JOHN AMIGOLAS YUKO MAHABUSU BAADA YA KUKUTWA AKIWA NA MWILI WA MFANYABIASHARA MAARUFU, GULAM, MARA BAADA YA KUPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI AMBAO WALIMVAMIA NA KUCHUKUA PESA ZAKE ZOTE NA KUKIMBIA NAZO HUKU WAKIMPIGA RISASI NA KUMUUA. JOHN ANASHIKILIWA NA POLISI.
ENDELEA ASUBUHI ya siku hiyo John alikuwa amesimama peke yake.nywele zikiwa timtim huku amepauka baada ya muda mrefu wa kutokuoga na mgomo wa kutokujishughulisha na chochote hadi atakapopata hatma ya jambo lililomleta hapo.
Mawazo yalikuwa yakimwandama baada ya usingizi wa mang’amung’amu ambao alikuwa hajauzoea. Hakuna aliyejali. Labda kwa kuwa hawakupewa taarifa juu. Juu ya hali aliyonayo. Hakuna aliyejua ni nini kilichomkumba.
Alipiga ndoo teke. Ndoo iliyokuwepo karibu na sehemu aliyokuwa amelala. Sababu za yeye kuwepo hapo pamoja na ndoo havikumwingia akilini. Alivuruga kitanda na kukaa chini huku akiwa ameshika kichwa chake.
Hasira zilikuwa zimempanda sana John ambaye alikuwa mahabusu kwa wiki moja sasa bila ya kupewa dhamana. Aliumia zaidi baada ya kuona hakuna msada wowote na kwamba alidhaniwa kwamba yeye ndiye aliyemuua mfanyabiashara mmoja wa magari.
Hiyo ni baada ya polisi kumwona yeye kwani ndiye aliyekutwa katika eneo la tukio pasipo kuwepo mtu mwingine. Eneo ambalo damu zilikuwa zimetapakaa baada ya watu wenye silaha kumvamia mfanyabiashara aliyekuwa tayari amekufa akiwa amelala chini.
Mfanyabiashara huyo, Gulam alikuwa akielekea benki kuweka fedha zake na mara alijikuta akiishia mikononi mwa watu wanne waliokuwa na bastola. Walimvamia na kumwibia hela zote na kisha kumuua. Watu hao walifanikiwa kukimbia na gari yao aina ya Mark II pasipo kukamatwa.
Katika kuwahi kumwokoa, John alikuta yule mfanyabiashara tayari ameshakata roho. Alijaribu kuwaita watu ili kusaidiana lakini baada ya mlio wa risasi kusikika watu walitawanyika na hivyo John alibaki pale peke yake hadi polisi walipofika dakika chache.
John alikuwa na bastola yake ambayo aliitoa mara tu baada ya kusikia mlio ule na kuishika. Hali hiyo alipelekea polisi kumkamata kwa kumshukia kwamba ni yeye aliyefanya mauaji yale baada ya kukutwa.
Bastola aliyokuwa nayo alikuwa akiitembea nayo siku zote kwani alikuwa na kibali cha kuimiliki. Wakati wa tukio hakuweza kuonyesha kibali na hivyo alifungwa pingu katika mikono yake.
Sasa aliishia mikononi mwa polisi kwani majambazi wale walifanikiwa kutoroka na pesa za mfanyabiashara yule. Alijaribu kujielezea kwamba siye yeye aliyefyatua risasi ile lakini polisi hawakumwelewa. Alipelekwa kituo cha polisi cha kati kwa ajili ya mahojiano na kupisha uchunguzi.
Gari lake aina ya Land Cruiser V8 liliachwa karibu na benki ambapo mauaji yalitokea. Hakujali na wala hakuwajulisha ndugu zake walifate. Aligundua kwamba alikuwa amelifunga vizuri na hivyo alielekea polisi.
***** John hakujua lililoendelea nyumbani kwao kwani alijua si rahisi ateseke mahabusu wakati Mzee wake anaweza kumwekea dhamana akawa huru. Akiwa bado kituoni ndani, siku inayofuata alipata taarifa juu ya kifo cha Mzee wake Amigolas. Baba yake mzazi. John alichanganyikiwa sana hadi kupoteza fahamu.
Hakuwa amemini kama ni kweli baba yake amefariki dunia. Baadhi ya askari walimsaidia kumpepea hadi akazinduka, alizinduka akiwa hajitambui vizuri. Bado alikuwa haamini kama ni mzee Amigolas aliyefariki.
“Amigolas, baba… Amigolas…baba,” ndio majina yaliyokuwa yakitajwa na John siku nzima. Hakujua juu ya familia yake kwani taarifa zilizokuja zilikuwa za baba yake kuuliwa.
Polisi walimwonea huruma lakini asingeweza kuachiwa kwenda kuona hadi uchunguzi wa tukio lake utakapokamilika.
Hakuna mtu aliyejua lolote kuhusu John kwani siku hiyo ndo siku ambayo nyumbani kwa kina John palipata pigo kubwa sana. Ni siku hiyohiyo John alikuwa aachiwe huru baada ya uchunguzi kuonyesha kuwa si yeye aliyeua.
“John aachiwe huru,” mkuu wa kituo alitoa kauli hiyo baada ya kupiga simu na kuongea na Afande Mushi.
“Naomba hilo file la John Amigolas, anatakiwa aje aweke saini. Na umtoe huko ndani. Taarifa kutoka kwa mkuu zinasema kwamba si yeye aliyeua. Afande Nicco, kamtoe huko aliko umlete hapa,” Afande Mushi alitoa amri na kusisitiza kwa afande Nicco ambaye alileta faili la John na kwenda kumtoa. Alikabidhiwa vitu vyake na kuruhusiwa japo alikuwa akionekana kutojitambua.
Alitoka nje ya Kituo cha polisi. Aliangalia uelekeo na kwanza alitaka kulifuata gari lake. Alitaka kujua ni kina nani waliotekeleza mauaji kwa baba yake na ni kwa sababu gani. Gari lake lilikuwa limeshaletwa hadi kituoni. Aliingia na kuwasha.
Aliifuata Barabara ya Uhuru kuelekea Hospitali ya Mount Meru, hospitali kubwa jijini Arusha. Alijua kwamba mwili wa baba ake utakuwa umehifadhiwa huko. Hakutaka hata kurejea kwanza nyumbani kwani angechelewa kupata uthibitisho kwa kuona kweli mwili uliopelekwa hospitali ni wa baba yake Mzee Amigolas. Alifika hospitali na kukuta umati wa watu ukiwa unafuatilia juu ya maiti zilizoingizwa hospitalini hapo asubuhi. Alisikia tu minong’ono ya watu ambao walikuwa wakisikitika kutokana na kuona maiti zikiingizwa na kupelekwa chumba cha kuhifadhia maiti.
Alisogea na kukutana na mmoja wa majirani zao ambaye alishirikiana na polisi kuzileta maiti hospitali hapo.
“Gaudence, ni…ni kweli maiti iliyoletwa ni ya baba yangu, tafadhali naomba niambie, we ni kama ndugu yetu. Tafadhali Bwana Gaudence,” John alikuwa akimuuliza Gaudence ambaye ni mmoja wa majirani zao huku akilia kwani alijua kuwapo tu kwa Gaudence hospitalini hapo kunadhihirisha ya kwamba mzee Amigolas amefariki kweli.
“Pole sana John, ni kweli na si baba tu, wameuliwa pia ndugu zako pamoja na mama yako Magdalena.”
“Unasemaje?” John aliishiwa nguvu na kukaa chini huku akilia. Gaudence alimsaidia kumwinua na kumpeleka katika gari lake alilokuwa amefika nalo hospitali.
“Usilie bwana John. Jikaze….hii ni kazi ya Mungu. Tuko pamoja.”
“Ina maana na wadogo zangu Isack, Neema na Jenipha?”
“Ndiyo John, wameshapelekwa chumba cha maiti, tunachosubiria ni taarifa za polisi kama watu waliowaua wanajulikana na itatangazwa pia katika vyombo vya habari baada ya uchunguzi,” Gaudence alimwambia John ambaye muda wote alikuwa amejiinamia huku akilia.
Aminata alikuwa ameshafika hospitali. Alikuwa anazunguka huku akifatwa na waandishi wa habari, alikuwa akielekea ndani kuonana na daktari mkuu wa hospitali hiyo. Baada ya muda alirudi akiwa anaangaza huku na huko. John alimtazama. Alihisi kukumbuka kitu lakini machungu ya kumpoteza mzee wake hayakumpa nafasi ya kutafakari lililotokea. Aminata alimfuata baada ya kujua kuwa ni John. Alimfuata ili kuthibitisha. “Habari yako kaka?” Aminata alimsalimia John ambaye alikuwa akimwangalia muda wote.
“Salama tu dada, karibu,” John alipata picha juu ya Aminata, alikumbuka kwamba alishawahi kumwona akiwa ameongozana na polisi wakati akikamatwa na baada ya hapo hakumwona tena hadi alipoachiwa huru.
“Inawezekana huyu ni mpelelezi,” aliwaza John huku akimwangalia Aminata aliyekuwa tayari amefika alipokuwa John.
“John, nadhani ndiyo wewe,” Aminata alimuuliza John jina lake kama kuthibitisha kweli alikuwa ndiye John mtoto wa Amigolas.
“Yes, ndiyo mimi. Kuna tatizo na mimi dada,” John hakuelewa Aminata alichomaanisha. Ndiyo kwanza ametokea mahabusu na sura ya Aminata aliikumbuka tayari. Hakujua Aminata alikuwa anashida gani na yeye.
“Nahitaji ushirikiano wako, baada ya kumaliza mazishi naomba unitafute,” Aminata alimaliza kuongea na kuondoka kulifuata gari lake. Aliwasha na kuondoka. John aliachwa na maswali kichwani. Alitakiwa amtafute Aminata baada ya mazishi ya ndugu zake.
***** Taarifa za vifo zilimfikia Antony ambaye alikuwa nchini Kenya. John ambaye ni pacha wake, alimfahamisha na hivyo Antony alipanga kurudi kumzika baba yake pamoja na ndugu zake. Maumivu yalikuwa makubwa sana kuwapoteza.
Baada ya siku mbili Antony aliwasili akitokea Nairobi nchini Kenya ambako alikuwa akifanya shughuli zake za biashara huko. Mzee Amigolas alikuwa amefungua maduka makubwa ya vitu mbalimbali vya umeme na nguo za kifahari. Maduka hayo yalisimamiwa na Antony.
Antony aliungana na ndugu zake katika mazishi huku akiwalilia sana. Ulikuwa ni msiba mzito sana kwa John na Antony ambao walibaki wenyewe. Antony alilia sana. Hakuamini macho yake kwa kuwapoteza watu wake wa karibu. Watu wengi walifika nyumbani kwa marehemu Mzee Amigolas. Na hii ni kutokana na kuwa maarufu kutokana na biashara zake.
Mzee Amigolas alikuwa ni mfanyabiashara maarufu wa madini aina ya Tanzanite. Alimiliki mgodi mkubwa wa madini hayo huko Mererani. Alikuwa ni tajiri mkubwa sana ambaye kutokana na utajiri wake na umaarufu wake, aliweza kushirikiana na matajiri wenzake kusafirisha madini nje ya nchi na kuyauza.
Utajiri wake ulijulikana kwa watu wengi. Alikuwa amewekeza kwa kujenga nyumba nyingi na hoteli mbalimbali mkoani Arusha pamoja na mikoani kama Dar ea Salaam. Pia maduka makubwa ya biashara nchini nan je ya nchi. Alikuwa ana nyumba kubwa sana maeneo ya Njiro aliyoishi pamoja na familia yake.
Alimuoa Magdalena na kufanikiwa kupata watoto watano yeye na pacha wake Antony, Isack, Neema pamoja na Jenipha.
Nyumba yake ilikuwa kubwa sana na yenye ulinzi mkali sana. Alimiliki magari mengi ya kifahari ambayo yalitumiwa zaidi na watoto wake. Watoto wake wawili mapacha John na Antony walikuwa wakisimamia baadhi ya biashara za baba yao. Antony ambaye ndiye aliyekuwa mdogo. Alikuwa akisimamia biashara za baba ake nchini Kenya. Wadogo zao Isack, Neema na Jenipha walikuwa wakisomea nchini Uingereza. Waliishi huko na mama yao Magdalena. Hadi mauti yanawakuta, walikuwa likizo kwa ajili ya sikukuu ya Chrismass na Mwaka Mpya. Hawakuwa na taarifa juu ya kuvamiwa usiku kwani wauaji walianza kuwaua walinzi wawili pamoja na mbwa wao kwa kuwapiga risasi kabla ya kufanikiwa kuingia ndani. Hakuna aliyesikia sauti ya risasi kwani walikuwa wameweka viwambo vya kuzuia sauti isitoke. Na huo ndiyo ukawa mwisho wa kuonana na ndugu zake ambao wote waliuliwa.
Hakuna taarifa za kukamatwa kwa wahusika japo polisi walikuwa wakiendelea na uchunguzi. Alitaka kumuuliza John kaka yake kama alikuwa akijua lolote linaloendelea kuhusiana na vifo hivyo. Hakujua wazo alilokuwa nalo John kwani alihisi John lazma atakuwa na la kufanya na yeye angetoa ushirikiano.
“Kaka, unampango gani baada ya haya yote,” Antony alimuuliza John siku mbili baada ya kumaliza mazishi.
Wakati huo John alikuwa akifikiria namna ya kumpata Aminata. John na Antony walianza kufatilia mali za baba yao ili wazirithi. Walizunguka kote na kuongea na watu waliokuwa wameachiwa na kujua maendeleo ya biashara hizo. Walifanikiwa kwenye mali nyingi isipokuwa mgodi wa baba yao.
Utata ukaanza kugubika kwenye suala la umiliki. Baada ya kifo cha baba yake mgodi ulisimama kufanya kazi. Hakuna kilichoendeshwa na wafanyakazi wote walitawanyika wasijue la kufanya.
Hata wachimbaji hawakuelewa. Tukio lililowashangaza wachimbaji wote. Baadhi ya watu walifika na kuwaamuru wasitishe uchimbaji wa madini hadi watakapoambiwa. Iliwashangaza sana. Wachimbaji wote walijua kwamba mwisho wao wa kufanya kazi umefika.
“Mgodi umeuzwa, hahitajiki mtu hapa…..ondokeni,” mmoja wa viongozi wa juu wa kundi la Mosses Ndula, Mbashala aliwapa taarifa. Hali hiyo ilileta sintofahamu huku baadhi ya wachimbaji wakilalamikia.
“Mbona tusipewe taarifa mapema, mnakuja kutuambia wakati tuko kazini, Mzee Amigolas hawezi kutufanyia hivyo, hata watoto wake hawana roho mbaya hivyo, na kama angekuwa anauza mgodi kweli angetufahamisha mapema na kujua hatma yetu, nyie mnakuja tu mnatuambia mgodi umeuzwa…. nendeni, sisi tuende wapi?” Mmoja ya wachimbaji aliyejulikana kama Mbago, ambaye alikuwa ndiye kiongozi wa wa wachimbaji ambaye anamjua sana bosi wake, Mzee Amigolas na watoto wake alikuwa akipingana na watu waliotumwa na Mosses Ndula.
“Tuonyesheni basi vielelezo siyo mnatuambia tu kwa mdomo, kama ni uongo je? Siku zote karatasi za uthibitisho zinatangulia….tutajuaje kama nyie ni matapeli.” Mbago aliwataka watoe vielelezo ili wapate uhakika wa kile walichoambiwa.
“Hizo nakala za maelezo hatujaja nazo, ila ukweli ndiyo huo. Mgodi umeuzwa na mnatakiwa mfuate utaratibu uliowekwa. Hakuna chenu hapa. Kuanzia sasa hakuna atakayewalipa,” Hakuna aliyemwelewa. Walianza vurugu. Mbashala na wenzake waliwanyooshea bastola wachimbaji lakini hawakurudi nyuma wala kutetereka.
Baada ya kuona wanazidi kusogea. Mlinzi wa Mbasha alifyatua risasi moja hewani. Hata hivyo wale wachimbaji walizidi kiusogea huku wakiokota mawe makubwa.
“Aaagh…mama n’kufaa,” mmoja wa wachimbaji alipiga kelele baada ya risasi nyingine kufyatuliwa na kumpata ya begani. Sasa waliamua kurusha mawe.
“Nani kakuambia upige risasi.” Mbashala alimfokea Yule mlinzi huku wakiingia haraka kwenye gari na kuondoka. Waliwarushia mawe na kufanikiwa kuharibu kioo cha gari lao.
Baada ya kufanikiwa kuwafukuza. Mbago aliwaita wenzake wote na kujikusanya kwa ajili ya kikao ambacho kngewasaidia kujua hatima yao katika machimbo hayo.
“Jamani sikilizeni, naomba tuzungumzie hili jambo,” Mbago aliwatuliza wachimbaji ili azungumze nao. Wachimbaji wote walitii na kukaa chini huku wengine wakiwa wamesimama kumsikiliza kiongozi wao. Yule aliyepigwa aliopelekwa hospitali na kuendelea na matibabu.
“Hili jambo sidhani kama tunakubaliana nalo wote, au siyo jamani?”
“Ndiyoo!Ndiyooo!” Wachimbaji walijibu kwa sauti za kelele kuashiria kuafikiana na kiongozi wao.
“Mwenzetu kapigwa risasi. Inaonyesha hawa watu wanataka kutuingilia kwa nguvu bila kufuata sharia. Wote tunaona kwamba hakuna ndugu au motto yeyote wa mzee wetu Amigolas aliyefika kutueleza. Hata hao wasaidizi wake hawajaja. Iweje wachukue tu mgodi. Lazima tujue.”
“Ndiooo! Ndiooo!” wote walishangilia kauli aliyoitoa Mbago.
Sasa, mi nadhani si jambo zito sana. Mi n’taenda hukohuko nyumbani kwa bosi n’kajue moja. Kama kuna kazi au hakuna. Sisi tumeajiriwa na kama mgodi umeuzwa walipaswa watuambie. Kwani watoto wa Mzee Amigolas si wapo. Mi nafahamiana na John, mtoto wa marehemu. Nitaenda kwao kuongea naye. Hata yeye anaweza kutusaidia. Kesho nitakwenda kujua moja.”
“Ndiooo!” Haki haitapotea. Tujue mojaaa,” wachimbaji walishangilia baada ya kusikia kauli ya kiongozi wao. “Nitaongozana na Masud na Baraka,” Mbago aliwateua wachimbaji wawili ambao angeongozana nao hadi nyumbani kwa Mzee Amigolas.
“Tukamjulieni hali mwenzetu aliyepigwa risasi.”
Polisi walikuwa wameshafika katika eneo hilo. Walihakikisha hali ya usalama inarudi. Mbago alikuwa ameshatoa taarifa polisi juu ya watu waliokuja kuuvamia mgodi na kuwafukuza kazi kwa nguvu. Polisi waliwapa taarifa juu ya mgodi ule. Mosses Ndula alikuwa polisi pamoja na wakili wake. Walikuwa wamepeleka hati ya kuonyesha kwamba kauziwa mgodi na Mzee Amigolas kabla ya kufariki na kwamba umiliki wake ungeanza baada ya miezi sita.
**** John alikuwa njiani akielekea kituo cha polisi cha kati. Hakuwa na taarifa zozote kuhusiana na yaliyotokea Mererani baina ya wachimbaji na watu wa Mosses Ndula. Kichwani kwake alikuwa akifikiria juu ya Aminata. Alitaka kujua ni vipi atampata Aminata.
Aminata Peter, ni mwanamke aliyesomea masuala ya upelelezi na kuwa moja wa wapelelezi wakuu wa jeshi la polisi. Taaluma yake ilimfanya ajuane na watu wengi ikiwapo kugundua njama mbalimbali za watuhumiwa.
Kama ilivyokuwa kwa John na Antony, Aminata alipata pigo kama lililowapata baada ya baba yake pamoja na mama na ndugu zake kufariki baada yua kuuliwa na majambazi wakati wakiwa njiani. Tukio hilo lilitokea baada ya kuwekewa mawe makubwa barabarani na hivyo kushindwa kupita na kuvamiwa.
Baada ya kufanikiwa kuwazuia kupita. Majambazi hao walipora vitu vyao vyote pamoja na kuwafyatulia risasi na kuwaua wote.
Wakati wa tukio hilo la kusikitisha Aminata alikuwa yuko shuleni. Shule ya bweni na hivyo hakuweza kusafiri pamoja na familia yao. Alilia sana kuwapoteza ndugu zake. Upelelezi ulikuwa ukifanyika lakini matokeo hayakumridhisha Aminata ambaye alikuwa na shauku kubwa sana ya kutaka kuwajua wauaji.
Baada ya kumaliza kidato cha sita, Aminata alijiapiza kufa na kupona hadi ajue mtandao wa wauaji wale. Ikiwezekana autokomeze kabisa. Hakumwambia mtu mwingine yeyote juu ya mpango wake huo. Alianza msako wake taratibu.
Alipenda kutoka mida ya usiku ili akakutane na baadhi ya vijana na kuzoeana. Alijua lazima watakuwa baadhi wanaufahamu huo mtandao.
Kwa mara ya kwanza Aminata anaingia ndani ya himaya ya Mosses Ndula. Anakutana na sura za watu wajuao kazi. Sura za kila aina ya wahuni. Haogopi.
Anakutana na kijana mmoja ambaye alikuwa anavuta sigara mlangoni. Anamwangalia sana kisha anapita. Yule kijana anamfuata.
“We nani?” anamuuliza Aminata.
“Mambo kaka angu, mi naitwa Stellah. Nimeshawahi kukuona mahali mjini karibu na Posta.
“Inawezekana,” yule kijana aliwaza huku akionyesha kuvutiwa na Aminata. Aminata alikuwa ni mzuri sana na hivyo kila aliyemwangalia alimtamani.
“Unataka nini huku?” alihoji yule kijana.
“Nadhani nitakuwa nimepotea njia. Samahani sijui huku ni wapi. Naomba unisindikize niweze kutoka huku. Samahani lakini kaka yangu.
“Aah, niko kazini hapa…lakini nitakusindikiza uweze tu kutoka hapa.” yule kijana alikuwa ndiye mlinzi wa mlangoni katika ngome ya Mosses ndula iliyokuwa eneo la Kambi wa Fisi. Huko ndiko Mosse alijua kwamba hasingeweza mtu yeyote kujua kinachoendelea.
“Asante kaka yangu,”aminata alimshukuru yule kaka na kisha alimuuliza jina lake.
“Naitwa Dula,” alisema yule kijana.
“Sasa Dula, nitakutafuta siku nyingine basi. Nimependa ulivyonisindikiza. Napenda tuwe marafiki zaidi. “Aaah, siamini,” Dula aliwaza huku akitabasamu kwa kutokuamini kama ni yeye. Hakujali kwamba ameacha mlango peke yake na kama atatafutwa na mkuu wake ambaye alikuwa ndani. Alimwacha Aminata akiondoka na kumwachia namba za simu ili wawasiliane.
Dula alirudi haraka. Alifika mlangoni na kwa bahati nzuri hakuna aliyefika hapo tangu atoke na Aminata. Aliendelea kusimama hapo hadi Mosses alipotoka na kuchukua gari lake na kuondoka pamoja na wapambe wake.
Aminata alifika nyumbani. Ilikuwa ni usiku wa saa tano. Hakuogopa kutembea mwenyewe. Baada ya kuondoka mitaa ya Kambi ya Fisi. Alichukua teksi iliyompekleka hadi nyumbani kwake Sakina. Alijilaza juu ya kitanda na kuanza kutafakari juu ya kumwingia Dula ili aweze kumwambia kuhusiana na Mosses pamoja na kundi lao wote.
***** Asubuhi alimpigia simu Dula na kumtaarifu kwamba wakutane Café la Azziz.
“Unapajua hapo.”
“Ndiyo, lakini ni sehemu hatari sana kwetu sisi hasa ukizingatia na jinsi tunavyojulikana mjini.”
“Unamaanisha nini Dula? Acha woga, we ni mwanamume. Njoo mjini bana. Huko kwenu mbali.”
“Ok poa bibie. Nakuja hapo.” “kumwacha mtoto mzuri kama yule…ni sawa na kuokota dhahabu alafu kuitupa ukiwa na akili zako timamu, waccha niende. Nitamdanganya bosi,” aliwaza Dula huku akitafuta kijana mwenye bodaboda ili aweze kumfikisha aliko Aminata.
Dula alichukua usafiri wa bodaboda hadi alipokuwa Aminata. Kutoka eneo la Kambi ya Fisi hadi Café la Azziz haikumchukua zaidi ya nusu saa. Alimkuta Aminata akimsubiri.
“Dula nikuombe kitu,” Aminata alimwambia Dula mara baada tu ya Dula kushuka katuika bodaboda. “Nini tena bibie?” alihoji Dula.
“Samahani lakini, sipendi harufu ya sigara.”
“Aaah, hilo tu bibie? ok nikiwa na wewe sitovuta hadi niondoke.”
“Ntashukuru sana.”
“Vipi bibie, za tokea jana?”
“Nzuri tu Dula.”
Dula alikuwa akimwangalia sana Aminata ambaye alikuwa akiendelea kunywa soda yake taratibu. Aliupenda uzuri wake. Alijiona mwenye bahati hasa baada ya kumwona Aminata akiomba msaada na kutaka kuwa marafiki. Hakujua lengo hasa la Aminata hadi kufanya hivyo.
Aminata aliutumia mwanya huo kuwajua vizuri. Alifurahia ushirikiano na Dula. Kila alipomhitaji Dula alikuwa akifika mara moja. Wakati mwingine alimfuata yeye ili Dula asijue lengo lake. Hata baadhi ya rafiki wa Dula walianza kumjua Aminata.
Wakiwa katika ukumbi wa starehe wa Triple A. Aminata alitaka kujaribu bahati yake kwa kumuuliza mengi kuhusiana na kundi lao. Kwa kipindi kifupi cha kujuana na Dula aliweza kuonana na wengi katika kikundi hicho akiwemo Mosses ambaye baada ya Dula kumtambulisha alionekana kumtamani sana Aminata.
“Unakaribisha sana shemeji. Wakati wowote.” Alisema Mosses kisha kutoka baada ya kumsalimia Aminata.
Aminata alimwangalia sana. Mosses alikuwa ni mrefu mweupe. Sura yake ilikuwa ikifanana na chotara wa Kiarabu. Ni Mnyamwezi wa Tabora lakini maisha yake alikulia Arusha. Alifanikiwa kusoma hadi kidato cha sita. Ni biashara za magendo ndizo zilizomfanya Mosses asiendelee na chuo kwa ni alifaulu vizuri lakini pesa ilimfanya asitamani tena kusoma. Na huo ndio ukawa mwisho wa kurejea yaliyo vitabuni.
Alianzisha kampuni ya magendo ambayo haikusajiliwa ya kununua magari na kuyauza. Baada ya miaka sita iligundulika lakini hawakuweza kumkamata kwani alikimbilia nchini Kenya na kuishi kwa miaka miwili. Baadaye Mosses alirudi na kuanza ujambazi. Ngome yake aliiweka katika msitu mmoja wa Kambi ya Fisi. Huko hakuweza kuonwa na yeyote kwani alijiimarisha kwa kuweka uzio na walinzi wa kutosha. Alianza kufanya ujambazi na utekaji wa magari akishirikiana na watu wake.
***** Aminata alifanikiwa kujua juu ya Mosses. Sasa roho yake ilitulia. Hakujali kuhusiana na kifo cha Dula ambaye baada ya kubainika ametoa siri za kundi.. Mosses alimpiga risasi na kufa. Aminata baada ya kusikia habari hizo aliamua kujificha kwa muda.
Alikimbilia jijini Dar es Salaam ambako aliamua kusomea masuala ya Upelelezi na jeshi. Alijua Dula hakumdanganya baada ya kumweluezea ukweli ya siku walivyoteka gari la mzee Peter na familia yake na kuwaua kisha kuchukua mali.
Aminata alitumia mbinu kubwa sana kumshawishi Dula ili amwelezee. Ni pale alipoamua kumvulia nguo akimaanisha kwamba ni wapenzi. Hapo sasa Dula alidiriki kuunyanyua mdomo wake na kumwambia Aminata kila kitu.
Usiku huo Dula alijua ungekuwa mrahisi sana. Baada ya kumwambia Aminata juu ya siri za kundi lake. Aminata alimtamkia Dula kuwa anampenda sana na kumwahidi kuwa wake. Dula alifurahi sana. Alimkumbatia Aminata kwa nguvu na kumbusu. Hapo ilikuwa ni kazi rahisi. Dula alijiandikia ushindi kwa mtoto mzuri Aminata.
“Mbona sikuelewi tena Aminata,” Dula alihoji baada ya kumwona Aminata akitoka kitandani na kukaa kitako katika moja ya masofa yaliyokuwa katika chumba cha hoteli waliyofikia.
“Hapana Dula, usijali. Siko tayari leo. Nimeumwa sana leo.”
“Kwa hiyo tutalala tu hivi hivi?”
“Siyo hivyo. Ni kwa leo tu. Wewe ni mpenzi wangu. Siku yoyote utanitumia uwezavyo.”
Dula alikubali kwa shingo upande na kulala.
***** Aminata alifanikiwa kumaliza mafunzo yake ya upelelezi. Alirudi Arusha na kujiunga moja kwa moja na Jeshi la Polisi. Ni ujanja wake na uchapaji kazi wake ndio ulipelekea kutunikiwa cheo cha Ofisa Upelelezi. Ilikuwa ni furaha kwake.
Kati ya mambo ambayo aliyafanya ni uchunguzi na kugundua biashara ya dawa za kulevya iliyomhusisha kigogo mmoja mkubwa serikalini.
Ni katika mpaka wa Tanzania na Kenya. Eneo liitwalo Namanga ndipo tukio hilo lilipotokea. Akiwa kati ya maafisa wapelelezi wadogo na walioibukia katika kazi hiyo. Aminata aliiamrisha kushushkwa moja ya mabegi ambalo ndani lilikuwa limesheheni nguo. Aliliangalia lile begi na hasa baada ya ofisa mmoja mkaguzi kuliwekea alama kumaanisha kwamba lilikuwa safi na kwamba hakukuwa na chochote kibaya. Ofisa huyo alizima alamu ya mashine ya kukagulia na kuipitisha juu ya begi hilo. Baada ya kumaliza aliiwasha. Aminata alikuwa ameona tukio hilo.
“Nasema shusha tena hilo begi. Sijaridhika na ukaguzi wake.” ofisa yule aliogopa kidogo na kumjia juu Aminata.
“Nimelikagua, halina shida. Haya mzigo mwingine.” yule ofisa aliamrisha baada ya lile begi kupakiwa kwenye gari.
“Nimesema, fungua begi,” Aminata alitoa tena amri ambayo safari hii yule ofisa aliitii na kufungua begi. Aminata alitumia kifaa maalumu na kugundua ndani ya lile begi kulikuwa na dawa za kulevya.
Haraka alichukua simu yake ya upepo na kuwasiliana na polisi ambao walifika maramoja na kuwachukua wale wahusika ambao walikuwa wamewekwa chini ya ulinzi mkali.
Walipelekwa Kituo cha Polisi cha Kati cha mjini Arusha kwa ajili ya mahojiano huku uchunguzi ukiendelea kuhusiana na biashara hiyo. Watuhumiwa baada ya uchunguzi walifikishwa mahakamani akiwemo kigogo wa serikalini ambaye ndiye aliyewatumia watuhumiwa wenzake kuziingiza dawa hizo zilizotokea nje ya nchi. Wakati wa sherehe moja kubwa ambayo iliwahusu maofisa wapelelezi. Aminata alipata bahati ya kupandishwa cheo na kuwa Ofisa mkuu. Baadaye alihamishiwa jijini Dar es Salaam. Alishindwa kupinga kwani mkuu wa polisi alitaka iwe hivyo. Aminata alihamia Dar es Salaam.
Huko Dar es Salaam, palikuwa hapakaliki. Mara nyingi alirudi Arusha kwa ajili ya kazi yake moja tu. Kazi ya kuuangamiza mtandao wa Mosses Ndula. Ulikuwa ni mtafutano baina yake na Mosses Ndula ambaye alidhamiria kumweka Aminata mikononi mwake.
***** John alikuwa hana raha. Alimfikiria sana wakati huo. Alikumbuka kwamba hakumwachia namba za simu Aminata bali alimwambia tu amtafute baada ya mazishi ya ndugu zake.
Alifikiria sana atampataje na mwisho aliamua arudi kituo cha polisi kwani mara ya kwanza kufika kituoni hapo alikuwa amefungwa pingu huku Aminata akiwa ni moja ya watu waliompeleka kituoni hapo kutokana na kesi yake kuwa kubwa japo iligundulika kuwa si yeye aliyemuua mfanyabiashara anayedaiwa kuuliwa. Aliingia na kumkuta Afande Nicco na kumsalimia.
“Habari yako afande.”
“Ahh! We mwalifu, umerudi tena, umejileta eeh?” Afande Nicco aliongea kwa mzaha uliosababisha John acheke.
“Karibu tena, leo umekuja kumshtaki mtu au kunisalimia tu?” Aliendelea na utani afande Nicco.
“Hapana nimekuja kukusalimia na kuulizia jambo moja. Kuna dada mmoja alikuwa pamoja na Afande Mushi waliponileta siku ya kwanza. Anaitwa Aminata.”
“Aminata, we unataka kutembea na ofisa upelelezi?” Alisema Afande Nicco kwa mshangao na kauli zake za utani. John alicheka kidogo.
“Hapana, kuna jambo anataka nizungumze naye, aliniambia nimtafute.”
“Kwani huna namba zake za simu?”
“Hapana, hakunipa siku hiyo. Kama unayo naomba unisaidie.”
“Sawa mi n’takupa namba zake za simu na kwa nini hakukuachia namba zake?” Alihoji Afande Nicco.
“Sielewi, ila alisema tu nimtafute.” Afande Nicco alimpa John namba za simu kisha waliagana. John aliwasha gari lake na kuelekea nyumbani. Alichukua zile namba na kumpigia Aminata.
“Haloo!”
“Habari yako, sijui nani mwenzangu?” Sauti ya upande wa pili ilikuwa ni ya Aminata ambaye alitaka kujua ni nani aliyempigia simu.
“John, mtoto wa Amigolas, marehemu sasa, tulikutana Hospitali ya Mount Meru na kunitaka n’kutafute baada ya mazishi ya ndugu zangu.”
“Ooh! John, pole sana. Ila umechelewa sana kunitafuta. Mimi nipo hapa McDonald’s Pub kama utaweza kufika hapa muda huu itakuwa vizuri zaidi.” Aminata aliongea kwa furaha baada ya kujua aliyempigia simu ni John.
“Nakuja hapo sasa hivi Aminata.”
“Sawa nakusubiri John.”
Aminata alikumbuka dhamira yake. alijua akiwa na John mpango wake utafanikiwa kwa asilimia mia moja. Alijua pigo alilolipata yeye ni sawa na alilolipata John na hivyo ingekuwa rahisi sana kufanya kazi pamoja.
Alikuwa tayari ameshaijua vyema familia yote ya mzee Amigolas. Aliijua baada ya kutaka kuwa katika upelelezi wa wauaji wa familia hiyo.
Japokuwa alishafahamu mtandao mzima lakini Aminata hakudiriki kuwaeleza polisi juu ya mtandao huo kwani lengo lake lilikuwa ni moja tu. Kulisambaratisha.
****** John aliwasha gari lake . Askari wa mlangoni aliwahi kufungua geti na John kuondoa gari kwa kasi ili amuwahi Aminata. Ilimchukua dakika 10 mpaka kufika McDonald’s Pub. Alikuta magari mengi nje. Alilipaki gari lake karibu na mlango wa kuingilia ndani. Aliteremka na kutoa simu yake na kumpigia Aminata.
“Haloo Aminata.”
“John, njoo moja kwa moja hadi counter, nipo peke yangu hapa.”
“Sawa Aminata, nakuja hapo sasa hivi,” John alielekea hadi counter na kumkuta Aminata akiwa ameshikilia glasi ya wine. Mhudumu alipomwona John alimkaribisha.
“Karibu kaka, n’kusaidie nini?”
“Hapana sitatumia chochote.”
“John, you should take something… mhudumu, mletee wine kama yangu,” Aminata alimwagizia John wine. Walikaa na kuanza kuongea baada ya wine kuletwa.
“John,” aliita Aminata.
“Yes Aminata, nakusikiliza.”
“Pole sana na msiba wa wazazi wako na ndugu zako. Nauhakika polisi bado wanaendelea na uchunguzi. Mimi ni ofisa upelelezi ndiyo maana uliniona siku ambayo ulikamatwa niliongozana pamoja na Inspekta Morris na Afande Mushi.
Wote kwa sasa wanafanya uchunguzi wa nani anahusika na vifo vya wazazi wako na ndugu zako.”
“Natamani sana kuwajua watu hao,” alisema John huku kainamisha kichwa chini na kusababisha huruma kwa Aminata.
“Utawajua John, kabla hawajakamatwa, mimi na wewe tutawakamata.”
“Tutawakamata vipi lakini?” Alihoji John kwa mshangao kwani hakuwa na uzoefu wa kukamata wahalifu. Iweje apewe jukumu hilo.
“Mi siyo polisi, n’tawezaje Aminata.”
“Namaanisha, nataka ulipe kisasi na si kuwakamata. Kama walivyoua ndugu zako, yapasa na wao waangamizwe. We ni mwanamume. Amka. Wale wakikamatwa na polisi baadaye watatoka. Inatakiwa wamalizwe kabisa.”
“Kumbe unawajua Aminata?” Alihoji John.
“Ndiyo John, ni mtandao mkubwa sana wa kihalifu, unaoogopeka sana. Kiongozi wao anaitwa Mosses Ndula, huwa hakai hapa nchini, anakuja bila yeyote kujua nakuondoka. Na huyo ndiye jabali lao. Ndiye aliyewatuma watu wake wawaue wazazi na ndugu zako. Inawezekana pia wakawa wanawatafuta na nyie wawili.”
“Sisi wawili, mi na nani?” “Unamfahamu pacha wangu, unamfahamu Antony?”
“Ndiyo John, kwenu nawafahamu japo nyie hamnifahamu. N’mefanya kazi nyingi sana kumsaidia baba yako. Na hiyo ilinifanya niwajue….. Nadhani ni muda wa kwenda. Nitakuelezea mengi tukifika kwangu.”
“Naomba tuongozane, twende pamoja nyumbani kwetu ukapafahamu,” John alimwambia Aminata ili waongozane kwenda kwao.
“Sawa John,” Aminata alikubali na kuongozana na John. Hakutumia usafiri wake. Aliliacha na kuondoka pamoja na John aliyekuwa na usafiri wake.
***** Walitumia dakika ishirini tu kufika Njiro nyumbani kwa kina John. Walikuta watu watatu wakiwa wamesimama nje ya geti. Mlinzi aliwafungulia na kuingia. John alikuwa bado hajawatambua hadi alipofikia geti kabisa. Mlinzi alifungua geti kubwa na kuliruhusu gari la John kuingia. John sasa alimtambua mmoja kati ya wale wageni.
“Hawa ni wachimbaji wa mgodi wa baba,” John alimwelezea Aminata.
“Namkumbuka mmoja tu, aliyevaa kapelo. Sijui wanataka nini.” John alishuka kwenye gari na kumfungulia Aminata mlango, alimkaribisha kisha kuwafuata wale wachimbaji.
“Mbago bila shaka,” John aliuliza.
“Ndiyo mkuu, ni mimi, habari za siku nyingi bosi?” Antony naye alikuwa akitoka nje baada ya kusikia gari likiingia na watu wakiongea. Alisimama mlangoni. Aminata alimwangalia sana kisha kumgeukia John. Hakuona tofauti kati yao. Walikuwa wamefanana sana.
“Salama tu, habari za Mererani bwana Mbago.” Aliwasalimia na wachimbaji wengine walioongozana na Mbago.
“Kule hali siyo nzuri kabisa bosi.”
“Kwa nini sio nzuri?” Alihoji John.
“Hatuelewi hatma yetu kwani mgodi umeuzwa bila ya kupewa taarifa. Ndio tumechukua uamuzi wa kuja kujua moja ikiwamo kuhoji imekuaje kimyakimya.” Alielezea Mbago kwa masikitiko huku wenzake wakiitikia kwa kichwa kuashiria anachosema ni kweli.
“Mgodi umeuzwa?” John na Antony kwa pamoja walitahamaki. Haraka Antony aliingia ndani na kutoka na hati ya umiliki wa mgodi inayoonyesha mmiliki halali wa mgodi ni baba yao Amigolasi.
John aliangaliana na Aminata kwa muda. Hakujua amwambie nini hadi pale Antony alipotoka nje na karatasi iliyoonyesha hati ya umiliki wa mgodi.
“Haiwezekani, hati hii hapa,” Antony aliwaonyesha. “Hii si ndo hati ya mzee? John embu itazame mwenyewe. Ni nani huyo anayeleta mchezo?” Antony alimkabidhi ile hati John ambaye aliiangalia kisha nay eye kumpa Aminata aiangalie.
“Nani kaja kuwapa hizo taarifa? Alihoji John huku akimwangalia Aminata kana kwamba Aminata alijua kinachoendelea. Aminata alikuwa kimya akisikiliza malalamiko na utetezi wa pande zote mbili. Wachimbaji na mabosi wao. Mbago aliwaelezea namna ilivyokuwa hadi wakaamua kuwafukuza kwa mawe na kisha kuitisha kikao cha kujadili safari ya kuja kuonana na wao.
“Mmefanya vizuri sana. nashukuru sana kwa hizo taarifa. Kuna watu wanataka kutudhulumu haki yetu. Labda sio mimi.” John alisema kwa ukweli huku akimrudishia Antony ile hati ili aipeleke ndani.
“Tutalishughulikia hilo, ila waambie wenzako kwamba mgodi haujauzwa, kazi ipo na mambo yakitulia m’taendelea kama kawaida.” Antony alihitimisha ili kuwaruhusu Mbago na wenzake wawawahi kuwajulisha wenzao.
“Tunashukuru sana bosi. Siye tunaenda. Mbaki salama.” Mbago na wenzake waliondoka baada ya kupata jibu. Hawakujua kwamba wamewaachia John na Antony kazi kubwa sana. John alionekana kuchanganyikiwa.
**** Ni aminata peke yake ndiye aliyeweza kumliwaza John. Aliamua kuwa naye karibu zaidi ili aweze kumtoa katika hali ile. Si kwa hilo tu bali pia Aminata alikuwa anaonyesha kila dalili za kumpenda John kimapenzi. Ni kwa kipindi kirefu sana amekuwa kattika hali hiyo ya upweke kwa ajili ya kazi.
Aminata alikuwa ameshapajua nyumbani kwa kina John na hivyo alifika mara kwa mara ili kuendeleza mipango yao.
Aminata alipata nafasi ya kuongea usiku huo. Hakwenda nyumbani kwake bali aliamua kulala nyumbani kwa kina John kwa ajili ya kuongea mengi. Aminata alimsimulia John yote yaliyomtokea hadi akaamua kuwa mpelelezi.
“Niliamua nikajiapiza kwamba sitawasamehe nan i lazima niwakamate na niwaangamize mimi mwenyewe. Baada ya kukufatilia na kujua wewe ni mtoto wa mzee Amigolas, na bada ya kuona pigo nililolipata mimi na wewe umelipata pamoja na pacha wako. Na pia John wewe unaonekana si lele mama. Wewe na Pacha mnaonekana mmeshiba sana. ni watu wenye nguvu za kupambana. Hivyo kwa mafunzo niliyoyapata tukichanganya na ninavyowaona nyie. Tutawamaliza hata kama wako wengi vipi.” Aminata alimwambia John huku akicheka kwa lengo la kumshawishi wawe pamoja.
John alisimama. Alijiona kama mshindi na asiyeogopa hatari yoyote. Alikumbuka wazazi wake na ndugu zake walivyouliwa. Aliwakumbuka Mbago pamoja na wenzake waliokuja siku chache zilizopita kuwaeleza juu ya migodi. Yeye kama mwanamume iweje akae nyuma wakati Aminata amejitoa kupambana dhidi ya dhulma.
“Tuko pamoja Aminata lazima tuwaangamize. Kesho asubuhi nitaongea na Antony tujue tunaanza lini kazi. Hata kama wameshajimilikisha mgodi lazima tuurudishe. Hizo ni dhuluma. Hatuwezi kuziacha zikatufilisi sisi. Walishachukua roho za ndugu zangu. Sasa wachukue na yakwangu nay a Antony kama wanaweza.” John alisema kwa hasira kali.
Aminata alimfuata na kumshika kisha kumkalisha juu ya kitanda. Pamoja na baridi kali ya mjini Arusha, John alitokwa na jasho kali. Joto lilisababishwa na hasira. Hapo Aminata alimwelewa John kwamba yu tayari kwa mapambano.
“John,” aliita Aminata…. “Wewe ni mwanamume unayeonekana shupavu. Ni mwanamume unayeweza kupambana na pia unamvutia sana mwanamke. Mvuto wako siwezi kuuvumilia pamoja na kwamba unayo hasira. Leo nipo kwako. Sitalala peke angu. Najua Antony ameshalala. Niazime mwili wako kwa usiku huu wa hii baridi,” Aminata alishindwa kuvumilia kila alipomwangalia John ambaye alikuwa amevua shati na kubakiwa na kaushi iliyombana vizuri na kufanya misuli yake itoke nje.
Aminata alipata nafasi ya kuushika mwili wa John kila alipokuwa akimbembeleza. Hapo alijihisi kumvamia John japokuwa alikuwa na hasira. Alijaribu umtuliza mpaka alipoweza kumwambia alichokitaka.
John aliyasikia aliyoyasemaAminata. Hakuonyeshwa kushangaa kusikia maneno yale. Hakuwa na kufanya zaidi ya kunyinyakulia ushindi murua wa mezani baada ya mpinzani wake kuweka mikono chini kuashiria hawezi kushindana.
Ukawa ni mgeuzano wa kila aina katika mbao za futi sita kila upande. Godoro la kisasa zaidi ya lilivyotumika kabla lilionja joto ya migusano na vilio vya mahaba kutoka kwa ofisa mpelelezi Aminata.
Tukio liliendelea tena na tena. Ukawa ni usiku wa bashasha uliolakiwa vizuri na miili iliyokuwa tayari kujifunga na kuwa pamoja. John alisahau hasira zake na kudhulumiwa kwa mgodi. Aminata naye akasahau kazi yake ya ofisa upelelezi. Mtifuano mkali ulimalizika pakiwa panaelekea kupambazuka. Wote walifurahia mchezo huo Asubuhi John alimfata Antony. Alimwelza juu ya kila alichoambiwa na Aminata. Antony hakuwa na pingamizi kwani alijua hakuna njia nyingine endapo wahusika walishajimilikisha mgodi. Hivyo alijiunga nao ili kuhakikisha wanafanikiwa.
John alimwita Aminata na kumweleza juu ya Antony kukubali. Aminata alifurahi sana. alimwangalia Antony vizuri kwa lengo la kuwatofautisha pindi watakapokutana. Antony ambaye ndiye aliyekuwa mdogo, alikuwa mweupe kidogo kuliko John. Pia Antony alikuwa ni mpole kwa zaidi ya John.
“Mmefanana sana nyie watu. Antony ni mweupe hapo ndo sitawachangamya.” Antony aliangaliana na John kisha wakacheka.
“Acha utania wako Aminata,” John alisema huku akimshika mkono Aminata na kumtambulisha vizuri Antony.
“Huyu anaitwa Aminata. Ni shemeji yako.”
“Nilishaelewa mapema, nilikuwa nasubiri tu nisikie kauli yako. Hongera kaka.”
“Asante.” Hapohapo Aminata nay eye akaongea kuwaambia John na Antony juu ya mpango wake.
“Nataka kwanza mjue kitu gani tutaanza nacho. Kazi ni kubwa sana kuliko huku kutambulishana. Inahitajika mfanye mazoezi hasa ya kulenga shabaha. John we ulikutwa na bastola lakini sidhani kama unajua kuitumia vizuri.”
“Najua sana, sema nakusikiliza.”
“Mmmh. Na mbona wale majambazi walikimbia hukuitumia wakati yule mfanyabiashara alivyovamiwa benki? Au hukujua kama uko nayo?” John na Antony walicheka sana kisha wakasema kwa pamoja.
“Basi tufundishe ofisa.”
Zoezi likaanza mara moja. Aminata aliwapeleka sehemu maalumu wa ajili ya kuwafundisha nyumbani kwake Sakina.
Jambo la kwanza alilofanya Aminata ni kuwafundisha mbinu mbalimbali za kutumia. Aliwafundisha kutumia silaha kwa kulenga shabaha pamoja na namna ya kuwa makini wakati unapokabiliana na adui yako anayekuhisi unamchunguza. Baada ya muda wote walijua.
AMINATA ANAFANIKIWA KUWASHAWISHI JOHN NA ANTONY KUJIUNGA NAYE KWA AJILI YA KUANGAMIZA KUNDI LA MOSSES NDULA. ANAWAPA MAFUNZO AMBAYO ALISHAYAPATA AKIWA KATIKA MAFUNZO YA JESHI.
JE WATAFANIKIWA KATIKA MPANGO WAO WALIOUDHAMIRIA…..
Ni story ya kiupelelezi inayomuhusu Afande Kalindimya ambae anahamishwa kutoka mkoa mmoja nje ya Dar na kuletwa Jijini Dar es Salaam. Anaingia kwa kasi na kutishia usalama wa wahalifu, Kasi yake inawafanya hata majambazi yaanze kugwaya na kuamua sasa kumchafua maksudi ili kumuharibia CV yake na kumvunja moyo, ili ikiwezekana aonekane hafai na kutolewa pale alipo ama kufukuzwa kabisa. Kazi ilikuwa ni ngumu sana, kila tukio lililotokea, Afande Kalindimya alipambana nalo hasa, ikafikia hatua kwenye vikao vya Parade, minong’ono ikasikika bila kujulikana ni nani anaesema, bali sauti zilisikika zikisema
‘AFANDE ANAHUSIKA!’
Je ni afande yupi anaehusika? Kwanini iwe ni minong’ono? Hebu twende pamoja mdau ili kumjua huyo afande anaehusika.
Sio ajabu kuingia ofisini na kuketi, baada ya sekunde chache simu kuita, lakini aghalabu mno kuingia ofisini na kukuta simu ikiita, hiyo ndio hali iliyomtokea Inspekta Kalindimya wa makao makuu ya Polisi kitengo cha Upelelezi. Alifungua mlango na kukutana na simu hiyo iliyokuwa ikiita, ilimshangaza, maana ilionekana kama ni simu ambayo ilikuwa ikisubiria yeye aingie ndani ndio ianze kuita, akaitazama na kujiuliza kulikoni hali ile? Mbona inamtia shaka? Moja kwa moja bila kuketi hata kwenye kiti chake, alielekea moja kwa moja kwenye mkono wa simu na kuunyanyua, mezani palikuwa na karatasi nae akatoa kalamu mfukoni, huwa ni kawaida sana simu za pale ofisini kutaka kuandikwa mara kwa mara, ni mara chache sana kukutana na simu ambazo hazina maelezo ama maelekezo. Baada ya kuweka sawa karatasi yake, akauweka sikioni bila kuongea chochote kile. Mtu wa upande wa pili alikuwa ni kama anaemuona vile Inspekta Kalindimya, hakumsalimia bali alimpa maelezo tu. “Afisa Mpelelezi, nina hakika ninaongea na Inspekta Kalindimya, hivyo basi, nenda mtaa wa Mikumi, eneo la Magomeni, Nyumba namba 14, Block DD, kaokoe maisha ya mrembo aitwae Mwanahamis, anaetarajia kuuawa muda mfupi toka sasa, namaanisha muda huu huu, fanya haraka nenda sasa hivi, ukichelewa kidogo ameuawa binti huyo” aliongea kwa harakaharaka na kukata simu bila hata ya kutoa nafasi kwa Inspector kuhoji. Inspector Kalindimya akabaki ameshika mkonga wa simu mkononi pasina kuwa na maamuzi ya haraka, tayari maeneo aliyotajiwa alikuwa ameyaandika kwenye karatasi aliyokuwa nayo, lakini kichwani alikuwa akijiuliza, je ni kweli kuna tukio? Isije kuwa ni katika michezo tu ya raia ambao hutumia vibaya namba za simu za sehemu za usalama ili tu kuwasumbua. Lakini kichwani akaamua ni heri tu atoke aende, hata kama amedanganywa huenda kuna chochote kitu ataokota hukohuko kuliko kukaa ofisini kusubiri matukio yamfuate. Akatoka nje hadi kwenye gari yake na kuingia ili kuanza safari ya kuelekea Magomeni Mikumi kwenye nyumba aliyo elekezwa. Alikuwa akitokea barabara ya Kawawa, amefika maeneo ya mataa ya Kinondoni Studio, simu yake ya mkononi ikaita, namba iliyotumika ilikuwa ni simu ya mezani, lakini kutokana na utambuzi alionao, aliweza kuijua kuwa ile namba si namba ya ndani ya nyumba, bali ni ya kwenye Call box. Roho ikamshituka, akahisi kuna jambo, basi akaipokea na kuichomeka kwenye spika za ndani za gari yake na kuongea na mpigaji hali ya kuwa akiwa na umakini wake barabarani vilevile. Mtu aliepiga simu hii, sauti yake ilifanana sana na mtu aliepiga simu awali, lakini safari hii aliongea kwa utaratibu na kuanza kwa kutupa lawama nyingi kwa Inspector Kalindimya “Inspector Kalindimya, kama leo nitaamua kukuburuza mahakamani kwa kosa la uzembe lililosababisha kifo cha raia mwema, mlipa kodi asie na hatia, nitakua nimekosea?” sauti yake ilikuwa ni ya upole sana. “Sidhani kuwa wakati huu umepiga simu kuniambia jambo hilo la kunilaumu,” “Ok! Wewe ndio utakuwa mshukiwa wa kwanza wa kifo hiki cha Mwanahamisi ambacho kimetokea kwa uzembe wako,” simu ikakatwa tena kama awali bila kuhoji lolote Inspector. Inspector alishtuka na kuongeza mwendo wa kasi ya gari lake ili kuwahi kufika eneo lile ambalo ameambiwa kuwa mauaji, hii simu ya pili ikamchanganya zaidi, alitamani kupaa ili awahi kufika eneo husika, lakini ikawa haiwezekani, maana gari si ndege. Kilichomsaidia ni kuwa muda ule hakukuwa na Jam kubwa sana barabara ya Kawawa, hivyo aliweza kutembea kwa kasi kubwa zaidi ili aweze kufika haraka eneo hilo aliloambiwa, alipofika Magomeni kanisani, akakata kona kushoto kuingia Morogoro Road, kama anaelekea eneo la Jangwani hadi eneo la Mikumi. Kufika kituoni pale ndio akasimamisha gari na kutoa ile karatasi yake ya maelekezo aliyo andika wakati akiongea na mtu aliempa jina la Raia mwema. Aliiangalia na kuiweka kichwani ramani ile kisha akashuka nje na kusogelea nyumba mbili tatu. Namba alizoziona ni zingine, lakini hizo namba ndio zikampa taswira ni wapi ilipo hiyo nyumba anayoitafuta. Kutokana na muonekano wa namba za nyumba zile zilivyokuwa, akajua kabisa nyumba anayoitafuta itakuwa upande wa barabara ya Kawawa. Hivyo akarudi na kuingia garini mwake, akaingia tena barabara ya Morogoro na kwenda mbele kugeuza ili kurudi kwenye mataa na hatimae akarudi Kawawa akiwa kama anaelekea mzunguko wa Kigogo. Mbele kidogo akakatisha kona na kuendesha gari taratibu huku akisoma namba za nyumba, akaweza kuiona nyumba anayoitafuta, hivyo akaenda mbele zaidi na kupaki mbele kidogo, akashuka na kuangalia usalama wa eneo lile na kulock gari yake. Taratibu kwa mwendo wa kiuenyeji, akaeleka kwenye ile nyumba aliyo elekezwa, alipoifikia aliona ni nyumba ambayo inaonekana ipo shwari kabisa, kwani nje palikuwa na kina dada kadhaa wamekaa wakisukana huku wakiongea kwa mabishano. Hali ile ikampa matumaini kuwa huenda ndio kile alichokuwa akihofu cha kusumbuliwa na raia ndio kilichomtokea nae kwa sasa, lakini akadhamiria tu kuingia ili aweze kumuona Mwanahamisi na ikiwezekana aongee nae, huenda kuna chochote akaambulia, wazo hili aliliamini zaidi. Kwa sura ya tabasamu pana, akawasogelea na kuwasalimia, walikuwa ni waungwana, waliitika na kumkaribisha huku wote wakionesha shauku ya kutaka kujua kilichomfikisha pale, nae kama mtu aliejua vile, hapo sasa ndio akamuulizia Mwanahamis, wakamwambia Mwanahamis ameingia ndani kwake muda uleule, kama vipi aende tu ndani mwake atamkuta. Akawauliza ni wapi kilipo chumba chake? Wakamuelekeza, akawashukuru na kuelekea huko kilipo hicho chumba, kwa mwendo wa taratibu na minyato, tena ya hatua ndogo ndogo huku mkono wake ukiwa umeigusa bastola yake aina ya Revolver 12, akausogelea mlango wa Mwanahamis ambao sasa tayari alikuwa ameujua kutokana na maelekezo aliyokuwa amepewa mwanzo hapo nje. Mabinti waliobaki nje wakaanza kuongea kwa ishara na sauti ndogo huku wakitabasamu na kugonga mikono yao kama ishara ya kuelewa kitu Fulani hivi, lakini Inspekta yeye hakuwepo kabisa pale, tayari alikuwa ametokomea ndani. Bahati mzuri mlango wa chumba cha Mwanahamis ulikuwa nusu wazi, akagonga zaidi ya mara tatu na kuwa ni kimya, akapata hofu kuwa huenda ni kweli kuna tukio limetokea, kwa tahadhari kubwa, akitumia mguu wake wa kushoto huku mkono wa kulia ukiwa umeshika bastola yake, akausukuma taratibu, na kuingia ndani. Baada ya kuingia ndani akakutana na maiti ya msichana mrembo kweli akiwa ameuawa kwa kuchomwa kisu kifuani, chini kidogo ya titi la kushoto, mahala ulipo moyo, hivyo kifupi alichomwa kisu cha moyo. Akairuka maiti ya mrembo huyo na kukikagua chumba vizuri kama kuna chochote, lakini hakuweza kuona kitu chochote ambacho aliona kina athari kwake wala kuona cha kumsaidia, akarudisha bunduki yake sehemu ya nyuma ya kiuno na kuisogelea tena maiti sasa. Awamu hii aliisogelea kwa ajili ya uchunguzi wa awali, pasina kuigusa maiti, akaikagua na kuiangalia kwa umakini, kuna kitu aliweza kukiona, kisu kilichochomwa kwenye mwili wa mrembo huyo kilikuwa ni kisu chenye mpini wa Plastic wenye rangi ya Pink.
“Inspector Kalindimya, kama leo nitaamua kukuburuza mahakamani kwa kosa la uzembe lililosababisha kifo cha raia mwema, mlipa kodi asie na hatia, nitakua nimekosea?” sauti yake ilikuwa ni ya upole sana.
Sauti ambayo ilimfanya Inspekta Kalindimya aulize kwa sauti ya kawaida sana isio hata na chembe ya hofu;
“Sidhani kuwa wakati huu umepiga simu kuniambia jambo hilo la kunilaumu,” Endelea;
“Ok! Wewe ndio utakuwa mshukiwa wa kwanza wa kifo hiki cha Mwanahamisi ambacho kimetokea kwa uzembe wako,” simu ikakatwa tena kama awali bila kuhoji lolote Inspector.
Inspector alishtuka na kuongeza mwendo wa kasi ya gari lake ili kuwahi kufika eneo lile ambalo ameambiwa kuwa mauaji, hii simu ya pili ikamchanganya zaidi, alitamani kupaa ili awahi kufika eneo husika, lakini ikawa haiwezekani, maana gari si ndege.
Kilichomsaidia ni kuwa muda ule hakukuwa na Jam kubwa sana barabara ya Kawawa, hivyo aliweza kutembea kwa kasi kubwa zaidi ili aweze kufika haraka eneo hilo aliloambiwa, alipofika Magomeni kanisani, akakata kona kushoto kuingia Morogoro Road, kama anaelekea eneo la Jangwani hadi eneo la Mikumi.
Kufika kituoni pale ndio akasimamisha gari na kutoa ile karatasi yake ya maelekezo aliyo andika wakati akiongea na mtu aliempa jina la Raia mwema.
Aliiangalia na kuiweka kichwani ramani ile kisha akashuka nje na kusogelea nyumba mbili tatu. Namba alizoziona ni zingine, lakini hizo namba ndio zikampa taswira ni wapi ilipo hiyo nyumba anayoitafuta.
Kutokana na muonekano wa namba za nyumba zile zilivyokuwa, akajua kabisa nyumba anayoitafuta itakuwa upande wa barabara ya Kawawa.
Hivyo akarudi na kuingia garini mwake, akaingia tena barabara ya Morogoro na kwenda mbele kugeuza ili kurudi kwenye mataa na hatimae akarudi Kawawa akiwa kama anaelekea mzunguko wa Kigogo. Mbele kidogo akakatisha kona na kuendesha gari taratibu huku akisoma namba za nyumba, akaweza kuiona nyumba anayoitafuta, hivyo akaenda mbele zaidi na kupaki mbele kidogo, akashuka na kuangalia usalama wa eneo lile na kulock gari yake.
Taratibu kwa mwendo wa kiuenyeji, akaeleka kwenye ile nyumba aliyo elekezwa, alipoifikia aliona ni nyumba ambayo inaonekana ipo shwari kabisa, kwani nje palikuwa na kina dada kadhaa wamekaa wakisukana huku wakiongea kwa mabishano.
Hali ile ikampa matumaini kuwa huenda ndio kile alichokuwa akihofu cha kusumbuliwa na raia ndio kilichomtokea nae kwa sasa, lakini akadhamiria tu kuingia ili aweze kumuona Mwanahamisi na ikiwezekana aongee nae, huenda kuna chochote akaambulia, wazo hili aliliamini zaidi.
Kwa sura ya tabasamu pana, akawasogelea na kuwasalimia, walikuwa ni waungwana, waliitika na kumkaribisha huku wote wakionesha shauku ya kutaka kujua kilichomfikisha pale, nae kama mtu aliejua vile, hapo sasa ndio akamuulizia Mwanahamis, wakamwambia Mwanahamis ameingia ndani kwake muda uleule, kama vipi aende tu ndani mwake atamkuta.
Akawauliza ni wapi kilipo chumba chake? Wakamuelekeza, akawashukuru na kuelekea huko kilipo hicho chumba, kwa mwendo wa taratibu na minyato, tena ya hatua ndogo ndogo huku mkono wake ukiwa umeigusa bastola yake aina ya Revolver 12, kuhakikisha kama ipo.
Akausogelea mlango wa Mwanahamis ambao sasa tayari alikuwa ameujua kutokana na maelekezo aliyokuwa amepewa mwanzo hapo nje.
Mabinti waliobaki nje wakaanza kuongea kwa ishara na sauti ndogo huku wakitabasamu na kugonga mikono yao kama ishara ya kuelewa kitu Fulani hivi, lakini Inspekta yeye hakuwepo kabisa pale, tayari alikuwa ametokomea ndani.
Bahati mzuri mlango wa chumba cha Mwanahamis ulikuwa nusu wazi, akagonga zaidi ya mara tatu na kuwa ni kimya, akapata hofu kuwa huenda ni kweli kuna tukio limetokea, kwa tahadhari kubwa, akitumia mguu wake wa kushoto huku mkono wa kulia ukiwa umeshika bastola yake, akausukuma taratibu, na kuingia ndani.
Baada ya kuingia ndani akakutana na maiti ya msichana mrembo kweli akiwa ameuawa kwa kuchomwa kisu kifuani, chini kidogo ya titi la kushoto, mahala ulipo moyo, hivyo kifupi alichomwa kisu cha moyo.
Akairuka maiti ya mrembo huyo na kukikagua chumba vizuri kama kuna chochote, lakini hakuweza kuona kitu chochote ambacho aliona kina athari kwake wala kuona cha kumsaidia, akarudisha bunduki yake sehemu ya nyuma ya kiuno na kuisogelea tena maiti sasa.
Awamu hii aliisogelea kwa ajili ya uchunguzi wa awali, pasina kuigusa maiti, akaikagua na kuiangalia kwa umakini, kuna kitu aliweza kukiona, kisu kilichochomwa kwenye mwili wa mrembo huyo kilikuwa ni kisu chenye mpini wa Plastic wenye rangi ya Pink.
Lakini pia kilikuwa kina maandishi kwenye mpini huo, maandishi yalikuwa ni meupe, akainama ili aweze kuyasoma vizuri zaidi, hayakuwa maandishi, bali zilikuwa ni namba, akaziangalia na kuzisoma namba zile kwa sauti 426474 na kusimama akiwa hajielewi.
Inspector akatoka nje hadi walipo wale wanawake na kuwaomba msamaha huku akiwataka wamfuate ndani haraka iwezekanavyo, wote wakanyanyuka kwa papara na kumfuata alipo, wakamkuta amesimama kwenye uwa wa nyumba ile katikati.
Kwa mara nyingine akawaomba wamuoneshe kilipo chumba cha Mwanahamis, karibu watu wote walimuonesha chumba kilekile alichoingia yeye, akatikisa kichwa na kuwaambia wote waingie ndani huku yeye akiwa ametangulia kuingia.
Baada ya kuingia mle ndani, walichokiona… Wanawake wale wakaangusha kilio.
Inspector Kalindimya akawanyamazisha na kuwauliza kama wanamjua Yule aliekufa pale, mmoja kati ya wale kinadada akasema huyo ndio Mwanahamis mwenyewe ambae yeye aliowakuta nje na kuwaulizia.
Akamteua mmoja amuite Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa, alifuatwa na kuja pale muda uleule akiwa na shauku ya kutaka kujua wito ule wa ghafla kama ni salama ama lah, japo aliemfuata alionesha kabisa kuwa hakuna kheri huko atokapo!
Inspector akaji tambulisha kwa Mwenyekiti wa Serikali za mitaa na kwa wale wengine pia ambao walikuwa hawajamtambua japo walikuwa wamehisi tu kuwa huyo ni askari, kisha akamwambia dhumuni la kumuita pale, pia akamueleza ni vipi alipata taarifa ya kifo kile na kisha akaanza kuwahoji wale aliowakuta.
Mtu wa kwanza kumuhoji ni Mwenyekiti mwenyewe wa Serikali kama anamjua marehemu, Mwenyekiti alikiri na kutoa historia fupi huku akionesha kumsifu marehemu kwa tabia njema, Inspekta aliporidhia akamshukuru.
Kisha akafuatia Yule ambae yeye alijitambulisha kwamba alikuwa akisukwa na marehemu, alikuwa ni mama wa makamo kiasi, akasema kuwa walikuwa wamekaa akimsuka kama ambavyo yeye aliowakuta wameketi, lakini simu ya Mwanahamis ikaita wakati akiendelea kumsuka.
Akaongea na kusema ngoja niangalie ndani basi, wote kila mmoja alikuwa na yake, maana story ilikuwa imepamba moto, hakuna alieshughulishwa na simu ya mtu, maada tu ndio ilikuwa na nafasi.
“Je alimuaga mtu yeyote?” alihoji Inspekta Kalindimya…
“Kwa kuwa ni mimi ndio aliekuwa akinisuka, kama unavyoona nywele zangu zilipofikia, akaniomba dakika 5 tu aingie ndani na kusema hachelewi,”
“Hapana, si mimi tu, kati yetu hakuna yeyote aliemuuliza wakati huwa si kawaida yetu, hupenda kuulizana kila wakati mwenzetu anapotoka, labda kwa kuwa tulimuona akiingia ndani na tulijua kama anataka kutoka ni lazima yeye mwenyewe tu angetuaga sisi hata kabla hatujamuuliza.” Alijitetea mama huyo aliekuwa akisukwa. “We mtu anakusuka, halafu anakuomba muda wako yeye aende sehemu, hukuhofu yeye kuchelewa japo alisema hachelewi?” aliendelea kuhoji afande mpelelezi.
“Sikuwa na hofu yoyote maana mimi leo Sikuwa na safari yoyote, nipo nyumbani tu na hata yeye niliamini hivyo, kuwa haendi mbali maana alionesha dalili ya kuingia ndani huku,”
“Ok! Sawa unaweza kuendelea…” huku akiandika Inspector akamruhusu aendelee kuongea.
“Dakika kama 5 hivi nawe ndio unafika, hapo sasa ndio picha ikaja kuwa ni wewe ndio ulikuwa ukiongea nae kwenye simu, na kama ulikuwa makini uliona ulipofika watu wote wakawa ni wakarimu sana kwako, waliamini wewe una ukaribu na Mwana, Masikini Mwanahamisi wangu,” mtu mzima akaanza kulia tena. Inspector akamtuliza na kumwambia wamalizie kwanza mahojiano.
“Tulishtuka pale uliporudi mara ya pili na kutuambia tukufuate haraka na tulipofika ukatuuliza tena kilipo chumba cha Mwanahamisi wakati sisi tayari tulikuonesha awali, hapo ndio tukapata shaka sote,” alimaliza mwanamke Yule na kumtazama Inspector kama ana swali lingine kwake.
Inspector Kalindimya alitulia kidogo na kuwatazama wengine kisha akamrudia tena mama Yule na kumuuliza;
“Ok! Unataka kuniambia kuwa pale alipokuwa akikusuka Mwanahamis, alinyanyuka kwa ajili ya simu tu? Na si kitu kingine?” lilikua ni swali jepesi kabisa.
“Hakuna mtu yeyote aliepita pale wakati nyinyi mkiwa hapo?” “Hapana,” hili swali sasa walijibu kwa pamoja, maana alivyouliza alikuwa akiwatazama kwa zamu
“Je huku ndani hakukuwa na mtu amabe alikuwa yupo huku? Yaani kama si chumba hiki chake, bali chumba kingine ama hapo uwani?”
“Hapana afande, mara nyingi sana sisi sote huja humu ndani kwa Mwanahamis asubuhi mara tu tuamkapo kwani yeye alikuwa ni mtu wetu sana na hivyo hata leo kabla ya kuwa hapo nje, sote uliotukuta hapo nje, tulikuwa humu ndani,” alijibu dada mwingine swali lile.
“Ni kipi mlichokuwa mkifanya humu ndani?” “Tulikuwa tukisikiliza taarabu na kisha tukanywa chai ndio hapo baadae tukamua tutoke nje afande,”
“Ni nini kiliwafanya mtoke nje wote kwa pamoja?” aliendelea kuandika maelezo yao.
“Tulikubaliana tuhamie nje kutokana na joto kuwa limezidi humu ndani kama unavyoona udogo wa nafasi yenyewe hapa chumbani,”
“Baada ya kuingia huku ndani yeye na kuwaacha nyie nje. Nini kilitokea?” “Hakuna chochote kilichoendelea hadi wewe ulipofika pale na kutusalimia na hadi sasa kilichojiri ni hiki…”
“Sawa, ni nani mmiliki wa nyumba hii?” swali hili lilimlenga Mwenyekiti wa Serikal za mitaa, akasema kuwa mwenye nyumba hayupo Jijini Dar es Salaam, anaishi mkoani Simiyu, ila pale ana mwakilishi wake tu ambae nae ni mpangaji aliedumu zaidi mle ndani.
“Ni huyu hapa dada, tumezoea kumuita Mamaa Kubwa” huku akimuonesha kwa kidole, afande akamtazama mwanamke huyo bonge la mtu ambae kwa wakati huu alikuwa akilia, huku wakiwa kwa sasa wametoka nje ya chumba na kuiacha maiti ikifunikwa shuka na Mwenyekiti wa Mtaa.
Afande akamwambia “Mamaa Kubwa, Naomba nikutambue kama mama mwenye nyumba, kwani hatuwezi kumuhusisha mwenye nyumba moja kwa moja kwa sasa, kwani bado ni mapema sana, nadhani umenielewa?” Alimuuliza huku akimtazama, nae akatikisa kichwa kukubali na Inspekta akamsemesha tena
“Kuna maswali kadhaa nitalazimika kupata majibu toka kwako, hivyo futa machozi na unipe ushirikiano wa kutosha ili tuweze kumjua muuaji wa shoga yako na kumtia nguvuni haraka iwezekanavyo,”
Akaitikia huku akijifuta machozi kwa kanga yake na kumtazama afande ambae bado kalamu ilikuwa mkononi mwake.
“Kuna mlango tofauti na huu ambao mimi nilipita wakati nikiingia humu ndani?” “Hakuna baba yangu, huku uwani njia tofauti na ile uliyopita wewe, haipo nyingine zaidi ya haya mabanda yaliyozunguka ambayo ni ya wapangaji wengine,”
“Hebu naomba tusogee na unioneshe,” wakasogea kule yalipo mabanda ambayo yamepangwa vema kama ni chumba na sebule kila banda moja.
Yalikuwa mawili na kila moja likiwa limejitosheleza kila kitu wakati lile la MwanaHamis likiwa ndio dogo, kwani lenyewe lilikuwa ni la chumba kimoja tu bila chochote, halikuwa na sebule, bafu wala jiko.
“Umeniambia mabanda haya ni ya wapangaji wengine, wapo wapi hao wapangaji wako?” hapa alihoji lakini hakuwa akiandika.
“Hili banda la kwanza ambalo ni chumba na sebule, kwa sasa hakina mtu, mwenyewe alihama tangu wiki iliyopita na hadi sasa bado dalali hajatuletea aina ya mtu tunaemtaka,” alimaliza kuongea huku akigeuka upande mwingine palipo na banda jingine.
“Banda hilo linamilikiwa na mwanadada mmoja ambae ni mwandishi wa habari za uchunguzi, kwa sasa anatakriban mwezi mmoja na nusu hajaonekana hapa akiwa amehamishiwa nje ya Dar kikazi,”
Maelezo ya Mamaa Kubwa yalijitosheleza na kumfanya Inspector amgeukie Mwenyekiti aliekuwa amesimama kushoto kwake na kusema
“Mwenyekiti na mama hapo, naomba tuzunguke kukagua mandhari ya nyumba,” huku akichora vitu Fulani kama ramani hivi kwenye daftari lake dogo la mkononi, wakaanza kuzunguka huku na kule. Waliizunguka nyumba nzima.
Baada ya kumaliza kuizunguka nyumba Inspector akatoa simu na kuwasiliana na wenzake waliopo kituoni ili kupata msaada wa usafiri kwa ajili ya kuiondoa maiti pale nyumbani ili kuipeleka hospitali kwa ajili ya maandalizi zaidi ya kiuchunguzi.
Alirudi chumbani na kukagua kila sehemu ajue ni wapi ambapo huenda muuaji alipitia, maana akili yake ilimgomea kabisa kusema kuwa Mwanahamisi amejiua
“Angejiua asinge andika namba hizi, bila shaka ameuawa, ndio maana hata simu nikapigiwa, lakini je muuaji amepita wapi hadi kumuua huyu mtu?”
Chumba kizima alikikagua, aliangalia dari wala halijatobolewa, akatoka nje na kuangalia juu ya bati, lakini pia hali ilikuwa ni shwari tu.
Kila eneo alilofikiria yeye alilikuta likiwa ni salama kabisa, alishindwa kabisa kung’amua ni wapi mtu huyu alipitia iwapo hakupita kwenye mlango ule? Na baada ya yale mauaji ni wapi muuaji amepita kutoka nje?
“Ama yawezekana akawa bado yupo humu ndani? Lakini mbona amenipigia simu na kunipa maelezo haya? Ni nani alienipigia simu? Ina maana ndio muuaji? Aliumiza sana kichwa Inspector Kalindimya na hakufanikiwa kupata jibu hadi gari ya Polisi kutoka kituo cha Oysteybay ikawa imewasili ikiwa na askari kadhaa walio kikazi zaidi.
Walipowasili walianza ukaguzi wa awali wa marehemu huku Inspector akiamuru simu ya marehemu itafutwe na apewe pindi ikionekana, lakini jitihada zote zilishindikana, ilionekana kama simu ile imechukuliwa, maana mle ndani haikuonekana.
Maiti ilichukuliwa na askari kwa ajili ya kuipeleka hospitali kwa uchunguzi zaidi juu ya chanzo cha kifo kile, huku ikiacha simanzi kwa majirani ambao tayari walianza kumiminika pale ndani.
Inspector akiwa bado hajaridhika kabisa na kile alichokiona kwenye nyumba ile, akamoumba namba ya simu Mwenyekiti na kisha akaingia ndani ya gari lake na kuliondoa taratibu huku akifikiria ni kwanini mpigaji wa simu alimwambia kuwa anahusika na kifo kile
“Na ukizingatia kuwa baada tu ya mauaji mimi nimekuwa ni mtu wa kwanza kuingia mle chumbani sehemu ambapo maiti nimeikuta, ama muuaji ana mpango wa kuniuzia kesi? Halafu kwanini alinijulisha mapema kabla ya tukio na kisha akapiga tena kunilaumu baada tu ya tukio ? Kuna nini hapa kati?”
Alikosa majibu na kuichukua tena karatasi ya ramani aliyochora na kuitazama upya akiwa kwenye mwendo wa taratibu.
Bado hakuweza kugundua ni wapi huyo mtu anaweza kuwa alipita, ndani ya nafsi yake aliweza kusikitika mno na kuikunja karatasi yake ya ramani akiwa anakaribia kituo cha Polisi. Aliingia ndani ofisini mwake na kujipweteka juu ya kiti chake kiuvivu kabisa, hakuwa sawa tena.
Akilini alipanga kurudi tena huko ili kujiridisha pindi atakapo maliza shughuli zingine za pale ofisini. Lakini akiwa anaiweka ramani ile ndani ya file alilofungua juu ya kesi ile ya mauaji, kuna msukumo Fulani ukamvaa, kuna kitu alikihisi.
Alijiuliza, akabidhi lile jalada kwa mkuu wa upelelezi wa mkoa ili lipangiwe mpelelezi kwanza au aende sehemu ile ambayo kuna wazo jipya amelipata? Akaona ni heri tu aende huko kwanza ili akikabidhi jalada liwe na mwanzo mzuri kwa yeyote atakae kabidhiwa.
Moja kwa moja hadi garini nje ya ofisi na kuelekea kulekule alipotoka, yaani nyumbani kwa Marehemu MwanaHamisi, safari hii hakuteremka kabisa wala hakusimama, bali alipita tu kama mpita njia na kuzunguka eneo lile.
Akiwa analiangalia kwa umakini mkubwa hasa alipofika upande wa pili wa jengo lile alilokuwa akiishi MwanaHamis, kwa usawa uleule wa ile nyumba palikuwa na jingo la ghorofa kadhaa.
Alipaki pembeni na kutoa simu yake kisha akampigia simu mwenyekiti wa Mtaa na kumtaka afike pale alipo yeye, akamuelekeza na kumwambia afanye haraka ili waweze kufanya kile kilichosababisha amuite.
Mwenyekiti alifika nae alishuka na kuelekea kwenye jumba hilo hadi ndani, alijitambulisha na kutoa kitambulisho chake, baada ya kujitambulisha akawaambia anataka kwenda usawa wa vyumba ambavyo madirisha yake yanatizama upande wa pili wa barabara ile.
Ilikuwa ni nyumba inayo milikiwa na Watanzania wenye asili ya Kiasia, walitoa ushirikiano wa kutosha, wakamuonesha kila sehemu ambayo alihitaji. Huku akichora ramani husika akaendelea tu kutazama usawa wa nyumba aliyoishi marehemu.
Hakuna ambacho aliweza kukigundua, kutokana na mandhari ya jingo lile isingewezeana kwa mtu kutoka Ghorofani na kwenda upande wa pili, maana ilikuwa imezibwa kabisa, sehemu zilizokuwa zimeachwa wazi zisingeweza kufanya mtu apitishe angalau mguu tu. Bado akili yake haikuweza kutambua ni vipi muuaji aliingia chumbani kwa Mwana, akashuka toka kwenye ghorofa ile na kuzama garini kwake kisha akaondoka kimyakimya akiwa na mawazo kedekede.
Hivyo ndivyo alivyoimaliza siku ile ya kwanza… **********
Siku ya pili ilikuwa ni siku ya mazishi ya MwanaHamis baada ya shughuli zote za uchunguzi wa mwili wa marehemu kukamilika, mazishi yakiwa yamepangwa kufanyika saa saba adhuhuri kwenye makaburi ya Mwananyamala hapo hapo Jijini Dar es Salaam.
Watu walifika kwa wingi hasa mara tu maiti iliporudishwa kutoka hospitali kwenye uchunguzi, Mwana alikuwa ni mtu wa watu hasa, hivyo hata habari ya kifo chake ili washtua wengi ambao bado walikuwa hawajaamini.
Wengi walifika pale wakidhani kuwa wanaweza kujua ni vipi Mwana aliuawa, nani alimuua na kwa njia gani kilitokea kifo hicho bila kujua kwamba hilo tukio huchukua muda mrefu sana hadi kumpata muuaji huku uchunguzi ukigharimu muda, pesa na hata maisha ya wengine.
Inspector Kalindimya alikuwepo pale msibani sambamba na maaskari wenzie kadhaa waliokuwa pale kufuatilia kama kuna lllote ambalo wanaweza kulipata likawasaidia kwenye uchunguzi wao.
Pembeni ya Inspekta Kalindimya, alikuwepo Inspekta Jitu, moja kati ya wasaidizi wakubwa wa mpelelzi aliekuwepo pale na kuhamishwa ili kupisha ujio wa Inspekta Kalindimya.
Walikuwa makini sana kufuatilia kila hatua iliyokuwa ikiendelea wakiwa na umakini mkubwa na wa hali ya juu, hawakupenda hata tukio dogo liwapite pale walipo, hivyo waligawana maeneo ya kufuatilia wakati taratibu za mazishi zikiendelea.
Mazishi ya waislamu, kwa kiasi kikubwa huwa ni tofauti na mazishi ya kikristo, maana waislam wanawake wao hawachanganyiki na wanaume japo msibani, na hata hapo ilikuwa hivyo, upande wa wanaume walikuwepo askari wawili wengine tofauti na Mainspekta hao.
Mmoja kati ya askari wale alikuwa akifuatilia tu kujua kama kuna mtu anawafuatilia wale mainspekta na hususan Inspekta Kalindimya. Wakati huyo askari mwingine nae alikuwa na kazi yake maalum aliyokuwa amepangiwa.
Kwa upande wa wanawake kule, Inspekta Kalindimya alikuwa amemuweka askari mmoja ndani kabisa ya chumba cha ndugu wa marehemu kufuatilia ili kujua ukaribu wa watu watakaokuja na huenda wakapata dodoso, alimtaarifu iwapo atamuwekea shaka mtu yeyote, basi asisite kumjulisha kwa njia yeyote.
Makubaliano yale yalimpa imani kubwa mno Inspekta akiamini kuwa amejipanga barabara, leo alijua kama itatokea kufuatiliwa ama kufuatilia juu ya mazishi ya Mewanahamis, basi huyo mfuatiliaji hatochomoka.
Saa 7 kasoro, kama kawaida waliwasili masheikh kwa ajili ya kuendesha ibada malum ya mazishi, wakati wao wakiendelea kusoma hitma ile, Inspekta akasikia simu yake ikiita. Ilimshitua sana, hakutegemea kabisa simu yake kuita muda ule japo haikuwa na mipaka ya kuita.
Alichokifanya ni kuitoa na kuangalia ni nani aliempigia, akaona kuna namba ya mezani, ikiwa ni ngeni kwake kabisa. Kabla ya kupokea alihisi kitu, akatazama kila upande, akianza mbele yake na kugeuka hadi nyuma akitazama kwa tahadhari kubwa na jicho pembe. bila kujua ani nini anaangalia pande hizo.
Pale mtu yeyote angemuuliza unaangalia nini hakika angesema hajui ni kipi anacho tazama. Alitaka kupokea,lakini akaona hatokuwa sahihi kupokea eneo lile ambalo bado kunaawatu wanafanya ibada ya kumsomea marehemu, kwa kulinda heshima, akanyanyuka na kusogea pembeni.
Hata Yule askari aliempanga kumfuatilia kwa ukaribu alimuona kwa mbali sana akiwa kama mtu ambae hana habari hata kidogo, kumbe nae alikuwa makini kuliko alivyojua yeye, lakini hakujali.
Akapokea sasa kwa sauti ya taratibu, maana tayari alihisi kitu, alikuwa ameshisi ni mtu yuleyule aliekuwa akimpigia awali, ndio huyo amepiga tena… na kweli hicho ndicho kilichotokea, sauti ilkuwa ni ileile, sasa ilikuwa ikimpa pole ya kushughulishwa na msiba wa Mwana.
Hakujibu lolote Inspekta, alikuwa yupo kimya tu hadi sauti ile ya kiume nzito safari hii tofauti na awamu zilizopita, ikamwambia
“Inspekta baada ya kukupa pole napenda kukwambia nakuonea huruma sana, maana nahisi utakuwa kwenye wakati mgumu mno kwa sasa,” ilisema sauti ile kwa kejeli, nae Inspekta akaijibu kwa dharau
“Ha ha haa! Unaonekana dogo una jeuri sana, lakini usiogope mimi nitakufundisha kazi…”
“Sawa, lakini tambua mimi kazi niliisha fundishwa huko CCP Moshi, na ndio maana sasa unaniona nipo kwenye ajira katika kupambana na wapumbavu na wajinga wajinga kama wewe.
Sasa kama huna cha kusema, ni heri ukampigia simu mkeo na kumtongoza upya, sawa?” aliongea maneno makali katika hali ya kawaida tu ili kumtia jazba Yule mtu aseme shida yake, maana moja kati ya masomo aliyopitia akiwa Chuo Cha Polisi Moshi.
Moja ya mbinu ya kumlazimisha mtu kusema jambo, walifundishwa ni kumtia mtu jazba wakati ambao anatoka kwenye hali ya kawaida, basi ni lazima ataropoka tu chochote lakini ni cha kweli.
Hiyo ndio iliyotokea, alipomwambia vile, jamaa akamwambia
“Inspekta tambua mara zote ninapokupigia simu mimi ujue nina habari njema kwangu na mbaya kwako,” akanyamaza kidogo kisha akaendelea
“…Inspekta hili ni game, kila siku kwenye game lazima mmoja ashinde, mimi daima huwa ni mshindi kwa sababu ndio ninae andaa hii game, ingekuwa ni bao, ningesema najua wapi pa kukufungia,
Lakini hii ni ‘Game of death’ huu ni mchezo wa kifo, kumbuka kuwa ni mimi ndio nimeuandaa, sasa basi wewe kwa kuwa umekuja kasi, nataka nikupumzishe kidogo nje ya ofisi ya Serikali, iwapo hutakubali kuachana na kesi hii.
Si umesikia Askari mwenzako mmoja aliuawa siku chache zilizopita? Basi ni kwa kimbelembele chake, achana kabisa na kazi hii, namaanisha kazi ya Upelelezi, we upo vizuri kwenye biashara, rudi uraiani acha watu wafanye kazi zao, sawa Inspekta?”
“Ha ha haa! Nilijua naongea na mwanaume mwenzangu, kumbe naongea na kibinti Fulani hivi kijoga joga? Sawa mrembo, nimekuelewa, nitafikiria ombi lako, maana sisi jeshini tumepewa option ambazo siwezi kumuambia mwanamke ambae sina hakika ya kuwa nae kwa muda Fulani…”
Maneno ya shombo aliyoyatoa Inspekta alijua dhahiri yatamkera mtu wa upande wa pili, lakini wala haikuwa hivyo, bali jamaa akajibu kwa kujiamini kabisa
“Hilo unaloiga wewe ndio lilipelekea kifo cha kizembe kabisa cha Inspekta mwenzio, nawe unapita mulemule, sasa Napata picha ya kweli kwamba nyote mmefundishwa mbinu ileile, sasa ole wako…” Inspekta akamkatisha
“Ndio hapo utakubali kuwa Serikali ni hatari, tambua kila kitu kuhusu wewe kipo mikononi mwangu sasa, na muda si mrefu nitakutia nguvuni,” aliongea kumtia hofu, na kwa sasa alifanikiwa, kwani jamaa akasema kwa kujitetea kwa haraka
“Unajidanganya Inspekta, na ili kukuonesha kuwa mimi nipo vizuri zaidi kuliko wewe, muda huu kuna tukio nafanya, na baada ya hao watu kunywa chai ambayo nimeigharamia mimi, yaani wakati jeneza la Marehemuu Mwana likitoka, andaa tena mazishi ya Mwana,”
“We ni mwendawazimu, naona hofu ya kutiwa mikononi tayari imeisha kuvaa,”
“Nisikilize Inspekta Kalindimya, mimi huwa sina utani kwenye kazi ninazopanga kufanya, hivi sasa ni saa saba na dakika moja, pishana na hilo jeneza la Mwana, si unaliona linatoka?” aliuliza mtu wa upande wa pili, kisha akaendelea
“Wakati lenyewe likitolewa nje, wewe nenda chumbani kwa Mwana, huko ndio kuna kila kitu, kwa heri, msalimie afande Jitu, naona anajiuliza tu unaongea na nani muda wote huu, ha ha haa!” alicheka kwa sauti iliokuwa kubwa na kumghasi hata Inspekta Kalindimya.
Kabla hajaongea lolote, Simu ikakatwa na kuanza kuwatazama watu waliopo pale kwa umakini wa hali ya juu mno, alikuwa akiangalia kama kuna mtu yeyote anaemtazama, lakini aliona kila mtu akiwa busy na kilichompeleka pale.
Sasa kweli tayari jeneza lilikuwa linaonekana kutolewa kupitia mlango mkubwa wa nje kutoka ndani, akaamua kuliwekea maanani lile lililosemwa na mpiga simu, akamtaka Inspekta Jitu amsubiri garini ili yeye aende ndani mara moja.
Kichwani alijipa moyo kuwa huenda huyo aliepiga simu ni mtu wa karibu na familia ya Marehemu, na yawezekana aliona maiti imeachwa nje ya jeneza na kuogopa kusema mbele yao, sasa amemtumia yeye kama mjumbe ili salamu zifike.
Kwanza akasogea hadi lilipo jeneza la Marehemu na kulikagua kwa macho, je maiti ipo mle ama lah! Alipoona maiti ipo kutokana na mfungo wa mkeka kama wanavyofanya waislamu, mfungo wa pipi.
Akasogea pembeni na kumuita mmoja wa wana ndugu aliekuwa yupo karibu sana na kumuomba amuhakikishie.
Kwanza alijitambulisha yeye ni nani na kumba wasogee pembeni na kisha akamueleza juu ya jambo hilo, jamaa baada ya kuridhishwa na utambulisho huo, ndio nae akasema kwamba ana hakika maiti ipo ndani ya jeneza, kwani hata nae ameshiriki kuiweka mle ndani ya jeneza.
Akamshukuru na kuachana nae.
Moja kwa moja akaelekea ndani hadi chumbani kwa marehemu Mwana, hapo akiwa na simu mkononi akiandika sms kumuuliza askari wa kike aliepo ndani vipi mazingira ya mle ndani yalivyo? Aliandika sms fupi tu lakini wenyewe walielewana.
Akarudisha simu mfukoni huku akiwaomba kina mama njia ya kupita, maana walikuwa ni wengi sana hadi kiasi ambacho aliamini hata sasa mpiga simu anamsumbua tu juu ya kumwambia aende huko chumbani kwa marehemu.
Alifika hadi kwenye mlango wa chumba cha marehemu na kukuta umefungwa, lakini haukufungwa na kitasa, bali ilikuwa umeshindikwa tu. Akanyonga kitasa na kuingia ndani tena kwa tahadhari. Alichokiona ndani alishtuka.
Alisimama na kuangalia kwa mshangao mkuu huku akionesha kabisa kushtushwa na tukio hilo.
Alikuwa na haki ya kushtuka, maana aliona maiti ya msichana mrembo kweli kweli ikiwa juu ya sofa ya watu wawili, ambao kwa mtizamo wa haraka haraka ilionekana kabisa maiti ile haina muda mrefu tangu kutokea kwa kifo kile.
Inspekta Kalindimya akahisi kuchanganyikiwa, mtu anafanya mauaji mbele ya watu wengi kiasi kile? Mtu huyu ni nani? Amefanikiwa vipi kumuua huyu mtu hapa kwenye kadamnasi? Alijiuliza maswali ya papo kwa hapo na kukosa jibu. Akatoa simu na kumuita Afande Jitu haraka ndani, afande ni kama alikuwa nje ya chumba, dakika moja tu mbele akawa yupo nae sambamba chumbani na alipoiona tu ile maiti….
Bila kujua lolote akajikuta amesema ‘Shit’ na kujipiga kofi pajani akiwa ameuma mdomo wa chini na hali kakunja ndita.
Hata Jitu nae alionekana kuchanganyikiwa, lakini hapo kabla alikuwa na hamu mno ya kutaka kujua mkuu wake wa kazi alikuwa kiongea na nani kwenye simu… Lakini hakukuwa tena na muda wa kuhoji juu ya jambo hilo.
Afande jitu alirudi garini na kuchukua Gloves pair mbili ili kuja kuanza kufanya uchunguzi wa awali kwanza wakati wakiomba usafiri wa kuja kuuchukua mwili wa Marehemu.
Kawa kawaida, kulikuwa na kisu cha rangi ya Pink kwenye mpini na sasa namba iliyowekwa ilisomeka 6352 huku ndani ya chumba pakiwa hakuna mtu yeyote, walikagua chumba kila sehemu hadi chini ya sofa, lakini wapi, hakaukuwa hata na mdudu.
Sehemu moja waliisahau, ilikuwa ni kwenye kabati ya nguo, nayo walipokumbuka na kuifungua..,
Hawakukuta chochote zaidi ya nguo zilizo pangwa vizuri ndani ya kabati, wakaishiwa pozi na kushusha pumzi kwa pamoja kwa mara nyingine tena, wakiwa hawajui ni wapi pa kuanzia.
Inspekta akatoa simu na kumuita Afande wa kike aliekuwa nyumba kubwa chumba ambacho maiti imeondokea kwenda malaloni, hakukawia akawa amefika, nae alishtushwa na kile alichokiona.
Inspekta akamwambia amfuate mama mwenye nyumba, anaitwa mama Kubwaa na kumwambia nahitajika chumbani kwa Mwana.
Mama Kubwaa alichukua dakika takriban mbili, kwani kulikuwa na mtu mmoja alikuwa amekuja kumpa pole, kwa kuwa alikuwa ni mwanaume alishindwa kumkatisha maongezi yake, hata afande Yule wa kike alimkuta nae japo hakumtazama kwa umakini, maana si hilo lililompeleka pale.
Mama mwenye nyumba akamaliza maongezi nae huyo kijana wa kiume ambae alitoa kiasi cha pesa na kuondoka akimuacha huru sasa Mama mwenye nyumba kuelekea chumbani kwa marehemu, alipoitwa na askari.
Akafika huku akiwa na imani kuwa itakuwa kuna jambo lolote jipya ambalo huenda jeshi la Polisi limefanikiwa kulipata kwa sasa tangu jana na hivyo anaenda kujulishwa ama wanataka msaada wake kwanza.
Alipoingia ndani tu, japo mwili wa Marehemu pale sofani ulikuwa umefunikwa, lakini ilijionesha tu ufunikaji ule, haukuwa salama, akajishika kichwa kwa mikono miwili na kusema Mwana kwa sauti ya juu na kuanza kulia.
Inspekta Kalindimya na Jitu wakatazamana usoni, wakajiuliza Mwana tena? Askari wa kike akamuuliza Mwana yupo wapi? Mama kubwaa akajibu huku akilia kwa kunyoosha kidole kwenye mwili wa Marehemu.
“Bi mkubwa, mwili wa mwana tayari tumeisha utoa hapa nyumbani na muda huu utakuwa maeneo ya makaburini,” aliongea Inspekta huku Jitu akitikisa kichwa kumuunga mkono. Mama Kubwa nae akaendelea kushikilia palepale
“Hapana bwana afande, huyu ni Mwana…” sasa hawakuwa na budi ila tu kukubaliana nae, maana yeye huenda anamjua vizuri zaidi kuliko wao “Sawa mama, hapa tuna maswali machache kuhusu Marehemu, tunaomba utusaidie kuyapatia majibu tafadhali,” aliongea Inspekta huku Jitu akiwa tayari na kalamu na karatasi ili kurekodi maongezi yao, mama Kubwa nae akatikisa kichwa kukubali kutoa ushirikiano huku akiitazama maiti ya Yule binti anae onekana alikuwa ni mrembo hasa.
“Jina lake nani?” “Anaitwa Mwana,” Alipojibu mama Kubwa, Inspekta Kalindimya akamuuliza kama hilo ndio jina lake halisi. Mama kubwa akaitika kwa kichwa akifuta machozi.
“Mwana nani? Maana kama ujuavyo haya majina ya kina Mwana, ni kifupi tu, hapo inaweza kuwa ni Mwana Hamisi, MwanaLisa na mfano huo, huyu sasa aliitwa Mwana nani?” aliomba ufafanuzi Jitu.
“Mmh kwa kweli sina ufahamu wa hilo, kwani hata hili jina la Mwana hatukuwahi kulisikia toka kwake moja kwa moja, bali kutokana na kuitana kwao wa jina wajina, ndio maana tukajua kuwa Yule nae jina lake ni Mwana, ila hakuna yeyote ajuae ni Mwana gani!” alieleza mama Kubwa kwa kirefu.
“Jina la baba yake?” aliuliza ili kupata maelezo kamili ya marehemu. “Kwa kweli hilo silijui, maana hata siku moja sijawahi kumuuliza na sikuona hata huo umuhimu,”
“Unamfahamu marehemu Mwana huyu kivipi?” “Ni rafiki mkubwa wa marehemu Mwana, na ndio alikuwa ni shoga yake kipenzi, kiasi ambacho haikuwahi kupita siku hata moja bila wao kuwasiliana ama kuwa pamoja,”
“Alikua akiishi wapi Marehemu?” “Nasikia tu ya kwamba alikuwa akiisi Manzese Tiptop, ila sifahamu ni nyumba gani,”
“Ok! Yeye amefika lini hapa?” “Ni mara tu baada ya taarifa ya msiba wa Mwana iliposambaa,”
“Nani alimjulisha juu ya msiba huo?” alihoji Inspekta Jitu, Kalindimya alikuwa yu kimya tu akisikiliza kwa umakini mahojiano. “Kwa kweli sifahamu, lakini kuna wengi wamesikia tu kwa watu tofauti hasa ukizingatia MwanaHamis alikuwa ni mtu wa watu,” alijibu tena mama Kubwa.
“Una maanishaa tangu alivyolala hapa jana hakuondoka tena kwenda popote? Ama alikuwa akitoka toka?”
“Ndio bwana afande, tangu alivyokuja jana jioni, hajatoka kwenda popote zaid ya kuhama vyumba tu lakini ni humu humu ndani, hadi mauti yamemfika.” Alijibu hivyo mama mwenye nyumba.
Inspekta alijikuta ameuliza maswali yote na mama alijibu bila kupepesa macho wala kutikisa masikio, lakini walipofika kwenye swala la muuaji walikwama.
Muda gani kuyo muuaji aliingia ndani na kufanya mauaji yale na hali watu walikuwa wengi wa kutosha. Hapa sasa alikuwa akijiuliza Inspekta…
“Ina maana Yule mwenda wazimu amenieleza kweli ama? Mbona kama ananichanganya vile?” akili yake ilikumbuka simu aliyopigiwa na na yule mtu alie mpa jina la raia mwema, lakini alikuwa ni mwanaume, na kawaida wanaume kuingia kwa wanawake ni shughuli pevu.
Sasa akapata pa kuanzia, akajituliza na kutengeneza koo kisha akamtazama mama Kubwa na kumuuliza
“Kuna mwanaume gani aliingia ndani ya chumba cha marehemu wakati shughuli za msiba zikiendelea?”
“Mwanangu siwezi kufahamu, maana tangu jana baada tu wewe na timu yako kuondoka, sisi tukakifunga chumba hihi na funguo ya chumba tukampatia Mwana, huyu marehemu ambae usiku wote wa jana hakukifungua,”
“Afisa kumbuka nimekwambia funguo anayo yeye na ndie umekuta maiti yake pia humuhumu ndani,” Inspekta aliposikia majibu yale, yalimtosheleza kumjibu kuwa mama Kubwa hana jibu la swali hilo.
Sasa ndio akaenda kwenye point yake moja kwa moja
“Unakumbuka kuonana na mwanaume yeyote tangu jana baada ya msiba hadi leo hii kabla ya mazishi ya Mwana?” aliuliza swali lile huku akimtazama kwa makini zaidi, hapa ndio aliamini kuwa kuna mwanga ambao utampeleka kwenye mafanikio.
“Hapana baba yangu, zaidi ya wanaokuja kunipa pole, sidhani kama kuna yeyote,”
“Hao waliokupa pole je? Unawafahamu kwa sura ama walikuwa ni wapya machoni mwako?”
“Mmmmh, Karibu wote ni walewale wa hapa mtaani, yaani ni watu tunojuana nao afande,” jibu lile kidogo lilimpa faraja Inspekta na kuona sasa angalau anaweza kufikiria kumpata muuaji kwa urahisi kiasi Fulani, nguvu ikaongezeka na kuendelea kuhoji;
“Kati ya hao watu, kuna mmoja wapo ni mtu tunae muhitaji sana, nawe pekee ndio unaemjua, sasa tutalazimika kuondoka hapa ili twende kituoni kwa mahojiano zaidi,” alisema inspekta huku akiwatazama wenzie ambao walitikisa kichwa kukubaliana nae huku akimpa wakati mgumu Mama Kubwa
“Afande, lakini mbona mi sina kosa lolote? Nimefanya nini hadi unipeleke Polisi?” alisema huku akiangusjha kilio.
“Hapana mama Kubwa, wewe huendi kuwekwa ndani, bali ninakwenda nawe kwa ajili ya mahojiano tu na baada ya kumaliza mahojiano utarudi nyumbani kwako, hivyo wala usiwe na shaka,” alimtoa hofu lakini bado hakuamini kauli ile, akasema kwa kukata tamaa,
“Ndio huwa mnasema hivyo hivyo, sawa bhana, basi niende na Joyce ili kama mkiniweka ndani aje kutoa taarifa nyumbani,” kauli ile ilitaka kumchekesha Inspekta Kalindimya, lakini akajizuia na kumwambia
“Hata wakienda na Joyce, hawezi kufika sehemu ambayo wewe utaenda kufanya mahojiano, nakuhakikishia utarudi ukiwa salama tu, nataka tutoke hapa kutokana na unyeti wa jambo lenyewe, we wala usiogope, tambua kule ni kituo cha usalama wa Raia na mali zao.”
Alimkata maini na Mama kubwa alipoambiwa asimame alikuwa amepoteza matumaini na sasa alihisi huu ndio mwisho wake wa kukaa uraiani, chozi lilikuwa likimtoka bila kificho. Wakati wakiongea hayo, tayari gari ya Polisi ilikuwa imefika na askari wakiwa na Camera na Stretcher, wakawatoa waliomo ndani huku Yule askari wa kike wakimtaka kuongozana na mama Kubwa hadi ndani ya gari la Inspekta Kalindimya.
Mama Kubwa alitoka huku akilia, watu tayari walikuwa ni wengi pale uani, wengi walimuonea huruma, hasa jinsi alivyotoka akiwa na huzuni usoni, alipowaona watu ni wengi pale nje, sasa akaangua kilio kabisa na askari akamfungulia mlango aingie ndani ya gari.
Waliomo ndani waliendelea na kazi zao kama walivyojipanga na baada ya kumaliza tu, wakatoka wakiwa na mwili wa marehemu hadi ndani ya pick up ya jeshi la Polisi na kuondoka.
Inspekta Kalindimya sambamba na Jitu wakatoka nao pia, Jitu akiwa ni wa mwisho kutoka, akiwa mlangoni, alichomoa funguo ya kitasa iliyokuwa mlangoni kwa ndani na kufunga mlango ule kwa nje huku akiwa na nia ya kuondoka na funguo hiyo.
Hivyo alimuita dada mmoja ambae alionekana kama ni mwenyeji na kumuuliza jina lake, akamwambia anitwa Joy, alilikumbuka jina hilo na kumuuliza
“Nafikiri wewe si mgeni ndani ya nyumba hii?” “Ndio, mimi ninaishi na mama Kubwa,” alijibu Joy akiwa naonekana kuwa na wasiwasi.
“Sawa, nimefunga chumba hiki na nimeondoka na funguo, tutarudi, kuweni makini, tukio lolote mkiliona lipo tofauti kidogo, naomba unijulishe kwa kutumia namba ambayo nitakupa, sawa Joy?” alisema huku akizama mfukoni na kutoa kalamu na diary ndogo ambayo alichana karatasi kiasi na kumuandikia namba.
“Hivyo wakati wowote, ukimuona mtu ambae unamtilia shaka ama ni mgeni kwenye macho yako na humuamini, nijulishe haraka iwezekanavyo, name nitafika muda huo huo, daima sitakuwa mbali na eneo hili, sawa Joy?” alipokea Joy huku sasa akiwa na amani kuwa yeye hachukuliwi kwenda kituoni.
Jitu alikuwa na funguo ile mkononi bado, sasa ndio akaiweka mfukoni mwake na kutika kuelekea nje na lakini mlangoni Inspekta Kalindimya alikutana na Mwenyekiti wa Serikali za mtaa na kumwambia anaondoka na Mama Kubwa kwa mahojiano nae ofisini ila atarudi baada ya muda watakapomaliza mahojiano yao.
“Vipi kuna haja ya kuongozana nae?” aliuliza Mwenyekiti. “Eer… Ni sawa tu lakini itakulazimu kutafuta usafiri wa binafsi kama hutajali, maana sisi tumeenea kwenye gari tulilokuja nalo,” alimjibu huku nae akitazama saa.
Mwenyekiti akasema atakuwa akija kwa nyuma yao kwani yeye ana usafiri wake binafsi ambao atautumia kufika huko, wakaagana na wale maaskari wakaingia kwenye gari lao na kutokomea kituo cha Polisi.
Nyuma wakiwa wamewaacha raia wakiwa na mshangao kwenye vikundi vikundi kadhaa wakijadili juu ya matukio mfululizo yaliyotokea nyumba ile. **********
Safari iliishia kituo cha Oysterbay, hapo ndipo ambapo waliketi na kuanza mahojiano yao. Inspekta alimkaribisha mama Kubwa ambae alikuwa akionesha wasiwasi mkubwa mno kutokana na kutokuwa na uzoefu wa kituo cha Polisi.
“Karibu mama Kubwa, jisikie huru kabisa, kwani hapa sio mahakamani, hapa ni kituo cha Polisi, maana ya kituo cha Polisi ni sehemu ya usalama kwa Raia na mali zao, hivyo amini upo sehemu salama kabisa, sawa raia mwema?” Inspekta alijaribu kumtoa hofu na alifanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Maana ile hofu iliyokuwa ikionekana usoni, ilionekana sasa kupungua kiasi Fulani na kuitika kwa kutikisa kichwa ishara ya kukubali. Jitu alikuwa pembeni kama kawaida na kalamu na diary ndogo, akiwa tayari kuandika maelezo atakayotoa kutokana na maswali atakayoulizwa na Inspekta.
Inspekta Kalindimya akamuuliza swali la kwanza kwa kumwambia kwamba anawakumbuka watu walioingia na kumpa pole? Jibu lake likawa ni lile lile, akaulizwa tena je anaweza kuwataja majina wanaume walioingia mle ndani kwake?
Aliwataja wanaume wasiopungua watatu, alipoambiwa ataje makazi yao akataja yote,
“Una ukaribu nao gani watu hawa?” akasema “Wote ni jirani zangu hawa,”
“Vizuri sana, tunaweza kwenda na kuwaona majumbani mwao?” aliuliza afande Yule wa kike akiwa kuna kitu amedhamiria.
“Hata sasa naweza kuwapeleka kwa mmoja mmoja, kwani wote nawajua wanapoishi,” walimaliza mazungumzo yao huku inspekta Kalindimya akimwambia Afande Yule wa kike ambae alimuita kwa jina la Marsha, aongozane nae sambamba na Jitu kwa hatua zaidi.
“Mkimaliza mahojiano nao watu hao aliowataja mumuache kwake huyu mama na kama kawaida, yeyote mtakaemtilia shaka tu, mleteni stoo kwa maelezo zaidi,”
Alimaliza maelekezo yake na kuwaaga akiahidi kuonana nao siku ifuatayo, alitaka siku hii arudi kwake muda ule akapumzike huku akifikiria juu ya mauaji ya wanawake wale.
Waliondoka na kueleka huko walipoagizwa, walifanya mahojiano na wote lakini hawakufanikiwa kuambulia chochote na mwisho wa siku wakaona ni kama kupoteza muda tu.
Wakamuacha mama kubwa na kuamua kurejea kazini kwao ili kuendelea na utaratibu mwingine hasa ukizingatia tayari usiku ulikuwa umeisha ingia. **********
Safari ya Inspekta iliishia kwake na kujitupia sofani aiwa amechoka kabisa, siku mbili za kazi ile nzito aliona ni kama siku milioni kwake. Akaanza kufikiria juu ya muuaji Yule ni nani, lakini bado hakuwa na jibu, akamua ajipumzishe ili kujipanga kwa ajili ya siku ifuatayo.
Asubuhi ya siku iliyofuata akawahi ofisini kuliko kawaida, lengo alitaka kujua ni nini siku iliyopita walikipata huko walipokwenda Jitu na afande Marsha. Aliwasili na kuwakuta wao tayari, Jitu akiwa amesimama na Marsha akiwa anaandika ripoti ile ya siku iliyopita.
Walimsalimia alipoingia kama zilivyo amri zakijeshi na kisha kumueleza habari nzima ya mahojiano ya siku ile iliopita, alichoka kabisa walipomueleza kuwa hawajaambulia chochote toka kwa watu wale.
“Mlimuuliza kuhusu mtu ambae aligharamia chai kwenye shughuli?” swali la Inspekta liliwafanya Jitu na Marsha watazamane na kukana kuwa hawajamuuliza.
“Hapo sasa nanyi ndipo mlipofeli, hilo swali mnaweza kuliona ni la kipuuzi sana, ila ni swali moja la msingi sana, hebu mmoja wenu anifuate twende huko kwa ajili ya hatua zifuatazo,” aliamuru Inspekta na Jitu na Marsha wakatazamana tena, wote wakawa tayari kwa kwenda, Jitu akamwambia Marsha
“Nendeni nyie, acha mimi niendelee na ile kesi nyingine ya wale majambazi wa Pori la Msanga,” Marsha kwa kuwa alikuwa akiitambua kesi hiyo, akakubali na kubeba diary ndogo huku akijihakiki kuwa yupo tayari na kutoka.
“Kama mtahitaji funguo ya chumba cha Marehemu Mwana, nimeiweka ndani ya file na kuifunga kwa gundi, ila kwa kuwa mnaenda huko unaweza tu kuibeba, inaweza kuhitajika huko,” ulikuwa ni ushauri mzuri mno ambao Marsha aliuchukua ulivyo na kuirudia funguo. Alipotoka Marsha akawakuta Jitu na Inspekta wakiwa kwenye maongezi, Jitu akiwa nje ya gari ya Inspekta akiwa ameinamia usawa wa kioo, na inspekta akiwa ndani ya gari akimsikiliza kwa makini.
Baadaya Marsha kuingia garini, wakaagana Jitu na Inspekta kwa ahadi ya kuonana wakati ujao hapohapo ofisini.
Safari ilishia nyumbani kwa mama Kubwa, hapo waliingia na kumkuta mama kubwa akiwa na mtoto mmoja hivi pamoja na Joyce, waliwaomba wawapishe na kisha Inspekta pasina kupoteza muda akamwambia mama kubwa kuwa mtu wanaemuhitaji hadi sasa hawajamjua na bado akasisitiza kwamba ni yeye pekee ndio anamjua na ndio naweza kuwasaidia.
“Baba yangu wee, mimi simjui muuaji, mbona tayari ningekuwa nimekwambia?” aliomboleza mama Kubwa kwa kudhani anaweza kugeuziwa kibao. Inspekta akaamua kumchanganya kidogo.
“Najua humjui muuaji kama ambavyo mimi simjui, lakini muuaji amekutaja wewe kuwa unamjua,” na kweli kauli ile ilimtikisa kabisa hadi Inspekta akaiona
“Kasema mimi ninamjua? Jamanii Sijui ananitakia nini mimi wallahi…” mama Kubwa akaangusha kilio.
“Mama Kubwa kilio hakina msaada wowote kwako wala kwetu kwa kipindi hiki, jambo la msingi ni kutusaidia tu sisi tumpate muuaji na amani irudi tena kwako kama awali, jana tuliomba utuoneshe watu wa kiume waliokuja kukupa pole na rambirambi, lakini tuliemtaka utuoneshe ulituficha, ni kwanini?”
“Hapana afande, mimi nilionesha watu wote na hadi makwao tulienda, kwanini niwafiche lakini?”
“Ok! Kuna mtu mmoja alikupa pesa juzi usiku kwa ajili ya kununua baaadhi ya vitu vya maandalizi ya mazishi, ni kweli ama lah?” aliuliza huku akiwa maemkazia jicho.
“Inspekta wote hao niliokutajieni walinipa pesa kwani wanajua kuwa Mwana hakuwa na pesa na mimi pia Sikuwa na pesa ya kuweza kusimamia mazishi bila ya msaada,”
“Una hakika ni hao tu uliotuonesha ndio waliokupa msaada wa pesa?” alihoji Inspekta baada ya kuanza kukata tamaa kutokana na kauli ya Mama Kubwa kuwa ni ya ukweli.
Kutokana na uzoefu wa kazi yake, aliweza kumjua mtu kwa kile asemacho, kuwa ni kweli ama lah! Sasa kwa mama Kubwa aligundua kuwa hakuwa akidanganya.
“Ni kweli, ila kuna mtu mmoja alikuja na sukari, akanipa sukari mfuko ule pale,” aliongea kisha akawaonesha mfuko wa sukari uliokuwa na uzito wa kilo 25 ambao kwa sasa ulipungua na kuwa ni wenye kilo kadhaa kwa sasa.
Baada ya kutazama huko, macho ya Inspekta na ya Marsha yalikutana na wakahisi kuna kengele ya hatari imelia vichwani mwao, walihisi kitu na sasa waliona ni wakati muafaka kukiachia.
“Huyo ndio mtu tuliekuwa tukimuhitaji, yupo wapi na kwanini hukutwambia mapema? Unaficha muuaji?” yalikuwa ni maswali mfululizo ambayo yalitoka kwenye kinywa cha afande Marsha.
“Hapana afande, ni vile nyie mliniuliza alienipa rambirambi ya pesa, huyu alikuja alileta tu hiyo sukari na majani ya chai, tena usiku uleule wa kifo cha MwanaHamis, hakunipa hata senti tano nyekundu mimi,” walimuelewa na kuendelea kumuhoji
“Huyo mtu unamjua?” “Hapana simjui bali alijitambulisha kama ni Mpenzi wa zamani wa Mwana,” “Alikuwaje? Yaani kama utamuona unaweza kumjua?” “Yap! Naweza kumjua kwani tayari amekuja mara mbili hapa ndani, ukiacha siku hiyo ya kuleta sukari na majani, lakini pia alikuja jana hapa wakati ule huyu dada amekuja kuniita,” aliongea mama Kubwa huku akimnyooshea kidole Marsha.
Inspekta Kalindimya akamuangalia Marsha ambae alionekana kupatwa na mshituko wa mbali ambao ni Inspekta pekee alieuona, Marsha akatikisa kichwa na kusema
“Ah! Ni kweli nilikukuta na mtu umesimama nae, nilimuona kwa mgongoni mwake tu, na wakati mimi nafika, yeye alikuwa akiondoka, naweza kumkumbuka kwa umbo tu maana sura sikuiona,” alisema Marsha kama vile ni mtu anaejuta hivi.
Inspekta alikuwa ameanza kupata matumaini ya kumjua mtu huyo, lakini kwa jibu lile la Marsha aliona kama bado tu wapo gizani, akamgeukia mama Kubwa na kumuuliza
“Ukimuona mara nyingine utamjua, lakini je anapokaa unapajua?” “Hapana wala sipajui, maana ndio ilikuwa ni mara ya kwanza kuonana nae siku hiyo, sikuwahi kumuona kabla,”
“Dah! Huyu muuaji amejipanga sana, anafuta nyayo zake kila alipopita, lakini hivi karibuni tutajua tu, hebu tuuone huo mfuko wa sukari aliouleta,” alisema Inspekta na kusogea pale ulipo.
Alipoukaribia tu aliweza kuziona namba zile walizozikuta kwenye mpini wa kisu kilicho muua marehemu Mwana, akapata uhakika kabisa kuwa alieuleta mfuko ule ndio muuaji halisi wa Mwana.
Alitoa diary yake ndogo na kulinganisha namba zile, kisha akamuita Marsha aje kuhakiki na hata nae akathibitisha sasa kwamba kuna uhusiano mkubwa matukio hayo mawili, wakarejea alipo mama Kubwa na kumuuliza kama ana hayo majani ya chai aliyoletewa.
“Ndio inspekta, alileta box kubwa sana kiasi isingewezekana kulitumia mara moja na kumaliza, ndani kuna pakti nyingi ambazo hata bado hazijatumika, zipo hapa, kama utalihitaji nitakuletea tu,” alisema Mama Kubwa huku akiwa tayari kunyanyuka kulifuata, alisubiri ruksa tu toka kwa Inspekta.
“Hebu fanya hivyo, lilete nilione,” alimjibu huku akijiweka vizuri kwenye sofa lake kusubiri hilo box liletwe.
Mama kubwa akawa tayari kunyanyuka kwenda nje kufuata box hilo, lakini akakumbuka na kumuita Joy ambae alifika punde tu wito ulipomfikia na mama kubwa akamwambia aende Store akalete box la majani ya chai. “Nilete paketi moja tu ama box zima?” joy aliuliza akiwa tayari amepiga hatua “Lete box lote tu na paketi zake bila kulitoa chochote ndani, yaani lilete kama lilivyo sasa,” alitoa maelekezo Inspekta. Joy akaitika sawa na kuondoka akimuacha mam akirudi kuketi chini alipokuwa ameketi awali wakimsubiri na kwa kuwa stoo yenyewe ilikuwa ni jirani tu na pale walipokuwa wameketi wao, alichukua dakika chache tu na kurudi na box hilo. Alilifikisha na kumkabidhi Inspekta mbae aliweza kuliona kwa mbali tu likiwa limeandikwa kwa nje kuwa ni dozen moja ya paketi za majani ya chai. Akalipokea na kuanza kulikagua kwa kuligeuza geuza huku na kule, kila upande. Muda wote huu Marsha alikuwa akifuatilia kila hatua ya mkuu wake anayoifanya, akiwa naelekea kwenye kuridhika kuwa kile alichodhania kuwa kipo pale, hakipo, sasa akakiona kwenye kipande cha karatasi kilichokuwa kikining’ing’inia huku kingine kikiwa kipo palepale kimeshika. Alivyo viunganisha tu, akapata kile ambacho alidhania kukiona pale, alipokiona tu akauma mdomo wake wa chini na kutikisa kichwa kama vile ameelewa kitu Fulani, kisha akampa box lile Marsha na bila kumwambia lolote nae akaanza kutazama eneo lile ambalo alimuona mkuu wake wa kazi akiliangalia. Akatazama na kisha akasogeza diary na kuandika tena namba zile, lakini Inspkta akamuuliza kama namba zile amezitambua? Akajibu ndio namba hizo amezijua na amezihakiki kama zina tofauti yoyote. “Sasa tunalazimika kuondoka na box hili lakini pia mfuko ule…” aliongea akimtazama Marsha kisha akageuza shingo kumwambia Mama Kubwa “…tunaweza kuupata mfuko huo wenye sukari?” kwa haraka bila hata kuhoji, Mama Kubwa akakubali, Inspekta akamwambia abadili na kutoa sukari iliomo mle ndani ili wao waondoke na mfuko mtupu. Joy aliekuwa yupo pale bado amesimama, akausogelea na kuusogeza kati na kisha akachukua kindoo kidogo na kumimina sukari ile na kisha akakunja mfuko huo na kumkabidhi afande Marsha ambae aliupokea na kuuweka chini. “Bado hilo box, nalo tunalihitaji kwa ajili ya shughuli zetu,” Joy akageuka na kulichukua na kutoka nalo kuelekea tena Stoo huku Inspekta akiwa anaaga kwa mama Kubwa kuwa wataendelea tu sana kufika pale, hivyo yeye asiwachoke. “Sawa baba, nitafurahi tu siku moja mkimtia nguvuni huyo muuaji, maana amani imetoweka na tunaishi kwenye mazingira ya wasiwasi mtupu,” “Msiogope kabisa, kwa sasa mpo salama kabisa, jeshi lenu linawalinda na chochote kitakacho kuwa kinaendelea hapa sisi tutajua hata kabla ya nyinyi wenyewe kujua, hivyo kuweni na amani tu mama Kubwa,” alimjibu huku tayari Joy akiwa amefika na kusimama nyuma ya Marsha ambae alionekana kuwa tayari kupokea box lile. Kama mtu aliekumbuka kitu hivi ama kumkumbuka Joy, akamuuliza “nakumbuka muda mchache kabla ya kutoka mwili wa marehemu MwanaHarusi wewe tulikuwa pamoja na ukaondoka na marehemu MwanaHeri, je nimekosea?” “Upo sahihi kabisa,” jibu lile lilimfanya Inspekta Kalindimya awaangalie kwa zamu Marsha na Joy, bila kujiuliza mara mbili akawaambia warudi kukaa ili waongee kidogo huku yeye akiwa ni mtu wa kwanza kuketi kwenye sofa lililokuwa jirani lakini likiwa ni tofauti na lile alilokaa awali. Baada ya yeye tu kuketi, wengine nao wakafuatia huku Marsha akiwa ni wa mwisho kuketi na aliketi jirani na alipo mama Kubwa. “Marsha ilikuwaje hapo? Mbona kama vile sijalielewa swali lako, unasema huyu Joy wakati mlipokuwa chumbani yeye akatoka na marehemu MwanaHeri kabla ya kukutwa na mauti, hebu fafanua kidogo ili nielewe,” aliuliza Inspekta akimtazama Marsha. “Yap! Ni kwa kuwa nae tunae hapahapa anaweza kutupa majibu,” kisha nae akamtazama Joy na kumuuliza “Nilikuona ukitoka na marehemu, hapo nikiwa namuona tu kama ni mtu tu ndani ya nyumba ile, Sikuwa nikimfahamu, wewe pia nilikuona ukishughulika mara kwa mara kitu ambacho kilinifanya niamini kwamba wewe ni muhusika ndani ya nyumba ile, lakini baadae ulikuja na kumuita Marehemu na bila kipingamizi yeye akanyanyuka kutoka chumbani na mkaelekea nje, je mlienda wapi?” “Tulipotoka chumbani mle tulikwenda moja kwa moja hadi nje ambapo nilienda kumuhoji marehemu kwani nilikuwa nimepata ujumbe wake kuwa alikuwa akinitafuta, ndio nikawa nimemuita ili kumsikiliza kwani mle ndani katu tusingeweza kuelewana,” “Alikuwa kweli akikuita ama ilikuwa ni habari ambayo si ya kweli?” alihoji Inspekta “Ni kweli alikuwa ana shida name,” “Shida gani?” “Mwana alikuwa amenunua simu mpya, ambayo bado hakuwa anajua kuitumia hivyo mara nyingi mimi nilikuwa nikimsaidia kumuonesha pale alipokwama, hata mara hiyo niliamini aliniita kwa ajili hiyo,” alisema Joy akikumbuka tukio hilo “Je ni kweli alikuita kwa ajili hiyo?”
“Ndio, aliniita kwa sababu hiyo hiyo, lakini Sikuwa na muda wa kutosha kufanya kile alichotaka, kwani muda ulikuwa hauruhusu,” “Ni kipi alichokuwa akikihitaji ambacho ulikuwa huwezi kukifanya muda huo?” “Kulikuwa na namba ya simu alitaka kuihifadhi kwenye simu yake, alitaka kuisave yaani lakini akawa hawezi, ndio akanifuata mimi kwa ajili ya jambo hilo,” “Kwani ilikuwa ni lazima sana kui save kwa muda huo wa kuelekea kwenye muda wa kutoka kwenda kuzika?” “Nilimuuliza swali hilo akaniambia kuwa kuna mtu amemuandikia namba hiyo na ipo kwenye screen anahofu ataifuta na wakati ni namba muhimu,” “ok! Nini kikafuatia baada ya hapo?” “Nikaona kwa kuwa mimi muda hauruhusu, yaani siwezi kumsaidia, basi acha nimtafutie mtu ambae anaweza kumsaidia juu ya jambo hilo, ndio nikamkumbuka Salma mara tu nilipomuona akiwa ameketi na wasichana wenzie jirani na pale tulipokuwa tumesimama mimi na marehemu, nikamuita.” hali ikazidi kuwa tete kwsa Inspekta na afande Marsha, wakatamani kumjua na huyo Salma sasa, Marsha akauliza “Salma huyo ni nani?” “Ni binti yangu afande,” mama kubwa akajibu haraka haraka akiwa hajiamin9i kabisa, mapigo ya moyo yalionekana kwenda kasi kuliko kipimo chake cha kawaida, Inspekta akomba aitwe pale haraka kama yupo. Kwa mara nyingine Joy akatoka na kurudi akiwa ameongozana na binti wa kiasi cha miaka kama 16 hivi, alifika na kuwasalimia kisha akaketi jirani na mama yake, ambapo afande alijitambulisha na kumtambulisha mwenzie, kisha mahojiano nae yakaendelea. “Salma unamfahamu marehemu MwanaHeri?” “Ndio ninamfahamu,” “Unamfahamu kivipi?’ “Ni rafiki kipenzi wa mpangaji wetu.” “Una taarifa juu ya kifo chake?” “Ndio ninazo,” “Sawa sawa, sasa unajua kuwa wewe ndio mtu wa mwisho kuonekana na marehemu?” lilikuwa ni swali gumu na zito kwa Salma, wote wakamtazama, nae akamtazama mama yake na kumkuta akimtazama yeye pia. Inspekta alitaka kujua tu kitu Fulani juu ya jambo hilo, alipoliona akarudi kwenye mahojiano. “Unakumbuka mara ya mwisho marehemu alipoonekana nawe, kabla alikuwa na nani?” salma tayari alikuwa maeathirika kwa swali lililopita, akajibu kwa kumuonesha kwa kidole Joy huku akiuma uma sehemu ya pindo la khanga yake. “wewe ulikuwa na nani wakati Joy na Mwana wapo pembeni?” “Nilikuwa na wanafunzi wenzangu ambao walikuja msibani kunipa pole,” “Baada ya kuwaona Mwana na Joy ni kipi kilifuatia?” “Dada Joy aliniita na kuniambia nimsaidie kusave namba kwenye simu yake iliyokuwa ipo chumbani kwa marehemu da MwanaHamisi,” “Ikawaje?” shauku ikawarejea tena. “Da Joy akaondoka na mimi na Dada Mwana tukaenda hadi chumbani kwa marehemu dada Mwana na kuingia ndani ambapo alitoa simu kabatini na kunipa,” “Kwa hiyo wewe ukai save hiyo namba?” aliuliza Inspekta na Marsha akaendelea tu kuandika. “Ndio nikaisave namba hiyo na kumrejeshea simu yake,” “Wakati huo yeye alikuwa wapi na anafanya nini?” “Yeye alikuwa kabatini akitafuta kitu Fulani hivi maana alikuwa akichakura chakura kwenye nguo,” “Alikwambia ni nini alikuwa akitafuta?” aliuliza Marsha na Salma alitikisa kichwa tu kukataa, “Baada ya hapo ikawaje?”Marsha akahoji tena. Mimi nae tukatoka tukiwa tumeongozana, mimi nikiwa mbele na yeye akiwa nyuma, lakini hatukuachana sana, hadi tulipofika nje akafunga mlango na sasa alikuwa na simu yake mkononi,” “Unaweza kuikumbuka hiyo namba ambayo uliisave?” aliuliza Inspekta Kalindimya. “Hapana kwa kweli, ila nakumbuka tu jina la Mtandao ila namba yenyewe siikumbuki,” “Hiyo namba wakati uki save ulisave kutoka kwenye namba zilizopigiwa ama kwenye missed calls ama kutoka kwenye namba alizopiga?” “Hapana, ile namba ilikuwa ipo kwenye screen, ilikuwa haijapiga wala kupigiwa, ni namba inaonesha iliandikwa tu na kuachwa ili mtu asave,” kengele ya hatari ikalia kichwani kwa Inspekta sasa akajidhihirishia kuwa mtu anae fanya mauaji yale si mtu wa taratibu, umakini mkubwa mno unatakiwa. “Mh… tunakusikiliza Endelea,” Marsha akamtaka aendelee tu na habari ile nyeti kwao. “Mi nilirejea kwa wenzangu na kuketi kama awali, Mwana nae alikuwa amepiga kama hatua tatu mbele hivi akielekea chumba cha wageni wa marehemu na wenyeji ambao ni kina mama, akatokea dada mmoja ambae alikuwa akilia pia, akamkumbatia Mwana na kumpa pole,” akatulia kumeza mate, kisha akendelea “Wakati huo hapo nje tulikuta jeneza la marehemu dada Mwana likianza kutoka uwani kwenda barabarani kwa ajili ya kuondoka kwenda makaburini, Mwana akaanza kulia kwa uchungu sana akiwa pembeni ya jeneza, akatokea dada mwingine mmoja hivi, tofauti na Yule wa awali, huyu alikuwa ni mweupe tena ni mrefu na mwembamba kiasi akamnong’oneza sikioni na kisha akamshika mkono, sote tulijua hawa wanajuana tu na hakuna alie shughulishwa nao,” alisema Salma kwa kujiamini kabisa.
“Wakaelekea wapi?” akauliza Inspekta kwa shauku, watu wote wakiwa wamemtolea macho Salma, hakuna yeyote mle ndani aliekuwa akijua juu ya jambo hilo. “Wakarudi kwenye mlango wa marehemu da MwanaHamisi, na da Mwana huyu aliefariki jana akatoa tena funguo na kufungua mlango, wakaingia mle ndani na tangu hapo sikujua tena kilicho Endelea hadi wewe ulipokuja na kuingia mle ndani,” “Alitoka saa ngapi huyo dada alie ingia na marehemu Mwana?” Inspekta Kalindimya aliendelea tu kuhoji huku akiwa makini na majibu ya Salma. “Noo! Sikuwa makini kabisa kumtazama tangu wakati ameingia hivyo sikujua kabisa niwakati gani alitoka, kwani tulikuwa busy na kutazama jeneza la marehemu likitoka mle ndani kuelekea makaburini,” alijibu binti kwa uhakika kabisa, afande Marsha na Inspekta Kalindimya wakatazamana kujiuliza nani aulize swali lifuatalo, Marsha akaelewa, akamuuliza Salma “Alikuwa amevaaje huyo mdada unaemzungumzia hapa?” “Alivaa Hijab nyeusi na miwani kubwa pia nyeusi, na kila muda alikuwa ameweka kitambaa chake usoni kama mtu anaefuta machozi vile na hata mara moja hakukitoa kitambaa hicho usawa wa pua na mdomo,” alizidi kufafanua Salma. “Ukimuona huyo mdada unaweza kumjua?” “Hapana nina hakika siwezi kumjua, maana sura alikuwa akiifunika sana kwa kitambaa usawa wa pua na mdomo na wakati mwingine akiwa anainama chini mara kwa mara,” “Je kwa hilo umbo ulilotutajia, kama tutamleta hapa unaweza kumtambua?” “Yeah!Kwa umbo hata usiku wa manane naweza tu kumjua ila kwa sura hata nisilidanganye jeshi letu, siwezi kabisa kumtambua.” Alimaliza Salma kujibu na Marsha aliekuwa akiandika mahojiano hayo akamtazama mkuu wake wa kazi. “Salma nashukuru mno kwa msaada mkubwa uliotupatia, huenda ukatupatia mwelekeo huko mbele japo kwa sasa bado unatuacha njia panda, ila tu wakati wowote tukikuhitaji, naomba utoe ushirikiano, sawa Salma?” aliuliza Inspekta na Salma akakubali bila kipingamizi. Akamgeukia mama Kubwa na kumuuliza “Mama Kubwa huyu aliekufa jana jioni nae jina laek ni Mwana, ama nimekosea?” “Wala hujakosea, huyu pia ni Mwana, tumejua kuwa anaitwa MwanaKheri,” alijibu mama Kubwa huku akijiweka vizuri, alijua sasa mahojiano yamehamia kwake. “Jana hadi usiku tunapo achana nawe, jina hilo la mbele ulikuwa hulijui, leo saa hizi ni asubuhi unasema mmelijua, umelijuaje?” aliuliza Marsha huku akifunua tena diary yake kuandika anayo yasikia pale. “Kama unavyojua tena misibani, mengi yanasemwa, hata jina hilo limesemwa semwa tu hadi yakanifikia kuwa jina lake halisi ni hilo,” mama Kubwa aliingiwa na hofu kutokana na kujichanganya na kuchanganywa na maswali ya wale maafisa upelelezi. “Ok! Kwa hiyo ni jina ambalo halina uhakika?” “Niseme tu hivyo kwa kuwa hatukumsikia mwenyewe, ila ninaamini itakuwa ni jina lake hilo,” “Ok! Na Yule mwana aliefariki awali ambae alikuwa ni mpangaji humu ndani, alikuwa akiitwa Mwana nani?” aliuliza Marsha Mauki. “MwanaHamisi, MwanaHamisi Rehani,” sasa aliamua kuwa awe anajibu kifupi ili tu asijichanganye. Wakatikisa vichwa kuoneshwa kuridhika na majibu yale na kujilaza kwenye sofa na kuangalia juu, akashtuka na kunyanyua shingo ghafla na kumuuliza Marsha Mauki “Funguo ya chumba cha Marehemu umekuja nayo?” “Ndio mkuu, ninayo hapa,” alijibu huku akinyanyuka na kuitoa kwenye Jeanz yake ya kike aliyovaa huku akimkabidhi mkuu wake. “Twende chumbani kwa Marehemu,” wakaongozana huku wakiwa na shauku, Marsha alitaka kujua kuna nini Boss wake amekipata pale ghafla vile na Inspekta nae alitaka kuhakikisha kile kilicho kuja ghafla kicwani. Walifungua na kuingia wao wawili tu chumbani, Mama Kubwa alibaki nje, kitu cha kwanza alichokifanya Inspekta ni kwenda moja kwa moja kwenye kabati ya marehemu Mwana na kupangua taratibu vilivyomo, kimoja kimoja. Alipofikia hatiua Fulani hivi akamuagiza Marsha aende kwenye gari yake akalete Kamera ili kuna kitu akihakiki mle ndani. Marsha akachukua dakika tatu tu kuwa tayari amerudi ndani akiwa na kamera mkononi, akamwambia kuopitia hizo picha zilizopo kwenye Kamera, ahakiki kama kuna mabadiliko yoyote mle chumbani toka walipo ondoka siku ya kwanza. “Usishughulishwe na kabati lakini, maana tayari hii nimeisha ivuruga, angalia tu tofauti ya juzi na jana, ama kama ina sumbua tukasafishe kwanza,” aliongea huku akiendelea kufanya kazi yake. Kila katratasi aliyoiona mle ndani aliipitia na kuifunua, aliyoiona ina manifaa kwenye kazi yake aliiweka na zile alizoona hazifai aliachana nazo. Marsha akasema ataendelea kuangalia taratibu akivuta subira wakati yeye akifanya kazi yake. Kuna karatasi moja Inspekta akaiona, ilikuwa na namba nyingi za simu, alijaribu kuangalia namba zile, zote zilikuwa na majina ya watu wenye namba hizo, aliona hiyo itamfaa, akaichukua na kuiweka kwenye mfuko wa koti lake. Lakini wakati akiiweka, akamsikia Marsha akishtuka kwa mshangao na kumuita “Inspekta…” huku akimsogelea mkuu wake, kamera ikiwa mkononi, Inspekta akageuka kumtazama, wakati huo tayari Marsha alikuwa pembeni ya ubavu wake, akampa Kamera na kumwambia…
“Mkuu picha hii ya juzi ipo tofauti na ile ya jana ambayo pia ni tofauti na mandhari ya sasa,” Inspekta alipokea Kamera na kuiangalia picha iliopo, baada ya kuiona tu, akatazama juu kwenye dari la nyumba ile, akaiona tofauti. Ilikuwa ni tofauti ndogo sana, ambayo ni mpelelezi pekee anaweza kuigundua ama mwenye chumba mwenyewe. Sehemu ya mlango wadari ilikuwa ipo wazi kwa ufinyu mdogo mno. Wakasogea pale pale chini na kuangalia kwa umakini zaidi, hapo ndio wakahakiki kuwa pale palivyo, hawakupa acha vile siku ya kwanza baada ya mauaji ya MwanaHamis, hapo ndio wakagundua kitu. “Ni kweli Marsha, juzi picha zinatuonesha palikuwa pamefunikwa vizuri sana hapa kwenye mlango wa dari, iweje leo uwe wazi kidogo? Nahisi hapa kuna uhusiano wa matukio haya ya mauaji yaliyotokea ndani ya chumba hiki” wakatafakari na kumuita tena mama Kubwa. Walichofanya sasa ni kumuonesha dari na kumuuliza tu kuwa juu ya dari ya nyumba ile kuna vitu huwa wanahifadhi? Akashangaa kwanza kwa kuoneshwa uwazi ule mdogo uliopo na kusema hakuna kitu chochote kinachowekwa darini. Wakamuuliza tena kuna mtu aliingia baada ya wao kuacha chumba kimefungwa siku ile ya kwanza? Akakana na kusema kuwa hakuna mtu yeyote alie ingia mle ndani zaidi ya MwanaKheri. Inspekta akamwambia mama mwenye nyumba amletee tochi kama ipo, mama Kubwa akasema anayo, akaifuata na kurudi nayo, wakati huo Inspekta tayari alikuwa amepanda juu na kufunua sehemu ile ya mlango wa dari. Kwa tahadhari kubwa akaingiza kichwa chae ili kutazama sehemu ya ndani ya dari, alipotazaama baada ya kupewa tochi, hakuweza kuona chochote, akaingia zaidi, alichoweza kuona ni alama ya kujivuta tu na kuweka mistari kuonesha kuwa kulikuwa na mtu kule juu hivi karibuni. Akashuka na kumtaarifu Marsha kile alichokiona na tangu hapo kukawa hakuna jipya tena, wakamuaga Mama Kubwa na kutoka wakimuahidi mama Kubwa kuwa atawaona tu sana hapo na ikiwa kuna jambo lolote, basi asisite kuwajulisha “Namba yetu si unayo?” aliuliza Marsha huku akimtazama Mama Kubwa. “Ndio ninayo ya Inspekta na Joy anayo nyingine ya Yule askari mwingine,” wakatoka na box tupu la majani ya chai na mfuko mtupu wa Sukari hadi garini kwao ili kuondoka. Wakiwa nje ya gari Inspekta alimrushia funguo Afande Marsh na kushika kitasa cha mlango akisubiri Marsha aingie garini na kumfungulia ili waondoke pale kurejea kazini. Marsha akashika Sterling na kuondoa gari ile kwa mwendo wa taratibu mno huku akionekana kama amesongwa na mawazo, kushoto kwake alikuwepo Inspekta Kalindimya ambae nae alikuwa kimya kabisa, hivyo kufanya safari kuwa ni ya Kimyakimya pasina yeyote kuongea. Kimya kilitawala hadi pale Inspekta alipokikata kwa kumuuliza Marsha anayaonaje matukio yale ya mauaji yanayo Endelea? Marsha akaonekana ni kama mtu alietwishwa mzigo mzito asio weza kuubeba. Lakini akanyanyua ulimi na kuseam inaonesha muuaji alikuwa amejipanga sawa sawa. “Ni kweli Marsha, kinacho nichanganya kingine ni kuwa vipi ile Cealing board jana hatukuiona?” “Mkuu umeona jinsi ilivyokuwa imewekwa? Kwa muda ule tulivyokuwa na haraka vile, isingewezekana kuona jambo hilo,” aliongea huku akipangua gear za gari na kunyamaza. “Inavyo onesha muuaji alijificha juu kwenye Sailing board, lakini sasa aliingiaje?” “Muuaji atakuwa alilala huko juu na kumuua MwanaKheri, lakini bado jibu halijapatikana, aliingiaje kumuua MwanaHamis?kabla hilo swali halikujibiwa, inspekta akaongezea “Kingine ambacho naweza kukitazama hapa kwa haraka ni juu ya mauaji, hadi sasa walio uawa ni watu wawili, tena ni marafiki, majina ya wahanga wote wawili yakiwa yana anziwa na Mwana, japo mbele ni tofauti,” “Na ukitazama kwa umakini utagundua tofauti ya vifo vyao ni masaa kadhaa wala si siku, tena ndani ya chumba kimoja, utata mtupu!” aliongezea Marsha. “Hapo sasa!Na ajabu zaidi anaaacha ujumbe kwenye visu vya aina moja, Sijui ni kipi amemaanisha hapo?” walikuwa wakijiuliza maswali mengi huku wakiwa hawana majibu hata chembe. “Inspekta kwa kweli maswali ni mengi sana…” “Na sisi ndio tunaopaswa kuyatafutia majibu,” aliongea Unspekta na kuufunga rasmi mjadala huo na kimya kikarudi kutawala tena. Kimya kifupi tu kikakatishwa tena na sauti ya Marsha alieuliza kuwa safari yao inaishia kituoni amam kuna sehemu nyingine? Inspekta akamwambia ampeleke tu nyumbani kwake akapumzishe kichwa maana anahisi tayari ameisha choka japo muda wa kazi haujaisha. Inspekta baada ya kufika kwake akamwambia Marsha aende tu na gari ila afanye kila linalowezekana wakutane ofisini saa kumi na moja jioni kuna mahali wanapaswa kwenda muda huo. “Sasa boss wewe utakuwa huna usafiri, unaonaje mimi nikipitia hapa ili kukuchukua?” “Pia si wazo baya, utafanya vizuri,” akafungua mlango na kutoka kuelekea ndani ya nyumba yake.
Lengo la kurudi nyumbani muda ule lilikuwa ni kujipumzisha kutokana na kuchoka kwa akili yake, lakini mara tu alipoingia ndani, hakujipumzisha kama alivyotamani, bali alipoketi kwenye sofa la watu wawili ambalo aliona ni muafaka kwa yeye kupumzika, akakumbuka kitu. Alikumbuka ile karatasi ya namba ya simu aliyochukua kwenye kabati la marehemu mwana na kuanza kuiangalia huku akiwa makiinanamba zile. Hakuwa anajua ni kipi anachokitafuta, bali alihisi kuna kitu atakijua kupitia namba zile. Kwa kuwa hakujua ni kipi akitafutacho pale, akatoa simu yake ya mkononi na kuangalia namba zile za simu zilizompigia ili kumpa taarifa ya vifo vya kina Mwana wote wawili. Aliziandika pembeni kwenye karatasi ileile ya namba zile za simu alizochukua kwa Mwana na kisha akapiga ofisini kwao na kumtaka mtu wa idara ya mawasiliano (Operator) amueleze namba zile za simu ya mezani ni za wapi. Alimtajia na upande wa pili ukamwambia utamjulisha baada ya dakika chache, akakata simu na kuendelea na kazi nyingine ndogondogo, uchofu hauku wepo tena, alitamani tu kuendelea kuieleleza ile kesi, aliamini kabisa kuwa muuaji ni mtu ambae haitowapa shida kumkamata. Operator wa jeshi la Polisi alifanya kazi ile ya kuzitafuta nmba zile ili kuzibaini zilikuwa ni za wapi, haikuchukua muda akampigia boss wake na kumueleza kwamba namba zile zote zilizotumika kumpigia simu zipo Wilaya ya Kinondoni, hizo Call box zake nazo zote mbili, yaani namba zote zilizotumika kumpigia simu yeye Inspekta, nazo zipo Mwananyamala ila ni sehemu tofauti “Namba iliotumika kukupigia juzi, ipo Mwana nyamala A, na hiyo nyingine haipo mbali, bali ipo Mwana Nyamala Hospitali, utaona kuwa zipo karibi karibu mno, haifiki hata mita mia tatu,” alielezea Operator na kunyamaza. “Ahsante sana kwa kazi nzuri,” Inspekta alijibu na kukata simu na kuanza tena uchunguzi mpya, maana sasa alibaini kitu kipya. Alibaini sasa kuwa katika yale matukio yote mawili, muuaji sio mtu mmoja, alitambua kuna watu zaidi ya mmoja ambao wanfanya mauaji yale, ama niseme anaeua na anaepiga simu ni watu wawili tofauti kabisa. Simu yake ya mkononi ambayo sasa alikuwa ameiweka mezani, akainyanyua na kumpigia simu Jitu kumuuliza alipo. Jitu akamwambia bado hajarejea kutoka huko alipokuwa, akakata simu Inspekta na kumpigia simu Marsha na kumwambia kuwa kitu anataka kuongea nae, aende kwake muda ule. Marsha akamwambia kuwa amefika ofisini na kumkuta mkuu ambae alimuita na sasa anaelekea huko, hivyo ampe kama nusu saa hivi atakuwa amefika huko kwake, wakakubaliana hivyo na kila mmoja akaendelea na hamsini zake. Inspekta akaketi vizuri mezani kwake na kuchukua karatasi mpya kabisa, alitaka sasa kucheza na namba zile ambazo zilikuwa zikiachwa kwenye mikono ya visu vya wauaji. Aliisumbua sana akili yake kwa kujaribu na kufananisha na namba za simu zile alizozichukua kwa Mwana, lakini wapi. Akajaribu kuzijumlisha zile za kwanza na zaz pili kwa kudhani atapata kitu Fulani, lakini bado. Mara ya tatu akajaribu kuzitoa namba zile zenyewe kwa zenyewe, lakini hakuambulia kitu, kila alichojaribu hakufanikiwa akaona anaichosha akili, aipumzishe kwanza. Hapo ndio akasikia sauti ya hodi kwenye mlango wake, alipotazama saa akajua huyo atakuwa ni Marsha amefika, alisogea mlangoni na kumfungulia aingie ndani, Marsha alitii na kutoa saluti kwa mkuu wake kisha wakaelekea sofani kuketi. “Marsha kuna kitu hapa tayari nimekijua, ndio maana nimekuita ili tujue tunafanyeje,” alianza Inspekta kuongea “Ni kitu gani hicho boss?” “Nimegundua hapa kwamba Muuaji wa Mwana heri na mtu alienipigia simu ni mtu mwingine, yaani ni watu tofauti kabisa,” “Kivipi Boss?” akauliza huku akijiweka vizuri kwenye sofa, Inspekta akachukua moja kati ya karatasi yenye maelezo na ramani aliyochora toka Mwananyamala hadi Magomeni, akampa Marsha huku akimuelewesha “Kwenye ile simu ya kwanza, yaani ya kifo cha Mwanahamis, yenyewe wala hainisumbui kichwa, kuna tofauti ya zaidi ya dakika thelethini tangu kupokea kwangu simu na kutokea mauaji…” akameza mate na kuendela “Lakini hii simu ya pili, ukiangalia umbali wa Mwananyamala Hospitali hadi Magomeni Mikumi, ndipo hapo ninapopata mashaka, maana ni umbali mrefu mno na kuna tofautiya dakika mbili tu toka nilipo pigiwa simu na tukio lenyewe la mauaji, ndio maana anapata shaka kuwa muuaji wa hili tukio la pili, sio Yule aliepiga simu,” alimaliza Inspekta kuongea na kumsikiliza Marsha nae ana maoni gani, kama alijua akadakia “Yeah! Ni kweli, haiwezekani kabisa hata kwa dakika 5, achana na hizo mbili ulizosema, ndani ya dakika 3 mtu awe ametoka Mwananyamala Hospitali aje Magomeni Mikumi na kufanya mauaji kisha apotee,” akatikisa kichwa kukataa. “Tena mpigaji wa simu aliekuwa akipiga si umesema ni mwanaume Inspekta?” “Ndio Marsha, mara zote amenipigia mwanaume,” alijibu na kumtazama Marsha.
“Kumbuka ile kauli ya Salma kule kwao, huenda ikawa sahihi kabisa hisia zako,” “Kwamba alimuona marehemu akiwa ameongozana na mtu alievaa hijabu?” alihoji Inspekta kama vile hajiamini hivi, Marsha akaitika kwa kichwa kukubali, lakini Inspekta akakanusha “Hapana Marsha, hicho wala sio kigezo cha kukikamatia, yawezekana tu akawa ni mwanaume alievaa mavazi ya kike ilimradi tu kukamilisha lengo lake,” “Dah! Eeh hapa kwazi kweli kweli,” ukimya ukatawala kidogo hadi Inspekta aliekuwa akiangalia ile diary ya upelelezi ule alipoifunga na kumtazama Marsha kisha akamuuliza “Vipi kwa Mkuu kulikuwa na kheri ama kuna tatizo linguine?” “Hapana alikuwa anasema kuhusu kesi hii ni kwa nini kesi leo inaingia siku ya nne nae hajui lolote? Nikamueleza tu kuwa hakukuwa na nafasi hata chembe ya kuweza kuonana nae na kuliongelea jambo hili pamoja nae,” “Sawa kabisa, ni jibu zuri, kwa hiyo amesemaje?” “Amedai kesho asubuhi kabla hatujatoka kwenda popote tuwasiliane nae, yeye atawahi kufika hivyo tukutane nae tukiwa pamoja mimi nawe,” “Sasa inategemea, anaweza kuchelewa kufika nasi tumeanza kuelekea kwenye mafanikio, yaani kumsubiri mtu ambae anataka kujua juu ya mauaji ambayo yote yapo kwenye file? Mimi nimepanga kesho tutaanzia sehemu moja hivi ili kwenda kasi na muda wetu,” “Kwa hiyo unataka kuniambia haitawezekana tena kesho kuonana na Mkuu?” aliuliza Marsh akitaka kupata kauli ya Inspekta. “No! sijasema hivyo bali nimeweka kama utangulizi, ikitokea tu kuwa tumepata dokezo ama fununu, iwapo itatokea habari yoyote kama emergency, italazimika sisi tuachane na mkuu twende kwanza huko, maana tupo pazuri sasa kwenye upelelezi wetu,” “Nimekuelewa, lakini nakushauri unapaswa kuonana na Mkuu, kwani inavyoonesha ni kama ana kitu Fulani hivi juu ya kesi hii, mtafute,” “Kweli Marsha? Kwanini asikwambie wewe ambae umeonana nae ana anajua kuwa mimi nawe sote ndio tunaofuatilia kesi hii?” “Ni kweli mkuu huenda ni jambo ambalo sijapaswa kulijua,” “Na kama hujapaswa kulijua basi ujue halihusu kesi hii, maana kama linahusu kesi hii ni lazima utalijua tu, lakini nitamtafuta baadae ama kesho,” alisema huku akikusanya makaratasi yake na kutaweka kwenye diry yake na kumshindikiza Marsha ambae tayari alikuwa akiaga ili kuondoka. “Lakini Marsha, mazishi ya Mwanakheri si ndio leo hii?” alikumbuka Inspekta na Marsha akakanusha kuwa maiti yenyewe wana ndugu watapewa leo jioni hii, hivyo mazishi wamewashauri yafanyike siku ifuatayo muda wowote. “Sawa, ushauri mzuri, sasa hakikisha kuwa hakuna chochote kitakacho tokea huko msibani, wapange vijana wa kutosha, kila tukio pale liwe lina mtu anaelifuatilia kwa ukaribu, vyumbani weka watu wetu kama kawaida, unanielewa afande?” Inspekta alitoa maagizo na kumfungulia mlangoa Marsha kisha akaendelea kumtazama. “Ndio mkuu, maagizo yako yatatekelezwa kama ulivyo sema,” kisha aktoka na kwenda zake akimuacha mkuu wake akijifungia ndani mwake. **********
Siku ya pili asubuhi na mapema Inspekta aliwasili kituoni na kumchukua Marsha ili kukutana na Mkuu waUpelelezi wa mkoa ambae alitaka kujua ni kwanini hadi wakati ule kesi ile ya mauaji ilikuwa haijamfikia yeye rasmi mezani kwake kwa ajili ya utambuzi na kupangiwa majukumu ya nani aiendeshe? Inspekta alijitetea kuwa majukumu ya kesi ile ndio sababu ya kufanya ichelewe kumfikia, lakini akamueleza tukio zima na hadi walipofikia sasa na nini mipango yao ya baadae iwapo wao ndio watakaopewa jukumu la kuiendesha kesi hiyo ama kumpa yeyote atake chagukliwa kuendesha kesi ile. “Sawa basi kama ni hivyo, maana nimeshangaa kuona ukimya ukitawala huku mauaji yakiendelea, hivyo wewe na Marsha mtaendelea na kesi hiyo, wakati ile ya utoroshaji wa Sukari, nayo si ilikuwa chini yako pia?” aliuliza mkuu huku akinyoosha kidole juu kama anaekumbushia kitu Fulani. “Ndio Mkuu, ile nilikuwa nae pia, Sikuwa peke yangu,” alijibu Inspekta Kalindimya. “Sawa, sasa hiyo kuanzia sasa ataisimamia jitu, nawatakieni kazi njema,” alimtakia kazi njema na kumpa mkono kisha Inspekta akatoka na kumpitia Marsha aliekuwa amevaa juba maalum kwa ajili ya kwenda kuhudhuria mazishi ya Marehemu MwanaHeri. Safari hii gari iliendeshwa na Inspekta mwenyewe, hadi maeneo ya Sinza nyumbani kwa kina MwanaHeri ambae ndio marehemu, walikuta watu ni wengi mno huku wengi wakionesha kama wamefuata kujua tu ni kipi kilicho sababisha kifo chake. Mazishi yalifanyika kwa amani na utulivu mkubwa huku ulinzi ukiwa umeimarishwa kwa kiasi cha juu mno lakini hadi wanamaliza kuzika, hakuna baya lolote lililotokea wala dalili yauwepo wa jambo hilo nao haukuwepo. Walipotoka makaburini wakarejea ofisini moja kwa moja ikiwa ni mchana wa jua kali, hakuna aliekuwa na wazo lolote muda ule zaidi ya kuhitaji kufika ofisini na kupokea taarifa mbalimbali kutoka kwa askari waliokuwepo kule eneo la msiba. Nao hawakuwa na jipya, siku hiyo amani ilitawala kila sehemu na hatimae wakaimaliza siku hiyo. ********** Zilipita siku tatu pasina habari yoyote huku wao wapelelezi wakiendelea na kazi yao ya kufuatilia muuaji Yule ni nani. Jioni moja wakati Inspekta akiwa maeneo ya Sinza nje ya nyumba ya kina MwanaHeri, alikuwa akitoka ndani y nyumba hiyo, alikwenda pale kupata namba ya Mpenzi wa Mwana. Alifanikiwa kuipata namba hiyo na kuondoka kuliekea gari lake ambalo alikuwa amelipaki upande wa pili wa barabara, kuna mtu akampita kasi sana akiwa na pikipiki aina ya Boxer, lakini mwendo wake ulimtisha kidogo Inspekta, kwani alionekana kama ni mtu ambae alikuwa akimsubiri yeye tu atoke. Kwa kuwa tayari alikuwa amemuona kwa mbali, alimkwepa lakini alishindwa kumzuia kuendelea na safari yaake, nae akaingia garini na kuondoka eneo lile haraka, tayari aliona lile eneo si salama kwake. Moja kwa moja akaelekea kituoni na kuketi peke yake ofisini mwake. Akili yake ili mtuma kumpigia simu Mpenzi wake MwanaHeri ambae aliambiwa kwa kipindi chote cha msiba hakuonekana kule nyumbani japo alionekana kwenye mazishi ya MwanaHamisi. Hapo ndio alipoona kama kuna tatizo, inakuwaje kwenye mazishi ya rafiki wa Mpenzi wake awepo na kwenye mazishi ya Mpenzi wake asiwepo? Akapata shaka na kutamani kumuhoji ili kujiridhisha, huenda alikuwa na tatizo ama alipata shock iliymsababishia ashindwe kufika msibani. Mwenyewe akajiuliza tu kichwani, kweli alishindwa kufika msibani, lakini hata baada ya kuzika kwanini asifike? Akatoa diary yake aliyo andika namba ile ya simu na kumpigia kwa simu yake ya mkononi. Simu iliita sana na haikupokelewa, akapiga tena lakini ikawa ni hivyohivyo. Mara ya tatu sasa ikapokelewa na kwa sauti ya kiume aliepigiwa akaipokea na kusema Hello! Inspekta Kalindimya akajitambulisha na kuomba kuongea na mtu aitwae Loren, aliepokea simu akasema kuwa Loren hayupo ametoka siku ya tatu leo hajaonekana nyumbani na simu aliiacha nyumbani. Kengele ya tahadhari ikalia kichwani kwa Inspekta Kalindimya, akamuuliza aliepokea simu yeye ni nani? Jamaa akamjibu kuwa yeye ni kaka wa Loren. “Mmeliripoti tukio hilo kituo cha Polisi?” “Ndio, na hata nilipoiona simu hii na wewe ulivyojitambulisha ni askari, nikajua huenda tukapata habari aidha ni nzuri ama mbaya, lakini tu nikajua una habari mpya,” aliongea kijana Yule wa upande wa pili akiwa na hofu. Inspekta akaligundua hilo na kumwambia kwamba ni kweli kuna habari mpya, anapaswa afike kituo cha Polisi Oyster bay kabla ya saa 10 jioni kwa ajili ya kupokea habari hizo ambazo zitakuwa ni nyeti kwake. “Afande ninaweza kuja hata sasa?” aliuliza akiwa na shauku ya kutaka kujua ni habari gani alizonazo afande, Inspekta akamwambia aende tu wala asihofu, yeye atamsubiri kituoni. Muda huo ilikuwa ni saa 6, ilipotimu saa 7 mchana, tayari huyo kijana akawa amewasili hapo kituoni na kumuulizia Inspekta, akapelekwa alipo na kuanza nae maongezi. Kwanza alitaka kujua jina la huyo kaka wa Loren, kijana akajitambulisha kwa jina la Chidy, kisha akamuuliza habari mbali mbali juu ya Loren na kazi yake. Chidy akamwambia kuwa ndugu yake ni mfanya biashara na husafiri mara kwa mara kufuata biashara zake mikoa mbalimbali na hasa huenda kwenye mikoa ile ambayo ipo pembezoni na nchi yetu. Alikua akiandika tu Inspekta kisha akamuuliza juu ya kutoweka kwa Loren na Chidy akasema hajuibali tangu siku ya juzi hawajamuona na walipoingia chumbani wakaikuta simu yake ikiita na hadi leo hajatokea tena. “Loren ana familia?” “Hapana, hakuwa na familia bali ana Mpenzi,” “Una mjua Mpenzi wake?” “Ndio ninamjua kwa picha iliopo kwenye simu yake kwani sijawahi kumuona ana kwa ana,” “Nahitaji kumuona,” Inspekta alimwambia Chidy huku akimtazama usoni, Chidy akazama mfukoni na kutoa simu ya mkononi na kumuonesha picha ya Mpenzi wa Chidy ambayo ilikuwa ipo kwenye display. Ilikuwa ni picha ya MwanaHeri, inspekta akamuuliza kama anamjua jina lake Yule mrembo. Chidy akasema kwamba hamjui jina lake ila alizoea kumuona ndugu yake akimuita baby. Hapo sasa ndio akamuuliza kama ana taarifa juu ya kifo cha mtu huyo. Chidy alishtuka sana na kuonesha mshangao tokana na taarifa hiyo na kumwambia Inspekta kuwa haji maana Chidy ndio mtu ambae angemwambia lakini kwa sasa ndio hayupo sasa. “Kuna mtu yeyote alipiga simu wakati wewe ukiwa nayo?” “Ni wengi sana na wote walikuwa wakimtafuta dogo na niliwajibu kwamba haonekani kwa sasa, wengi walisikitika na wamekuwa wakipiga simu mara kwa mara kutaka kujua kama ameonekana,” Waliendelea kuongea kidogo na kumtaka Chidy aiache simu pale kwa ajili ya uchunguzi zaidi na wakati wowote wakimuhitaji na yeye watamuita. Akafanya hivyo na kuiacha simu pale, akaacha namba yake na kusaini makaratasi ya kuthibitisha kuwa ameacha baadhi ya vitu hapo.
Inspekta alianza kuipekua simu ya Chidi ili kuangalia kama atapata chochote, kwanza alianza na namba za simu zilizoingia kwenye simu ile, alizichukua za wiki moja kabla ya tukio la vifo vile na hadi simu ile. Nyingi namba zilikuwa ni zilezile, lakini chache zilikuwa zimepiga mara moja moja, lakini zote alizi hifadhi kwenye karatasi nyingine huku akiandika hadi muda wa kupiga na kama iliongelewa muda mrefu aliandika pembeni pia. Kisha alienda kwa namba zilizopiga na kufanya hivyo pia, akahamia kwenye sms na kuanza kuzisoma, alikuta sms nyingi zilikuwa ni za kawaida tu, mwisho akaingia whatsApp, huko ndio hakukuta chochote cha maana. Alipoona kidogo kwenye kumfaa ni kwenye namba za simu tu. Mwenyewe akajisemea kuwa Loren anaonekana hakuwa ni mtu wa kuchat sana, hivyo hakuwa na lolote la kumuongoza huko, alkamaliza na kuiweka simu ila kwenye mfuko wa juu wa koti lake na kunyanyuka. Wakati kitoka nje ya jingo la ofisi simu yake ya mkononi ikaita na sasa tena ilitumika Call box, akapokea na kuweka sikioni, hakukuwa na salamu bali alikanywa tu kuwa aachane na ile kesi asijifanye ana kimbelembele, itampotezea kazi kabisa ama hata maisha yake iwapo atazidi kufuatilia. Alisonya na kumwambia mpigaji amebakiza masaa tu kumfikia hapo alipo, mpigaji akacheka na kumwambia hayo masaa anayosema yeye, basi ni masaa ya kukaa Inspekta ndani ya selo yao “Mlijenga selo kwa ajili ya wahalifu, sasa leo hiyo selo itakuhusu na wewe kutokana na kuwa na kimbelembele,” “Ok! Umemaliza? Maana najua ulipo ninasubiri muda tu ufike nije kukukamata kama kuku,” Inspekta alisha jua kuwa Yule muuaji tayari aliingiwa na woga kwa sababu amabzo yeyey mwenyewe anazijua. “Mimi nawe tutakutana jioni kwenye game yetu kama utakuwa nje ya selo, kwa heri.” Kisha akakata simu na kumuacha Inspekta akisonya na kubadili muelekeo, kutoka kuelekea nje, sasa akaelekea kwa mkuu wake wa upelelezi wa kituo. Alimkuta akiwa anaongea na saimu, lakini akamkaribisha na kumuonesha kiti huku akiendelea kuongea na simu ile. Alipomaliza akamuuliza kulikoni. Akamwambia tu kuwa anahisi muda wa kumtia nguvuni muuaji umekaribia sana, anahitaji msaada zaidi wakati wowote. Mkuu wake akamwambia kwamba yeye wakati wowote atakapokuwa na shida ya msaada asisiste kuomba.akatoka na kuahidi kuwasiliana na mkuu wakati huo utakapowadia. Moja kwa moja akaelekea kwenye ofisi ya Marsha na kumkuta akishughulika na namba za wale maiti, nae alikuwa akiaribu kuziangalia akama atapata ufunuo wowote, lakini wapi. Hadi anafika mkuuwa ke wa kazi, bado Marsha wala hakuwa hata na habari, alikuwa busy kweli. Alipomsemesha akawa ni kama amemshitua vile na kumtazama. “Naona ulikuwa mbali sana, lakini pamoja na hayo Yule mjinga amepiga simu tena akijaribu kunitishia na kunitaka kuachana nakazi hii, nimehisi tayari tumemshika pabaya, sasa sijajua ni wapi,” “Umeona mkuu?Hii itakuwa tayari tumeisha ingia kwenye njia zake na amehisi tumemsogelea, sasa nini cha kufanya?” aliuliza Marsha huku akimtazama usoni. “Tunatakiwa kwenda kwenye zile call box tukafanye mambo yetu na kuzifanyia uchunguzi wa kutosha, maana zote anazitumia huyo hayawani ni za Mwananyamala,” “Ooh! Kwa hiyo inabidi tuwasiliane na IT Master wetu?” “Yap! Kazi hiyo nitaifanya mimi kwanza wewe fanya kazi hii…” alisema huku akizama mfukoni na kutoa simu ile ya Loren na kumpa huku akimpana namba za simu alizochukua toka kwenye kabati la Mwana “Jaribu kuangalia chochote ambacho kitatufanya tupige hatua moja mbele, hapa lazima tuokote kitu muhimu, hivi vifo viwili vina uhusiano mkubwa na kutoweka kwa mtu huyu,” Marsha akapokea vitu hivyo huku Inspekta akitoka kwenda ofisi ya IT kuongea na master. Akiwa anaongea na IT Master, akafuatwa na Marsha na kuambiwa anahitajika haraka sana kwenye ofisi ya mkuu wa upelezi mkoa, yaani kwenye ofisi ya RCO, akamuaga IT Master akimtaka aandae vitu vya kufunga sehemu za Call box zaidi ya nne, kisha akatoka huku akimwambia Marsha kuwa akimaliza ama kuambulia chochote awasiliane nae, hapo ndio akaanza safari akiwa na hofu kidogo. Haikuwa ni kawaida kwa mkuu wake kumuita akiwa mbali na tena kwa wito wa kupitia mtu wa kati, mara zote huwa anampigia mwenyewe ama msaidizi wake ila sasa ndio ilitokea. Safari yake ilielekea makao makuu ya Polisi yaliyopo katikati ya Jiji jirani ana kituo cha Reli ya kati. Alimkuta RCO ambae alikuwa ameketi na baadhi ya makamanda wa Polisi wa maemneo tofauti akiwepo na Yule wa kituo chake cha kazi. Alishangaa kukuta mkutano ule usio rasmi, akawatazama na kuwasalimia kisha akaketi pasina hata kuambiwa kwenye kiti kimoja ambacho kilionesha kama ni kiti ambacho kilikuwa ni maalum kwa ajili yake.
Baada ya kuketi RCO akamuuliza ni vipi kuhusu kesi wanayoisimamia imefikia hatua gani? Akawaeleza na kujibu kuwa ipo pazuri na hadi sasa wamefikia hatua nzuri. Lakini RCO akamwambia inaonekana kama wanasuasua kwenye kesi ile hasa kwenye kumkamata muhusika, Inspekta alijitetea kuwa hapo walipo na wenzie wanajituma sana kiasi ambacho wanakosa hata muda wa kupumzika. Akaulizwa kama haoni kuna usaliti baina ya wao wenyewe kwa wenyewe? Akasema hakuna kitu kama hicho, RPC ambae nae alikuwepo mle akamwambia kwamba inasemekana kuwa yeye anahusika. “Inspekta akashangaa kidogo na kuuliza mimi nahusika? Akajibiwa ndio kuwa yeye ametajwa kuhusika na hapohapo akaitwa Jitu ambae alikuwa maeneo hayohayo na kuulizwa juu ya mawasiliano baina ya Inspekta Kalindimya na muuaji. Akaeleza kila kitu pasina kuongeza kitu, kisha RCO akatoa bahasha kubwa kutoka kwenye droo na kutoa karatasi moja yenye ukubwa wa A4 ndani yake na kumuita askari mmoja aliekuwa amesimama pembeni, bahasha kwa juu ilikuwa imeandikwa ‘AFANDE ANAHUSIKA’ akamwambia ampe Inspekta. Inspekta Kalindimya alipokea na kuisoma karatasi ile kwa pupa na alipomaliza, akamtazama RPC na kukuta akimtazama yeye, akamuuliza kama amekiona kilichoandikwa mle. Alijibu ndio na kuulizwa ni kipi. “Ni juu ya tuhuma ya kumdhulumu mfanya bashara wa kuuza visu,” akatulia kidogo, lakini RCO akawa kimya tu akimtazama, hatimae yeye mwenyewe akaendelea “…lakini mkuu mimi sikusiki na tuhuma hii wala sijawahi kununua visu mtaani…” akakatishwa “Lakini si umeisoma vizuri hiyo barua? Si umeona hadi namba yake ya simu na hadi mahala ulipomwambia aviweke, sasa unakataa vipi hapo?” RPC alimuuliza. “Mkuu hapa mimi sielewi chochote juu ya hivyo visu na hata huyu mtu alietajwa hapa mimi simjui pia,” “Unanithibitishia kwamba hata kwako mahala hapa tulipotajiwa hivyo visu hatutavikuta iwapo tutakwenda nyumbani kwako?” “Ndio mkuu, hizi zitakuwa ni mbinu chafu tu za watu wasiopenda kazi adhimu inayofanywa na jeshi letu la Polisi,” RPC na RCO wakatazamana na kisha RCO akamwambia kuwa wataongozana pamoja nae ili kwenda kujiridhisha. Wakanyanyuka huku RCO akimuahidi RPCkuwa watawasiliana baadae. Wakatoka wakiwa ni kundi la askari ambao walikuwa kwenye gari mbili hadi nyumbani kwa Inspekta Kalindimya, huku aakijiamini kabisa akafungua mlango wake wa barabarani na kuwakaribisha. Kwenye meza yake ya chakula pale pale walipo waliweza kuiona, juu ya meza hiyo palikuwa na kisu cha aina ileile ambacho kimekuwa kikitumika kwenye mauaji ya kina Mwana, hiki sasa kilionekana kama kinatumika mara kwa mara. Alipokiona tu mwenyewe akasema Shit, na kutamani kukificha, wakasogea wote kwa pamoja na kukitazama, Inspekta akatikisa kichwa tu akiwa kauma mdomo wa chini. RCO akamtazama na kama vile alitaka kumsemesha, akauchuna na kisha akawageukia vijana wake na kuwaambia waangalie tena sehemu nyingine, akamgeukia Inspekta sasa akamwambia “Inspekta, vipi kuhusu hivi visu? Aliekuletea anasema vipo 8 na hapa naona kuna kimoja, ukifanya kujumlisha na vile viwili vilivyotumika ina maana ni vitatu, sasa hivyo vitano vipo wapi?” “Mkuu, yaani hiki kisu mimi ndio ninakiona humu ndani mwangu kwa mara ya kwanza, sijawahi kukiweka humu, najua utaniuliza tunaishi wangapi, lakini kiukweli ni hivyo,” akiwa anatoa maelezo kwa boss wake, akaja askari mmmoja na kukakamaa mbele ya afande mkuu na kumwambia kuw wameviona visu vingine. “Vipo wapi sasa? Mbona hujavileta?” aliuliza RCO kwa shauku kubwa. “Mkuu vimefungiwa kwenye kabati ya vyombo sehemu ya chini yenye kioo, hivyo tumeviona kupitia hicho kioo,” “Hapo ndio mahala alipotaja kuwa alitumwa kuviweka na Inspekta, hebu twendeni akatufungulie…” Mkuu akaanza kuondoka huku akiamwambia Inspekta atangulie hadi ilipo kabati yake ya vyombo. Inspekta akiwa kama mtu ambae hajiamini vile, akatangulia hadi ilipo kabati yake ya vyombo huko jikoni, alipofika na kuinama hata nae aliweza kuviona visu hivyo ambavyo vilikuwa kama vile vimefichwa. Akamtazama mkuu wake wa kazi na akakutanisha nae macho, akamwambia afungue. “Mkuu wakati natoka niliacha funguo hapa, huwa sifungi humu jikoni wala milango ya kabati,” “Sikuelewi Inspekta, hebu nieleweshe vizuri, mimi shida yangu ni kutoa hivyo visu humo kabatini, sasa funguo ipo wapi?” “Mkuu, kabla sijatoka hapa palikuwa wazi, na funguo niliacha ikining’inia hapa kwenye mlango wake,” “Ok! Ulimuacha nani humu ndani?” lilikuwa ni swali la msingi sana lakini halikuwa na maana, kwa sababu Inspekta anaishi peke yake. Alijaribu kutoa maelekezo ya kutosha lakini hakueleweka, hata nae alijua kuwa hawezi kueleweka, hivyo akaamua awe mpole kwanza wakati akitafuta njia muafaka ya kufanya. Mkuu akaamuru askari mmoja avunje kioo na kutoa vile visu. Kweli walitoa visu vitano, vinne vikiwa havina alama yoyote ila kimoja kikiwa na namba zingine tofauti na zile za awali.
Inspekta alichoka ghafla, alitamani kufanya kitu ambacho hata hakijui ni kitu gani, ila alitamani kufanya jambo. RCO alivikagua visu vile na kuviweka kwenye mfuko waliokuja nao, kisha akawaambia askari wake watoke nje na kuanzia muda ule wamuweke mwenzao chini ya ulinzi. Aliwekwa chini ya ulinzi kama alivyoamrishwa na kisha ukachukuliwa ushahidi na kuondoka kuelekea kituoni huku askari wawili wakiwa wameachwa pale kwa ajili ya kuweka mazingira ya usalama. Akiwa ndani ya gari sasa ndio akili yake ikaanza kuchaji, alihisi sasa ile kauli ya Yule muuaji ni ya kweli, lakini akajiuliza ni vipi aliingia kwenye nyumba ile na hali funguo zote aliondoka nazo mwenyewe? “Ina maana huyu mtu ananifuatilia kwa kiasi kikubwa mno, ameamua sasa kuondoka hadi na funguo za mlango wa kabati yangu?Kuna nini hapa kati?Na kwanini aondoke nayo? Si angeiacha pale pale? Nahisi kuna kitu tena juu ya hii funguo, si bure,” mawazo mawazo yalikuwa ni mengi, hivyo hadi wanafika ofisi ya RCO yeye hana hata habari. Aliamriwa ataeremke na kuongozana moja kwa moja hadi kwenye ofisi ya RCO na kuingia ndani ili kufanya mahojiano mafupi. Akiwa hapo akapigiwa simu Marsha kwamba anahitajika huko haraka, aende akiwa na jalada la kesi za mauaji hayo anayofanyia upelelezi sambamba na Inspekta Kalindimya. Akajibu sana na akawasha gari ya Polisi na kwenda huko mkoani, aliwasili pale na kuwakuta wakuu wake wa kazi wakiwa wameketi wanajadiliana, yeye alikuwa yupo nyuma ya wakati lakini wakampa maelezo kidogo ambayo dhahiri aliyapinga. “Mkuu zaidi ya mara moja Inspekta amekuwa akipigiwa simu na kuambiwa juu ya suala la kuachana na kesi hii, nahisi ni mbaya wetu tu huyu anatumia vibaya udhaifu wetu ili kutusambaza,” Marsha alitetea huku akiwa na imani kauli yake itaweza kuwashawishi na kuweka mambo sawa. RCO alikaa kwa sekunde kadhaa akifikiri juu ya kauli ile na baada ya dkika takriban tatu hivi, akasema “Nilikuwa nimedhamiria kukuweka ndani kipindi chote cha ufuatiliaji, lakini kutokana na kauli ya Marsha, nitakusimmisha tu kazi kwa muda usiojulikana na hivyo tangu sasa mkabidhi makabrasha yote Marsha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli zingine,” “Sawa mkuu!” alijibu huku akisimama na kukauka kwa saluti. “Utakuwa unaripoti hapa kwangu kila siku saa moja na nusu asubuhi hadi pale nitakapothibitisha ukweli ni upi, sawa Inspekta?” “Ndio mkuu.” “Hutatumia gari binafsi tena muda wa kazi, tangu sasa gari ya ofisi itakufuata kukuleta huku na ndio itakayo kurudisha nyumbani baada ya kazi, nafikiri unanielewa?” “Ndio mkuu ninakuelewa,” Kisha wakatoka na Marsha ambae kichwani alihisi ni uonevu mkubwa amefanyiwa boss wake, lakini hakuwa na cha kufanya, maan ahuyu alie nae ni boss kwake, na aliefanya huo ambao yeye anauona kama ni uonevu, ni boss wao wote. Kimya kimya wakaelekea hadi kwenye gari ya Inspekta na kuingia, humo ndani ya gari ndio Marsha akampa pole mkuu wake wa akazi ambae alitabasamu na kusema vitu kama vile ni vya kawaida sana makazini “Jiandae tu nawe kukutana navyo, mafisadi na wazandiki ni watu ambao hatari sana, wakati mafisadi wanashika nchi, wazandiki wao huishika Serikali, basi inakuwa shida kubwa mno,” “Ni kweli boss, sasa Sijui nifanyeje na kazi hii halafu peke yangu? Alisema Marsha kwa huzuni, kwani tayari aliisha ingiwa na hofu moyoni. “Pambana tu binti, mbona unaweza? Jiamini tu, utakuza sana CV yako iwapo utalifanikisha hili jambo,” Marsha aliendelea kulalamika “Bila ya msaada? Peke yangu mimi siwezi, ujue mkuu hii ni kesi kubwa sana kwangu? Yaani inafikia hatua kwamba hata Sijui ni wapi pa kuanzia,” “Usijali, nafikiri hawatokuacha peke yako, lazima utapewa mtu wa kuendana nae,” Inspekta alizidi kumpa moyo, Marsha nae akaomba kuwa wakati wowote akihitaji msaada wake, basi asisite kumsaidia, “Sasa Marsha itategemea na msaada upi unataka, ule ulio ndani ya uwezo wangu na kama pia sintoingilia kazi zisizonihusu nitakusaidia, si unajua kuwa suala hilo halinihusu tena? Maana name sasa ni mtuhumiwa,” alijitetea Inspekta na kumfanya afande Marsha atikise kichwa kukubali. Tayari walifika ofisini kwao na kuingia ndani, huko ndani Inspekta akaliomba file kwa Marsha na kukopi baaadhi ya vitu alivyo hitaji na kumrejeshea pamoja na kumpa diary ambazo alizitumia kuandika maelezo muhimu. Alipomaliza akaitazama ofisi yake kwa umakini kama mtu ambae anaiaga vile, kisha akachukua alichoona anahitaji, akatoka nje na kuwaaga wenzie akimuacha Marsha kiwa na majonzi. Safari yake ikaelekea moja kwa moja nyumbani kwake na kuwakuta wale askari waliopangwa kulinda pale kwake wakiwa wanaendelea na jukumu lao. Walimfungulia geti na akaingia ndani, wakati akishuka garini wakakauka kwa saluti kisha yeye akaelekea ndani kwake ili kufanya uchunguzi zaidi juu ya nyumba yake, maana tukio lile la mtu kuingia ndani mwake, bado lilikuwa likimtafuna. Alijitupia kwanza sofani na kutoa simu yake iliyokuwa kwenye mfuko wa ndani wa koti lake, ilikuwa ipo kwenye silent tangu alivyoiweka wakati akiwa kwenye kikao, sasa alipoitazama akakuta kuna missed call moja tu, namba alihisi kuijua ijua hivi. Akatoa na kupiga namba hiyo, ilipokelewa na aliepokea safari hii hakuwa mtu mwingine, bali alikuwa ni mtu yuleyule ambae amekuwa akiwasiliana nae mara kwa mara kupitia Call box. Alipopokea tu cha kwanza akaanza kurekodi maongezi yake na huyo jamaa, alidhamiria sasa kurekodi kila simu ambayo ataona inastahili kuwa ni kumbukumbu kwake. Jamaa akaanza kwa kumpa pole nyingi na kumwambia anajua kila kitu kilichomtokea lakini ile inatokana na ubishi wake. Afande alimsikiliza tu. Mwisho akamuuliza ina maana alipiga simu kumueleza jambo hilo tu au amna jingine jipya? Jamaa akamjibu kuwa ipo sababu nyingine ambayo ataijua iwapo atakuwa makini na kumsikiliza hadi mwisho. “Tegemea kitu kipya leo hii ama kesho, maana mimi nilitaka wewe leo ulale ndani ili nikupunguzie kazi, lakini unaonesha kuwa unakubalika sana kwa huyo Mkuu wako wa kazi sasa basi nabadili mbinu, kesho tutaona nani atakaeshinda game yetu,” “We huna lolote, malizia tu siku zako za kuwepo uraiani kabla sijakufikia na kukutupua ndani,” Inspekta bado tu hutaki kunielewa? Game yetu Inaendelea na haitaki hasira, pia kumbuka ni mimi ndio mwenye funguo yako ya kabati… Sidhani kama umejisahaulisha,” Inspekta alikumbuka sana lakini aliona haina umuhimu tena, bali akacheka na kusema kiufedhuli akitaka kumkasirisha mtu wa upande wa pili “Haina kazi tena hiyo, nimeisha haribu kabati, sasa imebakikama scraper tu, ambayo wakati wowote tangu sasa nitaitupa kwenye dampo. vipi kuna kingine?” aliuliza Inspekta kwa kuamini kuwa amemtweza nguvu, lakini kumbe wala haikuwa hivyo, bali jamaa nae akacheka na kusema “huenda funguo hauihitaji tena, lakini tambua kuwa mimi sio mpumbavu kwa kiasi hicho unachodhani. Na katika kukudhihirishia hilo, nenda chumbani kwako juu ya kabati, kwaheri,” simu ikakatwa kimyakimya. Afande akashusha pumzi na kujiuliza aende ama lah! Akaamua aewnde tu akaangalie kwani hakuna athari yoyote ambayo ataipata iwapo atakwenda kuangalia hapo kabatini. Akanyanyuka na kuelekea chumbani kwake moja kwa moja na alipofika kwenye ile kabati hakuona kitu chochote kipya, basi akasonya na kuacha kuangalia kisha akaondoka kurejea kule sitting room kuendelea kujipanga zaidi. Akiwa ameketi pale Sitting room kama mtu vile aliekumbushwa kitu muhimu, akakurupuka tena. Moja kwa moja tena hadi kwenye kabati yake ya nguo kule chumbani, safari alichukua na stuli ili aweze kuona vizuri. aliweza sasa kukiona kila kitu kilichokuwepo juu ya kabati ile ya nguo. ni kitu kimoja tu alichokua akitaka kukiangania lakini alipokiangalia hicho kitu, hakukiona, akashtuka sana, hakutegemea kabisa kutokewa na kitu hicho. Alichukua simu yake ya mkononi na kupiga tena namba ile. Namba ilikuwa haipatikani, akarudia tena kwa kuhisi labda ni Mtandao lakini wapi… jibu likawa ni lilelile, akaitupia simu kitandani na kujishika kichwa kwa mikono miwili. “Ukisikia kuwa mateka ndio huku sasa, mtu unaweza kutumika bila kupenda, Mungu wangu.., ninajiokoaje juu ya kikombe hiki?” aliwaza peke yake huku akizunguka chumbani kwake kule na huku. Akili ilifikia ukomo wa kuwaza, alitamani kumpata huyo mtu aliekuwa akiwasiliana nae lakini hakuwa hewani, akapata wazo la kumpigia Marsha, ambae alimwambia atafika jioni pale nyumbani kwake. “Si utakuwepo mkuu ama una ratiba ya kutoka?” “Marsha sipaswi kutoka hapa, nipo kifungoni, natakiwa tu nije nikupe dondoo muhimu zimenifikia nikiwa ndani,” “Sawa boss, jioni nitafika.” Inspekta akakata simu na kisha akaanza kukagua tena upya chumba chake na kisha akakagua nyumba nzima, lakini hakukuwa na tofauti zaidi ya hiyo aliyoiona juu ya kabati. Wakati yeye akiwa nafanya uchunguzi kwenye nyumba yake, upande wa pili, Marsha alikuwa sasa nae ameanza kupata hofu juu ya mkuu wake wa kazi, inakuwaje sasa yupo nje ya ofisi na bado anasema anaendelea kupata dondoo? “Kiukweli Inspekta anapaswa kuchunguzwa, name nimeanza kupata hofu nae.” Alijisemea mwenyewe huku akikusanya makabrasha yake akitoka kwenda kuanza upelelezi wake kama alivyojipanga mwenyewe. Pasina kujua lolote, Inspekta alianza kazi ya kupeleleza juu ya zile namba, na hasa ile iliompigia, alichukua namba za simu alizochukua kwa marehemu Mwana na zile alizopewa Sinza na kuanza kuzilinganisha. Aligundua kuwa namba aliyopewa Sinza, ndio namba ambayo imempigia muda mchache uliopita, “Ahaa! Ina maana ni Loren ndio alieingia humu ndani kwangu? Na kipi kilichosababisha atumie namba yake kuwasiliana name? Huenda kuna kitu hapa kati?” aliwaza sana huku akiwa ameweka mikono yake mdomoni “Angalau sasa naweza kujua kuwa Loren yupo hai na ndio namuhusisha na matokeo yote haya ya mauaji, lakini Loren yupo vipi?” hapo sasa kaanza kujiuliza ni kipi afanye. Likamuijia wazo Wazo ambalo aliliona ni sahihi sana, wazo hilo lilikuwa ni kumsubiri Marsha afike jioni nyumbani kwake ili wakae na kulijadili jambo hilo bila kujua kichwani kwa Marsha kuna nini. Aliendelea kuandika hints zake kwenye diary yake na ilipotimu saa tisa mchana, akatoka kwenda kununua chakula, alipenda aje kula nyumbani kwake, hivyo alikwenda hotelini na baada ya muda akarejea na kukaa Mess. Wakati akianza tu kula, simu yake ikaita tena, akachukua headphones zake na kuzivaa, kisha akapokea na kuanza kurekodi mazungumzo yake. Mtu alikuwa ni yuleyule tena, sasa safari hii alikuja kivingine. “Inspekta pole sana kwa kuwa kwenye kifungo huru, hahahaaa! Leo nilikuwepo ofisini kwako na kukuulizia nikaambiwa umeenda nyumbani, lakini kwa kuwa name ni mfukunyuku zaidi ya wewe, nikaweza kusikia kuwa umepumzishwa, hongera sana bhana, wanakupenda mno! Maana pigo la leo ambalo lilikuwa linafuata lilikuwa baya zaidi, pumzika kwa amani!” “Ujue sasa ndio nipo kwenye wakati mzuri zaidi wa kukutia mikononi, nakuahidi kabla jua hili halijachomoza utakuwa kwenye mikono yangu.” Alisema Inspekta kwa ghadhabu, kwani alihisi kuna mtu ndani ya jeshi anawasaliti. “Huu ni mchezo tu Inspekta, umepangwa na kupangika, wewe wala usikasirike, japo nikiamua ninaweza kukutoa machozi mbele ya mkuu wako wa kazi, lakini any way. Leo nilikuja kukutembelea na kukuletea ule mzigo wako, kwa kuwa sikukukuta, nimelazimika kuondoka, maagizo zaidi anayo afande Marsha, kwaheri kwa sasa!” jamaa akakata simu kama kawaida yake. Inspekta alihisi kuchanganyikiwa sasa, aliona kabisa kama ni mchezo anachezewa huu sasa ulikuwa ni wa kijasusi, “Ina maana ni nani anampa taarifa zangu? Amefika kituoni na kuongea na Marsha, amempa maagizo gani tena?” maswali akayakosea majibu akaamua kukaa na kumsubiri Marsha kwa hatua zaidi, hamu ya kula ikakata. Saa moja usiku, afande Marsha ndio akafika na kuingia mle ndani, akamsalimia boss wake na kisha akaketi kwa maongezi ya awali. Lakini hata nae alionekana ana jambo, lakini tu akawa mpole kwanza. Inspekta akamueleza juu ya kile ambacho amekipata kutoka kwenye mazungumzo yale na mpigaji Hivyo Marsha nimegundua kuwa mtu alie ingia humu ndani alikuwa niLoren a ndio huyo ambae amekuwa akinipigia simu mimi mara kwa mara,” “Unamjua Loren?” “Hapana na kibaya hata picha yake nayo sijawahi kuiona,” “Kwa hiyo Inspekta wewe unashauri nini juu ya jambo hili?” “Mimi ninakushauri jambo la kwanza, nenda kwa kina Loren utafute picha yake na ujue kuna lipi linaendelea, kisha kwa nguvu zote ukisaidiwa na mitandao, uweze kumsoma ni kutoka wapi wapi anapiga simu kwangu, na mwisho unijulishe name ili niweze kuendelea na kazi yangu nikiwa nje ya ofisi,” alimaliza Inspekta na Marsha akatikisa kichwa kukubaliana nae, kisha akazama mfukoni na kutoa funguo mbili na kumkabidhi Inspekta. Wakati akimpa funguo zile alikuwa makini mnokumtazama kwa jicho la mbali mno, maana aliona kama Inspekta ameshtuka kidogo, akazipokea na kumuuliza amezitoa wapi? Marsha nae akamuuliza amezitambua? Inspekta akasema ameitambua moja tu ile ndogo ambayo ni ya kabati ile waliovunja kioo ilikutoa visu na ile nyingine haitambui. Lakini baada ya Inspekta kuiangalia kwa uzuri ndio akagundua kwamba ni funguo ya mlango wake mkuu, ilikuwa imefanana sana kiasi ambacho kama zingechanganywa basi mtu mwingine asingeweza kuzitofautisha, akamtazama Marsha na kumuuliza tena amezitoa wapi. Marsha akameza mate na kuegamia kwenye kiti chake kisha akamwambia kuwa mtu aliempa funguo zile ndio alimletea ofisini na wanafahamiana sana nae, na maagizo hayo yeye ndio alimpa kwamba aziache pale kwangu na bahati mbaya mimi sikuwepo. “Hivyo wakati mimi ninafika hapo ndio nikakutana nae akiondoka na funguo hizo akiwa ameziacha Kaunta, ila aliniambia kwamba hayo ni maagizo yako na ulimwambia afanye hivyo,” Inspekta aliishiwa pozi na kusema “Hili ni game na linaendelea kweli kama nilivyo ambiwa, jina lake je ulimuuliza ni nani?” “Ndio yeye ni Chidi jina lake na anaishi Sinza,” “Marsha, hilo jina la Chidy wewe ina maana hulikumbuki?” “Nalikumbuka sana si ndio jina la ndugu yake na Loren?” “Ndio, sasa imekuwaje awe na funguo zangu? Ina maana ameonana na Loren na kumpa funguo za nyumba yangu?” “Kwani wewe ulimpa Loren funguo za nyumba yako?” “Hapana mimi sijampa, lakini ndio kama nilivyo kwambia hapo awali kuwa katika uchunguzi wangu wa awali, inaonesha kwamba Loren anahusika na hili,” “Inspekta kwa hili hata mimi sasa naona unanichaganya, aliekuuzia visu alitaja hadi vilipo, na vikapatikana pakiwa funguo haipo na leo inakuja funguo ya kabati sambamba na ile ya mlango mkuu, tena inaletwa na mtu ambae ndugu yake haonekani, mbona mimi sikuelewi hapo?” alionesha dhahiri sasa Marsha kuchanganywa na yale Matukio. Inspekta hata nae sasa alishangaa kuona hata Marsha nae hamuamini juuya jambo hilo? Alianza nae kufa moyo taratibu, kwani hata mtu aliemuamini kuwa takuwa upande wake nae sasa anaonesha kuanza kuwa na hofu nae. Wakiwa kwenye maongezi hayo, ghafla simu ya Afande Marsha ikaita, akaipokea na kusikiliza upande wa pili. Aliepiga alimuuliza kamayupo kazini ama nyumbani, akajibu kuwa nyumbani kwa Inspekta Kalindimya, “Kuna nini huko hadi muda huu upo huko?” “No kuna habari ambazo alikuja kunipa, na ndio nilikuwa hapa bado sijaondoka,” wakaendelea kuongea kisha akasema “Sawa afande,” kisha akamgeukia Inspekta Kalindimya baada ya kukata simu na kumwambia, “Inspekta, RCO amenipigia simu na kuniambia kuwa unahitajika kituo cha Polisi sasa hivi, kaonane na RPC ofisini kwake lakini tuende pamoja,” “Kuna nini?” aliuliza kwa mashaka, kichwani akihisi kuwa huenda anaenda kurejeshwa kazini, akasimama na kujiandaa kisha akatoka na kumpitia Marsha aliekuwa nje akimsubiri garini. Wakati wakitoka akashangaa Inspekta kwa kuwakuta askari wengine tofauti na wale aliowaona mchana, akajiuliza ni vipi mabadiliko yamefanyika ghafla vile? Akamuuliza mmoja wao pale vipi wameenda wapi waliokuwepo? “Wamepangiwa kazi nyingine na sisi ndio tumekuja kushika nafasi zao,” akawaaga na kuwaambia wawe makini kisha akaelekea kwenye gari. Wakaondoka na kuelekea moja kwa moja kituoni na kumkuta Marsha akiwa tayari amewasha gari na kuelekea moja kwa moja kituoni na kuingia ofisini kwa RPC ambae pia alimkuta akiwa peke yake. Alimkaribisha akiwa ameketi kwenye kiti chake cha kuzunguka na kumuuliza alipotoka kazini pale alielekea wapi. Akajibu kuwa alipotoka pale alieklekea nyumbani kwake moja kwa moja na hakupita popote. Marsha akaingia na kuketi jirani na Inspekta ambae alikuwa amemuuliza swali lingine Inspekta kwamba alipofika kwake alitoka saa ngapi? Jibu likawa kuwa hakutoka kwani alikuwa na kazi nyingi za ndani mwake ikiwepo la usafi. Inspekta akamtazama Marsha na kumwambia Afande Marsha, ninazidi kupata mashaka na Inspekta Kalindimya, hapa anasema akuwa leo hajatoka kwake tangu alipokwenda, lakini kuna sehemu ameonekana akifanya mauaji asi tukapigiwa simu muda uleule, sasa nashindwa kuelewa hapa!” alishtuka mno Inspekta na kuuliza kwa mshtuko “Mimi?” Hakuna aliemjibu swali lake bali wakamtazama kama kwamba wanamuelewa sana kwa mchezo anaoucheza, kisha RCO akamwambia “Inspekta wakati nchi inakuaminina kukupa kazi ya kulinda usalama wa wananchi, haikuwa na lengo la wewe ndio uwe mtu wa kwanza kupoteza maisha yao, lakii kwa kuwa unakuwa unajaribu kupambana na jeshi ambalo unalitumikia, leo napenda ufahamu kuwa jeshi ni la nchi nzima, jeshi csio la mtu mmoja kusema kuwa kwa kuwa ni lake basi afanye anachotaka, hivyo nitakuweka ndani hadi uchunguzi utakapo kamilika,” “Sasa Mkuu mimi kosa langu nini?” “Ina maana kipi hujasikia hapo? Si nimekwambia kuwa umehusika na mauaji leo mchana? Nawe unakataa hujahusika, basi acha tuchunguze kisha tutapata ukweli na ndio utakao amua kipi kifanyike,” “Sawa Mkuu, lakini mimi si…” kabla hajamaliza kauli yake RPC akasema “Umenisikitisha sana kuniambia kuwa hujatoka wakati tayari askari nilio waweka kwako wanakiri kuwa ulitoka. Maana tayari wapo hapa niliwaita ili kuwahoji, wamekiri kuwa ulitoka, wewe unakataa kuwa hujatoka, sasa hapo ni kipi mimi nishike?” Bado Inspekta hakukumbuka kutoka hadi pale alipokumbuka kuwa alitoka na kwenda kuchukua chakula “Mwanzo ulikataa na sasa unakubali, unanijengea taswira gani? Nalazimika kukuchunguza sana. Maana muda huo uliotoka mle ndani kwako na ndio muda ambao mauaji yaliyotokea jirani na kwako,” “Afande ni nani alieuwawa?” “Ni Yule mtu ambae ulimpa funguo za nyumba yako na pia alikuuzia visu lakini pia ili kupoteza ushahidi ukamteka na ili kutusumbua zaidi, ukachukua simu yake na kuiingiza kama chanzo cha upelelezi wa kifo cha Mwana,” alitulia RPC na kuendelea “Ni kweli umefanikiwa kutusumbua kwa muda huu mchache, lakini kila mtu alishangaa sana wakati Loren, kijana ulie muua alipokuwa akipiga simu na kusema AFANDE ANAHUSIKA, ndio maana nikakusimamisha, lakini kumbe ndio nimekupa nafasi ya kupoteza ushahidi.” Marsha alikuwa akiandika. Marsha kuna chochote alichokuambia Inspekta?” “Ndio mkuu, Inspekta alinieleza kuwa na wasiwasi wa kuwa Loren anahusika na mauaji ya Mwana, hivyo alikuwa akiniambia nikitoka pale nifanye mpango wa kuitafuta angalau picha yake…” akamueleza yote aliyosema, kisha RPC akatikisa kichwa na kusema “Inspekta, unaweza kunieleza ni kwanini umeshiriki kwenye mauaji ya Raia halali wa Tanzania na wasio na hatia?” “Mkuu, nashangaa tu hapa, maana kwanza mimi sijaua mtu yeyote, pili Loren mimi simjui hata kwa sura na tatu, muda wote mimi nimekuwepo nyumbani ila huo muda tu wa kununua chakua tu pekee,” alijitetea Inspekta huku akiamini kabisa kuwa hawezi kueleweka, kama ambavyo yeye huwa hawaelewi wale anao wahoji. “Utanishawishi vipi Inspekta hadi nishindwe kuamini kuwa kinacho semwa si kweli?” alihoji RPC akiwa mikono kaweka kifuani.
“Ni kwa vile mimi siwezi kufanya hivyo, bali hizi ni mbinu chafu toka kwa watu ambao wamekuwa wakichukizwa na kazi nifanyayo na kuwaumbua,” alijitetea Inspekta na Mkuu akamwambia amthibitishie kile asemacho. Akatoa simu yake ya mkononi na kuweka sehemu ya maogezi aliyorekodi na kumsikilizisha Mkuu wake wa kazi ambae alimuuliza Inspekta “Kama ingekuwa wewe ndio Mimi hapa, yaani unaniletea ushahidi kama huo, wewe binafsi ungekubali?” “Hapana mkuu ila kwa sasa huu ndio ushahidi wangu wa awali,” “Sasa basi ajabu kitu kingine Inspekta kinachozidi kukutia shakani, ni juu ya kuuawa mtu huyo bila kukutwa kisu kifuani japo ameuawa kwa kisu, ningeweza kukuelewa tu iwapo huyu nae angekutwa na kisu mpfano wa vile aambavyo tumevikuta kwako, ningeweza kushawishika, ila kwa sasa…” alitikisa kichwa kukataa kabisa kumuelewa. Inspekta sasa alikubali matokeo, akasimama kwa unyonge, RPC akapiga simu sehemu na kuja askari mmoja na kumwambia ampeleke korokororni. Hii ni sehemu maalum wanaposhkiliwa askari waliofanya makosa, Wakati akitoka Marsha alikuwa amebaki amesimama akimtazama boss wake akipelekwa msambweni, hakuwa na jinsi ya kumuokoa, maana hakujua kama anachotuhumiwa ni kweli ama anasingiziwa. Alipopotelea mbele huko, Marsha akamuomba Mkuu wake waongee kidogo, alimjulisha kuwa hata nae hana imani na Inspekta Kalindimya, lakini pia bado anaamini Inspekta huenda anasingiziwa. “Kwa hiyo unasemaje?Unafikiri hastahili kufanyiwa hivi tunavyo mfanyia?” “Hapana, nafikiri ni lazima achunguzwe, na ili achunguzwe vizuri ninafikiri tumuachie simu yake huku ikiwa ipo kwenye mikono yetu, iwapo tunaweza kuwasiliana na Mtandao anaotumia, kuna baadhi ya mambo wayazuie kutumika kwenye simu hiyo bali yapitie kwetu moja kwa moja, unasemaje mkuu?” “Fafanua vizuri, bado sijakuelewa,” RPC alimwambia Marsha, ambae nae akamfafanulia mkuu wake wa kazi. “Sasa kwa swala hilo mbona wala haihitaji Mtandao anaoutumia? Ni suala la kuongea na wataalamu wetu wa teknolojia na Sayansi wanaliweka tu sawa, name nimeipenda hiyo, ni wazo zuri,” alikubali RPC na kumtaka ampe karatasi ili amuandikie barua ya uthibitisho toka kwake kwenda kwa watu wa idara ya Mawasiliano. Baada ya utaratibu wote kukamilika, alitoka Maarsha na kuelekea hadi kwenye ofisi ya RCO ambapo watu wa kitengo hicho walikuwepo, akawapa ile kazi na kuambiwa akae kama nusu saa hivi kisha awasiliane nao. Walichukua aina ya simu kwa kutafuta IMEI namba kisha wakafanya vitu vyao, baada ya muda wakamuita Marsha na kumwambia kuwa mambo tayarii mazuri. “Ok! Kwa hiyo mmefanya kama nilivyotaka mimi ama?” “Ndio afande, wewe si umetaka simu zote anazopiga na kupokea zipite ofisini?” Naam, lakini pia upande wa Email na Short Msg na Text zote nazo zipite ofisini, ila picha yoyote isiweze kutoka bali aweze kupokea,” “Yote hayo ndio yaliyofanyika mkuu kama ulivyotaka,” “Ahsanteni sana, na kwa herini,” wakati akitaka kutoka wakamuwahi na kumtaka asaini kwenye karatasi zao kwa ajili ya kumbukumbu zao za kiofisi, kisha akatoka kuekea tena ofisini ikiwa ni saa tatu usiku. Akiwa njiani akaghairi na kuelekea nyumbani kwake, kwani alitaka kwenda kituoni kumpa simu Inspekta, lakini akaamua kwamba atampa hata siku ijayo tu kwani si yupo sehemu salama. Alirejea kwake na kujitayarisha kwa kulala, lakini usiu wakati akiwa anapitia njozi zake akashtushwa na mlio wa simu, alipotazama simu ile akakuta namba ambayo kwake ilikuwa ni ngeni, alitegemea ataona jina kwenye namba hiyo, lakini haikuwa hivyo. Alipokea na kutengeneza koo, ila hakusema kitu, mtu wa upande wa pili akasema kumwambia kuwa leo anafurahi kwa kuweza kumsumbua kidogo kisha a akauliza “Mbona Inspekta sijakuona kwenye maiti ya Loren? Hilo maana lilikuwa ni kama pigo lako kuu, lakini usijali, kwa kuwa leo uliamua kujipumzisha na kuniletea kale kachangudoa, rorho yangu sasa imekuwa kwatu, ungekuja ningekufanyia kitu kibaya sana, ilikuwa nikuandalie pigo lingine takatifu kesho kama utazidi kuwa ni jeuri, nakupa masaa tu uniambie kama unaachana na mimi kabisa ama lah…” akanyamaza kimya tu Marsha, maana simu ile haikuwa yake, aliepiga akauliza “Ni ujeuri tu ama ni usingizi?Lakini usigope, kwa maelekezo zaidi tutawasiliana kesho, hahahaaa!” sauti ikakata bila kusubiri jibu. Sasa ndio Marsha akajua ni kwa nini Inspekta alisema hahusiki, nae sasa aliamini kabisa kwamba Inspekta Kalindimya hahusiki, baada ya kupokea simu ile ambayo ni ya huyo Inspekta. “Yaani mimi ananiita changudoa? Na ni kipi ambacho walipanga kumfanyia Inspekta? Sasa kwanza Inspekta aliwafanya nini hawa watu hadi wamtafute kiasi hicho?” alijiuliza maswali mengi sana na kukosa majibu. Akajilazimisha tu kulala akiazimia kesho kwenda kuongea na RPC na ikiwezekana pia na RPC ili Inspekta aachwe huru na aendelee kufuatilia jambo hilo. Akavuta shuka na kulala. Aliamka mapema na kujiandaa kwenda kazini akiwa na azma ya kuongea juu ya alichokisikia.
Moja kwa moja alianzia korokoroni na kumkuta Inspekta akiwa amekaa akitazama nje, chumba alichokuwa amewekwa ni chumb ambacho kilikuwa kipo ghorofani na aliweza kutazama nje bila kuleta madhara yoyte kwake wala kwa wengine. Ni eneo ambalo asingeweza kudhuru mtu wala kujidhuru mwenyewe, hiyo ndio korokoro ambapo waliwekwa askari wenye vyeo kupisha uchunguzi, sasa ndio Marsha alikuwa nje ya chumba hicho na kumuita Inspekta kwa sauti ya upole akiwa mlangoni. Inspekta akamsogelea akiwa anaonekana kama ni mtu ambae hajalala, nbalia alimsalimia na kumwambia kwamba anaomba msamaha jana alisahau kumpa simu yake “Usijali, lakini pamoja na yote haya Marsha, sielewi chochote kuhusu kifo cha Loren, hebu nieleze…” Masha akamkata kauli “Inspekta hata name najua kuwa wewe hujui lolote, ni usiku mmoja tu umenifanya nitambue hilo,” Inspekta akashangaa “Kivipi Marsha?” “Inspekta, chukua kwanza simu yako, acha nikafanye mpango nikutoe mengine tutaongea zaidi ofisini,” akasema huku akimpa smu hiyo kupitia kwenye mlango wa chuma uliowatenganisha kwa kati, mmoja akiwa ndani na mwingine akiwa nje “Sawa, mimi nipo humu,” nae akapokea ile simu na Marsha akaondoka kwa ahadi ya kurejea baadae. Akatoka tena na sasa akaingia kwenye ofisiya RPC na kukuta bado hajawasili, akarejea ofisini kwake hadi aliposikia wakijibu maswali kadhaa ambayo kila wakati anapofika pale huwahoji askari waliopo zamu. Akasubiri hadi alipohisi kwa muda ule atakuwa ameisha ingia ofisini mwake, nae akanyanyuka na kuelekea huko. Alikuta na kuongea nae akimpa maelezo juu ya kilichojiri tangu walivyo achana siku iliyopita. “Sasa simu hiyo ndio imekufanya uamini kuwa Inspekta hahusiki?” “Yap Boss, ni moja ya sababu,” “Haitoshi hiyo, huoni kama labda huenda tayari alikuwa amempanga mtu ampigie simu muda huo?” “Sasa Mkuu huyo amewasiliana nae saa ngapi hadi kumwambia hivyo? Maana tangu nimefika kwake hajaongea na simu yake hadi tunafika hapa na kukukabidhi simu wewe, hakuwa amejua ambacho kitakacho tokea, sasa huyo mtu amempanga saa ngapi? Hapana mkuu ni kama alivyosema mwenyewe kuwa hii ni sawa na usaliti kwa wasiopenda kazi anayoifanya,” “Kwa hiyo wewe una ushauri gani sasa?” RPC alimuuliza huku akitazama saa kama vile ni mtu ambae anasubiri muda ufike ama anacheleweshwa na kitu Fulani. “Mkuu ninashauri Inspekta aachiwe huru na aendelee na kazi hii kama awali, maana inaonekana hata muuaji anaweweseka pindi Inspekta anapoonekana sehemu,” “Sawa, hebu mlete hapa niongee nae,” “Marsha akatoka karibu akimbie na kumfuata Inspekta na kurejea nae baada ya dakika chache, wakati wakija wakakutana njiani na RPC akiwa anatoka “Aah, Inspekta kwanza pole sana, lakini nenda nyumbani kwanza kapumzike, mimi nina dharula mbaya ambayo imelazimika nitoke sasa hivi, nafikiri tutawasiliana, sasa Inspekta?” aliuliza huku akimpa mkono “Sawa mkuu,” “Baadae tutawasiliana,” hata kabla Inspekta hajajibu, yeye akawa anashuka ngazi kwa kasi na kutokomea moja kwa moja nje kwenye gari yake na kuwaacha Inspekta Kalindimya na Marsha wakiwa wamesimama wanatazamana, Marsha akauliza “Sasa Mkuu nipe ratiba yako,” “Ratiba yangu kwa sasa ni moja kwa moja kwa moja kwa kina Loren, wewe ulifika jana?” “Ndio nilikwenda mara tu baada ya kusikia hii taarifa ya kifo chake,” “Nani alitoa taarifa ya kifo hicho?” “Kwao wenyewe ambao walikuwa wakimtafuta nasasa walimkuta kwenye ghorofa moja lililokuwa likiendelea kujengwa huko maeneo ya Kijitonyama,” “Vipi ujumbe wowote ulipatikana kwenye maiti?” “Hapana wala haukukutwa ujumbe wowote, ila kupitia uchunguzi wa awali inaonekana aina ya kisu kilichotumika ni tofauti na vile vya awali, kiasi nahisi muuaji huyu nitofauti na Yule alie waua kina Mwana,” “Kwanini unasema hivyo?” “Kwanza hakuacha ujumbe na hiyo si kawaida yake na pili hakutoa taarifa juu ya mauaji yake, wewe unaonaje? Ama yawezekana amekuja kivingine?” “Kwani Marsha wakati unakuja kwangu tayari tukio lilikuwa limeisha tokea?” “Ndio, muda ule mimi nimekuja kwako ile ni mara ya pili, mara ya kwanza nilikuja na kuwachukua askari waliokuwa pale getini na kuondoka nao na kuwaacha hao waliopo kisha nikawaleta huku ili kuwahoji nao wakakiri kuwa ulitoka kama ambavyo ulisikia,” “Dah! Kwa hiyo muda niliotoka mimi na ndio muda alio uawa Loren?” “Yaani bila tofauti ya hata dakika kadhaa,” “Mh! Kazi ipo, huyu muuaji ni jasusi, na tukimuendea kasi huyu tutajikamata wenyewe, sasa la msingi hapa ni meme nawe kwenda hospitali kwenye maiti ya Loren kwa ajili ya uchunguzi zaidi,” alipendekeza Inspekta na Marsha akasema ni kweli hawajaendea hata hivyo kuchukua majibu ya utafiti wa chanzo cha kifo cha Loren. “Lakini Inspekta wewe ni heri tu ukapumzike, nahisi utakuwa haupo vizuri kabisa, niachie mimi niende kisha ukiwa vizuri utanijuza ulipo nitakuja kama ni nyumbani ama uytakuwa umekuja kazini,” alipendekeza Marsha naInspekta akakataa “Hapana kabisa, nichoke kwa kazi gani name nilikuwa nimeka tu muda wote huo, hapa suala la msingi ni moja kwanza, je muuaji amekujua nawe ama hajakujua?”
Swali la Inspekta lilimuelekea Afande Marsha moja kwa moja na kujikuta badala ya kumjibu mkuu wake akabaki akimshangaa, kisha ndio akakumbuka kujibu kuwa hafahamu kama amejulikana na muuaji ama lah! “Umeniambia kuwa amekwambia amekuona sehemu ya tukio la kifo cha Loren badala ya kuniona mimi, sasa tambua kwamba aekujua na ili tuhakikishe hilo, ngoja tufanye kitu, twende sehemu,” akamshika mkono kma vile anamburuta na kuongozana nae kuelekea nje kwenye gari moja kati ya gari za Polisi zilizokuwa nje na kumuita dereva waondoke. Walikwenda hadi Sinza na kupaki sehemu ya mbali kidogo na nyumbani kwa kina Loren na kuongea na Mwana “Marsha wakati ukiingia humu ndani kwa kina Loren, ulimkuta ndugu yake wa kiume aitwae Chidy?” “Hapana hakuwepo Chidy na kiukweli tu sikumuulizia, ok hapo una ona kuna watu wamekusanyika, hiyo ni ishara ya kwamba mazishi hayana muda mrefu, kwani maiti yao mmeihifadhi wapi?” “Mwananyamala,” “Uchunguzi umeisha kamilika?” “Ndio asubuhi hii inapaswa kwenda kuchukua majibu hayo,” “Hebu kabla ya kwenda huko tuingie mle ndani, nitaomba wewe ubaki kwenye gari ili tu kufuatilia kila ambacho kitakuwa kikiendelea hapa wakati mimi nikiingia ndani, sawa Marsha?” “Sawa Mkuu!” Inspekta akashuka na kuelekea ndani ya nyumba ile yenye msiba na kufika kuwasalimia kwanza aliowakuta nje na kisha akawaulizia alipo amam wa Marehemu. Walimuelekeza na kwenda kumpa pole kisha akawaomba watu faragha kwa dakika zisizozidi tano. Wakatoka wote na kuwaacha wao tu wawili, kisha hapo ndio mahojiano yakaanza, alimpa pole tena kwa mara ya pili kisha akamuuliza ni wapi walipouona mwili wa marehemu? Mama akajibu kwamba mwili ulionekana maeneo ya jirani tu pale. “Mama wewe ulienda kuushuhudia?” “Baba yangu wee… hata nilipata nguvu basi? Lakini nilishuhudia tu mavazi yale aliyotoka akiwa amevaa, ndio ambayo niliyaona na kumtambua mwanangu,” mama akaanza kulia, Inspekta akampoza na kumuhakikishia tu kwamba watampata muuaji siku chache zijazo. Naweza kumuona wapi Chidy?Maana hapo nje hata sijamuona?” “Mwanangu, Sijui mimi nina balaa gani? Chidy nae katoweka tangu jana usiku hata kabla ya mwili wa ndugu yake kuonekana,” “Mama unasema?” Inspekta alipata mshangao mkubwa sana kufanya mama azidi kuangusha kilio. “Ndio hivyo mwanangu, Sijui nae kimempata kipi!” alitoka anaenda wapi?” alitoka hapa akisema anaenda Polisi kuonana na Inspekta mmoja ambae pia anampelekea funguo yake,” “Alikwambia funguo hiyo aliipata wapi?” “Ndio, alisema amepewa na jamaa yake na huyo askari ambae amemwambia amuwahishie kabla hajatoka kazini,” “Sasa alikwambia ilikuwaje akampa yeye,” “Kama ulikuwepo mwanangu, name nilimuuliza hivyo akajibu kwamba huyo amtu anasema aliwaona pamoja ana ndio akaomba msaada huo, baada ya hapo akaondoka,” “Alipoondoka hapo ndio hajarudi hadi sasa?” “Ndio baba yangu, Sijui yupo wapi? Yeye hiyo sio kawaida yake, ni heri hata Loren ambae huwa anapitisha hata wiki mbili, lakini Chidy wala sio kawaida yake,” “Basi mama acha mimi niende, nafikiri huu ni muda sasa wa kwenda kuruhusu maiti ya Loren ije nyumbani kwa mazishi huku nasi tukiendelea na taratibu zingine, pole sana mama yangu,” akanyanyuka na kutoka akiwa hajielewi, moja kwa moja hadi nje na kuwaaga wale aliowakuta pale kisha akaelekea garini. Alipoingia tu ndani ya gari akakkumbatia kichwachake kwa mikono yake na kusema “Ah! Kwanini lakini?” “Vipi Inspekta?” “Dah!Kwanza hebu nieleze usalama hapa ni vipi?” alisema huku akimkata jicho Marsha. “Usalama upo vizuri tu ila hapa kuna mtu ninamuhofia, yulee alievaa T sheti na Pocket, amekuwa akingea na simu tangu uingie, pia amesogea hadi hapa ilipo gari, nikamwambia dereva atoke na kujidai anafunga mlango.” “Ili ajue kuwa hakuna mtu si ndio?” “Yah! Nilitaka kumuona ni lipi lengo lake, dereva huyo akaondoka na kuelekea dukani, huku nyuma huyo jamaa akaja na kusogea kabisa jirani na gari na kulizunguka huku akiongea na simu,” alimeza mate na kumalizia “Kisha akarudi huko akiwa amemaliza kuongea na simu yake hadi tena wewe ulipotoka nje nae ndio akaanza kuongea tena na simu,” “Anhaa!Kwa picha hilo ulilolisema wewe, ina maana sasa tambua kwamba sasa hivi tutaanza kufuatiliwa, wanajipanga hao, piga ua!” “Dah! Hapo Inspekta umenifungua akili sasa,” Marsha akawa kama alieshituliwa. “Tuwe makini tangu sasa, Dereva zidisha umakini wako muda huu, tunaelekea moja kwa moja Mwananyamala hospitali,” wakati akiwa anatoa maelekezo hayo, simu ya Marsha ikaita, ajabu wote wakamtazama Marsha, nae akama mtu alieiogopa simu ile, akaitazama tu hadi Inspekta akamuuliza vipi? “Hii namba ni ya simu ya mezani, halafu ni ngeni kwangu!” wakawa kama wameshangaa hivi. Simu ile iliendelea tu kuita kwa fujo vilevile. Inspekta akamwambia pokea, Marsha akapokea kwa hofu kidogo, aliepiga ndio aliesalimia na kumuuliza Inspekta imekuwaje simu inaita kwa muda mrefu vile? Akajitetetea kwamba alikuwa yupo mbali na simu hiyo. Inspekta akamwambia kwa ishara kuwa iwapo aa wasiwai na simu ile basi aweke ‘Loud Speaker’ ili wamsikie wote, nae kwa kuwa tayari alikuwa na hofu, akaweka hiyo sauti ya nje. Aliepiga alikuwa ni dakatari wazamu wa hospitali ya Mwananyamala, aliesimamia uchunguzi wa kifo cha Loren, na sasa alitaka kujua kuhusu kuiruhusu maiti ichukuliwe na ndugu wa marehemu ama bado kuna shida nyingine? Inspekta Kalindimya akamwambia huku akipunga mikono kwamba hapana, asiruhusu kabisa maiti kutoka, nae akamjibu hivyo na kumwambia wawaambie ndugu wa marehemu wasubiri kwa nusu saa nyingine. Daktari akakata simu na wao wakaanza kuondoka maeneo ya Sinza na kuelekea hospitali ya Wilaya ya Kinondoni, Mwananyamala huku akiwa makini kuangalia kama wanafuatiliwa, kuna wakati alifanya makusudi na kumwambia dereva akatishe kulia ama akushoto tofauti kabisa na waendako. Alifanya hivyo maksudi ilimradi tu kujua kama wanafuatiliwa na kidudud mtu chochote, lakini akaona kama hawafuatwi, wakaelekea moja kwa moja Mwananyamala Hospitali na huku akimuhadithia Marsha yaliyojiri mle ndani. Marsha alishangaa mno, hakuweza kuamini kile alichokisikia, na kuuliza kwa mara nyingine “Ina maana hata na Chidy nae ametoweka? Kuna siri gani hapo kati?” “Ndio hapo sasa!” wakawa tayari wamewasili kwenye geti la hospitali na Inspekta akamwambia dereva yeye anashuka na Marsha atangulie moja kwa moja kwa daktari huyo kwa ajili ya kuchukua majibu. Alidhamiria kujua ni nani anae wafuatilia na kama bado anaedelea, ndio maana akashuka pale, lakini hakugundua lolote, taratibu akaendelea kusogea na kutoa simu na kumpigia Marsha. Alimwambia amchukue daktari na kuelekea nae Murtuary watamkuta huko kwa ajili ya kuukagua mwili wa marehemu kwa mara ya mwisho kabla hawajaukabidhi kwa nduguze kwa ajili ya mazishi. Akajivuta taratibu hadi kwenye jingo la kuhifadhia maiti na kuwaona kwa mbali makundi makundi kadhaa ya watu yakiwa yamesimama kwa kujitenga, lakini ilionekana dhahiri kwamba kuna jambo wanasubiri. Hilo sio lililompeleka pale, lakini alijaribu tu kutafuta sura anayoijua ili aweze angalau kumsogelea na kupiga nae story ili kuvuta muda, lakini hakumuona pia muda. Alitazama saa tena na kuona kama muda unazidi kwenda, akaamua kusogea kabisa mlangoni kwa Mhudumu wa maiti na kumsalimia, akiwa anamuuliza amsaidie nini, ndio kwa mbali akawaona Daktari akiwa ameongozana na Marsha wakisogea eneo hilo. Alijitokeza nje baada ya kuona simu yake ikiita na kisha akanyoosha mkono kwa Marsha aliekuwa akimpigia na kurudi ndani. Waliwasili na kuungana nae huku wakiwa wamesimama, daktari huyo hakuwa mgeni kwa Inspekta na wala Inspekta hakuwa mgeni kwenye macho ya Inspekta, walikuwa wakitambuana maana walikuwa wameisha fanya kazi nyingi sana. Baada ya salamu na kujuliana hali, Marsha alimwambia mkuu wake kuwa daktari ameisha mkabidhi ripoti ya uchunguzi wao na inaonesha tu kwamba marehemu alipigwa na kitu kizito kichwani na kisha akakabwa shingoni na kisha akachomwa na kitu chenye ncha kali. “Doh!Daktari hakuna sumu iliyohusika pia?” ‘Hapana hatujaona athari yoyote ya sumu bali tulichokiona ni hicho tu tulichokiandika Inspekta,” alijibu daktari kwa kujiamini huku akijitikisa pale aliposimama. “Ok! Naweza kuiona maiti sasa hivi?” alimuuliza huku akimtazama, daktari akasema sawa, na kumuita muhudumu aliekuwemo mle na kumtaka kuwaongoza kwa maiti ile.walifika na kuvutiwa droo yenye maiti ile na kuiona. Muhudumu alisogea nyuma kidogo na kurejea na Gloves kama pea nne tofauti na kuwapa wote, wakazivaa ila tu daktari ambae alikuwa tayari mikononi ana gloves zake. Waliifunua na hawakushughulishwa sana na sura, kitu cha kwanza walichokihitaji ni pale kilipoingia kisu, walipoiona sehemu hiyo, wakatazamana Inspekta Kalindimya na Afande Marsha kisha akasema Inspekta kwamba tundu la kisu inaonesha kuwa safari hii hakikutumika kisu kidogo kama vile ambavyo vimekuwa vikitumika awali. “Ndio hata name hilo nimeliona, inaonekana ameamua muuaji kubadili mbinu,” “Ok! Tuapaswa kuongeza nguvu ya kumsaka huyu muuaji,” aliongea Inspekta akisogea nyuma ishara ya kuonesha ameridhika juu ya kile alichokuwa akikihitaji sasa amekiona, Marsha akamwambia muhudumu awape tu watu wenye maiti ile. Daktari akawaambia kuwa wakati wakifanya uchunguzi wamegundua kuwa sehemu ya sikio ya marehemu ilikatwa kidogo na kuwekewa dawa ya kukata damu, inspekta akaiomba tena maiti aione sehemu hiyo. Ikavutwa tena maiti na kufunuliwa toka kwenye mfuko wake maalum wa kuhifadhia maiti na hata kabla hawajaenda mbali zaidi, Inspekta akashtuka na kuguna kwa nguvu, “Ah! Huyu ni Chidy bhana, japo simjui Loren lakini huyu ni Chidy Marsha,” alisema huku akizidi kumtazama vizuri, Marsha nae akamsogelea zaidi na kumuweka sawa uso ukimtazama yeye. “Of Cuz ni kweli, kwani Chidy na Loren ni watu wawili tofauti?” “Yaah! Hao ni ndugu wawili tofauti,” alisema huku akivuta zipu kumfunika marehemu pasina tena hata kuliangalia hilo sikio lililokatwa. “Lakini mimi Sijui Chidy ni yupi na Loren ni yupi,” alijitetea Marsha
“Loren ni mtu aliepotea awali na Chidy ni nduguye aliepotea jana tu baada ya kuleta funguo kituoni,” alifafanua Inspekta Kalindimya “Shit! Huyu ndio alieleta funguo, hilo mimi mbona nalijua?” “Sasa alieleta funguo kwako, sio tunaemtaka sisi, maana huyo ndio mtu alieleta simu pia kwangu, alikuwa ni kiungo kwetu,” “Kwa hiyo alieuawa ni huyo alieleta funguo, si ndio mkuu?” alihoji Marsha akimtazama mkuu wake kwa umakini mkubwa. “Ndio! Sasa inaonekana kabisa kuwa tumerudi nyuma Marsha,” “Tena ni zaidi ya hata pale tulipokuwepo, kama huyu ni Chidy, ina maana Loren yu hai, iweje nguo zake avae ndugu yake?” wakamuaga daktari na kuondoka haraka eneo lile kurejea nyumbani kwa kina Loren. Njiani walijadiliana sana. Inakuwaje tena mauaji yahamie kwa mtu huyu mwingine ambae hahusiki? Tena ilionesha dhahiri kwamba Chidy alikuwa akimpenda sana mdogo wake maana aikuwa akiumizwa sana na kutokuonekana kwa mdogo wake. Huenda kuna siri kubwa hapa kati juu ya familia hii, ni kwanini Loren tu? Sasa hadi nguo? Dah! “Kwani wakati ametoka kwako kukuletea funguo alikuwa na mavazi ya aina gani?” alihoji Inspekta. “Alikuwa amevaa Tsheti moja nyeusi na Jeanz ya bluu, hakuwa na mavazi hayo tuliyo yaona,” alijibu Marsha. Safari hii tena waliingia wote hadi kwa mama wa marehemu na kumwambia muda sio mrefu maiti itawasili pale nyumbani, lakini wana maswali machache. “Mama unasema ulimuona Loren wakati wakiubeba mwili wake kuingiza kwenye gari, alikuwa amevaaje?” swali hilo ndio lilikuwa la kwanza na mama kataja nguo zile zile ambazo amekutwa nazo marehemu huko hospitali. “Je wakati akiwa ameondoka hapa alikuwa maevaaje?” “Hivyo hivyo ndio alikuwa amevaa,” wakaona kama vile wamemaliza maswali yao, sasa ndio wakampasulia kuwa wana imani kwamba maiti illiyo patikana pale sio ya Loren “Ni ya nani?” mama aliekuwa akilia kwa taratibu, sasa akanyamaza na hata kabla hajaelezwa ni maiti ya nani, akaingia dada mmoja akilia kwa sauti ya huzuni sana, mkononi alikuwa ameshika simu ndogo, inaonesha kama simu hiyo ndio ilimpa taarifa hiyo na kumtaja Chidy huku akimsogelea mama Loren “Mama eeeh, kaka yangu mimi… Mama ni kaka Chidy ndio amefariki,” mama hakusema kitu wala hakujibu lolote, palepale akaanguka kimgongo mgongo na kuzimia. Kwa haraka tu Inspekta akamwambia Yule aliekuwa akilia kwamba wamnyanyue na kumpeleka sehemu yenye hewa zaidi na kumpepea. Dakika chache mbele akazinduka na kuanza kulia kwa kelele zaidi ya awali. Inspekta na Marsha wao wakatoka wakiwa wamechanganyikiwa kabisa, wakiwa garini sasa walithibitisha kuwa muuaji huyo amejipanga. “Ujue huyu mtu habahatishi, huenda kuna mtihani alipewa Chidi na kushindwa kuutimiza sasa ndio hatma imekuwa hii, hawa wauaji ni watu wabaya sana,” aliongea Inspekta, dereva akamuuliza ni wapi wanaelekea? Marsha akamwambia waende moja kwa moja kituoni. Wote walikuwa kimya tu garini, Inspekta akaanza kujumlisha vile vifo na matukio jinsi yanavyotokea, alishindwa kabisa kupata picha ya matukio hayo. “MwanaHamisi alianza, akafuatia MwanaHeri na sasa Chidy, mbona nahisi kama Loren anahusika kwa asilimia mia moja bila kupepesa?” aliwaza Inspekta na wakati huo Marsha nae alifikiri “Huyu Inspekta nae amenichanganya sana, amemjuaje Chidy na kumgundua mapema mno wakati amemuona mara moja tu kama mimi? Ama ni kweli huyu mtu anahusika? Mbona nakuwa njia panda?Sasa kama kweli anahusika ni lini tutafanikiwa kumtia nguvuni?” Wakiwa katikati ya mawazo, dereva alisimamisha gari na kuwajulisha kuwa wamefika, lakini hakukuwa na hata mmoja ambae alimsikia, wote walikuwa mbali, akamgusa Marsha na kumwambia wamefika. Marsha alivyoshtuka ikawa na sababu ya Inspekta nae kuamka toka kwenye mawazo aliyokuwa nayo. Wakashuka na kuelekea ofisini, hawakukaa sana wakaagana kila mmoja kisema anaenda kupumzika wakati huo Inspekta akiwa wa kwanza kuondoka. Aliwasili nyumbani kwake na kwenda kujitupia kitandani, akakumbuka kuwa bado hajaoga, akaenda kuoga na kula kabisa, safari hii aliagiza chakula kupitia mmoja wa wale askari walinzi waliokuwepo pale. “Tunapaswa kuwa makini mno na maagizo tunayopokea, kosa moja magoli milioni, acha tu nitii sheria bila shuruti, nimuagize msosi jamaa nikaoge mimi, hadi nikimaliza nae atakuwa ameisha rejea,” aliwaza hivyo na kweli akatimiza. Akiwa mezani anakula, akachukua tena diary yake na kuanza kupitia tena siri za zile namba na kujumlisha na majina ya wahanga wa vifo vile. Hakuweza kuambua chochote. Bado ilikuwa ni mtihani kwake, akajikuta amechoka na kutokana na usingizi wa usiku uliopita aliokuwa kororkoroni, akalala mezani. Alishtuka usiku mnene na kuhamia kitandani kwake kulala. Wakati nae akiwa hivyo, Marsha nae alikuwa yupo macho akihangaika kufumbua fumbo lile la vifo, yeye kwa upande wake alikata tamaa mapema juu ya utafiti wa zile namba, kilichotokea ni kuanza kufuatilia nyendo za Inspekta kupitia namba yake iliyopo makao makuu ya Polisi. Ikapita wiki mzima pasina tukio lolote kubwa kutokea, siku moja wakiwa Inspekta Kalindimya na Afande Marsha wameketi sehemu moja wakipata kinywaji baada ya kutoka nyumbani kwa kina Loren, simu ya Inspekta ikaita. Inspekta akaiacha ikaita hadi ikakata na hata Marsha hakujua ni kwanini amefanya vile mkuu wake wa kazi. Ilipokata tu akamtaka Marsha anyanyuke na kuelekea nje “Twende Mwananyamala tukazihakiki zile Call box kama bado zipo salama, sina imani maana huyu mpumbavu anaendelea kucheza nasi tu huku wala hatumuoni kama ambavyo tulipaswa kuwa tunamuona,” “Lakini sasa mbona hujapokea hiyo simu mkuu? Huenda ana habari muhimu huyo,” “Marsha, ni mapema mno kwa wewe kulaumu, ni kwa vile bado hujakomaa katika kazi hii, kuna wakati unapaswa kufanya hivi ili mambo mengine yaende sawa, najua kwa sasa hutonielewa, ila tu siku chache mbele utajua,” wakiwa wanatoka nje ya hoteli hiyo, Marsha akaomba aoneshwe tu maana yake. Kwanza pale ni hotel na simu huyu jamaa anapopiga tanmbua kabisa kwamba ina tukio, ndio maana nimekwambia tuondoke,” kauli zile tata ndio zikazidi kumchanganya Marsha na kujiuliza tena ina maana ni kweli afande anahusika? Mbona anakwepa kuwasiliana na muuaji na ikiwa ni yeye ndio aiepiga? “Kifupi sasa hata name imani yangu kwa afande inazidi kupungua kama mvua inavyo pungua kiangazi,” aliwaza Marsha na kunyamaza huku akiingia ndani ya gari kwa upande wa abiria. Safari ikaanza kuelekea maeneo ya Mwananyamala, maana namba ile iliyotumika sasa ilikuwa ni ile ya Hospitali, sehemu ambayo Inspekta alitegemea kwamba jamaa akiingia tu yeye atajua lakini sasa hadi anapiga simu yeye huku hajui hata kidogo, akahisi kuna walakini. Walifika hadi kwenye Call box ya kwanza ya Maeneo ya Kwa mama Zacharia, walikuta mfumo mzima upo lakini haukuwa salama, Camera ilikuwepo, ila sehemu ndogo sana ya kipande cha waya hakikuwepo, waya ambao ulitumika kama antenna ya kurusha picha, ndio ulikatwa. Akaichukua Camera yake ikiwa haina kazi tena, kwa hasira akafyonya na kutoka kurejea garini ambapo alimkuta Marsha na kumuonesha, Marsha kwa kuwa nae sasa hakuwa na imani na Bosi wake, alimtazama tu na kujishangaza kidogo tu. Aliamini kabisa anachokifanya Afande sasa ni hadaa tu, kwani hawawezi kufanikiwa lolote iwapo tu Inspekta ataendelea kufanya mambo ya ulaghai kwa jeshi. “Hali ndio hiyo, sasa hebu twende A kisha tumalizie Hospitali, huenda huko tukapata pata,” “Inspekta, mimi sidhani kama tuna haja ya kwenda huko kote, maana ni kama tu tunakwenda kupoteza muda,” aliongea kama mtu aliekerwa na jambo hilo. “Marsha? Kwanini unasema hivyo?” “Inspekta mimi nahisi kuna mchezo tu unafanyika hapa huku tukipiga Mark time, tunaonekana tukifanya kazi lakini kumbe hakuna tunacho kifanya,” “KIVIPI Marsha? Hebu nielezee vizuri,” “Nina wasiwasi kuwa kuna usaliti kati yetu, maana kila tunapopiga hatua, tunajikuta tumerudi nyuma, hivyo miki binafsi sina imani na sisi wenyewe,” “Ni nani unahisi anafanya usaliti?” “Siwezi kujua bali ni mtu wetu tu wa karibu, inavunja sana moyo hali hii,” “Marsha kwakanuni za kijeshi hupaswi kukata tamaa na unapaswa kupambana mwanzo mwisho, hadi utakapomtia mikononi adui yako, usioneshe udhaifu wako kwa wenzako bali onyesha ujasiri wako kwa wenzako,” alimtia moyo na kuwasha gari kuelekea Mwananyamala A. Huko napo kulikuwa na Call box nyingine ambayo waliitegesha Camera na mic ndogo. Walitegemea angalau vyenyewe watavikuta vikiwa salama, lakini wala haikuwa hivyo. walikuta uharibifu ukiwa umefanyika kwa kiwango kilekile cha Call box ile ya kwa mama Zacharia. Marsha alitaka kuzungumza kitu lakini akahisi atamkwaza mkuu wake wa kazi, akanyamaza hadi walipofika Mwananyamala hospitali. Inspekta akashuka tena peke yake na kwenda kufanya yake. akarudi akiwa na hasira hadi garini na kujitupia huku akilaumu kuwa ni hatari sanaa. Akageuka Marsha na kumuuliza vipi? nae akajibu hali ni ileile tu haina tofauti na vile za kule. “kwani Inspekta ulihisi kutakuwa na utofauti wowote kati ya hizo Call box?” swali likuwa ni la kebehi na hata Inspekta alielewa hivyo lakini wala hakuonesha kupanic balia lisema kwa hali iliokuwepo pale alitegemea itakuwa hivyo. Akawasha gari na kuondoka wakiwa wameelewana waelekee moja kwa moja kituoni kwa ajili ya kujiandaa kwa ajili ya mipango mengine. Marsha alidhamiria kumchunguza zaidi bosi wake… “huenda mara ile ya kwanza nilikurupuka kama alivyosema mkuu, sasa napaswa kufuatilia kila step yake anayopiga, hakika mimi sasa nita deal nae tu!” aliwaza hadi wakiwa wamekaribia kituoni. Walishuka na kuelekea ofisini, wakiwa wameketi tu, Marsha akanyanyuka na kuelekea nje ambapo alielekea nje ya ofic yao na kuingia kwenye ofisi ya watu wa mahusiano na habari, akawaomba mawasiliano ya nambaya Inspekta. Mkuu wa zamu akampa na kuipitia, hakuona namba yeyote tofauti na zile ambazo zilipigwa wakiwa pamoja. aliporidhika hapo akachomoka na kuelekea ofisini kwa RPC ambapo huko napo akamkuta akiwa na RCO. Walipomuona wakamuuliza vipi? kuna mpya gani? Akawaeleza kila kitu juu ya hisia zake kwa Inspekta “Halafu wewe Afande ni mwenda wazimu eti? We si ndio ulimtetea na kusema hahusiki? Sasa imekuwaje?” RPC alimuhoji kwa mshangao. “Hapana sasa nimegundua kupitia baadhi makosa anayofanya kama hayo niliyo yaeleza kwenu,” “Ujue mimi sikuelewi, sasa unachotaka ni nini?” “Nataka nimchunguze yeye wakati akiendesha kesi hiihii, hivyo ningependa mimi nijiweke pembeni ili nipate wakati mzuri zaidi wa kumchunguza Inspekta,” wakatazamana RPC na RCO na kukubaliana kuwa swala lake ni la msingi sana. “Wazo lako zuri sana unataka tufanyejesasa? Hebu kuwa miwazi,” alisema RCO huku akitegemea Marsha kutoa wazo lake. “Naomba nikabidhi jukumu hili kwa Inspekta ambae nashauri asaidiane na Afande Jitu ambae nae asijue kama nawachunguza,” alimaliza Marsha na wao wakajadiliana kidogo kabla ya kukubaliana kuwa anachosema Marsha ni sahihi, wakamwambia aende kumkabidhi faili hilo na amwambie Jitu juu ya mabadiliko hayo pia Inspekta nae amjulishe. Akasimama na kupiga saluti kisha akatoka na kuwaacha wakiwa wanajadiliana juu ya kile ambacho amewaeleza. “Kamanda, kwanini tufanye kazi na mtu ambae ana tuhumiwa kuhusika na kesi anayoisimamia? Huoni kuwa tunakuwa tunaleta tatizo lingine?” aliuliza RPC. “Ujue kwamba Kati ya vijana wanao aminika kwa kitengo changu, basi yeye ni namba moja na namba mbili wake sijamuona, ninaamini kabisa anahusishwa tu, hebu tumuache afanye kazi wakati huohuo Marsha atatujibu,” wakakubaliana hivyo na kutoka wakiagana kwa ahadi ya kuendelea kuwasiliana. Marsha alipotoka pale moja kwa moja akaelekea kwa Inspekta Jitu na kumkuta akiwa ameketi peke yake akifunua makabrasha yake, alimsalimu na kumpa taarifa toka ngazi za juu, alipotaka kujua ni kwa sababu gani yeye amejitoa? Marsha akajibu kwamba “Inspekta hata sielewi niseme nini, bado mimi sina imani na mtu miongoni mwetu,” “Kwamba tunasalitiwa?” “Ndio Jitu, naona kabisa kuna wakati mambo yanakuwa mazuri lakini ikifikia tu sehemu za kuelekea mwishoni mambo yanaharibika na kuparaganyika kabisa, yaani nachoka kabisa,” “Sasa ukisikia upelelezi ndio huo, ingekuwa ukifika tu unamaliza, huo sasa sio upelelezi huo ni ukamataji, na hiyo ni hatua ya mwisho na pia amini tu kuwa tuataifikia,” “Sio kwa mwendo huu Inspekta,” “Afande kwa nidhamu za jeshi unafanya makosa sana kukata tamaa, hupaswi kukatishwa tamaa na jambo lolote, songa mbele hadi dakika ya mwisho,” alimpa moyo Marsha bila kujua kuwa mwenzie ana duku duku sana na Inspekta Kalindimya. “Hebu niambie ni nani ambae unamshuku,” “Siwezi kubashiri wala kufanya utabiri lakini tambua kuwa kwa njia ya kutazama tu mwelekeo sina imani na Inspekta Kalindimya,” “Kwanini labda?” alimuuliza huku akikunja faili lake na kumtazama kwa umakini zaidi ya ule wa awali. Marsha akamueleza juu ya tukio lililotokea Mwananyamala tangu mwanzo “Yaani nilikaa kimya tu kwa kuwa ni bosi wangu na hata tulipokuwa tumekosa pale sehemu ya kwanza, Inspekta akawasha gari na kuelekea A kwenye Call box nyingine na kukuta mazingira yaleyale na kumalizia ile ya mwisho iliopo maeneo ya Hospitali.” Jitu alikuwa akimsikiliza tu “Kote hali ilikuwa ni sawa, hakuna sehemu yoyote ambayo Camera zilikutwa salama, kote zilikutwa zikiwa zimeharibiwa lakini zimeachwa, ila sehemu moja ambayo aliitumia mhalifu kutupigia tukiwa nae, na hakupokea, hapo Mic hazikukutwa kabisa,” “Sasa Marsha huoni kuwa ungekuwa nae karibu zaidi ungeweza kumpatia kiulaini zaidi?” “No! Mkiwa nyinyi ndio mnawajibika mimi nitawafuatilia kwa ukaribu na lakini pia nitakuwa na chanzo kingine cha habari,” akatabasamu “We mwendawazimu kweli, yaani unigeuze mimi kama mic yako ili upaze sauti?” nae akacheka. “Nataka nikutumie, maana wewe unaweza kuona pia point muhimu za kumtia hatiani, mi hakika sina imani nae kabisa na sasa hivi naenda IT room kuwasiliana nao, wamfungulie kila kitu kwenye simu yake na ikiwezekana wamuingizie Data,” “Ok! Fanyeni hivi, nyie mawasiliano yake yote yapitie humu kwanza…” “Tayari hilo mbona? Yaani imebaki tu utekelezaji best,” alimaliza Marsha huku akisimama na kujiandaa kutoka. Inspekta akaingia na wote wakasimama na kumpa saloot kisha akawasemesjha kwa kuanza na Marsha “Nimesikia umebadilishiwa kazi? Amenipigia simu RCO muda huu, vipi lakini kuna usalama ama kuna tatizo?” alimuuliza huku akimtazama, nae akajichekesha na kujibu ni salama. “Basi sawa, umeisha mkabidhi kila kitu?” “Ndio nilikuwa nampa hapa Mkuu!” “Sawa, ulikuwa unatoka?” “Ndio mkuu, natoka sasa nafikiri ni hadi baadae,” “Ok! Sasa we unaweza kwenda, name nataka kuongea kidogo na Jitu hapa,”
Hapo ndio Marsha alikuwa akipataka, alitamani sana kujua ni nani aliepiga simu nje ya Yule mtu ambae Inspekta hakupokea. Akaelekea moja kwa moja kwa watu wa IT kujua kama anaweza kumtambua mtu huyo. Inspekta alipoketi akamwambia Jitu kuwa yeye alikuwa ni nyuma ya wakati, akamueleza baadhi ya matukio muhimu na kumtaka aseme nae wanajipanga vipi? Jitu akajitetea kuwa apewe muda. Lakini hata hivyo wakapanga siku ifuatayo asubuhi waende nyumbani kwa kina Loren kwa ajili ya uchunguzi zaidi hasa ukizingatia kwamba hawajarudi tangu waliyo ondoka siku ya msiba na hawajarejea tena. “Inspekta Jitu nashauri wewe uebnde peke yako ili kujua kama unafuatiliwa ama lah, maan inatambulika fika kwamba mimi najulikana,” “Umelenga nini kusema hivyo?” “Nataka nijue chanzo cha kuvuja upelelezi wetu, ni mtu wa ndani ya nyumba ile ama kuna chanzo kingine? Sasa wewe uende na kuingia bila kukaa muda mrefu, hapo tutajua, ama unasemaje?” Jitu akafikiria kwanza. Nae alipata kama wakati wa kujiuliza, ni vipi akatae kwenda yeye Inspekta ambae anajulikana na anataka aende yeye mgeni? Tayari Alisha jengewa shaka ya kutokumuamini Inspekta Kalindimya, Marsha alimuathiri kisaikolojia. “Inspekta kwa kuwa wewe tayari unajulikana kuwa ni nani, ni kwanini usiende na kutoa nafasi ya kuwatisha, kwani ni lazima wajiulize na hapo ndio watakurupuka,” “Huenda hujanielewa, ninachotaka mimi ni kupata chanzo cha kujulikana kwetu, Marsha tayari wamemuona japo wamehisi ni askari, ila walijuwa ni kama labda wa zamu tu, maana mtuhumiwa alipiga simu kunieleza juu ya kukosekana kwangu, kwenye tukio la mauaji ya kaka yake Loren,” alieleza kwa urefu. Ilionekana kama Jitu ameelewa lakini alikuwa na swali ambalo pia alishindwa kuliuliza, alitaka kumchana mkuu wake, lakini akaogopa na kumuuliza ni nani alimuuliza swali hilo? Akajibu ni mtuhumiwa na hapo Jitu akatikisa kichwa na kusema…
“Nimekuelewa Inspekta, lakini kwa maelezo tofauti mliyonipa, inapaswa kujipanga hasa kabla ya kukurupuka na kuna mambo inapaswa tujue sisi binafsi tu na yeyote asijue tofauti nasi,” “Na hiyo ndio huwa ni kawaida ya kazi hii ya upelelezi Jitu,” alimaliza na kuaga kwamba wataonana siku ifuatayo asubuhi na mapema wakutane hapo. Inspekta akatoka na Jitu akabaki ndani peke yake na kumtaarifu Marsha juu ya uwpo wa safari ya kuelekea nyumbani kwa kina Loren asubuhi ya siku ifuatayo, kisha akampa na mipango yote ilivyo huku akimsisitiza kuwa makini. *********-
Walifika nyumbani jwa kina Loren na kukaribishwa vizuri tu lakini ikiwa nyumba ni yenye simanzi sana, kila mmoja alionekana ni mtu mwenye huzuni mno, siku iliyopita walikuwa wamepanga aingie Inspekta Jitu peke yake, lakini kwa ushauri wa Jitu wakaingia wote. Waliketi kwenye viti vya ofisini ‘Office Chairs’ ambavyo vilikuwa uwani sehemu ya wazi na kutaka kuonana na mama yake marehemu, wakaambiwa yupo ndani amelala kwani hali yake sio mujarrab. Hali yake tangu kifo cha Chidy, ilipoteza mwelekeo na kuwa ni ya mashaka matupu, mara kichwa kinamuuma wakati mwingine anahisi presha, hiyo ndio ikawa ni hali yake. Sasa ikalazimu wafanye mahojiano na dada wa marehemu na kumswalika maswali mengi ya kutosha, lakini majibu yake yalionesha kutokujua lolote juu ya kifo cha ndugu yake. Nusu saa tu iliwatosha kuendelea kuwepo ndani ya nyumba ile, hivyo wakati inatimu saa tano asubuhi, nao wakawa wanatoka kuelekea ofisini kwao wakiwa hawajaambulia chochote. Wakatoka na kuendelea na shughuli zao mbalimbali wakiwa pamoja garini huku waki discuss juu ya mauaji hayo na muuaji ni nani. Kila walipokuwa wakifikiri na kujitahidi kumtafuta lakini wala hawakufanikiwa kupata walau fununu. Walirudi ofisini nakuendelea na uchunguzi wa kwenye faili lakini hawakuambulia lolote, walitamani tu siku iishe tu ili warudi majumbani mwao wakapumzike na kujipanga upya. Saa 10 jioni ilipotimu, afande akawa ni mtu wa kwanza kusimama ili kuelekea nyumbani huku akifuatiwa na Jitu ambae alitaka lift, wakatoka wakiwa wameisha funga ofisi na kuelekea nje ilipo gari. Kitendo cha kuingia garini tu, simu ya Inspekta ikaita. Gari ilikuwa iendeshwe na Jitu kwani ndio alikuwa na funguo ya gari na tayari alikuwa ameingia upande wa dereva, Inspekta akamzuia kuwasha kwanza. “Jamaa tena huyo,” akasema huku akimuonesha simu, kisha akatoa headfones na kuvaa sikio moja na upande mwingine akampa Jitu ndio akapokea simu kwa utulivu mkubwa. Mpigaji alipopokelewa simu yake akaongea bila papara na kumpa hongera Inspekta kwa kuwatembelea siku hiyo, Inspekta akamwambia anaona kabisa kwamba wala hana jipya kwa siku ile. Jitu akashangaa na kujiuliza tena imekuwaje? Mpigaji nae upande wa pili akacheka kwa sauti ya juu baada ya kauli ile ya Inspekta na kusema kwamba yeye hakosi jipya, “Inspekta kila.ukiona simu yangu, ujue kuna kitu kipya,” si inspekta Kalindimya wala Jitu walio ijibu kauli hiyo, wote walikuwa kimya wakimsikiliza kidume akitamba. “Muda mchacheujao, mwandishi wa habari na mfanya biashara mjasiriamali nitachukua pesa yake ili tu kukuonesha kuwa ninaiweza kazi na kwa kuwa hutaki kunielewa ninapokwambia kwamba achana na kazi hii nawe hutaki, sasa utawaponza wengi,” aliongea kwa kujitapa. “Kwa hiyo kwa sababu mimi nimekataa kujiondoa kwenye kazi hii ndio unaua raia wasio na hatia?” aliuliza Inspekta kwa kebehi. “Hakuna hasira hapo, kwa kuwa wewe ni jeuri acha tu tuucheze mchezo wetu hadi dakika ya mwisho mmoja wetu atakaeruhusu kushindwa ndio mchezo utakuwa umeishia hapo,” “Sawa kabisa, unaonaje tu tuumalize mchezo leoleo?” “Hapana!leo ni siku ya game, tucheze game yetu na Mwana, hahahaa!” alimaliza kauli yake kwa cheko kubwa, cheko iliyomkera mno Jitu na kutaka kuongea kitu lakini Inspekta akamzuia. “Unajua mwanaume wa kweli haogopi kukutana na kidume mwenzie? Sasa wewe itakuwaje uogope kukutana nami uso kwa uso na hatimae unaenda kupambana na mabinti tu? Maana mimi nina hakika kabisa kuwa wewe unaua mabinti tu,” aliongea Ispekta kwa nia ya kumpandisha jazba na ajikute ameropokwa tu maneno, lakini wala haikuwa hivyo, jamaa akaendelea kuongea bila jazba. “Inspekta tanbua kwamba kwa huyu meembo Mwana mimi wala sina nia nae mbaya, ni vile tu nahitaji pesa kwa ajili ya rambirambi ya mazishi ya Chidy bae aliuawa masikini ya Mungu bila kosa,” “Unajua kuwa unanipotezea muda tu bure?” ” Ila wewe huoni unavyojaribu kuingilia kazi za watu ambazo hazikuhusu kope wala jicho? Na ole wako uendelee kunifuatilia,” “Ndugu huwezi kulitisha jeshi la Polisi eti lishindwe kufanya kaziyake inavyo stahili kwa sababu yako…” “Afande unajua sana kuongea, ila nilipiga simu kukutaarifu tu kuwa leo sina nia mbaya na Mwana ila akileta ubishi nitamjeruhi, kwani huyu kwenye idadi yangu ya watu wa kuwaua yeye hayupo…” “Sasa umeniambia ili iweje?” awamu hii Jitu ndio aliuliza akiwa na jazba, alitamani mno kama vile angekuwa anamuona mtu huyo.
“Nimekwambia ili uwepo maeneo ya tukio ambalo nitalifanya maeneo ya Mwananyamala Studio, njoo ushuhudie tukio langu live leo hapo itakapo timu saa tatu usiku, mi nitakuwa Kigamboni, kwaheri!” Simu ikakatwa na kuwacha maafande wakitazamana na kushusha pumzi kwa nguvu. Jitu alikuwa ni mtu wa kwanza kutoa ile earfone sikioni mwake na kumuuliza Inspekta “Hivi huyu jamaa anaweza kuwa yupo seriuos kiasi hicho juu ya haya aliyo yasema?” “Yap!Huyu jamaa wala hatanii.lakini ujue kuwa kwasasa nahisi kuijua sauti yake?” “Sasa mkuu hapo tunafanyeje?” alihoji Jitu huku akijiweka vizuri kwenye siti yake. “Hatuna cha kufanya kwa sasa maana ni kama ulivyosikia tu hapo kwenye maongezi yake kuwa tukio litakuwa Studio, sasa jiulize hii studio inawaandishi wa habari wangapi?” aliuliza Inspekta na Jitu akajibu “Dah! Nahisi sasa kuishiwa mbinu, huyu jamaa ni hatari sana,” hupaswi kukata tamaa, sasa ni saa 11 jioni, muda aliousema yeye unakaribia, fanya mpango wa kuomba askari kituoni pamoja na usafiri, nataka uwapange eneo lote tajwa, acha nami niwake hadi Kigamboni,” “Sasa unaenda kufanya nini huko na mtu humjui na pia Kigamboni ni kubwa?” Jitu aliuliza kwa mshangao. “Huzijui tricks zao hawa? huenda tukio likatokea huko Kigamboni na halafu akawa ametupanga sisi huku Kinondoni,” alijibu kifupi tu lakini wakawa wameelewana. “Ok! Nimekuelewa Mkuu, acha nami nianze kujipanga tangu sasa, nafikiri tutawasiliana kila baada ya muda,” wakaagana na kila mmoja akashika kazi yake huku Jitu akirudi kituoni na Inspekta Kalindimya akielekea Kigamboni. **********
Marsha alikuwa akisikiliza mawasiliano yote ya Inspekta, mara tu baada ya kujua kwamba wameachana kati ya Inspekta Kalindimya na Jitu, yeye akajitokeza na kumvaa Jitu aliekuwa akiongea na baadhi ya askari. Alimsalimu na kumtaka faragha kidogo waongee. Jitu alisogea na kumsikiliza “Jitu kwa ukweli nimefuatilia maongezi yenu yote kwenye simu, nimezidi kupata uhakika kuwa sijakosea kuwa na mashaka na Inspekta Kalindimya juu ya kuhusika na vifo vya watu hawa,” “Kwanini Marsha?” “Maongezi yake yananishawishi niamini hivyo,” “Lakini mbona ameongea kawaida tu Marsha?” “Huenda wewe haukuwa makini ndio sababu, ulikuwa busy sana na kusikiliza anachojibu mtuhumiwa na sio anachokiongea Inspekta,” “Yawezekana, hebu nieleze kile ulichokisikia na kukushawishi uamini hivyo,” “Pale alipomwambia kuwa muuaji wa wanawake, yule jamaa wala hakubisha na Inspekta akazidi kunishtua baada ya kumwambia kuwa wakutane na kumaloza game.” Sasa Marsha hili kweli si ni game? japo upande wetu ndio tunatakiwa tushinde game hii, bado hoja yako haina mashiko,” Jitu sasa alimchana live. “Ok! nisikilize na hii nyingine… unakumbuka amemwambia mtuhumiwa kuwa ni muuaji wa wanawake?” “Ndio nakumbuka,” “Sasa kama muuaji si yeye huyo mtuhumiwa, ni nani sasa aliemuua Chidi?je ina maana Inspekta anamfahamu? na kama hamfahamu iweje amkatalie yule mtuhumiwa hata kabla ya yeye mwenyewe kukataa?” hapo sasa akawa ameongea point ambayo hata Jitu aliona ina mashiko. Akamwambia kuwa hapo sasa ndio pa kuanzia upelelezi wake na kwa upande wake amuachie yeye, wakaagana huku kila mtu akichukua muda wake kwa ajili ya kazi zake. **********
Inspekta Kalindimya akaelekea moja kwa moja Kigamboni, bahati yake ilikuwa ni njema kwani wakati anafika Ferry akaikuta Pantoni ikiwa haijajaa hivyo alipata nafasi ya kuvuka kwa haraka. Kituo kilikuwa ni Kituo cha polisi, hapo ndio ilikuwa ni sehemu muafaka kwake kwenda ili kuweza kuweka guide ili ikitokea kitu chochote kama vile kuhitaji msaada ama tatizo lingine basi apate msaada kwa wakati muafaka. Hivyo akakutana na mkuu wa kituo aliekuwa nje akimshindikiza mtu aliekuwa amesimaa nae akimpa maelezo fulani, ndio akasogea na baada ya salamu ndio akampa taarifa za Kiitelejensia. “Afande inasadikiwa kwamba kuna tukio huenda likatokea huku sijui una habari?” alimuuliza mkuu wa kituo. “Hapana mimi sina habari,” akamtazama Inspekta kwa mshangao. “Ohoo!sawa, kifupi ni kuwa kuna mtu mmoja anaehusika na yale mauaji mawili yaliyotokea Kinondoni, amepiga simu yupo huku,” “What? Unasemaje Inspekta?” Mkuu wa kituo aliuliza kwa mshangao utasema yeye ndio kaambiwa atauawa. “Naam! Na hiyo ndio sababu imenifanya niwe hapa muda huu,” “Hilo nalo hata nami nilihisi tu, ujaji wako wewe huku bila taarifa nilijua tu kuna jambo… kwanza ahsante kwa taarifa,” baada tu ya taarifa ile akanyanyua simu na kumpigia simu mtu fulani. Alimwambia awapange askari wake takriban mji mzima, “Hakikisha umewasambaza kila sehemu, sawa?” kisha akakata simu na kuanza kuzunguka hapa na pale. Dakika moja tu mbele yao ikarudi gari moja ya Polisi aina ya Diffender ikiwa nyuma na mbele yake kukiwa na RAV 4 nyeupe hadi pale kituoni. Kwa mbali Inspekta akaiona pikipiki aina ya Boxer ikipita kwa mwendo wa kasi sana na mtu aliekuwahajavaa kitu chochote cha usalama mwilini lakini kasi yake ilikuwa ni kubwa mno.
Wazo lake akalielekeza kwamba itakuwa mtu huyo anaiwahi Pantoni, kwani muda ulikuwa umekwenda sana, hilo ndio wazo ambalo alilipa nafasi ya kwanza. kwenye gari ile ya RAV 4 alishuka dada mmoja mnene hivi mweupe alikuwa na umbo zuri hasa la kike, alionekana nimrembo tena mwenye pesa zake. Kwa mwendo wa kawaida tu alielekea pale waliposimama wao na kuwasalimia kisha akamshukuru Mkuu wa kituo cha Polisi Kigamboni na kumwambia kuwa biashara imeshindikana. “Kwa hiyo itakuwaje sasa?” aliuliza mkuu wa kituo “Nafikiri nitakujulisha tena itakapokuwa tayari,” alimjibu huku akiwaaga na kuondoka huku Mkuu akimkaribisha tena. Wakati yeye akiondoka simu yake ikaita, akaanza kuongea na huku upande wa pili, Inspekta akamuuliza mkuu wa kituo kwamba usalama umeimarishwa? “Inspekta hapa huyo muuaji akigusa tu amekamatwa, tayari nimeweka ulinzi wa kutosha mji mzima na vitongoji vyake, pia watu wetu huku, yaani raia ni washiriki sana wa ile program yetu ya Ulinzi shirikishi,” “Dah!hongereni sana, hivyo mkuu unanihakikishia tu kuwa sasa naweza kwenda?” “Yap!we unaweza kwenda tu wala usihofu Inspekta,” wakashikana mikono kuagana huku wakianza kutembea taratibu kuelekea barabarani sehemu ambapo sasa alionekana yule kwanamke alkiongea na simu. Inspekta hakupenda kuongozana na yule mwanamke na hata muonekano wake kwa OCS – yaani mkuu wa kituo, ulimfanya Inspekta kujiuliza mwenyewe kuna nini? Akamuomba msamaha OCS na kumuuliza juu ya yule dada ambae sasa alikuwa tayari ameingia ndani ya gari na kuliwasha kwa ajili ya kuondoka. “Samahani Mkuu, huyo dada amekuja akiwa aneongozana na gari ya Polisi na kuja hadi hapa kukwambia kuwa biashara imeshindikana, kwani kuna biashara gani kati ya yeye na jeshi la Polisi?” alihoji. OCS huku akimshika begani kwa kujiamini kabisa akasema “Inspekta, kama raia wote wangefuata sheria ya fedha, kama huyu dada alivyo, basi amini matukio makubwa ya pesa yasingekuwepo abadan,” “Kwanini unasema hivyo mkuu?” “Huyu dada ni mfanyabiashara mkubwa sana hapa Jijini, japo biashara hufanyika huko bara, lakini mara zote mizigo hununua huku Kigamboni. Lakini kwa kuwa huja na pesa nyingi basi hufika hapa kuomba ulinzi, huchukua mzigo wake na kurudi nao hadi nyumbani akiwa salama chini ya ulinzi wa jeshi letu adhimu,” alieleza kwa kirefu OCS na Inspekta akamuelewa na kuhoji tena “Dah!heri yake anajua kuzitumia haki zake, ila tofauti na biashara ana kazi gani nyingine? maana katika mazingira ya kawaida ni vigumu mno kwa mfanyabiashara asie na elimu kuzijua haki hizo,” “Hahahaa kwanini unasema hivyo Inspekta?” “Ni kwa sababu wafanya biashara wengi wanafanya kazi zao kimazoea tu, hawajui kama muda unabadilika, sasa hilo ndio waliosoma wanajua, ndio maana nimeuliza nikiamini atakuwa amepita tu shule huyu,” wakacheka taratibu, OCS akasema “Eeh ni kwli Inspekta, mwanadada huyu ni msomi, ana masters ya MASS Com., yupo kwenye kampuni fulani ya habari…” kabla OCS hajamaliza kuongea, Inspekta kengele ya hatari ikalia kichwani mwake, akamkatisha maongezi kwa kumshika mkono na kumuuliza anakaa wapi. “Huyu dada atakuwa anaishi maeneo ya Kinondoni, ila sijajua ni Kinondoni…” kama mshale bila kujiuliza akachomoka Inspekta “Haa! Mkuu…” kitendo bila kuchelewa akakimbilia gari yake na huku akimwambia OCS kwamba huyo ndio mwanamke wanae muwinda hao wauwaji. OCS akashtuka na kupatwa na mshangao kwa ghafla, Inspekta akaingia garini haraka na kuliwasha kisha akaligeuza kwa kasi na kuondoka akiacha baadhi ya watu waliopo pale wabaki na mshangao. Alitaka kuwahi kumuepusha bi dada huyo kutokana na kifo ambacho kiliweza kuzuilika, aliamini inawezekana kabisa. OCS nae akili ikamuijia, nae palepale akawaamrisha askari wake waende Ferry kumuwahi Inspekta “Yule dada mliekuja nae anatakiwa hapa sasa hivi,” alitoa maelezo bila kuwaambia ni kwanini na amefanya nini? bali alitoa tu amri kwamba apelekwe hapo. Askari walewale waliomshindikiza sehemu ya biashara sasa ndio wakawa wanachomoka tena kumfuata, gari hii sasa iliondoka mbio zaidi hata ile ya Inspekta. Inspekta alikimbiza sana gari, lakini muda waliokuwa wameachana ulikuwa ni mkubwa sana ambao ina maanisha kwamba ni lazima dada yule atakuwa amefika mbali mno. Hadi anafika kivukoni, hakuweza kuiona gari hiyo ila kwa mbali aliiona kama vile ipo kwenye foleni, akaona sasa huenda ataiwahi. Lakini dhahiri baada ya kupiga hesabu zake, akaona kwamba hatoweza kumuwahi tena, iwapo ataendwlea kumfuatilia kwa gari, alitamani wawe wawili garini, lakini ndio hivyo… alikuwa peke yake garini. Alitamani kuiacha gari yake iliaiwahi ile gari ya yule dada, lakini hilo pia ikawa haiwezekani, ingekuwa ni sawa na kuzuia wengine wasipite, sasa akalazimika kutafuta mchepuko. Upande ule aliokuwa akipita yeye kuelekea Kivukoni, nafasi ilikuwa ni haba sana, haikuwezekana kabisa kupaki gari maana kulikuwa na majani marefu na vichaka vidogo vidogo maalum kwa ajili ya kupendezesha eneo hilo.
Hivyo upande huo ukawa haumfai yeye, akalazimika kuangalia upande wa pili, hapo sasa akachepuka pembeni, lakini kutokana na wembamba wa barabara alilazimika kusubiri sana gari za upande wa pili zilizotoka ndani ya kivuko zipite. Hapo muda ulizidi kulika na bi dada alizidi kusogea mbele. alipokuja kupata nafasi ya kuchepuka, akakutana na tatizo lingine, ni wapi apaki gari hiyo? Alikwenda umbali mrefu kidogo hadi karibu na majengo ya TanRoads kwa ajili ya kivuko na kutaka kupaki hapo, alizuiliwa lakini akalindwa na kitambulisho chake. Akashuka na kuanza kuelekea huko ilipo kuwa ile gari ya bi dada huyo. alikuwa mbiombio, gari takriban kumi bila kuliona, akajiuliza je huenda ameiacha nyuma? Akarudi kwa nyuma kidogo ili kuitazama kama ameivuka, lakini hakuiona. Uamuzi aliouchukua ni kuendelea kuangalia gari za mbele na iwapo ikatokea akaikosa, basi akaepalepale getini kusubiri hadi itakapomfikia gari hiyo ya huyo dada. Alipozimaliza gari zilizopo kwenye Mnyororo, aliona kundi.la watu likiruhusiwa kuingia kwenye pantoni, kutokana na kuwa na kigiza kilichokuwepo pale alihangaika sana kuiona gari. wakati ikipiga honi kuanza kuondoka, Panton inageuka upande kidogo kukata kona ili kuipata Angle yake vizuri, hapo ndio aliweza kuiona gari hiyo aina ya RAV 4. Akasogea mbele zaidi ili awahi hata kujirusha kwenye maji na kuingia kwa njia ya kuogelea, lakini akazuiliwa na askari wakiokuwepo pale, akatoa na kitambulisho lakini awamu hii hakikumsaidia. Waliendelea kumshikilia tu na kumzuia wakimwambia kuwa kina cha maji pale nibkirefu sana hivyo wao hawana ruhusa ya kumruhusu mtu yeyote. Rasmi akawa amechelewa, akaiona ilee… inapotea machoni mwake, akakasirika na kupiga ngumi kwenye paja lake na kujishika kiuno akiwa hajui la kufanya. Alishtuliwa na askari wawili waliofika pale na kumpigia saluti na kumuuliza kama amefanikiwa kumuona. Akawataka wajitambulishe kwanza, hawakubisha, wakajitambulisha. Baada ya kuwatambua akawapa maelezo kifupi tu na kuwataka warudi lindoni kwao yeye anavuka, wakageuza na kurejea kituoni huku yeye akianza kurejea ilipo gari kwa ajili ya maandalizi ya kuvuka. Akiwa garini akatoa simu na kumpigia Jitu, alipoipokea tu hata kabla ya salamu, akamuuliza alipo, nae akamjibu kuwa yupo Mwananyamala “Usalama upoje huko hadi muda huu?” “Nimesimama imara Mkuu, hapa nawazungukia kila sehemu ili kujua ni nini kinaendelea, kwani nimewasambaza sehemu zote kuzunguka Studio na maeneo ya Jirani,” “Safi sana, sasa hapo ulipo wewe ondoka muda huuhuu, elekea Ferry, lakini pitia njia hii ya Salender Bridge, maana Yule mwandishi nimepotezana nae,” alipo ongea hivyo Inspekta, moyo wake ukapiga mshindo na kumuuliza amemuona kwani? “Yap! Nimemuona lakini bahati mbaya tumepotezana kabla ya kuingia kwenye Pantoni, yeye alitangulia kabla yangu na mimi nikawa nimechelewa kumfikia hadi Pantoni inaondoka,” “Ok! Sasa tunafanyeje?” aliuliza Jitu kwa mshawasha. “Nenda kwenye barabara hiyo kama nilivyokueleza, kwani kama hana ratiba nyingine itakuwa ni lazima atakuwa anarudi kwake na hivyo ni lazima apite njia hii kwa kuwa anaishi kinondoni,” “Kinondoni ipi anaishi Mkuu?” “OCS wa Kigamboni amenieleza kuwa anaishi Kinondoni lakini hajui ni Kinondoni ipi, suala la msingi ni kumsimamaisha tu yeye pindi ukiiona hiyo RAV 4 nyeupe, ni new model, ina tairi za Sports,” baada ya maelezo hayo tu wakakata simu ili kila mmoja aweze kuwahi majukumu yake. Ilifika Pantoni nyingine na Inspekta akaingia, akiwa ndani ya Pantoni, inspekta Jitu akampigia simu na kumwambia kwamba kuna milio ya risasi imesikika maeneo ya inondoni Makaburini na hilo eneo yeye alikuwa tayari amelipita. “Kwa hiyo sasa Inspekta…” “Mkuu hapa tayari mimi nimeisha geuza, narejea huko kwenye milio hiyo huenda ndio mtu tumtakae,” alijibu Jitu huku akigeuza gari. “Sawa Jitu wewe rudi eneo la tukio haraka, mimi pia nipo njiani kuja hukohuko sasa hivi,” Jitu akapindua gari na kugeuza kwa mwendo wa kasi kuelekea maeneo ya Kinondoni Makaburini. Dakika 10 mbele Jitu akampigia simu Inspekta Kalindimya na kumwambia kuwa yeye yupo Mwananyamala hospitali, afike muda uleule bila kukosa, hakutoa kabisa nafasi ya kuulizwa zaidi akakata simu. Inspekta ambae nae muda huo alikuwa tayari ameisha toka ndani ya Pantoni, akanyoosha moja kwa moja kuelekea huko Hospitali kama alivyotakiwa. Alipita maeneo hayo ya makaburini kuangalia kama kuna chochote totauti, hakuona. Moja kwa moja hadi getini, akaingiza gari na kuipaki pembeni na kushuka, pale jirani na alipopaki yeye aliikuta gari moja ya Polisi aina ya Pick up ikiwa na Streacher, akasimama na kutazama ndani. Alikuwepo dereva peke yake akiwa ameegemea sterling, alionekana amechoka sana, nae hakutaka kumsumbua, maana anaijua kazi yao ilivyo. Alipotazama mbele kidogo akaiona gari ya Jitu ikiwa kwa pembeni kidogo. Huyo ndio mtu aliekuwa akimuhitaji, akaisogelea gari ile na alipoikaribia tu, Jitu aliekuwa mbali kidogo akamsemesha na kumsogelea.
Alipomkaribia akamjulia hali kisha akataka kumueleza yaliyotokea,Inspekta hakutaka kujua yote kwanza, alichotaka kujua ni kwanini wapo pale. “Tupo hapa kwa sababu MwanaMtama Abdul, yupo hapa,” “Mwanamtama?Ndio nani huyo MwanaMtama?” “Ndio huyo Mfanyabiashara ulienipa maelekezo yake,” “Mh! Yupo katika hali gani?Mzima ama amekufa? Hebu nielezee hilo kwanza,” “Ndio maana nilikwambia uje huku ili tulizungumzie jambo hilo kwa kituo,” “Sawa,” akajibu kifupi tu huku wakielekea kwenye gari la Inspekta Kalindimya na kuingia ndani ya gari hiyo. Walipoingia na kufunga milango, Inspekta akaiwasha gari na kuiweka Silence ili waweze kula kipupwe wakati wakiongea, maana ilionekana Inspekta alikuwa na hamu kubwa mno ya kutaka kujua. Jitu akautumia muda huo kumueleza kwa kirefu kabisa Inspekta kilichojiri. Baada ya kuongea nawe pale na kuniamuru nigeuze gari kurejea maeneo ya Kinondoni Makaburini, nakaribia makaburi pale, nikaona kuna kikundi cha watu, sikutaka kuwapita burebure, nikasimama na kushuka kuwafuata, maana hata name nilisikia milio ya risasi. Mara tu baada ya kuwasalimia pale pembeni nilimuona mlinzi mtu ambae nilimtambua kuwa ni mlinzi wa eneo lile kutokana na sare zake za kazi alizovaa, huyo ndio nikamuita pembeni na kumuuliza kuna nini kilichotokea. Mlinzi huyo ambae hakuwa akijua anaongea na nani, akanijibu kuwa mida ile akiwa lindoni kwake, yeye analind pale jirani kuna jengo la vioo kama utakuwa na kumbukumbu nzuri Inspekta,” “Sawa kabisa, linataka kuwa na usawa wa geti la kwanza kutokea mashariki,” “Haswaa! Ndio hapo huyo mlinzi alikuwa akilinda,” “Ok unaweza kuendelea,” alimtaka aendelee, maana tayari eneo alilielewa. “Sawa, basi anasema wakati akiwa anzunguka zunguka akasikia sauti ya risasi kwa nyuma kidogo ya eneo lao, na baada ya sekunde chache ikampita kasi sana gari ndogo aina ya RAV 4 Nyeupe huku nyuma ikifuatiwa na pikipiki aina ya Boxer.” Hapo akanyamaza kidogo na kumeza mate kisha akaendelea “Gari ile ilikwenda na kusimama mbali kidogo na eneo hilo la tukio na kisha wakati yeye akiwa hajajua ni nii afanye mlango ukafunguliwa na aliekuwa ndani ya gari akavutwa chini na aliemvuta ndio akaingia garini na kuondoka na gari hiyo kwa kasi sana,” “Aaaah!Kwa hiyo wewe ukawapigia kwa huko mbele waizuie?” sasa alikuwa ana shauku ya kutaka kujua. “Hapana mkuu, mimi wakati nafika hicho kitendo kimeisha tokea dakika kadhaa ziklizopita, hivyo hapa anakueleza tu maelezo toka kwa Yule mlinzi,” “Dah huyo Mlinzi nae boya kweli, we unaona mtu unaibiwa halafu una bunduki unashindwa kutoa msaada, haina maana sasa ya kuwa ni mlinzi, maana ya kuwa mlinzi ni kumlinda mtu na mali zake,” alijikuta akiongea vitu ahata visivyokuwepo, Jitu akamwambia kuwa asingeweza kufanya hivyo kwani pale yeye alikuwa lindoni na asingeweza kuondoka kwenda kushambulia huko na kuacha lindo likiwa wazi. “Na hivi wanatumia bunduki zenyewe za kizamani, mtu unalinda mali zina thamani ya mabilioni unatumia bunduki ya mwaka 30, inaweka risasi moja tu chemba, pumbavu! Hebu Jitu Endelea hao tuachane nao.” “Umeona eenh? Basi huyo mlinzi akiwa hajui ni ni afanye, ile RAV 4 ikatokomea mbele na kufuatiwa na pikipiki huku Yule mwanamke akiwa amebaki pale chini bila kutikisika, kiasi yeye kwa huko mbali alipokuwa, alijua itakuwa wamemuua. Akamuita mwenzie anaelinda upande wa pili na kumwambia amsaidie kulinda pande zote ili yeye aende akatoe msaada kwa Yule mtu pasina kujua kama yu hai ama ni maiti, basi mwenzie akamruhusu na yeye akaenda mbio, lakini akiwa hatua kadhaa kabla hajamfikia, ikatokea Bajaj na kusimama jirani na Yule mtu ambae sasa Yule Mlinzi aliweza kumuona kuwa ni mwanamke, aliekuwa akivuja damu maeneo mengi ya mwili wake. Akiwa ameshuka Yule dereva wa Bajaj, Mlinzi nae alikuwa sasa amefika, simu ya Yule mtu pale chini ikaita, Yule dereva wa Bajaj akaiokota tena bila hata ya woga na kupokea…” “Yule mlinzi nae anamtazama tu?” aliuliza Inspekta kwa mshangao. “Ndio, sasa unafikiri Inspekta masomo yetu sisi na wao yanalingana? Yaani ingewezekana tungeyafuta kabisa mambo haya ya walinzi wa…” kabla hajamaliza, simu yake ikaita, akamuomba samahani mkuu wake wa kazi ili apokee, nae akamuitikia kwa kichwa kukubali, Jitu akaipokea na baada ya mzungumzaji kuongea maneno machache, Jitu akasema “Ok! Tunakuja sasa hivi, maana wala hatupo mbali!” alipokata tu simu, akamwambia mkuu wake wa kazi kuwa huyo aliepiga ni daktari na anahitaji kuwaona, tena muda huohuo. “Kwa hiyo story yetu ndio imeishia hapo kwa sasa, acha tukamsikilize kwanza daktari, huenda kukawa na la maana zaidi ya hayo tuyajuayo,” aliongezea Inspekta na kutoka garini, huku Jitu akifuatia, wakafunga na kuelekea mbele zilipo ofisi za daktari. Waliwasili na kukuta mle ndani kuna mtu mwingine akiwa na majonzi, daktari aliwakaribisha na kumuomba Yule mtu awapishe kidogo, akatoka na kuwaacha wao wakikaa.
Daktari aliwakaribisha na kuanza kuwapa maelezo, hakuhitaji kufahamishana, maana wamekuwa wakionana mara kwa mara. Katika maelezo aliyowapa, aliwaambia kuwa baada ya uchunguzi wa awali, kuna kitu amegundua. Wameona kupitia vifaa vyao ikiwepo CT Scan kwamba Mfupa wa bega umevunjika na hivyo atahitaji operesheni kubwa zaidi ambayo inaweza kufanyika hospitali kubwa zaidi ya ile ya kwao. “Hivyo tangu sasa ninamuandikia barua ya rufaa na dakika chache zijazo tutamuondoa hapa kumpeleka Muhimbili,” alimaliza maelezo yake ambayo yalikuwa ni mafupi tu na hakukuwa na maoni zaidi ya kukubaliana na maamuzi ya daktari. Inspekta Kalindimya na Jitu wakatoka nje ikiwa ni saa tano usiku, Inspekta akamwambia Jitu afanye mpango wa kupeleka ulinzi sehemu atakayokuwepo mgonjwa wao. Wakaagana kila mmoja akiwa ameingia kwenye gari yake kwa ahadi ya kukutana siku ifuatayo, hawakukumbuka tena kumalizia story yao. **********
Siku ya pili asubuhi, wakati Inspekta akiwa amefika ofisini kwake, akamkuta tayari Jitu akiwa amewasili, lakini alikuwa nje ya ofisi akiongea na simu, Inspekta akamfuata hukohuko alipokuwa na kusimama mbali nae kidogo. Alipomaliza kuongea na simu, kila mmoja akafuata mwenzie huku wakiwa na shauku ya kukutana, wakasimama penuni mwa ukuta wa jengo la Polisi na kuanza kuongea mawili matatu. Wakiwa wanapiga soga, kuna kitu Jitu alitaka kukisema, lakini alipotaka tu kukitamka simu ya Inspekta Kalindimya ikaita, namba aliitazama na kuijua kuwa ni katika namba zilezile za usumbufu, akaipokea na kuweka ‘Loud Speaker’ ili Jitu nae asikie kinacho zungumzwa. “Hellow Inspekta,” sauti tayari waliijua kwani muonekano tu wa zile namba, ilikuwa ikijulisha kabisa kuwa ni mtu yuleyule anaepiga tena. “Sema,” alijibu kifupi huku akirekodi mazungumzo hayo “Kama nilivyokueleza jana mapema, mimi binafsi Sikuwa na mpango wa kumhuru MwanaMtama, lakini kiherehere chake kikamponza, na ana bahati sana kwamba alipata dhamana kwa niliekuwa nae, lah sivyo nae ningempoteza tu Yule kuku wa mayai,” aliongea kwa sauti ya kujiamini sana, Jitu akamuuliza kwa hiyo anasemaje “Nimekupigia simu kukujulisha kuwa hii sasa ni last Warning, onyo la mwisho, achana na kesi yangu hii, wewe huiwezi, hata DCI anaweza kuishindwa kesi hii ikimfikia, achana nayo haraka nimesema,” alitoa sauti ya kuamrisha, Inspekta akacheka kwa dharau na kusema “Yaani hicho ndio kimekufanya unipigie simu?” “Ndi Inspekta lakini nafanya hivi leo kwa faida ya MwanaJuma,” simu ikakatwa hapohapo na kuwaacha maafande wakiwa hawajui cha kufanya, hasa Inspekta Kalindimya ambae alionekana kama amechanganywa ghafla na maneno hayo. Wakaanza kutafakari, Jitu akamuuliza mwenzie huyo MwanaJuma ni nani? “Hata namjua basi Jitu?Simjui huyo mtu ni nani!” “Sasa kwanini atishie kwa mtu usiemjua?” “Hapo sasa name ndio ninaposhangaa, yaani hii kazi hadi ikaishe, tunapaswa kuchukua na likizo dah!” alijibu Inspekta na Jitu akamwambia mwenzie waende ofisini na kukaa kujadili. Vichwa viliwauma wote, Inspekta alichukua File la kesi ile na kuanza kulipitia upya huku Jitu akiwa ameshika visu vilivyopatikana kwenye mauaji na kulinganisha alama za vidole yaani Finger prints toka kwenye Computer iliokuwepo kwenye ofisi yao. “Ujue muuaji ni mmoja tu Inspekta, na hata sipati pisha kwanini alikishika kisu vibaya kabla ya kuvaa gloves,” “Inaonekana vipi kwani?” “Njoo uone na tujadili hapa, huenda tukaokoteza kitu hapa cha maana,” alijibu Inspekta huku akikunja file lake na kumsogelea mwenzie. Aliona nae alama za vidole zilionekana chini kwenye mpini huku sehemu ya juu ikiwa haionekani kwani gloves ilificha muonekano wake. “Sidhani kama kuna cha kutusaidia hapo, ila tu mimi nina swali moja kwako, hivi kwa MwanaMtama napo kilikutwa kisu?” “Hapana mkuu huko hapakuwa na kisu, lakini unakumbuka nilikueleza kwamba gari yake nayo ile RAV 4 nayo ilitekwa?” “Yap nakumbuka vema, ehee nayo vipi?”jana usiku nilipigiwa simu na kujulishwa na askari ambao niliwaweka kumlinda MwanaMtama kuwa wameletewa funguo na mtu akisema jina lake ni Loren alikuwa ameazima gari yako na amesema ikifika tu nipewe mimi,” alitoa maelezo marefu Inspekta. “He!mbona sijakuelewa? Yaani mtu kaleta funguo ya gari yangu halafu upewe wewe?” “Na ndio kilichofanyika hicho, nikapewa hiyo funguo leo asubuhi, lakini mimi sikuamini kama kuna mtu ulimuachia gari na alete kwangu,” “Dah huyu mtu sijui ananitakia nini?Kwa hiyo umegundua nini kupitia funguo hiyo?” “Ajabu sasa baada ya kuingia ndani tu kumuona MwanaMeka, hakuwa kwenye hali nzuri ya mahojiano lakini nikataka tu kumsalimu kwanza, niliingia nikiwa bado nina funguo ile mkononi, Mwana alipoiona tu kwa sauti ndogo akasema ile ni funguo ya gari yake,” “Duh! kama movie vile, ikawaje?” nikamwambia atulie kwanza hali ikiwa vizuri tutampa funguo yake, kisha nikakaa kwa sekunde kadhaa nikatoka,” Alimaliza huku akimwambia akaja ofisini na ndio walipokutana nje nae akiwa amefika.
“Sasa hiyo gari yenyewe ipo wapi?” aliuliza kwa msisitizo “Ndio pale nilitaka kukueleza ila ukapigiwa simu, hiyo gari nimepigiwa simu imeonekana maeneo ya Mwana Nyamala Kisiwani, na muda huu hapa itakuwa imeisha anza kuvutwa na Clain kuletwa hapa,” “Ok! Umeagiza iletwe hapa au ipelekwe kule Kilwa Road?” alihoji Inspekta. “Hapana nimewaambia wailete tu huku ili tuweze kufanya uchunguzi kwa uhuru zaidi,” alijibu Inspekta huku akichukua simu yake na kumwambia Inspekta kuwa anampigia simu afande aliempa kazi hiyo. “Ndio, mmefika wapi?” aliuliza na kisha akashangaa “Ha! Sasa mimi ningeotaje? Mbona hukunijulisha mapema?” “Sawa tunakuja!” akakata simu na kumwambia mkuu wake kuwa vijana wameisha fika kitambo sana ila walikuwa hawajawajulisha kama wapo nje tayari. “Ohoo!Kwa hiyo wapo nje na gari yenyewe?” aliendelea kuuliza Inspekta. “Ndio, na ninaona twende tuakaione,” akajibu Jitu huku akitoka nje kuelekea huko ilipo gari. Waliikuta gari ileile ambayo Inspekta aliiona kwa mara ya kwanza huko Kigamboni na kumwambia Jitu kuwa ni gari hiyo aliyokuwa ameihisi. Jitu akatoa funguo kimya kimya na kufungua mlango, kupitia mlango huohuo mmoja wote wakasimama na kuangalia ndani kuona kama kuna lolote ambalo wanaweza kuliona. “Inspekta Jitu, huyo aliefanya ukaguzi wa awali, yupo wapi?” Jitu akageuka nyuma na kumuita askari mmoja alliekuwa amesimam na karatasi mkononi na aliposogea tu akamuuliza vipi? Mbona hajawapa amaeekezo yoyote ya huko walipotoka?Akadai kuwa alikuwa akisubiri waangalie kidogo. “Ok! Hebu tueleze huko imekuwaje?” aliamua tu Inspekta kuyafupisha maana ilikuwa inataka kuwa ni habari ndefu na lawama , ndio akaamua kufupisha kwa kumuuliza walichokiona huko. Nae hakutaka tena kuhangaika, bali alichukua jalada alilo lifungua na kumkabidhi afande Jitu ambae alilifunua kidogo huku Inspekta akizidi kulizunguka lile gari kwa ajili ya ukaguzi. Alipomaliza tu kuizunguka akamrudia Jitu na kumwambia vipi kuna jipya gani? Akamwambia kwamba amegundua kwamba kua namba imeonekana mle kwenye kisu pia na kimeambanishwa mlemle pia. Inspekta akamwambia waende ofisini wakaketi chini kwa utulivu ili wapiti vizuri, hapo tayari walikuwa wame hemkwa vibaya kutokana na kuonekana mle kuna mambo nyeti. Wakaelekea moja kwa moja ofisinikwao na kuingia kwenye meza ya Inspekta ndio wakaketi na kuanza kulisoma lile faili, Inspekta akiwa ameketi na Jitu amesimama kwa pembeni yake wakisoma na kujadiliana. “Umeona kuwa muhusika ni yuleyule tu?” “Hilo linajulikana Jitu, sasa hebu tujaribu kuangalia kitu kipya, muite Yule kijana umuulize kama alikumbuka kuchukua alama za vidole kwenye sterling ya gari,” “Dah! Kweli, ndio maana ukawa ni Inspekta, nimekubali mkuu, sikuweza kufikiri hata sekunde 0 juu ya jambo hilo,” akajibu huku akitoa simu na kumpigia afande huyo ambae aliitika na kusema anakuja muda ule ule. Alipofika tu wakaanza kumshambulia na maswali mfululizo huku akijitahidi kuyajibu kwa uthibitisho na hata kwenye swali lile la kuchukua alama za vidole. “Ndio mkuu, wakati unanipigia simu nikakumbuka kuwaita watu wa alama za vidole na waliahidi hadi kufikia mchana huu watakuwa wamekamilisha uchunguzi,” alijibu akiwa amekakamaa, wakamruhusu aende kuendelea na majukumu mengine. “Angalia kitu hiki afande Jitu,” Inspekta akamwambia mwenzie huku akimuonesha kwa kidole sehemu ya maelezo yaliyo andikwa na Yule askari walie mruhusu aondoke, ile sehemu iliandikwa kuwa Kuna namba imekutwa kwenye kisu chenye mpini wa rangi na namba hiyo inasomeka kama 68262. Walizamisha akili na macho yao hapo kwenye namba hiyo kwa takriban dakika kadhaa, lakini kile kilikuwa ni kizungumkuti, suala la namba kwao kilikuwa ni kama mtihani. Hawakuweza kulifumbua fumbo hilo, lakini kidogo Inspekta aliweza kugundua kitu, kitu chenyewe ni kwamba walio uawa wote ni kina Mwana na katika matukio yote matatu yaliyo tokea ya mauaji na kutekwa, yamewahusisha kina Mwana. “Na halafu, miiili yote ya waliouawa, yaani kina Mwana wawili, namba zao za mwishozote zimeishia na 74, Sijui muuaji ana maanisha nini!” alihoji huku akimtazama Jitu. “Halafu matukio mengi anayafanyia Mwana Nyamala,” aliongeza Inspekta. “Duh! Hilo ni fumbo afande,” aliongea Jitu akistaajabu utundu na umahiri wa mkuu wake wa kazi wa kufuatilia vitu ambavyo yeye aliviona kama ni vidogo vidogo sana. “Kweli hilo ni fumbo, tena zito sana lakini ni sisi ndio tunaopaswa kulifumbua, tunafanyeje sasa?” Jitu tayari alikuwa ameanza kuondoka pale alipokuwa amesimama awali na kwenda maeneo ya dirishani kuangalia mandhari ya nje. Swali lile likambadili mwelekeo na kujikuta akigeuka na kumwambia mkuu wake kwamba, waende chumba cha uchunguzi wa alama za vidole ili kuchukua majibu, huenda yatawapa mwanga. Wakatoka kwa kuongozana moja kwa moja hadi ghorofa ya pili ndio ilipo ofisi hiyo, walikuta majibu yapo tayari. Alie yapokea ni Inspekta, akayatazama na kuguna, kisha akamuangalia Jitu, wakakutanisha macho…
Jitu akahoji vipi? Inspekta badala ya kumjibu swali lake, akamwambia “Jitu, umeisha kula mchana?” akiwa na mshangao akajibu “Mkuu, umesahau kuwa tumekutana hapa tangu saa mbili asubuhi na hatujaachana? Mimi hata chai bado sijanywa,” “Oh! Nilisahau, ujue nini? Tunaweza hata kufa kwa njaa, hebu twende kwanza nje tukatafute chakula, unaweza kujikuta umeanguka ghafla, dah! Hizi kazi hizi ni za kuzeeka kabla ya wakati,” alijibu huku akimpa karatasi kadhaa ambazo zilikuwa na majibu ya alama za vidole. “Watu wanakuwahisha hospitali kwa kujua kwamba huenda ikawa unaumwa, kumbe tatizo ni njaa,” wakacheka huku Jitu akiperuzi peruzi zile karatasi na kushuka ngazi taratibu. Wakatoka hadi kwenye kantini ya Jeshi la Polisi na kuagiza chakula, walikula kimya kimya tena kwa haraka kutokana na njaa kali ambayo ilikuwa imewanyemelea kwa kasi na walipomaliza kula tu wakatoka kurejea ofisini. Hapo ndio nafasi yao nyingine kwa wao kujadili juu ya ripoti toka uchunguzi wa awali, walipoifunua karatasi ile, walichoka kabisa maana ilionekana kwenye usukani kuna alama za mtu ambae kwao ni ngeni kabisa, ila kwenye upande mmoja wa gari, upande wa dereva, waliona alama ambazo hazikusomeka, maana zilifichwa na Gloves. Unaona kwamba muuaji anajua ni kipi anachofanya, kuna wakati unakuwa unahisi kabisa kuwa siku chache mbele kutokana na makosa yake madogo madogo afanyayo, tutamtia nguvuni, lakini anayafuta kabla ya kumtia nguvuni,” Inspekta Kalindimya aliweka wazi hisia zake. Hadi muda wa kazi unaisha, hakuna walicho ambulia zaidi ya kupiga soga tu na ilipofika saa 11 kamili jioni wakatoka wakiamini wanaenda kupumzisha akili kwani walikuwa wamechoka mno. ********** Usiku ulikuwa ni mrefu mno kwa Inspekta Kalindimya hasa akikumbuka tishio la mauaji toka kwa mtu huyo ambae alimtaka kuachana na kesi ile haraka iwezekanavyo. Akajiuliza ni kwanini muuaji amwambie hivyo? Ina maana kuwa yeye amefikia hatua ya mbali sana kuliko wengine ambao wamechunguza hizo anazo ziita ni kesi zake? Akakosa jibu na kunyanyuka kwenda kwenye meza yake ya kazi. Kwenye meza hiyo pindi anapokaa basi huwa yupo busy tu na kazi, wakati mwingine hata husahau kula na hata usingizi huwa unampitia akiwa ameketi hapo, suala la msingi kwake ni chai tu… Sasa ndio akaenda hapo kuketi kwa mara nyingine, ikiwa ni saa saba usiku akatoa zile namba na kuanza kuzifanyia kazi. Safari hii alibadili njia ya kuziangalia, akachukua zile namba na zigawa kwenye herufi. Alianza kwa kuzipa namba kwanza, hivyo ndivyo akili yake ilivyo mtuma, akaanza na A akiipa moja B ikiwa ni mbili hadi alipofika Z ambayo ilikuwa ni namba 30. Bado hakupata matunda yoyote yale, maana kuna namba zingine zilijichanganya, akaona hapo bado amefeli, akaacha na kunyanyuka, akili yake ikamtuma kwenda Mwana Nyamala kisiwani, sehemu ambayo ilionekana gari ya MwanaMtama. Akanyanyuka na kuelekea chumbani kwake, huko akafungua draw ya kabati yake ya kitandani na kuchukua kitu Fulani ambacho alikuwa akikihitaji muda ule, kisha akatoka na kufunga mlango wake vizuri, maana wale askari wa ulinzi aliokuwa amepewa awali tayari waliisha amriwa warejee kituoni kwao na waendelee na amjukumu mengine haraka. Alipohakikisha kuwa amefunga vizuri mlango wa nyumba yake, akaelekea hadi garini kwake na kuingia kuelekea huko alipo panga kwenda usiku huo. Kwa mwendo wa taratibu tu akatoka na kuelekea Mwananyamala akiwa peke yake njiani, barabara ilikuwa imetulia sana, aliwasili ile sehemu ambayo alisoma kama ni sehemu ambayo gari lilitelekezwa. Akashuka akiwa makini, maana ilikuwa ni sehemu ya hatari ikionesha dhahiri kuwa na vibaka na hata mateja pia, hivyo kwa tahadhari kubwa akateremka na kusimama nje ya gari lake. Kwa mbali aliweza kuona kundi la vijana ambao moja kwa moja akajua hao ni wezi tu wametoka kuiba na sasa wanagawana aidha wanaficha. Akaondoka kwa tahadhari akiwa na silaha yake mkononi akisogea kule walipo huku akijificha kwenye vichaka vilivyokuwepo pale. Aliweza kuwasogelea na kuwakaribia kabisa, kisha akawaweka chini ya Ulinzi, walikuwa ni vijana watatu tu kumbe, tofauti na alivyo kuwa akiona kwa mbali kuwa ni wengi sana. Akiwa amewaelekezea bastola yake aina ya Revolver 09/80 yenye uwezo wa kubeba risasi 12 kwa wakati mmoja, vijana wakatulia, hasa kutokana na mkwara aliokuwa akiwapiga. “Tulieni hivyohivyo, ujanja wowote au kujidai kujua kutasababisha kupoteza maisha ya Yule ambae atajidai kujua,” akawa anatoa simu na kupiga kituoni kuomba msaada wa gari la Polisi. Alipomaliza tu akawaambia walale chini vile vile walivyo, wawili wakalala bila hata vurugu, ila mmoja wao akajidai yeye ni mjuzi sana, akawa kama anataka kulala vile, akamrukia Inspekta ili kumpora bastola yake. Kumbe tangu anajiandaa kufanya shambulizi tayari mwenzie amemuona na amejitayarishaili aweze kumdhibiti, kijana akajirusha mzima mzima pale alipo Inspekta…
Kile kitendo cha yeye kujirusha tu akakutana na teke kali mno la tumbo na alipotua chini tu akamzima na mguu sehemu za kiuno. Ilitosha kabisa kumnyamazisha na kumkata ngebe zake, maana alitoa ukelele wa ajabu wa kuugulia maumivu huku akilia anakufa. Bastola yake Inspekta bado ilikuwa imewaelekea wale vijana waliokuwa pale chini. Akawaamuru wenye we wajifunge mashati yao, walikuwa ni dhaifu, tayari dawa za kulevya zilikuwa zime waathiri kwa kiasi kikubwa mno hawa wawili, ila Yule aliempiga, kidogo ndio alionekana kuwa na afadhali. Walijifunga hayo ma Tshirt waliyokuwa wamevaa huku Yule mwingine akiwa analalamika kuwaa ameumia, na baada ya muda sio mrefu sana, gari ya Polisi aliyokuwa ameiomba ikafika, haikuwa mbali sana, akawakabidhi watu wale. “Hawa wasitolewe na yeyote bila kuwasiliana name hiyo kesho asubuhi, mkuu akiuliza mwambieni kuwa ni nyeti, nitamtafuta mimi, sawa kuruti?” alimuuliza mmoja wa askari ambae alijibu sawa mkuu. Wakawaingiza kwenye Pick Up ile ya Polisi na kuanza kuondoka huku Inspekta nae akiingia garini mwake tayari kurejea kwake. Lakini akiwa anakaribia maeneo ya Mwana nyamala A, akakumbuka kitu, akakata kona ya ghafla na kuelekea kilipo kibanda cha simu, akashuka na kuchkua Camera maalum aiyopewa na mmoja wa wataalamu wa IT kutoka ofisini kwake. Hiyo alipopewa ndio akaja kuiweka nyumbani kwanza akisubiri muda kama huu ufike ili aweze kufanya hilo ambalo analifanya sasa. Aliposhuka na kwanza akakagua kama kuna mtu yeyote ambae anaweza kuwa anamtazama. Aliporidhika tu akaingia haraka, akaifungua simu iliokuwa mbela yake pale, alikuwa ameelekezwa kuwa afungue pale na kuifunga ndani ya Cover bila kujali kama itaonekena ama lah! Nae akafanya kama alivyoa amriwa kisha akategesha ware aliopewa sambamba na Camera ile na baada ya kumaliza kazi yake akaondoka ikiwa ni saa 10 ya alfajiri na kuelekea hospitali. Pale hakusumbuka kabisa, ilimchukua dakika chache zaidi na alipomaliza tu akaondoka na kwenda kumalizia ile ya mwisho iliopo maeneo ya Studio kisha akaelekea nyumbani kwake moja kwa moja. Nyumbani kwake, saa 11 alfajiri akiwa bado yupo nje hata hajaingia ndani, akahisi kuna mabadiliko, wakati akitoka alikuwa amezima taa, lakini sasa amerudi na kukuta taa zinawaka na hali hakuiacha katika hali hiyo. Kengele ikalia kichwani mwake, kwa tahadhari kubwa mno akateremka garini na hata kabla hajaufunga mlango wa gari, taa za nyumba nzima zikazimika kwa ghafla na kumfanya atetemeke na kujitupa chini ya gari na bastola yake mkononi. Taratibu akaanza kujivuta chini kwenye majani madogo madogo maarufu kwa jina la Ukoka huku akijielekeza nyuma ya nyumba yake ambapo alitegemea kuweza kujua ni nini kinaendelea. Kutokana na kuielewa vizuri nyumba yake, aliweza kuizunguka nyumba nzima na lakini hakuona tatizo lolote kwa nje, sasa akalazimika kujua kwa ndani napo kupo kwenye hali gani. Ndio sasa akaanza kuchungulia madirishani, aliporidhia ni salama, akaelekea mlango mkubwa wa mbele na kugusa kitasa cha mlango, ajabu akakuta upo wazi na hali aliufunga. Akarudi nyuma hatua kadhaa na kuingia kwa kasi huku akibiringita silaha mkononi. Ndani hakukuwa na mtu yeyote, bali juu ya Computer yake akakuta kisu chenye mpini wa rangi ya Pinki kikiwa na ujumbe mdogo kwenye karatasi. Ncha ya kisu ilikuwa imechoma karatasi kwenye ‘key board’ akawasha taa na kuikagua nyumba yake nzima kwa ndani, bahati mzuri kila sehemu mle ndani ilikuwa salama. Mwisho akarejea sitting room na kuelekea moja kwa moja hadi pale kilipo kisu na kukichomoa kwenye keyboard, akaichukua ile karatasi na kuanza kuusoma ujumbe ulio andikwa. Ujumbe ulikuwa sio mrefu sana na ulisomeka ‘Imebaki siku moja tu kwa ajili ya usalama wa MwanaJuma, ambae sina nia ya kumuua, ila ikinibidi nitafanya hivyo ikiwa tu nae hatokukufukuzisha kazi, kwani lengo langu ni wewe kuachana name, kwa hiari kabla ya kulazimishwa kurudi mitaani kuzurura,’ ilimaliza hiyo barua bila kuweka kingine chochote cha ziada. Roho ikapiga mshindo, Pah! Huyu MwanaJuma ni nani? Na ni kivipi anaweza kunifukuzisha kazi? Ina maana huyo mtuhumiwa ananijua sana mimi ama? Maswali yalikuwa ni mengi mnoakakoa majibu na kushusha pumzi kwa nguvu huku akiketi kwenye kiti kivivu. Alitamani iwe ni muda wa kazi ili atoke tu kwenda kazini kufanya mahojiano na wale vijana aliowakamata asubuhi ile, lakini muda ule wa saa 12 ilikuwa niu mapema sana kwa yeye kwenda kazini. Hivyo alicho amua kuwa ni heri tu aende akaoge na kujiandaa kwenda zake kazini. Akiwa ameshika tu mikono ya kochi lake, simu ikaita, ilikuwa ni simu yake ya mezani, ambayo ni nadra sana kuita. Akashtuka sana kwa wito ule, aliiangalia kama ndio mara ya kwanza kuiona, akaendelea kuitazama ahadi aliposhtuka kuwa ile ni simu imepigwa na inahitajika kupokelewa. Akaichukua na kuiweka sikioni.
“Inspekta, pole sana kwa kuhangaika usiku huu, napiga simu kutoka hapa A kwenye kile kibanda ulichotegesha Camera, umesahau kuwa mimi nipo kama upepo, kila sehemu wewe ulipo, tambua sasa kwamba mimindio nasaidia wewe kufika hapo, nakushauri njoo uziondoe zote tatu, maana hakuna msaada kwako kwa kupitia hizo,” halafu akacheka, Inspekta Kalindimya akamuuliza kwa taratibu tu “Umemaliza?” “Bado sana, ila cha mwisho ni kuwa leo ndio siku yako ya mwisho ya kuamua kuacha kazi kwa hiari yako, chagua tu moja…” akakata simu bila kumwambia achague nini. Alijaribu kuita Hallow… Hallow… Lakini bado wala haikupokelewa, kwani tayari ilikuwa imeisha katika. Japo kulikuwa na hali ya ubaridi, lakini jasho jembamba lilimtoka, akawa ni kama mtu ambae hajielewi elewi, akampigia simu Jitu na kumtaka ampitie wakati akitoka kuelekea kazini. ********** Saa moja asubuhi Jitu aliwasili nyumbani kwa Inspekta na kumkuta akiwa ameketi amatazama taarifa ya habari kupitia Televisheni ya Taifa. Hakuwa na jambo la muhimu sana kutazama bali alikuwa akivuta muda tu wa kumsubiri Jitu. Hivyo alivyofika tu Jitu na ratiba ya kuangalia TV ikawa imekufa rasmi na sasa alimkarimu na kumuonesha sehemu ya kukaa huku nae akijitengeneza vizuri. Akamuuliza kuhusu familia yake huko nyumbani alipotoka nae akamjibu ni njema tu. Sasa ndio akamueleza sababu ya kumuambia apite pale. Jitu alishangaa sana na kumuuliza kuwa wakati anatoka pale kuelekea kwenye hizo Call boxes alimueleza nani? Inspekta akamwambia kwamba hakumueleza yeyote hasa ukizingatia ilikuwa ni usiku mnene. “Isingewezekana kabisa kumwambia yeyote, maana usiku ulikuwa ni mkubwa san,” alisisitiza zaidi Inspekta Kalindimya. Sawa Boss, hapo nami sasa nimehakikisha kuwa kila hatua yako unayofanya hao watu wanaifuatilia, na nina hakika wamefanya hivyo ili tu kukujulisha kwamba kila hatua yako unayopiga,” “Of Coz, hiyo ni kweli! kama wangekuwa wananifuatilia ili wanidhuru nafikiri wangefanya hivyo maana inaonesha kabisa kwamba walikuwa na uwezo huo,” Inspekta alikubaliana na kauli ya Jitu ambae alikandamiza kwa swali “Sawa, tunafanyeje sasa?” huku akiegamia sofa akamtazama boss wake. “Jitu hiyo ndio sababu upo hapa, nimekuita ili tujipanfe tunafanya nini hata kabla hatujafika ofisini,” alieleza kiurefu. “Lakini si umesema kuwa kuna watu umewakamata mkuu?” aliuliza Jitu na Inspekta akakiri kuwa ni kweli na muda ule wapo kituoni. “Sasa ndio twende kwa hao watu ili tukawahoji huenda tukajua ni kipi kinaweza kutusukuma mbele,” “Wazo zuri sana Jitu, ngoja nifunge milango twende hukohuko,” akasimam na kwenda kufunga milango yote ya ndani kisha alipofika pale Sitting room akamkuta na Jitu ameisha simama nazima TV kisha wakatoka kwa pamoja na kisha Inspekta akafunga na huo mlango mkubwa na kutoka sambamba na Jitu. Walienda kazini kwa kutumia gari ya Jitu na garini walikuwa kimya wakitafakari hayo yanayotokea. Kila mmoja alikuwa na mawazo yake. Hakuna lililokuwa likimuumiza kichwakaa suala la huyo MwanaJuma ni nani ambae amekuwa akitumika kama nguzo. Hakuna kati yao hata mmoja aliekuwa akimjua huyo MwanaJuma, hawakuongea hadi walipowasili kituoni na bado walikuwa kimya wakielekea ofisini kwao. waliwasili ndani na kuketi kamawatu walio ambiana. Inspekta akanyanyua simu na kutoa maagizo ya kupelekwa kwake mara moja wale watuhumiwa aliowakamata usiku uliopita. baada ya kukata simu ile dakika mbili tu mbele wakaletwa vijana watatu wakiwa wameongozana. Jambo la kwanza alilolifanya ni kuomba na faili lao ambalo alilisoma na kumtupia Jitu nae akaliperuzi kwa sekunde chache na kulifunika. Inspekta akaanza kuwahoji na mwanzo walionesha kugoma kutoa ushirikiano wa kutosha lakini baada ya vitisho waliweza kufunguka. Walisema pale wao ni wafanyakazi tu na mida ile ndio hupata muda wa kufanya kazi zao na ndio kama vile walichomoka na kwenda kujitafutia chochote na waliporudi na chochote yeye sasa ndio akawakamata. Jitu akataka kujua bosi wao ni nani? wakakataa katakata kutaja na hapo Jitu akapandwa na jazba, akachukua Office pin moja Sisi tumezoea kuita Sindano urungu na kumsogelea mmoja akamuuliza atamtaja bosi wao wa kazi ama lah! Yule teja akakataa kuwa hamtaji, Jitu akasema yeye hupenda sana kukutana na watu wabishi kama huyo. akamwambia aweke mkono mmoja kwenye meza teja akaweka na ule mwingine Jitu akaukanyaga kwa mguu wake palepale kwenye kiti alichokaa na kkushika ule mkono ulioko mezani kwa mikono miwili, kisha akasema…
“Hivi ndio tunaanza, na ikizidi kunisumbua name nitaongeza adhabu,” akaichukua ile sindano na kuanza kuiingiza chini ya kucha, teja alipiga kelele za ajabu mno, Jitu akaendelea kuisukuma taratibu huku akimtazama usoni. Inspekta akamshika Jitu beaga na kumwambia asubiri sasa atasema, nae Jitu akamuuliza kama yupo tayari kusema, Teja akajibu kwa pupa kuwa atasema huku chozi likimtoka. “Haya sasa hebu tuambie, ni nani bosi wenu?” Inspekta ndie alieuliza swali. “Afande mkuu wetu anaitwa Jembe,” “Anaishi wapi Jembe?” “Sinza,” “Sinza ile ni kubwa sana, yeye anaishi Sinza sehemu gani?” “Afande hatujui wote anapoishi, kwanza tu huwa hapendi kuulizwa ulizwa maswali, akihisi tu unamchimba anaweza hata kukupoteza,” sasa walielewa kuwa anasema kweli, hapo ndio Jitu akamuachia. “Kumbe kiustaarabu hauendi wewe hadi kiuwenda wazimu ndio unatoa ushirikiano, pumbavu wewe,” Jitu akasonya baada ya kusema maneno hayo. “Tofauti na hii kazi Jembe anafanya kazi gani?” “Kiukweli afande mimi Sijui, yaani hapo nilivyoeleza mimi ndio nimejua hadi hapo,” “We usilete nyodo kwenye maswali ya msingi, sasa nitakubadilishia adhabu na kukupa kubwa zaidi, tueleze kazi nyingine anayofanya ama aliyowahi kuifanya hapo kabla,” Jitu aliingilia kati. “Kweli afande, mimi nimemjua Jitu wakati ametoroka gerezani na akafika maghetto pale kuomba hifadhi ndio hadi leo japo baadae alianza kazi za binafsi na ndio zikamtoa hadi sasa yeye ndio amekuwa mkuu wa kundi zima,” “Kazi gani binafsi anafanya?” “Anasafiri sana kwenda huko na kule kucheza madeal,” “Wewe umewahi kucheza nae deal lolote hivi karibuni?” “Hapana afande mimi sijawahi,” “Wewe hebu sema kweli, nitamuamuru Jitu akushughulikie sasa hivi,” alisema Inspekta Kalindimya na Teja alipomtazama Jitu akamkuta kakunja ndita kwenye sura yake, akarudisha macho yake kwa Inspekta na kumwambia yeye huwa anaachwa kwenye deal kwani ni dhaifu huwa wanakwenda na Dega. “Dega ndio nani?” Jitu alihoji. “Ni Yule alietaka kupigana nawe,” hapo akajibu huku akimtazama Inspekta japo swali aliulizwa na Jitu. Inspekta akageuka nyuma na kumuonesha Jitu huyo Dega, Jitu akapiga hatua kadhaa kuelekea kule alipo na kurudi nae baada ya kumfuata. Alipomfikisha tu mbele ya Inspekta, akawa mpole. “Dega, nataka ujibu maswali yangu kama nitakavyo kuliza, ole wako unizungushe ama ukwepe kujibu vile nitakavyo mie, nitakutonesha maksudi,” Inspekta alimwambia hivyo. “Afande naomba mnipeleke hospitali, mkono unaniuma sana,” alisema kwa majonzi huku akijikunja kunja kwa maumivu, Inspekta akamwambia kuwa amefanya vile maksudi ili atakapofika yeye kwa ajili ya mahojiano, basi asimsumbue “Yaani ukinisumbua tu ujue nagusa mkono tu huo mie, sawa?” “Nitakuambia ukweli mtupu, ila nakusihi nipeleke hospitali afande, naumia mno,” machozi yalikuwa wamemtoka mpaka basi, mkono nao ulikuwa umevimba, lakini hakupelekwa hospitali kwa amri ya Inspekta. “Sawa, nitakupeleka, tena ni mimi mwenyewe, kwanza niambie Jembe ni nani na yupo wapi?” “Jembe ndio mkuu wetu wa kazi anaishi Sinza, ila hakuna anaepajua ni wapi, mimi nimekujibu, Afande nipeleke hospitali,” aliendelea kuomba. “Bado hujanijibu, yupo wapi mkuu wenu?” “Sijui alipo kwa sasa!” “Kwa mara ya mwisho ulicheza nae deal lini na wapi?” “Juzi alikuja anaendesha gari Fulani hivi akanipa nijifunzie ndio nikaendesha endesha hadi ilipoishiwa mafuta nikaiacha pale kijiweni, nikafuata mafuta, kumbe ilikuwa imeibwa,” “Ulikuwa umelewa eti?” “Ndio afande!” alijibu kiufupi huku akigugumia kwa maumivu. “Nilijua tu katika mazingira ya kawaida utaendeshaje gari uliyoletewa na mwizi na kujiendeshea tu wakati hujawahi kumuona hata siku moja? Sasa ndio nieleze, hiyo gari ni ipi na alimuibia nani?” “Inspekta mimi Sijui ni wapi na ni nani alimuibia, aliniletea tu, nisaidie afande, mimi Sijui tena zaidid ya hapo,” alijitetea Dega. “Wewe ulikutana na DEga wapi hadi mkaunda hilo kundi?” “Tulikutana nae gerezani, mi wakati naingia yeye anatoka kisha akarudishwa tena na kunikuta, mimi nikatoka na kumuacha kisha tukaja kukutana miaka mitatu iliopita akiwa yupo tu mtaani ndio nikamkaribisha maskani,” “Alifungwa gereza gani?” “Ilikuwa Keko wakati tulipokutana mimi nae kwa mara ya kwanza,” “Mwaka gani huo ilikuwa?” Jitu ndie alihoji hapo. “Miaka mitatu iliopita afande,” “Alikuwa akitumia jina gani?” “Dah! Hata silikumbuki kwa sababu hata kule alikuwa akitumia jina hili hili la Dega, kwa hiyo jina lake lilikuwa likitajwa hakuna alie shughulishwa nalo,” “Namba gani ulitumia ukiwa huko?” Mimi nilikuwa nikitumia namba 427010” Walimuelewa na kisha wao wenyewe wakajadiliana, wakaamua sasa atolewe na kupelekwa hospitali, kwani msaada huo alioutoa umekuwa ni mkubwa sana kwao. Wakamuita askari mmoja wa zamu na kumpa maelekezo, kisha nao wakaamua waende magereza ya Keko kwa ajili ya uchunguzi wa mtu huyo na kwa hatua zaidi. “Inspekta unafikiri huko tunaweza kupata fununu juu ya mtu huyu muuaji kweli?” Jitu aliuliza akiwa ndie ameketi nyuma ya usukani. “Amini usiamini huyu mtu bila risasi wala ngumi, tunamtia nguvuni, hana siku mbili mbele,”
Jitu akatikisa kichwa tu kukubali, Inspekta akachukua file alilokuwa nalo mkononi na kuanzaa kulifunua funua huku akiendelea kuzungumza na Jitu. “Jitu amini usiamini, tunamtia nguvuni huyu muuaji ndani ya siku mbili kwa sababu ana tatizo la kukurupuka, japo anatuumiza sana vichwa lakini elewa fika kuwa hana maisha tena ya kuwa uraiani,” “Labda pia name nikukumbushe tu mkuu, unakumbuka ahadi yake ya leo?” ‘Ile ya huyo MwanaJuma Sijui MwanaEid?” “Ndio hiyohiyo,” “Mfamaji tu Yule hana lolote, angekuwa mtendaji kwa hilo si angefanya? Maana jioni haipo mbali.” Inspekta alikuwa akijiamini kupita kiasi, hadi Jitu mwenyewe akawa anashangaa. ‘Hivi huyu jamaa anategemea nini hadi kujiamini kiasi hicho? Ama ndio anatuhadaa? Mbona mimi simuelewi elewi?’ alijiwazia mwenyewe na wakati huo tayari walikuwa wamewasili mbele ya geti la kuingia ndani ya Fensi ya Magereza. Walitoa vitambulisho vyao na kuruhusiwa kuingia ndani ambapo walielekezwa hadi lilipo jengo la ofisi ya Bwana Gereza ambapo wakanyoosha hadi huko na kushuka ili kukutana nae. Aliwakaribisha na kuwapa siti za kukaa kisha wakajitambulisha baada ya salamu, Inspekta alielezea sababu ya wao kuwepo pale. “Hakika mkuu hapo ndio tulipokwama na tuna kila sababu ya kumtafuta mtu huyu na kumkamata kwa ajili ya usalama wa raia wetu, na sasa naona kama jukumu la kumjua muuaji ni letukwa kushirikiana nawe, sijui unatusaidiaje hapo?” alisema kama vile ni mtu anaejivua yeye na kumkabidhi jukumu mkuu wa gereza. Nae alionekana kamakufikiri kwa sekunde kadhaa kisha akawa kama amekurupuka hivi na kuuliza “Umesema namba yake yeye huijui wala jina alilotumia gerezani?” wakajibu wote kwa pamoja kwamba hawajui. lakini wakamtajia jina la utani tu alilokuwa akitumia. Mkuu wa gereza akaomba namba hiyo ya mtu waliemtia nguvuni. Jitu akavuta faili uliyokuwa mbele yake na kufunua ukurasa wa mtuhumiwa huyo na kumsogezea Mkuu wa gereza. hata kabla hajasoma jina la Mtuhumiwa, akasema mtuhumiwa huyo atakuwa alikuja pale kwa kesi ya utumiaji wa silaha za moto. “Hapa naona namba ya gereza letu hili, namba ya selo aliyokuwa amepangiwa na namba yake ya utambulisho kama mfungwa, kisha ndio akamtafuta jina. Baada ya kulisoma jina la huyo mfungwa akamtambua. “Sasa nashauri cha kufanya muende kwa huyo mliemkamata mlazimishe amtaje kwa namba ili tuweze kumtambua, na hapa kabla hamjaondoka nitawaonesha ni vipi mtamtambua huyo mtu ni nani na alikuwa gereza gani!” kisha akanyanyuka na kwenda pale walipokaa maofisa wale wapolisi. Pale alipofunua ilikuwa ni kwenye ile page ya mtuhumiwa walienae kituoni ambae namba.yake ilisomeka kama 427010 akaanza kuwafafanulia, akasema “Daima husomwa kwa namba mbili mbili kwa kuanzia mwanzo kwenda mwisho. Namba mbili za kwanza ni za gereza, yaani hiyo 42 ndio gereza leetu kama nilivyokuambia awali, namba hii huyolewa mahakamani kwani ni wao ndio hupanga gereza la mtu kufungwa, nafikiri tupo pamoja?” aliwauliza akiwatazama na wakatikisa kichwa tu kumkubalia, akaendelea “Namba ya kati hutolewa na gereza,kwani gereza ndio hupanga ni nani atafikia kwenye selo ipi pindi anapoletwa hapa, hivyo hiyo inayofuatia ni 70 hii ni namba ya Cell ambayo alikuwa akiishi humu ndani na kwa mujibu wa namba hiyo alikuwa yupo kusini magharibi, cijui mnanielewa?” alikuwa akifafanua kwa uhodari kabisa. wakamuitikia kuwa wanamuelewa vizuri sana aendelee tu. “Hiyo ya mwisho ni namba ya mfungwa mwenyewe, ambayo hutolewa na Nyapara na kusajiliwa kama namba rasmi ya mfungwa.” alimaliza kutoa ufafanuzi ambao waliona kama haujawasaidia lolote. Jitu akauliza kaa anaweza kumfahu dega ama lah wafungwa waliokuwepo miaka mitatu iliopita. Mkuu alishikilia palepale kuwa ni vigumu sana kwa jambo hilo. basi kwa shingo upande tu wakaaga huku wakiwa wanasimama na kumpa mikono yao na kutoka akiwa amewashindikiza. Inspekta akamueleza kuwa atahitaji namba yake ya siku na hasa ya mkononi ili ikitokea juwa kuna chochote ambacho watahitaji msaada, basi wawasiliane. Upande wa pili huku Jitu alikuqa akiona kama wamepoteza muda tu bure. Aliamini muda huo wangeweza tu kufanya mambo mengine na hata kwenye upelelezi wa ndani kwa ndani wangeweza kung’amua kitu tofauti na hiyo ya kwenda huko. Wakiwa wamechoka kabisa na muda wao, wakaelekea garini na Jitu kama kawaida akaingia upande wa usukani huku Inspekta Kalindimya akiingia kwa dereva na kuanza safari ya kurejea ofisini kwao. Ndani ya gari Inspekta aliendelea tu kupekuwa pekua faili ile. Lakini katika upekuzi wake akakumbuka kittu. harakaharaka kama vile ameamriwa afanye upesi, akarejea mwanzo kabisa na kuifunua namba ile ya mauaji ya mwanaHamisi. Namba ile ilisomeka 426474 nae akajaribu kuiweka kwenye makundi matatu vilevile kama alivyofanya Mkuu wa Gereza, akaguna na kumshika mkono mmoja Jitu aliekuwa makini akitazama mbele, akageuka na kumtazama, Inspekta nae akamtazama na kumwambia warudi gerezani Keko.
“Jitu faster turudi keko, muuaji tumemjua, haraka tumuwahi Mkuu kabla hajatoka,” Jitu kwa kasi aliyokuwa nayo aliipunguza kidogo na kulala na gari na kurejea kulekule alipotokea. Kabla hata hawajafika Inspekta akakumbuka kuwa alichukua namba ya simu ya Mkuu wa gereza, akampigia simu na kumuuliza kama yupo. badala ya kujibu kwanza nae akahoji kuna nini? Inspekta akamwambia kuna dharula hivyo wapo njiani wanarejea. Akawaambia wajitahidi wawahi jwani anapaswa kutoka muda ule kuelekea kwenye shughuli zingine za kitaifa. Wakamjibu dakika tano tu watakuwa pale. Kauli ya Inspekta aliisikia Jitu, akageuza kasi. Safari yao iliishia getini, hawakuongea garini hadi wanafika kwenye geti la kuingia ndani ya gereza ndio Inspekta akanyanyua mdomo na kusema mwisho wake huyo muuaji umewadia. Jitu akashusha pumzi kwa nguvu na kumuuliza boss wake kuwa ni kwanini amesema hivyo. Inspekta akamwambia anmuhakikishia kwa wakitoka mle ndani tayari watakuwa na jina la muuaji na kama watatulia ofisini hadi kufikia kesho kitakuwa kimeeleweka. “Amini usiamini huyu muuaji wa hawa watu ni mtu ambae anakesi hapo kwetu na nina hakika kabisa tukilijua jina lake tu nae amekwisha ndio maana nakueleza hivyo,” aliongea kirefu na maneno yake kiasi yalimuingia Jitu kichwani. Tayari walikuwa kwenye mlango wa mkuu wa magereza, akawakaribisha Secretary wake ambae tayari alipewa habari ya kurudi kwao na kuwaruhusu waingie. “Tena mna bahati sana, maana mkuu alikuwa na safari, hivyo jitahidini tu muwahi,” aliongezea huku akiwaonesha mlango ambao nao tayari wanaujua. “Ahsante,” alijibu Jitu wakiwa na haraka ya kuingia humo ndani. Walimkuta akiwa ameketi kama vile anawasubiri wao tu ili atoke, maana alikuwa amekaa kama amesimama vile, haraka haraka akawauliza shida kwani alikuwa na haraka. Inspekta akamwambia kuwa amepata namba Fulani kutoka kwenye chanzo chake cha upelelezi na kuifananisa na namba ya awali hivyo wamerudi ili apate kuwahakikishia. “Naomba niione Inspekta,” alikuwa na haraka sana na kila kitu alitaka kifanyike haraka haraka. Alipoitazama tu akasema ile namba kweli ni ya pale, akasimama na kuanza kuwangalia kwenye mafaili yaliyokuwa kwenye Self mbele ya macho yake lakini nyuma ya migongo ya wale maaskari wa upelelezi. Ilimchukua dakika kadhaa hivi hadi kuweza kuipata na kuja nalo pale mezani kwake na kuanza kulifunua funua. Alifunua kama kurasa mbili tatu hivi, akachomoa picha na kuinyanyua kuiangalia. Baada ya hapo akampa Jitu ambae alikuwa yupo karibu nae na kasha akarudisha macho yake kwenye faili lake kama kwamba hakuna kilichotokea. Jitu alipomtazama alie kwenye picha ile akampa Inspekta Kalindimya. Inspekta nae aliitazama picha ile kwa sekunde kadhaa na kuiweka mezani kasha akaelekeza maco yake kwa bwana gereza amabe alikuwa wala hahangaiki nao, kwani alikuwa anashughulishwa na lile faili tu. Baada ya kufunua funua kidogo akalifunika lile faili na kuwaangalia wale wapelelezi wawili na kuanza kusema “Namba hii mliyo ileta hapa ni mfungwa mmoja aliewahi kufungwa hapa gerezani na kuishi kwenye Selo namba 74 ambayo ipo mashariki kati ya miaka mitatu iliopita ana alikuwa akitumikia kifungo cha miaka mitano kwa kosa la unyang’anyi kwa kutumia silaha nzito, ila inaonekana hakikutimia kifungo hicho na akatoka,” wakashangaa. “Akatoka? Kivipi?” “Nasema akatoka kwa sababu kwa mujibu wa hii namba mliyo niletea inaonesha kwamba mtu huyo ni mzima, au sio?” Wote wakajibu ndio, wakiendelea kumtazama, Bwana Jela akaendelea “Lakini huku anaonekana alifariki kitambo sana, yaani hata mwili wake ulitoka humu kama unatolewa mwili wa maiti, ndio maana hata faili yake inaonekana ikiwa imepigwa ‘X” walichoka wale maafande na bila kuchelewa Inspekta akamwambia anapenda kumjua jina lake na alipoandikisha kuwa anaishi. “Jina lake ni Loren Malima, aliingia hapa miaka mitano iliopita akiwa na miaka 33 akiwa amehukumiwa kufungwa miaka mitano lakini ndani ya miaka miwili tu akawa amefariki na akachukuliwa na nduguze kwa ajili ya mazishi,” akliwasomea huku Jitu akiandika na Bwana Gereza alikuwa akitazama saa yake. Alionesha kuwa muda umemuishia sasa, nao wakamuelewa, Inspekta akatoa kamera na kuipiga picha tena ile picha na kumtaka Bwana gereza ampe nakala ya maelezo hayo kwa ajili ya uchunguzi zaidi. “Sawa, lakini samahani, nina mkutano na Waziri alasiri hii, sasa naomba nije niwakabidhi kwa Katibu wangu awashughulikie, samahanini lakini kwa kitendo hicho,” aliomba radhi kwani alihitaji kutoka. Wala usijali mkuu, jambo la msingi ndio hilo umetusaidia, nasi tunashukuru sana,” waljibu huku wakitoka nje na Bwana Gereza akiwa nyuma yao. Walipofika kwa Sekretari Yule, akamfahamisha watakacho kasha wakaagana akiwaomba wafike siku nyingine kwa maelezo zaidi, wakashukuru na kumuacha aende kwa amani, Dada Yule aliwasaidia kila walichohitaji, akawatolea copy kwa zile karatasi na kuwapatia, nao wala hawakukaa sana wakaaga na kuondoka, njiani ndio wakajadiliana na kuona kama bado wapo njia panda bado.
Waliwasili ofisini kwao moja kwa moja na kuanza kupitia majina yale waliyotajiwa, kwanza walianza kumchunguza na kutaka kumjua huyo Loren ni nani. Hivyo wakavuta Compuuter na kuanzaakumfuatilia kumjua, ajabu hakuonekana mle kabisa kitu ambacho hata wao kiliwaumiza kichwa “Haiwezekani kiu hicho, yaani mtu aliefungwa gereza kubwa kama Keko akosekane kwenye kumbukumbu za Polisi? Haiwezekani!” alisema Inspekta Kalindimya huku akiuma biki yake na kumfanya Jitu asimame kutoka kwenye kiti alichokuwa amekaa. “Hapa yawezekana ikawa kuna siri kubwa nyuma ya pazia, wizi wa kuku wapo humu, iweje huyu akosekane?” alisema Jitu na kujikuta akiropoka tu kuwa yeye anahisi ile kazi imemchosha. “Unaweza kujikuta unazeeka kabla hata ya muda,” Inspekta alikuwa yupo kimya tu, Jitu sasa ndio alikuwa msemaji. “Mkuu ninafikiri huu ni muda muafaka wa sisi kufunika haya makabrasha na kwenda kupumzisha akili maana hata kesho nayo ni siku, tusijiumize bure leo,” “Hilo nalo ni neon, maana hata utumie dawa nyingi kiasi gani, mguu wa bandia hauwezi kuota vinyweleo, hebu tukapumzishe akili,” akaungana na Jitu wakakusanya makabrasha ma kuzima na Computer pamoja na AC. Kwenye kutoka akanza kutoka Inspekta Kalindimya, itifaki ilizingatiwa na moja kwa moja yeye alielekea garini kwake n kusimama nje akiongea na simu na baada ya sekunde kadhaa akafika Jitu na kumuaga akaelekea kwenye gari yake. Kabla hata hajaketi kwenye gari yake Jitu, mlango ukiwa wazi huku akimuona dhahiri Inspekta nae akifngua mlango wa gari yake, aliweza kumuona pia Sekretary wa Inspekta akajitokeza akitweta kwa kuwa alikuja mbio. Alimsemesha na kwa umakini na uharaka wa ajabu Jitu akamuita Jitu ambae alishtushwa na ule ujaji wa Sekretary, hata naea lihisi kuwa hakuna jema, itakuwa kuna jambo tu. Kwa hatua ndefu ndefu Inspekta akatangulia na kufuatiwa na Sekretary wake huku mwisho akimalizia Jitu ambae alikwenda moja kwa moja kwa Sekretary na kumshika bega kumuuliza kuna nini? Akamwambia kuwa wanahitajika haraka sana ofisini kwa RCO muda uleule, bila kuguna wala kuuliza tena akanyoosha moja kwa moja hadi kwenye ngazi za ghorofa ya kwanza. Kila alivyozidi kupanda ngazi hizo, ndio na kasi nayo iliongezeka maana alitarajia kumuona Inspekta akiwa anapandisha ngazi hizo, lakini ilionesha kabisa kuwa alienda kasi kuliko yake. Inspekta akafika hapo na kugonga mlango kwa muda mrefu lakini hakuitikiwa, akalazimika kuingia tu hivyohivyo kwani alisikia sauyi ya nyayo zikihama toka sehemu moja kwenda nyingine. Hiyo ndio ilimchelewesha na kumfanya amkute Inspekta Mlangoni ndio anamuona Inspekta akimalizia kuingia nae akaongeza kasi zaidi na kuingia muda huo huo na kuwasalimia kasha akaketi sambamba na alipoketi Inspekta Kalindimya. Walimkuta mzee akiwa anazunguka tu hapa na pale kama vile mtu aliechanganywa na jambo fulani na alipowaona wamekaa akawakaribisha na kuwaonesha viti kwa mara nyingine. Wakatazamana na kujua kuwa itakuwa kuna jambo zito linamkwaza huyo mzee hadi anafikia hatua ya kutokujielewa. Ghafla kama mtu aliezinduliwa, akamgeukia Inspekta na kumuuliza anashughulika na kesi gani kwa sasa? Inspekta akamjibu kuwa anashughulikia kesi ya mauaji ya wasichana wawili waitwao kina Mwana. “Lakini pia kwenye kesi hiyo kuna majeruhi mmoja ambae yupobbado hospitali na tunafikiria…” kabla hajamaliza kutoa maelekezo zaidi, akakatishwa na Mkuu wake na kumwambia “asaaa tangu sasa hizo kazi zote fungia kwenye box kwa muda kwani kuna tukio moja kubwa na baya sana limetokea leo jioni hii, hadi Rais na baraza lake lamawaziri limepiga kelele na kutupa wakati mgumu mno jeshi la Polisi,” alisema na kushusha pumzi kwa nguvu. “Tukio gani hilo mkuu?” aliuliza Inspekta kwa shauku huku akiongeza umakini kwa RCO. “Waziri wa Jumuia ya Afrika na Muungano…” kabla hajamaliza Jitu akadakia “Bi MwanaJuma Eid,” “Yap! ametekwa maeneo ya Manjunju akiwa anaelekea nyumbani kwake maeneo ya Victoria.” “Boss hilo tukio limetokea leo saa ngapi?” alihoji Inspekta. “Tukio hili limetokea dakika chache zilizopita na tumezuia vyombo vya habari kutangaza juu ya jambo hilo hadi pale kila kitu kitakapo kuwa kipo vizuri…” akatulia kidogo na ukimya ukiwa umetawala kisha Inspekta akavunja ukimya na kusema “Mkuu, ninahisi kuna muingiliano wa kesi hizi mbili, yaani hii unayotueleza sasa na ile ambayo tumekuwa tukiishughulikia tangu awali” “Kivipi na unawezaje kutambua hilo?” aliuliza huku akiwa anamtazama kwa umakini, kwani kauli ile aliona kama huenda ikaleta unafuu kwa kiasi fulani. “Kesi ninayoisimamia sasa, muuaji aliniambia napaswa kujitoa kwenye hiyo kesi kabla sijafukuzwa na pia baada ya kuona simuelewi ndio jana akanipigia simu na kuniambia kuwa ananitaka niache kazi kwa faida ya Mwana, kibaya zaidi hakutaja ni Mwana gani ambae anae mtumia kama kinga yake,” aliongea kirefu Inspekta na kumfanya RCO afikirie kwa dakika kadhaa na kuhoji tena;
“Unafikiri ni kwanini alikwambia ujitoe kwenye kesi hii?” sasa alimuuliza huku akiwa anaketi kwenye kiti chake kuonesha kuwa anepata ahueni kiasi. “Nahisi ni kwa sababu amejua kuwa muda sio mrefu tutamtia nguvuni, sasa maekuwa na mashaka mashaka tu ambayo yanamfanya azidi kufanya makosa,” kauli hiyo ikawafanya wote wamuangalie Inspekta na Jitu akamuuliza “Kama lipi vile kosa ambalo amelifanya?” “Hiyo ya kumkamata Waziri ni dalili ya kutapatapa, na ndio kosa kubwa zaidi alilolifanya hilo Jitu,” wakakubali tu ili kujua ni muafaka gani ambao watafikia. “Najaribu kuchanganua maneno yako lakini hata sipati jibu, sasa hebu niambie, ni msaada gani naweza kuwapatia ili muweze kukamilisha zoezi hili ndani ya saa 24?” aliuliza Mkuu huku akiwaangalia kwa zamu. “Task force mkuu, naomba utuongezee uwezo,” “Upi huo?” “Ninahitaji sana kikosi kazi, kikosi maalum cha kukubaliana na uhalifu (Crime Response Team) kwani mhalifu amekuwa akitumia sana mawasiliano ili kutekeleza mambo yake,” aliomba Inspekta. “Sawa, nataka hadi kesho muda kama huu niwe na jibu kamili kuhusu huyo mtekaji nyara na lakini asubuhi nijulishe kuhusu Waziri, umenielewa?” alisema huku akisimama, itifaki ikazingatiwa, nao wakasimama na kukubali alichokisema, kisha nae akaongeza “Ninampigia simu RPC sasa hivi akuandalie hicho ulichotaka, lakini kumbuka, ninatoa masaa 24 tu uweze kumtia mbaroni huyo mhalifu na pia umuokoe Waziri akiwa yu hai, unanielewa?” “Sawa Mkuu,” akaitika Inspekta na kutoka kichwa kikiwa kinamzunguka, hakika alivurugikiwa akili, hasa akikumbuka hizo amri za mkuu wake wa kazi, ndio akachoka kabisa. Walikuwa wameongozana hadi ofisini, Jitu akiwa mpole kabisa, aliona kama wametwishwa mzigo wa mawe, walifika na kujitupia kwenye viti vyao vya kuzunguka, lakini leo wala havikuwa na staraham leo. Hakuna aliekumbuka kujizungusha, kila mmoja aliwaza ni wapi pa kuanzia, Jitu ndio akawa wa kwanza kupata wazo “Inspekta naomba niseme kitu,” Inspekta hakumjibu bali alimkazia tu jicho. “Nafikiri tuanze na utaratibu wa kumtambua huyo mtu ni nani na wapi tunaweza kumpata,” “Kivipi?” “Mimi sitaki kuamini kuwa Computer za Polisi zimeshindwa kumuhifadhi mtuhumiwa hadi inakosekena kumbukumbu kweli?” “Jitu bado hujatoa mwongozo, ni kipi tukifanye ili tuweze kulifanikisha hiyo,” “Sawa, mimi nilichokiwaza hapa ni kwenda kuanza na watu wa IT, tuwape jina na ikiwezekana na picha washughulikie hilo…” Inspekta nae akapata mwanga na kumkatisha Jitu. “Wazo zuri sana hilo Jitu, sasa name pia hapa nina wazo jingine, tukichanganya hilo lako na langu, ninaamini tutapata muafaka kwa urahisi sana,” “Wazo lipi Mkuu?” “Ninafikiria wewe uende kwa watu wa IT kisha mimi nielekee hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa Mwana,” hivyo ndivyo walivyogawana majukumuna kukubaliana kuwasiliana muda wote mmoja wao anapopata kitu kipya. Inspekta akatoka na kumuacha nae Jitu akijiandaa kutoka. Aliwasili hospitalini na kuingia kwa daktari kisha akajitambulisha, kwa kuwa haukuwa ni muda mzuri kwa wageni kuingia, akaomba aruhusiwe kwa sababu maalum. Daktari alimkubalia na kumuongoza hadi wadini na kumuacha huko wakiwa wao wawili tu. Alijitambulisha mbele ya Mwana na kumpa pole kisha akaanza mahoiano nae. Alimuuliza swali la kwanza kama anamfahamu aliemvamia? Mwana akakiri kuwa anamfahamu kwa sauti yake ambayo anajua fika kwamba anaitambua japo kwa upande wa sura hajui, kwani ilifichwa. “Wakati unavamiwa, ndani ya gari mlikuwa wangapi?” “Wakati nvamiwa ndani ya gari nilikuwa nipo peke yangu,” “Na wavamizi walikuwa wapo wangapi?” “Wao walikuwa wapo wawili tu, mwanamke na mwanaume,” “Anhaa! Ina maan a wote wawili walificha sura zao?” “Ndio afande, wote wawili walikuwa wamevaa mask, lakini Yule mwanaume sauti yake si ngeni kabisa kwenye masikio yangu,” “Na huyo mwanamke je?” “Yeye ni mgeni kabisa kwenye masikio yangu na hata bumbo lake kwenye macho yangu ni jipya kabisa,” akajiweka vizuri kwenye kitqanda ambacho kwa upande mmoja wa juu kiliinuliwa ili kumpa ahueni ya maumivu mgonjwa. “Lakini sina budi kumshukuru huyo mwanamke kwani nahisi huenda ndie alieniokoa na kifo,” aliendelea kusema Mwana. Habari ile ilikuwa ni mpya kabisa kwake, akamuuliza huyo mwanamke alimuokoa kivipi? “Baada ya kuchukua pesa, Yule mwanaume alitaka kuniua kabisa kwa kusema nimeponzwa, Yule mwanamke akamzuia na kusema kama ni pesa mbona nimetoa tena bila vurugu wala kelele? Ukatokea ubishi kidogo kati yao lakini wa muda mchache mno,” “Hakukuwa na mtu jirani?” alihoji Inspekta huku akiandika. “Hapana, kwa mbali niliona walinzi kwenye jingo la ghorofa la vioo pale karibu na makaburini, ila walikuwa ni mbali mno,” “Mh! Endelea, baada ya huo ubishi?” “Yule mwanaume akamuwekea bastola Yule mwanamke shingoni na kumwambia anipige risasi ya kichwa,” “Enhee! Ikawaje baada ya hapo?” “Hapo sasa Yule mwanamke akasogeza bunduki yake na kunipiga risasi ya bega na nakumbuka akanipiga na kitako cha bunduki kichwani, sikujua ni kipi kilicho Endelea hadi niliposhtuka nikiwa hospitali,” alimaliza kujieleza Mwana.
Inspekta alikuwa akiandika tu yale maelezo ya MwanaMeka, sasa akamuuliza “Umesema sauti ya Yule mwanaume sio ngeni si ndio?” “Ndio japo hata siikumbuki ni wapi nilipoisikia, ila hakika sio ngeni kabisa,” “Je ukiisikia tena unaweza kuitambua?” “Naam hata niwe taabani kiasi gani, naitambua vema kabisa,” alijibu Mwana kwa kujiamini na afande akatikisa kichwa kukubali akisemacho Mwana. Kisha akazama mfukoni na kutoa simu yake ya mkononi na kutafuta kitu Fulani hivi, alipokipata akanyanyuka pale alipokuwa ameketi na kumsogelea, akamsikilizisha audio Fulani ambayo alikuwa amerekodi. Yalikuwa ni mahojiano, Mwana alisikiliza na ilipofika sauti hiyo ambayo Inspekta alihisi kuwa Mwana ataijua, ni kweli aliijua na kutaka kulazimisha kunyanyuka kitandani na kusema hiyo ndio sauti yenyewe hasa. Inspekta akamtuliza na kumwambia apumzike tu vilevile hadi watakapomaliza mahojiano yao. Mwana akarudi chini na kulala kama awali, kisha Inspekta akahoji “Kama sauti si ngeni, ina maana huyo ni mtu ambae mnafahamiana nae vizuri, sasa hebu nifumbulie hili fumbo… je unafikiri huyu mvamizi aliekuvamia, alijuwa kuwa wewe una pesa kwenye gari ama ilitokea tu?” akamtazama usoni wakati Mwana akihangaika kutafuta jibu. “Mh! Afande kwa kweli hapo mimi siwezi kujua wala hata kupata hisia maana kilikuwa ni kitendo cha ghafla sana kwangu,” mahojiano yaliendelea kwa muda kidogo na huku akimbana kwa kila Nyanja kama ana fununu zozote. Lakini ilionekana kama vile hakuwa akijua lolote, Inspekta akachukua bahasha aliyokuwa nayo na kutoa picha moja ya wastani na kumuonesha MwanaMeka. MwanaMeka akaiangalia na kusema hamtambui kabisa mtu Yule. Inspekta akamwambia ajaribu kujikumbusha vizuri kama atamkumbuka, kisha akasimama na kutoa business kadi yake na kumwambia wakati wowote akipata kumbukumbu yoyote juu ya mtu Yule aliemuona kwenye picha, basi amshitue. “Wewe nijulishe wakati wowote, iwe mchana ama usiku, asubuhi ama jioni sawa Mwana?” alimuuliza huku akichukua bahasha yake na kuanza kutoka. Mwana aliitikia sawa na Inspekta alipopiga tu hatua moja akageuka na kusema “Pia ukikumbuka mtu mwenye sauti ile, basi ujue kuwa ndio mwenye picha ile niliokuonesha, nijulishe haraka iwezekanavyo,” Mwana akasema sawa na Inspekta akatoka kuelekea anapo pajua mwenyewe. **********
Ilikuwa ni saa moja jioni muda ambao alitoka nje ya hospitali ya Taifa, akampigia simu Inspekta Jitu kumuuliza matokeo ya huko alipokwenda na kujua ni kipi kilicho Endelea. Jitu akamwambia kuwa kiufupi ni kwamba data zilikuwepo na zikafutwa na haieleweki kama ni kwa maksudi ama ni bahati mbaya, lakini hakika inaonesha uwepo wa picha na jina lakini hakuna maelezo yoyote. “Hii inaonesha kuwa huyu msumbufu ana watu wake ndani ya Jeshi la Polisi, inatulazimu kwa sasa kuwa makini zaidi hasa kwa usiku huu wa leo,” aliongea Inspekta Kalindimya. “Sawa kabisa Inspekta na hata name nilikuwa na wazo kama hilo, wewe upo wapi kwa sasa?” alihoji Jitu. “mimi natoka Muhimbili hapa, sasa wewe fanya kila njia tukutane Ferry ili tuvuke kwenda Kigamboni, huko kuna dharula,” aliongea Inspekta huku akitazama saa yake, neon lake kwa Jitu, ambae kicheo ni mdogo na hata kiumri pia, lilikuwa ni sheria. Jitu akamuuliza kama yeye yupo nagari? Inspekta akamjibu ndio yupo na gari yake hivyo kama yeye anakwenda sasa hivi ni heri atumie pikipiki ya Polisi ili aweze kumuwahi na achukue dereva. Jitu akamwambia ampe dakika chache tu watakutana hapo Ferry, wakapanga akifika atamkuta kwenye gari yake ambayo atakuwa ameipaki getini kwa ndani, haitokuwa kwenye foleni. Dakika kadhaa mbele kweli Jitu alifika akiwa kwenye pikipiki ya jeshi la Polisi na kuelekea moja kwa moja ilipo gari ya Inspekta Kalindimya na kuingia, alimkuta akiwa anasoma maandishi aliyo yaandika yeye mwenyewe. “Tunaenda wapi mkuu?” aliuliza Jitu wakati Inspekta akiwasha gari kulielekeza kwenye njia ambayo ilikuwa inaishia ndani ya pantoni. “Nataka tukaanzie kituo cha Polisi Kigamboni, pale ndio safari yetu itapata muelekeo, kwa sasa hakuna muelekeo zaidi ya huo,” “Sawa, nipe habari za huko ulipo kwenda,” “Mh! Jitu… hatari sana! Amini usiamini kuwa kila mtu anamtambua jambazi lakini hamjui,” “Inspekta mbona sikuelewi? Inakuwaje anamtambua halafu hamjui?” “Namaanisha sauti yake kila mtu anaijua na lakini inapokuja suala la kumjua ni nani ndio inaingia kuwa ni shida,” akamueleza yote yaliyojiri kule kwa MwanaMeka na kumuacha na mshangao. “Mh! Hivi ina maana kuwa matukio haya yanashabihiana si ndio mkuu?” “Hicho kitu mimi ninakiamini, na hapa tulipofikia leo, ndio ilipokuwa point ya mtuhumiwa, alikuwa akimlenga waziri, kote kule alikuwa akizunguka tu,” “Ni kweli sasa name nimebaini, lakini je unafikiri muda huo tuliopewa unaweza kututosha kweli kumtia mikononi mwetu mkuu?” Jitu alikuwa akiuliza huku akionesha kabisa kuweka matumaini yake yote kwa Inspekta Kalindimya ambae alikuwa kijiamini mno. Gari ndio zilikuwa zinakamilisha utaratibu wa kutoka baada ya watu wote kuwa wameishatoka.
Alimjibu kuwa uwezekano ni finyu lakini hiyo haiwezi kusababisha kukata tamaa, bali pale ambapo unakatishwa tamaa na jambo Fulani basi hupaswi kuvunjika moyo, bali unalazimika kujituma zaidi. Waliwasili kituoni na kuomba kukutana na Mkuu wa kituo kile cha Kigamboni, wakaruhusiwa kumuona na kuketi nae ofisini na kumueleza kuhusu jambo lililowateta pale na kumkumbushia tukio la siku za nyuma lililitokea kule Kigamboni. “Hivyo Mkuu Yule mtu alikuwa ni MwanaMeka aliekuwa akiwindwa na huyo msumbufu, na sasa tumekuja huku kwa lengo maalum,” “Lipi hilo?” “Tunataka kukutana na askari wale waliompa Escort Yule mwanadada mfanyabiashara, kwenda sehemu ya biashara na kurudi nae,” Inspekta akasema huku akimtazama, Mkuu akatikisa kichwa kukubali na kunyanyua simu kumuita Katibu wake. Aliingia kwa unyenyekevu, Mkuu akamwambia ampigie simu askari aliekuwa zamu siku ile, akamtajia tarehe ya siku na muda husika. “Mwambie afike hapa haraka na wenzake aliokuwa nao, sawa?” alitoa amri ya kijeshi ambayo Katibu alitii bila shuruti na kujibu sawa huku akiwa amekakamaa. Akatoka na kuwaacha wakiendelea kuongea huku Mkuu wa kituo akiwauliza kama wanaweza kumkamata mtu huyo haraka iwezekanavyo? Jitu akajibu kuwa kuna asilimia kubwa za kumtia mikononi mwa vyombo vya usalama mapema. Wakati story zimenoga, akarudi Katibu Muhtasi wa Mkuu wa Kituo na kupiga saluti kisha akasema amewapata wawili kati ya wale waliokwenda huko, Mkuu hakujibu kitu akawatazama Jitu na Inspekta akitegemea jibu kutoka kwao. Inspekta akasema kwamba wao wawili hao wanatosha kabisa, akamruhusu tu Yule dada aende kuendelea na kazi nyingine wao wakamuomba Mkuu wafanye mahojiano mafupi. Akawapeleka kwenye chumba maalum ambacho kilionesha kama ni ukumbi wa mikutano hivi na kuwaambia kuwa wanaweza kufanya mkutano wao mle ndani, kisha yeye akatoka na kuwaambia atakuwepo ofisini kwake. Mahojiano yao hayakuchukua muda mrefu sana kwani wote kazi zao zilikuwa zimefanana na kila mmoja alikua akijua ni kipi kinachotakiwa kujulikana. Jitu aliuliza swali la mwisho na kisha akawataka wanyanyuke na kuelekea eneo la tukio walipompeleka huyo dada. Kwa pamoja wote wakanyanyuka na kutoka huku waitangulia nje na Inspekta pekee ndio akaenda ofisini kwa mkuu wa kituo na kumwambia kuwa anatoka na vijana hao kuelekea eneo la tukio. Aliwaruhusu na kumwambia kuwa iwapo atahitaji msaada wowote asisite kumjulisha kwani yeye hatotoka pale ofisini hadi wao watakaporejea, Inspekta akamwambia kuwa asijali, wapo pamoja. Wakati wanawasili eneo walilokwenda, ilikuwa ni saa tatu usiku, lakini eneo hilo lilionekana kama bado ni changamfu sana, mizigo mingi ikionekana kupakuliwa kutoka kwenye meli za magendo na watu wakitumia vinywaji vikali huku bangi na vitu vingi vya anasa vikiendelea eneo hilo waziwazi. Wakiwa bado hawajashuka garini kwa mwendo wa taratibu waliweza kuyaona yote hayo, mbele kidogo akasimama Inspekta na kugeuka nyuma walipokuwa wameketi wale askari wawili ambao ndio wenyeji wao na akawauliza huku akiwatazama ‘Hivi eneo hili limeruhusiwa kuwa katika mazingira haya tunayo yaona ama hamjui kinacho Endelea hapa? Mbona mimi sielewi?” “Yaani unaweza kusema imeruhusiwa kuvunja sheria, hii ni hatari sana,” aliongezea Jitu na Inspekta akasema kwa kuwa leo si kitu ambacho kimewapeleka huko. “Kilichotuleta leo hapa ni kumtafuta na kumjua ni nani ambae alikuwa akifanya biashara na Mwana, lakini hakikisheni kuwa jambo hili mnalidhibiti mara moja,” alisema huku akishika kitasa kwa ndani. Waliitikia sawa mkuu na kuanza kujipanga, Jitu akawauliza kama wanamjua Yule muuaji kwa sura? Wote wakasema hawamjui kwani walikuwa nae kwa mbali wakati akifanya mazungumzo na Mwana. “Labda kwa kumbahatisha tu tusogee eneo ambalo niliwaona huyo mfanya biashara na Yule jamaa wakiwa wamesimama,” alisema askari mmoja kati ya wale wawili na huku akionesha kwa kidole. “We ulimuona vizuri?” Jitu alihoji mguu mmoja ukiwa nje na mwingine ukiwa ndani ya gari. “Si mimi peke yangu bali ni sote tulimuona,” alipojibu hivyo na Yule mwingine alitikisa kichwa kumuunga mkono mwenzie. Wakajipanga kuwa waende wale wawili na kumuulizia kwa kumtaja umbo lake na alivyo kisha wakisha mjua wao watashuka na kuendelea nae. “Hakikisheni mkimjua mnamtoa pale na kumpeleka pembeni, hiyo itakuwa ni ishara kwetu, sawa makamanda?” Jitu ndio alikuwa akipanga kikosi kazi nae akamuambia afande kwamba anashuka garini na kusogea ambapo anaweza kuwa nao karibu ili kudadisi mazingira yale. Inspekta akabaki garini peke yake lakini macho yake yakiwa yanaangalia kule wanapoelekea wale askari wawili, alitamani mno kushuhudia mtu huyo akiwa amesimama nao. Jitu akiwa ameacha nafasi ya hatua zisizozidi tatu, kutokana na kuwa na shughuli nyingi eneo lile, hakuna aliekuwa akishughulishwa na mwingine, kila mtu alikuwa na jambo lake. Hiyo iliwapa nafasi mzuri zaidi kwa wao kufanya yao kwa nafasi, mbele kidogo ya macho yake Jitu, akaona Wale maskari wawili wakisimama ghafla na kumshika jamaa mkono, jamaa akasimama na kuwatazama kwa mshangao.
Walimsalimia na kumuulizia huyo mtu wanaemtafuta, alikana kumfahamu na kila walivyojaribu kumuelekeza hakumjua, wengi pia wakakana kumjua na hivyo walihisi kukata tamaa. Ikawalazimu kurejea garini ambapo ndio kilikuwa kituo chao, hapo ndio Jitu akatoa ushauri wa kuongea na MwanaMtama, ambae alikuwa ni mfanya biashara nyingine kabla ya kumjeruhi ikiwa kama ni kweli ndio yeye muhusika. Lilikuwani wazo zuri, Inspekta akampigia simu Mwana na bahati mbaya simu yake ikawa haipokelewai, ilikuwa ikiita hadi inakata, sasa hapo ikawa haina jinsi ila tu kurejea mjini. Waliwapitisha wale askari pale walipo watoa na wao kuelekea kwenye pantone ili kuvuka. Wakiwa ndani ya Pantoni simu ya Inspekta sasa ikaita, namba ya simu ilikuwa ni ya mezani, akamtazama Jitu na kumwambia ‘kumekucha’ Akaweka vitu vyake sawa ili kuweza kurekodi mazungumz yao na kupokea kwa neon moja tu “Nakusikiliza,” “Inspekta sasa naona unavuka kiwango, unakumbuka ahadi yangu ya jana kwako?” sauti ya leo ilikuwa ni kali tofauti na ile ya kila siku, Inspekta akajua kuwa leo amemshika pabaya, akazidi kumkera kwa kujidai amesahau na kumuuliza ni ahadi ipi aliyomuahidi jana. “Nazungumzia kuhusu Mwana,” Inspekta akazidi kumchanganya tu kwa maswali ya kebehi. “Mwana? Mwana yupi huyo?” “MwanaJuma Eid ambae wakati huu nipo nae sehemu,” “Ok! Amefanyaje huyo Mwana?” hakika ilikuwa ni ishara ya dharau, akapanic. “Una kiburi sio? Umepata jeuri kutokana na vijihabari ulivyopata si ndio? Sasa leo nakata mzizi wa fitna, na kesho utalipata jibu mapema tu maeneo ya kwa mama , uende ukaokota mzoga wa Mwana, Pumbavu kabisa,” alikuwa na jazba leo. “Name nakukumbusha kuwa leo utalala usingizi wa mwisho uraiani na huyo Mwana atakuwa ndio mtu wa mwisho kwako kumtoa roho, lakini jiandae nawe kwenda kuozea jela,” akacheka sasa Yule mtu kwa kujilazimisha na kusema “Na baada ya Mwana, kama utaendelea kunifuatilia basi jua usiku wa kesho utakua ni zamu yako, nitakutenganisha kila kiungo cha mwili wako, waambie nimesema kuwa kichwa chako nitakiweka Hospitali na mikono nitaipeleka sokoni, huku miguu yako nitaiacha kwako na kiwiliwili nitakipeleka ofisini kwako ili iwe ni fundisho kwa vimbembele wengine,” sauti ya sasa ilikuwa ni nzito sana na hata kufikia kumtisha Jitu. Alipomaliza tu kuongea safari hii akakata simu na kuwaacha wale wapelelezi wawili wakiwa wameketi wanajipanga, Jitu akajiwahi “Huyu mtu mara zote huwa hatanii, tunafanyeje mkuu?” Inspekta hakusema kitu bali akanyanyua simu na kumwambia RCO kuwa anataka kuwatumia wale askari wa kikosi cha CRT yaani Crime Response Team. Akamueleza kuwa amepanga kukitumia kikosi hicho huko maeneo ya Kwa mama Zacharia, akaruhusiwa na kisha yeye na Jitu wakajipanga kuwa usiku ule ni hakuna kulala. Walizunguka kila upande wakiweka ulinzi wa kutosha wakitumia askari wa kikosi tajwa hapo juu, ambacho mara nyingi huwa hakina vazi maalum wakiwa wamelichakaza kabisa eneo lile kwa ulinzi mkali. Saa nane usiku, inspekta alikuwa kituo cha Polisi akiwa na watu wa IT wakijaribu kumtafuta hewani huyo muuaji kwa njia ya mtandao, ghafla kwa mshtuko mkuu, akajishika mfuko wake wa suruali. Ni simu yake iliyoita, ambayo wala hakuitegemea muda ule, akaitoa haraka haraka huku mapigo yake ya moyo yakiwa na kazi zaidi ile ya damu yake, akaitazama na kugundua kuwa safari hii namba iliyompigia, haikuwa ya Yule hayawani. Hii sasa ilikuwa ni namba ya simu ya mkononi, akashusha kidogo munkari na kujilazimisha kutulia na kumsalimia aliepiga “Inspekta Kalindimya upo wapi?” hakujibu salamu mtu huyo bali aliuliza kwa haraka, sauti ilikuwa ni ya kike ikiongea kwa mashaka makubwa. “Wewe ni nani?” aliuliza huku akiitazama ile namba ya simu na kuwaambia wale watu wa mawasiliano waiunganishe kwao, nao wakaiunga na kumwambi aendelee. “Inspekta huwezi kunielewa kwenye simu, tambua leo nimeshinda nyumbani kwako hujaja hadi muda huu, nikatoka na kuelekea hadi kituoni, ofisini kwako napo sijakukuta, nahitaji kuonana nawe usiku huu, maisha yangu yapo mashakani!” aliongea huku akionesha wasiwasi ukiongezeka na tena kwa sauti ya haraka haraka. “Sawa, upo wapi kwa sasa?” alihoji Inspekta huku jamaa wengine nao wakisikiliza. “Wewe ndio uniambie mimi ulipo ili nije sasa hivi, maana mimi nipo mitani tu nikikimbia huku na kule kukutafuta wewe,” ilijibu ile sauti ya kike. “Hata kama nikitaka kukuelekeza mimi nilipo, kwanza ni lazima nijue upo wapi ili kuweka uzani wa kati, tuweze kukutana,” alimfafanulia Kalindimya. “Mimi kwa sasa nipo Manyanya, basi tukutane Studio baada ya muda mfupi,” “Hapana! Njoo vijana Hostel hapa kinondoni, kuna bendi ya Home alone inapiga, nitakuwa kwenye pembe ya mashariki kule nimevaa juba jeusi, ukifika mezani weka simu yako mezani mimi nitakufahamu kama ni wewe,” alitoa maelekezo marefu mtu wa upande wa pili. “Poa!” alijibu Inspekta na ilipokatika tu hiyo simu akampigia simu Jitu na kumwambia wakutane Vijana Hostel kisha akairudisha simu mfukoni.
Mashabiki wa mpira wa miguu wa timu ya Newcastle inayoshiriki ligi kuu ya mpira wa miguu nchini Uingereza walikuwa wamejazana kwa wingi ndani ya uwanja wao wa St’ James Park kwa ajili ya kutazama mechi kati ya timu yao na timu ya Manchester United ambayo ilikuwa ikitarajiwa kufanyika ndani ya uwanja huo. Kelele za mashabiki wa timu ya Newcastle zilikuwa juu sana, wengi walikuwa wameshika mabango mbalimbali ambayo yalikuwa yameandikwa maneno tofauti tofauti ya kumkaribisha mchezaji aliyetoka katika timu ya Genk ya nchini Ubelgiji. “YOU ARE THE BEST IN THE WORLD……MARRY ME FILBERT…..BE MY VALENTINE TONIGHT….WE ARE GOING TO BE CHAMPION THIS SEASON…..” Hayo yalikuwa baadhi ya mabango kadhaa ambayo yalikuwa yameshikwa na mashabiki wa timu ya Newcastle United, mashabiki wa kiume na mashabiki wa kike. Kelele zilikuwa zikizidi kuongezeka, zilikuwa zimebaki dakika ishirini kabla ya timu hizo kuingia uwanjani na kisha mechi hiyo kuanza. Kila shabiki wa timu ya Newcastle bado alikuwa na hamu kubwa ya kumuona mchezaji huyo ambaye alijulikana zaidi katika kuzifumania nyavu za timu pinzani. Filbert Martin, hilo ndio lilikuwa jina la mchezaji huyo ambaye katika siku hiyo ndio ilikuwa siku yake ya kwanza kuichezea timu ya mpira wa miguu ya Newcastle United hapo nchini Uingereza. Filbert alikuwa kijana kutoka nchini Tanzania, kijana ambaye alikuwa na shauku kubwa ya kucheza mpira wa kulipwa katika moja ya nchi ya Ulaya, katika miaka hiyo, ndoto zake zilikuwa zimekwishakamilika. Katika miaka ya nyuma Filbert alikuwa kijana wa kawaida sana ambaye alikuwa na ndoto ya kuwa mwanasheria nchini Tanzania. Alipokuwa akisoma kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Makurumla, kila siku ndoto yake ilikuwa ni kuwa mwanasheria mkuu nchini Tanzania. Kila alipokuwa akisoma, ndoto yake bado iliendelea kukua maishani mwake, alikuwa akijitahidi sana kusoma, hakuona kama angeweza kukamilisha ndoto ya kuwa mwanasheria mkuu nchini Tanzania bila kusoma. Nyumbani kwao hawakuwa na uwezo mkubwa, wazazi wake walifanikiwa kujenga nyumba lakini nyumba hiyo wala haikuwa kubwa, ilikuwa ni nyumba ya kawaida sana na alikuwa akiishi na wazazi wake pamoja na kaka yake mmoja, Denis na dada yake, Rachel. Maisha hayakuwa mazuri sana, mzee Martin hakuwa na fedha za kumfanya kufanya mambo makubwa kwa ajili ya familia yake au kuanzisha biashara kubwa, kitu ambacho kila siku alikuwa akiwasisitizia watoto wake ni kuhusu elimu tu. Ndoto za mzee Martin zilikuwa ni kuwaona watoto wake wakisoma kama alivyokuwa amesoma. Japokuwa hakuwa na fedha nyingi lakini kila siku alikuwa akiamini kwamba endapo mtu ukasoma basi kwa asilimia kadhaa maisha yako yangeweza kubadilika huko mbele kutokana na elimu uliyokuwa nayo kuweza kukubalisha katika mazingira unayoishi. Kila siku kilio chake kilikuwa hicho hicho, watoto wake wasome ili waweze kukamilisha ndoto zao ambazo walikuwa wamejiwekea katika maisha yao. Maneno ya baba yao ndio ambayo yaliwafanya kusoma sana, kila siku Filbert alipokuwa akilala mawazo yake yalikuwa yakifikiria kitu kimoja tu, kuwa mwanasheria mkuu nchini Tanzania. Ndoto yake iliendelea kukaa ndani ya moyo wake mpaka pale ilipokuja kufa na kuanza kujiwekea ndoto nyingine kabisa, ndoto ambayo wala haikuhitaji usome sana, alitamani kuwa mwanasoka mkubwa duniani. Hiyo ndio ndoto nyingine ambayo ilikuwa imekuja moyoni mwake. Ndoto hiyo ilianza kuja mara baada ya kuchaguliwa katika timu ya darasa la kidato cha kwanza shuleni hapo, japokuwa ilikuwa mara yake ya kwanza kucheza mpira katika uwanja mkubwa, Filebrt akaanza kusikia kitu cha tofauti moyoni mwake kuhusiana na mchezo wa mpira wa miguu. Uwezo wake katika ufungaji ulikuwa mkubwa sana, wanafunzi wenzake walionekana kumshangaa kwani uwezo ule ulikuwa umepanda kwa haraka sana. Akatamani kuwa mchezaji mkubwa wa kulipwa duniani, hakutaka kucheza soka nchini Tanzania, kitu alichokuwa akikitaka ni kucheza soka katika moja ya nchi za Ulaya. Kitendo cha kuwa na ndoto hiyo kikamfanya hata uwezo wake wa darasani kupungua, hakuona kuwa na sababu ya kusoma sana na wakati wachezaji wengi wa mpira duniani hawakuwa wamesoma sana. Hakujua ni kwa jinsi gani angeweza kukamilisha kile ambacho alikuwa amejiwekea moyoni mwake. Familia haikuwa na fedha za kutosha za kuweza kumsafirisha kumpeleka katika moja ya nchi za Ulaya kwa ajili ya kucheza soka la kulipwa jambo ambalo lilimfanya kubaki kimya kwani hata kama angemwambia baba yake bado asingeweza kumsafirisha kuelekea barani Ulaya kwa ajili ya kucheza soka. Bado kila siku alikuwa na ndoto ya kucheza mpira katika nchi mojawapo Ulaya. Japokuwa alikuwa na umri mdogo wa miaka kumi na tano, alijitahidi sana kufanya mazoezi huku akiamini kwamba kungekuwa na siku ambayo angepanda ndege na kuelekea Ulaya kwa ajili ya kucheza mpira wa kulipwa. Uwezo wake bado ulikuwa ukimshangaza kila mtu, kila alipokuwa uwanjani alionekana kuwa makini sana. Alikuwa hodari katika kufunga magoli ya kila aina. Alikuwa na uwezo mkubwa wa kutumia miguu yake yote miwili, alikuwa na uwezo mkubwa wa kutumia hata kichwa chake, pamoja na hayo yote, Filbert alikuwa hodari katika kupiga chenga. “Huyu dogo atakuja kuwa mchezaji mzuri sana hapo baadae” Jamaa mmoja ambaye alikuwa akiitazama mechi katik ya timu ya kidato cha kwanza na kidato cha tatu katika uwanja wa shule ya Makurumla alimwambia mwenzake. “Dogo anajitahidi sana. Sasa katika umri kama huu ndio anatakiwa kwenda Ulaya kucheza ila kwa hapa Tanzania, utakuta mpaka anakuwa babu bado yupo humu humu kwenye mechi za mchangani” Kijana mwingine alimwambia mwenzake. Uwezo wake ulikuwa ukiridhisha sana uwanjani kwa kila aliyekuwa akimwangalia. Umakini wake mbele ya goli ulikuwa mkubwa sana, ulimvutia kila mtu ambaye alikuwa akimwangalia. Bado ndoto yake ya kucheza mpira wa kulipwa Ulaya ilikuwa ikiendelea moyoni mwake. Alipoona kwamba bado muda unazidi kwenda na hakukuwa na kitu kilichobadilika, akaamua kumwambia baba yake. “Unajua kucheza mpira kweli?” Mzee Martin alimuuliza Filbert. “Najua sana” “Wewe unajua vipi kama unajua?” Mzee Martin alimuuliza Filbert. “Wengi wanaoniangalia wanasema ninajua” Filbert alijibu. “Sawa. Ila soma, nataka utimize ndoto yako ya kuwa mwanasheria mkuu hapa Tanzania” Mzee Martin alimwambia Filbert. “Sasa hivi nimebadilisha wazo baba” “Wazo gani?” “Nataka kuwa mwanasoka mkubwa duniani. Nataka niende nikacheze Ulaya” Filbert alimwambia baba yake ambaye alibaki akiwa amepigwa na mshangao. “Oooopppssss….!” Mzee Martin alijikuta akishusha pumzi ndefu. “Vipi tena baba? Haiwezekani?” “Inawezekana sana. Kama umeamua inawezekana sana” Mzee Martin alimwambia Filbert. “Nataka kukamilisha ndoto yangu baba” “Usijali. Nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kukufanya kuwa mwanasoka mkubwa duniani” Mzee Martin alimwambia Filbert. Kitu cha kwanza alichokifanya mzee Martin ni kumtafutia uhamisho Filbert kutoka katika shule ya sekondari ya Makurumla na kumpeleka katika shule ya sekondari ya Makongo. Hapo ndipo ambapo Filbert alitakiwa kufanya kile ambacho alikuwa akitaka kukifanya kila siku katika maisha yake. Kutokana na uwezo wake wa kucheza mpira kuwa mkubwa, katika mechi ya kwanza tu shuleni hapo akajikuta akiitwa katika timu ya shule. Mwaka huo alikuwa kidato cha pili. Timu ya shule ilikuwa imejaza wachezaji wa kidato cha tatu na cha nne na ni Filbert tu ndiye ambaye alikuwa mchezaji kutoka katika kidato cha chini. Uwezo wake wa kucheza mpira uliendelea kuonekana kila siku, akafanikiwa kufunga magoli mengi kitu ambacho walimu walionekana kuvutiwa nae. “Nimewaona wanafunzi wengi wakiwa wamepita hapa na kuwa wanasoka, ila kwako, umekuwa mtu wa tofauti sana” Mwalimu Kessy alimwambia Filbert katika kipindi ambacho alikuwa akijiandaa kwa ajili ya kucheza mechi katika mashindano ya Umitashumta. “Asante. Ninataka kutimiza ndoto yangu ya kuwa mwanasoka mkubwa duniani” Filbert alimwambia mwalimu Kessy. “Inawezekana sana. Cha msingi wewe jitume tu, hiyo ndio siri ya mafanikio” Mwalimu Kessy alimwambia Filbert ambaye alizidi kujituma zaidi na zaidi. Kadri muda ulivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo uwezo wake wa kufunga magoli ulivyozidi kuongezeka zaidi na zaidi. Wanafunzi kwa walimu wakatokea kumpenda, wasichana kama kawaida yao wakaanza kumletea shobo lakini Filbert hakuonekana kupenda wanawake, alichokuwa akikitaka ni kuwa mchezaji mkubwa. Japokuwa kila siku alikuwa akiwakataa wanawake lakini mwisho wa siku uvumilivu ukaonekana kumshinda kabisa mara baada ya kujikuta akiingia katika mikono ya mtoto wa kitajiri, Amanda Frank ambaye alikuwa akisoma katika shule ya Kenton iliyokuwa Sinza. Siku ambayo alikutana na msichana huyo ilikuwa ni siku ambayo shule ya Makongo ilipoomba kucheza mechi na shule ya Kenton maombi ambayo yalikubaliwa na wachezaji pamoja na mashabiki wa timu hiyo ya shule kuelekea huko. Wanafunzi wa shule ya Makongo hawakuonekana kuhofia, walikuwa wakijiamini sana, uwepo wa Filbert katika kikosi chao kuliwafanya kujiona kuwa washindi katika kila mechi ambayo walikuwa wakienda kucheza. Siku hiyo ndio ambayo Filbert akaonyesha uwezo wa juu, sauti za wakinadada ambazo zilikuwa zikisikika kwa kusema ‘USINIUMIZIE’ zilikuwa zikimchanganya sana na kujikuta akicheza kwa moyo mmoja. Filbert alionyesha uwezo mkubwa kitu ambacho kilimpelekea kufunga magoli matatu peke yake. Uwezo ule ukawafanya wasichana wengi wa shule ya Kenton kuvutiwa nae. Kila mmoja alikuwa akitaka kumfuata japo kumuomba namba ya simu ila hakukuwa na msichana ambaye alikuwa akijiamini, ni msichana Amanda ndiye ambaye alimfuata Filbert na kisha kuanza kuongea nae. “Hongera” Amanda alimwambia Filbert ambaye akauinua uso wake na kumwangalia msichana huyo, alikuwa Amanda, msichana ambaye alikuwa miongoni mwa wasichana wazuri shuleni hapo. “Asante” Filebrt alijibu na kisha kuyarudisha macho yake chini na kuendelea kufunga kamba za viatu vyake. “Unajua sana kucheza mpira, nani kakufundisha kucheza mpira?” Amanda alimuuliza Filbert ambaye akaachana na kazi ya kufunga kamba za viatu na kumwangalia Amanda usoni. “Sikufundishwa, nimejikuta tu nikijua kucheza mpira” Filbert alimjibu Amanda. “Sawa. Baba yako alikuwa ni mchezaji mpira?” “Hapana” “Au babu yako?” “Mmmh! Sijui” “Sawa. Nimefurahi kuongea nawe” “Usijali” “Ninaitwa Amanda Frank” “Mimi ninaitwa Filbert Martin” “Nimefurahi kukufahamu. Chukua hiki kikaratasi” Amanda alimwambia Filbert na kisha kumkabidhi kikaratasi. “Kina nini?” “Utaona tu kina nini. Utakachokikuta naomba ukifanyie kazi” Amanda alimwambia Filbert. “Naruhusiwa kukifungua hapa?” “Hapana. Kifungue nitakapoondoka” Amanda alimwambia Filbert. Katika kipindi chote ambacho Amanda alikuwa akiongea na Filbert wasichana wengine shuleni hapo walikuwa wakimwangalia kwa macho ya wivu. Nafasi aliyoipata Amanda ilionekana kuwa nafasi adimu sana ambayo kila mmoja alikuwa akiitamani kuipata. Baada ya dakika kadhaa, wanafunzi wa shule ya Makongo wakatakiwa kuingia ndani ya mabasi yao na kuanza kuondoka mahali hapo kupelekwa majumbani kwao. Filebrt alitulia katika kiti chake, kila mmoja katika kipindi hicho alikuwa akiizungumzia mechi hiyo pamoja na uwezo ambao Filbert alikuwa ameuonyesha uwanjani. Uwezo wake ule ndio ambao uliifanya timu ya shule ya Makongo kuibuka na ushindi mnene. Filbert hakuwa mtu wa makuu, hakuringa, alijiona kuwa sawa na wengine. Kile kikaratasi alichopewa na Amanda kilikuwa mkononi mwake, hakuonekana kuwa na habari nacho, stori za mechi ile zilikuwa zimeshika kasi na hivyo kusahau kabisa kukisoma. Gari lilipofika Kijitonyama, Filbert akateremka, akaagana na wenzake na kisha kuelekea nyumbani. Huku akiwa njiani, akakumbuka kwamba alikuwa amepewa kikaratasi na msichana Amanda, alipojiangalia mkononi, kilikuwepo, alichokifanya ni kukifungua na kisha kukiangalia kilikuwa na nini, kilikuwa na namba ya simu ambayo ilikuwa imeandikwa huku chini kukiwa na alama ya kopa, unajua alama hiyo ilimaanisha nini? Ilimaanisha MAPENZI.
Kitendo cha kuiona namba ile ya simu ya Amanda kilionekana kumshtua kupita kawaida, hakutegemea kama kungekuwa na msichana ambaye angeweza kumfanyia kitu kama kile. Katika maisha yake hakutaka kabisa kuwa na msichana yeyote yule lakini kwa jinsi Amanda alivyokuwa alionekana kuwa tofauti sana. Ni kweli alikuwa amewaona wasichana wengi warembo ambao walikuwa na mvuto kupita kawaida, wasichana ambao kila walipokuwa wakitabasamu basi ni lazima moyo wako ungesisimka sana. Kwa msichana kama Amanda, alionekana kuwa tofauti sana, kitendo cha Amanda kuja na kuongea nae na kisha kumgawia kikaratasi kile kilimfanya kufurahi japokuwa hakutaka kukitilia maanani. Hakutaka kumpa nafasi msichana katika maisha yake, aliwakumbuka wachezaji soka wengi ambao walishuka kiwango kwa asilimia kubwa kisa wanawake. Alimkumbuka Gerard Pique, Ronaldinho na watu wengine, kwa wanamichezo kama yeye, wanawake walionekana kuwa chanzo namba moja kwa mchezaji kushuka kiwango. Hakutaka kuwa na msichana kabisa, alijiona kuwa na safari ndefu mbele ya maisha yake, safari ambayo ilihitaji nguvu ya ziada mpaka kufika pale alipotaka kufika. Kitendo cha kuwa na msichana kilimaanisha kwamba angetumia muda mrefu kuwa na msichana kuliko kufanya mazoezi kitu ambacho hakutaka kabisa kitokee. Filbert alibaki akiziangalia namba zile, moyoni mwake taswira ya msichana Amanada ikaanza kumkaa kichwani na kuanza kujiona hali ya tofauti kabisa. Moyo wake ukaanza kujisikia kitu cha tofauti sana, kitu ambacho hakuwahi kukisikia katika maisha yake yote. Mchoro wa kopa ambao ulikuwa ukionekana katika kikaratasi kile ukaonekana kumchanganya kupita kawaida, akawa anauangalia mara mbili mbili huku akionekana kutokuamini kama msichana mrembo kama Amanda angeweza kumwandikia kitu kama kile. Filbert akainuka kutoka kitandani, akaifuata simu yake ambayo alikuwa ameiweka kwenye socketi ya umeme akiichaji na kisha kuichukua na kuiwasha. Katika kipindi hicho lengo lake kubwa lilikuwa ni kumpigia simu Amanda, alijiona kuwa na umuhimu wa kumpigia simu msichana huyo. Akaanza kubonyeza vitufe vya simu ile. Hata kabla hajabonyeza kitufe cha kijani kwa ajili ya simu kuita, Filbert akatulia kwanza na kuanza kufikiria mambo mengi katika maisha yake. Alikuwa akiupenda sana mpira, hakutaka kujihusisha na wanawake kabisa kwa kuamini kwamba uwezo wake wa kucheza mpira ni lazima ungeshuka. Orodha ya wachezaji wa mpira wa miguu ambao walikuwa wameshuka kiwango ikazidi kuongezeka kichwani mwake na mwisho wa siku akajikuta akiitoa namba ile na kuipotezea, kikaratasi akakiweka kabatini. Huo ndio ulikuwa uamuzi wake wa mwisho kujiwekea katika maisha yake, hakutaka kabisa kujihusisha na wanawake kwa kuona kwamba Amanda angeweza kumfanya kushuka kiwango chake na hatimae kuzima ndoto zake za kuwa mchezaji mkubwa wa kulipwa katika moja ya klabu barani Ulaya. “Haiwezekani. Nisije nikawa kama Ronaldinho” Filbert alijisemea. Akaachana kabisa na suala la Amanda na kuanza kufanya mambo yake. Kila siku akawa mtu wa kuamka asubuhi na mapema na kisha kuanza kufanya mazoezi kabla ya kwenda shuleni, Mwili wake ukajengeka sana na kujiona kufaa kabisa kuchezea katika moja ya klabu kubwa hasa za watoto walio chini ya miaka kumi na saba. Makali yake hayakupungua, kila siku yalikuwa yakizidi. Watu wa timu pinzani walikuwa wakimhofia sana Filbert, uwezo wake ulikuwa mkubwa sana kila alipokuwa akikutana na walinzi wa timu pinzani. Filbert hakuonekana kuwa mtu mwenye huruma kila alipokuwa akigusa mpira, mawazo yake katika kipindi chote kilikuwa ni kufunga magoli na kamwe hakuonekana kuridhika hata kama angefunga magoli zaidi ya kumi. Siku ziliendelea kukatika zaidi na zaidi mpaka kufikia simu ambayo wachezaji walio chini ya umri wa miaka kumi na saba ndani ya jiji la Dar es Salaam walikuwa wakihitajika kwa ajili ya kutengeneza timu ya mkoa ambayo ingeshiriki katika mashindano ya Copa Coca Cola. Kwa sababu shule ya Makongo ndio ambayo ilipewa kibali cha kuandaa kikosi cha timu hiyo itakayowakilisha jiji la Dar es Salaam, Filbert alikuwa mtu wa kwanza kujumuishwa katika kikosi hicho. “Kama kweli unajua kucheza mpira, hapo ndipo pa kuonyesha makali yako. Kila siku nitakuwa nakuja kuangalia mechi mnayocheza, ila lengo zaidi ni kukuangalia wewe” Mzee Martin alimwambia mtoto wake, Filbert. “Nitacheza kwa juhudi zote baba” Filbert alimwambia baba yake. “Nataka kila goli utakalofunga liwe zawadi kwa ajili yangu na mama yako” Mzee Martin alimwambia Filbert. “Nitafanya hivyo baba. Ninawapenda sana, hata kama nitafanikiwa kutimiza ndoto yangu, hakika nitakuwa nikiwakumbuka sana na kuwa nanyi bega kwa bega” Filbert alimwambia baba yake. Baada ya wiki tatu mashindano hayo yalianza rasmi. Kama alivyokuwa ameahidi mzee Martin ndivyo alivyofanya. Katika kila mechi ambayo timu ya vijana kutoka jijini Dar es Salaam ilipokuwa ikicheza amzee Martin alikuwepo uwanjani. Uwezo wa Filbert ulionekana kuwa mkubwa kupita washambuliaji wote ambao walikuwa wakicheza katika mashindano yale. Mpaka mashindano yale yanamalizika, Filbert akawa mfungaji bora pamoja na mchezaji bora wa mashindano yale. Hiyo ikaonekana kuwa furaha ndani ya jiji la Dar es Salaam kwa kutoa timu bingwa, mchezaji bora na mfungaji bora. Sherehe ikaandaliwa ndani ya hoteli ya Kilimanjaro ambapo huko rais akaamua kujumuika nao na kisha kuwaahidi watanzania kwamba ingetafutwa timu moja ya taifa ya vijana ambayo ingejumuisha wachezaji kutoka katika timu zote zilizoshiriki na kisha kuelekea nchini Ubelgiji kwa ajili ya kufanya majaribio na timu za huko. “Ni lazima tuwape changamoto wachezaji wetu, natumaini hii itakuwa timu bora ambayo haijawahi kutokea nchini Tanzania” Rais aliwaambia waandishi wa habari. “Wachezaji ambao watateuliwa watapelekwa nchini Ubelgiji, majina yataandaliwa na mchakato mzima utaanza kufanyika kwa ajili ya safari hiyo” Rais aliwaambia waandishi wa habari. Baada ya wiki moja majina ya wachezaji ambao walitakiwa kuunda timu ya taifa ya vijana ya Tanzania ikatangazwa na Filbert kuwa mmoja wa wachezaji hao. Hiyo ikaonekana kuwa furaha kwake na kwa familia kwa ujumla, hakuamini kwamba katika kipindi hicho nae alitakiwa kupanda ndege na kuelekea nchini Ubelgiji kwa ajili ya kwenda kucheza na timu za vijana za nchini humo. “Hapo ndipo pa kujitangaza Filbert” Mzee Martin alimwambia mtoto wake, Filbert. “Nitajitahidi baba. Nitacheza kadri niwezavyo” Filbert alimwambia baba yake. Filbert alijiona kuwa njiani kukamilisha kile alichokuwa akikitamani siku zote katika maisha yake, kuwa mchezaji mkubwa duniani. Kila siku alikuwa mtu wa kufanya mazoezi lakini bado kulikuwa na kitu ambacho kilimsumbua sana kichwani mwake, taswira ya msichana Amanda. Kila alipokuwa akifanya mazoezi, taswira ya msichana huyo ilikuwa ikimjia sana kichwani mwake. Hakuwa amemtafuta simu japokuwa ilikuwa imepita miezi miwili. Hakutaka kumtafuta kwa sababu moyo wake haukuwa tayari kujihusisha na msichana yeyote katika kipindi hicho mpaka pale ambapo angekuja kuwa mchezaji wa kulipwa barani Ulaya. “Amanda….subiri kwanza Amanda mpaka nikamilishe ndoto yangu” Filbert alikuwa akijisemea kila alipokuwa akiiangalia namba ya simu ya Amanda. Hayo yalikuwa ni maamuzi binafsi ambayo alikuwa amejiwekea katika maisha yake, hakutaka kuwa na msichana yeyote pale mpaka pale ambapo angefanikiwa kuwa mchezaji wa kulipwa barani Ulaya. Maisha yaliendelea kila siku mpaka kufikia wiki moja kabla ya wachezaji kuanza safari ya kuelekea nchini Ubelgiji. Filbert alikuwa na imani kubwa moyoni mwake kwamba asingeweza kurudi nchini Tanzania pamoja na wachezaji wenzake, aliamini kwamba kwa jinsi uwezo wake ulivyokuwa mkubwa basi ilikuwa ni lazima kuchukuliwa na timu yoyote ile nchini Ubelgiji. Kila siku alikuwa akiliamini jambo hilo kitu ambacho kilimpelekea kuwa na uhitaji wa kuwasiliana na Amanda hata kabla hajaondoka kuelekea Ubelgiji. ***** Amanda alionekana kuwa mwenye furaha katika kipindi chote hasa mara baada ya kumpa namba ya simu Filbert. Kila siku uso wake ulikuwa na tabasamu pana kwa kuamini kwamba Filbert angeweza kumpigia simu siku yoyote ile kuanzia siku ile ambayo alimkabidhi namba yake ya simu. Kila siku Amanda alikuwa makini na simu yake, kila alipokuwa akiiona namba ngeni ikiingia simuni mwake alikuwa akiipokea kwa mapozi yote lakini mpigaji wala hakuwa Filbert. Zoezi lake la kupokea namba ngeni kwa furaha liliendelea kwa takribani wiki mbili lakini hakukuwa na mafanikio yoyote yale, Filbert hakuweza kumpigia simu. Hilo likaonekana kuwa pigo kubwa moyoni mwa Amanda, moyo wake ukaanza kusononeka sana kwa kujiona kutokuthaminiwa na kusikilizwa. Kitendo kile cha kutokupigiwa simu ndicho ambacho kilimpelekea mara kwa mara kusimama mbele ya kioo na kisha kuanza kujiangalia. Kila siku alikuwa akiitwa msichana mrembo, alikuwaje mrembo na wakati mvulana ambaye alikuwa amempa namba yake ya simu hakuwa amemtafuta kama alivyotaka? Angejiita vipi mrembo na wakati mvulana ambaye alikuwa ametokea kumpenda hakuwa ameonyesha nia ya kuwa nae kama alivyokuwa ameionyesha yake? Amanda akaumia kupita kawaida, upweke ukaanza kumuingia moyoni mwake, hakujiona kuwa na thamani, japokuwa alikuwa mrembo lakini katika kipindi hicho akaanza kuupuzia urembo wake. Kitendo cha Filbert kutokumpigia simu kilikuwa kimemnyong’onyeza kupita kawaida. Amanda hakujua afanye nini, kwenda shuleni Makongo hakuweza kwa sababu kila siku shuleni alikuwa akipelekwa na gari la baba yake na kurudishwa na gari huku kila alipokuwa akiingia nyumbani hakuwa akitoka. “Filbert….Filbert mbona unanifanyia hivi?” Amanda aliuliza huku akilengwa na machozi. Mbele yake aliiona taswira ya Filbert, kila slichokuwa akikiongea aliamini kwamba Filbert alikuwa akimsikia. Siku zikaendelea kukatika kama kawaida, namba ya Filbert haikuingia ndani ya simu yake. Mwezi wa kwanza ukakatika na mwezi wa pili kuingia. Hapo ndipo ambapo aliliona tangazo kwenye gazeti kwamba mashindano ya Copa Coca Cola yalitarajiwa kufanyika ndani ya jiji la Dar es Salaam na hivyo jiji la Dar es Salaam kutoa kikosi chao. Hakujua ni kwa nini alivutiwa na kuliangalia tangazo hilo. Japokuwa hakuwa mfuatiliaji wa mpira kwa sana lakini akajikuta akianza kuliangalia tangazo lile, alipofika katika vikosi vya wachezaji ambao wangeliwakilisha jiji la Dar es Salaam, akapigwa na mshtuko mara baada ya kuliona jina la mtu ambaye alikuwa akimpenda sana, Filber. “Filbert mpenzi wangu….” Amanda alijikuta akiita huku akilitolea macho jina la Filbert ambalo lilikuwa katika gazeti lile. Amanda akaonekana kupewa kazi ya kuanza kufuatilia mashindano ya Copa Coca Cola ambayo yalitarajiwa kuanza baada ya wiki moja. Toka siku ya kwanza mashindano yalianza rasmi, Amanda alikuwa akikaa kitandani kwake chumbani na kisha kuanza kuangalia mpira. Hakupenda mpira na lengo lake halikuwa ni kuangalia mpira bali alikuwa akitaka kumuona mvulana ambaye alikuwa akimpenda kwa moyo wake wote. Kitendo cha kumuona Filbert kwenye luninga akicheza mpira kilimfariji sana, moyoni mwake alikuwa akijisikia amani kupita kawaida, hakuamini kwamba mwisho wa siku alikuwa amemuona mwanaume ambaye alikuwa akimpenda kwa moyo wake wote. “Filbert….Filbert kipenzi naomba unipigie simu mpenzi. Ninaumia moyoni, unaniumiza moyoni kipenzi” Amanda aliita kila alipokuwa akimuona Filbert kwa karibu. Maisha ndivyo yalivyokuwa. Kila siku Amanda alikuwa mtu wa mawazo tu, alimfikiria sana Filbert kiasi ambacho wakati mwingine alijiona akianza kukonda. Moyo wake ulikuwa katika mapenzi juu ya Filbert kwa asilimia moa moja, hakumtaka mwanaume mwingine, kwake, Filbert alionekana kuwa namba moja ambaye wala hakuwa na mpinzani yeyote. Siku ziliendelea kukatika na mashindano yake kumalizika. Zawadi alizozipokea Filbert zilimfurahisha sana Amanda kwa kuona kwamba hatimae mpenzi wake alikuwa amejinyakulia sifa kubwa nchini Tanzania. Moyo haukupoa, tena katika kipindi hicho ndio uliumia zaidi kwa sababu mashindano ya Copa Coca Cola yalikuwa yamemalizika na hivyo asingeweza kumuona tena Filbert. Kama kuumia alikuwa ameumia sana moyoni mwake na kama kuwa na mawazo alikuwa nayo mengi sana juu ya Filbert lakini hali haikuonekana kubadilika kabisa, bado Filbert hakuwa amepiga simu jambo ambalo lilikuwa likimuumiza sana Amanda. Siku zikaendelea kukatika mpaka kufikia siku ambayo Amanda aliisikia simu yake ikianza kuita, alipoichukua na kisha kuangalia kioo cha simu yake, ilikuwa namba ngeni. Kwanza akaonekana kukasirika kupita kawaida. Katika kipindi hicho ambacho alikuwa amechoka hakutaka kupokea simu ya mtu yeyote yule, kitendo cha kusumbuliwa na mtu ambaye namba yake haikuwa ndani ya simu yake kilionekana kumkasirisha kupita kawaida. Alichokifanya ni kubonyeza kitufe cha kijani na kisha kuanza kuita huku sauti ikisikika kuwa na uchovu. “Hallow” Amanda aliita mara baada ya kupokea simu ile. “Hallow! Habari yako Amanda” Sauti ya upande wa pili ilisikika. “Salama. Naongea na nani?” Ambanda aliitikia na kuuliza swali. “Unahisi unaongea na nani?” Sauti ya upande wa pili iliuliza. “Kuna wengi wananipigia siwezi kufahamu naongea na nani” Amanda alijibu. “Unaongea na Martin” “Martin! Martin ndiye nani?” “Filbert Martin” Sauti ya upande wa pili ilisikika. Amanda akauhisi moyo wake ukipiga kwa mshtuko mkubwa, hakuamini kile ambacho alikuwa amekisikia simu mwake. Mara baada ya kukaa kwa muda wa miezi mitatu kwa maumivu makali na majonzi yasiyokwisha moyoni leo hii alikuwa akiisikia sauti ya mtu ambaye aliamini kwamba alikuwa ndiye furaha yake na tumaini lake. Moyo wake ulioshtuka ukaanza kuingiwa na furaha kubwa moyoni mwake, hakuamini kwamba mwisho wa siku mtu ambaye alikuwa akitaka kuisikia sauti yake ndiye ambaye alikuwa amempigia simu. “Filbert….!! Filbert ni wewe?” Amanda aliita na kuuliza, tayari macho yake yakaanza kulengwa na machozi, furaha ikaonekana kumzidi uzito. “Ni mimi….” “Siamini” “Huamini nini?” “Miezi mitatu imepita, kwa nini haukunipigia simu jamani?” Amanda alimuuliza Filbert. “Nilikuwa bize Amanda” “Bize kiasi ambacho ulishindwa hata kuniandikia meseji?” “Naomba unisamehe” “Umeniumiza sana Filbert, nimekaa nikikufikiria wewe kila siku. Kwa nini umekuwa ukinifanyia hivi jamani?” Amanda aliuliza, machozi yakaanza kutiririka mashavuni mwake. “Naomba unisamehe” Filebrt alisikika simuni. “Usijali. Nimekusamehe” Amanda alimwambia Filbert. “Asante sana. Ninatarajia kusaifiri wiki ijayo ila kabla sijasafiri ningependa kuonana nawe” Filbert alimwambia Amanda. ”Hakuna tatizo. Tuonane wapi na lini?” “Nataka tuonane popote utakapo na muda wowote utakao” Filbert alimwambia Amanda. “Tuonane kesho saa tisa alasiri” Amanda alimwambia Filbert. “Hakuna tatizo. Utaweza kutoka nyumbani kwenu?” “Kwa ajili yako tu nitaweza” Amanda alimwambia Filbert. “Sawa. Tuonane sehemu gani sasa?” “Nitakwambia” Amanda alimjibu Filbert. Siku hiyo ikaonekana kuwa siku ya furaha kuliko siku zote katika maisha yake. Amanda hakuamini kama alikuwa ameongea na mtu ambaye alikuwa akimpenda sana, Filbert. Siku hiyo hakutaka kulala mapema, kitu ambacho alikifanya ni kuanza kuchati na Filbert tu. Tayari namba alikuwa nayo kwa wakati huo, tena hakuonekana kuridhika, kila alipokuwa akiiangalia alijiona kama angeweza kuipoteza, alichokifanya ni kuihifadhi katika kitabu chake cha kumbukumbu, kwenye kompyuta yake, akaiandika ndani ya kabati lake, akaandika kwenye email na kisha kujitumia, kwa kifupi ni kwamba hakutaka kuipoteza kabisa. Siku iliyofuatiwa ambayo walitakiwa kuonana, Amanda hakusoma kwa raha darasani, kila wakati alikuwa na mawazo juu ya Filbert tu. Masaa kwake yalionekana kutokwenda kabisa, kila wakati alikuwa akimfikiria Filbert tu. Kila mwalimu ambaye alikuwa akiingia darasani alionekana kutumia muda mwingi kufundisha, kitu ambacho alikuwa akikitaka ni kuona akiondoka shuleni na kwenda kuonana na mtu ambaye alikuwa akitamani sana awe mpenzi wake, Filbert. Dakika ziliendelea kwenda mbele, kila wakati macho yake yalikuwa katika saa yake ya mkononi, siku hiyo mshale wa dakika ulionekana ukisogea taratibu sana, alitamani kuushika na kuupeleka haraka haraka ili masaa yakatike na hatimae kuweza kutoka darasani na kwenda kuonana na Filbert. Dakika zikasonga zaidi na zaidi, vipindi vilipokwisha, akachukua simu yake na kisha kuanza kumpigia baba yake ambaye alikuwa na kawaida ya kumpigia dereva kwa ajili ya kwenda kumchukua Amanda shuleni. “Leo tutatoka saa kumi na mbili” Amanda alimwambia baba yake. “Kuna nini tena?” Sauti ya mzee Frank ilisikika simuni. “Kuna kazi tumepewa tuifanye kama kundi kwa sababu mitihani inakaribia” Amanda alidanganya. “Sawa. Kwa hiyo nimwambie aje saa ngapi?” “Saa kumi na mbili” “Sawa binti yangu. Soma sana utafanikiwa tu” “Usijali baba. Nakupenda” “Nakupenda pia” Hapo Amanda akawa na furaha, kitendo cha kumdanganya baba yake kwamba alitakiwa kufanya kazi pamoja na kundi mpaka saa kumi na mbili kilionekana kumfurahisha kwa kuona kwamba siku hiyo angekaa na Filbert kwa muda mrefu na kuongea bila kusahau kumwambia kile alichokuwa akijisikia juu yake. “Kwa hiyo tuonane wapi?” Sauti ya Filbert ilisikika simuni. “Mlimani City kwenye ukumbi wa Cinema” Amanda alijibu. “Kwa nini iwe huko?” “Nina nguo za shule Filbert” “Sawa. Hakuna tatizo” Filbert alimjibu Amanda na kisha kukata simu. “Oooopppsss…!!” Amanda alishusha pumzi ndefu.
Saa nane na nusu kengele ya kuondoka nyumbani ikagongwa na wanafunzi kutoka na moja kwa moja kuanza kwenda kwenye mabasi kwa ajili ya kupelekwa nyumbani. Amanda hakutaka kutoka darasani, alibaki darasani huku akitaka wanafunzi wapungue na kisha yeye kutoka na kuelekea katika jengo la Mlimani City. Wanafunzi walipopungua vya kutosha, Amanda akatoka darasani na kisha kuanza kuelekea nje ya shule. Moja kwa moja akaisimamisha bajaji ambayo ilikuwa ikipita mahali hapo na kumtaka dereva kumfikisha Mlimani City. “Elfu tano” Dereva alimwambia Amanda. “Usijali. Wewe twende tu” Amanda alimwambia dereva. Safari ya kuelekea Mlimani City ikaanza, muda wote Amanda alikuwa akimfikiria Filbert. Hakuamini kama siku hiyo alikuwa akienda kuonana na mwanaume ambaye alikuwa akitamani sana japo kukaa nae kwa dakika kadhaa, Filbert. Kama kummisi moyoni mwake alikuwa amemmisi vya kutosha na katika kipindi hicho alikuwa akitaka kumwambia ukweli kuhusiana na hali iliyokuwepo moyoni mwake. Mapenzi yalikuwa yamemlevya, alijihisi kuwa tofauti sana moyoni mwake, Filbert alionekana kuwa mwanaume maalumu ambaye aliletwa katika maisha yake na kuwa nae katika kipindi chote. Mzigo mzito wa mapenzi juu ya Filbert ulikuwa umemuelemea na alimhitaji mtu huyo kwa ajili ya kuushusha mzigo huo mzito. Mara baada ya kufika karibu na eneo la jengp la Mlimani City, Amanda akateremka, akamlipa dereva kiasi cha fedha alichokuwa akikihitaji na kisha kuanza kuelekea ndani ya eneo la jengo hilo. Muda wote Amanda alionekana kuwa na furaha, kitendo cha kutaka kuonana na Filbert siku hiyo kilionekana kumuwekea furaha moyoni mwake, furaha ambayo hakuwahi kuwa nayo kabla. Alichokifanya ni kuelekea katika sehemu ya kukata tiketi na kisha kukata tiketi za watu wawili kwa ajili ya kuangalia filamu mpya ambayo ilikuwa imetoka katika kipindi hicho, MY LATE MOM iliyokuwa imeigizwa na muigiza Matt Damon. Hakuishia hapo, alipokata tiketi zile, akanunua na bisi kwa ajili ya kula ndani ya ukumbi huo wakati wanatazama filamu. “Upo wapi?” Amanda alimuuliza Filbert katika kipindi ambacho aliamua kumpigia simu kwa kuwa aliona muda ukienda bila kuonekana mahali hapo. “Ndio nimeshuka kutoka katika daradala katika kituo cha Remmy, hapa ninatembea kuja huko” Filbert alimwambia Amanda. “Sawa. Wahi, filamu ishaanza” “Kuna filamu gani hapo?” “My Late Mom” “Mmmh! Hiyo sijawahi kuiona. Ina ngumi?” “Sidhani. Ni kama filamu fulani ambayo inahusu sana maisha” Amanda alimjibu Filbert. “Sawa nakuja. Ila ingekuwa in ina ngumi ingekuwa raha sana” “Usijali, siku nyingine tutakuja kuangalia filamu ya ngumi” Amanda alimwambia Filbert na baada ya maongezi ya hapa na pale kukata simu. Wakati huo Filbert alionekana kuwa kila kitu moyoni mwake, kitendo cha kuisikia sauti yake tu kiliuridhisha moyo wake. Amanda akaanza kuelekea katika sehemu iliyokuwa na mabenchi ya kisasa na kisha kukaa huku akimsubiria Filbert. Wala haukupita muda mrefu, Filbert akafika mahali hapo, kitu cha kwanza walichokifanya ni kukumbatiana japokuwa kwa Filbert alionekana kujishtukia. “Unanukia vizuri” Filbert alimwambia Amanda. “Asante Filbert. Umependeza” “Hahaha! Acha kunitania. Yaani kuvaa jezi ya Arsenal ndio nimependeza?” “Kweli tena. Halafu umebadilika sana” “Nimekuwaje?” “Mzuri. Mzuri zaidi ya kipindi cha nyuma” Amanda alimwambia Filbert ambaye hakuongea kitu chochote zaidi ya kubaki kimya. Wakaanza kupiga hatua kuelekea katika mlango wa kuingia ndani ya jumba la Cinema na kisha kutulia katika sehemu moja mpaka pale ambapo filamu hiyo ilipoanza kuonyeshwa. Katika kipindi chote cha kuangalia filamu hiyo, mawazo ya Amanda yalikuwa kwa Filbert tu, alikuwa akijifikiria ni kitu gani ambacho alitakiwa kuongea mahali hapo. Mtu ambaye alikuwa amemsubiria kwa kipindi kirefu tayari alikuwa amefika na kuwa karibu nae na ni yeye tu ndiye ambaye alikuwa akisubiriwa kuongea kile ambacho kilikuwa kikimsumbua moyo wake katika kipindi kirefu. “Sina hamu ya kuangalia filamu” Amanda alimwambia Filbert, filamu ndio kwanza ilikuwa imefika katikati. “Kwa nini? Mbona ni filamu nzuri tu?” “Natamani sana kuongea na wewe” Amanda alimwambia Filbert. “Ok! Hakuna tatizo” “Uliniambia kwamba unataka kusafiri, unataka kwenda wapi?” Amanda alimuuliza Filbert. “Nataka kwenda Ubelgiji” “Ubelgiji?” “Ndio” “Kufanya nini?” “Kucheza soka” Filbert alimwambia Amanda. “Na utarudi lini?” “Sijajua” “Mmmh!” “Nini tena Amanda” “Umepata timu huko au kuna ndugu yako?” Amanda alimuuliza Filbert. “Sina ndugu Ulaya” “Sasa nani atakupokea?” “Nitakwenda na timu ya taifa ya vijana wa Copa Coca Cola” Filbert alimwambia Amanda. “Ndio ile aliyoizungumzia rais?” “Ndio hiyo hiyo” “Sasa si wiki mbili tu jamani, au unataka kuzamia?” “Hapana. Ninaishi katika imani” Filbert alimwambia Amanda. “Kivipi?” “Kwamba nitapata timu” Amanda akanyamaza, maneno aliyoyaongea Filbert yalionekana kuwa mazuri kwa kila mtu ambaye angeyasikia lakini kwa Amanda yalionekana kuwa kama mwiba mkali moyoni mwake. Alikuwa akimpenda sana Filbert, hakutaka mwanaume huyo aondoke mikononi mwake, alikuwa akihitaji kuwa nae zaidi na zaidi na ikiwezekana hata kufunga ndoa kanisani na kuwa mume na mke. “Kwa hiyo ukipata timu ndio hatutoonana tena?” Amanda alimuuliza Filbert huku akionekana kuwa mpole. “Tutaonana. Kutakuwa na vile vipindi ambavyo msimu wa mechi unakwisha, nitakuwa nakuja na kuonana nawe Amanda” Filbert alimwambia Amanda. “Sawa” Amanda aliitikia kinyonge. Tayari furaha aliyokuwa nayo kipindi kifupi cha nyuma ikayeyuka moyoni mwake, alikwishajua kwamba hicho ndicho kilikuwa kipindi cha mwisho mwisho kuonana na Filbert na hivyo hakutakiwa kuifanyia mzaha kila nafasi ambayo alikuwa ameipata. Bila kutarajia na bila uoga wowote ule Amanda akaanza kumshikashika upaja Filbert hali ambayo ikamfanya kushtuka. “Vipi tena Amanda?” Filbert aliuliza huku akionekana kushtuka, akautoa mkono wa Amanda pajani kwake. “Ninakupenda Filbert” Amanda alimwambia Filbert. “Unanipenda? Nashukuru Amanda” Filbert alimwambia Amanda. “Filbert naomba uwe mpenzi wangu” Amanda alimwambia Filbert kwa sauti ya chini. “Amanda! Upo sawa kweli?” Filbert alimuuliza Amanda, yaani alijifanya kama kushtukizwa na wakati alikuwa akifahamu kila kitu ambacho kingeweza kutokea au kuambiwa na Amanda. “Nipo sawa Filbert. Ninakupenda sana na ninataka uwe mpenzi wangu” Amanda alimwambia Filbert kwa sauti ya chini iliyojaa mahaba. “Hapana Amanda. Hivi unajua kwamba mimi ni mcheza soka?” Filbert alimuuliza Amanda. “Najua” “Unajua matatizo wanayokutana nayo wanasoka mara wanapokuwa na wanawake?” Filbert alimuuliza Amanda. “Hapana” “Mwanasoka unapokuwa na mwanamke, kwanza uwezo wako uwanjani unashuka sana, magoti yatakuwa yakilegea sana” Filbert alimwambia Amanda. “Kwa hiyo mchezaji wa mpira hatakiwi kuwa na mwanamke?” Amanda alimuuliza Filbert. “Hiyo ndio maana yangu” “Mbona huko Ulaya wanaoa sasa?” “Wale wamekuwa professional Amanda ila si kwa mtu kama mimi ninayechipukia” Filbert alimwambia Amanda. “Nimekuelewa. Nikuulize swali?” “Uliza tu” “Unanipenda?” “Unamaanisha nini?” “Hivyo hivyo ulivyofikiria kichwani mwako. Unanipenda?” “Amanda….Amanda mbona unakuwa na haraka hivyo?” “Lazima niwe na haraka Filbert. Unaondoka kuelekea Ubelgiji na umesema kurudi huku mpaka msimu uishe, hauoni kwamba hii ndio nafasi yangu ya kukwambia kila kitu ninachojisikia kukwambia kuhusiana na mapenzi?” Amanda alimwambia Filbert. “Najua Amanda. Najua huu ni wakati wako” “Basi naomba uniambie” “Ila naona kama bado mapema sana” “Kivipi?” “Tuna nafasi ya kuendelea kuwa marafiki wa kawaida kabla ya kuingia katika mahusiano ya kimapenzi” Filbert alimwambia Amanda. “Tatizo lipo pale pale Fulbert. Unaondoka wewe na hautegemei kurudi karibuni, hivi unadhani utaniacha katika hali gani?” Amanda alimuuliza Filbert, wakati huo wote wawili walikuwa wakiongea kama watu wazima. “Amanda….!!” “Unataka kwenda kuoa mzungu?” “Hapana” “Labda ndicho unachokitaka na ndio maana unakataa kuwa nami Filbert” Amanda alimwambia Filbert, katika kipindi hicho alikuwa amekwishabadilika, macho yake yalikuwa yamekwishaanza kulengwa na machozi. “Umenielewa vibaya Amanda” “Nakuomba uwe mpenzi wangu Filbert” “Amanda….mbona unakuwa na haraka” “Nilikwishakwambia sababu zinazonifanya kuwa na haraka. Kwanza naomba unijibu swali langu, unanipenda?” Amanda alimuuliza Filbert. “Ooopppsss…!! Unaonekana kutokunielewa Amanda” Filbert alimwambia Amanda. “Naomba unijibu kwanza” “Nilikwishakujibu kabla” “Hapana, haukunijibu na hata kama ulinijibu sikusikia. Unanipenda?” Amanda alimwambia Filbert na kumuuliza. “Ninakupenda” “Asante. Naomba uwe mpenzi wangu” “Utavumilia?” “Kuvumilia nini?” “Nitakuwa mbali na Afrika. Utavumilia kuwa peke yako mpaka nitakaporudi?” Filbert alimuuliza Amanda. “Kama utachaguliwa na timu yoyote ile nitavumilia. Ukichelewa nitakuja huko huko Ubelgiji” Amanda alimwambia Filbert. “Kuja kufanya nini?” “Kukuona mpenzi wangu na pia kusoma chuo” “Mmmh! Aya” “Umemaanisha nini kusema aya?” “Nimeridhika na maneno yako” “Kwa hiyo umekubaliana nami?” “Sina jinsi. Kama umeridhika, nimekubaliana nawe Amanda” “Kwa hiyo leo hii ndio tumeufungua ukurasa wa kimapenzi pamoja?” “Bila shaka” Hiyo ikaonekana kuwa nafuu kwa Amanda, akashusha pumzi ndefu, hakuamini kwamba kile ambacho alikuwa akikitamani kwa muda mrefu leo hiyo ndio kilikuwa kimetimia. Kuanza mahusiano na Filbert kilikuwa ni kitu ambacho kilimfanya kuwa na furaha sana, bila kuogopa macho ya watu ambao walikuwa bize wakiangalia filamu, Amanda akambusu Filbert mdomoni. Huo ndio ukawa mwanzo wa mahusiano yao ya kimapenzi, huo ndio ukawa mwanzo wa mahusiano ambayo yalikuwa yenye kuumiza na kukera, yalikuwa ni mahusiano ambayo yalikuwa ni mwanzo wa moja ya filamu ya ngono ambayo ilirekodiwa na kutaka kusambazwa Tanzania nzima ili watu waone uchafu wa mtu ambaye alikuwa akiaminika na kukubalika sana nchini Tanzania. Yalikuwa ni mahusiano ambayo yalisababisha mambo mengi yenye kutisha. Hawakuonekana kujali, katika kipindi hicho kitu ambacho walikuwa wakikijali ni kuwa katika mahusiano ya kimapenzi tu, hawakujua kabisa kuhusiana na skendo ya video ya ngono ambayo ingeweza kurekodiwa kutokana na mahusiano hayo kuanzishwa siku hiyo ndani ya ukumbi huo wa Cinema ndani ya jengo la Mlimani City.
Je nini kitaendelea? Je mahusiano hayo yataweza kudumu? Je mahusiano haya yalisababishaje hii skendo ya filamu ya ngono?
Simulizi : A Sex Video Scandle Sehemu Ya Pili (2) Mawasiliano yakawa yameanza rasmi kati ya Filbert na Amanda. Kila siku walikuwa ni watu wa kupigiana simu na kuzungumza mengi kuhusiana na mapenzi. Kila mmoja alionekana kumjali na kumsikiliza mwenzake, mapenzi yao machanga yakaonekana kuanza kuchipua kwa kasi sana, kasi ambayo iliwashangaza hata wao wenyewe.Kila siku wakawa watu wa kupigiana simu usiku na kutumia muda mwingi wa kuzungumza pamoja. Katika kipindi hicho ndicho ambacho kilimfanya Amanda kuchelewa sana kulala, kila siku alikuwa akilala saa nane usiku kwani muda wote alikuwa akiongea na Filbert simuni. Filbert ndiye alionekana kuwa kipenzi chake cha moyo wake, kila siku Amanda alijiona kuwa malikia huku akimchukulia Filbert kuwa mfalme. Mapenzi yalikuwa yamewalevya wote, wakajikuta kila siku wakizidi kuogelea katika dimbwi kubwa la mahaba.Filbert hakusahau, alikuwa akikumbuka sana kwamba siku chache zijazo alikuwa akitarajia kusafiri na kuelekea Ubelgiji. Kwenda ulaya ndio ilikuwa sehemu ya ndoto ambazo alikuwa amejiwekea moyoni mwake, kwa sababu alikuwa mcheza soka, alikuwa akitamani kwenda kucheza soka katika nchi mojawapo ulaya.Filbert hakutaka kuikatisha ndoto yake kwa sababu ya mapenzi, japokuwa alijua fika kwamba alikuwa akimpenda sana Amanda lakini hakutaka kuikatisha ndoto yake hiyo kwa ajili ya msichana huyo. Bado mapenzi aliyaona kuwa na sehemu yake lakini hata mpira nao ulikuwa na sehemu yake.“Nataka tufanye mapenzi” Amanda alimwambia Filbert.“Tufanye mapenzi?” Filbert aliuliza kwa mshtuko.“Ndio” Amanda alijibu kwa sauti ya chini.“Haiwezekani Amanda. Kwa sasa hivi ni ngumu sana mpenzi” Filbert alimwambia Amanda.“Nakuomba mpenzi. Mwili unanisisimka kila ninapoisikia sauti yako” Amanda alimwambia Filbert.“Najua mpenzi lakini naomba unipe muda”“Muda wa nini tena?”“Wa kupata nafasi ya kucheza soka Ulaya”“Kwani si unakwenda huko keshokutwa mpenzi, kwani nimekuzuia?”“Najua haujanizuia. Ila tukifanya najua magoti yangu yatalegea sana. Acha nipate nafasi kwanza, baada ya hapo tutafanya mapenzi mpaka uchoke” Filbert alimwambia Amanda.“Ninapata tabu sana usiku mpenzi” “Najua Amanda. Vumilia kipenzi changu, vumilia tu” Filbert alimwambia Amanda.Amanda alikuwa akipata tabu kila siku, mwili wake ulikuwa ukimsisimka kupita kawaida, kila siku alikuwa akitamani kufanya mapenzi na mwanaume, mwanaume pekee ambaye alikuwa akimpenda na kumhitaji sana, Filbert. Amanda hakuwa akilala vizuri usiku, muda mwingi alikuwa akiyachezea matiti yake kila alipokuwa akilala kitandani, tena alikuwa akipenda kulala mtupu kabisa.Ndoto za kufanya mapenzi ndizo ambazo zilikuwa zimemtawala muda huo, hakutaka kuendelea kubaki katika hali hiyo na ndio maana aliamua kumwambia Filbert ukweli juu ya alivyokuwa akijisikia japokuwa Filbert hakutaka kuelewa kabisa.Filbert alikuwa na ndoto moyoni mwake, ndoto ambayo aliiona ikikaribia kukamilika kwa wakati huo, alikuwa akitaka kuwa mmoja wa wachezaji soka wa kulipwa katika nchi mojawapo ndani ya bara la Ulaya. Uwezo wake wa kucheza mpira ulikuwa mkubwa sana kiasi ambacho hakujiona kama alistahili kucheza mpira hapa barani Afrika. Kila siku alikuwa akiamini kwamba kuwa na mwanamke ndio kilikuwa chanzo cha wanasoka wengi kushuka viwango.Filbert hakuwa na lengo la kuwa na mwanamke lakini mara baada ya Amanda kumuonyeshea uhitaji mkubwa, akajikuta akikubali kuwa nae. Sasa hivi Amanda alikuwa amemwambia kitu kingine kabisa, kufanya mapenzi kama wapenzi wengine walivyokuwa wakifanya. Huo ukaonekana kuwa mtihani mkubwa kwa Filbert, ni kweli alikuwa amemkubalia Amanda kuwa mpenzi wake lakini hakujiona kama alikuwa tayari kufanya mapenzi na msichana huyo.Kitu ambacho alikuwa akikiogopa ni kushuka kiwango katika uwanja wa mpira. Alijua fika kwamba endapo angethubutu kufanya mapenzi na msichana Amanda basi kwa namna moja au nyingine ni lazima magoti yake yangepungua kufanya kazi na mwisho wa siku kulegea kabisa na hivyo kushusha uwezo wake wa kusakata kabumbu uwanjani. Hiyo ndio ilikuwa sababu kubwa ambayo ilimfanya Filbert kukataa katakata kufanya mapenzi na Amanda, kila siku alijiona kutaka kuwa katika uwezo wa juu mpaka pale atakaposajiliwa na timu kubwa yoyote ile barani Ulaya.“Kwa hiyo tutafanya lini?” Amanda alimuuliza Filbert.“Nikirudi kutoka Ubelgiji” Filbert alimwambia Amanda.“Sawa. Ila uliniambia kwamba usingerudi sasa hivi” Amanda alimwambia Filbert.“Nitarudi tu, wewe vumilia kwanza mpenzi, tatizo lipo wapi? Nimekuwa wako kwa hiyo hutakiwi kuhofia kitu chochote kile” Filbert alimwambia Amanda.“Sawa…ila unanifanya kujisikia vibaya sana mpenzi. Nina hamu sana” Amanda alimwambia Filbert.“Umekwishawahi kufanya mapenzi?”“Hapana”“Sasa hiyo hamu inatoka wapi?”“Jamani mpenzi, si nina mwili na pia nina kila kitu ambacho msichana anatakiwa kuwa nacho” Amanda alimwambia Filbert.“Kwa maana hiyo wewe ni bikira?”“Ndio”“Safi. Naomba uitunze mpaka nitakaporudi. Utaweza kuitunza?” Filbert alimwambia Amanda na kumuuliza.“Kwa ajili yako nitaweza mpenzi. Ila usichelewe kurudi” Amanda alimwambia Filbert.“Kwani nikichelewa nitakuta imetolewa?”“Hapana bali nitakuwa nikipata tabu zaidi ya kutamani kuwa pamoja nawe” Amanda alimwambia Filbert.“Naomba uitunze kwa ajili yangu”“Usijali laazizi…ila naomba usiniumize huko mbeleni”“Usijali. Sitokuumiza, nitayakumbuka mapenzi yako kila siku.Maneno mengi ya faraja ambayo walikuwa wakiambiana yalionekana kumfariji kila mmoja. Kila wakati walikuwa wakitamaniana sana kiasi ambacho walikuwa wakichukia sana kwa sababu gani mpaka katika kipindi hicho bado walikuwa wakiishi kwa wazazi. Kwa upande wa Amanda, darasani hakuwa akisoma kwa raha, kila wakati mawazo yake yalikuwa kwa mvulana wake ambaye katika kipindi hicho alionekana kuwa kila kitu, Filbert.Kama ambavyo mapenzi yalivyojulikana kwamba yalikuwa kikohozi, marafiki zake wakaanza kufahamu juu ya mapenzi hayo. Amanda akashindwa kabisa kujizuia jambo ambalo likamfanya kumwambia rafiki yake mpendwa, Happiness. Mara ya kwanza Happiness alionekana kushtuka sana, alimfahamu vilivyo Amanda, alionekana binti mrembo na mkimya sana ambaye wala hakuwa akijihusisha na mwanaume kabisa, katika kipindi hicho ambacho alisikia kwamba Amanda alikuwa na mpenzi, Happiness alionekana kushtuka sana.“Una mpenzi?” Happiness aliuliza huku akionekana kushtuka.“Ndio”“Yupo wapi?”“Makongo Secondary School”“Umeonana nae vipi na wakati huwa hautoki nyumbani?” Happiness alimuuliza Amanda.“Siku ile walivyokuja kucheza mpira”“Au unamzungumzia yule aliyefunga magoli siku ile?”“Yeah! Anaitwa Filbert”“Waoooo! Una bahati Amanda. Lucy na wenzake walikuwa wakimzungumzia sana” Happiness alimwambia Amanda.“Walisemaje?”“Eti ni mwanaume mzuri ambaye ana umbo linalomvutia kila mwanamke. Hebu niambie vizuri kuhusu yeye” Happiness alimwambia Amanda.“Unataka kujua nini kuhusu yeye?”“Chochote kile”“Ni mzuri sana, halafu anajua kupenda”“Kweli?”“Ndio hivyo”“Kweli una bahati sana Amanda kwani wanaume wengine majanga” Happiness alimwambia Amanda.“Kwani wewe na John vipi?”“Mmmh! Yaani ni balaa. Sijawahi kuwa na mwanaume anayependa sketi kama yule. Kila sketi inayopita mbele yake anaitamani. Yaani ni balaa” Happiness alimwambia Amanda.“Pole sana”“Asante sana”Hao walikuwa wanafunzi wa kidato cha pili, japokuwa walikuwa wadogo lakini katika masuala ya mahusiano walikuwa wakiyapenda na kushika nguvu katika maisha yao. Kila mmoja alikuwa na mpenzi wake ambaye alikuwa akimpenda kwa moyo wa dhati. Walikuwa wakiendelea kusoma huku katika upande mwingine wa maisha yao wakiwa wameyaacha mapenzi yachukue nafasi.Siku hiyo ikapita na kubaki siku moja kabla ya timu ya mpira ya vijana kuondoka kuelekea nchini Ubelgiji. Kwa Filbert ilikuwa ni furaha tupu, kila wakati alikuwa akiwaambia wazazi wake kwamba ile ndio ilikuwa nafasi yake ya kubadilisha maisha yake na maisha ya familia yake. Alionekana kuwa mwingi wa furaha, kila wakati alikuwa akiwataka wazazi wake wamtamkie maneno ya baraka hata kabla hajasafiri kuelekea nchini Ubelgiji.Wakati Filbert akiwa na furaha, kwa Amanda moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali mno. Alikuwa ahamini kama mpenzi wake ambaye alikuwa amedumu nae katika mahusiano kwa kipindi cha wiki mbili alikuwa akitaka kuondoka kuelekea nchini Ubelgiji na hivyo kumuacha katika hali ya mawazo na maumivu makali. Kila siku sala yake ilikuwa ni kuona akikaa na Filbert kwa zaidi na zaidi, hakutaka kumuacha na wala hakutaka kuona mtu huyo akienda mbali nae. Sala yake ikaonekana kutokujibiwa, yalikuwa yamebaki masaa ishirini na saba kabla ya Filbert kuondoka na timu nzima ya vijana kuelekea nchini Ubelgiji kwa ajili ya kuchukua mazoezi kwa muda wa wiki mbili.“Sina cha kufanya. Siwezi kusema nisiende huko mpenzi, ni lazima niende nikajaribu bahati yangu” Filbert alimwambia Amanda.“Nakupenda mpenzi”“Nakupenda pia. Ila hautakiwi kulia, yakupasa kufurahia kwani kama nitabadilisha maisha yangu na kuwa ya juu, basi amini hata maisha yako nawe yatakuwa hivyo hivyo” Filbert alimwambia Amanda.Katika kipindi hicho walikuwa Kijitonyama, katika mtaa ambao Filbert alikuwa akiishi lakini si ndani ya nyumba ya mzee Martin. Filbert alikuwa amekaa na Amanda katika chumba cha rafiki yake, Enock ambaye hakuwa akiishi mbali kutoka katika nyumba ya mzee Martin.Siku hiyo Amanda hakutaka kwenda shuleni japokuwa alikuwa ameaga kwamba angekwenda shuleni. Safari yake ya kuelekea shuleni iliishia katika mtaa wa Kijitonyama, alijiona kuwa na muda mwingi wa kukaa na mpenzi wake na kuongea mambo mengi kuhusiana na maisha yao ya mahusiano. Siku hiyo walikuwa kitandani, kipindi chote Amanda alikuwa amelala kifuani mwa Filbert. Mwilini alikuwa na nguo za nyumbani, nguo za shule ambazo alikuwa amezivaa siku alipotoka nyumbani kwao hakuwa nazo mwilini bali alikuwa ameziweka katika begi lake. Hakuona sababu ya kwenda shule na wakati mpenzi wake alikuwa akisafiri kuelekea Ubelgiji siku inayofuatia.“Hivi unajua kwamba hii ni kesi?” Filbert alimuuliza Amanda.“Kesi ipi?”“Kutokwenda shule na kuja kwangu”“Najua”“Sasa unataka niingie kwenye matatizo?”“Hapana”“Ulifika shule leo?”“Niliishia getini. Baada ya kushushwa kutoka garini, nikaondoka zangu” Amanda alimwambia Filbert.“Mchezo mbaya sana huo. Usijaribu kuufanya siku nyingine” Filbert alimwambia Amanda.“Kwani umekasirika kuniona mahali hapa?”“Hapana”“Sasa kwa nini uwe mchezo mbaya?”“Ungeweza kunifanya nisiende Ubelgiji, ungeweza kuzizima ndoto zangu mpenzi” Filbert alimwambia Amanda.Walibaki wakiongea mambo mengi, walibuasiana na kushikana hapa na pale lakini hawakufanya mapenzi. Japokuwa Amanda alikuwa aking’ang’ania mara kwa mara kwamba kama wapenzi walitakiwa kufanya mapenzi lakini kwa Filbert jambo hilo lilikataliwa kwa nguvu zote moyoni mwa Filbert. Bado mawazo yake yalikuwa juu ya mchezo wa mpira wa miguu, hakutaka kufanya mapenzi kwa kuona kwamba nguvu zake za miguu zingeshuka kwa kiwango kikubwa sana, alitaka kwanza kutafuta mafanikio.“Kwa hiyo, hiyo safari itakuwaje?”“Tunakwenda kulala hotelini leo na kesho asubuhi safari” Filbert alimwambia Amanda.“Unakwenda saa ngapi hotelini?”“Saa mbili usiku”“Kwa hiyo nikiondoka hapa ndio basi tena hatutoonana mpaka utakaporudi?” Amanda alimuuliza Filbert.“Nafikiri” Filbert alimjibu Amanda.Kama alivyosema Filbert ndivyo ilivyokuwa. Saa mbili usiku siku hiyo akawaaga wazazi wake na ndugu zake na kisha kuingia ndani ya gari la wachezaji na safari ya kuelekea hotelini kuanza. Ndani ya basi hilo kulikuwa na baadhi ya wachezaji kwani wengine bado hawakuwa wamepitiwa. Kila mmoja ndani ya basi alionekana kuwa na furaha, walikuwa wakiongea huku wakionekana kutokuamini kama kweli siku hiyo ndio ilikuwa siku ambayo walikuwa wakielekea Ulaya kwa ajili ya kufanya mazoezi ya kujiweka fiti.“Tukifika huko tutawaandalia mechi kadhaa, jitahidi sana kucheza kwa uwezo wa juu, huwezi jua, hii inaweza kuwa nafasi yako ambayo haitoweza kutokea tena katika maisha yako” Kocha wa timu hiyo, Abdulazak aliwaambia wachezaji.“Kama wewe ni mshambuliaji, funga magoli ya kutosha, kama wewe ni kipa, daka vya kutoka, kama wewe ni kiungo, kaba na kugawa mipra uwezavyo na hata kama wewe ni beki, zuia uwezavyo. Japokuwa tunakwenda ishirini na tano huko, nata turudi sisi tu, wachezaji wote tuwaache huko wakiwa wamenunuliwa na timu mbalimbali” Kocha mkuu aliongezea.Maneno hayo yalionekana kuwa kama sumu mioyoni mwa wachezaji, kila mmoja akaonekana kuwa na chachu ya kuonyesha uwezo mkubwa mara baada ya kuanza kucheza mechi za majaribio nchini Ubelgiji. Kila wakati wachezaji walikuwa wakipena amaneno ya hamasa ya kutiana nguvu.“Nitahakikisha nabaki Ubelgiji, huku bongo hakunifai” Filbert alimwambia rafiki yake ambaye nae alikuwa amechaguliwa, Steven.“Nakuamini sana, unaweza kufanya unachokisema, cha msingi jitume zaidi, funga magoli uwezavyo” Steven alimwambia Filbert.Filbert bado alikuwa na furaha isiyo kifani moyoni mwake, ndoto ambayo alikuwa ameipanga itokee katika maisha yake ilikuwa ikielekea kutimia na ni juhudi binafsi tu ndizo ambazo zilikuwa zikihitajika katika kipindi hicho. Moyo wake uliamini kwamba maisha yake yalikuwa ni mpira, aliamini mambo mengi katika maisha yake yangeweza kutimia endapo angeweza kufanikiwa kuwa mchezaji mkubwa wa kulipwa. Kwa sababu alikuwa amekataa kufanya mapenzi na msichana Amanda, alitaka kuhakikisha kwamba anachaguliwa kujiunga na timu yoyote ile ili aone kwamba kulikuwa na maana kubwa sana kukataa kufanya mapenzi na Amanda, msichana aliyekuwa akimpenda sana. Ulikuwa ni mwezi wa kumi na mbili, kipindi ambacho kilikuwa na baridi kali katikanchi nyingi barani Ulaya. Theluji zilikuwa zimemwagika ardhini, magari ambayo yalikuwa maalumu kwa ajili ya kusafisha barabara kwa kuondoa theluji ambazo zilikuwa zimefunika ardhi yalikuwa yakifanya kazi yake kama kawaida katika kutoa theluji zote ili barabara zionekane na hivyo magari yaweze kupita kama kawaida.Katika kipindi hicho ndicho ambacho ndege ya shirika la Fly Emirates ilikuwa ikitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Brussels uliokuwa ndani ya jiji la Brussel. Hali ya hewa bado ilikuwa ni ya ubaridi mkali katika kipindi hicho, wafanyakazi wengi wa hapo uwanja wa ndege walikuwa wamevaa makoti mazito huku wakiendelea kufanya kazi zao kama kawaida.Ukungu mzito ulikuwa umetawala katika sehemu kubwa ya jiji la Brussel, theluji ambazo zilikuwa zimedondoka kwa wingi zilikuwa zikionekana kukusanywa sehemu moja. Lami ndani ya uwanja huo wa ndege ilikuwa ikionekana vizuri japokuwa napo bado theluiji ilikuwa ikiendelea kudondoka kutoka angani.Wachezaji wa mpira wa timu ya taifa ya vijana walikuwa ndani ya ndege. Kila mmoja alikuwa amekabidhiwa koti zito kutokana na kujulikana kwamba mwezi wa kumi na mbili bara zima la Ulaya huwa katika kipindi cha baridi kali. Kila mmoja akaonekana kuhofia, hasa Filbert pamoja na baadhi ya wachezaji ambao walikuwa wametoka katika jiji la Dar es Salaam.“Mmmh!” Filbert alisikika akiguna huku macho yake yakiangalia nje kupitia dirishani.“Hii kweli balaa” Steven alimwambia Filbert.“Yaani bora ningekuwa nimeishi Arusha, Mbeya au hata Iringa. Kweli mpira utachezeka kaka?” Filbert alimuuliza Steven.“Hali itakuwa ni ya hatari sana. Hewa itakuwa nzito sana” Steven alimwambia Filbert.Kila mchezaji kwa wakati huo alikuwa akiangalia nje, hali ya hewa ikaonekana kuwaogopesha kupita kawaida. Walikuwa wametoka katika moja ya nchi iliyokuwa na joto kali na sasa walikuwa wameingia katika nchi nyingine kabisa, nchi ambayo ilikuwa na baridi kali. Hali ile ya hewa ikaonekana kuwa kikwazo katika kuonyesha uwezo wao uwanjani kutokana na hali hiyo kusababisha hewa kuwa nzito hasa pale unapokuwa uwanjani.Ndge iliposimama, ngazi zikateremshwa na kisha abiria kuanza kuteremka. Kila mmoja alikuwa na koti zito ambalo lilikuwa juu ya maswata yao ambayo walikuwa wameyavaa. Japokuwa walikuwa na nguo hizo mwilini lakini bado walikuwa wakisikia baridi kali ambalo liliwafanya kutetemeka kila wakati.Mizigo ikachukuliwa na wao kuruhusiwa kuondoka kuelekea ndani ya jengo la uwanja wa ndege. Walikuwa wakitembea kwa haraka haraka, theluji bado ilikuwa ikiendelea kudondoka jambo ambalo wakati mwingine lilionekana kuwa kama karaha miilini mwao huku wakiona kama walikuwa wakiongezewa baridi zaidi na zaidi.Kila hatua ambayo walitakiwa kupitia ndani ya uwanja huo wakaipitia na kisha kuanza kuondoka kuelekea nje ya uwanja huo ambapo wakakuta basi kubwa likiwa linawasubiria na kisha kuanza kuwapeleka katika hoteli moja kubwa ya Sheraton ambayo ilikuwa katikati ya jiji hilo la Brussel.Kila chumba walitakiwa kulala watu wawili, kwa sababu Filbert na Steven walikuwa marafiki wa karibu sana, wakakaa katika chumba kimoja. Kila mmoja ndani ya chumba kile alikuwa akifurahia, maisha kwao yakaonekana kuanza kubadilika, uwepo wao ndani ya hoteli ile uliwafanya kuanza kufikiria maisha mengine kabisa.Hiyo ndio ilikuwa ni mara ya kwanza kukaa ndani ya chumba ambacho kilikuwa kizuri namna ile, walikuwa wakikishangaa kila kitu ambacho walikuwa wakikitazama. Kitanda kilikuwa kikubwa tena cha duara ambacho kilikuwa na swichi ambayo mara unapobonyeza tu basi kitanda kile kilianza kuzunguka. “Mmmh! Hiki kitanda noma Steven. Unaweza kulala huku ukiwa umeelekea Magharibi, unaamka ukiwa umeelekea Mashariki” Filbert alimwambia Steven.“Kizuri sana. Unaweza kuamka asubuhi na ukaanza kujisikia kizunguzungu” Steven alimwambia Filbert.Hiyo kwao ikaonekana kuwa kama nyota njema ambayo ilionekana mapema sana. Chumba kile kikaonekana kuwatabiria maisha yao ya baadae kwamba walitakiwa kupanga chumba kama kile kwa kutumia fedha zao na si fedha za mtu mwingine. Kila mmoja akaanza kuiona ndoto yake ikianza kutimia, muonekano wa chumba kile na nchi ile kwa ujumla viliwafanya kujisikia vizuri.Siku hiyo wakabaki katika vyumba vyao. Usiku hawakulala, kwa sababu chumba chao kilikuwa ghorofani, wakafungua dirisha na kisha kuanza kuangalia mazingira ya jiji la Brussels. Ghorofa zilikuwa nyingi zilizopendezeshwa na taa za kila aina, walikuwa wakifarijika sana kuangalia mazingira hayo japokuwa kulikuwa na baridi kali sana wakati huo.Ndoto zao za kufika Ulaya zikawa zimetimia na ilikuwa imebakia ndoto moja tu, kuishi ndani ya bara hilo katika kipindi chote cha maisha yao. Hiyo ndio ndoto pekee ambayo ilikuwa imebakiwa, walimshukuru Mungu kwa kuwawezesha kufika ndani ya bara hilo lakini walijiona kuwa na shukrani zaidi endapo wangefanikiwa kukaa ndani ya bara hilo zaidi na zaidi.Asubuhi ya siku iliyofuata wakaanza kutembea sehemu mbalimbali kama kulizoea jiji la Brussels. Barabarani kulikuwa na wazungu wengi lakini nao watu weusi walikuwa katika idadi kubwa japokuwa haikuwa kama idadi ya wazungu. Watu weusi waliokuwa wakionekana katika mitaa mingi ndani ya jiji hilo walikuwa ni Wakongo ambao walitoroka kwao na kuzamia nchi hiyo au hata kupokelewa kutokana na nchi ya Kongo kuwa na mapigano ya mara kwa mara.Ukiachana na wakongo, pia kulikuwa na watu wa Rwanda pamoja na Burundi bia kuwasahau wasomali ambao kila siku walikuwa wakizidi kumiminika ndani ya nchi hiyo. Kwa waafrika, nchi ya Ubelgiji ikaonekana kuwa kama nchi yao, walikuwa wakijikusanya kwa wingi kila siku. Matembezi hayo yaliendelea zaidi na zaidi mpaka pale walipoamua kurudi saa sita mchana, muda wote huo wala jua halikuwa likionekana zaidi ya mawingu mazito ambayo yalikuwa yametanda angani.“Hii nchi nzuri sana. Nzuri sana, kumbe ukisikia Muafrika kaja kuzamia wala hautakiwi kumlalamikia” Filbert alimwambia Steven huku wakiwa wamekwisharudi ndani ya chumba chao.“Hivi hatuwezi kubaki huku?”“Kubaki tunaweza, ila tufanye juhudi katika kucheza mpira” Filbert alimwambia Steven.“Simaanishi kubaki kihalali, nataka tubaki kizurumishi” Steven alimwambia Filbert.“Unamaanisha tuzamie?”“Ndio”“Mchezo mbaya sana huo. Tunaweza tusifanikiwe”“Kivipi?”“Kucheza mpira”“Kwani si tunakimbia kuelekea mitaani”“Sawa. Una passport na viza?”“Hapana”“Sasa unafikiri utaweza kupata kazi kihalali huku?”“Daah! Yaani hapa nafikiri kama tukirudi, yaani kweli tukanyage Ulaya halafu turudi ndani ya jiji la Dar es Salaam, kweli haki hii Filbert?” Steven alimwambia Filbert na kumuuliza.“Haina jinsi. Hivi wamesema mazoezi tunaanza kufanya lini?”“Niliwasikia wakisema kesho”“Wapi?”“Sijui. Ila kama napo niliwasikia kwenye uwanja wa chuo”“Chuo gani?”“Mmmh! Wala sikijui” Steven alimwambia Filbert.Université Libre de Bruxelles,Hiki kilikuwa ni moja ya vyuo vikubwa sana nchini Ubelgiji ambacho kilikuwa kikipatikana ndani ya jiji la Brussels. Chuo hiki kilikuwa kaskazini mwa jiji la Brussels na kilikuwa kikichukua wanachuo wengi kutoka katika nchi mbalimbali duniani. Chuo hiki kilikuwa kikubwa na ni lugha mbili ndizo ambazo zilikuwa zikitumika ndani ya chuo hicho, Kifaransa ambayo ilikuwa ni lugha ya taifa ya nchi hiyo pamoja na Kiholanzi. Watu wengi wa hapo Ubelgiji hawakuwa wakifahamu lugha ya Kingereza, lugha yao kubwa ilikuwa ni kifaransa na hiyo ilikuwa moja ya sababu ambazo ziliwapelekea wakongo wengi kuingia ndani ya nchi hiyo. Kutokana na ukubwa huo, chuo hicho kilikuwa na wanachuo elfu thelathini na mbili na mia tano ambao walikuwa wakisoma chuoni hapo kila mwaka.Kilikuwa ni moja ya vyuo ambavyo vilikuwa vikiwafanya wanachuo kuwa bize sana na masomo, kila wakati wanachuo walikuwa wakikaa kimakundi kwa ajili ya kujisomea huku muda mwingi wakionekana kuwa bize kupita kawaida. Pamoja na kutoa elimu bora ndani ya chuo hicho, pia chuo hiki kilikuwa kikitoa wanamichezo bora ambao walikuwa wakicheza michezo mbalimbali kama soka, kikapu, raga na michezo mingine mingi.Chuo hicho kilikuwa chuo pekee kati ya vyuo themanini na tano ambavyo vilikuwa vikipatikana ndani ya nchi hiyo ambayo ilikuwa na timu ya soka ambayo ilikuwa ikiendelea kushiriki ligi daraja la kwanza nchini humo. Timu hiyo ilikuwa ikiundwa na wachezaji waliokuwa wamechanganyika, kulikuwa na wachezaji kutoka chuoni hapo pamoja na wachezaji kutoka mitaani ambao walikuwa na malengo ya muda mrefu kuchezea katika timu hiyo.Uwanja wa chuoni hapo ndio ambao ulikuwa ukitumika katika mazoezi ya timu yao ambayo walikuwa wameipa jina la Westerlo.Timu hiyo ya chuo ilionekana kuwa na kocha mzuri lakini kila siku ilikuwa na tatizo moja tu, wachezaji wake hawakuwa na uwezo mkubwa. Kocha pamoja na viongozi wa chuo hicho walikuwa wakijitahidi sana kuisukuma timu hiyo iweze kusonga mbele lakini bado haikuonekana kusogea hata kidogo, bado ilionekana kuwa nyonge sana kwa timu nyingine.Mishahara ambayo walikuwa wakilipa kwa wachezaji ilikuwa midogo mno na hiyo ndio ilikuwa sababu ambayo iliwafanya wachezaji kutokujituma sana jambo lililopelekea wachezaji wengi kutimuliwa na timu kudorora zaidi. Katika kipindi ambacho timu ya vijana wa Tanzani walipokuwa wameingia ndani ya nchi hiyo, timu hiyo ilikuwa ikishika nafasi ya kumi na sita kati ya na timu kumi na nane ambazo zilikuwa zikishiriki ligi daraja la kwanza. Hiyo ilionekana kuwa nafasi mbaya kwao, ilionyesha dhahiri kwamba kama kusingekuwa na wachezaji wenye uwezo kuongezeka basi timu hiyo ingeshuka, ingeshuka na kushuka mpaka kusahaulika katika ramani ya soka nchini Ubelgiji.Saa sita na nusu mchana basi la wachezaji wa kitanzania lilikuwa likisimama ndani ya eneo la uwanja huo kutokea hotelini ambapo walikuwa wamefika mahali hapo kwa ajili ya kuchukua mazoezi ambayo yangefanyika kwa muda wa wiki mbili hata kabla ya kurudi nchini Tanzania. Katika kipindi ambacho wachezaji walikuwa wakiteremka kutoka katika basi lile, wanachuo walikuwa wamesimama wakiwaangalia, vijana wale walionekana kuhisi baridi kali miilini mwao japokuwa walikuwa wamevaa makoti makubwa.Uwanja mzuri wa mpira wa miguu ulikuwa ukionekana machoni mwao. Kila mmoja akaanza kutabasamu, nyasi za uwanja ule zilikuwa zikivutia, uwanja ulikuwa umenyooka tofauti na viwanja ambavyo walikuwa wakivitumia nchini Tanzania. Kila mmoja akashikwa na kiu ya kutaka kucheza juu ya uwanja mzuri namna ile, wakaambiwa wajiandae huku viongozi wakipelekwa ofisini kwa ajili ya kwenda kutoa taarifa kwamba walikuwa wamekwishafika mahali hapo.Wanachuo wakaanza kukusanyika, kitendo cha kuwaona vijana wale wakijiandaa kuvaa kwa ajili ya kuanza mazoezi kilikuwa kikiwavutia. Watu wengi chuoni hapo walikuwa wakipenda sana kuangalia mpira na ndio maana walipowaona wachezaji wale wakijiandaa, wakakaa katika sehemu za mashabiki kwa ajili ya kuwaangalia vijana wale.“Hii ndio nafasi yetu” Steven alimwambia Filbert.“Hapa ndipo pa kuonyesha uwezo. Nikifanikiwa, kurudi Tanzania itakuwa kipindi cha likizo na mecho za taifa tu” Filbert alimwambia Steven.“Mimi nikichaguliwa kujiunga na timu mojawapo, Tanzania sirudi, nitachukua uraia wa huku huku” Steven alimwambia Filbert.Hiyo ndio ilikuwa siku ya kwanza kwa timu hiyo kuanza kufanya mazoezi ndani ya uwanja huo. Kila siku watu walikuwa wakijazana kuwaaangalia vijana hao ambao walionekana kuwa na uwezo wa juu katika kucheza mpira wa miguu. Kadri siku zilivyokuwa zikizidi kusonga mbele na ndivyo ambavyo watazamaji walivyokuwa wakiendelea kumiminika ndani ya uwanja huo kwa ajili ya kuangalia mazoezi ya timu hiyo.Baada ya wiki moja na nusu kupita huku wakiwa wamefanya mazoezi ya kutosha hapo ndipo ambapo timu mbalimbali zikaanza kuomba mechi kucheza na timu hiyo ya vijana kutoka nchini Tanzania. Uwezo ulikuwepo, vijana wenye uwezo walikuwepo nchini tanzania japokuwa vipaji vyao vilikuwa vimefichwa porini. Wachezaji wakajitoa, waliokuwa mabeki wakazuia vya kutosha, kipa akadaka kupita kawaida huku Filbert akifunga magoli zaidi ya manne katika kila mechi ambayo walikuwa wakicheza chuoni hapo.“Ces cing personnes deveraient se joindre à notre êquipe cette fenêtre transifer(Vijana wale watano wanatakiwa kujiunga na timu yetu katika kipindi cha usajiri)” Proffesa wa chuo alisikika akimwambia rais wa chuo huku akimnyooshea kidole Filbert, Steven, Godwin, Idrissa na Khatibu. Kwa jinsi wachezaji walivyokuwa wakifanya mazoezi walionekana kuwa fiti kupita kawaida, uwezo wao ulikuwa ukionekana dhahiri jambo ambalo liliwafanya maprofesa waliokuwa ndani ya chuo kile ambao walikuwa wakiangalia mazoezi yale kuvutiwa na baadhi ya vijana. Kila mwanachuo ambaye alipata bahati ya kuyaangalia mazoezi yale alionekana kukubali kwamba hapa duniani kulikuwa na watu ambao walikuwa na uwezo mkubwa wa kucheza mpira.Uwezo wa wachezaji wale ukawa gumzo chuoni hapo, kila mtu ambaye alikuwa akisikia kuhusu timu hiyo akatamani kwenda kuiangalia jinsi ilivyokuwa ikifanya mazoezi. Kila siku watu walikuwa wakizidi kuongezeka katika uwanja huo, mazoezi ya wachezaji hao yalionekana kumvutia kila aliyekuwa akiyaangalia.Sifa zao zikaanza kutapakaa katika sehemu mbalimbali nchini Ubelgiji, wanachuo wengine walikuwa wakiwapiga picha na kisha kuziweka katika mitandao mbalimbali ya kijamii na kuwamwagia sifa nyingi kitu ambacho kilipelekea hata wale ambao hawakuwa wamepata taarifa kuhusiana na uwepo wa timu hiyo kuelekea huko kuyaangalia mazoezi hayo.Viongozi wa timu nyingine hawakubaki nyuma, nao walikuja katika uwanja huo wa chuo kwa ajili ya kuangalia jinsi vijana wale walivyokuwa wakifanya mazoezi. Kila aliyekuwa akiwaangalia alikuwa akikubaliana na sifa hizo jambo ambalo kila mtu akataka vijana hao wajiunge na timu zao.Uwezo ule ambao walikuwa wakiuonyesha ndio ambao uliwafanya maskauti wa timu kubwa nchini Ubelgiji kutaka kucheza mechi pamoja na vijana wale. Maombi yao yalipokubaliwa, wakaziandaa timu zao za vijana ambazo zote hizo zilifungwa katika michezo yote waliyokuwa wamecheza.Hilo ndilo ambalo liliwatangaza zaidi, uwepo wao ukazidi kutangazwa ndani ya nchi ya Ubelgiji, watu wengi waliokuwa wakipenda mpira wa miguu walikuwa wakizidi kumiminika katika uwanja huo wa chuo kwa ajili ya kuwaangalia vijana hao huku kila mmoja akiwaona kuwa nyota wa miaka ya baadae endapo wangeendelea kufanya mazoezi zaidi na zaidi.Baada ya wiki ya kwanza kukatika, mtafaruku ukaanza kutokea. Katika siku ya kwanza ambayo Professa wa chuo hicho alipowaona vijana wale wakichukua mazoezi aliwasifia lakini hakuchukua hatua yoyote ile japokuwa alikuwa amewachagua kwa kuwaonyeshea vidole wachezaji watano ambao walionekana kuwa mwiba mkali. Ni kweli alikuwa amepanga kuwasajili katika timu yake wa Westerlo lakini mambo yake alikuwa akiyaendesha kwa taratibu sana.Katika ambacho maskauti kutoka timu nyingine walipokuja mahali hapo, hawakutaka kuchelewa, kwa sababu walikuwa na uhitaji mkubwa wa wachezaji waliokuwa na uwezo, wakaanza kuongea na viongozi wa timu ya taifa. Hapo ndipo ambapo professa alipoona kwamba alikuwa amekosea sana, aliona kwamba tayari alifanya kosa kubwa kujifanya yupo bize na wakati alikuwa amekwishawaona vijana ambao walikuwa na uwezo mkubwa uwanjani.Viongozi wa timu tatu ambazo zilikuwa zikishiriki ligi kuu ya Ubelgiji iliyojulikana kama Jupiler League, Genk, Standard Liege na Anderlecht tayari walikuwa wamekwishafika mahali hapo na kitu ambacho walikifanya ni kuanza mazungumzo ya kuongea na viongozi wa timu ya taifa ya Tanzania ili kujua ni kipi kifanyike na baadhi ya wachezaji waweze kubaki nchini hapo kwa kujiunga na timu zao.Vijana hao hawakuwa na mawakala, hilo likaonekana kuwa kama kipingamizi lakini kwa sababu kila kitu kilikuwa kwenye mipango, viongozi wakaambiwa kwamba ilitakiwa wachukue nafasi kama mawakala wa muda wa wachezaji hao kabla ya wao wenyewe kuamua ni nani na nani kuwa mawakala wao wa muda mrefu katika maisha yao ya soka.“Hakuna tatizo” Kocha msaidizi aliwaambia.Hapo ndipo kazi ilipoanza. Kwa haraka bila kupoteza muda mikataba ikaandaliwa, hakukuwa na suala la kupelekwa kufanyiwa majaribio, uwezo ambao wachezaji hao waliouonyesha mahali hapo ilitosha kabisa kuwaambia kwamba ni kwa kiasi gani walikuwa wameiva katika mchezo wa soka japokuwa walikuwa na umri mdogo.Mara baada ya wachezaji nane kuchaguliwa, wakapelekwa katika chumba maalumu ambapo huko wakawekwa kikao na kuambiwa kila kilichokuwa kikiendelea mahali hapo. Kwanza hakukuwa na mtu ambaye aliamini kile ambacho alikuwa amekisikia, kuchaguliwa na kujiunga na timu za hapo Ubelgiji ilionekana kuwa kama ndoto ya kila mtu mahali hapo.Filbert akatamani kusimama na kuruka ruka, hakuamini kwamba safari ambayo iliwatoa nchini Tanzania na kuwapeleka nchini Ubelgiji ndio ambayo ingewafanya kukamilisha kila ndoto ambayo walikuwa wamejiwekea maishani mwao. Baada ya kupewa darasa dogo na viongozi wao, moja kwa moja maskauti wa timu hizo tatu zinazoshiriki ligi kuu ya hapo Ubelgiji wakaingia, wanaanza kuongea huku kukiwa na mkalimani pembeni.Skauti wa timu hizo wakawachagua wachezaji wao na Filbert kujikuta akiangukia katika mikono ya timu ambayo ilikuwa ikiongoza ligi katika kipindi hicho, timu ya Genk huku rafiki yake, Steven akienda kujiunga na timu ya Anderlecht.Kwa wakati huo hakukuwa na muda wa kupoteza, kila kitu kilitakiwa kufanyika kwa haraka sana. Mchezo wa kuibiana wachezaji ulikuwa mkubwa sana barani Ulaya na ndio maana ilitakiwa kufanya mambo haraka haraka katika kuhakikisha kwamba wachezaji hao wanasaini mikataba.Kwa kuwa walikuwa chini ya miaka kumi na nane na pia walikuwa kama wachezaji huru, sheria ya soka ya shirikisho la soka la Ulaya, UEFA ikawaruhusu kujiunga na timu hizo huku wakiwa na mawakala wao wa muda mfupi.“Unataka nani awe wakala wako?” Kocha mkuu, Zakayo alimuuliza Filbert.“Kaka yangu, Dennis” Filbert alijibu na kocha yule kuandika.Kila mmoja akamtaja wakala wake ambaye alitakiwa kusimamia mikataba yao yote kuhusiana na soka pamoja na matangazo ya biashara endapo yangetokea katika maisha yao ya soka. Kwa sababu professa wa chuo hicho alikuwa amechelewa kutokana na uzembe wake mwenyewe, akaziomba timu hizo kubaki na wachezaji watatu kwa mkopo ili kuiwezesha timu yao kupanda daraja na kisha kuwaruhusu kuondoka kuelekea katika timu zao hizo mara ligi itakapomalizika.Hilo halikuonekana kuwa tatizo kabisa, kwa sababu bado wachezaji wale walikuwa wachanga, walionekana kuwa na uhitaji wa kukomaa katika ligi ndogo hata kabla ya kuja katika ligi kuu. Siku hiyo hiyo mikataba ikasainiwa na Filbert kuahidiwa kulipwa paundi elfu tano kwa wiki, kiasi ambacho kilikuwa ni sawa na milioni kumi na mbili na laki tano kwa fedha za kitanzania, hicho kilikuwa ni kiwango cha chini kabisa.Hapo ndipo ambapo maisha yao yalipotakiwa kuwepo. Kila mmoja alionekana kuwa na bahati na kwa wale ambao hawakuwa wamechaguliwa wakaonekana kuumia sana mioyoni mwao. Baada ya wiki moja, nauli pamoja na vibali vikaandaliwa na kisha mawakala wote ambao waliteuliwa kuwasimamia ndugu zao wakawa wamekwishafika nchini Ubelgiji, Dennis, kaka yake Filbert akiwa mmoja wapo.“Daaah!” Dennis alisema mara baada ya kumuona mdogo wake, Filbert, alionekana kutokuamini.“Vipi tena?” Filbert alimuuliza.“Una bahati sana. Aiseee, yaani kuja huku tu ndio imekuwa moja kwa moja” Dennis alimwambia Filbert.“Nilimwambia baba kwamba hii ndio ilikuwa ndoto yangu, uwezo wangu wa kucheza mpira haukutakiwa kuishia Tanzania” Filbert alimwambia Dennis.“Safi sana dogo. Siamini kama na mimi nimekuja Ulaya” Dennis alimwambia Filbert.“Ndio hivyo. Nimeamua kukuchagua wewe kuwa wakala wangu kwa sababu ninataka familia nzima iwe na fedha, yaani fedha zizunguke kwenye familia yetu” Filbert alimwambia kaka yake, Dennis.“Nimefurahi sana”“Na baba alisemaje mara baada ya kupata taarifa?”“Hahaha! Mzee wa watu angekufa kwa presha aiseee”“Ilikuwaje?”“Sijui niseme nini ila angekufa kwa presha, alishtuka sana” Dennis alimwambia Filbert.“Watanzania wamejua kila kilichoendelea huku?”“Hiyo ndio imekuwa gumzo ya jiji sasa hivi, kila kona mnazungumziwa nyie, ila wadau wengi wameonya msije kukubali kubadilisha uraia, nchi bado inawahitaji” Dennis alimwambia Filbert.“Siwezi kubadilisha uraia, ninaipenda sana nchi yangu” Filbert alimwambia Dennis.Siku hiyo walikaa hotelini huku wakiongea mengi, Filbert bado alijiona kuwa kwenye ndoto moja yenye kutia faraja kuliko ndoto zote maishani mwake ambapo baada ya muda angeshtuka kutoka katika usingizi mzito na kujikuta yupo Kijitonyama. Safari yake ya mafanikio akaiona kuanzia nchini Ubelgiji.“Kwa hiyo utacheza hapa maisha yote?” Dennis alimuuliza Filbert.“Haiwezekani. Nitatamani siku moja niende kucheza soka Uingereza” Filbert alimwambia Dennis.“Hahaha! Kumbe una akili sana”“Najua. Kule ndio pa kujitangaza zaidi. Huku porini sana” Filbert alimwambia Dennis.Siku ya kwanza ikapita. Baada ya wiki moja ya mapumziko Filbert akaanza kufanya mazoezi na timu ya soka ya Westerlo ambayo alikuwa ametolewa kwa mkopo kutoka katika timu mpya iliyomnunua ya Genk. Muda mwingi Filbert alionekana kuwa na furaha, kitendo cha kuanza kucheza soka la Ulaya kilimpa faraja sana, yaani kila kilichokuwa kikiendelea hakikuwa kikiaminika kabisa.Maskauti wa Genk hawakuwaacha wachezaji wao peke yao, walikuwa wakiwafuatilia kwa ukaribu sana. Katika kila mechi ambayo Westerlo walipokuwa wakicheza, maskauti hao walihakikisha wapo uwanjani kwa ajili ya kuwaangalia wachezaji wao wawili, Filbert na Idrissa ambao walikuwa wametolewa kwa mkopo.Uwezo wa Filbert ulionekana kuwa mkubwa sana ambao ulimshangaza kila mtu. Filbert alikuwa akilijua sana goli, alikuwa akijua sana kufunga kitu ambacho ndani ya mechi tano za kwanza akawa amefunga magoli sita jambo ambalo liliwaonyeshea maskauti wa Genk kwamba chaguo lao halikuwa baya, lilikuwa chaguo sahihi huku wakiona kwamba Filbert angekuwa mchezaji tishio katika siku za usoni.Japokuwa katika kipindi hicho alijiona kupata nusu ya kitu alichokuwa akikihitaji hakuweza kumsahau msichana wake, Amanda. Mara kwa mara alikuwa akiwasiliana nae kwa njia ya simu au hata kuwasiliana kwa njia ya mitandao ya kijamii. Kila siku Filebrti alionekana kuwa na furaha, kila kilichokuwa kikiendelea hakikuweza kuaminika katika macho yake.“Ninataka kuendelea na masomo Amanda” Filbert alimwambia Amanda.“Kwa hiyo unataka kurudi Tanzania?”“Hapana. Ninataka kusoma huku huku”“Lengo la kusoma ni nini na wakati una fedha na utakuwa tajiri mkubwa?” Amanda alimuuliza Filbert, katika kipindi hicho walikuwa wakiongea katika mtandao wa Skype.“Nina ndoto moja kubwa maishani mwangu” Filbert alimwambia Amanda.“Ndoto gani?”“Kuwa rais wa Tanzania. Hilo tu” Filbert alimwambia Amanda.“Unataka kuwa rais?”“Ndio. Miaka ijayo. Ninataka kuwa rais” Filbert alimwambia Amanda.“Sawa. Kwa hiyo unataka kuanza shule lini?”“Wiki ijayo”“Kwa hiyo utakuwa ukisoma na kucheza mpira?”“Hiyo ndio maana yangu” Filbert alijibu.Hivyo ndivyo Filbert alivyokuwa amepanga, kitu ambacho alikuwa akikitaka katika wakati huo ni kuingia darasani na kuendelea kusoma. Ndoto yake ambayo aliona iimebakia ilikuwa ni kuwa rais wa nchi ya Tanzania. Alipomfikishia wazo lake kaka yake, Dennis, wala hakupinga, kwa moyo mmoja akakubaliana nae na hata uongozi wa timu ya Weserlo na Genk nao wakakubaliana nae na hivyo moja kwa moja kuanza masomo yake katika shule ya St’ Phillip, shule iliyokuwa pembeni kidogo mwa jiji la Brussels.Maisha ya Ubelgiji yalikuwa mazuri, wachezaji walikuwa huru sana na baada ya miezi miwili Filbert akapangiwa nyumba ndani ya jiji la Westerlo, nyumba ambayo angekuwa akikatwa mshahara wake na mwisho wa siku nyumba hiyo kuwa yake. Kiasi cha fedha ambacho alikuwa akilipwa kilikuwa kikubwa sana, japokuwa milioni mbili kwa fedha za kitanzania zilikuwa zikitumika kulipia kodi lakini milioni kumi bado zilionekana kuwa nyingi.Akafanikiwa kununua gari huku akiendelea kuishi na kaka yake ambaye alikuwa kila kitu nchini Ubelgiji. Mazoezi hayakuonekana kuwa rahisi kwake, kila siku alikuwa akiacha usingizi, baridi kali na kisha kuelekea mazoezini na mchana kuelekea shuleni kabla ya kwenda mazoezini kwa mara nyingine jioni. Hali hiyo ilionekana kumuumiza sana lakini hakuwa na jinsi, ili kufikia malengo yako na mafaniko makubwa basi haina budi kupigana sana katika kipindi kigumu.“Excusez-moi (Samahani)” Msichana mmoja alimwambia Filbert katika kipindi ambacho alikuwa supermarket, alipogeuka na kumwangalia msichana huyo, alikuwa msicha mrembo, msichana aliyekuwa na mchanganyiko wa rangi, bila shaka baba yake alikuwa Mzungu na mama yake Msomali.“Mmmh!” Dennis ambaye alikuwa pembeni mwa Filbert alitoa mguno, msichana aliyekuwa amemuongelesha Filbert alionekana kuwa kama malaika.“Can you speak English? (Unaweza kuongea Kingereza)” Filbert alimuuliza msichana yule ambaye alikuwa ameongea lugha ya Kifaransa.“Yes. I can speak English (Ndio. Naweza kuongea Kingereza)” Msichana yule alimwambia Filbert huku akionekana kuwa na furaha.Filbert akabaki kimya kwa muda, kila alipokuwa akimwangalia msichana yule moyo wake ulikuwa ukijisikia hali ya tofauti sana, hali ambayo aliwahi kuisikia mara moja tu tena katika kipindi ambacho alikutana na Amanda katika jengo la Mlimani City. Kila alipokuwa akizidi kumwangalia msichana yule, alikuwa akimfananisha na muigizaji wa filamu za utupu Marekani, Skin diamond kutokana na urembo aliokuwa nao. Je nini kitaendelea?Je msichana huyo ni nani?Je Filbert ataweza kufanikisha ndoto yake ya kuwa rais? ITAENDELEA
Alikuwa mrembo sana ambaye alikuwa na kila sifa za kuitwa msichana mrembo. Alikuwa na wembamba wa kawaida, hipsi zake zilikuwa zimetokeza kidogo huku tumbo lake likiwa limeingia ndani. Ngozi yake ilikuwa nzuri, uso wake ulikuwa ni wa kitoto sana uliokuwa ukipendeshwa na kidoti kimoja ambacho kilikuwa juu ya mdomo pembeni ya pua yake nzuri ya kisomali.Mwendo wake ulikuwa ni wa kawaida sana lakini kutokana na mvuto ambao alikuwa nao kwa kila mwanaume ambaye alikuwa akimwangalia, alionekana kutembea kwa mwendo wa madaha kana kwamba alikuwa akitembea katika ardhi yake, ardhi ambayo ilikuwa imetengenezwa kwa dhahabu na madini mengine ya gharama.Sauti yake ilikuwa ikikamilisha uzuri wake, alipokuwa akiongea, alisikika vizuri masikioni mwa kila mtu ambaye alikuwa karibu yake. Wakati mwingine alikuwa akiiweka sauti yake kimahaba kama ilivyokuwa ya msanii wa maigizo kwa nchini Tanzania, Wema Sepetu. Kwa muonekano wa kawaida tu, msichana huyu alionekana kuwa tofauti sana na wasichana wengine, urembo ambao alikuwa nao ulikuwa mkubwa ambao uliwavutia wanaume wote ambao walibahatika kumtia machoni. Msichana huyu alikuwa akiitwa Saado.Saado alikuwa na urembo wa kipekee, uzuri wake ulionyesha kwamba kweli duniani kulikuwa na wasichana wazuri, wasichana ambao walihitaji kumpata mwanaume mwenye uwezo wa kuthamini, mwanaume aliyekuwa radhi kufanya jambo kwa ajili ya msichana mrembo kama huyo. Uzuri wa Saado wala haukujificha, ulionekana kwa kila mtu ambaye alikuwa akimwangalia huku marafiki zake wengi chuoni wakiwa wakimuita kwa jina la Cleopatra, mwanamke mwenye asili ya Misri ambaye anasadikiwa kuwa mwanamke mwenye mvuto kuliko wote waliopata kutokea katika dunia hii.Saado alikuwa akiishi hapo Ubelgiji ndani ya jiji la Brussels katika mtaa wa Hoogstaraat, mmoja wa mitaa ambayo ilikuwa ikikaliwa na Wasomali kwa wingi nchini Ubelgiji. Saado alionekana kuwa gumzo mtaani kwao, kila siku majirani zake walikuwa wakimsifia kutokana na urembo ambao alikuwa nao. Hakuwa na urembo uliochuja kwamba leo utamuona kuwa mzuri na baada ya kumzoea sana ungeona urembo kupotea machoni mwako.Sifa za urembo wake zilikuwa zikisikika katika kila kona, watu wengi walikuwa na hamu ya kumuona Saado kwani kwa jinsi sifa alizokuwa akipewa zilikuwa nyingi kiasi ambacho kila mtu alikuwa akitaka kumuona, alifanana vipi.“Anafanana na Angeline Jolie?” Mvulana mmoja alimuuliza mwenzake katika kipindi ambacho alikuwa amesikia sifa kuhusu msichana Saado.“Wewe twende, utamuona tu” Jamaa mwingine alimwambia mwenzake, alikuwa amemsifia sana Saado na sasa alikuwa akimpeleka Hoogstaraat.Vijana wale wakafika Hoogstaraat. Wasomali walikuwa wengi ndani ya mtaa huo huku wakiwa wamejengewa makazi na serikali, majengo marefu ambayo walitakiwa kuishi katika kipindi ambacho walikuwepo nchini Ubelgiji, kwa sababu wengi walikuwa wamezaliwa ndani ya nchi hiyo, nao wakachukuliwa kama raia wa nchi hiyo ambao walikuwepo toka katika kipindi cha nyuma.Mara baada ya kijana yule kuonyeshewa msichana Saado, kwanza alibaki kimya kwa muda, alikuwa akimwangalia Saado kwa umakini mkubwa sana. Saado alionekana kuwa mrembo, ni kweli kwenye maisha yake kijana huyo alikuwa ameona wanawake wengi warembo lakini kwa Saado alionekana kuwa tofauti kabisa.“Huyu ni binadamu au malaika?” Kijana yule aliuliza huku akimwangalia vizuri Saado ambaye wala hakuwa na habari, ndio kwanza alikuwa akichezea kompyuta yake ya mapajani.“Nilipokwambia kwamba Saado ni mzuri ulitakiwa kuniamini” Jamaa yule alimwambia mwenzake.Bado Saado aliendelea kuwa mrembo sana, baada ya siku hiyo, kuna watu wengi walikwenda mpaka Hoogestraat kwa ajili ya kujionea msichana huyo na kweli walipomuona, walikiri kwa midomo yao kwamba katika maisha yao walibahatika kuona msichana mzuri kama Saado na ndio maana hata muigizaji wa filamu za utupu, Skin Diamond alipoanza kuigiza filamu hizo na kuonekana, kila mmoja alimuona kufanana sana na Saado.Huyo ndiye alikuwa Saado. Alizaliwa mwaka 1992 nchini Somalia ambapo mara baada ya mapigano yaliyodumu muda mwingi nchini kwao wazazi wake, mzee Jaabir akaamua kuhama pamoja na familia yake na kuelekea nchini Ubelgiji kwa ndugu zake. Nchini humo wala hawakupata kipingamizi chochote kile, wasomali wengi walikuwa wameruhusiwa kuishi ndani ya nchi hiyo kwa kuwa walikuwa wakiepuka vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilikuwa vikiendelea nchini kwao.Kuzaliwa kwa Saado kulionekana kumkasirisha sana mzee Jaabir, alikuwa na watoto watatu ambao wote hao walikuwa wasichana, katika kipindi hicho alitarajia kupata mtoto wa kiume lakini mara baada ya mtoto kuzaliwa, alikuwa msichana. Kila wakati mzee Jaabir alionekana kuwa na hasira, kila alipowaona ndugu zake wakiwa na watoto wao wa kike moyoni alikuwa akijisikia wivu sana kwani tamaa ya moyo wake katika kipindi hicho ilikuwa ni kutamani kuwa na mtoto wa kiume.Hakuwa na jinsi, hasira zake hazikuweza kubadilisha kitu chochote kile, hazikuweza kumbadilisha Saado na kuwa mvulana, aliendelea kubaki kama alivyokuwa, aliendelea kubaki msichana tu.Baada ya miaka mitano kuishi nchini Ubelgiji, mzee Jaabir akaamua kurudi Afrika ndani ya nchi yake ya Somalia. Lengo kubwa la kurudi nchini Somalia lilikuwa ni kuchukua kila kitu ambacho kilikuwa ni mali yake hasa fedha. Baada ya kuingia nchini Somalia, hakukuwa na ndugu yeyote yule ambaye alijua ni kitu gani kilitokea huko kwani mzee Jaabir hakuweza kurudi tena na mwili wake haukuonekana kabisa.Bi Duddo alijaribu kuulizia kuhusu mume wake lakini wala hakupata jibu. Kila wakati alikuwa akiwasiliana na ndugu zake ambao waliamua kubaki nchini humo lakini wote walisema kwamba hawakuweza mzee Jaabir kwani hali ya nchini Somalia bado haikuwa imetulia, mapigano ya hapa na pale yalikuwa yakiendelea.Baada ya miaka kumi, Bi Duddo akaamua kusahau kila kitu, alijua fika kwamba mumewe alikuwa amefariki na hivyo alikuwa na jukumu lote la kuwalea watoto wake. Bi Duddo hakupata tabu sana katika malezi ya watoto wake kutokana na serikali ya Ubelgiji kuwajali sana, alipewa kila kitu ambacho alikuwa akikihitaji huku watoto wake wakisomeshwa shule, huo ndio ulikuwa mpango wa nchi ya Ubelgiji, kwa sababu nchi ilikuwa kubwa na watu wachache, walitaka watu waendelee kujazana ndani ya nchi hiyo.Alipofikisha miaka kumi, urembo wa Saado ukaanza kuonekana machoni mwa watu, nyota njema tayari ilikwishaanza kuonekana maishani mwake. Japokuwa watu wengine walikuwa wakimshangaa Saado kutokana na urembo ule mahali alipoupata lakini bado siri kubwa iliendelea kubaki moyoni kwa Bi Duddo, yeye ndiye ambaye alikuwa akifahamu kila kitu, Saado alikuwa na rangi mchanganyiko, alikuwa na asili kutoka kwa baba na mama.Katika miaka ya nyuma Bi Duddo hakuwa ametulia ndani ya ndoa yake, alikuwa ni mmoja wa wanawake waliokuwa kwenye ndoa ambao bado walikuwa na tamaa ya kutaka kutembea nje ya ndoa. Tamaa yake hiyo ndio ambayo ilimkutanisha na Bwana Reese, mwanaume mzungu kutoka nchini Marekani.Wakaanzisha mahusiano ya siri. Kila siku Bi Duddo alipokuwa akielekea katika mghahawa, mahali alipokuwa akifanyia kazi, alikuwa akiendelea kukutana na Reese ambaye kwa moyo mmoja wakaingia kwenye mahusiano ya kimapenzi ambayo yaliwapelekea kufanya mapenzi sana na mwisho wa siku kupewa ujauzito ambao baadae akaja kutoka Saado.Mzee Jaabiri hakuwa akifahamu lolote lile, kwa sababu yeye alikuwa mtu wa kukaa nyumbani tu huku akitumiwa fedha zamatumizi na ndugu zake waliokuwa Ubelgiji, hakuweza kugundua kwamba mke wake, Bi Duddo alikuwa akitembea nje ya ndoa na hata Saado hakuwa mtoto wake wa kumzaa.Hiyo iliendelea kuwa siri ya Bi Duddo, hakutaka mtu yeyote afahamu kuhusu Saado, mara kwa mara alikuwa akiwaambia kwamba mtoto wake huyo ndiye ambaye alikuwa amechukua urembo wake katika kipindi ambacho alikuwa binti wa miaka kumi na nne.Saado aliendelea kukua zaidi na zaidi, urembo wake uliendelea kuongezeka na watu kupeana taarifa. Alipofikisha umri wa miaka kumi na nane hapo ndipo alipoanza masomo ya chuo. Urembo wake huo uliendelea kuwa gumzo, vijana wengi chuoni hapo walikuwa wamevutiwa na Saado na kwa nia moja walikuwa wamejaribu kurusha karata zao lakini Saado hakuonekana kuwa mwepesi kuwakubalia.“Nakupenda sana Saado” Kijana mmoja alimwambia Saado ambaye alibaki akitabasamu tu.“Umenipendea nini?” Saado alimuuliza kijana yule.“Kila kitu ulichokuwa nacho”“Kama kipi?”“Kila kitu”“Sawa. Kwenye hicho kila kitu, nitajie vitatu tu”“Sura, tabia pamoja na umbo lako, umetokea kuuteka sana moyo wangu” Kijana huyo wa hapo chuoni alimwambia Saado.“Nashukuru”“Kwa hiyo umekubali kuwa mpenzi wangu?” Kijana yule alimuuliza.“Hapana”“Kwa nini tena?”“Siwezi kupenda”“Kwa nini hauwezi Saado?”“Sijafahamu kwa nini”“Nakuomba unikubalie, nakuomba uwe wangu Saado”“Hapana Willem, sihitaji kuwa na mvulana katika kipindi hiki” Saado alimwambia kijana huyo, Willem ambaye alionekana kutia huruma japokuwa Saado aliendelea kumuua nyani bila kumwangalia usoni.“Au unataka mpaka ningekuwa msomali?” Kijana yule aliuliza, tayari kwa mbali alionekana kuwa na hasira.“Hapana. Sina ubaguzi, kuna wasomali wengi wamekuja na nimewakatalia. Kwangu ninaweza kumkubali kila mtu, haijalishi ni mzungu, mtu mweusi au msomali. Ninaposema sitaki kuingia kwenye mahusiano wewe nielewe tu” Saado alimwambia Willem ambaye akakaa kimya kwa muda.Huyo ndiye alikuwa Saado, bado alikuwa msichana bikira, aliithamini bikira yake na hakuwa radhi itolewe na mwanaume yeyote yule. Kila alipokuwa akijiangalia chumbani kupitia katika kioo chake alikuwa akijiona kuwa mrembo ambaye alistahili kuendelea kukaa na bikira yake vile vile huku akijiahidi kwamba mwanaume wa kwanza kumruhusu kuitoa basi angekuwa yule mwanaume ambaye angekuwa radhi kumuoa tu.Huo ndio uamuzi ambao alikuwa amejiamulia. Maisha yaliendelea kwenda mbele zaidi na zaidi na ndipo alipokuja kuugundua udhaifu wake mkubwa. Saado akatokea kuvutiwa na wavulana ambao walikuwa na ngozi nyeusi. Japokuwa wazungu wengi pamoja na wasomali wenzake walikuwa wakimfuata lakini Saado hakuvutiwa nao ila kila alipokuwa akiwaangalia watu weusi, aliwaona kumvutia kupita kawaida.Saado akawa akihitaji sana kuwa na mwanaume mweusi. Hakujua kama wanaume hao walikuwa wameambiwa au la kwani baada ya mwezi mmoja kuugundua udhaifu wake, wanaume wengi weusi wakaanza kumtongoza. Saado hakujua afanye nini, wanaume ambao walikuwa ni ugonjwa wake wakawa wamekwishaanza kumfuata na kumwambia maneno mengi ya kimapenzi, alitamani kukubali lakini kuna kitu alijiona kutokuwa nacho kwa kia mwanaume ambaye alikuwa akimfuata, MAPENZI.Hali ile iliendelea zaidi na zaidi mpaka pale ambapo vijana kutoka nchini Tanzania walipokuja nchini Tanzania na kisha kuanza kufanya mazoezi katika chuo hicho alichokuwa akisoma Saado. Hakuwa akipenda kuangalia mpira lakini mara baada ya kusikia sifa kemkem juu ya uwezo wa wanaume hao uwanjani tena wakiwa na ngozi nyeusi, Saado akaamua nae kwenda huko.Mara baada ya macho yake kutua kwa Filbert, Saado akaanza kujisikia kitu cha tofauti moyoni mwake, mapenzi ambayo wala hayakuwepo moyoni mwake yakaanza kumuingia na kujikuta akiwa katika mapenzi ya dhati kwa Filbert.Kila siku akawa akiumia sana moyoni mwake, alijitahidi sana kutafuta kila nafasi ya kuongea na Filbert lakini nafasi hiyo wala hakuipata kitu ambacho kilimuumiza sana. Siku ambayo alikuwa ameamua kwamba ni lazima amwambie ukweli Filbert juu ya jinsi alivyokuwa akijisikia moyoni mwake, siku hiyo wachezaji hawakuja mazoezini, siku zao za kufanya mazoezi zilikuwa zimekwisha.Hiyo ikaonekana kuwa habari mbaya kwa Saado, alikuwa akipenda sana kupata japo dakika kadhaa kuongea na Filbert na kisha kumwambia ukweli juu ya moyo wake, alijiona kuwa na mzigo mkubwa wa mapenzi na ni mwanaume mmoja tu ndiye ambaye angeweza kuushusha, huyu alikuwa Filbert ambaye kwa wakati huo hakuonekana tena machoni mwake.Siku zikaendelea kukatika huku moyo wake ukizidi kuumia zaidi. Kila siku alikuwa akimuwaza Filbert, alimkumbuka sana lakini hakuwa akimuona machoni mwake. Siku ambayo alikuja kuonana nae katika supermarket moja iliyokuwa katikati ya jiji la Brussels, Saado hakuonekana kuamini, kwanza akaanza kumwangalia vizuri Filbert, alipokuja kuhakikisha kwamba ni yeye, akaanza kumfuata, Filbert alikuwa pamoja na kaka yake, Dennis.“Excusez-moi (Samahani)” Saado alimwambia Filbert“Mmmh!” Dennis ambaye alikuwa pembeni mwa Filbert alitoa mguno.“Can you speak English? (Unaweza kuongea Kingereza)” Filbert alimuuliza Saado ambaye alikuwa ameongea lugha ya Kifaransa.“Yes. I can speak English (Ndio. Naweza kuongea Kingereza)” Saado alimwambia Filbert huku akionekana kuwa na furaha. Wote kwanza wakabaki kimya, wakaanza kuangaliana kana kwamba walikuwa wakifananishana. Kwa Filbert, alikuwa ametulia na kuanza kuufikiria urembo ambao alikuwa nao Saado. Alionekana kuwa msichana mrembo kupita kawaida na kwa urembo ambao alikuwa nao, Amanda hakuwa akiingia hata nusu yake.Tabasamu pana lililotawala uso wa Saado ndilo ambalo lilimchanganya sana Filbert, akajiona kuhamishwa na kupelekwa sehemu moja nzuri sana, sehemu ambayo aliiona kuwa kama pepo ndogo. Kwa Dennis, alibaki akimwangalia Saado, alionekana kuwa msichana mrembo ambaye kwa mwanaume wa kisasa, mwanaume rijali hakutakiwa kumuacha hata mara moja.“Nakufananisha, sijui ndio wewe” Saado alimwambia Filbert huku akiachia tabasamu.“Inawezekana ndio mimi. Unanifananisha na nani?” Filbert alimuuliza Saado.“Na kijana mmoja hivi”“Yupi”“Alikuwa akicheza mpira chuoni. Alitoka Afrika”“Mmmh! Si mimi”“Hapana. Inawezekana kuwa wewe”“Sikuwahi kucheza mpira chuoni, yaani sijawahi kusoma chuo huku” Filbert alimwambia Saado.“Hapana. Haukuwa mwanachuo, ulikuja na timu na kuanza kufanya mazoezi, mlitokea Afrika” Saado alimwambia Filbert.Hapo ndipo ambapo Filbert akaanza kuvuta kumbukumbu zake na kugundua kwamba msichana ambaye alisimama mbele yake alikuwa miongoni mwa watu ambao walikuwa wakiwatazama katika kipindi ambacho walikuwa wakichukua mazoezi, hapo, furaha ikaongezeka moyoni mwake kwani kwa jinsi dalili zilivyokuwa zikionyesha, kulikuwa na kila sababu ya kumchukua msichana yule.“Nadhani ni mimi”“Unadhani au ni wewe?”“Nadhani. Tulikuwa wengi, inawezekana umenifananisha na mmoja wa wachezaji wengine” Filbert alimwambia Saado.“Hapana. Ni wewe” Saado alimwambia Filbert.Katika kipindi chote hicho Dennis alikuwa amekaa kimya huku akiwasikiliza. Kila wakati alikuwa akimuona Filbert akipoteza muda kwani kwake hasa huku Tanzania akitokea msichana wa hivyo huwa unakamilisha mambo haraka haraka bila kuchelewa hata kidogo. Kwa Filbert hali ilionekana kuwa tofauti, alikuwa akitoa maelezo marefu ambayo hakutakiwa kuyatoa mahali hapo zaidi ya kuelewana na Saado na kisha kuamua kipi kifanyike baada ya hapo.Waliendelea kuongea pamoja na hata kutambulishana majina yao, kila mmoja akaonekana kufurahia urafiki wao ambao ulianza mahali hapo. Huo ndio ulikuwa mwanzo, waliendelea kuwasiliana mara kwa mara huku katika kila mechi ambayo timu ya Westerlo ilipokuwa ikicheza Saado alikuwa akielekea uwanjani kwa ajili ya kumwangalia Filbert.Walikuwa ni marafiki wa kawaida japokuwa kila mtu moyoni mwake alikuwa akijisikia mapenzi juu ya mwenzake ila hakukuwa na mtu ambaye aliweza kulizungumzia suala hilo. Walikuwa wakipeana zawadi mbalimbali na hata kutembeleana mahali walipokuwa wakiishi.Kwa Filbert tayari umaarufu ukaanza kumsogelea, akaanza kujiona mtu wa tofauti kila alipokuwa akiyaangalia magazeti yakiwa yameandika habari zake kwamba alikuwa staa ajae katika ulimwengu wa mpira duniani. Hilo lilikuwa likimhamasisha sana, hakutaka kabisa kuvimba kichwa zaidi ya kuendelea kufanya mazoezi zaidi na zaidi.Timu ya Westerlo ikaonekana kupata bahati ya kumsajili kwa mkopo mchezaji huyo ambaye alionekana kuwa moto wa kuotea mbali. Filbert aliendeleza mwiba wake kama kawaida, alikuwa akifunga magoli mengi ambayo yalionekana kuwa muhimu katika timu yake jambo ambalo lilimfanya kupendwa sana na mashabiki wa timu hiyo, hasa wanachuo.Hapo ndipo ambapo Filbert alipoanza kuona matatizo ya kuwa mtu maarufu, kila alipokuwa akipita watu walikuwa wakimzunguka na kutaka asaini vitabu vyao. Mambo ambayo alikuwa akiyaona kwenye televisheni yakiwatokea masupastaa wengi kama David Beckham na wengine wengi tayari yakaanza kutokea katika maisha yake pia.Kila kitu kikaonekana katika maisha yake kikaonekana kubadilika. Kitendo cha kufanya vizuri uwanjani ndicho ambacho kilimfanya kuandikwa sana magazetini na hatimae kuwa mtu maarufu. Kila kona ndani ya jiji la Brussel lilikuwa likisikika jina lake kama mchezaji chipukizi ambaye alikuwa mwiba na ambaye angekuja kutisha sana siku za usoni.Kutokana na fedha ambazo alikuwa akizipokea kuwa nyingi, hakuwasahau wazazi wake, kila wiki alipokuwa akipokea mshahara alikuwa akiwatumia kiasi fulani kwa sababu aliamini kwamba bila wao asingeweza kuwa mahali hapo katika kipindi hicho. Vilevile Filbert hakutaka kumsahau Amanda, msichana huyo bado alikuwa msichana wake na hivyo alitakiwa kumuonyeshea mapenzi japokuwa katika kipindi hicho kulikuwa na mtu mwingine ambaye alikuwa ameleta mabadiliko moyoni mwake, Saado.“Hapa inakuwaje Filbert?” Dennis alimuuliza Filbert.“Kuwaje kivipi?”“Kuhusu huyu Amanda na Saado” Dennis alimwambia Filbert.“Mbona kawaida tu”“Kawaida?”“Ndio. Amanda mpenzi wangu na Saado rafiki yangu” Filbert alimwambia Dennis.“Acha masihala. Unasema Saado ni rafiki yako na wakati mnafanya mambo mengi kama wapenzi!” Dennis alimwambia Filbert.“Kama mambo gani?”“Hivi unafikiri mimi ni kipofu Filbert? Huu ni wakati wa kuchagua ni yupi uwe nae. Umekwishapata umaarufu, kuna wengi watakufuata tena ni wazuri kuliko Saado na Amanda, uamuzi ni wako” Dennis alimwambia Filbert.“Ninampenda sana Amanda”“Najua. Na vipi kuhusu Saado?”“Kama nilivyokwambia, ni rafiki tu” Filbert alimwambia Dennis.Huo ndio ukweli ambao ulikuwepo kwa wawili hao, bado urafiki mkubwa ulikuwa ukiendelea kama kawaida lakini kila mmoja alikuwa akijisikia mapenzi moyoni mwake. Kila mmoja alikuwa akiogopa kumwambia mwenzake kwa kuona kwamba asingeonekana mtu wa kawaida kwani wote wawili walikuwa wakitambua kwamba walikuwa marafiki wa damu.Kutokana na Filbert kutikisa sana jiji la Brussels, vyombo vingi vya habari vikaanza kuutangaza ukaribu ambao alikuwa nao pamoja na msichana Saado. Jambo hilo liliwafanya wengi kuona kwamba Filbert alikuwa amepata rafiki mzuri ambaye alikuwa akipendwa na watu wengi ambao walikuwa wakimwangalia. Katika kila mahojiano ambayo yalikuwa yakifanyika, Filbert alizungumza kweli kwamba walikuwa ni marafiki na yeye alikuwa na msichana wake aliyeitwa Amanda ambaye alikuwa nchini Tanzania.Maneno yake yakaonekana kumuumiza sana Saado lakini akavumilia kwa sababu hakuwa amemwambia Filbert ukweli kuhusiana na moyo wake na ndio maana mwanaume huyo alikuwa tayari kumtambulisha msichana Amanda kama msichana wake ambaye alikuwa akimpenda sana na alikuwa tayari kumuoa endapo angempa nafasi ya kufanya hivyo.Ukaribu ukaendelea na urafiki kusonga mbele kila siku. Mabadiliko yakaanza kutokea. Wakaanza kubusiana na kupeana kumbatio la tofauti kabisa. Mabusu ambayo walikuwa wakiyatumia kubusiana ni yale ya pajini pamoja na shavuni na wakati mwingine mikononi. Mabusu yaliendelea na kadri siku zilivyozidi kwenda kunogeshwa zaidi na kuanza kubusiana midomoni na walipokuja kujishtukia, midomo ilikuwa wazi na kuanza kubadilishana mate.Hao walikuwa marafiki, marafiki ambao wakajikuta wakianza kufanya vitu vingine kama wapenzi. Hali ile iliendelea zaidi na zaidi na mwisho wa siku kujikuta wakiwa kitandani watupu kabisa, kilichofuatia ni Filbert kuitoa bikira ya Saado ambayo ilishindwa kutolewa na wanaume wengi nchini Ubelgiji.Mahusiano ya kimapenzi yakaanza rasmi kati ya Filbert na Saado. Wote wawili waliamua kwa pamoja kwamba uhusiano huo wa kimapenzi uwe siri ya watu wawili na hakutakiwa mtu yeyote afahamu juu ya kilichokuwa kikiendelea, wakawekeana makubaliana kwamba hivyo ndivyo ilivyotakiwa kufanyika katika maisha yao ya mahusiano.Kila siku wakawa watu wa kulala pamoja huku wakifanya mapenzi ambayo yaliwafanya kujisikia vizuri na kujiona kwamba walikuwa wakikosa kitu fulani muhimu katika maisha yao. Kitendo cha kupenda kufanya mapenzi kila siku ndicho ambacho kikawafanya kuanza kutazama filamu za ngono. Hapo ndipo ambapo walionekana kuchanganyikiwa zaidi kwani filamu zile zilionekana kuwa kitu cha tofauti sana ambazho kiliiweka miili yao kuwa kwenye hali ya tofauti kabisa.“Mmmh!” Saado alimwambia Filbert katika kipindi ambacho walikuwa kitandani usiku huku mkanda wa filamu za ngono ukionekana kwenye televisheni yao.“Nini tena?”“Yaani nimeangalia kwa dakika kumi tu, tayari nishaanza kupata msisimko” Saado alimwambia Filbert.Filbert hakutaka kujiuliza, tayari alikwishajua Saado alikuwa akimaanisha nini, alichokifanya ni kumsogeza upande wake na kisha kama kawaida yao kuanza kufanya mapenzi. Maisha ambayo walikuwa wakiyaishi mahali hapo ndio ambayo yalimfanya Filbert kuanza kumsahau Amanda. Ni kweli katika kipindi cha nyuma alikuwa akimpenda sana msichana huyo lakini muda huo tayari Saado alikuwa amekwishachukua nafasi maishani mwake.Ni maisha ya ngono tu ndio ambayo yalikuwa yakiendelea. Filbert hakufikiria kuhusu kushuka kiwango, kila alipokuwa akifanya mapenzi na ndivyo ambavyo alikuwa akifanya mazoezi zaidi zaidi kitu ambacho kilimfanya kuwa katika nafasi nzuri uwanjani. “Kamera ya nini?” Filbert alimuuliza Saado katika kipindi ambacho alikuja chumbani huku akiwa na kamera.“Kila siku tunawaangalia watu wakifanya mapenzi, kwa nini na sisi tusiwe tunajitazama wakati mwingine?” Saado alimwambia Filbert.“Kwa hiyo unataka tujirekodi?”“Ndio”“Hapana. Huo ni upuuzi Saado” Filbert alimwambia Saado.“Upuuzi wa nini sasa? Mbona Ray J alijirekodi na aliyekuwa mpenzi wake, Kim Kardashian, mbona yule mwanamuziki Eve nae alijirekodi na mpenzi wake, au umesahau?” Saada alimwambia Filbert.“Sasa hauoni kama ile mikanda ilivuja na dunia kuiona na hata huu wetu utaonekana” Filbert alimwambia Saado.“Huu hauwezi kuvuja. Mikanda yao ilivuja kwa sababu waliachana” Saado alimwambia Filbert.“Sasa si umeona kwamba hilo ni tatizo”“Sasa kwani sisi tutaachana?”“Hapana”“Sasa unahofia nini?”“Ila hatuwezi kujua kipi kitatokea baadae Saado”“Kwa maana hiyo utaniacha na kisha kumrudia huyo Amanda?”“Simaanishi hivyo”“Kumbe unamaanisha nini?”“Mkanda unaweza kuonekana kwa staili yoyote ile na si lazima uvuje” Filbert alimwambia Saado.“Hapana. Hakuna atakayeweza kuuvujisha zaidi yetu sisi” Saado alimwambia Filbert.“Una uhakika?”“Asilimia mia moja”“Sawa. Ila lengo ni nini hasa kutengeneza mkanda huu?”“Kila siku umekuwa ukiangalia utupu wa wanawake wengine, najisikia wivu, nataka uwe unaangalia utupu wangu tu kwenye televisheni” Saado alimwambia Filbert.Kwa kila swali ambalo alikuwa akiuliza Filbert mahali hapo lilikuwa likijibiwa kisomi zaidi kitu ambacho kilimfanya Filbert kutokuwa na swali lolote lile zaidi ya kukubali kuutengenza mkanda huo wa ngono kati yake na Saado. Kila kitu ambacho walikuwa wameanza kukifanya kilikuwa kikirekodiwa jambo ambalo lilimfurahisha sana Saado.Huo haukuwa mwisho wala kuwa mkanda wao wa mwisho bali waliendelea kurekodi mikanda mingine zaidi na zaidi huku mikanda yote ile wakiifuta katika kamera na kuiingiza katika email zao. Mchezo huo ukaonekana kuwa siri, siri ambayo wala haikuweza kuvuja. Mpaka msimu unaishi na Filbert kuiongoza Westerlo kupanda daraja na kuingia ligi kuu, bado mchezo wao wa kujirekodi ulikuwa ukiendelea kama kawaida.Filbert na Saado wakaacha kuwaangalia Micky Blue, Skin Diamond, Victoria Allure na wasanii wengine wa filamu za utupu na kuanza kujitazama wao wenyewe. Hayo ndio yakawa maisha yao, kila siku ukawa mchezo wao, hakukuwa na mtu aliyefikiria kwamba mazoea hujenga tabia, na kama ni mazoea mabaya basi yangeweza kujenga tabia mbaya.Filbert hakuonekana kufahamu kitu chochote kwamba yale mazoea yangeweza kujenga tabia, tabia ambayo angeifanya hata sehemu nyingine na kumletea matatizo hasa katika maisha yake ya baadae, kwake, kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea mahali hapo alikichukulia kuwa kawaida tu, wala hakutaka kujali sana kwa kuwa filamu zote ambazo alikuwa akiigiza na Saado kitandani alikuwa akizihifadhi katika email yake.Je nini kitaendelea?Je nini hatma ya maisha yao?Je Filbert ataweza kumkumbuka Amanda? ITAENDELEA
Simulizi : A Sex Video Scandle Sehemu Ya Nne (4) Hayo ndio maisha ambayo walikuwa wakiishi kila siku, walikuwa ni watu wa kufanya ngono kila siku tena huku wakijirekodi na kisha kuzihifadhi video zile kwenye email zao. Wakaonekana kuzoea sana mpaka kuwajengea tabia ambapo waliona bila kujirekodi wakati wanafanya mapenzi tendo hilo halikuwa likikamilika.Filbert bado alikuwa akiendelea kwenda shuleni kama kawaida. Ndoto yake nyingine kubwa ambayo alikuwa amejiwekea ilikuwa ni kusoma sana na hatimae baada kuja kugombea urais katika chama chochote kile nchini Tanzania. Hilo ndio lilikuwa lengo kubwa ambalo alijiwekea katika maisha yake na kuhakikisha kwamba siku moja linakuja kutimia.Saado alikuwa ameuteka moyo wake, hakumfikiria tena Amanda ambaye alimuahidi mambo mengi likiwa la kutokumsaliti katika maisha yake. Filbert alionekana kusahau kila kitu, mapenzi ya Saado yalikuwa yakimlevya kila siku. Hakukumbuka kumpigia simu Saado, hakukumbuka kuwasiliana nae kwa kutumia mtandao wa Skype, mtu ambaye alikuwa muhimu kwake wakati huo alikuwa mtoto wa kisomali, Saado.Siku ziliendelea kukatika kama kawaida, jina lake liliendelea kuwa kubwa kila siku. Baada ya ligi hiyo kumalizika hapo ndipo Filbert alipotakiwa kuachana na timu ya Westerlo ambayo alikuwa akichezea kwa mkopo na hatimae kujiunga na timu ya Gent, timu ambayo ilikuwa imemsajili. Kutokana na jina ambalo alianza kujijengea, mashabiki wengi wa timu ya Genk wakaonekana kuturahia kwa kuona kwamba mchezaji huyo angeweza kuifanyia makubwa timu hiyo.Kitendo cha kupata jina kubwa nchini Ubelgiji, jina lake nalo lilikuwa likikua kwa kasi sana nchini Tanzania. Watanzania wakajivunia sana kuwa na mchezaji kama Filbert ambaye kila siku kazi yake ilikuwa ni kuitangaza nchi ya Tanzania. Kupitia jina lake, jezi nyingi za timu ya Genk zikaletwa nchini Tanzania, watu wakaanza kuzinunua kama njugu, jina la Filbert likaonekana kuwa kivutio kwa kila mtanzania.Huo ndio ulikuwa wakati ambao ligi hiyo ilipoanza dhahiri. Kila siku Filbert alikuwa akiamka asubuhi kama kawaida yake na kisha kwenda mazoezini hata kabla wachezaji wenzake hawajafika uwanjani hapo. Hiyo ilikuwa ni njia mojawapo ya kukamilisha ndoto yake ya kuwa mchezaji mkubwa zaidi ya pale alipokuwa. Mazoezini alikuwa akijituma sana kitu ambacho kilimfurahisha kila kiongozi wa timu ile.“WE LOVE U FILBERT, MARRY ME TONIGHT FILBERT, FILBERT AM FREE TONIGHT” Hayo yalikuwa ni baadhi ya mabango ambayo yalikuwa yameshikiliwa na wanawake ambao walikuwa wakiingia katika uwanja wa timu ya Genk. Mabango yale na sauti nyingi za mashabiki zikamfanya Filbert kupata nguvu ya kuzidi kucheza mpira.Katika kila mechi ambayo Filbert alikuwa akiingia uwanjani bado alikuwa akionekana kuwa mwiba mkali kwa timu pinzani. Katika kipindi hicho alikuwa ndio kwanza ameingia miaka kumi na nane, alionekana kuwa mshambuliaji machachari ambaye kila alipokuwa akisimama mbele ya goli wazo lake lilikuwa moja tu, kufunga.Hiyo ndio siafa ambayo ilimfanya kujulikana, watoto wa kike hawakuwa nyuma, kila siku walikuwa wakimsumbua huku wakimuonea wivu Saado kutokana na kuwa na mwanaume ambaye alionekana kuwa mvuto kwa kila mwanamichezo ambaye alikuwa akimwangalia. Filbert hakutaka kuwa na wanawake wengi, alichokuwa akikitaka ni kuwa na Saado tu.“Yaani sikusomi kabisa siku hizi” Dennis alimwambia Filbert.“Kivipi?”“Kuhusu huyu Saado. Hivi inakuwajekuwaje hapa?” Dennis aliuliza.“Kuwaje kivipi?”“Ni mpenzi wako au?”“Wewe unaonaje?”“Hapo ndipo unaponichanganya. Kila nikiangalia naona dalili zote za kuonyesha kwamba ni mpenzi wako, ila nilipokuwa nikikuuliza uliniambia kwamba ni rafiki yako. Hebu nieleze leo” Dennis alimwambia Filbert.“Saado ni rafiki yangu” “Hapana”“Sasa kwa nini hutaki kuamini?”“Rafiki! Hivi rafiki yako unaweza kulala nae chumba kimoja tena usiku?” Dennis alimuuliza Filbert.“Kwa nini nisiweze?”“Sisi ni waafrika na ngozi zetu zina joto, mambo hayo wanayaweza wazungu. Nadhani kuna kitu unanificha” Dennis alimwambia Filbert.“Huo ndio ukweli bro”“Hapna. Hebu niambie ukweli”“Sawa. Saado ni mpenzi wangu”“Sasa ulikuwa ukinificha nini?”“Mambo mengine siri sana”“Hapo hakuna siri. Na vipi kuhusu Amanda?” Dennis alimuuliza Filbert.“Hilo ndio linaniumiza kichwa”“Moyo wako umeamua nini?”“Kiukweli moyo wangu umeamua kuwa na Saado” Filbert alijibu.“Basi kuwa na Saado”“Kwa sasa hivi poa ila kwa baadae nadhani Amanda atanihusu sana” Filbert alimwambia Dennis.“Kwa hiyo Saado sio wa kuoa?”“Hiyo ndio maana yangu. Huyu ni wa kupita na kuacha?”“Hilo ni jibu”Hivyo ndivyo ambavyo Filbert alivyokuwa amejipangia, alijua fika kwamba alikuwa akimpenda sana Saado lakini hakuona kama kulikuwa na uwezekano wa kumuoa msichana huyo maisha yake ya baadae. Alionekana kuwa msichana mrembo lakini bado hakuwa na sifa za kuweza kuwa mke wake. Filbert alijua fika kwamba Saado alikuwa Msomali na hakuwa Mtanzania hivyo kama angemuoa basi asingeweza kujisikia uhuru kama ambavyo angekuwa na msichana wa kitanzania. Hiyo pamoja na sababu nyingine za msingi zikamfanya Filbert kuona kwamba Saado hakutakiwa kuwa mke wake.Shuleni alipokuwa akisoma mambo yalikuwa ni balaa. Watu wengi walikuwa wakimzunguka kila siku huku wengine wakitaka kusainiwa vitabu vyao. Sura ya Filbert ikaonekana kuwa dili kwa wakati huo, wanawake wengi walikuwa wakimfuata na kamera zao na kisha kupiga nae picha kwa ajili ya kuwaonyeshea marafiki zao.Ucheshi wake pamoja na kuwa na roho ya unyenyekevu kwa watu wengine ndivyo vilikuwa vitu pekee ambavyo vilimfanya kufagiliwa na watu wengi ambao walikuwa wakikutana nae. Kila alipokuwa akiingia katika supermarket mbalimbali hali haikuonekana kuwa ya amani kabisa, watu walikuwa wakimfuata na kisha kumzunguka kitu ambacho alikuwa akipigwa marufuku kuingia supermarket na kama alikuwa akitaka kuingia, watu walikuwa wakitolewa katika kila duka ambalo alitaka kuingia.Jina lake likazidi kuwa kubwa, Filbert akaonekana kuwa na nyota ya kupendwa sana na watu wa hapo Brussels. Ni kweli katika ligi kuu kulikuwa na wachezaji wengi lakini kwa Filbert alionekana kupendwa zaidi na kila mtu mahali hapo. Kila alipokuwa akipita alikuwa akisimamishwa na watu kwa lengo la kupiga picha hali ambayo ilimfanya kuanza kutembea na gari na kuanza maisha ya kujificha.“Kumbe kuwa supastaa raha sana” Filbert alimwambia Dennis.“Kwa nini?”“Heshima. Kila ninapopita ninapewa heshima kitu ambacho kinanifariji sana” Filbert alimjibu Dennis.“Ila kuwa makini na pia endelea kukumbuka kwamba ndoto zako hazitakiwi kuishia hapo, ikibidi tufanye mchakato uende Uingereza” Dennis alimwambia Filbert.Maisha yaliendelea zaidi, hakuacha kucheza mpira na wala hakuacha kusoma. Mwaka wa kwanza ukakatika, bado aliendelea kusakata kabumbu. Katika kila msimu wa ulipokuwa ukimalizika wachezaji walikuwa wakipewa likizo ya mwezi mmoja, kwa Filbert hakutaka kuja nchini Tanzania, alikuwa akiondoka zake na kuelekea nchini Marekani na kuponda raha huku akiwa pamoja na msichana wake, Saado.Katika kipindi hicho Filbert alikuwa na fedha nyingi na za kutosha huku akiwa kijana mdogo sana, hakuwa amezoea fedha hivyo alikuwa akizitumia kadri alivyotaka na wala hazikuisha kabisa. Kama starehe, katika kila mwisho wa msimu alikuwa akifanya starehe ya kila aina, alikuwa akitembelea katika kumbi zilizokuwa na gharama ambazo zilikuwa zikitembelewa na masupataa na watu wenye fedha tu.Filbert hakuchungulia mfuko wake, alikuwa akiendelea kuzitumia kila siku huku kila wiki kiasi kikubwa cha fedha kikiingizwa kwenye akaunti yake. Mtu mwenye ngozi nyeusi ambaye alikuwa katika maisha ya kimasikini akawa na fedha. Alifanya kila kitu alichokuwa akitaka kukifanya. Alifika mpaka nchini Marekani, nchi ambayo alikuwa akiisikia katika vyombo vya habari tu.Leo alikuwa akilala New York na kesho kuhamia Washington, leo alikuwa akienda kula chakula cha mchana Ohio na kesho alikuwa akienda kula chakula cha usiku Calfornia. Hayo ndio maisha ambayo alikuwa kiyapenda, katika kila sehemu ambayo alikuwa akienda, mpenzi wake, Saado alikuwa pembeni yake.Hayo yakawa maisha ya kisupastaa ambayo alikuwa akiishi. Baada ya kukatika siku kadhaa, msimu mwingine ukaanza, huo ulikuwa mwaka wake wa tatu kukaa nchini Ubelgiji bila kurudi nchini Tanzania. Kama kawaida yake, uwanjani hakuwa akitaka kuleta mbwembwe nyingi, kitu ambacho alikuwa akikitaka ni kuudhihirishia ulimwengu kwamba alikuwa mchezaji wa kipekee ambaye alistahili hata kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia.Makali yake yakaongezeka zaidi, starehe ambazo alikuwa amezifanya zikaonekana kama kumpa nguvu ya kucheza zaidi mpira. Mashabiki walivutiwa nae na hata kumuona kama mungu mtu kwenye timu yao. Kila alichokuwa akikitaka alikuwa akipatiwa bila kuulizwa swali lolote lile. Katika kipindi chote ambacho Filbert alikuwa ameichezea Genk, tayari walikuwa wamechukua kombe la ligi mara tatu.Jina lake likakuzwa zaidi, timu za Uingereza zikamuona, hapo ndipo purukushani zilipoanza rasmi. Manchester United, Arsenal, Chelsea na Liverpool zilikuwa miongoni mwa timu ambazo zilikuwa zikimhitaji sana Filbert ambaye alionekana kuwa kama lulu katika maisha ya soka. Fedha zikawekwa mezani kwa ajili ya kumsajiri mchezaji huyo ambaye aliitwa kwa jina la utani “Mtambo wa mabao”.“Ofa zimekuja nyingi tu, tena za fedha ndefu. Unataka nifanye mchakato na timu gani?” Dennis alimwambia Filbert na kisha kumuuliza.“Kuna timu zipi zimekuja?”“Zote kubwa unazozijua nchini Uingereza” Dennis alimwambia Filbert.“Hakuna timu ndogo iliyokuja?”“Labda na Newcastle”“Hiyo ndio nzuri.Nataka kwenda kucheza Newcastle” Filbert alimwambia Dennis ambaye akaonekana kushtuka.“Unasemaje?”“Nataka kwenda kucheza Newcastle”“Hapana. Nadhani utakuwa unanitania. Hebu kuwa serious kidogo Filbert” Dennis alimwambia Filbert.“Huo ndio ukweli”“Kwa hiyo umeichagua Newcastle mbele ya Arsenal? Umeichagua Newcastle mbele ya Manchester, Chelsea na Liverpool?” Dennis aliuliza huku akionekana kutokumuelewa Filbert.“Ndio”“Kuna nini Newcastle?”“Kuna fedha nyingi”“Fedha nyingi? Yaani Newcastle kuna fedha nyingi?”“Ndio”“Acha masihala”“Ndio hivyo. Kwani Manchester wameweka mezani bei gani?”“Wameweka paund milioni kumi na tano, Arsenal wameweka paund milioni kumi na nne, Liverpool paundi milioni kumi na saba Chelsea paund milioni ishirini” Dennis alimwambia Filbert.“Na vipi kuhusu Newcastle?”“Wameweka paundi milioni kumi”“Hapo ndipo ninapotaka kwenda”“Mungu wangu! Filbert, una akili?”“Kwa sasa utaona sina akili, ila baada ya miaka minne utaona kwamba nina akili” Filbert alimwambia Dennis.Huo ndio uamuzi ambao alikuwa ameuweka mahali hapo, aliichagua klabu ya Newcastle kwa moyo mmoja na wala hakutaka kwenda katika klabu kubwa ambazo zilikuwa zikimuhitaji kwa wakati huo. Baada ya tetesi za kutaka kuihama klabu hiyo zilipoanza kusikika, Genk wakaamua kuweka kikao pamoja nae huku wakimtaka kusaini mkataba mpya ambao ule wa zamani ulikuwa umebakisha miaka miwili. Hilo likaonekana kuwa gumu kwa Filbert, hakutaka kuongeza mkataba zaidi ya kutaka kuhama katika timu hiyo ambayo ilionekana kumthamini sana. Hilo likaonekana kuwa kama pigo kwa Genk jambo ambalo liliwafanya waandishi wa habari kuanza kumtafuta kwa ajili ya kufanya mahojiano nae, walikuwa wakitaka kujua sababu ya kutosaini mkataba na kama kulikuwa na timu anayotaka kuhamia ilikuwa timu ipi.“Nataka kwenda Uingereza” Filbert alimjibu mwandishi wa habari.“Kipi kimekupelekea kwenda nchini Uingereza?”“Nataka kucheza soka katika timu kubwa zaidi. Najua kwa hapa Ubelgiji hii Genk ni timu kubwa ila nadhani huu ni wakati wa kwenda kucheza klabu kubwa zaidi ya hii” Filbert aliwaambia waandishi wa habari.“Na si kwamba unafuata fedha Uingereza?”“Hapana. Nataka kujitangaza zaidi“Utakwenda timu gani kwa sababu naona timu zote kubwa nchini Uingereza zimeweka ofa mezani?” Mwandishi mwingine wa habari aliuliza.“Nitakwenda Newcastle”“Unakwenda Newcastle?”“Ndio”“Kwa nini isiwe Manchester, Arsenal au Chelsea”“Ni kwa sababu nataka kuwaonyeshea mashabiki wa Genk kwamba sikuondoka mahali hapa kwa sababu ninataka fedha zaidi, hapana, ninaondoka mahali hapa kwa sababu ninataka kuwa na changamoto mpya” Filbert aliwaambia waandishi wa habari.Kitendo cha kusema kwamba alikuwa akitaka kwenda kuchezea klabu ya Newcastle, mazungumzo ya malipo ya mshahara binafsi yakawekwa mezani na kuahidiwa kulipwa paund elfu sitini kwa wiki ambazo zilikuwa ni sawa na milioni mia ishirini na nne kwa fedha za kitanzania tena malipo hayo yakifanyika kila wiki.Katika kipindi hicho cha mapumziko Filbert hakurudi nchini Tanzania, alikuwa bize akishughulikia mambo yake ya uhamisho. Mpaka msimu mwingine unafunguliwa, Filbert alikuwa ndani ya jezi ya klabu ya Newcastle United ya nchini Uingereza. Kwake, hiyo ikaonekana kuwa ndoto kubwa ambayo alikuwa akiisubiria katika maisha yake.Picha nyingi zikapigwa, magazeti mengi yakatangaza ujio wake ndani ya klabu hiyo kwa paund milioni kumi. Mashabiki wengi wa mpira wakaonekana kumshangaa kwa kuzikataa klabu kubwa na kuamua kucheza katika klabu hiyo, kati ya watu ambao walikuwa hawamuelewi kabisa Filbert alikuwa Dennis.“Manchester walisema wangekulipa paundi elfu tisini, Arsenal paundi elfu themanini na Chelsea paund laki moja. Yaani umekataa huko na kuja hapa kwa paundi elfu sitini!” Dennis alimwambia Filbert.“Najua nilifanyalo. Nimekuja hapa ili tupate fedha zaidi, au wewe hautaki?” Filbert alimuuliza Dennis.“Tupate fedha nyingi, kivipi?”“Kihivyo hivyo”“Utakuwa umechanganyikiwa”“Najua, ila baada ya miaka mitano utaniona nina akili timamu” Filbert alimwambia Dennis.Jijini Newcastle, mashabiki wa timu hiyo hawakutaka kutulia, kila wakati walikuwa wakishangilia, kitendo cha kumpata Filbert kilionekana kuwafurahisha sana na kuwaona wapinzani wao, Sunderland kuwa si lolote lile. Filbert alionekana kuwa mwiba mkali uwanjani na kwa upande wa timu pinzani. Uwezo wake wa juu ndio ambao ulimfanya kila mtu kumwamini na kuona kwamba angekwenda kufanya mambo makubwa katika maisha yake ya soka ndani ya klabu hiyo.“Amanda….!” Filbert alijisemea katika kipindi ambacho alikaa kimya kwa muda chumbani kwake, picha ya Amanda ilikuwa imemjia kichwani mwake, akaanza kumkumbuka msichana huyo ambaye hakuwa amewasiliana nae kwa kipindi kirefu sana, miaka mitatu.
KWA WASOMAJI WAPYA. Filebrt alikuwa kijana wa kitanzania, kijana ambaye alikuwa na ndoto za kuwa mwanasheria mkuu nchini Tanzania. Ndoto yake hiyo ya kuwa mwanasheria ilikuja kukatika mara baada ya kugundua kwamba alikuwa na uwezo wa kucheza mpira wa miguu. Alicheza sana mpira wa miguu kiasi ambacho baba yake, mzee Martin akaamua kumpeleka katika shule ya vipaji vya michezo, Makongo.Huko aliendelea kusakata kabumbu mpaka pale alipochaguliwa kujiunga na timu ya mkoa wa Dar es Salaam na kisha kushiriki katika mashindano ya Copa Coca Cola. Timu hiyo ikachukua kombe na Filbert kuwa mfungaji bora na mchezaji bora pia. Timu ikachaguliwa kwenda nchini Ubelgiji. Siku kadhaa kabla ya kwenda Ubelgiji, Filbert akakutana na msichana ambaye alimpa namba ya simu, huyu alikuwa Amanda. Walipokutana wakaongea mengi na kujikuta wakiwa wapenzi waliopendana kwa dhati.Siku ya safari inapofika, Filbert anaondoka na kuelekea nchini Ubelgiji. Nchini humo, anafanikiwa kununuliwa na timu ya mpira wa miguu ya Genk ambayo inamtoa kwa mkopo na kuchezea timu ya Westerlo. Filbert anaonyesha uwezo wake, anafunga sana magoli, anapata umaarufu mkubwa uliompeleka kukutana na msichana wa kisomali, Saado.Wawili hawa wanaanza uhusiano wa kimapenzi huku wakijirekodi video katika kila kipindi walichokuwa wakifanya mapenzi. Japokuwa Filbert alikuwa akiwasiliana sana na Amanda lakini baada ya kumpata Saado, mawasiliano yanapungua na kufa kabisa. Yeye na Saado, Saado na yeye. Filbert akaamua kurudi darasani, lengo la kurudi darasani ni kwamba anataka kuwa rais wa Tanzania hapo baadae, anasoma na kucheza mpira.Timu zote kubwa za Uingereza zikamtaka lakini yeye akaamua kwenda Newcastle huku akisema kwamba baadae angepata fedha nyingi mno kitu kinachomchanganya wakala wake ambaye ni kaka yake, Denis. Maisha ya soka nchini Uingereza yanaanza na huku mahusiano yake na Saado yakiendelea kama kawaida. Filbert hamkumbuki Amanda, anayemkumbuka ni yule ambaye yupo nae katika kipindi hicho, Saado tu. Inatokea siku, siku ambayo alikaa na kulitamka jina ambalo hakulitamka katika kipindi kirefu cha nyuma, AMANDA. *******************Amanda hakuonekana kuwa na furaha nchini Tanzania, kila siku mawazo yake yalikuwa kwa mvulana ambaye alikuwa akimpenda kuliko mtu yeyote yule, Filbert Martin. Katika kipindi hicho Filbert hakuwepo nchini Tanzania, alikuwa amesafiri na kuelekea nchini Ubelgiji kwa ajili ya kufanya mazoezi ya mpira wa miguu pamoja na timu ya taifa ya vijana ya Tanzania.Usiku, mawazo yake yalikuwa yakimfikiria sana Filbert, kila wakati alikuwa akikosa raha, hakuwa akijisikia vizuri kwani alitamani kipindi chote cha maisha yake awe pamoja na Filbert kwani ndiye alionekana mfariji wa maisha yake. Filbert hakuwa pamoja nae, alikuwa akimfikiria kila siku lakini hali hiyo haikuonekana kubadilisha kitu chochote kile kwani Filbert aliendelea kuwa mbali na uwepo wa macho yake.Wakati mwingine Amanda alionekana kuchukia na kujuta kwa kuuruhusu moyo wake kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na Filbert, alijiona kama mtu ambaye alikuwa amefanya kosa kubwa la kumruhusu mwanaume huyo kuushika moyo wake kama kupita kawaida. Wiki ya kwanza ikakatika tangu Filbert aondoke na kuelekea nchini Ubelgiji, Amanda aliendelea kuvumilia kwa kuona kwamba ilikuwa imebakia wiki moja tu na hatimae mpenzi wake arudi nchini Tanzania na kuendelea kuonana kama kawaida.Wiki ya pili ikaingia na kumalizika lakini Filbert hakuwa amerudi nchini Tanzania. Maswali mengi yakaanza kumiminika kichwani mwake kwamba kulikuwa na kitu gani ambacho kilitokea nchini Ubelgiji mpaka mpenzi wake kutokuja ndani ya wiki hiyo, maswali hayo yalijibiwa na gazeti la michezo la Champion ambalo liliandika kwamba wachezaji kadhaa wa timu ya vijana wa Tanzania ambao walikwenda nchini Ubelgiji walikuwa wamesajiliwa na timu za huko.Taarifa hizo zikaonekana kuwa sifa kwa taifa zima la Tanzania lakini kwa Amanda ilionekana kuwa kama taarifa ya msiba kwani aliposoma majina ya vijana hao katika gazeti lile, Filbert alikuwa mmoja wapo. Amanda akashindwa kuvumilia, akaanza kutokwa na machozi, kitu ambacho alikifahamu ni kwamba Filbert asingeweza kuwa nae tena, alikuwa akimpoteza huku akimuona.Mawazo ya Amanda yakaonekana kuwa tofauti hasa pale ambapo Filbert alipoanza kumpigia simu mara kwa mara na kuanza kuongea nae. Hiyo ikaonekana kuwa kama faraja kwa Amanda, hakuamini kama angeweza kupokea simu kutoka kwa Filbert na kumwambia kwamba bado alikuwa akimpenda kupita kawaida na alikuwa akimhitaji zaidi ya msichana yeyote yule.Maneno yale yakamfariji na kumtia nguvu sana, akajiona kuwa msichana aliyekuwa na bahati kuliko msichana yeyote katika dunia hii. Mawasiliano baina ya watu hao wawili yalikuwa yakiendelea kama kawaida, mara kwa mara walikuwa wakiongea huku Filbert akimwambia Amanda juu ya kila kilichokuwa kikiendelea nchini Ubelgiji.“Utarudi lini?” Hilo lilikuwa swali kutoka kwa Amanda, alikuwa akimuuliza kila siku.“Nitarudi hivi karibuni, lakini kwanza subiri nikaekae kidogo huku mpenzi” Filbert alimwambia Amanda.“Sawa. Ila usinisahau tu kipenzi” “Hilo usijali, siwezi kukusahau, wewe ndiye mwanamke ambaye ninampenda kwa moyo wote maishani mwangu, naahidi kukuoa” Filbert alimwambia Amanda.“Nashukuru”“Kuna kitu nimekifikiria mpenzi”“Kitu gani?”“Nataka kuwa rais wa Tanzania hapo baadae” Filbert alimwambia Amanda.“Kwa nini umefikiria hivyo?”“Basi tu, nataka kuwa rais, ili kukamilisha ndoto yangu naomba uniunge mkono” Filbert alimwambia Amanda.“Hakuna tatizo mpenzi, nitafanya hivyo” Amanda alimwambia Filbert.“Nitashukuru”Hayo ndio yalikuwa maongezi ambayo walikuwa wakiongea kila siku, walikuwa wakipeana ahadi za kuishi pamoja baadae pamoja na kuwa na familia moja yenye amani na upendo. Walipendana na kusikilizana japokuwa walikuwa katika nchi mbili tofauti. Kila mmoja alionekana kumjali mwenzake, walikuwa wakipendana sana.Baada ya mwaka mmoja, mabadiliko yakaanza kutokea katika mahusiano yao, mawasiliano yakaanza kupungua na hayakuwa kama zamani. Hilo likawa swali gumu kujibika kichwani mwa msichana Amanda. Hakujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kikifanya hivyo lakini alipofikiria kwamba Filbert alimwambia kwamba angeanza kuingia darasani akaonekana kupunguza wasiwasi juu ya mahusiano yao kwa kuona kwamba Filbert alikuwa bize na masomo.Walizoea kuongea simuni, Filbert hakuwa akipiga simu, walizoea kuongea kupitia mtandao wa Skype lakini Filbert hakufanya hivyo. Hilo likaonekana kuwa kama pigo kwa Amanda, alikuwa amemkumbuka sana mpenzi wake lakini hakujua ni kipi kilikuwa kimesababisha jambo hilo kutokea. Huku akiwa analifikiria sana hilo, hapo ndipo akaanza kupata jibu, jibu la swali ambalo lilikuwa likimsumbua kichwani.Filbert alikuwa ameanza kupata umaarufu, mara kwa mara picha zake zilikuwa zikionyeshwa katika magazeti mengi Ulaya pamoja na magazeti ya kitanzania, hususani gazeti la Champion. Filbert alionekana kuwa mwanasoka ambaye alipenda sana starehe, leo alikuwa hapa na kesho alikuwa pale, alikuwa akitumia pesa bila kuwa na habari yoyote ile.Japokuwa alionekana kuwa hivyo lakini bado Filbert alikuwa kipenzi cha wapenda soka duniani, alikuwa akijituma sana mazoezini na hata kwenye mechi kitu ambacho kilimfanya kufunga magoli mengi. Amanda alikuwa akifuatilia kila kitu, kila siku ambayo gazeti la Champion lilipokuwa likitoka, Amanda alikuwa akilinunua, alihitaji kusoma taarifa nyingi kuhusiana na Filbert.Umaarufu, fedha vikaonekana kumsahaulisha Filbert ila pamoja na hayo yote, kulikuwa na kitu kimoja kikubwa ambacho kilimfanya Filbert kumsahau Amanda, kitu hiki kilikuwa ni mapenzi. Kwa mara ya kwanza Amanda alipoona taarifa kwamba Filbert alikuwa amempata msichana wa kisomali, Saado, mwili wake aliuhisi ukisisimka kupita kawaida, moyo wake ukawa na maumivu ya ghafla, maumivu ambayo yalifanana na kuchomwa msumali wa moto kwenye kidonda kibichi. Hilo likaonekana kuwa pigo kwa Amanda, akakosa raha, kila siku akawa mtu wa kulia tu. Katika kipindi hicho Amanda alikuwa kidato cha tatu, hakuweza kusoma vizuri, hakuweza kusoma kwa furaha kutokana na kile ambacho kilikuwa kikiendelea nchini Ubelgiji. Alimpenda sana Filbert na alikuwa tayari kufanya kitu chochote kwa ajili yake lakini Filbert alionekana kubadilika, akamsaliti na kuanza kutembea na msichana mwingine, msichana aliyeonekana kuwa mrembo sana, Saado.Mwaka huo ukakatika na kuingia kidato cha nne, bado hakuwa akipata simu kutoka kwa Filbert, hakumsahau mwanaume huyo, kila siku alikuwa akiendelea kununua magazeti ya Champion huku lengo lake likiwa ni kuzisoma taarifa mbalimbali za Filbert, alijua kwamba zilimuumiza sana lakini hakuwa na jinsi, alijisikia kuwa na mapenzi ya dhati moyoni mwake.“Ninashindwa kusoma mama” Amanda alimwambia mama yake, Bi Vanessa.“Kwa nini?” Bi Vanessa aliuliza kwa mshtuko.“Mapenzi mama” Amanda alimwambia mama yake.“Mapenzi! Yamefanya nini?” “Ninampenda mwanaume ambaye anaonekana kutokuwa tayari kunipenda kama ninavyompenda. Mwanaume huyu amekuwa mwanaume wangu toka kidato cha pili ila kwa sasa hayupo pamoja nami” Amanda alimwambia mama yake maneno ambayo yalionekana kumshtua.“Mwanaume gani?”“Filbert. Yule mchezaji wa mpira Ulaya” Amanda alimwambia mama yake.Bi Vanessa akashindwa kuvumilia kabisa, alionekana kukasirika sana lakini hakuwa na jinsi, alichoamua kukifanya ni kumwambia mume wake, mzee Frank juu ya kila kilichokuwa kikiendelea kwa binti yao. Kwanza mzee Frank akawa na hasira kali, hakutegemea kusikia kwamba binti yake alikuwa kwenye mahusiano na mvulana yeyote yule, alitaka binti yake asome kwa juhudi kubwa na hatimae kutimiza ndoto zake ambazo alikuwa amejiwekea toka kitambo. ITAENDELEA
“Umesema huwezi kusoma?” Mzee Frank alimuuliza Amanda kwa hasira.“Mapenzi baba”“Hebu nijibu swali langu kwanza. Umesema huwezi kusoma?” Mzee Frank aliuliza huku akiwa na hasira kali, kila alipokuwa akimwangalia Amanda alijiona kuzidi kuwa na hasira.“Ndio. Siwezi kusoma baba, nadhani nitafeli, kila ninapojaribu kusoma ninashindwa” Amanda alimwambia baba yakeMzee Frank hakusema kitu, akabaki kimya kwa muda, mwili wake ulikuwa ukitetemeka kwa hasira, hakutegemea kusikia maneno kama yale yakitoka kinywani mwa binti yake ambaye alimpa kila kitu katika maisha yake ili afanikiwe na kuwa mtu fulani hapo baadae. Hakuipenda kauli ya Amanda, alipenda sana kumuona binti yake akiendelea kusoma.“Mapenzi! Yaani mapenzi ndio ambayo yanakufanya kukataa elimu?” Mzee Frank alimuuliza Amanda.“Nitafeli baba, siwezi kusoma, saikolojia yangu imeharibiwa vibaya baba” Amanda alimwambia baba yake.“Haiwezekani, lazima uendelee kusoma, achana na mapenzi” Mzee Frank alimwambia Amanda.Maneno yake mengi hayakuweza kubadilisha kitu chochote kile, bado Amanda alizidi kung’ang’ania kwamba asingeweza kusoma kabisa. Ni kweli, akili yake haikuwa sawa, alikuwa katika mapenzi ya dhati na Filbert, alimpenda sana na ndio maana hata kile kitendo cha kumsaliti kilimfanya kuiharibu sana akili yake na kumuweka katika hali ya mawazo.Hakuona sababu ya kusoma, mapenzi yalikuwa yameuharibu sana moyo wake, hakujua kama angeweza kusoma na kufaulu, hakuwa akijisikia sawa kwa wakati huo. Huo ndio ukawa mwisho wa Amanda kusoma, hakwenda tena shule kitu ambacho kiliwakasirisha sana wazazi wake lakini hawakuwa na jinsi. Walikuwa wakimpenda sana binti yao na hawakuwa tayari kumuona akiwa katika hali ya majonzi kama ile ambayo alikuwa nayo katika kipindi hicho.Mwaka huo ukakatika na ndipo ambapo aliona taarifa gazetini kwamba mtu aliyekuwa mpenzi wake, Filbert alikuwa akihama kutoka katika klabu yake ya Genk ya nchini Ubelgiji na kuelekea nchini Uingereza na kuanza kucheza katika timu ya Newcastle United. Hiyo ikaonekana kuwa furaha kwa Amanda kwani aliamini kwamba kila wikiendi angeweza kumuona mpenzi wake wa zamani akicheza mpira. “Nakupenda Filbert” Amanda alijisemea kila alipokuwa akimuona Filbert luningani akicheza mpira.“Rudi kwangu mpenzi wangu, nimeacha shule kwa ajili yako, umeuumiza sana moyo wangu, ninakupenda sana, naomba usahau kila kilichopita, rudi kwangu, mimi nidye mtu pekee niliye kwenye mapenzi ya dhati, naomba urudi kwangu mpenzi, ninakupenda, nakupenda sana” Amanda alisema katika kipindi ambacho alikuwa akiziangalia picha mbalimbali za Filbert.Majonzi yake hayakuweza kubadilisha kitu chochote kile, bado Filbert aliendelea kuwa na msichana Saado nchini Uingereza na wala hakuonekana kuwa na dalili za kumrudia Amanda nchini Tanzania. Maumivu yake yaliendelea zaidi na zaidi moyoni mwake. Huo ulikuwa ni mwaka wa pili toka Filbert aache kuwasiliana nae lakini hakuweza kumsahau mwanaume huyo, alikuwa akizidi kumpenda kila siku na alikuwa tayari kwa chochote kile wakati huo.“FORGIVE ME, I MISS YOU AMANDA (NISAMEHE, NIMEKUKUMBUKA AMANDA)” Yalikuwa ni maneno ambayo yalisomeka vizuri sana katika fulana ambayo aliivaa Filbert katika kipindi ambacho alifunga goli safi wakati Newcastle ilipocheza na Manchester United. Filbert alionekana kama kuchanganyikiwa, alikuwa amekimbia mpaka katika sehemu kilipokuwa kibendera cha kona na kisha kuteleza kwa kutumia magoti yake na kuifunua jezi yake, fulana yake ya ndani iliyokuwa na maneno yale ikaonekana na kusomeka vizuri.Amanda akashtuka, akaikodolea macho televisheni ile na kuyasoma maneno yale, hakuamini, alikuwa akiyasoma mara kwa mara, alijiona kama alikuwa akiota na muda wowote ule angeamka kutoka katika usingizi wa kifo, Filbert alionekana kuanza kujirudi.*****Jina la Amanda ndilo ambalo lilikuwa likijirudia sana kichwani mwake, kila wakati alikuwa akimfikiria msichana huyo ambaye alitokea kumpenda kupita kawaida. Kila alipokuwa akikaa, jina la Amanda lilikuwa likimjia kichwani na hata alipokuwa akiendesha gari bado alikuwa akimfikiria Amanda. Msichana huyo alionekana kuwa wa muhimu katika maisha yake zaidi ya Saado ambaye alikuwa akipendana nae kwa sababu kulikuwa na kitu cha zaidi, umaarufu na pesa. Filbert alijua fika kwamba Amanda alikuwa akimpenda, hakumpenda kwa sababu alikuwa tajiri au maarufu bali alimpenda toka katika siku ya kwanza ambayo alikutana nae nchini Tanzania, ndani ya jiji la Dar es Salaam katika shule ya Kenton.Amanda alikuwa tofauti sana na Saado, msichana huyu wa Kisomali alionekana kuvutiwa na Filbert kwa sababu alikuwa maarufu na alikuwa na fedha nyingi, ila endapo asingekuwa na vitu hivyo, Filbert alijua fika kwamba Saado asingeweza kumpenda kama alivyokuwa akimpenda. Kwake, Amanda akaonekana kuwa kila kitu, alianza kuyarudisha mapenzi yake kwa Amanda ambaye alikuwa nchini Tanzania.Filbert hakuwa na nguvu ya kumpigia simu Amanda, alitamani kufanya hivyo lakini hakuiona kama ilikuwa njia sahihi. Kutokana na kuandikwa sana magazetini kuhusiana na mahusiano yake na Saado, alijua fika kwamba Amanda alikuwa akifahamu kila kitu kilichokuwa kikiendelea, hivyo alihitaji kumuomba msamaha na kisha kumtaka warudiane tena.Mahusiano yake na Saado hayakuwa imara kama yalivyokuwa katika kipindi cha nyuma nchini Ubelgiji. Mara baada ya kuingia nchini Uingereza Saado akaonekana kubadilika tofauti na alivyokuwa nchini Ubelgiji. Kutokana na uzuri wake ambao alikuwa nao alijiona kutamani kuwa na mtu ambaye alikuwa na fedha nyingi zaidi ya alizokuwa nazo Filbert.Kutokana na kutangazwa sana katika vyombo mbalimbali vya habari kwamba alikuwa msichana mzuri ambaye alikuwa akimilikiwa na mchezaji soka akaonekana kujisahau hasa pale ambapo alianzisha uhusiano na mmiliki wa timu ya Middlesbrough, Bwana Williams Adrian.Bwana Adrian alikuwa mzee maarufu ambaye alikuwa akimiliki kiasi kikubwa cha fedha. Yeye ndiye ambaye alikuwa ameinunua klabu hiyo ambayo ilikuwa na wachezaji wengi mashughuli ambao alikuwa akiwalipa mishahara mikubwa tofauti na klabu nyingine hapo Uingereza.Bwana Adrian alikuwa akimiliki majumba mengi ya kifahari, klabu za usiku, cassino na hata boti moja kubwa pamoja na ndege yake binafsi. Uchimbaji wa mafuta katika nchi za Uarabuni ndio ambao ulikuwa ukimuingizia fedha sana kiasi ambacho kila siku katika maisha yake alikuwa akitumia kiasi kikubwa cha fedha.Maisha mwake alikuwa akipenda fedha na alikuwa amezungukwa na fedha kila alipokuwa. Bwana Adrian alikuwa na kawaida ya kutembea na wanawake wazuri, wanawake ambao walionekana kuwa warembo sana. Mwaka huu alikuwa akitembea na mwanamitindo kutoka nchini Brazil na mwaka kesho alikuwa akitembea na mrembo wa Venezuela.Hayo ndio yalikuwa maisha yake, wanawake wengi wazuri alikuwa amekwishatembea nao na kila siku alitamani kuendelea kutembea na wanawake wazuri maishani mwake. Kitendo cha magazeti mengi nchini Uingereza kumsifia Saado tayari likaonekana kuwa kosa. Ni kweli Saado alikuwa na urembo mkubwa sana lakini sifa ambazo alikuwa akimwagiwa na magazeti mebgi ya Uingereza zikamfanya kuonekana mrembo zaidi na zaidi.Kama kawaida yake Bwana Adrian akaanza mishemishe zake, kila alipokuwa akijiangalia jinsi alivyokuwa na alipokuwa akimwangalia Saado, hakutegemea kumuona msichana huyo akimkatalia kuwa nae. Alichokifanya ni kuanza kuangaikia namba ya Saado, alipoipata, akaanza kuwasiliana nae.Waliongea mengi simuni na huku wakiahidiana kuonana katika siku ambayo ingekuwa maalumu kwa ajili yao tu. Ndani ya wiki moja tu, wakaonana katika boti ya Bwana Adrian na kisha kuanza kuongea mambo mengi. Utajiri wa Bwana Adrian ukaonekana kumlevya Saado, kila alipokuwa akiiangalia boti ile ilionekana kumshangaza kupita kawaida. Boti ilionekana kama nyumba ya kifahari, kulikuwa na bwawa la kuogelea pamoja na vitu vingine vingi.“Ninakuhitaji Saado” Bwana Adrian alimwambia Saado ambaye alikuwa akiumauma vidole tu.“Ila si unajua kwamba nina mpenzi”“Najua sana. Na nilifahamu hilo hata kabla sijakufuata” Bwana Adrian alimwambia Saado ambaye alionekana kutokuwa na ujanja siku hiyo.“Kwa sasa hivi siwezi kuwa na wanaume wawili”“Lakini hii itakuwa siri kati yangu na wewe”“Siri! Unadhani kuna siri hapa duniani? Kuna siku watu watafahamu tu” Saado alimwambia Bwana Adrian ambaye akaanza kumsogelea mahali pale alipokuwa amekaa.Tayari Bwana Adrian aliona kwamba asingeweza kumuua nyoka na wakati alikuwa amekaa mbali, alichokifanya ni kumsogelea Saado na kisha kuanza kumshika mkono. Saado alionyesha utulivu wa hali ya juu huku Bwana Adrian akiendelea kuongea maneno mengi ya kuchombezachombeza ambayo kwa kiasi fulani yalianza kumfanya Saado kuanza kumsahau Filbert.Hali ile iliendelea zaidi na zaidi, kila alipokuwa akiulizwa swali hili, alikuwa akiulizwa swali jingine kitu ambacho wakati mwingine ukampelekea kutokuwa na majibu yoyote yale. Kutoka mkononi, akashikwa mapaja na mikono kuzidi kusogea juu mpaka kifuani. Mguso wa mtu mwenye pesa ukaonekana kuwa tofauti na mtu mwingine, mguso ule ukamfanya Saado kuanza kutetemeka kwa hisia kali, akayafumba macho yake huku akihisi kama wadudu fulani walikuwa wakimtembelea, alipoyafungua, alikuwa mtupu.Hakukuwa na kilichoendelea mahali hapo, Bwana Adrian akafanya kile alichokuwa akikitaka, kwa mara ya kwanza Saado akamsaliti Filbert ambaye nae pia alionekana kuanza kubadilika. Huo ukawa mwanzo wa usaliti, Saado akawa akionana kisiri na Bwana Adrian huku Filbert akijua kwamba alikuwa peke yake.Katika kipindi ambacho Filbert alikuwa akikutana na Saado, kila mmoja alionekana kuwa na mabadiliko makubwa, mahusiano hayakuwa kama jinsi yalivyokuwa katika kipindi cha nyuma. Saado aliyaamishia mapenzi yake kwa mwanaume mwenye pesa, Bwana Adrian huku Filbert akiyaamishia mapenzi yake kwa msichana wake, Amanda.“Nitafanya kitu kwa ajili ya Amanda” Filebrt alijisemea.Siku hiyo akaamua kuondoka na kuelekea katika duka la nguo ambapo huko akanunua fulana nzuri nyeupe na kisha kurudi nayo nyumbani. Akaiweka juu ya kitanda na kisha kuanza kuiangalia. Kitu ambacho alikuwa akikitaka kilikuwa ni kuandika ujumbe mzito, ujumbe ambao aliuona kama ungemfurahisha Amanda na kujua kwamba ni kitu gani ambacho kilikuwa kikiendelea moyoni mwake kwa sasa.“Mbona umekuwa mwenye mawazo halafu unaiangalia sana fulana hiyo?” Denis alimuuliza Filbert.“Kuna kitu nataka kufanya” Filbert alimjibu Denis.“Kitu gani?”“Nataka nimuombe msamaha Amanda” Filbert alimwambia Denis.“Msamaha wa nini?”“Si unajua kwamba nilimsaliti”“Kwani haukuwa umemwambia kama basi?”“Hapana. Ilikuwa ghafla, sikutaka kuwasiliana nae” Filbert alimwambia Denis.“Kwa hiyo kuomba msamaha na hiyo fulana kuna uhusiano gani?” Denis alimuuliza Filbert.“Nitaiandika maneno ya kuomba msamaha na kisha kuivaa” Filbert alimwambia Denis.“Bado unanishangaza. Kwa hiyo utaivaa mitaani?”“Hapana” “Kumbe utaivaa wapi?”“Kwenye mechi ya jumamosi”“Mechi na Manchester United?”“Yeah!”“Sasa usipofunga goli?”“Nitafunga tu, nauamini uwezo wangu” Filbert alimwambia Denis.“Sasa Amanda ataionaje?”“Nadhani nae ataangalia mpira”“Sidhani”“Hata asipoangalia nadhani atasikia tu au kuona picha kwenye magazeti” Filbert alimwambia Denis.“Sawa. Kwa hiyo wewe na Saado mmeachana?”“Bado”“Sasa inakuwaje hapa?”“Wewe niachie mimi” Filbert alimwambia Denis.Hivyo ndivyo alivyokuwa ameamua, alitaka kumuomba msamaha Amanda kupitia fulana ambayo alikuwa akitarajia kuivaa kwa ndani siku ya jumamosi ambapo kungekuwa na mechi kali kati ya Newcastle na Manchester United iliyotarajiwa kuchezwa katika uwanja wa St’ James Park. Alichokifanya Filbert ni kuchukua maker pen yake yenye rangi nyekundu na kisha kuiandika jezi ile maneno yaliyosomeka “FORGIVE ME, I MISS YOU AMANDA (NISAMEHE, NIMEKUKUMBUKA AMANDA). Alipomaliza, akaanza kuiangalia na kisha kushusha pumzi ndefu.“Imependeza sana” Denis alimwambia Filbert.“Nashukuru kaka”Hiyo ilikuwa ni siku ya Alhamisi, Filbert alionekana kuwa na hamu ya kutaka kuuonyeshea ulimwengu kwamba alikuwa na msichana ambaye ni zaidi ya alivyokuwa Saado, hakujua watu wangeongea nini juu ya ujumbe ule lakini kitu ambacho alikuwa akikitaka ni kuuonyeshea ulimwengu kwamba kwa wakati huo alikuwa akimuomba msamaha Amanda.Siku ya mechi ikafikia na kisha Filbert kuichukua fulana ile na kuondoka nayo mpaka katika uwanja wa mazoezi na kisha kuingia katika basi la timu na kuelekea uwanjani. Kila mchezaji siku hiyo alionekana kuwa na mawazo mengi juu ya mechi ambayo ilikuwa mbele yao. Mechi hiyo ilionekana kuwa ngumu lakini kila mmoja alikuwa na kiu ya kutaka kushinda na hatimae kuwa miongoni mwa timu ambazo zimeifunga Manchester United msimu huo.Japokuwa wengi walikuwa wakiona kama wakielekea kufungwa lakini uwepo wa Filbert ukaonekana kuwaondoa wasiwasi. Walikuwa wakimuamini sana Filbert toka katika kipindi ambacho alikuwa akichezea Genk ya nchini Ubelgiji.Walipofika katika vyumba vya kubadilishia nguo, wakazikuta jezi zao ambazo zilikuwa zimewekwa tayari, akaichukua fulani yake kutoka ndani ya begi lake na kisha kuivaa, akaanza kumuonyeshea kila mchezaji.“Who is Amanda? (Amanda ni nani)” Mchezaji mmoja, Baines alimuuliza Filbert.“My Only Love (Mpenzi wangu wa pekee)” Filbert alijibu.“What about Saado? (Na vipi kuhusu Saado?)” Baines alimuuliza Filbert.“Just forget about her (Msahau tu)” Filbert alijibu.Mashabiki walikuwa wakisikika wakishangilia uwanjani, hiyo ilikuwa mechi ya pili kukutana na Manchester United na ndio mechi ambayo alitaka kuudhihirishia ulimwengu kwamba ukiachana na Saado, pia kulikuwa na msichana mwingine ambaye alionekana kuwa wa maana sana katika maisha yake na alikuwa hapo siku hiyo kwa ajili ya kumuomba msamaha.Katika kipindi ambacho wachezaji walikuwa wakiingia, Filbert alionekana kuchangamka sana, alikuwa akipiga makofi kila wakati huku akiwapungua mikono mashabiki wa timu yake ambao asilimia kubwa walikuwa wakilitaja jina lake kwa sauti kubwa.Mechi ilipoanza, wala haikuchukua muda mrefu, Filbert akafunga goli zuri, akakimbia mpaka sehemu ya kona ambayo ilikuwa na kamera nyingi, akateleza kwa magoti yake na kisha kuionyesha fulana yake mbele ya kamera ile na mbele ya mashabiki. Watu wakaripuka kwa furaha, kitendo kile kilionyesha kuwafurahisha sana watu. Goli hilo lilidumu mpaka mpira ulipokwisha.“Umeandika maneno ambayo yanaweza kuwa maswali sana kwa mashabiki wa soka duniani ambao wanaufahamu uhusiano wako na Saado. Hii ni ishara ya kuonyesha kwamba hampo pamoja kwa sasa?” Mwandishi wa habari wa Sky Sport alimuuliza Filbert mara baada ya mechi kumalizika.“Nadhani huu ndio mwisho wa kila kitu” Filbert alijibu kwa kujiamini.“Ulimwambia kabla?”“Nadhani mambo mengine ni ya kibinafsi zaidi, ila naomba ujue kwamba nilichokiandika ndicho nilichomaanisha kutoka moyoni” Filbert alimwambia mwandishi yule.“Sawa. Ila huyo Amanda ni nani?”“Ni msichana wangu”“Yupo wapi?”“Tanzania”Siku hiyo ndio ikaonekana kuwa mwisho wa kila kitu, Filbert na Saado wakaachana na kila mtu kuendelea na maisha yake. Wala haikuchukua muda mrefu, siri ikawekwa wazi na uhusiano kati ya Saado na Bwana Adrian kuwekwa wazi. Watu walishtuka, hapo ndipo walipoonekana kuhisi kwamba inawezekana hiyo ilikuwa moja ya sababu ya Filbert kuachana na Saado kwa sababu msichana huyo alionyesha kuwa na mahusiano na Bwana Adrian, mwanaume ambaye alikuwa na fedha nyingi.“Safi sana. Ujumbe umeonekana japo sina uhakika kama Amanda ameuona” Denis alimwambia Filbert.“Kama atakuwa ameuona, nadhani itakuwa poa sana. Kama hajauona basi itanipasa kuelekea Tanzania mwisho wa msimu” Filbert alimwambia Denis.“Hakuna tatizo”Siku zikaendelea kukatika, jina la Filbert lilikuwa kubwa kutokana na upachika mabao ambao alikuwa nao. Alifunga katika kila mechi ambayo alikuwa akiingia uwanjani. Timu kubwa zote Ulaya zikaanza kumendea, timu ya Real Madrid, Barcelona na timu nyingine zikafikisha dau mezani lakini timu ya Newcastle haikuweza kukubali kumuuza mchezaji huyo ambaye alionekana kuwa lulu.Uwezo wake haukumtangaza yeye tu bali uliitangaza mpaka nchi ya Tanzania. Kwa wale ambao hawakuwa wakiifahamu nchi hiyo wakaifahamu kupitia Filbert. Watu wakafahamu kwamba nchi iliyokuwa ikipatikana mlima wa Kilimanjaro ilikuwa ikiitwa Tanzania tofauti na wao walivyokuwa wakifikiria kwamba nchi hiyo ilikuwa ikiitwa Kilimanjaro.Mapenzi ya mashabiki wa Newcastle yalikuwa juu kwa Filbert. Walikuwa wakimpenda kuliko mchezaji yeyote yule. Kila siku walikuwa wakiwatambia wachezaji wa timu ya upinzani, Sunderland kwamba walikuwa wamepata mchezaji mzuri ambaye alikuwa na uwezo wa kubadilisha matokeo muda wowote ule. Pamoja na umaarufu huo, fedha nyingi alizokuwa nazo, bado Filbert alikuwa akimfikiria Amanda, hakutaka kuwa na msichana yeyote zaidi ya Amanda. Amanda hakuwa na cha kufanya zaidi ya kutokwa na machozi, kile alichokuwa amekiona katika televisheni yake hakuweza kukiamini. Ilikuwa imepita miaka mitatu bila kuwasiliana na mtu ambaye alimpa nafasi kubwa moyoni mwake, leo hii mtu huyo alikuwa ameandika ujumbe mzito katika fulana yake na kisha kuionyeshea dunia kwamba alikuwa amemkumbuka yeye na pia alikuwa akimuomba msamaha, bila shaka kwa kila kitu kilichotokea.Amanda akachukua mto na kisha kuufunika uso wake, machozi yalikuwa yakimtoka, hakufurahia kama alivyotakiwa kufurahia zaidi ya kushikwa na uchungu mkubwa, kitendo cha kuyasoma maneno yale kilionekana kumgusa kupita kawaida.Amanda hakutoka chumbani kwake, alibaki akilia tu kana kwamba alikuwa amefiwa. Mpaka katika kipindi ambacho wazazi wake walikuwa wamerudi kutoka kazini bado alikuwa amejifungia tu. Mama yake, Bi Vanessa akaonekana kushangaa, hiyo haikuwa kawaida kwa Amanda kuwa chumbani muda mrefu bila kuja sebuleni na kuanza kuongea nae kama kuwajulia hali. Kitu cha kwanza alichokifanya ni kuwauliza wafanyakazi kama Amanda alikuwepo chumbani kwake au alikuwa ametoka, alipoambiwa kwamba alikuwepo, akaanza kuondoka kuelekea chumbani humo. Akapiga hodi, hata kabla hajakaribishwa, akaufungua mlango na kuingia chumbani kwa Amanda.“Kuna nini Amanda?” Bi Vanessa alimuuliza Amanda ambaye alionekana kuwa kwenye hali isiyo ya kawaida, macho yake yalikuwa mekundu, hiyo ilionyesha kwamba katika kipindi kichache kilichopita alikuwa akilia.“Filbert mama” Amanda alimwambia mama yake.“Filbert! Amefanya nini tena binti yangu?” Bi Vanessa alimuuliza Amanda.“Ameniomba msamaha”“Amekuomba msamah?”“Ndio”“Alikupigia simu?”“Hapana”“Sasa amekuomba vipi msamaha?” BI Vanessa alimuuliza Amanda.Hapo ndipo Amanda alipoanza kuelezea kila kitu kilichokuwa kimetokea. Hakumficha kitu, alimwambia ukweli mpaka katika kipindi ambacho alikuwa akitazama mechi ambayo Filbert alifunga goli na kisha kuivuta kwa juu jezi yake na fulana ile iliyokuwa na maneno ya kumuomba msamaha na kumkumbuka yaliposomeka katika fulana ile.“Umeamua nini mpaka sasa?” Bi Vanessa alimuuliza binti yake, Amanda.“Sijajua niamue nini mama”“Wewe ndiye ambaye uliumizwa Amanda, ni lazima uwe na maamuzi yako mwenyewe, usimame kama mwanamke” Bi Vanessa alimwambia Amanda.“Nimsamehe kwa kila kitu”“Hakuna tatizo. Umeacha shule kwa ajili yake, litakuwa jambo lisilo na maana endapo utakuwa haumsamehi kwa kile alichokifanya. Kama amejirudi, hakuna tatizo” Bi Vanessa alimwambia Amanda.Huo ndio uamuzi ambao Amanda alikuwa ameuweka moyoni mwake, alijua fika kwamba Filbert alikuwa amemuumiza sana, aliishi kwa muda wa miaka mitatu pasipo kuwasiliana nae tena mbaya zaidi akiwa na msichana mwingine kabisa jambo ambalo lilimkasirisha na kuumiza sana moyoni, katika kipindi hicho hakutakiwa kukumbuka kitu chochote kile, alijiona kuwa na kila sababu za kumsamehe Filbert.Kitu ambcho alikuwa anakisubiria katika siku za karibuni ni kupokea simu kutoka kwa Filbert, aliombwa msamaha kupitia maandishi lakini aliona kulikuwa na umuhimu wa kuombwa msamaha kupitia sauti pia. Aliamini kwamba Filbert angekwenda kupiga simu kwa sababu alikuwa radhi kuionyeshea dunia kwamba alikuwa amekosea na hivyo alitakiwa kuomba radhi.Matarajio ya Amanda ndio yakaenda vile vile, siku iliyofuatia Filbert akampigia simu Amanda. Namba ilionekana kuwa ngeni tena ikiwa code za nchini Uingereza, Amanda hakutaka kujiuliza kwamba mpigaji alikuwa nani, alijua fika kwamba mpigaji huyo alikuwa ni Filbert. Moyoni mwake akajawa na furaha, hapo ndipo alipoamini kwamba Filbert alikuwa amemaanisha kile alichokuwa amekisema kwamba alikuwa akiomba msamaha kwa kila kilichokuwa kimetokea.“Halllow” Amanda aliita mara baada ya kuipokea simu ile.“Amanda…!” Filbert aliita.“Nakusikia Filbert”“Nilidhani labda sauti yangu utakuwa umeisahau” Filbert alimwambia Amanda.“Siwezi kuisahau. Nitaweza kusahau sauti za watu wote pamoja na za wazazi wangu lakini kamwe siwezi kuisahau sauti yako” Amanda alimwambia Filbert kwa sauti ya chini.“Naomba nikuulize swali” Filbert alimwambia Amanda.“Hakuna tatizo”“Uliitazama mechi ya jana?” Filbert alimuuliza Amanda.“Mechi gani?”“Manchester United na Newcastle”“Hapana” Alidanganya.“Daah! Ungeiangalia ungeona kitu fulani” Filbert alimwambia Amanda.“Kitu gani?”“Nadhani ungeangalia ningeanzia hapo. Ila usijali. Ninapenda sana kama tukianza upya mahusiano yetu ya kimapenzi, naomba unisamehe kwa kila nilichokifanya” Filbert alimwambia Amanda.“Nikusamehe?” Amanda alimuuliza Filbert.“Ndio Amanda”“Kwani umefanya nini mpaka kuomba msamaha?” Amanda alimuuliza Filbert.Kwanza Filbert akabaki kimya, sauti yake haikusikika japokuwa simu ilikuwa hewani. Alionekana kama mtu ambaye alikuwa akifikiria kitu fulani cha kuongea kwa Amanda ili aweze kueleweka zaidi. Swali alilouliza Amanda lilikuwa ni dogo lakini lilimaanisha kwamba Filbert kama Filbert ilimpasa aseme kwamba alikosea wapi na alihitaji msamaha kwa lipi.“Niliivunja ahadi niliyokuwekea” Filbert alimwambia Amanda.“Ahadi gani?”“Niliahidi kutokukuacha. Unakumbuka?” Filbert alimwambia Amanda na kisha kumuuliza swali.“Nakumbuka. Sasa kikatokea nini?” Amanda alijibu na kuuliza.“Nikakuacha kwa sababu ya tamaa ya macho yangu” Filbert alimwambia Amanda.“Hebu kuwa muwazi Filbert” Amanda alimwambia Filbert.Amanda alijifanya kama kutokufahamu kitu chochote ambacho kilikuwa kikiendelea katika maisha ya Filbert, hapo ndipo ambapo Filbert akaanza kuelezea kila kitu kilichokuwa kimetokea toka alipokuwa amekwenda nchini Ubelgiji. Kwa sababu katika kipindi hicho alikuwa akihitaji sana msamaha kutoka kwa Amanda, hakutaka kuficha kitu chochote kile, kile alichokuwa amekificha kilikuwa ni filamu ambazo alikuwa amejirekodi akiwa na Saado katika kipindi ambacho walikuwa wakifanya mapenzi.“Unajua kwamba uliuumiza moyo wangu Filbert?” amanda alimuuliza Filbert.“Najua Amanda na ndio maana nimeamua kukuomba msamaha” Filbert alimwambia Amanda.“Ok! Baada ya kukusamehe unadhani kipi kitafuata?”“Kunipa nafasi nyingine moyoni mwako, naahidi kutokuichezea” Filbert alimwambia Amanda.“Nitaamini vipi kama hautoweza kuichezea kama ulivyoichezea ya mara ya kwanza?” Amanda alimuuliza Filbert, kila swali ambalo lilikuwa likitoka mdomoni mwake lilikuwa gumu.“Sina cha kusema ila naomba uniamini Amanda”“Na vipi nikisema kwamba baada ya kuniacha kwa kipindi cha miaka mitatu nimempata mtu mwingine aliyeonyesha kunijali zaidi yako, mtu ambaye nimekuwa nae katika mahusiano kwa kipindi kirefu cha miaka mitatu zaidi yako?” Amanda alimuuliza Filbert ambaye akabaki kimya.“Umechelewa Filbert. Nadhani utaniumiza zaidi ya ulivyoniumiza” Amanda alimwambia Filbet.“Hapana. Siwezi Amanda. Nakuahidi” Filbert alimwambia Amanda.“Uliniahidi hivyo hivyo kipindi cha nyuma” Amanda alimwambia Filbert.“Nakuahidi. Sasa hivi ninakuahidi kiukweli Amanda” Filbert alimwambia Amanda.“Kwa hiyo zamani ulikuwa ukinitania na haukuniadisi kukweli?” Amanda alimuuliza Filbert.“Amanda pleaseeee, nakuhitaji moyoni mwangu” Filbert alimwambia Amanda kwani tayari alikwishaona kwamba kila swali alilokuwa akiulizwa lilikuwa gumu.“Nitaamini vipi kama hautoniumiza Filbert?”“Sijui nifanye nini ili uniamini. Labda niwe karibu na wewe zaidi” Filbert alimwambia Amanda.“Kumbuka zamani tulikuwa karibu. Ulikuwa ukinipigia simu kila siku na tulikuwa tukichati kila siku” Amanda alimwambia Filbert.“Nataka uje kuishi na mimi huku” Filbert alimwambia Amanda.“Unadhani hiyo itakufanya kutokuuvunja moyo wangu kwa mara nyingine tena?” Amanda alimuuliza Filbert.“Itasaidia kwa asilimia mia moja” Filbert alimwambia Amanda.****Filbert akaonekana kuwa na furaha, kitu ambacho alikuwa akikitaka tayari alikuwa amekwishafanikiwa kukipata. Alikuwa amemuomba msamaha Amanda na kutaka kurudiana nae mara baada ya kutengana nae kwa muda wa miaka mitatu. Hapo, hakujali kama watu wangemfikiria vipi kutokana na kumwacha mwanamke ambaye alikuwa akisifika sana kwa uzuri, Saado.Kwake alikuwa akimfikiria zaidi Amanda ambaye alionekana kuwa kama mwanamke wa ndoto katika maisha yake. Alimpenda Amanda na alikuwa akimhitaji kupita kawaida. Kila alipokuwa akikaa alikuwa akimfikiria msichana huyo kiasi ambacho akaona ilikuwa ni bora kama angemsafirisha na kumleta nchini Uingereza na kuishi pamoja nae.Hapo ndipo ambapo Filbert akaanza kufanya michakato yote kuhusiana na kumleta Amanda nchini Uingereza. Kwa sababu alikuwa na fedha wala halikuonekana kusumbua sana, ndani ya mwezi mmoja tu alikuwa amefanikisha kila kitu na hatimae Amanda kuelekea nchini Uingereza.Walipoonana kwa mara ya kwanza ndani ya uwanja wa ndege uliokuwa jijini London, uwanja wa kimataifa wa Heathrow, Filbert hakuonekana kuamini, alimwangalia Amanda mara mbili mbili huku akionekana kumshangaa sana. Amanda alionekana kuwa mrembo hasa, alikuwa mara mbili zaidi ya vile alivyokuwa amemuona kwa mara ya mwisho nchini Uingereza.Kwa mwendo wa haraka haraka akamfuata na kisha wote wawili kukumbatiana kwa furaha. Amanda akashindwa kujizuia, akaanza kutokwa na machozi mfululizo, hakuamini kwamba mara baada ya miaka mitatu ya kutengana, leo hii walikuwa wameonana kwa mara nyingine tena.“Vua kofia nikuone vizuri mpenzi” Amanda alimwambia Filbert.“Hapana. Utaniona tukifika. Nikivua kofia nitajulikana na watu kuanza kunizunguka zunguka” Filbert alimwambia Amanda.Akamchukua na kisha kuondoka nae kuelekea katika sehemu za kukata tiketi ya ndege. Hawakutaka kubaki hapo, kitu ambacho walitaka kukifanya ni kuondoka na kuelekea ndani ya jiji la Newcastle kwa ajili ya kuendelea na maisha kama kawaida. Ndani ya nusu saa, tayari walikuwa ndani ya ndege ya Fly Emirates ambayo ilikuwa ikitoka London kuelekea Manchester kwa kupitia Newcastle. Ndani ya ndege kila mmoja alionekana kuwa na furaha, walikuwa wamekumbukana sana kitu ambacho mara baada ya kufika nyumbani tu, wakaelekea bafuni kuoga na walipotoka kuanza kufanya kile ambacho mara nyingi wapenzi hufanya wanapokuwa peke yao chumbani. Ile ikawa mara ya kwanza kwa Amanda kufanya mapenzi, akaitoa bikira yake kwa mwanaume ambaye aliamini kwamba angekuja kuwa mume wake wa ndao.“Nitakuoa haraka iwezekanavyo” Filbert alimwambia Amanda huku akiwa kifuani kwake.“Mbona haraka sana?”“Ninataka kuendelea kuishi nawe kwa karibu zaidi” Filbert alimwambia Amanda.“Sawa. Na vipi kuhusu masomo yako?”“Nimebakisha miezi miwili. Baada ya hapo nitakuwa nimemaliza na kuanza kuchukua digrii ya kwanza” Filbert alimwambia Amanda.“Nakupenda Filbert”“Nakupenda Amanda” Filbert alimwambia Amanda na kisha kuendelea na mchezo wao.Hicho ndicho kitu ambacho wote wawili walikuwa wakikitaka. Walitaka kuonana na kuwa karibu kama zamani, walijua fika kwamba ukaribu wao ndio ambao ungewafanya kupendana zaidi na zaidi. Filbert hakutaka kumfikiria Saado, aliamua kusahau kila kitu kuhusiana na Saado. Zile picha za ngono ambazo zilikuwa kwenye email yake akawa amekwishazifuta, hakujua kama katika email ya Saado zile video ziliendelea kubaki. Filbert alikuwa kama kipofu, alisahau kwamba yeye ndiye ambaye alimuingiza Saado kwenye mahusiano ya kimapenzi, akasahau kama yeye ndiye alikuwa mwanaume wa kwanza kuzitoa damu za Saado kitandani, endapo angekumbuka mambo hayo, nadhani ilikuwa ni bora Amanda kubaki nchini Tanzania kuliko kutaka kuwa karibu nae kwa kuelekea nchini Uingereza.Je nini kitaendelea?Je ni majanga gani yatakayotokea hapo mbele?Je ni kweli Filbert ataweza kuoana na Amanda? ITAENDELEA
KUNGELE iliita mara ya pili, kwa muda ule na mazingiza ya nyumbani kwangu yalivyo nilijikuta nashtuka kupata mgeni pasipo kuwa na taarifa, nikainuka na kutoka kwa haraka kupitia mlango wa siri ulionifanya nimuone kwa ufasaha mgeni anayegonga bila ya yeye kuniona kisha nikarudi ndani kwa ajili ya kuufungua mlango unaogongwa.
Wakati nilipokuwa namchungulia Yule mgeni, sikuweza kumtambua kuwa ni nani, nilimuona tu kuwa ni mwanamke tena yuko peke yake. Swali lililokuwa limebaki kichwani ni kumjua ni nani na anataka nini. Nikaufungua mlango na kukutana mtu nisiyemtarajia.
Nilibaki nimeduwaa kwa maana ugeni ule nilikuwa siuelewi elewi, nilijiuliza maswali mengi yasiyo na majibu kutokana na namna nnavyofahamiana na kwa jinsi tulivyopoteana na mgeni yule. Nilijiuliza ‘Kutembelewa na Mwajuma! Mwajuma kipaplipapli? Tena nyumbani kwangu?’
Kwa kweli sikumkaribisha kwanza ndani. Sio kwamba niliamua kufanya hivyo bali ni kitendo kilichotokea bila kukifikiria kabla hajanishtua kwa maneno yake. “Hunikaribishi ndani Musa?”
Kwa kweli nilijikuta natetemeka. Sikutetemeka kwa sababu ya kuniuliza hilo swali, bali kwa kuniita jina ambalo kwa muda wote niliokuwa nikifahamiana na Mwajuma, hakuwa akilifahamu jina langu halisi. Nilijikaza kiume na kumkaribisha sehemu ya maongezi yenye viti vyenye vikalio vya kufumwa na ukili. Kwa mara ya kwanza baada ya miaka kadhaa nikakaa karibu na Mwajuma.
Labda kwanza nijitambulishe, naitwa Musa Njiwa, mpelelezi wa kimataifa mwenye rekodi ya mafanikio ya asilimia mia moja kwenye kazi yangu hiyo na kunifanya niwe mmojawapo ya wapelelezi bora hapa nchini pamoja na kuwa na miaka michache katika taasisi ya Usalama wa Taifa nimekuwa nikiaminiwa na kupewa kazi kubwa zenye maslahi kwa taifa.
Japo ninakiri kuwa na kaudhaifu mbele ya kinadada warembo, mimi ni mume wa msichana aitwaye Tausi binti Nurdin ambaye kwangu ni malkia wa warembo aliyeweza kuuteka moyo wangu kiasi cha kuuendesha anavyotaka.
“Niambie Mwajuma” nilipata ujasiri wa kuanza kumuongelesha mgeni wangu.
Mwajuma akatabasamu akiniangalia, kitendo hiki kilinikumbusha mbali sana lakini nilijikaza nikabaki kumwangalia usoni. Mwajuma ana macho ya paka na uso wake umepambwa na pua ya wastani na midomo yenye ‘lips‘ nene. Sio rahisi kuugundua uzuri wake kwa haraka, cha kwanza utakachogundua ni tabia zake za kike ambazo muda zote zinakukumbusha kuwa uko na mtoto wa kike anayehitaji uonyeshe uanamume wako.
Rangi yake asili ya kahawia ilikuwa inaifanya ngozi yake yenye afya ing’ae halafu kwa ujinga wake kavaa vile ambavyo alikuwa ananiacha hoi. Mi nilikuwa napenda sana akivaa kihasara hasara, kwa wasiofumba fumba maneno huwa wanasema kuvaa kimalaya.
Siku hiyo kabla ya kuja Mwajuma ilikuwa ni asubuhi tulivu, nyumba yangu ikionekana kujawa na upweke wa hali ya juu. Mawazoni nilikuwa sehemu tofauti na chumbani nilipokuwepo japo nilikuwa sipajui mahali nilipopelekwa na mawazo hayo. Ndipo ghafla nikashtushwa na kengele ya mlangoni iliyoashiria kuwa kuna mgeni.
Niliuhisi moyo ukinienda mbio mithili ya gari lililofeli breki. Moja kwa moja akili yangu ilirudi kwenye ugeni nilioupata siku nne kabla ya siku hiyo ambapo nilitembelewa na Mkuu wa usalama wa Taifa, tena bila taarifa yeyote. Kwa cheo chake, mtu huyu anaweza kuonana ama kuwasiliana na mheshimiwa Rais wakati wowote, ni mtu ambaye usalama wote wa nchi hii uko chini ya uongozi wake. Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza maishani kutembelea kwangu, na itakuwa ni mara yake ya mwisho bila shaka yeyote.
Mkuu alinitembelea ghafla akiletwa na usafiri maarufu kama bodaboda. Alikuwa amevaa suruari ya michezo, fulana nyepesi na raba kama aliyekuwa ametoka kwenye mazoezi ya kukimbia. Ni jambo la kustaajabisha sana lakini nilielewa kuwa hakuwa akitaka kujulikana kama anaenda mbali na nyumbani kwake japo kwa jioni ile sikujua ni kwa sababu gani aliamua vile. Siku hiyo Mkuu alionekana kama ana mzigo mzito sana wa mawazo. Baada ya kubabaika kwa muda, nilimkaribisha ndani lakini hakuchukua muda mrefu kukaa ndani, alitaka tutoke. Aliniambia tunyooshe miguu ufukweni kwa kuwa nyumba yangu haikuwa mbali na bahari ya Hindi.
Wakati tukinyoosha miguu ufukweni, mkuu alinieleza kuhusu hali ya nchi ilivyo. Sikutaka kuamini kuwa alifunga safari toka kwake Oysterbay kuja Boko ninapoishi kwa ajili ya kuniambia habari hizo ila kilichonitatiza zaidi sikujua ni kwa nini alikuwa ananieleza hayo, ila nilidhani kuwa alikuwa akijaribu kupunguza mzigo wa mawazo kichwani.
Uzito wa maneno yake nilikuja kuutambua siku moja baada ya yeye kunitembelea nyumbani kwangu, siku ambayo nilipata taarifa kuwa Mkuu amefariki kukotana na moyo wake kusimama ghafla. Kwa mtindo wa maisha aliyokuwa akiishi mkuu, hata wewe ungeambiwa taarifa hizo ungeishia kucheka kwa kutoamini lakini ndivyo ilivyoamuliwa itangazwe.
Kifo cha Mkuu kiliniuma sana na kujihisi mwenye deni kubwa la kumuenzi na kufanyia kazi maneno yake. Nilikuwa nimefiwa na mlezi wangu katika kazi, mtu ambaye nilimtegemea kwa kila kitu katika kazi yangu. Alikuwa akinichukulia kama mwanaye.
Kwa mara ya kwanza toka nipokee taarifa ya kifo cha mkuu, nilijikuta mawazo yangu yanahamia kwingine japo kwa muda mfupi kutokana na ujio huu wa Mwajuma.
‘Ina maana nilikuwa nampenda Mwajuma kiasi hiki au basi tu uchu umenizidi?’ Nikajikuta nikijiuliza bila jibu.
Katika maisha yangu yote, Mwajuma ndiye msichana pekee aliyeweza kunidanganya na nikaamini kuwa yeye ni mgeni katika ulimwengu wa mapenzi aliyetendwa katika uhusiano wa kwanza na kumfanya asipende kuwa katika mahusiano. Sababu hiyo ilinifanya nizame kwenye penzi lake.
“Eeh baba kikombe hiki kiniepuke, ila ikibidi kukinywa ntakinywa” nilijikuta nikisali ile sala yangu kimoyo moyo nikiwa namwangalia Mwajuma huku udenda ukitaka kunidondoka.
“Mwajuma! Mwenzio nimeoa sasa hivi” nilijikuta nikilalamika kibwege kwa maneno yasiyojulikana yalipotokea.
“Najua umeshangaa mimi kukujua hapa, na zaidi kulijua jina lako halisi. Ukipenda nitakueleza ila kilichonileta ni matatizo, baba yangu amekamatwa huu ni mwaka wa tatu akihusishwa na tukio la ujambazi” alianza kunieleza akipuuza malalamiko yangu ya ‘kiboya’ yasiyo na kichwa wala miguu kuwa nimeoa.
Nilimkazia macho alipotamka neno ‘baba yangu’, akajua namaanisha nini.
“Ni baba yangu kweli Nasibu, ule ulikuwa ni utoto. Mbona we ulinidanganya kuwa unaitwa Nasibu hadi leo likanikaa mdomoni?” alijitetea Mwajuma.
Mwajuma alishawahi kunipeleka kwa wazazi wake nikajitambulishe kumbe hawakuwa wazazi wake wa kweli, walikuwa watoto wa mjini kama yeye. Enzi hizo nilikuwa nimekolea mbaya kwa Mwajuma. “Unadhani kwa kunifuata mimi utapata msaada gani?” nilimuuliza kwa utulivu nikiiga mtindo wake wa kupuuzia baadhi ya hoja. “We unajuana na watu, pia una upeo mkubwa katika masuala ya sheria. Au na hilo ulikuwa unanidanganya?” alisema akiniangalia usoni.
“Yote ni kweli Mwajuma, unaweza kunieleza kwa ufupi kuhusu kesi yenyewe?”
Mwajuma alinielezea anavyojua yeye. Baada ya maongezi nilimuuliza amepajuaje pale ninapoishi , amefikaje na amejuaje jina langu.
“Usingeniuliza ningedondoka hapa hapa kwa mshangao”
“Na mimi ningekudondokea juu” niliropoka halafu nikaanza kujilaumu kwa kuonyesha uroho usio na tija.
Mwajuma alinielezea alivyoyajua mambo yangu japo sikuridhika na maelezo yake, niliamua kuufuata msemo wa ‘funika kombe mwanaharamu apite’. Alidai kuna siku aliniona maeneo ya Posta mpya nikiwa nasalimiana na mtu, mimi kwenye gari na huyo mtu alikuwa akitembea. Eti akashuka kumuuliza huyo mtu habari zangu akamweleza. Yaani kwa kifupi hadithi yake haikuwa na mashiko. Nikaamua kuwa na tahadhari kubwa kwa kila hatua ya utekelezaji jambo lililomleta pale. Japo nilikuwa na uwezo wa kumkatalia, niliona nijifanye mjinga ili nijue kitu halisi alichodhamiria. Ila kuna jambo moja lilikuwa linanikera katika maongezi yale, Mwajuma hakuonyesha dalili za kuwa bado ananipenda. Unajua hakuna jambo ambalo huwa linanipa mzuka kama msichana akiwa anaonyesha kunipuuzia, huwa najiuliza maswali mengi sana na kutaka kujaribu kuwa ni kweli hahitaji kulala kifuani kwangu au ‘anajishaua’ tu. Kujaribu huko ndiko ambako kulinipelekea kuwa katika mapenzi na wasichana wengi bila sababu za msingi. “Umekuja na usafiri gani, na una haraka kiasi gani?” nilimuuliza tukiwa tunaelekea ukingoni mwa kikao chetu kisicho rasmi. “Nilikuja na taxi”alinijibu kwa zile pozi zake zilizokuwa zinanipelekea kuwa nusu mwehu kwake. “Unaweza kunisubiri kidogo, nijiandae ili nikupeleke japo barabarani?” nilijikuta nikimuuliza kiuchokozi. “Mkeo akiridhia” Tulibaki tunaangaliana usoni, kisha nikajikuta nashusha macho yangu, nikashuhudia mapaja yaliyo wazi kwa sehemu kubwa kutokana na sketi yake fupi iliyochanua ambayo ameivaa. Wakati nainua macho kumtazama tena usoni, nikajikuta macho yangu yanakwamia kifuani kwenye matiti manene wastani yaliyo kwenye blauzi laini ambayo ukiwa na macho makali kama yangu, unaona ‘yaliyomo’. Mimi huwa ni mgonjwa sana wa matiti, sijui yana siri gani katika ubongo wangu. Huwa nikiyaona tu ubongo wangu unapigwa ganzi, mawasiliano kati ya akili na moyo yanakatika na kuuacha moyo uviamuru viungo vya mwili vishindwe kujikontroo na kuamua vitakavyo. Mwili ulinisisimka, nikainua macho kumtazama Mwajuma usoni. Tabasamu lilikuwa limefutika kwenye uso wa Mwajuma uso huo ukabaki na kivuli cha huruma kilichojaa ukarimu huku macho yake yakiwa yamelegea. Tukatazamana kwa muda, Mwajuma akashusha pumzi ndefu. Kwa muda ule mchache niligundua jambo moja kubwa, ‘sijapona ugonjwa wangu’. Mimi ni mdhaifu mbele ya kina dada warembo, lakini nilidhani kuwa baada ya kumuweka mikononi Tausi sitababaishwa tena warembo yaani nitakuwa mgumu kama ‘ukuta wa Berlin’ kumbe wapi ni kama ukuta wa udongo tu, nahitaji kufanya kazi ya ziada. Nikahisi mambo yanataka kuharibika, nikainuka kwa haraka na kuingia ndani. Kitu cha kwanza kukifanya baada ya kuingia ndani, ni kuinua simu na kumpigia mke wangu Tausi. Tukaongea mambo mengi kuhusu mapenzi yetu na yeye alitumia fursa hiyo kunipa habari kuhusu zoezi aliloenda kulifanya. Ni kama wiki moja ilikuwa imepita tangu Tausi asafiri kwa ajili ya kukamilisha program zake nchini Ufaransa ambazo alizianza wakati akiwa chini ya baba yake, Mzee Nurdin. Ilikuwa ni siku ambayo nilikutana na jambo ambalo lilinipa utata na shauku kubwa ya kutaka kulijua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam. Ndege moja ya abiria iliwasili, abiria wa kwanza kuteremka alikuwa kijana mmoja mtanashati ambaye alitembea haraka haraka na kukamilisha taratibu zote za kutoka kisha akaingia kwenye gari moja la kifahari lililoegeshwa nje ya uwanja. Kilichonitia mashaka ni kuwa baada ya kutoka tu yule kijana ndipo mbwa wa kugundua dawa za kulevya akaletwa na ukaguzi kuanza kama kawaida kwa abiria waliosalia. Nikanakili namba za lile gari bila kujali kama nitakuwa na kazi nazo ama lah kisha nikaendelea na shughuli yangu ya kumsindikiza Tausi. Baada ya kumaliza kilichonipeleka pale, yaani kumsindikiza Tausi nikapata shauku ya kufuatilia taarifa za kuhusu gari lile. Nilishtushwa zaidi na ukweli kuwa namba za lile gari hazikuwa zikiendana na gari lile, na mmliki wa gari halisi lenye namba zile ana ubini wa mmojawapo ya majina matatu ya kiongozi mmoja wa kisiasa. Nilipofuatilia zaidi nikapata taarifa kuwa mmiliki huyo aliwahi kuripoti kupotelewa na hilo gari lake lakini hakuwahi kufuatilia kama kuna taarifa yeyote iliyopatikana kuhusiana na gari lake alilodai limepotea. Cha kushangaza zaidi, baada ya kufuatilia nikalikuta ndani ya eneo lake la kuhifadhia magari likiwa limeegeshwa kwa mtindo wa kufichwa huku likiwa halina kibao cha namba. Kwa jinsi tukio lilivyoenda pale uwanja wa ndege na huu muendelezo wake nikajiridhisha kuwa mheshimiwa anahusika na ile ni biashara haramu. Nikabaki na swali moja tu, kwanini ajihusishe na mambo haramu wakati kwa nafasi yake anaweza kupata mahitaji yote muhimu? Huo ndiyo ukawa mtihani wangu mkubwa. Kwa siku mbili nilizofanya kazi ile nilijikuta nikipata maswali mengi zaidi kuliko majibu niliyoyategemea. Nilipata muunganiko wa ajabu sana uliotengeneza mtandao fulani ambao binafsi nilivutiwa kuujua mfungamano wao au kwa lugha nyepesi, japo linalowaunganisha hadi watengeneze mtandao huo. Ndipo nilipotatizwa na suala la Mkuu. Mwajuma alikuwa nje ananisubiri wakati naongea na Tausi. Nilipomaliza kuongea na mpenzi wangu nikajiandaa na kutoka nikiwa mpya kabisa kumsindikiza Mwajuma kwa gari yangu kisha tukakubaliana kuwa tuonane kesho yake ambayo itakuwa ndiyo siku ya kesi ya baba yake kuendelea mahakamani. Nilipotoka chumbani nilikuwa mpya kabisa tofauti na yule aliyekuwa akimtamani Mwajuma. Nadhani hata Mwajuma alishangaa kwa namna nilivyotoka na swaga tofauti na nilivyoingia chumbani. ******
Ngoja nikujuze kidogo kuhusu kisa cha Mwajuma ‘kipaplipapli’….. Miaka kadhaa iliyopita nilipewa kazi maalum kuipeleleza taasisi fulani ya fedha kama inatekeleza sera yao ya kuwawezesha kina mama wa kipato cha chini, sera ambayo iliifanya serikali kuipa ruzuku kubwa. Ili kuifanikisha kazi hiyo ilinibidi nikapange chumba eneo ya uswahilini ambalo ni mojawapo ya maeneo yaliyotajwa katika mipango yao ya utekelezaji. Huko ndiko nilikutana na Mwajuma. Hiyo ilikuwa ni kazi yangu ya kwanza toka nihitimu mafunzo ya upelelezi na ndiyo ilinifanya niamininike zaidi na kupewa majukumu makubwa ya ndani na nje ya nchi. Nilipokuwa maeneo yale nilikuwa nina kawaida ya kula kwa dada Salome, huyu ni mama lishe wa jirani ya pale nilipokuwa nakaa. Alikuwa akipika chakula kizuri sana na kwa usafi mkubwa hivyo wengi tulikuwa tunapenda kwenda kula pale. Na mara nyingi baada ya kula nilipenda kukaa na kupiga stori mbili tatu na dada Salome ambazo zilinisaidia katika kazi yangu. Siku moja wakati nakula, akaja Mwajuma ambaye alionekana amekwazwa na jambo fulani kubwa sana. Akaongea kwa muda na dada Salome kisha akataka kuondoka kabla dada Salome hajamwambia kwa sauti kubwa kuwa amsubiri amalize kazi waondoke wote. Sikuonekana kumtilia maanani sana Mwajuma, lakini alianza kugusa hisia zangu alipomsaidia dada Salome kazi ya kuninawisha mikono. Mtoto alipiga goti kwa heshima, nikakumbuka mabinti wa kisukuma nilivyoenda Sengerema kumtembelea rafiki yangu mmoja. Si kawaida ya mabinti wa uswahilini kuwa na heshima ya vile, nikawa nanawa mikono huku namkagua kitendo kilichomshtua dada Salome kiasi cha kunitupia maneno ya utani. “Nasibu vipi, kisu kimegusa mfupa?” Nikajikuta natabasamu bila kujibu neno, ila cha ajabu Mwajuma hakuonyesha kama aliyajali yale maneno. Sikujua kama alielewa akajikausha au hakujua dada Salome anaongelea nini. Jina la Nasibu ndilo nililokuwa nikilitumia katika kazi yangu ile na wengi walijua kuwa nafanya kazi kwenye ofisi ya wakili mmoja katikati ya jiji kama karani.
Baada ya kunawa nikaendelea kuwepo pale kama kawaida yangu kupiga stori lakini siku hiyo dada Salome hakuonyesha kama anahitaji stori kutokana na ule ugeni wa Mwajuma, nikaamua kuaga. “Mbona husubiri nikutambulishe? Huyu anaitwa Mwajuma au tumezoea kumuita kipaplipapli” Mwajuma akamwangalia dada Salome kwa jicho la kumkataza. Dada Salome akamgeukia Mwajuma. “Huyu anaitwa Nasibu, anatusaidia saidia mambo ya kisheria. Anafanya kazi ofisi ya mawakili mjini.” “Nashukuru kukufahamu Mwajuma” nilijibu nikimpa mkono ambao Mwajuma aliupokea akibonyea kwa heshima huku akinitupia jicho la wizi. “Usije kummezea mate bwana ‘angu” sauti moja mbaya ilisikika ikitokea upande wa jikoni kisha akatokea dada mmoja aliyebarikiwa kuwa na sura mbaya na umbile ambalo sio rahisi kujua mbele wapi, au nyuma wapi endapo angevaa nguo kubwa ya moja kwa moja halafu akasimama gizani. Kitu kilichokuwa kikinikera pale kwa dada Salome, ni Zaituni, huyu dada alikuwa anajifanya kumsaidia dada Salome lakini nadhani alikuwa akitafuta mabwana kwa maana alikuwa akinisumbua kila siku akitaka kulazimisha mapenzi au watoto wa mjini wanasema ‘kujiweka’. “Namimi nafurahi kukufahamu shemeji” alijibu Mwajuma na kumfanya dada Salome alipuke kicheko na kunifanya nizidi kukereka. “Njoo basi unichumu Nasibu wangu” aliniambia Zaituni akinisogelea na kusababisha harufu ya viungo vya mchuzi vilivyochanganyikana na jasho kutawala kwenye pua yangu. “Sipendi!” nilijikuta nikisema kwa hasira kiasi cha kumshangaza Zaituni mwenyewe na dada Salome kwa sababu mara zote akinitania huwa naishia kucheka tu na kuondoka. “Mnh! Leo?” aliguna dada Salome kisha akaendelea “ Zaituni, usije kunifukuzia mteja wangu. Kama hapendi huo utani ni bora ukauacha” Wakati wote Mwajuma alikuwa kama anaangalia sinema. Mi nikajifanya kutaka kuondoka kwa hasira. “Basi nisamehe Nasibu, sikujua kama hupendi utani huu” alijisemesha Zaituni kwa aibu. “Usijali, ili mradi ushaelewa kuwa sipendi hamna tabu” nilijikakamua kuongea. Ni kweli kuwa nilikasirika lakini kwa wakati ule sikuwa najua kama nilikasirika kwa vile alikuwa akihatarisha uwezekano wa kumng’oa mtoto Mwajuma. Kimsingi hata mwenyewe nilijishangaa kuwa hasira zile zilikuwa zimetokea wapi usiku ule. Inaelekea dada Salome alishajua kinachoendelea kichwani mwangu japo hata mimi mwenyewe nilikuwa bado sijakijua kwa kuwa alikuwa akiniangalia kama mtu anayenisoma mawazo yangu. Baada ya siku mbili tatu za kutomwona Mwajuma nilijikuta nikivunja ukimya kwa dada Salome na kumuulizia. “Ingepita wiki bila kumuulizia ningetembea bila nguo toka hapa hadi nyumbani” dada Salome alianza kujibu kwa maneno yake ‘mbofu mbofu’. “Hata yeye alikuulizia kutaka kujua habari zako, basi acha nikupambe mdogo wangu, yaani ungesikia maneno niliyomwambia ungeninunulia soda. Mwajuma kipaplipapli yupo nikupe namba yake?” aliendelea dada Salome na kuuliza swali la kizushi. “Kwanini mnamuita kipaplipapli?” nilimuuliza kuzuga kabla sijaichukua namba yake ya simu. “Sasa ukimpigia si ndio utamuuliza mwenyewe?” alinijibu dada Salome huku akinisogezea simu yake kunipa namba ya simu. Kama alijua kuwa nisingeweza kutamka kuwa naitaka namba yake, niliipokea simu ya dada Salome nikijifanya kuinakili namba ya Mwajuma kwa shingo upande kumbe moyo wangu ulikuwa ukinidunda kwa shauku ya kuipata namba yake. Kwa jinsi Mwajuma anavyoonekana, ni kama anamstahili mwanamme anayejua kulea mpenzi wake, mwanamme anayeweza kudekeza. Yaani nilijihisi kama ni mimi peke yangu mwenye sifa zinazostahili kuwa karibu na Mwajuma kutokana na huruma yangu kwa watoto wa kike. Ukimwona tu jinsi alivyo utatamani umkumbatie akulalie mabegani akuelezee mahitaji yake ili umtimizie. Kama Mwajuma anakuja na tatizo nawe mfukoni una hela ya kodi ya nyumba tu, lazima utampa. Anavutia kutatuliwa matatizo yake yote ili aishi kwa raha duniani. Nikamkumbuka mzee mmoja aliyewahi kunihadithia safari yake ya Tanga enzi hizo. Aliniambia kuwa kutokana na wema aliotendewa na mtoto wa kitanga aliyekuwa mwenyeji wake, alijikuta kila alichowaza kumpa dada yule anakiona kidogo, mwishowe akaamua kumtoroka alfajiri tena kwa kulisukuma gari kwa umbali mrefu ili asije kumshtua usingizini. Baada ya kutoka kwa dada Salome, nikajiandaa kabisa kulala na kujilaza kitandani ndipo nikampigia simu Mwajuma. Ndugu yangu, Mwajuma kajaliwa sauti ya kike! Yaani kama ndiyo hivyo una siku nyingi, unaweza kujikuta unajichafua. Tuliongea mengi ya kawaida hadi tukahamia idhaa ya hadithi za mapenzi. Tuliongea mengi na kimsingi aliniaminisha kuwa hayuko katika uhusiano wa kimapenzi kutokana na kuumizwa na mpenzi wake wa kwanza. Nilijikuta nikimshangaa mwanamme mwenzangu aliyeshindwa kumtunza binti mwenye mvuto wa kipekee kama Mwajuma. Nikikumbuka nilivyosumbuka siku ya kwanza kufanya mapenzi na Mwajuma akijifanya hajazoea, huwa najikuta nikijicheka mwenyewe. Ila aliweza kujikontroo na kuonyesha kuwa anazoea pole pole hadi akawa fundi kabisa. Nikajiona bonge la shababi kumbe ye alikuwa ananiona boya tu. Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa uhusiano wangu na Mwajuma. Kwa kweli nilikamatika kiasi cha kutangaza kuwa nataka ndoa na Mwajuma. Hapo ndipo nilipopelekwa kwa Mzee mmoja wa mjini maarufu kama Anko Kidevu, Mwajuma akidai kuwa ndiye baba yake. Kutokana na mapenzi yetu kuyaendesha kwa siri, nilichelewa sana kupata stori kuhusu Mwajuma. Na mwenyewe alikuwa anajitahidi sana kuniganda ili nisipate muda wa kongea ongea na watu na kweli alifanikiwa. Lakini mchezo mzima ulikuja kuwekwa wazi na Zaituni baada ya kutibuana na Mwajuma. Siku hiyo sitaisahau maishani mwangu kwa maana Zaituni alikuja nyumba niliyopanga akiwa ameongozana na mashoga zake na matarumbeta kuja kusutana na Mwajuma, ndiyo hapo siri zote zikafichuka na Mwajuma akanitoroka kabla sijamuona tena alipokuja nyumbani. Kumbe hilo jina la kipaplipali alikuwa alipewa na wenzake kwa kuwa kila mwanamme anayemjaribu huwa hamuachi hadi Mwajuma mwenyewe aamue kuvunja uhusiano wakawa wanamtania kuwa ana utamu wa ‘Fanta kipaplipapli’
*******
Tatizo la macho huwa hayana mipaka halafu tabia haina dawa, wakati naingia na gari langu katika viwanja vya mahakama ya Hakimu mkazi wa Kisutu, macho yangu yalitua moja kwa moja kwa binti mmoja aliyekuwa kanipa mgongo. Ili kupata figa kama ya binti huyo akinadada wengi hujikuta wakihudhuria kwenye ‘gym’ karibu kila jioni. Kwa kusema ukweli starehe yangu kubwa huwa ni kuwaangalia mabinti warembo, nakumbuka toka wakati nasoma sekondari nilikuwa kila nikitoka shule jioni hukaa pale Posta mpya na kuanza kuangalia wasichana warembo wakienda na kurudi. Nafsi yangu ikishiba napanda daladala kurudi nyumbani. Basi nimejikuta hata sasa napenda kukodolea macho warembo kisha nawaacha waende zao bila kuwasemesha. Baada ya kuegesha tu gari nikaanza juhudi za kuiona sura yake ili nione kama kuna uwiano kati ya sura na umbile lile, niliona kuwa ni vyema niitendee haki nafsi yangu kabla ya kuingia ndani kusikiliza kesi niliyoifuata. Nikajifanya natoa simu kuongea na mtu huku nikielekea upande aliopo mlimbwende yule aliyekuwa akionekana anamsubiri mtu. ITAENDELEA
NILIPOINGIA ndani ya nyumba ile kitu cha kwanza kilichovuta macho yangu katika nyumba hiyo inayodaiwa ni ya Mzee Kibwana ni picha ya baba wa taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye ni rais wa kwanza wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Ni picha inayoonekana kuwa ni ya siku nyingi iliyopigwa wakati kiongozi huyo akiwa kijana. Pamoja na kuonekana ni ya zamani sana lakini imewekwa kwenye fremu nzuri na kuonekana kutunzwa vizuri.
Jambo la pili lililonitia mashaka ni mapokeo ya wale watu wawili wakati Mwajuma ananitambulisha kwao, ni kama kuna mambo ambayo wanadhani kuingia kwa mtu kutoka nje kutayafanya yajulikane. Nikabaki najiuliza, ni kweli kuwa mzee Kibwana anahusika na ujambazi? Na kama anahusika na kwa umri alio nao ina maana kaanza toka ujanani, je ana maisha yanayoendana na ujambazi? Na kama kaanzia uzeeni, ni jambo gani lilimsukuma?
Ukweli ni kuwa ilikuwa ni kesi ndogo sana kufuatiliwa na mtu wa nafasi yangu, ile ni kazi ya wapelelezi walioko chini ya jeshi la polisi. Nilikuwa nafanya unoko tu wa ‘kiboya’ ambayo hata mwenyewe siupendi lakini upande mwingine uzoefu unaonyesha kuwa huwa hakuna jambo dogo.
Hadi baada ya muda mfupi tukiingia maeneo ya Kinondoni Shamba iliyopo nyumba ya mzee Kibwana, tayari nilishahisi uwezekano kuwa tukio la kupeleleza mwenendo wa lile gari nililoliona uwanja wa ndege linahusiana na kesi ya yule mzee pamoja na ujio mpya wa Mwajuma. Kwa maelezo ya mzee Kibwana, mwenendo wa mwajuma nnaoufahamu, na muonekano wa watu wale tuliokuwa nao mahakamani nilihisi kuwa kuna igizo kubwa lilikuwa linaendelea na mimi nimeingizwa katikati bila kujijua.
Mzee yule alidai kuwa kazi yake ya udereva wa taxi inamuwezesha kuhudumia familia yake ya watu saba, lakini pale walikuwa Mwajuma na ‘mama yake’ tu.
Kwa kusema ukweli starehe yangu kubwa huwa ni kuwaangalia mabinti warembo, nakumbuka toka wakati nasoma sekondari nilikuwa kila nikitoka shule jioni hukaa pale Posta mpya na kuanza kuangalia wasichana warembo wakienda na kurudi. Nafsi yangu ikishiba napanda daladala kurudi nyumbani. Basi nimejikuta hata sasa napenda kukodolea macho warembo kisha nawaacha waende zao bila kuwasemesha.
Baada ya kuegesha tu gari nikaanza juhudi za kuiona sura yake ili nione kama kuna uwiano kati ya sura na umbile lile, niliona kuwa ni vyema niitendee haki nafsi yangu kabla ya kuingia ndani kusikiliza kesi niliyoifuata. Nikajifanya natoa simu kuongea na mtu huku nikielekea upande aliopo mlimbwende yule aliyekuwa akionekana anamsubiri mtu.
Nilipofika kama hatua nne hivi kabla ya kumfikia, mrembo akanirahisishia kazi kwa kugeuka. Nilijikuta nimeshikwa na bumbuwazi nikimkodolea macho kama nimefumaniwa, kumbe alikuwa Mwajuma! Mwajuma alikuwa akinisubiri ili tuingie wote ndani. Tukaingia kwa kuongozana kama mke na mume wanaoingia kanisani kufunga ndoa. Hatukuongea chochote zaidi ya kusalimiana na Mwajuma kunishukuru kwa kuitikia mwito wake wa kufika mahakamani kutoka msaada.
Kwa kweli kwangu kama mume wa mtu mwenye ndoa changa, haikuwa dalili nzuri kuvutiwa namna ile tena na mtu ambaye alishawahi kuwa mpenzi wangu huku bado kukiwa kuna uwezekano wa kumrudisha kwenye himaya yangu. Ila nilipiga moyo konde na kumkemea shetani.
Ilikuwa yapata saa tatu hivi wakati kesi inaanza kwa washitakiwa kupewa nafasi ya kutoa maelezo yao ya utetezi kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitatu ya kuwekwa ndani. Waliongea kwanza watu watatu kati ya saba waliokuwa wakituhumiwa kufanya tukio la ujambazi kwa kuvamia benki mojawapo iliyokuwa katikati ya jiji pamoja na kuua askari wawili ndipo ikafika zamu ya baba yake Mwajuma.
Kwa mujibu wa maelezo waliyotoa wale waliotangulia na ushahidi wao haraka haraka ilinijia picha kuwa kilichofanyika baada ya tukio la ujambazi kutokea ni kwa polisi kuwakamata watu wenye rekodi za uhalifu na kuwapa kesi hiyo ya ujambazi.
Kimsingi maelezo ya watuhumiwa wale yalinikera sana, ilionyesha dhahiri kuwa kuna kazi ya ziada kulinoa jeshi letu la polisi hasa kitengo cha wapelelezi wa kesi. Ilionekana kama kuna uvivu fulani katika ufuatiliaji wa matukio ili kupata wahusika sahihi.
“Mimi ni dereva wa taxi toka mwanzoni mwa miaka ya themanini na ndiyo kazi inayonipa mahitaji ya kila siku mimi na familia yangu ya watu saba. Siku ya tukio nilikuwa nimeegesha gari eneo la stesheni, nikafuatwa na jamaa wanne waliokuwa na mabegi makubwa wakitaka niwapeleke Kimara. Tukaanza safari, kufika maeneo ya Ubungo Kibo kukawa na pikipiki ya askari inayokuja nyuma yetu.” Alianza kujieleza mzee huyo anayejulikana kwa jina la Jamali Kibwana.
“Kila tulipokuwa tukienda wale askari walikuwa kama wanatufuata sisi. Kufika Kimara Korogwe, ghafla nikasikia mlio. Kuangalia kwenye kioo nikakuta wale askari wanadondoka na pikipiki yao kisha wale jamaa wakaniamuru nisimame. Wakanirushia noti nne za elfu kumi kumi na kushuka wakikimbia kuingia njia mojawapo” aliendelea kujieleza kwa ufasaha.
“Nikapiga simu polisi kutoa taarifa, ila polisi walipofika pale wakanichukua kwa ajili ya kusaidia upelelezi kabla hawajaniunganisha na hii kesi.” Alimaliza kujieleza mzee Kibwana huku umati wote unaosikiliza kesi ile ukimsikitikia mzee huyo aliyekuwa akitia huruma kutokana na umri wake, kazi yake na mashtaka yanayomkabili.
Watu wakaanza kunung’unikia jeshi la polisi kwa chini chini. Pamoja na kuwa kila mtu aliamini yule mzee angeachiwa, watu walikuwa wakisikitika kutokana na muda aliopotezewa kukaa mahabusu na mateso ambayo huenda yalikuwa yakiipata familia yake.
Ila mimi nilikuwa na mawazo tofauti kwa kuwa kuna maswali mengi nilikuwa najiuliza bila kupata majibu. Nikajikuta napata hamu ya kuchunguza tukio hilo ila tatizo lilikuwa moja, ntamshirikisha nani ambaye atanielewa na mkuu ndiyo hivyo keshatoweka duniani? Wale waliobaki waliendelea kutoa maelezo yao kisha kesi ikaahirishwa hadi siku iliyokuwa ikifuatia. Tukatoka nikiwa nimeongozana na Mwajuma ambapo nje alinitambulisha kwa ndugu zake kadhaa kama mtu niliyesoma naye shule ya msingi ila nina ujuzi kidogo na mambo ya kisheria kwa hiyo aliniomba niwasaidie. Najua watu wazima walidhani kuwa mimi ni mpenzi wake kutokana na utambulisho ule usio na mashiko.
Baadhi walionekana kuufurahia ujio wangu, lakini kuna mzee mmoja ambaye nilitambulishwa kama rafiki wa karibu wa Mzee Kibwana alionekana kuniangalia sana kama aliyetaka kunifahamu zaidi ya alivyoelekezwa au kama anayetakakujua nilichohisi, pia kuna tatizo nililiona kwa kijana mmoja ambaye wana undugu na familia ya Mzee Kibwana. Huyu alionekana dhahiri kuwa hakufurahia ujio wangu pale.
“Umeionaje kesi baba?” aliniuliza kwa shauku niliyetambulishwa kama mama yake Mwajuma, au ‘mzaa chema’.
“Hana kesi mzee, naamini ataachiwa tu. Wala msipoteze gharama ya kutafuta mwanasheria” nilijibu kuwaridhisha wote, waliopenda ujio wangu na wale wasiopenda. Ila pamoja na kujibu ili kuwaridhisha, niliamini kuwa ni kweli mzee Kibwana angetoka kutokana na hali niliyoiona na uzoefu wangu.
Hapo kidogo nikaona naenda sawa hadi na ‘wapinzani’, nikawa nimefanikiwa kuwaondoa mashaka kwa kiasi fulani. “Mimi toka mwanzo nawaambia, mzee hana kesi, atatoka tu. Mmeona hata mtaalam anasema?” alijinadi yule kijana anayejulikana kama Mateso.
Baada ya maongezi mawili matatu nikaamua kumpa lifti Mwajuma, mama yake na yule mzee ambaye baadaye nilikuja kujua kuwa anaitwa Boimanda. Nilikuwa nishafikia uamuzi kuwa nipoteze muda fulani kujiridhisha kuhusiana na mambo niliyokuwa nayoyahisi.
Nadhani utanishangaa kwa nini nilipatwa na wasiwasi huo. Kwa namna mzee Kibwana alivyohadithia ni kwamba baada ya tukio lile alipiga simu polisi. Nikuulize wewe katika hali kawaida, una namba za polisi hapo ulipo? Na hata kama hizo namba unazo, tukio kubwa kama lile likikutokea hatua yako ya kwanza itakuwa ni kutoa ripoti polisi? Akili iliyonijia ghafla ni kwamba mzee Kibwana anahusika kwa namna moja au nyingine.
Jambo la pili lililonitia mashaka ni mapokeo ya wale watu wawili wakati Mwajuma ananitambulisha kwao, ni kama kuna mambo ambayo wanadhani kuingia kwa mtu kutoka nje kutayafanya yajulikane. Nikabaki najiuliza, ni kweli kuwa mzee Kibwana anahusika na ujambazi? Na kama anahusika na kwa umri alio nao ina maana kaanza toka ujanani, je ana maisha yanayoendana na ujambazi? Na kama kaanzia uzeeni, ni jambo gani lilimsukuma? Ukweli ni kuwa ilikuwa ni kesi ndogo sana kufuatiliwa na mtu wa nafasi yangu, ile ni kazi ya wapelelezi walioko chini ya jeshi la polisi. Nilikuwa nafanya unoko tu wa ‘kiboya’ ambayo hata mwenyewe siupendi lakini upande mwingine uzoefu unaonyesha kuwa huwa hakuna jambo dogo. Hadi baada ya muda mfupi tukiingia maeneo ya Kinondoni Shamba iliyopo nyumba ya mzee Kibwana, tayari nilishahisi uwezekano kuwa tukio la kupeleleza mwenendo wa lile gari nililoliona uwanja wa ndege linahusiana na kesi ya yule mzee pamoja na ujio mpya wa Mwajuma. Kwa maelezo ya mzee Kibwana, mwenendo wa mwajuma nnaoufahamu, na muonekano wa watu wale tuliokuwa nao mahakamani nilihisi kuwa kuna igizo kubwa lilikuwa linaendelea na mimi nimeingizwa katikati bila kujijua. Mzee yule alidai kuwa kazi yake ya udereva wa taxi inamuwezesha kuhudumia familia yake ya watu saba, lakini pale walikuwa Mwajuma na ‘mama yake’ tu. Nilipoingia ndani ya nyumba ile kitu cha kwanza kilichovuta macho yangu katika nyumba hiyo inayodaiwa ni ya Mzee Kibwana ni picha ya baba wa taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye ni rais wa kwanza wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Ni picha inayoonekana kuwa ni ya siku nyingi iliyopigwa wakati kiongozi huyo akiwa kijana. Pamoja na kuonekana ni ya zamani sana lakini imewekwa kwenye fremu nzuri na kuonekana kutunzwa vizuri. Ukiiangalia sebule yake kwa juu juu huwezi kuiona thamani yake kwa kuwa fenicha zake zinaonekana ni za kizamani sana, lakini ukitafakari mbao zilizotengenezewa zile fenicha, na mapambo ya kiasili yaliyopamba sebule ile utapata mtazamo tofauti. Sikuonyesha kushtuka na hali niliyoikuta mule, wakati huo Mwajuma na mama yake walikuwa wameingia ndani, nadhani kubadilisha mavazi wakiniacha na soda. Kwanza nilijaribu kuishia nje lakini wakaniomba niingie ‘kuwapa Baraka zangu’ japo kwa kunywa maji ya kunywa, hapo nikapata nafasi niliyoihitaji. Kitu ambacho kilikuwa kikitembea akilini mwangu ni kuwa pale sio kwa Mzee Kibwana, na uwezekano wa familia ile kuwa ya Mzee Kibwana ni ndogo sana. Kila kitu kilionekana kuwa kimepangwa vyema, ila kwa wenye upeo na michezo ya ajabu ajabu kama mimi utagundua tu kuwa hakukuwa na uhalisia. Nikaingiza mkono mfukoni, nikaibonyeza namba moja kwa muda bila kuiachia. Simu ilikuwa imejipiga kwenye mojawapo ya namba za dharura na kwa muda ule nikawa na uhakika kuwa niko hewani, kwa maana mtu wa upande wa pili atakuwa anasikia kila ninachoongea. “Hapa ndiyo nyumbani Nas… ah Musa” aliniambia Mwajuma akitokea chumbani kwake huku akionyesha kubabaika jina. “Lolote utakaloliita ni sawa, Naitwa Musa Nasib Njiwa” nililazimisha kuliingiza jina la Nasibu kujaribu kuondoa aibu ya kuonekana mwongo mwongo huku nikimalizia soda. Mwajuma akaniangalia kama anayekagua kama ninachosema kina ukweli, nami nikabaki namwangalia kabla hatujakatizwa na Boimanda aliyeingia kama mtu anayeingia kumfumania mkewe. Mzee huyu anayeonekana kuwa amejaaliwa ukorofi, tulimuacha nyumba takribani kumi kutoka pale kwa mzee Kibwana. “Ndiyo kijana, karibu sana” alikuwa anaongea huku akikaa kwenye mojawapo ya viti vilivyomo pale sebuleni. “Hapa wanapaita Kinondoni Shamba eeh?” niliwapiga swali lakini kwa mtindo wa kutoa maelekezo kwa mtu ambaye atakuwa amepokea simu upande wa pili. “Ndiyo bwana mdogo, ukitaka kumuelekeza mtu unamwambia tu Kinondoni shamba nyumba namba 288 karibu na kiwanda cha wachina” alijibu Boimanda huku akinikazia macho. Damu ilinisisimka kwa vile mzee yule alikuwa ananipa ujumbe kuwa anajua ujanja ninaoufanya. “Sawa sawa, mi ngoja niwaage sasa hivi” niliongea huku nikiinuka. “Nimekufukuza?” aliongea Boimanda kwa kujishtukia. Tukaishia kuzuga kucheka tu bila kujibu lolote. Nikamuaga mama Mwajuma kisha nikatoka na kuondoka zangu nikisindikizwa na Mwajuma hadi kwenye gari langu. “Nakumbuka tulivyokuwa tukilala kitandani huku tumekumbatiana tukihadithiana mambo mbalimbali, Mwajuma uliniahidi mambo mengi sana yaliyonifanya nikukabidhi moyo wangu na kuamini kila uliloniambia lakini mwisho wa yote uliamua kuondoka bila hata kusema kwa heri” nilianza kumueleza Mwajuma nikiwa kwenye gari na yeye amesimama chini. “Jamani, hayaishi?” aliuliza Mwajuma kwa aibu “Nakwambia yote haya kwa sababu nahisi umejitokeza ili uniongezee maumivu katika maisha yangu, na safari hii nadhani utaniua kabisa. Najua fika mwisho utakuwa siyo mzuri ila nimeamua kukusikiliza ili damu yangu iwe juu ya binti ninayempenda” nilimwambia makusudi maneno yale ili yamchome moyoni “Musa nakupenda sana ila yanayotokea yanakuwa juu ya uwezo wangu” Mwajuma aliongea maneno ambayo sikuwa na shaka kuwa yalimtoka moyoni kisha akageuka na kurudi ndani. Nilielewa Mwajuma alimaanisha nini, ina maana kuna watu wako nyuma yake wanampangia mambo ya kufanya na wakati wa kuyafanya. Nilipata uhakika kuwa simfahamu Mwajuma kama nilivyodhani, mbali na Boimanda, ni kina nani na kwa nini wameweza kumkontroo? Na Mwajuma hasa ni nani? Mzee Kibwana alikuja kuachiwa huru kama ambavyo kila mmoja alitarajia lakini hadi wakati huo kuna hatua kadhaa nilizokuwa nimezifanya ambazo zilipelekea kuzidi kuingiwa na mashaka na tukio zima lililopelekea mzee Kibwana kuwekwa ndani. Tatizo linaonekana lipo kwa Boimanda. Siku ya tukio, gari la mzee Kibwana lilikodiwa na Boimanda kwa ajili ya shughuli zake kitu ambacho ni nadra sana kutokea. Walipofika maeneo ya stesheni, Boimanda alimuacha mzee Kibwana pale amsubiri ila akampa tahadhari kuwa akimsubiri kwa nusu saa bila kutokea anaweza kuondoka. Na baada ya tukio la majambazi kuwapiga risasi polisi, simu ya kwanza kupokelewa na mzee Kibwana ilikuwa ya Boimanda kuulizia kama bado anamsubiri stesheni wakati huo saa nzima ilikuwa imepita toka amuache pale na kumwambia aondoke baada ya nusu saa. Boimanda ndiye aliyemshauri mzee Kibwana apige simu polisi na kumuelekeza namba za kupiga. “Boimanda ni nani?” hili ndilo lilikuwa swali ambalo nilipaswa kulijibu kabla ya kuendelea na chochote kuhusiana na uchunguzi wangu. Tatizo lililokuwa mbele yangu ni ruhusa ya kujiingiza kikamilifu kwenye kazi hiyo. Angekuwepo mkuu ingekuwa rahisi sana kumweleza na kupata msaada wowote ambao ningeuhitaji, lakini nafasi yake ilikuwa inashikiliwa na kiumbe mmoja aitwaye Kazikanda Moluwi ambaye sifa yake kuu ni mgumu kuelewa hasa kitu ambacho hakiko kwenye orodha ya kazi anazotakiwa kuzifanya. Kazikanda Moluwi alijulikana zaidi kwa jina la KM, na kabla ya kushika nafasi ya mkuu alikuwa anatumika sana kwenye shughuli za kulazimisha mambo yafanyike kwa namna yeyote. Mtu huyu hutumia nguvu zaidi kuliko akili kwa kuwa akili yake ni ya ‘kushikiwa’.
NILISHTUKA sana ila sikutaka kumuonyesha Mwajuma kuwa nimejali zile habari alizoniambia huku akionekana kuingiwa na hofu. Nilimvuta na kumkumbatia kwa nguvu nikimpiga busu kwenye paji la uso huku nikimpapasa mgongoni kisha nikamuachia na kuacha nafasi kati yetu. “Boimanda ni nani?” nilimuuliza kwa upole. “Hata mimi simfahamu vizuri, ila ndiye mratibu mkuu wa harakati zote zinazofanywa na mtandao huo. Ila kitu ambacho naweza kukuthibitishia ni kuwa Boimanda ni mtu hatari sana. Maneno yako uliyonieleza siku ile yalinichoma sana, toka siku ile nikawa nayatafakari, leo nikaona nikuite kwa vile hakuna anayejua kwa nimekuja kwenye hii kitchen party” “Ah achana na hizo habari” nilimjibu nikimkaribia kiasi cha kuhisi pumzi zake akiwa anahema. Kitendo hicho kilimfanya Mwajuma ashtuke na kuniangalia kama ambaye haamini anachoshuhudia. Nikauzungusha mkono wangu kiunoni mwake na kumkumbatia nikipeleka mdomo wangu kumnong’oneza jambo, kitendo kilichomfanya asisimkwe na mwili. Tatizo lililokuwa mbele yangu ni ruhusa ya kujiingiza kikamilifu kwenye kazi hiyo. Angekuwepo mkuu ingekuwa rahisi sana kumweleza na kupata msaada wowote ambao ningeuhitaji, lakini nafasi yake ilikuwa inashikiliwa na kiumbe mmoja aitwaye Kazikanda Moluwi ambaye sifa yake kuu ni mgumu kuelewa hasa kitu ambacho hakiko kwenye orodha ya kazi anazotakiwa kuzifanya. Kazikanda Moluwi alijulikana zaidi kwa jina la KM, na kabla ya kushika nafasi ya mkuu alikuwa anatumika sana kwenye shughuli za kulazimisha mambo yafanyike kwa namna yeyote. Mtu huyu hutumia nguvu zaidi kuliko akili kwa kuwa akili yake ni ya ‘kushikiwa’. Wakati nikitafakari namna ya kuiingia kazi hiyo, muda wa Tausi kurudi nchini uliwadia. Nikaenda kumpokea uwanja wa ndege nikiwa na shauku na hamu ya mahaba ya mke wangu. Nilipoona tu mfumo wa ulinzi pale uwanja wa ndege nikajua kuna mchezo unaotaka kuchezwa. Kwa haraka nikawasiliana na mtu ninayemuamini katika kikosi cha ulinzi wa viwanja vya ndege na baada ya nusu saa maaskari wote waliokuwa zamu walibadilishwa kwa dharura. Hadi wakati ndege iliyomleta Tausi ikiwasili, tayari kulikuwa na askari wapya tofauti na waliokuwa zamu tena waliongozwa na huyo mtu niliyemwamini na kulikuwa na pilika za hapa na pale kwa baadhi ya wapokeaji katika uwanja huo wa ndege. Abiria wote waliteremka akiwemo Tausi ambaye nilimpokea kwa furaha na mapenzi makubwa, nikawa namzubaisha ili nihakikishe abiria wote wameteremka kwenye ile ndege. Baada ya abiria kuwa kama wameisha, aliteremka msichana mrembo sana ila mwili wake unaonekana fika kuwa umetengenezwa kimazoezi. Nikamwangalia yule askari niliyemuamini, naye akajua namaanisha nini. Mimi nikaondoka na mpenzi wangu huku nikipanga kichwani namna ya kuburudika naye usiku huo. Laiti kama angejua mawazo niliyokuwa nayo kichwani angeona kweli ameolewa na mume ‘mcharuko’ kwa maana nilikuwa najitengeneza kisaikolojia. Usiku huo ilikuwa kama ndiyo mara ya kwanza kumuona Tausi. Unajua uzuri wa kuoa mwanamke mrembo? Hata ikifikia wakati maisha yamewapelekea kuchokana, unajikuta ukimtamani tu kwa jinsi alivyo. Sasa hebu fikiria mke wangu ni mrembo halafu penzi ndiyo kwanza limenoga, unajihisi kama upotelee humo humo. Kwenye vyombo vya habari katika siku iliyofuatia ilitawala habari za yule dada kuwa amekamatwa na shehena kubwa ya dawa za kulevya, Tausi alistaajabu sana kwa kua walikuwa wamepanda ndege moja. Moyoni nilijisifu kwa kazi nzuri niliyoifanya. Baada ya siku tatu toka nilipompokea Tausi, nilipigiwa simu iliyonishtua sana. Ilikuwa yapata saa saba za usiku niliposhtushwa na mlio wa simu yangu ya kiganjani. Kuangalia ikawa inaonyesha jina la Mwajuma, nikageuka kumwangalia Tausi ambaye naye alikuwa ameshtushwa na mlio wa simu hiyo kisha nikarudi kuiangalia simu hiyo. “Pokea mpenzi” aliniambia Tausi akiwa kwenye hali ya usingizi “Haloo!” Mwanamme nikajikaza kuipokea simu huku nikihisi jasho linanivuja. “Nifuate haraka niko kwenye kitchen party Kijitonyama” aliniambia akimalizia kwa kutaja jina la ukumbi. “Unajua unaongea na nani?” nilijikakamua kuuliza lakini ukweli ni kwamba kijasho kilikuwa kikinitoka. “Najua, wewe ni Musa au Nasibu na naamini utakuwa umelala na mkeo. Kuna jambo la muhimu sana kwako” aliongea Mwajuma na kukata simu. Nikageuka kumwangalia Tausi nisijue la kumwambia ila yeye alijua cha kuniambia. “Naijua kazi yako mpenzi na nakuamini, nenda tu kama utaona kuna umuhimu wa kufanya hivyo” aliniambia Tausi kwa utulivu. Wakati najiandaa kwenda aliponielekeza Mwajuma, mambo mengi yalikuwayakipita kichwani mwangu nikijaribu kutabiri kitakachojiri huku nikijaribu kupanga na kupangua hatua za kufanya kukabiliana nacho. Sikuwa na mashaka na Mwajuma ila hao walioko nyuma yake ndio walikuwa wananipa mashaka. Baada ya muda mchache nilikuwa aliponielekeza Mwajuma na kweli nilimkuta pale, sikujua kama alifanya makusudi kunitega au ndivyo alivyotakiwa kuvaa kwenye ile kitchen party, alivaa kigauni kifupi cha khanga, viatu vya chini na nywele zake alizitengeneza kirahisi mno. Japo alionekana simpo lakini alikuwa amependeza sana. Nilipomfikia sikutaka kuonyesha kama niliutilia mashaka wito wake, nikamshika mkono na kumvutia kwenye kisehemu chenye giza giza karibu na maegesho ya magari katika ukumbi huo kasha nikauzungusha mkono wangu kwenye kiuno chake na kumvuia kwangu ikawa kama kajibinua. Nikawa namtazama usoni kama ninayeomba ridhaa ya kumpiga busu. “Mke wako ana moyo sana, mimi nisingeweza” alianza kuniambia akionyesha kawivu kwa mbali “Anajiamini” nilimtupia kijembe Mwajuma. “Niambie kweli Musa, we unafanya kazi gani?” nilisisimkwa kwa swali la Mwajuma, nikajua kuna habari nzito nyuma ya swali hilo. “Kazi yangu unaijua Mwajuma, kuna nini?” “Nimekudanganya mengi Musa,ukweli ni kuwa katika maisha yangu siamini katika mapenzi. Sijawahi kukupenda kabla, nilikuwa na wewe kwa kuwa ilibidi iwe hivyo japo nikiri kuwa uliweza kunifanya niyafurahie mapenzi kwa mara ya kwanza katika maisha yangu. Muda wote tuliopoteana nilikuwa nakukumbuka sana hasa nilipokuwa na hamu ya mwanamme” alianza kujieleza Mwajuma huku nikiwa bado nimemshika kiunoni. Nilibaki nikimtazama usoni Mwajuma nikitafakari maneno yake yaliyokuwa kama kisu kinachoukata moyo wangu. Sikuwahi kudhani kuwa kuna mwanamke ambaye angeweza kufanya yote aliyokuwa akiyafanya Mwajuma bila ya kuwa na chembe ya mapenzi moyoni mwake. “Ina maana urembo wote wa Mwajuma ni kama mashine tu isiyokuwa na moyo ndani yake” nilijikuta nikijisemea moyoni nikikumbuka vitabu mbalimbali nilivyowahi kuvisoma kuhusu mahusiano ya kimapenzi upande wa mwanamke. Hadi wakati huo, nilichokuwa nikikijua mimi ni kuwa penzi la mwanamke hujengeka taratibu na likishakolea limekolea kwani kulitoa huchukua muda mrefu zaidi. Nilijikuta nikiutoa mkono wangu kiunoni mwa Mwajuma na kumfanya atabasamu kwa huzuni kisha akashusha pumzi ndefu. “Mimi ni askari Musa, na najua kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa na wewe ni askari lakini wa kiwango cha juu kwa kuwa muda wote niliokuwa na wewe nilishindwa kujua chochote kuhusu kazi yako ya uaskari” Mwajuma alinieleza maneno mazito ambayo yalinifanya nijihisi kutetemeka. “Kwanini umeamua kuniambia maneno hayo yote?” nilijikakamua kumuuliza “Nahisi uko hatarini kutokana na mambo unayoyafanya kuuingilia mtandao, kuna mtandao wa baadhi ya viongozi walioko madarakani unaojilimbikizia mali kwa njia haramu na halali ili uweze kuwa na nguvu kwenye uchaguzi ujao na kuchukua kiti cha urais” Mwajuma aliongea akiushika mkono wangu na kuukumbatia. “Kuna baadhi ya viongozi wa jeshi la polisi wanatumiwa na wanasiasa hao kwa kuwa waliingia madarakani kwa nguvu za hao wanasiasa, ila wenzangu na miye tunapewa tu amri na kazi za kufanya. Kwa kweli mimi nimechoka, niko tayari kushirikiana na wewe ili tuokoe nchi yetu. Tunakoelekea ni kubaya sana” Mwajuma aliongea maneno mazito sana kiasi cha kunifanya nikaribie kupoteza ujasiri wangu. “Kwanini ulitumwa kunifuatilia na nani aliyekutuma?” nilimuuliza Mwajuma “Hayo siyo ya umuhimu kwa sasa, ila cha muhimu ni kwamba matukio mengi ya ujambazi yanakuwa yamepangwa na biashara nyingi haramu zinajulikana na zina mikono ya baadhi ya wakubwa na zina lengo la kukusanya nguvu kwa ajili ya uchaguzi mkuu hivyo wewe unaonekana kikwazo na usipoangalia utapotezwa” aliniambia Mwajuma akionekana mwenye uhakika na anachokisema. ITAENDELEA
Nilijikuta nikiutoa mkono wangu kiunoni mwa Mwajuma na kumfanya atabasamu kwa huzuni kisha akashusha pumzi ndefu. “Mimi ni askari Musa, na najua kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa na wewe ni askari lakini wa kiwango cha juu kwa kuwa muda wote niliokuwa na wewe nilishindwa kujua chochote kuhusu kazi yako ya uaskari” Mwajuma alinieleza maneno mazito ambayo yalinifanya nijihisi kutetemeka. “Kwanini umeamua kuniambia maneno hayo yote?” nilijikakamua kumuuliza “Nahisi uko hatarini kutokana na mambo unayoyafanya kuuingilia mtandao, kuna mtandao wa baadhi ya viongozi walioko madarakani unaojilimbikizia mali kwa njia haramu na halali ili uweze kuwa na nguvu kwenye uchaguzi ujao na kuchukua kiti cha urais” Mwajuma aliongea akiushika mkono wangu na kuukumbatia. “Kuna baadhi ya viongozi wa jeshi la polisi wanatumiwa na wanasiasa hao kwa kuwa waliingia madarakani kwa nguvu za hao wanasiasa, ila wenzangu na miye tunapewa tu amri na kazi za kufanya. Kwa kweli mimi nimechoka, niko tayari kushirikiana na wewe ili tuokoe nchi yetu. Tunakoelekea ni kubaya sana” Mwajuma aliongea maneno mazito sana kiasi cha kunifanya nikaribie kupoteza ujasiri wangu. “Kwanini ulitumwa kunifuatilia na nani aliyekutuma?” nilimuuliza Mwajuma “Hayo siyo ya umuhimu kwa sasa, ila cha muhimu ni kwamba matukio mengi ya ujambazi yanakuwa yamepangwa na biashara nyingi haramu zinajulikana na zina mikono ya baadhi ya wakubwa na zina lengo la kukusanya nguvu kwa ajili ya uchaguzi mkuu hivyo wewe unaonekana kikwazo na usipoangalia utapotezwa” aliniambia Mwajuma akionekana mwenye uhakika na anachokisema. Nilishtuka sana ila sikutaka kumuonyesha Mwajuma kuwa nimejali zile habari alizoniambia huku akionekana kuingiwa na hofu. Nilimvuta na kumkumbatia kwa nguvu nikimpiga busu kwenye paji la uso huku nikimpapasa mgongoni kisha nikamuachia na kuacha nafasi kati yetu. “Boimanda ni nani?” nilimuuliza kwa upole. “Hata mimi simfahamu vizuri, ila ndiye mratibu mkuu wa harakati zote zinazofanywa na mtandao huo. Ila kitu ambacho naweza kukuthibitishia ni kuwa Boimanda ni mtu hatari sana. Maneno yako uliyonieleza siku ile yalinichoma sana, toka siku ile nikawa nayatafakari, leo nikaona nikuite kwa vile hakuna anayejua kwa nimekuja kwenye hii kitchen party” “Ah achana na hizo habari” nilimjibu nikimkaribia kiasi cha kuhisi pumzi zake akiwa anahema. Kitendo hicho kilimfanya Mwajuma ashtuke na kuniangalia kama ambaye haamini anachoshuhudia. Nikauzungusha mkono wangu kiunoni mwake na kumkumbatia nikipeleka mdomo wangu kumnong’oneza jambo, kitendo kilichomfanya asisimkwe na mwili. “Umeniamsha hisia za mapenzi juu yako, najihisi kukupenda kama vile mwanzo japo umekiri tofauti” nilimnong’oneza maneno hayo nikawa nahisi mikono yake ikinipapasa mgongoni mwangu. Nikamwangalia usoni huku nikiwa bado nimemkumbatia, Mwajuma alikuwa anaonekana kuhitaji jambo ambalo nililijua wazi. Nikampelekea mdomo na kumpiga busu zito la mdomoni, akauacha wazi mdomo wake kuuruhusu ulimi wangu upenye. Tukanyonyana ndimi kwa muda kabla ya kukatishwa na taa za gari lililokuwa likitoka katika maegesho. “Bado busu lako ni tamu vile vile” nilimwambia Mwajuma na kusababisha atabasamu. “Hujaacha tu mambo yako?” aliniambia kwa aibu. “Twende nikupeleke nyumbani mpenzi” nilimwambia nikimvutia nilipoliacha gari. Tulipofika nyumbani kwa kina Mwajuma, aliteremka akawa anaelekea mlangoni na mimi nikateremka na kumuwahi. Nikamvuta tukaanza tena kubusiana huku tukipapasana kabla ya jambo lililonitia mashaka kutokea. Tulimulikwa tena na taa za gari, hili la sasa hivi lilikuwa linapita. Nikahisi kuwa kuna kitu hakiko sawa ila sikujua ni nini. “Ntakutafuta kesho kwa namna ntakayoijua mimi kisha tutaongea vizuri zaidi na kuona kuwa tutawezaje kufanya kazi pamoja” nilimwambia maneno ambayo kwa mwenye kutafakari angejua moja kwa moja kuwa nimekiri kuwa mimi ni askari. Baada ya kuagana na Mwajuma nikarudi kwa Tausi wangu nikiwa nimejipa jukumu la kumjua Boimanda kupitia Mwajuma. Nilifika nyumbani na kumkuta Tausi wangu yuko macho akiwa amejilaza kitandani kajikunyata, alionekana kuwa alipatwa na hofu sana kwa kitendo cha mimi kuitwa usiku ule. Moyo uliniuma sana nilipokumbuka namna nilivyombusu Mwajuma. Niliapa kuwa haitatokea tena nifanye jambo kama lile na hata kwa kumjua Boimanda ntatumia njia nyingine badala ya kumuweka karibu Mwajuma. Nilimkumbatia Tausi wangu, nikamuona akijiachia na kuanza kurudi katika hali yake ya kawaida. “Kuna kazi italazimika niifanye kwa haraka” nilianza kujiongelesha nitafute pozi la kumhadithia kilichojiri ambacho kwa uhakika ningemficha ufisadi nilioufanya. “Umefikiriaje wazo langu?” aliniuliza swali ambalo sikulitarajia kwa muda ule. Tausi aliniambia kuwa angefurahi kama ningeacha kazi na kujihusisha na biashara ili niepukane na maisha ya hatari ninayoishi kutokana na kazi ninayoifanya. Kimsingi nilimkubalia kuwa wazo lake ni zuri ila utekelezaji wake unahitaji umakini wa hali ya juu ili nisije kujiingiza katika hatari zaidi kwa kuwa mengi nimeyaona na kuyajua, siwezi kondoka kirahisi. “Nishaanza kulifanyia kazi wazo lako mpenzi” nilimjibu huku nikimkumbatia kwa nguvu zaidi na kummiminia mabusu kadhaa kabla hatujaishia katika usingizi ambao ulitupeleka hadi saa tatu asubuhi. Kitu cha kwanza baada ya kuamka tu niliwatuma watu wangu wakamcheki Mwajuma na kufuatilia mienendo yake yote kwa masaa 24 kisha wakijiridhisha kwa vitu maalum ambavyo niliwaagiza waviangalie, wamchukue na kumpeleka sehemu ambapo ningekutana naye kwa mahojiano zaidi juu ya habari alizonipa. “Nimekwisha” niliongea mwenyewe baada ya kuwaza ‘kitakavyonuka’ endapo Tausi akiziona. Nikawa nazichambua moja baada ya nyingine, kikadondoka kikaratasi. Nikakiokota haraka na kukisoma. ‘Ukionyesha ushirikiano, Tausi hataziona na polisi hazitafika. Njoo ufukweni na usiwasiliane na yeyote. Kumbuka hapo ulipo tunakuona!’ Jasho jembamba lilianza kunitoka. Sikuwa nahofia kuuawa kwa kuwa kama nia yao ingekuwa hiyo, badala ya kunipiga picha wangenipiga risasi. Halafu ukiona mtu anajitahidi kutafuta mambo ambayo yatakutisha ujue anakuogopa. Niliamini kuwa ni watu wanaonifahamu fika ila ukweli ni kwamba wamenishika pabaya. Baada ya masaa machache nilipokea habari ambayo ilinishtua sana. Mwajuma alikutwa ameuawa chumbani kwake na watu wasiojulikana na polisi walikuwa katika uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo. Akili yangu ilisimama kwa muda kufanya kazi, nilijikuta natokwa na machozi bila kujijua. Nikawahi kutoka nje na kukimbilia ufukweni ili Tausi asije kushtuka. Kwa mujibu wa taarifa zilizokuwepo, majirani zake wanadai alirudishwa usiku sana na gari, baada ya muda gari hilo likarudi tena. Zikasikika purukushani za hapa na pale kisha kukawa kimya, wao wakajua ni mambo ya mapenzi tu, asubuhi wakashtuka kukuta damu zikichuruzika toka chumbani kwake ndipo wakatoa taarifa polisi. Kwa kweli nina muda mrefu sana sikuwa nimelia lakini siku ile nilijikuta nikilia kama mtoto mdogo, nililia haswa pale ufukweni. Niliwaza mambo mengi sana kuhusiana na Mwajuma, nilitamani kama kungekuwa na mtu wa kumhadithia kuhusu nilichojihisi kutokana na kifo cha Mwajuma. Kutwa nzima nilijitahidi kumficha Tausi lakini mwisho ilibidi nimwambie kuwa yule dada aliyenipigia simu kunipataarifa muhimu amekutwa ameuawa muda mfupi baada ya kuongea naye. Sikuweza kumwelezea kiundani kuhusu uhusiano wangu na Mwajuma lakini alihisi kuwa msiba ule ulinigusa sana. Tukalala na majonzi, sikuthubutu kwenda msibani japo ndiyo ingekuwa fursa ya kuwajua wazazi halisi wa Mwajuma. Baada ya siku mbili, walisafirisha mwili wa Mwajuma kwenda Mwanza kwa ajili ya mazishi na kama zilivyo taratibu za kiislamu hakuna aliyeuona mwili wa Mwajuma kwa kuwa ni watu maalum waliuandaa. Kama ilivyo kawaida yangu huwa ninaanza mazoezi mapema sana na kumaliza wakati jua linaanza kutoa mwanga hivyo baada ya mapumziko ya siku tatu ya msiba niliamka kama kawaida na kutoka nje kwa ajili ya mazoezi. Nilishtuka kuona bahasha ya khaki imelala karibu kabisa na mlango wangu. Nikaanza kuangaza huku na kule bila kuona dalili zozote za mtu. Nikaiokota kwa tahadhari na kuifungua. Kilichomo kilinifanya nitake kuzimia, ni picha zangu nikibusiana na Mwajuma pale nje ya ukumbi na kule nyumbani kwao. Kumbe wasiwasi wangu nilipomulikwa na taa za gari mara mbili haukuwa wa bure.
“Nimekwisha” niliongea mwenyewe baada ya kuwaza ‘kitakavyonuka’ endapo Tausi akiziona. Nikawa nazichambua moja baada ya nyingine, kikadondoka kikaratasi. Nikakiokota haraka na kukisoma.
‘Ukionyesha ushirikiano, Tausi hataziona na polisi hazitafika. Njoo ufukweni na usiwasiliane na yeyote. Kumbuka hapo ulipo tunakuona!’
Jasho jembamba lilianza kunitoka. Sikuwa nahofia kuuawa kwa kuwa kama nia yao ingekuwa hiyo, badala ya kunipiga picha wangenipiga risasi. Halafu ukiona mtu anajitahidi kutafuta mambo ambayo yatakutisha ujue anakuogopa. Niliamini kuwa ni watu wanaonifahamu fika ila ukweli ni kwamba wamenishika pabaya.
Nikaanza kutembea pole pole kuelekea ufukweni nikiwa na mawazo mengi kichwani, ila nilikuwa sina wasiwasi kutokana na utaratibu wangu wa kiusalama niliojiwekea. Kutembea kwangu pole pole ilikuwa ni kuvuta muda zitimie dakika tano.
Wakati nakaribia ufukweni, nilimuona mtu mmoja aliyesimama ufukweni hapo akimulikwa na mwanga wa mbalamwezi. Nilikuwa na uhakika kwamba hakuwa peke yake pale ila aliyekuwa anaonekana ni yeye tu.
“Musa Njiwa! Naamini hatutapata tabu ya kushirikiana na wewe kwa kuwa hutakuwa tayari kumpoteza Tausi wakati huo huo kushitakiwa kwa kesi ya mauaji” aliongea bwege yule akionekana kujiamini sana.
“Hakuna haja ya kunielezea jambo ambalo nalijua na wewe unalijua, nenda moja kwa moja kwenye jambo uliloniitia. Mnataka nini toka kwangu?” nilimjibu kwa kujiamini kwa kuwa ilikuwa imebakia dakika moja tu zitimie dakika tano za wao kujidai katika eneo langu. Pia nilimkatiza kuendelea kutoa historia kwa kuwa saa niliyoivaa huwa inarusha mawimbi ya sauti yanayonaswa kwenye mashine ya kurekodia sauti iliyoko ndani yangu.
Kutokana na kazi ambazo nimezifanya niliwekewa aina fulani ya ulinzi ili nisidhurike. Huwa nikiamka kwa mazoezi kuna vitu fulani huwa navifanya kumjulisha Tausi kuwa kila kitu kiko sawa.
Asiposikia chochote kutoka kwangu kwa muda wa dakika tatu kuna namba alizotakiwa kubonyeza na ndani ya dakika mbili au tatu tayari kikosi kinakuwa kimewasili. Endapo angeona kimya kinaendelea, kuna mtandao wetu wa siri aliotakiwa kuujulisha baada ya dakika nyingine tano.
“Tuko kwa ajili ya maslahi ya taifa na wananchi wote wa Tanzania kwa jumla, na wewe tunakutambua kuwa ni kijana mwadilifu na mchapakazi. Ila mienendo yako kwa siku chache hizi inatupa mashaka” aliongea kwa majivuno.
Wakati huo nilikuwa nikijihisi kutetemeka na ujasiri wangu wote ulianza kuyeyuka. Sio kwa sababu ya maneno aliyoniambia bali muda ambao tayari ningekuwa nimeokolewa toka mikononi mwa ile mijamaa. Hali hiyo ilinifanya nijue kuwa wale watu hawakuwa wa kawaida, walikuwa na nguvu kubwa.
“Ongea moja kwa moja, mnataka nini?” pamoja na wasiwasi ulioanza kuniingia nilijikuta nikimuuliza kwa hasira. Kwa kawaida huwa nachukia sana kufanya maongezi na watu ambao wanazunguka zunguka katika kuongea.
“Safi! Tunataka utuambie ni kazi gani unayoifanya sasa hivi na ni nani aliyekutuma?” “Sifanyi kazi yeyote, kwa hiyo hakuna aliyenituma” nilimjibu kwa kifupi bila kujifikiria
“Nadhani hujui unaongea na watu wa aina gani katika nchi hii”aliongea kwa majivuno mjinga yule.
“Napata shida ya kujua uwezo wenu katika nchi hii kwa sababu kama mngekuwa na uwezo mnaodhani mnao, usingeniuliza kuwa nafanya kazi gani na nimetumwa na nani, mngekuwa mnajua kuwa sifanyi kazi yeyote kwa muda huu na msingesumbuka kunitafutia vitu vya kunishinikiza” niliendelea kumjibu jeuri ili nimtie hasira afunguke.
Jamaa lilikaa kimya kwa muda kisha likajikohoza kusafisha koo lake, nikajua nishamkamata kwenye eneo nnalomtaka.
“Sikia kijana, tunajua unachunguza mienendo kadhaa ambayo kimsingi haikuhusu na hakuna agizo lolote ulilopewa kiofisi kufanya kazi hiyo, unahatarisha usalama wa taifa bila kujijua. Tumekuita kukufahamisha kuwa tunajua unachofanya na tuna uwezo wa kukushughulikia” aliongea jamaa yule kwa sauti iliyojaa chuki.
“Kitu ambacho napenda kukuthibitishia ni kuwa, sina lolote ninalotafuta, ila kubwa zaidi ninalotaka kukuthibitishia ni kuwa hamna uwezo mnaodhani mnao. Kwanza mna mbinu za kizamani za kutaka kubambikia watu kesi wakati iku hizi kuna kila aina ya teknolojia inayoweza kubainisha ukweli na mnajua wazi nna uwezo wa kuzitumia” nilimjibu kwa jeuri vile kwa kuwa nilishaona ishara za kuwasili watu wa mtandao wangu.
Jamaa akawa anaangaza huku na kule akitweta kwa hasira kisha akatoa amri kwa kujiamini, “hebu mchukueni huyu tukashughulikie”.
“Kamshughulikie baba ‘ako mzazi aliyeko shamba” nilimjibu kwa dhihaka.
“Wenzako wote tayari wako mikononi mwa wananchi wenye hasira kali na hivi sasa wanaweza kuwa tayari washauawa, umebaki peke yako. Umeamini kuwa waliokutuma hawana nguvu wanayodhani wanayo?” Nilimwambia kwa kujiamini ila kimsingi nilikuwa natoa maagizo kwa mtandao wangu juu ya hukumu ya wale wenzake.
Nikaanza kumsogelea huku yeye akirudi nyuma kwa woga, nikawa nazidi kumfuata kwa kuwa nilishamuona mmoja wa watu wangu akiwa kasimama kwa nyuma yake. Nikatisha kama nataka kumfukuza, akageuka kutaka akimbie, akajikuta yuko uso kwa uso na Jerome Masola.
“Kaa chini mbwa we” aliamrisha Jerome.
Jamaa lilikaa chini utafikiri limepigwa virungu vya magoti. Nikamuagiza Jerome amchukue yule ‘boya’ pamoja na picha zangu na Mwajuma wakamhoji sehemu yetu maalum kwa kuwa nilijua kuwa muda si mrefu watu kutoka ofisini wangekuja. Jerome akamchukua kutaka kutokomea naye wenzetu walipojipanga wakiwa na wale wengine waliokamatwa kabla.
Baada ya takribani dakika arobaini tangu mtandao wangu usafishe hali iliyotokea ndipo walikuja watu waliotumwa na idara ya usalama Taifa wakiwa na silaha, eti kuitikiwa wito wa hatari. Kwa kweli bila ya kuwa na malengo maalum, ningewatukana matusi ya nguoni.
“Hatukuwa na tatizo lolote na hakuna aliyetoa taarifa yeyote, labda mmepokea taarifa toka kwa mtu mwingine” niliwaeleza huku nikijifanya niko katika hali ya usingizi.
Wakajizungusha zungusha pale wakishindwa kuendelea kuniuliza chochote. Nadhani walikuwa wameshapewa majibu ya kunipa wakawa wanatafuta namna ya kunipa ila sikuwapa nafasi ya kuniambia upuuzi wao.
Lakini pia kikubwa nilikuwa najaribu kuwapa ujumbe kuwa na mimi ni mtu wa aina gani. Chezea mimi wewe?
Tukio la kuvamiwa nyumbani kwangu niliendelea kulikalia kimya, sikulitolea taarifa yeyote ofisini wala sikuilamu ofisi kwa kutochukua hatua ndani ya muda uliotakiwa ila tukio hilo na maneno ya yule lofa vilinipa ujumbe kuwa siko salama tena na ofisi inashiriki kwa namna moja au nyingine kwenda kinyume na mimi.
“Mi nadhani mtuache tupumzike na nyinyi mkaendelee kutafuta huyo mwenye matatizo” niliwaambia kuwafukuza kimtindo huku nikiingia ndani ya nyumba yangu na kufunga milango nikiwaacha wamechanganyikiwa wasijue mpango wao unaendaje au umeishia wapi.
Kutokana na aina ya kazi tunazozifanya na hatari inayotukabili kulingana na uadui tuliyojijengea, kuna baadhi yetu tunaoaminiana tulianzisha mtandao mdogo wa kulindana nje na utaratibu wa kiofisi. Na ndiyo uliniokoa siku hiyo mikononi mwa wanaojiita wanalinda maslahi ya taifa.
Siku hiyo kwenye taarifa za habari za usiku huo zikatangazwa habari kuwa majambazi sita wameuawa na wananchi wenye hasira kali maeneo ya Mbagala Majimatitu usiku wa kuamkia siku hiyo na polisi wanaendelea na uchunguzi.
KWA kweli pamoja na kutoka pale nyumbani, sikuwa na mahali pa kuanzia kumtafuta Tausi kwa kuwa mpango ule wote ulipangwa na Omari japo hakuna aliyekuwa anajua kama Omari ndiye anaratibu zoezi lile kwa kuwa alimtumia askari mmoja asiye na cheo chochote ambaye ni mmojawapo wa vijana wake waaminifu. Hiyo ilisaidia kuficha nguvu ya mtandao wetu. Uamuzi wangu wa kwanza ulikuwa ni kumtafuta Omari. Ghafla nikapokea simu iliyonishusha presha, nilipokea taarifa kuwa Tausi yuko salama… Kumbe alipoingia barabara kubwa tu kutoka pale nyumbani, Tausi alikutana na gari mbili zilizomuweka katikati na kulazimisha kumuongoza kuelekea Bagamoyo badala ya uelekeo wa mjini kama ilivyopangwa. Kutokana na aina ya kazi tunazozifanya na hatari inayotukabili kulingana na uadui tuliyojijengea, kuna baadhi yetu tunaoaminiana tulianzisha mtandao mdogo wa kulindana nje na utaratibu wa kiofisi. Na ndiyo uliniokoa siku hiyo mikononi mwa wanaojiita wanalinda maslahi ya taifa. Siku hiyo kwenye taarifa za habari za usiku huo zikatangazwa habari kuwa majambazi sita wameuawa na wananchi wenye hasira kali maeneo ya Mbagala Majimatitu usiku wa kuamkia siku hiyo na polisi wanaendelea na uchunguzi. Tukio la kuvamiwa nyumbani kwangu niliendelea kulikalia kimya, sikulitolea taarifa yeyote ofisini wala sikuilamu ofisi kwa kutochukua hatua ndani ya muda uliotakiwa ila tukio hilo na maneno ya yule lofa vilinipa ujumbe kuwa siko salama tena na ofisi inashiriki kwa namna moja au nyingine kwenda kinyume na mimi. Lakini pia kikubwa nilikuwa najaribu kuwapa ujumbe kuwa na mimi ni mtu wa aina gani. Chezea mimi wewe? Ila maneno aliyoniambia Mkuu siku aliyonitembelea yalirudi kichwani, “Nchi haitawaliki kijana wangu, kila kiongozi mwadilifu katika taasisi za ulinzi na usalama anatamani muda wake wa kustaafu ufike ili aachie ngazi kwa kuwa tunalazimishwa na wanasiasa kufanya watakavyo hata kama ni kinyume na taratibu na kanuni na sheria za nchi” aliniambia mzee yule kwa utulivu huku tukitembea pembeni ya bahari. Siku ile mzee yule aliendelea kunielezea kuhusu nguvu za kifedha walizonazo baadhi ya watu ambao wanajipanga kugombea urais, pia alinigusia kuhusu nguvu za vyama vya upinzani katika kubadilisha mawazo ya wananchi wa kawaida kiasi cha kutokea vurugu za mara kwa mara. Kwa jinsi alivyokuwa akiongea, hakuonyesha kama anahitaji nitoe mchango wowote wa mawazo. “Siasa na uroho wa madaraka ni sumu kubwa ambayo inaelekea kuangamiza taifa letu, watu wanajilimbikizia mali ili kupata nguvu ya kisiasa. Imefikia wakati taaluma zote zimemezwa na siasa, itafika wakati wanasiasa watalazimisha madaktari kuwaandikia dawa wagonjwa kwa namna wanavyotaka wao. Hii ni hatari sana” alinieleza mkuu. Baada ya kumsikiliza kwa muda, siku hiyo aliniambia sentensi moja ambayo ikawa inajirudia rudia kichwani mwangu kila mara “Epuka kutumiwa na wanasiasa, wewe ni mtoto wa Tanzania na hutakuwa na nchi nyingine ya kuiita nyumbani hata ukibadili uraia”. Sikujua aliniambia kwa sababu gani, ila alimaanisha alichoniambia. Nikaja kuelewa kwa ufasaha maneno ya Mkuu baada ya tukio lililonitokea. Inamaana kuwa Mkuu alikataa kutumika na hawa jamaa ndiyo wakamuua? Yuko wapi Mwajuma? Nilipowaza hivyo nilihisi damu ikikimbia kwa kasi isiyo ya kawaida mwilini, na kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nikakihofia kifo. Siku mbili zilipita kukiwa na ukimya kama vile hakuna kitu kilichotokea lakini upande wangu nilikuwa katika harakati za kujiwekea hali ya usalama hasa kwa ajili ya Tausi. Nilijua wakati wowote wangeweza kumvaa labda kwa kumdhuru au kumuonyesha picha zangu na Mwajuma ambaye ni marehemu kwa sasa. Mpango wakumuweka Tausi katika hali ya usalama ulikamilika. Jioni moja tuliiweka kwa ajili ya utekelezaji. Yolanda aliwasili nyumbani kwangu na gari dogo yenye vioo vya giza. Huyu ni mmojawapo wa vijana waliokuwa wakiaminiwa na Mkuu japo alikuwa bado ni mpya kwenye kazi yetu lakini alikuwa na mwenendo wa kizalendo haswa japo aliwahi ‘kuniboa’ wakati nna ‘stress’ zangu kuhusu Tausi. Eti mimi nna mawazo yangu, yeye akawa anabusiana na kijamaa chake mbele yangu. Ah! Lakini ulikuwa wivu tu wa kibwege. Japo hakuwa kwenye mtandao wetu wa kulindana, tulimshirikisha Yolanda kwenye zoezi hilo kwa kuwa hatukubahatika kuwa na mwanamke kwenye mtandao wetu. Na Yolanda alionyesha kupenda kuwa karibu sana na mimi na Tausi kwa kuwa alijua ni kwa namna gani tunapendana akawa anatufurahia. Yolanda aliingia nyumbani kwangu akakaa kwa muda, kisha akatoka Tausi akiwa na mavazi ya Yolanda na kuondoka na lile gari kuelekea sehemu ambayo angekutana na Omari, yule rafiki yangu mpenda wanawake Malaya. Omari alikuwa tayari na maagizo juu ya sehemu ya kumpeleka Tausi ili awe salama. Zilipita dakika kumi bila kupata mrejesho wowote toka kwa Omari. Kwa mujibu wa makubaliano yetu na mpango ulivyo, ndani ya dakika tano tayari Omari angeshanihakikishia kuwa Tausi yuko katika mikono salama na mimi nianze kazi mara moja. Mapigo ya moyo yakaanza kwenda kama mishale ya saa mbovu huku mawazo mengi yakipita kichwani nikajikuta nimezama kwenye mawazo mengi huku akili yangu ikifanya kazi haraka haraka na kusahau uwepo wa Yolanda pale kwa muda. Ghafla mawazo yalirudi kwa Yolanda. Nilipogeuka kumwangalia Yolanda, tukakutanisha macho na kuangaliana kwa muda. Macho yetu yaliambiana mambo ambayo hayakua mazuri, ghafla Yolanda akapeleka mkono kiunoni kutaka kutoa bastola yake. Nikamrukia teke ambalo nadhani liliupa mkono wake ullpata ganzi kwa sababu kwa dakika mbili ambazo tulizicheza baada ya teke lile, sikuuona mkono huo kushiriki chochote. Yolanda alikuwa mzuri katika mapigano lakini sio kiasi cha kunipa tabu tena wakati sehemu ya moyo wangu imeguswa. Nilimdhitibi na kumuweka kwenye chumba kidogo kisicho na kitu baada kumfunga na nyaya nyembamba kwenye mikono na miguu ambazo zingeweza kumkata kama angefanya harakati zozote za kujinasua. Ilionekana dhahiri kuwa Yolanda amenisaliti na ana uhakika pale alipo analindwa na watu waliomtuma kwa hiyo hakuwa na wasiwasi. Kwa jinsi Yolanda alivyo mrembo, ingekuwa wewe usingethubutu kumpiga hata kibao na angekuua, ni aina ya warembo ambao huwa wanachorwa kwenye majarida yaani amekamilika kila idara lakini mwanamme nilichapa kama napiga paka aliyeiba kitoweo cha ngama ambacho tayari ushakisongea ugali. “Yolanda! Wewe ni wa kunisaliti mimi?” nilijikuta namuuliza kwa uchungu binti yule “Taifa ni zaidi ya wewe na Tausi” alinijibu kwa macho makavu. Niligundua kwa haraka haraka kuwa amelishwa maneno ya sumu kiasi cha kuniona mimi ni adui wa taifa hili. Sikujisumbua kumhoji chochote kwa sababu nilijua wazi kuwa hata ningemuua asingenipa taaifa yeyote nnayohitaji. Badala ya kumchukia nilimuonea huruma Yolanda, nikapekua kwenye mashine ya kuhifadhia sauti, nikapata maongezi ya mkuu na maongezi ya yule mwehu wa wanaojifanya wanatetea usalama wa taifa. Nikamrekodia kwenye kifaa maalumu na kumuwekea Yolanda asikilize akiwa mule mule kwenye kijichumba nilichomhifadhi mimi nikiondoka. Kifaa nilichokitumia kumrekodia, kina sehemu ambayo unaweza kukiamrisha kifute kumbukumbu zote baada ya muda fulani na ndivyo nilivyofanya. Nilikiamuru kirudie mara mbili halafu kifute kumbukumbu zote. Nilijua baada ya mimi kuondoka wenye Yolanda wangefika muda wowote kumchukua mtu wao. Niliamini kuwa ile ndiyo tiba pekee inayomstahili Yolanda, japo nilifanya kwa faida yangu pia katika kupunguza idadi ya maadui. Kawaida yangu huwa narekodi kila maongezi nnayofanya na ugeni wowote unaokuja pale nyumbani kwa kutumia saa yangu maaalum ambayo huivaa mara zote nikiwa pale nyumbani. Nilijiandaa haraka haraka na kutoka pale nyumbani nikitumia gari yangu. Moyoni nilijawa na chuki ya hali ya juu kutokana na kugusiwa Tausi wangu tena kwa jambo lisilomhusu halafu sio la haki. Chuki hiyo ilichanganyikana na woga fulani kwamba wanaweza kumuonyesha zile picha na kumjaza sumu zitakazomfanya anichukie. “Vipi kama watamuua kama walivyomuua Mwajuma” nilijisemea moyoni maneno hayo yaliyonitia ghadhabu na kuona dhahiri umuhimu wa kuushambulia mtandao alionidokeza Mwajuma kabla ya wao kunimaliza. Kwa kweli pamoja na kutoka pale nyumbani, sikuwa na mahali pa kuanzia kumtafuta Tausi kwa kuwa mpango ule wote ulipangwa na Omari japo hakuna aliyekuwa anajua kama Omari ndiye anaratibu zoezi lile kwa kuwa alimtumia askari mmoja asiye na cheo chochote ambaye ni mmojawapo wa vijana wake waaminifu. Hiyo ilisaidia kuficha nguvu ya mtandao wetu. Uamuzi wangu wa kwanza ulikuwa ni kumtafuta Omari. Ghafla nikapokea simu iliyonishusha presha, nilipokea taarifa kuwa Tausi yuko salama… Kumbe alipoingia barabara kubwa tu kutoka pale nyumbani, Tausi alikutana na gari mbili zilizomuweka katikati na kulazimisha kumuongoza kuelekea Bagamoyo badala ya uelekeo wa mjini kama ilivyopangwa. Baada ya mwendo kama wa dakika nne, taarifa zilishasambaa kuwa binti ya rais katekwa na watu wasiojulikana na anatakiwa apatikane ndani ya nusu saa lakini namba za gari zikatangazwa ni zile za gari alilokuwamo Tausi. Ilikuwa ni kazi ya Omari kwa kutumia namna anayoijua mwenyewe alivujisha taarifa hizo za uongo. Hali hiyo iliwatisha sana mabosi wa watekaji ambao nao ni sehemu ya wakubwa walioko madarakani, wakaamua kutengua mpango wao kwa kuwa vyombo vyote vya usalama vilifungua macho na baada ya dakika zisizozidi kumi likajulikana gari lilipo na ndipo zikatolewa taarifa rasmi kuwa taarifa za awali zilitolewa kimakosa. Wakati huo vijana wa Omari walikuwa wameshamrudisha Tausi mikononi. Nilizipata habari hizo nikiwa njiani kwenda kwenye sehemu ambayo ningewasiliana na Omari bila yeyote kujua kama ni mimi ndiye nawasiliana na Omari. Nikajifikiria kurudi nyumbani lakini nikaona niwape muda maadui wamchukue Yolanda, nikatafuta sehemu yenye pilika pilika nikaegesha gari langu na kuingia nipate kinywaji. Mabosi wa watekaji walikuwa wamechanganyikiwa wasijue ni nani aliyetoa taarifa zile zilizouvuruga mpango wao. Ingawa mtu wa kwanza kumfikiria alikuwa Omari, muda wote wa pilika hizo Omari alikuwa akionekana kwenye hoteli moja akinywa na makahaba wawili. Na hakuwa anajishughulisha na mawasiliano yeyote. Wakajua hahusiki. Kitu ambacho mpaka wakati huo walikuwa na uhakika nacho ni kwamba nina nguvu kuliko walivyonifikiria awali kutokana na ukweli kuwa tayari walifeli katika mipango yao miwili dhidi yangu. Na kutofahamu huko ndiko kulifanya wasite kunipoteza duniani. Tuliamua katika mtandao wetu tusiwe na mawasiliano ya moja kwa moja nje na taratibu za kiofisi ili kuongeza wigo wa kujilinda, na sasa ndiyo tunaona faida yake. Wakati kinywaji changu kikiwa nusu, nikapokea simu toka kwenye namba nisiyoijua. Sauti niliyoisikia ndiyo iliyonishtua sana japo halikuwa jambo geni kutokea. Ilikuwa ni sauti ya Kazikanda Moluwi, mkuu mpya wa usalama wa taifa. Akaanza kuniita kwa jina. Hakuna anachonikera bosi huyu kama anacholiharibu jina langu, yeye badala ya kuita Musa anaita Msa. “We Msa, uko wapi?” aliita kwa sauti yake nzito ya kishamba shamba. “Niko Jojiz, maeneo ya posta” nilimjibu bila kusita. “Subiri hapo hapo” aliongea KM na kukata simu. Nikabaki nimeishikilia simu yangu mkononi. Nikaanza kuangaza milangoni kuona ni nani ataingia. Nikajikuta nashikwa bega na mlevi mmoja aliyekuwa akipiga stori sana na wenzake kwenye meza ya jirani yangu. Nikageuka kumwangalia, akatabasamu kisha akaniambia tuondoke kama vile tulikuja wote. Nilielewa moja kwa moja anamaanisha nini, nikainuka bila kumalizia kinywaji changu na kutoka naye huku akininukisha harufu yake ya pombe. Baada kama ya dakika kumi nilikuwa uso kwa uso na Kazikanda Moluwi au KM. Huwa sina mazoea kabisa na Mkuu huyu kwa kuwa sipendi watu wenye mitazamo isiyobadilika na hali halisi iliyo. Huwezi kumwambiakitu tofauti na anachoamini. “Msa, kuna kazi maalum ambayo taifa linataka uifanye” aliniambia baada ya kunipa sifa za kijinga kibao. “Nakusikiliza mkuu” nilimjibu kwa heshima huku nikiongeza umakini. “Mkuu wa nchi anataka uingie kwenye siasa, utaelekeza chama cha upinzani cha kuingia na shughuli utakayoenda kuifanya. Ni chama ambacho kinasumbua na kuhatarisha usalama wa taifa” alinielezea kwa utulivu KM na kumalizia kuniuliza kama nina swali. Nikakumbuka maneno ya Mkuu aliponitembelea kuwa kuna kundi ndani ya chama tawala linalopigiwa kelele na wapinzani kutokana na kujilimbikizia mali ambalo linashindwa kushugulikiwa na mamlaka kutokana na mizizi yake ilivyosambaa. Kundi hilo ndilo linatumia vibaraka wao kufanya mambo ya ajabu yanayomchafua Rais na serikali yake. “Agizo hili kalitoa mwenyewe au umeambiwa tu kuwa mkuu wa nchi kaagiza na kwa nini nitumwe mimi?” nilimuuliza maswali mawili ambayo yalimfanya ajiweke sawa kwenye kiti chake. Japo nilishajua atakachojibu lakini nilitaka kumuonyesha kuwa nafanya kazi kwa kufikiri sio kufuata tu maagizo. “Unachotakiwa ni kufanya kazi unayopangiwa bila kuhoji” alitoa jibu nililotarajia ila alikosea kwa kuniuliza kama kazi zote nilikuwa napewa sababu ya mimi kuchaguliwa kuifanya kazi husika. Nilimuelezea kazi moja moja na kumalizia kazi ya kumchunguza baba yake Tausi, Mzee Nurdin kwamba ilitokana na ukweli kuwa sikuwepo nchini kwa muda mrefu hivyo watu wengi ambao walikuwa kwenye mtandao wake wasingenigundua. KM alikaa kimya kwa muda kisha akaendeleza desturi yake ya utemi, “Hapa ni amri tu hakuna siasa”. Jibu lake lilinifanya nichekee moyoni, maana ananituma kazi ya siasa halafu ananiambia hataki siasa. Kwa kadiri ya mazoea yangu na ufahamu nilio nao, ukiona mtu anatanguliza kumtaja mkuu wa nchi ujue anataka kufanya jambo kwa maslahi yake ila anataka tu kutumia jina la rais ili kuwatisha watu wasihoji. “Mkuu” nilianza kuongea kabla hajanikatisha kwa ukali. “Nini!” “Siku hizi watu ni wafuatiliaji wazuri, ili tufanikiwe itabidi nijifanye nimeacha kazi na nilipwe stahiki zangu zote kisha nijifanye nimegeukia siasa. Hapo kila kitu kitaenda anavyotaka mheshimiwa rais” nilifanya jaribio la kumjaza kwenye mtego wangu. Akaniomba muda ajifikirie. “Ila nitalipeleka kama wazo langu kwa mheshimiwa ili alichukulie kwa uzito” aliniambia KM. nilifurahi sana kwa uamuzi wake wa kulipeleka kama wazo lake. Pamoja na yeye kufanya vile ila apate sifa kuwa ana mikakati bora, wazo kama hilo kutoka kwake lisingewafanya wanaomtuma kulitilia shaka na kufikiri mara mbili. Unajua watu wanaofanya mambo kama hawa wanaojiita watetea usalama wa taifa huwa hawana akili japo mara nyingi hujiona ‘vichwa’ sana. Kwa kuwa mioyo yao imetawaliwa na tamaa za mali na madaraka, akili zao zinaangalia eneo hilo tu. Nilijua watakubali kwa vile kwa akili zao ndogo watajua nikiwa nje ya mfumo rasmi itakuwa rahisi kwao kunipeleka wanavyotaka na ikiwezekana kuniondolea uhai wangu. “Utapigiwa simu kupata maelekezo” aliniambia KM. Nikageuza kurudi nyumbani nikimuomba Mungu kuwa kila kitu kiende ninavyotaka mimi. Hakuna kilichonishangaza kwa hali niliyoikuta nyumbani kwangu, sehemu zote nilizotarajia zingepekuliwa zilipekuliwa na Yolanda wao walikuwa wamemchukua. Sikuthubutu kuwasiliana na Tausi kwa ajili ya usalama wake ila kusema kweli nilikuwa na hamu naye. Kwa haraka ya ajabu nikapata taarifa zote nilizokuwa nazihitaji juu ya Boimanda, hii inatokana na mahojiano waliyoyafanya watu wangu na wale walionivamia. Boimanda alikuwa mtumishi mwadilifu wa serikali katika wizara kadhaa na kumalizia utumishi wake ofisi ya rais ambako alikuja kustaafu. Hakuwa na utajiri kutokana na usimamizi mzuri wa sera ya ujamaa na kujitegemea, pamoja na kupitia kwenye nafasi hizo pia Boimanda alikuwa usalama wa Taifa aliyestaafu akiwa kwenye ngazi za juu. Wakati akiwa usalama wa Taifa aliwaingiza vijana wake wengi sana, na mmojawapo alikuwa Kazikanda Moluwi ambaye sasa ndiyo Mkuu mpya. Kwa mara ya kwanza nikawa namtazama Boimanda kwa mtazamo mwingine, na nikaona bayana kilichokuwa kikimpa jeuri yule bwege aliyekuja kunihoji nyumbani kwangu.
KWA haraka ya ajabu nikapata taarifa zote nilizokuwa nazihitaji juu ya Boimanda, hii inatokana na mahojiano waliyoyafanya watu wangu na wale walionivamia. Boimanda alikuwa mtumishi mwadilifu wa serikali katika wizara kadhaa na kumalizia utumishi wake ofisi ya rais ambako alikuja kustaafu. Hakuwa na utajiri kutokana na usimamizi mzuri wa sera ya ujamaa na kujitegemea, pamoja na kupitia kwenye nafasi hizo pia Boimanda alikuwa usalama wa Taifa aliyestaafu akiwa kwenye ngazi za juu. Wakati akiwa usalama wa Taifa aliwaingiza vijana wake wengi sana, na mmojawapo alikuwa Kazikanda Moluwi ambaye sasa ndiyo Mkuu mpya. Kwa mara ya kwanza nikawa namtazama Boimanda kwa mtazamo mwingine, na nikaona bayana kilichokuwa kikimpa jeuri yule bwege aliyekuja kunihoji nyumbani kwangu.
Kwa kuanzia, ilibidi niwachukulie watu wote walioingizwa kazini na Boimanda pamoja na KM kuwa ni maadui zangu. Haikuwa rahisi kuwajua wote lakini kimsingi nikajua kuwa ndani ya taasisi yetu nyeti tayari tuna mitazamo tofauti kuusiana na mustakabali wa nchi yetu. Kwa kuogopa mtandao wetu kuvuja, tukapanga na Omari kuwaelezea vijana wetu kila kitu kuhusu mtazamo wetu na kuwa maadui zetu ni nani.
Kwanza nilikuwa nayafanya yote kwa mapenzi tu kwa nchi yangu lakini kwa sasa nafanya kwa kulipiza damu ya Mkuu na hasa damu ya Mwajuma, mrembo aliyetolewa uhai wake kwa vile tu alikuwa tu na dhamira ya kunisaidia. Kwa kweli nilikuwa naumia sana moyoni na nilijiona nina jukumu zito ila kazi ilikuwa ngumu kwa kuwa jamaa hawa ni kama wako juu ya sharia kutokana na mtandao wao ulivyo na nguvu.
Baada ya siku tatu niliitwa tena kwa Kazikanda Moluwi, ni tofauti na maneno yake ya awali kwamba nisubiri kupewa maagizo. Siku hiyo yalizuka mabishano makali sana kati yangu na KM baada ya kuniambia kuwa kashfa ya Mwajuma ndiyo itumike kama sababu ya kufukuzwa kazi ili kusiwe na mtu wa kuhoji uamuzi huo.
Maneno hayo yalikuwa ni kama uthibitisho rasmi kuwa KM, Boimanda na wenzao ndiyo walihusika na kumuua Mwajuma na uvamizi uliotokea nyumbani kwangu. Nilimwambia KM kuwa kama wanadhani nimehusika kwa namna moja au nyingine kwenye kifo cha Mwajuma wasiishie kufanya ni sababu ya mimi kufukuzwa kazi, wanifikishe moja kwa moja mahakamani.
“Unajiamini nini?” aliniuliza KM
“Sio suala la kujiamini, ni kufanya tu haki itendeke kwa kuwa inaelekea mnalijua sana jambo hilo sasa ni kwanini marehemu asipewe haki zake kwa kumkamata muuaji” nilimjibu kwa kujiamini.
“Hapa suala ni sababu ya wewe kufukuzwa kazi, usilete habari zako ningine” KM alijaribu kunitoa kwenye hoja.
“Kama uamuzi wa mimi kuingia kwenye siasa umetoka kwa mheshimiwa rais, kwanini zitafutwe sababu za kunifukuza kazi kwa kuogopa watu watahoji? Ni nani mwenye mamlaka ya kumhoji mheshimiwa rais? Labda ingekuwa nafanya kazi moja kwa moja na jamii mnesingizia kuwa wananchi watahoji.
Siwalazimishi kufuata ninavyotaka mimi ila kama mtataka kunikandamiza nitatutumia nguvu zangu zote kupata haki yangu.” Nilimwambia kwa kujiamini nikimtazama machoni. KM alinitaka niondoke ili atafakari uamuzi wa kuchukua lakini kwangu maneno yake yalikuwa yakimaanisha kuwa anaenda kuwaeleza waliomtuma ili wachukue uamuzi kutokana na hoja nilizozitoa.
Haikuchukua muda kupata uamuzi wa waliomtuma KM, maana nilipofika tu nyumbani nikapigiwa simu kuelezwa walichoamua. Nadhani alipopeleka hoja hiyo, waliomtuma wakajua waking’ang’ania hoja yao nitawashtukia. Ikakubalika kuwa niandike barua ya kuacha kazi. Nikafanya taratibu zote.
Siku ambayo nilimalizana na taasisi hii nyeti, tayari nilikuwa nishaandaa mpango wa namna ntakavyotekeleza majukumu niliyojipangia nikiwa nje ya ajira. Pia nilipangisha nyumba yangu niliyokuwa naishi pamoja na kutengeneza utambulisho mpya kabisa kwa ajili ya matumizi ya simu, mitandao na huduma za kibenki. Kifupi hadi wakati huo kulikuwa na watu wawili tofauti nje yangu.
Kitu ambacho viongozi hawakuwa wanakijua ni kwamba, badala ya kuwa kazi imeisha kwangu ndiyo ilikuwa imeanza rasmi. Baada ya siku kadhaa nilikuwa nikiishi sehemu tulivu nikiwa na mpenzi wangu Tausi, sehemu ambayo ilikuwa na mtandao wa ulinzi mkali kuliko nilipokuwa nakaa zamani kwa kuwa mtandao wetu ulijua kuwa nakabiliwa na hatari kubwa zaidi kuliko mwanzoni. Lakini kwa macho ya kawaida usingehisi kama sehemu hiyo ilikuwa na ulinzi wowote.
Nilitambulishwa kwa viongozi wa siasa ambao ni mamluki wenzangu kwenye chama hicho nilichoagizwa nijiunge nacho. Nilishangaa sana kuona kuwa ni wale walio mstari wa mbele kupiga kelele kwenye vyombo vya habari kila kukicha.
Inamaanisha kuwa na mimi natakiwa kuwa kimbelembele? Nilijiuliza kwa haraka haraka kabla sijapewa majukumu tofauti na ‘kutokelezea’ mbele ya waandishi wa habari kila mara, nikashusha pumzi.
Nilipewa kazi ya kuwasafisha viongozi wa chama tawala na chama kile cha upinzani waliokuwa na dhamira ya dhati katika kupigia kelele wizi unaofanywa na baadhi ya viongozi walio madarakani na wengine walio nje ya madaraka wanaotaka kurudi katika hatamu za kuishika nchi. Siku hiyo sikulala usiku kucha, pamoja na ushujaa wangu nilijihisi kupwaya katika jukumu hilo.
Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu toka nimfahamu Tausi, siku hiyo nilimpa mgongo nikijikunyata kwenye kona ya kitanda mithili ya watoto wa mitaani wanavyolala vibarazani wanavyokuwa wamejikunyata kwabaridi. Sikuwa nimemhadithia Tausi kilichojiri ila aligundua kuwa nina jambo zito kichwani, akanifunika shuka akalala pembeni yangu kwa utulivu.
Kikubwa nilichotakiwa kukijua kwanza, ni kiongozi mkuu wa harakati hizi. Kutokana na ukubwa wa mtandao, njia rahisi niliyoiona na kuiamnini ni ya kuling’oa shina na kuacha matawi yasambaratike yenyewe. Kazi ya kwanza ndiyo ilinishangaza zaidi. Nilipigiwa simu na kutaarifiwa kuwa nikachukue maagizo ya kazi ya kwanza kwenye sanduku langu la barua, nilicheka na kujiamini zaidi baada ya kupokea maagizo hayo kwa kuwa ilinipa picha kuwa wakina KM hawanijui vizuri. Sanduku langu la barua huwa liko pale kuzuga tu.
Jambo nililokuja kuligundua baadaye ni kuwawastaafu wa serikalini, waliaminishwa kuwa nchi ni yao na wakafanya kazi kwa uadilifu mkubwa na kuishia kwa na kipato duni. Sasa wanavyoona watumishi wa siku hizi wakitajirika kwa haraka kwa kutumia mbinu chafu, mioyo inawauma sana hivyo wanataka hatua kali zichukuliwe kwa haraka jambo ambalo halifanyiki kutokana na kinachoitwa ‘utawala wa sheria’.
Wenye uroho wa madaraka wakaligundua hilo na kuwaaminisha wastaafu hao kuwa wao wana uwezo wa kuisafisha hali iliyopo ili wapate sapoti kutoka kwao itakayowapeleka madarakani. Wakitumia hata njia chafu kupata utajiri huku wakiwadanganya wastaafu hao kuwa ni namna ya kujijengea uwezo ili waweze kuingia madarakani na kuisafisha nchi.
Walikuwa kwenye nafasi nzuri kweli kweli kwa sababu, serikalini walikuwa wakiaminika hata kwa mheshimiwa Rais mwenyewe, nje walikuwa wakiaminiwa na wastaafu na wao ndiyo watafuna nchi kwa kushirikiana na ‘mchwa’ wenzao wanaojinadi kuwa wanataka kuingia kuwashughulikia. Kazi ilikuwa ngumu sana. Nikaanza kuumiza kichwa ni kwa namna gani nitaweza kusambaratisha mtandao huo ili nisilazimike kuua watu wasio na hatia ambao wanatetea maslahi ya nchi yetu. Kikubwa nilichotakiwa kukijua kwanza, ni kiongozi mkuu wa harakati hizi.
Kutokana na ukubwa wa mtandao, njia rahisi niliyoiona na kuiamnini ni ya kuling’oa shina na kuacha matawi yasambaratike yenyewe.
Kazi ya kwanza ndiyo ilinishangaza zaidi. Nilipigiwa simu na kutaarifiwa kuwa nikachukue maagizo ya kazi ya kwanza kwenye sanduku langu la barua, nilicheka na kujiamini zaidi baada ya kupokea maagizo hayo kwa kuwa ilinipa picha kuwa wakina KM hawanijui vizuri. Sanduku langu la barua huwa liko pale kuzuga tu.
Barua na vifurushi vyote vinavyoelekezwa kuingia kwenye namba ya sanduku langu huletwa moja kwa moja mahali nitakapoagiza na kwa wakati ninaotaka. Kwa hiyo simu yao ilikuwa ni kama kuniambia tu kuwa kati ya vifurishi nilivyopokea muda mfupi uliyopita kuna kimojawapo kina kazi yao.
Nikavifungua kwa haraka haraka na kuikuta kazi yenyewe iliyonishangaza. Aliyetakiwa kuondolewa duniani hakuwa kiongozi wa upinzani bali alikuwa ni waziri wa serikali ambaye siku za karibuni alikuwa amevunja mtandao mmoja mkubwa sana uliokuwa ukiwaingizia watu wachache mabilioni ya hela kila mwezi.
“Hawa ni watetea maslahi ya taifa kweli?” nilijikuta najiuliza kwa sauti. Bahati nzuri hakukuwa na mtu karibu yangu. Tausi alikuwa jikoni akipika. Katika vitu ambavyo nilishindwa kumshawishi Tausi ni suala la kutafuta msichana kwa ajili ya kumsaidia kazi. Mara zote alikuwa akinijibu “nahitaji kumhudumia mume wangu mimi mwenyewe”.
Hapo ndipo anapowapiga bao wasichana wengine wasomi na waliotoka kwenye familia ya kitajiri kama yeye. Nadhani ni kwa ajili ya kumcha Mwenyezi Mungu.
Kichwa kilianza kuniuma kuhusiana na hiyo kazi. Nilipewa ratiba yake yote ikielekea kuwa mmojawapo wa wasaidizi wake wa karibu alikuwa anahusika na mpango huo. Wakati mzuri zaidi ilikuwa ni mkutano wake na waandishi wa habari kuhusiana na mikakati ya wizara yake katika kukabiliana na uhujumu wa uchumi. Kibaya zaidi mimi nilitakiwa kupanga tu mpango, watekelezaji walikuwa ni vijana wao na wakubwa hao walinisisitiza kuwa wanataka kazi safi.
Ilinibidi nipange mpango ambao haukuwatia mashaka yeyote, ilikuwa tutumie sumu ya kunusa ambayo ingewekwa kwenye kinasa sauti chake na walipangwa vijana wa kumuuliza maswali ya kukera ili aweze kuivuta nyingi iwezekanavyo. Pia nilipanga kuwa akizidiwa apelekwe hospitali ambayo ina daktari wao ili atoe taarifa za uongo kuhusiana na kifo chake. Kila kitu kiliandaliwa kama kilivyopangwa.
Hadi muda ambao ofisi zinafungwa, siku moja kabla ya mkutano huo ambao ulipangwa kufanyika kwenye chumba cha mikutano cha wizara yake kila kitu kilikuwa kimeandaliwa kwa umahiri mkubwa. Hadi wakati huo nilikuwa sijajua ni hatua zipi za ziada nizichukue. Ilipotimia saa 3 usiku likanijia wazo ghafla ambalo nililifanyia kazi kwa ukamilifu.
Siku ya tukio, waandishi walikusanyika tayari kumsubiri waziri huyo. Waziri akaeleza kwa kina alichowaitia waandishi wa habari kabla ya waandishi kuanza kuuliza maswali. Wakati anajibu swali la tatu waziri akaanguka na kuzua pilika pilika za hapana pale kabla hajachukuliwa na wana usalama kupelekwa kwenye hospitali mojawapo kati ya zinazohudumia viongozi na ndiyo aliyopangwa daktari wa ‘watetea maslahi ya taifa’.
Wazo nililolipata saa 3 usiku wa siku ya kuamkia mkutano wa waziri na waandishi wa habari lilinifanya nitoke usiku huo nikiwa tayari kwa lolote nikaenda moja kwa moja hadi kwenye jengo la wizara.
Nje niliwakuta askari wanne wakiwa na silaha, nikazunguka kwa nyuma ambako kuna jengo jingine. Nikafanikiwa kuwapenya walinzi wa jengo ambalo limepeana mgongo na jengo la wizara, nikapanda juu kabisa ya jengo hilo na kurukia juu ya jengo la wizara. Nikateremka pole pole hadi kwenye ghorofa ilipo ofisi ya wizara na chumba cha mikutano, nikakifungua chumba cha mikutano kwa namna ninayoijua mimi.
Moja wa moja nikatoa kinasa sauti chenye sumu, nikaweka nilichoenda nacho ambacho kinafanana na kile kwa kila kitu kabla ya kuenda kwenye kona moja ya dirisha na kutoa kifaa maalumu cha kurekodia picha Kama nilivyokuhadithia awali kuwa nilikuwa nawaza hatua za ziada za kuchukua, ni za ziada kwakuwa za awali tayari zilikuwa zimefanyika kwa kutumia watu wa mtandao wangu tulifunga kifaa hicho kwa ajili ushahidi wa siri ambao tulidhani ungetusaidia katika mipango yangu ya kuwamaliza wenye uchu wa mali na madaraka.
Nikatoka moja kwa moja hadi ilipo nyumba ya waziri ambayo iliimarishwa ulinzi na mheshimiwa rais kutokana na maamuzi makubwa aliyoyafanya waziri huyo. Nikatumia mbinu za kijasusi kuingia humo ndani, na baada ya kukagua vyumba kadhaa nikakigundua chumba cha waziri na kumkuta akiwa amelala na mkewe.
Nikawasha taa, wakakurupuka toka usingizini na kubaki wamehamaki wakiangaza huku na kule. Nikawahi kuwanyamazisha kwa kuwaonyeshea bastola na kuwaamuru wakae kitandani wakiwa kimya. Wakawa wanalalamika tu kuwa wako tayari kunipa chochote ili nisiwaue.
Nikawaamuru wainuke taratibu na wasogee mbali kidogo na kilipo kitanda, wakafanya hivyo huku mheshimiwa waziri akionekana kama anayepanga na kupangua mambo kichwani. “Mimi nakulinda mheshimiwa waziri, unatakiwa kuuawa kesho. Kuna watu ambao wana nguvu sana katika nchi hii wanaotaka ufe, kwa hiyo ukionyesha ushirikiano utaendelea kuwepo na nitaendelea kukulinda wewe na wenzio mnaolitakia mema taifa hili. Lakini ukijifanya mjanja kukwepa ninayokwambia ndiyo utakuwa unakimbilia kifo chako mwenyewe” nilimueleza kwa ufasaha nikimwangalia usoni.
Nilimweleza kwa kirefu na kumuonyeza picha za namna walivyofunga kinasa sauti chenye sumu na kumuelekeza cha kufanya na ndivyo alivyofanya na kudondoka. Pia nilimsisitiza mke wa waziri kuwa akifanya upumbavu wowote maisha ya mumewe yatakuwa hatarini na yeye ataisaidia polisi kwa kuwa ni yeye tu anayejua ninachowaambia pale. Japo walisisitiza kutaka kunijua na kujua nimetumwa na nani, hawakuweza kupata jibu lolote kisha nikaondoka kama ambavyo niliingia.
Baada tu ya waziri kufikishwa hospitali, lilikuja gari la Ikulu kumuondoa na kumpeleka kwenye chumba maalumu cha hopitali ya jeshi huku uvumi ukiwa umeshazagaa kuwa waziri huyo amefariki dunia. Ikaja kutangazwa kuwa yuko mahututi na mipango inafanyika kumpeleka nje ya nchi.
Kwa msaada mkubwa kutoka kwa mhehimiwa rais, maagizo yote ya waziri huyo yaliendelea kutekelezwa huku ikielezwa kuwa hali ya waziri huyo ni mbaya mno. Mambo yote alikuwa yakiratibiwa na maofisa ambao walionekana kuwa wasafi kutokana na taarifa za mtandao wetu wa siri. Lakini ukweli ni kuwa waziri huyo alikuwa ni mzima wa afya.
Upande wa wale wapuuzi wanaojiita watetea maslahi ya taifa waliamini kuwa nimefanya kazi vile ilivyotakiwa ila matatizo yalikuwa upande wao kwa kushindwa kumshikilia mgonjwa katika mikono yao ila hawakuwa na wasiwasi na mimi. Kilichonifurahisha zaidi ni uamuzi wao kuwa wasimamishe kwa muda opereseni yao ya kuwasafisha vimbelembele hadi hali itakapotulia, nikawa likizo isiyo rasmi. Likizo hiyo nikaitumia kuchunguza vyanzo vyao vyote vya mapato visivyo halali vya watu hawa kwa kushirikiana na mtandao wangu wa siri. Na kikubwa ni kumjua kiongozi wao, au ‘Rais mtarajiwa’.
Ndipo nikamgundua Mheshimiwa Dickson Malyato Ndagila, waziri wa za mani wa fedha aliyefukuzwa kazi serikalini kutokana na wizi mkubwa uliyotokea Benki Kuu na kumhusisha yeye kwa namna moja au nyingine japo hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja.
Simulizi : Mvuvi Bruno (Bruno The Fisherman) Sehemu Ya Kwanza (1)
Bruno The Fisherman (Mvuvi Bruno) Hali ya hewa angani ilibadilika ghafla, jua kali lililokuwa likiwaka lilifunikwa na mawingu mazito ya kijivu yaliyokuwa yametanda angani. Kwa jinsi hali ilivyokuwa ikionekana, kila mmoja aliamini kwamba mvua kubwa ingekwenda kunyesha. Mawimbi makubwa kiasi yalianza kupiga kwa nguvu ufukweni, kila mtu aliyekuwa akiiona hali hiyo aliogopa na kuona kwamba siku hiyo mvua hiyo ingekuwa kubwa kuliko hata zile ambazo ziliwahi kunyesha katika Kijiji cha Guolduvai kilichokuwa nchini Kenya pembezoni mwa bahari ya Hindi. Watu waliokuwa wakiogelea, wakatoka majini na kuelekea nyumbani kwao, kila mmoja alionekana kuwa na hofu kwani hali iliyokuwa ikionekana siku hiyo ilikuwa ni ya hatari tupu. Wavuvi waliokuwa wakivua samaki kama kawaida yao kwa nyakati za mchana, haraka sana wakaanza kurudisha mitumbwi yao kijijini kwani kwa kuwa walikuwa wakitumia mitumbwi ambayo haikuwa na nguvu ya kupambana na mawimbi makubwa, wakahisi kabisa kwamba kama mvua hiyo kubwa ingewakuta baharini basi hali ingekuwa mbaya zaidi. Wakati kila mtu akiogopa mvua kubwa iliyokuwa ikitarajiwa kunyesha, kijana masikini, aliyevalia fulana iliyokuwa imechanika ambayo kwa mbele iliandikwa 50 Cent huku ikiwa na picha kubwa ya mwanamuziki huyo alikuwa amesimama katika kichaka kilichokuwa kijijini hapo huku akiangalia huku na kule. Kwa muonekano wake tu haikuwa kazi kubwa kugundua kama kijana huyo alikuwa masikini wa kutupwa. Mbali na fulana yake hiyo iliyoonekana kuchakaa, chini alivalia pensi, kandambili zilizokuwa tofauti huku nywele zake zikiwa timtim. Kijana huyu aliitwa Bruno. Alikuwa kijana mkimya kijijini hapo, alimheshimu kila mtu aliyekuwa akiishi mahali hapo. Hakuwa mtu aliyekuwa na furaha, maisha yalimpiga, wazazi wake ambao walifariki miaka miwili iliyopita kwa kuzama na mtumbwi uliokuwa ukielekea Mombasa hawakumuachia kitu, alikuwa mikono mitupu huku akiendelea kufanya kazi ya uvuvi katika bahari ya Hindi. Alisimama mahali hapo huku macho yake yakiendelea kuangalia huku na kule. Hakuonekana kuogopa mvua kubwa iliyokuwa ikitarajiwa kunyesha, kile alichokuwa akikitaka ni kuongea na msichana aliyekuwa akimpenda kwa moyo wa dhati, Sharifa ambaye alimwambia kwamba angefika mahali hapo muda si mrefu. Mpaka mvua kubwa inaanza kunyesha bado msichana huyo hakuwa ametokeza. Mvua iliyoambatana na upepo mkali ilimnyeshea lakini hakukubali kuondoka, aliendelea kusubiri mahali pale mpaka alipomuona msichana huyo akija kutoka kule kijijini huku akikimbia. Uso wake ukajawa na tabasamu, kumuona Sharifa mahali hapo ndiyo lilikuwa lengo lake. Kila alipomwangalia, uzuri wa msichana huyo ulikichanganya kichwa chake. Sharifa akamsogelea mpaka pale alipokuwa, kama alivyokuwa Bruno, hata naye alikuwa amelowanishwa na mvua iliyokuwa ikiendelea kunyesha. Sharifa alipomfikia Bruno, akamsogelea, akamkumbatia na kuangaliana pasipo kuzungumza kitu chochote kile. Bruno alikuwa na mambo mengi ya kuzungumza na msichana huyo aliyekuwa amesuka mabutu kichwani mwake na viatu vyake ya chachacha vikiwa miguuni mwake. “Nimekusubiri sana!” alisema Bruno huku akimwangalia Sharifa, walipokuwa wamesimama, bado mvua kubwa iliendelea kuwanyeshea. “Pole sana! Nimechelewa kidogo lakini sidhani kama umekasirika,” alisema Sharifa kwa sauti ndogo huku akimwangalia mpenzi wake huyo kwa jicho lililoonyesha mahaba yote kwake. “Hakuna! Siwezi kukasirika! Ulizungumza na wazazi wako?” aliuliza Bruno. “Ndiyo! Nilizungumza nao, waliniambia vilevile.” “Kwamba?” “Hawataki kuona nikisimama na kuongea nawe. Kiukweli wanakuchukia, wanasema kwamba huna kitu, utanilisha nini? Utanipa nini? Huna chochote kile,” alisema Sharifa huku akimwangalia Bruno ambaye nguvu zilimuisha baada ya kuambiwa hivyo. Moyo wake ulikuwa na hasira tele, alimpenda sana Sharifa lakini kipingamizi kikubwa kilikuwa ni nyumbani kwa msichana huyo. Hakukubalika kwa sababu tu alikuwa masikini, wazazi wa msichana huyo walimchukia kupita kawaida. Sharifa alikuwa mzuri wa sura, alipendwa na kila mtu kijijini hapo, wanaume walimfuatilia, tena wale waliokuwa na mitumbwi yao ambao kila siku walipata pesa nyingi baada ya kuvua samaki. Wote hao, Sharifa hakuwakubali, kwake, moyo wake ulikuwa kwa mtu mmoja tu, Bruno ambaye alikuwa masikini wa kutupwa. Alichokuwa akikiangalia Sharifa hakikuwa pesa wala mali, hakuangalia mambo mengine zaidi ya mapenzi. Aliamini kwamba penzi lilikuwa kila kitu, hata kama Bruno hakuwa na kitu lakini aliamini kwamba angeweza kumpa furaha aliyokuwa akiihitaji. “Niambie tufanye nini! Sitaki kuolewa na mtu yeyote, ninataka kuolewa na wewe tu. Niambie Bruno unataka tufanye nini?” aliuliza Sharifa huku akitokwa na machozi yaliyokuwa yakitiririka mashavuni mwake ila ilikuwa vigumu kuyaona kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha. “Sijui tufanye nini! Labda unipe muda wa kujifikiria!” “Hatuna muda! Sema tufanye nini! Au tutoroke?” “Tutoroke?” “Ndiyo!” “Kwenda wapi?” “Popote pale. Nitahitaji kuwa nawe, sitaki kuona nikikukosa. Bruno, ninakupenda sana, wewe ndiye kila kitu katika maisha yangu, siwezi kuishi bila wewe,” alisema Sharifa, hapohapo akamkumbatia tena Bruno. “Sharifa! Sina pesa, sina kitu chochote kile. Nipo mtupu kama unavyoniona, hata tukitoroka, itakuwaje huko tutakapokwenda?” aliuliza bruno. “Vyovyote itakavyokuwa. Naomba tutoroke. Sitaki kukupoteza,” alisema Sharifa. Kwa jinsi alivyoonekana, Sharifa alikuwa tayari kutoroka mahali hapo. Moyo wake ulichoka na alihitaji kuendelea kuishi na mpenzi wake huyo. Hakutaka kubaki kijijini pale, wazazi wake walikataa yeye kuolewa na Bruno kwa kuwa tu alikuwa masikini. Hilo lilimuumiza mno na kitu alichokuwa amekifikiria ni kutoroka kijijini hapo. Kwa Bruno ilikuwa ngumu kukubaliana naye. Hakuwa na kitu, kilichomuumiza kichwa si kutoroka kijijini hapo bali ni maisha baada ya kutoroka. Alimwambia wazi Sharifa kwamba huo haukuwa uamuzi mzuri, walitakiwa kubaki hapohapo kijijini huku wakiamini kwamba kuna siku maisha yangekuwa kama wanavyotaka yawe. “Hatutakiwi kutoroka. Kama tatizo ni pesa, tutatafuta pesa, tutakuwa na pesa na kufanikiwa. Sharifa! Sitaki nikupoteze, kama kweli wazazi wako wanasema siwezi kukuoa kwa sababu sina pesa. Nitatafuta pesa tu, tena kwa nguvu zote,” alisema Bruno huku akimwangalia mpenzi wake huyo. Japokuwa ilikuwa vigumu kumshawishi msichana huyo lakini mwisho wa siku wakakubaliana kwamba hakukuwa na sababu ya kutoroka zaidi ya Bruno kupambana mpaka kuhakikisha kwamba anapata pesa na kumuoa msichana huyo. Walizungumza kwa dakika kadhaa, walipomaliza, Sharifa akaondoka kurudi nyumbani kwao. Huku nyuma Bruno alichanganyikiwa, bado hakufahamu ni kitu gani alitakiwa kufanya. Hali iliyokuwa ikiendelea ilimtisha mno, hakutamani kuona akimkosa msichana huyo kisa tu hakuwa na pesa. Alitaka kupambana mpaka kuhakikisha anapata pesa na kumchukua msichana huyo. Maisha yaliendelea, kama kawaida kila siku alikuwa akiondoka kuelekea baharini na rafiki yake, Abdul huku wakiwa kwenye mtumbwi wao. Huko, hasa nyakati za usiku walikuwa wakivua samaki na kwenda kuwauza kijijini kwao. Abdul alikuwa akifahamu kila kitu. Huyo ndiye alikuwa rafiki yake wa karibu, walipendana na kupeana siri ya kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika maisha yake. Abdul alimuonea huruma Bruno, alijua ni kwa jinsi gani mwanaume huyo alimpenda Sharifa, alijitahidi kufanya kila liwezekanalo kwa msichana huyo lakini bado wazazi wake hawakutaka kabisa kumuona binti yao akiwa na kijana masikini kama yeye. “Ila kuna siku nitapata pesa tu na kumuoa Sharifa,” alisema Bruno huku akimwangalia rafiki yake huyo, wakati huo walikuwa kwenye mtumbwi wao, chemli ilikuwa ikiwaka, walikuwa wakielekea mbali kabisa na bahari. “Unahisi utafanikiwa kwa kupitia hawa samaki?” aliuliza Abdul. “Inawezekana! Pia nitaanza kuangalia mpango wa kuelekea mjini Nairobi kwenda kuuza huko. Abdul, hujui ni kwa kiasi gani nampenda Sharifa,” alisema Bruno. “Najua. Unampenda sana. Ila hili suala la wazazi wake linaniumiza sana kichwa,” alisema Abdul. “Najua! Ila nitapambana tu!” Walikuwa wakipiga stori huku wakiwa safarini kuvua. Hayo ndiyo yalikuwa maisha yao ya kila siku. Walivua usiku kucha, walipigwa na maji, walipigwa na baridi na asubuhi walirudi kijijini huku wakiwa na samaki wa kuwauza kwa siku mbili. Mtu wa kwanza kabisa aliyekuwa akiwapokea na kuwasaidia kutoa samaki kwenye mtumbwi alikuwa Sharifa. Alikatazwa kuwa karibu na Bruno lakini hilo halikumfanya kumsaidia kazi hiyo. Wazazi wake walisema sana lakini hakutaka kusikia, alijitoa kwa kila kitu, kama kupigwa kwa ajili hiyo, alipigwa leo na kesho kama kawaida alifanya vilevile. “Pole sana mpenzi,” alisema Sharifa huku akimsogelea Bruno alipokuwa. Alionekana kuwa hoi. “Ahsante sana!” Wakawachukua samaki, wakamuita dalali na kwenda kutafuta wateja huku wakiwa wamekwishaelewana naye kabisa. Wakaondoka mahali hapo na kwenda nyumbani kwake, katika nyumba ya nyasi, ndani kitanda cha teremka tukaze na kutulia hapo. Walibaki wakiwa wameshikana mikono, waliangaliana kwa bashasha huku kila mmoja akionekana kuwa na hamu na mwenzake. Sharifa akaanza uchokozi kwa kukichezea kifua cha Bruno aliyekuwanaye kitandani hapo. “Ushaanza…” alisema Bruno huku akitoa tabasamu pana. “Kwani kuna tatizo mpenzi?” aliuliza msichana huyo, hapohapo akaanza kumvua fulana Bruno. Huku tayari akiwa amekwishavuliwa fulana yake, mara wakaanza kusikia sauti ya Adul kutoka nje ikimuita. “Bruno…Bruno fungua mlango…” ilisikika sauti ya Abdul. Wote wakashtuka, haraka sana Bruno akafungua mlango na kumwangalia rafiki yake huyo. Alikuwa akihema kwa nguvu, akamuuliza tatizo lilikuwa nini. “Mzee Jumanne anakuja na panga. Kimbia! Anakuja kukumaliza,” alisema Abdul. Bruno alivyosikia hivyo tu, haraka sana akachukua fulana yake lakini hata kabla hajatoka tu ndani ya kijumba chake cha nyasi, mzee huyo akatokea na kusimama mlangoni. Jasho lilikuwa likimtoka, alionekana kuvimba kwa hasira, mwili ulikuwa ukimtetemeka. Kitandani pale, alimuona binti yake akiwa amekaa, hasira zikamzidi zaidi, akalishikilia vizuri panga lake tayari kwa mashambulizi. Bruno aligundua hilo, akaona kabisa kwamba huo ndiyo ulikuwa mwisho wake kwani kwa jinsi mzee huyo alivyoonekana, hakuwa na masihara hata kidogo.
Mzee Jumanne alisimama mbali kidogo na nyumba yake, macho yake yalikuwa yakiangalia baharini namna mitumbwi ilivyokuwa ikiingia kijijini hapo baada ya wavuvi kutoka kuvua samaki. Moyo wake ulikuwa na hasira kali, alimchukia Bruno, kati ya watu wote aliotokea kuwafahamu maishani mwake, mwanaume huyo alikuwa mtu wa kwanza kumchukia kwa chuki kubwa moyoni mwake. Alimchukua binti yake, hakupendezwa na jambo hilo kwa sababu tu alikuwa kijana masikini ambaye alikuwa na uhakika kwamba angempeleka mtoto wake kwenye mzigo mzito wa umasikini kitu ambacho hakuwa radhi kukiona kikitokea. Alimkataza Sharifa kuwa na Bruno lakini binti huyo hakutaka kukubali hata mara moja, alimwambia baba yake wazi kwamba kuachana na Bruno lilikuwa jambo lisilowezekana hata kidogo na alikuwa tayari hata kufa lakini si kumwacha mwanaume huyo. Maneno hayo yalimchoma mno mzee Jumanne kiasi kwamba akaona kitu pekee cha kumfanya binti yake aachane na Bruno kilikuwa ni kumuua mwanaume huyo tu. Hakuogopa, alikuwa tayari kukaa gerezani hata kifungo cha maisha lakini si kuvumilia kumuona Bruno akiendelea kuvuta pumzi ya dunia na binti yake aliyekuwa akipendwa na wanaume wengi. Sharifa alimpenda sana Bruno, hakuwa radhi kuona akichukuliwa na mwanaume mwingine, katika maisha yake kila siku alimwambia wazi kwamba ilikuwa ni bora kufa lakini si kuona akiingia kwenye mapenzi na mwanaume mwingine. Mzee Jumanne alijaribu kwa nguvu zote kuwaleta wanaume waliokuwa na pesa kwa lengo la kumchukua binti yake lakini wote hao walishindwa kuuteka moyo wa binti huyo, kwake, hakukuwa na kitu kilichokuwa na thamani zaidi ya moyo wake kwa Bruno. Mzee Jumanne alipanga siku hiyo kuwa ya mwisho kumuonya binti yake kutembea na Bruno, alikuwa na uamuzi mmoja tu kichwani mwake, kumuua mwanaume huyo na yeye kuondoka zake hapo kijijini. Alitulia pembeni kabisa mwa bahari, macho yake hayakuacha kuangalia kule ambapo mitumbwi ilikuwa ikiingia. Alitulia, alimuona binti yake, Sharifa akiwa karibu na bahari, macho ya msichana huyo yalikuwa yakiangalia baharini. Alijua kabisa kwamba Sharifa alikuwa akimsubiri Bruno ili ampokee na kuondoka naye. Wala hazikupita dakika nyingi, mtumbwi wa Bruno ukaanza kuonekana kwa mbali, alijitahidi kujizuia kwani tayari hasira zilikuwa zimempanda na hata panga alilokuwa amelishika lilikuwa likitetemeka kwa kuwa mkono wake ulikuwa ukitetemeka kwa hasira. Akamuona Bruno akiteremka, akamuacha rafiki yake, Abdul na yeye kuondoka na binti yake. Moyo wake ukachoma, hasira zikampanda, akajipa nguvu kwamba alitakiwa kusubiri mpaka watakapoondoka na kwenda huko walipotaka kwenda. Baada ya dakika tano, naye akatoka mahali pale alipokuwa na kuanza kwenda nyumbani kwa Bruno ambapo aliamini kwamba binti yake alikuwa humo. Abdul alimuona mzee Jumanne, hakutaka kuchelewa, akaanza kukimbia kuelekea kwa Bruno kwa lengo la kumwambia kwamba mzee huyo alikuwa njiani akija na panga. Wakati Bruno akijiandaa kukimbia, tayari mzee huyo alikuwa amekwishafika ndani ya kibanda kile huku akiwa na panga lake mkononi. Bruno akabaki akitetemeka, alishikwa na hofu, kwa jinsi mzee Jumanne alivyokuwa akionekana ilionyesha kabisa alikuwa na hasira kali na kama asingefanya harakati za kukimbia mahali hapo basi angeweza hata kumkatakata kwa panga. Hakukuwa na sehemu ya kukimbilia, alitakiwa kupitia palepale mlangoni aliposimama mzee huyo. Alijua kuwa kwa nguvu alizokuwanazo mzee Jumanne asingeweza kumzuia hata kidogo. Hakutaka kujiuliza sana, hapohapo akamvamia kwa kasi, wote wakadondoka, haraka sana Bruno akasimama na kuanza kukimbia. Mzee Jumanne hakutaka kukubali, akasimama na kuanza kumkimbiza kwa panga. Ulionekana kama mchezo au filamu fulani hivi. Bruno alikuwa akikimbia kwa kasi kubwa kwani alijua dhahiri kwamba kama angesimama basi angeweza kukatwakatwa na lile panga. Akaongeza kasi zaidi, kasi ambayo mzee Jumanne hakuweza kumfikia hata kidogo. Mzee huyo akasimama, akashika kiuno huku akihema kama mbwa, macho yake yalikuwa yakimwangalia Bruno aliyezidi kukimbia kuelekea mtaani. Watu wote waliokuwa wakifuatilia tukio lile walishangaa na wengine kucheka kabisa. Walifurahishwa na jinsi mzee Jumanne alivyoinama na kushika magoti, panga lilikuwa chini huku akihema kwa nguvu. Bruno aliendelea kukimbia mpaka alipofika sehemu ambayo alihisi kwamba ilikuwa salama, akasimama na kupumzika. Hakujua ni mahali gani alitakiwa kwenda, alitulia huku akiangalia kila kona kuona kama mzee huyo alikuwa akija au la. Maumivu aliyokuwanayo moyoni mwake hayakuelezeka hata kidogo. Aliumia kuona akimpenda msichana ambaye wazazi wake walimchukia kwa sababu tu ya umasikini aliokuwanao. Siku hiyo hakurudi nyumbani, aliondoka na kuelekea nyumbani kwa rafiki yake, James ambapo akakaa huko na kumwambia kila kitu kilichokuwa kimetokea. Hakutaka kurudi nyumbani kwake kwani alijua kwamba piga ua mzee Jumanne ilikuwa ni lazima kurudi nyumbani hapo kumtafuta. Alikaa huko kwa siku hiyo na baadaye kuonana na Abdul na kutaka kusikia kilichotokea. “Sharifa alipigwa sana na baba yake,” alisema Abdul huku akionekana kuumizwa na kile kilichotokea. “Acha masihara!” “Yule mzee anapiga. Angemuua bila watu kumpoza,” alisema Abdul. “Daah!” “Ila ana msimamo mno. Alipigwa na kupigwa lakini bado alimwambia baba yake kwamba anakupenda na kamwe asingeweza kukuacha, yaani kila mtu alikuwa akishangaa,” alisema Abdul. Moyo wa Bruno ukauma zaidi, kitendo cha kuambiwa kwamba mpenzi wake alipigwa mno na baba yake kisa yeye, kiliuvuruga kabisa moyo wake kwani miongoni mwa vitu ambavyo hakutaka kabisa kuona vikitokea ni kuliona chozi la mpenzi wake. Japokuwa alikuwa nje ya nyumba yake lakini aliendelea kufanya kazi ya uvuvi kama kawaida. Kila siku jioni aliondoka na mtumbwi wa mvuvi mwenzake, James ambapo walikwenda mpaka baharini ambapo huko walikutana na Abdul na kisha kuingia kwenye mtumbwi wake na kwenda kuvua kama kawaida. Akawa akiishi kwa namna hiyo, hata alipokuwa akirudi, alipofika njiani kabisa alikuwa akikutana na akina James, anaingia kwenye mtumbwi wao na kurudi. Alifanya hivyo kwa wiki nzima. Mzee Jumanne hakuwa akijua kilichokuwa kikiendelea, alichoamini ni kwamba Bruno alikuwa amekimbia baada ya kumkosakosa kumkata kwa panga kama alivyokuwa amepanga. Wakati akijipa uhakika kwamba mwanaume huyo alikuwa amekimbia akapata maneno kwamba Bruno alikuwa akiendelea na shughuli zake za uvuvi kama kawaida. “Anafanyaje?” alimuuliza mvuvi mmoja aliyekuwa akiusimamia mitumbwi yake. “Watu wanasema kwamba anaonekana sana tu akivua,” alisema kijana huyo na kuanza kumwambia jinsi Bruno alivyokuwa akiingia baharini. Hilo lilitosha kabisa kumwambia kwamba Bruno aliendelea kuwepo kijijini hapo, alichokifanya ni kumtafuta James na kumwambia kwamba alitaka kufanya naye kazi moja kwa malipo makubwa ambayo asingeamini. “Kazi gani?” aliuliza James. “Umuue Bruno!” “Nimuue Bruno?” “Ndiyo!” “Nitamuuaje?” “Utamchukua kama unavyomchukuaga kwenda baharini, ukifika huko, mtupe baharini!” alisema mzee huyo. “Mmh!” “Unaogopa?” “Hapana! Ila si ataweza kuogelea, sasa akifika nchi kavu itakuwaje?” aliuliza. “Hakikisha siku ya tukio hauonani na huyo Abdul. Mnaondoka naye kwenda mbali kabisa, sehemu ambayo hata mkimtosa baharini, hawezi kupona,” alisema mzee huyo. “Hakuna shida. Kwa hiyo vipi kuhusu mfuko?” “Nawapeni elfu ishirini!” “Sawa.” Hilo halikuwa tatizo, akachukua shilingi elfu ishirini ya Kenya ambayo ilikuwa ni zaidi ya laki nne kwa shilingi ya Tanzania na kumpa. “Basi sawa. Hiyo kazi inafanyika usiku wa leo. Hutoweza kumuona tena,” alisema James. “Sawa. Nitashukuru sana!” alisema mzee Jumanne na kuondoka huku moyo wake ukiwa na furaha tele.
James alikuwa na furaha, hakuamini kama mzee Jumanne angetoa kiasi kikubwa cha pesa kwa kazi ndogo namna ile. Pesa alizopewa kwa upande wake zilikuwa nyingi mno kiasi cha kufanya utekelezaji haraka sana. Huyo Bruno aliyeambiwa amuue wala hakuwa ndugu yake, urafiki wao ulikuwa wa juujuu tu. Hakuona kama kulikuwa na tatizo lolote lile, kwake, kazi hiyo ilikuwa ni ya kutekeleza haraka sana pasipo kujiuliza. Akamwambia mwenzake aliyeitwa Kitula kwamba walitakiwa kufanya kazi ile huku pesa ile wangegawana. Maisha yao walijitahidi kufanya kazi kwa bidii mno, usiku na mchana kwa lengo la kupata pesa, leo huu, pesa ilikuja yenyewe na ni utekelezaji tu ndiyo uliokuwa ukitakiwa kufanyika. Walichokifanya ni kukubaliana kuifanya kazi ile kwa usiku wa siku hiyo kwa kumchukua Bruno na kuondoka naye mpaka mbali kabisa ambapo huko wangemtosa ndani ya maji na wao kuendelea na kazi yao ya uvuvi. Ilipofika jioni, kama kawaida wakamchukua Bruno na kuondoka naye. Hawakutaka kuonekana tofauti, walikuwa wacheshi vilevile, tabasamu yalitawala nyusoni mwao kiasi kwamba Bruno hakuona tatizo lolote lile wala kuhisi kwamba siku hiyo watu hao walitaka kumfanyia kitu kibaya. Wakaondoka mpaka mbali kabisa. Siku hiyo hali ilionekana kuwa tofauti na siku nyingine, kulikuwa na mawimbi mengi yaliyokuwa yakipiga hali iliyoonyesha kwamba bahari ingechafuka baada ya muda mchache. Waliendelea kupiga stori kama kawaida huku James na Kitula wakijifikiria ni kwa jinsi gani wangeweza kumtupa Bruno ndani ya maji na kuondoka zao. Siku hiyo hawakutaka kwenda upande wa Mashariki kama ilivyokuwa siku nyingine, waliondoka na kwenda upande wa Kaskazini ambapo waliamini kwamba wasingeweza kukutana na Abdul. Mtumbwi ulikwenda kwa umbali kama wa kilometa ishirini ndipo wakafika sehemu ambayo ilikuwa na kina kirefu mpaka zaidi ya mita elfu tatu. Waliona sehemu hiyo kuwa sahihi kwa kufanyia ule umafia waliotaka kufanya. Mpaka kufika hapo tayari Bruno alionekana kuwa na hofu, akahisi kabisa kulikuwa na kitu kilichotaka kutokea. Walikuwa wamekwenda kwa umbali mrefu sana pasipo kukutana na Abdul. Haikuwa kawaida, alijua kabisa kwamba kwa umbali fulani hivi walikuwa wakikutana na Abdul na kuingia katika mtumbwi wake lakini kwa siku hiyo mambo yalionekana kuwa tofauti kabisa. “Jamani! Huku tumekuja wapi?’ aliuliza Bruno huku akiwaangalia kwa uso uliokuwa na hofu nzito. “Baharini! Abdul mbona haonekani leo?” alijibu James na kujiuliza, yeye mwenyewe akajifanya hajui. Walizidi kwenda mbele kabisa, walipoona kwamba wamefika sehemu ambayo ni nzuri, hapohapo wakamgeukia Bruno na kuanza kumwangalia. Muonekano wao ulibadilika, hawakuwa kama wale ambao aliwazoea kipindi cha nyuma, walibadilika na kuwa watu wenye muonekano mwingine kabisa. Hilo likamtia hofu Bruno na kuhisi kwamba kulikuwa na kitu kilichotaka kutokea. Hata kabla hajafanya kitu chochote kile, wakamsogelea, wakamshika kinguvu na kumtosa baharini. Bruno alishangaa, hakujua sababu ya watu hao kufanya hivyo. Akabaki akielea ndani ya maji huku akiwaona James na Kitula wakiondoka mahali hapo na mtumbwi wao. Aliwaita, aliwaomba msaada lakini hakukuwa na mtu aliyerudi, wote waliondoka na mtumbwi huku wakipiga kasia ya nguvu kuondoka mahali hapo. Hilo lilimuuma, hakuamini kile kilichokuwa kikiendelea, hakuamini kama watu wale ambao kila siku alikuwa akiwaamini ndiyo waliokuwa wamemfanyia kitu kama kile. Hakutaka kukata tamaa, ilikuwa ni usiku sana, bahari ilitisha, mawimbi makubwa yalikuwa yakipiga kwa nguvu. Alipiga kelele lakini hakukuwa na msaada wowote ule. Kutokana na giza zito lililokuwa mahali hapo ilikuwa vigumu kuona hata hatua saba kutoka pale alipokuwa. Alijua kabisa kwamba siku hiyo ndiyo ungekuwa mwisho wake, alipiga mbizi mpaka mikono ikachoka na kubaki akiwa amekata tamaa kabisa. Alitulia hapo, wakati mwingine alizama, akaibuka na kuendelea kuelea juu ya maji tu. Muda ulizidi kwenda, kikafika kipindi bahari ikaanza kuchafuka, mawimbi makubwa yakaanza kupiga. Akapiga kelele lakini bado hakukuwa na mtu aliyetokea na kumpa msaada wowote ule. Alikuwa peke yake baharini, alipoangalia pande zote, hakukuwa na msaada wowote ule kitu kilichomfanya kuhisi kwamba siku hiyo ndiyo ungekuwa mwisho wake. “Mungu nisaidie,” alisema huku akiwa amekata tamaa. Alimuomba Mungu sana lakini hakukuwa na mabadiliko yoyote yale. Mawimbi yalimpeleka huku na kule, alizamishwa na kuibuliwa, alikunywa maji mengi, alijitahidi kujiokoa lakini akashindwa kabisa mpaka kufikia hatua akajiweka tayari kwa kufa. Alimkumbuka mpenzi wake, Sharifa, hakuamini kama huo ndiyo ungekuwa mwisho wa kumuona msichana huyo mrembo. Yaani kitendo cha kuchukuliwa na kuelekea baharini kilimaanisha kwamba huo ndiyo ulikuwa mwisho wake. “Sharifa mpenzi! Ninakufa pasipo kukuona. Bebi! Ninakufa,” alisema Bruno kwa uchungu mkubwa. Mawimbi yaliendelea kupiga, alikosa nguvu na baada ya dakika kadhaa, akaanza kuzama, alijitahidi kuibuka juu lakini ilishindikana kabisa, baada ya dakika tatu, mwili ukaishiwa nguvu, macho yakaanza kuwa mazito na hatimaye yakaanza kufumba, alijitahidi kujitingisha ili kuona kama alikuwa hai, akashindwa kabisa. Giza likaendelea kujaa machoni mwake na hakujua ni kitu gani kiliendelea baada ya hapo. *** Abdul alikuwa ndani ya mtumbwi wake, macho yake hayakutulia, yalikuwa yakiangalia huku na kule ili kuona kama mtumbwi wa akina James ungefika mahali hapo au la. Mitumbwi mingi ilikuwa ikipita mahali hapo, aliitolea macho kuona kama ilikuwa ni mtumbwi wa akina James lakini haikuwa huo. Moyo wake ulikuwa na hofu tele, kwa jinsi bahari ile ilivyokuwa imechafuka ilionyesha kabisa kwamba hali haikuwa nzuri hata mara moja. Hakwenda kuvua, alikuwa akisubiri, dakika zilizidi kwenda mbele kama kawaida huku akiendelea kuwasubiri watu hao lakini hakukuwa na mtu yeyote ambaye alitokea mahali hapo. Alihisi kwamba kulikuwa na tatizo, akajua kulikuwa na mchezo uliokuwa umefanyika ambao uliwafanya watu hao kuchelewa namna hiyo. Hakukata tamaa, aliendelea kusubiri mpaka ulipofika usiku mkubwa ambapo akaamua kuondoka zake huku akiwa na maswali mengi juu ya nini kilichokuwa kimetokea. Asubuhi ilipofika, alirudi kijijini kama kawaida. Alitaka kuonana na akina James, alitaka kujua ni kitu gani kilikuwa kimetokea mpaka watu hao kutokukutana nao usiku uliopita. Wakati akiwa ameweka mtumbwi wake pembezoni mwa bahari na kuufunga, kwa mbali akauona mtumbwi wa akina James ukija kule alipokuwa. Haraka sana akawafuata huku akiwa na shauku ya kutaka kufahamu ni kitu gani kilitokea. Alipowafikia tu na kuuwaangalia usoni, akabaini kwamba kulikuwa na tatizo lililokuwa limetokea kwani nyuso zao zilionekana kuwa tofauti na siku nyingine, zilikuwa ni sura zenye majonzi tele. “Msiniambie kama kuna jambo baya limetokea,” alisema hata kabla ya salamu. Wanaume hao hawakujibu, walibaki wakimwangalia tu huku kila mmoja akiwa kimya. Ukimya wao ukazidi kudhihirisha kwamba kulikuwa na jambo baya lililokuwa limetokea. Akawauliza kwa mara ya pili ambapo James akaanza kumwambia kwamba Bruno alikufa baharini. “Alikufa baharini?” aliuliza Abdul kwa mshtuko. “Ndiyo! Bahari ilichafuka, si uliona?” “Ndiyo!” “Mtumbwi ukapelekwa huku na kule na hatimaye ukapinduka. Tulijaribu kuogelea, tukaupindua na kuuweka sawa. Yeye alishindwa kuungana nasi, akapelekwa na maji, tulimuita lakini hakutumuona te…” alisema James hata kabla hajamaliza sentensi yake, akanyamza, machozi ya kinafiki yakaanza kujikusanya na kutiririka mashavuni mwake. Abdul hakuamini alichokuwa amekisikia, moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali mno, aliwaangalia akina James, maneno aliyokuwa akiambiwa yalionekana kama si katika ulimwengu halisi uliokuwa ukitokea, alihisi kwamba yupo ndotoni ambapo baada ya dakika kadhaa angeamka na kujikuta akiwa kitandani. Hakujua ni kwa jinsi gani alitakiwa kumwambia Sharifa. Msichana huyo alikuwa akimpenda Bruno kupita kawaida, kitendo cha kumfuata na kumwambia kwamba mpenzi wake, Bruno alikufa baharini aliona kabisa angesababisha maumivu makali moyoni mwa msichana huyo. Hakutaka kabisa kumfuata na kumwambia ukweli lakini baada ya kujifikiria sana, hakuwa na jinsi, alichokifanya ni kumtafuta Sharifa na kumwambia juu ya kile kilichotokea. Hakumwambia moja kwa moja kwamba alikufa baharini, alimwambia kama alivyoambiwa kwamba bahari ilichafuka, alitumbukia ndani ya maji na kupotelea huko kitu kilichomaanisha kwamba mwanaume huyo alikufa humo baharini. “Brunoooo…” Sharifa alijikuta akiita, akaufumba mdomo wake kwa viganja vyake na kuanza kulia kwa maumivu makali. Hakukuwa na kitu kilichotokea kumuumiza kama kitu hicho, kifo cha mpenzi wake kilikuwa na maumivu makali hata zaidi ya ambavyo wangekufa wazazi wake wote wawili. Alilia kwa sauti kiasi kwamba mpaka watu wengine wakabaki wakishangaa. Akaelekea chumbani kwake, hakunyamaza, aliendelea kulia mfululizo mpaka mafua yakampata. Alisikia kitu chenya ncha kali kikiuchoma moyo wake, maumivu aliyokuwa akiyasikia kipindi hicho hayakusimulika hata kidogo. Wakati Sharifa akiwa analia, upande wa pili baba yake baada ya kupewa taarifa kwamba Bruno alikuwa amekufa baharini moyo wake ukawa na furaha, hakuamini alichokisikia, alitabasamu na kumpongeza James kwa kazi nzuri aliyokuwa ameifanya. “Amekufa kweli?” aliuliza. “Ndiyo! Usiku bahari ilichafuka sana, mawimbi makubwa, yaani sikuwahi kuona hali kama ile tangu nizaliwe. Kwenye mawimbi hayohayo, mbali kabisa na bahari, tukamtosa majini, ataponaje hapo,” alisema James na wote kuangua kicheko. Kwao ilikuwa ni furaha tele, hakukuwa na mtu aliyehuzunika, mioyo yao ilikuwa na furaha kwamba hatimaye walikuwa wamefanikiwa kummaliza mwanaume huyo aliyeonekana kuwa mwiba mkali moyoni mwa mzee Jumanne. Hicho ndicho kilikuwa kipindi kibaya kwa Sharifa, kila siku alikuwa mtu wa kulia tu, moyo wake ulichoma, kila siku asubuhi alipokuwa akiamka alikwenda mpaka ufukweni na kusimama karibu kabisa na bahari na kuanza kuyaangalia maji. Hakuamini kama bahari hiyo ndiyo iliyommeza mpenzi wake aliyempenda kwa mapenzi ya dhati. Kifo cha Bruno kilisikika kila kona, kila mtu alimuonea huruma msichana huyo kwani mapenzi aliyokuwanayo moyoni mwake yalikuwa makubwa mno. Wengi hawakutaka kukutana naye kwani kwa jinsi alivyokuwa na huzuni, kila aliyekutana naye alikuwa akilia, Sharifa alisikitisha kupita kawaida. Wiki ya kwanza ikakatika, ya pili, ya tatu mpaka mwezi. Bado mwili wa Bruno haukupatikana. Alichokifanya Sharifa ni kwenda kuchimba kaburi kisha kuzizika nguo za mpenzi wake, Bruno kama ishara ya kumzika mwanaume huyo. “Nitakupenda maisha yangu yote hata kama umekufa. Siwezi kuolewa, siwezi kuwa na mwanaume mwingine tena,” alisema Sharifa huku akiwa kwenye kaburi hilo la mpenzi wake ambapo ndani yake kulikuwa na nguo tu.
Biashara ya madawa ya kulevya iliyokuwa imeshamiri duniani kote ilianza kuyumba. Kila mtu aliyekuwa akiifanya biashara hiyo alishangaa, mizigo mingi ilikuwa ikikamatwa, watu waliokuwa wakisafirisha ambao walijulikana zaidi kama punda walikamatwa na kufungwa gerezani huku wakipewa mateso makubwa. Marekani iliamua kuingia kazini, haikutaka kuona biashara hiyo ikiendelea kufanyika kwa kuwa watu waliokuwa wakiathiriwa zaidi walikuwa vijana ambao ndiyo walikuwa nguvu kazi ya taifa. Iliingia kazini rasmi, wasafirishaji waliokuwa wakipitia mipakani walikuwa wakikamatwa, Wamexico ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kusafirisha madawa na kuingiza nchini humo walikamatwa na kufungwa gerezani tena huku wakipewa mateso makali. Hali ilitisha, biashara iliyumba kupita kawaida. Wamarekani walichukiwa kwa kuwa walijifanya kimbelembele kuhakikisha kwamba wanazilaghai serikali za nchi nyingine kuhakikisha biashara hiyo inapotea haraka sana vinginevyo nchi ambayo ingepuuzia ingetolewa katika Umoja wa Mataifa. Hilo ndilo lililozifanya nchi nyingine kuwa makini na kutumia nguvu kubwa katika kuhakikisha wanatokomeza biashara hiyo iliyokuwa ikiwatesa sana vijana waliokuwa wakitumia. Ndani ya miezi sita tu, biashara ililala kwa kiasi kikubwa sana kiasi kwamba kila mmoja akahisi kwamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wa biashara hiyo haramu. Miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa waliokuwa wakifanya biashara hiyo walikuwa Samuel Maxwell aliyekuwa na umri wa miaka hamsini na mbili na Richard Todd aliyekuwa na miaka hamsini na nane. Wawili hao walikuwa mabilionea wakubwa nchini Marekani, Todd alikuwa na utajiri wa dola bilioni ishirini na nne ambazo zilikuwa ni zaidi ya shilingi trilioni arobaini na nane huku Maxwell akiwa na utajiri wa dola bilioni ishirini ambazo zilikuwa ni zaidi ya shilingi trilioni arobaini. Japokuwa walikuwa na biashara nyingi zilizokuwa zikiwaingizia pesa lakini biashara kubwa zaidi ambayo iliwafanya utajiri wao kukua kila siku ni biashara ya madawa ya kulevya waliyokuwa wakiifanya. Waliuziana madawa, walifanya biashara kama ndugu, walipendana kiasi kwamba mpaka mabilionea wengine wakashangaa kwani hawakuwahi kuwaona mabilionea ambao walikuwa wakishirikiana vizuri katika biashara zao kama wawili hao. Wakati Marekani ilipoanza kuleta figisufigisu katika biashara hiyo ndipo wawili hao wakatokea kugombana na kuonana kama paka na panya na chanzo kikubwa kikiwa ni biashara hiyohiyo ya madawa ya kulevya. Wakati watu wakihitaji sana madawa hayo na Todd kujiona kwamba hana kitu, haraka sana akawasiliana na Maxwell na kumwambia kuhusu mkakati wake ambao angeufanya kuhakikisha anapata mzigo na kuupeleka barani Afrika ambapo kulikuwa na uhitaji mkubwa wa madawa hayo. Maxwell hakuona kama kulikuwa na tatizo, alimwamini Todd, walikuwa wakifanya biashara hiyo kwa miaka mingi. Akampa mzigo wa dola bilioni mbili kwa lengo la kuupeleka Afrika na kufanya biashara hiyo na kumpelekea pesa zake. Todd akachukua mzigo na kwenda nao Afrika. Hakutaka kumwamini mtu yeyote, alitaka kuusafirisha yeye kama yeye na kuufikisha nchini Msumbiji salama kabisa. Akawasambazia watu wake na kuondoka zake. Alitegemea kupata pesa zake baada ya wiki mbili ambapo biashara hiyo ingekuwa imefanyika kikamilifu lakini kitu cha kushangaza kabisa, mpaka wiki mbili zinakatika bado hakuwa amepata pesa hizo alizoambiwa kwamba angepata. Kuwaamini watu wengine kukamgharimu, alikuwa akiwasiliana nao kwenye simu lakini bado watu hao hawakuwa wakipokea, hilo lilimchosha sana, lilimfanya kufadhaika kwa kuwa mzigo ule haukuwa wake, alikopeshwa na kuahidi kulipa pesa hizo mara baada ya biashara kufanyika. Waafrika wakamuingiza choo cha kike, hawakumlipa pesa zake. Kila siku Maxwell alikuwa akimpigia simu na kumwambia kuhusu pesa zake, hakujua ni kitu gani alitakiwa kumwambia kwani kama angemwambia ukweli kuwa hakuwa amelipwa, angeonekana tapeli na muongo mkubwa. Baada ya kukatika mwezi, Maxwell akachoka kufuatilia, japokuwa walikuwa marafiki lakini kwenye ishu ya pesa akaamua kuuweka urafiki pembeni na kuanza kumdai kibabe. Hilo halikumshangaza Todd, alijua dhahiri kwamba kuna siku kitu kama hicho kingetokea, alichomwambia ni kuendelea kusubiri kwani bado aliendelea kuwakumbusha watu hao kuhusu pesa zake. Akili yake ikavurugika, miezi miwili bila kulipwa kukamfanya kupaniki na hivyo kupanga kusafiri mpaka nchini Msumbiji kwa lengo la kwenda kuwaambia watu wake wamlipe. Wakati yeye akipanga kusafiri kwenda huko, Maxwell hakutaka kumuacha, aliona kabisa kwamba alikuwa akienda kutapeliwa. Hakuangalia tena urafiki, hakuangalia ni kwa kipindi gani walikuwa pamoja, alichokifanya ni kutuma watu kwenda kumteka, wamtese sana na awahamishie kiasi cha pesa alichokuwa akidaiwa katika akaunti yake. Vijana wakaondoka mpaka nchini Msumbiji. Walipofika, wakamwambia Todd kwamba aandae meli ambayo hapo ingewachukua mpaka Nigeria ambapo huko ndipo walipopanga kufanya mauaji hayo. Hilo halikuwa tatizo kwani kabla ya wao kwenda huko, tayari meli yake ya mizigo ilikuwa imeandaliwa kwa kufanya kazi hiyo na kipindi hicho ilikuwa ikitoka Afrika Kusini. Ilipofika, wakaambiwa kwamba imefika na hivyo kilichotakiwa kufanywa ni utendaji kazi kuhakikisha kwamba wanampata mwanaume huyo. “Mtafuteni mtu anayeitwa Robson Mautinho, huyo ndiye mtu aliyepewa mzigo huo, hakikisheni mwanaume huyo anapatikana,” ilisikika sauti ya Maxwell kwenye simu. Hilo ndilo lililofanyika, kumpata mwanaume huyo halikuwa jambo gumu kwa kuwa alijulikana kutokana na utajiri wake mkubwa. Walipoonana naye, hawakutaka kumficha, walimwambia kuhusu mpango wao wa kummaliza mwanaume huyo. Kwa Mautinho ilikuwa habari njema kwake, alikuwa akidaiwa pesa nyingi na hakuwa na mpango wa kuumlipa mzee Todd hivyo alivyoambiwa kwamba watu hao walikuwa na mpango wa kumteka, kwake ilikuwa ni furaha tele kwani kama wangemuua ilimaanisha kuwa asingesumbuliwa tena na mwanaume huyo. “Hakuna tatizo. Ameniambia kwamba kesho atakuja tuzungumze,” alisema Mautinho. “Basi sawa. Waambie vijana wako wamteke, wamfunge sehemu na tutakuja kumchukua mtu wetu,” alisema kijana mmoja aliyeitwa Phillip. “Sawa.” Hilo ndilo lililofanyika, siku iliyofuata, wakati mzee Todd amefika mahali hapo, akaanza kuzungumza na Mautinho na baada ya kumaliza mazungumzo, akajikuta akizungukwa na vijana wa mwanaume huyo, cha kwanza kilikuwa ni kuwaua walinzi wake aliokwenda naye na yeye kufunikwa uso wake na kitambaa kilichokuwa na umbo la kikapu. Hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, alijaribu kuuliza lakini mwanaume huyo hakumwambia kitu chochote kile. Akaamrisha apelekwe kwenye chumba kimoja cha giza na kuhifadhiwa humo. Alichanganyikiwa, alijiona kugeukiwa, akilini mwake hakuhisi kabisa kama Maxwell ndiye aliyefanya hivyo, alichoamini ni kwamba Mautinho ndiye aliyeamua kuucheza mchezo ule ili amtapeli pesa zake alizokuwa akimdai. Usiku mzima alikuwa akilia tu, moyo wake ulimuuma mno, akahisi kabisa kwamba watu hao walikuwa wakitaka kumuua. Kufa kwake halikuwa tatizo, ila tatizo lilikuwa ni kuiga familia yake tu. Alikuwa na mke aliyeitwa Juddie na mtoto wake wa kike aliyeitwa Martha. Kwake, kufa pasipo kuiaga familia yake alihisi ni maumivu mazito mno. Katika chumba alichokuwa amewekwa, hakikuonekana kuwa kizuri hata kidogo. Kilikuwa kichafu kilichokuwa na harufu ya damu. Hakupigwa, hakufanywa lolote lile lakini kukaa ndani ya chumba kile kulimfanya kuhisi mateso makubwa kupita kawaida. Ilipofika usiku, mlango ukafunguliwa na wanaume wawili kuingia, wakamchukua huku wakiwa wamemfunga kitambaa machoni na kuondoka naye. Hakujua alipokuwa akipelekwa ila alijua kwamba hakukuwa sehemu nzuri na kwa katika kipindi hicho ilikuwa ni lazima kuuawa. Aliingizwa ndani ya gari na kuondoka mahali hapo. Baada ya dakika kadhaa, akashushwa na kupelekwa sehemu huku akiwa ameshikwa na watu wawili kushoto na kulia. Akapelekwa sehemu iliyokuwa na ngazi na kuanza kupandishwa. Mlango ukafunguliwa na kuingizwa ndani ya chumba kimoja na kuwekwa humo. Hapo, kwa mbali alisikia kelele za watu wakicheka huku wengine wakigongesheana glasi, kwa jinsi vicheko vilivyokuuwa vikisikika ilionyesha kabisa kwamba walikuwa kwenye maisha ya raha kupita kawaida. Baada ya dakika kadhaa, honi ikaanza kupigwa, haikuwa ya gari wala treni, aliposikia vizuri ilikuwa ni honi ya meli, hapo akagundua kwamba alikuwa ndani ya meli ambayo hakujua ilikuwa ikielekea wapi, ndani ya dakika chache akaisikia ikianza kuondoka mahali hapo. Alichokifanya ni kutoa kitambaa kile usoni mwake. Chumba kilikuwa na mwanga hafifu, alibaki akiangalia huku na kule, hakujua mlango ulikuwa mahali gani. Akasimama na kuanza kuzunguka huku na kule, bahati nzuri kwake akagusa kitu ambacho alijua kabisa kilikuwa ni kama kitasa cha kufungua mlango wa kutokea ndani ya chumba hicho. Humo ndipo alipotakiwa kukaa mpaka atakapofikishwa mbali kabisa, Nigeria ambapo alitakiwa kuuawa. Hakujua mahali alipokuwa, na wala hakujua mahali ambapo meli hiyo ilipokuwa ikielekea. “Mungu naomba uniokoe! Naomba uniokoe Mungu,” alisema mzee Todd ndani ya chumba kile. Moyo wake uliogopa na muda wowote ule alihisi kwamba angeuawa na watu waliokuwa wamemchukua.
Maisha ya Sharifa yalibadilika na kuwa kama mtu aliyekumbwa na msiba mzito. Hakuwa na furaha, maisha yake aliyaona kuwa na giza kubwa mbele yake, moyo wake uliuma na kuuma, alilia usiku na mchana lakini machozi yake hayakuweza kumrudisha Bruno katika upeo wa macho yake. Kila siku ilikuwa ni lazima kwenda kwenye kaburi la mpenzi wake na kukaa huko, alikuwa mtu wa kulia huku muda mwingi akimlaumu baba yake kwamba ndiye aliyesababisha hayo yote. Bruno kutokuwa na pesa, kikabadilisha kila kitu, maisha yake yakaonekana kuwa si lolote na hata yule mpenzi aliyekuwa akimpenda aliambiwa aachane naye. Yote aliyokuwa akiyakumbuka yaliuumiza moyo wake, Sharifa aliumia kupita kawaida. Wakati mwingine alimuuliza Mungu kwamba kwa nini alizaliwa na baba yake, alitamani hata angezaliwa na mtu mwingine ambaye angemsapoti katika uhusiano wake na Bruno. Hakutaka kula, alikuwa kwenye maombolezo mazito. Mzee Jumanne hakujali, alichokuwa akikiangalia ni kuona mtoto wake akiachana na Bruno ambaye tayari muda huo alihesabika kama marehemu. Siku zikakatika, baada ya miezi mitatu, nyumbani kwa mzee Jumanne kukatokea ugeni kutoka jijini Nairobi, ugeni wa mzee Mohammed Olioh na ulifika hapo kwa kuwa walitaka kuzungumza mambo mengi kuhusu watoto wao. Mzee Olioh alikuwa mtu mwenye pesa zake jijini Nairobi. Alimiliki mabasi kadhaa yaliyokuwa yakifanya safari zake kwenda Tanzania, Uganda na mengine kwenda mpaka Rwanda. Alikuwa na pesa nyingi, aliheshimika kupita kawaida. Maishani mwake alibahatika kupata mtoto mmoja tu, aliyeitwa Rahman ambaye kipindi hicho alikuwa nchini Marekani akisomea sheria katika Chuo cha Kikuu cha Mississippi. Kipindi hicho Rahman alikuwa akijiandaa kurudi kutoka chuoni na kitu kimoja alichohitaji ni kutafutiwa mwanamke wa kuishi naye. Mtu ambaye alikuja kichwani mwa mzee Olioh ni msichana Sharifa aliyekuwa akiishi katika Kijiji cha Guolduvai kilichokuwa pembeni mwa bahari ya Hindi. Alimfahamu msichana huyo, alikuwa mrembo na baba yake alikuwa na heshima kubwa huko alipokuwa akiishi. Alichokifanya ni kuondoka na kuelekea huko. Alipofika, akaonana naye na kuanza kuzungumza naye. Alimwambia ukweli kuhusu mtoto wake aliyekuwa akitarajiwa kurudi nchini Kenya. Mzee Jumanne alipoambiwa hivyo, alishtuka, hakuamini kama mzee huyo angemfuata na kumwambia kitu kama hicho. Kumshawishi mtoto wake halikuwa tatizo, aliamini kwamba angekubaliana naye kwa sababu mtu aliyekuwa akimpenda, Bruno wakati huo alikuwa marehemu. Akamwambia mzee Olioh kwamba hakutakiwa kuhofia kitu chochote kwani yeye kama mzazi angezungumza na Sharifa na bila shaka msichana huyo angekubaliana naye. Mzee Olioh akaondoka kurudi jijini Nairobi huku akiwa na mategemeo mengi kwamba Sharifa angekubali na hivyo kuolewa na kijana wake. Huku nyuma, mzee Jumanne alikuwa na kazi kubwa ya kuzungumza na binti yake. Alijua kabisa kwamba alikuwa kwenye maumivu makali lakini hakutaka kuona akimkataa Rahman, ilikuwa ni lazima akubali kwa kuwa alitoka katika familia iliyokuwa na pesa. Sharifa alipoambiwa, akashtuka, hakuamini kama baba yake alifikia hatua ya kumtafutia mwanaume wa kumuoa. Hilo lilimuumiza mno moyoni mwake na bila kificho alimwambia baba yake kwamba hawezi kuolewa na mwanaume huyo. “Ila ana pesa! Anasoma Marekani!” alisema mzee Jumanne. “Siwezi kuolewa. Siwezi kuolewa na mwanaume yeyote baba,” alisema Sharifa huku akimwangalia baba yake. “Huoni kama umri unakwenda tu binti yangu?” “Kama unaona umri unakwenda, ungemkubali Bruno anioe, umeona amekufa ndiyo unakuja na kuniambia kwamba umri unakwenda. Kwa taarifa yako siolewi,” alisema Sharifa huku akimwangalia baba yake. Huo haukuwa muda wa kuogopa tena, alimwambia baba yake wazi kwamba hakutaka kuolewa na mwanaume huyo. Mzee Jumanne hakusema kitu, akakubaliana na mtoto wake na kuondoka. Alikwenda mpaka chumbani kwake, alivimba kwa hasira, hakuamini kama Sharifa angekataa kufanya kile alichotaka akifanye. Yeye ndiye alikuwa mzazi, sasa kwa nini amkatalie kuolewa na mwanaume aliyekuwa akimtaka? “Nitatumia mabavu kama mzazi! Si anakataa kwa hiari, sasa ataolewa kwa lazima,” alisema mzee Jumanne,. Alichokifanya ni kumpigia simu mzee Olioh na kumwambia kwamba kila kitu kilikuwa tayari, alizungumza na binti yake na kukubaliana naye na hivyo walitakiwa kupanga tarehe ya kufunga ndoa kijijini hapo. Haraka sana mzee huyo alipoambiwa hivyo, akampigia simu kijana wake nchini Marekani na kumwambia kile kilichojiri kwamba msichana waliyekuwa wamemchagulia alikubali kuolewa naye na hivyo alitakiwa kurudi Kenya haraka sana mara baada ya kumaliza mitihani. “Amekubali?” aliuliza. “Ndiyo! Haikuwa kazi kubwa.” “Ila ni binti mzuri?” “Niamini! Siwezi kumchagulia kijana wangu binti mbaya! Ni mzuri kama mama yako alivyokuwa kijana,” alisema mzee Jumanne na kuanza kucheka. “Sawa. Nilindieni mke wangu! Nikija tu ni ndoa na kuendelea kufanya mambo yangu,” alisikika Rahman. “Sawa. Hakuna shida.” *** Safari baharini ilikuwa ikiendelea, mabaharia walikuwa wamelala kwa kuwa usiku mzima walikuwa wamekunywa pombe kali. Ndani ya meli hiyo iliyokuwa na watu kumi na sita ni watu wawili tu ndiyo ambao hawakuwa wamelala, nahodha, mzee Sam Maskovich na mzee Todd aliyekuwa katika chumba alichohifadhiwa. Meli iliendelea kukata mawimbi, hapo walipokuwa, hakukuwa na nchi kavu yoyote iliyokuwa ikionekana. Meli ilikuwa katikati ya bahari ikiendelea na safari yake. Macho ya Maskovich yalikuwa mbele kabisa, alikuwa akiangalia kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Alichoka mno lakini hakuwa tayari kulala, yeye ndiye alikuwa kila kitu katika safari hiyo. Wakati akiendesha meli hiyo, pembeni kulikuwa na chupa ya pombe ambayo ndiyo ilikuwa ikimuweka sawa kila alipokuwa akisikia usingizi. Muda ulizidi kwenda mbele mpaka pale alipokiona kitu kikiendelea juu ya maji. Hakujua ni kitu gani, haraka sana akachukua darubini na kuanza kuangalia kwa karibu, alichokiona ni mwanaume akiwa anaelea juu ya maji. Alishtuka, hakujua ni kitu gani kilikuwa kimeendelea mpaka mwanaume huyo kuwa hapo. Alichokifanya ni kuwaamsha wenzake na kuwaambia kile kiliichokuwa kikiendelea. Wote wakaamka na kuangalia mbele, kweli walimuona mwanaume akiwa anaelea juu ya maji. “Chukueni boya,” alisema mzee Maskovich. Boya moja la duara lililofungwa kamba ngumu likachukuliwa na kutupwa baharini, mwanaume mmoja naye akajitosa baharini na kuanza kumfuata mtu huyo kule alipokuuwa. Alipomfikia, akamshika na kuwaambia wenzake wavute boya kitu ambacho kilifanyika kwa haraka sana. Mtu aliyekuwa kwenye maji akaokolewa na kuwekwa ndani ya meli, alikuwa Bruno ambaye hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea mahali hapo. Tumbo lake lilikuwa kubwa, alikunywa maji mengi, ngozi yake ilikuwa laini sana huku ikiwa inateleza kutokana na muda mwingi kuwa ndani ya maji. Huduma ya kwanza kabisa waliyompa ni kumlaza kifudifudi na kuanza kuukandamiza mgongo wake kwa lengo la kuyatoa maji aliyokuwa amekunywa. Hiyo ilisaidia kwani baada ya kukandamizwa mara kadhaa, maji yakaanza kutoka, walipohakikisha kwamba wamemaliza, wakamchukua na kumpeleka kitandani kupumzika. Kila mmoja alikuwa na maswali mengi, walijiuliza kuhusu mwanaume huyo, alikuwa nani na alikuwa akifanya nini mpaka kuwa baharini hapo. Wengi wakahisi kwamba inawezekana alikuwa kwenye meli na wenzake na meli kuzama. Wakaangalia mahali pale ili kuona kama wangeweza kuwaona watu wengine lakini hawakufanikiwa. Walipomaliza kumpa huduma ya kwanza, wakamchukua na kumpeleka katika chumba alichokuwemo mzee Todd na kumuacha humo. Mzee huyo alishtuka, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, alimwangalia kijana aliyekuwa ameletwa, hakuwa na fahamu, alionekana kuwa kwenye hali mbaya kwani hata kwa jinsi ngozi yake ilivyokuwa, ilionyesha alikuwa kwenye mateso makali ya kupigwa baridi. Akamsogelea pale chini alipokuwa na kuyasikiliza mapigo ya moyo wake, yalikuwa yakidunda kwa mbali sana hali iliyomfanya kugundua kwamba mwanaume huyo alikuwa hai. “Kwa nini wamemleta humu? Naye ni mateka au?’ alijiuliza mzee huyo huku akimwangalia Bruno aliyekuwa hapo chini. Hiyo ilikuwa siku ya kwanza, hakurudiwa na fahamu japokuwa alionekana kuwa hai. Vijana wa meli hiyo walikuwa wakiingia mara kwa mara ndani na kumwangalia kama alikuwa ameamka au la. Kila walipoingia, bado Bruno alionekana kuwa vilevile kama alivyokuwa kipindi cha nyuma. Walimuokoa kutoka baharini lakini baada ya kuona kwamba amechukua muda mrefu pasipo kurudiwa na fahamu, wakajadiliana ni kitu gani wafanye, wakakubaliana kwamba wamtupe baharini kwani tayari alionekana kuwa mzigo. “Tumtupe? Hakuna! Siwezi kukubaliana na kitu hicho,” alisema mzee Maskovich huku akiwaangalia watu hao. “Lakini amekufa!” “Bado mapigo yake ya moyo yanadunda.” “Lakini haamki! Inawezekana ndiyo hatua zake za mwisho kuishi ndani ya dunia hii,” alisema mwingine. “Hata kama. Tusubiri, kama kweli yeye ni wa kufa, atakufa na sisi kumtupa. Tumemuokoa, hebu tufanyeni lolote kuionyesha dunia kwamba tuna upendo wa ajabu,” alisema nahodha huyo maneno ambayo yaliingia kichwani mwa kila mtu. Siku nyingine ilipoingia ndipo Bruno akarudiwa na fahamu, akaanza kuwa kuyafumbua macho yake na kuangalia huku na kule. Alishangaa, alikumbuka kwamba mara ya mwisho alikuwa ndani ya bahari huku mawimbi yakimpeleka huku na kule na hatimaye kuzama, ila kilichotokea baada ya hapo, hakukijua. ”Nipo wapi?” lilikuwa swali la kwanza kabisa alilouliza mara baada ya kufumua macho na kumuona mwanaume mmoja akiwa amekaa pembeni yake. “Who the hell are you?” (wewe ni nani?) aliuliza mzee Todd. Aliposikia hivyo tu akajua kwamba mtu huyo alikuwa Mzungu, hivyo naye alitakiwa kuongea Kiingereza japokuwa kwa elimu yake ya kidato cha nne hakuwa akiifahamu vizuri. “Bruno!” alijibu huku akijitahidi kujinyanyua kutoka pale alipokuwa. “Bruno?” “Help me! I’m hungry…give me food, pleaseee…” (nisaidie! Nina njaa, naomba chakula tafadhali) alisema Bruno. “Want some food huh?” (unataka chakula huh?) “Yeah! Help me! Hunger is killing me,” (ndiyo! Nisaidie! Njaa inaniua) alisema Bruno huku akimwangalia mzee huyo kwa jicho lililokuwa la huruma kupita kawaida. Alichokifanya mzee huyo ni kusimama na kisha kuanza kupiga mlango kwa nguvu huku akiita kwa sauti. Hiyo ilisaidia, baada ya sekunde chache, mlango ukafunguliwa na kijana mmoja ambaye baada ya kuingia tu akamwambia kwamba kijana yule alizinduka na alikuwa na njaa kali. “Nakuja!” Kijana yule akaondoka, kule alipokwenda, akawaambia wenzake, vijana wanne wakaelekea kule huku wakiwa na chakula, walipofika, wakampa na Bruno kuanza kula kwa pupa kwani alihisi kama asingekula ndiyo ungekuwa mwisho wake. “Want some more?” (unataka kingine?) “Yeah!” Akaletewa, alikula na kula, baadaye akapelekewa soda na kunywa. Kidogo tumbo lake likapata nafuu na nguvu kuanza kurudi upya. Aliwaangalia vijana waliokuwa wamesimama mbele yake, hakujua ni wakina nani na hakujua ni kitu gani kilitokea. Vijana hao wakamnyanyua na kuondoka naye mpaka kwa wenzao, wakamuweka kati na kuanza kumuuliza sababu ya kuwa baharini. Hakutaka kuficha, alisimulia kila kitu, historia yake iliwakera watu wote kwa sababu kuchukiwa kwa mtu kisa umasikini kilikuwa kitu kibaya sana. “Pole sana! Kwa hiyo huna pa kwenda?” “Sina! Kama mtaweza, naomba mnirudishe!” alisema Bruno. ITAENDELEA
Simulizi : Mvuvi Bruno (Bruno The Fisherman) Sehemu Ya Pili (2) Kila mmoja alibaki akimshangaa Bruno, hawakuamini kama kungekuwa na mtu aliyekuwa radhi kumuua mtu mwingine kwa kumtosa baharini tu kwa kuwa upande wa pili kulikuwa na mzazi ambaye hakutaka binti yake aolewe na mwanaume huyo. Kila mmoja akahisi kwamba alikuwa akidanganywa, kitu walichohisi ni kwamba Bruno alikuwa mmoja wa waharamia waliokuwa wakiteka meli baharini kwa kushirikiana na makundi ya Kisomali. Walikwishawahi kukutana na watu wa namna hiyo, walikuwa wana roho mbaya, walitoa roho za watu pasipo kujali kama walikuwa watu wema, wachungaji au mashehe. Walimwangalia Bruno, kwa jinsi mikono yake ilivyojazia kutokana na kupiga sana kasia, wakahisi kabisa kwamba huyo alikuwa mmoja wa watu hao. Wakaanza kuongea pembeni kwamba ilikuwa ni lazima Bruno auawe kwani waligundua kwamba kile alichokuwa akikizungumza hakikuwa na ukweli wowote ule, aliwadanganya kwa kuwa tu alihitaji msaada kutoka kwao. Wakamchukua na kumrudisha ndani ya kile chumba, alibaki humo akiwa kimya, hakuzungumza na mzee Todd aliyekuwa pembeni ambaye naye alikuwa akishangaa sababu ya kijana huyo kupelekwa katika chumba kile kilichoonekana kuwa na mateso makubwa. “Why are you here?” (kwa nini upo hapa?) aliuliza mzee huyo huku akimwangalia Bruno. “My friends tossed me,” (marafiki zangu walinitosa) “Why did they do that?” (kwa nini walifanya hivyo?) Bruno hakuficha, alimwambia mzee Todd kila kitu kilichotokea kwa kuamini kwamba kwa kusema ukweli vile basi angeweza kuonewa huruma. Kwa mzee huyo, hata naye jambo hilo halikumuingia hata kidogo, alibaki akimwangalia Bruno kwa macho yaliyoonyeshwa kutokuridhishwa na majibu yake kabisa. “So, he sent people to toss you in the sea?” (kwa hiyo aliwatuma watu wakutose baharini?) aliendelea kudadisi mzee huyo. “Yeah! I am a poor. I have nothing, her parents dinied me to marry her!” (ndiyo! Mimi ni masikini. Sina kitu, wazazi wake walikataa nimuoe) alisema Bruno. Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa watu hao kuonana. Walizungumza mambo mengi huku mzee Todd akimwambia Bruno matatizo yote aliyokuwa akipitia na kwamba alikuwa njiani kuuawa na watu hao. Moyo wake ulimuuma, hakuogopa kufa bali kitu alichokuwa akikiogopa ni kuiona familia yake, mkewe Juddie na mtoto wake, Martha wakipata maumivu makubwa moyoni mwake. Muda ulizidi kwenda mbele, walikuwa ndani ya chumba kile, kila mmoja alifikiria kifo, walijua kabisa kwamba ilikuwa ni lazima wanaume wale wawamalize na kuondoka zake. Akili ya Bruno ilikuwa ikicheza kwa kasi, hakutaka kuona akifa, hakutaka kuona akipotea na mpenzi wake, Sharifa kujua kwamba alikufa, kama mwanaume, alitakiwa kupambana kuhakikisha kwamba anatoka salama ndani ya meli ile. Akasimama na kuanza kuzunguka huku na kule, macho yake yaliangalia kila kona, alitaka kujua ni mahali gani ambapo wangepatumia ili kutoroka ndani ya meli ile. Mzee Todd alimwambia kwamba alitakiwa kuuawa. Alijua fika kwamba mauaji yangefanyika baada ya meli kuvuka Afrika Kusini ambapo ilikuwa ni lazima meli ikaguliwe sana. Alimwambia hilo mzee huyo na kugundua kwamba kifo chake kingetokea baada ya kuvuka hapo Afrika Kusini katika bandari ya Cape Town ambayo hujulikana kama Table Bay ikiwa na maana ya Ghuba yenye mfanano wa meza. “Tuna siku mbili mpaka kuingia Afrika Kusini. Na kutokana na muda huo itakuwa ni lazima tuwe tumekwishapata majibu kabla ya kuingia katika nchi hiyo!” alisema Bruno. “Sawa. Ngoja nijifikirie!” *** “Innocent! Where are you?” (Innocent! Upo wapi?) “At home!” (nyumbani) “Did you contact with him today?” (uliwasiliana naye leo?) “Who?” (nani?) “Mr. Todd.” “No! Do you want me to contact him?” (Hapana! Unataka niwasiliane naye?) “Yeah!” Innocent ambaye alipigiwa simu na mke wa mzee Todd akachukua simu yake na kumpigia mzee huyo, simu haikuwa ikipatikana, hakuacha kumpigia zaidi na zaidi lakini majibu yalikuwa yaleyale kwamba mzee huyo hakupatikana. Haraka sana akampigia mtu aliyekuwa amempigia ambaye alikuwa ni mke wa mzee huyo, Juddie na kumwambia kwamba hakuwa akipatikana hivyo kumwambia kwamba waonane. Mwanamke huyo alikuwa na hofu kubwa moyoni mwake, hiyo ilikuwa inakatika siku nzima mumewe hakuwa akipatikana katika simu. Hilo lilimfanya kuwa na hofu kubwa, alimpigia simu zaidi na zaidi lakini majibu yalikuwa yaleyale. Hakuishia kumpigia kijana Innocent ambaye alikuwa mmoja wa vijana waliokuwa wakifanya kazi nyingi za mume wake, akawapigia wengine lakini nao hawakuwa wamewasiliana na mzee huyo na mbaya zaidi hata wale vijana aliokuwa amekwenda nao nchini Msumbiji hawakuwa wakipatikana. Hapo ndipo taarifa zikatolewa polisi ambao waliwasiliana na polisi wa Msumbiji kwa kupitia kitengo cha Interpol ambapo taarifa za awali zilisema kwamba kweli mwanaume huyo aliingia nchini humo kwani hata ndege yake ilikutwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maputo. “Sasa atakuwa wapi?” lilikuwa swali alilouliza mkewe. “Hata sisi hatufahamu chochote kile. Ngoja tufuatilie halafu tutakupa taarifa,” alisikika Innocent ambaye aliamua kusafiri mpaka Msumbiji kujua ukweli wa kile kilichokuwa kimetokea. Ilikuwa ni lazima kujua mahali bwana Todd alipokuwa. Ndege yake ilikuwa katika uwanja wa ndege, je, yeye mwenyewe alikuwa wapi? Walichokifanya ni kumtafuta rubani wake, kumpata haikuwa shida kwani alipouliziwa tu, alipatikana katika hoteli moja ya kifahari. Alipoulizwa kuhusu mzee huyo, hakufahamu kitu, aliwaambia kwamba alifika na mzee huyo mpaka nchini Msumbiji ambapo akamwambia akakae kwenye hoteli ile huku akilipia kila kitu. “Kwa hiyo hata wewe hujui yupo wapi?” “Sijui! Ndiyo kwanza mmeniambia nyie.” Polisi nchini Msumbiji wakaanza kuhaha kumtafuta mzee huyo, kila kona walipokuwa wakiuliza, hakukuwa na mtu aliyekuwa akifahamu ukweli. Zawadi nono ikawekwa kwa mtu yeyote ambaye angefanikisha kupatikana kwa mwanaume huyo lakini napo haikusaidia. Kikafika kipindi ambacho serikali ya Msumbiji ikahisi kwamba kundi la Boko Haram ndilo lililokuwa limemteka mzee huyo lakini katika hali ya haraka sana kiongozi wa kundi hilo akaibuka na kuzipinga taarifa hizo kwamba hawakumteka mzee huyo kwa kuwa hawakuona kama kuna ulazima wa kufanya jambo hilo. Taarifa za kupotea kwake zikaanza kuvuma kwenye mitandao ya habari, watu wengi walikuwa na maswali mengi kwamba ni nani alihusika kumteka mzee huyo? Kama alikuwa nchini Msumbiji, mbona alitafutwa kila kona lakini hakuwa amepatikana? Marekani haikubaki kimya, kupotea kwa mzee huyo iliwashangaza sana, walichokifanya ni kuwatuma maofisa wa CIA kuelekea nchini Msumbiji ambapo huko walitakiwa kufuatilia kila kitu na kugundua mzee huyo alikuwa wapi na ni kwa jinsi gani walitakiwa kumtafuta na kumpata. Maofisa wanne wakasafiri na kuelekea nchini humo. Kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kutafuta mawasiliano yake, walitaka kugundua ni watu gani alikuwa amewasiliana nao mara ya mwisho alipoingia nchini humo. Namba yake wakaipata na kuona namba ya bilionea mmoja kutoka nchini Msumbiji, Moutinho ambaye mara ya mwisho aliwasiliana naye. Huyo ndiye mtu wa mwisho ambaye aliwasiliana na huyo mzee siku mbili zilizopita. Walichokifanya ni kumfuata kwa lengo la kuzungumza naye. “Alikuja kwangu! Nilizungumza naye, hakuonekana kuwa sawa siku hiyo, alikuwa na hofu kubwa,” alisema Moutinho. “Sawa. Baada ya kuondoka hukujua alipoelekea?” “Sikujua kitu chochote kile.” “Sawa. Haina shida.” Hawakutaka kuzungumza naye zaidi, walichokifanya ni kuondoka huku wakiwa na uhakika kwamba bilionea huyo alikuwa akijua kile kilichokuwa kikiendelea. Walipofika hotelini, wakawasiliana na wenzao waliokuwa nchini Marekani na kuwaambia kuhusu bilionea huyo waliyezungumza naye kwamba alikuwa akifahamu kila kitu japokuwa alijifanya kutokujua lolote lile. “Hakikisheni anawaambia ukweli. Ikiwezekana, mrudieni na kuzungumza naye kibabe,” alisikika kiongozi wao. “Ondoa hofu. Tutakupa majibu kesho!” “Sawa.”
Innocent hakutaka kukubali, mbele yake kulikuwa na kazi kubwa ambayo alitakiwa kupambana nayo mpaka kuhakikisha anashinda. Alitaka kuwasiliana na vijana wake kwa kuamini kwamba wangegundua mahali alipokuwa Bwana Todd kwa haraka tofauti na maofisa wa CIA walivyotaka iwe. Watu wa kwanza kabisa kuwasiliana nao walikuwa ni vijana walioishi katika Jiji la Maputo nchini Msumbiji, wakawaambia kwamba kulikuwa na tukio la kupotea kwa bosi wao, vijana hao walikuwa wakifahamu kila kitu, walipata taarifa mapema sana kwamba bosi wao huyo alikuwa amepotea. Kulikuwa na makundi mengi nchini Msumbiji, waliamini kwamba kulikuwa na wanachama fulani katika kundi fulani ambao walikuwa wakifahamu mahali Bwana huyo alipokuwa, walitaka kuwafahamu watu hao, wakaanza kuwasiliana na vibaraka vyao mbalimbali kwa lengo la kuwaambia kuhusu taarifa juu ya mahali alipokuwa bosi wao. Baada ya kuulizia kwa siku mbili, tena huku wakitoa ahadi za kutoa kiasi fulani cha pesa kwa mtoa taarifa wakaambiwa kwamba kulikuwa na mtu alihusika katika utekaji wao, mtu huyo alikuwa bilionea Maxwell ambaye alimtumia bilionea mwenye kundi la kihalifu, Moutinho. “Kwa hiyo ikawaje?” aliuliza Innocent. “Tuliambiwa kwamba wanakwenda naye Afrika Kusini, wakipita katika ukaguzi, watamuulia huko na mwili wake kuutupa baharini,” alisikika kijana kutoka upande wa pili. “Basi sawa. Ngoja tufanye upelelezi zaidi,” alisema Innocent na kukata simu. Hakutaka kuchelewa, haraka sana akampigia simu mtu wake mwingine aliyekuwa Afrika Kusini ambaye kwa miaka zaidi ya kumi walikuwa wakishirikiana kuzipitisha meli zilizokuwa na mzigo wa madawa ya kulevya bandarini. Kijana huyo aliitwa Xuso. Alimwambia kila kitu kilichokuwa kikiendelea na kumwambia kwamba inawezekana kabisa ni meli ya Bwana Maxwell ndiyo iliyokuwa imetumika hivyo ilikuwa ni lazima kuhakikisha wanaipekua meli hiyo na kuingia ndani ambapo huko watamchukua mtu wao na kundoka naye. “Hilo si tatizo!” “Sawa. Hakikisha linafanikiwa!” “Haina shida. Nitawatumia polisi!” “Polisi?” “Si polisi halisi. Hao watakuwa vijana ambao watajifanya polisi, hilo usijali,” alisikika Xuso kwenye simu. Wakakubaliana na kukata simu. Hakukuwa na mua wa kupoteza, haraka sana mawasiliano yakafanyika na Xuso kuwaandaa vijana wake ambao walitakiwa kutafuta mavazi ya kipolisi tayari kwa kufanya kazi hiyo iliyokuwa mbele yao. Baada ya saa kadhaa, akapigiwa simu na kuambiwa kwamba vijana walikuwa tayari na hivyo walitakiwa kujiandaa kwa lengo la kuisubiri meli hiyo. Siku iliyofuata, asubuhi na mapema walifika bandarini, wakazugazuga huku wakizunguka huku na kule. Kila mtu aliwaona vijana hao waliojifanya polisi, walionekana kuwa wapya na si kama wale ambao kila siku hufika mahali hapo na kufanya ukaguzi wa meli. Baaa ya saa kadhaa, wakaambiwa kwamba kulikuwa na meli ilikuwa ikija, ilikuwa ni meli ya bwana Maxwell ambayo mara nyingi ilikuwa ikifanyiwa ukaguzi wa juujuu kwa kuwa alikuwa akibeba madawa ya kulevya. Siku hiyo kila mtu aliwaona polisi hao wa bandia kuwa na mzuka wa kufanya kazi. Kwanza walifika mapema lakini pia walionekana kuwa na uchu na meli hiyo kiasi kwamba baahi ya viongozi waliokuwa pale bandarini wakahisi kwamba watu hao waliambiwa mchongo mzima kwamba kulikuwa na ishu iliyokuwa ikichezwa mahali hapo. Meli ilipofika tu na kutua nanga, harakaharaka polisi wale wakaelekea kule pa kuingilia na kutaka kuingia. Vijana wa Maxwell walishangaa, haikuwa kawaida kwani kila siku walipokuwa wakifika ilikuwa ni lazima wapewe taarifa kwamba kulikuwa na polisi kadhaa ambao walikuwa wamekwishaingiziwa kias cha pesa mapema kabisa. Siku hiyo hawakupewa taarifa yoyote ile kwani hapo kabla walimalizana na mkuu wa polisi kwamba polisi hao hawakutakiwa kuja pale kwa kuwa walitaka kufanya mambo yao kwa urahisi zaii. “Who are you?” aliuliza Jackson, mmoja wa vijana wa Maxwell. “You must be kidding me!” (unanitania!) “What te hell is going on” (nini kinaendelea?) aliuliza Jackson, uwepo wa polisi wale ulimshangaza kupita kawaida. Hawakutaka kusikia kitu chochote kile, wakaingia ndani ya meli hiyo kibabe kwa kuwa walitaka kufanya kazi yao. Wazungu hao walibaki nje wakishangaa, siku hiyo waliona kabisa mabadiliko, polisi waliokuja hawakuonekana kuwa na urafiki hata kidogo. Wakaanza kuingia kwenye chumba kimoja mpaka kingine, walikuwa na bunduki zao mikononi mwao, wakapekua mpaka katika chumba cha mwisho kabisa ambacho ndicho Bwana Todd na Bruno walipokuwa wamefungwa. Walipoufungua mlango, macho yao yakatua kwa watu hao, polisi hao wakatabasamu, walichokifanya ni kuwachukua wote wawili na kuanza kutoka nao kwenda nje ya meli ile, wakati wakiwa wamekwishafika mlangoni tu, macho yao yakatua kwa polisi wenyewe waliokuwa wamefika mahali hapo huku wakiwa na bunduki mikononi mwao. “You are under arrest…” (mko chini ya ulinzi) alisema polisi mmoja, na polisi wote wakawanyooshea bunduki. *** Uwepo wa polisi wa bandia kuwepo mahali pale ulimshtua mkurugenzi wa bandari. Yeye kazi yake kubwa ilikuwa ni kucheza madili makubwa. Mkurugenzi huyo aliyejulikana kwa jina la Kumaro alipigiwa simu na Maxwell na kuambiwa kwamba ahakikishe meli yake siku hiyo inapita pasipo kukaguliwa. Hilo halikuwa tatizo, akakubaliana nao kwa kuwa tayari hapo kabla alipigiwa simu na Bwana huyo na kuambiwa kwamba siku hiyo hakutakiwa kuhofia kitu chochote kile kwa kuwa polisi wasingefika kabisa mahali hapo kwani tayari alimalizana na kamanda mkuu wa jeshi la polisi hapo Cape Town, Thambo. Kitendo cha vijana wa Xuso kufika bandarini, kilimshangaza Kumaro na hivyo kuamua kumpigia simu Thambo na kumlalamikia kwamba alichokifanya halikuwa jambo zuri kwa kuwa alimwambia kabisa kwamba kusingekuwa na polisi, sasa mbona kuna polisi walikuwa wamefika mahali hapo? “Polisi?” alisikika Thambo akiuliza. “Ndiyo!” “Sijatuma polisi hapo. Hebu ngoja niwatume polisi waje, nahisi kuna kitu,” alisikika Thambo na kukata simu. Polisi wa bandia walipoingia ndani ndiyo muda ambao polisi wa kweli walifika mahali hapo. Waliambiwa kila kilichotokea na hivyo kuwasubiri watu hao hapo nje. Walipotoka tu, hawakutaka kuchelewa, wakawaweka chini ya ulinzi lakini wakati huo wengine walikuwa kwa ndani hata mlango hawakuwa wameusogelea wakiwemo Bwana Todd na Bruno. Walipowaona wenzao wa mbele wamesimama, tayari wakahisi kulikuwa na kitu tena wakapata hofu kabisa baada ya kusikia wakiambiwa kwamba walikuwa chini ya ulinzi. Bruno hakutaka kubaki mahali hapo, tayari akili yake ilimwambia kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea, akamvuta Bwana Todd na kumwambia waondoke kwa kupitia ndani ya meli mpaka nje ya meli hiyo kwa kupitia ubavu wa meli ulioangalia baharini. “Tumepata msaada…subiri!” alisema Bwana Todd. “Tusubiri nini? Unajua nani polisi na nani adui yako? Huo aliyesikika akiwaambia hawa apo chini ya ulinzi ni nani? Kama ni polisi, sawa, je hawa ni wakina nani?” aliuliza Bruno huku akimwangalia Bwana huyo. Kidogo maneno hayo yakamuingia akilini na kuona kwamba kweli inawezekana kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea, akakubaliana na Bruno na hivyo kuondoka kwa kurudi nyuma. Hawakufika mbali, wakaanza kusikia milio ya risasi, wale watu walioamini kwamba walikuwa polisi walikuwa wakipambana kwa risasi na watu wengine kitu kilichoonyesha kwamba mahali hapo hakukuwa salama tena. “Tukimbie! Kimbia,” alisema Bruno na kuendelea kukimbia na Bwana huyo. Walikimbia, hakukuwa na sehemu ya kutokea, walichokifanya ni kuingia katika chumba kimoja miongoni mwa vyumba vingi vilivyokuwa ndani ya meli hiyo. Ndani ya chumba hicho walikutana na vitanda vya dabo deka, kwa kule pembeni kabisa kulikuwa na kidirisha cha kioo na hivyo kukifuata kwa lengo la kukivunja. Kilikuwa kioo kigumu mno na isingewezekana kukivunja kwa urahisi kama walivyofikiria. Bruno akaanza kutafuta kitu cha kuvunjia, kila kona aliyokuwa akiangalia kulikuwa na chupa tu ambazo hata kama angezitumia zote hizo asingeweza kuvunja kioo hicho. “Ni lazima tukivunje kioo hiki ili tutoroke,” alisema Bruno, nje ya kioo kile kulikuwa na bahari na uzuri ni kwamba wingi wa maji hayakuwa sawa na dirisha lile, yalikuwa kwa chini kidogo. Bruno hakutaka kukata tamaa, aliendelea kutafuta kitu cha kuvunjia kioo ndani ya meli ile na kwa bahati nzuri akakutana na kipande cha chuma, haraka sana akaelekea katika kidirisha kile na kuanza kukigonga. “Puu..puu…puu…” aliendelea kukigonga kioo kile huku Bwana Todd akiwa pembeni akimwangalia alivyokuwa akipambania maisha yao. Haikuwa kazi ndogo, ilikuwa ni kazi kubwa mno, alichoka lakini hakuacha kuendelea kugonga kioo kile. Wakati akiendelea kugonga, milio ya risasi ilikuwa ikizidi kuendelea kusikika kutoka kule walipotoka hivyo kumfanya Bruno kugonga kwa haraka zaidi kwa kuamini mara baada ya watu hao kupambana na wale watu waliotoka kuwachukua ndani ya chumba kile, basi watu ambao wangefuata wangekuwa wao. Alitumia dakika tano, tena kwa kukigonga kwa nguvu zote, kioo kile kikaanza kuvunjika taratibu, kikaanza kutoa alama za mvunjiko, Bruno hakutaka kuacha, akaendelea kugonga zaidi na zaidi hatimaye kioo kuvunjika. “Tupite kupitia hapa,” alisema Bruno, akachukua shuka lililokuwa kitandani na kuweka kwenye kidirisha kile kwa chini ili kuzuia vipande vya kioo vilivyobaki kutokuwakata. “Anza wewe kupita…” alisema Bwana Todd. “Hapana! Anza wewe. Ingia ndani ya maji, piga mbizi kwa nguvu tuelekee upande ule kule wenye meli ile kule kubwa, tukifika kule tutatoka. Ingia, hatuna muda wa kupoteza.Ngoja nikupe boya,” alisema Bruno, hapohapo akampa boya moja lililokuwa kitandani. “Na wewe?” “Nitaogelea. Usijali!” Bwana Todd akalichukua boya lile na kulivaa. Akapita katika kidirisha kile na kutumbukia ndani ya maji. Bruno hakubaki, naye akapita katika kidirisha kile na kutumbukia majini. Akamshika Bwana Bruno aliyeonekana kutokuwa na nguvu za kuogelea kwa kuwa umri ulienda sana na kuanza kumvuta kuelekea katika upande mwingine wa meli. Ilikuwa ni lazima kutoroka katika meli ile kama tu walitaka kuendelea kuwa hai.
Rahman alikuwa nchini Marekani, alikuwa akisoma katika Chuo cha Mississippi huku moyo wake ukiwa nchini Kenya tu. Alikuwa na furaha tele, kitendo cha baba yake kumwambia kwamba msichana alipatikana tena akiwa ni mzuri mno alisikia furaha ya ajabu moyoni mwake. Hakuacha kumpigia simu mzee Oloah na kumuuliza zaidi kuhusu binti huyo, leo alipokuwa akiambiwa hivi, kwamba alikuwa mzuri kama malaika, kesho alipiga simu tena na kuuliza alifananaje. Alichanganyikiwa kupita kawaida, mwili wake ulikuwa nchini Marekani lakini baada ya kuambiwa kuhusu msichana huyo, tayari moyo wake ukahama na kwenda nchini Kenya. Siku ziliendelea kukatika lakini kwake zilionekana kwenda taratibu sana, alitamani kuondoka kuelekea nchini Kenya ili aende kumuona Sharifa aliyeambiwa kwamba ni mzuri mno lakini hilo halikuwezekana. Baada ya mwezi mmoja, akamaliza masomo yake na kuanza safari ya kuelekea nchini Kenya. Njiani, mawazo yake yalikuwa kwa msichana huyo, hakuwahi kumuona lakini kichwani mwake kulitengenezwa picha ya msichana mmoja mrembo, aliyekuwa na umbo la kuvutia, sura nzuri na tabasamu lililomfanya kuvutia zaidi. Baada ya saa ishirini ndege ikafika mjini Dubai, akateremka na kupumzika kwa muda akisubiri kuendelea na safari ya kuelekea nchini Kenya. Hapo, akaelekea kwenye maduka ya nguo na kuanza kununua nguo kwa ajili ya wazazi wake na hata msichana ambaye hakuwahi kumuona. “Baba aliniambia ni mwembamba, mrefu kidogo, nadhani hizi nguo nitakuwa nimelenga,” alisema huku akichagua nguo kwa ajili ya Sharifa. Alipomaliza, baada ya saa mbili akapanda ndege na kuendelea na safari ya kuelekea nchini Kenya. Mapigo yake ya moyo yalikuwa juu, alikuwa na presha kubwa, moyo wake ulikuwa na shauku kubwa ya kumuona msichana huyo, alitaka kuona alifananaje, je, alikuwa kama msichana ambaye alimtengeneza kichwani mwake au alikuwa zaidi. Baada ya saa kadhaa, ndege ikaanza kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi. Akateremka na kuanza kupiga hatua kuelekea katika jengo la uwanja huo na abiria wengine huku mizigo yao ikichukuliwa na kupelekwa sehemu kwa ajili ya kuchunguzwa. Kila kitu kilipokamilika, akapewa mizigo yake na kuondoka mahali hapo. Alipofika nje, akawaona wazazi wake ambao walimfuata, wakamkumbatia na kumpongeza kwa kumaliza masomo yake. Alifurahi kuwaona, akawasalimia na kitu cha kwanza kabisa kuuliza kilikuwa ni juu ya Sharifa, alitaka kumuona haraka sana, hakuwa radhi kuona akipoteza muda wake pasipo kumuona msichana huyo ambaye kwa kipindi kirefu alichokuwa chuoni mawazo yake yalikuwa kwake tu. “Kesho tutakwenda kwao!” alisema mzee Olioh huku akimwangalia kijana wake. “Sawa. Nimemkumbuka mno. Ninampenda, nina uhakika ni mzuri na anastahili kuwa mke wangu!” alisema Rahman huku akiwaangalia wazazi wake. Furaha ikawa tele nyumbani kwa mzee huyo, kitendo cha kijana wake kurudi salama kutoka masomoni nchini Marekani kilimpa furaha kupita kawaida. Wakawa watu wa kuzungumza mambo mengi, Rahman aliwaambia mengi kuhusu maisha yake nchini Marekani, jinsi alivyosoma kwa kipindi kirefu na hata kujiepusha na wasichana wa huko ambao nao walikuwa wakimtaka kwa lengo la kulala naye lakini hakuonekana kuwa mwepesi hata kidogo. “Sina usingizi! Yaani ninatamani hata usiku huu tuondoke kwenda kumuona Sharifa! Hebu niambie tena baba! Anafananaje?” aliuliza Rahman, yaani kila alipokaa mawazo yake yalikuwa kwa Sharifa tu. “Ni mzuri!” “Kama?” “Malaika!” “Kweli?” “Niamini! Ni mzuri mno. Mtaratibu, anajielewa, yaani uzuri wake hakuna mfano,” alisema baba yake. Maneno hayo yakazidi kumtia presha kubwa, hakuamini kama kweli msichana huyo aliyekuwa akiambiwa alikuwa mzuri kiasi hicho, hakuacha kumuuliza baba yake zaidi kuhusu Sharifa kwani kesho yake aliona ni ndefu mno na saa zilikatika taratibu kama kinyonga. “Ni mweupe?” “Kama mwarabu!” “Mungu wangu! Ninavyopenda Waarabu mimi! Nadhani huyo atakuwa ni mzuri sana. Ninataka nimuone jamani! Nilishachanganyikiwa. Leo silali. Baba! Nataka kesho saa kumi na mbili asubuhi twende kwao,” alisema Rahman. Kama alivyosema ndivyo ilivyotokea, usiku hakulala, alibaki chumbani kwake huku akimfikiria msichana huyo mrembo. Ilipofika asubuhi, yeye ndiye alikuwa na jukumu la kumwamsha baba yake na kumwambia kwamba walitakiwa kujiandaa na kwenda kumuona Sharifa. Mzee Olioh alishangaa mno, aligundua kwamba kijana wake alitokea kumpenda mno msichana huyo japokuwa hakuwa amemuona. Hakukuwa na tatizo, akajiandaa na ilipofika saa mbili wakaondoka na kuelekea katika Kijiji cha Guolduvai. Kutoka jijini Nairobi mpaka Guolduvai kulikuwa na umbali wa kilometa mia nne, walitumia saa mbili njiani mpaka kufika huko. Mapigo ya moyo ya Rahman yalikuwa juu mno, macho yake yalikuwa na hamu kubwa ya kumuona Sharifa kuliko kitu chochote kile. Walipofika, gari likasimamishwa na kuelekea katika nyumba ya mzee Jumanne. Kwa jinsi wasichana wengine walivyokuwa wakionekana kijijini hapo, Rahman alipata hofu kwamba inawezekana baba yake alimremba tu lakini Sharifa hakuwa mrembo kama alivyokuwa ameambiwa. Wasichana wengine walikuwa wa kawaida kabisa, sasa ilikuwaje huyo Sharifa aliyekuwa akizungumziwa kuwa na uzuri kama ule aliokuwa ameambiwa? Wakakaribishwa ndani ya nyumba hiyo kwa furaha na kutulia. Muda wote macho ya Rahman hayakutulia, alikuwa akiangalia huku na kule, kila mtu aliyekuwa akiingia ndani ya nyumba hiyo alikuwa akimwangalia mno. “Tumekuja kumuona Sharifa kwanza!” alisema mzee Olioh. Hilo halikuwa tatizo, Sharifa ambaye alikuwa uani akaitwa mahali hapo. Jinsi alivyoitikia, hiyo Beee alivyoitoa moyo wa Rahman ukamlipuka na kuanza kudunda kwa nguvu kana kwamba ulitaka kuchomoka. Wala hazikupita sekunde nyingi, Sharifa akatokea sebuleni hapo. Macho ya Rahman yalipotua kwa msichana huyo hakuamini kama alikuwa akimwangalia binadamu au malaika. Alikuwa msichana mrembo mno, msichana wa ajabu ambaye alikuwa na uhakika kwamba wakati Mungu alipokuwa akimuumba alihakikisha amemaliza kazi zake zote na kuanza kumuumba msichana huyo tena kwa udongo maalumu. Alikuwa na uzuri wa ajabu. Moyo wa Rahman ukazidi kudunda na kuchanganyikiwa, alishindwa kuamini kama yeye ndiye ambaye angemuoa msichana huyo, kulala naye kitanda kimoja na hatimaye kuzaa watoto. Akashindwa kujizuia, tabasamu pana likaonekana usoni mwake, akatamani kusimama na kwenda kumkumbatia kwani kwa jinsi alivyoonekana, alikuwa bab’ kubwa. “Sharifa…” Rahman alijikuta akiita, baba yake akamminya kwa mguu na kumtaka atulie. Si kwamba aliliita jina hilo kwa makusudi, lilimtoka tu mdomoni kwani ule uzuri aliouona kwa msichana huyo hakika ulimchanganya. Sharifa akakaa kochini na baba yake kuanza kutoa utambulisho. Akamwambia Sharifa kuhusu ugeni ule, mzee Olioh hakuwa mgeni machoni mwake, alimfahamu, alikuwa mzee yule aliyekuja mahali pale mwezi uliopita na kuzungumza na baba yake kuhusu kijana wake aliyetaka kumuoa na bila shaka kijana aliyekuwa naye ndiye ambaye alitaka kumuoa. Alibaki akiangaliana na Rahman. Kwake, hakukuwa na mwanaume mzuri kama Bruno, pamoja na umasikini aliokuwanao kijana yule bado alikuwa akimpenda vilevile, kwake, hata kama angekuja mwanaume mzuri kuliko wote katika dunia hii, moyo wake ungeendelea kuwa kwa Bruno tu. Walizungumza mno, baadaye akapewa nafasi Rahman, kama kawaida akaanza kushukuru na mwisho wa siku kumshukuru baba yake kwa kuamua kumchagulia msichana ambaye alikuwa mzuri zaidi ya alivyokuwa akifikiria. “Sharifa ni msichana mzuri, msichana ambaye naamini atakuwa bora katika maisha yangu, mke bora ambaye nitakuwa naye kwenye shida na raha,” alisema Rahman huku akimwangalia Sharifa kwa jicho lililoashikilia mapenzi makali aliyokuwanayo juu yake. Kila mtu aliongea lake, mzee Jumanne alionekana kuwa na furaha tele, kitendo cha binti yake kuwa mkimya mahali hapo kilionyesha kabisa kwamba alikubaliana na kile kilichokuwa kikiendelea. Walichokifanya kama wazazi ni kuwaachia nafasi wawili hao sebuleni wakae na kuzungumza kwa muda, wazoeane ili mapenzi yaanze huku mipango ya kufungwa ndoa ianze kufanyika. “Nimetokea kukupenda sana Sharifa. Nilipoambiwa kuhusu wewe, hakika sikuwa na swali kwani naamini kwamba baba yangu huchagua vilivyo bora kabisa,” alisema Rahman huku akimwangalia Sharifa ambaye alikuwa kimya kabisa. “Ninakupenda Sharifa. Upo tayari kuwa mke wangu wa ndoa?” “Hapana!” “Kwa nini tena jamani? Tatizo nini Sharifa!” “Hapana! Umeniuliza, nimekwambia hapana! Kuna swali tena katika hilo?” aliuliza Sharifa huku akimwangalia Rahman. Moyo wa Rahman ukanyong’onyea, hakuamini alichokuwa amekisikia. Mategemeo yake yalikuwa tofauti na jinsi alivyodhani hapo kabla, alihisi kwamba baba yake alimaliza kila kitu na ni yeye tu ndiye aliyekuwa akisubiriwa kwa msichana huyo. Hilo lilimuuma lakini hakutaka kukata tamaa, alijua kwamba huyo alikuwa msichana na kama angeendelea na msisitizo wake basi kuna siku angekubaliana naye. Mpaka wazazi wanarudi mahali hapo, hakukuwa na kitu kilichobadilika lakini Rahman aliona ni muda wake kupambana. Maisha yaliendelea, hakuacha kwenda Guolduvai, mara kwa mara alikuwa akienda huko na kuonana na Sharifa, alimuonyeshea kwamba alimpenda kupita kawaida, kila alipokuwa akienda alibeba zawadi kwa ajili ya msichana huyo. Bado hakuweza kuubadilisha moyo wa Sharifa, msisitizo wake ulikuwa uleule kwamba hakutaka kuwa na mwanaume huyo. Mwezi mmoja ulipokatika, ndipo kidogo moyo wa Sharifa ukaanza kulegea na hatimaye akaanza kumkubali Rahman kwani alionekana kuwa mwanaume mpole na mwenye uvumilivu mkubwa mno. Tabasamu likaanza kuonekana usoni mwake na hatimaye kumwambia kwamba alikubali kuolewa na yeye lakini kwa sharti moja tu, kama lingeshindikana basi amuache na kufa akiwa hajaolewa. “Nipo tayari kwa sharti lolote lile,” alisema Rahman. “Ni kwamba nilikuwa na mpenzi!” “Niliambiwa. Si huyo Bruno?” “Ndiyo! Inasemekana alikufa baharini. Ila mimi siamini hilo hata kidogo. Najua atakuwa hai sehemu fulani,” alisema Sharifa. “Labda! Hakuna ajuaye.” “Sasa basi. Kama kuna siku atarudi tena na kugundulika hakufa! Huo ndiyo utakuwa mwisho wangu mimi na wewe hata kama utakuwa umenioa na kukuzalia watoto,” alisema Sharifa. “Haina shida.” “Unahisi utaweza kuniacha nikaendelea na maisha yangu na mpenzi wangu?” “Nitakuruhusu! Nakuahidi kukuruhusu endapo atarudi.” “Sawa. Kama ni hivyo hakuna tatizo!” Wakakubaliana na maisha kuendelea. Walikuwa wakifanya kila kitu isipokuwa mapenzi tu. Waliahidiana kwamba wangefanya mapenzi siku ambayo wangeoana na kuwa mume na mke. Kwa Rahman hilo halikuwa tatizo hata kidogo, alichokuwa akikiangalia ni kuwa na msichana huyo tu. Siku zikaendelea kukatika, wazazi wakafurahia na hatimaye tarehe ya kufunga ndoa ikapangwa na wawili hao kujiandaa. Kwa mzee Jumanne ilikuwa ni furaha tele, hakuamini kama hatimaye alifanikiwa kumlaghai mtoto wake na hatimaye alikuwa akiolewa na kijana kutoka katika familia ya kitajiri. “Hakika umenifanya nijisikie baba! Nakupenda sana binti yangu! Naomba usahau yote yaliyopita,” alisema mzee Jumanne. “Asante baba! Nimekusamehe!” alisema Sharifa. Siku zikakatika na hatimaye siku ya harusi kufikia. Kila mmoja alionekana kuwa na furaha tele. Sharifa alichukuliwa na kupelekwa Nairobi, akafanyiwa shopping ya maana huku ikiwa tayari imepita miezi sita tangu alipopewa taarifa ya kifo cha mpenzi wake. Akarudi Guolduvai akiwa Sharifa mwingine, alibadilika, alikuwa mrembo. Chakula kikapikwa, watu wakajiandaa kusherehekea sherehe hiyo. Simu ikapigwa na kuambiwa kwamba msafara wa bwana harusi ulikuwa njiani kuja kuchukua mke. Wanawake walikuwa wakicheza ngoma, siku hiyo hakukuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea kijijini hapo zaidi ya kusherehekea harusi hiyo kubwa. Bwana harusi alipofika tu, kitu cha kwanza kilikuwa ni kupelekwa katika uwanja maalumu wa kucheza ngoma za kitamaduni na kuanza kucheza. Madrasa ikaanza kazi yake, ikapiga madufu na dua ya maana kupigwa. Wakati bwana harusi akijiandaa kufunga ndoa huku mzee Jumanne akiwa amekwishakaa kwenye mkeka tayari kwa kufungishwa ndoa hiyo, kwa mbali alionekana Abdul akiwa anakimbia kwa kasi, shati lilikuwa mkononi mwake, watu walimshangaa, hakuwa akikimbia kimya kimya, alikuwa akipiga kelele kwa nguvu huku akiliita jina la Sharifa. Shekhe aliyetaka kufungisha ndoa ikabidi anyamaze na kumwangalia kijana huyo ambaye alipitiliza mpaka katika chumba alichokuwamo Sharifa kitu kilichomfanya kila mtu kupigwa na butwaa. “Sharifa…Sharifaaa…Sharifaaa…” aliita Abdul huku akiwa ameingia, Sharifa aliyekuwa kitandani na shela lake akashtuka baada ya kuona mlango umefunguliwa. “Kuna nini?” “Bruno yupo hai! Bruno yupo hai Sharifa….” alisema Abdul huku akimwangalia Sharifa aliyeonekana kushtuka. “Yupo wapi?” “Sijui! Ila yupo hai! Tuondoke! Bruno yupo hai,” alisema Abdul huku akimshika Sharifa mkono na kumvuta. Kitendo cha kusikia Bruno yupo hai, Sharifa alichanganyikiwa. Hakukuwa na ndoa tena, huyo ndiye alikuwa mwanaume wa maisha yake, alikubaliana na Rahman kwamba kama mwanaume wake angerudi tena kusingekuwa na ndoa. Wakatoka ndani, wakapita katika umati wa watu waliokuwa nje ambapo ndoa ilitaka kufungwa. Mzee Jumanne alibaki akishangaa, akasimama na kumuita binti yake aliyekuwa akikimbia na Abdul. “Sharifa…Sharifa kuja hapa…” alisema mzee huyo. “Siwezi! Siwezi baba! Bruno yupo hai…” alisema Sharifa huku akikimbia, maneno hayo yalimfanya kila mtu kushtuka, iliwezekanaje mwanaume huyo awe hai na wakati alikufa baharini tena miezi sita iliyopita. Hata kuwakimbiza wakashindwa kwani watu hao walikuwa wakikimbia kwa kasi huku shela likiwa mwilini mwa Sharifa. Ni ndani ya dakika moja tu, wakapotea machoni mwao. Ubwabwa ukawa mchungu. Pale Rahman alipokuwa, alitamani ardhi ipasuke atumbukie ndani.
Hawakuchukua muda mrefu baharini wakafanikiwa kufika nchi kavu ambapo moja kwa moja wakaanza kuondoka huku eneo zima likiwa halina mtu kutokana na milio ya risasi iliyokuwa ikisikika mahali hapo. Wakaondoka mpaka katika geti namba sita la kuingilia bandarini hapo, hawakutaka kupoteza muda, haraka sana wakaondoka mahali hapo na kwenda barabarani. Bruno hakujua kitu chochote kile, hakujua ni mahali gani walitakiwa kuelekea, alibaki huku akiangalia huku na kule, kazi yake kubwa ilikuwa ni kumtoa mzee yule ndani ya meli ile na baada ya hapo basi mzee huyo ndiye angeshikilia usukani kwa kuwa alipafahamu Afrika Kusini tofauti na yeye ambaye ilikuwa ni mara ya kwanza kufika mahali hapo. “Where to?” (twende wapi?) aliuliza Bruno huku akimwangalia mzee yule. “Wait?” (subiri) Akasubiri. Mzee Todd akatulia, alionekana kama mtu aliyekuwa akijifikiria kitu fulani hivi. Baada ya dakika moja, akauinua uso wake na kumwambia Bruno kwamba walitakiwa kwenda sehemu, katika Mtaa wa Kloof ambao ulikuwa na maduka mengi, mtaa pekee ambao ulikuwa ukiongozwa kutembelewa na wakazi wengi wa hapo Cape Town. Mzee huyo aliendelea kumwambia kwamba huko kulikuwa na mtu aliyekuwa akimfahamu ambaye angewasiliana naye na kuondoka kurudi nchini Marekani. Wakaanza safari ya kuelekea huko huku kila mmoja akiwa hana kitu kabisa mfukoni mwake. Kwa jinsi walivyokuwa wakionekana, hakukuwa na mtu aliyeamini kama watu hao walitakiwa kutembea katika jiji hilo la kitalii, jiji lililojaza watu wenye pesa ambapo kila mtu aliyekuwa akionekana barabarani alikuwa na muonekano wa pesa. Safari ya kwenda Kloof haikuchukua muda mrefu, wakafika. Ulikuwa mtaa uliokuwa na watu wengi waliokuwa wakizunguka huku na kule, wengine walikuwa wakijipiga picha za ukumbusho huku wengine wakifanya manunuzi yao. Wakaelekea mpaka katika sehemu iliyokuwa na nyumba nyingi za kifahari, mageti makubwa, sauti nyingi za mbwa zilikuwa zikisikika, wakalifuata jengo moja na kuanza kugonga geti, wala hazikupita sekunde nyingi, sauti ya mlinzi ikaanza kusikika kutoka katika kipaza sauti kidogo kilichokuwa kimepachikwa ukutani. “Wewe nani?” alisikika mlinzi huyo. “Todd.” “Nikusaidie nini?” “Ninataka kuonana na Brown.” “Una miadi naye?” “Hapana! Naomba kuonana naye.” Alichokifanya mlinzi ni kupiga simu ndani ambapo akalisema kama alivyoambiwa. Alimwambia mzee huyo kwamba kulikuwa na mtu aliyekuwa akimuulizia aliyeitwa Todd. Mtu ambaye alikuwa akimfahamu mwenye jina hilo alikuwa mmoja tu, mfanyabiashara maarufu aliyekuwa na utajiri mkubwa. “Todd! Haiwezekani kuja bila taarifa, hebu subiri,” alisema Brown. Hapohapo akaelekea katika chumba kilichokuwa na kompyuta mbili na kuanza kuangalia nje kupitia kamera ndogo za CCTV zilizokuwa getini. Aliwaona watu wawili waliokuwa wamesimama, mmoja alimfahamu vilivyo, alikuwa ni mzee Todd lakini kwa jinsi alivyoonekana, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea. Hakutaka kubaki ndani, akaondoka na kuelekea getini, akamwambia mlinzi afungue geti, akafanya hivyo na watu hao kuingia. Alimwangalia Todd, hakiamini kama alikuwa yeye, alibadilika, alionekana mchafu, hakuwa yule Todd aliyekuwa akimfahamu. “Kuna nini kimetokea?” “Ni habari ndefu sana. Naomba tuingie ndani kwanza,” alisema Todd. Hilo halikuwa tatizo, wakaingia ndani na kuanza kumuhadithia kila kitu kilichokuwa kimetokea. Alimwambia kuhusu mpango uliokuwa umesukwa, mpango ambao alikuwa na uhakika kwamba nyuma yake kulikuwa na mtu lakini bahati mbaya hakumgundua mtu aliyekuwa nyuma yake. “Na huyu?” “Ni kijana ambaye naye aliletwa ndani ya meli ile,” alijibu Todd kuhusu Bruno. Brown akanyamaza, akamwangalia Todd, hakuamini alichokuwa amekisikia, alihisi kudanganywa. Akamwambia kwanza asubiri aende chumbani ambapo angempa pesa na kwenda kumfanyia harakati zote za kusafiri na kurudi nchini Marekani. “Nitashukuru sana,” alisema Todd. Brown akaondoka. Sebuleni walibaki wawili. Bruno alimwangalia Todd, alikuwa mwanaume mzee, aliyehitaji sana msaada wake, alijua kabisa kwamba kama angemuacha pasipo mtu huyo kufika nchini Marekani basi ingekuwa vigumu sana kufika kwa kuwa tu wale watu ambao waliwatoroka wangemtafuta na kumuua. Walikuwa wamezungumza na Brown, kwa jinsi alivyoonekana, Bruno alihisi kulikuwa na kitu. Akamwambia Todd kwamba walitakiwa kuondoka mahali hapo kwa kuwa moyo wake haukuwa na amani na mwanaume huyo aliyekuwa amewakaribisha. “Ni rafiki yangu!” “Una uhakika?” “Ndiyo!” “Unamwamini?” “Asilimia mia moja. Tusubiri!” alisema Todd ambaye alionekana kutokuwa na hofu hata kidogo. “Hapana! Simuamini. Nahisi kuna jambo. Tuondoke!” alisema Bruno lakini mzee huyo aliendelea kukataa kwa kumwambia kwamba waendelee kubaki kwa kuwa msaada pekee uliokuwa umebaki ulikuwa ni kwa rafiki yake huyo. Huku wakiwa wamejiachia kwenye kochi na Kituo cha Televisheni cha SABC kikiendelea na matangazo huku kikiwa kimejiunga na Kituo cha Habari cha CNN cha nchini Marekani, wakaona taarifa ya habari ambayo ilimshtua kila mmoja. Kulikuwa na mtu aliyekuwa akitafutwa kwa kuhusishwa na madawa ya kulevya. Nyumbani kwake kulikutwa na kilo tano za madawa ya kulevya, nakala ambazo zilionyesha kabisa kwamba alikuwa akiifanya biashara hiyo kupeleka Mexico, Cuba na sehemu nyingine. Polisi waligundua hilo baada ya kwenda kupekua nyumbani kwake na kukuta vitu hivyo vyote. Wote wawili walishangaa kwani mtu huyo aliyekuwa akitafutwa alikuwa Todd. “Nini?” aliuliza Todd huku akisimama na kuisogelea televisheni. Hakuamini alichokuwa akikiangalia, alishangaa, ni kweli alikuwa akifanyya biashara ya madawa ya kulevya tena kwa siri kubwa, na hakuwahi kuyapeleka madawa hayo nyumbani na hata familia yake haikuwa ikijua kilichokuwa kikiendelea, sasa iweje mzigo wa madawa hayo yakutwe nyumbani kwake? Nani aliyaweka na wakati hakuwahi kufanya kitu kama hicho? “Tuondoke,” alisema Bruno, bado hakuwa na amani. “Hapana! Brown atanisaidia,” alisema mzee huyo huku akianza kutokwa na machozi, alitia huruma. Bruno hakuwa na imani na Brown, alihisi kabisa kwamba mtu huyo kulikuwa na jambo alilotaka kulifanya. Akayapeleka macho yake katika televisheni ambapo ilitangazwa kwamba kwa yeyote ambaye angefanikisha kukamatwa ka mzee huyo basi angepewa kiasi cha dola milioni mbili. “Tuondoke!” alisema Bruno kwa hasira, hakutaka tena kuona mzee huyo akikataa, akamshika na kuanza kumvuta kwenda nje. Todd alikataa lakini hakuwa na jinsi, akakubaliana na Bruno na kuondoka naye mahali hapo kwani hakuwa na jinsi, kama kweli mwanaume huyo alikuwa na hofu na Brown, basi hakuwa na jinsi. *** Bilionea Maxwell alishika simu yake na kuanza kuongea na Innocent, kijana ambaye alikuwa karibu sana na mzee Todd. Alimpigia simu kwa lengo moja tu la kutaka kucheza mchezo fulani ambao aliamini ungeweza kumpoteza kabisa Todd. Alimwambia kuhusu mpango wake aliokuwa nao, alihitaji mtu wa kumsaidia na hakuona kama kungekuwa na mtu mwingine zaidi ya Innocent. Alimwambia wazi kwamba alitenga kiasi cha dola milioni moja kwa ajili yake kama malipo kwa kazi kubwa aliyoitaka aifanye. Dola milioni moja kilikuwa kiasi kikubwa cha pesa ambacho kiliichanganya mno akili ya kijana huyo. Haraka sana akamuuliza kuhusu kazi hiyo, hakutaka kumficha, alimwambia kwamba alitakiwa kumsaliti mzee Todd. “Kivipi?” “Ninataka kuiteka familia yake, si kwa nia mbaya, hapana, ni kwa nia nzuri sana na baadaye nitaiachia,” alisema Maxwell kana kwamba alikuwa mtu mzuri. “Mmh!” “Ndiyo! Unaweza kunisaidia katika hilo. Nitakulipa dola milioni moja keshi,” alisikika mzee huyo. Hilo lilionekana kuwa jambo gumu lakini kiasi cha pesa alichokuwa ametajiwa kilikuwa kikubwa mno, kilimchanganya, hakutaka kuona kiasi hicho cha pesa kikipita mbele yake, kama alitakiwa kumsaliti basi hakukuwa na tatizo lolote lile. Alikuwa bosi wake, alimfanyia kazi, hakuwa ndugu yake, kama alikuwa bosi wake, aliamini kuna siku mzee huyo angekuwa na uwezo wa kumfukuza na kumuajiri mtu mwingine kwa kuwa tu alihitaji pesa na hata muda mwingine kubana matumizi. Alijitoa kafara na kumwambia Maxwell kwamba alikubaliana naye hivyo hizo pesa ziandaliwe, hilo halikuwa tatizo. Alichokifanya Maxwell ni kuwasiliana na vijana wake na kuwaambia kwamba alihitaji mzigo wa madawa ya kulevya kilo tano, akapelekewa na kuanza kuwapa maelekezo juu ya nini kilitakiwa kufanyika. Akapigiwa simu Innocent na kuambiwa kwamba kuna vijana wangekwenda nyumbani hapo na kuingia ndani, walinzi wasingeweza kuwagundua kwa kuwa yeye mwenyewe alitakiwa kusema kwamba alikuwa akiwafahamu kama marafiki wa Todd. Hilo likafanyika, vijana wakaelekea huko. Innocent mwenyewe hakuona jinsi madawa yalivyokuwa yamebebwa kwani yalibebwa kwa siri sana tena kwa vifurushi vidogo. Wakati wameingia mpaka sebuleni na vijana wanne, Innocent akaenda kumuita mke wa Todd. Kitendo cha kuondoka sebuleni hapo kilionekana kuwa kosa kubwa, hapohapo vijana wale wakachukua vifurushi vile vya madawa na kuanza kuvificha katika makochi na sehemu nyingine. Mpaka Innocent na mkewe wa Todd wanafika sebuleni, tayari walikamilisha kila kitu. Wakamwambia mwanamke huyo kwamba walitakiwa kwenda sehemu kuonana na mume wake kwa kuwa alikuwa amejificha kwa kuogopa kutafutwa na wabaya wake. “Mnasemaje?” “Mzee yupo! Amejificha, alikwenda nchini Msumbiji. Kuna watu walimteka na kutaka kumuua, alifanikiwa kuwatoroka na kuja huku. Wabaya wake wapo hapahapa jijini New York, ameogopa kuja nyumbani kwani anaamini kwamba wanaweza kuja hapa na kumuua,” alisema kijana mmoja kwa sauti ya unyenyekevu, tena kwa suti aliyokuwa amevaa, ilikuwa vigumu kugundua kama alikuwa mtu mbaya. “Yupo wapi?” “Kwenye jumba lake la mafichoni. Mama! Mzee yupo kwenye hatari sana,” alisema kijana huyo, akabadilisha muonekano wa sura yake, akawa na huruma ghafla kama Papa John Paul wa Pili alivyokuwa. “Jamaniiiiii!” “Mama hatuna muda,” alisema kijana huyo. Hakutaka kuchelewa, kwake, mume wake alikuwa kila kitu moyoni mwake, alimpenda kuliko kitu chochote kile. Kwa kuwa aliambiwa kwamba mumewe alikuwa akimsubiri, akamuita na binti yake kwa lengo la kwenda huko kuonana naye. Wakaondoka kwa kuwa alimwamini kijana yule lakini la zaidi ni kwa sababu alimwamini Innocent. Walinzi hawakujua chochote kile, wakawaruhusu kuondoka, wakaingia ndani ya gari na kuondoka. Baada ya Maxwell kuambiwa kwamba kila kitu kilikamilika, akapiga simu polisi na kujidai akitoa taarifa ya madawa ya kulevya. Polisi walivyosikia tu, haraka sana wakaelekea huko, walipofika na kufanya upekuzi, wakayakuta madawa hayo ya kulevya na hivyo mtu wa kwanza kushukiwa alikuwa mzee Todd. Taarifa ikatolewa kwamba mzee huyo alikuwa akitafutwa, na mbaya zaidi ilitoka taarifa iliyosema kwamba alikwenda Afrika kupeleka mzigo mwingine. Kiasi cha dola milioni moja kikawekwa mezani kwa kila mtu ambaye angefanikisha kukamatwa kwake. Mke wa mzee Todd, Juddie na mtoto wake, Martha walipelekwa mpaka katika chumba kilichokuwa na mwanga hafifu na kuambiwa watulie kwenye viti vilivyokuwa ndani ya chumba hicho. Hawakuelewa mahali walipokuwa, walikuwa wakiangalia huku na kule, chumba hicho kiliwaogopesha kwani mbali na kuwa na viti hivyo pekee, kuta za chumba hicho zilikuwa na michirizi ya damu ambayo ilionyesha kabisa kwamba hakikuwa chumba cha mchezo hata kidogo. Waliogopa, hawakujisikia amani. Japokuwa waliambiwa kwamba Todd alikuwa huko na ndiye ambaye alikuwa akiwahitaji, hawakuhisi kama kweli hilo jambo lilikuwa hivyo, walihisi kabisa kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea. Walimwamini Innocent, hawakuwa na hofu naye hata kidogo. Watu waliokuwa wamewachukua hawakuwafahamu lakini kwa kuwa Innocent alihusika katika kila kitu, hawakuhofia kitu chochote kile. Wanaume wale walikuwa wakiingia kwa zamu, kila walipowauliza, walijibiwa kwamba walitakiwa kutulia kwani kila mtu aliyekuwa ndani ya chumba kile hakutakiwa kupiga kelele kwa kuwa ukimya ndiyo ulikuwa ulinzi wao pekee. “Tell us, where is Todd?” (tuambie, Todd yupo wapi?) aliuliza Juddie. “I told you to shout the hell up,” (nimekwambia nyamaza) alisema mwanaume huyo kwa hasira na sauti kubwa iliyomfanya Juddie na mtoto wake, Martha kuogopa. Wote waliogopa, waliwaona watu hao kuwa mahatili ambao wangewatoa roho yao muda wowote ule kama tu wangeendelea kuongea kitu ambacho hakikutakiwa kufanyika ndani ya chumba hicho. Waliendelea kukaa mpaka ilipofika usiku wa manane. Hawakulala, bado walikuwa wakiamini kwamba Todd angetokea lakini mpaka inafika alfajiri hakukuwa na dalili za mwanaume huyo na kugundua kwamba kulikuwa na jambo jingine lililokuwa likiendelea. Asubuhi, wakaletewa chai na kuanza kunywa. Hawakunywa kwa raha, walikunywa huku wakiwa na hofu nzito mioyoni mwao. Ilipofika majira ya saa nne, mwanaume mmoja akaingia na kuanza kuzungumza nao. Huyo ndiye aliyewaambia kilichokuwa kikiendelea, walikuwa mahali pale kwa kwa sababu Todd alikuwa amewafanya jambo baya ambalo hakutaka kuwaweka wazi. Walishangaa, waliuliza kuhusu jambo hilo baya, hawakuambiwa kitu zaidi ya kuambiwa watulie tu. Maxwell alipigiwa simu na kuambiwa kwamba kila kitu kilikuwa tayari. Akaridhika na hivyo kuanza kumtafuta Todd kwenye simu lakini akamkosa. Hakutaka kujali sana, alichokifanya ni kuwapigia vijana wake na kuwauliza kilichokuwa kikiendelea. Kitu ambacho kilimchosha ni baada ya kusikia kwamba mwanaume huyo alikuwa ametoroka. “Ametoroka?” aliuliza Maxwell, hakuamini alichokuwa amekisikia. “Ndiyo mkuu!” “Inawezekana vipi? Hivi kweli anaweza kutoroka ndani ya meli? Anaweza kuogelea?” aliuliza Maxwell huku akionekana kuchanganyikiwa. Kijana huyo akaanza kumwambia kila kitu kilichokuwa kimetokea bandarini mpaka Todd kutoroka akiwa na kijana waliyemuokota baharini kwa lengo la kumsaidia. Maxwell alichanganyikiwa, hakuamini alichokisikia, akahisi kabisa alikuwa akidanganywa au kulikuwa na mchezo uliokuwa umechezwa. Si kwamba hakufahamu kuhusu mapigano ya risasi yaliyotokea bandarini huko Cape Town, alifahamu kila kitu lakini kilichomshangaza ni namna ambavyo watu hao walitoroka. Kwa hasira, akawaambia wawatafute na kukata simu. Kichwa chake kilichanganyikiwa. Kutoroka kwa Todd kilimaanisha kitu kibaya kwake, hakutaka kuona mwanaume huyo akiendelea kuwa hai, kuendelea kuwa hai kungemaanisha mwisho wake kwani kwa namna moja ama nyingine ilikuwa ni lazima kumtafuta na kulipa kisasi. Wakati huo, taarifa za habari katika vituo mbalimbali vya televisheni vilikuwa vikitangaza kuhusu kutafutwa kwa mwanaume huyo. Kila kona, picha yake ilionekana. Dunia ilipigwa na butwaa, kile kilichokuwa kikionekana kilimshangaza kila mmoja. Wengi hawakuamini kama utajiri wa mzee huyo ulitokana na biashara ya madawa ya kulevya aliyokuwa akiifanya. Wema wake, ukasahaulika, chuki za Wamarekani dhidi yake zikaanza kutawala katika mioyo yao. Kila kona watu walikuwa wakiongea kuhusu jambo hilo tu, waliandika mabango, kwenye mitandao walitoa maoni yao huku wakiitaka dunia iseme mahali alipokuwa mwanaume huyo aliyekuwa akiwapoteza vijana wengi kwa kuwauzia madawa ya kulevya. Maofisa wa FBI (Federal Bureau Of Investigation) wakaanza kumtafuta nchini Marekani huku wale wa CIA (Central Interlligence Agency)wakiondoka kwenda barani Afrika ambapo waliambiwa mtu huyo alikuwepo kwa lengo la kumtafuta. “We have one week! We have to arrest this dude,” (tuna wiki moja! Inapaswa tumkamate huyu mshikaji) alisema ofisa mmoja. “Did you find out where he is by now?” (ulikwishajua mahali alipokuwa sasa hivi?) “Nope! But we have to,” (hapana ila inabidi tumkamate) Wakati picha zake zilipokuwa zikitoka katika vyombo mbalimbali vya habari ndipo kipindi hichohicho ambacho Brown aliona kwenye televisheni. Alichoamini ni kwamba Todd alikuwa nchini Marekani lakini baada ya kuambiwa na mlinzi kwamba alikuwa akihitajika na mwanaume huyo getini, hakuamini. Kiasi cha pesa kilichokuwa kimewekwa kilikuwa kikubwa mno, hakutaka kuona akikikosa, kwake, pesa zilikuwa muhimu kuliko hata urafiki. Alikwishawahi kuua watu wengi kwa sababu ya pesa, aliwasaliti watu wengine kwa sababu ya pesa, sasa kumsaliti Todd na kumchoma kwa polisi hakukuwa na tatizo lolote lile. Kule chumbani alipoelekea, akachukua simu yake na kuwapigia polisi. Aliwaambia kwamba alimuona Todd yule aliyekuwa akitafutwa na muda huo aliokuwa akizungumza nao alikuwa ndani ya nyumba yake, hivyo walitakiwa kufika haraka sana kumkamata. “Una uhakika ni yeye?” lilikuwa swali la kwanza kutoka kwa polisi aliyekuwa akizungumza naye kwa njia ya simu. “Acha ushamba! Sasa kama sina uhakika ningewapigia?” aliuliza Brown, swali alilokuwa ameulizwa lilimkasirisha kupita kawaida. Simu ilipokatika, akaondoka na kurudi sebuleni, alitaka kupiga stori na watu hao mpaka pale ambapo polisi wangefika na kumkamata. Alipokwenda sebuleni, kilichomshangaza ni kwamba mwanaume huyo hakuwepo. Alichanganyikiwa, akatoka na kwenda kwa mlinzi, akamuuliza na kumwambia kwamba watu hao wawili waliondoka. “Kwa nini uliwaruhusu?” “Hukuniambia niwazuie mkuu! Nilidhani umemalizana nao,” alijitetea mlinzi. Hilo lilimchanganya mno, aliona kabisa mamilioni ya dola yakiondoka mikononi mwake katika hatua ya mwisho kabisa. Hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya, alitoka mpaka nje ya nyumba ile na kuangalia huku na kule, si Todd wala Bruno aliyekuwa akionekana. Njiani, Todd na Bruno walipishana na gari mbili za polisi zikienda kule walipokuwa wametoka. Hapo, ndipo Todd akaamini kwamba Brown hakuwa mtu mzuri, alikuwa amewachongea kwa polisi kwa kuwa kukamatwa kwake kungemfanya kupata kitita cha dola milioni moja. *** Rahman alihisi kuchanganyikiwa, pale alipokuwa hakukukalika hata kidogo, alimwangalia mzee Jumanne ambaye naye kwa kumwangalia tu alionekana kuchanganyikiwa kama alivyokuwa. Alimpoteza mwanamke aliyekuwa akimpenda, tena katika hatua ya mwisho kabisa kabla ya kufunga ndoa. Alinyong’onyesa, pale alipokuwa alihisi kabisa akipigwa na baridi kali na kuanza kutetemeka, Uso wake ukajawa na aibu, kila mtu aliyemwangalia, akamuonea huruma kwani hakuvumilia, ni ndani ya sekunde chache machozi yakaanza kutiririka mashavuni mwake. Alimpenda mno Sharifa, kwake, msichana huyo alikuwa kila kitu. Alimuahidi mambo mengi mno, na kweli angeyatimiza kwa kuwa alikuwa akimpenda lakini cha kushangaza, msichana huyo akakimbia huku akipiga kelele kwamba hataki kuolewa kwa kuwa Bruno alikuwa hai. “Who is this man?” (huyu ni nani?) alimuuliza baba yake huku akionekana kuchanganyikiwa. “Bruno! The poorest fella in the village,” (Bruno! Mwanaume masikini kabisa hapa kijijini) alijibu baba yake kwani aliambiwa na mzee Jumanne kwamba Bruno alikuwa masikini mno. Mzee Jumanne alihisi miguu ikimtetemeka, alihisi kama angeanguka muda wowote ule kwani kile kilichokuwa kimetokea, hakukiamini hata mara moja. Hakutaka hata kumwangalia Rahman, alijua ni kwa jinsi gani mwanaume huyo alikuwa amechanganyikiwa, mtu muhimu kabisa ambaye alitakiwa kuzungumza naye alikuwa James, yeye ndiye aliyemuagiza kwenda kumuua Bruno, kama hakufa, nini kilitokea. James alikuwa kwenye harusi hiyo, yeye mwenyewe alikuwa amepigwa butwaa, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea mpaka Abdul kufika mahali hapo na kusema kwamba Bruno alikuwa hai. “James! Nini kimetokea?” aliuliza mzee Jumanne. “Sijui ni kitu gani kimetokea.” “Wewe si ulisema ulimuua?” “Hapana! Nilisema tulimtupa baharini!” “Ikawaje?” “Bila shaka alikufa kwani mawimbi yalikuwa yakipiga makubwa mno, bahari ilichafuka,” alisema James huku akimwangalia mzee huyo. “Niambie kitu kiimoja. Bruno alikufa au hakufa?” aliuliza mzee Jumanne. “Nahisi alikufa!” “Sikiliza. Sitaki uhisi. Niambie alikufa au hakufa?” “Kwa kweli ni ngumu kujibu ila kwa jinsi mawimbi yalivyokuwa, alikufa,” alijibu James, yeye mwenye hakuonekana kujiamini hata kidogo. Hilo likawa gumzo kijijini hapo, kila mtu alikuwa akiliongelea suala hilo kwamba iliwezekanaje Bruno yule waliyeambiwa kwamba alikufa baharini miezi sita iliyopita awe hai? Kila mmoja akashikwa na hamu ya kumuona, walitaka kuamini baada ya kumuona lakini si kusikia kama walivyokuwa wamesikia. Alipokimbia Sharifa na Abdul, hakukuwa na mtu aliyepafahamu, wote walikuwa wakisikilizia kumuona mtu huyo, je, ni kweli alikuwa hai au mchezo tu uliokuwa umepangwa? ITAENDEL
Simulizi : Mvuvi Bruno (Bruno The Fisherman) Sehemu Ya Tatu (3) Bruno na mzee Todd walikuwa wakitembea kwa kasi kuelekea Upande wa Kaskazini, vichwa vyao vilikuwa vikifikiria maisha yao yangekuwaje nchini Afrika Kusini huku yeye, Todd akitafutwa dunia nzima kwa makosa ambayo hakuwahi kuyafanya. Kichwa chake kilimfikiria mke wake na mtoto wake, aliwakumbuka, alitamani kuungana nao tena lakini kwa kipindi hicho haikuwezekana kabisa. Ukiachana na yeye, Bruno kichwa chake kilikuwa kikimfikiria mpenzi wake, Sharifa tu. Hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea huko, alitamani kurudi haraka nchini Kenya ili kwenda kuonana naye kwa mara nyingine lakini hilo halikuwezekana kabisa. Hakujua ni kwa jinsi gani angeweza kurudi nchini humo na wakati mfukoni mwake hakuwa na pesa yoyote ile. Hapo Cape Town walitembea kwa kujificha sana mpaka walipofika katika kituo cha treni za umeme cha Bellstar Junction. Hapo walitaka kupanda treni na kuondoka jijini Cape Town na kuelekea Johannesburg ambapo huko waliamini kwamba wangepata msaada wa kuondoka nchini humo. Hawakuwa na pesa mfukoni lakini mzee Todd alikuwa na pesa nyingi katika akaunti yake. Aliogopa kwenda benki na kuchukua pesa kwani sura yake ilikuwa dili kila sehemu na watu walimtafuta kwa nguvu kubwa. “Ninataka kuelekea benki kuchukua pesa, ila nahisi nitakamatwa. Unadhani unaweza kwenda kwa ajili yangu?” aliuliza Todd huku akimwangalia Bruno. “Kwenda benki?” “Ndiyo!” “Sawa. Benki gani?” aliuliza. “Barclays!” “Haina shida.” Alichomwambia ni kwamba alitakiwa kwanza kwenda huko kwa lengo la kuchukua karatasi ya kuandikia hundi (cheque) na yeye kuipeleka benki. Hilo halikuwa tatizo, akaelekea benki ambapo huko akakutana na dada mmoja wa Kizulu na kuanza kuongea naye. Alizungumza naye huku akionekana kuwa mchangamfu mkubwa, alijua kumteka mtu kupitia mazungumzo yake kiasi kwamba msichana huyo aliyeitwa kwa jina la Susan akabaki akikenuua tu kwani kila neno alilolizungumza Bruno kwake liliukuna moyo wake. “Umetoka wapi?” aliuliza Susan, hakuwahi kukutana na mwanaume aliyekuwa akiongea kama Bruno. “Kenya!” “Ooh! Kumbe Afrika Mashariki. Nawapenda watu wa huko, wanaongea sana, ni wachangamfu mno. Si ndiyo ilipo Tanzania?” aliuliza msichana huyo. “Ndiyo!” “Ninawapenda sana Afrika Mashariki!” Hilo likampa uhakika wa kukamilisha kile alichokitaka. Akamwambia kwamba lengo la kufika mahali hapo lilikuwa ni kuchukua kitabu cha hundi. Hilo halikuwa tatizo, Susan akampa kitabu hicho na Bruno kuondoka mahali hapo. Huko alipokwenda, alimfuatan mzee Todd na kumpa kile kitabu. Mzee huyo akakichukua na kuandika kiasi cha dola milioni moja apewe mkononi. Bruno alipokichukua kitabu hicho na kuangalia, hakuamini, alimwangalia vizuri mzee Todd, alihisi kama kiasi kile cha pesa alichoandikiwa kilikuwa ni uongo. “Dola milioni moja?” “Ndiyo! Hakikisha unakwenda na kufungua akaunti yako. Utazichukua hizi pesa na kuziingiza kwenye akautnti yako, tutakuwa tunazitumia kupitia akaunti yako,” alisema mzee huyo. Bruno alichanganyikiwa mno, hakuamini alichokuwa akikisoma kwenye cheki ile. Kiasi kile, kwa pesa za shilingi ya Kenya kilikuwa ni sawa na bilioni moja, milioni mia mbili na senti kadhaa huku kwa shilingi ya Kitanzania ikiwa ni zaidi ya shilingi bilioni mbili. Akaondoka mahali hapo na kumuacha mzee huyo akiwa sehemu amekaa kwa kujificha sana. Alipofika, kama kawaida yake akamfuata Susan na kuanza kuongea naye. Kitu cha kwanza alichohitaji kilikuwa ni kufungua akaunti. “Una randi elfu ishirini?” aliuliza Susan. “Ya nini?” “Kufungulia akaunti!” “Sina! Ila nitakuwa nazo baada ya kufungua akaunti!” “Kivipi?” Alichokifanya Bruno ni kumuonyeshea Susan ile hundi aliyokuwa ameandikiwa. Msichana huyo hakuamini, kilikuwa kiasi kikubwa cha pesa ambacho kilitakiwa kuingia mara baada ya kufunguliwa kwa akaunti hiyo. Haraka sana Susan akampeleka sehemu ya kupiga picha, akafanya hivyo na kufuata taratibu zote na kiasi hicho cha pesa kumlipia yeye mwenyewe kwani aliamini kwamba angelipwa kwa fadhilla alizokuwa ameonyesha. Mchakato ulipokamilika, hundi ile ikachukuliwa na pesa kutolewa katika akaunti ya mzee huyo na kuingizwa katika akauti ya Bruno, akatoa kiasi cha dola elfu ishirini na dola elfu moja na kumpa Susan kisha kuondoka zake. Hilo likamfurahisha mzee Todd na kuona kwamba walikuwa wakienda kufanikiwa kile walichokuwa wakikitaka. Wakawa na pesa, walichokifanya ni kukata tiketi na safari ya kuelekea Johannesburg kuanza. Njiani, mzee Todd alikuwa na kofia, hakutaka kugundulika na mtu yeyote yule kwani aliamini kwamba dunia nzima ilikuwa ikifahamu kama alikuwa akitafutwa. Treni hiyo ilichukua saa moja mpaka kufika katika Jiji la Johannesburg ambapo wakateremka na kufikiria kwenda kupumzika hotelini. Kitu walichokifanya ni kununua simu. Kila mmoja akanunua yake pamoja na laini ambazo zilisajiliwa kwa jina la Bruno. Kila kitu kilipokamilika, kwa kuwa namba ya mke wake aliifahamu, akaanza kumpigia. Simu haikuita muda mrefu ikapokelewa na mkewe. Sauti yake haikuwa ya kawaida, alikuwa akizungumza huku akilia. Alihitaji msaada kwani pale alipokuwa hakukuonekana kuwa salama kabisa. Wakati akizungumza naye, mara simu akapokonywa na sauti ya mwanaume kusikika kutoka upande wa pili. Iliongea kibabe, sauti ambayo haikuonekana kuwa na mchezo hata kidogo. “Tunakuhitaji ndani ya saa arobaini na nane. Mbali na hilo, utaziona maiti za familia yako ufukweni. Una saa arobaini na nane kujisalimisha kwetu,” alisema mwanaume huyo kwa sauti yenye utetemeshi. “Wewe nani?” “Si lazima unifahamu. Fanya kama nilivyokwambia,” alisema mwanaume huyo na kukata simu. Mzee Todd akabaki akitetemeka, hakujua mwanaume huyo aliyekuwa akizungumza upande wa pili alikuwa nani. Akachoka, akatulia kwenye kiti huku akitetemeka kupita kawaida. Hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya. Maneno aliyozungumza mwanaume huyo yalionyesha kabisa kwamba familia yake haikuwa salama huko ilipokuwa. “Halo…halo…” aliita lakini hakukuwa na sauti iliyosikika upande wa pili. Bruno alibaki akimwangalia mzee huyo, alikuwa akilia, machozi yalitiririka mashavuni mwake. Alionekana kuumizwa na kile kilichokuwa kimetokea. Aliipenda familia yake na mara kadhaa alikuwa akiizungumzia kwamba aliikumbuka na alitamani sana kuonana nayo. Akamuuliza kilichokuwa kimetokea, akamwambia kwamba familia yake ilitekwa na mtu asiyemfahamu na alimuhitaji ndani ya saa arobaini na nane kitu ambacho kilikuwa ni vigumu kufanyika. “Kwa hiyo?” aliuliza Bruno kwa sauti ya upole. “Sijajua ni kitu gani kinatakiwa kufanyika. Familia yangu itauawa! Familia yangu itauawa!” alisema mzee Todd huku akilia kama mtoto. *** Hakukuwa na mtu aliyekuwa muhumu kwa kipindi hicho kama mzee Todd. Maofisa wa CIA walikuwa wakimtafuta kila kona, walimtaka mzee huyo kwa udi na uvumba. Walihangaika kila kona kumtafuta lakini hawakujua mahali alipokuwa. Wakati mwingine waliambiwa kwamba alikuwa nchini Msumbiji, walisafiri na kwenda huko lakini hawakufanikiwa kumpata. Mzee huyo aliwasumbua kichwa kupita kawaida. Dunia ilikuwa kimya, kila mmoja alitaka kuiona nguvu ya Marekani kwamba kama ingeweza kumpata mwanaume huyo au la. Walihangaika, kwenye simu hakuwa akipatakana na hata walipojaribu kuitraki simu yake hawakuambulia kitu chochote kile. Walisumbuka kwa muda wa wiki nzima ndipo siku moja wakafanikiwa kuiona simu ya mke wake ikiita, ilikuwa ikipigiwa na simu kutoka nchini Afrika Kusini. Waliifuatilia simu ya mkewe bila yeye mwenye kugundua. Walijua kwamba ilikuwa ni lazima kwa mzee huyo kuwasiliana na familia yake na ndiyo maana walikuwa makini sana kuhakikisha wanakamata mawasiliano kutoka kwa watu hao. Simu iliyopigwa katika simu ya mwanamke huyo ilitoka Afrika Kusini walichokifanya ni kuiunganisha na kuanza kusikiliza mazungumzo ya watu hao. Maneno waliyoyasikia yaliwashangaza, Juddie alisikika akilia huku akiomba msaada kuonyesha kwamba alikuwa kwenye hatari na baada ya hapo wakasikia sauti ya mwanaume ikimwambia kwamba alimpa saa arobaini na nane tu awe amejisalimisha. Maofisa wa CIA hawakujua kilichokuwa kikiendelea, hawakujua ni kitu gani kilikuwa nyuma ya pazia. Ili kujua kile kilichokuwa kikiendelea ilikuwa ni lazima kumkamata Todd na kumuuliza kuhusu hayo yote yaliyotokea na huku wakiwa wameandaa kesi kwa lengo la kumpeleka mahakamani. “Simu imetoka Afrika Kusini karibu na kituo cha treni cha Johannesburg Park. Waambie vijana waende huko, wamuwahi mzee huyo na kumtia mikononi mwao,” alisema mwanaume mmoja, haraka sana simu ikapigwa Afrika Kusini, maofisa wa CIA waliokuwa huko, wakawataarifu kwamba mahali walipokuwa hakukuwa mbali na kituo hicho, hivyo walikuwa wakienda haraka sana kuhakikisha mzee huyo anatiwa mikononi. Johannesburg haikuonekana kuwa sehemu salama kwa maisha yao, ilikuwa ni lazima waondoke nchini humo huko Bruno akimwambia mzee Todd kwamba walitakiwa kuelekea nchini Kenya kwani alikuwa akizijua sehemu nyingi za kujificha ikiwemo kijijini kwake. Hilo halikuwa tatizo, lakini kabla ya kuondoka kuelekea nchini humo ilikuwa ni lazima wapate mtu ambaye angewaunganishia na meli yoyote ile ili waondoke kuelekea Kenya. Kwa Bruno, kwake lilionekana kuwa suala kubwa na gumu kwani humo Afrika Kusini, hakuwa na ndugu, rafiki au mtu yeyote yule. Walitamani kukutana na mtu yeyote ambaye angewaambia mahali pa kwenda kwani kwa jinsi mzee Todd alivyokuwa akitafutwa, walijua kabisa kwamba wasingeweza kupanda ndege, ilikuwa ni lazima kuondoka nchini humo kwa kutumia gari au meli. “What should we do?” (Tufanye nini?) aliuliza mzee Todd. “Let’s go to Soweto. I’m sure there are people who can help us out,” (Au twende Soweto, naamini huko kuna vijana wengi ambao wataweza kutusaidia,” alisema Bruno. Hakuwahi kufika Soweto lakini alisikia tu kwamba huko kulikuwa ni uswahilini mno, kulikuwa na wahuni wengi ambao walikuwa wakipanga madili yao ya kuvamia benki na hata kufanya uchafu wa kila aina. Ilikuwa ni lazima kwenda huko kama tu walikuwa wakihitaji msaada wa kuondoka nchini humo. Soweto ilikuwa ndani ya Johannesburg hivyo haikuwa vigumu kwao kufika huko. Kwa kuwa walikuwa na kofia, miwani hawakuhofia kumuuliza mtu yeyote mahali ilipokuwa Soweto. Walipouliza kwa mtu mmoja tu, akawaambia mahali kulipokuwa na kuanza kwenda huko. Walikuwa na hofu, waliijua Soweto, kulikuwa na fujo za kila aina, watu walikuwa wakiuawa kila siku, haikuwa sehemu salama ya kuishi kwani watu wote waliokuwa wakiishi humo walikuwa waswahilini ambao waliamini zaidi katika fujo. Baada ya dakika kadhaa, wakaingia Soweto. Sehemu hiyo haikutofautiana na sehemu nyingine za uswahilini. Kulikuwa na nyumba mbovu, barabara za vumbo na kitu pekee ambacho kilipendezesha mtaa huo ni uwanja wa timu ya Orlando Pirates. Kila mtu alikuwa akiwaangalia jinsi walivyokuwa wakitembea mtaani. Walikuwa wakiangalia huku na kule, kwa kuwaangalia tu ilikuwa ni rahisi kugundua kwamba watu hao walikuwa wageni. Walitembea kwa kujishtukia huku muda mwingi wakiangalia huku na kule. Walitembea mpaka walipokuta sehemu iliyokuwa imefungwa kamba kwa mbele. Hiyo ilikuwa ni kuingia ndani kabisa ya mtaa huo wa Soweto. Watu waliokuwa wakipita hapo walikuwa wale wa kitambo au wahuni ambao kutoa roho za watu ilikuwa ni sawa na kuua mbu. Magari yote yaliyokuwa yakiibwa mjini, yalipitia hapo na kamba ile kufungwa. Hao ndiyo walikuwa chanzo cha mashirika ya umeme kuanzia mfumo wa luku kwa kuwa hawakuwa wakilipa na kila siku watu wa umeme waliokuwa wakienda huko walikuwa wakipigwa na wengine kuuawa. Walisimama pale barabarani huku wakijifikiria kama iliwezekana kuvuka mahali pale au la. Kwa kupaangalia, palionekana kuwa pa kawaida, hakukuwa na mtu yeyote, barabara ya vumbi haikuwa hata na gari moja. “Kuna kamba! Hii inamaanisha haturuhusiwi kuingia?” aliuliza Bruno, hakujua maana ya kamba ile. “Nahisi kwa magari! Sisi tuingie,” alisema mzee Todd. Hicho ndicho walichokifanya, wakaingia kwa kuivuka kamba ile, wakateembea kwa mwendo wa kawaida kusonga mbele huku kila mmoja akionekana kuogopa mno. Walipopiga kama hatua mia moja, mbele wakamuona mwanaume akijitokeza na kusimama barabarani. Mkono wa kulia alishika panga huku wa kushoto akiwa na bunduki aina ya AK-47. Mwanaume huyo alivalia usongo kichwani kama Rambo huku akiwa na kaoshi na kipenzi kilichokuwa kimechanikachanika. Wakasimama na kuanza kuangaliana na mwanaume yule. Kabla hawajachukua hatua yoyote ya kufanya, wakageuka nyuma, wanaume wengine waliokuwa na muonekano kama wa mwanaume yule aliyekuwa mbele yake wakatokea, walikuwa zaidi ya wanne. Mpaka kufikia hapo, wakajua maana ya Mtaa wa Soweto. Walisikia tu kwamba ndani ya mtaa huo mauaji yalikuwa waziwazi, halikuwa jambo la kushangaza kuwaona watu wakipigwa au miili yao kutupwa barabarani kama mizoga. “Hey! White! What are doing here?” (Hey! Mzungu! Unafanya nini hapa?) lilikuwa swali la kwanza alilouliza mmoja wa wanaume waliokuwa nyuma yao. Hakukuwa na Mzungu aliyejaribu kwenda Soweto. Watu hao hawakupendwa huko kwa kuwa weusi waliamini kwamba walikuwa katili na ndiyo waliokuwa wakiwatesa watu weusi wengi nchini humo. Kulikuwa na mapigano ya chini kwa chini baina ya Wazungu na watu weusi. Walitafutana kimya kimya, Wazungu walikuwa wakiokotwa wakiwa wamekufa na hata wakati mwingine nao watu weusi waliokotwa wakiwa wamekufa. Hakukuwa na mtu aliyemaliza uhasama huu, ulikuwa ukiendelea huku kila mmoja akijiona kuwa sahihi na kusingekuwa na mtu yeyote wa kumbabaisha. Soweto haikuwa na maendeleo makubwa na watu hao waliamini kwamba Wazungu ndiyo waliokuwa wakiinyima maendeleo kwani pamoja na kuwa katika jiji la biashara la Johannesburg lakini uswahilini bado kuliendelea kuwa Soweto. Wazungu wengi waliwahusisha wanawake weusi katika biashara ya ngono. Walikuwa wakiwachukua na kuwapeleka katika madanguro ya Kizungu na hata cassino na kuanza kuwafanya walivyotaka. Wanawake hao walitafuta pesa, walijua kwamba walikuwa wakijidhalilisha lakini hawakuwa na jinsi, kwa kuwa walikuwa wakaiingiza pesa, kwao Kitendo cha mzee Todd kuonekana humo ilikuwa ni hatari kwa maisha yake, aliulizwa swali lakini hakuwa na jibu lolote lile. Wakawasogelea na kuanza kuwaangalia vizuri, waliporidhika, wakawachukua, wakawafunga kamba na kuanza kuondoka nao. Wote wakajua huo ndiyo ulikuwa mwisho wao, walikuwa na hofu na kuona kwamba huo ungekuwa mwisho wao. Walipitishwa mitaani, kila mtu aliyekuwa akiwaangalia, alishangaa na zaidi kuliko yote walikuwa wkaimshangaa mzee Todd, ilikuwaje ajiamini aende Soweto na wakati Wazungu wote walikuwa wakiogopa kwenda huko? Ni mwendo wa dakika tano tu wakafika katika jumba moja bovu na kuingizwa humo na kuamriwa watulie kwani kulikuwa na kiongozi wao aliyetakiwa kuwaona na kuwauliza maswali machache kabla ya kutoa uamuzi kwamba baada ya kuuawa huyo Mzungu, naye Bruno alitakiwa kuuawa au la. “Do they want to kill us?” (wanataka kutuua?) aliuliza mzee Todd huku akionekana kuchanganyikiwa. “Yeah! They really want to kill us. Let’s get prepared,” (Ndiyo! Wanataka kutuua hasa. Tujiandae tu) alisema Bruno kwani kwa jinsi watu wale walivyokuwa wakionekana, walionyesha kila dalili za kutaka kuwamaliza watu hao. Kitu walichokifanya ni kuwapokonya simu zao na kwenda kuzifungia ndani. Wakawapekua na kuwakuta na pesa, dola aambazo napo wakazichukua na kadi ya benki ambayo kwao ilikuwa muhimu kuliko kitu chochote kile. “How much do you have?” (mna kiasi gani?) aliuliza mwanaume mmoja huku akiwa ameshika kadi ya ATM. “We have nothing…” (hatuna kitu) alijibuu Bruno. “You must be kidding me,” (utakuwa unanitania) “Serious brother, we have nothing,” (siriazi kaka, hatuna kitu) alijibu Bruno, hakutaka kumuacha mzee Todd aongee kwani kwa hofu aliyokuwanayo ingekuwa rahisi kusema kiasi chote kilichokuwa kwenye akaunti na wakati yeye mwenyewe alikuwa akikitaka. “Give me the password,” (nipeni namba ya siri) alisema mwanaume huyo.
Hilo lilikuwa jambo gumu ambalo lisingeweza kufanyika. Kitendo cha kumpa mwanaume huyo namba ya siri ya kadi ile ilimaanisha kwamba wangekwenda kuchukua kiasi chote cha pesa ambacho kilikuwa kikubwa mno. Bruno hakutaka kukubali, kwake, zile pesa zilikuwa kila kitu, alizitaka na ndiyo maana aliamua kumpambania mzee Todd kumfikisha salama alipokuwa akipataka yeye lakini si kuona akipoteza pesa zile. Jamaa huyo aliona kama alifanyiwa kiburi kwa kutopewa namba ya siri ya kadi ile, akachukua bastola yake na kuwanyooshea huku akitaka aambiwe kuhusu namba hizo. Wakati kila mmoja akijua kwamba walikuwa wakipigwa risasi, ghafla mlango ukafunguliwa na wanaume wawili kuingia humo. Mmoja alikuwa yule kiongozi wao aliyekwenda kuitwa kwa lengo la kuja kuwaona watu waliokuwa wamewakamata. Kiongozi huyo alipofika hapo, akawaangalia watu hao. Ghafla, akashtuka, hakuamini kumuona mtu huyo mahali hapo. Hakuwa mzee Todd, bali alikuwa Bruno. Akamsogelea na kumwangalia vizuri. Alimfahamu mtu huyo japokuwa ilipita miaka kumi hawakuwa wameonana. Bruno alibaki akimshangaa mtu huyo, hakumfahamu na aliona kabisa kwamba siku hiyo ndiyo ilikuwa ya kwanza kumuona mbele ya macho yake. “Bruno!” aliita mwanaume huyo kitu kilichomfanya Bruno kushtuka, si yeye tu bali hata watu wengine waliokuwa mahali hapo. “Who the hell are you?” (wewe nani?) aliuliza Bruno huku akimwangalia mwanaume huyo. “Niangalie! Hunijui kweli?” aliuliza mwanaume huyo kwa Kiswahili kilichomfanya Bruno kugundua kwamba mtu huyo alitoka Afrika Mashariki. Bruno alimwangalia, hakuweza kumkumbuka mwanaume huyo, kwake, alionekana kuwa mgeni kabisa. Aliyaangalia mavazi aliyokuwa ameyafaa, yalimuonyesha jinsi alivyokuwa katili na mtemi katika mtaa huo. “Bruno! Umenisahau Ibrahim Onyango! Kiongozi wa watoro shuleni!” alisema mwanaume huyo. Alipolitaja jina la Onyango tu, kumbukumbu za Bruno zikaanza kurudi nyuma. Akamkumbuka mwanaume huyo, aliwahi kusoma naye sekondari mpaka pale walipomaliza shule na kufeli vibaya huku yeye akianza kazi ya uvuvi. Onyango alikuwa kiongozi wa watoro shuleni kwao, hakupenda kusoma, kila siku aliwaambia wazazi wake kwamba shule ilimkataa na ilikuwa ni lazima kuondoka Kenya na kuelekea Afrika Kusini kutafuta maisha. Wazazi wake walizungumza naye sana, walikuwa ni wazazi waliokuwa na uuwezo mkubwa, walimpa kila kitu lakini Onyango hakutaka kukubali, mali zile alisema ni za wazazi wake na yeye ilikuwa ni lazima kutafuta mali zake, hakuona sehemu ambayo angepata maisha mazuri zaidi ya kwenda Afrika Kusini. Alitoroka Kenya na kuelekea Afrika Kusini. Watu walishangaa lakini yeye aliamua kuwa na maisha yake. Miaka zaidi ya kumi ilikuwa imepita, leo, Bruno alikutana na Onyango Afrika Kusini huku akiambiwa kwamba huyo ndiye alikuwa kiongozi wao. “Unafanya nini huku?” aliuliza Onyango huku akimwangalia Bruno. “Ni habari ndefu sana! Tunaweza kwenda sehemu kuongea nje ya hapa manake hizi bunduki zinanikosesha amani kabisa,” alisema Bruno. “Haina noma!” Bruno hakutaka kubaki peke yake, aliamini kwamba kama angemuacha mzee Todd ndani ya chumba kile basi angepigwa mikwara na kutoa namba za siri za kadi, alichokifanya ni kuondoka na mzee huyo kwenda uani na kuanza kuzungumza na Onyango. Waliongea kwa furaha, walicheka na kukumbushiana mambo mengi ya nyuma. Muda wote huo mzee Todd alikuwa akiwasikiliza tu, hakuelewa Kiswahili, alibaki kimya huku mawazo yake yakiwa yanaifikiria familia yake tu. “Ikawaje?” “Washikaji wakanitosa baharini! Mtu wangu nilipiga mbizi mpaka nikaokolewa na Warusi,” alisema Bruno. “Na huyu mzee vipi?” “Nilimkuta kwenye meli hiyo, wana walitaka kumuua, ila nilipotoroka, nikatoroka naye!” “Wewe ninja! Yaani ulitoroka kwenye meli, wewe ninja mchizi wangu,” alisema Onyango huku akitoa tabasamu pana. Waliendelea kukaa uani na kuendelea kuzungumza. Wakati mazungumzo yakiwa yamepamba moto, wakaanza kusikia kelele kutoka mtaani, hawakujua kulikuwa na nini. Wakati wakiwa wanajiuliza, wakaanza kusikia milio ya risasi, ilikuwa ni kama milio ya majibizano. Kila mmoja akaogopa, Onyango akachukua bunduki yake, akapanda ukuta na kuangalia kwa nje kuona kulikuwa na nini. Macho yake yakatua kwenye gari moja jeusi, lilikuwa jipu, kulikuwa na Wazungu wanne waliovalia suti ambao walikuwa wakipambana na vijana wake. “Kuna nini?” aliuliza Bruno huku akiogopa. “Wazungu! Wamekuja kupambana! Sijui kuna nini!” “Tufanye nini?” “Njooni huku!” Aliwachukua na kuwapeleka katika mlango mwingine wa kutoka ndani ya eneo la nyumba hiyo na kuwaambia wakimbie kwani hawakujua watu hao walikuwa wakina nani na walihitaji nini. Hilo halikuwa tatozo, wakaagana na kuanza kukimbia mahali hapo. Milio ya risasi iliendelea kusikika kila kona. Wazungu wale walikuwa hatari, walikuwa na shabaha kupita kawaida, kila risasi iliyokuwa ikitoka, ilitoka kwa malengo na kumpata mtu. Japokuwa Soweto kulizoeleka kusikika milio ya risasi lakini siku hiyo hali ilionekana kuwa tofauti. Soweto ilibadilika na kuwa kama uwanja wa mapambano. Watu weusi wengi waliuawa na hakukuwa na mtu aliyejua sababu iliyowafanya Wazungu hao kufika humo na kuanza kushambulia. Bruno na mzee Todd waliendelea kukimbia, hakukuwa na mtu aliyesimama, kila mtu alikuwa akiokoa maisha yake. Wakakimbia mpaka mlimani na kuanza kuangalia kwa chini kwa mbali. Waliwaona watu wakipambana, milio ya risasi iliendelea kusikika kwa sauti kubwa huku watu wengine wakikimbilia kule walipokuwa. “Mungu wangu! Nimesahau kadi ya ATM kwa yule jamaa,” alisema Bruno mara baada ya kujipekua mifukoni kuangalia kadi ile. “Unasemaje?” “Kadi na simu! Tumesahau ndani ya nyumba ile,” alisema Bruno huku akionekana kuchanganyikiwa, kwake, ilikuwa ni afadhali kusahau simu lakini si kadi ya ATM. “Tuondoke! Achana navyo! Tuondoke!” alisema mzee Todd, kwake, pesa zilizokuwa katika akaunti aliyofungua Bruno kilikuwa kiasi kidogo sana cha pesa. “Haiwezekani!” “Bruno! Tuondoke!” “Siwezi kuondoka na kuacha kadi ile. Ni lazima nirudi!” “Urudi?” “Ndiyo!” “Kule kwenye mapambano?” “Hukohuko!” “Haiwezekani!” “Siwezi kuendelea mbele pasipo ile kadi. Kuna hela nyingi sana, hatuwezi kuacha kadi kiholelea,” alisema Bruno. Walikuwa wakivutana, mzee Todd alimwambia Bruno kwamba walitakiwa kuondoka lakini kijana huyo hakutaka kuelewa kitu chochote kile. Alichomwambia ni kwamba amsubiri pale na yeye kwenda kule kuchukua kadi. Alikuwa akikimbia kuteremka mlima. Alipishana na watu waliokuwa wakipandisha, kila mmoja alikuwa akimshangaa, wao walikuwa wakikimbia risasi lakini ndiyo kwanza Bruno alikuwa akizikimbilia. Walimuona kama mtu aliyechanganyikiwa lakini mwenyewe hakuwa tayari kuona akirudi nyuma, kwake, kadi ile ilikuwa muhimu kuliko kitu chochote kile. Milio ya risasi iliendelea kusikika lakini hakujali, alipofika, akaanza kupita kwenye vichochoro. Alikuwa peke yake, watu wengine walikuwa wamejifungia vyumbani mwao na wengine kukimbia. Hakukumbuka mahali nyumba ile ilipokuwa lakini baada ya kukumbuka kwamba ndipo mahali watu wale walipokuwa wakipambania, akaanza kufuatilia milio ya risasi hiyo. Alitembea harakaharaka kwa kujificha mpaka alipofika mahali ilipokuwa nyumba ile. Hakutokea kule ilipokuwa nyumba ile bali alipotokea ni nyuma ya gari la Wazungu wale waliokuwa wakipambana. Akawaangalia vizuri Wazungu wale, jinsi walivyokuwa wakipambana na hata kukwepa risasi, akagundua kwamba hawakuwa watu wa kawaida hata kidogo, mafunzo waliyokuwa nayo yalikuwa hatari mno. “Who the hell are these people?” (hawa ni wakina nani?) alijiuliza swali alilokosa jibu, kijasho chembamba kilikuwa kikimtoka mfululizo. *** Mawasiliano yakafanyika haraka sana kutoka nchini Marekani, maofisa wa CIA waliokuwa nchini Afrika Kusini walitakiwa kwenda kule simu ilipopigwa ambapo wakaelekezwa na kuelekea huko. Walipofika katika kituo cha treni jijini Johannesburg ambapo ndipo mzee Todd alipokuwa amepiga simu, hawakuweza kumuona mzee huyo. Haraka sana wakawapigia simu maofisa waliokuwa nchini Marekani na kuwaambia kile kilichokuwa kikiendelea kwamba mwanaume huyo hakuwa mahali hapo. Hilo halikuwa tatizo, kwa kutumia satalaiti yao kwa mfumo wa GPS, wakaweza kuiunganisha simu ya mzee Todd na wao kuweza kuona jinsi simu ile ilipokuwa kipindi hicho. Waliona ikiwa inatoka sehemu moja kwenda nyingine, hawakutaka kubaki mahali hapo kwani kutoka katika kituo hicho mpaka mahali simu hiyo ilipokuwa hakukuwa mbali. Wakaondoka na kumfuata mahali alipokuwa kwani simu ile ilionyesha kwamba ilikuwa katika Mtaa wa Soweto. Hawakuchukua muda mrefu wakawa wanakaribia kuingia katika mtaa huo. Walipoangalia tena kifaa chao wakaona kwamba simu imetulia sehemu moja kitu kilichowafanya kujua kwamba ilikuwa imewekwa ndani, sehemu fulani na watu hao kutulia. Waliijua Soweto, walijua tabia za watu wa huko kwamba hawakuwa na mchezo hata mmoja, walizijua chuki zao kali dhidi ya Wazungu, walijua kabisa kama wangekwenda kimama basi ilikuwa ni lazima kuuawa. Wakakaanda bastola zao na kuingia ndani huku wakiwa na gari lao ambalo vioo vyake havikumruhusu mtu wa nje kuona ndani. Walipofika katika eneo ambalo halikuwa mbali na mahali simu ilipokuwa, wakasimamisha gari lao. Nyumba iliyokuwa mbele yao ndiyo ambayo ilikuwa na mtu waliyekuwa wakimtafuta, nje ya nyuumba ile kulionekana vijana mbalimbali wakifanya mambo yao, wengine walikuwa wakipiga stori na wengine kujitenga pembeni huku wakivuta bangi. “Tufanye nini?” aliuliza jamaa mmoja. “Tukavamie!” “Ila tuwe makini kwanza, tunaweza kufa na mbaya zaidi hatujui wale jamaa wana nini,” alisema mwingine. Wale vijana waliokuwa nje ya nyumba ile walionekana kulishuku gari lile, lilikuwa limekuja mahali pale na kusimama, hawakujua kulikuwa na kitu gani kilichokuwa kikiendelea lakini wakahisi kabisa kwamba watu waliokuwa humo ndani hawakuwa watu wema. Wakachukua bunduki zao na kuanza kulisogelea. Maofisa wale wa CIA walipowaona wanakuja, wakaziandaa bastola zao kwa lengo la kushambuliana kwani walijua kwamba kama wale vijana wangejua kwamba ndani ya gari lile walikuwemo wao, Wazungu basi ilikuwa ni lazima kuwamaliza. “Paa!” ulisikika mlio mmoja wa risasi, jamaa mmoja wa pale Soweto miongoni mwa wale vijana waliokuwa wakipiga hatua akaanguka na damu kuanza kumtoka kifuani. Vijana wale wakashtuka na kugundua kwamba kweli watu wale hawakuwa wazuri kwao, wakajificha na kuanza kushambuliana nao. Milio ya risasi ilisikika kila kona mahali hapo, wale waoga, wakakimbia lakini waliokuwa na bunduki nao wakajiweka sawa na kuanza kupambana na watu hao. Bruno alikuwa amekwisharudi na kuwa nyuma ya gari la maofisa wale wa CIA, hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya kwani kwa jinsi alivyokuwa mweusi, kama angejitokeza mbele ya watu wale ilikuwa ni lazima kumuua kwa kuwa wangehisi kwamba naye alikuwa adui. Hakuondoka mahali hapo, alijibanza kwenye ukuta huku akifuatilia kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Baada ya dakika kadhaa, milio ya risasi ikaacha, Wazungu wale wakajua kwamba watu weusi waliokuwa wakipambana nao, wote walikuwa wamekufa na hivyo kuanza kuingia ndani. Walipofika, ni maiti tu ndizo zilizokuwa zikionekana huku zikiwa zimetapakaa damu. Ndani ya nyumba ile, wakaanza kumtafuta mzee Todd ambaye walijua kwamba alikuwa humo kwa kuwa bado GPS ilionyesha kwamba simu ile ilikuwa humo ndani. Wakafanikiwa kuipata lakini kitu cha ajabu, mzee huyo hakuwepo. Wakaanza kuangalia katika kila chumba, wakafungua milango na kuingia ndani lakini hawakuweza kumuona mzee huyo ambaye walifika hapo kwa lengo la kumtaka yeye tu. Walipohakikisha kwamba hakuwepo, hawakutaka kupoteza muda kubaki mahali hapo, walichokifanya ni kuondoka na kuziacha maiti mulemule ndani ya nyumba ile. Wakati wanatoka, wanaingia ndani ya gari lao na kuondoka mahali hapo, bado Bruno alikuwa amejibanza kwenye kile kiukuta, alipoona gari limeondoka mahali hapo, haraka haraka akatoka na kwenda ndani ya nyumba ile. Hali aliyoikuta humo ilimuogopesha mno, hakuwahi kufikiria hata siku moja kwamba katika maisha yake kuna siku angeweza kuziona maiti nyingi zikiwa zimetapakaa kama ilivyokuwa siku ile. Akaziruka na kumfuata yule mwanaume ambaye aliichukua ile kadi na kuanza kumpekua mifukoni mwake, akabahatika kuikuta kadi ile ambayo aliichukua na kuondoka zake. Bado mtaa ulikuwa kimya, hakukuwa na mtu aliyethubutu kutoka ndani ya nyumba yake kwa kuhofia maisha yake, kila mtu alibaki ndani huku dakika zikiendelea kwenda mbele. Bruno alipoondoka hapo, moja kwa moja akaelekea kule mlimani, alikuwa akikimbia, alichoka lakini hakutaka kusimama, kwake, mzee Todd alikuwa kila kitu, alihitaji kumsaidia mzee huyo kwa kuwa alionekana kuhitaji msaada kupita kawaida. Alipofika kule juu, akamkuta pale pale alipomuacha na kumuonyeshea kadi ile kwamba alifanikiwa kuipata kitu kilichoonekana kumfurahisha mzee yule. “Kwa hiyo?” aliuliza mzee Todd. “Tuondoke tukapange vyumba hotelini,” alisema Bruno na kuanza kuondoka hapo. Mzee Todd hakutaka kuvua miwani wala kofia aliyokuwa ameivaa, hakutaka kugundulika na mtu yeyote yule, alijua kwamba alikuwa akitafutwa kila kona hivyo kama angeendelea kujificha hivyo basi ingemsaidia kuwa salama mpaka siku ambayo angefanikiwa kufika nchini Marekani. Alijua kwamba kutafutwa kwake ni Maxwell ndiye alikuwa amefanya hivyo, alihisi kitu hicho kwani mbali na kuwa na urafiki wa mashaka lakini kila mmoja alihitaji kuwa na nguvu ya kibiashara kitu kilichoonekana kuvuruga kila kitu. Hawakuchukua muda mrefu wakafika sehemu iliyokuwa na hoteli ndogo iitwayo Elizabeth Royal, moja kwa moja wakaelekea mpaka mapokezi ambapo wakafanya harakati za kuchukua chumba. “Tutakaa kwa siku tano,” alisema Bruno ambaye akachukua ile kadi na kumpa dada wa mapokezi ambaye akaingiza namba za kadi katika kompyuta yake na kuchukua kiasi kilichotakiwa kama malipo kwa muda huo. Alipomaliza, akawapa kadi zilizotumika kama funguo na kuondoka mahali hapo kuelekea vyumbani kupumzika. Maxwell alichanganyikiwa, mpaka kipindi hicho hakujua mahali mzee Todd alipokuwa. Alihisi kabisa kichwa chake kikichanganyikiwa, mwanaume huyo alikuwa muhimu mno kwake, alimtaka kwa udi na uvumba na ndiyo maana alihangaika kwa nguvu zote kuhakikisha kwamba anauawa kwa gharama yoyote ile. Vijana waliokuwa nchini Afrika Kusini nao hawakuweza kumsaidia kwa chochote kile, kila alipowapigia simu walimwambia kitu kimoja kwamba bado waliendelea kumtafuta na hawakujua mahali alipokuwa. Alikuwa na familia yake, ilikuwa ni lazima kuhakikisha kwamba watu hao hawaondoki mikononi mwake, alihakikisha kwamba anawafanyia umafia wa nguvu hata kama mzee huyo hakuonekana. Alimpa saa sabini na mbili ambazo zilikuwa ni siku tatu, alijua kwamba kwa jinsi alivyokuwa akiipenda familia yake, ilikuwa ni lazima mzee Todd afanye kila liwezekanalo kufika nchini Marekani. Siku ya kwanza ikakatika, ya pili ikaingia na kukatika lakini bado majibu yalikuwa yaleyale kwamba Todd hakuonekana na vijana wake walikuwa wakiendelea kumtafuta kila kona bila mafanikio. “Kwa hiyo?” aliuliza kijana mmoja kwenye simu, alitaka kusikia kutoka kwa bosi wake kama ilikuwa ni muhimu kuimaliza familia yake hata kama hakuwa amerudi au walitakiwa kusubiri. “Tuongeze siku mbili, inawezekana akafika,” alisema Maxwell. Hawakuwa na jinsi, wakaongeza siku mbili huku wakiendelea kuitunza familia yake kwa chakula na vitu vingine. Kila siku Juddie alikuwa kwenye maumivu makali, hakujua mahali mume wake alipokuwa, alitamani kumuona, hata kama asingemuona akiwa hai basi aione hata maiti yake na kujihakikishia kwamba mume wake alifariki dunia. Siku hizo zilipokwisha, Maxwell hakuwa na jinsi, akamwambia kijana yule awamalize na kisha kuipiga picha miili ya watu hao ili baadaye amtumie mzee Todd na kumwambia kwamba aliiteketeza familia yake na alibaki yeye tu, na ilikuwa ni lazima amtafute na kumuua. “Kill them both,” (waue) alisema Maxwell kwenye simu. “Hakuna shida bosi!” alisema kijana huyo na kukata simu, utekelezaji ulitakiwa kufanyika mara moja. *** Japokuwa walikuwa wamepatana kukaa mahali hapo kwa muda wa wiki moja lakini mpaka kipindi cha mwezi nzima Bruno na mzee Todd walikaa ndani ya hoteli hiyo waliyokuwa wamechukua chumba. Hawakuonekana kuwa na hofu yoyote ile kwani kwa jinsi walivyokuwa ilikuwa vigumu sana kumgundua mzee Todd kwamba alikuwa mtu aliyekuwa akitafutwa mno kutokana na sakata la madawa ya kulevya lililokuwa likimkabiri. Waliishi kwa amani japokuwa muda mwingi mzee huyo alikuwa akimfikiria mke na mtoto wake. Hakujua kama watu hao walikuwa hai au la kwani tangu alipopewa muda wa saa sabini na mbili mwezi uliopita, hakuwasiliana nao tena. Hakuonekana kuwa na raha hata kidogo, kichwa chake kilikuwa na mawazo tele. Alitamani kuondoka barani Afika, hakutaka kuendelea kuishi huko na wakati hakujua familia yake ilikuwa ikiendeleaje nchini Marekani. Dada wa mapokezi, Thandi ambaye aliwapokea katika hoteli waliyokuwa wamechukua chumba alionekana kuwa na wasiwasi na wateja hao. Mtu aliyemtia hofu alikuwa mzee Todd ambaye muda wote aliokuwa akiongea, kofia na miwani haikutoka mwilini mwake. Alikuwa akijiuliza mambo mengi kuhusu mtu huyo, hakujua sababu ya kufanya hivyo, alijaribu kumwangalia vizuri zaidi lakini hakupata jibu juu ya mwanaume huyo, hakujua alikuwa nani na kwa nini hakutaka kuondoa kofia wala miwani aliyokuwanayo. Alijaribu kuvumilia, alitaka kuona kama ingetokea siku moja mzee huyo kuvua kofia yake lakini jambo hilo halikuweza kutokea, kila alipokuwa akitoka chumbani kwake kofia yake ilikuwa kichwani. Japokuwa lilionekana kuwa jambo la kawaida lakini kwa mhudumu huyo likaonekana kuwa jambo moja kubwa sana kwani katika kipindi hicho kulikuwa na matukio mengi ya kigaidi yaliyokuwa yakitokea nchini Afrika Kusini, akahisi kwamba inawezekana mzee yule alikuwa mmoja wa magaidi waliotaka kuilipua hoteli yake. Kukosa amani kwake kukampeleka kumuhadithia mpenzi wake nyumbani. Alimwambia ukweli kuhusu wageni hao waliokuwa wamechukua mwezi mzima kazini kwake lakini katika kipindi chote hicho hakuwahi kuona kofia ikitoka kichwani mwa mzee Todd. “Mwezi mzima?” aliuliza mpenzi wake. “Ndiyo! Ni mwezi mzima ile kofia ipo kichwani,” alijibu Thandi. “Mmh! Labda kuna kitu hapo, umejaribu kufuatilia kwa karibu kujua sababu?” aliuliza mpenzi wake. “Hapana! Ila anaonekana ana pesa sana kwani hivyo vinywaji anavyokuywa, ni balaa,” alisema Thandi kwa lengo la kumsifia mzee Todd. Wakati wakizungumza mambo kuhusu wageni hao, kichwa cha mpenzi wake kikaenda sehemu nyingine kabisa. Yeye alikuwa mmoja wa vijana waliokuwa wamewekwa nchini Afrika Kusini kwa lengo la kumtafuta mzee Todd. Alikuwa kijana wa Maxwell ambaye aliamua kuwatawanya wengi nchini humo kwa kuamini kwamba mzee Todd alikuwa ndani ya Afrika Kusini. Alipoambiwa na Thandi kuhusu jambo hilo, hakutaka kubaki nalo bali alichokifanya ni kwenda kuwaambia vijana wenzake kile alichoambiwa na mpenzi wake kwani hata naye alikuwa na hofu tele kwa kuhisi kwamba inawezekana huyo Mzungu alikuwa ni yule Todd waliyekuwa wakimtafuta. “Sasa kofia si jambo la kawaida tu,” alisema mwenzake baada ya kupewa taarifa. “La kawaida? Unajua kwamba inawezekana akawa Todd tunayemtafuta?” “Ni vigumu! Hivi Todd anavyotafutwa anaweza kuwa hotelini kweli?” “Inawezekana kwani hayupo peke yake, yupo na kijana mwingine. Mmesahau tulivyoambiwa kwamba kwenye meli Todd alikuwa na kijana mwingine wa Kiafrika?” aliuliza mpenzi wa Thandi. Hilo kidogo likawaingia vichwani mwao. Ilitakiwa kuanza kufuatilia na kujua watu hao walikuwa ni wakina nani na kwa nini mwanaume huyo wa Kizungu alikuwa akivaa kofia muda wote. Walichokifanya ni kuwatuma vijana wawili na kuanza kuwafuatilia katika hoteli hiyo. Vijana hao wakaenda na kupanga vyumba huku wakitakiwa kufuatilia kila hatua ambayo watu wale walikuwa wakichukua. Baada ya siku mbili, vijana hao wakafanikiwa kumuona Bruno na mzee Todd wakiendelea na maisha yao kama kawaida hotelini pale. Kwa kumwangalia mzee Todd, kwao halikuwa na ugumu kugundua kama huyo alikuwa mzee huyo. Haraka sana wakawaambia wenzao kwamba walimwangalia mzee huyo na kugundua kwamba alikuwa yuleyule waliyekuwa wakimtafuta na hivyo vijana hao kupiga simu kwa Maxwell na kumwambia kilichokuwa kikiendelea. “Safi sana! Hakikisheni haondoki ndani ya hoteli hiyo,” alisikika Maxwell kwenye simu. “Kwa hiyo tumuue au?” “Hapana! Atekwe, msimuue hapo hotelini, watu wakikusanyika mnaweza kukamatwa na kuniletea matatizo,” alisikika Maxwell. Mipango ya kutekwa kwao ikapangwa, hawakutakiwa kutekwa wakiwa vyumbani mwao bali walitakiwa kutekwa wakati wakiwa katika mgahawa wa hotelini hapo walipokuwa wakila. Hilo wala halikuwa tatizo, walichokifanya ni kusoma ratiba yao kwanza. Wakagundua kwamba watu hao wawili walikuwa wakishuka mgahawani saa nne asubuhi, saa sita mchana na saa mbili usiku, hivyo kama walitaka kuwateka basi hiyo ndiyo mida yao waliyokuwa wakitoka kwenda kula. “Tuwatekeni usiku, nadhani hiyo itakuwa salama zaidi,” alisema kijana mmoja na kukubaliana. Siku iliyofuata ndiyo ilikuwa siku ya kufanya tukio hilo, kuanzia asubuhi mpaka jioni walikuwa wakiwafuatilia kwa makini sana. Majira ya saa moja hata kabla hawajakwenda kwenye mgahawa, tayari vijana hao walikuwa wamefika mahali hapo huku wakiwa na bastola zao viunoni. Wakati Bruno na mzee Todd wakishuka kwenda kula, walikuwa wakiwaangalia tu, wakawaona wakiifuata meza moja, wakakaa na kuanza kula huku sehemu yote hiyo ikiwa na watu. “Kwa hiyo? Tuwafuate sasa hivi?” aliuliza jamaa mmoja. “Umewaambia washikaji waandae gari?” “Ndiyo! Walisema gari lipo tayari hapo nje ya hoteli,” alijibu mwingine, walikuwa wakiongea kwa sauti ya chini. “Basi sawa. Twende!” Wakainuka na kuanza kuwafuata watu hao, walipowafikia katika meza ile, wakatoa bastola zao kisiri sana na kuwaambia wasimame. Kwanza walitaka kubisha lakini hata kabla ya kufanya hivyo, wakaziona bastola hizo kitu kilichowafanya kuogopa. Waafrika Kusini hawakuwa watu wa mchezo, waliwafahamu, walikuwa na michezo ya kutisha na bastola zao, walikuwa wepesi kuua, kwao, kumwaga damu ilikuwa ni kama kumchinja kuku au kumuua panzi. Wakainuka na kuanza safari ya kuelekea nje ya mgahawa ule huku wakiwa wametangulizwa mbele. Hakukuwa na mtu yeyote aliyegundua kitu kilichokuwa kikiendelea mahali hapo, walichokiona ni marafiki wanne walikuwa wamewafuata wenzao na kuondoka mahali hapo. Walipofika nje, tayari wenzao walikuwa katika gari moja mahali hapo, walichokifanya ni kuwataka kuingia garini na baada ya hapo, gari likawashwa na kuondoka mahali hapo kwa mwendo wa kawaida kana kwamba hakukuwa na kitu kibaya kilichokuwa kimetokea. Hata kabla hawajafika mbali, kijana mmoja aliyekuwa amebaki ndani ya gari lile na dereva akachukua simu yake, akabonyeza namba fulani, baada ya sekunde kumi akaanza kuzungumza na mwanaume wa upande wa pili ambaye alikuwa Maxwell. Alimwambia kwamba mtu aliyekuwa akihitajika alikuwa mikononi mwao hivyo walitaka kufuata maelekezo ya juu ya nini cha kumfanya mtu huyo. “Just kill him,” (muueni tu!) “And the other guy?” (na huyu mwingine?) “Who is he?” (nani huyo?) “He was with him, should we kill him too?” (alikuwa naye, naye tumuue pia?) aliuliza. “Kill them both,” (waueni wote) “Ok sir,” (Sawa bwana mkubwa) alisema kijana yule na hapohapo akaanza kuikoki bunduki yake, kilichotakiwa kufanywa ndani ya gari hilo ni mauaji tu. Bruno na mzee Todd walijua kile kilichokuwa kikienda kutokea kwani waliisikia sauti iliyokuwa ikizungumza na kijana yule, wakajua kabisa kwamba walikuwa wakienda kufa humo garini. Walitamani kuruka kupitia dirishani lakini walishindwa, vioo vilifungwa na mbaya zaidi walikuwa wamewekwa mtu kati hivyo wasingeweza kufanya kitu chochote kile. Wakaanza kuomba msamaha, hawakutaka kufa kikatili ndani ya gari. Bruno ndiye aliyekuwa akilia sana, moyoni mwake alimkumbuka mpenzi wake, Sharifa, ilikuwa ni lazima aondoke Afrika Kusini kwenda nchini Kenya kumuona mpenzi wake aliyekuwa akimpenda kwa moyo wa dhati. Wakati wakiwa wanasali sala zao za mwisho, tayari vijana waliokuwa mule garini walikwishamaliza kuzikoki bastola zao na kilichosikika baada ya hapo ni milio ya risasi tu huku gari likiwa kasi. “Paaa! Paaa! Paaa!” milio ya risasi ikasikika na damu kutapakaa garini. *** Bado msichana Thandi alikuwa na hofu tele juu ya watu waliokuwa wamefika katika hoteli yao na kuchukua chumba, mwanaume yule wa Kizungu kila siku alikuwa na kofia kichwani mwake na miwani, hakutaka kuitoa, alipokuwa akifika mapokezini, alikuwa na vitu hivyo na hata alipokuwa akiingia ndani ya gari pia alikuwa na vitu hivyo. Hilo lilizidi kumtia hofu msichana huyo, hakutaka kukubali, aliona kabisa kwamba ilikuwa ni lazima amwambie bosi wake juu ya kile kilichokuwa kikiendelea kwani kwa muda wa mwezi mzima mwanaume huyo kuwa hivyohivyo, lilionekana kuwa jambo gumu. Mbali na kuzungumza na mpenzi wake, akazungumza na meneja wa hoteli hiyo ambaye naye akaanza kufuatilia na kugundua kwamba kulikuwa na ukweli kwa kile alichokuwa akiambiwa. Hakutaka kuchelewa, meneja huyo akazungumza na polisi na kuwaambia kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Polisi hao walitaka kuthibitisha kile kilichokuwa kikiendelea na hivyo kwenda katika hoteli hiyo kujionea kwa macho yao. Siku ambayo walikwenda na kuonyeshewa watu hao ndiyo siku ambayo Bruno na Todd walikuwa kwenye mgahawa wakila. Polisi waliokuwa na nguo za kiraia walikuwa mahali hapo, bastola zilikuwa viunoni mwao, walijiandaa na kitu chochote kile ambacho kingetokea mahali hapo. Baada ya dakika kadhaa, wakawaona wanaume wawili wakisimama na kuwafuata watu wale waliowafuata, walisimama karibu nao na kuanza kuzungumza nao. Walikuwa polisi, walijua kila kitu alichokuwa akikifanya adui. Japokuwa watu wengine hawakuwa wameziona bunduki walizozionyesha watu hao kisiri na kuwataka kusimama, wao waliziona vizuri kabisa. “What the hell is going on?” (nini kinaendelea?) aliuliza polisi mmoja huku jicho lake likiangalia kule kwa wizi. “I don’t know, let’s keep waiting,” (sijui, hebu tuendelee kusubiri) alijibu mwenzake. Baada ya sekunde kadhaa wakawaona watu wao wakisimama na kuanza kupiga hatua kwenda nje huku wale jamaa wakiwafuata kwa nyuma. Haikuwa ngumu kwao kugundua kwamba watu wale walikuwa wamewekwa chini ya ulinzi na hivyo kuanza kuwafuatilia. Walipofika nje, wakawaona wakiingia ndani ya gari na kuondoka mahali hapo. Nao hawakutaka kubaki, wakaingia ndani ya gari lao na kuondoka kwa kulifuatilia gari lile. Walilifuatilia gari hilo ambalo lilichukua Barabara ya Western Bypass ambayo ilikuwa ikielekea Upande wa Kaskazini mahali kuitwapo Woodmead kulipokuwa na makorongo makubwa. Magari yalikuwa yakitembea kwa mwendo wa kawaida, hawakusubiri sehemu yoyote ile, ilikuwa ni lazima kulifuatilia na kujua mwisho wa safari hiyo ilikuwa wapi. Hawakuwa mbali kutoka katika gari hilo, ilikuwa ni sawa na hatua tano za miguu ya binadamu. Wakati wakiwa wamekwishafika Bryston, wakashangaa kuona mwanaume mmoja akitoa bastola yake ndani ya gari. Hawakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea lakini waliangalia vizuri kabisa na kumuona mtu huyo akiwa na bastola yake dakika chache baada ya kuongea kwa simu. “Stephen, take your gun and do the work,” (Stephen, chukua bastola yako ufanye kazi) alisema mwanaume aliyekuwa akiendesha gari. Hilo halikuwa tatizo kwa huyo mtu aliyeambiwa kwani alikuwa miongoni mwa polisi waliokuwa na shabaha kubwa, alichokifanya, kama muvi vile akatokeza nusu ya mwili wake nje ya gari kupitia dirishani na kisha kunyoosha mkono wenye bastola kuelekea katika gari lile. Watu waliokuwa pembeni walishangaa, hawakujua sababu ya mwanaume yule kufanya hivyo lakini hata kabla hawajapata majibu, Stephen akaachia risasi kadhaa ambazo zilipenya katika kioo cha nyuma, mwanaume mmoja akapigwa risasi ya shingo kwa nyuma, kwa kupagawa, wenzake wakaanza kurushiana risasi na Stephen ambaye alikuwa kwa nyuma na alikuwa akiwaona vizuri kabisa. Kila mmoja akawasahau watu wao na hivyo kuanza kupambana na Stephen aliyeonekana kuwa si mtu wa mchezo hata kidogo. Mwenzake aliyekuwa ameshikilia usukani alijua vilivyo namna ya kupambana na watu waliokuwa kwenye gari hivyo alichokifanya ni kuendesha kwa kasi na kusimama upande wao wa kulia na hivyo kumpa nafasi Stephen kufanya kile alichokitaka. Watu waliokuwa pembeni wakaanza kukimbia, kila mtu alikuwa akiyaokoa maisha yao kwani hali ilionekana kutisha na ilionekana kabisa kwamba muda wowote ule risasi zile zingewapata. “Deal with the driver,” (shughulika na dereva) alisema dereva. Hilo halikuwa na tatizo hata kidogo, haraka sana Stephen akaanza kushughulika na dereva aliyekuwa ameambiwa. Ni ndani ya sekunde thelathini tu, risasi mbili zikaingia katika mikono ya dereva, hakuendelea kuushikilia usukani na hivyo gari hilo kutoka barabarani na kuanza kuingia korongoni kwa kasi. *** Abdul na Sharifa walikuwa wakikimbia kwa kasi, nguo ya harusi tena huku akiwa amepambwa vizuri ilikuwa mwilini mwa Sharifa lakini hakutaka kujali, alikuwa akikimbia huku akimfuata Abdul ambaye alimwambia kwamba mpenzi wake, Bruno alikuwa hai na hakufa kama alivyokuwa ameambiwa. Moyo wake ulikuwa kwenye majonzi mazito, hakuamini kama alithubutu kukubali kuolewa na mwanaume mwingine na wakati hakuwa na uhakika kama mpenzi wake aliyempenda kwa mapenzi ya dhati alikufa kweli au la. Walichukua dakika kumi kukimbia, wakasimama nje ya nyumba moja ambapo Abdul alimwambia kwanza wapumzike kwani walikuwa wamekaribia kufika kule alipoambiwa kwamba bruno alikuwepo. Walipumzika pasipo kuongea kitu chochote kile, baada ya dakika kadhaa, ikambidi Sharifa aulize vizuri kama kweli kile alichokuwa amemwambia kule harusini kilikuwa kweli au alimdanganya. “Bruno yupo wapi?” aliuliza Sharifa huku akimwangalia Abdul. “Nimeambiwa alipiga simu. Twende kwa Alfred, yeye ndiye aliyepokea simu kutoka kwake na kumwambia kwamba Bruno yupo hai,” alisema Abdul. Sharifa alionekana kukakasirika lakini hakuwa na la kufanya, walichokifanya ni kuanza kwenda kwa huyo Alfred huku akitaka kujua ukweli juu ya kile alichokuwa ameambiwa. Walipofika, kijana huyo akawaweka kwenye kochi na kuanza kuzungumza nao. Aliwaambia kwamba alipokea simu kutoka kwa Onyango na kumwambia kwamba Bruno alikuwa hai, tena aliongea naye mwenyewe. “Onyango?” aliuliza Abdul huku akionekana kutokuamini alichokisikia. “Ndiyo! Onyango huyohuyo!” “Yule aliyekimbilia Afrika Kusini?” “Ndiyo! Sijui wamekutana vipi lakini inaonyesha kwamba Bruno naye yupo Afrika Kusini,” alisema Alfred maneno yaliyomfanya kila mtu kushtuka. “Afrika Kusini?” aliuliza Sharifa huku akionekana kutokuamini. “Ndiyo!” Hilo halikumuingia akilini hata kidogo, alijaribu kufikiria namna ambavyo mpenzi wake huyo kufika Afrika Kusini kutoka nchini Kenya, alijaribu kujifikiria na kuunganisha safari ya kufika nchini humo lakini alikosa jibu kabisa, alibaki akishangaa, aliuliza mara nyinginyingi na Alfred alimwambia vilevile kwamba alikuwa Afrika Kusini. “Kuna kingine sasa! Kama unashangaa yeye kuwa Afrika Kusini, basi hili jingine utazimia,” alisema kijana huyo. “Lipi?” “Bruno ni bonge moja la bilionea!” alisema Alfred. “Bilionea?” aliuliza Abdul. “Ndiyo!” “Kivipi yaani?” “Huo ni umbeya niliopewa na Onyango, kawa bilionea kivipi, sijui, ila ni bonge la bilionea. Atakapotoka nchini Marekani, atakuja Kenya,” alisema Alfred. “Nchini Marekani?” “Ndiyo!” “Sasa Alfred unatuchanganya. Umesema Afrika Kusini, ukasema ni bilionea, sasa hivi unasema nchini Marekani, mbona hueleweki?” aliuliza Sharifa huku akimwangalia Alfred kwa macho yaliyojaa mshangao mkubwa. “Yaani hata mimi mwenyewe sikumuelewa Onyango mpaka pale aliponihakikisha kwamba jamaa kweli ni bilionea,” alisema. “Kivipi?” “Alimwambia Onyango kwamba anahitaji namba yangu ya akaunti ili akutumie pesa. Nahisi zitakuwa zimefika manake nimeona mlio wa meseji, nafikiri ni pesa hizo,” alisema Alfred. “Mimi ndiyo sikuelewi kabisaaaa, naona kama unaongea Kirumi,” alidakia Abdul. “Hebu subiri!” alisema Alfred, akaingia mkono mfukoni na kutoa simu yake. Kulikuwa na ujumbe wa simu umeingia, hapohapo akaufungua na kuanza kuusoma. Uso wake ukajawa na tabasamu pana, baada ya hapo, akampa Sharifa ausome ujumbe huo, ulikuwa ujumbe mfupi uliosomeka ‘You have received 100,000 dollars from bank account number 0987225677890, (umepokea kiasi cha dola laki moja kutoka akaunti ya benki namba 0987225677890). “Umeona! Amesema hizi pesa amezituma kwa ajili yako,” alisema Alfred, hilo likawachanganya zaidi. Wakahisi kama kile kilichokuwa kikiendelea kilikuwa ni ndoto ambapo baada ya mudua mfupi wangeamka na kujikuta wakiwa kitandani. ITAENDELEA
Simulizi : Mvuvi Bruno (Bruno The Fisherman) Sehemu Ya Nne (4)
Gari liliseleleka mpaka kule korongoni ambako hakukuwa na urahisi kwa mtu kufika huko mpaka uzungukie sehemu nyingine ya mbali. Kila mtu alikuwa hoi na wote walikuwa wakitokwa na damu. Bruno na Todd walikuwa kimya, damu ziliwatoka kichwani mwao na hawakujua ni kitu gani kilikuwa kimeendelea mpaka kuanza kushambuliwa kwa risasi. Walichokifanya ni kuanza harakati za kutoka ndani ya gari lile lililokuwa limegeuka chini juu, juu chini. Wakazisogeza maiti zile na kisha kufungua mlango. Mzee Bruno akaanza kutoka, alipoanza kusimama, akashangaa akishindwa kutokana na maumivu makali aliyokuwa akisikia mguuni. “Aauughh..” alijikuta akipiga kelele. Damu zilikuwa zikimtoka mguuni, alipoangalia vizuri aligundua kwamba alipigwa risasi ambayo ilizama kabisa ndani ya mguu wake. Alisikia maumivu ambayo hakuwahi kuyasikia kabla, akashindwa kabisa kusimama, ili kusonga mbele ilikuwa ni lazima kushikwa au kubebwa. Haraka sana Bruno akateremka na kuanza kuelekea katika upande aliokuwa Todd na kumshika kisha kumpeleka pembeni. Akamlaza chini na kuanza kumpa huduma ya kwanza. Kitu cha kwanza kabisa alichotakiwa kufanya kilikuwa ni kuitoa risasi iliyokuwa katika mguu wa mzee huyo. Alishindwa kwa kuwa hakuwa na kifaa chochote kile hivyo kumwambia kwamba walitakiwa kuondoka mahali hapo kuelekea nje ya eneo la eneo hilo. Akamshika kwa kuupitisha mkono wa mzee huyo kwenye bega lake na kuanza kuondoka mahali hapo. Walichukua nusu saa wakafika juu kabisa barabarani. Hawakujua ni mahali gani walitakiwa kwenda, walichokifanya ni kuanza kuelekea upande wa Kaskazini ambapo waliamini kwamba hakukuwa na mtu yeyote hatari. Walitembea kwa mwendo mrefu, baada ya dakika ishirini na tano, wakaanza kupigiwa honi, walipoangalia nyuma, gari ndogo aina ya Vitz ilikuwa nyuma yao. Gari hilo likasimama na dereva aliyekuwa humo ndani kuanza kuwaangalia, kwa jinsi walivyoonekana, ilionyesha dhahiri kwamba walikuwa wakihitaji msaada, akawafungulia mlango na kuwaambia waingie ndani. “Nini kimetokea?” aliuliza dereva huyo huku akiwaangalia kupitia katika kioo cha mbele, aliwaweka kiti cha nyuma. “Tulitekwa,” alijibu Bruno. “Mlitekwa?” “Ndiyo! Bosi wangu wakampiga risasi ya mguu. Tunaomba utusadie,” alisema Bruno huku akimwangalia mzee huyo. “Haina shida. Nitawapeleka hospitali sasa hivi!” “Hospitali?” “Ndiyo!” “Hapana! Naomba utupeleke sehemu yoyote ile lakini si hospitali,” alisema Bruno. “Kwa nini? Mzee ana risasi mguuni, inabidi iende ikatolewe,” alisema dereva. “Hapana! Naomba utupeleke popote pale.” Bruno alimwambia dereva huyo aliyejitambulisha kwa jina la Jonathan jinsi maisha yao yalivyokuwa hatarini. Alimwambia kuwa kulikuwa na mtu mwenye mkono mrefu alikuwa akiwatafuta, aliwatuma watu kwenda kuwamaliza lakini walishindwa na gari lao kupata ajali na kutumbukia korongoni. Hakuishia hapo, aliendelea kumdanganya kwamba kama mzee Todd angepelekwa hospitali inamaanisha kwamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wao kwa kuwa jamaa huyo aliyekuwa akiwatafuta alikuwa na watu wengi, kila kona alikuwa amesambaza watu wake kwa leo la kumlinda na hata kumfanyia kazi. Kidogo hiyo ikamuingia Jonathan, akatokea kuwaamini na kuwaambia kwamba angewapeleka nyumbani kwake. Safari iliendelea, baada ya dakika arobaini wakafika nyumbani hapo ambapo akawateremsha na kuelekea ndani. Akamuita mke wake aliyeitwa Magdalena na kumwambia kile kilichokuwa kimetokea, jinsi alivyokutana na watu hao nje mpaka kuomba msaada wake. Hilo halikuwa tatizo, kwa kuwa mkewe huyo alikuwa na ndugu yake aliyekuwa daktari akampigia simu na kwenda nyumbani hapo. Baada ya dakika kadhaa, Sophiane ambaye ndiye alikuwa daktari aliyepigiwa simu akafika nyumbani hapo na kumwangalia mzee Todd aliyekuwa hoi kitandani. Akaangalia jeraha, akaandika vifaa ambavyo vilihitajika kwa lengo la kumfanyia upasuaji na kutoa risasi hiyo. “Inahitajika randi elfu ishirini,” alisema Sophiane. “Mbona kiasi kikubwa hivyo?” aliuliza Jonathan. “Ni vifaa vya gharama kwa kuwa ni risasi ndiyo inayotakiwa kutolewa, ila pia vifaa hivyo haiviuzwi kiholela kwani serikali ilitangaza majeraha yote ya risasi yalitakiwa kutibiwa hospitalini,” alisema Sophiana huku akiwaangalia watu hao. Jonathan hakuwa na pesa za kutosha ila hilo halikuonekana kuwa tatizo lolote lile, Bruno akamwambia kwamba pesa ilikuwepo na kitu kilichohitajika kilikuwa ni hivyo vifaa tu. Yeye, Jonathan na Sophiana wakaondoka kwenda mjini ambapo huko Bruno akaenda katika mashine ya ATM na kutoa kiasi cha pesa kilichotakiwa na cha ziada kwa ajili ya matumizi yao na kumkabidhi Sophiana ambaye alikwenda na kununua vifaa hivyo tena kwa kutumia vyeti vya udaktari. “Twendeni nikaanze kazi,” alisema mwanamke huyo. Baada ya dakika kadhaa wakafika nyumbani hapo na kuanza kazi. Risasi ikatolewa, kila mtu akafurahi na mzee huyo kuanza kutibiwa nyumbani hapo na hata alipopona, Jonathan akawaambia kwamba maisha yao yalikuwa hatarini hivyo walitakiwa kukaa mahali hapo kwa mwezi mzima jambo ambalo halikuonekana kuwa tatizo. “Kwa hiyo huu ni mwezi wa pili tupo Afrika Kusini! Nitarudi lini nyumbani kuwaonyesha wakina James kwamba sikufa?” alijiuliza. Mwezi huo pia wakatakiwa kukaa hukohuko Afrika Kusini. *** Maxwell alikuwa na presha kubwa, alitaka kusikia kile kilichokuwa kimeendelea nchini Afrika Kusini. Hakutulia nyumbani kwake, muda wote alikuwa akipigia simu nchini humo na kutaka kujua kile kilichokuwa kikiendelea. Alitaka kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa, na kwa sababu aliona kama kudharauliwa kwa kile alichokuwa ameagiza, alichokifanya ni kuwapigia simu vijana wake na kuwaambia wammalize Bi Juddie na mtoto wake, Martha. Hilo halikuwa tatizo, vijana hao walipoambiwa hivyo, wakawachukua watu hao na kwenda kuwaua na kuitupa miili yao ufukweni mpaka pale polisi walipopewa taarifa na kwenda kuichukua. Ilikuwa ni taarifa mbaya mno kwa kila mtu, hakukuwa na aliyejua kama kulikuwa na mtu aliyekuwa nyuma ya kila kitu kilichokuwa kikiendelea, wengi walimchukulia mzee Todd kama muuza madawa ya kulevya lakini kwa kile kilichotokea kilimgusa kila mtu. Moyo wa Maxwell ukaridhika lakini bado kichwa chake kilimfikiria huyo Todd, hakujua vijana wake walifikia wapi kwani kila alipowapigia simu alipewa majibu ambayo hayakumridhisha hata kidogo. Siku zikakatika mpaka mwezi mmoja kumalizika, bado hakukuwa na kitu kilichoendelea mpaka pale alipopigiwa simu na kuambiwa kwamba vijana walikuwa njiani kwenda kutekeleza suala la kumuua mzee huyo kwani walipewa taarifa kwamba alikuwa hotelini. Hilo lilimfurahisha na kuahidi kulifuatilia kwa karibu sana. Walipokuwa ndani ya gari, akawapigia simu, akaambiwa kwamba walikuwa na watu hao na hivyo walikuwa njiani kwenda kuwamaliza. Moyo wake ukajisikia furaha ya ajabu, akakata simu, akachukua chupa ya mvinyo na kuanza kunywa huku muziki ukipiga taratibu kwenye redio yake sebuleni kwake. Baada ya saa moja alipoona kwamba kazi ile ilifanyika, akaanza kuwapigia simu vijana wake ili apate mrejesho kama kazi ile ilifanyika au la. Alipiga simu, haikuwa ikipokelewa, iliita na kuita lakini hali ilikuwa kimya kabisa. Hilo lilimchanganya, haikuwa kawaida kwa vijana wake kutokupokea simu zake, alihisi kwamba kulikuwa na tatizo na hivyo kupiga zaidi na zaidi lakini majibu yalikuwa yaleyale kwamba simu haikupokelewa. “Nini kinaendelea huko? Mbona hawataki kupokea simu zangu?” aliuliza, hakupata jibu, kichwa chake kilichanganyikiwa kupita kawaida. Baada ya dakika kadhaa, akapiga tena simu, haikuita muda mrefu, ikapokelewa na sauti ya mwanamke kusikika upande wa pili. Huyo ndiye aliyemwambia kwamba kulikuwa na ajali mbaya ilikuwa imetokea ambapo watu waliokuwa ndani ya gari hilo walikuwa wamekufa wote. “Wamepata ajali?” “Ndiyo! Ila kilichowaua si ajali,” alisikika mwanamke huyo. “Ni nini?” “Risasi,” alipoambiwa hivyo, moyo wake ukapiga paa, hakuamini, aliuliza zaidi na zaidi kwa kudhani kwamba majibu yangebadilika lakini yaliendelea kuwa vilevile kwamba vijana wake waliuawa na gari kuingia kwenye korongo. “Haiwezekani! Haiwezekani!” alisema Maxwell huku akiwa amechanganyikiwa.
Bruno na mzee Todd hawakuwa na cha kufanya zaidi ya kuendelea kukaa nchini Afrika Kusini kwa mwezi mwingine wa pili. Hawakupenda kukaa nchini humo, kila mmoja alihitaji kuondoka kuelekea nchini mwao lakini hawakuwa na jinsi, waliendelea kubaki nchini humo nyumbani kwa Jonathan huku mzee Todd akiendelea kupatiwa matibabu. Siku ziliendelea kukatika, Bruno hakutakiwa kutoka ndani, alikuwa na hofu kubwa kwa kuhisi kwamba bado watu hao walikuwa wakimtafuta kila kona hivyo angeweza kuuawa. Alikuwa kama mwali, kila siku ilikuwa ni kuamka ndani na kubaki humohumo mpaka jioni. Yalikuwa ni maisha ya shida, hakujua ni kwa jinsi gani angeweza kuwasiliana na Abdul aliyekuwa nchini Kenya kwa lengo la kumwambia kuwa hakufa, ili taarifa hiyo ampe Sharifa ambaye bila shaka alikuwa na wasiwasi mkubwa huko alipokuwa. Kupata simu halikuwa tatizo ila tatizo kubwa lilikuwa ni kupata simu ya mtu mmoja aliyekuwa nchini Kenya ambaye angemuunganishia kuzungumza na msichana huyo. Kila siku alizungumza na mzee Todd ambaye alimwambia jinsi alivyokuwa akiumia kuona akiwa mbali na familia yake. Hao ndiyo walikuwa watu aliokuwa akiwategemea, hakuwa na ndugu, maisha yake tangu alipokuwa kijana mpaka alipopata utajiri, mkewe na mtoto wake ndiyo walikuwa watu pekee. “Unahisi tutaweza kuondoka hapa salama?” aliuliza mzee Todd. “Ninatumaini hilo mzee! Cha msingi ni kumuomba Mungu katika hili, ila ni lazima tuondoke salama hapa,” alisema Bruno, alimwambia mzee huyo maneno ya kumfariji kiasi kwamba akahisi kwamba Bruno alikuwa malaika aliyetumwa kwa lengo la kumtia moyo pale alipokuwa akimevunjika moyo. Wakati akiendelea kuugua kitandani pale ndipo alipopewa taarifa juu ya kifo cha familia yake ambapo maiti zao zilikutwa ufukweni. Ilikuwa taarifa mbaya iliyouumiza moyo wake, hakuamini kile alichokuwa akikiona, moyo wake ulimwambia kwamba ni Maxwell ndiye aliyefanya hivyo. Lawama zake zilikuwa kwa mwanaume huyo, aliuumiza moyo wake na kuhisi kabisa kwamba alifanya hivyo kwa kuwa alihitaji mali zake, aliutaka utajiri wake na hata kushikilia biashara nyingi alizokuwa akizifanya. Hakulia sana, hakuhuzunika sana kwani mahali walipokuwa hakutaka wenyeji wao wagundue kwa kuamini kwamba kama ingetokea hivyo basi ilikuwa ni lazima wakatoe taarifa katika kituo cha polisi na kukamatwa. Siku ziliendelea kukatika huku mawazo juu ya familia yake yakimuumiza moyoni mwake. Hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya, hakuwa na watu wengine wa karibu sana kwani tangu alipokuwa akifanya biashara ya madawa ya kulevya hakuwa anajiamini kuwa na watu wa karibu zaidi ya familia yake, yaani hata walinzi wake hakuwa akiwaamini. Waliendelea kuwa hapo mpaka mwezi ulipokatika ambapo wakakubaliana kwamba ni lazima waondoke kuelekea nchini Kenya kwa kupitia njia za panya mpaka kufika huko. Hilo halikuonekana kuwa tatizo, alichokifanya Bruno ni kuzungumza na Jonathan na kumwambia kile walichokuwa wakikitaka. Jonathan akawaambia kwamba halikuwa jambo zuri kupitia njia za panya, kwa kuwa walikuwa na pesa na hati zao za kusafiria zilipotea basi lingekuwa jambo jema kama wangekwenda uhamiaji kwa lengo la kukabidhiwa nyingine. “Hapana! Nadhani kwa njia za panya ni vizuri zaidi,” alisema Bruno. “Hapana! Njia hizo si salama, mnaweza kuuawa,” alisema Jonathan. Walimwambia Jonathan kwamba walitaka kuondoka nchini humo kwa njia za panya lakini mwanaume huyo aliendelea kuwasisitizia kwamba hizo hazikuwa njia nzuri kwenda nazo kwani watu wengi ambao walikuwa wakitumia njia hizo walisafiri kwa hofu kubwa kitu ambacho hakutaka kuoana watu hao wakikutana nacho njiani. Wakaambiwa wasubiri wakati Jonathan akifuatilia hati zao za kusafiria uhamiaji. Hilo likaonekana kama kwa kosa kubwa, hawakutaka kuendelea kubaki nyumbani hapo, katika kipindi ambacho Jonathan alikuwa ameondoka kuelekea huko, huku nyuma nao wakatoroka nyumbani hapo. Sehemu ya kwanza kabisa ambayo walitaka kwenda ilikuwa ni katika Jiji la Pretoria ambapo waliamini kwamba safari yao ya kuelekea nchini Kenya ingeanzia hapo. Walipoondoka, wakaelekea mpaka katika Kituo cha Treni cha Sandton ambapo hapo wakapanda treni na kuanza safari ya kuelekea Pretoria. Ndani ya treni hakukuwa na mtu aliyewagundua, walivalia kofia na miwani kiasi kwamba ilikuwa vigumu sana kwa nyuso zao kuonekana. Ndani ya treni walikuwa kimya kabisa, hawakutaka kuzungumza jambo lololote lile. Walijifanya kufuatilia safari huku wakiwa wameviinamisha vichwa vyao. Kutoka hapo Johannesburg mpaka Pretoria walitumia saa mbili na dakika kadhaa, wakafika ambapo hawakutaka kukaa sana, ilikuwa ni lazima waunganishe safari mpaka Polokwane. Hapo hakukuwa na treni ya kwenda huko, walitakiwa kuchukua basi ambalo lingewapeleka mpaka huko. Bado hilo halikuwa tatizo, wakakata tiketi na kuanza kuelekea Polokwane. Ndani ya basi hilo kulikuwa zaidi ya abiria hamsini, kila mmoja alionekana kuwa na jambo lake, wote walikuwa bize huku wengine wakiwa na mizigo mikubwa, hakukuwa na mtu aliyemfuatilia mwenzake, kila mmoja alikuwa bize na mambo yake. Walichukua saa nne ndio wakaingia huko. Giza tayari lilianza kuingia na kulikuwa na baridi kali, wakatafuta vyumba na kwenda kulala. Huko, kila mtu aliendelea kuwa na mawazo juu ya watu wake. Mzee Todd alikuwa kwenye maumivu makali, bado hakuamini kama kwelii familia yake ilikuwa imeuawa kinyama, alikuwa na hasira mno na hakuona kama kweli Maxwell alistahili kuishi, kwa kuwa aliimaliza familia yake, naye ilikuwa ni lazima ammalize kwa gharama yoyote ile. Upande wa pili na Bruno alikuwa na mawazo yake kuhusu mpenzi wake, Sharifa. Moyo wake ulikuwa na shauku kubwa ya kumuona kwa mara nyingine tena na kumwambia kile kilichotokea na kwamba hakufa. Kwa kiindi hicho, kwa esa ambazo zilikuwa katika akaunti yake aliyokuwa ameifungua hao Afrika Kusini zilikuwa nyingi mno ambazo angeweza kuzitumia kwa kufungua biashara nyingi nchini Kenya. Wakati mwingine alitamani hata kumkimbia mzee Todd na kupotea zake lakini kila aliofikiria hali ya mzee huyo, hatua alizokuwa akipitia katika maisha yake, hakuona kama lilikuwa jambo jema kufanya kile kilichokuwa kikimjia kichwani mwake. Asubuhi iliofika, wwakajiandaa kwa ajili ya kuendelea na safari yao kama kawaida. Hapo Polokwane Mjini walitakiwa kuanda basi mpaka sehemu iitwayo Mankweng ambao hao wangeunganisha mpaka Tzaneen, Nkowankowa hadi Phalaborwa ambao hao wangekutana na vijana waliokuwa wakifanya shughuli ya kuwaitisha watu miakani kwa njia za anya kuelekea nchini Msumbiji. Hawakutaka kuoteza muda, baada ya kula na kuchukua kiasi cha esa kilichoonekana kuwatosha, wakaondoka kuendelea na safari yao. Ilikuwa ndefu mno, waliondoka asubuhi lakini mpala inafika majira ya saa kumi na mbili jioni bado hawakuwa wameingia Phalaborwa ambao wangetakiwa kulala. Kila mtu ndani ya gari alichoka kuita kawaida, waliofika Nkowankowa, kama kilometa mia nne mpaka Phalaborwa wakaamua kulala hao. Hakukuwa na abiria aliyeruhusiwa kutoka ndani ya gari, walitakiwa kubaki humohuko kwani sehemu za vijiji kama hizo hazikuwa nzuri kwa usalama wao. Abiria wakalala usingizi wa mang’amung’amu hadi asubuhi ambao safari ikaendelea kama kawaida. Hapo, kutokana na ubovu mkubwa wa barabara walitumia saa sita kufika Phalaborwa. “Nyie mnataka kwenda wapi?” aliuliza kijana mmoja. “Msumbiji!” alijibu Bruno. “Msumbiji! Kwa njia za halali au?” “Kama ingekuwa kwa njia ya halali unahisi tungekuja huku?” aliuliza Bruno, alichoka, hakuhitaji maswali yoyote yale. Kijana yule akawachukua na kuwapeleka katika jumba moja chakavu ambapo huko wakakutana na vijana watatu ambapo yule kijana mmoja akawaelezea shida yao na kupewa maelekezo kwamba walitakiwa kuyafuata kama walitaka kufika nchini Msumbiji salama kabisa. “Yapi hayo?” aliuliza Bruno. “Kwanza mna randi elfu tano?” aliuliza kijana mmoja huku akiwa ameshika kipande cha bangi. “Pesa si tatizo,” alisema Bruno na kutoa kiasi cha pesa kilichokuwa kikihitajika na kumpa. Kijana yule akaanza kuwaambia kuhusu safari yao ambayo wangewaelekea mpaka katika msitu wa Kruger na wao kuunganisha mpaka nchini Msumbuji. Kruger ulikuwa moja ya misitu hatari sana iliyokuwa na wanyama wakali. Waliwaambia kwamba wao wangewapeleka mpaka mwanzo wa msitu huo na safari ya mbele walitakiwa kwenda peke yao ila wangewaambia njia nzuri na salama mpaka kufika nchini humo. Hilo halikuwa tatizo hata kidogo, mchana huohuo wakaanza safari ya kuelekea katika msitu huo ambao ulikuwa ni kama kilometa kumi kutoka hao waliokuwa. Njiani walikuwa wakipiga stori na Bruno kuwaambia kwamba wao walikuwa maharamia ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kuteka meli Afrika Kusini na kukomba mizigo yote lakini kwa kipindi hicho walitakiwa kurudi Msumbiji kwa kuwa kule Cape Town hakukuonekana kuwa salama kabisa. “Na kama mimi nikitaka kuwa mharamia?” aliuliza jamaa mmoja. “Kwanza ni lazima ujue kuigana, uwe japo na mkanda mmoja wa karate, ujue kuua kwa kumpiga mtu sehemu hatari mwilini mwake lakini la zaidi ni lazima ujue kuambana na watu hata sita waliokuwa na bunduki,” alisema Bruno huku akionekana kuwa makini sana. “Wewe umefuzu?” “Ndiyo! Nakumbuka mtu wa kwanza kabisa kumuua alikuwa The Ruler! Mnamfahamu?” aliuliza Bruno. “Haana! Ndiye nani?” “Eeeh! Hamumfahamu mtu aliyekuwa akitisha sana kwa mauaji Somalia, yule ambaye alimteka mpaka mtoto wa rais?” aliuliza Bruno. “Hapana!” “Fuatilieni, mtajua mtu huyo alikuwa ni hatari kiasi gani. Ndiye mtu wa kwanza kumuua,” alisema Bruno. Kila kitu alichokuwa akiongea mahali hao kilikuwa ni uongo asilimia mia moja. Aliwaangalia vijana hao, hawakuwa wakieleweka, kwa jinsi walivyoonekana, alihisi kabisa kama wangeweza kuwageukia baada ya kuona pesa. Aliliona hilo na ndiyo maana alikuwa akiwaambia stori za uongo zilizowafanya vijana hao kuanza kuogoa na kuhisi kwamba walikuwa na watu hatari sana ambao wangeweza kuwapiga ndani ya dakika kadhaa tu. “Na huyo Mzungu?” aliuliza jamaa mmoja kwa sauti ya chini. “Huyo ndiye mafia mwenyewe. Muitalia, hana maneno mengi lakini ana roho ya kinyama zaidi ya Musolini,” alisema Bruno, wote wakashtuka. “Mmh!” “Huyo ni mtu hatari sana, unamuona anachechemea, alipigwa risasi tano mguuni, lakini mpaka leo bado anatembea, huyo ni mtu hatari sana,” alisema Bruno, vijana wale wakawa na hofu zaidi na kuona kwamba muda wowote ule wangeweza kugeuziwa kibao. Wakaona safari ikiwa mbali mno, hawakutaka kuwaamini tena watu hao, walionekana kuwa hatari na hawakuwa na mchezo hata kidogo. Baada ya saa moja, wakafika waliokuwa wakielekea na kuwapa maelekezo kuhusu njia walizotakiwa kupita. “Ila kumbukeni kwamba kuna wanyama wakali sana,” alisema jamaa mmoja, Bruno akaanza kucheka. “Wanyama wakali? Hahaha! Hawana nafasi, tuna uwezo wa kupambana na simba zaidi ya watano, usijali,” alisema Bruno maneno ambayo yaliwafanya vijana wale kuhisi kwamba mtu huyo alikuwa jasiri sana. “Basi sawa. Safari njema,” alisema mmojawao. “Sawa,” aliitikia Bruno na kuanza safari ya kuelekea katika mbuga ya wanyama ya Kruger iliyokuwa ikisifika kuwa na wanyama wakali. *** Hawakutakiwa kuogopa kuingia msituni, ilikuwa ni lazima wavuke na kusonga mbele mpaka nchini Msumbiji. Mbuga ya Kruger ilitisha mno, kila walipokuwa wakipiga hatua ni sauti za ndege na wanyama tu ndizo zilizokuwa zikisikika kila kona. Waliendelea kusonga mbele, walikuwa makini, mioyo yao ilikuwa ikimuomba Mungu wasiweze kuingia mikononi mwa wanyama wakali kama simba, chui na wengineo. Ndani ya saa tatu walikuwa wakitembea tu, walichoka lakini hawakutaka kupumzika. Njiani walikutana na wanyama wa kawaida kama nyumbu, swala, tembo na wanyama wengi wanaokula majani. Baada ya kutembea kwa umbali wa kilometa kama thelathini ndipo wakabahatika kuiona hoteli moja kubwa na ya kitalii iliyoandikwa King Lion kwa juu ambayo ilikuwa maalumu kwa watalii waliokuwa wakitembelea mbuga hiyo. Wakaanza kuifuata, walipoifikia, getini wakasimamishwa na walinzi walioonekana kuwashangaa mno. Hawakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea mpaka watu hao kutembea katika mbuga hiyo ambayo ilikuwa ikitisha kupita kawaida. “Nyie mmetoka wapi?” aliuliza mlinzi mmoja huku akiwashangaa. “Huko mbugani!” “Mmewezaji kutembea katika mbuga hii?” aliuliza mlinzi mwingine. Kulikuwa na matukio kadhaa yaliyokuwa yakitokea huko, watalii walikuwa wakiuawa hovyo kila walipokuwa wakitembea, katika hoteli hiyo, kulizungushwa nyavu ngumu kwani hapo kabla simba walikuwa wakiingia na kuwashambulia watalii. Kitendo cha wao kutembea mbugani na kuonekana kuwa salama kabisa kilionekana kama muujiza fulani kwa walinzi wale. “Tumekuja kupanga vyumba,” alisema Bruno, aliamua kuwakatisha kwani walichokuwa wakikizungumza kilikuwa ni usalama wao tu wakati walipokuwa wakipita mbugani. Hilo halikuwa tatizo, wakachukuliwa na kupelekwa ndani mpaka mapokezi ambapo hapo wakachukua vyumba na kutulia. Kabla ya kwenda kila mtu chumbani kwake, mzee Todd akataka kukaa na Bruno kwa lengo la kuzungumza naye mambo mengi, hilo halikuwa tatizo, Bruno akakubaliana naye na hivyo kuanza kuzungumza. Kitu kikubwa kabisa alichokisema mzee huyo ni kumshukuru Bruno kwa kile alichokuwa amemfanyia, alipambana naye, alimsaidia pasipo kuangalia kama walikuwa wakifahamiana kabla au la. Walikutana kwenye meli lakini kwa jinsi alivyokuwa akimsaidia ilikuwa ni kama ndugu yake wa karibu au rafiki ambaye walikutana tangu miaka mingi nyuma. “Ni upendo tu! Nitahakikisha unafika nyumbani kwako salama,” alisema Bruno huku akimwangalia mzee huyo. “Nitashukuru sana. Sina familia, unalijua hilo?” aliuliza mzee Todd. “Nalijua, sitaki kukumbuka, inaniuma sana kila nikikumbuka kile nilichokuwa nikikiona kwenye televisheni,” alisema Bruno huku uso wake ukionyesha ni kwa jinsi gani alikuwa na huzuni moyoni mwake. “Kuna jambo jingine muhimu nitakwambia siku nyingine, labda baada ya kufika nchini Kenya,” alisema mzee huyo na kumruhusu Bruno kuondoka. Bruno hakujua ni kitu gani mzee Todd alitaka kumwambia, hakutaka kufikiria sana, kichwa chake kikaanza kumfikiria mpenzi wake, Sharifa ambaye alikuwa nchini Kenya huku akijua kwamba alikuwa marehemu. Alitamani sana kumpigia simu lakini hilo lilishindikana kwa kuwa hakuwa na namba ya mtu yeyote kutoka nchini Kenya. Hapo, wakakaa siku ya kwanza, wakakaa siku ya pili mpaka ya kumi, hawakutaka kuondoka haraka kwani waliona kuwa hiyo ilikuwa sehemu salama na ya kujificha ambapo kusingekuwa na mtu yeyote ambaye angebaini kwamba walikuwa mahali hapo. *** Watalii waliendelea kumiminika ndani ya hoteli hiyo, kila siku kulikuwa kunaingia idadi kubwa ya watalii waliofika nchini Afrika Kusini kwa lengo la kuangalia wanyama waliokuwa katika mbuga hiyo. Wakati hao wakiendelea kuingia humo, wengine walikuwa wakiondoka huku wakiwa wamelipa kiasi kikubwa cha dola kilichoifanya nchi hiyo kupiga hatua kubwa kwenye sekta ya utalii. Wazungu hao hao waliokuwa wakiingia ndiyo walioweza kumbaini mzee Todd. Siku ya kwanza kumuona tu, hawakutaka kujiuliza, walimfahamu mzee huyo, walikuwa wakifuatilia sana kwenye televisheni kuliko Waafrika ambao mtu huyo alikuwa barani kwao. Hawakutaka kuchelewa, haraka sana simu ikapigwa mpaka jijini Johannesburg ambao wao wakawasiliana na polisi waliokuwa katika mbuga hiyo na kuanza kufanya harakati za kumtia mzee huyo mikononi mwao. Walikijua chumba alichokuwa amepanga, wateja walisema walimuona mzee huyo akiingia chumbani kwake lakini hakukuwa na mtu aliyejua kama mwanaume huyo alikuwa mzee Todd aliyekuwa akitafutwa dunia nzima. Polisi hawakutaka kuchelewa, haraka sana wakaelekea katika chumba alichokuwa amepanga na kuanza kugonga huku wakihitaji kufunguliwa mlango. Hakukuwa na mtu aliyefika kuufungua kitu kilichowapa uhakika kwamba inawezekana mzee huyo alikuwa amelala au alikuwa bafuni akioga. Kwa kutumia kadi ya kuingilia ambayo waliichukua kwa mhudumu, wakaufungua mlango na kuingia ndani. Humo, hawakukutana na mtu yeyote yule, kitanda kilikuwa kimetandikwa huku juu ya meza kukiwa na kikombe kilichokuwa na kahawa, walipokwenda kukiangalia, kwa jinsi mule ndani kulivyokuwa ilionyesha kabisa kwamba mtumiaji wa kikombe kile hakuwa ameondoka muda mrefu uliopita, hivyo wakazidi kumtafuta. Walimtafuta kila kona lakini hawakuweza kumpa. Wakatoka ndani na kuelekea nje, huko, wakaliona gari moja la watalii likitaka kuondoka mahali hapo kuelekea mbugani zaidi kwa lengo la kuangalia wanyama. Wakahisi kwamba mzee huyo alikuwa humo, wakalifuata na kuanza kuwaangalia watalii wote waliokuwa wamesimama na wengine kukaa kwa nyuma, waliangalia kwa makini sana lakini mwanaume huyo hakuonekana. Wakajua kabisa kwamba hakuwa humo, wakaondoka kurudi hotelini na kuanza kumtafuta tena. Walitumia nguvu nyingi sana lakini hawakuwa wamefanikiwa hivyo kuwauliza tena wale Wazungu kujua kama kweli mtu waliyekuwa wamemuona ndani ya chumba kile alikuwa mzee Todd au walimchanganya. “He was the one!” ( alikuwa yeye?) “Madam, we have tried to look for him i every corner but we didn’t find him,” (mama, tumejaribu kumtafuta kila kona lakini hatukumpata) alisema polisi mmoja. “But I saw him, he was the one,” (lakini nilimuona, alikuwa mwenyewe) alisema mwanamke huyo huku akionekana kuwa na uhakika wa kile alichokuwa akikizungumza. Walimwamini, wakaelekea tena na kuanza kumtafuta lakini hawakufanikiwa kumpata. Hilo liliwashangaza sana, wakatoka na kuanza kuangalia mpaka nje ya hoteli ile, walipomkosa, wakaamua kwenda kuangalia kwenye orodha ya magari yaliyoondoka na watalii kwenda kuangalia wanyama. “Yameondoka magari mawili tangu saa moja,” alisema mwanaume aliyekuwa akitoa ruhusa ya kuyaondoka magari hapo kuelekea ndani kabisa ya mbuga hiyo. “Sawa.Ila ninachokijua mimi ni kwamba magari huwa yanakwenda upande wa Magharibi, si ndiyo?” aliuliza polisi. “Ndiyo! Huenda huko kwa kuwa ndiyo kulipokuwa na wanyama.” “Sasa mbona kuna moja limekwenda Mashariki?” aliuliza. “Mashariki?” “Ndiyo!” “Haiwezekani!” “Kwani wewe unaporuhusu magari yaondoke, huwa huyaangalii?” “Nayaangalia. Dereva alivyopiga simu kuhitaji gari nilimwambia aende ofisini kwangu kuchukua ufunguo kwani nilikuwa nimebanwa na haja hivyo nilikwenda chooni,” alijibu. “Basi habari ndiyo hiyo! Kuna moja limekwenda upande wa Mashariki,” alisema polisi huyo, mwenzake akaingilia: “Ila si tumeangalia kwenye lile gari lililokwenda Mashariki na tukamkosa?” “Ndiyo! Ila kwa nini lielekee Mashariki? Nahisi kuna kitu! Hebu tulifuatilieni,” alisema polisi huyo, wakatoka kwa kasi, wakachukua gari lao na kuanza kulifuatilia gari hilo katika upande ule wa Mashariki huku kila mmoja akihisi kwamba ndani ya gari lile alikuwepo mzee Todd, ila kila walipokuwa wakikumbuka kuwa walipokwenda kuwaangalia watu waliokuwemo mule hawakuweza kumuona, walichanganyikiwa, kwa hiyo safari yao ilikuwa ni kama kwenda kubahatisha tu.
Tangu walipoanza kukaa katika Hotel ya King Lion hawakuwa na amani kabisa, walikuwa na hofu kwa kuhisi kwamba watu waliokuwa hapo wangeweza kuwagundua. Hawakuwa na wasiwasi na watu weusi, waliwajua kwamba hawakuwa wafuatiliaji, hata kama wangeonyeshewa picha sasa hivi kwamba mtu huyu anatafutwa basi ndani ya dakika ishirini kama wangekutana naye ingekuwa vigumu sana kumkumbuka. Walichokuwa wakikiogopa ni hao Wazungu waliokuwa wakiingia na kutoka katika hoteli hiyo. Ni kweli mzee Todd alikuwa akivaa kofia na wakati mwingine miwani lakini hilo halikumfanya kuwa na amani moyoni mwake, alihisi kabisa kwamba kuna siku tatizo fulani lingeweza kutokea. Walikaa hapo kwa siku kadhaa, baada ya hapo, kuna mtu alionekana kumtilia shaka kwani kila alipokuwa akimwangalia, hakuwa akiyahamisha macho yake kwa haraka, ilikuwa ni kama alikuwa akimfahamu au waliwahi kukutana naye kwa siku chache zilizopita. Hiyo haikuwa mara ya kwanza, ilikuwa ni mara nyingi Mzungu huyo alikuwa akionekana kuwa na wasiwasi naye. Walichokifanya ni kuanza kusuka mipango ya kutoroka kwani wasingeweza tena kuendelea kubaki mahali hapo. Hiyo ilikuwa ni mbuga kubwa ya wanyama, kwa ile iliyokuwa upande wa Afrika Kusini iliitwa Kruger ila kwa upande wa Msumbiji iliitwa Limpopo. Kutoka Kruger mpaka Limpopo kulikuwa na umbali wa kilometa zaidi ya hamsini, ilikuwa ni mbali mno hivyo walihitaji usafiri wa kuondoka nao kuelekea katika mbuga hiyo. Alichokifanya Bruno ni kuanza kufuatilia, alitaka kujua jinsi madereva wa magari yale ya kuwatembeza watalii mbugani walikuwa wakipata vipi ufunguo. Kwenye kufuatilia kwake akagundua kwamba kulikuwa na ofisi maalumu waliyokuwa wakienda na kuchukua ufunguo huko. Humo kulikuwa na meneja wao, hakuishia hapo, aliendelea kufuatilia na kugundua kwamba meneja huyo hakuwa na choo ndani ya ofisi yake, alipokuwa akitaka kujisaidia, alikwenda katika choo cha wafanyakazi na kujisaidia. Mbali na hayo yote, alihitaji nguo. Akapeleleza na kugundua mahali ambapo nguo za madereva zilipokuwa zikikaa. Akaanza kufuatilia ratiba za madereva hao na kugundua kwamba kwa siku kati ya magari nane yaliyokuwa mahali hapo yalikuwa yakiondoka magari sita na mawili kubaki. Akajipanga na mzee Todd, siku ambayo walitakiwa kuondoka, Bruno alikuwa akiangalia saa yake tu huku akiwa amemwambia mzee Todd ajiandae. Alikaa katika kiti kilichokuwa karibu na ofisi ya meneja wa hoteli hiyo, watu walikuwa wakiingia na kutoka ndani ya ofisi hiyo. Hakuwa na haraka, alichokuwa akikiangalia ni idadi ya magari yaliyokuwa kule nje, alikuwa akiyafuatilia kwa karibu kabisa. Baada ya saa nne kukaa katika kiti kile, mlango wa ofisi ile ukafunguliwa na meneja kutoka. Akamsalimia na kuelekea chooni kujisaidia. Hiyo ndiyo ilikuwa nafasi yake, haraka sana akasimama, akachungulia dirishani, gari iliyokuwa imebaki ni Jeep moja na Toyota 110 tatu. Akaingia ndani ya ofisi ile, akaangalia huku na kule, funguo zilikuwa zimewekwa kwenye ubao uliopigiliwa ukutani. Akaangalia ufunguo wa Jeep, akauchukua, akaelekea katika chumba kidogo ambacho kilikuwa kikitumika kuhifadhia nguo za wafanyakazi, akachukua shati moja na kutoka harakahara. Alipofika nje, akamuita mzee Todd, akamfuata, Wazungu wengine walipomuona mzee Todd akielekea kule kulipokuwa na gari, wakahisi kwamba zamu yao ilikuwa imefika hivyo kuifuata gari ile na kupanda huku mzee Todd akiwa mbele na Bruno. “Tutafanyaje kama hawa wamepanda?” aliuliza mzee Todd huku akionekana kuwa na hofu. “Tunaondoka nao!” “Mbugani?” “Hapana! Mjini,” alisema Bruno. Hakutaka kuchelewa, hapohapo akaliwasha gari hilo, alipotaka kuliondoa tu, akashtukia akisimamishwa na polisi waliokuwa wakija kule kwa kasi, akatulia na kuwasikilizia huku akionekana kuwa na hofu nzito. Polisi wale walifika mahali pale na kuanza kuwaangalia Wazungu wale waliokuwa nyuma, walimwangalia mmoja baada ya mwingine, waliporidhika wakaliruhusu pasipo kuangalia mbele kwani walijua watu waliokuwa wakikaa mbele walikuwa muongozaji na dereva tu. Bruno akapiga gia na kuanza kuondoka mahali hapo. Hakuendesha kwa mwendo wa kasi kwa kuwa hakujua kuendesha gari vizuri, pale mbele alikuwa akipewa maelekezo na mzee Todd ambapo kila alipokuwa akiyafuatisha, gari lilikuwa likiondoka mpaka alipozoea. Wakaondoka mahali hapo, Wazungu wale nyuma hawakujua mahali walipokuwa wakielekea, walionekana kuwa na wasiwasi kwani walizoea kuona wakiondokea upande wa Magharibi lakini siku hiyo walikuwa wakienda upande mwingine kabisa, upande wa Mashariki. Hawakuuliza, gari lilikuwa kwenye kasi, njiani walikuwa wakipishana na wanyama, waliamini kwamba gari lingesimama na wao kuwaangalia wanyama hao na hata kuwapiga picha lakini haikuwa hivyo. Hawakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, gari liliendeshwa kwa kasi mpaka lilipofika katika eneo lililokuwa na kibao kilichoandikwa “Welcome Limpopo” yaani wakikaribishwa katika Mbuga ya Wanyama ya Limpopo. Ulikuwa ni mwendo mrefu mno, walitumia saa moja na nusu ndani ya hilo gari huku likiwa kwenye mwendo wa kasi. Walipofika sehemu ambayo waliamini kwamba ingekuwa salama, wakateremka na Bruno kuwafuata wale watu kule nyuma. “Nisikilizeni,” alisema, kila mtu akawa kimya huku akiogopa. “Kana kuna mtu anajua kuendesha gari, aende mbele aendeshe mrudi hotelini, sisi tushafika,” alisema Bruno. Hawakutaka kubaki mahali hapo, wakaondoka kusenga mbele ambapo waliamini kwamba kungekuwa salama kabisa. Mtalii mmoja akaelekea mbele ya gari lile na kuanza kuliendesha kurudi hotelini huku kila mmoja akishangaa juu ya watu wale, walikuwa wakina nani? Na kama walikuwa wabaya kwa nini hawakuwajeruhi? Kila walichojiuliza walikosa majibu. Polisi wale waliokuwa wakielekea kule lilipokwenda gari lile, baada ya nusu saa wakakutana na gari la watalii likirudi hotelini kwa mwendo wa kawaida. Wakalisimamisha na kuwauliza kuhusu watu hao, wakawaambia kila kitu kilichotokea na kusisitiza kuwa watu wale hawakuwa hatari kwa sababu kama wangekuwa hatari ilikuwa ni lazima wawafanyizie au hata kuwaibia kila kitu walichokuwanacho. “Ni watu wema sana, sidhani kama walikuwa na malengo mabaya, ila ni watu wazuri mno, hawakutujeruhi wala kutuibia,” alisema jamaa mmoja huku akionekana kumaanisha kile alichokuwa akikizungumza. *** “Ni wakina nani hao?” “Sifahamu.” “Hebu vuta kamera kwa karibu zaidi. Hapohapo, hebu waangalie vizuri!’ alisema mwanaume mmoja. Watu wanne walikuwa ndani ya chumba kilichokuwa na kompyuta kadhaa ambazo ziliunganishwa na baadhi ya kamera zilizokuwa zimefungwa katika Mbuga ya Wanyama ya Limpopo. Walikuwa wakifuatilia kila kitu kilichokuwa kikiendelea kupitia katika kompyuta zao. Waliweza kumuona Bruno na mzee Todd wakipiga hatua katika mbuga hiyo. Walipowaangalia, kitu cha kwanza kabisa kilichokuja kichwani mwao ni kwamba watu hao walikuwa majangili. Mikononi hawakuwa na bunduki yoyote ile lakini walihisi kwamba inawezekana walikuwa wamezificha sehemu kwa kuwa tu hawakutaka kuonekana nazo. Haraka sana simu ikapigwa kuelekea katika kitengo maalumu cha ulinzi na kuwaambia kilichokuwa kikiendelea. Taarifa iliyotolewa ni kwamba watu hao walikuwa majangili na hivyo walitakiwa kufuatiliwa haraka sana. Hilo halikuwa tatizo, vijana waliokuwa na bunduki nzito wakaanza kuelekea huko, upande wa Magharibi ambapo kila mmoja aliamini kuwa walipewa taarifa ya watu hao kwa kuwa walikuwa majangili. *** Bruno na mzee Todd hawakuwa na habari, walikuwa wakiendelea kusonga mbele huku wakiwa makini kuangalia kila kona. Walimuomba Mungu awalinde kwani mbuga hiyo ilikuwa na wanyama wakali na wakati mwingine walikuwa na sifa ya kuwashambulia watalii waliokuwa wakienda huko. Walitembea kwa mwendo wa haraka uliojaa umakini, kila walipokuwa wakiwaona wanyama wanaokula majani, waliongeza umakini zaidi kwani waliamini kwamba pembeni yao kulikuwa na wanyama wala nyama kama simba, chui na wengine wengi. Hawakuwa wakiongea, kwa jinsi walivyokuwa wakionekana, walihisi kabisa kwamba wangesikiwa na wanyama ambao kuna uwezekano walikuwa wamejificha mahali fulani. Waliendelea kupiga hatua na baada ya kufika katika mto Mturuma, wakasimama na kuanza kujadiliana kama ilikuwa ni sahihi kuvuka mto huo au la. “Ila unahisi kutakuwa na mamba?” aliuliza Bruno. Mzee Todd akauangalia kwa makini zaidi, maji yake yalikuwa yamesimama, aina ya mito hiyo huwa hatari kwa sababu mamba hupendelea kukaa humo. Hawakutaka kuuvuka kwanza, ilikuwa ni lazima kuufanyia upekuzi kabla ya kuchukua uamuzi wa kuuvuka. Wakati wakiwa wanajadiliana ndiyo kilikuwa kipindi ambacho askari pori walikuwa wakija kule walipokuwa kwa kasi kubwa. Walikuwa ndani ya magari yao, walishikilia bunduki na kuona kabisa huo ulikuwa muda wa kuwakamata watu hao na kuondoka nao kwani miongoni mwa vitu vilivyokuwa vikipigwa marufuku na ambavyo kesi yake ilikuwa kubwa ilikuwa ni ujangili. Wakati wamekaa hapo, wakasikia mlio wa magari kutoka nyuma yao, waliogopa, walijua tu kwamba walikuwa maaskari, wakabaki wakiwa wamesimama, walikuwa na uwezo wa kuingia ndani ya mto ule lakini mioyo yao ilikuwa migumu kabisa kuchukua uamuzi huo. Wakabaki wakiwa wamesimama, magari hayo mawili yakafika, maaskaro watano waliokuwa na bunduki wanateremka na kuanza kuwafuata, walipowafikia, hawakutaka kuzungumza nao jambo lolote lile, wakawachukua na kuondoka nao. “Mna bahati sana, yaani mngeingia ndani ya ule mto, tungeipata mifupa yenu tu,” alisema askari mmoja huku akiwaangalia watu hao. Ndani ya gari ndipo wakaambiwa kwamba walikuwa chini ya ulinzi kwa kuwa iligundulika kwamba walikuwa majangili. Walishangaa, walijitetea kwamba hawakuwa majangili lakini hakukuwa na mtu aliyewaelewa. Walifungwa pingu na kupelekwa mpaka katika kituo cha polisi cha hapo mbugani na kuambiwa kusubiri. Humo, hawakunyamaza, waliendelea kusisitiza kwamba hawakuwa majangili na hivyo walitakiwa kuachwa na kuondoka lakini askari hawakutaka kuwaacha. Ilipofika mchana, mlango wa mahabusu ukafunguliwa na kuambiwa kutoka ndani ya mahabusu ile. Wakachukuliwa na kuelekwa katika ofisi ya mkuu wa kituo kwa lengo la kuhojiwa maswali kadhaa. Mkuu huyo aliwaangalia, alijua kabisa kwamba watu hao hawakuwa majangili kwa kuwa walipokuwa wamewafuatilia hawakuwakuta na silaha yoyote ile ambayo ingewaonyesha kwamba walikuwa majangili. Aliwaweka ofisini kwake na kuanza kuzungumza nao, kitu pekee alichotaka kufahamu ni sababu ya watu wale kuwa mule mbugani, walikuwa wakitafuta nini na walikuwa wakielekea mahali gani. “Tulipotea njia,” alisema mzee Todd, alimwambia Bruno kwamba hakutakiwa kuzungumza kitu chochote kile. “Kutoka wapi?” Wakaanza kumwambia stori nyingine kabisa ambayo ilikuwa ni uongo mtupu, walimwambia kwamba walikuwa na wenzao kutoka nchini Afrika Kusini ambao walikuwa wakitembea katika mbuga ya wanyama kwa lengo la kutafuta dawa za mitishamba lakini wakati wakiwa huko, walikimbizwa na wanyama wakali na kupotea na hata pale walipokuwa hawakujua walikuwa mahali gani mpaka walipofikishwa kituoni. Kwa sababu aliongea mzee Todd, aliaminika kwa asilimia mia moja na hiyo kuambiwa kwamba warudi kwanza mahabusu kabla ya kutolea ambapo moja kwa moja wangechukuliwa na kurudishwa Afrika Kusini. “Ila sisi siyo Waafrika Kusini!” alisema Bruno. “Nyie mmetoka wapi?” “Kenya!” “Kwa hiyo mnataka mrudishwe Kenya?” “Ikiwezekana mkuu kwani tulikwenda Afrika Kusini kwa ajili ya hizo dawa za mitishamba tu!” alisema Bruno. “Basi sawa!” Wakati wakiwa ofisini kwa mkuu wa kituo, polisi wengine walikuwa katika chumba kingine wakiangalia televisheni. Huko ndipo walipoweza kuiona picha ya mzee Todd akiwa mmoja wa watuhumiwa waliokuwa wakitafutwa kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya nyumbani kwake. Polisi wakabaki wakiangalia, mwanaume aliyekuwa akionyeshwa walimfahamu sana, alikuwa yuleyule ambaye walikuwa naye katika kituo hicho. Haraka sana wakainuka na kuelekea ofisini kwa mkuu wao na kumwambia kile kilichokuwa kimetokea. Haraka sana naye akafungua televisheni na kuangalia kile alichoambiwa, ni kweli alikuwa mzee Todd, mwanaume aliyekuwa akitafutwa na CIA kwa udi na uvumba. Wakafurahi, kiasi kilichokuwa kimetolewa kilikuwa kikubwa mno, lingekuwa kosa kubwa kama wangemuachana mwanaume huyo aondoke mikononi mwao. Mkuu akawaambia vijana wake kwamba hawakutakiwa kuwashtua, ili waweze kumpata vizuri na kuondoka naye mpaka mjini ambapo huko wangempeleka mpaka katika kituo kikuu cha polisi kilichokuwa Limpopo. Ndani ya saa moja, wakawatoa katika mahabusu kirafiki kabisa, waliwaambia kwamba walitakiwa kusafirishwa haraka sana kuelekea nchini Kenya waliokuwa wakitaka kuelekea. Kwa jinsi mkuu wa kituo alivyokuwa akiongea, alionekana kumaanisha alichokuwa akiwaambia na hakutaka kuwaonyeshea dalili zozote za kuonekana walikuwa na la jambo. Njiani, walikuwa wakizungumza, waligongesheana mikono lakini mioyoni mwao walijua kile ambacho kingekwenda kutokea mbele ya safari. Walipanga kupita nao mjini, kwenda sehemu fulani ambao huko wangewaweka chini ya ulinzi na kuwachukua kuwaeleka katika kituo kikuu cha polisi. Gari liliendeshwa kwa mwendo wa kawaida kabisa, walikuwa wakipiga mahesabu jinsi ya kuwaweka watu hao chini ya ulinzi kwani kwa jinsi mabosi wa madawa ya kulevya walivyokuwa watu hatari, walihisi kabisa kwamba kama wangefanya mchezo wangeweza kuuawa wao. Gari lilibakiza umbali kama wa mita elfu moja kufika katika kituo hicho cha polisi, polisi hao wakaanza kuandaa bunduki zao kitendo kilichowashtua Bruno na mzee Todd na kuhisi kwamba kulikuwa na kitu kilichotakiwa kutokea. “Mmh!” aligunda Bruno, polisi hao wakawanyooshea bunduki zao na kuwaambia kwamba walikuwa chini ya ulinzi. “Jamani! Tumefanya nini?” aliuliza Bruno huku akiambiwa alale chini haraka sana. “Todd! Kila mtu anakujua kama wewe ni mtu hatari sana. Upo chini ya ulinzi, ulidhani ungeisumbua dunia kwa kipindi kirefu? Ni muda wako kwenda kuhukumiwa kwa kile kilichotokea, ila pole sana kwa vifo vya familia yako, sikuwa nimekugundua mpaka nilipoambiwa kwamba ni wewe,” alisema mkuu wa kituo huku akitabasamu, polisi wote nane waliokuwa ndani ya gari hilo waliwanyooshea bunduki. Simu ikapigwa makao makuu ya polisi na kuambiwa kwamba yule muuza madawa ya kulevya aliyekuwa akisumbua alikamatwa na hivyo walikuwa njiani kuelekea katika kituo kikuu cha polisi hapo Limpopo. Polisi wa makao makuu hawakuamini kile walichoambiwa kwamba muuza madawa huyo alikuwa amekamatwa, taarifa zikaanza kusambazwa katika kituo hicho kwamba kila polisi alitakiwa kujiandaa kumuweka chini ya ulinzi mwanaume huyo kwa kuwa alikuwa mtu hatari sana. “Wapo wapi?” aliuliza polisi mmoja. “Vasco Da Gama,” alijibu polisi mmoja sehemu ambayo haikuwa mbali sana kutoka katika kituo hicho. Polisi wote wakaweka bunduki zao tayari na walichokuwa wakikisubiria ni mwanaume huyo tu. ***
Safari ya kuelekea katika kituo kikuu cha polisi ilikuwa ikiendelea kama kawaida. Ndani ya gari lile polisi wote walionekana kuwa na furaha kupita kawaida, kwao, kumpata mzee Todd iliwafurahisha na kujiona wakipata pesa ambazo ziliahidiwa kwa yeyote ambaye angefanikisha kupatikana kwa mtu huyo. Bunduki zilikuwa mikononi mwao, walimpa ulinzi wa kutosha kwani walichokijua ni kwamba mwanaume huyo alikuwa hatari sana, kama wasingemlinda kama walivyofanya basi hali ingekuwa ya hatari mno. Mzee huyo alikuwa na Bruno humo, walimwangalia kijana yule, hawakumjua alikuwa ni nani kwa yule mzee lakini kitu walichohisi ni kwamba alikuwa kijana wa mzee Todd ambaye alikuwa akishirikiana naye kuuza madawa ya kulevya barani Afrika. Wakati wakiwa wamekwishafika katika eneo maarufu kwa kuuza vitanda, Vasco Da Gama wakashtukia wakianza kumiminiwa risasi mfululizo. Hawakujua watu hao walikuwa wakina nani, walipigwa risasi lakini hawakuwaona watu waliokuwa wakiwashambulia. Mpaka wanainama na kujificha, polisi wanne walikuwa chini, damu zilikuwa zikiwatoka. Watu waliokuwa karibu na eneo hilo, hawakutaka kubaki mahali hapo, wakaanza kukimbia kuyaokoa maisha yao. Vijana ambao waliwashambulia polisi hao, wakatoka walipokuwa wamejificha, walikuwa vijana saba wenye silaha kali aina ya AK 47, walitembea kwa mwendo wa kujiamini huku wakiendelea kulifuata gari lile. Walipolifikia, wakalizunguka na mwanaume mmoja kuwatangazia polisi waliokuwa humo kwamba walitakiwa kutupa bunduki zao vinginevyo wangelilipua gari hilo. Polisi walivyosikia hivyo wakaogopa na kufanya kama walichoambiwa. Walifanya hivyo kwa sababu mbili. Moja ni kwamba walihisi kwamba wangelipuliwa kweli lakini kubwa zaidi ni kwamba hawakuwa wakifahamu watu hao walikuwa wangapi. Walipozitupa tu, wanaume hao wakalisogelea gari hilo, wakawaangalia polisi wote, walikuwa wamelala huku wakiwa na mzee Todd na Bruno ambao nao walikuwa kimya. Vijana hao hawakutaka kupoteza muda, walichokifanya ni kuwamiminia risasi polisi wote. “Na hawa tuwafanye nini?” aliuliza mwanaume mmoja. “Nao wamalize,” alisema mwingine, wakakoki bunduki zao tayari kwa kuwamaliza mzee Todd na Bruno. *** Milio ya risasi ilikuwa ikiendelea kusikika kama kawaida. Baada ya mzee Todd na Bruno kukimbia kwa kuruka ukuta, Onyango akabaki ndani ya jumba lile na wenzake. Alijua kwamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wake, hakujua ni wakina nani walikuwa wakipiga risasi hizo, alichanganyikiwa ndani ya jumba lile kiasi kwamba wakati mwingine alitamani hata ardhi ipasuke atumbukie ndani. Alitamani kwenda kupambana lakini kwa jinsi risasi zile zilivyokuwa zikirushwa, alijua kabisa kwamba watu hao walikuwa hatari, kwani risasi zilipigwa kwa malengo na nyingi ziliwapata wenzake. Hakutaka kuona akifa, alitakiwa kupambana mpaka anashinda, njia pekee ya kuyaokoa maisha yake ilikuwa ni kuingia katika dari ndani ya nyumba hiyo. Hilo ndilo alilolifanya, haraka sana akaufungua mlango wa dari na kuingia ndani kujificha. Huko juu, kulikuwa na harufu chafu, joto lakini alitakiwa kuvumilia kwa sababu tu alitakiwa kuupambania uhai wake. Baada ya dakika chache, mlango ukafunguliwa na wanaume kuingia ndani ya jumba hilo. Aliwasikia vilivyo, wanaume hao wakaanza kuongea ndani ya jumba hilo kwamba watu wote walikuwa wamekufa. Kwa jinsi Kiingereza chao walivyoongea, alijua kabisa walikuwa Wamarekani, hawakuwa Wazungu wa Afrika Kusini, hakujua sababu za watu hao kuwa mahali hapo na kuwashambulia kiasi hicho. Baada ya dakika moja tu, wanaume hao wakaondoka baada ya kuhakikisha kwamba kila mtu aliyekuwa ndani ya nyumba ile alikuwa amekufa. Huku akijiandaa kuteremka, akasikia mlango ukifunguliwa tena, muda huo alikuwa Bruno ambaye alifuata kadi ya ATM. Hakumuona, alichokijua ni kwamba alikuwa mmoja wa Wazungu wale hivyo akajificha kama kawaida. Baada ya sekunde kadhaa, mlango ukafungwa na mwanaume huyo kuondoka. Baada ya nusu saa, Onyango akateremka kutoka ndani ya dari, kile alichokiona kilimsikitisha kupita kawaida, hakuamini kama marafiki zake wote walikuwa wamekufa ndani ya nyumba hiyo. Hali iliyokuwa ndani ndiyo iliyokuwa na nje pia, kila kona kulitapakaa miili ya marafiki zake. Siku hiyo hapo Soweto kulikuwa na msiba mzito, watu walilia sana na kuwachukua Wazungu kupita kawaida. Siku iliyofuata, Onyango akawatafuta watu wengine wa kuunda kundi jingine. Alikuwa na hasira mno na hakutaka kabisa kuona wakiendelea kushambuliwa na Wazungu, ilikuwa ni lazima wahakikishe wanapambana vilivyo. Kundi jingine likaundwa, ingawa alikuwa Mkenya lakini kila Msauzi alikuwa akimpenda, alikuwa mkorofi sana, alijua kupambana na hata kuwalaghai watu wengine waungane naye. Kuunda kundi kubwa tena haikuchukua siku moja, ilichukua wiki mbili, vijana ishirini wakajikusanya na kuunda kundi jingine kubwa la wahuni. Walichokuwa wakikihitaji zaidi kilikuwa ni silaha tu. Walizokuwa nazo, hazikutosha, walitakiwa kujipanga na kutafuta nyingine. Baada ya kundi kutimiza mwezi, wakaamua kuondoka hapo na kwenda nchini Msumbiji. Walichokuwa wakikihitaji kilikuwa ni bunduki tu. Waliogopa kufanya uhalifu Afrika Kusini kwa kuwa walihofia maisha yao na kutafutwa. Hawakutaka kuharibu huko, walitakiwa kuharibu sehemu nyingine kabisa, hivyo wakaenda huko. Watu waliokuwa na bunduki walikuwa polisi hivyo kuanza kuchunguza na kugundua kwamba kulikuwa na gari la polisi lililokuwa likitoka katika Mbuga ya Limpopo na kuelekea mjini huku wakiwa na bunduki ndani ya gari hilo. Hiyo ikawa nafasi yao, wakaelekea mjini na kutafuta sehemu kujificha. Hakukuwa na mtu aliyeonekana kuwa na hofu nao, walivaa kiheshima na walikuwa wakirandaranda mpaka kipindi ambacho gari la polisi lilipoanza kuonekana. Hawakutaka kuchelewa, walichokifanya ni kuanza kulishambulia, watu waliokuwa mahali hapo wakakimbia kwani walijua kabisa kwamba watu hao walikuwa hatari. Kwa kuwa mule kulikuwa na polisi nane, waliamini kwamba kungekuwa na bunduki za idadi hiyo ambazo zingewafanya kuwa na idadi kubwa ya bunduki na hivyo kuendelea kufanya uhalifu. “Na hawa tuwafanye nini?” aliuliza mwanaume mmoja. “Nao wamalize,” alisema mwingine, wakakoki bunduki zao tayari kwa kuwamaliza mzee Todd na Bruno. Huku kijana yule akijiandaa kuwafyatulia risasi watu hao, Onyango akaamuru waache kwani alitaka kuwaona kwanza. Hilo halikuwa tatizo, kijana huyo akaacha, Onyango akasogea mpaka kule, watu aliowaona, yeye mwenyewe akashtuka. “Bruno!” aliita huku akionekana kushtuka. “Onyango!” “Vipi tena? Mbona sielewi?” aliuliza Onyango huku akiwaangalia kwa mshangao mkubwa. Bruno hakujibu kitu, kitendo cha kumuona Onyango tu kilimaanisha kwamba maisha yao yangekuwa salama. Hilo lilikuwa eneo la tukio, hawakutakiwa kukaa sana mahali hapo, walichokifanya ni kuchukua bunduki walizokuwa wakizitaka na kuondoka mahali hapo. Wakaingia ndani ya gari na kuanza kuelekea nchini Afrika Kusini kupitia katika Mbuga ya Wanyama ya Limpopo. Walijua njia za panya, walijua njia ambazo hakukuwa na kamera. Asubuhi ya siku iliyofuata wakafika huko, wakaelekea mpaka Soweto na kupumzika. Huko ndipo Bruno akaanza kuwaambia kile kilichokuwa kimetokea, kwamba walikuwa na mpango wa kwenda Kenya lakini wakajikuta wakikamatwa. “Mnataka kurudi Kenya?” aliuliza Onyango. “Ndiyo!” “Basi subiri nifanye mpango! Endeleeni kukaa hapa.” Hawakuwa na jinsi, waliambiwa kwamba walitakiwa kusubiri na hivyo kufanya hivyo. Waliendelea kubaki mahali hapo huku siku zikiendelea kukatika. Alichokuwa akikifanya Onyango ni kuwatafutia watu ambao aliwaamini ambao wangewachukua watu hao mpaka nchini Kenya. Bruno alikuwa na mawazo tele, kwake, siku moja ilionekana kuwa na saa arobaini na nane kwani alikuwa akisubiri sana lakini hakukuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea. Wakati mwingine Bruno alikuwa akimuuliza kuhusu namba za simu za watu aliokuwa akiwafahamu nchini Kenya. Kwa Onyango, hilo halikuwa tatizo, aliwafahamu watu hao kwani kulikuwa na Wakenya wengi kutoka katika Kijiji cha Guolduvai. Onyango akawa na kazi mbili, kwanza kuwatafuta vijana ambao wangefanikisha wao kufika nchini Kenya lakini pia vijana ambao walitoka katika kijiji hicho. Baada ya mwezi kukatika ndipo akafanikiwa na hivyo kuwasiliana na Onyango na kumwambia kwamba kila kitu kilikuwa tayari. Hata kabla Onyango hakumpelekea namba ya simu ya Alfred, mwanaume ambaye alimpata Afrika Kusini, akaamua kumpigia simu yeye mwenyewe na kuanza kuzungumza naye. Alimwambia kwamba Bruno, mwanaume ambaye bila shaka alisadikiwa kufariki dunia nchini Kenya alikuwa hai nchini Afrika Kusini, ila mbali na hilo, alimwambia kwamba inawezekana Bruno akaja kuwa bilionea mkubwa kwa kuwa alikuwa na bilionea mkubwa ambaye alimsaidia kwa kila kitu. “Bruno namkumbuka! Kijiji kizima kinajua kwamba amekufa,” alisema Alfred. “Hajafa! Tupo naye huku!” “Wapi?” “Afrika Kusini!” “Inawezekana vipi?” “Ndiyo hivyo, ni stori ndefu, nafikiri akija huko atakwambia nini kilitokea,” alisema Onyango. “Kwa hiyo nifanyeje?” “Amesema mtafute rafiki yake anayeitwa Abdul, umwambie kwamba yupo hai!” “Na nimwambie kuhusu ubilionea wake?” “Hilo juu yako sasa!” alisema Onyango na kukata simu. Baada ya hapo, akarudi nyumbani na kumwambia Bruno kwamba kila kitu kilikuwa tayari hivyo walichotakiwa ni kuanza safari siku inayofuata. Hilo halikuwa tatizo, wakajiandaa, ilikuwa ni lazima waondoke nchini humo kwani walikuwa wamekaa mno huku wakinusurika vifo na vifungo. Bruno hakutaka kuridhika, alihitaji kuzungumza na huyo mwanaume kutoka nchini Kenya, hilo halikuwa tatizo, akapewa namba ya simu na kumpigia lakini kwa bahati mbaya, siku ya Alfred haikuwa ikipatikana. Mpaka kesho yake inafika na kuondoka, bado simu ya mwanaume huyo haikuwa hewani. Vijana wanne walikuwa wakiondoka nao kuelekea nchini Kenya, hawakutakiwa kufika huko, walitakiwa kuishia njiani lakini pia hawakutakiwa kupitia Msumbiji, walitakiwa kupitia Botswana, Zambia, Tanzania na kuingia nchini Kenya. Waliiona hiyo kuwa safari ndefu lakini walikuwa na uhakika kwamba watu hao wangeweza kufika huko salama kabisa. Baada ya kujiandaa kwa kila kitu, wakaanza safari hiyo kwa siri kubwa sana kuelekea nchini Kenya. Wakati huo, tayari Bruno alikwishachukua kiasi cha dola laki moja benki ambapo dola elfu ishirini alimgawia Onyango kama shukrani huku akimuahidi kumtumia kiasi kingine cha pesa baada ya kufika nchini Kenya. Safari ikaanza, ilikuwa ni ndefu na yenye kuchosha sana. Waliondoka kwa kujifichaficha sana mpaka wakatoka nje ya Afrika Kusini na kuingia Botswana. Huko, njiani kote ni pesa tu ndiyo iliyokuwa ikitumika. Walipokuwa wakiona mambo magumu, walitoa kiasi cha pesa na kuwahonga polisi hivyo kuruhusiwa kupita katika sehemu ambazo hawakutakiwa kufika. Walipoingia huko nchini Botswana, kitu cha kwanza kilikuwa ni kuchukua hoteli ya kawaida na kutulia. Bruno aliendelea kumpigia simu Alfred lakini hakuwa akipatikana, hilo lilimchanganya, alichokuwa akihitaji ni kuzungumza na mwanaume huyo na kumwambia kuhusu kwenda kule alipokuwa akiishi na kumwambia Abdul kwamba alikuwa hai. Safari hiyo ilichukua wiki tatu mfululizo na ndipo wakafanikiwa kufika Tunduma nchini Tanzania. Hapo, wakachukua basi Mbeya Mjini ambapo huo ndiyo ungekuwa mwanzo wa kuelekea nchini Kenya. Njiani, walichoka mno, walitamani hata Tanzania uwe mwisho wao, hawakutaka kuendelea zaidi lakini hawakuwa na jinsi. Walikuwa na pesa za kutosha, walipofika Mbeya Mjini, wakaelekea katika duka la kubadilisha pesa na kuchukua pesa za Kitanzania kiasi cha shilingi milioni sita na kuendelea na safari yao. Kidogo kuwepo nchini Tanzania kuliwapa amani. Watu wa huko hawakuwa wakiangalia televisheni sana, walizipata taarifa kuhusu mzee Todd lakini hakukuwa na yeyote yule aliyeonekana kujali kuhusu mzee huyo. Hapo Mbeya Mjini, walikaa kwa usiku mmoja na asubuhi wakapanda basi na kuanza safari ya kuelekea jijini Tanga. Safari yao ilichukua saa kumi na mbili wakafika jiji humo ambapo wakatulia katika nyumba ya wageni huku wakijiandaa safari ya kuelekea Mombasa. “Tunaingia Kenya kesho, ila pia tutatakiwa kuingia kwa njia za panya kama tulivyofanya huko nyuma,” alisema Bruno. “Ila Kenya si kwenu?” “Ndiyo! Sina hati ya kusafiria, nahisi litakuwa tatizo!” “Sawa. Basi tutatumia pesa kama kawaida,” alisema mzee Todd. Hilo ndilo la msingi lililotakiwa kufanywa. Walichokifanya siku iliyofuata ni kuanza safari kwa njia ya basi kuelekea nchini Kenya. Njiani, hawakuonekana kuwa na hofu, waliamini kwamba wangefika nchini humo salama kabisa. Basi lilitembea kwa mwendo wa kasi kuelekea mpakani mwa Tanzania na Kenya. Japokuwa huko kulikuwa na ulinzi mkubwa lakini walikuwa na uhakika wa kupita pasipo tatizo lolote lile. Ndani ya basi walikuwa wakizungumza mambo mengi, mzee Todd alimshukuru mno Bruno kwa kuwa alimsaidia sana mpaka kipindi hicho kuwa hai. Hakuwa na familia yake lakini kitendo cha kuwa hai kipindi hicho kilimpa uhakika wa kuendelea kuishi na kujipanga kwa ajili ya maisha yake ya mbele. Kulikuwa na kesi ya kuuza madawa ya kulevya, hakutaka kufikiria hilo sana kwani alikuwa na uhakika wa kulishinda, kitu pekee na cha umuhimu kabisa kilikuwa ni kuelekea nchini Marekani na kuendelea na maisha yake. “Nakushukuru sana Bruno, bila wewe nadhani sasa hivi ningekuwa marehemu,” alisema mzee huyo huku akimwangalia Bruno. “Tumesaidiana! Hata mimi nakushukuru sana! Naamini kila kitu kilitokea kwa mpango wa Mungu!” alisema Bruno huku uso wake ukiwa na tabasamu pana. “Unahitaji nini nikufanyie?” aliuliza mzee huyo. “Unifanyie?” “Ndiyo!” “Mimi ni masikini sana, mkwe hanitaki kwa kuwa mimi ni masikini!” alisema Bruno. “Hilo si tatizo! Kuna jingine ambalo unataka nikufanyie?” aliuliza mzee Todd. “Labda kukitengeneza Kijiji cha Guolduvai ninapoishi, hakuna zaidi,” alijibu Bruno. Walikaa na kuzungumza mengi, wakati huo safari ilikuwa ikiendelea kama kawaida. Baada ya saa kadhaa, wakakaribia katika mpaka wa Tanzana na Kenya kwa upande wa Tanga ulioitwa Horohoro. Siku hiyo ilionekana kuwa tofauti na siku nyingine, kulikuwa na idadi kubwa ya magari yaliyokuwa yakisubiri kuingia nchini Kenya. Mbali na magari hayo, pia kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakitaka kuingia na kutoka. Kila basi, abiria walitakiwa kuteremka na kuangaliwa hati zao za kusafiria. Kwao, hawakuwa na kitu chochote kile, walichokuwa wakikitegemea kilikuwa ni pesa tu walizokuwanazo. *** Mzee Hamidu alichanganyikiwa, alimwangalia binti yake, Ashura aliyekuwa kitandani ambaye alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifua kikuu (TB), moyo wake ulimuuma mno. Ugonjwa huo ulikuwa ukimsumbua kwa kipindi cha mwezi mzima, aliambiwa na daktari hapo Mombasa kwamba alitakiwa kumpeleka Nairobi kwa ajili ya matibabu lakini hakuwa na pesa. Kumpeleka Ashura huko kulihitaji kiasi kikubwa cha pesa, shilingi elfu hamsini ya Kikenya ambazo zilikuwa ni kama milioni moja kwa pesa za Kitanzania. Kilikuwa kiasi kikubwa cha pesa ambacho hata kama angefanya kazi kwa mwaka mzima bado asingeweza kupata kiasi hicho. Alimwangalia Ashura, moyo wake ulimuuma mno, alihitaji pesa kuliko kitu chochote kile. Japokuwa alikuwa mkuu wa polisi mpakani lakini bado mshahara wake haukuwa ukitosha kwa kuwa alikuwa akikatwa madeni mengi ambayo aliwahi kukopa serikali. Mke wake alikuwa ni mtu wa kulia tu, moyo wake ulimuuma, kila siku alikaa pembeni ya binti yake aliyekuwa akikohoa madonge makubwa ya makohozi, alitumia dawa mbalimbali lakini zote hizo hazikuweza kumtibu Ashura. Siku zikakatika, mzee Hamidu akawa ni mtu mwenye mawazo tele na hata ufanyaji kazi wake haukuwa kama ule ambao ulitakiwa kuwa kwa kuwa muda mwingi alikuwa akimuwaza Ashura aliyekuwa akiteseka kitandani. Wakati hali ya binti yake ikiendelea kuwa hivyo huku akiwa anaendelea na kazi yake ofisini ndipo akapelekewa watu wawili ofisini kwake, mmoja alikuwa Mzungu na mwingine mtu mweusi aliyejitambulisha kwa jina la Bruno. Watu hao walichukuliwa kutoka ndani ya gari lililokuwa likiingia nchini Kenya kupitia mpakani hapo. Hawakuwa na kitu chochote kile, walikuwa wakiingia nchini Kenya pasipo kibali na hata huyo aliyekuwa akisema kwamba alikuwa Mkenya, hakuwa na kitu chochote kile ambacho kingemtambulisha kwamba alikuwa raia wa nchi hiyo. Mzee Hamidu aliwaangalia, kichwa chake kilivurugika kabisa, hakuwa na hamu ya kuendelea kufanya kazi, alifikiria sana nyumbani kwake, hali aliyokuwa ameiacha kwa binti yake, ilikuwa mbaya mno. Bruno na mzee Todd waliogopa, walitamani sana kuingia nchini Kenya lakini kwa jinsi hali ilivyokuwa, waliona kabisa wangerudishwa au kwenda kufungwa gerezani kwa kile kilichotokea. Walibaki wakimwangalia mzee Hamidu, alikuwa kimya huku akiwaangalia kwa zamu. Kitu ambacho kilikuja kichwani mwa Bruno kilikuwa ni pesa tu. Walikuwa watu watatu ndani ya ofisi ya mzee huyo, hiyo ilikuwa nafasi ya Bruno kuhakikisha anampa rushwa mzee huyo ili wavuke salama mpakani hapo. Hakuamini kama kungekuwa na Mwafrika ambaye angekataa pesa, kila mtu alihitaji pesa kwa kuwa mishahara ya wafanyakazi wa Afrika haikuwa ikitosha kabisa. “Mlikuwa mnavuka mpakani pasipokuwa na vibali, ni kweli?” aliuliza mzee Hamidu huku akiwaangalia. “Ni kweli ila…” “Hakuna cha ila, suala ni kwamba mlikuwa mnavuka bila vibali, tena mkajiamini kwa kuona kuwa polisi hawawezi kuwababaisha, mkaona kabisa kwamba sisi si kitu na ndiyo maana mkajiamini, si ndiyo?” aliuliza mzee Hamidu, alionekana kuwa siriazi kupita kawaida, na kila alipokuwa akizungumza, alionyesha na vitendo kabisa. Kwa jinsi alivyoonekana, ilikuwa vigumu kwa Bruno kuhisi kama mzee huyo angekubali kupokea rushwa, alionekana mwanaume mkakamavu ambaye aliiheshimu mno kazi yake. Aliwaambia mambo mengi mno, aliwatisha lakini mwisho wa siku Bruno akamuonyeshea noti ya dola mia moja na kumwambia kwamba awaruhusu kupita mahali hapo. Mzee Hamidu akatulia, aliiangalia dola ile, akasimama na kwenda pembeni kabisa ya ofisi ile, akasimama na kuuangalia ukuta. Hakukuwa na kitu ambacho alijiahidi kutokukifanya katika kazi yake kama kupokea rushwa, kitendo cha kuiona dola ile, kilimkumbusha mtoto wake aliyekuwa nyumbani ambaye alisumbuliwa na ugonjwa wa kifua kikuu. Alikaa katika hali hiyo kwa dakika moja na nusu, akayageuza macho yake kwa Bruno na mzee Todd, alikuwa akilia kitu kilichomfanya kila mmoja kumshangaa. Hakutaka kuwaficha, aliwaambia kwamba hakuwa na lengo la kupokea rushwa, angewaruhusu kuondoka na kuingia nchini Kenya kwani kwa jinsi walivyoonekana, walionekana kuwa na kiu kubwa ya kuingia nchini humo, ila kutokana na hali aliyokuwanayo binti yake, hakuwa na jinsi, ilikuwa ni lazima kuichukua pesa hiyo. “Ninaichukua kwa sababu ya mtoto wangu!” alisema mzee Hamidu. “Amefanyaje?” “Ni mgonjwa mno! Leo mnaponiona hapa, sijajua ni kitu gani kitaendelea nyumbani,” alisema mzee Hamidu, hakupanga kuwaambia watu hao suala hilo lakini alijikuta akiwashirikisha. Kwa jinsi alivyozungumza, alitia huruma mno, alionekana kuguswa na kile kilichokuwa kikiendelea. Bruno na mzee Todd wakajikuta wakishikwa na huruma, mioyo yao ikajawa na simanzi. “Tutakusaidia, atakwenda hospitali, atatibiwa na kupona kabisa,” alisema mzee Todd maneno ambayo yalimshtua sana mzee Hamidu. “Kweli?” aliuliza huku akionekana kutokuamini. “Niamini!” alisema. Mzee Hamidu akasimama, akawasogelea na kuwakumbatia. Kwake, kilichokuwa kikiendelea aliona kama ndoto fulani hivi ambapo baada ya muda angeshtuka kutoka usingizini. Hakukuwa na kesi tena, wakaondoka na kuelekea nyumbani kwa mzee huyo. Walipoonyeshewa Ashura, wao wenyewe walikiri kwamba msichana huyo alikuwa kwenye matatizo makubwa na alihitaji msaada. Wakachukua gari na kuondoka kuelekea jijini Nairobi. Walitumia saa tatu, wakaingia jijini humo ambapo Bruno akaenda kubadilisha pesa na kuchukua pesa za Kenya na kumpeleka hospitalini. Walipofika huko, mzee Todd hakuteremka, alibaki ndani ya gari. Bruno, mzee Hamidu, Ashura na mke wa mzee huyo wakaingia ndani ya hospitali na kuonana na daktari, malipo yakafanyika na msichana huyo kulazwa. “Hiki kitakusaidia wewe na familia yako,” alisema Bruno na kumpa mzee huyo dola elfu kumi na kuondoka zake. Mzee Hamidu hakuamini, akamsogelea mke wake na kumkumbatia, kwa kiasi alichopewa kilikuwa kikubwa mno ambacho kama angeamua kumtibu mtoto wake, basi wangempa matibabu yote na hata chenji kubaki, tena nyingi tu. Upande wa pili, Bruno na mzee Todd wakakodi teksi na kuanza kuelekea Mombasa katika kijiji cha Guolduvai. Njiani, mawazo ya Bruno yalikuwa yakimfikiria mpenzi wake, Sharifa, hakujua ni kitu gani kingetokea huko, moyo wake ulikuwa na furaha tele, alitaka kumuona tena, alitaka kuzungumza na mzee Jumanne na kumwambia kwamba alitaka kumuoa msichana huyo kwa kuwa tu alikuwa na pesa, hakuwa masikini kama alivyokuwa kipindi cha nyuma. “Siamini kama ninakwenda kumuona Sharifa, ni kipindi kirefu sana kimepita,” alisema Bruno huku akionekana kutokuamini. Barabara haikuwa mbaya, dereva aliendesha gari kwa mwendo wa kawaida kabisa. Ndani ya teksi, kila mmoja alikuwa kimya, vichwa vyao vilikuwa na mawazo tele na kitu pekee alichohitaji Bruno ni kufika nyumbani huko haraka iwezekanavyo. *** Sharifa alibaki akimwangalia Alfred, hakuamini kile alichokisikia kwamba Bruno alikuwa na pesa na alikuwa amemtumia kiasi fulani cha pesa kwa ajili ya ya matumizi yake. Dola laki moja kilikuwa kiasi kikubwa sana, angeweza kukitumia mwaka mzima na pesa nyingi zingebaki, kwake, hizo pesa hazikuwa tatizo, hazikuweza kumletea furaha zaidi ya kumuona mpenzi wake huyo. Alimuuliza zaidi Alfred kuhusu Bruno, angefika lini kwani alikuwa amkataa kuolewa kwa ajili ya mwanaume huyo hivyo alitaka kufahamu ukweli. “Atafika tu,” alijibu Alfred. “Lini?” “Sijajua ila atafika tu!” Moyo wa Sharifa ukanyong’onyea, hakutaka kurudi nyumbani kwa kuwa tayari alikataa kuolewa kwa ajili ya mwanaume huyo ambaye moyo wake ulitokea kumpenda kwa kiasi kikubwa mno. Walichokifanya ni kwenda benki ambapo Sharifa akafunguliwa akaunti na kiasi kile cha pesa kuhamishiwa katika akaunti yake huku akimwachia Alfred kiasi cha dola elfu kumi kama shukrani kwake. Alikaa nyumbani kwa Alfred mpaka ilipofika usiku ndipo akaondoka na Abdul kurudi nyumbani kwao. Mzee Jumanne alipomuona, akamfuata na kuanza kumpiga vibao mfululizo, kwa kile kilichokuwa kimetokea, kilimdhalilisha na kumfanya kuonekana hana maana. Watu walitoka jijini Nairobi mpaka kijijini hapo kwa ajili ya kufunga ndoa lakini kilichotokea hapo, msichana huyo akakimbia. Kwake ilikuwa ni aibu kubwa, hakuamini kama binti yake wa kumzaa angeweza kufanya kitu kama kile. Sharifa alilia mno, akaondoka na kuelekea chumbani kwake. Huku nyuma mzee Jumanne alikuwa mtu wa kulalamika tu, alimwambia mke wake kwamba Sharifa aliwadhalilisha sana. Mke wake alimpoza lakini hakupozeka, hasira alizokuwanazo hapo zilikuwa ni za kiwango cha juu kabisa. Kijijini hapo, habari ikawa ni Sharifa tu, kile alichokifanya hakikuwa kitu kizuri na watu wengi walimlaumu kwa kuwa alikataa kuolewa na mwanaume mwenye pesa kisa Bruno ambaye mpaka kitu hicho hakukuwa na mtu aliyejua mahali alipokuwa, na hata kama alikuwa hai, kila mmoja alijua kwamba alikuwa masikini wa kutupwa. Siku zikaendelea kukatika, bado Sharifa alikuwa na hamu ya kumuona mpenzi wake, hakutaka kumwambia baba yake kuhusu pesa alizokuwa nazo kwenye akaunti, kila kitu kiliendelea kuwa siri huku akitamani kumuona Bruno akirudi kijijini hapo na kuanza maisha wote wawili. “Bruno! Rudi mpenzi, ninakukumbuka mno, sikutaka kuolewa kwa ajili yako, rudi mpenzi, nimekukumbuka,” alisema Sharifa. Hayo ndiyo maneno aliyokuwa akiyazungumza kila siku. Kiasi kile cha pesa kilichokuwa benki hakutaka kutumia pesa yoyote ile, alitulia nyumbani huku sala yake ikiwa ni kumuona mwanaume huyo. Siku ziliendelea kukatika, mpaka mwezi unakatika, bado Bruno hakuwa amerudi kitu kilichoanza kumtia wasiwasi moyoni mwake. *** “Bruno….Bruno…Bruno….” zilisikika kelele za watu kutoka mitaani, wanawake waliokuwa wakichota maji kisimani wakaacha na kuanza kuelekea kule kelele zile zilipokuwa zimesikika. Kila mtu alikuwa na shauku ya kumuona huyo Bruno aliyekuwa akishangiliwa na watu waliokuwa mitaani. Watu waliokuwa ndani ya nyumba zao wakatoka na kwenda kushuhudia kile walichokuwa wakikisikia, waliokuwa pembezoni mwa bahari nao wakaelekea kule kujionea kwa macho yao. Kila kona gumzo lilikuwa ni Bruno, alisababisha kasheshe mtaani na ndiyo maana watu walipolisikia jina lake wakatoka kwenda kujionea kwa macho yake. Bruno alisimama nje ya teksi huku akiwa na mzee Todd, alikuwa akikiangalia kijiji hicho, uso wake ulikuwa na tabasamu pana, hakuamini kama alirudi kijijini humo baada ya kupotea kwa miezi kadhaa. Alikuwa amekonda, hakuwa kama alivyoondoka kipindi cha nyuma. Watu walimsogelea na kumwangalia, walitaka kuamini kama alikuwa yeye au mtu mwingine. Wengine wakamsogelea na kumshika, walitaka kuona kama alikuwa mtu halisi au mzimu. Pembeni yake alikuwepo mzee Todd, watu hawakutaka kufahamu kuhusu mzee huyo wa Kizungu, walitaka kufahamu kuhusu Bruno, ilikuwaje mpaka awe hai kipindi hicho? Wakati watu walipokuwa wakipiga kelele za Bruno, Sharifa alikuwa nyumbani kwao akiendelea na kazi zake kama kawaida. Alikuwa mnyonge, hiyo haikuwa siku hiyo tu, hayo yalikuwa maisha yake ya kila siku. Akiwa anaosha vyombo akasikia kelele nje huku jina la mpenzi wake likisikika. Alichanganyikiwa, vyombo havikuosheka tena, akasimama, akavalia khanga yake na kutoka ndani huku akikimbia. Alichanganyikiwa, alitaka kuona kile alichokuwa amekisikia, alikimbia mpaka mahali kulipokuwa na teksi, alipoanga vizuri, alimuona mpenzi wake akiwa amesimama na mwanaume mmoja wa Kizungu, hakutaka kubaki alipokuwa, akaanza kumfuata kwa kumkimbilia, alipomkaribia, akamrukia, wakaanguka chini huku watu wengine wakibaki wakiwa wamepigwa na butwaa. “Bruno! Bruno…” aliita Sharifa huku machozi ya furaha yakianza kutoka. Kwake ilikuwa ni vigumu kuamini moja kwa moja kwamba mtu aliyekuwa amemkimbilia na kudondoka naye chini alikuwa Bruno. Alimpenda, alikuwa mwanaume wa ndoto yake ambaye hakutaka kumuacha hata siku moja. Machozi ya furaha yalikuwa yakimtoka, hakuamini alichokuwa akikiona, wakati mwingine alihisi kama yupo kwenye ndoto. Watu walizidi kukusanyika, kila mtu aliyekuwa akimuona Bruno, hakuyaamini macho yake. Hazikupita dakika nyingi Abdul akatokea, uso wake ulikuwa kwenye tabasamu pana, alichanganyikiwa kwa furaha, rafiki wake wa kipindi kirefu, aliyepotea, Bruno alikuwa mbele ya macho yake. Akamsogelea, akamsalimia na kumkumbatia. Siku hiyo ilikuwa ni furaha kijiji kizima, kila mmoja alionekana kuwa na furaha kupita kawaida. Kabla ya kufanya jambo lolote lile, Abdul akamuuliza kilichokuwa kimetokea baharini kwani waliambiwa na akina James kwamba alizama. “Walinitupa baharini, sikujua lengo lao lilikuwa nini,” alisema Bruno. “Walikutupa?” “Ndiyo! Walitaka nife, nahisi walitumwa, ila sitaki kukumbuka, nimesamehe kila kitu,” alisema Bruno huku akiwa na tabasamu. Mzee Jumanne alikuwa nyumbani kwake, si kwamba hakusikia kelele kuhusu Bruno, alizisikia sana, moyo wake ulijawa na hasira nyingi, hakuamini kama mwanaume huyo alikuwa amerudi kijijini akiwa mzima kabisa. Mule alipokaa, alishindwa hata kutoka kwenda nje, uso wake ulikuwa na hasira mno na hakukuwa na kitu chochote alichohitaji kusikia kutoka kwa mwanaume huyo. Aliwahi kumpiga mkwara mwingi kuhusu kuachana na binti yake lakini kijana huyo hakusikia, ilimuuma sana kwa kuwa hakutaka binti yake aolewe na Bruno kisa tu alikuwa masikini. Kule walipokuwa, Bruno akamtambulisha mzee Todd kwa Abdul kwani aliamini kwamba hakuwa akimfahamu na baada ya hapo wakaanza kwenda nyumbani kwa mzee Jumanne huku Sharifa akiwa pembeni yake. Walipofika, wakaingia ndani, wakakaribishwa na kukaa kwenye makochi yaliyoonekana kuanza kuchakaa. Mama yake Sharifa alipokuwa akimwangalia Bruno, hakubadilika, alikuwa vilevile kama alivyokuwa kipindi cha nyuma. Nyumba nzima walimchukia, hawakumpenda kwa kuwa yeye ndiye aliyemfanya Sharifa kukataa kuolewa na kijana kutoka katika familia ya kitajiri mwezi uliopita. Mzee Jumanne akaitwa, akaelekea sebuleni, alipofika hapo, macho yake yakatua katika nyuso za watu hao, hakucheka wala kuonyesha tabasamu, alitaka kuonekana kwa watu hao kwamba alikuwa akimchukia Bruno kupita mtu yeyote katika dunia hii. Walikaa na kuzungumza, kitu ambacho Bruno alimwambia mzee Jumanne ni kwamba alitaka kumuoa Sharifa na kuondoka naye kuishi Nairobi ambapo aliamini kwamba biashara zake zingekuwa huko. “Umuoe Sharifa?” aliuliza mzee huyo. “Ndiyo!” “Kivipi? Huna kitu chochote kile, unataka uende kumuua binti yangu kwa njaa? Hakuna ujinga kama huo,” alisema mzee Jumanne huku akionekana kukataa kabisa binti yake kuolewa na Bruno. “Mzee! Mimi si Bruno niliyeondoka! Hicho ni kitu cha muhimu sana ambacho unatakiwa kukifahamu. Niambie unahitaji nini,” alisema Bruno. Mzee Jumanne akanyamaza, kwa jinsi Bruno alivyoongea alionekana kujiamini kupita kawaida. Hakujua sababu ni yule Mzungu au la. Alimwangalia, bado muonekano wake haukuonekana kuwa kama mtu mwenye pesa, alimdharau na aliona kabisa kijana huyo hakustahili kuishi na binti yake. “Baba! Nitakupa kitu chochote utakachohitaji. Nitakununulia boti za kuvulia samaki zaidi ya tano, achana na mitumbwi, hizo sitokununulia kama kujipendekeza, nitakununulia kama zawadi za kunitunzia huyu Sharifa. Na boti hizo zitaingia hapa kesho,” alisema Bruno huku akimwangalia mzee huyo. Mzee Jumanne hakuamini alichokisikia, akamwangalia Bruno, kwa jinsi alivyokuwa akiongea, alionekana kumaanisha mno lakini kwake ilionekana kama kichekesho fulani hivi. Hakutaka kusema kitu chochote kile, akapuuzia na kunyanyuka kuelekea chumbani kwake. Bruno hakutaka kujali, yeye pamoja na wenzake wakasimama na kutoka ndani, huko nje walipokwenda, watu walijikusanya nyumbani hapo, kila mtu alitaka kumuona Bruno kwa mara nyingine, walitamani hata kumgusa ili kuona kama alikuwa yeye au mzimu. “Bado kuna mambo mengi tunahitaji kufanya! Nitakuja ndani ya siku mbili pamoja na hizo boti za mzee,” alisema Bruno. “Hivi kweli unataka kumnunulia boti?” “Sharifa! Ninahitaji baba yako awe na furaha, amekuwa akinichukia kwa kipindi kirefu sana kwa sababu ya umasikini wangu. Nataka nafsi yake imsute kwamba yule masikini ndiye ambaye amekuwa msaada mkubwa kwake,” alisema Bruno. Siku hiyo hawakutaka kukaa kijijini, wakaondoka na kuelekea Nairobi huku wakiwa na Abdul. Walipofika, wakachukua chumba katika hoteli ya kawaida na kutulia humo. Bruno alikuwa amekwishafika nchini Kenya alipokuwa akihitaji ilikuwa ni zamu ya mzee Todd tu kuondoka na kuelekea nchini Marekani. Bado mzee huyo alikumbuka wema aliokuwa ametendewa na Bruno, jinsi alivyokuwa amemsaidia kwa kiasi kikubwa, alichomwambia ni kwamba alitaka kumuachia kiasi cha dola milioni mia tatu kwa ajili ya maisha yake. Hicho kilikuwa ni zaidi ya shilingi bilioni mia sita. Kilikuwa ni kiasi kikubwa mno ambacho Bruno hakuwahi kufikiria katika maisha yake. Kiasi hicho cha pesa kilitakiwa kuhamishwa haraka sana kutoka katika akaunti ya mzee huyo na kuingizwa katika akaunti ya Bruno. Bila kuogopa kitu chochote kile, wakaondoka na kuanza kuelekea katika tawi la Benki ya Barclays. Walipofika huko, Bruno akateremka, akaelekea ndani ya benki hiyo na kuchukua kitabu cha kuandikia hundi na kurudi kwenye taksi ambapo akamwandikia hundi ya kiasi hicho na hivyo pesa hiyo kuanza kuhamishwa kwenda katika akaunti ya Bruno kitu kilichochukua dakika chache tu. “Bruno! Ninashukuru kwa kila kitu, pamoja na yote hayo, ninahitaji unisaidie kitu kimoja tu,” alisema mzee Todd. “Usijali! Kitu gani?” “Nitahitaji uwe shahidi katika kesi yangu inayonikabiri. Wewe ndiye umeona kila kitu kilichokuwa kikiendelea, jinsi nilivyokuwa nimetekwa na kutakiwa kuuawa, najua kwamba dunia inatamani kuona nikiuawa, ninahitaji uwe shahidi wangu, usimulie kila kitu kilichokuwa kimetokea kuanzia ndani ya meli,” alisema mzee huyo. “Haina shida. Nitakusaidia pale nitakapohitajika,” alisema Bruno.
Maofisa wa CIA walikuwa makini kufuatilia kila kitu kilichokuwa kikiendelea kuhusu mzee Todd, hawakutaka kuiambia dunia moja kwa moja kwamba bado walikuwa wakiendelea kumtafuta mzee huyo. Waliwatuma baadhi ya maofisa nchini Afrika Kusini, walikwenda huko mpaka sehemu ambayo waliamini kwamba mwanaume huyo alikuwepo lakini baada ya kufika, baada ya kupambana sana na watu wa hapo, hawakuweza kumpata. Wakarudi na kutoa ripoti juu ya kitu kilichokuwa kimetokea, kila mmoja alihuzunika lakini hawakuwa na jinsi. Siku ziliendelea kukatika, waliendelea kumtafuta kila kona lakini hawakufanikiwa kumuona. Baada ya siku chache wakapewa taarifa kwamba mwanaume huyo alikuwa ametoa kiasi fulani cha pesa katika akaunti yake na kukihamishia katika namba nyingine. Hilo likawafanya kuwa na hofu kwamba inawezekana mwanaume huyo aliamua kuhamisha pesa hizo kwa kuwa alihitaji kufanya manunuzi yake kwa ajili ya kujilinda. Waliwasiliana na benki ya Barclays na kuwaambia kuhusu kuifunga akaunti hiyo lakini hilo halikuwezekana kwani kwa masharti makubwa ya benki hiyo, kitu cha kwanza kabisa hakikuruhusu akaunti yoyote ya mtu kufungwa kwa maslahi ya mtu fulani au shirika fulani. Wakaiacha, baada ya miezi mitano wakapata taarifa tena kwamba kulikuwa na muamala ulikuwa umefanyika katika tawi la benki hiyo lililokuwa chini Kenya. Hawakutaka kuchelewa, haraka sana wakawasiliana na vijana wao waliokuwa Nairobi na kuwaambia kufuatilia kila kitu kilichokuwa kikiendelea huko kwani tayari walikuwa na wasiwasi kwamba mzee Todd alikuwa huko. Ndani ya dakika tano tu, maofisa wa CIA walikuwa katika tawi la benki hiyo na kuingia ndani, macho yao yalikuwa yakiangalia huku na kule lakini hawakuweza kumuona mzee Todd. Hilo likawachanganya, wakatoka hapo na kuelekea nje, walipofika huko, wakamuona kijana mmoja akitembea kwa mwendo wa kujiamini kabisa kuifuata teksi moja iliyokuwa ikimsubiri. Huyo alikuwa mtu pekee ambaye alitoka ndan ya benki hiyo na kufuata teksi, wakahisi kitu na kuanza kuifuatilia. Alipoifikia teksi ile, akafungua mlango na kuingia ndani. “Kuna nani mwingine ndani ya teksi ile?” aliuliza ofisa mmoja. “Naona watu kama watatu hivi!” “hebu twende!” Walitaka kuiwahi hata kabla haijaondoka mahali hapo. Mikononi walikuwa na bastola zao, walipoifikia tu, wakaushika mlango wa dereva na kumuamuru atulie kama alivyokuwa na kuufungua mlango. Walinzi waliokuwa mahali hapo walionekana kushtushwa na kilichokuwa kikiendelea, mawazo yao yaliwaambia kwamba watu hao walikuwa majambazi, wakaandaa bunduki zao lakini ofisa mmoja akawaonyeshea kitambulisho ambacho kilionyesha kwamba walikuwa ni maofisa wa CIA. “Settle down,” (tulieni) alisema mwanaume mmoja na walinzi wote kutulia. Wakamshusha mzee Todd, akateremka na kuinyoosha mikono yake ambapo moja kwa moja wakamfunga pingu. Haikuonekana kuwa kazi kubwa, mzee huyo hakuonyesha ishara yoyote ya kiburi kwani alijua kabisa kwamba kitu hicho kingetokea na hata kama kisingetokea yeye mwenyewe aliamua kujipeleka katika ubalozi wa Marekani ambapo huko angechukuliwa na kusafirishwa kuelekea nchini Marekani. Kwa jinsi kitendo kile kilivyokuwa cha haraka na siri kubwa, hakukuwa na mtu yeyote yule ambaye aliona kilichokuwa kimetokea zaidi ya walinzi wawili, wakamchukua mzee huyo tu, wakampakiza ndani ya gari. “Help me! You have to do what I’ve told you to do,” (nisaidie! Fanya nilichokwambia kufanya) alisema mzee Todd huku akimwangalia Bruno. “I will!” (nitafanya) *** Mzee Todd alikuwa ndani ya ndege akipelekwa nchini Marekani. Taarifa za kukamatwa kwake zilikuwa ni za kimyakimya na hakutakiwa mtu yeyote afahamu kama mwanaume huyo alikuwa amekamatwa kwa kuogopa kuvamiwa na wauzaji wa madawa ya kulevya. Humo ndani ya ndege, hakuwa na raha hata kidogo, alijua kwamba kila kitu kilichokuwa kimefanyika kilikuwa ni mchezo ambao ulichezwa na Maxwell kwa ajili ya kumpoteza. Hakuona kama angeweza kutoka katika kesi hiyo kubwa. Mbele yake kulikuwa na ugumu lakini watu pekee ambao aliamini kwamba wangeweza kumsaidia kutoa ushahidi walikuwa wawili tu, Innocent na Bruno. Alikuwa akisafirishwa kuelekea nchini Marekani huku matumaini yake yakiwa kwa watu hao wawili tu. Hakuzungumza kitu chochote kile, alikuwa kimya na kichwa chake kilikuwa kikifikiria ni kwa jinsi gani angeweza kupambana na kesi hiyo ambayo dunia nzima iliamini kwamba kweli madawa ya kulevya yalikutwa chumbani kwake na kulikuwa na uwezekano mkubwa kwamba alihusika katika kuiteketeza familia yake. Baada ya saa zaidi ya ishirini, hatimaye ndege ikaingia nchini Marekani. Hapo, alikuwa akisubiriwa na maofisa wa CIA ambao walimchukua, wakampakiza ndani ya gari na kuondoka naye. Walipoona kwamba amefika salama ndiyo taarifa zikaanza kutolewa kwa waandishi wa habari ambao wote hawakuamini kile walichokuwa wamekisikia. Mwanaume huyo aliwasumbua kwa miezi sita, hawakuwa wamempata japokuwa walimtafuta kila kona, kukamatwa kwake ikawa shangwe, watu kwenye mitandao ya kijamii wakaandika sana kuhusu mwanaume huyo na kila mmoja alikuwa akimuhukumu kwa nafasi yake kama mtuhumiwa ambaye alitakiwa kunyongwa mpaka kufa. Kwenye vyombo vya habari, ni picha zake tu ndizo zilikuwa zikitawala. Wamarekani walijua kucheza na akili za watu, walijisifia kwamba hakukuwa na mtu yeyote ambaye angethubutu kuichezea nchi hiyo na kutafutwa asipatikane. Walihitaji watu wao warudishe matumaini kwao kwa mara nyingine kwani kulikuwa na watu wengi ambao walikuwa wakitafutwa na maofisa wa CIA lakini cha ajabu kabisa hawakuwa wakipatikana. Kitendo cha kumkamata mzee Todd kikawahakikishia kwamba wangesifiwa kila kona kwani wangeonekana mashujaa ambao hawakulala usiku mzima kwa ajili ya mtu huyo. Mzee Todd akawekwa ndani ya chumba cha mahojiano na kuanza kuulizwa maswali kadhaa. Hakufumbua mdomo wake kujibu swali lolote lile, kila kitu alichoulizwa, aliwaambia kwamba asingeweza kuongea lolote lile mpaka mwanasheria wake kuwa mahali hapo. Hilo halikuwa tatizo hata kidogo, haraka sana mwanasheria wake, Harry Donny akapigiwa simu na ndani ya dakika chache alikuwa ndani ya chumba hicho na mzee Todd kuanza kujibu kila swali alilokuwa akiulizwa. Aliulizwa zaidi ya maswali hamsini ambayo yote aliyajibu kwa ufasaha na hivyo kesi hiyo kutakiwa kufika mahakamani haraka sana. Wakati huo kila kona duniani walikuwa wakimzungumzia mzee huyo, kesi yake hiyo nzito ilizua mambo makubwa mno, kila kona, watu wote walitaka kuisikiliza na kuona hatima ya mzee huyo ingekuwa nini. Asilimia kubwa ya watu walitaka kushuhudia mzee huyo akifungwa kifungo cha miaka mingi gerezani kwani kwa miaka hiyo kulikuwa na idadi kubwa ya vijana waliokuwa wakipotea kutokana na matumizi mabaya ya madawa ya kulevya. Waandishi wa habari walikuwa wakimiminika mahali hapo huku wakiwa na hamu ya kutaka kuzungumza na mzee huyo au hata kupata picha zake kwani picha nyingi ambazo zilikuwa zikitumika kipindi hicho zilikuwa ni picha za zamani tu. Hakukuwa na mtu aliyepata nafasi hiyo, waliambiwa kwamba suala la picha walitakiwa kusubiri mpaka siku ambayo angepandishwa mahakamani. Mwanasheria wake ambaye ndiye huyohuyo angekuwa wakili wake akaanza kumuuliza maswali mengi juu ya kilichokuwa kimetokea. Hakutaka kumficha, alimwambia ukweli kuhusu kila kitu kwamba hakuwa ameweka madawa ya kulevya ndani ya nyumba yake bali kulikuwa na mwanaume aliyeitwa Maxwell ambaye ndiye alikuwa nyuma ya mchezo wote. Yeye ndiye aliyeratibu kila kitu na hata alipokwenda Afrika, yeye ndiye aliyepanga mipango ya kuuawa lakini ilishindikana baada ya kukutana na kijana aliyejitambulisha kwa jina la Bruno. “Alisuka mipnago ya kunimaliza, nikasaidiwa kwani nilichukuliwa kwenye meli yake na kupelekwa sehemu kwa lengo la kuuawa ila tukatoroka bandarini,” alisema mzee Todd. “Na huyo kijana kuna uwezekano wa kupatikana?” “Ndiyo! Kuna uwezekano, yeye atatoa ushahidi wa kila kitu kilichotokea,” alisema mzee Todd huku akiwa na uhakika wa kumpata Bruno. “Sawa. Haina shida!” Walizungumza mambo mengi na baada ya kukamilisha kila kitu, tarehe ya mahakama ikapangwa tayari kwa kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo. Mzee Todd alikuwa mtu mwenye huzuni tu, kila alipokuwa selo kichwa chake kilikuwa kikiifikiria familia yake tu, hakuamini kama aliipoteza kwa tamaa za mwanaume mmoja tu aliyetaka afutike ndani ya dunia hii. Alihuzunika mno lakini alijiahidi kwamba kamwe asingelipa kisasi kwa kuwa aliamini kwamba kulikuwa na Mungu ambaye alisema kwenye maandiko yake kwamba visasi vyote vilikuwa juu yake. Siku ziliendelea kukatika, baada ya siku kadhaa, hatimaye siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu ikawadia. Zaidi ya watu elfu tatu walikusanyika katika viunga vya mahakama kwa lengo la kusikiliza kesi hiyo. Hapo, kulikuwa na waandishi wa habari ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kupiga picha kila kitu kilichokuwa kikiendelea mahali hapo. Mashirika makubwa ya habari duniani, CNN, BBC, Sky News na mengi yalikuwa bize kuonyesha moja kwa moja kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika viunga vya mahakama huku wakijaribu kufanya mahojiano na baadhi ya watu waliokuwa mahali hapo. “Namkumbuka mpenzi wangu, Jericho, alikuwa mtu mwema kabisa lakini baada ya kuanza kutumia madawa ya kulevya, nikampoteza, moyo wangu uliniuma sana, ninapomuona huyo mzee, ninatamani hata nimuue kwa mkono wangu,” alisema msichana mmoja huku akionekana kuwa na hasira mno. “Nilimpoteza kijana wangu baada ya kuingia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya. Nilimpa kila kitu, hakutaka kusoma, alichanganyikiwa kabisa na madawa. Halafu leo mniambie kwamba huyu mzee aachiwe huru, nadhani nitamuua hata mtaani,” alisema mwanaume mmoja, kwa kumwangalia tu isingekuwa vigumu kuamini kwamba angefanya kile alichokuwa akikisema. Kila mtu aliyekuwa akihojiwa alimshutumu mzee huyo moja kwa moja, hakukuwa na mtu aliyetaka kumuona mwanaume huyo akiachiwa huru, kila mmoja alitamani kuona akihukumiwa jela kwa kosa alilokuwa amelifanya. Baada ya saa moja, gari moja lililokuwa likiongozwa na baadhi ya magari ya CIA lilikuwa likiingia mahakamani hapo. Haraka sana waandishi wa habari wakasogea kule lilipokuwa na kuanza kulipiga picha. Kila mtu aliamini kwamba huyo alikuwa mzee Todd, walipiga picha nyingi mpaka mlango ulipofunguliwa na mwanaume huyo kuteremshwa huku akiwa na pingu mikononi mwake. Hakuuficha uso wake, alikuwa na uhakika wa kushinda kesi hiyo, alikuwa akiangalia huku na kule, hakutabasamu, alikuwa kwenye hali ya kawaida, alizungukwa na maofisa wa CIA mpaka alipoingizwa ndani ya jengo la mahakama. Humo ndani, kulikuwa na watu zaidi ya mia saba waliokuwa wamekaa na wengine kusimama, kila mmoja alitaka kujua kile kilichokuwa kikiendelea, siku hiyo ilikuwa ni ya kusikiliza kesi lakini hakukuwa na mtu yeyote yule aliyetaka kukosa kesi hiyo. Baada ya dakika kadhaa, mzee Todd akapelekwa kizimbani na hakimu kuingia. Kwa heshima kila mtu akasimama, alipokaa tu kwenye kiti chake, akagonga kinyundo na watu wote kukaa. Kesi ikaanza mara moja. Siku hiyo haikuwa ya kusikiliza mashahidi, haikuwa siku ya kusikilizwa utetezi wake, ilikuwa ni siku ya kusomewa mashtaka, makosa aliyoyafanya na baada ya hapo kesi kuahirishwa mpaka baada ya wiki moja na nusu. “Ninaiahirisha kesi hii mpaka tarehe 10/08,” alisema hakimu na kugonga kinyundo chake, akasimama na kuondoka mahali hapo. Watu wakatoka nje lakini hawakutaka kuondoka mahakamani hapo, walitaka kumuona mzee Todd akiondolewa na kupandishwa ndani ya gari lake. Polisi mmoja akamfuata pale kizimbani, akamchukua na kuanza kuelekea naye nje huku akiwa amemfunga pingu. Kila kona mahali hapo kulikuwa na ulinzi mkali, walijua kwamba mwanaume huyo alikuwa na watu wengi hatari ambao wangeweza kufanya kila liwezekanalo mpaka kuhakikisha wanamtoa mahali hapo. Walichokuwa wakikifikiria kilikuwa tofauti kabisa, mzee Todd hakuwa na kundi lolote lile, alikuwa yeye kama yeye na hakukuwa na kitu ambacho aliamini kama mashahidi ambao wangeeleza kila kitu kilichokuwa kimetokea na hivyo kushinda kesi hiyo. Alipotolewa nje, watu wakachukua simu zao na kuanza kumpiga picha, waandishi wa habari walikuwa wakihangaika, hawakutulia, kila mmoja alihakikisha anapata picha ambayo ingeyafanya magazeti yao na tovuti zao kutembelewa na watu wengi. Mzee huyo hakuuficha uso wake kama watu wengine, hakuona kama alikuwa na hatia na muda wote alikuwa kimya tu, akachukuliwa na kupakizwa ndani ya gari na kuanza kuondolewa mahali hapo. Wakati akiondolewa, wakili wake, Harry alikuwa akimwangalia, moyo wake ulimuuma mno, alimuonea huruma mteja wake lakini alikuwa na uhakika kwamba hao mashahidi ambao alimtajia basi wangeweza kumsaidia kutoka katika mikono ya kifungo kilichokuwa kikimkabiri. Baada ya gari lile kuondoka, akalifuata gari lake na kuondoka mahali hapo. Wakati gari likiwa limefika katika Barabara ya Brooklyn, akaangalia kwenye kioo, kwa nyuma kulikuwa na gari lililokuwa likimfuata. Alikuwa na wasiwasi nalo kwani kila alipokuwa akijaribu kwenda huku na kule, gari lile lilikuwa likimfuata kitu kilichomfanya kuhisi kuwa watu waliokuwa humo walikuwa wabaya ambao wangeweza kumfanya lolote lile. Akaanza kuliendesha gari kwa mwendo wa kasi, hilo halikuweza kumsaidia kwani gari lake halikuwa na kasi kubwa kama gari lililokuwa likimfukuza kwa nyuma. Aliendesha lakini hakuweza kuliacha, gari hilo likamfikia na kuanza kuendesha ubavuni mwake. Mwanaume mmoja akatokeza na kumnyooshea bastola na kumtaka asimamishe gari vinginevyo angeanza kumshambulia kwa risasi. Harry akaogopa, hakutaka kuona akifa, mule ndani ya gari alipokuwa akaanza kutetemeka kwa hofu, akaanza kupunguza mwendo na kusimama. Gari lile likasimama, wanaume wawili wakateremka na kumfuata huku wakiwa na bastola mikononi mwao, baada ya kulifikia, wakafungua mlango na kumteremsha na kumpeleka ndani ya gari lao. “Don’t dare to open your fucking mouth,” (usithubutu kufungua wako) alisema mwanaume mmoja huku akimgongagonga na bastola kichwani. Harry akanyamaza, kijasho chembamba kikaanza kumtoka na kuhisi kwamba huo ungekuwa mwisho wake. ***
Simulizi : Mvuvi Bruno (Bruno The Fisherman) Sehemu Ya Tano (5) Maxwell alikuwa nyumbani kwake, moyo wake haukuwa na amani hata kidogo, kitendo cha vijana wake kushindwa kumteka mzee Todd kilimuhuzunisha kupita kawaida. Alichanganyikiwa, alijua hatari ambayo ilikuwa mbele yake, alijua kabisa kwamba kama asingefanya kila liwezekanalo kuhakikisha mwanaume huyo anatekwa basi mbele yake kungekuwa na hatari kubwa mno. Hakutaka kutulia, kila wakati alikuwa akiwasiliana na vijana wake lakini walichokuwa wakimwambia ni kwamba hawakuwa wamefanikiwa kumpata mwanaume huyo. Hakutaka kuona akikubali, bado aliendelea kuwasisitiza vijana wake kumpata mzee Todd lakini mpaka siku hiyo ambayo alikuwa sebuleni kwake mwanaume huyo hakuwa amekamatwa. Baada ya dakika kadhaa kukaa sebuleni, macho yake yakatua kwenye taarifa ambayo ilimshtua sana. Kupitia kituco cha televisheni cha CNN kulikuwa na habari ambayo iliyokuwa imefika hivi punde kwamba mzee Todd alikuwa amekamatwa nchini Kenya na muda huo alikuwa amefikishwa makao makuu ya CIA kwa ajili ya kujibu kesi yake iliyokuwa ikimkabiri. “Amekamatwa! Mungu wangu!” alisema Maxwell huku akisimama na kuangalia vizuri televisheni ile. Hakuamini alichokuwa akikiangalia, hapohapo akampigia simu mmoja wa vijana wake aliyeitwa Dragon na kumwambia kuhusu taarifa ile kwamba mzee Todd alikuwa amekamatwa hivyo walitakiwa kufanya kila kitu kujua namna kesi hiyo ilivyokuwa ikiendeshwa. Hilo halikuwa tatizo, vijana wakaanza kufanya kazi yao kufuatilia, walihitaji kujua mambo mengi kuhusu huyo wakili ambaye angemsimamia, walijua kuwa kama kulikuwa na kesi ilikuwa ni lazima kuwa na mashahidi wa kumtetea mzee huyo. Hao ndiyo waliotaka kuwajua, walitaka kuhakikisha wanawatafuta mashahidi wote na kuwamaliza ili mzee Todd ashindwe kesi hiyo iliyoonekana kuwa ngumu kwa upande wake. Siku ambayo kesi ilikuwa ikisikilizwa, walikuwa mahakamani hapo, lengo lao lilikuwa ni kuhakikisha wakili anakamatwa na kupelekwa sehemu kwa ajili ya kuulizwa maswali kadhaa. Hilo likafanyika na muda huo walikuwa na Harry ndani ya gari lao. Walimwambia anyamaze kwani vinginevyo wangeweza kummaliza. Walikuwa wakizunguka naye tu huku wakimuuliza baadhi ya maswali kuhusu kesi hiyo na hata mashahidi ambao walitakiwa kwenda mahakamani. Harry hakutaka kuwaambia ukweli, alichokisema ni kwamba bado kesi ilikuwa mahakamani na hata mashahidi hawakuwa wamejulikana hivyo walitakiwa kusubiri. “Unatudanganya! Hebu kifumue kichwa chake,” alisema mwanaume mmoja maneno yaliyomfanya Harry kuogopa. “Naomba msiniue! Naomba msiniue, mimi ndugu yenu,” alisema Harry huku akianza kulengwa na machozi. “Muue bwana, anatuchelewesha,” alisema jamaa huyo na mwenzake kukoki bunduki. “Subiri nawaambieni ukweli,” alisema Harry. “Tatizo unahisi kwamba tumekuja hapa kucheza na wewe. Sikiliza mshikaji wetu, tumekuja kufanya kazi, ukituzingua, tunakuzingua,” alisema jamaa aliyeshika bastola. Harry hakutaka kunyamaza, ilikuwa ni lazima awaambie vijana wale kila kitu kilichokuwa kimetokea hasa upande wa mashahidi ambao walitakiwa kwenda mahakamani kutoa ushahidi wao kuhusu kile kilichokuwa kimetokea. Mtu wa kwanza aliyemtaja alikuwa Innocent, huyo walimfahamu, kummaliza halikuwa jambo gumu hata kidogo na mtu wa pili aliyemtaja aliiitwa Bruno ambaye waliambiwa kuwa alikuwa nchini Kenya. Walipoambiwa hivyo hawakutaka kumshikilia Harry, wakamuacha na kumuonya kwamba hakutakiwa kumwambia mtu yeyote yule kuhusu kile kilichokuwa kimetokea. Wakampigia simu Maxwell na kumwambia kila kitu kwamba katika kesi ile kulikuwa na watu wawili ambao kama asingehakikisha wanamalizwa basi angeweza kufungwa. Akatajiwa majina ya watu hao, alimfahamu Innocent, kwake, huyo hakumsumbua ila mtu ambaye alikisumbua kichwa chake alikuwa Bruno, mwanaume ambaye hakuwahi kumuona na hakujua alifananaje. “Alisema anaishi Kenya?” aliuliza. “Ndiyo!” “Sehemu gani?” “Mombasa!” alijibu. Hilo halikuwa tatizo, kwa sababu walijua mahali pa kumpata walihakikisha wanafanya kila liwezekanalo kabla ya wiki mbili na kumuua. Alichokifanya ni kuwalipa vijana hao kiasi cha dola laki mbili na kuwatuma kwenda nchini Kenya huku wakijifanya watalii na wengine kutakiwa kumuua Innocent hapohapo Marekani. Baada ya siku mbili, vijana watatu, Kelly, Adson na Tim walikuwa ndani ya ndege wakielekea nchini Kenya. Walipewa maelezo yote juu ya kile walichotakiwa kufanya, kwa Mombasa, hawakujua eneo hilo lilikuwa na ukubwa gani lakini walikuwa na uhakika wa kukamilisha kazi hiyo ndani ya siku chache kabla ya kurudi nchini Marekani. *** Kama kudharaulika, Bruno alidharaulika sana, alikejeliwa kila kona, hakupendwa kutokana na umasikini uliokuwa umemtafuna. Kipindi hicho kila kitu kilionekana kubadilika, hakukuwa na mtu aliyeamini kwamba mwanaume aliyekuwa ameagiza boti mpya kutoka jijini Nairobi alikuwa Bruno yule ambaye alionekana kuwa si lolote lile. Mzee Juma alijisikia aibu moyoni mwake, hapokuwa Bruno alimuonyeshea kutokujali lakini hakuwa na raha hata kidogo. Alihisi kila mtu alikuwa akimcheka baada ya kumpuuza kijana huyo na mwisho wa siku kutaka kumuozesha binti yake kwa mtu mwingine na wakati Bruno alikuwa akimpenda kwa mapenzi ya dhati. Alizipokea boti zile, machozi yalikuwa yakimtoka, hakuweza kuvumilia, hapohapo akaanza kububujikwa na machozi, hakukuwa na kitu kilichomuuma kama hicho, akaanza kumuomba msamaha Bruno ambaye bila kupepesa macho alimwambia kwamba alimsamehe. Jina la Bruno likaanza kukua, kila mtu aliyesikia kile kilichotokea alitaka kumshuhudia Bruno mwenyewe, walitaka kuona alifananaje kwani taarifa walizozisikia ni kwamba alikuwa kijana mdogo aliyekuwa na utajiri wa kutisha. Hakutaka kuishia hapo, alichokifanya ni kuanza kujenga nyumba kubwa hapo kijijini na kuwawekea bomba maji ya kunywa na kufulia, akawa na mipango ya kununua magari lakini pia akanunua jumba kubwa jijini Nairobi na kuanzisha biashara zake nyingi. Maisha yake yalionekana kama kulala masikini na kuamka tajiri. Hawakujua sababu iliyomfanya mzee Todd kumpa pesa nyingi Bruno ambaye alikuwa akiziendesha kwa kufanya biashara nyingi na kubwa. Ndani ya wiki moja tu tayari jina lake likawa kubwa na wengi kutabiri kwamba angekuwa bilionea mkubwa sana hapo baadaye. Kwa kuwa alikuwa masikini na alijua jinsi masikini walivyokuwa na maumivu mioyoni mwao hasa katika kupata matibabu, akaanzisha taasisi yake ya kusaidia wagonjwa wasiojiweza kujilipia aliyoiita Bruno & Sharifa Foundation. Aliwekeza kiasi kikubwa cha pesa, akaanza kuwaita madaktari kwa lengo la kuwasaidia wagonjwa waliokuwa wakihangaika kupata matibabu. Alitumia kiasi kikubwa cha pesa lakini hakujali, kwake, moyo wake ulijitolea kumsaidia kila mtu. Hilo likamfanya kujulikana nchini Kenya, watu wakatamani kumuona kwani kwa masikini wasiokuwa na uwezo alionekana kama Mungu. Umaarufu wake ukawa mkubwa, kwa jinsi alivyokuwa na pesa, alivyosaidia watu kwa kipindi kifupi cha wiki moja na nusu tayari kila kona alikuwa akisikika yeye tu. Magazeti yakamuandika yeye na mkewe, jinsi walivyokuwa wameyabadilisha maisha ya watu wengi kwa kipindi kifupi. Hawakuringa, hawakujiona, kwao, ni upendo wa dhati tu ndiyo uliokuwa umetawala mioyoni mwao. Bruno hakuacha kufuatilia kesi ya mzee Todd, tangu siku ya kwanza ilipoanza kusikilizwa, alipokuwa akihojiwa na hata mashahidi walipokuwa wakihitajika alikuwa akifuatilia kila kitu. Alisahau kabisa kama alitakiwa kuwa shahidi katika kesi hiyo hivyo kuendelea na maisha yake huku akimuomba Mungu ampiganie mzee huyo ili ashinde kesi ile. Baada ya wiki moja, akapokea ugeni kutoka nchini Marekani. Watu hao walikuwa madaktari kutoka katika Hospitali ya St. Andrew iliyokuwa jijini New York na lengo lao kubwa la kufika nchini Kenya ni kusaidia watu waliokuwa wakisumbuliwa na magonjwa mbalimbali. Watu hao walikuwa ni Tim na wenzake. Walipofika Nairobi, kitu cha kwanza kilikuwa ni kulisikia sana jina la Bruno. Hawakujua kama mwanaume huyo ndiye waliyekuwa wakimtaka au alikuwa mwingine. Walifuatilia na kugundua kwamba alikuwa mwenyewe kwani alikuwa akiishi katika Kijiji cha Guolduvai kilichokuwa Mombasa. Mbali na kulisikia jina lake, wakapewa taarifa nyingi kuhusu mwanaume huyo, taasisi aliyokuwa ameifungua ambayo ilionekana kuwa gumzo kila kona. Hilo likawasadia na kuona kwamba kama wangejifanya madaktari kutoka nchini Marekani basi ingesaidia sana kukutana na mwanaume huyo na kutimisha lengo lao. Wakasafiri kutoka Nairobi mpaka Mombasa. Walipofika huko, haraka sana wakamuulizia mwanaume huyo, kumpata halikuwa tatizo hata kidogo, wakaelekezwa na kuanza kumfuatilia kwa ukaribu. Siku iliyofuata, walikuwa mbele yake. Bruno alipowaona, alifurahia kwa sababu aliamini kwamba watu hao wangemsaidia mno kuwatibu wagonjwa wengine. Akawakaribisha nyumbani kwake, akawatambulisha kwa mpenzi wake, kwa kifupi akatokea kuwaamini kupita kawaida. Walizungumza mambo mengi kuhusu matibabu, walimwambia kuhusu ujio wao nchini Kenya, hawakuwa wamefika kwa kuwasaidia watu bali walifika kwa ajili ya kutembelea nchi hiyo kama watalii ila kwa sababu walisikia kuhusu taasisi yake basi nao wakaona kulikuwa na umuhimu wa kutoa msaada ili wachangie baraka. “Hakika ni Mungu!” alisema Bruno huku akionekana kuwa na furaha kupita kawaida, hakujua kama watu hao walitumwa nchini Kenya kwa lengo la kummaliza kama maagizo kutoka kwa Maxwell.. Kitendo cha Bruno kuwaamini Wazungu wale kilionekana kuwa kosa kubwa kwa kuwa hawakufika nchini Kenya kutangaza dini au kutoa msaada, walifika mahali hapo kwa kufanya kitu kimoja tu, kumuua yeye na kurudi nchini Marekani. Kumpata Bruno na kumuua lilionekana kuwa jambo gumu mno, mara nyingi hakuwa akishinda nyumbani, kwa kuwa alikuwa na mambo mengi ya kufuatilia, kazi yake kubwa ilikuwa ni kwenda huku na kule na kuhakikisha hakuna kitu chochote kile kinachoharibika. Tim na wenzake wakawa kwenye wakati mgumu, kila walipopanga wamteke na kwenda naye sehemu kwa lengo la kufanya mauaji, jambo hilo lilionekana kuwa gumu mno. Mtu waliyekuwa wakibaki naye alikuwa Sharifa. Yeye ndiye walisaidiana naye kuhakikisha huduma ya afya ilikuwa ikiendelea vizuri na kila mtu kuhudumiwa kama ilivyotakiwa kuhudumiwa. “Tufanye nini?” aliuliza Adson. “Hivi kweli imeshindikana kumteka kabisa?” aliuliza Tim huku akiwaangalia wenzake. “Ni suala gumu sana! Yaani kumuua ni vigumu kuliko hata tulivyokuwa tunajifikiria,” alisema Kelly. “Kwa hiyo?” “Kama vipi tumteke mkewe!” “Halafu?” “Tumuonye asiende Marekani kwa ajili ya kutoa ushahidi vinginevyo tutamuua mke wake,” alisema Adson. Hawakutaka kufanya jambo hilo kwa haraka, walitakiwa kusubiri mpaka siku mbili kabla ya kesi ile kuunguruma tena nchini Marekani. Kumteka Sharifa halikuwa jambo gumu, lilikuwa jepesi mno ambalo lingefanyika ndani ya dakika chache tu na kufanya mambo mengine. Wakakubaliana na hatimaye kwa pamoja kuanza kuhesabu siku. Hawakumuonyeshea Sharifa tofauti yoyote ile, nyuso zao zilikuwa na tabasamu pana na kila wakati walipokuwa wakiongea waliongea kwa mbwembwe kiasi kwamba msichana huyo akawaona kuwa watu muhimu sana. “Una mimba?” aliuliza Tim huku akimwangalia Sharifa. “Umejuaje?” “Unavyoonekana tu! Kweli au uongo?” aliuliza. “Kweli!” “Ooh! Safi sana!” Hiyo ikawa sababu nyingine kwao kufanikisha kile walichokuwa wakikihitaji, walijua kabisa kwamba mwanamke anapokuwa na mimba ya kwanza, mwanaume huwa anachanganyikiwa na anakuwa radhi kufanya lolote lile lakini si kumpoteza mke wake. Wakaambiana kilichokuwa kikiendelea na hivyo kusuka mipango yao vizuri. Tim akaanza kuangalia ramani, ilikuwa ni lazima kumteka mwanamke huyo na kukimbia naye mbali kabisa na kijijini hapo. Sehemu ambayo aliiona kuwa nzuri kukimbilia ilikuwa ni ni Tanga ambapo huko kulikuwa na mapango ya Amboni, wangekaa huko mpaka kipindi ambacho kesi ile inamalizika pasipo Bruno kuelekea nchini Marekani. “Ni mpango mzuri sana, naamini kama tutafanikiwa, basi tutakuwa tumeshinda vita kubwa mno,” alisema Adson huku akitoa tabasamu pana. Wakati wao wakiendelea kujadiliana na kupanga mipango yao, upande wa pili watu walizidi kumiminika katika kila kituo ambacho taasisi ya Bruno na mkewe ilianzisha. Madaktari waliokuwa na uwezo waliendelea kufanya kazi yao kama kawaida huku wakipata usimamizi wa karibu kutoka kwa Sharifa. Kila siku Bruno alikuwa na kazi ya kumpigia simu mke wake na kumuuliza kuhusu maendeleo yake. Kipindi hicho ndicho msichana huyo alipomwambia mpenzi wake kwamba alikuwa mjauzito. Bruno aliposikia hivyo, hakutaka kuendelea kubaki Nairobi, haraka sana akaondoka na kuelekea Mombasa kwa lengo la kumuona mpenzi wake huyo. Alipofika, akapokewa kwa mabusu kemkem na kukumbatiwa. Alimwangalia Sharifa machoni na kumuuliza kama kile alichomwambia kilikuwa kweli au alikuwa akimtania tu. “Ni kweli! Nilikwenda kupima,” alisema Sharifa huku akimwangalia mpenzi wake huyo. “Wa kike au wa kiume?” “Bado sijajua! Ila ninachojua atakuwa mtoto mzuri sana,” alisema Sharifa na kumkumbatia Bruno. Ujauzito huo ulimchanganya Bruno, hakuamini kama naye alikuwa akikaribia kuitwa baba. Kila alipomwangalia Sharifa, msichana huyo alionyesha tabasamu pana huku muda mwingi akilishika tumbo lake. Mapenzi aliyokuwanayo Bruno ni kama yalikuwa yamechochewa na kuchipuka upya moyoni mwake. Alizidi kumpenda mpenzi wake na kumwambia kwamba angempenda milele hata kama kingetokea kitu gani. Hakukaa sana Mombasa, siku iliyofuata akarudi Nairobi huku Tim na wenzake wakiendelea kupanga mipango yao. *** Wakati akina Tim wakiwa nchini Kenya, huku Marekani Maxwell alitakiwa kufanya jambo jingine la msingi, kwa kuwa kati ya mashahidi waliokuwa wametajwa alikuwepo Innocent, ilikuwa ni lazima kuhakikisha kijana huyo anauawa mara moja. Akampigia simu na kumwambia kwamba anataka kuonana naye, kwa kuwa Innocent hakuwa na hofu na alishirikiana na Maxwell kwa mambo mengi, akakubali na kwenda kuonana naye. Hiyo ndiyo ilikuwa siku ambayo Maxwell alitakiwa kummaliza kijana huyo, hakutaka kuona akiendelea kuishi, ili kwenye kesi ile ionekane kwamba kweli mzee Todd alifanya mauaji hayo, hakuwa na jinsi kuanza na kijana huyo. Baada ya dakika arobaini na tano Innocent akaibuka nyumbani hapo na kuanza kuzungumza. Hakutaka kumficha, alimwambia ukweli jinsi kesi ilivyokuwa ikiendelea mahakamani na ilitakiwa wafanye kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba mzee huyo hachomoki. Hilo halikuwa tatizo kwa Innocent, akakubaliana naye lakini kwa upande mwingine, akajua kabisa kwamba angeweza kusalitiwa. Akachukua simu yake na kumtumia ujumbe mfupi kijana aliyekuwa nje, ujumbe ambao alimwambia kuwa alitakiwa kuhakikisha anamchukua Innocent na kwenda naye sehemu kumuua akiwa na wenzake. Hilo halikuwa tatizo, wakakubaliana na wakati wakiagana na Innocent kutoka nje, wanaume wawili wakamsogelea na kuanza kumzongazonga huku wakiwa na bastola. Alishangaa, lilikuwa jambo geni kabisa kwake, akahoji lakini akajibiwa kwa kupigwa na kitako cha bastola kichogoni hapohapo akaanguka na kupoteza fahamu. Wakambeba na kumuingiza ndani ya gari. Hawakutaka kupoteza muda kusubiri mahali hapo, wakaondoka na kuelekea katika jumba moja lililokuwa Manhattan hapohapo jijini New York. Huko, hawakutaka kuchelewa, wakamuingiza katika chumba cha mateso na kumuweka kitini kisha kumfunga kamba. Aliporudiwa na fahamu, alishangaa kuona akiwa kwenye chumba hicho kilichoonekana kutisha kupita kawaida kutokana na mazingira yake yalivyokuwa. Hakujua kosa lake lakini hakuwa na budi kuomba msamaha, wanaume hao waliokuwa na miili iliyojazia hawakutaka maswali wala maelezo walichokifanya ni kutekeleza kazi ya bosi wao na hivyo kumpiga risasi kadhaa kifuani na kumpigia simu Maxwell. “Kazi imekamilika,” alisema jamaa mmoja. “Amekufa?” “Kama ulivyotuagiza.” “Sawa. Ahsanteni! Ngoja niwasiliane na akina Tim nione wamefikia wapi,” alisema Maxwell na kukata simu, hakutaka kupoteza muda, hapohapo akampigia simu Tim kwa lengo la kumuuliza mahali walipofikia. “Kila kitu tayari,” alisikika Tim kutoka upande wa pili. “Mmemuua?” “Hapana! Ila tumemchukua mke wake, hapa tupo tunaelekea nchini Tanzania,” alisema. “Kufanya nini?” Tim akaanza kumuelezea kile kilichokuwa kimetokea, walimwambia hali aliyokuwanayo Sharifa kwamba alitakiwa kuchukuliwa na mumewe kupigiwa simu na kuambiwa kwamba hakutakiwa kwenda nchini Marekani kwa gharama yoyote ile. “Kazi nzuri! Na akija Marekani tu, hakikisheni mnamaliza huyo mke wake, sawa?” alisema na kuuliza. “Ndiyo mkuu!” “Kazi njema,” alisema na kukata simu. *** “Today is the day,” (leo ndiyo siku yenyewe) alisema Tim huku akiwaangalia wenzake. Walikaa nchini Kenya kwa siku kadhaa wakisubiri kufanya mipango ya kumteka Sharifa na kuondoka naye. Kwao, kazi hiyo haikuonekana kuwa ngumu tena kwa kuwa waliaminika na kila mtu aliyekuwa akiwaangalia aliwaamini kwamba walikuwa madaktari kutoka nchini Marekani. Siku hiyo ambayo ndiyo waliyotaka kufanya tukio wakamwambia Sharifa kwamba lingekuwa jambo jema kujiunga nao kwani kesho yake wangeweza kuondoka kurudi nchini Marekani kuendelea na kazi zao nyingine. Hilo lilimshtua Sharifa kwani kitu alichojua ni kwamba watu hao wangeendelea kukaa nchini Kenya kwa siku kadhaa. Kuhusu kuungana nao na kula chakula cha mchana halikuwa tatizo hata kidogo, akakubali na hatimaye kwenda sehemu fulani iliyokuwa na hoteli na kuanza kunywa. Kichwa cha Sharifa hakikuwaza ubaya wowote ule, aliwaamini watu hao kwamba walikuwa wema kwa kuwa tangu walipofika nchini humo na kutoa msaada wa kuwasimamia wagonjwa wengine katika vituo vya afya walivyokuwa wamevianzisha. Walikula na kunywa, walizungumza mambo mengi, walifurahia mno na kugongesheana mikono lakini vichwa vyao vilikuwa vikifikiria kitu kimoja tu, kumteka msichana huyo na kuondoka naye kuelekea Tanga. Walipomaliza, wakaingia ndani ya gari. Humo ndipo Sharifa akagundua kwamba watu aliokuwanao hawakuwa wa kawaida, walibadilika, vile vicheko walivyokuwa wakicheka, vikapotea, sura zao zikawa na muonekano mwingine na kuanza kumtia hofu. “Kuna nini?” aliuliza. “Tulia hivyohivyo,” aliambiwa na kutolewa kisu, Tim akakishika na kumwamuru anyamaze kwani vinginevyo angemchoma tumboni, msichana huyo akafanya kama alivyoambiwa. Gari likawashwa mahali hapo na kuanza kuondoka kuelekea katika barabara inayoelekea nchini Tanzania. Njiani, Sharifa alitakiwa kunyamaza kwani vingine angeuawa kama alivyoambiwa. Hakukuwa na tatizo lolote lile barabarani, waliendelea na safari yao huku kila mmoja akitarajia kufika nchini Tanzania pasipo kupata kipingamizi chochote kile njiani. Muda wote huo Sharifa alikuwa na hofu, hakujua kilichokuwa kikiendelea, aliwaamini watu hao lakini ghafla walibadilika na kuwa watekaji. Kila alichokuwa akijiuliza juu ya kile kilichokuwa kimetokea alikosa majibu. Kila alipotaka kuuliza kitu, aliambiwa kunyamaza, hakutakiwa kuzungumza jambo lolote lile kwani kama angekaidi basi angechomwa kisu kama alivyokuwa ameambiwa. Hivyo akanyamaza. *** Muda ulikuwa ukienda, kila mmoja nyumbani alijua kwamba muda wowote ule Sharifa angerudi nyumbani hapo na kuendelea na majukumu lakini msichana huyo hakutokea. Nyumbani kwake, wafanyakazi walikuwa na hofu, wakahisi kwamba alipitia sehemu fulani hivyo kuendelea kumsubiri lakini kitu cha ajabu kabisa msichana huyo hakutokea mahali hapo. Mpaka inafika majira ya saa mbili usiku, bado hakuwa amefika. Hilo likawatia wasiwasi na kuhisi kwamba kulikuwa na jambo lilikuwa limetokea, haikuwa kawaida na mbaya zaidi kila walipokuwa wakimpigia simu haikuwa ikipatikana. Walichokifanya ni kumpigia Bruno na kumwambia kilichotokea. Alipoambiwa hivyo, hakutaka kuendelea kubaki jijini Nairobi, ni kweli alikuwa bize lakini kwake, familia ilikuwa ni zaidi ya pesa na mali hivyo akarudi haraka sana Mombasa ili kuangalia ni kitu gani kilikuwa kikiendelea. Njiani, alijaribu mara kadhaa kumpigia simu Sharifa, hazikuwa zikipatikana, Hilo lilimtisha na kumfanya kuogopa, akahisi kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea, akapiga simu zaidi na zaidi lakini majibu yaliendelea kuwa yaleyale. Hakutaka kuchelewa, alichokifanya ni kuripoti polisi na kuwaambia kile kilichokuwa kimetokea. Kila polisi alishangaa, hawakuamini kama Wazungu waliokuwa wametajwa wangeweza kushirikiana kumtena msichana huyo. Wakamuuliza maswali kadhaa kuhusu Wazungu hao, akawaambia kwamba walitoka nchini Marekani na walifika huko kwa kuwa walitaka kuwasaidia wagonjwa waliokuwa wakiteseka na magonjwa mbalimbali nchini humo. “Mh! Sasa Wazungu wamemteka au kuna watu wamewateka na hao Wazungu?” aliuliza polisi mmoja huku akionekana kushangaa. “Hatuna jibu. Naomba mfuatilie,” alisema Bruno huku akionekana kuchanganyikiwa. Hilo ndilo lililofanyika, mtu ambaye mchumba wake alikuwa ametekwa alikuwa Bruno, mwanaume aliyeibuka ghafla na pesa na kuwa mtu mwenye heshima kubwa mno. Polisi hawakutaka kusubiri, hawakutaka kuona suala hilo likifika mbali zaidi mpaka rais kujua, ili kuwe na amani, waokoe vibarua vyao ilikuwa ni lazima kupambana kuhakikisha msichana huyo anapatikana mara moja. Simu zikapigwa katika vituo vya polisi na kuambiwa kilichokuwa kikiendelea, walitakiwa kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha Sharifa na Wazungu wale wanapatikana haraka iwezekanavyo. Bruno hakuwa na furaha tena, moyo wake ulinyong’onyea na kuona kabisa kwamba asingeweza kumuona tena mpenzi wake. Hakulala, usiku mzima alikuwa akiongea na wakubwa wa vituo kuhusu mpenzi wake kama alikuwa ameonekana sehemu au la. Wakati hayo yote yakiendelea, zilikuwa zimebaki siku mbili kabla ya kesi ya mzee Todd kuendelea nchini Marekani. Akiwa katika hali hiyo, akapigiwa simu kutoka moja kwa moja nchini Marekani na kuambiwa kwamba alikuwa akihitajika nchini Marekani kwa ajili ya kutoa ushahidi katika kesi ya mzee Todd. Alipoambiwa hilo tu, akaanza kupata picha, akaunganisha tukio lililotokea la kutekwa kwa mchumba wake na kesi ile ya mzee Todd, akahisi kabisa vitu hivyo vilikuwa vimepangwa, kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea. Huku akiendelea kuwa katika hali hiyo, akapigiwa simu tena, akaichukua na kuangalia kioo, mpigaji hakuwa mwingine bali ilikuwa ni namba ya mchumba wake, muda huo ulikuwa ni saa sita usiku. “Halo! Sharifa upo wapi?” aliuliza mara baada ya kuipokea simu ile. “Unatakiwa kufanya kitu kimoja tu,” ilisikika sauti ya mwanaume mmoja kutoka upande wa pili, alikuwa Tim. “Unasemaje?” “Sikiliza maelezo yetu kwanza,” alisikika Tim. Akamwambia kilichokuwa kikiendelea, alikuwa akihitajika nchini Marekani kwa lengo la kwenda kutoa ushahidi katika kesi ya mzee Todd, hapo, Tim alimwambia kwamba alitakiwa kutokwenda nchini humo kwani kama angekwenda, mchumba wake angeuawa kwa kuchomwa visu kwa kuwa alikuwa mikononi mwao. Bruno aliposikia maneno hayo, akaogopa, akahisi kabisa mwanaume huyo hakuwa akitania kwani hata sauti yake ilivyokuwa ikitoka, ilionyesha ni kwa jinsi gani alikuwa siriazi kwa kile alichokuwa akikizungumza. “Naomba msimuue mpenzi wangu,” alisema Bruno huku machozi yakianza kumtiririka mashavuni mwake. “Hatutomuua kama tu hautokwenda nchini Marekani, vinginevyo, tutamuua yeye na hata hicho kiumbe kilichopo tumboni mwake,” alisikika Tim, maneno aliyokuwa ameyazungumza yalimfanya Bruno kuogopa kupita kawaida. *** Mzee Bruno alitulia huku masikio yake yakiwa kwa wakili wake, Harris. Mwanaume huyo hakumwambia kitu chochote kuhusu kutekwa kwake, alijua kwamba kama angemwambia ukweli basi hali ingekuwa mbaya zaidi na inawezekana watu wale wangemrudia tena na kumteka kama walivyofanya. Alizungumza naye kwa utaratibu, hakutaka kumuonyeshea dalili kwamba kulikuwa na kitu kilichokuwa kimetokea, alimpa matumaini kwamba angeshinda kesi ile pasipo kumwambia kuwa mashahidi waliokuwa na nguvu ya kumtoa walikuwa njiani kuuawa. Yeye ndiye aliyekuwa akimwambia hali ilivyokuwa ikiendelea. Hakumficha, alimwambia kuwa Wamarekani walimchukia na kila mmoja kwa kipindi hicho alikuwa akitaka kuona akihukumiwa kifo kama watu wengine. Hilo lilimuhuzunisha mzee huyo kwani hakuwa amefanya jambo lolote baya, hakuwa ameua wala yale madawa ya kulevya yaliyokutwa ndani ya nyumba yake hayakuwa yake. Kila alipokuwa akimuuliza kuhusu mashahidi wake kama walipigiwa simu, Harris alikuwa akijiumauma kana kwamba kulikuwa na jambo baya sana ambalo mzee huyo hakutakiwa kulijua. “Waliwasiliana nao,” alisema. “Ikawaje?” “Waliniambia kwamba watakuja!” “Watakuja? Washaanza safari? Serikali ndiyo inatakiwa kuwasafirisha! Wameanza hiyo safari?” aliuliza. “Hata sijajua!” “Harris! Inakuwaje usijue na wakati wewe ndiye wakili wangu ninayekutegemea?” aliuliza mzee Todd. Harris hakuwa na cha kujibu, hofu ilimtanda moyoni mwake. Mpaka kufikia hatua hiyo, tayari mzee Todd akahisi kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea ambacho mtu huyo aliyemtegea hakutaka kumwambia ukweli. Siku hazikuwasubiri, zikaendelea kukatika kama kawaida. Mpaka siku ya kupanda tena mahakamani, bado mashahidi hawakuwa wamefika mahakamani na kwa taarifa ambazo zilianza kuzagaa ni kwamba mtu aliyetajwa kama shahidi namba mbili, Innocent alipotea katika mazingira ya kutatanisha, na hakukuwa na mtu aliyejua mahali alipokuwa. *** Ilikuwa ni lazima kwa Tim na wenzake kuondoka Mombasa na kuelekea Tanga nchini Tanzania. Hawakuona kabisa kama kungekuwa na watu wangeweza kuwasumbua njiani kwa kuwa walikuwa na kiasi kikubwa cha pesa ambacho wangekitumia kwa polisi yeyote yule ambaye angediriki kuwazuia. Njiani, walikuwa wakiendelea na safari yao, hakukuwa na mtu aliyekuwa na wasiwasi, waliwapigia simu wenzao waliokuwa nchini Marekani na kuwaambia kwamba walifanikiwa kumpata mchumba wa shahidi namba mbili ambaye kwake alikuwa hanywi, hali wala hafanyi kitu chochote kile, kwa mapenzi aliyokuwa akimpenda msichana huyo, alikuwa tayari kufanya jambo lolote lile. Walichukua saa kadhaa wakaanza kukaribia Horohoro huku ikiwa ni saa nne usiku, mahali kulipokuwa na mpaka wa Kenya na Tanzania. Mpaka kufikia hapo wakawa na uhakika kwamba wangeingia nchini Tanzania kwa kuwa kusingekuwa na mtu yeyote yule ambaye angediriki kuwasimamisha. Ndani ya gari Sharifa alipewa masharti kwamba hakutakiwa kuonyesha hali yoyote ile ya kuwatia wasiwasi watu wengine, kama alivyokuwa ndivyo alivyotakiwa kuwa, yaani sura yenye tabasamu ambayo ungeonyesha kwamba hakukuwa na jambo lolote baya ambalo lilikuwa likiendelea. Baada ya kubakiza mita mia mbili kabla ya kuingia mpakani hapo wakaanza kuyaona magari kadhaa yakiwa yameweka foleni na kwa kuwa hawakutaka kusababisha jambo lolote ambalo lingewafanya kugunduliwa, nao wakaweka foleni kwa ajili ya upekuzi. Magari yalikwenda taratibu sana mpaka baada ya saa moja nao ndiyo wakafanikiwa kufika mahali pa kuvuka ambapo hapo wakatakiwa kuonyesha vibali vyao kabla ya kuendele. “This is our passports,” (hizi ni hati zetu za kusafiria) alisema Tim huku akimwangalia polisi aliyekuwa akikagua hati za kusafiria. “What about hers?” (vipi kuhusu yake?) aliuliza akimaanisha Sharifa. Tim hakutaka kuzungumza sana, alichokifanya ni kuchukua kibunda cha dola kilichokuwa na dola mia moja kama ishirini na kumuonyeshea polisi yule kisiri. “We have no time friend,” (hatuna muda rafiki) alisema Tim huku akimwangalia polisi huyo ambaye naye kwa siri kubwa akakichukua na kukichikichia chini ya kitabu chake cha maelezo na kuwaambia jamaa waliokuwa wameshikilia vyuma vya kuzuia magari kuliruhusu gari hilo, na kwa kuwa ilikuwa ni usiku, hakukuonekana kuwa na tatizo lolote lile. Wakaondoka huku wakiwa wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa, pesa zile walizozitoa zilibadilisha kila kitu na kuonekana kwamba walikuwa watu wema. Walipofika kama umbali wa miaka mia tano kutoka mpakani pale, simu ikapigwa na taarifa kutolewa kwamba kulikuwa na Wazungu watatu walikuwa ndani ya gari na mwanamke mmoja, Wazungu hao hawakutakiwa kuvuka mahali hapo. Polisi yule aliposikia tangazo lile, akajua kabisa kwamba watu waliokuwa wakiuliziwa ni wale ambao aliwaruhusu mpakani hapo lakini hakutaka kusema kitu chochote kile kwa kuhofia kuharibu kila kitu na hata zile pesa alizokuwa amepewa, mwisho wa siku zingeweza kugundulika na kumletea matatizo. Safari ilikuwa ikiendelea huku kila mmoja akijiona kuwa bingwa kwa kile kilichokuwa kimetokea. Kutoka hapo Horohoro mpaka Tanga Mjini ilikuwa ni umbali wa kilometa 172, Tim hakutaka kuendesha kwa mwendo wa taratibu, ilikuwa ni lazima kuwahi hivyo kuendesha kwa mwendo wa kasi kana kwamba walikuwa wameliiba gari hilo. Walitumia dakika arobaini na tano mpaka kufika tanga Mjini ambapo moja kwa moja wakaenda uswahilini na kuchukua vyumba katika gesti moja na kujificha huko huku wakiwasiliana na wenzao ambao walikuwa wakihitaji kujua kile kilichokuwa kimeendelea nchini Kenya. Ilipofika saa sita usiku, Tim akachukua simu ya Sharifa na kumpigia simu Bruno na kumwambia kwamba hakutakiwa kwenda Marekani kwani vinginevyo mpenzi wake ambaye walikuwanaye wangeweza kummaliza. “Umemwambi?” aliuliza mwenzake. “Ndiyo! Akibisha basi hatutokuwa na jinsi! Tutamuulia mbali,” alisema Tim maneno yaliyomtisha Sharifa. *** Polisi walichachamaa, kila kona walikuwa wakiwaulizia Wazungu hao walioonekana kuwa mwiba mkali kwa Bruno. Alichanganyikiwa, usiku huo alikuwa akiwatafuta lakini mpaka asubuhi inaingia hawakuwa wamefanikiwa kwa lolote lile. Hilo liliwachanganya polisi, walichokiamini ni kwamba watu hao walikuwa hapohapo Mombasa hivyo kuendelea kuwatafuta kwa nguvu zote. Asubuhi hiyo walipoona kwamba hawakufanikiwa, wakawapigia simu polisi waliokuwa mipakani na kuwaulizia watu hao kama walikuwa wamepita huko au la lakini kwa bahati mbaya, kila walipokuwa wakiuliza waliambiwa kwamba watu hao hawakuwa wamepita hivyo kuendelea kuwatafuta ndani ya Kenya tu. “Hawa watu watakuwa wameondoka Kenya, haiwekani kila kona hawapo japokuwa tumehakikisha ulinzi kila sehemu,” alisema mkuu wa kituo kikuu cha polisi cha hapo Mombasa, kwa jinsi alivyoongea alionekana kuchanganyikiwa kwani suala la mchumba wa Bruno kutekwa halikuwa la kawaida hata kidogo, kichwa chake kilikuwa kikimfikiria rais endapo tu angepata taarifa hiyo. Wakati polisi wakiendelea kumtafuta Sharifa, Bruno alikuwa akijua kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Moyo wake ulitamani sana kumsaidia mze Todd lakini kila alipofikiria upande wa pili kwamba mpenzi wake angeuawa mara baada ya kwenda nchini Marekani akabaki akiwa hajui ni kitu gani alitakiwa kufanya. “Hii haiwezi kuwa siri tena, ni lazima nimshirikishe Bartazar,” alisema Bruno. Hilo ndilo alilolifanya, haraka sana akampigia simu mkuu wa polisi nchini Kenya, Bartazar na kumwambia kile kilichokuwa kikiendelea. Mkuu huyo wa polisi alipoambiwa, alichanganyikiwa, akauona ugumu wa kazi uliokuwa mbele yake, hakutaka kuchelewa, kwa kuwa alikuwa na namba za rais, akampigia na kumuhadithia kila kitu kilichokuwa kikiendelea. “Yaani ilikuwaje?” alisikika rais akiuliza hivyo kuanza kuhadithiwa tena. Hakuwa akijua kitu chochote kile, kwake, jambo hilo lilionekana kuwa geni kabisa. Bartazar alichokihitaji kilikuwa ni kitu kimoja tu, rais huyo wasiliane na ubalozi wa Marekani kwa lengo la kuwapa taarifa maofisa wa CIA ambao walitakiwa kufanya kila linalowezekana kuhakikisha Sharifa anapatikana kwani wao kama wao wasingeweza kuwapata. Rais hakusubiri, kama alivyoambiwa ndivyo alivyofanya, haraka sana simu ikapigwa mpaka ubalozini na kuwaambia kilichokuwa kimetokea. Balozi wa Marekani nchini Kenya, akapiga simu nchini Marekani na kuwaambia kila kitu. Haraka sana maofisa wa CIA waliokuwa nchini Kenya, wakapigiwa simu na kuambiwa kila kitu na walitakiwa kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha huyo msichana anapatikana kwa udi na uvumba ili mpenzi wake asafirishwe na kuelekea nchini Marekani kwa ajili ya kutoa ushahidi wa kesi hiyo. “Ila tumechelewa, kesi yenyewe ni kesho,” alisikika jamaa mmoja. “Itaahirishwa. Tutapeleka taarifa mahakamani,” alisema mkuu wa CIA nchini Marekani. *** Siku ya kesi ambayo ilitarajiwa kusikilizwa kwa upande wa mashahidi ilikuwa imefika. Watu wengi walifika mahakamani hapo kwa kuwa walitaka kusikia kile kilichokuwa kimetokea mpaka mwanaume huyo kuamua kuyaficha madawa ya kulevya nyumbani kwake na mwisho wa siku kuhusishwa katika vifo vya familia yake. Watu wengi waliohudhuria kesi hiyo siku hiyo walikuwa na hamu kubwa kusikiliza kwa upande wa mashahidi. Wale waliokuwa wakitakiwa kusimama kwa upande wa jamhuri walikuwa tayari lakini kitu cha ajabu mpaka siku ya kesi inafika jaji hakuwa amepokea taarifa yoyote kuhusu mashahidi kwa upande wa mshtakiwa. Mahakamani kukaanza kuzuka minong’ono, hakukuwa na mtu aliyejua kilichokuwa kikiendelea, walikuwa wakiangalia huku na kule kuona kama mzee Todd alikuwa na mashahidi mahakamani hapo. Yeye mwenyewe alishangaa, hakujua kama kweli Bruno alikuwa na taarifa au la. Alimsaidia sana kijana huyo na alikumbuka kabisa kwamba siku ya mwisho kuzungumza naye alimwambia kuwa angependa sana siku ya kesi yake aende Marekani na kusimama kama shahidi lakini kitu cha kushangaza kabisa kijana huyo hakutokea. Hilo lilimsikitisha sana, upendo wote aliokuwanao kwa Bruno ukapotea, akahisi kugeukiwa na mtu ambaye hakumtarajia kufanya jambo kama hilo. Moyo wake ukaanza kuwa na chuki dhidi ya Bruno, japokuwa kijana huyo alimsaidia sana lakini muda huo hakuwa hakuona thamani ya msaada alioutoa kwake kwa kuwa alihitaji kusaidiwa zaidi katika hali ngumu kama aliyokuwanayo kipindi hicho. “Bruno! Why do you do this to me?” (kwa nini unanifanyia hivi Bruno?) aliuliza mzee huyo kwa sauti ya chini huku machozi yakimtoka kwani aliamini kwamba Bruno alikuwa mtu muhimu hata zaidi ya alivyokuwa Innocent. Baada ya dakika kadhaa, jaji akapokea kikaratasi kutoka kwa mwanaume mmoja, akaanza kukisoma, alipomaliza, akayainua macho yake na kuielezea mahakama kwamba kesi hiyo iliahirishwa mpaka baada ya wiki mbili kwani mashahidi wawili waliokuwa wakitarajiwa kusimama kizimbani kumtetea mzee Todd hawakufika mahakamani hapo. “What? Just hung him,” (nini? Nyie mnyongeni tu) alisikika mwanaume mmoja mahakamani hapo.
CIA watatu, Andrew Putt, Gilbert Michael na Richard Bull wakaianza kazi yao nchini Kenya kuhakikisha Sharifa anapatikana haraka iwezekanavyo. Kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kwenda Mombasa katika kijiji cha Goulduvai alipokuwa akiishi Sharifa kwa muda huku akiwahudumia wanakijiji kwa afya zao. Walipofika huko, kila kona watu walikuwa wakilizungumzia tukio hilo. Hakukuwa na mtu aliyekuwa na furaha, kila mmoja alihuzunika kwani kwa kile kilichokuwa kimetokea hawakukitegemea hata kidogo. Hapo, wakazungumza na Bruno na kumuuliza maswali kadhaa. Aliwasimulia kila kitu alichokuwa akikifahamu kuhusu Wazungu wale na mwisho kabisa akawaambia kwamba lengo la watu hao ni kwamba hakutakiwa kwenda nchini Marekani kutoa ushahidi kwa yaliyokuwa yametokea kwa mzee Todd. “Someone is behind this,” (kuna mtu yupo nyuma ya hili) alisema Bull huku akiwaangalia wenzake. Wakahitaji simu ambayo Bruno aliwasiliana na Tim, walipopewa, wakachukua namba, wakasogea pembeni hidogo huku Putt akichukua tablet yake na kufungua sehemu ya ramani na kuanza kuangalia. Bruno alitulia pembeni, alibaki akiwaangalia Wazungu hao walioonekana kuwa hatari katika kumtafuta mtu yeyote waliyekuwa wakimtaka. Walikaa huko kwa zaidi ya nusu saa huku wakizungumza na wakati mwingine wakiangalia tablet ile kwa lengo la kujua zaidi kuhusu watu hao walikuwa mahali gani. “Hivi kweli wanaweza kwenda Nairobi?” aliuliza Putt huku. “Sidhani! Haiwezekani mtu afanye tukio kama hili halafu akaelekea Nairobi,” alisema Bull huku akiwaonyeshea wenzake ramani katika table. “Kwa maelezo ya mumewe alisema kwamba alipigiwa simu, lakini haikuwa ya kawaida, ilipigwa kwa mtandao wa WhatsApp, mnajua kwa nini mpigaji alifanya hivyo?” aliuliza Gilbert. “Hapana!” Gilbert alikuwa miongoni mwa maofisa wa CIA waliokuwa na utaalamu mkubwa wa kumtafuta mtuhumiwa yeyote yule. Alikuwa mtaalamu wa hisia ambaye kama kulikuwa na tukio limetokea ndani ya nyuma na mtuhumiwa kutoweka, aliweza kusimama na kukwambia kila kitu kilichokuwa kimetokea ndani ya nyumba hiyo. Alikuwa mtaalamu na makao makuu walimpeleka nchini Kenya kwa lengo la kuhakikisha kwamba Kundi la Al Shabaab linateketezwa haraka sana kwa kuwaambia kila kitu kilichokuwa kimetokea. Kwa akili yake, akagundua kwamba watu hao hawakuwa nchini Kenya, walikuwa wameondoka na kuelekea katika nchi nyingine na ndiyo maana waliamua kupiga simu kwa kutumia Mtandao wa WhatsApp. “Kivipi?” aliuliza Bull. “Ni kwa sababu hawakutaka kupatikana katika minara ya simu za mkononi. Kama wangetumia simu ya kawaida, tungejua wapo wapi, ila kwa WhatsApp, bila shaka watu hawa wameamua kuficha mawasiliano ili tusijue wapo wapi,” alisema Gilbert huku akionekana kumaanisha alichokuwa akikizungumza. Alichokisema ndio ulikuwa ukweli wenyewe kwamba watu hao waliondoka na kuelekea nje ya Kenya. Hakukuwa na maswali mengi kwamba ni nchi gani walikuwa wameelekea, moja kwa moja wakagundua kwamba ilikuwa ni Tanzania na hivyo ilikuwa ni lazima waende huko. “Kwa nini isiwe Somalia?” “Ni kwa sababu kuna mapigano huko. Kwa akili ya kawaida tu, ungeweza kukimbilia Somalia?” aliuliza Gilbert. “Haiwezekani!” “Kama haiwezekani, basi watu hao watakuwa wamekimbilia Tanzania,” alisema. Hawakutaka kupoteza muda, ilikuwa ni lazima kuondoka na kuelekea nchini humo. Hawakuaga bali walimwambia Bruno kwamba watakaporudi watarudi wakiongozana na mpenzi wake hivyo alitakiwa kuwasubiri hapohapo Mombasa. Njiani, walikuwa wakizungumza mambo mengi, kwao, kazi ile haikuonekana kuwa ngumu tena, waliamini kwamba kwa namna moja ama nyingine wangefanikiwa kwa kuwa tu walijiona kuwa na uwezo mkubwa kuliko hata hao watu waliokuwa wamemteka Sharifa. Hawakuchukua muda mrefu wakafika katika mpaka wa Horohoro kwa upande wa Kenya. Wakateremka na moja kwa moja kuelekea katika ofisi ya kiongozi wa maaskari hapo mpakani, mzee Hamidu na kumuuliza kuhusu watu hao waliokuwa wamepitia mahali hapo kuingia Tanzania. “Hakuna watu waliopita,” alisema mzee Hamidu huku akimwangalia Bruno. “Si kweli!” “Huo ndiyo ukweli, au kama mmekuja na ukweli wenu mwingine,” alisema mzee Hamidu huku akisimama kwenye kiti, yote hayo ilikuwa ni kutaka kuwaonyeshea watu hao kwamba alikuwa mwanaume imara na kile alichokuwa akikisema ndicho kilikuwa sahihi. “Hapana! Bado tunajua kwamba walipita hapa, ila walipitaje? Inawezekana wewe hufahamu lakini kuna mtu hapa atakuwa anafahamu,” alisema Gilbert. “Kwa hiyo kuna mtu alichukua rushwa?” “Huwezi kujua!” “Hizo ni dharau,” alisema mzee huyo. Gilbert hakutaka kubaki ndani ya ofisi hiyo, kwa jinsi mzee Hamidu alivyokuwa akiongea, alihisi moyo wake ukipatwa na hasira kali, na ili kuepusha matatizo, akaamua kutoka ndani ya ofisi ile. Pale nje akasimama na kuanza kuangalia huku na kule, aliwaangalia jinsi ambavyo askari walivyokuwa wakipekua magari, alikuwa na uhakika kwamba watu hao walipita mahali hapo kwani hata upekuzi ambao ulikuwa ukifanyika, ulifanyika kizembe sana. “Tuingieni nchini Tanzania, bado moyo wangu una uhakika kwamba watu hawa walipita mahali hapa,” alisema Gilbert, wakaingia ndani ya gari lao na kuingia nchini Tanzania, hapo wakaanza kuitafuta Tanga Mjini. *** Kila kona katika Tanga Mjini kulikuwa na stori moja tu iliyokuwa ikianza kuzagaa kila kona. Wazungu watatu ambao walichukua chumba kimoja katika nyumba ya wageni iliwashangaza kila mtu aliyekuwa ameisikia. Watu walijua kwamba Wazungu walikuwa miongoni mwa watu waliokuwa na pesa, watu ambao mara baada ya kufika barani Afrika basi wangekuwa wakiishi katika hoteli nzuri lakini Wazungu waliokuwa wameingia Tanga kwa siku hizo walionekana kuwa tofauti na wenzao kabisa. Hali hiyo ikaanza kuwatia wasiwasi watu wa hapo Tanga kiasi kwamba wengi wakahisi kwamba kulikuwa na kitu cha siri kilichokuwa kikiendelea ambacho kingeweza kuwa hasara au hata kupoteza maisha kwa wakazi wa hapo. Walichokifanya siku iliyofuata ni kuwasiliana na polisi. Waliwaambia kila kitu kilichokuwa kimetokea kwamba inawezekana kabisa Wazungu wale hawakuwa watu wazuri na ndiyo maana hawakutaka kupanga katika hoteli kubwa kwa kuogopa kukamatwa. Polisi walipoambiwa, hawakutaka kusubiri, wakaondoka na kuelekea huko kwa lengo la kuwaona Wazungu hao. Walipofika, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kuzungumza na mmiliki wa gesti hiyo na kumuuliza maswali mengi. Hakuwaficha, aliwaambia kila kitu kuhusu Wazungu hao na hivyo kuhitaji kuzungumza nao. Hilo halikuwa tatizo, alichokifanya ni kuwaita, wanaume hao, wakatoka chumbani, wakafunga mlango kwa ufunguo ili Sharifa asitoke, wakawafuata polisi na kuanza kuzungumza nao. Waliwaambia kwamba walifika hapo Tanga kwa lengo la kuingia katika mapango ya Amboni lakini kabla ya kwenda huko walijikuta wakiibiwa kiasi cha pesa walichokuwanacho cha dola elfu themanini, laptop na saa zao za mikononi na vijana wa mitaani ambao waliwafuata na kuwatolea visu. “Poleni sana! Kwa nini hamkutoa taarifa polisi?” aliuliza polisi mmoja, kwa jinsi Tim alivyokuwa akielezea, ilikuwa ni vigumu kuamini kwamba alikuwa akidanganya. “Tulichanganyikiwa! Hatupo sawa, hata nauli ya ndege kurudi nyumbani hatujui tutaipataje, hapa mnapotuoni, tupo hivihivi pamoja na msichana wa nchini Ghana ambaye tumekuja naye, hatuna kitu,” alisema Tim. Polisi wakaangaliana, kile alichokuwa amekisema kilionekana kuwagusa kupita kawaida hivyo kuwaambia kwamba wanaondoka na kurudi baadaye huku wakiwa tayari wamejua ni kitu gani walitakiwa kufanya kuwasaidia Wazungu hao. Walipoona polisi wameondoka, hawakutaka kuendelea kukaa kwenye gesti hiyo, ilikuwa ni lazima waondoke kwani walihisi kwamba mara baada ya kuondoka, wangekwenda kupata ukweli wa wao kuwa hapo na kurudi huku wakiwa na sura nyingine. Wakaufungua mlango na ufunguo, wakaingia ndani, kilichowashtua ni kwamba Sharifa hakuwemo chumbani humo. Hilo liliwatia hofu kwani walipokwenda nje kuzungumza na polisi walimuacha humo ndani na zaidi ni kwamba waliufunga mlango kwa ufunguo, sasa kama ameondoka, atakuwa amepitia wapi? “Kwenye dari! Tuangalieni kwenye dari,” alisema Adson na kwa kuwa pale kulipokuwa na mlango wa dari kulikuwa na meza, wakajua kabisa msichana huyo alipanda juu ya meza hiyo na kuingia humo kwa lengo la kuwatoroka hotelini humo. “Jamani! Ili tuwe salama, huyu msichana ni lazima apatikane,” alisema Kelly, wakautoa mlango wa dari na Tim kuingia huko kumtafuta Sharifa. *** Sharifa alikuwa ndani ya chumba kile huku akiwa na wasiwasi tele, hakujua ni kitu gani kingeendelea kama tu watu hao wangeendelea kumshikilia kama ilivyokuwa. Hakutaka kuona akiwa mikononi mwa watu hao, alitamani kuona akiondoka na kurudi kwa mpenzi wake. Kama kulia, alilia sana lakini muda huo haukuwa wa kulia tena, ilikuwa ni lazima kufanya kila liwezekanalo kuondoka ndani ya chumba hicho. Alikuwa humo, Tim na wenzake walikwenda nje walipokuwa wakihitajika na polisi, yeye mule ndani ilikuwa ni lazima afanye kila linalowezekana kuhakikisha anatoka ndani ya chumba hicho. Akaufuata mlango, akakishika kitasa na taratibu kuanza kukitekenya kwa lengo la kukifungua. Mlango haukufunguka kuonyesha kwamba ulifungwa kwa nje. Haraka sana akaacha. Akaangalia huku na kule, akafanikiwa kuuona mlango wa dari ukiwa umefungwa. Kichwa chake kikamwambia kwamba hiyo ndiyo ilikuwa njia pekee ya kuweza kuondoka ndani ya chumba hicho. Akachukua meza, akaiweka chini ya mlango wa dari na kupanda, akaanza kuufungua mlango huo kwa kuusukuma, ukafanikiwa kufunguka. Kazi kubwa ilikuwa ni kupanda juu ya dari. Ilikuwa ni kazi ngumu ambayo aliamini kwamba asingeweza kuifanya hata kidogo lakini kitu cha kushangaza kabisa ambacho hata yeye kilimwachia maswali ni kwa namna ambavyo alipanda na kuingia darini, akaurudishia mlango ule wa dari. Ndani kulikuwa na giza, hakuwa na simu, hakuwa na kitu chochote kile ambacho kingemfanya kumulika mule ndani lakini hilo halikumfanya kubaki mahali pale, kwa kutumia magoti yake akaanza kusonga mbele, sehemu ambayo aliamini kulikuwa na mlango mwingine. Humo darini, alisikia milio ya panya, hakuoga hata kidogo, kitu alichokuwa akikimbia kilikuwa ni hatari hata zaidi ya panya aliokuwa akiwasikia. Baada ya dakika mbili akafika katika mlango mwingine wa dari na kuufungua. “Mungu nisaidie,” alisema huku akiangalia ndani ya chumba hicho. Alisikia sauti za watu wakiongea bafuni kwa furaha, hakutaka kujiuliza kuhusu watu hao, akahisi kabisa kwamba walikuwa wapenzi waliokwenda kuyafurahia maisha yao na muda huo walikuwa wakioga tayari kwa kuondoka. Bahati ilikuwa upande wake kwani pale kulipokuwa na mlango wa dari kulikuwa na kitanda, haraka sana akaruka mpaka juu ya kitanda. Akaondoka na kuufuata mlango, akaufungua na kuanza kuangalia nje. Alipoona koridoni hakuna mtu, hakutaka kusubiri, hara sana akatoka na kuelekea nyuma ya gesti hiyo na kuanza kukimbia. Mule ndani, Tim aliendelea kutambaa ndani ya dari na kufanikiwa kuuona mlango wa kushukua katika chumba kingine. Haraka sana akaufuata, haukuwa umefungwa hivyo akarukia ndani ya chumba hicho. “She was passing through this room,” (amepitia chumba hiki) alisema Tim na kuufungua mlango na kutoka ndani. Kichwa chake kilimwambia kwamba msichana huyo alikuwa ameondoka kupitia katika mlango wa nyuma na hivyo kuanza kukimbilia huko. Alichanganyikiwa, msichana huyo alikuwa mtu muhimu mno, aliwafanya kufika nchini Kenya, wakatoroka mpaka Tanzania na walikuwa wamelipwa kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya kuhakikisha mpenzi wa msichana huyo, Bruno haondoki kuelekea nchini Marekani. Kule nje aliwakuta watu wakiwa wamepigwa na taharuki, kilichokuja kichwani mwake ni kwamba walimuona Sharifa akiwa amekimbia na hawakujua sababu iliyomfanya kukimbia na ndiyo maana walikuwa kwenye hali hiyo. Akaanza kuelekea katika njia iliyokuwa na watu wengi waliokuwa wamesimama kwa kuamini kwamba msichana huyo alipitia njia hiyo. Watu wote wakaanza kumwangalia na yeye, ni kweli walimuona msichana mmoja akiwa amekimbia lakini ghafla, baada ya sekunde kadhaa wakamuona mwanaume wa Kizungu naye akikimbia kuelekea kule alipokimbilia mwanamke yule. “Jamani! Kuna nini tena?” aliuliza jamaa mmoja aliyekuwa amevaa msuli kama mtu aliyekuwa na busha. “Hata mimi nashangaa! Hawa watoto wetu siku hizi wana visa sana, utakuta huyo Mzungu kamtoa Instagram halafu anamkimbia,” alisema mzee mwingine. Tim alikimbia mpaka katika barabara kuu kabisa lakini hakuweza kumuona Sharifa. Alichanganyikiwa, kwa wakati huo msichana huyo alikuwa muhimu kuliko kitu chochote kile. Akamtafuta na alipoona hajafanikiwa, akarudi kule gesti na kuwaambia wenzake kile kilichotokea. Kila mmoja alichanganyikiwa, kitendo cha kumkosa msichana huyo kilimaanisha kwamba Bruno angekwenda nchini Marekani na kuweka ushahidi juu ya kile kilichokuwa kimetokea. “Ni lazima tuondoke kurudi Marekani haraka sana,” alisema Tim huku akiwaangalia wenzake, yeye alionyesha kuchanganyikiwa zaidi ya wenzake. “Tukiulizwa?” “Tunakwenda kimyakimya!” “Halafu?” “Huyu mtu tutamvizia uwanja wa ndege, najua tutajua siku ambayo atakwenda nchini Marekani, nadhani hapo ndipo tutakapofanya utekaji hukohuko mbele ya safari! Mnaonaje?” alisema na kuuliza. “Linaingia akilini! Hakuna kuchelewa, kama vipi kesho tuondokeni,” alisema Kelly. Hivyo ndivyo walivyokubaliana, hakukuwa na sababu ya kuendelea kubaki nchini Kenya na wakati kulikuwa na kazi kubwa ambayo walitakiwa kuifanya haraka iwezekanavyo. Usiku huohuo wakaondoka na kuelekea katika hoteli ya kifahari ya Jumanji iliyokuwa Tanga Mjini na kuchukua vyumba hapo. Siku iliyofuata, wakapanda ndege na kuelekea Dar es Salaam ambapo huko wakaunganisha mpaka nchini Marekani. Ndani ya ndege kila mmoja alikuwa akifikiria lake, mbele yao kulionekana kuwa na kazi kubwa lakini ilikuwa ni lazima kuhakikisha wanaikamilisha kwa haraka sana. Hawakutaka kuzungumza mambo mengi kuhusu jambo hilo ila walipanga kuzungumzia zaidi mara baada ya kufika nchini humo. Baada ya saa ishirini na tano, wakaingia nchini humo. Wakafikia hotelini, hawakutaka kuwasiliana na Maxwell, walitaka kukamilisha kila kitu haraka sana pasipo mwanaume huyo kufahamu jambo lolote lile. Wakajipanga na baada ya siku tatu tangu wafike nchini Marekani wakapata taarifa kwamba Bruno alikuwa njiani akielekea nchini Marekani. Kwa kuwa walitakiwa kukamilisha mpango wao haraka sana, wakajipanga kwa kwenda uwanja wa ndege na kufanya uchunguzi ili wagundue ni ndege ipi ambayo ingemfikisha hapo nchini Marekani. Wakapewa taarifa kwamba Bruno alipanda ndege ya Shirika la American Airlines na angeingia mahali hapo majira ya saa 05:43 usiku, hivyo walitakiwa kusubiri. *** Gilbert na wenzake waliingia nchini Tanzania katika jiji la Tanga na kuanza kufanya upelelezi kugundua kile kilichokuwa kikiendelea. Walianza kuzunguka katika vituo vya polisi kwa lengo la kupata ukweli juu ya kile kilichokuwa kikiendelea. Huko, wakaambiwa kwamba hakukuwa na taarifa yoyote ile juu ya mtu waliyekuwa wakimtafuta lakini kama wangewapa muda, basi bila shaka wangejua kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Japokuwa walikuwa katika kituo kikuu cha Tanga, wakaondoka na kuelekea katika vituo vingine vidogo, walikuwa na uhakika kwamba kama Sharifa alikuwa amepelekwa nchini humo basi ilikuwa ni lazima kupatikana hata kama kungetokea jambo gani. Huko, wakapewa taarifa kuhusu Wazungu waliokuwa wamefika hapo Tanga na kuchukua chumba katika gesti moja ya uchochoroni ambapo huko walionekana wakiwa na mwanamke mmoja kutoka nchini Ghana. “Mwanamke kutoka nchini Ghana?” aliuliza Gilbert. “Ndiyo!” “Ulimuona huyo mwanamke?” “Hapana! Ila tuliambiwa na mwenye gesti kwamba walikuwa watalii,” alisema polisi aliyekuwa akijibu maswali kwa niaba ya mkuu wa kituo ambaye hakuwa mahali hapo. Hapo hakukuonekana kuwa msaada tena, wakahisi kabisa kwamba watu hao ambao waliambiwa kuhusu stori zao na kwamba walikuwa na mwanamke kutoka nchini Ghana iliwezekana kabisa wakawa watu waliokuwa wakiwatafuta, wakaelekea katika gesti hiyo huku wakisindikizwa na polisi, walipofika, wakaingia ndani. Wakakutana na mhudumu na kumuuliza kuhusu Wazungu hao, aliwaambia kwamba walikuwa ndani hivyo kwenda katika chumba walichokuwa wamechukua huku Gilbert na wenzake wakiwa na bastola mikononi mwao kwa ajili ya jambo lolote baya lile ambalo lingetokea huko. Walipokifikia chumba, wakaufungua mlango na kuingia ndani huku wakiwa na bastola zao. Walipofika, hakukuwa na mtu yeyote yule, Wazungu wale ambao waliambiwa kwamba walikuwa humo na mwanamke mmoja, hakukuwa na yeyote yule, chumba kilikuwa kitupu kabisa. “Wapo wapi?” aliuliza polisi. “Mmh! Walikuwa humu! Sijui wapo wapi!” alisema jamaa mwenye gesti. Wakatoka kwa kuhisi kwamba watu hao walikuwa wamekwenda sehemu fulani hivyo walitakiwa kuwawahi. Nje, kila kona hawakufanikiwa kuwaona watu hao zaidi ya wananchi kuwashangaa tu kwani kwa tukio lililokuwa likitokea siku hiyo kila mtu lilimshangaza kwani haikuwa na kawaida kwa Wazungu kuwa katika hali kama waliyokuwa wale wa mwanzo na hata hao wa kipindi hicho. “Wametoroka! Wamekwenda naye wapi?” aliuliza Gilbert, kwa kumwangalia tu usoni alionekana kuwa na hasira kupita kawaida. ***
Sharifa alikuwa akikimbia huku akiangalia nyuma, kila mtu aliyekuwa akipishana naye alimshangaa, hawakujua kitu kilichokuwa kimetokea mpaka msichana huyo kukimbia huku akionekana kuwa na hofu kubwa. Alikimbia mpaka alipofika mahali kulipokuwa na nyumba nyingi zilizokuwa milango wazi, hakutaka kuendelea kukimbia tu kwa kuona kwamba angekamatwa kwa kuwa hakuwa na kasi, hivyo akaingia ndani ya nyumba moja na kuomba msaada. Watu walikuwa vyumbani mwake, wakatoka na kumwangalia Sharifa aliyekuwa ukumbini, aliwaambia watu hao kwamba alihitaji msaada kwa kuwa alikuwa akikimbizwa. Wakati akiwa hapo ukumbini, akamuona Tim akipita nje kwa kasi huku akikimbia, Sharifa akajificha kwani hakutaka kuonekana na mwanaume huyo. Watu wote wakabaki wakimshangaa, kwao, alionekana kama mtu aliyekuwa na matatizo fulani, yaani kama changudoa aliyemkimbia mteja gesti. “Bibie vipi?” aliuliza mwanamke mmoja. “Kuna mtu ananikimbiza anataka kuniua,” alisema Sharifa huku akiangalia huku na kule, kwa kifupi alikuwa na wasiwasi. Kwa lafudhi yake tu, kwa jinsi alivyokiongea Kiswahili chake hakukuwa na swali kwamba msichana huyo alikuwa Mkenya. Mwanamke mmoja akamchukua na kumuingiza chumbani mwake na kumuuliza tatizo alilokuwanalo ambapo akaanza kumwambia kila kitu kilichotokea. Alishangaa, hakuamini kama kweli kungekuwa na watu ambao wangetoka nchini Marekani mpaka Kenya kwa lengo la kumteka mtu fulani, haikumuingia akilini, wakati mwingine aliona kama alikuwa akidanganywa na msichana huyo lakini akaamua kukubaliana naye. “Nikusaidie nini?” aliuliza mwanamke huyo baada ya kusikiliza maneno ya Sharifa. “Nataka kuwasiliana na mume wangu! Naomba unisaidie,” alisema. Hilo halikuwa tatizo hata kidogo, akampa simu na msichana huyo kumpigia Bruno aliyekuwa nchini Kenya, baada ya sekunde kadhaa alikuwa akiongea naye. Alimwambia mahali alipokuwa, Bruno aliposikia hivyo, alichanganyikiwa, hakuamini kama mpenzi wake alitoroka mikononi mwa watu hao na hivyo kuanza safari ya kuelekea Tanga. Hakuwa akienda peke yake, aliwasiliana na polisi na kuwaambia kila kitu kilichotokea kwamba mpenzi wake alikuwa salama kabisa nchini Kenya hivyo alitakiwa kwenda huko na kumchukua. Njiani, Bruno alikuwa na presha kubwa, moyo wake ulikuwa umekwishakata tamaa na alihisi kabisa kwamba huo ungekuwa mwisho wa kumuona mpenzi wake huyo akiwa mzima, kitendo cha kumwambia kwamba aliwatoroka watu wale kilimfanya kuwa na furaha kupita kawaida. “Ila kawatoroka kweli au wanamtumia ili kunipata mimi?” alijiuliza Bruno, upande wake mwingine ulionekana kuwa na wasiwasi. “Haiwezekani! Kama ingekuwa wanamtumia, wangemwambia aniambie niende peke yangu,” alijijibu. Polisi hao wa Kenya walichokifanya ni kuwasiliana na polisi wa Tanzania kupitia Interpol na kuwaambia kile kilichokuwa kikiendelea. Wao, yaani polisi wa Tanzania walitakiwa kwenda mahali alipokuwa Sharifa na kumchukua lakini baada ya Bruno kuambiwa hivyo, hakutaka kabisa hilo litokee, alichohitaji ni kwenda yeye mwenye mpaka alipokuwa mpenzi wake na kumchukua. Baada ya saa kadhaa, wakafika Tanga. Akampigia simu Sharifa ambaye alimpa mwenyeji na kumuelekeza mahali nyumba yake ilipokuwa. Kutoka hapo walipokuwa mpaka kulipokuwa na nyumba hiyo hakukuwa mbali sana kwani ni mwendo wa dakika ishirini kwa gari wakawa wamekwishafika. Wakamkuta mwenye nyumba nje, wakamfuata na yeye kuanza kuwapeleka ndani ambapo huko Bruno akakutana na Sharifa, kwa furaha aliyokuwanayo, akamsogelea na kumkumbatia. “Walitaka kuniua,” alisema Sharifa huku akilia, alikuwa amekumbatiana na Bruno tu. “Wasingeweza. Nipo pamoja na wewe, kukumaliza wewe inamaanisha walihitaji vita na mimi,” alisema Bruno huku akiwa amemkumbatia mpenzi wake huyo. Wakamchukua na kuanza safari ya kurudi Mombasa. Njiani, kila mmoja alionekana kuwa na furaha, mioyo yao ilifurahia kuungana tena kwa mara nyingine tena. Baada ya saa kadhaa wakafika Mombasa ambapo huko, kitu cha kwanza kilikuwa ni kwa Bruno kuwasiliana na akina Gilbert na kuwaambia kile kilichotokea na hivyo kukutana na kuzungumza. Wao wenyewe walifurahi lakini bado walionekana kuwa na hofu na usalama wa maisha ya Bruno. Walijua kabisa kwamba kama lengo la kumteka Sharifa lilikuwa ni kuhakikisha kwamba Bruno haendi nchini Marekani basi ingekuwa ni lazima watu hao wafanye jambo lolote lile kuhakikisha mwanaume huyo hatoi ushahidi katika kesi hiyo. “This is not the end,” (huu si mwisho) alisema Gilbert huku akimwangalia Bruno. “What do you mean,” (unamaanisha nini?) “They are going to look for you,” (watakutafuta) “And kill me?” (na kuniua?) “That what they want. Bruno, we have to take you to USA by ourselves,” (Hicho ndicho wanachokitaka. Bruno, tutakupeleka Marekani sisi wenyewe) alisema Gilbert. Hicho walichokifanya, baada ya siku mbili wakaanza safari ya kuelekea nchini Marekani. Kwa kuwa walikuwa na uhitaji wa kuwapata watu hao, hawakutaka kujionyesha, ilikuwa ni lazima na wao wajifanye abiria ili iwe rahisi kwao kufanikiwa kwa kile walichokuwa wakikitaka. Ndege ilichukua saa zaidi ya ishirini angani na ndipo ikaanza kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JFK. Abiria wakaanza kuteremka akiwemo Bruno. Walitembea kwa mwendo wa taratibu kuufuata mlango uliokuwa ukielekea katika jengo la uwanja huo. Hakuonekana kuwa na hofu hata kidogo, alijiamini mpaka alipochukua begi lake lililokuwa limechunguzwa na kuanza kutoka nje ya jengo lile. Alipofika, harakaharaka mwanaume mmoja akamfuata na kumwambia kwamba alikuwa dereva teksi ambaye alitumwa na mwanaume aliyeitwa Todd kwa lengo la kumpokea. “Alikuagiza?” aliuliza Bruno. “Ndiyo! Au nimekuchanganya?” “Ni mimi! Nilidhani ungekuwa na bango lililokuwa na jina langu,” alisema Bruno huku akiachia tabasamu pana. “Hapana! Alinionyeshea picha yako. Karibu,” alisema mwanaume huyo huku akimpa mkono, wakaanza kuifuata teksi iliyokuwa maeneo hayo. Bruno akaingia ndani ya teksi ile, hakuonekana kuwa na hofu hata kidogo, aliamini maneno aliyoongea mwanaume yule kwamba alitumwa na mzee Todd kwenda kumchukua hapo uwanjani. “Ni mara yako ya kwanza kufika hapa?” aliuliza mwanaume huyo. “Ndiyo! Ni mara yangu ya kwanza, nimekuja kutoa ushahidi kwenye kesi yake kisha nitarudi Kenya,” alijibu huku tabasamu likiwa usoni mwake. “Ooh! Sawasawa! Nadhani atafurahi sana akisikia umefika salama,” alisema dereva, safari ikawa inaendelea kama kawaida.
Tim na wenzake wakajipanga vilivyo, ilikuwa ni lazima Bruno atekwe uwanjani na kupelekwa sehemu kwa lengo la kuuawa na kisha mwili wao kuutupa. Hilo likapangwa na hivyo kuanza kumtafuta dereva ambaye walimwambia kuwa ingekuwa vizuri kama angekwenda uwanjani hapo na kumchukua Bruno na kujifanya kwamba alikuwa ametumwa. Siku ilipofika, Tim akaenda na dereva huyo mpaka uwanja wa ndege, akachukua namba yake ya simu na wakati abiria wanatoka ndani ya jengo la uwanja huo, alikuwa akizungumza naye na alipomuona Bruno, akamwambia kwamba alikuwa mwenyewe na ndipo dereva huyo alipoanza kumfuata. Alifuatilia kila hatua mpaka alipoingia ndani ya teksi na kuanza safari ya kuondoka mahali hapo. Mipango yao ilikuwa ni kwenda katika jengo moja lililokuwa hapohapo New York. Hawakuchukua muda mrefu, wakafika, dereva akasimamisha gari, hapohapo akateremka na Kelly na mwenzake, Adson kutokea na kuanza kuifuata teksi ile, walipoifikia, wakaufungua mlango na kumtoa kwenye gari. “What is going on?” (nini kinaendelea?) aliuliza Bruno huku akionekana kushangaa. “Shiiiiiiiiii!” alimnyamazisha Kelly huku akiwa na kipande cha nondo mkononi mwake. Wakambeba na kuondoka naye, wakamuingiza ndani ya jumba hilo, kitu kilichokuwa kikitakiwa kufanywa haraka ni kumuua na kisha kuuacha mwili wake hapohapo na wao kuondoka. “Don’t kill me, please,” (tafadhai, msiniue) alisema Bruno lakini hakukuwa na mtu aliyejali, kila mmoja alichokuwa akikihitaji mahali hapo ni kuona mwanaume huyo akifa haraka sana. *** Gilbert na wenzake walikuwa wakifuatilia kila kitu, waliteremka kutoka ndani ya ndege huku wakimwangalia Bruno, walikuwa makini naye na waliamini kwamba kwa namna moja ama nyingine ilikuwa ni lazima watu wamfuatilie kwa sababu kile alichokuwa akienda kukifanya nchini Marekani kilionekana kuwa kitu hatari. Waliingia ndani ya jengo la uwanjani hapo huku wakiwa pamoja naye, walijifanya abiria na ilikuwa vigumu kwa watu wengine kugundua kwamba watu hao walikuwa pamoja kwani walijitenga naye kupita kawaida. Walipofika nje, wakamuona akiongea na dereva teksi, kwa jinsi walivyoongea, walionekana kama watu waliokuwa wakifahamiana, akaambiwa aingie ndani ya gari, akafanya hivyo. Gilbert na wenzake hawakutaka kuchelewa, walikuwa na uhakika kabisa kwamba dereva teksi yule alikuwa ametumwa hivyo kuanza kuifuatilia teksi ile. Walikuwanayo kwa umakini kabisa, hawakutakiwa kuwa na presha yoyote ile, ila walitakiwa kuwa makini kwa kuwa kama wangekosea hatua moja basi Bruno angeweza kuuawa. Waliifuatilia teksi ile mpaka ikafika mahali fulani, nje ya nyumba moja, kwa jinsi walivyoangalia huku na kule, haikuwa vigumu kugundua kwamba eneo hilo lilikuwa la hatari sana, wakazima taa za gari lao na kisha kulisimamisha kwa mbali kidogo huku macho yao yakiwa katika teksi ile iliyokuwa imesimama. “Tufanye nini? Tupige risasi?” aliuliza Putt. “Hapana! Subiri kwanza!” alisema Gilbert. Hapohapo wakamuona Kelly akielekea ilipokuwa teksi ile, akaufungua mlango huku akiwa na kipande cha nondo. Hakuwa peke yake, alikuwa na Adson ambapo wakambeba Bruno na kuingia naye ndani ya jumba lile. “Tuwafuate?” aliuliza Bull. Wakati wakiwa wamejiandaa, wakashtuka kuliona gari jingine likifika mahali hapo, mlango ukafunguliwa na mwanaume mmoja kuteremka. Alikuwa Tim ambaye alikwenda uwanja wa ndege kuhakikisha kwamba Bruno anakamatwa. Alipofika maeneo yale, akasimamisha gari na kuteremka, naye akaingia ndani ya jumba lile. Haraka sana Gilbert na wenzake wakateremka na kuanza kuelekea lilipokuwa jumba lile. Walikuwa na bastola mikononi mwao ili kuhakikisha wanafanya mauaji pale ambapo ingewabidi kufanya hivyo. Walipofika katika dirisha la jumba lile wakaanza kuchungulia ndani. Wakawaona vijana wale wakiwa wamemuweka Bruno chini tayari kwa kuanza kumpiga. Hawakuwa na bunduki, kama kumuua ilikuwa ni lazima wafanye hivyo kwa kutumia vipande vya nondo walivyokuwanavyo. Kilichotokea ni kuanza kumshambulia Bruno na vipande vya nondo walivyokuwanavyo. Gilbert na wenzake walikuwa wakiangalia na kila walipotaka kuingia, Gilbert alikuwa akiwazuia kwa kuwaambia kwamba hawakutakiwa kuwa na presha hata kidogo. “Watamuua!” alisema Putt huku akionekana kuchanganyikiwa. “Tunakusanya ushahidi, subiri!” “Tunakusanya ushahidi?” “Ndiyo! Subiri!” Bruno alizidi kupigwa na vipande vya nondo ile mpaka akawaida hoi. Wakati wakijiandaa kummalizia, haraka sana Gilbert akanyoosha mkono wake uliokuwa na bastola, zilitoka risasi tatu mfululizo, kila mtu akapigwa, wakaanguka chini. Gilbert na wenzake wakatoka kule walipokuwa na kuingia ndani, wakawafuata wanaume wale, wote watatu walikuwa chini wakiugulia maumivu, Gilbert hakutaka kuchelewa, hapohapo akawapiga risasi za vichwa Adson na Tim kisha kumuacha Kelly akiwa peke yake huku akiugulia maumivu. Wakamshika Bruno pale alipokuwa, alikuwa amepasuliwa, alipigwa vibaya, hawakutaka kumuacha, wakamchukua na kumpeleka ndani ya gari huku wakiwapigia simu polisi na kuwaambia kwamba walitakiwa kuelekea katika jumba lile kuchukua maiti za waharifu ambao waliwashambulia kwa risasi. “Na huyu?” aliuliza Putt huku akimaanisha Kelly. “Tunaondoka naye!” Japokuwa alikuwa na maumivu makali, hawakutaka kujali, walimchukua kwa kumshika hovyohovyo mpaka ndani ya gari na kuliondoa mahali hapo. Njiani Kelly alikuwa akilia, alisikia maumivu makali katika paja lake la kulia, damu zilikuwa zikimtoka lakini hakukuwa na mtu yeyote aliyejali. Walimchukua mpaka hospitalini na kumtaka kutibiwa huku akiwa chini ya ulinzi mkali. Kwanza risasi ikatolewa na kuendelea na matibabu mengine. Wakati huo, pia Bruno alichukuliwa na kupelekwa katika chumba kingine na madaktari kuambiwa kwamba walitakiwa kuhakikisha mwanaume huyo anapona haraka iwezekanavyo kwa kuwa walikuwa na kazi naye. Wakati hayo yote yakiendelea, mzee Todd alikuwa selo, kama kawaida yake alikuwa akilia mno, moyo wake ulimuuma kwa kuwa aliona kama Bruno alimsaliti kwa kile kilichokuwa kikiendelea. Hakupokea taarifa yoyote ile, moyo wake uliumia kwani miongoni mwa watu aliokuwa akiwaamini alikuwa Bruno, na yote hiyo ni kwa sababu alikuwa naye kwa kipindi kirefu na hata kumpa kiasi kikubwa cha pesa. Siku zikaendelea kukatika, baada ya siku ya kusikiliza tena kesi hiyo kwa upande wa mashahidi ilipofika, Bruno akachukuliwa na kupelekwa mahakamani huku akiwa amefungwa bandeji katika sehemu kubwa kichwani mwake kwani alikuwa amejeruhiwa mno. Watu wengi hawakujua sababu ya mwanaume huyo kufika mahakamani, wengi walihisi kwamba inawezekana alikuwa na kesi kama watuhumiwa wengine ambao walikuwa wakifika hapo huku wakiwa wamejeruhiwa. Baada ya dakika kadhaa, gari lilobeba watuhumiwa ambao walitakiwa kusimama kizimbani na kujibu mashtaka yao wakafika mahali hapo. Haraka sana waandishi wa habari wakaanza kusogea na kuanza kupiga picha. Mtu waliyekuwa wakimtaka alikuwa mzee Todd, waliihitaji picha yake mno kwa kuwa ndiye mtu aliyekuwa akijulikana kuliko wote ambao walikuwa wakifikishwa mahakamani katika kipindi hicho. Kwa kumwangalia tu isingekuwa vigumu kugundua kwamba moyo wake ulivunjika nguvu, mwili wake ulipungua kwa sababu ya kuwa na mawazo mengi. Alikuwa akiifikiria familia yake lakini pia aliifikiria kesi hiyo ambayo ilikuwa ikimuelemea. Akaingia ndani, akawekwa katika kiti kimoja na kuambiwa kutulia hapo. Hakujua kama Bruno alikuwemo mahakamani, alichohisi ni kwamba alikuwa amesalitiwa na mwanaume huyo. Wakili wake alikuwa mbele kabisa, yeye mwenyewe alionekana kuwa na hofu moyoni mwake, kila alivyokuwa akiiangalia kesi ile alikuwa na uhakika kwamba mteja wake angeshindwa kesi ile. CIA walifanya kila kitu kwa siri kubwa, hakukuwa na mtu aliyetakiwa kujua kilichokuwa kikiendelea kuhusu mashahidi kwani walimficha Bruno kwa nguvu zote na ndiyo maana hata mzee Todd hakuambiwa kitu chochote kile, alitakiwa kumuona Bruno kwa kushtukiza mahakamani hapo. Hakimu alipokuwa akiingia, watu wote wakasimama kama kumpa heshima na alipokaa, wakakaa na kutulia. Kesi ikaanza, kama kawaida ikaanza kusomwa kwa dakika chache, ilipoanzia mpaka siku hiyo ambapo mashahidi walitakiwa kusimama na kusema kile kilichokuwa kimetokea. “Shahidi namba moja anaitwa Bruno,” alisema hakimu, mzee Todd akashtuka kulisikia jina hilo, alikuwa ameinama, akauinua uso wake. Akamuona mwanaume mmoja akisimama na kuanza kuelekea kizimbani, kwa kumwangalia tu ilikuwa ni rahisi kugundua kwamba alikuwa kwenye maumivu makali, alitembea kwa msaada wa Gilbert ambaye alikuwa pembeni yake na kumpeleka mpaka kizimbani. Kila mtu aliyekuwa mahali pale alikuwa akishangaa, hawakumjua mwanaume huyo, alikuwa amezungushiwa bandeji, na kwa usoni yalionekana macho tu kwani alikuwa amejeruhiwa vibaya. Akanyoosha mkono wake wa kulia na kisha kujitambulisha na kuiambia mahakama kwamba kila kitu ambacho angekwenda kukizungumza mahali hapo kilikuwa cha kweli kabisa na asingezungumza uongo hata kidogo. “Naitwa Bruno Mike Onyambe!” alijitambulisha na mahakama kuanza kusikiliza ushahidi wake. Alianza kusimulia kila kitu baada ya yeye kutoswa ndani ya maji na baadaye kuokolewa na watu waliokuwa katika meli ambayo aliikumbuka kwa jina lake, iliitwa Britannian Cargo P56 kwani iliiandikwa ubavuni. Mule ndani, akaepelekwa ndani ya chumba ambacho akakutana na mzee huyo akiwa amefungwa huko na hivyo kuanza kuzungumza. Hakutaka kuishia hapo, alisimulia kila kitu mpaka mzee huyo alivyokuwa akitafutwa na vijana ambao walipokea maelekezo kutoka nchini Marekani na hata wakati familia yake ilipokuwa ikiuawa, walikuwa Afrika Kusini na waliiona taarifa hiyo kwenye televisheni. “Hakukuwa na kipindi kigumu kwa mzee Todd kama kipindi hicho. Alilia sana, hakuamini alichokuwa akikiona, iliniumiza sana moyoni mwangu, kwa nilivyokuwa nikimwangalia, niliyaona mapenzi yake makubwa aliyokuwanayo kwa familia yake. Mara nyingi aliniambia kitu kimoja tu kwamba kuna mtu anaitwa Maxwell ndiye aliyekuwa amesababisha yote hayo, alitaka kumuona akiingia gerezani ili afanye biashara zake kwa uhuru zaidi,” alisema Bruno, mahakama nzima ilikuwa kimya. Alitumia dakika arobaini na tano, alipomaliza, akashuka kizimbani. Mzee Bruno alikuwa akilia, hakuamini kilichokuwa kikitokea. Ushahidi wa Bruno ulimkumbusha mbali kabisa, ulimkumbusha familia yake na mateso makubwa aliyoyapata alivyokuwa ndani ya meli. Alipomaliza, akanyamaza. Akaanza kuulizwa maswali kutoka upande wa jamhuri na kila alipokuwa akiulizwa, alijibu kama ilivyokuwa ikitakiwa. Alipomaliza, akateremka na kisha hakimu kusema kwamba kulikuwa na ushahidi kutoka CIA ambao ulikuwa ni wa kina kwa kuwa ulifuatiliwa kwa hatua zote. Akaanza kuusoma ushahidi huo ambao ulieleza mambo mengi kuhusu mchezo ulivyokuwa na moja kwa moja ulikuwa ukimuweka hatihani mzee Maxwell. “Vijana walifuatilia kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Ni kweli mzee Maxwell alikwenda Afrika, alipofika huko, akatekwa na kuingizwa katika meli iitwayo Britannian Cargo P56 ambayo ina usajili wa jina la Maxwell anayemiliki kampuni kadhaa nchini Marekani,” ulisema sehemu ya ushahidi huo na kuendelea: “Nchini Afrika Kusini kulikuwa na kijana aliyekuwa akishirikiana naye, huyu aliitwa Xuso ambaye aliuawa siku chache zilizopita. Pale bandarini, Pretoria ndipo alipotaka kumalizia kazi yake kwani aliamini kuwa endapo angemuua Todd pale ingekuwa ni rahisi kwao kuupoteza mwili huo kwa kuwa walikuwa na watu wengi.” “Walifanikiwa kwa kila kitu. Baadaye baada ya kugundua kwamba mzee Todd amekamatwa, alichokitaka ni kupoteza mashahid, hapa tunapoongea, kijana ambaye alikuwa karibu na Todd, Innocent, ameuawa na tulivyofuatilia tukagundua kwamba kijana huyo alianza kuweka ukaribu na Maxwell na alihusika katika kuweka madawa ya kulevya ndani ya nyumba ya Todd.” “Yeye alifanikisha kutekwa kwa familia ya Todd, alihakikisha anashirikiana nao kwa ukaribu lakini waliposikia kwamba naye alitakiwa kuwa shahidi, wakamuua na mwili wake kuutupa baharini.” “Bruno ambaye ni raia wa Kenya alipitia vikwazo vingi. Kwanza hakutakiwa kufika Marekani kwa kuwa Maxwell alijua kwamba mtu huyu alikuwa mwiba hatari sana. Wakamteka mchumba wake ili baadaye atishwe kwamba angeuawa kama tu angekanyaga nchini Marekani, bahati nzuri baadaye msichana yule alitoroka walipofika nchini Tanzania.” “Hiyo haikutosha, wakapanga mipango wamteke uwanjani, walifanikiwa ila kwa kuwa maofisa wetu ni watu hatari, walifanikiwa kumuokoa katika mikono yao na kuwaua vijana wawili na kumbakiza mmoja,” ulisema sehemu ya ushahidi huo.
Mahakama nzima ilikuwa kimya ikisikiliza ushahidi uliotolewa na Shirika la Kijasusi la CIA. Kila mtu alikuwa makini kusikiliza, kile ambacho kilizungumzwa mahali hapo kilionekana kumshangaza kila mmoja. Baada ya kutolewa kwa ushahidi huo mrefu ambao ulichukua saa moja, ndipo mahakama ikasimamishwa kwa muda kwani baraza la wazee lilitakiwa kulizungumzia jambo hilo kabla ya kutoa uamuzi wa kukamatwa kwa Maxwell. Muda huo mzee Todd alikuwa akitokwa na machozi ya uchungu, hakuamini kile alichokiona kikiendelea, mbali na Bruno, hata CIA walikuwa upande wake kumtetea kwa kila kitu kilichokuwa kimetokea. Alitamani kusimama na kumfuata Bruno na kumkumbatia kwani kwake, alikuwa mwanaume shujaa ambaye alimtetea mpaka pumzi ya mwisho kabisa. Baraza hilo la wazee lilikaa kwa nusu saa nzima ndipo likatoka na mahakama kuendelea. Kitu cha kwanza kabisa kilichoamuriwa na mahakama ni kuachwa huru kwa mzee Todd lakini vilevile Maxwell alitakiwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani huku akitakiwa kusomewa mashtaka ya kushiriki katika mauaji ya familia ya mzee Todd na hata kifo cha Innocent. Kesi ilipofungwa, mzee Todd akamsogelea Bruno na kumkumbatia, hakuamini kama alishinda kesi hiyo ambayo iliibua chuki kubwa mioyoni mwa Wamarekani kwa kuwa waliamini kwamba aliua na kukimbia nchini humo. Akamshukuru sana kiasi cha kutokwa na machozi, walizungumza kidogo na kisha kuondoka ndani ya mahakama hiyo huku Bruno akiwa chini ya ulinzi mkali kwani hakukutakiwa kuachwa hata kidogo kwa ajili ya usalama wake. Siku hiyohiyo Maxwell akakamatwa na siku iliyofuata kupelekwa mahakamani. Kesi yake ilikuwa nzito na iliyonguruma kwa miezi miwili na mwisho wa siku kukutwa na hatia na kuhukumiwa kifo kwa kuchomwa sindano ya sumu ya cynaide. Kwa Bruno, aliendelea kutibiwa hospitalini nchini Marekani huku akiwa chini ya ulinzi mkali. Hakukutakiwa mtu yeyote kuingia ndani ya chumba chake zaidi ya daktari, mzee Todd na Sharifa ambaye alisafirishwa mpaka Marekani kwa ajili ya kumuona mpenzi wake. Mzee Todd hakuacha kumshukuru Bruno, kwake, mwanaume huyo alionekana kuwa mkombozi aliyemuokoa katika mdomo wa kifo, hakutaka kumuacha hivi hivi kwani hata alipopona, akamuingizia kiasi cha dola bilioni moja kwenye akaunti yake ambapo kwa pesa za Kitanzania ilikuwa ni zaidi ya shilingi trilioni mbili. Maisha ya Bruno yakabadilika, alikuwa masikini, aliyedharauliwa lakini mwisho wa siku alikuwa bilionea aliyeheshimika sana nchini Kenya. Hakuacha kuwasiliana na mzee huyo, kwake, alikuwa kama baba yake kwani ndiye mzee ambaye alikaa naye kwa kipindi kirefu na kumfundisha maisha kuhusu umiliki wa pesa, biashara na mambo mengine mengi. Baada ya miezi tisa kutimia, hatimaye Sharifa akajifungua mtoto wa kike na kumpa jina la Grace, yaani Rehema akiwa na maana kwamba kwa kile alichokuwa nacho, maisha aliyokuwa akiishi ni kama alipewa rehema tu kutoka kwa Mungu wa mbinguni. Kutoka katika maisha ya dhiki, kuishi katika kijumba kibovu alichoachiwa na wazazi wake mpaka kuishi kwenye bangaloo kubwa, hakika ilikuwa ni ndoto moja ya kusisimua kupita kawaida. “Kila kitu kilipangwa na Mungu. Mtu wa kwanza kumshukuru ni baba yako, bila yeye, nisingekutana na mzee Todd, bila yeye nisingekuwa hapa nilipokuwa,” alisema. Aliendelea kufungua kampuni nyingi, kwa kuwa aliamua kuwekeza kwenye uvuvi pia, akanunua meli kubwa iliyokuwa ikisafiri mbali kwenda kuvua huku akimuweka Abdul kuwa kiongozi lakini pia hakuangalia ubaya, akamchagua James na mwenzake ambao ndiyo waliomtosa baharini na kuwapa vyeo kwa kuamini kwamba pia watu hao wawili walichangia kuyabadilisha maisha yake. Hakuangalia kisasi, alisahau kila kitu, nguvu ya upendo ilikuwa na uwezo wa kubadilisha kila kitu, hicho ndicho alichokikumbuka ambacho alihubiriwa mara kwa mara kanisa “Upendo unapozidi, kisasi kinakufa, namshukuru Mungu kwa kuyabadilisha maisha yangu na kuniweka hapa. Tulimuomba Mungu sana siku moja tuishi pamoja, na hapa tunaishi pamoja, siku si nyingi kuanzia leo tutafunga ndoa,” alisema Bruno huku akimwangalia Sharifa. “Nakupenda sana, nakupenda zaidi kwa kuwa umekuwa mtu wa msamaha kwa kila aliyekutendea ubaya,” alisema Sharifa. “Hilo ndilo ambalo Mungu anatuagiza kila siku. Tunatakiwa kusamehe hata kama tulikasirishwa na kupata maumivu makubwa kiasi gani,” alisema Bruno, hapohapo akamkumbatia mpenzi wake huyo na kujifunika shuka, kilichoendelea, hakifai kuandikwa mahali hapa.
Usingizi uligoma kabisa, alijigeuza upande huu, akarudi upande ule, hali ikabaki ileile usingizi kumgomea.Hakuona sababu ya kuendelea kuteseka, alimgeukia mama Zainath, na kumgusa mabegani kwa mara nyingine tena.
“Nimesema niache!, sitaki, kwa leo sijisikii, labda siku nyingine “,mama Zainath alifoka kwa hasira.
“Sawa mke wangu, unayosema ni sahihi kabisa, lakini……”,
Raisi Jonsoni Mtemvu alijitetea,lakini mke wake aliendelea kusimamia msimamo wake wa kutokidhi haja za mume wake. Alijifunika shuka, na kuuchapa usingizi.
Bwana Jonsoni Mtemvu, raisi kijana kabisa,moyo wake ulikata tamaa ya kupata penzi la mke wake kwa usiku huo, alitazama saa yake ya mkononi, saa ya dhahabu ambayo aliinunua kwa mamilioni ya pesa.
“Saa tatu na nusu! bado mapema sana, kanikomoa na mimi namkomoa mara mbili zaidi, “raisi aliongea, huku akionekana kufikilia jambo. Akiwa na nguo ya kulalia, alishuka kitandani, akatembea hatua chache kulisogelea kabati lake, kabati ambalo lilisheheni suti za bei kali, suti ambazo zilimtofautisha yeye pamoja na wananchi wake.
“Hii itanifaa, lakini ngoja nimpigie bwana Januari Sasamba, anipe mwongozo! bila hivyo usiku huu utakua mrefu kwangu ……”,Jonsoni Mtemvu alizungumza peke yake, bila mke wake kutambua. Mkono wake wa kulia ulizama mfukoni na kutoka na simu, iPhone7 ilisomeka kwenye kioo cha nyuma.
Alibonyeza namba kadhaa, bila shaka alikuwa akiitafuta namba ya mtu huyo. Waziri January, namba ilisomeka kwenye sehemu ya majina. Alibonyeza sehemu ya kupiga, kisha akaisogeza simu yake katika sikio lake la kulia.
“Kulikoni mheshimiwa, mbona usiku usiku! “,sauti ilisikika upande wa pili, baada ya kupokelewa.
“Usiku una mambo mengi ndugu, anyway! naomba unijibu haraka sana ujumbe wa sms ninao kutumia “,mheshimia Jonsoni Mtemvu, raisi wa nchi ya Goshani aliongea. “Sawa boss, nitafanya hivyo! “,upande wa pili wa simu ulizungumza, kisha simu ikakatwa, na kumuacha na shauku kubwa ya kutaka kufahamu ni nini ambacho kilimfanya mkuu wake wa kazi, raisi Jonsoni apige simu wakati wa usiku, tena mida ya kupumzika!
“Samahani waziri na rafiki yangu kipenzi,mke wangu kanigomea na ninataka kukidhi haja zangu, wewe ni rafiki yangu na hatufichani kwa chochote kile, nahitaji msaada wako. “,ujumbe wa meseji uliingia kwenye simu ya waziri Januari Sasamba, waziri mkuu wa nchi ya Goshani, cheo ambacho alikipata kwa kuteuliwa na rafiki yake ambaye walisoma wote chuo kimoja, chuo kikuu cha “Goshani university “,miaka kumi iliyopita.
“Kazi ndogo sana,sijawahi kukuangusha, ngoja nikusaidie bila hivyo unaweza kujikuta umembaka mkeo …”,mheshimiwa January Sasamba alizungumza peke yake, aliwasha data, akaingia katika ukurasa wa instagram, macho yake yakaishia sehemu ya kutafuta jina la mtu unayemuhitaji.
“Changudoa Goshani”,aliandika, kisha akabonyeza kitufe cha kuruhusu kutafuta mtu anayetumia jina hilo. Msururu wa majina ulitokea, macho yake yakaishia kwenye jina la kichina, Yuan Liang, akiwa na shauku ya kutaka kujua mengi kuhusu jina hilo, akaenda kwenye taarifa zote kuhusu ukurasa huo.
“Yuan Liang,chinese girl, Living in Goshani, self employed as a prostute, call; 0248698653”,(Yuan Liang,binti wa kichina,nimejiajiri kama malaya,piga;0248698653) ,
Macho ya mheshimiwa Januari yalimtoka,mapigo ya moyo yakaongezeka,moyo ukamjaa tamaa.Hakuamini kama kuna mtoto mzuri na mrembo kiasi kile,isitoshe raia wa kigeni,anajiuza katika nchi ya Goshani.Haraka haraka alikopi namba ya Yuan Liang,akaenda upande wa meseji ,na kuanza kulitafuta jina la mheshimiwa raisi.
“Raisi Jonsoni”,jina lilisomeka,bila kuchelewa alimtumia ujumbe,kisha akaendelea na shughuli zake za kutazama mpira,starehe ambayo aliipenda kwani alikuwa bado hajaoa,licha ya kuwa na cheo kikubwa nchini Goshani.
“Huyu mwanamke mbona simfahamu,siku zote nachukua wanawake lakini sijawahi kukutana naye?,mchina kweli anaweza kuwa maskini kiasi hiki,tena ajiuze katika nchi maskini,nchi ambayo hawezi kupata mteja wa kumlipa dola kumi kwa usiku mmoja?anyway,ngoja nijue mwisho wake,mkuu akifanikiwa,nitamfahamu tu binti huyu
“, akiwa mwenye mawazo,waziri mkuu bwana Januari Sasamba aliendelea kunywa wisky taratibu,huku macho yake yakiwa bize kufuatilia mpira kati ya Real Madrid na Livrpool,fainali ya ligi ya mabigwa barani Ulaya.
…………………………………
“Ni msichana mrembo wa kichina,anaitwa Yuan Liang, yuko hapa Goshani,kwa mawasiliano 0248698653,kazi kwako mkuu,usiku mwema!”,ujumbe wa sms ulisomeka,katika simu ya mheshimiwa raisi,bwana Jonsoni Mtemvu kutoka kwa waziri Januari Sasamba.
Akiwa amepigilia suti nzuri ya kifahari,suti iliyopambwa kwa mistari ya kupanda na kushuka,alitoka nje bila kumsemesha mke wake,huku mapigo ya moyo wake yenye uchu wa kingono yakienda kasi.
“Mkuu unahitaji ulinzi?,safari ya wapi?”,kamanda mkuu,kamanda aliyeongoza jopo la walinzi katika ikulu ya raisi aliongea.
“,Makamanda wawili wanatosha,naelekea Serena hoteli kuna mtu muhimu nahitaji kuzungumza naye”,mheshimiwa Jonsoni Mtemvu alizungumza huku akiwa bize na simu yake.
“,Nipo afande,”inspekta mwenye bunduki kubwa ya smg aliitikia.
“,Inspekta Junior”,kamanda mkuu aliita tena.
“,Nipo afande” ,inspecta mwingine mwenye bastola kiunoni aliitikia.
“Hakikisheni usalama wa raisi,kazi ikiharibika ,kifungo au kunywongwa halali yenu…”,kamanda mkuu aliongea,huku sura yake ikiwa haioneshi utani hata kidogo.
“,Sawa afande,tuna ahidi atarudi salama,kibaya kikitokea tunakubali kufa au kunyongwa”,inspecta Amiry pamoja na inspecta Junior waliitikia.
“,Nafurahi kuskia hivyo,kazi njema”,kamanda mkuu aliongea,huku vijana wake wakitembea kwa ukakamavu kulisogelea gari la kifahari aina ya V8,gari ambalo mheshimiwa raisi alikwisha pakizwa ndani yake.
…………………………………
Green pick hotel; 10;30pm
Mikono yenye uzoefu mkubwa wa kuchezea kompyuta, ilikuwa bize kucheza na kompyuta ya kifahari, maarufu kama “macboock air “,kioo cha kompyuta kilionesha watu mbalimbali duniani, watu ambao waliibiwa vitu vya thamani kisha kuuawa kikatili.
“Nina masaa arobaini na manne ya kuishi hapa Goshani,kwa sasa ninapaswa kwenda China nikafahamu ukweli kuhusu wazazi wangu,kwani pesa tayali nimekusanya ya kutosha “,msichana mrembo,aliyeimudu vizuri lugha ya Kiswahili,lugha maarufu Afrika mashariki,aliongea huku akitazama kompyuta yake yenye matukio mbalimbali ambayo amekwisha yafanya.
“Ndrii,ndrii!ndrii!ndriii!”,mlio wa simu ulisikika.
“Nani tena huyu,meseji za nini usiku huu nimechoka!,kama ni kazi yenye pesa za madafu sifanyi mimi siku ya leo…”,msichana mrembo wa kichina aliongea,huku akinyanyuka kutoka kwenye kitanda alipokuwa ameketi,na kuisogelea simu yake juu ya meza.
“Aim president Jonsoni Mtemvu,the president of Goshani ,i want to be with you this night, i promise to pay u well…”,(Mimi ni raisi Jonsoni Mtemvu,raisi wa Goshani,nahitaji kuwa na wewe usiku huu,nakuahidi nitakulipa vizuri…”,) meseji ilisomeka katika kioo cha simu,huku akisoma mara mbili mbili ujumbe huu uliotumwa kwa sms.
“Sawa mheshimiwa,nikukute wapi?”,Yuan Liang akiwa mwenye wasiwasi,huku machale yakimcheza,alijibu meseji bila kuchelewa,huku mapigo ya moyo wake yakimuenda mbio.
“Oooh kumbe unajua Kiswahili, Niko Serena Hotel,chumba namba 20,karibu sana “,mheshimiwa raisi, bwana Jonsoni Mtemnvu alijibu ujumbe wa sms.
“Dakika kumi nitakua hapo, sasa hivi ni saa nne na nusu, saa nne na dakika arobaini nitakua hapo, onyo!! polisi wakae umbali wa mita tano na eneo la chumba …”,Yuan Liang aliandika ujumbe wa sms wenye masharti mazito ndani yake, kisha haraka haraka alianza kujiandaa kwa ajili ya kazi.
“Nimeshawaibia watu wa kubwa duniani na kuwaua, leo naenda kufanya historia nyingine, nachohitaji ni pesa tu, ukahaba ni kuficha uhalisia tu, ole wake avunje masharti, atakufa yeye na ukoo wake, ikiwezekana serikali yote, watakufa! “,kwa malingo, mwanadanda mrembo sana, mwenye asili ya kichina, aliongea huku akiivaa sura ya bandia usoni mwake.
Alichukua mkanda wake, mkanda wenye visu vidogo vidogo takribani ishirini na kuupachika kiunoni mwake, kisha alivaa koti kubwa na jeusi, mkononi alivaa gloves nyeusi, zenye sindano ndogo ndogo zisizo onekana kwa macho ya kawaida. Mguuni alivaa kiatu chenye kisigino, kisigino kilichofungwa kifaa kidogo maalumu kwa ajili ya kukata mawasiliano ya simu pale kitakapotumika kwa kubonyeza kibatani kilichofungwa kwenye miwani ya Yuan Liang.
“Ooooh shit! nimesahau miwani, !!ilikua kazi bure ” ,alizungumza baada ya kupiga hatua kadhaa, kisha alirudi chumbani, aliangaza huku na kule hakuona chochote kile.
Ghafla tabasamu liliipamba sura yake, miwani yake ilikua kitandani, aliifata na kuivaa, kisha alitoweka haraka sana kutoka chumbani mwake.
…………………………………
Serena hotel;. 11;00pm
“Sikilizeni vijana,kuna mgeni wangu muhimu anakuja, pesa hizi hapa, agizeni kinywaji! kuhusu ulinzi msijali sana, mgeni mwenyewe ni mwanamke, sizani kama atakua mtu mbaya kwangu, akizingua hata mimi naweza mdhibitii ……”,raisi Jonsoni alizungumza na vijana wake, umbali wa takribani mita nane kutoka chumba namba ishirini.
“Hahahaa, sawa bosi! ,sisi tupo, kuhusu kukulinda tutakua makini pia, tumekula kiapo cha kifo au kifungo kwahyo usjali …”,inspecta Junior pamoja na inspecta Amiry walicheka, huku wakiwa makini kuangaza huku na kule kudumisha ulinzi.
“Sawa vijana, asisogelee chumba mtu yoyote mpaka nitoke “,mheshimiwa Jonsoni aliongea, huku akielekea chumba namba ishirini.
“,Sawa mkuu, kuwa makini “,vijana waliitikia, huku macho yao yakimsindikiza raisi wao, raisi wa kwanza kijana kati ya watatu, tangu nchi ya Goshani ipate uhuru kutoka kwa Wachina mwaka 1994.
…………………………………
Pikipiki kubwa aina ya baja, ilipaki nje ya geti la Serena hoteli. Mtoto wa kike mwenye sura ya kizungu alishuka, kisha kuwasogelea walinzi ambao walionekana kuwa na wasiwasi sana.
“Mimi itwa Elizabeth, iko kuja Gosheni toka Uingereza, kuja ona geni wangu, wewe angalia motorcycle yangu, mimi kupa wewe dola kumi “,Yuan Liang aliongea, huku akiwa amevaa sura bandia ya kizungu.
“Sawa mzungu, karibu sana, ukihitaji chakula cha kimataifa na vyumba vya kisasa vinapatikana, pikipiki yako nitakuangalizia mpaka kesho “,mlinzi mmoja, miongoni mwa walinzi wa nne waliokuwepo getini, mlinzi mwenye tamaa ya pesa aliongea, bila kutambua kuwa mgeni anayemkaribisha alikuwa na sura ya kondoo, lakini moyo wake ulikua mubaya uliojaa ukatili kupita kiasi.. .
Serena Hotel;
Yuan Liang aliruhusiwa kuingia hotelini, hakuna mlinzi yoyote aliyekuwa na mashaka naye, alibonyeza batani kwenye miwani yake upande wa kulia, kuruhusu kifaa kilichofungwa kitaalamu kwenye kisigino cha kiatu chake kufanya kazi yake, mawasiliano ya simu yakakatika eneo lote la hoteli.
Aliangalia saa yake ya mkononi, “Saa tano na nusu! “,Yuan Liang alizungumza, akaongeza mwendo, “RECEPTION “(MAPOKEZI “) ,kibao kilisomeka katika chumba kidogo cha vioo, akasogea ili kuongea na muhudumu,
“,Welcome! tukusaidie nini? “,muhudumu wa mapokezi alizungumza.
“,Mimi iko nenda chumba namba twenty, taka ona mgeni wangu “,Yuan Liang alizungumza kwa rafudhi ya kizungu.
“,Ohooo! kumbe ni wewe, karibu sana, karibu, panda juu ghorofa ya pili, kunja kushoto, kisha kulia, utaona chumba kikubwa chenye vioo vya rangi ya dhahabu “,muhudumu alizungumza, baada ya kugundua mgeni wa raisi aliyesubiliwa kwa hamu tayali aliwasili, alinyenyua simu ya mezani, akabonyeza namba kadhaa, akaweka sikioni, “Dear customer, there is network error, try again later, “(Ndugu mteja, kuna matatizo ya mtandao, jaribu tena baadae) “,upande wa pili wa simu ulizungumza …
“,Oooh shit! hakuna mtandao, anyway! hakijaharibika kitu, nenda tu chumbani utamkuta “,muhudumu alizungumza, kwa ishara ya mkono, akamuelekeza Yuan Liang njia ya kupita kuelekea juu ghorofani.
“Kazi imefanyika! mawasiliano hakuna tena!”,Yuan Liang alizungumza peke yake bila sauti kusikika, tabasamu lilionekana usoni mwake, safari ikaanza, akapanda ngazi taratibu kwa umakini wa hali ya juu, huku macho yake yakiangaza huku na kule kuangalia kamera za ulinzi na njia za kutorokea baada ya kukamilisha kazi.
“,Sorry sister, my name is Amiry, the police inspector “,(Dada samahani, naitwa Amiry, inspecta wa jeshi la polisi) “,inspecta Amiry alizungumza.
“,My name is Junior, the police inspector “,(Naitwa Junior, inspecta wa jeshi la polisi) “,inspecta Junior alijitambulisha.
“,Mimi itwa Elizabeth, kuja ona mgeni wangu ,chumba hiyo hapo ……”,Yuan Liang alijitambulisha, mara baada ya kuzuiwa na walinzi alipojaribu kusogelea mlango wa chumba namba ishirini.
“,Ohoo! kumbe ni wewe, samahani sana bosi! tuko kazini, ni wajibu wetu, samahani kwa usumbufu ……”,inspecta Junior pamoja na inspecta Amiry waliomba samahani baada ya kutambua mwanamke huyu wa kizungu hakuwa adui, bali mgeni wa mheshimiwa raisi aliyesubiliwa kwa hamu. Walisogea pembeni, Yuan Liang akapita, baada ya hatua kadhaa, akafika mlango wa chumba, akabonyeza kengele ukutani, sekunde mbili tu, mlango ukafunguliwa, akatumbukia ndani …
…………………………………
00;00pm
Mheshimiwa raisi alikosa usingizi,pepo la ngono liliendelea kumsumbua,alitazama saa yake,muda ulikimbia,alilala kidogo,akashuka kitandani,akatembea huku na kule ndani ya chumba,akaangalia saa tena,”saa sita kamili…!,hee!au haji?,kanidanganya mwanamke huyu,nita……”,kabla hajamaliza kuzungumza,alihisi hatua za mtu kuusogelea mlango wa chumba,akatega masikio kusikiliza kwa makini.
“,tiririii!tiririi……”,mlio wa kengele ulisikika,mapigo ya moyo ya raisi yakaongezeka,furaha ikarejea tena.Akausogelea mlango,akazungusha kitasa cha mlango chini na juu,mlango ukafunguka…
“,Mpenzi,mimi penda wewe sana,leo kupa wewe penzi nzuri……”,Yuan Liang alizungumza baada ya mlango kufunguliwa,alimsogelea raisi,akamkumbatia…
Raisi Jonsoni Mtemvu alisahau kuwa mgeni aliyepaswa kuonana naye ni mchina na wala sio mzungu,huku akizungumza kiswahili kilicho nyooka.Hakuwa na hofu juu ya mwonekano mpya wa mgeni wake pamoja na kiswahili kibovu cha rafudhi ya kizungu alichozungumza mgeni wake,Jonsoni Mtemvu alihitaji penzi na wala sio kitu kingine.Alimsogelea Yuan Liang,akamkumbatia na kumtupia kitandani.
“O…oo…oo…oh”,Jonsoni Mtemvu alilalamika na kupoteza fahamu, pua na mdomo wake vilibanwa ghafla,mshipa wa fahamu ulipigwa kifuti cha mkono,pigo ambalo lilifanywa kwa sekunde moja tu,kitanda kikageuka uwanja wa mauaji…
“,Pumbavu!mnakula pesa za walalahoi,pesa zote mnanunua makahaba,kufa mpuuzi wewe!”,Yuan Liang alizungumza,huku akimsachi raisi Jonsoni Mtemvu,kwenye mifuko wapi!kwenye waleti wapi!,hakuna kitu!
“Raisi gani unatembea bila pesa!ungenilipa nini sasa?”,Yuan Liang alifoka,mkono wake ukiwa bize kukagua waleti ya mheshimiwa Jonsoni Mtemvu.
“Free of charge,special card for president” ,(Hakuna malipo,kadi maalumu kwa ajili ya raisi)”,kadi ilisomeka,kadi ya raisi iliyomuwezesha kupata huduma bure mahala popote pale.
“,Ohoo!ndio maana,kwahiyo hata mimi ulitaka unifanye bure?,stupid president!”,Yuan Liang alibwatuka,akatupilia waleti kule! kadi kule!,akachukua saa ya raisi kwenye mikono yake,akaichunguza kwa makini,akabonyeza batani mbili za saa ya kifahari kwa wakati mmoja,taa ya saa ikabadilika rangi,nyekundu!kijani,njano!,kisha ikawaka nyeukundu tena,memory card(diski) ikatoka!
“,Yes!nitajua mengi kupitia diski hii,siri zote za nchi nitazifahamu,nitapata mabilioni ya pesa!”,Yuan Liang alizungumza kwa furaha, akaitelekeza saa, akaingia chooni, akachomoa visu viwili kwenye mkanda wake, akakata kioo cha dirisha, akapenya na kuruka kwa serekasi hewani mpaka chini. ” ,Kazi imekwisha! “,Yuan Liang alizungumza, hakuna aliyemshuhudia wakati akitekeleza tukio hilo, alitoka getini, akawapatia dola ishirini walinzi, wakachekelea kwa furaha, akawasha pikipiki yake, akatokomea kusikojulikana …
…………………………………
08;00am
Taharuki ilitanda nchini Goshani, kila kona watu walikaa makundi, tukio la raisi Jonsoni Mtemvu kuibiwa na kuvunjwa shingo kiligusa hisia za wengi, huyu alisema hili, yule akasema lile.
“,Hotelini alifata nini usiku, au mikataba mibovu ya madini wanaifanyia huko eee?? “,raia mmoja aliongea.
“,Hapana! raisi huyu hana shida kabisa,anawajali wananchi na kupiga vita mauaji ya albino pamoja na ufisadi katika nchi yetu, tumwombe Mungu amjalie afya njema, japo hatujui kaibiwa nini?na walinzi walikuwa wapi? “,raia mwingine wa pili alizungumza.
“,Kweli kabisa! raisi hana shida, lakini tuache serikali ifanye uchunguzi, lazima tutafahamu kila kitu ……”,raia wa tatu alizungumza, huku mchezo wa karata ukiwa umepamba moto,miongoni mwa kundi la wazee watano waliokaa kwenye kijiwe kupata kahawa,kabla ya kuelekea kwenye shughuli zao…
…………………………………
Ikulu;9;30am
“,Jambo la kwanza,inspekta Amiry pamoja na Junior wawekwe mahabusu,bila shaka wameshiriki kwa namna moja au nyingine!jambo la pili,hakikisheni mtuhumiwa,anakamatwa!fanyeni uchunguzi,aletwe kwangu akiwa hai au amekufa,diski iliyoibiwa ina siri zote za taifa,zikiwekwa wazi,usalama wa nchi yetu utakua matatani”,raisi Jonsoni Mtemvu alitoa amri kwa askari wapelelezi,askari wa serikali ya Goshani wakiongozwa na inspekta Gupta.
Askari watano walitoka nje ya chumba cha siri,katika ikulu ya raisi,mahali ambapo matibabu ya Jonsoni Mtemvu yalikuwa yakifanyika.Mheshimiwa Jonsoni Mtemvu hakua na amani ,hofu ya maovu yake kufichuliwa ilimtawala,mikataba yote ya biashara haramu alizojishughulisha nazo ,kuuza siraha,madawa ya kulevya,kuuza viungo vya albino,mikataba yote ya biashara hizi ilirekodiwa katika saa ya mheshimiwa Jonsoni Mtemvu kwa siri kubwa,wananchi walimwamini,hawakutambua chochote kile,aliwaza ,akawazua,kichwa kikamuuma!,alijilaumu kutokuwa makini siku iliyopita,hakujua aanzie wapi kumtafuta adui yake,yote aliwaachia askari wake……
Green pick hotel; Masaa tisa nyuma ,
Pikipiki aina ya baja ilifunga breki, Yuan Liang aliwasili katika hoteli aliyoweka kambi, akakusanya kilicho chake kutoka katika chumba namba kumi na tano, “muhudumu amelala? ,funguo za chumba ataziona mezani akiamka “,Yuan Liang aliongea, akiwa na sura yake halisi ya kichina, aliweka funguo za chumba chake juu ya meza ya mapokezi, akatoweka!
Begi lake lenye kila kitu chake alilipakiza kwenye pikipiki yake,akapiga stata pikipiki yake,ikagoma kuwaka!, akapiga tena, ikakubali, akavuta moto, akaachia, ikaacha vumbi eneo lote na kuwakera walinzi wa geti la hoteli kwa moshi mzito. Alinyosha barabara kuu kuelekea nje ya jiji la Costa, kaskazini mwa nchi ya Goshani. Alidhamiria kutoka nje ya jiji, kabla raisi hajapata fahamu na kuanza kumsaka muhusika aliyemuibia na kumjeruhi.
…………………………………
Huwei; masaa sita nyuma
Pikipiki kubwa aina ya baja liliwasili mji mdogo wa Huwei, nje kidogo ya jiji la Costa,kaskazini mwa nchi ya Goshani, baada ya kumaliza masaa matatu njiani.
“,Karibu! utapata vinywaji, chumba, na starehe za kila aina mahali hapa ……”,mzee wa makamo aliongea, umri wake yapata miaka hamsini,heleni zilikua nasikioni, shingoni alivalia cheni,chini alivalia jinsi, juu akavalia tisheti iliyoandikwa jordani na kuchorwa mpira wa kikapu, bila shaka mzee huyu alipenda ujana japokuwa alikula chumvi nyingi.
“,Casabranka Casino “,kibao kilisomeka, huku taa katika kibao zikiwaka kufuatana na mdundo wa wimbo wa “sorry “ulioimbwa na mwanamuziki wa rnb Justin Bieber kutoka Amerika. Yuan Liang alipotosheka kusoma kibao, akaridhika na makazi yake mapya ya muda, kama kawaida yake siku zote, huhama kila wakati anapotekeleza tukio la wizi au mauaji.
“,Nahitaji chumba cha ghorofani, lakini dirishani! “,Yuan Liang alimjibu muhudumu yule, huku akiisogeza pikipiki yake mahali salama pa kuhifadhia magari ya wateja. Siku zote alitumia vyumba vya dirishani, vyumba rahisi kutoroka anapovamiwa na polisi.
“,Kimebaki kimoja, chumba namba therathini, kiko ghorofa ya tatu, maana ghorofa ya pili kuna ukumbi na klabu ya muziki! “,muhudumu yule alimjibu Yuan Liang,kichwa chake kikishangazwa na utofauti wa mchina huyu, alikuwa mswahili haswaa licha ya ngozi nyeupe na macho madogo aliyokuwa nayo.
“,Ewala! hicho kitanifaa, sitasumbuka kutembea hatua nyingi kutafuta muziki, napenda sana kucheza disko! “,Yuan Liang aliongea kwa utani mwingi ndani yake,alipaki pikipiki yake, wakatembea mpaka mapokezi, akalipia, akakabidhiwa funguo, akaanza kupandisha kuelekea juu kwa kutumia lifti ya umeme.
…………………………………
Jiji la Gosta; 11;00am
Makao makuu ya nchi ya Goshani, msongamano uliendelea kama kawaida, huyu alifanya hili, yule akafanya lile, kila mmoja alikuwa bize kutafuta ridhiki bila kumfatilia mtu mwingine, siunajua mjini bwana!
“,Woouu! woou! woou! “,Kingo’ra cha polisi kilisikika, kamanda Gupta akiwa kama dereva,kamanda Yasini alikuwa ameketi pembeni yake,nyuma walikaa polisi wa kawaida watatu wenye silaha,walikamatilia mikononi bunduki aina ya smg.
Difenda ilikimbia kwa kasi, magari mengine yalipisha pembeni, watembea kwa miguu walisogea mbali na barabara waliposikia sauti ya king’ora. Kamanda Gupta aliendelea kukanyaga mafuta kuwahi kabla mtuhumiwa hajatoweka.
“,Watalaamu wa mawasiliano wa kujitegemea, watunza siri za muheshimiwa raisi, wanasema ujumbe wa mwisho, raisi akiwasiliana kuhusu mgeni wake halisi,ulitoka chumba namba kumi na tano katika hoteli ya Green pick, kwahiyo ndiyo tunaelekea huko, mkifika ni kuonesha vitambulisho na kuzama ndani, sawaa? “,kamanda Gupta alitoa maelekezo.
“,Ndio afandee! “,askari wote wakiongozwa na kamanda Gupta waliitikia, safari ikaendelea.
…………………………………
Green pick hotel; 12;05pm
Difenda ilifinya breki kwa fujo, vumbi likatimka, askari wakalukia nje wakiongozwa na kamanda Gupta, wakaonesha vitambulisho kwa walinzi getini, wakaingia ndani.
Askari watatu wenye bunduki walibaki nje, kamanda Gupta pamoja na kamanda Yasini wakaingia ndani. ” ,Reception “(Mapokezi) “,maandishi yalisomeka, wakasogelea dirisha la chumba cha mapokezi.
“,Sisi ni maafande wa jeshi la polisi kutoka makao makuu, “,Kamanda Gupta alizungumza, akatoa kitambulisho akaonyesha, kamanda Yasini na yeye akafuatia, akatoa kitambulisho akaonyesha.
“,Karibuni sana, sijui tuwasaidie nini? “,muhudumu wa kike, akiwa amevaa shati nyeupe, tai nyekundu ya kipepeo shingoni, usoni alijirembea na kuvutia mteja yoyote yule, aliongea kwa tabasamu zuri kwa makachelo hawa wawili wa jeshi la polisi.
“,Raisi alivamiwa jana usiku, akaibiwa katika hoteli ya Serena,tetesi zimeenea kila kona, nazani unatambua hilo,,kabla ya tukio alifanya mawasiliano na simu kutoka chumba namba kumi na tano katika hoteli yenu! “,kamanda Gupta alifafanua kwa kina.
“,Jana usiku tuliamka na kukuta funguo za chumba mezani, ambazo ni hizi hapa, mteja tayali ameondoka, mnaweza kwenda kufanya uchunguzi! “,muhudumu aliongea.
“,Itapendeza zaidi, lakini sijui mwenye chumba alikuwa anaitwa nani? “,kamanda Gupta aliuliza.
Muhudumu akapekua karatasi, wiki mbili nyuma, siku ya jumanne, akaliona jina la mtu aliyechukua chumba hicho.”anaitwa Yweon Lee “,anatokea Japan, hata rafudhi yake inadhibitisha hilo, anaongea kiswahili cha kigeni ambacho hakijanyooshwa vizuri.”,muhudumu aliongea. Kamanda Gupta akatikisa kichwa, wakaelekea juu ya ghorofa, baada ya dakika tano wakafika, wakakiona chumba, chumba cha mwisho, upande wa kushoto, karibu na dirisha. Wakafungua na kuingia ndani. Dakika kumi mbele, walikuwa wamepekua kila kona, hawakutambua chochote kile, wakafunga chumba, wakarudi mapokezi, wakakabidhi funguo na kutoweka.
…………………………………
Kituo kikuu cha polisi jijini Costa; 2;20pm
“Poleni sana, lakini ndio majukumu yalivyo, mtusaidie ,na sisi pia tuwasaidie! “,Kamanda Gupta aliongea, aliketi kwenye kiiti, karatasi ya maswali ikiwa juu ya meza, mbele ya meza waliketi inspekta Junior pamoja na inspekta Amiry, baada ya kutolewa mahabusu kwa mahojiano. Mkono wa kulia wa kamanda Gupta, aliketi kamanda Yasini.
“,swali la kwanza, mnaweza kutwambia ni nani aliyemvamia mheshimiwa raisi nyinyi kama walinzi wake siku hiyo?, “kamanda Gupta alihoji.
“,Hatumfahamu muhusika, lakini tunamuhisi mwanamke mmoja wa kizungu aliyeitwa Elizabeth,alisema anatokea Uingereza na alikuwa mgeni wa raisi, kwakuwa awali raisi alitupatia maelekezo kukaa mita tano mgeni wake akifika tulifanya hivyo, kwakuwa alituonya tusiingie chumbani kwake mpaka asubuhi, tulifanya hivyo na kumgongea asubuhi, tulipo ona kimya, tuliingia ndani, tukakuta amezimia, muhusika alitoweka kupitia dirishani, tukatoa taarifa serikalini, huku sisi tukiwekwa mahabusu! “,kamanda Amiry alitoa maelezo mazuri kwa kina, huku kamanda Gupta akilinganisha majina aliyoambiwa, raisi alimtajia mgeni wake aliitwa Yuan Liang, hotelini aliambiwa muhusika wa chumba aliitwa Yweon Lee kutoka Japan, lakini katika hoteli ya Serena, anayehisiwa anaitwa Elizabeth kutoka Uingereza.
“,Kimbembe hapo!, kazi hii ngumu kwelikweli! ,asante kwa ushirikiano wenu,msijali tutawasaidia,mtakua huru”,kamanda Gupta hakuona haja ya kuendelea kuhoji,kazi haikuwa rahisi kama alivyofikilia,aliwashukuru inspekta Amiry pamoja na inspekta Junior kwa muda mfupi wa mahojiano,wakanyanyuka,wakapigiana saluti za heshima,wengine wakarudishwa mahabusu,wengine wakatoka kuendelea na majukumu kumsaka muhusika.
…………………………………
Chumba cha siri, Ikulu; 05:00pm
Shingo ilifungwa bandeji,kichwani aliegemea mto kunyoosha shingo yake, nesi alikua bize kutimiza majukumu yake, alimpatia dawa, akampatia na maji.
“,Inatosha!, nitafanya mwenyewe, nipishe nizungumze na vijana wangu “,Jonsoni Mtemvu, raisi wa nchi ya Goshani aliongea, huku akipokea maji pamoja na dawa,akiwatazama kwa shauku ya kutaka kujua upelelezi ulipofikia kutoka kwa kamanda Gupta pamoja na kamanda Yasini, wakiwa wameketi sentimita chache, kutoka katika kitanda alicholazwa mheshimiwa raisi ,bwana Jonsoni Mtemvu.
“,Sawa, haina shida mkuu! “,kwa sauti yenye nidhamu ya kazi, nesi aliyejulikana kwa jina la Upendo aliongea, akachukua makolokolo yake, akatoka nje.
“,Bosi kazi ni ngumu! Green pick hoteli wanasema muhusika wa chumba cha simu iliyokupigia anaitwa Yweon Lee kutoka Japan,wewe unasema anaitwa Yuan Liang, kilichonifanya nichoke zaidi, Amiry na Junior tumewahoji wanasema mgeni wako wa Serena hoteli anaitwa Elizabeth kutoka Uingereza, ndiye wanamshuku maana alipotea ghafla baada ya tukio, nashindwa kuelewa mkuu! “,Gupta aliongea, huku kamanda Yasini akitikisa kichwa kuashiria kukubaliana na maneno ya askari mwenzake.
Raisi Jonsoni Mtemvu alichoka, nguvu zikamuishia, lakini akapiga moyo konde na kujikaza kisabuni. “,Sawa, inabidi niwaongezee nguvu, nitawasiliana na waziri mkuu Januari Sasamba, aombe msaada haraka sana wa wapelelezi wa kundi la “the super three soldiers” kutoka Tanzania, nina imani watawaongezea nguvu!, “raisi Jonsoni Mtemvu aliongea.
“,Ndio mkuu, itakuwa vema zaidi na kazi itakamilika kwa wakati! “,kamanda Yasini aliongea, akakubaliana na wazo raisi.
“,Kweli kabisa, wakifika hata kesho hapa nchini, siku moja tu inatosha kurudisha nyaraka za nchi zilizoibiwa mikononi mwako! “,kamanda Gupta aliendelea kukazia.
“,Sawa, nitafanya hivyo! “,raisi Jonsoni Mtemvu aliongea,kamanda Gupta pamoja na Yasini wakapiga saluti kwa heshima, kisha wakatoweka kusikojulikana.
Ikulu; Costa, Goshani
Mama Zainath, mke wa mheshimiwa Jonsoni Mtemvu, raisi wa nchi ya Goshani alikosa furaha, alijuta kwa kitendo alichokifanya cha kumnyima unyumba mume wake na kumsababishia matatizo, alijuta, kila wakati alijilaumu, alijiona hajui kutunza mume. “,Lazima nikamuombe msamaha, nampenda mume wangu, sio vema ahudumiwe na manesi wakati mimi nipo,hata kama alitaka kunisaliti nakosea, napaswa kusamehe na kusahau ili kuinusuru ndoa yangu ……”,mama Zainath alijishauri, akanyanyuka sebureni alipokua ameketi, sebure iliyojaa kila aina ya samani, samani zenye hadhi na heshima. Akaelekea kwenye chumba cha siri, chumba ambacho mume wake alifanyiwa matibabu.
“,Karibu mke wangu, nafurahi kukuona, nisamehe kwa yote niliyotaka kukufanyia,naomba tusahau yaliyopita na tugange yajayo ……”,Jonsoni Mtemvu akiwa ameketi kitandani, alimuangalia mke wake upande upande, shingo lake lilipinda kuelekea kulia mwa jicho lake, kifuti alichopigwa na Yuan Liang alimanusura kivunje mfupa wa shingo lake. Aliongea kwa sauti ya upole yenye kujaa busara kama kawaida yake, sifa ambazo zilimwezesha kuficha maovu aliyoyafanya, alifanya biashara haramu ya viungo vya albino, kuuza silaha na madawa ya kulevya, yote hayo hakuna aliyefahamu zaidi yake na rafiki yake waziri Januari Sasamba.
“,Nimekuelewa mume wangu, sitarudia tena, nakupenda baba Zainath …”,mama Zainath aliongea kwa huzuni,akadondosha chozi, Jonsoni Mtemvu akamfuta chozi lake kwa kutumia mikono yake, wote wakakumbatiana.
…………………………………
Huwei;Casabranka Casino
Msichana mrembo wa kichina, asiyechosha kutazamwa alikuwa ameketi kwenye kitanda chake,chumba namba therathini katika hoteli ya Casabranka.
“,Shit! Kumbe raisi Jonsoni Mtemvu ni mtu mubaya kiasi hiki, anaua albino, anauza silaha za serikali, isitoshe anauza madawa ya kulevya, kweli umdhaniaye siye kumbe ndiye,mimi naua watu wenye hatia, watu wabaya kujipatia pesa, siui viumbe wasio na hatia kama albino, lazima Jonsoni Mtemvu alipie damu hizo ……”,Yuan Liang alikasirika, japo alikuwa muuaji lakini alikuwa na moyo wa huruma, siku zote aliua watu wabaya na kuwaibia pesa, ndiyo maana hata raisi hakumuua, alizani ni mtu mzuri kumbe mubaya.
Alichomoa diski kwenye kompyuta,diski aliyoiba na kuichomoa kutoka kwenye saa ya raisi,alimaliza kusikiliza sauti na maongezi mbalimbali yaliyorekodiwa, akaweka pembeni kompyuta yake, akabonyeza namba kadhaa, kisha akaweka simu sikioni.
“,Unaongea na Doungso! ,diski yako iko mikononi mwangu, nahitaji bilioni kumi kesho jioni, saa tano kamili usiku, nitakuelekeza mahali pa kunikuta, ukipuuzia nafichua maovu yote kwa serikali na wananchi wako, utanyongwa, onyo! polisi yoyote yule asije akanifuatilia, nitawaua nyote ……!”,kama kawaida yake ya kudanganya majina, alimpigia raisi Jonsoni Mtemvu, akampatia maelekezo namna ya kuirudisha diski mikononi mwake, kisha akakata simu.
“,Ole wake asifuate maelekezo, nitamuua, huyu sio mtu mzuri wa kumwacha hai “,Yuan Liang aliongea peke yake, akarudi kitandani, akaendelea na shughuli zake za kuchezea kompyuta yake.
…………………………………
Ikulu; Costa, Goshani.
Simu yake ikiwa pembeni ya kitanda chake ilianza kuita, akaitazama kwa jicho lililojaa maswali, hakumfahamu aliyekuwa anapiga simu, namba ilikua mpya mbele ya macho yake. Akamtoa mke wake mwilini mwake,mama Zainath akaacha kumkumbatia, akamruhusu apokee simu, akasimama akaanza kutoka chumbani kumpatia uhuru mume wake, aliamini simu ilihusu maswala ya kiofisi na serikali kwa ujumla.
“,Unasema??,we ni nani?, uko wapi?, haloo, haloo!, “,Jonsoni Mtemvu hakuamini alichokisikia, akauliza aweze kumjua zaidi aliyempigia, alichelewa sana,Yuan Liang alikuwa tayali amekata simu.
“,Kuna nini mume wangu?,”,mama Zainath alikuwa hajafika mbali,alirudi haraka,alitaka kujua kitu ambacho kilimshtua mume wake baada ya kupokea simu.
Jonsoni Mtemvu alishindwa amjibu nini mke wake,alitafakari, akaamua kudanganya,”,Nyaraka za serikali kuhusu mikataba ya madini imepotea, sijui serikali itanielewa vipi, nimesaini juzi tu! “,alidanganya, jasho jembamba lilimtoka usoni,mke wake akamfuta jasho kwa kanga yake, aliamini maneno ya mume wake, akamuondoa shaka, “Usjali mume wangu, nyaraka zitapatikana, kila kitu kitakua sawa, ngoja upone kwanza, “mama Zainath aliongea, huku fikra za mume wake zikiwaza mbali sana.
Askari watatu wa kundi la wapelelezi nchini Tanzania, “the super three soldiers ” walikubali kutoa msaada nchini Goshani, ili kumnasa mtuhumiwa aliyemuibia na kumjeruhi raisi wa nchi hiyo bwana Jonsoni Mtemvu.
“,Msaada wenu ni muhimu kwa nchi yetu, mtuhumiwa kaiba diski yenye siri za nchi yetu, kunaswa kwake ni faida kwenu na kwetu, kwani mtaokoa usalama wa raia wetu kwa namna moja ama nyingine, karibuni sana Goshani, ni mimi waziri mkuu wa nchi ya Goshani, Januari Sasamba ……”,Kamanda Kendrick alisoma barua iliyotumwa kwa njia ya barua pepe (email), huku wenzake wawili wakimtazama na kumsikiliza kwa makini.
“,Inabidi tukawasaidie, hiyo ni hatari sana, nchi yao iko hatarini! “,kamanda Philipo, kamanda namba mbili na mtaalamu wa kompyuta na mawasiliano aliongea.. “,Lazima usiku huu wa leo tukanyage ardhi ya Goshani, misheni ifanyike masaa matano tu, kisha kesho jioni turejee Dar es Salaam ……”,kamanda Catherine aliongea,kamanda namba tatu, mtaalamu wa mawasiliano na tehama, taaluma moja na kamanda Philipo.
“,Asanteni sana, nafurahi kuskia hivyo, tukutane saa tano kamili usiku, mahali hapa “ofisi ya ukombozi ” ,saa tano na nusu tutapanda chopa na kuelekea nchini Goshani. “,kamanda Kendrick aliongea, wote wakanyanyuka, wakapigiana saluti, kila mmoja akaelekea alikokujua yeye.
Waziri mkuu Januari Sasamba, pembeni yake alisimama waziri wa ulinzi, nyuma yao walisimama wapelelezi wawili waliotegemewa na nchi ya Goshani, Kamanda Gupta pamoja na kamanda Yasini. Bila shaka kuna ujumbe muhimu walimletea raisi Jonsoni Mtemvu, bila kujua siri nzito aliyoificha moyoni mwake, alionywa, akisema, atauawa, alipaswa kumwambia mtu mmoja tu wa kupeleka pesa, pesa nyingi sana ambazo zilizidi bajeti ya nchi…
“,Mkuu, tumefanikiwa kupata msaada, usiku wa leo tunategemea kupata wapelelezi wa kimataifa kutoka Tanzania, the super three soldiers, kama ulivyonipatia maelekezo awali ……”,Januari Sasamba aliongea, akimtazama raisi aliyekuwa ameketi kitandani, uso haukuwa na tabasamu, alikosa furaha, Januari Sasamba alitambua jambo hilo, uso wa rafiki yake aliutambua nyakati zote za furaha na huzuni, tangu wakiwa masomoni, chuo kikuu cha Goshani.
“,Vipi mkuu uko sawa kweli? “,Jonsoni Mtemvu aliuliza.
“,Hayuko sawa, ugonjwa wa shingo bila shaka unamuumiza! “,waziri wa ulinzi, Saidi Mbeku aliongea.
“,Msijali niko sawa, hakikisheni mnawapokea vizuri na kushirikiana nao kwenye kazi ili mtuhumiwa apatikane na diski ipatikane, mnaweza kwenda! lakini waziri Januari Sasamba naomba ubaki mahali hapa ……”,raisi Jonsoni Mtemvu aliongea.
“,Sawa mkuu, saluti! “,saluti zilipigwa, waziri wa ulinzi akatoka nje, akifuatiwa na kamanda Gupta pamoja na kamanda Yasini, waziri Januari Sasamba akabaki ndani ya chumba cha siri.
…………………………………
“,Tunapata wapi bilioni kumi?, zinahitajika kesho saa tano usiku, na wewe ndiye unapaswa kuzipeleka hakuna mwingine, ili kuikomboa diski, anasema tusipopeleka pesa, au tukaenda na polisi, ataweka wazi kila kitu, atatuuwa ……”,Jonsoni Mtemvu aliongea, akiwa amechanganyikiwa.
“,Pesa zote hizo zinaenda wapi?, bajeti tu ya nchi bilioni moja,nani anahitaji? “,akiwa amejawa na mshangao, Januari Sasamba aliuliza.
.
“Mwanamke yule mwizi kanipigia nusu saa iliyopita,amesema atatupatia taarifa mahali pa kupeleka pesa ,japo hatuna pesa hizo, ni nyingi sana! “,raisi Jonsoni Mtemvu aliongea.
“,Ngoja nikwambie, pesa za bandia zipo,mzigo tayali umeingia, tutatumia kumpekea na kumnasa! “,Januari Sasamba aliongea.
“,Hapo sawa, itakua rahisi kumkamata, kama atakua hajakamatwa na wapelelezi kutoka Tanzania, naomba uwapatie ushirikiano wakifika, kazi njema, tutazidi kuwasiliana, “raisi Jonsoni Mtemvu aliongea, kisha akamruhusu Januari Sasamba kuondoka.
…………………………………
01:20pm, Goshani
Helikopta yenye chapa ya Tanzania, ilitua makao makuu ya jeshi nchini Goshani, makamanda watatu walishuka, usoni walivaa miwani ya rangi nyeusi, chini walivaa suti nyeusi, miguuni walivaa viatu vyeupe, walifanana kwa kila kitu.
“,Karibuni sana, karibuni sana Goshani! “,waziri wa ulinzi,Saidi Mbeku aliongea, akawasalimu wageni wake, “,Asante sana, tumekaribia! “,Kendrick, kamanda namba moja alijibu kwa niaba ya wenzake,kisha waziri akawaongoza mpaka kwenye difenda za polisi, wakapakiwa, wakapelekwa hotelini.
Costa;Goshani
Difenda ya polisi ilisimama pembeni na hoteli, “High Classic Hotel “,ilisomeka, mabegi yao yakashushwa kwa msaada wa askari,moja kwa moja mpaka kwenye vyumba vitatu vilivyokuwa vimeandaliwa kwa ajili ya wapelelezi kutoka Tanzania. “,Funguo zenu hizi hapa, mmoja atalala namba 20,mwingine 21 na watatu atatumia chumba namba 22,karibuni sana, tutaonana kesho asubuhi, salutii …”,Waziri wa ulinzi Saidi Mbeku aliongea, akakabidhi funguo kwa kamanda Kendrick, wakapigiana saluti, kisha akatoweka yeye pamoja na msafara wake.
“,Karibuni sana,kila huduma mtaikuta ndani ya vyumba vyenu, chakula na kila kitu kwa ajili yenu kimeshalipiwa, mkiwa na tatizo tupigieni kupitia simu za mezani ndani ya vyumba vyenu, “muhudumu wa hoteli,alitoa maelekezo, huku akiwaongoza askari wa tatu wa kundi la the super three soldiers, kuelekea kwenye vyumba vyao.
“,Hiki ni chumba namba ishirini, kinachofuata ni namba ishirini na moja, cha mwisho ni ishirini na mbili …”,muhudumu yule wa kike aliongea, alivutia kwa kila kitu, hakuchosha kutazamwa na kamanda Kendrick pamoja na kamanda Philipo.
“,Asante, tumekuelewa! vipi nikiwa na shida binafsi na wewe nakupataje? “,Kamanda Kendrick alijikuta ameropoka, kilicho ndani ya moyo wake.
“,Naitwa Ansie, napatikana vyumba vya wahudumu ghorofa ya mwisho, namba zangu ni zero saba ……”,muhudumu alimjibu Kamanda Kendrick,huku akibetua betua midomo yake, akiyarembua macho yake.
“,Bwanaaaeee,hebu ingia ndani uko, umalaya wako mpaka nchi za watu! “,Kamanda Catherine aliona wivu, siku zote alimnyemelea kamanda Kendrick bila mafanikio, kazi zilimbana, alishindwa kuwa muwazi kuelezea hisia zake kwa Kendrick, aliamua kuvumilia,aliapa kusema ukweli siku moja. “,Muone sura, wivu tu unakusumbua, “Kamanda Kendrick aliongea, huku muhudumu wa hoteli aliyejitambulisha kwa jina la Ansie akiondoka zake, huku makalio yake yakipepesuka huku na kule.
“,Nikuonee wivu wewe, kwa pesa gani uliyonayo, mwanaume pesa bwanaa, “,Catherine aliongea,vidole vyake viwili alivichezesha hewani,mkono wake wa kushoto ulishika kiunoni.
“,Hahahaaa “,kamanda Kendrick pamoja na
kamanda Philipo walicheka, kisha wakaingia ndani ya vyumba vyao.
…………………………………
Chumba namba 22:
Kamanda Catherine aliingia, akafunga mlango wake kwa ndani,”Duuuh walijuaje hawa, napenda sana chumba chenye gym ya kufanyia mazoezi,”akiwa amesimama alitabasamu, baada ya kuona chumba cha gym pembeni kabisa na mlango wake, akakifungua akakitazama, akazidi kutabasamu,akakifunga,akatembea kuelekea upande wa pili wa chumba, uso kwa uso na friji ya vinywaji, akaifungua,hakua mlevi, alifurahia juisi ya matunda, haikuwemo, akasonya, akachukua maji ya baridi kukata kiu.
“,Washenzi kweli, wanafikiri sote walevi, nikiwa mlevi na kazi yangu hii, ata teke ntapiga kweli? “,kamanda Catherine aliongea, akanyanyua chupa ya maji, akanywa, sekunde tu, chupa ilikua tupu.
Akavua suti yake ya bei ghari, akavaa nguo za kulalia, akajitupa kitandani, akauchapa usingizi …
…………………………………
Chumba namba 21:
Kamanda Kendrick alikuwa bize akinywa bia, alipenda sana pombe licha ya kuonywa mara kadhaa na rafiki zake, lakini alishindwa kuacha tabia hii ambayo muda mwingine ilirudisha nyuma ufanisi wake wa kazi.
Alifurahi sana kusogezewa vinywaji karibu yake, friji ilijaa pombe kuliko maji na juisi. Dakika tano tu tangu aingie chumbani,chupa tupu tatu za bia aina ya Safari, zilitelekezwa pembeni.
Dakika kumi baadae alikuwa amekunywa bia sita, akatosheka, akajitupa kitandani, tai yake ilikuwa shingoni, suti yake ilikuwa mwilini, viatu vyake vilikuwa mwilini …
…………………………………
Chumba namba 20;
Kendrick, the super three soldier namba moja, kiongozi mkuu wa kundi, alingia ndani ya chumba chake, kilikuwa na mwonekano mzuri sana, akaangaza huku na kule, akatabasamu, alifurahi sana kuona chumba cha kufanyia mazoezi (gym room).
“,Walijipanga sana, wamedhamiria kutuandaa vizuri, tutajitoa kuwasaidia, wametupokea vizuri sana …”, Aliongea, akakikagua chumba chake vizuri, akapanga vifaa vyake vizuri, akavua suti yake,akavaa nguo za kulalia na kujipumzisha kitandani, huku akitafakari namna ya kuianza kazi yake jua litakapochomoza.
…………………………………
Huwei; Costa, Goshani
Harakati ziliendelea kama kawaida katika mji mdogo wa Huwei, kaskazini mwa jiji la Costa nchini Goshani, watu wa eneo hili hawakuwa na muda wa kulala,asubuhi, mchana na usiku harakati ziliendelea, biashara haramu ndizo zilipelekea mji huu kukua kwa kasi.
“,Dada unaenda wapi, lipia pesa kabla hatujakuchafua sasa hivi, kama unaishi ndani ya jengo hili, onesha funguo za chumba ……”,pande la baba liliongea, lilikuwa na urefu wa futi saba, kifuani lilijazia, kwa kukadiria mtu huyu alikuwa na uzito wa takribani kilo mia moja.
“,Ninaishi chumba namba therathini, sina historia ya kutembea na funguo, “Yuan Liang aliongea kwa kujiamini, bila wasiwasi wowote.
“,Kama huna funguo, toa pesa, “jibaba lile liliongea, mikononi na kila sehemu ya mwili wake ilijaa tatoo na michoro ya kila aina.
“,King of Huwei, Mfalme wa Huwei) “,Yuan Liang alisoma maandishi kwenye mkono wa kushoto wa jibaba lile lililokuwa limesimama mlangoni, akacheka kwa kejeli, akatoa dola kumi mfukoni,mara mbili zaidi ya pesa za kiingilio cha club ya muziki, ghorofa ya pili, akamrushia.
“,Acha dharau we mwanamke, ntakutwanga ngumi sasa hivi ……”,jibaba lile liliongea, huku likiokota pesa lilizorushiwa, Yuan Liang akasonya tena kwa dharau, akaingia ndani.
“,Unanisonya eee? tutaona utapita wapi wakati wa kurudi! “,jibaba lile liliongea, likaendelea na shughuli zake.
………………………………
Casabranka Casino;
Yuan Liang aliingia ndani ya club ya muziki, watu walibanjuka kwa staili mbalimbali, wengine walicheza nusu utupu huku wakirushiwa pesa na wanaume wenye pesa zao.
Yuan Liang akajisogeza kaunta, aka agiza kinywaji, dakika mbili mbele, pombe kali aina ya konyagi ilisogezwa mbele yake, akaifungua, aka agiza maji pamoja na glasi,dakika moja mbele akaletewa glasi pamoja na chupa ya maji, maji ya Kilimanjaro kutoka nchini Tanzania. Akachanganya kwenye glasi, akaanza kunywa, huku midume na watu wenye pesa zao wakimtamani, wengine walikuwa makapuku, wengine walikuwa na pesa zao.
“,Samahani dada tunaweza kukaa pamoja, “pedeshee mmoja mwenye kitambi kikubwa aliongea, kichwani alikuwa na kipara, hakuwa mfupi sana wala mrefu sana, alikuwa na kimo cha wastani.
“,Usiwe na shaka! “,Yuan Liang aliongea, akiyalegeza macho yake yaliyojaa huba.
“,Sijui dada unaitwa nani? “,mwanaume yule aliuliza, huku akiusogeza mkono wake kupapasa paja la Yuan Liang ambalo lilibaki wazi akiwa amekaa kwenye kiti.
“,Usiongee sana sema una shilingi ngapi,? kama una dola mia mbili, utaonja penzi la mwanamke chotara wa kichina “,Yuan Liang aliongea.
“,Nitakupatia dola mia tano, kwa saa moja tu! “,mwanaume yule aliongea, akafungua briefcase, noti nyingi zilipangwa zikapangika, Yuan Liang aliziona, akatikisa kichwa, akaashiria kukubali.
“,Sisi kila kitu tunafanyia kwenye vyoo vyetu, twende huko! “,mwanaume yule aliongea, akanyanyuka, akaongozana na Yuan Liang.
…………………………………
Yuan Liang alifika katika vyoo vya kasino la Casablanca, akiwa ameongozana na pedeshee mwenye uchu wa mapenzi, kila mmoja alikuwa na mipango yake kichwani.
“,Nikirekodi filamu ya ngono na mwanamke huyu, nitauza sana, nitapata pesa nyingi “,Mwanaume yule aliongea peke yake ndani ya nafsi yake, akaufungua mlango wa choo, akawa wa kwanza kuingia, Yuan Liang akafuatia, wakafunga mlango kwa ndani.
“,Namuua kwa dakika moja, napitia dirishani, narukia ghorofa ya juu mpaka chumbani kwangu, natoweka na pesa zake, nahama hoteli hii, anakosa penzi na pesa vyote kwa pamoja! “,Yuan Liang aliongea, huku akikichunguza chumba cha choo, ghafla akashtuka, machale yakamcheza.
Aliiona kamera ya tofauti sana, ikiwa juu imefungwa mithili ya taa, akaitambua, akatabasamu, akachukua miwani yake, akaivaa, akabonyeza batani katika miwani yake,miwani iliyounganishwa na kifaa kidogo katika kisigino cha kiatu chake kilichofanya kazi ya kukata mawasiliano ya simu na kifaa chochote kile cha mawasiliano ,kama kompyuta na Kamera.
Pedeshee yule akatabasamu,akaweka begi la pesa pembeni, akaanza kutoa mavazi yake, akabaki na nguo yake ya ndani, Yuan Liang akacheza na hisia za mwanaume yule, Yuan Liang akavua kimini chake, akavua brauzi yake, akabaki akiwa na matiti yake yaliyomsimama vilivyo, akamsogelea pedeshee yule, wakakumbatiana, wakaanza kunyonyana ndimi, Yuan Liang alipoona hisia za mwanaume yule zilimepanda, akachomoa kisu kidogo alipokuwa amekificha katikati ya kiatu chake, akamfunga mdomo ghafla huku akiwa amempiga kabali, pedeshee alishindwa kujitetea, alirusha miguu huku na kule, akachomwa kisu cha mgongoni, ndani ya sekunde kumi tu, roho ya pedeshee yule ikaacha mwili …
Yuan Liang akajifuta damu kwa kutumia suti za pedeshee yule,chumba cha choo kilitapakaa damu kila kona, akavaa harakaharaka, akachukua briefcase ya pesa, akajaribu kufungua dirisha likakubali, akapenya kwenye nondo, akaruka serekasi,akatua ghorofa ya tatu, akatokezea mbele ya chumba chake, akaangaza huku na kule hakuona mtu, akaingia ndani ya chumba chake ……
…………………………………
Costa; Goshani, 7;50am
Kamanda Kendrick alikuwa amemaliza kupiga mazoezi,alikuwa na dakika kumi tangu akurupuke usingizini, akaelekea bafuni, akaoga, akamaliza, akachukua suti yake, akaivaa mwilini, suti nyukundu tofauti na aliyokuwa amevaa usiku uliopita, akachukua bastola yake, akapachika magazine,akachukua kisu chake kidogo kilicho chongoka kama msumeno,silaha zake akaziweka katikati ya koti lake,tayali alikuwa amekamilika,akatoka nje.
Uso kwa uso akakutana na kamanda Catherine,utazani walijiandaa kwa pamoja,mtu mmoja tu alikuwa amekosekana,kamanda Philipo.
“,Niko poa, ngoja tumuamshe huyu mvivu! “,kamanda Kendrick aliongea, akaanza kugonga mlango wa kamanda Philipo, aligonga kwa takribani dakika tano bila mafanikio, akausukuma, ukafunguka, wote wakaingia ndani huku bastola zikiwa mikononi, Kendrick pamoja na Catherine, waliingiwa na hofu kwa kugonga mlango wa kamanda Philipo kwa muda mrefu bila mafanikio …
“,What, nini hiki shiit! “,kamanda Kendrick aliongea, macho yake yalikutana na chupa sita za bia zikiwa zimesambaa sakafuni.
“,Yaani nilijua tu, tangu jana nilipo ona friji iliyojaa bia, nilijua lazima ndugu yetu tumpotezee, hahahaa ……”,kamanda Catherine alicheka sana, akimcheka kamanda Philipo aliyekuwa amelala na viatu baada ya kuzidiwa na pombe, wote kwa pamoja walirudisha bastola zao mahala pake, kamanda Kendrick akimhurumia rafiki yake kwa ulevi uliozidi kipimo, huku Catherine akicheka, alishindwa kujizuia.
Huwei;Masaa sita nyuma
Yuan Liang alifika ndani ya chumba chake,alihema kwa kasi sana, tayali alikuwa ametekeleza mauaji, akafungasha kila kitu cha kwake,akavua kimini chake, akavaa suruali nyeusi ya jinzi, akachomoa kifaa kidogo cha kwenye kiatu chake, kifaa maalumu cha kukata mawasiliano, akakipachika kwenye kiatu kingine chekundu, kisha akakivaa, tayali mizigo yake ilikuwa sawa, akatoka ndani ya chumba chake, akafunga, akashuka ghorofani akiwa na haraka sana …
“,Funguo zako hizi hapa, nashukuru sana “,Yuan Liang aliongea, alikutana na mzee aliyempokea, mzee ambaye alipenda ujana pasipo kawaida.
“,Mind your own business (jali shughuli zako) “,Yuan Liang alijibu kwa jeuli, mzee yule akakasirika.
“,Fuck you son of bitch …”,mzee yule alifoka, akamtukana Yuan Liang kwa kizungu, akamshika makalio yake, alimtukana na kumdharau. “,Puuuuuu ……”,Yuan Liang aliacha mabegi yake, akaruka mateke mawili, yakampata usoni mzee yule, kishindo kikasikika, akaanguka mita kadhaa eneo la mapokezi,uso wake ukavimba. “,Unanitukana mi malaya unanijua vizuri, pumbavu wewe, jitu zima ovyoo! “,Yuan Liang alimkejeli mzee yule, watu walianza kukusanyika katika mlango wa mapokezi kushuhudia, Yuan Liang akatoka haraka, akapanda pikipiki yake, akatoweka eneo lile la Casabranka Kasino.
…………………………………
Chumba namba 25;
Mitambo yao ilizima ghafla,mara tu kijana wao alipotaka kuanza mchezo mchafu wa ngono na kumrekodi,machale yakawacheza,walichunguza mitambo yao, hawakuona tatizo, mitambo yao ilikuwa sawa kabisa.
“,Nenda kachunguze nini kimetokea, hakikisha mwanamke yule hagundui kama alitaka kurekodiwa mkanda wa ngono “,bilionea Xavery, raia wa Italiano aliongea, akamtuma kijana wake aliyekuwa akiongoza mitambo ya kurekodia filamu chafu za ngono.
“,Sawa bosi, ngoja nikaangalie nani anataka kutuharibia kazi yetu, video zingine tumerekodi vizuri isipokuwa hii ambayo imezingua tu kabla hatujaanza ……”,kijana yule aliongea, akatoweka chumba namba ishirini na tano.
“,Vipi dogo mbona mapepe sana, “jibaba aliyehusika kulinda mlango wa kasino aliongea, huku akimtazama kwa macho yaliyojaa udadisi kijana yule aliyehusika na kurekodi filamu za ngono.
“,Kazi ilitaka kuanza, kamera ikazima ghafla, hatujui nini tatizo, nd’o naenda kukagua bro …”,kijana yule aliongea, jibaba lile la mlango wa Casino likampisha, akaingia ndani ya ukumbi wa muziki.
…………………………………
Kijana yule aliyekuwa na sura halisi ya Kiafrika, huku rasta ndefu zikining’inia vizuri katika mgongo wake, alipenya katikati ya watu waliokuwa wanacheza mziki bila wasiwasi wowote,wanawake waliokosa heshima kwa wazazi wao, walikua uchi wa mnyama wakicheza na kurushiwa pesa na mapedeshee wenye pesa zao, walirekodiwa kwa ajili ya video zao kuuzwa kila kona ya dunia,shughuli mbalimbali za kuuza silaha pamoja na madawa ya kulevya ziliendelea ndani ya Kasino.
Alifanikiwa kuvuka makundi ya watu waliocheza muziki, akakunja kulia, akakunja kushoto, “TOILETS “,kibao kilisomeka,akaingia, moja kwa moja mpaka kwenye vyumba walivyotumia kurekodia filamu zao.
Akakagua choo kimoja baada ya kingine, “Puuuuu! “,alidondoka mweleka, aliteleza kwenye damu baada ya kufungua choo kimoja, mwenzao alikuwa ameuawa kikatili.
“,Yalaaaaa! ,wameuwaa, amekufaaa! “,alipiga kelele, akatoka akikimbia, suti yake ilikuwa imetapakaa damu baada ya kudondoka,watu wote ndani ya kasino waliacha shughuli zao, walikimbia kuziokoa nafsi zao.
“,Mbona unakimbia dogo, nini kimetokea?,damu hizo zimetoka wapi? “,jibaba lile la mlango wa kasino liliongea, huku likiwapisha raia waliotoka ndani ya kasino kwa fujo kuyaokoa maisha yao.
“,Wamemuua Bensoni, wamemuua! “,kijana yule aliyehusika na kurekodi filamu za ngono aliongea.
“,Unasemaje?? nenda kamwambie bosi haraka sana …”, mlinzi yule wa kasino aliongea, sura yake ilitisha,kutokana na mwili mkubwa aliokuwa nao.Alipomaliza kuongea, kijana yule alitimua mbio kuelekea kwa bosi wake, bilionea Xavery aliyemiliki jengo lote la Casabranka,pamoja na biashara zote ndani ya jengo hili, kasino la muziki lilibaki tupu, isipokuwa wafanyakazi wa kasino hili.
…………………………………
Wafanyakazi wa kasino pamoja na hoteli ya Casabranka walikaa kikao,walitaka kujua ninani alihusika na mauaji.
“,Kuna mdada alisema anakaa chumba namba therathini, ni chotara wa kichina, anaongea kiswahili bila tatizo lolote, alinipita mlangoni kwa jeuri, sikumuona wakati wa kutoka, bila shaka ndiye muhusika …”,jibaba la mlango wa kasino la muziki aliongea.
“,Huyo ndiyo anakaa chumba namba therathini, nilimpokea jana tu, lakini amekabidhi funguo nusu saa baada ya mauaji, akanipiga na mateke akaondoka, sina shaka, huyo ndiye ameua! “,mzee aliyependa ujana aliongea, akitoa maelekezo kwa bosi wake Xavery.
“,Muuaji apatikane haraka sana,sina shida na pesa wala mauaji aliyoyafanya, nataka aungane na sisi kwenye kundi letu, mbinu alizotumia zitatufaa sana, anafaa kwa shughuli zetu, akipatikana nitawalipa pesa nyingi kama zawadi ya kumtafuta …”,bilionea Xaviery aliongea, vijana wake wakamuelewa.
…………………………………
Mexic;
Yuan Liang aliendesha pikipiki yake,ndani ya nusu saa tu, alifika katika makazi mapya, alipaki pikipiki yake ndani ya hoteli ya hadhi ya chini,hoteli zote kubwa eneo la Mexic,kilomita tano kutoka mji wa Huwei zilikuwa zimejaa.
“,Shilingi elfu kumi tu chumba! “,mama mmoja umri wa miaka arobaini alimpokea Yuan Liang, akamkaribisha katika nyumba yake ya kulalia wageni.
“,Umeme upo?, napata mahali pa kuhifadhia pikipiki yangu? “,Yuan Liang aliuliza maswali mawili kwa wakati mmoja.
“,Vyote vinapatikana, usjali mwanangu! “,mwanamke yule alimpatia maelekezo Yuan Liang, Yuan Liang akalipia shilingi elfu hamsini, akapaki pikipiki yake mahali alipoelekezwa, kisha yeye akelekea ndani kupatiwa chumba cha kupumzika, ikiwa yapata majira ya saa kumi usiku.
“,Unalala sana kama mwanamke,siwezi nikaolewa na mwanaume mlevi,anayelala sana kama wewe,”kamanda Catherine alimtania kamanda Philipo.
“,Hahahaaa”,wote walicheka sana,kamanda Philipo akanawa uso,akapiga mswaki,akiwa na suti yake aliyolala nayo tangu jana,wakatoka kuelekea Ikulu kuonana na raisi wa nchi ya Goshani,tayali kwa ajili ya kuanza kazi. …………………………………
Ikulu; Chumba cha siri 9;20am
“,Naitwa kamanda Kendrick, kiongozi wa kundi, huyu anaitwa kamanda Philipo, na huyu anaitwa kamanda Catherine “,kamanda Kendrick aliwatambulisha wenzake mbele ya raisi Jonsoni Mtemvu, akiwa amelala kitandani.
“,Karibuni sana, nazani kila kitu kuhusu kazi mlishapatiwa maelekezo, tutatoa ushirikiano wowote mtakapohitaji, msisite kunijulisha “,raisi Jonsoni Mtemvu aliongea.
“,Sawa mheshimiwa,sisi tunaomba tupate askari wa kutuongoza, tufike hoteli aliyokuwa akiishi mgeni wako, kisha tufike hoteli mliyokutana, mwisho tuonane na walinzi wako waliokuwa zamu kukulinda “,kamanda Kendrick aliongea.
“,Waongozeni askari hawa wapelelezi, wapatieni ushirikiano kila hatua “,Jonsoni Mtemvu aliongea.
“,Sawa mkuu “,wakaitikia, wakaanza kutoka nje, wakiwa pamoja na kundi zima la the super three soldiers.
Green pick hotel; 10;02
Difenda mbili za polisi zilifunga breki kwa mara nyingine tena, katika hoteli ya green pick. Kamanda Kendrick akiwa ameongozana na kundi lake, mara baada ya kutoka ikulu kuonana na raisi Jonsoni Mtemvu, walianza kazi haraka sana kwa kufika maeneno muhimu kwa ajili ya kufanikisha upelelezi wao.
“,tumefika et ee, “
“,yes afande, tumefika …”,
“,Hapa ndipo mheshimiwa aliwasiliana na mgeni wake kwa simu? “,
“,Ndio afande, ni hapa! “,
“,Sawa,tupelekeni kwenye chumba alichokuwa anaishi mgeni huyo …”,
“,Usjali afande, tufuateni …”,
Yalikuwa ni mazungumzo kati ya kundi la the super three soldiers, pamoja na kamanda Gupta na mwenzake kamanda Yasini. Wote wakashuka kwenye difenda yao ya mbele, wakaelekea ndani ya hoteli, kamanda Gupta pamoja na kamanda Yasini walitangulia mbele, kamanda Kendrick, Catherine pamoja na kamanda Philipo wakawafuata kwa nyuma.
Wakafika mapokezi, wakajitambulisha, wakaonesha vitambulisho kama kawaida, kisha wakaanza safari kuelekea chumba namba kumi na tano.
“,ana umri gani? na alikaa hotelini kwa siku ngapi …”,
“,kuhusu umri,sifahamu! lakini amekaa hapa kwa wiki mbili …” ,
“,Kwa nini usijue taarifa muhimu kama hizo, majambazi wanatumia sana vyumba vya wageni kama hivi, watakuja kufanya mauji ya kikatili siku moja, anyway tuyache hayo! kazi njema …”,
Yalikuwa ni mazungumzo kati ya kamanda Kendrick pamoja na muhudumu wa mapokezi, katika hoteli ya Green pick. Wote wakiwa wanapanda juu ghorofani kuelekea chumba namba kumi na tano, wakafika mbele ya mlango, akamuacha muhudumu aendelee na majukumu yake, wenyewe wakafungua chumba na kuingia. Wakachunguza kila kona,kamanda Philipo akapiga picha muonekano wa chumba,kamanda Catherine akafungua dirisha la vioo, akachungulia nje, akaona alama za viatu na makucha katika ukuta, machale yakamcheza.
“,Kendrick …”,
“,yes afande “
“,njoeni muone hapa …”,
Askari wote, Gupta, Yasini, Philipo pamoja na Kendrick wakasogea ukutani.
“,mnaona nyayo za miguu, unaona makucha, harafu dirisha limelegea tofauti na madirisha ya vyumba vile, maua kule chini yamekanyagwa kanyagwa”,kamanda Catherine aliongea.
“,Ndio afande, tumeona “,askari wote walijibu.
“,ok, pigeni mahesabu ya kijasusi, mnafikiria nini katika vichwa vyenu …?”,kamanda Catherine akauliza tena.
“,mtu wa chumba hiki, hakua anatumia njia halali kuingia chumbani mwake, kuna baadhi ya siku alipitia dirishani “,kamanda Kendrick alijibu.
“,Exactly,fikra zangu zinaniambia mtu aliyekuwa anaishi katika chumba hiki si wa kawaida, kuna siku aliruka kwa serekasi kutoka kwenye maua yale, akakanyaga hapa ukutani kwa miguu au makucha ya mikono kama unavyo ona, kisha akaingia ndani, “kamanda Catherine alipiga mahesabu ya kipelelezi,wote wakakubaliana na mawazo yake.
“,Kweli we ni hatari mama, sijawahi juta kukufahamu, ngoja tuendelee na upelelezi, tutajua tu …”,Kendrick aliongea.
“,kweli kabisa, “Philipo akaitikia.
“,Maana haiwezekani dirisha hili liwe wazi, mengine yawe yamefungwa tena hoteli kubwa kama hii, “Catherine aliongea kwa mara nyingine tena.
“,Tuliwambia wasi ingize mteja katika chumba hiki wala kubadili chochote ndani ya chumba hiki,nazani ndio maana hawajafunga dirisha hili…”,Gupta na Yasini,askari wapelelezi wa nchi ya Goshani waliongea.
“,Ndio maana nikasema,dirisha hili lina tatizo,siku zote lilikuwa lina achwa wazi,ndiyo maana mtu wa chumba hiki aliondoka kwa haraka akasahau kufunga dirisha kwani ni mazoea yake,anyway,tuondokeni katika hoteli ya pili…”,Catherine aliongea,akafunga dirisha,wote wakatoka nje,wakafunga mlango wa chumba wakashuka ghorofani.
…………………………………
“,Samahani muhudumu,wakati chumba mnampatia mwanamke huyo,dirisha lilikuwa bovu?”,
“,Hapana mheshimiwa,lilikua zima kabisa…”,
“,Mbona limelegea,halifungi vizuri…”,
“,Mmmh,kuhusu hilo sifahamu,kwasababu tulikatazwa kuingia mpaka uchunguzi ukamilike,kwahiyo hatujui chochote,lakini lilikua zima kabisa…”,
“,Vipi kuhusu nyayo za viatu ukutani,karibu na dirisha la chumba namba kumi na tano,kulikoni?”,
“,kama nilivyo kwambia awali,hatujui chochote kile,kama kuna nyayo za viatu ukutani,chumba hakikua hivyo awali…”,
“,Ok thank you,sasa naanza kupata mwanga,tuondokeni,muhudumu asante ,na kazi njema,mnaweza kusafisha chumba na kumpatia mteja mwingine…”,
“,Sawa mkuu,karibuni tena…”,
Yalikuwa ni mazungumzo kati ya kamanda Kendrick pamoja na muhudumu wa hoteli,kwa mara nyingine tena.Mazungumzo yakamalizika,askari wote wakatoka nje ya hoteli,wakatoweka walikokufamu wao.
…………………………………
Serena hoteli;
“Hiki ndicho chumba namba ishirini, kama mnavyo kiona, tangu tukio litokee hatujakifanyia hata usafi, tuliambiwa tusikanyage humu mpaka uchunguzi utakapo kamilika …”,meneja mkuu wa hoteli ya Serena, mheshimiwa Vandmir Gomez aliongea, suti nyeusi, tai nyeusi pamoja na viatu vyeusi viliupendezesha mwili wake,kila kona alipopita aliitwa kwa jina la bosi Gomez, jina sahihi kabisa ambalo liliendana na mavazi yake ya kifahari pamoja na pesa nyingi alizokuwa nazo, takribani dola za kimarekani bilioni moja, pesa ambazo zilipelekea atajwe katika jarida la Forbes Afrika mwaka 2017 ,kama tajiri pekee kijana barani Afrika mwenye umri wa miaka ishirini na tano tu.
“,Usjali mheshimiwa, kuanzia leo kila kitu kitakua sawa …”,kamanda Catherine aliitikia, huku akitembea kuelekea bafuni, akawaacha makamanda wenzake wakifanya uchunguzi chumbani,huku kamanda Philipo akiwa bize kuchukua picha ambazo zingewasaidia baadae kwenye uchunguzi.
“,nyote njoeni huku, asibaki hata mmoja …”,kamanda Catherine alikuta nondo imekunjwa,dirisha limekatwa, huku akiangalia kipande cha kioo kilichokatwa na kutelekezwa.
“,Kuna nini tena? “,Philipo na wenzake waliuliza.
“,Hapo ndipo mtuhumiwa alitorokea baada ya kumjeruhi mheshimiwa raisi,…”,bosi Gomez, meneja wa hoteli ya Serena aliongea.
“,bila shaka, hata mimi nimeona, kamanda Kendrick na wenzako, naomba mchungulie dirishani harafu mniambie mmeona nini! “,kamanda Catherine aliongea, kamanda Philipo akiwa na shauku kubwa ya kutaka kujua kilichotokea, akawa wa kwanza kuchungulia dirishani, akafuta kendrick, kisha Gupta na Yasini wakamalizia.
“,mneona nini? “,kamanda Catherine aliuliza swali kama kawaida yake.
“,makucha na viatu, “walijibu.
“,tayali tumeshamjua muuaji, aliyekuwa amepanga katika chumba namba kumi na tano kule Green pick, ndiye alimshambulia raisi …”,Catherine aliongea, huku akichunguza vioo vilivyokatwa dirishani, mtuhumiwa akapita.
“,tena ni muuaji hatari sana, hiki ni kisu kigumu kuliko vyote duniani, kinaitwa the magic knife, kisu cha maajabu, kilitengenezwa nchini Marekani mwaka 1935,kilitumika katika vita ya pili ya dunia na kuua mamilioni ya watu, kina uwezo wa kukata chuma pamoja na vioo vigumu, kwani kina madini ya almasi ndani yake ……”,kamanda Catherine alionesha utalaamu wake katika upelelezi,wote wakimsikiliza kwa makini, huku kamanda Kendrick akitikisa kichwa, akikubaliana na maelezo ya kamanda Catherine, mpelelezi mtata wa kike, kutoka katika kundi la the super three soldiers la nchini Tanzania. “,tuondokeni, twendeni mahabusu tukaonane na walinzi wa mheshimiwa raisi, kisha tuhitimishe uchunguzi wetu, tukamkamate mtuhumiwa, maana sizani kama ni vigumu kumpata …”,kamanda Kendrick aliongea,wakatoka nje,wote wakamfuata,wakaaga uongozi wa hoteli, wakatoweka haraka sana katika hoteli ya Serena.
Kamanda Junior pamoja na kamanda Amiry walikuwa wameketi mbele ya meza, huku Kamanda kendrick na wenzake wakiwa upande wa pili wa meza, pamoja na waziri wa ulinzi bwana Saidi Mbeku.
“,swali la kwanza, raisi aliwambia anaenda kuonana na nani? “,
“,hapana, lakini alitwambia mgeni wake ni mwanamke “,
“,alitegemea mgeni wake atamjeruhi? au ni mtu mbaya kwake ?…”,
“,Hapana, ndiyo maana alitwambia tusogee mbali na chumba chake, alimwamini mgeni wake kwa asilimia mia moja…”,
“,mgeni huyo alikuwa ni mzungu, Muafrika, na alijiamini kiasi gani? ,”
“,Alikuwa mzungu, alijiamini sana …”,
“,Asanteni kwa ushirikiano wenu, kwa upelelezi tulio ufanya awali, tukilinganisha na huu, nyie hamna hatia, waziri wa ulinzi kwa vile yuko hapa, muachiwe haraka iwezekanavyo, muendelee na majukumu yenu ya kulijenga taifa, pia serikali iwalipe fidia, mtuhumiwa ni mwanamke, mzoefu wa mauaji, mwenye tabia za kujigeuza geuza, tutamkamata kwani tuna watalaamu wa kompyuta mahali hapa, twendeni tukaonane na raisi Jonsoni Mtemvu, kisha tukamtafute mtuhumiwa mahali alipo kabla ya saa kumi na mbili jioni …”,
Jopo lote la maaskari wapelelezi wakasimama, wakaondoka, huku kamanda Amiry na mwenzake Junior wakiachiwa huru kwa amri ya waziri wa ulinzi,Saidi Mbeku, baada ya ukweli kuhusu muuaji aliyemjeruhi raisi na kumuibia kufahamika.
Mexic; 11;00am
Yuan Liang alikurupuka kutoka usingizini, alikuwa amechoka sana kwa purukushani za hapa na pale usiku uliopita, aliiba, akaua na kutoroka eneo la kasino ya Casabranka hoteli, lililopatikana katika mji mdogo wa Huwei, akakimbilia kilomita tano, katika mji mdogo wa Mexic, kaskazini mwa jiji la Costa, nchini Goshani.
“,Nimelala sana, haijawahi kunitokea hata siku moja, I have to look for money, muda wa kazi sasa …”,Yuan Liang alijigeuza kitandani, akanyanyuka, akaisogelea simu yake, katika kabati chakavu, kama ujuavyo hoteli za uswazi, akaitazama simu yake, “11;00” saa yake ilisomeka, ilikuwa saa tano asubuhi, akapigwa na butwaa akishangaa jinsi masaa yalivyofyatuka kama umeme.
“,Ngo ngo, ngo ngo, hodii! wenyewe! “,
“,karibu, nakuja! “,
Muda mfupi tu, akiwa bado amesimama akitafakari, mlango wa chumba chake ukaanza kugongwa, akaitika, akausogelea mlango wake, akachungulia kupitia tundu la mlangoni, akajiridhisha, aliyegonga mlango hakuwa adui yake, akafungua mlango.
“,Umelala sana, pole na uchovu …”,
“,Asante, “
“,Jana umetoa pesa nyingi, hapa tunatoa huduma ya chakula pia, sijui nikuandalie chakula gani siku ya leo? “,
“,Oooh, ok, nisubili kidogo, nakuja …”,
Yalikuwa ni mazungumzo kati ya Yuan Liang pamoja na mwanamke aliyempokea usiku uliopita, Yuan Liang akarudi ndani, akasogelea mabegi yake mawili, akafungua, akachukua noti tano za elfu kumi kumi, akarudi tena mlangoni, kuzungumza na mwenyeji wake.
“,Jana nilikupatia elfu hamsini, ile ni kwa ajili ya chumba, hii hapa ni kwa ajili ya chakula, “
“,Sawa dada, hapa kuna chapati, ndizi nyama, wali,pamoja na chipsi, sijui tukuletee msosi gani? “,
Mama yule aliongea, akamuaga Yuan Liang,akaondoka zake. Yuan Liang akafunga mlango wa chumba chake, akabonyeza bonyeza simu yake, akaweka sikioni.
“,Haloo “,Yuan Liang aliongea.
“,Hallow nani mwenzangu? “,upande wa pili wa simu uliitikia.
“,Saa tano usiku nipate pesa zangu, mpate diski yenu, mtanikuta Mexic, mji mdogo kaskazini mwa Goshani, nitawambia pesa mumpatie nani, na diski mtaipataje, “Yuan Liang aliongea.
“,Haloo, haloo, halooo! “,upande wa pili wa simu ukaongea, simu haikujibiwa, Yuan Liang akabonyeza tena simu yake, akakata simu.
“,Mshenzi kabisa, anazani natania, niko siliasi, ngoja aone,”Yuan Liang aliongea, akachukua kompyuta yake, akakaa kitandani, akaendelea na shughuli zake za kuchezea kompyuta yake.
…………………………………
Ikulu; Saa moja iliyopita
Waziri mkuu Januari Sasamba, alikuwa ameketi kitandani, pembeni na rafiki yake kipenzi, raisi Jonsoni Mtemvu. Walikuna vichwa vyao, wakatafakari bila kupata majibu, walitafakari kuhusu namna ya kurudisha diski yenye siri nyingi haramu,irudi katika himaya yao.
“,Kachukue pesa, anza safari ya kuelekea huko, hakikisha haumwambii mtu yoyote yule …”,
“,lakini mkuu, vipi kuhusu makachelo hawa kutoka Tanzania,situwaachie wafanye kazi wao! “,
“,Itakua vizuri zaidi tukiipata sisi kama sisi, bila kupitia wao, kwani wakiipata wao wanaweza kuichunguza diski hiyo, mambo yakawa mabaya zaidi, “
“,Sawa bosi, nimekuelewa “,Januari Sasamba aliitikia, akasimama kutaka kuondoka, huku raisi akiipokea simu yake iliyoonekana ikiita kwa muda mrefu, bila kupokelewa.
“,Haloo,nani mwenzangu? “,raisi aliongea, akasikiliza maelezo kutoka upande wa pili wa simu.
“,Haloo, haloo, halooo!”,Jonsoni Mtemvu aliongea, akaongea tena, alikuwa amepagawa, simu ilikuwa tayali imekatwa, waziri mkuu Januari Sasamba alikuwa bado hajaondoka, alikuwa amesimama mlangoni, akisikiliza maongezi kati ya raisi, pamoja na mtu aliyempigia simu bila kumfahamu.Akajongea taratibu, akarudi katika kitanda alicholazwa rafiki yake.
“,Kapiga tena! “,
“,Anasemaje? “,
“,kasisitiza kuhusu pesa zake, anasema pesa zipelekwe katika mji mdogo wa Mexic, atatutarifu mahali pa kuonana naye …”,
“,duuuh, haina jinsi, ngoja nikajiandae, nifike huko …”,
“,Sawa,jitahidi, kazi njema! “!
Januari Sasamba alimaliza kuongea, akaagana na rafiki yake, akasimama, akaondoka zake.
………………………………… 12;45pm
The super three soldiers walirejea tena ikulu, wakiongozana na kamanda Gupta, pamoja na kamanda Yasini. Waka keti katika sofa, karibu kabisa na kitanda cha mheshimiwa raisi Jonsoni Mtemvu.
“,unaendeleaje mheshimiwa? “,
“,naendelea vizuri, nipe ripoti! “,
“,Upelelezi unaendelea vizuri, mtuhumiwa ni hatari sana, walinzi wako hawahusiki na chochote kile, tunaomba utusaidie saa yako, saa ndio kila kitu kwa sasa, tumalizie hatua ya mwisho ya uchunguzi! “,
Kamanda Kendrick aliongea,akitoa ripoti ya upelelezi kwa raisi Jonsoni Mtemvu, dakika mbili tu, raisi akavua saa yake mkononi,kamanda Philipo akaipokea, akaipachika katika kifaa kidogo kilichokua na taa nyekundu, taa nyekundu ikiwaka na kuzima.
Kamanda Philipo akachukua kompyuta yake, kwenye begi dogo, akaifungua, akachomeka waya wa USB, akaunganisha na kifaa kidogo, kifaa kilichokuwa na saa ya raisi, akaanza kazi yake, kamanda Catherine akiwa pembeni yake, wote walikuwa wataalamu wa kutumia kompyuta.
“,Connection loading ……”,kioo cha kompyuta kilisomeka kwa kizungu.
“,Vipi, mahali ilipo diski ya saa mmepatambua? “,kamanda Kendrick aliuliza.
“,hapana, bado inasachi,ngoja tusubili …”,kamanda Philipo aliongea.
‘,link connected, the related disc available in Mexic,Costa, Goshani “,(imeunganishwa, diski inayohusiana inapatikana Mexic, Costa, Goshani …)”,maandishi yalisomeka tena katika kioo cha kompyuta,picha kubwa ya ramani ikaonekana.
“,tayali, sogeeni muone,diski iko Mexic, bila shaka mtuhumiwa yuko huko Mexic…,”Catherine aliongea, macho yake yakiwa bize kutazama kompyuta.
“,Mexic!! “,raisi alishtuka, alisikia jina ambalo lilitajwa awali kwenye simu na mtu aliyempigia, akihitaji pesa apatiwe diski yake, akatafakari jambo, katika kichwa chake.
“,Basi kamateni silaha, tuondoke! “,kamanda Catherine aliongea, kamanda Philipo na wenzake wakaacha kutazama ramani katika kompyuta, wakasimama, “tunaondoka mheshimiwa, salutii “,kamanda Kendrick aliongea, wakapiga saluti, wakatoka nje, kuelekea Mexic, kaskazini mwa jiji la Costa, nchini Goshani.
Mara tu baada ya the super three soldiers kutoka nje ya chumba chake, alichokuwa anapatiwa matibabu,mheshimiwa raisi, Jonsoni Mtemvu alichukua simu yake, akalitafuta jina la waziri Januari Sasamba,akapiga simu, simu ikaita, ikaita tena na tena bila mafanikio.
“,huyu vipi, mbona hapokei simu? “,aliongea, akapiga tena, dakika mbili tu, ikapokelewa.
“,Haloo, niko ndani ya gari, ndio maana sikusikia simu, nambie, “upande wa pili wa simu ulisikika.
“,Kuwa makini, makamanda wanakuja huko,mitambo yao inaonesha mtuhumiwa yuko huko, hakikisha unachukua diski kabla yao, ikishindikana, wakawahi kuichukua, hakikisha wanakupatia kabla hawajagundua siri zetu, mpaka najuta kwanini niliwaleta, tukizubaa watatugeukia!!”Jonsoni Mtemvu aliongea, akakata simu.
“,Usjali mkuu, nitakua salama …”,upande wa pili wa simu uliongea, simu ikakatwa, angalau raisi Jonsoni Mtemvu akawa na amani moyoni.
…………………………………
Gari lilikanyagwa mafuta, kamanda Gupta kama kawaida yake, alifahamu kila kona za jiji la Costa, alikuwa ameshika uskani,barabara kuu, kuelekea nje ya mji, kaskazini mwa jiji la Costa. Kadri walivyozidi kusafiri, masaa yakazidi kwenda, ndivyo kilomita za eneo, mahali diski ilipo, ziliweza kupungua.
“,Bado kilomita kumi, endelea kukanyaga mafuta, tukifika mji unaoitwa Huwei, tutaupita, tutasogea kilomita tano mbele, tutafika eneo la Mexic, mahali diski ilipo, “kamanda Catherine aliongea, akifuatilia ramani kupitia kompyuta yao.
“,Sawa mkuu, nusu saa inatosha, tutafika …”!,kamanda Gupta aliwatoa hofu, akaendelea kukanyaga mafuta ya difenda yao, gari ikafyatuka kama umeme, na kuwaacha midomo wazi, raia pamoja na askari wa usalama barabarani kandokando ya barabara, king’ora juu ya gari kilipiga kelele na kutahadharisha watumiaji wengine wa barabara kuwa makini na gari hilo la polisi.
…………………………………
Huwei;
Kikundi cha majambazi, maarufu kama “Casablanca gang ” ,kikichomilikiwa na bilionea Xavery, mfanyabiashara wa madawa ya kulevya, silaha pamoja na filamu chafu za ngono,kilianza safari kutoka Huwei, kuelekea Mexic, mahali iliposemekana Yuan Liang alitorokea huko.
Vijana sita, wawili wazungu, mmoja mjapani, na watatu Waafrika tena waswahili wa nchini Goshani, walikuwa wamepanda pikipiki zao, miwani rangi nyeusi pamoja na suti nyeupe, wakielekea kumtafuta Yuan Liang, wamshawishi ajiunge nao kwa lazima au hiari, kama walivyoelekezwa na bilionea Xavery.
Mexic; 1;00pm
Yuan Liang alikuwa ameketi kwenye kitanda chake,machale yalimcheza, kichwa chake hakikutulia hata kidogo, muda wote alikuwa anasimama na kuchungulia dirishani, kuchunguza usalama wake.
“,Siko sawa, kuna kitu sio bure! ninapaswa kujiandaa, muda wowote kuna kitu kinaweza kutokea …”,Yuan Liang aliongea, akatelekeza kompyuta yake pembeni, akasogelea mabegi yake ya nguo pamoja na vifaa muhimu. Akavaa jinsi yake aliyoitumia siku zote kwenye mauaji, akavaa mkanda wenye visu vidogo vidogo maarufu kama “magic knives ,akachukua bastola yake, akaiweka kiunoni,akavaa koti lake kubwa lililokaribia kumfika miguuni, akachukua miwani yake,akaivaa,akasogelea viatu vyake vyenye visigino
virefu,akavivaa,dakika tano tu zilitumika, tayali alikuwa amekamilika.
Akapekua tena begi lake, akauona mkoba wake, akaufungua, akachukua diski, kisha akarudisha mkoba na kulifunga tena begi lake, akatoka nje na kutokomea.
“,Hapa si salama tena, ngoja niondoke, nitarudi baadae, “aliongea baada ya kufunga mlango wa chumba chake, akaanza kupita koridoni, akakunja kushoto, akakunja kulia, akatoka nje ya hoteli aliyokuwa amepanga, akachukua pikipiki yake, mahali alipokuwa amepaki,akawasha, akaondoka haraka sana eneo lile kama upepo.
Akakamata barabara kubwa ya kuelekea mji wa Huwei,alikuwa anatafuta mahali salama, aweze kufanya biashara na serikali ya raisi wa nchi, bwana Jonsoni Mtemvu, ampatie diski, kisha yeye apate bilioni kumi kama walivyokubaliana.
“,Kuna kibanda cha baa, nilikipata jana, nikifika pale, nitamjulisha aniletee pesa mahali hapo, maana ni nje ya mji, hakuna watu wengi,tunaweza kufanya biashara vizuri tu, akinizingua, na mimi namzingua! “,Yuan Liang aliongea, akiwa amekamatilia pikipiki yake, akatoweka mbali na mji mdogo wa Mexic,akiwa ameshika njia ya kurudi jijini Costa, kupitia mji wa Huwei.
Baada ya robo saa, akiwa ametembea kilomita tatu, zikiwa zimesalia kilomita mbili tu afike mji wa Huwei, alifika katika baa aliyokuwa akiifikiria, akapunguza mwendo wa pikipiki yake,akapaki pikipiki yake, akashuka, akaisogelea kaunta.
“,Samahani dada,nikusaidie nini! “,muhudumu wa baa aliuliza.
“,Konyagi pamoja na maji,shilingi ngapi? “,Yuan Liang akauliza.
“,elfu kumi na tano tu …”,muhudumu akajibu, Yuan Liang akaingiza mkono mfukoni, akatoa noti mbili za elfu kumi kumi,akampatia muhudumu, kisha akarudishiwa shilingi elfu tano..
“,hapana, hiyo baki nayo, itakusaidia! “,Yuan Liang aliongea.
“,asante dada yangu …”,muhudumu akashukuru, akachukua chupa ya konyagi iliyojaa vizuri, akampatia na chupa ya maji ya Uhai kutoka nchi jirani ya Tanzania, akampatia. Yuan Liang akapokea, akasogelea meza moja yenye viti takribani sita, akaketi mahali hapo, akachanganya konyagi na maji kwenye glasi, akaanza kunywa, huku mziki wa rumba taratibu ukipigwa katika baa hiyo, na kupenya vilivyo katika moyo wa Yuan Liang. “,Nilipopatwa na ajari, nililia sana, fanya hima, nisaidieee!,”,
Ni moja ya mistari iliyopenya katika nafsi ya Yuan Liang, japo hakuwa mwanaume, lakini nyimbo ilimgusa bila kutegemea, akajikuta anatikisa kichwa kufuata biti la wimbo huo, ulioimbwa na bendi maarufu ya Msondo ngoma, kutoka nchini Tanzania, Afrika ya Mashariki. Akaendelea kunywa, akisubili muda ufike, aweze kumjulisha raisi Jonsoni Mtemvu, aweze kuleta pesa zake, ajipatie diski yake kabla hajaivujisha na kuweka mambo yote hadharani.
…………………………………
Huwei;
Kamanda Gupta aliendelea kukanyaga mafuta,wakafika mji wa Huwei, wakakata kona kidogo, wakanyosha barabara kubwa iliyopita pembeni ya jengo kubwa la Casablanca kasino, hawakusimama, wakanyosha moja kwa moja kuelekea mji ndogo wa Mexic, kilomita tano kutoka Huwei.
“,Kuweni makini, oneni! diski imehamishwa tena, adui yuko kilomita tatu kutoka mahali alipokuwa awali,kilomita mbili kutoka hapa tulipo, bila shaka machale yamemcheza! “,kamanda Philipo aliongea, wote macho yao yakahamia katika kompyuta.
“,Huyu mpuuzi anaonekana ni hatari eee!, lakini leo itakua mwisho wake! “,kamanda Kendrick aliongea,huku akiikoki bastola yake.
“,Bado dakika tano, tufike eneo hilo, kilomita mbili kutoka Huwei, lakini tutajuaje mahali diski ilipo?, na nani anayo? “,kamanda Gupta aliuliza.
“,tukifika,kompyuta itaonyesha,kumjua mtuhumiwa, itabidi tutumie mbinu za kipelelezi pamoja na uzoefu, muuaji anajulikana popote pale …”,kamanda Catherine alisisitiza, kisha ukimya ukatawala,safari ikaendelea …
dakika tano zikakatika,walikuwa bado hawajafika, dakika saba sikafika, ” ,link connected, the disc related is available in this area …,”limeunganishwa,diski inayohusiana inapatikana eneo hili)”,maandishi yalitokea katika kompyuta,ikaonesha ramani ndogo,ambayo hawakuielewa vizuri.
“,Tumefika,lakini hatuoni majumba mengi mahali hapa,hebu paki gari hapo baa,tuanze upelelezi…”,kamanda Catherine alitoa maelekezo,wakazima kin’gora wasiwashtue watu,wakachukua silaha zao ndogo,bastola pamoja na vizu,wakaweka katika nguo zao,wakatoka na kuisogelea baa,wakiwa makini kupeleleza kila sura waliyo iona!”,
…………………………………
Yuan Liang aliendelea kunywa bia yake,lakini ghafla alisikia mlio wa king’ora cha polisi kwa mbali,kelele za king’ora zikaongezeka kadri muda ulivyozidi kwenda,difenda ya polisi ikafunga breki kwa fujo, king’ora kikazimwa, difenda ya polisi ikakata kona na kupaki pembeni ya baa.
“,Shit! damu itamwagika, mimi ni wa kuniletea polisi? Jonsoni Mtemvu are you serious?, kwa nini umekiuka maagizo yangu, why? “,Yuan Liang aliongea pekeyake, akiwa amejaa na hasira ghafla, polisi wakashuka na kuingia ndani ya baa, waka angaza huku na kule, wakasogea kaunta, “muhudumu, tupatie juisi kila mmoja, mi pia nipatie na maji, “Kamanda Kendrick aliongea, macho yake yakiwa bize kumtazama raia wa kichina, aliyekuwa ameketi mita takribani tano kutoka eneo la kaunta…
“,Huyu namuhofia, wageni wote wa raisi, walikuwa raia wa kigeni! tena wanawake kama huyu, harafu mavazi ya mwanamke huyu si ya binadamu wa kawaida ,”kamanda Kendrick alipiga mahesabu kichwani mwake, akimtazama mwanamke ambaye alikuwa bize kunywa bia yake, bila wasiwasi wowote.
“,Saa yake ni ya kipelelezi, miwani yake ni automatiki mashine, inabatani mkono wa kulia wa jicho, viatu vyake, kisigino chake kinafanana na kile kisigino cha kiatu, katika hoteli zote mbili, nina wasiwasi na mwanamke huyu, tukienda vibaya, hakuna atakaye rudi salama nchini Tanzania “,kamanda Catherine aliwaza.
“,Huyu mwanamke mavazi yake, kama komandoo, sio huyu kweli, mbona koti kubwa kama jambazi, ila wachina sio watu wazuri, wanapiga karate kama mashine, tusipokuwa makini, kama ni yeye atatushambulia kabla hatujashtukia …”,kamanda Philipo aliwaza.
“,Gupta, Guptaa! yule mwanamke mi namuhofia, anaonekana tu ni hatari, kama sio yeye muuaji, ninani sasa eneo hili …?”kamanda Yasini alimnongoneza kamanda Gupta.
“,Hakuna, atakua ni yeye tu! “,kamanda Gupta aliitikia kwa sauti ya chini, mazungumzo ambayo hakuna mtu yoyote aliyasikia, zaidi yake na kamanda Yasini. Wote walikuwa bize wakitafakari,fikra zikiwatuma kuwa mwanamke aliyekuwa mbele yao, ndiye muuaji waliyekuwa wakimtafuta.
“,Vipi wateja wangu, vinywaji nimeshawaletea muda mrefu, chukueni mkanywe,!”,
“,aaa…a…aah sawa kabisa, asa…nte …”,
Muhudumu aliwashtua, wote wakashtuka, wakaitikia kwa kigugumizi,wakachukua vinywaji vyao, wakaenda kuketi meza moja na Yuan Liang, muuaji mkatili, chotara wa kichina,walikaa karibu naye, ili wampeleleze kwa undani zaidi.
“,Samahani dada, sijui unaitwa nani? “,
“,Hwan Lee …”,
“,Ohoo, kumbe unajua kiswahili, we unatokea nchi gani hapa Afrika mashariki …”,.
“,Goshani is my mother land, China is my father land! “,.
“,ohoo, nice! ,kumbe mchina pia, unaonekanaa…”,
“,Hahaahaa “,
Wote walicheka kwa kicheko cha kinafki, Catherine alikuwa ameshagundua mtu aliyekuwa mbele yao alikuwa ni hatari sana, aliuona mkanda wenye visu, visu ambavyo alivitambua vizuri sana, kisu kimoja cha aina hiyo kilitumika kukata kioo katika hoteli ya Serena, mapigo ya moyo wake yakaanza kukimbia kwa kasi sana.
“,Mbona mna maswali mengi, nyinyi ni polisi? “,
Yuan Liang aliwauliza swali la mtego, huku fikra zake zikiwa tayali kwa mashambulizi,kamanda Kendrick na wenzake hawakutegemea swali hilo, wakakosa jibu la kumpatia kwa haraka, wakaangaliana, wakakonyezana, Yuan Liang alizitambua fikra zao, akaendelea kujifanya mjinga mbele yao, awatie adabu vizuri, bila kujua kuwa askari mbele yake sio askari mdebwedo aliowazoea.
“,Uko chini ya ulinzi!, usitikisike, kaa hapo hapo …”,ghafla, bastola sita zilikua kichwani mwake, akatii maelekezo, akipiga mahesabu namna ya kuwashambulia, kisha atokomeee.
…………………………………
Vijana sita wa kundi la Casabranka gang walipoteza mwelekeo,hawakufanikiwa kumuona adui yao maeneo ya Mexic walikoelekezwa, hoteli zote kubwa za starehe walikagua bila mafanikio, wakafunga safari kurudi katika makazi yao ya Huwei, kumpatia ripoti bosi wao, bilionea Xavery.
Walifika katika baa waliyopita awali, wakataka wapoze kiu zao kwa mara nyingine tena,ghafla wakashtuka, kabla hawajapaki pikipiki zao, waliona gari la polisi, wakaogopa kupaki pikipiki zao, walipochunguza kwa makini, walimuona msichana waliyemtafuta, kwani jibaba wa mlango wa kasino alimtambua vizuri,akawajulisha wenzake…
Jibaba lile la mlango wa kasino la Casabranka lilipiga kelele, liliitambua vizuri sura ya Yuan Liang,wote wakashambulia, wakiwa bado juu ya pikipiki zao..
Yuan Liang akiwa amenyoshewa silaha, ghafla alisikia mlio wa pikipiki nje, alipogeuza shingo lake kutazama pikipiki hizo, alimtambua mmoja kati ya vijana sita, walivalia miwani myeusi na suti nyeupe, walipoiona sura yake, wakachomoa silaha zao, wakashambulia askari waliomnyoshea silaha Yuan Liang, Yuan Liang akatumia fursa hiyo kujiokoa, aliruka serekasi mara mbili, akapiga mateke sita,Catherine akapangua,bastola yake ikadondokea kule, kamanda Kendrick akalipangua teke hilo, lakini likamzidi nguvu, akaangukia upande wa pili, Gupta, Yasini pamoja na Philipo wakatandikwa na kuangukia kule, Yuan Liang alikuwa ameshika rimoti ya pikipiki yake, akaibonyeza huku anakimbia, pikipiki ikawaka, akakimbia na kuirukia, akapanda, akaondoka, huku vijana wa Casabranka gang wakimsaidia kushambulia, wakapiga risasi taili za difenda ya polisi, wakatoweka zao …
“,Jikaze, jikaze, ngoja nikusaidie, tayali wametuponyokaaa,ama zao ama zetu…”,kamanda Catherine aliongea, akasogea kumsaidia kamanda Kendrick, risasi ilipenya katika bega lake, alipojaribu kumzuia Yuan Liang asikimbie, akajikuta anagaagaa kwa uchungu.
Mexic;
Waziri mkuu, Januari Sasamba, alikuwa na masaa mawili, akiwa ndani ya mji mdogo wa Mexic. Alikodi chumba cha kifahari kwa siku moja tu,katika hoteli ya kitalii maarufu kama” Mexic garden hotel “,hoteli yenye mandhari mazuri ya kuvutia, hasa maua yenye rangi nyekundu na njano, yaliyopandwa kuzunguka maeneo yote ya hoteli,vipepeo wakiruka na kuzidi kupendezesha uzuri wa eneo hili.
Wageni wote katika hoteli hii walikuwa na nyuso za furaha,isipokuwa mtu mmoja tu, ambaye muda wote alijishika kichwani, akijikuna kipara chake, midomo yake ilicheza cheza, bila shaka alikuwa akiongea mwenyewe, si mwingine, ni waziri mkuu wa nchi ya Goshani, waziri ambaye alitambulika kila kona kwa utendaji wake mzuri serikalini, licha ya kuwa na siri nyingi moyoni mwake, siri ambazo iwapo zitagundulika, hakustahili kuendelea kuishi, adhabu ya siri zake nzito alizozificha ni kunyongwa …
“,Usafi uimarike,mpatieni huduma nzuri, aitangaze vizuri hoteli yetu …”
“,Sawa bosi! “,
“,Haya mnaweza kwenda, kuendelea na majukumu yenu …!”,
Alikuwa ni meneja wa hoteli ya Mexic garden,akizungumza na wafanyakazi wake, baada ya kuitisha kikao cha dharula,walipopata mgeni mkubwa kutoka serikalini, ndani ya dakika kumi tu, kikao kifupi kilimalizika, wote wakatawanyika …
……………… …………………
Waziri Januari Sasamba alisimama, akatembea huku na kule, akachungulia dirishani, hakuona chochote kile, zaidi ya vipepeo walioruka kufurahia maua, pamoja na watu wachache walioketi katika bustani, wakifurahia na familia zao, akatoka katika dirisha, akaketi kwenye sofa ndani ya chumba chake, chumba namba tatu, akachukua simu yake, akaanza kupangusa kioo cha simu yake,bila shaka alichunguza kitu fulani …
“,Mbona hapigi? Mbona hasemi nimkute mahali gani?, ok, let me call him, ngoja nimpigie! “,
Waziri, mheshimiwa Sasamba aliongea,akanyenyua simu yake, akaweka sikioni, akapiga, simu ikaanza kuita, ikaita tena mpaka ikakata,haikupokelewa,akapiga tena, ikaita, sekunde mbili tu ikapokelewa …
“,Haloo, naitwa Waziri Januari Sasamba, nimetumwa na muheshimiwa raisi kuleta pesa zako, kisha unipatie diski, nikuletee pesa wapi?? “,waziri mkuu, mheshimiwa Sasamba aliongea.
“,Pumbavu kabisa, wewe na raisi wako nyote mtakufa, nitawaua, kisha nitaanika kila kitu wazi! Haiwezekani mniletee polisi mimi, mnataka kuniua?, I say you can’t, you can’t kill me, hamuwezi kuniua hata siku moja! “,upande wa simu uliongea kwa kufoka, kisha simu ikakatwa.
“,Haloo, haloo, haloo! “,Januari Sasamba aliongea, akaongea tena, simu ilikuwa imeshakatwa. Hakuamini alichokisikia, mwili wake ukafa ganzi, akaanza kutetemeka kwa woga.
“,Nini kimetokea? mbona sielewi?, au the super three soldiers walitaka kumnasa?, tumekwishaa! bora tusingewaleta! kazi imekua ngumu kwelikweli!,”Januari Sasamba aliongea mwenyewe, kama mtu angemtazama, alivyokuwa akiongea peke yake, hakuwa na tofauti na kichaa, mheshimiwa waziri siku zote hakua mwepesi kukata tamaa, alinyanyua simu yake kwa mara nyingine tena, akampigia simu jambazi hatari wa kike,ambaye hakuwahi kumuona uso kwa uso hata mara moja, japo yeye ndiye alikuwa chanzo cha matatizo, kwa kumtafuta kahaba huyu kupitia mtandao wa Instagram ili amridhishe rafiki yake, raisi Jonsoni Mtemvu, bila kutambua kuwa mwanamke huyo alikuwa zaidi ya hatari, jambo ambalo lilimfanya ajutie kila siku iendayo kwa Mungu …
“,Nimesema sitaki maongezi na nyinyi! sitaki pesa zenu! hukumu yenu ni kifo tu, ……”,sauti ya kufoka ilisikika, simu ikakatwa, waziri Sasamba akanyongonyea, maneno aliyoyasikia yalikuwa machungu na mazito.Hakuwa na haja ya kupiga tena simu, alijilaza kwenye sofa bila kupenda,akiwa hajui nini cha kufanya…
………………………………
Nusu saa iliyopita;
Yuan Liang alifanikiwa kuponyoka mikononi mwa the super three soldiers, kwa msaada wa kikundi cha uhalifu, kikundi kilichojihusisha na biashara haramu maarufu kama Casablanca gang,wote kwa pamoja waliendesha pikipiki zao kwa kasi sana,wakanyosha barabara moja kwa moja,kuelekea mji wa Huwei,baada ya dakika kumi,walikuwa tayali wamekimbia kilomita mbili,wakafika katika kasino lao,makao makuu yao yaliyopatikana katika jengo lao kubwa la hoteli,wakaingiza pikipiki zao,wakaingia mafichoni,chini ya ardhi,kwenye mahandaki yaliyojengwa kwa siri miaka mingi iliyopita…
“,Nahitaji kuondoka!,nambie niwalipe kitu gani,pesa au kitu gani,kwa msaada mlio nipatia…!”,
“,Tunataka ujiunge na sisi,nd’o lengo kuu la sisi kukutafuta na kukusaidia…”,
“,Hapana,hilo halitawezekana!”,
“,tunaomba utii maagizo yetu,bila hivyo utakufa!”,
“,Mnanitisha si ndio?,death is nothing to me,siogopi kufaaa!,kabla sijafa mimi,nyote mtakua mmeshaoza na kuanza kunuka!”,
“,Unatutukana si ndio?”,
“,drii,drii,drii……”,
“,Hebu niache nipokee simu,cool down please!”,
Mazungumzo yaliendelea kati ya bilionea Xavery,kundi lake pamoja na Kahaba Yuan Liang,walishindwa kufikia makubaliano,Yuan Liang alikataa kujiunga nao,wakaanza kumtisha kifo,na yeye akawa mkali,hakuogopa mtu yoyote chini ya jua,aliahidi kuwaua kabla yeye hajafa kama wakijaribu kumshambulia,ghafla simu yake ikaita,akaipokea,kisha akaiweka sikioni.Ndipo alipokuwa mkali kama pilipili,mtu aliyempigia alikuwa na hasira naye,kwa kumtumia polisi,tofauti na walivyokubaliana,akakataa pesa zao,akakataa kuwarudishia diski yao,akaahidi kuwaua wote na kuweka siri zote hadharani…
Kundi la bilionea Xavery walisikiliza mazungumzo kati ya Yuan Liang pamoja na serikali ya raisi Jonsoni Mtemvu,wivu ukawajaa,tamaa ya pesa ikawaingia,wakawa na shauku kubwa ya kuungana na Yuan Liang,ili baadae wamgeuke,pesa wakizipata ziwe zao,akikataa wamteke,kisha awaambie mahali diski ilipo,waichukue wao…
“,Tutakupatia bilioni tano,ungana na sisi binti,unataka matatizo ee?”,
“,Wee mzee nakuheshimu ujue,nimesema sitaki sitaki,narudia tena sitaki,sitaki kushirikiana na nyinyi……”,
“,Unaleta jeuri ee?,fungeni milango yote ya chumba cha siri,mkamateni hakikisheni hatoki ndani…!”,
Milango yote ya chumba cha siri,milango ya umeme ikafungwa,vijana wa bilionea Xavery,vijana takribani arobaini wakamzunguka Yuan Liang,vijana wawili walikuwa wazungu, mmoja mjapani na wote waliobakia walikuwa Waafrika weusi, wenye miili iliyoshiba ipasavyo.
Yuan Liang alijiweka sawa kwa mapambano, aliingiza mkono kwenye mkanda wake, akachomoa kisu kimoja, akakishika kikamilifu, akavua miwani yake, alitaka isivunjike, akaiweka kwenye mfuko wa koti lake, akakunja ngumi, miguu yake ilijikunja kama inge, alijiandaa kwa mapigano, yoyote atakaye msogelea amtie adabu …
…………………………………
“,Haloo, haloo bosi, mambo yameharibika,mwizi wa diski kashambuliwa na polisi, anasema sisi ndio tumewatuma hao polisi, kwahiyo ameahidi kutuua muda wowote, harafu kila kitu atakiweka wazi kwa wananchi!! “,
Mheshimiwa Jonsoni Mtemvu alipigiwa simu na rafiki yake, aliipokea haraka sana, aweze kujua nini kilikua kinaendelea, alichanganyikiwa, kazi ya kurudisha diski yake katika mikono yake ilizidi kuwa ngumu, alijuta kwanini alitaka kuchepuka na kuangukia katika mikono ya kahaba Yuan Liang, alijuta kwanini aliwaleta the super three sordiers nchini kwake kufanya upelelezi wa kesi yake …
“,What!, hawa wanataka nini tena, sina pesa za kuwalipa kwa sasa, nina mambo mengii ……”,
“,Haloo bosi! “,
“,Haloo vijana! “,
“,Polee na matatizo, naskia diski yako imeibiwa, ina siri zote zako, mbaya na nzuri! “,
“,Ndio vijana, lakini sina pesa za kuwalipa! “,
“,Usjali, wewe ni mwenzetu, tumefanya biashara ya silaha na madawa ya kulevya muda mrefu,sina haja na pesa ndugu yangu, kesho natuma vijana, watatoka msituni katika maficho yetu, watakuja kukusaidia, diski itakuwa mikononi mwako! “,
“,Nitashukuru sana,sasa hivi ananitishia mpaka kifo,kama vita na iwe vita,poteleaa mbalii……”,
“,Sawa kabisa,itabidi afe huyo mwanaharamu,hawezi kukudhalirisha kiasi hiki…”,
“,kweli kabisa,ok,kwaheri bosi!”,
“,sawa,sawa,kazi njema!”,
Kikundi cha kigaidi cha M27,kikundi cha magaidi 27,magaidi waliouziwa silaha za serikali na mheshimiwa Jonsoni Mtemvu walisikia tetesi za mteja wao kujeruhiwa na kuibiwa diski yake muhimu,wakampigia simu,wakaahidi kumsaidia,akafurahi sana,hakutegemea msaada huo,aliwaamini sana magaidi hawa kwa umakini katika kazi,hawajawahi kumuangusha hata siku moja,mheshimiwa Jonsoni Mtemvu akatabasamu,akaketi kitandani,akaanza kufanya mazoezi ya shingo yake,akageuka huku,akageuka kule,moyo wake ulipata matumaini mapya kwa mara nyingine…
Casablanca hoteli;
Yuan Liang alizungusha macho yake kila kona,akitafuta upenyo wa kupita, haukuwepo, vijana arobaini wa bilionea Xavery walimzunguka ipasavyo, hakukuwa na uwazi wowote kumruhusu hata panya kupita.
“,Mkamateni! tukimpata tutapata pesa nyingi, amekataa kujiunga na sisi, sawa!, lakini inasemekana ana diski, mkamateni atwambie diski ya serikali ameificha wapi?,tukiipata mambo yatakua yamenyooka”,bilionea Xavery aliongea.
Vijana wake wakapata nguvu, mioyo yao ikajaa shauku ya kupata pesa nyingi, mikononi mwao walishika mapanga, visu na wengine nyundo ndogo, wakamvamia Yuan Liang wote kwa pamoja …
“,Kwachaaa! “,
“,Yalaaa …”,
“,Kwachaaa …”,
“,Uwiiiii …”,
“,Kwacha, kwachaaa …”,
“,Msimuogope, mvamieni nyote, shambulia! mwanamke mmoja tu ndiyo anawashinda, shambulia washenzi msipomkamata na nyie mnakufa! “,
“,Kwachaaa! “,
“,Yalaaa, uwiiii! “,
“,Kwachaaa, kwachaa! “,
“,Puuu, puuu “,
Vijana wa kundi la Casabranka gang, walimavia Yuan Liang, bila kutegemea, aliruka serekasi, akawapiga mateke yaliyovunja shingo zao,wakalia kwa uchungu,wakamvamia tena, huku wengine wakigaa gaa chini, wakampiga na panga zao akakwepa, wakampiga tena, akakwepa, akaruka serekasi na kutua upande wa pili,wakamfuata, wakarusha mateke yao akakwepa, wakarusha tena, akadaka mguu wa mmoja wao, akaupiga na kifuti, mguu ukavunjika,jambazi la kiafrika lenye kiduku kichwani likapiga kelele za uchungu, dakika kumi tu, vijana takribani kumi na tano, vijana wa bilionea Xavery walikuwa wamelala chini wakiugulia maumivu. Bilionea Xavery akafoka, akawahimiza vijana wake waendelee kumshambulia Yuan Liang,huku wengi wao wakisogea nyuma, Yuan Liang akaingiza mfukoni mikono yake, akatoa gloves,gloves zake hatari zenye misumali midogomidogo, akazivaa,kijana wa kijapani akiwa ameshika panga lake, akamsogelea Yuan Liang, Yuan Liang akaruka mateke mawili, yote yakapanguliwa, akaruka serekasi ya kinyume nyume, kisha akarudi na mateke manne mfululizo, matatu yakapanguliwa, moja likampata shingoni, kisigino cha kiatu chake kirefu kikamjeruhi,akaangukia upande wa pili kama mzigo, shingo yake ikivuja damu, vijana wote wakamvamia tena Yuan Liang, hapo ndipo walijuta kuzaliwa, walipigwa gwala, mateke, ngumi nyingi mfululizo, mapigo ya karate za kichina,wote wakadondoka chini, vijana wawili wa kizungu licha ya kupigwa mateke vifuani na kudondoka chini, walisimama tena, hawakukubali kushindwa, wakatupa visu vyao, wakakunja ngumi …
“,Nawaomba mniache niende, nitawafanya kitu kibaya, sitaki kuua mtu siku ya leo ……!”,Yuan Liang aliongea, huku jicho lake la kushoto likimtazama bilionea Xavery, jicho lake la kulia likiwatazama vijana wawili wa Kizungu, vijana ambao walikuwa wamesimama kizembe, huku wakipepesuka, Yuan Liang licha ya kuwapiga na mateke vifuani, alikuwa ameshawategua miguu yao ya kulia …
“,Hutoki humu ndani malaya weee! “,
“,You call me malaya eee!, mnanijua maskini wa kizungu nyie! “,
“,Yes, wewe malaya!,your finished, we are going to kill you now,fuck you son of bitch…! “,
Majambazi mawili ya kizungu yalijitamba, yalimtukana Yuan Liang matusi ya nguoni, matusi ambayo Yuan Liang aliyachukia siku zote,siku zote waliomtukana na kumwita malaya waliambulia kichapo kikali, sura ya Yuan Liang ilikuwa imekunjamana kwa hasira,akajitayalisha kutoa pigo kali la kuua mtu, wazungu wale wakamvamia, wakaruka mateke mawili angani,akapangua mateke yote, wakaruka tena, alikuwa anawasoma staili zao za mapigano, akapangua tena mateke yao…
“,Tayali nimeshaweka mapigo yao kichwani, wakijiroga wakaruka tena mateke, wamekwisha!”,
Yuan Liang aliongea peke yake moyoni mwake, bila kutambua fikra za Yuan Liang, wazungu wale wakaruka tena mateke, Yuan Liang akakwepa kwa kuinama chini kidogo ,kabla hawajatua chini, wakiwa bado hewani, akadaka miguu yao, akawagonganisha,wakapigana vikumbo, wakadondoka chini kama mizigo wakiugulia maumivu, akaruka serekasi, akatua kwenye matumbo yao, akachomoa visu viwili hatari, kutoka kwenye mkanda wake, akawachoma kwenye macho yao, macho yao yakatoboka, yakatokeza kwa nje, wakafa palepale, kifo cha kikatili …
“,Mnaniita malaya, hata huko kuzimu mlikoenda, msisuthubutu kuniita Malaya, nitawafuata huko huko, haya na wewe bosi wao!!, bado hutaki kuniacha nikaenda zangu ……”,
Bilionea Xavery aliongea kwa kigugumizi,hakufahamu Yuan Liang kama alikuwa mtu hatari kiasi kile, akamruhusu kwa shingo upande, akipiga mahesabu yake kichwani, bila kutambua kuwa Yuan Liang alikuwa na uwezo wa kufikiria fikra za mtu, kama akimtazama macho yake …
Yuan Liang akaanza kuondoka, baada ya kufika umbali wa mita tano, bilionea Xavery akanyanyua bastola yake,akajiandaa kumshambulia kwa risasi kahaba Yuan Liang,alipotaka tu kuvuta taiga ya bastola yake, Yuan Liang alichomoa kisu chake, akaruka serekasi na kurusha kisu hewani, kisu kikatua kwenye mkono wa bilionea Xavery, kikafyeka vidole vyake vinne, damu zikamwagika kama maji, bastola yake ikadondokea kule, akapiga kelele za uchungu na maumivu.
“,Siku nyingine ukisamehewa uwe na adabu, jinga kabisa wewe! “,Yuan Liang alitukana,akaondoka zake, akafika kwenye mlango wa chumba hiki cha siri, chumba kilichojengwa chini ya ardhi katika hoteli ya Casablanka, “,Shiit! milango ni ya chuma, tena imefungwa kwa umeme! anyway! hakijaharibika kitu,”Yuan Liang aliongea, akachukua kisu chake kimoja, kisu aina ya magic knife, kisu cha maajabu, visu vilivyojipatia umaarufu vita ya pili ya dunia kwa umahili wake, akaanza kukata chuma cha mlango, akatengeneza duara dogo lililomuwezesha kupita, dakika kumi tu alimaliza, akatoka nje na kutoweka, kurudi katika hoteli yake, hoteli ya hadhi ya chini, katika mji mdogo wa Mexic, kilimita tano kutoka mji wa Huwei.
Kamanda Kendrick alikuwa amelazwa kitandani,daktari wa jeshi la nchi ya Goshani alikuwa ameshika mkasi wake, akitoa risasi katika bega la kamanda Kendrick,baada ya kumchoma sindano ya ganzi, aliingiza mkasi wake kwa utaalamu wa hali ya juu eneo la jeraha, akaibana vizuri risasi, akaivutaaa …
“,Yalaaaa! “,kamanda Kendrick alipiga kelele.
“,Paaaaaa! “,
“,Keleleee, unapiga makelele kama uko leba ebooo! makelele yote utazani mwanamke anajifungua bwanaa! “,
“,Hahaaaaa …”,
Askari wote walicheka,kamanda Catherine alimchapa kibao kama Kendrick,alipipiga kelele baada ya risasi kuchomolewa, siku zote walipenda kutaniana, huku wakiwa wamebeba mzigo mzito wa mapenzi katika nafsi zao, kutokana na majukumu kuwabana,kila mtu alitunza siri yake moyoni mwake.
“,Lakini jamani, huyu adui si wa mchezo mchezo,hatuna budi kuongeza masaa arobaini na nane ya kukaa nchini hapa! “,kamanda Philipo aliongea.
“,Kweli kabisa, hili jinga lipone tu, turudi kazini kesho! “,kamanda Catherine aliongea, akichanganya na utani ndani yake.
“,Msijali, masaa mawili yajayo atakua vizuri,atakuwa na nguvu pia za kufanya kazi ndogondogo! “,daktari aliongea, huku akishona jeraha la kamanda Kendrick.
“,Sio kazi ndogo ndogo, bunduki atashika, vita atapigana, akifa kazini sio mbaya, atakufa kishujaa, “kamanda Catherine aliendelea kuongea kwa utani.
“,Kweli kabisa, uko sahihi, hata mimi nilikatika miguu yote na mikono, lakini nilipigana vita vya kagera na kushinda ……”,kamanda Philipo aliongea, wakizidi kutaniana, huku kamanda Gupta pamoja na kamanda Yasini wakiwa pembeni, wakitazama vituko vya wenzao, wapelelezi kutoka Tanzania, na kujikuta wakicheka muda wote …
“,Na wewe naye toa uongo wako huko, this is too much! umetudanganya sana, inatosha, umefika mbali ……”,kamanda Catherine aliongea, akamkejeli kamanda Philipo.
“,Hahaahaaa ……”,wote walicheka sana kwa mara nyingine tena, kamanda Kendrick alikuwa na furaha kuwa na wenzake karibu, licha ya jeraha alilokuwa nalo, hakuhisi maumivu, huku nguvu zikirejea kadri muda ulivyozidi kwenda …
…………………………………
Msitu wa mikoko;
Hali ya ubaridi ilikuwa imetawala ndani ya msitu wa mikoko, msitu uliopatikana mashariki mwa nchi ya Goshani, kandokando na bahari ya hindi.Magaidi wa M27 walianza kujiandaa,wakapakia silaha zao ndogo ndogo, bastola pamoja na mabomu, wakaanza kutoka msituni, kwenda kumsaidia rafiki yao, raisi wa nchi ya Goshani, mheshimiwa Jonsoni Mtemvu, msitu huu wa kihistoria, ulihusika katika vita ya kupigania uhuru mara mbili mfululizo, mara ya kwanza, Waafrika na Waingereza walipigana mwaka 1990,Wachina wakatoa msaada katika vita, wakapigana na Waafrika, wakashinda, wakafanya figisu na kuua watawala wa Kiingereza waliokua madarakani, kisha wao wakatawala koloni hili kwa miaka minne tu,Waafrika walikubali kutawaliwa na Wachina kwa miaka minne tu,huku wakiendesha harakati za siri kupigania uhuru wao, wakaingia msituni, wakiongozwa na wazee wawili machachali walioshiriki vita ya kwanza na Waingereza,mzee Ishimwe pamoja na mzee Mpuzu Yahimana, wakapigana vita, wakashinda vita hiyo, Goshani ikapata Uhuru mwaka 1994 chini ya wachina,mzee Mpuzu Yahimana akawa raisi,mzee Ishimwe akawa waziri mkuu, wote wakiwa na miaka takribani sabini, lakini hawakuwafukuza wakoloni wa kichina, walikaa nao kwa miaka mitano wakiendesha shughuli mbalimbali, viwanda na mashamba makubwa ya mkonge.
Idadi ya watu ikaongezeka nchini Goshani,baada ya kupata uhuru, walizaliana kwa kasi bila kuzingatia uzazi wa mpango, sera ya kuzaa watoto wawili tu chini ya uongozi wa kichina ikafutwa, Waafrika wakakosa ardhi, serikali ikaamua kuwafukuza wachina wote nchini Goshani ili kupata makazi ya kutosha, huku baadhi wakiwa tayali wameoa Waafrika, akiwemo aliyekuwa gavana wa kichina, Liang Xung, hakutaka kurudi kwao na ngozi nyeusi, pamoja na mtoto wake mwenye asili ya Kiafrika, akatoroshwa na helikopta yake pamoja na ndugu zake wa kichina usiku wa manane, mke wake Eliza akashtuka asubuhi hakumkuta mume wake Liang Xung wala ndugu zake, akamwachia mtoto aliyeitwa Yuan Liang mwenye umri wa miezi kumi tu,mama yake hakutegemea jambo hilo, akapata presha na mshituko kwa kuachwa na mume wake kipenzi na kufa palepale, Yuan Liang akalelewa na kanisa katoriki mpaka kukua kwake …
Mexic; 6:20pm
Msichana mrembo, hatari sana, mwenye sura nzuri ya kichina, sura isiyo chosha kumtazama,alipaki pikipiki yake, baada ya kutumia dakika kumi na tano tu kwa pikipiki yake, kutoka Huwei mpaka Mexic, aliteremka kwenye pikipiki yake, akaipaki mahali alipoelekezwa na mwenyeji wake, kisha akaanza kuusogelea mlango wa chumba chake …
“,Nilijua tu, machale yalinicheza na kutoweka mahali hapa, kumbe nasakwa na polisi, isitoshe hawa wahuni tena walikuwa wananitafuta, eti nijiunge nao pumbafu kabisa!, mimi sio muuaji, naua watu wabaya, nawaibia pesa na mimi nipate kuishi, siwezi kujiunga na majambazi tena!, dhambi nilizofanya miaka iliyopita zinatosha, ninapaswa kujua ukweli kuhusu wazazi wangu kwa sasa, kazi hii ya diski ikiisha, nikapata pesa zangu, naondoka haraka sana kuelekea China, lazima niwafahamu wazazi wangu………,Yuan Liang aliongea peke yake moyoni mwake, akipita katika korido ndefu, kuelekea katika chumba chake.
“,Ohoo, umerudi mwanangu, siku nzima tulileta chakula haukuwepo, tukuletee chakula gani usiku huu? “mama aliyempokea Yuan Liang, mmiliki wa hoteli hii ya uswazi alimuuliza, baada ya kukutana uso kwa uso koridoni,akimtazama Yuan Liang chini mpaka juu,akifikiria jambo fulani …
“,Polee na kazi! maana nyie askari kazi zenu simchezo, muda wote mnakimbia huku na kule, usiku na mchana ………”,mama yule aliongea tena, alifikiri Yuan Liang alikuwa askari, kumbe sivyo, alikuwa amefikiria mbali sana.
“,Usjali mama yangu, majukumu tu ya kazi yamenibana, niletee ndizi nyama na coke ya baridi kama ipo ……”,Yuan Liang aliongea, akaufungua mlango wake, akaingia ndani ya chumba chake.
“,Coke ya baridi ipo, usjali kabisa, nakuletea ndani ya dakika tano mwanangu, ule ushibe ……”,mama yule aliongea, kisha akatoweka, akamwacha na maswali mengi kichwani.
“,Hakuna kitu nilichokuwa nakipenda duniani kama kuwa askari na kuitumikia serikali, lakini sasa hivi kila kona kumejaa waovu, sina wa kumwamini, hiyo serikali tu, raisi wake anaua albino, anauza silaha, madawa ya kulevya na isitoshe ni mzinzi, je askari wake si ndio wanaharamu kabisaa! bora niishi hivi, nikiiwaibia hawa matajiri, nipate pesa,tena huyu mpuuzi atanitambua mimi ni nani, leo namfata mpaka ikulu, si ananichukulia natania, naenda mpaka ikulu usiku huu ……”,Yuan Liang aliongea, akachukua visu kwenye begi lake, visu takribani kumi, akavipachika kwenye mkanda wake, mahali ambapo alitoa visu na kuvitumia kwenye mapambano na kundi la Casablanca gang…
Akachukua bastola yake, akachomoa magazini, akapachika magazini nyingine, akachomoa kitambaa chake kidogo, leso rangi nyeusi, akapaka mafuta kidogo ya bunduki,akaanza kusafisha bastola yake taratibu, akipiga mrusi na kuchezesha kichwa chake, kuendana na biti la mlio wa mrusi wake.
“,Ngo ngo ngo, ngo ngo ngo, hodiii… “,ghafla mlango wa chumba chake ulianza kugongwa,akachomeka bastola yake kwenye koti lake, akausogelea mlango wake kwa umakini, kwa sasa hakupaswa kumwamini mtu yoyote yule …
Alichungulia mlangoni, kwenye nyufa ndogo za mlango, akafungua mlango, alimtambua mgeni wake, aliyekuwa akigonga.
“,Chakula chako hiki hapa, vyombo nitachukua kesho……”,mama yule aliongea,alitokea kumpenda na kumjali sana Yuan Liang,kwani alikuwa mteja wa kwanza kumpatia pesa nyingi,tangu aanzishe hoteli yake yenye vyumba vitano tu vya kulala wageni.
“,Usjali mama,nikimaliza kula nitatoka kidogo,nitakupitishia vyombo vyako!”,Yuan Liang aliongea,akapokea chakula chake alichoagiza,kisha akafunga mlango.
“,Sawa mwanangu!”,sauti ilisikika upande wa pili,mama yule alimjibu Yuan Liang,kisha akaondoka zake.
…………………………………
Gari kumi za kifahari,zenye rangi nyeusi,maarufu kama benz,zilitoka msituni,kupitia njia za siri ambazo walizifahamu wao wenyewe tu,njia ambazo zilikuwa na makona mengi,barabara nyingi zikiwa zimekutana msituni,kama ni mgeni wa msitu huu,akipita barabara moja,anaweza kutembea baada ya muda,akajikuta anarudi palepale alipoanza safari awali.
Gari la mbele,lenye bendera ndogo nyekundu,karibu na taa ya mbele mkono wa kulia,bendera ikiwa na mchoro wa bunduki pamoja na silaha mbalimbali za kivita,iliongoza msafara,ilishika barabara ya vumbi msituni,ikakunja kushoto,ikakunja kulia,ikanyosha tena barabara ya vumbi,ikakutana na barabara sita mbele, ndani ya msitu,ikapita barabara ya pili kutoka mkono wa kulia,barabara ambazo zilitengenezwa makusudi kuwachanganya maadui wanaoingia katika msitu wao wa mikoko,gari hilo lenye bendera ya M27,bendera ambayo wengi walizani ni pambo tu la gari,ilitembea kwa kasi sana,ikakutana na barabara nne,ikapita tena barabara ya pili kutoka mkono wa kulia,ikanyosha tena barabara,ikakunja kulia,ikakunja kushota,uso kwa uso na barabara kubwa ya lami,barabara kuu inayoelekea nchi jirani mkono wa kulia, Tanzania na Kenya, huku mkono wa kushoto ikielekea katikati ya jiji la Costa, nchini Goshani.
Dereva akaangalia kushoto,akaangalia kulia,barabara ilikuwa imejaa magari,akaangalia tena kushoto,magari yalikuwa yamepungua,dereva akapata upenyo,akakata kushoto, akaingia barabarani,magari yote yakamfuata,magari kumi,gari la kwanza lilikuwa na magaidi wa tatu,mkuu wa kikundi, mlinzi pamoja na dereva, gari lililofuatia lilikuwa na magaidi wanne, huku magari mengine yaliyofuata nyuma yakiwa na magaidi wawili wawili kila gari, safari ya kuingia jiji la Costa, nchini Goshani, ilianza …
…………………………………
Mexic; 8;02
Yuan Liang alikuwa amejiandaa kama kawaida yake,alikuwa amevaa suruali nyeusi ya jinzi, viatu vya visigino vyeusi, viatu vyenye kifaa maalumu cha kukata mawasiliano ya simu, pamoja na vifaa vya umeme.Koti lake jeusi lilikuwa mkononi mwake,akatoka nje ya chumba chake, akapanda pikipiki yake, akavaa koti lake, akawasha pikipiki na kuondoka …
“,Nusu saa tu inanitosha, napaswa kuwa jijini Costa, niingie Ikulu wakiwa bado macho, nidhihirishe ukomando wangu,si wananitumia polisi bwanaa!,nawafata polisi hukohuko”,
Yuan Liang aliongea, akiwa amekamatilia uskani wa pikipiki yake, akiendesha na kufyatuka kama ndege, huku akikwepa magari kwa ustadi wa hali ya juu,wakati mwingine akirusha pikipiki yake, ikatua upande wa pili, alipokutana na foleni, ndefu, akawaacha watu wengi midomo wazi …
“,Mungu wangu weee! anaendeshaje huyu, si atakufaa! “,mwanamke mmoja aliongea,akiwa na familia yake ndani ya gari, wote macho yakiwatoka, wakitazama nje ya gari, licha ya magari kuwa kwenye foleni, Yuan Liang aliruka juu ya magari na kuendelea na safari yake, akapita juu ya magari, akawaacha watu wote midomo wazi … …………………………………
Hospitali ya jeshi;
Kamanda Kendrick alikuwa amefungwa bandeji begani, alikuwa amepata nafuu na kuruhusiwa,akatoka nje ya chumba cha hospitali,akiwa sambamba na kamanda Catherine, nyuma yao alikuwa kamanda Gupta, Yasini pamoja na kamanda Philipo.
“,Tunaelekea wapi? “,kamanda Kendrick aliuliza.
“,Hotelini, tunaenda kupumzika, kesho asubuhi na mapema, kazini kama kawaida, kumsaka huyu malaya! “,kamanda Catherine alimjibu kamanda Kendrick, akamtukana Yuan Liang kwa kumwita malaya, tusi ambalo Yuan Liang alilichukia, kama angekuwepo, sijui ingekuaje ,tungeongea mengine kabisa …
“,Kweli kabisa, cha muhimu kamanda Philipo awahi kuamka, asinywe pombe na kulala na viatu, ataharibu kila kitu ……”,kamanda Gupta aliongea kwa utani.
“,Hahahaa, “wote walicheka,wakaingia ndani ya difenda yao, wakatoweka …
…………………………………
Ikulu; 8;50pm
Yuan Liang alipaki pikipiki yake, katika maegesho ya jiji(public parking),kilomita moja kutoka ikulu ya raisi wa nchi ya Goshani.
“,Nitaichukua pikipiki yangu saa tano usiku, pesa yako hii hapa, linda pikipiki hii kama dhahabu ……”,
“,Sawa bosi, ondoa shaka! nd’o kazi yetu hii ,chenji yako hii hapa…”,
“,Hapana, hiyo utamuhonga wifi,baki nayo tu…”,
“,Hahaa, “
Wote walicheka, Yuan Liang alitaniana na mlinzi, eneo la kupakia magari na pikipiki katikati ya jiji, karibu na ikulu ya raisi, akaanza kuondoka,akavuka barabara, akaingia upande wa pili wa barabara, akakunja kulia, akaanza kufuata njia ya kwenda ikulu …
“,tapu! “,mlio ulisikika, alibonyeza batani ya miwani yake mkono wa kulia,miwani iliyounganishwa na kifaa maalumu cha kukata mawasiliano,alikata mawasiliano ya simu,kamera zote za ulinzi ikulu zikazima ghafla …
Ikulu; 9:02pm
Mama Zainath, mke wa raisi Jonsoni Mtemvu, alikuwa ameketi sebuleni, akifuatilia kipindi cha taarabu kwenye televisheni yake kubwa. Mawazo yalikisumbua kichwa chake, akimfikilia mume wake, tangu avamiwe, ajeruhiwe na kuibiwa diski ya saa yake, amekua mwenye wasiwasi,akiwa hana furaha hata kidogo, muda wote alipokea simu kwa siri, tofauti na jinsi alivyomzoea.
“,Haiwezekani!, kuna kitu, sio bure, kuna kitu, ngoja nimpigie rafiki yake, waziri Januari Sasamba,kesho tukutane, tuzungumze, atakua anafahamu matatizo ya mume wangu ambayo hataki mimi nijue au mtu yoyote ajue, haiwezekani akitaka kuongea na simu, tutoke nje, yaani hata mimi mke wake!, haiwezekani kabisa, mbona hakua hivyo hapo kabla?…”,mama Zainath alifoka peke yake,akaingiza mkono kwenye matiti yake, akaichomoa simu yake,akabonyeza namba kadhaa, akaweka simu sikioni.
“,Network error! ,try again later …(mtandao unasumbua,jaribu tena baadae) “,sauti ilisikika, hakuamini alichokisikia, akabonyeza namba nyingine, akapiga tena.
“,Network error!,try again later…(mtandao unasumbua, jaribu tena baadae) “,sauti ya simu yake ilisikika kwa mara nyingine tena,”,mbona hapatikani?, anyway, nitamtafuta kesho! lazima nionane naye ainusuru ndoa yangu eboo! “,mama Zainath aliongea, huku akirudisha simu yake, katikati ya matiti yake,akajilaza kwenye sofa, akaendelea kuangalia televisheni.
“,Bosi, bosi, bosi, kuna tatizo! “,askari mkuu wa kitengo cha ulinzi ikulu aliingia kwa fujo,akiita bila mpangilio.
“,tatizo gani?, ambalo linakufanya uingie bila hodi wala nidhamu katika nyumba ya muheshimiwa bosi wako ……”,mama Zainath aliongea, huku akimtazama kwa jicho baya lililojaa dharau, askari mkuu wa kitengo cha ulinzi ikulu.
“,Bosi, mfumo wa ulinzi ni hafifu kwa sasa!, kompyuta zote za ulinzi zimezima ghafla, kamera za ulinzi zimezima na zenyewe,kwahiyo asitoke mtu nje wala kuingia ndani kwa sasa, fungeni milango na madirisha, sisi tutakua nje tunadumisha ulinzi …”,askari yule aliongea, sura yake ikiwa yenye kujaa wasiwasi.
“,Ok, sawa, ngoja nimpigie injinia wetu, aje atengeneze na kurekebisha tatizo hili …”,mama Zainath aliongea, akachukua simu yake, akaitafuta namba ya injinia wa mifumo yote ya umeme ikulu ya raisi.
“,Hata mawasiliano hatuna,hatuwezi kufanya mawasiliano yoyote yale !…”,askari yule aliongea, mama Zainath akampuuzia, akaendelea na shughuli zake za kupiga simu.
“,Network error!, try again later, (mtandao una matatizo, jaribu tena baadae) “,sauti ya simu ilisikika, mama Zainath akakunja sura, akayaamini maneno ya askari wake, wasiwasi ukamvaa ghafla.
“,Hapa kuna shida, sio bure! Ok, kampatie taarifa mheshimiwa raisi, katika chumba chake cha matibabu …”,mama Zainath aliongea,kisha akaendelea na shughuli zake za kuangalia taarabu, huku akijiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu..
…………………………………
Yuan Liang akiwa amevaa gloves zake zenye misumali midogo midogo, aliutazama ukuta mrefu wa ikulu, ukuta wa futi hamsini kwenda juu, huku juu yake kukiwa kumepambwa na waya za umeme (electric wire fence),ambazo zilizidi kuimarisha ulinzi.
Yuan Liang alitazama mita mia moja mkono wa kulia, hakuona kitu chochote, zaidi ya kamera ambazo alikuwa tayali ameshakata mawasiliano yake, pamoja na taa kubwa ambayo iliangaza eneo lote la ikulu, bila kuficha kitu chochote, mende wala panya yoyote yule. Akatazama tena mita mia moja mkono wake wa kushoto, hakuona askari yoyote yule,akatabasamu, akaanza kupanda ukuta, akikwea na kujivuta kama nyani, akitumia gloves zake ambazo zilinasa ukuta na kumuwezesha kupanda bila tatizo lolote lile, ndani ya dakika tano tu, alikuwa amefika juu, usawa wa nyaya za umeme, akaruka serekasi, akatua upande wa pili wa ukuta, ndani ya ikulu ya raisi wa nchi ya Goshani.
“,Puuuuuu! “,kishindo kilisikika, Yuan Liang alifika chini kama mzigo, akalala chini, akajificha kwenye maua kama nyoka, akiwa kimya kama maji mtungini.
“,Kamanda Amiry! “,
“,Yes kamanda Junior, nambie! “,
“,Hujaskia kishindo nyuma ya nyumba, siunajua mifumo ya ulinzi, kompyuta na kamera zimezima, twende tukaangalie kishindo hicho ni cha nini,isije ikawa tumevamiwa!”,
“,Kweli kabisa kamanda,”
“,John na Jacob, nawaomba mara moja! “,
“,Sawa kamanda Junior, haina shida, tunakuja! “,
“,Kuna kishindo kimesikika nyuma ya nyumba, piteni mkono wa kushoto, mimi na Amiry tutapita mkono wa kulia, silaha zenu ziwe mkononi, adui yoyote shambulieni, tutakuja kuwasaidia …”,
“,Sawa afande …”,
Kundi la askari walinzi wa ikulu wakiwa wameshika silaha zao,walielekea nyuma ya nyumba, ikulu ya raisi haraka iwezekanavyo,macho yao yalikuwa makini, kuangaza kila kona ya jengo, mahali ambapo adui anaweza kujificha.
Yuan Liang alinyanyua shingo yake, hakuona askari yoyote yule, akanyanyuka, akatembea mita takribani tano, akajibanza kwenye ukuta, akachungulia, aliwaona askari wawili, wakija wanakimbia, akajiandaa kwa shambulio,askari wale wakapitiliza, baada ya mita takribani mbili mbele wakasimama, wakaangalia huku na kule, hawakuona mtu, wakaangalia kwenye maua hawakuona mtu, zaidi ya maua yaliyokanyagwa na kuvunjika. Wakahisi uwepo wa mtu nyuma yao, wakageuka kizembe, bila tahadhari yoyote ile, walipigwa ngwala wowote wawili, silaha zao wakazitupa kule, Yuan Liang akazidaka zikiwa hewani kwa ufundi wa hali ya juu.
“,Yalaaa…a …”,
“,Acha kelele wapuuzi nyie kabla sijasambaratisha ubongo wenu, mikono juu nasema, mikono juu! geukeni, ongozeni njia mpaka chumba cha raisi mshenzi dunia nzima, atakaye kiuka maagizo yangu, namwaga ubongo wake mara moja …”,
Yuan Liang alifoka, akiwa ameshika bunduki mbili za smg, moja mkono wa kulia, nyingine mkono wa kushoto, kamanda John pamoja na kamanda Jacob, wakatii amri, wakaanza kutembea, wakifuata maelekezo ya Yuan Liang.
“,Angalia chini ya magari, chini ya magari yote matatu! “,kamanda Junior aliongea.
“,Hakuna kitu,kila mahali kuko salama! “,
“,Chini ya bustani hizo za maua! “,
“,Kote hakuna kitu, labda kwenye bustani zile pale, lakini nazani kamanda Jacob na John wameshamaliza kukagua na tayali wamesharudi getini! “, “,Basi sawa, twende getini tukaendelee na majukumu ya ulinzi !”,
Mazungumzo kati ya kamanda Amiry pamoja na kamanda Junior yalimalizika, wakaacha zoezi la ukaguzi, wakaanza kutembea kwa maringo, kurudi getini, bila wasiwasi wowote, wakipiga stori mbili tatu, bila kutambua kuwa wenzao walikuwa chini ya ulinzi.
…………………………………
Mama Zainath alishtukaa, akaamka kwenye sofa kama mwendawazimu,jasho jembamba lilimtoka, akatetemeka kama mgonjwa wa degedege, moyoni alimwomba Mungu kimoyomoyo, akamkumbuka kwa mara ya kwanza tangu waingie ikulu yeye na mume wake …
“,Shiiii!ukipiga kelele umekwisha! ungana na hawa maboya, atakayejaribu kutoroka, atakufa! “,Yuan Liang alifoka kwa sauti ya chini, sauti iliyomezwa na mziki wa taarabu kwenye televisheni, macho yake yalitazama kila kona ndani ya sebule, “TOILETS “,aliona kibao kizuri, chenye maandishi rangi ya dhahabu, akatafakari cha kufanya, akapata jibu.
“,Nyote simameni, tembeeni kuelekea chooni, ole wenu nisikie mtu yoyote anapiga kelele, mtanitambua! …”,Yuan Liang aliongea, akiwa amewanyoshea silaha askari pamoja na mama Zainath, baada ya dakika mbili walikuwa mbele ya vyoo pamoja na mabafu. Akatabasamu, aliziona funguo za vyoo na mabafu katika vitasa vya mlango …
“,Nikujue inisaidie nini, jambazi mkubwa wewe, nakuhakikishia hutoki humu salama ……”,kamanda John aliendelea kujibizana na Yuan Liang, bila kuogopa mtutu wa bunduki karibu na kisogo chake, mama Zainath akiwa amejawa na uoga, akaufungua mlango wa choo, ukabaki wazi kama hotelini …
“,Puuuu, puuuu ……”,kishindo kilisikika, Yuan Liang aliruka mateke mawili, moja likampata kamanda John kwenye kichwa,lingine likampata kamanda Jacob shingoni, wote wakadondokea chooni kama mizigo, kiatu cha Yuan Liang chenye visigino virefu kikawajeruhi, damu zikawatoka kama maji, kila mmoja akiugulia maumivu, kamanda John alijishika kichwani, kamanda Jacob alijishika shingoni …
“,Na wewe mwanamke ingia humo chooni,kabla sijakufanya kitu kibaya kama hao skauti wenu, na nyie sisimizi, ole wenu mumfanyie kitu kibaya huyo mwanamke huko chooni, nitawakata mipira yenu ya kukojolea bila huruma, mtanikumbuka mpaka kabulini ……”,Yuan Liang aliongea, akafunga mlango, akachomoa funguo kwenye kitasa, akaziweka katika koti lake, akaanza kutembea, kukitafuta chumba cha raisi Jonsoni Mtemvu.
…………………………………
Akiwa amejawa na tabasamu, aliruka na kufanya mazoezi katika chumba chake, aliinyosha shingo yake, akaizungusha kulia na kushoto, mbele na nyuma, akazidi kutabasamu, afya yake ilizidi kuimarika siku hadi siku. Kitendo cha marafiki zake, kundi la kigaidi la M27 kumpigia simu masaa takribani matatu yaliyopita,wakampatia taarifa ya ujio wao kilizidi kumfurahisha.Akasahau kabisa salamu za vitisho kutoka kwa rafiki yake waziri Januari Sasamba, vitisho ambavyo vilitoka kwa Yuan Liang, baada ya kuwasiliana naye kwenye simu …
“,Hapana bosi, mifumo ya ulinzi yote haifanyi kazi, kamera za ulinzi zimezima, kompyuta za ulinzi zimezima, isitoshe hata simu hatuwezi kupiga wala kupokea simu! “,
“,Unasema? ina maana kuna attack yoyote inataka kufanyika ?,ina maana tumevamiwa? “,mheshimiwa Jonsoni Mtemvu aliongea, uso wake ulibadirika ghafla, furaha yake ikapotea,akakumbuka vitisho vya kifo kutoka kwa Yuan Liang, akazidi kuchanganyikiwa!
“,Shiiii! kaa kimya mheshimiwa, sikia kelele huko sebuleni, chukua bastola yako, atakaye ingia humu chumbani kwako, kama ni adui mshambulie, ngoja mimi nikaangalie nini kinaendelea ,vipi kuna nesi wala daktari yoyote mahali hapa……”,askari mkuu wa kitengo cha ulinzi ikulu aliongea,bastola yake ilikuwa mkononi,huku akiusogelea mlango aweze kutoka nje ya chumba cha siri.
“,Hapana, wote wameondoka, watarejea tena kesho! “,raisi alijibu kwa wasiwasi, huku akisikia sauti za kelele sebuleni, sauti ambazo zilichanganyikana na mziki wa taarabu, akachomoa bastola yake chini ya kitanda, akajiandaa kushambulia kiumbe chochote kile kitakacho ingia chumba cha siri, chumba cha matibabu ya raisi.
Ikulu; 9:45
Kamanda Amiry, pamoja na kamanda Junior, wakaingiwa na wasiwasi. Mkuu wao wa kitengo cha ulinzi, tangu aingie katika chumba cha siri,chumba cha matibabu ya raisi, saa moja lilikuwa limepita, alikuwa bado hajarejea. Kamanda John pamoja na Jacob,na wenyewe nusu saa ilikuwa imepita, bila kujulikana mahali walipoelekea,vichwa vyao vikajaa maswali yasiyokuwa na majibu.
“,Kichwa hakijatulia kabisa, kuna tatizo, sio bure, haiwezekani tangu aingie ndani mpaka sasa hajatoka, kuna kitu sio bure! “,kamanda Amiry aliongea.
“,Wewe baki hapa getini, ngoja mimi niingie ndani nikajue nini kinaendelea, inawezekana kamanda John pamoja na kamanda Amiry wako ndani! “,kamanda Junior aliongea, akatoka kwenye chumba cha ulinzi, pembeni ya mlango, akatembea kuelekea ndani,ajue nini kinaendelea.
Baada ya dakika tano, alikuwa mlangoni, akafungua kitasa kikagoma, akazungusha tena kitasa, kikagoma. “,Au tayali wamelala, mbona wamefunga kitasa kwa ndani, na kama wamelala, kwanini walale wakati mkuu wetu wa ulinzi akiwa ndani?, haiwezekani, kuna tatizo …”,kamanda Junior aliongea, akabonyeza kengele kwenye ukuta wa mlango, akasubili waweze kufungua, dakika mbili zikapita, tatu zikapita, hakuna aliyefungua mlango. Akabonyeza tena kengele ya ukutani,akasubili,dakika tano zikapita, hakuna aliyemfungulia mlango, akakata tamaa, akarudi kwenye kibanda chao cha ulinzi, akiwa amechanganyikiwa …
…………………………………
Huwei; 10;02
Bilionea Xavery alikuwa ameketi kwenye sofa, katika ofisi yake, ndani ya hoteli ya Kasabranka. Daktari wake aliendelea kumpatia matibabu,baada ya vidole vyake vya mkono wa kulia, kufyekwa na kisu cha Yuan Liang,vidole vikabaki kama mgonjwa wa ukoma.
“,Haijalishi umeumia kiasi gani, lakini natambua kuwa nimeumia zaidi yenu,hivyo basi! usiku huu kabla jua halijachomoza hakikisheni mnamkamata msichana huyu, msakeni kila kona, pembe zote za nchi hii, Huwei, Mexic mpaka jiji la Costa! Mkirudi mahali hapa hakikisheni mnavidole vyake vya mkono wake wa kulia, pamoja na diski ya serikali, yaani ni kisasi juu ya kisasi! tumeelewana? “,bilionea Xavery aliongea,huku akiugulia maumivu makali yasiyo elezeka.
“,Ndiyo mkuu! “,vijana wake, waliitikia,huku nyuso zao zikiwa zimejawa na hasira, wakiwa wamepania kulipiza kisasi, baada ya kuaibishwa ndani ya kasri lao.
“,Haya poteeni! “,bilionea Xavery, bosi wa kikundi cha majambazi cha Kasabranka gang aliongea,vijana wake wote wakapotea mbele yake,vijana takribani ishirini ambao hawakupata majeraha makubwa, wakiongozwa na jibaba la mlango wa kasino,lenye mwili wa kutisha usio na faida yoyote ile, Yuan Liang alilipiga na kulitegua mguu licha ya umbo lake dogo la kike.
………………………………
Ikulu;
Yuan Liang alijibanza ukutani,akachungulia pembe zote za sebule, kulia na kushoto, akachungulia tena na tena, hakuona mtu yoyote yule, akafuata korido ndefu, akaona ngazi iliyoelekea ghorofani, mahali kulipokuwa na vyumba pamoja na ofisi ya raisi,akapanda ngazi, bila kutegemea, akakutana uso kwa uso na askari mwenye bunduki, akawekwa chini ya ulinzi, Yuan Liang alikuwa ameshatelekeza chooni bunduki zake mbili alizowanyanganya askari polisi.Akanyosha mikono juu, akipiga mahesabu namna ya kushambulia na kujiokoa.
“,Mikono juu! wewe ni nani? na umefuata nini?, nijibu kabla sijatawanya kichwa na kiwiliwili chako kwa risasi! “,kamanda mkuu wa kitengo cha ulinzi ikulu aliongea,hakujibiwa, Yuan Liang alikuwa kimya, akimtazama askari yule kwa dharau.
“,Pyuuuuu ……”,
“,Aaa…ak…yala…aa…a! “,
Yuan Liang alimuangalia askari yule machoni, askari yule alipojaribu kuangalia pembeni kidogo, Yuan Liang alichomoa kisu kwenye mkanda wake kama umeme,akakirusha, kikatoboa vidole vya kamanda mkuu wa ulinzi ikulu, kikatokea upande wa pili wa viganja vyake, kamanda yule akapiga kelele, sauti haikutoka, damu pekee ndiyo ilitiririka na kumlaani Yuan Liang kwa ukatili alioufanya, akadondoka chini kama mzigo, huku bunduki yake ikiangukia kule. Yuan Liang akachomoa bastola yake, akamsogelea, akamuwekea kisogoni “,Simama mshenzi wewe, nipeleke chumba alichopo raisi! “,Yuan Liang aliongea, kamanda mkuu akasimama, akaanza kutembea,akapita chumba cha Kwanza, akapita tena chumba cha pili, akafika mbele ya chumba cha tatu, akasimama …
“,Ingia, unaniangalia nini?, unataka kunitongoza?, sijawahi kupenda mimi, hebu ingia ndani……”,Yuan Liang alifoka, lakini kamanda hakutii amri yake, alikuwa amesimama kama sanamu. Yuan Liang akakasirika, akampiga kifuti cha mgongoni, kamanda yule akagaa chini kwa uchungu, mkono ulimuuma, mgongo ukamuuma,mwili wake wote ulijawa na maumivu.
“,Yala…aa,aaaghh”kamanda alilia kama mtoto, maumivu aliyoyasikia hayakuwa ya kawaida.
“,Kelelee huko! tatizo lenu ni wabishi, nilikua staki hata kukuumiza …”,Yuan Liang aliongea, akasogele mlango wa chumba cha siri, akaufungua,…
“,Siwezi kukuua kwa sasa,nimekuja kukupatia onyo,usinitumie polisi tena,harafu nakupatia masaa ishirini na manne kuanzia sasa,usipo leta pesa zangu,kila kitu nakiweka wazi,nimekufata hapa ujue ni kiasi gani najiamini,siogopi kitu chochote kile,shenzi kabisa wewe…”,
Yuan Liang alifungua mlango wa chumba,akakutana uso kwa uso na raisi Jonsoni Mtemvu akiwa na bastola mkononi,akafyatua risasi,Yuan Liang akaruka serekasi kama umeme,risasi ikamkosa,ikamtandika kichwani kamanda mkuu wa kitengo cha ulinzi,akafa palepale,Yuan Liang akakasirika,akamtandika ngumi nyingi raisi Jonsoni Mtemvu,akampiga kifuti cha mkononi,akamtegua mkono wake wa kulia,akampiga vifuti vya miguuni,akamtegua miguu yote miwili,akagaagaa chini,akipiga kelele kwa maumivu makali,Yuan Liang akachomoa kisu chake,akatoboa vioo vya dirisha,akapenya,akaruka serekasi,akatua chini,akapanda ukuta,akaruka serekasi tena,akatua upande wa pili,akatokomea,tayali alikuwa amekamilisha kazi yake…
…………………………………
Costa; 10;20pm
Magari kumi ya kifahari,yakiwa yamepangana, yalisimama na kupaki katika hoteli kubwa ya kifahari,” Costa intertantinal hotel “,haikuwa mara yao ya kwanza kufika mahali hapa, walifika katika hoteli hii mara kwa mara, huku wakiwa na vyumba vyao vya kudumu, vyumba ambavyo walivilipia kwa mwezi. Milango ya gari la kumi ilifunguliwa, magaidi wawili wakatoka,wakasimama mlangoni, wakiwa na makoti yao marefu,gari la tisa likafuatia, magaidi wakatoka, wakasimama mlangoni, magari yote yakafuatia,magaidi wote wakatoka, isipokuwa gari la kwanza,gari lenye bendera ndogo karibu na taa za mbele. Magaidi baada ya kutoka, wakakagua aneo lote, kwa kutumia vifaa vyao, wakaridhika, kulikuwa hakuna maadui wowote wale, wakafungua mlango wa gari la bosi wao, akatoka, akaanza kutembea kuelekea hotelini, kila kona akiwa amezungukwa na vijana wake, wakaingia kwenye lifti, wakapanda mpaka ghorofa ya kumi, mahali kulipokua na vyumba vyao …
Costa; 11;03pm
Yuan Liang alifanikiwa kutoka nje ya jengo la ikulu bila kukamatwa, akavua gloves zake mikononi, akaziweka katika mifuko yake, “,Shiit! nimetoka na funguo za wale washenzi kule chooni,potelea mbali! watajua wenyewe namna ya kutoka ……”,aliongea, akiwa anakimbia, akitoka eneo la ikulu, alipokaribia barabara, akabonyeza batani ya miwani yake, akaruhusu mawasiliano ikulu, akavuka barabara,dakika mbili tu alitumia, akafika maegesho ya magari, mahali alipopaki pikipiki yake …
“,Saa tano na dakika nane, umewahi, nilizani utarudi kuichukua kesho, maana nyie maafande hamtabiriki, kazi zenu ngumuu! “,mlinzi wa magari,katika pakingi ya jiji aliongea,hata yeye alifikiri Yuan Liang ni askari kutokana na mavazi yake, Yuan Liang akampuuzia,alikuwa kazini, sura yake haikua ya matani hata kidogo, alikuwa ameikunja kama bibi kizee wa miaka themanini,mlinzi yule akaogopa,hakuendelea kuuliza tena, Yuan Liang akaingiza mkono wake mfukononi, akatoa funguo za pikipiki yake, akawasha pikipiki, akatoweka, kuelekea mahali alikokufahamu yeye.…
…………………………………
Ikulu; robo saa iliyopita
Kamanda Amiry pamoja na kamanda Junior walishtuka,mlio wa risasi ulisikika, ndani ya jengo la ikulu, ikulu ya raisi Jonsoni Mtemvu. Wakapagawa,wakakimbia bila mpangilio.
“,Daaah, nimesahau,mlio huo wa risasi umenichanganya, twende tukajue kuna nini? “,kamanda Junior aliongea, akarudi katika kibanda cha walinzi, pembeni kabisa na geti la kuingilia ikulu,akachukua bunduki yake, wakaanza kulisogelea jengo la ikulu.
“,Puuuuuu! “,kishindo kilisikika nyuma ya nyumba.
“,Pita huku na mimi nipite huku …”,kamanda Amiry aliongea,jasho jembamba likimtoka.
“,Ok afande! “,kamanda Junior alijibu, akapita mkono wa kushoto, mwenzake akapita mkono wa kulia, macho yao yakiwa makini kuangalia mita hamsini mbele, mita hamsini nyuma, kulia na kushoto. Wakatembea huku wakijibanza kwenye ukuta, wakachungulia tena, hawakuona mtu, wakapiga hatua kadhaa harakaharaka, wakajibanza kwenye ukuta, wakachungulia …
“,Mbona hakuna mtu! yule pale, pigaa! “,
“,paaaa! paaaa! “,
“,Shiiit! ameruka, katuponyoka!, huyu sio raia wa kawaida!, raia wa kawaida hawezi kuruka ukuta kimafia namna hiyo …”,
“,Amiry, Amiry, angalia kule juu! “,
“,Mungu wangu weee! tumekwisha! alipita dirishani kule juu, chumba cha raisi, kama raisi ameuawa tumekwisha! lazima tufe! “,
“,Twende ndani,twende! “,
Kamanda Amiry pamoja na Junior walifika nyuma ya nyumba, waliopoangaza huku na kule hawakuona kitu, walipoangalia vizuri, walimuona adui anatokomea, wakashambulia, hakuna risasi yoyote iliyomjeruhi adui, adui yao aliruka serekasi na kuvuka ukuta mrefu, wakabaki wakiwa wameduwaa,wasiwasi ukawajaa, kamanda Junior akageuka, akaangalia juu, usawa wa ghorofa ya ikulu,dirisha lilikuwa limetobolewa, akamtaarifu mwenzake, wote wakazidi kuchanganyikiwa, wakakimbia kimbia kama wendawazimu.
“,Itakua vizuri zaidi! “,kamanda Amiry akajibu,kamanda Junior akakimbia kuelekea kibanda cha walinzi, akachukua kamba ndefu ya mkonge, akarudi akiwa ameishika, wote wakakimbia nyuma ya nyumba.
“,Irushe kwenye nondo za dirisha !”,
“,Ndio nafanya hivyo, tayali imekaza! “,
“,Jaribu kubembea tuone kama imekaza! “,
“,Imekaza afande!”,
“,OK, tupande juu! “,
Kamanda Junior alianza kujivuta kuelekea juu,dakika mbili tu alitumia, kamanda Amiry akafuatia, na yeye alitumia dakika mbili tu, akafika juu, wakapita dirishani, kwenye tundu lililokatwa na Yuan Liang, wakaingia ndani ya chumba cha siri, chumba cha matibabu ya raisi Jonsoni Mtemvu.
“,What!mheshimiwa ,nini kimetokea?”,kamanda Junior na kamanda Amiry waliongea kwa mshangao,hawakuamini kile walichokiona mbele ya macho yao.
“,Nisaidieni,nisaidieni,nakufa!nakufa!”,hali ya raisi Jonsoni Mtemvu ilikua mbaya,alihema kwa shida sana,huku akilia kwa uchungu kama mtoto mdogo,wakamnyenyua,wakamuweka kitandani.
“,Ndii,ndii,ndii……”,kamanda Junior alibonyeza simu yake ndogo,nokia ya tochi,akaiweka sikioni.
“,Unampigia nani tena?”,kamanda Amiry aliuliza.
“,Madaktari wa ikulu wafike haraka mahali hapa kutoa msaada,harafu nataka nitoe taarifa wizara ya ulinzi na usalama wa taifa…”,kamanda Junior alijibu.
“,Jaribu lakini sizani kama mtandao unafanya kazi,mmh angalia kule,damu nzito inatokea wapi hiyo?……”,kamanda Amiry aliongea,huku akiangalia kila kona ya chumba,ghafla akashtuka,aliona damu nzito ikitiririka kuingia chumbani,akausogelea mlango taratibu,kamanda Junior aliahirisha kupiga simu,macho yake yalikuwa yamemtoka,akiitazama damu nzito na mbichi sakafuni
“,Hali imeshakua mbaya, kamanda John yuko wapi?, kamanda Jacob yuko wapi?, vipi kuhusu mke wa raisi, yuko wapi? “,kamanda Junior aliongea, huku akiutazama mwili wa mkuu wao wa kitengo cha ulinzi ikulu,damu ilitiririka kichwani kama maji,sehemu aliyopigwa risasi.
“,Nakufa, nakufa, nisaidieni, nisaidieni! “,raisi Jonsoni Mtemvu alipiga kelele za maumivu kwa mara nyingine tena, wote wakageuka kumtazama, wakachanganyikiwa!
“,Nenda kawatafute, John, Jacob pamoja na mama Zainath, mimi ngoja niwataarifu madakari wa raisi pamoja na serikali yote kwa ujumla kuhusu tatizo hili, bora tufe tu, japo hatujahusika na chochote kile, ukweli utatuweka huru siku zote! “,kamanda Junior aliongea, akachukua simu,akabonyeza bonyeza kisha akaweka sikioni …
“,Mhhh, mtandao unapatikana!, simu inaita! Kweli leo wametuweza! “,kamanda Junior aliongea kimoyo moyo, akiwa anasubili simu iweze kupokelewa.
…………………………………
11;30pm
Magari yalipishana ikulu, magari yaliingia na kutoka, waandishi wa habari waliendelea kuchukua picha za matukio mbalimbali, huku kamanda Amiry pamoja na kamanda Junior wakiwekwa chini ya ulinzi kwa mara nyingine tena.
“,Hatujaua sisi,hatuja mjeruhi raisi, hatuhusiki na kitu chochote kile! “,kamanda Amiry pamoja na kamanda Junior walipiga kelele, walipigwa virungu bila huruma, wakapakiwa kwenye karandinga la polisi.
“,Wapelekeni! haiwezekani sote tutekwe, wao waachiwe, harafu waje kutupatia msaada, hawajajeruhiwa popote pale, isitoshe hata tukio la kwanza la mume wangu kujeruhiwa ilitokea hivi hivi, naomba sheria ichukue mkondo wake, sikubali! sikubali! “,mama Zainath alifoka, licha ya kusaidiwa kutolewa bafuni, mahali alipokuwa amefungiwa na Yuan Liang, hakuwaamini kabisa askari wake wa kitengo cha ulinzi, kamanda Junior pamoja na kamanda Amiry, aliamini walihusika kwa namna moja ama nyingine …
Ghafla,difenda ya polisi yenye king’ora cha hatari, iliingia ikulu kwa fujo, kamanda Catherine akashuka kwenye gari, kamanda Kendrick akafuatia, kisha Philipo, Yasini na Gupta wakashuka ndani ya gari.
“,Jamani mmeniamsha usingizi ukiwa bado haujaisha, lakini hakijaharibika kitu! “,kamanda Philipo aliongea.
“,Acha masihara kazini! wote tumeamshwa usingizini bila kupenda, lakini tunapaswa kutimiza majukumu ,tunapaswa kujua nini kimetokea ……”,kamanda Catherine aliongea. “,Wote tuelekee ndani ya jengo la ikulu kwa ajili ya uchunguzi, lazima tupate jibu kuhusu muuaji, lazima tujue siri iliyofichika hapa katikati, sizani kama tatizo ni diski tu, kutakua kuna siri kubwa imefichika ndani yake ……”,kamanda Kendrick aliongea, wote wakaongozana kuelekea ikulu, waandishi wa habari walitaka kuzungumza nao, lakini hawakua tayali kuongea kitu chochote kile, taarifa walizopokea kwa simu kuhusu mauaji ikulu yaliwachanganya na kuwavuruga akili zao.
Mexic; 00;20am
Waziri mkuu, mheshimiwa Januari Sasamba aliendelea kuuchapa usingizi,mawazo lukuki yaliyomjaa kichwani, yalimfanya akorome na kulala fofofo.Hakujua chochote kile ambacho kilimtokea rafiki yake, ghafla simu yake ikaanza kuita.
“,Ndriii, ndriii, ndriiii! ndriii, ndriii ……”,mtetemo wa simu ulisikika katika masikio yake,akakurupuka kutoka usingizini, akapapasa kitanda chake huku na kule,mikono yake ikagusa simu yake, akaichukua, akaitazama, “Shemeji mama Zaina “,kioo cha simu yake kilisomeka, mke wa rafiki yake, mke wa raisi Jonsoni Mtemvu alikuwa anampigia.
“,kulikoni usiku huu?, mbona tunasumbuana?,nitamtafuta kesho, kwa sasa nimelala zangu! “,waziri Januari Sasamba aliongea, akakata simu, akajilaza kitandani, huku akiwa amekerwa na simu iliyomshtua kutoka usingizini.
“,Ndriii, ndriii, ndriii “,mtetemo wa simu ukasikika tena,akakurupuka tena kwa hasira, akachukua simu yake, akaitazama, mama Zainath alikuwa amempigia kwa mara nyingine tena, akaipokea, akaisogeza sikioni.
“,Shemeji uko wapi?,tumevamiwa ikulu, baba Zainath kapigwa nusu mfu, hajiwezi kabisa, mkuu wa kitengo cha ulinzi ameuawa, mimi na askari wawili tuliponea chupuchupu, jambazi hilo la kike lilitufungia bafuni,namshukuru Mungu hatujajeruhiwa! nakuomba kesho asubuhi njoo hapa nyumbani tuzungumze, kuna kitu nataka nikushirikishe…”,sauti ya kike, sauti iliyojaa jazba, ilisikika upande wa pili wa simu, mara tu baada ya waziri Januari Sasamba kupokea simu, akachanganyikiwa, jasho jembamba likamtiririka mwilini, akaanza kutetemeka kwa hofu.
“,Au amekuja ikulu?,ni yeye au mwingine! “,waziri aliongea, akiwa amesahau kama alikuwa anaongea na simu.
“,Unaongea nini?,mbona sikuelewi?”,sauti ya mama Zainath ilisikika.
“,Hapa…ana,hapaa…na,siongei kitu,sawa,nitakuj…aa,nakujaa sasa hivi!”,waziri aliongea kwa kigugumizi,akitetemeka kwa hofu.
“,Utakuja?,au unakuja sasa hivi?,kwa nini umeshtuka na unahema kwa hofu,mbona sikuelewi…”,mama Zainath aliongea,akajiuliza maswali kichwani,aligundua kuna siri waziri Januari Sasamba aliifahamu,yeye pamoja na mume wake,lakini walikuwa hawataki kuiweka wazi.
“,Kwa sasa niko Mexic,mji mdogo kaskazini mwa jiji la Costa,siwezi kuja usiku huu,nitakuja kesho asubuhi na mapema…”,waziri aliongea,akijikaza kisabuni,akaificha hofu yake asiweze kugundulika.
“,tumekwisha!,tayali yule mwanaharamu ameshafanya yake,nilizani anatania,hapa sio mahali salama kwa sasa,i have to go back to the city now!,lazima nifike Costa usiku huu……”,waziri aliongea,akaiweka simu yake pembeni,akashuka kitandani,akavaa suti yake,akavaa viatu,akachukua briefcase yake yenye pesa za bandia,bilioni kumi taslimu,akachukua simu yake kitandani,akatoka chumbani haraka sana,akiwa kama mwendawazimu…
…………………………………
Costa;00;30am
Mkuu wa kikundi cha magaidi,kikundi cha M27,aliwaita vijana wake katika chumba cha mikutano,ndani ya hoteli ya kimataifa ya Goshani,hoteli ambayo waliizoea kama nyumbani kwao,kwani walifika mara kwa mara kwa ajili ya kufanya biashara mbalimbali.
“,Wote mmekamilika?”,mkuu wa kikundi hiki aliuliza,sigara yake ya kizungu ilikua mdomoni,alikuwa amekunja nne,huku akichezesha chezesha mguu wake.
“,Tumekamilika bosi,!”,wote walijibu kwa heshima, wakiwa wameketi kwa makini, wakisubili kumsikiliza bosi alitaka kuwambia nini, baada ya kuitisha kikao cha dharula.
“,Nimewaita, nimewaamsha usiku huu katika vyumba vyenu, hali ni mbaya kwa rafiki yetu,tusipomsaidia, biashara zetu zitagoma, hata hoteli hii tusinge kaa kwa uhuru kiasi hiki, anatulinda sana! “,mkuu aliongea kwa hisia kali, vijana wake wakawa na shauku kubwa kutaka kumsikiliza,ukimya wa hali ya juu ukatawala.
“,Ndio bosi, tunalitambua hilo! “,magaidi ishirini na sita wakaitikia.
“,Habari ya mjini kwa sasa, ikulu imevamiwa!,askari mmoja ameuawa, rafiki yetu, mheshimiwa raisi, amejeruhiwa vibaya sana, isitoshe alikua hajapona vizuri”,mkuu aliongea, vijana wake wakashangazwa na taarifa hiyo,wakabaki midomo wazi.
“,Nani huyo alikuwa na jeuri ya kuingia ikulu?, hata kama kuna askari mdebwedo, wanavifaa maalumu vya ulinzi kumnasa adui kabla hata hajaisogelea ikulu ……”,gaidi namba mbili aliongea,wote wakageuza macho yao kumsikiliza.
“,Hata mimi nashangaa,ok tuyaache hayo! tumekuja kumsaidia, na ndio lengo kuu lililotutoa msituni, hivyo basi, tunapaswa kuanza kazi haraka iwezekanavyo! “,mkuu aliongea,akataka kazi iweze kuanza haraka,kuitafuta diski iliyopotea na kumuua adui kabla hajaleta madhara makubwa zaidi.
“,Lakini bosi! adui tutamfahamuje?,hata sura yake hatuifahamu, muhusika ndio huyo kajeruhiwa, bila shaka atakuwa na ulinzi mkali kwa sasa,tutaanzia wapi? “,gaidi namba tano aliuliza swali, swali la msingi sana.Wote wakamgeukia bosi, wakisubili majibu kutoka kwake.
Bosi akachukua simu yake, akaibonyeza bonyeza, akaiweka sikioni, vijana wake wakamshangaa, walikuwa hawajui anampigia nani usiku huu. “,Eee haloo! M27 namba moja hapa, nimekuja na kundi langu, tumekuja kutoa msaada, lakini ndio hivyo raisi kafanyiwa shambulio lingine, hatuwezi hata kuonana naye, sasa adui tutampataje?, tunaomba maelekezo kama unamfahamu ……”,mkuu aliongea, huku akijizungusha kwenye kiti chake,moshi wa sigara ukimtoka mdomoni, ukazidi kuwaburudisha majirani zake, kwani wote walikuwa wavutaji.
“,Niko njiani na gari langu, natokea mji mdogo wa Mexic, ndiyo napata taarifa za shambulio ikulu muda huu, namba ya huyu muhusika anayetusumbua vichwa ninayo, nawatumia sasa hivi! “,upande wa pili wa simu ulisikika, bila shaka alikuwa ni waziri mkuu Januari Sasamba.
“,Sawa mheshimiwa, tunasubili namba hiyo! kuwa makini, maana inawezekana mtu wa pili kushambuliwa na adui ni wewe “,mkuu aliongea,kisha akakata simu.
“,Nazani mmesikia, tunatumiwa namba ya adui sasa hivi, kisha kazi itaanza mara moja! “,mkuu aliongea,akiwatazama vijana wake usoni, mmoja baada ya mwingine.
“,ndrii, ndrii, ndriii! “,mlio wa simu ulisikika, mkuu akaitazama simu yake, akatabasamu.
“Tayali namba imetumwa! ,M27 namba tatu chukua hii namba, mpigie huyu mwanamke kahaba, mwambie bosi anataka kulala naye kwa milioni mia moja! “,mkuu aliongea, akampatia simu yake gaidi namba tatu, akampatia maelezo namna ya kufanya. Gaidi namba tatu hakuwa na muda wa kupoteza, alikopi namba, akapiga, simu ikaanza kuita.
“,Haloo! “,sauti ilisikika.
“,yes haloo!, uko wapi? “,gaidi namba tatu aliongea.
“,Unapiga simu, hujajitambulisha, halafu unaniuliza niko wapi?, kaka we mzima kweli? ……”,Yuan Liang aliongea kwa jeuli, bila hofu yoyote ile.
“,Samahani dada, bosi anakuhitaji,kuna milioni mia moja mezani, sema uko wapi afike aonane na wewe! “,gaidi namba tatu aliongea kwa upole, akizuia hasira zake, asije akaharibu kazi, hakupenda wanawake wenye dharau kama Yuan Liang. Alitamani kumtukana lakini hakuwa na jinsi, ilibidi ajizuie, mipango isije ikavurugika.
“,Niko Mexic, onyo! kama mmetumwa, hamna lengo zuri na mimi, nitawafyekelea mbali, mtajuta kunifuata wenyewe! “,Yuan Liang aliongea kwa dharau,kisha akakata simu.
“,Hahahahaaaa”,kundi la M27 walicheka,walimdharau sana Yuan Liang, walimuona kama panya anayetaka kupigana na tembo, wakaahidi kumkomesha.
“,Haya, safari ianze mara moja! hakikisheni mnamdhibitishia kuwa sisi ndio M27,hatunaga maneno ya taarabu kwenye kazi “,mkuu aliongea, akanyanyuka kwenye kiti, akaongoza msafara.
“,Sawa bosi! “,magaidi wote waliitikia, wakanyanyuka kwenye viti vyao, wakaungana na bosi wao kwa ajili ya kuelekea mji mdogo wa Mexic, usiku wa manane, majira ya saa saba usiku.
Kundi la majambazi, kundi la Casabranka gang, waliendesha msako mzito, nyumba zote za kulala wageni, katika mji mdogo wa Mexic. Mkononi walikuwa na picha ya Yuan Liang, picha ambayo waliichukua katika akaunti yake ya instagramu.
“,Nawambia tutakesha, tutakesha! mimi nashauri, angalieni kwenye akaunti yake ya instagram, bila shaka ameweka namba ya biashara yake ya ukahaba, tujifanye kama wateja,tujue yuko mahali gani,tukamfyekelee mbali…”,mmoja kati ya vijana ishirini,vijana wa Kasabranka gang walioenda kumsaka Yuan Liang alitoa ushauri,baada ya kupekua hoteli zote bila mafanikio.
Ikulu;
Hali ya raisi Jonsoni Mtemvu ilikua mbaya sana,chumba cha siri alichokuwa anafanyiwa matibabu awali kilikuwa kimevurugika, damu ilitapakaa kila kona, huku dirisha likiwa limepasuliwa kitaalamu na kumuwezesha adui kutokomea.Askari walimnyenyua mheshimiwa raisi, akahamishiwa chumba kingine, madaktari bingwa wanne, wawili wazungu, mmoja muhindi, na wa mwisho muafrika. Kila mmoja alikua bize akijitahidi kuokoa maisha ya raisi wa nchi ya Goshani, bwana Jonsoni Mtemvu.
“,Ana high blood pressure,isitoshe anapumua kwa shida sanaa! “,daktari wa kihindi aliyefanya kazi idara ya afya serikalini, kwa mika takribani kumi aliongea.
“,Vipi kuhusu picha ya X-ray aliyopigwa, majibu yanasemaje! “,daktari wa kizungu, daktari mkuu wa raisi Jonsoni Mtemvu aliongea.
“,Hana tatizo,bila shaka ameteguliwa, hajavunjwa mahala popote pale! “,daktari aliyekuwa amevalia suti nyeusi, suti iliyofanana na rangi ya ngozi yake aliongea,akatoa maelezo ya kina, wote wakatikisa vichwa, walikubaliana na ripoti aliyoitoa, wote wakiwa wamezunguka kitanda cha raisi.
“,OK,tatizo kubwa ni hili la difficult in breathing, tuhakikishe upumuaji wake unarudi katika hali ya kawaida, blood pressure ya mwili wake iwe normal kufikia saa mbili asubuhi, bila shaka ulimwengu wote utataka kusikia ripoti kuhusu afya ya raisi wetu,! “,daktari wa kizungu aliongea,kisha wote wakaanza kazi,nje ya chumba kipya cha matibabu ya raisi, askari kumi wenye silaha nzito walikuwa makini kudumisha ulinzi,hakuna mtu yoyote aliruhusiwa kusogelea chumba hiki bila kitambulisho pamoja na sababu maalumu.
…………………………………
2;20am
Kamanda Kendrick aliongoza msafara,askari wezanke wakamfuata nyuma yake,huku mwisho kabisa mama Zainath akiwa amefunga kanga yake kiunoni, akitoa ushirikiano wa hali ya juu kwa wapelelezi hawa, wenye siku moja tu nchini Goshani. Wakapanda ngazi, wakafika ghorofani, uso kwa uso na damu nzito ambayo haikusafishwa makusudi, kwa ajili ya uchunguzi.
“,Hapa ndipo kulikuwa na maiti ya askari wetu, alipigwa risasi kichwani! “,mama Zainath aliongea,sura yake ikiwa haina hata chembe ya tabasamu.
“,Wakati anapigwa risasi nyie mlikua mahali gani! “,kamanda Catherine aliuliza.
“,Tulikuwa tumefungiwa chooni, mimi pamoja na askari wawili wa ulinzi, ndipo baada ya tukio kukamilika, adui akiwa ameshatoroka, kamanda Junior pamoja na kamanda Amiry walikuja kututoa chooni kwa kuvunja kitasa cha mlango! “,mama Zainath aliendelea kuongea kwa huzuni.
“,Hawa askari inabidi wahojiwe, inawezekana wanahusika, kuna jambo wanafahamu, haiwezekani tukio la kwanza litokee wakiwepo halafu wasijeruhiwe, tukio la pili vivyo hivyo! lazima tuwahoji kwa mara nyingine tena! “,kamanda Kendrick aliongea..
“,Kweli kabisa afande, lakini tayali wameshakamatwa na kuwekwa rumande! “,mama Zainath aliongea.
“,Basi ni vizuri, kesho tutafanya nao mahojiano, watapata mateso makali mpaka watasema ukweli! “,kamanda Kendrick aliongea, alikuwa na hasira sana,wote kwa pamoja wakaingia ndani ya chumba cha siri, chumba alichokuwa anapatiwa matibabu muheshimiwa raisi, kabla ya tukio.
“,The same person, the same killer, muuaji ni yule yule, ona visigino vya viatu vyake, ona jinsi alivyokata kioo, kama alivyofanya hotelini ……”,kamanda Catherine aliongea, wote wakatikisa vichwa, viatu vya Yuan Liang vilionekana kukanyaga damu baada ya askari kupigwa na risasi,kila alipokanyaga, mpaka eneo la dirishani alipotorokea, kulikuwa na alama za visigino vya viatu vyenye damu, wakapata majibu haraka sana!
“,Mama usjali, masaa kumi yajayo tutakua tumemtia nguvuni, aliyefanya tukio hili ndiye aliyefanya na hili tukio lililopita,ngoja tukamtafute adui, lakini tutapaswa kufanya mahojiano na mume wako akipata nafuu, inaonekana kuna siri nzito imefichwa hapa katikati, inawezekana tatizo sio diski, kutakuwa na jambo lingine kabisa linaloibua matukio yote haya! “,kamanda Kendrick aliongea, akaanza kutoka nje, askari wote wakamfuata,safari ya kumsaka adui ikaanza haraka iwezekanavyo.
Walishuka ghorofa ya ikulu kama wendawazimu, wakatoka nje ya jengo la ikulu, wakajipakia ndani ya difenda yao, kamanda Gupta akakamatilia uskani.
“,Kamanda Philipo pamoja na Catherine fanya majukumu yenu, tumieni kompyuta yenu kujua lokesheni ya diski kwa sasa! ,kamanda Gupta ondoa gari mahali hapa, tutajua tunaelekea wapi mbele kwa mbele, tutakapo fahamu mahali adui alipo “,kamanda Kendrick aliongea, kila askari akatimiza majukumu yake kama alivyo elekezwa. Kamanda Gupta akawasha gari, geti likafunguliwa, akaliondoa gari kwa kasi, akawaacha midomo wazi waandishi wa habari ambao walisimama nje ya geti la ikulu kwa ajili ya kukusanya taarifa, kuwahoji watu mbalimbali walioingia na kutoka ikulu…
” ,Connected!, the related disc is available in Mexic …”,(imeunganishwa, diski inayohusiana inapatikana Mexic) “,ujumbe ulisomeka kwa mara nyingine tena katika kompyuta ya the super three soldiers,mara baada ya kamanda Catherine kuunganisha saa ya raisi na kompyuta yao, wakatambua mahali diski ya raisi ilipo, mahali ambapo adui alikuwa anapatikana.
“,Duuuh huyu mwanamke ni hatari sana! muda huu kafanya tukio na tayali yuko Mexic! ,anyway, Gupta nazani umesikia, kanyaga mafuta kuelekea Mexic haraka iwezekanavyo! “,kamanda Kendrick aliongea, akionekana kushangazwa na mbinu mbalimbali alizokuwa anatumia adui kwenye shughuli zake.
“,Nimesikia afande! dakika ishirini tu,tutakua tayali tumetia nanga! “,Gupta alijibu, macho yake yakitazama mita mia moja mbele, akikwepa na kuovateki magari makubwa barabarani, akapenya katikati ya magari, huku king’ora cha gari yake kikimsaidia kuwataarifu madereva wa magari mengine kukaa mbali na gari lake. Alikuwa dereva mzuri kwenye mashindano ya olimpiki mwaka 2005,akatwaa taji kama dereva namba moja wa dunia, serikali ya Goshani ikampenda, ikampatia pesa nyingi, ikamuajiri kama dereva mkuu wa jeshi, akiwa kitengo cha upelelezi …
…………………………………
Mexic; Nusu saa iliyopita
Kundi la majambazi la Casabranka gang walitabasamu, walifanikiwa kupata namba ya simu, namba ya kahaba Yuan Liang kupitia akaunti yake ya instagramu, wakakopi namba, wakampigia.
“,Haloo! mimi raia ya kigeni, iko toka Italiano, mimi taka penzi lako, iko lipa wewe dola mia tano kwa saa moja, this night, before morning! “,jibaba la mlango wa kasino, kasino la Kasabranka liliigiza sauti,baada ya kumpigia Yuan Liang. “,Ok, kwangu nahitaji pesa tu! njoo, niko Mexic, but hata mimi nimeigiza sana drama kama hizo za kujibadirisha sauti, kubadirisha nchi yangu n. K, kwahiyo kama umetumwa, una lengo baya na mimi, nitakuua! “,sauti ya simu ilisikika.
“,ok mama, no problem! wewe iko hoteli gani, chumba namba ngapi ?”,jambazi liliuliza tena, likijitahidi kuigiza sauti na rafudhi ya kigeni, lisije likashtukiwa.
“,Niko chumba namba tano, hoteli ya Mtakuja,pembeni ya barabara kuu, mwanzoni mwa mji mdogo wa Mexic! “,sauti ya simu ilisikika.
“,Ok mama, mimi kuja hapo now, wewe nipa penzi zuri, mimi kupa wewe mapesa mingi, a lot of money!……”,jambazi liliongea,likakata simu,kundi lote likatabasamu kwa furaha, wakajipakia katika pikipiki zao, wakatoka katika hoteli ya Suncity mwisho wa mji wa Mexic,baada ya kukagua bila mafanikio na kumaliza hoteli kubwa za mji wote, wakaanza kurudi katika hoteli ya hadhi ya chini, waliyoelekezwa na Yuan Liang.
…………………………………
Mexic; 3;01am
Kahaba Yuan Liang alikuwa na masaa takribani mawili akiwa amekamilisha kazi na kurejea Mexic katika makazi yake, ndani ya hoteli ya hali cha chini. Alijaribu kulala, kujipumzisha katika kitanda chake, lakini malengo yake yakashindwa kukamilika,alipigiwa simu ya kwanza, akakurupuka usingizini, akaipokea, akazungumza na baada ya mazungumzo akalala tena, saa moja likapita, akapigiwa tena, akakurupuka usingizini, akapokea simu, watu wawili wenye malengo ya kufanana walimpigia kwa muda uliokaribiana, akatafakari, machale yakamcheza …
“,Kuna kitu, huu ni mtego sio bure,siwezi kukaa hapa tena!, ngoja niondoke, napaswa kuondoka mahali hapa, napaswa kukaa sehemu ambayo itaniwezesha kuona mtu yoyote atakaye sogea hotelini hapa kunitafuta …”,Yuan Liang aliongea, huku akitafakari haraka haraka, akapata jibu.
“,Ngoja nikakae na ombaomba hapo barabarani, nitajivika gunia, mizigo yangu na pikipiki yangu nitaipaki hapo sheli, kando ya barabara, nitalipa pesa, watanihifadhiaa katika pakingi yao,kama ni maadui nitawatandika, kisha nitaelekea kwenye sheli, nitachukua pikipiki yangu, nitatoweka! “,Yuan Liang alimaliza kutafakari,alimaliza kupiga mahesabu mazito ndani ya kichwa chake, akanyanyuka kitandani, akafungasha virago vyake, akatoka nje ya chumba chake, akiwa na kila kilicho chake mkononi …
Mexic; 4;02
Yuan Liang alikuwa amebeba mabegi yake,koti lake kubwa lilikuwa mwilini mwake, akatoka katika hoteli ya Mtakuja,akiwa amepania kuihama hoteli hii na kutokomea mbali,atakapomaliza kuwatandika maadui zake.
“,usiku huu unaelekea wapi mwanangu? “,mama muhudumu na mmiliki wa hoteli ya Mtakuja, hoteli isiyokuwa na madirisha ya vioo, huku pazia chakavu zikiipamba milango yote ya hoteli hii yenye vyumba vitano tu vya kulala wageni, alimuuliza swali Yuan Liang baada ya kukutana naye uso kwa uso ,akiwa anafanya usafi, majira ya asubuhi …
“,Naondoka! asante kwa huduma zako, lakini kuna watu wanaweza kufika hapa kunitafuta,siunajua kazi zetu za kiaskari bwanaa! watakao niulizia waambie nimeondokaa, nimehama hoteli, ikiwezekana waonyeshe hata chumba nilichokuwa nalala, usionyeshe jeuli yoyote ile, watakuua! “,Yuan Liang alimpatia maelekezo mama yule, akaisogelea pikipiki yake, akapakia mabegi yake, akawasha pikipiki, akatokomea, huku akimwachia maswali mengi mama yule yasiyokuwa na majibu.
“,Sawa mwanangu, Mungu akulinde! “,mama yule liongea, akaendelea na shughuli zake za usafi.
Yuan Liang aliwasha pikipiki yake, akavuka barabara upande wa pili, akaingiza pikipiki yake katika sheli, “PURE OIL “,kibao cha sheli kilisomeka,akasimamisha pikipiki yake, akashuka, akatembea kwa mwendo wa haraka, akazisogelea ofisi za sheli …
“,Naomba mnihifadhie pikipiki yangu, shilingi ngapi bosi? “,Yuan Liang aliuliza, macho yake yakimtazama muhudumu wa kike, akiwa amevaa ovaroli la bluu, lenye chata kubwa ya “PURE OIL ” mgongoni.
“,dola tano kwa siku! “,muhudumu yule alimjibu Yuan Liang.
“,Sawa, nitaichukua baada ya saa moja tu, saa kumi na mbili nitakua hapa! “,Yuan Liang aliongea, akaingiza mkono mfukoni, akatoa shilingi elfu kumi na mbili, pesa halali za nchini Goshani,kisha akatokomea.
Alitembea huku akiangaza pembe zote za barabara, akafika pembeni na hoteli ya Sun city, hoteli ya kifahari iliyoangaliana uso kwa uso na hoteli ya Mtakuja,hoteli zote zikiwa zimetenganishwa na barabara kubwa!
“, Pesa hizi hapa, nisaidieni magunia nijifiche hapa, kuna majambazi wananitafuta, nataka nijifiche mahali hapa, nijifunge magunia, nionekane kama mwenzenu”,Yuan Liang aliongea, akachukua noti kumi za elfu kumi kumi, akawagawia omba omba kumi waliokuwa wamelala kando kando ya barabara, karibu kabisa na hoteli ya Sun city.
Yuan Liang aliwapatia omba omba pesa nyingi sana, siku zote walipewa pesa za sarafu, leo ilikua bahati yao, walishika noti kabla hata jua halijachomoza, walimuona Yuan Liang kama mkombozi wao,kila mmoja akampatia gunia moja japo aliomba magunia matatu tu, akayachana vizuri, akajifunika,dakika moja tu ilipita, msafara wa pikipiki takribani ishirini zikapaki pembeni ya hoteli ya Mtakuja, wakaingia ndani ya hoteli, Yuan Liang aliwaona vizuri sana,…
Dakika tano zilipita, kumi zikapita, dakika ya kumi na tano, majambazi ishirini ya Kasabranka gang yakatoka ndani ya hoteli ya Mtakuja,sura zao zikiwa zimekunjamana kwa hasira,jambazi moja lenye kiduku kichwani, midomo ikiwa imebabuka kwa kuvuta bangi bila kipimo maalumu, lilikuwa limemshika mwanamke mmiliki wa hoteli hii, mama ambaye alimpenda sana Yuan Liang tangu akanyage katika hoteli yake.
“,Paaaaaa, twambie malaya mwenzako kaenda wapi?, bila hivyo tunakuua! “,jambazi lilifoka, lilimtandika kofi zito mwanamke yule, akajitupa mweleka, akagaa gaa chini kwa uchungu.
Yuan Liang alishindwa kuvumilia, alishuhudia kila kitu ambacho mama mwenye umri sawa na mama yake alikuwa anatendewa, alidharilishwa sana kwa kutukanwa matusi ya nguoni, “twambie, malaya mwenzako kaenda wapi, twambie, malaya mwenzako kaenda wapi? “,maneno aliyotukanwa mama yule yalijirudia mara mbili mbili katika kichwa chake, siku zote alilichukia sana tusi hili,Yuan Liang aliibuka kama mzuka, akiwa amevaa magunia, visu viwili vikiwa mikononi mwake, akavuka barabara huku akikimbia, akawasogelea majambazi wale.
“,Kill him fyeka vidole vyake tumpelekee bosi! “,sauti ya amri ilisikika, majambazi wote wa kasabranka gang wakamvamia Yuan Liang, aliyekuwa amejifunga magunia kama kichaa.
“,Mnanitukana mi malaya et eee! mtajuta kunifata mahali hapa, “Yuan Liang alifoka, sura yake haikuonekana, macho yake na mdomo wake ulionekana kupitia matundu yaliyokatwa katika gunia,alionekana zaidi ya kituko.
“,Kwachaa! “,
“,Yalaaa! “,
“,Kwachaa! “,
“,Uwiiii! “,
“,Kwachaa, kwachaaa! “,
“,Yalaabiii! “,
“,Kwachaa! “,
“,Nakufaa! “,
Yuan Liang alipiga mapigo ya kuua mtu, kila jambazi aliyemsogelea alivujwa vunjwa mifupa ya mkono wake, huku akichanwa chanwa na visu shingoni, hakuna aliyeinuka tena baada ya kipigo kutoka kwa Yuan Liang, kahaba hatari katika mapigo ya karate.
“,Nisogelee uone kati ya wewe na mimi nani malaya! “,Yuan Liang aliongea kwa kejeli, akipiga mahesabu kuwashambulia maadui zake ,akiwatazama kupitia matundu madogo kwenye gunia lake.
“,Iyaaaa! nakuuwa malaya wewe, nakuuwa! “,jambazi lile lenye mnyororo lilipiga kelele, likaruka mateke mawili hewani, Yuan Liang akapangua mateke yake, likampiga na mnyororo akakwepa, likampiga tena na mnyororo akainama chini, akaudaka mnyororo wake, akauvuta, akalipiga na vifuti, akalinyonga kwa mnyororo wake, likafa palepale.
“,Tukimbie! kimbieniii!Yuan Liang ni shetani, hatumuwezi, atatuua!”,amri ilisikika tena, majambazi takribani kumi na mbili waliokuwa wazima, walijipakia katika pikipiki zao, wakaziwasha kwa rimoti, zikawaka, wakatokomea,kila mmoja akitaka kuiokoa nafsi yake mbele ya kahaba hatari, Yuan Liang.
………….………………………
Mexic; dakika kumi zilizopita
Kundi la magaidi ishirini na saba ,M27,walifika katika mji mdogo wa Mexic, kaskazini mwa jiji la Costa. Gafla msafara wao ulisimama,kulikuwa na magari takribani matano mbele yao, yakiwa yamesimama barabani, na kusababisha foleni.
“,Bosi hatuwezi kuendelea na safari, ngoja nishuke nikaangalie foleni hii inasababishwa na nini! “,gaidi namba tisa, dereva wa mkuu wa kikundi aliongea, akafungua mlango wa gari lake, akashuka.
“,Kuwa makini! miji hii imejaa wahuni kama wewe, ukienda kizembe utashambuliwa na vibaka …”,bosi wa kikundi cha M27 aliongea, dereva akatikisa kichwa, bila shaka alimuelewa, dereva akaanza kupenya kwenye magari, gari la kwanza, la pili, kisha la tatu,uso kwa uso na kundi la vijana wakipigana, mtu mmoja aliyejifunika magunia akipiga karate na kuwashambulia vijana takribani kumi na tano kwa mpigo, akavutiwa naye, akarudi haraka kwa bosi wake huku anakimbia.
“,Bosi, bosi, kuna mapambano barabarani, kandokando ya hoteli mita mia moja kutoka hapa! kuna mpiganaji atatufaa kama akiungana na sisi, twende ukamuone, “dereva alifika huku akihema, bosi akatoka nje, magaidi wote wakashuka kwenye magari yao kwa ajili ya kumlinda bosi wao, wakaanza kusogea eneo la tukio, tukio ambalo lilisababisha msongamano wa magari mengi barabarani.Bosi wa kundi la magaidi la M27 alivutiwa sana na mpiganaji huyu, alitamani sana aungane naye kwenye kundi lake, akiwa tayali kumlipa pesa zozote zile, akaendelea kutazama mpambano huo huku akisubili mapigano yaishe, amweleze mtu huyo aliyejivika magunia aweze kujiunga na kundi lake.
“,Tukimbie, kimbieni!, Yuan Liang ni shetani, hatumuwezi, atatuua …”,sauti ilisikika, ikapenya katika masikio ya bosi mkuu wa kundi la M27,jina lililotajwa halikuwa geni masikioni mwake, ni jina la mwanamke ambaye walikuja kumtafuta,akiwa anatafakari, Yuan Liang alivua magunia yake, akabaki na sura yake halisi ya kichina, akiwa amevaa koti jeusi, suruali nyeusi ya jinzi pamoja na viatu vyake vya visigino virefu, mkononi alikuwa ameshika visu vyake viwili, maadui wake wakipanda pikipiki na kutokomea kama wendawazimu, wakimkimbia msichana huyu!
“,Mkamateni!, huyu ndiye tumekuja kumtafuta, huyu ndiye mpuuzi Yuan Liang aliyemjeruhi rafiki yetu Jonsoni Mtemvu …”,bosi mkuu wa kundi la M27 alitoa amri, magaidi wake ishirini na tano wakatoa nyundo zao ndogo kwenye mifuko ya makoti yao, wakaanza kumsogelea Yuan Liang ili wamshambulie, huku gaidi mmoja akiwa amesimama sambamba na bosi kumpatia ulinzi. Watu walikuwa wamefurika, mji huu haukua na watu waoga, ikiwa majira ya saa kumi na moja asubuhi, watu waliamshwa na kelele, wakafungua madirisha yao, wengine milango, wakashuhudia mapigano haya, wenye magari barabarani walisimamisha magari yao, hawakua na haraka,wengine walitoka nje ya magari yao kushuhudia mapigano haya, huku baadhi wakibaki ndani ya magari yao na kuendelea kuushuhudia mpambano huu mkali …
Ikulu; 6:00am
Waziri Januari Sasamba aliwasili jijini Goshani, hakua na muda wa kupoteza, alifika moja kwa moja ikulu, aweze kumjulia hali rafiki yake kipenzi raisi Jonsoni Mtemvu,kisha azungumze na shemeji yake, mama Zainath, aweze kufahamu kile ambacho alitaka kumweleza tangu usiku uliopita.
“,Anaendeleaje? “,raisi Jonsoni Mtemvu aliwauliza madaktari watatu ambao walikuwa wanampatia matibabu rafiki yake.
“,Kwa sasa anaendelea vizuri, muda mfupi uliopita nd’io amepata usingizi, akalala fofofo, akiamka tutakujulisha uongee naye! “,daktari wa kizungu alimjibu Januari Sasamba, akatikisa kichwa,kukubaliana na kile alichoelezwa, kisha akatoka nje ya chumba cha matibabu ya raisi, akashuka ghorofani, akafika sebureni, akaketi.
“,Shemeji nimekuita hapa! bila shaka unajiuliza maswali mengi bila majibu,ukitaka kujua nini hasa nimekuitia?”,mama Zainath alizungumza,macho yake yakiwa bize kumtazama Januari Sasamba usoni, kusoma hisia na fikra zake.
“,Ndiyo maana sikutaka kufika nyumbani kwangu, nataka nijue jambo ambalo umeniitia, maana hali sio shwari kwa sasa! “,Januari Sasamba alijibu, akikwepesha macho na mama Zainath, asije akapoteza uwezo wake wa kujiamini, akaharibu kila kitu.
“,Mume wangu tangu apate tatizo mara ya kwanza anaongea na simu kwa wasiwasi sana, na wewe umekua naye bega kwa bega kama rafiki wa karibu, isitoshe mtu anayemvamia na kumjeruhi ni yule yule!, je unafahamu kitu chochote hapa katikati kilichojificha! “,mama Zainath aliuliza swali, akionekana kubadirika kabisa, sura yake haikuonesha tabasamu hata kidogo.
“,Hapaana, hapana, sijui choc…hote, sijui kabisa…aa, labda um…uulize mwenyewe! “,waziri Januri Sasamba alijibu kwa kigugumizi, akiwa na wasiwasi.
“,Muuaji yuko Mexic, ndipo alipotorokea mara ya kwanza baada ya kufanya tukio, tukio la pili kalifanya na amerudi huko huko Mexic, lakini pia, nimekupigia simu usiku uliopita ukaniambia uko Mexic, ulienda kufanya nini huko? “,mama Zainath aliuliza tena.
“,Nilienda kwenye shughuli zangu zingine kabisa, kwahiyo siwezi kulizungumzia swala hilo! ” ,Januari Sasamba aliongea, alitambua tayali shemeji yake alianza kuhisi jambo fulani,wasiwasi wa siri zao kuvuja ukazidi kuongezeka nafsini mwake, akawa mkali kama pilipili!
“,Sawa shemeji yangu, tusije tukakwazana bure! lakini kama kuna mambo mabaya mmeyafanya na mume wangu, yanapowageukia na kupata matatizo msinishirikishe kwa jambo lolote lile …!”,mama Zainath aliongea ,akasubili majibu kutoka kwa shemeji yake.
“,Sawa shemeji usjali, ngoja mimi nifike nyumbani mara moja! “,waziri Januari Sasamba aliongea, akanyanyuka kwenye sofa, akausogelea mlango, akaufungua,akutoka nje na kuondoka zake.
“,Kuna tatizo, ona alivyotoka ndani kama anakimbizwa!, anyway! mtakapo kufa kwa aibu ndipo mtakapo sema ukweli, haiwezekani kila kukicha kuvamiwa na kupigwa tena na jambazi hatari, jambazi linaloshinda nguvu jeshi la serikali, haiwezekani kabisa, kuna kitu! “,mama Zainath aliongea, akajilaza kwenye sofa, tangu usiku hajapata usingizi kabisa, muda wote aliketi sebureni na kuangalia televisheni, akisubili kupokea wageni mbalimbali walioingia na kutoka ikulu, kumjulia hali mume wake, raisi Jonsoni Mtemvu.
…………………………………
Mexic; Nusu saa iliyopita
Yuan Liang alikuwa ameshayatupilia mbali magunia aliyokuwa amejifunika, wakati akipambana na kundi la majambazi maarufu kwa jina la Kasabranka gang, akafanikiwa kuwashinda,majambazi nane aliwajeruhi vibaya sana, kumi na mbili wakamkimbia.
Akiwa bado hajapumzika,kundi lingine la majambazi asio fahamu mahali walikotokea walimzunguka,wote walivalia makoti marefu na meusi, mkononi wakiwa wameshika nyundo ndogo kwa ajili ya mapambano..
“,Nasema mshambulieni, hakikisheni mnaipata diski, kisha mnamuua! “,sauti ilisikika kutoka jambazi mmoja akiwa amesimama nyuma kabisa, pembeni yake akiwa amesimama komandoo aliyekuwa na mwili mkubwa, bila shaka alikuwa ni mlinzi wake. Yuan Liang aliendelea kuwatazama, akisubili kujibu mashambulizi, huku akiahidi kumfyekelea mbali Jonsoni Mtemvu,kwani aliamini ndiye aliyemtumia makundi ya majambazi, waweze kumuua.
“,Nazani umesikia kauli ya bosi,kama unataka kuishi, tukabidhi diski,M27 hatujawahi kushindwa na mtu yoyote yule, tena wa kike kama wewe! “,jambazi mmoja aliongea,Yuan Liang akawahesabu majambazi wale,walikua ishirini na saba, akatabasamu, akatikisa kichwa, bila shaka aligundua kitu fulani…
“,Kumbe nyie ndiyo magaidi wa M27,nyie ndiyo mnauziwa silaha na serikali ya Jonsoni Mtemvu, nyie ndio mnahonga serikali kupitia kivuli cha raisi Jonsoni Mtemvu pamoja na waziri mshenzi Januari Sasamba, mnapitisha madawa ya kulevya bandarini bila kukaguliwa mkitumia kibali cha raisi!, sasa leo ulimwengu wote utajua maovu yenu, siku ya leo ijumaa, dunia nzima itakua bize kufuatilia habari pamoja na vifo vyenu …”,Yuan Liang alifoka, raia waliokuwepo pembeni kwa ajili ya kushuhudia mapambano ya ngumi bila malipo yoyote, wote walikimbia kujificha,kila mmoja aliwatambua magaidi hawa kwa ukatili, japo hawakuwahi kuwashuhudia machoni uso kwa uso. Yuan Liang hakutaka pesa tena, alitaka kuipigania haki iweze kupatikana, hakuwa tayali kuitoa diski mikononi mwake na kupoteza ushahidi.
“,Anasema nini huyo mshenzi, mkamateni tuondoke naye, akatwambie diski ameficha wapi!! “,bosi wa kikundi cha magaidi cha M27 alifoka, baada ya kusikia Yuan Liang anaweka wazi siri zao, alipaswa kunyanganywa diski na kuuawa kabla mambo hayajaharibika. Baada ya kutoa amri, magaidi ishirini na tano walimvamia Yuan Liang, kila mmoja akiwa na nyundo yake mkononi, katika mkono wake wa kulia.
Yuan Liang aliruka mateke,magaidi yakakwepa, akaruka tena yakwakwepa, yakamtandika na nyundo, akaruka serekasi, akatua upande wa pili, yakamvamia yote kwa pamoja, akayatandika ngumi yakwepa, akatumia kisu chake, akaruka mateke manne mfululizo, yote yakapanguliwa kwa ufundi na magaidi watano waliokuwa mbele kuongoza kundi …
“,Hawa washenzi nikizubaaa wataniumiza, isitoshe nimechoka tangu jana niko kazini!! “,Yuan Liang aliongea, akarudisha visu vyake kwenye mkanda wake, akainama, akafunga vizuri kiatu chake, akakunja ngumi, akajiandaa kutumia pigo lake la kifo, pigo ambalo siku zote liliwaacha maadui zake viwete.
“Naomba asinisogelee mtu yoyote,nitamuua ……”,Yuan Liang aliongea, mguu mmoja alikuwa ameuning’iniza juu, mikono yake miwili ilishika chini, alikuwa kama ng’e anayejiandaa kumshambulia adui.
“,Hahaaaaa, usijitetee malaya wewe, na leo wote tunakulala bureee!! “,gaidi moja lenye mwili ulioshiba kwa mazoezi lilimkejeli Yuan Liang, likamsogelea huku mkononi likiwa linacheza na kurusha rusha nyundo yake.
“,Paaaa! “,
“,Yalaaa! “,
“,Vuuuu, puuuu! “,
“,Yalaaa! “,
“,Kwachaa! “,
“„Yalaaa!, umeniumiza mseng* wewe! “,
“,Mseng* mama yako, nimewaambia msinisogelee mkazani nawatania, leo ndio mtajua mimi na nyie nani malaya! “,Yuan Liang alifoka, huku akikunja ngumi, akijiandaa kutumia pigo la kifo kwa mara nyingine tena, baada ya kulitumia kwa sekunde tano tu, akaruka hewani na kuvunja vunja mikono ya kila jambazi aliyemsogelea,magaidi takribani watano walikuwa chini wakiugulia maumivu ya mikono yao, wengine wakitukana matusi ya nguoni, huku baadhi ya magaidi wakirudi nyuma baada ya wenzao kujeruhiwa vibaya kwa sekunde tano tu.
…………………………………
Mexic;
Difenda ya polisi ikiwa na king’ora juu, ilipita barabarani na kufyatuka kama ndege, the super three soldiers walikuwa wamepania kukamilisha kazi haraka iwezekanavyo, waweze kurudi nchini Tanzania.
“,Tunaingia Mexic, hebu angalia kama bado adui yuko eneo hili …… !”,Kamanda Kendrick alitoa amri, kamanda Catherine akabonyeza batani ya kompyuta yake,akatazama kwenye kioo.
“,Connected, the related disc is available in Mexic, “(Imeunganishwa, diski inayohusiana inapatikana Mexic …)”,ujumbe uleule ulikuwa bado unaonekana kwenye kompyuta, akatabasamu, huku akijiweka sawa kwa ajili ya kuanza kazi.
“,Afande, bado mtuhumiwa yuko hapa Mexic, mwanzo wa mji! “,kamanda Catherine aliongea, wote wakatoa bastola zao, wakajiandaa kwa ajili ya kuanza kazi haraka iwezekanavyo, dakika tano zijazo, watakapoingia mji wa Mexic.
…………………………………
Magaidi yaliendelea kumnyemelea Yuan Liang, huku Yuan Liang akimsubili yoyote yule atakayemsogelea aweze kumtia adabu, ghafla king’ora cha gari la polisi kikasikika, magaidi hawakutaka sura zao kuonekana mbele ya macho ya polisi,wakaanza kukimbia kuyasogelea magari yao waweze kutoweka haraka sana.
“,Chukueni wenzenu walio jeruhiwa ,huyu mshenzi tutamtafuta baadae, ngoja tuwapishe hawa watoto wanaotupigia ving’ora! “,amri ilisikika, magaidi wote wakajipakia kwenye magari yao, wakatoweka, barabara ikiwa kimya, wananchi wote wakiwa wamejifungia kwenye majumba yao, uwepo wa M27 maeneo hayo uliwatisha sana.
“,Mikono juu!ukijitikisa, au ukifanya lolote lile tunakushambulia ……”,Yuan Liang hakutaka kukimbia, alitaka kujisalimisha ili awaeleze polisi ukweli kuhusu ukatili wa raisi wao Jonsoni Mtemvu pamoja na Waziri wake Januari Sasamba.
“,Sitaki shari na mtu, naomba mniache, nitajifunga pingu mwenyewe, nitaingia kwenye gari mwenyewe! “,Yuan Liang aliongea, bila wasiwasi wowote, akitoa masharti kwa askari wa the super three soldiers, pamoja na kamanda Gupta na Yasini waliokuwa wamemnyoshea silaha zao wakimsogelea.
“,Nawaomba mtii masharti yangu, sina lengo baya kujisalamisha, na mimi sio mtu mubaya, nasema hivi!nitajifunga pingu mwenyewe, nitaingia kwenye gari mwenyewe! “,Yuan Liang aliongea kwa upole, akatoa maelekezo kwa mara nyingine tena, kwa askari waliokuwa wanamsogelea.
“,Pumbavu kabisa, umeua, umemshambulia raisi, umeiba diski, halafu unatuwekea masharti ya kukumata! “,kamanda Gupta aliongea. Wote walimtambua Yuan Liang, baada ya kuitazama sura yake na mavazi yake, walimkumbuka siku alipowatoroka kwenye baa nje ya mji wa Mexic, wote walikuwa na hasira isipokuwa kamanda Kendrick. Kamanda Gupta akamvamia Yuan Liang, kamanda Catherine akafuatia, kisha wote wakafuatia, Yuan Liang alikwepa mateke matatu kutoka kwa Gupta, Catherine pamoja na Yasini, kisha akaruka mateke manne yaliyotupilia mbali bastola zao, wote wakabaki bila silaha mkononi.
Mexic; 6:24am
Kamanda Kendrick japo alikuwa hajapona vizuri bega lake, hakua na budi kuingilia mapigano kati ya askari wake na kahaba hatari sana, Yuan Liang. Askari wake wote walikuwa wanahema kama mbwa, piga nikupige, licha ya Yuan Liang kuwa peke yake, lakini alikuwa hapigiki kizembe.
“,Puuuuuh “,kishindo kilisikika.
Kamanda Kendrick aliruka teke, Yuan Liang akainama chini, akaruka tena mateke matatu mfululizo, Yuan Liang akayapangua yote kwa mikono yake ,kabla kamanda Kendrick hajatulia chini, alimpiga ngwala Yuan Liang, akadondoka chini kama mzigo! wakamvamia na kumfunga pingu pale pale chini, kamanda Gupta alishika mguu mmoja, kamanda Yasini akashika mguu mwingine, kamanda Philipo akamshika mikono Yuan Liang, kamanda Catherine akamvalisha pingu huku kamanda Kendrick akiwa ameshika bastola, tayali kwa ajili ya kumshambulia Yuan Liang atakapotaka kuleta vurugu. “,Tatizo nchi za Kiafrika zinatetea sana wahalifu, mnakamata wasio na hatia,haya kabla ya kwenda kituoni, naomba tuchukue pikipiki yangu hapo sheli ……”,Yuan Liang aliongea, hakuna aliyemjibu, wote walimuona kama jambazi hatari aliyestahili adhabu ya kunyongwa.
Walimpakia kwenye gari, wakamtupa kama mzigo, difenda ya polisi ikasogezwa katika sheli ya “pure oil “,ikajazwa mafuta, kisha wakapakia kwenye difenda pikipiki ya Yuan Liang, wakatoweka kwa fujo eneo hili,raia wakafungua milango na madirisha, kushuhudia difenda ya polisi ikitoweka mbele ya macho yao!
…………………………………
Costa; kituo cha polisi
Tetesi za jambazi hatari kukamatwa, jambazi hatari aliyemshambulia raisi mara mbili mfululizo, zilienea kila kona ya jiji la Costa na nchi jirani. Raia walijaa nje ya kituo cha polisi wakitaka kumshuhudia jambazi huyo wa kike, huku waandishi wa habari wakiwa bize kuchukua taarifa kwa ajili ya kupamba vyombo vyao vya habari, wengine redio, wengine televisheni.
“,Naomba majaji wote, balaza la mawaziri, na askari wote wawe mahali hapa, washuhudie mahojiano haya,waandishi wa habari wawe hapa kurusha matangazo laivu, bila hivyo sitaongea ukweli wowote ule,”Yuan Liang aliongea, akiwa amefungwa na kutundikwa kwenye mlingoti kama yesu msalabani, mkono wake ulifungwa kaskazini, mwingine ukafungwa kusini.
“,Dakika tano kila mtu uliyemuhitaji atakua mahali hapa! “,kamanda Kendrick aliongea, kamanda Catherine na wenzake wakatoka nje, dakika kumi mbele,mawaziri na waandishi wa habari walijaa kituo cha polisi, mahali alipokuwa amefungwa Yuan Liang,alifungwa kwa kamba na minyororo migumu, asipate upenyo,akaua watu na kutoroka.
“,Unaweza kutwambia historia fupi ya maisha yako? “,kamanda Catherine aliuliza swali, waandishi wa habari wakiwa bize kurekodi matukio, huku majaji wakiwa makini kuskiliza kesi, watoe hukumu mara moja bila hata kuipeleka kesi mahakamani.
“,Naitwa Yuan Liang,nililelewa na kukulia katika kituo cha watoto yatima cha mtakatifu Petro chini ya kanisa katoriki, nilipo fikisha miaka kumi na nane, niliingia mtaani kutafuta pesa, nikiwa barabarani, ghafla nilivamiwa, nikazibwa mdomo na kupakiwa kwenye gari,sikujua naelekea wapi,gari ilifika bandarini, nikapandishwa kwenye boti, mpaka kwenye kisiwa ambacho sikikumbuki jina, nikakuta watoto wengi kama mimi, wanafundishwa mapigano na mbinu mbalimbali za kujilinda, walikuwa magaidi, nikajifunza kwa miaka miwili, nikafikisha miaka ishirini,nilikuwa nimeiva, nikatumwa mzigo wa madawa ya kulevya, sikuwa tayali kurudi tena kwa magaidi hawa, nikajitupa majini, na kuogelea, walinitafuta bila mafanikio, nikaibukia pwani ya nchini Goshani, nikaingia mtaani tena, hapo ndipo nilianza wizi, niliwaibia pesa watu wabaya hasa wafanya biashara, wanasiasa na viongozi wa dini waliotaka kuninunua kama kahaba, hapo ndipo niliwaibia na kuwatia adabu ili waache tabia zao kulingana na vyeo vyao ……”,Yuan Liang alimaliza kutoa historia yake fupi, historia iliyomwacha mdomo wazi jaji mkuu, mwenye umri wa miaka themanini.
“,Wewe ni mtoto wa gavana wa kichina, mtawala wa Goshani enzi za ukoloni, baba yako alikua anaitwa Liang Xung, mama yako alikuwa ni muafrika, ndio maana wewe ni chotara! baba yako alitoroka na kurudi China, hakutaka kwenda na ngozi ya kiafrika huko, akamuacha mama yako, mama yako akapatwa na mshituko akafa palepale! wewe ukapelekwa kituo cha watoto yatima, ndipo ulipotoweka katika mazingira ya kutatanisha! “,jaji yule alimaliza kusimulia, watu wakazidi kuachwa midomo wazi
“,Mungu wangu! is this true?, anyway! yameshapita, napaswa kusahau! “,Yuan Liang alishtushwa na historia kuhusu wazazi wake, akapiga moyo konde na kujikaza kisabuni,ili aweze kusahau yaliyopita.
“,Mungu wangu, maajabu haya, jambazi kumbe alikuwa mtoto wa gavana! “,kelele zilisikika, watu walizidi kushangaa.
“,Tuambie! kwa nini ulimshambulia na kutaka kumuua raisi Jonsoni Mtemvu! “,swali lilisikika kutoka kwa waziri wa ulinzi,ukimya ukatawala, kila mtu alitaka kujua kuhusu jambo hilo.
“,Raisi ni muuaji, yeye na waziri Januari Sasamba, ni wauaji wakubwa na wauzaji wa silaha za serikali! “,Yuan Liang aliongea, askari wote wakamnyoshea silaha,tayali kwa ajili ya kupokea amri kumshambulia.
“,Acha kumkashifu raisi mbele ya majaji watukufu, utahukumiwa kifo! “,jaji mkuu aliongea.
“,Nitahukumiwa kifo, baada ya raisi na waziri mkuu kuhukumiwa, msipowahukumu, nitawahukumu mimi mwenyewe,!”,Yuan Liang aliongea, watu wote wakabaki midomo wazi.
“,Silahaa chini! “,Kamanda Kendrick, akiwa kama askari mwenye cheo kikubwa kuliko wenzake alitoa amri, askari wote wakashusha silaha zao chini …
“,Hujajibu swali, kwanini ulitaka kumuua raisi ?”,waziri wa ulinzi akauliza swali kwa mara nyingine tena.
“,Raisi alininunua kama kahaba, lakini mimi sio kahaba, sijawahi kulala na mwanaume yoyote yule, mtu anaponihitaji, mimi naenda kwa lengo la kumuibia, na kumzimisha kabla hajatimiza lengo lake, akishtuka, anakuta ameshaibiwa na mimi nikiwa nimeshatoweka!! ndivyo ilivyotokea, nilimzimisha raisi Jonsoni Mtemvu kabla hajafanikiwa kulala na mimi, nikamuibia diski ya saa yake ambayo ni ya dhahabu, nilijua nikiiuza nitapata pesa nyingi, nilipoenda kuichunguza nikagundua siri na maovu yote ya raisi, ndiyo maana nasema niwauaji! naomba televisheni iletwe hapa mara moja! “,Yuan Liang aliongea, dakika mbili tu, televisheni kubwa ililetwa, ikaunganishwa, walikuwa wameshamsachi kila kona, hwakuona diski, alikuwa ameshaificha mbali sana.
“,Askari mmoja abonyeze batani ya miwani yangu, mkono wa kushoto, kisha atazame kisigino cha kiatu changu, kikijifungua, achukue diski ya raisi wenu mshenzi kuliko wote duniani! “,Yuan Liang akaendelea kutoa maneno ya kejeli kwa raisi,akatoa maelekezo, kamanda Kendrick akasogelea miwani ya Yuan Liang, akabonyeza kama alivyoelekezwa, kisigino cha kiatu cha Yuan Liang kikafunguka, ndani ya kisigino kulikuwa na mashine ya kukata mawasiliano, akaachana nayo, akachukua diski, akabonyeza tena batani, kiatu kikajifunga, akasogelea televisheni, akachomeka diski, diski yenye ukubwa sawa na flashi, wakaanza kusikiliza sauti na kutazama matukio ya kihalifu yaliyofanywa na Jonsoni Mtemvu pamoja na Januari Sasamba.
“,Zima televisheni, wakamatwe mara moja, haijalishi ni mgonjwa au amekufa wote wakamatwe! “,amri ilitoka kutoka kwa waziri wa ulinzi, askari wakatoka nje haraka sana, wakiongozwa na kamanda Kendrick, kila kitu kiliwekwa wazi, ukweli ulikuwa umejulikana
…MWISHO … Jonsoni Mtemvu na Januari Sasamba walihukumiwa kunyongwa, Yuan Liang akapewa bilioni kumi na serikali kama zawadi, akaachana na wizi, akafungua kampuni ya ulinzi, mke wa raisi, mama Zainath alikufa kwa presha baada ya kutambua ukweli kuhusu maovu ya mume wake.
GEREZA LA NYUMBA YA GIZA KATIKATI YA MILIMA IRINGA
Fujo ndani ya gereza hili zilikuwa zimeshamiri katika upande ambao ulikuwa na sehemu za kufulia nguo, makelele ya wafungwa wa kiume waliokuwa wakishinikiza kupigwa kwa mtu ndiyo yalikuwa yakisikika yakipaa kwa nguvu . Kulikuwa na kundi kubwa sana la wafungwa waliokuwa wamezunguka duara katika eneo la jirani na sehemu mojawapo ya kufulia nguo ndani ya gereza hilo, kulikuwa na mapigano makali sana yaliyokuwa yamezuka ndani ya sehemu ya kufulia nguo ambayo ilipelekea hao watu wakawa wamezunguka kuweza kutazama. Mfungwa gani ambaye alikuwa hapendi kuona Askari akipigwa ndani ya gereza hili, walikuwa wakipigwa sana na maaskari hao waliokuwa wameshindikana. Ndani ya gereza hilo ambalo halina hata muongo mmoja tangu lianzishwe, lilikuwa likisifika kwa kuwekwa watu watukutu sana ambao walikuwa wameshindikana na wauaji wakubwa. Hata Askari wenyewe wengi wao walikuwa ni watu walioshindikana kuwekwa kwenye magereza mbalimbali kutokana na ukatili wao waliokuwa wakiufanya. Walitokea kuwa ni watu wenye kuchukiwa sana ndani ya gereza hilo kutokana na huo ukatili wao waliokuwa wakiufanya humo ndani, wafungwa wajeuri baadhi walikuwa wakiwahofia sana na kutokana na kipigo kizito walichokuwa wakiwapa. Ndiyo maana hata kupigwa kwa huyo Askari mmojawapo wa magereza aliyekuwa yupo humo ndani ya chumba chenye kufuliwa nguo, walibaki wakishangilia sana. Walikuwa wakiona ni burudisho Askari huyo akipewa kipigo na Mfungwa mwenzao, muda huo Askari wa magereza ambaye alikuwa yupo katikati alikuwa ameshindwa kabisa kuweza kujihami. Alipojairbu kutoa rungu ambalo alikuwa akilitumia mfungwa mmojawapo alimpokonya rungu, aligeuzwa gunia la mazoezi baada ya hapo kutokana na kushindwa hata kujihami. Mfungwa huyo ambaye alikuwa akimfanya gunia la mazoezi naye alijua kumpiga, alikuwa akitumia ujuzi wake wote katika kurusha ngumi ambazo zilikuwa zikimuonesha ni jinsi gani alivyokuwa fundi katika mapigano. Kila alipotumia mbinu mpya kabisa katika kumshmbulia huyo Askari ndiyo wafungwa wenzake ambao walikuwa ni wahalifu wazito, walivyozidi kusngilia kwa ufundi aliokuwa akiuonesha. Askari aliyekuwa akipigwa naye alikuwa amelowa damu uso mzima kwa jinsi alivyochakazwa, alipewa pigo moja la mwisho ambalo lilimtupa chini na ikawa ndiyo mwisho wake na hakusimama tena. Mfungwa ambaye alikuwa akitoa kipigo kwa Askari alikuwa ni mwenye sura ya kutisha, aliyejichora michoro mbalimbali mwilini mwake na alikuwa ni mwenye mwili mkubwa sana. Alipoona kaanguka chini aliamua kumfuata ili amalize kabisa mchezo, alikuwa akionekana kabisa kuua halikuwa jambo kubwa sana kwake. Alipomkaribia Askari huyo taa za humo ndani zote zilizimika kwa ghafla, kutokana na gereza hili kujengwa katikati kwenye shimo la mlima. Mwangaza wa kawaida haukuwa ukifika kwenye maeneo yote, hivyo mwangaza wa sehemu za ndani ya gereza ulikuwa ukitolewa na taa maalum zilizokuwa zikiwaka masaa ishirini na nne. Kuzimika kwa taa hizo ni giza linalofuata, kuzimika kwa taa hizo kuliambatana na ukimya wa ghafla sana uliowaingia wafungwa wa eneo hilo. “Ohoo! Afande Nkongo” Baadhi ya wafungwa waliropoka Haikupita hata dakika mbili kulianza kusikika milio ya kupigwa watu eneo hilo, sauti za watu waliokuwa wakilalamika kuumia pamoja na kuachia miguno ya maumivu. Ndiyo zilitawala ndani ya eneo hilo la kufulia nguo. Sauti za kupigwa watu humo zilidumu kwa muda mrefu, taa zilipokuja kuwaka asilimia kubwa ya wafungwa ndani ya gereza hilo walikuwa wana manundu na wengine walikuwa wamepasuka katika sehemu mbalimbli za miili yao Wote walikuwa wakigaragara chini na kiumbe pekee aliyekuwa amesimama alikuwa ni Askari mmoja ambaye hapo awali hakuwepo kwenye tukio hilo. Alikuwa ni Askari ambaye ameenda hewani haswa, mwenye mwili wa kimazoezi, alikuwa ni mweusi na alikuwa na nyota tatu kwenye bega lake. Alikuwa amesimama huku rungu likiwa lipo kwenye mkononi, macho yake makali ambayo yalikuwa yameficha kabisa uzuri wa kiume aliokuwa nao kwenye uso wake ndiyo yalikuwa yakiangaza kwenye eneo ambalo wafungwa wote walikuwa wakigaragara kwa maumivu. Hakika ndiye yeye aliyeshusha dhahama hiyo kwa wafungwa wote waliokuwa wakishangilia, muda huohuo kikosi cha maaskari mbalimbali waliokuwa wameshika virungu kiliingia hapo eneo la kufulia nguo ndani ya gereza hilo. Kiongozi wa kikosi hicho alitoa saluti kwa Askari huyo ambaye alikuwa, baada ya hapo walimchukua Askari mwenzao ambaye alikuwa amejeruhiwa na kuondoka naye mahala hapo. Waliwaondoa wafungwa hao waliokuwa wakiugulia kipigo huku Yule Askari akiwa ameweka mikono nyuma akiangalia hadi pale wafungwa wote waliporudishwa vyumbani mwao Walimuacha Askari huyo akiwa amesimama pekee akiwa ameweka kirungu alichotolea adhabu nyuma, alikuwa akiyatazama mazingira ya eneo hilo kama vile alikuwayaona kwa awali. Macho yake yaliyojaa ukali hadi yakawa mekundu, hayakuwa yakiisha kabisa kuyatazama mazingira ya hapo. **** Upande wa pili ndaniya gereza hilihili upande wa vyumba vya maofisa wanawake kulikuwa na mjadala mzito sana uliokuwa ukiendelea, maaskari wanawake waliokuwa na urembo lakini waliosheheni kila aina ya balaa. Walikuwa wamekaa kwenye ofisi hiyo wakiwa wanajadili waliyokuwa wanayajua wao, yalikuwa yakiwahusu wao tu ndani ya ofisi hiyo ndiyo maana wakakusanyika kwa pamoja wakijadilia. Ulikuwa ni muda ambao hawakuwepo kwenye eneo husika kutokana na wafungwa wa kike wengi kuwepo ndani ya vyumba vyao, porojo za kusogeza muda ndiyo zilikuwa zikijadiliwa hapo “Jamani mimi kuna kitu nimekiweka ila uzalendo uanishinda” Aliongea mmoja wao “Wacha wee Teddy hebu tuambie” Alidakia mwingine “Kusema ukweli ASP James nimechizika kwake” Teddy aliongea “Wee! Teddy hilo utabaki nalo mwenyewe moyoni bibi” Mwingine kabisa alidakia “Kwanini Jamila au hana moyo yule” Teddy aliuliza “Mtu mwenyewe yule hata kuongea na mtu tabu utaanzia wapi kumfuata senia kama yule” Jamila aliongea “Potelea pote siwezi kukaa kimya kwenye maisha yenyewe haya kutoka hutoki humu” Teddy aliongea “Sasa hata kama hivyo utaanzia wapi?” Yule wa kwanza alidakia “Rose usinikatishe tamaa shosti” Teddy aliongea “Si kama nakukatisha tamaa sote tunamjua yule hadi wewe mwenyewe” Rose aliongea Muda huohuo kengere ya dharura ikalia ndani ya gereza hilo, taa ya kengele hiyo ambayo ilikuwa imeunganishwa humo kwenye ofisi yao ilwajulisha kabisa kuwa dharura hiyo ilkuwa imetokea kwenye gereza la wanawake ndani humo. Ilikuwa ni kawaida sana ndani ya gereza hilo na ilikuwa haipiti siku mbili bila kutokea fujo ndani ya gereza hilo kutokana na wafungwa watukutu waliokuwa wakiwekwa humo ndani, iliposikika kengele hiyo kila mmoja alinyanyua kirungu chake. Wote kwa pamoja ambapo walikuwa wamevaa gwanda za mfumo wa suruali walikimbilia kwenye gereza la wanawake. Lilikuwa ni gereza ambalo lipo chini kabisa ya ofisi yao, iliwabidi washuke kwa haraka sana na kiukakamavu kuelekea huko. Walipokaribia eneo la magereza ya wanawake walisikia sauti ya fujo kubwa sana, hiyo iliwafanya wote kwa pamoja waufungue mlango wa mbele wa kuingia kwenye sehemu ambazo zilikuwa na vyumba vingi vyenye wafungwa. Teknolojia ya umeme ya ndani ya gereza hilo haikuwawia vigumu kuufungua mlango huo, walipoufungua tu baadhi ya wafungwa wa kike ambao walikuwa wakiwatambua balaa lao walitawanyika na waliingia vyumbani mwao. Wachache wajeuri waliendelea kusalia huku wakishangilia kama hawajawaona maskari hao. Maafande hawa wa kike wenye balaa tofauti na muonekano wao ulivyo, walianza kuwasogelea wale wafungwa wajeuri waliokuwa wapo wamezunguka duara huku wakiwa wanashangilia. Kilichofuata hapo ilikuwa ni kupiga virungu bila kuangalia mahali popote, wale waliokuwa wakijifanya wabishi na wakajaribu kuwakabili walijikuta wakichezea kipigo cha haja kutoka kwa maaskari hao ambao walikuwa ni wajuzi pia pia kwenye masuala ya mapigano. Muda mchache baadaye fujo yote ilikuwa imetulia na hakukuwa na yeyote ambaye alikuwa akileta ukaidi. Wale ambao walikuwa wakisababisha mkusanyo huo uwepo, walipewa kipigo cha haja. Kupigana kwao walipaona hapana maana kabisa kutokana na kipigo hicho wallichokuwa wamepewa, wote waliingia gerezani wakiwa na manundu kwenye miili yao kutokana na kipigo hicho walichokuwa wamepatiwa kwa kuleta mkusanyiko usio na maana na kupelekea fujo. **** Upande wa gereza la wanaume chumba kimojawapo cha wafungwa kulikuwa na wafungwa wawili waliokuwa wamepasuka vichwani, wengi walikuwa na manundu kwenye sehemu mbalimbaliza miili yao. Mmoja tu ndiyo hakuwa na nundu wala alama ya kuumia baada ya kuwa alikuwa amebakia humo ndani katika muda ambao wenzake walikuwa wakishangilia kupigwa na Askari, huyo alikuwa ni mtu wa makamo ambaye alikuwa na mwili mwembamba sana pamoja na kimo kirefu. Alikuwa aakiwangalia sana nwekzaek waliokuwa wameumia humo ndani na alikuwa akisikitika sana, alipowaona wengi wao wakijikanda manundu yao alikuwa akiwaonea huruma sana kwa kitu ambacho walikuwa wamekifuata kikiwapa hali hiyo. “Aisee Nkongo hafai kabisa yule” Mfungwa mmoja ambaye alikuwa na nundu jirani kabisa na utosi aliongea. “Tatizo mlienda kule hakukuwa na haja ya kwenda mngemuachia jamaa balaa lake mwenyewe” Mtu huyo ambaye alikuwa akiwasikitia alisema. “Kamishna Wilfred ungejua tulivyokuwa tunawachukia hawa majama wacha tushngilie” Aliongea “Ndoni mimi nilikuwa polisi hao nawatambua fika ndiyo maana nikatulia hapa, najua wote humu tumeingia sababu ya uhalifu lakini angalieni na maaskari wa kuwagomea. Si Segerea ile humu wapo walioshindikana watupu” Kamishna Wilfred aliongea “Kamishna ingekuwa wewe unaona yule anayekuonea anapigwa ungefanyaje?” Aliulizwa “Ningefurahi lakini haina maana kama kufurahi huko nipayuke nafikiri Nkongo nyinyi hamumjui kabisa yaani” Aliwaambia “Tena yule jamaa muache asiingie kwenye anga zangu atajuta kabisa” Aliongea mwingine aliyekuwa amepasuliwa. “Aisee Godi yule siyo Askari wa kawaida hana hata maelewano mazuri na rafiki zake ana jambo lipo moyoni mwake na nalijua tangu nipo kazini. Usicheze naye kabisa” Kamishna Wifred aliwaonya “Ngojea tu jamaa nitamtaimu yule” Godi alipania “Kama unaona ni sawa kumpiga basi ungempiga alipowapiga kundi zima akiwa peke yake, si kiumbe yule nitakuja kuwaambia habari yake” “Kamishna mbona unamsifia sana jamaa huyo tupe habari yake” Ndoni aliongea akiwa amekaa mkao wa kusikiliza “Muda hautoshi kwa leo majamaa watazima taa soon tu na kupita kuzingua, tufanye kesho kama baada ya kutoka kibaruani” “Poa” Waliitikia na kisha wote wakabadili mada na kuongea mambo mengine. *** Afande Nkongo muda huo alikuwa yupo kwenye eneo la chini kabisa ya gereza hilo, ni ndani ya eneo ambalo lina mawe mengi sana ambapo kulikuwa na sehemu iliyokuwa imevunjwa kuingia ndani ilikuwa haijamaliziwa. Mbele yake kulikuwa kuna Mfungwa yule ambaye alikuwa akimpa kipigo Afande mwenzake, alikuwa akivunja mawe kwa nyundo kubwa kuelekea ndani ambapo alikuwa akitengeneza njia ya kuweza kuwekwa reli mpya kabisa. Ndani ya gereza hilo Mzabuni aliyekuwa na jukumu la kuwalisha alikuwa akiingiza chakula kupitia njia hiyo ya reli, vyakula vilikuwa vikingizwa kwa Viberenge. Hivyo hiyo ilikuwa ni sehemu mojawapo ambayo ilikuwa ikitazamiwa kuja kuwekwa reli mpya, kufanya kosa la kumpiga Afande ndiyo lilifanya apewe kazi ya kupasua miamba ya ndani ya milima hiyo ili iweze kupatikana uwazi utaokuwa ukitumika kupitishia chakula na mahitaji mengine muhimu. Mkanda ambao ulikuwa umekunjwa kisawasawa ulikuwa umeshikiliwa mkononi na Afande Nkongo, alikuwa ni mwenye cheo kikubwa ndani ya gerza hilo lakini sehemu kazi kama hizo juu ya wafungwa watukutu kabisa alikuwa akizichukua yeye. Ndiyo maana hata huyo aliyediriki kumpiga Askari alimpa yeye adhabu hiyo na alikuwa akisimamia mwenyewe. Kicheo ni mrakibu msaidizi wa jeshi la magereza(ASP), uwepo wake ndani ya gereza hilo kulitokana na ukorofi ambao aliokuwa nao kama walivyo maaskari wenzake. Muda huo alikuwa akimtazama yule Mfungwa ambaye alikuwa akipasua mawe kwa nguvu , hakuwa akipepesa macho kabisa na macho yote yalikuwa yapo kwa mfungwa huyo ambaye alikuwa mkosefu. Haikufika hata muda mrefu tangu ampe adhabu hiyo alichoka, ukubwa na ugumu wa miamba ulimfanya asimame kwa ghafla ashindwe kuendelea na kazi. Hapo alitoa ushawishi kabisa kwa Afande Nkongo, akiwa anajishika kiuno kwa kuchoka alisikia mkanda mgumu wa kijeshi ukitua kwenye mgongo wake. Alipoushikilia mgongo mkanda huo ulihamia kwenye kiunoni, akiwa anaugulia maumivu hayo ndiyo alivyozidi kuongezewa maumivu mapya kabisa kutoka kwa. Alipoendelea kujishika katika sehemu ambazo alikuwa akipigwa ndiyo kipigo kilizidi kabisa na akajikuta akishika nyundo mwenyewe na kuendelea kupasua mawe. Pumziko la kipigo ndiyo lilifuata baada ya kuishika nyundo na kuendelea kupasua mawe, alikuwa akisikia maumivu sana lakini mbele ya Afande huyu asiyejua hiko hakuwa na huruma naye hata kidogo. Aliendelea kupasua kwa nguvu na hata nguvu zilizpomuishia alijikuta akapigwa mikanda pamoja na virungu ili asimame aendelee kupasua mawe, haikuwa na kupumzika kabisa mbele ya Askari huyu ambaye hakuwa ni mwenye huruma kabisa likija suala la adhabu. “Leo utatoka hapa ukipasua tobo la urefu wa mita 100, hutakiona kitanda mpaka ufikie hapo” Afande Nkongo aliongea kwa hasira kama ilivyo kawaida yake akiudhiwa. “Afande nimechoka” Alilalamika “Kukuonea huruma ni kujipelekea matatizo, nasema pasua mawe hayo. Nilishasema siwapendi watu kama nyinyi sasa ukiendelea kunisemesha ni kichapo” Hakuwa na ujanja tena zaidi ya kuendelea kupasua mwamba huo kupatikane nafasi ya umbali huo aliokuwa akitakiwa aupasue, ugumu wa miamba ya mlimani ilikuwa ikimuweka kwenye wakati mgumu sana. Alipofikiri kipigo alichokuwa akipatiwa kila akisitisha kazi ilimbidi tu aendelee. Sura ya msimamizi wa zoezi hilo haikuwa yenye kuwa na huruma naye, ilikuwa imezidi kuchukia sana tofauti na ilivyokuwa hapo awali jambo ambalo lilimfanya asilelemae hata kidogo. Jasho lilikuwa likimtoka si kidogo hadi hata mikono ikawa inateleza, hii ilisababisha aangushe nyundo mara kwa mara. Alikimbilia kuiokota kuhofia kuongezewa dhahama isiyo na lazima, aliendelea kupasua miamba hiyo kwa nyundo kuelekea ndani. Nusu saa ilipita na hakukuwa na dalili yeoyte hata ya kuonewa huruma, mtuhumiwa huyu wa ugaidi na mauaji kama walivyo wengine hakuwa na mtetezi wake. Alikuwa yupo ndani ya shimo lenye urefu, mtetezi wake ndiyo huyo alikuwa akiiteketeza ngazi yake ya kumfanya kuokoka ndani ya shimo.
Afande huyu alikuwa akitulia kimya tu akimuangalia Mfungwa wake, mlio wa kupasuliwa kwa mawe ndiyo kama ulikuwa ni burudani yake. Ulipokatika huo mlio basi kilichokuwa kikifuata ilikuwa ni kipigo, hakutaka kabisa mlio huo ukatike katikati ya kazi hiyo. Macho yaliyokuwa ni mekundu ambayo yalionekana dhahiri kutokana na kuwepo kwa mwangaza humo ndani ya mlima, yalikuwa yakitua sehemu moja tu katika eneo ambalo alikuwepo yule Mfungwa aliyeleta kadhia kwa Askari mwenzake, Yalikuwa ni kama yalikuwa yamegandishwa, mboni haikusogea pembeni juu wala chini. Zilikuwa zipo usawa ule ambao alikuwa yupo huyo mbishi ambaye hadi muda huo alikuwa ni mwenye kujuta kutokana na ubishi wake. Afande Nkongo alikuwa akiutazama kwa umakini sana mgongo wa mfungwa huyo,ilikuwa ni kama alikuwa akiburudishwa sana kwa kuangalia jinsi ambavyo ulikuwa uking’ara kwa jasho. Kugongana kwa chuma kigumu na mawe ya milima hiyo, kulitoa makelele lakini hakukumfanya aache kukaa kwenye eneo hilo kumsimamia huyo Mbishi. Muda huo mwenye kufanya adhabu hiyo alikuwa hajafika hata mita kumi ya kutoboa kuingia ndani kati ya mita mia moja alizokuwa amepatiwa, muda ulikuwa ukiyoyoma kama kipande cha mpira kilichokuwa kimetiwa kwenye moto. Bado alikuwa hajafika asilimia moja ya eneo ambalo alikuwa amepatiwa kama adhabu, misuli yake imara ya kimazoezi ilituna kwa jinsi alivyokuwa akilazimisha uchovu uliokuwa umeanza kumuingia. Ujengekaji wa mwili wake kimazoezi ulionekana barabara kwa jinsi ambavyo alikuwa ameshikilia nyundo hiyo kwa nguvu nyingi sana akigonga miamba, kuhema napo kulikuwa naye mithili ya bolti na gurudumu la chombo cha moto. Alijuta kuingia kwenye mikono ya mtu huyu ambaye alimuona ni Malik ndani ya dunia hii, aliona ukatili wake haukuwa na tofauti kabisa na Malik yule ambaye aliwahi kumsikia kwenye vitabu vya dini akilinda lango la Jahannamu. Kutokuwa na usikivu juu ya hali ya mtu, ni sifa tosha kabisa iliyomfanya amfananishe huyo na Mlinzi wa moto mkali kuliko wote, ingawa Malik huyu kwenye roho yake alikuwa akisikia tofauti na yule ambaye alimsoma kiimani ambaye hakuwa akisikia hata kidogo. Sifa za huyo afande ambazo alikuwa akizisikia kila siku zikiwakumbwa wengine, aliweza kukabiliana nazo kwa mara ya kwanza. Alikiri kabisa alikuwa ameingia kwenye anga ambayo haikuwa ikimfaa kabisa. Ilipotimu nusu saa akashindwa kujizuia kwani uchovu ulikuwa umezidi kiwango, hatimaye alianguka chini akawa sura ikiwa juu huku macho yake yakiangalia sehemu ya juu ya eneo hilo. Kuanguka huko kulifuatia na hatua nzito za Afande Nkongo, Mfungwa huyo akiwa kwenye uchovu alifunga macho kwa mara moja na alipofungua alikutana na kivuli kikiwa kimekinga taa hiyo aliyokuwa akiitazama. Akiwa bado hajakielewa hicho kivuli alisikia kitu kigumu sana kikitua kwenye bega lake na kisha kikafuata kifuani, hakutaka kujiuliza mara mbili kitu hicho kilikuwa ni nini. Alitambua kabisa huo ulikuwa mkanda mgumu wa kijeshi, alibiringisha kutokana na maumivu aliyokuwa ameyapata. Aliuweka mgongo juu na hapo ni kama alikuwa amemuwekea Afande Nkongo sehemu ya kupiga, mkanda huo ulitua kwenye mgongo wake. Maumivu zaidi aliyapata na hata akafumba macho kwa nguvu, kufumba macho namna hiyo bado hakukushwishi aweze kuonewa huruma na Afande huyu asiye na huruma. Aliendelea kupokea kipigo kizito na muda huo akiwa amechanganyiwa na virungu, kipigo hiko kilidumu hata fahamu zilipomtoka kiliendelea vilevile. Usitishwaji wa kipigo hicho ulikuja kutokea baada ya kusikika ukelele mkubwa, huo ulikuwa ukitokea katika upande ambao kulikuwa na njia ya kurudi gerezani. Sauti hiyo kubwa ilikuwa ikifahamika vyema na Afande Nkongo,ilikuwa ni sauti ya nguvu ambayo ilikuwa ikimkataza asiendelee kufanya hivyo alivyokuwa akifanya. Naye alisitisha mara moja na kisha akasimama kuangalia nyuma, alikutana na sura ya Mtu mzima wa makamo mwenye mwili mkakamavu akiwa amesimama. Alipomuona huyo mtu alisimama kisha akatoa heshima, alibaki akiwa amesimama huku akimtazama Mkatazaji wake ambayo alikuwa yupo mita kadhaa kutoka hapo alipo. “nini unafanya kijana wangu?” Aliulizwa hakujibu “Keshapoteza fahamu huyo, kama ni hatia aliyokuwa ameifanya ungecha” Sauti ya kumlaumu ilirudi tena kumuambia lakini hakushughulika kutia neno. Yule Mzee ambaye alikuwa akimtambua vilivyo afande huyo aliyewakuwa amempa heshima, hakushughulika kumuuliza juu ya kimya chake. Alichoamua ni kutoa simu ya upepo ya kisha akatoa amri wa vijana wengine, dakika takribani mbili baadaye waliingia vijana wengine ambao walikuwa na sare za kiaskari na walienda kumnyanyua Mfungwa huyo na kisha wakamtoa eneo hilo na kumuacha akiwa Mkuu wao yupo pamoja na Afande Nkongo. Aliamua kumsogelea Askari huyo wa chini yake ambaye hakuwa akiishiwa hasira, alipomfikia alimkuta akiwa na macho yaaleyale ya kihasira akiwa anamtazama. Hasira hizo hazikuwa zenye kumtisha hata ukali wa sura alionao mmiliki wake, alimshika bega lake la kuume na kisha akamtazama kwa sura ya upole. “Najua una machungu sana kijana wangu, ila ukumbuke waliokufafanya uwe katika hali hii si hawapo. Chuki usihamishekwa wengine” Alimuambia “Ni ngumu sana kuisahau hii, kila nikiona mwenye nguo kama zangu akiwa anafanya kitu kisichostahiki au hawa watuhumiwa wakifanya haya” Aliongea kwa uchungu “Lakini si hao waliokufanya uwe katika hali hii kijana wangu, usichukie maelfu kwa kosa la wachache” “Siwezi nawachukia wote hawa” “Hiyo siyo sahihi kijana wangu, hebu tutoke tuelekeee kule Bwaloni” Wote kwa pamoja waliifuata njia ndefu ambayo iliwapeleka hadi eneo lenye mlango wa chuma, mlango huo ulifunguliwa na Askari wa cheo cha chini na kisho wote wakapita. Walifuata njia nyingine iliyokuwa ikielekea eneo lenye ngazi ambazo walipanda, walitembea wakizipita kona nyingi sana ndani ya gereza hilo. Hatimaye walifika kwenye eneo la juu ya gereza hilo ambako anga lilikuwa likionekana, wote walienda hadi ndani ya Bwalo la chakula la maaskari waliokuwa na vyeo vikubwa ndani ya gereza. Walitafuta mahali pa kuketi kwenye eneo lenye viti vilivyopangwa kimpangilio, muda huo humo ndani kulikuwa na watu wengine kabisa waliokuwa wakiangalia mpira na kushangilia kwa nguvu sana. Afande Nkongo naye alipoona kulikuwa na mechi ya kukata na shoka alijikuta akielekeza macho yake huko hulipo Luninga, taratibu ule uso wa kujaa chuki ukapungua na akawa na sura ya kawaida na hapo alianza kuongea na Mkuu wake huyo akiwa hana hasira yeyote ile. Hakika kulikuwa na mechi ya timu mojawapo ambayo alikuwa akiipenda, wote waliangalia huku wakiongea mambo mbalimbali. Haikufika hata muda mrefu timu yake ambayo alikuwa akiipenda iliweka mpira wavuni, alishindwa kujizuia na akajikuta akishangailia kwa furaha sana hadi Maaskari wengiena ambao hawakuwahi kuliona kabisa tabasamu lake wakamtazama. Waliona ilikuwa ni maajabu kwa ASP huyo kutoa kicheko cha kushangilia kwa nguvu. Wengi walikuwa wakidhani kuwa alikuwa hana kiungo ambacho kingemfanya acheke kwenye mwili wake ndiyo maana alikuwa ni mwingi wa kununa, kucheka huko kuliwafanya waamini kuwa walikuwa wakiwaza tofauti kabisa na alivyo. Uzuri wake sura yke ulionekana ndani ya siku hiyo ikiwa ni siku ya kwanza kabisa kuangalia mpira akiwa na maofisa wenzake tofauti na kuangalia mpira ndani ya nyummba yake katika gereza hilo. Wengi wao walikuwa ni wenye kumtazama kwa kuibia sana akiwa ni mwenye furaha, hakika alipendeza sura akiwa katika hali hiyo ambayo hakuwa akipenda kujiweka siku zote. “Unajua unapendeza sana ukiwa ni mwenye kutabasamu hivyo” Mkuu wake alimuambia huku akitabasamu na yeye, Hakujibu chochote alipoambiwa maneno hayo yeye alijikuta akitabasamu, hilo halikumzuia Mkuu wake kuache kuendelea kumsemesha kwani alikuwa ni mtu pekee ambaye alikuwa akipikika naye chungu kimoja naye ndani ya gereza hilo. “Unajua sababu ya kukuleta huku, umekuwa ni mwingi wa mawazo hadi unasahau siku muhimu kama ya leo” Alimuambia kisha akatoa kadi akampatia Afande Nkongo aliifungua kadi hiyo kwa utulivu wa hali ya juu, alikutana na kadi iliyopambwa vizuri ikiwa na ujumbe wa kumtakia furaha ya siku ya kuzaliwa. Alibakia akishangaa kwani alikuwa hajui kabisa kuwa ilikuwa ni siku muhimu ya kuzaliwa kwake. Mambo mengi yaliyokuwa yamemtinga yalimfanya hata ashindwe kutambua kuhusu hilo, wingi wa mawazo ndani ya ubngo wake nao ulikuwa ni sababu nyingine kabisa ambayo ilimfanya ashindwe kutambua siku yake muhimu sana. “Happy birthday, hongera kwa kutimiza miaka 35” Alipongezwa akiwa bado yu ndani ya Mshangao. Muda huo huo luninga ikazimwa kwa ghafla na maofisa wote waliokuwa wapo ndani humo, waligeuka nyuma na wakamtazama yeye na kisha wakaanza kupiga makofi huku wakimuimbia kumtakia furaha ya siku ya kuzaliwa. Afande Nkongo alijikuta akiingiwa na tabasamu alipotazama maafisa wenzake wachache waliokuwa wamevaa mavazi ya kiraia wote kwa pamoja wakimuimbia, maofisa hao nao walisogea hadi karibu yake huku wakiendelea kuvigombanisha viganja vyoa na kupelekea kutokea kwa sauti hizo zilizokuwa zikiendana na wimbo huo waliokuwa wakiuimba. Si wanaume wala wanawake miongoni mwa maofisa hao waliokuwa wamevaa vyenye kupendezesha, wote walisogea hadi karibu yake na kila mmoja akiwa na zawadi yake mkononi. Ilionekana wazi lilikuwa ni jambo ambalo lilikuwa limeandaliwa muda mrefu na yeye hakuwa amelitambua, muandaji wa jambo hilo alikuwa ameliandaa vya kutosha hadi kufikia hatua ya Afande Nkongo kutabasamu akiwa na wenzake. Hakika alikuwa ameviondoa vile vyenye kuukera moyo wake, ndiyo maana alikuwa na tabasamu namna hiyo. Alikumbatiana na wengi waliokuwa wakihitaji kufanyiwa hivyo, haswa watoto wa kike ambao walikuwa wakihitaji hilo jambo. Hilo halikuwa neno kabisa kwa Afande Nkongo yeye aliona ilikuwa ni jambo la kawaida tu kukumbatiana nao, muda mfupi baadaye alikuwa na zawadi nyingi sana kwenye eneo ambalo alikuwa amekaa. Hilo lilimpa faraja sana na akajikuta akifurahia nao, ilikuwa ni mara ya kwanza kwa yeye kujishngaa sana kwa jinsi alivyobadilika na hata kutabasamu akiwa yupo na hao watu. “Napenda niwahukuruni sana, sina cha kuwalipa” Aliongea baada ya kupokea zawadi na kisha alimtazama Mkuu wake wa Kazi akamwambia, “Baba sina cha kukulipa” Furaha ilikuwa imefana ndani ya jengo hilo la Bwalo hadi pale alipoaga kwenda kumtazama mwenzake aliyekuwa hospitsli, aliondoka akiwa amekabidhi zawadi kwa mkuu wake. Aliahidi kurejea tena kuzifuata. Hilo lilikubaliwa na wote waliokuwa humo ndani, alipotoa mguu humo ndani kilichofuata ilikuwa ni mjadala kuhusu yeye. “Mkuu leo Afande ana nini namuona siyo kawaida yake, nilijua atachukia” Afisa mmoja aliongea. “Cha muhimu niliwaambiwa ukitaka uwe na urafiki naye, la si hivyo hutaongea naye na ukilazimisha ni ugomvi” Mkuu aliongea “Kwanini aliulizwa?” Aliulizwa “Hilo suala ni gumu kuwaeleza hivi sasa, usije ukaenda kuongea naye kirafiki ukiwa umevaa sare za kazi hamtaelewana labda uwe kikazi” Alieleza “Ila unatutisha mkuu” “Eleweni hilo, kila mtu ana kipindi alichopitia kwenye maisha yake ndiyo kama Nkongo” Alieleza “Ni kijana mzuri mwenye umbo zuri ila ukaaji wake wa kuwa namna ile kila muda kununa kunanishangaza kwa kweli” “Huyu ni mtu mmoja mnapaswa mumuelewe jamani” “Sawa mkuu” **** Muda huo Afande Nkongo alikuwa yupo ndani ya chumba kimojwapo cha wodi,ni hospitali maalum ya jeshi la Magereza iliyokuwa imejengwa ndani ya Gereza la Nyumba ya Giza. Alikuwa akitazamana na kitanda cha Askari mwenzake aliyekuwa yupo chini kicheo, alikuwa ni mwenye majeraha mengi sana kwenye mwili wake na kupelekea hata sura yake isitambulike vyema. Afande Nkongo alipouona huo uso wake mwenzake alijikuta akiingiwa na huruma na zile hasira dhidi ya yule Mfungwa zikamjia. Alitamani muda ururdi nyuma ili aweze kumuongezea adhabu Mfungwa yule ambaye alikuwa amesababisha maafa hayo. Hilo halikuwezekana kabisa kwani huyo Mfungwa pia hakuwa ni mwenye fahamu hadi inafikia mida hiyo, yote ni kutokana na kipigo ambacho alikuwa amempatia kutokana na kushindwa kuendelea na kazi. Alibaki hapo akimtazama mwenzake pasipo kukupesa jicho, alikaa kwenye hali hiyo kwa muda mrefu sana hadi pale aliposikia sauti ya mtu akiguna nyuma yake. Hapo aligeuka nyuma na kukutana na Afande Teddy akiwa ni yu mrembo kuliko alivyokuwa akionekana, huyu alikuwa ni yule Askari ambaye alikuwa akiwaambi wenzake juu ya kumuhusudu Afande mmojawapo wa humo ndani. Afande Nkongo alipokutana na Afande huyo wa kike alipokea heshima yake kutokana na kuwa mkubwa kicheo kwake, alitikisa kichwa kuikubali heshima hiyo na kisha alirudisha macho kwa mwenzao aliyeo kitadani. “Mkuu anaendeleaje?” Aliulizwa “Hali ndiyo hiyo kama unavyoiona” Alijibu “oooh! God hawa wafungwa dawa yao ni kuwavunja na miguu tu hii too much” “Hii atailipia huyo Bazazi, subiri azinduke apate nguvu lile eneo kwa ajili ya reli mpya atalibomoa yeye lote hadi njia ipatikane” Afande Nkongo alipoongea maneno hivyo alisogea hadi jirani na kitanda. Alikishika kiganja cha Mgonjwa kwa sekunde kadhaa kisha aligeuka na kuondoka humo ndani akimuacha Afande Teddy akiwa pekee yake. Macho ya Afande Teddy yote yalikuwa yapo kwake kipindi alipokuwa akitoka humo ndani, hadi anapotea kwenye upeo wa macho yake ndiyo alipokumbuka kugeuza macho na kumtazama Mgonjwa. Haukupita muda mrefu tangu atoke Afende Nkongo, aliingia Askari mwngine wa kike ambaye alikuwa si haba kama alivyo huyo aliyekuwa yupo hapo ndani. Huyu hakuwa mwingine ila alikuwa ni Afande Rose mmojawapo wa maafande wa kike aliokuwa nao ofisini. “Naona shosti leo ulikuwa naye humu” Aliambiwa “Yaani imekuwa maajabu kabisa” Alisema “Kivipi tena?” “Yaani leo kaongea na uso wake chuki sijauona” “Bahati yako bibi huenda kalainika” “Mh! Usinitie moyo tu nikaenda kuingia pabaya, ujue nilikuwa najikaza tu hapa ila namuogopa sana” “Mh! Haya tuachane na hayo shosti, vipi Kamugo anaendeleaje?” “Yaani hali ndiyo kama unavyoiona hapa, hii Minguruwe tunayoichunga ni tabu tupu” “Yaani hawa wa kuwavunja miguu kabisa, nasikia huko huyo jamaa kampa kibano hadi kanyamaza kwenye kitanda hadi sasa” “Ni bora tu yaani wametukusanya sisi wakorofi tuje kuchunga hawa manguruwe vichaa, ikileta ujinga ni dawa hiyo tu” “Ndiyo kazi hii shosti” Muda huo walibaki kimya na wakawa wanamtazama Afande Kamugo, walisikitika sana kumuona akiwa kwenye hali hiyo ingawa wao wenyeji walikuwa ni wenye roho ambazo siyo za kawaida.
Hawakukaa sana kwani muda muda ambao walikuwa wakihitajika kupumzika, ulikuwa ndiyo muda ili waweze kujiandaa na siku mpya. Ulikuwa ni muda wao wasio na zamu kutokana na kupangiwa zamu ya asubuhi Usiku huo walihitajika kupumzika kama ilivyo kwa wanadamu wengine ili waweze kujiandaa kukabiliana na siku mpya. Waliondoka humo wodini bada ya kumuona Askari mwenzao aliyekuwa yu mahututi, hasira zao kwa wafungwa zilikuwa ni kubwa sana pindi walipokuwa wakitoka humo ndani. Walikuwa wakitamani hata wafungwa waliokuwa wamemfanyia hivyo mwenzao wangekuwa wanatoka upande wa kike,ili waweze kuwapa kipigo kizito. ALFAJIRI ILIYOFUATA Majira ya alfajiri mlio wa kengele ya kuamsha wafungwa ilisikika ikilia kwa fujo, wafungwa walikuwa tayari wameshaanza kuamka na kutoka kwenye vyumba vyao. Walikuwa wakitoka kwa haraka sana kuhofia kipigo kutoka wa maafande ikiwa watachelewa kutoka vyumbani. Maasakari nao hawakuwa nyuma kabisa katika kupita kwenye vyumba mbalimbali vya gereza hilo kuhakikisha habaki mtu humo ndani. Muda mfupi baadaye wafungwa wa kiume makundi kwa makundi walikuwa wapo kwenye ngazi zilizokuwa zikishuka chini wakiwa na vifaa mbalimbali vya kazi, walikuwa wakishuka kwa haraka sana kutokana na kupelekeshwa na maafande ambao walikuwa wapo nyuma yao. Walifika hadi eneo ambalo lilikuwa na njia kama ya kupitisha reli ambayo ilikuwa ni tofauti na ile ambayo alikuwa akipewa adhabu yule Mfungwa aliyempiga Askari. Walipofika eneo hilo ambalo kulikuwa na upana wa kutosha waligawanywa makundi, kila kundi lilikuwa na Askari wake ambaye alikuwa akilichunga. Rokoo ilianza kupita kwenye kila kundi hadi pale maaskari walipohakikisha kuwa wapo idadi kamili. Baada ya hapo kila mmoja alishika kifaa chake cha kazi na kazi ikaanza, ilikuwa ni kupasua mawe kutengeneza njia ya kupitisha reli ziingiazo ndani ya jengo hilo kuleta huduma mbalimbali. Wengine walikuwa wakifanya kazi ya kuzoa vipande vya miamba vilivyopasuliwa na kuvipeleka eneo jingine, kila mmoja alikuwa na jukumu lake katika kazi hiyo ngumu ambayo walikuwa wakiifanya humo ndani. **** Muda huo Afande Nkongo ndiyo alikuwa akitoka kwenye ofisi yake, alikuwa amevaa gwanda la kikazi kama kawaida yake huku mkononi akiwa na rungu ambalo lilikuwa la muhimu kwake. Aliingia moja kwa moja kwenye njia ile ambayo aliipita siku iliyopita, alishuka ngazi hadi kwenye ambalo alikuwa amempa adhabu yule Mfungwa. Alikuwa anayo taarifa ya kuzinduka kwake na muda huo alikuwa akiendelea na adhabu yake, hapo alimkuta akiwa amesimamiwa na maaskari wawili ambao walikuwa wapo chini yake na pembeni kukiwa na Mkuu wake wa kazi ambaye alikuwa amevaa sare za ofisini za kijani. Maaskari hao walipomuona waliendelea na kazi ya kusimsmia eneo hilo, Afande Nkongo alitoa saluti kwa mkuu wake na kisha akasogea jirani kabisa na eneo ambalo Mfungwa huyo alikuwa akipasua mawe kufikia umbali ule aliokuwa amemwambia aufikie. Kitendo cha kuiona ile nguo ambayo ni sare ya wafungwa wekundu ulianza kujengeka kwenye macho yake, mishipa midogomidogo ilianza kujitokeza kwenye macho yake. Mkono wake uliokuwa umeshika rungu ulikakamaa sana kuashiria alikuwa na hasira sana, alipofika hapo aliwatazama maasakari wa chini yake waliokuwa wakimsimamia kwa macho ya kihasira sana hadi wenyewe wakaingiwa na hofu. “Kaendeleeni na kazi zingine huyu niachieni” Aliwaambia huku akiwatazama kwa macho yake makali. “ASP” Mkuu wake wa kazi alimuita “Afande” Aliitika na kisha akaageuka nyuma kuelekea alipoitwa, alipofika alisogea kando na Mkuu wake huyo kuteta jambo. “Mwanangu wachie hao waendelee naye, wewe kaendelee na kazi za kiofisi” “Lakini Baba” “Hakuna na lakini naomba fanya hivyo kama unaniheshimu, usiwe na hasira na hawa siyo waliokukosea” “Sawa” “Pitia ofisi zote za junior wako uhakikishe kama wanafanya kazi kiutiifu” Alitoa saluti alipopokea jukumu hilo na kisha alipanda ngazi akiwa ameamua kumridhisha Mkuu wake wa kazi, alipitia kwenye ofisi moja moja ndani ya gereza hilo akianzia kwa wanaume na hatimaye alifika kwenye ofisi za Maaskari wanwake waliokuwa wapo ndani ya gereza hilo. Kitendo cha kufungua mlango wa ofisi hiyo aliwakuta maaskari hao wakike wakiwa wanaongea, wote walipomuona walikakamaa na mkubwa kuliko wao aliyekuwa yupo huo ndani alitoa saluti kwake. “Hamna kazi ya kufanya siyo?” Aliwauliza wote walikaa kimya “Si nawauliza nyinyi hapo, yaani mnageuza sehemu ya kupigia domo hii ofisi. Haya kila mmoja afanye kazi yake iliyomuweka humu ndani” Alipomaliza kutoa mmri hiyo alitoka nje ya chumba hicho cha ofisi. Moja kwa moja alielekea kwenye ofisi zingine ndani ya gereza hilo akiwa anakagua kazi zinavyoendelea, alizimaliza ofisi zote akiwa anawaonya wale wote waliokuwa wakifanya uzembe na hatimaye alishuka hadi eneo ambalo kulikuwa na wafungwa wengi waliokuwa wakifanya kazi. Huko alikuta kazi zikiwa zinaendelea vizuri katika kila upande ndani ya gereza hilo, aliridhishwa na maaskari wale waliokuwa wakisimamia wafungwa kufanya kazi mbalimbali ndani ya gereza hilo. Alipomaliza kupita na kukagua alianza kuridi kupita ofisi moja moja kupanda juu kurudi ndani ya ofisi yake, ilikuwa ni kawaida yake akimaliza kukagua kuanza kupita kuhakiki kwa mara ya pili. Ukaguzi wa aina hii alikuwa akiulenga sana kwenye ofisi za maaskari wa juu kidogo ambapo walikuwa na kawaida ya kuendelea kutegea pindi anapoondoka, baada ya ukaguzi huo wa mara ya pili alirudi tena ndani ya ofisi yake. Kuifikia ofisi yake ilikuwa ikimlazimu kupita kwenye vyumba tofauti vya ofisi vya gereza hilo, eneo ambalo lilikuwa linaanza vyumba hivyo kulikuwa na picha mbili ambazo kila akiingia ndani ya ofisi hiyo lazima mojawapo aitazame sana. Picha ya kwanza ilikuwa ni picha ya Mheshimiwa Rais Zuber Ameir na picha ya pili ilikuwa ni picha ya Mkuu wa jeshi la magereza nchini, Kamishna Jenerali. Macho yake yalikuwa yakitua kwenye picha hiyo ya pili kuliko hata picha ya Amiri jeshi mkuu ndani ya nchi hii. Alipochoka kuitazama picha hiyo macho yake huwa mekundu na jambo hilo maaskari waliokuwa wapo chini yake walikuwa wameshaanza kumzoea ingawa hawakujua ilikuwa ikitokana na kitu gani. Aliingia ofisini kwake akavuta kiti na kisha akakaa kuendelea na kazi muhimu, umakini wote ulikuwa kwenye kazi kutokana na utulivu ambao ulikuwa upo ndani ya ofisi hiyo. **** Muda ambao Afande Nkongo alikuwa akitoka kwenye upande ambao walikuwa wakisimamiwa wafungwa, wale ambao walikuwa wakikaa gereza moja na Kamishna Wilfred walitoa macho kumtazama na kisha wakageuza macho kumtazama mwenzao huyo aliyekuwa ameahidi kuwasimulia juu ya Afande huyo. Wale waliokuwa wamepigwa siku iliyopita walimtazama kwa macho yenye chuki sana, hawakuwa na lolote la kumfanya kutokana na mamlaka ambayo alikuwa nayo ndani ya gereza hilo. Walitokea kumchukia sana lakini chuki yao ilikuwa ni sawa na kazi bure tu, hawakuwa na lolote la kuzituliza chuki zao. Wakisema wajaribu kumpiga hawakuwa na uwezo wa kupigana naye, walikuwa wakijua sana jinsi alivyo hatari kwenye mapigano ya mikono mitupu na hata ya kushika silaha. “Kamishna mtu wako huyo” Mfungwa mmoja alimwambia. “Inaonekana hamumpendi sana nyinyi majamaa” Aliwambia huku akiendelea kupasua mawe kwa nyundo kubwa sana. “Ulisema utatuammbia kuhusu yeye kumbuka Kamishna” Mmoja alimkumbusha “Msihofu jamani nitawaambia kila kitu kuhusu yeye subirini wa chai ufike” “Hamna noma jamaa” Waliedelea na kazi yao ngumu ndani ya gereza hadi ulipofika muda wa chai, kengele maalum ililia na wote wakaweka vifaa chini wakaelekea kwenye eneo la kupata kifungua kinywa. Wafungwa mbalimbali walikuwa wamepanga mistari kueleka kwenye eneo la kuchukua kifungua kinywa chao, mistari ilikuwa ikisogea taratobu sana kutokana na ugawaji wa chakula hicho kutokuwa wa kasi. Ulifika muda wa kupata chakula kwa wale wafungwa waliokuwa wapo pamoja na Kamishna na Wilfred. Baada ya hapo wote walielekea kwenye eneo ambalo walikuwa wamelitenga kwa ajili ya kunywa chai, wote kwa pamoja walikuwa na wahka wa kusikia juu ya Afande ambaye alikuwa ni mkatili kuliko wote ndani ya gereza hilo. Walipoketi tu kila mmoja akiwa na chakula chake walipeleka macho yote kwa Kamishna Wilfred ambaye alikuwa ameshikilia mkate na kikombe cha bati chanye chai. “Kamishna tunakusikilia sasa” Aliongea mfungwa mmoja na kumfanya Kamishna Wilfred aweke kikombo chini. Akianza kuuweka mkate wake ili upite kwenye mashine za usagaji mdomoni alisimulia, “Japo miaka imesogea sana lakini ndani ya siku hii sitasahau kabisa, ilikuwa ni siku ambayo nilikuwa nimemaliza kidato cha sita. Siku ambayo nilikuwa nimekaa nyumbani kwa muda wa majuma kadhaa, siku hiii ilikuwa ni siku chache tu tangu nifanye maandaalizi ya kujiangaa kujiunga na jeshi la kujenga Taifa. Siku hiyo nilitoka vizuri nyumbani hadi kituo cha mabasi Ubungo na kisha nilipanda basi la Tanga, kituo cha kushuka ilikuwa ni Kabuku wilayani Handeni. Niliposhuka hapo nilikutana na wanafunzi wengi waliohitimu kidato cha sita wakiwa wanasubiria wapate muongozo. Wote tulikuwa hatujui kambi tuliyokuwa tumepangiwa ilikuwa ipo wapi ndiyo maana tulikaa hapo kwani huko Kambini tayari walikuwa wamepata taarifa ya ujio wetu hivyo ilikuwa ni lazima wafike. Haikuchukua mida tuliona gari la rangi ya kijani kibichi likifika hapo, lilikuwa ni Gari kubwa sana na mara nyingi hutumiwa kubeba mizigo ndani ya kambi za jeshi. Gari hilo lilipofika tu hapo na kusimama mlango wa upande wa mbele ulifunguliwa, alishuka Mwanajeshi aliyekuwa amevaa fulana ya kijani maarufu kama ‘greenvest’ na kombati la kijeshi. Kichwani alikuwa ameva kofia nyekundu ambayo ilikuwa ikumuonesha kabisa alikuwa ni MP. Huyo alitupa ishara ya kupanda ndani ya gari hilo na wote tukafanya hivyo hatukutaka kabisa kusubiri kutokana na wingi wetu eneo hilo. Nilifanikiwa kupata nafasi ndani ya gari hilo ambapo tulikuwa tumebanana sana. Hapo safari ya kuondoka kwenye eneo hilo kuingia ndani ya kambi ndiyo ilianza, safari ilikuwa ni ndefu sana na njia ilikuwa ni isiyo na lami. Mashimo madogo pamoja na kukutana na miwaruzo mbalimbali kwenye barabara hiyo ya udongo mwekundu uliokauka ndiyo ilifuata. Ilituchukua mwendo wa takribani dakika kumi na tano kufika kwenye eneo la mwanzo la kambini kutokana na barabara hiyo ilivyo. Hapo tulishuka kila mmoja akiwa na mizigo yake aliyokuwa amekuja nayo, mwanzoni mwa eneo la kambi hiyo tulikutana na kibanda ambacho kilikuwa na foleni tofauti za wanafunzi waliokuwa wakiandikishwa kuingia ndani ya kambi hiyo, niliposhuka kwakweli nilichanganyikiwa kabisa na sikujua ni wapi nilipotakiwa kwenda. Ilinibidi nisogee jirani na wanafunzi wenzangu na kisha niulize utaratibu wa hapo, nilisogea hadi kwenye eneo ambalo kulikuwa na mstari mrefu sana na mtu wa mwisho alikuwa ni kijana aliyekuwa amepanda hewani akiwa mwili uliokuwa ukitangaza mazoezi aliyokuwa akiyfanya. “Oyaa niaje” Nilimsabahi “Safi tu kaka, ishu vipi?” Alinijibu “Safi aisee hivi hapa utaratibu vipi maana sielewi?” “Kaka unavyoona hapa ni foleni kulingana na mkoa ambao shule uliyotoka ipo, we wa mkoa gani?” “Dar kaka sijui foleni yke ni ipi?” “Yaani kaka kama uliotea vile foleni ndiyo hii ya watu wa Dar” “Doh! Bora maana mistari mingi nilikuwa nawaza kuzunguka” “Umefika kituo chako, naitwa James sijui mwenzangu nani?” Alijitambulisha huku akinipatia mkono “Wifred” Huo ndiyo ukawa mwanzo wa kujuana na James kijana ambaye alikuwa na historia nzito katika kipindi cha nyuma cha maisha yake aliyopitia. Tulifanikiwa kumaliza kujiandikisha na kisha tulizisalimisha simu zetu kama sheria ya jeshi linavyotaka. Baada ya hapo wote tuliyokuwa tumemaliza kujiandikisha tuliingia ndani tukiwa tumeongozana na Afande ambaye alikuwa yupo nje katika eneo tulilokuwa tukijiandikisha. Tulipelekwa hadi eneo ambalo lilikuwa na jengo moja kubwa sana. Jengo hilo lilipofunguliwa tulikutana magodoro mapya ambapo kila mmoja wetu alichngua alipendalo. Baada ya hapo kila mmoja alipewa shuka yake mpya kabisa yenye rangi ya bluu, muda huo wote nilikuwa pamoja na James na tulikuwa tukiongea mambo mbalimbali katika kila muda wote. Tulipomaliza hapo tulirudishwa juu tulipokuwa tumetoka na tulienda kuwekwa kwenye eneo ambalo lilikuwa na uwanja mkubwa sana. Hapo tuliitwa majina tena na kisha tuliingizwa ndani na kupelekwa kwenye eneo ambnalo lilikuwa na vyumba vya kulala ambavyo badaye tulikuja kuvitambua kwa jina la anga. Bado James nilikuwa nipo naye karibu katika kipindi chote cha muda tukiwa tumetokea kuwa marafiki wakubwa sana. Nilikuja kulitambua jina lake la ukoo ambalo ni jina la watu wa watu wa kaskazini magharibi, ni James Nkongo ambaye ndiye huyu Anfande Nkongo ambaye mnachukia nyinyi”. “Dah! Kumbe mmetoka naye mbali namna hiyo ila wewe uliingia jeshi la polisi na yeye kaja huku Magereza ilikuwa vipi?” Alulizwa “Kuweni na subira sasa huko kote nakuja kuwaleza” “Mzee tunasubiri kwa hamu sana si unaona muda mwenyewe wakunywa chai na kupumzika ni mdogo sana” Aliambiwa “Kipindi chote ambacho nilikuwa nikifahamiana naye nilikuwa nikimuona ni mtu mwenye furaha sana, mwenye kutabasamu kila muda hata sura yake yenye mvuto ilianza kuonekana kwa wasichana tuliokuwa tupo nao mafunzoni na hata maafande wa kike wale waliokuwa wakiishi kambini maarufu kama ‘service girls’. Pamoja na kunyolewa upara na kukaa kwenye eneo ambalo halikuwa na matunzi mazuri, bado alionekana ni mwenye mvuto sana kwa wasichana. Hili lilimfanya awe karibu sana na wasichna ndani ya kambi hiyo na hata hao maafande katika muda ambao tulikuwa tukikutana wote sehemu ya kula chakula, hili jambo pia lilinifanya na mimi niwe karibu na wasichna hao kwani alikuwa yupo nami katika kila kipindi cha muda. Alikuwa ni mcheshi sana katika kila muda ambao tulikuwa tukikaa naye, hili lilifanya hata kuruti wenzetu tuliokuwa tupo nao Kombania moja kuwa na maelewano nao mazuri sana. Hakuna ambaye alikuja kufikiria huyu pamoja na ucheshi wake mkubwa aliokuwa nao alikuwa na historia nzito ambayo ilikuwa imejificha kwenye maisha yake. Masihara mengi aliyokuwa nayo kumbe alikuwa ni mtu ambaye alikuwa jambo ambalo alikuwa ameliweka moyoni mwake, jambo ambalo lilikuwa ni lenye kusikitisha sana ingawa hakuna aliyekuwa akiwaza kama alikuwa hivyo. Muda wa awali wiki sita za mafunzo magumu ziliposiha kuanza kufanya kazi za kawaida, ndipo nilipokuja kujua kuwa huyu alikuwa na zaidi ya jambo katika maosha. Nakumbuka kabisa ndani ya siku ambayo nilikuja kujua kuhusu hili ilikuwa ni katika muda ambao tulikuwa tukienda shamba, muda huo tulikuwa tumeshamaliza mafunzo ya ulengaji shbaha na hata yale ya ushikaji silaha kwenye gwaride. ______________TIRIRIKA NAYO Jane ndiyo chanzo cha mimi kujua mengi kuhusu Nkongo nikiwa tupo ndani ya kambi hiyo, binti huyu alikuwa akitoka Kombania tofauti kabisa na sisi tuliyopo. Muda wa kula alikuwa haachi kuja kukaa na sisi kwenye kombania yetu ili apate kuongea na Nkongo, kiukweli alikuwa akimuhusudu sana lakini hakuweza kumwambia. Wala Mhusika hakuwa amewaza kabisa kumpenda huyo binti. Ucheshi mwingi aliokuwa nao ndiyo chanzo cha kumuweka kuwa karibu naye katika kipindi chote ambacho alikuwa akija hapo, hakika alitokea kupendezwa sana na rafiki yangu huyu ambaye alikuwa akificha kitu kigumu sana ambacho hata mimi hakuthubutu kuwahi kunieleza kuhusu hicho kitu hapo awali. Nakumbuka vizuri siku moja majira ya usiku muda ambao maafande walikuwa wameitwa kwenye kikao cha dharura na Kamanda kikosi wa Kambi hiyo, ilikuwa ni majira ya jioni ambapo tulichelewa sana kutoka ndani ya Bwalo la kulia chakula. Siku hiyo Jane aliongea sana na Nkongo tofauti na siku nyingine nyingi, kutokana na kumuhusudu sana aliamua kujisifia sana kuhusu mamlaka ya wazazi wao. Hapo ndipo binti huyu alipojichanganya na kutaja kuwa alikuwa ni mtoto wa Mrakibu mwandamizi wa magereza, jambo hilo lilifanya Nkongo amtazame kwa mshangao sana kama alikuwa amepokea taarifa ya kushtusha. Binti huyo kuendelea kumuonesha kuwa alikuwa akitoka familia inayojiweza ndipo alipotaja jina la Mzazi wake, liliposikiwa vyema kwenye masikio ya rafiki yangu kipenzi. Macho yake yalibadilika rangi na kuwa mekundu ghafla, mishipa ya damu midogo sana ikaonekana kwenye macho ikiwa imewekwa rangi nyekundu. Ilikuwa ni mara ya kwanza kumshuhudia akiwa kwenye hali hiyo mimi na hata waliokuwa wapo eneo hilo, wote tuliingiwa na mshangao. Yeye hakujali mshangao wetu zaidi ya kunyanyuka na kuondoka akiwa haongei neno lolote, hata maafande wa kike ambao hawakuwa wakihusika kwenye kikao waliokuwa wakiongea na sisi waliiingiwa na mshangao mkubwa sana. Alipoondoka wote waligeuza macho na kunitazama mimi, macho yalionesha ni jinsi gani walikuwa wakihitji kujua kile kilichomuondoa eneo hilo. Sikuwa na jibu la kuwapa kwakuwa sikuwa najua chochote kinachoendelea, nilishindwa hata niwaambie nini kuhusu huyo rafiki yangu kipenzi ambao wote walikuwa wakiamini kabisa kuwa mimi nilikuwa nikijua chanzo cha kilichomtoa eneo hilo. “Wil rafkki yako ana nini yule?” Afande mmoja wa kike aliniuliza “Mwenzangu leo James nimemuogopa kabisa sikuwahi kumuona akiwa vile” Ndawili mmoja aliongea, hili ni jina ambalo wasichana huitwa huko jeshini. “Jamani mshangao uliowakumba nyinyi ndiyo ninao mimi sijui chochote jamani kuhusu James” Niliwaambia “Si rafiki yako yule” Niliambiwa “Hata kama jamani kuwa rafiki haimaanishi unajua ya moyoni mwa mtu, ngoja nikamcheki huko” Niliwaeleza kisha nikanyanyuka na kutoka Bwaloni nikiwaacha wakiwa na mshangao kila mmoja. Nilienda kumtafuta Nkongo kwenye eneo ambalo tunakaa Kombania yetu, sikumuona na wala sikujua alikuwa yupo wapi. Nilihangaika sana katika kumtafuta na hatimaye nilimkuta akiwa yupo kwenye eneo lenye michungwa akiwa amekaa chini amejiinamia, niliposogea karibu na kukaa naye ndipo nilipobaini alikuwa akilia. Sikuwahi kumuona akiwa analia tangu nijuane naye. Hata huzuni pia sikuwahi kuiona kwenye uso wake, hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kumuona akiwa yupo kwenye huzuni kubwa. “Mzee vipi mbona unalia?” Nilimuuliza kwa upole. “Wil yule Jane sitaki hata kumuona kwenye maisha yangu, nilikuwa najiuliza nimemuona kila nikimuona kumbe kafanana na Ibilisi” Aliongea kwa hasira “Mbona sikuelewi mtu wangu kuna kitu gani kingine ulichonificha?” Nilimuuliza “Huwa sipendi kuelezea suala hili kabisa, we niache tu” “James inamaana tumeanza kufichana siyo poa mtu wangu” “Ok, ngoja nikueleze” Siku hiyo ndiyo nilijua sababu ya Nkongo kuondoka akiwa amebadalika ghafla na pia ndiyo siku ambayo nilijua alichokificha, jambo hilo nililolijua ndiyo chanzo cha yeye kuwa hivi alivyo hadi hii leo. Ooooh! Alarm imelia turudini kwenye kazi nitawaeleza baadaye muda umeisha” Kamishna Wilfred alikatisha kuelezea baada ya kusikika kengele maalum ya kuisha kwa muda wa kupata kifungua kinywa na hata kupumzika, alikuwa amebakisha kipande kidogo cha mkate ambacho alikimalizia kwa haraka. Aliongozana na wenzake kutoka mahala hapo kwenda kwenye eneo lao la kazi, nyuma yao walikuwa wakifuatwa na maafande kama ilivyo kawaida ambao walikuwa wakihakikisha wanafika eneo la kazi na kutimiza jukumu lao. **** Kipindi ambacho muda wa kupumzika ulikuwa ukikaribia kuisha ndiyo muda ambao Teddy aliingia kwenye bwalo la chakula la maofisa wakubwa ndani ya gereza hilo, aliangaza macho ndani ya bwalo hilo na kisha akayatuliza macho kwa Afande Nkongo ambaye alikuwa akimalizia kifungua kinywa chake akiwa amekaa peke yake kwenye meza. Alijipa ujasiri na kujongea hadi kwenye meza hiyo ambapo alisimama mbele yake, alitoa heshima kwa mkubwa wake huyo na kisha alivuta kiti akaketi. Ndani ya siku hii aliamua kabisa kujitoa mhanga kuliko kukaa na jambo ndani ya moyo wake, ndiyo maana alifika hapo pasipo kuhofia jambo olote. “Samahani Afande” Aliomba radhi na kupelekea Afande Nkongo anyanyue uso na kumtazama, Teddy alikutana na jicho kali kabisa ambalo lilitazama sare yake na kisha likatua usoni. “Ndiyo” Hatimaye sauti ya mkubwa wake huyo ilitoka. “Afande nilikuwa na mazungumzo muhimu sana wewe kama hutojali” “Ya kikazi au nje ya kazi?” “Nje ya kazi” “Sasa hivi ni muda wa nini?” “Wa kazi” “Sasa maongezi ya nje ya kazi yatahusika vipi muda huu wa kazi, ndani ya wakati ambao muda huu wa kupumzika unaisha” “Najua Mkuu ila..” “Hakuna cha ila rudi Bwalo lenu si muda wake hayo maongezi yako unayoyahitaji” Ilipotoka kauli hiyo Teddy alibaki akiwa ameumia sana, alishindwa kunyanyuka hata kwenye kiti ingawa alikuwa amepewa amri ya kuinuka hapo kwenye kiti. “Unapinga amri ya mkuu wako siyo, nimesema rudi Bwaloni kwenu kabla sijakugeuzia kibao” Ilipotoka kauli nyingine kwa mara ya pili, mwenyewe alisimama akaondoka humo ndani akiwa ameumia sana kwa maneno aliyokuwa ameambiwa. Afande Nkongo hakuonesha kabisa ni mwenye kujali hilo yeye aliiona ni sawasawa kutokana na binti huyo kuwa na kitu ambacho alikuwa akikichukia sana, kitu hicho ndiyo alikuwa amekuja nacho huyo binti bila ya kujijua yeye mwenyewe. Gwanda ndiyo kitu ambacho kilifanya akose kabisa hata dakika ya kuongea na mkuu wake huyo, aliondoka akiwana maumivu akiona ameonewa pasipo kujua kilichokuwa kimefanya hayo. **** Teddy alirudi hadi ndani ya ofisi ambapo walikuwa wapo wenzake waliokuwa ametoka Bwaloni mapema, alikuwa akitokwa na machozi na alipoingia na kukaa kwenye kiti. Alikumbuka kuchukua kitambaa chake na kufuta machozi hayo kisha akaegemea mgongo wa kiti na kutazama juu, alibaki akiwa ameelekeza macho yake juu kuitazama taa yenye mwanga mkali iliyopo ofisni humo. Alikuja kuacha kuitupia macho taa hiyo baada ya kusikia sauti ya mwenzake ikimuita. “Teddy” Jamila alimuita na kupelekea ageuza macho na kumtazama. “Una nini shosti?” Aliulizwa “Yaani hata sijui kwanini Afande James ananitesa namna hii” Alipotoa kauli hiyo chozi lilianza kumtoka tena tena, ule ukatili pamoja na jeuri aliyokuwa nayo kwa wafungwa hapo haukionekana kabisa. “Imekuwaje kwani?” Alitupiwa swali kwa mara nyingine, aliamua kuwaleza juu ya kilichotokea. “Shosti sasa usilie jamani tulia utamfuata baada ya kutoka ofisini” Alishariwa na rafiki mwingine, muda huo huo kengele ya kuisha muda wa mapumzika ndiyo ililia. Ulikuwa ni muda ule ambao Kamishna Wilfred alikuwa amekatisha kuwasimulia wenzake juu ya kilichotokea katika mingi iliyopita. ****
Upande wa wafungwa wanawake wao walikuwa wakivunja mawe katika upande mwingine ambao haukuwa na mawe magumu sana, gereza hili lilikuwa halina jinsia kabisa katika suala la kzi ndiyo maana hata wanawake walikuwa wakifanya kazi ngumu pia. Ni ndani ya eneo la chini ya gereza hilo ambako ilikuwa ikihitajika kupanuliwe zaidi gereza hilo, walikuwa wakichakarika huku waikisimamiwa na maafande wa kike. Getu, Frida na Stella wale wasichna waliokamatwa kwenye kisa cha Shujaa kilichoandikwa na mtunzi Mahiri Hassan O Mambosasa. Walikuwa wapo eneo moja wakiwa wamekaa na rafiki yao Josephine mwanamke tishio aliyekamatwa ndani ya kisa cha Wito wa kuzimu baada ya kuua maelfu ya watu jijini Dar es salaam. Wote walikuwa wakivunja mawe huku wakiongea mambo mbalimbali ambayo yaliwafanya wasione kazi ngumu, wakati wakiendelea kuchakarika na kazi ilifika muda Josephine alisimama kwa muda wa dakika kadhaa akiwa ameshika kiuno huku wenzake wakiendelea kufanya kazi. Kitendo hicho kilisababisha apigwe na kirungu cha bega na mmoja wa Maafande ambao walikuwa wakisimamia eneo hilo, ilikuwa ni tendo ambalo lilimuudhi na alijikuta akifytua teke la shukrani ya punda ambalo lilimpata Afande huyo kifuani akaanguka chini. Aligeuka nyuma akaona kundi maafande watatu wakiwa wanamjia kwa kasi, hakutaka kabisa kuwahofia yeye alitupa nyundo chini na kisha akasimama akiwa hana hofu. Afande wa kwanza kumfikia alikutana na pigo la karate akaenda chini, mwingine alileta rungu ambalo lilimkosa baada ya kuyumba na kisha akamuachia ngumi nzito ya kidevu. Shangwe za wafungwa ziliamka muda huo kutokana na maafande hao kupewa kipigo,waliendelea kushuhudia wale maaskari ambao walikuwa wakiwanyanyasa wakipewa kipigo na mwenzao. Fujo za kelel zao ilikuwa ni jambo ambalo lilisababisha waje wale wasichana ambao walikuwa wamempokea na kumleta gerezani, wasichana hao hawakuwa wengine ila ni kina Teddy. Hakuna ambaye alikuwa hawajui walivyo wajeuri na makatili hao maafande, Josephine alijipanga kupigana nao lakini alipopangua pigo la mmoja basi alionja kirungu cha mwingine. Alipigwa sana virungu ambavyo vilimkumbusha siku ya kwanza kuingia ndani ya gereza hili alipoleta ubishi. Aliongezwa na mabuti baada ya kuanguka akiwa haonewi huruma, hakika aliingia ukanda wa wajeuri wenzake. Alipokuja kuachiwa baada ya kupewa kipigo alikuwa na manundu mengi sana, alikuwa hana tofauti na mcheza masumbwi akitoka kwenye pambano. Baada ya hapo aliburuza mithili ya gunia na kupelekwa eneo jingine kabisa, aliburuza hadi kuingia kwenye eneo hilo ambalo lilikuwa na kila uchafu ndani yake ambao ulimfanya yule mwenye kinyaa kutapika. Alikuja kuhisi kutoburuza baada ya kufika eneo lenye unyevu ambalo lilikuwa na harufu kali sana. Alipoangza vizuri alikuja kubaini kuwa alikuwa yupo jirani na mtaro unaopitisha kinyesi ambao ulikuwa umefunguliwa, unyevu huo ulimbainishia kabisa kuwa mtaro huo ulikuwa umeziba na muda huo ulikuwa ukitoa uchafu nje. Hapo aliinuliwa kwa nguvu sana na kisha kichwa chake kikatazamisha kwenye mtaro huo uliokuwa ukichukua uchafu vyooni, aliona takamwili za ndani miili ya mwenzake zikiwa zimejazana na kuweka taswira isiyo ya kawaida. Takawmili hizo zilikuwa zimeganda sehemu moja ambapo ziliweka taswira isiyopendeza, chepe ambalo lilikuwa kuukuu liliangushwa mbele yako hapo. “We si kiburi humu ndani tupo viburi zaidi yako, sasa utachota mavi na chepe hili kuahimishia upande wa pili wa mtaro huu ambako hakujaziba. Uzibuke na huo uchafu wenu ulioganda hapo nisiuone” Teddy alimuambia kwa jeuri kisha akamsukuma kungia ndani ya mtaro huo. Josephine na jinsi ilimbidi yeye mwenye aingie kwenye mtaro huo na kuanza kuyachota hayo yasiyopendezeka kuyatazama, alikuwa akisimamiwa hapo hadi kazi hiyo ambayo haikuwa ngumu lakini ilihitaji moyo iweze kuisha. Harufu kali ilitoka alichota koleo la kwanza tu lakini hakuwa hata na uwezo wa kuziba pua zake, alivumilia harufu hiyo akiendela kuyachota. Koleo la mwisho kulichota ndiyo alijuta kabisa kuleta jeuri yake, yale maji yaliyokuwa yamezibwa yalizibuka kwa kasi sana na kumvamia hata yeye kwenye mwili wake. Alitoka juu kwa haraka akiwa amelishiia chepe hilo, kazi aliyopewa alikuwa tayari ameshaimaliza ila alikuwa hatamaniki kwa kutoa harufu mwilini mwake. Aliondolewa eneo hilo baada ya adhabu hiyo kuisha akiwa ananuka na alienda kujiafisha moja kwa moja, alirudishwa eneo lile ambalo wenzake walikuwa wakifanya kazi baada ya kubadili nguo na aliongezewa kazi mara mbili ya wenzake. **** Usiku kama kawaida maofisa wote walikuwa wapo ndani ya Bwalo la chakula wakingalia vipindi mbalimbali vya luninga, wote wenye vyeo ngazi ya juu walikuwwepo kasoro Afande Nkongo ambaye alikuwa yuo ndani ya nyumba yake iliyomo humo gerezani. Ukimya ndiyo ulikuwa umetawala katika muda ambao walikuwa wakiangalia Luninga, ukimya huo ulikuja kuondoka baada ya mitambo kukata ghfla baada ya kuvurugika kwa hali ya hewa. Ukimya huo ulizusha maongezi mengine kabisa, ndani ya maongezi hayo ndipo walipokuja kubaini kuwa mmoja wao hakuwepo. Walipoangalia meza aliyokaa Mkuu wao hawakumuona Afande Nkongo, hapo walibaini ni yeye tu ndiye alikuwa amekosekana humo ndani. “Mkuu mwano yupo wapi?” Afande mmoja wa kike aliuliza “Mbona unamuulizia sana Hollo au ndiyo mkwe?” Mkuu huyo aliuliza kimasihara na wote wakaanza kucheka humo ndani. “Lakini mkuu hujawahikutumbia kabisa sababu ya Nkongo kuwa vile zaidi ya kutuambia kila kila siku kila mtu ana historia yake katika maisha” Mwingine aliongea “Ni jambo ambalo ni zito sana vijana wangu msilione rahisi sana kuliongea, kwanza mna vifua?” “Mkuu tupo tayari kulitunza ila tujue tu kipi kinamsibu mwenzetu” Aliambiwa “Ok naomba hata yeye mwenyewe asijue kuhusu hili, hapendi kabisa mwingine ajue” “Ondoa shaka kuhusu hilo” Alitolewa hofu kuhusu hilojambo. “Ok sasa ngojeni niwaelezeni” Alipoongea hivyo wale ambao walikuwa wapo mbali naye walisogea karibu zaidi waweze kusikia, ukimya ulitawala wakiwa wanajiandaa kusikiliza kuhusu hilo jambo ambalo walikuwa wakitaka kulifahamu zaidi. Kila mmoja alikuwa amekaa mkao mzuri kuweza kulisubiria jambo hilo kwa hamu sana aweze kulisikia, habari za kukatika mitambo ya televisheni walikuwa wameshazitoa ndani ya vichwa vyao na kusikiliza historia muhimu ndiyo walilipa kipaumbele
MIAKA KADHAA ILIYOPITA Kundi kubwa la watoto wa shule walikuwa wakitoka darasani majira ya saa nane, walikuwa ni watoto wa darasa la saba ambao walikuwa wakitoka m ndani ya msingi inayotumia Kingereza katika kufundisha. Miongoni mwa watoto waliyokuwa wakitoka darasani, James alikuwa yupo akiwa amebeba begi lake nadhifu kabisa. Makelele ya watoto hao ya hapa na pale ndiyo yalisikika katika muda huo waliokuwa wakitamani kwenda nyumba kuliko kitu chochote, wengi walikuwa wakiongea kwa sauti katika muda huo huku wengine wakicheza na kufukuzana kama ilivyo kawaida yao. James alikuwa yupo katika kundi la marafiki zake wakubwa wawili ambao alikuwa wakiwapenda sana, wote kwa pamoja walikimbilia kupanda kwenye gari la shule ambalo huwa linawarudisha majumbani mwao. Baada ya muda mfupi safari ya kuondoka kurudi nyumbni ndiyo ilianza, wanfunzi wote walikuwa wametulia ndani ya gari hilo kutokana na uwepo wa mwalimu mkali ambaye hakuwa akitaka kabisa makelele. Gari hilo lilizunguka mitaa mingi sana na kuwashusha wanafunzi tofauti na hatimaye likafika maeneo ya Tameko ambalo ndiyo kituo cha kushuka James. Hapo aliagana na marafiki zake halafu akashuka jirani kabisa na lango la nyumbani kwao. Alibonyeza kengele langoni hapo kisha akasubiri kwa muda hadi pale mlango ulipofunguliwa, alitokea Mwanamke ambaye alimfanya James amkimbilie na kumkumbatia kwa furaha. Alikuwa ni mama yake mzazi ambaye alikuwa akimpenda sana, alibebwa ingawa alikuwa amefikia umri wa kutobebwa na kisha aliingia naye hadi sebuleni. “Mama huyo mwanao unamdekeza” Mvulana mabye alikuwa ni mkubwa kiumri alimuambia mama yake baada ya kuona mdogo wake anabebwa. “Niachie mziwanda wangu huyu wacha nimdekeze” Alongea huku akimshusha chini na kuanza kumfungua kamba za viatu, alimvua na begi lake la shule na kisha alimpeleka kwenye meza ya chakula na akaanza kumlisha kama vile alikuwa hawezi kula **** “Hivi hizi habari ni za ukweli Philipo mbona sielewi?” Mwanaume mmoja aliyekuwa na nyota moja pamoja na ngao begani mwake aliongea “Hapana siyo za ukweli mkuu nafikiri wewe unatambua kazi yangu” Philipo ambaye alikuwa na nyota tatu mabegani mwake akiwa na nguo za maaskari magereza kama mwenzke alijitetea. “Ujue hii ni skendo kubwa sana” “Elius nafikiri unanijua tangu tukiwa shule hebu fikiri nitaweza vipi kufanya haya, mimi ni Philipo yuleyule sijabadilika kitu” “Hata fikiria jinsi Kamishna General huko alivyo mkali akisikia habari hii unafikiri itakuwaje” “Sasa sina hatia Elius, wewe ni mkuu wangu na pia rafiki yangu wa siku nyingi nisaidie ndugu” “Ngoja nikamsikilize huyo Mwandishi ambaye alikuwa ameandika kuhusu habari hii vizuri ndiyo nijue nitakusaidia vipi” “Sawa ndugu ila usiwaamini sana hao waandishi si unajua ni hatari kiasi gani kuzusha mambo” “Ngoja kwanza nikaone ana ushahidi gani huyo na tuhuma hiyo anayokutuhumu kabla hayajafika huko” Yalikuwa ni maongezi kati ya Mrakibu Mwadamizi wa jeshi la magereza SSP Elius Nkongo na rafiki yake kipenzi pia askari wa chini yake Mrakibu msaidizi ASP Philipo Lutonja. Tuhuma ambayo ilikuwa imemkumba ASP Lutonja kupitia gazeti pendwa maarufu nchini ndiyo lilifanya aitwe kwenye ofisi hiyo na Mkuu wake huyo. Ilikuwa imekaa kama habari ya kidaku kwa jinsi ilivyokuwa imeandikwa kwenye gazeti, habari hyo haikudharauliwa mara moja kwani ingeweza kabisa kulipa sifa mbaya jeshi la Magereza. Ilipofika ofisi kwa SSP Nkongo aliamua kuivalia njuga kwani lilikuwa likimuhusu rafiki yake, hakutaka kabisa kuona habari hiyo ikimuacha na sifa mbaya rafiki yake. Pia hakumuamini asilimia mia moja na ndiyo maana alimuita hapo na kuanza kumuuliza juu ya suala hilo, tayari alikuwa na miadi na Mwandishi aliyeandika habari ile ambaye alikuwa amethibitisha kabisa kuwa alikuwa na ushahidi wote kuhusu habari aliyoandika. Kabla hajaenda kwa mwandishi huyo ilimbidia fanye mahojiano kabisa na ASP Lutonja. Majira ya alasiri yalimkuta akiwa yupo ndani ya mgahawa katikati ya jiji la Dar es salaam akiwa yupo uso kwa uso na mwandishi huyo. Alikuwa ni mwandishi mkongwe ambaye alikuwa na jina kubwa ndan ya nchi hii, ndiyo huyo aliyekuwa akidai ana na ushahidi wa kila kitu juu ya jambo ambalo aliliandika kwenye gazeti alilokuwa akilimiliki. Gazeti ambalo lilikuwa limebatizwa jina na kuitwa gzeti la kidaku kutokana na habari zao walizokuwa wakiziandika, hakuna mwananchi ndani ya Tanzania ambaye alikuwa hamtambui kabisa mwandishi huyu ambaye alikuwa akisifika kwa umahiri wake katika uandikaji habari kwenye magazeti mbalimbali makubwa mbali na gazeti lake. Akiwa yupo hapo mbele alikuwa amekuja na mkoba wa kubeba mgongoni ambao muda huo alikuwa ameupakata, alikuwa akitazamana ana kwa ana na SSP Nkongo ambaye alikuwa amefuata huo aliokuwa akiuita ushidi wake. “Ndiyo Bwana Kizigo nimekuja nilikuwa nahitaji kujua kila kitu kuhusu ilichokiandika kwenye gazeti lako” SSP Nkongo alifungua mjadala “Ndiyo SSP kama nilivyokuambia ushahidi upo na niliutafiti mwenyewe, huwa siandiki habari bila ushahidi” Kizigo aliongea “Unao hapo hapo tuuone?” Kizigo alipoulizwa swali hilo hakujibu na badala yake alifungua mkoba wake akatoa picha ambazo alizimwaga kwenye meza. “Kwa muda mrefu ndani ya nchi kulikuwa na wimbi la uuzaji wa silaha kinyume cha sheria. Kipindi hicho chote kumekuwa kukitokea matukio kupungukiwa kwa silaha katika ghala zenu tofauti na hata za majeshi meingine, wasamaria wema wa kwanza kulijua hili suala walitoa taarifa kwa mwandishi mwenzangu Marehemu Kibiti ambaye alifariki siku cchache tu alipotangaza kuwa alikuwa akilifuatilia hilo swala, alikutwa amefariki kwenye kiti chake cha ofisini na haikueleweka kifo chake kilitokana na nini zaidi ya kumsikiliza Dokta Nasibu ambaye alidai alikufa kwa shinikizo la damu.. Ndugu SSP napenda utambue kuwa kabla ya kifo chake Kibiti aliwahi kuniambia kuwa maisha yapo hatarini kupita simu ya mkononi na maongezi yake niliyarekodi ni haya hapa” Kizigo aliongea na alipomaliza alitoa simu yake na kisha akafungua kwenye faili la maongezi hayo. Alibonyeza kitufe kuyacheza maongezi hayo mbele ya SSP Nkongo, yalisikika vizuri maongezi hayo ambapo walikaa kimya wote. Baada ya kuyasikiliza kwa umakini sana hadi yakaisha, Kizigo aliendelea na maelezo. Jambo ambalo halikufahamika ni kwamba picha hizo zilikuwa tayari zimeshapigwa na Kibiti mwenyewe, alizihifadhi hizo picha nyumbani kwa mdogo wake na kumpa maelekezo yote ikiwa atauawa. Alipouawa ndiyo picha hizo zikafika kwenye mikono yangu kama maelekezo yalivyomtaka. Ndugu SSP nafikiri unaona kabisa hapo ni jinsi gani hao maaskari waaminifu ndani ya jeshi la magereza wakiondoka na wafungwa majira ya usiku kwenda kuwapelekea huko kwenye biashara zao. Wengi wao wanaopelekwa huko waliingizwa gerezani hapo kwa sababu hiyo tu kuweza kufanya zao, nilipopata ushahidi huo wa awali niliamua kuingia kazini mwenyewe nikiwa sijulikani kabisa kama ninafuatilia suala hili. Wahusika waliona hili suala lilikuwa limeisha kabisa, kupunguza umakini kwenye suala hili ndiyo kulinifanya mimi niweze kufika mbali kabisa kiasi cha kujua mengi zaidi” Kizigo alieleza. “Sawa nimeyasikia maelezo yako na pia ushahidi wa picha nimeuona, je Lutonja anahusika vipi hapa maana sijaona ushahidi wa kumtia hatiani” Aliuliza “Ndugu SSP tunaenda hatua kwa hatua hadi huko utapajua kote we kuwa na subira” “Enhee! Ndiyo” “Jirani yangu ni mmoja wa maaskari wa gereza ambalo ofisi zako zipo, ndiyo aliweza kutoa siri hii. Aliniambia jinsi ambavo wafungwa huwa wanatolewa usiku na magari tofauti ya magereza ambayo huja hapo gerezani. Alieleza kuwa huwa wanaambiwa warudi nyumbani katika muda ambao wa kazi pindi yanapoingia magari hayo, yeye aliamua kunieleza hayo kutokana na kuhisi ni kinyume cha utaratibu na pia alikuwa ni mdogo kicheo alikuwa akihofia maisha yake. Hapo ndipo mimi nilipofunga safari hadi hapo gerezani muda huo wa usiku nikiwa nimevaa nguo zake za kazi, kama kawaida nilishuhudia yakija magari ya mizigo makubwa na yaliingia hadi ndani. Nikiwa nimebandika kamera yangu kwenye kifungo cha shati, tuliamriwa wote kwa pamoja tuondoke hapo gerezani kurudi nyumbani eti tulitakiwa kuwa off. Ndugu SSP napenda utambue kuwa sikutaka kuondoka hapo gerezani bali nilijibana mahali nikiwa nashuhudia jinsi ambavyo wafungwa walivyokuwa wakitolewa na kisha hupewa nguo nyingine na kupanda hayo magari na kisha kuondoka. Kwenye siku hiyo ndipo nilipoweza kumshuhudia ASP Lutonja akiwa yupo katika nguo za kiraia akiwaongoza wafungwa hao kuingia kwenye magari. Siku hiyo niliwafiatilia hadi walipifika kwenye gereza la Ukonga ambapo walichukua wafungwa wengine, safari yao hiyo iliendelea hadi Kisarawe porini. Huko nilishuhudia kukiwa na magari makubwa ya mizigo mawili, moja la jeshi la polisi na jingine la JWTZ. Yote mawali yalikuwa yana mizigo ndani yake ambayo sikuweza kuitambua hadi pale waliapoanza kuishusha. Niliweza kushuhudia kwa macho yangu silaha mbalimbali zikishushwa na kisha kuingizwa ndani ya magari hayo yalikuwa yamewachukua wafungwa hao hadi zikaisha, kazi hiyo yote walifanya wafungwa waliochukuliwa ambao walionekana kuwa na maelewano mazuri na maasakari hao kwani walikuwa wakiongea nao kama marafiki. Picha zote za ushahidi ni hizi hapa jionee mwenyewe” Alipomaliza kuongea maneno hayo alitoa picha zingine akampatia SSP Nkongo. Alibaki kutoamini kwa picha hizo ambazo zilimuonesha rafiki yake kipenzi ambaye alikana kabisa kujihusisha na tuhuma hizo, msaliti alikuwa ni rafiki tena zaidi ya ndugu ambaye walishibana kwa kipindi kirefu cha muda tangu wakiwa hawajijenga kimaisha. Ilikuwa ni aibu sana kuwa rafiki ambaye alikuwa akiliasi taifa pasipo kujali kiapo ambacho alikiweka. SSP Nkongo alikuwa akimpenda sana rafiki yake lakini kwa hilo jambo ni heri hata urafiki ufe kuliko kuwa na msaliti. “Sawa Bwana Kizigo nimekuelwa naomba uniachie hili suala nilifanyie uchunguzi, pia huo ushahidi naomba usitoke kwenye gazeti kabla sijamaliza upelelezi wangu nitakaouanza mwenyewe” Alimuambia “Sawa SSP hilo halina shida ushahidi mwingine video hizi hapa nafikiri ni muhimu kwako” Kizigo alimpatia na mikanda ya video ambayo alikuwa ameirekodi kuhusu tukio hilo la usaliti wa afisa wa ngazi ya juu kabisa wa magereza. Waliagana hapo na kisha kila mmmoja akaondoka kuelekea alipokuwa amepanga kwenda katika majira hayo, hawakujua kabisa ushahidi huo ungekuwa ni chanzo mengine ndani ya maisha yao. Pia hawakutambua kuwa walikuwa wakipambana na mtandao mkubwa kiasi gani ambao ulikuwa nyuma ya kila kitu walichokuwa wakikichunguza. Utayari wa kufanya jambo lolote katika uchunguzi huo ndiyo uliwafanya hata wasijali kuhusu uhatari wa kazi waliyokuwa wakiifanya, Askari aliyekuwa yupo tayari kufa kwa ajili ya nchi yake. Alikuwa amekutana na mwandishi ambaye yupo tayari kufa kwa ajili ya kutetea jamii yake, hakika walishabihiana kwa kila kitu. **** Jioni yake ilikuwa ni ambapo giza lilianza kuzidi kwa wafuatiliaji wa sakata hili kabla majira ya usiku wa manane hayajafika, kubisha hodi kwa giza kwa wafuatailiaji hawa. Kulianza nyumbani kwa Bwana Kizigo ambaye alikuwa hana hili wala lile na wala hakutarajia kama yangekuja kuwa hayo. Majira ya saa moja jioni akiwa anaangalia luninga nyumbani kwake, mlango mkuu wa mbele katika nyumba hiyo ambayo alikuwa anaishi uligongwa kwa taratibu sana. Ugongwaji wa mlango huo ulisababisha mke wake ambaye alikuwa yupo jikoni akiendelea na shughuli zake za upishi atoke mbio hadi mlangoni kwenda kumsikiliza huyo mgeni. Alipoukaribia mlangoni alifungua kiuwazi kidogo na kisha akaangalia nje, alipomuona mgongaji wa mlango huo aliamua kufungua kwani hakuwa na hofu yeyote kwake. Aliingia ASP Lutonja akiwa ameongozana na watu wawili ambao walikuwa waemvaa suti nyeusi, Mke wa Kizigo aliwatolea tabsamu akiona walikuwa ni wageni wa kawaida. “Karibuni” Aliwakaribisha zaidi lakini karibu yake ilijibiwa na mmoja wa wale watu waliokuwa wamevaa suti kuchomoa bastola ndani ya koti lake la suti. Kzigo alishuhudia kwa macho yake mawili bastola hiyo ikikohoa na kupasua kichwa cha mke wake kipenzi, aliuona mdomo huo wa bastola ukimuangalia yeye baada ya kuachia kikohozi chenye maafa. “Kizigo napenda nikuambie kuwa uropokaji una ubaya wake, tulianza na Kibiti kwakuwa alikuwa ni mbishi kama wewe. Sasa ni zamu yako” ASP Lutonja aliongea kifedhuli “Lutonja ndiyo unaniua nipo radhi uniue lakini jua hamna siku nyingi nyinyi mtaozea jela” Pamoja na kuwekewa silaha aliwajibu kijeuri “Tunayo miaka mingia ya kuishi vyombo vyote vya dola vipo chini yetu siku nyingi. Jiulize huo ushahidi wako utaenda wapi wewe” “Ndiyo mnavyojidanganya siyo tayari haupo mikononi mwangu na upo kwenye mikono ya mtu ya mwaminifu sana katika vyombo hivyo vya dola. Mkuu wako hakuniamini nimeupeleka kwingine kabisa” “Unachekesha wewe rafiki yangu kipenzi anayeniamini SSP Nkongo akuamini wewe na gazeti lako linaloropoka hadi tumelipakazia sifa na kuonekana la udaku linalodandia siasa” “Sasa tuone mtapata faida gani na kuniua mimi, nipo tayri niueni kama mke wangu ila mjue kiama chenu chaja” “Hebu dawa yake naona anachonga sana na huyo mwenye ushahidi tutampata” ASP Lutonja aliongea na hapohapo ile risasi ilikohoa tena, paji la uso la Kizigo lilitobolewa na na ukawa ndiyo mwisho wake. “Kiama ni chako kimefika sisi chetu bado hata ungekuwa na mtoto angeota mvi sisi bado hakitafika, boys chomeni nyumba yake ionekane ni tukio la ajali ya moto. Mimi nitahakikisha ripoti itayofanywa ya kifo hiko inapindishwa” Alipoongea maneno hayo alitoka hadi nje ya nyumba hiyo akiwaacha wale vijana ndani. Muda mfupi baadaye wale vijana walitoka nje kujongea hadi mahali walipokuwa wameegesha gari, walipolifikia tu gari lao nyumba ile ililipuka kwa moto mkubwa sana. Wao waliachia matabasamu kisha wakaingia ndani ya gari na kuondoka. **** Majira hayo SSP Nkongo alikuwa amekaa sebuleni akiwa yupo na mtoto wake wa miaka kumi na mbili ambaye ni James, kaka yake mkubwa alikuwa yupo kwenye meza akijisomea kutokana na kuwa yupo kwenye masomo ya sekondari. Muda huo alikuwa akiangalia Luninga lakini tafakari zote zilikuwa zipo kwenye ushahidi aliokuwa amepewa na Kizigo, alikuwa akitafakari jinsi mbavyo mtu mzima yule mwenye taaluma ya habari alivyojitoa mhanga ili kuweza kupata ushahidi muhimu kama huo. Macho yote yakiwa yameelekea kioo cha luninga, moyo wake ulikuwa ukimpongeza kabisa kwa kazi nzuri aliyokuwa ameifanya yeye na Marehemu Kibiti.
Hakuwa hata na taarifa ya mwenzake ambaye alikuwa amempa ushahidi muda mfupi uliopita, hakujua alikuwa amebaki peke yake tu ambaye alikuwa akiujua ushahidi ule ambao ungewaweka wote wale matatani. Alitafakari kuhusu suala hilo ambalo lilikuwa limemfanya aanze kumchukia rafiki yake kipenzi, tafakuri hizo za ndani ya kichwa chake ziliambatana na upangaji wa jambo jingine. Hakika alidhamiria kwa nguvu zake kuhakikisha ASP Lutonja anaishia nyuma ya nondo kwa usaliti aliokuwa ameufanya hakuona umuhimu wa mtu huyo kuendelea kuwa uraiani ikiwa alikuwa amefanya usaliti mkubwa. Akiwa kwenye tafakari hizo kwa mara nyingine aliweza kulikumbuka jina ambalo lilikuwa limeanza kumtoka ndani ya kichwa chake, usaliti wa mwenzake ndiyo chanzo kikubwa cha yeye kulikumbuka jina ambalo lilikuwa limesahaulika tayari kwenye kichwa chake. Bond ndiyo jina pekee ambalo alikuwa ameanza kulisahau ndani ya kichwa chake, hatimaye lilikuwa limerudi kichwani mwake kwa mara nyingine. Asili ya neno Bond ilikuwa ni miaka thelathini iliyopita ndani ya Shule ya sekondari ya Usagara Tanga, jina hli lilikuja baada ya wanafunzi wa shule hiyo kusoma kitabu cha kipelelezi maarufu kilichoandika na mwandishi Ian Fleming. Urefu wa jina hili ulikuwa ni James Bond lakini lilikuja kufupishwa ndani ya shule hiyo. Jina hili lilikuja kubandikwa na kuficha jina la mwanafunzi mwingine kabisa ndani ya shule hiyo. Sifa za huyu mwanafunzi ambaye alikuwa ni kibaraka wa walimu, mwanafunzi huyu hakuweza kufahamika ukibaraka wake kwa walimu hapo shuleni. Haikuweza kufahamika jina halisi la mwanafunzi huyo ambaye alikuwa akifanya upekuzi wa siri zao na hatimaye kuzianika kwa walimu na kuwapa wakati mgumu wa kukabiliana na adhabu ngumu, waliishia kumbandika jina mtu huyo kama Bond kutokana na kumtomjua na pia jinsi alivyokuwa akiwapeleleza. Ilifika kipindi wanafunzi wenyewe kwa wenyewe wakawa hawaaminiani kutokana na mtu huyo ambaye alikuwa akiuza siri zao kwa walimua kila kukicha. Kila mmoja alikuwa akimuhisi mwanafunzi mwenzake kuwa alikuwa akihusika na jambo hilo ikiwa siri zao walizokuwa pamoja zikagundulika. Hakika walikuwa wakimuogopa Bond huyo waliyembatiza jina kila siku, hawakuwahi kumjua kwa sura lakini sifa zake ilitosha kuwatia hofu kabisa. Hawakujua kabisa huyo alikuwa akifanana namna gani, zaidi ya kuishia kujenga picha vichwani mwao kuhusu muonekano wake. Kila mwanafunzi ambaye alikuwa yupo makini sana katika mambo yake walikuwa wakikaa kimya kila mtu apitapo mbele yao, walihisi huenda huyo ndiyo alikuwa Bond huyo aliyekuwa akiwaharibia mambo yao yaliyokuwa yapo kinyume na miiko ya shule. Walipoweka jicho la umakini kila waongeapo kwa kuwa wamemuhisi fulani bado mipango yao ilikuwa ikiharibika kila kukicha, hakika walibaki wakichnganyikiwa wakijiuliza huyo Bond alikuwa na uwezo gani. Wengi wa wanafunzi wa mkoa wa Tanga kwa kipindi hicho walikuwa wakimuhusisha sana na ushirikina huyo mwanafunzi, hata viranja wasio waaminifu ambao walikuwa wanawaibia siri ya wanafunzi mbalimbali walikuwa hawajui alikuwa akifanana vipi. Imani za kishirikina zilizokuwa zimetawala ndani ya mkoa hu zilitosha kabisa kwa wao kumuhusisha na ulozi. Bond mwenyewe aliyekuwa akiwanyima raha wale wavunjifu wa sheria za shule, alikuwa ni mwanfunzi wa kawaida sana hapo shuleni. Asiye na cheo cha uongozi wa serikali ya wanafunzi wala uongozi wa darasa, hakuna ambaye angedhania kwamba huyo mwanafunzi ndiye alikuwa akiwaharibia kila siku mipango yao. Wengi walizoea kumtania kutokana na urefu aliokuwa nao, alikuwa ni mu ambaye alikuwa hakasiriki kila anaapotaniwa. Kipenzi cha watu ndani ya shule hiyo, aliyependwa na wanafunzi karibu vidato vyote kutokana na kupenda kuwajali watu pamoja na ucheshi aliona nao. Ndiye huyu aliyekuwa akiitwa Bond kutokana na kupeleleza maisha ya wanafunzi hao shuleni, hakuna ambaye alikuwa hamfahamu huyu mwanafunzi kutokana na ucheshi aliyo nao. Aliitwa Elius Nkongo kwa jina lake halisi, ndiye huyu ambaye alikuwa akiwanyima usingizi wavunjifu wa sheria za shule. Kijana ambaye alizaliwa na uwezo wa juu katika kufuatilia mambo ambao ulikuja kubainika kwa wazazi wake wenye asili ya Kagera waliokuwa wakifanya kazi mkoani Tanga, kabla walimu wa shule hiyo hawajaufahamu kuufahamu. Hadi anaondoka ndani ya shule hiyo hakuna ambaye alikuja kuikaimu nafasi yake ya kupeleleza wavunjifu wa sheria za shule, alibaki kuwa historia tu jina lake ndani ya shule hiyo kwa wanafunzi wa miaka aliyokuwepo. Mwaka aliyohitimu kidato cha sita ndiyo mwaka ambao habari hizo za kukamatwa kwa watu ziliisha, wengi walijua kabisa kuwa huyu Bond alikuwa ametoka kwenye mwaka wa wanafunzi hao waliomaliza ingawa hawakumjua kwa sura. Kilichofuata hapo ilikuwa ni kupooza kwa ufuatiliaji wa wanafunzi na hata ule wasiwasi ukapungua kutokana na kuondoka kwake. Bond huyu alikuja kuhamia kwenye mafunzo ya jeshi la kujenga Taifa ya awali kabisa, yalikuwa ni mafunzo ambayo walikuwa wakikaa mwaka mzima ndani ya kambi. Mafunzo hayo nayo bado hakuacha ile asili yake ambayo alikuwa ameianza tangu kipindi akiwa yu mdogo, huko napo alipokea sifa ya aina yake akiwa yupo huko jeshini. Ilifikia hatua ya kutaka hata kuchukuliwa akimaliza mafunzo hayo lakini Mzazi wake hakupenda kabisa. Alikuwa akihitaji mwanae aendelee na masomo na si kujiunga na jeshi hilo, majibu ya kidato cha sita hayakuwa mazuri kwake jambo ambalo lilifanya ashindwe kujiunga na chuo. Hili suala lilimfadhaisha sana mzazi wake na Bond akabaki mtaani alipotoka mafunzoni, aliendelea na tabia yake ileile ambapo kwa muda aliokuwa amekaa hapo mitaa ya nyumbani kwao alifanikiwa kugundua uwepo wa kikundi cha uhalifu. Maaskari wa jeshi la polisi walimpongeza sana kwa kuweza kufanikisha huko kugundulika kwa kikundi hicho, lakini aliporudi nyumbani ilikuwa ni ugomvi mkubwa. Mzee Nkongo alikuwa hataki kabisa mtoto wake afanye huo upelelezi wake ambao alikuwa akiufanya tangu yupo mtoto, alkizidi kumuonya na hapo akaona hakusikilizwa. Alipochoshwa na tabia hiyo mbayo alikuwa akimuonya mwanae ilimbidi tu aongee naye kuhusu kujiunga na jeshi la polisi, aliona ndipo kunamfaa. Aliamini kuwa jambo hilo litasikilizwa na kuuungwa mkono na mwanae huyo, aliona kabisa alikuwa na mwangaza wa kuelekea huko. Ule msemo wa kuwa kipaji huonekana kwa mtu angali mdogo, aliuamini kabisa na akaamua ni bora ampeleke sehemu ambayo inamfaa kwa yeye kuendeleza hicho kipaji chake. Alikuwa na uhakika kabisa Bond angelipokea suala hilo kwa mikono mwili, muda wa jioni akiwa yupo ndani ya nyumba yake aliyopewa na serikali alimuita mwanae na kumueleza kuhusu suala hilo. Tofauti na alivyotarajia suala hilo lilipokewa kwa namna nyingine kabisa, kupingwa kwa suala la kujiunga na jeshi la polisi ndiyo alipopakea. Mzee Nkongo alichoka na hakumuelewa kabisa mwanae huyo, aliyekuwa akikaa nyumbani huku muda ukiwa unaenda sana. Alitakiwa awepo masomoni au awe na ajira yeyote kwa kipindi hicho, lakini masomo yameshindikana na ajira nayo alikuwa ameikataa. Hakuweza kumuelewa na ikambidi amuulize kile apendacho kukifanya, hapo ndipo Bond alichagua kujiunga na jeshi katika kikosi kingine tofauti ambacho baba yake hakudhania kabisa. Elius maarufu kama Bond hatimaye alichagua kujiunga na jeshi la Magereza kwa mafunzo mafupi kwani tayari alikuwa amepitia mafunzo imara ya kijeshi. Nafasi kipindi hicho za kujiunga na jeshi hilo zilikuwa zimetoka, alipoomba kutokana na kuwa katika jeshi la kujenga taifa kwa muda mrefu. Alipita bila kikwazo chochote na akajiunga kwa mara ya kwanza ndani ya jeshi hilo, pamoja na kujiunga kwake ndani ya jeshi hilo bado hakuacha kabisa tabia yake ya kupeleleza. Huku jeshini ndiyo alikuja kukutana na rafiki yake waliyepotezana wakiwa shuleni, huyu hakuwa mwingine ila ni Philipo Lutonja. Bond huyu alikuja kulala usingizi katika kipindi ambacho alikuwa amepata mchumba,tabia hii ilionekana kumkera kabisa mwanamke ambaye alikuwa amempata katika umri wake aliokuwa akihitajika kuwa na mwenza. Kipindi hicho alikuwa tayari amehamishiwa jijini Dar es salaam akiwa pamoja na rafiki yake Philipo, ajira alikuwa nayo na cheo alikuwa ameshapata japo hakikuwa kikubwa sana. Tabia hii ilikuja kujulikana na mchumba wake ambaye ilimchukiza sana, alimuonya kuhusu hiyo tabia ya kufuatilia vitu lakini haikukoma. Mwishowe alitishiwa kumuacha ndipo alipoamua kuiacha tabia, hapo ndipo Bond alilala na akabaki Elius yule mcheshi na mpenda kuzungumza na kila mtu. Miaka thelathini sasa imepita tangu Bond alale akimuacha Elius akiwa yupo huru, akiwa ameacha ile tabia yake ya kupeleleza. Sasa akiwa amekaa hapo kwenye kochi ndiyo aliamka tena, uamkaji huu ulikuwa ni wa kimyakimya sana bila hata kumshtua mwanae wa mwisho James akiwa yupo naye. Hakika asili haifi hata kwa kushikiwa silaha, humrudia mtu kutokana na sababu maalum. Ndiyo ilivyokuwa kwa SSP Nkongo asili hiyo ilirudi katika muda ule ambao yule Mchumba wake anaitwa mke wake na wala hakuwaza kabisa kama ingeweza kurudi, hakukaa sana hapo kwenye televisheni yeye aliinuka na kuingia ndani. Huko ndani napo hakukaa sana, alitoka akiwa mkononi na funguo pamoja na mkoba wake wa kazini, alielekea kwenye maktaba yake ambayo alikuwa akifanyia mambo muhimu ya kiofisi kipindi akiwa yupo nyumbani kwake. Kitendo cha kuketi mezani kiliambatana na utoaji simu yake ndogo ambayo haitumii kwa mawasiliano makubwa, alibonyeza vitufe vya simu hiyo na hatimaye alipata kitu alichokuwa akikitafuta. Alikuwa akitafuta ni faili muhimu la sauti ambayo alikuwa ameirekodi kipindi akiongea na Kizigo, alicheza sauti hiyo ikawa inasikika vyema katika muda huo aliokuwa amejifungia humo ndani. Aliisikiliza sauti kwa umakini kabisa akifuatilia hadi jinsi iliyokuwa ikizalishwa, alijenga taswira ya Kizigo na kipindi akiongea na hapo akapata akakumbuka lugha ya mwili kipindi alipokuwa akiongea naye. Lengo lake ilikuwa ni kupima kuwa huyo mtu alikuwa yu miongozi mwa ukweli au siyo, ushahidi pekee wa picha haukutosha kumthibishia kuhusu hilo pasipo yeye kuchunguza. Uchunguzi wake hakuona shaka ndani ya maneno ya Kizizo, hakika alikuwa ni miongoni mwa wakweli. Bado hakutaka kujiridhisha kuwa ushahidi wote uulikuwa umekamilika, alitaka ajithibitishie na yeye. Hakuwa mtu wa kuridhishwa na ushahidi utakaoletewa pasipo na kujiridhisha, hapo aliamua kupanga mikakati muhimu ya kazi yake. Vitu muhimu ambayo alikuwa akivifanya aliamua kuvinakili kwenye kitabu chake cha siri ambacho alikuwa akikitumia kuhifadhia mambo muhimu, usiri uliomo ndani ya kitabu hicho ulikuwa ukijulikana na yeye mwenyewe tu na hata mke wake hakuwa akijua. Aliponakili mammbo muhimu ya kuanzia alifunga kitabu hicho, alitoka na kurudi ukumbini kwani muda wa kula tayari ulikuwa umewadia. Siku iliyofuta kama kwaida alienda ofisini kwni ilikuwa ni siku ya Ijumaa, ilikuwa ni siku ya kazi ilimbidi awe kazini. Asubuhi ya siku hiyo alikuwa ameshapata taarifa za kifo cha Kizigo mtu muhimu aliyemfumbua macho. Magazeti muhimu ndani ya asubuhi hiyo yalikuwa tayari yameshaandika habari juu ya kifo hicho, magazeti mengi yalikuwa yameandika sababu maalum juu ya kifo hicho. Alijikuta akivutika na gazeti moja kati ya magazeti mengi yaliyokuwa yameandika juu ya kifo hicho, lilikuwa ni gazeti muhimu sana ambalo huandika mambo mazito kuhusu matukiom balimbali ndani ya nchi hi. ‘KIZIGO AULIWA NA WASALITI WENZAKE Muuaji aeleza kila kitu’. Hicho kilikuwa ni kichwa cha habari kikubwa na maandishi madogo yalifuatia chini yake. Gazeti hilo lilimvutia kabisa pindi aliposhuka kutazama meza ya magazeti siku hiyo, alilipita hela na kisha akarudi ndani ya gari akaendeleana safari ya kuelekea ofisini. Kitendo cha kutia mguu ndani ya ofisi yake tu na kufunga mlango, alitupa gazeti hilo kwenye meza yake na kisha akaweka mkoba chini ya meza. Alipoweka kiungo cha kukaa kwenye kiti chake, alikamta gazeti hilo na kuanza kuipitia habari hiyo kwa umakini sana. Alimaliza kuisoma habari hiyo na akaona ni jinsi gani ilikuwa imetengenezwa kiufundi zaidi, alinakili vitu muhimu kwenye habari hiyo na kisha aliendelea na kazi zingine zilizomuweka kwenye jeshi hilo. **** Muda wa kifungua kinywa ulimkuta akiwa yupo meza moja na rafiki msaliti, ilikuwa ni kawaida kwenda pamoja katika maeneo kama hayo na hakutaka kabisa kuuvunja utaratibu huo. Alijua wazi laiti angeuvunja ingekuwa ni mwanzo wa kuweka fikra mpya kichwani mwa ASP Lutonja. Hakutaka hilo litokee mapema kabisa, aliamua kutobadilisha tabia zote ambazo alikuwa akizoeleka kuonekana nazo akiwa naye. Lengo ni kuzidi kuivuta amani ya moyo wake, kuonesha hakuwa anajua chochote ili aweze kumchunguza. Bond alikuwa yupo kichwani mwake na ule umakini wake uliongezewa na hamasa za kusoma riwaya za James Bond ulikuwa umerudi tena, ucheshi ulikuwa ukitawala kwenye maneno yake. Si yeye wala ASP Lutonja aiyekuwa amegusia juu ya tuhuma iliyowasili siku iliyopita, walipomaliza kupata kifungua kinywa ndipo Msaliti wake alipoanzisha mada hiyo. “Elius vipi jana ulienda kukutana naye?” Aliulizwa “Aaaah! Nilienda hana lolote lile waandishi wa habari wanaleta janjajanja tu” Alijibu “Nilkwambia mimi rafiki jana hukutaka kunielwa aisee, siwezi kusaliti kiapo nilichokiweka wakati najiunga na jeshi hili” “Aisee nimekuamini kabisa si umesikia kumbe naye alikuwa akihusika kwenye mchezo huo” “Unaona sasa! Alitaka kunigeuzia mimi mpira yaani mambo yamekuwa mabaya kwake wenzake wamemuuua, si umesikia Mhusika yupo kituo cha kati kasema katumwa kumuua na kaichoma nyumba yake moto” “Mshahara wa dhambi ni umauti na kaupata” “Kabisa kabisa hata angepona bado angekuwa na kesi ya kujibu, kwanini anichafue Assistant Superintendent of prison” “Ujue habari ya kizigo alivyokuwa akinisimulia imenikumbusha ishu ya Bond kipindi kile tupo shuleni” “(huku akicheka) Aisee Elius una kumbukumbu, unajua sikuwahi kumjua ni nani yule mtu aliyekuwa akipeleka taarifa kwa walimu hadi namaliza pale shuleni” “Hata mimi simjuia hadi leo hii,naona huyu Kizigo ndiyo likuwa akileta ujanja huo. Bahati mbaya hata kupangilia maelzo hajui yaonekane kweli, body language imemuonesha ni muongo” “Achana naye huyo si wa kumsema tena, Elius unajua wiki ijayo ni Kipaimara ya Jane” “Sasa nitajuaje bila wewe kunifikia taarifa, nina tunguli za kunijulisha” “Haaaah! Huachi mambo yako, sasa ndiyo nakujulisha hivyo ni wiki ijayo jumapili sherehe nyumbani” “Usihofu nitaleta mangoko yangu haya nije kukusaidia kupunguza kilo za pilau ili usipate akiba ukamwaga” Kicheko kilimtoka ASP Lutonja kutokana na vituko vya rafiki yake, alicheka sana huku akimtazama lakini hakukuta cheko kwenye uso wa SSP Nkongo zaidi ya tabasamu. Alicheka hadi alipomaliza hakusikia kicheko chake, alikuwa amemzoea kabisa rafiki yake ambaye hupenda kumchekesha pasipo yeye kucheka. “Hivi Elius hivyo vituko utaacha lini?” Alimuuliza “Mamba akiacha kuwinda kwenye maji na mimi ndiyo nitaacha” Alipewa jibu “Yaani tupo shule hivyohivyo, JKT nahisi ulikuwa hivyohivyo. Tunaingia mafunzoni hivyohivyo hadi huku kazini aisee” “Yaani nimekuambia Mamba akiacha kutegea mawindo ndani ya maji na kuja kutega na kushika nchi kavu. Basi nitaacha pia” “Ushawaambukiza hadi watoto wake aisee, yaani Fred ndiyo huyo vituko James sipati picha aisee” “Hivi Paka kuchimba shimo kabla ya kujisaidia anaambukizwa na mzazi wake?” “Hamna ni tabia asili” “Basi Fred naye ni tabia asili kama yangu” “Mshindi wewe, time hii imekimbia tayari tuondoke” Wote walismama kwenye viti walivyokuwa wamevikalia wakiwa wanaongea na kutaniana, kila mmoaja aliingia ofisini wake na kuendelea na kazi kama kawaida. Muda wa kutoka kila mmoja alielekea nyumbani kwake na baadaye jioni walikutana tena, walikutana kwenye bar moja ambayo walikuwa wakipenda kukutana kila ufikapo mwisho wa wiki. Ndani ya Bar hiyo walikuwa wakipenda kupata kinywaji kutuliza machungu ya wiki nzima, walikunywa na kula nyoma choma wakiongea mambo mbalimbali. Muda huo SSP Nkongo alikuwa akitafuta kila mbinu aweze kumchimbua huyo Msaliti wake, pombe iliendelea kunyweka kwa taratibu sana kiupande wake lakini kwa mwenzake alikuwa akinywa kwa fujo san. Haikufika muda mrefu ASP Lutonja alikuwa amelewa tayari na uchangamfu mkubwa ulikuwa umemvaa na hata akafikia kupiga makelele kwa nguvu. Hiyo ilikuwa ni hatua mbaya sana kwao kutokana na kujulikana vyeo vyote, ili kuiokoa hatua hiyo SSP Nkongo alimchukua rafiki yake hadi kwenye gari yake ambayo ndiyo walikuja nayo pamoja. Ilikuwa ni muda ambao giza lilishaanza kuingia na kuiondoa nuru ambayo ilikuwa iking’ang’ania kuwepo ingawa muda wake ulikuwa umeisha. SSP Nkongo aliliondoa gari kwa mwendo wa wastani hadi alipofika eneo ambalo lilikuwa ni mitaa kadhaa kutoka nyumbani kwa ASP Lutonja, hapo alisimamisha gari na kisha akamtazama rafiki msaliti aliyekuwa haishiwi kuropoka akiwa yupo ndani ya gari. “Unajua hii kazi nishaanza kuona haina faida kiupande wangu vipi wako mzee” Alimuuliza kimtego huku akitambua kiwango cha unywaji pombe alichofikia hakikuwa na utunzaji siri. “Mimi nishatambua hilo kitambo sana ndiyo maana nikaungana na wakina Meja Ibrahima Salim wa JWTZ” ASP Nkongo aliropoka “Yaani Philipo wewe rafiki yangu upo kama ndugu yangu wa damu unanificha hili” “AaaaaH! Tatizo wewe Elius unajifanya mzalendo kulinda kiapo, kiapo kitu gani viongozi wa dini tu wanasaliti imani zao ndiyo sembuse sisi” “Nipe mpango upo vipi maisha yanapanda gharama si unajua hilo” “Aaaaah! Kitu simpo kabisa Elius, ni kuiba silaha za kambi zote za kijeshi na kuziuza tuna mawakala wakubwa” “Duh! Mtu wangu si hatari hiyo au kupo vipi” “Hakuna hatari yeyote ile, polisi na hata usalama wa taifa wapo viganjani mwetu hawana tabu kabisa. Umeona kama Kizigo kajifanya mjuaji jana tumemfuata na tumemuua kisha tumemuuzia kesi mwingine kabisa na kalazimishwa akakiri. Eti aje kunisemea kwako” “Ndiyo hapo hata mimi nameshngaa kabisa, mimi na wewe toka lini tukawekana pabaya” “Aaaaah! Si ndiyo hapo yule jamaa hebu muache na ujinga wake” “Sasa nipe ramani nipo tayari kujiunga na wewe nisogeze maisha” “Usijali wewe kama ndugu kwangu kesho nitakuja kukupa taarifa kila kitu” “Hamna shida. SSP Nkongo alipoondoa gari baada ya kuridhishwa na majibu ya mwenzake ambaye alikuwa amelewa, alimpeleka hadi nyumbani kwake na kisha alimshusha na kuingia naye ndani. Alipomkabidhi kwa mke wake kisha aliondoa gari na kuelekea nyumbani kwake akiwa na ushahidi mwingine, ASP Lutonja alikuwa hatambui kabisa kile ambacho kilikuwa kimetokea kutokana na kuzidwa kilevi. Hakujua sababu ambayo ilimfanya rafiki yake huyo asinywe kilevi kingi zaidi ya kunywa kidogo akiwa na kinywaji chenye kupunguza makali kilevi hicho, lengo lilikuwa limeshatimia mtegwaji alikuwa hatambui kama alikuwa ametegwa. SSP Nkongo alipofika nyumbani hakukaa hata kidogo aliaga na kutoka, aliongoza gari yake kuelekea kwenye eneo ambalo hisia zake zilikuwa zimemtuma. Safari yake alifuata muongozo wa aliokuwa ameukuta kwenye picha ya Kizigo mojawapo ambao ulikuwa umewekwa nyuma. Muongozo huo ndiyo ulimfikisha hadi kisarawe na alipitliza kwenye eneo alilokusudia hadi mbele kidogo ambako alikuta kulikuwa na mji mdogo. Aliegesha gari yake pembeni ya duka hio na kisha akaomba kuangaliziwa, alitoa ahadi ya kurejea muda mfupi na kisha alianza kukita hatua zake ndefu ardhini kusogea alipopakusudia. Alifika kwenye eneo alilokuwa amelikusudia na alitembea kuingia kwenye njia ya kujificha kulingana na muongozo wa picha aliokuwa ameukariri, aliingia kwenye kichaka na akajibana hapo. Alikaa kwenye eneo hilo kwa muda mrefu na hata alifikia kukata tamaa ya kuendelea kukaa hapo, muda mfupi baadaye aliweza kushuhudia gari mbili kubwa za kijeshi zikiingia kwenye njia ambayo ilikuwa ikiingia kwenye eneo la pori ambalo alikuwa amejibana. Alishuhudia watu wanne wakishuka baada ya magari hayo kuegeeshwa, watu hao walienda moja kwenye eneo lenye majani mengi. Kilikuwa ni kichaka kilichokuwa kimejifunga ambacho watu hao waliingia na hawakuonesha dalili ya kutoka. Alikaa hapo kwa muda wa dakika kadhaa ili kuhakiki kama watu hao ndani ya mgari walikuwa peke yao. Alipoona kimya kwenye magari hayo taratibu alijitoa kwenye kichaka hicho, alitembea kwa mwendo wa kunyata mithili ya simba aliyekuwa akinyatia wingo lake. Alikuwa yupo makini sana asiweze kupatwa na Yuda mmoja miongoni mwa Mayuda wengi waliokuwa wakihusika na eneo hilo, kituo cha kwanza cha mnyato wake ilikuwa kwenye magari hayo ya kijeshi yaliyokuwa yameegeshwa na kuzimwa taa. Ubond ulikuwa umempanda kichwani akajikuta akiyaangalia magari hayo vizuri aweze kutambua umiliki wake ulikuwa ni jeshi gani, pamoja na uwepo wa giza eneo hilo aliweza kutambua gari mojawapo ni aina ya Iveco na muundo wake alibaini kabisa lilikuwa ni gari la jeshi la wananchi, jingine aliona lilikuwa ni aina ya Leyland hapo alitambua lilikuwa ni mali ya jeshi la polisi kutokana na kuchunguza sehemu za bati za namba kwa macho yake makali gizani. Hakutaka kulala nyuma baada ya hapo alisogea hadi kwenye eno ambalo lilikuwa na kichaka, taratibu alifungua kichaka hicho akaingia akiwa na tahadhari kubwa. Alikutana na njia iliwekwa mawe ambayo ilikuwa ikishuka chini ya ardhi. Alishuka chini kuifuata njia hiyo hadi alipofika kwenye eneo ambalo lilikuwa na mlango, alijaribu kuufungua mlango lakini alishindwa kutokana na kufungwa uimara. Alipoutazama sehemu ya pembeni alibaini kuwa ulikuwa umefungwa na namba za siri, ugumu wa kufungua mlango huo alianza kuuona na hakutaka kubaki tena eneo hilo kwani hakuwa na njia nyingine ya kuufungua huo mlango. Aliondoka kwa kupitia njia aliyoingia nayo eneo hilo hadi barabarani na kisha alirudi hadi pale alipokuwa ameeegesha gari lake, alitoa noti moja ya shilingi elfu tano na kumpatia aliyemuomba kumlindia gari. Baada ya hapo aliondoa gari lake kwa mwendo wa kasi awahi kufika nyumbani kwake, dakika ishirni baadaye alikuwa tayari ameshafika nyumbani kwake kwa ajili ya kupumzika na familia yake. **** Asubuhi iliyofuata AS Lutonja aliamka akiwa ni mchovu sana kutokana na kilevi cha siku iliyopita, pamoja na uchovu huo hakutaka kabisa kukaa ndani kwani ilikuwa ni muda ambao alikuwa akifanya mazoezi ya kukimbia akiwa pamoja na rafiki yake. Alivaa nguo za mazoezi baada tu ya kusafisha kinywa chake na kisha akatoka nyumbani kwa akiwa ameongozana pamoja na kijana wake wa kiume, wote walikimbia taratibu kuelekea nyumbani kwa SSP Nkongo. Baada ya mwendo wa takatibani robo saa waliweza kufika nyumbani hapo, walimkuta tayari akiwa amejiadnaa akiwa na kijana wake Fred ambaye alikuwa akikimbia naye mazoezi. Familia hizo mbili kwa pamoja zilijiunga na kuanza kukimbia kuelekea kwenye uwanja wa mpira ambao walikuwa wakipenda sana kufanya mazoezi hapo, muda mfupi baadaye walifika uwanjani hapo wakikimbia huku mmoja akiwa ni mwenye amani moyoni mwake lakini mwingine hakuwa na amani. Mmoja alikuwa amejawa na umakini mkubwa katika kumchunguza mwenzake, umakini huo aliokuwa amejawa nao alikuja kupata uhakika na kisha akaondoa hofu. Alikuwa ni SSP Nkongo alikuwa na hofu huenda mwenzake angekuwa na kumbukumbu wa kile kilichotokea usiku uliopita, kulewa haikumaanisha ndiyo ingeweza kutokuwa na kumbukumbu zote. Alihisi angeweze kukumbuka chochote. Alipopata uhakika hakuwa akikumbuka chochote aliondoa hofu yote aliyokuwa nayo, aliendelea kufanya naye mazoezi kuweka mwili sawa kwani hawakutaka kabisa kuwa na miili ya kizembe ingawa walikuwa na vyeo vikubwa ndani ya jeshi la Magereza. Mazoezi yaliwachukua muda mfupi na hadi saa moja asubuhi wakawa tayari wameshamaliza, walianza kukimbia kwa mwendo wa taratibu wakirejea majumbani mwao kwa ajili ya kujiandaa. Ilikuwa ni siku ya jumamosi na wote walikuwa wakielekea kazini kwa kufanya kazi kama kawaida, siku hii ya leo ilikuwa na masaa machache ya kufanya mazi hivyo walikuwa wakihitajika wawepo makazini kwa ajili ya kutimiza wajibu wao. **** Majira ya saa nne asubuhi ofisini kwa SSP Nkongo aliingia Inspekta, alitoa saluti kwa mkubwa wake huyo wa kazi na kisha aliamriwa kuketi kitini. Ulikuwa ni ujio ambao ulikuwa ukimaanisha kuwa kulikuwa na taarifa au shida kutoka kwa aaskari huyo ambaye alikuwa yupo chini yake kicheo. SSP Nkongo alijiandaa kusikiliza shida ya huyo Inspekta, aliacha kufanya kazi ili aweze kumsikiliza. “Ndiyo Mwambe” Alimpa wasaa wa kuongea “Afande kuna jambo sijalipenda nimeamua kuliripoti kwako” Inspekta Mwambe aliongea akiwa ni mwenye hofu “Kwa siku ya nne mfululizo kuna kijana wa chini yangu alikuwa akinilalamikia juu ya utolewaji wafungwa usiku Gerezani na kupelekwa kusikojulikana. Hii siyo kwake tu hata ndugu yangu mmoja ambaye ni Askari gereza la Ukonga amenithibitishia” “Ndiyo nipe maelezo kamili” “Juzi nimeamua kuja mwenyewe hapa gerezani nikashuhudia mkuu wangu akiwaondoa wafungwa wa zamu wasilinde usiku na kisha yeye huwatoa wafungwa wale wanaotuhumiwa ujambazi wa benki na kuondoka nao. Jana sikumuona Mkuu akifika lakini walikuja maafande wengine ambao nahisi siyo wa kambi hii wakawachukua wafungwa wale na kuondoka nao” “Mkuu ni nani maana wapo wakuu wengi hapa” “Ni Mkuu Lutonja” Kauli hiyo iliposikika kwenye masiko ya SSP Nkobgo alionesha kushtuka ingawa haikuwa taarifa ngeni kabisa, aliweka vignja vya mikono usoni mwake kwa sekunde kadhaa na alipovitoa alimtazama Inspekta Mwambe. “Mwambe hili suala ni serious, gazeti limetoa tuhuma hiyo lakini uchunguzi haujaonesha hatia yake” “Mkuu hata mimi nilitaka kuamini hivyo lakini hata kabla huo uchunguzi haujatoka. Tayari nimelibaini hili. je kushuhudia na uchunguzi kipi ni ushahidi sahihi” “Kwako wewe uliyesema umeshuhudia ila siyo kwangu Mwambe” “Natambua hilo Mkuu ila nakuomba tu hata na wewe uje usiku huku ujibane mahali uone mambo yanayofanyika” No Inspketa usiseme maneno hayo inaonesha unaona sijakuamini, lakini utafiti kwangu pia ni muhimu. Mtu mkubwa kama Lutonja hatuwezi kumkamata kienyeji, lazima nikusanye ushahidi” “Sawa mkuu, ukinihitaji kutoa msaada nipo tayari kukusaidia” “Nikikuhitaji nitakuita uwe msaidizi wangu ila kwa sasa wacha niingie kazini peke yangu kwanza. Unaweza kwenda kuendelea na kazi Mwambe” “Mkuu” Alinyanyuka na kwenye kiti akatoa heshima baada ya kupokea amri ya kurudi eneo lake la kazi, baada ya hapo alitoka ofisini akiwa tayari amefikisha dukuduku lake Alimuacha SSP Nkongo akianza kuona uhatari wa urafiki wake na ASP Lutonja, usaliti wake ndani jeshi la magereza ukigundulika basi na yeye angehusika moja kwa moja. Urafiki wake na Yuda ndiyo ungeweza kumtia hatiani jambo ambalo hakuwa tayari litokee, kufikia wakati huo alikuwa yupo tayari urafiki ufe lakini si yeye kuingia kwenye aibu. Jambo hilo hadi kumfikia Inspekta alikuwa na uhakika kwa asilimia mia moja lilikuwa limefika kwa Maaskari wengi waliokuwa wapo chini yake. Kugundulika kwa jambo hilo kwa wakubwa zake aliona ungekuwa mwanzo wa yeye kuanza kunyooshewa vidole na maaskari wa chini yake, hakika kutembea na mwizi nawe utaitwa mwizi. Ndiyo hili alilihofia kutokea, kuonekana ni ndani ya mnyororo mmoja na rafiki wa tangu shuleni. Urafiki wao ulioshibana hadi kufikia kila mmoja kuwa msimamizi wa mwenzake kwenye ndoa, aliona ndiyo ulikuwa ukielekea kumtia doa kutokana na kuambatana naye kila sehemu kama kumbikumbi. Lazima angehisiwa hata huko kwenye uhaini aliyokuwa anaufanya angeambatana naye, hata kama ushahidi wa kumtuhumu yupo kwenye hatia haukuwepo. Bado aliona angehukumiwa na hukumu ya wanadamu wasiyojua hata uhalisia wa jambo, wanadamu wasio acha kuongea kitu kinachopita mbele yao hata kama hawakukijua uhalisia wake. Hao ndiyo aliokuwa akiwahofia kabisa kuweza kumshushia heshima yake, rekodi nzuri ambayo alikuwa anyo kwenye jeshi hilo hata kiasi cha kuwa nishani kadhaa kwenye vazi lake. Alihisi zitakuja kuonekana hazina thamani kwa raia ambao walikuwa wakimuheshimu pia, pia hakutaka kuona linatokea kwani alikuwa akihitaji heshima za pande zote mbili “Sitokubali” Alijisemea moyoni mwake alipoyafikiria masuala hayo yaliyokuwa yakikaribia kuchafua heshima yake, akiwa hapo mezani aliiingiza mkono mfukoni mwake. Alifungua na picha ya familia yake pamoja na ile aliyopiga na rafiki Yuda zilionekana. “Ni bora unione sifai kwa familia yake kuliko jamii inione sifai, majukumu na heshima hazina urafiki” Alijisema huku akiitazama picha aliyokuwa yupo pamoja na ASP Lutonja, alipochoka kuitazama picha hiyo aliitazama picha aliyokuwa yupo pamoja na familia yake. “Ukigundulika wewe kabla ya mimi kukuweka hatiani nitaonekana nilikuwa nakufuga, hata nikitoa ushahidi hautokuwa na maana. Nitaanza kukuweka pingu mwenyewe ili familia yangu isije kudharaulika kisa urafiki wetu” Aliendelea kusema na moyo wake huku akizitazama picha hizo kama vile zilikuwa zikitambua kle akisemacho.
Hatimaye muda wa kurudi nyumbani baada ya kutimiza majukumu ya kiofisi uliwadia, siku hii aliondoka akiwa mwenyewe tofauti na ilivyozoeleka kuondoka akiwa yupo na Yuda wake. Safari yake ilikuja kuweka kituo cha kwanza kwenye nyumba yake ambayo alikuwa akiishi na kisha alichukua kitu muhimu. Alitoka tena na kuondoka akiwa hakuaga kabisa alikuwa akielekea wapi. Alikuja kuishia kwenye nyumba nyingine ya kwake ambayo ilikuwa ipo shambani kwake, SSP Nkongo aliingia ndani ya nyumba hiyo ambayo ilikuwa na kila kitu ndani yake kasoro tu makazi ya viumbe hai. Alielekea hadi kwenye chumba kimojawapo ndani ya nyumba hiyo ambacho kilikuwa kimejaa vitabu pamoja na mafaili mbalimbli, hapo alitua mkoba wake ambao alikuwa ameubeba na kisha akasogelea kabati kubwa la vitabu. Macho yaliyokuwa yakizunguka mithili ya kurunzi ya ulinzi mpakani, yalitua kwenye faili jipya kabisa miongoni mwa mafaili kadhaa yaliyopo humo kabatini. Alilitoa faili ambalo lilikuwa limefungwa kamba na kisha alifungua kamba hiyo, yaligawanyika na kuwa mafaili mawili ambapo moja alilirudisha mahala pake na kisha jingine alilichukua. Faili hilo moja ambalo alilichukua alikwenda nalo mezani na kisha akalitua, macho yake yaliyokuwa yamejaa umakini yalikuwa yametua juu ya faili hilo lilipokuwa hapo mezani kabla hata ubongo haujashurutisha mikono yake kuweza kufungua.’Msaliti’ ndiyo kichwa kilichokuwa kipo juu ya faili hilo, alikisoma kama vile alikuwa akikiona kwa mara ya kwanza na kisha alilifungua faili hilo kuangalia ndani yake. Ushahidi wote aliokuwa ameukusanya ulikuwa upo ndani ya faili hilo, alipofungua aliongezea na ushahidi mwingine kwa kuandika vitu vyote ambavyo alikuwa amevifanyia utafiti. Aliambatanisha na ushahidi wa kurekodi ambao alikuwa ameufanya kwa watu mbalimbali ambao walikuwa wamethibitisha juu ya kile alichokiona. Alipomaliza kunakili kila kitu kwenye karatasi za ndani ya faili hilo alihakiki maandishi yake, usahihi wa maandishi hayo uliporidhishwa na macho yake aliyoyapitisha juu yake aliamua kulifunga faili hilo kisha akalirudisha pale alipokuwa amelitoa. Kuliweka faili hilo kuliambatana na kuchomoa faili jingine ambalo lilikuwa limefungwa pamoja na faili hilo, nalo alilifungua na kuandika kama alivyofanya kwenye faili lililopita. Baada ya hapo alilifunga faili hilo lakini aliingiwa na utaribu mpya tofauti na utaratibu ambao alikuwa ameufanya kwenye faili la awali. Utaratibu huu ulimpelekea kutolirudisha faili hilo mahala pake na akabaki nalo mezani. Alipomaliza alitoka humo ndani na kisha alielekea kwenye sebule ya nyumba hiyo, alilitua faili mezani pindi tu alipofika kwenye sebuleni na kisha alijibwaga kwenye kochi. Alijipekua mfukonni akiwa ni mwenye kutafuta kitu, alijipekua kwa namna hiyo kwa sekunde kadhaa akibadili mifuko tofauti. Hatimaye alifika mfuko wa mwisho kabisa na kupata kile ambacho alikuwa akikitafuta, hakika ilikuwa ni bangili ya rangi ya fedha ambayo ilikuwa imetengenezwa kwa madini magumu. Pingu za kufungia watuhumiwa ndiyo alikuwa akizitafuta na hatimaye zilikuwa zipo mikononi mwake. Aliiweka juu ya faili hiyo pingu na kisha aliinuka na kuliendea jokofu ambalo lilikuwa lipo jirani kabisa na sebule hiyo, ufunguaji wa jokofu hilo ndiyo ulifuata na aliinama kutafuta miongoni mwa cupa kadhaa ambazo zilikuwa zipo ndani ya jokofu hilo. Alipoinika mikono haikuwa mitupu kama ilivyokuwa hapo awali kipindi akilisogelea hilo jokofu, iliibuka ikiwa na chupa moja ya pombe kali ambayo alizoea kuinywa kabla hajaingia kwenye kazi ngumu tangu akiwa yu na cheo kidogo ndani ya jeshi hilo. Alirudi na chupa hiyo mezani na aliifungua huku huku akilitazama faili lilipo mbele yake, kifuniko kilipotii amri ya kufunguka alipeleka chupa hiyo mdomoni na kisha alipiga mafunda kadhaa. Alipoishusha ilikuwa imepungua mililita za ujazo kutokana na kumezwa na kinywa chake, aliipeleke hiyo chupa kwa mafundo kadhaa na hatimaye ikaisha. Alipoitua alichukua faili lake na kisha alitoka ndani ya nyumba hiyo, adhma iliyokuwa ipo ndani ya kichwa chake ilikuwa ni kumtia nguvuni Msaliti wake tu. ****
Majira ya moja jioni James alikuwa yu sebuleni akiangalia luninga, mama yake alikuwa yupo jikoni na kaka yake alikuwa yupo chumbani. Mlango wa kuingia sebuleni kwao uligongwa mara mbili jambo ambalo lilimpeleka kuinuka kwenye kochi na kwenda kuufungua, akili yake ya utoto aliyokuwa nayo hakuwa ameuliza huyo aliyokuwa akigonga mlango huo alikuwa ni nani. Wala hakushughulika kujiuliza huyo aliyekuwa akigonga mlango huo alikuwa ameingiaje ndani hapo bila kufunguliwa lango la magari ambalo mara nyingi sana huwa linafungwa majira yote na hufunguliwa baada ya kugongwa. Akili yake yote ilikuwa imemtuma kuwa huyo aliyekuwa amegonga mlango huo alikuwa ni Baba yake kipenzi ambaye hakuwa amerejea nyumbani ,alitekenya kitasa kwa kutumia ufunguo uliokuwa upo kati yake na hatimaye kitasa hicho kikatii amri. Aliponyonga kitasa na kukifungua kilichofuata hapo ilikuwa ni kuandikwa kwa historia mpaya katika maisha yake, ulikuwa ni mwanzo wa ukurasa wa maisha ambao ulikuwa ni zaidi ya jeraha kwake. Ugeni uliotangulia baada ya yeye kufungua mlango ilikuwa ni gesi nzito, ugeni ulivamia macho yake na kumpa muwasho wa ajabu sana ambao hakuustahimilia alipiga kelele kutokana na maumivu aliyoyapata huku akitaja jina la mama yake. Kilichofuata hapo ilikuwa ni kutoona kilichopo mbele yake, akiwa kwenye hali hiyo ya kupiga kelele alipokea msukumo wa nguvu sana ambao ulimrudisha ndani ya nyumba. Mama yake na kaka yake walipotoka tu kilichofuata ilikuwa ni kila mmoja kuoneshewa bastola na mtu ambaye alikuwa na silaha, mtu huyo ambaye hawakumtambua na wala hawakuwahi kuiona sura yake aliwaamuru wakae kimya na kisha walale chini. Haikupita hata dakika tangu walazwe chini aliingia mtu mwingine ambaye alikuwa amevaa suti nadhifu sana kama wa awali, mtu huyu alifunga mlango na kisha akabaki akitabsamu sana. “Salam kwako mke wa SSP” Aliongea mtu huyo wa pili kuingia ambaye alikuwa na upara pamoja na ndevu nyingi kidevuni. Salamu yake haikujibiwa na alioneshewa sura zilizojaa woga kama vile ndiyo lilikuwa jibu la salamu hiyo, hilo halimkufanya huyu mtu awazingatie na badala yake aliachia tabasamu pamoja na mwenzake ambaye alikuwa amewawekea silaha. Huyu alikuwa na nywele nyingi sana huku kidevuni mwake hana ndevu tofauti alivyo mwenzake, naye alirudisha tabasamu alilopewa na Madevu kisha akawatazama mateka wake walikuwa wamejaa hofu sana. “Mdomo mzito sana kujibu salamu Bibi wa SSP lakini iliyotuleta hapa si salamu yako utakijua tu” Madevu aliongea kwa mara nyingine kisha akaenda mahali ilipo sebule ya chakula, alirudi akiwa na kiti ambacho alikiweka jirani kabisa na eneo ambalo James alikuwa ameangukia baada ya kuingiliwa na hewa asiyoijua kwenye macho yake. Akiwa na tabasamu lilelile alimnyanyua mtoto huyu ambaye alikuwa amejigonga vya kutosha baada ya kusukumwa, amlishika kwa namna isiyopendeza kabisa na kisha akamuwekea mkono jirani na uso wake. Aliupitisha mkono mara mbili kwenye uso wake James, macho hayakupepepsa kuashiria alikuwa haoni. “Hongera sana jamaa ile gesi imefanya kazi sasa hawezi kumtambua yeyote yule kati yetu” Aliongea na kisha alimsukuma kwa nguvu hadi akajigonga kwenye kabati la vyombo akaanguka chini, yowe ya uchungu lilimtoka mama yake lakini aliwahiwa na kidole cha shahada kilichowekwa mkono kumuashiria akae kimya. Wakiwa wapo ndani ya nyumba hiyo mngurumo wa gari ulisikika na hatimaye ukavumia kwenye lango la kuingia ndani ya nyumba hiyo, wote walitambua mhusika aliyekuwa akiiingia eneo hilo hakuwa mwingine ila ni SSP Nkongo. Milio ya honi hapo getini ilisikika ambayo haikuwatia hofu watu wale waliokuwa wapo humo ndani, sekunde kadhaa lango kuu lilisikika likifunguliwa kisha gari hiyo iliingia hadi ndani. Wete humo ndani walisikiliza sauti hadi pale gari hiyo ilipoenda kuegesha na kuzimwa, milio ya viatu ya watu wengi si tu mmoja alisikika ikisogea kwenye eneo la barazani kwenye mlango. Haukupita muda mrefu mlango ulifunguliwa na, aliingia SSP Nkongo akiwa amefuatana na mtu ambaye alikuwa amevaa nguo za kifungwa akiwa amemuwekea bastola kisogoni. Alipoingia tu alifuatana na mwingine ambaye alikuwa amevaa nguo za kifungwa akiwa amesokota rasta, yeye naye alitulizwa chini kama ilivyo familia yake. Wavamiaji wale waliokuwa wapo humo ndani walitazama wote mlangoni, hiyo ilikuwa ni ishara kuwa walikuwa hawajatimia idadi yao kuna mwingine alikuwa akiingia. **** Umbali kutoka kule shamba alipokuwa amejenga ile nyumba hadi katikati ya mji, ulikuwa ni mkubwa ambao ungemgharimu kupoteza dakika nyingi njiani. SSP Nkongo aliamua kuongeza mwendo wa gari na hatimaye alikuwa amefika katikati ya jiji, dhumuni kubwa ilikuwa ni kwenda kituo cha kati kwenda kuchukua maaskari wa jeshi la polisi ili aongozane nao kwenda kumtia nguvuni ASP Lutonja. Alipokuwa yupo kwenye foleni katikati ya jiji ndiyo akakumbuka alikuwa amesahau kitu muhimu sana, silaha yake aliyokuwa akiitumia ndiyo alikumbuka alikuwa ameisahau. Aliamini kabisa angeongozana na maasakri hao kwenda kumkamata lakini isingewezakana kuwa mikono mitupu, silaha ilikuwa ina umuhimu wake. Mtuhumiwa akiwazidi nguvu maaskari basi silaha hiyo ingewaku na wajibu, hakutka kujiaminia kisa alikuwa ameongozana na Maaskari. Hakika aliona amefanya uzembe mkubwa sana kuisahau silaha pindi alipoingia nyumbani kwake alipotoka kazini, alifikia hatua ya kujitukana mwenyewe alipokuwa yupo humo garini kwenye foleni. Yale mazoea ambayo sasa amekuwa tabia kila ifikapo nyumbani ni kutoa silaha yake ndani ya gari na kuihamishia ndani, sasa yalikuwa yamemgharimu ndani ya siku hiyo muhimu. Alikuwa amezoea kutotoka tena aingiapo ndani ya nyuumba yake na sasa mazoea hayo yalikuwa yakimgharimu yeye mwenyewe, hakuwa na jinsi zaidi ya kugeuza gari kuiwahi silaha yake a bila ya kujua alikuwa akienda kulikabili balaa jingine kabisa lililokuwa likimgoja ndani kwake. Kutokana na uwepo wa foleni katika barabara za jijini aliweza kufika nyumbani kwake majira ya Saa moja ikiwa inaelekea saa mbili, huu ulikuwa ni muda ambao nyumbani kwake tayari kulikuwa kumevamiwa na yeye alikuwa hajui kuhusu hilo. Alipofika kwenye lango kuu la kuingilia nyumbani kwake kutokana na wahka aliokuwa nao, alipiga honi kwa fujo. Haikupita muda lango hilo lilifunguliwa huku mfunguaji akiwa hamuoni na wala hakujali kuhusu kumuona yeye alisogeza gari hadi kwenye maegesho na alishuka akiwa ni mwenye haraka. Kitendo cha kukanyaga mguu kwenye ardhi ya maegesho ya nyumbani kwake, kuliambatana na kukutana mdomo wa bastola. “Geuka nyuma na utulie hivyohivyo” Aliamriwa na mtu ambaye alikuwa amevaa sare za wafungwa, hakutaka kubisha aligeuka kama alivyo na kisha alikuja mtu mwingine ambaye alimpekua halafu akaamriwa aingie ndaani. Ndipo alipoingia ndani akakutana na familia yake ikiwa imewekwa chini, naye aliongezewa hapo chini na kuwekewa silaha. Muda huohuo vilisikika viatu vya mtu akikanyaga kwenye sakafu ya barazani kuashiria kuwa alikuwa akiingia ndani ya nyumba hiyo, wavamizi wale walitokwa na matabasamu waliposikia sauti hizo. Aliingia ndani ASP Lutonja akiwa amevaa nguo za kazi akionekana ni mwenye tabasamu pana, wale ambao walikuwa hawajui kabisa kuhusu upande wa pili wa afande huyu walionekana kutoamini kabisa kama angeweza kuwafanyia hivyo. “Elius unajidai mjanja sana, huu mtandao ni mpana wewe umeona sasa” ASP Lutonja aliongwa na kisha alijongea hadi pale alipo Madevu ambaye alikuwa amekaa kwenye kiti, alipishwa kwenye kiti hicho na kisha akaketi yeye. “Napenda utambue hivi kila sehemu tuna vibaraka wetu ili kuhakikisha usalama wetu, maaskari wote waliokuwa wamejua ukweli wetu sasa ni hivi ni marehemu. Ujinga wa maaskari hao walikuwa ni kuwaeleza wenzao kuwa walikuwa wanaenda kumuambia mkuu wako Mwambe, wamemwambia na alipokuja kukuambia wewe nilikuwa nina taarifa tayari na nilitega sikio kusikiliza kile chote mlichokuwa mkikiongea. Sasa hii ndiyo zawadi yako na wewe, huyo Mwambe namuacha hana madhara kabisa sasa hivi” ASP Lutonja aliongea huku akitabasamu kwa dharau. “Mwanaharamu mkubwa wewe” SSP Nkongo aliropoka akiwa hana uwezo wa kufanya chochote “Ndiyo na uanaharamu wangu ndiyo leo nimekuja kuuonesha kwako, najua umeandika faili kuhusu uchunguzi wako. Lipo wapi?” “Faili ninalo lakini siwezi kukupa hata ufanyeje” “Alaaaaah! We nunda siyo, Manywele mpe demo kwanza” ASP Lutonja alipotoa kauli hiyo yule mwenye nywele nyingi aliyekuwa na silaha alimpiga risasi ya kichwa mtoto wake wa kiume mkubwa akaondokwa na uhai papo hapo. “Noooooo! Fred my son” SSP Nkongo alishindwa kuvumilia akapaza sauti na machozi yakaanza kumtoka, mke wake naye ilikuwa ni hivyohivyo kutokana na uchungu wa kumpoteza mwana. “Elius usilete ubishi kumbuka umebakiwa na mtoto mmoja tu yule pale ambaye haoni,leta faili hilo” “Natoa! Natoa! Lipo kwenye gari” “Mpe ufunguo Bwana Nyapara akalilete upesi sana” Hakuleta ubishi alitoa ufunguo wa gari na kisha aliurusha mbele bado akiwa analia, Yule ambaye alikuwa amevaa nguo za kifungwa aliyesokota rasta aliuchukua na akatoka nje. Alirejea baada ya muda mfupi akiwa amebeba faili hilo ambalo lilikuwa limeambatanishwa na pingu, alimpa ASP Lutonja faili hilo. “Anhaaaaah! Naona ulijiandaa kabisa kuniweka nguvuni hadi na pingu ulikuwa nazo, lakini umeshachelewa tayari ndugu. Faili ninalo mkononi” “Faili unalo tayari naomba iache famili yangu bado nahitaji iendelee kuishi” “Ngamia akiweza kupita kwenye tundu la sindano ndiyo suala hilo litawezekana, leo nataka ushuhudie kwa macho yako ile mikanda ya wazungu isiyohitajika nchini katika uhalisia. Madevu chukua silaha ya Nyapara umuangalie huyu firauni” ASP Lutonja alipoongea maneno hayo yule Nyapra mmoja aliyekuwa amemtuliza SSP Nkongo alimpa silaha Madevu, baada ya hapo wale manyapara wawili walimchukua mke wa SSP Nongo na kumlaza chini kinguvu. Nguo zake zilichanwa mbele ya mume wake akiwa anashuhudia ambaye alitamani kuinamishwa kichwa chini lakini alilazimishwa kutazama, uchanwaji wa nguo na manyampara hao kulimwacha akiwa mtupu ndani ya muda mfupi tu. Mmoja alimshikilia na kisha mwingine alianza kumuinmgilia kinguvu katika njia zote mbili huku mume wake akishuhudiaa, aliporidhika alikuja kumkamata na kisha mwenzake akawa anamuingilia kinguvu vilevile hadi walipotosheka. Damu zilikuwa zimetapakaa kwenye eneo ambalo alikuwa akiingiliwa kutokana na kuingiliwa njia zisizo stahiki, alikuwa akilia kwa uchungu kutokana na maumivu aliyoyapata huku akiwa hana hata nguvu ya kusimama. “Nkongo umeona mkanda wa X huo natumai umekuburudisha” ASP Lutonja aliongea kwa kejeli.
Lilikuwa ni tukio ambalo halikuwa likifaa kabisa kuangaliwa na macho ya SSP Nkongo, mke wake ambaye alikuwa akimpenda. Aliyekuwa akimpa hadhi kama ya malkia ndani ya majira hayo alikuwa amedhalilishwa vya kutosha, mwanamke ambaye alimpenda na kumuheshimu alimuona akiwa amefanywa kama kahaba ambaye alikuwa amevamiwa na wahuni. Jambo lenye kuumiza ambalo hajawawahi kufanyiwa kwenye maisha yake, lilikuwa ni hilo kuliko yote mazito ambayo aliwahi kuyapitia. “Annaaaa!” Aliita jina la mke wake kwa uchungu sana lakini kelele zake hizo zilizua mengine kabisa, bastola ambayo ilikuwa ipo mikononi mwa Madevu ilikohoa baada ya ASP Lutonja kutoa ishara. Kichwa cha mke wake kilitobolewa kama ilivyofanya kwenye kichwa cha mtoto wake mkubwa Fred. Alilia sana huku akikumbuka jinsi ambavyo alikuwa akiishi na mke wake huyo, upendo wote alioneshewa na mke wake hapo ndiyo ulikuwa ukipita kama mkanda wa sinema kwenye kichwa chake. Alitamania hata tukio lile liwe halijatokea aweze kuwa na mke wake, lakini lilikuwa ni jambo ambalo haliwezekani kwani lilikuwa limetokea tayari. Alilia kama mtoto mdogo na kusababisha hadi James ambaye alikuwa amebaki peke yake naye alie kutokana na kilio cha baba yake, kilio hicho cha mtoto wake mmoja tu aliyekuwa amebakia kilimfanya geuze uso kumtazama mtoto huyo. Kitendo cha kumuona tu mtoto wake akiwa ni mwenye kupapasa kilizidi kumtia uchungu,kujigonga kwa mtoto wake kwenye sehemu mbalimbali kulifanya aone kama alikuwa akijingonga yeye. Hakukuwa na msaada mwingine ambao ungeweza kumsaidia, kilio ndiyo ulikuwa msaada wake kwa muda huo aliokuwa amefikwa na makuu zaidi kwenye maisha yake. “Vipi Nyapara mmeupenda na mzigo huo nini, mkiutaka ni juu yenu tu” ASP Lutonja aliongea maneno hayo huku akiwatazama wale wafungwa wenye vyeo gerezani. Ilikuwa ni jambo la neema sana kwa Wanyapara hao na hawakutaka kupoteza muda, kwa kasi ya jabu walimuendea SSP Nkongo wakiwa a lengo moja tu ndani ya vichwa vyao. Ilikuwa ni kumuingili na si kitu kingine, walipomfikia walitaka kumkamata kwa nguvu na hapo walikutana na sekeseke jingine kabisa. SSP Nkongo hakuwa akitaka kabisa kufanyiwa kitu hicho, alikuwa yupo radhi afe lakini si kuingiliwa na wafungwa wale walio na uchu kutokana na kukaa gerezani. Mmojwapo alipomgusa tu alimzoa akanguka chini kisha akajifyatua na kusimama wima, wa pili alipomfuata alimuachia masumbwi ya maana yakampeleka chini. Alipotaka kumfuata kulekule chini alipokuwa ameanguka alipigwa risasi ya mgongo, bado hakutaka kukata taama kwa kupigwa risasi hiyo aliamua kujirusha na kumfuta hukohuko. Aliitwa shingo ya Nyapara na kumkaba kwa nguvu zake zote, wale waliokuwa wana silaha walikuwa wakifanya kazi ya kupiga risasi za mabega lakini mikono hiyo haikutoka . Nyapara alikuwa akitapatapa huku akirusha miguu kutokana na kukabwa huko, waliendelea kumpiga risasi mbalimbali kwenye viungo vyake ili aachie lakini ni kama vilikuwa si viungo vyake. Hakuachia kabisa hadi pale Nyapara aliposhiwa nguvu kabisa akawa haleti fujo kabisa, Nyapara mwingine alisogelea karibu akajaribu kumtoa mwenzake lakini alikutana na mikono imara zaidi ya chuma.
Kitendo cha Nyapara yule Marasta kusogea karibu kujaribu kumtoa mwenzake, wale wenye silaha wakaacha wote kutumia silaha zao. Hapo ndipo walipokuwa wamehalalisha kifo chake kwenye mikono ya SSP Nkongo ambaye alikuwa akitokwa damu sehemu mbalimbali, mwenzake akiwa anavutana naye ndiyo muda ambao Nyapara yule alikata roho akiwa yupo kwenye mikono ya adui yao. Mikono ilipokuja kulegea na kufanikiwa kumtoa, waliopoa mwili ambao haukuwa na uhai tofauti na kutarajia kuwa wangeopoa mwili wenye uhai. Hilo liliwatia hasira sana na wakamiminia risasi sehemu mbalimbali za mwili SSP Nkongo, mwili wake ulipoingiliwa na risasi hizo ulikuwa ukifanya kazi ya kuhaha kuhakikisha uhai hauondoki. Uhahaji huo wa kubaki na uhai haukufanikiwa kutokana na uhai kuwa na nguvu ya kutoka kuliko kubaki ndani ya mwili, SSP Nkongo aliaga dunia bila ya kutamka neno lolote na shingo yake iliangukia upande. Macho yake yalikuwa yakimtoka kuelekea eneo ambalo alikuwa amelala James, huo ndiyo ulikuwa mwisho wa Askari mzalendo ambaye aliondoka sambamba na watu wake muhimu wawili akimuacha mmoja hana msaada. “Vipi ASP tummalize na huyu mtoto?” Madevu aliuliza “Aaargh! Achana naye huyu, hajaona chochote na wala hajui kuhusu chochote kuhusu sisi. Tuondokeni haraka eneo hili, we Nyaparra beba mwenzio tutaenda kutengeneza kifo chake gerezani” ASP Lutonja aliongea na kisha alianza kupiga hatua kuelekea nje ya nyumba hiyo, wenzake walifuata nyuma kutoka nje.
**** Matukio yote yaliyokuwa yakitokea James hakuwa akiyaona kwa ufasaha kutokana na gesi ya sumu aliyokuwa amepulizwa kwenye macho yake. Gesi hiyo haikuwa imemuathiri sehemu kubwa ya macho yake kiasi cha kumfanya kutoona kabisa, alikuwa akiona maumbile ya watu pamoja na ukungu mwingi sana. Sauti zote zilizokuwa zikitoke alikuwa akizisikia barabara, aliweza kushuhudia maumbile ya watu hao yakifanya unyama pamoja na kelele nyingi ambazo zilikuwa zikitoka kwa wazazi wake. Nguo za rangi ya machungwa pamoja na sare za kazi alizovaa ASP Lutonja, aliziiona rangi yake lakini hakuweza kuwatambua wavaaji wake walikuwa ni kina nani, Kunyanyaswa na wale wavamizi napo kulinyima kabisa wasaa wa kuweza kusimama. Alikuwa akilia kwa uchungu katika muda ambao wavamizi hao walikuwa wakitenda unyama hadi wanaondoka, kelele za wazazi hadi zinatulia alikuwa akiendana nazo kwa kilio cha uchungu. Pamoja na kuwa bado alikuwa hajapevuka na alikuwa akielekea umri wa kupevuka, hakuwa na akili ya kitoto kiasi cha kutotambua kilichokuwa kikiendelea eneo hilo kilikuwa ni nini. Wavamizi walipotoa miguu yao na kutokomea kusikojulikana, tayari alikuwa amejua hakuwa na ndugu yeyote ambaye alikuwa amebakia hai. Hilo lilimfanya aendelee kulia kimyakimya kutokana na sauti kumkauka kwa kulia muda mrefu, nguvu nazo kwenye mwili wake zilimuishia taratibu kila alipozidi kulia na mwishowe alipoteza fahamu na hakujua kitu gani kilichokuwa kikiendelea. Alikuja kuamka katika majira ambayo hakuyajuakabisa, alipofungua macho yake aliona giza tu na hakuwa na uwezo wa kuona kabisa. Alipiga kelele kwa nguvu huku akiwaita wazazi wake, kelele hizo ziliambatana na sauti za kuhimizwa Msichna aende kumtuliza asifanye fujo. Akiwa hajui kinachoendelea alijikuta akilishikiliwa kwa nguvu sana, alihisi kukamatwa na mikono laini ya kike ambayo ilikuwa imemshinda nguvu alizonazo. Mikono hiyo ilipokuja kumuachia taratibu alipungukiwa nguvu na kisha aliiingiwa na usingizi wa ghafla ambao hakuutarajia kma uneweza kumpata. **** Zilipita siku tatu ndani ya nchi nzima habari iliyokuwa imetawala ilikuwa ni kifo cha SSP Nkongo pamoja na mke wake ambaye liingiliwa kabla ya kuuliwa. Ilikuwa ni habari ya simanzi sana kwa watu waliokuwa wakimpenda afisa huyu wa jeshi la Magereza ambaye alikuwa amejizolea sifa lukuki, kifo chake hicho kilipelekea hata wale ambao walikuwa hawamjui kuanza kumfuatilia. Wengi walipobaini utendaji wake wa kazi pamoja na pongezi nyingi ambazo alikuwa amepatiwa na Mheshimiwa Rais walihuzunika sana, majira ya jioni ya siku hiyo habari zikiwa zimesambaa kuliibuka kwa msiba mwingine mzito sana ambao uliwafanya watu wabaki na hurum sana kwa kizazi cha Mzee Nkongo. Mama yake Mzazi SSP Nkongo naye aliaga dunia kwa shinikizo la damu ambalo lilichangiwa na kifo cha mtoto wake, ilikuwa ni misiba minne iliyokuwa ipo nyumbani kwa Mzee Nkongo Tanga. Siku iliyofuata mazishi yaliyohudhuriwa na watu wengi sana yalifanyika kwenye Makaburi ya Bombo, watu waliokuwa wakitoka kwenye mikoa tofuti walikuja kuhudhuria kwenye mazishi hayo ya Afande Mzalendo. Viongozi mbalimbali wa kiserikali nao walikuwa wapo kwenye mazishi hayo kuifariji famili ya wafiwa ambayo ilikuwa imebaki Babu na Mjukuu tu. ambao walikuwa hawana muangalizi yeyote. Ilikuwa imepita miaka mingi sana Mzee Nkongo hakuwa ameenda nyumbani kwao, umri huo alikuwa ameshasahau ndugu zake wote waliokuwa wapo huko kwa Kagera kutokana kulowea Tanga tangu apangiwe ajira huko. Hivyo ndugu waliokuwa karibu yake walikuwa ni yeye, mjukuu wake pamoja na familia ya mkewe ambao walikuwa wenyeji wa mkoa huo. Mazishi ya SSP Nkongo yalihudhuriwa hata wakuu mbalimbali wa majeshi nchini wakiongozwa na Amiri jeshi mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Marehemu wote wanne walipumzishwa kwenye nyumba zao za milele ndani ya siku hiyo, mazishi yalipokalimika watu wote walitawanyika na wachache wakaja kuifarijia familia ya Marehemu. **** Siku ilishia hatimaye ikaingia siku ya pili na hadi ikaingia juma, nalo halikukaa na hatimaye likaja la pili yake hadi ukatimia mwenzi. Taratibu watanzania walianza kusahau kuhusu tukio hilo ambalo lilikuwa limemkuta kijana mdogo James ikimuacha akiwa hna wazazi, alikuwa akilelewa na babu yake Mzee Nkongo huku Inspekta Mwambe akiwa anakuja kumuona siku moja moja. Upofu ndiyo ulikuwa ni maisha yake kutokana na dawa aliyokuwa amewekewa na wavamizi wa nyumbani, unyonge ndiyo ulikuwa rafiki yake mkubwa ingawa alikuwa na rafiki mkubwa sana ambaye alikuwa akimchekesha kila siku. Ucheshi wa marehemu baba yake hata babu yake alikuwa nao na ndiyo huo alikuwa akiutumia kumchekesha lakini haikusaidia kitu katika kumuweka kuwa ni mwenye furaha. Bado aliendelea kuwa yu mwenye huzuni uliokuwa umezidishwa na kutokuwa na uwezo wa kuona ilihali alizaliwa akiwa anaona. Ahadi za kumsaidia ambazo zilikuwa zimetolewa na viongozi wa juu wa kiserikali zikaungwa mkono na wananchi zilikuwa zimeyeyuka tayari, msaada wowote haukuja nyumbani hapo. Mzee Nkongo alizidi kuilaani serikali hiyo na akawa akiishi na Mjukuu kwa shida sana, pamoja na na shida hizo bado alimpenda sana James na alimona ni Elius wake wa pili baada ya kwanza kufariki. Alikuwa akihisi bado alikuwa ana huzuni kila akitazama hali ya Mjukuu wake ambaye ilikuwa ni yenye kusikitisha, alikuwa ni mwenye kupelekwa chooni na hata kufanyiwa huduma zingine muhimu katika maisha yake kutokana na kutojiweza. Mzee Nkongo aliendelea kutaabika naye na hakutaka kuona msaada wa yeyote zaidi ya Inspekta Mwambe ambaye alijitolea kuwasaidia tangu siku ya kwanza, wengine ambao walikuwa wakiahidi kumsaidia alikuwa akiwaona wanafiki. Hakuwa akiacha kuilaani serikali ambayo alikuwa ameifanyia kwa miaka mingi hadi anastaafu, ambayo pia mwanae aliitumikia kwa moyo wote hadi anafikwa umauti. Aliona kuwa hayo ndiyo yalikuwa malipo ya hiyo serikali katika kujituma kwake kwenye ajira, moyoni msemo wa fahila za punda ni mateke haukuwa ukimtoka kwa hayo aliyofanyiwa. Mwaka mmoja baadaye ilikuwa ni pigo ingine kwa James katika maisha yake, Mzee Nkongo ambaye alikuwa msaada kwake naye hakukaa muda mrefu Mungu akamchukua akabaki akiwa peke yake. Taarifa za kifo cha Mzee Nkongo zilimfikia Inspekta Mwambe akiwa yu mgonjwa na hata alipokuja kupona na kwenda nyumbani kwa Mzee huyo, alipewa taarifa ya kucukuliwa James na ASP Lutonja ambaye alikuwa ameahidi kumlea. Hiyo ilikuwa ni taarifa mbaya ambayo inasikitisha sana kwake, alimuonea huruma sana mtoto yule ambaye alikuwa ametelekezwa na ndugu wa mama yake baada ya kubaki yatima. Sasa alikuwa ameangukia kwenye mikono ya mtu ambaye alikuwa akihisi kabisa hakuwa mtu sahihi, aliumia sana lakini hakuwa na nguvu ya kuzuia hilo kwani hakuwa na nguvu ya kupinga hilo kutokana na kuwa mdogo kicheo na wala haikuwahi kujulikana kama alikuwa na urafiki mkubwa na Marehemu baba yake. **** Maisha ndani ya nyumba ya ASP Lutonja yalianza kwa furaha kabisa, alianza kupata faraja kwa kuwa pmoja na mtu ambaye alikuwa akikaribiana naye rika. Malezi mazuri aliyokuwa nayo kwa Mke wa ASP Lutonja alianza kuona kama alikuwa akilelewa na mama yake, aliishia akiwa ni mwenye kuhudumiwa kwa kila kitu huku akipewa kila hitaji muhimu na rafiki wa Marehemu baba yake ambaye sauti yake hakuwa akiipenda kusikia. Kila akiisikia sauti yake alikuwa ni mwenye kukereka lakini upendo aliokuwa akipewa ulimuondolea kero yote ambayo alikuwa nayo kwa kusikia sauti hiyo, alipata raha ya maisha ile ambayo aliikosa kwa kundokewa na wazazi wake. Upendo wa kinafiki aliokuwa akioneshwa na ASP Lutonja haukudumu kwa muda mrefu, muda huo hakujua kabisa kuwa alikuwa akisukiwa mpango wa kuweza kumuondoa ndani ya nyumba hiyo ili aonekane hafai. Jambo jingine alikuwa halitambua ni shinikizo la mama mwenye nyumba hiyo aliyekuwa akimpenda kwa dhati, huyo ndiyo chanzo cha yeye kuletwa ndani hapo. Pamoja na mwenye nyumba hiyo kudanganya vya kutosha kuwa alikuwa akiletewa msaada kipindi alichokuwa yupo kwa babu yake ili asiletwe hapo, hakuweza kushawishi kabisa kuzuia kuletwa hapo baada ya kufariki kwa Mzee Nkongo. Alikuwa akikereka kila anapomuona ndipo siku moja akamua kumfanyia hila, alikula njama na mfanyazi wa nyumba hiyo kumpakazia hila mbaya James. Akiwa hana hili wala lile siku ya siku ulipotimia muda wa kulala akiwa ni mwenye kuongozwa kutokana na kutoona, alipelekwa chumbani kwa Jane mtoto wa kike pekee wa familia ya ASP Lutonja. Hakuwa akijua muundo wa vyumba ndani ya nyumba hiyo ulivyo yeye alipandishwa kitandani na kulala moja kwa moja katika kitanda kisicho chake, kutokana na kulala vibaya kwa Jane pia ambaye alikuw akichipukia yule Msaidizi wa kazi alitoa nguo zote na kisha akamvizia James akiwa tayari ameshalala kumtoa nguo pia. James alilala akijina yu huru kitandani alipozeoa kulala pasipo kujua mpango uliokuwa umesukwa, usingizi wake ulikuja kukatika baada ya kusikia kitu chenye ugumu kikitua kwenye mwili wake. Alipatwa na maumivu makali lakini hakuwa na wa kumsikiliza, bado aliendelea kushushiwa kipigo tu. Ugumu wa kitu ambacho kilikuwa kikitua mwilini mwake kwa nguvu, hakujua ulikuwa ni mkanda wa kijeshi ambao ulikuwa umeshikiliwa na ASP Lutonja. “Mamaaaa!” Alilia kwa uchungu sana “Baradhuri wewe umfuate huko kaburini kukuzaa kiumbe chenye laana kama wewe, yaani kukusaidia kote unadiriki kuja kumlala mwanangu wewe mtoto” Ilikuwa ni sauti ya Mke ASP Lutonja ikiambatana na kipigo alichokuwa kikishusha mume wake. Masikini ya Mungu James hakuwa akiona na wala hakujua ni wapi akimbilie alipokuwa amekaa hapo kitandani, alipojaribu kusogea pembeni kutokana na kuumizwa sana na mkanda huo. Loh! Alianguka chini kama mzigo kutoka kwenye kitanda, huko kulimfanya apigwe kama mtu mzima na kuongezewa mateke, ASP Lutonja alimpiga bila hata ya kujali kuwa nafsi yake ilikuwa ikimsuta kwa hila aliyokuwa amempakazia
Nani ambaye angekuwa ni mtetezi kwenye siku hiyo ngumu ilihali wale waliokuwa wakiujua ukweli walikuwa wakitaka kumuona akiendelea kupata tabu, hakuna na msaada katika hali hiyo ya upofu ambao alikuwa nao. Kilio tu ndiyo ulikuwa msaada wake hakujua ni wapi pa kukimbilia, pande zote zilikuwa ni giza kwake na hakuona pa kwenda zaidi ya kulala chini hapo alipokuwa amelala bila ya kuwa na nguo huku akiendelea kupigwa kwa nguvu . Mkanda mgumu ambao alikuwa akipigwa nao ulianza kuleta athari kwenye mwili wake, haikupita muda alianza kusikia maumivu zadi kutokana na kuchanika sehemu mbalimbali za mwili wake. Bado ASP Lutonja hakuonesha dalili ya kusitisha kumpiga, alipokuwa akisogea uapnde ambao mkanda ulikuwa haufiki basi alionja teka la nguvu. Kipigo kizito cha mtu mzima kilidumu kwa muda mrefu na hakikuonekana dalili ya kutulia.
Baada ya muda mrefu wa maumivu ya sehemu mbalimbali za mwili wake, hatimaye James alipoteza fahamu akiwa bado anaendelea kupigwa. Aliendelea kupigwa hadi pale alipogeuka kama guni katikati ya kipigo ndipo mpigaji akajua kuwa alikuwa amesababisha mengine. “Mungu wangu Baba jane hujaua kweli mtoto wa watu huyu?” Mke wa ASP Lutonja aliuliza kwa wasiwasi mkubwa, alipelekea mumewe asogee hadi karibu ya James na kumchunguza. “Kazimia huyu mke wangu, hebu leteni nguo zake” ASP Lutonja alitoa amri baada ya kuto uhibitisho wa hali ya James. Haraka sana nguo hizo zililetwa kwani zilikuwa zipo humohumo ndani, alimvalisha nguo hizo na kisha alichukua fimbo ambayo James alizoeleka kuitumia katika upofu wake. Alimnyanyua na hakutaka kabisa kusikiliza neno la mwingine, alipomuweka begani vizuri alimtazama mke wake.
Naenda kumtupa jalalani akiamka ajikute hukohuko, hatuwezi kukaa na mtoto firauni kama huyo” Aliongea na hakukuwa na mtu yeyote aliyepinga suala lile. Alitoka naye hadi nje lilipo gari lake na kisha akamuweka sehemu ya mizigo, aliliondoa gari hilo kwa kasi sana akikata mitaa mbalimbali. Safari yake ilikuja kuishia kwenye eneo la kutupa uchafu ambayo lilikuwa lipo mbali kidogo na makazi ya watu, hapo alifungua sehemu ya kuwekea mizigo ya gari lake na akamtoa James halafu akamtupa kwenye eneo lenye uchafu mwingi sana. Alipohakikisha hakuwa ameonekana na mtu yeyote aliingia garini na kupotea kwenye eneo hilo, moyoni alishukuru sana kwa kuodokewa na kiumbe ambacho hakuwa akikitaka kukiona katika maisha yake. Aliona atakuwa huru sana na si kila siku kutazama sura ambayo alihisi ilikuwa imemgundua kuwa yeye ndiyo Mhusika mkuu wa mauaji, sasa aliona mke wake atakuwa ametulia na kuacha na tabia yake kukazania watoto ambao hawakuwazaa.
James alipokuja kuzinduka bado alijikuta akiwa yupo jalalani akiwa na maumivu sehemu mbalimbali za mwili, aliijua kwa tabu aa kajaribu kupiga hatua kuelekea mahali ambapo hakuwa akipajua. Loh sallaleh! Upande ule ambao alikuwa akielekea kulikuwa na mteremko mkali sana ambao ulikuwa umejaa uchafu mwingi,kutokana na kutoona alijikuta akiporomoka huko yeye na fimbo yake. Alibiringita kwenye kifusi cha uchafu huku akilia kwa uchungu akitaja majina ya wazazi wake, alikuja kutua kwenye kitu kigumu sana ambacho hakukielewa kilikuwa ni nini. Maumivu yalimpta zaidi na kitu hicho kigumu alichokuwa ameangukia kilimpigiza karuka juu na katua upande wa pili akaendela kubiringita, hakuwa akiona alikuwa akielekea wapi ndani ya rundo hilo la uchafu zaidi ya kuvaana na kila aina uchafu ambao ulimbadilisha harufu na kunukia harufu inayotoka hapo.
Kubiringita huko hatimaye alikuja kuingia sehemu ambayo ailikuwa ina maji, alihisi kupelekewa na maji hayo yaliyokuwa na nguvu. Alipojaribu kujizuia hakuweza na hata ile fimbo aliyokuwa nao ilimtoka mkononi, alipiga kelele sana alipokuwa akipelekwa na maji hayo kwa nguvu lakini hakukuwa na aliyekuwa akimsikiliza. Ilikuwa ni kipindi ambacho mito ilikuwa imejaa kutokana na mvua zilizoanza kunyesha mikoani, ndiyo maana maji hayo yalikuwa na nguvu sana kutokana na kuwa mengi kupita kiasi. Alikuja kupelekekwa na maji hovyo na hatimaye alikuja kujigonga kwenye kitu kigumu kichwani, fahamu zilimtoka baada ya kujigonga kwenye hapo huku akianza kusikia kelele kwa mbali za watu.
**** Harakati za kumfuatilia James akiwa yupo nyumbani kwa mkuu ndiyo ziliendelea, alipopata uhakika alikuwa akipendwa sana na familia hiyo na alikuwa akionekana kama mmoja wa familia ile. Inspekta Mwambe aliamua kuacha kumfuatilia kwani aliona alikuwa yupo kwenye mikono salama, mara chache alizokuwa akikutana nao mjini wakiwa wapo pamoja naye na wakifurahia naye. Zilitosha kumpa uhakika alikuwa yupo mahali salama, kunawiri kwa James nako kulizidi kumdanganya akaaacha hata kumfuatilia. Muda alioacha kumfuatili ndiyo muda ambao Jmaes alikuwa akikaribia kukumbwa na dhahama, alipokuja kukumbwa na dhahama hakujua kabisa hadi pale alipokuja kusikia kwa majirani kuhusu kufukuzwa kwake.
Sababu ya kutaka kumuingilia binti wa pekee wa familia bado ilikuwa haingii akilini kake kutokana na hali aliyokuwa nayo, James huyu ambaye hata chooni alikuwa akipelekwa ni jambo ambalo haliingii akilini mwake kabisa. Siku hiyohiyo alianza kumtafuta asijue alikuwa ameenda wapi kutokana na wingi wa watu ndani ya jiji hili,, alihangika sana katika kumtafuta lakini hakupata hata fununu juu ya mahali ambapo James alikuwepo. Majukumu ya kazi ya siku nzima nayo yalimfanya hata azidi kupata tabu katika kuutmia muda wake vizuri, alipotoka kazini napo mazi ilikuwa ni hiyohiyo ya kumtafuta lakini hadi giza linaingia hakuwa amefanikiwa.
**** James alikuja kurejewa na fahamu zake kwa kuhisi ugumu uliokuwa umeukumba mgongo wake kutokana na sehemu aliyokuwa amelala, alipoinua kichwa chake na akajaribu kufungua macho yake huenda atabapata bahati ya kuona. Alikutana na giza zito kuashiria kuwa alikuwa bado yu katika upofu, akiwa katika hali hiyo alisikia sauti ya Mwanamama akiimba nyimbo zaa kikabila akiwa yupo umbali fupi kutoka hapo alipo. Kusikia sauti hiyo ngeni kulimfanya ahisi hakuwa kwenye mazingira salama, aliinuka kwa haraka sana lakini aliwahiwa kukamatwa kisha alisikia sauti ya Mzee ambayo ilimmshawishi kukaa chini. Alipokaa chini taratibu alianza kupapasa akiwa ni mwenye kutafuta kitu, hali hiyo iliwafanya wenyeji wake ambao walikuwa wnamtazama wasikitike. Walikuwa wameshajua kuwa huyo mtoto alikuwa ni kipofu, Mzee huyo kabisa ndiyo aliiingiwa na moyo wa huruma huku akimtazama jinsi alivyokuwa akihangika. “Unatafuta nini?” Aliulizwa “Fimbo yangu ipo wapi? Nitatembea vipi?” Aliuliza maswali mfululizo “Mbona hukuwa na fimbo kabisa mwanangu” Mzee alimuambiwa “Kwanza mbona siwajui nyinyi kina nani?” “Sisi ni wasamriawema tu, tumekuokota hapo bondeni Darajani ulipelekwwa na maji ukajigonga kwenye ukingo wa daraja” Maneno hayo yalimfanya James aanze kulia baada ya kumbukumbu kumrudia “Hapana usilie kwani kuna nini kimetokea” “Sijui nimekosa nini jamani? Baba na Mama mnaniacha, nateseka hadi nasingiziwa kubaka. Kipofu kama mimi nitaanzaje wakati hata sioni hata kitu” “Kijana umepatwa na nini?” Alipoulizwa swlai hilo ndiyo alipoanza kusimulia kila kitu juu ya kilichomtokea hadi inafika siku hiyo, Mzee huyo kila kitu kuhusu familia ya James alikikumbuka na hata sura ya kijana huyo ikamjia kwa mara ya mwsiho kumuona kwenye magazeti.
“Mungu wangu kumbe wewe ndiyo mtoto wa Nkongo yule aliyeuawa” Mwanamama aliyekuwa akipika alipayuka kwa nguvu.
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa James kukaa na wazee hao kwenye nyumba yao iliyochoka, alilelelwa kama mtoto wa hapo akiwa mwenye kupewa upendo. Alijihisi amani moyoni mwake ingawa hakuwa kwenye mazingira yaliyokuwa mazuri. Alikuwa ni mwenye kufuatana na Mwanamama ambaye alitokea kuwa mlezi wake mkubwa kwenye shughuli mbalimbali, alimpenda Mmwanamama huyo kama mama yake kutokana na jinsi alivyokuwa akimpenda. Chakula alicholishwa na mikono ya Mwanamama huyo ingawa hakikuwa kizuri kwake aliona ni chenye kufaa kuliko kula kile kizuri kwenye mazingira hatarishi. Adabu aliyokuwa nayo taratibu alianza kupendwa na watu mbalimbali, uzuri wa sura ambao ulikuwa umepotea kutokana na wingi wa makovu nao ulirudi na kumfanya aonekane kijana mwenye kuvutia. Kipindi hicho alikuwa tayari ameshapevuka na akawa ni mwenye mvuto zaidi, upofu wake ukawa si sababu ya yeye kuanza kuvutia wasichana wa huko Uswahilini alipokuwa akielelewa. Pamoja na hyo yule Mwanamama bado alikuwa yu imara kumlinda, alimpenda kama mwanae.
**** Mwangaza katika maisha ya James ulianza kuonekana kwa hatua ndogo kabisa, kufikia hatua ya kuwa mwenye kujihisi na amani ndiyo ulikuwa hatua ya awali ya mwangaza kwenye maisha ya James. Hatua ya pili ilikuja kuonekana ilikuwa ni baada ya majuma kadhaa, siku akiwa yupo pamoja na Yule mwanamama kwenye biashara yake pikipiki aina ya boxer iliegeshwa kando. Alishuka mtu mzima ambaye alisogea hadi kwenye kibanda cha matunda iliyokuwa ni biashara yao, alikuwa ni mnadhifu ambaye alionekana kabisa alikuwa na nia ya dhati ya kununua matunda. “Matikiti bei gani? Haaaah! James?” Aliuliza huyo mtu kuhusu matikiti maji lakini alishtuliwa na kumuona James.
“We nani?” James aliuliza aliposikia jina lake likiitwa. “Anko Mwambe mimi” Aliongea mtu huyo ambaye hakuwa mwingine ila ni Inspekta Mwambe. “Baba Mwambe” James alimtamka kisha akasimama akiwa na lengo la kumkimbilia Inspekta Mwambe asijue ni wapi alipo. “James tulia kwanza utaumia, Anko hivi huyu unafahamiana naye kivipi? Mwanamama yule aliuliza huku akimshika James mkono. Ilibidi Inspekta Mwambe aeleze na kisha james naye akaeleza, hapo ndipo aliporuhusiwa kwenda kwake. Baada ya hapo Yule Mwanamam alifunga kibanda chake na kisha aliongozana na Inspekta Mwambe hadi nyumbani anapoishi, huko walikutana na mume wake ambaye walimueleza kila kitu. Ilikuwa ni katika siku ambayo walikuwa wakikubali kutenganishwa na James waliyekuwa wamemzoea lakini hawakutaka kumuacha kirahisi, walihitajia kujua kuhusu usalama wake kutokana na mazingira aliyopelekwa akateseka. Ilikuwa ni zamu ya Inspetka Mwambe kuwaelewa uhakika wa usalama wake, katika muda huu ndipo alipotumia wasaa kumueleza kuwa nyumba yao waliyokuwa wakiishi tayari imeuzwa na watu wasiojulikana huku tuhuma nyingi zikienda kwenye familia ya mama yake mzazi, aliwaleza pia uwepo wa nyumba moja ambayo ilikuwa imebakia. Hii ilikuwa ni ile nyumba ya kule shamba ambayo Marehemu SSP Nkongo alikuwa akiitumia kupanga mikakati yake. Hapo wote walikuja kubaini kuwa baba yake kabla hajafikwa na umauti akiwa njiani kuufuta huo umauti, alikuwa tayari maeshampa taarifa ya uwepo wa nyumba ile kitahadahari. Yeye ndiye aliyeaminiwa akaambiwa kukitokea la kutokea basi ushahidi upo kule na funguo ya kule alielekezwa mahali ilipo. Inspekta Mwambe alitumia wasaa nuo kuwaeleza ile ndiyo nyumba pekee iliyobaki na haijulikani na yeyote.
Pamoja na maelezo hayo bado hawakutaka kumuachia James kirahisi nmna hiyo, iliwabidi waongozane hadi huko shamba kwenda kuishuhudia nyumba hiyo. Huko walifika na kuiona nyummba hiyo ya kisasa ambayo ilikuwa imesalimika. Hapo waliridhia kumuachia James lakini walipewa ombi. Waliombwa wamtunze hapohapo watalipwa chochote na humo watakuwa wanaishi, hilo ombi lilipita. Kuanzia siku hiyo wakaanza kuishi ndani ya nyumba hiyo yenye kila kitu wakimtunza James, uswahilinmi walipasahau kabisa na hapo ndiyo yakawa makazi yao.
Majuma kadhaa baadaye tatizo lile la kutoona iliwabidi kwenda kwa Daktari, gharama zote zilisimamiwa na Inspekta Mwambe. uchunguzi wa kitabibu ulionesha tatizo hilo lilikuwa likibika kabisa na huo ndiyo ukawa mwanzo wa furaha kwanza, miezi kadhaaa mbele James alitibiwa tatizo lake la kuona. Alifurahi sana kurudi kwenye ulimwengo waliokuwa wakiona kwa mara ya pili, malezi yote aliyokuwa akipewa na wale waliomuokota yalikuwa yamefikia tamati lakini hakuruhusu waondoke na hao aliwaheshimu kama wazazi wake wa hiyari. Inspekta Mwambe alikuwa akija kuwaona kila siku akiwa na nguo za kiraia na walikuwa wakikaa naye kwa furaha sana, siku moja aliamua kuja na nguo zake za kazi na ilikuwa ni mara ya kwanza kwake kuvaa nguo hizo James akiwa yu anaona. Siku hiyo maelewano hayakuwepo kabisa. Ulizuka mtafaruku isieleweke chanzo kilikuwa ni nini, hawakuelewana kabisa na hadi alipooondoka. Alipokuja siku inayofuata akiwa na nguo za kraia walielewana vizuri tu na hakukuwa na mkwaruzano. Hili ilimfanya aanze kumchunguza kwa ukaribu ilitokana na nini, alipogundua chanzo ilikuwa ni vazi lake ilibidi apelekwe kwa mataalamu wa Saikolojia ndipo hapo walipobaini kuwa alikuwa akikumbuka tukio la kuuawa kwa wazazi wake na kaka yake. Tiba ya ushauri kutoka kwa mtaalam huyo wa Saikolojia aliipata na hatimaye alirudi kwenye hali ya kawaida ambayo ilisaidia hata asiwe na hasira kila anapoiona nguo ya kazi ya Mlezi wake mkuu. furaha iliendelea huku ASP Lutonja akiwa hajui lolote kwa mtoto wa mwenzake ambaye alikuwa amemfanyia hila akampiga na kumfukuza kwake. Mwaka uliofuata James alianzishwa kidato cha kwanza katika shule ya bweni , ilikuwa ni furaha kwake kwa kurudi kwenye mazinmgira ya kielimu tangu alipoikacha shue akiwa darasa la saba. Aliendekeza nguvu zake katika usomaji na alikuwa ni mwenye bidii huku akikumbuka kuwa alikuwa akihitajika kuyajenga maisha yake mwenyewe, tabia ya baba yake ya ucheshi ambayo alikuwa ameirithi ndiyo illirudi akiwa yupo ndani ya shule.
Ucheshi wake huo ulimfanya kutokea kuwa kipenzi cha watu ndani ya shue hiyo, si wasichana wala wavulana ndani ya shule wote walikuwa wakipenda kukaa karibu naye kutokana na ucheshi aliyokuwa nao. Moyo wake wa kusaidia mwanafunzi mwenzake yeyote atakayepatwa na matatizo nao ulimfanya azidi kupendwa, shule nzima jina lake ilikuwa midomoni mwa watu akiwa tu kidato cha kwanza. Upande wa walimu napo alitokea kujizolea umaarufu mkubwa sana akawa akipendwa na kila mwalimu, utiifu wake ndiyo ilikuwa chanzo cha kupendwa na walimu hao ndani ya shule aliyokuwa akisoma. Mwaka unaofuata wa kidato cha pili ulikuwa ni mwaka ambao ulitosha kabisa kushawishi walimua na hawa wanafunzi kumpatia uongozi James, uchaguzi mkuu wa serikali ya wanafunzi ndani ya shule hiyo ulipofanyia. Alipata uongozi wa kawaida na hapo ndipo alipozidi kujizolea umaarufu, bado hakuacha bidii yake ya masomo pamoja na umaarufu huo aliokuaw aamejizolea shuleni. Alikuwa amebeba sifa ambazo alikuwa nazo marehemu baba yake kipindi akiwa shule, ubond ndiyo kitu pekee ambacho hakuwa amebeba kwenye sifa alizokuwa nazo baba yake. Jina la James lilikuwa ni mithili ya mate kwenye vinywa vya wanafunzi kwa jinsi lilivyokuwa limekaa kwenye vinywa vyao, pamoja na kuwa ni mwenye madaraka makubwa sana ndani ya shule aliyokuwa akisoma. Bado hakuwa mtu mwenye kujikweza sana, alijona yu mwanafunzi kama wanafunzi wengine. Mwaka wa pili uliisha akiwa ni mwenye sifa kedekede ndani ya shule yao, ulipoingia mwaka wa tatu akiwa yu kidato cha tatu uchaguzi wa serikali ya wanafunzi ulifanyika kwa mara nyingine tena. Shinikizo kubwa la wanafunzi ndani ya shule hiyo lilimfanya aweze kugombea nafasi ya uongozi kwa mara nyingine, safari hii alitaka kuchukua nafasi ileile lakini shinikizo la watu lilipelekea agombee rais wa serikali ya wanafunzi.
Hakuwa na mpinzani hata kwenye nafasi hiyo na hatimaye alipita bila upinzani mubwa, akawa ni rais wa kwanza wa wanafunzi kutoke kwenye shule hiyo akiwa yu ngazi ya kawaida(o-level). Ilizoeleka wanafunzi wa shule hiyo wenye nafasi hiyo walikuwa wakitoka kwenye daraja za juu kielimu(o-level), hakika yeye ndiye aliyevunja rekodi hata kwenye uongozi wake kwa kuweza kuwaongoza wale waliokuwa wapo daraja za juu kielimu na hata daraja moja naye bila kupindisha chochote. Demokrasi ndiyo ilikuwa imetawala katika uongozi wake, ndiyo maana alikuwa ni kiepnzi cha watu sana. Hakwenda kinyume na miiko ya uongozi wake na alikuwa ni msikivu sana wa wanafunzi wengine, sifa zake zilikuwa ni zilezile ambazo zilikuwa zimempa jina kbwa katika shule hiyo. Suala la wasichana lilikuwa ni urafiki wake wa kawaida kutokana na malengo aliyokuwa amejiwekea, alikuwa ni mwenye kuongoza kwenye masomo mbalimbali darasani hivyo hakutaka ashuke kidaraja kutokana na kuendekeza wasichana. Wapo wengi sana waliokuwa wakimpenda lakini hakulegeza msimamo wake, hata wasichana wengine walipokataliwa na kumzushia kutokuwa sawa kimwili bado hakuweza kuharibikiwa na heshima yake. Yote kutokana na kuwa kipenzi cha watu, yeyote ambaye angezusha uzushi kwake basi alikuwa na aibu ambayo ilikuwa ikimkumba yeye na hata kujitia matatizo. Bado aliendelea kuwavutia wengine wengi na hata waliokuwa wamemzidi vidato lakini waliishia kapa, miezi nayo ikakatika hatimaye mwaka huo ukaisha ukaingia mwaka mwingine.
Likizo ya mwisho wa mwaka ilipoisha mwaka mwingine ulifuata katika kipindi cha mwaka wa mwisho wa elimu ya daraja la kawaida, mwake huo nao alikuwa akiishi kwa misingi aliyokuwa amejiwekea hapo shule na hadi akahitimu kidato cha nne katika shule hiyo. Baada ya kuhitimu maisha ya nyumbani ndiyo yalifuata na akawa ni mwingi wa kukaa ndani sana, hakuwa mtu mwenye marafiki kutokana na kupoteza muda mwingi akiwa shule. Pia uwepo wa nyumba aliyokuwa akiishi eno la shamba, ulifanya awe na urafiki mkubwa na Mwambe ambaye alikuwa ni na cheo cha ASP(Mrakibu msaidizi). Yeye ndiye alikuwa akija kutoka naye na kutembea naye katika sehemu mbalimbali za katikati ya jiji zenye kuvutia, huyo ndiye aliyekuwa rafiki yake mkuwa sana. Alipokosekana alikuwa ni mwenye kutoka na kwenda mwenyewe mjini katika sehemu ya kutuliza mawazo, alirejea nyumbani akiwa ametuliza akili yake vya kutosha huko mjini na alijumuika na wazazi wake wa hiyari ambao walikuwa wamekuwa na mionekano ya wenye nazo na si namna ile ambayo walikuwa wakiishi uswahilini. Miezi ilisogea na hatimaye matokeo ya kidato cha nne yakatoka akwa ni aliyefaulu kwa daraja la kwanza, muda wa kujiunga na kidato cha tano hakutaka kurudi tena kwenye shule ile bali alijiunga na shule ya sekondari ya Tambaza na akawa anakaa katikati ya jiji. Alisoma kwa miaka miwili na hatimaye alihitmu na alipangiwa kujiunga na jesi la kujenga taifa kambi ya Mgambo Kabuku jijini Tanga.
Huko ndipo alipoenda kukutana na Wilfred ambaye alikuja kuwa rafiki yake mkubwa, tabia ileile aliyokuwa nayo ndiyo ilimfanya we kipenzi cha watu ndani ya kambi hiyo. Si afande wala kuruti ambaye hakuwa akipenda kuwa naye. Kipindi hicho tayari alikuwa akijua kila kitu kuhusu Philipo Lutonja ambaye alikuwa ni Mrakibu mwandamizi wa jeshi la magereza(SSP), uchunguzi uliofanywa na ASP Mwambe kuhusu kifo cha baba yake alikuja kubaini kuwa huyo ndiye alikuwa mhusika mkuu wa mauaji ya wazazi wake. Hakuwa na la kufanya tena zaidi ya kuliacha suala hilo kama lilivyo, upana wa mtandao ambao ulikuwa ukihusika na kila kitu ulimfanya abaki na kidonda moyo lakini si kutafuta tiba. Ndani ya kambi hiyo ndipo alipokuja kumuona msichna ambaye alikuwa akimfananisha hakujua alikuwa kamuona wapi, alidhani alikuwa tu kamfananisha na mtu. Hivyo aliacha kabisa kufuatilia suala hilo la kutaka kumjua kindani, aliendelea na mafunzo yake ya miezi mitatu ndani ya kambini. Uhalisi wa msichana huyo alikuja kuujua siku ambayo alijitaja mwenyewe bila kuulizwa lolote, hakika alikuwa ni Jane Philipo Lutonja. Msichana ambaye aliambiwa alimuingilia chumbani katika kipindi ambacho alikuwa yupo kwenye ulimwengo wa vipofu, siku hiyo ndiyo alijeruhiwa na mtu ambaye anamtaja hapo na kisha kutupwa Jalalani. Ubaya aliofanyiwa na familia hiyo ndiyo ulirudi kwenye kichwa chake, aliwahi kudhalilika kiasi cha kupigwa hana nguo mbele yake akiwa yupo ndani ya nyumba yao. Hakutaka kukaa eneo hilo alipokumbuka hayo, aliona alikuwa hahitajiki kabisa kuongea na mtoto muuaji ambaye alimuweka yatima. Alienda kukaa huko eneo tulivu akiwa analia ndipo Wilfred akamfuata na kuamua kumsimulia kila kitu kuhusu maisha yake, siri ambayo hakuwahi kumsimulia yeyote yule zaidi ya watu wake wa karibu.
“Dah! Pole sana aisee, inamaana yule demu ndiyo chanzo cha kutekeseka kwako” Wilfred alimuambia
“Ndiyo Wil yani bila yule na baba yake sasa hivi ningekuwa nipo wazazi wangu wote na nisingekuwa nimepitia magumu niliyopitia” Alijibu
“Pole sana mtu wangu” “Yaani mwanangu inauma sana hivi kipofu kubaka ataweza wapi, ikiwa kuona penyewe haoni” “Man mpotezee kama vipi na kaa mbali naye” “Yaani mana nitaanza kumpotezea lakini najua ni suala gumu sana kutokana na yeye kunifuata kila muda” “Si unajua kanasa kwako tayari ndiyo yupo hivyo, ila mwanangu kupitia hali fulani ya maisha kuna sababu zake. Hata haya yanayotokea ukiwa hapa kambini yasingetokea ikiwa hiko kipindi ulichopitia hukukipita, ona ni sehemu ya maisha tu”
“Najua hilo Wil ila ngumu sana, hebu fikiri wewe kusikia kilio cha wazazi wako kipindi wanakufa tena mama yako abakwe ndiyo afe. Halafu mtu mwenyewe ni huyo ambaye anakuweka kwake na kukutesa” “Naelewa mtu wangu hebu chukulia kama halijatoke ukabiliane na wakati wako wa kimaisha uliobakia duniani” “Poa mtu wangu, wewe ni zaidi ya ndugu”
“Hamna noma twendo kombania sasa hivi si unasikia filimbi hiyo, maafande wamerudi kwenye kikao” Wote walinyanyuka na kwenda kukaa kwenye kombania yao katika kukaa mstari maarufu kama kufoleni, kutokana na kutotimia kwenye foleni hiyo walikumbana na adhabu ya kukunja ngumi chini. Walikaa namna hiyo hadi walipotimia wote ndiyo utaratibu mwingine ukafuata wakiwa hapo kwenye Kombania, saa nne kamili waliruhusiwa kwenda kulala kujiandaa na siku mpya. Uchovu wa siku nzima walilala usingizi mzito, saa kumi na moja alfajiri walikuja kuamshwa wote ulikuwa ni muda wa kujiandaa kwenda shamba. Mujibu wa ratibu ilikuwa ni kupanga mistari na kuhesabiwa idadi na ilipotimu saa kumi na mbili wote walielekea shambani, njia ya kuelekea shambani wengi walikuwa wakitembea sambamba na James kutokana na kuzoea vituko ambavyo alikuwa navyo. Siku hii ilikuwa ni afadhali kidogo kutokana na kutokuwa na watu wa kombania nyingine wakiwa wapo njiani. Hii ilimuwezesha kutoiona sura ya Jane hadi wanaingia shamba na kufanya kazi ambazo zilikuwa zimewaweka huko, majira ya saa nne walipokuwa wakinywa chai ndipo alipomuona na alipotaka kumfuata Wilfred alimuwahi na kusoge naye pembeni. Aliongea kwa muda mfupi na kisha alirudi pale alipo James, aliketi na aliendelea akunywa chai akiwa yupo kimya. “Vipi umemuambiaje naona kageuza kaondoka?” Alimuuliza “Mtu wangu unafikiri kuna kumficha tena yule, nimemuambia hutaki kukaa karibu naye tu kasepa” Wilfred aliongea
“Safi sana aisee, tumalizie turudi tukapige kazi” Waliendelea kunywa chai ambayo ilikuwa ikiwapa nguvu ya kuingia shambani kwa mara ya pili, walipomaliza tu kunywa walisogea kando kwani muda ulikuwa bado na waliamua kuongea mambo yao mengine yaliyokuwa yakiwahusu wao. Hawakujalia kabisa Jane alikuwa ameumia namna gani kwa maneno ambayo alikuwa ameambiwa na Wilfred, ilikuwa ni kawaida tu kwa James kutokana na jinsi alivyokuwa akimchukia Jane. **** Upande wa Jane ilikuwa ni maumivu makubwa kuambiwa maaneno yale na Wilfred, aliona kama alikuwa akiambiwa uongo lakini alipomtazama Mhusika alikuwa hana habari naye ndiyo hapo akajua kama ilikuwa ni ukweli. Moyo wake tayari ulikuwa umeshapenda kwa kijana huyo, hakuwa akijua kuwa kijana huyo ndiye yule ambaye alikuwa akiishi ndani ya nyumba yao miaka mingi iliyopita. Wala hakujali kuwa siku ambayo hakuwa ameingiliwa ila kutokana na ukali wa baba yake ilibidi tu akae kimya tu kulifanya suala hilo lionekane kweli, alipelekea mtu ambaye likuwa ameunasa moyo wake ndiyo ateseke akiwa kwenye hali ya upofu na hatimaye kwenda kutupwa jalalani.
Laiti angeliyajua hayo wala asingejileta karibu yake katika muda huo ambao alikuwa akichukiwa, aliona ni mwenye kuonewa na muda huo akiwa ameshika kikombe chake cha chai baada ya kumaliza kunywa chai. Machozi yalikuwa yakimlanga na hata marafiki zake wa karibu walipooona hali hiyo ilibadi wamuulize, hakutaka kuwaficha aliwaeleza kila kitu hadi wenyewe wakashangaa kabisa kwani haikuwahi kutokea hiyo. Kutokana na urafiki aliokuwa amejengeana nao akiwa yupo humo ndani ya kambi, aliwaomba wamsaidie nao walikubali ombi hilo. Muda wa kurudi kambini ulipowadia wote kwa pamoja walirudi wakiwa makundi tofauti, muda huu ndiyo rafiki yake mmoja wa karibu alipotumia wasaa wa kuongea na James na kumueleza kuhusuhali hali halisi aliyo nayo rafiki yake. Alitumia kila aina ya ushawishi ya kuweza kumfanya James akubali kuongea naye lakini ilishindikana, walipozidi kumuambia hivyo neno la mwisho ambalo lilitoka kinywani mwa James ndiyo lilimfanya akose la kuongea. “Namchukia!” James alitamka neno hulo akimuacha msichana huyo akiwa ameingiwa na mshangao, hakuujali mshangao huo yeye alikaza mwendo na kumfuata Wilfred ambaye alikuwa ametanguliwa mbele.
**** Siku zilisogea wakiwa wapo ndani ya kambi na Jane alibaki akiumia mwenyewe ndani ya moyo wake, muda kujiandaa na gwaride la mwisho hatimaye ulifika. Kipindi hicho ndipo Jane liweza kupitisha siku pasipo kumuona James kutokana na yeye kutokuwepo kwenye mazeozi ya gwaride, alikuwa akifanya kazi bustanini katika muda wote wa asubuhi hadi mchana. Aliweza kumuona kwa mbali akiwa na kundi la watu wakiongea na kufurahia mambo mbalimbali, lakini hakuweza kutia mguu na kusogea karibu yake kuongea naye kwa jinsi alivyokuwa na hofu naye. Aliedelea kuvumilia hali hiyo akiwa hapo kambini kuhofia kumkera James na hatimaye yakafika kwa wakubwa wa kambi. Sheria ya kambi ilikuwa ikikataza kuwa na mahusiano laiti ikujulikana hatua kali zinachukuliwa, hilo aliogopa sana kuweza kujiharibia na hatimaye kukosa cheti chake na kupoteza tu muda wa kuwa hapo kambini kisa mapenzi. Siku ya kuhitimu mafunzo kwenye mahafali hayo ndiyo ilikuwa siku ambayo wote walitembelewa na wazazi wao, siku hii SSP Lutonja pia alikuwa yupo ndani ya kambi hii akiangalia jinsi vijana walivyokuwa wakipiga gwaride. Siku hiyo James ndiye liyekuwa kiongozi wa gadi zote zilizopo uwanjani na alitendea haki nafasi aliyokuwa amepewa, alikuwa kivutia kikubwa sana kwa wahudhuriaji wa shereha hiyo. Gwaride lilipoisha pamoja na taratibu zingine za kawaida, ulifuata muda wa kujikusanya pamoja na wazazi na wageni mbalimbali. Muda huu ndipo James alipopokea pongezi kutoka kwa wazazi mbalimbali kutokana na uwezo ambao alikuwa ameuonesha, SSP Lutonja naye alijikuta akimpongeza huku akiwa hamtambui kabisa kuwa huyo ndiye alikuwa ameharibu maisha yake katika kipindi cha miaka kdhaa nyuma. James aliupokea mkono huo wa pongezi lakini ana hasira kubwa sana moyoni mwake, alipoombwa kujumuika na familia hiyo iliyomuharibia maisha yake. Aligoma na kutoa udhuru wa uongo ili asikae nayo karibu tu na kisha alienda kwa wazazi wake wa hiyari ambao walikuja kumtebelea baada ya kumaliza mafunzo.
Siku liyofuata baada ya mafunzo kila Mhitimu alikabdhiwa cheti chake pamoja na posho yake, baada ya hapo wote waliruhusiwa kuondoka wakitumia magari mbalimbali ambayo yalikuwa aymekuja kukaa nje ya kambi hiyo. Kila mmoja alipanda gari ambalo lilikuwa likimfikicha huko alipokuwa akiishi, siku hiyo ndiyo siku ambayo moyo wa Jane ulimuuma kwa kuondoka ndani ya kambi hiyo liliyokuwa ni eneo rahisi sana kuonana na mwanaume aliyekuwa akimpenda.
Muda wa kukaa nyumbani kusubiria majina ya kujiunga na chuo ndiyo ulifuata kwa James yeye alieendelea kufurahia kukaa akiwa na familia yake na akimtembelea Mtu muhimu katika amsiha yake ASP Mwambe. Tayari muda huo hakuwa akimuita anko kama ilivyokuwa zamani, alibadili jina kabisa na kumuita baba kutokana na mchango mkubwa alioutoa kwenye maisha yake. Alikuwa akimuheshimu kama baba yake na hata mke wake alikuwa akimuita mama yake, ASP Mwambe alikuwa na mtoto wa kike ambaye alimuona kama dada yake lakini maono hayo yalikuja kubadilika hapo awali kutokana mazoea yaliyokuwa yamejengeka baina yao. Binti huyu alikuwa akiitwa Sara, katika mazoea yaliyokuwa yapo baina yao wote wawili walijikuta wakipendana. Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa James kuingia kwenye mapenzi, alifanya mapenzi hayo kwa siri akiwa yupo na binti huyo wa baba yake wa kumlea. Ulikuwa ni uhusiano uliojaa mapenzi ya dhati baina yao wawili, walianza kwa kukutana kwa siri na hatimaye wakajumuika katika sehemu mbalimbali kwa matembezi wakiwa wawili. ASP Mwambe wala hakuona uajabu kwa jinsi walivyokuwa wakitoka pamoja, yeye aliona ni mazoea ya kawaida ambayo walikuwa nayo tangu muda mrefu. Hakujua mazoea hayo tayari yalikuwa yamepiga hatua na kujenga kurasa mwingine baina ya wawili hao, wote wawili walikuwa wakingoja majibu ya chuo ingawa Sara alikuwa ametangulia mwaka mmoja kumaliza kidato cha sita.
Walifuatana kama kumbikumbi waliyokuwa wakitafuta sehemu ya kuanzisha kichuguu kila waendapo, walikuwa wakipendezana kwa jinsi wote walivyokuwa wana mvuto. Kila mmoja alijiona ni mwenye bahati kwa kuweza kumpata mwenzake, jambo hili lilifanya wawe ni wenye furaha muda wote. Hitaji la mioyo yao ndiyo lilisababisha wawe pamoja, haya yalikuwa ni mapenzi ambayo James hatakaa ayasahau kwenye maisha yake kwa jinsi yalivyomfsnya ajione yu kiumbe tofauti. Alizidi kuwa na furaha kutokana uwepo wa mwanamke huyu, hakujiona ni mwenye mapungufu katika maisha yake kila akifikiria alikuwa akipendwa na mwanamke mmoja mrembo miongoni mwa warembo. Mapenzi yao yalishamiri katika kipindi chote walichokuwa wakisubiri majina ya chuo, hata yalipotoka bado yaliendelea kushamiri ingawa walikuwa wamepangiwa vyuo tofauti ndani ya jiji la Dar es salaam.
Umbali hauleti athari yeyote kwenye mapenzi ya kweli na waliokua na malengo makubwa, hii ilijidhihirisha kutokana na kupangiwa vyuo tofauti ndani ya jiji la Dar es salaam. James alipangiwa chuo kikuu cha Dar es salaam huku Sara akipangiwa chuo cha usimamizi wa fedha IFM. Waliendelea kusoma kwa bidii na kila mwisho wa wiki walikuwa pamoja, walitembeleana sehemu mbalimbali za kupumzika wakiwa pamoja kila walipokuwa mapumzikoni. Mawasiliano baina yao nayo hayakufa kabisa kila walipokuwa mbali, haikupita muda wa siku nzima pasipo kuwasiliana zaidi ya mara moja kutokana na kila mmoja alivyokuwa akimjali mwenzake. Hii ndiyo ilikuwa nguzo la penzi lao na kulifanya lidumu, marafiki wa karibu wa kila mmoja ambao walikuwa wakisoma nao walikuwa wakijua kuhusu uhusiano wao. Kila mmoja alimuonesha rafiki yake ni jinsi gani ambavyo alikuwa akijiona ni wa fahari zaidi kuweza kuwa naye kimahusiano, marafiki wa karibu wa kila mmoja walikuwa wakiitambua vyema sura ya shemeji yao ambaye alikuwa akiuchengua moyo wa mwenzao. Kuonesheana huku picha kulikuja kuibuka kwa athari kubwa kipindi hicho wakiwa wapo mbalimbali, mwanzo wa atahri hizo ulianza katika chuo cha IFM ndani ya kozi ambayo alikuwa akiichukua Sara. Picha hizo zilikuwa zipo kwenye simu ya marafiki zake ziliweza kujulikana na watu wa pembeni ndani ya chuo hicho, wengi walisifia kuweza kumpata mvulana huyo. Wengine walivutika kutokana na utanashati wake, lakini mmoja aliumia alipobaini hilo hata alipoweza kuiona iicha ya wawili wakiwa pamoja kupitia marafiki wale wapendao kusambaza mambo. Utanashati wa James uligeuka mada ndani ya chuo hicho miongoni mwa wanafunzi wa kike waliokuwa wakipenda kufuatilia watu, huku ndipo kulipelekea kumfikia Jane ambaye alikuwa akisoma masomo hayohayo kujua. Usiri wa taarifa hiyo katika kipindi cha wali ulimfanya asiweze mujua chochote kilichokuwa kinaendelea, hakuwa na mazoea na Sara ndiyo maana ilipelekea asijue kinachoendelea kwa muda mrefu hadi pale zilipoanza kusambaa. Jane kutokana na kuwa ni mtoto wa mzazi ambaye alikuwa na uwezo wa juu kifedha, majigambo na majivuno yalikuwa hayamuishi. Hasa alipoanza kusumbuliwa na wavulana hapo chuoni kuliko wanafunzi wengine, ndiyo akawa anajiona mwenye hadhi ya kipekee kabisa. Hili lilisababisha amdharau Sara na hata iwe ngumu kusalimiana naye, ndiyo maana mwanzoni kabisa aliukosa uhondo wa kufahamu kuhusu hili. Mazoea waliyonayo baadhi ya marafiki zake ndiyo yalifanya ajue kuhusu Mvulana ambaye alikuwa akimpa hadhi ya kipekee Sara, sifa lukuki alizokuwa akimwagiwa juu ya mvulana huyo alitamani kabisa kumuona akiamini alikuwa hana hadhi ya kusifiwa hivyo kutokana na dharau alizonao kwa Msichana mwenzake. Siku alipokuja kuiona picha ya James akiwa pamoja wamekumbatiana na Sara tena ikiwa imepigwa kwa ufundi wa hali ya hali ya juu, ndiyo alipoanza kumchukia zaidi kutokana na kumpenda mwanaume tangu alipomuona katika mafunzo ya JKT. Hakujua alipo huyo mwanaume zaidi ya kujua alipo mpenzi wake, kundi la pamoja la Whatsapp la darasa lao ndiyo lilizidi kabisa kumuumiza kutokana na jinsi ambavyo Sara alikuwa akipenda kumtuma mpenzi akiwa naye karibu katika picha mbalimbali. Alijikuta akiumia sa kila anapopakua picha hizo na kuangalia, macho yake yalipokutana na picha hizo alikuwa kizifuta. Ilipotumwa picha ya James akiwa peke yake ndiyo alikuwa akiipakua na kuitia kwenye simu, moyoni alikuwa amejenga adhma ya kumtafuta James kwa nguvu zote aweze kuonana naye hakujali yale yaliyokuwa yametokea jeshini baina yao. Alidodosa awezavyo na hatimaye akajua mahali ambapo James alikuwa akisoma, alijiona alikuwa ameanza kupata mwangaza wa kumpata lakini alipofikiri ukubwa wa chuo hicho pamoja na wingi wa wanafunzi. Aliingiwa na ugumu wa kuweza kumpata kutokana na kutojua alikuwa akisoma masomo gani, mtu peke ambaye alikuwa akijua hayo alikuwa ni Sara. Huyu ambaye alikuwa akimdharau kila siku, kumuuliza hilo suala ilikuwa ni ngumu sana kutokana na huyu mhusika tayari alikuwa ameshajenga chuki naye. Hata kama angekuwa hana chuki naye angeanzia wapi kumuuliza, alitambua ni jinsi gani wanawake walivyokuwa wana wivu wakipenda. Alihofia wivu huo ungepelekea hata awe katika matatizo ikiwa suala hlo litafika kwa baba yake, hofu ya kuchafua jina la baba yake ambalo lilikuwa limekua kwa kasi ndiyo ilikuwa ipo ndani ya moyo wake. Mtoto wa mkubwa wa magereza kuingilia penzi la mtu ingekuwa ndiyo habari ambayo ingebeba vichwa vya magazeti mbalimbali, hakuna ambaye hakumtambua kuwa alikuwa ni mtoto wa mkubwa huyo ambaye alikuwa ameshajizolea umaarufu jijini. Kulinda heshima ya baba yake alikujali sana lakini kutafuta penzi napo hakuacha kupajali, hii ilifanya awe ni mwenda chuo kikuu cha Dar es salaama mara kwa mara. Aliamini ipo siku angeweza kumtia machoni, ukubwa wa chuo pamoja na wingi wa wanafunzi ulimkatisha tamaa hata ashindwe. Hakujua alikuwa akikaa sehemu gani jambo jingine ambalo lilimpa ugumu katika kumfuata, alikuwa ni mwenye tabia ya kuja ndani ya chuo kikuu hicho hata katika kipindi cha kati ya wiki lakini hakufanikiwa kumpata. Aliendelea kuwa na tabia hiyo karibu mwezi lakini mwisho wake alikata tamaa kumuona James kwa njia hiyo, aliona njia iliyobaki ilikuwa ni kuwatumia marafiki wa Sara ambao walikuwa ni watu wake wa karibu. Alijaribu kutumia mbinu hiyo kuweza kupata namba ya simu ya James lakini hilo nalo alishindwa, wivu aliokuwa nao mwenye mpenzi ulikuwa mwingi sana kutokana na sifa ambazo alikuwa amemwagiwa kila walipoiona sura yake. Hilo lilisababisha hata Jane akose namba hiyo kutokana na hofu ya mwenye mali kuporwa, hivyo hakugawa namba kwa watu wengi. Waliokuwa na namba hiyo walikuwa ni marafiki wa ksribu wsara. Ambao aliwadharau kipindi kwa kirefu kutokana na familia aliyokuwa akitokea. Taratibu alijikuta akianza kumsalimia Sara bila mwenyewe kutaka ili aweze kuwa karibu naye, alikuwa akinyamaziwa mara nyingi sana alini bado hakuchoka kumsalimia. Alipokea dharau kama alivyokuwa akifanya dharau lakini hakukata tamaa, lengo ilikuwa ni kupata mawasiliano ya James hata kukutana naye. Wasichana hao walimtenga nao kutokana na tabia za kike ambazo walikuwa wameumbwa nazo, asili ya baadhi ya wenye jinsi ya kike kuweka visirani katika mioyo yao ndiyo ilisababisha hata ashindwe kukaa karibu nao. Alikata taama na hata akawa ni mwingi wa kuwafuatilia bila ya sababu yeyote, dharau zake ambazo alikuwa akizifanya aliziona hazina maana kabisa. Alijuta kuishi maisha ya kiumaarufu kisa kulewa pesa za baba yake, aliona laiti kama angekuwa na maisha ya kawaida ya kujichanganya na watu kama ilivyokuwa kwa Sara. Angekuwa ameshapata hata namba ya James na kuweza kukutana naye,dhumuni la moyoni mwake la kumpata James kwa namna yeyote ile ndiyo lilifanya hata awe mwenye kufikiria kumpindua mwanamke mwenzake kwa namna yeyote.
**** Maisha ya James ndani ya chuo kikuu Dar es salaam akiwa ni mkazi wa hostel za Mabibo Ubungo Kibangu, yalikuwa na furaha sana kila kukicha. Alikuwa amepata rafiki mpya kabisa ambaye alikuwa akisoma naye chuo hicho, wote walikuwa wakisoma masomo tofauti. Alikuwa ameingia kwenye urafiki na Norbert Kaila mwanafunzi wa chuo kikuu hicho anayechukulia masuala ya uandishi wa habari. Huyo ndiye alikuwa rafiki yake ambaye walikuwa wakipendana, ndiye pia rafiki pekee ambaye alikuwa na maelewano mazuri na mpenzi wake. James alimpenda sana rafiki huyu ambaye alikuwa ni mkware wa wanawake, hakumuhofia kabisa kuweza kumpindua kwa mpenzi kwa kutokana na heshima aliyokuwa akimpa shemeji yake. Matembezi aliyokuwa akiyafanya James basi mpenzi wake au Norbert alikuwa yupo,hakika walipendezana sana kwakuwa wote wawili walikuwa ni watanashati na wenye mvuto. James alikuwa akiishi na rafiki yake huyo katika chumba kimoja ambapo muda mwingine ilimlazaimu kulala nje, yote ni kutokana na uingizwaji wanawake tofauti na rafiki yake huyo. Hakuwahi kumuambia neno lolote baya kuhusu tabia yake hiyo kutokana na yeye kuwa anapishwa kila akija Sara awe naye. Pamoja na kubadili wasichana namna hiyo James alikuwa akitambua wazi rafiki yake huyo alikuwa na mwanamke ambaye alikuwa masomoni nje ya nchi, mwanamke huyo ndiye ambaye alikuwa akimpenda kwa dhati. Aliishia kuziona picha za mwanamke huyo ambaye aliambiwa anaitwa Norene, aliendelea kuishi naye huku akivumilia kila kitu kuhusu tabia ambaye alikuwa nayo Norbert asiyepitiwa na mwanamke mrembo akakaa bila ya kumfuata. Hayo ndiyo yalikuwa maisha yao wakiwa wapo chumbani kwao, alikuwa ameshamsahau kabisa Wilfred ambaye alikuwa ameamua kujiunga na jeshi la polisi baada ya kumaliza mafunzo ya jeshi la kujenga taifa. **** Inavyojulikana kuwa mtafutaji hatoki mikono mitupu hata siku moja, ndiyo ilijidhihirisha katika siku moja ya mwisho wa wiki amapo Sara alikuwa yupo pamoja na rafiki yake wa karibu wakiwa wanatoka na kuelekea kwenye matembezi yao. Siku hiyo walikuwa na miadi ya kukutana na James pamoja na Norbert, walitoka pamoja majira ya saa tano asubuhi kwenda hadi jirani na hostel za kina James. Waliwakuta wakiwa tayari wamejiandaa na walikuwa wakisubiri ujio wao, siku hiyo ndiyo ilikuwa siku ya kwanza ya Norbert kuweza kumuona rafiki yake Sara na baada ya kutambulishwa tayari alikuwa ameingiwa na tamaa naye. Walipochukua usafiri na kuondoka huko walipokuwa wakielekea tayari mtafutaji ambaye alikuwa na tumaini la kutotoka mikono kapa alikuwa amewaona, Jane alikuwa amemfuatilia Sara tangu anatoka kwenye hostel alizokuwa akiishia hadi anafika hapo na kukutana na James.
Ilikuwa ni mara ya kwanza kumuona na James akiwa yupo mvulana mtanashati kama yeye, aliamua kuwafutilia akiwa amekodi teksi hadi walipofika kwenye ufukwe wa Coco. Hapo aliwashuhudia wakikumbatiana na wakitembea kwa upendo katika muda wote waliokuwa wakielekea kwenye eneo la kunywea vinywaji kwenye ufukwe huo. Vitendo vyote ambavyo vilikuwa vikifanywa nao vilikuwa vikimuumiza kila alipokuwa akiviona. Ilifika muda akiwa amekaa mbali na eneo hilo alikuwa akilia sana kila alipowaona, walipokuwa wakicheka pamoja huku wakilaliana kiupendo yeye alijiona alikuwa akitobolewa kwenye moyo wake. Kila kitendo kilichokuwa kikifanyika hapo kilimuumiza zaidi na hatimaye alishindwa kustahimili akaondoka, alitumia usafiri kama aliyokuwa amekuja huku njiani akiwa haishi kulia kutokana jinsi alivyokuwa akimpenda James.
**** “Yaani shem huyo mwenzako sijui umemlisha nini?” Rafiki wa Sara aliuliza huku akiwa amekaa pembeni ya Norbert. “Unajua inabidi niulize shem kamlisha nini Jem maana kamkaa kinywani kila muda utafikiri mate” Norbert naye alitia maneno wote wakacheka “Heeeh! kumbe wote nilijua huku” Rafiki yake Sara mshangao ulimtoka “Ukisikia nyota zenye kuendana ndiyo hizi ndiyo maana tunapendana,Gilda shosti upo hapo?” Sara aliinggilia naye “Sina usemi kwenu nyinyi kumbikumbi” Gilda alisema “Kumbikumbi huwa wawiliwawili tu, hapa kuna wengine wanaotakiwa kusogezana karibu tu” Norbert aliropoka hukua akimbania jicho James kiutani, kicheko kilimkuta rafiki yake huyo ambaye alikuwa ameelewa maana ya fumbo hilo. “Shem nawe usiongee mafumbo, nimekuelewa kabisa unachokisema” Sara aliongea “Halafu shem huyo rafiki yako hajatulia” Gilda aliongea huku akicheka “Sasa ninarukaruka au namna gani?” Norbert alitia masihara “Kutulia ni jukumu la maji ya mtungini yanyweke wewe” James naye aliropoka “Kumbe na wewe ndiyo zakoeh!” Sara alikuja juu “Situlii kwako tu kuhakikisha unafurahi kwenye kila siku ya maisha yako” James alichombeza huku akimshika kidevu mpenziwe “Loh! Wivu mwingi” Gilda aliweka jicho la kumsuta alipongea maneno hayo.
“Akaa we! Mwenye mali hulinda chake bibi” Sara
Waliendelea kufurahi siku hiyo huku wakiongea mambo mabalimbali, ilikuwa ni katika siku ambayo pia Norbert aliyekuwa mcheshi kama James aliendekeza tabia yake ileile ya kupenda wasichana. Wapendanao walipotoka kwenda faragha yeye alitumia wasaaa huo kumchembeza Gilda aliyekuwa wamekuja kwa mwaliko wa shoga yake, hadi wapendanao hao wanarudi tayari alikuwa ameshamzidi mrembo kwa maneno yake hadi akakosa usemi wa kuongea. Utani uliendelea kati yao wakiwa wapo hapo mezani, Gilda alianza taratibu kuwa karibu na Norbert na hata wakawa wanatania matani ambayo yalikuwa ni tofauti na walivyokuwa hawajabaki wawili. Mazoea hayo yalifanya James amkate jicho kwani alikuwa ameshatambua rafiki yake huyo, Norbert alirudisha jicho hilo kwa kumnyanyulia nyusi moja juu. Hiyo ilikuwa ni ishara tosha kuwa alikuwa tayari ameshaanza kumuingiza kwenye anga zake, hakika alikuwa akimtambua vyema huyo rafiki yake. Moyoni alibakia na mshangao kwa muda mfupi ambao alikuwa ameutumia kuweza kumshawishi, hakika alimuona alikuwa ni mtu ambaye alikuwa na kizizi. Kutokana kuwa na mazoea ya kiheshima hadi kuwa na mazoea kama walikuwa na ukaribu ndani ya muda mfupi, hakika alimvulia kofia Norbert akamuona ni kiumbe wa ajabu sana. Hakuwahi kuona akitumia muda mfupi kumpata mwanamke na hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza, waliendelea kuifurahia siku hiyo ya mwisho wa wiki lakini bado mshangao wake haukuwa umetoka kichwani mwake. “Jamanieh! Kama vipi leo twendeni klabu tukafurahia siku hii” Norbert alitoa wazo” “Enhee! Shem umeongea hapo twendeni jamani tukitoka hapa” Sara naye alidakia
“Mtu na shema wake akili zinafanana, haya limepita hilo sijui kwa shem hapo” James aliongea huku akimtazam Gilda
“Sina neno kabisa” Gilda aliridhia “Raha iliyoje tunaingia kama jozi za viatu vile” Norbert aliropoka “Huyu naye muone” Gilda aliongea huku akimpiga singi Norbert
Majira ya jua kutua wote walinyanyuka kwenye viti vyao na kuchukua usafiri, wakiwa katika muundo wa wawiliwawili walipanda usafiri ambao uliwapeleka moja kwa moja hadi kwenye klabu maarufu jijini Dar es salaam. Walifanikiwa kufika na wote waliingia ndani ya klabu ya muziki wakiwa ni wenye hamu sana ya kuucheza, muda huo muziki ulikuwa bado haujachangamka kutokana na kutokuwa muda wake wa kuchangamka. Wakiwa wanasubiri muda wa kuchangamka muziki huo walitumia kukaa chini na kuongea mambo mbalimbali. Muda wa kuucheza muziki huo ulipofika waliingia kati ya kuucheza wakiwa wawili wawili, uchangamfu ndiyo uliingia kwenye akili zao kwenye kipindi chote walichokuwa wakiucheza muziki huo wa ujana. Wakiwa kwenye kundi la watu walikuwa wakiucheza huku wakiwa na furaha tele, James alikuwa yu karibu na Sara wakiucheza muziki na Norbert alikuwa yu karibu ya Gilda. Hakika walipendeza kutokana na walivyoendana na jinsi walivyokuwa wakicheza kiufundi zaidi, wote waliujua kuucheza ingawa wengine walikuwa wakionekana hawakuwa wachezaji muziki. Usiku mnene uliwakuta wakicheza muziki huku wakipumzika kwa vipindi chache,fujo zilipoanza kutawala kwenye muziki taratiou walijitoa na wakakaa pembeni wakiendelea kuongea. Muda ulipoanza kuyoyoma zaidi hatimaye walinyanyuka kwenye makochi maalum ya ndani ya klabu hiyo na wakaondoka. Wakiwa wawili vilevile waliondoka na kuelekea katika sehemu moja ya kuumzika, kinamna ya ajabu tu James alikuwa akimshngaa Norbert kwa jinsi alivyokuwa hafai kwa wanawake. Alikuwa bado haamini kama alikuwa ameweza kuongozana naye hadi kwenye nyumba ya kupumzikia, ahata alipochukua chumba na Sarah bado alikuwa anaona kama ulikua mchezo wa kuigiza. Kumuona rafiki yake huyo alikuwa ameingia chumba kimoja na Gilda, hakika hakutarajia ndani ya kipindi kifupi cha muda tangu waonane. Asubuhi ya siku iliyofuata wote walikutana tayari wakiwa wametoka kulegeza uimara ya vitanda vilivyopo katika nyumba hiyo ya kupumzikia. Siku hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kupumzika na walikuwa hawataki kwenda sehemu yeyote ile, wanaume hao wawili waliwasindikiza wanwake wao hadi kwenye hostel zao. Walipowafikisha ndiyo ikawa mara ya kwanza kwa James pamoja na Norbert kuonekana kwenye kundi la wasichana waliokuwa wakiishi hostel, siku hiyo ilikuwa ni usumbufu kwao kwani walisalimiana na wasichna tofauti ambao walikuwa wakiwachangamkia hadi wasichna wao waliingiwa na wivu. Nao kutotaka kuwaudhi waliondoka kwa haraka,kuondoka eneo hilo tayari Norbert alikuwa ameshaanza kutamani baadhi ya wasichana warembo aliowaona. “Mwanangu huku kuna mashori balaa” Norbert alimuambia James baada ya kushuka kwenye kituo cha daladala Ubungo. “Dah! We mtu mwisho kabisa ushatamani na kule” James aliongea huku akianza kucheka “We unafikiri nani asitamani watoto micharuko wale, yaani kuingia tu walivyotupapatikia” “Mtu wangu hivi lini utatulia na msichna mmoja?” “Muda wa kugeuka jua kuzama mashariki labda” “Haya haya ni maisha yako siwezi kukuhukumu kwakuwa mimi mwenye sina ukamilifu kwenye ya kwangu”
“Yaani ndiyo nakukubali hapo tu mwanangu, ndiyo maana hata wewe sikukulaumu kuwa na mmoja huna sababu ya kuwa kama nilivyokuwa hivi” “Halafu kila siku neno lako ni hilo tu ila huniambii una sababu gani iliyokufanya uwe hivyo”
“Mwanangu ni stori ndefu sana ila napenda ujue hata mimi nilikuwa na msichana mmoja kama ulivyo wewe na nilimpenda sana” “Sasa si unipe habari mtu wangu yaani mimi wako wa damu pia unanificha, ilikuwaje hadi ukakutana naye huyo msichana na kipi kimekufanya uwe namna hiyo” Maneno hayo walipokuwa wanayaongea tayari walikuwa amefika kwenye eneo la Ubungo maziwa jirani na ilipo mitambo ya umeme nchini.
Norbert alimtazaa rafiki yake na kisha alieleeza, “Nilikuwa ni kijana mmoja nisiyejua hata ujanja kwenye masuala haya, yote yalianza nikiwa kidato cha tatu nilipokuja kumpata msichana ambaye aliushika moyo wangu sana. Nakumbuka nilikuwa na kawaida sana ya kutoroka kwenye shule ya bweni niliyokuwa ninasoma na kuingia mtaani kwenda kujilia vitu vidogo kutokana na kukinaishwa na mlo mmoja wa bweni, kutoroka kwangu huku ndiyo ilikuwa sababu ya kuweza kukutana na msichana huyu. Ingawa nilikutana naye katika mazingira ambayo yalikuwa si mazuri bado haikuwa sababu kwa sisi kuja kushindwa kuanzisha pendo katika siku za mbeleni, alikuwa ni msichana ambaye alikuwa amenizidi kiumri kidogo. Siku ya kwanza kukutana naye ilikuwa ni kama kawaida yangu ya utoro katika mwisho wa wiki nipo mitaani. Siku hiyo majira ya jioni nikiwa naelekea shuleni upande wa nyuma wa ukuta ndipo nilipoweza kumshuhudia mtu akiwa ameanguka barabrani akiwa aangaliwa hali yake na Mwanamke mzee, nilitaka niwapuuzie lakini nafsi ilisita na kusogea karibu na eneo hilo. Upungufu wa mwangaza majira ya jioni haukuweza kunifanya nishindwe kumuona msichana huyu ambaye alikuwa ana majeraha kwenye sehemu mbalimbali za mwili wake. Kitu cha kwanza nilichokifanya ni kumuuliza yule Mwanmke mzee kuuhusu hali ya huyo na sababu zake, kutokana na kuaanza kumuuliza kiheshima haikumuwia vigumu kwa Mwanamke huyo kuniambia alikuwa amemuona eneo hilo akiwa ameanguka. Aliniomba nimsaidie kumbeba niende naye nyumbani kwake nami sikuona sababu ya kukataa nilifanya kama alivyotaka, nilimbeba na nikaelekea hadi huko alipokuwa akiishi kwenye nyumba ambayo ilikuwa imechakaa. Nilielekezwa kwa kumuweka binti huyo na mimi nikamuweka, alianza kupewa huduma nami nilikaa eneo hilo hadi inafika majira ya saa mbili. Chakula nilipewa nikala hapohapo na niliaga nikarudi shule nikiwa nimemuacha akiwa bado hajarejewa na fahamu, siku hiyo nilikuta wenzangu wakiwa wapo madarasani wanajisomea lakini nilipitiliza moja kwa moja hadi bwenini nikaenda kulala kutokana na kuchoka. Oyaa Jem gari hilo mtu wangu mbona huangalii hata mbele yako” Norbeet alisimulia na kisha alisitisha baada ya kuona gari likiwa linakuja mbele, James alikuwa akimsikiliza huku akiwa anamtazama pasipo kuangalia mbele. “Dah! Mtu wangu nimenogewa endelea basi kunipa mkasa”
“Utoro kama kawaida nilikuwa nikiufanya lakini siku hizi nilipunguza kwenda mitaani na nilikuwa nakuja kwenye nyumba hii niliyomleta yule binti, nilimkuta akiwa bado ni mgonjwa lakini sikuwa nikichoka kuja kumuona. Hadi alipokuja kupatwa na nafuu na akaambiwa na Yule Mwanamke ambaye tayari nilikuwa anamuita mama juu ya mimi, alinishukuru sana na hapo ndipo ukaanza urafiki baina yetu. Alipokuja kupona kabisa niliweza kujua alikuwa ni mmoja wa wasichna warembo ambao walikuwa wamekosa matunzo, mioyo yetu taratibu ilianza kuzungumza na hatimaye siku moja nikaja kuingia kweny pendo lake. Sikuwahi kupenda kama nilivyopenda hapa nakuambia mtu wangu, Mwanakombo alikuwa ni kila kitu kwangu kama ningekuwa ni Askari basi huyu angekuwa ni Kamanda wangu. Mambo yote ya kitandani nilikuwa chekechea lakini nilikuja kupata shahada kabisa. Nilifurahi kuwa ndani ya penzi lake lakini sikuja kudumu kabisa mtu wangu, lilikuja kusambaratika kutokana na ujio wa mdada mmoja katika shule yetu kumleta mwanafunzi mpya. Huyu dada ambaye nilimuona kama jinamizi kwenye penzi letu alikuwa akiitwa Ester, alikwa ni sawa na mimi kiumri kimtazammo lakini alikuwa ameyaanza maisha mapema na alikuwa na usafiri wa maana. Huyu dada naye alikuja kunitamani lakini kutokana na kunogewa na Mwanakombo mtoto wa Kitanga nilipiga chini sikutaka mahusiano naye. Hapo ndiyo mwanzo wa matatizo ulipoanza, sikuwa nafikiria kama kabisa angekuja kufanya hivyo. Alipokuja kujua kuwa nina mahusiano na Mwanakombo alipanga mpango mbaya sana wa kuweza kumkomesha, alikuja siku akiwa na lengo la kumuambia ana kwa ana aniache. Siku hiyo alipokuja kumuona huyo Mwanakombo amuambie aliondoka bila ya kuaga, siku hiyo nilipokuwa nikiwatazama wote wawili niliweza kujua kuwa alikuwa wakifanana sana. Siku hiyo pia niliweza kujua kuwa huyo Ester alikuwa ni ndugu wa damu wa Mwanakombo, nilisimuliwa kila kitu juu ya undugu wao na jinsi walivyotengana. Haikuchukua muda mrefu tangu nifahamu hilo kipenzi changu aliuawana mhusika akawa ni Ester. Tangu siku hiyo Mwanamke alipokuwa chnazo cha kumkosa mpenzi wangu, nilianza kulipiza kwa kuwabadili tu kama nguo sikuwa na mapenzi nao. Rafiki yangu ambaye tulikuwa tukisoma naye shule moja ambaye anaitwa John kwa sasa yupo mafunzoni jeshi la polisi alinishauri lakini sikubadilika, hata huyo Ester mwenye nilikuja kumuweka katika orodha ya niliowachezea. Hivyo mtu wangu hii ndiyo sababu ya kuwa na wasichana wengi ingawa yupo mmoja Norene ninayempenda kwa dhati” Norbert alihitimisha kusimulia na muda huo wakiwa wamefika kwenye lango la kuingia hostel. “Dah! Pole mtu wangu” “Usijali jamaa ndiyo maisha haya ila hawa viumbe waache watakoma” “Il sijapendelea unavyofanya mtu wangu” “Tuiache hii habari” Wote waliingia kwenye jengo lililokuwa na chumba chao ndani yake, waliingia kwenye chumba na walipumzika kutokana na shughuli ya usiku uliopita. **** Kujua makazi ya James ilikuwa ni ushindi mkubwa sana kwake na aliamua kutopoteza nafasi hiyo, Jane alitoka nyumbani kwao majira ya jioni akiwa ameaga alikuwa anarudi Hosteli lakini haikuwa hivyo. Alikuwa na safari nyingine ya kuunganisha ndiyo aweze kupita na kwenda hostel, alipitia moja kwa moja hosteli za Mabibo ambapo alikuwa amepanga kwenda. Akiwa ameamua liwalo na liwe aliingia hadi ndani ya uzio wa hosteli hiyo, ukubwa wa hostel hizo ulimfanya yeye kutosonga mbele zaidi ya kuuliza wenyeji wa hapo. Aliamua kumtafuta Mlinzi na alimuuliza kuhusu mtu aliyekuwa akimtafuta, kutokana na James kuzungumza na watu wa aina tofauti hata wafanyakazi wa ndani ya jengo hilo. Haikumuwia vigumu Jane kuambiwa alikuwa anamjua huyo aliyekuwa akimfahamu. Hiyo ndiyo ilikuwa bahati yake baada ya kuhangaika kwa muda mrefu na hatimaye alikuwa ameweza kupata kile alichokuwa akikitafuta, alielekezwa moja kwa moja jengo alilokuwa anapatikana na chumba chake. Alimshukuru san Mlinzi huyo na moja kwa moja alipiga hatua kwa madaha akiwa yu ndani ya mavazi yaliyokuwa yakimpendeza, alielekea ndani ya jengo aliloelekezwa na kisha alienda kugonga kwenye chumba ambacho alitajiwa na Mlinzi h. Mlango ulifunguliwa na alikutana na mtu mwingine tofauti na aliyekuwa amemkusudia hadi kufunga safari na kufika hapo, alikutana na Norbert ambaye alikuwa yupo kifua wazi kavaa nguo ya mazoezi akiwa na taulo begani. “Karibu” Alikaribishwa “Asante, mambo” Aliiitikia ukaribisho na akasabahi “Poa tu, nikusaidie nini mrembo?” “Samahani nahisi sijakosea nilivyoelekezwa, James anaishi hapa?” “Haaah! Usiulize mashuzi kwenye shibe ya kunde mrembo, ndiyo anaishi ila una bahati mbaya sana” “(Alicheka kwa sekunde kadhaa) Kwanini?” “Ametoka muda si mrefu amepigiwa simu kuna jambo la muhimu ameitwa na mzazi wake” “Hee! Jamani, kwahiyo atarudi?” “Ndiyo imetoka hiyo kesho tena atapitiliza moja kwa moja chuo” “(akionekana mwenye unyonge) Sawa huu mguu ulikuwa wake, wacha niende hivyo” “Sasa si ungeukata tu uuache hapahapa akija nitampatia” “(Akacheka tena) Mmmh! Mcheshi sana wewe kama James, wacha niende sijui unaweza kunipatia namba yake” “Dakoka sifuri tu ninarudi” Norbert alipongea hivyo aliingia ndani ya chumba na alipotoka alikuwa na simu, alimpa akachukua namba hizo na kisha alizihifadhi kwenye simu yake. “Asante mkaka wacha niende” “Aaaaaah! Dadaeh! Vibaya hivyo sasa” “Jamani kwanini?” “Yaani unakuja na kuondoka bila ya kujuana kweli, hivi akija na wewe ukamkosa kwenye simu nimuambie nani sasa” “Ooooh! Sorry nina haraka ndiyo maana hata nimesahau, mwambie Jane alikuja” “Wapo wengi sana anaowafahamu wana majina hayo nimuambie Jane yupi?” “Mwambie Jane wa mgambo Tanga au Jane Lutonja” Alipotaja jina lake hakutaka kubaki hapo kwani aliyekuwa amemlenga hakuwepo, kuondoka ndiyo ulikuwa uamuzi na hakuwa na jingine la ziada. **** Muda wa chakula cha usiku James alikuwa yupo meza moja na ASP Mwambe wakiwa wanakula chakula, jambo ambalo alikuwa ameitiwa tayari walikuwa amezungumza. Alikuwa pembeni ya Mke wa ASP Mwambe ambaye ni mama mzazi wa Sara, wote walikuwa wanakula chakula kwa furaha lakini furaha za wote zilikuwa ila ya Jmaes iltumbukia nyongo baada ya simu yake kuita. Kutokana na kutoona umuhimu wa kuipokea simu hiyo kando aliipokea huku akiwa ameshika kijiko cha chakula, aliisikia sauti nyororo ikimsabahi. “Safi nani mwenzangu……Jane yupi najuana na wengi……nani kakupa namba yangu……..Ok sasa sikia, iwe mwanzo na mwisho wa kunipigia simu sihitaji hata kuongea na wewe” James aliongea kwa upole, alipojua kuwa aliyekuwa akimpigia simu alikuwa ni Jnae alibadilika na alikata simu kisha akaizima. “Vipi mwanangu mbona hivi?” Mama Saraha aliuliza lakini hakujibiwa na badala yake alimuona James akiinamisha kichwa chini “James si umeulizwa au siku hizi na wewe ushaanza tabia ya kuficha mabo” ASP Mwambe aliingilia. “Baba wacha niwaambie tu, huyu aliyepiga simu ni Jane lutonja sijui ananitafutia nini yaani waliyonifanyia kwao hawajatosheka tu” Alilalamika “James kama ni huyo mimi nikiwa ni baba yako mlenzi nakushauri kaaaa naye mbali kabisa, SSP Lutonja akijua una mawasiliano tu na binti yake ni kero. Wangapi nimewashuhudia wapo gerezani kisa huyo binti, najua wewe ni kijana wa kiume ila hapo jali maisha yako” ASP Mwambe aliongea “Sawa baba” Alitii Hamu yote ya kula chakula ilikuwa imemuisha kabisa na aliinuka kwenye kiti na kuingia chumbani, aliwaacha walezi wake hao wakiwa wanamshangaa lakini hawakuamuambia kitu kitu chochote hadi pale alipoingia ndani. Uliposikika mlango wa chumbani kwake ukifungwa ndipo mume na mke hao walitazamana, walikaa kwa muda mfupi wakitazamana hivyo hivyo bila ya kuongea chochote. Walipochoka kutazamana kila mmoja alirudisha macho kwenye sahani yake ya chakula na wakaendelea kula, ukimya ulitawala kwa muda mfupi na sauti na vijiko vikigonga sahani kipindi wanakula ndiyo ilisikika. “Baba Sara” Mama Sara aliuvunja ukimya huo. “Ndiyo mke wangu” ASP Mwambe aliitikia “James inabidi uwe mshauri wake mzuri sana la si hivyo tutampoteza huyu” “Sitoruhusu hilo lipotee nampenda kama mwanangu wa kumzaa ndiyo maana nipo naye kwa miaka yote hii” “Hata mimi pia, sina mtoto wa kiume lakini kwa ujio wake kwenye familia hii najihisi nina mtoto wa kiume” “Tutamlinda mke wangu usijali” Asubuhi ya siku iliyofuata James aliamka mapema na alipelekwa na Baba yake mlezi hadi chuoni, aliendelea na masomo kama kawaida ile namba akawa ameifungia kabisa. Siku hiyo nayo iliisha na kisha siku mpya ikafuata, Norbert alikuwa ameshaambiwa kila kitu juu ya Jane na kuwahi kuishi ndani ya nyumba yao huku akifichwa baadhi ya vitu ikiwemo uhusika wa baba yake Jane. Yeye naye aliunga mkono hilo suala na akitumia nafasi hiyo kumsaidia James. Alimua kumuambia ukweli huku akimtajia kila kitu juu ya asili ya James, Norbert alifanya tofauti na alivyofanya Wilfred alipokuwa jeshini. Alimua kumtuhumu kwa jinsi alivyochangia James kuharibikiwa na maisha kipindi akiwa na upofu, huo ulikuwa ni mwiba mchungu sana kwa Jane na hakuthubutu kabisa kuendelea kumfuata James kwani nafsi yake ilikuwa imemsuata tayari kwa hatia aliyokuwa ameifanya.
Kukaa kimya ilihali hakuwa ameingiliwa ukweli na James ilikuwa na hatia kubwa iliyohalalisha kupigwa kwake, kumbukumbu za jambo hilo zilimuumiza sana hasa akikumbuka alimshuhudia akipigwa uchi hadi ngozi yake ikachanika. Hakuwa na namna ya kujitetea kabisa kutokana kulitazama suala hilo likiwa linatokea hadi bila kutoa utetezi wowote, hofu dhidi ya baba yake ndiyo ilimfanya hata ashindwe kuongea chochote. Alipokuwa akitendewa jambo hilo tayari alikuwa ameanza kupata viashiria ya ukubwa ndani ya mwili wake, hakuwa mtoto hadi aseme kuwa alikuwa hajui kama maeneo yake yalikuwa hayajaguswa. Mwenyewe alianza kuacha kumfuatilia na huo ndiyo ukawa mwanzo wa kuwa ni mwenye kuumia, masomo alikuwa akiendelea nayo na aliweza hata kuwa na mwanaume mwingine lakini bado hakuweza kumsahau James. Alikuwa na lengo lile la kuwa naye, upendo wa kweli kwa mtu aliyekuwa hana haja naye ndiyo ulikuwa unamsumbua sana. Uzuri ule aliokuwa akiuona ni silaha na ni sababu tosha ya kuwa na jeuri, hakuona sababu yeyote ya kuendelea kuwa nao ikiwa aliyekuwa akimthamini hana haja naye.
Jane huyu alibadilika kuwa ni binti mkimya muda wote aliyekuwa yupo kwa ajili ya masomo tu, mwanaume aliyekuwa naye alikuwa akikidhi haja ya mwili wake tu na si kuwa naye kimaisha. Hii ilifanya abadili wanaume kila kukicha akiona alikuwa amechoka kuwa na mwanaume mmoja, hakuona haja ya kujithamini ilihali hatahminiwi na yule aliyekuwa akimthamini. Hitaji la mwili lilipokuwa likimsumbua basi ilikuwa ni kwa mwanume yeyote yule, atakayeleta jeuri kwenye uhusiano wake kisa alikuwa amelala naye alikuwa akiishia kuachana naye. Hayo ndiyo yalikuwa maisha yake hadi anahitimu katika chuo hicho kwa kusoma miaka mitatu, siku ya mahafali alisherekea na familia yake huku akishuhudhia jinsi Sara Alivyokuwa yupo karibu na James. Siku hiyo pia aliweza kushuhudia familia nzima ya ASP Mwambe ambaye alikuwa akimJua ikiwa ipo karibu na James, siku hiyo ndipo alipoweza kutambua kuwa huyo aliyekuwa amemchukua mwanaume wa maisha yake alikuwa ni mtoto wa Afisa wa Magereza kama ilivyokuwa yeye.
James baada ya kumaliza masomo yake ya chuo mwaka huo aliohitimu mpenzi wake, aliamua kwenda kujiunga na jeshi la magereza kwa maamuzi yake mwenyewe. Aliingia kwenye mafunzo ya jeshi hilo, Jane naye alipopata habari kuwa James alikuwa amejiunga na jeshi la magereza naye aliamua kujiunga nalo. Walikutana kwenye mafunzo lakini hali ilikuwa ni ileile hakukuwa na maelewano kati yao, hadi muda wa mafunzo unaisha na wote kuajiriwa katika sehemu tofauti ndani ya jeshi hilo. Jane bado alikuwa na nia ileile ya kumpata James, kutimiza nia hiyo aliongea na baba yake ambaye alikuwa ni Kamishna msaidizi tayari. Akitumia hila aliweza kufanikisha kuhamishwa James katika ofisi gereza ambalo alikuwa akifanya kazi jijini Dar es salaam. Bado hakuwa ameweza kumshawishi James kuwa naye pamoja na kuwa yupo naye ndani ya ofisi moja. Ofisi ambayo alikuwa akiogopwa kutokana na kuwa ni binti wa afisa wa juu wa jeshi hilo, alikuwa ameona alikuwa ameweza kutimiza hila yake kumbe ndiyo kwanza alikuwa ameweza kufanikisha kuwa karibu kwa Sara na James ambao walikuwa maeneo tofauti ya ajira.
Wapenzi waliokuwa wametenganishwa na majukumu ya kazi sasa walikuwa wapo pamoja, hiyo ilikuwa ni hatua nzuri kwao lakini pia ilikuwa ni mbaya sana kwa Kwa Inspekta msaidizi Jane. Alikuwa ameanza kujuta kuweza kumuhamisha Inspekta msaidizi James ambaye alikuwa akitambulika kwa jina la Nkongo kuja jijini tena. Aliona ni bora hata angebaki hukohuko kuliko kuendelea kuwa kwenye ofisi moja naye akiwa hajatimiza kile ambacho alikuwa akitaka kitimie, uhasama wa James kwake bado ulikuwa ukiendelea na hakukuwa na hatua yeyote ya kuja kuongea naye na hata kufikia kuwa naye karibu. James alikuwa ni kipenzi cha watu ndani ya ofisi hiyo kutokana na kujiheshimu na pia kuwa mcheshi, alikuwa akiongea na kila mtu lakini si Jane ambaye alikuwa yupo kwenye orodha ya watu aliokuwa akiwachukia ndani ya dunia hii.
Kipindi hiko ndiyo alikuwa amepalilia kabisa mahusiano ya James na Sara, yalifikia hatua baba mzazi wa Sara ambaye alikuwa Mrakibu wa jeshi la magereza kwa wakati huo kujua. SP Mwambe alishangazwa sana na uhusiano huo lakini kutokana na wote kuwa wanapendana na yeye anawapenda, aliamua kuubariki uhusiano wao. Mama Sara naye hivyohivyo aliamua kuubariki uhusiano huo, sasa wakawa wapo huru kabisa na uhusiano na siyo wa kujibana kama ilivyokuwa awali. Mwezi mmoja baadaye katika shereha ya kuzaliwa James ambayo ilihudhuriwa na maaskari wenzake wengi, alimvisha pete ya uchumba Sara na hilo lilizidi kuwa pigo kubwa kwa Jane. Aliumia sana na hata ufanisi wa kazi ukapungua kabisa akawa si makini kabisa katika ufanyaji wa kazi kama ilivyokuwa hapo awali, hii ilikuja kusababisha hata baba yake alitambue hilo na alipojua binti yake alikuwa ni mwenye msongo wa mawazo bila ya kujua sababu yeyote. Aliamua kufanya mipango aende kujiendeleza kielimu zaidi nje ya nchi akiamini hio litaweza kumuokoa, Jane hakuwa na jinsi naye alikubali safari hiyo ili kwenda kutuliza akili yake huko na si kukaa na kuzidi kuumia akiwa yupo kazini.
Kipndi hicho kilikua tayari Kamishna msaidizi Lutonja alikuwa ameshatambua juu ya James kuwa ni mtoto wa aliyekuwa rafiki yake, aliamua kumuacha tu kwani aliona hakuwa na madhara ya yeyote. Hakuona haja ya kumuua mtu ambaye alikuwa anamuona hana hatari kwenye maisha yake,aliendelea na maisha yake akiwa bado yupo kwenye kikundi haramu tofauti na kile cha awali ambacho kilisambaratika baada ya umakini kurudi kwenye vyombo vyua dola. Uhaini na ujambazi aliokuwa ameufanya hakuwa ameuacha kabisa katika kipindi chote. Alikuwa akiendelea na uhaini huo kwa namna tofauti ya kuuza magendo. Alitokea kuwa Afisa mwenye fedha sana tofauti na mshahara wake, hilo liliweka mawswali ambayo mwenyewe baadaye aliyajua kuyazima kwa kujieleza alikuwa amewekeza kwenye shughli zingine tangu akiwa yupo kijana kabisa. Maswali ya mali zake yaliishia hapo na akawa akipata heshima yake kutokana na kuwa afisa mkubwa, hakika aliishi kwa raha sana pamoja na familia yake. **** Maisha ya uchumba kati ya James na Sara yalidumu kwa muda mrefu hadi walipokaa na kuamua waweze kufanya mipango ya ndoa, walilifikisha suala hilo kwa wazazi nao waliliafikia bila ya pingamizi lolote. Wakishirikiana na wale wazazi wa hiyari wa James ambao walimuokota, walianza kufanya maandalizi taratibu. Taarifa zote za maandalizi ya ndoa hiyo tayari yalikuwa yamejulikana kazini kwa James na Sara, marafiki wa pande zote mbili walikuwa wakishirikiana nao bega kwa bga katika kufanya maaandalizi. Norbert, Wilfred ambaye alikuwa ni mrakibu msaidizi wa jeshi la polisi. Walikuwa ni marafki wakubwa wa upande wa James, Gilda pamoja na marafiki wengine nao walisimama upande wa Sara.
Wote walikuwa wakiwatakia la heri kwenye maandlizi yao hayo ya ndoa, walijitoa katika kila kitu ilimradi shughuli hiyo ikamilike. Siku zilisogea na hatimaye siku ya harusi ikafika Jane akiwa yupo nje ya nchi kimasomo, hakuwa na taarifa yeyote juu ya kilichokuwa kikiendelea nchini. James na Sara kwa mara ya kwanza kwenye maisha yao walifikia ndoto ambayo walikuwa wakiisubiri kwa siku nyingi sana, siku waliyokuwa wapo mbele ya Mchungaji ambaye alifungisha ndoa yao walikuwa hawaamini kama wangeweza kufikia siku hiyo. Maisha ya uchumba kwa muda mrefu hatimaye walikuja kuwa kwenye hatua ya kuwa mwili mmoja, mbele ya Mcnungaji wote walikiri kutaka kuwa kwenye ndoa na mwenzake bila hata kusita. Lilipoulizwa pingamizi halikuwepo na hiyo ndiyo ikawa tikiti ya wao kuwa mwili mmoja, hatimaye walifanikiwa kuwa mume na mke na pete za ndoa wakavishana. Waliweka sahihi kwenye cheti chao cha ndoa, nderemo na vifijo zilitawala baada ya kufunga ndoa hiyo na sasa wakawa wa halali kwa Muumba wao. Sherehe kubwa ilifuata baadaye kwenye ukumbi mmoja maarufu jijini Dar es salaam, ndugu na marafiki pamoja na jamaa walihudhuria sherehe hiyo wakitoa pongezi zao. Wale wanafunzi waliokuwa wakisoma nao chuo kimoja ambao walitambua jinsi walivyokuwa wakipendana, waliwapa hongera kwa kufikiaa hatua hiyo kwa kutoa zawadi mbalimbali.
Zawadi nyingi kwenye sherehe zilitoka ikiwemo nyumba ya kisasa waliyokuwa wamekabidhiwa na SP Mwambe, wengi walikunywa na kufurahi ndani ya sherehe hiyo na hata muda wa kuisha kwa sherehe ulipofika. Walitamani iendelee lakini wakati ulikuwa haurudi nyuma, fungate ya mahaursi ilipangwa kwenye hoteli ya kifahari iliyopo visiwani Zanzibar. James na Sara kwa pamoja wakiwa wapo kwenye likizo walisaifri kwenda visiwani humo, ujio wao tayari ulikuwa umeshajulikana na kwa pamoja walipelekwa hadi hotelini hapo. Walikula fungate yao katika hoteli hiyo huku wakiwa ni wenye kujiona viumbe waliozaliwa upya, huduma zote muhimu ndani ya hoteli tayari zilikuwa zimegharamiwa katika kipindi chote walichokuwepo hotelini hapo.
Fungate ilipoisha katika muda ambao likizo zao zilikuwa zikikaribia kuisha, walirudi kwa pamoja jijini Dar es salaam. Waliamua kuweka makazi yao katika nyumba waliyokuwa wamepewa na SP Mwambe kama zawadi kwa kufunga ndoa. Maisha ya ndoa waliyaanza katika nyumba yao hiyo mpya ambayo ilikuwa ina kila kitu ndani yake, ndugu na jamaa walikuwa hawaishi kuja kuwatembelea hapo nyumbani kwao katika siku ambazo walikuwa wapo mapumzikoni. Hatimaye likizo waliyokuwa wamepewa kila mmoja iliisha na wote walirejea kazini, maisha ya ndoa yalikuwa ni matamu sana kwao hawakuwahi kuuona uchungu wake tangu walipoyaanza. Kila mmoja alikuwa akiitambua thamani ya mwenzake ndiyo siri ya kuwa na furaha katika ndoa yao, pia kila mmoja aliona alikuwa amepata mwenza sahihi kwenye maisha yake ndiyo maana waliianza ndoa yao kwa furaha sana. Kila muda walikuwa wakitamani kuwa karibu lakini majukumu ya kikazi yalikuwa yakiwafanya wawe mbalimbali, yalipoisha majukumu walikuwa pamoja katika muda wote. Kinai ya kuwa karibu na mwenzake haikusikika kwenye ndoa yao kwa jinsi walivyokuwa wakipendana, maisha yalizida kuwa mazuri wakiwa ameunganisha na kuwa mwili mmoja na hata mafanikio yao walikuwa wakichangia pamoja. Ndani ya ndoa hiyo kutokana a kuwa mmunganiko uliokuwa unajali maisha yao ya baadaye, waliweza kujenga nyumba ya pili kwa ushirikiano wao na pia walinunua magari mawili ambayo wote walikuwa wakiyatumia kwa ajili ya usafiri.
Bado hawakuwasahau wazazi katika kila siku ndani ya maisha yao kwani ndiyo walikuwa ni nguzo kwao, walienda kuwaona kila inapopatikana wasaa wa kufanya hivyo kutokana na upendo waliokuwa nao kwao. Wazazi wa hiyari wa James ambao walikuwa wakiishi shamba katika kipindi hiki tayari walikuwa wamezeeka, umri ulikuwa umewatupa mkono zaidi, wao utani mkubwa kwa wanandoa hawa ilikuwa ni kupatikana kwa mtoto tu ili wamuone wakiwa na mvi zao kichwani. Walikuwa wakifurahia sana kila wanapotembelewa na wapendanao, dua zote njema walizokuwa wakizijua wao waliwaombea ili wazidi kuwa na ndoa imara na itakayodumu kwa muda mrefu. Maisha marefu pia walizidi kuwaombea wanandoa hao ambao walikuwa wakiyafurahisha macho yao kila wanapowaona, walitamani hata waendelee kuishi milelele ili waionje furaha ya ndoa.
Haikupita miezi mingi sana kiasi cha kutahadharisha upunguaji wa mwaka, ndani ya mwaka huohuo Muumba aliiwaona katika maombi yao waliyokuwa wakitaka yatimie kila siku. Kujibiwa kwa ombi hilo walilokuwa wakiliomba kila siku na kuzidisha juhudi ya kulipata, ilizidisha furaha ndani ya ndoa yao. Mtoto ndiyo ombi ambalo walikuwa wakiliomba kila siku katika maisha yao pamoja na maombi mengine, hili lilijibiwa kwa Sara kunasa ujauzito katika kipindi hiko. Mapenzi baina yao yalizidi katika kipindi hiko ambacho James tayari alikuwa na cheo cha Inspekta ndani ya jeshi la Magereza, Sara alizidisha kudeka kila alipokuwa yupo karibu na mume wake katika kipindi hiko cha ujauzito. Habari ya ujauzito aliyokuwa nao Sara ilifika kwa kila mtu wa karibu na hata ofisini kwa kila mmoja, hongera nyingi ndiyo walizipokea kutokana na kuishi vizuri sana na watu.
Kipindi hiki ndiyo Jane alirejea kutoka nje ya nchi alipokuwa yupo kimasomo, alifikia nyumbani kwao ambapo alipokelewa vizuri sana kutokana na jinsi walivyomkumbuka kwa kukaa nje ya nchi kwa muda mrefu . Alipumzika nyumbanni kwao akiwa hana hili wala lile juu ya ndoa aliyofunga James, moyoni bado hakuwa amemsahau alikuwa akimkumbuka na bado nia ya kuwa naye kimaisha ilikuwa ipo. Alipokuwa masomoni aliweza kutuliza akili yake kutokana na msongo wa mawazo, lakini hakuweza kuufanya moyo wake usiwe na hitaji la kuwa na James. Hilo ndiyo jambo ambalo alilishindwa kutokana na moyo kuwa na ushawishi mkubwa kulikoa akili katika mwili wake, alikuwa ameshakataa kuolewa na wanaume wengi na alikuwa akifikiria tu kuolewa na James. Hakuwa akijua bahati haikuwa yake kabisa na alikuwa akiwaza yasiyowezekana.
Aliporejea kazini alipandishwa cheo na kuwa Inspekta kamili na siku aliyokuwa akiripoti ofisini watu wote walikuwa wakitambua ujio wake, James akiwa mmojawapo na katika muda huo alikuwa yupo juu yake kicheo kutokana na kutangulia kupandishwa cheo. Alikaa pamoja na wafanyakazi wengine ndani ya ofisi hiyo katika kumpokea, muda smbao walionana ana kwa ana James hakuwa na chuki ile aliyokuwa nayo hapo awali. Alipopewa heshima yake kama mkubwa yake aliipokea, alipopewa mkono naye aliupokea na ikawa kwa mara ya pili wanashikana viganja kabla ya kuwahi kufanya hivyo wakiwa pamoja mafunzo ya JKT. Kupokea mkono wa James ilikuwa ni faraja kutosha kwa Jane hadi akajikuta akiutazama mkono huo akihisi haukuwa wenyewe, kitendo cha kutazama kiganjani mwake alipokuwa ameshikana. Aliweza kuuona mkono wa kushoto wa James ukiwa na pete ya rangi ya dhahabu iliyokuwa ya duara, hii ilikuwa ni pete ya ndoa hata bila ya mtu kuambiwa ilikuwa inajulikana tu. Aliuhisi moyo wake kama ulikuwa ukipasuka alipoiona bangili hiyo ndogo ya kidoleni ambayo ni sehemu ya pingu ambayo hufungwa maisha, wazo la kumkosa James lilimjia kichwani mwake lakini hakutaka kuliamini kabisa. Aliona ni kama utani vile kila akilifikiria wazo hilo, alijikaza kiafande na akaweza hata kumaliza kusalimiana na Inspekta mwenzake na kisha akahamia kwa maaskari wengine wa hapo Gerezani. Aliwasalimia mmoja baada ya mwingine huku akili yake ikiwa ipo kwenye pete ya ndoa aliyoiona, alipomaliza kuwasilimia wote aliingia kwenye ofisi yake nyingine ambayo ilikuwa ni eneo moja na ilipo ofisi ya Inspekta James. Alikaa kitini na akili yote ikawa ipo bado kwa mwanaume yule ambaye alikuwa akimuhitaji kwa kila hali kwenye maisha yake na sasa alikuwa amemkosa. Akiwa yu ndani ya mawazo rafiki yake kipenzi aliingia ofisni kwake, kutokana na kuwa alikuwa amemzidi cheo alipewa heshima yake. Alimruhusu kuketi kwenye kiti naye aliketi huku akitabsamu kudhihirisha urembo aliokuwa nao, Jane alibaki akimtazama rafiki yake huyo ambaye alikuwa amemjia ofisini hapo akionekana alikuwa na jambo.
“Shosti nikupongeze Ulaya imekupenda kwakweli” Alipongezwa
“Asante shosti niambie naona una jambo huo ujio wako si kawaida” Alimuambia
“Shosti umekosa vingi sana kwenda masomoni”
“Enhee! Wacha wee, kwanza nipe habari za hapa tangu nilipoondoka”
“Yapo! Mengi sana kikubwa ni Afande Nkongo kaoa”
“Unasema!”
“Ndiyo hivyo shosti yaani bonge la sherehe ofisi nzima tulikuwepo kasoro wewe tu” Maneno hayo yalikuwa ni yenye kumchoma sana lakini ilibidi ajiweke kwenye hali ya kawaida ingawa huyo shoga yake alikuwa akijua vizuri kama alikuwa akimpenda James
“Shosti ndiyo hivyo umeshawahiwa tayari tena ni yule Mdada wa TRA uliyesoma naye chuo”
“Sara!” “Enhee! Kama ulikuwepo vile ni huyohuyo aliyekuwahi” Aliposikia hayo ndiyo aliweka kabisa mikono usoni mwake
“Shosti usihuzunike wanaume hawajaisha nilikuwa nakutaarifu tu, sasa hivi Afande James ni baba kijacho”
“Sawa” Unyonge ulimuingia ingawa alijilazimisha kutabasamu na kisha aliendelea na kuongea na rafiki yake huyo, hakukaa sana alinyanyuka kwenye kiti na kutoka nje.
Inspketa Jane ndipo uchungu uipomshika na hata chozi likamdondoka kwa kuwahiwa kila kitu, muda huo wa kazi alijikuta akilia kwa sauti ya chini iliyokuwa imembatanishwa na kwikwi. Alilia sana na hata kilio kikamchoka na hakuona maana ya kulia ikiwa ilikuwa haimrudishi tena James kwenye mikono yake. Aliamua ajikaze na kutimiza wajibu wake uliokuwa umemuweka ndani ya ofisi hiyo, muda wa mapumziko mafupi ulipofika alienda kupata kifungua kinywa. Eneo la kupata kifungua kinywa alimuona Inspekta James akiwa amekaa na baadhi ya maofisa wakipata kifungua kinywa kwa pamoja, aliamua kujumuika nao huku macho yame yakiwa hayaishi kuitazama pete ya ndoa iliokuwa ipo kidoleni.
Ucheshi alikuwa nao mwanaume ampendaye ulikuwa ukimchekesha pia lakini kicheko hicho kilikuwa kikiyeyuka kila aitazamapo pete ile ya ndoa iliyopo kidoleni, kifungua kinywa chake alikimaliza lakini alijikuta akishindwa kukaa hapo mezani pamoja naye na aliinuka na kuondoka. Alirejea ofisini akiwa ni mwenye majonzi sana kwa kupoteza muda sana na akose alichokuwa akikitaka, muda wa mapumziko ulipoisha aliendelea na majukumu ya ofisni kama ilivyo kawaida. Ulipofika muda wa kutoka aliamua kuondoka akiwa ni wa kwanza kutoka ndani ya ofisi hiyo, alimuacha Inspekta James akiwa yupo ofisini kwake hajatoka. Safari yake baadaya kutoka ofisni hapo ilikuja kuishia kwenye jengo la mamlaka ya Mapato jirani kabisa na Stesheni, hapo alitafuta sehemu nzuri ya kuegesha gari na alishuka huku akiacha macho ya watu yakishangaa jinsi msichana mrembo kama yeye aliyevaa vazi la jeshi la magereza lenye nyota. Hakujali macho ya watu kwani aliamini cheo alichokuwa ncho ndiyo kiliwafanya wabaki hivyo, aliingia ndani ya jengo la TRA na kisha alienda hadi mapokezi na kumuulizia aliyekuwa akimtafuta.
Umaarufu aliokuwa nao Sara ndani ya ofisi hizo haikumuwwia vigumu kuweza kumpata, alielekezwa hadi ilipo ofisi yake. Akiwa ni mwenye mwendo wa kimadaha alipiga hatua kuelea huko ofisini, alipofika alimkuta Sara akiwa ndiyo anakusanya vitu muhimu atoke ofisini. Alipomuona moyo ulizidi kupata maumivu lakini alijikaza na kisha akaguna alipokuwa yupo mlangoni, mguno huo ulimfanya Sara ambaye alikuwa ameanza kunenepa kutokana ujauzito kugeuka. Inspekta Jane aliachia tabasamu huku akimtazama mwenzake ambaye alikuwa amefanikiwa kupata anachokitaka, alipokewa na tabasamu pia kutoka kwa Sara ambaye alikuwa hana chuki ile aliyokuwa nayo chuo. Yote aliyokuwa akifanyiwa chuoni na Inspekta Jane alikuwa ameshayasahau tayari, Sara alijikuta akienda kumkumbatia kutokana na kutoonana kwa muda mrefu sana.
“Jamani ni wewe kweli au naona ndiyvyo sivyo” Sara aliongea kwa furaha
“Ndiyo mimi huyohuyo hakuna mwingine” Inspekta Jane aliongea huku akilazimisha tabasamu.
“Nyota hizo begani hapo si mchezo kama shemeji wako”
“Kawaida tu mwanamke kujituma unaipata hii, kama wewe tu ulivyo ndani ya ofisi hii” “Nikupe hongera shosti wangu kwa hilo, haya nilisikia ulikuwa Ulaya umerudi lini?” “Yaani hivi unavyoniona ndiyo naingia kazini kwa siku ya kwanza” “Kumekupenda sana huko Ulaya”
“Halafu nyinyi mna tabia mbaya sana, yaani mmenivizia nimeondoka ndiyo mkafanya harusi yenu”
“Shosti sasa hapo sina kosa maana ulitutoroka wewe mwenyewe, yaani harusi ya Afande wako mwenyewe umeingia mitini”
“Ila hongera sana, Baba kijacho na Mama Kijacho”
“Asante shosti, wewe vipi mwenzetu lini tunakula pilau na sisi”
“Mwenzangu yaani hata mpango sina sasa hivi”
“Shosti usiseme hivyo umri unakimbia huu”
“yote mipango ya Mungu, nilikuja mara moja kukuona wacha nikukimbie mida hii nahitaji niwahi nyumbani nina ishu muhimu”
“Haya shosti, namba yako kwanza basi”
Walibadilishana namba za simu na waliagana, Inspekta Jane ndiyo alikuwa wa kwanza kutoka ndani ya ofisi hiyo na kuondoka. Sara alifuata baada ya kufunga ofisi yake akiwa na furaha sana kwa kutembelewa na aliyekuwa hapatani naye akiwa chuo, alifurahi sana kuweza kuongea naye. Aliamini kabisa zile zilikuwa ni akili za kitoto tu kipindi wapo masomoni na sasa zilikuwa zimewaondoka, kinyongo alichokuwa nacho kipindi kile kilikuwa kimemuisha. Hakujua kabisa kuwa huyo aliyekuja hapo alikuwa ana kinyongo bado kisa Mwanaume aliyekuwa naye, hakujua kabisa huyo alikuja kumsalimia lakini si kwa nia ya urafiki.
Siku hiyo ilipita na siku nyingine ikafuata hatimaye nayo ikakatika na hata juma nalo likafutika, Inspekta Jane alikuwa tayari ana mawasiliano na mke wa Afande mwenzake. Urafiki wa kinafiki tayari alikuwa ameuanzisha tangu alipoenda siku ile ofisini kwenda kuhakikisha kama kweli alikuwa mjamzito. Mazoea yalienda na hatimaye iikafikia hatua akakaribishwa nyumbani kwa Afande mwenzake, napo alipazoea na hata alipomkuta Afande huyo alikuwa akimchangamkia ingawa alikuwa akijua alikuwa hahitaji uchangamfu ule aliokuwa nao. Sara akiwa hajui chochote kilichokuwa kimetokea kwenye maisha ya nyuma ya Mume wake alikuwa ni mwenye kuona walikuwa ni wana maelewano mazuri, Inspekta James naye alijua kulificha hilo suala na hakutaka mke wake awe na chuki na mtu mwingine. Aliweza kumficha na hata wakwe zake walipojua kuhusu hilo bado mke wake hakuwa akijua chochote kile, jinsi mke wake alivyokuwa akimpenda aliona kutakuwa na mtafaruku mkubwa sana ikiwa itajulikana. Alikuwa akijulikana aliwahi kupata na upofu lakini hakuwa akijulikana aliwahi kunyanyaswa na hata kutupwa jalalani, yote yalibaki siri yake ingawa hakutakiwa kukaa na siri kwa mke wake.
Chuki aliyokuwa nayo kwa Inspekta Jane bado alikuwa nayo na haijaisha hata kidogo, moyo wake ulikuwa unagoma kabisa kuwa na ukaribu na mtoto wa adui yake ambaye aliwaua wazazi wakena kumtia upofu. Kugoma kwa moyo ndiyo kulimfanya hata asihitaji kuwa karibu na binti huyo, hakutaka kuulazimisha moyo kwani alikuwa akijua wazi kufanya hivyo ni kujidanganya. Aliamua kuendana na moyo jinsi ulivyokuwa ukitaka na si alivyokuwa akitaka yeye. Kila alipoiona sura yake alikuwa akikumbuka jinsi alivyopigwa nyumbani huku akifokewa, kumbukumbu ya tukio hio ilimkumbusha na jinsi alivyokuwa akisikia sauti za wazazi wake siku ambayo waliuawa. Kutokana na kumbukumbu hizo kiukweli kabisa hakutaka kabisa kuiona sura ya Inspekt Jane, uwepo wa ajira nao ulimfanya awe anamuona kila siku.
**** Upande wa Inspekta Jane kadri siku zilivyokuwa zikizidi kwenda alikuwa akijaribu kumsahau Inspekta James lakini ilishindikana. Alianzisha hata uhusiano na mwanaume aliyekuwa na mvuto kama Inspekta James lakini bado alishindwa kumsahau, hii ilifanya hata aweze kuachana na mawanume huyo kwa ugomvi mkubwa san. Ugomvi huo ulitokana na yeye kutaja jina la ‘James’ akiwa yupo kunapo kati ya raha na mwanaume huyo, mtafaruku huo uliotokea kwenye chumba cha hoteli ulikuwa ukielekea kumuumiza na laiti kama angekuwa si Asakri basi angeumia vibaya. Siku hiyo aliondoka kwenye chumba hicho cha hoteli akiwa ametumia mafunzo yake ya kijeshi kumjeruhi huyo Mwanaume wake aliyeingiwa na wivu akataka kumpiga. Tangu siku hiyo aliona hana haja ya kuudanganya moyo wake ikiwa alikuwa akilikumbuka jina la aliyekuwa akimpenda akiwa yupo na mwingine.
Jina la James lilikuwa limemkaa kichwani na hata kinywani na hakuwa na namna ya kulisahau kabisa,hitaji la kuwa la kuwa na Inspekta James lilikuwa limezidi upande wote na akaona alikuwa akimhuhitaji zaidi. Taratibu hitaji hili lilikuja kumfanya ajihisi na wivu kila akimuona Inspekta James akiwa yupo na mkewe, aliona kama alikuwa akidhulumiwa na mwanamke mwenzake ambaye alikuwa na haki. Jambo hili llimfanya aitie vituko ndoa hiyo kila mara lakini kutokana uimara wa wapendao nao hao, waliweza kuvikabilia vituko vyote. Inspekta Jane hakuchoka aliendelea na harakati za kuifanya ndoa hiyo isidumu kabisa, yote alishindwa kwani alikutana Mwanamke ambaye alikuwa na moyo thabiti katika kumpenda mume wake. Alifikia hata hatua ya kuwatuma wanawake waje nyumbani kwa Inspekta Jame wakijifanya ni mahawara zake walikuwa hawahudumiwi, yote alishindwa kabisa kwani kila walichokuwa akiambiwa aliamini ni uongo kabisa. Walipozidi kuja mara kwa mara ndiyo aliamini walikuwa wakitumwa, upendo na kuaminiana ndiyo ilikuwa silaha ya ndoa hii ndiyo Inspekta Jane alishindwa kuishambulia hadi iyumbe.
Alipoona alikuwa hawezi kumuweka Inspekta James kwenye himaya aliamua kuvuruga kila kitu, alikuwa yupo radhi amkose na mke wake pia amkose kuliko kumuona akimuumiza moyo wake. Hii ilimfanya apange mpango wa kutaka kumuangamiza Inspekta James akiona roho yake itatulia ikiwa ataondoka kwenye uso wa dunia hii, alianza kuutekeleza mpango kwa kutaka kumuwekewa sumu mara mbili alipokuwa akija nyumbani kwake lakini jaribio hilo lilishindikana. Muumba alikuwa yupo na wanandoa hawa ndiyo maana hata majaribio hayo yalishindikana, alijairbu tena kumuwekea kwenye kinywaji sumu alipojumuika nao kwenye matembezi. Siku hiyo alifanikiwa kumuwekea sumu lakini bahati mbaya kinywaji hicho kilimwagika kabla hata hakijatumiwa na Inspekta James. Bado hakuchoka na aliamua kuumiza kichwa kwa mra nyingine, alitafuta mbinu nyingine ya kumuua Inspekta James na hatimaye akaona jaribu bahati yake kwa siku ya mwisho. Alijiapiza akishindwa kwa mbinu hiyo basi hatojaribu mbinu nyingine tena, ukatili aliokuwa nao baba yake naye tayari ulikuwa umeshavamia moyo wake. Siku ya siku ambayo alikuwa amedhamiria kumuua Inspekta James kwa mbinu nyingine kabisa, ilikuwa ni siku ambayo Mama yake mzazi alikuwa akija kumuona kazini ili amuage kwani alikuwa akisafiri ghafla. Pia ilikuwa ni siku ambayo Sara akiwa pamoja na Mama yake walikuwa wametoka kuwachukua wakwe wa hiyari wa kule shamba walikuwa wakija nao mjini, siku hiyo ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa Sara hivyo walikuwa wakija kuhudhuria sherehe ambayo ingefanyika hapo baadaye nyumbani kwa Inspekta James. Majira ya kufanya hila ilipokaribia ilikuwa ni muda ambao Inspekta Jame alikuwa akitoka ofisini mara moja, Insekta Jane alikuwa amelitambua hilo na tayari alikuwa ameharibu breki ya gari.
Inspekta Jame alitoka hadi ndani nje na akaingia ya gari lake na alipoingia aliliwasha, alipotoka kuondoka alikumbuka alikuwa amesahau kitu muhimu ofisini kwake. Kutokana na haraka aliyokuwa nayo aliacha gari ikiwa inawaka na kisha alikimbia ndani ili awahi aje kuendelea na safari. Muda ambao anatoka kulikuwa na mahabusu waliokuwa wakishushwa kwenye gari baada ya kutoka mahakamani, kitendo cha kuacha ufunguo namna ile kilikuwa kimeonwa na Askari mmoja bandia aliyekuwa amechomekwa kumuokoa Mhalifu mwenyewe aliyekuwa anatoka mahakamani. Walitazama kila upande na kwa kasi ya ajabu yule Askari bandia aliwashambulia Maasakari halisi na kisha alikimbia pamoja na Mahabusu ndani ya gari ya Inspekta James, waliliondoa kwa kasi sana huku wakiacha risasi zikituia juu ya bati la gari hilo. Lango muda huo lilikuwa lipo wazi na walilivuka sasa wakawa wanakaribia barabarani, ilimbidi Yule Mhalifu aliyekuwa akiliendesha gari hilo akanyage breki kupunguza mwendo. Hawakujua kama gari hilo lilikuwa limeshaharibiwa breki, loh! alipokanyaga breki ilikuwa hakuna hata ya kupapasia. Mhalifu huyo alijikuta akikanyaga breki hata kasahau kuangalia mbele kwa jinsi alivyochanganyikiwa, mwenzake ambaye alijifanya Asakri alikuja kumgusa kumfanya aangalie mbele alikuwa tayari ameshachelewa. Alikutana uso kwa uso na gari aina ya toyota landcruiser, kishindo cha kugongana kilifanya hata magari hayo yayumbe na kulivamia gari jingine ambalo lilikuwa likipita kwa kasi likitokea njia iliyokuwa ikielekea nje ya mji. Ilikuwa ni ajali ya magari matatu ambayo iliwacha midomo wazi wote waliokuwa hapo karibu kutokana na jinsi magari hayo yalitoa kishindo. Maaskari magereza ambao walikuwa wakiwafukuza wale Wahalifu kwa risasi waliwasili hapo wakaikuta gari ya mkuu wao ikiwa haitazamiki kwa jinsi ilivyoharbika, pia walizishuhudia gari zingine mbili ambapo moja ilikuwa ikijulikana wazi kwao. Wote walipigwa mshangao na hata walibaki wakiwa wamezubaa kwa sekunde kadhaa, walikuja kushutuliwa na kelele za Inspekta James ambaye alikuwa ameyaona magari hayo.
“Saraaaa!” Inspekta Jame alipiga kelele kwa nguvu huku akiliendea gari dogo moja lililokuwa limepondeka kutokana na ajali hiyo. Loh! Aliliona gari la mke wake ambalo alilitambua kupitia bati la namba za usajili, Inspekta James siku hiyo alichanganyikiwa kabisa. Makelele yalimtoka kama mwendawazimu huku akilisogelea gari la Sara ambalo alilizunguka, kupondeka kwa gari hilo ndani aliona taswira ya kimiminika chekundu jambo ambalo lilifanya ndiyo azidi kuchanganyikiwa hata akajaribu kuvuta kuvuta mabati hayo yaliyokuwa yakipondeka. Ugumu wa mabati ulikuwa si kuvutika na mikono ya mwanadamu, hivyo Inspekta James alionekana ni mwenye kucheza tu na si kufanya chochote. Alipokuwa akipiga makelele hayo alisikia sauti ya makelele mengine kabisa, makelele hayo yalimfanya anyamaze kwa ghafla na aangalie kule ambapo kelele hizo zilikuwa zikitoke. Aliweza kumuona Inspekta Jane naye akilia akiwa amesimama kwenye landsruiser ambaye ilikuwa imepatwa na ajali hiyo, aliisikia sauti yake akilalalamika kwa kutaja jina la mama yake. Aliganda kwa sekunde kadhaa akimtazama hadi plae akili yake ilipokaa sawa na kurudisha macho kwenye gari la mke wake. Inspekta James naye alijikuta akilia kwa uchungu sana hadi maaskari wa chini yake wakaja kumkamata na kumshikilia kiuimara zaidi, muda huo tayari kikosi cha uokoaji cha jeshi la magereza pamoja na jeshi la polisi kilikuwa kimewasili.
Kazi ya utoaji miili kwenye magari ilikuwa ni ngumu sana kutokana na jinsi yalivyokuwa yamepondekza magari yote, kutokana na magari hayo kuwa katika kasi kipindi yanagongana. Inspekta James akiwa ametulizwa chini kwa nguvu sana aliweza kushuhudia ndani ya gari lake kukitolewa miili ya wale waliokuwa wameiba gari lake na kujaribu kutoroka. Hao ndiyo walikuwa chanzo cha ajali na kila alipowatazama mmojawapo alikuwa amevaa sare kama zake, loh! Alianza kuliona vazi ambalo alikuwa amevaa lilikuwa limefanya mauaji hayo. Saikolojia yake ilikuwa tayari imevurugika kama alivyokuwa akiziona sare hizo kipindi cha nyuma, alipowatazama wale maaskari waliomshikilia aliona kama alikuwa ameshikiliwa na wauaji vile. Vazi la pili la kifungwa aliliona ni mojawapo ya vazi ambalo lilikuwa likihusika na tukio hilo baada ya kuliona kupitia mwili wa Yule Mahabusu ambaye alikuwa anatoroka. Alianza kupiga kelele huku akituhumu lakini hakuachiwa kutokana na kuonekana alikuwa amechanganyikiwa, akiwa kwenye kupiga kelele huko ambako kulichnganyika na kilioo. Aliweza kushuhudia pia gari ya mke wake ikikatwa mabati na kisha mwili wa kwanza ukatolewa ukiwa hauna uhai.
Hakika alimuona Sara akiwa ameumia sehemu mbalimbali za mwilini, mwili wake ulikuwa haujengi taswira nzuri kutokana na kujaa damu sehemu mbalimbali. Inspekta James alilia zaidi akimtazama mke wake aliyekuwa na ujauzito akifunikwa na shuke jeupe, aljaribu kufurukuta kwenye kundi la Askari waliokuwa wamemshikilia lakini hakufua dafu. Uokoaji uliendelea na hata aliishuhudia miili mingine mitatu ambayo ilikuwa ikitambulika kwenye macho yake ikitolewa, alizidi kuchnganyikiwa aliipoiona miili ya wazazi wake wa hiyari pamoja na Mama mkwe wake ikifunikwa na shuka pia. Kilio kilimtoka hadi nguvu zikaanza kumuishia, akiwa yupo kwenye hali hiyo alijikuta akishtuka baada ya kusikia makelele mengine ya mtu ambaye alikuwa amechnganyikiwa.
“Uwiiiii! Nimemuua Mama yanguuuuu!” Sauti ya Inspekta Jane akiwa akiwa ameshikiliwa alipouona mwili wa mama yake nayo ilipaa hadi ikafika mwenye masikio yake, hasira zilimpanda aliposikia kauli hiyo na akaona kabisa ajali hiyo ilikuwa ikihusika na mikono ya Inspekta Jane.
Kutokana na kuwa mwenye kuishiwa nguvu Maaskari waliokuwa wamemshikilia walilegeza mikono, walipokuja kutahamaki Inspekta James alikuwa tayari ameshawachomoka ghafla. Walimuona akitoka mbio huku akielekea kwenye eneo ambalo alikuwepo Inspekta Jane aliyekuwa amevaa mavazi kama yake, alipomkaribia alirusha ngumi ya nguvu sana lakini mkono wake uliwahi kudakwa na Maasakri wengine waliokuwa wapo pembeni ambao walimuwahi. Hapo alishikiliwa na watu wengi zaidi kuliko awali kutokana na kuonekana alikuwa amechnganyikiwa, kundi kubwa la Maaskari waliokuwa wamemshikilia walikuwa wakijaribu kumrudisha nyuma kutoka kwenye eneo hilo. Inspekta James alipoona hakuwa amepata wasaa wa kuweza kumtia adabu mbaya wake aliishia kupayuka na kumtuhumu kwa kile alichokuwa akikifanya, alikuwa akiwapa faida watu waliokuwa wamekuja kushuhudia tukio hilo la ajali.
“James nisamehe mimi sikujua kabisa, kukupenda ndiyo chanzo cha haya. Niliona bora tukose wote kukuua wewe kumbe natafuta matatizo mengine zaidi” Inspekta Jane aliropoka huku akipiga kelele kwa nguvu sana, haikupita muda alipoteza fahamu na maaskari waliokuwa wamemshukilia walimpeleka kwenye eneo la huduma ya kwanza.
Hali ilikuwa tete kwa Inspekta James pia kutokana na kuusikia ukweli, shinikizo la damu ambalo halijawahi kumsumbua kwa mara ya kwanza lilimsumbua na alipoteza faamu akiwa yu mwenye hali mbaya sana. Alianza kupatiwa huduma ya kwanza na maaskari wenzake lakini hali ilizidi kuwa tete kila walipokuwa wakihakiki vipimo vya shinikizo la damu, lilikuwa likishuka kila muda waliokuwa wakihangaika naye kumpatia huduma ya kwanza. Hali hii ilifanya gari la wagonjwa liitwe upesi na yeye kukimbizwa hospitalini ili kuokoa maisha yake. Zoezi la kutoa mili ndani ya magari yote baada ya kukamilika, gari la kuchukua miili hiyo liliibeba kwa jili ya kwenda kuhifadhiwa. Baada ya gari hilo kuondoka mabaki ya magari yaliondolewa eneo lote na babrabra ilisafishwa, gari lenye kubeba magari yaliyopatwa na ajali lilifika hapo. Magari yote matatu yalibebwa kwa kifaa maalum na kuwekwa kwenye gari hilo, yaliondolewa eneo hilo na barabara ikabaki ikiwa ni yenye mabaki madogo ya vioo.
**** Taarifa za kutokea kwa vifo hivyo zilimfikia SP Mwambe akiwa yupo ofisini kwake, ilikuwa ni siku ambayo alilia kama mtoto mdogo alipoipata taarifa hiyo akiwa ofisini. Kazi zote hazikufanyika kabisa na hata usafiri wake mwenyewe alishindwa kuuendesha, siku hiyo alishikiliwa na kupelekwa hadi hospitalini ambako miili ya awapendao ilikuwa imehifadhiwa. Akiwa ni mwenye kuongozana na kijana wa chini yake kicheo aliweza kupelekwa kuona miili hiyo, kilio kilizidia baada ya kuiona miili yote. Hakuwahi kuwaza kama ipo siku watu hao awapendao watakuja kuondoka ndani ya dunia hii na kumuacha peke yake akiwa hana ndugu yeyote. Mke wake na mtoto wake wa pekee wote walikuwa wamefarikia siku moja, ni pigo ambalo hajawahi kulipata kwenye maisha yake yote ambayo aliyapitia. Pigo la kwanza kulipata kwenye maisha yake ilikuwa ni kufiwa na mtoto wa kiume aliyefariki akiwa bado mchanga kabisa, alipopta mtoto wa kike katika uzao wa pili moyo wake ulitulia na upendo aliuweka kwa mwanae. Sasa mtoto wake huyo pekee ndiyo alikuwa amemuacha bila hata kusema hata kwaheri, utuzima wake aliokuwa nao siku hii alilia kama mtoto mdogo
Hali ilikuwa ni hiyohivyo kwa Kamishna Msaidizi Philipo Lutonja alipopokea taarifa za kifo cha mke wake, alilia sana kwa kumpoteza Mwanamke ambaye alikuwa akimpenda sana. Mwanamke ambaye alihangaisha moyo wake kumpata na hata akasaidiwa na rafiki yake Marehemu SSP Nkongo katika kumpata, sasa hakuwepo naye kabisa ndani ya dunia hii. Upweke tu ulikuwa ukiuvaa moyo wake pindi alipokuwa akiondoka mbali naye, alikuwa akitamani arejee hata alipokuwa yupo safarini kutokana na kutamani kuwa naye kila dakika. Sasa alikuwa ameondoka kiumjumla na hatarejea tena, hakutarajia kabisa jambo kama hilo kama litaweza kuja kumpata. Kilio chake naye kilipelekea kupoteza fahamu kama Inspekta James kutokana shinikizo la damu kupanda, siku nzima hakuamka alikuwa yupo mahututi kitandani. Matabibu walikuwa wakihangaika katika kuyaokoa maisha yake, alipokuja kuzinduka kutoka kwenye kuzimia huko alikuwa hawezi hata kutembea. Msiba tayari ulikuwa umewekwa na yeye alikuwa yu kwenye kiti cha magurudumu katika muuda wote aliokuwa yupo msibani, alikuwa ni mkimya ana asiyetaka kuongea na mtu yeyote. Huduma zote muhimu alikuw akifanyiwa kutokana na mshtuko huo aliokuwa amepata, hakuwa na tofauti kabisa na Mlemavu. Binti yake aliyekuwa amesababisha tukio hilo alikuwa tayari amerukwa na akili, alikuwa amefungwa kamba ndani ya chumba komoja cha nyumba hiyo huku akifanyiwa huduma zote kama ilivyo Baba yake. Mtoto wake mkubwa ndiyo aliongoza kila kitu kutokana na ndiye mtu pekee ambaye angeweza kusimamia, hakukuwa na mwingine ambaye alikuwa anajiweza ndani ya nyumba hiyo isipokuwa yeye tu.
**** Inspekta James alipokuja kurejewa na fahamu hakuwa na tofauti kabisa na mtu ambaye alikuwa amerukwa na akili, alikuwa akihudumiwa kila kitu katika kipindi chote cha msiba. Tofauti yake hakuwa mtu mwenye fujo yeye alikuwa kimya tu huku akiongea maneno ambayo yalikuwa hayana maana katika muda wote, alikuwa haishi kulitaja jina la mke wake. Hali hiyo ndiyo ilizidi kumuumiza SP Mwambe, mtu pekee wa karibu aliyekuwa amebakia alikuwa ni huyo ambaye amerukwa na akili. Wazee aliokuwa amesaidiana katika malezi ya Inspekta James nao walikuwa wapo kwenye vyumba vya kuhifadhi miili wakisubiria kwenda kupumzishwa kwenye nyumba zao za milele. Hatimaye siku ambayo ilikuwa imepangwa kuipumzisha miili ya marehemu wanne walioaga dunia ndani ya siku moja ilitimia, huu ulikuwa ni msiba wa pili kwa James kufiwa na watu wake wa karibu wenye idadi kama hiyo tangu walipoanza wazazi wake na Bibi yake. Muda wa kuaga miili hiyo kabla ya maziko James aliletwa akiwa ameshikiliwa kutokana na kurukwa na akili, marafiki zake wa karibu walikuwa akimuonea huruma sana kutokana na hali hiyo ambayo walikuwa nayo. Alifanikiwa kuuaga mwili wa mke huku akicheka kama ilikuwa habari ya kufurahisha kutokana na kurukwa na akili, miili mingine aliiaga kinamna hiyohiyo na kisha aliondolewa na taratibu zingine zikafuata. Mazishi ya miili yote minne yalifanyika jijini Dar es salaama kwenye Makaburi ya KInondoni, watu wengi waliokuwa wameguswa na tukio hilo walihudhuria huku wakimshudia Inspekta James alivyo.
Upande wa nyumbani kwa Kamishna Msaidizi Lutonja mazishi yalifanyika siku inayofuata baada ya kufanywa mazishi ya watu wa karibu wa SP Mwambe, watu wengi nao waliokuwa wameguswa na hali ambayo ilikuwa imempata Afisa huyo wa jeshi la Magereza walihudhuria kwa wingi. Ulikuwa ni msiba mkubwa lakini haukua umeuzidi ukubwa msiba ulifanyia siku iliyopita, wanahabari waliokuwa wakisaka habari kwa udi na uvumba kama ilivyokuwa kwenye msiba uliopita, walifurika kwa wingi sana kwenye msiba huo. Mazishi yalifanyika kwenye makaburi yaleyale yaliyofanyika mazishi siku iliyopita, Mume wa marehemu alishuhudiwa akiwa yu kwenye kiti cha magurudumu kutokana na kupatwa na hali mbaya kwa kifo cha mke wake. Watoto wote wa marehemu walikuwa wapo eneo hilo la maziko, Inspekta Jane waliweza kumuona akiwa yupo kwenye mikono ya maaskari imara wa jeshi hilo kutokana na kurukwa na akili. Wengi waliomuona walimulaani sana kutokana na kusababisha kifo cha mama yake mzazi, hawakujali hali ya kuchnganyikiwa ambayo ilikuwa imemkumba wao waliangusha laana zao pasipo kuzitamka waziwazi kutokana na kuingiwa na hasira. Binti kusababisha kifo cha mama yake kisa kutaka kumpoteza Mwanamke aliyekuwa hana mapenzi naye, ilikuwa ni jambo ambalo waliona alikuwa si kiumbe wa kawaida. Wengi walimuhukumu huku wakisahau hakuwa ni malaika bali alikuwa mwanadamu kama wao, alikuwa anakosea kama wanavyokosea wao. Maneno ya wanahabari wa magazetini yalikuwa tayari yamewapa sumu, hiyo ilikuwa ni habari ambayo ilitawala jiji zima na hata picha zake zilikuwa zimeshasambaa kwenye magazeti mbalimbaoli. Hakuna ambaye alikuwa haijui sura yake kutoka na jinsi magazeti yalivyoichapisha, wengi waliitambua vyema sura hiyo na haikuwapa shida kuanza kumnyoooshea vidole huku wakimuongelea vibaya. Pamoja na kurukwa huko na akili bado hawakumuonea huruma kabisa, wao waliendelea kumfanya mada katika eneo hilo la msiba hadi mazishini.
Maisha ya Inspekta James baada ya mazishi yalikuwa ni wa kuwekwa ndani akilelewa kama mtoto, SP mwambe alikuwa ameajiri wafanyakazi waliokuwa wakimuhudumia kwa gharama kubwa. Alikuwa akiendelea kumfanyia mipango ya kumpata Daktari ambaye angeweza kumpatia tiba, alihangika kwenye hospitali tofauti kila alipopata muda ilmradi tu James aweze kupona na arudi kwenye hali ya kawaida. Hakufanikiwa katika kipindi hicho alichokuwa akihangaika lakini hakukata tamaa naye, upendo aliokuwa naye kwa kijana huyo ambaye alikuwa akimheshimu kama baba yake mzazi. Ulimfanya asichoke kumuhudumia wala kutafuata matabibu tofauti, alikuwa akifanya kazi na kila muda wa kupumzika alikuwa akihangaika naye. Baada ya kuona tiba za hospitalini zilikuwa zikishindikana, alidiriki hata kwenda kwa waganga wa kienyeji ilimradi mwanae wa kumlea aweze kuwa sawa. Waganga wa kienyeji ambao hawakuwa wakiweza kulitibu tatizo hilo nao walijua kuila pesa kwa kumdanganya mambo mbalimbali, alijikuta akimaliza pesa kwa waganga na hatimaye akajikatia tamsa. Marafiki wakubwa wa Inspekta James ambao ni Norbert Kaila pamoja na ASP Wilfred nao hawakuchoka kabisa kuja kumuona rafiki yao, walikuwa wakimtia moyo sana SP MWambe juu ya hali ambayo alikuwa nayo kijana wake. Hawa nao walifanya hata asichoke kumlea kijana wake, alikuwa nao bega kwa bega pale ambapo panahitajika msaada wowote ule kutoka kwao. Nao walisaidia katika kumtafutia wataalamu mbalimbali,wote walikuwa wakihitajia kumuona rafiki yao akirudiwa na hali ya kawaida.
**** Upande wa Inspekta Jane hali ilikuwa ni mbaya zaidi hadi ikafikia hatua ya kufungwa kamba, alishawahi kutoroka zaidi ya mara moja akiwa yu katika hali ya kurukwa na akili. Pia alishajaribu kufanya jaribio la kujiua baada ya kushika kisu pindi alipovamia jikoni, alikuwa akitunzwa kwa jicho la umakini sana. Baba yake naye alikuwa amepewa mapumziko kutokna na hali ambayo alikuwa nayo huku akiendelea na matibabu, wote wawili walikuwa ni watu wenye kuhudumiwa kila muda. Mtu pekee ambaye alikuwa akiweza kwenda kuendelea na majukumu alikuwa ni mtoto mkubwa familia hiyo, ilikuwa ni familia ambayo ilitawaliwa na ukimya mkubwa sana kutokana na huzuni ambayo walikuwa wanayo. Furaha ile ambayo ilikuwa ipo hapo awali ilitoweka kabisa, ukimya ndiyo ulikuwepo katika kipindi chote. Ulipita mwaka hali ikiwa ni hiyohiyo huku Mzee Lutonja akiwa ameanza kutembea lakini kwa shida sana, Binti naye ukichaa ndiyo ulikuwa umemkomaa kabisa. Hawakuweza kukaa naye hapo ndani ya nyumba hiyo kwa balaa alilokuwa akilileta, ilibidi apelekwe kwenye hospitali maalum ya kutunza watu wenye ulemavu wa akili.
Ndani ya mwaka huo mpya SP Mwambe aliweza kupandishwa cheo akawa Mrakibu mwandamizi wa jeshi la magereza(SSP), mwaka huohuo pia ikiwa imetimia mwaka mmoja tangu Inspekta James arukwe na akili. Norbert alipendekeza apelekwe barani Ulaya ambapo kulikuwa kulikuwa na mtaalamu ambaye angemtibu, gharama zake zilikuwa kubwa lakini kutokana na wote kumuhitaji aweze kupona walichanga na kikapatikana kiasi ambacho kilisaidia kusamfirsha hadi huko. Alikaa huko kwa nusu mwaka akiwa ameongozana na Norbert, hatimaye aliweza kurudi kwenye hali yake ya kawaida taratibu. Alipopona kabisa aliruhusiwa kurudi nyumbani Tanzania akiwa na rafiki ambaye alimpa shukrani kubwa sana, uwanja wa ndege alipokewa na watu wake wa karibu na kisha alipelekwa hadi nyumbani kwa Baba yake mlezi. Ilikuwa ni siku ambayo ilikuwa ya furaha sana kupona kwake, jioni ya siku hiyo walifanya tafrija fupi katika kumkaribisha tena kwa mara nyingine nyumbani. Tafrija ambayo bado Inspekta James aliona mapungufu yaliyokuwa yapo, hakuwa amezoea kufurahia ndani ya nyumba hiyo ila uwepo wa Sara na Mama yake. Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza na alijitahidi sana kuikabili hali hiyo ingawa ilikuwa ni jambo ambalo gumu sana kwake, watu wachache wa karibu waliokuwa wana faraja kwa kupona kwake ndiyo walihudhuria tafrija hiyo. Inspekta James aliweza kuwaona Maafisa wenzake wakiwa wapo kwenye nguo za kiraia ndani ya tafrija hiyo, wale waliokuwa wapo karibu na Marehemu Sara nao aliwaona pia. Faraja iliingia ndani ya moyo wake kwa kuwaona wakiwa wamefurahi kwa yeye kupona, alijumuika nao kwa pamoja katika kuifurahia siku hiyo. “Kikubwa ni kumshukuru Mungu kwani yeye ndiyo kila kitu ndani ya dunia hii, bila yeye nisingeweza kurudi katika uzima huu. Kaniacha na kidonda kikubwa sana lakini sipaswi kuilaumu kazi yake. Watu niliowapenda kawachukua kwa awamu lakini bado ninapswa kumshukuru kwani ameweza kunifanya niwe na pumzi hadi muda huu, amenilinda panapo hatari. Napaswa ni mshukuru. Pia nitakuwa mchoyo wa fadhila kama nikimsahau Baba hapa, Norbert na Wifred kwa kuchngia niweze kurudi katika hali ya kawaida. Hakika bil ya juhudi zao hawa nisingeweza kuwa mzima hadi leo hii, napenda nitamke kuwa ninawapenda sana” Inspekta James aliongea katika tafrija hiyo alipopewa nafasi ya kusema chochote, makofi yalipigwa baada ya kumaliza kutoa machache na kisha watu wakaendelea kufurahia. Siku iliyofuata habari kubwa iliyokuwa imetawala magazeti ilikuwa ni kupona kwa Inspekta James, kila gazeti lilikuwa na habari hiyo ingawa aikueleweka walikuwa wameipata vipi kutokana na jambo hilo kuwa ni siri kwa watu wa karibu waliokuwa wakitambua ujio wake nchini akitokea Ulaya. Siku iliyofuata ilikuwa ni muda wa kumiminika kwa watu ndani ya nyumba ya SSP Mwambe kuja kumuona huku waandishi wakitaka kumuona, hakuna ambaye alikuwa hajasahau tukio lilimkuta na wengi wao walikuja kumpa pole hapo nyumbani. Usumbufu wa wanahabari ulizidi na hatimaye wakaamua kuwazuia ili James aweze kupumzika kabla hajaripoti ofisini, hakuna ambaye alikuwa akimtakia mema hakufurahishwa na habari hii ya kurudi kwake katika hali ya kawaida. Siku zilisogea hatimaye alikuja kuripoti kazini baada ya kuwa nje kwa muda mrefu sana, ilikuwa ni kipindi ambacho kulikuwa na utawala wa Rais mpya nchini Tanzania ambaye alikuwa akiitwa Zuber Ameir. Kipindi hiki ndipo James alipobadilika na kuwa si yule wa awali hata marafiki aliyokuwa nao hapo ofisni walianza kumuogopa. Kumbukumbu ya kifo cha mke wake ndiyo ilimfanya awe hivyo, kila alipokua akivaa vazi lake la ofisini alijikuta akiwa anajichukia yeye mwenyewe akilitazama kwenye kioo. Alipoyaona mavazi ya wenzake ndiyo kabisa hakukuwa kuna maelewano, alikuwa akijaribu kujibu maongezi yao walipokuwa kikazi tu. Ucheshi wake aliokuwa nao hapo awali uliondoka kabisa, sura yenye hasira katika kila muda akiwa yupo ofisni ndiyo ilimtawala. Ule uzuri wake wa sura ulipotea kabisa kutokana na kuwa mwenye kukunja sura muda wote, alikuwa si Afande yule muelewa ambaye alikuwa amezoeleka na wafungwa kama ilivyokuwa hapo awali.
Kitendo cha kifo cha wazazi wake, mke wake na wale wote aliokuwa akiwapenda kusababishwa na nguo kama zake za kazi pamoja na nguo za wafungwa. Alianza kuwachukia wafungwa wote waliokuwa wapo humo ndani pamoja na maaskari wenzake,kazi alikuwa akizitekeleza kama kawaida lakini hakuwa na maelewano na Askari yeyote aliyekuwa yupo kwenye sare za kazi. Jambo hili lilikuwa tayari limeshagundulika kwa SSP Mwambe lakini alishindwa pa kuanzia kwenda naye hospitali kutokana na hali hiyo. Kipindi hiki ndipo marafiki zake wa karibu walipogombana kutokana na tuhuma ambayo alikuwa amebebeshwa mmoja, Norbert na Wilfred walikosana baada ya kuchapishwa tuhuma dhidi ya Wilfred. Taaluma ya uandishi aliyokuwa nayo Norbert ndiyo ilisababisha waweze kufarikiana, Inspekta James alikuwa akiongea nao kwa pamoja na hata alipojaribu kusuluhisha ilishindikana. Muda baada ya kazi katika kipindi cha kuwa mwenye kuwa na sura ya huzuni kila wakati, alikuwa akiutumia katika kucheza ngumi na mazoezi ya viungo. Hakuwahi kuwaza kuwa na Msichna yeyote yule katika maisha yake baada ya kuondokwa na mke wake, nyumbani kwake aliongeza vifaa vingi vya mazoezi. Hakuwa mtembeai kabisa kila alipokuwa nje ya kazi, yeye alikuwa ameelekeza nguvu katika mazoezi kila siku. Mwili wake ulijengeka na kuwa mkakamvu zaidi na wenye kukaa kimazoezi zaidi, alikuwa ni mwenye kifua kipana. Kimo kirefu ambacho alikuwa amerithi kutoka kwa baba yake kilimfanya azidi kuonekana ni mwenye mwili mkubwa, maisha yalikuwa yakiendelea huku wafungwa ndani ya gereza wakiwa wamembatiza jina la Mnoko kutokana na kutokuwa na huruma nao. Kila ilipotokea fujo yeye ndiyo alikuwa akiingia ndani ya gereza hayo ikiwa wafungwa watukutu watawazidi nguvu maaskari, aliogopwa sana ndani ya gereza kutokana na ukatili aliokuwa akiufanya katika kupiga wafungwa waliokuwa watukutu.
**** Ndani ya kipindi hiki ndiyo Mzee Lutonja alipona kabisa na alirejea tena kazini, kama kawaida vyombo vya habari viliitoa habari hiyo ya kurejea kwake kazini baada ya kupona. Nyumbani nwaandishi walikuwa hawaishi kuja kumuhoji katika kipindi cha mwanzo alichokuwa na faya njema kabisa, aliendelea na kazi kama kawaida lakini hakuweza kuacha tabia yake . Kuisahau tabia yake ya uhaini ilikuwa ni ngumu sana, ni sawa na nyani kulisahau pori, aliunda kikundi kipya kabisa akachana na kikundi ambacho kilikuwa kipo chini ya Mtandao ambacho alikuwepo baada ya kujitoa kwenye genge la Ibrahim aliyekuwa na cheo cha Luteni Jenerali tayari na alikuwa ni mnadhimu mkuu wa majeshi. Uuuzaji wa unga ndiyo ilikuwa biashara yake kubwa ambayo ilimuingiza pesa na akawa ni mwenye pesa nyingi kuliko awali, kipindi hicho tayari alikuwa ameshaanza kujenga chuki ka Inspekta James akimuona yeye ndiyo chanzo cha kufa kwa mke wake. Aliamini bila ya yeye kumfanyia matesomakubwa binti yake, mambo hayo yasingetokea kabisa. Alikuwa kila siku ya maisha yake akitafuta sababu ya kuweza kumuondoa kazini, alitaka amchafue ndani ya nchi hii kwa watu waliokuwa wakimuonea huruma baada ya kukutwa na matukio ya kusikitisha Tuhuma za kwanza dhidi ya Inspekta James ilikuwa ni juu ya unyanyasasi wafungwa, tuhuma hiyo ilitupilia mbali kabisa na mkuu wa jeshi la magereza baada ya kuulizwa wafungwa wanyonge gerezani. Wengi wa wafungwa wanyonge walikuwa wakisema alikuwa amewafanya waishi kwa amani, walikuwa hawaonewi kabisa kutokana na uwepo wake ndani ya gereza. Hii ilifanya tuhuma hiyo isiwe na nguvu kabisa, aliendelea kutafuta nafasi nyingine ya kuweza kumuharibia kazi kijana mabaye hakuwa na hatia yeyote ile kwake.
**** Mwaka miwili baadaye James alikiacha cheo cha Ukaguzi na hatimaye akawa Mrakibu msaidizi wa jeshi la magereza (ASP), kipindi hiko ndipo kulitokea mauaji ya mkuu wa majeshi nchini Jenerali Kulika. Tuhuma zote zilishushwa kwa Professa kijana Moses Gawaza, mwezi mmoja baadaye ilikuja kujulikana kuwa tuhuma hiyo alisingiziwa na wale wote waliokuwa wakihusika walijulikana. Kipindi hiki ndipo alipotambua rafiki yake kipenzi ambaye alidai alikuwa akipakaziwa habari na Norbert aliingizwa gerezani, alikuwa ni Wilfred ambaye alikuwa na cheo cha ukamishna tayari katika jeshi la polisi. Kuanzia siku ambayo alivaa vazi la Wafungwa ndiyo ulikuwa mwisho wake wa kuwa na urafiki naye. Hakuwa akimchukulia kama rafki yake na hata pale lilipofanyika kosa kubwa na yeye akihusika basi kipigo kilikuwa kinamhusu. Ndani ya mwaka huo ndiyo gereza jipya la wafungwa wenye makosa mazito lilifunguliwa, Maaskari wote watukutu waliamishiwa kwenye gereza hilo huku ASP James ambaye alizoeleka kuitwa ASP Nkongo akibaki gerezani hapo. Alibaki na wafungwa wenye akosa ya kawaida sana, wao nao walipokuwa wakileta ubishi walikuwa wakpewa kipigo kizito. Tabia hii ya kupiga wafungwa ndipo Kamishna Lutonja alipokuja kupata njia ya kuweza kumpakazia jambo. Aliletwa gerezani mfungwa mtukutu mmojawapo gerezani hapo, Mfungw huyo ilikuwa n imtego ambao ulikuwa umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kufikia lengo lake. Mfungwa huyo alifanya utukutu akiwa yupo gerezani, taarifa zilipomfikia ASP Nkongo alimpa kipigo kizito sana ambacho kilipelekea alazwe hospitali. Akiwa yupo huko hospitali tayari Tabibu ya jeshi hilo alikuwa ameshakula hongo, alimmaliza kabisa na hapo ikawa ni tuhum nzito ambayo haikueleweka ilisambaa vipi uraiani. Magazeti mbalimali yaliandika habari ile huku mengi yakisema alikuwa ameonewa, rekodi za gerezani zilikuwa zikionesha alikuwa ni mtuhumiwa wa wizi ambaye alikuwa yupo Mahabusu. Kukuzwa mambo kwa habari hiyo na magazeti zilifika hadi kwa Kamishna Jenerali wa jeshi la Magereza, huyo aliagiza uchunguzi ufanyke na kisha ASP Nkongo akaitwa na kuhojiwa. Tuhuma ilionekana kuwa nzito ambayo ilimuelemea kabisa, makamishna walikuwa kama wameambizana kwa jinsi walivyokuwa wakishusha shutuma juu ya kulichafua jeshi la Magereza. Aliyekuwa akimtetea alikuwa ni Kamishna msaidizi mwandamizi Mwambe, huyu ndiye alisimama peke yake katika kumtetea ili asiharibikiwe na kibarua. Utetezi wake uliokuwa na mshiko ulisikilizwaa na hatimaye uchunguzi kwa mara ya pili katika mwili wa Mfungwa ukafanyika, kilichosabaisha kifo chake kilionekana kilikuwa ni kitu kingine kabisa baada ya uchunguzi huo kumalizika. Ilionekana alikuwa amekabwa na kuuliwa akiwa amelazwa, tuhuma hiyo ndipo ilipohamia kwa kuitwa Daktari aliyekuwa akimtibu kuja toka maelezo yake siku inayofuata. Siku ya kutoa ushahidi wake Dakati huyo alikutwa akiwa amefariki nyumbani, hapo kulionekana na kulikuwa na mchezo mchafu uliokuwa ukihusika na ASP Nkongo hakuonekana na hatia yeyote ile. Ili kuepusha maneno zaidi ya wanahabari ilibidi ahamishiwe Gereza jipya ya Nyumba giza kuwafuata Maasakri watukutu waliotangulia. Baaada ya uhamisho huo kufanyika ulipita mwaka mmoja ndipo Mzee Mwambe akapandishwa cheo na Mheshimiwa Rais kuwa Kamishna kamili, aliteuliwa kuwa mkuu wa gereza la Nyumba ya giza akichukua nafasi ya aliyekuwa mkuu wa gereza hilo ambaye alifikia umri wa kustaafu. Alipewa muda wa kujiandaa na maisha kuianza safari yake ya kwenda kuripoti eneo jipya la kazi ambalo kulikuwa na Mwanae wa kumlea, katika kupandishwa huko ndipo mkuu wa magereza alistaafu na nafasi yake ikachukuliwa na Mzee Lutonja aliyekuwa Kamishna baada ya kupandishwa cheo na kuwa Kamishna Jenerali. Uteuzi huo hakuupenda kabisa Kamishna Mwambe lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kuukubali, hakuwa na mamlaka ya kuingilia uteuzi wa Amiri jeshi mkuu. Muda wa kuripoti kwenye eneo jipya la kazi ulipotimia alichukuliwa na helikopta maalum kutokana na gereza hilo kutokuwa na njia nyingine ya kuweza kuingia, siku hiyo akiwa kwenye vazi lake la ofisini alipokelewa na Maafisa wa jesi hilo katika kituo kipya cha kazi. Ilikuwa ni siku ya furaha kuweza kuungana na mwanae mlezi, walipoonana furaha ilizidi hata wakakumbatina kutokana na kukaa muda mrefu bila kuonana. Kamishna Mwambe aliyaanza maisha mapya ndani ya ofisi yake mpya na akatokea kuheshimiwa sana na vijana wa chini, upendo aliokuwa nao na pia kukaa na watu tofauti ndani ya gereza hilo. Kulimfanya ajichukulie heshima hiyo, maaskari wote walifurahi sana kumpata kiongozi kama yeye ambaye alikuwa akikaa nao kama marafiki baada ya muda wa kazi, huko alianza maisha mapya akiwa hana cha kupoteza alichokiacha huko uraiani. Mtu wake muhimu alikuwa yupo ndani ya gereza hilo tu, aliyekubai maisha hayo na aliona ni afadhali hata aendelee kuishi hukohuko miaka yote. Kipindi hiko ndipo alipopokea lawama juu ya ukimya aliokuwa nao ASP Nkongo, ukaribu wake na kuelewana naye kuliwafanya wengi walalamikie juu ya tabia yake. Kutoongea na mtu ndiyo tabia ambayo ilikuwa ikiwakera sana maofisa wenzake, walimuona mwanzoni alikuwa na maringo lakini kuwa na hasira kulikuja kuwaaminisha hakukuwa na maringo yeyote yale kwenye nafsi yake. Wapo waliojaribu kukaa naye karibu katika kipindi cha kazi lakini walishindwa, wapo wale waliojaribu kuongea naye katika kipindi cha mazoezi wote wakiwa wana nguo za kiraia na walifanikiwa kuelewana naye. Walipoleta urafiki huo kipindi cha kazi wakiwa na sare waliambulia kutoleelewana, wapo waliodhani alikuwa akivuta bangi kutokana na tabia hiyo aliyokuwa nayo. Ila haikuwahi kuonekana akiivuta hiyo bangi jambo ambalo walishindwa kumtuhumu hivyo, walipoleta malalamiko hayo kwa Kamishna Mwambe alikuwa akiwaambia kila kitu kina sababu yake. Aliwaomba sana wamzoee huyo kwani hakupenda kuwa hivyo, kauli hiyo iliwafanya mwanzo wahisi alikuwa na ugonjwa wa akili. Habari zilipomfikia Kamishna alikanusha kabisa na akasema alikuwa na akili timamu kabisa na hakuwa kama hivyo wanavyodhani, hiyo iliwafanya wamuache ASP Nkongo kama alivyo na wakamzoea kama walivyoambiwa na mtu huyo ambaye alikuwa akielewana naye. Walikuwa wakiongea naye muda wa mazoezi tu katika kipindi wote wakiwa na nguo za kiraia, ingawa hakuwa na ucheshi kabisa.
Hamu ya kutaka kujua kile ambacho kilisababisha akawa hivyo ndiyo walikuwa nayo, walikuwa wakimsumbua sana Kamishna Mwambe juu ya kuwaeleza karibu kila siku. Hii ilipelekea nyakati hiyo ya mapumziko aamue kuwaeleza kisa cha yote hadi akawa akitoa sharti na kutojua mwenyewe kama wanajua habari zake
WAKATI ULIOPO
“Sasa jamani najua mmesikia yote kuhusu kisa cha James, niambieni sasa ingekuwa ni wewe ungekuwa kwenye hali gani” Kamishna Mwambe aliuliza
“Kwakweli mkuu hata mimi ningekuwa kenye hali hiyo” Mmojawapo alijibu “Yaani wazazi wako wauliwe uishi katika upofu kwa muda mrefu, unakuja kuwa na furaha lakini mwingine anakuja kuiharibu furaha hiyo” Kamishna Mwambe aliongezea “Kwakweli mkuu inamuma sana” Afisa mmoja wa kike aliongea huku machozi yakimtoka “Ndiyo mtambue sababu ya yeye kuwa hivi Nkongo wote wawili kuanzia baba na mwana si wananunaji wa hivyo” Aliwaambia “Jana hapa alipotabasamu nilimuona ni mwenye sura isiyo na ukatili hata kidogo,kwakweli namsikitikia sana” “Ndiyo ujue hakuna kiumbe aliyezaliwa na ukatili au roho ya kutokuwa na huruma, chanzo cha yote ni wanadamu” Aliwapa somo “Mkuu tumekuelewa” “Sasa ikiwa mnataka kuongea naye basi na tuwe na urafiki naye” “James ukitaka kuongea naye zingatia yafuatayo utaweza kuwa rafiki yake mkubwa sana, usije ukavaa sare za kazi kipindi unaenda kuongea na maongezi yenu yawe baada ya kazi. Nguo za kazi hizi za rangi ya brown akiziona nakumbuka matukio ya kifo cha mke wake na pia cha wazazi wake, waliosababusha haya wote walikuwa wamevaa nguo za aina hiyo pamoja na za wafungwa” Alimuambia “Sawa mkuu” “Ohoooo! Naona mitambo imekaa sawa kaeni angalieni mbele kuna mpira anaweza kuja muda wowote” Kamishna Mwambe aliongea baa baada ya mitambo ya televisheni kurudi tangu ilipoaktika, haikupita muda mrefu ASP Nkongo aliingia na kuja kuketi jirani na Baba yake mlezi. “Naona leo leo umekuja kwa mara ya pili kuja kuangalia mpira huku” Kamishna alimuambia huku akimtazama “Kuangalia mpira ndani muda mwingine kunaboa sana” ASP Nkongo alijibu huku akishangaa jinsi maofisa wenzake walivyokuwa wamekaa karibu na mkuu wao. “James” Afisa mmoja aliita na kupelekea atazamwe usoni,kutazamwa huko kulimpelekea amsifie kwa muonekano wake akiwa kwenye mavazi ya kiraia. Wengine nao walisifia hivyohivyo na kisha wakawa wanaangaia mpira huku wakiongea naye, ASP Nkongo ndani ya siku hiyo alishangaa sana kuona hadi maofisa wa kike wakiwa wanaangalia mpira. Mazungumzo kila muda ambao mpira ulikuwa ukibadilika muelekeo wake ndiyo yalitawala, waliokuwa wanajua mpira kiundani walikuwa wakitoa maelezo yao ambayo yalizusha mjadala huku mpira ukiwa unaendelea. Mechi ya siku hiyo iliyokuwa ikioneshwa kwenye luninga ilikuwa ikiwahusu mahasimu wakubwa wa timu ambayo anaishabikia ASP Nkongo, alikua akiiombea sana hiyo timu ambayo alikuwa akiishababikia iweze kufungwa. Kila muda timu pinzani ilikosa goli kwenye lango la mahasimu wa timu anayoishabikia alikuwa akiona walikuwa wamefanya uzembe mkubwa sana, haikupita muda mrefu mahasimu aliokuwa akiwachukia walishambuliwa sana na hatimaye wakafungwa. ASP Nkongo aliruka juu kwa nguvu huku akishangilia, alipokaa chini alimkata jicho Kamishna Mwambe alivyokuwa ametulia kimya kwani timu iliyofungwa ilikuwa ni timu ambayo anaipenda. Maafisa wote nao walimtazama jinsi alivyotulia kimya huku wengine kwa wakicheka, ama kweli kuangalia mira na hasimu wako tabu tupu. “Leo siku yenu Baba lazima mlale” Alimuambia Baba yake mlezi ambaye alikuwa amekaa kimya tu. “Haya mjanja wewe” Kamishna Mwambe hatimaye aliongea na wote walicheka kwa nguvu sana.
****
“Jamani huyu James msimuone hivihivi tu kapitia mengi sana hebu fikiria ungekuwa wewe ungefanyaje hapo?” Kamishna Wilfred ambaye alikuwa akiwasimulia kile ambacho anakijua kuhusu ASP Nkongo aliwauliza. “Yaani tumehangaika naye sana alikuwa ni chizi kabisa bila ya mimi na Kaila pamoja na Mzee Mwambe asingekuwa hivi leo” Aliendelea kuwaambia alipoona wamekaa kimya. “Yaani siku ya kwanza kuingia gerezani nilidhani mshkaji yupo atanisevu niende vizuri na life ya huku, siku nikajiona nina urafiki na Afande Nkongo si nikaleta fujo. Aisee jamaa alinipiga marungu na mabuti juu hadi nikatoka nundu yaani sitasahau, hapo ndipo nilipojua kuwa huyu si mtu. Mwanzo nilimchukia pia kama mnavyomchukia nyinyi lakini baadaye Mzee Mwambe nilipata bahati ya kuongea naye ndiyo akaniambia chanzo cha yeye kuwa hivyo, jamani yule ukijifanya ujuaji ukiwa umevaa haya manguo yetu au za maafande utaumia. Waliwaua wazazi wake na pia waliosababisha mke wake akafariki walikuwa wamevaa nguo za aina hii hii, kuziona hizo nguo jua anaona kama ndiyo anatazamana na wauaji wake” Aliwaambia “Ebwanaeh! Sasa nimekupata vizuri kabisa,jamaa kapitia mengi kweli hadi kuwa kipofu” Mmoja alidakia “Yaani yule pale nahisi roho yake itatulia mpaka huyo mbaya wake aingie kaburini” Aliwaambia “Hivi huyu mkuu wa magereza na mambo aliyoyafanya mbona hakamatwi yaani?” Mmoja aliuliza “Hivi utaanzia wapi kumkamata na mtandao mpana aliokuwa nao, mara ya mwisho nikiwa kazini nilikuwa najua mzee alikuwa nauza unga yule lakini mtandao ni mpana aliokuwepo” Aliwaambia “Ama kweli hii nchi mwenye kauli si mwenzako, nimekuwa muuaji lakini anayenituma ndiyo kanifanyia fitina hadi nimeingia ndani mwaka wa nane huu” “Yaani ndiyo hivyo ila huyu Mkuu wa magereza hana muda mrefu ndani ya uraia kwa mfumo huu wa uongozi” Kamishna Wilfred aliwaambia “Sasa kaweza kuishi miaka yote hiyo hawajamuweza” “Majamaa sasa hivi kuna viumbe vitatu ni hatari sana, kuna Norbert Kaila nilijua mwandishi wa habari tu lakini ni mpelelezi. Kamishna John Faustin naye ni jasusi, kuna Professa Moses Gawaza naye ni mpelelezi. Hawa watu wameisambaratisha timu yetu hadi mimi nipo humu ndani” Aliwaambia huku akipiga muayo halafua akamalizia, “oyaa wacha tulale aisee kazi ya kesho si mchezo tukichelwa kulala imekula kwetu” Kila mmoja alijilaza kwenye kitanda chake kutokana na muda kuwa umekwenda, uchovu waliokuwa nao kwa siku nzima baada ya kupasua sana miamba. Uliwafanya waupate usingizi ndani ya muda mfupi, kulianza kusikika mikoromo kwa baadhi yao baada ya kuchotwa na usingizi.
****
Utaratibu ulikuwa ni kama kawaida ndani ya gereza hili kila ikitimia muda wa alfajiri, wafungwa wote walikuwa macho na walikuwa wameshajiandaa. Wote walielekea maenno yao ya kazi wakiwa wanasimamiwa na Maaskari waliokuwa zamu, muda huu ASP Nkongo naye alikuwa yu macho na tayari alikuwa yupo maeneo ya juu ya gereza hilo kwenye nyumba yake akijiandaa kutoka nje na kuingia kazini. Muda mfupi baadaye alitoka huku akitembea kwa mwendo wa taratibu akiwa amevaa sare zake nadhifu, mkononi alikuwa na mkoba muhimu, aliingia kwenye ofisi yake na akautua mkoba huo na kisha alitoka huku akikunja mikono ya sare yake. Alishuka moja kwa moja chini ya ardhi kama ilivyokuwa kawaida yake na kupitia katika ofisi mbalimbali. Siku hii kidogo maofisa waliokuwa wapo chini yake walimfurahisha sana, hakumfokea mtu yeyote kwenye eneo lake la kazi. Aliporidhika na utaratibu ulivyokuwa ukienda alirudi ofisini kwake mara moja, kawaida ya gereza hili ilikuwa maofisa wanaingia kazini mapema sana tofauti na ilivyozoeleka kwenye magereza mengine. Hii ilitokana na wote kuwa na makazi ndani ya eneo hilohilo, walikuwa wakiwahi kutoka kuliko magereza mengine lakini masaa ya kazi yalikuwa ni yaleyale. Maofisa wa ngazi za chini kabisa wale ambao walikuwa hawashughuliki na sehemu hizo za ofisni ndiyo walikuwa wakifanya kazi kizamu. Walikuwa na siku nzima ya zamu ya kusimamia wafungwa na kisha siku inayofuata walikuwa walipumzika na wengine walichukua zamu. Huo ndiyo ulikuwa utaratibu wao kila siku kwa maafande wa kawaida. Maafande hao wa kawaida ndiyo waliyokuwa wakipendwa sana na ASP Nkongo ufanisi wao wa kazi, hao walikuwa hawana muda wa kuzembea katika eneo la kazi tofauti na wale wengine ambao walikuwa wapo maofisini.
*****
Majira ya muda wa kifungua kinywa baada ya Kamishna Mwambe kumaliza kupata kifungua kinywa chake alikuwa akitoka na kurudi ofisini kwake, akiwa yu njiani alikutana na Teddy ambaye alimpatia heshima yake. Aliipokea heshima hiyo huku akimtazama kwa tabasamu, Teddy hakutaka kujibaraguza aliamua kujieleza juu ya kuhitaji maongezi naye. Aliweka wazi kabisa alikuwa na maongezi naye ambayo yalikuwa si ya kiofisi, Kamishna Mwambe kwakuwa alikuwa akipenda sana kusikiliza maaskari wa chini yake aliamua kutafuta mahali palipokuwa patulivu akaketi naye chini na kusikiliza hiyo shida yake. “Ndiyo binti” Alimuitikia “Mkuu najua wewe ni kama baba yangu hivyo sitoona haya kukuambia kuhusu hili suala kwani ninahitaji sana msaada wako” Teddy aliongea “Wewe ni kama mwanangu upo huru kuongea nakusikiliza, hata ukiniita Baba ni sawa” “Mkuu kwa muda mrefu nimekuwa ninateseka kisa James, nimejaribu kila niwezalo lakini nimeshindwa hata kukaa kuongea naye. Nahitaji kuwa na mume mkuu na nahitaji kuwa familia, mwanaume peke nimuonaye ni yeye tu sina mwingine lakini ndiyo siyo muelewa. Naamini wewe anakuheshimu kama baba nimeamua kukufikishia hili kwako” “Je unampenda kwa dhati kabisa?” “Ninampenda kwa dhati” “Ok nimekusikia najua na yeye ni muda wa kupata mke pia nitaongea naye ila nitakupa masharti ukiongea naye jaribu kuyazingatia” “Sawa” “Unaweza kwenda binti suala hili limefika kwangu tayari nitajua namna ya kukusaidia” Kamishna Mwambe alipotoa ruhusa hiyo kwa Teddy aliondoka na kurejea eneo lake la kazi kwa haraka, alimuacha Mzee huyo akiyatafakari maneno hayo. Haikuwa mara ya kwanza kusikia tetesi juu ya binti huyu kumtaka ASP Nkongo, zilikuwa ni tetesi ambazo hakuwa na uhakika nazo na sasa alikuwa amejiwekea uhakika nao. Hakutaka kukaa eneo hilo kwa muda mrefu aliamua kuelekea ofisini kwake moja kwa moja.
****
Baada ya muda wa kufanya kazi kuisha ndani ya ofisi zao kila mmoja alirejea kwenye makazi yake, muda huu ndiyo muda ambao Kamishna Mwambe aliutumia kujongea hadi nyumbani kwa ASP Nkongo. Kutokana na kupazoea na pia kuuzoea utaratibu wa kijana wake wa kumlea, alijua ndani ya muda huo alikuwa akifanya nini humo ndani. Hakutaka kubisha hodi alipitiliza moja kwa moja hadi ndani, alipoingia ndani ya sebule ya nyumba hiyo ambayo ilikuwa ina samani kadhaa ikiwa na idadi kubwa ya vyuma vya kunyanyua vikiwa vimezagaa jirani na meza ya sebuleni. Jambo hilo halimkushngaza kabisa alikuwa tayari ameshamzoea Mwanae huyo tabia yake, alipongia alienda kuketi kwenye kochi mojawapo na kisha akatulia kwa sekunde kadha halafu akapaza sauti kumuita. ASP Nkongo alitokea akiwa amevaa kaptula huku akiwa kifua wazi, kutokana na kuitambua sauti ya mlezi alienda kuketi hadi jirani yake kwani alishatambua alikuwa na jambo ndiyo maana kamuita. “James mwanangu unajua miaka inakimbia hii sana, kamwe haitorudi nyuma” Alimuambia “Natammbua hilo Baba” “Sasa basi napenda uanze kuijenga familia kwa mara nyingine mwanangu, hivi unataka uondoke duniani hapa hata uzao hujaacha kweli” “Baba tatizo mazingira” “Mazingira yana nini mwanangu, yaani hadi nakuja kutamkiwa na binti ameamua kuweka haya zote pembeni anataka uwe mume wake” Maneno hayo yalipotoka ASP Nkongo alikaa kimya akawa amekosa la kuongea. “Si kama nakulazimisha mwanangu hebu fikiria kuhusu hilo, Teddy yule binti ambaye huwa unamjibu kiukali ni msichana ambaye anakupenda sana. Hivi ushawahi kuona mwanamke akitoka huko na kuja kumtamkia mzazi wa kiume wa fulani anampenda” “Hapana sijawahi kuona” “Sasa jiulize ni kwanini yeye kaja kunitamkie kuwa anakupenda, maana yake kashindwa kuvumilia kabisa” “Lakini” “Hakuna cha lakini hebu niambie yule binti unamuona vipi?” “Ni msichna mrembo sana na mwenye mvuto” “Saa ule urembo wake na mvuto wake wote jiulize wangapi wanamtaka lakini kaja kwako, James usifikiri humu ndani hakuna anayemtaka yule” “Sawa nimekuelewa” “Siyo unielewe tu hebu tafuta namna ya kuweza kuwa pamoja naye yule, unahitajiwa ukiwa hivi bado upo ujanani fikira ukija kuwa kama mimi na bado hutaki kuoa itakuwaje. James najua ulimpenda Sara tena sana lakini naomba ukubali ameshakwenda tayari muda mrefu, usiishi kama mimi niliyechoka wewe bado unahitaji Mwanamke kuliko kitu kingine chochote” Kamishna Mwambe aliongea huku machozi yakiwa yanamlenga, hali hiyo ilimfanya ASP Nkongo ainamishe uso wake chini mwenyewe hakutaka kumuangalia. “Mimi sina cha kupoteza James nimeshakuwa mtu mzima kuona sioni umuhimu lakini katika umri kama wako niliona umuhimu wake. Najua una uchungu umefiwa na kiumbe kilichokuwa kipo bado tumboni, hebu fikiria mimi nilifiwa na mtoto tena nikiwa nimemuona jinsi alivyochukua sura yangu lakini sikukata taama nikampata ambaye alikuwa mke wako” Maneno hayo yalimchoma sana Jmes hadi chozi likawa linakaribia kumtoka. “Baba nimekuelewa nipo tayari kuoa kwa mara nyigine” “Sasa huo ndiyo uanaume James, Mkuu Nkongo ameondoka na kuacha alama yake duniani basi na wewe uache ya kwako. Upo tayari kumuoa je ni nani? Maana si lazima unaweza kuchagua mwngine” “Teddy ndiye atakayekuwa mtu pekee anayenifaa, hata kama nikichagua mwingine nitaleta matatizo kama ya mwanzo. Nilikuwa simuhitaji Jane nafikiri matokeo yake umeyaona nimepoteza familia. Sipo tayari litokee hili ikiwa najua kuna ambaye ataumia nikichukua mwingine” Baada ya hapo Kamishna Mwambe alianza kumpa somo kijana wake juu ya maisha yake kwani aliona bado alikuwa akimkumbka tu mke wake. Alitumia muda huo kuongea naye kirefu zaidi huku akimuusia mambo mbalimbali, alikuwa akitaka aingie kwenye njia iliyo sahihi na si kufuata pasipo sahihi aje kupotea. Huyu kijana kuwa naye aliona kama alikuwa na mtoto wa kumzaa, hakutaka kumpoteza kinamna yeyote ie. Alikuwa akimlinda sana na hata zilipoibuka chuki dhidi yake alikuwa akimkingia kfua, upendo wote aliokuwa ameupoteza kwenye ajali ya gari la binti yake. Aliuhamishia kwa kijana wake wa kumlea ambaye alikuwa na kidonda kimoja naye katika ajali hiyo, kutokana na uzito wake aliokuwa akipewa na ASP Nkongo haikuchukua muda kuweza kukubaliwa maneno yake. Heshima aliyokuwa akipewa ilikuwa ni kubwa kutokana na mchango aliyonao katika maisha yake, hakutaka kumuangusha kwa kitu chochote kama yeye ambavyo hakuwahi kumuangusha. Mambo mengi ambayo alikuwa amefanyiwa yalikuwa hayalipiki, njia ambayo ingeweza kumuhisi kidogo alikuwa akirudisha fadhila ya yale aliyofanyiwa ilikuwa ni heshima na utiifu tu kwa Mlezi wake.
_______________TIRIRIKA NAYO
Teddy Andrew au wengi walivyokuwa wamemzoea kumuita kwa jina la Modo Teddy kutokana na wembamb wake aliyokuwa nao, jina hilo lilikuja kupotea baada ya kuupata mwili uliyokuwa na mvuto zaidi hata ya huo uwembamba aliyokuwa nao. Binti huyu alikuwa ni mmoja kati ya mabinti wapole, alikuwa ni mtoto wa pekee kwa tajiri Andrew ambaye alikuwa akisifika sana jijini Arusha. Alilelewa na kukulia katika maisha ya raha na wala hakuwahi kuijua shida, elimu yake aliisoma kwenye shule ya kimataifa kuanzia yu mtoto hadi anaingia sekondari. Alikuwa ni mwenye kipawa cha akili katika masomo yake, haikuwahi kutokea akashuka kimasomo kipindi akiwa yupo shule. Hii ilimfanya Mzee Andrew ambaye ajivunie kuwa na binti kama yeye na kumuongoza katika msingi wa kufuata katika masomo, baba yake alikuwa ni tajiri ambaye alikuwa akitilia mkazo suala lake la kujielimisha na pia alifuatilia kwa kina masomo yake. Teddy alifanikiwa kumaliza kidato cha sita katika shule ya kimataifa hapahapa nchini, kumaliza kwake shule nchini Tanzania hakukuweza kumkwepesha kutoingia kwenye mafunzo ya JKT kutokana na ulazima wake. Mzee wake alilipinga sana suala hilo kutokana na kumlea mwanae katika maisha ya kudekeza, lakini hakuweza kufua dafu mbele ya mfumo ambao ulikuwa umewekwa. Ilikuwa ni akose nafasi ya kujiunga na chuo kikuu au aingie jeshini aende chuoni, ilimbidi tu akubali tu aingie jeshini huko akiwa anamuonea huruma sana kutokana na kasumba mbaya ambayo ilikuwa imesambzwa dhidi ya jeshi. Kutoruhusiwa kwa mawasiliano ndani ya kambi muda wa mafunzo kulizidi kumtia hofu lakini aliamua kuwa na subira moyoni, mawasiliano alipokuja kuyapata na mwanae ilikuwa ni muda ambao alikuwa akitakiwa kwenda kufanya maombi ya chuo katikati ya mafunzo hayo. Mzee Andrew alipoweza kutuliza hofu aliyonayo baada ya kupata taarifa Binti yake alikuwa yupo mzima wa afya kabisa, muda wa mafunzo ulipoisha ndipo alipoweza kuja kumuona Binti yake katika siku ya Mahafali alivyopungua mwili. Ndipo siku hiyo alipofanikiwa kuja kuyaona mazingira ya kambi aliyokuwa akiishi, yalikuwa ni mazingira ambayo yalikuwa si ya kilelemama ambayo yalifanya ashangae kwa binti yake kuweza kuishi maisha kama hayo wakati alikuwa amezoea sana kudeka. Hatimaye siku inayofuata alirudi ndani ya jiji la Arusha na akayaanza maisha baada ya kutoka jeshini, katika muda huu ndipo alipoachiwa huru sana na Baba yake kutokana na kuwa amekua mtu mzima. Kipindi hicho ndipo Teedy alikuwa yupo katika mahusiano mazito sana na kijana wa hadhi ya kawaida ambaye alikuwa amekutana naye jeshini, walikuwa wapo ndani ya penzi la siri sana. Walikuwa wakipanga muda vizuri na kukutana na watu wa kawaida na kufurahi sana, alitokea kumuamini sana huyo kijana. Ilikuwa ni mara ya kwanza kujiingiza kwenye mahusiano ya mapenzi hivyo alijitoa mzima kabisa kwenye mahusiano hayo, mahusiano hayo ambayo yalikuja kujulikana na baba yake aliyapinga kwa nguvu zote lakini Teddy hakutaka kabisa kuyaacha na aliendelea nayo. Baba yake hakutaka kushindana naye kwa jinsi alivyokuwa akimpenda ilimbidi akae kimya tu, hakutaka alete matatizo mengine kisa kulazimisha. Muda wa mahusiano hayo haukufika hata mbali na Teddy alijikuta akijuta ndani ya maisha yake, ilikuwa katika muda ambao majina ya chuo yalikuwa yametoka na alikuwa akisubiri siku zisogee aweze kujiunga na chuo. Kipindi hicho ndipo alipogundua kuwa alikuwa amependa mtoto wa Mhalifu mkubwa sana jijini Arsuha ambaye aliambiwa ni mfanyabiashara wa kawaida, mambo yalikuja kujulikana siku ambapo alikuja kujulikana kuhusu utajiri wa baba yake na huyo Mhalifu. Alitekwa nyara na kushinikizwa mzazi wake alete pesa, Mzazi wake alipoleta jeuri tu Teddy alijikuta akibakwa na mtu ambaye alikuwa akimuona ni atakuja kuwa mkwe wake huku akishirikiana na Mwanae. Msako baadaye uliendeshwa na hatimaye watu hao wawili Baa na Mwana walikuja kuvamiwa kwenye maficho yao, walipojaribu kutoroka waliishia kuuacha uhai wao. Askari wa jeshi la polisi ambao walikuwa makini zaidi waliwashambulia, kuanzia siku hiyo Tedy alibadilika na kuwa mnyongea na asiye na furaha. Chuo ulipotimia muda hakikuendeka kabisa, aliathirika kisaikolojia kwa kitu alichofanyiwa na Mtu ambaye alimpenda sana. Hali yake ilitishia kabisa wazazi wake na kuona alikuwa akielekea kuchanganyikiwa, chuo hakukitaka tena na akawa ni wa kukaa ndani. Baba yake alipojaribu kumtafutia kazi nyingine za kufanya kutokana na ushawishi wake wa kifedha, aliishia kuzikataa na hakukuwa na wa kumlazimisha. Kipindi hiko mawazo yalipomzidi ndipo alipoamua kubadili maisha na kuwa ni wa kwenda mazoezini, alifanya mazoezi ili kupunguza mawazo lakini haikusaidai kitu. Ufanyaji huu mazoezi ndipo ulipopelekea akaingia kwenye uchezaji wa ngumi, suala hilo halikumfurahisha Baba yake lakini hakuwa na uwezo wa kulipinga. Aliamua kukubaliana na matakwa ya binti yake na si kushindana naye, Teddy kuanzia hapo aligeuka kuwa mwanamke ambaye alikuwa akijua vizuri sana kuitumia mikono yake katika kupigana ingawa mwili wake haukuwa mkomavu kutokana na kufanya mazoezi kwa muongozo wa walimu.
Maisha ya kukaa nyumbani kwa muda mrefu yalimfanya baba yake kutoyafurahia kabisa, alikuwa akitamani awe masomoni au awe kwenye shughuli ambayo ingemuingizia kipato. Alipoona hakuwa na uelekeo wa kufanya vile anavyotaka ilimbidi amuulize juu ya akitakacho, siku hiyo ndipo Mzee Andrew aliingiwa na mshangao mwingine baada ya binti yake kulichagua jeshi la wananchi. Hakutaka kupingana naye alijaribu kumtafutia nafasi lakini kwa bahati mbaya nafasi hazikuwa zimetoka, kulikuwa na nafasi ndani ya jeshi la Magereza ambalo pia alikubali tu kujiunga nalo hivyohivyo kutokana na kulipenda pia. Huo ndiyo ulikuwa mwanzo kwa binti wa kitajiri kuingia ndani ya jeshi la magereza, baada ya mafunzo mafupi aliweza kupata kazi kwenye Gereza moja ambalo lilikuwa lipo Arusha. Alipatiwa nyumba na wazazi wake na pia sehemu ya kampuni kubwa ambayo wazazi wake walikuwa wakiiimiliki, aliendesha maisha yake peke yake na hakutaka kuwa mwenza. Teddy akiwa na cheo cha RSM naye alikuwa ni mmoja wa maaskari wa kike ambao walikuwa wakorofi, alikuwa akiogopeka na wafungwa. Alikuwa ni rafiki mzuri sana wa maaskari wenzake lakini alikuwa ni adui mkubwa wa wafungwa, ujeuri wowote utakaofanywa na wafungwa alikuwa akimpa dhabu kubwa na hata kipigo kizito. Ukorofi huo aliokuwa nao ulimfanya awe anashughulika na wafungwa wale ambao walikuwa na makosa makubwa gerezani, huko alikuwa akiingia na rungu au muda mwingine alikuwa akiingia bila ya rungu. Hatari yake ilikuwa ni ileile kutokana na kuwa mjuzi sana katika mapigano, aliweza kuwa kipenzi cha wafungwa wanyonge ndani ya gereza. Utukutu wake ulikuja kumfanya ahamishiwe kwenye gereza la Nyumba ya giza akiambatana na maaskari wengine watukutu, Baba yake alihuzunika kuwa mbali na binti yake lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kuridhia tu na ile kampuni ambayo alikuwa amempa akamsaidia usimamizi. Alipokuja ndani ya gereza hili na kukutana na marafiki wapya waliokuwa watukutu kama yeye, alianza kujihisi yupo kwenye dunia ya watu kama yeye. Huko ndipo aliporejewa na furaha kwa mara nyingine na akanawiri kuliko awali, haikupita muda mrefu aliweza kumshuhudia afande mpya mtanashati asiyecheka na watu akiwasili ndani ya gereza hilo. Huyo ndiyo Afande ambaye alifanikiwa kuuteka moyo wake kwa mara ya pili tangu alipojeruhiwa, alijitahidi kila awezavyo kumpata lakini alishindwa. Hakuwa mwingine ila ni ASP Nkongo ambaye alikuwa mwenye sura ya hasira muda wote, aliposhindwa kumpata kwa kipindi kirefu cha muda ndipo alipoweza kumuomba msaada Mkuu wake ambaye alikuwa akielewana naye.
**** ASO Nkongo baada ya kuondoka baba yake mlezi tangu amalize kufanya naye mazungumzo, moyoni mwake alikuwa tayari amekiri kuwa mke wake alikuwa tayari amekwenda na hatorejea tena. Aliamua tu kuweza kuwa na mahusiano na binti huyo ambaye alikuwa akimpenda, alipoyatazama mzingira ya nyumba yake aliyokuwa akiishi aliona kabisa yalikuwa yakimshawishi aweze kumuongeza ndani humo. Kutokuwa sawa kwa baadhi ya vitu kutokana na kutojali kwake aliona akifaa awe na mwenza ambaye atamuongoza kuweza kuwa na maisha mengine, mfumo wa maisha aliyokuwa akiufuata aliona ulikuwa ukihitaji kubadilika na kuingia katika mfumo mwingine lakini hakuwa akiweza kuubadili mfumo huo akiwa anaishi maisha ya upweke ndani ya Nyumbani yake. Uwepo wa ubavu wa kushoto ndiyo kitu pekee ambacho kingeweza kumbadilisha katika aliyokuwa akiishi, utaratibu aliokuwa amejiwekea ndani ya eneo hilo akiwa yupo peke yake ulikuwa ni utaratibu mgummu kwa yeye mwenyewe kuubadili pasipo kuwepo kwa mwingine. Siku zote mwanadamu hubadili mfumo wa maisha mabo alikuwa ameuzoea kutokana uwepo wa mwingine katika mazingira anayoishi, uwepo wa mtu mwingine hufanya atoke kwenye mazingira ya upweke na kuingia mazingira ya namna nyingine. Hapa ndipo ule mfumo wa maisha aliokuwa ameuzoea kipindi yu mpweke hubadilika, ASP Nkongo naye alionekana alikuwa akimuhitaji Teddy kuweza kubadilisha yake kutokana na kuingiwa na maneno ya baba yake. Majira yale ya kuangalia mpira kutokana na kipindi hiko na michuano ya Klabu bingwa ya dunia yalifka, siku hiyo kwa mara ya kwanza Teedy aliletwa humo ndani ya Bwalo la maofisa ambao walikuwa wamemzidi cheo. Kwa mara ya kwanza aliweza kumuona ASP Nkongo akiwa ni mwenye tabasamu na si kununa kama alivyozea, hakika siku hiyo ilikuwa ni faraja kwake hasa alipokaribishwa kukaa jirani naye muda wa kuangalia luninga. Yote hiyo ilikuwa ni mipango ya Kamishna Mwambe aliyokuwa ameifanya. Wengi waliokuwa wapo humo ndani walibaki na maswali kwa Askari mwenye cheo cha kwaida kuweza kuingia humo ndani, walishindwa kuendelea kujiuliza maswali zaidi baada ya kujua alikuwa amekaribishwa na mkuu wao. Waliendelea kuangalia mpira huku wale walengwa wawili wakiwa wameingiwa na ukimya baada ya kukutana kwa mara ya kwanza, Teddy alikuwa yu mwingi wa kumuangalia usoni ASP Nkongo katika muda ambao alikuwa akiongea na kucheka na wenzake. Alipotazamwa yeye jamo la kwanza kulikimbilia ilikuwa ni kuangalia pembeni kutokana na kuingiwa na aibu kubwa , muda kadri ulivyoenda walijikuta wakiongea maneno machache wenyewe. Kamishna Mwambe alipoona wameanza kuongea wawili alizuga mwenye udhuru akatoka nje, aliporejea hakukaa sehemu aliyokuwa amekaa awali na alienda kuketi kwenye kiti kingine kabisa. Mpira uliendelea kuangaliwa huku ASP Nkongo na Teddy wakiwa wanaongea kwa pamoja, ilifika muda wote wawili wakawa na furaha kutokana na mioyo yao kuwa tayari ilikuwa imeanza kuzungumza. Muda wa mapumziko ya mechi waliyokuwa wakiitazama ndipo walipoazama kabisa kwenye mazungumzo huku wakicheka, wengi waliokuwa wakiangalia mpira pamoja nao walibaki wakishngaa lakini walikaa kimya kutokana ilikuwa ni habari ambayo haikuwa ikiwahusu.
Mazungumzo waliyokuwa wakiyaendeleza yalipopiga hatua nzuri hatimaye walikaa karibu na kupunguza sauti wakawa wanaongea yao ya moyoni, kicheko kilichokuwa kipo mara ya kwanza kilipungua na hatimaye wakawa wanaongea bila ya kuwepo kicheko hicho na sauti ya chini sana. Muda wa kipindi cha pili katika mechi mbayo walikuwa wakiingalia ulipoanza, ASP Nkongo alirudisha macho yake kwenye luninga lakini hakuacha kuongea na Teddy kutoka na walikuwa wamefikia hatua nzuri ya mazungumzo. Alikuwa akitupia jicho luninga huku akiongea na Teddy ambaye alikuwa amesogea karibu zaidi kutokana na mazungumzo kuwa yao kibinafsi, kufikia hatua hiyo na jinsi walivyokuwa wamekaa hakuna ambaye hakuwa akijua kuwa watu hao walikuwa na zaidi ya ukaribu mioyoni mwao. Tayari maofisa wengine walikuwa wameshajua kinachoendelea ingawa walikaa kimya kutokana na kuwa yalikuwa hayawahusu, waliwaachia wahusika na nafsi zao wayatawale mazungumzo yao. Hatimaye dakika tisini zikatimia na maafisa mmoja baada ya mmoja alitoka humo ndani ya Bwalo na kurejea kwenye nyumba zao, muda mfupi baadaye ndani ya Bwalo hilo walibaki wawili tu waliyokuwa wamezama kwenye maongezi yaliyojaa ukaribu zaidi. “Mkuu kwakweli sikutarajia kama upo hivi” Teddy walipokuwa amebaki wawili “No niite James tu hilo jina sitaki kulisikia nje ya ofisi” ASP Nkongo alikataa kuitwa jina hilo “Ok” “Sasa nafikiri hakuna ambacho hujanielewa hapo Teddy” “Nimekuelewa James nipe juda kwanza siwezi kukupa jibu kwa haraka” “Lini jamani wanadamu siku kuziona ni bahati je unatarajia kesho utaniona?” “No usiseme hivyo James” “Ndiyo ukweli hiyo” “Kuwa mwenye kusubiri nafikiri sitokuweka sana nitakuwa jibu lako” “Ok nimekuelewa” “Sasa?!” “Tutoke muda umeenda huu” ASP Nkongo aliongea huku akinyanyuka na kumpa mkono Teddy amuinue, tabasamu lilimtoka binti huyo aliponyooshewa mkono naye kwa madaha alimpa kiganja chake akamuinua. Walitoka wakiwa wameshikana mikono kwa namna ya upendo huku Askari ambaye alikuwa akihusika na kuzima taa humo Bwaloni akiiingia, walitembea kufuata njia ambayo ilikuwa ikienda eneo ambalo kulikuwa na nyumba za maaskari wa jeshi hilo pamoja na wafanyakazi wa mzabuni. Ilikuwa ni siku ya kwanza kwa wote wawili kuongozana pamoja, kila mmoja alijisikia ni kiumbe tofauti kwa kufutana na mwenzake. Waliongozana kwa pamoja hadi walipofika kwenye eneo ambalo lilikuwa likitenganisha njia, hapo walisimama na wakabaki wameshikana viganja vya mikono yao huku wakitazamana. “Sasa?!” Teddy aliuliza “Kesho kama vipi?” ASP Nkongo alimwambie hukua akitaka kuitoa mikono yake lakini Teddy hakuwa tayari. “Ngoja nikusindikize” ASP Nkongo aliamua kuongea na kisha akaanza kuongozana naye kuelekea kwenye eneo ambalo alikuwa akiishi, wote walienda hadi kwenye nyumba ya wastani ambayo ilikuwa imejengwa kisasa zaidi. Walipofika hapo bado walikuwa walikuwa wameshikana vignja vya mkono, ASP Nkongo alimpeleka hadi mlangoni kabisa. “Nikutakie usiku mwema” Alimuambiwa huku akimtazama usoni, katika namna ya kiajabu aliuachia mkono wake na hapo kukatokea jambo ambalo hakutarajia kama litatokea. Teddy baada ya kuachiwa kiganja cha mkono alijivuta mbele kwa nguvu, alitulizaa papi za midomo yake kwenye papi za musomo ya ASP Nkongo. Wote kwa pamoja alijikuta wakiwa wameingiwa kwenye hali nyingine kabisa, walidumu kwenye tendo hilo kwa muda mfupi na walipoachiana na walikumbatiana kila mmoja akiwa na hisia kwa mwenzake. “Nakupenda sana James nipo tayari kuwa nawe” Hatimaye Teddy alihalalisha mwanzo wa ukurasa mwingie kwake.
Maisha ya mapya kati ya wale waliyokuwa wamepitia kwenye chungu kipindi cha nyuma yalichipuka kwa kasi kubwa , mtu wa knzwa kuyajua mahusiano hayo alikuwa yule ambaye alipelekea wakawa pamoja. Teddy alikuwa akijua kabisa kuishi naye mpenzi wake, alifuata kile ambacho aliambiwa na Kamishna Mwambe kilikuwa kikimkera ASP Nkongo. Hii ilifanya waishi kwa furaha na hata utaribu wa maisha ya ASP Nkongo ukaanza kubadilika, nyumbani kwake kukawa mahali palipokuwa pana usafi wa kipekee. Uhusiano huu ulianza kwa kujulikana na maofisa wa juu ambao waliwaona kwa siku ya kwanza pamoja na marafiki wa Teddy waliokuwa wakijua kila kitu. Taratibu ulianza kujulikana kwa baadhi ya maaskari wa chini na hatimaye Maafande wote wakawa wanatambua, kufikia kipindi hiko wote waili walijumuika kwa pamoja mazoezini. Wote wawilikwa kuwa pamoja walijiona ni viumbe ambao walikuwa wamezaliwa upya, walifuatana kama kumbikumbi katika kila sehemu walipokuwa wakielekea.
Haikukaa muda mrefu sana hatimaye Teddy alihamisha makazi yake kabisa nyumbani kwa ASP Nkongo, huko walianza kuishi kama mume na mke. Utaribu mzima wa maisha ya ASP Nkongo ndiyo ulibadilika kabisa, kuishi na mwanamke ambaye alikuwa akimuelewa jinsi alivyo kulimfanya awe James yule ambaye alikuwa ni mcheshi sana katika kipindi cha nyuma. Hatimaye alianza kujijengea marafiki wengi sana kutokana na maofisa hao nao kujua jinsi ya kukaa naye na kuongea naye, muda mfupi tangu aweze kuwa na marafiki wengi alitokea kuwa kipenzi cha maofisa wengi kutokana na ucheshi aliokwua ameupoteza kurudi. Pamoja na hayo bado alikuwa hapendi kabisa maelewano na Askari aliyekuwa yupo ndani ya vazi la kazi, hii ilifanya Tedy kutovaa kabisa vazi hilo akiwa yupo naye ndani na muda wa kwenda kazni alikuwa akimuacha atangulie ndipo na yeye huvaa na kutoka. Huo ndiyo ulikuwa mfumo wa maisha yao na Teedy akawa kila siku akitaka hali hiyo iondokane ili aweze kuishi naye kiuhuru zaidi, suala hili aliamua kulifikisha kwa Mkwe wake ambaye aliahidi kulishughulikia. Suala hili pia lilikuwa limeshagunduliwa na baadhi ya maaskari ambao waliahidi pia kulishughulikia ili mwenzao arudi kwenye hali ya kawaida, haikupita muda mrefu sana tangu kuambiwa hatimaye maofisa wote waliungana na mkuu wa gereza wakamuita mtaalamu wa Saikolojia. ASP Nkongo aliposikia kuhusu ujio wa mtu huyo mwanzoni alionekana kutotaka suala hilo, Tedy alitumia ushawishi wake na hatimaye alikubali. Tiba alianza kupewa huku Teddy akiwa yupo karibu naye, kutoka na utaalamu wa mtu ambaye walikuwa wamemuajiri alianza kuridi katika hali yake ya kawaida. Taratibu aliona si kila aliyekuwa akivaa vazi kama lake alikuwa ni mtuhumiwa wa mauaji ya aliowapenda, hatua hiyo ilifikia pazuri sana na hata akwa anakaa na wenzake wakiwa wamevaa mavazi ya kazi. Tiba iliendelea na hata akwa anawaona wafungwa wengine waliokuwa ndani ya gereza hilo si wwaliosababisha awe hana furaha katika maisha yake, hatua ya mwisho ya tiba hiyo ilipokamilika alikuwa ni kiumbe mpya kabisa si yule ambaye alikuwa na ukatili. Hapo ndipo mapenzi baina yake na Teddy yalipizidi kuliko hata awali,pia ndiyo alizidi kuwa kipenzi cha Maaskari wote ndani ya gereza si wakubwa wala wadogo kutokana na kuwa mtu mwenye kupenda kuongea na atu. James wa zamami mwenye ucheshi aliamka kwa mara nyingine hakuna ambaye alikuwa akimfahamu vizuri hakujua hilo, hata Kamishna Wilfred ambaye alikuwa yupo gerezani alifahamu kuhusu hilo. Pia wafungwa nao waliokuwa wakimuona katili walifahamu kuhusu hilo, alianza kukubalika miongoni mwa wafungwa kutokana na tabia yake. Ilifika kipindi alikuwa akienda kuka pamoja na wafungwa walipokuwa wapo kwenye mapumziko baada ya kupata chakula na kuongea nao, hii ilifanya wafungwa waliyokuwa wakimchukia wampende na hata kuongea nao kwa urafiki. Kutokana na tabia yake hiyo jeuri miongoni mwa wafungwa ikapungua, alikuwa akijua kuongea nao na kuwafanya wawe watiifu wakubwa kwa Maaskari waliokuwa wakiwasimamia. Kuongea kwake pia kulikuwa ni kwa maasakri waliokuwa na vyeo vya chini ambao walikuwa hawaonani naye mara kwa mara kutokana na mfumo wa utaritibu wa maisha wa hapo gerezani, ASP Nkongo alikuja kuwa askari ambaye alikuwa amevunja rekodi kwenye gereza hilo kwa kukaa sehemu moja na maasakari wa chini yake. Alidiriki hata kuingia kwenye bwalo lao la chakula na kukaa nao, muda mwingine alikuwa akila chakula ambacho walikuwa wakila wao. Aliongea nao kama alikuwa akiongea na mtu mwingine wa karibu naye, kutokana na tabia yake hiyo jina lake lilikaa vinywani mwa wengi sana kila wakati alikuwa akizungumziwa. Sifa zake za kulibadili gereza hilo hatimaye zilivuma nje ya gereza na akawa mwenye kujizolea heshima kubwa, vyombo vya habari vilikua vikitaja habari zake kila kukicha na hata ikafikia wanahabari wakafungga safari hadi ndani ya gereza hilo kuja kujionea hali halisi ilivyo. Hakupokea sifa nzuri kutoka kwa Kamishna jenerali Lutonja kutokana chuki ambayo alikuwa nayo, alipokea sifa hata kwa Rais Zuber Ameir ambaye alikuwa akilitembelea gereza hilo. Wafungwa wale waliyokuwa watukutu walikuwa watiifu sana kutokana na kujua namna ya kuishi nao, kwenye maonesho ikiwa sherehe itaandaliwa ndani ya gereza hilo wafungwa walitumika pia kuonesha ujuzi mbalimbali walikuwa nao. Mwezi mmoja baadaye hatimaye ASP Nkongo alimvalisha pete ya uchumba Teedy katika sherehe ambayo ilihudhuria na maskari watupu waliokuwa wapo gerezani humo, siku hiyo ilikuwa ni ya furaha sana kwake na mpenzi wake kutokana kufikia hatua nyingine kabisa ya uhusiano wao. Baraka zote walizipata kutoka kwa Kamishna Mwambe na pia wenzao waliwatakia maisha mema, baada ya kuisha kwa sherehe hiyo lilipita juma moja hatimaye Mzee Andrew akiwa na mke wake walikuja hapo gerezani kumuona binti yao. Siku hiyo nao walizidi kuwa na furaha kumuona binti yao alikuwa amerejewa na hali ya furaha ambayo aliikosa kwa kipindi kirefu, walikaribisha nyumbani kwa ASP Nkongo ambaye alikuwa ni mkwe wao mtarajiwa. “Lakini sijapenda mlivyovishana pete kiwizi namna hiyo” Mzee Andrew aliongea wakiwa wamekaa pamoja sebuleni. “Umeona Baba Teddy hawa watoto walivyo waone vile” Mama Teddy nay alidakia “Dady na Mummy jamani” Teddy alilalamika “Jamani nini naona siku hizi umemisi sana kudeka kama ilivyokuwa tabia yako” Mzee Andrew aliongea huku akitabasamu. “Haaah! Kumbe na ukubwa huo unadeka” ASP Nkongo naye aliongea huku akiweka uso wa mshangao. “Yaani huyu kwa kudeka ndiyo menyewe kabisa” Mzee Andrew alidakia “Daddy si nimeacha nimekua mimi” Teddy alionga huku akiziba uso wake. “Haya wanangu sisi tunasubiri pilau tule na wajukuu tuwaone lini sasa” Mama Teddy aliuliza “Tunafanya mipango hivyo Mungu akitujalia hatutamaliza mwaka huu tayari kila kitu” ASP Nkongo alijibu “Sisi pamoja nanyi kwenye kila hatua yenu, James asante sana” Mze Andrew alisema “Asante ya nini Baba?” ASP Nkongo aliuliza “Umeweza kunirudishia Teddy wangu yule ambaye alipotea miaka iliyopita sina budi nikushukuru” Aliambiwa
Baba na Mama sina budi niwashukuru nyinyi kwani mmeweza kunipatia Teddy ambaye amenirudisha James yule ambaye nilipotea” ASP Nkongo aliongea huku akiuzungusha mkono wake begani kwa Teddy ambaye alimlalia kwenye bega lake.
Wazazi hao hawakutaka kukaa muda mrefu kutokana na majukumu waliyokuwa nayo, ilipofika majira ya alasiri Helikopta ambayo iliwaleta hapo awali ilirudi tena na kuwachukua. Waliondoka wakiwa ni wenye furaha kubwa sana kwa kumuona binti yao akiwa yupo kwenye furaha, moyoni walikuwa wakishukuru ana ujio wa James kwenye maisha ya binti yao ambayo yalikuwa yamepoteza dira kutokana na kuathiriwa na maumivu aliyoyapitia kwenye maisha yake.
Hazikupita siku nyingi rafiki yake James kipenzi ambaye walikuwa hawajaonana kwa muda mrefu alifika naye kuja kuwaona, ilikuwa ni furaha sana kwa kuweza kuonana na Norbert kwa mara nyingine akiwa nimwenye furaha. Siku huyo walijikumbusha kipindi cha nyuma cha maisha yao walichokuwa wamepitia, ucheshi baina yao uliokuwa umepotea kwa kipindi kirefu cha muda ulirejea tena.
“Mzee hongera kwa kuopoa humuhumu” Norbert alimpongeza wakiwa wanaongea wawili baada ya kupishwa na Teddy. “Asante aisee, vipi wewe huko bado hujaoa?” ASP Nkongo alizipokea pongezi na kisha akauliza. “Bdo niponipo aisee” “Aaah! Come on unangoja nini?” “Bado haijafikia muda muafaka ingawa tayari nina familia” “Norbert aisee umri unaenda huo na Norene una mtoto naye na unaishi naye, hebu muweka ndani” “Nipo kwenye mpango huo si unajua kila kitu mipango” “Aisee najua kwa mtindo huo ile tabia yako hutaacha kabisa” “(Norbert akacheka) Aisee wewe yaani hujasahau” “Akusahau nani we jamaa unapenda sketi balaa kama ndiyo zinakupa pumzi duniani” “Nitapunguza jamaa si unaona umri unakimbia huu” “Siyo upunguze uache kabisa na uwe mtu mpya kabisa” “Poa poa aisee nataka niwe kama wewe sasa hivi” “Ujibadili rangi uwe mweusi kama mimi au vipi?” “(Akacheka) Aise James hubadiliki wewe, vipi Wil anaendeleaje?” “Yupo poa sasa hivi ila anajuta kwa njia aliyopitia hadi anaacha familia na kuwa gerezani” “Keshachelewa tayari sasa, hatoliona jua la uraiani milele” Marafiki hao waliopotezana muda mrefu waliweka mazungimzo wakiwa wapo nyumbani, ASP Nkongo alikuwa hajaenda kazini siku hiyo na alikuwa akimpokea mgeni wake huyo. Si yeye tu hata Teddy naye hakuwa ameingia kazini, muda mfupi baadaye Teddy alirejea baada ya kuonga mambo yao mengine. Waliifurahia hiyo siku wakiwa pamoja. majira ya mchana Norbert aliwaaga na kuondoka baada ya kusalimia na Kamishna Mwambe.
**** Hakuna kibaya ambacho hakina mwisho duniani, si kwa ubaya tu kila jambo lina mwisho wake. Ikiwa umebaki mwezi mmoja tu ASP Nkongo na Teddy wapate likizo kwa ajili ya kukamilisha shughuli ya kufunga pingu za maisha, ubaya wa Kamishna Jenerali wa magereza ulifahamika kwa wanausalama wa siri wa EASA na hapo huo ndiyo ukawa mwanzo wa kusakwa. Mambo yalipomzidi kombo alijaribu kutoroka lakini alishindwa kutokana na umakini wa wanausalama hao, alipoona hivyo aliamua kupamba nao kwa silaha aweze kutoroka. Huu ndiyo ulikuwa mwanzo wa yeye kupigwa risasi na kufariki dunia, baada ya kifo chake ndiyo mabaya yake yote yalijulikana aliyokuwa akiyafanya. Ilikuwa ni aibu kubwa kwa mtu kama yeye, habari hiyo ilifika kwa James akiwa yupo kazini. Hakuifurahia wala kuhuzunika kwa taarifa jiyo aliposikia, alishindwa kuifurahia taarifa hiyo kutokana yeye alikuwa na mwanadamu kifo kilikuwa kinamuhsu na pia alishindwa kuhuzunika kutokana na huyo aliyeuawa alikuwa ni mbaya wake. Alikuwa akimchukia sana lakini baada ya kifo chake hicho chuki yake iliisha papo hapo, hakuona sababu ya kuendelea kumchukia. Mazishi ya Kamishna Jenerali wa magereza yalifanyika kwenye makaburi ya Kinondoni na yalihudhuriwa na Kamishns Mwambe tu yeye hakuuhudhuria kabisa. Juma chache baadaye walisahau kabisa na hatimaye siku zilisonga, hatimaye muda wa likizo ulifika na wote wawili wakaenda likizo ambako walikuwa wakienda kukamilisha taratibu zote za ndoa. Walipotoka ndani ya gereza hilo kwa mara ya kwanza wakiwa na nguo za kiraia, walieleka jijini Arusha moja kwa moja nyumbani kwa Mzee Andrew. Walipokewa kwa mapokezi makubwa sana kutokana na ujio wao kuwepo taarifa zake kwa tajiri huyo, hiyo ilikuwa siku ya kwanza kwa ASP Nkongo kuweza kufika nyumbani kwa wakwe zake ambao walikuwa matajiri kupitiliza. Furaha aliyokuwa nayo haikuwa ikielezeka kabisa kutokana na jinsi alivyokubalika ukweni, alikaa hapo ukweni kwa siku kadhaa na kisha aliondoka kwenda kwenye nyumba ya mchumba wake ambako walifanya makazi kwa kipindi chote walichokuwa wapo jijini hapo. Hazikupita siku nyingi sherehe za awali zilianza katika kipindi hicho pia Kamishna Mwambe alikuwa ameomba likizo kwa ajili ya kusimamia shughuli hizo. Baada ya majuma mawili tangu shereha za awali kukamilika siku ya harusi iliwadia, ilikuwa ni mara ya pili kwa ASP Nkongo kufikia hatua hiyo na mara ya kwanza kwa Teddy. Hatimaye ndoa ilipita kanisani baada ya wote kuridhia na kutokuwepo pingamizi, shereha kubwa ilifuatia katika ukumbi uliokuwa mali ya Mzee Andrew. Wale wote walikuwa watu wa karibu wa pande zote walikuwa amefika ndani ya sherehe hiyo kubwa ambayo ilikuwa imehudhuriwa na viongozi wakubwa kutoka na ushawishi aliyonao Mzee Andrew kama mmoja matajiri nchini. Kamishna Mwambe alijikuta akitokwa machozi ndani ya sherehe hiyo kutokana furaha ambayo ilipitiliza, hata alipopewa kipaza sauti aongee aliishia kutoa shukrani kwa Mkwe wake kutokana na kumfanya kijana wake kurudi katika hali ya kawaida.
“Sina mengi ya kuongea napenda niwatakie kila la heri kwenye maisha yao, mkwe wangu wangu Teddy napenda niseme asante sana kwa kumfanya James kuwa mpya” Kamishna Mwambe aliongea huku akijifuta machozi ya furaha ambayo yalikuwa yakimtiririka huku shangwe zikisikika, baada ya hapo Mzee Andrew naye alishika kipaza sauti kuongea machache. “Narudia tena kusema neno lile ambalo niliwahi kukuambia, James asante sana kwa kunirudishia Teddy wangu aliyepotea bila wewe asingekuwa hivi. Sijutii uamuzi wangu wa kukukabidhi jumla Teddy wangu ikiwa umemrudisha, nashindwa hata nikupe zawadi gani kwa hilo kijana wangu. Teddy mwanangu kila la heri mheshimu na umpende Mumeo ” Mzee Andrew aliongea na shangwe zikafuata baada ya kumaliza. Sherehe kubwa ilipoisha fungate ambayo ilikuwa imepangwa kufanyika kwenye hoteli ya Singita ndiyo ilifuata, maharusi waliondoka kuelekea huko hotelini usiku huo huo kwa kutmia ndege ya kukodi ambayo walikuwa wameandaliwa. Walikaa huko kwa muda waliotakiwa kukaa na hatimaye walirejea Arusha tena, walikaa jijini hapo kwa siku kadhaa na hatimaye walirejea kazini baada ya muda wao wa likizo kuanza kuyoyoma. Gerezani napo kulikuwa na shangwe kubwa walipowasili, waliandaliwa sherehe fupi ya kuwapongeza kwa hatua waliyofikia. Waliyaanza maisha ya ndoa wakiwa huku wakiendelea na kibarua chao, Askari jhela aliyepitia mazito aliishi maisha yenye furaha na mke wake wakaanzisha familia.
Safina alikuwa peke yake na aliuona usiku huo kuwa mbaya sana katika maisha yake kwani mvua kubwa ilikuwa inanyesha na yeye alikuwa amejibanza kwenye kibanda kilichokuwa kinavuja. Hakuwa na pakwenda tena kwani kwao alishafukuzwa. Kwakweli Safina alilia sana usiku huo. “kifo, kwanini kifo? Umemchukua baba, umemchukua mama na kuniacha peke yangu ndani ya dunia hii. Ona sasa mvua kubwa inanyesha, nipo hapa peke yangu nalowa. Kwanini kifo usimrudishe baba na mama yangu ili niishi nao kama zamani?” Safina alilia sana bila ya kupata msaada wowote hadi panakucha. Asubuhi yake mvua ilikatika na Safina akaingia mtaani ili kutafuta chakula kwani alikuwa hajala chochote, ilikuwa si rahisi tena kwa mtu yeyote kutambua kama yule ni mtoto wa Sam na Latifa.
Mchana wa saa saba, Safina alichoka kutembea huku na kule kwahiyo akajikalia kwenye gogo na kujiinamia chini huku akilia. Ndipo alipoguswa bega na mtu ambaye kwa muda huo Safina hakumjua ni nani.
Mchana wa saa saba, Safina alichoka kutembea huku na kule kwahiyo akajikalia kwenye gogo na kujiinamia chini huku akilia. Ndipo alipoguswa bega na mtu ambaye kwa muda huo hakumjua ni nani. Safina akageuka nyuma ili kuangalia ni nani aliyemshika bega, akamuona ni mtoto wa kiume aliyekuwa mchafu sana. Mtoto huyo akamuuliza Safina, “unalia nini?” Safina akamjibu, “njaa inaniuma” Yule mtoto akamwambia Safina, “usijali nifuate” Safina akainuka na kuanza kumfuata yule mtoto, wakafika chini ya mti na yule mtoto akamwambia Safina asimame hapo ili amsubiri kwani anaenda kuleta hela ili waende kula. Safina alikuwa akimsubiri huyo mtoto bila ya kujua hiyo hela anaenda kuchukua wapi. Safina akiwa mahali pale akimngoja yule mtoto mara akasikia sauti za watu, “mwizi huyo jamani nimeibiwaaa” Alipokuwa akisikiliza vizuri ili ajue zile kelele zinatokea wapi, mara akamuona yule mtoto akija na kumshika mkono huku akienda naye haraka haraka. Walitoka sehemu hiyo na kwenda hadi kwa mama ntilie ambapo yule mtoto aliagiza sahani mbili za chakula na kuanza kula, alipodaiwa pesa akatoa noti ya shilingi elfu kumi, kwakweli Safina alishangaa sana kwa mtu kama yule kuwa na hela ya aina ile. Walipomaliza kula, yule mtoto akaondoka na Safina, wakafika sehemu moja chini ya mti na kukaa huku wakifahamiana vizuri. “mimi naitwa Musa, je wewe mwenzangu unaitwa nani?” SAFINA: Mimi naitwa Safina. MUSA: Sasa nini kimekukumba hadi ukawa unalia? Safina akamuelezea Musa kuhusu kifo cha wazazi wake na jinsi alivyofukuzwa na ndugu zake, huku machozi yakimtoka. MUSA: Dah!! Pole sana Safina, hayo ndiyo maisha yanayotukumba watoto yatima. SAFINA: Na wewe pia ni yatima? MUSA: Ndio mimi ni yatima sina baba wala mama. SAFINA: Pole sana, nao walikufa kama wazazi wangu? MUSA: Historia yangu ni tofauti kidogo Safina, ila kwa kifupi simjui baba na wala sijawahi kumuona, mama alinambia kuwa baba alinikataa tangu tumboni ila hata hivyo mama yangu alishakufa. SAFINA: Mmh!! Na ndugu zako je? MUSA: Walinifukuza, hawakutaka kuniona tena. Wakanisingizia mambo mengi ambayo sikuwahi kuyafanya, nimekuwa mtoto wa mitaani na mitaa ndio baba, mama na ndugu zangu. SAFINA: Inasikitisha sana. MUSA: Ndio maisha yalivyo Safina. Musa na Safina wakazoeana, wakajenga ukaribu kama wa ndugu. SAFINA: Na ile pesa uliipata wapi? MUSA: Safina, maisha ya mtaani ni kuhangaika tu. Ile pesa niliiba. SAFINA: Uliiba? Si unajua kuiba ni dhambi! MUSA: Najua ndio ila tufanyeje ikiwa ukiwaomba hawakupi? Bora kuwaibia tu. SAFINA: Lakini Musa jua ukikamatwa utafungwa. MUSA: Kufungwa ni kawaida kwa watoto wa mitaani Safina. Musa na Safina wakaongea mambo mengi ya hapa na pale ili Safina aweze kujisikia amani tu.
Basi Musa akamchukua Safina na kwenda kumtambulisha kwa watoto wengine wa mtaani. MUSA: Jamani, huyu ni mwenzetu anaitwa Safina. (halafu akamgeukia na Safina), Safina, hapa kuna Mirium, Tizo na Shida. Halafu kuna wengine, Sikuzani na Siza nadhani watakuwa mitaa mingine. Safina akaweza kufahamiana na watoto hao ambao walionekana kuwepo tu duniani bila matumaini yoyote ya maisha. MUSA: Safina maisha yetu pa kulala shida, pa kula shida. Sisi mvua yetu na jua letu kwahiyo naomba utambue hilo na taratibu utazoea. SAFINA: Sawa Musa. Siku zote tangu Safina aingie mtaani alikuwa akilia tu kwa ugumu wa maisha kwani hakuzoea kuomba wa la kuiba kwahiyo maisha yakawa magumu sana kwa upande wake, hakujua la kufanya kwakweli. Alitamani Mike aende kumchukua ili akaishi nae tena Marekani. “Anko Mike kwanini hata siku moja usiote kuwa mimi napata shida huku? Natamani uji kunichukua ili twende tukaishi wote Marekani” Mambo hayo yalikuwa kama ndoto tu kwa Safina, mara Musa akamshtua Safina toka kwenye lindi la mawazo. MUSA: Safina! Usipende kulia kila muda Safina, utaumwa na kichwa. SAFINA: Inaniuma Musa, yani kufukuzwa kwenye nyumba ya wazazi wangu!! Inaniuma sana. MUSA: Ni kweli inauma Safina ila Mungu yupo atatusaidia. SAFINA: Kwanini watoto yatima tunateseka hivi jamani? MUSA: Safina, mwanzoni nilijua kwamba mimi nimeteseka sana kwavile mama yangu hakuwa tajiri kwahiyo alivyokufa wakaona kuwa mimi nitakuwa ni mzigo kwao, ila nimeshangaa wewe Safina yani wazazi wako na utajiri wote ulioniambia bado ndugu wanathubutu kufanya hivi!! Kweli binadamu wengi hawana utu Safina ila jipe moyo tutashinda. SAFINA: Najaribu kufikiria ila nakosa jibu la mwisho wa maisha yangu. MUSA: Usiwaze sana Safina, inabidi ujitahidi kwenda kuombaomba ili tupambane na maisha haya. SAFINA: Musa, siwezi. (huku akilia). MUSA: Jitahidi Safina utaweza tu. Musa alimuhurumia sana Safina ingawa wote walikuwa kwenye matatizo lakini Musa alionyesha huruma kubwa sana juu ya Safina hadi watoto wengine wa mtaani walimshangaa Musa kwani yeye ndiye aliyejulikana kuwa na roho mbaya kuliko wote, ila alionekana kumuhurumia sana Safina. Na taratibu Safina akaanza kuzoea vile wanavyoishi watoto wengine wa mtaani. Musa hakutaka mtu yoyote kuonekana akimuonea safina.
Suzan katika pitapita zake, akakutana na rafiki yake aliyesoma naye kitambo. SUZAN: Pendo rafiki yangu, unafanya kazi wapi? PENDO: Nafanya kazi hospitali, mwenzio siku hizi nimekuwa nesi. SUZAN: Mmh! Pendo kwa elimu gani? PENDO: Mbona niliendelea kusoma mwenzio. SUZAN: Basi shoga yangu ukisikia mahali wanatafuta msaidizi, nipo jamani naomba unishtue. PENDO: Hata pale hospital walikuwa wanahitaji mtu wa usafi ngoja nitaulizia. SUZAN: Dah!! Utakuwa umenikomboa kweli rafiki yangu. Siku zote Suzan alijilaumu kwa kutosikiliza ushauri wa dada yake Latifa, ambaye alikuwa akimshauri mara kwa mara kuwa asome lakini yeye hakufatilia, ila sasa anajutia kwani kila anapoomba kazi wanataka cheti, alijilaumu sana kwa kutnkukubali kuendelea na masomo. Suzan akapata bahati ya kupata kazi ya usafi kwenye hospitali anayofanyia kazi Pendo. Aliwekwa kwenye usafi na baadae mapokezi akiwaandikisha majina wagonjwa wanaoingia hospitalini hapo Alikuwa hodari sana kitendo ambacho kilimvutia daktari mkuu wa hospitali hiyo na kuamua kumuweka mapokezi. Kwakweli Suzan alifurahi sana kitendo cha yeye kupata kazi kwenye hospitali hiyo na akaamua kuhamia nyumbani kwa Pendo na kuishi wote. PENDO: Hivi Suzy hunaga mpenzi? Sijakusikia hata mara moja ukimtaja shemeji yangu. SUZAN: Wee Pendo acha tu, nilikuwa nae anaitwa Frank ila akaenda masomoni Ujerumani, na tangu kipindi hiko sijawahi kuwasiliana nae hadi leo nadhani atakuwa amepata msomi mwenzake. PENDO: Na mbona hujatafuta mwingine sasa? SUZAN: Sitaki mtu yeyote, najipanga na maisha yangu kwanza. PENDO: Ila usijari, kama kweli huyo Frank alikupenda atakutafuta tena tu. SUZAN: Sidhani, mtu ameshaenda nje kusoma halafu arudi amkumbuke Suzy asiyesoma? Haiwezekani, acha tu nijipange kwa maisha yangu. PENDO: Sawa ila badae mi nitatoka na shemeji yako. SUZAN: Sawa shoga yangu hakuna tatizo. Suzan na Pendo wakaishi pamoja kama ndugu wa damu, na hapo ndio tunapata urafiki mwema kwani mnasaidiana kwa shida na raha.
Watoto wa mtaani walijikuta, wakimshangaa sana Musa kwajinsi alivyobadilika. MIRIUM: Jamani, toka Musa akae na Safina, siku hizi amekuwa na huruma ya ajabu hata wizi kapunguza. SHIDA: Namshangaa sana sijui anafikiri ataishije bila ya wizi! SIKUZANI: Usimshangae, bora awe hivyo hivyo jamani, Musa alizidisha roho mbaya hadi sisi alikuwa anatufanyia unyama. Safina alikuwa hapendi kabisa tabia ya wizi ndiomana Musa akapunguza wizi sababu ya Safina.
Siku moja baada ya mvua kubwa kunyesha, Safina alianza kuumwa, alikuwa akitapika na kutetemeka yani alikosa nguvu kabisa. Basi Musa alikuwa anamuangalia Safina tu, hakutaka kwena kudhurula na kumuacha Safina katika hali aliyokuwa nayo. Muda wote alikaa naye tu chini ya mkorosho kwani ilikuwa ndio sehemu kubwa ya kupumzika kwa watoto wengi wa mitaani. MUSA: Safina, ngoja nikaombeombe angalau nipate hata mia mbili ya kununua panadol. SAFINA: Sawa Musa. Musa akaondoka eneo hilo na kuanza kutafuta tafuta Pesa ya kununulia dawa. Safina akabaki mwenyewe akijisemea, “Hivi kwanini? Shida zote zinipate mimi? Naumwa mimi, hakuna msaada wowote. Mvua yangu na jua langu. Nitaishi hivi mpaka lini? Au ndio mpaka nitakapokufa kama wazazi wangu?” Safina alikuwa akilia lia tu mahali pale. Musa akaenda kwa watu ili apate msaada. MUSA: Saidia jamani, rafiki yangu anakufa. Naomba hata mia. MTU 1: Kama una hela ndogo si umpe! MTU 2: Wee siwezi kutoa hela yangu kuwapa hawa watoto, nakwambia hawa ndio vibaka wa mjini. Musa aliomba na kuomba bila ya kupata msaada wowote, akakumbuka hadi ule usemi usemao kuwa ‘siku ya kufa nyani miti yote huteleza’ Kwakweli Musa aliona ni mtihani mkubwa sana kwake, akaamua kurudi pale chini ya mkorosho. Akamkuta Safina akiwa na hali mbaya zaidi, Musa akaamua kufanya uamuzi wa haraka na kujisemea liwalo na liwe. Musa aliporudi pale chini ya mkorosho akamkuta Safina akiwa kwenye hali mbaya zaidi, akaamua kufanya uamuzi wa haraka zaidi na kujisemea kuwa liwalo na liwe. Musa akaamua kumchukua Safina na kumbeba mgongoni mwake, akamfunika na kipande cha khanga huku akijisemea, “naenda nae hospitali hivihivi hata kama sina pesa” Musa akaanza safari ya kwenda hospitali, takribani hospitali kama tatu alifukuzwa yeye na mgonjwa wake kwani hakuwa hata na pesa ya kumuona daktari. Akaanza kukata tamaa ila akajipa moyo kuwa lazima apate hospitali ya kumweka Safina tu. Alipofika hospitali ya nne iliyoitwa hospitali ya Nile, alishangaa kupokelewa vizuri na moja kwa moja yeye na mgonjwa wake mgongoni wakapelekwa kwa daktari na yule muhudumu akatoka, kwakweli Musa alishangaa sana kwa kutokuulizwa pesa ya kumuona daktari. Yule daktari akamwambia Musa amlaze yule mgonjwa kitandani, halafu akamfanyia baadhi ya vipimo na Musa akangojea vipimo vya daktari akiwa na mgonjwa wake mule ndani. DAKTARI: Mgonjwa ameanza kuumwa lini? MUSA: Tangu juzi. DAKTARI: Hamkumpa dawa yoyote? MUSA: La, sikumpa dawa yoyote. DAKTARI: Ok, mgonjwa anaonekana kuwa na malaria kali sana, kwahiyo itabidi alazwe. MUSA: (Akashtuka), alazwe? DAKTARI: Ndio alazwe, mbona unashtuka? Musa alishtuka sababu hata hela ya kumuona daktari alikuwa hajalipa, sasa gharama za kulazwa je!! Baada ya hapo, daktari akamuandikia Safina matibabu na kuwapeleka sehemu husika ya kulazwa wagonjwa. Musa akatakiwa kwenda kuandikisha taarifa za mgonjwa, akaandikisha taarifa anazoelewa yeye kuhusu Safina basi. Nesi wa zamu akamuita Musa ili aweze kulipia gharama za kumuhudumia mgonjwa wake mahali hapo. Musa akamuomba kwa kuwa hana pesa yoyote. Nesi huyo aliyejulikana kwa jina la Rose. ROSE: Hivi wewe utamletaje mgonjwa kwenye hospitali binafsi wakati huna pesa? MUSA: Nihurumie dada yangu, si unaona hali yangu ilivyo. ROSE: Hali yako mimi inanihusu nini? Unafikiri hospitali ya bure hii? MUSA: Simaanishi kuwa hii ni hospitali ya bure, ila sina pesa kwasasa. ROSE: Sasa nakwambia, nenda uendako ukalete pesa hapa lasivyo mgonjwa wako hatumuhudumii chochote. Umesikia wewe? MUSA: Sawa nimesikia. Musa akawa anaondoka eneo lile, ndipo Suzan akamuona na kukumbuka kuwa alimpeleka yule na mgonjwa wake moja kwa moja kwa daktari bila kumuandikisha, akaamua kumuita na Musa akasogea pale dirishani akijua ndio yaleyale ya pesa. SUZAN: Unaitwa nani? MUSA: Naitwa Musa. SUZAN: Na yule mgonjwa wako anaitwa nani? MUSA: (Akijibu kwa hasira), nishamwandikisha kule kwingine. SUZAN: Mbona unajibu kwa hasira hivyo? Inabidi na hapa aandikishwe. MUSA: Msinichanganye bhana. Halafu akaondoka, kwakweli Suzan alimshangaa sana Musa na majibu yake na alijishangaa kwanini hakumuandikisha tangia mwanzo, akawa anajisemea, “mmh!! Wagonjwa wengine wamevurugwa kweli jamani.” Musa nae alijiuliza sana kuwa kwanini amemjibu vibaya yule dada wa mapokezi wakati hakuna baya alilomtendea. “yule dada anaonekana kuwa na huruma, ila ndio hivyo tena nishamjibu vibaya dah” akaendelea na safari yake ya kutafuta pesa ya huduma kwaajili ya Safina.
Kule hospitali nako Rose akamfata Suzan pale dirishani. ROSE: Hivi Suzy kazi imekushinda au?? SUZAN: kwanini jamani dada Rose? ROSE: Unapokea wagonjwa ovyo ovyo, unawapeleka kwa daktari bila kadi wala nini.! Ona sasa yule chokoraa kamleta chokoraa mwenzie tena bila hata ya pesa. Unadhani yule mgonjwa atalipiwa na nani huduma hizi? SUZAN: Jamani dada, alikuwa hapa na mgonjwa wake akiwa hoi sana nikaona kuwa niwawaishe halafu maelezo nichukue wakitoka. ROSE: Kweli akili zako ni fupi sana, yani unangoja watoke ndio uchukue maelezo loh!! Umewekwa hapo mapokezi ili ufanye nini? SUZAN: Nipokee wagonjwa, na si ndio nimewapokea jamani. ROSE: Ngoja tu, huyu chokoraa asipoleta pesa tutakata mshahara wako kwa uzembe. Kwakweli Suzan alishangaa sana na hakujua cha kufanya ikambidi tu awe tayari kwa lolote. Suzan alipompokea Musa na Safina, hakujishughulisha kabisa kumuangalia yule mgonjwa ila aliwapeleka moja kwa moja, laiti kama angewaangalia angeweza kumgundua Safina mtoto wa marehemu dada yake.
Musa akajaribu kuomba msaada kwa watu. MUSA: Naomba nisaidie japo pesa kidogo tu. MTU: Bora hiyo pesa nikaitupe baharini kuliko kukupa wewe. Musa alikata tamaa kabisa ya kupata pesa kwa njia hiyo ya kuomba, “hata kama Safina amenikataza maswala ya wizi lakini lazima nikaibe tu ili nipate pesa ya kupeleka huko hospitali” Akaamua kwanza aende kwa wenzie pale mtaani ili akapate ushauri. Alipokuwa anakwenda, wenzie nao wakawa wanaongea, SHIDA: Mmh jamani Musa anavyotia huruma utafikiri anayeumwa ni yeye kumbe Safina. SIKUZAN: Eti anamuhurumia Safina kisa mpeni wa maisha haya. Hivi nani mwenyeji wa maisha haya jamani? Mmh!! MIRIUM: Kwanza huyo Safina kila siku ni mgeni kwa lipi haswa jamani!! Kashazoea jamani, miaka nenda rudi tupo naye sasa huo ugeni usioisha ni upi? TIZO: Labda kwavile ni kadogo dogo ndomana anakahurumia jamani. Musa akawafata pale walipo na kuwaeleza kuhusu Safina, MUSA: Jamani, Safina kalazwa. WOTE: Kalazwa? MUSA: Ndio na hospitali wamesema kuwa nisipopeleka pesa basi hawatamuhudumia. MIRIUM: Musa usijali, watamuhudumia vizuri, wewe kwa hali yako hiyo wanafikiria pesa utaitoa wapi. MUSA: Sio nisijali Mirium, hapa tufikirie maisha ya Safina kwani yako hatarini. MIRIUM: Lakini si umesema kuwa amelazwa? MUSA: Ndio amelazwa. MIRIUM: Sasa wasiwasi wako ni nini? Akifa si atakufa mikononi mwao? MUSA: Ndio atakufa mikononi mwao lakini hasara atapata nani? SHIDA: Hasara gani sasa? MUSA: Shida, kuwa na akili. Tunampoteza mwenzetu, tunapoongea hapa mkumbuke kuwa tunaongelea uhai wa Safina! MIRIUM: Sawa, sasa tufanyeje? MUSA: Hilo ndio jambo la kusema, tukae chini na tujadiliane kitu cha kufanya ili mwenzetu aweze kurudi katika hali yake ya kawaida. Basi wakaanza kujadiliana namna ya kupata pesa, SHIDA: Jamani, naona mnapoteza muda tu. Musa wewe ni shujaa kwa wizi kwanini basi tusiende kupora watu pesa? MIRIUM: Shida, kumbuka juzi ulitaka kukamatwa! SIKUZAN: Ila hakuna njia nyingine rahisi zaidi ya hiyo, itabidi Musa uende kupora tu na hilo ndio suluhisho. Waliongea mengi na kuafikiana kuwa wakafanye uporaji tu.
Manesi walishindwa kumuhudumia Safina aliyekuwa amelazwa kwani madawa yote aliyoandikiwa yalikuwa hayajalipiwa bado. Usiku wa siku hiyo ilikuwa ni zamu ya Pendo, na kama kawaida yao akiingia nesi mwingine anapewa maelekezo juu ya wagonjwa waliolazwa. Pendo na Suzan walikuwa wanaonana mara chache kamavile hawaishi nyumba moja, hii ilitokana na muda wa kuja kazini ambavyo ulitofautiana kati yao, mmoja akiingia mwingine anatoka. Mara nyingi wanakuwa pamoja ile siku ya mapumziko tu. Kwahiyo Pendo alipofika mahali hapo alimkuta Suzan akiwa amejiandaa kutoka, wakasalimiana tu na kuagana, halafu Suzan akaondoka kwenda nyumbani. Pendo alishangaa sana kumuona binti mdogo akiwa mgonjwa sana na bila ya kuhudumiwa kwa chochote, ikambidi Pendo akamchukulie binti huyo dawa na sindano kwa dhamana yake mwenyewe, akamuhudumia sana usiku wote wa siku hiyo, hadi ilipofika alfajiri alionekana kuendelea vizuri kwani dripu aliyomuweka ilimsaidia sana. Kama kawaida yake Pendo, kabla hajaondoka akawatembelea wagonjwa wote, PENDO: Unaendeleaje? SAFINA: Naendelea vizuri, asante sana kwa huduma yako. PENDO: Usijali, nipo kwaajili yenu. Alipomaliza akajiandaa na kuondoka ili kuwapisha manesi wengine na yeye kwenda kupumzika. Pendo alipofika nyumbani, Suzan alikuwa tayari ameshaondoka, hiyo ilikuwa ni kawaida kwao kwani mara nyingine zinaweza kupita hata siku tatu bila ya kuonana. Siku hiyo, Pendo akawa anafanya usafi, mara albamu ya Suzan ikadondoka, basi akaichukua na kuangalia picha, ndipo alipokutana na picha aliyopiga Sam, Latifa, Suzan na Safina. Basi akajikuta akimkazia macho sana yule mtoto na kuona kuwa hata hajabahatisha pale. “mbona sura hii inafanana na sura ya mtoto aliyelazwa hospitali? Au nimemfananisha? Hapana huku sio kufanana. Hivi inawezekana akawa ndiye huyu? Kama ndiye huyu inawezekana hata Suzan asimjue jamani?” Pendo alijiuliza maswali mengi kwani anajua wazi kuwa Suzan ndiye anayepokea wagonjwa, iweje sasa asimuone huyo mtoto. Pendo aliishika sana sura ya yule mtoto kutokana na kumuhudumia sana usiku huo. Pendo alipofika hospitali siku hiyo alikuwa na hamu sana ya kuonana na Suzan ili amweleze kuhusu ile sura ya yule mtoto, lakini alipofika tu akaambiwa kuwa Suzan alishaondoka kitambo kwani kuna vitu ameenda kufatilia. Mara Pendo akafatwa na Rose na kuanza kuambiwa, ROSE: Yule mgonjwa wa kitanda namba kumi na moja…. Kabla hafamaliza, Pendo alishtuka sana kwani hicho kitanda ndicho alicholazwa Safina. PENDO: Amefanya nini? Mara Pendo akafuatwa na Rose na kuanza kuambiwa, ROSE: Yule mgonjwa wa kitanda namba kumi na moja….. Kabla hajamalizia, Pendo alishtuka sana kwani hicho kitanda ndicho alicholazwa Safina. PENDO: Amefanya nini? ROSE: Kheee!! Mbona una haraka kama mkojo wa asubuhi!! Si unisikilize kwanza. PENDO: Sawa, amefanya nini? ROSE: Mwanzoni nilitoa amri kuwa asihudumiwe ila sasa nimeona bora muendelee kumpa huduma tu. Ila kesho asubuhi kuna kikao cha wafanyakazi wote wa hapa kwahiyo usiwahi kuondoka. Pendo sasa akapumua kwa amani maana mashaka yalimjaa sana kuhusu Safina. Na usiku wa siku hiyo akaendelea kumuhudumia kwa ukaribu zaidi ili amkariri vizuri ila hakuweza kumuuliza maswali mengi sababu ya wingi wa wagonjwa usiku huo.
Suzan alipofika nyumbani alikuwa amechoka sana, alipoangalia mezani akaiona picha aliyopiga yeye, Latifa, Sam na Safina. Aliikuta pale mezani kwavile Pendo alisahau kwenda nayo. Aliichukua picha ile na kuiangalia, huku akijisemea, “Hivi kwanini Sam na Latifa mlikufa? Na Safina je unaishije huko ulipo? Umenisahau hata mimi? Ni bora shemeji na dada wangeendelea kuishi hukohuko Marekani kuliko walivyorudi hapa nchini, ona sasa wameteketea, loh kifo kweli hakina huruma” Asubuhi alipofika kazini kukawa na kikao cha wafanya kazi ambacho kiliwahimiza kufanya kazi kwa bidii, na pia kuacha uzembe katika kazi. Kwahiyo Pendo hakuweza kuzungumza tena na Suzan. ROSE: Hii ni hospitali ya mtu binafsi sio ya serikali kwahiyo mjue kwamba hospitali hii inalipiwa kodi hivyobasi kila mgonjwa anatakiwa achangie gharama za matibabu. Muache huruma za kijinga. Alipomaliza aliwataka wote waende sehemu zao za kazi kwani Rose ndiye aliyekuwa msimamizi mkubwa wa hospitali hiyo.
Suzan alipokuwa pale mapokezi mara akaja mtoto mchafu mchafu, huyo mtoto alikuwa ni Shida mwenzake na Safina huko mitaani. SHIDA: Kuna mgonjwa kalazwa hapa anaitwa….. Kabla hajamaliza, Suzan akadakia kumjibu. SUZAN: Kama unaulizia wagonjwa waliolazwa nenda dirisha la pili. Kwahiyo Shida akaondoka hapo na kwenda kuulizia hilo dirisha la pili. SHIDA: Kuna mgonjwa kalazwa hapa, anaitwa Safina. Je amelazwa sehemu gani? Basi yule mdada akawa anapekua daftari la wagonjwa waliolazwa pale na kumuuliza, MDADA: Kalazwa lini? SHIDA: Juzi MDADA: Umesema anaitwa nani? SHIDA: Safina MDADA: Nenda wodi ya wanawake chumba cha tatu, kitanda namba kumi na moja. SHIDA: Sawa asante. Shida akaenda moja kwa moja hadi alipoelekezwa na kumkuta Safina kalala, akaamua kumuamsha. SHIDA: Safina, Safina, amka. SAFINA: Kheee! Shida umekuja. Musa yuko wapi? SHIDA: Pole sana, unaendeleaje? Je wanakupa huduma? SAFINA: Naendelea vizuri na huduma wananipa ndio. SHIDA: Pole sana, Musa ndio kanielekeza kuwa uko hapa. SAFINA: Kwani yeye yuko wapi? Sijamuona tangu juzi aliponileta hapa. SHIDA: Musa kakamatwa na polisi. SAFINA: Kafanywa nini? Kwani kafanyaje hadi kakamatwa? SHIDA: Kuna jamaa mmoja tulipanga kumpora kwa bahati mbaya Musa akakamatwa, mimi nilibahatika kukimbia. Yani hivi tunavyoongea hapa yupo kituoni. SAFINA: Masikini Musa, najua alikuwa anaiba kwaajili yangu. Nahitaji kumuona, kwahiyo itabidi nitoroke hapa hospitali. SHIDA: Hata mimi nilitaka kukushauri hivyohivyo kwani ukiwaambia kwamba unataka kutoka watakudai pesa wakati sisi pesa hatuna. Kwahiyo Shida na Safina wakawa wanapanga jinsi ya kutoroka hapo hospitali. SHIDA: Safina, hebu nijifanye kama nakufanyisha mazoezi halafu tukifanikiwa kufika nje tunatimua mbio. Sawa? SAFINA: Sawa, nimeelewa. Shida akajifanya kamshika Safina mkono huku anatembea naye taratibu hadi wakafanikiwa kutoka nje, na ikawa rahisi kwao sababu muda huo kulikuwa na watu wengi wakiingia na kutoka kuwaona wagonjwa wao. Walipofika nje wakaanzisha safari ya kwenda kituoni na wala hawakurudi tena hapo hospitalini.
Pendo alipofika nyumbani, sura ya Safina bado iliendelea kutembea kichwani mwake. Ulipofika mchana akajiandaa ili aende hospitali kuzungumza na Suzan kuhusu yule mtoto kwani mchana huwa hakuna wagonjwa wengi. Na alipofika hospitali, akamkuta Suzan kapumzika sababu kulikuwa hakuna wagonjwa wa kupokelewa muda huo. Basi wakasalimiana na Pendo akatoa ile picha na kumuuliza Suzan. PENDO: Suzan, hivi hawa ni wakina nani? SUZAN: Aaah!! Hapa kuna marehemu dada yangu na shemeji ambao kipindi kile nilikwambia wapo Marekani pamoja na mtoto wao. PENDO: (Akionyesha sura ya Safina), umesema huyu ni mtoto wao? SUZAN: Ndio ni mtoto wao, vipi leo unawaulizia hao ndugu zangu kama vile umewahi kuwaona? PENDO: Hapana bhana, huyu mtoto wao anaitwa nani? SUZAN: Ooh! Anaitwa Safina hata sijui anaendeleaje jamani. PENDO: Umesema anaitwa Safina? SUZAN: Ndio anaitwa Safina, mbona unashangaa au umewahi kumuona kwenye Tv hapo zamani? Maana kanajua kuimba kweli yani. PENDO: Unajua Suzy, yule binti wa kitanda namba kumi na moja kafanana kweli na huyu halafu nae anaitwa Safina. SUZAN: Acha masikhara bhana Pendo, binti gani huyo? Mbona mimi sijamuona wakati mimi ndio napokea wagonjwa? PENDO: Si yule binti waliyesema mwanzo tusimuhudumie sababu ya pesa! SUZAN: Khaaa! Kwani kafanana na huyu? (akionyesha ile sura ya Safina) PENDO: Ndio, kwani wewe hujamuona? SUZAN: Ndio sijamuona. PENDO: Basi twende ukamuone. Suzan na Pendo wakaenda hadi wodini lakini Safina hukuwepo pale kitandani, wakaamua kumuuliza nesi wa zamu ya mchana siku hiyo. PENDO: Zena, hivi yule mgonjwa wa namba kumi na moja yuko wapi? ZENA: Kuna muda nilimuona na ndugu yake, ila sijui sasa atakuwa ameelekea wapi. Basi wakaamua kumtafuta kila mahali pale hospitali lakini hawakumuona. ROSE: Au ametoroka? ZENA: Pengine. PENDO: Hapana bhana, hawezi kutoroka. ROSE: Usikatae, yule binti anajua wazi kuwa anadaiwa inawezekana akawa ametoroka ili kukimbia deni. Rose akawaita kikao cha dharura na kuwaambia kuwa wanatakiwa kuwa makini na wagonjwa hapo hospitali kwani hawatatakiwa kutoka bila ruhusa ya daktari. ROSE: Wagonjwa wengine lawama tu, sasa kametoroka bila hata ya kumaliza dozi. Umakini wenu manesi ni muhimu sana la sivyo itakuwa tunatoa huduma zisizo na maana hapa kama wagonjwa hawamalizi dozi. ZENA: Masikini, kaliogopa kudaiwa. ROSE: Ndio lazima kaogope, kwani hospitali ya baba yake hii!! Baada ya hapo, Pendo na Suzan wakatoka nje. PENDO: Pole Suzan, kwani hujaweza kumuona. SUZAN: Nashindwa hata kuelewa kwanini sikumuangalia wala kumuhoji? PENDO: Kwani ilikuwaje? SUZAN: Alikuwa amebebwa mgongoni na yule kijana na mimi nilimpeleka moja kwa moja kwa daktari halafu nikatoka nje dah!! PENDO: Je, hukumuuliza huyo kijana wanakaa wapi? SUZAN: Yule kijana aligoma kunijibu halafu cha kushangaza wala sikumfatilia tena. PENDO: Usijari Suzy kila jambo na wakati wake na kila tukio maishani hutokea kwa sababu fulani, huwezi jua kwanini imekuwa hivyo ila Mungu pekee ndiye ajuaye. Ila amini kwamba milima haikutani lakini binadamu ukutaka, kwahiyo ipo siku mtaonana tena na tutaendelea kumtafuta huyo Safina. SUZAN: Asante sana Pendo, nashukuru. Pendo na Suzan walikuwa ni watu wa kupeana moyo sana katika mambo yote wanayoyafanya.
Modesta alipata habari zilizomuumiza sana ikabidi aende nyumbani kwa dada yake Aisha kuuliza. MODESTA: Nasikia mmeuza mali zote za marehemu! AISHA: Ndio tumeuza kwani wewe tatizo lako nini? MODESTA: Dada, mtapata laana nyie!! Sina ubaya ila mmechafua sana ukoo kwani kuna tetesi nimesikia kuwa mmewaroga Sam na Latifa ndiomana wamekufa. AISHA: Hayo mambo ya kuroga nenda kamuulike kaka yako Juta kwani mi sihusiki. MODESTA: Na mbona Safina hayupo huko kwa kaka Juta? AISHA: sasa umekuja kumuulizia kwangu, kwani umesikia kuwa hiki ni kituo cha kulelea watoto yatima? MODESTA: Ila dada, utayakumbuka maneno yangu, ipo siku tu. Haki ya mtu haiendi bure bure, nitajitahidi hata me mwenyewe kumtafuta huyo Safina hadi nimpate. AISHA: Nenda kamtafute bhana eeh hunipunguzii kitu wala huniongezei. MODESTA: Nitamtafuta ndio maana nyie mashetani msije mkammaliza na yeye bure. Kwakweli Modesta aliumizwa sana na matendo ya ndugu zake, na akaamua yeye kama yeye kuanza kumsaka Safina.
Musa akiwa rumande, alipigwa sana na maaskari kama kawaida yao ila huko rumande akaenda kukutana na kitu tofauti kilichobadili taswira nzima ya maisha yake.
Musa akiwa rumande alipigwa sana na maaskari kama kawaida yao ila huko rumande ndio alipoenda kukutana na kitu tofauti kilichobadili taswira nzima ya maisha yake.
Musa akaitwa kuhojiwa na askari kama kawaida yao kwani unaweza kujikuta unahojiwa hata mara kumi. ASKARI: Wee kijana mwizi unaitwa nani? MUSA: Musa Israel ASKARI: Nani? MUSA: Musa Israel. Ndani ya ofisi kulikuwa na askari mkuu wa hapo amekaa kwenye meza, gafla akajikuta kuna jambo linamjia kichwani baada ya kusikia jina hilo. “Nakwambia, hii mimba si umeikataa!! Basi huyu mtoto nitakayejifungua nitamwambia kuwa baba yake anaitwa Israeli, na wala sitakutaja wewe. Na hiyo Israel si jina la mtu yeyote kama unavyodhani bali namaanisha yule malaika mtoa roho za watu kwani wewe ni muuaji na unafanana nae” Hiyo sauti ya kike ikajirudia kama mara tatu katika akili yake, akajikuta akiwaamuru wale maaskari waache kumpiga yule mtoto na wamuingize ofisini kwake ili amuhoji. Musa alipoingizwa ofisini hapo akakalishwa chini, basi yule askari akawaamuru wale maaskari watote na akaanza kumuhoji Musa. KAMANDA: Umesema unaitwa nani? MUSA: Naitwa Musa. KAMANDA: Musa nani? MUSA: Musa Israeli. KAMANDA: Baba yako yuko wapi? MUSA: Simjui wala na yeye hanitambui. KAMANDA: Je! Israeli ni jina lake? MUSA: Hapana. KAMANDA: Sasa mbona unajiita Musa Israeli ikiwa Israeli si jina la baba yako? MUSA: Mama aliniambia nijiite hivi sababu baba alinikataa. KAMANDA: (Akapumua kidogo), mama yako anaitwa nani? MUSA: Anaitwa Sada Mwinyi. KAMANDA: Sada Mwinyi? MUSA: Ndio Sada Mwinyi. KAMANDA: Yuko wapi kwasasa? MUSA: Amekufa. KAMANDA: (Akashtuka sana), amekufa? Dah! Pole sana. Kwahiyo sasa unaishi wapi? MUSA: Naishi mitaani tu. KAMANDA: Mitaani? Kwanini? MUSA: Ndugu wa mama walinifukuza baada ya mama yangu kufariki. KAMANDA: Na kwanini unaiba? MUSA: Maisha ya mtaani ni magumu sana ndio yanayotufanya watoto wa mitaani tuibe. Yule kamanda akajikuta amekosa raha kwakweli, mara wakaingia wale maaskari ili kumchukua Musa wamrudishe rumande ila yule kamanda akawazuia na ikawabidi watoke nje. KAMANDA: Musa, nataka nikuchukue ili ukaishi nyumbani kwangu. Je uko tayari. MUSA: kweli muheshimiwa? Niko tayari tena nitafurahi sana. Basi yule kamanda akamchukua Musa ili aondoke naye, akaenda kuifuta kwanza kesi inayomkabili na kujiandaa kuondoka naye.
Safina na Shida walipokuwa katika harakati za kwenda kituoni, ni hapo gafla Safina akawaona ndugu wawili wa baba yake kwa mbali. SAFINA: Shida tujifiche sitaki wale wanione. SHIDA: Kwanini Safina? SAFINA: Siwataki wale ni ndugu wa baba nawachukia sana. SHIDA: Ila si ndugu zako? SAFINA: Ndio, yule mwanamke ni shangazi Modesta na yule mwanaume ni bamkubwa Jese. Sitaki kabisa wanione. Basi Safina na Shida wakajificha hadi pale Modesta na Jese walipopita ndipo Safina na Shida wakatoka na kuendelea na safari. MODESTA: Kwakweli kaka sijafurahishwa kabisa na vitendo vyenu, na sitachoka kumtafuta Safina hata kama itapita miaka kumi. JESE: Tatizo lako Mode huna kazi za kufanya, yani wewe kila mwaka habari ni Safina Safina kama wimbo wa Taifa vile. Hata Nuhu alitengeneza safina kama vipi na wewe tengeneza yako. MODESTA: Nyie kweli mmevurugwa jamani. Ila siku zote nitawakumbusha hili kwamba jasho la mtu haliendi bure. JESE: Nimegundua kwanini wewe Mode hupatani na Aisha, kumbe ndio unaakili mbovu kiasi hicho loh!! Achana na mtoto wa Sam, mwache ahenye aone dunia ilivyo. MODESTA: Hivi ungekuwa wewe ndio umefanyiwa hivyo ungejisikiaje? JESE: Ushasema ingekuwa, kwahiyo fanya mambo yako, yangu niachie mwenyewe. Roho ya Modesta ilikuwa inamuuma sana juu ya upotevu wa Safina, amakweli si wote wabaya kwenye ukoo. Mara gafla Modesta akageuka nyuma na kwakweli akamuona mtu kama Safina, akamuangalia kwa makini na kuhakikisha kuwa ni yeye, Safina alipogundua kaonekana akageuka nyuma, ndipo Modesta akaanza kuita “Safina, Safina” Safina hakugeuka kumuangalia tena bali alianza kutimua mbio huku Shida akimfata kwa nyuma. Walipofika mahali wakapumzika. SAFINA: Nilikwambia Shida wale si watu wazuri. SHIDA: Huwezi jua, labda hakuwa na lengo baya. SAFINA: Huwajui ndiomana, haya tuendelee tu na safari yetu ya huko kituoni. Modesta aliumia sana moyo kwahiyo akaamua kwenda kwa kaka yake Peter. MODESTA: Kaka usiku wa jana nimemuota Latifa. PETER: Sasa mimi nifanyeje? MODESTA: Kaka tafadhari, nisaidie kumtafuta Safina. Tafadhari simama nami kwenye kumtetea Safina. PETER: Nilishindwa kumtetea wakati anafukuzwa na mke wa kaka sembuse sasa? Ila alitia huruma sana. MODESTA: Kaka, kumbuka hakuna kibaya tulichotendwa na Sam wala Latifa. Tumuhurumie mtoto wao basi PETER: Kweli huruma inanijia, ila inawezekana Safina ameshakufa sababu ni muda mrefu sasa. MODESTA: Natambua hilo ila Safina yu hai. Naomba tukimpata uwe nami katika kumtetea, nakuomba kaka yangu. Kwakweli sina amani wala raha kwa miaka yote hii naumia tu juu ya Safina. PETER: Umejuaje kama yu hai? MODESTA: Nimemuona mjini akiwa kachakaa sana dah!! Namuhurumia Safina kwakweli. Peter akajikuta naye akimuhurumia Safina ingawa ni muda mrefu umepita hata alikosa matumaini kuwa Safina yu hai, lakini kwavile Modesta alimuhakikishia kuwa Safina yu hai kwahiyo akaamini hivyo.
Yule kamanda na Musa walipokuwa wanatoka pale kituoni, kufika nje tu mara Safina na Shida nao wakafika mahari pale. Musa alipomuona Safina alimkimbiria kwa furaha na kumkumbatia, lakini yule kamanda hakuelewa kinachoendelea basi Musa akawaelezea wenzake kuwa kuna kamanda amejitolea akaishi kwake. Basi akawavuta Safina na Shida ili nao waweze kusalimianda na yule kamanda na labda na wao wamuombe kuishi kwake. Ila kitendo cha Safina kumuona yule kamanda kikazua taswira mpya, kwani Safina alishtuka sana kumuona mtu huyo kwani hakumtarajia kabisa.
Kitendo cha Safina kumuona kamanda huyo kilizua taswira mpya, kwani Safina alishtuka sana kumuona mtu huyo ambaye hakumtarajia kabisa. Safina akamuita yule kamanda, kitendo kilichowashangaza wote kuwa Safina anamjua yule kamanda. SAFINA: Bamdogo Frank!! Yule kamanda akashtuka sana kwani hakutarajia kama anafahamiana na binti huyo. Ilikuwa ni ngumu kwa Frank kumtambua Safina kwani alimuacha akiwa mdogo sana na sasa amekua ila amechakaa sana. FRANK: Umenijuaje? SAFINA: Nakujua, wewe si ndiye mchumba wa mamdogo Suzy? FRANK: Kwani wewe ni nani? SAFINA: Mimi ni Safina, mtoto wa Sam na Latifa. FRANK: Ooh!! My God, yani wewe ndiye yule mtoto uliyekuwa unaimbaimba vizuri!! Dah, nini kimekupata Safina? SAFINA: Ni historia ndefu. FRANK: Ok, twendeni mkapande gari niwapeleke kwangu. Wote wakaenda kupanda gari ya Frank na kwenda nyumbani kwake.
Walipofika nyumbani kwa kamanda Frank, ikabidi kamanda huyo amuulize vizuri Safina kwani hali ya Safina ilimshangaza sana. FRANK: Safina hebu nielezee kilichokupata. SAFINA: Baba na mama walikufa (huku akilia). FRANK: Dah!! Pole sana Safina, inamaana Sam na Latifa walikufa?? Mmh hebu nieleze vizuri Safina. Safina akamueleza kila kitu kilichomtokea hadi kuwa na maisha aliyokuwa nayo sasa, maisha ya mtaani. Alimueleza yote hayo huku machozi mengi yakimbubujika. FRANK: nyamaza Safina, hii ni hali ya dunia ila siku moja itaisha. SAFINA: Sijui hiyo siku moja itakuwa lini? Miaka inakuja na kupita nikiwa natangatanga mitaani. Safina mimi wa leo si Safina yule aliyeweza kuonekana nchi za ulaya akionyesha vipaji vyake, Safina wa sasa ana kipaji cha ombaomba na kula majalalani. FRANK: Safina usijari, ilimradi mimi nipo hautakula tena majalalani. Sawa mama!! SAFINA: Nashukuru sana bamdogo, kwani mamdogo Suzy yuko wapi? FRANK: Sijaonana naye kwa kipindi kirefu sana na hata sijui anaishi wapi? SAFINA: Kwani umeachana na mamdogo? FRANK: Hapana, sijaachana nae, ni maisha tu ndio yakanitenga nae. SAFINA: Sasa mbona hujui aliko? FRANK: Nilisafiri, nikaenda India kimasomo. Tangu kipindi hiko mawasiliano na Suzy yakakatika na niliporudi sikujua Suzy anaishi wapi hadi leo hii sijui. SAFINA: Je, ulijaribu kumtafuta? FRANK: Ndio nilimtafuta, maana nilipoenda kwenu nikadhani labda nitamkuta Sam nimuulize ila nilikuta sura ngeni na wakaniambia kuwa Sam haishi pale. SAFINA: Inamaana shangazi kauza nyumba yetu? FRANK: Usijari Safina, jipe moyo utashinda. Safina akaongea mambo mengi sana na kamanda Frank, naye Frank akawaambia Safina, Musa na Shida kuwa amejitolea kuwalea kwahiyo wataishi hapo nyumbani kwake huku akiwa na lake moyoni kuhusu Musa. FRANK: Ningependa wote mniite baba, sawa eeh!! WOTE: Sawa tumekuelewa. Kwahiyo Frank akaishi nao hapo kama watoto wake.
Sikumoja Modesta akiwa katika pita pita zake akakutana na Suzan, akaamua kumuita. MODESTA: Suzy jamani za miaka?? SUZAN: Hata nikikwambia wewe itakusaidia nini? MODESTA: Sisi ni ndugu Suzy. SUZAN: Undugu wa mimi na nyie ulikufa pale dada yangu alipoingia kaburini. MODESTA: Najua una hasira Suzy, ila jaribu kunielewa. Nia yangu ya kukuongelesha ni Safina. SUZAN: (Kusikia habari ya Safina, ikabidi awe mpole), eeh Safina kafanyaje tena? MODESTA: Kuna siku nilimuona Safina mjini, kwahiyo inamaanisha Safina yupo. Ni bora tukasaidiana kumtafuta ili mtoto asitangetange. SUZAN: Hapo umeongea la maana sasa, eeh unafikiri tufanyaje? MODESTA: Suzan hakuna namna zaidi ya kumtafuta tu. Kama tungekuwa na pesa labda tungemtangaza. Basi nipe namba yako ya simu ili tuwasiliane. SUZAN: Mweeeh!! Hata hiyo simu ninayo basi!! Niliona inanitia gharama ya vocha tu bila umuhimu wowote kwahiyo nikaiuza. Labda wewe unipe yako. MODESTA: Nadhani hapa tumekutana majanga matupu sababu hata mimi sina simu. Ikabidi Suzan amuelekeze Modesta sehemu anayofanyia kazi ili kama akipata taarifa yoyote afike kumwambia. Kama kawaida ya Modesta akaenda tena kwa kaka yake mkubwa kumlalamikia. MODESTA: Hivi kaka roho yako haikuumi kabisa kuhusu Safina?? JUTA: Ila wewe Mode sijui akili yako ikoje? Unataka kufufua mambo yaliyopita na kusahaulika kabisa kama yalikuwepo. MODESTA: Hata kama mud mrefu umepita kaka, wakati bado upo. Safina atafutwe na mmuombe msamaha. JUTA: Kweli wewe ulikosea kuzaliwa jamani, mbona akili yako haina akili Mode, yani mimi na akili zangu timamu nianze kumtafuta Safina?? Hebu kafie mbele huko wewe na huyo Safina wako. MODESTA: Najua mnaniona mimi kama chizi sasa ila ipo siku mtayakumbuka maneno yangu. Kama kufa nitakufa tu, wangapi wameshakufa sembuse mimi!! JUTA: Tatizo mdogo wangu hujielewi wewe. MODESTA: Kaka unajua wazi mkeo ana roho mbaya, alinifukuza mimi hadi Safina kamfukuza. JUTA: Nitolee mashetani yako hapa kwangu, kama umekosa ya kusema naomba uende. Na utakufa masikini wewe. MODESTA: Ndio nitakufa masikini lakini masikini shujaa, mtu nisiyechoka kupambana na maisha yangu mwenyewe sio kupambana na mali za watu. JUTA: Nenda bhana, umewehuka wewe sio bure. MODESTA: Naenda ndio ila siku zote nitaendelea kulilia haki ya Safina. Roho ya Modesta ilikuwa inamuuma sana kila akifikiria mambo mema aliyofanyiwa na Sam na Latifa. Akaondoka huku akijisemea “sitachoka na sichoki mpaka pale haki itakapotendeka juu ya Safina”. Wakati anawaza hayo, mbele yake akamuona Latifa amesimama na mara gafla akampungia mkono na kupotea, kwakweli Modesta alihisi kama kuwehuka na hisia kubwa ikamjaa kuwa kaka zake wanahusika vilivyo na kifo cha Sam na Latifa, lakini akajiuliza kuwa hata kama angefungua mashtaka ya mauaji angewashtaki vipi wakati watu hao wameuwawa kishirikina na kikubwa zaidi ni kuwa serikali haiamini ushirikina. Imani ya Modesta inamuachia Mungu hiyo kesi ya kishirikina ila bado anajitolea kupambana na haki ya Safina, huruma kubwa inamjaa akikumbuka pale njiani alipomuona Safina na jinsi alivyopauka, moyo wake unazidi kumtuma tu kuwa anapaswa amsaidie Safina.
Siku moja Kamanda Frank alishika picha ya Suzan akawa anaiangalia na kujiuliza kimoyomoyo, “hivi Suzy uko wapi jamani? Hata sijui nianzie wapi kukutafuta. Mawazo mengi yananisonga, natumai uwepo wako ungenisaidia kuyatatua” Mara Safina alienda pale alipokaa Frank, na kumkuta na picha ya Suzan mkononi. SAFINA: Ni picha ya mamdogo Suzy hiyo? FRANK: Ndio ni wewe, nilikuwa nawaza hapa pakuanzia kumtafuta. SAFINA: Hebu niione. Kamanda Frank akampa Safina ile picha, wakati Safina anaiangalia mara Musa na Shida wakasogea eneo lile. Na Musa nae akajiunga na Safina kuitazama. MUSA: Mmmh!! SAFINA: Mbona unaguna Musa? MUSA: Huyu dada kama namjua? SHIDA: Dada gani huyo? Wakampa picha na Shida nae akaitazama. SHIDA: Hata mimi namjua. Frank kusikia vile akashtuka, FRANK: Mmemjuaje? SHIDA: Mimi nilimuona hospitali, na wewe Musa je? MUSA: Hata mimi nilimuona hukohuko hospitali. FRANK: Hospital gani? Na anafanya nini? MUSA: Huyu dada yupo mapokezi kwenye ile hospitali aliyolazwa Safina. FRANK: Kweli?? Basi kesho twendeni tukamuangalie, pengine ni yeye. Safina alibaki na mshangao tu kwani yeye hakubahatika kumuona huyo dada.
Kesho yake Suzan akiwa pale kazini mara kuna mtu akamfata huku akiwa na haraka nyingi sana ilionyesha sehemu anayopelekwa kulikuwa na tukio la hatari limetokea. Hakuweza kuendelea kubaki eneo hilo bali alienda kuchukua ruhusa haraka haraka na kuaga. Kwahiyo akaondoka na huyo mtu aliyemuita.
Kesho yake Suzan akiwa pale kazini mara kuna mtu akamfata huku akiwa na haraka nyingi sana ilionyesha sehemu aliyopelekwa kulikuwa na tukio la hatari sana. Hakuweza kubakia hapo kazini bali alienda kuchukua ruhusa na kuondoka haraka haraka pamoja na yule mtu aliyemuita. Pendo alipofika pale hospitali nae alishangaa kumkosa Suzan mahali pale kwani siku hiyo aliwahi kufika. Alipouliza akaambiwa kuwa Suzan ameomba ruhusa kuwa kuna mahali anaenda mara moja. Hakujua kwakweli mahali alipoenda Suzan.
Kamanda Frank kama alivyopanga jana yake, ikabidi aondoke na wakina Musa ili waweze kumuulizia Suzan kwenye hospital ambayo walisema kuwa wamemuona. Walipofika pale hospitali ikabidi amtume Musa ili aende kumuulizia na kumuita. Musa akaingia pale hospitali, akakuta mapokezi kuna wadada wawili wamekaa wanaongea. Ikabidi awafate na kuwasalimia, kisha akawauliza. MUSA: Samahani, namuulizia yule dada wa mapokezi. PENDO: Nani huyo? Suzy au? MUSA: Ndio ni dada Suzy. PENDO: Ooh!! Ametoka, kwani unataka nini? MUSA: Kuna mgeni wake pale nje anamwita. PENDO: Nipeleke nikaongee naye. ZENA: Loh!! Pendo kwa umbea sikuwezi. PENDO: Ushaanza maneno yako na wewe loh, hebu nipeleke mwaya. Basi Musa akaongozana na Pendo hadi alipo Frank kwani alitoka nje ya gari na akawa amesimama chini ya mti. FRANK: Habari yako!! PENDO: Nzuri tu ila Suzy ametoka ila mimi ni rafiki yake, niambie tu shida yako pengine naweza nikakusaidia. FRANK: Hivi wewe sio Pendo kweli? PENDO: Ndio mimi ni Pendo, kwani wewe nani? FRANK: Yani Pendo umenisahau Frank!! Dah! PENDO: Frank?? Aaah!! Kumbe wewe ni Frank jamani. Dah ulinipotea kabisa. Wote wakakumbukana na kukumbatiana. PENDO: Umebadilika sana Frank hata sikukutambua. Uko wapi siku hizi? FRANK: Nipo tu kwani masomo nishamaliza kitambo. Basi Pendo na Frank wakaongea mengi sana kwani ni kipindi kirefu tangu waonane. FRANK: Inamaana Pendo upo hapa na Suzy? PENDO: Kwanza umejuaje kuwa Suzy yupo hapa? FRANK: Ni stori ndefu, kwani yuko wapi? PENDO: Si nimekwambia kuwa ametoka!! FRANK: Sawa, kwani unamjua Safina mtoto wa Latifa? PENDO: Nilimuona kwenye picha tu. FRANK: Basi ngoja. Kamanda Frank akaenda kuwaita wakina Safina, Pendo alipomuona Safina alishangaa sana. PENDO: Huyu ndie Safina? FRANK: Ndio ni huyo. PENDO: Ooh!! Jamani nilikuwa namuhudumia hapa bila hata kumjua, pole sana Safina, na vipi unaendeleaje? SAFINA: Naendelea vizuri, asante. PENDO: Frank, umempata wapi huyu? FRANK: Ni stori ndefu. PENDO: Mmh nawe umezidi sasa kila kitu ni stori ndefu tu. FRANK: Na wewe kwa kupenda umbea, huachi tu tabia yako ya shule? PENDO: Hahaha, ila bora Safina kapatikana maana Suzy alikosa raha kabisa. Basi Pendo akaenda kuomba ruhusa ili awapeleke wakina Frank mahali anapoishi yeye na Suzy, aliporuhusiwa akawapeleka. PENDO: Hapa ndio tunapoishi. FRANK: Kwahiyo na Suzy anaishi hapa? PENDO: Ndio tunaishi wote. FRANK: Aah!! Hamuachani nyie yani hadi leo mko wote. PENDO: Urafiki wangu na Suzy ni wa kudumu. Basi wakaongea mengi, ikabidi Frank ampe Pendo ramani ya kumuelekeza nyumbani kwake ili aweze kufika na Suzy. Hadi muda wanaondoka, Suzy alikuwa bado hajafika nyumbani.
Suzan akiwa na yule mtu aliyempeleka, mara akamuona Modesta akiwa mbele yake. SUZAN: Khee!! Vipi tena Mode nini kimekupata? MODESTA: Huwezi amini Suzy, nimemuona Latifa kabisa kwa mcho yangu ndiomana nikamtuma mtu akufate ili nawe umuone. SUZAN: (Akiangalia huku na kule), mbona hayupo? MODESTA: Ametoweka ila alikuwa hapa, nimemuona kabisa Suzy. SUZAN: Mbona makubwa haya, miaka yote hii bado dada anatokea.? MODESTA: Hawezi kuacha mpaka pale mtoto wake atakapopewa haki anayostahili. Mara Modesta akaanguka eneo hilo, ikabidi Suzan amuinue hata kushangaa ni kipi kimemuangusha. SUZAN: Pole jamani Modesta, kwani ni nini kimekuangusha? MODESTA: Sijui ila hisia zangu zinanituma kuwa kuna nguvu mbili zinavutana Suzy. SUZAN: Kivipi Mode! MODESTA: Kwasasa sijui ila ipo siku nitajua tu. Ikabidi Suzan amsindikize Modesta hadi nyumbani kwake anapoishi. MODESTA: Suzy tafadhari, ukimpata Safina kuwa nae makini sana. Nahofia wasije wakamtenda vibaya. SUZAN: Sawa Mode, nimekuelewa. Ila hata sijui nimkinge vipi? MODESTA: Kuna mambo mengi yanacheza kwenye ulimwengu tusioweza kuuona kwa macho yetu cha muhimu ni kwamba kuwa makini na Safina ukimpata, maadui ni wengi sana. SUZAN: Nakuahidi Modesta, nitajitahidi kwa hilo. Suzan akamuaga Modesta na kuanza kurudi mahali anapoishi.
Suzan alipofika nyumbani, akamkuta Pendo yupo kwenye harakati za kurudi tena kazini. PENDO: Suzy leo kuna ugeni tuliupata. SUZAN: Ugeni gani huo? PENDO: Ni Frank na Safina ila nitakwambia vizuri nikirudi. Pendo akaondoka na kumuacha Suzan akiwa kwenye lindi la mawazo. “mmmh!! Mbona sielewi, Frank na Safina? Frank yupi na Safina yupi? Mbona Pendo kaniacha njia panda. Lakini leo anawahi kurudi nitamsubiri hadi arudi ili aniambie hata hivyo kesho ni siku yetu ya mapumziko.” Suzan alikuwa na hamu kweli ya kujua kuhusu huo ugeni, kwahiyo akamsubiri Pendo ili aongee nae ingawa alichoka sana siku hiyo. Pendo aliporudi akamueleza vizuri Suzan na akamwonyesha ramani ya kwenda nyumbani kwa Frank. PENDO: Basi kesho twende pamoja huko kwa Frank. PENDO: Usijari, kesho tutaenda pamoja kwani ni siku yetu ya mapumziko. SUZAN: Nitafurahi sana nitakapomuona Safina. PENDO: Na Frank je? SUZAN: Nitafurahi pia. PENDO: Nilitaka nishangae, usimfurahie kipenzi chako tena. SUZAN: Mmh na wewe Pendo loh!! Wakajadili na kujipanga vyema kwenda kwa huyo Frank.
Basi kesho yake Pendo na Suzan wakajiandaa na safari ya kwenda kwa Frank ikaanza. Walipokaribia kufika ikabidi waulizie vizuri, wakampata kijana mmoja wa kumuuliza. PENDO: Samahani, tunaulizia nyumba ya mtu mmoja anaitwa Frank iko mtaa huu. KIJANA: mnaulizia kwa kamanda Frank? SUZAN: Kamanda? Mmh!! Pengine ndio huyo huyo. Basi yule mtu akawaelekeza nyumbani kwa Frank, wakamshukuru na safari ikaendelea huku wakisemezana. SUZAN: Inamaana siku hizi Frank kawa kamanda? PENDO: Labda, maisha hubadilika Suzy. Walipofika, wakagonga mlango na kufunguliwa na Shida ambaye aliwakaribisha hadi ndani. Mara Frank akatoka na kuwakuta, kwakweli Frank alifurahi sana kumuona Suzan, alimsalimia na kuongea ya hapa na pale. Wote walifurahi pamoja na Pendo. SUZAN: Jamani nataka kumuona na Safina sasa, yuko wapi eti Frank! FRANK: Kuna muda alitoka na Musa, sijui hawajarudi. Ngoja niwaulizie. Kabla Frank hajainuka kwenda kuuliza, mara Musa akaingia ndani huku jasho jingi likimtoka. FRANK: Musa vipi? Kuna nini? MUSA: (Huku akihema sana) ni Safina. FRANK: Safina kafanyaje? MUSA: Safina kapata ajali. WOTE: Nini? MUSA: Safina kagongwa na gari na sasa yupo hospitali. Suzan alikaa chini, miguu yote iliishiwa nguvu kabisa kwani hakuelewa chochote wakati huo, ni Pendo tu ndiye aliyekuwa akimtuliza.
Suzan alikaa chini miguu yote iliishiwa nguvu kabisa kwani hakuelewa chochote wakati huo. Ni Pendo tu ndiye aliyekuwa akimtuliza. Suzan aliwaza mengi sana, akaikumbuka na kauli ya Modesta kuwa amlinde Safina. Frank akamwambia Musa awapeleke huko hospitali, kwahiyo wakapanda kwenye gari lake hadi hospitali alipolazwa Safina. Walipofika pale wakaulizia kwa daktari ili waweze kumuona. DAKTARI: Sitaweza kuwaruhusu mkamuone kwa sasa, maana hali yake ni mbaya na bado tunamshughulikia. SUZAN: Dokta, atapona kweli? DAKTARI: Msijari yote ni mapenzi ya Mungu. Daktari alivyosema hivyo Suzan akajikuta machozi yakimtoka, Pendo akaendelea kumbembeleza tu. Frank akaanza kumuhoji Musa maswali. FRANK: Musa, kwani ilikuwaje? MUSA: Tulikuwa tunavuka barabara, mi nilikuwa mbele ya Safina na nyuma gafla nikasikia amegongwa. Ila yule dereva alishuka harana na tukasaidiana kumpakiza kwenye gari na kumleta hapa hospitali. FRANK: Huyo dereva yuko wapi? MUSA: Sijui labda uwaulize madaktari. Frank akaenda kuwauliza madaktari na wakamuonyesha alipokaa dereva. FRANK: Hivi kwanini unakosa umakini barabarani hadi unasababisha ajali? DEREVA: Haikuwa kusudio langu kaka hata mi mwenyewe nimeshangaa nimeshagonga. FRANK: Sasa nakwambia omba sana Mungu mgonjwa apone kwani asipopona utaozea segerea. DEREVA: kweli kaka sikudhamiria. Mara Frank akapiga simu kituo cha polisi ili waje wamkamate yule dereva, na walipofika hawakutaka maelezo mengi zaidi ya kumkamata tu. Hali ya Safina iliwakosesha raha kwakweli na kujiuliza maswali mengi sana kuwa kwanini iwe vile ilivyokuwa. Wote walimuombea Safina apone ili waweze kwenda nae sambamba. Suzan alijikuta safari ya kumuona Safina hapo hospitali imepamba moto kiasi kwamba alibakiza kiasi kidogo tu kufukuzwa kazi, alitamani hata Safina ahamishiwe hospitali anayofanyia kazi ili awe anamuona kila mara.
Safina alikaa miezi miwili hospitali kwenye chumba cha pekee na uangalizi mkubwa sana. Suzan alienda kwa Modesta kupata ushauri ila alimkuta Modesta akiumwa umwa. SUZAN: Mode, Safina amepatikana ila amepata ajali mbaya sana na mwezi huu ni wapili sasa yupo hospitali. MODESTA: Suzy cha muhimu ni kumuombea tu apone, naimani Mungu atamsaidia Safina. SUZAN: Na wewe vipi hali yako mbona haieleweki? MODESTA: Naumwa Suzy tangu kipindi kile uliponiacha. Mara Aisha dada wa Modesta akafika mahali hapo. Akashangaa sana kumkuta Suzy akiwa hapo. AISHA: Kheee kwani undugu bado unaendelea kati yenu? MODESTA: Kwanini usiendelee? AISHA: Ila wewe Suzy unapenda sana kujipendekeza. SUZAN: Sijipendekezi bali hata mimi naijali afya ya Modesta. AISHA: Hahaha, mwenzio Mode hapa ana ukimwi ndo mana kanyorodoka ila haya mambo ya kifamilia kwahiyo wewe Suzy hayakuhusu. Kwavile lililompeleka pale lilikuwa limeisha ikabidi Suzy aage na kuondoka. Akabakia Modesta na Aisha mahali hapo. AISHA: Sikia mode, kuna nyumba moja ya marehemu Sam imeshindikana kabisa kuuza, sasa kaka akasema itakuwa sababu ya mdomo wako, hebu tupe baraka wenzio ili na wewe ung’arishe maisha yako. MODESTA: Dada nilishakwambia, na tena nakwambia sitaki kugombania mali za marehemu, nyie endeleeni tu. AISHA: Yani mdogo wangu maradhi yote hayo yanayokusumbua bado hutaki msaada? MODESTA: Kama kusaidiwa basi nisaidiwe kivingine na si kwa kudhurumu mali ya marehemu ipo siku itawarudi tu. AISHA: Kweli mdogo wangu umevurugwa jamani, pole sana. Swala la kushindikana kuuzwa kwa hiyo nyumba kiliwapa mashaka sana ndiomana wakaweka wapangaji wao huku wakitafuta namna ya kuiuza nyumba hiyo.
Hali ya Safina ikaanza kubadilika hadi akawa na hali nzuri na kuweza kuruhusiwa kurudi nyumbani. Ndipo na yule dereva aliyewekwa rumande na Frank akaruhusiwa kutoka. Walimshangaa sana wenzie alivyokonda, akawa anajisemea, “na kazi ya udereva siitaki tena kwani nimekaa rumande bila hata kusomewa mashtaka.” RAFIKI: Umekonda sana John. JOHN: Jela si mchezo na ukizingatia sijazoea kabisa. RAFIKI: Pole sana ndio mambo ya ajali hayo. JOHN: Ndio hivyo wangu, siku zote ajali ikitokea dereva ndio unaonekana mwenye makosa dah!! Hata kama chanzo ni aliyegongwa. RAFIKI: Ndio maisha hayo. JOHN: Nashukuru Mungu amepona na mimi nimeweza kuwa huru. kwakweli yule dereva siku zote alijiuliza chanzo cha ile ajali ni nini kwani hakuelewa kabisa zaidi ya kujikuta kashaponga tayari.
Safina akiwa amerudishwa pale nyumbani kwa Frank, Suzan akawa anaenda kila siku kumuangalia Safina. SUZAN: Unaendeleaje mama? SAFINA: Naendelea vizuri mamdogo saivi nimepona, si unaona nimeanza hata kutembea! SUZAN: Kweli umepona mwanangu. SAFINA: Hivi mamdogo kwanini usije kuishi hapa na bamdogo? SUZAN: unapenda nije kuishi hapa? FRANK: (Akadakia), ndio napenda tuishi pamoja Suzy, Safina endelea kumshawishi mamako mdogo akubali na sisi tufurahi. Suzy akatafakari na kuona bora tu afanye maamuzi ya kuishi hapo. Kwahiyo baada ya wiki Suzy akahamia mahali hapo, huku akiendelea kumpa Safina mazoezi ya hapa na pale mpaka pale ili aweze kutengemaa. Ilimchukua muda kurudi katika hali ya kawaida, ila Mungu alimsaidia Safina na kujikuta amepona kabisa.
Moyo wa Frank ulizidi kumsumbua kuhusu Musa, ikambidi amuite Suzan na kumueleza kila kitu kuhusu Musa. SUZAN: Unamaanisha ni mtoto wako? FRANK: Ndio ni mwanangu. SUZAN: Unaweza kuniambia sababu kubwa ya wewe kukataa mimba! FRANK: Nilikuwa bado nasoma Suzy na huyo Sada mwenyewe alikuwa ni mwanafunzi, ningekubali ningefungwa Suzy. Niliogopa hilo. SUZAN: Ila ni haki yake kabisa huyo binti kukufananisha na Israeli maana hata yeye atakuwa amekufa kwaajili ya msongo wa mawazo juu yako. FRANK: Jamani Suzy!! SUZAN: Hakuna cha jamani sasa, cha msingi ni Musa atambue ukweli na amjue baba yake. FRANK: Sielewi nitaanzia wapi kumwelewesha. SUZAN: Musa ni mtoto wa kiume, itakuwa rahisi kukuelewa mwanaume mwenzie haswa wewe Israeli, hahaha. FRANK: Suzy acha masikhara bhana, mwenzio nipo serious. SUZAN: Basi ngoja tufikirie namna ya kumwambia. FRANK: Hapo sawa. Kwakweli swala hili lilimuumiza sana kichwa Frank kwani alifikiria vitu vingi na mambo mengi.
Siku hiyo Suzan akaamua kumuuliza Musa kiutaniutani kuwa endapo atamjua baba yake atafanya nini. Akakutana na majibu ya ajabu sana yaliyojaa kwenye kichwa cha Musa.
Siku hiyo Suzan aliamua kumuuliza Musa kiutani utani kuwa akimjua baba yake atafanya nini. Akakutana na majibu ya ajabu sana yaliyojaa kwenye kichwa cha Musa. MUSA: Unajua ni vigumu sana mimi kumjua baba yangu kwani mtu pekee anayemjua ni mama ila nae ameshakufa. SUZAN: Musa dunia ni pana sana, huwezi jua siku moja ukamtambua baba yako, hapo utakapomtambua utafanyaje? MUSA: Kwanza nitamuogopa sana huyo mtu, pili kwavile mama yangu alimfananisha na Israel mtoa roho nadhani huyo baba atakuwa ni mtu mbaya sana na mkatili, ataweza kuniua muda wowote. SUZAN: (Akapumua kidogo), ila Musa yote ni mapito katika maisha. Mama yako alimuita Israel labda sababu ya hasira zake juu ya baba yako kipindi hicho ila haimaanishi kuwa baba yako ni mtu mbaya kiasi hicho. MUSA: Atakuwa mbaya tu, kwamaana alinikataa tangu tumboni. Si mtu mzuri kwakweli. SUZAN: Musa, mimi unavyoniona ni mtu wa aina gani? MUSA: Wewe ni mtu mzuri sana sijapata kuona, mtu mwenye upendo na kujari. SUZAN: Nashukuru, je kamanda Frank naye unamuonaje? MUSA: Kwakweli ni mtu wa kipekee sana kwani amebadilisha maisha yangu. SUZAN: Kwamfano ikatokea kwa bahati mbaya tukafanya kitu na kukokosea je unaweza kutusamehe? MUSA: Kwakweli siwezi kuwa na kinyongo na nyie, na sidhani kama kuna baya la mimi kushindwa kuwasamehe. Nyie ndio wazazi na walezi wangu sasa. SUZAN: Basi Musa, mwenzio mimi nilikataliwa na baba yangu kama wewe, na hata nilipokua kua akaendelea kunikataa ila najua ipo siku atanikubali nami niko tayari kumsamehe kabisa. MUSA: Unamaana gani mamA? SUZAN: Maana yangu ni kuwa hata wewe pindi ukibahatika kukutana na baba yako na akakubali kuwa wewe ni mwanae, basi jifunze kumsamehe. Maana maisha ya ujana hufanya watu wafanye vitu bila kufikiri ila badae hujutia ila hilo liwe funzo kwako na kwamaisha yako. MUSA: Nimekuelewa, na mimi siko tayari kukataa damu yangu kwani mtaani ni mateso sana. SUZAN: Sawa sawa, na unapokuwa na tatizo lolote usisite kunieleza. Musa alijikuta akimuelewa sana Suzan na alijikuta akimpenda sana kwani Suzan alikuwa ni mtu mwenye huruma.
Frank aliendelea kujifikiria namna ya kumueleza Musa ukweli. SUZAN: Ni vyema sana mtu akaujua ukweli wa maisha yake kwani kunamuwezesha kujitambua kuwa yeye ni nani? FRANK: Sasa nifanyaje ili niweze kumweleza ukweli? SUZAN: Nakushauri mchukue Musa na kwenda nae sehemu tulivu, uwe kama unapiga nae story za hapa na pale na hapo umwambie ukweli naimani Musa atakuelewa tu. FRANK: Nitaweza mwenyewe kweli Suzy? SUZAN: Wewe ni mwanaume na Musa nae ni mtoto wa kiume atakuelewa tu. Hata hivyo nilishajaribu kumvuta kifikra. FRANK: Ila nadhani itakuwa vyema tukaenda wote, hata kama nitaongea na Musa, wewe utakuwa hata pembeni kutungoja. SUZAN: Usijari Frank, wee nenda nae yeye tu. Frank akamuomba Musa kuwa amsindikize mahali, Musa akajiandaa na kuondoka nae. Frank akampeleka Musa kule alipokusudia kumpeleka. Frank akamueleza Musa kila kitu kilivyokuwa na sababu ya kumkataa kabla hajazaliwa. FRANK: Tafadhari Musa mwanangu nisamehe, kwakweli najutia makosa yangu. MUSA: Kwanza hadi sasa nahisi kuwa naota, yani nimeweza kukutana na mtu aliyejulikana kama Israeli!! FRANK: Kwakweli sikukusudia mwanangu. MUSA: Hivi unajua shida nilizopata wewe? FRANK: Naelewa mwanangu, nisamehe. MUSA: Niachie muda kufikiria. Musa akamuomba Frank warudi, na waliporudi nyumbani Musa akajikuta amekosa amani, akamfata Suzan. MUSA: Kumbe baba uliyekuwa unanieleza ndio huyu ninaeishi nae? Kwanini awe yeye jamani? SUZAN: Musa yote ni katika mapito ya ujana tu, unapaswa kumsamehe. MUSA: Nimsamehe mtu aliyefananishwa na Israeli mtoa roho na mama yangu? SUZAN: Kila jambo hufanywa kwa makusudi flani, mama yako alikupa jina la mbele kama Israel akijua ipo siku utafahamiana na baba yako na hiyo ndio itakuwa furaha yake. MUSA: Kwahiyo inawezekana aliniita hivi kwasababu hiyo eeh!! SUZAN: Hiyo ndio maana yake na ndiomana baba yako akakutambua. Musa akainama na kutafakari sana, akajikuta akiinua kichwa na kusema “Nimemsamehe baba” Kwakweli Suzan alifurahi sana na akamuita Frank, kufika pale Musa akamkumbatia baba yake. Ikawa ni furaha kubwa sana kwa Frank. Usiku wake ikabidi amtambulishe rasmi Musa kwa Safina na Shida kuwa ni mwanae mzazi. Wakafurahi sana kwa kutambuana. Kwakweli Frank alijivunia kuwa na mtu kama Suzan ndani ya nyumba yake na moyo wake ukakiri kwamba yule ndiye mwanamke wa kumuoa.
Musa akajikuta amekuwa ni mtu wa furaha muda wote. MUSA: Nimefurahi sana kumjua baba yangu na hii inaonyesha kuwa hivi karibuni Safina maisha yako yatabadilika kabisa. SAFINA: Kwanini unasema hivyo wakati ndoto za maisha yangu zilishakufa.? MUSA: Safina, leo usiku nimeota kuwa wewe unaishi katika maisha mazuri sana, na mimi naamini ndoto zangu kwani nilipokuwa mtaani nilishawahi kuota kuwa nitamjua baba yangu na imekuwa kweli. SAFINA: Unaamini sana ndoto? MUSA: Ndoto zangu nikiota zaidi ya mara moja daima huwa kweli. SAFINA: Napenda ziwe kweli ila sijui ni nani atakayeweza kunirudisha katika maisha yangu ya zamani labda anko Mike. MUSA: Anko Mike ndio nani? SAFINA: alikuwa rafiki mkubwa wa baba yangu ila ni mzungu na anaishi Marekani. MUSA: Pengine siku moja anaweza kufika nchini kwetu. SAFINA: Mmh sidhani. Mara Suzan akawa amerudi na kuwasalimia kisha kuingia ndani. MUSA: Kwakweli Safina, huyo mamako mdogo ana roho nzuri sana. SAFINA: Ndiomana nampenda, ila siwapendi ndugu wa baba kwakuwa wana roho mbaya kama mashetani. MUSA: Mmh!! Usiwaze sana Safina yote yataisha tu. Musa na Safina wakaongea mambo mengi, kumbe Shida alienda kuwachukua wenzie wengine wa mtaani ili wapate kumuona baba yake na Musa. SHIDA: Karibuni, hii ndio sehemu tunayoishi sisi kwa sasa. SIKUZAN: Khee, pazuri kweli. Mmepata bahati sana Shida. SHIDA: Hapa ni nyumbani kwa babake Musa. MIRIUM: Babake Musa? Kwani Musa ana baba? SHIDA: Ndio kampata babake. TIZO: Kweli Musa ana bahati. Hivi anaweza kuturuhusu na sisi tuishi hapa? SHIDA: Anaweza kwani ana roho nzuri sana. Shida akawakaribisha basi Musa na Safina wakafurahi sana kuwaona wenzao. Na wakaongea mengi. Suzan alipotoka nae akashangaa kuona wamekuwa wengi, baada ya salamu wakamtamburisha, na baadae wakamuomba kuwa watoto hao waishi mahali hapo. Frank aliporudi ikabidi Suzan amweleze kuhusu wale watoto na ombi lao la kuishi hapo. FRANK: Hivi Suzy nitaweza kweli kukaa na familia yote hiyo? SUZAN: Itabidi uweze na iwe njia yako ya kujutia yale yote ambayo mwanao amepitia akiwa mtaani. FRANK: Suzy ila ni wengi sana kwakweli, nitafilisika jamani. SUZAN: Frank, hawa si watoto wadogo kusema kwamba utahangaika nao, ni wakubwa sasa hawa. Ungewaruhusu tu ili wapate mwangaza wa maisha yao. FRANK: Umenipa mtihani mkubwa sana Suzy. SUZAN: Huu mtihani ni saizi yako Frank, tena unakufaa kabisa. Kila kitu huwa na sababu, kubali tuwalee tu hao watoto, watakula tunachokula sisi. FRANK: Sawa nimekubali. Basi watoto hao wakawa wanaishi nyumbani kwa Frank, jumla wakawa kama watu kumi nyumbani kwake.
Suzan akaamua kumpeleka Safina nyumbani kwa Modesta ili akamsalimie na pia Modesta nae ajisikie vizuri kwa kumuona Safina, ila walipofika hawakumkuta na walipouliza wakaambiwa kuwa Modesta alihama na hata hawaelewi ni wapi alipohamia. Wakiwa njiani wanarudi, mara wakakutana na mtu aliyeonyesha kuwa anamjua vizuri Safina. Mtu huyo aliita na kuwafanya Safina na Suzan wageuke nyuma.
Wakiwa wanarudi, gafla akatokea mtu aliyeonyesha kuwa anamjua vizuri Safina. Mtu huyo aliita, kitendo kilichofanya Safina na Suzan wageuke nyuma. Ndipo hapo Safina akapatwa na mshangao kuona amekumbukwa na mtu huyo, kumbe walipishana nae kwanza na ndipo kufika mbele huyo mtu akageuka na kumuita Safina. SAFINA: Aaah madam Lucy!! Basi wakakumbatiana. LUCY: Unajua nilipowapita hapo sura yako ikanijia sana ndiomana nikajaribu kukuita nijue kama ni wewe, kumbe ni wewe kweli jamani! SAFINA: Ndio ni mimi madam. LUCY: Umebadilika sana Safina, ni sura yako tu ndio haibadiliki. Unaishi wapi kwani? SAFINA: Naishi na mamdogo (huku akimuonyeshea kwa Suzan). Basi Suzan na Lucy wakasalimiana na kufahamiana pia. LUCY: Kwahiyo wazazi wako bado wako Marekani? SAFINA: Hapana (huku machozi yakimlengalenga), walishakufa kitambo sana. LUCY: Jamani Safina, pole sana mama. SAFINA: Nimeshapoa madam, vipi siku hizi bado unaendelea kufundisha pale shuleni? LUCY: Hapana, nipo na biashara zangu tu. Ila kuna watu wametoka ulaya huwa wanakuja kwangu kujifunza kiswahili. SUZAN: (Akaingilia kati), Safina hebu nitambulishe vizuri. SAFINA: Mmh!! Mamdogo nawe, huyu alikuwa mwalimu wangu, anaitwa madam Lucy. LUCY: Ni vizuri kufahamiana, ila kwangu sio mbali na hapa tafadhari naomba niwapeleke mpafahamu. Kwahiyo Safina na Suzan wakaenda hadi kwa Lucy kupafahamu. LUCY: Ingieni basi ndani mnywe hata maji! SUZAN: Usijali mwalimu, tutapanga tu siku nzuri ya kuja kukutembelea. SAFINA: Madam, hao wanafunzi wako huwa wanakuja hapa kujifunza? LUCY: Hapana, huwa nawafata mahali walipofikia ila hapa huja mara moja moja kunitembelea. Walikuwa na maongezi mengi sana ila Suzan akaona waage ili waweze kuwahi kurudi nyumbani. Kwahiyo Lucy akawasindikiza na wao wakaenda zao. Kwakweli Lucy nae alimsikitikia sana Safina. “Ama kweli maisha yanabadilika, yani Safina alivyokuwa mzuri ndio amechusha vile!! Dah, inaonyesha kapitia magumu sana. Eeh Mungu mrehemu.” akajikuta ananyoosha mikono juu na kumuombea Safina.
Kesho yake Suzan akiwa kazini, Pendo akamfata. PENDO: Kheee mwenzangu, una tenda ya kulea watoto yatima? SUZAN: Na wewe kwa umbea, umewaonea wapi? PENDO: Jana nilifika kwako Suzy. SUZAN: Wale hawana pa kwenda Pendo. PENDO: Sasa pale pana raha gani zaidi ya karaha na kero. Hapo ulipo huna mtoto halafu unaishi na mijitu yote ile loh!! Pale ilitakiwa uishi na watoto wawili tu Musa na Safina. Ila huruma yako itakuponza Suzy. SUZAN: Pendo, fikiria kwanza wale watoto hawana wazazi, hawana pa kuishi wala pa kwenda. PENDO: Lakini wale wameshazoea maisha ya mitaani Suzy, kumbuka kunguru hafugiki. SUZAN: Jamani Pendo maisha ya mtaani si mazuri. PENDO: Hivi unataka ndoa kweli wewe rafiki yangu? Nakwambia pale Frank hafurahii chochote, usije kujikuta umekazana kulea mitoto isiyokuhusu wakati mwenzio anatafuta mwanamke wa kujiliwaza nae. SUZAN: Jamani Pendo, usiseme maneno hayo. Unafikiri mi nifanyaje? PENDO: Wapelekee wanapolelewa yatima wenzao, hilo ni wazo tu kama hutaki lipotezee. Kwakweli Suzan alijiona yupo kwenye wakati mgumu ila bado aliendelea kuwaonea huruma watoto hao.
Mtaa mpya aliohamia Modesta kipindi hiko akajikuta akiwa na urafiki na mdada aliyesadikika kuwa na maruhani. Mdada huyo alikuwa na asili ya kiarabu ila chotara kwani alikuwa ni mchanganyiko wa mwafrika na mwarabu, alijulikana kwa jina la Yusra. Wakiwa wanapiga stori kuna mtu alimdokeza Modesta kuwa Yusra akipandisha maruhani ana uwezo wa kuzungumza mambo mengi yaliyopita na yanayowazunguka. Kwavile Modesta alijihisi kuwa na matatizo kwa kipindi hiko akajiweka karibu zaidi na huyo binti ili pengine aambiwe matatizo yake hata kwa njia ya stori. Siku moja akiwa yupo ndani kwake na huyo binti, akatokea mtu mwingine aliyeitwa Rhoda na kuwasha marashi ambayo yalimuhamasisha Yusra kuongea kile anachokiona. MODESTA: Unajua kaka na wifi yangu walikufa kifo cha gafla sana. YUSRA: Kifo chao ni mipango ya wanadamu, tena ni ndugu zako, wabaya sana. MODESTA: Na mbona wifi anapenda kunitokea mimi? YUSRA: Ule ni mzimu wake, na katika wote kwenye ukoo wako amekuona ni wewe mwenye huruma. MODESTA: Na ile ajali niliyoambiwa mtoto wao amepata? YUSRA: Ile haikuwa ajali ya kawaida kama mnavyodhani, ulikuwa ni mpango wa ndugu zako kumuangamiza na yule mtoto ila mwenyezi Mungu amemponya. MODESTA: Jamani amepona kweli?? Hata siamini. YUSRA: Amini kuwa amepona, ila ndugu zako wanajua amekufa. Usiwaambie chochote hadi pale mtoto mwenyewe atakapoamua kujitokeza kwao. MODESTA: Na vipi kuumwa kwangu mimi? YUSRA: Ulikuwa na ugonjwa wa kawaida ila badae ndugu zako wakauzidisha ili kufanga mdomo wako. MODESTA: Mmh!! Inamaana ndugu zangu ni wachawi? YUSRA: Hapana si wachawi ila wanatabia za kichawi, yote hayo wamefanya kwa ushirikina wakisaidiwa na mganga mmoja hivi, ila tambua kwamba siku zote Mwenyezi Mungu ndiye muweza. Kwakweli Modesta alisikitika sana kuhusu ndugu zake, akajisemea “yote haya ni sababu ya tamaa za mali” kwakweli alimuhurumia sana Safina, huku akiwachukia na kuwaogopa ndugu zake.
Siku hiyo Frank akatembelewa na shangazi yake na dada yake aliyeitwa Mwasiti. Walipofika nao walishangaa kuona vijana na mabinti nje ya nyumba ya Frank. SHANGAZI: Mwasiti, vile visichana na vivulana vinatafuta nini pale nje ya nyumba ya Frank? Wakati Frank hana hata mtoto wa kusema watacheza naye. MWASITI: Hata mimi nashangaa shangazi. Walipofika, wale watoto wakawasalimia na Suzan akatoka nje na kuwakuta, akawakaribisha ndani. Suzy alikuwa anawajua ndugu karibia wote wa Frank na wao walikuwa wanamjua ila hawakujua kama anaishi na Frank kipindi hicho kwani ni muda mrefu hawajapata habari zake. MWASITI: Suzy!! Usiniambie sasa hivi unaishi na Frank!! SUZAN: Ndio naishi naye. MWASITI: Ndio hatakuja kututembelea! SUZAN: Nilipanga kuja na Frank ila mambo yakaingiliana. SHANGAZI: Kwani Frank yuko wapi na wakati tumemwambia tunakuja? SUZAN: Ametoka mara moja ila atarudi muda si mrefu. SHANGAZI: Samahani kwanza nataka niulize kitu. SUZAN: Bila samahani shangazi. SHANGAZI: Suzy sijaelewa hao watoto hapo nje wanafanya nini, je ni majirani? SUZAN: Hapana, tunaishi nao humu ndani. SHANGAZI: Mnaishi nao!! Kivipi?? Mara Frank akawa amerudi, basi akasalimiana nao. Ile kukaa tu, shangazi mtu akaendelea na hoja yake. SHANGAZI: Niambie Frank, hao watoto unaishi nao kivipi? FRANK: Hao ni watoto yatima shangazi. SHANGAZI: watoto yatima? Sasa hiki ni kituo cha kulelea watoto yatima? FRANK: Hapana ila nawasaidia tu. SHANGAZI: Kumbe wewe ni mtoa misaada? Mbona kuna ndugu zako wanateketea huko huwasaidii?? FRANK: Jamani shangazi!! SHANGAZI: Siwezi kabisa kukubaliana na jambo hili najua hata kaka hawezi kukubali. Ngoja niondoke zangu. FRANK: Shangazi yani ndio unaondoka? SHANGAZI: Ndio naondoka, unataka nifanye nini hapa? Nitazame ujinga wako huu! Mwasiti inuka twende. MWASITI: Jamani kwaherini. Shangazi yake akamvuta kwa hasira ili waondoke kabisa eneo hilo, nao wakaondoka. Frank nae akainuka na kwenda chumbani, Suzan akamfata nyuma. FRANK: Suzy haya yote umeyataka wewe. SUZAN: Nimeyataka mimi kivipi? FRANK: Wewe ndiye umewaalika hawa watoto hapa nyumbani? SUZAN: Nimewaalika kivipi wakati wewe mwenyewe ulikubali kuwa waishi hapa! FRANK: Nilikubali sababu ulinilazimisha. SUZAN: Ila hakuna haja ya kubishana Frank, cha muhimu ni kujua tunabebaje huu mzigo wetu. FRANK: Ngoja kichwa changu kitulie kwanza maana hata sielewi kitu chochote.
Frank akiwa kazini kwake akatembelewa na Shangazi na baba yake, akajua wazi ni juu ya uwepo wa wale watoto nyumbani kwake.
Frank akiwa kazini kwake akatembelewa na shangazi na baba yake, akajua wazi ni juu ya uwepo wa wale watoto nyumbani kwake tu. BABA: Hivi mwanangu huo upolisi ndio umekufundisha kufuga wezi ndani? FRANK: Baba nitafugaje wezi wakati mimi napingana nao? BABA: Hao watoto wa mitaani ndio wanaoongoza kwa kuibia watu na wewe umeenda kuwaweka ndani kwako unategemea nini wewe? FRANK: Baba unajua wale watoto wanaiba sababu ya maisha magumu lakini sasa sidhani kama wataiba tena. SHANGAZI: Usiwe mjinga wewe, watu husema kuwa mtu haachi asili yake, sasa wale toka utotoni wanaiba sasa waje kuacha leo? FRANK: Basi niacheni nifikirie mliyoniambia. SHANGAZI: Ufikirie nini? Tunachotaka ni uwafukuze pale nyumbani. FRANK: Dah! Kuwafukuza siwezi. BABA: Kwanini huwezi? FRANK: Maana kwa kupitia wale watoto nimeweza kumjua mwanangu. Wote wakashtuka na kumuuliza,”mwanao? Kwani una mtoto wewe?” FRANK: Ndio mwanangu tena mwanangu mzazi. WOTE: Kivipi? Basi Frank akaamua kuwaeleza kila kitu kuhusu Musa na wote wakabaki wanastaajabu. Pia akawaeleza kuhusu Safina na kuwafanya waendelee kushangaa. SHANGAZI: Safina mtoto wa Sam? FRANK: Ndio mtoto wa Sam. SHANGAZI: Aaah maskini, kumbe ameishi maisha ya mtaani wakati baba yake ni tajiri sana na ana mali nyingi. FRANK: Lakini wazazi wake hao wameshakufa. SHANGAZI: Yani Sam na Latifa walikufa!! Maskini mbona Aisha hajaniambia wakati nimekutana nae mara nyingi tu. FRANK: Tena huyo Aisha ndiye aliyemfukuza Safina kwenye nyumba ya wazazi wake. SHANGAZI: Kumbe Aisha ni mtoto mbaya kiasi hicho!! Hafai kabisa katika jamii. Walijikuta wakisikitika sana, nao wakahitaji kuwaona Safina na Musa. Kwahiyo wakaondoka hapo na Frank hadi nyumbani kwake, na Frank akawaita Safina na Musa kuwatambulisha kwao. SHANGAZI: Poleni sana watoto wazuri jamani. MUSA na SAFINA: Asante bibi. SHANGAZI: Si halali kabisa kumnyang’anya mtoto wa marehemu urithi wake, Frank wazijua sheria msaidie Safina kupata kilicho chake. FRANK: Najitahidi kutafuta wakili atakae saidia ila mambo yanabana sana. SHANGAZI: Kila mtu ana haki hata kama ni mtoto. Waliongea mengi na walifurahi sana kumjua mtoto wa Frank na wakapanga kufanya sherehe ya kumkaribisha Musa kwenye ukoo wao kwani walimuona kama vile mwanampotevu.
Baada ya wiki, familia ya Frank wakafanya sherehe ya kumualika Musa kwenye familia hiyo, ilikuwa ni siku ya furaha sana. Frank akaitwa na dada zake, MWASITI: Inabidi uoe sasa kwani ushakuwa mtu mzima kaka. FRANK: Unanishauri nimuoe nani? MWASITI: Nani mwingine zaidi ya Suzy!! ESTA: (Akadakia), kwakweli kwa mimi hapana hata sikushauri umuoe Suzy. FRANK: Kwanini dada yangu? ESTA: Frank, tafuta mwanamke anayekwenda na wakati, unajua Suzy ana mambo ya kishamba sana!! MWASITI: Acha zako Esta, wewe mjanja mbona hujaolewa? Mwache kaka amuoe Suzy. ESTA: Ili azidi kumrundikia mitoto ya kuokoja. MWASITI: Kwanza hiyo mada ya watoto ilishaisha. ESTA: Ila na mimi ni mawazo yangu, sipendi kaka amuoe Suzy. Wakagombana sana ikabidi Frank awaamulie. FRANK: Acheni ujinga jamani, leo ni siku ya furaha. Frank hakufurahishwa kabisa na ule ugomvi kwani yeye ndiye wa kuamua kuwa atamuoa nani.
Frank akatafakari sana na kweli akagundua kuwa umri wake umeenda na anahitajika kuoa kweli. FRANK: Suzy nahitaji tujihalalishe kabisa. SUZAN: Kivipi Frank? FRANK: Nataka tufunge ndoa Suzy. SUZAN: Kweli Frank? FRANK: Ndio hivyo Suzy au wewe unaonaje vipi?? SUZAN: Mi niko tayari Frank. Frank akafurahi sana na kumkumbatia Suzan. Tatizo la watu wengine ni vie kuingilia mambo yasiyo wahusu.
Frank aliamua haswa kufunga ndoa na Suzy na ndicho kitu alichofanya, akaamua kumuoa Suzy ili wawe mke na mume kwa uhalali kabisa. Harudi yao nzuri ilifanya sana, huwa MC hakosei pale anaposema wenye wivu wajinyonge kwani anajua wazi kuwa kuna watu wenye wivu mahali hapo. Baada ya ndoa, shangazi wa Frank akamfata Frank na kuzungumza nae. SHANGAZI: Mwanangu sasa sina ubaya ila nina jambo zuri tu. FRANK: Jambo gani hilo? SHANGAZI: Napenda kuwaona wewe na Suzy mkiwa na furaha, ila watoto wengi namna ile hamuwezi kuwa na furaha nakwambia. FRANK: Sasa shangazi unataka nifanyeje? Lakini kuwafukuza hapana. SHANGAZI: Hapana, sina nia kwamba uwafukuze, ila nakushauri kama unaweza wale watoto wapeleke shule ya bweni ili wawe wanalala huko huko hiyo pia itaimarisha ndoa yako. FRANK: Mmh shangazi!! SHANGAZI: Najua unapata shida kunielewa maana yangu, ila ukifanya hivyo utatambua. Wawe wanakuja kukaa kipindi cha likizo tu, itakusaidia sana Frank. FRANK: Gharama za hizo shule za bweni je? SHANGAZI: Usijari utapata msaada tu, ila fanya hivyo kwanza. FRANK: Sawa shangazi nitafikiria. Frank akafikiria sana kuhusu ushauri aliopewa na shangazi yake, na kujisemea kuwa anatakiwa aufanyie kazi. Akakumbuka matukio ya ugomvi wa wale watoto mule ndani ambapo kuna siku alimkuta mmoja kamshikia kisu mwenzie akimtishia kumuua, akafikiria sana na kuona kwamba itakuwa ngumu kwa yeye kuwalea watoto hao hapo kwake, ni bora wakakae shule ambapo watakuwa karibu sana na walimu katika kuwaangalia na kugundua matatizo madogo madogo waliyonayo na kuyatatua. Akaona wazo la kuwapeleka shule za bweni ni nzuri sana.
Frank akaamua kuwaita watoto wote wa mule ndani na kuwaambia kuwa wanatakiwa kusoma kwa makini sana, kwahiyo ameamua kuwatafutia shule za bweni. Nao wakafurahi sana kwani waliona kubanwa sana wanapokaa mule ndani bila kujua kama shuleni ndio kubanwa zaidi. Akawapeleka shule tofauti tofauti, hakutaka kuwapeleka wote shule moja, alifanya hivyo ili na wao wapate uelewa unaotakiwa. Kwahiyo wote wakapelekwa shule za bweni kasoro Safina na Musa.
Modesta alikuwa ni mtu mwenye mawazo sana na alijiuliza mambo mengi baada ya kugundua ukweli halisi, kwani ulimsaidia kuwagundua ndugu zake kuwa ni watu wa aina gani, jinsi walivyo na roho za kinyama. “kwakweli hawa wanaweza kuniua hata mimi jamani, roho zao si za binadamu wa kawaida.” alijisikia vibaya sana moyoni, akamkumbuka sana marehemu baba yao na jinsi alivyokuwa anaongea kuwa watoto wake hao ni watu wakatili, kwasasa ndio Modesta ameelewa kuwa ukatili wa ndugu zake hao uko wapi.
Suzan akapata ujauzito na kufanikiwa kujifungua watoto wawili mapacha waliowaita Jeni na Jerry. Walifurahi sana kuwapata watoto hao, ilikuwa ni furaha kubwa kwenye familia. Safina alitamani sana kwenda kumtembelea madam Lucy ila alimngoja mamake mdogo ili waende wote kumtembelea. SAFINA: Mama, naona Jeni na Jerry wamekua sasa. Kwanini tusiende kumtembelea madam Lucy? SUZAN: Unahitaji kumuona? SAFINA: Ndio, nahitaji kuongea nae. SUZAN: Basi sawa tutaenda kesho kutwa. Siku ilipofika Suzan na Safina wakajiandaa na kwenda kumuona madam Lucy, na walipofika kule wakakutana na kitu ambacho hawakukifikiria kabisa.
Siku ilipofika Suzan na Safina wakajiandaa na kwenda kumtembelea madam Lucy. Na walipofika kule wakakutana na kitu ambacho hawakukitarajia kabisa kwani waliona kama vile kutakuwa na ugeni mwingine kwenye nyumba hiyo, Lucy aliwakaribisha kwa furaha sana. Baada ya salamu akawakaribisha vizuri sana. LUCY: Karibuni sana jamani, kwakweli leo nimekuwa mtu mwenye bahati sana. SAFINA: Bahati ya nini madam?? LUCY: Yani nyie mmekuja kunitembelea na wale wanafunzi wangu nao wamekuja kunisalimia na kuniaga. SAFINA: Wanataka kurudi ulaya? Kwani washajua kiswahili? LUCY: Wanataka kurudi ulaya ndio, yani wamejua kiswahili kabisa. SUZAN: Kumbe wewe ni mwalimu bora sana, hadi watu wanaelewa duh!! Wote wakacheka na kufurahi, huku madam Lucy akiendelea kuwakaribisha sebleni. Walipofika sebleni, wakakaa kwanza ili kupata utambulisho vizuri. LUCY: Karibu sana jamani, ngoja niwatambulishe kwa wageni wangu. SUZAN: Itakuwa vizuri sana. LUCY: Jamani hawa ndio wale waliokuwa wakijifunza lugha kiswahili kwangu, hapa kuna Joseph, Chuck na Blenda. Safina akawa anawaangalia kwa makini huku akitafakari anayoyaona kwani hakuamini amini. LUCY: Jamani na huyu anaitwa Safina ni…… Kabla hajamaliza Blenda alipatwa na mshangao kwani muda wote alikuwa kamkazia macho Safina na kujiuliza ni yeye au sio yeye. BLENDA: Safina? LUCY: Yes, Safina. Mbona unashangaa Blenda?? BLENDA: Safina Samwel? Blenda aliuliza kwa mshangao, hadi Safina akashtuka na kutambua kuwa kweli anamuona ni Blenda na amemkumbuka vilivyo kwani ndio jina ambalo huwa anatumia, jina la Safina Samwel. SAFINA: Ndio mimi ni Safina Samweli, nilikutana nawe Germany na USA. BLENDA: Yes, i know you. Wakakumbatiana kwa furaha, ndipo Blenda akawaambia Joseph na Chuck kuhusu Safina. Na wote wakajikuta kumkumbuka na kumkumbatia kwa furaha. Wakajikuta wakijadili mambo mengi na kumuuliza maswali mengi kuwa kwanini hakutokea kwenye lile tamasha kubwa. CHUCK: Nilikutafuta sana Safina ili nikuombe msamaha kwani ni mimi niliyecrush gari yenu ukiwa wewe na mama yako pale supermarket. SAFINA: Usijari Chuck yashapita hayo. JOSEPH: Tulikungoja sana Safina kwenye ile tamasha but hukuja. BLENDA: Kweli Safina tulikungoja sana, whats happen to you?? Safina akajaribu kuwaelewa kwa muhtasari kilichomfanya ashindwe kurudi tena Marekani na kushindwa kuhudhuria lile tamasha. BLENDA: Pole sana Safina. SAFINA: Namuhitaji prof. Mike ndio msaada wangu kwa sasa. BLENDA: Safina, we promise you. Tutafanya the best as we can hadi tumpate prof. Mike. Wakamuahidi Safina kwa kila hali kuwa watamsaka Mike hadi wampate ili wamweleze kama Safina mwenyewe alivyowaambia. Walifurahi sana kuongea na Safina siku hiyo, ikabidi na waagane mahali hapo kwani wakina Blenda walishajiandaa kwaajili ya Safari kwa kesho yake. Wakampa matumaini makubwa sana ya kuonana na prof. Mike na wote wakawa wenye furaha. Ilikuwa ni siku njema sana kwao kwani hata uwanja wa mazungumzo waliutawala wao wengine walibakia kucheka pa kuchekesha na kuhudhunika pa kuhudhunika.
Waliporudi nyumbani, Safina alikuwa na furaha sana, tena sana. SAFINA: Mamdogo, unajua mimi kukutana na wale watu kunanipa matumaini makubwa ya kukutana na anko Mike. SUZAN: Kwani wanajuana nae? BLENDA: Anko Mike anajulikana sana kwahiyo ni rahisi wao kumjua. SUZAN: Inamaana huyo Mike ni mtu tajiri sana? SAFINA: Ana uwezo ndio tena ni mwanasheria anayetambulika na wengi. SUZAN: Utafurahi kuonana nae eeh!! SAFINA: Nitafurahi sana kwani nitapata mwangaza mpya wa kushughulika na hawa ndugu zangu walionitesa. Nawachukia sana. Waliongea mambo mengi sana. Kipindi chote ambacho Safina ameanza kukaa hapo, muda mwingi Frank alikuwa akitumia kujua ukweli wa mali zote za Safina, ila kwa mali alizozijua alikutwa zimeshauzwa. Yeye alijua nyumba na maduka makubwa mawili aliyoacha Sam ila vyote vina wamiliki wapya. Aliporudi alimuita Suzan chumbani na kuzungumza nae. FRANK: Suzy, unajua kitendo cha kvotambua mali alizoacha marehemu kinatupa shida kujua urithi halali wa Safina. SUZAN: Naelewa Frank, kazi ni ngumu sana. Sijui itakuwaje? FRANK: Unajua Safina aliachwa akiwa mdogo sana. Na sasa miaka kama nane imepita bila ya kushughulika na chochote. SUZAN: Naelewa hilo swala ila haki ya mtu ni yake tu. FRANK: Halafu wale ndugu zake wameuza kila kitu jamani. SUZAN: Hivi wamewezaje kuuza kila kitu? Walikuwa na hatimiliki kweli? FRANK: Sidhani, kwanza Sam alikuwa ni mtu msomi bhana halafu tajiri. Inawezekana alikuwa na mwanasheria wake wa kujitegemea. SUZAN: Inawezekana, tatizo Safina hamjui yoyote hapa nchini zaidi ya huyo mzungu walieishi nae Marekani. FRANK: Ni haki yake kutokumkumbuka wa huku, alienda Marekani akiwa mdogo sana ndiomana anamjua huyo huyo. Wakamuita Safina na kumuuliza tena, nae akawatajia huyo huyo Mike anayeishi Marekani ikabidi wakubali tu kumngoja huyo Mike kwani Safina aliwahakikishia kuwa huyo Mike akipata habari zake lazima atafika tu.
Siku moja Safina na Musa wakaenda kuwatembelea wenzao kwenye hizo shule za bweni, siku hiyo wakaifanya maalum kwa matembezi hayo tu. Na kila walipowatembelea hao wenzao walionyesha kumshukuru sana Frank kwa wema aliowafanyia. TIZO: Sikutegemea kabisa kama nitasoma mwenzenu, hii imekuwa furaha kwangu, ingawa wenzangu wananiona kuwa nimekuwa mtu mzima ila nitasoma tu niweze kupata mwangaza wa maisha. MUSA: Ni kweli Tizo, madarasani wanatuona kuwa tumewazidi umri ila tusikate tamaa, tusome tu ili tuweze kutoa ujinga. MIRIUM: Kwakweli kamanda Frank ametufuta machozi na ujinga. TIZO: Uzuri ni kuwa katuahidi kila mmoja kumsomesha fani aipendayo, ni furaha sana kumfahamu mtu huyu. Wote walifurahia na kumsifia kamanda Frank. Musa na Safina wakarudi nyumbani, wakamsikia Frank akizungumza na Suzan. FRANK: Unajua inaniuma sana kuona tunashindwa kumsaidia Safina kwenye mali zake. SUZAN: Tatizo ni kuwa tutampataje huyo Mike!! FRANK: Hapo pa kumpataje ndio mtihani. Mara Safina akaingilia mazungumzo yao, SAFINA: Mmenisaidia sana jamani hata Mungu mwenyewe anaona, iliyobaki ni kumwachia yeye kwani ndiye mtatuzi wa matatizo yetu. SUZAN: Inaonyesha umekata tamaa mwanangu. SAFINA: Pengine lakini najua ipo siku moja Mungu atamshuhudia anko Mike hata kwa ndoto ila sijui ni lini, ninachojua atakuja tu. SUZAN: Ila usikate tamaa mwanangu. SAFINA: Naelewa mama, ila niliwapenda sana wazazi wangu kupita chochote ulimwenguni, ni bora wangechukua mali zote na kuniachia wazazi wangu. SUZAN: Usijari, Mungu atakulipia. SAFINA: Natambua hilo, kama ni ni huyu Mungu ninayemuomba kila siku ndiye muumba vyote basi haki itapatikana. FRANK: Pole sana ila yote yataisha. SAFINA: Chozi langu mimi Safina najua limefika kwa Mungu naye atawahukumu hawa ndugu zangu. Kwakweli Safina alikuwa akiwasikitisha na maneno amcyo aliongea, walimuhurumia sana.
Modesta akaona afanye uwezekano wa kukutana na Suzan ili aweze kumuona Safina. Ilimbidi aende kwenye hospital ambayo Suzan alimuelekeza, kufika pale hospital hakumkuta Suzan, akaelekezwa na kwenda kuzungumza na rafiki wa Suzan ambaye ni Pendo, naye akamwambia siku ya kwenda ili ampeleke anapoishi Suzan. Siku ilipofika Modesta alifika kwa Pendo na kumkuta Pendo ameshajiandaa kwahiyo wakafanya safari ya kwenda kwa kamanda Frank. Walipofika wakamkuta Suzan na kufurahiana sana, naye akawakaribisha ndani, ile Safina kumuona Modesta tu akakimbilia chumbani na wote wakamshangaa, kwakweli Safina hakuwataka kabisa ndugu wa baba yake. Suzan akaongea nao mambo mengi, Modesta akamuomba Suzan akamuitie Safina japo amsalimie kidogo tu. Ikabidi Suzan aende chumbani aliko Safina ili kumshawishi akamuone shangazi yake. SAFINA: Siwataki siwataki kabisa ndugu wa baba. SUZAN: Safina usifanye hivyo jamani, Modesta hana nia mbaya. SAFINA: Siwataki kabisa ndugu wa baba, wote ni sawa. Sitaki kuwaona. Suzan akajitahidi sana kumshawishi ila Safina akagoma kabisa. Ikabidi Suzan arudi tu sebleni na kumueleza Modesta. SUZAN: Amekataa kabisa Mode. MODESTA: Usijari Suzy, ipo siku ataelewa kuwa sina nia mbaya. Kwakweli Modesta aliumia sana kwa kupata hukumu ya vitendo vya nduguze ila akajisemea hatokata tamaa. Akamuaga Suzan na kuondoka na Pendo waliyeenda naye.
Blenda na wenzie walipofika Marekani ikabidi wafanye kile walichomuahidi Safina. Ikabidi Blenda aende kumuulizia Mike, akaelekezwa nyumbani kwa Mike. Kwahiyo akaamua kwenda, ila alipofika akaambiwa kuwa Mike hayupo pale na sehemu ambayo ametajiwa kuwa yupo ilimsikitisha sana.
Ikambidi Blenda aende kumuulizia Mike, akaelekezwa nyumbani kwa Mike na kuamua kwenda huko. Ila alipofika nyumbani kwa Mike akaambiwa kuwa hayupo pale, mahali alipotajiwa kuwa yupo palimsikitisha sana. Kwani aliambiwa kuwa Mike amelazwa kwa muda mrefu sana. Blenda akawaambia mwenzake habari hiyo. Basi wakaenda huko kwenye hiyo hospitali waliyoelekezwa. Kwakweli hali ya prof. Mike haikuwa nzuri hata kidogo kwani alikuwa amepalalaizi. Wakamweleza kila kitu lakini kwa hali ile hakuwa na uwezo wa kufanya kitu chochote zaidi ya kufanyiwa, kwahiyo kukawa hakuna kitu chochote cha kumsaidia Safina kwani prof. Mike mwenyewe alikuwa hajitambui.
Safina alikuwa ni mtu wa kusikitika sana kwa kipindi hicho kwani ni muda mrefu ukawa umepita bila kupata taarifa yoyote kuhusu prof. Mike. SAFINA: Ni mwaka sasa tangu wakina Blenda waondoke lakini sijapata taarifa yoyote. MUSA: Usijali Safina kwani mvumilivu hula mbivu. SAFINA: Nakubaliana na wewe Musa ila siwezi kusahau mambo yote waliyonitendea ndugu zangu. Yaani wamenifanya nijute kuwa na ndugu kama wale. MUSA: Yote ni mipango ya Mungu Safina. SAFINA: Ndio nakubali kuwa yote ni mipango ya Mungu, lakini kwanini mimi? Kwanini Safina? Inamaanisha watu wote duniani hawajaonekana ila Safina pekee ndiye aliyeonekana kuwa anastahili kupata adhabu hii, maana hii ni adhabu kwenye maisha yangu. Kwakweli Safina alikuwa anaona kuwa ni mtu anayeonewa sana kwenye maisha yake. Tangu wazazi wake wafariki anaona kuwa maisha yake hayana muelekeo mzuri. Ingawa anaishi na Frank lakini moyo wake unaumia sana hasa akikumbuka alivyofukuzwa na ndugu zake. Safina akabaki akimuomba Mungu tu ili amsaidie katika maisha yake. “Nakuomba Mungu wangu unisaidie kwani wewe ndiye msaada pekee nilio nao. Ulikuwa nami toka hapo mwanzoni hadi leo hii naamini uko nami maana hamtupi mja wako. Endelea kuwapa moyo bamdogo Frank na mamdogo Suzy wa kuendelea kunilea mimi kwani mimi ni mzigo wao sasa. Pia nakuomba umwezeshe anko Mike popote pale alipo asikie kilio na sauti yangu, kama ni mgonjwa basi malaika wako wakashughulike naye ili apone. Wewe ndiye msaada wangu na kimbilio langu, nionyeshe mlango wa kutoke. Amen!!” Alimaliza kuomba na kumshukuru Mungu, kumbe alipomaliza kuomba tu ndio wakati huo huo prof. Mike alipata uwezo wa kuamka kitandani, watu wote walimshangaa kwani ilikuwa ni kitu cha ajabu sana, walishapoteza matumaini ila ni kweli Mike aliamka siku hiyo na kuweza kuinuka. Kweli ulikuwa muujiza, hapo inaonyesha jinsi gani imani hufanya kazi.
Prof. Mike akafanya mazoezi ya hapa na pale na baada ya siku kadhaa akaweza kuwa mzima kabisa. Akapata ruhusa na kurudi nyumbani kwake. Blenda akaamua kwenda tena hospitali lakini akaambiwa kuwa prof. Mike ameshatoka na alikuwa mzima wa afya njema. Kwakweli alifurahi sana kusikia hivyo, ikabidi afunge safari na kwenda nyumbani kwa prof. Mike ili amweleze kikamilifu kuhusu Safina. Alipofika akamkuta prof. Mike, kwakweli Blenda alifurahi sana, ikabidi aanze kujitambulisha kwake na kumueleza kila kitu kuhusu Safina. Mike alishangaa sana kusikia yote hayo, akamwambia Blenda kuwa itabidi aende nae ili kumsaidia Safina.
Safina aliendelea kumuomba Mungu bila kuchoka. Na alikuwa akiwashukuru sana wanaomlea. SAFINA: Mamdogo, naona faraja sana kuwa na ninyi hapa. SUZAN: Usijari ni jukumu letu kukulea. SAFINA: Maisha ya mtaani ni magumu tena magumu sana, uyasikie tu kwa watu kwani kule mvua yetu, jua letu, pa kulala shida, pa kupumzika hakuna na chakula vilevile kukipata ni bahati nasibu. SUZAN: Acha kufikiria sana ulikopitia iliyobaki ni kusonga mbele. Suzan alipenda sana kumfariji Safina ili asijione kuwa mpweke. Musa nae alikuwa akimsifia Suzan mara nyingi anapoongea na Safina. MUSA: Tangu mama yangu alipokufa sikudhani kama nitakuja tena kupata mapenzi ya mama. Lakini huyu amekuwa kama mama yangu mzazi yani ananipenda, ananilea na ananitunza. SAFINA: unajua mamdogo Suzy ana moyo wa kipekee sana. MUSA: Kweli kabisa, nimekuwa nikiteseka mitaani zaidi ya miaka kumi. SAFINA: Kwani mama yako alikuacha na umri gani? MUSA: Miaka mitano, toka nikiwa na umri huo nimeweza kujua maisha ni kitu gani. SAFINA: Pole sana Musa, mie miaka michache niliyokaa mtaani nimeweza kuuona ugumu wa maisha. Je wewe uliyekaa zaidi ya miaka kumi!! Dah. MUSA: Machozi na maombolezo yangu na mambo yote mabaya niliyoyapitia sasa yamefutwa na furaha na amani niliyoipata hapa nyumbani. SAFINA: Kwakweli tumshukuru Mungu kwa kutuondoa kwenye lile jana. MUSA: Nitamshukuru Mungu milile kwani nilijua yale ndio maisha yangu daima. Kwakweli Musa alikuwa na furaha sana kwa upendo alioupata toka kwa Suzan. Suzan alikuwa ni mwanamke mfano wa kuigwa kwani alijua kuwa wale watoto wanahitaji faraja ndiomana akazidi kuwapenda sana na sana. Kwakweli mateso na vilio vya watoto wale vilizimwa na furaha aliyonayo.
Modesta hakuridhishwa kabisa kwa kitendo cha kuchukiwa na Safina, ikabidi afunge safari tena na kwenda kuwasalimia. Siku hiyo alifunguliwa na Safina mwenyewe, Safina alipomfungulia Modesta mlango tu, Safina akageuka na kutaka kukimbilia chumbani ila Modesta akawahi kumshika mkono Safina. MODESTA: Tafadhari Safina usinifanyie hivyo. SAFINA: Sioni sababu ya kuongea na wewe. MODESTA: Safina, niangalie Tafadhari. SAFINA: Ili iweje? MODESTA: Wee niangalie tu. SAFINA: (Akageuka na kumtazama), haya nishakuangalia. MODESTA: Je! Kuna lolote baya ambalo mimi nimewahi kukutenda? SAFINA: Hapana, ila ndugu zako wamenitenda vibaya. MODESTA: Je! Ni halali kumuhukumu mtu kwa kosa la ndugu zake? SAFINA: Si halali ila inategemea. MODESTA: Safina, hakuna baya nililowahi kukutendea. Na si haki kunihukumu kwa kosa la ndugu zangu, nitazame mimi kama Modesta na si mtu mwingine kama unavyofikiria. Sina ubaya wowote na wewe Safina, tafadhari usinihukumu kwa kosa nisilotenda. Safina akafikiria sana maneno aliyoambiwa na Modesta kwani yalimwingia vilivyo kwenye akili yake. Ikabidi amkumbatie kwa kumuonyesha kuwa hana kinyongo nae tena. Na hapo akamkaribisha ndani vizuri na mazungumzo ya hapa na pale yakaendelea. SAFINA: Ni hasira tu ndio zinafanya niwe vile. MODESTA: Naelewa Safina, ila yote yataisha. SAFINA: Yataishaje? MODESTA: Cha muhimu hapa ifunguliwe kesi tu hata mimi nitakuwa shahidi. SAFINA: Kesi hiyo itahusu nini sasa? MODESTA: Ihusu kukunyang’anya mali na kukufukuza kwenu. Safina aliongea mengi sana na Modesta, kwakweli Modesta alipata faraja ya kusamehewa na Safina.
Blenda na prof. Mike wakapanga safari ya kuja nchini. Siku ya safari wakiwa uwanja wa ndege, wakashangaa kuwakuta watu wawili nao wakiwa pale kuwangoja.
Blenda na Prof. Mike wakapanga safari ya kuja nchini. Siku ya safari wakiwa uwanja wa ndege wakashangaa kuwaona watu wawili pale wakiwangoja. Wakawashangaa sana kwani hawakupanga nao safari, watu hao ni Joseph na Chuck. Watu hawa wakawaambia kuwa wameona vyema kuambatana nao, kwani bado wanahitaji kuwa nchini na pia wanahitaji kumuona tena Safina. Wazo kubwa la prof. Mike ni kumuona Safina tu, mtoto wa rafiki yake kipenzi mr. Sam. Kwanza hakuamini kabisa alichoambiwa na Blenda, alichotaka Mike ni kuyasikia kwa Safina mwenyewe. Muda ulipofika wakaingia kwenye ndege tayari kwa safari ya kwenda kumuona Safina.
Ilikuwa siku ya Jumatatu ambapo Suzan aliwashangaa Musa na Safina kutokwenda shule. SUZAN: Mbona leo hamjaenda shule? MUSA: Tumefunga shule. SUZAN: Kumbe mmefunga! Nilikuwa sijui. SAFINA: Mmh! Mamdogo umesahau kuwa huu ni mwezi wa sita!! SUZAN: Mwenzenu nimesoma kipindi cha mkoloni halali yangu kusahau, kipindi kile cha muwa uliozamisha meli. Akawafanya Safina na Musa wacheke. SAFINA: Mamdogo nawe una vituko. SUZAN: Naomba niwatume basi. MUSA: Tutume tu mama. SUZAN: Naomba mniendee kwa Pendo kuna makaratasi atawapa mniletee. MUSA: Sawa hakuna tatizo. Basi Musa na Safina wakajiandaa na kwenda nyumbani kwa Pendo.
Frank akiwa kwenye ofisi yake akashangaa kufikiwa na ugeni, nao wakajitambulisha kwake. Ikabidi Frank aanze nao safari ya kuwapeleka nyumbani kwake. Kitendo cha Safina kuwaelekeza wakina Blenda ofisi ya kamanda Frank ndio kilichowasaidia kwenda moja kwa moja na kumpata mahali hapo. Walipofika nyumbani kwa Frank, Suzan aliona sura moja ya tofauti nayo ilikuwa ya prof. Mike kwani Blend, Chuck na Joseph alishawaona kwa madam Lucy. Akawakaribisha sana nyumbani hapo. Wakaongea mengi ila walisononeka baada ya kuambiwa kuwa Safina hayupo, ila wakapewa uhakika wa kurudi muda sio mrefu. Frank akamuuliza Mike maswali ya hapa na pale na kupata mwangaza wa haki ya Safina kwani prof. Mike alimuelezea kuwa Sam alikuwa na wakili wake hapo nchini, wakaongea mengi na kushauriana mambo mengi. Wakina Blenda wakaamua kuaga ili waweze kwenda kumtembelea madam Lucy, kwahiyo wakaondoka na kumuacha Mike mahali hapo.
SAFINA: Mamdogo Pendo sisi tunakwenda. PENDO: Loh jamani nishawazoea, kaeni basi kidogo hadi jioni. MUSA: Tulimuaga mama kuwa hatuta chelewa sana. PENDO: Basi sawa, mwambieni nitakuja kesho kutwa. Safina na Musa wakaanza safari ya kurudi, walipofika njiani wakakutana na mtoto wa jirani yao. MTOTO: Kaka Musa, nyumbani kwenu kuna mzungu kaja. SAFINA: Mzungu? MTOTO: Ndio mzungu nimemuona yupo nyumbani kwenu. SAFINA: Mmh!! Atakuwa nani jamani? MUSA: Twende tukajionee hukohuko Safina. Basi Safina na Musa wakaanza kutembea haraka ili wakamshuhudie huyo mzungu. Walipoingia ndani Safina hakuamini macho yake kwa alichokiona. SAFINA: Uncle Mike!! Basi Mike akainuka na kumkumbatia Safina kwa furaha. MIKE: How are you Safina? SAFINA: I am fine, and how are you doing? MIKE: Fine and very happy to see you again. SAFINA: I’m very happy too my uncle. Basi Mike na Safina wakaongea mengi. Safina akamueleza kila kitu kilichotokea tangu siku ambayo yeye na mama yake walipoingia hapo nchini, akamueleza na misukosuko yote aliyopitia, kwakweli Mike alimuonea huruma na kumsikitikia sana Safina. Wakapanga mikakati ya kuweza kumpata wakili wa Sam ili waweze kufungua kesi ya dhuluma na kudai haki vizuri. Prof. Mike akawapatia jina la wakili huyo ili waweze kwenda kumuulizia kwenye ofisi za mawakili.
Pendo kama alivyowaambia wakina Musa, na siku hiyo akaenda kumtembelea Suzan. Kufika wakaongea mengi na Suzan akamweleza Pendo kila kitu kilichojiri kuhusu Safina. PENDO: Umesema wakili mnayemtafuta anaitwa nani? SUZAN: Prof. Mwambe. PENDO: Kama ndio huyo basi mimi napajua hadi kwake. SUZAN: Basi itakuwa vizuri kutupeleka. Suzan akampa habari hiyo Frank na akafurahi sana. Kesho yake wakafunga safari hadi nyumbani kwa prof. Mwambe. Wakamkuta nae ndio siku hiyo amerudi nchini kwani alikuwa nchi jirani. Kwakweli Mwambe alishangaa kuuona ugeni huo wa gafla. Baada ya salamu wakamueleza kilichowapeleka pale. MWAMBE: Kumbe mr. Sam alikufa? SUZAN: Ndio tena kifo cha gafla sana. MWAMBE: Maskini Sam!! Mawazo yangu nilijua bado yupo marekani jamani dah!! FRANK: Na tangia yeye na mkewe waiage dunia huu ni mwaka wa nane sasa. MWAMBE: Ooh!! Jamani, kumbe ni muda mrefu sana. Mr. Sam alikuwa rafiki yangu mkubwa sana hata kwenye harusi yake mimi nilikuwa bestman wake. Ningejua yote haya kabla wala binti yake asingeteseka kwani Sam alikuwa na mali nyingi sana, waliozichukia itakuwa wamefojisha tu. Basi Mwambe akaanza kuwaelezea kuhusu mali za Sam hapo nchini hadi wakabaki wanashangaa tu, wakakubaliana kuwa lazima ifunguliwe kesi ili waliomfanya Safina ateseke nao wapate fundisho.
Juta ambaye ndiye kaka mkubwa wa Sam, akapokea barua kuwa wanahitajika mahakamani. Ikabidi amuite Aisha na Jese azungumze nao. JUTA: Nashindwa kuelewa kabisa, eti twende mahakamani. AISHA: Kufanya nini tena kaka? JUTA: Eti kuhusu mali za Sam. AISHA: Mali za Sam? Mali gani wakati Sam alikufa kitambo! JUTA: Wanadai eti Safina ndiye aliyekuwa mrithi halali wa mali hizo. JESE: Jamani kaka si mlisema kuwa Safina alikufa? JUTA: Ndio, hata mi nashangaa hapa. AISHA: Kaka lazima kuna uzembe umefanyika mahali. JESE: Kama swala la uzembe atakuwa ni Peter tu, nimemuona akiwa pamoja sana na Modesta siku hizi. JUTA: Huu ni ujinga sasa, lazima tufanye kitu mapema kabla mambo hayajaharibika. Mara kuna sauti ikasikika ikicheka nyuma yao.
Wakiwa wanajadili mara ikasikika sauti ikicheka nyuma yao, kila mmoja alishtuka na kuwa na bumbuwazi. Ile sauti ilicheka tena ilicheka sana. Mara ile sauti iliyocheka wakasikia ikisema, “Huu ndio ule wakati nilioungoja kwa hamu” Mara kimya kirefu kikatanda hakuna aliyeweza kuongea hata kidogo, walijikuta wote wakikimbilia ndani. Kwavile hapo ilikuwa ni nje ya nyumba ya Juta kwahiyo wakaingia moja kwa moja ndani ya nyumba kwavile walikuwa nje. Baada ya kimya kifupi wakaanza kuulizana kuhusu ile sauti. JUTA: Hivi ile sauti inaweza kuwa ya nani? AISHA: Mmh!! Ile sauti ni kama ya marehemu wifi Latifa. JESE: Acha zako bhana Aisha, huyo Latifa alishakufa kitambo sasa sauti yake ifanye nini? Mi nahisi ni mtu tu alitaka kututisha. JUTA: Inawezekana, ila je mtu huyo wa kututisha ni nani? AISHA: Basi atakuwa Modesta jamani maana ana akili mbovu sana yule. Wakaamua kuuficha ukweli kwa fikra zao za uongo. Mke wa Juta akawa anawashangaa tu. SARAH: Mbona kama kuna mabishano hapa? AISHA: Wifi, kuna barua hapa inatutaka twende mahakamani, eti kesi ya kuhusu mali za Safina. SARAH: (Akashtuka), Safina? AISHA: Ndio Safina, wewe si ulimfukuza hapa! SARAH: Sikumfukuza wifi, aliondoka mwenyewe. Yule mtoto ana kiburi sana. AISHA: Mmh!! Wifi ulimfukuza wewe. JUTA: Jamani hapa tusirumbane, cha msingi tujue jinsi gani tutakabiliana na kesi hii. Ikabidi wajadiliane kwanza na kuona kwamba kuna ulazima wa kuweka kikao cha familia ili wajadili namna ya kukabiliana na hiyo kesi.
Juta akaamua kuitisha kikao cha familia, na kuwaeleza wote kuhusu hiyo kesi. PETER: Hapo hakuna cha kufanya zaidi ya kwenda mahakamani tu. JESE: Upeo wako wa kufikiri ni mdogo sana Peter. PETER: Nakubali nina upeo mdogo na ndiomana mkakubaliana ninyi watatu kutengeneza hati feki na kuuza mali za marehemu. JUTA: Peter, unaongea vitu gani wewe? Umekuwa kama poyoyo! AISHA: Huyu Peter nae anakuwa mjinga kama Mode tu. MODESTA: Mimi sio mjinga ila nataka nisikie huo ujinga wenu wa leo. JESE: Hii miwatu mbili imevurugwa hii. Juta na Aisha wakawa wanacheka. JUTA: Tuacheni marumbano basi, cha msingi tujue tutafanya nini. JESE: Hivi kwanini Safina hakufa jamani? AISHA: Hata na mimi nashangaa. MODESTA: Kwanini msife nyie watu wazima? Mnataka afe mtoto kwa lipi? Kama kufa kufeni nyie. JUTA: Hata wewe kufa tu, maana maneno yako ni ya kufa kufa. JESE: Tumekaa na watu wasio na akili kabisa hapa, jamani twendeni tukasikilize mashtaka kwanza halafu tuamue cha kufanya. Ila cha muhimu ni kupinga mashtaka yote tutakayoambiwa. MODESTA: Hata kama mkipinga, ukweli utabaki pale pale. Halafu akainuka na kuondoka. JUTA: Huyu Mode hana akili kabisa na hafai kwenye ukoo ndiomana elimu yake ni ziro. PETER: Tafuteni na wakili wa kuwatetea kwanza. AISHA: Kwahiyo wewe unajitenga?? PETER: Hakuna baya nililolitenda. JUTA: Tutaenda huko mahakamani kusikiliza jamani. Kwahiyo wakajipanga kwaajili ya kwenda mahakamani.
Wakaamua kwenda kusikiliza mashtaka kwanza, na huko mahakamani wakamkuta Suzan na Frank. Wakasomewa mashtaka yao na kupinga yote, kwahiyo kesi ikapangwa siku nyingine kwaajili ya ushahidi. Walipotoka, Aisha akamfata Suzan. AISHA: Nilijua tu wewe kidudu mtu ndio umefanya yote haya. SUZAN: Maneno hayasaidii na lazima mtakuwa hatiani tu nyie. Aisha akaondoka na kuwafata ndugu zake ili wapate kujadili. JESE: Jamani hii kesi ni ngumu, wakili peke yake hatoshi lazima tutafute mganga wa kutusaidia. JUTA: Umesema vyema Jese, hilo ndio jambo la kufanya. Kumbe Modesta aliwasikia maneno yao, kwakweli alisikitika sana. AISHA: Jamani ishu ya mganga msiwashirikishe Modesta na Peter, hawa wataharibu tu mipango yetu. Wakakubaliana kwenda kwa mganga kumbe Modesta alishawasikia tayari. Walipoondoka ikabidi Modesta amfate Suzan na kumueleza. SUZAN: Sasa tufanyeje Mode? MODESTA: Cha muhimu ni maombi tu, kwani kwa Mungu hakuna linaloshindikana. Wale ni sawa na mfamaji kwahiyo wanatapatapa. SUZAN: Ila ndugu zako wana mambo sana. MODESTA: Wana mambo balaa ila nitachunguza tu, usiache kuomba juu ya Safina, Suzy. SUZAN: Sawa Mode nimekuelewa. Wazo kubwa la Modesta alitaka kwenda kwa yule binti wa kiarabu, Yusra ili ajue mambo ambayo ndugu zake wameyapanga kwa Safina safari hii.
Siku ya kesi na ushahidi ilikuwa tayari, na prof. Mwambe akaweka tayari kila kitu kwaajili ya kesi hiyo. MWAMBE: Usijari Safina, kesho ndio siku yenyewe. Wewe jielezee tu bila uoga wowote. SAFINA: Sawa nimekuelewa. Basi Mwambe akawaaga na kuondoka. Wakabaki Safina na Musa pale nyumbani. SAFINA: Musa sijui kama nitaweza kujieleza. MUSA: Acha uoga Safina, utaweza tu. Jipe moyo utashinda, kwa Mungu hakuna lisilowezekana. SAFINA: Naelewa Musa ila ndugu zangu ni wabaya sana jamani, yaani kuwaua wazazi wangu sababu ya mali! MUSA: Usiwaze sana Safina, ila ubaya ni kuwa serikali haitambui uchawi. Kama ingetambua, basi hata kesi ya mauaji ingewakabili hao jamaa. Ila cha msingi ni upate haki yako Safina. SAFINA: Ni kweli Musa ila napenda wale ndugu zangu na wao wateseke maisha. MUSA: Hukumu lazima iwakabili nduguzo Safina. Wakiwa wanajadili hayo, mara gafla Safina akaanguka sakafuni huku damu zikimtoka puani. Hofu kubwa ikamtanda Musa na kumpigia simu Suzan. Naye Suzan alihisi kuchanganyikiwa, akampigia simu Modesta. MODESTA: Suzy, nakuja hapo nyumbani sasa hivi. Msimpeleke hospitali. SUZAN: Sawa. Akakata simu haraka na kumpigia Musa.
Musa akiwa kamuweka Safina begani ili ampeleke hospitali, anashangaa akipigiwa simu na Suzy na kukatazwa kufanya hiyo. Ikambidi amlaze kwenye kochi. Suzan aliharakisha na kurudi nyumbani, akamkuta Safina akiwa kwenye hali mbaya sana, hata na yeye wazo la kumpeleka hospitali likamjia. Wakati anataka kufanya hivyo mara Modesta akafika. SUZAN: Mode ona, tutafanyaje sasa? MODESTA: Tulia Suzy, ngoja nifanye nilichoambiwa kwanza. Modesta akachukua kipande cha mkaa na kukisaga halafu ule unga unga akachanganya na chumvi. Akachukua kidogo na kuchanganya na maji, halafu akaanza kumpaka Safina kwenye paji la uso. Na ule ung uliobaki akamnyunyizia puani, mara wakamuona Safina akijigeuza geuza na kupiga chafya mfululizo. Alipiga chafya kwa sana na mara akainuka na kukaa, akiwa haelewi chochote kilichotokea. SAFINA: Kwani kuna nini hapa? MODESTA: Hakuna kitu mama, usijari mwaya. Safina alikuwa anajishangaa tu kwani alipojigusa usoni alijiona ana vitu vyeusi vyeusi. SAFINA: Na hii ni nini? Ikabidi Musa amueleze Safina kilichotokea, kwakweli Safina alishangaa sana. Suzan nae alikuwa akishangaa yote. SUZAN: Mode, umejifunza wapi hiyo dawa? MODESTA: Suzy hayo ni mambo ya asili, yule Yusra ndio ameniambia nifanye hivi kwasababu nilienda kumuuliza. SUZAN: Mmh!! Walitaka kumpoteza Safina eeh!! MODESTA: Ndio, ila Mungu mkubwa Suzan. Hawatafanikiwa tena na hila zao mbaya, tena bora mmenisikiliza kutokwenda hospitali kwanza. MUSA: Kwani hospitali ingekuwaje? MODESTA: Mambo kama haya ukipeleka hospitali unammaliza mgonjwa sababu hospitali wangemchoma sindano na hapo ndipo pabaya. MUSA: Haiwezi kujirudia tena. MODESTA: Haiwezekani tena, kwani wenyewe watadhani Safina ameshakufa ila watashangaa kumuona kesho mahakamani. Wakasikitika sana, kwani ndugu hao walikuwa wabaya kwakweli bila hata huruma kabisa, ila siku zote mwisho wa ubaya aibu. Na ndiomana Mungu amewaaibisha.
Juta, Aisha na Jese wakiwa kwa mganga wao, mganga huyu ndio yule yule aliyewasaidia kuwamaliza Sam na Latifa. Walihakikishiwa kuwa kila kitu tayari. Sasa kilichobaki ni kwenda kumzika Safina. Wakiwa wanajiandaa kuondoka mara hali ya hewa ikabadilika kwenye kile kibanda cha mganga, kwani yule mganga alianguka gafla na kuanza kutapatapa huku na kule.
Wakiwa wanajiandaa kuondoka mara hali ya hewa ikabadilika kwenye kile kibanda cha mganga, kwani mganga alianguka gafla na kuanza kutapatapa. Wote watatu wakapatwa na bumbuwazi kwani mganga alikuwa akihangaika kama vile mtu anayekabwa. Gafla akatulia tuli, wakabaki wanaangaliana bila ya kujua cha kufanya. Mganga akiwa katulia pale chini, wakajaribu kumuamsha lakini hakuamka, walipomtazama vizuri wakagundua kuwa ameshakufa. Hofu kubwa ikatanda mioyoni mwao. AISHA: Jamani mbona sielewi kitu!! JUTA: Hata mimi sielewi kitu. JESE: Tutafanyaje sasa? AISHA: Tuite watu waje watusaidie. JESE: Halafu tutawaambia kuwa imekuwaje? Mara gafla mke wa mganga aliyeitwa Rhoda akaingia kwenye kile kibanda, akamuona mumewe kalala chini akiwa hajitambui. Akamkimbilia pale chini na kumtikisa akiwa kimya kabisa, Rhoda akaanza kulia huku akipiga kelele, “mmemfanya nini mume wanguuuuu?” Wakaona hapo itakuwa khatari, ikabidi wakubaliane kukimbia na kumuacha mke wa mganga na mganga akiwa pale chini. Rhoda aliendelea kupiga kelele iliyofanya watu kujaa kwenye kibanda hicho, kila mmoja alibaki kushangaa tu. Rhoda nae aliendelea kupiga kelele kuwa wamemuua mume wake. Watu wakambeba hadi hospitali ambako daktari alithibitisha kuwa yule mganga ameuwawa kwani inaonyesha kuwa kuna mtu amemnyonga. Rhoda akasema, “sikubali lazima watu waliohusika na kifo cha mume wangu washtakiwe”
Juta, Aisha na Jese wakakimbilia moja kwa moja nyumbani kwa Aisha. JUTA: Mbona makubwa haya ya leo jamani!! AISHA: Makubwa tena makubwa haswaaa. JESE: Ila bora kazi ya Safina imeisha. JUTA: Ndio kazi ya Safina imeisha, ila je ni kitu gani kimemuua mganga? AISHA: Mmh!! Jamani labda ni uoga wetu tu. Usikute mganga hajafa, labda alienda kuongea na mizimu yake. JUTA: Inawezekana kweli hajafa, na bora iwe hivyo maana ndiye tegemeo letu yule. JESE: Ila kaka hakuna tatizo ilimradi Safina kafa unadhani kuna mtu atakaefika mahakamani hapo kesho? Ni moja kwa moja tutashinda kesi tu. JUTA: Ila mi nadhani hiyo kesho tutokee hapa hapa kwa Aisha. Sidhani kama ni salama kurudi kwangu. JESE: Kweli kabisa kaka, kwako pale wengi wanapajua. Hapa itakuwa rahisi hata kufanya dawa tulizopewa. AISHA: Ila jamani tuombee mganga asiwe amekufa maana mkewe chizi yule balaa. JESE: Jamani msilete mada za kufa tena, mshasema hajafa sasa hilo la kusema kama amekufa linatoka wapi tena? Halafu hata kama akifa sisi tutahusishwa vipi? JUTA: Hamna bhana Aisha amesemea tu. Ila kama akifa tunaweza kuhusishwa kwavile sisi ndio tulikuwa nae. AISHA: Sawa basi tufanye hajafa na hakuna chochote kilichotokea. Wakawa wanajipa moyo kuwa mganga hajafa. Wakaendelea kufanya dawa zao za kushinda kesi.
Nyumbani kwa Frank wakawa wanajiandaa kwaajili ya kwenda kwenye kesi. SUZAN: Hivi watakuwa na cha kujitetea kweli wale? FRANK: Watajiuma uma tu kama kawaida yao ila hawataweza chochote. SUZAN: Na wewe umejuaje kama watajiumauma? FRANK: Nilipata habari kuwa Aisha ni maneno mengi, ila leo atapatikana. Wakaingia kwenye gari pamoja na Safina na Musa, na safari ya kwenda mahakamani ikaanza. Kufika njiani, gari yao ikagongwa kwa nyuma kitu ambacho kiliwachelewesha kidogo mahakamani kwani walikuwa wakitatua kwanza lile tatizo la gari kugongwa. Walipofika, wakaingia mahakamani, na kukuta watu wote wameshafika. Hakimu alipoingia, ndipo kesi ikaanza kusomwa ikiwa kila upande kuna mashahidi na wakili wa kuwatetea. Wakili wakina Safina alikuwa Bwana Mwambe na wakili wakina Juta alikuwa Bwana Maneno. Kesi zilizowakabili washtakiwa zilikuwa nyingi, kwanza kudhurumu mali ya Yatima, pili kutengeneza hati feki na kuuza mali za marehemu na tatu kumfukuza mtoto wa marehemu na kumfanya ateseke mitaani. Kesi zote ziliwabana sana washtakiwa hata hawakujua ni wapi pa kupumulia.
Baada ya kesi kusomwa, na mawakili kusema yao mbele ya mahakama. Mwendesha mashtaka akawataka mashahidi wa kesi hiyo waweze kueleza. Ndipo Bwana Mwambe alipomwambia Safina apande kizimbani na kujieleza. Kitendo cha Safina kupanda pale kortini, kiliwafanya wakina Juta kukosa amani na kushindwa kuelewa kuwa imekuwaje hadi Safina yupo hai hadi muda huo, hawakumuona kama kafika mahakamani kutokana na kwamba wakina Safina walifika nyuma yao. Safina akaelezea yote yaliyomtokea kwenye maisha yake tangu wazazi wake walipofariki, alielezea kwa uchungu sana, kila aliyekuwepo pale mahakamani alisikitika. Musa nae akaelezea jinsi alivyokuwa akiishi na Safina mitaani. Frank akaelezea hali halisi aliyomkuta nayo Safina. Suzan nae akaeleza mambo yaliyosibu hadi Safina kunyang’anywa mali zake.
Basi na upande wa washtakiwa nao wakaanza kutoa maelezo yao. AISHA: Huyu mtoto ni wa kaka yetu kwahiyo mimi namuona kama mwanangu wa kumzaa, siwezi kumtenda vibaya kwani mimi na Sam ni ndugu tena wa damu. Kaka Juta alimchukua Safina na kumlea kama anavyolea watoto wake lakini Safina alitoroka. MWAMBE: Alitoroka au walimfukuza? Na si akaja kwao na kukukuta wewe na kaka yako halafu ukamfukuza pia! AISHA: Lakini…….. MWAMBE: Lakini nini? Aliwakuta na mkamfukuza siyo? AISHA: Unajua Safina…… MWAMBE: Jibu swali nililokuuliza, mlimfukuza? AISHA: Hatukumfukuza bali aliondoka mwenyewe. MWAMBE: Kwahiyo Safina alijiamulia kwenda kupata shida na kuacha kwao? AISHA: Alikuwa na akili za kitoto enzi hizo. Kama kawaida ya kesi, ikahairishwa hadi kesho.
Kesho yake kesi ikasomwa tena, shtaka ambalo waliamua kupingana nalo vilivyo ni swala la kumfukuza Safina kwani waliona kuwa hilo swala litawatia hatiani zaidi. Bila kutegemea, wakamuona Modesta nae akipanda kizimbani na kutoa ushahidi kuwa ndugu zake walimfukuza Safina. Na katika kulitia nguvu swala hilo, Modesta aliweza kumtafuta mtu aliyekuwa mlinzi wa nyumbani kwa Sam aje kutoa ushahidi kwani ndiye aliyeshuhudia. Mlinzi huyo aliitwa Juma. Naye akapanda kizimbani na kuapa kisha kuelezea ilivyokuwa. “Ilikuwa ni Jumamosi majira ya saa moja jioni, nilisikia mtu akigonga geti, nilipofungua alikuwa ni Safina. Kwakweli nilihudhunika kwa hali aliyokuwa nayo kwani alikuwa amekonda sana na alikuwa mchafu. Nilimkaribisha ndani na kuendelea na shughuli zangu, mara baada ya muda kidogo nikasikia dada Aisha akigomba mara nikamwona kamshika mkono Safina huku akisukumana nae hadi getini, akafungua geti na kumsukumia nje. Nikamsikia akimwambi kuwa “usirudi tena hapa na ukithubutu kukanyaga mguu wako tena mahali hapa nitakuchinja”. Dada Aisha alisimama pale pale getini hadi Safina alipopotelea gizani kabisa ndipo akafunga geti na kuniambia “ole wako umkaribishe tena huyu mtoto ndani, nitakufunza adabu”. Kwakweli niliumia sana moyoni ingawa sikuwa na la kufanya kwa wakati huo.” Kila mmoja pale mahakamani alisikitika sana, jaji akaahirisha kesi hadi mchana wa siku hiyo ili ije kutolewa hukumu kwa wahusika.
Wakiwa nje wanangoja hukumu ya kesi yao. JUTA: Jamani hivi Modesta ana akili kweli? JESE: Yule ni mlemavu wa akili, yani anaangamiza ndugu zake kwaajili ya watu baki dah!! AISHA: Ngoja tushinde halafu tuone atakimbilia wapi. Wakiwa wanazungumza mara wakamuona Rhoda akiwa na maaskari, RHODA: Hawa hapa ndio waliomuua mume wangu.
Wakiwa wanazungumza mara wakamuona Rhoda na maaskari. RHODA: Hawa hapa ndio waliomuua mume wangu. Wale maaskari wakachukua pingu na kuwafunga watuhumiwa walioonyeshwa, kwahiyo Juta, Jese na Aisha wakafungwa pingu. AISHA: Jamani kosa letu ni nini?? ASKARI: Nyie ni wauaji, mmemuua mume wa huyu mama. JESE: Lakini sisi hatumjui huyo mama. Wakaamua kumkana Rhoda pale kwa maaskari. RHODA: Kheee!! Kweli Wauaji ni wauaji tu yani leo hii Jese unanikana mimi!! JESE: Hatukujui bhana, tunakushangaa unamaana gani kusema sisi ni wauaji. RHODA: (Akamgeukia askari) Askari mimi nina mashahidi kabisa kuwa hawa ndio wahusika wa kifo cha mume wangu. Akatokea askari mwingine aliyeitwa Juma na kuwaambia. JUMA: Jamani hao watuhumiwa tayari kwani wana kesi yao inasomwa mchana kama vipi na hiyo ipelekeni kwa hakimu moja kwa moja wahukumiwe tu hawa. JUTA: Haiwezekani jamani, tena haiwezekani kabisa. Mnataka kutubambikizia kesi nyie. Modesta akaona nduguze wakiwa na pingu halafu wamezingirwa na maaskari, ikabidi aende kusikiliza. Akaambiwa kuwa nduguze wanashtakiwa kwa mauaji ya kumuua mganga. MODESTA: Vizuri sana, dhambi uliyofanya huwa haikimbiwi kirahisi hivyo. Mliwaua wale wengine kishirikina sasa imetokea aliyeuwawa kweli, amakweli hukumu ni hapahapa duniani, mbinguni kuhesabiwa tu. JUMA: Waliua kishirikina? MODESTA: Ndio, na bahati yao serikali haiamini uchawi. RHODA: Ila mume wangu hawajamuua kiuchawi, wamemkaba kiuhalisia kabisa hadi kufa. MODESTA: Kwani mume wako ni nani yao? RHODA: Mume wangu ni mganga wa jadi, wamemuua hawa halafu leo wananikana. MODESTA: Oooh!! Nimekuelewa mama, kama ndio hivyo basi watakuwa wamemuua kweli kwani niliwasikia kuwa wanaenda kwa mganga. JESE: Wee Mode wewe, acha maneno yako hayo. Nani wa kwenda kwa mganga kati yetu hapa? Sisi sio watu wa imani za kishirikina. ASKARI: Hapa sio pa marumbano, swala ni kwamba mmeua basi na hukumu lazima ihusike hapa. Juta, Jese na Aisha walikuwa ni watuhumiwa tayari ikawa ni ngumu kwenda kufanya mambo mengine kwani mchana walikuwa wanatakiwa kusomewa mashtaka.
Basi mchana wa siku hiyo ulipofika, watu walijaa mahakamani hapo ili kujua hatma ya kesi hiyo, wengi walimuonea huruma Safina kwa maisha aliyopitia. Wengine waliwaza kuwa endapo wakinaJuta watashindwa kesi itakuwaje kwa mali walizonunua kwao. Kesi nyingine ikatajwa ikiwahusu Juta, Jese na Aisha ilikuwa ni kesi ya mauaji ila wakaikana kesi hiyo. Kesi ya mauaji ikapangwa kusomwa tena kesho wakati ushahidi kamili ukiletwa. Kwa hitimisho la kesi ya Safina, jaji akatoa hukumu ya kesi hiyo. “Kwakweli inasikitisha sana kwa mzazi kutafuta mali kwa shida kwaajili ya mtoto wako halafu mtoto huyo apate shida ambazo hukuzitegemea. Nbmini kuwa hata wazazi wa huyu binti watakuwa wamehudhunishwa sana kwa jambo hili. Watuhumiwa wamedhurumu jasho la mtu tena wamemtenda vibaya yatima wakati wanajua wazi yatima anapaswa kupewa upendo, watuhumiwa ndio walikuwa watu muhimu sana wa kumuendeleza huyu yatima kimaisha lakini kvokana na uroho wa mali wakatamani hata kumuua na hili ni kosa la jinai. Kutokana na hatia mliyokutwa nayo, mahakama hii inawahukumu kifungo cha miaka kumi na tano jela na adhabu kali. Na hili liwe fundisho kwenu na kwa wote wenye tabia kama za kwenu. Na Safina arudishiwe mali zake zote.” Jaji alimaliza na kutoka, ikawa nderemo na furaha huku wakimpongeza Safina kwa ushindi. Wale walionunua mali za marehemu Sam, walisikitika sana kwani wengine waliuziwa bila vibali na wengine kwa hati feki. Na wao wakaamua kufungua madai ya pesa zao kwa watuhumiwa kwani walikuwa wametapeliwa.
Ilikuwa ni furaha kweli kwa Safina na wengine wote walomuhurumia. Na kesho yake wakaamua kwenda tena mahakamani kusikilizia kesi ya mauaji. Kule mahakamani kesi ikasomwa tena, wakaipinga kabisa. Mashahidi wakatoa ushahidi wao kuwa waliwaona nyumbani kwa mganga, ubaya zaidi ni ushahidi alioutoa mtoto wa mganga kwani aliwapiga picha siku hiyo wakati wapo na baba yake. Kwahiyo wakakuta na hatia. Mahakama ikawahukumu kifungo cha maisha, na kuhusu kesi ya madai ya wale walionunua mali za marehemu Sam. Mahakama ikatoa tamko kuwa mali za Juta, Jese na Aisha zinadiwe halafu wanunuzi hao wapewe nusu hasara ili iwe fundisho kwao la kununua vitu bila ya vibali vinavyoeleweka. Kwakweli ilikuwa ni kilio kikubwa kwa Aisha, Juta na Jese. Walipokuwa wanapelekwa gerezani Peter na Modesta wakawafuata. JUTA: Tafadhari Peter nitunzie wanangu. PETER: Usijari kaka nitawatunza. MODESTA: Hata na mimi nitawatunza, sina roho mbaya kama mnavyodhani. Nimeshukuru kuwa mnaenda kuyalipia makosa yenu sasa. Na siku zote mkumbuke kuwa MWISHO WA UBAYA NI AIBU. AISHA: Mode jamani, kweli tumeaibika. Hata hatutazamiki na watu tena. Najutia mimi, najutia yote niliyoyafanya ila yote nilishinikizwa na hawa kaka zangu. JESE: Hakuna cha kushinikizwa hapa, sema tujutie tu kwani aibu na fedheha vimetupata. Sarah na watoto wake wanne aliozaa na Juta, wote walikuwa wakilia na kuomboleza tu. Jese aliwahurumia watoto wake wawili aliokuwa anawalea. JESE: Na mimi nitunzieni wanangu. PETER: Usijari kaka, nitawatunza. Aisha hakuwa na mtoto ila alikuwa mjamzito, muda wote machozi yalimtoka kwani ameshajua kuwa mwanae atamzalia gerezani.
Safina akakabidhiwa mali zake zote, kwakweli ilikuwa ni furaha sana. Na akamteua kamanda Frank na Suzan kuwa wasimamizi wa mali zake. Wakaamua kufanya sherehe kubwa sana ya kumpongeza Safina. Kwakweli Safina aliwashukuru sana, aliwashukuru wote. Akaamua kumkabidhi nyumba moja shangazi yake Modesta ili asihangaike. Maisha yalimuwia vigumu sana Sarah, akaenda kumuomba Safina kwani hakuwa na mahali pa kwenda na watoto wake. SAFINA: Wanao ni ndugu zangu, watakaa na shangazi. Ila wewe tafuta pa kwenda. SARAH: Nihurumie Safina, tafadhari nihurumie. SAFINA: Mbona wewe hukunihurumia? SARAH: Ni shetani tu alinipitia Safina. SAFINA: Ngoja nimuulize shangazi kama atakukubali wewe na roho mbaya yako. Safina akamuuliza Modesta, naye akasema ataishi nae ila Safina akamwambia Sarah kwamba ataishi kwa Modesta kama mfanyakazi wa ndani tu.
Baada ya kukarabati nyumba yao, Safina akamuomba kamanda Frank kuwa wahamie huko na wote wakahamia pale kwenye nyumba ya marehemu Sam, ikawa ni furaha sana. Safina akamwambia kamanda Frank kuwa kiwanja kimoja kitumike kujengwa kituo cha kulelea watoto yatima na watoto wa mitaani, fedha iliyokuwa kwenye account ya baba yake ndio aliona kuwa itafanikisha shughuli hiyo. FRANK: Umeamua vyema Safina. SAFINA: Maisha ya mtaani ni magumu sana bamdogo, kuliko kupata shida ni bora wafurahie maisha kwa pamoja na mahali pazuri. FRANK: Sawa sawa Safina. Ikabidi Frank azianze hizo harakati. Siku Modesta akiwa amelala akatokewa na Latifa ndotoni na kumwambia. “kwaheri Mode, sasa mtu wangu atapumzika kwa amani” Halafu akampungua mkono kama ishara ya kumuaga. Modesta alishtuka na kusema, “Latifa” Modesta alifurahi moyoni kuona sasa ukweli na uongo umejitenga.
Prof. Mike akapanga mipango ya kusafiri na Safina kwenda naye Marekani ili akamkabidhi vitu ambavyo wazazi wake waliviacha huko na kuendelea kuboresha maisha yake. Safina akaacha kila kitu chini ya Frank na Suzan. MUSA: Safina nitakumiss SAFINA: Hata na mimi nitakumiss Musa. MUSA: Ninachoomba usitusahau huko. SAFINA: Usijari kwa hilo Musa, nitawakumbuka siku zote. Tena nikiweza kule nitakualika na wewe uje Musa MUSA: Kweli Safina? Nitafurahi sana na mimi siku nitakayofika huko. SAFINA: Usijari, tuombeane uzima tu. MUSA: Nitakuombea daima. SAFINA: Asante Musa, machozi yetu yote yamekauka sasa. Safina na Musa wakakumbatiana kwa furaha.
Ikafika siku ya safari, Safina na Prof. Mike wakajiandaa. Basi Suzan, Frank, Musa, Modesta na Peter wakawasindikiza hadi uwanja wa ndege. Wakaagana, halafu Safina na prof. Mike wakaenda kupanda ndege. Safina alifurahi sana kwani hakuamini kama maisha yake yanajirudia, ingawa aliwapoteza wazazi wake lakini aliamua kusonga mbele ili wazazi wake waendelee kujivunia kuwa nae hata huko walipo. Safina akajikuta akisema kwa furaha. “I can’t believe that i’m going back to USA”
Ilikuwa Ijumaa ya tarehe kumi mwezi Desemba ambayo hali yake ya hewa ilikuwa tulivu kabisa. Nyakati hizo za asubuhi mambo hayakuwa shwari katika nyumba ya mzee Kibudo ambayo watu kadhaa walikuwapo nje wakilia kwa huzuni juu ya kifo cha mzee huyo aliyeuawa na watu ambao hawakujulikana. Watu hao wa kijiji cha Magugu wilaya ya Babati mkoani Manyara waliungana na familia ya mzee huyo katika tatizo hilo la msiba. Maswali mengi yalikuwapo vichwani mwa watu juu ya mtu aliyefanya mauaji hayo kwa mzee huyo aliyekuwa mkarimu licha ya utajiri wake aliokuwa nao kijijini hapo. Jeshi la polisi lilifanya uchunguzi juu ya kifo cha mzee huyo na mwishoe familia yake ilihurusiwa kufanya mazishi wakati wahusika wa tukio hilo wakiendelea kupelelezwa. Hatimaye mzee Kibudo ambaye ilielezwa kuwa aliuawa kwa mapanga alizikwa, tukio hilo lilishuhudiwa na mkewe na watoto wake watatu pamoja na ndugu na jamaa waliofika msibani hapo. Mara baada ya msiba huo familia ya marehemu Kibondo ilikuwa ikisubiri maelezo yeyote kuhusiana na wauaji wa mzee huyo lakini hakuna taarifa zozote zilizopatikana kutoka jeshi la polisi. James Kibudo ambaye alikuwa mtoto wa mwisho wa marehemu ndiye pekee alifanikiwa kupata nafasi ya kusoma katika shule moja mkoani Arusha. Kaka yake mkubwa alikuwa akiwasaidia wazazi wake kazi za shamba na uchungaji wa ng’ombe vitu vilivyomfanya mzee Kibudo kuwa na uwezo kifedha kijijini hapo. Baada ya msiba huo James aliondoka nyumbani kwao kurudi shuleni mara baada ya kuagana na familia yake akiwamo dada yake aliyetarajiwa kuolewa. Kichwani alikuwa na mawazo juu ya mtu aliyehusika na mauaji ya baba yake jambo lililomkosesha raha mara kadhaa. Alitamani jeshi la polisi lifanikishe kukamatwa kwa watu hao na sheria kali juu yao ichukuliwe. Katika nyakati tofauti aliwasiliana na familia yake kwa njia ya simu akiulizia jitihada zilizofanywa na jeshi la polisi lakini jibu lilibaki kuwa watuhumiwa wa mauaji hayo hawakupatikana. Mwezi mmoja baadaye James akiwa amebakiwa na siku chache ili shule yao ifunge kwa ajili ya likizo fupi, alishtushwa na ujio wa mjomba yake shuleni kwao. Jambo lililompa hofu ni hali ya wazi aliyoionyesha iliyompa hisia za tatizo nyumbani kwao. Mjomba yake huyo hakumweleza kitu zaidi ya kumwambia kuwa ajiandae kwa ajili ya safari kuelekea kwao, baada ya kubisha kwa muda mfupi akitaka kujua sababu ya kufanya hivyo alikubali na kujiandaa. Safari ilianza kuelekea kwao, muda wote wa safari James alikuwa na mawazo akiwa haelewi jambo lililokuwa limetokea hali iliyopelekea aanze tena kumuuliza mjomba yake huyo. Baada ya kuona usumbufu ulizidi alimjibu kwa ufupi kuwa kulikuwa na matatizo nyumbani kwao hivyo uwepo wake ulihitajika. Baada ya safari hiyo ya masaa kadhaa walifika kijijini kwao Magugu, walianza kutembea taratibu kuelekea nyumbani kwao muda wote alikuwa na hofu akiwa haelewi kilichokuwa kinaendelea. Hofu hiyo ilimzidi na kujikuta akianza kulia baada ya kuona kundi la watu wakiwa wamezunguka eneo la nyumba yao na kelele za vilio zikiendelea.Alijitahitidi kutembea lakini miguu yake ilimwishia nguvu na hatimaye alianguka chini kabla ya kusaidiwa na watu waliokuwapo eneo hilo la msiba. Alipelekwa mpaka ndani na kuwakuta ndugu zake kadhaa waliomtaka atulie na kujipa ujasiri kama mwanamme. Walianza kwa kumweleza kuwa familia yake yote ilikuwa imeuawa usiku wa siku hiyo. Jambo hilo lilimfanya James kulia kwa uchungu baada ya kuelewa yeye pekee ndiye alikuwa amebakia katika familia hiyo zaidi hakuelewa chanzo cha mauaji hayo yaliyofanywa. Kama kawaida polisi walifanya uchunguzi wao juu ya tukio hilo na kuondoka na vielelezo wakiahidi kufanya upelelezi zaidi. Hatimaye miili ya wanafamilia hao waliouawa kwa kukatwa na mapanga ilizikwa kijijini hapo. James alijawa na mawazo juu ya muuaji wa familia hiyo na wazo la kuhakikisha muuaji anapatikana linamkaa zaidi kichwani mwake. Akili yake ilikuwa tayari kuua katika kulipiza kisasi kwa mtu yeyote ambaye angethibitika kuhusika na mauaji hayo. Wakati huo alikuwa kidato cha nne akiwa amebakiwa na miezi kadhaa ya kumaliza shule, baada ya likizo aliondoka akirudi shule akitarajia kupata taarifa za wauaji kutoka jeshi la polisi. Mali za familia hiyo ya marehemu Kibudo zilianza kusimamiwa na mdogo wake ambaye hakubahatika kuwa na mtoto katika maisha yake. Zaidi alikuwa ni mtu mlevi ambaye pia hakuwahi kuoa. Alichaguliwa kusimamia mali hizo wakati James akisubiriwa amalize shule ili akabidhiwe, hiyo yote ilitokana na hofu waliyokuwa nayo ndugu wa familia hiyo ya kuuawa iwapo wangesimamia mali hizo. Ndugu wengi waliogopa hata kulala katika nyumba hiyo ya marehemu mzee Kibudo wakihofia kuuawa. George Kibudo alisimamia mali hizo katika misingi mibovu kutokana na tabia yake ya ulevi aliyokuwa nayo. Baada ya miezi mitatu James alirudi kijijini hapo na kuungana na baba yake mdogo huyo kusimamia mali hizo akiwa ameshamaliza kidato cha nne. Tatizo lililomsumbua kichwani mwake lilihusiana na kutokamatwa kwa mtu aliyehusika na mauaji ya familia yake. Pia aliingiwa na hofu juu ya sababu ya mauaji hayo, lakini jambo lililokuwa kichwani mwake siku zote aliamini baba yake hakuwa na kosa lolote alilomfanyia mtu. Aliamua kuanza upelelezi wake kwa utulivu kumfuatilia mtu aliyehusika na mauaji hayo kwani aliamini alikuwapo kijijini hapo. Alianza tabia ya ulevi ambayo awali hakuwa nayo lengo likiwa ni kuwa karibu na watu ili kufanikisha upelelezi wake. Baada ya kipindi kifupi alibaini baba yake alishawahi kufanya biashara ya pamoja na mzee mmoja aliyejulikana kwa jina la Samola miaka mingi iliyokuwa imepita. Katika biashara yao hiyo walimalizana kwa kufikishana mahakamani baada ya kushindana katika kugawana n`gombe walizokuwa nazo. Baada ya mzozo huo wa kugawana n`gombe kumalizwa na mahakama, baba yake hakuwa na uhusiano wa karibu na mzee huyo ambaye alifilisika miaka kadhaa baada ya kugawana kwao. Upelelezi huo uliompa shaka ndiyo ulimfanya James amweleze baba yake mdogo aliyeishi naye wakati huo ambaye alipinga kuhusishwa kwa mzee huyo katika mauaji hayo ya familia yao. Waliendelea na shughuli zao za kila siku, wakati upelelezi wa James dhidi ya muuaji wa familia yake ukiendelea. Siku moja akiwa amelewa akirudi nyumbani kwao akitokea eneo lililouza pombe za kienyeji ikiwa yapata saa saba usiku, James alishtushwa na kelele zilizotoka nyumbani kwao za mtu aliyeonekana alikuwa akipigwa. Kutokana na hali ya kulewa aliyokuwa nayo hakuingiwa na hofu zaidi ya hasira zilizompanda akiamini kuna watu walikuwa wakifanya mauaji. Alichomoa panga lake aliloliweka kwenye koti ambalo siku zote alikuwa akitembea nalo akihofia usalama wake, alianza kukimbia kwa kasi akielekea nyumbani kwao huku akipiga kwa sauti ya juu kelele ambazo hazikueleweka. Mara baada ya kuukaribia mlango wa nyumba yao, aliwaona watu wawili wakitoka kwa kasi, mmoja akiwa na shoka na mwingine akiwa na panga. Alisimama pembeni kidogo na mlango wao akiwa anatafakari afanye nini, punde kidogo alitoka mtu mwingine kwa kasi ndani kwao akiwa amebeba panga mkononi. James alitoka mbio akimfukuza mtu huyo aliyekimbia kwa kasi ya ajabu, baada ya kuwa mita kadhaa nyuma akimfukuza akiwa anahisi hawezi kumkamata aliamua kurusha panga lake lililompata sawasawa mtu huyo shingoni. Mtu huyo alianza kukimbia kwa kupepesuka kabla ya kuishia kuanguka, James alimsogelea na kuanza kumpiga kwa mateke. Mtu huyo alianza kujiviringisha chini akipiga kelele baada ya panga lililompata kutoka shingoni na damu nyingi ilikuwa ikimtoka. “leo utasema anayewatuma kufanya unyama…” alisikika James ambaye alikuwa na hasira. Akiwa anaendelea kumpiga mtu huyo katika eneo hilo la giza huku akili yake ikiwa haijatulia kutokana na kulewa kwake alishtushwa na kitu kizito kilichotua begani kwake. Alianguka chini wakati mkono wake wa kulia akielekeza kwenye bega lake la kushoto na kushika panga lililomkata sawasawa. Akiwa anapiga kelele kwa maumivu aliwashuhudia watu wawili wakimbeba mwenzao aliyemkata shingoni na kuanza kuondoka naye kwa kasi eneo hilo wakielekea katika vichaka vilivyokuwa karibu na eneo hilo.
James akiwa anaendelea kulia kwa maumivu aliyoyapata, kundi la watu lilikuwa likielekea kwa kasi eneo alilokuwapo baada ya watu hao kusikia kelele zilizopigwa kwa muda mrefu. Hatimaye walifika eneo hilo na kumchukua kabla ya safari ya kumpeleka hospitali kuanza, wakati huo James aliendelea kulia pasipo kuelezea jambo lolote lililokuwa limetokea. Watu hao waliomchukua ambao walikuwa majirani walitoka kutoa msaada baada ya kuamini kuna mauaji yalikuwa yakifanyika katika nyumba ya marehemu Kibudo. Walikuwa wamebeba zana mbalimbali na zaidi kwa pamoja walikuwa na shauku siku zote za kumfahamu mtu aliyekuwa akifanya mauaji katika familia hiyo. Waligawana kwa wengine kwenda kumpeleka James hospitali wakati wachache walibaki wakijadiliana juu ya matukio hayo yaliyokuwa yakiongozana. Mmoja wao alimkumbuka George Kibudo, baba yake mdogo na James jambo lililowapa hisia za kuanza kumtafuta kwa vile waliishi pamoja. Waliingia katika eneo la sebule la nyumba hiyo wakiwa wamebeba taa za mafuta kutokana na ukosefu wa umeme eneo hilo. Walishtushwa na mauaji yaliyokuwa yamefanyika sebuleni hapo dhidi ya George, alikuwa ameuawa kikatili na damu nyingi ilikuwa imemtoka ikiwa imezunguka eneo alilokuwapo. Wanawake walioshuhudia tukio hilo walianza kulia kwa sauti huku wakitoka eneo hilo la sebuleni ambalo mauaji hayo yalikuwa yamefanyika dhidi ya George. Watu waliokuwapo nje nao walipata shauku ya kuona kilichokuwa kimetokea ambao nao pia hawakuwa na hamu ya kumtazama George mara mbili kwani alikatwa mapanga kila eneo la mwili wake. Siku iliyofuata ndugu na jamaa walifika nyumbani hapo kwa marehemu mzee Kibudo wengi wakiwa na mshtuko baada ya taarifa za mauaji hayo. Ndugu wachache ambao awali walipendekezwa kusimamia mali hiyo ya marehemu mzee Kibudo walionekana wakijisifu kwa kukataa kwao kutokana na hofu ya kutokea kwa mauaji ambayo awali walikuwa nayo. Bado kulikuwa na kitendawili juu ya muuaji wa familia hiyo na wachache walihisi huenda James alipata ufumbuzi kidogo. Baada ya uchunguzi wa jeshi la polisi mwili wa bwana George Kibudo ulihurusiwa kuzikwa, siku iliyofuata zoezi hilo lilifanyika ambalo pia lilihudhuliwa na James ambaye alikuwa amepata matibabu ya awali. Muda wote wa mazishi James alikuwa na hasira juu ya mtu aliyehusika na mauaji hayo, mkono wake wa kushoto ulikuwa ndani ya koti lake baada ya kufungwa ili usichezecheze. Bado hisia zake zilikuwa zikimtuma na kuamini mzee Samola alihusika na mauaji hayo. Mbali na mahudhurio ya mzee huyo katika misiba ya ndugu zake bado hisia zake zilibaki palepale. Jambo lililompa taabu ni uwezo wake wa kufikiri alioufanya ili kumkumbuka mtu aliyefanikiwa kumkata na panga shingoni lakini hakufanikiwa kumkumbuka. Aliamini hiyo yote ilitokana na kulewa kwake siku hiyo ya tukio zaidi alipanga kuhakikisha mtu aliyehusika na mauaji hayo anagundulika na kufikishwa katika vyombo vya sheria. Baada ya mazishi hayo askari wa upelelezi walimwita James kando na kuhitaji kujua mambo kadhaa yaliyohusiana na tukio zima lililopelekea kuuawa kwa baba yake mdogo. James alitoa maelezo yake kwa askari hao ingawaje hakuhusisha hisia zake juu ya mzee Samola, alipanga kufanya upelelezi yeye mwenyewe juu ya mzee huyo. Askari hao ambao pia waliahidi kufanya upelelezi walimweleza pia kuwa wangetoa taarifa katika zahanati na hospitali ili mtu aliyeumia shingo asipatiwe msaada wa matibabu pasipo maelezo ya kutosha. Baada ya siku tatu, katika kikao cha familia James aliwaomba ndugu zake kadhaa wamsaidie kusimamia mifugo na mashamba ambavyo vyote vilikuwa vya marehemu baba yake. Hakuna hata ndugu mmoja alithubutu kukubali kumsaidia kusimamia mali hizo kwani kila mmoja alihofia uhai wake akiamini angeuawa. James alijitahidi kuwaeleza ndugu zake juu ya mwenendo wa marehemu baba yake akiwahakikishia kuwa alikuwa mtu mwema lakini hakuna hata ndugu mmoja aliyethubutu kuamini. Wengi walikuwa wameiingiwa na hofu hata watu wazima hawakuwa tayari kumsaidia. Aliendelea kusimamia mwenyewe mali hizo akiwatumia watu aliowaajiri kama vibarua. Baada ya wiki moja akiwa katika matembezi yake ya jioni, wakati ambao pia mkono wake ulikuwa haujapona alimuona mzee Samola kwa umbali katika eneo ambalo liliuzwa pombe za kienyeji. Aliendelea kutembea akiwa hana wazo la kumsalimia mzee huyo ambaye alikuwa akimtazama kwa makini na hatimaye alimwita James. Alitiii wito kwa kuanza kutembea kuelekea eneo alilokuwa amekaa mzee huyo, mara baada ya kumfikia na kumsalimia, aliketi katika kiti kilichokuwa upande wa pili uliotazamana na mzee huyo. “Kijana pole sana kwa matatizo yaliyokukuta, naomba ujipe moyo” Aliongea mzee Samola akiwa ameinamisha kichwa chake chini. “aah! mambo ya kawaida tu haya mzee, mimi nimeshatulia” alijibu James akiwa amemkazia macho mzee huyo. “Askari wanaendeleaje na upelelezi?” Aliuliza tena mzee huyo swali ambalo James hakuchelewa kulijibu. “upelelezi unaendelea vizuri na tunatarajia watuhumiwa watafunguliwa mashtaka ndani ya mwezi huu” alijibu swali hilo na kumpandisha mzee Samola hofu ya waziwazi aliyoigundua kutoka kwa mzee huyo. James mara baada ya kumjibu aliaga na kuanza kuondoka akimwacha mzee Samola akiwa na nia ya kuwafahamu watuhumiwa wa tukio hilo lakini James alimweleza alikuwa na haraka wakati huo. Akilini aliingiwa na hisia za kuamini ya kuwa mzee Samola alihusika na mauaji ya familia yake kwa namna moja au nyingine, zaidi alihitaji ukweli juu ya hisia zake upatikane. Aliamua kuanza kurudi nyumbani kwake ili akapange jambo la kufanya kuhakikisha anaupata ukweli unaomhusu mzee Samola. Mara baada ya kufika nyumbani kwake alikaa sebuleni akiwa anawaza jambo la kufanya, punde alisikia sauti ya mwanamke akipiga hodi jambo lililomfanya afungue mlango na kumkaribisha. Alikuwa ni mwanamke aliyemfahamu kwa sura lakini hakutambua alikaa maeneo gani kijijini hapo. Baada ya kuzungumza kwa muda mfupi, mwanamke huyo ambaye alionekana kutokuwa na furaha alimtaka James waongozane naye nyumbani kwake. Alimweleza kuwa kulikuwa na jambo muhimu ambalo alipaswa kulitambua. James bila uoga alikubali na mara baada ya kufunga mlango wa nyumba yake walianza kutembea na mwanamke huyo kuelekea nyumbani kwake. Hatimaye walifika nyumbani kwa mwanamke huyo baada ya nusu saa ya kutembea, alikuwa akiishi katika nyumba iliyokuwa eneo la peke yake, waliingia katika nyumba hiyo na James alikaribishwa kiti na kuketi. Mwanamke huyo alianza kwa kuhitaji utulivu wa James juu ya yote ambayo alidai yangetokea siku hiyo, jambo ambalo aliahidi kulitekeleza. Alianza kumwelezea juu ya mume wake ambaye alidai alikuwa amefanya mambo ya kusikitisha, wakati akieleza hayo mwanamke huyo alikuwa akilia. Jambo hilo lilimfanya James ahitaji kujua kuhusu mambo ambayo mume wake huyo aliyafanya, mwanamke huyo alisimama na kumwambia amfuate. Alitimiza jambo hilo na walianza kutembea kuelekea chumba cha pembeni alichohisi kilikuwa chumba cha kulala, alikuwa na shauku ya kujua jambo ambalo lingetokea. Mara baada ya kuingia katika chumba hicho James alimshuhudia mwanamme mmoja aliyelala kitandani akiwa amezungushiwa vitambaa shingoni mwake. Kwa akili ya haraka aliamini mtu huyo ndiye aliyefanikiwa kumdhuru kwa panga siku ya mauaji ya baba yake mdogo.Alibaki na shauku ya kutaka kujua mtu huyo alitaka kumweleza nini. “Denis nimekuja na James unayemhitaji” aliongea mwanamke aliyeongozana naye mara baada ya kuingia kwao. Mwanamme huyo aliyemgundua muda huo kuwa aliitwa Denis alianza kunyanyuka taratibu, “James karibu sana bwana” alisikika akiongea kwa taabu mara baada ya kuketi katika kitanda chake. Baada ya salamu alianza kwa kumwambia kuwa alimwita ili kumweleza mambo yaliyohusu mauaji ya familia yake.Jambo hilo ambalo awali James alilihisia lilimfanya moyo wake ulipuke kabla ya kuanza kutokwa mishipa usoni iliyotokana na hasira, hali hiyo haikugundulika na wenyeji hao. “mtu anayehusika kwa aslimia zote ni mzee Samola…..” alitulia kidogo wakati mapigo ya moyo ya James yakiwa yameanza kwenda mbio. “yeye ndiye aliyemuua baba yako kwa mkono wake akidai alidhulumiwa mali” Aliongea mwanamme huyo kwa sauti ya chini na polepole, alionekana alipatwa na tatizo lililopelekea ashindwe kuongea vizuri
“yeye ndiye aliyemuua baba yako kwa mkono wake akidai alidhulumiwa mali” Aliongea mwanamme huyo kwa sauti ya chini na polepole, alionekana alipatwa na tatizo lililopelekea ashindwe kuongea vizuri. Wakati huo James alikuwa ametoa macho akimwangalia mwanamme huyo aliyesimulia mauaji ya familia yake. “nimeamua nikueleze kwani siamini kama nitapona na zaidi nahitaji msamaha wako kwani nilihusika katika mauaji ya mara ya pili ya familia ya…” kabla hajamalizia sentensi hiyo James alimvamia na kuanza kumpiga ngumi mfululizo mwanamme huyo akitumia mkono wa kulia ambao hakuumia. “James usimpige, usimpige kama nilivyokuomba kuwa mtulivu naomba utulie” alipiga kelele mwanamke aliyempeleka hadi eneo hilo jambo ambalo alitii. Alikuwa akitokwa na jasho kama alinyeshewa na mvua wakati huo mwanamme huyo alikuwa akikoroma mara baada ya kupigwa. James aliondoka eneo hilo kwa kasi akiwa haelewi la kufanya hasira zilimpanda na aliweza kumuuwa mzee Samola kama angekutana naye njiani, alielekea nyumbani kwake ili kwenda kufikiri jambo ambalo alipaswa kulifanya. Aliamua kupiga simu kituo cha polisi cha wilayani Babati, askari walimwahidi kufika katika kijiji hicho cha Magugu ndani ya nusu saa.. Baada ya dakika arobaini na tano gari la askari lilifika nyumbani kwake hapo na aliwaongoza mpaka nyumbani kwa bwana Denis baada ya kutoa maelezo ya muda mfupi. Walimkuta akiwa amezidiwa sana ingawaje aliweza kuwathibitishia kuhusika na mauaji ya familia ya mzee Kibudo akiwa anatumwa na mzee Samola. Walimchukuwa na kuanza safari ya kumpeleka hospitali ya wilaya ili akapatiwe matibabu, mara baada ya kufika katika hospitali hiyo madaktari walielezea uwezekano mdogo wa kupona kwake kwani kidonda chake kilichimbika sana. Hiyo yote ilitokana na aina ya dawa ya kienyeji aliyokuwa akiitumia, alikuwa akihofia kukamatwa kwake akienda hospitali jambo lililomfanya atumie dawa hizo. Askari mmoja alielezwa amlinde mgonjwa huyo na gari hilo la polisi liliondoshwa kwa kasi na kuanza kurudi kijijini Magugu. Askari hao waliokuwa wameongozana na James, lengo lao kubwa lilikuwa ni kwenda kumkamata mzee Samola aliyehusishwa na mauji ya familia ya mzee Kibudo kwa kiasi kikubwa. Mara baada ya kufika nyumbani kwake mzee huyo alishtushwa na ujio wa askari hao jambo lililowapa imani juu ya kuhusishwa kwa mzee huyo na mauaji hayo. Askari hao walimkamata mzee Samola na kumpakia kwenye gari la polisi, wakati hayo yakiendelea watoto wake pamoja na wajukuu kadhaa walikuwa wakilia kwa uchungu juu ya tukio hilo lililokuwa likiendelea. Hata majirani walishtushwa na tukio hilo kwani walimtambua mzee Samola kama mtu mwema, vilio vyao hivyo havikuwazuia askari kutekeleza kazi yao kwani waliondoka na mzee huyo. Walimpeleka kituo cha polisi cha wilaya hiyo ya Babati na mashtaka dhidi yake yalitarajiwa kufunguliwa siku iliyofuata. James aliruhusiwa kurudi nyumbani huku moyoni akiwa na amani ambayo aliikosa katika kipindi kirefu. Mawazo yake yalimtuma kuhakikisha haki inatendeke katika kesi ambayo ilitarajiwa kufunguliwa hakutaka aina yeyote ya upendeleo. Alihitaji mzee Samola ahukumiwe adhabu ya kunyogwa kwa vile alifanya mauaji katika familia yake, alikuwa tayari kuua endapo mahakama ingeshidwa kufanya kazi. Jioni ya siku hiyo James alipigiwa simu na mtu ambaye namba yake haikuonekana aliyemweleza awe mwangalifu kwani alikuwa akitafuta matatizo. Alipuuzia kauli hiyo na kuamini ilitoka katika familia ya mzee Samola. Siku iliyofuata askari walimfuata kijana Denis aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya wilaya wakihitaji maelezo zaidi, lakini alikuwa amezidiwa na kushindwa kuongezea jambo lolote. Masaa machache baadaye hali yake ilizidi kuwa mbaya zaidi na askari waliwaomba madaktari wajitahidi kuokoa maisha ya kijana huyo ili atoe maelezo yaliyohusiana na kesi ya mauaji. Hiyo yote ilitokana na mahojiano ya awali ambayo askari walifanya na mzee Samola aliyekana kuhusika na mauaji ya familia ya mzee Kibudo. Hatimaye kesi iliyohusu mauaji ilifunguliwa dhidi ya mzee Samola na kijana aliyeitwa Denis ambaye pia alikuwa bado hajapona. Wiki tatu baadaye kijana huyo alipata nafuu baada ya jitihada kubwa zilizofanywa na madaktari na alikuwa na uwezo wa kupanda kizimbani. Jambo hilo lilikuwa faraja kwa James ambaye muda wote alikuwapo na askari hospitalini hapo ili kumlinda mtuhumiwa huyo. Baada ya hali ya mtuhumiwa huyo kuwa nzuri kiasi alimtaja mtu mwingine ambaye alikuwa mtoto wa mzee Samola kuwa alihusika pia na mauaji ya familia ya mzee Kibudo. Kijana huyo aliyeitwa Frank alikamatwa na kuongeza orodha ya watumiwa waliobakiza siku chache kupandishwa kizimbani. * * * Jackson John Samola alikuwa mtoto wa nje ya ndoa wa mzee Samola ambaye alikuwa katika harakati za kutafuta maisha jijini Nairobi nchini Kenya. Katika maisha yake aliishi mkoani Shinyanga na mama yake na hakuwahi kuishi pamoja na baba yake mzee Samola. Alimheshimu baba yake huyo kwa vile alikuwa akimtimizia mahitaji yote aliyokuwa akiyahitaji wakati akiwa shule. Jambo hilo lilimjengea tabia ya kumtembelea mara kadhaa baba yake huyo mkoani Manyara. Akiwa bado yuko jijini Nairobi alishtushwa na taarifa alizopewa na ndugu yake aliyemweleza kuwa baba na kaka yake walikuwa wakishtakiwa kwa kosa la mauaji. Jambo hilo lilimchanganya sana na hakuamini kama ni kweli walikuwa wakijihusisha na mambo kama hayo. Aliwaeleza ndugu zake wajitahidi kufanya kila waliwezalo kuhakikisha baba na kaka yake wanashinda kesi hiyo. Kutokana na kubanwa kwake na kazi aliamua kutuma fedha ili ziwasaidie katika kutoa rushwa ikibidi ili baba na kaka yake wasigandamizwe katika kesi hiyo. Ndugu zake walijitahidi kufanya jitihada mbalimbali ikiwamo ya kujaribu kumuua kijana Denis aliyetarajiwa kuelezea uovu huo lakini jitihada zao zilishindikana. Hatimaye kesi hiyo iliposomwa kwa mara ya kwanza watuhumiwa hao walionekana kuhusika na mauaji ya familia ya mzee Kibudo na hukumu ya kifo ilitolewa dhidi yao. James alifurahishwa na tukio hilo lililofanywa katika misingi ya haki, watu wengi waliohudhulia kesi hiyo walihuzunika ingawaje ukweli ulijieleza kuwa watu hao walikuwa na hatia. Jambo kubwa ambalo liliwafanya watu kuhuzunika ni imani waliyokuwa nayo awali kuwa mzee Samola, mwanaye pomoja na Denis walikuwa wakionewa. Watu wa kijiji cha Magugu waligawanyika pande mbili kwa wale waliofurahia kutendeka kwa haki na wengine wachache waliungana na familia ya mzee Samola iliyokuwa na hasira juu ya hukumu hiyo. James akiwa nyumbani kwake jioni ya siku hiyo lilifika kundi la wazee na kuhitaji kuongea naye, jambo ambalo alilitii. Wazee hao waliokuwa upande wake walimtaka ahame kijiji hicho haraka iwezekanavyo ili kuokoa maisha yake, wazee hao walimweleza juu ya mbinu za mauaji ambazo lazima zingepangwa na familia ya mzee Samola dhidi yake. Watu walizidi kuongezeka katika kikao hicho cha ghafla na zaidi ndugu zake waliungana na wazee hao wakidai walichoka kushuhudia mauaji dhidi ya familia yao. James alikubali ushauri huo na siku iliyofuata aliondoka akielekea mafichoni mkoani Arusha akiwa amewapa jukumu ndugu zake kuuza kila kitu alichokuwa nacho kijijini hapo. Alihitaji wamuuzie n`gombe zaidi ya mia aliokuwa nao na mashamba yote, fedha hizo alitaka zimsaidie kwenda kuanza maisha sehemu nyingine. Jambo hilo lilianza kutekelezwa na vitu hivyo vilianza kuuzwa kijijini hapo na sehemu nyingine tofauti. Familia ya mzee Samola iliyokuwa na hasira iliweka kikao juu ya jambo la kufanya wakati watoto wa kiume wa mzee huyo walidai walimsubiri mwenzao kutoka Nairobi nchini Kenya ili wajue jambo la kufanya. Siku tatu baadaye kijana Jackson John Samola aliwasili kijijini hapo akiwa na hasira juu ya tukio lililokuwa limetokea, alikaa na kaka zake wengine ambao kwa pamoja walijadiliana. Mtu aliyeonekana kusababisha hukumu ya kaka na baba yao hakuwa mwingine bali ni James Kibudo huku kaka zake Jackson wakihitaji kulipiza kisasi. Kilichowachanganya zaidi ni taarifa walizozipata kuwa mtu huyo alikuwa ameondoka kijijini hapo“msipate taabu kaka zangu, kama mtu huyu yuko katika dunia hii niachieni kazi, miaka hata kumi na tano itapita lakini adhabu yake iko palepale” alisikika akiongea Jackson akiwa na hasira. Kupitia elimu yake aliwaeleza kaka zake kuwa huo haukuwa muda muafaka wa kulipa kisasi kwani ingekuwa rahisi kwa wao kugundulika jambo ambalo walimwelewa.
Baada ya kuuzwa kila kitu kilichokuwa chake kijijini kwao Magugu, James alielekea jijini Dar es salaam akiwa na lengo kubwa la kwenda kunzisha biashara hilo liliwezekana kwani alikuwa amepata kiasi kikubwa cha fedha. Ndugu zake aliwaeleza wagawane mashamba kadhaa ambayo hakuyauza na kichwani mwake hakuwa na wazo la kurudi kijijni hapo akihofia kuuawa kama aliyokuwa amepewa ushauri. Moyoni alijiona hana kosa na alichoshukuru zaidi ni haki iliyokuwa imetendeka juu ya wauaji wa familia yake. * * * * Baada ya miaka kumi James alikuwa miongoni mwa matajiri wakubwa jijini Dar es salaam kupitia biashara tofauti alizokuwa nazo. Hakuwahi kurudi kijini kwao hata siku moja ingawaje ndugu zake walimtembelea mara kadhaa. Tayari alikuwa ameowa na alibahatika kupata watoto wawili wakiume, mambo yaliyojili miaka kumi iliyokuwa imepita alianza kuyasahau na aliwaza maendeleo zaidi. Wakati huo alikuwa na marafiki zake kadhaa ambao baada ya mikakati yao tofauti ya kujikwamua kimaisha waliamua kuanzisha kampuni ya utengenezaji wa vyombo vya ndani. Taratibu zote zilifanyika na kampuni hiyo iliyosajiliwa kama JAJHO Company Limited ilianza kufanya kazi. Kampuni hiyo iliitwa hivyo ikitokana na kifupisho cha majina yao ambayo yalikuwa James,Amos,Jackson,Hamis na Onesmo. James ndiye alikuwa na hisa nyingi zaidi ya aslimia arobaini akifuatiwa na Jackson mwishoe wengine. Katika kipindi kifupi cha biashara kampuni hiyo ilionekana kukubalika na watu walionyesha uzalendo kwa kununua bidhaa zake zilizotengenezwa hapahapa nchini. Jambo hilo lilikuwa faraja kwa James aliyekuwa kiongozi wa kampuni hiyo kutokana na hisa nyingi alizokuwa nazo, lakini pia wenzie walionyesha furaha juu ya mafanikio hayo. Mafanikio yake ndiyo yalimfanya James awapeleke mapema watoto wake nchini Marekani kwa ajili ya masomo. Walianza masomo katika shule iliyokuwa Chicago katika jimbo la Illinois iliyoitwa American Academy School iliyochukua watoto wa shule ya msingi mpaka sekondari. Moyoni hakuwa na shaka akiamini alikuwa amefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika maisha yake. Jackson wa kampuni hiyo ya JAJHO Company Limited hakuwa mwingine bali ni Jackson John Samola ambaye lengo lake lilikuwa ni kulipiza kisasi kwa James. Hakuwahi kukutana na James zaidi ya kumuona kwenye picha kwa vile hakuishi katika kijiji cha Magugu ambacho James aliishi awali. Watu wote waliomiliki kampuni hiyo walikuwa rafiki zake na walikubaliana naye kuhakikisha wanamuua James. Lengo lao lilikuwa ni kusubiri kampuni hiyo ikue na James kuwa na kiasi kikubwa cha hisa na hatimaye kufanikisha zoezi la mauaji. Hakuna mtu aliyekuwa akijua siri hiyo zaidi yao wanne, Jackson siku zote za maisha yake alikuwa akiamini James angekufa kizembe na tayari alinasa katika mtego wake. Baada ya mwaka mmoja Jackson na wenzake waliona ni muda muafaka wa kuuawa kwa James wakati ambao walikuwa na mafanikio makubwa katika kampuni yao. Walikuwa wakitafuta mbinu mbalimbali za kuhakikisha wanamuua James na mwishoe walipata jibu la kufanikisha zoezi hilo. Jackson alipendekeza kuwa waandae ziara ya kufurahia mafanikio yao wakiwa na familia zao na mwishoe waiangamize familia ya James. Aliwataka ziara hiyo ifanyike nchini Kenya kwa vile aliifahamu vizuri nchi hiyo na ingekuwa rahisi kufanikisha mauaji hayo. Wamiliki hao wa kampuni hiyo mbali na James walimheshimiana sana na Jackson na walikuwa tayari kumsaidia malipizi ya kisasi. Hawakuwa watu wema kwani walishawahi kufanya kazi za ujambazi na kwao kuuawa kwa James waliamini kungewapa kipato kikubwa kupitia hisa ambazo zingeongezeka.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Baada ya kikao chao hicho cha awali walichokifanyia nyumbani kwa Jackson, walipanga Amos ambaye alikuwa miongoni mwa wamilikiwa kampuni hiyo atoe maoni ya ziara hiyo katika kikao chao cha kampuni kilichofanya kila mwisho wa wiki. Kama ilivyokuwa kawaida yao kuwa na kikao siku ya Ijumaa, James alijumuika na wamiliki wenzie wa kampuni hiyo katika kikao. Mara baada ya mambo muhimu kuzungumziwa Amos alitoa maoni ya kufanyika ziara nchini Kenya wakiwa na familia zao katika kumaliza mwaka huo na kufurahia mafanikio yao. Jambo hilo lilionekana kupokelewa vizuri ingawaje James hakulifikilia kabla alikubaliana na wenzake kufanyika ziara hiyo mwishoni mwa mwaka. Wakati huo ilikuwa ni mwezi wa kumi na ziara yao ilipangwa kuanza mwishoni mwa mwezi wa kumi na mbili. Makubaliano hayo yalionekana kuwa faraja kwa Jackson na wenzie walioamini kuwa mipango yao ilielekea kukamilika. Kila siku iliyokuwa ikienda walikuwa wakiendeleza vikao vyao vya siri vya kukamilisha mauaji hayo hiyo ilitokana na umaarufu aliokuwa nao James. Tayari alikuwa na jina kubwa hivyo mauaji dhidi yake yalihitaji usiri mkubwa ili kushindikana kwa jitihada zozote za upelelezi. Jackson bado alijijengea tabia ya kuwaeleza kaka zake kuwa mambo mazuri yalikuwa hayahitaji haraka akiwahakikishia kukamilisha malipizi ya kifo kama James alivyochangia kunyongwa kwa baba na kaka yao. Siku sita kabla ya ziara ya wamiliki wa kampuni ya JAJHO Company Limited, James alipokea taarifa za mwanae mmoja aliyekuwa akisoma American Academy School. Alielezwa mwanae huyo wa kwanza aliyekuwa na miaka tisa ambaye aliyeitwa Geofrey alikuwa akipatwa na homa za mara kwa mara jambo lililowafanya walimu wa shule hiyo wamshauri mwanae huyo arudishwe Tanzania. James hakushangazwa sana na taarifa hizo kwani alilitambua hilo kwa vile mwanae huyo alikuwa akipatwa na maradhi tofauti tokea utoto wake. Alikubaliana na walimu kuwa mwanaye huyo arudishwe Tanzania lakini mdogo wake aliyeitwa Robert alitakiwa kubaki nchini humo kuendelea na masomo. Alielezwa mwanaye angefika Tanzania baada ya wiki moja, hiyo ilitokana na ratiba ya ndege ambayo alikatiwa tiketi. James aliyaelewa maelezo hayo lakini aligundua mwanaye angefika yeye akiwa ziarani nchini Kenya, Alipanga kuacha taratibu zote za mapokezi ya mwanaye zikiwa sawa. Hatimaye siku ambayo wamiliki wa kampuni ya JAJHO Company limited waliipanga kwa ziara ilifika na waliamua kutumia usafiri wa gari lengo lao kubwa likiwa ni kupita katika vivutio tofauti vya nchi katika kanda ya kaskazini. Asubuhi ya siku hiyo James alifika na gari lake katika ofisi ya kampuni akiwa na mkewe ambaye walipendana sana tayari kwa ziara hiyo. Katika ofisi za kampuni yao zilizokuwapo maeneo ya Posta tayari wamiliki hao walikuwa wamefika na alikuwa akisubiriwa Hamis na familia yake ambao walikuwa hawajafika. Lilikuwa limeandaliwa basi maalumu kwa ajili ya safari hiyo na wamiliki hao walionyesha furaha wakisubiri safari hiyo ianze. “mzee hata mtoto tu, inakuwaje?” aliongea Jackson akimuuliza James katika hali ya utani kwani alielewa watoto hao walikuwa masomoni nchini Marekani. “acha hizo bwana kwani hujui wako wapi?, ila mwanangu Geofrey yuko njiani akirudi tutapishana naye” aliongea James akijibu utani huo. Baada ya dakika kadhaa Hamis alifika ofisini hapo akiwa na familia yake na safari ilionekana ilikuwa imesha kamilika. Waliingia kwenye basi lililokuwa limeandaliwa na safari ilianza wakiwa wamepanga kupitia hifadhi ya taifa ya Serengeti na mwishoe walipanga wapitie mkoa wa Mara wakielekea nchini Kenya. Walimtumia dereva mmoja ambaye alikuwa akiaminika sana na kampuni hiyo, James hakuwa na hofu kwani alishamwandaa mtu wa kumpokea mwanaye siku mbili zilizofuata hivyo aliamini mambo yote yangekuwa kama yalivyopangwa. Hawakuwa na haraka kwani siku hiyo walilala Moshi mjini wakiwa na lengo la kupata maelezo ya hifadhi ya mlima Kilimanjaro siku iliyofuata. Walitekeleza zoezi la kutembelea hifadhi hiyo siku iliyofuata na baada ya maelezo mafupi yaliyohusu mlima huo waliendelea na safari wakipitia hifadhi ya Serengeti na siku tatu baadaye walikuwa nchini Kenya. Walitumia siku mbili kutembelea maeneo tofauti ya jijini Nairobi na siku ya tatu walielekea Machakos kwa ajili ya kuendeleza ziara yao wakiwa na furaha tele juu ya tukio hilo. Walifikia katika hoteli ya kifahari ambayo walikuwa wameikodi kwa ajili yao kwa siku kadhaa wakiwa sehemu hiyo. Kila familia ilipewa vyumba vyake na kila hitaji lilikuwa likitimizwa na wahudumu wa hoteli hiyo.
Kila familia ilipewa vyumba vyake na kila hitaji lilikuwa likitimizwa na wahudumu wa hoteli hiyo. Jackson ndiye aliyefanya mipango yote na wakati huo aliona ulikuwa ni muda muafaka wa kuuawa kwa James na mkewe. Alikuwa ameongea na kundi la majambazi lililopaswa kuwasaidia kukamilisha mauaji hayo, majira ya saa tatu usiku watu hao walifika hotelini hapo wakiwa na gari zao tatu. Mara baada ya kufika walimpigia simu Jackson ambaye aliwaahidi kutoka nje baada ya muda mfupi. Baada ya kupigiwa simu Jackson alimuaga mkewe na watoto wake akiwaambia kuwa alikuwa na kikao kifupi na wamiliki wenzie wa kampuni yao. Alipotoka nje aliwapigia simu Amos, Hamis halikadhalika Onesmo akiwaeleza watoke nje. Walitekeleza jambo hilo kwani walielewa zoezi ambalo lilifuata, nao waliaga familia zao wakieleza kuwa walikuwa na kikao. Walipofika nje walipanda katika gari moja lililokuwa la mwisho kati ya hayo matatu ya majambazi yaliyokuwa yamefuatana, Jackson alimpigia simu kiongozi wa kundi hilo aliyekuwa gari la mbele na kumweleza jambo walilotakiwa kufanya. Mara baada ya zoezi hilo Jackson alichukua tena simu yake na kumpigia James na punde ilipopokelewa alianza kwa kusikika “haloo James, njoo nje hapa na mkeo ikibidi kuna tatizo limetokea” “tatizo? tatizo gani tena!” aliuliza James kwa mshangao. “njooni tu jamani mtaliona tusipoteze muda” “sawa tunakuja” alimaliza James akiwa ameahidi kutoka na mkewe. Baada ya dakika tano James alitoka na mkewe wakiwa na nguo za kulalia, walisimama katika mlango wa kuingilia katika hoteli hiyo. Jackson na wenzie walishuhudia vizuri tukio hilo, alichukua tena simu yake na kumweleza James aende katika Range Rover iliyokuwa ya kwanza kati ya tatu zilizokuwa zimeegeshwa zikiwa zimeongozana. James alifanya hivyo na alianza kutembea akielekea katika gari hilo na hakuonyesha hofu yeyote. Alikuwa amemwacha mkewe akimwangalia hatimaye James aliingia katika gari hiyo aina ya Range Rover. Baada ya dakika tano Jackson alielewa mpango alioufanya ulikuwa umefanikiwa alichukua tena simu yake na kumpigia mkewe James ambaye walimwona vizuri akiwa katika mlango wa hoteli hiyo. Hatimaye walimshuhudia akipokea simu “shemeji vipi? mbona unakaa nje, kuna mgonjwa hapa tunashauriana cha kufanya njoo” alisikika Jackson akimweleza mkewe James. “hee! kumbe mgonjwa nakuja” alijibu kabla ya kuanza kutembea akielekea kwenye Range Rover aliyoelekea mumewe. Hatimaye naye alipanda gari hilo, Jackson na wenzie walipiga kelele za kupongezana wakiamini kazi ilikuwa imeisha. Ziliwashwa gari zote tatu huku lao likiendeshwa na jambazi aliyekuwapo toka awali, mara baada ya kufunguliwa geti la hoteli walianza safari kwa mwendo wa kasi wakiwa na lengo la kuelekea eneo la Garrissa lilokuwa kando ya mto Tana walikopanga mauaji ya James na mkewe yaende kufanyika. Mr. Tyoso kama alivyofahamika kutokana na matukio yake tofauti haramu ndiye aliyehusika katika mpango huo wa kutekwa kwa James na mkewe huku safari ikiendelea kuelekea eneo walilopanga kumfanyia mauaji. Mara baada ya James kupigiwa simu aelekee kwenye gari aina ya Range Rover, Walijiandaa na kijana wake mmoja wa kazi aliyekuwa kwenye gari hilo na punde alipoingia walimpiga na kitako cha bunduki na kumfanya azimie walimfanyia hivyohivyo mkewe ambaye pia alikuwa amezimia. Wakati huo mr. Tyoso alipanga kufanikisha mauaji hayo ili kutimiza matakwa ya wateja wake na mwishoe alihitaji kuendelea na shughuli zake akiwa na kundi lake hilo. Walikimbiza gari zao na masaa mawili baadaye walikuwa katika eneo la Garrissa lililokuwa na giza nene kando ya mto Tana, wakati huo ilikuwa yapata saa tano na nusu. Waliegesha gari zao katika eneo hilo ambalo pia halikuwa na njia ila vichaka na mti kadhaa iliyokuwapo. Lilikuwa ni eneo lenye giza nene ambalo mtu mwoga asingevumilia kukaa. Gari moja kati ya hizo tatu walizokuwa nazo liliwashwa taa zake na kufanya eneo hilo liwe na mwanga kama ilikuwa mchana. James na mkewe walishushwa na kuwekwa eneo la mbele ambalo taa hizo za gari zilielekezwa, kwa umbali James alianza kurudiwa na fahamu ila kichwa kilimuuma sana. Hali haikuwa hivyo kwa mkewe ambaye bado alikuwa amezimia, mr. Tyoso aliwaamuru vijana wake wakachote maji katika mto Tana ambao ulikuwa umbali mfupi toka hapo, lengo lao likiwa ni kuwamwagia maji. Walitaka kufanya hivyo ili kurudisha kumbukubu za James na mkewe. Baada ya dakika tano vijana wake hao watatu ambao walikuwa na bunduki mabegani mwao walirudi na madumu matatu ya maji ambayo walianza kwa kuwamwagia James na mkewe. Wakati hayo yote yakiendelea Jackson alikuwapo eneo la tukio na wenzie, alikuwa na hasira akihitaji kuuwa lakini alitulizwa na mr Tyoso aliyemtaka asiwe na haraka. Dakika kadhaa baada ya kumwagiwa maji ambayo yalikuwa ya baridi sana James na mkewe walishtuka na kukutana na picha mbili zilizonekana vizuri. Mkewe James hakuzitambua picha hizo ila mumewe alionyesha kushtuka, wakati huo walikuwa wako chini eneo walilokuwa wamemwagiwa maji. Waliponyanyua vichwa vyao walikutana na sura waliyoifahamua ya mtu aliyekuwa ameshika picha hizo ambaye alikuwa Jackson. James na mkewe walishtushwa na hali halisi iliyokuwapo eneo hilo, watu zaidi ya watano walikuwa na bunduki, aliwashuhudia wamiliki wenzie wa kampuni wakiwa eneo hilo mbali na Jackson aliyekuwa ameshika picha. Tayari alijua kulikuwa na shari kwani aliiona picha ya mzee Samola na mwanaye Frank ambao wote kwa pamoja walihukumiwa kunyogwa kwa kosa la mauaji ya familia yake. Muda huo wote hakuna mtu aliyekuwa akiongea zaidi ya Jackson aliyeshika picha huku akitetemeka. “ulizani ungepona kwa kusababisha kunyonga kwa baba na kaka yangu?” alisikika Jackson baada ya kimya cha muda mrefu, kabla hajajibiwa kitu wakati huo James na mkewe wakitetemeka alikurupuka na kuchukua moja ya bunduki ya kijana wa mr. Tyoso na kimumiminia kifuani mkewe James risasi zaidi ya saba. James alipiga kelele juu ya tukio hilo, na kwa kasi ya ajabu alikurupuka kumvamia Jackson aliyekuwa na bunduki akiwa na lengo la kumpiga, kabla hajafanikisha lengo hilo alikamatwa na Amos aliyesaidiana na Hamis kabla ya kususkumwa tena chini. “wewe ni kama muuaji unadhani utatuweza” Aliongea Onesmo aliyekuwa ameshika nondo mkononi na alianza kumpiga nayo, Amos na wenzie nao walijumuika naye kumpiga James ambaye alilia kwa uchungu akiwa haelewi kosa alilowafanyia wenzie hao waliomiliki kampuni moja. Baada ya dakika tano James alikuwa ameumizwa sana na damu nyingi ilikuwa imemtoka nguo zote alizokuwa amevaa zilikuwa zimelowa damu. “ mfungeni kamba huyu kinyago..” alisikika Jackson baada ya kuwasitisha wenzie wasiendelee kumpiga. Baada ya agizo hilo vijana wa mr. Tyoso walitekeleza jambo hilo na kuanza kumfunga kamba, muda wote matukio hayo yakiendelea hawakuingilia kitu kazi yao ilikuwa ni kuhakikisha usalama wa wateja wao. Mara baada ya kufungwa kamba kwa James aliyekuwa akilia kwa sauti ya chini Jackson na wamiliki wa kampuni wenzie waliopanga mauaji hayo walichukua bunduki kila mmoja. Walianza kuzikoki tayari kwa kufyatua risasi wakiwa wamezielekeza eneo alilokuwa amelala James akiwa hatazamiki mara baada ya kipigo. Jackson aliwaeleza wenzie wakae tayari kwa kufyatua risasi akihesabu mpaka tatu “ moja….! mbili….! ta…” * * * * * George Johnson alikuwa ni kijana ambaye alizaliwa nchini Kenya na baada ya masomo yake ya shule ya msingi na sekondari alianza kujishughulisha utengenezaji filamu. Mara kadhaa alifanya kazi hiyo katika sherehe mbalimbali jijini Nairobi zikiwamo harusi na mahafali. Aliishi akitegemea kazi hiyo na mara nyingine alikuwa akiwafanyia kazi ya kuwapiga picha watalii kadhaa waliokuwa wakitembelea nchini Kenya. Alikuwa akiwaandalia filamu za ziara zao watalii nchini humo na hatimaye walikuwa wakimlipa pindi walipokuwa wakirudi katika nchi zao. Mwezi wa kumi na mbili wakati sikukuu zikiwa zimekaribia alipigiwa simu na shirika moja lililohusika na watalii. Alielezwa kuwa kuna watalii walikuwa wakimhitaji awapigie picha za filamu kwa ajili utafiti wa viumbe vilivyoishi kando ya mto Tana. George alitaka kupuuza ombi hilo kutokana na sikukuu zilizokuwa zimekaribia lakini aligundua baadaye kazi hiyo ilikuwa muhimu zaidi. Aliwajibu watu hao kuwa alikuwa tayari kwa kazi hiyo, na hatimaye utafiti huo ulienda kuanzia eneo la Kipini ambalo ndipo Mto Tana ulikuwa ukiishia kuingia bahari ya Hindi.
Aliwajibu watu hao kuwa alikuwa tayari kwa kazi hiyo, na hatimaye utafiti huo ulienda kuanzia eneo la Kipini ambalo ndipo Mto Tana ulikuwa ukiishia kuingia bahari ya Hindi. Watalii hao wanne waliokuwa wazungu wakitokea Norway walianza utafiti wao huo wakiwa na George aliyechukua picha kila jambo aliloambiwa kuchukua. Alikuwa akipiga picha vyura wa aina tofauti waliokuwa kando ya mto huo na hilo lilikuwa ndilo lengo kubwa la watalii hao walitaka kujua aina za vyura waliopatikana kando ya mto huo. Walikuwa wakitumia gari aina ya Land Cruiser na kila ilipofika jioni walikuwa wakiweka mahema na kulala. Maisha hayo yalimchukiza George lakini jambo hilo lilikuwa la kawaida kwa wazungu hao waliozoea kazi hizo za utafiti. Siku iliyofuata walikuwa eneo la Burra wakiendelea na utafiti huo, hali kadahalika George alikuwa akipiga picha kwa ajili ya kuandaa filamu ya watafiti hao waliokuwa wakitokea Norway. Siku ya tatu walikuwa eneo la Garrissa na mara baada ya utafiti wao huo liliwekwa hema na walilala tena eneo hilo wakiwa na gari lao katika sehemu hiyo iliyokuwa na miti pamoja na vichaka, walikuwa wakiweza kupita kutokana na uwezo mkubwa wa gari walilokuwa nalo. Muda wote waliokuwa wakilala George hakuwa na mazoea ya kufanya hivyo kutokana na uoga aliokuwa nao, lakini haikuwa hivyo kwa watafiti aliokuwa ameongozana nao ambao walikuwa wakilala pasipo hofu. Alikuwa na kamera yake kifuani ambayo kamba ya kibegi chake ilikuwa imemkaa shingoni, alitamani kazi hiyo ikamilike ili waondoke maeneo hayo ya mto Tana. Majira ya saa tano na nusu usiku alishtushwa na kelele za magari yaliyonguruma upande wa magharibi wa eneo walilokuwapo. Jambo hilo lilimshtusha kwani hakufikiria kama kuna gari lingeweza kufika eneo hilo aliamua kutoka nje na alishuhudia mwanga uliotokana na taa za gari na kufanya eneo hilo lililokuwa na giza nene liwe kama mchana. Dakika kadhaa akiwa hajagungua jambo la kufanya alishuhudia taa kadhaa za gari hizo zikizimwa na mwanga wa kawaida ulibaki katika eneo hilo. Alipata ujasiri wa ghafla uliomtuma aende eneo hilo bila kijiuliza mara mbili alianza kutembea eneo la pembeni na mwanga huo akiwa anausogelea. Lengo lake lilikuwa asionwe na watu hao waliokuwa wamefika eneo hilo nyakati hizo za usiku, mara baada ya kukaribia eneo hilo na kuanza kuyaona magari hayo vizuri alilala chini na kuanza kujiburuza kwa tumbo akisogea zaidi eneo hilo.Hatimaye alikuwa umbali wa kama mita nane na alishuhudia kila kitu kilichokuwa kikiendelea eneo hilo lililokuwa na mwanga kama wakati huo ilikuwa mchana. Aliwashuhudia watu kadhaa wakiwa na bunduki mabegani mwao na wengine wawili mwanamke na mwanamume walikuwa chini kama vile walikuwa wamepotelewa na fahamu. Baada ya dakika chache aliwashuhudia watu wengine watatu wenye dunduki zao wakiwa na madumu aliyohisi yalikuwa maji kwani walikuwa wametokea eneo la mto Tana. Walianza kuwamwagia watu hao maji ambao walishtuka baada ya muda mfupi, George alihisi kuna jambo lilitaka kutokea juu ya watu hao na aliamua kuwasha kamera yake ya filamu ili ajumuike nayo katika kushuhudia tukio hilo. Taratibu aliiegesha na ilianza kuchukua picha za kila kitu kilichoendelea eneo hilo, alimshudia mtu mmoja akiwa anawaonyesha watu hao waliomwagiwa maji picha.Baada kimya cha muda mrefu mtu huyo aliongea kidogo kabla ya kukurupuka na kuchukua bunduki kisha kumumiminia mwanamke aliyekuwapo chini na mwanamume kwa risasi zaidi ya saba. George alishtushwa na unyama huo uliokuwa ukiendelea hata hali ya hofu juu yake ilianza kumwingia lakini alijikaza akiamini alikuwa mwanamme kamili. Aliigeukia kamera yake na kushuhudia ikiendelea kuchukua kila tukio lililoendelea. Alimwona mwanamme aliyekuwa chini na mwanamke huyo aliyepigwa risasi akijaribu kumvamia mtu aliyekuwa amefanya tukio hilo. Hakufanikiwa zoezi hilo kwani alisukumwa chini na alianza kupigwa na watu hao ambapo mmoja wao alionekana alichukua kitu kizito kama chuma. Dakika chache baadaye mtu huyo alikuwa ameumizwa vibaya na aliamriwa afungwe kamba, baada ya kufungwa kamba aliwashuhudia wanaume wanne wakizikoki bunduki zao wakiwa tayari kwa kumuua mtu huyo aliyefungwa kamba. Mmoja wao alianza kuhesabu akisikika “moja….! Mbili…! tatu…!” mara baada ya kuhesabu mara tatu watu hao walianza kummiminia risasi mtu huyo kama vile walikuwa vitani walikuwa hawana huruma hata kidogo. Wakati tukio hilo likiendelea George aligeuza kichwa chache asishuhudie tukio hilo, aliiacha kamera yake ikipiga picha kila kilichoendelea. Katika maisha yake alikuwa akidhani matukio kama hayo yalikuwa ya filamu za kuigiza lakini alishuhudia kwa macho yake na kubaini kuwa yalikuwa yakitokea. Baada ya zoezi hilo watu hao waliwasha gari zao na kuondoa kwa kasi eneo hilo la tukio, George alijikuta akilia peke yake juu ya mauaji hayo yaliyokuwa yametokea. Aliikumbuka tochi aliyokuwa nayo baada ya giza nene kutanda eneo hilo ikiwa ni baada ya kuondoka kwa magari hayo, alichukua kamera yake na kuanza kusogea taratibu eneo la tukio. Mara baada ya kufika eneo hilo alitumia tochi akiendelea kuwapiga picha watu hao waliokuwa wameuawa, moyo ulimuuma sana na hakuelewa kosa walililokuwa wamefanya. Akiwa anaendelea kizichukua vizuri picha za sura za watu hao waliouawa alishtushwa na mngurumo wa gari lililokuwa likirudi kwa kasi eneo la tukio. Alitoka mbio na kwenda kufichama katika kichaka cha karibu, aliwashuhudia watu sita wakishuka katika gari hilo na mmoja wao aliwaamuru wenzie wakaitupe miili hiyo katika maji ya mto Tana. Walitii maagizo hayo na kuibeba miili hiyo, walianza kuelekea upande uliokuwa na mto huo. Baada muda mfupi walikuwa wametimiza zoezi hilo waliwasha tena gari zao na kuondoka kwa kasi. George alikuwa amechanganyikiwa na katika maisha yake hakuwahi kushuhudia mauaji kama hayo, aliingiwa hofu juu ya uhai wake kuhusiana na picha hizo alizozipiga. Siku iliyofuta ambayo ilikuwa ya mwisho aliendelea kuchukua picha zilizohusiana na utafiti uliofanywa na raia wa Norway. Hakujaribu kumwambia mtu juu ya tukio alilokuwa amelishuhudia usiku wa siku iliyopita, hakuwa na furaha sana jambo lililofanya watafiti hao wamwulize mara kadhaa kama alikuwa na tatizo. Hakuthubutu kutoa siri hiyo aliyokuwa ameishuhudia, mara baada ya utafiti huo aliandaa filamu ya watalii hao na hatimaye aliikabidhi na kupewa malipo yake. Tayari pia alikuwa ameandaa filamu ya dakika ishirini na tano iliyohusiana na mauaji aliyoyashuhudia, alikuwa akisubiri asikie tukio lolote lililohusiana na mauaji hayo ili aipeleke filamu hiyo kituo cha polisi. Matukio ambayo yalikuwamo katika filamu hiyo ilikuwa na vigumu kwa mtu kuamini kama yalikuwa ni mauaji ya kweli, alifanikiwa kuzipata picha za watu ambao walionekana vizuri mwanzo mpaka mwisho. Siku kadhaa zilipita pasipo kusikia jambo lolote lililohusiana na mauaji hayo, alipata wazo la kupeleka kituo cha polisi filamu hiyo lakini kabla hajafanya hivyo aliamua kuomba ushauri kwa mjomba yake aliyekuwa mwanajeshi mstaafu. Alisimulia tukio lililoendana na lake na kujifanya akiomba ushauri wa tukio kama hilo, mjomba yake huyo alimtisha akimwambia matukio kama hayo ni hatari. Aliongezea kuwa angefanikisha kukamatwa kwa watu hao lakini mwisho wake lazima ungekuwa kifo. George jambo hilo halikumwingia akilini hata kidogo, moyoni aliumia juu ya mauaji aliyokuwa ameyashuhudia na alipanga kuifikisha filamu hiyo kituo cha polisi endapo angesikia mauaji yeyote yaliyohusina na tukio alilolishudia. Suala la kutafutwa na wauaji hakuliogopa lakini mawazo yake yalimtuma kuhakikisha haki inatendeka juu ya wauaji. * * * * Mara baada ya kukamilisha mauaji ya James na mkewe, Jackson na wenzake pamoja na kundi la vijana wa mr. Tyoso waliondoka eneo la tukio na gari zao kwa kasi kubwa. Wakiwa wametembea kilomita moja Tyoso aliamua kutoa wazo la kutupwa miili ya watu hao waliokuwa wameuawa katika maji ya mto Tana na waliamua kutekeleza zoezi hilo. Gari moja liligeuzwa kurudi eneo la tukio likiwa na Jackson pamoja na vijana watano wa mr Tyoso, mara baada ya kufika eneo la tukio walifanikisha kutupwa kwa miili ya James na mkewe katika maji ya mto Tana na hatimaye safari ilianza wakirudi eneo walilowaacha wenzao.
Mara baada ya kufika eneo la tukio walifanikisha kutupwa kwa miili ya James na mkewe katika maji ya mto Tana na hatimaye safari ilianza wakirudi eneo walilowaacha wenzao. Walipofika walianza safari ya kuelekea Machakos eneo waliloziacha familia zao, majira ya saa nane usiku walifika eneo hilo na Jackson alichukuwa jukumu la kumlipa mr. Tyoso alyesaidia kufanikisha mauaji hayo akiwa na kundi lake. Mara baada ya tukio hilo mr Tyoso aliondoka akiwa na kundi lake katika hoteli hiyo waliokuwa wamefikia. “sasa mmeona watu wangu kazi imeisha na utajiri ule ni wetu” alisikika Jackson mara baada Tyoso kuondoka na kundi lake. “mwache aende kuzimu mtu gani anamikiki nusu ya hisa za kampuni” aliongezea Hamis jambo hilo, wote walikumbatiana na kupongezana na walirudi katika vyumba vya familia zao kama vile walitoka kwenye kikako kirefu cha kampuni. Siku iliyofuata kama ilivyopangwa ilikuwa na siku ya kuanza safari ya kurudi nchini Tanzania, asubuhi kilifanyika kikao cha safari hiyo. Jackson aliwaeleza wanafamilia hao kuwa James na mkewe walikuwa na mambo ya ziada ya kufanya nchini humo Kenya hivyo wangerudi Tanzania wiki moja baadaye. Jambo hilo lilieleweka na safari hiyo ilianza, siku tatu baadaye walikuwapo nchini Tanzania. * * * * Robert ambaye alikuwa mtoto wa pili wa James hakufurahishwa na safari iliyokuwa imeandaliwa dhidi ya kaka yake Geofrey aliyetakiwa kurudi nchini Tanzania kutokana na homa za mara kwa mara alizokuwa nazo. Baada ya maandalizi ya safari ilikuwa ikisubiriwa siku hiyo wakati Robert akiwa hayuko tayari kuachana na kaka yake huyo ambaye pia hakupenda tukio hilo. Siku ya safari ilipofika Robert akiwa na mwalimu wake waliondoka shuleni hapo kuelekea uwanja wa ndege wa Chicago kwa lengo la kumsindikiza Geofrey. Walikuwa wakilia wakiwa hawaamini kuwa wangetengana kwa miezi kadhaa iliyokuwa imebakia kabla ya likizo. Hatimaye walifika katika uwanja huo wa ndege na Robert aliagana na kaka yake na kuishia kupanda ndege akiwa na mwalimu wao. Walikuwa wakielekea jimbo la Washington ambako safari ilitarajiwa kwenda kuanzia. Robert alirudi shule akiwa na dereva wa gari hilo la shule ila hakujisikia vizuri muda wote kutokana na tukio hilo la kuagana na kaka yake. Alijipa matumaini akiamini angerudi Tanzania wakati wa likizo yake ndefu jambo lililomfanya ajipe moyo wa kubaki shuleni hapo kuendelea na masomo yake. Hatimaye majira ya saa moja jioni Geofrey alikuwa akiagana na mwalimu wake tayari kwa safari ya kurudi Tanzania. Ndege aliyopanda ilikuwa ikitarajiwa kupita katika bara la Amerika ya kusini katika jimbo la Rio de Jeneiro nchini Brazil kabla ya kupita Uingereza na mwishoe Afrika. Geofrey alielezwa kuwa taratibu zote za mapokezi yake zilikuwa zimeshakamilika na angepokelewa mara baada ya kufika Tanzania. Safari ya ndege hiyo ilianza mara baada ya muda uliopangwa kutimia, Geofrey mtoto wa miaka kumi alikuwa akiona mwisho wa kuyaona maghorofa ya kifahari ya nchi hiyo ulifika. Aliamini angeikumbuka sana Marekani hususani jimbo la Illinois ambalo alikuwa akisoma, hiyo yote ilitokana na kuumwa kwake mara kadhaa akaamua kukubaliana na kila lililokuwa limetokea. Mbali na mabegi yake ya nguo yaliyokuwa yamehifadhiwa eneo la mizigo alikuwa amebeba begi lake dogo alilokuwa akihifadhi vitu vyake muhimu. Moja ya vitu alivyohifadhi humo zilikuwa picha za familia yake ambayo aliipenda sana, alikuwa na picha zidi ya ishirini zikiwamo ambazo alikuwapo mdogo wake Robert.Safari iliendelea kukiwa na kila raha ambazo siku zote alitambua kuwa zilikuwa za kawaida katika usafiri huo wa ndege. Baada ya masaa kadhaa ya safari hiyo alishtushwa na hali ya mtikisiko ambayo ndege hiyo ilianza kukumbana nayo. Jambo hilo pia liliwashtua hata abiria wenzie waliohofia hali hiyo ya mtikisiko, hakuna taarifa zozote zilizotolewa na dakika kadhaa baada ya mtikisiko huo kuzidi. Walitoka wahudumu wa ndege ambao pia walikuwa na hofu na walianza kutoa maelezo ya hatari ambayo ndege yao ilielekea kukumbana nayo. Walieleza kuwa kila mtu asali kwa imani yake kwani ndege ilikuwa imepoteza mwelekeo kutokana na ukungu mzito uliokuwa umetanda angani. Taarifa hizo ziliwashtua abiria hao ambao kila mmoja alianza kufanya jambo lake, wengine walikuwa wakilia, wapo waliokuwa wakiomba pasipo kumaliza sala zao kutokana na hofu iliyokuwa imetanda. Kuna wengine walianza kuzunguka zunguka katika ndege hiyo ambayo haikuwa na raha tena kutokana na mtikisiko uliongezeka na kuwafanya watu wengine washikilie vizuri viti walivyokuwa wamekalia. Marubani wa ndege hiyo walikuwa wamechanganyikiwa baada ya ndege yao kupoteza mwelekeo walikuwa hawaelewi walichokuwa wakikifanya kutokana na ukungu uliokuwa umetanda angani. Katika harakati zao hizo za kujiokoa walishtushwa na mlima uliokuwapo umbali mfupi toka eneo walilokuwapo. Jambo hilo liliwaogopesha na waliishia kufumba macho baada ya kuamini haikuwezekana kuukwepa mlima huo wakiwa tayari kwa lolote ambalo lingetokea. * * * * Hali haikuwa shwari katika milima iliyokuwa eneo la jimbo la New Amsterdam nchini Guyana bara la Amerika ya kusini kwani kulikuwa na ajali mbaya ya ndege iliyokuwa imetokea katika eneo hilo. Askari wa jimbo hilo walitumia usafiri tofauti kufika katika eneo hilo lililozungukwa na misitu ambalo lilitumiwa zaidi na wawindaji. Hali iliyokuwapo eneo hilo ndiyo iliyowakatisha tamaa askari hao kwani kulikuwa na miili ya watu saba tu ambao walikuwa wameokolewa wakiwa wamejeruhiwa vibaya. Watu wengi walikuwa wamepoteza maisha katika ajali hiyo ya ndege iliyokuwa inabeba abiria zaidi ya mia moja ishirini. Askari waliwakimbiza hospitali watu walikuwa wamejeruhiwa vibaya na walikuwa wakiendelea kuwatafuta watu wengine na tayari miili ya watu zaidi ya sabini ilikuwa imepatikana. Ndege hiyo ilikuwa imesambalatika katika vipande vidogo vidogo na sehemu yake kubwa ilikuwa imelipuka kwa kuwaka moto. Mpaka jioni ya siku iliyofuata zoezi hilo liliendelea kuleta matuamaini japo kuwa watu wengi walikuwa wamepoteza maisha. Eneo ambalo ajali hiyo ilitokea lilikuwa halipitiki kirahisi kutokana na miti iliyokuwa imebanana sana jambo lililowachosha sana askari na kuamini huenda watu waliokuwa katika ndege hiyo tayari walikuwa wameisha. Ndipo walipohitaji orodha ya abiria waliokuwapo kwenye ndege hiyo iliyoonyesha zaidi ya watu saba walikuwa hawajapatikana. Taarifa za awali zilizofanywa zilieleza ndege hiyo ilipata ajali kutokana na ukungu ulikokuwa umetanda angani siku ya tukio. Siku tatu baadaye bado miili ya watu wawili ilikuwa haijapatikana na askari baada ya kuitafuta kwa muda mrefu walitoa tamko lao la kuamini miili hiyo ilikuwa imelipuka na sehemu kubwa ya ndege hiyo. Hatimaye zoezi hilo lilisitishwa na ndugu wa marehemu hao walianza kuwasili nchini Guyana ili kuitambua miili ya ndugu zao waliopata ajali katika tukio hilo lililojawa majonzi. Viongozi mbalimbali wa nchini Guyana walitembelea eneo la tukio lakini pia walikuwapo waliotembelea mochuari ya hospitali ya mji mkuu wa nchi hiyo wa Georgetown ambako miili yote ilihifadhiwa. Siku iliyofuata aliwasili mwanamke mmoja mzungu ambaye mara baada ya kujitambulisha aliongoza eneo ambalo kulikuwa na watu waliojeruhiwa katika ajali hiyo.Mara baada ya kumkosa mtu aliyemtafuta kati ya hao waliokuwa wamejeruhiwa alianza kutembea kwa haraka akielekea mochuari huku akilia, alionekana akiamini mtu huyo alikuwa miongoni mwa wale waliokuwa wamefariki. Mkononi alikuwa na picha ya ndugu yake huyo aliyekuwa akimtafuta, mara baada ya kufika mochuari alianza kuzunguka kila sehemu ambayo miili ya watu hao ilikuwa imehifadhiwa. Alizunguka kwa mara tatu lakini hakufanikiwa kumwona ndugu yake huyo jambo lililopelekea aanze kuonyesha picha ya ndugu yake aliyemtafuta lakini hakuna aliyemwona mtu huyo. Baada ya kuona jitihada zake zikigonga ukuta aliamua kuelekea katika kituo cha polisi ili kukutana na mkuu wa kikosi kilichotumika kutafuta miili ya watu hao waliopatwa na janga hilo la ajali ya ndege. Huko alijitambulisha kama Lashay na alieleza kuwa alikuwa akitokea Marekani, alidai alikuwa akimtafuta mwanafunzi wake aliyeitwa Geofrey James ambaye alikuwa safarini kuelekea Tanzania. Mara baada ya maelezo hayo askari aliyeongoza kikosi cha kuitafuta miili ya wahanga hao alitoa masikitiko yake akidai mtu huyo ni mmoja kati ya wawili ambao miili yao haikupatikana eneo la tukio.
Mara baada ya maelezo hayo askari aliyeongoza kikosi cha kuitafuta miili ya wahanga hao alitoa masikitiko yake akidai mtu huyo ni mmoja kati ya wawili ambao miili yao haikupatikana eneo la tukio. Hiyo ilitokana na taarifa ya majina waliyopewa na shirika la ndege iliyopata ajali na baada ya kufanya utambuzi wa miili waligundua Geofrey ni mmoja ya watu hao ambao hawakupatikana. Zaidi alitoa maelezo ya imani yao kuwa Geofrey alikuwa amepoteza maisha katika ajali hiyo ya ndege. Baada ya taarifa hiyo Lashay aliyeeleza kuwa alitokea shule ya American Academic School aliondoka katika kituo hicho cha polisi na kurudi katika hoteli aliyofikia katika jimbo hilo la Georgetown. Alikuwa na majonzi juu ya tukio zima la mwanafunzi wake Geofrey James aliyesoma katika shule yao ambaye alikuwa akirudishwa Tanzania kutokana na homa za mara kwa mara. Alikaa jimboni hapo kwa siku tatu akiamini huenda angepata taarifa za kupatikana kwa Geofrey lakini haikuwa hivyo, baada ya kuona hakuna dalili zozote za mafanikio aliamua kuanza safari ya kurudi Marekani. Mra baada ya kufika alitoa taarifa za kila kitu kilichokuwa kimetokea katika uongozi wa shule yao na taarifa za kuaminika alizozitoa zilieleza Geofrey alikuwa amefariki katika ajali hiyo ya ndege. Robert James pia alielezwa taarifa hizo alizozipokea kwa majonzi hali iliyopelekea aanze kulia muda wote akiwa shuleni hapo. Mwalimu wao Lashay ambaye awali James aliwahi kumkabidhi watoto wake ndiye aliyechukuwa jukumu la kumpeleka Robert nyumbani kwake akimfariji juu ya tukio hilo. Uongozi wa shule ulikuwa ukijaribu kufanya mawasiliano na James ambaye hakupatikana muda wote katika namba yake ya simu hali kadharika mkewe alikuwa hapatikani. Hatimaye waliamua Lashay aongozane na Robert kurudi Tanzania ili kutoa taarifa zilizohusiana na kifo cha Geofrey, mikakati yote ilifanyika na safari hiyo iliandaliwa. Siku husika ilipofika walianza safari ingawaje Robert kwa kiasi kikubwa alikuwa ametawaliwa na mawazo juu ya kifo cha kaka yake. Siku ya Jumatatu majira ya saa kumi na moja jioni Lashay alikuwa ameongozana na Robert wakitembea kutoka katika eneo la uwanja wa ndege wa mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Lashay alikuwa na mabegi kadhaa wakati Robert aliyeonekana mchovu na alikuwa hajabeba kitu, waliongoza hadi eneo la lililokuwa na teksi za kukodishwa na kupata moja wapo. Safari ilianza kuelekea nyumbani kwao maeneo ya Masaki ambako Robert aliyekuwa na miaka saba alikuwa akikukumbuka vizuri, wakati huo Lashay alikuwa akitizama mandhari ya Tanzania aliyokuwa akiisikia tu kupitia vyombo vya habari juu ya utajiri wake wa maliasili. Baada ya saa moja walikuwa nje ya geti la nyumba ya James ambalo lilifunguliwa baada ya kupigwa honi ya gari hilo walilokuwa nalo. Mara baada ya kuingia walishtushwa na kundi la watu waliokuwapo eneo hilo ambao walionekana walikuwa wakijadiliana jambo. Robert alishtushwa na kelele za vilio zilizompokea kutoka kwa majirani kadhaa na ndugu zake wachache aliowatambua ambao awali walikuwa wakiwatembelea nyumabni kwao. “jikaze mwanangu baba na mama wamepotea na hivi zimepita wiki mbili” aliongea mama mmoja aliyemtambua kama shangazi yake. Taarifa hizo zilimshtusha zaidi Robert ambaye alianza kulia kwa sauti na mwishoe aliishia kupoteza fahamu walimchukua na kumpeleka katika miti ya kupumzika iliyokuwa na kivuli na kuanza kumpepea. Mwalimu wake Lashay ambaye alikuwa ameongozana naye hakutambua chanzo cha kupoteza fahamu kwa Robert kwani hakuelewa kitu. Alikaribishwa na mwanamme wa makamo aliyejitambulisha kwa jina la Jackson ambaye alidai awali walimiliki pamoja na James kampuni ya JAJHO Company Limited. Alimweleza Lashay kila kitu kilichohusiana na mazingira ya kupotea kwa James akiwa na mkewe nchini Kenya. Zaidi alidai mchakato wa kutafutwa kwao ulikuwa ukiendelea, Lashay naye alieleza kuhusiana na kifo cha Geofrey aliyekuwa mtoto wa James. Jackson aliwatangazia watu wote waliokuwapo nyumabni hapo kuwa James aliyeaminika kuwa huenda alikuwa ameuawa na mkewe, pia mwanaye alikuwa amefariki katika ajali ya ndege iliyotokea nchini Guyana. Taarifa hizo ziliangua vilio vya watu waliokuwapo eneo hilo zaidi majirani ambao walimtambua vizuri mwanae huyo wa James. Siku tatu baadaye wakiwa wanaendelea kusubiri jitihada za vyombo vya habari na polisi ambao walikuwa na taarifa za kupotea kwa James, ndugu zake waligundua jambo lililowafanya waondoke nyumbani hapo kimyakimya. Waligundua Jackson aliyesimamia zoezi hilo la kutafutwa kwa James na mkewe ambaye pia alikuwa mmoja wa wamilikiwa JAJHO Company Limited alikuwa ni mtoto wa marehemu Mzee Samola aliyekufa kwa kunyongwa. Hisia za kulipizwa kisasi ziliwajia na hofu zaidi ilitanda juu ya uhai wao walimwacha Lashay aliyedai alihitajika kurudi Marekani na Robert ambaye ada aliyolipiwa ilikuwa ni ya miaka mitatu na zaidi msimu wa masomo ulikuwa haujaisha. Lashay alihisi jambo juu ya tukio hilo la ndugu zake na James kuondoka wakati taratibu za kumtafuta ndugu yao zikiwa bado zinaendelea. Siku iliyofuata hata majirani wachache ambao walikuwapo nyumbani kwa James kwa muda siku kadhaa wakisubiria taarifa zozote zilizomhusu na mkewe waliamua kuondoka. Jambo hilo lilimshangaza Lashay ambaye alibaki na Robert sambamba na wafanyakazi wawili waliokuwapo nyumbami hapo. Majira ya saa saba mchana Jackson alifika na watu kadhaa na kumwita Lashay kando na kumweleza kuwa jambo lililokuwa likifuata wakati huo ni uuzaji wa nyumba ya James. Alimweleza kuwa James alikuwa akidaiwa na kampuni yake ya JAJHO na kulikuwa hakuna njia nyingine ya kulipa deni hilo zaidi ya kuuza nyumba yake iliyokuwapo baada ya kupotea kwake. Zaidi alidai kuwa hata hati ya nyumba hiyo ilikuwa mikononi mwao kama dhamana ya deni alilokuwa nalo. Mnada wa nusu saa ulifanyika na nyumba hiyo iliuzwa, waliamriwa wahakikishe wametoka katika nyumba hiyo ndani ya masaa matano. Lashay alizidi kuchanganyikiwa na zaidi ni Robert aliyemshangaa mr Jackson kwa maamuzi yake, alikuwa akimtambua kama mjomba kutokana na biashara aliyofanya na baba yake lakini aligundua ukosefu wa utu wa mjomba huyo. Hilo lilitokana na kutowajalia kwani hakuzingatia ni wapi wangelala siku hiyo zaidi aliondoka na watu waliokuwa wamenunua nyumba hiyo wakiwa wamepewa agizo la kuondoka kwao. Lashay hakuwa na la kufanya zaidi ya kuchukuwa mizigo yake hali kadharika Robert alichukuwa mizigo yake. Aliamua kuwalipa wafanyakazi ambao walikuwa wakifanya kazi nyumbani hapo kwa James kwa vile walionekana kutokuwa na mwelekeo na jambo lililofuata hakujua kwani hakuwa na mawasiliano yeyote na ndugu zake James. Aliamua kupanga katika nyumba ya kulala wageni akiwa na Robert aliyekuwa amechanganyikiwa juu ya kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika familia yake. Lengo kubwa la Lashay lilikuwa ni kuvuta subira akiamini huenda James na mkewe wangepatikana. Baada ya kutopatikana mafanikio yeyote ndani ya siku tatu aliamua kuanza safari ya kurudi Marekani akiwa na Robert, hisia za mauaji dhidi ya James na mkewe zilianza kumwingia. Nafsi yake ilikuwa ikimtuma kuwa mtu ambaye huenda alihusika na mauaji hayo ni Jackson hiyo ilitokana na kukosa utu na kuonyesha ukatili wake waziwazi. Tayari aliingiwa na hisia akiamini alikuwa na kazi juu ya Robert ambaye hakuwa na msaada kwa wakati huo. * * * * Jeshi la polisi nchini Kenya lilikuwa na taarifa juu ya kupotea kwa watanzania wawili mtu na mkewe wakati wakiwa katika ziara yao binafsi. Taarifa hizo ndizo zilizowafanya polisi kadhaa waanze upelelezi juu ya tukio zima la kupotea kwa watu hao, wiki moja baadaye kulikuwa hakuna dalili zozote za kupatikana kwa watu hao jambo lililopelekea askari hao waachane na upelelezi wao. Wiki ya nne tangu kupotea kwa watu hao polisi walipata taarifa za kupatikana miili ya watu wawili kando ya mto Tana katika eneo la Burra ikiwa imeharibika vibaya. Taarifa za awali zilidai watu hao walikuwa ni mwanamke na mwanamme ambao walibakiwa na mifupa kwa kiasi kikubwa kutokana na muda mrefu waliokuwapo majini. Miili hiyo ilichukuliwa mpaka jijini Nairobi kwa uchunguzi zaidi, askari hao walituma taarifa kwa askari wa Tanzania wakihitaji vielelezo zaidi juu ya James na mkewe ambao walikuwa wakitafutwa hadi muda huo. Hiyo yote ilitokana na kutokuwa na taarifa zozote za kupotea au kuuawa kwa raia wa nchi hiyo, siku mbili baadaye walipokea vielelezo zaidi vilivyomuhusu James na mkewe na mwishoni uchunguzi ulibainisha kuwa watu waliouawa walikuwa ni wenyewe.
Siku mbili baadaye walipokea vielelezo zaidi vilivyomuhusu James na mkewe na mwishoni uchunguzi ulibainisha kuwa watu waliouawa walikuwa ni wenyewe. Taarifa hizo zilitumwa kwa jeshi la polisi nchini Tanzania juu ya James na mkewe waliopatika wakiwa wameuawa. Jeshi la polisi lilitoa taarifa kwa kampuni ya JAJHO juu ya kupatikana kwa mwili wa James na mkewe na liliwahitaji wahusike na taratibu zote za mazishi. Jackson alitoa taarifa kwa wazazi wa mke wa James akiwaeleza juu ya kupatikana kwa maiti ya mwanao lakini hakufanya hivyo katika familia ya James ambayo alielewa ilijua juu ya kila kitu kilichoendelea. Kitendo cha ndugu zake hao kuondoka bila kuaga katika nyumba ya James aliamini kilitokana na kugundua kwao ugomvi uliokuwapo baina ya familia zao mbili za marehemu mzee Kibudo na Samola ambaye alikuwa baba yake. Aliondoka na wamiliki wenzie wa kampuni sambamba na ndugu kadhaa wa mkewe James kwa usafiri wa ndege wakielekea jijini Nairobi. Lengo lake alihitaji ahakikishe James na mkewe wanazikwa nchini Kenya, japo kulikuwa na maswali mengi juu ya vifo hivyo lakini aliamini hakuna mtu ambaye angeliweza kutegua kitendawili cha vifo hivyo. Mara zote alionyesha huzuni juu ya tukio hilo lakini moyoni alikuwa na furaha kupindukia, alikuwa amefanikiwa kuwafukuza watu waliokuwapo nyumbani kwa James akiwamo mtoto wake. Alifanya hivyo akijifanya anaiuza nyumba hiyo kwani aliamini hakuna ndugu ambaye angethubutu kuifuatilia. Hilo lilijidhihirisha wazi kwani hata vyombo vya habari vilitangaza juu ya kupatikana mwili wa James na mkewe lakini hofu ya ndugu zake iliwafanya asijitokeze hata mmoja. Hatimaye walifika nchini Kenya na mara baada ya kuishuhudia miili ya James na mkewe walipewa kibali cha kuizika. Amos ambaye alikuwa miongoni mwa wamiliki ya kampuni yao alijifanya akitoa wazo la kuizika miili hiyo nchini humo. Alitoa mtazamo wake juu ya mazishi ya watu hao ambayo yalipaswa kufanyika katika kijiji cha James lakini hakuna ndugu yeyote aliyefika kwa ajili ya kufanikisha zoezi hilo. Hilo lilikuwa ni wazo lao toka awali na hawakutaka kurudi na miili hiyo nchini Tanzania wakihofia maswali mengi na zaidi uchunguzi ambao ungejitokeza. Waliwaeleza ndugu zake na mkewe James kuwa kampuni yao ilikuwa na matatizo ya kifedha wakati huo hivyo kupunguza gharama katika miili hiyo iliyokuwa ikizidi kuharibika waliomba waizike hapohapo nchini Kenya. Jambo hilo lilikubalika ingawaje kwa shingo upande na miili hiyo ilizikwa katika eneo walilopewa kibali cha kuzika. Jeshi la polisi lilidai kuwa liliendelea na uchunguzi juu ya watu waliokuwa wakihusika na mauaji hayo kwa namna moja au nyingine. Jackson na wenzie hawakuwa na hofu na walisisitiza kuwa walihitaji jeshi la polisi lifanye kazi yake kadri liwezavyo ili watuhumiwa wakamatwe. Walieleza hayo kwa vile walielewa hakuna mtu mabaye angeweza kutambua tukio zima la mauaji ya James na mkewe. Baada ya siku tano safari ya kurudi Tanzania kwa usafiri wa ndege iliandaliwa na siku iliyofuata walitakiwa kuwa safarini wakirudi. Jackson na wenzie waliona huo ulikuwa muda muafaka wa kumwachia kazi mr. Tyoso ambaye walishirikiana kufanikisha mauaji ya James na mkewe ili afuatilie zoezi la upelelezi huo. Walifanya hivyo katika hali ya kujihami lakini aslimia zote walizokuwa nazo waliamini hakuna mtu aliyeshuhudia mauaji hayo. Baada ya makubaliano hayo hatimaye siku iliyofuata walianza safari wakirudi Tanzania wakiamini hakuna jambo lolote ambalo lingeweza kujitokeza. Mr. Tyoso aliipokea kazi aliyopewa na wateja wake na kuwahakikishia kuwa siri hiyo isingeweza kuvuja. Kwa vile mtandao wake wa ujambazi ulikuwa mkubwa na alikuwa akishirikiana na askari kwa kiasi kikubwa aliamua kuongea na askari kadhaa ili wafuatilie kwa karibu kila kilichoendelea katika upelelezi huo. Kila siku nyakati za jioni alikuwa akiwapigia simu askari aliyokuwa amewaachia kazi hiyo na kuwauliza jambo lililokuwa likiendelea na hakupata taarifa yeyote iliyotoa hofu ya kuvuja kwa siri hiyo.Baada ya siku chache wakati upelelezi huo ukiendelea alisikia simu yake ikiita na aligundua mtu aliyepiga alikuwa ni askari aliyempa jukumu la kufuatilia kwa karibu upelelezi wa mauaji ulioendelea. Wakati huo ilikuwa yapata saa tano na nusu usiku “haloo mr. Tyoso kuna jambo limejitokeza mkubwa” alisikika askari huyo mara baada ya simu yake kupokelewa “jambo gani hilo?” aliuliza Tyoso kwa mshtuko “kuna mtu anadai ana filamu ya mauaji ya James na mkewe na ataileta kituo cha polisi kesho”. Baada ya kusikia hayo Tyoso alishtuka zaidi akiwa haamini juu ya jambo hilo aliloelezwa, alimwomba askari huyo afuatilie nyendo za mtu huyo haraka na zaidi alihitaji jina na namba yake ya simu. Alipatwa na mawazo ghafla na hakutaka kuwaeleza wateja wake juu ya jambo hilo lililokuwa linaendelea aliamini hakuna kitu ambacho kingeweza kufanikiwa. Aliwaza kuhakikisha filamu hiyo haifiki kituo cha polisi na zaidi mtu aliyekuwa na filamu hiyo alihitaji auawe kwa vile alikuwa na uwezo wa kuitoa siri hiyo muda wowote. Dakika kumi baadaye ujumbe mfupi wa maneno uliingia katika simu yake na mara baada ya kuusoma aligundua ulitoka kwa askari ambaye alikuwa amempigia simu. Alikuwa amemtumia namba ya simu na jina la mtu huyo aliyedai kuwa alikuwa na filamu ya mauaji aliyeitwa George Johnson. Bila kupoteza muda Tyoso alichukua simu yake na kumpigia mtu huyo akimweleza kuwa alikuwa askari wa upelelezi aliyehusika na uchunguzi wa mauaji ya James na mkewe. Alimweleza aliihitaji filamu hiyo ya mauaji usiku huo kwani ilikuwa ni muhimu sana kutokana na maagizo waliyopewa na mkuu wa upelelezi. Walielewana vizuri na baada ya Tyoso kuelekezwa eneo ambalo George alishi alianza kijiandaa kwa ajili ya kumfuata. Jambo kubwa alilolihitaji kwa mtu huyo ni uhai wake na kikubwa zaidi ni filamu aliyoelezwa ilikuwa na mauaji ya James na mkewe. Aliiandaa bunduki yake na kuweka risasi za kutosha akiamini jambo lilofuata lilikuwa ni mauaji, aliiweka katika koti lake kubwa alilovaa na kufanya mtu asiweze kugundua kirahisi kuwa alikuwa amebeba bunduki. Alivaa miwani yake iliyopoteza mwonekano wake wa sura na alipanda pikipiki yake na kuanza safari kuelekea eneo alilokuwa ameelekezwa. George alikuwa amepata taarifa zilizohusiana na kuokotwa kwa miili ya watu wawili waliokuwa wameuawa ambao aliamini taarifa zao alikuwa nazo kupitia filamu ya dakika ishirini na tano aliyofanikiwa kuipata katika mauaji hayo. Jambo lililomuogopesha ni ushauri ambao awali alipewa na mjomba yake kuwa asitoe siri kama hiyo akidai lazima angefanyiwa jambo baya. Baada ya kufikiria kwa siku kadhaa aliamua kufikia uamuzi wa kutoa siri hiyo, kufanikisha hilo siku moja majira ya saa nne usiku alipiga simu kituo cha polisi na kueleza juu ya filamu ya mauaji aliyokuwa nayo. Alielezwa aipeleke siku iliyofuta na masaa kadhaa baadaye aligiwa tena simu akielezwa filamu hiyo ingefuatwa usiku huo na mtu aliyekuwa askati wa upelelezi. Hakuwa na pingamizi juu ya jambo hilo alikuwa akimsubiri mpelelezi huyo aifuate filamu hiyo ya mauaji aliyoyashuhudia. Nusu saa baadaye mlango wa geti la nyumba yake aliyoishi peke yake uligongwa ilikuwa nyumba ambayo hata shughuli za uandaaji wa filamu alizifanyia humo mara baada kupiga picha sehemu tofauti. George alisimama na kuanza kutembea taratibu akielekea getini akiwa na imani kuwa mgeni aliyekuwa amegonga geti lake alikuwa askari mpelelezi. Mara baada ya kufungua geti mtu huyo aliingia akiwa na pikipiki yake na kuiegesha mbele ya nyumba hiyo ya George. “samahani kwa muonekano wangu, kazi hii inatuhitaji tuwe makini sana”aliongea mpelelezi huyo kama alivyo jitambulisha awali kwenye simu. “usijali karibu….” Ajibu George ambaye kwa kiasi alianza kuonyesha hofu na mgeni wake huyo. Mara baada ya kuingua ndani walianza kuongea mambo tofauti mbali na lile kubwa lililohusu filamu ya mauaji. Wakati huo mgeni wake alikuwa amevaa miwani ambayo haiku mwonyesha vizuri sura yake, baada ya dakika kadhaa mtu huyo alitoa miwani yake na sura yake ndiyo ilimuongeza hofu zaidi na kuanza kuingiwa na mawazo kuwa hakuwa askari. Alimfananisha na mtu mmoja ambaye alikuwapo kwenye tukio la mauaji ambayo aliyashuhudia kwa macho yake. Jambo hilo ndilo lilimfanya amuulize swali huku akiwa na uoga. “samahani askari kabla ya yote, naweza kukiona kitambulisho chako cha kazi?” aliuliza George ambaye hakujiamini.
“Samahani askari kabla ya yote, naweza kukiona kitambulisho chako cha kazi?” aliuliza George ambaye hakujiamini. Mtu huyo alisimama na kuelekeza mkono wake kwenye koti lake kubwa alilokuwa amevaa alitoa bunduki na kuielekeza kwenye paji lake la uso wa George ambaye alichanganyikiwa ghafla. “hiki ndiyo kitambulisho changu, sasa mimi siyo askari sihitaji chochote toka kwako zaidi ya kila kitu kinachohusiana na mauaji uliyoyashuhudia” alisikika mtu huyo akiwa ametoa macho. Kwa uoga George alianza kutembea mpaka kwenye chumba alichokuwa akiandalia filamu hizo na alikuwa akifuatwa nyuma na mtu huyo. Mara baada ya kuingia kwenye chumba hicho aliitoa filamu iliyokuwa na mauaji aliyoyashuhudia na kuikabidhi ikiwa imeandikwa juu yake ‘MAUAJI’. “bado sehemu gani nyingine kuna picha za hii filamu” alisikika mtu huyo kwa ukali na kumfanya George ampe kamera yake aliyokuwa akipigia picha akidai picha hizo hazikufutwa kwenye hiyo kamera. Mara baada ya kuchukua vitu hivyo alimumiminia risasi tatu George tumbomi na kumfanya aangue huku damu nyingi ikimtoka. Mtu huyo aliye jitambulisha kama mpelelezi ambaye hakuwa mwingine bali ni mr. Tyoso aliichukua kamera na filamu hiyo na kuviweka katika boksi moja lililokuwa na filamu nyingine. Mawazo yake yalimtuma akiamini kuwa filamu hiyo ilikuwa imehifadiwa sehemu nyingi hivyo ingekuwa ni rahisi kupatikana tena. Alizipiga risasi kompyuta tatu zote zilizokuwapo katika chumba hicho akiamini zilitunza filamu hiyo. Wakati akifanya hayo yote George alikuwa akitupatupa mikono na miguu baada ya kupigwa risasi, tayari damu nyingi ilikuwa imemtoka. Mr. Tyoso aliondoka kwa kasi eneo hilo la nyumba ya George akiwa na boksi alilobebea filamu zote alizoziona katika kile chumba pamoja na kamera. Aliendesha pikipiki yake akiamini alikuwa amefanikisha ushindi wa siri hiyo iliyokuwa inataka kuvuja. Jambo ambalo bado lilikuwa linamuumiza kichwa ni kuhusiana na filamu hiyo alihisi ilikuwa haihusiani na mauaji waliyokuwa wameyafanya. Kumbukumbu zake zilimpa aslimia chache na filamu hiyo jambo alilokuwa akilisubiria kwa hamu lilikuwa ni kuiona filamu hiyo kama ni kweli ilikuwa ikihusiana na mauaji waliyokuwa wameyafanya na wateja wake. Saa nane kamili usiku aliwasili nyumbani kwake na kabla ya yote alianza kuiangalia filamu hiyo, baada ya dakika tatu tu za kuiangalia alisikika akiongea peke yake “Mungu wangu alituonaje mbwa huyu” . Alishangazwa na filamu hiyo ambayo aligundua ilionyesha kila kitu walichofanya siku ya mauaji. Haraka aliamua kuanza kuangalia filamu nyingine ambazo nazo alikuwa amezichukua, alishuhudia sherehe za harusi na nyingine ikiwamo misiba na filamu moja ilikuwa ikionyesha vyura wa aina tofauti. Baada ya muda mfupi wa kuziangalia kwa haraka pasipo kumalizia aliigeukia kamera ambayo aliweza kukutana na picha nyingine za mauaji alizokuwa amezishuhudia. Aliichukua filamu hiyo pamoja na kamera kisha akavichoma usiku huohuo, hakutaka kubakia na kumbukumbu za mauaji hayo ambayo na yeye alihusika akihofia usalama wake na wateja aliowafanyia kazi hizo. Filamu nyingine aliziacha kwani aliona zilikuwa hazina jambo lolote la hatari kwa usalama wao mara baada ya zoezi hilo alichukua simu na kumpigia Jackson. Ilikuwa yapata saa tisa usiku lakini aliona umuhimu wa mteja wake huyo kujua jambo ambalo lilitaka kuwatokea. Alipongezwa sana kwa kazi hiyo aliyokuwa ameifanya zaidi Jackson alishtushwa na taarifa hizo za kuwa kulikuwa na mtu aliyewafuatilia siku ya tukio la mauaji waliokuwa wameyafanya. Alimuahidi Tyoso kumtumia fedha siku iliyofuata kama pongezi juu ya zoezi hilo alilokuwa amelifanya. * * * * Mzee Rogart alikuwa miongoni mwa raia masikini walioishi nchini Guyana, alikuwa mkazi a jimbo la New Amsterdam aliyefanya shughuli kuu ya uwindaji pembezoni mwa mlima ambao kulitokea ajali ya ndege. Katika maisha yake mzee Rogart alikuwa na mke na watoto wawili ambao walikuwa wamemkimbia miaka kadhaa iliyokuwa imepita, walimwacha porini huko kutokana na ugumu wa maisha ambayo hawakuyaweza. Mzee Rogart alikuwa wa kwanza kufika katika eneo la ajali hiyo ya ndege na kushuhudia ajali hiyo, jambo alilolifanya siku hiyo ya tukio alimckukua mtoto mmoja aliyekuwa amejeruhiwa vibaya kutokana na ajali hiyo na alimpeleka mpaka nyumbani kwake akiwa na lengo haswa la kumtibu na hatimaye aanze kuishi naye. Aliamini hilo lingewezekana kutokana na vifo vya watu wengi vilivyokuwa vimetokea eneo la tukio na aliamini mtoto huyo naye angedhaniwa alifariki. Alikuwa akihitaji kuwa na mtoto kwa vile mkewe na watoto wake wawili waliokuwa wamemtoroka, walimpa imani iliyomkaa kichwani kuwa hawangerudi tena. Alianza kumtibu mtoto huyo kwa majani ya porini ambayo aliyatambua kama dawa kutokana na maisha ya miaka mingi aliyokuwa akiishi porini huko. Wakati akifanya hayo kila siku alikuwa akienda eneo ambalo ajali ya ndege hiyo ilitokea na kujumuika na askari waliotafuta miili ya watu waliokuwa wamefariki. Hatimaye zoezi lao lilikamilika pasipo kugundulika kuwa alimwiba mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo. Alikuwa akiishi umbali wa kilometa zaidi ya saba toka eneo ambalo ajali ilitokea, muda wote alikuwapo nyumbani kwake akisubiri kwa hamu mtoto aliyekuwa amemwokota arudiwe na fahamu. Alikuwa amevunjika mkono na mguu akiwa amepatiwa matibabu ya kufungwa vizuri na miti midogo midogo iliyoenda sambamba na maeneo aliyokuwa amevunjika. Mtoto huyo pia alikuwa na majeraha mengi sehemu tofauti za mwili wake, suala lililomuumiza kichwa mzee Rogart lilihusiana na kuchelewa kuzinduka kwa mtoto huyo aliyekuwa na shauku ya kumfahamu. Alipunguza kasi yake ya uwindaji na muda mwingi alikuwapo nyumbani kwake hapo akihakisha mtoto huyo anakuwa salama. Hakufanikiwa kupata vielelezo vyovyote vilivyohusiana na mtoto huyo zaidi ya picha akiwa na wazazi wake ambazo alizipata kwenye begi pembeni kidogo ya eneo ambalo alimchukua. Baada ya siku nne tangu kuchukuliwa kwa mtoto huyo toka eneo la ajali hatimaye alizinduka akiwa anashangaa eneo alilokuwapo na mtu aliyekuwa na ndevu na nywele nyingi zenye mvi. Kilichomshangaza zaidi ni eneo hilo la porini ambapo pia nyumba aliyokuwapo ilijegwa kwa miti na kuezekwa kwa majani. Hakuna jambo ambalo walielewana na mzee Rogart aliyezungumza lugha ya Hindu zaidi waliweza kutambuana majina. Rogart alifurahishwa na kuzinduka kwa mtoto huyo aliyebaini alikuwa raia wa Tanzania ambaye pia aliitwa Geofrey, aliendeleza matibabu yote aliyokuwa akiyafanya kwa mtoto huyo na hatimaye alipona baada ya miezi mitatu. Tayari alianza kuifahamu lugha ya Hindu aliyokuwa akiitumia, mara kadhaa Geofrey alionyesha nia ya kutaka kurudi Tanzania ila alipoelezwa nchi ambayo walikuwapo alikatishwa tamaa kabisa. Hiyo ilitokana na imani aliyokuwa nayo kuwa ingekuwa vigumu kwake kuondoka eneo hilo na kumfanya aanze kujifariji kuwa hayo yalikuwa makazi yake mapya. Suala la shule lilikuwa limepotea kabisa kichwani mwake, ingawaje hakuwahi kutembea na kukutana na watu wengi zaidi ya wawindaji wachache waliokuwa wakikutana mara kadhaa porini. Chakula chao kikubwa ilikuwa nyama na wakati huo alikuwa mwindaji mzuri akishirikiana na mzee Rogart ambaye alimpenda sana. Hakuthubutu kuisahau familia yake na alikuwa akizitizama picha za familia yake hiyo kila siku akiwa anaamini miujiza pekee ndiyo iliweza kumkutanisha tena na familia yake. Baada ya miaka mitano akiwa tayari na miaka kumi na tano alikuwa amepata mambo tofauti kutoka kwa mzee Rogart aliyekuwa na historia iliyojaa mikasa. Moja ya mambo aliyoyatambua toka kwa mzee huyo ambaye miaka ya nyuma alikuwa jambazi wa kutisha lilihusiana na mauajia aliyowahi kuyafanya dhidi ya mke wa rais wa nchi hiyo ya Guyana. Alimweleza miaka kumi na tano iliyokuwa imepita mzee Rogart akiwa jambazi wa kutisha nchini humo alipewa jukumu na chama cha upinzani cha nchi hiyo cha DPG ‘Democratic Part of Guyana’ la kumuuwa rais wa nchi hiyo aliyeitwa Zakheem Pirjah. Alikubaliana na kazi hiyo baada ya kupewa fedha za kutosha na siku ya tukio alisababisha ajali iliyomuua mke wa rais. Msako mkali ulifanywa wa kutafutwa kwake na rais huyo ambaye mpaka wakati huo alikuwapo madarakani akitumia ubabe. Alidai wakati huo alikuwa na umri wa miaka arobaini na tano, hivyo baada ya kuona mambo yalikuwa magumu aliamua kukimbilia porini hapo akiwa na familia yake. Aliacha mazoea aliyokuwa nayo ya kunyoa nywele na muda wote alikuwa na nywele ndefu zilizopoteza mwonekano wa sura yake.
Aliacha mazoea aliyokuwa nayo ya kunyoa nywele na muda wote alikuwa na nywele ndefu zilizopoteza mwonekano wa sura yake. Aliishi na familia yake kwa muda mfupi porini hapo wakiwa hawajui mauaji hayo aliyoyafanya kwa mke wa rais zaidi ya vile walivyomtambua kuwa alikuwa jambazi. Baada ya kuona maisha ya porini yalikuwa magumu mkewe na watoto wake waliamua kuondoka na hawakuwahi kurudi tena porini hapo. Geofrey alishtushwa na historia hiyo ambayo mwishoe aliichukulia kama kitu cha kawaida kutokana na heshima aliyokuwa ameijenga kwa mzee Rogart akimchukulia kama mzazi wake. Muda wote wakiwa porini hapo katika shughuli za uwindaji walikuwa wakitembea na bunduki ambayo waliitumia siyo katika uwindaji tu bali ilitumika kama tahadhari ya usalama wa mzee Rogart aliyeamini rais wa nchi hiyo Zakheem alikuwa akimtafuta. Mara kadhaa pia walikuwa wakikumbana na wanyama wakali kama Simba hivyo waliitumia kujiokoa Walikuwa wakipata risasi kwa kununua kwa wawindaji wengine ambao walikuwa hawaishi porini huko na hivyo ndivyo walivyoendeleza maisha yao. Siku moja Geofrey aliondoka peke yake akimwacha mzee Rogart aliyekuwa na homa nyumbani hapo. Alikuwa akifuatilia mitego waliyokuwa wameitega dhidi ya swala na wanyama wengine hususani nguruwe pori ambao haswa walikuwa nyama yao kubwa wakiwa porini hapo. Akiwa ametembea umbali wa kilometa kadhaa toka nyumbani kwao alishtushwa na askari waliokuwapo eneo hilo ambao mara baada ya kumwona walianza kumfuata. Alikuwa amevaa bukta pekee na kuacha eneo la juu kuwa wazi zaidi alikuwa hajavaa hata viatu, begani alikuwa na upinde sambamba na mishale mingi aliyoishika katika mfuko mdogo aliokuwa nao. Alitaka kukimbia lakini alijipa ujasili, mawazoni alihisi watu hao walitaka kuwakamata kutokana na uwindaji waliokuwa wakiufanya. Askari hao walianza kumshangaa kwa jinsi alivyokuwa amevaa lakini yeye kwake lilikuwa jambo la kawaida kwa miaka yote aliyokuwapo porini hapo. Mara baada ya kumfikia walimsalimia kwa lugha ya Hindu na hatimaye walitoa picha wakiashiria kuwa walitaka kumwuliza jambo. Mara baada ya kumwonesha picha hiyo ambayo aligundua ilikuwa ya mzee Rogart moyo wake ulishtuka ingawaje hakuonyesha hali yeyote ya mshtuko. Walimuuliza kama alimfahamu mtu huyo au yeyote aliyefanana naye lakini aliwajibu alikuwa hamfahamu na hakuwahi kukutana naye porini hapo. Picha hiyo ilionekana ilichukuliwa miaka mingi wakati mzee Rogart akiwa hana nywele nyingi kama alizokuwa nazo wakati huo. Baada ya majibu hayo polisi hao waliokuwa sita waliendelea na msako wao dhidi ya mtu huyo, Geofrey aliamua kuacha zoezi lake la kufuata mitego waliyokwa wameitega na kuanza kurudi nyumbani. Mara baada ya kufika katika nyumba waliokuwa wakiishi alishtusha na moto mkubwa uliokuwa ukiwaka ukiwa umeshia nyumba yao. Pembeni kulikuwa na madumu ya mafuta aina ya petroli ambayo yalionekana kuteketeza nyumba hiyo. Alizunguka maeneo yote ya sehemu hiyo waliokuwa wakiishi akiwa naimani huenda mzee Rogart alikuwa ameuawa lakini hakubahatika kuiona maiti yeyote. Hisia za kuwapo kwa kundi kubwa la polisi msituni hapo zilimwingia na kuamini kuwa mzee Rogart alikuwa amekamatwa. Aliongeza mishale mingine na wakati huu aliamua kuchukuwa dawa ambayo walikuwa wakiipaka katika ncha ya mishale ambayo ilikuwa ikiwafanya wanyama wapate usingizi pindi wakiwa mawindoni. Dawa hiyo ya majani ilikuwa katika kikopo kidogo na ilikuwa ikiwasaidia kuwapata wanyama hata kama walichubuliwa kidogo na mishale. Hakuwa tayari kuishi porini bila mtu aliyemheshimu kama mzazi wake na mazingira aliyoyaona eneo la tukio aliamini askari hao hawakuwa mbali na mzee Rogart. Aliondoka kwa kasi ya ajabu ambayo ilikuwa ya kawaida kwake kutokana na shughuli hiyo ya uwindaji waliyofanya. Aliachana na njia ambayo awali alikuwa ametokea na kuanza kufuata njia nyingine na baada ya kukimbia kwa muda mfupi alifanikiwa kuyaona makanyagio ya viatu vya kiaskari na hapo imani ya kukamatwa kwa mr. Rogart ilimkaa zaidi kichwani. Akili yake ilimtuma kufanikisha hata mauaji ili kuhakikisha anampata mzee huyo, alikimbia umbali wa zaidi ya kilometa thelathini pasipo mafanikio ya kuwaona askari ambao aliamini walikuwa wamemkamata mzee Rogart. Alianza kuingia hofu ya kushindwa kufanikisha lengo lake la kumuokoa mzee huyo wakati huo ikiwa jioni, alianza kutembea taratibu akiamini zoezi hilo lilielekea kushindikana. Hofu ya kuuawa kwa mzee Rogart ilizidi kumkaa kichwani na aliamini rais Zakheem Pirjah wa nchi hiyo asingeweza kumwacha hata kidogo. Tayari giza liliingia na hakukuwa na dalili zozote za kuweza kufanikisha kwake kumwokoa mzee huyo. Akiwa bado anaendelea kutembea porini humo huku akiwa amekata tamaa kwa kiasi kikubwa alishtushwa na chanzo cha moto kilichotoa moshi karibu na eneo alilokuwa akitembea wakati huo. Hisia zake zilimtuma akiamini kulikuwa na jambo lililokuwa likiendela eneo hilo wakati huo, japo hakuwashuhudia watu waliokuwapo kwenye chanzo hicho cha moto lakini aliamini kuwa ndiyo waliohusika na kukamatwa kwa mzee Rogart. Alianza kusogelea taratibu eneo ambalo moto huo ulikuwa ukiwaka huku akijificha kwenye miti alitaka kuwaona watu waliokuwapo eneo hilo. Hatimaye alitulia sehemu na kuweza kuwaona vizuri lakini pia akishuhudia kila kitu kilichokuwa kikiendelea eneo hilo. Walikuwa askari wanne waliokuwa wamezunguka chanzo cha moto kutokana na baridi iliyokuwapo muda huo, akili yake kwa haraka ilimpa jibu kuwa hao ndiyo walihusika na kukamatwa kwa mzee Rogart. Jambo lililomtatiza hakuweza kumwona mzee huyo eneo hilo, akaanza kuzungusha macho kila upande akiwa na lengo la kuhakikisha kama alikuwapo eneo hilo. Baada ya muda mfupi alimwona mzee Rogart kwa umbali akiwa amefungwa kwenye kwenye mti mkubwa uliokuwa pembeni na eneo ambalo askari hao walikuwa wakiota moto. Geofrey alianza kufikiri jambo la kufanya baada ya kuamini kuwa huo ulikuwa wakati muafaka wa kumuokoa mzee Rogart. Alichuchumaa taratibu baada ya kugundua jambo la kufanya na baada ya kufanya hivyo alianza kutoa matawi ya miti ambayo yalikuwa mengi chini ya miti iliyokuwa imezuguka eneo hilo. Mara baada ya kuyatoa alipata shimo lililomwezesha yeye kuingia kwa kiasi kikubwa akiwa ameweka mishale yake na upinde pembeni kidogo na eneo alilokuwapo. Alikuwa amebakiwa na mishale mitatu na dawa ambayo ilileta usingizi pindi walipokuwa wakifanikiwa kuwadhuru wanyama. Mara baada ya kujihakikishia usalama wake akiwa na mshale mmoja ambao tayari ulikuwa na dawa kwenye ncha yake alianza kupiga kelele kama za paka. Alizipiga kelele hizo kwa sekunde kadhaa na kuwafanya askari waliokuwapo kwenye chanzo cha moto washtuke na kuanza kutazama eneo ambalo kelele hizo zilitoka. Waliacha mazungumzo yao waliyokuwa wakiyazungumza na kuanza kuangalia eneo ambalo kelele hizo zilitoka. Baada ya muda mfupi mmoja wao aliwaondoa shaka akiwaambia kuwa hakuna jambo lolote, walikaa tena chini na kuendelea na mazungumzo yao. Dakika mbili baadaye walizisikia kelele hizo zikiwa zimeanza tena jambo lililomfanya mmoja wao achukue bunduki yake na kuanza kutembea kuelekea eneo ambalo alisikia kelele hizo. Ghafla hakusikia tena kelele hizo lakini aliendelea kutembea akielekea eneo ambalo alikuwa amesikia kelele hizo zikitoka. Alitembea mpaka eneo la ndani toka sehemu iliyokuwa na chanzo chao cha moto lakini hakuweza kuona kitu na alibaki amesimama huku akiwa anacheka akiwaeleza wenzake kuwa hapakuwa na kitu. Wakati huo Geofrey alikuwa amejifukia chini katika matawi ambayo askari huyo alikuwa pembeni yake akiwaeleza wenzie, walikuwa katika eneo lililokuwa na giza mbali na eneo lenye chanzo cha moto. Alianza kwa kujitoa kichwa taratibu na mara baada ya kutoka vizuri kwa kasi alimchoma yule askari na mshale katika mguu wake wa kulia, kabla ya kuuchomoa mshale huo kwa haraka na kurudi tena katika shimo alilokuwapo. Askari huyo alipiga kelele akitupa bunduki yake pembeni na kuanza kujiviringisha kwa maumivu aliyokuwa akiyapata. Wenzake walitoka mbio eneo walilokuwapo na kwenda kumshuhudia damu zikimtoka katika mguu wake wa kulia, hisia alizozipata askari huyo alidhani ni nyoka jambo lililowafanya askari wenzie wambebe mpaka kwenye chanzo cha moto. Walianza kumpa huduma ya kwanza kwa kumfunga kamba eneo la juu na sehemu aliyokuwa amepata jeraha hilo. Wakati huo kwa kasi akijiburuza kama nyoka, Geofrey alitoka na kuelekea eneo alilokuwa ameweka mishale yake na upinde akiwa amebakiwa na mishale miwili pamoja na dawa aliyitumia katika zoezi hilo. / Geofrey alitoka na kuelekea eneo alilokuwa ameweka mishale yake na upinde akiwa amebakiwa na mishale miwili pamoja na dawa aliyitumia katika zoezi hilo. Alikimbia upande mwingine wa pembeni na kujilaza akiwa ameshaweka dawa ile iliyosababisha usingizi katika mshale mwingine na aliupachika kwenye upinde tayari kwa kuuachia. Alielewa kwa vyovyote vile watu hao wangerudi eneo lile kuangalia nyoka ambaye alikuwa amemdhuru askari mwenzao. Aliwasikia wakijadiliana jambo la kufanya huku wakiwa wamechanganyikiwa, hilo lilifuata baada ya kuona askari mwenzao akiwa amepatwa na usingizi wa ghafla. Walishauriana waendelee na safari ili wampeleke mwenzao hospitali, lakini umbali wa kilometa zaidi ya arobaini zilizokuwa zimebaki kuuacha msitu huo ndizo ziliwakatisha taama. Mmoja wao aliwaeleza wenzie kuwa rais Zakheem asingewaelewa hata kidogo endapo mzee Rogart angewakimbia, wakati huo mzee huyo aliangalia kila kilichoendelea.Baada ya makubaliano hayo waliona wabaki eneo hilo kutokana na hofu kubwa juu ya mzee Rogart waliyeamini hakuwa mtu wa kawaida kwa vile alitafutwa kwa miaka mingi pasipo kupatikana. Askari hao waliendelea kumpa huduma mwenzao aliyepatwa na usingizi wa ghafla wakiamini alikuwa ameg`atwa na nyoka. Baada ya muda mmoja wao alianza kutembea kuelekea eneo lililokuwa limetokea tukio hilo, mkono mmoja alibeba bunduki na mwingine alikuwa amebeba ukuni uliokuwa umeshika moto huku ukiendelea kuwaka. Mara baada ya kufika eneo hilo aliziona damu ambazo zilikuwa zimemtoka askari mwenzao na aliamini eneo hilo alikuwapo nyoka, aliendelea kuzungusha macho kila upande wa eneo hilo akijaribu kumtafuta nyoka huyo. Wakati huo kwa umbali mfupi katika eneo lililokuwa na giza Geofrey alimwona vizuri askari huyo aliyekuwa na ukuni wenye moto ulioangaza vizuri sehemu aliyokuwapo. Bila kuchelewa aliivuta kamba ya upinde wake iliyokuwa na mshale huku akiwa ameupima sawasawa akielekeza katika mguu mmoja wa askari huyo. Punde aliachia upinde huo ulioenda kutua sawasawa kwenye mguu wa kushoto wa askari huyo na ulizama kiasi cha kutaka kutoka upande wa pili wa mguu huo. Alitoka mbio na kuelekea upande mwingine uliokuwa karibu kabisa na eneo alilomwona mzee Rogart akiwa amefungwa. Askari huyo alipiga kelele na kutupa bunduki na ukuni uliokuwa na moto akiwa ameumia mguu wake na kuushuhudia mshale uliompata sawasawa. Kelele hizo ziliwashtua askari wenzie waliokimbia kuelekea eneo alilokuwapo na kumwona akiwa amedhuriwa na mshale huo. Askari mmoja alianza kumvuta kuelekea eneo ambalo lilikuwa na chanzo cha moto na mwingine alimua kuzima moto uliotaka kushika eneo hilo baada ya ukuni wenye moto kutupwa chini na mara baada ya kuzima alienda kuungana na mwenzake. Hisia za nyoka tena ziliwatoka kichwani mwao na walianza kuingiwa na hofu kubwa kuwa eneo hilo kulikuwa na adui, askari mmoja alianza kumpiga mzee Rogart akimshutumu alihusika na matukio hayo. Mara baada ya kumtoa mwenzao mshale na kupunguza kasi ya damu iliyokuwa ikimtoka wote wawili walishika bunduki zao wakiwa tayari kwa shari hiyo iliyoendelea. Muda mfupi mwenzao naye aliingia katika usingizi mzito, jambo hilo liliwachanganya na kuamini wenzao walikuwa wanakufa. Mzee Rogart alionekana kupata faraja kidogo moyoni akihisi huenda kuna mtu alikuwapo eneo hilo kumwokoa lakini bado alikuwa akihofia maadui zake kadhaa wa miaka mingi iliyokuwa imepita na kuwahusisha na tukio hilo lililokuwa likiendelea. Mawazo yake hata kidogo hayakumweka akilini kijana wake Geofrey aliyemchukulia kama mwanaye kuhisika na jambo hilo. Askari mwingine alimfuata kwa mara ya pili na kuanza kumpiga tena ngumi za tumbo akimtaka aseme mtu aliyehusika na tukio hilo. Wakati huo askari mwenzie alikuwa kwa mbali akizunguka eneo hilo akiwa na tahadhari kubwa ya usalama wake. Akiwa anaendelea kumpiga mzee huyo alishtushwa na mshale uliotua kwa kasi na kupenya sawasawa katika makalio yake na kumfanya aanze kupiga kelele kutokana na maumivu aliyoyapata. Bunduki aliyokuwa ameishika aliitupa chini na alianza kujivingisha kwa kelele za maumivu. Askari mwenzie aliyebakia kwa kasi alimfuata na kumvutia eneo walilokuwapo wenzake, aliingiwa na hofu ya ghafla na imani aliyoipata haraka ilimbainishia alikuwa katika hatari ya kupoteza maisha muda wowote.Akili yake ilikuwa haijatulia hata kidogo akiwa bado hajagundu jambo la kufanya askari huyo aliyejeruhiwa aliingiwa na usingizi kama wenzake. Jambo hilo lilimshtua askari huyo aliyekuwa amebakia akamua kutoka kwa kasi akikimbia kuondoka eneo hilo ambalo wenzake aliamini walikaribia kufariki. Aliongoza upande ambao walikuwa wakielekea na mzee Rogart na aliondoka bila hata kumsemesha jambo lolote akiwa na hofu kubwa. Mzee Rogart alikuwa bado katika mti aliokuwa amefungwa kando kidogo na chanzo cha moto huku hofu tele ikiwa imemjaa baada ya askari pekee aliyebakia kukimbia. Hofu yake ilitokana na mtu huyo aliyemwokoa alikuwa na lengo gani, zaidi aliamini hakuwa na mtu yeyote waliyefahamiana wakati huo ambaye angeweza kumsaidia. Kilichomtisha zaidi alikaa dakika kama kumi pasipo kuona dalili za mtu huyo akitokea, jambo hilo lilimtia hofu zaidi na alihisi na yeye mwisho wake ulifika. Akiwa na mawazo tele alishtushwa na mshale ulitoka kwa kasi ya ajabu upande wa mbele yake uliokuwa na giza na kutua juu kidogo na kichwa chake katika mti huo aliokuwa amefungwa. Hofu yake iliongezeka na hali ya ketetemeka ilifuata alipogeuza kichwa chake kuutazama mshale huo alishuhudia wote ukiwa umezama kwenye mti. Jambo hilo lilimfanya mzee huyo aanze kulia peke yake, baada ya kuanza zoezi hilo la uoga alishtushwa kumuona Geofrey akitoka katika eneo hilo la miti lililokuwa na giza huku akicheka juu ya hofu aliyoionyesha. Mzee Rogart hakuamini macho yake baada ya kugundua aliyekuwapo eneo hilo alikuwa ni Geofrey, aliacha kulia akiwa tayari ametokwa na machozi. Alimfungua haraka kabla ya kukumbatiana kwao, akili yake ilimrudia kichwani mzee Rogart na kuamini kuwa kila kitu alichokiona kilifanywa na mwanae huyo ambae alimtambua kwa uhodari wa kutumia upinde na mishale. Alikuwa hakosi pindi wakiwa katika shughuli zao za uwindaji, kila mshale siku zote ulikuwa lazima umpate mnyama. Walichukua bunduki zote nne za askari hao ikiwamo na ile ya askari aliyekimbia eneo hilo baada ya kuingiwa na hofu ya kuuawa walianza kukimbia kwa kasi kurudi eneo ambalo lilikuwa na makazi yao. Lengo lao kubwa lilikua ni kwenda kupanga na kujua jambo ambalo lingefuata wakati huo. Mzee Rogart ambaye alikuwa na umri wa miaka sitini alikuwa akijitahidi kukimbia kama vile alikuwa kijana mdogo ukimlinganisha na Geofrey. Tayari ilikuwa imegundulika kwamba waliishi porini na agizo la kukamatwa kwa mzee Rogart lilikuwa limetoka kwa rais wa nchi hiyo Zakheem Pirjah akiwa na machungu juu ya kifo cha mkewe miaka kadhaa iliyokuwa imepita. Rais huyo alionekana alihitaji kwa hamu Rogart akamatwe akiwa hai na lengo lake lilionekana kuwa alihitaji kumuua ili kulipiza kisasi katika kifo alichomsababishia mkewe. Majira ya saa kumi usiku wakikuwa wamefika eneo waliloishi huku wakiwa wamechoka sana na eneo hilo lilikuwa limeungua lote kiasi cha kukosekana kwa mabaki hata kidogo. Hiyo yote ilitokana na miti iliyotumika kuijengea nyumba hiyo na zaidi mafuta ya petroli ambayo askari waliyatumia kuichoma. Mzee Rogart alimweleza Geofrey kuwa alihitaji waelekee jimbo la Linden lililokuwa eneo la kusini mwa nchi hiyo ya Guyana. Mawazo yake yalikuwa ni kwenda kutafuta msitu mwingine katika jimbo hilo ili wakaendeleze maisha yao kama ilivyokuwa awali. Hakukuwa na pingamizi kutoka kwa Geofrey ambaye muda wote alimsikiliza mzee huyo aliyemchukulia kama mzazi na alikuwa tayari kufanikisha lolote ili apone. Kilichomuuma sana ni kuungua kwa kumbukumbu ya picha zake za familia alizokuwa akitembea nazo siku zote. Ila alifarijiwa na mzee huyo aliyempa imani kuwa siku moja lazima angerudi Tanzania kuwaona wazazi wake. Waliamua kulala eneo hilo ambalo lilikuwa na joto kutokana na moto uliounguza nyumba yao wakiwa wanapumzika baada ya kukimbia kwa muda mrefu. Siku iliyofuata waliamka majira ya saa tatu asubuhi na walikuwa na hofu wakihisi muda wowote askari waliotumwa na rais wangerudi tena eneo hilo.
Siku iliyofuata waliamka majira ya saa tatu asubuhi na walikuwa na hofu wakihisi muda wowote askari waliotumwa na rais wangerudi tena eneo hilo. Walianza kujiandaa kama walivyokuwa wamepanga kuondoka eneo hilo, kulikuwa na shati moja ambalo lilikuwa la mzee Rogart lililokuwa limechakaa sana ndilo alimpa alivae Geofrey. Shati hilo lilikuwa nje ya nyumba hiyo hivyo halikuungua katika janga la moto, alimpa kwa vile hakuwa na mazoea ya kuvaa shati akiwa porini hapo. Wote walikuwa katika mavazi duni kwani hata mzee Rogart alikuwa amevaa shati lililokuwa limechakaa sana na suruali iliyojaa viraka zaidi walikuwa hawavijui viatu. Mtu wa kawaida angewachukulia kama watu waliokuwa masikini wa kupindukia, walianza kutembea kwa tahadhari kubwa wakielekea eneo la kusini mwa eneo hilo walilokuwapo ambapo walipanga kuelekea jimbo la Linden. Mzee Rogart alikuwa amebeba bunduki tatu zilizokuwa na risasi, wakati Geofrey alikuwa amebeba upinde na mishale mingi iliyokuwa kwenye mfuko wake lakini pia hakuacha dawa aliyoitumia ambayo ilisababisha usingizi. Moyoni kwa kiasi alikuwa na furaha kwani alikuwa amelichoka eneo hilo alilokuwa ameishi kwa miaka kadhaa. Walikuwa wakiongea mambo tofauti ya hapa na pale wakati wakiendelea kutembea kwa kasi lengo likiwa ni kupunguza umbali wa msitu huo uliokuwa mkubwa. Majira ya saa kumi na mbili jioni walikuwa wametembea umbali wa kilometa nyingi wakiwa wamekutana na wawindaji wachache pasipo kuwaona askari. Bunduki moja kati ya tatu walizokuwa nazo walibadilisha na chakula kwa wawindaji waliokutana nao ambao walikuwa wakitokea makwao. Kubadilisha vitu wakiwa porini hapo lilikuwa jambo la kawaida kwani wawindaji wachache waliokuwa wakitokea vijiji vya karibu walikuwa na mazoea ya kuweka kambi porini kwa muda na baada ya kuwanasa wanyama walikuwa wakirudi katika vijiji vyao. Njiani walikuwa wanakutana na wanyama ambao wengine walikuwa wakali ili kutokana na uzoefu wao walikuwa wakiwafukuza wasiwadhuru. Hatimaye wakati wa nyakati za jioni walifika katika eneo waliloamua kulala lilikuwa pembezoni kidogo na mto mdogo wa maji, walikuwa wamechoka sana na malengo yao yalikuwa ni kuhakikisha siku iliyofuata wanatoka katika msitu huo. Waliamua kukata miti na kuikusanya sehemu moja lengo lao likiwa ni kuzuia upepo na baridi vilivyokuwapo eneo hilo. Mara baada ya zoezi hilo walianza kula chakula walichokuwa wamepata kwa wawindaji, walipokamilisha zoezi hilo walilala wakisubiri safari yao iendelee siku iliyofuata. Muda wote wakati mzee Rogart akiwa amelala Geofrey alikuwa hapati usingizi, mara kadhaa alisinzia lakini alirudi katika hali yake. Mkononi alikuwa na upinde na mshale alivyoviweka sawa kwa shari muda wowote, hakuwa na amani ya kulala na hakumshangaa mzee Rogart kwani aliamini mzee huyo alikuwa amezeeka baada ya harakati kama hizo wakati wa ujana wake. Majira ya saa sita usiku akiwa amesinzia kwa muda mfupi alishtushwa na miale ya tochi aliyoiona kwa mbali upande wa mbele walikoelekea baada ya kuvuka mto mdogo uliokuwapo. Jambo hilo lilimpa shauku ya kutaka kujua mwanga huo ulikuwa ukitolewa na nani. Wawindaji wachache aliwafahamu hawakuwa na mazoea ya kutumia tochi pasipo kumwamsha mzee Rogart alitoka mbio akiwa na upinde sambamba na mishale yake akielekea eneo alilouona mwanga huo. Hatimaye aliukaribia mwanga huo na taratibu alianza kusogea akijificha kwenye miti akiwa na lengo la kuwona wau ambao walikuwapo eneo hilo. Aliziona tochi kadhaa zikiwa zimeegeshwa maeneo tofauti ya eneo hilo lililokuwa na mahema lakini pia aliwaona askari wakizunguka zunguka eneo hilo wakiwa na bunduki zao. Hisia za msako uliokuwa ukiendelea zilimjia kichwani na aliamini askari hao walikuwa wengi. Akili yake iliona huo ulikuwa muda muafaka wa yeye na mzee Rogart kuondoka eneo hilo ili kuokoa uhai wao, taratibu alianza kuondoka eneo hilo na alipofiaka umbali mrefu alikimbia kwa kasi akirudi eneo walilokuwa wamelala. Alipofika eneo hilo alishtuka baada ya kuona sehemu aliyokuwa amelala mzee Rogart ikiwa wazi hata bunduki zake hazikuwapo, hofu ilimwingia akiamini tayari mzee huyo alikuwa amekamatwa. Alibaki ametulia akiwa hana jambo la kufanya, baada ya dakika kadhaa alishtushwa na sauti ya mzee Rogart akimwita ambaye naye alionekana alitokea sehemu ambayo ilikuwa na askari hai. Alifurahi kumwona mzee huyo na walikubaliana safari iendelee usiku huo kwani eneo hilo lilikuwa tayari na matatizo. Walibeba vitu vyao vichache na waliendelea na safari yao wakiwa wamechoka lakini waliamini kupona kwao kulikuwa bora zaidi kuliko kitu kingine. Siku iliyofuata majira ya saa sita mchana waliweza kutoka katika barabara kuu iliyoelekea jiji la New Amsterdam na mwishoe jimbo la Georgetown. Walificha silaha zao pembeni kidogo na barabara na walianza kusimamisha magari tofauti yaliyopita eneo hilo yaliyoelekea Linden walikopanga kuelekea. Magari mengi yalisimama ila baada ya kuwaona watu hao na hali zao kiujumla madereva walikuwa wakiingiwa hofu na kukataa kuwapa msaada. Hata magari ya abiria yaliposimama yalikataa kuwachukuwa wakiamini huenda walikuwa majambazi, watu wengi walimshangaa zaidi Geofrey kwa vile alikuwa mwafrika na zaidi katika mavazi machafu. Hofu yao pia ilikuwa kwa mzungu mwenzao mzee Rogart aliyekuwa na ndevu pamoja na nywele nyingi vyote vikiwa na mvi lakini pia sura yake ilikuwa haionekani vizuri kutokana na nywele hizo. Baada ya kukaa barabarani hapo pasipo kupata msaada kwa zaidi ya saa zima huku wakiwa na hofu ya kukamatwa wakiwa eneo hilo, mzee Rogart alitoa ushauri wa kufanya unyan`ganyi wa gari ili waweze kuondoka eneo hilo. Alielekea katika kichaka kilichokuwa pembeni kidogo ya barabara na kutulia na bunduki yake akiwa amemwacha Geofrey ajaribui kuendelea kusimamisha magari ambayo yangepita eneo hilo. Magari mengine yalikuwa hayasimami na baada ya muda mfupi gari moja lilisimama lilokuwa la kutembelea, teski aina ya Toyota. Alikuwamo kijana mmoja ambaye baada ya kuelezwa kuwa walihitaji msaada alipuuza akiimhofia kwani hata kioo alishusha kidogo alianza kulisogeza gari lake barabarani tayari kwa kuendelea na safari. Geofrey alibweka kama mbwa ishara iliyomtoa mzee Rogart kwa kasi kichakani na kuelekezea bunduki yake eneo la mbele la uskani ambapo dareva huyo alikuwapo. Alimuamru ashuke haraka jambo ambalo alitekeleza, wakati huo Geofrey alianza kupakia upinde na mishale yake na bunduki nyingine aliyokuwa nayo mzee Rogart kwenye gari hilo ambavyo walikuwa wamevificha pembezoni mwa barabara. Mara baada ya zoezi hilo mzee Rogart alimweleza kijana aliyekuwa na gari hilo aanze kukimbia bila kugeuka kurudi na barabara sehemu aliyokuwa ametoka. Alitekeleza jambo hilo akiwa na hofu huku akiamini watu hao aliowachukulia kama majambazi wangemuua, alitoka mbio akitekeleza masharti hayo. Mzee Rogart aliamini kazi ilikuwa imeisha aliingia kwenye gari na kulitoa kwa kasi eneo hilo akielekea upande wa jimbo la Linden, alikuwa na uzoefu mkubwa wa kuendesha magari hiyo ilitokana na enzi za ujana wake akiwa jambazi mkubwa. Geofrey alikuwa haamini kilichoendelea zaidi alifurahishwa na gari hilo, alikumbuka mara ya mwisho kupanda gari ilikuwa wakati ambao alisindikizwa na mwalimu wake wa American Academic School katika uwanja wa ndege wa Washington. Hakuwahi kupanda tena gari kwa zaidi ya miaka sita aliyokuwepo porini na mzee Rogart. Alikimbiza gari lao huku wakiwa na imani ya kufika jimbo la Linden baada ya masaa machache. Muda wote wakiwa kwenye gari walikuwa wakizungumza mambo tofauti zaidi walijisifia kwa kuukwepa mkono wa askari waliowafuata porini. Wakiwa wamebakiwa na kilomita kadhaa ili wafike katika jimbo hilo, walishtushwa na gari la askari lililokuwa likija nyuma yao kwa kasi na hisia zote za kukamatwa kwao zikawaingia. Furaha waliyokuwa nayo iliwaishia ghafla na mzee Rogart aliongeza kasi ya gari lao akiwa na hofu. Dalili zote za kukamatwa kwao zilianza kuonekana na tayari kulikuwa na vipaza sauti vilivyotumiwa na askari hao waliowataka wasimamishe gari lao. Baada ya muda mfupi huku wakiwa hawatii amri hiyo ya askari walifika aktika eneo la mpaka lililotenganisha jimbo la Linden na lile la New Amsterdam eneo ambalo lilikuwa na askari wengi na geti lake lilifungwa kutoruhusu gari lolote kupita kwa wakati huo.
Baada ya muda mfupi huku wakiwa hawatii amri hiyo ya askari walifika aktika eneo la mpaka lililotenganisha jimbo la Linden na lile la New Amsterdam eneo ambalo lilikuwa na askari wengi na geti lake lilifungwa kutoruhusu gari lolote kupita kwa wakati huo. Mzee Rogart alisikika akiongea kwa machungu akimweleza Geofrey kuwa wakati wake wa kuishi ulikuwa umeisha. Jambo hilo lilimfanya Geofrey aanze kulia kwa uchungu akiwa hayuko tayari kutenganishwa na mzee huyo. Mwishoe aliamua kusimamisha gari hilo wakiwa umbali mfupi na geti hilo, alianza kwa kumshukuru Geofrey akiamini asingepewa adhabu kama ambayo angepewa yeye ambayo aliamini ilikuwa ni kifo. Baada ya muda mfupi mzee Rogart akiwa hajaongea mambo aliyotaka kumweleza Geofrey, tayari kundi la askari walikuwa wamelizunguka gari lao wakiwa wamewaelekezea bunduki zao wakiwaambia watoke. Mzee Rogart na Geofrey walitekeleza amri hiyo na wote kwa pamoja walitoka wakiwa wamenyoosha mikoni juu, askari waliwafunga pingu kila mmoja na walipakizwa katika gari tofauti kabla ya kuanza kuondoka gari hizo za polisi eneo hilo. Siku iliyofuata vyombo vya habari nchini Guyana vilitawaliwa na habari za kukamatwa kwa jambazi sugu aliyetafutwa kwa zaidi ya miaka kumi na tano pasipo kupatikana. Zaidi vilielezea kuwa mtu huyo ndiye aliyesababisha ajali iliyopelekea kifo cha mke wa rais bwana Zakheem Pirjah. Magazeti tofauti yalichapisha picha ya mzee Rogart akiwa na kijana aliyeishi naye porini aliyekuwa mwafrika. Mwonekano wa mavazi yao na jinsi walivyokuwa vilikuwa kivutio kwa raia wa nchi hiyo walionunua magazeti wakihitaji kujua habari zao zaidi. Tayari kesi dhidi yao ilifunguliwa wakati Geofrey akiwa na kosa la kufanya unyan`ganyi wa gari pamoja na kuishi na mtuhumiwa huyo. Geofrey hakuwa na shaka sana juu ya hukumu ambayo ingeenda kutolewa ila alimwonea huruma mzee Rogart akiamini kesi yake ilikuwa kubwa ambayo usalama wake ulikuwa mdogo. Kilichompa shaka zaidi ni vile muda akiwa anashikiliwa na askari katika kituo cha New Amsterdam hakuelewa kituo ambacho mzee Rogart alikuwapo. Siku yake ya kesi alipelekwa mahakamani na baada ya kukubali makosa yake alihukumiwa kwenda jela kwa miaka mitatu. Geofrey aliumia kufuatia adhabu hiyo na aliona mpango wa kurudi Tanzania kuiona familia yake ulikuwa unapotea kabisa. Kichwani aliingiwa na imani ya kuwapo nchini Guyana kwa miaka mingine zaidi ya mitano, kwani alielewa mara baada ya kutoka jela alipaswa atafute fedha kwa ajili ya nauli kurudi Tanzania. Askari walimchukuwa tayari kwa safari akiwa na wafungwa wenzie kuelekea katika gereza kubwa lililokuwapo kusini mwa nchi hiyo katika jimbo la Biloku. Safari ilianza wakiondoka mahakamani hapo akiwa pia haelewi mahali ambapo mzee Rogart alikuwapo zaidi alikuwa hajui kesi yake ilikuwa ikisomwa siku gani. Ndani ya gari hilo la magereza alikuwa mwafrika peke yake na alitulia pasipo kuongea na mtu ingawaje wenzie wachache walikuwa katika maongezi. Mawazo yake alikuwa ameyarudisha nchini Tanzania akiwa anaikumbuka familia yake. Siku zote alikuwa akiamini familia yake ilimtambua kuwa alikufa katika ajali ya ndege na hilo ndilo lililokuwa likimpa hamasa ya kutaka kurudi nchini Tanzania. Hatimaye walifika gerezani na aliweza kukutana na wafungwa weusi kama yeye kadhaa ambao walikuwa rafiki zake. Gereza hilo lililokuwa na taabu nyingi lakini kwake aliona kila kitu kilikuwa sawa kwa vile maisha aliyokuwa akiishi porini yalikuwa magumu zaidi. Baada ya wiki moja alipata taarifa kutoka kwa wafungwa kadhaa waliokuwa wakiingia gerezani hapo baada ya hukumu zao ambao walimweleza kuwa mzee Rogart alifariki kwa maradhi siku moja kabla ya hukumu yake. Geofrey alilia kwa uchungu juu ya taarifa hizo lakini pia hakuamini kama ni maradhi yalipelekea kifo chake, kichwani mwake aliaminii kifo hicho kilipangwa na rais wa nchi hiyo bwana Zakheem Pirjah. Wafungwa gereza hilo walikuwa wanamwogopa sana Geofrey, kwani kwa muda mfupi alifahamika kutokana na jitihada zake za kuwasaidia wafungwa waliokuwa wanaonewa. Alikuwa na mwili wa kawaida lakini alikuwa tayari kupigana na mfungwa yeyote aliyekuwa mkorofi na kumpiga. Baada ya miezi sita Geofey alizoea zaidi mazingira ya jela na hakuwa na imani kama angemaliza muda wake na kuondoka eneo hilo. Alijifunza kusahau kurudi Tanzania na zaidi juu ya kifo cha mzee Rogart, siku moja akiwa anaendelea na kazi za shambani gerezani hapo alishtushwa na kauli ya askari aliyemweleza kuwa alikuwa na mgeni. Geofrey alimkabidhi mfungwa mwenzie jembe alilokuwa akilitumia na aliongozana na askari magereza kuelekea chumba cha wageni. Hakupata picha juu ya mtu aliyefika gerezani hapo akiwa na nia ya kutaka kumwona, hiyo yote ilitokana na vile alivyokuwa akiamini jambo hilo lilikuwa gumu akiwa gerezani hapo. Mara baada ya kufika katika chumba hicho cha wageni alimwona msichana mmoja mrembo aliyeonekana alikuwa na mchanganyiko wa damu ya kiafrika na ya kizungu akiwa amekaa katika mojawapo ya kiti kilichokuwapo. Akili yake kwa haraka ilimtuma akiamini mtu huyo hakumfuata yeye, hata siku moja hakuwahi kuingiwa na fikra juu ya ujio wa mtu kama huyo aliyevutia kwa mwonekano. Alibaki kimya akimsikiliza askari amwekekeze kuhusu mgeni wake na wakati huo alihisi mgeni huyo alikuwa nje. Askari huyo alimweleza Geofrey akimwonyesha kwa kidole msichana aliyekuwa ameshangazwa naye kuwa ndiye mgeni wake, alimpa dakika kumi za maongezi. Alianza kutembea kuelekea katika meza ambayo msichana huyo alikuwa amekaa, hatimaye alifika na kuketi katika kiti cha upande wa pili akitazamana uso kwa uso na msichana huyo huku wakitenganishwa na meza ndogo.Kabla hajaongea kitu alishangazwa kuona msichana huyo akimsalimia kwa lugha ya kiswahili ambayo hata askari aliyekuwapo pembeni kidogo hakuielewa. “Geofrey mambo, mzima?” alisikika msichana huyo mara baada ya kuketi kwake “mimi mzima sijui wewe” alijibu Geofrey akiwa hajiamini na zaidi alikuwa hajaitumia lugha hiyo toka aingie nchini hapo Guyana. Msichana huyo alianza kwa kujitambulisha kuwa aliitwa Magreth na alikuwa raia wa nchini Tanzania, alimweleza kuwa alikuwapo nchini humo Guyana kwa vile baba yake alikuwa balozi wa Tanzania nchini humo. Aliendelea kumweleza jinsi alivyomfahamu Geofrey kupitia vyombo vya habari baada ya kukamatwa kwake jambo lililomfanya apange siku moja kumtembelea gerezani hapo. Alihitaji kufahamu juu ya mkasa uliomfika Geofrey mpaka alikuwa gerezani hapo akidai kuwa aliwajali waafrika wote waliokuwapo nchini humo. Muda wote wakati Magreth akisimulia hayo kuna jambo alilokuwa ameligundua ambalo tayari lilianza kuwa kikwazo moyoni mwake. Baada ya maelezo hayo mafupi ambayo Geofrey aliyaelewa alianza kumsimulia mkasa wa mambo yote aliyokutana nayo hadi wakati huo akiielezea pia familia yake. Muda wote akimsimulia, Magreth alipatwa na uchungu akionyesha dalili zote za kutokwa na machozi. Akiwa anaendelea kumwelezea, askari magereza aliyekuwa kando ambaye pia hakuelewa walichoongea alimweleza Geofrey kuwa muda uliisha, alisimama tayari kwa kurudi tena kwa wafungwa wenzie. “ahsante dada Magreth kwa kunijali..” alisikika Geofrey akiwa na anavutwa na askari huyo. “usijali kuna chakula nimekuletea watakupatia, lakini pia nitarudi siku nyingine uumalizie mkasa wako” alisikika Magreth akiwa na huzuni akimweleza Geofrey aliyeanza kuondoaka eneo hilo na hakujibiwa. Kichwani alipata hisia za ugumu wa maisha ya Geofrey ingawaje alimsimulia mpaka wakati anaokotwa kwenye ajali ya ndege na kwenda kuishi na mzee Rogart. Mbali na huzuni aliyokuwa nayo Magreth alishtushwa na hisia zake za ghafla juu ya Geofrey, alimhitaji awe mwanamme wake wa ndoto. Alikuwa ameishi kwa miaka mingi nchini humo Guyana lakini hakuwahi kuwapo katika mahusiano, jambo hilo lilimshangaza kuona alivutiwa na mtanzania mwenzake aliyekuwa gerezani. Geofrey alikuwa tofauti na yule aliyemwona kwenye vyombo vya habari siku anakamatwa, kwa vile alikuwa mwanamme aliyevutia. Baada ya kuelezwa kuwa chakula alicho mpelekea angekipata aliondoka gerezani hapo na kuelekea uwanja wa ndege kwa safari ya kurudi jimbo la Georgetown ambalo alikuwa akiishi na familia yake. Mara baada ya kufika nyumbani kwao hakumweleza mtu juu ya zoezi alilolifanya la kumtembelea mfungwa wa kitanzania. Jambo lililomkaa kichwani mwake na kutawala mawazo yake lilikuwa juu ya mfungwa huyo, hakuelewa sababu iliyopelekea jambo hilo. Siku tatu baadaye aliondoka nyumbani kwao na kusafiri tena kurudi jimbo la Biloku lengo kuu likiwa kwenda kukutana na Geofrey ili amumalizie mkasa wake lakini zaidi alikuwa amemkumbuka kupita kiasi. Kama ilivyokuwa awali alifanikiwa kupata nafasi ya kuongea naye ingawaje Geofrey alishtushwa na bahati aliyoipata ya kutembelewa tena zaidi alishukuru juu ya chakula alichokipata. Hatimaye alimumalizia mkasa wake na kumfanya Magreth akose raha akiwa hana njia ya kumsaidia lakini alimweleza kuwa angejaribu kwenda kufanya jitihada za kuwatafuta wazazi wake Geofrey. Alimweleza kuwa angempa mtu jukumu kutoka Tanzania ili awatafute jambo ambalo alifurahi kulisikia. Hatimaye Magreth aliondoka na kuanza kurudi nyumbani kwao, akiwa na furaha ya kumwona Geofrey wakati lengo lake likizidi kujengeka zaidi moyoni. Wakati huo alikuwa akisoma chuo kikuu cha Guyana akisomea udaktari na alikuwa katika likizo fupi. Tayari alikuwapo nchini humo na wazazi wake kwa zaidi ya miaka saba, mama yake alikuwa na asili ya Uingereza wakati baba yake alikuwa mtanzania akiwa balozi nchini humo kutoka Tanzania. Mara baada ya kufika nyumbani kwao alimpigia simu rafiki yake wa karibu aliyekuwapo nchini Tanzania na kumwomba aulizie mtu aliyeitwa James Kibudo kama Geofrey alivyolitaja jina la baba yake.Baada ya kumpa rafiki yake huyo kazi hiyo alianza kusubiri taarifa zozote kutoka kwa mtu huyo ambaye mwishoni alidai kulikuwa hakuna mtu aliyeitwa jina hilo. Bila kuchelewa alimpa taarifa hizo Geofrey ambaye alichukulia jambo hilo kama la kawaida na aliamini siku ambayo angerudi Tanzania mambo yote yangekuwa sawa.
Bila kuchelewa alimpa taarifa hizo Geofrey ambaye alichukulia jambo hilo kama la kawaida na aliamini siku ambayo angerudi Tanzania mambo yote yangekuwa sawa. Magreth alikuwa amejiwekea utaratibu wa kumtembele gerezani kila mwisho wa wiki jambo lililompa sana faraja. Geofrey naye tayari alianza kuingiwa na mshtuko wa moyo juu ya Magreth kutokana na ishara za wazi alizozipata lakini aliona jambo hilo haliku wezekana kwa yeye kuwa na uhusiano na mrembo huyo. Siku zote alimchukulia kama msichana mwenye huruma na aliamini hakuna jambo ambalo lingeweza kutokea kuhusiana na hisia zake. Muda ulikwenda na hatimaye Geofrey alibakiwa na wiki mbili za kutumikia adhabu yake, hakuamini hata kidogo kuwa angeliacha gereza hilo na kuwa huru. Furaha yake iliongezeka zaidi kutokana na ahadi ambayo Magreth alishampa ya kufanikisha safari yake kurudi Tanzania. Zilibaki siku mbili, hatimaye moja na mwishoe siku ya Jumapili majira ya saa nane alipewa nguo za kuvaa alizoelezwa aliletewa na mtu aliyefika gerezani hapo kumchukua. Geofrey hakujiuliza maswali mengi akiamini nguo hizo zilitoka kwa Magreth aliingia katika chumba cha kubadilishia nguo na kuanza kuvaa nguo hizo. Lilikuwapo shati moja rangi nyekundu pia viatu na soksi vilikuwa vya rangi hiyo pamoja na jinzi moja iliyovutia kwa muonekano. Geofrey alivivaa na kuanza kutembea akitoka katika chumba hicho askari magereza walishtuka na kuanza kumshangilia kwa mwonekano mzuri aliokuwa nao. Mkuu wa gereza alimsifia kwa tabia yake nzuri aliyokuwa nayo kipindi akiwa gerezani hapo zaidi kitendo chake cha kuwatetea wanyonge. Alimaliza akimwambia aliamini toka wakati huo angekuwa raia mwema na mwishoe alimhurusu aondoke. Geofrey alianza kutembea kuelekea geti kuu la gereza hilo kwa haraka akiwa hajiamini kwani alihisi angeitwa tena kurudi kifungoni. Mara baada ya kutoka katika geti hilo kidogo moyo wake ulitulia lakini alihitaji kuondoka kabisa eneo hilo. Alikuwa akimwangalia Magreth kama alikuwapo eneo hilo kumchukua kama alivyoelezwa na askari magereza. Alizungusha kichwa kila upande eneo hilo pasipo kumuona zaidi ya gari lililokuwa na rangi nyekundu ambalo lilikuwa kando yake kidogo ambalo vioo vyake havikuhurusu mtu wa nje kuona ndani. Akiwa anatafakari juu ya jambo la kufanya alishtushwa mlango wa gari hilo uliokuwa ukifunguliwa, alielekeza macho yake ili aone mtu ambaye angeshuka. Alishuhudia mguu wa mwanamke ukiwa na kiatu rangi nyekundu ukitoka kabla ya mtu huyo kutoka kabisa. Mshtuko wake uliongezeka zaidi baada ya kuona mtu huyo alikuwa Magreth, alikuwa amevaa vitu vyenye rangi nyekundu toka chini hadi juu. Alikuwa na gauni la kuvutia na zaidi mkononi pia alikuwa na maua ya rangi hiyo, alianza kutembea akielekea eneo ambalo Geofrey alikuwa amesimama. Mara baada ya kumfikia alimkubatia kabla ya kusikika “ pole sana Geoffur…..” “ahsante lakini zaidi nashukuru kwa kunijali muda wote nikiwa jela” Alijibu Geofrey ambaye mapigo yake ya moyo yalimwenda mbio hakuelewa jambo lililoendelea siku hiyo lakini rangi nyekundu ndiyo ilimpa shaka zaidi. Aliongozwa mpaka kwenye gari hilo lililokuwa Range Rover, kabla ya kuondoka kwao Geofrey aliamua kuuliza jambo lililomtatiza ingawaje lilimpa hisia za ushindi moyoni mwake. “kwa nini kila kitu kina rangi hii..” aliuliza Geofrey baada ya kushindwa kujizuia, Magreth alicheka kidogo kabla ya kumgeukia akimtizama usoni “Geoffur leo ni tarehe kumi na nne mwezi wa pili siku ya wapendanao duniani, naamini tunapendana” alimjibu jambo lililomfanya Geofrey acheke kwa furaha ingawaje hakujibu kitu ila aliona kama vile alikuwa amelala masikini na kuamka mfalme. Tayari alijipa aslimia mia za kuwa na Magreth mpaka mwisho wa maisha yake. Waliongoza mpaka hoteli ya kifahari iliyokuwapo katika jimbo hilo la Biloku na huko ndipo uhusiano wao ulianza rasmi baada ya ahadi nyingi walizowekeana. Siku iliyofuata Magreth alianza kumtafutia Geofrey hati ya kusafiria kurudi Tanzania. Mara baada ya taratibu zote kukamilika alimsindikiza Geofrey uwanja wa ndege tayari kwa safari kurudi Tanzania, alimweleza angerudi pia mara baada ya masomo yake ya mwaka mmoja uliobakia. Magreth alikuwa akilia kwani alihisi huo ndiyo ulikuwa kama mwisho wa yeye kuonana na Geofrey, mara baada ya kuagana alikuwa amempa namba ya simu na fedha za kutosha akiwa amemweleza mara baada ya kufika Tanzania amjulishe. Safari hiyo ilianza na mwishoe walifika Tanzania wakiwa wamepita Uingereza, Ethiopia na nchi nyingine. Geofrey bila kupoteza muda alikodi teski na alimweleza dereva ampeleke eneo lililokuwa na kampuni ya JAJHO, halikuwa jambo gumu kwa dereva huyo kwani alidai kampuni hiyo ilikuwa kubwa sana wakati huo. Alihitaji kufikia katika kampuni hiyo kwani bado Geofrey kumbukumbu alikuwa nazo juu ya kampuni hiyo aliyoiacha akiwa anaelekea Marekani na ilikuwa chini ya umiliki wa baba yake na wenzie wanne. Hatimaye walifika katika foleni ya magari iliyokuwapo maeneo ya posta akiwa ameelezwa walikaribia kufika katika eneo lililokuwa na ofisi hizo za kampuni ya JAJHO. Alikumbuka kumtaarifu Magreth kuwa tayari alikuwa amefika Tanzania, wakati huo alikuwa amekaa upande wa mbele wa teski hiyo akiwa na dereva na kioo cha gari kilikuwa wazi. Alichukua simu yake na kumpigia mara baada ya kuita mara moja ilipokelewa “nimeshafiaka Tanzania na niko nae…..” kabla hajamalizia sentesi hiyo mara baada ya kusalimiana kwao kibaka mmoja aliinyan`ganya simu hiyo kwa nguvu na kuondoka kwa kasi eneo hilo la foleni na tayari magari yalikuwa yamehurusiwa. Geofrey alichanganyikiwa ghafla juu ya tukio hilo zaidi hakuwa na namba ya mawasiliano ya Magreth ambayo ilihifadhiwa kwenye simu hiyo. Baada ya jitihada za haraka za kuipata simu hiyo kushindikana aliamua kukubaliana na tukio hilo na alimhurusu dereva waendelee na safari akiwa na imani kuwa angeitafuta namba hiyo. Mara baada ya kufika eneo hilo aliongozwa mpaka kwenye ofisi ya mmiliki mkuu wa kampuni hiyo aliyekuwa na hisa nyingi, aliamini alikuwa anaenda kuonana na baba yake. Mara baada ya kuingia katika ofisi hiyo alikutana na sura tofauti na baba yake ila kumbukumbu zake zilimjia kwa mbali juu ya mtu huyo. “ samahani namuulizia James Kibudo” Alisikika Geofrey mara baada ya kuketi, mtu huyo alishtuka kidogo kabla ya kumuuliza “unamuulizia kama nani katika kampuni hii” alijibu mtu huyo “kama mmoja wa wamiliki wa kampuni hii” alijibu “sikiliza kijana James Kibudo alifilisika miaka mingi iliyopita na hayupo kwenye orodha ya wamiliki wa wa kampuni hii, alituuzia hata jina lake ndiyo maana hatujabadili jina la kampuni hii ya JAJHO tukihofia soko letu mtaani, zaidi alikutwa ameuuawa nch…” kabla hajamalizia kuongea Geofrey alikurupuka na kumvamia akitaka kujua vizuri sentesi ya mwisho iliyohusu mauaji. Walinzi kadhaa waliitwa ofisini hapo na kumkamata zaidi mtu huyo aliyekuwa bosi aliyejitambulisha kama Jackson aliwaita wamiliki wenzie Amos, Hamis na Onesmo ili wamhoji mtu huyo. Geofrey baada ya kutulia kidogo alijieleza vizuri na mwishoe watu hao walimpa taarifa za kuuawa kwa baba na mama yake miaka kumi iliyopita na mdogo wake Robert walidai hawakujua eneo alilokuwapo na imani yao ilikuwa alikuwapo Marekani. Walimweleza juu ya taarifa walizokuwa nazo juu ya kifo chake baada ya ajali ya ndege iliyotokea nchini Guyana. Baada ya maelezo hayo Geofrey akiwa na majonzi aliaga na kuondoka eneo hilo la ofisi za JAJHO, mawazo yake yalikuwa ni kuhakikisha anaenda Kenya na kushuhudia kabuli la baba na mama yake.Jackson na wamiliki wenzie waliitana na kushangilia juu ya tukio hilo la maelezo ya kifo cha James na mkewe waliyoyatoa kwa mwanaye na waliamini siri yao isingevuja. Alielekea katika nyumba moja ya kulala wageni maeneo hayo ya Posta na muda wote alikuwa akilia juu ya tukio hilo alillolisikia, siku iliyofuata alianza safari akielekea Kenya kwa lengo la kwenda kuliona kabuli la baba na mama yake. Mara baada ya kufika jijini Nairobi aliongoza katika kituo kikuu cha polisi cha jiji hilo na kuomba kuonyeshwa makabuli hayo. Tayari alishaelezwa awali na mr. Jackson kuwa askari wa kituo hicho wangemsaidia kwani walihusika kwa kiasi kikubwa na mazishi ya wazazi wake.
Tayari alishaelezwa awali na mr. Jackson kuwa askari wa kituo hicho wangemsaidia kwani walihusika kwa kiasi kikubwa na mazishi ya wazazi wake. Askari hao walimwelewa na mara baada ya kurejea kumbukumbu zao aliongozwa na askari mmoja hadi eneo la makabuli hayo. Geofrey alilia kwa uchungu mara baada ya kuona vibao ambavyo rangi yake ilikuwa ikikwajuka vikiwa na majina ya wazazi wake na aliamini aliloelezwa kuwa waliuawa. Siku iliyofuata aliwatafuta mafundi ujenzi kadhaa na kuwataka wamjengee makabuli hayo yaliyokuwa katika hali mbaya ya kuweza kupoteza kumbukumbu yake. Mara baada ya zoezi hilo aliweka mataji kama ishara ya kushiriki kwake katika msiba huo na kwa wakati huo aliamini hata mdogo wake Robert angeweza kwenda kuiona kumbukumbu hiyo ya kifo cha wazazi wao. Tayari alikuwa ameishiwa fedha zote alizopewa na Magreth kabla ya kuondoka kwake nchini Guyana na wakati huo aliona hana njia ya kuweza kumuokoa. Aliamua kumpigia simu mr. Jackson wa kampuni ya JAJHO akiomba uwezekano wa kupatiwa kazi lakini alijibiwa kwamba hawakuwa na nafasi hiyo. Aliumia juu ya jibu hilo lakini alijipa moyo ingawaje kuna wakati aliwahisi vibaya wamiliki wa kampuni hiyo. Jambo lililomkaa kichwani aliwaza kuwa ni lazima atafute fedha kwa ajili ya kufuatilia watu waliofanya mauaji dhidi ya familia yake. Akili yake ilimtuma kuua kama akiwagundua watu waliohusika na mauaji hayo kwani aliamini jeshi la polisi la nchi zote mbili za Tanzania na Kenya lilishindwa kazi yake. Baada ya kujibiwa vibaya na mr. Jackson alijichanganya katika mitaa ya jiji la Nairobi ili kutafuta maisha akianza kwa kuuza vitu tofauti barabarani. Wiki moja baadaye aligundua kuwa alijichelewesha kufanya malipo ya vifo kwa watu ambao walihusika na kifo cha wazazi wake. Kwani aliamini ilimbidi apate fedha ili afanye upelelezi na mwishoe apange malipizi hayo, aliamua kuanza kutafuta kundi la majambazi nchini humo akiamini aliweza kazi hiyo kwani alipata mafunzo mengi toka kwa mzee Rogart akiwa nchini Guyana. Baada ya wiki moja alikutana na mtu aliyejulikana kama mr. Tyoso ambaye alikuwa na kundi lake la majambazi, hivyo alianza kazi na watu hao. Ndani ya mwezi mmoja kundi la mr. Tyoso lilipata mafanikio kupindukia kupitia uwezo mkubwa aliokuwa nao Geofrey. Kikubwa ni utumiaji wake wa bunduki na zaidi upinde na mishale walivyofanyia unyan`ganyi sehemu tofauti nchini Kenya. Alikuwa akiishi na mr. Tyoso mwenyewe kwa vile hakuwa na nyumba katika jiji hilo. Baada ya miezi mitano ya mafanikio tayari Geofrey pia alikuwa ni mtaalamu wa kuendesha magari hata pikipiki. Siku moja Geofrey alipatwa na homa ya malaria na hivyo alibakia nyumbani kwa mr. Tyoso wakati kundi hilo likiendelea na ujambazi. Muda wote akiwa nyumbani hapo alikuwa akisikiliza redio na mwishoe nyakati za jioni aliamua kuigeukia luninga ya mr. Tyoso. Alianza kuchagua filamu mbalimbali ambazo angeweza kuangalia lakini alivutiwa na moja iliyoonekana ilikuwa ya wanyama kwani iliianza kwa kuonyesha vyura. Ilimvutia zaidi kutokana na maisha ya porini aliyokuwa ameishi kwa muda mrefu nchini Guyana, ilionyesha ilikuwa imeandaliwa na George Johnson raia wa Kenya miaka kumi iliyokuwa imepita. Aliendelea kuangalia filamu hiyo huku akifurahia aina ya vyura walioonyeshwa, ghafla filamu hiyo ilikatishwa katikati na maneno yaliyoandikwa ‘MAUAJI YA KUTISHA’ yalitokea. Geofrey alikaa vizuri ili aone kilichokuwa kikifuata, alishtushwa na filamu hiyo iliyoendelea na baada ya sekunde chache aliwaona wazazi wake wakiwa porini kama wametekwa. Alikaa vizuri zaidi na kutoa macho, alimwona Jackson,Hamis,Amos na Onesmo wote wakiwa wamilikiwa kampuni ya JAJHO wakiwa katika eneo hilo la tukio na zaidi bosi wake mr. Tyoso alikuwapo. Jasho lilimtoka kama maji mara baada ya kuanza kushuhudia mauaji ya wazazi wake, aliwashuhudia jinsi wamiliki wa JAJHO walivyommiminia risasi baba yake wakati mama yake akiuawa na mr. Jackson. Zaidi aliona kila kitu katika tukio hilo kwani mpiga picha aliwachukua wazazi wake kwa karibu sana na kamera yake kabla ya wauaji hao kurudi na kuwatupa wazazi wake katika mto Tana. Geofrey hakuamini vizuri na wakati huo alichukua upinde na mishale yake tayari kwa shari aliwaza kuanza mauaji na mr. Tyoso aliyeonakana kuhusika. Tayari ilikuwa yapata saa moja jioni, alikuwa ameirudisha kwa mara ya pili filamu hiyo akiiangalia tena. Ghafla wakati akiendelea kuangalia filamu hiyo mr. Tyoso aliingia lakini Geofrey hakusikia chochote kutokana na hali ya kuchanganyikiwa aliyokuwa nayo juu ya filamu hiyo. Shati lake lilikuwa limelowa jasho kama vile alikuwa amenyeshewa na mvua, mr Tyoso alishtushwa na filamu hiyo iliyompa hisia za mauaji waliyoyafanya miaka mingi iliyokuwa imepita. Alikurupuka na kwenda kuitoa filamu hiyo kabla ya kuivunja akikanyaga na buti lake lililokuwa kama la jeshi, jambo hilo lilipelekea filamu hiyo kugawanyika katika vipande. Geofrey akili yake kidogo ilianza kumrudia sawasawa akiwa amegundua kuwa mtu aliyepaswa kuanza naye kumuua alikuwa amefika. Mr. Tyoso akilini hakuwahi kuhisi wala kuambiwa kuwa watu waliouawa katika filamu hiyo walikuwa ni wazazi wa Geofrey. Hata baada ya kuivunja filamu hiyo alielewa lilikuwa jambo la kawaida kwani walikuwa wamefanya mauaji kadhaa na Geofrey hivyo aliamini alikuwa mtu muuaji kama yeye. Wakati huo Geofrey mishipa ya hasira ilikuwa imemtoka shingoni na usoni na alikuwa kimya bila kusema kitu akiwa ameshika upinde na mshale alioupachika sawasawa lakini pembeni na eneo alilokaa akiweka mishale mingine mingi. “ebwana hili dili kuna mzushi alituona tulivyokuwa tunawasaidia watanzania fulani wa kampuni ya JAJHO kumuua mwenzao, kwa hiyo huwa siipendi hiyo filamu kwanza sikujua kama bado ipo” aliongea mr Tyoso baada ya ukimya kwa muda mrefu. Geofrey alisimama akiwa na mshale wake na upinde akiwa amemwelekezea mr. Tyoso usoni , “piga magoti haraka sana” aliongea kauli ambayo mr. Tyoso hakuitekeleza akijua ni utani. “vipi tena tunataniana toka…..”alisikika akijibu kauli ya Geofrey lakini kabla ya kumalizia sentensi yake alipigwa teke la uso lililompeleka mpaka chini. Hapo mr Tyoso aligundua kulikuwa na shari hivyo alitekeleza amri ya kupiga magoti, Geofrey aliivuta kamba ya upinde wake ambao alipachika mshale akiwa ameuelekeza kifuani kwa mr Tyoso. “jina langu ni Geofrey James Kibudo kwa hiyo wewe ulishiriki kuwaua wazazi wangu sina zawadi ya kukupa zaidi ya hii….” Aliongea Geofrey kauli iliyomshangaza mr Tyoso na mara baada ya kuimaliza kauli hiyo aliachia kamba ya upinde na mshale wake kwa kasi ya ajabu ulielekea kifuani mwa mr Tyoso na kupenya sawasawa ukiwa umeingia zaidi ya nusu. Mr. Tyoso alianza kupiga kelele za maumivu aliyoyapata wakati damu ilianza kumtoka, Geofrey aliingia kwenye chumba chake na kuchukua fedha zake zote. Mara baada ya kufanya hivyo alielekea katika chumba cha mr. Tyoso na kuchukua bunduki mbili walizozitumia kwa ujambazi lakini pia alichukua fedha ambazo aliziona. Alirudi na kuchukua funguo za gari katika suruali aliyokuwa ameivaa mr. Tyoso ambaye bado alikuwa akilalamika kwa maumivu makali. Alifanikisha mambo hayo ndani ya dakika saba na alitoka mbio nje akiwa pia amebeba upinde na mishale, mara baada ya kupakia vitu vyote kwenye gari alilitoa kwa kasi eneo hilo la nyumba ya mr Tyoso. Alikuwa amebeba bunduki, upinde na mishale sambamba na fedha za kutosha kwani alielewa jambo lililofuata lilikuwa malipizi ya vifo vya wazazi wake. Alikimbiza gari hilo aina ya ‘Land Cruiser’ akiwa na mpango wa kuvuka mipaka kuelekea Tanzania na hatimaye kuingia Dar es salaam kwa ajili ya kufanya malipo ya mauaji. Wakati akiwa anaendelea kuliacha jiji la Nairobi kuna jambo aligundua lilikuwa la muhimu kulitekeleza, alichukua simu yake na kumpigia mr Jackson ambaye baada ya simu kuita kwa muda mfupi aliipokea “baada ya kumuua mr. Tyoso nakuja kuwaangamiza na nyinyi wote nawapa siku saba za uhai wenu” alisikika Geofrey mara baada ya simu kupokelewa kabla ya kukata na kuizima. Aliendeleza kasi ya kuendesha gari lake, hakuwa na mpango wa kuwashirikisha polisi jambo hilo kwani aliamini walishindwa kufanya kazi yao kwa zaidi ya miaka kumi, alipanga kuwauwa wamiliki wa kampuni ya JAJHO wote kwa mkono wake. Mr. Jackson alishtushwa na kauli aliyoipokea toka kwa mtu ambaye namba yake aliihifadhi kama Geofrey akiwa mtoto wa marehemu James. Hisia za kugundulika kwa siri yao zilimjia jambo lililopelekea ampigie simu tena Geofrey ili ajue kama alikuwa ameigundua siri hiyo lakini simu ya kijana huyo haikupatikana.
Hisia za kugundulika kwa siri yao zilimjia jambo lililopelekea ampigie simu tena Geofrey ili ajue kama alikuwa ameigundua siri hiyo lakini simu ya kijana huyo haikupatikana. Aliamua kumpigia simu mr Tyoso ili ahakikishe kama kweli alikuwa ameuawa, simu yake ilipokelewa na mtu mwingine aliyemthibitishia kifo cha mr. Tyoso. Upelelezi wa haraka alioufanya mr Jackson aligundua Geofrey alikuwa akifanya kazi kama jambazi chini ya usimamizi wa mr Tyoso. Uthibitisho wa siri hiyo kuvuja ulikamilika na aliwaita wenzie na kuwaeleza juu ya jambo hilo lakini zaidi aliwataka wajiweke katika tahadhari ili wafanikishe kumuua Geofrey kabla ya kuuawa kwao. Walitafuta vijana wakakamavu zaidi ya ishirini na kugawana watano kila mmoja na zaidi waliwatafuta wengine zaidi ya thelathini waliopewa jukumu la kufuatilia nyendo za Geofrey waliyeamini bado alikuwa hajaingia Dar es salaam. Jackson na wenzie walijipa matumaini wakiamini kuwa ni lazima Geofrey angeuawa kabla yao kutokana na mikakati waliyoiweka. Baada ya siku tatu Geofrey alikuwapo nchini Tanzania, alikuwa amefikia wilaya ya Bagamoyo katika kijiji cha Fukayosi akiwa amejitambulisha kama mpangaji katika nyumba yenye vyumba vitatu aliyoishi mzee mmoja. Alikuwa amepewa chumba kimoja kati ya hiyo vitatu wakati vingine vilitumiwa na mzee huyo, alimtoa hofu mzee huyo akidai kuwa alikuwa akifanya utafiti katika maeneo hayo na angeishi kwa muda wa wiki mbili. Mzee huyo hakuwa na ubishi kwani alipea fedha za kutosha, tayari Geofrey alikuwa na pikipiki aliyoinunua njiani wakati akitokea Kenya. Siku iliyofuata aliondoka na pikipiki akielekea jijini Dar es salaam ambako alifanya zoezi la kuzitambua nyumba za wamiliki wa kampuni ya JAJHO ambalo halikuwa gumu kutokana na umaarufu na utajiri waliokuwa nao. Tayari aliamua kuanza mauaji na Onesmo baada ya kuona uwezekano wote wa kufanikisha zoezi hilo, alikuwa amepanga kuwauwa wamiliki hao ndani ya usiku mmoja siku iliyofuata. Siku iliyofuata majira ya saa tatu usiku aliondoka Bagamoyo na pikipiki akielekea jijini Dar es salaam akwa na lengo moja la kwenda kuwauwa wamiliki wa kampuni ya JAJHO. Alikuwa amebeba upinde na mishale sambamba na na bunduki moja iliyokuwa na risasi za kutosha, vyote alikuwa ameviweka kwenye begi kubwa alilokuwa amelibeba mgongoni lakini pia alikuwa na tochi pamoja visu kadhaa vilivyozunguka kiunoni mwake. Alikuwa hajatumia dawa zozote za kulevya lakini akili yake kwa ujumla ilimtuma kuua, alikuwa mtu aliyeathirika kisaikolojia ambaye ilikuwa vigumu kuubadili msimamo wake. Saa tano usiku alikuwa nje ya geti la mr. Onesmo akiwa ameshaiegesha pikipiki yake na bila kuchelewa aligonga akiwa amejitega kwa shari pembeni na mlango mdogo wa geti hilo. Alisikia vishindo mlinzi akijongea getini na kuanza kufungua mlango mdogo wa geti hilo, alijiweka tayari akiamini alipaswa kuanza na mlinzi huyo akiwa ameshika moja ya kisu kilichon`gaa kutokana na ukali wake. Mara baada ya kutoka mlinzi huyo aliyekuwa na bunduki yake alipokelewa na teke zito la usoni lililomrudisha ndani ya geti hilo akiwa ameanguka. Kabla hajafanya jambo lolote alinyan`ganywa bunduki aliyokuwa nayo, Geofrey alimwelekezea bunduki hiyo mlinzi huyo kabla ya kuambiwa aongoze kwenye chumba chake cha ulinzi kilichokuwa getini hapo. Alitekeleza jambo hilo na kwa haraka aliingia kwenye chumba hicho akifuatwa na Geofrey ambaye alimuhoji maswali kadhaa na aligundua Onesmo alikuwa hajarudi nyumbani kwake. Alieleza lengo lake la kumuhitaji Onesmo na si mlinzi huyo hivyo alitumia kamba zilizokuwapo katika chumba hicho na kumfunga mikono na miguu. Baada ya kufanikisha zoezi hilo alimpiga mlinzi huyo na kitako cha bunduki yake katika mishipa yake ya fahamu ya shingoni iliyopelekea mlinzi huyo aanguke chini akiwa amepoteza fahamu. Alitoka nje kwa kasi na kuchukua pikipiki yake na kuiingiza ndani katika chumba hicho cha cha mlinzi alibadilisha shati lake na kuvaa la mlinzi huyo sambamba na kofia yake hakubadili suruali kwa vile iliendana na ya mlinzi huyo.Wakati akitafakari jambo la kufanya alishtuhwa na honi za gari zilizopigwa nje ya geti hilo. Bila kujiuliza mara mbili aligundua mtu huyo alikuwa Onesmo akirudi nyumbani kwake, alielekea katika geti hilo na kulifungua kwa kasi la kwanza na hatimaye la pili ambalo alijificha nyuma yake. Alishuhudia gari mbili zikiingia na kwenda kuegesha eneo la mbele la nyumba ya hiyo alishuka Mr Onesmo na watu zaidi ya kumi walioonekana walikuwa wakimlinda. Tayari alikuwa amefunga geti hilo na kurejea katika kibanda chake, kwa sauti ya chini alisikia maongezi yaliyoendelea “bosi leo tunaomba tukapumzike ili turudi kwa kasi mpya ya kesho lakini pia huna haja ya kumuogopa Geofrey huyo ni mtu mdogo sana hatuwezi” alisikika mmoja wa watu hao aliyeonekana alikuwa kiongozi wao. “sawa kwa leo tu ila saa kumi na moja muwe mmefika hapa” Aliwajibu Onesmo ambaye alianza kutembea akielekea katika nyumba yake kabla ya kufunguliwa na kuingia. Watu hao walioonekana kama walinzi wa Onesmo waliingia kwenye gari hizo Mercedez Benz mbili walizofika nazo na walianza kuziendesha wakiziondoa eneo hilo. Geofrey alijua jukumu lake kwa kasi alifungua geti na watu hao waliondoka. Hapo aliamini mchezo ulikuwa umeisha bila kupoteza muda alichukua visu vitatu na bunduki moja iliyokuwa na risasi za kutosha aliongoza hadi kwenye mlango wa kuingilia wa nyumba hiyo na kuanza kugonga. Aliamini mtu aliyekuwa amemfungulia Onesmo lazima angerudi kumfungulia baada ya muda mfupi akisikia vishindo vya mtu huku akiongea “jamani mlinzi nini tena….” Aliongea dada huyo ambaye mara baada ya kufungua mlango alipokelewa na bomba la mbele la bunduki. “kwa usalama wako tulia naomba unionyeshe chumba anacholala mr Onesmo” Aliongea Geofrey akiwa amemkazia macho dada huyo ambaye alinyosha mkono akionyesha ghorofa ya kwanza ya nyumba hiyo. Baada ya maelezo hayo Geofrey akitumia nguvu alimpiga msichana huyo na kitako cha bunduki na kupelekea kuanguka kwake kabla ya kupoteza fahamu. Bila kupoteza muda Geofrey alikimbia akielekea ghorofani mwa nyumba hiyo alipofika aliuona mlango mmoja ambao ulikuwa haujafungwa vizuri huku taa yake ikiwaka aliingia na kumshuhudia mr. Onesmo akibadilisha nguo za kulalia huku mkewe akiwa amelala “mamaaa weeee nafwaa huwiiiii” alipiga kelele mr Onesmo ambazo zilimwamsha hata mkewe. “tulia mbwa wewe nisije nikakuua kabla ya wakati” aliongea Geofrey akiwa amemwelekezea bunduki yake jambo lililoleta utulivu hata kwa mkewe Onesmo ambaye hakujua jambo lililoendelea. “ nipe simu yako haraka iwezekanavyo” alitoa agizo hilo ambalo Onesmo alilitekeleza. “ulidhani mlivyowauwa wazazi wangu nisinge wagundua” aliongea Geofrey wakati akikipitisha kisu chake tumboni katika hali iliyoonyesha alikisafisha na bado alikuwa amemwelekezea bunduki mr Onesmo. Alikuwa ameshika kisu kirefu mithili ya panga kilichon`gaa kupindukia, ghafla alikurupuka na kumvamia Onesmo akiwa amelekezea kisu hicho tumboni kilichompata sawasawa. Wote alianguka chini huku Geofrey akiwa bado amekishikilia kisu, alikitoa kwa kasi na bila huruma alishindilia mara tatu zaidi akichoma na kuchomoa. Damu iliyotoka na kuruka ilikuwa ni zaidi ya machinjio, jambo hilo ndilo lililopelekea mkewe Onesmo kuzimia. Geofrey akiwa amebeba bunduki yake alitoka mbio chumbani hapo na kuongoza moja kwa moja hadi kwenye kibanda cha mlinzi ambaye alikuwa hajarudiwa na fahamu. Aliwasha pikipiki na kuchukua vitu vyake vyote kabla ya kuiondoa pikipiki hiyo kwa kasi eneo hilo la nyumba ya Onesmo. Baada ya saa moja alikuwa maeneo ya Kimara katika hoteli iliyotambulika kwa jina la `Mwalon West` ambako bila kupoteza muda alilipia chumba kimoja.Tayari ilikuwa yapata saa saba na nusu usiku bado lengo lake lilikuwa ni kuhakikisha anakamilisha mauaji kwa wamiliki wa kampuni ya JAJHO katika usiku huo. Aliamini simu ya Onesmo aliyoichukua kabla ya kumuua ndiyo ingekamilisha zoezi hilo, aliandaa visu, bunduki yake sambamba na upinde na mishale ambavyo aliviweka chini ya uvungu. Alikuwa amechanganyikiwa na hakuwaza jambo lolote zaidi ya kuua, alichukua simu ya Onesmo na kufanikiwa kuziona namba za simu za Jackson, Hamis na Amos. Baada ya kuziona namba hizo alifungua sehemu ya ujumbe mfupi wa maandishi na kuanza kuandika.
Baada ya kuziona namba hizo alifungua sehemu ya ujumbe mfupi wa maandishi na kuanza kuandika. Alipanga kuwatumia wamiliki hao ujumbe wa maandishi ili wafike hotelini hapo akiamini wangeshawishika. Baada ya dakika tatu alikamilisha ujumbe huo uliokuwa hivi ‘Mkubwa Nimefanikiwa Kumkamata Mshenzi Geofrey James Kibudo, Fanya Haraka Uje Katika Hoteli Ya Mwalon West Chumba Namba 25 . Njoo Peke Yako Kama Unavyojua Inatubidi Tuue Na siri Hii Asiijue Mtu…..! Nakusubiri!’ Alikamilisha Geofrey ujumbe huo wa simu na kuutuma kwa namba za watu hao kwa pamoja. Ujumbe huo ulionyesha kupokelewa na Hamis pamoja na Amos lakini haikuwa hivyo kwa Jackson. Geofrey alijaribu kumpigia namba yake ilikuwa haipatikani. Baada ya dakika tatu akiwa anatafakari jambo la kufanya alishtushwa na mlio wa simu hiyo kabla ya kushuhudia ujumbe wa maandishi toka kwa Hamis ulioandikwa ‘Msimuue Huyo Mshenzi Nakuja Sasa Hivi…’ dakika moja baadaye Amos naye alithibitisha kufika hotelini hapo. Geofrey alijua kazi ilielekea kuisha aliandaa upinde na mshale tayari kwa mauaji, alikuwa akiwasubiri kwa hamu ili aendelee kukamilisha ndoto yake ya kuwaua wote usiku huo. Baada ya nusu saa alisikia mlango ukigongwa, jambo lililompa hisia kuwa mmoja wa watu hao alikuwa amefika, kwa kasi alienda kusimama kando ya mlango huo akiwa na upinde na mshale uliotegeshwa tayari kwa shari. “tafadhari ingia…” alisikika Geofrey na kumfanya mtu aliyekuwa angonga kufungua mlango na kuanza kuingia. Mara baada ya kuingia alianza kuangalia huku na huku akionekana kama alitafuta kitu, Geofrey alikuwa ametulia huku akiwa amegundua mtu huyo alikuwa Hamis. Akiwa bado hajatulia vizuri alishtushwa na sauti ya mtu aliyekohoa alipogeuka alitoa macho kabla kuanza kupiga kelele “siniue usiniue tafadhari..” alipiga kelele Hamis baada ya kumshuhudia Geofrey akiwa tayari kwa kumuua “tulia we mbwa huna muda wa kupoteza inakupasa uuangane na mwenzio Onesmo…” alisikika Geofrey kabla kuachia mshale ulioenda kumpata sawasawa Hamis tumboni, akiwa hajatulia vizuri alisindikizwa na teke la uso lililompeleka mpaka chini, alianza kulalamika kutokana na maumivu aliyoyapata. Geofrey alichukua bunduki chini ya uvungu wa kitanda akiwa anahofia usalama wake baada ya kelele zilizotolewa na Hamis, aliiweka vizuri baada ya ya kusikia vishindo vya mtu akija kwa kasi eneo la chumba hicho. Punde alishtushwa na sura mtu huyo aliyeingia bila kugonga baada ya kuona alikuwa ni Amos “mikono juu kunguru mkubwa na taratibu sogea kwa mwenzio…” alisikika Geofrey kwa jazba na kumchanganya Amos aliyetetemeka kupindukia baada ya kumwona Hamis akiwa ametokwa na damu nyingi na bado alikuwa akihangaika. Jambo hilo lilimfanya Amos achanganyikiwe ghafla na kushindwa kutimiza amri aliyopewa, hasira za Geofrey ziliongezeka na kuamua kuanza kumiminia risasi Amosi ambaye alianguka baada ya muda mfupi. Alimgeukia Hamis na kumpiga naye risasi ya kichwa na kumfanya atulie kabisa. Kulikuwa na kelele za watu waliohofia uhai wao baada ya kusikia milio hiyo ya risasi. Bila kuchelewa Geofrey alichukuwa funguo za pikipiki yake pamoja na bundu ki hiyo aliyokuwa bado kaishika alianza kukimbia akitoka katika hoteli hiyo. Aligongana na watu waliokuwa wamechanganyikiwa wakizunguka katika hoteli hiyo, alipiga risasi nyingine mbili sakafuni ambazo ziliwafanya hata walinzi wakimbie. Geofrey alifanikiwa kuichukua pikipiki yake na kuondoka kwa kasi eneo hilo la hoteli ya Mwalon West. Alikimbiza pikipiki yake akielekea Bagamoyo alikokuwa amepanga chumba, tayari aliona ndoto zake zilikuwa zimeingia dosari kwa vile hakufanikisha mauaji ya watu wanne. Alikuwa anawaza kuhakikisha anaenda kujiandaa kwa ajili ya kurudi kumalizia mauaji na Jackson. * * * * Magreth alikuwa ameshtushwa na kukatika kwa mawasiliano ghafla kati yake na mwanamme wa ndoto zake, Geofrey. Muda wote alikuwa akilia akiwa hajui jambo lililokuwa limemtokea, kuna wakati alikuwa akihisi mwanamme huyo alikuwa amemsaliti. Alikuwapo katika chuo cha Guyana akiwa amebakiza muda mfupi ili amalize elimu ya chuo, wakati huo maendeleo yake kitaaluma yalikuwa mabovu kutokana na mawazo aliyokuwa nayo juu ya Geofrey muda wote. Baada ya miezi kadhaa alishindwa kuvumilia na aliamua kuondoka chuoni hapo pasipo kuaga na kuandaa safari yake ya kurudi Tanzania. Hatimaye siku hiyo ilifika na safari ilianza akiwa hajatoa taarifa ya safari hiyo hata kwa wazazi wake. Baada ya wiki moja alikuwapo nchini Tanzania akimtafuta Geofrey kila kona ya jiji la Dar es salaam pasipo mafanikio yeyote, jambo lililomkatisha tamaa kwa kiasi kikubwa.Alikuwa amefikia katika nyumba yao na kila siku alitumia gari lake kumtafuta Geofrey akiwa anatembea na picha yake lakini hakuna mtu aliyemfahamu. Hapo ndipo Magreth alipozidi kuchanganyikiwa zaidi akiamini alikuwa amepoteza mwelekeo wa kumpata. Siku moja akiwa Kariakoo katika mizunguko yake hiyo ya kumtafuta, alishtuka baada ya kumuona kwa umbali mtu aliyeamini alikuwa ni Geofrey. Alishuka kwenye gari na kuanza kumkimbilia mtu huyo huku akimwita. “Geoffur!, Geoffur……..” alimwita mtu huyo ambaye hakuitika na baada ya sekunde kadhaa kelele za kuita zikiwa zimeongezeka mtu huyo alisimama. Magreth akiwa anakimbia alimrukia na kumkumbatia na wote waliaanguka chini, watu waliokuwa katika pilikapilika zao walianza kushawashangaa. “ wewe dada vipi? mbona unanirukia inakuwaje?” Alisikika mwanamme huyo mara baada ya kusimama. “samahani kaka unafanana sana na mchumba wangu” aliongea Magreth huku akiwa na anajisikia aibu ikiwa ni baada ya kugundua mtu huyo hakuwa Geofrey ila walifanana sana. “samahani naomba tuondoke wote maana watu wanatushangaa nitakueleza vizuri niko na gari” Alisikika Magreth na walianza kutembea na mwanamme huyo hadi kwenye gari na kuondoka eneo hilo. Baada ya muda mfupi wa maongezi Magreth aligundua jambo lililompa matumaini, mwanamme huyo alikuwa mdogo wake Geofrey aliyeitwa Robert. Alikuwapo Tanzania kwa miezi zaidi ya sita akiwa na mchumba wake wakitokea Marekani na kazi aliyoifanya alikuwa akipeleleza juu ya tukio la mauaji ya wazazi wake zaidi alikuwa anaamini kaka yake Geofrey alikufa katika tukio la ajali ya ndege nchini Guyana. Robert alikuwa ameacha biashara zake nchini Marekani na jambo lililopelekea hayo yote lilihusiana na upelelezi juu ya kifo cha wazazi wake. Magreth pia aligundua juu ya kifo cha wazazi wa Geofrey na zaidi alimweleza Robert kuwa kaka yake bado alikuwa hai na alimsimulia kisa kizima cha maisha ya kaka yake huyo na zaidi alimwonyesha picha zake. Jambo hilo lilimfurahisha kwa kiasi kikubwa Robert, alijiona kama hakuwa mpweke kutokana na uhai wa kaka yake. Siku iliyofuata waliendeleza zoezi la kumtafuta Geofrey wakati Robert alikuwa na mchumba wake aliyeitwa Annie ambaye alitoka naye Marekani. Ni siku ambayo ilikuwa ngumu na iliwachanganya zaidi kwani vyombo vingi vya habari vilitawaliwa na kisa cha kuuawa matajiri wakubwa watatu wakitanzania. Muuaji alitajwa kwa jina la Geofrey James Kibudo, ingawaje picha zake hazikupatikana lakini polisi walikuwa wakiendelea na msako mkali ili kumnasa. Magreth alichanganyikiwa hata hamu ya kumtafuta Geofrey ilianza kupungua lakini Robert naye hakuwa ametulia kwani alishtushwa juu ya taarifa hizo. Annie aliwapa moyo akiwaeleza huenda Geofrey hakuhusika na waliendelea na zoezi lao hilo la kumtafuta Geofrey. Muda wote Magreth alikuwa akilia na kuonekana kujuta kukutana na Geofrey lakini bado alithibitisha kuwa Geofrey alikuwa mwanamme wa ndoto zake. Siku tano zilikatika na kulikuwa hakuna taarifa zozote kutoka jeshi la polisi juu ya kupatikana kwa muuaji lakini bado Magreth na wenzie walikuwa wakiendelea na zoezi la kumtafuta Geofrey. Walikuwa wakilala kwenye gari na walitembelea kila sehemu waliyohisi wangempata, siku hiyo majira ya saa mbili usiku walikuwa maeneo ya Bagamoyo katika kituo cha kuuza mafuta ya gari.Walikuwa wakiongeza mafuta katika gari lao baada ya mizunguko mingi, wakati zoezi hilo liliendelea kuna mtu alifika na pikipiki na kuegesha eneo la mbele yao akiwa na nia ya kuongeza mafuta. “Geoffur, Geoffur…..” alipiga kelele Magreth huku akishuka kwenye gari walilokuwa nalo na kumfuata mtu aliyekuwa kwenye pikipiki ambaye pia alishtuka kabla ya kushuka katika pikipiki. Magreth alimkimbilia na kumkumbatia Geofrey aliyeanza kulia baada ya kumwona.
Magreth alimkimbilia na kumkumbatia Geofrey aliyeanza kulia baada ya kumwona. Hatimaye Robert na Annie walijongea eneo hilo, Robert alikurupuka kwa kasi na kumkumbatia Geofrey na wote walianguka chini. Geofrey ambaye alikuwa mnyonge huku akiwa amebeba begi kubwa, hakuuliza na alionekana kumkumbuka mdogo wake.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Magreth nisamehe nadhani nimeharibu ahadi yetu kwa vile sidhani kama ndoto zetu zitatimia kama tulivyopanga, bado nahitajika kuua mtu wa mwisho aliyewaua wazazi wangu” alisikika Geofrey huku akiweka begi lake vizuri alilolibeba mgongoni kabla ya kuisogelea pikipiki na kupanda. “ nakupenda sana Magreth lakini yanipasa niondoke, Magreth, Roby aamh! Annie naenda, lakini muwe waangalifu” Alisikika Geofrey kabla ya kuwasha pikipiki yake na kuiondoa kwa kasi eneo hilo. Wote walibaki wamepigwa na butwaa na zaidi Magreth aliyeonekana akilia, ghafla aliacha kulia akasikika akisema “hapana, hapana Geoffur nampenda…,haiwezekani..! kama kufa tufe wote” alitoka akikimbia na kwenda kuingia kwenye gari kabla ya kuliwasha na kuliondoa kwa kasi eneo hilo akiwa amemwacha Robert na Annie wakiwa hawaelewi jambo la kufanya. Annie alimtuliza Robert aliyechanganyikiwa kwa kiasi kikubwa na alimtaka waende wakatulie ili watafakari jambo la kufanya na ikawa hivyo. Walipata chumba katika hoteli moja na walikuwa wakitathimini juu ya matatizo hayo waliyokumbana nayo. Siku iliyofuata majira ya saa moja asubuhi walipata taarifa za kifo cha Magreth aliyepata ajali mbaya mara baada ya kuondoka akiwa na lengo la kumfukuzia mchumba wake Geofrey. Baada ya dakika tano walipata taarifa nyingine iliyoeleza Geofrey James Kibudo alikuwa katika hali mbaya akiwa amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili baada ya kushambuliwa na askari wakati akijaribu kumuua tajiri Jackson. Ilielezwa alikuwa amepigwa risasi zaidi ya nane, bila kupoteza muda Robert na Annie walikodi teksi na kuondoka maeneo ya Bagamoyo wakiwa na lengo la kwenda kumuona. Robert alikuwa na hasira na mpaka wakati huo alikuwa hajui juu ya jambo lililoendelea juu ya mkasa huo. “waliowaua wazazi wetu ni wamiliki wa kampuni ya JAJHO na amebaki Jackson John Samola hakikisha unamumaliza mwenyewe kwa vile naamini jeshi la polisi lilishindwa kazi hiyo” ilikuwa ni kauli ya Geofrey aliyeongea kwa taabu sana mara baada ya Robert na Annie kufika hospitali. Alikuwa hajazungumza kitu kwa askari waliokuwa wanamlinda zaidi ya kauli hiyo aliyoitoa kwa Robert.Hata hivyo hakuna askari aliyesikia maelezo hayo, na Geofrey alionekana hakuwa na imani na jeshi la polisi. Baada ya dakika chache alifariki na Robert alilia kwa uchungu juu ya tukio hilo lililomuuma na aliamini kuuawa kwa Jackson ilikuwa ni kazi iliyokuwa mikononi mwake. Alitoka mbio eneo hilo la hospitali kabla ya kwenda kukodi teksi akihitaji apelekwe Masaki katika nyumba aliyoishi Jackson. Alikuwa hana silaha ya aina yeyote lakini imani yake ilikuwa ni kufanikisha mauaji hayo. Annie aliamua kuwaeleza askari juu ya kila kitu alichokisikia na askari waliondoka naye wakiwa na lengo la kwenda kumkamata Jackson kwa kuhusika na mauaji. Teski aliyokodi Robert ilienda kusimama nje ya geti la nyumba ya Jackson, kulikuwa na kundi kubwa la watu maeneo hayo. Mara baada ya kumlipa dereva wa gari hilo alishuka na kujichanganya na watu hao “du! yani jamaa amejiua… aah! hii kali kaka…” alisikika mmoja wa watu waliokuwapo eneo hilo na kumfanya Robert aliyekuwa na hasira kuuliza swali “nani kajiua na kwa nini….” “Aah.. Mr Jackson Samola amejipiga risasi kichwani…” alijibu mmoja wa watu hao. Robert alianza kulia kwa sauti kama na yeye alikuwa mfiwa wa tukio hilo, lakini hiyo yote ilitokana na hasira alizokuwa nazo. Baada ya dakika kadhaa askari walifika eneo hilo na kukamilisha taratibu zote zilizohitajika. Hatimaye Geofrey na Magreth walizikwa mjini Moshi eneo ambalo baba yake Magreth alizaliwa. Hiyo yote ilitokana na ombi la Robert aliyependa watu hao wawekwe karibu ingawaje hawakuwa katika ndoa. Jambo hilo lilikuwa la kusikitishwa hasa kwa watu waliopata kisa cha Magreth na Geofrey.Baada ya maombolezo ya msiba huo Robert alipanga safari tayari kwa kurudi na mchumba wake Marekani kuendeleza biashara zake. Siku moja kabla ya safari alipigiwa simu na askari waliomhitaji, alitii agizo hilo na mara baada ya kufika kituo cha polisi alipewa ujumbe mfupi ulioandikwa kwenye karatasi ambao Mr Jackson aliandika kabla ya kujiua alianza kwa kuusoma “…nilikuwa mpumbavu kwa kupingana na mkono wa sheria ya nchi yangu, kwani sheria ikiamua inapaswa itekelezwe lakini nilipinga adhabu ya kunyongwa aliyopewa kaka na baba yangu mzee Samola…, mwishoe walinyongwa. Niliamua kulipa kisasi cha vifo hivyo kwa James Kibudo na mkewe wasio na hatia lakini nimesababisha madhara makubwa kwani watoto wake nao wananitafuta waniue. Nimeamua kujiua kwa vile mimi pekee ndiye ‘MUUAJI ALIYEBAKIA’, hata nikisubiri mkono wa sheria lazima nitanyongwa na siri zangu zimeshagundulika.Naomba nusu ya utajiri wa kampuni ya JAJHO wapewe wanawe James Kibudo…….” Alimaliza Robert kusoma ujumbe huo ulioandikwa na Mr Jackson kabla ya kujiua. “du! sichukui kitu kutoka kampuni ya JAJHO, sihitaji kuona damu ikimwagika zaidi, nawaachia kila kitu” alisikika Robert mara baada ya kutoka kituoni hapo. Hakuwa tayari kuchukua mali ya kampuni hiyo iliyokuwa na historia ndefu ya mauaji, aliona jambo la msingi ni kutochukua kitu na zaidi biashara zake aliamini zilimtosha. Baada ya miaka kumi Robert alikuwa tajiri mkubwa katika jimbo la Illinois, Marekani na tayari alishaanza kusahau matatizo yaliyoikumba familia yake miaka kadhaa iliyokuwa imepita. Tayari alikuwa na watoto wawili na alikuwa akifurahia maisha ya ndoa na Annie, kumbukumbu zake zilikuwa hazimtoki kichwani juu ya kifo cha familia yake na mchumba wa kaka yake Magreth. Siku zote katika maisha yake sala zake alimaliza kwa kusema ‘Mungu Azilaze Roho Zao Mahali Pema Peponi’.
Simulizi : Anga La Washenzi (2) Sehemu Ya Kwanza (1)
ILIPOISHIA
Alipomaliza kula akalipia na kunyookea ubalozi wa China. Humo ndani hakumkuta balozi bali msaidizi wake. Wakateta kwa lisaa limoja kabla Jona hajatoka ndani ya jengo hilo.
Kitendo cha kutoka tu, ikachukua dakika mbili, Sheng akaarifiwa juu ya ujio wa Jona. Na shuku zake zote alizozileta ubalozini!
ENDELEA
Sheng akaweka simu yake chini kisha akashusha pumzi ndefu akiwaza. Akawasha sigara yake kubwa na kuinyonya akijizungusha na kiti kwenda huku na kule.
Jona … Jona … Jona … kichwa chake kiliimba hili jina. Inawezekanaje mwanaume mmoja akamwangaisha na kumkosesha amani kiasi hiki? Mtu mmoja? Chawa mmoja kwenye nywele?
Hapana! Akang’ata sigara yake na kuitafuna kwa hasira. Huu ulikuwa ni udhalilishaji wa hali ya juu! Na hauvumiliki. Kabla hajanyanyua simu yake kupiga, mara ikaita, akapokea.
Walikuwa ni vijana wake waliopo Nairobi wakimuuliza kama kuna haja ya kuendelea na zoezi lao la kummaliza bwana Kamau Githeri ama waachane naye kwa sasa.
Akawaamuru warudi nyumbani kwanza. Hali si shwari. Lazima bwana Kamau atakuwa analindwa kwa hali ya juu, na macho ya wanausalama yatakuwa kwake muda mwingi tangu tishio hilo.
Aliposema hayo, akawataka vijana warudi nyumbani, kuna kazi ya kufanya. Tena warudi upesi mara moja!
Akaweka simu chini na kutumbukiza mikono mfukoni. Akafuata dirisha kubwa lililopo ofisini mwake alafu akatazama nje akitafakari.
Baada ya kama dakika kumi na tano, akampigia simu mhasibu na kumuagiza atenge shilingi milioni mia moja kwa ajili ya oparesheni kabambe. Majira ya jioni kabla hawajafunga ofisi kuondoka, ahakikishe pesa hiyo inafika ofisini kwake pasipo kukosa.
**
“Hodi!”
Ilibishwa mara moja na kuitikiwa. Ni ndani ya nyumba ndogo ya wastani ipatikanayo maeneo ya Kimara, Dar es salaam.
Kwa kuitazama tu, nyumba hii ilikuwa na takribani vyumba vitatu. Na kama kuna cha zaidi basi ni jiko, choo na bafu. Jona alipekua kwa macho ya haraka akingoja afunguliwe mlango.
Mazingira ya hapo hayakuwa tulivu sana. Si kwasababu ya kelele toka ndani, lah! Bali toka kwa majirani. Uzio kuzunguka nyumba hiyo ulikuwa umejengwa ndani ya muda mfupi. Na kwa Jona alidhani pengine ni sababu ya makelele hayo ayasikiayo, mwenye nyumba alikuwa anataka kujitenga kidogo na muingiliano mkubwa ndani ya eneo hili.
“Karibu,” alisema mwanamke mmoja mnene mweupe aliyevalia dira akikatisha uchambuzi wa Jona kichwani. Mwanamke huyu kwa makadirio ya Jona alikuwa na miaka 45 – 50. Na ndiye shangazi yake Miriam.
“Ahsante.” Jona akaingia ndani wakasalimiana.
“Nimemkuta Miriam?”
“Ndio, yupo anaoga. Baada ya muda mfupi atakuwa hapa.”
“Ahsante. Nitangoja.”
“Unatumia kinywaji gani?”
“Maji yanatosha.’
Mwenyeji akamletea Jona maji ya kunywa na kisha akaketi.
“Wewe ndiye Jona?”
“Ndio, ni mimi.”
“Naomba umsaidie mwanangu, tafadhali. Naomba sana baba. Hana amani wala raha. Amedhoofu mno. Wale washenzi wamemchakaza haswa!”
“Amekuambia nini kuhusu hao watekaji wake?”
“Mengi tu, nadhani atakueleza mwenyewe kwa undani. Ana taarifa za kutosha kabisa zitakazowasaidia kuwatia nguvuni.”
Jona akamiminia maji kwenye glasi na kunywa mafundo matatu akipeleka macho yake hapa na pale. Ndani ya muda mfupi akagundua mama huyo ni mjane kwa kuona picha za mumewe zikiwa zimetundikwa ukutani na maandishi ya kumtakia kheri huko aliko.
Zaidi akafahamu mama huyu ajihusisha na shughuli za utengenezanaji bidhaa kwa mikono baada ya kuona vyeti kadhaa za maonyesho na tuzo za utambulisho pia toka SIDO.
“Ulikuwa unayafahamu mahusiano kati ya Miriam na huyo mwanaume aliyemteka?” Jona akauliza.
Shangazi akanyamaza kwanza kidogo. Kuna kitu kilimkaba kuropoka. Alikodoa macho yake na kuyafumba, akang’ata lips.
“Kusema ukweli nilikuwa nayafahamu, japo sikuyaridhia kwakuwa Miriam alikuwa tayari ndani ya ndoa. Japo aliniletea mashtaka kadhaa toka kwa mumewe, sikuona haja ya kumshauri aachane naye, sisi ni wakristo, ndoa ni moja tu.”
“Huyo mwanaume ashawahi kuja hapa? Mnajuana?”
“Hajawahi kufika hapa japo namjua kwa sura.”
“Ulimwonea wapi?”
“Kwenye simu ya Miriam.”
“Miriam alivyopotea ulikuwa unafahamu alipo?”
“Nilikuwa najua yupo Arusha lakini sikujua haswa ni wapi.”
“Kwanini Miriam ameamua kuja kwako baada ya kutoka Arusha na si kwenda kwa maa mdogo wake aishiye Kinondoni?”
Kabla shangazi hajajibu hili, Miriam akafika. Alitabasamu kumwona Jona, tabasamu la matumaini. Akamsalimu na kumkaribisha. Shangazi akawapisha.
Pasipo kuchelewa wakaanza maongezi yao. Miriam kwa hisia sana akaeleza namna alivyokuwa anatendewa mpaka alivyojinasua. Akamweleza Jona nini Nyokaa anafanya na wapi anapatikana.
Habari hizo zikamtosheleza Jona. Sasa akapata wapi pa kuanzia kumuwinda Nyokaa. Kufanikisha hilo, Miriam akamuahidi kumuunga mkono kwa asilimia zote, lakini pia hakusita kumpatia tahadhari.
“Kuwa makini, si watu wazuri kabisa. Hawaoni shida yoyote kumuua mtu kisha wakamnyofoa viungo vyake na kwenda kuviuza.”
Hili kwa Jona lilikuwa jipya. Hakujua kama Nyokaa, mbali na biashara ya madini, anafanya pia na biashara ya viungo vya binadamu akivisafirisha kwenda Afrika ya kusini.
Kwasababu hii basi, amekuwa akiteka nyara watu na kuwahifadhi baada ya muda kisha akiwaua na kwenda kuuza viungo vyao kama vile: figo, maini na moyo.
Hata hapo wanapoongea na Miriam, kulikuwa kuna watu huko waliotekwa na wengine wakiwa watoto.
Hili likamgusa Jona katika namna ya kipekee.
“Sasa unahitaji kwenda rehab, Miriam,” Jona akashauri.
“Nataka, lakini nahofia sana usalama wangu. Hata hapa ninapokaa, Nyokaa anapafahamu, anaweza akatuma watu waje kunimaliza.”
Jona akajaribu kumtoa hofu kwa kumwambia atamuweka chini ya ulinzi kwa wakati wote huo atakaokaa hapo lakini bado kwa Miriam hilo halikutosha kabisa.
Hakuna mtu aliyekua anamwamini anaweza kumlinda isipokuwa Jona mwenyewe.
“Usijali, nitakuwa nakuja kukutembelea na tutakuwa tunawasilana mara kwa mara, sawa?”
“Sawa.”
Kwa namna Miriam alivyoitikia ilikuwa ni kama anataka kumridhisha Jona. Hata Jona naye alilitambua hilo. Hakupuuzia yale maelezo aliyoyasema Miriam juu ya usalama wake lakini aliona kwa hatua hiyo itakuwa njema huku akitafuta namna bora zaidi.
Akamuaga Miriam anaenda zake. Alikuwa amechoka mno kwa siku hiyo, aliona ni kheri aende nyumbani kupumzika.
Lakini kabla ya kunyookea huko akaenda kituo cha polisi cha karibu na kutoa taarifa juu ya Miriam akitaka mwanamke huyo pamoja pia na makazi yake yatazamwe kwa jicho la kipekee kwani wapo hatarini.
Alipokamilisha zoezi lake hilo akajiweka kwenye daladala kurudi nyumbani.
Akiwa njiani akatathmini kazi yote aliyofanya kwa siku hiyo. Haikuwa mbaya, akajivunia. Kila kesi iliyokuwa mikononi mwake ilikuwa imefikia pazuri na ufumbuzi wake unaonekana.
Akafika nyumbani na kumkuta Marwa akiwa ameketi sebuleni.
“Pole kwa upweke.”
“Nilikuwa na mke wangu, sikuwa mpweke.” “Mke wako?”
“Ndio.”
Marwa akaonyeshe tarakilishi yake mezani. Jona akacheka.
“Msalimie mkeo, mwambie shemeji anamsalimu.”
“Na wewe pia, msalimu wa kwako aliyeko ndani ya jokofu,” Marwa akatania. Jona akacheka tena, akamwambia mwanaume huyo ni namna gani hawezi kulala mpaka atie kinywaji mdomoni.
Kichwa chake kimekuwa kikifikiria sana familia yake, haswa wakati wa usiku.
“Huoni sasa ni muda wa wewe kutafuta mtu mwingine?” Marwa akauliza. Jona akamtazama mwanaume huyo na kumkubushia yale maelezo aliyompatia yeye kipindi kile.
Akimpata huyo mwingine, atamuweka hatarini. Alafu kwa sasa yu bize hatokuwa radhi kusumbuliwa na ‘calls’ na jumbe za mara kwa mara.
“Unajua wanawake muda mwingine wana matatizo. Unaweza ukawa unafuatilia kesi nyeti sana, pengine raisi ameuawa, lakini yeye akakutumia ujumbe ukiwa kazini ‘ina maana raisi ni muhimu kuliko mimi?'”
Wakacheka. Jona akaendea jokofu na kutoa kinywaji, akatafuta na glasi akaviwek mezani. Akawambia Marwa kuwa amechoka sana lakini hataweza kulala pasipo kinywaji.
“Nikuwekee kidogo?”
“Hapana!”
“Najua imekupelekesha sana asubuhi ya leo. Wewe si mlevi.”
“Umejuaje?”
“Hakuna swali ninaloulizwa sana kama hilo. ‘Umejuaje?’,” Jona akatabasamu na kuongezea: “Anyways, hauna sura ya pombe. Niambie kama nadanganya.”
Wakaendelea kuteta kidogo, na jambo la maana walilozungumza kabla Jona hajapitiwa na usingizi wa kilevi, ni kesho yake waende kuwatembelea wazazi wake Marwa.
Jona alikuwa anataka kuona antidote wanayoitumia. Pengine anaweza kuifutia ufumbuzi.
Marwa akajikuta anapata moyoni. Alitokea kumuamini sana Jona. Aliamini mwanaume huyo atalipatia swala lake ufumbuzi japo hakujua ni kwa namna gani.
Hii inaitwa imani.
Alimtazama Jona akiwa amelala kwenye kiti, akamnyanyua na kumbeba kisha akaenda kumlaza kitandani. Akamfunika na shuka jepesi.
**
Saa mbili asubuhi.
“Jona, hili ni kushangaza kabisa!” Alipayuka Kamanda. “Leo punde nilipofika tu ofisini, nimepokea ujumbe toka kwa mtu nisiyemjua akijiita ‘msamaria mwema’. Taarifa zake zimeniogopesha sana, na zaidi zimenifanya nikatafakari kwa kina ni nani mtu huyo na kama ujumbe alionitumia unaweza kuwa kweli.”
Kamanda akabofya tarakilishi yake wakati Jona ‘aliyekula’ suti akimtazama kwa umakini. Kidogo Kamanda akamkabidhi Jona tarakilishi yake apate kusoma ujumbe huo.
Jona akaupitia kwa wepesi kisha akamtazama Kamanda.
“Umeupata ujumbe huu mwenyewe?” Akauliza.
“Sijajua. Ila huyu mtu amejuaje akaunti yangu ya barua pepe?”
Kabla Jona hajajibu, simu ya mezani ya Kamanda ikaita. Akainyofoa kwenye kitako chake na kuiweka sikioni. Alikuwa ni Kamanda mkuu. Naye amepata ujumbe kama alioupata Kamanda kwenye akaunti yake.
Wakateta kwa dakika kadhaa. Kisha,
“Sawa mkuu,” Kamanda akamalizia simu yake na kuirejesha kwenye kitako chake alafu akalaza mwili kitini.
“Jona,” Kamanda akaita. “Sheng Li ana kesi nzito ya kujibu. Hizi tuhuma si nyepesi hata kidogo. Muite kituoni na hii kesi utaibeba wewe.”
Kisha akamtazama Jona kwa macho ya pole, yenye kiini cha msisitizo.
“Anza upelelezi mara moja!”
Sasa tunda lilikuwa limekwiva. Kifuani Jona akatabasamu akiona sasa muda wa kumuingia Sheng kwa miguu yote umeshawasili.
Alikuwa analingoja hili kwa muda.
Akanyanyuka akibeba jukumu hilo na kurudi ofisini kwake alipotulia na kumpigia simu Marwa. Akamwambia njia yake imezaa matunda. Wamepata kile walichokuwa wanakitaka!
“Sasa mji wa Roma unaanza kuanguka. Kwa ushahidi tulio nao Sheng haweza kututoka abadani!” Jona akatilia muhuri.
Baada ya lisaa limoja akatoka ofisini, akiongozana na wenzake wawili, wakaelekea kwenye ofisi ya Sheng. Huko wakamkuta mwanaume huyo akiwa ana kikao kifupi na wafanyakazi wake wawili wenye asili ya China.
Akapewa taarifa ana ugeni toka polisi. Alipotazama kwenye kamera, akajikuta anatabasamu baada ya kumwona Jona!
Tabasamu lake hili halikuwa la furaha, bali kifo. Hasira na chuki. Alitetemeka kwa hasira na hata kikao chake hakuweza tena kuendelea nacho, akakivunja mara moja akihaidi watakifanya tena pale atakapotoa taarifa.
Jona akaingia ofisini.
“Bwana Sheng, naitwa inspekta Jonathan toka makao makuu, polisi,” Jona akaonyeshea kitambulisho chake kisha akaelezea dhumuni la ujio wake kumtaarifu Sheng kuwa yupo chini ya upelelezi maalum kwa kuhusishwa na tuhuma kadhaa za mauaji, biashara za magendo, vilevile umiliki haramu wa jeshi.
Jona akamtajia orodha ya viongozi anaotuhumiwa kuwaua hapa nchini na nchi jirani, Kenya. Akamtajia ‘kambi zake za jeshi’ iliyopo hapo makaoni na Nairobi na biashara zake anazofanya.
Sheng akabadilika rangi kuwa mwekundu. Lakini akamudu kutabasamu na kumtazama Jona kwa utararibu. Akamuuliza:
“Mbona sielewi unachokiongelea inspekta?”
“Unaelewa kila kitu,” Jona akasema kwa hakika. “Kila nilichokieleza hapo kina uthibitisho na ushahidi. N jambo la muda sasa uovu kukaa wazi. Hakuns linalodumu milele, Sheng!”
Sheng akashindwa kuzuia hasira zake, akakunja sura sasa. Moyo wake uligeuka kuwa barafu. Mikono yake ilitetemeka akiwaza kama ana haja ya kutoa bunduki yake kwenye droo awamalize polisi hawa mara moja alafu awazike kwenye himaya yake.
Lakini hapana! Kwa kufanya hivyo ataharibu zaidi. Mpaka polisi hao wamefika hapo ni wazi huko makaoni kuna taarifa zao. Endapo akiwaua, atawakaribisha nzi zaidi kwenye kidonda ambacho anaweza kukificha.
Leo Sheng akawa amejifunza somo moja muhimu sana. Si kila mahali wapaswa kutumia bunduki. Pale mbu anapotoa juu ya korodani, ndipo unapoelewa kwamba si kila jambo husuluhishwa kwa nguvu.
Akairudishia vizuri droo yake yenye bunduki alafu akatabasamu.
“Ni tuhuma,” akasema kwa lafudhi yake ya ki-Mandarin. “Sishangazwi na tuhuma hizo, najua mimi ni mfanyabiashara mkubwa siwezi kukosa maadui wa kuniharibia.”
Akaonya.
“Endapo tuhuma hizi zitakapobainika ni za uongo basi wanasheria wangu watahakikisha serikali inanilipa fedha nyingi sana kama fidia ya kunisumbua … na utambue kabisa, Jona. Hili litahatarisha uhusiano uliojengwa kwa muda mrefu kati ya nchi hizi mbili. Na sina haja ya kukuelezea ni kwa namna gani mnavyonufaika na uhusiano huu, kila mwananchi anajua.”
“Lakini si kila mwanachi anajua mnayoyatenda,” Jona akamkatiza. “Hawajui pia mnavyonufaika katika haya.”
Akanyanyuka na kumtaka Sheng afike kituo kikuu cha polisi kesho yake asubuhi na mapema. Kushindwa kufanya hivyo kutamuweka matatani vilevile kutaweka bayana asubuhi na mapema kuwa tuhuma zake ni za kweli.
Aliposema hayo Jona akaaga na kwenda zake. Sheng akabaki akisaga meno. Alishindwa hata kuongea. Moyo wake ulikuwa unamuenda kasi. Jona alimfanya ajione ni mtoto mdogo asiye na kitu, mdhaifu na hana akili!
Hakuwahi kudhalilishwa kiasi hiki. Akalalama kifuani. Haikuwahi kutoka hata siku moja.
Alinyanyuka akaendea jokofu akafungua na kutoa maji makubwa, akanywa yote kana kwamba alikuwa na kiu cha karne!
Alitaka kupooza hasira zake. Alihisi kifua kinawaka moto. Baada ya hapo, angalau akijihisi ana unafuu, akarejea kitini, akawaza namna ya kufanya.
Ilimbidi awe mwangalifu sasa. Hata kama anataka kumwangamiza Jona basi afanye hilo kwa pole, kwa ustadi, mikono yake isinuke damu kualika nzi.
**
“Mlitumwa na nani kwenda kumvamia Marwa?” Aliuliza Jona akiwatazama wanaume wawili mbele yake. Wanaume hawa mmojawao alikuwa ni dereva, na mwingine akihusika moja kwa moja kwenye tendo la utekaji wa Marwa. Walikuwa wamevalia suruali zao za vitambaa huku vifua vikiwa wazi, mikono na miguu imefungiwa vitini.
“Hatukutumwa na yeyote yule!” Dereva akaropoka. “Tumeshasema tulikuwa tunamdai kwa muda mrefu, tulikuwa tunataka pesa yetu!”
“Nimeshaambiwa ninyi ni wabishi. Hampo tayari kusema lolote. Mmefunzwa kukaa kimya, mmefunzwa kupambana na mateso, lakini mimi pia mimefunzwa kutesa. Ebu tuone nani mshindi.”
Jona akatumia robo saa tu, akapata kila anachokihitaji. Wanaume wale hawakuweza kustahimili mateso aliyowapa wakaweka bayana kila jambo kwamba walitumwa na Sheng kumchukua Marwa wampeleke akajibu mashtaka yake.
Jona akataka maelezo zaidi kutoka kwao, ni wapi Sheng anapozikia wafanyakazi punde anapowaua? Hapa watumishi hao wakaleta tena ka ubishi, Jona akarejea zoezi lake la kuwabana pumzi akiwapiga nyundo za mbavu!
Hawakustahimili, wakalegea. Wakaeleza. Maelezo yote hayo Jona akayaandika na kumfikishia Kamanda.
“Hakikisha kesho atakapofika hapa, unamtia ndani kisha unaenda fanya msako kwenye himaya yake nzima. Utakapokuta miili hiyo ardhini utakuwa ushahidi mzuri sana. Itasaidia ku ‘finalise’,” Kamanda akapendekeza.
“Sawa, mkuu, nitalifanyia kazi!” Jona akalibeba hilo kisha akatoka zake nje ya ofisi.
“Wo genben bù xihuan ta,” (Simpendi kabisa,) sauti nyingine ikajibu. “Wo suoyào de zhishì siwáng!” (Ninachokitaka afe tu!)
Kukawa kimya kidogo.
“Nàme ni you shé me jìhuà?” (Kwahiyo nini umepanga?)
“Wo xiang qieduàn ta yilài de shou,” (nataka kukata mkono anaoutegemea,) kisha akaongezea, “Ni huì bang wo ma?” (Utanisaidia?)
“Wo huì bangzhù,” (Nitasaidia,) mwingine akajibu.
“Názhe ta. Ni huì zài jiudiàn de àn bian kàn dào ta.” (Chukua hii. Utamwona kwenye fukwe ya hotel.)
Baada ya muda wa dakika tano, ndani ya ofisi ya Sheng akatoka mchina aliyebebelea mkoba mkubwa mweusi. Akapanda Range rover modeli ya zamani, rangi ya grey, akaelekea Sea View hotel.
Baada ya mwendo wa dakika kadhaa akawasili, akaingia hotelini na asichukue muda mrefu akatoka akiwa na mikono mitupu. Akazama ndani ya gari na kupiga simu.
“Ta xiang yào duoshao?” (Anahitaji kiasi gani?) Sauti ikauliza simuni.
“Ba jiàgé fan bèi nàme gàosù ni zenme xiang!” (Ongezea mara mbili alafu sema unatakaje!) Mtumishi akajibu.
“Méiguanxì!” (Sawa!) Sauti ikamjibu simuni.
Baada ya kuteta huko na kukubaliana, mtumishi akawasha chombo chake na kutimka. Sheng akatabasamu akiwa ofisini. Sasa mambo yalienda kama alivyotarajia.
Akajilaza kwenye kiti na kunyanyua simu kumpigia mhasibu, akamwambia amletee tena milioni mia moja. Alipoirudisha simu mezani, akatabasamu tena. Hakika hakutegemea kama siku hiyo ingeisha vizuri.
**
Bado mpaka saa moja usiku …
“Tuondoke, muda umewadia,” akasema Jona akimtazama Marwa. Walikuwa wameketi ndani ya sebule ndogo ya kawaida lakini ikiwa imepambwa kwa usafi wa hali wa juu.
“Hatumngojei baba?” Marwa akauliza.
“Muda umeenda, Tutakuja siku nyingine,” Jona akashauri na mara kidogo akatokea mama mtu mzima, makadirio miaka sitini kasoro kidogo. Alikuwa mwembamba mwenye nywele za mvi, lakini akiwa mwenye nguvu na uchangamfu.
Akaketi kitini.
“Naona baba amechelewa sana leo,” akasema. “Sijui atakuwa amepitia wapi!”
“Usijali, mama,” Marwa akamtoa hofu. “Tutakuja siku nyingine kumwona. Kwa sasa tunaomba tukukimbie.”
“Mbona mnawahi hivyo na mmekuja muda si mrefu?” Mama akashangaa. “Kaeni mumngoje kidogo. Nadhani ndani ya muda mchache, atawasili.”
“Kuna mahali tunatakiwa kupitia mama,” Jona akaeleza. “Tungekaa mpaka usiku mzito.”
Mama hakuwa na budi, akawatakia safari njema lakini kabla hawajaondoka akahitaji aongee kidogo na Marwa. Jona akatangulia kwenda nje.
“Vipi? Mbona unaondoka haujatupatia dawa?” Mama aliuliza, na kuongezea. “Unajua imebakia kiasi kidogo sana!”
Akafungua fundo lake la kanga na kutoa kachupa kadogo kumwonyeshea.
“Unaona?”
Ndani ya kachupa hako kulikuwa na kama katone hivi ka maji ambacho kukaona ilihitaji umakini wa hali ya juu.
“Nimeona, mama,” Marwa akasema kwa upole. “Nitakuletea tu.”
“Kaburini?” Mama akastaajabu. “Unadhani haka katatuweka hai mpaka lini, Marwa?”
Marwa hakuwa na la kusema, akatazama chini.
“Kuna shida gani, Marwa? Naomba uniambie. Dawa imeisha?”
“Hapana.”
“Sasa nini shida? Niambie mwanangu.”
Marwa akajikuta macho yake yanakuwa mekundu. Sauti ya mama yake ilikuwa inatafuna moyo wake. Alitamani kumwambia hayupo tena kule apatapo dawa lakini alihofia. Angeweza kumuua mamaye kwa presha.
Akamtia tu moyo ampe kitambo kidogo, atakuwa ameshaleta dawa hapo nyumbani.
“Kama kuna shida tuambie,” Mama akamwambia akimshika bega. “Sisi ni wazazi wako, hauna mtu mwingine wa kumwaminini.”
“Hakuna shida mama,” Marwa akakazana. Alikaza uso wake usionyeshe majonzi. Akamkumbatia mama yake na kumuaga. Lakini alipogeuka tu chozi likamshuka haraka. Moyo wake ulikuwa unamuuma. Alikuwa anashuhudia wazazi wake wakifa mbele ya macho yake.
Alienda kukutana na Jona wakaenda zao. Hakusema jambo mpaka wanafika nyumbani.
“Marwa, it’s going to be ok!” Jona akamfariji. “Tutapata antidote tu.”
Marwa akajikuta anadondosha chozi. Akamtazama Jona na kumwambia shida si kuipata, bali muda. Antidote aliyoiona inawatosha kwa usiku huo wa leo tu. Kesho yake hawatakuwa na cha kutia mdomoni, wataanza kuteseka mno.
“Kwa umri wao ilibidi wawe wamepumzika, si kupitia shida hizi,” alisema Marwa kwa uchungu.
Jona akamtazama kwa huruma. Baada ya mafikirio kidogo, akamuuliza:
“Unajua antidote hiyo ilipo?”
“Kivipi?”
“Unafahamu mahali wanapoihifadhi antidote hiyo kule kwa Sheng?”
“Si mbaya,” Jona akateta. “Basi jiandae saa tano tunaenda huko!”
“Wapi?” Marwa akatahamaki kwa woga.
“Ilipo antidote!” Jona akafafanua. Na asingoje maelezo zaidi, akaenda zake chumbani. Marwa akabaki anamtazama kwa mshangao.
**
Baada ya kunyata kidogo,
“Upande huu!” Marwa akaelekeza kwa sauti ya chini. Alikuwa amevalia nguo nyeusi na kinyago usoni. Na Jona pia.
Walikuwa tayari wameshazama kwenye ngome ya Sheng katika majira haya ya saa sita usiku. Lengo lao likiwa moja, kwenda kuinyaka antidote ndani ya maabara.
Wakatembea tena kwa utaratibu wakichukua kila tahadhari, walipokaribia maabara, wakamwona mwanaume mmoja aliyebebelea bunduki kubwa ndefu mkononi. Jona akaitambua ni SMG.
Mwanaume huyo alikuwa ni mlinzi. Alikuwa ameketi kwenye kibaraza cha jengo la maabara akichokonoa meno yake kwa kijiti.
Jona akampanga Marwa.
“Utatoka na kunyata kuelekea upande huu,” akamwonyeshea upande wa kushoto. “Lazima atakutazama na aidha anaweza kukuita. Lakini kabla hajafanya kitu, atakuwa tayari yupo mikononi mwangu.”
Marwa hakupewa muda wa kufikiri, Jona akaanza kutekeleza mpango. Haraka akanyanyuka na kutembea upesi kuelekea upande wa kulia, lakini akifanya hayo miguu yake haikutoa sauti hata kidogo.
Basi muda mchache, mlinzi akamwona Marwa akikatiza, haraka akanyanyuka na kuishikilia vema silaha yake. Akapaza sauti:
“Wewe nani?”
Marwa akasimama na kumtazama.
“Mimi? Mimi naitwa Marwa!”
“Marwa?” Mlinzi akatahamaki. Hakuwa analijua jina hilo katika orodha ya walinzi. Akamtaka Marwa anyooshe mikono juu na kupiga magoti.
“Sina tatizo na wewe,” Marwa akasema akishuka chini. “Mwenye tatizo ni huyo aliyepo nyuma yako.”
Haraka mlinzi akageuza shingo kutazama. Mara shingo hiyo ikadakwa na kuendelezewa safari. Akadondoka chini kama mbuyu.
Wakamficha, kisha chap wakaufuata mlango mzito wa maabara. Ulikuwa ni mlango wa chuma wenye kitasa kipana. Wakajaribu kuufungua pasipo mafanikio.
“Jona, inabidi tukachukue funguo!”
“Wapi?”
“Stoo. Kule wanapozihifadhi.”
“Hatuna muda huo Marwa. Mlinzi mwingine anaweza kutokea akagundua uwepo wetu. Na endapo akirusha risasi moja tu, atakuwa keshatibua mambo.”
“Sasa tunafanyaje?”
Jona akavua mkanda wake na kuchomoa kichuma cha kushikilia vitundu mkandani. Akakipinda kichuma hicho kwa mdomo, akitumia sekunde kadhaa kama ishirini, alafu akakidumbukiza hicho kichuma ndani ya kitasa.
Akapeleka mkono kushoto na kulia, mara mlango ukalia – kat! Wakajaribu kuufungua. Hola! Mlango haukufunguka.
“Shit!” Jona akalaani.
Akakirepea tena kile kichuma kwa kukibadili muundo wake, alafu akajaribu tena. Mlango ukalia tena – kat! usifunguke.
“Hapana, Marwa,” Jona akatikisa kichwa. “Mlango huu umelokiwa mara tatu, utafunguka tu … ngoja uone …”
Jona akachokonoa tena kitasa, mlango ukalia tena – kat! Na mara hii walipougusa ukatii amri! Wakazama ndani.
Maabara ilikuwa kubwa. Wakitumia kurunzi kuangaza, wakaanza kupekua upesi upesi. Wakachukua dakika nyingi humo. Baadae ndipo wakaona chumba kidogo ndani ya maabara kikiwa kimeandikwa antidote mlangoni.
Jona akafanya ufundi kufungua kitasa kisha wakazama humo ndani, baada ya muda kidogo wakatoka Jona akiwa amebebelea flask – chupa ya kioo yenye mdomo mwembamba chini ikiwa imejitanua mithili ya pembe tatu. Ndani ya chupa hiyo kulikuwa na kimiminika mithili ya maji.
Kwa haraka wakajongea kuufuata mlango wa maabara, lakini kabla hawajaufikia, Marwa akajikwaa. Mguu wake ulidumbukia ndani ya vifereji vidogo vya kutolea uchafu, akajikuta yu chini kwa kukosa namna ya kujiokoa!
Kabla hawajafanya jambo, ndani ya muda mfupi, wakasikia chupa kadhaa nazo zikidondoka na kusababisha kelele!
Mara huko nje, sauti nzito ikauliza:
“Nani huyo?”
Alikuwa ni mjibaba wa miraba minne, mkononi akiwa ameshikilia bunduki ndogo.
Mwili wake mpana kama gogo ulikuwa umesitiriwa na nguo nyeusi. Chini ana buti kubwa rangi ya kaki. Kichwa chake kinameremeta kwa kukosa nywele. Na mdomo wake ukiwa umefunikwa na mustachi mzito wenye afya tele.
Jibaba hilo likalalama.
“Yani hawa panya sasa naona wananipanda kichwani!”
Likapiga hatua nzito kuufuata mlango lakini kabla hajaugusa, akauliza:
“Isak yupo wapi?” Akitazama huku na kule kisha akalalama;
“Hawa panya watamaliza vitu vyote humu ndani. Experiment gani hizo za kila siku kutumia panya!”
Akasonya.
“Hakuna mnyama namchukia ka –“
Akashtuka kuona mlango una upenyo. Asiamini macho yake akausukuma kwa kidole, mara ukafunguka na kuachama. Akapata wasiwasi. Akashikilia vema bunduki yake na kuzamisha mkono ndani, akabofya switch, taa zikawaka!
Akaangaza akinyooshea bunduki yake huko. Kwa mbali akona chupa kadhaa zikiwa zimepasuka. Akapiga hatua kusonga.
Pembeni ya chupa hizo zilizopasuka, kwa chini ya meza za sementi zilizokuwa zimejengwa humo, alikuwa amelala Marwa.
Alikuwa ameubana mdomo wake kwa nguvu akijitahidi kutulia lakini alikuwa anasikia maumivu makali sana. Chupa zile zilizoanguka zilimrushia kemikali usoni na alikuwa anahisi kuungua!
**
Yule mtu wa miraba akafika eneo hilo lililopasukia chupa, akaangaza akisukuma sukuma vyupa kwa buti lake jeusi akiwa amebinua mdomo. Akatazama kushoto na kulia. Akasonya lakini kabla hajapoga hatua akauona mguu wa Marwa. Akashtuka kana kwamba ameona nyoka kwenye majani.
Akaamuru upesi Marwa atoke kwa uhai wake kabla hajamwaga ubongo.
Kwa uoga Marwa akaanza kujisogeza akiomba asiuawe. Akatoka akiwa ameshikilia uso wake alioukunja kwa kuhisi maumivu makali.
“Wewe nani?” Akauliza mtu mnene. Bwana, hakukaa sawa akala jiwe la kichwa!
Si jiwe unalolijua wewe bali ngumi. Akadondokea chini kama kiroba cha tani. Kuangaza akamwona mwanaume akiwa amesimama mbele yake hatua kadhaa.
Akaguna kwa kebehi. Akatazamia bunduki yake, akatahamaki Marwa ameshaikomba na kuijaza kiganjani.
Akacheka. Akapangusa eneo alilopigwa kisha akasimama!
Kwa mtu wa kawaida kwa ile ngumi aliyopewa, asingeamka abadani. Kwa unafuu angezirai, ila kawaida ni kufa tu.
“Najua hamuwezi nipiga risasi!” Jamaa akagamba. “Mkipiga risasi mtashtua jengo zima hili, na ndani ya sekunde tu mtageuzwa bucha. Kama nyie ni wanaume kweli, kunja!” Akatapa akitoa macho yake makubwa mithili ya bundi.
Kwakweli alikuwa anaogopesha. Mwili wake ulijawa na misuli na kwa kumtazama tu ungetambua amekomaa haswa. Nguo zilikuwa zimembana.
Jona akamtaka Marwa ashushe bunduki, na asogee kando. Wakatengeneza ka uwanja kadogo kwa ajili ya pambano.
“Utatambua kwanini nilipewa jina la Baba!” Akatapa jamaa akijitambulisha. Akanyoosha shingo yake kisha mabega, ka!-ka!-ka! Akanyoosha vidole ka!-ka!-ka!
Alafu kama fuso akamfuata Jona. Akatupa mawe ya maana. Ngumi nzito haswa. Jona akazikwepa akisogea nyuma na pembeni.
Baba akaendelea kurusha ngumi za mfululizo, mwishowe Jona katika kukwepa miwani yake ikadondoka chini. Kosa! Akala ngumi tatu zenye uzito wa tani! Akadondoka chini akiachama kwa maumivu makali! Kinyago kilipasuka. Akavuja damu mdomoni na puani kidogo.
Baba akatabasamu kiushindi.
“Amka!”
Jona akapapasapapasa chini kuitafuta miwani yake, Baba akaisukumizia kando kwa mguu, kisha akamnyanyua Jona kama unyoya na kumsogeza karibu na uso wake.
“We ni mtoto kwangu. Mimi ni Baba! Mimi ni nani?”
Jona alikuwa anona maruweruwe kana kwamba mtu anayetazama akiwa chini ya maji ama ameingiliwa na maji machoni. Alikuwa anahangaika kuona lakini hakufanikiwa. Macho nayo yalikuwa yanamvuta.
Baba akamrusha kwa juu alafu akamtwanga ngumi! Akabidukabiduka hewani kabla hajadondokea chini kama mzigo!
Tih!
Akahisi mwili mzima umevunjika. Akagugumia kwa maumivu akijikusanya. Mdomoni alikuwa anamwaga damu.
“Amka!” Baba akasema kwa kejeli akimtazama Jona. Haraka na kwa ukimya, Marwa akatambaa kuifuata miwani ya Jona. Haikuwa mbali sana na yeye. Alipoikamata mkononi akaificha alafu akamwita Baba.
“Hey!”
Baba akageuka kumtazama.
Marwa bado alikuwa anagugulia maumivu ya kemikali, jicho lake moja akiwa amelifunga. Akamkebehi Baba kwa makusudi. Baba akakasirika na kumfuata. Marwa kwa kulenga, akairusha miwani juu ya mwili wa Jona.
Jona akapapasa na kuikamata. Akaivaa.
Baba akamnyanyua Marwa juu kama alivyofanya kwa Jona. Lakini kabla hajafanya kitu, akaguswa begani. Kugeuka likawa kaburi lake. Akapokea ngumi nzito ya shavu, akapepesuka.
Asikae vema, Jona akampatia dabo bundle za teke. Akapepesuka akijakakamua kwa hali na mali asianguke chini.
Jona akaamua sasa kumpatia KATAUTI – Mateke mawili yanayoyofyatuliwa baada ya kiumbe kupaa hewani kwa namna ya mzungusho. Baba akashindwa kustahimili! Akadondoka chini kama tembo.
Jona akamuwahi Marwa kumjulia hali.
“Upo ok?”
“Yah! Am ok!” Marwa akajibu bado akiwa ameficha jicho lake moja.
“Sure?” (Hakika?) Jona akasisitiza.
“Yah! Niko ok!” Marwa akajibu lakini hali aliyomo ikimsaliti. Baadhi ya sehemu zake za uso zilikuwa zimeanza kubadili rangi, Jona aliliona hilo na akapata hofu.
Kabla hajasema kitu, Marwa akamshtua Baba anakuja. Jona akasaga meno na kumwambia:
“Ningoje hapa twende nyumbani.”
Bwana we! Kama kuna kosa aliwahi kufanya Baba tangu azaliwe, lilikuwa ni hili. Kuamka tena. Na hatokuja kulisahau kosa hili maisha yake yote.
Kwa kasi ya ajabu, Jona alimrushia ngumi zisizo na idadi. Akajitahidi kupangua mbili tatu lakini baadae akashindwa. Jona alikuwa haraka mno. Kasi yake ilikuwa ya ajabu!
Mpaka Jona anamaliza, Baba akajikuta hawezi kusogeza kiungo chochote cha mwili. Akadondoka kama mbuyu asiamke tena!
Jona na Marwa wakatoka ndani ya maabara wakiwa wamebebelea antidote waliyoifuata. Wakatembea kwa tahadhari mpaka ukutani, wakaambaa na ukuta huo kwenda mbele, kidogo wakasikia sauti za watu wakiwa wanateta.
Jona akaangaza, akaona watu wakikatiza. Akamuagiza Marwa amngoje kidogo, akasonga na kuchungulia, akawaona wanaume kama kumi kwa idadi. Wote walikuwa weusi. Walikuwa wanatoa maboksi toka chumba fulani hivi na kuyaweka nje.
Kidogo, Jona akamwona mwanaume mwenye asili ya kichina akija hapo. Akafungua maboksi kadhaa na kuyatazama alafu akashika kiuno akiwatazama wanaume waliokuwa wanaendelea kuyaleta.
Hawakuchukua muda mrefu, wakasitisha zoezi. Mchina akayahesabu maboksi yale alafu akapiga simu. Ndani ya muda mfupi, gari aina ya Van jeusi likaja hapo maboksi yakaanza kupakiwa.
Kabla zoezi hilo halijakamilika, mara mlio wa tahadhari ukaita kwanguvu kuhabarisha hali si salama. Wanaume wale wakatazamana, kisha haraka wakaacha kupakia maboksi na kusambaa kila eneo.
Baada ya muda mfupi wakagundua maabara ilikuwa imekwapuliwa, mlinzi mmoja amefariki na mwingine yu hoi hajiwezi.
Kufuatilia nyayo za viatu na matone ya damu wakafika mpaka pale Jona alipokuwa anawachungulia. Wakagundua wameshatokomea.
Taarifa zikamfikia Sheng. Akiwa amevalia ‘casual’ akafika eneo la tukio na kushuhudia kila kitu. Akang’ata meno kwa hasira. Kwa akili yake yote akaamini ni Marwa wakishirikiana na Jona ndiyo wamefanya hayo.
Mosi, Marwa hawezi kupigana kuwaangusha wanaume wale, hivyo alimhitaji Jona. Pili, Jona hakuwa anajua mazingira hayo, hivyo alimhitaji Marwa.
Walikuwa wanaisaka antidote. Si kwasababu nyigine bali kuwapelekea wazazi wa Marwa.
Sheng akaagiza wazazi wa Marwa waangamizwe kabla ya jua la kesho halijazama. Na kuhusu Jona, awachiwe yeye anajua dawa yake.
**
“Inabidi twende hospitali,” alisema Jona akimtazama Marwa kwa muda mfupi kabla hajarudishia macho yake mbele waendako.
Walikuwa ndani ya gari Jona akishikilia usukani.
“Nitakuwa poa tu usijali,” Marwa akasema akiwa amelaza kichwa kitini.
“Hapana, lazima twende hospitali! That is chemical!”
Marwa hata kuongea hakuweza. Alikuwa anasikia maumivu makali. Alihisi kuna michanga na changarawe jichoni huku upande huo wa uso ukiwa unawaka moto.
Wakashika barabara ya kwenda hospitali, wakasonga nayo kwa kwa dakika kadhaa, kabla ya kukata kona kwa mbele kuingia hospitalini, Jona akatazama sight mirror. Akakunja ndita na kusema:
“Nahisi tunafuatwa!”
Marwa akakodoa jicho lake moja lililozima ila ghafla akaliminya kwa kuhisi maumivu. Ni kama vile alipigwa na shoka kichwani.
**
Wakakata kona kuzama ndani ya hospitali, na lile gari ambalo Jona alikuwa analishuku likanyoosha na barabara. Wakatambua kumbe ilikuwa hofu yao tu, hakuna anayewafuata. Ndani ya muda mfupi wakaonana na daktari na kisha kujieleza.
Marwa akaafanyiwa uchunguzi na ikabainika ameathirika na kemikali, mishipa midogo midogo ndani ya macho imeathirika na hivyo jicho lake hilo linaweza kuwa kipofu kabisa ama kufifia uwezo wake wa kuona.
“Kama msingeliwahi zaidi basi lingepasuka ama kulika kabisa akawa chongo,” alieleza daktari. Jona akapata shaka kwa Marwa kuwa na hali kama ya kwake.
Baada ya muda mfupi wakaruhusiwa kutoka hospitalini wakiwa wamepatiwa dawa ya kutia jichoni na kupaka usoni.
Kwa maumivu aliyokuwa nayo na ‘ka ahueni’ alikokapata baada ya kufanyiwa dawa, Marwa akalala akimwacha Jona peke yake anaendesha gari.
Waliwasili nyumbani, Jona akamsaidia Marwa kushuka ndani ya gari na kumpeleka mpaka chumbani akapumzike alafu yeye akajirudisha sebuleni kana kwamba ilikuwa ni saa kumi na mbili jioni wakati muda ulikuwa umeshaenda.
Kwa sasa ilikuwa inaelekea saa tisa na nusu usiku.
Alifungua jokofu atoe kinywaji, akatahamaki hakukuwa na kitu. Vilikuwa vimekwisha. Akalaani vikali. Vimeishaje hata hakutambua? Akaketi kitini akiwa amekangangikiwa na akijilaumu kwa kutotambua hilo mapema.
Uzembe wa aina gani.
Mwili wake ulikuwa unamuuma kwa zoezi alilotoka kufanya ndani ya himaya ya Sheng. Na kichwani pia alikuwa ana mawazo. Alihitaji kinywaji apate kulala.
Awe anakunywa taratibu huku akiichambua siku yake nzima mpaka anapotelea usingizini. Kwa kufanya hivi huwa kunamsaidia kesho aamkapo ajue ni nini cha kufanya.
Akakaa hapo kochini kwa muda mrefu sana. Macho yalikuwa meupe na yenye nguvu lakini mwilo ukowa hoi. Hata akajilaumu kwanini hakuteka vidonge vya usingizi kule hospitali.
Alibadili kila mkao kitini mwishowe akaenda kitandani kujilaza. Muda mfupi akapitiwa na usingizi. Alipolala hapo kwa muda mfupi akakurupuka baada ya kuota ndoto mbaya.
Huwa hivi kila alalapo pasi na kinywaji. Anaota familia yake. Anakumbuka siku aliyowaona wakiteketea ndani ya nyumba yao iliyogeuzwa tanuru.
Akatazama saa, saa kumi na moja! Hata hivyo akashukuru ndoto hiyo kwa kumwamsha ndani ya muda. Akajiandaa kwenda kazini.
Hakutaka kumsumbua Marwa, alijua amechoka sana na kitambo kifupi tu amelala. Akamtazama tu kwa kumkagua na macho yake alafu akaondoka.
Lakini alipokuwa huko ofisini, bado akajihisi mchovu mno. Hakuweza kufanya kazi yake vema. Mwili ulikuwa mzito, alihisi pia kichwa kimeongezeka ukubwa anahangaika kukimudu.
Haikutakiwa awe hivyo siku hiyo. Siku hiyo ilikuwa muhimu mno kwani Sheng alikuwa anafika kituoni kwa ajili ya mahojiano na pia atazamie kama kuna haja ya kumtia ndani.
Alitakiwa awe mwenye nguvu, mwenye hari, lakini haikuwa hivyo.
Akatazama saa yake. Akamuwaza kidogo Sheng na kile walichokifanya jana. Akajikuta anagutuka! Macho yalimtoka kwa kukumbuka jambo. Akabamiza meza.
Shabash! Wazazi wake Marwa!
Haraka akatoka ofisini, akajipakia ndani ya gari na kutimka haraka. Alijilaumu sana kwa uzembe alioufanya. Kivipi aliwasahau wazazi hao?
Bayana hawatakuwa salama kwani Sheng atakuwa ameshagundua kwamba wameiba antidote. Moyoni akawa anasali akute kila jambo jema.
Kwa kasi kubwa akaendesha gari akili yake ikiwa bize. Alipowasili, akakimbilia ndani na kuangaza. Hakukuta mtu sebuleni. Akaita, napo kimya.
Akaenda chumbani. Akajikuta uchungu unamkaba baada ya kuona maiti mbili kitandani!
Wazazi wake Marwa walikuwa wameshauwa. Walididimiziwa risasi kwenye mapaji yao ya uso.
Jona akashindwa kuzuia machozi. Akaishiwa nguvu kabisa. Aliketi kitandani akishikilia kichwa chake kwa manung’uniko na lawama. Kazi yote waliyoifanya ilikuwa bure. Tena ikiwagharimu mara mbili yake.
Kwa muda kidogo akawa hajui cha kufanya. Alihisi kichwa kimeacha kufanya kazi. Hana hisia wala wazo lolote.
Hakufahamu ni kwasababu gani, ila baada ya muda, akajikuta anamkumbuka mkewe. Alijihisi mtupu. Mpweke rohoni. Alikumbuka tabasamu lake na namna alivyokuwa anamkumbatia kila arudipo kazini. Akimbebeleza alale na akimsihi aamke.
Pengine alikuwa anahisi anakosa hayo mambo kwa kipindi kama hiki kigumu. Haikuwa la kuficha, muda huu alikuwa anamhitaji sana mke wake kuliko kipindi kingine chochote.
Akiwa kama mtu asiyejitambua wala kuonyesha kujali akalala hapo na maiti hizo mbili.
Alikuja kushtuliwa na kurejeshwa fahamuni baada ya ujumbe kuingia ndani ya simu yake. Simu ilitetemeka mfukoni, akaichomoa na kuitazama. Ilikuwa ni ujumbe toka kwa Marwa.
‘Naomba unisaidie kuwapelekea wazee antidote’
Jona akatikisa kichwa chake kwa masikitiko. Akaamka na kuidumbukiza simu mfukoni kisha akaendea gari na kujipakia.
Akiwa njiani, simu ikaita. Kamanda.
“Upo wapi na unajua leo Sheng anakuja kituoni?” Kamanda alifoka.
“Nipo njiani, mkuu,” Jona akajibu alafu akakata simu.
Muda mfupi akawa ameshafika na mbele yake, ndani ya ofisi, yupo mwanaume mchina. Mfanyabiashara mkubwa nchini, bwana Sheng tayari kwa ajili ya mahojiano.
Lakini Jona hakuwa sawa. Asingeweza kufanya kazi yake inavyotakiwa. Akamwomba radhi Sheng na kumtaka aje siku nyingine atakayompa taarifa kwani kuna dharura.
Sheng akatabasamu, kisha akamuuliza:
“Unaenda msibani?”
Jona akamtazama kwa jicho kali. Alitamani amrukie mwanaume huyo na kumnyofoa macho kisha ayatafune. Lakini akadumisha hari yake.
“Ndio, naenda msibani,” akajibu. “Bila shaka unaufahamu mi wa nani.”
Sheng akatabasamu tena kisha akasema:
“Mlichofanya jana haikuwa good move. It was one of the most stupid step.”
Jona akamtazama Sheng kwa kitambo kidogo kabla hajamsogelea mwanaume huyo na kumtazama machoni.
“Siku yako ipo karibuni. Nitakuvunjavunja kwa mkono wangu. Utalipa kila tone la damu ulilolimwaga.”
“Siku yangu!” Sheng akacheka. Akatikisa kichwa chake na kupepea kwa kidole. “Yako ndiyo ipo karibuni kuliko udhanivyo. Siku hiyo nitaimark kwenye kalenda na kuisherehekea kila mwaka.”
“Sheng,” Jona akaita. “Mimi ni mfupa mgumu, wewe fisi huniwezi. Umeniwinda mara ngapi nikakurudishia maiti zako?”
“Mara hii haitakuwa kama hapo mwanzo,” Sheng akajitapa. “Hilo nakuahidi.”
Alafu akanyanyuka na kwenda zake Jona akimtazama kwa macho batili. Alifikiria kumsweka mwanaume huyo ndani mpaka atakapomaliza mchakato wa msiba, akaona hamna haja hiyo. Hajafikia hatua ya kumwogopa kiasi hiko!
**
Baada ya siku mbili.
Walikuwa wameyapa mgongo makaburi wakitembea kuondoka zao. Walikuwa wamevalia nguo nyeusi juu mpaka chini. Nyuso zao zikipambwa na miwani, Jona ya macho na Marwa ya jua.
Uso wa Marwa kwa upande wa kushoto ulikuwa mwekundu na hakuweza kustahimili jua, akauelekezea chini. Mikono yao ilikuwa ndani ya makoti marefu waliyoyavaa.
Anga lilikuwa jeusi kiasi, jua kwa wastani, na kulikuwa kuna kila ishara ilkionyesha mvua ilinyesha muda kidogo hapo nyuma.
Walipoyaacha makaburi kwa urefu mdogo wakielekea barabarani, simu ya Jona ikaita ndani ya koti. Akaichomoa na kuitazama, ilikuwa namba mpya. Akapokea na kuiweka sikioni.
Jona hakujua nini maana ya ujumbe huo na hakutaka kujishughulisha nao sana. Wakaendea usafiri wa daladala na kujipakia. Leo hawakuwa na gari kwani alilirudisha kituoni.
Wakiwa humo ndani ya daladala, muda mchache mbele, ndipo Jona akaukumbuka ujumbe ule aliopewa kwenye simu baada ya kusikia taarifa redioni kuwa Kamanda wa polisi mkoa, ameuawa na watu wasiojulikana, usiku wa kuamkia leo!
Akashangazwa sana na habari hizo. Akamtaka Marwa aelekee nyumbani, watakutana baadae. Akaenda moja kwa moja kituoni.
***
Huko inspekta Jona akapata maelezo kuwa Kamanda aliuawa usiku na mtu aliyefika nyumbani kwake na mojawapo ya gari iliyopo kituoni.
Jona akatahamaki. Kwa maelezo hayo maana yake Kamanda aliuawa na polisi? Alitaka taarifa zaidi lakini hakuna aliyempatia. Ilionekana kila mtu ana taarifa nusu nusu, na hakuna mwenye uhakika.
Akiwa amekaa ofisini kwake akitafakari, akakumbuka hata maneno ya Sheng. Je ndiye kammaliza? Hapana. Mbona Sheng alisema atammaliza yeye na si Kamanda?
Au hiyo ndiyo mojawapo ya njia ya kumtafuta? Akawaza sana. Akatamani apatiwe hii nafasi ya kufuatilia hili tukio. Akakaa humo ofisini mpaka majira fulani walipotoka kwenda kuonana na kamanda mkuu wa polisi. Alikuja kuwatembelea.
“Wewe ndiyo Jona?” Kamanda mkuu akamuuliza kana kwamba hamjui. Akampatia mkono.
“Ndiyo, ni mimi, afande,” Jona akajibu kwa ukakamavu.
“Oooh! Nilikuwa nikipata taarifa zako toka kwa bwana Chisanza.”
Bwana Chisanza ndilo jina la Kamanda aliyefariki dunia.
“Alikuwa anakubali kazi zako. Ameondoka ametuachia pengo kubwa sana.” Kamanda mkuu aliendelea kuongea na Jona. Akamshika bega lake la kulia alafu akaenda kwa mtu mwingine afuataye kwenye mstari walioupanga kumpokea mkuu huyo.
Baada ya kusalimiana na kila mmoja, wakapata kuwa na kikao kidogo ndani ya kituo kikuu.
“Hili jambo si la kuvumilika kabisa kabisa!” Alibweka Kamanda Mkuu. “Haiwezekani tukaenda kwa namna hii, lazima jambo lifanyike tena haraka iwezekanavyo, mambo yakae hadharani upesi ili wananchi wasipoteze imani kwa jeshi lao.”
Akanywa maji kupooza koo alafu akaendelea kunguruma.
“Isipite wiki moja … isipite wiki moja huyu muuaji hajakamatwa! Haiwezekani RPC auawe alafu hili jambo likachukuliwa wepesi wepesi tu. It is a serious issue. Na watu wote, nchi nzima wajue hilo. This is a serious issue.”
Baada ya maongezi hayo Kamanda Mkuu akapendekeza Jona apatiwe kesi hiyo mikononi mwake. Akamsihi aitendee haki, na ndani ya muda mfupi awe ameshaonyesha matunda.
Kwa moyo mkunjufu, Jona akabeba jukumu hilo.
**
Aliyapekua mazingira yote ya ndani baada ya kufanya mahojiano na wanafamilia, mahojiano ambayo hayakuwa na matunda mengi kwake.
Kwa ufupi akagundua muuaji alifika na gari na kulipaki nje, akazama ndani kwa kuruka ukuta kisha akamuua mlinzi kwa kumnyonga, na kutulia hapo kwa muda kidogo kabla hajarahisishiwa kazi kwa Kamanda kutoka nje akiongea na simu.
Kamanda alikuwa anaongea na nani kwa muda huo? Na kwanini alitoka nje?
Kwa haraka Jona akaelezwa na kumbukumbu yake kuwa ni yeye ndiye alikuwa anateta na Kamanda kwa muda huo. Kuhakikisha akatazama ‘call log’ kwenye simu yake. Na kuhusu kutoka nje, ni Kamanda alimweleza hivyo baada ya kuona mtandao unasumbuwa awapo ndani.
Kwahiyo basi kwa upesi na wepesi kabisa, muuaji akamaliza tukio lake kwa kumpiga Kamanda risasi tatu za kichwani alafu akatumia tena ukuta na kuyeya.
Sehemu za ukuta alizotumia kuingia na kutoka nazo zililuwa zimechafuka. Na kwa nje ya uzio alipokuwa anatua, aliacha alama za viatu.
Mwanaume wa makamo, kwa mujibu wa ukubwa wa kiatu, na ni mwanaume mzito, kwa mujibu wa kutitia kwa nyayo za viatu ardhini.
Ubaya hakuna aliyekuwa anajua kimo wala mjazo wake wa mwili kwani mtu ambaye angeweza kuwa shuhuda, yani mlinzi, aliuawa na wanafamilia wengine walikuwa ndani wakati wa tendo.
Yani mwanaume mmoja tu alifanya haya, Jona aliwaza akiwa anatazama nyayo za viatu. Akapata wazo. Akapiga picha nyayo hizo na kuondoka zake kwenda kwa majirani kuuliza uliza kama kuna shuhuda yeyote aliyeona jambo.
Lakini akawaza akiwa njiani. Mwanaume huyo muuaji alikuwa anategemea kumuua Kamanda hapo nje au ilitokea kama bahati ya mtende?
**
Alitazama viatu vya wale wanaume aliowakamata kule kwa Marwa akivilinganisha na picha yake ya nyayo za viatu alizozipiga nyumbani kwa Kamanda, akagundua vyafanana.
Hapo Jona akapata kutengeneza picha yake kichwani kwamba mtu huyo alikuwa pia amevalia suti na kinyago usoni kama wafanyavyo wafuasi wa Sheng pindi watakapo kufanya tukio.
Sasa angalau akawa amepata pa kuanzia. Sheng atakuwa anahusika na mauaji haya lakini kwanini amuue Kamanda?
Simu ikaita na namba ngeni. Akapokea.
“Halo … ndio, ni mwenyewe …”
Simu ikakata. Huenda ni salio. Jona akaamua kuipigia namba hiyo na kuendelea kumskiza.
” … usijali, enhe ulikuwa unasema … ndio … una uhakika? … ndio mida ya usiku … sawa, nashukuru kwa taarifa.”
Mtu huyo aliyekuwa anaongea naye alijitambulisha kwa jina la Deo. Alikuwa ni mwanaume mwenye sauti nzito aliyejinasibu kuwa shahidi wa tukio. Ametumia namba ambazo Jona aliziacha kwa majirani kwa maelezo kuwa wakipata cha kumshirikisha basi wasisite kumtafuta.
Bwana Deo akamwambia Jona kuwa alishuhudia gari la watu waliofanya tukio. Na alipolielezea gari hilo lipoje, Jona akajikuta anashangaa kwa kufananisha taarifa hizo na gari walilokuwa wanalitumia yeye na Marwa hapa karibuni.
Habari hizi zikamshtua. Akataka kuonana na bwana Deo lakini mwanaume huyo akamwambia hana muda huo. Amejitolea tu kama msamaria mwema.
Jona akashusha pumzi ndefu ya uchovu.
**
“Karibu,” Jona alimwonyeshea Marwa chupa kubwa whisky akiiweka mezani.
“Hapana, nashukuru,” Marwa akamjibu akitabasamu kwa mbali. Jicho lake la kushoto lilikuwa limefunikwa na pamba na plasta. Walikuwa ‘wamejiachia’ sebuleni wakipigiwa muziki laini kandokando.
“Poleni kwa msiba, wanasafirisha?” Marwa akauliza.
“Nadhani,” Jona akajibu akitazama chupa yake ya kileo. “Wataupeleka Morogoro.”
Kukawa kimya kidogo Jona akimiminia kinywaji kwenye glasi.
“Vipi mmebaini chochote?”
“Yah! .. ” Jona akajibu pasi na uhakika ndani yake. “Kiasi chake. Natumai mengi yatakuja kwa mujibu wa muda.”
Kisha hawakuongea kwa muda mrefu kidogo Marwa akiwa anachezea simu na Jona akiwa anakunywa kinywaji chake.
“Hii kesi inaonyesha dalili ya kuwa controversial sana,” Jona akauvunja ukimya. Alikuwa ameshakata nusu chupa ya kileo chake. “Lakini nitaimaliza tu,” akajihakikishia. “Nitashinda.”
Alikuwa kana kwamba anajiongelesha mwenyewe. Marwa alimuitikia kwa tabasamu tu na kupiga kimya. Pengine kwasababu hakujua nini Jona anamaanisha.
Jona hakufunguka kwa undani.
**
“Unahitajika ofisini kwa Kamanda,” alisema afande fulani mwanamke aliyechungulia mlangoni mwa ofisi ya Jona baada ya kugonga mara tatu.
Jona asijiulize sana, akanyanyuka na kwenda huko alipokutana na kaimu Kamanda, ambaye kwa sasa tunaweza kusema yeye ndiye aliyekuwa katika nafasi ya marehemu Kamanda japokuwa bado hakuapishwa na kutangazwa.
Lakini hakuwa mwenyewe, ofisini pia alikuwapo mwanaume mzungu aliyevalia suti rangi ya grey. Nywele zake zilikuwa za gold ‘blonde’. Lips ya juu ya mdomowe ilifunikwa na mustachi, macho yake yakifanana na ya paka.
Jona akaketi na kutambulishwa, yule mzungu alikwa anaitwa Elliot Parker. Ni mpelelezi mashuhuri toka kwenye shirika la viwango vya juu duniani kwenye maswala ya ujasusi na upelelezi.
Akaambiwa kuanzia muda huo kesi ya mauaji ya Kamanda itakuwa mikononi mwa mzungu huyo, Elliot Parker. Ampatie ushirikiano wote.
“Utamweleza ulipofikia na kila kitu ulichokipata huko,” Kamanda akatoa agizo. Jona akiwa amepigwa na butwaa akauliza:
“Kamanda, kwani kuna shida gani imetokea mpaka kufikia hatua ya kumpatia kesi mpelelezi wa kigeni?”
“Kwasababu mojawapo ya mtuhumiwa ama watuhumiwa ni watu toka jeshi letu la polisi,” Kamanda akajibu. “Hivyo kufanya kazi hii kwa ufanisi zaidi, pasipo na aina yoyote ya upendeleo ama kupindisha mambo, tulihitaji mtu toka nje.”
Jona akahisi hapa kuna jambo halipo sawa.
Ni nani huyo mtuhumiwa toka jeshi la polisi? Mbona upelelezi wake mfupi umeonyesha tofauti? Alijiuliza maswali haya kichwani kwa haraka. Ila hakuwa na namna zaidi ya kufuata agizo alilopewa na mkuu wake.
Hakuwa katika nafasi ya kupinga agizo bali kutekeleza agizo. Akaongea na Elliot Parker mpaka alipofikia na kisha akisindikizana naye akampeleka mpaka nyumbani kwa marehemu Kamanda.
Elliot Parker akitumia vifaa vyake vya kitaalamu akachukua ushahidi kwa ‘kuscan’ eneo ambalo mtuhumiwa alilishika wakati anaingilia na kutokea ndani kwa lengo la kupata alama za dole gumba.
Alipomaliza hilo akatumia “magnifying glass’ kupekulia njia na nyayo za mtuhumiwa. Akaandika taarifa na kisha wakaondoka na Jona kurudi kituoni.
**
“Marwa, things are not ok. Nasense kuna mchezo unafanyila nyuma ya mgongo wangu,” alisema Jona akiwa ameshikilia kichwa chake amejilaza kitini.
“Ni kuhusu ile kesi?” Marwa akauliza baada ya kuvuta juisi ndani ya glasi kwa mrija wake mwembamba. Mezani kulikuwa kuna dumu la lita tano likiwa limesheheni juisi ya embe. Kila mtu alikuwa na glasi yake ya juisi ila ya Jona haikuwa imepungua hata kidogo tangu ijazwe.
Mrija ulikuwa unaeleaelea juu ukikosa mteja.
“Yah ni kuhusu hiyo kesi,” Jona akajibu. Macho yalionyesha yupo mbali kifkra. “Sielewi kuna nini hapa kati, lakini …” Jona akatikisa kichwa. “Mambo hayapo sawa kabisa kabisa.”
“Nini shida haswa?” Marwa akauliza akimtazama Jona na chongo lake.
“Nimefanya uchunguzi, na kwa clue ndogo niliyoipata, muuaji ni miongoni mwa watu wa Sheng kwa mujibu wa sare za viatu. Lakini ajabu ni kwamba, baadae shahidi anakuja kunambia gari aliloliona likiwa limebeba watuhumiwa ndilo lile tulilotumia hapa karibuni.
Kama haitoshi, Kamanda naye ananiambia mmoja wa watuhumiwa ni mtu toka jeshi la polisi, nastaajabu amejuaje kama mmoja wa watuhumiwa ni polisi na huku hajafanya uchunguzi, mpaka anafikia hatua ya kumleta mtu mgeni? Na alafu ilikuaje watuhumiwa hao wa mauaji wakapata gari ambalo lipo kituoni? “ Marwa akaguna. Akaweka glasi chini na kukiri kuna jambo.
“Hapo lolote linaweza kutokea. Sasa lazima na wewe uwe na nafasi ya kujihami. Uwe na maelezo yenye mantiki ya kukuweka salama na kulimaliza hili.”
Ujumbe huu ukapenya kwenye masikio ya Jona. Kweli ulikuwa na mashiko. Aliona ana haja ya kujua kila kitu kitakachoendelea kwenye kesi hiyo. Na si tu kujua, bali awe amemtangulia bwana Elliot Parker kwenye harakati zake.
Ajue alichokiona mzungu huyo, alichokisikia, alichokiandika na kukisoma.
Baada ya hapo, angalau Jona akapata unafuu wa mawazo. Akanyanyua juisi na kuigida mapafu kadhaa. Sasa kichwani mwake alikuwa anafikiria namna gani atahakikisha anamweka bwana Elliot Parker mgongoni mwake.
Mara simu ikaita, akaitazama, alikuwa ni Miriam . “Hallo … yes, habari yako? … safi tu. Unaendeleaje? … niko poa, nihabarishe … saa hii? … serious? …”
Jona akatazama saa yake ya mkononi, saa moja usiku.
” … ok, nakuja. Nipe dakika chache.”
Akakata simu na kumtazama Marwa.
“Nadhani nimepata kazi ya dharura.”
**
“Yupo wapi?” Lilikuwa swali la kwanza Jona kuuliza baada ya kuingia ndani mwa Shangazi yake Miriam. Alitumia kama nusu saa kufika hapo. Miriam, aliyekuwa ana uso wa hofu na macho mekundu, alimpokea na kumkumbatia kwanguvu. Hakuamini kama Jona angefika.
“Ahsante sana kwa kuja, Jona,” alisema kwa toni ya uoga. “Naogopa, naogopa!”
“Usijali,” Jona akamtoa hofu. “Yupo wapi?” Akarudia tena swali lake. Miriam akamwonyeshea mlango wa chumba kwa kidole, Jona akakimbilia huko kutazama akimwacha Miriam sebuleni.
Baada ya muda mfupi akarejea.
“It is not that serious,” Jona alisema akiketi kochini. “Itakuwa ni Malaria tu si kingine.”
“Kweli?” Miriam akauliza akitoa macho.
“Yah its true.”
“Tumpeleke basi hospitali!”
“Hapana. Hamna haja hiyo. She is not in that critical situation, Miriam.”
“Ndo’ ulikuwa ukiishi hivi na wanao?” Jona akauliza. Miriam akatabasamu kabla hajajibu.
“Mimi muoga sana. Eliakimu ndiyo alikuwa akisumbuka nao sana kipindi wanaumwa. Mimi mmh mmh mwoga sana.”
“Hujawamiss watoto wako?”
“Nimewamiss mno. Ila naona ni kheri kwao wakawa na mimi mbali kwa muda huu. Natumai huko kwa shangazi yao wanaishi vema japo kuna muda huwa nawakumbuka sana!”
“Pole mama. “
“Vipi kuhusu wewe?”
“Mimi sina familia.”
“Haiwezekani. Serious?”
“Ndio. Walifariki kwenye ajali ya moto miaka miwili iliyopita.”
“Oh my God. Pole sana,” alisema Miriam akimtazama Jona kwa sura ya huruma. Jona hakutaka kuendelea na simulizi hizo, huwa zinamuumiza sana pindi anapozikumbuka, akabadili mada kwa kumtaka Miriam amwonyeshe jokofu lao apate kutengeneza dawa ya mgonjwa.
“Dawa?” Miriam akatahamaki. “Hamna dawa kwenye friji.”
“Najua haipo, ndiyo maana nataka kutengeneza,” Jona akamjibu na kuongezea: “Nikiona vilivyomo nitajua cha kufanya. Usiku huu haitakiwi aachwe hivi hivi.”
Wakaongozana mpaka jikoni, ndani ya jokofu Jona akatoa tunda moja la chenza na kulikata robo kipande kisha akakichemsha. Maji yake akampatia Miriam ampatie shangazi anywe.
“Akimaliza atalala vema.”
Baada ya muda mfupi Miriam akarejea na kikombe kitupu. Akamwambia Jona tayari Shangazi amemaliza.
“Una uhakika itamsaidia?”
“Asilimia zote. Ndani ya kinywaji alichokunywa kuna unmodified natural quinine, itamsaidia.”
Miriam akamkumbatia tena Jona.
“Nashukuru sana.”
“Nadhani napaswa kwenda sasa,” Jona akasema akijipapasa mifuko.
**
Ngo! Ngo! Ngo!
“Ingia,” Jona alirusu hodi akitazama mlangoni. Akamwona bwana Elliot Parker akiingia ndani, amevalia suti nyeusi na kwenye mkono wake wa kushoto amebebelea mkoba wa kahawia.
Wakasilimiana, Elliot akaketi na kueleza dhamira ya ujio wake. Yupo pale kwa ajili ya kumuuliza Jona maswali kadhaa juu ya kesi ya mauaji ya Kamanda.
Jona hakuona shida, akamkarimu kwa mikono yote. Akamuahidi bwana Elliot atampatia ushirikiano wote autakao.
Elliot Parker akafungua mkoba wake na kutoa karatasi kadhaa. Akazitazama kwa zamu alafu moja akaiweka mezani na zingine akazirudisha mkobani.
Akaitazama tena ile karatasi aliyoiweka mezani alafu akaanza kumuuliza Jona maswali.
“Do you know the last person Chisanza communicated with?” (Unamjua mtu wa mwisho aliyewasiliana na Chisanza?)
“No, I dont,” (Hapana, simjui,) Jona akajibu kwa kujiamini.
“Are you sure?” (Una uhakika?)
“Yes, I am.” (Ndio, nina uhakika.)
“The last person was you,” (mtu wa mwisho alikuwa wewe,) akasema Elliot Parker. “And it happened a few minutes before Chisanza was killed. Anything to say about that?” (Na ilitokea muda mfupi kabla Chisanza hajauawa. Chochote cha kusema kuhusu hilo?)
“I dont know anything about that,” (sijui lolote kuhusu hilo,) alisema Jona. “I only contacted him about the case he gave me to deal with.” (Niliwasiliana naye kuhusu kesi tu aliyonipa nihangaike nayo.)
“But you know that his house troubles them with network, right? And one has to go out to talk clearly?” (Lakini unajua nyumba yao inawasumbua mtandao, sio? Na mtu inambidi aende nje aongee vizuri?)
“Yes, I do.” (Ndio, najua.)
Elliot Parker akaandika karatasini. Alafu akamuuliza Jona kuhusu gari linalosadikika kutumiwa na wauaji. Lini ilikuwa mara yake ya mwisho kulitumia na kama kuna mtu yeyote anayemjua ameshawahi kutumia gari hilo tangu lije kituoni.
Jona akaeleza hakuna aliyekuwa analitumia isipokuwa yeye tu ila kwenye shughuli zake za kazi. Baada ya maelezo hayo, bwana Elliot Parker akapaki vitu vyake na kuaga.
Akamwacha Jona akiwa na maswali kichwani. Hakuelewa kinachoendelea.
Ndani ya muda mfupi, wakaja polisi watatu, wakamuweka chini ya ulinzi. Akatiwa pingu mikononi.
Alikuwa ni mtuhumiwa namba moja wa mauaji.
Akatiwa lupango akichangamana na wahalifu wengine humo. Akaenda ukutani kabisa akaketi na kushika kichwa asiamini. Alidhani pengine ni ndoto, akafikicha macho yake lakini bado mambo yalikuwa yaleyale.
Alikuwa lupango.
Wamemchongea njia. Wamemzamisha mtegoni. Yale yote yalikuwa yamepangwa atiwe ndani. Ndivyo akili yake ilivyoamini.
Wakatumia gari alilolitumia. Wakaua muda alioutumia.
Kila kitu kilikuwa kimeshapangwa. Walimsoma. Walimfuatilia. Wakamzamisha!
Kwa mara ya kwanza Jona alikuwa ametanguliwa mbele. Alifanywa mjinga. Alilambishwa mchanga. Kwa mara ya kwanza alizidiwa akili!
Akawaza hii kesi yake itakwendaje. Je, wamejipanga kumsingizia sababu gani amemuua Kamanda? Akakosa jibu. Alihisi moyo wake umenyauka. Alihisi uchungu mno hata akashindwa kuzuia chozi lisimtoke.
Alikuwa amefanya makosa kurudi jeshini. Hakutakiwa kurudi tena huku. Kaburi lake sasa limechimbwa na wanataka wamfukie kabisa.
“Afande Devi,” Jona akapaza sauti. “Naomba nifanyie mpango niongee na ndugu zangu.” Alikuwa kifua wazi ana suruali pekee, miguuni peku. Mkono alikuwa ameutoa nje ya nondo za lupango akimwonyeshea polisi aliyekuwa anakatiza koridoni.
“Jona,” polisi huyo akashangaa. Akatazama pembeni alafu akarudisha macho yake kwa Jona. “Mwanangu, itakuwa msala. Si unajua ishu yako ilivyo hot.”
“Nifanyie bana Devi. Humu leo mimi kesho wewe. Hamna hata mtu anayejua kama nipo humu. Nifanyie msada,” Jona aliteta kwa huruma.
Afande Devi akaguna. Alikuwa ni mwanaume mwembamba asiyezidi miaka ishirini na tano. Alitazama kushoto na kulia kwake alafu akasema:
Jona akakaa hapo akishikilia vyuma huku akimngojea afande Devi. Akawa anachungulia mara kwa mara akisimamisha masikio yake asikie kila jambo.
Ikapita dakika kumi.
Robo saa.
Nusu saa.
Lisaa limoja.
Jona akakata tamaa. Akarudi ukutani na kuketi. Akainamisha uso wake chini.
“Oya Jona!” Mara akasikia sauti ya chini ikimwita. Hataka akanyanyua uso wake kutazama. Alikuwa ni afande Devi. Haraka akanyanyuka na kwenda langoni.
“Sikia. Vitu vyako sijaviona kabisa yani, sijui vimefichwa wapi havipo pale pa siku zote. Sasa kama vipi wewe tumia simu yangu. Umeshika namba kichwani?”
“Ndio,” Jona akawahi kujibu. Afande Devi akampatia simu yake kwa tahadhari alafu akawa anaigiza kuzungukazunguka maeneo hayo.
Jona akampigia Marwa na kumpasha habari juu ya kilichotokea. Lakini akamwonya asije akakanyaga pale kituoni. Alihofia Sheng na kundi lake wanaweza wakam ‘trace’ na kummaliza.
“Usijali, mi ntakuja,” alisema Jona. “Nadhani unajua kila kitu hapo nyumbani. Ukihitaji akiba ya pesa utaikuta chumbani mwangu kabatini.
Lakini naomba unifanyie kazi moja usiku huu. Naomba utafute kila unachokijua kuhusu mtu anayeitwa Elliot Parker. Ni mpelelezi toka shirika kubwa la ujasusi na upelelezi duniani.”
Akiwa amesindikizwa na wanaume wawili, mikono na miguu ikiwa imetiwa kwenye vitanzi vya pingu, akaingizwa ndani ya ofisi na kuagizwa aketi.
Ofisini alimkuta Kamanda mkuu akiwa amejaa kwenye ‘sofa’ lake. Amekusanya viganja vyake viwili na kuviwekea kidevu kwa juu. Akamtazama Jona kana kwamba uwanja wa bao. Kisha kwa ishara, akawataka wale wasindikizaji waende nje. Wakatii agizo.
Kwa muda wakatazamana na Jona kabla hajavuta pumzi ndefu na kuishusha.
“Nilikuamini Jona kukupa nafasi hii, kukupa kesi hii. Ulikuwa ni mfano wa kuiga kwa uhodari na uchapaji wako wa kazi. Ufanisi na utendaji wako ulikupatia sifa kedekede, ukavuna imani za watu. Kwanini ukayafanya haya?”
“Sihusiki Kamanda kwa lolote lile,” Jona akajibu. “Sijatia mkono wangu kumwangamiza RPC. Na sikuwa na sababu ya kufanya hivyo hapa karibuni.”
“Una maanisha nini kusema hapa karibuni?” Akauliza Kamada mkuu. “Ina maana ulikuwa umedhamiria kufanya hivyo hapo baadae?”
“Hakuna anayejua ya baadae, Mkuu. Yote ni vitendawili. Lakini kwakuwa tunaongelea ya sasa na yaliyokwishatokea, basi mimi sijahusika kwa namna yoyote ile. Sijajua kwanini nachezewa mchezo huu!”
“Mchezo?” Akauliza Kamanda kwa kebehi. “Unauona huu ni mchezo? Wake up Jona, this is reality. Unaenda kuozea jela. It is better ukawa muwazi nijue nakusaidiaje.”
“Mkuu,” Jona akaita. “Kama kuwa muwazi ni kudanganya, basi sitaweza kamwe. Nasimamia kwenye ukweli siku zote. Sihusiki na haya mauaji.”
Kamanda mkuu akashusha pumzi. Akamtazama Jona kea sura ya huruma.
“Ushahidi wote upo against you. Kila kitu kinanyooshea kidole kwako. Mpaka finger print inasema ni wewe. Utabishana na ukweli mpaka lini? … anyways.” Kamanda mkuu akalaza mgongo wake kwenye kiti.
“Naweza nikakusaidia, ila kubali kwanza ukweli huu. Kubali haya mashtaka alafu mengine niachie mimi. Nitajua namna ya kuyamaliza. Sawa?”
Jona akamtazama Kamanda mkuu kwa macho ya kitabe. Akatikisa kichwa chake mara tatu kisha akasema:
“Kamwe sitakubali kitu ambacho sijafanya. It will never ever happen. Nawashauri msingoje kabisa.”
“Jeshi la polisi limefanikiwa kumtia nguvuni mtuhumiwa namba moja wa mauaji ya aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoa, bwana Chisanza, ambaye aliuawa kwa risasi usiku wa kuamkia jana maeneo ya nyumbani kwake, Mbezi: Goba.
Kwa taarifa zaidi tuungane na ripota wetu Jack Chiwelu.”
“Tumesikitishwa sana sana sana … ” alinguruma Kamanda mkuu wa polisi akiwa amezingirwa na vinasa sauti vya kila aina ya chombo cha habari hapa nchini. “Baada ya kufanya upelelezi yakinifu, tena tukishirikiana na vyombo vya kipelezi toka nje ya nchi kwa ufanisi zaidi, na kugundua kuwa mwenzetu mmoja, afahamikaye kama inspekta Jonathan Mchau, amekidhi viwango vyote vya kuwa mtuhumiwa namba moja wa kesi hii. Akitumia ujuzi wake aliofundishwa na jeshi kutekeleza mauaji kinyume kabisa na kazi yake.”
Picha ya Jona ikarushwa hewani.
“Sababu yake ya kutenda mauaji hayo bado haijajulikana. Linafanyiwa uchunguzi na punde utakapokamilika basi tutawajulisha na mtuhumiwa kufikishwa mahakamani sheria ifuate mkondo wake.
Na kwasababu basi sheria ni msumeno, itakata kila inapotakiwa. Na hili liwe onyo kwa maaskari wote nchini kuwa kofia zao za uaskari haziwafanyi wao kutenda wanachokitaka bali kufuata, kulinda na kutekeleza sheria tu!”
“Nikiripoti toka hapa makaoni, mimi ni Jack Chiwelu, Mambosasa TV.”
Sheng akacheka kwanguvu sana. Hakika alikiona alichokuwa anakitaka. Alipata pia alichokuwa anakitaka. Usiku huu kwake ukawa mwanana kabisa kuliko zote alizowahi kuzipitia.
Akanyanyua glasi yake ya mvinyo na kupiga ‘cheers’ na Elliot Parker aliyekuwa amekaa pembeni yake. Mbuyu ulikuwa umedondoshwa pasipo jasho.
“But the work is not yet done,” (Lakini kazi bado haijaisha,) Elliot akasisitizia. “We have to sink him into the jail as soon as possible.” (Inabidi tumzamishe jela haraka iwezekanavyo.)
**
Wakati wote wakiwa wamelala ndani ya lupango, yeye alikuwa macho. Si kwasababu ya mbu na kunguni waliokuwa wanasumbua bali mawazo kichwani mwake. Alikuwa anahisi maumivu kwa kuonewa.
Haki kuna muda dunia haipo ‘fair’. Si kila anayetupiwa lupango ama jela basi mikono yake ina hatia.
Leo hakuwa na pombe ya kumsaidia kulala. Leo hakuwa na Marwa wa kupiga naye soga. Leo alikuwa mwenyewe. Si akiegemea kochi bali ukuta.
Usiku wa aina yake.
Saa tisa jioni, Ramada hotel.
Vx nyeusi iliingia na kupaki, ndaniye wakatoka Boka na Miranda walioshikana mikono kuingia ndani ya hoteli. Wakapata chakula na kujikuta wamejilaza kwenye vitanda vyembamba karibu na swimming pool.
Walikuwa hapo kurefresh akili zao baada ya kupitia magumu kadhaa hapo nyuma. Boka akifiwa na mumewe wakati Miranda akiwa kwenye kiti-moto baada ya mauaji hayo.
Lakini hatimaye yote yamepita. Yote yamekuwa kheri sasa. Ulikuwa wakati wa kukaa tena pamoja na kuangazia yajayo, tena katika namna ya pekee kabisa haswa baada ya kuachwa na nafasi sasa ya kujivinjari pasipo woga.
Hakukuwa na mtu wa kuwanyima kumeza mate tena.
“Unapenda sana kuja hapa?” Aliuliza Miranda ndani ya bikini. Umbo lake lilikuwa linaonekana vema na pengine kukushawishi ukamwona Boka hakufanya makosa kabisa kuwa ‘zezeta’ hapa.
Alikuwa anavutia hasa. Kwa rangi yake, uso mpaka na umbo. Na hata namna alivyokuwa anaongea, alivutia kusikilizwa.
“Pametulia sana hapa kuliko kwengine, haswa nyakati za siku za wiki. Ukija hapa you get a real refreshment,” alieleza Boka aliyejivunia kuwa na mwanamke mrembo pembeni yake.
Miranda akadaka glasi juu ya kameza kadogo pembeni ya kitanda, akanyonya mafundo mawili kabla hajalaza kichwa chake na kuuliza:
“So nini plan yako kwa sasa?”
Boka akatabasamu kwa mbali. Akageuza mwili wake na kumtazama Miranda.
“Kukuoa,” akajibu kwa ufupi.
“Are you serious?” Miranda akaigiza kustaajabu.
“Why not, nipo serious.”
Miranda akanyamaza kidogo akiwaza kichwani. Kwa wanawake wengine hii ilikuwa ni ‘a million dollar chance’. Sio tu kwenye swala la kuolewa kama kila mwanamke ambavyo angependa kuwa na mume na familia yake, la hasha, bali kuolewa na mtu mwenye nafasi serikalini.
Mtu mzito mwenye pesa. Haikuwa jambo dogo hata kidogo. Lilikuwa ni jambo la kutetemesha mwili na kuukimbiza moyo upesi haswa ukifikiria zile ‘shopping’ za Dubai, safari za China na Afrika ya kusini.
Lakini kwa Miranda, hili halikuwahi kuwa lengo. Kuolewa. Achilia mbali kuolewa na Boka. Mwanaume huyu hajawahi kumvutia hata chembe. Hamsisimui. Alikuwa hapo kwa ajili ya kufanikisha malengo yake tu.
Hapa akamkumbuka mke wa Boka.
Japokuwa alikuwa ni adui kwenye ‘mishe’ zake, lakini kwa njia moja ama nyingine alikuwa anamhitaji. Kumtuliza mumewe asifikirie maswala ya kumuoa.
Sasa mke huyo amefariki. Boka atakuwa mwepesi kutafuta mwanamke mwingine na hata kumuoa.
Sasa nini maana yake hii? Inabidi kazi itendeke haraka iwezekanavyo kabla ya mambo haya ya kuoana. Aliwaza Miranda.
Akanyanyua tena glasi ya juisi na kupeleka mrija mdomoni akiwa amejilaza. Akanywa mafundo mawili mepesi akichambua cha kunena.
“Nadhani unajua cha kufanya, mheshimiwa. It is obvious baba yangu hatokukubalia kama hutomfanyia kazi yake.”
“Najua!” Boka akadakia. “Si nimeshamkubalia?”
“Kazi moja!” Miranda akajistaajabisha. “You have to show wewe ni mtu anayeweza kumuamini na kumtegemea. Unajua hawa wazungu ni ngumu sana kumwamini mtu, lakini akishakuamini tu basi.”
“Kwahiyo unanishauri nini?”
“Mpe sababu ya kukuamini. Tena si moja, kadhaa.”
“Nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu. Ila vinataka muda. Huoni nitakawia kukuoa?”
“Kwanini wahofu kuhusu hilo swala? Wadhani kuna mtu atakuja niiba au?” Miranda aliuliza kwa mishebeduo ya kike. “Mimi ni wako tu. Wala usiwe na papara. Hata kwa muda huo utakaokuwa unafanya mambo yako, mimi nitakuwa pembeni yako. Kuna shida?”
Japo Boka hakujibu, alionekana kuafiki alichoambiwa. Hakuwa na usemi.
“Vipi ile safari ya Afrika kusini?” Miranda akauliza. “Umeischedule lini?”
“I think nitaenda huko wiki ijayo Jumatatu.”
Alivyojibu hivyo ni kana kwamba Jumatatu hiyo ilikuwa mbali. Siku hiyo ilikuwa ni Alhamis, kwahiyo Jumatatu ilikuwa ni hatua tatu tu kuifikia. Miranda akatabasamu. Hili halikuwa jibu baya kwake kabisa. Lilimaanisha ajiandae.
Lakini kama haitoshi, Boka akamwambia anataka kumkabidhi biashara ya mkewe aiendeshe. Kampuni ile ya vipodozi na urembo, iliyosambaa Afrika mashariki, iwe chini yake.
Swala hili likawa mtambuka kwa Miranda. Hakutaka kuingia kichwakichwa hapa. Alihofia kilichomkuta Mke wake Boka. Lakini pia kujianika kwa maadui zake.
“Huoni tunapaswa kungoja kwanza kesi ya mkeo iishe?” Akauliza.
Kichwani kwake akiwaza mpaka kesi hiyo ikiisha, Jona atakuwa amemsaidia ku ‘clear’ maadui zake hawa akawa salama.
Hakujua Jona kwa wakati huo alikuwa rumande. Na kesi imesharudishiwa mikononi mwa inspekta Geof, ambaye hafahamu yale aliyokuwa anayafahamu Jona.
Hata kidogo!
**
Baada ya mahojiano yake ya muda mfupi kulingana na muda aliopewa na daktari, inspekta Geof alisafisha koo lake na kusimama akimtazama mwanamke aliyejilaza kitandani.
Mwanamke huyu alikuwa ni shoga yake marehemu mkewe Boka.
Alikuwa anapata wakati mgumu sana kuongea. Mwili wake ulijawa na majeraha makubwa. Na maumivu aliyokuwa anayapata hayakuwa yanamithilika. Kama si sindano za kupunguza maumivu alizokuwa anadungwa, angekuwa analia muda wote.
Ukimtazama ungemuonea huruma. Na kama ungekuwa na moyo mdogo basi isingekuwa ajabu ukajaza machozi machoni.
Hii likazidi kumfanya inspekta Geof aone kuna haja ya kumtafuta mtu aliyehusika na hili kwa nguvu zote. Awajibishwe kwa mujibu wa kile alichokitenda.
Akashusha pumzi ndefu. Mkono wake wa kuume ulikuwa umeshikilia notebook na kalamu.
“Ahsante sana. Ugua pole. Nitakuja kukuona tena karibuni.”
Akatoka ndani ya hospitali na kuonana na daktari, kisha akaenda zake kwenye gari lake na kutulia humo kwa dakika kadhaa. Akapitia yale maelezo aliyopewa.
Yote yakamjengea mantiki kumbe mauaji yale ya mkewe mheshimiwa yalikuwa ni kisa cha kimapenzi. Yalikuwa yamesukumwa na wivu wa mapenzi.
Akatikisa kichwa chake kisha akazungushia duara kwa jina la Miranda kwenye notebook, na kuandika kando: ‘the primary target’.
**
“Nilikuambia usije,” Jona alilalama akiwa amekunja sura. Mikono yake ilikuwa imebana nondo za lupango kwanguvu kana kwamba anataka kuzing’oa.
Alimtazama Marwa kwa macho makali. Lakini Marwa aliyekuwa amebebelea mfuko mweusi wa rambo, amesimama mbele yake, alikuwa akimtazama kwa huruma.
“Lakini nitawezaje kukaa nyumbani kwa amani na wewe upo humu?” Marwa aliuliza.
“Ni hatari, Marwa,” Jona akamjibu akilalama. “Unadhani nakutania ninavyokuambia hivyo?”
“Kama ni hatari basi tuwe wote. Siwezi nikakaa nyumbani na sijui huku unaendeleaje. Unataka nije nisikie wamekuua na kukuzika pasipo kukuona? Nitakaaje nyumbani nikila na kunywa huku sijui kama tumbo lako limepata kitu? Chakula kitashuka? Kama ni hatari na kuniua, basi waniue! Nimeshapoteza wazazi wangu, sina cha kupoteza tena. Na wewe upo ndani, ntajificha milele?
Ukifa nitapata nguvu ya kulia na wakati ukiwa hai nilishindwa hata kunyoosha mkono kukusaidia? … siwezi Jona.”
Marwa akafungua mfuko wake. Ndaniye kulikuwa kuna hotpot la wastani na chupa ya maji. Akampatia Jona ale.
Ni kama vile alikuwa anajua mwanaume huyo hakula tangu alipowekwa humo ndani.
“Wamekuruhusu kuja humu?” Jona aliuliza.
“Hapana,” Marwa akajibu. “Hawakuniruhusu, nikakaa hapo nje siku nzima mpaka askari fulani akaniita na kuniuliza kama nina shida yoyote. Nilipomweleza nimekuja kukuona wewe, akanisadia. Lakini ameniambia nifanye upesi.”
“Askari gani huyo?” Jona akauliza akila. Marwa akampatia maelezo yaliyomfanya Jona kutambua ni Afande Devi.
Baada ya muda mfupi, akampatia Marwa vyombo aende zake upesi.
“Kuwa makini sana,” akamsisitizia. Marwa akapokea vyombo na kabla hajaenda, akamkumbushia Jona jambo.
“Nilitafuta kuhusu Elliot Parker.”
“Ukapata nini?” Jona akawahi kuuliza kufupisha maongezi.
“Nimetafuta kote lakini sijaona hilo jina kama ni mpelelezi wa aidha FBI, CIA, au INTERPOL.”
“Nilijua tu!” Jona akajisemea. “Sasa nenda. Fanya upesi! Kuwa makini sana.”
**
“Ni nani yule?” Aliuliza koplo Massawe akimtazama Marwa anaishia. Kaunta alikuwa ameketi afande Devi akiwa anapekua daftari kubwa.
“Ni kijana flani hivi,” Afande Devi akajibu akifanya jitihada za kukatisha maongezi hayo kwa kufunguafungua daftari kujifanya yupo ‘bize’.
“Kijana gani na alikuja hapa kufanya nini?” Koplo Massawe akasisitizia. Alimtazama afande Devi kwa macho ya mashaka. Na kabla afande Devi hajajibu, akasema:
“Unajua tumekatazwa kumruhusu yoyote kumletea chakula yule jamaa. Kwanini ukamruhusu aende huko na mimi nilimzuia?” Massawe akafoka.
“Sikujua,” afande Devi akajitetea. “Nilimkuta hapo nje kwa muda mrefu. Nikamuuliza akasema haja yake. Nikaona si vibaya ku-“
“Usirudie tena!” Massawe akamkatiza. “Sawa?”
“Sawa afande!”
**
Baada ya muda kidogo koplo Massawe akaondoka zake na kumwacha afande Devi peke yake. Devi asipoteze muda akaenda kumwona Jona rumande na kumwonya kuhusu watu wanaomtembelea.
“Hawataki upatiwe chakula, Jona. Utakapoona nimewazuia wageni wako jua nimekosa namna ya kuwaruhusu.”
Jona akafadhaishwa sana na hili. Kwanini wanamfanyia hivyo? Nini lilikuwa kosa lake ndani ya jeshi? – uweledi wake?
“Usijali,” afande Devi akamtoa mashaka. “Nitakuwa nakusaidia kadiri ya uwezo wangu. Nitakapokuwa napata muda ntakuwa nakupenyezea hata kidogo. Lakini kwa siri sana.”
“Ahsante sana Devi,” Jona akachonga. “Ila nakuomba uachane na hivi vitu. Wewe bado kijana mdogo na ndiyo kwanza umeanza kazi mwaka huu. Hili linaweza kukugharimu.”
“Wala usijali, Jona,” Devi akamtoa mashaka. “Wewe ni miongoni mwa watu wachache sana walionipokea vema hapa kituoni wakaniheshimu japokuwa ni mdogo kwao kiumri na kicheo. Hustahili haya. Naamini hauna roho hiyo. Mimi nitakusaidia kadiri ya uwezo wangu.”
Afande Devi hakukaa sana hapo, akaenda zake kurudi anapotakiwa kuwapo. Alihofia koplo Massawe anaweza akarudi asimkute ikawa taabu.
**
Kamanda mkuu akiwa anaongozana na maaskari wengine wawili, mmoja akiwa amevalia kiraia, wakakomea langoni mwa rumande ya Jona. Kamanda akamtazama Jona kwa jicho la huruma kisha akadaka vyuma vya lango.
Jona alikuwa amekaa mbali ukutani.
Kamanda akatikisa kichwa kwa masikitiko. Kwa ishara, akamtaka mwanaume Jona ajongee karibu naye. Jona akatii. Akamsogelea mkuu wake huyo na kumtazama machoni.
“Jona,” Kamanda akaita. “Kwanini umekubali kuteseka kiasi hiki? Fanya yaishe. Niruhusu nikusaidie. Haustahili kabisa kuwapo humu ndani.”
Jona akamtazama Kamanda kwa sekunde kadhaa kisha akamjibu akiwa anang’ata meno.
“Anayestahili kuwepo humu ndani ni wewe pamoja na wenzako. Nitakapofanikiwa kutoka humu, basi jua ni wewe ndiye utakayeingia.”
Kamanda mkuu akatabasamu.
“Shida yako ipo hapo, Jona. Unashupaza sana shingo. Unajua kisa cha chui na chungu? … chui alizamia kijijini kwa watu akiwa anatafuta chakula kwa ajili ya wanae. Hakutaka kumla mtu kabisa bali apekue majikoni aone kama atapata chochote kitu.
Huko akafanikiwa kusikia harufu nzuri kabisa ya chakula toka kwenye chungu kidogo. Kuonja … alah! Kilikuwa kitamu sana. Akaona kinafaa kupelekea watoto wake porini.
Lakini si bahati, chui akazamisha kichwa chake ndani ya chungu hicho hata akashindwa kukitoa. Akahangaika huku na huko kujinasua asifanikiwe mpaka wanakijiji wakamsikia. Wakajaa kumzunguka.
Walitaka sana kumsaidia, lakini silka ya chui iliwaogopesha kufanya hivyo. Je, Kucha zake zingewaacha salama? Walihofia. Na je wakishatoa hiko chungu kichwani, meno yake hayatawararua?”
Kamanda akaweka kituo. Akameza mate na kumwambia Jona.
“Badili hulka yako, uruhusu kusaidiwa. Kushupaza kwako shingo hakutakupelekea popote zaidi ya shimo la tewa.”
Jona akasaga meno.
“Kama ungelibadili hulka yako kwanza, nisingelikuwepo humu ndani,” akasema kwa kujiamini, kisha akaita, “Kamanda, kwa makusudi ulitengeneza kidonda kwasababu una dawa mkononi Sawa dawa yako yaweza kuponya lakini vipi maumivu niliyoyapata? Na je kovu utakaloniachia?”
Akahitimisha.
“Silambi mkono unaoniadhibu. Tena pasipo na hatia. Si kwamba ni kiburi, la hasha! Bali itanifanya niwe na hatia. Kamanda, acha nitapambana mpaka tone la mwisho.”
Kamanda mkuu akabinua mdomo wake kisha akamtazama mmoja wa watu alioongozana nao kuja hapo, yule aliyevalia kiraia. Akamuuliza:
Kamanda akamtazama Jona kisha akarudisha macho yake kwa yule mwanaume aliyemuuliza. Akampatia maagizo.
“Hakikisha hali kwa siku zote anazokaa humu ndani!”
“Ndio, mkuu!” Akajibu mwanaume huyu kwa ukakamavu.
**
Asubuhi …
Mlango ulipofunguka, alitoka inspekta Geof akiwa amebebelea notebook yake mkononi. Nyuma yake alikuwapo mwanadada Miranda akimsindikiza.
Wakasimama kibarazani, Inspekta akampatia Miranda mkono wa kheri kisha akamkumbusha hatakiwi kuondoka nje ya mji mpaka pale upelelezi utakapokamilika, na kesho atakuja tena kumwona.
Aliposema hayo, inspekta akaondoka zake Miranda akimtazama mpaka anatoka nje ya geti. Akarudi sebuleni na kuketi akikuna kichwa chake kwa mawazo. Nywele zilikuwa timtim, na mwili wake ndani ya dira angavu ulikuwa unahangaika kuweka kila mkao. Aliwaza. Hakuona kama una upenyo wa kuchomoka katika kesi hii. Kama upo basi ni kama ule wa tundu la sindano. Mambo yamekuwa magumu zaidi. Kwa dalili za wazi, inspekta alionekana kudhamiria kumtia ndani.
Mawazo yake yakaenda mbali. Akamuwazia Jona. Kwanini kesi hii amepewa mtu mwingine mbali na yeye? Aliamini Jona ni mwerevu kung’amua muuaji na si huyu Geof ambaye macho yake yanakomea juu ya zulia.
Akawaza afanyaje? Mawazo yake yote yakamuelekezea msaada wa pekee ni Jona. Akanyanyua simu na kupiga. Hakuwa anafahamu kuwa Jona yupo nyuma ya vyuma.
Simu ikaita pasipo mafanikio. Akaamua kumpigia Kinoo amshirikishe habari zake kwa mara ya kwanza. Hata akisikia amekamatwa basi asije akastaajabu na aje kumtembelea rumande.
Simu ikaita mara mbili kabla ya kupokelewa. Kulikuwa na makelele kuonyesha Kinoo alikuwa mjini kwenye pilika za magari na watu. Miranda asijali hilo, akatimiza adhma yake ya kumhabarisha Kinoo.
“Sidhani kama kesho akija ataniachia huru. Maswali yake yote nilikuwa nababaika kujibu. Najiona kabisa nikitenga shingo kwa mchinjaji.”
“Sasa tunafanyaje?” Kinoo akauliza.
“Tumtafute Jona. Naamini anaweza akanisaidia!”
“Jona? Yule polisi?”
“Ndio! Alikuwa ndiye mpelelezi wa hii kesi, ila wamembadilisha!”
“Miranda, kwani hujasikia habari za Jona?”
“Zipi?
Kinoo akamhabarisha Miranda kwamba Jona amekamatwa anatuhumiwa kumuua RPC hivyo asitegemee kumsikia tena.
Miranda akachanganyikiwa. Tumbo likamvuruga. Alikata simu akaiweka kando na kulaza kichwa chake kwenye kiti.
Jona amekamatwa? Jona amemuua RPC? Maswali haya yakazunguka kichwani. Akajikuta anatikisa kichwa chake kama mwehu.
Hapana.
Hakuamini hata chembe.
Akanyanyuka upesi na kwenda ndani.
**
“Jona, naamini hujaua,” Miranda alisema kwa sauti ya chini akimtazama Jona kwa macho ya huruma. “You have been framed. Na ubaya si tu inakuumiza wewe bali hata na sisi. I need you out. Things are not the same.”
Macho ya Miranda yalibadilika rangi na kuwa mekundu.
Jona alikuwa amesimama akishikilia nondo kwa mkono wake wa kuume akitazama chini. Sijui alikuwa anawaza nini. Ila ungemtazama ungeona moyo wake unaungua. Kifuani alikuwa ana moto mkali.
Alikuwa anasikia maumivu aliyoyaonyesha kwa kung’ata meno yake.
“Jona, Miranda akaita. “We have to do something. Usikae ukaridhika na hii hali. Najua you are innocent.”
“Nitafanya nini Miranda nikiwa humu rumande nimebanwa na vyuma?” Jona akauliza. Macho yake yalikuwa mekundu. “Nimedhamiria kweli kufanya kitu, lakini nafanyaje na nipo humu ndani?”
Kabla Miranda hajasema kitu, afande Devi aliwasili eneoni akiwa amebebelea chakula kwenye mfuko. Akamkabidhi Jona.
Akamtazama machoni.
Akamtazama na Miranda kisha akarudisha macho yake kwa Jona.
“Kula upesi!” Akasema kwa kunong’oneza kisha akaenda zake.
**
“Umempatia?” lilikuwa swali la kwanza kutoka kwa koplo Massawe.
“Ndio, nimempa,” akajibu afande Devi. Uso wake alikuwa ameukunja. Macho yake yalionyesha mawazo. Aliketi akafungua daftari kubwa la hapo kaunta akaigiza kulitazama ila kiuhalisia alikuwa mbali sana kimawazo.
Ndani ya muda mfupi, Miranda akafika hapo kaunta akiwa anatembea kwa madaha. Mwanamke huyo aka ‘sign out’ na kuwaaga.
Massawe akanyanyua simu na kupiga.
“Ndio, ameshakula kile chakula … sawa, mkuu.
Massawe aliongea akimtazama Miranda anayeyoyoma. Punde akakata simu akiwa anasikia sauti ya kicheko.
Sasa alikuwa ameshakamilisha kazi yake. Anachongoja ni malipo tu toka katika mkono mchafu!! Akatabasamu alafu akamuagiza afande Devi aende ndani kuhakiki kama kweli Jona amekula na kumaliza kile chakula walichompatia.
Afande Devi akatii amri. Upesi akaenda huko na baada ya muda mfupi akarejea akiwa ameshikilia mfuko wa nailoni mkononi.
“Amekula … amemamaliza!”
“Una uhakika?” Massawe akahakiki. Alikwapua mfuko wa nailoni toka mikononi mwa Devi na kuupekua kama kuna mabaki.
“Ndio, nina uhakika,” Devi akajibu akitazama chini. Akaendea daftari kubwa la mapokezi, akaketi na kuanza kulipekua.
Macho yake yalionyesha yupo mbali kimawazo. Hata daftari hilo hakuwa analipekua bali analifungua tu kuigiza.
Hakudumu hapo muda, akalifunga daftari na kwenda zake kantini. Si kwamba alikuwa na njaa. Alienda kutafuta amani.
**
“Una uhakika?” Akauliza Kamanda mkuu. Macho yake yalikuwa na mabaki ya furaha katika hali hii ya kushangazwa.
Alikuwa amevalia tisheti jepesi jeupe na suruali ya traki rangi ya bluu. Mbele yake, kiti kinachotazamana, alikuwa ameketi mwanaume mchina, Sheng, akiwa ndani ya shati jeupe, tai na suruali nyeusi ya kitambaa.
Katikati yao kulikuwa kuna meza ndogo ya kioo. Juu yake kulikuwa na chupa kubwa ya wiski yenye mfumo wa kipekee ikiwa inafanana na viglasi vyake kwa kando.
Viglasi hivyo vilikuwa vimejaa pomoni lakini havikuwa vimeguswa hata kidogo. Soga za hapa na pale zilikuwa zimenoga zikiyaweka makoo yao bize.
“Uhakika kabisa,” akajibu Sheng. Lafudhi yake ya kimandarin haikukoma kuonyesha asili yake. “Yani hatutohangaika hata kidogo, utakuja nambia menyewe.”
Basi Kamanda mkuu akacheka.
“Yani mimi nilikuwa nimepanga kumpa mateso ya kila aina mpaka alainike. Unajua kijana yule ni mgumu sana?” Akauliza Kamanda mkuu kiretorikali. “Mgumu sana! Sasa nilikuwa nafikiria nimuingize kwenye tanuri gani asichomoke.”
Akacheka kidogo kama mtu anayeumwa kifua.
“Kumbe kuna njia nyepesi bana.”
“Yes!” Sheng akatikisa kichwa. “Nakupa siku mbili tu, utaona matokeo yake.”
Kukawa kimya kidogo wote wakiwa na matabasamu usoni. Sasa wakapata wasaa wa kutia kinywaji mdomoni na kunywa fundo moja moja.
“Lakini kuna jambo takuomba,” alisema Sheng akiweka glas yake mezani.
“Karibu, nakusikiliza,” Kamanda akamkarimu akimtazama kwa macho ya umakini.
“Naomba, ufanye kila ujhualo. Huyu mtu asitoke ndani kabisa! He stopped most of my things when he was out. Sitaki kabisa arudi uraiani!”
Kamanda akatabasamu. Na kabla hajajibu akanywa kwanza fundo moja la wiski kisha akanguruma kupooza koo linaloungua.
“Yani kuhusu hilo?” Akatikisa kichwa. “Usijali kabisa. Ondoa kila aina ya shaka. Nitahakikisha anabakia nyuma ya vyuma maisha yake yote. Na hata itakaposhindikana, basi atoke akiwa mfu.”
Sheng akakunwa sana na hilo jibu. Akanywa kwa pupa kimiminika kilichobakia kisha akabamiza kiglas mezani.
“Ntashukuru sana. Now I can spend my night peacefully!”
“Kabisa yani, ondoa hofu. Namfahamu vema yule kijana. Nafahamu uwezo wake vizuri sana. Akitoka mule ndani kwa njia yoyote ile, vitanda vyetu vitageuka kuwa jehanamu. Siwezi kabisa nikaliruhusu hilo.”
Bas mara Sheng akaingiza mkono wake mfukoni kana kwamba anatafuta kitu. Akaingiza kushoto kisha kulia. Akatoa pochi yake na kuitazama. Ilikuwa imesheheni fedha. Haikuwa na uwezo wa kufungwa. Kamanda akaitazama pochi hiyo akiimezea na kinywaji chake.
Mara Sheng akamuuliza:
“Unahitaji fedha yoyote ile?”
Kamanda hakujibu, akabaki anajichekesha. Sheng akaiweka pochi yake mezani na kumsogezea Kamanda.
“Ya soda hiyo.”
**
“Mara yako ya mwisho kuonana naye ilikuwa lini?” Aliuliza Geof aliyejiveka suti matata ya kisasa rangi kahawia. Macho yake ya kazi yalikuwa yanamwangazoa Boka machoni.
“Ni muda mrefu sasa sijaonana naye!” Boka akadanganya. Hapa walikuwa wanamwongelea Miranda na kwa akili zake tayari alifahamu wapi inspekta huyu anapoelekea na yeye hakuwa radhi kabisa kudhalilika.
Kubainika kuwa mkewe alikufa kutoka na mahusiano na ‘mchepuko’ hakikuwa kitu anachotaka kimtokee hata kidogo.
Ni fedheha. Aibu.
Alishapata picha namna gani magazeti yatakavyomsakama na kumchora mbele za watu. Haswa magazeti ya udaku!!
Hili kwake lilikuwa ni jinamizi alilokuwa anajitahidi kuliokoka. Japokuwa bado hakujua ni kwa namna gani jambo hilo lilivyo na kina kirefu.
Hakuwaza ni kwa namna gani hili swala la Miranda kuhusika na kifo cha mkewe linaweza kuwa kweli, bali namna ambavyo atabaki salama kulinda heshima yake kwanza.
Japo pia hakutaka Miranda ahusike na hili. Kwanza, hakuwa anaamini kama Miranda atakuwa ametia mkono kwenye mauaji ya mkewe.
Kwake Miranda ni msichana mrembo asiye na makuu. Msichana ambaye hata kushika kijiko ama uma vizuri hawezi, sembuse kuua. Hakujua alikuwa anajidanganya.
Mwanamke huyo alikuwa ni mafia haswa!!
“Lakini mnawasiliana, sio?” Inspekta aliuliza ncha ya peni ikitoboa karatasi.
“Ndio, tunawasiliana lakini …” Boka akazimbazimba. ” … sio sana …”
“Unajua kama alikuwa anawasiliana na mkeo?” Inspekta akatupa swali jingine.
“Sifahamu,” Boka akajibu upesi. Inspekta akamtazama kwa muda kidogo machoni.
“Mheshimiwa, huyu binti alikuwa ni mfanyakazi wa mkeo, ilikuwaje ukawa na mawasiliano naye ya karibu?”
“Si karibu kihivyo,” Boka akajitetea. “Unajua Miranda ni mwanamke mchangamfu sana na mwepesi kuzoea mtu. Mke wangu alinikutanisha naye, akanizoea!”
“Mkeo akakupatia na namba yake?”
“Ha … hapana…! Niliipata namba yake sababu za kikazi, maana ndiyo alikuwa kaimu kwa company.”
“Na ukawa unakutana naye pasipo mkeo kujua.”
“Hapana. Unajua mke wangu ana wivu sana. Anapenda sana kuumba mambo ambayo hayapo! Mahusiano kati yangu na Miranda yalikuwa ni ya kikazi tu, si vinginevyo.”
“Kwa mujibu wa maelezo ya shuhuda namba moja wa ajali, rafiki yake mkeo aliyelazwa hospitali, amesema mkeo alishuhudia jumbe kadhaa za mapenzi kwenye simu yako toka kwa huyo mwanamke. Ni kweli?”
“Kwenye simu yangu? – mimi? Mmmh mmh sidhani! … chukua hata wewe utazame kama utaona!”
Inspekta hakuuliza tena jambo, akanyanyuka na kuaga aende zake. Akamhusia mheshimiwa asitoke nje ya mkoa ama kukaa mbali na makazi yake kwa muda wote huu wa upelelezi.
Akaenda akiwa sasa kichwani ameshamuongea mheshimiwa kama mtuhumiwa namba mbili wa mauaji. Maelezo yake yanayojikanganya na yale aliyoyatoa Miranda yalimtia hatiani.
Pengine walishirikiana na Miranda kutimiza mauaji waishi pasipo na shida, inpekta Geof aliwaza.
**
“Mi — mi — skuona haja ya …” Miranda aliongelea puani. Alikuwa ameibinyia simu sikioni, yupo sebuleni akitazama kwa macho ya kukanganyikwa.
“Nisamehe, sikujua kama yangekuwa makubwa kiasi hiki. Kweli tulikuwa na ugomvi, but nilichukulia simple tu,” Miranda aliruruma. Alisimama akashika kiuno chake akienda huku na huko. Mara akikuna nywele na kuminyaminya lips zake.
“I am sorry nimekuingiza kwenye a big mess … ndio, tulishawahi kukutana … yes … laki … eeenh … I didnt do it! Yeye ndo’ alikuwa anatak …”
Simu ikakata.
Miranda akaketi chini akishusha pumzi ndefu.
“Bila Jona hapa naenda ndani huku najiona,” akajisemea mwenyewe kama chizi.
Hakuwa na amani. Tumbo lilikuwa linamkoroga. Mwili mzima anauhisi umekuwa dhaifu.
**
“Yes, Miranda,” BC alinguruma baada ya kuchomoa simu yake mfukoni na kuiweka sikioni. Alikuwa ndani ya Mlimani City malls ndani ya duka la simu kama kawaida akiwa amenawiri na kupendeza hali iliyomfanya aonekane kijana zaidi kinyume kabisa na namba za umri wake.
Alikuwa ametinga kaunda suti ya bluu. Kifuani amechomeka ua dogo jekundu spesheli. Chini miguu akiihifadhi ndani ya kiatu madhubuti cha ngozi.
“What problem?” (Shida gani?) BC akauliza akiangazaangaza simu. Mara kidogo akaacha zoezi zima na kuisikiliza simu yake kwa umakini zaidi. Punde akatoka nje ya duka akiwa amekunja ndita.
“That is real serious shit!” (Hilo ni jambo kubwa kweli!)
Akatulia kidogo akiskiza. Kisha akasema kwa sauti ya agizo.
“Let’s meet immediately and see what we can do!” (Tukutane mara moja tutazame nini tunaweza fanya!)
Akaskiza tena. Kisha akahitimisha.
“It is either we get the door or make it by ourselves” (Ni aidha tuupate mlango ama tuutengeneze wenyewe!)
***
Akakata simu na kuirejesha mfukoni. Hamu ya kuendelea na ‘shopping’ ilikata. Akatoka kufuata gari lake akakwea na kuhepa.
**
“Upo sawa mzee?” Aliuliza mahabusu mmoja akimtazama Jona kwa macho ya wasi.
Jona alikuwa amelala chini akiwa ameshika kichwa kwa kuhisi maumivu makali. Pua yake ilikuwa inachuruza damu. Macho yake hayakuwa yanaona vema ingawa alivalia miwani.
Alikuwa anajihisi mdhaifu mwili mzima. Haswa kwenye maungio ya mwili. Mishipa ya damu ilikuwa inamvuta, na kwa wakati huohuo akihisi baridi kali!!
Wenzake, wanne, waliokuwepo ndani wakawa wanamtazama kwa hofu. Walikuwa wameshamtambua kama mtu asiyelala nyakati za usiku, ila hii ya leo ilikuwa mpya. Walihofu huenda amezidiwa. Haikuwa hali ya kawaida!
Alikuwa ananguruma na kugugumia kwa maumivu. Mwili unamtoka jasho jingi, alafu bado anajikunyata!!
“Muite afande,” mmoja akashauri. Yule aliyekuwa karibu na langoni akapaza sauti kuita afande afande kuna mtu kazidiwa. Ndani ya muda mfupi afande fulani akafika hapo na kumtazama Jona.
Akashtuka! Haraka akaenda kaunta na kumpasha habari koplo Massawe aliyekuwa ameketi hapo.
“Afande, kuna mtu kazidiwa mahabusu. Tufanye namna!”
“Nani huyo?”
“Jona!”
“Jona?”
“Ndio. Anatokwa na damu puani. Anamiminika jasho.”
Massawe akaguna na kufikiri kidogo. Akachomoa simu yake na kupiga. Baada ya muda mfupi ikapokelewa. Akaelezea hilo jambo la Jona.
“Nimesema achana naye. Hujasikia nini hapo?” Massawe akapandisha sauti. “Achana naye atarejea kwenye hali yake mwenyewe!”
Afande yule mpasha habari akanyamaza na duku lake kifuani. Na hii ndiyo moja ya shida ya jeshi. Pale mkubwa wako anapoamuru jambo huna nafasi ya kulikosoa zaidi ya kulifuata tu. Hata kama waliona halipo sahihi!
Na kwa afande huyu alifanikiwa kulimeza duku lake akaendelea na mengine kwani alifundishwa kufanya hivi huko mafunzoni. Hata ‘mkubwa’ akikuagiza usukume jengo mpaka lianguke, huulizi kama inawezekana, bali unaweka mikono yako ukutani na kupoteza nguvu yako bure!
Lengo kulazimisha tu utii ustawi ndani yako. Lakini pengine pia, kwa kujua ama kutokujua, huchochea hisia za uoga na unyenyekevu zoba.
“Afandeee!” Sauti za mahabusu iliendelea kuita. “Mtu amezidiwa huku jamani!”
Massawe kama vile hakusikia hayo akaendelea na kazi zake, afande mwingine akiwa anamtazama kwa kuibiaibia, alitumai pengine Massawe angeguswa hivi karibuni.
Lakini alikosea. Massawe alitia pamba masikioni. Hakuwa anasikia wala kujali.
**
“Amekufa?” Aliuliza mwanaume aliyekuwa amesimama langoni. Macho yake yalikuwa yanamtazama Jona akiwa ametulia tuli hachezi wala hatikisiki!!
Haraka akatoka langoni na kusogea karibu kuwakuta wenzake waliokuwa wanamtazama Jona kwa macho ya maulizo.
“Amekufa nini?”
“Sijui! Mbona ametulia hivi?”
“Huyu atakuwa amekufa!” Akauliza mmoja kisha akaweka kiganja chake shavuni mwa Jona. “Wa baridi kweli!”
Mwingine akaweka sikio kifuani, “bado mzima!” Akalipuka. “Nasikia mapigo yake ya moyo kwa mbali sana!”
“Atakuwa kazirai nini?”
“Labda. Unajua mwili wa binadamu ukishindwa kuhimili maumivu, unapoteza fahamu!”
“Ndo maana yake. Inasemekana ndo kamuua RPC. Sasa naona wenzake kama vile wamemshit! Si unajua ile? … wanamkomoa flani hivi!”
“Duh! Noma kweli mwanangu. Ila akifia humu itakuwa soo.”
“Hamna soo wala nini. Mbuzi atakuwa kafia kwa muuza supu!”
Maongezi haya yote Jona alikuwa anayasikia kwa mbali sana … mbali sana …
Kwa mbali sauti hizi zilivuma masikioni mwake katika mfumo wa mwangwi kana kwamba zinatokea ndani ya chungu ama pango kubwa. Hakuweza hata kutambua nani aliyekuwa anaongea hapa au pale japo alikuwa anawafahamu wote waliopo mule rumande.
Alitamani kutikisa mwili wake lakini hakuwa anaweza hata kidogo. Mwili ulikuwa mzito mno! Kichwani alikuwa anasikia kana kwamba sauti ya panga ama jembe likiwa limekita kwenye mwamba mgumu!
… Kaaaaaangggg’ … kaaaaaanggggggg’
Hakujua nini kinaendelea ndani ya mwili wake. Alifahamu fika tatizo litakuwa kile chakula alichokula. Ila hakutambua hii ilikuwa sumu gani. Na lengo lake mwilini lilikuwa ni nini.
Mbona bado yupo hai? Lakini akalitilia mashaka hili. Pengine amekufa na yeye bado hajalitambua. Kama hawezi kusogeza kiungo chochote cha mwili, ni nini huko kama si kufa sasa?
“Naaammmuuuuoooonnnnaaaa ….” alisikia sauti kwa mbali ikinong’ona kwa kujivuta. Neno moja alilisikia likiwa refu mno. Sauti hii akaitambua kuwa ya kipekee tofauti na zile alizokuwa anazisikia hapo awali.
Lakini bado fahamu zake hazikuweza kumjuza ni ya nani haswa! Akakodoa macho, lakini alikuwa anaona kizakiza cha kina cha maji. Watu awaona kama vivuli kwenye kioo.
“You are on time!” (Upo ndani ya muda!) Alisema BC akitazama saa yake mkononi. Alishafika nyumbani kwake, ameketi kibarazani penye viti na meza vya kupumzikia. Hakuwa amebadili nguo. Hakuingia hata ndani tokea amefika, zaidi ya kuketi hapo kumngoja mwanamke huyu,
Miranda. Ambaye alifika hapo akiwa amevalia jeans ya bluu na tisheti jeusi.
Uso wake haukuwa na furaha.
Alivuta kiti akaketi kisha pasipo kupoteza muda akaendea kilichomleta hapo.
“As I told you earlier. What should we do now?” (Kama nilivyokuambia hapo mapema. Nini tufanye sasa?)
“It is simple. We want him out, right?” (Ni rahisi. Tunamtaka atoke, sio?)
“Yes, we do! But do you think it will be that easy? He is charged of murder. Murder of a big man!” (Ndio, tunataka! Lakini unadhani itakuwa rahisi? Anashikiliwa kwa mauaji. Mauaji ya mtu mkubwa!)
“Maybe we should try to bail him out. Even if it may cost much!” (Pengine tungejaribu kumtoa kwa dhamana. Japo inaweza kugharimu mno!)
“What if that way won’t work?” (Vipi kama njia hiyo haitafanikiwa?)
“Then we’ll try the other one.” (Basi tutajaribu nyingine.)
Miranda akachipua tabasamu. Lakini BC akampatia tahadhari.
“That other way will only be possible if Jona complies with my conditions.” (Hiyo njia nyingine itawezekana kama tu Jona atakubaliana na vigezo vyangu.”
**
Majira ya asubuhi … kama saa nne hivi.
Kwa mbali kidogo Marwa anatazama kwenye lango la kituo kikuu akiwa amesimama na mfuko wake wa nailoni wenye chakula.
Alikuwa amevalia suruali pana ya kitambaa na shati lililokunjamana kwa uhaba wa pasi.
Akiwa anatazama huko akamwona afande Devi akitoka akiwa anaongozana na mwanamke fulani hivi, wakasimama langoni, na mara wakamtazama kwa pamoja, afande akamnyooshea kidole.
Punde mwanamke huyo akaanza kuchukua hatua kumfuata Marwa. Alipomfikia akamsalimu na kujitambulisha kama rafiki yake Jona. Yupo hapo kumtembelea na kumjulia hali.
Naye Marwa akajitambulisha kama ndugu na mkazi mmoja na Jona.
Lakini haikuchukua muda mrefu, Miranda akatambua Marwa hakuwa sawa. Macho yake yalikuwa mekundu, pia hakuonyesha yupo ‘comfortable’ kuongea naye.
Pengine alikuwa anamshuku anaweza akawa si mtu mzuri, akawaza. Kumwondoa hofu Marwa, Miranda akajipambanua kwa undani namna anavyoielewa kesi ile ya Jona kama ilivyopandikizwa mahususi kumteketeza, na mtuhumiwa wake mkubwa akiwa ni Sheng.
“Hata atakapoyashinda haya hatakuwa Jona wa awali.”
“Una maanisha nini?” Miranda akawahi kumuuliza.
“Tayari wameshamtilia virus mwilini!” Marwa akajibu machozi yakibubujika. “Hataweza kudumu muda mrefu, labda tu awe anapewa antidote! … Antidote ambayo anayo Sheng pekee!”
Miranda akakaukiwa na mate mdomoni.
“Umejuaje wamemtilia virus? Na kwanini wafanye hivyo?” Akauliza kwa kinywa chake kikavu.
Marwa akafuta kwanza chozi lake alafu akamwambia alijua hilo punde tu alipomwona Jona. Hali yake aliyokuwa anaipitia ilikuwa ndiyo ileile ambayo wazazi wake waliipitia kwasababu ya kutiliwa virus.
“Atapata shida sana,” akasema Marwa akijaribu kukumbuka namna wazazi wake walivyokuwa wanahanya. “Namwonea huruma. Na Sheng atamgeuza mtumwa!”
“Kivipi?” Miranda akawahi kuuliza.
Marwa akaeleza namna gani Sheng hutumia silaha hiyo ya virusi kumteka mtu akimfanya mtumwa wa antidote. Endapo unataka unafuu dhidi ya maumivu makali unayojisikia basi atakupatia antidote lakini kwa mabadilishano na kazi yake anayotaka utende.
Miranda akapatwa na woga. Hata akaishiwa na nguvu. Akamtaka Marwa waende kantini wakaketi na kuongea zaidi.
Wakaagiza chakula na kuendeleza soga. Miranda akamsikiliza vema Marwa akijieleza. Naye akaja kujinasibu kuwa yu mpangoni kumsaidia Jona atoke ndani, japo hajajua ni kwa namna gani.
“Afande wameniambia hawezi kupata dhamana hata kidogo, wala nisijisumbue popote pale. Nawaza namna ya kumng’amua mule.”
“Dada yangu,” Marwa akaita. “Naomba tu utafute namna yoyote. Na hata kama ukihitaji msaada toka kwangu, nipo radhi kukusaidia kadiri ya uwezo wangu wote … Jona atapata shida sana mule ndani. Watamtesa haswa kwa wale virus kwa maana hata antidote tuliyonayo haitoshi hata zaidi ya siku nne!”
Miranda akakuna kichwa chake kwa ukucha. Alikuwa anawaza. Alisonya kisha akatoa simu yake mfukoni na ‘kuchonga’ na BC. Akampasha habari namna alivyogonga mwamba kuhusu mambo ya dhamana.
“Ok, but it should be as fast as possible!” (Sawa, lakini inabidi iwe haraka iwezekanavyo!)
Miranda akakata simu kisha akamuaga Marwa, aenda zake. Wakabadilishana namba mwanamke huyo akayeya akionekana kuwa na haraka.
Punde kidogo, Marwa akiwa bado yu kantini, akapokea ujumbe toka kwa Miranda.
‘Ukifika home, nishtue!’
Akaujibu ujumbe huo kisha akarejesha simu mfukoni. Hata hakula. Hakuwa na hamu hiyo akitazama chakula alichomletea Jona hakikuguswa.
Alikuwa anawaza ni muda gani Jona atarejewa na fahamu apate kumpa chakula. Alikuwa radhi kungoja hapo mpaka usiku alimradi lengo lake litimie.
**
“Kaka, naweza nikatoa vyombo?” Sauti ilimshtua toka usingizini. Marwa akafikicha macho yake na kumtazama mhudumu, mwanamke mwembamba mweupe. Kisha akiwa na wenge lake la usingizi, akatazama mezani. Bado kulikuwa na chakula alichoagiza lisaa nyuma.
Akatikisa kichwa.
“Chukua tu, dada, hamna shida.”
Mhudumu akakusanya chombo na kwenda nacho. Marwa alipotaka kugeuza shingo kumtazama mhudumu huyo ndipo alipogundua shingo yake ilikuwa inauma!
Alikuwa amelalia kiti kwa muda mrefu. Shingo ilikuwa inamvuta kana kwamba amevunjika.
Akiwa anahangaika nayo, mara akamwona afande Devi akiwa anaingia kantini. Akajikuta anataka kujua hali ya Jona. Lakini kabla hajafanya lolote lile, afande Devi akamwona mwanaume huyo, bila hiyana, akamjongea karibu.
“Bado upo?” Akaigiza kushangaa.
“Bado nipo, mkuu,” Marwa akateta kinyonge akijitengenezea kitini. “Nitaenda wapi na sijampatia chakula ndugu yangu?”
Afande Devi akatikisa kichwa. Mara akanyoosha mkono wake kumuita mhudumu, upesi akaja hapo na kumwagiza amletee soda.
“Natamani sana kukusaidia ndugu yangu, sema nashindwa,” alijieleza afande Devi. “Nakuonea huruma sana. Namwonea huruma pia na Jona, yupo kwenye shida kubwa sana kwakweli.”
Marwa akainamisha kichwa chake chini. Akakizuia na mkono kutengeneza tama.
“Dawa ya nini?” Afande Devi akauliza akipokea soda yake toka kwa mhudumu.
“Hamuoni anaumwa?” Marwa akastaajabu. Afande Devi akanywa kinywaji chake fundo moja alafu akatikisa kichwa.
“Ninavyokuambia siwezi kumsaidia unadhani nakutania?” Akaifunika soda yake na kizibo isijazwe inzi. “Kwanza Jona haumwi magonjwa ya hospitali. Shida ni moja tu. Akitaka kupata unafuu inabidi akiri kutenda lile tukio.”
“Hata kama hajafanya!” Marwa akatahamaki.
“Ni kwa uhai wake lakini!” Afande Devi akamsabahi akikodoa macho. “Kufa na huku bado hajahusika ama kuishi kipi bora?” Akauliza Devi.
Marwa hakuwa na jibu, akakaa kimya. Devi akanywa mafundo kadhaa ya soda mpaka kuifikisha karibu na kikomo.
“Anyway, lete chakula hicho nitampatia. Wewe nenda kapumzike. Siku nzima upo hapa.”
“Sure?” Marwa akahakiki.
“Yeah. Leta tu wala usijali,” afande Devi akamtoa mashaka. Marwa akamkabidhi chakula.
‘Nimefika nyumbani’ Marwa alituma ujumbe kwa Miranda kama mwanamke huyo alivyomtaka.
Lakini kiuhalisia hakuwa bado amefika nyumbani bali karibia na maeneo ya nyumbani. Alikuwa amesimama dukani akinunua baadhi ya mahitaji yake, mojawapo likiwa hilo la vocha lililomwezesha kutuma ujumbe.
Muda si mrefu, Miranda akampigia simu. Akapokea na kuipachika sikioni.
“Ndio, nimefika … kesho? Mida ya saa ngapi na wapi? Ooh! Unapafahamu? … basi nakutumia ujumbe kukuelekeza … sawa, n’tajitahidi!”
Simu ilipokata alimalizia kuchukua vitu vyake hapo dukani, mkate na majani ya chai, alafu akashika zake barabara kwendelea na safari.
Lakini kuna mtu alikuwa anamtazama!! Kuna mtu alikuwa anamfuatilia. Mwanaume huyu alikuwa amevalia kapelo nyeusi, shati jeusi na suruali ya jeans. Alikuwa ameweka mikono yake mfukoni.
Kila Marwa alipokuwa anasogea, akasogea naye na mpaka akahakikisha Marwa aingiapo. Kazi yake ikawa imekomea hapo.
**
‘Nimeshapaona mkuu.’ ujumbe ulitumwa toka kwenye simu ndogo aina ya Samsung.
‘Safi, sasa ngoja mpaka ntakapokupa agizo’ ujumbe ukaingia kwenye simu hiyo.
‘Sawa’ ujumbe ukajibiwa.
**
Kwa dirishani moshi wa sigara ulikuwa unafuka. Kama ungelikuwa kwa nje ungeweza dhani kwa ndani kuna kitu fulani kimeshika moto.
BC alikuwa anavuta sigara yake kubwa kwa fujo. Hufanya hivi akiwa na mawazo lukuki kichwani mwake. Pembeni alikuwa ameketi Miranda akipooza koo lake na kinywaji ghali, John Walker.
Kulikuwa kuna ukimya hapa. Kama vile shetani alikatiza. Kwa muda kidogo kila mmoja alikuwa akishughulisha mdomo wake.
“What if we kill the inspector?” (Vipi kama tukimuua inspekta?) Aliuliza BC akiwa amefunikwa na moshi wa sigara. Uso wake alikuwa ameugeuzia dirishani.
“No!’ Miranda akatikisa kichwa. “You know what. Getting Jona out is our no-escape plan. Not only because Jona will save my ass, but will keep Sheng too obstracted to be comfortable. Without Jona, Sheng can even swallow us. We need him out, for me for us!” (Unajua nini. Kumtoa Jona ni mpango wetu usioepukika. Sio tu kwasababu Jona atanisaidia, lakini atamzuiza sana Sheng asiwe huru. Bila Jona, Sheng anaweza hata akatumeza. Tunamhitaji atoke, kwa ajili yangu, kwa ajili yetu!) Miranda alinguruma.
“But Jona will be police no more!” (Lakini Jona hatakuwa polisi tena!) BC akatahadhari.
“It doesn’t matter!” (Haijalishi!) Miranda akatema cheche. “Jona will make Sheng pay for all he has gone through in whatever way!” (Jona atamfanya Sheng alipe kwa yote anayoyapitia kwa njia yoyote ile!)
Miranda akasafisha koo na kuongezea:
“This is the best chance to get Jona in our side!” (Hii ni nafasi yetu kubwa kumpata Jona kwenye upande wetu!)
**
BC akasafisha koo lake. Hakuwa anajua mengi kumhusu Jona ukilinganisha na Miranda. Miranda akachukua fursa hiyo kumweleza BC juu ya uwezo wa Jona.
Ni mwanaume wa shoka. Mwanaume ngangari, mtu wa kazi!! Endapo wakimpata mwanaume huyo basi wasijali kabisa kuhusu ulinzi na usalama. Na wala Sheng hatakuwa tena mtu wa kumhofia.
“Let’s get the best out of this. It is obvious Jona’s lost all of his interest in Police army. To him, they are now traitors and cruel organ.” (Tufaidike na hili. Ni wazi Jona ameshapoteza hamu yake yote ndani ya jeshi la polisi. Kwake, sasa ni wasailiti na wakatili.)
Maelezo haya kwa namna fulani yakagonga kichwa cha BC. Alitokea kuvutiwa nayo. Akampa Miranda kazi ya kuhakikisha hilo linatokea. Yaani kumshawishi Jona aingie upande wao.
Hapo Miranda akakumbuka na agizo la Kinoo juu ya wale wanawake wawili: Sarah na Sasha. Akataka kumweleza BC lakini akaona huo si muda sahihi.
Wacha kwanza wapambane na hili lililopo mezani. Hili lililo kubwa. Hayo mengine yatafuata baadae. Hata hakumtonya BC juu ya hali ya Jona kule gerezani kuwa yu hoi na ameshapandikiziwa virusi.
Alihofia BC anaweza akabadili mawazo. Aidha akamchukulia Jona anaweza kuwa mzigo badala ya msaada kwao.
“So what way we gonna use?” (Sasa njia gani tutatumia?) Akauliza Miranda. Aliona wameshakubaliana wanataka kumtoa Jona. Kitu pekee kilichobaki ni namna tu.
BC akavut sigara kwa dakika kama mbili pasipo kusema kitu. Alipoweka sigara yake chini akabinua mdomo wake mkavu alafu akajitengenezea vema kumtazama Miranda.
“We need plan in this,” (tunahitaji mpango kwenye hili,) akanza kutambulisha wazo lake. Miranda akamuazima masikio yote.
“We have to force him out. You know we can’t do it while he’s in the police station. It is better if we get the chance to have him in the truck!” (Inabidi tulazimishe atoke nje. Unajua hatuwezi akiwa ndani ya kituo cha polisi. Ni bora kama tukipata nafasi akiwa ndani ya gari!)
Mpango wa BC hapa ulikuwa ni kumchomoa Jona toka garini kwa kuliteka gari hilo ama kulipindua, aidha likiwa linatoka mahakamani ama kwenda!!
Lakini kwa Miranda alikuwa ana wazo jingine. Hili la BC aliliona ni gumu kutekelezeka kwa minajili kwamba polisi watampeleka Jona mahakamani pindi tu atakapokiri kama kweli alihusika na tukio la mauaji ya RPC kitu ambacho Jona hatakifanya abadani.
Japo wanatumia virusi kumlazimisha afanye hivyo, Miranda aliamini Jona atakuwa mgumu kuridhia.
Sasa wafanye nini?
Akili yake ikawa hii: wamchomoe Jona akiwa hapo hapo kituoni!!
“Serious??” BC akatahamaki. Lakini kabla hajamkatisha mwanamke huyo, akampatia nafasi kwanza amweleze.
Miranda akafunguka kuwa anahitaji ‘tiny gas containers’ kwa gharama yoyote ile. Atahitaji kama kumi hivi na ndani ziwe zijazwe na Fluothane, Neothyl pamoja na Penthrane’.
Kwa kutumia watu wawili atakaoongozana nao, basi atakamilisha zoezi la kumtoa Jona ndani ya rumande!!
“Are you sure??” BC alikuwa na wasiwasi. Kupata gesi hizo haikuwa shida hata kidogo, lakini utendaji ulimstaajabisha.
Hakutaka kumkatisha tamaa Miranda. Japo hakuelewa namba mpango huu utakavyotekelezwa, akaamua kumwamini na kumpatia nafasi. Ila akampa tahadhari.
“You have to be very careful!” (Inabidi uwe makini sana!)
“I know to keep my ass safe!” (Najua kujiweka salama!) Miranda akajibu kwa kujiamini.
Kwa asilimia zote alikuwa anaamini mpango wake utatimia!!
**
Usiku wa saa tatu…
“Naomba utupatie faragha,” Miranda aliongea akimtazama Sarah. Ilikuwa ni punde kidogo tu baada ya kusalimiana na Kinoo na kujuliana hali. Sarah akanyanyuka na kuwapisha kwa kwenda nje lakini hakuwa anapenda kitu hichi hata kidogo.
Alikunja sura yake, akabinua mdomo na kutembea kwa kasi kuelekea huko nje. Mimba nayo ilikuwa inachangia. Aliona anasumbuliwa, na aidha Miranda hakuwa anajali hali aliyomo.
Kinoo akamtazama Sarah akiishia akijaribu kuhisi alichonacho mwanamke huyo kifuani. Alijua wazi Sarah alikuwa amekwazika na hakupenda kitu hicho kitokee.
Alikuwa anampenda Sarah. Na mimba yake tumboni ilimfanya amjali maradufu.
“Kama nani?” Miranda akajibu kwa swali, kisha akaongezea: “mahusiano baina yako na yeye hayahusiani hata kidogo na kazi yetu!”
“Ndiyo maana nikakusihi uwaingize!” Kinoo akatema cheche. “Tutaendelea kumtoa hivi kila tukiwa tunaongea mpaka lini? Anajihisi vibaya.”
“Kinoo,” Miranda akaita. “Unadhani sijali? I do care but it takes time. Be patient. Kuna kazi tunatakiwa kuifanya hapa, tuweke nguvu zetu zote hapo, punde itakapokamilika, mambo yote haya yatakuwa mepesi kama kumsukuma mlevi!”
Kinoo akatikisa kichwa akishushia pumzi puani. Akajaribu kutuliza moyo wake.
“Kazi gani hiyo?” Akauliza.
“Kumtorosha Jona kituoni!” Miranda akamjibu kana kwamba ni kazi ya kumuua mbu.
Kinoo akashangazwa. Ulikuwa ni mpango hatari huo. Yani sawa na kwenda kucheza na domo la mamba!!
Miranda akamtuliza.
“Inawezekana. Na kama kila kitu kikifanyika poa, tutatumia dakika tano tu kukamilisha zoezi hilo pasipo kumwaga tone lolote la damu!”
Kisha mwanamke huyo akatiririka kumwelezea Kinoo namna gani watafanikisha zoezi lao. Kinoo akasikiliza kwa umakini.
**
“Siku nyingine usinilete huku, uje mwenyewe!” Sarah alifoka akimtazama Kinoo kwa jicho la vita. Walikuwa ndani ya gari wakirudi nyumbani baada ya kumalizana na Miranda. Kinoo alikuwa ameshikilia usukani asionyeshe kukwaza na kauli ya ‘mkewe’.
“Haitojirudia tena, usijali.”
“Mara ya ngapi hii?” Akabweka Sarah. “Ya pili! Nikija mwanitoa nje. Wanileta huku ili un’toe nje?”
“Ila nilikuambia ubakie nyumbani ukakataa,” Kinoo akajitetea akiwa anatazama barabara.
“Kwahiyo ndiyo maana ukaamua kuja kunikomoa, sio?” Miranda akatema cheche. “Wewe ulitarajia uniache nyumbani na nani? Nikae peke yangu nimekuwa mchawi na unajua kabisa hali yangu?”
“Nisamehe, Sarah,” Kinoo akaamua kukatisha maongezi. “Halitajirudia tena nimekuahidi.”
Lakini hilo halikuwa jepesi kwa Sarah. Na si tu Sarah, bali kwa wanawake. Kuna muda unaweza jikuta unahitaji ‘earphones’ kwani wakianza kuongea hawatakupa hata mapumziko ukanywa maji!
Kinoo hakujua ni muda gani Sarah aliacha kuongea. Alihamishia akili yake yote barabarani. Na akiwaza kazi ambayo ipo mbele yao.
Aliporudi fahamuni kuwa yupo na mtu pembeni yake, tayari mazingira yalikuwa kimya. Angalau akahema. Akamwambia sasa Sarah kuwa kuna kazo wanatakiwa kuifanya hapo mbeleni japo hakumuweka wazi ni ipi hiyo.
Sarah akapuuzia. Alikuwa analipiza kile Kinoo alimfanyia kwa kumnyamazia wakati anaongea hapo nyuma. Kinoo naye akalitambua hilo, hakuangaika naye.
“Naomba tupitie kwa Sasha,” baada ya dakika mbili Sarah akanena.
“Kufanya nini huko saa hii?” Kinoo akauliza.
“Nataka nikalale huko leo. Sina hamu kabisa ya kuwa na wewe.”
“Eh!” Kinoo akaguna.
Hakutaka kusema jambo akaamua kutimiza agizo la mpenzi wake huyo kuepusha maneno. Lakini bado alikuwa amekosea. Sarah akawaza pengine Kinoo alikuwa amemchoka.
Yani amemwambia akalale kwa dada yake alafu anakubali pasipo hata kubisha? Akavuta mdomo mpaka wanawasili. Walipofika ndipo akatoa ya moyoni.
“Naona umefurahi mimi kuja huku!”
Kinoo akatikisa kichwa asiseme jambo. Aliona angeongea angesababisha vingine ambavyo hakuvitarajia. Akaongoza njia mpaka getini, akagonga na wakakaa kungoja.
Ndani ya muda mfupi geti likafunguliwa na akatoka mwanamke mmoja mtu mzima. Wakamsalimu na kumwambia haja yao, kumwona Sasha.
“Mbona amehama hapa siku nyingi!” Mwanamke huyo akawaeleza. Sarah akastaajabu. Inawezekanaje dada yake akahama hapo makazi yao ya muda mrefu pasipo kumwambia??
Lakini pia atakuwa ameenda wapi na ilhali pesa hakuwa nayo? Hakupata majibu.
“Amehamia wapi?” Sarah akauliza. Yule mwanamke akamwambia hafahamu. Kitu pekee anachojua ni kwamba mwanamke huyo amehama.
“Ahsante sana,” Kinoo akashukuru na kumtaka Sarah warejee kwenye usafiri waondoke zao.
Lakini wakiwa wapo njiani, Sarah hakuwa na amani. Alikuwa anamuwaza pacha wake. Alihisi atakuwa shidani. Alikosa kabisa furaha.
“Usijali, ni mtu mzima yule. Hawezi akawa amepotea,” Kinoo akamtoa hofu.
Angalau hili swala likawaleta pamoja baada ya kuhitilafiana hapa nyuma.
“Mara yake ya mwisho kuonana naye alinambia hayuko vizuri kifedha. Hata nikamtoa nauli. Leo naambiwa amehama. Inashangaza!” Sarah aliongea kwa hisia.
“Au kafukuzwa kodi?” Kinoo akauliza. Lakini kabla Sarah hajajibu, Kinoo akapuuza wazo lake hilo. “Ila haiwezekani! Si angekuja pale nyumbani??”
Sarah akabaki kimya. Punde akatafuta simu yake na kumpigia dada yake. Sijui alikuwa anawaza nini akachelewa kufanya hilo. Aliweka simu sikioni kusikilizia, baada ya ukimya wa sekunde kadhaa, sauti ikamwambia anayempigia hapatikani!
Akajaribu kama mara nne, yote majibu yakiwa hayohayo, HAPATIKANI!! Sarah akazidi kujawa na hofu.
Mpaka wanafika nyumbani alikuwa kimya. Ila kheri alipokuwa anaingia ndani, simu yake ikaita. Kutazama alikuwa ni Sasha! Mwanamke huyo alimtafuta baada ya kukuta taarifa ya kutafutwa punde baada ya kuwasha simu yake.
“Hallow!”
“Hey nambie sis!”
“Mambo?”
“Poa. Unaendeleaje dear?”
“Safi tu. Upo wapi?”
“Mie? Ntakuwa wapi pengine zaidi ya nyumbani saa hii?
“Nyumbani?”
“Ndio. Nipo kwa bi Mwenda hapa.”
Bi Mwenda alikuwa ni yule mwanamke aliyewafungulia geti Sarah na Kinoo walipoenda kumtembelea Sasha kule makazini.
“Sasha,” Sarah akaita. “Kwanini unaniongopea?”
“Nakuongopea? Kivipi dear?”
“Umehamia wapi?”
Kidogo kukawa kimya.
“Najua umehama. Nambie umehamia wapi?”
“Sarah, yah nimehama. It’s a long story. Ntakutafuta tuongee.”
Simu ikakata. Sarah akaachwa na bumbuwazi. Akajaribu tena kupiga akaambiwa haipatikani!!
Sasha ana nini?? Akajiuliza akiduwaa.
**
Usiku mzima alikuwa analia kwa maumivu makali! Mifupa ilikuwa inamuuma mwili mzima. Kichwa bado kinagonga na pua inamimina damu!!
Kila alipotaka kusogeza kiungo chake cha mwili, akaishia kulalama na kushindwa. Haki mateso yalikuwa makali mno. Hakuwahi kujihisi mdhaifu kiasi hiki tangu azaliwe.
Hakuwahi kuhisi maumivu makali kiasi hiki tangu atambulishwe duniani. Haya yalikuwa kiboko!! Ni kama vile alikuwa amevunjwavunjwa mwili mzima kisha akadumbukizwa kwenye bwawa la barafu akae humo kwa masaa!
Hakuwa anahisi chochote kwa ngozi yake. Kichwa kilikuwa hakigongi tena bali kinampigia kelele kali! Ushawahi kusikia paka akikwarua bati? Ndivyo Jona alivyokuwa anasikia makelele sikioni!!
Meno yalikuwa yanamuuma. Jasho lilimwagika.
Wenzake hawakuwa na la kumsaidia zaidi ya kumtazama tu kwa huruma. Japo hawakuwa wanajua nini Jona anahisi mwilini, walimwona anateseka sana.
“Jooonnnaaaa!” Sauti kwa mbali ilimfikia masikioni. Kama kawaida sauti hii alikuwa anaisikia kwa mbali sana. Kwa taratibu sana.
Alitamani ajue sauti hii ni ya nani ila hakuweza. Maumivu alikuwa anayasikia. Kelele sikioni iliyokuwa inamuumiza, ilimnyima nafasi hiyo.
Langoni alikuwa amesimama Kamanda mkuu. Alikuwa yu ndani ya sare yake ya jeshi iliyokuwa imechafuka kwa urembo na vyeo. Macho yake yalikuwa yanamtazama Jona aliyekuwa amelala chini.
Kidogo akaungana na vijana wawili waliokuwa wamevalia kiraia. Walikuwa ni maaskari pia. Miongoni mwa vijana hao alikuwa ni yule ‘jamaa’ aliyemfuatiliw Marwa kuyafahamu makazi yake.
Wote wakamtazama Jona kwa muda mchache kabla Kamanda mkuu hajaagiza wamlete ofisini kwake ana maongezi naye.
**
“Jona!” Kamanda akaita akimtazama Jona kitini. Jona alikuwa amekaa hapo akiendelea kuchuruza damu puani. Alikuwa ameketi kana kwamba mgonjwa wa utindio wa ubongo. Alikuwa ameng’ata meno, amekunja ndita, mabega ameyapandisha juu. Macho amefumba kusikilizia maumivu pomoni anayosikia.
Kwa mbali sauti ya Kamanda ikamfikia:
“Jona, utaendelea na mateso haya mpaka lini? Kubali yaishe. Si kila mara utaibuka kuwa mshindi! … naweza nikakusaidia. Nipatie nafasi.”
Jona hakuwa na uwezo wa kujibu. Aliendelea kukaa vilevile kana kwamba hajasikia kitu.
“Ukifanya mchezo utafia rumande kwa ubishi wako!” Kamanda akatishia. “Sasa chagua moja nikakutupie huko uendelee na maumivu yako ama nikusaidie upate unafuu??”
Japo Jona hakuwa na uwezo wa kupambana, na alikuwa anasikia maumivu yasiyo na mithili, akafungua macho na kumtazama Kamanda. Macho yake yalikuwa mekundu mno!
Alimtazama Kamanda kwa macho ya umauti. Macho ya kisasi!!
Akiwa anahisi maumivu ya kufa, akanyoosha mkono wake akitaka kumkamata Kamanda. Ila haukufika, akashindwa kustahimili maumivu.
“Unajifanya mgumu eenh?” Kamanda akamuuliza akibinua mdomo wake. Akagonga meza mara mbili.
Puh! Puh!
**
Mlango wa ofisi ukafunguliwa, wakatoka vijana wawili wa Kamanda wakiwa wamembelelea Jona. Kwa upesi wakayoyoma naye wakielekea rumande kwenda kumtupia huko.
Mlango wa ofisi ulipofunga, Kamanda akanyaka simu yake na kupiga.
“Bado ni mgumu. Nadhani tuangalie namna ya pili sasa,” Kamanda alisema kwa hakika.
“Hapana,” sauti ikavuma simuni. “Ngoja tutazame na kesho kama bado ataendelea kuvumilia. Virus hao wanatafuna kila siku inavyokwenda. Hataweza kuvumilia zaidi ya kesho. Na itapendeza zaidi kama yule rafiki yake atamletea antidote!”
“Kivipi?” Kamanda akauliza.
“Hao virus ambao wapo mwilini mwake hawaondolewi na antidote waliyonayo. Endapo atakampopatia, basi ataharibu mambo zaidi. Atapata maumivu maradufu!!”
Kamanda akaridhika na hayo maelezo. Akakata simu.
**
“Nipo tayari kwa kila kitu,” alisema Marwa akimtazama Miranda. Walikuwa wapo ndani ya nyumba ya Jona majira haya ya mchana. Miranda alifika hapo muda si mrefu hapo nyuma akiwa katika harakati zake za kuwezesha zoezi la kumtoa Jona kituoni.
“Sawasawa!” Miranda akatikisa kichwa. “Hili zoezi inabidi lifanyike kesho kwa namna yoyote. Wewe kazi yako ni ndogo sana. Kule kituoni wameshakuzoea sasa kuwa unaleta chakula mara kwa mara.
Sasa kesho yake nitakupatia hotpot la chakula ulipeleke huko. Utakapofika, utafanya njia zozote ulifungue pale kaunta, kwa muda wa sekunde kumi tu. Kisha ukifanikiwa kulipeleka kwa Jona, umtahadharishe asile.
Ataliweka wazi kwa dakika moja, inatosha. Mengine mimi na Kinoo tutamalizana nayo.”
“Sawa, hamna shida,” Marwa akapokea maelekezo. Kisha pasipo kupoteza muda akamwambia Miranda kuwa anataka kwenda kituoni kumpelekea chakula Jona.
Na pia vilevile antidote!!
“Hamna shida, naweza kukuwahisha,” Miranda akamkarimu. Wakanyanyuka toka sebuleni na kwenda nje walipodumbukia ndani ya Range Rover sport nyeupe na kutimka.
** Kwa kasi waliyoitumia hawakuchukua muda kuwasili, Marwa akashuka garini na kwendaze kituoni baada ya kuagana na Miranda aliyesema anaenda kushughulikia na kuweka mambo sawa.
Marwa akaingia mapokezi na kukutana na afande Devi aliyempokea kwa ukarimu na kumjulia hali.
“Nimekuja kumletea chakula jamaa ‘angu,” alisema Marwa kisha akafungua chakula na kukionyesha.
“Najua umekuja sababu hiyo,” alisema afande Devi pasipo kutazama chakula hicho. Ni kheri akuwapo koplo Massawe, basi akamruhusu akamwone mtu wake upesi huko rumande.
Chap Marwa akafika huko na kumkuta Jona akiwa amejilaza hoi. Akamuita mara tatu akisaidiwa na mahabusu wengine. Jona akaamka na akiwa hajiwezi kwa lolote, wenziwe wakamburuta kusogea langoni.
Kwa namna ambavyo Marwa alimwona Jona, akashindwa kuzuia machozi machoni mwake. Jona alikuwa amepungua. Ni mdhaifu. Hana afya wala havutii kumtazama.
Si Jona yule umjuaye.
“Jona,” Marwa akaita. “Kula angalau.” Akambembelezea chakula. Jona akatamani sana kumjibu lakini hakuwa anaweza.
Alimtazama Marwa akamwona kwa mbali. Alitabasamu kumpa matumaini lakini Marwa akaishia kulia.
“Nitashinda,” Jona alisema kwa sauti ya chini. “Usijali, Marwa.”
Akala tonge mbili tatu, akashindwa kuendelea. Alilalama anasikia kichefuchefu, na kadiri anavyotafuna anasikia kichwa kinamuuma maradufu!!
Japo ni kweli alitamani kula, tumbo lilikuwa tupu, hakuweza abadani!
“Nimekulete antidote!” Marwa alimwambia kwa macho ya furaha. Alikuwa amemshikilia na mkono wake kumzuia aketi.
Kabla Jona hajasema kitu, Marwa akatazama kushoto na kulia alafu akachonoa kichupa kidogo mfukoni, akamtaka Jona afungue mdomo.
Akamminia chote kisha akamruhusu ajilaze chini.
“Utakuwa sawa,” Marwa aliamini.
Jona akalala asiseme kitu. Muda si mrefu akakata fahamu kabisa!! Hakuwa anasikia, kuona wala kuhisi chochote.
Maumivu yalizidi mwilini mpaka fahamu ikashindwa kustahimili. Marwa asiwe anajua hilo, akamtazama Jona kwa sekunde kadhaa. Na hata alipoona kimya akatambua mwanaume huyo atakuwa katika hatua za kuwa sawa. Hivyo hana haja ya kuhofu.
Akamuaga Jona na kisha kwenda zake.
**
“Afandeee!” Sauti ikavuma ndani ya rumande. Si kwamba kulikuwa kimya, bali sauti hii ilikuwa kubwa kupita kiasi.
“Afandee, kuna mtu anakufa huku!” Alipaza sauti jamaa mmoja aliye ndani ya chumba kimoja na Jona.
Jona alikuwa anatoa damu masikioni, puani, mdomoni na machoni kama machozi!! Hakuwa anatikisika hata kidogo. Hakuonyesha dalili zozote za uhai.
Hata mwili wake ulikuwa wa baridi kana kwamba ametoka kwenye jokofu!!
Haraka afande Devi aliwasilia akamtazama Jona. Mahali alipokuwa amelaza kichwa chake palikuwa pametapakaa damu.
Hata afande huyu akashtushwa sana na hili. Upesi akamweleza na kumsisitiza Massawe akamwambia mkuu wa kituo kuwa wanatakiwa kuchukua hatua upesi la sivyo mtu atawafia rumande iwe tabu!
Taarifa zikafika kwa OCD, ila ikawa bure. Jona hakuruhusiwa kutoka kituoni kwa namna yoyote ile labda awe mfu tu!!
“Nenda kaendelee na kazi yako. Kama kufa mwache afie humo. Alivyomuua RPC alidhani atastarehe??” Alisema OCD akiwa anachokonoa meno yake kwa toothpick.
**
“Ewaah … naona ameshapatiwa ile antidote!” Alisema Kamanda mkuu akitabasamu na simu.
“Yes … he is in critical situation … hawezi akafa? … ooh sawa. Hamna shida nitafanya hivyo.”
Kamanda akakata simu kisha akacheka. Alipewa maagizo ya kuyatimiza.
**
“Naomba uningoje hapa,” alisema Sarah kwa sauti ya kuamuru. Macho yake yalimtazama Kinoo kabla hajabanduka toka kwenye kiti cha gari na kwendaze ndani ya jengo maeneo ya Msasani.
Kinoo akamtazama mwanamke huyo akizamia humo aliposema anaenda kukutana na dada yake, Sasha, kama walivyopeana maelekezo.
Akawaza kidogo akijiuliza maswali kadhaa. Sasha alikuwa anafanya nini katika hilo jengo maeneo ya Msasani na kwanini Sarah hakutaka kuongozana naye kwenda humo.
Kwani Sasha si shemeji yake??
Hakuwaza wala kujihangaisha sana kwani alidhani pengine Sarah anataka tu kulipiza kisasi kwa vile anavyomfanyia akiwa anaongea na Miranda akimtaka atoke nje.
Akajikuta anatabasamu na kupuuza. Kosa ambalo hakutakiwa kulifanya hata kidogo.
Kwenye ulimwengu wa kijasusi, hakuna kitu kidogo hata siku moja. Kila tendo laweza kugeuka na kuwa sumu kali ys kumshusha tembo ndani ya sekunde kadhaa tu!!
Kusogezea muda wake wa kungoja, akawasha redio na kulaza kiti, akajilaza.
Akatazama dirishani kisha akarudisha macho yake kwa Sarah.
“Sijasema tumuue yeyote yule, Sarah!”
“Sasa unadhani hizo taarifa utakazokuwa unapeleka huko zitaishia kwenye nini?” Sarah akamkatiza.
Hakutaka kumwelewa dada yake hata kidogo. Alitoka zake ndani ya nyumba pasipo kuaga akamwacha Sasha akiwa ameduwaa.
Akang’ata meno na kukunja ngumi kwanguvu. Mpango wake ulikuwa umefeli!!
Sasa atafanyaje?? Kichwa chake kilikuwa moto. Hakuna mtu yeyote anayetakiwa kujua siri hiyo ila tayari ashamweleza dada yake.
Hapa akapata shaka kubwa. Hakuamini kama Sarah atautunza mdomo wake asiseme kitu. Kama tu akiufungua mdomo wake basi kazi itakuwa imekwisha!!
“Damu nzito kuliko maji,” alijipa moyo. Ila kama mambo yasipoenda kama inavyotakiwa, basi hamna budi.
Hamna budi.
Itabidi amtoe sadaka dada yake!!
Aliwaza.
**
Usiku mzito, ndani ya chumba chenye giza …
Waaaaa!! Jona alimwagiwa maji ya baridi na kuamriwa aamke upesi. Hakujua hapo alipo amefikaje. Alijaribu kufungua macho yake kutazama lakini hakuwa anaona kitu.
Si tu kwamba kulikuwa ni giza, hakuwa na uwezo wa kuona kabisa mbali na kutokuwa miwani. Hata masikio yake yalikuwa yamepoteza uwezo wake wa kawaida. Pia ngozi yake yake, ilikuwa hafifu kwenye kuhisi.
Lakini ajabu alipomwagiwa maji hayo ya baridi, alilia kwa maumivu makali ambayo hajawahi kuyapata!!
Ni kama vile maji hayo yalikuwa na visu ama viwembe. Yalimfanya ang’ate meno kwa ukali wa maumivu yaliyopitiliza. Alihisi amechanjwa chanjwa kila sehemu ya mwili wake iliyoonja maji hayo ya baridi.
Alihisi maji hayo yameingia mifupani. Yanamtafuna!!
Japo alikuwa dhaifu, akatapatapa kujinasua. Akahangaika huku na kule lakini hakuweza kufua dafu kwenye kamba ngumu alizokabwa nazo kitini.
Lakini kama haitoshi, ndani ya chumba hicho kulikuwa na ndoo tatu za maji baridi kabisa. Zote zilikuwa zinamgojea yeye.
Zinamngoja akileta ukaidi.
“Mzee, hatuna muda wa kupoteza hapa na wewe. Tunataka kitu kimoja tu. Kiri na sisi tutaenda zetu. Ukileta ujuaji, tutasema na wewe usiku huu mzima.”
Jona alisikia sauti hiyo kwa mbali mno. Hakumjua anayemwongelesha ni nani. Alikuwa amekunja shingo yake kana kwamba kaelemewa na kichwa.
“Sisemi kitu,” akasema kwa kunong’oneza. Mtesi wake akatabasamu kuonekana meno kizani.
Baada ya hapo Jona akamwagiwa ndoo mbili za maji baridi. Maji haya si kwamba yalimfanya asikie baridi, ila mchanganyiko wake na virusi vilivyomo mwilini mwa Jona, ulizalisha maumivu makali yasiyomithilika!!
Haikupita muda mrefu, Jona akazima.
Simu ikapigwa.
“Hatujafanikiwa, mkuu.”
“Sawasawa,” sauti ikatoka simuni. Sauti nzito ya Kamanda mkuu ikiashiria kutoka usingizini. Mwanaume huyo alisafisha koo lake kisha akasema:
“Sasa tuhamie kwenye njia ya mwisho. Kesho hakikisha mnamteka yule kijana anayemletea chakula kisha mumpatie machaguzi mawili, aidha tumuue huyo kijana ama afanye tunachokitaka.”
**
Kesho yake, asubuhi ya saa mbili …
“Kila kitu kipo tayari,” alisema Miranda akimtazama Kinoo kwa jicho la kazi. Kinoo akabinua mdomo wake na kutengua vidole.
“Basi na kazi itendeke!” Akasema kwa kujiamini akinyanyuka.
“Hakikisha hakuna kosa hata moja linafanyika,” Miranda alisisitiza. “Hii ni kazi ya kufa ama kupona. Kama tukiharibu basi tumetia mchanga kwenye wali wa kula mwaka mzima.”
“Usikonde, bibie,” Kinoo akamtoa shaka. “Kila jambo litaenda kama lilivyopangwa. Lakini usisahau ahadi yangu.”
Miranda hakusema kitu, akachomoa simu yake na kupiga. Punde akasema:
“Nikukute hapo hapo.” Alafu akakata simu na kusimama.
**
“Bila shaka unakumbuka maelezo?”
“Ndio.”
Miranda akamshika Marwa mkono wake wa kuume.
“Hakikisha unafanikiwa,” akamsihi. “Hatuna nafasi ya kufanya kosa lolote leo. Aidha kama tunataka kupoteza yote.
Marwa akatikisa kichwa.
“Ntajitahidi kadiri ya uwezo wangu.”
Miranda akatabasamu, kisha akanyanyuka na kwendaze.
**
Kwenye majira ya saa kumi jioni …
Baada ya mlio wa gari huko nje, mara Marwa anafungua geti na kuzama ndani. Mkononi amebebelea hotpot ya chakula. Mwendo wake ni wa ukakamavu na usoni hakuonyesha shaka.
Ni katika kituo hiki cha kati. Watu walikuwa kadhaa wakiwa wamesimama huku na kule aidha wakingojea watu wao watoke nje ama wakingoja kuingia ndani.
Kwa haraka haraka Marwa akatazama mazingira hayo alafu akazama ndani. Hakumkuta afande Devi wala koplo Massawe. Alimkuta hapo afande fulani wanne waki wapo bize na kazi za hapa na pale.
Akaeleza dhumuni lake kumwona Jona na kumpatia chakula. Afande wale wakatazamana kisha mmoja akamwambia haitawezekana.
“Kwanini?” Marwa akauliza. Afande wale hawakumpa sababu, wakamwambia tu haiwezekani. Kwa ufupi.
Basi Marwa akatoka zake hapo kaunta na kuelekea kantini akiwaza ni kwa namna gani atafanya. Kwa muda wote aliokuwa pale kaunta roho ilikuwa inamdunda haswa.
Alikuwa ana kauoga ndani yake. Kama wale polisi wangemtazama vema wangelibaini hilo na huenda wakamtia mashakani.
Alivuta kiti akaketi. Akachojoa simu yake na kumtumia ujumbe Miranda kumweleza hali iliyopo. Punde Miranda akampigia.
“Do it,” sauti ya kike ilisihi. “You must do it, Marwa. Alafu utatuhabarisha.”
Kabla Marwa hajajieleza sana, mara simu ikakata. Marwa akashusha pumzi ndefu. Moyo ulikuwa unamwenda mbio.
Jasho kwa mbali lilianza kutambaa usoni mwake.
“Samahani, naweza nikakusaidia?” Sauti ya mhudumu ilimgutua mawazoni.
“Naomba maji makubwa,” akaagiza na kuendelea kutafakari. Kama bahati akamwona afande Devi. Hapa angalau akajikuta anapata ahueni. Lakini haikutakiwa Devi amwone pale kantini!!
Kama Devi angelimwona pale kantini basi afande huyo angeishia kuchukua hotpot na kumtaka aende, yeye atasimamia zoezi.
Hivyo, haraka akanyanyuka na kujificha. Afande Devi hakuketi hapo kantini akateka soda na kulipa kisha akayeya eneo ambalo Marwa aliamini itakuwa ni kule kaunta.
“Pesa yako hii hapa,” alisema Marwa pasipo kumtazama mhudumu. Macho yake yalikuwa yanatazama njia asiwaze hata kama kuna chenji anatakiwa kungoja.
“Chenji!”
“Kaa nayo tu,” akasema akiondokaze.
Aliwasili kaunta na kama alivyowaza, afande Devi akawa tayari amejaa pale. Kabla hajamsalimu, mmoja wa wale afande waliomfukuza hapo awali akamtazama na kumfokea:
“Haukuerewa enh? … nitakutia sero sasa hivi ukamkute mwenzako huko!!”
Marwa hakujibu. Alimtazama afande Devi kwa macho ya mhitaji, afande huyo akaingilia kati.
“Chacha,” Devi akaita. “Jamaa ‘angu huyu bana.”
Basi Marwa akacheza karata dume hapa hapa. Haraka akafunua chakula chake alichokiweka pale kaunta na kuzuga analalama kuwa chakula ki safi. Hamna tatizo lolote na hata akitakiwa kuonja atafanya hivyo.
“Huna haja hiyo, ndugu yangu,” Afande Devi akamtoa shaka akimwekea mkono begani. “Its ok. Funha tu chakula chako.”
“Hapana!” Akasema Marwa akitikisa kichwa. “Labda ana hofu na hiki chakula. Tazama afande … nipo hapa kumsaidia tu rafiki yangu.”
Marwa akaigiza mpaka pale alipoona muda ni sahihi kwake kufunga hotpot, zoezi lake la kwanza likawa limefanikiwa. Lakini la pili, kwenda kumpelekea Jona chakula. Kidogo ikawa tabu.
“Wewe liache tu hapa. Nitalipeleka,” alisema Afande Devi akivuta hotpot.
“Lakini afande, tafadhali naomba ulipeleke saa hii. Najua hajala tangu jana na hata leo nikakawia kuleta chakula. Atakuwa naa njaa sana.”
Marwa akaenda zake. Akatoa simu yake mfukoni na kutua ujumbe kwa Miranda.
‘ABC’
Akimaaanisha mambo matatu yamekwishafanyika. Alipoletea ujumbe wa ‘delivery report’ akaweka simu mfukoni na kwenda kukaa mbali kidogo na kituo lakini eneo alilohakikisha anapata hewa ya kutosha kwani ni kama alianza kuhisi kichwa kimeanza kuwa kizito.
**
Wiu!-Wiu!-Wiu!-Wiu!-Wiu!!
Ilikuwa sauti kali ya king’ora.
Mara gari la wagonjwa lililokuwa katika kasi kubwa liliingia ndani ya eneo la kituo na mara wakashuka watu wawili waliovalia sare za kiuguzi. Wakashusha machela harakaharaka na mmoja wao akazama ndani!
Punde wakatoka na Jona na akiwa amebebwa. Na wasiwe na haraka sana, yule muuguzi aliyebakia nje akaweka sikio lake kifuani. Akachopeka dripu na kumwingiza Jona ndani.
Alafu kukatisha utepe, muuguzi yule awali akarudi tena ndani na kumtoa afande Devi. Hakuonekana kama mtu anayejielewa. Alikuwa anarembua akikokotwa. Mkono wake wa kuume ulikuwa shingoni mwa muuguzi.
Naye wakamzamisha ndani na kisha gari likahepa!!
Hata wale maafande waliokuwepo mlangoni wakiwa wamebaki na butwaa.
**
“Habari zilizotufikia hivi punde!” mwanamke mrembo nyuma ya kioo cha televisheni alinguruma kwa sauti yake ya kuvutia watazamaji na wasikilizaji.
Alikuwa amevalia suti rangi ya damu ya mzee. Na kwa namna alivyokuwa amependeza, ungeliweza kupuuza habari anayoitangaza na badala yake ukamtazama yeye.
Lakini kwa ukubwa wa habari hii, hakuna ambaye angeweza kudiriki kufanya hivyo. Habari hii iliyowafikia hivi punde ilikuwa ni ya moto!!
Ya kustaajabisha na kuvuta watu wasonge karibu na vyombo vyao vya habari.
“Mtuhumiwa nambari moja wa mauaji ya aliyekuwa mkuu wa polisi mkoa, ametoroshwa kituoni na watu wasiojulikana … watu hao wakiwa wamefika hapo kwa kutumia gari la wagonjwa, walifanikiwa kuondoka na mtuhumiwa huyo pia na polisi mmoja ambapo mpaka sasa haijajulikana wamepelekwa wapi … tukutane saa mbili usiku kwa habari zaidi.”
Taarifa hiyo ikazua gumzo kubwa haswa jijini. Watu wakapigwa na bumbuwazi na kwa namna wahalifu walivyowazidi akili polisi mpaka kufanikiwa kukwapua mtu tena kituo kikuu!
Watu waliosikia habari hiyo wakiwa ndani ya madaladala wakapata mada ya kusogezea muda angalau kuwasahaulisha foleni ya kukera nyakati kama hizi.
Na wale wa mitandaoni wakazisambaza upesi. Si katika namna ya kusikitika bali kushangazwa!!
**
“Kamanda siwezi nikakuelewa hata kidogo!” Alifoka Sheng kana kwamba anaongea na mtoto wake. Na kadiri akiwa na hasira basi lafudhi yake ya ki-mandarin inafanya asieleweke kabisa nini anaongea.
Kila mara Kamanda akawa anamuuliza simuni ni nini anaongea.
Uso wake ulikuwa mwekundu. Jasho jembamba lilikuwa linakatika kwenye paji lake la uso.
Akatoa agizo:
“Namtaka! … I want him kabla siku ya kesho haijakwisha. La sivyo …” akakata simu na kuibamizia mezani.
Kutazama mlangoni alikuwa amesimama mdada mchanga wa kichina ndani ya sare, sketi nyeusi na form six nyeupe, akiwa amebebelea trey yenye chupa kubwa ya mvinyo na glasi yake.
Mdada huyo alikuwa amesimama kwa hofu akimtazama Sheng kwa mashaka. Bila shaka alishaona mambo yametibuka.
Sheng, kwa hasira, akavuta droo na kutoa bunduki yake ndogo. Pasipo kujiuliza mara mbili, akamtwanga risasi tatu mwanadada huyo, akafa papo hapo!!
Mwanadada ambaye hakuwa na hatia bali akitimiza tu kazi yake.
Punde wakaingia wanaume wawili na pasipo kuuliza wakanyanyua maiti na kuipeleka inapotakiwa kuwapo.
Sheng akabaki akizunguka kitini kwake akiwa na mawazo makali sana. Hakujua namna ya kufanya. Alihisi kichwa chake kimeganda. Amechanganyikiwa. Hakupata cha kufanya japo aliwaza sana.
Mwishowe akaamua kunyanyua simu na kupiga. Simu ikaita mara mbili kabla ya kupokelewa. Akasemakwa ufupi, nakuhitaji ofisini na punde muda usiende sana hapo ofisini akaingia mwanaume mmoja mwenye asili ya China.
Alisalimu na kuketi. Mwanaume huyu alikuwa ndiye yule waliyejadiliana na Sheng kipindi kile mpaka kufikia kumpelekea pesa Kamanda mkuu hotelini.
Alikuwa amevalia suti yake nyeusi. Imemkaa vema japo hakupendeza. Alikaa kitini kwa muda kidogo kabla Sheng hajamwongelesha.
Kwa muda wote huo Sheng bado alikuwa anawaza tu lakini kitu kisichoeleweka. Unajua namna mtoto mchanga aandikavyo karatasini?? Ndivyo Sheng alivyokuwa anahisi kichwani.
Yaani vuruguvurugu tupu!
Baada ya muda kidogo, akanyanyuka na kuendea jokofu. Akatoa maji madogo na kuyanyonya kama ndama afanyavyo ziwa la mamaye. Si kwamba alikuwa anahisi kiu kali, hapana. Alitaka angalau kifua chake kipoe.
Kwani la sivyo angeweza hata kuchojoa bunduki kwenye droo na kumtwanga mtu aliyemuita mwenyewe hapo.
Alipokunywa na kumaliza maji hayo, angalau kwa mbali akapata ahueni. Akamweleza yule jamaa, jinale Shao, juu ya kikichotokea. Na hakika hata Shao akapigwa na bumbuwazi zito!
Ila akatafuta namna ya kukabiiana nalo apate kumshauri mkuu wake ambaye alikuwa amekwama. Kwanza akamtoa hofu juu ya Jona.
“Women huì dédào ta!” (Tutampata!) Akasema kwa kujiamini.
“Rúguo women bù yuànyì dehuà, ta huì si de!” (Na kama tusipofanikiwa basi atajifia) Kwa minajili kwamba virusi waliomuingizia mwili hawatadumu naye kwa muda mrefu. Kadiri anavyokaa navyo ndivyo watakavyomdhoofisha na mwishowe kufa!!
“Tamen yongyuan bù zhidào cóng nali dédào jie yào!” (Kamwe hawatajua wapi pa kupata antidote!) Akasema Shao kwa msisitizo. Maneno hayo yakaingia ndani ya kichwa cha Sheng lakini bado hayakumkosha. Akauliza kama antidote ipo ndani ya kambi yao.
Shao akamjibu ni kiasi kidogo sana kilichopo. Hakiwezi kudumu hata zaidi ya juma moja.
“Méiyou! Wo yào lìjí mái xià suoyou de jiedú jì!” (Hapana! Nataka antidote zote zifukiwe mara moja!) Sheng akabweka akigongesha kidole chake mezani. Alihofia pengine antidote hizo zinaweza kupatikana na kumsaidia Jona.
Shao akalipokea hilo agizo na kuapa kulitekeleza. Kisha akamsihi mkuu wake kutumia fedha yake sasa kama chambo cha kumpatia Jona. Aweke matangazo kote mitandaoni akitangaza kutafutwa kwa mwanaume huyo na mtu atakayetoa taarifa zitakazofanikisha upatikanaji wake basi apatiwe donge nono la pesa.
Sheng akaridhia hilo wazo kwa moyo mkunjufu. Lakini pia akaagiza vijana wake wote wa vitengo vya usalama wakutane naye usiku wa saa nne. Ana mambo kadhaa anataka kujadili nao.
**
“Hatujafanikiwa mpaka sasa, mkuu!” Sauti ilivuma kwenye simu ya Kamanda. Alikuwa amesimama koridoni akiwa amevalia taulo. Ameshikilia kiuno chake kipana.
Si sebuleni wala chumbani kulipokuwa kunakalika. Tumbo lilikuwa joto. Kama kuna kipindi kigumu alichowahi kupitia akiwa kazini, basi ni hiki.
Mwili ulikuwa unamtetemeka na kila simu iliyokuwa inapigwa alikuwa akiidaka upesi na kuiweka sikioni. Zaidi ya hapo alikuwa mbogo haswa. Hata mkewe na watoto walienda kujifungia ndani baada ya kuona hapakuwa panakalika.
“Hamjafanikiwa mnafanya nini sasa huko??” Akafoka. “Ni kazi gani mwafanya huko ina maana mmeshindwa kui-trace hiyo ambulance mkajua imeelekea wapi??”
“Tumefanya hivyo mkuu,” sauti ikajitetea simuni. “Tumefuatilia na hata kwenda mpaka hospitali ambayo jina lake lilikuwa ubavuni mwa ambulance hiyo …”
“Wakasemaje??” Kamanda akakatiza.
“Hawaitambui hiyo ambulance! Haipo kwenye orodha ya usafiri wao. It means ilifojiwa tu!”
“Na namba?? … hizo plate nu-number je??” Kamanda akauliza upesi.
“Namba tumezifuatilia, ni za biashara. Gari lilisajiliwa kama daladala ila kuhusu mwenye mali nayo alikwisha fariki muda sana. Hata hili gari halikuwa likifanya kazi hiyo ya daladala kwa muda mrefu hapa jijini kutokana na marufuku ya vyombo vya aina hiyo kufanya kazi hiyo jijini.”
Kamanda akashusha pumzi ndefu kisha akauliza:
“Sasa mmefanyaje?”
“Bado tunaendelea na upelelezi mkuu, tutakapopata chochote kitu basi tutakutaarifu.”
Kamanda akakata simu na kurejea sebuleni. Akakaa hapo akiwaza na kuwazua nini afanye. Akiwa hapo, mara simu yake ikaita. Akatazama alikuwa ni Sheng. Akapokea simu na kuiweka sikioni.
Sheng akampa taarifa ya kumhitaji ofisini kwake majira ya saa nne usiku.
**
“This is disgrace to Wu family!” (Hii ni fedheha kwa familia ya Wu!) Sheng aliwaka. Macho yake yalikuwa mekundu. Hakuketi kitini, alihisi hataeleweka. Aliongea kwa hasira na jazba.
“Siwezi kukubali kudhalilishwa kiasi hiki na kikundi kidogo cha watu. Kamwe!”
Akatazama kushoto na kulia akipekua rundo la wafanyakazi wake wanaomtazama kwa umakini. Ukumbi ulikuwa kimya. Hata mbu angelikatiza hapo angelisikika.
Vijana watabe, vijana wa kazi, wachina kwa weusi, walikuwa wametega sikio kumsikiliza mkuu wao. Na wakiwa tayari kubeba agizo lolote lile watakalokabidhiwa.
“Sasa ni hivi,” Sheng akaelekeza kwa mkono. “Kwa sasa kazi zote zitasitishwa. Hakuna kufanya kazi nyingine yoyote isipokuwa moja tu! Kumtafuta Jona popote alipo. Yeyote atakayeleta kichwa chake ofisini kwangu, nitampatia cash shilingi milioni mia nane!
Zoezi hili lisizidi mwezi mmoja tangu sasa.”
Baada ya hayo akawataka waende. Akabaki na Shao aliyejadiliana naye kwa sekunde kadhaa kabla hajamuuliza kumhusu Lee.
“Ta zài nali?” (Yuko wapi?)
Shao akapandisha mabega akisema hana taarifa naye.
Kabla hawjajadiliana zaidi, kijakazi akaja na kumpasha habari Sheng kuwa ana mgeni. Kamanda mkuu ameshafika ofisini kwake.
**
“Nimekuita hapa kwa jambo moja,” Sheng alifungua kijikao chake cha dharura. Mbele yake alikuwa ameketi Kamanda mkuu akiwa ndani ya shati la kitenge na suruali nyeusi ya kitambaa.
“Nahitaji silaha zaidi kwa ajili ya kazi zangu. Nataka unisaidie kwenye hilo.”
“Silaha?” Kamanda akadakia. “Nitakusaidiaje bwana Sheng. Ni ngumu kutoa silaha stock na kukupatia. Itaweza leta suspicions!”
“No! No! No!” Sheng akatikisa kichwa. “Sihitaji silaha zako. Kuna mzigo mkubwa utafika bandarini ukiwa kwenye meli ya wauguzi wanaokuja kutoa huduma ya matibabu bure hapa nchini. Ndani ya meli hiyo kubwa kuna kontena zangu mbili za silaha. Ninachojitaji wewe ufanye ni kuzipitisha kwa kutumia jina la jeshi. Basi!”
Kamanda akameza mate.
“I need them kwa ajili ya kumsaka Jona!” Sheng akamalizia habari.
**
Sasa shauri lilikuwa limekatwa na kesi imefikishwa mahakamani. Boka na Miranda wakataarifiwa kuhitajika kituo cha polisi mara moja.
Ikiwa ni majira ya jioni, Miranda na Boka wakawasili hapo kila mtu akija na usafiri wake lakini ikionyesha bayana kuwa walikuwa na mawasiliano.
Boka alikuwa ameongozana na mwanasheria wake, Bwana Manyanja Mayanja, ambaye yeye ndiye alikuwa akihusika na kila kitu hapo huku mteja wake akiwa msikilizaji tu.
Kwa msaada wa mwanasheria bwana Mayanja Mayanja, wakapewa dhamana na zaidi tarehe za kuhudhuria mahakama kwa ajili ya kusikiliza kesi yao.
“Tutakaposhinda kesi hii, jamhuri italazimika kulipa fidia ya muda na usumbufu na pia kusafisha taswira ya mteja wangu kwa kupitia vyombo vyao vyote vya habari!” Bwana Mayanja Mayanja alinguruma.
Baada ya hapo wakatoka kituoni, ila kabla hawajakwea kwenye vyombo vyao vya usafiri, mara Miranda akaitwa.
Alipogeuka akakutana uso kwa uso na Koplo Massawe.
Moyo wake ukashtuka. Macho ya koplo Massawe yalikuwa yanamtazama kwa yamkini.
Akageuza shingo yake kumtazama Boka kisha akamsihi amngojee yeye akienda kukutana na koplo Massawe.
“Habari yako?”
“Safi, afande.”
Massawe akamtazama Miranda machoni. Miranda naye akajitahidi kuyakaza macho yake. Ila moyo ulikuwa unampwita haswa. Kama koplo Massawe angeligundua hilo, basi angeliweza kumshukumu kindakindaki.
“Kama nishawahi kukuona hapa, bibie,” alisema Massawe kwa uso wa mashaka. “Ndiye wewe?”
“Mimi?” Miranda akajiwekea kiganja kifuani. Akabinua mdomo wake na kusema: “labda, inawezekana ikawa ni mimi … kuna kesi yangu nafuatilia hapa kwa inspekta.”
“Oooh!” Massawe akatikisa kichwa. “Basi sawa. Unaweza tu ukaenda.”
Miranda asiamini macho yake, akageuka na kuenda zake. Massawe akamtazama akiyoyoma kichwani akijaribu kukumbuka alipomuonea mwanamke huyo.
Alikuwa tayari ameshamtilia mashaka akidhani anaweza kuwa na mahusiano na Jona. Na kama angelithibitisha hilo basi Miranda angekuwa na mashtaka ya kujibu. Asingelitoka hapo kituoni kwendaze.
Ni kama bahati Miranda kuwa na kesi mbadala hapo kituoni. Alichoropokea tundu la sindano.
**
Mikono yake ikiwa ndani ya mifuko ya koti la ngozi, Lee alitazama huku na huko kukagua majengo marefu ndani ya Hongkong.
Macho yake yalikuwa yamezibwa na miwani ya jua. Mdomoni alikuwa ana pipi ndogo ya kijiti akiimung’unya taratibu.
Kuna kitu alikuwa anatafuta. Mkononi mwake alikuwa ana karatasi ndogo nyeupe yenye ‘address’ ya kufika mahali anapopataka. Na huko si kwengine bali kumfuatilia Chen Zi!!
Wamkumbuka mwanaume huyo?? Mwanaume wa mwisho kuwasiliana na kutumiwa nyaraka kwa njia ya mtandao na yule mchina aliyekwiba nyaraka ya siri ya Lee??
Sasa Lee alikuwa ndani ya Hongkong kumtafuta na hata kumuangamiza kwa mkono wake mwenyewe!! Alifanya yote haya kwa siri kubwa asiwataarifu hata wenzake. Aliona huo ndiyo muda wa kufanya hivyo, la sivyo hatalifanya hilo milele!
Tangu Jona alipotiwa gerezani, alidhani angeweza kufanya misheni yake hii pasipo kusumbuliwa na Sheng. Hivyo mpaka sasa hakuwa anajua chochote kile kuhusu yaliyotokea kwa Jona.
Hakuwa anajua kuwa mambo hayapo tena ‘under control’ bali ‘over control’. Anahitajika na kutafutwa na mkuu wake huko nchini!
Alikuwa anatimiza siku ya tatu akiwa Hongkong. Katika upelelezi wake wa akitumia mtandao wa Facebook alikuwa amepata pa kuanzia kumtafuta na kumpata Chen Zi amtakaye.
Chen Zi ambaye anadhani anaweza akawa ni shabiki wa mwanamuziki Chen Zi halisi ambaye alikuwa mwanamuziki maarufu chini China aliyeripotiwa kufa kwa kuzidisha dozi ya madawa ya kulevya.
**
Ngo! Ngo! Ngo! Lee alibisha hodi kisha akatoa pipi yake mdomoni. Punde akafunguliwa mlango na kikongwe wa kichina aliyemkarimu kwa upole.
Akazama ndani na kuketi. Akafanya ‘survey’ kukagua sebule ya bibi huyo. Ilikuwa hafifu na yenye vitu vya kale na haikuchukua muda akagundua kuwa bibi huyo anakaa hapo na binti mdogo anayetunza.
“Wo zhao chén Zi!” (Namtafuta Chen Zi!) Lee akasema hitaji lake. Yule kikongwe akafikiri kidogo kisha akatikisa kichwa chake.
Chen Zi yupi unayemuongelea? Akauliza. Lee akafungua simu yake na kumwonyesha kikongwe yule picha aliyoipakua toka kwenye mtandao wa Facebook.
Kikongwe akavalia miwani na kuitazama picha hiyo kwa ukaribu. Akamuita na yule dada anayekaa naye, akamkabidhi picha hiyo aitazame. Dada akaiangazia na punde akatikisa kichwa.
“Women bù rènshì ta!” (Hatumjui!)
Lee akaitazama tena ile picha kisha akairejesha simu yake mfukoni.
“Ni shì shéi?” (Wewe ni nani?) Akauliza yule kikongwe akimtazama Lee kwa umakini.
“Wo shì ta de péngyou,” (Mimi ni rafiki yake,) Lee akajieleza. “Ta gàosù wo ta zhù zài zhèli.” (Aliniambia anaishi hapa.)
Kikongwe yule akatikisa kichwa. Basi Lee akashukuru na kwenda zake. Kichwani akiwa anawaza pengine mtu huyo aliyechat naye alimlaghai kama ilivyokuwa kwa mtu yule wa mwisho kumfuatilia jana yake.
Hii ndiyo shida ya Facebook. Watu hata mia wanaweza wakawa wanatumia jina moja. Kwa kupitia mtandao huo, Lee aliwang’amua watu wanne wakitumia jina la Chen Zi na wote wapo China!
Tayari mmoja ashamwendea na kukuta sipo anapoishi. Alipofuatilia address’ aliyopewa na mtu huyo akajikuta anafika nyumbani kwa mwanamke mmoja mjane!
Na leo amefuatilia address ya mtu mwingine wa pili, ameishia kufika mlangoni mwa kikongwe! Akawaza nini shida. Lakini hakujali sana. Alikuwa ana muda wa kutosha siku hiyo hivyo hivyo atawamalizia na hao wawili aliowabakiza kwenye orodha.
Akiamini kati ya hao basi mmojawao atakuwa ni Chen Zi anayemtafuta yeye. Moyoni akiwa anaomba nyaraka hiyo isiwe imezagaa ama kufika kwenye mikono ya maadui.
**
“Huanyíng!” (Karibu!) Sauti ya kiume ilifika masikioni mwa Lee. Hakupata wasaa wa kuitafakari sauti hiyo, mara mlango ukafunguliwa na mwanaume mwenye umri wa makadirio 40 – 45. Mwanaume huyo alikuwa amekalia ‘wheel chair’. Mkono wake wa kushoto ulikuwa umelemaa na mdomo wake ulikuwa umepindia kushoto pia.
Akamsalimu Lee na kumuuliza ni kwa namna gani atamsaidia. Lee akaeleza haja yake, kumtembelea rafikiye aitwaye Chen Zi.
Mwanaume yule aliyemkarimu akatahamaki. Hakuwa anamjua mtu huyo. Kwa mujibu wa maelezo yake anaishi na mkewe anayefanya kazi kiwandani, hata simu hana, na huwa yupo bize sana kumhudumia akiwa nyumbani.
“Wo hen bàoqiàn raoluàn!” (Samahani kwa usumbufu!) Lee akaenda zake. Kichwani akiwaza haya matukio. Ina maana Chen Zi wote aliochat nao wamemlaghai??
Alitoa simu yake akaitazama. Akairudisha tena mfukoni.
**
“Wo bù rènshì ta!” (Simjui!) Alisema mwanamke mwembamba mwenye tumbo kubwa la ujauzito. Alikuwa amesimama mlangoni akimtazama Lee machoni.
Nywele zake zilikuwa hovyo. Alionyesha kuchoka. Kama si wa kushusha vitu kesho basi keshokutwa haipiti.
“Wo yigè rén zhù zài zhèli!” (Naishi peke yangu hapa!) Alisema mwanamke huyo mjamzito akizika matumaini yote ya Lee! Sasa rasmi idadi ikawa imetimia ya watu wanne aliochat nao na kati ya wote hao hakuna Chen Zi anayemtafuta.
Ilimshangaza hili. Lakini ilimshangaza zaidi kwa namna alivyokuwa anakutana na watu wasiojiweza kwenye kila pango alilokwenda kumtafuta Chen Zi.
Kwanini watu hao walimdanganya kama vile alivyoaminishwa na wenyeji wake?? Kwanini wafanye hivyo ilhali hakuwa ameeleza taarifa zake binafsi, badala yake akitumia picha ya kike??
Hapa akabishana na akili yake. Ina maana amebumburukiwa?? Hapana! … kivipi?? Hakuwa ameacha nyayo zozote za kuhisiwa kombo.
Ila …
Akawaza.
Kuwaomba wanaume hao ‘address’ zao kutakuwa kuliwapa mashaka?? Yani mwanamke aliyejirahisisha kupita kiasi?? Hapana. Akatikisa kichwa. Sidhani.
Aliagiza juisi hapo mgahawani. Akatoa simu yake na kuitazama. Haikuwa na ujumbe wowote ule. Akaiweka mezani na kunywa juisi yake taratibu akifikiria namna ya kufanya.
Punde hapo mgahawani wakaingia wanaume watatu waliovalia nguo nyeusi juu mpaka chini. Walikuwa ni wanaume wenye miili mikubwa, wawili miongoni mwao walikuwa ni wachina, mmoja alikuwa ni mtu mweusi ti.
Jamaa huyu mweusi hakuwa na nywele hata moja kichwani. Wenzake walikuwa nazo ila chache, kwa mbali.
Wakakaketi eneo moja. Upande wa kushoto wa Lee kwa umbali wa hatua kama nne hivi za mtu mzima. Nao wakaagiza juisi.
Ikapita kama dakika tatu wakiwa hapo. Ila walikuwa wanamtazama Lee si mara moja wala mbili, wala tatu.
Na kuna kitu walikuwa wanateta midomoni mwao kisisikike hata kwa majirani.
Basi Lee akiwa hapo, hakuwatambua hao watu hata akatoka na kulipia kisha akaenda zake. Lakini wale watu wakatoka nao wakiwa wameacha hata vile walivyoagiza hapo mgahawani. Hao wakaongoza kumfuata Lee kama mkia.
Lee akapanda gari na kuketi akiwa peke yake nyuma kabisa. Alipoketi akachomoa kitabu fulani kilichokuwapo kwenye vijindoo vidogo vijishikavyo ukuta mwa gari, akakunja nne na kukipitia kitabu hiko kilichokuwa na mambo matamu yaliyovutia.
Kilikuwa ni kitabu kilichoonyesha mambo kadhaa kadhaa ya kitalii ndani ya China. Maeneo ya kutembelea na vivutio kadhaa ndani ya nchi hiyo. Milima na mabonde. Uoto na utamaduni. Na pasipo kusahau ukuta ule mkuu ‘great wall’ wa China.
Lee akavutiwa sana na kitabu hicho, akapanga kutembelea moja ya vivutio vile kwani alikiri kifuani mwake kuwa japo alikuwa yu mchina, hakuwa anajua mambo mengi kuhusu nchi yake, maana amekuwa wa kutembea sana huku na kule.
Hakutulia nchini mwake tangu alipotwaliwa na familia ya Wu, baada ya hapo akasafiri na kwenda kuishi nchi nyingine kabisa, kwa hivyo amekuwa mgeni katika nchi yake. Na ana hamu ya kujua mambo kadhaa zaidi.
Kwa muda akatekwa na hicho kitabu, gari likasonga na kusonga. Alifungua kurasa na kurasa akivutiwa na anachokiona. Hata hakujua kama ndani ya gari lile walipanda wale wanaume watatu ambao kwa namna moja ama nyingine walikuwa wanamzingatia.
Akafika kituoni na kushuka. Akatembea kuelekea jengo fulani lenye urefu wa wastani. Nyuma yake kama hatua kadhaa, wale wanaume nao wakawa wanajongea taratibu kumfuata.
Lee akapapasa mifuko yake, na mara akatoa kiasi fulani mfukoni mwake na kuzama ndani ya duka moja kubwa ‘Mi Hao supermarket’, humo akapate kutazama baadhi ya mahitaji yake kabla hajarejea nyumbani.
Alipozama humo ndani wale wanaume wakasita kuzama. Wao wakaamua kungoja kwa nje. Lee akazurura taratibu ndani ya duka akipitia shelvu moja baada ya nyingine. Hakuwa na haraka. Hakuwa na ratiba nyingine zaidi ya kurejea nyumbani kupumzika, na kwa namna moja ama nyingine mahali pale palimsahaulisha mawazo yake kwa muda kidogo.
Basi akiwa anautumia muda wake kiasi humo, mara mlinzi aliyekuwa amekaa ndani akatoka nje kwenda kuwakuta wale mabwana kule nje maana aliona wamekaa kwa muda mrefu hapo wasionekane kama wana shughuli yoyote ya maana.
Na kwa kiasi kimoja ama kingine, mwonekano wao ulizua mashaka. Walionekana wahuni. Si watu wa kuamini. Japo mlinzi alikuwa mwembamba asiye na nguvu, akatumia madaraka yake kuwauliza wanaume wale majabali ni nini walikuwa wanafanya hapo.
Basi wakatazamana na kisha mmoja akasema, wanamngoja mwenzao aliyeingia humo ndani na maelezo waliyotoa wakamlenga Lee. Basi mlinzi akaachana nao na yeye akazama ndani.
Moja kwa moja akamwendea Lee na kumuuliza kuhusu hilo. Hapo ndiyo akawa ametibua mambo. Sasa Lee akajua kuna watu. Na kwa kutumia kamera za mapokezi akawaona watu hao. Hakuwa anawatambua. Na kwa kumbukumbu yake hafifu, aliwaona mahali.
Hakujua ni wapi, ila kama aliwaona, aliwaza.
Basi akamaliza kuchukua vitu vyake naye akalipa na kutoka nje, hakuwasemeza wale wanaume. Alitaka kuona kama watahangaika naye. Nao hawakusumbuka. Ila wakaunga nyuma kama mkia.
Lee akatembea akiwa anawaza kichwani mwake namna ya kufanya. Na akiwa anawaza wale watu ni wakina nani. Akaona si busara kwenda nyumbani kwake moja kwa moja. Na hakuwa na haja ya kuwakimbia wale wanaume maana wapo ndani ya uwezo wake kabisa.
Basi akatafuta kichochoro alipozama humo. Ilikuwa ni kaupenyo kadogo kakuongoza kutokezea upande wa pili ambapo huko kuna bahari kwa kama umbali wa hatua hamsini kwa mbele.
Njia ilikuwa nyembamba, na kwa wale wanaume majabali iliwawia vigumu kidogo kupita kwa kujinafasi kama walivyokuwa wakifanya barabarani.
Humo njiani Lee akaona ni mahala pema pa kufanya alichokuwa anawaza kichwani – kuwakabili wale wanaume ambao aliamini kuwa maadui.
Basi akasimama na kuweka vitu vyake kando. Kisha akakung’uta mikono na kugeuka kuwatazama wale wanaume ambao nao walisimama punde Lee alipofanya hivyo.
Akawauliza wao ni wakina nani na kwanini wamfuata. Wanaume wale kwa kebehi wakamwambia kabla hawajamfuata, yeye ndiye aliyewafuata. Lee akashangaa.
Hakuwa anataka kusumbuka sana, akawauliza wanataka nini toka kwake. Wale wanaume wakasema wana maongezi naye, na kama hatojali basi aongozane nao kwenda huko wanapomtaka kuteta.
Lee akasita. Vipi kama watu hawa wanatafuta mahali pa kummalizia? Kama kweli walikuwa na hitaji basi ni kwanini walikuwa wakimfuata kimya kimya hivyo? Akakataa, akema kama wana hitaji basi walieleze hapo hapo na si vinginevyo.
Wale wanaume wakatazamana. Na basi akasema kama hakuwa anahitaji kwenda kwa hiyari, basi watamlazimu maana wametumwa vivyo.
Wakamfuata wakitaka kumnyakua, lakini Lee akajiandaa kwa mapambano. Akajiweka sawa na kuanza kupambana. Alikuwa mwepesi kukwepa na kuutupa mwili tofauti na maadui zake.
Japo ilikuwa pevu, akaimudu ndani ya dakika kadhaa. Alikuwa amechoka kwani wale majamaa walikuwa majabali haswa kwa hivyo kuwalaza chini wakiwa hawajiwezi, haikuwa kazi rahisi hata kidogo.
Akakusanya vitu vyake na kuondoka. Ikiwa hakuonekana na yeyote yule zaidi ya wale waliobakia hoi sakafuni.
**
“We are already here!” Sauti ilivuma garini. Lilikuwa ni gari refu jeusi, Limousine. Dereva akashuka na kwenda kufungua mlango wa nyuma, akatoka mwanaume mfupi mchina aliyevalia suti nyeusi. Mkononi mwake alikuwa ana sigara kubwa iliyokuwa inafuka moshi mwingi. Na macho yake yalikuwa yamefunikwa na miwani meusi.
Mwanaume huyo akavua miwani na kuangaza huku na huko. Mara akawaona wale wanaume majabali wanne wakiwa wanajikongoja kuja garini. Mwanaume huyo ndani ya suti akawatazama kwa uso wa ghafira, alafu akaingia ndani ya gari na kutulia.
Wale wanaume nao wakaingia na kisha gari likahepa wasipate hata kuongea. Kwa muda kukawa kimya.
Baada ya muda wa dakika kadhaa humo katika gari hilo la kifahari, mwanaume yule jabali mwenye rangi nyeusi, akamtazama yule bwana aliyekuja kuwachukua, akamsihi mambo hayakuwa kama vile walivyotaraji.
Lakini yule bwana hakujali. Mdomo wake aliutumia kuvuta sigara badala ya kuteta. Alikuwa ‘bize’ uso wake ukitazama mbele, na ubaya miwani yake iliyokuwa imeficha macho, haukutuonyesha wapi au nani anamtazama.
Hatukupata uhakika kilichoendelea maana baada ya dakika kadhaa hivi, limousine hiyo ikazama ndani ya jengo moja refu hapo Hongkong, likaendea eneo la maegesho ya gari.
Lakini kitu pekee ambacho tulikuja kupata hakika nacho ni kuwa, wale mabwana, majabali waliogaragazwa na Lee, waliuawa na maiti zao zikafungiwa mawe makubwa na kutupiwa baharini!
Aliyesalimika akawa ni mmoja tu, yule bwana mweusi. Naye usiku akajikuta kitandani akiwa amefunikwa mdomo wake na karatasi pana. Akainyofoa akilalama kwa maumivu makali.
Na kwenye ile karatasi kulikuwa kuna ujumbe ulioandikwa kwa wino mweusi kwa lugha ya kichina ukimtaka ahakikishe anampata Lee ndani ya siku mbili tu, la sivyo maisha yake yatakuwa katika rehani kubwa.
**
Alipoweka glasi yake ndefu mezani, akakohoa kidogo kisha akamtazama Miranda aliyekuwa amekaa kando. Akamuuliza;
“How is he now?” (Anaendeleaje sasa?)
Miranda akanywa kwanza naye kinywaji chake glasini. Ulikuwa ni mvinyo mwekundu. Akagida mafundo matatu, alafu akamtazama Bwana Brown almaarufu, BC, ambaye kama kawaida yake alikuwa ndani ya suti tamu iliyomkaa mwilini. Mguu ameukunja nne, na vidoleni amebebelea sigara kubwa.
“He is still far from being ok,” (Bado hayuko sawa,) Miranda akasema kwa vuli la huzuni, alafu akashusha pumzi ndefu na kuufumbata mdomo wake.
“We have to get the cure, otherwise he will die in our hands,” (inabidi tupate tiba, vinginevyo atafia mikononi mwetu,) Miranda alisema akiwa anamtazama BC kwa kina.
Kukawa kimya kidogo. Wakinywa na pia BC akivuta sigara yake. Baada ya muda kidogo, BC akaulizia kuhusu antidote iliyoletwa na kijana aliyemfahamu kwa jina la Marwa.
Alipata kumwona kijana huyo hapo kwa Miranda na kisha akatambulishwa kama mkazi wa eneo moja na Jona.
“That antidote makes things worse! He almost died the last time I gave it to him!” (Antidote huaribu mambo kabisa! alikaribia kuca nilipompatia mara ya mwisho!”) Miranda alitema cheche. Basi BC akanyamaza kidogo. Na kama ilivyo hulka yake akiwa mawazoni, akawa anavuta sana sigara kuliko kunywa.
Kwa hivyo, Miranda akanyamaza akingojea jibu maana alikuwa ana uhakika bwana huyo atateta baada ya muda fulani.
Hakuwa amekosea, baada ya muda BC akafungua mdomo wake mkavu kuteta. Akamwambia Miranda, Bwana Sheng atakuwa ametambua kuwa Marwa alikuwa na antidote hivyo akabadili virusi vya kumtilia mwilini.
Basi wasihangaike sana, yeye anahitaji kiasi kidogo cha mate ya Jona, akienda nyumbani kwake ayafanyie utaratibu wa kuyapembua kwenye maabara yake binafsi wajue cha kufanya.
“I am sure, after two days he will be dead if he wont be taking antidote.” (Nina uhakika baada ya siku mbili atakufa kama hatakuwa anatumia antidote.) Bwana BC akateta. Na huu ulikuwa ukweli mtupu mana Jona alikuwa amekwisha mno, hajiwezi kitandani.
Kama ungelikuwa na roho nyepesi, machozi yangalikutoka ukimwona.
Na basi kwa uzito wa swala hilo, hata ule mvinyo aliokuwa anakunywa Miranda hakuwa unasuuza koo lake kabisa. Hakuufurahia maana kichwa chake kilikuwa kimetingwa na mawazo lukuki.
Basi wasipoteze muda hapo, ndani ya muda mfupi baada ya BC kumaliza sigara yake, Miranda akapata mate ya Jona kwenye kijifaa kidogo cha chupa, na haikuwa ngumu kwake kupata mate hayo kwani Jona alikuwa akiyatiririsha ya kutosha.
Akamkabidhi BC na bwana huyo akaondoka zake.
**
“Nadhani amelala sasa,” alisema Marwa akirudishia mlango wa chumba alicholazwa Jona. Mbele yake alikuwa amesimama Miranda akiwa amekumbatia mikono yake, ametazama chini akizimeza lips zake.
Alikuwa amesimama hapo koridoni maana hakuwa anataka kwenda kumtazama Jona chumbani akihofia kusononeka moyo. Kila alipomwona Jona macho yake yalibadilika rangi kuwa mekundu, na akihisi moyo wamuuma haswa.
Baada ya kupewa taarifa taarifa hiyo na Marwa, wakaongozana kwenda sebuleni. Na punde alipoketi, simu yake ikaita. Alikuwa ni BC. Akapokea na kuiminyia simu sikioni.
“I have never seen such a virus like this before!” (Sijawahi kuona kirusi kama hiki hapo kabla!) Sauti ya BC ilinguruma simuni. Miranda akabana pumzi kwa mshangao. Moyo wake ulianza kwenda mbio.
Akauliza kwa hofu, “So what shall we do??” (Sasa tutafanya nini??)
***
BC akaguna kidogo alafu akasema inabidi wafanye kuipata antidote hiyo kwa namna yoyote maana la sivyo Jona atakufa. Ila kwa kusogezea muda, atampatia antidote mbadala. Hiyo itampatia Jona ahueni ila si ya kudumu!
Na ubaya ni kwamba kadiri atakavyoendelea kutumia antidote hiyo basi ataishia kuwa kilema hapo baadae kwani si nzuri sana.
“Send that man to my house. I will give it to him. (Mtume huyo mwanaume nyumbani kwangu. Nitampatia.) BC alihitimisha maongezi yake kisha akakata simu.
Miranda akateta na Marwa aende kwa BC, akamkabidhi na funguo ya gari kisha maelekezo ya namna ya kufika huko.
“Usikawie,” akamsihi. “Inabidi ulete hiyo antidote upesi Jona apate unafuu.”
Marwa akafichama funguo kiganjani mwake.
**
“You are welcome!” BC alimkaribisha Marwa sebuleni. Mwanaume huyo akaketi kwenye sofa zenye nyama na kumtazama Bwana huyo mzungu pasipo kutia neno. Aliamini anajua kilichomleta hapo.
BC akakung’utia mabaki ya sigara kisosini, kisha akavuta pafu ndefu na kuzima kabisa sigara yake. Akapuliza moshi angani na kumtazama Marwa.
“So you are the man?” (kwahiyo wewe ndiye mwenyewe?)
Marwa akatikisa kichwa chake, akasema, “Yes, I am.”
“Ok, so listen to me very carefully,” (sawa, sasa niskize kwa umakini,) BC akafungua dibaji yake ya maongezi. Akajitengenezea vema kitini kisha akamtazama Marwa aliyekuwa amemwazima masikio.
“You have to follow instructions properly. Time and diet. I didn’t have time to write them down so I’ll just tell you orally!” (Inabidi ufuate maelekezo vema. Muda na mpango kula. Sikuwa na muda wa kuviandika kwahiyo nitakuambia kwa mdomo!)
Baada ya hapo akamwelekeza Marwa dozi, muda na chakula anachotakiwa kupewa Jona. Marwa akavi- note vyote kichwani pasipo kubakisha hata chembe. Akashukuru, na kuaga. Alikuwa ndani ya upesi. Hakutaka kupoteza hata sekunde.Lakini bwana BC akamtaka avute subira kwanza.
Kuna jambo anataka kujadili naye kwa ufupi.
“I know you dont know but I want to let you know, I spend a lot of money on him. And it is clear that I will even spend more and more to get him on his feet. The question is, will I get his loyalty?” (Najua hujui lakini nataka kukujuza, natumia fedha nyingi juu yake. Na ipo wazi kuwa nitatumia zaidi na zaidi kumfanya asimame kwa miguu yake. Swali ni, nitaupata uaminifu wake?)
Hapa Marwa akasita. Si tu kwamna hakuwa na jibu, bali alihofia kuteta. Hakuwa anajua lililopo kichwani mwa Jona, wala mwa Bwana BC. Hakutaka kutibua mambo mapema hii, akaomba muda kidogo. Itakuwa vema Jona akisema mwenyewe punde atakapopata uwezo wa kutamka.
Bwana BC akaguna akisafisha koo lake. Akalamba lips zake kavu akimtazama Marwa kwa sekunde kadhaa akiwa kimya.
“You are his friend. I hope you know him inside out. I adopted him when he was abandoned by the world. When he was no one. So he should be someone under my shadow. Deliver this message to him.” (Wewe ni rafiki yake. Natumai unamjua ndani nje. Nilimuokota akiwa ametelekezwa na ulimwengu. Akiwa si mtu. Kwahiyo inabidi awe mtu chini ya kivuli changu. Fikisha huu ujumbe.)
Marawa akatikisa kichwa kwa kuridhia, alafu akaaga na kwenda zake.
**
Akiwa kwenye mataa, akapata kufikiria yale maneno ya BC. Alilaza kichwa chake akitazama ‘sight mirror’. Na kwa muda kidogo akawa amesafiri kwenda ulimwengu mwingine. Ulimwengu wa mawazo na fikra.
Akaumauma midomo yake akijaribu kupembua. Akisikia sauti ya Bwana BC na kwa muda huo akiyaweka maneno yake kwenye mizani na hulka ya Jona.
Je, Jona ataridhia masharti ya BC? Hili swali lilimuumiza kichwa kidogo. Vipi kama Jona atakaidi na kuamua kufuata njia yake, BC atachukua hatua gani? Naye atakuwa upande gani?
Mawazo haya yakaonyesha kutokuwa na komo zaidi ya kujiumiza kichwa. Asingeweza kuyapatia majibu kwa muda huo, ila alishindwa kuyafukuza kichwani mwake.
Alikuja kushtuliwa na honi kali za magari yaliyo nyuma yake maana taa zilisharuhusu na alikuwa bado hajasogeza matairi ya chombo. Haraka akapangua gia na kukanyaga pedeli ya mafuta.
**
Tip! Tip! Vidole vilibonyeza vitufe kiooni, mara ujumbe ukaenda na muda si mrefu tiki ikatokea ujumbeni kuashiria ujumbe umefika.
Lee akaweka simu yake pembeni kisha akajilaza akitazama dari. Muda ulikuwa unazidi kwenda akiwamo Hongkong pasipo mafanikio. Endapo akiendelea kukaa huko, basi Sheng atafahamu hayupo na hata akarudi akawa na wasaa mgumu wa kujieleza.
Akashusha pumzi ndefu. Akafikiri kidogo na akili yake mtambuka ikamletea majibu. Kidogo akajiona mjinga. Kama kulikuwa kuna njia ya yeye kupata anachokitaka, basi ilikuwa kwa kupitia wale majamaa watatu!
Akatikisa kichwa chake kwa masikitiko. Kwa akili yake mtambuka wale majamaa watakuwa wana mahusiano na hichi anachokitafuta. Hakuamini kama wanaweza kuwa vibaka wa kawaida tu, wakimtaka akaonane na mkuu wao.
Huyo mkuu ni nani? Na amemfahamuje ingali hapa Hongkong yeye ni ‘mgeni?’ Hapa mawazo yakampeleka mbali sana. Hata akaanza kuwatilia mashaka wale watu aliokuwa anawakuta kule majumbani kumtafuta Chen Zi.
Je, na wao watakuwa wanahusika na wale mabwana watatu?? Akatambua hapa kutakuwa kuna kitu, na kama akipata wasaa basi ana haja ya kuzitazama nyumba zile katika namna ya kipekee. Atagundua jambo.
Akatazama kesho yake, hakuwa na muda. Alipanga kwenda mahali ambapo marehemu Chen Zi halisi, yule aliyekuwa maarufu nchini, alikuwa akifanyia mazoezi yake. Aliamini huko anaweza akapata lolote jambo likampa mwanga.
Akaendelea kuyapanga mawazo hayo kichwani mpaka akapitiwa na usingizi.
**
“Boss, tumemaliza kazi,” alisema mwanaume ndani ya suti nyeusi akimtazama Sheng kitini.
“Una uhakika mmefukia kila kitu?” Sheng akauliza. Macho yake yalikuwa yanamtazama kijana huyo mjumbe kwa ukali.
“Ndio, mkuu. Kila kitu tumemiminia shimoni!” Akaapa mjumbe. Uso wake ulikuwa umepooza. Macho yake yamelegea. Na mara akaanza kukohoa kwa pupa mpaka akatoa damu. Akamuaga Sheng kwa ishara kisha akatoka zake.
Sheng akalaza kichwa chake kitini akifikiria kwa sekunde kadhaa. Punde simu yake ikaita, akainyakua na kuweka sikioni.
“Sawa, nakuja,” alisema kwa ufupi kisha akaiweka simu mezani. Akaendelea kufikiria kwa muda kidogo, na kisha akanyanyua simu yake ya mezani na kulonga, “tazameni hao vijana waliozika hizo antidotes! Kama watakuwa wameanza kubadilika, wawekeni kwenye cages. Ntakuja kuwatazama kesho mapema.”
Alipotoa agizo hilo akasimama na kutoka ofisini.
**
Bandarini, usiku wa saa nne …
Meli ya kichina inayojinasibu kuja kutoa huduma za afya bure nchini, haswa jijini. Ilikuwa tayari imeshatia nanga. Ndani yake ilikuwa imebeba wafanyakazi alfu moja na mia. Miongoni mwao vikosi vya wanajeshi wa kichina takribani vitatu kila kimoja wapo kikiwa na askari hamsini.
Ilikiwa ni meli kubwa. Juu yake ikipeperusha bendera ya nchi, na ubavuni ikiwa ina chapa ya msalaba mkubwa rangi nyekundu.
Gari jeusi, Ford Ranger modeli ya 2016 ikiwa imefunikwa bodi ya nyuma, ikasimama eneoni na punde akashuka Sheng. Kisha wanaume kadhaa watatu wenye asili ya China wakiongozana naye.
Sheng akatembea kwa ukakamavu akifunga kifungo cha koti lake la suti. Alikuwa anaelekea kule ambapo Meli ilituama. Akiwa ametazama mbele aendako, mara akasikia sauti:
“Kiongozi,” kutazama, akamwona Kamanda mkuu akitokea upande wa gizani. Alikuwa yu mwenyewe akiwa amevalia nguo za kiraia. Akasogea, ila wale wanaume waliokuwa wanaongozana na Sheng wakamzuia.
Sheng akawaamuru wamwachilie.
Kamanda akampatia Sheng mkono. Akasema, “nimekuwapo hapa kwa muda.”
Lakini uso wake ulionyesha shaka.
“Lakini sikuwa nafahamu kuwa si silaha tu umeleta. Umeleta pia na watu na chemicals!” Kamanda akakunja uso akitoa macho. Sheng akasimama na kumtazama.
“Kamanda,” Sheng akaita, “kwani kuna shida nikiongezea kidogo mzigo wangu?”
Kamanda akabanwa kwanza na kigugumizi. Akatafuta neno la kuongea, akasema, “Hapana bwana Sheng. Lakini nilipaswa kuwa na taarifa rasmi. Namma hii inaweza kututia hatiani!”
Sheng hakumjibu Kamanda. Akaendelea kutembea akiwa anawaza mambo yake kichwani. Alipofika getini, akasimama na kumtazama Kamanda. Akasema, “ni hatia gani hiyo waizungumzia? Kwani nakulipa kwa kazi gani?”
Kamanda akataka kujibu, ila Sheng akasimamisha kidole chake kama ishara ya kumtaka asimuingilie. Alafu akaendelea kunena, “fanya kazi yako, Kamanda.”
Kisha akazama getini na ndani ya muda mfupi yakatoka magari mawili makubwa yaliyobebelea kontena rangi za kijani. Zilipotokomea eneoni, Sheng akaonana na Kamanda na kumpatia mkono wa kheri, anataka kwenda zake.
“Samahani,” Kamanda akasafisha koo na kuuliza; “Mmefikia wapi kwenye swala la Jona?” Sheng akamtazama kwa sekunde mbili kisha akamwekea mkono begani.
“Kamanda, kati yangu nawe, nani wa kumuuliza mwenzake hilo swali?”
“Aahm pengine unaweza ukawa umepata jambo. Si mbaya kunishirikisha.”
“Sijapata kitu. Na nilidhani hata hilo jambo wewe ndiye utakuwa wa kwanza kuling’amua maana limeshusha hadhi ya jeshi lenu.”
Sheng aliposema hayo, akamwacha Kamanda pasipo kumuaga. Akatembea hatua tano, ila mara akageuka na kumtazama Kamanda. Akasema, “fom today, hilo swala la Jona, niachie mimi, sawa?”
Kabla Kamanda hajasema jambo, Sheng akageuka na kwenda zake. Kamanda akabaki akimtazama mwanaume huyo anayoyoma.
Akalaani sana. Aliona amedharaulika. Thamani yake imeshuka. Juzi tu, alikuwa akinywa na Sheng kwa furaha, leo anaongea naye kana kwamba kakijana ka mtaani!
Akang’ata meno. Punde akajikuta ndani ya gari lake, akatekenya shina la usukani na kutimka eneoni baada ya kuhakikisha kila jambo limeenda sawa.
Alijua wazi kesho yake vyombo vyote vya habari vitakuwa hapo bandarini. Na hata yeye atakuwapo hapo akiwakilisha jeshi la polisi. Ila akiwa kama mtu asiyejua kinachoendelea hapo. Akiwa ni miongoni mwa wageni rasmi!
**
Saa nane usiku …
“Kila kitu tayari, unaweza kwenda kupumzika, boss,” alisema mwanaume mrefu mweusi, kijakazi wa Sheng. Alikuwa amevalia ‘ovaroli’ la bluu na kichwani akiwa amejiveka kofia ngumu na usoni amevalia miwani kubwa ya kumkinga macho na mikononi ana glovu ngumu rangi ya njano.
Sheng na Shao walikuwa wamesimama pamoja wakiwa wametia mikono mifukoni. Macho yao yalikuwa yanatazama magari yale mawili makubwa yaliyotoka bandarini, na watu kadhaa wakiwa wanashughulika hapa na pale kwenye upakuaji.
Baada ya kijakazi huyo kusema hayo, wanaume hao wa kichina wakaongozana kwenda kutazama kama kila kitu kipo sawa. Wakakuta kontena limebakia tupu, na ndani ya maabara kulikuwa kumesheheni vitu kadha wa kadha.
Wakatazama maabara ile kwa kitambo kidogo, kisha Sheng akamuuliza Shao, “unadhani vitasaidia?”
Ni nadra kwao kutumia lugha ya kiswahili katika maongezi yao. Ila Sheng aliamua kufanya hivi maana alitaka kumpa Shao mazoezi zaidi ya kutumia lugha hii. Imekuwa ikimsumbua, na kwakuwa yupo ndani ya nchi itumiayo kiswahili katika maongezi ya kila siku, hakuwa na budi kukifahamu.
“Nadhani vitasaidia sana,” Shao akajibu kwa sauti ya puani. Kama ungelikuwa unamsikia usingelimwelewa kabisa kwa namna anavyoongea. Ila kwa mwenzake Sheng ilikuwa haina shida maana wanashea lugha.
“Lakini, Shao,” Sheng akasema akimtazama mwenzake. “Naona kuna haja ya kuagiza vijana toka China kuja kufanya kazi huku. Hawa vijana wa hapa siwaamini kabisa, haswa ukizingatia Lee sijui alipo.
Tuna haja ya kutuma maombi nyumbani watukabidhi baadhi ya vijana waliowapika huko kwa mafunzo magumu, waliojawa stadi za mapambano, waje kutusaidia.”
Shao akaminya lips zake nyembamba. Akatoa mkono wake mmoja mfukoni na kufikicha pua yake kidogo kama mtu mwenye mafua.
“Sishani kama itawezekana kwa shasha,” akasema Shao akitikisa kichwa. “Unajhua shasha hivi kule nyumbani kumekuwa na shiida shana. Li wameamka na kuwa ngufu kuba tofauti na mwashoni. Inasemekana wanafadhiliwa na matafa ya magaribi. Wanapambana shana kuhakksha Wu inakufa na waon ku-rise.”
Li ni wakina nani?
Miaka kadhaa huko nyuma koo ya Li ilikuwa ni moja ya koo ya kawaida sana ndani ya nchi ya China. Hakuna mtu aliyekuwa anaizungumzia wala kuipa uzito kwenye maongezi yao. Ilikuwa ni koo iliyoundwa na wakulima na wafanyabiashara wadogowadogo.
Na katika kipindi chao, koo hiyo ikashuhudia koo ama familia ya Wu ikipanda kwa kasi sana mbele ya macho yao haswa baada ya kuonekana kuvutia serikali katika namna ambavyo ilikuwa ikiwasaidia kupata na kulinda mikataba ya China. Vilevile ikihakikisha dola ya China inakua kiuchumi kwa kutumia mkono wowote, aidha wa damu ama kitabu!
Na kwasababu hiyo basi, Wu wakatengewa kitengo maalum ndani ya chemba za serikali. Kitengo ambacho kiliikabidhi koo ya Wu ofisi ya ujasusi wa kiuchumi dunia nzima. Kwa hivyo basi, koo hii ikawa si siri tena ndani ya nchi ya China japo biashara zao zingine zilikuwa haramu kama vile utumwa wa kileo, madawa na utekaji.
Sasa basi kwa kuitambua hili, nchi za magharibi ambazo hazipo tayari kuona dola zao zinawekwa miguuni na China, zikaamua kufanya jambo kujinasua na kuwadhoofu wachina wajao kwa kasi. Na njia bora waliyoichagua ikiwa ni ile ile ya ‘kikulacho ki nguoni’. Wakiwa wanafahamu nguvu ya China ni familia koo ya Wu, basi wao wakaungana na koo ya Li kuhakikisha wanamtokomeza na kumdhoofisha Wu! Na basi kwasababu Li walitaka umaarufu na pesa (Fame n’ money), kwao hili hawakuliona gumu. Wakalipokea wakiwa vichwani wamedhamiria kifuta kiburi cha Wu, na kuirejesha koo ya Li kama koo yenye nguvu zaidi kama ilivyokuwa kabla ya mapinduzi ya nchini China ya mnamo mwaka 1945 mpaka 1950.
Na sasa, Li wamekuwa wakiitawala Hongkong. Taratibu wakijipanga kutanuka na kwenda kuikabili Wu popote ilipo.
Je, vipi kuhusu ile nyaraka ya Lee na saga la Chen Zi huko Hongkong??
Tuurudi kwa Sheng na Shao …
Sheng alitikisa kichwa chake. Alikuwa ameelewa nini Shao amemaanisha. Akalaani. Akalaani tena maana aliona ni uzembe umefanyika mpaka kufikia hali kama hiyo ya sasa. Hakuwa anaamini kama Li ingefikia kipindi kuwa tishio na hata sasa Wu ikashindwa kusambaza wapambanaji wake na basi wakabakizwa hukohuko China.
Akafikiria kidogo na kuona kuna haja ya kwenda huko China. Akakutane na viongozi wake juu na kujadili mambo kadhaa. Lakini Shao akampa tahadhari. Haitakuwa vema kama akienda huko akiwa hajakamilisha kwanza kazi yake ya kumtia Jona mikononi.
Toa boriti kwenye jicho lako ndipo utazame ya wengine. Sheng akakubali shauri hilo. Punde atakapomalizana tu na Jona, atasafiri kwenda China angalau kwa juma moja tu.
Na aliamini hilo la kumshughulikia Jona halitachukua muda maana ameshaleta vifaa vya kazi.
Wakatoka maabara na kwenda kwenye ghala za silaha. Napo wakatazama ingizo jipya na kufurahishwa nalo. Baada ya hapo wakatoka na kwenda kupumzika maana muda ulikuwa umeshaenda sana.
**
Asubuhi Redioni …
” … kwa hivyo basi, mimi kama kiongozi mkuu wa mkoa, ningependa kutoa rai kwa wananchi wangu kutumia fursa hii adhimu. Kuanzia majira ya saa mbili asubuhi kesho mpaka majira ya kumi jioni, wafike pale kwenye meli ya kichina ili wapatiwe matibabu na vipimo bure kabisa!
Hili lamaanisha na kuonyesha namna gani serikali yao inavyowajali, na kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata afya bora akaijenge nchi kwa kufanya kazi.”
Ilikuwa sauti ya mkuu wa mkoa.
** Na kweli fursa ikachangamkiwa ipasavyo. Watu wenye matatizo mbalimbali wakajaa kwenye meli na kutibiwa bure kabisa. Lakini changamoto ikizuka kuwa wagonjwa walikuwa wengi mno hata wengine wakarejea majumbani pasipo kupata huduma wanayoihitaji.
Baadae usiku kwenye televisheni, habari ikaruka na baadhi ya wananchi waliopata huduma wakoipongeza serikali kwa msaada huo toka nje kwa namna ambavyo walipata mapokezi na huduma za kisasa.
Na hapohapo habarini, kiongozi wa meli hiyo akapata kuongea, pamoja pia na kiongozi mkuu wa mkoa. Wakanena namna uhusiano wao unavyoimarika na kwa namna gani wataendelea kusaidiana zaidi.
**
Saa tatu usiku, Hongkong
Siku yake nzima haikuwa na mafanikio, tunaweza tukasema hivyo kwani kitu alichokuwa amekiendea hakuwa amekipata hata kidogo. Bwana Lee akashusha pumzi, kisha akadaka kiuno. Akatazama saa yake, majira yalikuwa yamemtupa mkono.
Akawaza kuondoka sasa. Pengine akirudi kesho anaweza kumkuta huyu meneja ahusikaye na uwanja huu uliopo ghorofa ya tatu, ambapo ndipo Chen Zi alikuwa anafanyia mazoezi enzi za uhai wake.
Na endapo siku hii ikienda bure, itakuwa hasara kubwa sana kwake maana muda unazidi yoyoma. Alijua wazi hatakiwa kupoteza hata sekunde huko Hongkong maana anaweza hitajika na Sheng mara moja akakosekana.
Akanyanyuka, na kuvaa miwani yake meupe isiyo ya macho bali urembo wa kuficha identity yake. Akachomeka mikono yake mfukoni, kisha akatembea kufuata lifti. Akangoja kidogo, mara ikafunguka na mzee mmoja mfupi mnene mwenye nywele nyeusi na kiwaraza kwa mbali, akatoka kwenye lifti akitembea kwa ukakamavu.
Lee akamtazama mzee huyu. Alikuwa mwenyewe. Amevalia shati na koti la kizibao lililofumwa na ngozi. Chini alivalia suruali brown ya kadeti na kumalizia na raba.
Lee akahisi pengine huyu mwanaume ndiye anahusika na uwanja huu. Mavazi yake yaliakisi mtu wa michezo. Basi akaachana na lifti na kumuita huyu Bwana. Hakugeuka, akanyoosha tu mkono wake kumwambia Lee amefunga hilo eneo, na kwa sasa haitaji mteja yeyote.
Lee akamweleza yeye si mteja, yupo hapo maana ana shida fulani, anaomba amsikize. Yule Bwana akasimama na kumtazama kwa shari. Kisha akamuuliza shida gani hiyo?
Lee akatabasamu kwanza. Hakutaka kumhofisha bwana huyu. Alijitahidi kuwa rafiki kadiri alivyoweza. Akasema kwa ustaarabu kuwa alipewa taarifa kwamba Chen Zi alikuwa akifanyia mazoezi hapo. Basi kwa namna gani atapata mtu anayefahamiana na huyo jamaa?
Yule Bwana akadhani pengine Lee ni polisi. Akastaajabu na kumwambia akiwa amekunja uso, ni kwa mara ngapi watakuja hapo kumsumbua na maswali ya mara kwa mara? Amechoka.na hana muda tena. Na basi ndiyo maana ameamua kutokujihusisha tena na mambo ya burudani.
Lee akatabasamu na kumuahidi hiyo itakuwa mara yake ya mwisho kuja hapo. Hatopenda kumbughudhi, ila kama asipojali amsaidie, naye kwa namna fulani atamfurahisha.
Aliposema hayo alikuwa akigusa mfuko wake. Yule Bwana akatabasamu. Akakunjua uso wake na kumtazama Lee kisha akampasha habari muhimu.
Anajua mengi kuhusiana na Chen Zi, ila swala la kifo chake kimekuwa ni utata hata kwake. Lilikuwa la ghafla mno! Kwa mara zote ambazo Chen Zi alikuwa akifanya mazoezi hapo, alikuwa anakatazama hata washirika wake kutumia sigara, ilikuwa ni ajabu kuja kupewa taarifa kuwa amekufa kwa kuzidisha dozi ya madawa!
Bwana yule akatikisa kichwa. Akatazama chini kwa masikitiko. Alikuw amemkumbuka Chen Zi, si tu kama mteja wakw bali kama mwanae kwa namna alivyokuwa mkarimu.
Lakini asipoteze muda zaidi, akamwelekeza Lee kumhusu mpiga gitaa wa Chen Zi. Huyo anaitwa Chong Pyong. Ni kijana mfupi aliyetoboa kila sehemu ya uso wake. Tangu Chen Zi alipokufa, alijiunga kwenye bendi moja maarufu Hongkong na Shanghai. Wamekuwa wakipiga muziki wao kwenye hoteli mbalimbali!
Akamtajia baadhi ya hizo hoteli. Lee akamshukuru kwa kumpatia kiasi fulani cha pesa kisha akaenda zake.
Basi akashika njia ya kuelekea kituo cha mabasi maana muda bado ulikuwa unaruhusu upatikanaji wake, pia hii itamsaidia kutunza fedha zaidi, kichwani akipanga kutumia taksi wakati wa kurudi tu.
Baada ya muda mfupi, akawa amefika kwenye moja ya hoteli aliyoambiwa na yule Bwana. Bahati akakuta tangazo likinadi uwepo wa ile bendi aliyoambiwa kuwa ndaniye ndo’ yupo Chong Pyong.
Ikamlazimu alipie kiingilio kikubwa sana kuingia humo maana ilikuwa hoteli ya ‘watu wazito’. Akatafuta mahali pa kukaa, na kisha macho yake yakaangaza mbele kwa wale watumbuizaji.
Hakuchukua muda mrefu, akamwona mlengwa wake kwani kwa kadiri muziki ulivyokuwa unapigwa, Chong Pyong alikuwa anaonekana kwa wepesi maana alijiri mbele kila muda akionyesha umahiri wake kwenye upigaji wa gitaa.
Sasa Lee akaanza kupanga namna ya kumchomoa bwana huyo apate kuteta naye. Ila siku hiyo ikajiri kama bahati, hakungoja sana, mara muziki ukazima na wale watumbuizaji wakaingia kwenye mtindo wa utofauti kidogo.
Sasa alisimama mwimbaji nyuma ya kidaka sauti, akaanza kuimba kwa mtindo wa ‘akapela’ – sauti kavu pasi na vyombo. Bila shaka walikuwa wamelenga wasikilizaji wapate ladha halisi ya sauti tamu toka kwa mwimbaji, lakini pia kuwapa mapumziko wale wengine wapate kuvuta pumzi baada ya kutumbuiza kwa muda.
Hapo sasa, Lee akamwona Chong Pyong akielekea nyuma ya ukumbi. Akanyanyuka akitazama usalama. Walikuwa wamesimama walinzi kadhaa konani wakiwa wamevalia suti nyeusi na masikio yao yakizibwa na vifaa vya mawasiliano.
Lee akahesabu idadi yao, sita. Na basi akatambua kuwa walinzi hao watakuwa wanamtazama mienendo yake. Na hakuwa amekosea. Walirusha macho kumtazama, na hatimaye wakamtilia shaka. Haikuruhusiwa mtu kueleka kule nyuma ya ukumbi kama wewe si mhusika.
Wale walinzi wakawasiliana, kisha mmoja akanyanyua mguu wake mzito kumfuata Lee kule aelekeapo.
Lee akaongeza mwendo. Na yule mlinzi naye akaongeza mwendo, na akazidi kumtilia Lee shaka. Akapaza sauti kidogo akimtaka Lee asimame hapo hapo alipo. Alijitahidi sauti yake isiwatie hofu wateja wengine waliokuwa wametulia, aidha wakila ama kuburudishwa na sauti tamu ya mtumbuizaji.
Ila Lee akakaidi. Akaendelea kutembea. Na baada ya muda kidogo, akazama nyuma ya jukwaa. Sekunde tano nyuma, na yule Bwana mlinzi naye akakazamia humo.
Akaangaza, ila hakumwona Lee! Kwa umbali wa hatua ishirini walikuwapo baadhi ya wale wahusika wa bendi, kwa idadi watu watano, wawili walikuwa wanatazama baadhi ya vifaa, wawili walikuwa wakiteta na mmoja anakunywa maji.
Mlinzi huyu akapata shaka zaidi juu ya Lee. Akapaza sauti kuwauliza wale wasanii kama wamemwona mtu mgeni humo, wote wakasema hawajui!
Mlinzi akatazama kushoto kwake, kulikuwa kuna korido ndogo inayoelekea stoo, na ’emergency exit door’. Akawaza pengine Lee atakuwa ameenda huko. Ila kabla hajanyanyua mguu, mara king’ora kikaanza kuita kwanguvu!
Kilikuwa ni king’ora kinachoashiria moto kuzuka ndani ya hoteli, mara sauti za watu wakipiga mayowe zikaanza kusikika huku na kule, na watu wakaanza kukimbia kama wehu kila mmoja akitaka kunusuru roho yake.
Hata yule mlinzi akaachana na kumtafuta Lee, akaenda kule kwenye hall kubwa kuhakikisha usalama.
Ila kiuhalisia hakukuwa na moto. Ni kwamba Lee aliwasha ‘lighter’ karibu na ‘sensor’, hivyo ikapeleka taarifa ya moto ambao kumbe aliuzima na kutia lighter mfukoni.
Hapa kwenye vurumai ya watu, sasa akageuka kuwa chui aliye mawindoni, jicho lake lilimwagukia Chong Pyong lisimwache. Na baada ya muda mfupi akawa amemtia mkononi. Akamzimisha na kutoka naye kwa kupitia emergency door.
Baada ya muda mfupi Lee akawa amefanikiwa kufika na Chong Pyong mahali alipoweka makazi, akamlaza hapo na kwenda kuoga kuondoa uchovu. Alipomaliza akakumbuka kuwa hakuchukua chakula, akashuka chini kuendea.
Aliporejea akakuta kitanda kitupu! Chong Pyong hakuwapo. Hamaki kugeuka nyuma, mara kiti kikarushwa kwanguvu kumfuata. Haraka akakwepa, kiti kikakita ukutani na kuvunjika.
Chong Pyong akajaribu kurusha mateke na ngumi, lakini hakuwa na mafunzo ndani yake, hakuweza kufua dafu kwa Lee, akatulizwa punde na kujikuta sakafuni akiugulia maumivu.
Akamuuliza Lee yeye ni nani na nini anahitaji kwake? Lee akamwambia ingekuwa busara kama angemuuliza kabla hajaamua kumshambulia. Lakini kwa wakati huo, Chong Pyong akadhani aidha Lee ni afisa wa polisi, na basi kama sio, atakuwa jambazi aliyetumwa amuangamize.
Basi akaanza kujitetea akijieleza yeye hana makuu na mtu. Anacharaza zake gitaa tu kwa ajili ya kuingizia kipato familia yake na si kingine. Kama haitoshi, akaendelea kubwabwaja kwa hofu, akasema mpaka mengine ambayo Lee hakuwa na haja nayo.
Kwa maelezo hayo Lew akatambua Chong Pyong alikuwa mtu wa aina gani. Mpenda starehe na anasa. Alafu pia ni mwongomwongo.
Basi akamtaka anyamaze. Yeye hayupo hapo kwa ajili ya kumdhuru ila ana shida na mtu mmoja tu ambaye anafahamu atakuwa na taarifa zake, naye si mwingine bali Chen Zi!
Chong Pyong akatoa macho kusikia jina hilo. Kwa sekunde kidogo akatulia akimtazama Lee kwa uso wa maulizo. Akamuuliza Lee yeye ni nani? Lee akamjibu shabiki mpenzi wa Chen Zi. Chong Pyong akamtazama tena kwa sekunde kama tano pasipo kunena kitu.
Mosi, kuna kitu alikuwa anafahamu. Pili, kuna kitu alikuwa anaogopa. Mara akatikisa kichwa akasema, Chen Zi ni mfu. Hana taarifa zozote juu yake.
Lee akamdaka shingo na kumbamizia ukutani, alafu akamning’iniza kwa mkono wake mmoja akitazama uso wa Bwana huyo ambao ulijawa na vipuli.
Akamwambia kwa sauti ya chini, hana masikhara naye. Na hapo walipo ni ghorofa ya kumi, haoni soni kumtupia nje akajifia endapo asiposema anachokihitaji. Tena haraka asimpotezee muda. Ni nini kilimuua Chen Zi?
Basi bwana yule akiwa amekabwa kwanguvu asiweze hata kuhema, akapambana kunena huku jasho likimchuruza. Lee akamwachia avute hewa akiwa amempatia dakika moja tu kueleza, la sivyo waendelee na zoezi!
Chong akavuta hewa kwa pupa huku akikagua shingo yake. Baada ya sekunde kadhaa, akamtazama Lee kwa macho yake mekundu. Akameza mate. Akasema hajui kitu. Kitu pekee ajua ni kuwa Chen Zi alizidisha dozi ya madawa ya kulevya.
Lee akamdaka tena shingo na kumbamiza ukutani! Mara hii hakumkaba, akabadili zoezi, akadaka moja ya kipini puani mwa Chong Pyong, akakinyofoa kwanguvu. Damu zikaruka! Chong Pyong akapiga kelele kali za maumivu.
Ila Lee hakukoma, wala hakumwongelesha, akadaka kipini kingine kwenye nyusi ya Chong Pyong, nacho akakivuta kwanguvu, damu zikachuruza!
Chong Pyong akalalama kwa maumivu. Lee, sasa mkono wake ukiwa umejawa damu, akadaka tena kipini kingine cha Chong Pyong, sasa cha mdomoni, Chong Pyong akapaza sauti, nasema! Nasema! Uso wake ukiwa umejawa na damu.
Lee akamwacha na pasipo kuongeza neno, akamtazama kwa macho yenye kiu na neno. Basi Chong Pyong akavuta kwanza pumzi kisha akasema kuwa Chen Zi hakufa kwa madawa, bali aliuawa na watu wasiojulikana. Akasema anaamini watu hao walikuwa ni wapinzani wake kimuziki.
Lee akamuuliza, sasa ilikuwaje vyombo vyote vya habari nchini na vya kimataifa vikatangaza kuwa amekufa kwa kuzidisha dozi ya madawa ya kulevya? Chong Pyong akahema kwanza. Kisha akamwambia Lee kuwa huo ni mchezo tu ulipangwa kwani Chen Zi alipewa sumu, na alipopoteza fahamu, wakamvutisha madawa na kuacha baadhi mezani mwake, mpaka mauti kumkuta.
Lee akashangazwa na hiyo taarifa. Akamuuliza bwana huyu, aliyajuaje hayo, na kwanini hakuchukua hatua kuripoti huo ukweli?
Chong akabanwa na kigugumizi. Akajitetea alikuwa anaogopa pengine angefanya hivyo, watu hao wangemuwinda na kummaliza. Aliamua kunyamazama kunusuru roho yake.
Na kitendo cha kwamba alijuaje, alipata kushuhudia hayo yakitukia. Hapa Lee akamuuliza swali jingine, hao wauaji akiwaona ataweza kuwatambua kwa kuwatazama?
Kabla Chong hajajibu, simu yake ikaita mfukoni. Hapa wakatazamana kwa sekunde kama tatu. Lee akazamisha mkono wake mfukoni mwa Chong na kutoa simu. Ilikuwa ni iphone 8 rangi ya fedha. Akapokea na kuweka ‘loud speaker’, kisha akamuwekea Chong Pyong mdomoni.
Sauti iliyotoka simuni ilikuwa ni nzito. Na mara moja ilimuuliza Chong yupo wapi muda huo? Chong akalaghai yu mgahawani. Sauti ikauliza tena wapi amefikia kwenye lile swala la yule jamaa anayemtafuta Chen Zi?
Hapo Chong Pyong akabanwa na kigugumizi. Alimtazama Lee wakakutana jicho kwa jicho. Lee akamkazia ndita na kumpa ishara aendelee kuongea na simu.
Chong Pyong akasema bado hajafanikiwa, kisha akakohoa mara tatu. Mara simu ikakata. Lee akaelewa kile kikohozi kilikuwa ni ishara.
Na sasa akatambua kuwa Chong Pyong alikuwa ana mengi ya kumjuza. Kwa namna moja ama nyingine ni adui anayemtafuta. Akamuamuru ampatie nywila za simu yake. Hili swala likawa gumu kidogo kwa Chong Pyong.
Lakini baada ya Lee kunyofoa vipini vyake vitatu, akashindwa kustahimili maumivu, akatoa nywila, Lee akafungua simu na kuzama ndani. Akaingia Facebook na kukuta Chong Pyong akitumia jina la Chen Zi!
Akaelekea kwenye kona ya ujumbe, huko akakuta ‘conversation’ kati yake na Chong Pyong akiigiza kuwa Chen Zi! Kumbe Chong alikuwa miongoni mwa wale watu ambao Lee aliwaomba anwani na wakampatia kisha Lee alipoitafuta akaishia kujikuta katika nyumba ya yule kikongwe mjane!
Kama haitoshi, kumbe Chong Pyong alikuwa anawasiliana na wale Chen Zi wengine wote ambao Lee aliwasiliana nao na kisha wakampatia anwani ya uongo!
Kwanini Chong Pyong anatumia jina la Chen Zi huko Facebook? Kwanini na wenzake wanayatumia majina hayo? Na kwanini walimlaghai?
Kabla hajapata majibu ya maswali hayo, Lee akaamini kuwa Chong Pyong atakuwa anahusika na mauaji ya Chen Zi halisi, kwa namna moja ama nyingine! Kwanini walimuua? Na hao ma – Chen Zi wengine ni wakina nani?
Akamkaba Chong Pyong na kumwamuru amueleze kila analolijua, la sivyo atanyofoa roho yake ndani ya sekunde moja tu! Aliminya mishipa ya koo la Chong mpaka mwanaume huyo akatoa ulimi nje, macho yakitumbuka!
Alipomwachia, akadondoka chini akipapatika kuhema! Lee akamwambia ana sekunde tatu tu za kusema, la sivyo ataendeleza zoezi na mara hii hatalisitisha kamwe mpaka atakapogeuka kuwa mfua
Mara wakiwa hapo, Lee akasikia vishindo vizito mlangoni mwake. Vilikuwa vya watu waliotoka kukimbia kisha wakasimama ghafula!
Vishindo hivyo vilipokoma, sauti nzito zikaulizana. Lee akatambua hapo si salama. Ndani ya sekunde tatu mbele, mara mlango ukavunjwa na wanaume watatu majabali wakaingia ndani wakiwa wamebebelea bunduki mikononi. Miongoni mwao alikuwapo yule jabali mweusi aliyepewa agizo la kumtafuta Lee.
Wakatazama huku na kule, hawakumwona mtu zaidi ya Chong Pyong aliyekuwa amelala chini akihema kama bata. Kutazama dirishani, wakaona li wazi, Lee alikuwa ametoroka kwa kutumia shuka!
** Yule jabali mweusi akaghafirika akipiga ngumi kiganja chake. Haraka akaamuru wenzake washuke kule chini kumtafuta mwanaume huyo wakati yeye akiwa amebaki na Chong Pyong ndani ya chumba.
Akamuuliza Chong Pyong maswali kadhaa. Ma maelezo yake yakazidi kumtia Lee hatiani na kuthibitisha kuwa si mtu wa kubaki hai hata kidogo.
Lazima auawe! Maana tayari atakuwa amefahamu siri yao kuwa Chen Zi aliuawa na si kuzidisha madawa kama vile watu wadhaniavyo.
Lakini pia, wakammaliza na Chong Pyong kwa usalama zaidi. Waliona endapo mtu huyo akiendelea kuwa hai, basi Lee atamtafuta na kupata kila anachokitaka. Kitu ambacho hawakuwa radhi kitokee, hata kidogo!
Yule jabali mweusi baada ya kutimiza agizo la mkuu wake, kummaliza Chong Pyong, akaamriwa aende polisi na kuripoti hilo tukio katika namna ambayo Lee ataonekana kuwa mtuhumiwa wa mauaji hayo tangu amekuwa mkazi wa hilo eneo ambapo Chong amefia.
Jabali hilo likatii na kufanya kama alivyoagizwa. Ndani ya muda mfupi, polisi wakafika eneo la tukio, wakapiga picha kadhaa, wakachukua maelezo toka kwa Jabali yule mweusi kama shahidi, kisha wakaondoka na mwili wa Chong Pyong.
Na kwa msaasa wa kamera za CCTV, zilizokuwako maeneo ya koridoni na huko nje, polisi wakapata picha ya Lee iwasaidie kwenye msako.
**
Saa mbili asubuhi …
“Vipi? Unaendeleaje?” Marwa alimuuliza Jona aliyekuwapo kitandani akitazama kana kwamba mtu aumizwaye na mwanga mkali.
Ndani ya chumba walikuwa wenyewe tu, na tayari Marwa alikuwa amembembelezea chai mgonjwa na kufanikiwa kwa kiasi chake. Alikula kidogo akasema ameridhika.
Kabla Jona hajajibu, alimtazama Marwa kisha akafumba macho yake kwanguvu kama mtu auguliaye maumivu, alafu akasema kwa kunong’ona:
“Naendelea vizuri.”
Mdomo wake ulikuwa mkavu. Macho yake madhaifu yalikuwa yamezungukwa na duara jeusi kwa mbali. Uso wake ulikuwa umekonda na kudhoofika.
“Nipo wapi hapa?” Akauliza akijitahidi kuchanua macho yake. Ila akashindwa. Haraka akayaminya na kuyafumba.
Marwa akamwambia, “Upo kwa Miranda. Unamkumbuka?”
Jona akakunja ndita kwa mbali, alafu akauliza, “Miranda?”
“Ndio, Miranda,” Marwa akamjibu akimtazama na tabasamu kwa mbali. Jona hakusema tena, akanyamaza.
Marwa akamtazama kwa muda. Kisha akarudia tena swali, “unamkumbuka?”
Jona akabaki kimya. Ni kama vile alikuwa amepitiwa na usingizi. Marwa akaondoa vyombo na kumwacha peke yake. Ila muda kidogo akarudi na kumtazama. Bado Jona hakuonyesha dalili ya kuamka.
Akaketi kitandani na kuendelea kumtazama kwa muda wa dakika tano, akasikia hodi mlangoni na sauti ya kike. Alikuwa ni Miranda. Akanyanyuka kwenda kukutana naye.
“Vipi hali yake?” Akauliza mwanamke huyo. Marwa akageuza uso kumtazama Jona, kisha akatoka ndani ya chumba na kukifunga.
“Angalau,” akajibu akipandisha mabega. “Ameweza kuongea leo, japo kwa muda mchache … ile antidote imemsaidia!”
Marwa akatabasamu kwa mbali, ila Miranda akatazama chini. Marwa akamuuliza, “Vipi?” Miranda akatikisa kichwa kisha akaongoza mpaka sebuleni. Wakaketi.
“Ile si antidote ya kumpatia,” Miranda akasema kisha akalaza kichwa chake kitini. “Itampa ahueni kwa sasa, kwa kitambo kidogo, ila inabidi atafutiwe antidote ya kudumu. Endapo akiendelea kutumia hii ya sasa, ataishi kupooza mwili.”
Marwa akatoa macho kwa mshangao.
“Mbona hukuniambia mapema?”
Miranda akamtazama. “Ingesaidia nini?” Akauliza. Kisha kama mtu aliyejishtukia aidha atakuwa amemkwaza Marwa, akashusha pumzi yake na kunyanyua mkono.
“Inabidi tutafute antidote halisi,” Miranda akasema. Ila uso wake haukuwa na lepe la matumaini. “Tusipofanya hivyo, tutatibu tatizo moja kwa kuleta jingine.”
“Tutaitafutia wapi sasa?” Marwa akauliza. Mara simu ya Miranda ikaita. Kutazama alikuwa ni BC.
**
Saa nne asubuhi …
BC alichomoa leso yake mfukoni akijifikicha pua. Mafua yalikuwa yanamsumbua. Aliporudisha leso yake mfukoni akanywa fundo moja kubwa la whisky kisha akamtazama Miranda na Marwa waliokuwa wameketi pembezoni mwake.
Walikuwa wapo nje ya nyumba ya bwana huyo wa kizungu. Meza mbili zilikuwa mbele yao, ila ya Bwana BC pekee ndiyo ikiwa na kinywaji. Wote walikuwa kimya wakimtazama bwana huyo wa kizungu kwa hamu.
BC akawatazama kisha akapooza koo lake kwa kunguruma. Akalaza mgongo wake kwenye kiti kidogo cha chuma alichokalia, na kusema kwa sauti kakamavu:
“We have to prepare for any risk so far. To get the actual antidote won’t be an easy task at all!” (Inabidi tujiandae kwa hatari yoyote. Kupata antidote halisi haitakuwa kazi ndogo kabisa!)
Miranda na Marwa wakaendelea kumtazama kwa umakini. Na sura zao hazikuonyesha kama watu wanaohofia hatari hizo. Bali wana kiu na kupambana nazo. Na Bwana BC aliliona hilo.
Akanywa fundo moja tena la whisky na kuwaambia haswa lengo lake la kuwaitia hapo.
“Did you hear about that Chinese ship?” (Mmesikia kuhusu ile meli ya wachina?) Kabla hajajibiwa, akasema, “for sure, it might have brought something huge. And I fear, amongst them, is what we need.” (Kwa uhakika, itakuwa imeleta kitu kikubwa. Na nadhani, miongoni mwavyo ni kile tunachokohitaji.)
Akaweka kituo akitazama chupa yake ya kinywaji chake. Akafikiri kidogo na kuwataka Miranda na Marwa wafanye jambo kuhusu kile kitakachokuwa kimeletwa na ile meli. Kama kutakuwa na namna ya kuingia ndani ya kambi ya Sheng na kisha kupekua.
“Though it is risky. It worths it.” (Japo ni hatari. Ina manufaa.)
Lakini vipi kama hawataikuta antidote huko? Akauliza Miranda.
“Then you will surely see something else!” (Basi kwa hakika mtaona kitu kingine!) Akajibu BC. Na kuongezea, “and it will be equally important!” (Na kitakuwa na umuhimu sawa!)
Lakini pia akawaambia kama njia hiyo haitafanikiwa, basi atawaeleza plan B. Na kwasababu plan A itakuwa haijafanikiwa, basi Plan B itakuwa ndiyo njia pekee iliyobaki na kwa namna yoyote ile iliyopo duniani, lazima itimie!
**
Saa nne usiku …
“Una hofu?” Miranda aliuliza akimtazama Marwa. Mwanaume huyo alikuwa ameketi kwenye kiti nje ya nyumba akiwa anafikiri na kuyajenga kichwani.
Akamtazama Miranda na kutikisa kichwa. “Hapana, nipo ok.” Ila uso wake ulimsaliti. Alikuwa na hofu. Na tumbo lake lilikuwa linauguza woga.
Miranda akamsogelea na kuketi karibu yake. Akamwambia, “usijali. It will be ok. Hatutakufa. Tutafanikiwa kutoka hai na salama.”
Lakini kumbukumbu ya Marwa eneo lile haikuwa nzuri. Mara ya mwisho almanusura apate ukilema. Na ni ustadi tu wa Jona ndiyo uliowatoa hai. Hakuwa anaamini kama yeye na Miranda wataweza mudu.
Miranda hakusema kitu. Akamgusa mgongoni na kumtaka akajiandae kwani muda umeshafika.
Baada ya muda kidogo wakawa tayari wakiwa wamevalia sweta nyeusi zinazobana, suruali nyeusi za kombati na buti. Miranda akajiweka kwenye gari. Ila Marwa akaenda kwanza kumuaga Jona.
Akamtazama kwa sekunde kama tatu. Hakuonekana kama ana fahamu. Akaketi kitandani na kumshika mkono wake. Akamuita, “Jona.” Kisha akasema kwa sauti ya chini, “nakuacha kidogo. Mungu akijaalia tutaonana, tukiwa na dawa mkononi.”
Alipomaliza kusema hayo akaendelea kumtazama Jona kwa muda kidogo. Mlango ukagongwa.
“Twende, Marwa!”
Marwa akanyanyuka na kwenda kumkuta Miranda huko nje. Wakakwea garini na kutimka.
Baada ya robo saa wakawa wamefika karibu na eneo. Miranda akaliegesha gari lake eneo aliloona ni salama, eneo fulani la baa walilolipia kiasi fulani, kisha wakatembea kwenda mahali husika. Wote migongoni mwao walikuwa wamwmevalia vibegi vidogo vyeusi.
Kwa mwendo wao wa upesi, wakatumia kama dakika kumi tu kuwasili, wakaelekea upande wa kushoto wa jengo na kukwea ukuta baada ya kukata nyaya za umeme, Miranda akisimamia zoezi hilo.
Kama nyani, Miranda aliudaka ukuta na kisha akamvuta Marwa, wakazama ndani na ‘kunyuti’ kwa muda kidogo kusoma rada.
Eneo lilikuwa linalindwa mara mbili ya hapo mwanzo tangu mzigo mpya ulipoletwa na pia tangu antidote ziibwe mara ya kwanza na Jona na Marwa.
Kwa hivyo walitakiwa kuwa makini sana. Makini zaidi. Na hata Marwa alimkubusha hilo Miranda mbali tu na kumuelekeza ramani ya eneo maana yeye ni mwenyeji.
Wakaficha nyuso zao na vinyago. Na kisha wakaanza songa taratibu kuelekea upande wao wa kulia. Mahali walipo kulikuwa na vijumba vidogo vidogo visivyokuwa na watu. Ndani humo kulikuwa na majengo majengo kadhaa na kila jengo likiwa na kazi yake. Aidha ghala ama sehemu pa kupumzikia watu au ofisi.
Eneo lilikuwa kubwa sana! Na lote lilikuwa limezingirwa na uzio. Na kwa makadirio ya haraka, ndani ya eneo hilo kulikuwapo na watu takribani mia mbili hamsini!
Miongoni mwao wakiwa vijakazi, pamoja na walinzi wanaolinda hapo mchana na jioni. Na kila kijipande cha eneo, kilikuwa na kikosi cha walinzi wake. Na kila kikosi kikiwa na kiongozi wake mkuu.
Eneo kubwa lilikuwa linamulikwa na mwanga mkali wa taa. Mahali pachache pachache palikuwa na kiza. Na huko ndiko ambako Miranda na Marwa walikuwa wanajiegeshea huku maeneo yale yenye mwanga wakiyakwepa ama kuyapita kwa upesi sana.
Mpaka kufikia maabara kulikuwa na umbali wa kama nusu na robo ya kilomita. Na hapo katikati walinzi wakiwa wamejaa. Wanarandaranda. Wamebebelea bunduki nzito.
Basi taratibu. Tazama. Pita. Simama. Tazama tena. Pita. Ngoja. Tazama. Pita. Huo ndiyo ulikuwa mchezo. Wakafanikiwa kupita salama robo kilomita.
Ila wakiwa wanatafuna tena umbali huo, kuna mlinzi akahisi jambo. Alikuwa ni baba la miraba minne. Amevalia kibodi cheusi kinachobana misuli na suruali ya jeans ‘dark blue’. Bwana huyu alihisi msogezo wa vitu nyuma ya kibanda kimoja cha mawasiliano.
Akasimamisha masikio yake na kukodoa macho. Akashikilia bunduki yake vema mkononi. Akasonga kueleka huko alipopatilia shaka. Akatazama tazama, hakuona kitu. Ila kugeuza shingo, akastaajabu kumkuta mtu amesimama.
Akashika shavu lake linalomimina damu. Akakodoa kwa hasira. Akanyanyuka na kujipanga. Kutazama vema akamwona ni mwanamke. Akaguna.
Basi akarusha ngumi, Miranda akayeya kisha akanyaka mkono huo na kuuviringita kama anauvunja. Mwanaume akabinua mgongo akiugulia, Miranda akamzawadia teke la kifua na kumcheusha damu bwana huyo aliyepepesuka kana kwamba kakumbwa na dhoruba.
Hajasimama vema, Miranda akazunguka na kutuma mguu wake wa kulia, akakata koo la bwana huyo kwa kisigino cha kiatu chake. Mwanaume akalala chini mauti!
Damu zinamwagika haswa. Miranda na Marwa wakamficha kwenye kachombingo fulani cha hilo jengo kisha wakaendelea na safari yao.
Wakakata tena robo kilomita. Wakiwa wanaenda kwa tahadhari kubwa. Simama. Ngoja. Tazama. Tembea. Simama. Ngoja. Tembea.
Wakafikia mahali ambapo palikuwa kama uwanja. Mahali hapo palikuwa na mwanga mkali. Pia kwa mbali, kule konani ya uwanja, walikuwa wamesimama wanaume watatu wakivuta sigara. Mikononi mwao walikuwa wameshikikia kamba za zilizofunga mbwa shingoni.
Bahati Miranda na Marwa waliwaona wanaume hao kwa kutumia hadubini. Wakiwa wamejilaza chini wakajadili namna ya kufanya. Na ilikuwa lazima wakatize hapo kuendelea na safari yao kutokana na mahali walipoingilia.
Miranda akatazama tena na hadubini yake. Kushoto na kulia. Kushoto na kulia. Kwa mbali wakaona kuna walinzi wengine wakiishilia kwenda kaskazini ya mahali walipo.
“Sasa tunafanyaje?” Marwa akauliza.
“Tungoje kidogo,” Miranda akamjibu macho yake yakiwa ndani ya tundu za hadubini. “Muda si mrefu watamaliza ile sigara wanayoshea. Tutajua watatawanyika ama lah!”
Basi wakangoja kwa muda wa kama dakika tatu, kweli wale wanaume wakawa wamemaliza kile kipisi walichokuwa wanashea. Mlinzi mmoja akabaki hapo wakati wawili wakitawanyika. Mmoja akaelekea kushoto na mwingine kulia.
Sasa wakaona huo ndiyo mwanya wa kusonga hapo mataani wakiingiza kuwa kama walinzi, wakitumai kwa umbali ambao yule mlinzi mmoja alipo, itamuwia vigumu kutambua wao ni wavamizi.
Ila kabla hawajanyanyuka, wakastaajabu sauti nyuma yao, “tulia hivyo hivyo!”
Marwa akaogopa sana. Moyo wake ukaanza kupiga makasia.
Basi wakatii. Wakiwa wananyanyuka, Miranda akaigiza kupaliwa na kikohozi kikali. Mlinzi kutazama, upesi Miranda akakanyaga ukuta kisha akajibidua! Mguu wake wa kushoto ukapiga bunduki, na wa kulia ukachana uso wa bwana mlinzi kama kiwembe! Bwana huyo akapiga yowe kali la kuugulia.
Aaaaghh!!!
Mara Miranda akamwamuru afunge mdomo wake upesi akiwa amemnyooshea bunduki. Kisha akamkita na kitako cha bunduki na kumzimisha. Wakamficha na kundelea na safari.
Ila sauti ile ya mlinzi akigugumia maumivu, haikuwa imeishia kwenye masikio yao. Kuna wengine pia walisikia. Nao walitambua hilo, kwa hivyo walitakiwa kuondoka eneo hilo upesi.
Wakakatiza ubavuni mwa uwanja wakiwa wanatembea kwa haraka. Mlinzi yule aliyekuwa mbali konani akarusha macho yake kuangaza, ila hakutia shaka sana. Zaidi alitazama wale wenzake wawili kama wamepotelea, kisha akachomoa sigara nyingine mfukoni na kuiwasha. Akaitia mdomoni.
Akainyonya kwa nguvu na kutema moshi juu kama kiwanda.
“Sasa, tupite njia hii!” Marwa akamwelekeza Miranda. “Hii ni shortcut. Tutavuka barabara mbili, kisha tutakunja kushoto. Kama hatua hamsini hivi, tutakuwa tumewasili.”
Wakafuata hayo maelekezo. Wakashika barabara nyembamba iliyowakatisha chochoro. Wakaibuka kwenye njia pana. Wakatazama huku na huko. Salama. Wakavuka na kudaka chochoro nyingine. Napo wakapita, wakakutana na njia kubwa. Wakatazama huku na huko. Hawakumwona mtu. Ila kabla hawajapiga hatua, wakasikia kishindo cha mtu.
Wakasita. Kidogo akakatiza mwanaume mrefu mwenye mwili uliojengeka. Mkononi mwa mwanaume huyo alikuwa ameshikilia kamba ya mbwa. Kabla ya mwanaumr huyo kupita, mbwa akanusa jambo na mara akasimama!
Akatazamatazama huku na huko akinusanusa. Mara akabweka akiangazia kule kwenye uchochoro! Akawa anavuta kamba akitaka kwenda.
Mwanaume yuple aliyemshikilia akatazama kule uchochoroni. Kulikuwani giza, hakuona vema. Mbwa akawa anamvutia huko kwanguvu sana. Mwishowe, akaamua kuacha kamba, mbwa akakimbilia huko upesi na kuzama kichochoroni.
Mwanaume yule akawa amekaa tenge akiwa ameshikilia bunduki yake. Sekunde kama tano, kimya. Hakusikia sauti ya mbwa. Akapata shaka. Akachomoa bunduki yake pajani na kuishika vema. Akaanza jongea kwenda uchochoroni.
Hatua ya kwanza … hatua ya pili … hatua ya tatu … hatua ya n … mara akashtuka kumwona mbwa anatoka uchochoroni! Akaruka na kusogea kando. Akamwona mbwa amebebelea mfupa mdomoni. Mara ameulaza chini na kuanza kuulambalamba.
Hajakaa vema, akasikia kishindo cha mtu upande wake wa kushoto. Kugeuka, akashanga tu ghafla yupo gizani. Hata hakujua katendwa nini. Akadondoka chini puh! Kama gunia la mkaa.
“Twende!” Miranda akamsihi Marwa kwa sauti ya chini. Mara mwanaume huyo skachomoka alipokuwa amejificha, wakaendelea na safari. Mpaka wakafanikiwa kufika maabara.
Tatizo ni kwamba, hapo wakakuta walinzi takribani sita! Wote wakiwa wamebebelea bunduki mikononi mwao. Warefu na waliojaza miili kwa misuli minene!
Marwa akatikisa kichwa. “Hatutoweza, Miranda!”
Miranda akaminya mdomo wake na kukuna kichwa.
“Lazima kutakuwa na njia.”
***
“Njia gani hiyo na pale waliposimama ndipo kuna mlango?” Marwa akauliza. Miranda hakumjibu, akaendelea kutafakari namna ya kuenenda. Namna ya kuzama mule ndani pasipo kuzuiwa na pande zile za baba.
Baada ya dakika mbili, akamuuliza Marwa, “Kule nyuma hamna njia ya kuingilia?”
Marwa akamwambia hakuna, isipokuwa dirisha tu. Miranda akatulia akiendelea kuwaza. Akamtaka Marwa wangoje hapo kwa muda kidogo. Aliamini wale walinzi sita hawatakaa pale kwa muda mrefu.
Basi wakavuta subira kidogo. Kama dakika kumi hivi, mlinzi mmoja akachoropoka na kuacha wenzake watano. Ila hao walioachwa hawkauonyesha dalili ya kuondoka maana walilaza kabisa miili yao, wakipiga soga za hapa na pale.
Sasa ikabidi Miranda atafute namna ya kuwaondoa hapo maana la sivyo watakesha. Wanaweza kujikuta wanakaa hapo mpaka mambo yakagutukiwa!
Akamuuliza Marwa ampatie ramani ya wapi ilipo ‘main switch’. Kidogo Marwa akasita. Hakuwa na kumbukumbu nzuri juu ya wapi ilipo ‘main switch’ kwa hivyo akamtajia mwanamke huyo sehemu tatu, akibashiri mojawapo itakuwa sahihi.
“Unaenda kufanya nini huko?” Marwa akauliza. Miranda hakujibu, asipoteze muda akamtaka Marwa ajifiche kisha yeye aende huko. Akanyata na kusonga. Akatazama usalama. Akaendea njia yake kwa tahadhari na baada ya muda mfupi akawa amefika kwenye eneo moja ambalo aliambiwa na Marwa.
Kutazama, hapakuwa penyewe! Akasonya na kuanza kufuata mahali pa pili alipoelekezwa na Marwa. Kwa upesi ila kwa tahadhari akasonga akielekea huko. Kabla hajafika akawaona wanaume wawili wakikatiza. Akajibanza. Wanaume wakapita.
Akatazama kondo na kondo, kukawa salama. Akashika tena njia na kutembea. Akanyata kama mende ukutani, hakutoa sauti. Kuchungulia, akaona chumba kidogo chenye tahadhari ya umeme. Akashukuru. Hapo ndipo alikuwa anataka.
Akatazama tena kushoto na kulia. Upesi akatembea kwenda kwenye kichumba hicho. Hapo kwa nje kulikuwa na mwanga kwa hivyo hakutakiwa kukaa hapo kwa muda. Akajaribu kufungua kichumba hicho, mlango ulikuwa umefungwa!
Haraka akavuta begi lake mgongoni akachomoa chuma chembamba alichokizamisha nyuma ya mlango alafu haraka akautegua mlango. Basi ukafunguka. Akazama ndani na kutulia humo.
Muda si mrefu, kama sekunde tatu tu kupita tangu Miranda aingie ndani, mlinzi mmoja akatokea akikatiza hapo. Miranda akatulia kimya ndani ya kijichumba. Mlinzi yule kabla hajapita, akasita, aliona mlango ukiwa wazi.
Akasonga na kuutazama. Akaushika na kuusukuma mbele na nyuma. Na asijiulize sana akaurejeshea mlango ule sawa, kisha akaendelea na safari yake ya lindo.
Miranda akashusha pumzi ndefu, kisha akachomoa miwani ya mpira na kuiveka machoni. Sasa akawa anaona mule kizani, japo kwa mwanga wa kijani.
Akafungua kebo ya swichi.
**
“Marwa!” Sauti ikanguruma sikioni kwa kupitia kifaa kidogo Marwa alichokichomeka sikioni.
“Bado wapo hapo?” Sauti ya Miranda ikauliza kifaani.
“Ndio.” Akajibu Marwa kwa kunong’oneza. “Bado wapo, wanne sasa!”
“Sawa,” sauti ya Miranda ikajibu.
“Unafanya nini huko, Miranda??” Marwa akauliza akishikizia kifaa chake sikioni. Miranda akamwambia, “nakuja!” Kisha akakata mawasiliano. Marwa akahisi umeme utakata muda si mrefu. Akatazama taa akihesabu muda na akiwaza ni nini Miranda anapanga kichwani.
Ikapita dakika kama tatu, Miranda akawa amefika hapo. Akamwambia Marwa, “tulia, muda si mrefu, ntakwambia cha kufanya!”
Basi wakatulia hapo, muda si mrefu taa zikaanza kufinyafinya. Wale walinzi wakatazama na kuanza kuulizana. Taa zikazidi kufinyafinya maradufu. Miranda akamtazama Marwa na kumtaka avae miwani yake ya kiza kisha akamkabidhi pini nyembamba na kumpa maelekezo mafupi ya kueleweka juu ya kitu cha kufanya.
Marwa alipokwisha fanya hivyo tu, taa zote zikazima baada ya mlio mkubwa wa mlipuko. Kukawa kumejawa na kimuhemuhe. Walinzi wale wakatazamana na kisha upesi wakakimbilia kule kwenye mlipuko wakimwacha mlinzi mmoja pale eneoni.
Na kwakuwa kulikuwa ni kiza na vishindo vya watu vilikuwa vinasikika huku na kule, basi Miranda na Marwa wakasonga eneo la maabara pasipo kugutukiwa upesi. Wakamfikia yule mlinzi, Marwa akakimbilia mlangoni wakati Miranda akimkabili yule bwana mlinzi.
Hakupoteza naye muda, mitupo yake mitatu ikamlaza mwanaume chali. Anavuja damu. Na pasipo kupoteza muda, akamburuza mwanaume huyo mpaka mlangoni. Marwa alikuwa tayari ameshaufungua mlango. Wakamzamisha ndani kisha wakafunga mlango.
Haraka Miranda akamweleza fomula ya kemia wanayohitaji kuitazama maabarani humo. Na basi upesi wakaanza kusaka fomula hiyo huku na kule. Maabara ilikuwa imeshona kwa kujaa vitu lukuki hivyo kazi haikuwa nyepesi kutazama huku na kule kutafuta kitu kimoja.
Wakachoma dakika mbili … tatu … nne … tano … mpaka kumi na tano, hakuna kitu walipata. Mpaka wakaanza kusikia sauti za walinzi wakisongamana huko nje.
Huko nje walikuwa wamefika walinzi watatu wakiwa wamebebelea kurunzi kubwa mikononi kupambana na kiza. Walinzi hao wakasimama hapo mbele, mmoja akapanda kibaraza na kutupa miale ya kurunzi ndani ya dirisha la maabara. Akalipeleka kushoto na kulia. Hakuona kitu.
Miranda na Marwa walikuwa wamejihifadhi chini ya meza wakiwa wamefunikwa na mizigo kadhaa. Wakangoja hapo, kurunzi likapita. Walipoona salama, wakanyanyuka na kuendelea na msako wao walioufanya kimya kimya.
Ikapita dakika tano, Miranda akaona kitu ndani ya chupa ndogo aina ya ‘test tube’. Kutazama vema, akaona kuna seti hapo za chupa hizo zikiwa na vimiminika rangi ya ‘pinki’ iliyopauka.
Uzuri alikuwa ni mtu mwenye ujuzi na mambo ya kemikali. Si tu kuwa alisomea mambo hayo darasani akiwa na diploma, bali pia aliyafanyia kazi kwa muda mrefu akiwa na bwana BC.
Akanong’ona, “Marwa, nahisi ndiyo hizi.” Marwa akatazama na kuuliza, “mbona haina badge?”
“Ndio, ila hii ndiyo rangi yake,” Miranda akasema kwa uhakika kisha akageuza begi lake na kutoa vizibo vidogo vya mpira, akaziba midomo ya test tube kisha akatia seti hiyo begini na kuweka begi mgongoni.
“Tuondoke,” Miranda akamsihi Marwa.
“Tunapitia wapi?”
Miranda akasimama kidogo na kuangaza nje. Wasingeweza kupitia pale mlangoni. Basi akamwambia Marwa watumie dirisha maana ndiyo njia pekee iliyobakia.
Kabla Mara hajatia neno, mara Miranda akatambaa kama mende kufuata dirisha la kusini, mbali kabisana mlango. Alipofika hapo, akajaribu kufungua dirisha hilo. Akagundua lipo ‘sild’, basi akafungua begi lake kwa mkono hata asitazame. Akapapasapapasa na kutoka na chuma fulani kilichojichanua kama mbawa za ‘helikopta’.
Akakinasisha pale dirishani, kisha akaanza kunyongorota mashine ndogo iliyo nyuma ya mbawa hizo. Basi hicho kifaa kikanguruma kidogo, Miranda akatoa mikono upesi, basi zile mbawa za kifaa hicho zikainama na kukuta kioo. Zikazunguka upesi na kabla hazijamaliza kutengeneza tundu, Miranda akakizima na kukinyofoa.
Akamtazama Marwa na kumpa ishara asogee. Marwa akatii. Ila akamuuliza kuhusu kile kioo. Hakitatoa sauti wakashtukiwa?
Miranda akatikisa kichwa, kisha akampatia kidude kidogo chekundu alichokitoa mfukoni, na kumwambia, “utakibonyeza ikifika tatu. Sawa?”
Marwa akapokea agizo. Moja … mbili … tatu! Marwa akabonyeza kitufe hicho na hapohapo ikasikika sauti kubwa ya mlipuko. Sauti hiyo kuja kuzima tayari Miranda alishadondosha dirisha zima, wakatoka!
Sauti za watu zikarindima huku na huko. Watu wakawa wanapishana ama kusimamishana wakijiuliza nini kinatokea humo. Kulizuka hali ya taharuki, na ukizingatia bado mwanga haukuwa umerudi.
Basi Miranda na Marwa wakatumia fursa hiyo kufika kwenye uzio, wakanyaka na kujitupia nje baada ya Miranda kufanya kazi yake ya kukata nyaya za umeme. Miranda alitua chini katika namna ambayo alihakiki hakuna kitu kitakachovunjika begini. Mkono wake wa kushoto ulishikilia begi akitua kwa kishindo.
Ila kabla hawajanyanyuka na kuhepa, Miranda akamtaka Marwa atulie hapohapo tuli, la sivyo wangeharibu chakula mwishoni.
“Shhhhhh!!!” Miranda akampa ishara kisha akakagua eneo zima kwa macho yake mepesi.
Wakiwa wametulia hapo kwa muda kidogo, wakaona watu kwa mbali wakiwa wanasonga kuzama ndani ya uzio. Na pale getini palikuwa na hekaheka.
Basi Miranda akamtaka Marwa wabadili njia, nao hawakwenda mbele bali wakarudi nyuma na kufumbukia njia huko. Baada ya muda wa dakika nane, wakawa wamelifikia gari lao. Wakapanda na kulitia moto upesi.
Hapo Miranda akatabasamu na kucheka. Walikuwa wamekamilisha kazi yao. Hata moyo wake ukawa wa baridi sasa na Marwa akalaza kichwa chake kwenye kiti akitabasamu. Alihisi ametua mzito wa toni kadhaa kichwani. Haikuwa kazi nyepesi hata kidogo.
Ila kabla hawajaikuta barabara kuu, mara risasi tatu zikalia! Pah! – pah! – pah! Kioo cha nyuma cha gari kikapasuka na kuwa unga.
Wakawehuka. Kumbe walikuwa wanafuatiliwa! Nyuma yao kulikuwa kuna gari jeusi, Toyota Harrier, imeshusha vioo vya madirisha ya nyuma.
Miranda akamtazama Marwa. Hawakuongea kitu. Kumbe walikuwa wamekosea sana. Vita bado haikuwa imeisha. Bado refa hakuwa amepuliza kipyenga cha kuhitimisha mchezo.
Sasa hapo wakawa na zoezi la kukabili lile gari ambalo ndani yake hawakuwa wanajua wapo watu wangapi.
“Marwa,” Miranda akaita. “Inabidi tuwamalize hawa watu wote. Endapo tukiwatorola ila tukawaacha salama, itakuwa rahisi kutufuatilia na kutujua. Wameshalijua gari letu.”
Marwa akataka kuuliza watawamalizaje, ila akaamua tu kunyamazama. Pengine Miranda alikuwa ameshapanga namna ya kufanya. Akawaza.
Na ni kweli, mwanamke huyo alikuwa tayari ameshayapanga yake kichwani. Alihakikisha hajai kwenye macho na tageti ya adui, na baada ya muda fulani akamwambia Marwa, “shika usukani!”
Hakurudia mara mbili, akachumpa kwenda nyuma ya gari. Haraka Marwa akalazimika kuudaka usukani na kusonga hapo kwenye kiti cha dereva kwa tahadhari.
Risasi zikarushwa tena. Zikabangua gari kando na kando. Marwa akawehuka kwa uoga. Akayumbisha gari huku na huko. Ila akamudu na kuliweka sawa tena. Mwendo ulikuwa mkubwa sana.
Akatazama kwenye ‘sight mirror’, akamwona Miranda amelala kochini. Hakujua mwanamke huyo anafanya nini maana hakuwa na muda wa kubakiza macho kiooni.
Baada ya muda kidogo, Miranda akanyanyuka toka kitini, akachungulia kutazama gari linalowafuata. Kisha akarudi tena chini. Sauti ya kukoki bundiki ikaita. Na mara kidogo akanyanyuka na kuchomoa mikono yake nje ya gari kwa kupitia uwazi uliosababishwa na kioo kuvunjwa.
Mikononi alikuwa amebebelea bunduki fupi, kama vile ‘sub-machine gun’ ila hizi zilikuwa fupi zaidi, zimechomekwa risasi pomoni.
Basi akaelekezea mikono yake katika lile gari liwafuatalo na kilichofuatia hapo kikawa kufuru. Alimwaga ‘njugu’ kama mvua ya masika. Alichokuwa anakifanya ni kupeleka mikono kushoto, kulia. Kulia, kushoto.
Risasi zikatoka pasipo kupumzisha koo la bunduki. zikachakaza kioo cha gari lile linalowafuata. Zikachomoa uhai wa dereva na mtu aliyekaa naye mbele mara moja wasiombe hata maji!
Gari likayumba. Likayeya. Mara likapiga kona ya ghafla na kubinuka, likabiringita mara ya kwanza, ya pili, ya tatu, juu kukawa chini!
Matairi yalizunguka na kukoma. Punde ndani ya gari ikasikika sauti ya mwanaume akikohoa. Kisha akaguguma kidogo kwa maumivu aliyokuwa anayapata. Si kwamba yalikuwa madogo, la hasha, mbavu zilikuwa zimembana. Anachuruza damu. Amevunjikavunjika kuanzia kiunoni kushuka chini.
Basi mara mlango wa gari hilo ukasukumwa kwanguvu, akatoka mwanaume aliyekuwa amechafuka damu kichwani. Akajivuta na mikono kutoka ndani ya gari. Akatoa mwili mpaka kiuno, kisha akalala hapo akiwa hoi!
Alilalama sana kwa maumivu makali. Hata kuhema ilikuwa tabu. Alikuwa ndiye mtu pekee aliyesalia kwenye ajali hiyo. Wenzake wote walikuwa wameshakata kauli.
Akiwa hapo chini, anagugumia, mara akasikia kishindo cha miguu kikimsongea. Akajikakamua na kunong’ona, “nisaidieee …”
Mara kishindo cha miguu kikakomea mbele ya kichwa chake. Kutazama akaona kiatu kirefu cha kike, rangi nyeusi. Akakazana kurusha macho yake kutazama juu. Hakuona vema, ila akapata kutambua ni mwanamke waliyekuwa wanamkimbiza. Bunduki yake bado ilikuwa inanuka moto.
“Nisa ….”
Hajamalizia kauli, akala risasi tano za kichwa! Sina haja ya kusema kuwa alikufa papo hapo maana unajua kilichotokea. Damu zikamwagika kutengeneza kadimbwi.
Miranda akachuchumaa na tazama ndani ya gari, akaona kimya. Hama dalili ya uhai. Basi akaondoka zake akirusha miguu upesi.
Ila hakuridhika. Pengine mule ndani kunaweza kukawa na watu waliopoteza fahamu tu na si maisha. Basi alipokaribia gari lake, akatema tena risasi kadhaa kulenga uvungu wa gari, mara chombo kikalipuka.
Wakayeya upesi.
Kukawa kimya ndani ya gari kwa muda wa dakika kumi na, hakuna mtu aliyemwongelesha mwenzake. Ni kama vile walikuwa wanawaza na kuchambua kilichotoka kutokea. Na kama vile bado hawakuwa wanamini kama kazi imekwisha.
Walifika kwenye makutano ya barabara, Marwa akatazama ‘sight mirror’ baada ya kusimamisha gari lao kupisha gari kubwa lililobebelea kontena kubwa rangi ya bluu.
Nyuma yao akaona daladala moja, costa, akashusha macho yake na kumtazama Miranda aliyekuwa amejilaza kitini. Alikuwa anatazama nje akiwaza jambo.
Hakumwongelesha. Ila baada ya kukanyaga mafuta na kuondoa chombo baada ya gari lile kubwa kukatiza, akamwita mwanamke huyo na kumwambia, “You were amazing! Really amazing! I didn’t expect … oh God!” Marwa akatikisa kichwa na kumalizia, “Nifundishe na mimi!”
Miranda akatabasamu. Akaguna puani asiseme kitu. Wakafika nyumbani. Miranda akaweka ile set ya test tube mezani.
“Vipi anaendeleaje?” Marwa akamuuliza dada wa kazi akionyeshea kichwa chake kule chumbani alazwapo Jona.
“Nahisi yupo sawa,” dada akajibu.
“Hauna uhakika. Hukwenda kumtazama?” Marwa akauliza. Dada akapandisha mabega. “Nilienda kumtazama jioni. Sasa kila nikimtazama naona tu yu vilevile. Sijamtazama tena mpaka muda huu!”
Marwa akatazamana na Miranda kisha akaelekea chumbani kumwona Jona. Mwanaume huyo alikuwa amekaa vilevile kama alivyomuacha. Akamshika mkono na kumwita. Hakuitika. Ila hakujali, akamtazama kidogo alafu akatabasamu na kusema, “Nimerudi, Jona. Tumefanikiwa kupata antidote.”
Akatabasamu zaidi, na kuendelea kunena kwa sauti ya chini, “haikuwa rahisi hata kidogo. Miranda alikuwa so magnificient. Siamini hata kama sasa nipo na wewe. Nilijua sitakuona tena, ila Mungu si Athumani …” akanyamaza kidogo. Kuna kitu kilikaba koo lake. Akajaribu kumeza mate kisha akaendelea kunena, “… Mungu ana makusudi nawe. Ana makusudi na sisi. Muda si mrefu utaacha kitanda na mikono yako itafanya kazi iliyozoea.”
Aliposema hayo, akamtazama tena Jona kwa muda kidogo kisha akamuaga. Ila kabla hajatoka ndani ya chumba, akasikia sauti ya Miranda huko sebuleni. Alikuwa anaongea na simu.
Basi akatoka na mpaka kufika sebuleni akamkuta mwanamke huyo ameshamalizana kuteta na simu. Akaketi na kumtazama. Alikuwa ana uso wa mafikirio. Akamuuliza, “vipi kila kifu kipo sawa?”
Miranda akashusha pumzi alafu akasema, “nimetoka kuongea na BC. Nimemwelezea kuhusu hii chemical. You know what? Amesema si yenyewe …”
Marwa akahisi baridi la ghafla limempitia. Koo limemkauka. Na joints zote za mwili zimeishiwa nguvu.
Akatoa macho. Ila kabla hajanena, Miranda akamwambia, “ngoja kwanza …”
*** Miranda akanyanyuka akishika kiuno chake. Akang’ata kidole akifikiria. Kisha akamtazama tena Marwa na kumwambia.
“I know it can’t be!” Akatikisa kichwa. “It can’t be kabisa! Lazima hii iwe yenyewe.”
Alikuwa kama mtu aliyewehuka, na Marwa aliogopa kumwongelesha. Akabaki anamtazama aone ataishia wapi. Ila na yeye alikuwa amegawanyika nafsi.
Alikuwa amejihisi mtupu kabisa. Akifikiria shurba alizopita, tundu la sindano, kisha kazi ikawa bure, anachoka kabisa. Alitamani alie, ila hapana. Hata macho yalikuwa makavu.
Miranda akaketi kitini. Akashika kichwa. Akatazama zile seti pale mezani kisha akainamisha tena kichwa chini. Hapa Marwa akatambua mwanamke huyu alikuwa ana roho ngumu.
Haki ingekuwa ni mwanamke mwingine, angeweza kujaza ndoo kwa machozi. Angekuwa tayari ameshanyofoanyofoa nywele zake akisaga meno.
Pengine alikuwa anaugulia kwa ndani, ila kitendo cha kuweza kubakiza gulio hilo kifuani asilitoe, bado kulimfanya Marwa ashangae.
“Sasa tunafanya nini?” Marwa akauliza.
Miranda akashusha pumzi na kukodoa macho. Akaminya lips zake kama apendavyo, alafu akasema kwa sauti ya chini, “tungoje, labda akiziona anaweza kubadili mawazo.”
“Una maanisha BC?” Marwa akauliza. Miranda akatikisa kichwa na kujibu kifupi, “yah!”
Kukawa kimya kidogo. Punde Miranda akamuita dada wa kazi na kumuagiza amletee maji ya kunywa. Haraka dada huyo akatii agizo, akamletea Miranda jagi kubwa la kioo na glasi kwa pembeni.
Miranda akafakamia glasi mbili kwa mpigo kana kwamba kilevi, wakati huo Marwa akiwa anamtazama. Angalau akahisi ahueni kifuani mwake.
Marwa akasafisha koo na kumwambia, “pole. I know how you feel.”
Miranda akatanua lips zake kama mtu anayetabasamu, hakusema kitu.
“Natumai ile kazi uliyoifanya haitakuwa bure. Naomba Mungu iwe hivyo. Unastahili pongezi sana, ila si bahati kuna muda dunia huwa katili … si kila saa ipo fair. Na tukio lile linaweza kupita ila kwangu litaacha nyayo maishani mwangu yote. Sitalisahau.
Si tu kwamba niliona ulivyo mkufunzi kwenye sanaa za mapambano, bali namna ulivyokuwa unahangaika kumrudishia uhai mtu aliye hoi kitandani. It was remarkable!”
Miranda akaguguma na kusema, “ingekuwa remarkable kama ningefanikiwa. All of that was useless!”
Kisha akanyanyuka na kwenda zake chumbani. Marwa akabaki peke yake. Akatazama yale maji kwenye jagi kwa sekunde kadhaa kisha akayavuta upande wake.
Ikapita kama dakika tano. Mara akasikia vishindo vya miguu koridoni. Kutazama akamwona Miranda akiwa amevalia taulo kifuani. Uso wake ulikuwa ‘fixed’.
Akaita, “Marwa.” Kisha akaongezea akinena kwa sauti ya chini, “Thanks kwa compliments. Nisamehe kwa maneno yangu.”
Kwa namna moja ama nyingine Miranda alikuwa amejiskia vibaya kumsemesha Marwa vile. Roho ilimsuta.
Marwa akajibu kwa tabasamu lile nesi ampalo mgonjwa. Miranda akaenda zake na ndani ya muda mfupi Marwa akasikia mtu akijimwagia maji kwa ‘shower’, naye akaamua kumwagia maji ndani ya mwili wake.
Akakaa hapo sebuleni kwa muda mpaka akaanza kusinzia. Kwa mujibu wa saa ya ukutani, ilikuwa ni saa tisa usiku.
Hakujua alikurupushwa na nini, akaamka na kuangaza kisha akajikokota kwenda chumbani alipolazwa Jona, akajimwaga kwa pembeni ya mgonjwa huyo na kuanza kujiongelesha mwenyewe.
“I am sorry, Jona … I am so sorry … bado hatujafanikisha … hatujafanikiwa.”
Hakunena tena jingine usingizi mzito ukambeba pasi na huruma. Akakoroma kwa uchovu.
** “Marwa!” Sauti iliita. Haikuwa sauti ya kike bali ya kiume. Kabla hajaitika, akajaribu kuifikiria ni sauti ya nani, akakosa jibu.
Ikajirudia tena, “Marwa, amka! … Marwa!”
Mara hii alipofikiria kuhusu hii sauti, akagutuka baada ya kupata majibu. Ilikuwa ni sauti ya Jona! … hapana! … akakataa … akatega sikio asikie tena kuhakiki.
“Marwa!” Sauti ikaita tena. “Marwa!” Ikarudia kuita. Na hapa Marwa akapata kweli uhakika wa kile alichokiwaza. Kweli ilikuwa ni ya Jona.
Basi kichwa chake kilikuwa kizito sana. Alikuwa bado ana usingizi pomoni kichwani. Ila akapambana kukinyanyua na kufungua macho aone amwitaye.
Hakuona mtu! Kutazama kando, Jona alikuwa yupo vilevile kama alivyomuacha. Amelala. Dirisha lilikuwa jeupe kuashiria pamekucha.
Sasa nani alikuwa akiniita? Akawaza. Punde akapata jibu.
“Marwaa!” Sauti iliita mlangoni. Na sauti hii akaitambua kuwa ni ya Miranda, na si Jona kama alivyokuwa anasikia! Akasonya na kujibandua kitandani. Akaendea mlango.
“He! Ulikuwa umelala au umekufa?” Miranda akauliza akistaajabu. Alikuwa amevalia gauni refu jeusi lililobana kifua na kumwaga chini. Nywele zake alikuwa amezifichama ndani ya mfuko fulani wa nailoni.
“Sorry, yani nlikuwa usingizini kweli,” Marwa akajitetea.
“Na mbona ukalala huko kwa mgonjwa badala ya chumba chako?”
“Aaahm! Unajua nilizidiwa na usingizi, hata huko chumbani nikaona mbali kufika.”
Miranda akaguna, kisha akamwambia ajiandae kwani BC amefika. Itakuwa vema wakiwa wote. Basi Marwa akaenda kuoga na kuosha uso kisha akajivuta sebuleni. Ila usingizi bado ulikuwa unamsumbua. Macho yalikuwa mekundu. Na kichwa kizito sana.
Alipotazama saa ya ukutani, akaona ni saa nne kasoro asubuhi. Akastaajabu. Si bure Miranda alimuuliza kama amelala ama amekufa.
Sebuleni alikuwa ameketi BC ndani ya suti ya kijivu na kando yake aliketi Miranda. Mwanamke huyo hakuonyesha dalili ya kuwa na hata lepe la usingizi, hali hii ilimshangaza kidogo Marwa ukizingatia muda waliolala. Ila hakuwa na muda wa kujiuliza sana.
Mezani kulikuwa kuna seti ya zile test tube Miranda alizozikwapua toka maabara ya Sheng, kwa hivyo ilikuwa rahisi kubashiri mada mezani ilikuwa ni hizo kemikali.
“They are not the one,” (sio zenyewe,) BC alinena akimtazama Marwa. Ilionekana alishateta tayari na Miranda hapo kabla.
“It seems Sheng did not want to risk. And perhaps, the antidote is not there at all, or it wasnt brought as we thought. But …” (inaonekana Sheng hakutaka kujiweka hatari. Na pengine, antidote haipo kule kabisa, au haikuletwa kama tulivyowaza. Lakini …)
Bwana huyu mzungu akaweka kituo, kisha akakunja nne na kuumwaga mgongo wake kwenye ukuta wa kiti.
“… In one way or the other, this may be our starting point.” (… kwa namna moja ama nyingine, hili linaweza kuwa kianzio chetu.)
Japo Marwa alikuwa na usingizi kichwani, hakupepesa macho hata kidogo. Alisimamisha masikio yake na kujaribu kukaza macho. Pengine kumsikiliza mzungu akiongea kunahitaji juhudi za ziada kusikia kila analolitamka kwasababu ya ung’ataji wao wa maneno.
“Though this is not the antidote we want, it can act as a great ingredient we need to make one … the real one.” (Japo hii si antidote tunayoihitaji, inaweza kutumika kama kiungo kikubwa tunachokihitaji kutengeneza yenyewe. Ile ya ukweli.)
Hapa Marwa akajikuta anatabasamu. Hatimaye ile kazi haikuwa bure, akawaza. Ila kama kuna kitu hakuwa anakijua ni kuwa ndiyo kwanza kazi ilikuwa inaanza! Maana walitakiwa kupata viungo vingine viwili kutimiza antidote inayohitajika kumtibu Jona.
“So you mean we have to go there again?” (Kwahiyo unamaanisha inabidi turudi tena kule?) Marwa akauliza akiwa na uso wa hofu.
BC akatikisa kichwa na kusema, “No! Maybe it’s somewhere more dangerous than there.” (Hapana! Labda ni mahali hatari zaidi kuliko kule.)
Marwa akamaliza mate.
“Where is it?” (Ni wapi huko?) Akauliza.
BC akatazamana na Miranda.
Kisha wakacheka. Miranda akamtoa hofu Marwa.
“Anakutania tu. Kuna mahali panapotisha kuliko pa Sheng?”
“Ni wapi huko anasemea?” Marwa akauliza kwa uso ‘serious’. Miranda akatasabamu kwanza, kisha akamwambia, “ni MSD. Medical Store Department.”
“Ghala la dawa la serikali?” Marwa akatahamaki.
“Ndio,” Miranda akamjibu. “Huko ndiko tutapata mojawapo ya dawa tunayoihitaji ili tuichanganye na hii kumtibu Jona.”
Marwa akatulia. Napo haikuwa rahisi.
“Kama tusipofanikiwa kukipata hiko kitu, basi mambo yatakuwa magumu zaidi. Itatulazimu twende ughaibuni.”
“Leo usiku,” Miranda akamjibu. “Hatuna muda wa kupoteza, Marwa. Unaona hali ya Jona ilivyo. Sio?”
Marwa akaafiki. Wakateta kidogo, baada ya muda wakarudi tena kwenye mada yao, mara hii BC akiongea kwa msisitizo.
Akasema punde dawa hiyo atakapoitengeneza, basi ataitoa kwa awamu na kwa masharti. Anataka kujua kama Jona atakuwa upande wake ama lah! Anahofia kuhangaika ‘for nothing’.
“You two must make sure, he allies. It is the only thing I can afford to hear.” (Ninyi wawili lazima mhakikishe, anashirikiana. Ni kitu pekee ninachotaka kukisikia.)
Miranda akatazamana na Marwa, kisha akarudisha uso wake kwa BC. Akamhakikishia kila jambo litaenda sawa. Hakuna la kutilia shaka. Kwa sasa wazingatie kumkomboa Jona, na kila kijacho kitaangukia panapostahili.
BC akaafiki akitoa onyo. Hakukaa tena sana, akaaga na kwenda zake.
**
“Chai ipo tayari, nakwambia kwa mara nyingine. N’kuletee?” Akauliza Kinoo kwa uso wa kughafirika. Macho yake yalikuwa yanamtazama Sarah aliyejilaza kitandani.
Ni robo saa sasa tangu amwambia mwanamke huyo kuwa chai ipo mezani, na wala hajasogeza msuli wake hata mmoja. Chai inaelekea kupoa sasa ingali iliandaliwa kwa haraka baada ya mwanamke huyo kulalama njaa.
“Nimeshakusikia,” Sarah akajibu kwa kujivuta. Na badala ya kuamka aende, akajigeuzia upande wa pili.
Kinoo akatikisa kichwa. Kifuani mwake alijawa na hasira. Aliondoka akaenda zake sebuleni alipoketi na kutazama chai iliyokuwepo mezani. Chapati, mayai manne ya kuchemshwa, soseji tatu, chai ya maziwa.
Kikombe cha chai hakikuwa kikifuka moshi tena.
Akasonya. “Tabu zingine bana,” akalalama. Akashika tama akiendelea kungoja. Alichoshwa na hizi kero za mwanamke wake, ila hakuweza kuchukua hatua hata moja.
Lakini cha ziada, hakujua Sarah anateswa pia na msongo wa mawazo juu ya dada yake, Sasha. Alikuwa yu njia panda ya kuchagua aidha asimame na ndugu yake wa damu ama mpenzi, baba wa mtoto wake. Mambo haya yalikuwa magumu. Na hakuweza kuomba ushauri.
Baada ya muda kusonga, mtu hatoki chumbani, Kinoo akakomba vitu vyake mezani na kuvipeleka jikoni. Akavitumbukiza ndani ya ‘microwave’ na kuvipasha huku chai akiinywa kama maji.
Baada ya dakika kadhaa, akavitoa na chai akamimina nyingine, ya moto, alafu akaongozana na vyakula hivyo, vikiwa kwenye trey, mpaka chumbani. Akaviweka kando ya Sarah na kumtaka aamke ale.
“Kinoo, sijisikii kula.”
“Unamaana gani hujisikii kula?”
“Nahisi tumbo limejaa.”
“Kwa kitu gani na hujala?”
Sarah akanyanyuka na kuketi kitako. Akamtazama Kinoo.
“Muda si mrefu nitakuwa na ugeni. Sasha anakuja. Nadhani nitakula naye.”
Kabla Kinoo hajafunua mdomo wake, hodi ikagongwa huko nje. Wakatazamana na Sarah kisha asiongee kitu, akanyanyuka kuendea mlangoni. Alikuwa ni Sasha. Alivalia blauzi ya zambarau na suruali ya jeans rangi ya bluu iliyokolea rangi.
Akamsalimu na kumkaribisha ndani. Akaketi sebuleni. Punde Sarah akatoka chumbani na kukutana naye. Walikumbatiana na muda si mrefu wakajumuika kwenye kunywa chai.
Kinoo akawapa faragha kwa kuaga anaenda dukani.
“Anakujali sana unh?” Sasha aliuliza kimbea punde Kinoo alipofunga mlango na kupiga hatua kama nne hivi akijiendea.
Sarah akatabasamu na kuguna. “Kwakweli. Namchosha sana. Ila huu ndiyo muda wa kumsumbua.”
Wakacheka.
“Hongera sana,” Sasha akampongeza. “Wenzako hawapati bahati kama hii!”
Wakateta maongezi hayo kwa muda wa kama dakika tatu, kisha Sasha akaanza kuelekea kwenye lengo lililomleta hapo.
“Vipi? Mmefikia wapi kwenye lile swala? Jamaa amefanikisha?”
“Hapana,” Sarah akajibu akitikisa kichwa. “Ameniambia mazingira bado hayajatulia.”
“Mazingira yapi hayo?”
“Sasha, sifahamu. Muda mwingine akinijibu kama hivyo, nashindwa kuendelea kuuliza sana.”
“Hapana, Sarah!” Sasha akapiga kofi paja lake la kulia. “Unajua nakutegemea wewe. Unataka nife, eti? Upo kwenye nafasi nzuri sana ya kumshawishi. Najua hatotaka kukuudhi ukiwa kwenye hali kama hii.”
Sarah akatikisa kichwa. “Unajua si kazi nyepesi kabisa, sister. Inabidi ufahamu kuwa nikimuuliza sana ama kumshawishi sana, anaweza akahisi kuna jambo. Hufikirii hilo?”
“Hamna. Unatumia tu akili, Sarah. Laiti, kama isingelikuwa kule makaoni kuna jambo wanalishughulikia kwa sasa, nisingelikuwa hai. Wangeshanimaliza maana muda wangu wa kufanya nililoagizwa, umeshakwisha.”
Sasha akamshika mkono Sarah.
“Maisha yangu yapo mikononi mwako. Know that. Wewe niingize tu nami nitajua namna ya kuenenda … na na kuhusu Kinoo, nitafanya kadiri ya uwezo wangu kumweka salama.”
Mara mlango ukafunguliwa akaingia Kinoo. Wakashtuka, ila hawakuteta. Kinoo akapitiliza kwenda chumbani.
“Unadhani anaweza akawa amesikia?” Sarah akauliza akinong’ona.
“Hapana,” Sasha akajibu. “Tulikuwa tunaongea kwa sauti ya chini. Hawezi akawa amesikia.”
“Una uhakika?”
“Ndio. Sasa mimi naomba niondoke, tutawasiliana baadae. Ila nakuachia kazi moja, unajua hatujamaliza maongezi yetu, ila hatuna budi kuyakatisha. Mpeleleze na unambie ni nini sasa hivi wanahangaika nacho?”
“Unamaanisha nini?”
Sasha akatazama mlango wa chumbani kisha akarudisha macho yake kwa dadaye.
“Nataka kujua wanahangaikia kitu gani sasa hivi. Lazima kitakuwapo, kimoja ama viwili. Ukivijua, nijuze upesi. Sawa?”
Sarah hakujibu, Sasha akasimama na kusema kwa sauti. “Niitie basi shemeji nimuage!”
Sarah akapaza sauti kumwita Kinoo, akafika na Sasha akamuaga, akaenda zake.
“Sarah,” Kinoo akaita muda mfupi baada ya kuketi kitini wakitoka kumsindikiza Sasha. Sarah moyo ukampwita. Alihofu.
“Kuna kitu unanificha?” Kinoo akauliza. Moyo wa Sarah ukazidi kwenda mbio. Vidole vyake navyo vilianza kutetemeka.
Kinoo akamtazama Sarah ndani ya kiini cha macho yake kwa sekunde tano asiseme jambo, kisha akanyanyuka na kwenda zake chumbani. Akamwacha Sarah akiwa na mawazo lukuki kichwani.
Akahisi pengine mwanaume huyo amesikia kile walichokuwa wanaongea. Habari hiyo ikamtisha. Ikamfanya ahofie hata kwenda huko chumbani kukutana naye.
**
Saa tatu usiku …
“Hatuna muda wa kuzubaisha mambo,” alisema Miranda. Walikuwa ndani ya gari pamoja na Marwa. Gari hili lilikuwa dogo, Toyota IST rangi nyeusi.
“Tunachotakiwa kukifanya ni kufika hapa,” akaonyeshea kidole kwenye ramani kubwa aliyoiweka mapajani. “Tutapita njia hii, ni fupi zaidi. Walinzi wapo wanne tu, na hupendelea kukaa maeneo haya …” Miranda akaonyeshea kidole maeneo matatu kwenye ramani.
“Na kama ikitokea dharura, basi tutatokea kwa njia ya huku kusini. Ni njia ndefu, ila ina uhakika wa kutoka nje baada ya kukwea makontena yaliyokaribu na kuta.”
Kabla hawajatoka, wakavalia barakoa kuficha sura.
Lakini waliposonga muda mchache baada ya kutoka kwenye gari waliloliegesha umbali wa kilomita kadhaa toka eneo la tukio, mara likafika gari moja lililotembea kwa mwendo mdogo na kukoma. Halikuwa limewashwa taa.
Gari hili lilikuwa ni Nissan Patrol rangi nyeupe. Vioo vyake vilikuwa vyeusi usiweze kuona ndani. Punde gari hilo likazimwa na mwanaume mmoja akatoka ndani.
Akalisogelea lile gari lililowaleta Miranda na Marwa.
**
Akalikagua na kisha akarudi kwenye ile Nissan Patrol waliyokuja nayo. Ndani ya muda mfupi wakashuka wanaume wanne, wote walikuwa wamevalia nguo nyeusi kuanzia juu mpaka chini. Nyuso zao hazikuwa za kuvutia, bali kutisha.
Walikuwa na miili mipana wakionyesha waja wa shari. Na wasiwe na papara, wakaegemea gari lao na kungoja kwanza muda. Mmoja wao, ambaye alikuwa dereva, akatoa simu mfukoni na kupiga.
Ikaita mara mbili kabla haijapokelewa.
“Yes, boss. Tumewakuta … ndio, sawa … tutahakikisha hatufanyi makosa.”
Kisha akakata simu na kuidumbukiza mfukoni. Alikuwa ni nani huyo aliyeongea naye? Najua bila shaka unadhani ni Sheng. Hujakosea. Ndiye yeye, lakini alijuaje ‘move’ hii ya Miranda na BC?
Turudi nyuma kidogo, si mbali sana, bali usiku wa kuamkia leo.
Baada ya taarifa kufika kwake kuwa wamevamiwa, watu kadhaa wameuawa na pia kusababisha hasara kubwa, Sheng hakufurahishwa kabisa na hili. Alikuwa mwekundu kwa hasira, na kwa mkono wake wa kulia akawamiminia risasi wanaume kumi waliokuwa wanahusika na lindo.
Ilikuwa awamalizs wote ila jamaa yake akamsihi asifanye hivyo maana itakuwa hasira ya samaki kujitumbukiza mtegoni. Atamaliza nguvu kazi ambayo bado ingemea matunda.
Lakini haikuwa rahisi hata kidogo kwa Sheng kuwabakizia uhai. Ilibidi mawazo mbadaka yatumike kumshawishi kwamba bado adui anaweza kutiwa mkononi. Hajatokomea kama alivyowaza.
Kwa kuwa, maadui hao waliowavamia waliiba chemical ndani ya maabara basi ni wazi watakuwa washirika wa Jona wakihaha kumtafutia ahueni. Kwahiyo, moja, Jona yu hai.
Na basi kama watu hao watakuwa wana ujuzi wa kemia, watatambua kuwa chemical waliyoichukua, haitakuwa suluhisho, bali kipande chake. Kwa hivyo, watataka kukamilisha antidote. Hapo watatafuta kipande kilichokosekana.
Na kwa mawazo ya haraka, sehemu ya kuipata ni MSD. Watege hapo, watawakamata wahitaji wao. Watu waliowatia hasara kubwa. Watu watakaowasaidia kumpata Jona na kummaliza ‘for good’.
Ila likatoka onyo toka kwenye kinywa cha Sheng. Kama mpango huo hautafanikiwa, kama mpango huo hautamea matunda, basi atamwaga damu za wale wote aliotaka kuwamaliza pasi na simile.
Hivyo, ndiye wewe uliyetumwa hapa kuhakikisha unafanikisha kazi, ukitambua kuwa roho yako ipo rehani, utafanya mzaha?
“Itawachukua kama dakika tano tu kufika mahali wanapopataka,” alisema Dereva akitazama saa yake ya mkononi. “Kwa makadirio mepesi, baada ya dakika ishirini, inabidi tujiandae. Haijalishi watatokea wapi, ila lazima watarejea kwenye chombo chao cha usafiri.”
Huyo dereva aliponyamaza, alimtazama mmoja wa jamaa aliongozana nao, pasipo kusema neno, jamaa huyo akafungua mlango na kutoa begi jeusi, ndani yake akatoa kifaa fulani cheusi chenye umbo la duara.
Akasonga karibu na gari la wakina Miranda, akalala chini na kupachika kifaa hicho uvunguni. Alafu akakibonyeza tip! … tip! Ikasikika sauti kama ya kitu kinachozunguka kwa kasi, kisha ikanyamaza.
Jamaa huyo akanyanyuka na kurejea garini. Yule dereva akanyoosha mkono wake ndani ya gari, akatoa kifaa kipana mithili ya tablet. Akakibofya bofya mara tatu, mara kiooni ikaonekana ramani, na mahali pale palipokuwa gari la wakina Miranda.
Kumbe walikuwa wameliwekea ‘tracking chip’. Sasa hata gari hilo litakapoenda popote pale wataliona na kulifuatilia vema.
Ikapita muda kidogo wakakwea gari lao na kusogea mbali kidogo na hilo eneo.
**
Ndani ya Bohari …
Miranda akatoa ishara ya mkono, Marwa akasimama upesi akimtazama kwa umakini. Mwanamke huyo akachungulia, akaona mwanaume mmoja aliyevalia ovaroli la bluu na kofia, akikatiza.
Mwanaume huyo alipoyoyoma, Miranda akampa ishara Marwa, wakaendelea kutembea.
Majengo haya yanayohifadhi dawa, yalikuwa yamepangwa katika mistari kana kwamba bweni. Na kila jengo lilikuwa lina milango miwili, mmoja mbele, mmoja nyuma.
Miranda alikuwa anafahamu ni jengo gani wanaliendea, walishayavuka mawili, na lile moja kabla ya la mwisho ndilo alilokuwa analitaka.
Basi wakaendelea kunyata. Walikuwa makini maana si tu walinzi ndiyo waliokuwepo humo, bali pia na baadhi ya wafanyakazi, ambao wengi wao walikuwa wamevalia ovaroli na kinyago cha kuziba pua na mdomo.
Hawakuwa wengi, ila kikwazo kikubwa kilikuwa ni mataa yaliyokuwa yanamulika huku na kule. Mataa makubwa yenye nguvu ya mwanga.
“Tutaingia mule ndani,” alisema Miranda akinyooshea kidole jengo la mbele. “Nadhani unajua cha kufanya. Kama kawaida, hatuna muda wa kuchomesha!”
Miranda akachungulia tena, njia ilikuwa nyeupe, akachoropoka haraka akitembea asitoe kelele. Alipofika jengoni, akatazama nyuma. Alikuwa amemwacha Marwa. Upesi akampa ishara ya kumtaka aje.
Marwa akachungulia, kulikuwa shwari. Akatoka mbio, ila akiwa katikati, akajikwaa na kudondoka chini. Akaguna kwanguvu kwa maumivu maana alidondokea sakafuni.
Kishindo chake na sauti ya kugugumia, ikamshtua mmoja wa wafanyakazi wa Bohari aliyekuwa amesimama kwa mbali, akiwa kwenye bomba akinawa mikono yake.
Akatazama na kumwona Marwa akijinyanyua. Akapata shaka. Uso wa Marwa ulikuwa umefunikwa na barakoa. Na hata nguo alizokuwa amevaa, hazikuwa zile za walinzi wala wafanyakazi.
Basi akasonga karibu na lile jengo, akibeba kila tahadhari pamoja naye. Aliposimamisha masikio yake, akasikia lango likifunguliwa, na pia sauti ya watu wawili wakinong’ona.
Akapata shaka zaidi. Kwa hofu, asije jitia hatarini zaidi, akachomoka mpaka kwenye kibanda cha walinzi akatoa taarifa kuwa kule ameona wezi, wamevalia barakoa na nguo nyeusi. Wanazama ndani ya ghala pili toka mwisho!
Ndani ya kibanda hicho cha walinzi, kulikuwa kuna walinzi takribani watatu. Mmoja mwanamke. Mezani kwao kulikuwa kuna bunduki mbili kubwa kuukuu, daftari na virungu viwili.
“Wana silaha?” Akauliza mlinzi akitoa macho kana kwamba pera.
“Niliyemwona mikono yake ni tupu,” akasema yule mfanyakazi, na pasi kupoteza muda, wakatoka walinzi wawili waliobebelea silaha, wakaongozana na bwana yule aliyewaletea silaha.
Wakasonga mpaka eneoni.
Walipofika wakanyamaza na kutumikisha masikio yao. Hawakusikia jambo. Wakatazama mlango, ulikuwa umetenguliwa kufuli. Hapa wakaamini wamevamiwa.
Basi wakatumia mafunzo yao ya kijeshi, wakazama ndani ya jengo na kutanguliza midomo ya bunduki. Wakaangaza, hawakuona kitu!
“Wako wapi?” Akauliza mlinzi mmoja akipepesa macho yake makubwa.
Punde, wakasikia sauti huko nje, ya yule bwana aliyekuja kuwapasha habari,
“Wale kulee!”
Basi haraka wakatoka ndani na kwenda huko nje. Yule bwana akawaelekeza, kule mbali kwenye makontena. Ameona kitu huko. Basi walinzi wakakimbilia huko upesi.
Sekunde tano mbele …
“Twende,” sauti ya Miranda ikasema kwa kunong’ona. Kumbe hawakuwa kule ambako walidhaniwa wapo. Ulikuwa ni mtego. Walikuwa wapo nyuma ya jengo walilotoka kukwapua walichokifuata, na walitazama wale walinzi wanapoelekea.
Wakatoka hapo mafichoni, na haraka wakakimbia kwa muda wa sekunde kumi na tano, Miranda akadanda ukuta na kujivuta juu. Akamvuta pia na Marwa wakadondokea nje ya eneo la Bohari!
Hawakupoteza muda, wakaendea usafiri wao. Wakakwea na kutimka.
Sekunde kumi mbele …
Gizani ndani ya gari, kifaa kikawaka na kuonyesha ‘tracking chip’ ikiwa inatembea. Dereva akaguna puani. Kisha akasema,
“Wameshatoka.
Gari likawashwa na taratibu likaanza kusonga.
** Basi Miranda pamoja na Marwa wakiwa hawana habari yoyote, wakaswaga na chombo chao wakikata mitaa. Na sasa mioyo yao ikiwa misafi maana wameshakamilisha kazi.
Sasa walikuwa wanatazamia Jona apone, kisha arejee kwenye uwanja wa mapambano. Ni wazi walikuwa wanamhitaji. Ni wazi picha zake enzi za ‘uhai’ wake zilikuwa zinasumbua akili zao.
Basi kupunguza kuboreka ndani ya gari, Marwa akanyoosha mkono wake na kuwasha redio kisha akajilaza kitini akikonga moyo kwa nyimbo zilizokuwa zinarushwa.
Miranda akatabasamu, akamtazama mwanaume huyo na kumuuliza; “ni wapi unakumbuka?”
Redioni kulikuwa kunarushwa nyimbo za kale ya miaka ta themanini na tisini za mapema.
“Mbali sanaa!” Marwa akasema akitikisa kichwa. Na huku macho yake akiwa ameyafumba anasikiza muziki kwa hisia.
“Mbali wapi na wakati wewe ni wa juzi?” Miranda akatania. Marwa akaamka na kumkodolea macho.
“Wa juzi? Nani wa juzi?” Akauliza.
“Wewe ‘apo wa juzi. Unataka kubisha nini sasa?” Miranda akatamba. “Unamjua mwenye hii gari?”
Marwa akalaza kichwa kitini kisha akafumba macho akiendelea kula muziki.
“Si yule jamaa wako wa vibodi?”
Miranda akacheka. “Sasa huwezi amini yule ni mdogo wangu, tena wa pili!”
Marwa akaitikia kwa kumridhisha.
“Nakwamba ukweli. Sikutanii!”
“Haya, dada. Shikamoo.”
“Ewaa. Marhaba. Sasa umekua.”
“Hivi …” Marwa akanyanyuka na kuketi vema kitini. “Unataka kunambia tunapeleka gari kwa yule jamaa?”
“Ndio,” Miranda akajibu akitazama mbele. “Umesahau makubaliano yetu?”
“Kesho? Hapana! Siku nyingine hutopewa ukiomba. Tutunze ahadi tuliyoiweka.”
Marwa hakuridhia, ila hakuwa namna. Aliona uvivu kushuka na kuanza kutafuta usafiri mwingine. Kweli lilikuwa ni swala la kuchosha.
Basi akakaza macho yake saa hii akiwa amegemea kioo. Sijui nini alikuwa anawaza. Macho yake yakatazama ‘side mirror’ kwa muda mrefu na akili yake ikiwa inawandawanda huku na kule.
Japo hakuweka mazingatio kiooni, baada ya muda fulani, alitambua jambo. Alitilia shaka kuwa wanafuatwa. Kuna kitu cheupe chaenenda kila wanapokwenda.
Akakaa vema na kutazama. Akaweka mazingatio. Akatambua kitu hicho cheupe ni gari aina ya Nissan patrol.
Akasema, “Miranda, ile hadubini yako ipo begini?”
Miranda akamwambia ndio. Na akauliza anaitakia nini? Marwa hakujibu. Akarukia nyuma na kufungua begi, akatoa hadubini na kuivesha machoni. Akajitengenezea kitini na kubakisha hadubini tu juu. Akatazama.
Miranda akapata walakini. Akamtazama mwanaume huyo kwa kutumia ‘sight mirror’ ila hakupata wasaa wa kumzingatia kwa kina maana gari lilikuwa kwenye mwendo.
Baada ya muda kidogo, Marwa akarejesha hadubini kwenye begi kisha akatazama akiwa na uso wa hofu.
“Marwa, kuna nini?” Miranda akauliza. Ilikuwa imebakia dakika kama sita tu kuwasili kwa Kinoo. Tayari njia ya vumbi ya kuelekea huko walikuwa wameshaishika.
Marwa akashusha kwanza pumzi, kisha akamjuza Miranda kuwa wanafuatiliwa na Nissan huko nyuma. Miranda akaangaza, kweli akaliona.
“Sure?”
“Yah! Kwa muda mrefu sasa. Ndani kuna wanaume zaidi ya watatu waliovalia mavazi meusi.”
Hapa kichwa cha Miranda kikaanza kuzunguka kama tiara. Nini afanye. Ni wazi sasa endapo akilipaki gari hilo kwa Kinoo, atakuwa ameuza kesi. Na inaweza ikawa huo ndiyo mwisho wao endapo adui wao anatafuta tageti ya kuwamaliza.
Basi akakanyaga mafuta kwanguvu, gari likaanza kupepea. Akaendesha kama mwehu, ila kwa ustadi na japo njia ni nyembamba.
Ndani ya muda mrefu akatokea kwenye barabara ya lami, akakata kona kuchubua barabara, akajiweka sawa, akatimka kama kishada. Ndani ya muda mfupi akawa amewapoteza maadui zake.
Haikujalisha namna gani Marwa alitazama na hadubini, hakuwaona abadani.
Ila hawakuwa wanajua. Wanaweza kukimbia ila si kujificha. Na maadui zake wakiwa wanatambua hilo, hawakuangaika kukimbizana naye. Kikubwa walichojua ni kwamba tayari Miranda ameshafahamu kuwa wameunga mkia.
Basi wakiwa wanaendesha gari lao kistaarabu kabisa, wakawa wanatazama kifaa chao namna kikienenda. Mara kinakata kona. Mara kinanyoosha.
Yule bwana dereva akawaamrisha washike silaha zao vema maana tukio linalofuata huenda likahusisha kutupiana risasi kwani tayari tageti yao imebumburuka. Wale wanaume walipofanya hivyo, basi dereva akaongeza mwendokasi.
**
Gari lilitulia tuli na kuzima. Kisha kukawa kimya kana kwamba hamna kitu hapo. Miranda na Marwa wakatazamana. Kisha wakatazama huko nje. Walikuwa wamezingirwa na nyumba zilizotulia kimya na vichaka vya hapa na pale.
Walidhani wapo eneo salama. Hakukuwa hata na watu waliokuwa wanakatiza. Miranda akamwambia Marwa hapo ni sehemu sahihi kwao kutulia wasome na kutazama mambo yanavyoenenda.
Endapo kukiwa shwari, basi wanaweza kutoka na kuendelea na safari yao. Na wakitoka hapo, waelekee moja kwa moja nyumbani, si kwa Kinoo tena.
Basi dakika zikasonga. Hawakusikia wala kuona kitu cha kutilia mashaka. Ila ilipohitimu dakika ya nane. Wakastaajabu watu watano wanasimama wakinyooshea bunduki gari lao!
Watu hawa walikuwa wamevalia barakoa na nguo nyeusi ti. Miili yao ilikuwa imetuna kwa misuli. Bila shaka walikuwa ndiyo wale jamaa wa Nissan Patrol!
Kufika hapo waliacha gari lao kwa umbali kisha wakatambaa chini kama nyoka. Ni kuja tu kustaajabu watu wananyanyuka na silaha!
“Tokeni nje upesi!” Wakaamuru. Miranda akataka fanya ujanja, ila wakamwonya. Wanamwona kila anachofanya. Aweke mikono juu na atoke nje kwa usalama wake kabla hawajamiminia risasi gari likawachakaza na wao waliomo ndani.
Basi sasa wakina Miranda wakawa hawana ujanja. Wakatoka wakiwa wameanika mikono yao juu. Na kama walivyoamriwa, wakapiga magoti. Wanaume wawili wakazama ndani ya gari lao na kupekua, mmoja wao akatoka na begi la Miranda ambamo humo ndimo kuna dawa waliyotoka iba bohari.
“Mwisho wenu umewadia. Mlidhani ninyi ni werevu sana, sio?” Akasema jamaa mmoja. Kisha akatazama zile dawa zilizokwapuliwa kule bohari kama uhakiki. Jamaa huyu ni wazi alikuwa ndiye yule dereva.
Aliporidhika na zile dawa, akazirejesha mkononi mwa aliyemkabidhi kisha akamtazama Miranda na kumwambia,
“Sasa tutafanya biashara kati yetu nawe. Upo tayari kubadili maisha yako kwa yale ya Jona?”
Miranda akamuuliza, “una maanisha nini?”
Basi yule bwana akajibu, “nikabidhi Jona nami nitakuacha na uhai wako.”
Miranda akamtazama Marwa. Marwa akamtikisia kichwa akiwa amekunja uso. Miranda asijali, akarudisha uso wake kwa yule bwana na kusema, “nimekubali!”
Marwa akapayuka, “Hapana! Hapana, Miranda usifanye hivyo!!”
Miranda hata hakumtazama. Akarudia kusema kuwa ameridhia.
“Miranda!” Marwa akaita kwa uchungu. “Mirandaa!” Na mara akazirai.
“Vipi huyu?” Akauliza yule bwana.
“Ana matatizo ya kupoteza fahamu akiwa over excited!” Miranda akajibu. Basi mabwana wawili wakambeba Marwa na kumtia garini. Naye Miranda akaamrishwa asimame waelekee huko alipo Jona.
Wakamtia garini na safari ikaanza. Wakatembea kwa umbali wa kilomita moja, bwana dereva akauliza:
“Ni wewe ndiye ulimtoa Marwa kituoni?”
“Ndio, ni mimi.” Miranda akajibu na kisha kukaa kimya.
“Unaonekana mwerevu sana wewe. Na jasiri haswa. Ila umefanya makosa sana maana upande uliopo si sahihi. Hakuna aliyeanzisha vita na Sheng akashinda.’
Miranda akakaa kimya.
“Ni nani bosi wako wewe? Na kwanini ulimtoa Jona kituoni?”
“Sina bosi,” Miranda akajibu. “Jona ni rafiki yangu mkubwa, bila shaka hiyo ni sababu ya kumhangaikia.”
Yule bwana dereva akaguna kwa cheko.
“Unajifanya mjanja sio? … laiti usingekuwa umeingia makubaliano nami basi ningelikuwa nishakumaliza muda mrefu uliopita. Ila ntaheshimu makubaliano yangu nawe …”
Akaendelea kulonga na kulonga, ila sasa Miranda akawa hamsikii tena. Alikuwa amezama fikirani akiwaza mambo kadhaa. La kwanza ikiwa ni namna gani atajinasua.
Alikuwa amezungukwa na ‘mababa’. Na kando yake akiwa amelala Marwa. Kule viti vya mbele walikuwa wamekaa tena wababa wawili.
Ni wazi mazingira yalikuwa magumu kujikomboa hapa.
Miranda akakosa la kunena. Pasipo kungoja wale wanaume wakashuka toka kwenye gari, dereva akitaka kuwa mtu wa mwisho, abaki garini ili afunge na kuweka kila kitu sawa.
Kabla Miranda hajashuka akamgusa kidogo Marwa, mara mbili mguuni mwake katika namna ambayo hakuonekana, kisha akasimama kandokando ya mlango akitazama wanaume wale ambao tayari wameshajongea getini, ni yeye tu ndiye anangojewa awafungulie wazame ndani.
Akakohoa mara mbili, kisha akaanza kujongea. Na kabla hajafika mbali, yule dereva akauliza, “vipi huyu mtu wako?”
Akimaanisha Marwa. Miranda akabinua mdomo kisha akasema, “nadhani twende tukamtoe kwanza huyo mnayemhitaji kisha tukirejea tutamtoa huyo. Au mwaonaje?”
Yule dereva akagutuka na jambo. Akiwa bado garini akauliza, “kwanini tusimtoe tukaenda naye kabisa ndani?”
Miranda akapandisha mabega kupendekeza kwamba lolote ni kheri tu. Kisha akakohoa tena mara tatu na kupigapiga kifua chake kama mtu asikiaye maumivu.
Wale wajamaa waliokuwa wameshuka, wakajiteua wawili wauendee mwili wa Marwa. Miranda akasimama akitazama kwa makini. Na kwa macho ya wizi, akamtazama mwanaume mmoja aliyekuwa amesimama kando yake.
Basi katika namna ya ajabu, haraka ya radi, milio miwili risasi ikavuma. Mara wale wajamaa walioenda kumbeba Marwa wakajikuta chini. Na ni ajabu kama walibakiwa na uhai maana walitulia tuli ya maji mtungini!
Na katika namna hiyo hiyo, yani haraka ya kustaajabisha, Miranda akamsulubu yule jamaa aliyekuwa amesimama naye kwa teke barabara, akajikuta kama mkungu wa ndizi uliochoropoka mgombani! Tih!
Na mara, “tulia hivyohivyo!”
Ilikuwa ni sauti ya Marwa. Sura yake ameijaza ndita na akikodoa kutishia amani. Mdomo wa bunduki ameuelekezea kichwani mwa dereva.
Akampa sisitizo, “ukitingisha hata nywele, basi uhai wako mali yangu!”
Dereva akaweka mikono juu akiwa amefura. Miranda akarejea ndani ya gari na kisha akachukua bunduki aliyokuwa ameishikilia Marwa. Akambonda dereva na kitako chake, akazirai.
“Umefanya kazi nzuri sana, Marwa!” Miranda akampongeza. “Umekuwa mwanafunzi mwepesi sana kushika mambo. Najivunia kuwa nawe.”
Basi wasipoteze muda, wakawafungasha wanaume wale ndani ya gari kisha Miranda akamtaka Marwa azame ndani na yeye akamalizane na maadui hao.
Kazi haikuwa ya kulala! Hawana mahali pa kuhifadhi maiti hizo, na huenda ikaleta kesi. Bila shaka majirani watakuwa wamesikia vishindo vya risasi. Amelenga kuwapeleka mahali salama na kisha ampatie ujumbe murua bwana Sheng.
“Basi twende wote!” Marwa akabweka. “Ya nini uje kuniacha kwenye tisa na kumi i-karibu?”
Wasizoze na jamvi, wakakwea na Miranda akatimua chombo mpaka maeneo yapatikanayo makao ya Sheng. Huko akaliweka gari kwenye maegesho yasiyo rasmi, alafu akashuka na kwenda … baada ya dakika kama tano akarejea na kumwambia Marwa kila kitu kipo sawa japo hakusema alienda kufanya nini.
Na kabla hawajaliacha gari hilo, mwanamke huyo akaandika baadhi ya maneno kwa ‘marker pen’ nyekundu kiooni.
Kisha wakayoyoma eneo hilo.
**
Zikapita kama dakika kumi na tano, na jamaa mmoja mrefu mwembamba mwenye asili ya kichina akakatiza eneoni akiwa anavuta sigara kwa hisia.
Pengine alikuwa anasikia baridi. Sigara yamsaidia kuiondoa. Ila ambacho alikiona sekunde chache mbele yake, nadhani kilimsaidia zaidi kupasha mwili joto.
Alisita, akatazama. Akapekua na kugundua ile ilikuwa gari ya makaoni. Mbona ipo huku? Akajongea kutazama. Akaangalia na mule ndani. Haki alichokiona kikamfanya aachame, sigara ikadondoka chini.
**
“Mkuu, kunaa … kuna …” alimwemweta bwana mweusi akijawa na puzo la hofu usoni. Mbele yake alikuwa amesimama bwana Shao, yule jamaa wa karibu na Sheng. Yule jamaa aliyemshawishi Sheng kurusha ndoano kwenye zoezi lingine badala ya kuwamaliza wafanyakazi kwa kuwaua.
Japo ilikuwa ni usiku mkali, bwana huyu hakuwa amelala. Macho yake yalikuwa meupe na uso wake upo moto.
Alikuwa ameketi sebuleni. Usiku huu mzima alikuwa anakaa na kungoja kuja kupewa mrejesho wa zoezi aliloliasisi. Akiwa anategemea mambo yataenda bambam.
Ila kwa namna mtumishi huyu aliyemtoa ndani alivyokuwa anaongea, akaanza kupata shaka. Hata moyo wake ukaanza kuchanganyia kasi.
Haiwezekani akafeli! Haki Sheng hataelewa.
“Kuna nini?” Shao akauliza kwa lafudhi yake ya kimandarin. Macho yake madogo alikuwa ameyakodoa.
Basi mtumishi yule akajikaza na kusema,
“Kuna ujumbe wako … kule!”
Ikachukua dakika tano tu, Shao akawa ameshajua yale yote ya habari za watu walioagizwa. Ya kwamba wameuawa, na wengine wakazimishwa fahamu.
Na ujumbe akaandikiwa kiooni, “Nenda kaukute ujumbe wako ndani ya kibanda cha mlinzi!”
Akavuta mafundo mawili ya hewa, na tayari ujumbe huo alioambiwa upo kibandani mwa mlinzi ukawa umewasili mkononi mwake. Kuna mtumishi alikuwa tayari anao mkononi.
Ulikuwa ni ujumbe wa maneno machache tu ukiwa umeandikwa kwenye kikaratasi kidogo, ukisema, “Tumepata antidote. Mmepata kifo!”
Shao akaghadhabika haswa. Dharau ya aina gani hii? Ina maana mtu alileta gari hapo, mosi, pili, akazama ndani ya uzio wao na kwenda kwa mlinzi, akaweka karatasi ndani ya droo!
Alafu … alafu akatoka salama!
Shao akajihisi amevuliwa nguo. Na kwa bayana akatambua jambo hili likimfikia Sheng, hakuna atakayekuwa upande salama hata punje! Sheng hana moyo wa kubeba kejeli kiasi hiki! Ni mwepesi wa maamuzi. Ni mwepesi wa kushika hasira.
Basi bwana Shao akawaita watumishi kumi, akawaagiza wawazike wale watu upesi. Na wale ambao walikuwa amezirai, akawamalizia kwa kuwadunga risasi za kichwa akitumia bunduki yenye kiwamba cha kumeza sauti.
Akasihi jambo hilo liwe la siri mno. Na akatishia endapo likisikika basi ata-deal na hao watumishi kumi aliowapa kazi. Wahakikishe Sheng hajui lolote lile, na yeye anajua cha kufanya!
Wakatii agizo.
Makaburi yakachimbwa, watu wakazikwa kupumzishwa.
**
Asubuhi ya saa mbili …
“Marwaa!” Sauti nyembamba iliita mlangoni baada ya hodi ya kistaarabu. “Dada anakuita!”
Marwa akafungua jicho moja na kuangaza. Bado alikuwa ana usingizi pomoni. Kwanini jua linawahi kuchomoza kiasi hiki? Alilalama.
Hapa karibuni amekuwa akilala robo usiku. Anachoka. Hii haikuwahi kuwa mfumo wa maisha yake hapo kabla. Yeye ni mtu wa kulala mapema, aghalabu huchelewa sana endapo akibanwa na kazi za hapa na pale, tena haizidi saa sita usiku.
Miranda anawezaje?
Akajikusanya na kuamka. Akajianda kwa muda mfupi na kisha kwenda sebuleni. Huko akamkuta Bwana BC na Miranda. Sebule nzima ilikuwa imejawa na moshi wa sigara za BC.
“Pole, naona bado umechoka!” Miranda alimpokea kwa tabasamu. Akashukuru. Akiwa anaketi, naye BC akampongeza kwa kazi aliyoifanya usiku wa kuamkia siku hiyo. Akashukuru tena.
Basi BC akamwambia kazi imeshakwisha. Ndani ya siku tatu tu, Jona atarejea kwenye hali ya kutia matumaini. Na pasipo kuzidi mwezi, atakuwa amesharejea kuwa Jona kamili.
Habari hizi zikamfurahisha sana Marwa. Akatabasamu mpaka gegoni. Ila BC akamwonya. Akamkumbusha yale makubaliano ya awali waliyoyaweka.
Atampatia Jona antidote, ila wataandikishiana makubaliano. Na atakuwa akitoa kidogo kidogo akitazama kama makubaliano yake yataheshimiwa.
**
Marwa angelisema nini? Hakuwa na la kusema zaidi ya kuafiki kile ambacho BC alikuwa anamwambia japo ndani ya moyo wake alijawa na hofu. Hakuwa anamwamini kabisa Jona. Alihofia anaweza kiuka vifungu hivyo na kuleta tafrani.
Misukosuko waliyopitia inatosha. Pengine Jona anaweza akalitambua hilo, alijipa moyo. Basi baada ya muda mfupi BC akaaga na wakaondoka pamoja na Marwa kwa makubaliano kwamba aende kumpatia antidote.
Walipofika nyumbani kwa BC mwanaume huyo akazama maabara na kufanya kile anachokijua zaidi. Ikamchukua kama robo saa akatoka akiwa amebebelea kemikali ndani ya chupa maalum ya kioo. Akamkabidhi Marwa na kumpa maelekezo.
Marwa hakupoteza muda, akamuaga na kwenda zake BC akimsisitizia kuwa makini na chupa hiyo iliyobebelea antidote.
Alipowasili nyumbani, akampatia Jona kiasi alichoelekezwa kisha akajikuta sebuleni pamoja na Miranda.
Aliketi akiwa ana mawazo kichwani. Miranda alimtazama na kisha kumuuliza, “Marwa, kuna tatizo?”
Marwa akatikisa kichwa akiminya lips. Hakusema kitu. Miranda akamtazama na kisha akamjongea akiachana na kutazama televisheni.
Akamwambia, “Najua unachowaza.”
Marwa akamtazama. Bado hakusema kitu.
“Hata mimi kinanipa hofu kama wewe. Ila natumai kila kitu kitakuwa fresh. Usiwaze sana.”
Marwa akamuuliza, “una uhakika?”
Akajibu, “Hata kama sina uhakika, ila ya nini kufikiria yajayo ambayo bado hayajafika? Don’t worry …” akamshika Marwa bega. “Kama tumepita kule kwenye bonde la mauti, tutashindwa hapa?”
Marwa akashusha pumzi. Akauliza, “ila vipi kama Jona hataridhia? BC atammaliza?”
Miranda akatulia kwanza akiwaza. Kwa kama sekunde tano, akasema, “pengine hiyo inaweza ikawa kazi kubwa kuliko zote tulizozifanya..”
Miranda akashusha pumzi. “Endapo kama Jona akikataa, tutakuwa njia panda. Tuna kazi ya kumshawishi. Na naamini inawezekana … yah! Inawezekana.”
Miranda akatabasamu. Naye Marwa akatabasamu.
“Leo jioni tutatoka out for a dinner. Angalau tukatefresh minds na kujipongeza. Au unasemaje?” Miranda alichombeza. Marwa akajibu kwa kuongeza upana wa tabasamu lake.
**
Akiwa anakula chakula cha mchana ndani ya mgahawa mdogo jijini Hongkong, mara akaona askari wawili wakiingia ndani ya mgahawa huo. Mmoja wao alikuwa mrefu, kijana, mwenye nguvu, na wa pili alikuwa mzee kidogo, kofia yake alikuwa ameishikilia mkononi hivyo mvi na uso wake uliochoka ulionekana vema.
Walinyookea kaunta, wakaskizwa na kisha wakaketi kwa mbali kidogo.
Wakiwa wanafanya yote haya, Lee alikuwa anawatazama chini ya kofia yake ‘kapelo’ kwa macho ya kuibiaibia.
Alikuwa anafahamu anatafutwa na hata huko kwenye vyombo vya habari wamekuwa wakimrusha akihusishwa na kifo cha Chong Pyong, mpiga gitaa maarufu jijini.
Sasa anaishi kama ndege. Na hata juhudi za kujikomboa kurudi alipotoka zinakuwa ngumu zaidi kwani huko viwanja vya ndege watamtambua na kumweka chini ya ulinzi.
Basi akaendelea kula, na kwa macho ya kuibia akaendelea kuwatazama wale askari ambao nao muda si mrefu wakaletewa chakula na kuanza kushibisha matumbo wakipiga soga za hapa na pale.
Akiwa anaelekea kumaliza chakula, mhudumu akaja. Alikuwa ni mama mtu mzima anayejitahidi kujiweka vema. Alikuwa amemletea bili yake ya chakula.
Akaipokea na kuitazama, kisha akatoa pesa mfukoni na kuiweka mezani. Hakutaka hata kumtazama yule mhudumu usoni.
Mhudumu akakusanya pesa yake na kushukuru. Akaenda zake. Ila akiwa na shaka juu ya Lee. Kwanini alikuwa ana-behave namna ile? Kwa utaratibu wa kichina, si adabu, haswa ukifanya vivyo kwa mtu mzima.
Basi yule mhudumu, pasi na kujenga hoja ya kumhisi Lee, akaenda kusema kule kaunta na jikoni namna vijana wanavyobadilika siku za karibuni. Na pasipo kujua basi akaalika macho zaidi kwa Lee. Wakamtazama. Ila hawakujali sana.
Ilipopita dakika tatu, ndipo kidogo mambo yakaanza kubadilika. Televisheni iliyokuwa imepachikwa ukutani kwa ajili ya kusogezea muda wateja na kuwavutia kwenye eneo hilo dogo, ikarusha matangazo ya kutafutwa kwa Bwana Lee!
Picha yake ambazo zilikuwa zimedakwa na CCTV nazo zikarushwa, ila napo haikujalisha sana, ni watu wawili ambao walikuwa wamekaa karibu na wale askari ndiyo waliupokea ujumbe huo wa televisheni na kuanza kuujadili.
Wale askari nao wakaungana nao, wakawa wanne. Na kwasababu eneo hili halikuwa kubwa, basi kila mtu ndani ya mgahawa alisikia vema kilichokuwa kinazungumzwa, akiwamo Lee.
Napo haikujalisha sana, ila tabu halisi ikaanzia pale ambapo yule mhudumu aliyeenda kuchukua pesa toka kwa Lee kugundua kwa namna moja yule mtu aliyetangazwa kideoni anafanana na Lee!
Si kwa sura, la! Bali vazi. Lee alikuwa amebadili mavazi yake yote isipokuwa shati lake la ndani ambalo kwa juu alilifunika na koti ambalo hakulifunga zipu.
Sasa yule mhudumu akaunga taarifa kichwani kwake. Huenda yule kijana amejifunika uso na hataki kutazama watu maana anahofia kugundulika.
Hakumwambia mwenzake yoyote, taratibu akaenda kwa wale askari, kisha akawatonya akielekezea macho kwa Lee. Lee akagundua hilo.
Askari wote walitazama upande wake, pamoja na yule mhudumu.
Wale askari wakatoka nje na kuangaza. Kushoto … kulia … kushoto … wakamwona yule kwa mbali! Yule askari kijana akachomoa filimbi na kuipuliza kwanguvu akimkimbilia Lee.
Akipiga kelele asimame! Asimame!
Lee akakimbia kwa kasi sana. Na baada ya punde fupi, akajibana sehemu, kwenye kuta ndogo ya kauchochoro, hapo akabana mpaka na pumzi asisikike.
Baada ya dakika moja, yule askari akawa amefika eneo hilo. Alikuwa anatembea, anahema kwanguvu, macho yake yanaruka huku na kule kuangaza na kupekua watu.
Alitilia shaka kiuchochoro, akatupia macho huko, hakuona mtu. Ila kabla hajapita, mara simu ya Lee ikaita mfukoni! Askari akashtuka na kuangaza. Moja kwa moja akahisi mtuhumiwa wake atakuwapo hapo.
Akajongea akiwa ameshikilia kipochi kidogo cha ngozi kiunoni mwake kilichobebelea bunduki ndogo.
Alipopiga hatua ya nne, Lee akamuwahi! Hafla! Akampiga ngumi tatu za haraka, askari akapoteza nguvu! Akamchomolea bunduki, na kunyofoa risasi zote kisha akamwachia kasha tupu akiondoka zake kwa mwendo wa wastani.
Askari akabaki chini akilalama kwa maumivu.
Lee aliposonga kwa mbali kidogo, akatazama simu yake. Akagundua ni Sheng ndiye alikuwa anampigia. Akastaajabu imewezekanaje? Amepata wapi mawasiliano yake? – ina maana ameshafahamu yuko China?
Simu ikaita tena. Akasita kupokea. Akajiuliza kwa kama sekunde nne, akakata shauri na kupokea.
Swali la kwanza, unafanya nini China? Na la pili, kwanini umemuua Chong Pyong?
Kumbe Sheng alishafahamishwa habari za kutafutwa kwa Lee. Habari zake ambazo zimezagaa ndani ya Hongkong zilishafika mpaka makao ya Wu family, nao wakamjuza Sheng kumhusu mtu wao.
Sasa Lee akawa njia panda. Mosi, hakuaga. Pili, atasema anafanya nini huko Hongkong? Kufuatilia nyaraka ya Sheng iliyopotea??
Akajikaza na kulaghai. Akasema amekuja China kusalimia na kujizoeza na mazingira. Ila bwana Sheng hakujali sana hiyo sababu wala hakumpeleleza zaidi, akamwambia kuna kazi anataka kumpatia.
Na kwakuwa yupo huko China, anaamini ataifanya vema.
**Lee akatega sikio apate kusikia kazi hiyo, ila pia kwa wakati huo huo akiwa na tahadhari juu ya mazingira yake asije akawa anafuatiliwa na askari.
Alikuwa anatazama huku na kule. Akatafuta mahali pazuri pa kujishkiza, akatazama chini akifunikwa na kofia. Akaendelea kuteta na simu.
Basi Sheng akamwambia kuwa huko Hongkong afanye namna, juu ama chini, ahakikishe anaenda makao makuu ya Wu family kukutana na viongozi. Watakuwa na kazi ya kumpatia.
Lee akapeleleza kuhusu kazi hiyo, ila Sheng hakuwa tayari kumwambia. Akamsisitizia tu aende huko. Maelezo yote atapewa.
Na kabla hajakata simu akamwambia ahakikishe anafanya kazi hiyo. Na ahakikishe anakwenda kabla siku hiyo haijakoma.
Yeye ni nani akatae agizo la bosi? Akaweka simu mfukoni na kisha akaanza kufanya utaratibu wa kwenda mahali ambapo ndipo alipokuzwa punde baada ya kuokotwa mtaani.
Mahali palimpofunza yale yote anayoyajua. Kumpandikiza roho ya unyama, na ujuzi wa kutisha kabisa kabla hajaanza kusafiri kwenda kutenda kazi.
Ikamchukua masaa matatu na dakika arobaini kuwasili mbele ya geti kubwa lililofunikwa na paa yenye mitindo ya tamaduni za kijenzi za China. Na chini ya paa hiyo, kulikuwa kumening’inizwa kibao cheusi chenye maandishi ya kichina ndani ya rangi ya dhahabu. Yakisomeka kwamba eneo hilo ni milki ya WU DRAGON.
Lee akatazama sana hapo akikumbuka mbali. Kipindi kile akiwa kijana mdogo zaidi. Akajikuta anatabasamu na kukiri kwamba muda ni upepo. Unakimbia haswa.
Akiwa hapo, mara sauti ya kichina inapaza. Anatazama sauti hiyo inapotokea na kumwona mwanaume mmoja aliyevalia gauni jeupe za michezo ya mapambano. Kiunoni amefungia mkanda mweusi.
Jamaa huyo akamuuliza Lee ni nini anafanya hapo na yeye ni nani? Kabla hata Lee hajajibu, wakatokea tena wanaume watatu toka msituni. Jengo hili lilikuwa limezungukwa na msitu mpana. Na hata Lee akiwa njiani kuja, alikuwa tayari ameshaonekana.
Watu hawa, wanne kwa idadi, walikuwa kama chambo tu. Wengine zaidi bado walikuwa mafichoni na Lee alilitambua hili. Akatanua mikono yake na kutabasamu.
Akajitambulisha yeye ni wa Wu familu. Ila wale watu wakatilia mashaka. Wakamtaka athibitishe kauli yake kwa kupambana na mmoja wao maana wanatambuana kwa mitindo na mienendo ya mapigano.
Basi pambano likazuka, yule jamaa aliyemshtua Lee mwanzoni kabisa akijitolea kupimana ubavu, huku wenzake wakibakia kama watazamaji.
Wakajitenga bayana, na pambano likaanza! Kijana yule mgeni machoni mwetu, hakuwa haba. Alidumu kwenye ulingo kwa dakika tatu akimpa changamoto kubwa Lee, kwa wepesi wake wa maamuzi na mwili.
Ila ngoma ya watoto haikeshi, Lee akamtuliza kwa kuisimamisha ngumi yake nzito kandokando ya shavu baada ya kumshambulia kwanguvu mno!
Yule bwana akatabasamu na kuafiki. Haki Lee ni wa Wu family. Akampatia mkono na kumkaribisha. Ila mara wakashtuliwa na sauti kavu ya kizee ikiwapongeza.
Kutazama getini hawakuona mtu, bali alikuwapo juu ya ukuta akiwa ameketi kwa kukunja miguu! Ilikuwa ni ajabu kwa namna mtu alivyokaa hapo. Alikuwa ni mzee asiye na nywele kichwani, ila mustachi mwembamba mrefu, na kidevuni ana ndevu nyembamba zilishoshuka mpaka kitovuni. Nywele hizi zote zilikuwa nyeupe kama sufi.
Alikuwa amevalia joho la mapambano, rangi ya karoti iliyofubaa.
Kwa jina alikuwa anaitwa Shifoo Nieng, yaani master Nieng. Mkufunzi aliyewalea, na anayewalea vijana wote watokao kwenye ‘temple’ ya Wu family. Japo ni mzee, kwa makadirio miaka sabini na, ila bado ni mwenye nguvu akitenda kazi yake inavyotakiwa.
Na kama kuna kitu cha ziada kuhusu yeye, basi ni kumbukumbu. Haikujalisha ametoa vijana mamia kwa mamia, alikuwa ana uwezo wa kuwakumbuka vijana wote kwa sura!
Hakupata shaka kabisa kumwona Lee. Na alifurahishwa kuona bado kile alichomfundisha kipo ndani yake.
Akamkaribisha Lee nyumbani.
**
Saa nane mchana … nchini.
Punde Sheng aliporejea kitini akitoka kwenye jokofu, mlango wake uligongwa mara mbili. Akiwa anatambua ni nani yupo mlangoni, akapaza sauti ya kusafisha koo.
Mlango ukafunguliwa na Shao akaingia. Kama vile walikuwa wameambizana, walikuwa wamevalia suti ya kijivu wote, ila Sheng yeye alikuwa amechomeka ua dogo jekundu upande wake wa kuume.
Wakasilimiana, na Sheng asiseme kitu, akamtazama Shao katika namna ambayo Shao alielewa ni nini mwanaume huyo anataka. Si kingine bali taarifa ya ile misheni ya Bohari.
Shao akasafisha kwanzo koo alafu akakunja nne. Akamwambia Sheng kuwa vijana walienda kutenda kazi waliyotumwa, ila hawakufanikiwa. Hapa kwenye ‘hawakufanikiwa’ alipaongea kwa sauti ndogo, kisha akamtazama Sheng.
Akashuhudia Sheng akikunja ndita alafu akajilaza kitini, akibinua mdomo. Shao akabashiri Sheng atakuwa anapapasapapasa droo yake yenye silaha.
Akajawa na hofu. Moyo wake ulimwenda mbio ila akajitahidi kujikaza. Akaweka mkono wake mezani, akiigiza kujiamini, na kumweleza Sheng kuwa vijana walishindwa kufanya hiyo kazi kwakuwa walengwa wao hawakwenda bohari la dawa kama walivyotarajia.
Sheng hakusema kitu. Bado uso wake ulikuwa umetindwa na ndita na macho yake ameyafinyanga kuwa madogo zaidi.
Basi Shao akaendelea kujieleza. Isingeliwezekana tukio kufanyika pasipo watu. Na mwishowe akaomba apewe muda. Atakamilisha kazi.
Bado Sheng hakusema kitu. Uso wake ulikuwa vilevile. Sasa alikuwa anatisha na usijue nini anawaza kichwani!
Shao akaendelea kusisitiza ampatie nafasi nyingine. Ila akiwa anaongea, akasikia sauti ya droo ikifunguka. Akanyamaza. Akasema moyoni hayupo radhi kupoteza uhai wake.
Na kichwani akapiga mahesabu, endapo Sheng akichomoa bunduki, basi atapambania uhai wake mpaka tone la mwisho. Akaweka miguu yake tenge.
Sheng akauvuta mkono wake na mara juu akaweka faili rangi ya zambarau. Angalau Shao akapata amani. Sheng akafungua lile faili na kisha akatoa wino ndani ya droo. Akaandika jambo, kisha akasukumia faili alipo Shao.
Akalipokea na kulitazama. Ilikuwa ni HATI YA KIFO. Sheng alikuwa anamtaka atie sahihi kwenye makubaliano ya kumpata Jona, la sivyo atammaliza kwa mkono wake mwenyewe!
Ila kwanini Sheng alimsitiri Shao? Ni wazi angelikuwa mtu mwingine angelitoka mfu humo ofisini. Kwanini Shao?
Kwa mara ya kwanza, Sheng alitumia akili dhidi ya hasira. Kumuua Shao kungemuweka matatani na kwa namna iliyo bayana, ingesababisha mgogoro ndani ya familia ya Wu. Hivyo, akataka kuweka mikono yake safi.
Shao asaini kuridhia.
Shao akamtazama kwanza Sheng. Wakatazamana kwa kama sekunde tatu, kisha Shao akasema kabla ya kutia sahihi, apewe kwanza kila kinachohitajika kumpata Jona.
Sheng akamuuliza ni kipi ambacho hana na hali jeshi zima alimkabidhi? Shao akasema bado havitoshi, anahitaji ‘access’ ya maabara kwa muda wowote ule.
Hapa kidogo Sheng akasita.
Akamtazama Shao kwa jicho la shaka na kumuuliza kwanini anataka hilo aliloomba. Shao akamjibu kwa ufupi, amwamini. Sheng akafikiri kidogo kisha akapandisha kichwa chake juu kama ishara ya kuafiki, basi Shao akatia sahihi katika hati ile na kisha akamrudishia Sheng kisha akaaga na kwenda zake.
Sheng akabaki akifikiri. Hata naye Shao akaenda akifikiri. Alikwazwa na kile kitu. Alifika kwenye makazi yake na kuketi akiwaza haswa. Baada ya muda kidogo akaita vijana wake kumi na kuwaeleza kile kilichotukia.
Akawaonya na kuwasisitiza ya kwamba sasa misheni ya kumkamata na kumuua Jona si tu ni kazi bali utetezi wa uhai wao. Wafanye kila wakijuacho kuhakikisha wanamtia mkononi.
Na zaidi akawaambia ana mpango. Ila atawashirikisha muda si mrefu baada ya kukutana na mtu mmoja nyeti kabla siku hiyo haijaisha. Kwa hivyo, akawaambia wale vijakazi wakutane nae majira ya saa nne usiku palepale walipokutania.
Agizo hilo likapita, watu wakatawanyika. Kwenye majira ya saa mbili usiku, mwanamke mmoja aliyevalia baibui, akaja kwenye makazi ya Shao. Aligonga mlango mara mbili, Shao aliyekuwepo ndani akatazama saa yake ya mkononi, akagundua ndiye mgeni anayemngojea, akatabasamu akinyanyuka. Akauendea mlango na kufungua.
Alikuwa ni Sasha! Mwanamke huyo akazama ndani na muda si mrefu maongezi ya kiini yakachukua nafasi. Lengo kuu la Shao kumwita hapo mwanamke huyo ni kuwa anaamini kwa namna moja ama nyingine, wakina BC wanaweza wakawa wanahusika na tukio la kukombolewa kwa Jona.
Japo hakuwa na uhakika, aliona jambo hilo sio la kulipuuzia. Na sasa alikuwa anataka mrejesho wa Sasha amefikia wapi kuomba ‘access’ ya kuzama ndani ya kundi hilo akitumia mgongo wa dada yake, Sarah.
Sasha akanywa maji kwanza kupoza koo kisha akamwambia Shao kuwa kazi haikuwa nyepesi hata kidogo. Na kwa namna moja, wakuu wa kitengo hicho wanaonekana kutingwa na kazi kiasi kwamba maombi hayo yamewekwa kwenye mangojeo.
Hapa Shao akazidi kuamini aidha ‘kazi’ hizo ambazo zimewatinga zinaweza zikawa zinamhusu Jona. Akang’ata lips zake akitafakari.
Akanyanyua glasi yake ya kinywaji akanywa mafundo mawili alafu akakuna kidevu chake cheupe.
Akamwambia Sasha hawana muda wa kupoteza. Inabidi jambo lifanyike kuhakikisha makazi ya watu hao wanaowashuku yanapelelezwa kama yamemuhifadhi Jona. Na kazi hiyo ataifanya yeye, Sasha, kwani atakuwa ana ufahamu wa maeneo hayo.
Hata alipojitetea hayafahamu, Shao hakumwelewa. Akamsisitizia amtumie dada yake, Sarah, kuyafahamu na kisha afanye kazi hiyo ndani ya siku mbili tu!
Punde atakapofahamu kuwa Jona amelazwa miongoni mwa majengo hayo, atoe taarifa na wao watalifanyia kazi mara moja!
Simulizi : Anga La Washenzi (2) Sehemu Ya Tatu (3)
Usiku wa saa nne …
Simu iliita, ila Sarah alihofia kuipokea. Alikuwa kitandani pamoja na Kinoo, na ni dada yake ndiye aliyekuwa anapiga.
Akamtazama Kinoo, hakuwa anatikisika. Alimpatia mgongo akitazama ukutani. Ila naye hakuwa amelala. Na alisikia simu hiyo ikiita. Lakini hakusema wala kufanya kitu.
Sarah akakata simu. Kisha akatulia kwanza asiseme jambo kwa kama dakika mbili akisikilizia pengine Kinoo atafanya jambo. Hakufanya!
Basi akafungua simu yake na kwenda moja kwa moja upande wa ujumbe. Akaandika kwa haraka akitumia vidole vyake vyepesi kumwonya Sasha asimpigie muda huo kwani yupo na Kinoo.
Kisha akatuma tena ujumbe wa pili kumuuliza anataka nini usiku wote huo?
Akangoja kwa sekunde tano ujumbe kuingia. Sasha akianzia mbali kwa kumuuliza nini kinakawiza zoezi lao la kuungwa kundini. Je watu wao wametingwa na kazi gani?
Sarah akasonya, kisha kwa pupa akabofya kioo cha simu kumwambia dadaye mbona hilo alishamwambia kuwa hajui, na Kinoo amekuwa mgumu kujipambanua?
Sasa Sasha akaenda kwenye lengo lake, akamwomba dada yake amweleze makazi ya watu wanaohusika na Kinoo. Sarah akamwambia kuhusu Miranda tu, maana ndipo anapopafahamu. Kisha asipoteze muda akamuaga dada yake na kuzima simu kabisa.
Akalala baada ya kuchoma dakika kadhaa akiwaza nini Sasha amepanga kufanya. Akapotelea kabisa usingizini.
Ila Kinoo bado alikuwa macho! Alivuta tena dakika kadhaa alafu akavuta simu ya Sarah na kuiwasha. Akatia nywila na kubonyeza OK. Simu ikakataa kufunguka.
Akajaribu tena kuweka nywila, akabonyeza OK, majibu yaleyale, simu imegoma! Kumbe Sarah alibadilisha nywila ya simu yake. Kinoo akalalama. Akairejesha simu alipoikuta kisha akaendelea kuwaza.
Ni nini mwanamke huyu alikuwa anafanya nyuma ya mgongo wake? Tena yeye na dada yake?
Haki alipata shaka. Na aliona alichukulie hatua hilo.
Ila atawahi kabla ya madhara kutokea? Hili ni la mimi na wewe kujiuliza.
**
Saa moja kasoro asubuhi…
Baada ya kupata kifungua kinywa, Lee alienda kukutana na Nieng, Shifoo Nieng, aliyekuwa ametulia ndani ya bustani aki-meditate kama afanyavyo kila siku kuanzia majira ya saa kumi na moja alfajiri.
Alipofika hapo, akatulia na kungoja. Alishaambiwa zoezi hilo la Nieng huwa linakoma saa moja kamili hivyo alijua hatakaa hapo kwa muda mrefu kungoja.
Hakukosea, muda si mrefu akaungana na Nieng ambaye alimtaka waende kufanyia maongezi yao ndani. Ofisi yake ilikuwa imekaa mbele ya dojo, ndani hakukuwa na kiti wala meza, bali mito midogo chini ambayo ndiyo hutumika kama kiti.
Wakaketi humo katika mtindo wakaao wanafunzi wa sanaa ya mapambano ndani ya dojo kisha maongezi yakachukua nafasi. Nieng akaanza kwa kumuuliza Lee kwanini alimuua Chong Pyong.
Lee akaeleza kila kitu. Hakuhusika na kumuua Chong Pyong. Amesingiziwa tu akiwa katika harakati za kumtafuta Chen Zi.
Nieng akastaajabu kusikia Chen Zi. Akamuuliza Lee ana mahusiano gani na Chen Zi? Lee akalaghai kuwa ni rafiki. Alihofia kusema kuhusu nyaraka ile aliyokuja kuitafuta.
Basi Nieng akamwambia Lee kuwa Chen Zi aliuawa na familia ya Li. Wala hakuwa amezidisha madawa kama inavyosemekana. Na sababu kubwa iliyopelekea Chen Zi kuuawa ni kuhisiwa ana mahusiano na Wu family.
Nieng akaenda mbali akamwambia Lee kuwa kuna mengi sana yanatukia ndani ya China, watu kuuawa na wengine kupotea. Familia ya Li imekuwa yenye nguvu mno hapa karibuni, na kama wasipofanya jitihada basi wataifutilia mbali kabisa familia ya Wu.
Mpaka hivyo wanapoongea, tayari wameshapokonywa jiji la Hongkong. Na hata Shanghai imekuwa matatani. Haitachukua pia muda mrefu kuwa chini ya Li, kama vile Beijing.
Ajabu ni kwamba, japo familia ya Wu inaungwa mkono na serikali, bado tu Li wanawasumbua. Inasadikika kuna baadhi ya vibaraka ndani ya serikali, na wao wamekuwa wakitoa taarifa zote kwa Li family.
Sasa kuwadhibiti inabidi liwe kipaumbele chao kikubwa. Kuna baadhi ya viongozi inabidi wauawe, kuna baadhi ya watu inabidi wapotezwe.
Japo wanawajua watu hao, bado kazi imekuwa ngumu! Ila Nieng akaendelea kwa kusema sasa amepata matumaini. Anaamini Lee atakuwa mwarobaini wa tatizo hilo.
Anaamini kwenye uwezo wake, atamkabidhi jeshi na orodha ya watu wa kuwamaliza.
Kwa Lee halikuwa gumu hilo. Akaliafiki. Ila shida kidogo ilikuja pale alipoambiwa mtu wa kwanza wa kummaliza.
Alikuwa ni makamu wa raisi!
Nieng akamwambia Lee kuwa makamu huyo wa raisi ndiye kikwazo cha kwanza katika mambo yao. Yeye ndiye amekuwa kibaraka wa Li family kinyume kabisa na serikali ilivyo. Amekuwa akichukua taarifa na mipango yao yote na kuifikisha mezani mwa familia ya Li.
Yeye ndiye ambaye amekuwa kiungo kikubwa cha Wu family kudhoofika ndani ya nchi na hata huko ulimwenguni.
Lee alitakiwa kummaliza mwanaume huyo pasi na simile hata kidogo. Ahakikishe habaki na uhai na hata kama kutakuwa na uwezekano basi familia yake nayo itokomee kisibaki kitu.
Hiyo itakuwa salamu mwanana kabisa kwa familia ya Li. Na kwa namna iliyo kubwa itawapa kimuhemuhe na joto miilini.
Ila Nieng akaenda mbele zaidi kwa kumwambia Lee kuwa kazi hiyo haitakuwa nyepesi kabisa maana makami huyo mbali tu na kulindwa na serikali kama afisa mkubwa, pia analindwa na ulinzi binafsi unaopewa nguvu na familia ya Li.
Basi Lee baada ya kupewa maelekezo hayo pamoja pia na anwani ya makazi ya makamu wa raisi akaenda kuonana na watu atakaofanya nao kazi. Walikuwa wengi mno, kadiri kama watu alfu mbili wenye mafunzo.
Ila kwasababu alitaka wanaume waliokomaa kimafunzo ili kazi ikawe rahisi na kwa ufanisi, basi akafanya ‘interview’ kidogo akisaidiwa na Nieng, wanaume wale wakapewa fursa ya kupambana wenyewe kwa wenyewe, mwishowe Lee akachagua watu watano wa kazi.
Akawataka waonane baadae usiku kwa ajili ya kuyapanga. Yeye akatoka kwenda kukagua makazi yale ya makamu wa raisi ambayo alikuwa amelenga kufanya tukio kesho yake.
Ilikuwa ni umbali uliomgharimu masaa maana kiongozi huyo alikuwa anakaa Beijing na si Hongkong. Alipofika huko akatumia tu macho yake kuchambua eneo, kwa dakika kumi, kisha akayeya.
Baadae usiku kama alivyopanga miadi akakutana na wale watu wake watano wa kazi, akaanza kuwapanga namna ya kuenenda. Ila wakiwa maongezini, shifoo Nieng akaingilia kwa kumhitaji Lee dakika chache.
Akamweleza kuwa mambo yamebadikika. Amepata taarifa kuwa kiongozi huyo hayupo nchini, amesafiri kikazi kwenda Mongolia, nchi jirani na China kwa upande wa kusini. Hivyo basi inabidi aende huko kufanya kazi, na pia itakuwa wepesi zaidi kwa maana ulinzi wake utakuwa hafifu.
Basi kwa maelezo hayo, Lee akaona ni kheri akaenda mwenyewe kutekeleza hiyo kazi. Ila Nieng akamwambia kuwa taarifa juu ya wapi anakaa huko Mongolia, haijapata. Ni jukumu la Lee sasa kuitafuta atakapokuwa huko.
Kumbuka ilikuwa usiku. Lee akiwa peke yake baada ya maongezi hayo alijikuta anaugawa muda wake wa kupumzika kwa kufuatilia mitandaoni ziara ya kiongozi huyo huko Mongolia.
Akagundua alienda kufungua balozi yao huko na pia miradi kadhaa. Kwa makadirio akaona kiongozi huyo atadumu ndani ya nchi hiyo kwa siku zisizozidi mbili. Hivyo basi kesho anatakiwa kumaliza kila kitu.
Atatumia njia za vichochoro kuzama ndani ya Mongolia, mosi kwasababu ya usalama. Anaenda kufanya mauaji huko, hakutaka kubakiza harufu yoyote maana endapo akitumia njia rasmi anaweza akatiliwa shaka na hata atakapotafutwa ikawa rahisi kupatikana.
Pili, hakuwa na nyaraka stahiki.
**
Baada ya Miriam kukaa nje kwa muda mrefu, shangazi yake alimfuata na kumjulia hali. Alikuwa na uso uliopooza na macho yanayohakisi mawazo kichwani.
Shangazi akamuwekea mkono begani na kumuuliza kama ni lile lile ndilo linalomtatiza. Miriam akatikisa kichwa kuafiki. Alikuwa anamuwaza Jona.
Hapa siku za karibuni hakuwa na furaha hata chembe maana hakuonana na mwanaume huyo. Na zile taarifa za kuhusishwa na kumuua Kamanda na pia tena kutoroka jela, zilimtia kimuhemuhe sana.
Alikuwa anahofia sana maisha ya Jona. Aliona si mtu anayestahili hayo anayoyapitia kwa namna alivyo mtu wa kujali. Na hata pasipo kusita, kwa moyo wake wote, alikuwa anaamini Jona hakuhusika na mauaji ya Kamanda kwa namna yoyote ile. Japo hakuwa anajua kuna mchezo gani nyuma ya pazia.
Anajiuliza sana Jona yupo wapi. Na ana hofu kama mwanaume huyo atakuwa mzima wa afya kwani kama ingelikuwa yu mzima, anaamini angelikuja kumtembelea na kumjulia hali.
Ila hofu haijengi.
Hofu yanyima kula hata kunywa. Yanyima amani. Na hichi ndicho Shangazi yake alikuwa anamweleza. Kuendelea kuwaza namna ile hakutamfanyia chochote chema zaidi ya kumuumiza.
Akamsihi waende ndani. Na kama chambo kitaungua, basi watasikia tu harufu. Kama Mungu alivyomlinda yeye alipokuwa mikononi mwa wale wadhalimu, basi ndivyo atakavyomlinda na Jona kama vile wanavyomwombea kila uchwao.
Wakaenda ndani.
Basi kama ni kheri hii ilikuwa ya asubuhi. Kwenye majira ya saa mbili asubuhi mlango ukagongwa shangazi akaenda kufungua. Akamkuta Marwa mlangoni.
Akapatwa na hofu. Hakuwa anamtambua mtu huyo. Akiwa amekunja sura akamuuliza Marwa nini anataka, Marwa akamtaka kwanza amwambie kama hapo ni makazi ya Miriam. Alipomjibu akamweleza kuwa ametumwa na Jona kufikisha salamu.
Basi shangazi akamruhusu Marwa kuingia ndani na kumkutanisha na Miriam. Akamweleza kuwa Jona anamsalimu sana. Alikuwa hoi na pindi alipopata ahueni akamuulizia na kumwelekeza aje kumwona.
Miriam akafurahi sana. Akataka kumwona Jona ila Marwa akamwambia haitawezekana kwa sasa. Na ahakikishe hilo jambo linakuwa siri kupita kiasi. Jona atakuja kumtembelea yeye mwenyewe atakapotengemaa.
Marwa hakukaa sana, akaaga aende zake. Ila Miriam akamtaka angoje kwanza. Akaingia ndani na kutoka na karatasi na peni, akaandika ujumbe na kumkabidhi Marwa ampelekee Jona. Akamsisitizia sana ujumbe huo ufike mikononi mwa Jona.
Marwa akamuahidi. Kisha sasa akaenda zake.
**
Saa tatu usiku …
Jona alitabasamu punde aliposoma ujumbe wa Miriam. Hakika ulimgusa moyo wake na kumpa ahueni sasa ya kuwa mwanamke huyo ni mzima wa afya maana alikuwa anahofia huenda wakina Nyokaa wakawa wamefanya jambo kumdhuru.
Bado hakuwa na afya tenge, ila angalau kwa siku moja ya kutumia antidote, aliweza kutazama, kutambua na hata kunena. Pia kujisogeza huku na pale japo kichovu.
Alifurahi sana kumwona Marwa ni mzima. Kila saa alikuwa anamkumbatia kwa kutoamini. Alimshukuru pia na Miranda kwa kazi waliyofanya. Hata kabla hajaelezwa alikuwa anafahamu ni kazi kubwa imefanyika mpaka yeye kuwa pale.
Ila kutokana na hali yake bado kuwa si nzuri, Miranda na Marwa hawakuona kama ni muda sahihi wa kuanza kumchanganya mwanaume huyo mapema yote hiyo. Bado alikuwa anastahili kupumzika, tena sana.
Ndo maana hata huu ujumbe wake alikuja kuusoma saa hizi japo uliletwa kwa muda mrefu sana maana ndo muda aliofungua macho.
Marwa akamletea chakula na kisha akakaa naye kwa muda kidogo wakiteta. Akamuuliza kuhusu Miriam. Jona akamweleza kwa ufupi.
Marwa hakutaka kumpeleleza sana. Akatoa vyombo na aliporejea akamkuta Jona amekwisha lala. Antidote zilikuwa zinamchosha.
Basi akakaa pembeni yake na kuchukua ile karatasi ya Miriam na kuisoma. Akajikuta anatabasamu. Miriam alikuwa ana hamu sana ya kumwona Jona. Na akiapa siku hiyo itakuwa ya furaha sana kwake.
Marwa akaikunja vema hiyo karatasi, kisha akaiweka chini ya mto wa Jona. Akatoka chumbani.
Ila siku hii bado haikuwa imekwisha. Ndiyo kwanza ilikuwa imeanza. Kabla ya jua la kesho kuchomoza, kuna misheni mbili kubwa zilikuwa zinatakiwa kumalizika.
Mosi, Sarah kutambua kama Jona anaishi kwa Miranda. Na pili, Lee kummaliza makamu wa raisi ndani ya nchi ya Mongolia.
Litakalojiri, si mimi wala wewe anayejua. Ila ni wazi kiti kilikuwa cha moto.
Basi na muda ukasonga kama ilivyo ada. Ilipogonga saa nne ya usiku, mtu mmoja akazama ndani ya jengo la Miranda. Mwanaume huyu alikuwa amevalia suti nyeusi na barakoa nyeusi usoni.
Ni ajabu mtu kuvaa suti katika kazi kama hizi. Mtu huyu alijibana nyuma ya ukuta, akatazama usalama. Kulikuwa ni kimya na sebuleni alikuwa amekaa Miranda na Marwa wakitazama televisheni.
Huku vyumbani kote kulikuwa gizani. Na kule getini mlinzi alikuwa amejilaza kwenye kiti chake akichokonoa meno. Hakuwa anajua kinachoendelea.
Mwanaume yule mwenye barakoa akajongea dirisha la kwanza, akachungulia. Akatoka hapo akaizunguka nyumba kwa nyuma, kisha akatazama tena dirisha lingine.
Mara akasikia sauti ya kitu kikitembea. Akajibania kwenye ukuta kwanguvu, mkono wake wa kuume akiushikizia kiunoni ambapo aliweka silaha, bunduki ndogo.
Alipotulia hapo kwa sekunde nne, akagundua hamna hatari yoyote. Basi akaendeea tena lile dirisha na kuchungulia. Chumba hicho ndicho alalacho Marwa. Tayari ameshatazama anacholala Miranda, na anacholala Jona, ila hakugundua kitu. Kulikuwa na giza na pupa zake hazikumfanya akaona jambo zaidi tu ya mwili uliofunikwa nusu shuka.
Basi alipotoka tena hapo akawa amebakiza sehemu moja tu. Matumaini yake yote yakawepo hapo kuwa ndiyo itakuwa mahali penye kitu wanachokitaka.
Ila hakujua chumba hicho kilikuwa ni cha mfanyakazi wa ndani. Na msichana huyo hakuwa amelala. Ni muda mfupi ametoka kuoga na kumbe ndiye yeye ambaye vishindo vyake vilisikika hapo kabla.
Basi bwana yule mwenye barakoa, akachungulia. Akameona mwanamke huyu akijifuta. Napo akagundua si penyewe. Ila sasa akashindwa kutoka hapo upesi. Macho yake yaliganda kwenye mwili wa mwanamke ulio uchi.
Japo ilikiwa ni giza, akatumbua macho aambulie chochote kitu.
Akachukua hapo kama sekunde sita, msichana akagundua jambo. Akageuza shingo yake kutazama dirishani, mwanaume yule mwenye barakoa akajificha upesi.
Hakufanikiwa kumwona.
Mwanaume yule akanyata na kurudi kule alipojibania mara ya kwanza alipozama ndani. Akatulia hapo kwa sekunde kama nne tena, kisha akaanza kurejea zoezi lake kwa mara nyingine ili ahakiki kabla hajaondoka na jibu la mtu wanayemtafuta hayupo hapo.
Akapitia dirisha la kwanza. Salama salmin. Akiwa kwenye dirisha la pili, akasikia vishindo vikubwa! Haraka akajivuta na kujibana kwenye kona ya mbele.
Alisimama hapo kwa tahadhari sana. Na vishindo vile alivyosikia havikukoma, vikaendelea kujita kumfuata. Akatambua wazi kuwa ajaye ni mlinzi.
Sasa zoezi likawa linaendea kubadilika. Hakutaka kuacha alama yoyote hapa ila ikaanza kuonekana itashindikana maana endapo mlinzi huyu akimwona, basi hatoweza kumwacha hai.
Vishindo vikaendelea kusonga. Miguu hii ya mlinzi ilikuwa inaburuza haswa. Sijui alijifunzia wapi ulinzi huyu bwana. Alipiga hatua nne zaidi, na hamaki akajikuta mikononi mwa mvamizi!
Kilichosikika hapo ni mtu akigugumia tu, na mlinzi akawa amemaliza habari yake. Akatuliwa chini taratibu na yule jamaa sasa akawa yupo huru zaidi. Sasa akatazamia madirisha yaliyobakia.
Akanyata na kunyata. Akatazama lile dirisha la chumba anacholala Jona, hapo akasita kidogo. Akajiwa na fikra. Kamaa kule sebuleni yupo mwanaume na mwanamke, na kile chumba kingine yupo mwanamke, hichi yupo nani?
Kabla hajaacha dirisha hili, akachomoa kurunzi yake ndogo na kumulika ndani. Mwanga wa kurunzi hii ulikuwa mdogo, kaduara kake ka mwanga kalikuwa chenye ukubwa wa sarafu ya mia mbili.
Akaangaza usoni mwa mtu yule aliyekuwa amelala, akagundua ni Jona! Akajikuta anatabasamu.
Ila sasa alivyo mjinga, asiondoke akataka kwenda kwenye lile dirisha la msichana wa kazi akatazame tena. Basi akanyata na kufika hapo, akachungulia. Hakumwona mwanamke.
Akazubaa hapo kwa sekunde kama tano akiangazaangaza maana ilikuwa giza. Ila punde akasikia sauti ya mguu ukiburuza. Akaangaza upesi. Kidogo akatokea mtu konani, alikuwa ni Miranda!
Mwanaume yule mwenye barakoa akatupa risasi mbili. Miranda akawahi kujificha ila alikuwa tayari amejeruhiwa. Bega lake la kushoto lilikuwa linachuruza damu!
Bwana yule mvamizi asipoteze muda akadaka ukuta na kurukia nje. Miranda naye akajaribu, ila maumivu ya mkono yakampatia shida. Japo alifanikiwa, ila hakuwa ndani ya muda. Kwa mbali akaona gari likiyoyoma kwa kasi!
Akarudi zake ndani. Sebuleni akamkuta msichana wa kazi ma Marwa. Haraka wakampatia huduma ya kwanza kwa kumtia dawa ma kumfunika jeraha. Uzuri risasi haikupenya ndani, bali iliparaza bega na kwenda zake.
Wakiwa wanampatia huduma hiyo, msichana wa kazi akaeleza namna alivyotilia shaka kwamba kuna mtu nje. Na zaidi hisia zake hizo zikathibitishwa na sauti ya mguno. Kumbe ndo ile iliyokuwa ya mlinzi.
Hapo Miranda akapata maswali. Ni nani yule mtu na alikuwa anafanya nini. Kwa akili ya kawaida, baada ya kujadili, wakagundua watakuwa ni watu wa Sheng. Na hapo walikuja sababu ya kumtafuta Jona ndiyo maana walikuwa wanapeleleza dirishani.
Sasa wakapata shaka. Kama watu hao watakuwa wamegundua kuwa Jona yupo hapo, watafanya nini?
**
Ngo! Ngo! Ngo!
Shao akafungua mlango. Uso kwa uso akakutana na kijakazi wake aliyevalia suti. Akamkaribisha ndani na wakaketi sebuleni. Kijakazi yule akampa mrejesho wa kazi waliyotoka kufanya.
Amemwona Jona, yupo mikononi mwa kijakazi wa BC. Ila akaeleza pia ameonekana alipokuwa akifanya kazi hiyo. Hapo Shao akaghafirika!
Akalalama kazi imeharibika kwani watu hao watachukua tahadhari kutokana na tukio hilo. Hapo hamna kazi yoyote iliyofanyika!
Akamtaka kijakazi huyo aende zake amwache mwenyewe afikirie cha kufanya. Kijakazi akaenda zake. Shao akafikiri sana. Mwishowe akaona sasa cha kufanya ni kuanza kupanga mipango ya kuwashambulia wakina BC maana ameshajua Jona yupo mikononi mwao.
Akawaza kama kazi hiyo anapaswa kumshirikisha Sheng, akaona haina haja. Ataifanya na kuimaliza mwenyewe.
**
Hakuwa amepumzika siku hii nzima. Kutwa allikuwa kwenye safari, na hata usiku huu hakuwa mtu wa kupumzika bali yupo kazini.
Tayari Lee ameshazama ndani ya Mongolia, kitambo tu. Na tayari alishasonga eneoni ambapo anatakiwa kufanya tukio. Eneo ambapo makamu wa raisi wa China yupo kimalazi.
Eneo hilo lilikuwa linalindwa na watu lukuki hapo nje. Na pia huko ndani walikuwa watu kadhaa wakienda huku na kule.
Lee akatoa hadubini na kupekua eneo hilo kila pande. Alikuwa umbali wa kama kilomita mbili na nusu. Aliporidhika na alichokipata kwa hadubini, akairejesha begini alafu akavalia barakoa.
Mwanaume akazama kazini.
Ni mwendo wa dakika chache kuwasili ndani ya eneo la tukio kwa namna alivyokuwa anatembea. Alitulia kidogo na kuangaza, eneo lilikuwa linalindwa haswa. Akapiga hesabu kama anaweza kufanikiwa kuingia ndani pasipo kuleta taharuki.
Ilikuwa ngumu. Kila mahali palitapaka walinzi na taa nazo zilikuwa zinaharabu mahesabu. Ilikuwa ngumu kujibanza ukiwapo ndani.
Basi akawa mvumilivu kidogo, akatazama wale walinzi wanaozunguka kwa nje na kutambua mienendo yao. Akasogelea mti uliokuwapo karibu, akakwea kwa haraka alafu akapekua tena mazingira.
Akavuta subra. Kisha kidogo akatoa kakifaa kwenye mkoba wake, kakitu kama kafilimbi rangi nyeusi, akakiweka mdomoni na kukipuliza kwanguvu. Ndani yake kulikuwa na kakipini kadogo chembamba.
Kaliruka na kumkita mlinzi mmoja shingoni kwa usahihi wa hali ya juu! Yule mlinzi akaguna akikunja sura. Kabla hajanyofoa kapini hako shingoni, akajikuta amedondoka chini na kupoteza fahamu!
Lee akataka kurukia ndani, ila akawahi kusita. Alimwona mlinzi mwingine akija upande ule aliokuwa amelala mwenzake chini. Akafika na kustaajabu. Haraka Akaweka kidole chake sikioni akiminyia kufanya mawasiliano na wenziwe.
Ila kabla hajafungua kinywa, chap! Kipini kikamchoma na yeye shingoni, akadondoka chini baada ya sekunde mbili tu!
Sasa Lee akajitupia ndani, akafikia kwa kujituliza na sarakasi. Kisha upesi akaikusanyia miili ya wale watu ukutani, akaifunika na shuka jeusi alilotoa begini, ikaonekana kama kamlima fulani kadogo.
Alafu haraka akasonga akifuata mlango akichomoa kapini fulani ambacho alifungulia kitasa na kuzama ndani.
Kulikuwa kimya.
Alitulia kwa sekunde kama nne akiwaza namna ya kufanya na pia akiskizia huko nje kama wamebashiri lolote. Zilipokwisha sekunde hizo nne, akajongea taratibu.
Ndani kulikuwa na mwanga lakini ilikuwa ngumu kubashiri kama watu wamelala ama lah maana palikuwa kimya na kwa wakati huohuo taa zikiwa zinawaka kila eneo.
Kazi ikawa kwa Lee kutambua ni wapi alipo mtu anayemlenga. Hapa alihitaji kuwa mwangalifu na msikivu mno. Alipotulia kwa sekunde kama tatu, kazi ikawa nyepesi kuliko alivyodhani.
Alisikia sauti ya mtu bafuni akisafisha koo. Bila shaka akamtambua kama ndiye mlengwa wake. Basi akanyata kufuata bafu. Akatulia hapo kidogo, kama baada ya dakika hivi, mlango wa bafu ukafunguliwa.
Akatoka bwana mmoja wa kichina, ana kiwaraza hafifu na mwili wake umemomonyoka kizee. Basi haraka Lee akamminya bwana huyo na kumweka ndani ya uwezo wake. Hata kelele hakuwa anaweza kupiga!
Ila alipomtazama … alipomtazama akagundua hakuwa makamu wa raisi! Akastaajabu. Basi akiwa amemminya bwana huyo, akamuuliza yeye ni nani? Na makamu wa raisi yupo wapi?
Bwana yule akiwa amebanwa na hofu kuu, na akiwa amebanww mbavu katika namna ambayo hawezi kuongea kwanguvu, akasema yeye ni msaidizi wa makamu, ila akasema hajui makamu alipo!
Lee akaghafirika maana alijua wazi bwana huyo anaongopa. Ni lazima tu atakuwa anajua mlengwa wake alipo. Akamminya zaidi, ila bwana yule hakuwa tayari kusema!
Lee akamziraisha alafu akamlaza chini, akaenda kukagua vyumbani. Akatazama chumba cha kwanza, humo akakuta wanawake wawili wembamba wakiwa wamelala. Ina maana wanawake hawa walikuwapo hapo kumhudumia msaidizi yule wa makamu au makamu mwenyewe.
Lee akaenda chumba cha pili. Taa ilikuwa inawaka ndani, huenda makamu akawa hajalala, akawaza. Basi cha kufanya akagonga mlanga mara mbili na kuskizia.
Akasikia sauti nzito ikimwamuru aingie ndani. Akafungua mlango na kuzama. Kutazama, uso kwa uso na mlengwa wake! Alikuwa mwanaume mwembamba mwenye makadirio ya miaka sitini ya mwishoni ama sabini za mwanzoni.
Usoni alikuwa amevalia miwani ya macho. Nywele zimekuwa kama za kahawia kwa mvi za mbali. Alikuwa amevalia kaushi nyeupe na bukta fupi. Amekalia kakiti kadogo kalichopakana na meza ya saizi yake. Juu ya meza hiyo ndogo kulikuwa kuna karatasi kadhaa nyeupe, na diary yenye kava gumu jeusi.
Basi ile kutazamana, bwana makamu akapatwa na woga sana! Akatazama kando upesi kama mtu atafutaye silaha, ila upesi akatupiwa pini shingoni, akanyeta. Punde akaanza kuona mbilimbili, mara kichwa puh mezani!
Lee akafunga mlango na kumsogelea. Akakusanya kila kitu chake na kisha akatengua shingo kumfanya mfu! Akatoka na kwenda kumkuta yule bwana aliyemziraisha. Naye hakumwacha salama, akamtengua shingo kumfanya mfu!
Sasa akabakia na kazi ya kutoka mule ndani. Pengine inaweza ikawa kazi kubwa kuliko kuingia, akatazama kushoto na kulia, wakapita walinzi wawili. Alipoona mazingira murua, akatoka chap kwenda ukutani.
Ila alipofika na kabla hajatoka, mlinzi mmoja akamwona! Akagutuka. Haraka mlinzi akachomoa bunduki yake ndogo na kuifyatua risasi mara mbili! Ila bahati haikuwa kwake, haikumpata mlengwa!
Lee akachumpa nje na kuanza kukimbia kwa kasi. Wale walinzi nao wakajikusanya na kumkimbiza Lee ambaye alikimbilia huko msituni.
Walitoka hapo kama wanaume kumi. Wote wakiwa wamebebelea silaha. Ila hawakufua dafu msituni humo Lee akafanikiwa kuwapotea na kwenda zake salama salmini.
Alikuwa ameegesha pikipiki kubwa mahali, akaiwasilia na kuitia moto, safari ikashika hatamu. Hakutaka hata kubaki Mongolia kabisa, alikuwa amelenga siku hiyohiyo kutoboa mpaka China.
Kazi aliyotumwa alikwisha itekeleza. Tena kwa ustadi mkubwa.
Haikuwa hata na haja ya kuitangaza kwani jua likipanda kesho yake tayari habari zitakuwa zimeshasambazwa na vyombo vya habari kuwa makamu wa raisi na msaidizi wake wameuawa huko nchini Mongolia na mtu asiyejulikana!
**
Saa tatu asubuhi …
Shao alikuwa na kikao kifupi na vijakazi wake kumi. Walikuwa katika mpango mkakati wa kufanya jambo, tena kubwa na lenye madhara.
Vijakazi wote walikuwa tuli wakimsikiliza mkuu wao, na yeye Shao akatumia huo mwanya kueleza kinagaubaga jambo la kufanyika. Naam. Hakutaka muda upotezwe, bali uhai wa adui.
Alichotaka ni kuletewa kichwa tu. Haijalishi risasi ngapi zitatumika ila jambo litekelezeke, yupo tayari kugharamia kila risasi kugharamia kila risasi itakayopotea kwenye uwanja wa vita.
Basi na wasipoteze muda, kikao kikafungwa na wakaahidiana kukutana tena hapo majira ya saa sita usiku.
**
Saa tatu usiku …
Gari aina ya Subaru iliyobebelea wanaume watano ilisimama na kuzimwa kabisa. Wanaume hao wakateta kidogo kisha wakatoka wote garini isipokuwa dereva.
Wote hawa walikuwa wamevalia mavazi meusi na kofia za soksi kichwani. Na hata kwa kuwatazama upesi ungeligundua walikuwa wamefichilia silaha za moto.
Wanaume hawa wakatokomea dereva akiwatazama mpaka wanaishilia. Walikunja kona kama mbili kufika mahali walipokuwa wanaelekea. Wakaruka ukuta, na kuzama ndani.
Kulikuwa ni makazi ya Miranda!
Kimya.
Wakagawana pande. Wakachomoa na silaha zao kuziweka vema viganjani kwa ajili ya kazi. Wawili wakaendea kibanda cha mlinzi, kutazama hamna mtu.
Kwa ukimya wa hali ya juu, wakasonga kuufuata mlango. Na wale wa nyuma na wao wakasonga mlango wa ziada. Wakatulia hapo.
Ndani taa zilikuwa zimewashwa. Na sauti moja ya kike ilikuwa inasikika kwa mbali kuashiria kuna mtu humo.
Basi wale wavamizi, wakahesabu mpaka tatu, wakazama ndani kwa kuvunja mlango kwa mateke yao mazito.
Wakaangaza huku na kule. Hamna kitu! Ila bado ile sauti ya kike ilikuwa inasikika.
**
Wakatazamana kwa duwazo. Kisha wakiwa wamebebelea silaha zao, wakasonga kwenda mavyumbani. Wakapekua kivita, hawakuona kitu! Ila mule chumbani sauti ilipokuwa inatokea, wakaukuta mdoli kitandani.
Aaagh!
Mdoli ulikuwa umerekodiwa na kuachwa hapo ucheze wenyewe. Wote wakakusanyika na kuutazama mdoli huo. Ulikuwa ni wa kike, nywele ndefu za kupendeza na macho makubwa yenye nyusi ndefu. Nyuma ya mgongo wake alikua ana kitu fulani kigumu. Wakamfunua nguo na kumtazama. Ilikuwa spika! Basi bwana yule aliyemshikilia mdoli huyo akasonya na kumminya huyo mdoli kwa mkono wake mpana.
Yule mdoli akasinyaa na kuvunjika. Ila baada tu ya sekunde nne, wakaanza kukohoa mno. Kumbe yule mdoli alitoa hewa fulani na hiyo hewa kwa upesi ikasambaa ndani ya kile chumba.
Hao mabwana wakakohoa sana. Wakatoka ndani ya chumba wakiwa wanajikokota wakipaliwa na kikohozi. Hata macho yakawa mekundu kwa kukohoa!
Hawakupata wanachokitaka, na zaidi wakapata matatizo. Walijikokota mpaka kwenye gari yao wakazama ndani. Wakaendelea kukohoa sana kiasi cha kushindwa kuongea.
Baada ya dakika kama kumi, bado wakiwa hapohapo hawajaenda popote, angalau wakapata ahueni. Wakamweleza yule dereva kuwa mule ndani hamna mtu! Hawajamwona yoyote yule na huenda kabisa likawa tego. Walengwa wao watakuwa waligutuka mapema kuwa watakuja kuwatembelea.
Basi dereva akaleta ubishi. Akawauliza kama kweli walipekua vema. Wale mabwana wakasema walitazama kila eneo na walichokiambulia ni mdoli tu kitandani ukiwa umerekodiwa sauti!
Sasa kukawa hamna namna. Ikabidi waende zao, wale mabwana wakiendelea kukohoa sana na sana.
**
Basi zikapita kama dakika chache. Ndio, ni chache si nyingi, Miranda na Marwa wakawa wamezama ndani ya jengo lao ambalo lilitoka kupekuliwa muda si mrefu.
Walifika katika kile chumba, kile ambacho kilikuwa na mdoli, Miranda akamwokota yule mdoli chini akitabasamu. Akamtazama Marwa na kumwambia kwamba mpango wao umeitika. Kile walichokipanga kimezaa matunda.
Wasipoteze muda, wakaondoka hapo isijulikane wameenda wapi.
**
Baada ya mlango kuita mara moja tu, Shao akafungua na kukutana na kikohozi cha watumishi wake. Hata ndani hakuwakaribisha akawauliza kwa pupa imekuwaje?
Wakamweleza ya kuwa kule hawajapata kitu chochote, zaidi wameambulia maradhi! Shao afanye nini zaidi ya kukasirika?
Alikasirika mno, akang’ata meno yake na sasa akaridhia na akili yake kwamba maadui zao watakuwa walishatambua kuwa watatembelewa.
Sasa afanyaje? Akajiuliza. Akawataka wale watu waende zao wamwache afikiri na kupanga lingine. Asubuhi na mapema atawajuza namna ya kufanya.
Basi wale wajakazi wakaenda zao.
***
Hali haikuwa nzuri kabisa kwa usiku huu mzima. Wale mabwana wanne walikohoa sana na hawakupata nafasi haya ya kufumba macho kufurahia lepe la usingizi.
Walikohoa mno. Kadiri muda ulivyokuwa unasonga ndivyo walivyozidi kukohoa, mwishowe wakakosa pumzi na kujifia!
Yani kama vile mchezo. Mpaka jua linachomoza kesho asubuhi yake, watu hao wakawa wamekauka kaukau!
Maiti zao zilikakamaa kama mibuyu! Shao akapewa taarifa na akaenda kuwaona kabla hawajawazika. Akatahamaki na akasihi mwili mmoja ubakizwe kama sample watazame ni nini kiliwakumba.
Baadae walipofanya hivyo, wakagundua kuwa watu hao walikuwa wamevuta hewa mbaya ya ukaa. Mapafu hayo yalikuwa meusi kama mkaa na koo lao la hewa lilikuwa limetobokatoboka!
Hapa Shao akatambua kuwa hata wale wakina BC wako vema kwenye ‘chemical weapon’. Ilimpasa awe makini zaidi.
Ila kama kuna kitu ambacho alikuwa anaridhia na nafsi yake ni kwamba hajashindwa vita.
Bado ana uwezo wa kumpata na kummaliza Jona. Cha kufanya ni kuja tena na mpango mwingine. Na sasa anatakiwa kutumia sana maabara kumaliza kazi yake.
**
Majira ya kumi na moja jioni …
Shao alizama maabara na kuvalia mavazi yake ya kazi. Koti jeupe na maski ya kubana pua na mdomo, pia na glovu za mikononi kujilinda.
Akatumia kama masaa matatu akiwa humo maabara. Alikuwa peke yake. Na macho na mikono yake ikafanya kazi barabara kuitikiwa wito akili yake. Alichukua hiki akachanganya na kile, kile akachanganya na hiki na mwishowe akajikuta anapata kimiminika cha kijani iliyokolea.
Akakitikisa na kukitazama kikiwa ndani ya tube. Kukihakiki, akatwaa panya watatu wakubwa, na mmoja wao akamminyia kemikali hiyo mwilini akitumia bomba la sindano.
Yule panya akadumu kwa sekunde moja, mara akaanza kutapatapa akimimina damu. Na isichukuwe muda akafa! Ila hata baada ya kufa, Shao hakumtoa, badala yake akaendelea kuwatazama wale panya mpaka zilizopohitimu dakika tatu.
Hakuona mabadiliko! Akasonya. Si hicho alichokuwa anataka. Basi akamtoa panya yule aliyekufa kisha akawabakiza wale wawili.
Akarudi tena kwenye ‘experiment’ zake na baada ya punde akawa amepata mchanganyiko mwingine ambao ulikuwa ni wa kijani kupitiliza hata kuelekea kuwa nyeusi!
Akaifyonza na bomba la sindano na kumdunga panya mmoja, kisha akatulia na kuangaza.
Yule panya akadumu kwa sekunde tano tu, na tofauti na yule wa kwanza, huyu hakutapatapa kabisa, alidondoka chini ghafla baada ya moyo kusimama!
Ila Shao hakumtoa na badala yake akaendelea kumtazama panya huyo. Na kama vile dakika moja, yule panya mwingine ambaye hakuwa amedungwa kemikali, akaanza kudhoofu! Alianza kuyumba kama chombo kiendacho mrama, na mara akadondoka na kufa!
Shao akatabasamu. Sasa alikuwa amepata anachokitaka.
**
Majira ya saa mbili usiku ..
Kwa huku nje kulikuwa kumetulia tuli. Ni hatua tu nzito za walinzi hapa na pale ndizo zilikuwa zinasikika.
Ni hapa karibu na ofisi ya Sheng.
Taa za ndani ya ofisi zilikuwa zimezimwa kuashiria hakuna mtu humo ndani. Ila …
Ni kama vile ungetulia vema ungesikia sauti za watu kwa mbali. Labda ungewaza ni masikio yako ila ndani ya muda mfupi sauti ya kitasa ilijita, na mlango ukafunguliwa kistaarabu akatoka bwana mmoja aliyekuwa amevalia nguo nyeusi kama walinzi wengine wazungukao eneoni.
Bwana huyo alitoka kwa tahadhari, na baada ya punde akanyanyua miguu yake kutokomea.
Lakini …
Huyu bwana hakuwa mgeni machoni petu. Kama kumbukumbu zi vema, huyu bwana ni mmoja wa wale wateuzi kumi wa bwana Shao kwa ajili ya kazi yake. Sasa nini alikuwa anafanya ofisini kwa Sheng tena wakiwa kizani?
Vilevile taa ikiwa haijawashwa, mule ndani ya ofisi ya Sheng, simu ya mezani ikanyakuliwa na kupachikwa sikioni kisha punde sauti ya Bwana Sheng ikauliza kama aongeaye naye ni makao polisi.
Baada ya hapo, akatoa taarifa ya kwamba Jona anashikiliwa na mwingereza bwana Brown Curtis hivyo wakafanye msako kwenye nyumba yake haraka iwezekanavyo!
Aliposema hayo akapachika simu mezani. Tulipata kutambua hilo kwa sauti, kisha akaketi na kusema kwa lugha ya kichina, acha tuone nani atakayekuwa ndege wa alfajiri.
** Ni nini alimaanisha bwana huyu? Ni nini anadhamiria kufanya na mbona jambo hili hakumshirikisha Shao? Kwanini alifanyia maongezi haya ndani ya kiza?
Pengine unawaza hali ya Jona na wenzake ukasahau kujiuliza maswali hayo.
Basi siku hii ikaenda. Kesho yake majira ya asubuhi tu, Shao akaamkia ndani ya maabara. Akachukua ile kemikali yake aliyoitengeneza jana yake na akaanza kuifanyia taratibu kuigeuza kuwa katika mfumo wa hewa.
Alifanya zoezi hilo kwa muda wa masaa matatu, kumbuka alikuwa yu mwenyewe, na hatimaye alipogeuza kemikali hiyo kuwa hewa, akaijaribisha kwa panya aliowatoa kwenye hifadhi yake, na punde tu panya hao, watatu kwa idadi, walipovuta hewa ya kemikali hiyo wakafa pasipo kuomba maji!
Shao akatabasamu. Kazi ilikuwa kufyonza tu hewa hiyo na kuiswekwa kwenye kontena zake maalum.
Aliazimia kemikali hiyo kutumika usiku wa siku hiyo. Kwa matarajio yote aliamini itamletea matunda anayoyataka.
**
Saa tano asubuhi …
Gari, defenda kama yalivyozoeleka kuitwa, ya polisi ilitua mbele ya geti na honi ikapigwa mara nne, geti likafunguliwa na gari likazama ndani.
Lilikuwa limebebelea askari wanaume watano kwa nyuma, na wawili upande wa dereva ambao wao walikuwa wamevalia nguo za raia. Gari hili liliposimama tu, askari wale wakashuka upesi.
Watatu miongoni mwao walikuwa wamebebelea bunduki na mmoja ameshikilia redio koo mkono wa kuume.
Kibarazani alikuwa amesimama BC akishangazwa na ujio huu. Alikuwa amevalia gauni la bafuni alilolifungia vema kiunoni. Alidaka kiuno chake akijiuliza maswali kichwani, punde askari wakamfikia na kumweka chini ya ulinzi, na wakamweleza haja yao kuwa ni kufanyia upekuzi eneo hilo lote maana wanahisi litakuwa linahifadhi mtu wanayemtafuta.
BC akashangaa na hata akawaambia kwamba hamna mtu wanayemhitaji humo. Pia hawana haki ya kumweka chini ya ulinzi kama madai yao hayajathibitishwa.
Pia akawasihi wangoje ampigie na kuongea na mwanasheria wake kwanza.
Madai yake yote hayo yakapuuzwa, askari hawakumzingatia hata kidogo. Wakamweka chini ya ulinzi na kumtia pinguni kisha wakaanza kufanya upekuzi hadidi.
Wakapekuwa kila pande ya nyumba na wakagundua kuwa mwanaume huyo alikuwa na baadhi ya kemikali maabarani mwake. Ila hawakufanikiwa kumpata yeyote yule. Hata yule waliyekuwa wanamdhania yumo.
Basi wakambeba BC na pia wakawasilisha kemikali zake zote walizozitoa maabara na kuzipeleka moja kwa moja kwenye ofisi ya mkemia mkuu kwa ajili ya uchunguzi na maelezo zaidi ya kitaalamu.
Bwana yule mzungu akaswekwa rumande.
Na kama haitoshi, kamanda wa mkoa akaitisha ‘press conference’ kuwaambia waandishi na wananchi nini kimetokea. Lengo kuu hapa lilikuwa ni kufanya jeshi lionekane ‘linashughulika’, halijashindwa na kila kitu kipo kwenye ‘mikono yao.’
Hivyo japo hawakumpata Jona, bado kutangaza kwenye vyombo vya habari ilikuwa ni turufu! Hata bwana Sheng hili jambo lilimpendeza machoni.
Na baadae kwenye majira ya jioni, bwana huyo wa kichina akaenda kuonana na Kamanda mkuu. Akamweleza kuwa bwana huyo wa kizungu waliyemtia kizuizini anajua fika wapi alipo Jona. Wanachotakiwa kufanya ni kumbana mpaka aseme.
Kamanda akamwambia aondoe shaka, atalisimamia hilo kwa nguvu zake zote. Ila akamsisitizia tena kuwa jambo lao liwe la siri, hata wenzake hawatakiwi kulijua.
Kamanda akamtoa hofu. Na Sheng hakukaa sana, akaenda zake kurudi makaoni.
**
Baadae majira ya usiku …
Hodi iligonga mara mbili kwenye makazi ya Sheng. Alipopokea hodi hiyo, akazama ndani Bwana Shao aliyekuwa amevalia suti ya traki rangi nyeusi. Akaketi na kumwambia Sheng juu ya habari zile za polisi kumvamia na kumkamata BC.
Akaeleza namna alivyoshangazwa na habari hiyo maana walikuwa katika mpango. Ila akamuuliza bwana Sheng kama amehusika kwa vyovyote na hiyo oparasheni.
Sheng akakataa, na hata akasema aliwaza pengine ni yeye, yaani bwana Shao, ndiye aliyefanya hilo.
Basi baada ya kwenda tofauti kimaudhui, Shao akamuuliza Sheng kuhusu hilo jambo. Ni nini msimamo wao kwenye hili? Watafanya nini sasa?
Sheng akatikisa kichwa kwanza alafu akamwambia Shao kuwa yeye ahusiki na wala hatahusika na chochote kile kwani kila kitu alimkabidhi yeye.
Na hata akamkumbusha kuhusu ile HATI yao ya kifo. Shao akashangazwa. Asiseme kitu, akaaga na kwenda zake!
**
majira ya saa tano asubuhi …
Mwanaume mzungu aitwaye Henry Marshall alifika kituoni akiwa amebebelea briefcase nyeusi na pia amevalia suti nyeusi iliyomkaa vema mwilini.
Mwanaume huyu alikuwa ni mwenye nywele rangi ya ‘brown’. Macho yenye kiini cheusi. Mwili wake ulikuwa mwembamba na wenye nishati ya kutosha. Alikuwa anatembea kwa ukakamavu. Na macho yake ndani ya miwani nyeupe ya macho, yalikuwa yanaangazaangaza huku na kule.
Akajitambulisha kwa jina na pia dhumuni lake kuwapo hapo. Yeye ni mwanasheria wa Bwana Brown Curtis. Amekuja hapo kwa dhumuni la kumtetea mteja wake.
Na bwana huyo akawachachafya askari hao akiwaambia wamekiuka sheria kwa kumsweka ndani mteja wake kwa mashauri yasiyo na uthibitisho na hata pasipo kuongea naye kama mwanasheria.
Japo bwana Henry alijieleza vema kutokana na nafasi yake, wale askari hawakutaka kumwelewa kabisa. Hata kuonana na Brown Curtis hakuruhusiwa. Basi akaenda zake akisema atalipeleka shauri hilo mahakamani.
Na ana uhakika atashinda, na hilo shauri litaigharimu serikali pesa kubwa!
Hakuwa anatania. Alikuwa ni mwanasheria wa hadhi yake toka Uingereza. Tena anayefahamu vema sheria nje na ndani. Aliapa kulifanyia kazi jambo hili kuonyesha thamani ya pesa anayolipwa na mteja wake.
**
Saa nane mchana …
Simu iliita kwa muda mfupi tu, Kinoo akapokea na kuiweka sikioni. Alikuwa ni Miranda anampigia na tayari alikuwa anajua mwanamke huyo anataka kuongelea nini.
Nalo si jingine bali swala la BC. Akapokea simu na kuteta. Miranda akamtaka waonane haraka iwezekanavyo kupanga namna ya kufanya kwa ajili ya bosi wao.
Ikachukua kama nusu saa tu, wakawa wamekutana na kujiweka ndani ya gari kunena mawili matatu. Basi Miranda akamwambia Kinoo kuwa inabidi aende kumtembelea BC kule kituoni maana yeye wanaweza kumhisi kwa namna moja ama nyingine kuwa anahusika na Jona kwani alishawahi kufika huko mara kadhaa.
Ila Kinoo naye akasita, akaeleza hofu yake. Vipi kama naye akikamatwa? Miranda akamsihi hamna muda wa kuhofu, na hawana machaguzi mengine zaidi ya kutenda.
Na hapo anapoteta naye, tayari ashafikisha habari za Brown Curtis makao makuu, hivyo wanaweza wakatumwa mawakala hivi karibuni.
Basi Kinoo akaridhia, ataenda kuonana na BC kesho asubuhi na mapema. Ila akamuuliza Miranda, vipi kuhusu bwana yule, Jona? Wapi alipo na anaendeleaje?
**
Katika namna ya ajabu, Miranda akasita kumweleza Kinoo juu ya maswali hayo. Akamtaka aende akajiandae na yeye aende zake maana kuna eneo anapitia.
Kinoo akashuka toka garini na kisha akasimama akishuhudia gari la binti huyo likitokomea.
Ila kuna jambo lilimjia kichwani. Ni kama radi jambo hilo lilikuja upesi. Akawaza namna ambavyo Miranda amekuwa kama mtu wa ‘kumtenga’ siku hizi.
Amekuwa si wa kumshirikisha na wala kumhitaji kama ilivyokuwa huko nyuma. Kwa namna moja ama nyingine alipata wivu wa kiume. Aliona kama vile Jona na mwenzake Marwa wametenganisha familia yake.
Nafasi yake imezibwa na hao watu.
Akawaza.
Kama hali ipo hivyo na huyo Jona bado yupo kitandani, vipi akiamka na kurejea kwenye hali yake? Atakuwa na nafasi hata robo?
Alihofia.
Aliwaza akiwa anatembea kurejea nyumbani kwake. Alipofika ndipo mawazo hayo yakaenda zake na kuacha nafasi ya kuwaza mengine. Ya mkewe.
Hakuwa amemkuta hapo nyumbani na hakuwa anajua wapi kaenda. Akalalama yaani kutoka kidogo tu naye keshafungua mlango!
“Mwanamke huyu!” Akatikisa kichwa. Akanyakua simu na kumpigia. Nayo ikaita mara tatu pasipo majibu. Akasonya na kujiongelesha mwenyewe.
“Sijui nimfanye nini. Na hivi ana ujauzito, basi keshapata sababu haswa!”
Akalalama na kulalama. Hata kama angelitukana isingelisaidia kwani mtuhumiwa hakuwapo wala hakuwa anasikia, wala kujali.
**
“Kama nilivyokuambia, kumbe yule muuaji alikuwapo huko,” alisema Sasha kisha akashushia na juisi. Akamtazama dada yake, Sarah, na kuendelea kumwambia,
“Wewe umekaa siku zote hizo, umekalia pesa dada yangu. Ina maana hujui kama donge nono lilitangazwa kwa mtu atakayetoa taarifa zitazosaidia upatikanaji wake?”
Sarah akapandisha mabega akisema hana habari kabisa. Na hata kama angelikuwa na habari asingelifanya lolote kwani hakuwa anajua kama wakina Kinoo wamemuhifadhi jamaa huyo.
Basi Sarah akaendelea kumpasha habari. Akamwambia taarifa zake zilishafika polisi na hata walipoenda kumsaka, hawakumwona, tayari wameshamuamisha!
“Sasa dada yangu, nataka tupige hela kama wehu! Najua wewe utakuwa unajua wapi alipo. Tumbua basi tupige hizo milioni kisha twende zetu Ibiza huko mbali na ulimwengu.”
Sarah akatikisa kichwa. Akatazama kinywaji chake mezani, juisi ya embe, ambayo haikuwa imeguswa kabisa, kisha akasema:
“Yani wewe unakuwa kama sio dada yangu yani. Mbona unakuwa zoba zoba wewe bana! Unashindwaje kujua na wakati unaishi na yule mwanaume?”
“Sasha!” Sarah akaita kwa tahadhari. “Nakuapia kwa Mungu wangu, yule mwanaume muda si mrefu atahisi huu mchezo tunaoufanya. Kabisa nakwambia. Ndipo anapoelekea.”
Sasha akapeleka mdomo wake pembeni. “Uoga wako tu huo! Unadhani atakufanya nini na umebeba mimba yake? … hana ujanja wowote.”
Sarah hakusema kitu. Akajaribu kunywa kinywaji chake ila hakikupanda. Alipokunywa fundo moja tu, akarejesha glasi chini. Akasema,
“Naomba niende.”
“Nimekuudhi?” Sasha akajishuku.
“Hapana,” Sarah akajibu. “Naona tu muda umeenda. Nahisi yule bwana atakuwa amerejea nyumbani isije kuwa nongwa bure.”
“Ok!” Sasha akasema na kisha akanywa fundo za nguvu kumalizia juisi yake mezani, alafu akanyanyuka.
“Twende nikusindikize.”
Akampeleka Sasha hatua kadhaa akiendelea kumshawishi afanye kazi yake ya kupeleleza alipo Jona. Sarah akaahidi kulifanyia kazi, ila si kwa haraka hivyo. Akajikweza kwenye gari na kuondoka zake.
Sasha akatoa simu yake ya mkononi na kupiga. Akaongea na huyo wa kuongea naye kwenye simu ya kwamba ameshapiga hatua moja. Wavute subira kuona matokeo yake, kisha akakata simu.
**
Kesho yake, majira ya saa nne, central …
“Nimekuja kuonana na mfanyakazi mwenzangu,” alisema Kinoo akimtazama askari machoni pasi na woga. Askari akamtazama kwa jicho la uchovu wa kebehi na kumuuliza,
“Nani huyo mfanyakazi mwenzako?”
“Yule mzungu aliy …”
“Yule jambazi!” Askari akaropoka.
“Hapana, si jambazi,” Kinoo akamtetea.
“Ni nani basi?” Askari akauliza. “Mtu anayemficha jambazi ni nani kama sio na yeye ni jambazi?”
“Afande, hakuwa amemficha yeyote. Sidhani kama mtu huyo mnayemwongelea alionekana kwenye jengo lake baada ya msako mlioufanya.”
“Sawaa? … kwanza nenda zako kabla sijakuweka ndani na wewe. Wewe mwenyewe unaonekana jambaka tu. Ebu nenda bwana! … Nenda, husikii!?”
Kinoo akashusha pumzi na kisha akageuka aende zake. Akatwaa simu mfukoni na kumpigia Miranda.
“Wamenikatalia kuonana naye.”
“Kwanini?”
“Sijajua.”
“It’s ok. Naona wameamua hivyo. Na itakuwa ni agizo wanatekeleza. Sasa achana nao, tutafanya njia nyingine.”
“Ipi hiyo?” Kinoo akatazama nyuma yake kisha akarudisha macho mbele. “Usinambie ni kama ile tuliyofanya mara ya kwanza? Kwa sasa haitawezekana. Ulinzi umekuwa mkali kupita kiasi!”
“Hapana, si njia hiyo bali nyingine ya kidiplomasia zaidi. Anyways, tutaongea baadae.”
Miranda akakata simu.
**
Simu ya mezani ya bwana Sheng iliita, akainyofoa toka kwenye kitako chake na kuiweka sikioni. Alikuwa ni kamanda akimpigia majira haya ya jioni.
“Mkuu, naomba mambo yataenda kombo,” alisema Kamanda simuni.
“Naona hili swala la bwana Brown litatoka nje ya mikono yangu.”
“Kivipi?”
“Mahakama imeamuru aachiliwe. Amekamatwa kinyume na taratibu!”
“You can’t be serious!”
“Sure! Na si hivyo tu, hata waziri wa sekta hii amenipigia simu na kuniagiza nitende kama nilivyoambiwa maana hili swala limeanza kuvuta hisia za kimataifa, haswa Uingereza juu ya namna raia wake alivyokuwa treated offensively!”
Sheng akashusha pumzi, kisha akauliza, “na vipi kuhusu zile kemikali? Hauwezi ukapata chochote huko?”
“Hamna kitu. Hata tukipeleka mahakamani, hatutashinda. Tutashindwa kutetea hoja zetu na mwishowe itaonekana kuna dhamira binafsi katika hili!”
Sheng akakosa cha kunena. Akiwa anatetemeka mkono akapachika simu yake ya mezani kwenye kitako chake na kisha akalaza kichwa kochini akiwaza.
Alihisi kuchanganyikiwa.
**
Saa mbili usiku …
Bwana Henry Marshall alimfikisha BC nyumbani kwake alafu akaingia ndani na kuteta kidogo kuhusu swala lake, akimtoa hofu kabisa kwani kila kitu kipo sawa mikononi mwake.
BC akamshukuru sana, na akamtakia usiku mwema akapumzike maana amefanya kazi nzito siku hiyo. Bwana huyo akaenda zake.
BC akaenda kukoga na kisha akavaa vema. Akafungua jokofu lake la kuteua chupa moja ya kinywaji. Alikuwa ana kiu nacho haswa. Akafungua na kunywa kwa mtindo wa tarumbeta mpaka pale alipobakiza robo chupa ndiyo akaenda nayo mezani.
Akanywa taratibu akitafakari. Akawaza lile tukio la yeye kukamatwa, na akakubaliana na akili yake kuwa tayari wakina Sheng watakuwa wanafahamu kuwa Jona yupo mikononi mwake.
Hii ilikuwa ni vita. Na yeye kuachiwa huru na polisi si kwamba ndiyo ilikuwa imekoma, bali ndiyo inaanza.
Amejipangaje kupambana? Alikuna kichwa chake. Lazima Sheng atakuja na njia nyingine baada ya hii. Itamgharimu kiasi gani kumsimamisha Jona asimame mwenyewe?
Alikuwa amechoka sana. Hata hakuwaza vema, akamalizia kinywaji chake na kwenda kulala. Kesho yake asubuhi na mapema akamwita Miranda aje nyumbani.
Ila alipokata simu hiyo, akapewa taarifa kuwa bwana Henry Marshall amefariki dunia.
** Jambo hili likageuza maisha yake haraka, juu chini chini juu! Hata akasimama apate kuzisikia vema. Hakuamini kabisa. Na hata huyo mtu aliyempa taarifa akamwona mwehu.
Akakata simu. Ila punde kidogo ndipo akagundua kuwa jambo hilo ni kweli baada ya kumpigia simu Henry Marshall na kuita pasipo majibu, alafu akaona mtandaoni habari za mwanasheria wake.
Ajabu iliyoje hii! Alihisi mwili mzima umekuwa wa baridiii, ila kichwa kinawaka moto haswa!
Gari la Henry lilikuwa zima kabisa, isipokuwa kioo tu cha mbele ndicho kilipasuliwa na risasi zilizomwagwa kama njugu kumpasua na kumtoboa Bwana Henry, akalala pasipo msaada.
Suti yake imefyonza damu mpaka ikashiba na kuchuruza nyinginezo. Uso wake umeshindiliwa risasi tatu hivyo kufanya ugumu kidogo kutambulika!
Hakika hizi zilikuwa habari mbaya sana kwa Bwana Brown. Hakuwahi kupata habari hizi hapa karibuni isipokuwa hii. Alijikuta anapata hasira sana. Tena sana, hata akahisi hataweza kuendesha gari.
Akamwita kijakazi wake na kumpatia funguo ampeleke eneo la tukio.
Alipofika huko akakuta gari la bwana Henry likiwa linakusanywa na gari ‘breakdowns’ na mwili wake ushapelekwa hospitali.
Akawasiliana na baadhi ya watu wake na wakaliongelea jambo hilo kwa kukubaliana kupeleka maiti nchini Uingereza ikazikiwe huko.
Na wakakubaliana baadae majira ya usiku wakutane wapate kuteta jambo.
**
Baadae majira ya saa nne usiku, nyumbani kwa Brown Curtis.
Wanaume watatu walikuwa wamekalia sebuleni. Wawili walikuwa ni sura ngeni machoni na mmoja wao alikuwa ni Brown Curtis (BC). Wote walikuwa wamevalia suti nyeusi, si muda mrefu walikuwa wametoka kwenye makazi ya muda ya marehemu bwana Henry Marshall.
Wanaume hawa wageni inakuwa vema na rahisi kuwatofautisha kwa rangi za nywele zao. Mmoja nywele zake zilikuwa nyeusi ti, aitwa McKnight na mwingine alikuwa na nywele ‘blonde’, aitwa Woodman
Pengine majina yao si ya muhimu sana maana hatutahangaika nayo sana katika simulizi hii, ila kwa hapa wana umuhimu fulani.
Basi wakiwa wanateta hapo, BC akionekana waziwazi kuwa ana hasira na anajua fika aliyetenda jambo hilo la kidhalimu, akasema anahitaji watu kadhaa wa ‘kazi’.
Na watu hao waagizwe toka Uingereza mara moja pasipo kupoteza muda hata punje!
Ila mabwana wale wakawa wastaarabu kidogo, “slow down, Brown,” alisema yule mwenye nywele nyeusi. “Our government will respond on this, we don’t need to rush in!”
Brown akatikisa kichwa. “No! It is enough. I am done with this and now my patience is gone! I want to end things immediately! Enough is enough!”
Hakutaka kusikia wala kungoja namna Uingereza itakavyochukua hatua. Alitaka hatua achukue mwenyewe mkononi.
Siku zote hakuwa mtu aliyekuwa amepanga wala kudhamiria kummaliza Sheng. Ila kwa sasa hilo ndilo litakuwa lengo lake la kwanza kabisa!
Sheng aende kaburini!
Basi mabwana wale wengine wawili, kwa kuona sikio hili lilikuwa la kufa, wakaafikiana naye na kumwahidi kumuunga mkono. Watatimiza kile bwana huyo anataka.
***
Kesho, saa sita mchana.
Hodi ilibishwa na kabla Sheng hajatia neno akastaajabu mlango unafunguliwa, anazama Kamanda mkuu!
Uso wake haukuwa katika pumziko. Mweusi kuliko kawaida. Alikuwa amevalia nguo za kiraia, shati ya kitenge na suruali nyeusi ya kitambaa, na kichwa chake akikihifadhi ndani ya kofia ‘cowboy’ rangi ya kahawia.
Akaketi na kumuuliza Sheng, “ni nini umefanya?”
Sheng akatabasamu, alafu akajisukuma na kiti kwenda mpaka ukutani. Akaweka viganja vyake tumboni na kumtazama Kamanda kana kwamba mama wa kambo anavyomtazama mtoto wa mumewe akiwa anaongopa.
Akauliza, “kwani kuna nini Kamanda?”
“Sheng!” Kamanda akatahamaki. “Ina maana hujui ulichokifanya? Kulikuwa kuna haja gani ya kummaliza yule mwanasheria?”
Kimya kidogo.
” … na nilishakwambia Sheng. Nilishakwambia. Waziri aliniambia hili jambo linaweza kuleta utata sana na serikali ya Uingereza. Tuachane nalo tu, tuangazie namna zingine. Hujataka kunisikia kabisaaaa, ndugu!
Huoni umeiingiza serikali yetu matatani. Dunia nzima watalichukuliaje hili tukio? Si wataona Bwana Henry kauawa na serikali! Na mimi nikiambiwa nipeleleze huoni nitaingia matatizoni!”
Sheng akashusha pumzi ndefu puani kisha akarembua macho na kuyakodoa.
“Kamanda, dharau kwangu zina mipaka,” akasema kwa sauti ya wastani. “Zile zilikuwa ni dharau. Kuna muda a king has to remind fools that he is a king!”
Kamanda akasikitika sana. Akakunja ndita na kumweleza bwana Sheng,
“Umekosea sana na uniweka kwenye wakati mgumu mno. Bila shaka mimi na wewe tumemalizana, hatudaiani. Kwa hivyo, naomba kila mtu sasa ashunghulike na mambo yake. Pesa zako zinanuka, Sheng!”
Kamanda akasimama kwa kiburi. Akafungua mlango na kwenda zake. Sheng akatabasamu, kisha akacheka.
Ikapita dakika tatu, mlango ukagongwa tena. Na kama ilivyokuwa awali, kabla Sheng hajasema kitu, mlango ukafunguliwa. Akajiuliza kuna nini leo?
Kutazama akamwona Shao.
Bwana huyo aliketi pasipo kusalimu. Akakunja nne akimtazama Sheng na kisha akamuuliza,
“Ni wewe ndiye uliyewaita polisi kwa bwana yule?” Aliongea kiswahili kilichonyooka. Bila shaka alifanyia mazoezi maswali haya kwa msaada wa wale watu wake.
“Unasema nini wewe?” Sheng akauliza.
“Unajua ninachokiongelea, Sheng. Unajua kila kitu, na nashangazwa nia yako ni nini?”
Wakatazamana kwa sekunde mbili.
“Shao, kama umeshindwa kazi yako, usitafute mlango wa kutokea, sawa?”
“Sijashindwa,” Shao akasema kwa kujiamini. “Ila wewe unataka nishindwe. Nimeligundua hilo. Sijajua utafaidika na nini katika hili. But its ok. Kama unataka kunimaliza, nimekuja. Niue.”
Sheng akatabasamu. Akatikisa kichwa chake mara mbili alafu akamtazama Shao.
“Sina shida ya kukuua. Na kama nitakuua basi ni kwa mujibu wa makubaliano tuliyoweka mimi na wewe. Si vinginevyo, Shao … kama hutojali, naomba unipishe nina kazi nyingi za kufanya.”
Kabla Shao hajaamka toka kitini akamtazama kwanza Sheng na macho yanayoongea husda, kisha akanyanyuka na kwenda zake.
**
Baadae, majira ya saa tano usiku..
Kwa umbali wa kama hatua nane hivi za mtu mzima, kuna mtu alikuwa amejificha hapo akitazama mlango wa ofisi ya Sheng.
Kuna kitu alikuwa anakingoja hapo. Na ni kama muda ulikuwa unasogea kuendea hilo tukio. Mazingira yalikuwa kimya haswa.
Zikapita dakika tano, mara mlango wa ofisi ya Sheng ukafunguliwa akatoka mwanaume mmoja aliyekuwa amevalia nguo nyeusi.
Mwanaume huyu alikuwa ndiye yule. Bila shaka unamkumbuka. Miongoni mwa wale ‘vijakazi’ kumi wa bwana Shao.
Mwanaume huyo alitazama huku na kule, kule na kule kisha akashika njia kujiendea. Ila hakuwa anajua kuwa leo zilikuwa zimetimia zile arobaini zake.
Akiwa anatembea, hana hili wala lile, akajikuta amedakwa shingo. Kabla hajashangaa, akatenguliwa kuvunjwa!
Akadondoka chini mfu.
Aliyemuua akamtemea mate na kusema, “tangulia kuzimu sisi twaja.”
Kisha akaenda zake.
Baada ya dakika kadhaa, maiti hiyo ikagundulikana na taarif akafikishiwa Sheng.
*** Ilikuwaje? Hilo ndilo lilikuwa swali la kwanza la Sheng. Mwanaume huyo alikuwa ametoka kumjulia hali hivi punde na sasa amekufa? Alishangazwa.
Akawaita walinzi na kuwaliza nini kilijiri. Wote hawakuwa wanajua. Swala hili likamtia hofu Sheng. Huenda mwanaume huyo kauliwa na Shao? Aliwaza. Na kama kweli anachokiwaza ndicho, ina maana Shao atakuwa anafahamu kuwa anamzunguka?
Akashusha pumzi ya mawazo. Pasipo kulifanya jambo hilo kuwa la hadhara, akamzika mtu huyo kisiri na kisha akaendelea kutafakari. Sasa hakuwa na daraja la kumfanya ajue kinachondelea kwa Shao. Hawezi kukaa hivi. Lazima afanye namna.
Akiwa anawaza hivyo, kule upande wa Shao nao wakiwa wamekutana katika usiku huu huu wakawa wanapanga mipango yao. Kuna mwanaume mmoja alikuwa amesimama mbele na ndiye huyo aliyetoka kumuua yule mwanaume aliyetoka kwa Sheng. Ungeweza kumtambua mtu huyo kwa nguo alizokuwa amevaa.
“Tuwe makini sana,” alisema Shao. “na zaidi ya kuwa makini tuwe na uahirikiano. Najua Sheng atamfuata mwinginewe ili awe anajua ninachokipaga na kukifanya. Na itakuwa ngumu kwenu kukataa, cha kufanya kubali ila utoe taarifa kwangu nami nitakuwa nakuelekeza namna ya kuenenda.”
Baada ya Shao kusema hayo, akawataka waende zao na kumwacha peke yake. Vijakazi hao wakatii.
**
Ni asubuhi, katika makazi yasiyojulikana…
Marwa akamkalisha Jona kitako akitabasamu. Jona alikuwa anavuja jasho jingi na Marwa akitiririka kiasi. Wote walikuwa wamevalia nguo nyepesi chini traki rangi ya bluu zinazofanana.
“Sasa hivi inabidi uwe unafanya kila siku!” Alisema Marwa akimtazama Jona. Angalau afya yake ilikuwa imeanza kurejea. Macho yanaonekana ila bado akiwa mdhaifu kiasi.
Angalau sasa, tunaweza tukasema hivyo kwani hakuwa hivyo hapo awali. Na mtu aliyemwona ingemuwia vigumu kuamini kama mwanaume huyo angelikuja kusimamia miguu yake siku moja.
Alitabasamu na kumwambia Marwa, “Dah! Si mchezo.” Akafuta jasho kwa kiganja chake. Alikuwa anahema kwanguvu.
“Ila unajitahidi sana!” Akasema Marwa. “sikutegemea leo kama ungefanya mazoezi kiasi kile. Hata Miranda akija nikamweleza hataamini!”
Jona akatabasamu. “Nataka kurudi kwenye hali yangu kwa udi na uvumba.”
“Naona kwakweli,” Marwa akabinua mdomo. “hautachukua hata juma moja kila kiungo kitakuwa sawa mwilini. Uanze yale mambo yako yale!”
“umeanza sasa, Marwa. Mimi nimechoka hapa sina hata nguvu ya kunena. Naomba nikaoge tutaongea zaidi najua una mengi ya kunambia maana mengi yametokea kipindi sipo ulimwengu huu.”
Jona akajiendea kukoga. Alipomaliza akajifuta vema na aliporejea sebuleni akamkuta Marwa akiwa pamoja na Miranda. Mwanamke huyo alikuwa amevalia shati na suruali nyeusi ya jeans. Alipomwona Jona alitabasamu toka moyoni.
“naona umepona sasa!”
Jona akatabasamu na kuketi kitini. Akatet kidogo na Miranda kuhusu hali yake na maendeleo yake yakamtia hamasa Miranda. Alifurahi sana kumwona Jona anarejea kwenye hali yake.
Walipomaliza maongezi hayo, Miranda akatazamana na Marwa katika namna fulani ya kuwasiliana kisha Marwa akasafisha koo na kusema;
“Jona, kwakuwa sasa angalau umerejea kwenye hali yako, tunaona ni muda muafaka kukushirikisha jambo.”
Marwa akaweka kituo baada ya kusema hayo. Alafu akamtazama tena Miranda kabla hajaendelea.
“sidhani kama nina haja ya kusema sana juu ya namna gani Miranda na mkuu wake, bwana Brown, walivyotusadia mpaka sasa. Hilo liko wazi. Ila sasa, kuna jambo, ama naweza kusema mkataba wa maneno ambao kwa namna moja kubwa kwasababu ya kuhitaji msaada, niliuingia mimi pamoja na mr. Brown.
Bwana huyo alinisihi sana kuwa atakusaidia sana kwa kadiri ya uwezo wake, nawe unaweza ukaona. Ila akaniambia kwamba atahitaji umrudishie fadhila kiasi kidogo.”
Hapa Marwa akasita kidogo. Akamtazama Miranda na kisha akaendelea.
“sasa bwana Brown anataka uwe mtumishi wake. Ni hilo tu ndi…”
“haitawezekana!” Jona akamkatisha Marwa. Akasema kuwa hilo jambo kamwe halitatokea japo anashukuru sana kwa msaada aliopatiwa.
“siwezi kufanya kazi chini ya BC. Haitakaa itokee hata siku moja hata kwa dau gani!”
Miranda akashusha pumzi ndefu alafu akatia neno, “Jona, naomba ulifikirie hili swala kwa mapana zaidi. Ni bwana Brown pekee ndiye aliyekuokota wakati wengine wakiwa wamekitekeleza. Tafadhali fikiri mara mbili.”
Jona akatikisa kichwa. “Marwa, Miranda, huo ndiyo msimamo wangu na hautabadilishwa na chochote kile. Siwezi kufanya kazi na bwana Brown kwa sababu yoyote ile! Ila…”
Akanyamaza kwanza akitazama chini. Akakunja ngumi.
“lazima wale wote walionilaza chini walipe kwa gharama yoyote ile. Wamenitesa mno na kuharibu maisha yangu. Kamwe sitawaacha salama. Iwe kwa kunuka ama kunukia. Nitawasaka kama mbwa mwenye njaa na nitawaua kwa mkono wangu nwenyewe pasipo na tone la huruma.
Niliapa kwa Mungu wangu. Siku nitakayotoka kwenye mateso yale itakuwa kiama chao hakika. Sitabakiza hata mmoja. Na kila ninapokumbuka hilo, napata nguvu ya kufanya mazoezi zaidi niwe kamili.”
Jona akisema haya, machozi yakamjaa machoni. Alikuwa anaongea kwa uchungu mno na kwa hisia kali. Aliminya ngumi yake mpaka akahisi maumivu.
“sijui kwakweli!” Miranda akatikisa kichwa. “naona mambo yanakuwa magumu zaidi.”
“kabisa! Ila hata mimi nililihisi hili jambo. Halijanishangaza kabisa. Ni asilimia ndogo sana niliihifadhi kuwa Jona ataridhia hili jambo. Kichwa chake anakijua mwenyewe.”
Kukawa kimya kidogo. Miranda akanyanyuka na kumwambia Marwa,“acha nikapumzike kidogo. Baadae nitaenda kuonana na Bwana Brown “
“utamwambia nini?” Marwa akauliza upesi.
“nimwambie nini zaidi ya nilichoambiwa na Jona,” akasema akienda zake. Marwa akaachwa akiwa na hofu. Aliona kabisa mambo yanapoeleka si kwema. Ila afanye nini sasa?
Alihisi tumbo linavuruga. Hakutaka kuona kazi yote ile waliyoifanya inageuka kuwa vumbi.
**
Saa mbili usiku …
Ndege kubwa ya kampuni ya BRITISH AIRWAYS ilitua kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius K. Nyerere. Ndege hiyo ikatema watu kadhaa ikiwemo wanaume kumi na mbili waliovalia suti nyeusi kali na wamebebelea mikoba mikononi.
Wanaume hawa waingereza kw utaifa, walikuwa wametokea jiji la London na hapa nchini walikuwa wamekuja kwa agizo la bwana Brown Curtis.
Walitoka nje ya uwanja, wakapokelewa na Bwana Brown mwenyewe ambaye alikuja na gari kubwa la kuwatosha wote, Noah nyeupe yenye vioo vyeusi. Wakajitweka humo na safari ikaanza ya kuelekea nyumbani kwa bwana Brown.
Pasipo kupoteza muda baada ya kuwasili, BC akawaeleza kuwa wamekuja nchini kwa kazi moja, kummaliza Sheng na utawala wake hapa nchini.
Lakini kwakuwa watu ha walikuwa wamechoshwa na uchovu wa safari, bwana Brown akawataka wapumzike kisha kesho itakapofika watayajenga na kuyapanga vema.
Basi wanaume hao kumi na wawili wakaenda kukoga wafanye mpango wa kupumzika. Hawakuwa watu wa soga nyingi, bali matendo. Miili yao ilikuwa imejengeka kimazoezi na macho yao yalionyesha kweli wao ni watu wa kazi.
Wakiwa wanajishughulisha huko, Miranda akafika nyumbani kwa BC. Akaelezwa juu ya ujio wa hao watu na hata wakaitwa na kutambulishwa kwa mwanamke huyo. Baada ya hapo, Miranda akasema lengo la ujio wake.
“Jona doesn’t want to join with us.”
BC akatabasamu. Sigara yake iliyokuwa kwenye kisosi ilikuwa haijazima, akainyakua na kuifyonza.
“ok, he’s chosen death over life. He wil pay!”
Akafyonza tena sigara. “in fact I dont need him anymore. The men are already here, I know they will do the work effectively. But I won’t leave Jona alive. He must die!” Miranda hakusema kitu. Alikuwa anamtazama tu BC akivuta sigara na kunena.
“did you hear me? He must die. And you are the one who’s gonna do it.”
Miranda akatahamaki, “me!”
“yes, you!” BC akabweka. “kill him!” Alisema akiwa ametoa macho. Akasisitiza zaidi, Jona auawe. Na isichukue hata siku mbili awe amemletea kichwa cha mwanaume huyo mfukoni!
**
Jambo hili lilikuwa si jepesi hata kidogo. Miranda alienda zake akiwaza mno namna gani atalitekeleza. Yaani ina maana kazi yote ile waliyoifanya, wakahatarisha na uhai wao, ni bure!
Alikosa usingizi. Hata alimtazama Jona kwa macho ya maswali hata wenzake wakajua hayuko sawa.
“vipi hujapenda chakula?” Marwa akauliza. Alijua wazi shida si chakula. Alitafuta pa kuanzia tu.
Miranda akatabasamu kiuongo alafu akaguna. Akasema, “hamna bana. Chakula ni kitamu sana tu.”
Akakaa kimya kidogo. Alafu akaendelea. Hakuwa anamtazama mtu bali chakula chake.
“kuna mambo flani tu nawaza. It’s not a big deal!”
“ni kuhusu Mr. Brown?” Jona akauliza akimtazama mwanamke huyo ambaye hakutaka kumtazama. Aliendelea kuangushia macho yake kwenye sahani yenye chakula alichopika Marwa. Wali na njegere.
“hapana,” Miranda akatikisa kichwa. “si kuhusu yeye. Ni mambo mengine tu yananitatiza. Ila kama nilivyosema …” Hapa akawatazama upesi. “it’s not a big deal, guys. Msijali!”
Kukawa kimya kidogo. Sauti za sahani na kijiko zikivuma, na kwa mbali watu wakitafuna.
Kama dakika mbili hivi, Jona akauliza, “bila shaka ulienda kuonana na BC. Anasemaje kuhusu taarifa yangu?”
Miranda akangoja atafune na kumeza kwanza. Ila pia awaze cha kusema kichwani.
Akasema, “sikufanikiwa kuonana na BC. Alikuwa ametoka hivyo sijapata kujua msimamo wake kwenye hili. Japo najua litamkwaza kwa kiasi kikubwa.”
Jona akanyamaza. Aliendelea kutafuna na baada ya muda kidogo, Miranda akanyanyuka na kuwaaga anaenda kulala.
“Unadhani yupo sawa?” Marwa akauliza punde baada ya kusikia Miranda akifunga mlango.
“hayupo sawa,” akajibu Jona. “na ni kwasababu ya BC.”
“BC?”
Jona akatikisa kichwa kuafiki. “japo hakutuaga, atakuwa alikwenda kwa BC. Na bila shaka alichomwambia ndicho kinamnyima raha. Najua BC hatakubali kwa urahisi kile nilichokisema.”
Ila akapuuzia.
“tule bana,” akamwambia Marwa. “kila kitu kitajulikana kutokana na muda. Hatuna haja ya kuhofia sana mwisho tukapoteza appetite ya kula chakula kitamu kama hiki!”
Ila kiuhalisia Jona hakuwa ‘amelipotezea’ hili jambo. Na tangu hapa alifahamu fika kuwa inabidi awe makini zaidi maana lolote linaweza kutokea.
**
Saa tano asubuhi … Shanghai, China.
Katika asubuhi hii, Lee alikuwa yupo katika chumba fulani ndani ya ghorofa refu katika jiji la Shanghai. Ndani ya chumba hichi, kitandani kulikuwa kuna begi jeusi na kuna bunduki moja ndefu, yenye kiwamba chembamba cha kumezea sauti.
Na juu kidogo ya bunduki hiyo kulikuwa kuna kifaa cha kumwekea mlengwa ‘targetini’. Kioo cha ku-zoom. Hapo mtu anapojaa kiooni na mlengaji akabofya kitufe, basi tunahesabu ashakuwa mfu!
Bunduki hii, Lee aliipa jina la ‘Death lullaby’ kumaanisha wimbo mzuri wa kubembelezea kifo. Wimbo huu unapopigwa basi lazima mpigiwaji alewe na afe kifo kitamu kisicho na maumivu.
Na hicho ndicho ambacho Lee amekuja kukifanya hapa Shanghai. Amekuja kumletea mtu wimbo wa kifo. Mtu huyo aitwa bwana Chow, balozi wa Umoja wa mataifa.
Alishapata taarifa kuwa mtu huyo yupo katika hoteli hii maarufu. Yani si hii ambay Lee yupo bali ile ambayo anaitazama tangu saa kumi na mbili asubuhi.
Katika hoteli hiyo chumba namba mia thelathini, bwana Chow alikuwa amechukua hifadhi na ndani alikuwa na mwanamke kahaba. Hivyo basi ujio wake hapo hotelini ulikuwa ni wa faragha, hata mwanamke huyo alikuja hapo kama mteja mwingine tu, na chumba akalipia kabisa.
Yote hayo kwasababu ya kutotengeneza ombwe la siri kuvuja. Na pale mlangoni kulikuwa kumesimama wanaume wawili walinzi. Wamevalia suti nyeusi wakisimama kama masanamu.
Basi baada ya kungoja sana, hatimaye Lee anapata anachokitaka. Anamwona mwanamke yule kahaba akielekea ndani ya bafu akiwa amefunga taulo kifuani.
Haraka anazamisha jicho lake kwenye kioo cha lenzi na kumweka mwanamke huyo tagetini. Ila si yeye anamtaka, lah! Alifahamu tu kama mwanamke huyo anaelekea bafuni basi nyuma yake atakuwapo bwana Chow.
Na kweli. Bwana huyo akiwa amevalia taulo kiunoni naye alitokezea kwenye kamwanya kadogo kiooni akielekea bafuni. Alipita kwa kasi sana. Lee alitaka kubofya kitufe cha bunduki, ila akawahi kujizuia.
Akatulia kwanza. Akaona ni vema akavuta subra kwani endapo akitupa risasi na ikamkosa bwana huyo basi atakuwa amefanya kosa kubwa sana. Na itamgharimu muda na pesa kumpata tena bwana huyo kimyani.
Akashusha pumzi ndefu alafu akaendelea kukaa tenge kungoja. Hapa hakutaka hata mbu amsumbue. Ni kazi iliyohitaji uangalifu wa hali ya juu. Ana sekunde kama tatu tu za kufanya hilo tukio kwani kamwanya kadogo kalicho dirishani kangechukua sekunde tatu tu mtu kukapita asionekane tena.
Kwa hivyo, japo hakujua Bwana Chow atatoka muda gani bafuni, alilazimika kukaa tayari muda wote kwa jicho lake kuwa kiooni na kidole chake kupapasa kitufe tayari kwa ajili ya tukio.
Moja … Mbili … Tatu … Nne … Alikuwa anavuta pumzi akiwa ametulia katika hali ya juu. Ni pumzi yake tu ndiyo iliyosikika. Zaidi ya hapo hakuna kitu. Hata yale magari yaliyokuwa yanakatiza huko chini yakipiga honi ama kunguruma, hayakuwa yanasikika!
Lee hakuwa anayasikia.
Basi baada ya kungoja kama mwendo wa dakika ishirini na kitu hivi, mlango wa bafuni ukafunguka. Binti akatoka kutangulia. Lee akakaza kidole kwenye kitufe cha bunduki.
Sekunde mbili mbele, akatoka bwana Chow. Mlengwa. Akapiga hatua mbili tu kufika kwenye kale kamwanya ka dirisha. Alipofika hapo hakunyanyua hata mguu, Lee akafyatua risasi, ikatoboa paji la uso la bwana Chow.
Asipige hata kelele, akadondoka chini mfu. Yule mwanamke kahaba akapaza kelele za hofu kwanguvu! Wale walinzi wawili wakazama ndani. Mmoja akamtazama bwana Chow, mwingine akaangaza macho yake dirishani. Akaona tobo la risasi!
Akapaza sauti, ni mdunguaji! Basi wale wanaume wakatoka na kuanza kukimbilia kule kwenye jengo alilokuwa Lee.
Hata kabla hawajatoka ndani ya hoteli yao walikuwa tayari wameshachelewa sana. Kwani Lee ‘alishayeya’ muda mrefu ndani ya sekunde kumi tu baada ya tukio.
Alitumia kamba kutoka katika dirisha la chumba chake hivyo akapotea ndani ya eneo hilo pasipo hata mapokezi kujua.
Sasa akawa ametimiza mtu wa sita kumuua kwa mkono wake. Kwenye orodha alibakiza watu wawili tu ambao kimahesabu alipangia kuwamaliza msibani.
Yaani watakapohudhuria msiba wa bwana Chow.
**
Saa kumi na mbili jioni ..
BREAKING NEWS!
Sauti nzito ilivuma redioni. Kisha ikatafsiri, habari zilizotufikia hivi punde… Baada ya hapo sauti ya kike ikadakia ikisema,
‘kamanda mkuu wa polisi nchini, amekutwa mfu nyumbani kwake baada ya kusemekana amevamiwa na watu wasiojulikana ambao walimshindilia risasi nane kifuani mwake kabla hawajaondoka katika namna ya ajabu. Habari zaidi itawafikia majira ya saa mbili usiku.’
Taarifa hiyo ikasambaa kwa upesi sana ndani ya jiji na ndani ya nchi. Ikazidi kuzua tafrani na hofu kwa wananchi kwani hata lile la mauaji ya Kamanda wa mkoa halikuwa limepatiwa ufumbuzi.
Ni nani aliyemuua Kamanda mkuu? Je ni yule yule aliyemmaliza Kamanda mkoa?
Na basi katika namna ambayo ilileta hoja nzito, serikali ya Uingereza ikahusishwa kwenye hili ikihesabiwa huenda ikawa ni kisasi cha kifo cha bwana Henry Marshall na ukamatwaji wa mtu wao, yaani Bwana Brown Curtis.
Ila hayo yote hayakuwa sahihi, kwani aliyemuua Kamanda huyo alikuwa ni bwana Sheng. Sasa yupo ofisini kwake na habari alishazipata.
Kamanda ilibidi afe tu, hakukuwa na namna. Ilibidi afe kwani anajua siri za Sheng na alijitoa mkondoni. Atabaki vipi hai?
Sheng akazima redio baada ya taarifa hiyo na kwa kujipongeza, akachomoa mvinyo kwenye jokofu akajimiminia na kupiga mafundo kadhaa.
Na akiwa hapo anakunywa, mara mlango wake ukagongwa. Akameza kwanza kinywaji kisha ndio akaruhusu mgongaji azame ndani …
Bwana huyo mlangoni alikuwa anahema kwanguvu mpaka Sheng alisikia akiwa ndani. Na kwa kujihami alishavuta droo yake yenye silaha…
***
“we’ve finished!” Alisema bwana mzungu akimtazama bwana Brown aliyekuwa amekaa kitini. Walikuwa wamesimama wanaume watatu waliovalia suti, warefu na wenye miili mipana.
Wanaume hawa ni miongoni mwa wale waliotoka Uingereza wakija hapa nchini kutenda kazi. Na sasa walikuwa wameshaifanya. Wapo hapa krejesha ripoti.
“are you sure about that?” Brown Curtis aliuliza akijitengenezea kitini. Hata sigara aliacha kuvuta akawatazama watu wake kwa makini.
“yes, we are sure,” akasema mwanaume mwingine. “his head’s swallowed ten of our bullets!”
Bwana Brown akacheka sana mpaka akakohoa. Hakuamini kama bwana Sheng angekufa kwa urahisi hivyo. Alicheka na kulaani sana. Ila pia akawapongeza vijana wake kwa kuwamiminia kinywaji kwenye glasi.
Basi wakanywa sana na hata wakapiga soga ndefu kuhusu Uingereza. Ila ikafikia mahali bwana Brown akawaambia, “there is one simple task I want you to do.”
Wale wanaume wakampatia masikio. Bwana huyo akawaeleza juu ya Jona. Anataka mwanaume huyo afe kwani aliyempatia hiyo kazi haamini kama ataitekeleza.
Pia akawasihi, “if the woman trouble you, jus kill her.”
Wale wanaume wakabeba maagizo hayo na kwasababu usiku ulikuwa umeingia, wakaenda kupumzika wakilenga kufanya kazi hiyo kesho na huku wakitaka kazi nyingine itafutwe mapema kwani hiyo waliyopewa haitawia hata dakika.
Basi BC akafurahishwa na hilo. Huu usiku wake ukawa mwororo kabisa. Alivuta sigara mpaka akajichokea. Pia akanywa kwa raha zake kamili.
**
Saa saba usiku …
Japo Shao hakuwa kwenye mipango yake, jambo hili la kuuawa kwake kulimshtua haswa bwana Sheng. Inakuwaje adui anaingia ndani na kummaliza mtu kama Shao?
Adui huyo ni nani na anajiamini kiasi gani hivyo?Na ni kweli alikuwa amemlenga Shao ama yeye?
Akiwa amesimama kandokando ya kaburi la Sheng ambalo lilikua limetoka kuchimbwa muda si mrefu, aliwaza sana. Hata siku hiyo hakuwa na hasira kama kawaida yake.
Alikuwa ametulia na kwa kumtazama tu alionekana kumezwa na lindi kubwa la mawazo. Macho yake yalikuwa mekundu, lips kavu na uso wa njano.
Mwili wa Shao ukazama ndani ya ardhi na kisha ukafukiwa upesi. Yote hayo Sheng akitazama ila asione chochote kwani alikuwa mbali haswa.
Hata kila kitu kilipokamilika, ilibidi Sheng ashtuliwe kwamba kila kitu kimekwisha na sasa akapumzike.
Wakati huo walinzi wakiwa wanatetemeka kwa hofu. Walijua Sheng atawamaliza kwa kile anachokiita uzembe.
Ila kinyume kabisa na mawazo yao, Sheng hakutia neno. Na kwa ukimya kabisa akajigeukia na kwendaze. Akajiweka kitini sebuleni na kuendelea kuwaza sana.
Alikosa amani na raha kabisa. Alijitathmini namna mambo yalivyoenda hapa karibuni. Pasipo kutarajia akajikuta anatoa chozi. Chozi la simba.
Aling’ata meno yake kwanguvu akimeza mate yaliyokuwa na ladha ya klorokwini.
Mara hodi ikagonga. Hajasema kitu, mtu akazama ndani. Alikuwa ni mwanaume yule aliyekuja kumpasha habari ya kifo cha Sheng. Mwanaume mrefu aliyevalia tisheti nyepesi nyeupe na suruali ya kadeti rangi nyeusi.
Alikaa kitini na kumtazana Sheng kwa sekunde kadhaa kabla hajashusha pumzi ndefu na kuanza kuteta. Ni kama vile Sheng hakuwa anajali anachosema kwani alikuwa anatazama pembeni kwa umakini.
Ila masikio yake yalikuwa yanadaka kila jambo hapa. Yalikuwa makini kuliko kawaida.
“Wauaji walikuwa ni wazungu. Waliruka ndani na kuwamaliza walinzi takribani nane kabla hawajafika nyumbani kwa Shao. Ni watu wenye ujuzi wa hali ya juu. Walikuwa ni watatu ila walifanya tukio hilo kwa muda mfupi.
Na japo waliua watu wengi, ilifanyika ndani ya muda mchache mno kiasi cha kutokujulikana! Na baada tu ya kummaliza Shao waliondoka zao. Hatujajua walitumia usafiri gani kwani hawakubakiza alama yoyote ile.
Na hatujajua kwanini wamemuua Shao. Na walilenga haswa kummaliza yeye kwani walimnyookea na kummaliza na kisha wakapotea!”
Sheng akafikicha pua yake pasipo kusema jambo. Akamtazama kijakazi wake huyo na kumwonyeshea ishara ya kichwa akimtaka aende, naye kijakazi akaenda zake kumpatia faragha.
Sheng akaendelea kuwaza. Na baada ya muda ndipo akafungua kinywa na kusema neno moja, “Brown!”
Kisha hakusema tena neno lingine lolote mpaka usiku huu unaishilia zake.
**
Saa nane usiku…
Tap! Sauti ya chupa ililia baada ya kugonga meza. Kinoo akanguruma kama simba kupooza koo lake kwa pombe kali aliyogida.
Akapiga kichwa chake kofi na kukitikisa kisha akamtazama mkewe, bibie Sarah. Macho ya mwanaume huyu yalikuwa mekundu haswa yakirembua.
Kwenye sebule yao mezani kulikuwa kuna ‘bapa’ mbili na kopo kubwa la juisi ya embe. Juisi hii ilikuwa ni ya Sarah na bapa hizi zilikuwa ni za Kinoo. Tayari alishamaliza moja, hii ya pili ilikuwa nusu sasa.
Tayari Kinoo alishachanganya waya kichwani. Hakuwa sawa na alikwishalegea, ila kwa upande wa Sarah bado alikuwa ngangari. Japo macho yake yalikuwa mekundu kwa usingizi, alikuwa anajitahidi ‘kukaza’.
Kuna lengo alitaka litimie. Hakutaka kulaza jahazi.
“ah-ah! Mimi sio bwege unajua!” Kinoo akajitapa kilevi. “mimi natazama tu. Najua watazama kwenye anga zangu tuuu … Mimi,” akajipigapiga kifua. “mimi ndiyo Kinoo wa Kunikavu! Kisiki walichoshindwa wakata mkaaa!”
Aliposema hayo akatulia kama mtu aliyepitiwa na usingizi.
“ila mume wangu mi’ n’na wazo,” Sarah akateta akichezea kifua cha Kinoo. “wewe sasa hivi si waekutenga, wanakuona hufai, huna mana! … Unaonaje na sisi tukamwaga mboga kabisa!”
Kinoo akaguna kwa mbali kuitikia. Sarah akaendelea kunena,
“Unaonaje tukatoa taarifa za yule jamaa, tukapiga mpunga mrefu tukafanya yetu mbele kwa mbele huko. Nani atajua?”
Kinoo akagunia kooni, “mmmmhhh!” Kisha akapambana kufungua macho yake ya kilevi. Akamtazama mkewe.
Sarah akaendelea kunena, “usiwe kama boya, watu washakuchoka, shika lako tembea mbele. Utakuja kujuta baadae nakwambia.”
Kinoo akanyaka kwanza chupa ya kileo, akanyonya mafundo kadhaa kana kwamba anakunywa juisi. Kisha akaiweka chupa mezani na kusema, “tatizo nini unajua .. Sijajua wapi walipomweka huyo bwege!” Akakohoa kidogo na kusema, “ila ngoja…” Akayoosha kidole juu.
“nitafanya mchongo mmoja, mmoja tu, nitajua kila kitu alafu kama mbwai na iwe mbwai tu,” akajivuna kilevi kisha akanyanyua tena kilevi na kupiga fundo kadhaa, sasa akamaliza na yeye akalala papo hapo.
**
Saa tano asubuhi …
“Kino! Kino!” Sauti ya kike ilisikika kwa mbali ikiita. “we Kino, amka bana simu yako inaita!”
Kinoo akaufinyanga uso wake na kuangaza. Kichwa kilikuwa kinamgonga haswa, alijilaza palepale kitini kwa usiku huo mzima.
Macho mekundu na mwili wa kichovu.
Kabla hajasema kitu Sarah akamkabidhi simu inayoita mkononi. Kutazama akaona ni Miranda. Akapokea na kuiweka sikioni.
“… Nipo home! … Saa hii? … Kuna ishu gani? … Basi nipe kama robo saa …”
Simu ikakatwa.
“kuna nini?” Sarah akawahi kuuliza. Kinoo akajikusanya na kunyanyuka zake. Alisema maneno kadhaa tu, “mambo yameharibika huko!” Kisha akayeya zake.
Sarah akapaza sauti kumkubushia kile walichoongea usiku wake.
“usisahau basi ile ishuu!”
Kinoo akafungua geti na kwenda zake. Sijui kama alisikia ama alipuuzia.
**
Saa nane mchana …
“I think there is something for you, boss,” alisema jamaa mmoja wa wale wanaume wa kazi toka Uingereza. Mkononi alikuwa amebebelea mfuko mkubwa mweusi wa rambo. Macho yake yalikuwa yanamtazama BC aliyekuwa ameketi kwenye kiti cha mbao bustanini.
“what is that?” BC akauliza kabla hajapokea mfuko huo.
“I don’t know. Somebody on a bike delivered it,” alisema bwana yule wa kizungu. Bado mkononi akiwa ameshikilia mfuko huo.
“we have scanned it. It is not a bomb.”
“Open it,” BC akaagiza.
Bwana yule aliyeleta mzigo akauweka chini na kuufungua. Ndani akakuta kichwa cha binadamu!
Kichwa hiki kilikuwa cha bwana Graham, bwana aliyeenda zake asubuhi ya siku hii kwenda kutimiza agizo la Bwana Brown la kummaliza Miranda na Jona.
Kwenye mdomo wake alikuwa ana karatasi yenye ujumbe.
**Bwana Brown akatahamaki haswa kuona haya. La haula! Akatoa karatasi hiyo mdomoni mwa kile kichwa cha bwana Graham na kukisoma.
‘Don’t you ever do that again!’ Kikaratasi kiliandikwa vivyo. Bwana Brown akakichanachana kwa hasira akiwa amepaliwa na ghadhabu kuu kifuani mwake.
Akang’ata meno na kutazama huku na kule. Mbili haikuwa inakaa wala tatu haikuwa inasogea. Alikasirika mno na akawaza mawazo kadhaa kichwani mwake. Nani aliyemuua Graham?
Jona asingeweza kufanya haya, aliamini hilo. Wala si yule rafiki yake, yaani Marwa. Hakuwa na uwezo huo wa kumwangusha mtu kama Graham.
Hapa ni Miranda pekee.
Kichwa hiki na huu ujumbe anamaanisha nini? Bwana Brown aliwaza. Ina maana Miranda amekaidi maagizo yake? Ina maana …
Ina maana Miranda ameamua kumkingia kifua Jona?
Bwana Brown akajikuta anatabasamu katika haya. Alimtuma kijakazi wake amletee sigara yake kubwa na alipoitia kinywani akainyonya kwanguvu na kutema moshi kando.
Alivuta sigara hii kama kichaa. Nadhani unajua huwa anafanya hivi akiwa kwenye hali gani. Alipovuta sigara mbili na kuzimaliza ndiyo angalau kichwa chake sasa kikatulia.
Akawaza na kukubaliana mambo kadhaa na kichwa chake. Ahitaji tena kufanya kazi na WASWAHILI. Sasa kazi zake atazifanya na waingereza wenzake tu.
“where is Randon? Call him for me!” Aliagiza kwa mdomo wake mkavu utemao moshi. Punde kidogo kijana mrefu, mwili mpana ndani ya suti kana kwamba mwanasheria mahakamani, akawasili.
Akasimama kwa ukakamavu akimtazama bwana Brown.
“from today, you will be my assistant supervisor. You will monitor your colleagues and make sure all things are under control,” alisema Bwana Brown kisha akamtaka mwanaume huyo awaite wenzake wote hapo.
Akalitekeleza hilo na ndani ya muda mfupi, wakawasili na bwana Brown akawaambia juu ya uteuzi wake. Wote wakaafiki.
Sasa bwana Brown akampatia kazi bwana Randon. Kazi yake ya kwanza. Yeye pamoja na wenzake wawili, hivyo jumla watatu.
Kazi hiyo ikiwa ni kummaliza Jona na Miranda. Hakuwapa hata muda wa kujivuta. Akaagiza ndani ya masaa matano kazi iwe imekwisha!
**
Saa kumi jioni …
Gari la Miranda, Range rover sport, ilitua mbele ya nyumba ya Kinoo, bwana huyo akashuka wakaagana na kisha akaenda zake ndani.
Hakumkuta mkewe, ila punde akawasili akiwa amebebelea mfuko mweusi wa rambo. Alisema ametokea sokoni.
Na alipoketi akamuuliza kuhusu ile gari kama ni ya Miranda. Alipojibu ndiyo. Akamuuliza, “umefanikisha ile ishu?”
“ishu gani?” Kinoo akatoa macho.
“naweee! Ina maana tuliyoongea jana umeshayasahau?” Sarah akatahamaki.
“nini tuliongea jana?” Kinoo akauliza. Sarah akasonya na kisha akanyanyuka na kujiendea zake pasipo kusema kitu. Kinoo akabaki akiduwaa.
Akawaza kidogo kabla hajashusha pumzi ndefu na kwenda zake kujinywea maji. Akarejea sebuleni kisha akatulia kwa muda kidogo. Hapa akakumbuka ‘ujinga’ alioufanya jana usiku wa manane pamoja na mkewe.
Akatikisa kichwa chake na kuzama zaidi kwenye mawazo. Akawaza sana hatma yake na maisha haya. Akafikiria kile Miranda alichomwitia, kuwa ameamua kuachana na Bwana Brown na anamtaka wafungue ukurasa mpya wa maisha yao.
Akawaza sana na mwisho wa siku hakuona anga nyeupe kabisa. Maisha yalikuwa yanaelekea kuyumba. Kila kitu BC ndiye anatia mkono, leo wakiwa ‘yatima’ mambo yataenda?
Ni wazi yatachukua muda. Na hata zaidi, roho zao zitakuwa rehani kwani vipi kama bwana Brown akiazimia kuwasaka na kuwamaliza?
Akashusha pumzi.
“Sarah!” Akaita akiwa amelaza kichwa chake kitini. Mkewe akaja pasipo kuitika.
“mke wangu, nimefikiria kuhusu lile jambo tuliloliongea jana usiku, na nimeona lile wazo lako ni vema. Mambo hayapo kwenye mstari na huenda tukicheza tukakosa yote haya.”
Sarah akatabasamu. Bado hakutia neno.
“nimeshapata ninachokitaka,” alisema Kinoo. “nimeshajua wapi wanapoelekea pia kuweka makazi yao mapya. So kilichobakia hapa ni kutoa tu siri hiyo tupate cash tufanye mambo mengine. Ikiwezekana tuondoke kabisa katika mji huu!”
Hapa sasa Sarah akafungua kinywa, “hayo ndiyo maamuzi ya kiume sasa?”
Akamkumbatia mumewe kwa furaha.
“Shetani akikosa namna, humtuma mwanamke.”
***
Saa kumi na mbili jioni kuelekea saa moja usiku …
Gari aina ya Toyota Prado nyeusi ilitoka kwenye makazi ya bwana Brown Curtis ikiwa katika mwendo wa wastani.
Gari hiyo ilivuma na barabara kwa dakika tano, ikafika mahali pa kona ili kuishika barabara iliyonyooka kwenda mpaka huko kuitafuta town.
Ilipokata kona hii … Mambo yakabadilika haraka mno! Badala ya kukutana uso kwa uso na barabara, gari hii ya bwana Brown ikakutana uso kwa uso na kifo!
Ni katika namna ya ajabu. Mbele limesimama gari, Subaru, ikiwa imetanua mbawa zake kama mwewe anayetaka kupaa. Na kwenye mbawa hizo walikuwa wamesimama wanaume sita kwa ujumla. Kumbuka ni hatua chache tu toka kwenye kona.
Wanaume hawa kila mmoja alikuwa amebebelea bunduki aina ya short machine gun (SMG) ambazo zimejawa na risasi za kutosha. Na tayari zimesha-kokiwa kwa ajili ya kazi.
Ee bwana weh!
Baada ya kitendo kilichochukua sekunde tatu tu cha gari la Bwana Brown kuchomoza, ikaanza kunyesha mvua za risasi haswa. Gari liliminiwa ‘njugu’ za kutosha. Kioo kilikuwa nyang’anyang’a. Uso wote wa gari uliharibika vibaya mno.
Kioo kilikuwa chekundu kwa damu.
Gari lilitulia likifuka moshi.
Hakukuwa na alama ya uhai.
Wale wanaume baada ya hili tukio lililodumu kwa dakika tano tu, wakajitweka ndani ya gari lao na katika zile mbio uzionazo runingani kwenye mashindano, wakatimka! ***
“Good job. Are you sure he was in?” Sheng aliuliza.
“hapana. Tulichokifanya ni kumiminia tu risasi gari lake katika namna ambayo haitamwacha salama yeyote aliye ndani.”
Si haba kwa Sheng. Aliwapongeza vijana wake kwa kufanya kazi hiyo vema, mengine atayaona kwenye taarifa ya habari.
Ila kabla hajawaruhusu vijana hao waondoke, simu yake ya mezani ikaita. Akapokea na kuiweka sikioni.
“yes … Serious? … Tell me the address … Ok!”
Alipokata simu akatabasamu na kuwatazama vijana wake wa kazi. Akawaambia kuna kazi ya kufanya imepatikana. Na kazi hii haitakiwi kulala hata kidogo.
Akawatajia eneo ambalo inabidi wakafanye tukio. Na kazi hiyo ni kummaliza Jona na Miranda! Taarifa imeshatolewa juu ya wapi wanapopatikana.
Basi vijana wale wakiongozwa na ‘waskaji’ wake Lee, wakapokea agizo hilo na kuahidi kulitekeleza. Bwana Sheng akawaahidi endapo watatekeleza kazi hiyo, kila mmoja atapata kiasi cha milioni hamsini taslimu!
Pesa shetani. Nani asingetaka mambo haya?
***
Usiku wa saa tano …
Usiku wa saa sita …
Sheng alitazama saa yake. Ilikuwa vema haimdanganyi. Akachukua mvinyo na kuumiminia kweye glasi. Akagida na kuumaliza wote kabla hajamiminia tena glasini.
Akapiga simu. Iliita. Haikupokelewa. Akaendelea kunywa zake kinywaji. Baada ya punde chache, akasikia hodi mlangoni. Akasimama upesi na kuendea mlango.
Alipofungua alikutana na sura ngeni. Zaidi akakutana na mdomo wa bunduki.
Macho yakamtoka pima. Asiseme kitu akaamriwa,
“get on your seat!”
Basi akajongea kwenye kiti chake na kuketi. Uso umejawa na hofu na macho yamejawa na maulizo.
Mwanaume huyu aliyemnyooshea bunduki hakuonyesha kama ana utani. Alikuwa amekuja hapa kwa ajili ya kutenda kazi tu.
Alikuwa ni mzungu.
Alikuwa ndani ya suti.
Alikuwa ni bwana Brown!
“you can’t kill me you Asian bastard!” Bwana Brown alibweka. “you are so fucking young to me. You are jus’ nothing, nobody to me!” Bwana Brown aliwaka. Macho yake yalikuwa makali na mdomo wake anaupindisha.
Ila bwana huyu hakuonekana mzima. Hakuwa mzima. Upande wake wa kushoto ulikuwa unavuja damu iliyochuruzika mpaka kidevuni. Jicho lake la upande huohuo lilikuwa jekundu.
Suti yake ilikuwa chafu. Na hata shati lake jeupe lilikuwa lina mabaki ya damu ya moto kabisa. Na ungemtazama vema mkono wake wa kuume huu uliobebela bunduki, nao ulikuwa unachuruza damu. Kwa chini matone yalikuwa yanadondoka dondoka.
Na hata huu mwendo wake haukuwa wa yule bwana Brown tumjuaye.
“now who’s laughing at last, you bitch!” Bwana Brown alisema aking’ata meno. “I ask you, who’s laughing now??” Akapaza sauti akifoka.
Bwana Sheng alikuwa kimya akimtazama. Bila shaka bwana huyu alikuwa ana jambo analifikiri kichwani. Alitakiwa kuwa mwangalifu mno hapa maana bwana Brown alikuwa ameweka kidole chake kwenye kifyatuo cha risasi.
Akihema tu, risasi inapasua kichwa ama kifua chake na kumpeleka jehanamu mara moja!
“All over England know me!” Bwana Brown aliendelea kunguruma. Chumba kizima alikuwa anasikika yeye tu. Ungejiuliza je wale walinzi wa bwana Sheng wanaojaa eneo hilo, wako wapi muda huo!
“I am an abandoned rock. But look! Here I am still standing. I am on top of the hill and nobody can fall me down!”
Bwana Brown aliposema hayo, akafuta pua yake kwa mgongo wa kiganja cha mkono wa kushoto kisha akatoa neno lake la mwisho.
“now I am done talking. Send my wishes to hell!” Akafyatua risasi!
Haraka Sheng akajitupa na kufyatua miguu yake kupiga mkono wa bwana Brown wenye bunduki na kisha katika upesi akamkita na teke la kifua lililomwangusha Bwana Brown chini! Kisha akacheka. “who’s laughing now?” Akauliza kwa kebehi. Bwana Brown akajikusanya na kunyanyuka. Akajipanga kupambana. Ila asingeweza. Alikuwa amechoka. Alikuwa hajiwezi. Alikuwa ana majeraha.
Alijaribu kutupa shambulio la ngumi, ila kwa Sheng akaona mchekechea. Akamlamba bwana huyo mateke mawili tu, akadondoka chini akiwa mfu!
Ni baada ya punde tu maiti ya bwana Brown ikaanza kumwaga damu kuchafua sakafu.
“send my wishes to hell,” bwana Sheng alinung’una akiwa amebinua mdomo kisha akaendea jokofu lake na kutoa kinywaji. Akakiminia kwenye glasi na kuketi kitini.
Haki alikuwa ana haja ya kusherehekea kwa maana aliponea chupuchupu haswaa kutolewa roho. Alijipongeza kwa mafundo manne ya kinywaji kisha akashusha pumzi ndefu na kuegesha kichwa kitini.
Akawaza kama angelikuwa ameuawa. Hakuna mtu aliyekuja kichwani mwake isipokuwa mkewe na mtoto wake. Aliwaza sana vipi kama leo ingekuwa ndiyo mwisho wa pumzi yake?
Akaona kuna haja ya kuwasiliana na mkewe na mwanae ambao wote wapo China, Beijing. Ila asingeweza kuwapigia simu muda huo. Na ubaya ni kwamba asingeweza hata kuacha ujumbe wakapelekewa kwani familia yake hii ilikuwa ni ya siri.
Hakuna mfanyakazi wake yeyote aliyekuwa anayeijua kwani ilikuwa ni mwiko haswa! Viongozi wote wa juu wa familia hii ya Wu hawakutakiwa kuwa na familia kabisa. Na yote haya ni sababu ya kutotoa mwanya wa udhaifu.
Endapo kiongozi akiwa na familia, maadui watapata fursa ya kumkamata kwa urahisi wakitumia mke na watoto kama chambo.
Ngo! Ngo! Ngo!
“Mkuu!” Sauti ilisikika mlangoni na kumtoa Sheng kwenye kawimbi ka mawazo kalichokuwa kamemchukua. Hakuitikia, alingoja asikie tena sauti hiyo na alipohakikisha anaifahamu, akaendea mlango na kuufungua.
Alikuwa ni kijakazi wake
“Upo salama, mkuu?”
“Ulikuwa wapi mpaka maadui wanafika kwenye makazi yangu??” Sheng akafoka.
“mkuu umesahau kuwa uliniagiza?”
“vipi wenzako wamesharudi?”
“hapana, bado hawajarudi.”
“umefanya nao mawasiliano yoyote?”
“hapana! Sijawatafuta tangu walipoondoka. Kwani hawajakupigia?”
“hapana. Hawajanipigia.”
Sheng akaangaza macho yake huku na kule, hakuona watu. Alistaajabu akauliza walinzi wako wapi. Yule bwana aliyemjia akamwambia wengi wao wameuawa. Maiti zao zinazagaa huko mazingirani.
Ina maana Bwana Brown ndiye aliyewamaliza hao wote?
“kuna maiti mbili pia za wazungu!” Akaeleza kijakazi yule akionyeshea uelekeo. Basi akiongozana na bwana Sheng, wakaenda huko.
***
Asubuhi ya saa mbili … Kwa mbali redio ya simu inanguruma …
“ulifanikiwa?” Akauliza Sarah akimtazama mumewe. “maana hata hukunambia namna mambo yalivyoenda.”
“yah!” Akasema Kinoo kisha akadaka kikombe cha chai na kunywa fundo moja. “nilifanikiwa. Niliwapata nikawapasha habari.”
“sasa?”
“nasikilizia. Walinambia watan’tafuta wakithibitisha kama habari hizo ni za kweli.”
“watathibitishaje sasa?”
“si wataenda kumkamata huko! Huoni redio ipo on hapa nataka nisikie kila kitu.”
Sarah akaguna.
“vipi kama wakimkamata alafu wasikupe hiyo pesa?”
“hawawezi bana.”
“unajuaje? Wakikuzunguka na kwenda zao?”
“Sarah, unaweza ukaniacha nikanywa chai basi?”
“chai gani? – Hii ya rangi? Si tujadili vya maana lakini Kinoo?”
“ningoje basi nimalize! Kwani nachukua mwaka hapa!”
Kabla Sarah hajatia neno, mara sauti ikasikika redioni kutangaza habari zilizowasili hivi punde. Wote wakajikuta wananyamaza kusikiliza kwa umakini.
“maiti sita za wanaume pamoja na bunduki nne zimekutwa kandokando ya mto Msimbazi na kusababisha taharuki kwa wakazi wa karibu na maeneo hayo. Mpaka sasa maiti hizo hazijatambulika, na uchunguzi unaendelea.”
Habari ikakata. Kinoo akatazamana na Sarah.
“wanaweza wakawa wakina Miranda au?” Kinoo aliuliza kana kwamba kuna mtu mwenye majibu. Haraka akanyakua simu yake na kupiga, ikaita mara mbili na kupokelewa na sauti ya kike.
“halo Miranda! … Vipi? Unaendeleaje? … Safi, upo salama? … Kabisa? … Umesikia hiyo habari ya watu waliokutwa mtoni? … Poa, sawa!”
Alipokata simu akanyanyuka na kuacha chai.
“wapi sasa? Umejua ni wakina nani?” Sarah aliuliza. Kinoo hakujibu, akazama chumbani na baada ya dakika moja akatoka akiwa amebadili nguo ya juu, amevalia kibodi cheusi.
Habari hii ya maiti mtoni ikiwa imesambaa na kukamata jiji na nchi zima, Sarah aliipata mwanya wa kuifaidi kwa kupitia mitandao ya kijamii ambayo haikuwa nyuma kabisa kwa mfululizo wa picha na vimaelezo vya hapa na pale.
Alipekua kila picha aliyoiona mtandaoni na akasoma kila neno lililoandikwa. Kila mtu akaeleza yake na kusimulia katika namna yake, ila kwa upande wa Sarah bado hakupata alichokuwa anahitaji.
Japo alipekuwa picha zile zote, hakuona sura ya Jona. Hii ikampa maswali kidogo, ina maana Jona atakuwa hajakamatwa na polisi? Na wale watu waliouawa, watakuwa wanahusika naye kwa namna yoyote ile?
Akiwa mawazoni, mlango unagongwa. Anaacha simu na kwenda anamkuta mwanaue aliyevalia helmet akiwa amebebelea mfuko mweusi.
“mzigo wako nimetumwa kukuletea.”
Sarah alipoupokea, mwanaume huyo hakukaa, akaenda zake. Sarah akaketi kitini na kufungua mzigo huo.
***
Akakuta boksi kubwa jeupe. Akalifungua na ndani akakuta rundo kubwa la pesa zilizo katika mfumo wa dola za kimarekani. Akatabasamu, na mwishowe akaangua kabisa kicheko.
Alifurahi mno kuona pesa hizo. Alihisi moyo wake unamwenda mbio, haraka akanyanyuka na kuzipeleka chumbani. Akajifungia huko, na kuhesabu kibunda kimoja baada ya kingine.
Hakuwa anajua ni kiasi gani cha pesa hicho ila alifahamu ni pesa nyingi. Nyingi za kuweza kutia mtu kiburi. Ila akiwa anatazama pesa hizo, akaona na kipande cha kikaratasi.
Haraka akakichomoa na kukisoma maana kilikuwa na ujumbe.
‘Habari yako ilikuwa ya kweli, ila hatujafanikiwa kumpata mlengwa. Tunatumai utakuwa na taarifa zaidi. Kila taarifa itakuwa na thamani ya pesa hizi.’ Baada ya maelezo hayo, ikaandikwa namba ya simu kwa chini. Namba mbili.
Basi Sarah akajikuta anataka pesa zaidi. Alitamani Kinoo arejee nyumbani upesi ampashe habari hizi na kumtia hamasa.
Ila wakati huu anamngoja mumewe, acha sisi tujifikirishe kidogo. Mtu huyu aliyemletea hizi pesa ametumwa na nani? Bila shaka ni Sheng. Na mwanaume huyo tayari ameshapokea taarifa za kuuawa na kutupwa kwa vijakazi wake huko mtoni.
Na hata zaidi ameshatambua kuwa taarifa hizo za Jona na Miranda zimetoka kwa nani kwa kupitia Sasha. Bwana huyu anajua atapata zaidi mambo ya Jona kwa kumtumia mwanaume huyu.
Na mara hii akipata taarifa, ataingia mwenyewe uwanjani kucheza mziki ambao vijana wamefeli.
Simu ikaita. Sarah akapokea baada ya kuitazama kiooni na kujua ni ya dada yake, Sasha.
“Hallow!”
“mambo?” Sauti ya Sasha ilisikika vizuri kwenye simu.
“fresh. Vipi wewe?”
“niko poa. Vipi upo mahali salama?”
“yah! Niko fresh.”
“jamaa yupo wapi?”
“ametoka kidogo. Ila nadhani anakaribia kuja.”
“vipi umepokea mzigo wowote?”
“yah! Nimepokea eenh!”
“poa. Nitakutafuta baadae au kesho. Uwe karibu na simu yako, sawa?”
“Poa!”
Simu ikakata.
**
Majira ya saa mbili kasoro usiku … Mahali fulani tulivu …
“Kwahiyo sasa mtafanyaje?” Aliuliza Kinoo. “maana maisha yenu yamekuwa kama swala.”
Miranda akashusha pumzi ndefu, alafu akanywa kinywaji chake ndani ya glasi, juisi ya dhabibu, kisha akasema;
“Tutazama kipi cha kufanya. Jona anarejea wa kasi kwenye hali yake na nadhani njia nyepesi sasa ya kuwa salama ni kwa kum-face adui yetu badala ya kumkimbia.”
Akanywa kwanza kinywaji kisha akaendelea na maneno, “kadiri tunavyokimbia ndivyo anavyozidi kutuwinda. Hakuna mahali tutakayokuwa salama. Ila kwa sasa hatutaweza kwenda kukabiliana naye.
Nadhani tunahitaji siku kama tatu au nne hivi za kujipanga na Jona kuwa sawia kabisa.”
“sasa kwa muda wa hizo siku, mtakuwa mnakaa wapi?” Kinoo akauliza.
“hatuwezi tukapata mahali pa kudumu. Tutajiegesha hotelini kwa siku hizo. Ntakupa habari ni wapi tutakapokuwa punde tu ntakapopapata.”
“Sawa.”
Kinoo akatazama saa yake ya mkononi. Muda wa kuondoka ulikuwa umekaribia. Ila kabla hajaaga akamuuliza Miranda,
“umepata habari zozote za BC?”
“hapana,” Miranda akajibu na kisha akauliza, “vipi kuna mpya yoyote?”
“hapana. Ila auhisi anaweza pia akawa amehusika kuleta hao watu kuwavamia?”
“hapana. Watu waliotumwa walikuwa ni wanaume weusi. Endapo wangekuwa ni wazungu basi ningemshuku bwana Brown moja kwa moja. Na hivi tangu wazungu hao wamekuja, sidhani kama atakuwa anatukumbuka.”
Kinoo akatazama tena saa yake kisha akasimama. Sasa akaaga na kwenda zake. Baada ya dakika tatu Kinoo hakuonekana, Miranda akanyanyua simu yake na kupiga.
**
Majira ya saa nne usiku …
“Hallow!” Bwana Sheng alipaza sauti akiongea na simu yake. Alikuwa ameketi sebuleni mwa nyumba, amekunja zake nne. Amevalia nguo nyepesi za kulalia.
Simu ilipokatika, akapiga na kusema maneno machache tu kisha akakata. Baada ya muda kidogo wakaja wanaume wawili vijakazi wa Sheng. Wakasalimu na kuketi kitini kusikiza wito.
“kesho tutakuwa kazini. Nimeshapata taarifa nyingine ya makazi ya Jona. Jiandaeni maana muda wowote nitawataka twende huko! Muwataarifu na wenzenu sita.”
Baada ya kusema hayo, wale vijakazi wakaenda zao. Bwana Sheng akabakia hapo sebuleni akinywa taratibu kinywaji chake na akiwaza kwa mbali.
Punde kidogo simu yake ikaita, alipotazama akaona ni mkewe toka Beijing. Akashangaa kuona amempigia majira haya. Akapokea na kuibandika simu sikioni.
Mkewe alikuwa amemkumbuka na anamuulizia ni lini atarudi China kumwona kwani hata mtoto amekuwa akisumbua sana. Hata shule haendi anakesha akilia anataka kumwona baba.
Kwa sauti ya upole kabisa, bwana Sheng akaongea. Akamwahidi mkewe kuja kumwona pindi atakapomaliza kazi fulani kubwa mbele yake.
Japo mwanamke hakumwamini, alimsisitizia zaidi. Lazima aje kuwaona muda mfupi tu baada ya kumaliza kazi hiyo. Kisha simu ikakatwa.
**
Majira ya saa saba mchana …
Limousine nyeusi ilingia ndani ya uwanja wa hoteli. Dereva akashuka na kufungua mlango wa nyuma akatoka mwanaume fulani mweusi aliyevalia suti rangi ya kijivu.
Mwanaume huyu alikuwa mrefu, na kichwa chake hakikuwa na nywele. Suti yake ilimkaa vema na kwa kumtazama upesi ungesema ni mtu fulani mkubwa taasisi fulani.
Mdomoni alikuwa ana sigara kubwa na kwenye mkono wake wa kushoto alivalia saa ya dhahabu.
Mwanaume huyo, akiwa anapiga hatua za kikakamavu, akaendea mapokezi na kujitambulisha anaitwa bwana Lorenzo Kagula, anahitaji mapumziko kwa muda wa siku tatu hotelini hapo.
Basi mhudumu, mdada fulani mweupe aliyevalia sare, akiitwa Lidia Kombo kwa mujibu wa kibandiko kifuani mwake, akatazama orodha ya vyumba na kisha akampatia bwana huyo chumba namba 114.
“Samahani, unaweza ukanibadilishia. Nishawahi kuja hapa na sikupenda hiko chumba. Unaweza ukanitazamia chumba namba sabini na kitu hivi?”
“usijali,” akasema mhudumu kisha akatupia macho yake kwenye orodha tarakilishini, baada ya punde akasema, “aaahm … Kuna chumba namba 74!”
“si mbaya”
Bwana huyo akalipia na akageuka aende baada ya kukabidhiwa ufunguo. Na kwasababu alisema ni mwenyeji basi hakuhitaji kusindikizwa.
Ila upesi akarejea kwa mhudumu na kumwambia,
“samahani, dada. Kuna wageni wangu pia ningependa wafikie hapa. Vipi kuna vyumba vya kutosha?”
“pasipo shaka,” akasema mhudumu kwa tabasamu. Basi bwana Lorenzo akaenda zake akipiga mluzi.
Baada ya kama dakika kumi na tano, gari aina murrano nayo ikaja hapo hotelini, wakashuka wanaume watatu waliobebelea briefcase. Waliingia ndani ya hoteli na kisha wakauliza kuhusu ujio wa bwana Lorenzo hapo hotelini.
Walipohakikisha yupo, wakaweka oda ya vyumba.
“naomba utupatie chumba namba 75 au 76 ili tuwe karibu naye. Ni mwenzetu.”
Yule dada mhudumu akasikitika akiwaambia vyumba hivyo vina watu, kwa kuwasaidia akawatafutia na kuwapatia vya namba 80 na 86.
Basi wakalipia na kwenda zao wakisindikizwa na mhudumu mpaka milangoni. Mhudumu akaenda zake akiwakabidhi funguo.
Wote wakaingia chumba namba 80, na baada ya dakika chache wakatoka na kwenda kwenye kile chumba cha Lorenzo. Mmoja akasema,
“vile vyumba viina watu. Bila shaka watakuwamo humo kama tulivyopewa maelezo.”
Bwana Lorenzo akatikisa kichwa kisha akasema, “ila ni vema tukahakiki, usiku tumalize zoezi. Si umekuja na vile vitu nilivyokuambia?”
“ndio.”
Mmoja wa wale mabwana waliokuja ‘kumcheki’ Lorenzo akafungua briefcase. Ndani kulikuwa na nguo, sare zinazofanana na za wahudumu wa hoteli.
Bwana huyo akazivaa na kufanana vilevile na wahudumu, kisha akatoka ndani kuendea mlango wa chumba namba 75.
Alipofika hapo akabisha hodi.
“mhudumuu!” Akapaza na sauti.
*** Baada ya muda kidogo mlango ukafunguka, akachungulia mwanamke mmoja mweupe mwenye nywele mtindo wa afro.
Yule dada akatazama ndani kisha akarudisha uso wake kwa huyo mhudumu na kumwambia,
“mataulo si mmeshachukua? Au mwayabadilisha mara ngapi kwa siku?”
Huyu bwana akatabasamu alafu akaomba radhi na kusema, “kama yameshachukuliwa hamna shida, kuna tatizo lingine lolote?”
Dada yule akatikisa kichwa kisha akafunga mlango na mhudumu yule akaenda zake. Alirejea kule alipowaacha wenzake na kuwaambia yale aliyoyakuta huko.
“ina maana hawatakuwapo?” Akauliza yule mwanaume aliyejinasibu kwa jina la Lorenzo Kagula.
“hapana!” Akasema mwanaume mwingine. “tusikate tamaa kiuwepesi hivyo! Kwani kufungua mlango mtu mwingine kunazuia mlengwa watu kuwepo ndani?”
Basi wakakubaliana kwamba inabidi wafanye vivyo hivyo alimradi misheni yao ikamilike. Inabidi tu wavute muda na kisha baadae, majira ya usiku, wakakague vyumba vyote viwili ambavyo wamepewa taarifa kuwa vinawahifadhi watu wao.
Basi Lorenzo akampigia simu mkuu na kumpa mrejesho wa kinachoendelea. Na kwasababu za kuvutia muda, wakaagiza vinywaji vikali kupooza makoo yao.
Wakanywa na kujilaza.
Baadae wakati giza likiwa limeingia, ni majira ya saa mbili usiku, bwana Lorenzo akashtuka na kutazama saa yake ya mkononi.
Kichwa kilikuwa kinamgonga kwa mbali. Wenzake wote walikuwa wote walikuwa wamejilaza hoi. Akataka kuwaamsha ila akasita. Muda wa misheni bado haukuwa umefika.
Basi kurejea usingizini, akapiga tena kinywaji, chupa nzima yeye mwenyewe. Hapo akalala kama mfu wa kale. Hata mwivi angeweza kumnyanyua na kuiba godoro kisha akamrudisha na asisikie lolote lile!
Masaa yakaenda. Ilipohitimu majira ya saa sita kasoro usiku, mmoja wao, yule aliyeigiza mhudumu, akaamka. Akawakurupua wenzake na wote wakaamka isipokuwa Lorenzo.
Walijitahidi sana kumwamsha ila wapi. Hata kama angeamka asingeweza kufanya kitu kwa hali aliyomo. Basi ikabidi wale wengine wapange kufanya tukio pasipo yeye maana isingewezekana misheni hiyo kutokufanyika siku hiyo.
Na hapo tayari Lorenzo, ambaye yupo hoi hajiwezi, alikuwa ameshamwambia bwana Sheng kuwa misheni hiyo ipo chini ya uwezo wao, haina haja ya yeye kusumbuka.
Basi mabwana hawa wakaweka kila kitu sawa. Walikuwa na bunduki mbili zilizojaa risasi. Wakavalia na nguo nyeusi za kazi isipokuwa mmoja ambaye alitumwa akatazame usalama kwanza.
Bwana huyo akatoka na kwenda, baada ya dakika kadhaa akarejea na kuwaambia kila kitu kipo sawa. Basi akavalia sare za wahudumu na kisha wakaenda huko chumbani wanapohisi watu wao wapo.
Yule bwana aliyevalia sare akagonga hodi na kusema, “mhudumuu!” Kisha akangoja.
Kimya.
Akagonga tena na kupaza sauti ya kujitambulisha kuwa mhudumu, ila napo ikawa kimya. Akawatazama wenzake. Ni kama vile waliwasiliana kwa macho, bwana ‘mhudumu’ akarudia tena kugonga.
Napo bado kimya. Ila kwa ndani taa ilikuwa inawaka na hili ndilo liliwapa imani kuwa kuna watu ndani.
Wakatazamana.
Mmoja wao aliyekuwepo nyuma, akachomoa kitu mfukoni kisha akachokonoa kitasa. Sauti ikasikika tas-tas! Na alipobinya kitasa, mlango ukaitika kwa kufunguka.
Wakatazama huku na kule. Hakukuwa na mtu. Wakapekua chumba kizima, kila kona, hakukuwa na kitu!
Basi wasipoteze muda, wakatoka na kwenda kile chumba kingine, cha pili yake. Huko hawakupoteza muda kama ilivyokuwa kwenye hiki cha kwanza, wakachokonoa kitasa na kuzama ndani.
Kulikuwa ni kiza. Waliwasha taa na kuangaza. Hamna kitu! Wakasaka kila kona, hakukuwa na kitu! Hapa wakatazamana kwa butwaa.
Iliwezekanaje hili? Au taarifa walizopewa hazikuwa sahihi? Ilibidi wajiulize mara mbilimbili. Wakatoka chumbani mule na kurejea chumbani mwao.
Wakamkuta bado Lorenzo amelala. Hawakuhangaika naye, wakateka simu na kupiga kwa mkuu wao kumweleza yaliyojiri.
“ndio, namba ni hizohizo! … Hamna mtu mkuu, saa zile mara ya kwanza kulikuwa kuna kabinti flani hivi. Sasa hivi hata naye hayupo maana hata tungempata yeye kwa namna moja angeweza kuwa na majibu … Ndio, mkuu … Sawa.”
Simu ikakata.
“anasemaje?”
“turudi makaoni!”
“saa hii?”
“ndio.”
“na hii mishe vipi?”
“amesema huenda taarifa sio sahihi au watakuwa wameshashtukia. Anampigia mtu aliyempa taarifa kwa maongezi zaidi.”
Wapoelezana hayo, wakaanza kujipanga waende zao. Walipotia kila kitu kwenye begi, wakamwamsha Lorenzo. Bado hakuamka.
Walimpigapiga makofi na kumvutavuta lakini bado haikusaidia. Ila wakiwa katika huo mchakato, mmoja wao akaona kama rangi nyekundu shukani.
Kutazama vema, damu! Wakamgeuza Lorenzo aliyekuwa amelala kifudifudi, wakagundua mwanaume huyo alikuwa ameuawa! Tumbo lake lilikuwa limejawa na damu ambayo bado ilikuwa ya moto kabisa!
Kutazama vema zaidi, alikuwa ana jeraha la kisu, matundu matatu tumboni! Wakapata kitendawili. Nani aliyemuua Lorenzo ndani ya muda mfupi ambao walitoka?
Hapa wakajikuta wanaamini kuwa walengwa wao walikuwapo mulemule ndani ya hoteli. Na si tu kuwapo bali pia walikuwa wanawafuatilia kiasi cha kujua kuwa wametoka na wakaenda kummaliza Lorenzo!
Haraka wakatoka nje na kuanza kuangaza huku na huko. Na hapa wakashirikiana na walinzi wa hoteli baada ya kuwapa taarifa, msako ukafanyika kote hotelini.
Na hata baadae wakapitia taarifa za watu wote waliokuwamo humo ndani ya hoteli ili wapate kubaini nani hakuwapo au aliyetoka hivi karibuni.
Wakagundua kuna watu wawili tu waliotoka, nao wote wakiwa ni wanaume, kwa majina Zebedayo na Derick, wakiwa ni wakazi wa chumba namba 200.
Zaidi ya hapo hakuna kingine kilichopatikana.
Mabwana wale wakampigia simu mkuu wao na kumweleza habari hizo ambazo zilimshangaza na kumghafirisha sana.
Ila mchezo huu ulianzia wapi na ulifanyikaje?
Ni hivi, wakati mhudumu yule feki wa kwanza kabisa alipokuja kwenye chumba walichokuwa wanakishuku kuwa kina watu wao, akamkuta mwanamke mgeni hapo, ndipo mambo yalipoanza kuchanganyia.
Kwanza, mhudumu huyu hakuwa na kibango cha jina lake kama ilivyo kwa wahudumu wote hapa hotelini. Pili, japo sare yake ilijitahidi sana kufanana na za wahudumu wa pale, bado zilikuwa na kasoro kidogo kwenye ukoleaji wa rangi.
Na tatu, kuja kuulizia taulo kwa majira yale, tena ikiwa tayari yashabadilishwa asubuhi, kulileta shaka. Basi mwanamke huyo aliyempokea, akafikisha taarifa kwa mtu aliyemwomba afanye hivyo kwani alitegemea kutakuwa kuna ugeni mahali hapo.
Na alipotoa taarifa hiyo tu, mwanamke huyo akaondoka zake maana alishamaliza kazi.
Baada ya hapo, mengine yote yakawa historia. Mwindaji akawindwa kwa ustadi.
**
Saa tano asubuhi …
Hodi sasa ilikuwa inagongwa kama fujo mno mlangoni. Hata Kinoo aliyekuwa amelala usingizi wa mfu akaamka. Akghafirika akipaza sauti yake nzito kuuliza kwa kufoka.
Hakujibiwa.
Akatazama kando, mkewe hakuwapo. Kichwa nacho kilikuwa kinamuuma sana. Alipata hata tabu kusimama. Alijikongoja mpaka sebuleni akitaka kuelekea mlangoni, ila mezani akaona unga fulani mweupe.
Akaujongea na kuutazama. Akaubinyia kwenye kidole chake na kunusa. Akapata shaka. Kabla hajauendea mlango, akaenda jikoni. Akarudi tena chumbani. Akagundua nguo za mkewe hazikuwapo!
Mwanamke ametoroka? Alijiuliza. Ina maana jana usiku alintilia dawa kwenye kinywaji? Akawehuka. Akili yake ikamtuma moja kwa moja kwenye pesa. Tazama pesa kama zipo!
Akatazama, hola! Patupu!
Akahisi miguu imemwishia nguvu. Akahisi mwili umekuwa wa baridi kama barafu. Akahisi haja zote kwa mpigo!
Bam! Bam! Bam! Mlango ukabamizwa tena na tena.
***
Akajikakamua na kuuendea. Alipofungua akakutana na mwanadada Miranda. Moyo wake ukapiga fundo kubwa, ila akajitahidi kubana hisia.
“Miranda!” akaigiza kutahamaki. “mbona bila taarifa mama?”
Miranda hakujibu. Akazama ndani na kwenda kuketi kitini. Akakunja nne.
“Habari yako?”
“Salama,” akajibu Miranda na kisha akauliza, “vipi wewe?”
“Mimi niko poa tu,” akasema Kinoo. Ila kiuhalisia hakuwa salama. Hata uso wake ulimsaliti. Alijawa na hofu. Na kwa namna fulani alikuwa anasutwa roho.
Akajichekesha.
“karibu bana. Naona Leo umeamua kun’tembelea!”
“Kinoo,” Miranda akait kisha akamtazama mwanaum hiyo machoni na kumuuliza, “mkeo yupo wapi?”
“yah! Hayupo ndani. Vipi kwani kuna shida yoyote?”
“Hamna shida kwangu. Ila shida ipo kwako.”
“shida gani?”
Miranda hakusema kitu. Akabaki akimtazama Kinoo kwa sekunde kadhaa. Akatazama chini na kisha akashusha pumzi ndefu.
“Kinoo,” akauvunja ukimya kwa kuita. “Kama isingalikuwa wewe ni jamaa yangu niliyetoka nawe mbali, hata sasa ningekuwa nishakumaliza. Sijui ni nini kimekukalia kichwani mpaka ukadiriki kututoa sadaka kiasi hiki.”
Kinoo akakunja sura kwa mkanganyiko.
“Sijakuelewa. Ni nini unamaanisha?”
“Unajua kila ninachokisema hapa, Kinoo. Wewe si mgeni hata kidogo. Unajua ulichokitenda na kama nakusingizia, nitazame unambie haujui.”
Kinoo akatazama chini.
Kukawa kimya kwa sekunde kadhaa.
“Ni yule mwanamke, sio?” Miranda akauliza. Kabla hajapewa jibu, akaendelea kunena, “tangu alipoingia mwenye maisha yako nilijua vitu havitakuwa kama vilivyokuwa hapo awali. Nilifahamu fika, na ndiyo maana hata kukushirikisha tena kwenye mambo yangu nilisitisha.”
Akanyamaza. Kinoo bado alikuwa anatazama chini.
“sasa yupo wapi hiyo mwanamke? unajua hata alipo hivi sasa? ila mimi nipo hapa. Nipo hapa kama nilivyokuwapo tangu nyuma. Je kama ningaliuawa, nani angalikuwa nawe hapa?”
Kinoo hakusema kitu. Ila macho yake yalianza kuwa mekundu.
“Hata pesa si hajakuachia?” Miranda akaendelea kunena. “Amekuacha kama alivyokukuta … Nimeshangaa sana ni kwa namna gani alivyokufanya mjinga. Ulikuwaje mjinga kiasi hiki ndugu?”
Kimya. Miranda akasimama.
“Nakutakia maisha mema,” akasema na kwendaze kuelekea mlango, ila Kinoo akamdaka mkono na kumsihi akae. Sasa macho yake yalikuwa mekundu zaidi.
“Miranda,” akaita. “Nisamehe sana. Nastahili kuadhibiwa vikali. Siku zote umekuwa mkarimu na kama dada kwangu ila nikachagua kukuangamiza. Nimekabwa na hayà, hata uwepo wangu ni unafki mtupu. Tafadhali, naomba uniangamize. Nami nimeridhia kwa hali zote.”
“Sina haja ya kukuua, Kinoo,” Miranda akajisemea. “Nina damu nyingi za kuziangamiza ila yako si mojawapo. Niliona tu tuachane kwa amani. Kila mtu akawa na maisha yake. Inatosha.”
Ila Kinoo bado hakuwa radhi kumruhusu Miranda aende zake. Akiwa amemng’ang’ania mkono akamsisitiza amsamehe. Na yupo tayari kufanya lolote lile kama nauli ya msamaha wake.”
Baada ya hiyo kauli, Miranda akaketi na kusema,
“Kuna kazi ya kufanya. Upo tayari?”
**
Saa nane mchana …
“Kwahiyo una mpango gani na hiyo mimba?” Aliuliza Sasha kisha akapooza koo lake na kinywaji kikali.
Walikuwa wameketi sebuleni. Nyumba hii ni kubwa na ya kupendeza. Samani zake pia ni za gharama kubwa.
“Sijui nafanyaje!” Akasema Sarah. Alikuwa amejilaza kiuchovu kochini. “Siwezi kusema niitoe. Ni kubwa sasa. Ni hatari!”
Sasha akanyamaza kwanza. Akajinywea mafundo mawili kisha akasema, “kwahiyo utaubeba huo mzigo mpaka lini?”
Sarah akabinua mdomo. “Mpaka pale nitakapoutua. Hamna namna.”
“You are not serious!” Sasha akang’aka. “Alafu huyo mtoto unakuja kumwambia baba yake nani?”
“Amekufa.”
Sasha akacheka.
“Anyway, inabidi ufanye namna. Mimi sijaona haja ya kubeba mzigo huo. Na kuhusu ukubwa wa mimba, sio shida. Madaktari wapo, wazuri tu ninaowaamini. Nakupa muda wa kufikiri, utanambia. Sawa?”
Sarah hakujibu. Alitazama zake kando. Sasha akanywa mafundo kadhaa na kumaliza chupa yake, ndipo Sarah akanena, “kwahiyo itakuwaje kuhusu Kinoo?”
Sasha akanyamaza kana kwamba hakusikia. Sarah akarudia kuuliza, “una maanisha nini? Mtamuua?”
“Bado unampenda? Mbona unajali sana?”
Sarah hakujibu. Macho yaliyomtazama dada yake yalionyesha anataka majibu na si maswali.
“Ana nafasi moja tu ya kujitetea. Kama asipotoa taarifa yenye kuzaa matunda hivi sasa, nadhani Sheng atamuangamiza.”
“Ila taarifa anazotoa ni sahihi!” Sarah akang’aka.
“Sijakataa. Ila hazizai matunda. Na Sheng anawaza kuwa huenda akitoa taarifa huwapasha pia na wenzake!”
“Hapana. Hafanyi hivyo!”
“Sijabisha, Sarah. Ila ndivyo ambavyo nimekwambia kuhusu Sheng.”
Kukawa kimya kidogo.
“Ole wako umwambie Kinoo haya n’lokwambia,” Sasha akatahadhari.
**
Saa nne usiku …
“Una uhakika?” Aliuliza Sheng akiongea na simu.
“Ndio, nina uhakika. Na mara hii sitataka pesa yako mpaka pale utakapohakikisha maneno yangu.”
“Sawa. Tutawasiliana.” Sheng akakata simu.
Baada ya kama lisaa limoja akawa na wajakazi wake kumi na mbili. Wakajiweka kwenye chombo cha usafiri na kwenda zao.
Wakanyookea eneo fulani mbele ya hoteli. Tutaita eneo hili hoteli ila haikuwa na hadhi hiyo, ila ilizidi hadhi ya guest house au lodge.
Hapo baada ya kukaa ndani ya gari kwa muda kidogo, wakatoka wanaume wanne na kuzama ndani ya hoteli.
Punde kidogo sauti za bunduki zikavuma! Wanaume wengine watatu wakatoka garini na kuzama ndani. Milio mingine ikavuma. Kisha kukawa kimya.
Sasa kwenye gari wakawa wamebakia wajakazi watatu tu pamoja na Sheng. Hawakuwa wanaelewa nini kinaendelea ndani. Na Sheng, kwa kuhisi kuna jambo halipo sawa, akawazuia watumishi wake wasiende tena ndani.
Wakangoja hapo kwa muda kidogo. Lakini katika hali ya ajabu, mara hoteli nzima ikazima taa na kuwa kiza!
Na mwanga uliporejea, Sheng akashuhudia watu wakiwa wamesimama mbele ya gari! Na watu hao walikuwa wamebebelea bunduki kubwa mikononi mwao, wakiwanyooshea!
“Shuka upesi garini!” Amri ikasikika. Sheng akatazamana na watumishi wake. Hakuwa tayari kutii amri ya yeyote. Basi wale wafanyakazi, katika namna ya kipekee, wakamziba Sheng, kisha mwanaume huyo wa kichina, akasukuma gia na kukanyaga mafuta kwa pupa!
Gari likamchupa kuwafuata wale watu waliowanyooshea bunduki. Na kabla watu wale hawajanusuru roho zao, wakagongwa na kusinywa!
Sheng akaangua kicheko. Na kama haitoshi, akarudisha tena gari na kuwasinya tena aliowagonga.
Kisha akashuka na kuwatazama. Usoni mwake alikuwa na tabasamu.
“Hakuna mtu wa kupambana na …” kabla hajamalizia kauli yake hiyo, akakaukiwa na maneno ghafla baada ya kugundua aliowaua ni miongoni mwa wafanyakazi wake.
Lakini iliwezekanaje hili?
Hakujua kumbe wafanyakazi wake hao walikuwa wametolewa mhanga. Viunoni walikuwa wamefungiwa mabomu na hata bunduki walizokuwa wamebebelea hazikuwa na risasi hata moja.
Kabla hajafanya jambo, akashangaa kuona alama ya kitaa chekundu cha bunduki kikiwa kifuani mwake. Na kisha akaamriwa na mtu ambaye hakumwona,
“Weka mikono yako juu!”
***
Haraka akaweka mikono yake juu kutii amri.
Dakika … watu wakamveka kinyago cheusi akawa gizani. Akapakizwa ndani ya gari ambalo hakulifahamu, safari ikaanza kwenda mahali ambapo hapafahamu.
Kama mwendo wa lisaa limoja. Akashushwa ndani ya eneo fulani hivi, kiwanda ambacho kimetekelezwa. Akaingizwa ndani ya chumba fulani na kuvuliwa kinyago.
Hakuwa anaona kitu maana kulikuwa ni giza totoro. Dirisha moja lililo juu kabisa halikutosha kuingiza mwanga kabisa ndani kwahiyo watu hawaonani.
Baada ya kutupiwa humo, mlango ukafungwa na kukawa kimya kwa kama dakika tatu, hakuna kinachofanyika.
Baadae kidogo, Bwana Sheng anasikika akijikusanya na anajinyanyua. Anaangaza huku na kule kisha anapaza sauti kuita,
“Heeeey!” Kimya. Ni mwagwi tu wa sauti ndiyo ulimjibu. Akarudia kuita na kuita, ila ni bure. Hakukuwa na kitu. Na hata alidhani hakuna mtu anayemsikiliza.
Akanyamaza. Ila baada ya kama dakika mbili hivi, mlango ukafunguliwa. Vikasikika vitu fulani vikidondoka kang!-kang! Na kisha mlango ukafungwa.
Sheng akaita, hakuna aliyemjibu wala kuhangaika naye. Punde baada ya muda hewa ikaanza kuwa nzito. Akawa anahangaika kuhema.
Hakuchukua muda mrefu, akajihisi mdhaifu na hatimaye akapoteza fahamu.
Kama vile watu wale waliotupia vile vitu ndani walikuwa wanahesabu muda kwani punde walikuja kufungua mlango na nyuso zao zilikuwa zimefunikwa na vinyago vya kuzuia gesi.
Wakamtazama bwana Sheng wakitumia kurunzi. Wakamwona amelala hajiwezi. Wakatazamana na kutikisiana vichwa. Wakamjongea, na kumnyanyua.
Wakatoka naye ndani wakielekea kusikojulikana.
**
Beijing, mishale ya saa tano asubuhi …
Baada ya kufanya kazi yake vema, kumaliza wale wote waliopo orodhani, sasa Lee alikuwa ndani ya jiji la Beijing kwa dhumuni la kuonana na afisa fulani wa serikali kwa ajili ya kujadili vitu kadhaa.
Mezani alikuwa ameweka glasi yenye mvinyo. Ila hakuwa anahangaika nayo sana, bali simu yake ambayo alikuwa anaandika text na kutuma.
Anapokea na kutuma. Baada ya muda kidogo, simu yake ikazima charge. Akalaani. Akaiweka simu yake mezani na sasa akahamishia mawazo yake kwenye glasi yake ya mvinyo.
Akanywa mafundo matatu alafu akatazama nje ya kioo. Huko nje watu walikuwa bize kila mtu akihangaika na yake. Watu walikuwa wanapita huku na kule. Kila mmoja na yake.
Hapa bwana Lee akapata wazo. Alimwona mzee fulani akikatiza akiwa amebeba briefcase mkononi. Akaitazama briefcase yake na kuinyakua kuiweka mezani.
Akafungua na humo ndani akatoa diary fulani ambayo alilenga asome kusogezea muda. Diary hii ilikuwa ni ile ambayo aliitwaa toka kwa makamu wa raisi aliyemmaliza kule nchini Mongolia.
Aliperuzi diary hiyo kwa muda kidogo. Kuna kitu kikavutia macho yake. Akatazama kwa umakini, ila kabla hajakata kiu chake, akahisi kiganja begani mwake. Kugeuka akakutana uso kwa uso na afisa yule aliyekuwa anamngojea.
Afisa huyo akatabasamu pasipo kusema kitu. Akampatia Lee ishara ya kichwa kisha akatangulia kwenda zake. Lee akalipia kinywaji chake kisha akamfuata afisa huyo.
Mpaka nje kulikuwa kuna gari limesimama, Lee akajiweka na safari ikang’oa nanga.
Ila afisa yule alikuwa mtu mkimya sana. Gari lilitembea kwa takribani robo saa na hakutia neno lolote.
Alikuwa anatazama nje ya gari na alionekana mtu aliyetingwa na mawazo kiasi. Lee alimtazama afisa huyu, na hakuona kama kuna haja ya yeye kusumbuana naye.
Akatulia tuli akiangaza huko nje. Ila baada ya muda kidogo afisa huyo akamwongelesha akitaka kumjua Lee kwa undani.
Lee hakujiweka wazi sana. Hakuona sababu ya yeye kufanya hivyo, basi akawa anamjibu afisa huyu kwa ufupi tu.
Afisa huyu kama mtu aliyegundua hilo, akaacha kusumbuana na Lee. Akanyamaza kama alivyofanya hapo awali. Safari ikaendelea.
Baada ya kama dakika ishirini, wakiwa wameacha jiji la Beijing kwa kiasi kidogo, gari ikasimama na kujiegesha pembeni. Kisha dereva pasipo kupewa maelezo yoyote, akaizima gari na kutulia tuli.
Yule afisa akafungua briefcase yake na kutoa karatasi kadhaa. Akamkabidhi Lee pasipo kusema jambo.
Naye Lee akatoa karatasi kadhaa kwenye briefcase yake na kumpatia afisa huyo kisha wakapeana mkono.
Ila kabla Lee hajatoka ndani ya gari hilo, afisa huyu alipomaliza kukagua karatasi alizopewa kwa haraka, akamsihi Lee kwa maneno machache sana. Awe makini.
Kabla Lee hajatia neno, mlango wa upande wake ukafunguka. Akaenda nje na gari la afisa likatimka akilishuhudia.
Akatazama mwanzo na mwisho wa barabara. Kulikuwa kuna safari ndefu ya kuelekea jijini Beijing. Hakika alihitaji usafiri.
Ila kwanini afisa yule alimtupia mbali huko? Aliwaza. Alikokotoa kichwani akajikuta akiamini pengine ni sababu za kiusalama.
Angalau mawazo hayo yakampa unafuu. Ila akawaza tena, kama ni sababu za usalama, je ni sahihi kwake kutelekezwa eneo kama hilo akiwa na nyaraka muhimu na nyeti hivyo?
Aliendelea kuwaza akijongea. Alitembea kwa mwendo wa dakika kumi, na mara ghafla akasikia sauti ya breki kali! Akashtuka na kutazama kando yake. Akaona gari aina ya Ford ranger nyeusi. Ilikuwa imeshusha vioo na ndani yake walikuwa wanaume kadhaa.
Kabla hajawajua wanaume hao ni wakina nani, wapo wangapi, akastaajabu wakitoa mitutu ya bunduki na kumwonyeshea.
Wakamimina risasi kadhaa. Zikatoboa na kujeruhi mwili wa Lee vibaya! Akadondoka chini kama mzigo asiyeonyesha dalili za uhai.
Wanaume wawili wakashuka toka kwenye lile gari, wakampoka Lee briefcase yake na kisha wakatimka zao kwa kasi wakirudi kule walipotokea, yaani kule mbali na jiji.
Baada ya muda asioujua. Akiwa gizani, Lee anasikia sauti za watu. Anakakamaa na kufungua kope za macho yake. Anamwona mwanamke mmoja na wanaume wawili. Anataka kusimama, anashindwa.
Watu wale wakamtaka atulie kwani amejeruhiwa vibaya. Akajitazama, tumbo lake lilikuwa limejawa damu. Alihisi maumivu makali sana.
Hakudumu tena muda mrefu, akapoteza fahamu.
**
Saa nne usiku, nchini …
Mlango ulifunguliwa, Bwana Sheng akaingizwa ndani ya chumba chake akiwa hajiwezi kwa lolote. Alibwagwa chini na kisha mlango ukafungwa.
Watu hawa waliomleta walikuwa ni wanaume wawili waliovalia suti nyeusi na vinyago usoni. Vinyago vya kuzuia gesi yenye sumu hivyo nyuso zao hazikuwa zinaonekana haswa ni wakina nani.
Walikuwa wanatembea kwa ukakamavu. Miili mirefu na yenye nguvu.
Baada ya kuufunga mlango waliondoka zao wakielekea upande wa kulia wa mahali alipohifadhiwa bwana Sheng. Baada ya mwendo wa dakika tano, wakavua vile vinyago vyao na punde wakawa wametoka ndani ya eneo hili.
Huko nje napo palikuwa kiza, hivyo hawakuonekana vema watu hawa. Walijipaki kwenye gari, cadillac nyeusi, wakatimka.
Kule chumbani, kizani, baada ya dakika tatu tangu gari lile litimke, Bwana Sheng alianza kugugumia. Na mara akakohoa kama mara sita kabla ya kunyamaza na eneo zima likawa kimya kana kwamba ni chini ya shimo.
“We are eagerly waiting for your command, sir,” sauti ilisikika toka garini. Punde gari likasimama na wanaume watatu wakashuka.
Gari hii lilikuwa ni ile cadilac nyeusi iliyotoka kule kwenye kiwanda kilichotelekezwa. Hivyo basi tuna kila sababu ya kuamini kuwa, wanaume hawa ndiyo wale waliomtia Sheng mikononi.
Walikuwa ni wazungu. Watu wanaoonekana wamestaarabika kabisa. Ila kwa yale matendo yao machache tulioyaona, inatosha kuwaweka kwenye kundi la wauaji maarifa.
Wauaji maarifa ni watu stadi wenye uwezo wa kupanga tukio la kuua kwa fomula za kisayansi. Yaani wakammaliza mtu na kubakishwa maswali mengi sana kwa washuhudiaji ama wapelelezi juu ya namna gani wametekeleza hilo.
Kama wewe ulivyobaki hapo ukiwa hutambui ni kwa namna gani watu hawa wamefanikiwa kumtia kimyani bwana Sheng. Na hata pengine ungeweza kushupaza shingo kuwa watekaji si hawa, maana hawakuwapo mafikirioni.
Hawa ni wauaji wasomi. Wamekaa darasani kufundishwa namna ya kuua, kuteka na hata kutesa. Kila kitu chaenda kimahesabu.
Na punde tu unapoona jambo linatokea kwa bahati, basi kwa upande wao hapo ndipo mambo yalipoenda kombo maana hawaamini kwenye bahati, bali nguvu za akili na miili yao.
Kwa jina la pamoja waliitwa ‘the intellect instinct’. Na wapo watano tu kwa idadi. Nguo zao ni suti tu, na pengine ungeweza kuwatofautisha na wengine kwa ua dogo jekundu wanalolipachika kifuani upande wa kushoto.
Waliposhukia ilikuwa ni ndani ya nyumba maridadi sana. Si kubwa, bali ya wastani na rangi zake za kupendeza. Ni kama jengo la vyumba vinne ama vitatu mbali na jiko, choo bafu na stoo.
Hapa nje kwenye uwanja wa kuegeshea magari, kulikuwa kuna cadillac nyingine nyeusi imetulia.
Wanaume hawa watatu wa kizungu wakaingia ndani na kujumuika na wenzao wawili ambao walikuwa sebuleni wakihangaika na tarakilishi.
Na mmoja wao wale waliozama ndani alikuwa anaendelea kuongea na simu hata alipozama ndani na kuketi.
“Yes it does … I think tomorrow I’ll be very sure, sir … no any reason for that … ok, thanks.”
Simu ikakata.
***
Saa tisa jioni …
“Mara ya ngapi sasa?” Aliuliza Miranda akitazama bahari. Upepo ulikuwa unapuliza haswa na fukwe ilikuwa na watu wachache kwasababu haikuwa mwisho wa wiki.
Mwanamke huyu alikuwa amevalia tisheti nyeusi, na suruali ya jeans. Unaweza ukasema kama ilivyo ada yake. Miguuni alikuwa peku akikanyaga mchanga na kuoga maji ya bahari.
Kwa mbali kidogo, alikuwa amepaki gari lake. Ni kama umbali wa hatua ishirini na tatu au na nne hivi. Na hapa alipokuwa amesimama, kando yake alikuwepo mwanaume, Kinoo.
Kifua chake kilikuwa kimebanwa na kibodi cheusi na suruali yake ya kadeti rangi ya udongo ilikuwa imeminya mapaja yake manene.
“Kutakuwa na tatizo gani?” akauliza Miranda. Bado alikuwa anatazama bahari, na kabla Kinoo hajajibu, akaendelea kwa kusema, “Nahisi kuna tatizo hapa. Tena si dogo. Ni jambo la muda tu tatizo hili kuwa bayana. Haya matukio yaliyotukia hapa karibuni, yanafikirisha.”
“Ni kweli. Huenda kwenye ile …” Kinoo hakumaliza hiyo kauli, wakasikia sauti kubwa ya mluzi toka upande ule ilipo gari la Miranda. Wote wakatazama na kumwona Marwa huko. Akawafanyia ishara ya kuwaita.
“Nadhani nina kitu kwa ajili yenu!”
Wakajongea huko. Ndani ya gari alikuwapo Marwa pamoja na Jona. Wote walikuwa wamevalia mashati meupe na suruali za jeans, zikitofautiana rangi tu, bluu na nyeusi.
“Nadhani tulikuwa sahihi kwenye lile jambo. Ni wazi Sheng atakuwa ametekwa, ama amehifadhiwa mahali,” alisema Marwa ambaye mbele yake, juu ya dashboard, kulikuwa na tarakilishi iliyounganishwa na mtandao.
“Mmejuaje?” akauliza Miranda.
“Hapa karibuni mtandao wa wachina hawa, haujawa katika namna nzuri kiulinzi na hata kiutendaji. Nimeweza kuzama tena katika mtandao wao na kudukua taarifa ambazo zinakiri upoteaji wa bwana Sheng, lakini zaidi tumefanikiwa kupata code itakayotusaidia kumtia kimyani.
Ni hivi, kila kiongozi mkubwa wa wachina hawa ana jina lake la siri ‘code name’ ambalo humtambulisha popote pale kwenye himaya yao. Na tulipolipata hilo jina, tumefanikiwa kuli-trace kwa kuongezea baadhi ya taarifa, satellite ikatuonyesha wapi yupo!”
“Imewezekanaje katika namba hiyo?” Kinoo akauliza.
“Imewezekana kwasababu hiyo ‘code name’ si jina tu ambalo mlengwa hupewa, bali pia ni chip ambayo hushindiliwa ndani ya mwili wake ambayo itasaidia upatikanaji wake popote pale atakapopotea, ama kutokujulikana yupo wapi.”
“Kama ni hivyo, kwanini wafuasi wake hawajampata na kumwokoa mpaka sasa?” Miranda akatia shaka.
“Kwasababu taarifa ya kupotea kwa Sheng haijafiikishwa makao makuu, China,” Jona akajibu. “Ni huko makao makuu pekee ndipo kwenye ‘wing’ kubwa ya kimtandao ambayo hu-monitor wings zote za familia na koo ya Wu.”
“Kwasababu ni sisi,” Marwa akajibu kiwepesi na kisha akatazamana na Jona na kujikuta wanacheka.
“Ok, guys, sasa tunafanyaje?” Miranda akauliza. “Kuna haja ya kwenda huko kumkomboa Sheng?”
“Hapana,” Jona akajibu. “Endapo tukifanya hivyo, ni wazi kuna mambo fulani tutakayoyakosea majibu. Kwanza, ni kwanini chamber ya Sheng hawajatuma taarifa huko China juu ya hili? Ni kipi wamepanga kufanya? Alafu, ni nani anayehusika na utekaji huu? Na amepanga kufanya nini na Sheng?
Maana kama wangelikuwa na lengo la kumuua, wangelifanya hivyo toka pale hotelini.
Kuna mengi ya kujifunza hapa. Watu wale waliomteka Sheng, si wa kawaida. Haiwezekani kwa yale yote yaliyotukia, hakuna hata shahidi wala maelezo yoyote yaliyotolewa mpaka sasa.
Hatujui wamejipangaje. Hatujui ni wakina nani. Kumjua adui yako ni nusu na robo ya kumshinda. Inabidi tuwe wapole hapa, ama twaweza kuzamisha mguu kwenye kisima chenye maji meusi.”
“Jona!” Miranda akaita. “Twende kwa Mr Brown!”
“Are you serious?” Kinoo akawahi kuuliza akitoa macho.
“Yes, I am totally serious!” Miranda akajibu. Na kabla hajamngoja yeyote aseme jambo akakalia kiti cha dereva, akatia moto, safari ikaanza.
***
Baada ya honi ya gari kupigwa mara mbili, geti dogo linafunguliwa kidogo. Mwanaume mmoja mzungu anachungulia nje na kukagua usafiri kwa macho akitumia sekunde tatu, kisha anatupa swali,
“Who are you?”
“Mr. Brown associates!” Miranda akajibu. Yule bwana mzungu akatoka vema getini, alikuwa amebebelea bunduki kubwa mkononi.
“How can I prove that?”
“Kit-kat is the play of the cat, pat it before cut it out of its curiosity. Then hat it and give it to a big fat rat,” Miranda akasema maneno hayo upesi, basi bwana yule wa kizungu akaridhia, akafungua sasa geti kamili wageni wakazama ndani.
Baada ya dakika chache wakawa wameketi sebuleni, na kuwakarimu wageni, akawepo bwana mmoja mzungu pamoja nao. Bwana huyo ni mtu wa pili aliyekuwapo hapa, mbali na yule aliyewafungulia mlango.
“We are here to see Mr. Brown,” akasema Miranda kwa kujiamini.
“I am sorry,” Bwana yule mwenyeji akasema akitikisa kichwa, “Mr Brown is not here anymore. He was killed.”
“Killed?” Miranda akatahamaki.
“Yes, and that’s all I can tell. He was killed. So he’s no more.”
“Who killed him?”
“Madam,” bwana yule akaita akimtazama Miranda kwa macho dhalili, “I said that was all I can tell. He was killed. Enough. We are done here. The business with him is over.”
Basi Miranda na wenzake wakawa hawana lingine la kusema hapa, wakaondoka zao.
“Sheng amemuua Brown,” Miranda akasema akiwa anatazama mbele waendako.
“So waliyemteka Sheng watakuwa ni watu wa Mr Brown?” Marwa akauliza.
“Nadhani,” Miranda akajibu. Alisimamisha gari kwenye foleni, akaweka kiwiko kwenye dirisha na kucha mdomoni akifikiri.
“Ila mbona bwana yule hakutaka kusema zaidi? Ina maana hawakuamini?” Jona akauliza.
“Pengine wanaweza wakawa hawaniamini, ila pengine pia hata na wao wanaweza wakawa hawafahamu linaloendelea.”
“Unamaanisha nini kusema hivyo?” Jona akaendelea kueleza. Na kwa macho yake ya kijanja ndani ya miwani akaona mikono ya Miranda ikiwa inatetemeka kwa mbali. Na hata uso wake ukiwa umejawa na mashaka.
“Ni bora wakawa hawaniamini,” Miranda akajibu, “Kuliko wakawa hawajui linaloendelea.”
Akavuta hewa na kusema, “Kama hawajui linaloendelea, basi kazi itakuwa kubwa sana kuliko tunavyowaza. Kazi kubwa kuliko tunavyoweza kuwaza, kwani watakuwa wametumwa watu wa kikosi kingine kuja kumaliza kazi.”
“Ni tofauti na wale?” Jona akauliza.
“Ni tofauti kama ardhi na mbingu,” Miranda akateta. “Na sasa ndo’ napoanza kupata majibu, kwa mujibu wa lile tukio, watakuwa ni watu hao ndiyo wamelifanya, hawa watu wa siri ambao inawezekana hata wenzao hawajui kama wapo nchini.”
“Kuna haja ya kuhofia kuhusu hilo?” Jona akauliza.
“Ipo!” Miranda akajibu akimtazama. “Jona, watu hawa ni wachawi.”
“Wachawi? – Kivipi? Unamaanisha nini?”
*** Miranda akanyamaza kwanza. Foleni likaruhusiwa kwendaze, basi akatia gari moto wakaendelea na safari. Baada ya kutembea kwa dakika tatu, bado akionekana mtu anayebughudhiwa na mawazo, akasema:
“Kuna kipindi Mr Brown alinieleza kidogo juu ya watu hawa. Tulikuwa tunaongelea mambo yetu tukiwa tumetoka kufanya kazi fulani hivi kubwa. Siku hiyo nilimfurahisha sana kwa utendaji wangu wa kazi, akaniambia kama nikiendelea hivyo hivyo, basi siku moja angalinipeleka Uingereza.
Huko nitapata mafunzo zaidi na kama nikifuzu basi nitakuwa HS, yaani Headquarter Servant. Nitapata kila ninachokitaka, na nitafanya kazi mataifa mbalimbali kutimiza adhma ya kundi.
Sikuweza kumuuliza sana kwani alikuwa amelewa, na hata yale maongezi yake kwa namna moja ama nyingine nilidhani yanachochewa na pombe, hivyo sikuzingatia sana. Lakini kwa sasa naona yalikuwa na mantiki ndani yake.
Na zile simulizi alizokuwa ananipa, hazikuwa za uongo wala kutiwa chumvi. Alikuwa anasema ukweli.”
“Ni simulizi gani hizo alikuwa anakupa?” Jona akataka kujua.
“Alikuwa anaongea kwa kujivuna na kucheka mara kwa mara. Ni wazi alikuwa anapendezwa na simulizi hizo. Alijipambanua akinieleza ni namna gani vijana hao wamekuwa wakifanya kazi kwa ufanisi, na hata akan’tolea mifano kedekede ya watu mashuhuri na maarufu waliouawa na hao watu mpaka sasa hakuna aliyekamatwa.
Anyways, sitamaliza kama tukiongelea haya. Ila yatupasa kuwa makini sana.”
Baada ya lisaa limoja na nusu, wakawa wamewasili kwenye nyumba fulani yenye ghorofa moja. Wakazama ndani na walipoketi wakajihudumia glasi glasi za juisi na maongezi yakaendelea.
“As long as hawa watu hawaonekani ku-pose threat, Inabidi tungoje kwanza ni kitu gani kundi la Sheng litafanya,” alisema Jona alipoweka glasi mezani. “Hatua yao ndiyo itatupa mwanga sisi tufanye nini.”
Marwa akaguna na kisha akatia neno, “Mimi kuna kitu nahisi. Kwa akili yangu yote na kwa moyo wangu wote, siamini kama watu hawa, kama Miranda alivyowaongelea, watahusika na Sheng pekee kisha wakajiondokea zao. Nahisi mbali na hili la Sheng, kuna la ziada.
Na hapo ndipo ndipo utata utakapotokea.”
Jona akabinua mdomo, “Inawezekana unalolinena ni kweli. Si la kulipuuza hata kidogo. Kama kuna uwezekano, inabidi kufuatilia nyendo zao hatua kwa hatua.”
**
Saa nane usiku …
“Tunaenda siku nyingine sasa, naona kuna haja ya kuchukua hatua,” alisema jamaa mmoja mweusi. Macho yake yalikuwa yanamtazama mwanaume wa kichina aliyekuwa ameketi kwenye kiti kirefui akinywa whiskey.
Mwanaume huyu wa kichina alikuwa ndiye yule aliyekuwa akiwasimamia wakina Marwa walipokuwa kwenye kitengo cha SPACE BUTTON. Sasa ndiye yeye amekuwa mkuu baada ya Sheng kutoonekana.
Alikunywa tena fundo moja la whiskey kisha akamtazama mwanaume huyo aliyempa taarifa, akamwambia kwa sauti yake nyembamba yenye lafudhi ya ki-mandarin,
“That’s none of your business. Najua cha kufanya na ni kwa muda gani nifanye. So can you please get away from my face?”
Mwanaume yule aliyemfikishia taarifa akageuka aende zake, ila huyu bwana wa kichina akamwita na kumwambia,
“Ole wako ufanye kitu ambacho sijakwambia,” alisema akiwa anarembua kilevi. “Nitakuambia nini cha kufanya. Usidhani mimi ni chizi, I am not crazy. I am not craaazy, ok?”
Mwanaume yule mweusi akaenda zake akimwacha huyu bwana wa kichina hapa anaendelea kunywa. Baada ya kama dakika tano, bwana huyu akamalizia kinywaji chake, akanyanyuka na kujikokota kwenda ndani.
Alipofika akajitupia kitandani akitabasamu. Akatazama simu yake. Akabofyabofya kutazama akaunti yake ya benki, mara punde ujumbe ukaingia kumwambia ana shilingi milioni mia nane taslimu. Akatabasamu na kukumbatia simu yake.
Alikuwa ana furaha sana. Huu ulikuwa ni muda wake. Na akiwa anaamini kabisa kuwa bwana Sheng hatarudi akiwa hai, basi aliazimia kujiweka sawa kabla mambo hayajarudi kwenye mstari.
Simu ikaita.
Akaitazama akikunja sura. Akajiuliza kwa sekunde kadhaa kisha akapokea na kuiweka sikioni. Alikuwa ni wakala toka makao makuu, Hong Kong, China.. Na alibashiri bwana huyo atakuwa amempigia kumuuliza kuhusu Sheng.
Maongezi yao yakadumu kwa muda wa dakika kumi. Na kama alivyobashiri, mada ilikuwa Sheng kwani hajatuma mrejesho wa maendeleo kwa muda wa ‘masiku’ sasa. Na bwana huyo akaenda mbele kwa kuuliza sababu zinazomfanya bwana Sheng kutokuwapo eneo la kazi kwa siku zote hizo.
Kumbe walishatazama kwenye ‘tracing’ zao wakabaini kwa siku zote hizo ambazo bwana Sheng hajawasilisha mrejesho wa kazi, hakuwapo eneo la kazi.
Basi kwa maswali hayo, huyu bwana wa kichina akashindwa kuficha. Ikabidi sasa aweke bayana kuwa Sheng hayupo eneo la kazi, na hawafahamu wapi alipo.
Basi haikuwa taabu, bwana yule aliyewapigia simu akasema anatuma taarifa za location aliyopo Sheng, na kufikia kesho majira kama hayo apewe ‘feedback’.
“****!” Bwana huyu wa kichina akalaani. Sasa mipango yake ilikuwa imeharibika. Usiku wake uligeuka kuwa wa maruwani ghafla na hata pombe zilizokuwa zimemwingia kichwani, zikapotea!
Akabaki akiwaza nini cha kufanya.
**
Saa nne na robo asubuhi …
“He is weak enough!” aliongea mwanaume wa kizungu, mmoja wa kundi la ‘intellect instinct’ akiwa ndani ya eneo lile la kiwanda kilichotelekezwa.
Mwanaume huyu alikuwa ametoka ndani ya chumba kile walichomhifadhi bwana Sheng. Na hapa akiwa anaongea alikuwa ametia mkono wake wa kuume mfukoni, yu ndani ya suti nyeusi matata.
“We have already done each and everything. It’s just a matter of time for us to interrogate and kill him … we need at least eight final hours … ok. I’ll be in touch.”
Bwana huyo akakata simu, akageuka arejee kule chumbani, ila alipopiga hatua nne, akasikia kama sauti ya mlio wa gari. Haraka akasimama na kutulia tuli kuhakikisha kama alichokisikia ni kweli.
Hakusikia tena sauti yoyote, ila akawa tayari ana shaka. Badala ya kwenda kule chumbani akatembea kwa ustadi kwenda nje ya kiwanda. Alipofika mlangoni, akajibana mahali na kutazama nje.
Hakuona kitu.
Ila akiwa amejiweka kwenye mazingira ya utulivu mkubwa, masikio yake yakampa taarifa kuwa kuna jambo halipo sawa. Akanyanyua mkono wake wa kuume na kuongea kwenye saa yake kwa sauti ya chini,
“Alert.”
Kisha akachomoa bunduki yake ndogo na kuikamata vema mkononi. Baada ya kama dakika mbili za utulivu, akasikia sauti ya kitu cha chuma kikidondoka chini. Sauti ilitokea upande wake wa kushoto.
“Umeona kitu?” aliuliza mwanaume mmoja rangi maji ya kunde. Hawa walikuwa ni wafuasi wa bwana Sheng. Kwa idadi wanaume watano wakiwa wamekuja hapa kumkomboa mkuu wao.
“Hamna kitu,” mwenzake akamjibu.
Basi wakasonga tena wakiwa wananyata. Wakasonga na kusonga, na baada ya dakika kama sita, wakawa wamefika kwenye mlango wa chumba ambacho amehifadhiwa bwana Sheng.
Na kwa muda wote huo hawakuwa wamemwona mtu yeyote yule. Kitu pekee walichokiona ilikuwa ni gari aina ya cadillac nyeusi ikiwa imeegeshwa kwa nje ya kiwanda hiki.
Basi wakafungua mlango, haukuwa umebanwa na komeo wala loki, wakazama ndani na kumwona Sheng akiwa amejilaza chini hajielewi. Ni pumzi tu ndiyo huashiria kuwa yu hai.
Wakambeba na kuanza kujongea kwenda nje. Wanaume wawili walifanya hivyo, na wengine watatu wakiwa wanawalinda wenzao wakitazama huku na huko kwa tahadhari kubwa. Mikono yao iliyobebelea bunduki ikienda kushoto na kulia, juu na chini.
Wakafanikiwa kutoka nje pasipo mushkeli. Wakasonga zaidi kulifuata gari lao, ila ajabu hawakulikuta. Pale walipoliacha hakukuwa na alama yoyote ile ya gari.
Na hata lile cadillac nyeusi waliyoiona wakati wanakuja, nayo haikuwapo. Wakatazamana kwa bumbuwazi.
Wakatazama huku na kule, hakukuwa na kitu mbali na kiwanda kilichochoka na kufubaa. Mazingira yalikuwa kimya mno. Majani na matawi ya miti yaliyumbishwa na upepo, kisha yakatulia.
***Ndani ya dakika moja na sekunde mbili, watu wale watano waliokuwa wamembebelea Sheng kumwokoa, wakawa wamedondoka chini isijulikane nini kiliwaangusha.
Alah! Baada ya muda kidogo vichwa vyao vikaanza kuvuja damu kulowanisha nyasi na mchanga. Na kumbe vilikuwa vimetobolewa na ncha za risasi!
Risasi hizi zilikuwa zimetokea wapi? … kwa umbali wa kilomita moja na hatua kadhaa, kule juu kabisa ya chumba kimojawapo kilichopo ndani ya kiwanda, ndipo risasi zilipotoka.
Na basi hazikupiga kelele hata kidogo maana midomo ya bunduki ilikuwa imemezwa na viwamba vya kumezea sauti.
Watu hao watano, the intelectual instinct, wakatoka wakiwa wanatembea mwendo wa kubarizi fukweni mwa bahari, wakawaendea watu hao wavamizi, ambao kwa sasa wamekuwa miili tu, wakamnyanyua bwana Sheng na kurudi naye ndani.
“How did they know we are here?” akauliza mwanaume mmoja wa kizungu. Nadhani kwa sasa ni vema tukawatambua kwa majina ili iwe vema, huyu aliyeuliza aitwa Denmark, wenzake wanne ni, Sweden, Ireland, Scotland na Wales.
“We have to know that,” akasema Scotland kisha akamtazama bwana Sheng aliyekuwa amelala hajiielewi. “And we have to before it’s too late.”
“There must be a thing here,” akadakia Denmark. Naye pia akimtazama bwana Sheng. Macho yao wote yalikuwa ya kijanjajanja sana. Na sura zao za watu wa mafikirio ya mbele. “I think we have to take him home,” akashauri bwana Denmark.
Basi wakamtoa bwana Sheng na kumweka kwenye gari yao mpaka eneo wanapokaa. Huko wakamfanyia bwana Sheng ‘scanning’ ya mwili na kubaini ana chip ndani yake. Wakaitoa na Denmark akadhamiria kuiharibu.
“No, don’t do that,” akasema Scotland. Alikuwa ni mwanaume mwenye mwili mpana kuzidi wote. “We need that chip.”
“Yah!” akadakia Wales na kuongezea, “It’ll help us getting the rest of them.”
***
Saa nane mchana ….
Beep … beep … beep … beep
Sauti kwa mbali ilisikika masikioni mwake. Alihisi mwili wake mzito. Alijaribu kufurukuta ila alishindwa. Alihisi viungo vyake vya mwili huenda vimepooza.
Ila hakuchoka kujaribu kupambana kutoka katika wimbi hili la giza. Alihangaika na hatimaye, kama mtu aliyetoka kunusurika kuzama kwenye maji ya kina kirefu, akakurupuka akivuta hewa mafundo makubwa makubwa.
Akatazama kushoto na kulia. Tumbo likamvuta kwa maumivu makali ambayo alishindwa kupambana nayo, akajikuta anarudisha kichwa chake upesi kwenye mto akigugumia maumivu.
Tumboni alikuwa ana bandeji iliyohifadhi jeraha lake la risasi. Pia kwenye mguu wake wa kushoto alikuwa na jeraha la risasi iliyomparasa. Kichwa kilikuwa kinamuuma na fikira zikiwa nzito kuvutika.
Akashusha pumzi ndefu. Akaperuzi chumba alichomo, akagundua ni hospitali tena ya kisasa. Akajiuliza amefikaje hapo, kuna mtu aliyemleta? Hakukumbuka hata tone. Akatazama tena kushoto na kulia.
Kidogo baada ya kutulia akakumbuka namna alivyoingia matatizoni. Mara ya mwisho kuwa na fahamu alivamiwa na kupokonywa kila alichokuwa nacho. Kulitambua hilo kukamfanya azame zaidi mawazoni. Ilikuwa ni kama vile amechokoza fikra.
Akawaza tukio zima na namna ilivyokuwa. Ina maana yule afisa wa serikali alimzunguka? Alijiuliza. Mara mlango ukafunguliwa akaingia nesi, mwanadada mchanga wa kichina. Uso wake ulikuwa mfupi wenye miwani ndogo ya kumsaidia kuona.
Alipomwona mgonjwa wake, akatabasamu na kumuuliza hali yake. Lee, ambaye ndiye mgonjwa, akamwambia anaendelea vizuri. Ila naye akarusha swali juu ya nani aliyemleta hapo maana kuwapo hospitali kama ile, yenye hadhi, haileti mantiki kuletwa na wasamaria.
Nesi akatabasamu, akiwa ameweka mikono yake kwenye mifuko ya koti, akamwambia Lee kuwa ni wasamaria ndiyo walimleta. Na kwasababu ya kitambulisho chake ndiyo maana wakamleta mahali hapo.
Baada ya kujibu hivyo, akamuaga na kumtaka apumzike. Atakuja kumwona tena baadae. Basi akaendaze.
Lee akabaki akiwaza kuhusu hicho kitambulisho ambacho nesi alikiongelea. Akakumbuka ni cha ‘member’ wa familia ya Wu. Alikiweka kitambulisho hicho nyuma ya mfuko wake wa suruali baada ya kusisitiziwa afanye hivyo kabla hajatoka makao makuu.
Akiwa bado fikirani, ghafla anasikia sauti ya kelele na mara inakoma na kuwa kimya kama awali! Anapata shaka. Punde kidogo, anaona kivuli cha mtu mlangoni. Kwa maana mlango ulikuwa umegawanywa nusu ya chini ‘material’ ya mbao na ile nusu ya juu, kioo cha kufifia.
Kivuli hicho kilikuwa ni cha mwanaume mwenye mwili mpana, na kichwa chake alikuwa amekihifadhi na kofia ya wale wapanda farasi.
Mlango ukafunguka …
**
Saa tatu usiku …
Sauti ya mtu akiteta kwenye simu akitumia lugha ya kichina ilisikika toka dirishani. Sauti hiyo ilidumu kwa dakika tatu tu alafu simu ikakata. Baada ya muda mfupi wakaja wanaume watano ndani ya hiyo nyumba, na maongezi yakafanyika.
Bado sauti zao zilikuwa zinatoka dirishani. Na kwasababu dirisha lilikuwa mbali kidogo na sebule, hawakusikika vema nini wanateta. Baada ya kama robo saa, wale wanaume wakatoka na kwenda zao. Nyumba hii ikadumu mwangani kwa dakika kumi, kisha ikawa gizani.
**
Saa nne usiku …
“It’s time,” Wales alimtonya Denmark aliyekuwa ameketi sebuleni. Mwanaume huyo wa kizungu akanyanyuka na kwenda moja kwa moja kwenye chumba cha mwisho. Hata sasa kwakuwa ni usiku wa kulala wote walikuwa wamevalia nguo nyepesi na si suti zao kama ilivyo ada.
Kwenye chumba hicho cha mwisho, ndani alikuwapo Sheng akiwa amewekwa kitini. Alionekana mdhaifu asiye na nguvu. Macho yake yalikuwa yanarembua na hata mdomo wake alikuwa anapata shida kuufumba.
“Hey …” Denmark akaita akimpigapiga Sheng vikofi vya shavu. Kisha akaketi kwenye kiti mbele ya Sheng, nyuma yake Wales na Scotland wakiwa wamesimama.
“Don’t worry it is going to be easy and fast. I won’t last long,” alisema Denmark akimtazama Sheng ndani ya macho yake madhaifu.
“So tell me who are you?” Denmark akauliza.
“My name is Sheng Ping. The East African zonal manager of Wu clan and family from Hongkong, China,” Sheng akajibu vema, hata Denmark akatabasamu na kuwatazama wenzake., “I think we’ve got it.”
Kila alilouliza, Sheng akawa mwepesi wa ndimi basi akafunguka anavyotakiwa. Watu wale walipopata kila walichokitaka katika ‘tape’, Denmark akanyanyuka na kukoki bunduki yake.
“It’s time to die, pal.” akainyooshea mdomo wake kwenye paji la uso la mwanaume huyo, ila kabla hajaifyatua, Scotland akamgusa bega lake na kumwambia, “We still need him.”
“Are you sure?” Denmark akauliza. Kidole chake kilikuwa tufeni.
“Yes, I am sure, we do,” Scotland akajibu. Basi Denmark akashusha silaha yake na kuichomeka kiunoni.
***
Saa nne asubuhi …
“Ndiyo hapa!” akasema mwanaume mmoja mwenye sura mbovu. Alikuwa ni dereva wa gari hili, Murrano rangi ya fedha. Ndani yake kulikuwa na wanaume watano waliobebelea silaha. Na hapa walipokuwa wamesimamisha gari ilikuwa mbele ya nyumba fulani, ghorofa, ambayo haijamaliziwa.
Basi wanaume wale wakashuka wote, na hao wakazama ndani ya jengo hilo. Ndani ya muda mfupi wakatoka wakiwa wamembeba Sheng.
Walimkuta akiwa amelala chini hajiwezi. Wakamsweka ndani ya gari na kutimka pasipo kupoteza muda.
Basi Scotland akatokea mbali kidogo na nyumba hiyo akiwa anatazama gari likiyoyoma, na simu yake ipo sikioni, akasema, “It is on the right track.” kisha akakata simu na kuidumbukiza mfukoni.
Baada ya dakika moja tangu mlango ulipogongwa, ukafunguliwa na kichwa cha mchina kutokeza nje. Kutazamana, akaona Sheng akiwa kabebelewa na wanaume aliowaagiza basi akawapokea na Sheng akaingizwa ndani na kisha maongezi machache yakachukua nafasi.
“Hatukukuta mtu yeyote, isipokuwa mwili wake tu,” yule dereva mwenye sura mbovu aliteta.
“Hatujajua wamemfanyia nini, na hatujajua ni wakina nani kwa lengo gani.”
Basi yule mchina akaguna akimtazama Sheng kwa macho makini. Akatulia kidogo na kusema mawazo yake.
“Kwa asilimia zote watakuwa ni watu wa yule mzungu ambaye Sheng alimuua. Ila kwanini hawakummaliza kwa muda wote huo? Ni nini walikuwa wanafanya naye?” Hata yeye akapatwa na maswali.
Basi isiwe na haja kwa muda huo, ilikuwa ni lazimu bwana Sheng apewe huduma haraka asije fia kwenye ‘mikono salama’. Daktari wa mule mule ndani akaitwa na kumfanyia ‘diagnosis’, baada ya hapo akamtundikia dripu na kutaka kufanya maongezi machache na yule bwana wa kichina.
Daktari huyu alikuwa ni mwanaume mzee mwenye kiwaraza kichwani. Sura ya upole na macho ya hekima za utu uzima. Alivalia koti jeupe ambalo lilionekana kumvaa kutokana na ufupi wake.
Akasafisha koo na kusema, “Bwana huyu ametiliwa sumu.” Aliongea kwa uhakika, ila sauti yake ikiwa chini. “Afya yake ni dhalili hivyo anahitaji uangalizi wa juu mno.” aliposema hayo akakohoa kidogo na kuvuta hewa ndefu kwa pua, kisha, “Namhitaji kule eneo langu la kazi kwa uangalizi zaidi.”
Sasa ameshasema daktari, yule bwana wa kichina akawa hana kipingamizi. Kikubwa akaongozana na daktari mpaka huko ambapo Sheng alipelekwa, akaingizwa ndani ya chumba maalum, ndani ya jengo litumikalo kama sehemu ya kutoa huduma za matibabu ndani ya eneo hilo.
Humo ndani kulikuwa kuna mazingira tulivu, na hata wahudumu wa kutosha, wa China na hata wa hapa nchini.
“Inatosha, yupo mikono salama, waweza kwenda,” alisema Daktari akimtazama bwana yule wa kichina. Naye pasipo kubisha akaendaze. Ila akiwa na maswali kichwani.
Sasa ufisadi wake ulikuwa hatiani. Endapo Sheng akisimama kwa miguu yake ni wazi hatabakizwa na pumzi. Hata akajikuta tumbo likimuuma na kichwa pia.
Baadae, kwenye majira ya saa mbili usiku, akatoka ndani, akiwa amejipaki ndani ya gari nyeusi aina ya discovery, akaelekea zake viwanja akiwa ameongozana na vijana wake watatu wa kazi.
Alilenga kupumzisha kichwa chake kwa mawazo, lakini pia alikuwa na mawazo fulani ambayo alitaka kuwashirikisha hawa vijana wake watatu ambao alikuwa amependezwa nao.
***
Saa sita kuelekea saa saba usiku …
Kuna sauti kubwa ya muziki hapa. Watu wengine wapo ndani ya kiwanja wakijibetua na kunengua kwa mujibu wa midundo ya muziki huo. Wengine walikuwa wamekaa kwenye makochi, na wengine wakiwa wameshikana, wanatomasana ama wamesimama tu wakiongea kana kwamba wanasikiana dhidi ya muziki huu mkubwa.
Mwanga ulikuwa hafifu, ila hewa ya kutosha. Kote palikuwa pametawaliwa na kiza, ila vijitaa vidogodogo vyekundu, vya njano, vya kijani na vya kila rangi vikipitapita huku na huko.
Mahali hapa palikuwa ni klabu ya usiku.
Wakiwa wamekaa kaunta, kila mmoja ana kinywaji chake, na hapo tayari wameshakunywa kadha wa kadha, yule bwana wa kichina, aidha kwa kuona sasa ni muda muafaka wa kuteta, akasema,
“Mmetosheka?”
Wale mabwana alioongozana nao wasiseme kitu, wakatabasamu. Ishara ya kwamba bado ni muda mchanga. Basi yule bwana wa kichina akawaambia wanywe mpaka waseme wenyewe basi.
Lakini wakiendelea huku kunywa, akaendea adhma yake.
“Nataka muwe watu wakubwa sana. Nafikiria kuwapa nafasi nyeti sana pale kitengoni. Mwaonaje?” japo muziki ulikuwa mkubwa, sauti yake nyembamba ya kichina ilipasua na kusikika vema. Wale mabwana wakatabasamu.
Ni wazi pande la nofu la nyama liliwekwa mezani mwa mabwana fisi.
“Yah! Sisi hatuna shida kabisa!” wenzake wakamuunga mkono na tena huku usoni wakijawa na matabasamu ya kiroho, na hata kujichekesha pasipo na msingi.
“You know, nimetazama nikaona mnanifaa sana,” akasema bwana yule wa kichina. “kati ya watu wote nikaona ninyi ndiyo watu wa kutenda kazi na mimi … mna nguvu, na intelligent …” bwana huyu wa kichina akaweka kituo kwa kunywa kwanza fundo moja la kinywaji chake, kisha akaendelea wakati hadhira wake wakimsikiza kwa umakini.
“Ila sasa kuna tatizo moja, moja tu, moja!”
“Lipi hilo?” akauliza mmoja wa mabwana wale. Basi yule bwana wa kichina akanyamaza kwanza, kama mtu anayefikiria, kisha akauliza,
“How far can you go to get this?”
“Uncountable miles,” akasema bwana mmoja. Huyu alikuwa karibu zaidi na bwana huyu wa kichina. Na maneno yake haya yakamfurahisha bwana huyo, akatabasamu, “That’s nice. If then, I have a work for you to do.”
Basi akawaeleza kazi hiyo na alipomaliza kuwaeleza, wakapeana mikono ya kukubaliana. Ila bwana mmoja, yule aliyekaa mbali na bwana huyu wa kichina, akawa na shaka. Akauliza,
“Vipi kuhusu wengine?”
“Wengine!” mwenzake aliye jirani akatahamaki. “Hapa duniani ulizaliwa na nani? Jiangalie wewe ndugu yangu, acha ufala!”
Kuliunga hilo mkono, wengine wakacheka na kisha wakaendelea kunywa na kunywa. Baadae kwenye majira ya saa nane kasoro, bwana yule wa kichina akaona inatosha, basi akawataka waondoke. Ila akaona ni vema kama akipata mwanamke mmoja wa kwenda kumpunguza uzito kwa usiku huo.
Akamwamgiza mmoja wa wale jamaa aliokuja nao amtafutie mwanamke mzuri wa kwenda naye. Pasipo hiyana mwanaume huyo akafanya kazi na ndani ya muda mfupi akarejea na mwanamke mzuri kabisa, mweupe mwenye figa ya kuzembesha.
Na mwanamke huyu, kama bahati au nuksi, alikuwa ni Glady.
Bwana yule wa kichina akapendezwa naye hakika, wakaondoka naye kwenda kujipaki garini warudi makaoni.
**
Mazingira haya hayakuwa mageni. Ni kama vile aliwahi kufika huku, kumbukumbu zake zilimweleza bayana. Alijitahidi kutazama barabara na mazingira, akajikuta anapata picha fulani.
Na kweli hakuwa amekosea kabisa. Macho yake hayakuwa yanamdanganya, hili eneo si geni kwake. Na alipotuliza kichwa vema sasa akakumbuka. Mahali huku alishawahi kumleta yule mwanaume wa kichina aitwaye Lee.
Glady akaminyua mdomo wake. Hapa kidogo akamkumbuka mwanaume yule wa kichina, Lee. Na basi akajikuta anachukua simu yake na kupekua kama jina lake lipo kwenye simu. Akaliona.
Akataka kutext, akasita. Litakuwa jambo la kipumbavu akifanya hivyo. Basi akatulia kwanza akiwaza ujinga fulani kichwani mwake. Punde sauti ya honi ikamtoa fikirani. Walikuwa wameshafika getini. Geti likafunguliwa, wakazama ndani.
Ndimo humu humu! Akaendelea kuhakikisha. Ndimo humu humu alipomleta Lee. Macho yake ya wizi yakawa yanaangaza sana, huku na kule mpaka gari kusimama na kuongozana na wanaume wale kwenda kwenye makazi ya yule mchina.
Yeye akaamriwa aingie ndani, na yule bwana wa kichina akabaki na wale mabwana wengine pale mlangoni. Akateta nao kwa sauti isiyosikika vema, na kisha wakafunga mjadala kwa mchina yule akisema, “Msiniangushe!” wanaume hao wakaondoka zao, bwana yule wa kichina akazama ndani.
Akavua nguo na kwenda kuoga akimwacha Glady peke yake.
Glady akatazama huku na kule. Kimini chake akakivuta akibadilisha pozi la kukunja nne. Punde akanyanyuka na kuchungulia dirishani. Akaangaza nje akijaribu kufikiria ni upande upi yalipo makazi ya Lee. Muda kidogo, akasikia mlango wa bafu ukifunguliwa, basi akarejea kitini.
“Kaoge,” yule mchina akamwambia Glady. Glady akanyanyuka na kwenda bafuni. Akaoga akiwaza kuhusu Lee. Kabla hajatoka, akasikia sauti ya yule mchina huko chumbani. Alikuwa anaongea na simu.
“Hakikisha anakufa kabisa, sawa?”
Glady akashtuka. Akapatwa na maulizo kichwani. Sasa akapata picha juu ya nini yule bwana wa kichina alikuwa anaongea na wale wajamaa. Akaguna. Akapiga moyo konde na kutoka bafuni. Akaketi kitandani.
Bado bwana yule wa kichina alikuwa anaongea na simu.
*** Alikuwa anatoa maelekezo na huku akisisitiza kuwa mlengwa lazima amalizwe kwa namna ya siri isije zua utata. Basi baada ya muda, akanyamaza na kisha kumgeukia bibie Glady. Ila macho yake yalieleza namna gani alivyokuwa yupo nje ya ‘mood’.
“Umekwishaoga?”
“Ndio, kama unavyoniona,” akajibu Glady ila naye akiwa na sura ya woga na maulizo.
“Kuna shida yoyote?”
“Mmh mmh hamna.”
“Mbona unaonekana haupo comfortable?”
“Wala, niko ok tu.”
Kukawa kimya kidogo. Bwana yule wa kichina akatazama chini kisha akashusha pumzi ndefu puani na kuuliza, “Haujaja na nguo nyingine mbali na zile?” huku akitazama nguo za Glady zilizopo kwenye kiti.
“Hapana, sijaja na zingine. Kwani vipi?”
“Nothing. Nilidhani umekuja na zile nguo za kusisimua, zile zaaa … you know? Anyway, usijali. Nipe muda kidogo. Sawa?”
“Kwani tulikubaliana nilale huku?”
“Kulala itakuwa shilingi ngapi?”
“Utaongezea mara mbili ya ile tuliyokubaliana.”
“Haina shida.”
Bwana yule wa kichina akakwapua simu yake na kusimama, “Ningojee hapa.”
Akaenda zake sebuleni. Glady akatulia pale kitandani kwa muda kidogo kisha akasimama na kwenda mlangoni kutega sikio. Kulikuwa kimya. Ila baada ya muda kidogo akasikia sauti ikianza kuteta na simu.
Kuna wazo likamjia kichwani. Haraka akaendea simu yake na kutafuta jina la Lee. Akajaribu kubipu. Alipoona haiiti, akazama upande wa ujumbe, ila akatoka tena na kwenda kwenye mtandao wa whatsapp, huko akamsaka Lee na kumtumia ujumbe.
**
“Kuna ulinzi, ila tutafanikisha,” alisema bwana mmoja mshirika na yule bwana wetu wa kichina. Aliposema hayo akaweka simu mfukoni kisha akatazama kando, kulikuwa na jamaa yake mwingine. Walikuwa wameazimia kufanya kazi hii watu wawili tu kuepusha msongamano ambao ungelipeleka kushtukiwa.
Akampatia ishara ya kichwa, na huyo mwenzake, kwa haraka, akaenda nyuma ya jengo. Jengo hili ni lile ambalo amelazwa bwana Sheng kwa matibabu zaidi. Na halipo pweke, bali limezingirwa na walinzi kadhaa.
Basi huyu bwana baada ya kutia simu yake mfukoni, akaanza kujongea, punde akamfikia mlinzi na kusalimiana naye, akaumulizia hali ya mgonjwa.
“Anaendelea vema,” akajibu mlinzi, na kisha kama mtu asiye na habari au shaka, akatazama zake kando kuendelea na kazhi yake.
“Naweza kumwona?” bwana yule akanena. Mlinzi akamtazama kwa kukunja ndita.
“Saa hii?”
“Kwani kuna shida?”
“Huoni kama kuna shida? Mgonjwa anatazamwaje saa hii. Daktari amesema anahitaji ma …” upesi akadakwa shingo, kak! Akavunjwa. Akadondoka chini kama mzigo.
Basi bwana yule haraka akasonga ndani asionekane na mlinzi mwingine yeyote. Akadaka korido na kusonga kwa hatua kadhaa kubwa kabla hajakutana na nesi.
“Nikusaidie nini, mlinzi?”
Alikuwa ni nesi wa kichina. Mfupi na mdogo kwa umbo. Sura yake ilikuwa thabiti na macho yenye mkazo. Basi bwana huyu akatabasamu na kusema, “Samahani, ni usiku mkubwa. Nimekuja kumtazama mkuu, kuna machache ya kusema naye.”
“Siwezi nikakuruhusu kwa sasa. Njoo kesho asubuhi.”
“It’s urgent, please. In fact nimeagizwa na mkuu. Hatonielewa kama nikimwambia sijafanikiwa.”
Nesi akashusha pumzi na kuminya lips zake nyembamba. “Ok, ni muda mfupi nakupa.”
Hakujua amempatia kibali muuaji. Bwana yule akatabasamu na kwenda zake upesi akakamilishe kazi. Ila bahati isiwe kwake, hakuwa anajua wapi alipolazwa mlengwa wake. Hivyo ikamlazimu kupoteza kama dakika mbili kabla hajawa mbele ya mtu anayetakiwa kumuua.
Kabla hajafanya hilo, simu yake ikanguruma mfukoni. Akaitoa na kutazama, alikuwa ni mtu aliyemuagiza akafanye tukio. Akapokea na kumwambia kwa kunong’oneza, “I am in, wait.” kisha akakata simu.
Sasa ikawa imebakia kumaliza tu kazi, bwana Sheng akawe historia ya kale inayotisha.
Alikuwa amelala kitandani hajielewi hata linaloendelea. Dripu ilikuwa ipo kwa juu ikidondosha matone, na usoni alikuwa ana ‘nyago’ ya kumpatia hewa ya oksijeni. Mwili wake wote ulikuwa umefunikwa n shuka isipokuwa shemu yake ya kichwa na mikono tu.
Kando kando yake kulikulikuwa na vifaa kadhaa vinavyobeba uhai wake kwa ncha ya kidole. Na pia kulikuwa na kifaa kioo kionyesha maendelea ya mapigo yake ya moyo. Ama kwa hakika yalikuwa hafifu.
Bwana yule akaweka mikono yake shingoni mwa Sheng. Hajaminya, mara akasikia kipyenga cha ‘hafla, Prrrrriiiiiii!!!! prrrrrrrriiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii! Prrrrriiiiiiiiiii! Akatoa macho. Huko nje akasikia vishindo vya watu vikitesa ardhi!
Kwa muda kidogo akawa ametekwa na buwazo. Akimbie? Au amalize kazi yake? Alihisi kutetemeka. Kama angeendelea kumnyonga bwana Sheng, wazi ingelimchukua muda kidogo na yeye huo muda hakuwa nao. Basi afanye nini cha haraka kunusuru roho yake na huku atimize wajibu?
Akanyofoa waya za mashine zimsaidiazo mgonjwa, kisha upesi akatoka nje akikimbia. Kufika nje, akakutana na watu taribani kumi kwa idadi ya haraka. Wote wakiwa wamemnyooshea bunduki, akaamriwa anyanyue kwapa. Akatii.
Kule ndani nesi akawahi chumba cha mgonjwa. Huko akakuta ‘alarm’ zalia kwa fujo na mgonjwa akiishilia uhai. Haraka akarejesha mashine katika hali ya kawaida, na akaokoa maisha ya mkuu wake kwa ncha ya sindano. Mashine ya mapigo ya moyo ikaanza kusoma upya. Akatip! … akatip! … akatip! … akatip! http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Mgonjwa akihema kwanguvu ndani ya kinyago.
***
Ngo! Ngo! Ngo! Bwana wa kichina alisikia hodi hiyo, ila akasita kwanza. Macho yalikuwa yamemtoka. Jasho jembamba lilikuwa lamchuruza. Na moyo wake ulikuwa unakita kwanguvu kubisha hodi mbavu.
Hodi ikarudiwa tena. Na hakuwa na namna ya ziada sasa zaidi ya kwenda kuiitikia. Akiwa na kibukta chake, na mwili unamtetemia, akajonga na kutengua kitasa. Nje akawaona wanaume wawili anaowatambua wakiwa wamepigishwa magoti, na wanaume wengine takribani kumi wakiwa wamewasimamia na bunduki.
“Walitaka kumuua mkuu Sheng!” shtaka likatolewa kwa sauti kuu. “Wamevamia hospitali na kuua walinzi wanne katika jaribio hilo!”
“Inawezekanaje jambo kama hilo?” akashangaa bwana huyu wa kichina, kisha akawatazama walengwa na kuwauliza kwa sauti ya ukali kidogo,
“Ni kweli yanayozungumzwa?”
Wale watu wawili wakamtazama. Na kwa soni, akaepusha macho yake kutazama kando.
“Mkuu, wanastahili kuuawa mara moja!” akasema mmoja wa wale mabwana waliowaleta wale mateka. Akaungwa mkono na wenzake wote. Ndio! Wanastahili kuuawa. Na hiyo ndiyo ilikuwa sheria. Hamna anayebakiziwa uhai akidiriki kufanya jaribio la kummaliza mkuu. Na adhabu yake yafanyika mbele ya umati.
Hata bwana huyu hakuweza kulikataa hili kwani litazua mjadala mkubwa na hata kumweka rehani. Basi akakbidhiwa bunduki kutimiza agizo. Bunduki ilikuwa na risasi kumi na nane.
Wakati hayo yote yanaendelea, Glady alikuwa anashuhudia kwa kupitia dirisha. Mambo haya yalikuwa yanamtisha mno. Ametoa macho na kinywa chake kipo wazi.
Risasi zikavuma mara mbili! Wale watu wakadondoka wafu. Wakabebwa na kwenda kuzika kana kwamba mizoga, na huku nyuma wakimwacha bwana yule wa kichina majuto na maumivu makubwa sana kifuani.
Aliingia ndani akamtaka Glady aondoke zake upesi. Na baada ya punde akakutana na jamaa wake mmoja mpangoni aliyebaki. Akiwa amekabwa na donge la uchungu kooni, akasema, “Mpango wetu ulikuwa wa kipumbavu na wenye papara. Sasa tumeshawapoteza wawili.”
Yule bwana akamuuliza, “Una mpango mwingine?”
“Pengine ninao,” akasema bwana huyu wa kichina. “Na sasa nitaufanikisha mwenyesha jua likiwa linawaka.”
Basi hawakuongea sana, jamaa yule akaendaze. Watakutana baadae.
***
Saa tatu asubuhi …
“Do we need to hold on more?” aliuliza Wales akimtazama Denmark. Wote walikuwa wameketi sebuleni, vichwani wa earphones zilizokuwa zinawaletea taarifa toka kwenye kifaa maalum kidogo walichomfungia Sheng. Na mpaka sasa kifaa hicho kiilikuwa kimeshawatanabahisha makazi aliyopo Sheng na hata sauti ya yale yanayozungumwa ndani ya duara la robo kilomita toka kila pande ya dunia ya mahali alipo Sheng. Tena kwa usikivu mzuri.
“No,” akajibu Denmark. “Perhaps we should wait a bit. It seems the are more and more to discover.”
Saa nane mchana.
Japo ilikuwa ni katikati ya siku, yaani mchana, jua halikuwa linaonekana na hali ya hewa ilikuwa ya abridi kana kwamba kuna mvua yaja muda si mrefu. Upepo ulikuwa unapuliza na angani hakukuwa kweupe ama kweusi sana, wastani.
Muda huu, ndani ya jengo ambalo ndilo makao makuu ya familia ya Wu kulikuwa ni kutulivu haswa. Si kwamba watu hawakuwa wanapita, lah! Watu walikuwa huku na kule, wanakatiza kutoka kushoto na kwenda kulia wakiwa wamevalia mavazi yao ya majoho rangi ya karoti,
Hata zaidi wakiteta, lakini kwa ukimya kiasi kwamba ni ngumu kujua kama hapa pana watu kama umefumba macho.
Katika utulivu huu, mara mtu mmoja anakuja kwa kasi akikimbia. Anasimama malangoni na kufungua, kisha anazama ndani upesi. Anaenda moja kwa moja kuonana na ‘master’ na kumweleza kuwa kuna jambo nje anapaswa kwenda kuliona.
Basi pasi na ajizi, master, tumtambue kwa jina hilo, anatoka akiongozana na kijana huyo mpaka nje. Huko wakitembea umbali mfupi, wanakutana na vijana wengine watatu wakiwa wamembelea mwanaume asiyejiweza.
Ni Lee. Master anamtambua. Kabla hajauliza nini kilichotokea, vijana wale wanasema wamemkuta akiwa njiani, amejilaza, hajiwezi. Mgongoni ana matundu mawili ya risasi na mwili wake umejawa majeraha.
Lee anapelekwa kwenye chumba fulani kidogo chenye uhaba wa mwanga, analazwa chini na kisha vijana wale wanaondoka wakimwacha master peke yake. Anawasha mishumaa, na kisha anaanza kuandaa madawa.
Anatwanga hiki. Anamiminia kile. Anachuma hiki. Anaweka pale. Anachanganya hili na lile na mara anapata uji mzito wa rangi ya kahawia. Anampakaa Lee shingoni, kisha anachukua pini kali ndefu, anamchanja na kutoa risasi mwilini.
Kwenye majeraha anatia majani fulani aliyoyaponda na kuyachanganya na unga alioutoa kwenye kibakuli fulani cha udongo juu ya shelfu. Baada ya hapo, anawasha moto kwenye vijiti viwili vyembamba na kisha anaviwacha ndani vikiwa vinafuka moshi mzito.
Anarejea mahali pake pa kazi na anaketi akitafakari kilichomsibu kijana yule, yaani Lee. Akatengeneza mawazo mengi sana kichwani ila akaona ni bora avute subira, alimradi amerejea salama, atapata tu kujua kilichotokea kwa kupitia kinywa cha mlengwa.
***
Saa kumi jioni, Hongkong …
Mlango wa kioo unafunguliwa na anazama ndani jibaba jeusi la miraba minne. Jibaba hili ndilo lile lililopewa kazi ya kumtafuta na kummaliza bwana Lee tangu kipindi kile alichoingia anga za wenyewe.
Anaketi kitini, kiti kinabonyea kidogo. Anasafisha koo lake na kumtazama mwanamke mrembo wa kizungu aliyekuwa mbele yake akitafuna ‘bubblegum’ kwa pozi za kike. Macho ya mwanamke huyu, ndani ya miwani kubwa nyeupe, yalimwangazia huyu mgeni na kumuuliza kwa sauti ya chini ila sikivu,
“Cany I help you, Rob?”
“Surely, you can. You know why I am here.”
Mwanamke huyu akapuliza puto na kulipasua, kiisha akaendelea kutafuna na sasa macho yake yakiangazia tarakilishi yake ya mezani.
“I don’t see any appointment here. Are you sure you’re supposed to be here at this time?”
“Yikes!” jibaba likalaumu. “Please can you do something? You know it gat to be serious issue for me to be here, ayt?”
Mwanamke yule akanyanyua simu yake na kupiga. Akaleza kuna mgeni papo. Basi alipoweka simu mezani akamtazama mgeni wake na kumpatia ishara ya kichwa. Jibaba akanyanyuka na kwenda zake ndani kukutana na bosi.
Bosi huyu alikuwa amevalia suruali ya kitambaa rangi ya bluu na kiatu cheusi safi. Hakuonekana kwa juu na hivyo basi tutamtambua kwa sauti yake nzito kwa sasa.
“I am done,” akasema yule jibaba.
“Sure?” bosi akauliza kwa sauti yake ya kukoroma.
“Sure. Now the document is within our hands and the man is down.”
“Perfect. One step at a time.”
“So what’s next?”
“Future is so exciting, Rob. Full of bloodshed. But now I can confidently declare the death of Wu family. Confidently. It’s just a matter of time.”
Rob akacheka.
“Let me see what I can do today,” akasema bosi na mara Rob akanyanyuka na kwenda zake.
***
Saa kumi na mbili jioni, nchini, kambi ya wachina.
Bwana yule wa kichina alirejeshea mlango wa maabara na kutengenezea suti yake vema. Akapiga hatua kubwa na dhahiri mgongoni akiwa amewekelea kitu fulani ambacho hakutaka kionekane.
Punde akawa ameshafika kwenye makazi yake na baada ya dakika kama kumi hivi, akatoka na kuelekea kule hospitali ya kambi kwenda kukutana na Sheng. Ulinzi ulikuwa umeimarishwa maradufu tofauti na hapo awali. Idadi ya walinzi ilikuwa imeongezeka, takribani kama watu kumi wakiongezwa lindoni.
Akakutana na daktari na kupewa ripoti ya maendeleo ya mgonjwa. Na baadae akapewa ruhusa ya kwenda kumwona mgonjwa. Fursa adhimu aliyokuwa anaitaka. Daktari alimsindikiza ila hakukaa ndani, akamwacha mgeni mwenyewe na mgonjwa.
Bado Sheng alikuwa kwenye hali ya kutojielewa. Ni mashine tu ndizo ambazo zilikuwa zimeshikilia uhai wake. Macho yake hayakuwa yamefumba vema, na alikuwa anahema kwanguvu.
Bwana yule wa kichina akatulia humo kwa kama dakika tano hivi kisha akachomoa sindano ndogo ndani ya mfuniko yenye kimiminika rangi ya manjano. Akatazama usalama. Akasogelea dripu, na kisha akadungia sindano ile ndani ya mfuko na kutikisa fuko hilo la dripu mpaka pale ambapo hali ya kimiminika ilirejea kwenye mazingiira yake ya awali.
Alafu akamwita daktari na kumwambia amemaliza haja yake.
“Anatia matumaini. Amenishika mkono japo hajasema jambo,” alisema bwana yule wa kichina akitabasamu. Hakukaa sana akaenda zake.
Usije dhani bwana huyu ni mjinga kujiweka rehani kiasi cha ‘kifala’. alikuwa anajua anachokifanya na anakijua fika.
Alipofika nyumbani, muda si mrefu akaja yule jamaa wake mmoja aliyebaki, akamweleza, “Nimeshakamilisha kazi. Sasa itachukua juma moja kwa Sheng kufa. Kuanzia sasa atakuwa anakufa taratibu taratibu.”
Yule jamaa mwingine akatabasamu na basi akampatia mwenzake mkono wa pongezi.
**
Saa tatu usiku …
“They have poisoned him,” alisema Scotland. Tayari wanaume hawa wa kizungu wakawa wameshalijua hilo kwa kupitia kifaa chao ambacho wamekipandikiza kwenye mwili wa Sheng.
Katika namna ya kitaalamu, baada ya mabadiliko kadhaa kutokea mwilini mwa mhusika, kifaa hicho kilitoa taarifa kwa waliokiweka.
“But why they did this?” akauliza Wales. “Why do they want to kill their master?”
“There’s something behind here,” akasema Denmark akikuna kidevu. Kwa sekunde kama mbili hivi wakatazamana. Ila punde wakasikia kitu nje. Wakapata shaka.
Walipokuja kutoka, wakagundua kulikuwa kuna mtu ndani ya eneo lao. Kwenye perving, kulikuwa kuna nyayo mbichi za viatu.
Wakatoka hata kutazama nje ya uzio wao wapate kutambua kama kuna yeyote, ila hawakufanikiwa abadani. Walichoambulia ilikuwa ni alama za matairi ya gari kuashiria kwamba mtu huyo alikuja papo na usafiri.
Wakabaki kwenye buwazo na shaka kiasi chake. Mtu huyo atakuwa amesikia kitu gani toka kwao? Ametumwa na nani na amepafahamuje hapo kwenye makazi yao?
Hata waliporudi na kuketi sebuleni wakaendelea kujiuliza. Walikuwa wanaamini wamefanya kila kitu kistadi kiasi cha kutokubakiza kivuli, sasa hii ishara ya mtu kutembelea eneo lao haikuwa njema kabisa.
Sasa ikawalazimu wawe makini sana. Na kwa kuhakikisha hilo, wakaona ni vema wakifunga kamera zao ndogo maeneo mbalimbali ya jengo hilo ili basi iwe rahisi kupata taarifa za uvamizi kabla matokeo hasi hayajachukua nafasi.
Zoezi hilo likafanyika upesi, na kila kitu kikawa kwenye mstari wakiamini kuwa mvamizi yule atarejea tu. Na punde atakapofanya hivyo basi hilo litakuwa kosa lake la mwisho kulifanya kabla hajaenda jehanam.
Ila hawakuwa wanajua. Hata wakati wanafanya ‘installation’ hiyo ya kamera, mtu yule ambaye walimkosa alikuwa anawatazama na hivyo basi akiwa anajua si muda wa yeye kufanya tena jaribio la kuzama mule.
Si kwamba mtu huyu alikuwa karibu, lah! Alikuwa ndani ya gari, kilomita kadhaa tu mbali na ile nyumba ya walengwa. Na macho yake yalikuwa yanasaidiwa na hadubini kalii yenye uwezo wa kupambana na kiza kupekua eneo analolitaka.
Alipotosheka na alichokipata, akaweka hadubini chini na kutabasamu. Na kumbe alikuwa ni Jona. Lakini alipajuaje hapa? Si muujiza. Jona na wenzake walikuwa ni watu wa kwanza kutambua utekwaji wa bwana Sheng na hata makazi ambayo alihifadhiwa kwa kutumia chip ndani ya mwili wa mchina huyo.
Na hivyo basi, watekaji hawa pasipo kujua lolote lile, wakafanya kosa la kumpeleka mateka wao nyumbani ili wamhoji na hatimaye kumtia kifaa chao kitakachowasaidia kuwapatia data.
Kiupofu wakarahisisha kazi ya wakina Jona. Sasa jicho la tai lilikuwa linawamulika kwa karibu zaidi.
“Sasa?” akauliza Miranda. “Kuna haja ya kufanya mambo?”
“Hapana,” akajibu Jona akitikisa kichwa. “Hivi Miranda hujajua kuwa hapa kuna faulo ya mchezo inachezwa? Bado tunatakiwa kuwa watazamaji kwa sasa. Muda utakapofika wa kuvaa jezi basi tutalitenda.”
“Ila kule upande wa Sheng bado wapo kimya,” sauti ya Marwa ilivuma. Kumbe alikuwa kwenye viti vya nyuma vya gari. “Unadhani na wao watakuwa wanapanga kitu?”
‘Sidhani,” akajibu Jona kisha kubinua lips zake. “Kama yule jamaa alivyosema, kuna something behind hapa. Kule kwa kina Sheng kuna jambo linafichwa, ila naamini muda si mrefu mambo yatakuwa bayana. Kama si hivyo, basi wale wazungu wasingekawia kuchukua hatua.”
Basi gari likawashwa, wakatimka. Ila si kwamba jicho la tai lilikuwa linawaacha walengwa wake wapweke, hapana. Kuna namna hapa kamilifu.
***
Saa kumi na moja asubuhi …
Kwa mbali alianza sasa kupata ufahamu. Masikio yake yalisikia sauti ya ndege wakilia huku na kule kumjuza kuwa asubuhi imewasili. Ni kweli mwili wake ulikuwa umechoshwa na purukushani za kuinusuru roho yake, ila bado alikuwa ana nia ya kurudi tena ulimwenguni kujua yanayoendelea.
Akafungua macho japo yalikuwa mazito. Akatazama kushoto na kulia na kisha akajitahidi kunyanyuka akipambana na maumivu aliyokuwa anayasikia. Alipoketi kitako, sasa akasikia vema. Huko nje sauti za watu walio kwenye mafunzo zilikuwa zinavuma. Kiwanja cha kufanyia mazoezi hakikuwa mbali sana na pale alipokuwapo. Lakini hata hivyo sauti hizi zimeanza kuvuma muda si mrefu kwani angelizisikia mapema kabla ya zile za ndege masikioni.
Akapambana kusimama. Akaweza. Ilikuwa ni ajabu mno, na kama ungelimwona jana basi ungelisema mtu huyu, kama kweli angelinusurika uhai, basi ingemchukua miezi kama mitatu au minne au mitano kusimama tena.
Hakika dawa za ‘master’ zilikuwa kali na zenye kufanya kazi mapema mno. Akajivuta kudaka shuka na kujisitiri, kisha akajikokota mpaka nje. Bado hakuwa na mwendo sawia, ila angalau husogea. Na kwa kasi ile ya dawa, basi hata juma lilikuwa kubwa kwake kutengemaa.
Taratibu akajivuta mpaka eneo alipokuwa master, akiwa anafanya meditation kama ada yake kila asubuhi ya mapema, na kusimama hapo pasipo kusema jambo. Alingoja master amalize. Ila ajabu, kama dakika mbili kukatiza, master bado akiwa amefumba macho na hata amempatia mgongo bwana Lee, akamwita kwa jina.
Akamuuliza, ina maana umepona kiasi hicho? Kisha akatabasamu na kugeuka kumtazama. Ni baridi na ametoka na shuka, tena mtu mgonjwa. Akamwelekeza waende mahali penye joto zaidi, wakapate pia na kifungua kinywa.
Baada ya muda kidogo wakawa wapo ndani ya chumba kidogo chenye zulia na mito chini, wakaketi. Punde fupi akaja mwanadada aliyebebelea trey ya kioo na vikombe viwili vya kahawa. Akawapatia.
Walipoanza maongezi Lee akaeleza staajabu yake kuwa pale maana alidhani amekwisha kufa kwenye mikono ya wadhalimu. Vita ilikuwa kali na walikuwa wamedhamiria haswa kumtoa roho.
Basi master wake akamwambia ni kama bahati. Na kama yuko sahihi, basi wadhalimu wale waliolenga kumuua, walishindwa kutimiza hilo kwa uhakiki zaidi baada ya yeye kuzama ndani ya himaya ya Wu, hivyo walivyotupa hizo risasi zao, wakaona inatosha wakajiendea.
Ila zaidi ya hapo, Lee akaeleza mkasa mzima ulivyokuwa. Namna alivyosalitiwa na yule afisa na hatimaye kukwapuliwa nyaraka zote hata zile ambazo alitakuwa kuja nazo.
Master akamtoa shaka kwa kumwambia watajua namna ya kumalizana na afisa huyo. Kwakuwa amepona dhidi ya kifo, basi ni huyo afisa ndiye ambaye ataonja kifo. Na kwa kuanzia muda huo, akamtawaza kuwa kamanda mkubwa wa kamandi ya makao makuu.
Akampa majukumu ya kuongoza kikosi chote kilichopo hapo makaoni, cha watu takribani alfu ishirini. Na hivyo akamtaka baadae nyakati za jioni wakalifanye jambo hilo kuwa rasmi kwa kuliweka bayana kwa kila mtu anayetakiwa kulifahamu.
Basi baada ya kuteta hayo kidogo, wakanyamaza na kupambana na baridi iliyopo kwa kunywa kahawa zao vikombeni. Zikapita kama dakika tatu, Lee akauliza swali, umepata chochote kile toka kule Afrika?
Master akatulia kwanza kidogo kabla hajajibu. Alishusha pumzi ndefu puani alafu akasema kwa maneno machache, hali si shwari. Lee alipotaka kujua zaidi, akamweleza kuwa kuna taarifa walizipata za kutekwa kwa Sheng na watu wasiojulikana. Ila kwa sasa mambo yapo vema kwani ameshapatikana, japo si mzima kiafya.
Lee akapata shaka hapa. Wakina nani hao waliomteka bwana Sheng? Alipoeleza shaka lake, Master akamtoa hofu kwa kumweleza kuwa anaamini Sheng atalimaliza jambo hilo kwani kama lingekuwa kubwa basi angeshalieleza huku makaoni.
Basi kikao kikawa kimezizimia hapo.
Baadae majira ya mchana, Lee akiwa peke yake anakula chakula, jambo lile la Sheng likamjia tena kichwani. Aliona kuna haja ya kuhofia sana kuhusu kile kitu. Ni mtu gani ambaye alikuwa ana uwezo wa kumteka Lee? Je ni wakina Jona? Ama watu wa bwana Brown Curtis?
Akiwa hapo anakula, akaja mtumishi mmoja kumwona. Msichana mchanga wa kichina aliyekuwa amebana vema nywele zake, mwili wake ameusitiri kwenye nguo za kitamaduni.
Msichana huyo alikuwa amebebelea nguo za Lee alizotoka nazo shurbani. Kabla hajaziweka chini akamuuliza Lee kama nguo atazihitaji tena ama akazichome. Lee akafikiri kidogo, akamruhusu msichana huyo akazichome.
Ila mwanamke huyo kabla hajatokomea, Lee akakumbuka jambo. Akamwita mwanamke huyo na kumwambia atazame mfukoni mwa nguo hizo kama kuna simu yake. Alikuwa anabahatisha tu, na kama angeliambiwa hamna,a singeshangaa.
Ajabu, msichana yule baada ya kufanya msako mdogo, akahisi kitu kigumu mfukoni. Alipozamisha mkono na kuchomoa, akatoka na simu. Akamkabidhi Lee na kisha akaenda na zile nguo akachome.
Lee, akiwa haamini, akaipekua simu yake. Na baada ya muda kidogo, kwakuwa alikuwa na hamu kujua zaidi mambo yaliyotokea kule Afrika, aka-‘switch’ laini yake ya kimatumizi kule mtandao wa whatsapp.
Muda kidogo, akapokea jumbe kadhaa. Ikiwemo zile za Glady!
***
Saa saba na nusu mchana, Shanghai, China. Kwenye ghorofa ya ishirini ya nne …
Kulikuwa kuna kikao cha watu wasiozidi watano. Watu hao wote wote walikuwa wamevalia suti nyeusi, na sura zao zikiwa kapuni. Miguu yao ilikuwa imetambaliwa na soksi nyeusi pia na chini wakimalizia na viatu barabara vya ngozi!
Ndani ya eneo hili kulikuwa tulivu, na kiyoyozi chapuliza kwa mbali.
“It is now or never,” sauti nzito ilisema. Na sauti hii kama wewe ni mtu wa kumbukumbu basi ilikuwa ndiyo ile ambayo ilikuwa inateta na Rob jana yake tu baada ya kupewa taarifa ya zoezi la kummaliza Lee.
Bwana huyo alikuwa hapa kikaoni na wenzake. Na mjadala hapa ukiwa ni kumaliza kabisa familia ya Wu kwenye uso wa dunia ili basi kuruhusu wabepari kufanya kazi yao vema na kuondoa kabisa tishio la China kushikilia uchumi wa dunia na kuiendea kombo Amerika.
“This is the time for us to finish the game,” alisema bwana yule mwenye sauti nzito. Wenzake wakaunga mkono hoja. Na hivyo basi wakakubaliana wanaume wale waliopo Afrika, the intellectual instinct, waanze kutekeleza kazi ya kufutia mbali mamlaka ya China ukanda wa Afrika ya mashariki na kati.
Sasa mambo yalikuwa yameanza kupamba moto na vita rasmi ilikuwa imetangazwa, ambapo mataifa makubwa ya kibepari yameazimia kumwangusha tembo huyu mkubwa wa mlengo wa pili kabla hajazidi kutapanya na kuharibu shamba lao.
Kwa namna Uchina ilivyokuwa inakuja juu, si kitu cha kuwaza kuwa hofu kuu inatokota kwenye mioyo ya mabepari. Hii ni alama ya kushindwa. Alama ya kuzidiwa maarifa. Kitu ambacho kamwe hawako radhi kukiafiki.
Basi kikao baada ya muda kikafungwa na mabwana wale wakatawanyika. Ila bwana mmoja, si yule bosi wa Rob, alipokuwa kwenye gari aliongea na simu yake kwa muda mfupi akitoa maagizo. Anataka kambi ya wachina imalizwe haraka iwezekanavyo.
Bwana huyu alikuwa anatimiza tu kile walichokubaliana. Na hao aliokuwa anaongea nao hawakuwa wengine bali the intellectual instinct, kundi haramu la mauaji na mienendo ya kimafia, sasa likiwa limeshaweka makazi yake nchini.
**
Baada ya siku mbili … Dar, Uwanja wa ndege.
Ni majira ya mchana. Lee akiwa anakokota kibegi chake kidogo anaongea na simu akiwa ameweka sura ya kazi. Macho yake yamezibwa na miwani ya jua, na mtindo wake wa nywele ameubadili kidogo. Alikuwa amezilaza, na kwa wingi wake zikawa zinakaribia kugota mabegani mwake.
Punde alipotoka ndani uwanja wa ndege, yaani kuikuta barabara, akatia simu yake mfukoni na kuangaza kushoto kwake. Akaliona gari fulani likiwa laja. Range rover sport nyeusi. Ikasimama mbele yake, akakwea.
Gari likatimka kwa mwendo wa wastani uliokuwa unachanganyia kwenda kasi.
“Vipi, mmemwambia yeyote yule?” akauliza Lee.
“Hapana, hakuna anayejua,” akajibu jamaa aliyekaa kando na dereva.
“Safi sana,” Lee akapongeza na kuuliza, “Sheng anaendeleaje?”
“Yuko kama jana tu. Sioni kama kuna mabadiliko,” akaendelea kujibu yule jamaa aliyeketi karibu na dereva. Wakati akiteta akikunja kunja shingo yake kutazama nyuma alipokuwa ameketi Lee.
“Mpaka sasa hamjajua nani anayehusika na utekwaji wake?”
“Hatujajua. Wala sababu za wale wenzetu kujaribu kumuua.”
Lee akanyamaza. Kitu pekee alichokuwa amewaambia hawa watu ni ujio wake na ufanywe kuwa siri. Hakuna la ziada. Hivyo watu hawa hawajui kama Lee alinasa habari zozote toka kwa dada poa Glady.
“Si huko naelekea, tushike barabara ya kushoto,” Lee alielekeza.
“Kwani hatuendi makaoni?” dereva akauliza.
“Tunaenda,” Lee akajibu, “ila baada ya kutoka kwanza huku.”
**
Ngo! Ngo! Ngo! Ngo!
Glady alifunua shuka akaangaza kwa jicho moja. Bado alikuwa yu kitandani majira haya ya mchana na si ajabu kwani amelala asubuhi ya saa nne. Chumbani alikuwa na mwenzake ambaye alikuwa amelala vibaya kiasi cha kuacha maungo yake wazi.
Mwanamke huyo alikuwa ananuka pombe na hata miguuni bado alikuwa ana viatu vyake vya visigino virefu. Na hapo kitandani kulikuwa na chupa tupu ya Vodka.
“We Esther! Esther!” Glady aliita akimsukumasukuma mwenzake. “Wewe si nilikuambia ukalale kwako? Nani kakuruhusu ulale hapa?” Glady aliuliza. Ila alikuwa anaongea na mfu. Huyo Esther alikuwa hasikii hata tone. Mdomo wake unukao kileo, ulikuwa wazi akikoroma kama amekabwa.
“Wewe!” Glady akaendelea kusumbuka na Esther. “Si naongea na wewe Esther!”
Hodi ikagongwa tena. Sasa akili ya Glady ikakumbuka kuwa ameamka kwasababu ya hodi na si Esther. Akasonya. Kichwa kilikuwa kinamgonga kwa mbali na mwili wake ulikuwa umejawa na uchomvu. Alivuta shuka kwanguvu kumpokonya Esther kisha akajifunika na kwenda mlangoni.
Baada ya kuondoa loki zake duni, akakutana uso kwa uso na Lee.
“Kumbe ni wewe?”
“Ndio ni mimi?” Lee akajibu akiegemea ukuta. Alikuwa ameegesha gari lake mbali kidogo na hapa alikuwa mwenyewe.
“Mbona saa hii jua kali?” Glady akauliza na kisha akapiga mhayo.
“Nina maongezi kidogo na wewe,” Lee akajinasibu. Glady akatikisa kichwa chake akifinyanga lips zake.
“Mchina, nimechoka. Kwanza kama unadhani utanipeleka kule kwenu, sahau kabisa. Kwa niliyoyaona siku ile, yanatosha kabisa!”
“Ndiyo maana nipo hapa,” Lee akateta.
“Ina maana wewe huyajui au?”
“Pengine wewe unayajua zaidi … Sikia, Glady, serious, sina muda sana wa kukaa hapa. Tunaweza tukaongea tafadhali? Sidhani kama itachukua muda mrefu.”
“Ulikuwa wapi siku ile nakutumia message? Hukusikia mlio wa risasi?”
“Sikuwapo hapa, nilikuwa China.”
“Oooh!” Glady akakuna kichwa chake kwa kidole kimoja alafu akapiga tena mhayo. ‘Nimechoka, nataka kupumzika.”
Lee akazamisha mkono wake mfukoni na kutoka na ‘wekundu’ kama sita hivi, akamwonyeshea Glady. Glady akatabasamu.
—
“Alinichukua, ila hakufanya chochote na mimi. Alikuwa bize sana kuongea na simu kupanga mikakati ya mauaji. Ila bahati si yake, wale watu aliowatuma walirejeshwa na akawaua kwa mkono wake mwenyewe,” alieleza Glady akiwa ameketi kwenye ngazi. Lee naye akiwa pembeni yake.
“Ulisikia sababu ya yeye kufanya hivyo?” Lee akauliza. Glady akapandisha mabega yake juu na kusema, “Hapana. Ila nilichosikia ni kwamba usiku ule ungekuwa mkubwa sana kwao. Na hata mimi alin’chukua ili akafurahie siku yake hiyo japo haikuishia kuwa nzuri nadhani.”
“Ahsante,” Lee akasema akisimama. “Nitakuhitaji tena karibuni. Namba yako si ile ile?”
“Umenimiss eenh?” Glady akauliza akimkonyeza Lee.
“Ni kwa kazi. Si kama ufikiriavyo,” Lee akamweleza na kisha akaenda zake.
***
Majira ya saa mbili usiku …
Kulikuwa na ukimya eneo hili. Kwa mbali, kwa mbali sana, maongezi yalikuwa yanasikika kwenye makazi ya bwana yule wa kichina aliyefanya hila ya kummaliza bwana Sheng.
Maongezi haya yalichukua muda mfupi, kama vile dakika mbili tu, na muda mwingi kulikuwa ni kimya. Yaani ukimya ulitawala dakika tano za maongezi haya ambayo kwa jumla na zile mbili zilikuwa saba za makutano.
Baada ya dakika hizo, sauti kubwa ya risasi ikavuma … na tena … na tena! Tatu kwa ujumla. Baada ya hapo, wanaume wawili wakatoka ndani ya makazi hayo wakiwa wamebebelea mwili wa bwana yule wa kichina na kwenda kuufukia, Lee akishuhudia.
Baada ya hilo tukio, akaenda zake hospitali kumwona Sheng aliyekuwa amelala kitandani kwa masiku sasa. Bado hakuwa na nguvu. Na mashine ya oksijeni ilikuwa iimefunika mdomo na pua yake.
Kwa mbali mashine ya kuhesabu mapigo ya moyo ilikuwa inafanya kazi, ikilia.
Lee akamsogelea Sheng na kumtazama kwa huruma. Ndani ya kifua chake akijiuliza ni nini kilijiri. Alikuwa anatamani sana kujua. Kichwani alikuwa ana maswali kadha wa kadha.
Akiwa amekaa hapo, mara Sheng akafungua jicho lake la kushoto kwa mbali. Akanyanyua vidole vyake kupapasa mkono wa Lee. Lee akashtuka kwa faraja kuona hilo. Akadaka mkono wa Sheng na kumtazama usoni akikodoa.
Kuna kitu Sheng alikuwa anataka kuongea. Uso wake ulionekana kuhangaika akitaka kusema jambo.. Basi Lee akamwondoa mask yake ya kumvutisha hewa, na kisha akasogeza sikio lake kwenye mdomo wa Sheng uliokuwa unamamata kwa mbali ukiwa umeegemia kushoto.
Sheng, akiwa anakoroma na akisikika kwa mbali sana, akamwambia Lee maneno kadhaa ya kichina. Na baada ya kusema hivyo, akakaa kimya. Lee akawahi kumrejeshea kinyago chake cha kuhemea. Ila hakufungua tena jicho wala kuchezesha tena vidole vyake wala kiungo chochote.
Lee akapata shaka, akamwita Daktari haraka. Naye alipokuja, akaenda kungoja nje. Kwa takribani kama nusu saa, daktari na nesi wakawa wapo ndani, vitu vikiingizwa na kutolewa. Baada ya hapo, daktari akiwa amenyong’onya akamwita Lee ofisini.
“Hali inakuwa mbaya kila uchwao. Ilikuwa ni ajabu sumu inaendelea kumtafuna mwili pasipo kujali juhudi zote hizo tulizofanya.” Daktari akatengeneneza miwani yake na kutazama baadhi ya karatasi ndani ya faili, kisha akasema kwa sauti ya chini;
“Tumekawia. Na hili linaelekea kugharimu maisha yake. Tumegundua ndani ya dripu kulikuwa na sumu. Hatujui imefikaje, na mbaya zaidi majibu yake yameshaanza kuonekana mwilini. Amepooza upande wake wote wa kulia. Matumaini yake ya kupona ni hafifu hafifu mno.”
Akiwa hapo, bado taarifa hizi zikiwa ngumu kuzimeza, mara akasikia king’ora cha hatari kikilia kwanguvu! Punde akaja mwanaume mmoja hapo akiwa amebebelea silaha mkononi. Akasema, “Tumevamiwa!”
Lee akamtazama daktari na kumwambia, “Ningoje hapa, nakuja.” kisha akaenda zake na yule jamaa aliyekuja kuleta taarifa. Wakaelekea mpaka huko inaposemekana kuna mashambulizi. Lakini hawakukuta kitu chochote. Zaidi kulikuwa kweli kuna miili ya watu waliokufa ikiwa imezagaa huku na kule.
Jambo hili likamshangaza sana Lee. Walipata kusikia sauti za milio ya bunduki na hata kilio na magugumizi ya watu wakililia uhai lakini kila walipokwenda kutazama, hawakukuta mtu huko zaidi ya maiti.
Lee akatahamaki. Basi akapata wazo. Haraka akaenda control room apate kutazama kinachoendelea kwa kutumia rekodi ya kamera za cctv ambazo zimetundikwa ndani ya jengo hilo maeneo mbalimbali. Lakini alipofika huko, napo akakuta maiti za watu wanaohusika na kitengo hicho. Wote, sita kwa ujumla, walikuwa wameshindiliwa risasi kadhaa wakiwa chini wanamwaga damu. Alipotazama televiisheni, hakuona kitu. Zote zilikuwa na rangi ya bluu kuonyesha kwamba hakuna kinachodakwa na kurushwa kwa muda huo.
Ina maana wavamizi walikuwa tayari wameshaharibu mifumo yote ya kamera! Bado akiwa hapo, mara umeme ukakatika ghafla na eneo lote likabakia totoro gizani. Hapo sasa mambo yakawa magumu kupita kawaida.
Watu wakaendelea kuuawa na maadui wakiwa wanafanya namna ya kutoonekana kwa wepesi. Kwa takribani nusu saa, watu wengi mno wakawa wameuawa. Lee hakuwa na msaada wowote ule, zaidi ya kila mahala kushuhusia maiti na maiti na maiti.
Sauti ya mtu akigugumia ilisikika, na mara ikanyamaza kimya. Upande wa kushoto, akadondoka mtu akiwa anamimina damu kifuani mwake baada ya kukitwa na kisu kirefu chenye ncha nyembamba ndefu.
Hapo muuaji akaonekana akiwa mwanaume aliyevalia mavazi meusi ya kubana kana kwamba wale watu wazamao ndani ya maji. Muuaji huyo hakuwa amebakiza sehemu yoyote ya mwili wake wazi. Nguo yake hiyo ilikuwa imefunika mpaka kinywa na pua, macho yakiwa yamemezwa na miwani iliyobana kuta za uso.
Miwani hiyo ilikuwa inamwezesha kuona vema katika giza hili. Kwenye nyonga zake, alikuwa amebebelea mkanda mwembamba ulioning’iniza bunduki mbili ndogo. Na mikononi alikuwa ana visu viwili vinzvyochuruza damu.
Upesi, baada ya mtu yule aliyekitwa na kisu kudondoka chini, akatokea mtu mwingine mlinzi wa jengo. Alipomwona mvamizi, hakujiuliza mara mbili akarusha risasi kama tano kwa mfululizo. Lakini ajabu hakufanikiwa kumpata mlengwa wake kabisa.
Bwana yule mvamizi alichumpa na kujibiduabidua hewani, na mara kufumba na kufumbua akawa haonekani. Kuja kutahamaki, yule mlinzi akiwa anatazama huku na huko, mara akasikia kishindo cha mtu nyuma yake. Akatazama upesi kwa woga. Na katika haraka ya ajabu, kabla hajabinya kitufe cha risasi, akachomekwa kisu cha shingo.
Akiwa anapapatika na kifo, akabinya kitufe cha risasi kwanguvu, risasi zikamiminika kama mvua, lakini zote zikaenda kombo maana mvamizi alikuwa ameshaelekezea mdomo wa risasi pembeni. Basi bwana yule mlinzi alipoishiwa nguvu, akadondoka chini na kujifia.
Mvamizi akaweka kidole chake sikioni na kuuliza,
“What’s your position?” Sauti ikamjibu kwa mbali isisikike vema isipokuwa kwake mwenyewe. Basi akaongezea kwa kusema. “The building is under control. Seize the man and let’s finish the business.”
Akatoa kidole chake kwa sikio na kupotelea gizani.
**
Kulikuwa ni kimya sasa kupita kiasi. Hata watu hawakuwa wanaonekana wakikatiza huku wala kule tofauti na ilivyozoeleka siku zote.
Hata hapa hospitali palikuwa kimya. Ila hali hiyo haikudumu kwa muda mrefu, wanaume watano wakajiri wakitoa upande wa kushoto wa jengo. Wote walikuwa wamevalia sare, nguo nyeusi zinazobana miili na usoni wakiwa na miwani zilizobana na kushikilia vema nyuso zao.
Wakazama ndani ya hospitali, wakinyookea chumba alichokuwa amelazwa Sheng. Kufungua mlango kutazama, hakukuwa na mtu! Kitanda kilikuwa tupu. Mashine, mipira na waya, zilikuwa pembeni.
“Shit!” akalaani Denmark. Alitambulika kwa sauti yake. Sheng hakuwa ndani!
Basi akamgeukia mwenzake na kusema, “Scot, go look where he is.”
Haraka aliyepewa agizo hilo, Scotland, akatoka ndani na kwenda kule walipokuwa wamepaki gari lao, nje ya Jengo upande wa kulia, kama kilomita moja na nusu hivi. Alienda huko kwa kukimbia. Na hawakutaka kwenda wote kwa maana Denmark alikuwa anaamini Sheng atakuwa amefichwa ama amejificha ndani ya jengo.
Hivyo ni swala la kupewa taarifa na kuifanyia kazi tu.
Baada ya punde, Scotland akatoa taarifa, “He is out of the building!”
Hakuongezea ttaarifa nyingine, akasikia kiganja cha mtu kikimgusa begani. Kutazama, alikuwa ni Lee.
“I’ve got a little problem here,” Scotland akasema akiwa amebinyia kidole chake sikioni. “Let me deal with it, be in touch.” akamalizia taarifa na kisha akaufunga mlango kumkabili Lee.
“Who sent you here? Are you are the one who kidnapped Sheng?” Lee akauliza tena. Bwana Scotland akasikika akiguguma kwa kicheko, kisha akasema, “Hell yeah!” na kuongezea, “I don’t think if you have to know who sent us here ‘coz you are going to die in anyway. What help will it give?”
Aliposema hayo, Scotland akachomoa visu vyake nyuma ya kiuno.
“Where’s Sheng?” akauliza.
“You have to go through me to get him,” Lee akajibu kwa kujiamini.
“Ok, if that’s what you want,” akasema bwana Scotland na vita ikaanza. Lee hakuwa na silaha yoyote mkononi mwake. Aliamini kwenye uwezo wake kumlinda na hata kummaliza adui.
Na kwakuwa hakuwa anafahamu uwezo wa adui yake, akaona ni vema ampatia nafasi ya kumuanza. Kwa wakati huo akiwa anaamini adui wake huyo hatakuwa mtu mwepesi kutokana na matukio waliyoyafanya ndani ya jengo.
Hakuwa amekosea. Scotland alikuwa mwepesi mno na zaidi akiwa mwenye nguvu. Lee alijitahidi kukwepa lakini bado akajikuta akipokea ngumi kadhaa na mateke yaliyomrudisha nyuma.
Akaona endapo naye asiposhambulia basi muda si mrefu atajikuta yu hoi na kuwa chakula cha adui. Akaanza naye kujikakamua.
Akatupa ngumi, ikayeya, akatupa tena nyingine nayo ikadakwa, kabla hajaviringitwa, akaruka juu na kuchoropoa mkono wake kisha akajifyatua mateke. Nayo yakapanguliwa.
Scotland akatuma mikono yake yenye visu, Lee akajitahidi kuizuia, lakini Scotland akamzidi ujanja na kumchanja mkono wake wa kuume. Kisha haraka akaviringita miguu ya Lee na kumwangusha chini. Lee akapiga kiwiko mkono wa kushoto wa Scotland, kisu kikaangukia kando, sasa akabaki na kisu kimoja cha mkono wa kuume.
Akawa analazimisha kumtoboa Lee kifuani, Lee naye akikazana kuzuia mkono huo kwa mikono yake yote miwili. Ila ni dhahiri alikuwa anaelekea kushindwa. Ncha ya kisu ilikuwa inasogea taratibu, na ilibakiza kama robo sentimeta kugusa paji la uso la Lee.
Ilibidi afanye jambo la sivyo alikuwa anakufa. Basi akatumia akili yake. Kwakuwa nguvu kubwa Scotland alikuwa ameiweka kisuni, Lee akaachilia mikono yake upesi na kukunja shingo yake haraka. Kisu kikatoboa chini. Na sasa kwakuwa mikono ya Lee ilikuwa huru kwa muda huo mfupi, akagonga shingo ya Scotland maeneo ya pembeni chini kidogo mwa taya, Scotland akalegea.
Lee akachojoa miguu yake na kumkita mwanaume huyo kwenye kende, na kabla hajalalama kwa maumivu, akawa ameshasomba kisu na kumkita nacho shingoni. Akamsukumia pembeni bwana huyo na kuhema kwanguvu. Kazi haikuwa nyepesi hata kidogo!
Alimpofunua usowe na kumtazama hakuwa mtu anayemfahamu.
Akiwa amemaliza kazi hiyo pevu, akampoka bwana huyo funguo wa gari atumie usafiri wao kuyeya na Sheng. Akazama ndani na kutekenya gari, akaweka ‘gear’, kabla hakanyaga mafuta, akasikia kitu kisogoni.
“shut the the car off,” akaamriwa. Basi akatii amri. Akazima gari na kuweka mikono yake juu. Kukawa kimya kidogo. Alipotazama sight mirror, kioo kikaacho juu ya kichwa cha dereva, akaona sura nyeusi na si ya kizungu kama ambavyo alikuwa anawaza. Na kama haitoshi, sura ile aliyoiona haikuwa ngeni machoni pake.
“Sheng yupo wapi?” sauti ikauliza. Basi Lee akasita kidogo kusema. “Nimekuuliza Sheng yupo wapi?” Swali likarudiwa. Lee akajifikiri kidogo, kisha akasema, “Yupo upande wa kaskazini wa mahalii tulipo.”
“Tumwendee,” akaamriwa. Basi akatia moto kwenye gari na kutimka kwenda huko ambapo Lee alipasemea. Lakini kichwani mwa mchina huyu hakukuwa salama. Alikuwa anawaza mambo ya hatari. Alikuwa anawaza namna ya kujinasua hapa ahepe zake salama.
“Kamwe usije ukafikiri ujinga,” mwanaume yule aliyemwonyeshea bunduki akamtahadharisha. “Punde tu utakapofanya ujinga wako, basi nitatoboa kichwa chako na kukuacha mfu uliwe na mbwa koko!”
Basi hapa Lee akasitisha kwanza mipango yake. Akawaza huyu mtu ni wa namna gani na kivipi aliwaza alchokuwa anakiwazia yeye kichwani. Katika fikra hizo ndipo sasa fahamu zikamjia, kumbe mwanaume yule alikuwa ni Jona.
Ndio! Akili yake ikawa inazoza yenyewe. Ni Jona huyu. Ina maana naye amekuja na wale wazungu au amekuja kwa mambo yake binafsi? Lakini amejuaje haya? Akajikuta akipata mawazo maradufu.
Lakini zaidi akajikuta pia ana sababu ya kuhofia mara mbili. Kwake Jona hakuwa mtu wa masikhara hata kidogo. Kabla ya songombingo lolote lile, alikuwa ni mwanaume waliyemtafuta na kuhangaika kummaliza pasipo mafanikio.
Gari likasimama.
“Yupo pale!” Lee akasema akionyeshea kwa kichwa.
“Shuka, kamlete!” Akaamriwa. Naye pasipo ajizi akashuka na kutembea hatua tano kwendea kizani. Alipotazama kwa macho yake ya wizi, akaona mdomo wa bunduki ukimuelekea. Hakuwa anaweza kutoroka. Aidha akifanya hivyo aenende akiwa majeruh kama atafanikiwa kunusuru roho yake.
Ni kweli. Mwanga wa mbalamwezi haukuwa unamdanganya. Alichokiona kiliikuwa ni sahihi kabisa.
Basi akamnyanyua bwana Sheng aliyekuwa amelala chini, pengine katika hali ya kutojitambua. Akauweka mkono wa Sheng begani mwake na kisha akaanza kujongea kuuendea usafiri.
Ila akilini mwake bado akiwaza. Bado akifafanua. Na macho yake yakiwa yanaangazaangaza kule dirishan ambapo mdomo wa bunduki ulikuwa umetokeza nje tayari kwa ajili ya shambulio.
Akawaza kumtelekeza Sheng. Amweke mbele kama ngao yake kisha yeye akapotea zake salama. Ila akaona si kheri. Hata kama angelifanikiwa kutoka hapo, nini kingelifuata? Si kwamba kazi na juhudi zake zote zitakuwa za kutwangia maji kinuni?
Aliweza kuyawaza haya yote kwasababu ya mwendo wa taratibu aliokuwa anakokotana na mgonjwa Sheng. Mgonjwa huyo alikuwa mzito, na tena hivi hajiwezi, basi uzito ndiyo huwa maradufu. Ilimpasa Lee kutumia nguvu nyingi sana kusonga.
Basi akiwa bado hajafika mlangoni mwa usafiri, mara ghafla akasikia jambo la kumshtua. Ilikuwa ni kama sauti ya kishindo na kaupepo pia. Akatazama upande wake wa kaskazini kwa mashaka. Huko akaona mtu mmoja kwa mbali kama kweli macho yake yalikuwa yanaona sawia.
Mtu huyo alikuwa mweusi kwanzia kichwa mpaka miguu na mkono wake wa kuume ulikuwa umebebelea bunduki yenye mdomo mrefu. Yalikuwa ni mang’amun’amu ya giza? Akajiuliza. Hapana! … Hapana! Sauti ikateta kichwani mwake. Na kwa kumwondoa shaka, mara taa za gari alilomwacha Jona akiwa ndani likawasha ‘full light’, akamwona mtu huyo vema.
Ni kweli alikuwa ni mtu. Ni kweli mkononi alikuwa amebebelea bunduki. Na ni kweli alikuwa amevalia mavazi meusi kuanza juu mpaka chini. Mavazi haya yalikuwa ndiyo yaleyale ambayo alikuwa ameyavaa yule bwana wa kizungu aliyetoka kumuua muda muda si mrefu.
“Panda upesi!” Jona akafoka. Na haikuchukua punde, risasi zikaanza kumwagwa haswa kushambulia gari! Ni kheri Jona alikuwa amefungua mlango wa gari na basi risasi zilizokuwa zinamwelekea Lee na Sheng zikagotea mlangoni. Takriban risasi nane!
Lee alipojitupia humo, pamoja na Sheng, gari likakanyagwa mafuta na kuchomoka kwa kasi mno! Hata mlango ukafungwa wakiwa mwendoni. Gari, kwa pupa na kwa kasi, likamfuata bwana yule aliyekuwa anawashambulia kwa nia ya kumsomba.
Kabla halijafanikiwa, bwana huyo akatoweka. Ilikuwa ni upesi mno kiasi cha kuweza dhani pengine ameyeyuka, ila la hasha! Bwana huyu alikuwa amekwenda hewani mithili ya paka mweusi wa misitu ya Amazonia.
Na kama vile ngedere, akatua kwenye paa la gari liendalo kasi, na akalikamata kwa nguvu mno. Wakati nguo yake ikiwa imeshaji – tune na kuwa yenye mabakamabaka yenye matobo madogomadogo yaliyovimba. Na mikononi kucha zilikuwa zimetokama kana kwamba chui.
Hivyo basi haikujalisha gari lilipelekwaje, hovyo kiasi gani, bwana huyo akawa bado yu paani. Jona akayumbisha gari kwanguvu, akaendesha kwa mwendokasi wa hali zote, bado hakufanikiwa kumng’oa njemba huyo paani!
Na kutulia kidogo, njemba huyo akaanza kumwaga risasi akitoboa paa. Shukrani gari lilikuwa na paa gumu. Waliolitengeneza walilenga liwe hivyo, na si tu kwenye paa, hata huko pande zingine, gari lilikuwa gumu kumeza risasi.
Na punde bwana huyo alipokuwa akishambulia paa kwa risasi, Jona akatambua kuwa adui huyo kwa huo muda atakuwa ameshikilia paa kwa mkono moja, mwingine akiutumia kuushambulia, hivyo akaongeza kuyumbisha usafiri huo kwa pupa na kumnyima nafasi ya kufanikisha zoezi lake.
Akafanikiwa kwa hilo. Na pale adui alipopata upenyo wa kushambulia tena, Jona akafanya mahesabu ya upesi kichwani. Ni hivi, wakati anamwona adui yule akiwa amebebelea bunduki wakati ule alipomulika full light, adui huyo alikuwa amebebelea bunduki mkono wake wa kuume.
Kwahiyo basi adui huyo hutumia mkono huo, wa kuume, kushambulia. Na kwa maana hiyo mkono wa kushoto ndiyo hudaka paa. Na kwa makadirio yake basi, itakuwa vigumu sana kwa adui huyo kuangukia upande wa kulia, kwani atakuwa kajaza balansi upande huo. Hivyo … hivyo upande wa kumwangushia ulikuwa ni huu huu wa kushoto alipoekea mkono.
Basi akamwacha adu afyatua risasi. Akazihesabu, moja … mbili … tatu … nne! Akabinya breki ya ghafla na kuliemazia gari upande wa kushoto kwa kukata kona ya ghafla mno! Mpango ukaitika. Adui alikawia kudaka paa kwa mkono wake wa kuume, na hivyo akawa sasa ananing’inia na mkono wake wa kushoto, upande wa kushoto wa gari.
Bado akawa ngangari. Akanyooshea mdomo wa bundki ndani ya gari. Lakini kabla ajafyatua, Jona akatupa teke lake kutengua mlango wa gari, mlango ukatenguka na kumsomba adui huyo na kumwaga chini! Akabiringita mara tano kabla hajatulia tuli akiskizia maumivu makali. Na huku akitazama gari likiyoyoma.
“****!!” akalaani akipiga kofi ardhini kisha akaweka kidole chake sikioni na kusema, “I’ve lost them!”
**
Gari lilisimama na pasipo kupoteza muda, Jona akachumpa nje na kumwamuru Lee ashuke pamoja na Sheng. Wakatii amri. Lee akiwa anajikokota, akamtua Sheng na kisha wakafuata amri ya Jona ya kumfuata aelekeapo.
Baada ya hatua kadhaa. Wakakuta gari lingine, range rover sport nyeupe. Ndani alikuwapo Miranda, Marwa na Kinoo. Wakapanda humo na kuhepa wakiwa wamelitelekeza gari lili la maadui lililowaleta mpaka hapo.
Zikapita kama dakika nane, na mara gari lingine likafika hapo likiwa na wanaume wanne. Wale ‘the intellectual instinct’. walishuka na kulitazama gari lao, hakuna mtu. Wakanyofoa mfumo wa GPS na kifaa fulani kilichokuwa kinafuatilia ‘chip’ aliyopandikiziwa Sheng mwilini.
Basi wakarejea ndani ya gari lililowaleta na kutimka. Wakaendelea kufuatilia mahali alipo Sheng kwa kutumia chip ile. Na baada ya kama robo saa, wakawa wamefika mahali ambapo ilionyeshwa kwenye ramani kuwa ‘chip’ ipo hapo.
Basi wakashuka na kusogelea hilo eneo. Ajabu wakakuta kuna kikopo kidogo cheupe chenye mfuniko mwekundu. Mmoja akakiokota na kuifunua. Ndani akakuta ‘chip’ yao na karatasi nyeupe yenye ujumbe uliosomeka,
“Welcome to the sky of the damned.” Kumaanisha karibu kwenye anga la washenzi.
Wakaghafirika sana kukumbwa na kadhia hiyo. Aibu iliyoje hiyo? Waliona wamevulia nguo mbele ya umati. Waliona wamedhalilishwa haswa. Wanashindwaje na watu duni kama hawa? Na tena kwa wakati huo wakiwa wamempoteza mpambanaji mmoja vitani?
Basi wakarejea ndani ya gari lao na wasiende popote bali wakae na kujadili cha kufanya kwa maana sasa hawakuwa na namna mbadala, chip ilikuwa imetolewa mwilini mwa Sheng na hata lile gari lao, ambalo kama lingechukuliwa basi wangelifuatilia, nalo limetelekezwa.
Lakini japo walikuwa ndani ya gari kujadili nini kifuate, ajabu wakajikuta ukimya umewatawala. Vinywa vilikuwa vizito na pengine vichwa navyo viligoma kufikiri kwa muda. Wakakaa hapo kwa muda wa kama dakika kumi hivi, kukiwa kimya. Kitu pekee kilichojuza kuwa kuna watu ni sauti za pumzi.
“Let’s go home,” akapendekeza Wales. “It’s not safe out here.”
Basi gari likawashwa, wakatimka. Wakatembea barabarani kwa mwendo wa kama nusu saa, na wakiwa wamekwama kwenye mataa, kwa nyuma, dereva akaona gari la polisi. Akalitazama kwa umakini kwa kupitia side mirror, punde wakaruhusiwa kwenda. Wakaenda.
Na lile gari la polisi huku nyuma likawa linawafuata. Gari hili lilikuwa la modeli kama zile za corola, lakini lenyewe ubavuni lilikuwa lina rangi nyeusi na maandishi makubwa meupe, POLISI, na kwenye paa kulikuwa na taa ziang’azo, nyekundu na bluu.
Hapa bwana Denmark, dereva, akapata shaka juu ya gari hilo. Akafikiri kuliweka gari lao kando wapate kuteta na polisi ila akaona chaguzi hilo halitakuwa jema. Mazingra hayakuwa mazuri kwa wao kufanya tukio eneo hilo endapo wakikosana na hao wanausalama, basi akaendelea kutembea, na kwa tahadhari akaongeza mwendokasi wa gari.
Alipofika mahali alipoona ni ‘salama’ kwao, basi akaegesha gari kando na kungoja. Punde nalo gari la polisi likafika na kuegesha pembeni pia. Akashuka mwanaume mmoja aliyebebelea bunduki mkononi, na kidogo akashuka mwingine. Huyu yeye alikuwa amevalia sare za polisi.
Yule mwenye nguo za kiraia, akaamuru,
“Shuka chini na weka mikono juu!”
Akisema hayo alikuwa amejiweka mbali kidogo na usafiri huo. Na mikono yake imekaa tenge kujihami. Basi kidogo, Denmark akashuka. Ajabu tayari mwili wake ulikuwa umevalia suti nyeusi na si zile nguo ambazo walifanya nazo tukio.
“Is there any problem, officer?” akauliza.
“Yes, there is!” akajibu yule polisi aliyevalia nguo za kiraia. Bila shaka alikuwa ni mpelelezi.
“Raise up your hands!” akaamuru. Bwana Denmark akatii amri.
“Are you alone in that car?”
“Uuuuhm, no! I am with friends.”
“Tell them to get out! Hands up!”
Denmark akawatazama wenzake na kuwapa ishara ya kichwa. Wote walikuwa wamesikia amri ile, basi wakatoka wakiwa wameweka mikono juu. Na wote walikuwa tayari wamevalia suti zao kama yule mwenzao, Denmark.
“Who are you? And where are you coming from?” Afisa polisi akauliza. Denmark akawatazama wenzake kisha akapaza sauti, “We are just tourists. We are from beach.”
“Beach at this time? … may I see your documents?”
“Aahm, sure you may, but they are not here with us. They are where we live in, would you mind taking you there to see?”
Yule afisa akatazamana na mwenzake kwa macho ya mashaka. Alafu akaurudisha uso wake kwa wale wazungu, akawaamuru wageukie na kushika gari kwa ajili ya ‘search’, wakatii. Basi wale polisi wakajongea na kuanza kuwapekua wakipapasapapasa mifuko na maungo yao.
Walipomaliza, wakawakata wanaume hao wasonge kando na gari nalo lipekuliwe. Wakatii. Polisi wakaangaza ndani ya gari na kurusha macho huku na kule. Hakuna walichopata.
“We are sorry. You can just move on with your journey,” akasema bwana polisi akimpatia mkono Denmark.
“Never mind, it’s just normal,” Denmark akasema kwa tabasamu. Yule polisi na mwenzake wakajongea kufuata gari lao, na hawa wakina Denmark wakazama garini waende.
“ … sio wenyewe, sio wenyewe over …” polisi yule mkaguzi akateta na radio call. Lakini hapa ndipo akagundua kuna kitu hakipo sawa. Mkono wake wa kuume uliobebelea radio call ulikuwa na damu! Kutazama vema, ni kweli na si macho yake.
Hapa moja kwa moja akajua damu hiyo alikuwa ameitoa mkononi mwa Denmark. Basi akashuka upesi, lakini kabla hajasema jambo, gari la wakina Denmark likawa limeng’oa nanga na kujiendea. Akarudi garini na kuanza kulifuatilia.
Kwa ishara wakataka gari hilo likae kando. Lakini kwa sasa wakawa wamenoa, gari halikukaa tena kando na badala yake vita ikaibuka!
“Ndio wenyewe! Ndio wenyewe, over! …” polisi aliteta na radio call yake. Macho yakiwa yamemtoka pima kutazama gari walikimbizalo. “… plate number T 457 AAA, New Bagamoyo road! … T 457 AAA New Bagamoyo road, Over!”
Alipomalizia kusema maneno yake hayo akastaajabu kuona gari lile walikimbizalo, likikata kona ya ghafla, likasimama na kurudi nyuma upande wa kushoto. Pap! Wakatazamana na wale polisi. Kilichofuata hapo ikawa ni simulizi ya kusisimua. Risasi zilitupwa haswa, tena ndani ya muda mfupi tu, ila wale polisi hakuna aliyetoka na uhai wake hata mmoja! Wote wakamiminwa damu na kuachwa na matobo matobo kana kwamba karatasi. Kisha wazungu wakapotea!
Na walipofika huko mbele, wakavamia na kukwapua gari lingine kwa usalama. Sasa wakaondoka pasipo mushkeli mpaka kwenye makazi yao.
***
Saa tano usiku …
Ni nje ya nyumba lakini ndani ya uzio. Hapa Lee alikuwa amepigishwa magoti na Sheng akiwa amelazwa chini. Mbele yao kuna watu watatu nao ni Jona, Miranda, Marwa na Kinoo. Mkononi mwa Jona kuna bunduki ndogo na mdomoni mwa bunduki hiyo kuna kiwamba cha kumezea sauti. Na bunduki hiyo tayari ilikuwa ‘imekokiwa’ kwa ajili ya tukio.
Hapa nje ni baridi. Kuna manyunyu ya mvua. Na kwa namna anga lilivyokuwa limefungamana kwa uweusi, kulionyesha kuna dalili ya mvua kubwa kushuka muda wowote ule.
“Mbio za sakafuni huishia ukingoni,” akasema Jona akimtazama Lee. “Kiko wapi sasa? Leo upo mbele yangu ukiwa huna msaada, na huyo punda wako akiwa amejilaza kama mwana kuku aliyenyeshewa na mvua. Kuna lolote la kusema kabla ya risasi zangu mbili kung’oa uhai wenu usio na maana kwangu?”
Lee akatazama kwanza chini, na kisha akamtazama Sheng ambaye hakuwa na uhakika kama kweli yu hai au lah, kisha akasema, “Mbele ya macho yenu naweza nikaonekana si wa maana kwa sasa kama ukitazama hapa na si mbele. Lakini …” akamtazama Jona machoni. “Lijalo ni kubwa kuliko hili unalolimaliza. Linatisha, na limedhamiria kuuteka ulimwengu mzima.
Kama wataka kweli kulimaliza, kuyamaliza yote for the good of this country na ulimwengu kwa ujumla, basi unanihitaji.”
“Ni kitu gani hicho unachokiongelea?” Jona akauliza.
“Umeona kile kilichokuwa kule,” akasema Lee. “Umewaona wale waliotuvamia na kwa namna walivyofanya kuteketeza kambi nzima ndani ya muda usiozidi lisaa limoja. Kama haitoshi, watu hao si tu kwamba watatumaliza sisi na kwenda zao, la! Bali wataanzisha ngome yao hapa.
Na kwa kupitia ngome hiyo basi watateka kanda hii like never before. Mtashuhudia mauaji makubwa na hata vita kuzuka ili wapate vile vilivyomo ndani ya nchi hii kabla ya kuikausha kuwa jangwa.
Sidhani kama unawafahamu vema watu hawa zaidi ya kuwaonea hapa. Wameanza huko Uchina, na sasa wamefikia hapa. Wataufikia ulimwengu mzima na kuuweka kiganjani. Kisha watamgeuza kila mtu kikaragosi kabla ya kuwa maiti. Amini nakwambia.”
Jona akatulia kidogo kisha akauliza, “Kwahiyo wewe utawamaliza watu hao?”
“Siwezi kufanya hilo hata kidogo. Mimi ni kama chawa tu ndani ya msitu huo mkubwa. Ila ninachoweza kukifanya ni kuwatambua, na hata kuonyeshea wapi wanapatikana. Pengine mkiwa mmedhamiria, mkapate kuwamaliza kabla maji hayajawafika shingoni.”
Kabla Jona hajatia neno, Lee akasema akiwa anatazama chini, “Pengine sisi twaelekea kuisha, lakini lijalo linatuhofisha hata sisi.” Akanyanyua uso wake na kuendelea kuteta, “Nakupa maisha yangu kwa hii ahadi. Niruhusu nikusaidie kuwamaliza watu hawa, na punde tutakapokamilisha hilo, utanipatia bunduki hiyo mwenyewe, nami nitajimaliza.”
Jona, akiwa amefinyanga macho yake, akamtazama Sheng. “Siwezi kumwacha huyu hai. Hana sababu yoyote ya mimi kumbakizia pumzi.”
Akamnyooshea bunduki, lakini Miranda akaishika bunduki hiyo na kusema, “Ngoja kwanza …”
***
“Pengine kabla ya kumuua, tuntamhitaji,” akavuma mwanamke huyo. Watu wote wakamtazama lakini Jona ndiye akamuuliza, “Tutamhitaji kwa kitu gani na ilhali yupo huyu mwingine?”
Miranda akamnong’oneza Jona sikioni, na basi mwanaume huyo akaridhia kumbakiziauhai bwana Sheng, ambaye bado kiuhalisi hakuwa anaonekana kama mwenye matarijio ya kupona. Hata hapa wakati watu wanajadili juu ya uhai wake, yeye hakuwa anafahamu lolote lile.
Tendo pekee la uhai alilokuwa analifanya ni kuhema tu.
Basi Lee na Sheng wakakusanywa na kuingizwa ndani, Lee akahifadhiwa kwenye chumba cha peke yake, kwakuwa bado hakuwa anaaminika. Na Sheng akawekwa pia kwenye chumba chake. Bado usimamizi ukionyeshwa kwa kufungiwa mlango.
Sasa hapo vikawa vimebaki vyumba viwili tu ambavyo viliwapa mawazo wenyeji juu ya namna gani watalala kwa sasa.
Asubuhi ya saa tatu …
“Kinoo, inabidi uende town kuchukua double decker,”alisema Miranda. “Lakini pitia kwanza kwa Kilonzo, chukua pesa hapo. Usijali, ntamtaarifu akupatie.”
Kinoo akapokea maagizo hayo na kwenda zake. Angalau hivyo ndivyo namna walivyokuwa wanaendesha familia yao. Kwakuwa mirija yote ilikuwa imezibwa na hakukuwa na yeyote miongoni mwao ajihusishaye na shughuli rasmi, Miranda alikuwa akichakarika kufufua na kuendeleza vibiashara vyake vya hapa na pale.
Jambo hili lilikuwa linamkwaza sana Jona. Alitamani kusaidia lakini Miranda hakutaka kabisa hilo maana Jona bado hakuwa amesahaulika kwenye taswira za watu, tena kama muuaji wa kamanda wa polisi, na lile tukio lake la kutoroshwa toka kituoni.
Ilikuwa ni hatari kwake kwenda huko nje na kuzurura. Lakini mbali na yote hayo, bado Jona aliona anapaswa kuwa na cha kufanya kumsaidia mzigo wote ulioangukia kwenye mabega ya mwanamke huyu, japo kitu chenyewe hakuwa anakifahamu. Hakuwa anajua ajihusishe na nini awe salama na atoe mchango.
“Hey,” Miranda aliita kumng’oa Jona mawazoni. “Are you ok?”
“Yes, I am,” Jona akajibu akimtazama Miranda kwa tabasamu ambalo halikuwa laendana na macho yake.
“Sure?” Mirand akauliza.
“Yeah! No problem,” Jona akasema akitikisa kichwa. Walikuwa wenyewe sebuleni maana Kinoo aliongozana na Marwa kwenda huko kwa mtu ajulikanaye kama Kilonzo.
“You think about Sheng? … listen, its going to be alright. We need him at this time. Unahitaji antidote kumbuka. Na zaidi we can use him kama frontline wetu kukamilisha kazi. Don’t you think about that?”
Wakati Miranda anasema hivyo, alishika mikono ya Jona na kuiminyaminya. Alikuwa anamtazama Jona kwa macho yanayoongea, kwa macho yanayomaanisha akitamkacho.
“Naelewa,” Jona akajibu. “You don’t have to repeat that, Miranda. Thanks. I appreciate kila unachokifanya for me. Unajitolea sana. Nina deni kubwa sana kwako.”
“No no no. Hauna deni lolote kwangu. Jona, mpaka sasa tupo hapa ni kwasababu yako wewe. Umetupa tumaini na kitu cha kukipigania. Umetufanya tuwe tayari kufa lakini kwa heshima tukiacha historia kuwa tulipambania upande ulio mwema. We thank you for that.”
Basi wakakaa hapo na kuteta kwa kama nusu saa. Kinoo akapiga simu akiwa eneo la kununua kitanda, akamweleza Miranda kuwa kwa pesa waliyoipata kwa Kilonzo, basi aina ya kitanda wanachoweza kukipata si kile alichokuwa anatamania.
Hapo ikawa hamna namna, Miranda akamwambia achukue kilichopo, atajua nini cha kufanya. Alipokata simu, akamwambia Jona, “Inabidi niende.”
Akanyanyuka na kwenda chumbani. Baada ya muda kidogo, akatoka akiwa ameshajiandaa. Amevalia gauni lake matata likabalo kiuno na viatu vyake vya visigino virefu. Mkononi amebebelea pochi ndogo.
“Natoka kidogo. Nitarejea muda si mrefu sana.”
Jona akaitikia kwa kichwa, Miranda akaenda zake akimsindikiza kwa macho.
**
Saa tano asubuhi …
“Miranda, Miranda, ulikuwa wapi siku zote hizo? … ulinikimbia si ndio?”
“Hapana, mpenzi. Sikukumbia. Kwanini nifanye hivyo?” Miranda alijitetea kidhaifu akimtazama Boka usoni. Boka alikuwa ofisini kwake, ameketi kwenye kiti chake kikubwa akizunguka zunguka huku na kule. Amejaa.
“Hivi unajua hata kesi iliendaje, iliishaje?” Boka akamuuliza Miranda.
“Hapana, sijui. Lakini Boka, hatuna haja ya kuongelea yaliyopita tena mpenzi. Yashapita, right? Let’s focus kwa yajayo. Here I am.”
Boka akatabasamu. Akagongagonga kalamu yake mezani mulipojaa mafaili kadha kwa kadha na kusema, “Baba yako mzungu alikutorosha nchini?”
Miranda akatazama chini kwa sekunde tano pasipo kusema jambo. Aliporejesha uso wake juu, macho yalikuwa mekundu na punde yakaanza kumwaga chozi.
“Amefariki,” akasema kwa sauti ya chini. Boka akashikwa na huruma. Akakunja ndita zake kumtazama Miranda kwa pole.
“Amefariki lini na mbona hukunambia, Miranda?”
Basi hapo Miranda akapata upenyo wa kupenyesha ulaghai wake. Akamwambia Boka kuwa hata ukimya wake ulisababishwa na msiba huo. Ilimpasa aende Uingereza kinyume na masharti aliyopewa. Na hata aliporejea hakuwa sawa kabisa. Imemchukua muda kurejea halini.
“Pole sana, mpenzi. Sikuwa nafahamu yote hayo,” Boka alijinasibu. “Ila usijali. Mambo yako sawa sasa. Baada ya yule Kamanda aliyepita kufariki, huyu wa sasa ni rafiki yangu sana. Na hata ndiye yeye aliyefanya jitihada mimi kuwa huru. Kwahiyo hakuna tena haja ya kuhofia.”
Baada ya maongezi haya machache, Boka akafunga ofisi kwa muda na kutoka na Miranda kwenda mahali patakapowa- ‘refresh’. mahali tulivu watakapoweza kuongea kwa uhuru. Huko wakaongea sana, na mwishowe Boka akampatia Miranda pesa taslimu.
“We are still looking for …” simu ikakata. “Shit!” Denmark akalalama. Akaweka simu chini na kuwatazama wenzake. “Boss is so mad!” akasema kwa ufupi kisha kukawa kimya kwa sekunde kadhaa. Ni wazi walikuwa katika hali ngumu. Lazima wampate na kummaliza Sheng ili kazi yao isemekane kumalizika.
Denmark akamtazama Wales na kumuuliza, “Anything?”
Wales alikuwa ni mtu ahusikaye na mitandao na mambo ya teknolojia. Ndiye yeye hata aliyehusika na kumpandikiza Sheng chip ndani ya mwili wake. Na kwa kutwa nzima, alikuwa bado anahangaika na tarakilishi yake kuona kama anaweza kupata namna ya kumpata Sheng.
“No,” akasema akitikisa kichwa. “Not yet. I think we should wait more.”
“No, Wales!” akafoka Denmark. “We have no time to waste more. We have limited days here, remember! You have to do something.”
“I do!” Wales akajibu. “I do it everytime. When I tell you to wait just wait because I am on to something. Can’t you see? I don’t just sit and do nothing.”
Basi maongezi haya y kutupiana mipira, yakaendelea mpaka pale majira ya saa moja usiku, ambapo Wales alikuja kutoa taarifa kuwa kuna jambo amelipata kwa kutumia ‘satellite’. Wenzake wote wakajongea na kumskiza.
“I think I’ve found him,” akasema kwa kujiamini.
“Sure?” Ireland akauliza akitoa macho.
“Yes, sure.”
Lakini kabla hajasema jambo hilo, simu ya Denmark ikaita. Kupokea akaambiwa sentensi moja,
“Kill the president before the next night.”
Na kisha simu ikakata. Kabla hajawaambia wenzake jambo, akapiga simu na kuuliza, “What about the chinese man?”
“Kill both of them. The president has already signed many Chinese huge contracts that we cant allow any of them to operate. It is very dangerous. So kill him.”
Simu ikakata tena. Denmark akafikisha taarifa hizo kwa wenzake. Bado wakiwa katika joto hilo, wakasikia sauti ya honi getini.
***
Basi kwa tahadhari kabla hawajakwenda huko getini, wakatazama taarifa za kamera kadhaa walizokuwa wamezipachika kwenye makazi yao. Na walipotazama wakapata kujua kuwa wageni waliopo getini ni polisi.
Wamekuja kufanyaje hapo? Ina maana walijua makazi yao? Hawakuwa na muda mrefu wakujipanga. Denmark akatoka ndani akiwa hajabebelea silaha yoyote. Wenzake wakabaki ndani kwa miadi ya kutazama kinachoendelea na kuchukua hatua pale watakapoona panastahili.
Geti likafunguliwa.
“You are under arrest!” akafoka polisi mmoja akimnyooshea Denmark bunduki. Akamwamuru mwanaume huyo aweke mikono yake kichwani na aongoze kwenda ndani kuwatoa wenzake.
Jumla ya polisi walikuwa sita. Wanne wamevalia sare zao na wawili wakiwa ndani ya mavazi ya kiraia. Basi wakaongozana na Denmark na kuzama naye mpaka ndani. Lakini kabla hawajafanya ukaguzi wao, Denmark akataka kwanza kujua nini kinaendelea kama moja ya haki ya mtuhumiwa.
“You are the suspect of murder of two policemen,” polisi mmoja akaeleza.
“Me?” Denmark akatahamaki. “Ok, may I contact my lawyer, please?”
“After issue us your all valid documents of being here and bring us all of your mates here,” polisi akatoa sharti. Denmark akamtazama pasipo kusema jambo, kisha akaomba ruhusa ya kwenda ndani kuleta vitu vinavyohitajika.
Hapo akakabidhiwa polisi wawili wa kumsindikiza. Sebuleni wakabakia polisi wawili, na kule nje wakiwa wawili wengine. Baada ya muda, Denmark akarudi akiwa amebebelea nyaraka zake, ila wenzake hawakuwapo hapo.
“Where are your mates?” akauliza polisi.
“They are out,” akajibu Denmark. Basi polisi huyo amuulizaye maswali, akawaamuru polisi wale waliomsindikiza bwana Denmark kwa mara ya kwanza, wafanye upekuzi wa nyumba nzima. Agizo likaanza kutekelezeka.
Wakazama vyumbani na kupekuapekuwa huku na kule. Chini na juu. Mikononi mwao wakiwa wamebebelea silaha za moto.
Baada ya muda mdogo, polisi mmoja aliyekuwa anafanya upekuzi akagundua jambo lililomshtua. Alipotazama dirishani kule nje, aliona miili miwili ikiwa imelala chini. Akatahamaki.
Kutazama vema akagundua miili hiyo ilikuwa ni ya wenzao wawili ambao walikuwa wamekaa nje. Akahisi kusisimka. Vinyweleo vikasimama na macho yakamtoka. Wameuawa!
Basi kugeuka aende kutoa taarifa, akakutana uso kwa uso na Ireland. Kabla hajavuta pumzi, akawa ameshambuliwa na kulazwa chini mfu. Ireland akakwapua silaha yake.
Yule polisi mwingine wa pili, akiwa huko chumba kingine, akiwa hana hili wala lile, hajui liendealo. Akaendelea kupekua na kupekua. Kuja kutahamaki amezibwa mdomo. Akafurukuta. Mara akakitwa na kitu kichwani, akadondoka kama mzigo.
Sasa polisi wanne wakawa wapo chini. Walibakia polisi wawili tu ambao wapo sebuleni.
Kwakuwa muda ulikuwa umeenda na wale walioagizwa hawakurejesha taarifa, basi yule polisi, ambaye alionekana ni mkubwa kuliko wenzake kwa cheo, akamtazama polisi aliyekuwa naye hapo sebuleni na kumpatia ishara ya kichwa kuelekea chumbani.
Yule mwenzake pasipo kusita akaenda huko asijue aenda kujitoa uhai. Alipopotelea huko, akapotelea kweli. Sasa Denmark akabaki na yule mmoja pale sebuleni. Muda ukaenda. Akaanza kutabasamu.
Polisi yule akatia shaka. Na muda si mrefu akapewa sababu ya kuhofia zaidi baada ya washirika wote wa Denmark kutoka chumbani, yaani Ireland, Sweden na Wales.
“Would you mind putting your gun down, officer?” akasema Denmark. Polisi akagoma kutii hilo agizo. Akiwa aliyeshikwa na woga, akasonga nyuma mpaka dirishani. Akafungua dirisha na kuchungulia upesi. Akaona wenzake wakiwa chini. Wamekufa!
Mikono yake ikaanza kutetemeka. Na mate yakawa magumu kumezeka. Alikuwa hana ujanja tena, alikuwa hana cha kufanya. Risasi zake kadhaa ndani ya bunduki zisingeweza kumwokoa dhidi ya wadhalimu wale.
***
Usiku wa saa mbili …
“Wameondoka,” alisema Marwa akimtazama Jona. Mwanaume huyo alikuwa ametoka kutazamia kwenye tarakilishi yake kufuatia vifaa walivyoviweka kule kwa wale wazungu.
Ndani ya nusu saa, Jona na Kinoo wakawa wamefika kwenye eneo husika. Jona akamwambia Kinoo atulie nje kusoma ramani, yeye atazama ndani. Basi akaingia na kupembua. Akakuta maiti za wale polisi, nje, sebuleni na vyumbani. Akapiga picha za maiti hizo na kisha akamtumia Marwa kwa kupitia mtandao, alafu akamtumia ujumbe kumuuliza,
“Watakuwa wameenda wapi?”
Akiwa anangoja majibu, akatoka ndani ya nyumba hiyo na kwendaze mbali pamoja na Kinoo. Muda kidogo ujumbe ukaingia toka kwa Marwa, “Wapo karibu na sisi!”
“Karibu na wakina nani?” Jona akauliza. Punde ujumbe ukaingia toka kwa Marwa ukisema, “Naona kama wanajongea kuja kwenye makazi yetu!”
“Serious, Marwa?”
“Yes. I think they are coming!”
Yote aliyokuwa anayaongea Marwa hayakuwa ya kutilia shaka kwani gari walitumialo wazungu wale lilikuwa limepachikwa kifaa tambuzi cha GPS hivyo wakijua mwenendo wake. Zoezi la upachikaji wa kifaa hicho lilifanywa na Jona kipindi kile almanusura kukamatwa.
Sasa hapa kwenye kioo cha tarakilishi ya Marwa, ‘GPS tracker’ ilikuwa inaonyesha gari hilo likisonga kuja walipo. Na kasi yake ilikuwa kubwa ajabu!
“Kinoo, we have to go! Haraka!” Jona akabwatuka kisha upesi wakaanza kukimbia kufuata chombo chao cha usafiri. Walipokwea, wakatimka upesi, Jona akikamata usukani.
Alikimbiza gari kwa kasi mno. Macho yake yalituama barabarani, mikono yake ilikamatia usukani kwanguvu na miguu yake ikikanyagia mafuta na breki kwa zamu.
“Call Miranda!” Jona akamwagiza Kinoo. Kinoo akafanya hilo jambo upesi. Simu ikaita mara moja na mara ikapokelewa, ikawekwa ‘loudspeaker’.
“Miranda!” Jona akaita. “Ondokeni hapo nyumbani upesi!”
“Hatuwezi!” Miranda akajibu. “Hatuwezi kuondoka kwa sasa, it’s too late! Wameshawasili. Yatupasa kupambana nao.”
“Hamuwezi kupambana mkiwa wawili, hamtaweza kuwamudu. Just escape!” Jona akazidi kusisitiza akitamani gari igeuke kuwa ndege ya kivita.
“No, Jona. Hatuna namna! Huwezi jua huko nje ni hatari kuliko humu ndani. Vipi kama wata ….” simu ikakata.
“Miranda! Miranda!” Jona akaita. “Piga tena!” akamwamuru Kinoo. Simu ikaita tena, haikupokelewa. Walipopiga kwa mara nyingine, ikawa haipatikani. Jona akazidi kuchanganyikiwa. Aliamini Miranda na Marwa wasingeweza kuwazuia watu wale, tena wanne na waliokubuhu kwenye sekta ya mauaji.
Kwake ikawa mtihani mkubwa. Na hata akajuta kwanini alitoka kwenda kule kwenye makazi ya wale wazungu. Ubaya zaidi ni kwamba hakuweza kutoa taarifa hizo polisi. Katika vita hii walikuwa wenyewe tu.
***
“Let’s spread!” akasema Denmark, kisha akamalizia, “Show them no mercy!”
Basi wanaume watatu, Ireland, Wales na Sweden wakagawanyika kuizingira nyumba ya wakina Miranda. Wakati huo wakiwa tayari wameshajivika nguo zao za kazi.
Punde kidogo, umeme ukakatika katika nyumba hiyo na kuwa kiza totoro isijulikane mlango na dirisha lipo wapi. Hapa sasa wale ‘the intellectual instinct’ wakawa wanaona kana kwamba mchana mkavu wa saa nane.
Hakuna huruma. Hakuna mtu yeyote kutoka na uhai.
Basi ndani ya dakika kadhaa, watu hao wakawa wamezama ndani ya nyumba kwa kuvunja milango. Wakafanya msako wao, na ndani ya muda mfupi wakawa wamegundua kuwa wamezamia mtegoni.
Ndio, mtegoni! Ndani hakukuwa na mtu isipokuwa Sheng aliyekuwa amelazwa kitandani. Swala hili likawashtua. Lakini wakiwa werevu wa kutosha, wakang’amua na kujinasua. Wakitumia teknolojia kubwa ya miwani waliyoivaa, wakatambua kuwa kuna nyayo za miguu mahali kadha wa kadha.
Na kama wakina Miranda wakiwa watu waliolitambua hilo jambo, wakajitokeza bayana, yeye pamoja na Lee huku Marwa akiwa ameendelea kufichama.
“Oh! Now you are here!” akasema Denmark, nyuma yake wakiwa wamesimama wenzake kwa ukakamavu. Mandhari yalikuwa ya giza, ila kwakuwa hapa walikuwa nje, basi angalau waliweza kuonana, haswa Miranda na mwenziwe, Lee, ambao hawakuwa wakitumia miwani ya kuonea.
Mbali na giza hilo, kulikuwa kimya.
“We could have killed Sheng already and left, but I wanted to see you, the people who outwitted us,” aliendelea kusema Denmark kwa dharau. Akamtazama Miranda na kisha akahamishia macho yake kwa Lee. Hapo akaganda kwa muda kana kwamba mtu amjuaye ama anamfananisha.
“The Chinese man,,” akasema na kisha kuguna kama mtu aliyekabwa na kicheko. “I think I know you, don’t I?”
Lee hakusema kitu. Kwa namna alivyokuwa anamtazama kulisema nini kipo kifuani mwake. Alikuwa ana pande la chuki. Mikono yake ilikuwa imekunja ngumi kwanguvu. Na pumzi yake ilikuwa inaenda juu na chini kwa kasi.
Denmark akanyoosha mikono juu akisema, “You don’t know who we are, lads! You don’t know anything about us, right?” akatabasamu. “Maybe you are braver more than we could imagine, stronger and bolder … but … but don’t ever mess with us.” Denmark akasema akitikisa kichwa chake na kidole akikipeleka kushoto na kulia. “Don’t ever ever do that. We are not of the same ground.”
“Neither do we,” akadakia Miranda kwa ujasiri. Basi Denmark akamsogelea na kumuuliza, “What do you say?”
“You heard me,” Miranda akamjibu akimtazama usoni. Denmark akatabasamu. Kisha akawatazama wenzake na kupiga makofi. “Wow! What’s so special about you sweet lady?”
“More than you can ever imagine,” akajibu Miranda. “More than you can ever handle.”
“Sure?” akauliza Denmark.
Kabla Miranda hajajibu, Lee akamshika bega mwanamke huyo kama ishara ya kumtaka anyamaze. Miranda hakujali, akajibu, “Totally sure.”
“Miranda,” Lee akaita. “Hatuna haja ya kufanya hili. Mwache mwanakharamu apite. Tuko outnumbered!”
“Kama kufa acha tufe,” akasema Miranda. “Tunakufa mara moja tu, Lee. Siwezi kuwa mdhaifu kiasi cha kudhihakiwa kiasi hiki.”
Lee akashindwa kumtuliza mwanamke huyo. Kwa macho yake akashuhudia wale washirika wa Denmark wakisogea nyuma kidogo kutoa uwanja, na Denmark akasema akimwambia Miranda, “Show me what you have.”
Miranda akamtazama Lee na kumpatia ishara ya kichwa kuwa ampatie nafasi. Lee akasita. Akauliza kwa kunong’ona, “Are you sure?” Miranda akajibu kwa kupandisha kichwa chake, basi Lee akasonga nyuma kwa hatua mbili tu na kisha akasimama akitazama kwa umakini.
Miranda akajiweka tenge, Denmark akamtazama. Mwanamke huyo akatanua miguu yake kutafuta balansi na kisha akakunja ngumi. Denmark akaguna kwa kebehi kisha akamwonyeshea Miranda ishara ya kumkaribisha.
Miranda akaanza kutupa ngumi zake nyepesi za kasi. Denmark akazihepa kama mchezo, ilan kwa makusudi akatengea uso wake ngumi moja iliyomkita upande wa shavu lake la kulia na kumgeuzia uso kando.
“Not bad,” akasema. “Any more than that?”
Miranda akakwazika na kauli hiyo. Sasa akafunguka kwa umahiri wake wote, akazirusha ngumi na kujifyatua mateke kama mitego ya porini. Hamaki akamkita Denmark mateke mawili ya kifua na almanusura kumwangusha chini.
Hapa sasa Denmark akatambua mwanamke apambanaye naye hakuwa wa kumpuuzia wala kumdharau. Si bure alikuwa anajiiamini. Sasa akakunja ngumi na kutanua mapaja yake kujisimika ardhini. Akamkaribisha tena Miranda.
Miranda akaja tena akionyesha umahiri wake. Na sasa akidhamiria kumwangusha mwanaume huyu kumkata ngebe. Ila hakujua … Hakujua anatakiwa kuwa mwangalifu mno kuliko anavyodhani.
Sasa akarusha ngumi zake za upesi. Pengine akimweka ‘busy’adui yake huyu ili ampatie shambulio kubwa la hatari litakalomlaza hoi. Lakini hakuwa anafahamu kuwa akiwaza hivyo, naye adui alikuwa akiwaza kingine. Sasa Denmark hakutaka kukwepa ngumi yoyote ya Miranda, na badala yake akaanza kumdhoofisha mwanamke huyo.
Kila Miranda alipotupa ngumi yake, kwa kasi ya umeme, Denmark akatengua ngumi hiyo kwa ngumi yake nzito. Miranda aliporusha ngumi kama sita na tendo hilo toka kwa Denmark likirudia, akaanza kuchoka. Mikono ikamuuma.
Basi kujikomboa, akaanza kutumia miguu yake. Akarusha mateke mfululizo na kwa mkupuo. Napo mchezo ukawa uleule. Denmark alimuumiiza miguu yake wa kupangua kila shambulizi na ngumi zake nzito za upesi. Sasa Miranda akawa amechoka, na hapo bado Denmark hajaanza kumshambulia!
Mwanaume huyo asiwe na huruma, baada ya kutambua kuwa Miranda alikuwa hoi, na sasa anahisi maumivu maungoni mwake, akaanza kutupa mashambulizi. Ngumi zake zilikuwa nyepesi ila nzito maradufu. Hata Miranda alipojitahidi kuzizuia baadhi, bado aliyumba kwa kushindwa kustahimili.
Alipojiweka bayana, akala ngumi mbili, moja ya kifua na nyingine ya tumbo, akacheua damu. Akadondokea chini na kunguruma kwa nguvu kwa maumivu makali. Denmark akatikisa kichwa chake.
“C’mon lady. We are about to start!”
Miranda akatema mate yenye damu pembeni. Akataka kusimama, viungo vilikuwa vinamuuma. Lee akammwekea mkono wake begani kumtuliza kisha akasema kwa sauti ya chini,
“Let me …”
Kisha mwanaume huyo akamtazama Denmark na kujipanga kwa ajili ya pambano. Denmark akatikisa kichwa chake kwa masikitiko. Akampatia ishara mwanaume huyo kumkaribisha. Lee akakataa. Akairudisha ishara hiyo kwa Denmark. Alitaka mwanaume huyo awe wa kwanza kushambulia.
Basi Denmark hakuona tabu. Akaanza kurusha ngumi, viwiko na kila kiungo chake cha mwili kupambani. Mapigo yake yalikuwa ya kasi na mazito. Ilimlazimu Lee awe ‘intensive focused’. Macho na akili yake iwe nyepesi kwenye kufanya maamuzi yenye tija.
Walidumu kwa kama dakika tatu pasipo yeyote kufanikiwa kufikisha shambulizi lake kwa mwenzake. Lakini kwa muda wote huo Lee alikuwa anafanya kazi ya ziada kwani alikuwa anazingatia sana na kujilazimu kufanya maamuzi mepesi mno.
Alikuwa anatumia akili yake kwa kiasi kikubwa huenda tofauti na adui yake, hivyo ilifikia mahali akawa kama mtu aliyechoka kuendana na kasi kama hapo awali. Hapa Denmark akampatia ngumi tatu na kumwangusha chini!
Akang’ata meno kwa hasira. Akanyanyuka upesi na kujiweka tenge kwa ajili ya pambano sasa akiona ni vema kushambulia kuliko kushambuliwa. Njia nzuri ya kujilinda ni kwa kushambulia kwa kasi.
Akaweka nguvu zake zote kwenye mikono yake. Akajitutumua kwa muda. Denmark akawa matatizoni, ila bado akafanikiwa kuyeya na kukwepa, akienda kushoto na kulia, chini na juu … kushoto, kushoto .. kulia, chini! Kando na kando, kushoto, chini!
Alipokaa wazi, Denmark akatumia fursa hiyo kumtwika teke zito na kummwaga chini! Denmark akacheka kidogo na kudhihaki, “that woman his better than you!”
Lee akapandwa na hasira lakini kheri kabla hajafanya lolote, akatambua hilo ni kosa. Kutwaliwa na hasira ukiwa kwenye uwanja wa mapambano hudumaza utumiaji wa akili. Huchochea utumiaji wa nguvu kwa fujo na basi hatimaye kuangamia.
Basi kwanini asitumie njia hii? Akaona kuna haja ya kufanya jambo kumkwaza bwana Denmark. Kuna sababu ya kumpandikiza mwanaume huyo hasira ili amtoe ‘mchezoni’.
“Yes, she is better than me. But at least I look like a man, not like you sweet pie. You are more beautiful than her!” Lee akasema kwa dhihaka akitabasamu kwa mbali akinyanyuka taratibu.
Denmark akabinua mdomo. “I am going to shut that piece of shit forever!” akafoka akimjongea Lee. Akamrushia ngumi nyingi sana kwa hasira. Lee akajificha kukwepa ngumi hizo. Sasa shida kwake ikiwa nguvu kubwa ya Denmark. Mashambulizi yake yalikuwa ya kilo haswa!
Ila sasa hakuwa akitumia akili tena kama hapo mwanzo. Fundo la hasira lilikuwa limemkaba na alitaka kumkomoa mpambani wake ndani ya muda mfupi! Alitaka kumtia adabu.
Huu sasa ndiyo ukawa mwanya kwa Lee. Mwanya wa kutumia akili yake zaidi ya adui yake. Alijua fika unapokuwa na hasira, mazingatio ya kujilinda hupungua, mtu huzingatia zaidi kushambulia. Basi akatafuta mwanya wa kushambulia dhidi ya ‘mvua’ alizokuwa anatumiwa.
Na alipoupata mwanya huyo, akatuma ngumi tatu za haraka, zikamlaza Denmark chini! Wenzake wakamsogelea haraka kumjulia hali.
“Let go of me!” Denmark akawaka akiwasukumia wenzake kando, Alipatwa na hasira maradufu. Uso wake ulikuwa mwekundu. Aling’ata meno yake kwanguvu, akasimama na kumtazama Lee akihema kana kwamba mbogo.
Lee akamkaribisha tena kwa kumuita kwa ishara na kusema,
“Camon my lady.”
Holala! Denmark akanguruma kama simba. Akiwa amekunja uso wake, macho ameyafuma kwa ndita, mdomo ameubinua kama upinde wa mshale, akamsogelea Lee kwa kasi akitengeneza vishindo kana kwamba tembo. Alikuwa amefura haswa. Hakuna alichokuwa anakitaka zaidi ya kummaliza Lee.
Hakika zile dharau zake hakuweza kuzistahimili. Alikuwa amemvua nguo. Alikuwa amemdhalilisha mbele ya wenzake, tena awaongozao.
Basi akatupa ngumi zake kwa fujo. Kwanguvu. Haraka!! Lee akapata kibarua kikubwa cha kujikomboa. Ilikuwa ni kazi kubwa sana kwake kujikiinga dhidi ya mashambulizi haya. Hata kama hakuwa amekubwa, bado mikono yake ilipata maumivu kwani Denmark alikuwa na nguvu mno.
Pale Lee alipokuwa anaona anazidiwa kwa maumivu, basi akawa anasonga nyuma ama kuyeya ‘mazima’ kukwepa kombeo anazotupiwa. Alidumu kwa kama dakika tano, anashambuliwa tu. Anashambuliwa tu! Alishangazwa ni pumzi ya namna gani aliyokuwa nayo Denmark.
Hakuonekana kuchoka wala kupunguza kasi. Kama vile alivyoanza ndivyo alivyokuwa anaenenda. Hakuonekana mtu wa kuchoka muda mfupi ujao, hivyo basi kama Lee hatopata upenyo wa kushambulia, basi muda si mrefu atashindwa tena kujilinda. Atazidiwa. Na huo ndiyo utakuwa mwisho wake.
Akainjika mkono wake wa kuume kukinga ngumi ya Denmark, akainjika na wa kushoto, akarudi nyuma. Akainjika mguu wake kumzuia Denmark kurusha teke. Akainjika tena mkono wake kuume kukinga shambulizi. Akainamisha kichwa, akakipeleka kulia, akakirudisha kushoto kukwepa ngumi.
Alafu akasonga tena kando!
Denmark, kama mtu aliyetambua kuwa Lee anaanza kuzidiwa, akamsongea upesi na kuendelea kumtupia mambo mazito mazito. Mateke, viwiko, ngumi, na hata magoti. Na kweli taratibu mbinu yake ikaanza kuzaa matunda. Sasa Lee akawa akikwepa hii na ile, ijayo inamkomba.
Bahati si kwake, alipochelewa kidogo tu kujikinga, akakumbana na ngumi ya haja ya bwana Denmark iliyofukua taya zake na kumnyanyua juu kama unyoya! Na kabla hajagusa chini, Denmark akapanua mguu wake wa kulia kwenda juu, kisha akamsigina tumbo na kumgotesha sakafuni. Lee akapiga kelele kali!
Aaaaaaggh!! akajikunja kugugumia maumivu makali ya tumbo. Akakunja sura yake akisaga meno.
“Get up bitch!” Denmark akafoka akikodoa macho. Kinywa kilitema mate kana kwamba manyunyu ya mvua ya masika.
“I said get uupp!!”
Akamfuata Lee kwa upesi. Akamzaba mateke mawili ya tumbo. Miranda akashindwa kuvumilia kumwona Lee anashambuliwa kiasi kile. Akapaza sauti, “Stoop!” akisonga kumfuata Denmark, ila kabla hajafika, akastaajabu teke likimsomba kichwa, akajikuta hewani, sekunde, akadondokea chini kama mkungu!
Akapiga yowe la maumivu.
Basi hapa akawa kana kwamba amemtonesha Lee kidonda. Mwanaume huyo akanyanyuka akisema, “Is that the best you have?”
Denmark akaguna kwa kebehi. Akapiga hatua mbili kumfuata Lee. Akatupa mashambulizi yake kama ilivyo ada. Ila kwa sasa Lee hakupumbazia kama muda ule. Ndani ya dakika moja akawa ametambua cha kufanya.
Denmark akazama kosani. Lahaula! Lee akamkandika ngumi tatu za haraka mno. Akiwa anaugulia, Lee akapanda kwa hewa. Baba, akafyatuka teke lililoadhibu taya za Denmark. Na kama haitoshi likafuatia teke lingine. Denmark, na uzito wake, akanyanyuka juu kabla ya kumwagikia chini.
Yote hayo yalitokea ndani ya sekunde tatu tu! Sekunde tatu tu!
Denmark akachumpa kwa mikono yake na kusimama. Hasira zimemjaa pomoni. Akaja kwa kasi kumfuata Lee. Naye Lee hakumngoja kwa sasa. Akajikuta chini ndani ya muda mfupi, akafyagia miguu ya Lee kwa miondoko ya mdudu nge! Na kwa namna miguu yake ilivyokuwa inazunguka kama feni baridi, Denmark akajikuta akiadhibiwa vilivyo.
Sasa akalazwa chini na kutulia. Alikuwa amezidiwa.
“Hey, are you fine?” Sweden akamuuliza Denmark.
“Do I look like that?” Denmark akafoka na kuamuru, “Kill him!”
Basi wale wanaume watatu, Ireland, Sweden na Wales wakapoke agizo hilo la kushambulia. Ila kabla hawajafanya hilo, mara wakasikia gari huko nje. Wakatazamana. Punde si punde geti likafunguliwa na wanaume wawili wakazama ndani!
“We have to go!” akapaza Denmark. Basi mara Ireland akachomoa cha kuchomoa kwenye nyonga yake na kukibamiza chini. Muda si mrefu moshi ukatanda. Watu wakapotelea! Moshi ulipokoma, hawakuonekana wapi wameelekea.
***
“Inabidi tuwe makini sana. Uzembe kama huo unaweza kutugharimu maisha!” alifoka Jona. Walikuwa wote wamekaa sebuleni isipokuwa Sheng aliyekuwa amelala ndani. Ni tulivu haswa. Na hata umeme uliokuwa umekatika, sasa ulirejea.
“Nitahakikisha halitokei tena kosa kama hilo,” akajitetea Marwa. “Sijui nilipitiwaje? Tulikuja kutahamaki wakiwa karibu haswa. Hata kukimbia hatukuweza.”
Kukawa kimya kidogo. Jona akamtazama Lee aliyekuwa anatazama chini. Uso wake ulikuwa umejaa majeraha na hata mwili wake ulikuwa na maumivu ya hapa na pale. Alikuwa ametulia tuli kana kwamba maji mtungini.
“Ahsante sana, Lee,” akasema Jona. “Sitasahau ulichokifanya siku ya leo, unastahili pongezi.”
Lee akatikisa kichwa chake pasipo kusema jambo. Kisha akaendelea tena kutulia.
“Sasa nini kinafuata? Inabidi tuwe na mipango ya kuwamaliza hawa watu kabla hawajaleta madhara.”
Hapo Lee akateta jambo. “Tafadhali,” Kila mtu akamtazama na kumpa masikio.
“Inabidi tuwe makini sana. Watu wale si wepesi kama pengine tudhaniavyo. Tuhakikishe mipango hiyo inakuwa ya akili zaidi kuliko nguvu. Endapo tukisema twende battle na wao, tutapoteza, na haswa sasa hivi wakiwa wameshindwa kuonyesha umwamba wao kwa mara ya kwanza.
Lazima watajipanga zaidi ya mara hii.”
“Lakini,” akasema Jona. “Wamejuaje makazi yetu?”
Akauliza akimtazama Marwa. Marwa akamtazama Lee na kusema, “Nadhani Lee anaweza kutupatia majibu.”
“Mimi?” Lee akatahamaki. “Nitapata wapi majibu hayo?”
“Lee,” Marwa akaita. “Ulikuwa wapi wakati Sheng alipokuwa ametekwa?”
“China,” Lee akajibu.
“Huko nini kikatokea?”
“Mambo mengi tu yalitokea. Siwezi kusimulia yote.”
“Lipi lililokuwa kubwa?”
Lee akafikiri kidogo na kisha akasema, “Nilitawazwa kuwa kiongozi.”
“Na hiyo ndiyo sababu,” Marwa akateta. Lakini bado kila mtu akwa kwenye bumbuwazi. Hawakuwa wameelewa jambo.
“Unamaanisha nini kusema hayo?” Lee akauliza. Uso wake ulihakisi namna ambavyo alikuwa kwenye mkanganyiko.
“Utakuwa una chip mwilini mwako. Kama ile aliyokuwa nayo Sheng. Ujio wenu hapa ndiyo ambao umetuweka sisi bayana. Tumekaa hapa kwa muda, na kama wanaume wale wangekuwa wana namna ya kututambua, basi wangeshalifanya hilo tangu pale Jona aliponusurika kukamatwa nao.
Na kwa upande wa Sheng, chip tulishatoa, sasa nini kinabakia hapo kama kielelezo isipokuwa Lee?”
Basi kuthibitisha hilo, Lee akakaguliwa mwili, na kweli ikagundulikana ana chip mwilini mwake. Akajaribu sana kukumbuka nini kilitokea na ni muda gani aliwekewa chip hiyo. Akili yake ikamweleza kuwa itakuwa muda alivyokuwa yu hoi anaumwa!
Lakini kwanini ilifanyika kwa siri hivyo? Mbona hakushirikishwa? Na je kwa Sheng ilikuwa vivyo hivyo? Maswali haya hakuwa na majibu nayo.
“Sasa tunafanyeje?” akauliza Miranda. “Tuiharibu hiyo chip?”
“Alafu?” Jona akauliza.
“Ili wasiweze kututrace!”
“Hapana,” akasema Jona. “Kwakuwa watu wale itakuwa ngumu kuwatambua mahali walipo endapo wakiacha kutumia ule usafiri, hii chip itakuwa nyenzo nzuri ya kutambua na kuwacontrol.”
“How na ipo mikononi mwetu?” Kinoo akauliza.
“Kama walitumia chip hii kuwaongoza mpaka kuja hapa, basi wataitafuta tena. Tena sasa kwa kulipiza kisasi. Hivyo itakuwa rahisi kuwazamisha mtegoni kwa kuitumia.”
Wazo hilo likaonekana kuwa na hekima ndani yake.
“Na punde tutakapowatia mikononi, basi tutapata getaway nzuri sana ya kuwamaliza pamoja na genge lao!”
***
Saa nne asubuhi …
Sauti ya Denmark akifoka ilisikika chumbani. Baada ya muda mfupi, mlango ukafunguliwa akatoka akiwa na sura nyekundu. Mkononi alikuwa amebebelea simu.
Akaelekea sebuleni na kuketi. Wenzake pia walikuwa huko. Na alipofika, wote wakamtazama kana kwamba wanatarajia jambo kutoka kwake. Ila kukawa kimya kwa muda. Denmark alikuwa amefura. Na kutua fundo lake kifuani akaendea maji ya kunywa na kujijaza mafundo manne makubwa makubwa.
Kisha akahema.
“We have to kill him today. So get prepared.” akasema Denmark. Na asiwe mtu wa kungoja maoni, akaenda zake kurudi chumbani. Wenzake wakabaki wakitazamana.
Ni wazi hali ilionekana si shwari.
***
Majira ya saa kumi na mbili jioni …
“Jona!” Marwa akaja chumbani akiita. Uso wake ulikuwa umepaliwa na hofu. Jona alishtuka toka kitandani na kumtazama. “Vipi?”
“Kuna jambo unatakiwa kuona. Upesi!” Marwa akasisitiza na kisha wakaongozana mpaka sebuleni. Jona akakalia kiti na kutazama tarakilishi. Lakini kabla hajaona kitu, Marwa akasema:
“Wapo karibu na Ikulu. Nadhani ….”
“Watakuwa wameenda kumuua Raisi?” Jona akakatiza kwa tahamaki.
Saa moja na robo usiku, Ikulu.
Walinzi lukuki walikuwa wamesimama kwa nje na hata kutembea ndani. Wengi wao walikuwa wamevalia kaunda suti na kuna baadhi wamevalia sare za jeshi. Watu hao walikuwa na silaha mikononi, japo si wote. Na wale waliovalia kaunda suti walikuwa wana vifaa vya mawasiliano vimepachikwa masikioni.
Mbali na walinzi hao kulikuwa na kamera za ulinzi hapa na pale. Kulionekana kunalindwa haswa. Sidhani kama kunahaja ya kueleza sana namna mahali akaapo Raisi panavyolindwa.
Kulikuwa kumetulia haswa. Na pengine unaweza kusema kuwa mahali hapa ndipo salama kuliko mahali pengine popote nchini. Huenda ikawa kweli, lakini pia yaweza kuwa sio sahihi. Kuna muda yule asiyelindwa ndiye yupo salama zaidi kuliko yule alindwaye. Masikini hulala milango wazi na wakati wale walio juu wakilindwa na binadamu na teknolojia za hali ya juu!
Basi, huwezi amini katika rundo hili la walinzi, watu huthubutu kuja kupavamia. Tena wakiwa wanne tu! Ilikuwa ni ajabu na kweli. Na watu hao wasiwe wajinga kubeba hatari kama hiyo, walikuwa wamejikamilisha ipasavyo.
Masaa kabla ya tukio hili walikuwa wameshatumiwa taarifa zote wanazotakiwa kuzijua kuhusu eneo hili kwa kukusanya taarifa toka kwenye mfumo wa satelaiti. Pili, watu kadhaa washawahi kuja kutembelea eneo hili la Ikulu, si kila mtu ni mwema.
Hukusanya taarifa kidogo kidogo, pengine zinaweza zikawa kidogo, lakini nini hutokea pale kidogo na kidogo huungana? Na tatu, watu hawa kabla hawajavamia hapa, waliitumia vema pwani ipakanayo na jengo vamiwa kutimiza haja zao.
Lakini mbali na yote hayo, kuna kosa moja tu walikuwa wamelifanya. Lipi hilo?
Taratibu taratibu walinzi wakawa wanapunguzwa. Wanadondoshwa chini na kufichwa. Ni kama vile mchezo wa kuigiza uonavyo kwenye televisheni. Wavamizi hawa walikuwa wanafanya mambo yao kwa ustadi wa hali ya juu na pasipo kupoteza muda kwa aina yoyote ile.
Kila kitu kwenye mahesabu. Hata hatua wapigazo. Walitakiwa kuwa humo eneoni pasipo kuzidi dakika arobaini na tano! Na katika hizo, nusu saa pasipo kufahamika kama wapo humo.
Walifanikiwa sana kutimiza hilo. Mpaka dakika ya kumi na mbili hakuna aliyekuwa anafahamu kama nyumba ya Raisi ipo chini ya uvamizi. Na pale ilipogundulikana ikawa hivi …
Mwanaume mmoja, afisa usalama, mweusi mwenye mwili mrefu kakamavu, alisikia sauti za ajabu za wanyama waliomo ndani ya eneo. Akapata hamu kutazama kama moja ya jukumu lake. Aliposonga, akafanikiwa kuona mguu wa mtu ukiwa chini.
Basi haraka akapaza sauti yake kwenye kifaa kutoa taarifa ya tahadhari. Alipofanya hivyo hakungoja majibu, akasonga kuufuata ule mguu, akagundua kuna mwili wa mwenzake umelala hapo pasi na fahamu!
Alikuwa tayari amesachomoa bunduki yake. Akakimbia ila hakufika mbali akakutana na mvamizi aliyevalia barakoa. Mvamizi huyo hakuwa na kitu mkononi isipokuwa glovu zake nyeusi. Macho yake alikuwa ameyafunika na miwani yenye mshikio wa mpira na mgongoni ana begi.
“Weka mikono juu!” afisa akamwamuru kisha akateta na kifaa chake cha mawasiliano, “Nimemkamata mmoja wao! … nimemkamata mmoja wao!”
Alipomalizia kauli hiyo, akastaajabu kukitwa na kitu kichwani. Akadondoka hoi hajiwezi hata ukucha. Lakini je vipi kuhusu taarifa yake aliyoitoa kwa wenzake?
Habari mbaya ni kuwa, hakuna taarifa yoyote ile iliyokuwa inaenda wala kufika kwa yeyote yule! Kabla ya wavamizi hawa kufanya kazi yao, walishahakisha hilo jambo la mawasiliano ya walinzi linapatiwa ufumbuzi. Walipachika vifaa vinne vyeusi, ukubwa wa tofali la kuchoma, kwenye pande nne za dunia zizungukazo Ikulu.
Wakazipanga vema kwa kuzificha alafu wakaziwasha wakiwa tayari wameingia eneoni. Vifaa hivyo vilikuwa vinazalisha nishati kali sana mithili ya ‘radioactive’ ambayo ilikuwa na uwezo wa kupumbazisha ama kuchelewesha jitahada za mwasiliano ndani ya eneo husika.
Na kutokana na kuzalisha nishati hiyo kali, haikuweza kudumu kwa muda mrefu. Hukaa kwa nusu saa tu kabla ya kuzima na kufanya mawasiliano kurudi kwenye hali yake ya awali baada ya dakika tano.
Basi dakika zikaendelea kuyoyoma na kuyoyoma. Na sasa zikiwa zimebakia dakika mbili tu kwa vile vifaa vya mawasiliano kuzima lakini bado haja ya tukio ikiwa bado haijamalizika.
“We have a few minutes!” alitoa tahadhari mmoja wao. Walikuwa wameshashika korido wakielekea chumba walichoamini watamkuta mlengwa wao.
Mara ghafla mbele wakatokea wanaume wawili walinzi, afisa wa usalama. Katika hali hiyo hiyo ya ghafla, mmoja wa wavamizi akachojoa visu vitatu nyuma ya mgongo wake na akavitupa kwa utaalamu wa hali ya juu, vikawakita wale walinzi na kuwadondosha chini.
Ti ti ti ti ti ti! ‘Alarm’ ikalia kutaarifu vifaa vya kuminya taarifa vimezima! Hivyo basi wakawa na dakika tano tu za kutoka na kutokomea hapo kabla ujumbe wa uvamizi haujawafikia wahusika, aidha kwa mfumo sauti au mfumo picha wa kamera za CCTV.
“We have to go!” mmoja akasisitizia.
“No! We aren’t going anywhere till we finish this!” sauti nyingine ikasema ikiwa na mamlaka ndani yake. Ilikuwa ni sauti ya Denmark.
“He is not here!” sauti nyingine ikatahadharisha. “Just let’s go!”
“He must be here,” Denmark akafoka. “Its whether we get him or we die in here! Let’s search!”
Kiongozi alishasema, hakukuwa na kupinga. Agizo likabebwa na utekelezaji ukaanza mara moja. Wanaume hao wakaanza kupekua huku na kule.
Na hilo ndilo lilikuwa kosa lao kubwa, hawakuwa wanajua haswa Raisi yupo wapi. Taarifa ya kuwa yupo Dar es salaam haikutosha kudhihirisha kuwa atakuwa Ikulu.
Dakika tano zikapita. Mawasiliano yakaanza kurejea. Maafisa wa usalama waliomo ndani ya jengo wakaanza kupata taarifa kadha wa kadha. Japo zilikuja kwa kasi, walitambua kuwa hali si shwari. Na wale wanaohusika na kuendesha mitambo ya CCTV wakaanza kuona taswira mbalimbali viooni.
Sasa taarifa rasmi ikawa wazi kuwa ngome ipo chini ya uvamizi!
Katikati ya taharuki hiyo, king’ora kikasikika kikilia. King’ora hicho kilifika kwenye sikio la kila mtu aliyekuwapo mule ndani ya jengo. Na hali isiwe tenge, king’ora hicho ndiyo kikazidi kuwatia watu vimuhemuhe kupita kiasi kwani kilimaanisha Raisi alikuwa anarejea jengoni.
Kwenye jengo ambalo lilikuwa na wavamizi!
Basi taarifa zikazuka, na Afisa aliyekuwa anahusika na Ulinzi jumla wa Ikulu, bwana Kulanga Hassan, akawapasha wale maafisa wanaokuja na Raisi ya kuwa wasitishe zoezi lao haraka mno na Raisi apewe ulinzi maradufu maana wapo chini ya uvamizi.
Na wakati wao wakifanya maamuzi hayo, wale mabwana wavamizi, wakaona sasa hiyo ndiyo ilikuwa nafasi adhimu ya wao kumaliza kazi. Ilikuwa ni lazima Raisi auawe! Sasa wameshapata uhakika kuwa yupo ndani ya eneo la karibu.
“Mwingize Raisi ndani … narudia, mwingize Raisi ndani. Huko nje si salama. Fanya hivyo haraka iwezekanavyo!” amri ilisikika kwenye masikio ya maafisa waliomo msafarani.
Na punde baada yake, afisa aliyeitoa amri hiyo akavunjwa shingo na wavamizi baada ya kazi yake kuisha. Basi mara punde, gari limbebealo Raisi likiwa limeongozana na magari mengine, likazama ndani.
Ilikuwa ‘too late’ wanasema wazungu. Raisi alikuwa ameshazama eneoni. Kitendo tu cha bwana Kulanga kumaliza kuongea, umeme ukakatika! Eneo lote likawa giza kana kwamba ni chini ya handaki.
Hapa sasa wale wavamizi wakawa mithili ya majini!
Basi katika hali hiyo ya giza na purukushani, maafisa usalama wakawa wanawasiliana na jitihada zao kubwa zikiwa ni kwenye kurejesha kwanza umeme ndani ya eneo. Nuru ilikuwa muhimu sana kwa wakati kama huo.
Lakini papo hapo wawe pia wanawasiliana kwa ajili ya kumdhibiti adui. Ila shida inakuja wapi? Utamdhibitije mtu usiyemwona? Mtu usiyejua yupo wapi?
Kurunzi kubwa zikawashwa na kumulika huku na kule, ila Ikulu ina eneo kubwa, bado haikutosha kutoa kile kinachohitajika haswa. Kwahiyo basi kwasababu hapa mlengwa mkubwa alikuwa ni Raisi, basi afisa wa usalama wakamzingira kumhakikishia usalama.
Wakati huo wengine wakiwa wanachakarika, aidha kwa kumtafuta adui ama kutafuta mwanga, wao wakawa wanahakikisha mkuu huyo wa nchi yupo kwenye mazingira swalama kabisa.
Ukapita muda kidogo. Bado purukushani zilikuwa zinaendelea, zavuma, hapa na pale. Katikati ya purukushaniyo, mara sauti ikasikika kwenye vitega sauti vya maafisa wa usalama ikionya,
“Hakuna kupokea amri kutoka kwa mwingine yoyote isipokuwa kwa mkuu peke yake …. Narudia amri, maagizo hutoka kwa Kulanga pekee … Kulanga pekee!”
Sauti hiyo ikakata. Zikapita kama dakika nne, mara sauti ya Kulanga ikavuma, “Mwingizeni Raisi kwenye chumba cha dharura. Haraka, chumba cha dharura!”
Basi baada ya amri hiyo, maafisa usalama nane wakiwa wanamziba Raisi wakaongozana naye mpaka chumba cha tatu ndani ya jengo Ikulu ambapo walimfungia Raisi humo na wakabaki maafisa watatu ndani yake, na watano kwa nje.
“Raisi yupo ndani? Raisi yupo ndani?” sauti ikauliza kwenye vitega sauti.
“Ndio, mkuu. Raisi yupo ndani. Narudia tena, Raisi yupo ndani.”
“Vizuri!”
Sauti ikakata na kisha kuwa kimya kwa wale maafisa waliokuwa beneti na Raisi, na hata wale ambao wamekaa nje mlangoni.
Lakini huko upande wa pili, mambo hayakuwa mambo. Watu walikuwa wanauawa kwa bunduki zenye viwamba vya kumezea sauti. Damu zilikuwa zinamwagwa kana kwamba jinamizi lenye nguvu pagani limeshuka kwenye uso wa dunia. Maiti zilikuwa mahali kadha wa kadha na ubaya ni kwamba hakuna mtu aliyekuwa anafahamu wauaji wapo upande upi wa dunia!
Walikuwa si watu wa kutuama. Walitumia paa, walitumia silaha ndogo ndogo zisizo na madhara ya sauti. Walitumia maarifa na ujuzi wao kwa hali iliyotukuka kabisa. Ilikuwa inashangaza kwa namna ambavyo watu wachache walivyokuwa wanasumbua wale walio wengi.
Mpaka ‘backup’ iliyoombwa kuja kutoa msaada iwasili, basi uharibifu mkubwa utakuwa umetokea hapa.
“Afisa afisa …. afisa afisa…” bwana mmoja alibweka. “Taa zimezimwa zote, imebaki moja tu! Zimezimwa zote imebaki moja tu!” Taarifa ikatolewa na kusambazwa. Kurunzi zote zilikuwa zimezimwa kwa kupasuliwa na watu ambao hawakuwa wanaonekana.
Sasa ilikuwa imebaki kurunzi moja tu iliyo kubwa! Zingine zilikuwa zimegeuzwa kuwa ‘skrepa’ kwa kutobolewa na vifaa vidogo vya vyuma vyenye ncha kali mduara.
Hakuna aliyewaona watu waliotupa vifaa hivyo. Na kwa namna hiyohiyo ndivyo ambavyo watu walikuwa wanauawa. Wengi wao walikuwa wanakutwa wakiwa wametobolewa vifua, shingo au vichwa vyao kwa vifaa vyenye sumu kali iliyokausha miili ya wahusika kwa haraka mno.
“Afisa … Afisa!” sauti ikaita. “Afisa Kulanga amekutwa ameuawa na kupoa … narudia, amekutwa akiwa ameuawa na kupoa!”
Habari hizi zikazidi kuwachanganya maafisa. Lakini zaidi kuwatia hofu!
Mara ya mwisho Kulanga anaonekana ilikuwa ni ndani ya chumba cha kuangazia taswira za CCTV. Huko alikuwa na wataalamu wanne wakiwa wana ‘monitor’ mipango ya kuhakikisha jengo zima linakuwa linaangazwa.
Lakini muda mfupi kabla ya Kulanga kuuawa, kamera zilianza kupoteza mwelekeo. Zilianza kugomagoma na aidha hata kurudia picha. Na kabla tatizo halijafanyiwa kazi, mara kamera zikakaa vema. Kumbe ulikuwa ni mchezo wa mapumbazo.
Ulikuwa ni mchezo wa ulaghai! Na kweli mtegwaji akazama anapotakiwa kuzama.
Ni hivi, wakati video hizo zasumbua, ‘attention’ za watu zilihama. Macho na masikio yao yalikuwa yanaangazia kwenye video na namna ya kukabili tatizo. Kumbe basi mlango unafunguliwa! Hawakujua mlango ulifunguliwaje, kwa kutumia nini, ila wanakuja kutahamaki kuna mtu mlangoni.
Hawajafanya jambo, wakaona vitu vipo hewani, navyo hawakuwa wanajua ni vitu gani, ila wakaja kuvijua baada ya kutua kwenye miili yao. Vilikuwa ni vyuma vyenye ncha na sumu! Japo vyuma hivyo vilitupwa vingi, havikumgusa Kulanga isipokuwa tu kuuchanja mkono wake wa kuume uliobebelea silaha, hivyo akadondosha silaha yake na kuwa mtupu!
Hapo wenzake wote wakiwa tayari wamehamia ulimwengu wa wafu. Walikuwa tayari wamehudumiwa na zile silaha ipasavyo.
“Now we are going to do it by my rules if you want to live, officer,” sauti ya mvamizi ikaruruma. Bwana Kualnga kabla hajataka kuleta ubishi, akatazama mkono wake uliochanjwa. Ulishaanza kubadili rangi kuwa wa zambarau!
***
Afisa usalama wakatazamana. Habari ya kuwa Afisa Kulanga amekutwa mfu iliwatibua akili. Hapa wakapata shaka, mmoja akagonga mlango na kuuliza kama waliomo ndani wako salama. Hawakupata majibu!
Wakagonga zaidi na zaidi, bado kulikuwa kimya. Na kwasababu basi ya kuimarisha usalama, wale maafisa waliokuwemo ndani walikuwa wameufunga vema mlango. Kumbuka hiki kilikuwa ni chumba cha dharura endapo hatari itajiri ndani ya Ikulu hivyo kilikuwa kimesanifiwa katika namna ya ulinzi.
Mlango ulikuwa mzito na makufuli yake yalikuwa kana kwamba vile visanduku vihifadhivyo vitu vya thamani. Si ya kuvunja kwa wepesi hata kidogo.
Basi mabwana hawa, ambao tayari wameshahisi mambo hayako sawa, wakaanza kuhangaikia mlango, na huku wakitoa taarifa juu ya hali waliyomo ili wapate msaada.
***
Ilikuwa ni muda mfupi sasa tangu waone kazi huenda ikawa imekamilika. Basi wakawasiliana na kupanga kutoka ndani ya eneo la Ikulu haraka iwezekanavyo.
Kila mmoja akiwa kwenye ‘angle’ yake wakachoropoka na kukutania upande wa mashariki ya Ikulu. Muda huo sasa vikawa vinaingia vikosi vingine vya wanajeshi na hata maafisa wengine wa usalama.
Wavamizi walipoukaribia ukuta, wakaanza kuchumpa kujikuta nje dhidi ya ukuta mkubwa wa Ikulu walioufanya watakavyo. Wakiwa wamebakia wawili ndani ya eneo la Ikulu, wakaonekana!
Wanajeshi watatu waliokuwa wamebebelea bunduki mikononi, wakawaonyeshea silaha na kuanza kuwafyatulia risasi. Risasi zikaruka kama kumi hivi, na miongonizo zikafanikiwa kumwangusha mmoja wa wavamizi wakati mmoja akifanikiwa kuchumpia nje.
Ila naye alikuwa amejeruhiwa! Alikuwa anakimbia akivuja damu.
Wakaliendea gari lao na kujipaki upesi. Kuwasha gari, halikuwaka! Wakawasha na kuwasha. Bado hakukuwa na amfanikio. Ilikuwa ni hatari mno kubakia hapo kwa usalama wao. Eneo hilo lilikuwa limechafukwa. Lilikuwa ni eneo ambalo lipo ‘busy’ kuliko eneo lolote lile nchini kwa muda huo.
“What’s wrong!” akauliza Denmark, sauti yake ilimtambulisha. Alikuwa anauliza kana kwamba kuna mtu anayejua kinachoendelea hapo ukizingatia yeye ndiye alikuwa dereva.
Alijitahidi sana kuwasha gari pasipo mafanikio. Walipoona wanapoteza tu muda hapo, wakashuka. Kabla hawajaenda popote, wakawa wamezingirwa na watu watatu waliovalia barakoa na kubebelea silaha za moto. Wakapewa na amri ya kunyoosha mikono juu upesi!
Lakini hapahapa, tena ikiwa ni kama sekunde kadhaa tu toka wavamizi wawekwe chini ya ulinzi, vikasikika vishindo vya watu! Mara, “Wale pale!”
Risasi zikaanza kutupwa kwa fujo kuwalenga wavamizi pamoja na wale waliowaweka wavamizi chini ya ulinzi!
Basi hapa ndiyo ikawa salama ya wavamizi. Kushambuliwa kwa pamoja na wale waliokuwa wamewaweka chini ya ulinzi kuliwafanya wote watafute upenyo wa kuokoa maisha yao. Kwahiyo basi wakajikuta wakitawanyika huku na kule.
Wakajikuta wote wakiwa watuhumiwa na wahanga wa risasi zilizokuwa zinamwagwa kama njugu, baada ya kama dakika tano mvamizi mmoja akawa yupo chini kwa kushindiliwa risasi, yule aliyekuwa amejeruhiwa wakati wanafanya jitihada za kuuvuka ukuta wa Ikulu. Wengine wawili wakawa wapo mbioni kutafuta usafiri mwingine wa ziada kuwatoa eneo la hatari.
Na wakati huo wakipambana kwa kurudisha majibu ya risasi walizokuwa wanarushiwa na wale wanajeshi waokozi.
Vita ilikuwa si ndogo. Wanajeshi waokozi walikuwa wengi na hivyo basi mashambulizi yao kuwa makubwa. Kwa muda wote huu wa mashambulizi, eneo lililo karibu la Ikulu lilikuwa limesimama kwa muda. Taharuki ilikuwa imetawala, hofu, vilio na watu kupatwa maruhani!
Eneo hili liligeuzwa kuwa uwanja wa vita ndani ya muda mfupi. Kwa watu wa nchi hii ikawa jambo la kushtusha sana, na habari hizi zikasambaa na kupamba moto huko kwenye mitandao ya jamii na kutengeneza hamu kubwa ya watu kutaka kujua kinachoendelea.
Basi wale wavamizi, wawili waliokuwa wamebaki hai, wakakimbilia baharini na kupoka boti ndogo ya mvuvi. Wakamteka mwenye nayo na kumweka chini ya ulinzi kisha wakawasha mashine na kutimka kuyakata mawimbi.
Muda mfupi kabla hawajatokomea kuacha ‘war zone’, boti zingine mbili, kubwa kuliko ya wavamizi, zikajiri zikiwa zinawafukuza kwa kasi. Mwendo wa boti hizo ulikuwa mkubwa sana, zilikuwa za kisasa na za kivita. Haikuhitaji ufahamu mkubwa kutambua kuwa zilikuwa za jeshi la wana maji.
Mbali na kuwafukuza wavamizi, walikuwa wakiwatupia risasi za moto kuwanyima nafasi ya kupanga mashambulizi ama kutimiza adhma ya kutoroka japokuwa risasi nyingi zilizama majini kuliko kudhuru.
Ndani ya boti hizo kulikuwa kuna kama wanajeshi kumi na mbili, sita kwenye kila mojawapo! Kulikuwa kuna madereva na watu waliobaki wakifanya kazi za ushambulizi. Macho na akili zao zilikuwa zinafanya kazi, huenda, kwa hatua yao ya juu kabisa. Lengo hapa lilikuwa ni kuhakikisha wavamizi hawafanikiwi kuponyoka mkono wa dola.
Basi wakazidi kuwafukuzia na kuwafukuzia. Na kwakuwa boti zao zilikuwa za kisasa zaidi, zilikata mawimbi na kupambana na nguvu ya bahari inavyotakiwa hivyo wakazidi kuwasogelea walengwa wao. Zaidi … zaidi … na zaidi!
Mara …
“Acha kufyatua! Acha kufyatua!” amri ilisikika toka kwa mkubwa wa kikosi, wakiwa sasa wameshaisogelea kwa ukaribu mno boti ya wavamizi.
Ajabu ni kwamba, boti hiyo ya wavamizi ilikuwa bado yayoyoma, mashine yafanya kazi, ila ndani ni kama vile kulikuwa na mtu ambaye hakuwa anatikisika, mtu kama sanamu!
Basi wanajeshi walipogundua hilo wakapatwa na kiwewe. Walipoangaza vema, wakagundua mtu huyo alikuwa amekufa. Na hata hakuwa mvamizi bali mvuvi tu. Hapa wakajita, japo walifanya jitihada, bado wavamizi walikuwa wametoroka!
“Huenda tukawa tumewaua!” Hoja hii kidogo ikaleta mashiko, lakini ikawapunguziia machungu wanajeshi wale dhidi ya kuonekana wamefanya kazi ya kutwanga maji kinuni.
Ila kwa kamanda wa kikosi bado hakuwa ameridhia na hili.
“Tafuteni miili hiyo mpaka pale itakapopatikana. Kinyume na hapo, tutakuwa tumefanya kazi ya kukimbiza pepo.”
Basi wakaanza kurandaranda huku na kule huku na kule kutafuta ushahidi wa miili kuthibitisha kuwa wamefanikiwa kuwamaliza wavamizi. Hawakuambulia chochote kwa masaa mawili.
“Wametoroka,” akasema kamanda wa kikosi. “Hata boti lao halina viashiria vyovyote mbali na huyu mvuvi waliyemuua!”
Habari hizi zikawa za simanzi. Punde, mwanajeshi mmoja akamwita kamanda na kumwambia kuna jambo wanahitaji alitupie macho. Basi kamanda akaitikia wito na kwenda mpaka kwenye kachumba kadogo ka boti hii ya kisasa ambayo nchi ilipatiwa kama msaada toka nchi zilizokwisha endelea. Kwenye kachumba hako kulikuwa kuna mifumo na mashine ya kusaidia mawasiliano. Kilikuwa ndiyo sehemu kitovu ya kupokea na kutuma mawasiliano ndani na hata nje ya boti ikiwa na uwezo mkubwa wa kutimiza majukumu yake hata maeneo ya mbali na yenye ufinyu wa mtandao.
Humo kulikuwa na watu wawili, mmoja wao alimwelekezea kamanda kwenye ‘screen’ ya ukubwa wa wastani iliyokuwa imepachikwa ukutani akamwambia,
“Wakati kurunzi inamulika mara ya kwanza, inaonyesha kulikuwa na watu. Unaweza ukawaona kwa mbali …”
Hapa kamanda akafinya macho yake kutazama.
“Lakini baada ya boti kukwepa kurunzi kwa muda wa dakika moja tu, hawakuonekana tena!” mwanajeshi alitoa maelezo kamanda akitazama kwa umakini.
“Ebu rudisha hiyo video nyuma,” kamanda akaagiza. Video iliporejeshwa, akaitazama kwa ukaribu zaidi. Hapa akagundua jambo. Si kwamba wavamizi walikuwa wamepotea baada ya kurunzi la boti yao kwenda kombo, bali watu wao walitoroka mapema zaidi.
Walikuwa wamechezewa akili. Na muda wote ule wakidhani wanawakimbiza wavamizi, walikuwa tayari wamejitosa kwenye maji wakiacha nyavu na vifaa vya mvuvi pamoja pia na mwili wake katika namna kuwalaghai kuwa bado wapo botini.
Hapa kamanda akajiona mjinga sana. Ni kwa namna gani walikuwa wamefanywa kuwa watoto tena karibia na mbele ya macho yao. Lakini pia akawaza, watu hao, yaani wavamizi, watakuwa wameelekea pande ipi ya dunia, nchi kavu ama bado wapo majini?
Taarifa ikasambaa kwa vikosi vingine maeneo mbalimbali kufanya doria ya kuhakikisha wavamizi hao hawatoki salama kwenye pwani yote hii ya Afrika ya Mashariki.
Basi punde kidogo baada ya kufanya hivyo, boti ikatikisika kwanguvu kana kwamba imekumbwa na wimbi kali! Kufumba na kufumbua, ‘alarm’ kali ya hatari ikaanza kulia!
Duuiiiil! Duuiiil! Duuuiiil! Duuuiil! Duiiiil!
Haraka wahusika wakatazama kwenye ‘boat operation system’ kung’amua nini tatizo. Ajabu machoni mwao, wakaona boti yazama! Kando kidogo ya mashine ya kukatia maji kulikuwa na tundu kubwa ambalo laingiza maji ndani kwa fujo haswaa!
Hawajakaa vema, wakasikia milio ya risasi. Kutazama yatokea wapi, wakagundua ni kutoka kwenye boti mwenza. Risasi zilikuwa zinarushwa kwa fujo haswa. Zinapasua vioo na kutoboatoboa boti kuwa chujio.
Risasi hizi zikawanyima kabisaa wanajeshi hawa fursa ya kuikomboa boti yao inayozama kwa kuwafanyia wazingatie zaidi uhai wao dhidi ya ncha za risasi zilizokuwa zinarindima.
Mpaka zinakoma, boti ilikuwa imeshazama nusu na robo. Sehemu yote ya nyuma ilikuwa ndani ya maji. Boti yabinuka juu! Boti ile mwenza ikatokomea kama kishada.
Simulizi : Anga La Washenzi (2) Sehemu Ya Tano (5)
Kwenye korido za hospitali …
Waziri mkuu anaingia, bwana Sospeter Mhenga. Ametoka kutumbukiza simu yake mfukoni muda si mrefu. Mwendo wake ni wa kasi na uso wake umepaliwa na mashaka. Kando yake anaongozana na ‘bodyguard’ wake lakini pia maafisa usalama wawili.
Baada ya muda mfupi akaonana na maafisa kadhaa waliokuwepo kwenye tukio, kisha daktari anayehusika, bwana Mahenge, ambaye aliyeongozana naye mpaka chumba alimolazwa Raisi.
Humo Waziri mkuu akapata shaka. Macho yake madogo yalitumbua ndani ya lenzi ya miwani.
“Atapoa kweli?”
Mheshimiwa Raisi alikuwa amezingirwa na mashine za kumsaidia kupumua na mashine za kumsaidia kusukuma mapigo yake ya moyo. Ndani ya chumba kulikuwa kuna milio ya ‘bip-bip’ ya mashine kadha wa kadha kumnusuru raia namba moja wa nchi.
Ngozi yake ilikuwa imebadilika rangi kueleka zambarau wakati lips na kope zake za macho zikiwa na rangi ya njano.
Waziri mkuu akaongozana na Daktari kutoka ndani ya chumba cha mgonjwa, koridoni wakakutana na familia ya Raisi, mke na mtoto wake mkubwa wa kiume. Wasitete sana, wakiwa katika hali ya haraka, Waziri mkuu akaongozana na Daktari mpaka ofisini kwake na kuketi.
“Hali yake ….” Dkt Mahenge akabinua mdomo, “… si nzuri kabisa. Amevuta sumu kali sana. Mapigo yake ya moyo yanapungua kadiri na muda, napata shaka kama mashine ile itasaidia kwa kitambo.”
“Kwahiyo tunafanyaje dokta kunusuru maisha yake?” akauliza Waziri akiwa na kimuhe.
“Tutajaribu kadiri na uwezo wetu,” akasema Dkt Mahenge. “Ila kwa sasa, haraka iwezekanavyo, anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa kupunguza pande la virusi linalotafuna mapafu na kuziba njia zake za fahamu. Baada ya hapo tutajua kama abakie hapa nchini ama aende nje kwa matibabu zaidi.”
“Dokta,” Waziri akaita kwa upole. “Kuna nafasi ya yeye kupona lakini?” akauliza.
Dokta Mahenge akameza kwanza mate kisha akatikisa kichwa chake kuafiki, “Natumai atakuwa sawa. Tutafanya kadiri tunaloliweza arejee kwenye hali yake.”
Basi baada ya kusema vivyo, Daktari akaenda zake. Walikuwa ‘bize’ sana, kama unavyojua mgonjwa huyu hakuwa wa kawaida. Ni Raisi. Ni raia namba moja ndani ya nchi.
Madktari wote walikuwa kazi waliyo nayo mbele ni kubwa, si ya mchezo kabisa. Na huenda kazi hii inaweza kuwavumisha ama kuwayoyomesha kwenye medani hii. Madaktari hawa, wakiongozwa na Dkt Mahenge, walikuwa wamedhamiria kwenye hili. Walikuwa wanataka kuuonyeshea umma kuwa hata wataalamu ndani ya nchi wana uwezo mkubwa pia.
Hii ilikuwa ni nafasi yao adhimu. Lakini ilikuwa wazi kuwa mambo hayakuwa mepesi hata kidogo. Shughuli iliikuwa pevu haswa.
Basi usiku mzima, madaktari wakawa wanahangaika wakitumia maarifa yao yote kumwokoa mheshimiwa Raisi. Oparesheni ilidumu kwa masaa tisa, watu wakiwa nje wanangoja kwa hamu kubwa taarifa za chumba hicho. Watu hao wakiwamo familia ya Raisi, Waziri mkuu na pia makamu wa Raisi ambaye alifika papo, pia maafisa kadhaa na wafanyakazi wengine wakubwa wa serikali.
Walikuwa wanapeana habari na simulizi za hapa na pale juu ya mambo yalivyokuwa yametukia. Ilikuwa ni simulizi ya kuogofya haswa ambayo hakuna hata mtu aliyewahi kuwaza kuwa siku moja mbele ya macho yake atashuhudia Raisi kufanyiwa jaribio la kuuawa tena wavamizi ambao walidiriki kuivamia ngome yake kuu.
Ni wakina nani hao, wametumwa na nani? Na nini walikuwa wanakitaka kwa Raisi? Kumshambulia Raisi ni kuishambulia nchi nzima!
“Mmewatambua watu hao?” akauliza makamu wa Raisi, bwana Mrutu. Uso wake mnene mweusi wenye vioo vyembamba vya macho ulikuwa umefumwa kwa hofu na mkanganyiko.
“Bado,” akajibu Mkuu wa idara ya Usalama wa taifa, bwana Jovetic Holombe. “Ila tutajua tu ndani ya muda, vijana wanaifanyia kazi.”
“Ila unahisi ni wakina nani?” akauliza makamu wa Raisi. Mara Waziri mkuu naye akasonga karibu.
“Makisio ni mengi, mheshimiwa. Naomba mtupatie muda tutatoa majibu ya uhakika, ila tu kitu nachoweza kusema kwa sasa ni kuwa watu hawa watakuwa ni makomando kabisa maana ni watu wenye ujuzi mkubwa sana. Lazima watakuwa wametumwa na watu wenye maslahi mapana.”
Haikupita muda wakapata taarifa kuwa wanajeshi wale waliowafukuzia wale wavamizi wameuawa na wengine wapo majeruhi hawajiwezi. Na kama haitoshi, boti ya maafisa wa jeshi la majini imekombwa na kuwatorosha wavamizi. Habari hizi zilitolewa na mkuu wa kamandi hiyo.
***
Saa kumi na mbili asubuhi, Bagamoyo …
Maafisa wanne wa polisi walikuwa ufukweni wakipulizwa na pepo ya bahari. Wawili walikuwa wamebebelea bunduki mikononi na wamevalia sare. Wawili wengine walikuwa wamevalia nguo za raia ila mmoja ndiye aliyebebelea silaha miongoni mwao.
Huyu ambaye hajabebelea silaha, alikuwa ameshikilia ‘radio call’ mkono wake wa kuume. Alikuwa anaongea na radio call hiyo akiwa amekunja ndita, sura ya kazi. Sauti yake ilikuwa kavu na yenye ‘punch’ ya juu.
Mbali na maafisa hawa wa jeshi la polisi, kwa upande wao wa magharibi, kulikuwa na boti nyeupe ikiwa inaeleaelea. Boti hiyo, kwa ubavu wake wa kushoto, ilikuwa na chapa ya jeshi, kamandi ya maji. Pasi na shaka ndiyo ile iliyowatorosha wavamizi.
“… ndiyo, afande …” aliteta yule afisa polisi mwenye radio call. “…sawa, afande, nimekupata vema, over!” akashusha chini mkono wake wenye kifaa cha mawasiliano kisha akawatazama wenzake na kuwapasha agizo walilopewa.
“Watu hawa inabidi wapatikane. Naamini bado watakuwa ndani ya Bagamoyo hii. Vituo vyote vipewe taarifa hii na askari wote wafanye kazi hii leo hii.”
Habari hii haikuwa nyepesi kabisa. Bagamoyo ni mojawapo ya eneo la kitalii. Wazungu wamejaa hapa wakizunguka kwenye fukwe, wakijilaza kwenye vitanda vya mabwawa ya kuogelea, ama wakifurahia huko kwenye vivutio mbalimbali.
Kumtafuta mzungu mtuhumiwa ndani ya eneo hili haikuwa rahisi, achilia mbali ukubwa wa eneo.
Basi kwakuwa jambo hili lilikuwa zito, maafisa wa jeshi la polisi, wanajeshi na maafisa wa usalama wa taifa walishirikiana kulitekeleza. Walisambaa huku na huko, wengine wakiwa wamevalia nguo za kiraia kuchangamana na watu.
Vyombo vya usafiri vikawa vinasimamishwa na kukaguliwa kabla ya kutoka ndani ya Bagamoyo. Huko baharini, boti za wanausalama zinazungukazunguka kufanya doria. Na hata baadhi ya hoteli zikawa zinavamiwa na wana usalama, wageni wote wanakaguliwa.
Msako huu ulikuwa mkali haswa. Uliwapa hofu raia waishio eneo hilo, lakini zaidi wageni ambao huenda wengine walikuja nchini kutokana na sifa walizosikia kuwa mahali hapa ni kisiwa cha amani. Sasa mambo yalikuwa yanageukia mbele ya macho yao.
Kwenye majira ya saa nne asubuhi, taarifa ndipo zikaanza kuvuma sasa kuwa Ikulu ilivamiwa na Raisi yupo hoi hospitalini. Sauti ya makamu wa Raisi ilisikika redioni na sura yake ikaonekana kwenye televisheni kutangaza habari hiyo iliyowashtua watu haswa!
“ … Mpaka sasa wana usalama wanafanya kazi yao kuwatafuta wadhalimu waliohusika na tukio hilo. Natoa rai kwa wananchi wote, tuungane kwenye hili, kutoa taarifa zozote zitakazosaidia upatikanaji wa wahalifu hao. Pia tumweke Raisi wetu kwenye maombi ya salama. Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.”
Taarifa hizo zikazua soga kila mahali ambapo watu walikutana. Si kwenye daladala, ofisini wala vijiweni, hiyo ndiyo ikawa habari kuu! Watu wakijiuliza na wengine wakibashiri nani atakayekuwa anahusika na tukio hilo kubwa kabisa kuwahi tokea tangu nchi ipate uhuru.
Basi mambo yakaendelea kuwa katika hali hii ya homa ya matumbo. Ilipofika kwenye majira ya saa saba, kwenye hoteli moja kubwa, jina kapuni, inayopakana na bahari huko katika mji wa Bagamoyo, ikasikika sauti ya risasi! Ikachukua tena dakika moja, ikasikika sauti nyingine ya risasi, tena na kisha tena!
Mara sauti za kilio zikasikika, na ndani ya dakika moja tu baada ya sauti hizo za risasi, gari moja ya Tour, Toyota Landcruiser Safari, ikatoka kwa fujo na kuvamia geti! Likiwa kwenye mwendo kasi, likadaka lami! Kwa pupa likakimbia likitawala barabara yote.
Lilipokaa sawa, likatimka haswa na kuzua tafrani kubwa. Wanausalama wakapeana taarifa ndani ya eneo zima la Bagamoyo, na magari matano yakaungia kulifukuzia kwa nyuma.
Wanausalama waliamini ndani ya gari hilo kulikuwa na watu wanaowahitaji hivyo kwa hali na mali ilibidi wawatie nguvuni. Hata vyombo va habari navyo vikaanza kurusha taarifa kuwa jeshi la polisi, kwa muda huo, lilikuwa njiani kufukuzana na watuhumiwa.
Basi gari lile, Toyota Landcruiser Safari, likaendelea kukimbia sana. Ni kama robo saa tangu likae barabarani tangu kukwapuliwa kwake likiwa linatafuta njia ya kutokomea toka Bagamoyo. Likiwa linakaribia kutimiza adhma yake, mara matairi yakapasuka baada ya kutwangwa risasi!
Matairi ya nyuma yakawa bazoka. Gari likaanza kuyumba, kwenda mrama! Halijakaa vema, matairi ya mbele nayo yakapasuka, sasa gari likayumba kupita kiasi, hatimaye likapinduka likibiringita mara nne na kisha kutulia. Wanausalama wakalizingira wakiwa wamelijalia silaha.
Walipotazama ndani, wakamwona mzee mmoja wa kizungu akiwa anavuja damu lukuki. Hata hakukaa vema, mzee huyo akakata pumzi. Kusaka ndani ya gari, hakukuwa na mtu mwingine yeyote. Ila kulikuwa na simu iliyopo ‘on’.
Wakaichukua simu hiyo na kuongea kujua nani aliyekuwa anaongea na mzee huyo kabla hajafa. Walichoambulia,
“You are too stupid to catch us. Mind your president!” kisha simu ikakata. Baadae walipokuja kufanya mchakato wa kujua simu hiyo ilikuwa inapigwa tokea wapi, wakaja ipata kandokando mwa bahari.
Na kumbe yule mzee alipewa agizo la kukimbiza gari kwa ajili ya kunusuru familia yake, mke na watoto wake watatu, waliokuwa wametekwa na wavamizi wa Ikulu, yaani bwana Denmark na mweziwe. Na asingeweza kudanganya kwani wavamizi hao waliifungia gari ‘tracking’, na huku wakimpa fursa ya kuwasiliana na watoto wake waliokuwa wakilalamika kubonyezewa tundu za bunduki vichwani.
***
Saa kumi na mbili jioni …
Dkt Mahenge anaweka simu yake ya mezani chini na kumtazama Makamu wa Raisi aliyekuwa amejawa na hamu ya kusikia neno toka kwake. Akashusha pumzi kwanza kisha akakuna kichwa chake chenye upara.
“Mheshimiwa,” alafu akabinua mdomo wake. “Imeshindikana. Hamna namna, inabidi apelekwe nje kwa matibabu zaidi.”
Makamu akatikisa kichwa chake kwa masikitiko.
***
Baada ya masaa mawili, Uwanja wa ndege wa Julius K. Nyerere, Dar es salaam.
Ilikuwa ni jioni ya saa moja. Ndege kubwa ya AIR TANZANIA nambari B. 20BC348 ilikuwa inangurumisha injini zake. Feni zilizo mbawani zilikuwa zinachanganyia taratibu kuelekea kwenye kasi kubwa.
Punde kidogo ndege hiyo ikaanza kukaa tenge kwa ajili ya kupaa. Rubani alitoa maelekezo, tahadhari na pia taarifa kuwa ndege hiyo kituo chake cha kwanza itakuwa ni India moja kwa moja.
Ila rubani huyu aliyejitambulisha kwa jina la Kassim Tolabora, alizingumza kutoa taarifa kwa lugha ya kiingereza pasipo kutia kiswahili kama ilivyozoeleka. Hili laweza likawa si tabu. Lakini lafudhi yake ilitia shaka. Ni wazi aliyekuwa anaongea hakuwa mswahili, alikuwa mzungu.
Hakukuwapo na hilo kwenye ratiba.
Ndani ya ndege kulikuwa na Daktari na manesi kadhaa wa ziada kwa ajili ya kumhudumia Mheshimiwa akiwa anaenda kupata huduma zaidi. Lakini pia kulikuwa na maafisa usalama waliokuwa wanamsindikiza, wanaume nane kwa idadi. Walikuwa wamevalia kaunda suti rangi ya majivu.
Basi ndege ikaenda na kudumu kwa lisaa limoja hewani. Kasi yake ilikuwa kubwa ikikata pepo haswa. Watu waliokuwa ndani wakawa wanamtazama Raisi na taarifa yake ikitolewa kila muda, dakika na sekunde kuwa anaendeleaje. Huko aelekeapo pia wakapashwa taarifa kuwa anakuja mtu mkubwa kiasi hata maandalizi yalianza kufanyika.
Lakini pia wakati hayo yanaendelea, vyombo vya habari vya nje navyo vilianza kurusha habari juu ya kile kilichotokea Tanzania. Habari hii ilikuwa ya moto na ilivuta wasikilizaji na hata watazamaji wengi. Mpaka muda huo ambao Raisi alikuwa anasafirishwa kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu, hakuna aliyekuwa amekamatwa kwa kuhusika na tukio hilo kubwa. Ilikuwa ni ajabu kwa namna yake.
Lakini pia swala hili likafukua makaburi, watu wa kawaida, wataalamu wa historia na hata wataalamu wa mambo ya siasa za Afrika wakaanza kulitafutia vyanzo kwa kutazama na kuchambua misimamo ya Raisi ambayo walikuwa wanadhani kwa namna moja ama nyingine ndiyo ambayo imemwadhibu.
BBC – Idhaa ya kiswahili majira ya saa nne usiku …
Mtangazaji, bwana Paul Chisanja, alikuwa beneti na Profesa Robert Waulaya wa chuo kikuu cha Mzumbe kuzungumzia jambo hilo. Kwa kujitanua na kutumia uhuru wao wa kujieleza, Profesa huyo akadadavua na kuhusisha jaribio hilo la kuuawa kwa Raisi na msimamo wake aliokuwa ameuweka kwenye mkutano wa Umoja wa Afrika uliofanyika hivi karibuni kuwa ni muda sasa wa nchi za Afrika kuanza kukataa misaada toka nje kwani yawafanya watumwa.
Lakini akaenda mbele kwa kusema kuwa fukuto lililopo baina ya serikali ya saa na nchi za Magharibi huenda sasa ikawa sababu ya kutaka kumwondoa mwanaume huyo Ikulu.
Swala hili likapokelewa pia na vyombo kama vile CNN na Deutchvelle wakijaribu kuhoji na kuwahusisha watu kadhaa kwenye mahojiano hayo, ilimradi tu swala hili limetawala habari.
Basi ndivyo ilivyokuwa, wakati huo ndege ipo hewani kumsafirisha mkubwa wa nchi.
Ila huko Uingereza, Birmingham, kwenye ofisi kumi na mbili zilizopo nchi ya ardhi kulikuwa ni mahali ambapo pametingwa na shughuli nyomi. Ofisi hizi za siri ambazo zilikuwa zimewamudu watu takribani hamsini zilikuwa zimefumwa katika namna ya sayansi ya juu kabisa. Tarakilishi zilizokuwa zinatumika hapa zilikuwa ni nyepesi kwenye michakato lakini pia ziki-access hata mitandao ya kiza (dark web) ambazo hazikuwa zimezoeleka na watumiaji wa kawaida bali wahalifu.
Ndani ya ofisi hizi, mawasiliano yalikuwa kabambe na nadhifu. Huduma ndogondogo kama vile kuletewa chakula, maji, kahawa na hata ‘gluecose’ zilikuwa zinafanyika na roboti ndogo za matairi. Watu walikuwa ‘busy’ kuendesha na kusimamia mitambo.
Taarifa zilikuwa zinatolewa hapa kwenda pale katika vitengo tofauti tofauti ambavyo vyote vilikuwa vinasimamiwa na wanawake waliokuwa wamevalia suti na miguuni viatu vyeusi vya visigino virefu. Wanawake hawa vifuani mwao walikuwa na vibandiko vya vioo vilivyokuwa vimeandikwa majina yao.
Haya majina hayakuwa ya kawaida kama ujuavyo, lah! Yalikuwa yameandikwa kufuatia silaha. Mmoja, aliitwa Dagger, mwingine bullet, mwingine bomb, mwingine swords, mwingine arrow na kadhalika na kadhalika. Kwa idadi vitengo vilikuwa kumi, hivyo na wanawake kumi juu yao.
Juu ya wanawake hao kulikuwa kuna mwanaume mmoja, mkuu wa kila jambo, ama tumwite mkurugenzi mtendaji. Yeye ofisi yake ilikuwa pweke kwa juu kidogo ya hizi zingine. Ndani ya ofisi yake, kulikuwa na kiti kirefu na meza ya kioo basi. Kwa macho ya kawaida ungesema ofisi hii ina uhaba wa vitu ukilinganisha na ukubwa wake.
Ila ungekuwa umekosea haswa. Ndani ya ofisi hii kulikuwa na vitu lukuki ila vikiwa vimehifadhiwa kwa teknolojia ya juu. Kuta za ofisi hii zilikuwa zinabiduka na kuleta kinachoagizwa baada ya kubofya button ambazo zimejaa mezani.
Bwana huyu mkubwa aliyekuwepo hapa, hakuwa na jina kamili. Na kama vile wale wanawake ambao wapo kule chini wakisimamia vitengo mbalimbali, jina lake lilikuwa la ajabu kwenye kibandiko kinachoning’inia upande wake wa kuume wa kifua.
Kibandiko chake kilikuwa kirefu na maandishi yake rangi ya dhahabu kikisomeka ‘all of them’, kwa kifupi mabanoni A.OT. Kumaanisha kwamba yeye alikuwa ni mjumuiko wa vile vyote ambavyo wasimamizi wake walikuwa, yaani dagger, swords, bullet, arrow na kadhalika.
Mwanaume huyu wa kizungu ambaye amejawa na ndevu lukuki kwenye taya zake, alikuwa amevalia suti nyeusi, amejilaza kwenye kiti chake na miguu yake mifupi ameilaza mezani, nyayo zikifunikwa na viatu vya Italia (Italian shoes).
Alikuwa ‘amerelax’. uso wake haukuonyesha shaka. Masikioni alikuwa ana ‘earphone’ na kinywani ana ‘bubblegum’ anayoitafuna kwa kubadilisha pande za meno. Alikuwa mtulivu haswa.
Ila punde akanyanyua mkono wa kushoto na kutazama saa yake ya mkononi. Kuna kitu alikuwa anatarajia. Punde mlango wake ulifunguliwa akaingia mwanamke mwenye kibandiko kisomekacho ‘Sword’, alitembea kwa madaha na kukomea mbele ya mkuu wake. Akamwambia,
“They are on air with the President.”
Mwanaume yule akatulia kana kwamba hajasikia. Alitafuna bubblegum yake mara tatu alafu akauliza, “So?”
“They will finish their task,” akajibu mwanamke yule mleta habari. Mkuu akatafuna kwanza kama mara nne kisha akasema, “They better do that.”
Basi mwanamke yule aliyeleta habari akashika hatamu kwenda zake, ila kabla hajafika mlanggoni mkuu akasema, “Make sure you are on touch.”
“We are!” mwanamke akajibu na kwenda zake.
***
“Make sure he doesn’t survive. That’s your order,” sauti ya kike ilisikika kwenye earphone kubwa za rubani mkuu, mwanaume mzungu aliyevalia sare za rubani. Naye mwanaume huyo hakuwa mwingine bali Bwana Denmark, na kando yake, alikuwa rubani wa pili msaidizi, naye si mwingine bali bwana Wales.
Ilikuwa ni ajabu kwa wao kuwapo hapa. Hakuna aliyekuwa anadhania kuwa watuhumiwa wa jaribio la mauaji ya Raisi ndiyo haohao waliopewa dhamana ya kumpeleka mtu huyo nje ya nchi kwa matibabu.
Kiuhalisia hakuna aliyepanga wala kuyajua haya, hata wale waliokuwemo ndani ya ndege hiyo hawakujua liendealo. Wanaume hawa, Denmark na Wales, walikuwa wamewavamia marubani na kuwamaliza muda mfupi kabla ya Raisi kupakiwa na safari kuanza.
Maiti za marubani halisia waliotakiwa kupaisha ndege hii zilikuwa zimeachwa kulekule kwenye uwanja wa ndege. Hakuna aliyekuwa amelijua hilo mpaka sasa.
“Let’s do it,” akasema Denmark akimtazama Wales. Wanaume hawa walikuwa wamekwishaandaa parachuti kwa ajili ya kutokomea wakishamaliza kazi yao. Basi walipoweka mitambo sawa, wakatoka ndani ya chumba cha marubani na kuelekea kule upande wa raia kukutana na wana usalama lakini pia Raisi wammalize kabisa.
Mikononi walikuwa wameshikilia bunduki ndogo kwa ajili ya kurahisha kazi. Hawakupanga kutoana jasho, ni tendo na kuhepa tu.
Basi baada ya kutoka kwenye eneo lao la kazi, tendo ambalo lilichukua sekunde nne tu, uso kwa uso wakakutana na kitu ambacho hawakukitarajia kabisa. Hii ilikuwa ni ‘surprise’ ambayo iliwaacha midomo wazi na kuwafanya watazamane.
Uso kwa uso walikutana na Jona, Lee na Miranda wakiwa wameketi. Watu hao walikuwa wamebebelea bunduki mikononi mwao. Na kwenye viti vingine, maafisa usalama wote, nane kwa idadi, walikuwa wamelala hawajielewi hata chembe.
Ilibidi Denmark na mwezake wapite kwenye bonde hilo la umauti kwenda kumkuta Raisi kwenye chumba chake maalumu. Humo alipofungiwa yeye na wahudumu.
Basi ghafla, risasi zikaanza kutupwa. Watu hawa wakarushiana risasi kwa fujo sana. Na kwa kuona kuwa ilikuwa ngumu kukabiliana na hali ya hapa, basi bwana Denmark na Wales wakarudi upesi kwenye chumba cha rubani na kujifungia humo.
Wakapasua mitambo yote mezani kwa rubani kwa kutumia risasi na sasa ndege ikaanza kwenda kombo. Wakati huo mlango wa chumba hicho ulikuwa unabamizwa kwanguvu, Jona na wenzake wakitaka kuzama humo.
Ilikuwa ni fujo kubwa! Jona na wenzake walishindwa kubomoa mlango kwa kukosa nafasi kwani ndege sasa ilikuwa inayumbayumba hovyo kana kwamba mtu aliyevamiwa na maruwani. Walitupiwa huku na kule, hata silaha zao hazikubakia mikononi!
Basi kwa wakati huo huo, wakina Denmark wakatumia mlango mdogo wa dharura uliokuwapo upande wa rubani, wakachoropoka toka kwenye ndege baada ya kupambana na pepo kali mno. Sasa wakawaacha wakina Jona wakipambana kwenye ndege inayoenda kuanguka.
Hakukuwa na cha kufanya kunusuru ndege hii, hilo lilikuwa bayana. Ndege ilishapoteza mwelekeo na si tu hivyo, ilikuwa inaelekea kuanguka vibaya sana hivyo kubeba roho za wote wale waliokuwa ndani yake.
Si Jona, Miranda wala Lee waliokuwa na la kufanya hapa. Upepo ulikuwa unaingia mwingi sana kwenye ndege, na muda si mrefu bawa la kulia likapata moto na kukatika, likaacha tundu kubwa kwenye ndege ambalo nalo likazidi kuzamisha upepo uso na kifani.
Hata jitihada za kuchoropoka toka kwenye ndege haikuwa inawezekana. Upepo uliokuwa unaingia ndani ya ndege ulikuwa mkali sana. Uliwabamizisha na kuwang’ang’anizia watu kwenye kuta za ndege. Hata kuhema ilikuwa ni kazi kubwa. Kama ndege hii ingeendelea kufanya hivi kwa muda, basi watu wangekufa kabla haijagota chini.
Kama baada ya dakika kumi na moja tangu ndege ianze kwenda mrama, Miranda akaanza kupoteza fahamu. Macho yake yalipanda juu na kifua chake kikihaha kuhema. Alikuwa anapitia wakati mgumu sana, na zaidi alikuwa ni mwenye ugonjwa wa kuhofia vimo virefu.
Jona alimtazama mwanamke huyo akiwa hana la kufanya. Alichokuwa amekifanya Jona ni kujificha nyuma ya kiti ngangari cha ndege ambacho kilimziba na upepo mkali. Hali haikuwa njema hata kidogo.
Alitazama kushoto na kulia kwake akiwaza namna ya kumkomboa Miranda. Hakutaka kukubali kuwa hamna jinsi. Alifikiri kutambaa aking’ang’ania viti mpaka atakapomfikia Miranda. Ila alipoanza tu kufanya hivyo, akajikuta anatupwa na upepo punde tu baada ya kutoka kwenye mgongo wa ‘siti’.
Alibamiziwa ukutani na upepo ukawa unamsulubu ipasavyo. Alishindwa kuhema kabisa, upepo ulikuwa mwingi mno kiasi kwamba hakuweza kutoa hewa nje bali kuingia tu.
Akiwa anatazama kwa mbali kama mtu aishiaye na uhai wake, macho yanatoa machozi, mdomo ameukaza, masikio hayafanyi kazi, akaona ndege ikiwa inakaribia kufika chini. Na kheri ndege hiyo ikiwa inaelekea baharini!
Sekunde mbili tu, ndege ikakita juu ya uso wa bahari kwanguvu kana kwamba nyangumi mkubwa wa bluu. Ikazama, na taratibu mno ikaanza kusonga kwenda chini kabisa.
Ndege hii wakati yachapa maji ya bahari, ilisababisha mfarakano mkubwa, vioo vilipasuka, viti vilingoka na kadhalika. Lee na Jona walikuwa ni wahanga wa hili, walichanjwa na vioo na hata kukitwa na vitu mbalimbali.
Lakini hapa ndipo palikuwa mahali pa kuokoa roho zao. Ni kheri hata ndege hii ilikomea baharini maana kama ingeliangukia mahali pengine basi ilikuwa ni uhakika kuwa asingenusurika yeyote yule.
Jona aliogelea kumfuata Miranda ambaye alikuwa ameishiwa na nguvu na aelekea kufa. Si kwamba mwanamke huyo hakuwa anajua kuogelea, lah! Bali hakuwa na nguvu kabisa. Mwili wake ulikuwa umeteseka sana angani hivyo hakuwa na nguvu ya kupambana na mawimbi ya bahari.
Jona akambeba na kutoka naye ndani ya ndege. Akapiga mbizi kwenda mpaka juu, alipofika akavuta hewa fundo kubwa. Akamsaidiza pia na Miranda kuhema. Mara kidogo Lee naye akachomoza juu, Jona akampatia kazi ya kumtazama Miranda ambaye alikuwa ameanza kupata ‘momentum’.
“Nata kurudi kule chini kutazama wengine!” alisema Jona na basi akavuta pumzi kadhaa za kutosha, akazama chini akiogelea kana kwamba samaki.
Ila kinyume na alivyokuwa ametaraji, ndege ilikuwa imeenda chini zaidi, ilibidi afanye jitihada za ziada kuifikia na kuzama ndani kufanya uokozi. Na kwa muda huo huo afanye jambo hilo kwa wepesi kabla hajakaukiwa na pumzi kifuani.
Basi akazama ndani ya ndege na moja kwa moja akapiga mbizi kufuata chumba alimokuwemo Raisi na wahudumu wake. Akafungua mlango huo kwanguvu. Kutazama ndani, akaona wahudumu wale pamoja na Raisi wakiwa hawana dalili ya uhai. Akamfungua Raisi toka kwenye kitanda chake na kumnyanyua pamoja na mhudumu mmoja, daktari, akaanza kupiga mbizi kwenda nje ya ndege.
Ndege ilikuwa imeshuka chini zaidi ya mara alipoingia hivyo safari ya kupanda juu ilikuwa ni ndefu sana. Na kama haitoshi hakuwa peke yake, alikuwa pamoja na watu wawili mabegani, watu wazima wenye kilo zao.
Akajitahidi sana kupiga mbizi, lakini taratibu pumzi yake ikaanza kufikia kikomo. Bado alikuwa mbali na uso wa bahari. Alijitahidi kuongeza nguvu lakini bado hakuwa anaweza kutoboa kabisa. Hata yeye aliliona hilo, basi akawa hana budi kumwachia mtu mmoja apande na mwingine.
Akamwachia daktari, sasa akabaki na Raisi peke yake. Akaongeza kasi maradufu lakini bado hakuwa na uwezo wa kumaliza hili zoezi. Juu kulikuwa mbali. Mbali haswa. Hata kama angelimwachia Raisi aende mwenyewe bado uwezekano ulikuwa mdogo.
Ila hakukata tamaa. Hakutaka kushindwa kwenye hili kabisa. Aliamua ajitahidi kadiri awezavyo, na pale atakapoishia basi ndiyo uwe mwisho wake.
Akaogelea tena na tena, akasonga kama mita tano tu, nguvu zikaanza kumwishia mwilini. Sasa akajihisi mwisho wake umefika. Hakuwa anasonga mbele tena, alianza kuhisi anarudi nyuma kwenda kwenye sakafu ya bahari ambayo hata ndege yenyewe bado haikuwa imefikia.
Mapigo yake ya moyo yalianza kunyamaza. Mikono yake ilianza kupoteza nguvu kumwachia Raisi. Macho yake yalianza kupoteza uwezo wake akielekea kufa.
Sasa akiwa amekata tamaa na amekubali kuwa anakufa, akahisi mkono wake umeshikwa! Akavutwa kwanguvu kuelekea juu. Na punde, sekunde kadhaa, akajikuta yupo juu. Mkono wake wa kuume bado ulikuwa umemshikilia Raisi. Akahema kwanguvu sana. Kwa muda wa kama dakika tano akawa anahema tu … anahema tu.
Alipokuja kutulia, alimwangazia Raisi ambaye alikuwa amepokelewa na Lee na Miranda. Mwanaume huyo alikuwa amekwishafariki. Haikujalisha walifanya jitihada gani, hakukuwa na muitikio wowote ule toka kwake. Hata mapigo yake ya moyo yalikuwa yameshazizima.
Asingeweza kudumu kwenye maji kwa muda wote ule ukizingatia hali yake iliyomfanya asiwe kwenye fahamu zake. Lakini pia inawezekana mwanaume huyo akawa alifariki hata kabla ya ndege kuzama majini. Yote yawezekana kuwa majibu.
Basi Jona akaona ni kheri wautunze mwili wa mheshimiwa huyo kwani inawezekana kuja kuwa na matumizi kwa hapo baadae. Ni vema hata watakapopata nafasi ya kurudi nchini warudi na mwili huo kama kielelezo kuwa walijaribu, angalau walipambana kumnusuru mkuu wa nchi.
Jua lilikuwa lataka kuchipukia, lakini likazongwa sana na mawingu.
***
Saa mbili asubuhi, Julius Nyerere Airport.
Wanaume wawili, maafisa Usalama waliokuwa wamevalia kaunda, walikuwa wamesimama kandokando na uwanja patuapo na paondokeapo ndege.
Mmoja aliyekuwa mfupi na mweusi kuliko mwenzake, alikuwa ametia mkono wake wa kushoto mfukoni na wa kulia ukiwa umeshikilia simu yake kwa maongezi. Alikuwa anaongea na mkubwa wa kazi aliyekuwepo huko makaoni.
“ … ndege imepaishwa na watu wengine, huenda ni maadui. Marubani wote waliotakiwa kuwapo ndnai ya ndege wamekutwa wamekufa! … ndio, mkuu. Tumejaribu lakini mpaka sasa hamna mafanikio. Ndege haionekani kwenye rada yoyote ile, na kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, mara ya mwisho kupatikana ilikuwa ni juu ya bahari ya Atlantiki, upande wa Kaskazini Mashariki … sawa … sawa, mkuu!”
Alipokata simu hiyo, wanaume hao wakaelekea kwenye ofisi ya mawasiliano ya ndege ipatikanayo kwenye Uwanja huo kwa ajili ya taarifa zaidi.
Baada ya masaa mawili, taarifa ikawa rasmi sasa kuwa Ndege iliyokuwa imembebelea Raisi imepotea. Hakuna inapoonekana. Hata kule India ambapo ndipo ilitakiwa kuwapo kwa muda huo, hawana habari nayo.
Taarifa hizi zikazidi kuweka watu kwenye hali ya taharuki na mshangao. Kwasababu za ndani, ikabidi wakubwa wa vyombo vyote vya Usalama wakutane kwa ajili ya kikao cha dharura. Makamu wa Raisi naye akhudhuria kikao hicho kutazamia nini cha kufanya kutoka na hali hii ya kustaajabisha.
***
Miranda alikohoa akiwa amejikunyata. kwa muda wote huo, bado walikuwa kwenye maji. Mvua ilikuwa inanyesha, hali ya hewa ilikuwa baridi sana. Ukungu ulikuwa umetawala kiasi cha kutoona vema pande zao nne za duni.
“Inabidi tumwache,” akasema Lee akimtazama Jona aliyekuwa amesmshikilia Raisi. “Umechoka sana. Anakutia uzito zaidi.”
Jona akatazama mwili wa Raisi. Ulikuwa ni wa zambarau ukiwa na uweupe kwa mbali wa barafu. Ulikuwa ni wa baridi mno kana kwamba jiwe lililotoka kwenye jokofu. Hata mwili wa Jona ulikuwa wa baridi ila si kwa kiasi hiki.
“Labda tutapata msaada,” akasema Jona. Ila sauti yake ilionyesha kabisa kuwa na upungufu wa matumaini. Walikuwa wamepiga mbizi sana lakini mpaka muda huo hawakuwa wameona kitu chochote isipokuwa maji tu. Watakaa humo kwenye maji mpaka muda gani na huku ni ya baridi chini ama karibu na nyuzi sifuri sentigredi?
“Jona,” Miranda naye akaita. “Hatuna namna. Mwache tupambanie maisha yetu kwa mara ya mwisho au tufe wote.”
Jona akashusha pumzi ndefu. Akatazama mwili wa Raisi kwa macho ya huruma, ila kabla hajauachia mwili huo uzame kwenda sakafuni mwa bahari, wakasikia mlio wa risasi! Kutazama wakamwona Miranda akiwa ametoa macho na kuachama kinywa.
Jambo hilo lilimshtua sana Jona, alidhani Miranda atakuwa ametwangwa risasi. Akamshika akiwa ametoa macho, akamuuliza, “Miranda, nini?”
Ni kama vile walisahau kuwa risasi yaweza kupigwa kwa mara nyingine tena na kuwadhuru. Miranda akamtazama Jona na kumwambia, “Risasi!”
“Imefanyaje? Imekupiga?” Jona akauliza kwa pupa. Miranda akatikisa kichwa akiwa ameachama kinywa. Akasema kuwa risasi imempitia sikioni muda si mrefu ulopita. Na alikuwa anashangaa kwa kudhani aidha amekufa.
Basi Jona akamzamisha, wote wakazama kwa haraka na kusonga ndani ya maji. Walikuwa wamepata nguvu ghafla, lakini pia tumaini kwenye wakati huu mgumu. Japo walikuwa wanashambuliwa kwa risasi, walipata kujua kuwa hapo karibu na wao kutakuwa na sehemu kavu ya ardhi ambayo husimamiwa na hao watu wanaotaka kuwaua.
Na ni kweli walichokuwa wanadhani. Kwa umbali wa hatua kadhaa toka walipo kulikuwa na kisi kikubwa sana, lakini hawakuwa wamekiona kwasababu ya ukungu. Kisiwa hicho pweke kilikuwa kimejawa na misitu iliyofungamana kwa umbijani.
Kwenye fukwe, mchanga mweupe unaovutia na hata pia matumbawe yakushangaza. Lakini papo hapo kulikuwa na wauaji waliokuwa wamebebelea bunduki, nao ni Denmark na mwenzake Wales.
Wanaume hawa wa kizungu walikuwa wametua mbali kabisa na hiki kisiwa baada ya kujirusha toka kwenye ndege. Walijikuta baharini na hivyo basi wakafanya jitihada za makusudi kufika hapa.
Lakini kinyume kabisa na matarajio yao, wanawaona watu waliowaacha kwenye ndege wakiwa hai. Jambo hili si tu kwamba linawashangaza, bali linawakasirisha mno.
Haraka baada ya kubaini hilo, wanafanya jitihada za kuwamaliza kwa kuwatupia risasi lakini nazo bado hazikufua dafu. Na hapa tuongeapo tayari walikuwa wameshawapoteza watu hao wakiwa hawajui wapo upande upi wa maji.
“You should have killed her!” aling’aka Denmark akimweleza Wales juu ya kosa lake la kumbakiza Miranda. Lakini Wales akajitetea kuwa ni sababu ya upepo. Upepo ulikuwa mkali na hivyo mahesabu yake yakaenda kombo.
Basi hawakuwa na la kufanya hapa zaidi ya kutupa macho yao huku na kule kuwatafuta walengwa wao kwa kutumia hadubini yao. Wakafanya swala hilo kwa muda wa takribani dakika tano, hawakufanikiwa kuona kitu. Ni kama vile walikuwa wameshawapoteza watu wao kabisa.
“Now what we do?” akauliza Wales.
“Search them!” akafoka Denmark, kisha akamzaba Wales kibao cha kichwa. “Fool!”
Wales akakwazika na hiko kitu, lakini hakuwa na la kufanya. Akazamisha macho yake kwenye matundu ya hadubini na kuendelea kusaka wapi walipo watu wao, wakati huo Denmark akaenda kujipumzikia chini ya mti akimtazama.
Alisaka lakini hakufanikiwa. Jona na wenzake walikuwa tayari wameshazunguka upande wa nyuma wa kisiwa na kukomboa nafsi zao. Jona akiwa bado amembebelea Raisi wakazama ndani ya misitu kwa usalama zaidi. Wakatulia kuvuta hewa na kupumzika.
Lakini walijuaje kama upande huu kuna kisiwa mbali na ukungu uliokuwa unasumbua macho yao?
Punde walipopata nafasi ya kuongea baada ya kuzama ndani ya maji kuepuka risasi, Lee alimuuliza Miranda ni upande upi wa sikio risasi ilmpuliza. Naye Miranda alipojibu, basi wakapata kutengeneza jografia ya wapi risasi ilipotokea, na basi huko ndiko kwenye ardhi kavu.
Sasa wamefanikiwa japo hawajui wapi adui alipo na nini amepanga. Kama litakuwa ndani ya uwezo wao, basi wahakikishe wanawahi kummaliza adui kwani endapo maadui watawawahi wao, basi itakuwa tabu sana maana wao hawana silaha mikononi mwao.
Basi baada ya muda mfupi kupumzika, Jona akauficha mahali mwili wa Raisi na kuwataka wenzake waanza kuwasaka maadui zao kwa tahadhari. Sasa wakaanza kunyatanyata na kuangaza macho yao huku na kule. Ila bado miili yao ilikuwa mizito, na zaidi walikuwa wamechoka. Kupambana kwenye maji kwa muda mrefu, kuliwapunguzia nguvu kwa kiasi kikubwa na hawakuwa na muda wa kutosha wa kupumzika.
Basi wakaendelea kutembea. Kisiwa hiki ni kikubwa, hapa sasa wakaanza kujua. Walitembea kwa muda mrefu lakini bado hawakuwa wamefikia kikomo. Na basi kwasababu walikuwa wamechoka mno, Lee akapendekeza wapumzike maana hata watakapokutana na maadui hawataweza kufua nao dafu kutokana na kuwa dhaifu.
Wazo hilo lilikuwa jema ila hatarishi, watapumzikia wapi? Vipi wakiwa mapumzikoni wakavamiwa? Iliwalazimu kuwa waangalizi maradufu hapa.
“Pengine tupumzikie juu ya miti,” Miranda akashauri, walipoona ni wazo jema, Jona na Lee wakaanza kukata matawi kuunda viota. Walidumu kwenye hilo zoezi kwa dakika kadhaa, walipomaliza wakavifunga viota hivyo mitini na kupumzika.
Haikuwa rahisi kuonekana. Viota hivyo vilifanana na matawi ya miti. Miti ilikuwa mingi sana hapa, kwa mtu kung’amua kuwa kuna makazi huko juu ya miti basi ni juhudi kubwa zimefanyika.
Na kabla hawajajipumzisha, Jona alihakikisha kuwa eneo hilo lipo vema kiulinzi, mbali na macho ya watu.
Basi isichukue muda, wakapitiwa na usingizi. Ila usingizi wa mashaka. Walikuwa wanafumbua macho yao kila muda kutazama, haswa pale walipohisi huenda kuna shaka.
Zikapita dakika kumi na tano, hatimaye wote sasa wakapitiwa na usingizi. Hawakuweza kudumu kutazamatazama tena. Walikuwa wamechoka mno, miili iliwazidi uwezo wao kumudu.
Basi dakika zikasonga zaidi na zaidi. Kama baada ya nusu saa, kule fukweni, bwana Denmark na Wales wakagundua kulikuwa na nyayo za viatu vya binadamu. Walikuwa wamefika ule upande ambao Jona na wenzake walikuwa wameingilia.
“You see,” akasema Denmark. “Now they are here. They are in the island!”
Wakatupa macho yao ndani ya kisiwa. Kilikuwa ni kikubwa sana. Watu wao watakuwa kwa upande gani? Hicho kilikuwa ni kitendawili kikubwa kuking’amua.
Wakafuatilia nyayo zile ambazo zilizama ndani ya msitu, lakini hazikudumu sana zikamezwa na majani. Haikuwa tena rahisi kuona nyayo za watu. Hapa sasa wakalazimika kwenda tu kwa hisia. Kitu pekee kilichokuwa kinawapa imani ni kuwa, walengwa wao hawakuwa na silaha kama wao.
Lakini wakiwa njiani, Denmark aliendelea kumsema Wales kwa uzembe aliokuwa ameufanya. Alikuwa anamtupia lawama na hata kumtusi. Na si tu yeye, hata wale wengine ambao tayari walikuwa wamekufa, akisema kuwa wao ndiyo chanzo cha kasi hiyo kuzorota. Laiti kama wangelikuwa wametilia maanani, basi kwa muda huo wangekuwa wapo Uingereza.
Maneno hayo yakawa yanamkwaza sana Wales. Hakuona hoja ya wao kulaumiana wakati walikuwa wapo pamoja kwenye kazi, na zaidi hakuona haja ya Denmark kumwendesha kiasi hicho ingali wote ni watu wa daraja moja. Denmark ni mkubwa kwasababu tu ya kuteuliwa, lazima awapo kiongozi, ila si kusema ana uwezo kushinda wenziwe.
“I am sick and tired of your bullshit, Den!” Akafoka Wales. “Can I have a moment of peace, please?”
“What did you say?” Denmark akauliza akimsogelea Wales.
“You heard it!” akajibu Wales akimtazama Denmark machoni. Basi Denmark akapandwa na hasira na kumzaba kofi kali Wales mpaka kudondoka chini. Mwanaume huyo uso wake ukawa mwekundu kwa hasira.
Akanyanyuka pasipo kusema jambo. Akajikung’uta, na ghafla akamwelekezea bunduki bwana Denmark na kumwagia risasi tatu. Denmark akiwa ametoa macho kwa kutokuamini, akadondoka chini na kufa macho yakiwa wazi.
“Die you bitch!” akafoka Wales kisha akamkandika teke Denmark aliyekuwa mfu tayari. Alipomaliza hapo akachojoa chombo cha mawasiliano toka kwa Denmark na kutoa taarifa makaoni juu ya eneo walilopo, lakini pia kuwa wamepungukiwa idadi ya watu hivyo wanahitajika watu kadhaa kumsaidia.
Alipokata mawasiliano akamtemea mate Denmark na kwenda zake. Ila milio ile ya risasi iliyomuua Denmark iliwashtua na kuwafanya wakina Jona kuwa tenge.
***
Saa tano asubuhi …
Makomandoo sita walikuwa wameshajipaki kwenye ndege ya kivita tayari kwa ajili ya kusafiri kwenda kumtafuta Raisi huko baharini mwa Atlantiki. Makomandoo hawa walikuwa wametoka kuongea na mkuu wao muda mfupi uliopita wakipewa hamasa ya kutenda kazi yao. Ilikuwa ni lazima warejee na Raisi nyumbani. Hata kama amekufa basi warejee na mwili wake.
Basi pasipo kupoteza muda, ndee ikanyanyuka na kwenda kwa kasi sana. Makomandoo wale wakiwa wametulia ukutani mwa ndege wakiwa wamefungia mikanda yenye nguvu. Walikuwa ni wanaume walioshiba haswa. Miili mirefu iliyojengekea. Vifuani wamevalia vijishati vyeusi vilivyobana vifua vyao, miguu imekabwa na kombati za jeshi na vichwa vikiwa vimemezwa na kofia nyekundu za jeshi.
Walikuwa wamejiandaa kwa lolote lile.
Lakini pia kwa wakati huohuo, kuitikia wito wa Wales, Underground office kule Uingereza ilikuwa imeshatuma watu wake kadhaa kwa ajili ya kwenda kumsaidiza Wales kumaliza kazi. Hivyo lilikuwa ni swala la muda tu kwa tu hawa kukutana na kuonyeshana ubabe.
Kisiwa hiki kilikuwa kinaenda kumezwa na damu.
Basi kufikia usiku kukawa bado kimya kisiwani. Hakukuwa na tabu wala shaka sana, Wales hakuwa amekutana wala kuonana na wakina Jona, na hii ilikuwa ni kwasababu hawakutafutana. Baada ya kupungukiwa na mtu, Wales aliona afanye stara kungoja, na kwa wakati huohuo wakina Jona wakiwa wamejihifadhi ndani ya giza.
Usiku ukakomaa zaidi na zaidi. Kwenye majira ya saa saba hivi usiku, makomandoo wa kitanzania wakawa wa kwanza kuwasili karibu na eneo la tukio. Wanaume hao walitua ndani ya maji na kisha kupiga mbizi mpaka kwenye kisiwa.
Kulikuwa ni baridi sana na upepo ulikuwa unapuliza sana. Ila kwa makomandoo hawa halikuwa shida hata kdogo. Walikuwa ni watu walofundwa kuishi mahali mbalimbali na kukabiliana na hali mbalimbali. Kuitwa jina la komando halikuwa jambo la lelemama. Ni kuzoeza mwili na patashika na kila shurba za dunia.
Wanaume hao ‘walipotimba’ hapo kisiwani wakatulia na kujadili kwa muda kidogo. Hawakuwa wanafahamu kama hapa palikuwa pana watu, dhumuni kubwa haswa ni kuangazia upande upi wa dunia ambapo ndege hiyo ilikuwa imeangukia ama kupotelea.
Basi baada ya muda wakawasiliana na makaoni na kuwataarifu wapo juu ya ardhi kavu ndani ya bahari iliyosolemba. Kule makaoni walipozama kwenye ramani ya dunia iliyopo kwenye vifaa vya elektroniki, wakabaini eneo walilopo. Na hata walipo ‘trace’ ile ndege, wakabaini kuwa ukanda ule ndiyo ambapo ndege ilikuwa imepotelea kwenye rada.
Kwa taarifa hizo, makomando wakaona ni vema basi vifaa viwahishwe ili wapate kuwandawanda kwenye bahari kuangaza. Vifaa hivyo vikahaidiwa kufika haraka iwezekanavyo.
Mawasiliano yalipokata, wanaume hao wakaona wasipoteze muda, kwa wakati huo ambapo hawawezi kutanga baharini, basi wahakikishe pia na pale kisiwani ni mahali salama. Kwakuwa ndiyo ardhi pekee ipatikanayo karibu na ukanda wa kupotea kwa ndege, huenda ikawa na watu ambao wanawatafuta ama wanahitaji msaada.
Huenda.
Basi wakaanza kuzama ndani, mikononi mwao wakiwa wamebebelea silaha na macho yao yakiangaza dhidi ya msitu. Giza lilikuwa kubwa. Waliwasha kurunzi nzao na kuendelea na kazi. Wakatembea kwa umbali mrefu, kisiwa kilikuwa kipana. Wakiwa wanatembea, mtu wa kwanza kuwatia machoni akawa ni Wales.
Mwanaume huyo aliyekuwa amejibana nyuma ya mti, aliwatazama vema kuwang’amua kuwa wale hawakuwa watu wake, yaani wale ambao alikuwa amewaomba waje kumsaidia. Akapata mawazo, ina maana maadui zao, yaani wakina Jona, na wao watakuwa wamewatuma watu wa kuja kuwasaidia?
Basi akaona ni vema kama akiwatia watu wale machoni muda wote ili ajue nini watakuwa wanapanga na vilevile iwe rahisi endapo watu wake wakifika awapashe habari eneo ambapo walengwa wake wanapatikana.
Sasa akawa anawafuatilia, taratibu akihama toka kwenye mti mmoja kwenda mti mwingine. Kwa hali ya utulivu kabisa na kwa tahadhari. Basi wakaenda kwa kama dakika tano, ila ikafikia muda mmoja wa wale makomandoo akahisi kuna kitu.
Alisikia kitu kikitembea na si mara moja, zaidi ya mara tatu. Basi akiwa hajawaambia wenzake, akaanza kutilia maanani yale alokuwa anayasikia. Muda si mrefu, akagundua kuna mtu.
Hakutaka kuwashtua wenzake na pia hakutaka kuanza kumwaga risasi kwanza kabla hajajiridhisha. Akapaza sauti, “wewe nani? Jitokeze!”
Ila mtu yule, ambaye alikuwa ni Wales, akanyuti nyuma ya mti akiwa ametulia. Na sasa kutokana na sauti ile ya maulizo, makomandoo wengine wote wakawa nao wameelekezea nyuso na hata silaha zao huko.
“Kuna mtu,” akasema yule komando aliyemwona Wales. Macho yao yaliganda eneo la tukio na wakiwa tayari kwa ajili ya lolote lile litakalojiri, aidha mtu huyo awe rafiki ama adui.
Kwa wakati huo Wales akawa anawaza namna ya kufanya. Kama akikimbia, basi risasi zitatupwa kwa wingi kumfuata. Lakini pia kama akiendelea kukaa hapo, ni wazi wale watu watajongea kumfuata.
Kichwa chake kikawa kimetingwa. Macho yake yakawa yanaangaza huku na kule kukimbizana na muda apate fursa ya kuokoa maisha yake. Hali ilikuwa tete.
Baada ya sekunde kadhaa za ukimya, Wales akiwa bado hajafanya maamuzi, makomandoo wakaanza kujongea kuufuata mti alipojifichia. Kurunzi zao zilimulika hapo kuhakikisha hawapitwi na kitu. Miguu yao iliyovekwa buti kubwa ikawa inajongea ikipiga hatua kubwa na kwa upole.
Bado Wales akawa amekwama hajui la kufanya. Alihema kwa sauti ya chini ila upesi upesi. Akashikilia bunduki yake vema na kuamua kupigania maisha yake kwa kupambana na maadui uso kwa uso. Hakukuwa na namna sasa.
Basi ikiwa imebakia hatua kama sita tu kufikiwa, mara sauti kubwa ikasikika tokea baharini. Ilikuwa ni sauti ya boti lililokuwa linaendeshwa kwa kasi. Makomandoo wale wakasita na kutazamana kwa namna ya maswali.
Kama haitoshi wakasikia na sauti kadhaa za watu wakizungumza. Usiku ulikuwa mtulivu hivyo basi sauti ilikuwa inavuma katika namna ya kusikika pasipo tabu, ukijumuisha na upepo wa bahari.
Sauti hizo zilizokuwa zinavuma zilikuwa si za kiswahili bali za kiingereza hivyo basi zikazalisha shaka kwa wale makomandoo kwamba huenda hao watu wakawa ni miongoni mwa maadui walioshiriki na mpango wa kummaliza Raisi.
Basi kitendo hicho cha kuzubaa, kikampatia mwanya bwana Wales. Akachoropoka upesi baada ya kujitupia kwa samasoti mbugani, na kwa upesi akaanza kukimbia akikakatiza mitini.
“Ni mzungu!” akasema Komandoo mmoja aliyekuwa amebebelea kurunzi, kisha akaongezea, “Amevalia nguo za rubani!”
Basi hapa wakawa na uhakika kuwa bwana huyu ni mmoja wa maadui wanaowatafuta, wakaanza kumrushia risasi pasi na kifani na hata kumkimbiza kwa kasi.
Bwana Wales akakimbia mno akikatiza hapa na pale. Nyuma yake vyuma vya risasi vilikuwa vinapiga na kutoboa ama kuchana miti. Aliinamishia chini kichwa chake na kunyoosha mapaja haswa.
Akaruka kuvuka matawi, majani na hata visiki. Muda mwngine kurunzi ya wanaomkimbiza ilikuwa inamsaidia juu ya wapi apite na kukanyaga. Akakimbia kwa kama dakika moja kabla hajachomoa chombo chake cha mawasiliano na kuanza kuwaelekeza watu waliokuja kumsaidia wafuate milio ya bunduki.
Akiwa anatoa maelekezo hayo, akastaajabu kadunguliwa bega lake la kushoto. Akalalama kwa maumivu makali, ila hakusimama. Akaendelea kukimbia kwa kasi, akivuka, akipambana, akikumbatiana na miti na matawi yake.
Mara akadondoka chini! Kama kheri alipodondokea palikuwa na korongo la wanda wa majani, akabiringita kama tairi na kwenda kujikuta chini akiangukia bega lililoumia. Akasaga meno kwa maumivu makali mno. Kabla hakanyanyuka, akasikia, “Yule kule chini!”
Mara risasi tena zikaanza kumwagwa. Mojawapo ikamtoboa mguu wake wa kulia, hivyo hata alipoamka, akajikuta hawezi kukimbia tena kama awali! Makomandoo wakaserereka kwenye kile kikorongo na kuendelea kumkimbiza.
Lakini kama kuna kosa walilofanya mabwana hawa basi ni kumkimbiza bwana huyu kwa wingi, takribani makomando wanne walikuwa wanalifanya hilo zoezi wakimkimbiza pasipo kujua ama kujali kwamba wanajiweka bayana kwa ajili ya shambulizi la kushtukiza.
Kama inegeliwezekana, kwakuwa watu hawa walikuwa na mawasiliano, wangejigawa, na watu wawili tu wangetimiza hiyo kazi, kiasi kwamba hata wakishambuliwa na kuuawa, ‘gape of number’ isiwe kubwa.
Basi hatua ya kwanza, ya pili, tatu … saba na nane, mara makomandoo wakawa wamempoteza bwana Wales. Hawakumwona wapi ameelekea. Alikuwa amjificha lakini bado sauti yake ya kuugumia maumivu ilikuwa inasikika kwa mbali.
Makomandoo wakatembeza kurunzi yao huku na kule. Hili pia ikiwa ni mojawapo ya kosa kwenye vita za msituni kwani hukuweka wazi upo eneo gani hata pale adui anapokuwa mbali. Walipoyumbisha kurunzi juu mitini,, wakawaona watu nane kwa ghafla. Watu hao walikuwa wamevalia barakoa na macho yao yamezibwa na miwani.
Bwana we, kabla hata hawajasema suuh! Wakamiminiwa risasi kana kwamba mvua ya vuli. Zikawatoboa vichwa na kupasua miili. Zikavujisha damu na kuwageuza bucha ndani ya kasi ya kufumba na kufumbua! Hakuna aliyeibuka salama! Wote wakalala chini wakiwa wamefunikwa na damu nzito.
Wauaji wakatua chini na wawili miongoni mwao wakaelekea upande wao wa kushoto ambapo huko walimkuta Wales akiwa amelala chini. Upesi wakamfanyia huduma ya kwanza kwa kuziba majeraha yake, begani na mguuni, kisha wakambeba na kumpeleka kwenye boti waliyokuja nayo, huko tena kulikuwa na watu wawili, wanaume wa kizungu.
***
“Siwapati!” akasema Komandoo mmoja akitikisa kichwa punde baada ya kushusha radio call yake toka sikioni. Alikuwa ametoka kuwatafuta wenzao wanne walioenda kumfukuzia Wales.
“Jaribu tena,” mmoja akashauri. Komandoo yule mwenye radio call akaruda tena hilo zoezi, majibu yakawa yaleyale. Hawakuwa wanawapata walengwa wao. Basi hapa wakapata shaka kuwa huenda milio ile ya risasi waliyokuwa wanaisikia iliwamaliza wenzao.
Wakiwa bado hawajaamua la kufanya, mara wakasikia sauti toka kwenye radio call. “Your friends are dead. Would you want the same service?”
“Yes, you bitch!” akafoka komandoo mwenye radio call. Uso wake mweusi ulijawa na ndita na kona za mdomo wake zilishuka chini. “If you are a man, show yourself up!” akatema mate kwa kufoka.
“Then come down where you heard shots. I will be waiting!” sauti ikamjibu.
Bwana yule komandoo akasonya na kukata mawasiliano kisha akawatazama wenzake na kuwaambia kile alichoambiwa ya kuwa watu hao, waliowamaliza wenzao, wanataka washuke kufuata sauti ya mlio wa risasi ilipotokea.
Ila wakakabwa na tahadhari. Kama wakienda huko, wanajuaje namna ambavyo watu hao wamejipanga? Ilibidi waibuke na namna ya kukabiliana nao kwanza kabla ya kwenda. Kama inawezekana wajue pia na idadi na hata silaha walizo nazo.
Ila yote hayo watayafanyaje? Basi wakakubaliana kumtuma mmoja kama chambo, yeye aende kwa siri huko ambapo wanahisi hao watu wapo kisha atoe taarifa na basi wenzao wataenda kutimiza kazi.
Mtu huyo akateuliwa, na pasipo kuuliza akaenda kutekeleza kazi yake. Wakati akienenda akawa anawasiliana na wenzake barabara juu ya wapi alipofikia.
Basi wakiwa wanafanya hilo na wakitaraji matunda ya kazi yao, hawakujua ya kwamba tayari walikuwa ndani ya mpango kabambe wa kumalizwa.
Watu wale, wauaji, ambao walikuwa wameongea nao kwenye mawasiliano walikuwa na vifaa bora kabisa vya mawasiliano. Kwa kupitia vifaa hivyo wakatambua makomandoo wale wapo pande gani ya dunia, na hata mipango ya kuwamaliza ikasukwa na sasa inatekelezwa.
Wanaume hao wauaji wakajigawa kwenda kila pande kuwazunguka makomandoo. Walikuwa wananyata kiasi cha kutokutoa sauti yoyote. Watu hawa walikuwa wataalamu haswa. Kila nyendo yao ilikuwa ni ‘professional’. mikononi mwao walikuwa wamebebelea bunduki na masikioni mwao walikuwa wamechomelea waya za mawasiliano.
Waya hizo zilikuwa hazionekani kwa haraka kwasababu ya barakoa walizokuwa wamezivaa. Ila ungetazama vema upande wa masikioni mpaka kinywani, basi ungepata kuziona.
Basi watu hawa wakiwa wananyata, wakawa wanazungumza kwa sauti ya kunong’ona. Na baada ya kama robo saa, wakawa tayari wamewazunguka walengwa wao. Lakini kwa namna walivyotenda kazi yao, hakuna komandoo hata mmoja aliyebaini hilo!
Hali ilikuwa tulivu sana. Baridi bado lilikuwa linatawala. Usiku huu ulikuwa mrefu sana. Na kabla haujakoma, wazi kulikuwa kuna mambo mengi yanakuja.
Mwanaume huyo alikuwa tayari kwenye eneo ambalo wenzao wameuawa. Aliiona miili yote ya wenzao ila hakuona watu wengine wa ziada. Miili hiyo ambayo tayari ilikuwa imeanza kuvutia wadudu, ilikuwa inatisha. Japo komando huyu alikuwa amefundwa kuzoeza mambo haya, hili jambo lilimsisimua.
Namna ambavyo miili ile ilikuwa imetifuliwa pasi na huruma kulimfanya akajita na hofu.
Mara akasikia sauti ya kitu kikitembea. Haraka akageuza uso wake kutazama. Hakuona jambo. Akawasha kurunzi kuangaza akiwa amekodoa macho haswa. Napo hakuona kitu. Ila pale alipotazama juu, mara akavamiwa na mtu mzito aliyemwangusha chini. Mtu huyo alikuwa amebebelea kisu chenye mpini mdogo na ncha ndefu.
Kwenye makali ya kisu hicho kulikuwa na mawimbimawimbi yaliyochongoka. Upande wake wa pili kulikuwa kumenyooka kisha kukajipindia kama upinde wa mshale kuelekea kwenye ncha. Kilikuwa ni kisu kizito na cha kutisha.
Yule mvamizi akajitahidi akitaka kumchoma komandoo kichwani. Komandoo akakidaka na kumzuiza. Wakapambania nguvu, mwishowe komandoo akamzidi na kumtupia kando kisha akanyanyuka upesi. Akatazama kando na kando kutafuta silaha yake, akaiona! Kabla hajainyanyua, kisu kikarushwa kwanguvu kumchoma mkono. Akalalama kwa maumivu makali!
Hajakaa vema, akakitwa teke la kifua na kujikuta chini kama kifusi. Hakukaa hapo, akachomoa kisu mkononi akiugulia maumivu, akakitupa kikaenda kombo, akasimama na kujipanga kwa ajili ya kupambana. Mkono wake wa kulia ulikuwa unamwaga damu, alikuwa anahisi maumivu makali sana, lakini hakuwa na wa kumdekea hapa la sivyo atatolewa uhai!
Basi yule bwana mwenye barakoa nyeusi akaguna kwa cheko. Akatazama mkono wa yule komando unaovuja damu kisha akatikisa kichwa chake akiigiza masikitiko. Alipokaa tenge, akamkaribisha komandoo aje kupambana.
Komandoo akatupa mitupo yake mizito, bwana yule akakwepa. Naye bwana yule alipotuma mashambulizi yake, komandoo ‘akazitoa’ kwa ustadi. Ila sasa shida ilikuwa ni mkono wake. Alikuwa anahisi maumivu makali. Kisu kilitoboa kabisa mkono wake na kutokezea upande wa pili.
Alijituma kukwepa, kukinga na hata kushambulia lakini kasi yake ilikuwa inazorota. Kuna muda pia alikuwa anashindwa kujikinga kwa mashambulizi ya upesi kwasababu alikuwa anahisi maumivu makali mkononi hivyo akawa anabaki ‘uchi’ mbele ya adui.
Na bwana yule, mwenye barakoa, akiwa ametambua udhaifu huo, akautumia ipasavyo na mwishowe akamdhibiti komandoo na kumlaza chini. Akamtwanga risasi tatu za kummalizia kabla hajauacha mwili hapo na kuondoka zake.
***
“Don’t fire!” sauti ya kunong’ona ilisikika kwenye vipokea sauti. “I think we need them.”
Wanaume hawa, saba kwa idadi, walikuwa wamelala chini wakifunikwa na majani yaliyojawa na umande. Hawakuwa wanaonekana kabisa kwa kumezwa na majani pia ukiongeza na rangi zao za nguo.
Macho yao yalikuwa yamezama kwenye tundu za hadubini za bunduki wakiwa tayari wameshawaweka walengwa wao kwenye rada kwa ajili ya shambulizi, na tayari walishawazingira makomandoo.
Basi baada ya amri ile kutoka, wakasimama na punde, “Hands up!” amri ikapazwa. Makomandoo kutazama, walikuwa wamezingirwa na watu saba kwa idadi. Kila pande ya dunia ilikuwa ina matundu ya bunduki!
Wakaamriwa watupie bunduki kando ya mbali na kisha walale chini upesi, wakatii! Wakafungwa kamba mikononi na safari ikaanza kwenda kule ufukweni kukuta boti yao wapate kwenda.
Wakatembea kwa muda wa dakika kadhaa, kama dakika kumi na hivi, wakafika fukweni. Huko wakawatweka makomandoo wale kwenye boti na kutaka kuondoka.
“There are still more!” akasema Wales punde baada ya kuwaona wale makomandoo wakiingizwa botini, na akaendelea kwa kusema kuwa watu hao bado watakuwa huko kisiwani, ndiyo waliokuwako kabla ya hawa wengine kufika.
“Those are more dangerous,” akatahadharisha akimtazama yule kamanda wa kikosi kilichokuja kumwokoa. “Worry out,” akasema kamanda kisha akauliza, “How many are they?” “Three!” akajibu Wales. Basi kamanda wa kile kikosi akateua watu wake sita na kurudi nao kisiwani kwenda kuwatafuta hao waliobakia, hivyo basi hapa botini wakabakia wawili, mbali na Wales wa tatu.
** “You go to this side! … you two go over that one!” alisema kamanda wa kikosi akiwagawa watu wake. Wawili wakaenda upande wa mashariki wa kisiwa, wawili wakaenda upande wa magharibi wa kisiwa na yeye pamoja na mmoja wakazama katikati ya kisiwa.
Msako ukaanza.
Wakati huo majira yalikuwa bado ni ya usiku. Mwezi ulikuwa unaangaza lakini kwa ufifu sana ndani ya kisiwa kwani miti iliyofungamana matawi yalikuwa yanazuia mwanga usipenye.
Hivyo kwa humu ndani, kulikuwa kuna kagiza katotoro, isipokuwa tu kwenye sehemu moja moja hapa na pale palipokuwa hapajazongwa na matawi magumu ya miti.
Wanaume wakasonga kwa tahadhari na huku wakijiweka kwenye mawasiliano. Kwa kama mwendo wa dakika kumi, wakawa bado hawajaambulia jambo. Kulikuwa patupu. Ni kiza na ndege, matawi na popo.
**
“How long will this take?” akuliza mwanaume mmoja aliyekuwa amevalia barakoa kule botini, akiwa ni miongoni mwa wale wawili walioachwa pamoja na Wales. Hata kwa sasa walikuwa wamevulia barakoa zao, ila tutawaita kwa majina hayo tupate kuwatambua vema.
“No one knows!” akajibu mwingine mwenye barakoa. Alikuwa amejegemeza akiwa anavuta sigara yake aliyoichoropoa kwenye droo moja ndani ya boti.
“You know we have to be at the bay before the dawn,” akasema tena yule mwanaume wa kwanza. Ni yeye ndiye alikuwa karibu na usukani wa boti, bila shaka ni dereva. “We must be on time, otherwise we may miss the plane.”
“I know that story, pal,” akajibu mwenzake. “But do you think we can do anything about this?”
“Perhaps there was no need to go back for the others. If we leave them here, they will just die! Was there a need?” akang’aka yule mwanaume karibu na usukani kisha akamtazama Wales aliyekuwa amelala chini kwa uchovu, akamuuliza, “was there?”
“Yes, it was,” akajibu Wales. “It is better we finish what we’ve started. If we leave these punks alive, I surely tell you they will come back knocking at our door.”
Alipomaliza kusema hayo, wakahisi boti inapepesuka. Wakatazamana pasipo kusema jambo. Pengine wakahisi ni pepo ama maji ya bahari. Ila hapana, boti ikapepesuka zaidi na zaidi! Mmoja akalazimika kwenda kutazama.
Ila alipoenda hakurejea ndani ya muda. Mwenzake, yule aliyekuwa karibu na usukani, akapata shaka. Kabla hajaenda kutazama huko nje, Wales akamsimamisha na kumwambia, “Be careful.”
Mwanaume yule hakujali sana, akaenda zake huko nje na kumfanya Wales akae tenge kuskiza nini kitakachotokea. Alitamani kwenda lakini majeraha aliyonayo yasingemruhusu kufanya hivyo. Alitega sikio pasi na kusikia jambo. Ikapita dakika moja, akaamua kuita.
Kimya.
Hapa akapata sababu ya kuwa na shaka. Akajikongoja kusimama aende huko nje. Mkononi alikuwa na bunduki ya kumlinda dhidi ya shambulizi. Kufika huko nje hakuona mtu! Akastaajabu. Kugeuka akajikuta amekitwa nyuma ya shingo, akadondoka chini kuzirai! Hakupata hata wasaa wa kumwona aliyemshambulia.
Alikuwa ni Miranda.
“Mpo sawa?” mwanamke huyo akawauliza wale makomandoo waliokuwako ndani wakiwa wamefungwa. Akawafungulia toka kwenye kamba kuwaweka huru.
“Wewe ni nani?” komandoo mmoja akauliza.
“Msijali, mtanijua. Siko mwenyewe.”
Baada ya muda mfupi, Lee naye akiwa ametokea upande wa pili wa boti, akajiri akiwa amelowana chepechepe kama ilivyokuwa kwa Miranda. Watu hawa ndiyo walikuwa wakiwavutia wale watu kwenye maji na kuwamaliza. Naye akajitambulisha kwa jina tu.
“Nanyi mlikuwapo kwenye ndege?” akauliza Komandoo.
“Ndio, tulikuwamo pamoja kwenye ndege kabla ya kuanguka,” akajibu Miranda.
“Vipi kuhusu mheshimiwa? Yupo wapi?” akauliza Komandoo.
Miranda akanywesha sura yake akisema, “Bahati mbaya alifariki safarini.”
“Vipi mwili wake? – upo wapi?”
“Msijali, upo. Utakuja hapa muda si mrefu bila shaka.”
Makomandoo wakatazamana na mmoja kuuliza, “Utakujaje na umesema amefariki?”
“Kuna mtu atauleta,” akajibu Miranda na kuongezea, “Kuna mwenzetu yupo huko nje. Yeye atakuja nao.”
“Anafanya nini huko?” Komandoo akaulizia.
“Anamalizia kazi kabla hatujandoka,” akasema Lee.
Lakini ilikuwa inaleta mantiki kwa Jona kuwapo huko nje? Pengine waweza kuona hii ilikuwa ni fursa adhimu kwake kujiondokea pamoja na wenzake baada ya kushikilia boti hii, ila kinyume na hapo yupo kule kisiwani! Msituni!
Atapambana na wanaume wale sita wenye silaha na ujuzi wa hali ya juu yeye mwenyewe?
Dakika nane nyuma …
“Nendeni,” alisema Jona baada ya kuchomoza nyuso zao toka kwenye maji, yeye pamoja na wenzake. Macho yao yaliyokuwa mekundu kwasababu ya kula chumvi ya bahari yalikuwa yanawashuhudia wanaume wale watano wakiwa wanazama msituni kisiwani kwenda kuwatafuta.
“Twende wapi?” akauliza Lee wakimtazama Jona.
“Nendeni kwenye boti,” Jona akasema. “Mimi nitarudi kule kisiwani kukabiliana nao.”
“Mwenyewe?” Miranda akadakia.
“Ndio, mwenyewe. Kuna haja gani ya kwenda wote kama kazi inaweza kufanyika na mmoja wetu?” Jona akasema akiwatazama wenzake kwa macho ya uhakika.
“Una uhakika?” akauliza Miranda. Uso wake ulikuwa na mashaka.
“Ndio, nina uhakika. Ikipita dakika arobaini na tano sijafika, basi nyie nendeni.”
“Hatuwezi kwenda tukakuacha, Jona,” aliteta Miranda kisha akamshika Jona mkono na kumwambia, “Please, be safe.”
“I will be safe,” akasema Jona na kabla mtu mwingine hajaongeza neno lingine, mwanaume huyo akazamia kwenye maji asionekane ameelekea upande upi wa dunia. Basi Miranda na Lee wakafanya kama vile walivyoambiwa, wao waende botini. Jona yeye ataenda kukabiliana na wale wanaume walioenda kule msituni mpaka arudi na kitambulisho, gate-pass (kama itakuwapo) na chombo cha mawasiliano alichobebelea yule mkuu wa kikosi kilichokuja kumwokoa Wales. Walijua mwanaume huyo alikuwa navyo kwani walishawafuatilia watu hao kwa muda fulani huko msituni. Yaani siri ilikuwa sirini. Wakati wanaume hao wakiwa wanajificha na kufanyia siri kwenye mashambulizi yao, na wao sirini walikuwa wanatazamwa ama kufuatwa! Kifuani mwa mwanaume yule aliyekuwa kamanda mkuu wa wenzake, kulikuwa kunaning’inia karatasi fulani iliyokuwa ‘laminated’. kwenye karatasi hiyo kulikuwa na picha ndogo na pembeni ya picha hiyo taarifa kadhaa. Ilikuwa ni jambo linaloleta maana masikioni kuona wakina Jona wanawinda namna ya mawasiliano ya mkuu huyu. Walijua watu hawa wametoka kutumwa na hivyo basi mawasiliano yao na makaoni huwa yenye nguvu na tija kuliko yale ya Wales. Walijua watu hawa watakuwa na cha ziada. Cha ziada ambacho kitawasaidia kuangusha ngome mbeleni.
Lakini wote twajua kuwa kupata vitu hivyo haitakuwa nyepesi. Tena ikifanywa na mtu mmoja ambaye silaha yake ni mikono pekee.
**
Alipochomoza toka kwenye maji alipanda haraka ardhini. Alikuwa kwenye ubavu wa magharibi wa kisiwa. Alitazama huku na kule kabla upesi hajakimbia na kuzamia kwenye miti.
Na basi akiwa amebeba tahadhari zote, akatazamia ardhi na kuona alichokuwa anakitaka baada ya hatua kadhaa, nacho si kingine bali alama za watu anaowatafuta. Majani yalikuwa yametawanyika mahali walipopita, na pengine ambapo hapakuwa na majani akaona nyayo za viatu.
Akafuatilia kwa muda wa dakika sita. Akajibana kwenye kwenye mti baada ya kusikia sauti ya wanaume wakiongea. Aliporusha macho yake, akaona watu wawili. Ni wale ambao walipewa kukagua upande wa magharibi.
Akaendelea kunyata kuwajongea. Ilikuwa ni hatari kwake kuwaonyesha alipo mapema maana walikuwa na silaha za moto, wangeweza kuzitumia kummaliza kabla hajatimiza adhma yake.
Basi alipoona sasa amekaribia vya kutosha, akanyanyua tawi moja la mti lililo kavu, lakini kabla hajamaliza kunyanyuka, tawi lile likameguka kuvunjika! Likatoa sauti iliyowashtua wanaume wale na kuangazia upande huo upesi!
Jona akatulia tuli nyuma ya mti akihema taratibu. Wanaume wale wakatazama eneo hilo kwa sekunde kadhaa. Na wasipuuzie jambo, wakatazamana na kupeana ishara ya kwenda kutazama kupata uhakiki. Taratibu wakajongea, ila ghafla wakasikia sauti ya kitu upande wao wa kushoto. Haraka wakageukia huko!
Kutazama wakaona ni kipande cha tawi la mti. Kilikuwa ni kipande ambacho Jona amekirusha. Kabla hawajarejewa na akili, Jona akawa ameshawafikia. Kurejesha nyuso zao kule walipokuwa wanaelekea, bunduki zikakamatwa na kuviringitwa duara kamili, mikono yao ikachina, sasa haraka silaha hizo zikavutwa pasipo kipingamizi.
Hawajakaa vema, silaha zao zikatumika kuwabondea vichwa na kuwaangusha chini wakiwa hawana fahamu. Jona akachojoa vyombo vyao vya mawasiliano na kuzihifadhi silaha zao kwa ajili ya matumizi ya baadae.
“ … thirteen … fourteen … Fifteen!” alisema Jona kisha akapiga ngumi kiganjani mwake. Mpaka muda huo alikuwa ametumia robo saa. Hivyo ana nusu saa tu kutimia dakika arobaini na tano za kumaliza kazi yake. Muda ambao amewaambia wenzake kuwa ukifika na bado hajarudi, basi wawashe boti kwenda zao.
** “Sure? … ok, we’re coming!” alisema yule kamanda mkuu wa kikosi kisha akamtazama mwenzake aliyekuwa anashirikiana naye kwenye ukaguzi wa kisiwa eneo la katikati. “They’ve got them in the West!” akamwambia kisha akawasiliana na wale wengine wa upande wa Mashariki kuwa hawana haja ya kuendelea kusaka kwani watu wao wamepatikana.
Basi wakaanza funga safari kuelekea kule upande wa magharibi. Walikuwa wanatembea kasi wakiwasiliana. Baada ya dakika kama kumi na moja, wakawa wamefika upande huo wa magharibi wakiwa wote wanne.
“Hey, where exactly are you?” akauliza kamanda mkuu. Punde akajibiwa, akawatazama wenzake na kuwapa ishara ya kichwa kuwataka wasonge mbele zaidi. Wakasonga kwa dakika mbili. Ila ghafla kamanda akawataka wasimame kwani alihisi kitu! Wote wakasimama!
Kwa utulivu mkubwa akaskiza. Macho yake yalienda kushoto na kulia. Juu na chini. Hamaki! Akatokea Jona mbele yao toka nyuma ya mti mkubwa uliopo hatua nane tangu walipo.
Mwanaume huyo alikuwa amebebelea bunduki kwenye mikono yake yote miwili na tayari tunduze ameshawaelekezea maadui. Basi kamanda kuona vivyo, kabla Jona hajabinya vitufe vya bunduki, upesi mno akamkamata mmoja wa wenzake na kumweka mbele yake kujikinga.
Basi risasi zikanyesha haswa!! Ilikuwa ni ti!-ti!-ti!-ti!-ti!-ti!-ti!-ti! Wanaume wale wakizungu wote wakala za kutosha isipokuwa yule kamanda mkuu ambaye akiwa amejikinga, akawa anasonga kumfuata Jona.
Aliposonga karibu kidogo, akamrushia Jona mtu yule aliyekuwa anamkingia. Jona kumkwepa mtu huyo na kukaa vema, kamanda akawa ameshamfikia akatengulia bunduki zake kando. Akachomoa bunduki yake ndogo, ila Jona naye akawahi mkono wake na kuutengua, bunduki ikadondokea chini. Sasa wote wakawa hawana bunduki mikononi.
Wakatupiana mikono, ila wote wakafanya ustadi kujilinda. Wakakaa tenge kutazamana kana kwamba majogoo. Kamanda akauliza, “So you are the dangerous one?”
Jona hakujibu akamvamia. Alikuwa hana muda. Alikuwa anakimbizana na muda na mpaka muda huo alikuwa amebakiza dakika kumi na mbili tu.
Wakatupiana makonde ya nguvu. Wote walikuwa wana nguvu za kupambana na ustadi wa aina yake. Ilikuwa ni mapambano ya mafahali wawili ambayo yaliumiza majani. Waliparangana kwa muda wa dakika kadhaa asionekane nani aliye mwamba. Wakasimama tena kutazamana.
“Anything left?” akauliza yule kamanda. Jona akatazamia muda. Sasa amebaki na dakika tano tu! Akapiga kelele kwanguvu na kumvamia kamanda kwa mashambulizi makali.
Kamanda akajizuiza, akatupa pia na yake, Jona akajikinga na upesi akambana kamanda miguu kumwangusha chini. Kabla kamanda hajafurukuta, Jona akawahi kunyanyua silaha na kumtwanga nayo risasi tatu kifuani! Kamanda akaenda na ubabe wake.
Jona akamkagua na kuchukua kila alichokiona kinastahili alafu akaanza kukimbia kwenda kuikuta boti waliyomo wenzake.
Kupiga hatua mbili, akadakwa mguu na kuanguka chini. Kumbe kulikuwa na adui mmoja aliyebakia na uhai. Aling’ang’ania mguu wa Jona na upesi akavuta silaha yake iliyokuwa pembeni apate kumuua, ila Jona kwa haraka akatumia mguu wake uliokuwa huru, akatengua mkono wa adui uliobebelea bunduki na kisha akammaliza mtu huyo kwa kummiminia risasi nne za uhakika.
Akanyanyuka na kuendelea kukimbia kwa kasi. Sasa alikuwa amebakiza dakika mbili tu kwenye muda wake. Hakutazama nyuma wala pembeni bali mbele aelekeapo!
**
“Tuondoke,” alisema Lee akimtazama Miranda aliyekuwa anaangalia msitu wa kisiwa.
“Hapana,” Miranda akatikisa kichwa. “Hatuwezi kuondoka tukamwacha.”
“Alisema ikifika daki ya arobaini na tano twende kama atakuwa hajafika,” Lee akakumbushia. Japo uso wake nao ulikuwa na huzuni kuyasema haya.
“Najua alisema hivyo, ila hatutaondoka pasipo yeye,” Miranda akasisitizia. Muda si mrefu macho yake yakaanza kujawa na machozi. Jicho lake la kushoto likadondosha maji.
“Najua atarudi,” akasema kwa sauti ya chini. Alikuwa anatazama miti kama vile mtu asomaye ramani. “Najua hatafia huko … atarudi tu.” akamtazama Lee na kumwambia, “Atarudi, si ndio?”
Lee akashusha pumzi ndefu. Akatazama saa ya mkono wake, ilikuwa ni dakika ya sitini sasa na Jona hajaonekana. Akakosa cha kusema.
“Atarudi, si ndio?” Miranda akauliza tena akiwa ameng’ata meno. “Na kama hatorudi, basi hapahapa nitawangoja waliomuua na kuwaadhibu.”
Wakakumbatiana Miranda akiegamisha kichwa chake kwenye bega la Lee. Machozi yaliendelea kumtoka. Hakuwa anataka kuamini kwamba msitu ule umemmeza Jona.
Basi punde wakiwa vivyo wamekumbatiana, wakasikia sauti, “Heey!”
Miranda akasema, “ni Jona!” akaangaza kule msituni na akamwona mwanaume akiwa anakuja akikimbia, mikononi mwake alikuwa amebebelea mwili wa Raisi. Akamtazama Lee kwa furaha kubwa na kumwambia tena. “Ni Jonaa!”
Basi wakaruka na kwenda kumlaki, Lee akapokea mwili wa Raisi na kuutanguliza botini. Miranda akafurahi sana kumwona Jona, hata akambusu mwanaume huyo shavuni na kumwambia, “Nilijua utarudi tu,” akasema akiwa na tabasamu pana. Akamkumbatia tena Jona kabla hawajakwenda botini.
“Umepata kitu?” Lee akamuuliza.
“Nimepata kila kitu,” Jona akajibu. “Sasa ni muda wa kwenda kumaliza kazi.”
Basi wakatia moto boti na kuondoka zao. Wakiwa njiani Jona akawasiliana na makao makuu na taarifa ikawa ni kwenda kwenye ‘bay’ kama ilivyokuwa awali. Huko watakutana na ‘helicopter’ ya kuwachukua na kuwarejesha makaoni.
Basi safari yao ikadumu kwa mwendo wa saa moja na nusu mpaka kufika ‘bay’ ya barafu kuu. Hapo kulikuwa na wanaume wawili ndani ya helicopter ambao walikuwa wanawangoja.
Basi kwakuwa haikutakiwa wanaume hao wagundue mapema kuwa si wenyewe waliokuja hapo, wakawataarifu kwa njia ya mawasiliano kuwa kuna majeruhi wa kuja kuwasaidia kuwabeba, hivyo waje kuwapatia mkono.
Wanaume wale wakashuka pasi na hiyana na kusonga kwenye boti. Tena walikuwa hawana hata silaha mikononi mwao. Wakajikuta wakiwekwa chini ya ulinzi na kuamriwa waanike mikono yao juu upesi! Kwa woga wakatii amri. Lee na Miranda wakawaswaga kwenda kwenye helicopter wakimwacha Jona peke yake na wale makomandoo.
“Nadhani sasa mtarudi nyumbani kupeleka mwili wa mheshimiwa. Sisi tunaenda England kumaliza mzizi wa yote haya,” Jona aliwaambia wale makomandoo, watatu kwa idadi, watano wakiwa waliuawa kule msituni.
“Tumekubaliana ataenda huko mmoja, na sisi wawili tutaongozana na nyinyi kwenda huko kupambana,” akasema yule kamanda wa kile kikosi cha makomandoo.
Basi kwakuwa tayari ndege yao iliyokuwa inawasiliana nayo ilikuwa njiani, wakawasiliana nayo kuwaelekeza walipo, kisha walipofanya hivyo makomandoo wawili wakaondoka na wakina Jona wakitumia ile helicopter waliyoiteka. Wakadaka anga kwenda kuwatafuta na kuwamaliza washenzi.
**
Saa tano asubuhi …
Baada ya mlango kufunguka, walitangulia wanaume wawili ambao ni wale waliokuwa madereva wa ile helicopter iliyotekwa. Wanaume hawa wazee waliokuwa wamevalia makoti meusi ya ngozi na jeans zilikoza kwa rangi ya bluu, walikuwa wamenyoosha mikono juu na nyuso zao zikiwa zimejawa na hofu.
Nyuma yao alikuwapo Jona na wenzake, Miranda, Lee na Makomandoo wawili. Basi wakaketi na Jona akawauliza wale mateka juu ya taarifa zao. Wakajitambulisha kuwa ni madereva waliokodiwa kwa ajili ya usafirishaji. Hakuna kingine wanachokijua.
Jona na wenzake wakafanya msako ndani ya makazi ya wanaume hao na wakabahatika kupata nyaraka na picha kadhaa ambazo zilithibitisha kuwa mateka walitoa taarifa za uongo. Walikuwa ni miongoni mwa wafanyakazi wa taasisi ya siri ya Uingereza, ila kwenye kitengo cha usafirishaji.
“So you were lying, unh?” Jona akamnyooshea mmoja wao tundu la bunduki kichwani. “So choose one, to speak or die?”
Mwanaume huyo akatetemeka kwa hofu. Jasho likamchuruza. Akabanwa na kigugumizi asijue nini aseme.
“I’m gonna count up to five seconds!” Jona akafoka kisha akafungua bunduki yake na kutoa risasi nne, akabakiza risasi moja tu ndani ya bunduki alafu akaifunga na kumwekea mateka wake kichwani.
“One …” Jona akahesabu kisha akafyatua kitufe cha bunduki. Bunduki ikalia kak! Kumaanisha imekosa risasi.
“Two …” akahesabu tena na kufyatua kitufe cha bunduki, bunduki ikalia kak! Kumaanisha imekosa tena tundu la risasi.
“Three! …” akahesabu tena na kufyatua kitufe. Tena, kak! Bunduki ikalalamika kwa kukosa risasi! Hapo mwanaume yule mateka akawa amelowana jasho ndembendembe. Alikuwa kwenye vuli la umauti. Pengine kwenye wakati mgumu zaidi tangu aingie duniani.
Jona aliposema “Four! …” kabla hajafyatua, mateka akapiga kelele, “I’ll speak! … damn! I’ll speak!”
Jona akafungua bunduki na kutazama, tundu lenye risasi ndilo lilikuwa limekaa tenge. Kwahiyo endapo angebonyeza kitufe basi mateka yule alikuwa anapasuliwa ubongo na kulazwa mfu!
“Okay, one after another,” akasema Jona akiketi. “Tell us about your boss.”
Mateka akamtazama na kumuuliza, “What do you want to know about him?”
“Important things,” akajibu Jona. “Let’s start with where he lives, where he likes to go and what he likes to do.”
Basi mateka akasema kila alichoulizwa, kwa ufasaha na kwa uoga. Ofisi za bosi ziko wapi, makazi yake yapo wapi na viwanja anavyopenda kutembelea. Pia pasipo kusahau nini huwa anapendelea kufanya.
Sasa Jona na wenzake wakawa wana kazi ya kuanza kusuka mipango ya kutekeleza na kumaliza. Ila Lee akapata wazo, akaita,
“Jona,” na kisha akasema kwa uhakika, “nadhani kuna mtu tunamhitaji kuturahisishia kazi yetu.”
“Nani huyo?” Jona akauliza.
“Mwanamke mmoja aitwa Glady,” Lee akajibu akimtazama Jona machoni.
“Glady? Ni nani huyo na atatufaa vipi?”
Lee akachukua zamu kueleza ni kwa namna gani Glady anaweza kuitenda kazi kwa kutumia kaliba yake ya kujiuza na kujua kushawishi, Jona akavutiwa na maelezo hayo, ila kwa namna gani Glady atakuja kuwakuta na pesa hata ya kumsafirisha hawana?
“Usijali,” akasema Lee. “Nitamwelekeza Marwa aliyekuwepo nyumbani nini afanye na pesa atazipata. Zipo nyingi sana chini ya akaunti yangu na hata ya Sheng mwenyewe.”
Wakakubaliana na Lee akafanya mpango wa kuwasiliana na Glady kwenye mtandao wa whatsapp. Kheri alikuwa anakumbuka namba ya mwanamke huyo. Alimpata ndani ya muda mfupi na akamweleza haja ya moyo wake. Jambo hilo likamshangaza na kumtisha Glady, ila akapata uthubutu baada ya kuambiwa kauli hii na Lee:
“Nitakupa pesa unayotaka.”
Akajichekesha na kuridhia dili hilo ambalo mbele ya macho yake lilionekana ni nono haswa. Uzuri alikuwa ana passport na kuhusu visa Lee akamwambia afike ubalozini, kuna mtu wake pale atakayempanga kufanikisha hilo ndani ya muda mfupi.
Wakaelewana kila kitu na ikawa ndani ya mipango kuwa Glady atafika Uingereza keshokutwa kama mambo yakienda vile yanavyotakiwa.
Basi baada ya hapo, Jona na wenzake wakaona ni vema wakienda kutembelea jiji la London na hata basi watakapopata fursa waende na kuyaona na yale maeneo ambayo wale mateka wao wamewaeleza.
Ndani ya muda mfupi wakawa wamejiandaa. Wakawafungia wale mateka wao ndani ya chumba na kisha wakaondoka kwenda kubarizi jiji. Wakafanya vivyo ndani ya masaa matatu, walipomaliza kutalii huko wakaanza kupitia eneo moja baada ya lingine ya yale waliyopewa taarifa nazo. Uzuri Lee alikuwa msanifu mzuri kwenye uchoraji, akachora kila linalotakiwa, haswa muonekano wa majengo, njia na hata vituo.
Kwahiyo kwenye majira ya jioni ndipo walirejea kwenye makazi yao, ya wale wakazi waliowateka, wakiwa wamefanya kila linalotakiwa. Ila walipofika walikuta mazingira tofauti, na jambo hili kidogo likawazusha shaka.
Mosi, walikuta mlango u wazi. Pia walipotazama eneo walipowahifadhi wale mateka wao, hawakuwakuta! Zilibakia kamba tupu pasipo cha kufungia. Swala hili likawafanya damu zao zianze kuchemka!
Kulikuwa na nyayo kadhaa za viatu kwenye zulia. Kwa harakaharaka nyayo hizo zilikuwa za watu watatu. Ina maana ndiyo hao waliokuja kuwakomboa mateka!
Hawajakaa vema risasi zikaanza kurushwa kupasua vioo vya dirisha! Haraka Jona na wenzake wakalala chini. Risasi zikaendelea kutupwa kuchafua na kuharibu kabisa jengo. Zilikuwa ni risasi za mfululizo na nyingi!
Watu waliokuwa wanashambulia walikuwa watano. Wanaume watatu na wanawake wawili. Wanaume walikuwa wamevalia makoti marefu rangi ya kaki, pengine ni sababu ya mvua za hapa na pale na baridi. Wanawake walikuwa wamevalia makoti ya ngozi yaliyobana miili yao na kufanya waendane na fasheni na kwa wakati huohuo kujiweka salama dhidi ya baridi.
Nyusoni walikuwa wamevalia miwani meusi, ilikuwa ajabu ukitazama na muda huu wa giza. Labda, tuseme labda, miwani hizi hazikuwa za jua kama tujuavyo tuonapo kila miwani meusi.
Basi mashambulizi yakaendelea kwa fujo. Ilikuwa ni kitu cha kushangaza maana Jona na wenzake hawakuwa wamkitarajia hili kwa ghafla hivi. Hawakudhani pengine vita ingeanza mapema kiasi hiki.
Sasa maadui watakuwa wanajua kuhusu ujio wao, si ndiyo hivyo? Na pengine pia washajua kuwa wale makamanda wao waliowatuma tayari wameshauawa.
Ndio, hilo lilikuwa bayana. Kumbe muda mfupi baada ya wao kuondoka, watu hawa wa kazi walifika kwenye makazi ya hawa madereva kwa ajili ya kukusanya taarifa toka kwao baada ya ukimya wa ajabu tangu watumwe. Ukimya pia kwa wale makamanda ambao hawakuwa wanapatikana hewani kwa ajili ya mawasiliano.
Walichokikuta ni madereva hao wakiwa kambani na wakiwa tayari wametoa taarifa nyeti. Haraka wakapasha habari kule makao makuu na agizo likatolewa kwamba watu hao wamalizwe haraka kabla haijaleta kizazaa ndani ya nchi.
Kumbuka taasisi hii ni ya siri. Hata waingereza wenyewe hawakuwa wanafahamu juu ya uwepo wake isipokuwa kwa watu kadhaa nyeti, tena wachache. Na ilitakiwa kuwa hivyo milele na milele, aamin.
“Fuata silaha!” akapaza Jona. Kulikuwa kuna kelele sana. Risasi zilizokuwa zinapasuapasua madirisha zilifanya usikizani uwe hafifu. Ilibidi umtazame mtu anayeongea mdomoni ujue anasema nini au basi mpeane ishara.
Taratibu wakasonga kwenda vyumbani. Kila mmoja na alipoweka silaha yake akachukua na kuziweka vema kwa ajili ya kujikomboa. Sasa wakaanza kupekua huku na kule kuangazia maadui zao wapo pande gani.
“Wawili wapo upande wa mashariki …” akasema Komandoo mmoja, Blanko kwa jina la vitani. Mwingine naye, Chombo, akasema kuna wawili upande wake wa magharibi. Jona akamalizia kwa kusema kuna mmoja upande wa kaskazini. Basi baada ya jitihada hizo za kufahamu walipo maadui zao kufanikiwa, japo ilikuwa ni tabu wakipunyuliwa na ncha za risasi madirishani, wakagawana majukumu ya kuwashuhulikia. Makomandoo wawili, Chombo na Tito, wakapewa shavu la upande wa magharibi. Blanko na Miranda wakapewa upande wa mashariki na Lee akapewa upande wa Kaskazini.
Jona yeye akabaki kuwa ‘free roller’ kazi yake ikiwa ni kuangazia na hata itakapobidi kwenda nje kuangalia kama kuna wengine na kupambana nao!
Basi mashambulizi ya kutupiana risasi yakadumu kwa muda wa dakika sita. Wakafanikiwa kuwaangusha maadui watatu na kuwabakiza wanaume wawili tu. Ila hao wawili wakiwa wamefahamu kuwa wamezidiwa na mipango ya kimashambulizi, wakajificha, na basi wakawa wanatupa risasi zao kwa kutegea.
Wakitupa mbili tatu, wanajiziba ama kuinama kusikizia majibu yaliyokuwa yanakuja kwa mkupuo.
“We need backup!” alisema mmoja. Walikuwa wameweka migongo yao nyuma ya kuta wakihema kana kwamba wametoka mbio.
“We are outnumbered! We need damn backup!” akafoka. Mwenzake akamtazama na kumwambia, “we need to go, not backup! Police are going to be here soon!”
Hawajakaa vema, wakasikia king’ora cha polisi. Sasa wakaanza kutazamia nafasi watoroke kabla hawajatiwa nguvuni. Haikutakiwa kujulikana kama ni wao ndiyo walihusika na hilo tukio. Na hata kama wakikamatwa basi watajieleza kuwa wao ni majambazi na si wahusika wa taasisi yao ya siri.
Walipotazama na kuona mazingira ni sawia, mmoja akachoropoka upesi akimwacha mwenzake nyuma. Mwenzake naye akatazamia usalama, mara naye akachopoka, ila alipokata kona akifuata upande ule alipokimbilia mwenzake, akastaajabu kumkuta mwenziwe chini!
Hajakaa, mara akajihisi hana nguvu! Akajihisi analegea. Akadondoka chini asielewe kitu. Alikuwa gizani. Sauti ya king’ora cha polisi ilififia masikioni mwake na hatimaye ikakoma kabisa. Punde Jona akamsachi na haraka akatokomea hapo.
**
Saa tatu usiku …
“We failed!” alifikisha taarifa mwanamke mwenye kibandiko cha upanga, yaani Sword., kifuani Alikuwa amesimama kwa ukakamavu akimtazama mkuu wao aliyekuwa amekaa vema kwenye kiti chake akiwa ameziba mdomo wake kwa kiganja chake kipana.
“You failed,” mkuu akarejea kusema kauli hiyo kisha akatabasamu. “They’ve killed all our commanders. Kidnapped our drivers and got almost all information … Moreover, they are on our playground, at our home! … and you come here to tell me about failure!”
Mkuu akabamiza ngumi mezani. Akasimama na kumkwida mwanamama aliyemletea taarifa, akamsogeza karibu na uso wake uliokuwa umegeuka kuwa mwekundu.
“Don’t tell me that shit, okay? I am not used to failure, my dear. And don’t make me be, my dear. Got me?”
“Yes, sir!”
Mkuu akamsukumiza mwanadada huyo kando na kumfokea akimyooshea kidole.
“I want them within reasonable time! Nobody can hide in this country as far as I know it like the palm of my hand! … And when you get them, bring them here to face me.”
“Yes, sir!”
Mwanamama akageuza mgongo wake kuufuata mlango. Mkuu akatoa agizo la mwisho. “Don’t return here with empty hands as I shall kill you with my bare hands, my dear.”
Mwanamama akalipokea agizo na kwenda zake. Akakusanya kikosi cha wapambanaji kumi na wawili, na kabla hajatoka makaoni wakaingilia mifumo yote ya kamera zilizo mitaani na za utambulisho wa watu mahotelini. Hivyo punde watakapoona nyuso za walengwa wao zifanyiwe kazi haraka iwezekanavyo. Jambo hilo halikuwawia ugumu kwani nyuso za Jona na wenzake zilikusanywa upesi baada ya kufanya utaalamu wao wakizitoa kwenye kamera zilizokuwa zimefungwa kwenye nyumba za wale madereva waliotekwa.
**
Na basi sasa kazi inakuwa rahisi na pengine kabla ya jua kuchomoza kila jambo linaweza likawa limekamilika.
Kwakuwa kumi na wawili ni watu wengi sana, kiongozi wao akaona si busara wakiongozana pamoja hivyo wagawane ipate kuwa rahisi kufanya kazi. Endapo taarifa zitakapotoka kuwa walengwa wapo upande fulani, basi waliopo karibu watafanya hiyo kazi wakati msaada zaidi ukiwa njiani waja.
Kila kitu kikawa chema. Ni taarifa tu ndiyo ilikuwa inangojewa hapa na si kinginewe. Muda ukasonga mpaka majira ya saa kumi na mbili hivi ndipo mtandao ukatoa taarifa kuwa walengwa wamepatikana!
Tiiiii! Tiiiii! Tiiiiii! Tarakilishi ya yule jamaa aliyebakizwa makaoni kwa ajili ya kuendesha mitambo ililia. Alikuwa anasinziasinzia. Alikurupushwa na alarm hiyo akarusha macho yake kwenye kioo.
Akaona jina ni Queenland Hotel. Nyuso ambazo zilikuwa zimetunzwa kwenye ghala ya tarakilishi yake zilifanana kwa asilimia tisini na nane na zile ambazo zimeonekana kwenye hoteli ya Queenland!
Akanyanyua simu ya mezani na kumpasha habari mkuu wa kikosi kilichopo huko mtaani pasipo kujali ukubwa wa usiku. Akamweleza bayana kuwa waelekee Queenland na watapata wanachokitaka.
Basi taarifa ikapokelewa na kutumwa tena kwa watu wanne waliokuwa karibu na ilipo hoteli hiyo. Waende huko upesi na wenzao wapo njiani kuwafuata.
Watu hao wanne, wawili majibaba na wawili wakiwa ni wadada, wakaenda mara moja kutekeleza agizo. Walikuwa ndani ya gari aina ya BMW x6 nyeusi ambayo vioo vyake vilikuwa vimefungwa kuwa giza.
Gari likaenda kwa kasi, na lilipofika kwenye uwanja wa hoteli hiyo, kabla ya kushuka watu hawa wakafungia bunduki zao vyuma vya kupunguzia sauti, alafu wakahakikisha mifumo yao ya mawasiliano ipo sawia.
**
“Nimekipenda!” alisema Komandoo Chombo akitazama kuangaza chumba walichotoka kuingia muda si mrefu. Kilikuwa ni chumba kipana kilichokuwa na rangi mbalimbali za kuvutia. Taa kubwa na ya urembo ikining’inia na madirisha mawili ambayo yana mwonekano mzuri wa maghorofa mengine yaanayopakana nayo. Mbali na hapo kuna bafu pana lenye kila aina ya huduma.
Ama kwa hakika vilikuwa vinavutia machoni na viliendana haswa na gharama zake. Wanaume hawa watatu, Komandoo Chombo, Tito na Blanko, wote kwa pamoja walivutiwa nacho.
Wakawa wanaendelea kupekua, isipokuwa Chombo yeye akawa amejitupia kitandani alipopokelewa na godoro laini kubwa lililomhakikishia mapumziko ya furaha.
Muda si mrefu, hodi ikagongwa. Kwakuwa wengine, yaani Tito na Blanko, hawakuwapo mazingira ya karibu, Tito alikuwa bafuni na Blanko akiwa ameenda mpaka kwa nje kuangalia mazingira, Chombo ikampasa kuitikia hodi hiyo.
Akanyanyuka kivivu kujongelea mlango. Alipofika akauliza kabla hajafungua,
“Who’s it?”
Akaitikiwa ni mhudumu. Basi akafungua na kuangaza. Akakutana na mwanadada mrembo aliyekuwa amevalia sare. Mkononi alikuwa amebeba trey ya mvinyo na glasi zake nne.
“Are you alone?” akamuuliza akiwa anatazama huku na kule. Chombo akatabasamu kidogo na kusema. “No. I am wrih my friends!”
Mhudumu akatabasamu na kusema, “Oh! It’s sweeter when it’s shared.” kisha akaenda zake kuufuata mlango Chombo akimtazama. Alikuwa anatembea kwa madaha kiasi cha kuvutia kumtazama, achilia mbali urembo wake maridadi.
“Anything else, Mr.?” akauliza mhudumu akiwa ameshikilia mlango.
“No! … Nothing,” akajibu Chombo kwa sauti ya kutokumaanisha.
“Ok, I will be here so soon to take leftovers,” akaaga mhudumu kwa namna hiyo, na Chombo akamsindikiza kwa macho malaini kabla hajaufunga mlangowe kisha akarudi na kuungana na wenzake ambao walikuwa tayari wameshatoka huko walipokuwa.
“Jamani kuna mambo yenu hapo,” akasema akionyeshea ule mvinyo ulioletwa na mhudumu.
“Oooh!” akadakia Tito. “Ila nimekuona ulivyokuwa unamtazama yule mhudumu!” akatania wakacheka. Na basi kwakuwa mhudumu alisema kuwa atakuja kuchukua mabaki muda si mrefu, wanaume hawa hawakukawia wakabwia kinywaji na kuacha chupa i nyeupe ndani ya sekunde kadhaa tu.
Vinywa na makoo yao yalikuwa yamezoea vinywaji vikali. Hii ‘wine’ ilikuwa ni kama sharubati tu. Hata glasi hawakutumia bali waligida kwa mtindo wa tarumbeta.
Ila walipomaliza walijikuta wakihisi vichwa ni vizito sana. Hawakuweza kudumu tena, wakajilaza kana kwamba ng’ombe waliokuwa hoi kwa kulimishwa siku nzima.
Lakini mabwana hawa, mbona si kujiuliza kuletewa kinywaji hicho muda kama huo wa usiku mnene? Pengine imani yao ilikuwa kubwa. Ama tuseme kiu za makoo yao zilizidi uwezo wa wa kufikiria.
**
Akiwa bafuni, anasikia hodi. Miranda anazima bomba lake la maji na kuskiza vema kama kweli akisikiacho ndicho. Ni kweli. Alijiuliza kidogo kabla hajavuta taulo lake akajifuta uso na kulikaza vema kifuani.
“Comiiiing!”
Akatoka kwenda mlangoni. Kabla hajafungua, akachungulia kwanza na kumwona mwanamke aliyevalia sare za wahudumu. Mkononi mwake alikuwa amebebelea trey lenye mvinyo mwekundu pamoja na glasi mbili.
“You’re welcome!”
“Thanks. Sorry for my disturbance.”
“Never mind.”
“Mam, it’s my pleasure to serve you with the finest and royal wine in the country. Hope you are going to enjoy it the same to your stay in our hotel.”
“Thanks,” akasema Miranda akitabasamu kinafki. Mhudumu akazama ndani na kwenda moja kwa moja kwenye meza alipoweka mvinyo aliouleta na kisha akaaga.
“I will be back soon to take leftovers.”
Miranda asijali sana, akarudishia mlango na kurudi bafuni kumalizia zoezi lake. Lakini mhudumu yule, ambaye ndiye yuleyule aliyewapa wale makomandoo mvinyo, hakuwa amekomea kwake.
Sasa akiwa amebebelea mvinyo mmoja wa mwisho akaelekea chumba kilichokuwa kimewahifadhi Jona na Lee. Mvinyo huo mmoja ulikuwa unasindikizwa na glasi mbili pia pembezoni. Kama kawaida akagonga na muda si mrefu akafunguliwa.
“Hey!” alikuwa ni Lee. Kiunoni alikuwa amefungia taulo. Na kabla hajafungua alihakikisha kwanza mhudumu huyo yupo peke yake kwa kuchungulia.
Mhudumu akaomba samahani na kuteta haja yake, amekuja kuwaletea mvinyo bora kabisa. Basi pasi na hiyana, Lee akamkaribisha azame ndani. Mhudumu huo akiwa anatembea kwa maringo, akaingia na kunyookea meza.
Kitandani Jona alikuwa amelala ila si usingizi. Alikuwa anahisi uchovu na pengine isingezidi dakika tano angekuwa ameshapitiwa na usingizi. Hata hivyo kitu pekee kilichomfanya akadumu kwa muda akiwa amcho, ni kumngoja Lee atoke bafuni naye ajimwagie maji.
Basi macho yake yakiwa bado ni mazima, yakamtazama yule mhudumu. Kichwani akajiuliza maswali kadhaa haswa la kuletewa mvinyo wakati ule. Ila akili yake ilikuwa imechoka, zembe kwa muda huo. Hakujali sana. Labda wanataka wateja wao walale unono, akawaza kaupumbavu.
Ila wakati mhudumu anaweka mvinyo mezani, Jona akaona jambo lililompatia shaka. Alidhani pengine ni macho yake ila la hasha, alikuwa sahihi! Kwenye nyonga ya kulia ya mhudumu kulikuwa na bunduki!
Bunduki hiyo ilikuwa imezibwa na sketi ya sare. Ni kuinama kwa mhudumu ndipo kulifanya silaha hiyo ihakisiwe tena endapo kama ungetazama kwa umakini.
Mhudumu akamtazama Jona na kutabasamu, kisha akaanza safari yake ya kimadaha kwenda mlangoni.
Kwa namna alivyokuwa anatembea na namna anavyovutia, mwanaume ungepata wapi wasaa wa kumdhania mwanamke huyu ni hatari? Macho yako yote yangekulevya kufaidi uumbwaji wa Mungu uje kutambua unamalizwa ukiwa unakufa!
Akiwa amebakiza hatua tatu kuufikia mlango, sauti ya kiume ikakoroma, “Please, stop!”
Akasimama.
Akasikia Jona akitoka kitandani na kusimama, basi akaanza kujongesha mkono wake kwenda kwenye silaha. Huenda mambo yamebuma.
Jona akasonga na akasimama hatua mbili nyuma yake. Mwanaume huyo alikuwa amevalia suruali pekee. Macho yake yaliyokuwa na uchovu sasa yalikuwa yanatazama kwa mashaka.
“Who are you?” Jona akauliza.
“I am the waitress!” akajibu mhudumu. Hakuwa amegeuka. Alikuwa anatazama mbele kuangazia mlango. Pale mlangoni alikuwa amesimama Lee, bado hajajua kinachoendelea hapa uzuri.
“Why do you bring wine at this time?” Jona akauliza kwa sauti ya amri.
“It’s our schedule,” akajibu mhudumu, alafu akageuka kumtazama Jona. Bado mkono wake ulikuwa karibu na nyonga yenye silaha.
“Can you please taste it for us?” Jona akaomba. Mhudumu akatabasamu na kuuliza, “Why? You think we want to kill our clients?”
“Maybe!” Jona akajibu akipandisha bega la kulia. “You never know.”
Hapa mhudumu akamtazama Jona machoni, wakatazamana kwa sekunde nne pasipo kufanya jambo.
“Okay!” Mhudumu akabinua mdomo. “I will do what you wish.” kisha akasogelea mvinyo na kumiminia kwenye glasi.
**
Kabla hajautia kinywani, akasita. Akamtazama kwanza Jona na kisha Lee. Nyuso za wanaume hao tayari zilikuwa zimebeba shaka. Mambo hayakuwa sawa.
Basi mhudumu huyu akapeleka glasi kinywani, ila kabla hajafyonza, akachomoa upesi bunduki yake toka kiunoni. Alifunua sketi yake upesi kiasi kwamba hata nguo ya ndani haikuonekana. Kabla hajawanyooshea wakina Jona na kufyatua, Jona akawa amemfikia! Ila bado akafyatua. Risasi ikaruka na kutoboa mlango.
Kabla tena hajafanya jambo, Jona akawa amempokonya bunduki. Ila naye mhudumu akawa na upesi, hakumruhusu Jona amshambulie, akamng’ang’ania mkono wake, Jona akauvuta kwanguvu na kumtandika kiwiko, akadondoka chini!
Alikuwa anavuja damu puani. Kichwa kilikuwa kinamgonga sana. Hakuweza kunyanyuka tena na kupambana. Jona akamfunga kinywa na mikono kwa kutumia mkanda wake kisha akaenda upesi kwenye chumba cha Miranda kwani alihisi huenda mhudumu yule akawa ameshapitia huko kwani chumba chake kilikuwa cha mwisho kwenye utaratibu wa namba.
“Who’s it?” sauti ya Miranda iliuliza.
“It’s me, Jona!”
“Jona?” Miranda akajiuliza kwa sauti yake ya chini. Alikuwa ameketi kitandani akiwa bado hajatoa taulo mwilini mwake. Kwa ujumla alikuwa amejifunga mataulo mawili, moja kifuani na lingine kichwani, ila kuendea mlango, akajivesha taulo kiunoni kutimiza matatu.
“Umekunywa wine?” lilikuwa swali la kwanza la Jona. Aliuliza akiwa ametoa macho na akizama ndani kwa kuusukuma mlango. Alipotupa macho akaona chupa ya wine mezani. Haikuwa imefunguliwa. Hatimaye akashusha pumzi.
“Kuna nini Jona?” Miranda akauliza kwa uso wa mashaka.
“Tupo under attack,” Jona akamjibu akimtazama kwa macho ya hakika. Ila hakusema sana, akaenda kuufuata mlango atoke, ila kabla akamtazama Miranda na kumwonya, “Usinywe hiyo wine!” kisha haraka akauendea mlango kuelekea kwenye chumba cha wale makomandoo.
“Vipi, amekunywa?” Lee aliuliza. Alikuwa ni punde ametoka kwenye chumba. Ameshavalia suruali na shati jepesi.
“Hajanywa!” Jona akajibu akiwa na haraka. Akauendea mlango wa wale makomandoo akiwa anaongozana na Lee kwa nyuma. Akaukuta mlango ukiwa umefungwa. Akagonga pasipo mafanikio. Akauvamia kuuvunja.
Kutazama ndani akawaona mabwana wale wakiwa wamelala kitandani. Hawakuonekana kujielewa. Na kama wangelikuwa wazima basi wangelikuwa wamedamka punde waliposikia mlago ukigongwa, hata basi ukivunjwa.
Chupa ya wine ilikuwa tupu, haina kitu!
“Wamekunywa!” Lee akaropoka. Walitazamana na Jona, Jona upesi akawafuata wale makomandoo na kuwanusa. Walikuwa wananuka pombe!
Lakini zaidi hawakuwa wanapumua! Mapigo ya moyo yalikuwa yamezima! Kiufupi, walikuwa wamekufa.
“Tunafanyaje, Jona?” Lee akauliza.
“Sijui!” Jona akasema akiketi kwenye kitanda. Alishika kichwa chake kwa mawazo.
Ila upesi akiwa amekumbuka jambo, akamtazama Lee na kumwambia, “Tuondoke hapa upesi! Wauaji wameshajua wapi tulipo.”
“Na vipi kuhusu hii miili?” Lee akauliza.
“Inabidi tuondoke nayo. Hatuwezi kuiacha hapa!” Jona akasema akisimama.
“Hapana, Jona!” akasema Lee akitikisa kichwa. “Ni hatari sana kufanya vivyo. Hatujui maadui wapo wapi, wapo wangapi. Tutawezaje kujiokoa na huku tuna miili mitatu?”
“Sasa tutafanyaje?” akauliza Jona. Alikuwa ni kama mtu aliyechanganyikiwa. Kwa muda akili yake ilikuwa haifanyi jambo. Alikuwa anawaza mambo mengi kwa wakati mmoja.
“Tutapiga picha na kuzituma mtandaoni,” akasema Lee. “Tutaandika caption, najua picha itasambaa mtandaoni na watapata namna.”
“Seriously?” Jona akatia shaka.
“Ndio. Jona hatuna muda hapa. Lazima tufanye maamuzi ya hekima ama wote tuwe wafu!”
Kabla Jona hajasema jambo, wakasikia sauti za vishindo. Wakahisi si shwari. Haraka Lee akachomoa simu na kupiga picha miili ya wale makomandoo …
Huko nje koridoni kulikuwa na wanaume wawili na mwanamke mmoja. Watu hawa waliokuwa wanatembea sambamba walikuwa wamebebelea bunduki mikononi mwao. Nyuso zao zilikuwa za kazi na macho yao yalikuwa yanaangazia milango mitatu inayofuatana.
Milango mitatu ya vyumba vya Jona na wenziwe.
Basi punde walisimama mbele ya chumba cha wale makomandoo. Chumba hicho kilikuwa wazi tu. Hawakuona mtu. Basi wakausogelea mlango, walipofika, wale wanaume wawili, ghafla mlango ukafungwa kwanguvu na kuwakumba!
Wakaweweseka. Walimparamia mwanamke aliyekuwepo nyuma yao na huo ukawa mwanya mzuri kwa wakina Jona kushambulia. Haraka Jona na Lee wakawarukia, na kwa ustadi wao, wakawapokonya silaha na kuwalalisha chini kwa maumivu.
Haraka wakamshtua Miranda na kumwambia waende upesi kwani mambo yameharibika. Upesi Miranda akatoka na wakaelekea kaskazini mwa hoteli. Muda si mrefu, kwenye eneo la tukio, pale walipokuwa wameachwa wale watu walio hoi kwa kipigo, akawa amewasili mwanamke kamanda, Sword, akiwa ameongozana na watu wanne wengine.
“Where are they?” Mwanamke huyo akauliza. Mwanaume mmoja akanyooshea kidole chake upande wa kaskazini, basi haraka mwanamke huyo kamanda akiwa ameongozana na watu wake wakaelekea huko.
Walisaka, hawakuona mtu! Kabla hawajarudi kwa wale wenzao, wakasikia sauti ya mtu anagugumia. Kwenda kutazama, wakamkuta mlinzi akiwa amefungwa mdomo.
“They’ve escaped!” Mwanamke kamanda akaropoka. Geti la uani lilikuwa wazi. Wakina Jona walikuwa wametoroka, na ni wazi haikuwa muda mrefu. Bado geti lilikuwa linachezacheza!
Basi haraka kamanda Sword na wenzake wakakimbilia huko. Kutazama kushoto na kulia, kwa mbali mkono wao wa kuume, wakaona mtu anaishilia. Wakaanza kukimbia kuelekea huko, kufika hawakuona mtu!
“Shit!” akalaani kamanda Sword akipiga kofi paja lake. Mazingira yalikuwa tulivu mno. Ni usiku huu tena mzito. Magari machache yalikuwa yanaonekana barabarani, watu wanaotembea kwa mguu hawakuwapo.
Basi punde, mawasiliano yakaungana toka kule makaoni. Mwanaume yule aliyekuwepo kwenye mitambo akawaambia wapi alipowaona walengwa wao. Ni mtaa wa pili toka walipo. Wapo barabarani bado hawajapata usafiri!
Lakini pia akawaonya kuwa mmoja wao ameshikilia bunduki.
“Let’s go!” akaamuru kamanda. Moja kwa moja wakaenda huko walipoambiwa.
Asubuhi na mapema kila kituo cha habari kikarusha taarifa juu ya watu waliokutwa wakiwa wafu kwenye moja ya mtaa wa London. Watu hao walikuwa ni wale waliokuwa wanawafukuzia wakina Jona, kwa idadi watu wanne! Wawili miongoni mwao wakiwa majeruhi wapo hospitali kupokea huduma.
Mbali na hayo, pia hata ile miili ya wale makomandoo na kile kilichotokea kule hotelini kikarushwa na watu wakajua. Hata watu wa Tanzania nao wakapata habari juu ya wanajeshi wao kwenye nchi ya kigeni. Kuitikia hilo, shughuli za kufuatilia miili hiyo ikaanza mara moja.
Basi, mambo yakazidi kupamba moto. Kwakuwa kikosi nambari ‘wani’ kilikuwa kimeshashindwa kufanya kazi yake ya kuwamaliza wakina Jona, ikabidi sasa kitumwe kikosi cha pili. Cha sasa pia kilikuwa kinaongozwa na watu kumi chini ya kamanda mwanamke mwenye jina la Arrow.
Nao wakadumu kwa siku moja. Wote wakapukutika. Kikatumwa kikosi cha tatu na cha nne, nao hawakuwa wameambulia kitu. Wote wakamalizwa kana kwamba maji. Ilikuwa ni kama utani, lakini watu wakienda hakuna aneyerejea zaidi ya taarifa ya habari ya watu kukutwa kwenye mahoteli, ama barabarani!
Kabla ya kikosi cha tano hakijatumwa, Kamanda mkuu, akaona ni kheri kabla hawajafanya hilo, watulie kwanza kuona wapi wanakosea. Ni wazi sasa wakina Jona watakuwa wanafahamu wanachokifanya.
Wakapanga mipango madhubuti ya kuwa, punde wakina Jona watakapoonekana kwenye kamera basi watoe taarifa polisi kwanza. Wahakikishe watu hao wanahitajika na serikali. Na basi picha zao zitazagaa kutangazwa kwenye vyombo vya habari.
Hapo watakuwa wameihamishia kesi mikononi mwa serikali. Ila,
“Don’t you think it will be risk even for us?” akauliza mmoja. Walikuwa wanafahamu wakina Jona watakuwa ni watu wanaujua nyendo zao, vipi wakikamatwa na polisi, hawatatoa taarifa zao huko kituoni?
“No!” akasema Kamanda mkuu akitikisa kichwa. “Before doing that I will have already killed them!” Basi kikao cha dharura kikawa kimeishia hapo. Na siku hii ikaenda salama mpaka kwenye majira ya saa tano usiku.
Kamanda mkuu akatoka kwenda kwenye tafrija fupi iliyokuwa imeandaliwa na Malkia kwa ajili ya kumpongeza mmoja wa vijana wake, kwa jina Prince Henry, kwa kupata mtoto wao wa kwanza na mwanamke aitwaye Diana Lavik, mwanamke mwenye asili ya kilatini.
Tafrija ilikuwa imehudhuriwa na watu wakubwa na wazito. Ulinzi ulikuwa mkubwa. Watu walikuwa wamependeza kwa suti na magauni ya kumetameta aghali.
Basi bwana Kamanda alipoiingia, haikuchukua muda kupata kinywaji mkononi mwake. Na pia watu wawili watatu wa kupiga naye soga za hapa na pale. Ila akiwa anafanya hivyo, mara akasikia sauti ya mwanamke nyuma yake.
“Hey, gentleman.”
Sauti hii ilikuwa kavu ila tamu masikioni. Haikumchukua muda kamanda akageuka kutazama. Hamaki uso kwa uso akakutana na mwanamke mwenye rangi ya dhahabu. Nywele zilizofundwa vema na macho ya kuvutia. Kiuno kimekabwa na gauni na amepanda kwa viatu virefu nyeusi.
Mwanamke huyu alikuwa ni Glady.
“Do I know you, madam?” Kamanda akauliza.
“Yes, you do!” akajibu Glady akirembua. “Would you mind a dance?”
“Off course!”
Glady akamkwapua Kamanda na kusonga naye kando kucheza wimbo wa taratibu uliokuwa unapiga. Sikioni mwake sauti ya mbali ikamwambia, “Hakikisha unamuua.”
Kamanda alimtazama Glady machoni akamwona mwanamke mrembo haswa. Mwanaume huyu hakuwa mtu wa kupenda rangi nyeusi, ila hapa kwa Glady akachina haswa. Hakuwahi kumwona mwanamke mrembo kama huyu. Kwenye mikono yake alikuwa anampatia joto fulani analolihitaji.
Na zaidi ya yote Glady alikuwa na kitu ambacho wanawake wote wa kizungu aliokuwa nao hawakubahatika kuwa nacho – shepu! Kiuno kinajulikana kipo wapi, na baada ya kiuno basi nini kinafuatia.
Hakika hapa bwana Kamanda alikuwa ameshikwa. Ugumu na ukatili wake wote ukawa ni sponji chakavu mbele ya mwanamke kubuhu. Mtambo. Bibie Glady.
Kwa kujiamini kabisa mwanamke huyo alikuwa anamtazama mwanaume huyo machoni. Lakini siyo kumtazama kama ujuavyo wewe, lah! Kumtazama kiuanamke. Kumtazama kwa macho yanayoomba huba. Macho yanayolilia mapenzi ya ndani!
Ama kwa hakika chunusi ilipata kucha ndefu. Kiuno cha Glady kilichokuwa kimeshikiliwa na mkono mpana wa Kamanda kilikuwa kinaenda kutoka na midundo ya muziki. Nyonga yake iliaga kila melodi.
“Who are you?” Kamanda akajikuta anauliza. Alishindwa kuvumilia zaidi. Hakutaka muziki ukome. Hakutaka mwanamke huyu atoke mikononi mwake. Na hii ndiyo ilikuwa sababu ya Glady kulipiwa kila kitu aje Uingereza. Hata wale waliokuwa wanatilia shaka, sasa walianza kusadiki. Kila kazi na mkono wake.
“My name is Rebentha…” akasema Glady pasipo kutumia nguvu. Lips zake zilizokuwa zimechovya ‘lipstick’ hazikuwa zikihangaika bali ulimi.
“Rebentha?” Kamanda akaguna. “Rebentha from?”
Glady akatabasamu. Kamanda akahisi amepigwa shoti, kwa muda kidogo akasahau hata alichouliza, akasema, “You are so beautiful, Rebentha!”
“Thanks,” Glady akaipokea kwa madaha na kusema, “I am from Caribbean.”
“Caribbean! Wow! I have never been there. How did you know me?”
“How long does it take to see a handsome lonely man in the party?”
Kamanda akatabasamu pasipo kutia neno.
“Honestly I don’t know you. But my eyes just fell on you. Is it wrong?”
Kabla Kamanda hajatia tena neno, Glady akatazama kushoto kwake kwa mbali na kusema alikuwapo kule akinywa kinywaji kabla hajamtia machoni mwanaume huyo aliyependeza akiwa mpweke, aongea tu na wazee hapa na pale.
“You are so confident!” akasema Kamanda.
“Doesn’t that turn you on?” Glady akauliza. Basi Kamanda akaishia kutabasamu, akamkumbatia kwanguvu mwanamke huyo na kucheza naye kwa muda kabla hajamwomba wakapumzike kidogo na kufanya maongezi zaidi.
Lakini kabla ya kwenda huko, Glady akamlaghai wacheze zaidi kwani bado ana hamu ya kufanya vivyo. Akiwa nyumbani huwa hapati huo muda na yeye kucheza ndicho kitu anapenda zaidi.
Basi Kamanda hakuona tabu. Hakutaka kumghafirisha mwanamke huyo mrembo, akampatia dakika tatu za ziada. Wakacheza na akiwa anamuuliza maswali ya hapa na pale, wapi ametokea na amekuja na nani?
Wakiwa hapo wanacheza kutafuna hizo dakika tatu za ziada, ndipo Glady akawa anapanga namna ya kufika kwenye kilele cha kazi yake. Wigi lake refu lilikuwa linamziba masikio yaliyokuwa yana ‘earphone’ za mawasiliano na pia hereni zake zenye ncha kali.
Baada ya kutazama huku na kule, akiwa anapiga mahesabu kichwani, akatengeua mguu wake wa kuume, kisigino cha kiatu kikameguka, akaangushia kichwa chake kwenye bega la Kamanda. Mara Kamanda akaguna kutoa sauti ya maumivu akiwa amekunja sura.
“I am sorry! … shit! Its my earring!” Glady akasema akitoa kichwa chake akijitahidi kusimama. Shingo ya Kamanda ilikuwa imechanjwa kidogo. Kwa mbali kulikuwa kuna kamstari kekundu. Na punde, damu ikaanza kuchuruza.
“It’s okay, never mind!” Kamanda akasema akishika eneo lenye maumivu. Kutazama vidole vyake akaona alikuwa anavuja damu, basi akamwomba mrembo muda mchache akapate kujiosha, atarejea.
“Its ok. I will be waiting,” akasema Glady akiwa na sura ya taharuki na huzuni. Mwanamke huyu aliigiza haswa. Basi Kamanda akaenda zake ‘washroom’ Glady akimtazama mwanaume huyo akiishia, kisha akaweka kidole chake sikioni na kusema,
“Nimemaliza kazi!”
Ama kweli vitamu ndivyo venye sumu.
**
Alijihakikisha kama yupo sawa. Anhaa akaridhika. Damu ilikuwa haitoki tena hata tone. Basi akajifuta kwa mara ya mwisho na kitambaa chake kilicholowana maji alafu akajitengenezea vema. Bado alikuwa amependeza na suti yake toka Italia.
Kamanda akajirekebisha nywele zake kabla ya kwenda kukutana tena na mrembo. Alipojihakikishia kuwa yuko sawia kwa kila kitu, akatoka kuuendea mlango. Ila kabla hajaufikia, akahisi kichwa chake kinagonga. Alisimama na kuskizia, akajiona bado yu vema, basi akaendelea na safari yake.
Alipofika kwenye uwanja akaangaza huku na kule, hakumwona Rebentha! Lakini punde , si Rebentha tu, hata watu wengine akawa hawaoni. Walianza kuwa maruweruwe, asione cha kueleweka! Kichwa kikamgonga sana, na damu zikaanza kummiminika toka puani kwa fujo.
Hakudumu kwa muda mrefu akiwa amesimama, akajikuta chini!
Watu wakamtazama na kumsogelea. Damu hazikukatika, zikaendelea kummiminika zaidi na zaidi kuchafua suti yake aghali. Kwa muda kidogo shughuli ikawa imesimama. Mwili wa Kamanda ukanyanyuliwa na upesi ukatiwa kwenye gari la wagonjwa lililokuwapo eneoni kuwahishwa hospitali, huku nyuma tukio hilo likiwa limeacha zogo.
Gari hilo la wagonjwa likatimka haswa, ving’ora vikitawala barabarani. Lakini kumbe waliopo humo ndani si wahudumu bali ni Jona na wenzake. Walikuwa wamevalia sare na vichwa vyao vimemezwa na kofia zenye chapa ya huduma.
Sasa watu hawa walikuwa wamempata Kamanda. Tena kwa ulaini kabisa. Gari hilo la wagonjwa baada ya kutembea kwa takribani dakika kumi na tano, likazima ving’ora na kutoka kwenye barabara kuu.
Likapotelea huko kusikojulikana.
Baada ya juma moja … Dar es salaam, kituo kikuu cha polisi. Sauti ya kishindo cha miguu yenye buti ilikomea mbele ya lango la nondo za chuma, hapo akasimama Askari mnene mweusi mkononi akiwa amebebelea bunduki na kiunoni mwake amening’iza pingu.
Akatazama ndani ya chumba cha mahabusu, macho yake makubwa yakaangukia kwa mtu mmoja aliyekaa nyuma kabisa. Jona. Akampa ishara ya kichwa kumtaka asonge karibu. Jona akafanya hivyo. Akashika nondo na kumuuliza askari,
“Mmefanya nilichokiomba?”
Askari hakumsemeza jambo, akachojoa ufunguo na kufungua lango, Jona akatoka. Akaongozana naye mpaka kaunta ambapo huko alikutana na Makamu wa Raisi, ambaye kwa sasa ndiye alikuwa amekaimu kiti cha Raisi.
Akamsalimu na Makamu akamuuliza, “Ndiyo wewe Jona?”
“Ndio, mheshimiwa.”
“Hata kama usingeliomba kuonana na mimi, ningekuja kuteta nawe maana nahisi nina mengi ya kusikia toka kwako.”
Basi Jona akapatiwa nafasi ya kuteta pamoja na Makamu wa Raisi kwa faragha. Akamweleza yote toka herufi A mpaka Ze. Na kama haitoshi, akamkutanisha mheshimiwa huyo na wenzake: Miranda, Lee na Marwa. Nao kila mmoja kwa nafasi yake akaeleza yote yale ya kweli, na hata kuthibitisha wayasemayo kwa nyaraka na shahidi mbalimbali zilizokuwa mikononi.
Makamu wa Raisi akapigwa na butwaa na yale yote aliyoyasikia. Ilikuwa ni ngumu kuyakataa kwani hata matukio yaliyokuwa yanatukia ndani ya nchi pasipo na majibu ya uhakika, yaliungana mkono na maelezo na shahidi zilizotolewa.
Akaamuru wale wachimba madini, wakina Nyokaa, watiwe nguvuni upesi. Pia akatoa agizo wakina Jona waachiwe huru, lakini akamtaka Jona aonane naye faragha baada ya majuma mawili. Zaidi akawapatia kiasi fulani cha fedha kama motisha kwa kupigania nchi yao kwa dhati.
Siku hiyo Jona na wenzake wakafanya tafrija nyumbani kwa kujipongeza. Wakamwalika pia Glady na Miriam ambaye hakusita kuja upesi. Tafrija ikafana sana na kila mtu akafurahia isipokuwa kwa Sheng ambaye alikuwa mlemavu wa kudumu kwa kupooza.
Yeye alikuwa kwenye ‘wheelchair’ akitokwa na machozi. Hakuwa anaweza kusogeza mwili wake hata kidole. Alikuwa ni wa kufanyiwa kila kitu, na kwakuwa hakukuwa na mtu mwenye muda huo, wote walishakubaliana kuwa mwanaume huyo atatumwa kwenda kwao China kukutana na familia yake.
Kwa mujibu wa daktari hakuwa anaweza kudumu hai zaidi ya miezi miwili tangu sasa.
“Samahani sana, Sheng,” alisema Lee. “Sitaweza kuwa nawe tena kwa sasa maana nimepata familia mpya. Nasikitika maana utakuwa mpweke sana, na mikono yako iliyozoea kuua haiwezi tena kufanya kazi hiyo.
Ila nina furaha pia maana kwa sasa hatimaye utakuwa huru kuwa na familia yako. Hautakuwa na haja ya kujificha tena maana wote wameshamalizana wenyewe kwa wenyewe. Pengine kwa muda kidogo tutaiona dunia ikiwa tofauti.
Kwaheri Sheng.”
Lee aliposema hayo, akambusu Sheng kwenye paji la uso na kurudi tafrijani alipokutana na Glady na kukumbatiana kwa huba. Ila muda si mrefu, Jona akamwita na kumtaka faragha.
“Kuna lolote?” akauliza.
“Ndio, lipo,” Jona akajibu na kisha akatazama kushoto na kulia kuhakikisha kama wapo wenyewe. Akamnong’oneza jambo Lee, Lee akatabasamu. Ghafla, Lee akamshika mkono Jona na kumvutia tafrijani kisha akapaza sauti,
“Naomba tuskizane tafadhali!” muziki ukazimwa. Watu wote wakawatazama. “Jona hapa ana kitu cha kuwaambia…”
“Mimi?” Jona akatahamaki.
“Oooh basi nitakusaidia kusema …” Lee akapayuka. “Jona wants to marry Miranda!”
Watu wakalipuka kwa shangwe, ila Miranda akaziba mdomo wake akiwa ametoa macho kwa kutoamini. “Serious?” akauliza akitahamaki. Basi Jona akamtazama na kujikaza akimwambia, “Yes, serious!”
Simulizi : Anga La Washenzi (1) Sehemu Ya Kwanza (1)
Mvua ilikuwa inanyesha sana. Hali ya hewa ilikuwa baridi ikiambatana na upepo wa wastani. Watu wengi hawakwenda kazini, na hata wanafunzi pia wakitega shule kwa kisingizio cha barabara kufurika maji. . . . Pengine watu hawa walikuwa na hoja kutokana na miundombinu dhaifu ya jiji la Dar es Salaam ambayo haiwezi kurandana na mikikimikiki ya mvua. Ila kwa mwanaume Jonathan Mchau, hilo halikuwa na mashiko kamili kwani yeye alikuwa ofisini akiendelea na kazi zake kama ilivyo ada. . . . Ni ndani ya chumba kidogo kinachopatikana maeneo ya mwenge. Kwenye kuta za chumba hicho kulikuwa kumetundikwa picha kadhaa za kuchorwa kwa mikono. Picha hizi zilikuwa zimeundwa kimafumbo lakini pia zikibeba utajiri wa tamaduni za Afrika kwa ujumla. . . . Kama ungelipata nafasi ya kutembelea hapo basi ungepatwa na kamshangao kidogo kutazama picha hizo zilizofumwa na rangi mbalimbali za kuvutia kiasi kwamba ukasahau kuwa eneo hilo limepakana na barabara yenye makelele lukuki ya magari. Na hata kuta za jengo hilo zina nyufa kadhaa. . . . Mwanaume huyu ajulikanaye kwa jina la Jonathan, joh, ama Jona kama wamuitavyo watu wa karibu, alikuwa ni mwanaume mweusi mtulivu mwenye mwili wa kujaa, macho makubwa mabovu yasaidiwayo na vioo vya miwani, nywele ndefu kichwani na ndevu alizozichonga umbo la ‘o’. . . . Hakuwa mtanashati sana, pengine kwasababu alikuwa kazini na kazi yake aihitaji unadhifu wa hali juu ilhali unacheza na rangi. Ila alikuwa mtulivu sana, na macho yake yaliganda kwenye karatasi aichorayo kwa umakini wa hali ya juu. . . . Alikuwa ndani ya ulimwengu wa peke yake asijali kabisa yanayoendelea nje ya karatasi. Unaweza kudhani mwanaume huyu hakuwa anajua kama kuna mvua ilikuwa inanyesha. Umaanani huu kupita kiasi ukamfanya asifahamu kama kuna mgeni ameingia eneo lake na kusimama kwa sekunde kadhaa. . . . Akashtuliwa, “Hello!” . . . Akatazama na kumkuta mwanamke fulani mrembo, mrefu mwenye rangi maji ya kunde. Alikuwa amevalia sweta rangi ya kijivu iliyofunika blauzi yake nyeupe, pamoja na suruali ya jeans iliyobana vema umbo lake la figa. Miguuni alivalia raba nyekundu. . . . Nywele na masikio yake alikuwa ameyaziba kwa kofia kubwa jeusi la soksi. Mgongoni alikuwa amebebelea begi kubwa jeusi, haya ya kuhifadhia tarakilishi mpakato. Uso wake ulikuwa mfupi na mpole. Macho yake yalikuwa ya wastani ila makali. Mdomo wake mdogo alioupaka rangi ya kahawia ulichanua kwa tabasamu. . . . “Samahani kwa kukutoa kazini,” akasema mwanamke kwa sauti ya kumlaghai nyoka. . . “Usijali,” akadakia Jonathan, “karibu sana.” Akaacha kazi akasimama kumlaki mgeni. “Ahsante. Hapa ndiyo kwa Joh?” “Yes, ndiyo hapa.” “Na wewe ndiye Joh mwenyewe?” “Ndio, ni mimi.” “Ook, nimeagizwa na Beatrice Shauri kuulizia mzigo wake.” “Bite?” “Ndio!” . . . Jonathan akatabasamu. Akafuata mfuko mmoja mkubwa mweupe wa rambo, ndani yake ulikuwa na kitu cha umbo la mstatili, akaunyanyua na kumkabidhi mgeni. . . . “Unaweza ukatazama.” . . . Mgeni akatazama mzigo huo kisha akaurudisha ndani ya mfuko. . . . “Ahsante sana. Unamdai?” “Hapana.” “So naweza nikaondoka nao?” “Hapana.” Jonathan akatikisa kichwa. “Siwezi nikakupatia maana sijapata ridhaa ya mmiliki.” “Bite ni dada yangu.” “Taarifa hiyo haijitoshelezi kukupa mzigo wake, dada. Hakunipa agizo hilo.” . . . Mwanamke yule akaguna na kubinua mdomo. Akapandisha mabega na kuzungusha macho. . . . “Ok,” akasema kwa kupitia puani kisha akaenda zake. Ila punde anarejea tena. “Kaka mbona unakuwa si mwelewa lakini?” Alilalama. Macho yake yalikuwa yamelegea, mdomo wake ukitepeta. “Nimekwambia Bite ni dada yangu, ameniagiza. Simu yangu imezima chaji unajua umeme unavyosumbua siku hizi, ningempigia uongee naye!” . . . Joh alipigwa na bumbuwazi. Kuna kitu alikikokotoa kichwani. . . . “Dada,” akaita. “Siwezi nikakupa kazi ya mtu. Na hii ni kwasababu sikupewa agizo hilo. Ni swala la uaminifu tu. Sikufahamu, siwezi kukuamini namna hiyo.” . . . “Basi ntakuongezea pesa mara mbili ya aliyokulipa Bite,” akasema mwanamke huyo kwa kujiamini. Hapo sasa ndiyo Jonathan akapata wasiwasi zaidi. Kwanini mwanamke huyu anataka mzigo huu kiasi hiki? . . . Aliona haja kubwa ya mwanamke huyo ndani ya macho yake. Alikuwa anataka ule mzigo kwa hali na mali. “Sema basi,” mwanamke akasisitiza. Uso wake ulikuwa umekunjana. Alitazama majira ya saa yake kana kwamba mwanafunzi aliyechelewa zamu ya mwalimu mnoko. “Unataka shilingi ngapi?” Akauliza. “Sitaki pesa yako,” Jonathan akajibu na kuongezea: “Naomba uende, dada.” . . . Mwanamke akashusha pumzi ndefu. Akavua begi lake na kuzamisha mkono wake wa kuume ndani. Jonathan akapata shaka. Alitazama mkono huo vema. Alidhani huenda ukatoa silaha. . . . Kabla mkono huo haujatoka ndani ya begi, sauti ya wanaume ikasikika. Jonathan na mgeni wake wakatazama sauti hiyo inapotokea. Mlangoni wakawaona wanaume wawili waliovalia makoti marefu meusi ya kuwakinga na mvua. . . . Wanaume hawa walikuwa warefu na weusi. Mmoja alikuwa na mustachi mnene, mwingine kidevu na mashavu yake yakiwa hayana harara za ndevu. Miili yao ilikuwa imejaa wakitembea kikakamavu. . . . Haikuchukua muda mrefu Jonathan akagundua wanaume hao walikuwa ni wana usalama. Kwa namna walivyokuwa wanaongea, kutembea na muonekano wao pia ulisadifu hiyo dhana. . . . Alirudisha macho yake kwa yule mwanamke, akaona mwanamke huyo akifunga begi lake na huku mkononi akiwa mtupu. Mwanamke akamtazama Jonathan kwa jicho baya kisha akaondoka zake akisonya. . . . Jonathan alimsindikiza mwanamke huyo mpaka alipotoka mlangoni, kisha akahamishia macho yake kwa wageni wapya. . . . “Karibuni.” “Ahsante,” aliitikia mwanamume mmoja kisha kwa pamoja wakamsalimu Jonathan. “We ni Jonathan Mchau?” Aliuliza mwanaume mwenye mustachi. Sauti yake ilikuwa ya madaraka. Walikuwa wanamtazama Jonathan kana kwamba wanamfananisha na mtu waliyemuona kitambo. “Ndiye mimi,” Jonathan akajibu. . . . Leo ilikuwa ni siku ya tofauti sana kwa Jonathan. Ugeni wa pili sasa huu unamtembelea. Kazi iliyomfanya asijali hali ya hewa akaja ofisini, ilikuwa imesimama. ‘Karoho’ kalikuwa kanamuuma. Aliona anapoteza muda. . . . “Tuna maongezi kidogo na wewe,” akasema mwanaume mwenye mustachi. Yeye ndiye alikuwa muongeaji mkubwa mwenzake akiwa kimya. “Karibuni,” Jonathan akasema akinyooshea mikono yake ndani. “Tunaweza tukafanyia hayo maongezi kwenye gari?” “Kwenye gari!” Jonathan alistaajabu. “Ni maongezi gani hayo? Na nyie ni wakina nani? – hamjajitambulisha.” “Sisi ni polisi.” Wanaume wale wageni wakaonyeshea vitambulisho vyao. “Hivyo usijali.” “Sijali, ila ningependekeza tufanyie hayo maongezi hapa hapa ofisini kwangu,” Jonathan alisema akiketi kitako. Wanaume wale wawili wakatazamana kisha muongeaji akasema: “Sawa.” . . . Wakavuta viti vilivyoko kando, walionyeshewa na Jonathan, wakaketi. . . . “Jonathan, sisi sio wakaaji sana. Kwa majina naitwa inspekta Norbet Mlanje na huyu mwenzangu ni inspekta Nombo tumetokea kituo kikuu, central.” “Karibuni inspekta.” “Ahsante kwa mara nyingine. Nadhani mpaka hapo utakuwa ushajua tumekuja kufanya nini.” “Sijajua,” Jona akasema akitikisa kichwa. “Sawa, si mbaya tukaliweka wazi,” akasema Inspekta Norbet akikuna ndevu. “Kama tulivyosema hapo awali, tumetoka central, na tumeagizwa kuja hapa kwa ajili ya kukuomba kurejea kundini. Mkuu anakuhitaji sana.” . . . Jona akatabasamu. . . . “Siwezi kurudi,” akajibu kwa ufupi na kisha akasimama. “Nina kazi nyingi zinaningoja. Mnaweza mkanipa nafasi?” . . . Inspekta wakatazamana alafu wakanyanyuka kishingo upande. . . . “Jona,” inspekta Norbet aliita. “Taifa lako linakuhitaji kwa sasa. Nadhani ni wakati wa wewe kuacha ukaidi na kusikiza wito huu.” “Inspekta Norbet,” Jona akaita. “Sihitaji kazi yenu, naomba umwambie mkuu hilo. Tena umsisitizie. Sihitaji kazi yenu hata kidogo.” . . . Inspekta wakatazamana kwa macho ya paka. . . . “Sawa, ila utakapobadili mawazo yako usisite kututaarifu.” . . . Jonathan hakujibu, inspekta wakaondoka. Walifika mlangoni Norbet akamtazama tena Joh kana kwamba mama aliyekata tamaa juu ya mwanaye. Kisha wakatokomea. . . . Jonathan alitafakari kwa dakika mbili, akaketi kuendelea na kazi yake aliyokuwa anaifanya hapo awali. Ila kwa sasa akili yake haikuwa imetulia. Mawazo yalimpoka atensheni. Alimfikiria yule mwanamke, alafu pia na wale inspekta. Alijikuta anakosea kutenda kazi kila mara. . . . Mwishowe aliacha, akasimama na kwenda nje kutazama madhari, pengine angechangamsha akiliye. Alitazama namna mvua inavyokita ardhi, barabara ilivyolowana. Alitazama jinsi matairi ya magari yanavyotapanya maji barabarani. . . . Alitazama anga lilivyojibana na kuwa jeusi. Namna palivyokuwa tulivu usidhanie kama hapo ni Dar, tena majira hayo. . . . Akiwa anarandisha macho yake mithili ya mtalii mbugani Serengeti, kuna kitu alikiona kikamvutia. Mara ya kwanza alikipuuzia, na hata ya pili pia. Mara hii ya tatu akaamua kukitilia maanani. Ilikuwa ni gari kubwa, Range Rover Sport nyeusi, lililosimama hatua ishirini na tano za mtu mzima toka kwenye banda lake. . . . Taa za nyuma za gari hilo zilikuwa zinawaka. Gari lilikuwa linachemka, ungeliona hilo kwa wepesi kwa kutazama bomba lake la kutolea moshi. Pleti namba ya Kenya. Vioo vyake vilikuwa vyeusi, hivyo hata kama ungekuwa karibu usingeona walio ndani. . . . Jona alilitazama gari hilo akijiuliza maswali mepesi kichwani. Lipo hapo tangu muda gani? Linafanya nini hapo? Mbona haliondoki? Linamsubiri nani ama nini ilhali mabanda yamefungwa? Mara gari hilo linatiwa moto na kuondoka. Jona analisindikiza likiyoyoma kisha anarudi zake ndani kuendelea na kazi. Angalau akili yake ilikuwa freshi. . . . Alidumu kazini mpaka majira ya jioni akiwa ameisogeza sana kazi yake. Alifunga banda kwenye majira ya saa kumi na mbili, akapanda bodaboda mpaka kwenye baa moja isiyo na jina, maeneo ya karibu na makazi yake, Mbezi beach GOIG. Hapo akatulia akiwa ameagizia Alvaro baridi. . . . Watu walikuwa wachache, bila shaka sababu ya hali ya hewa. Jona alijitenga mbali na watu, akiketi kwenye meza pweke. Macho yake yalikuwa yanachambua mazingira huku mdomo wake ukipiga mafundo kadhaa ya kinywaji. . . . Taratibu akiwa hapo, anamezwa na tafakuri na taswira mithili ya ndoto. Haikuchukua muda mwingi kuhamishwa toka kwenye fahamu zake mpaka ulimwengu huo mwingine. . . . Hii ndiyo sababu mwanaume Jona hapendi kuketi pasipo shughuli. Kila anapokuwa huru, akili yake humkumbusha yaliyopita. Na yaliyopita si mema. Humuumiza. Humtonesha kidonda sugu kisichotaka kupona. . . . Anajiona kwenye nyumba kubwa inayoungua moto. Anavuja jasho jingi akitoa macho huku na kule. Anaita jina lisilosikika. Anazunguka huku na kule. Mbao za paa zinaanguka. Hewa inakuwa nzito ndani ya nyumba anashindwa kuhema. Macho yake yanamwaga machozi. Anajikuta anaishiwa nguvu akikohoa kwa pupa. . . . Haraka anatoka ndani. Anatembea hatua kadhaa kuacha kibaraza, mara anaanguka chini. Anajitahidi sana kuhema. Jasho bado linaendelea kummiminika. Punde fahamu zinaacha mwili wake, anazirai. . . . “Kaka!” kwa mbali sauti ya kike ilipenya kwenye ngoma ya masikio ya Jona. “Kakaa!” sauti hiyo ikajirudia, mara hii kwanguvu ikiambatana na kupigwa kwa meza. Jona akashtuka. Mbele yake alikuwa amesimama mhudumu, mwanamke mtu mzima mwenye uweupe mwekundu wa kujichubua. .
*** *** *** “Vipi, kaka kuna tatizo?” Mwanamke aliuliza. Alikuwa amevalia suruali ya jeans na tisheti nyeupe ya bia ya Serengeti. Mkono wake wa kuume alikuwa ameshikilia sahani ndefu ya plastiki iliyobebelea kinywaji cha Balimi. . . . “Hamna tatizo dada,” Jona alijibu akipangusa uso. Alinyanyua kinywaji chake akapiga mafundo mawili. Mwanamke alimtazama kwa mashaka. Ni wazi alikuwa anastaajabu kutingwa kule kwa mwanaume huyo. . . . “Samahani,” akasema. “Nilitaka kujua kama utahitaji chochote toka jikoni.” “Ooh, kuna chakula gani?” Jona akauliza akiketi vema kitini. “Nyama ya kukaanga, rosti, ndizi, chips na ugali.” . . . Jona akatazama saa yake ya mkononi. Muda ulikuwa umeenda, na pia alihisi uchovu. Aliona ni vema akabeba chakula moja kwa moja aende nacho nyumbani, hivyo akaagizia na kungoja. . . . Baada ya muda mfupi, chakula kikaletwa, akalipia na kuondoka. Toka hapo bar mpaka nyumbani kwake si mbali. Mwendo wa wastani ungekufikisha kwa takribani dakika kumi. Kama ukikazana unaweza kuchukua hata dakika tano tu. Ila Jona hakuwa na haraka na nyumbani. Hakuwa na cha kuwahi, labda kama kungekuwa kuna mvua ingemkimbiza. . . . Mvua ilikuwa imekata, manyunyu tu ndiyo yalikuwa yanashuka. Nyumbani hakukuwa na mtu wa kumngojea, anaishi peke yake. Miguu yake ilitembea taratibu akitazama chini. Alipokaribia nyumbani kwake, akaona kuna gari limesimama kwa mbele, shaka likampata. Alisimama upesi, akalichambua gari hilo. Alisogea kidogo apate kuliona vema. Mara akagundua ni lile lile aliloliona kule kazini likiwa limesimama, na kisha kuondoka. . . . Lilikuwa ni Range Rover Sport, pleti namba yake ya Kenya. Jona akajikuta anapata maswali. Akiwa hapo anaendelea kutazama, akamuona mwanamke mmoja akitokea gizani, akapanda ndani ya gari hilo upesi. Mavazi ya mwanamke huyo yalimfanya Jona aamini ndiye yule mwanamke aliyemtembelea kazini akidai mzigo wa Beatrice. . . . Ina mana amenifuata nyumbani? Alijiuliza. Kumbe ndiye yeye aliyekuwa ndani ya gari hilo kule nje ya mabanda! . . . Hakutoka hapo alipokuwa amejibanza. Macho yake yaliendelea kutazama gari akingojea liondoke. Aliminya mfuko wa chakula, akasonya. . . “Chakula kinapoa.” . . Punde anamuona mwanaume mmoja mrefu akiwa kando na gari. Hakujua ametokea wapi. Mwanaume huyo aliegeza mikono yake dirishani mwa gari akasimama hapo kwa muda kidogo. Bila shaka alikuwa anaongea jambo na mtu ama watu waliomo ndani ya gari. . . . Alitazama huku na kule, akapanda kwenye chombo wakaondoka. Jona alisindikiza hilo gari mpaka lilipoyoyoma kisha akatoka alipokuwa na kuenenda nyumbani kwake. . . . Ilikuwa ni nyumba ya wastani, sebule na vyumba viwili, yenye uzio mfupi wa tofali na geti dogo jeusi. Ilikuwa kimya na tulivu sana, pia ilikuwa giza. . . . Jona alikula kisha akaelekea chumbani kwake pasipo kupoteza muda. Kilikuwa ni chumba kipana kidogo, kitanda kikubwa na kabati moja kubwa la nguo lenye kioo kipana. Pembezoni mwa kabati hilo kulikuwa kuna kitu kikubwa chenye pembe nne kikiwa kimefunikwa na shuka la kijivu. Jona alioga, kisha akafungua kabati lake na kitoa kisanduku fulani cha mbao, kidogo kwa umbo. Alikifungua, ndani yake kulikuwa kuna brashi kadhaa za kuchorea, mirija kadhaa ya rangi na penseli za mikaa, charcoal pencils. . . . Alikiweka kisanduku hicho juu ya stuli aliyosogeza karibu na kitu kilichofunikwa na shuka, kisha akalibandua shuka hilo. Kumbe hapo kulikuwa kuna makaratasi lukuki meupe marefu, mahususi kwa ajili ya kuchorea. . . . Karatasi ya kwanza kabisa ilikuwa ina picha ya mwanamke mrembo mwenye nywele za rasta. Jona aliitazama picha hiyo kwa sekunde kadhaa akifikiria jambo. . . . Mwanamke alikuwa anatabasamu, macho yake yaliangaza. Jona naye akajikuta anatabasamu, ila macho yake yakiwa mekundu. . . . Alifungua picha nyingine, picha ya mtoto wa kiume mwenye makadirio ya miaka mitatu. . . . Alitazama picha hiyo kwa sekunde kadhaa kabla hajaigeuza na kukutana na karatasi mpya isiyo na mchoro wowote. Hapo akaanza kuchora kwa kutumia penseli. . . . Hakutazamia popote pale isipokuwa alirejea kichwani mwake. Alichora picha ya mwanamke, yule aliyekuja kumtembelea ofisini akidai mzigo wa Beatrice. Alimchora mwanamke huyo hivyo hivyo kama anavyoonekana kuanzia kichwani mpaka kifuani asisahau hata vazi. . . . Alipomaliza aliketi kando, akitazama picha hiyo kwa umakini. Alijiuliza maswali kadhaa lakini hakuyapatia majibu. Alitamani Beatrice angekuwepo karibu ili amuulize, au basi angekuwa na simu ampigie. Mwishowe anaamua kuipuuzia, anafuata jokofu sebuleni na kutoa chupa kubwa ya whisky anayoanza kuigida akielekea chumbani. Alikunywa chupa yote, kisha akalala. . . . Hawezi kulala pasipo kufanya hivi. Hujaza jokofu lake mara kwa mara kwa vileo vikali, kwa kazi moja tu, kumsaidia alale. . . . Asipokunywa, usingizi huwa mrefu kupitiliza. Ataamka na kushtuka kila mara. Hatapata amani. Amekuwa akifanya hivi kwa takribani miaka mitatu sasa. Tangu pale alipoacha kazi yake ya uaskari, akiwa inspekta mwadilifu. . . . Ni miaka hiyo ya nyuma, mwanaume huyu alikuwa na furaha akitenda kazi yake kiufanisi. Alisuluhisha kesi kedekede zilizoonekana ngumu na zisizowezekana mbele ya macho ya wengine. Alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kumaliza makundi ya majambazi yaliyokuwa yameweka makazi yake ndani ya jiji la Dar es salaam. . . . Alifahamika kwa jina la Joh ‘the knife’, moto wa kuuotea mbali. Mwanaume mwenye mateke mazito, ngumi za kasi na matumizi mazuri ya silaha, haswa kisu. Hata kivuli chake kilikuwa kinaogopesha. . . . Simulizi hiyo ya kupendeza ilikuja kuhitimishwa muda mfupi baada ya baba yake mzazi alipofariki akiwa kazini, kituo cha polisi. Babaye alikuwa ni miongoni mwa maafisa polisi waliouawa kwenye mashambulizi ya majambazi vituoni vya polisi kwa dhumuni la kupoka silaha. . . . Ilikuwa bado miezi mitatu tu mzee huyo astaafu, adha hiyo ya kifo ikamkumba. Jambo hili lilimuuma sana Jona, akaapa kutafuta wahusika wote na kuwatia nguvuni. Ilimgharimu mwezi tu kufanikisha adhma hiyo. Alipomaliza akaamua kuacha kazi papo hapo. Maamuzi haya hakushawishiwa na yeyote yule isipokuwa akili yake. Alirudisha kila kitu cha jeshi akiandika barua ya kushindwa kuendelea na majukumu. Barua hiyo haikueleza sababu, bali tu hitaji. . . . Kiuhalisia, Jona alisononeshwa sana na namna jeshi la polisi lilivyomhudumia na kumjali marehemu baba yake. Aliona anastahili zaidi ya kile alichopewa na jeshi hilo. Alilipigania sana, alilitendea kazi kwa uadilifu na kwa uaminifu. Heshima aliyopata, haikuwa hata theluthi ya yale aliyotenda. . . “Nami nikifa nitatendwa hivi hivi,” alikuwa anasema Jona. “Kama wameshindwa kumthamini baba yangu aliyewatumikia miaka nenda rudi, vipi kwangu? Familia yangu itaachwaje?” . . . Aliona kazi hiyo haimfai. Aliamua ahamishie nguvu zake kufanya mambo mengine yatakayomletea faida zaidi, ambayo ni kujihusisha na biashara. Kuwepo ndani ya jeshi la polisi kulikuwa kunamkumbusha baba yake na kifo chake. Mara kadhaa alijikuta anajiuliza endapo angekuwa katika nafasi ya baba yake, familia yake ingebakije, ingeishije? Upuuzi. . . . Alitaka kupumzisha akili yake na purukushani. Alikuwa na ndoto za kufanya biashara, atengeneze faida kisha aende mbali kabisa, ulimwengu mwingine ambapo hakutakuwa na simu za kuitwa ofisini wala kazi za kutumikishwa. Atakuwa na familia yake tu, karibu kabisa na maji ya bahari, visiwa, samaki, moto na miti. Ila matarajio hayo yote yanakatwa ghafla kana kwamba kibatari mbele ya kimbunga. Familia yake inauawa kwenye moto mkali ulioteketeza nyumba. Biashara yake ya kusafirisha korosho nje ya nchi inakufa, mtaji unakata. . . . Mambo haya yanatukia kwa haraka sana. Yanamwacha Jona katika fikirishi kali maisha yake yakigeuka juu chini, chini juu. Ni ndani ya muda mfupi anapoteza mihimili yake ya maisha. Anageuka kuwa fukara, na ombaomba. . . . Katika kipindi hicho cha ukata mnene, jeshi la polisi likatupa ndoana kwa Jona kumtaka arejee kazini kabla hajafa kibudu. . . . Lakini, ingawa Jona hakuwa na mbele wala nyuma, akakataa kata kata, wakati huo hana hata uhakika wa chakula mezani. Lakini je nani aliyapanga mambo haya yote kwa Jona? Yalitukia tu? . . . Taarifa ya kikosi cha zimamoto na uokoaji, ilisema nyumba iliungua kwa hitilafu za umeme. Sababu ambayo haikukuna kabisa kichwa cha Jona kwani aliamini aliweka makazi yake katika usalama kwa kufunga vifaa vya kuzima umeme punde tu hitilafu inapobainika. . . . Isitoshe, kama ukimuuliza leo hii kwanini biashara yake, iliyoanza kuchanua, ilikufa hatakupa jibu la kueleweka. Hajui. Ni ndani ya juma moja tu, mtandao wake wa biashara ukakata huko Vietnam, mizigo yake ikazuiliwa bandarini na kugubikwa na urasimu mkubwa. . . . Kama haikuwa kipaji chake cha kuchora, hakujua maisha yake yangeenda wapi. Angalau alipata chakula na hata nauli za kumsogeza toka eneo moja kwenda lingine. Japokuwa pesa ilikuwa finyu! Sasa kivipi mtu huyu atalala pasipo kilevi? Kwake, haikuwezekana. Alishuka chini kama embe lidondokavyo mtini. Alikuwa kama bado yu kwenye bumbuwazi. . . . Ikiwa ni kwenye komo la usiku, majira ya saa kumi na moja, gari nyeusi Mark X, inasogea mbele kidogo ya geti la Jona na kusimama. Anashuka mwanamke mmoja mrefu aliyevalia kimini kifupi cheusi na viatu vyenye kisigino kirefu. . . . Mwanamke huyo alikuwa na nywele nyingi alizozikusanya na kuzibana kwa kamba nyekundu, uso wake mnene ulikuwa una miwani ya macho yenye fremu nzito. . . . Aliegemea gari akitazama nyumba ya Jona. Punde akamwona mwanaume huyo akifungua mlango na kutoka ndani. Ilikuwa rahisi kwake kumuona Jona kuliko Jona kumuona kwani yeye alikuwa gizani wakati Jona akiwa kwenye mwanga. . . . Jona alifika getini ndiyo akajua kuna mtu yupo kando. Alishtuka, lakini hakumpa faida hiyo mgeni. Alisogea kwa kujiamini akasimama akimtazama mwanamke aliyekuwa hapo. . . . “Wewe nani?” Aliuliza pasipo salamu. Macho yake yalikuwa mekundu. Alikunja ndita. “Habari yako?” Mwanamke akasalimu kwa sauti tamu. “Nzuri,” Jona akajibu. “Samahani kwa kukusumbua, Jona. Najua huu ndio muda pekee wa kukupata maana umekuwa ukishughulika na kubanwa kwa siku nzima. Kwa jina naitwa Nade, ni mtumishi wa Mheshimiwa Eliakim Mtaja, nimekuja kukufikishia wito wake binafsi kwako. Anakuhitaji. “Ananihitaji kivipi?” Akauliza Jona. “Nadhani ingekuwa vizuri ukaongea naye, sina majibu ya kukuridhisha. Naweza nikakupeleka?” “Hapana, huwezi.” “Jona, sasa mheshimiwa atakupataje?” “Sijui.” “Una simu?” “Hapana.” . . . Mwanamke alifungua gari mlango wa nyuma akatoa Nokia xperia nyeusi akamkabidhi Jona. . . . “Ina kila kitu. Bila shaka mtawasiliana kwa kutumia hiyo.” Jona akapandisha kichwa juu. “Sawa,” alijibu kiufupi. “Naweza nikakupeleka job?” Mwanamke aliuliza. “Hapana,” akajibu Jona. “Nashukuru.” Jona alifika kazini akiwa tayari amechoka. Amechoshwa na mawazo. Hakushika kazi yoyote akitafakari kwa dakika kadhaa. Alitoa kiti ndani akakiweka nje alipoketi kutazama mazingira. Hii ndiyo ilikuwa desturi yake. Kila anapokumbana na jambo analohitaji kulifikiria vema, basi hutafuta mahala tofauti atakapopata hewa safi na kumtoa kwenye mazingira ya mazoea.
Bado mazingira yalikuwa ya giza, giza la asubuhi. Magari yalikuwa yanakatiza barabarani mara kwa mara watu wakienda makazini. Fremu za maduka zilikuwa zinafunguliwa, sauti za milango ya bati zikasikika huku na kule.
Lakini yote hayo hayakutosha kumuondoa Jona fikirani. Alijikuta anasonya kisha akachomoa simu mfukoni, ile aliyokabidhiwa na mwanamke aliyenadi kuagizwa na bwana Eliakimu Mtaja.
Akaifungua na kuzama mtandaoni. Akaperuzi vichwa vya habari vya magazeti apate kujua kinachoendelea nchini na duniani kwa ujumla. Kwa muda mrefu sana hakufanya hilo zoezi. Alijiweka mbali na ulimwengu kabisa, si kwasababu ya kutokuwa na simu bali kwasababu ya kutotaka bughdha za ulimwengu. Aliuchoka, akataka mapumziko. Ila kwa sasa, kwa namna mambo yalivyokuwa yanatukia, aliona kuna haja ya kupitia na kufahamu mambo kadhaa. Pengine anaweza pata jambo muhimu la kumpa mwongozo.
Alipitia vichwa vya magazeti nane. Miongoni mwao kichwa kimoja kikamgonga kichwa na kumpa hamu ya kutaka kujua zaidi. Kichwa hiki kilijirudia kwenye magazeti matano. Kilikuwa kinahusu mauaji ya mfanyabiashara ndani ya jiji la Dar es salaam. “Mfanyabiashara auawa na majambazi.” “Mfanyabiashara, almaarufu Bite wa China, auawa kwa risasi na watu wasiojulikana.” “Majambazi wamvamia na kumuua Bite!” Kusaka undani zaidi wa taarifa hiyo, Jona akazama tena mtandaoni. Akaperuzi blogu kadhaa zilizojaribu kuelezea tukio hilo, hatimaye akakata kiu yake ya habari. Kwa msaada wa picha za mlengwa na taarifaze, aligundua kumbe aliyeuawa ni Beatrice Shauri! Hili likamshtua. Si muda mrefu sana nyuma mwanamke huyo alionana na Jona akamkabidhi kazi ya kufanya aliyoahidi kumlipa pesa nzuri. Bado Jona alikuwa anamkumbuka vizuri mwanamke huyo kwa tabasamu na sauti tamu. Alikumbuka hadi nguo alizokuja nazo siku hiyo alipoingia naye kwenye mahusiano ya kibiashara. Alikuwa amevalia suruali ya jinsi ya kubana na topu ya pinki. Nywele zake zilikuwa fupi, amezikata na kuzirepea vema.
Ameuawa!? Jona aliacha shughuli zake akaufuata ule mzigo wa Beatrice Shauri, akautazama kwa kina. Ni kana kwamba kuna kitu alikuwa anatafuta. Japokuwa kazi hiyo aliifanya yeye mwenyewe kwa mikono yake, ila hakuwa amepata wasaa wa kuiperuzi. Mzigo huo ulikuwa mkubwa. Picha kubwa ya kuchorwa kwa mkono ambayo kama ungeitazama vibaya, basi ungesema imechukuliwa na kamera, tena yenye uwezo wa hali ya juu. Ilikuwa ni picha ya kisiwa kilichozingirwa na maji ya bahari. Kisiwa hicho kilikuwa cha kijani. Kilivutia machoni. Ukitazama vizuri pia hapo hapo pichani utaona ndege wekundu na weupe, upande wa kusini mwa kisiwa, wakiwa wanaruka pamoja. Kulikuwa kuna vialama na viashiria vingi pichani. Jona alishindwa kuving’amua. Kwa mara ya kwanza, wakati anavichora, hakuvijali ila kwa sasa anapata mushkeli na kuumiza kichwa.
“Kwanini hii picha inatafutwa?” alijiuliza. Alitafakari kwa sekunde tano kabla hajaamua jambo kichwani: “Ni lazima itakuwa na mahusiano na kifo cha Bite.”
Akaketi kitini akiendelea kutafakari na picha ipo mkononi. Akili yake ilimwambia kabisa wale watu aliowaona jana usiku nyumbani kwake watakuwa wanahusika na kifo cha Bite kwa namna moja ama nyingine. Lakini je sababu itakuwa ni hii picha? akaitazama tena. Maswali hayo yalikuwa magumu na majibu yake yalihitaji jitihada. Kama kuna siku mwanaume huyu alitamani kurudia kazi yake ya upelelezi basi ni hii. Alitamani kujua zaidi kuhusu Beatrice na ile picha. Alikuja kuondolewa kwenye lindi hilo la mawazo na mlio mkali wa simu. Alikuwa ni Mh. Eliakimu Mtaja. Pasipo kufikiria mara mbili, Jona akapokea na kuitweka sikioni. “Naongea na Johnathan Mchau?” Sauti kavu iliuliza. “Ndiye mimi.” “Kijana, naomba tukutane, nina shida nawe. Nimekutafuta kwa muda mrefu sana.” Jona hakuona tabu, akakubali wakapanga miadi. Bwana Eliakimu alimsisitizia na kumwomba sana asije akakosa. “Nakutegemea sana,” alisema kisha akakata simu. Ilikuwa ni saa moja sasa ya asubuhi. Mwanga wa jua ulishatawala na kuangaza. Haikupita muda mrefu, akaja mwanaume mmoja mfupi rangi maji ya kunde. Macho yake makubwa, ndevu lukuki kwenye taya. Mwanaume huyu anaitwa Jumanne. Ni mfanyakazi mshirika na Jona ndani ya banda moja. Ni maarufu sana kwa uchoraji, haswa michoro ya tingatinga. “Afadhali umekuja,” Jona akasema baada ya salamu. “Kuna mahali nataka kwenda mara moja!” Akaaga na kuondoka na mzigo wa Bite alioupitishia kwenye makazi yake. Baada ya nusu saa akawa ndani ya nyumba kubwa ya kuvutia. Mlinzi alimkaribisha na kumuelekeza mahali pa kukaa punde alipojitambulisha. Ilikuwa ni eneo dogo lililopo kwenye bustani, lina viti na paa dogo la kigae.
Muda si mrefu akatoka mwanaume mnene, mfupi, mweusi mwenye panki. Alikuwa amevalia tisheti nyeupe iliyobinuliwa na kitambi chake kikubwa, bukta na viatu vyepesi.
Akatazama kushoto na kulia kabla hajaenda kukutana na Jona bustanini. Walisalimiana na kujuliana hali kisha wakaelekea kwenye kiini cha mkutano. “Jona, nina shida kubwa, na nimeambiwa wewe ndiye unayeweza kun’saidia. Ni muda mrefu sasa nimeliripoti polisi, lakini naona hamna kitu. Kama bahati tu, afisa mmoja akanambia nikutafute japokuwa alikuwa hana namna yoyote ya kukupata. Alichokuwa anakijua kuhusu wewe ni makazi yako tu, napo hakuwa na uhakika sana.”
Eliakimu akaweka kituo. Jona alikuwa anamsikiliza kwa umakini mkubwa. “Ila naamini yote yatakuwa historia sasa maana nimeshakupata,” Eliakimu akaendelea kunena. “Ni takribani mwezi mmoja sasa tangu mke wangu apotee. Nimemtafuta maeneo yote ninayoyajua, sijampata. Kwao na kwa marafiki zake! Napata mashaka sana juu ya hili. Nahofia usalama na uzima wake. Jona, naomba unisaidie kumpata mke wangu. Nipo radhi kwa gharama yoyote ile ilimradi tu apatikane. Hata kama ameuawa, basi nijue na nani amehusika.” “Mzee,” Jona akaita. “Sidhani kama ninafaa kufanya hiyo kazi. Sipo tayari kwa sasa.” Uzuri bwana Eliakimu alishataarifiwa mapema juu ya ukaidi wa Jona. Mwanaume huyu alikuwa mgumu na mwenye msimamo mkali. Ilikuwa inahitaji roho ya nanga kumbadili fikra na mwenendo. “Jona, nimekuomba hili kama mume anayemhitaji mke wake, baba anayemtafuta mama wa watoto wake. Si kwamba nakupa kazi, la hasha! Tafadhali naomba unisaidie. Nipo radhi kukusaidia kwa namna yoyote ile. Nina mtandao mpana, ninafahamiana na watu lukuki wakubwa. Bila shaka itaweza kukurahisishia kazi.” Uso wa bwana Eliakimu ulikuwa umenyong’onyea. Usingeweza kuamini kama mtu huyu, waziri wa Habari na michezo, angewahi kuja kuomba kitu kwa mtu wa kawaida kiasi hiki. Watu hawa walikuwa wamezoa kutoa amri na maagizo na kisha jambo hutendeka. Ila kwa leo ilikuwa kinyume, alikuwa anaomba, tena kwa unyenyekevu. “Mheshimiwa,” Jona akaita. “Hili jambo si la kukurupukia kabisa, linanihitaji niwe mtulivu. Ningeomba unipatie usiku huu nilitafakari, nitakupa majibu.”
Bwana Eliakimu hakupendezwa sana na hilo jibu. Aliona kama vile Jona ametumia njia ya kistaarabu kukataa ombi lake. Ila hakuwa na namna, alipiga konde, akaamini. “Sawa,” akasema kishingo upande. Jona akanyanyuka na kumpatia mkono wa kwaheri, akahepa zake.
Baada ya robo saa akawa ameshafika kazini. Alimkuta Jumanne akiwa ameketi anabofya kioo cha simu yake kubwa isiyo na jina. “Vipi, kila kitu kipo sawa?” aliuliza. “Shwari tu,” Jumanne akajibu na kuongezea: “Kuna mgeni alikuja kukuulizia. Yani ile we umetoka tu, akaingia.” “Nani?” akauliza Jona akiwa anaketi.
Kwa mujibu wa maelezo ya Jumanne, Jona alipata picha halisi. Mgeni huyo alikuwa ni yule dada aliyekuwa anataka mzigo wa Bite.
“Bonge la ndinga mwanangu alikuja nalo, nikasema yees leo si ndo’ leo!” alisema Jumanne akitabasamu meno yote nje. “Ulivyomwambia sipo akasemaje?” Jona alipeleleza. “Akaniuliza vipi nyumbani kwako, nikamjibu haupo home.”
Jona akawa kimya akitafakari. Tabasamu la Jumanne lilififia akiuliza: “Vipi mzee, kuna usalama?”
Jona hakutaka kumpa mashaka Jumanne. Alilazimisha tabasamu usoni akapachika kiganja begani mwa mwenzake. “Kila kitu kipo sawa, J. Huna haja ya kuhofia.” “Haya bana, ila huyo manzi ni mkali! Nifanyiefanyie basi na mie mwenzako ning’aze.” “Sina hata namba yake. Hatujuani.” “We si ndo’ zako hizo. Wazungu wewe, hadi na wabongo wewe. Sijui mie hawanioni?”
Kidogo Jona akapumzisha akili yake alipokuwa ananena na Jumanne. Walitabasamu na kucheka. Na siku ilikuwa hivyo mpaka jioni walipofunga wakiwa wameingiza USD 900 toka kwa watalii fulani wa kiamerika.
Kama kawaida Jona akapitia bar aliipoketi kwa masaa mawili akinywa Alvaro baridi. Hapa ni mahala pake mahususi pa kupunguzia muda wa kwenda kuwa mpweke nyumbani.
Alipomaliza akajikusanya na kuelekea nyumbani akitembea ado ado. Kichwani alikuwa na fikra mbalimbali zilizokuwa zinakatiza kwa awamu.
Alifika nyumbani, akashika geti. Ajabu likafunguka pasipo kungoja funguo. Moyo wa Jona ukakita, akili yake ilimkimbiza haraka kwenye usalama wa mzigo wa Bite.
Milango yote ilikuwa wazi. Kulikuwa kuna chapa za viatu sakafuni, na mazingira yalikuwa shaghalabaghala kuonyesha upekuzi ulitendeka.
Moja kwa moja akaenda kwanza chumbani kwake karibia na eneo la kabati, akafunua zulia na kukutana na kamlango kadogo alikokafungua na kuzama chini.
Ilikuwa ni handaki. Tena kubwa tu kutosha kabisa sebule na chumba kimoja. Humo kulikuwa kama stoo kwa kujazwa vitu kadha wa kadha.
Jona akawasha taa apate kuona, kisha kama mtu anayejua anachofanya, akanyookea kwenye kona ya handaki.
Akakuta picha ya Bite. Ilikuwa imefunikwa na kitambaa kikubwa ikiwa imetulia kabisa kama ilivyowekwa.
Jona akashusha pumzi ndefu kwanza. Alijihisi amepata amani ya moyo. Alijikuta mpaka anatabasamu mwenyewe.
Aliifunika tena picha kwa kitambaa na kuirejesha palepale alipoiweka. Alipaona hapo ni salama sasa. Mahali anapopaamini panaweza kumhifadhia jambo lake nyeti.
Bila shaka wavamizi hawakuwa wanajua kama ndani ya nyumba hiyo kuna handaki. Kiufupi, hawakuwa wanajua lolote kuhusiana na nyumba hiyo.
Walidhani ni ya kawaida kama zingine, ujinga ambao uliwagharimu. Walimchukulia Jona kiuwepesi, hawakumpa haswa uzito anaostahili.
Nyumba hii japokuwa i ndogo kwa juu ya ardhi, yani kwenye macho ya kawaida ya binadamu, kiuhalisia ilikuwa kubwa sana kutokana na mambo kadha wa kadha yaliyowekwa katika muundo wa siri.
Ukiachana na handaki ambalo nalo lina sebule na chumba, kuta za nyumba hii zina milango nyuma ya makabati ya vyombo na nguo. Huwezi ukalifahamu hili kama hujafundwa. Ukisogeza makabati haya pembeni, unakuta milango ya vyumba vidogo vidogo sana ambavyo vinatunza nyaraka na vifaa vya siri.
Chumba kilichopo nyuma ya kabati la jikoni, kilikuwa kina nyaraka na makabrasha yake muhimu. Pia vitu vingine ambavyo hakutaka kuvipoteza, mathalan vifaa alivyokuwa anachezea marehemu mtoto wake. Na hata pia vile alivyokuwa anavipenda mkewe.
Kwahiyo ndani ungekuta mipira ya kuchezea, midoli, marashi mbalimbali, nguo, viatu na kadhalika.
Chumba cha siri kilichojificha nyuma ya kabati lake la nguo la chumbani, kilikuwa kina silaha tu, na si kingine cha ziada.
Silaha hizi zilipachikwa ukutani zikipangiliwa vema. Zilikuwa ni silaha moto na baridi. Bunduki aina kadha wa kadha, mapanga, visu, mashoka, nondo, jambia na kadhalika.
Ila silaha ya kisu ikiwa imetamalaki kuliko zingine. Kulikuwa kuna visu takribani mia moja! Vya kila aina. Vyenye mipini ya kila rangi na muundo wake.
Hii ndiyo silaha Jona anaipenda. Silaha anayoimudu vema. Silaha ambayo hakuweza kwenda vitani pasipo kurandana nayo.
Jona akishika kisu, ni hatari kuliko akishika bunduki. Kinachomfanya apende silaha ni sababu mbili. Mosi, hufanya kazi pasipo kukoma. Hakuna kusema imeishiwa kama utumiapo bunduki na risasi.
Pili, aliona ndiyo silaha isababishayo maumivu anayoyataka kwa adui. Maumivu ya taratibu. Maumivu makali. Risasi humuondoa mtu haraka. Kuna watu hawastahili kifo cha haraka, aliamini.
Alitoka kwenye handaki akarejeshea vitu kama vilivyokaa, akaenda kuketi sebuleni.
Baada ya kupata picha hiyo sasa alikuwa ametua hofu. Lakini akajitwika mawazo zaidi. Mawazo ambayo aliona yanahitaji ufumbuzi wa haraka.
Alichomoa chupa ya kileo ndani ya jokofu, akamiminia kwenye glasi na kuanza kunywa taratibu akikokotoa mambo kichwani.
Alipomaliza kinywaji kwenye glasi, akabebelea chupa mkononi na kuanza kurandaranda ndani ya nyumba.
Alitazama na kuchambua nyayo za viatu alizozikuta. Alienda nje ya jengo napo akatazama chini. Akaenda pia nje ya uzio.
Akagundua nyumba yake ilivamiwa na watu watatu: mmoja alikuwa mwanamke, mwingine mwanaume. Wa tatu hakujua jinsia yake, yeye alikuwa dereva.
Alijua hilo kwa kutazama alama za viatu vilivyotoka kwenye gari. Upande wa kulia wa gari, viatu vya kike vilitokea, ila kwa nyuma, si kwa dereva, kama ilivyokuwa kwa viatu vya kiume upande wa kushoto wa gari.
Na viatu hivyo vikarudi na kuingia garini kwa mtindo uleule uliotokea. Gari ikarudishwa nyuma na kutimka. Ndiyo maana ikawa rahisi kwa Jona kujua kuwa dereva hakushuka.
Kama gari lingeenda mbele lisirudi lilipotokea, ingemuwia vigumu kujua kuhusu mambo ya dereva, na watu waliotokea nyuma.
Zaidi akagundua ni aina gani ya gari ilikuja hapo. Si nyingine bali ni ile ile Range Rover Sport. Aling’amua kwa ufananisho wa alama za matairi.
Akarudi zake ndani akifunga milango yote. Akaoga na kujilaza kitandani. Hata hakula. Akiwa anangoja usingizi umchukue kwa msaada wa kileo alichopiga, akafanya maamuzi. Aliona ana haja ya kurudi kazini.
Aliona ana hitaji la kufanya jitihada za kuutafuta ukweli uliojificha na kugubika swala la hil la picha na kifo cha Bite.
Lakini pia kumsaidia bwana Eliakimu Mtaja, kumwepusha na hadha ya kuwa kama yeye, asiye na mtu anayempenda, maana uchungu wake anaujua.
Lakini kabla hajaanza kuchambua kivipi atayafanyia kazi hayo mambo, usingizi ukampokonya fahamu. Alijikuta asubuhi ya saa kumi na moja.
Kila yanapofika majira haya usingizi kwake hukata hivyo huamka na kuanza kujiandaa kwa ajili ya kukabiliana na siku mpya.
Alihisi njaa sana, ilimbidi atengeneze na kunywa chai, kitu ambacho si kawaida yake.
Alipika chai na mayai. Kulikuwa kuna ubaridi wa mvua siku hiyo, kwahiyo alitaka apate joto.
Akiwa anakunywa chai, mvua ikaanza kunyesha, tena kubwa haswa. Kwahiyo hata alipomaliza ikambidi angojee kidogo kuona kama itapungua.
Alitazama nje akitumia dirisha la jikoni. Alikagua mazingira ya nyumba kwa macho kama mtu ambaye alikosa cha kufanya.
Mvua ilikuwa inamiminika. Na baridi lilikuwa linaongezeka. Alistaajabu ni kwa namna gani ataenda kazini. Alitamani mvua ile ingemkutia akiwa kazini kama ilivyokuwa hapo juzi, lakini haikuwezekana.
Alirudi zake kitandani akajilaza kwa malengo atafakari sasa alichokiachia njiani jana usiku. Alijifunika shuka na kuangaza darini. Hakukaa muda usingizi ukambeba tena. Hali ya hewa ilimshinikiza. Shuka alilojifunika ukijumlisha na hali ya baridi iliyozuka, hakuweza kujisaidia.
Akalala. Ila usingizi tofauti na ule anaolala kila usiku, usingizi wa kushinikizwa na pombe. Usingizi huu ulikuwa halisi. Usingizi anaoukwepa kila uchwao kwani huwa unamletea matatizo, majinamizi ya kale.
Alidumu kwa takribani dakika kama ishirini usingizini. Mara akaanza kupata njozi. Alijiona akiwa kwenye uwanja wa vita anapambana na watu waliovalia sare za jeshi. Ila hakujua jeshi la wapi.
Watu hawa walikuwa wengi, ila yeye akiwa peke yake. Hakuwa na silaha, alitumia mikono na miguu yake tu. Aliopambana nao walikuwa na bunduki. Lakini akifanikiwa kuwamudu vema.
Alizikwepa risasi. Aliwavunja na kuwatengua maadui pasipo huruma. Alikuwa kila anapommaliza mmoja, anakazana kwenda mbele zaidi kwa kukimbia.
Baada ya muda, akiendekea kupambana kwa juhudi na kusogea mbele, akaona kijumba fulani kidogo, cha mbao chumba ghorofa mbili, umbali wa kama kilomita mbili.
Kijumba hicho kilikuwa kimekaa kwenye mwinuko ulitosha kuona vema kwa chini. Yani kule ambapo yeye na hao watu wengine wanaparangana.
Kwenye sakafu ya ghorofa hiyo, Jona aliona watatu. Hakuwa na uwezo wa kuwaona vizuri, lakini alijua mmoja atakuwa mkewe na mwingine mwanaye.
Alizidi kupambana na kujongea. Kila aliposogea akatupa macho kwenye lile jengo. Punde akaona vizuri. Alikuwa sahihi. Mkewe na mwanaye walikuwepo hapo.
Walikuwa wamefungwa kamba mikono na miguu wakifungwa pia na vinywa. Mwanamke alikuwa amepiga magoti, mtoto akiwa amesimama.
Pembezoni yao alikuwa amesimama mwanajeshi mrefu aliyekuwa amebebelea bunduki ndogo, amewanyooshea mwanamke na mtoto waliofungwa.
Basi Jona akazidi kuchanganyikiwa. Alipambana maradufu. Alizidi kujongea na kujongea. Alipokaribia jengo akasikia sauti kuu inapaza: “Simama hapo hapo, la sivyo nawateketeza hawa washenzi wako!” Akatii. Alisimama na kusalimu amri. Alipigishwa magoti kwa lazima akinyooshewa midomo ya bunduki. Macho yake yalitazama familia yake kwa uchungu. Yalivuja machozi. Alitamani kugeuka malaika akawaokoe lakini hakuweza.
Alijitahidi kuwa mpole awanusuru. Mara giza likagubika asione jambo kabisa. Hakujua limetokea wapi. Punde tu, akasikia milio miwili ya risasi. Pah! – Pah!
Akashtuka toka usingizini akihema kwanguvu. Alikunja ndita. Macho aliyatoa. Alimeza mate akitafakari. Mara akashtushwa na mlio wa simu iliyoita kandokando yake.
Akaichukua na kuitazama. Alikuwa Mh. Eliakimu Mtaja. Akapokea na kuiweka simu sikioni. “Nakuja mheshimiwa!” Akasema na kujinyanyua.
Mvua ilikuwa imepungua, manyunyu tu ndiyo yalikuwa yanarasha. Bado baridi lilikuwa linapuliza tena kwa kiasi kikubwa.
Jona akavaa koti refu jeusi kisha akatoka. Alitumia usafiri wa daladala kwasababu ya mvua. Baada ya lisaa moja akawa amefika nyumbani kwa Mh. Waziri Eliakimu Mtaja. Alipokelewa wakafanyia maongezi ndani ya nyumba.
“Nipo tayari kufanya kazi. Ila kwa masharti kadhaa,” akasema Jona. “Naomba niyasikie,” Mh. Eliakimu akatega sikio asikie vema. “Nataka nifanye kazi hii kwa namna nijuavyo, pasipo kuingiliwa na yeyote yule. Nitakusanya taarifa, nitazichambua, nitazifanyia hariri na kuchukua hatua. Sitahusika na jeshi la polisi, wala sitashirikiana nao. Nitafanya kazi kwa weledi wa siri mkubwa. Na ningependa iwe hivyo mpaka mwisho.
Lakini zaidi, naomba ushirikiano ulio kamili.” Jona akaweka kituo.
Mheshimiwa akashusha pumzi ndefu, akajibu: “Sawa, nimekuelewa na nimeridhia.” Lakini akapendekeza. “Najua kuna muda utakuwa unanihitaji, aidha nikupe baadhi ya taarifa ama nikusaidie kufanya jambo fulani litakalokusaidia. Sasa si kila muda nakuwa na fursa, nakuwa nabanwa na kutingwa na mambo mengi tena muhimu. Hivyo basi, kuna mtu ningependekeza uwe naye karibu. Anajua karibia kila kitu kunihusu.
Atakusaidia sana kwenye kufanya kazi yako.” Aliposema hayo akaita: “Hey!” Mara tokea ndani akaja mwanamke mrefu aliyevalia sketi ya kaki ya kumbana. Topu nyeusi iliyofunikwa na koti jeusi la kifungo kimoja.
Mwanamke huyu hakuwa mgeni mbele ya macho ya Jona. Alimtambua upesi kuwa ndiye yule aliyekuja nyumbani kwake na kumpatia wito wa Mheshimiwa.
Anaitwa Nade.
Uso wake mpana. Nywele zake nyingi anazozibana. Na miwani ya macho yenye fremu nzito nyeusi, vilimtambulisha upesi. Alitambulishwa kwa Jona kama mlinzi binafsi wa Mheshimiwa. Jambo hilo likamshtua kidogo Jona. Hakulitarajia.
Mwanamke huyu hakuonekana kama mlinzi. Alikuwa mrembo sana kuwa mlinzi. Aidha kazi ya ukarani ofisini, au mapokezi hotelini ndizo ambazo ungezifikiria punde ungemwona.
Jona alijiuliza ni nini kilichofanya mwanamke huyo apewe kazi kubwa kiasi hicho. Hiyo ikawa mojawapo ya sababu ya kukubali kufanya naye kazi.
Alitamani kumuona akiwa kazini. Alitamani kuona nini kipo nyuma ya ulimbwende wa mwanamke huyo kikamfanya aaminike.
Cha kwanza alichokifanya Jona ni kuulizia taarifa zote za mtandaoni kumhusu mke wa Mheshimiwa. Alitaka kujua majina na akaunti zake. Asiwe na bahati, Mheshimiwa akawa hajui lolote kuhusu hayo. Cha kufanya Jona akaomba jina kamili kisha akaendelea na mengine ambayo aliona yangeweza kumsaidia kwenye kazi. “Waweza nijuza anapendelea nini? Kwenda wapi? Kufanya nini?” “Anapenda sana kuogelea. Alikuwa anaenda kuogelea kila mwisho wa juma. Pia, ni mtu wa lakshari sana.” “Unaweza ukamuelezea ni mtu wa aina gani kwa ujumla?” “Yah! Muongeaji, mchangamfu, anayependa starehe na kujishughulisha pia.” “Na vipi kuhusu mavazi?” “Aaahm … kwa kifupi anapenda kwenda na wakati.” “Kabila lake?” “Mnyaturu.” “Naomba unipatie picha yake.” Mheshimiwa akaelekea chumbani na kutoka na albamu ya picha, akamkabidhi Jona. Jona akatazama na kuchagua picha tano. “Naweza nikaenda nazo zote hizi?” “Bila shaka,” akajibu Mheshimiwa. “Ana ndugu yeyote hapa Dar?” “Ndio. Shangazi yake anaishi Kimara suka, nyumba namba 102. Na pia mama mdogo yake anaishi Kinondoni, kama nakumbuka vema, ni nyumba namba 52. Ghorofa moja rangi nyeupe. Hao ndiyo ninaowafahamu kwa hapa Dar.” “Kwao ni wapi?” “Arusha; Mianzini.” “Asante sana,” Jona akasimama. “Nadhani nimepata pa kuanzia hii safari.” Wakapeana mikono na Mheshimiwa. “Vipi hautahitaji fedha kufanikisha hili?” Mheshimiwa aliuliza. “Usijali nitakutaarifu punde nitakapokuwa nahitaji msaada,” akasema Jona.
Ila kabla hajaondoka, Mheshimiwa akamuita na kumwambia: “Nahitaji kumpata huyo mwanamke, si kingine. Mtafute na umlete hapa. Usihangaike na mengine kumhusu. Bila shaka tumeelewana.” Jona akaitikia kwa kupandisha na kushusha kichwa chini. Ila uso wake ulikuwa na mashaka.
Kauli ya Mheshimiwa ilimpatia maswali kadhaa. Alijiuliza nini kipo nyuma ya angalizo hilo. Alitoka ndani ya nyumba, akaenda kufuata daladala. Bado hali ya hewa ilikuwa ya manyunyu na baridi pia. Hivyo koti lake lilikuwa na faida.
Alienda kazini akamkuta Jumanne ameketi akifanya kazi fulani kwa mkono. Akamsalimu kisha naye akaketi.
Akatoa simu na kuzama mtandaoni. Akatafuta jina la mke wa Mheshimiwa ndani ya mtandao wa Facebook. “Mariam Jullian,” akaandika hivyo na kusaka. Yakaja majibu mengi mno. Watu kutoka maeneo mbalimbali, ndani ya nje ya nchi.
Ikamchukua muda kumpata aliyekuwa anamuhitaji akitumia mfanano wa picha za mtandaoni na zile alizokuwa nazo.
Akapekua taarifa za mlengwa wake huyo lakini pia picha na matukio. Picha ya mwisho kurushwa mtandaoni humo ilikuwa ni jana yake tu. Hilo jambo likamshangaza Jona. Kumbe mwanamke huyu alikuwa hai, tena mwenye furaha.
Akaipakua picha hiyo aitazame vizuri. Akaikagua mazingira akagundua ni ya hoteli. Alihangaika kujua ni hoteli gani na ipo wapi, ila ndani ya picha ile hakufanikiwa. Akarudi tena mtandaoni na kupekuwa. Akapakua tena picha mbili nyuma ya ile picha ya mwanzo, zote aliona zinarandana mazingira.
Akaanza kuzikagua kwa undani. Katika hizo picha akafanikiwa kumuona mwanamapokezi wa hotel kwa mbali. Ni wazi zilipigwa malangoni mwa hoteli.
Alikuwa ni mwanaume aliyevalia shati jeupe na tai ya mistari mistari. Alikuwa amezingirwa na meza kubwa inayong’aa.
Mbele yake kulikuwa kuna tarakilishi nyeusi isiyo na chogo.
Kwenye picha moja, mfanyakazi huyo alikuwa amefunikwa nusu ya kifua na tarakilishi, ila ya pili kidogo alikuwa wazi. Hiyo Jona ikamfaa.
Akaivuta kwa ndani akilenga kifua cha mfanyakazi huyo. Alipokipata kwa karibu akapata kujua jina la hoteli.
Lilikuwa limeandikwa juu kidogo ya mfuko pamoja na chapa yake.
Ilimchukua umakini Jona kung’amua hilo kwani kuvuta picha kwa ndani kunaharibu ubora wa picha kimuonekano.
Baada ya muda mfupi akawa ameshafika mbele ya hoteli anayoitaka. Akazama ndani mpaka mapokezi.
Bahati akamkuta mwanampokezi yule aliyemuoma pichani, ila alikuwa njiani akitaka kuondoka baada ya kumuachia mwenzake zamu. “Samahani kidogo,” akasema Jona akimsimamisha mlengwa wake. Akachoropoa kitambulisho cha polisi ndani ya koti na kuonyeshea. Kilikuwa kitambulisho feki, ila kwa macho ya raia wa kawaida asingeweza kugundua abadani. Hii ilikuwa ni mojawapo tu ya nyaraka feki alizonazo Jona. Ndani ya ghala lake, anazo nyaraka feki lukuki, kwa kazi lukuki kama mwenyewe asemavyo.
Baada ya kutoka jeshini aliona anahitaji nyaraka hizo ili mambo fulani yaende, nyakati fulani. “Naitwa Inspekta Maganga. Kuna taarifa nazihitaji kutoka kwako.” Mfanyakazi yule wa hotel akaonyesha hofu. Bila shaka hakuzoea madhila za polisi. Aligeuza shingo akamtazama mwenzake aliyemuachia zamu kwa macho ya maulizo. Alikuwa mwanamke mrembo mweupe ndani ya sare. “Karibu, inspekta,” kisha akasema. Wakasogea karibu na kaunta. Wafanyakazi wa hoteli wakajitambulisha.
Inspekta akatoa simu na kumuonyeshea mlengwa wake picha ile ya mke wa Mheshimiwa aliyoipiga karibu na malango. “Nahitaji taarifa za huyu mtu. Alikuja hapa jana majira ya saa nne asubuhi.” Haikuwa ngumu kwa mfanyakazi yule wa hoteli kumng’amua mgeni huyo. Picha ilimsaidia kurejesha kumbukumbu haraka.
Akaendeea tarakilishi na kupekua taarifa za wageni ndani ya muda husika. Punde tu akazipata. “Anaitwa Salome Gerald. Alikuwa ameongozana na mwanaume, kwa jina Mushi Gadi,” akasema mhojiwa. “Ina maana wameshaondoka tayari?” Jona akauliza. “Ndiyo, wameondoka asubuhi na mapema leo hii.” “Wametokea wapi? Na wanaelekea wapi?” “Wametokea Arusha, wanaelekea Iringa,” mhojiwa akasoma taarifa za wageni ndani ya tarakilishi. “Walikuja na usafiri?” “Sijajua. Pengine tungetazama videos za cctv.” Mchakato huo ukawachukua kama nusu saa, Jona akawa amepata kila anachokitaka. Akaaga na kuondoka.
Akiwa ndani ya daladala akaendelea kupekua mtandaoni juu ya mke wa mheshimiwa. Miongoni mwa picha, akamuona mwanaume fulani aliyemtilia shaka. Mwanaume huyu alikuwa amefanana na yule aliyemuona kwenye video hotelini akiwa ameongozana na mke wa mheshimiwa.
Akapakua picha hiyo na kuitunza. Akapakua pia na nyingine iliyoonyesha gari aliloliona pia kwenye video ya hotelini.
Japokuwa picha hizi zilikuwa za muda mrefu nyuma, zilikuwa na manufaa. Zilimfanya Jona apate mwanga kidogo wa jambo lake.
Aligundua mke wa mheshimiwa alikuwa ana mahusiano na yule mwanaume kwa muda mrefu. Akagundua pia Arusha ndipo mahali wanapokuwa mara nyingi.
Zaidi akapata jina alitumialo mwanaume huyo. Japokuwa halikuwa halisi ila angalau litamsaidia mbali na lile feki alilotumia kujisajilia hotelini.
Mwanaume huyu alikuwa anajiita Black Nyokaa mtandaoni. Alilijua hilo kwa kutazama picha moja ya mke wa mheshimiwa aliyomwalika mwanaume huyo.
Basi Jona akazama tena kwenye profaili ya jamaa huyo apekue. Bahati isiwe kwake, hakukuta jambo la maana.
Hata picha haikuwepo, bali jina tu na akaunti tupu.. Alisonya akazima simu. Akaacha sasa kichwa chake kitafakari mambo aliyotoka kuyaona.
Alitafakari mambo hayo nusura apitilizwe na gari. Alikurupuka akashuka na kukwea gari lingine akayookea moja kwa moja kwenye msiba wa Bite.
Akiwa njiani alinunua kofia aliyoivaa kufunika uso wake usitambulike. Alifika eneoni akakuta magari na watu wengi, ilikuwa ni siku ya kuaga kabla mwili haujasafirishwa kwenda nyumbani mkoa wa Morogoro.
Makazi ya Bite yalikuwa makubwa na ya kuvutia. Nyumba yenye uzio mzito mpana. Geti refu jeusi likiwa wazi kukaribisha waombolezaji.
Jona alitafuta eneo akaketi kwanza asome namna mambo yanavyoenda.
Lengo lake hapo lilikuwa ni kutafuta lolote jambo litakalomsaidia kwenye ung’amuzi wake juu ya kinachoendelea kumhusu Bite.
Alijua hatoweza kutoka hapo msibani mtupu, anaweza kupata mwanga angalau akajua nini chanzo cha mauaji ya Bite na kama kina mahusiano na ule mzigo wake alionao.
Penye wengi hapakosi jambo, walisema waswahili. Jona aliamini hilo na ndiyo maana yupo hapa.
Alitazamatazama huku na kule, na hatimaye akapata eneo lililokuwa kijiwe cha stori. Walikuwa wamejikusanya wanaume kadhaa hapo wakiteta.
Akajisogeza taratibu mpaka hapo. Akaketi akitega vema sikio.
Kwa muda mfupi aliokuwa hapo akagundua Bite alikuwa anamiliki kampuni ya magari. Kampuni hii haikuwa na muda mrefu tangu ianzishwe, na mtu aliyeshirikiana naye kuianzisha alishakufa.
Akiwa hapo bado anaendelea kuskiza, akamuona mwanamke fulani ndani ya hijabu. Alimtazama vema mwanamke huyu akamgundua ni yule anayemfuatilia – mwanamke aliyekuwa anataka mzigo wa Bite.
Haraka Jona akanyanyuka na kuhakikisha macho yake hayabanduki toka kwa mwanamke huyo, kila alipoenda ma kuongea na watu akawa anamtazama.
Haikuchukua muda mrefu akamuona huyo mwanamke akiwa anaongea na mwanaume fulani aliyekuwa amempa mgongo.
Mwanaume huyo alikuwa mrefu mwenye mwili wa kujengeka. Kichwa chake hakikuwa na nywele ila mwingi wa ndevu.
Jona alimtazama kwa umakini huyo mwanaume, kichwa chake kikamwambia mwanaume huyo ndiye yule aliyemuona siku ile nje ya nyumba yake wakiwa na Range Rover Sport nyeusi.
Alipata hamu ya kujua hawa watu zaidi, malengo yao haswa ni nini na ni wakina nani. Alihakikisha hawatoi kwenye mboni ya macho yake.
Aliwaweka kwenye uangalizi mpaka mwisho gari lililobebelea jeneza likiondoka. Watu hao wakajipaki kwenye gari lalo, Range Rover na kuhepa.
Jona akakodi pikipiki na kuanza kulifuatilia gari hilo kwa nyuma akilipa umbali kidogo.
Alilifuatilia mpaka maeneo fulani hivi ya Kawe gari hilo lilipoacha njia kuu ya lami na kushika ya vumbi.
Likatembea kwa dakika nane. Hapo sasa dereva kwa urahisi akajua anafuatiliwa. Alikuwa ni yule mwanaume pande la mtu akishikilia usukani.
Mwanamke akatazama nyuma, akaona pikipiki. Alijitahidi kuing’amua sura ya Jona lakini akashindwa, kofia ilimkinga.
Alisonya kisha akauliza; “Ni nani huyu?” Hakukuwa na mwenye majibu. Ila walijua tu hawapo salama, na ni lazima jambo lifanyike.
Dereva akadaka njia zingine za kuchepukia, ndani ya muda mfupi wakatokea baharini, wakasimamisha gari.
Jona naye akasimamisha pikipiki na kuwatazama. Mpaka hapo alikuwa amehisi huenda akawa ameshtukiwa.
Alijifanya anatazama maji ya bahari kwa muda kidogo kisha akakwea tena pikipiki na kupotea.
Pande lile la mtu na mwanamke aliyeongozana naye wakamtazama mpaka alipoyoyoma. Walishindwa kujua nini haswa lengo la huyo mtu, ambaye ni Jona sasa.
Walikaa hapo eneo la bahari kwa muda wa dakika kumi kusoma mambo. Walipojihisi wapo salama, wakaondoka zao, lakini wakiwa waangalifu sana.
Walisogeza chombo mpaka kwenye nyumba namba 89. Nyumba kubwa yenye uzio mrefu. Wakazama ndani na geti kufungwa nyuma yao.
Walijua sasa wapo salama. Waliketi sebuleni wakajadili kuhusu pikipiki ile iliyokuwa inawafuata. “Kuna haja ya kumfikishia taarifa, mkuu?” Akauliza pande la mtu ambaye ndani ya maongezi haya jina lake lilijiweka wazi, Kinoo.
Na la mwanamke lilikuwa Miranda. “Hapana, ni mapema sana,” alijibu Miranda akiliza mifupa ya vidole vyake. Macho yake yalionyesha yupo mbali kifikra. “Tunahitaji kujua kwanza ni nani anayetufuatilia na anahitaji nini,” akaendelea kueleza Miranda. “Endapo tukimwambia mkuu kwa taarifa hizi robo robo, hatatuelewa, atatuona wazembe.” Kukawa kimya kidogo. “Shida ni kwamba tuna maadui wengi, ni ngumu kubashiri,” alisema Miranda. “Ni kweli,” akaitikia Kinoo. “Ila tuna jukumu la kujua ni adui gani ameanza kunyoosha mkono tusije tukawaamsha wengine usingizini.” Miranda akaitikia kwa kutikisa kichwa. Alinyanyuka akaendea chupa ya kinywaji, wiski, akaiweka mezani pamoja na glasi mbili. “Sasa yule mshenzi ameshaenda, nini sasa kinafuata?” Akauliza Kinoo akijinyoosha kuiteka glas ajipatie kinywaji. “Hali inakuwa ngumu zaidi,” akajibu Miranda. Alimimina kinywaji akanywa kwanza fundo moja kupoza koo. “Nani kammaliza Bite? Unajua hilo swali linanitatiza sana,” alisema Miranda akimtazama Kinoo. “Na kamuua kwasababu gani? Amekufa kabla hajatusaidia kupata ile picha na kutufafanulia.” “Picha si ipo kwa yule mchoraji?!” Akasema Kinoo. “Umeipata?” “Hapana, ila angalau tuna uhakika ipo.” Miranda akanywa fundo mbili. “Hata nguvu za kuitafuta hiyo picha zinaniisha,” akasema akitikisa kichwa. “Hapana!” Kinoo akawaka. “Mimi naamini yule mchoraji atakuwa anajua jambo. Sema wewe ndiyo unazingua?” “Mimi?” “Ndio!” “Kivipi nazingua?” “Unamremba sana yule boya, tunajikuta watakatifu sana yani.” “Kwani wewe ulikuwa unatakaje, Kinoo? Tutengeneze kesi zingine? … Si kila kitu chaendeshwa na mdomo wa risasi!” “Sasa kwa hiyo system tutapatia wapi hiyo picha? Tumekagua nyumba nzima hamna kitu! Ukimwomba akupe, hata kwa fedha, hataki! Sasa?” Miranda akashusha pumzi ndefu. Akanywa tena mafundo mawili. “Tujaribu tena,” akashauri. “Unajua nini Kinoo, tatizo ni kwamba nataka kuepuka vyombo vya habari kabisa. Nataka tufanye mambo haya kwa siri, tumalize kwa siri. Unajua mwenyewe namna gani hii ishu ilivyo ngumu.” “Una maanisha nini?” “Endapo hili jambo la huyu mchoraji likivuma, basi wale wabaya wetu watalifahamu, watajua kuna jambo na watalifuatilia.
Huoni kama hapo itakuwa nongwa? Wakifuatilia wakajua ni kuhusu picha, basi watatusumbua zaidi. Watataka kujua kilicho kwenye picha.
Kama waliweza kummaliza Bite kuficha siri, vipi wakisikia kuna jambo litakalovujisha neno?” Kukawa kimya. Kinoo alimalizia kinywaji chake glasini kisha akalaza mgongo kitini. “Miranda,” akaita. “Mimi bana nakuachia hili jambo mwenyewe. Wewe utakavyoona, sawa. Utantaarifu.” “Usijali,” alisema Miranda kisha akanyanyuka. “Leo hatuendi?” Aliuliza. “Wapi?” Kinoo akatoa macho. “Nawe acha uoga, unadhani ni wapi?” Akaangua kicheko. “Ni klabu tu hapo!” “Siendi,” Kinoo akajibu na kuongezea: “Hivi wewe hujachoka enh? Siku nzima msibani na bado unataka kwenda klabu! We kiboko.” Miranda akatabasamu. Akanyanyua chupa kubwa ya wiski na kumiminia mdomoni. “Tena usinikumbushe huo msiba wa kis*nge. Nimekaa hapo kutwa nzima na wala sijapata chochote. Nimepoteza muda tu!” Kinoo akatabasamu. Akanyanyuka na kujinyoosha. “Maisha ndivyo yalivyo. Si kila mara wapata, la hasha! Kuna muda wakosa na kuna muda wapata. Cha msingi ni kutokata tamaa. Tuendelee kupambana.” “Ila roho inaniuma sana, Kinoo,” akasema Miranda akipiga kifua chake ngumi. “Kwanini?” “Kila mara tunazidiwa hatua, kwanini? Ina maana sisi ni wajinga na wazembe kiasi gani?” “Hapana, Miranda. Kila mbwa ana siku yake. Kuna siku wataingia kwenye anga letu. Anga la washenzi. Hakika watajuta!” Kinoo aliposema hivyo akapiga mihayo. Miranda alitabasamu na kumtaka aende akapumzike. “Usiku tuna kazi ya kufanya, bila shaka unakumbuka,” akasema Miranda. “Tena?” “Ndio, kwani iliisha?” “Poa, mida!” Kinoo akatoka ndani, Miranda akaingia chumbani.
Kinoo akaelekea nyuma ya nyumba ambapo kulikuwa kuna chumba kikubwa kilichojitenga ambacho kilifungwa na mlango wa bati.
Akafungua mlango huo kwa kutumia funguo aliyoitwaa dirishani. Akatoa pikipiki moja matata, Ducati Monster nyekundu modeli ya 2016 aliyotia moto na kuhepa nayo.
Alivalia kofia ngumu na uso wake ukazibwa na kioo cheusi cha kofia hivyo ikawa ngumu kumng’amua uso. Lakini Jona alimjua mwanaume huyo upesi. Alikuwa amejibanza kwenye jengo moja karibu sana na jengo alimotoka huyo mwanaume, yaani Kinoo.
Lakini pia na nguo alizovaa Kinoo zilimfanya Jona, mwanaume mwenye macho mabovu ndani ya miwani, amkumbuke na kumtambua kwa usahihi.
Alimtazama Kinoo anavyoyoyoma, kisha akaurudisha uso wake getini mwa jengo. Akatazama kwa muda pasipo kuona jambo.
Akaamua kuondoka, ila akiapa kurudi na kufanyia jengo hilo upelelezi zaidi. Alitaka kujua uhusiano wa hao watu na kifo cha Bite,na picha pia.
Ilimradi sasa alishajua makazi yao, kwake hii ni hatua muhimu kuelekea kupata majibu yake. Hivyo hakupoteza muda.
Akajirudisha nyumbani asiende kazini. Alikoga na kula kisha akapumzika kidogo kabla ya kuanza kuchora picha kadhaa kwenyw makaratasi yake marefu.
Leo hii hakuchorea chumbani, bali sebuleni. Alijivika earphone masikioni akisikiza muziki laini huku akitenda.
Macho yalitazama katatasi, mkono wake ukienda kwa ustadi. Alikuwa anarejelea kwenye kumbukumbu zake, na baada ya muda picha ya mtu sasa ikaonekana vizuri.
Alikuwa ni mwanaume mrefu mwenye mwili mpana. Alikuwa amevalia shati lililobana mwili. Kichwa chake hakikuwa na nywele, ila ndevu lukuki. Alikuwa ni Kinoo! Hata mtoto mdogo angekueleza hivyo kwa kutazama tu mara moja. Kama haitoshi, akachora pia na picha ya Bite vilevile kama alivyoichora awali. Alipomaliza akaketi na kuanza kuitazama picha hiyo kwa umakini kama fumbo. Hakudumu hapo muda mrefu, simu ikamshtua. Akaichomoa mfukoni na kutazama. Ulikuwa ni ujumbe toka kwa Nade.
Kabla hajaujibu ujumbe huo, akajiuliza ni namba ngapi zilizotunzwa ndani ya simu hiyo. Ni mara ya pili sasa amekuwa akiona majina yanatokea katika njia ya kumrahisishia kufahamu.
Ina maana namba hizo zilitunzwa kwa ajili ya matumizi yake? Ndio, akili yake ikamjibu.
Ile simu alikuwa ameandaliwa, na hata watu wa kuwasiliana naye walishaainishwa. Alitumia muda wake kuperuzi majina yaliyotunzwa simuni, akayakuta manne tu. 1. Mh. Eliakimu Mtaja 2. Mama Mdogo (Kinondoni) 3. Nade 4. Shangazi (Kimara)
Ikamshangaza kidogo. Alipewa simu hiyo akiwa hamjui yeyote kati ya hao, labda tu Mheshimiwa. Ina maana watu hao waliwekwa simuni kabla hata hajaipokea? – Hadi Mama Mdogo na Shangazi wa mke wa mheshimiwa!
Alipuuzia maswali hayo akauendea ujumbe wa Nade na kuufungua. “Habari?” Ujumbe uliuliza. “Njema,” Jona akajibu. Hata salio lilikuwa kedekede kwenye simu. “Kuna kitu umepata?” Ujumbe ukaingia. “Ndio,” Jona akaandika, ila kabla hajajibu akasita. Akaufuta ujumbe huo na kuuandika mwingine. “Hapana, bado.” “Kweli?” “Ndio.” Kimya kidogo. “Haya sawa. Naomba unishirikishe utakapopata jambo. Hata kama kidogo. Sawa?” “Sawa.” Jona akaweka simu chini. Alistaajabishwa na namna alivyoulizwa kuhusu upelelezi wake ndani ya masaa machache tu. Alijiuliza ni hofu ama hamu iliyosukuma maswali hayo. Hakutaka kuumiza kichwa chake zaidi. Alifunga zile picha alizokuwa amechora kisha akazipeleka chumbani.
Baadae kwenye majira ya usiku akiwa yupo kitandani, na tayari amejishindilia kilevi, akazama kwenye mtandao wa Facebook na kuanza kuperuzi akaunti ya mke wa mheshimiwa.
Akafungua akaunti yake upesi akiipa jina la Giovanni Lacatte. Akaweka taarifa bandia akijinadi anaishi Italia na anahusika na mitindo mavazi.
Akarusha picha kadhaa za wanawake wanamitindo. Baada ya hapo akadukua akaunti mifumo na mara punde akawa ana wafuasi wengi waliomfuata.
Wafuasi laki tatu! Wafuasi hawa wote walikuwa feki. Ila usingeweza kutambua mpaka uanze kuwatazama.
Alikuwa ni mtu mmoja tu aliyezidishwa mara elfu!
Jona alipoona kila kitu kipo sawa, akamuomba urafiki Mariam Jullian, mke wa Mheshimiwa.
Haikupita muda mrefu, kabla hajaanza kusinzia, ombi lake likakubaliwa. Akiwa amefungua jicho moja, akamtumia Mariam ujumbe.
Waliwasiliana wakitumia lugha ya kiingereza wakijuliana hali. Jona akamlaghai amempemda na angependa kumtumia kutangazia mavazi yake.
Jambo hilo likamvutia sana Mariam. Akaingia mkenge akitaka kufanya kazi hiyo. Ila alishikwa tahadhari, akauliza kama kutakuwa kuna malipo yoyote anayotakiwa kufanya.
Jona akamtoa shaka. Lakini pia kutengeneza mazingira ya ‘kiprofesheno’ hakutaka kuzoeana ghafla na ‘mteja’ wake, akamwambia atamtafuta tena siku za usoni. Mariam akiwa mwenye furaha, akaridhia na kuaga.
Jona alikuwa sasa anasinzia mno. Akaiweka simu kando na kulala. Dakika tano kupita, akashtuka. Alisikia sauti ya mlango wa geti.
Akakurupuka na kusimamisha masikio. . . . Hakusikia kitu. Akaamua kunyanyuka na kwenda mpaka jikoni alipochungulia nje. Hakuona jambo.
Hakuridhika, akatoka nje. Aliangaza kila pande ya nyumba, hamna kitu. Sasa ni nini? Akajiuliza.
Alitulia hapo nje kwa dakika kama tano kama atasikia ama kuona jambo lolote. Hola! Akaamua kujirejesha kitandani na kujilaza.
Haya sasa ni mawenge, si bure. Aliongea na nafsi yake. Kabla hajalala akawaza kuhusu mambo yake anayoyafanyia kazi. Alikumbuka yale yote aliyoyatenda, akagundua siku ilikuwa ndefu sana.
Ndani ya siku hiyo yalitukia mengi. Aliwaza nini kitajiri siku inayofuata. Akiwa dimbwini mwa fikra, usingizi ukambeba sasa pasipo taarifa. — Ndani ya usiku huo huo. Majira ya saa tisa usiku, pembezoni mwa klabu ya usiku ya Masai.
Nje ya uzio ilikuwa imepaki Range Rover sport, ile wanayoitumia Miranda na Kinoo. Gari hiyo ilikuwa imezimwa na haikuwa na mtu ndani yake.
Muda kidogo mbele, Miranda anatoka ndani ya klabu. Alikuwa amevalia gauni fupi jeusi linalobana mwili. Viatu virefu vyekundu.
Nywele zake ndefu za bandia alikuwa amezichana na kuzilazia pembeni. Kwenye mkono wake wa kushoto alikuwa ana kapochi kadogo chekundu. Wa kulia ana funguo ya gari.
Alitazama kushoto na kulia kisha akaminya funguo, gari ikalia na kuwaka taa. Akafungua mlango na kuzama ndani.
Alichoropoa simu ndani ya kipochi, akatuma ujumbe kwa Kinoo. “Fanya fasta, usiuweke usiku.” . . Ndani ya muda mfupi, ujumbe ukaingia kumjibu; . . “Poa najitahidi. Tunaelewana bei.” . . Haikupita muda mrefu, kama dakika tano, Kinoo akatoka naye ndani ya klabu akiwa ameongozana na mwanamke mweupe mrefu mwembamba.
Alikuwa amenyoa upande mmoja, upande mwingine akiwa na nywele ndefu rangi ya bluu. Alitoga kila sikio mara tano na kuvisha hereni.
Alivalia sidiria nyekundu na sketi fupi ya kuchanua rangi ya pinki aliyofananisha na mkoba wake aliouweka begani.
Alikuwa na uso mwembamba usiovutia, ila aliupamba ukawa angalau. Akiwa ameshikwa kiuno na Kinoo, wakaelekea kwenye gari na kupanda, gari likaondoka.
Usingejiumiza kichwa kujua mwanamke huyu alikuwa anajiuza, yani malaya ama tuseme changudoa. . “Hukunambia kama mtakuwa wawili!” Alisema malaya akimtazama Miranda aliyekuwa anaendesha gari. “Unajua mkiwa wawili bei yake ni tofauti.” . . “Nipo peke yangu tu,” akasema Kinoo. “Huyo ahusiki na mambo yetu.” . . Malaya akaitikia kwa kutikisa kichwa akibinua mdomo. Akachoropoa sigara kwenye mkoba. . . “Unataka ufanye nini?” Kinoo aliwahi kumuuliza. Hakungoja jibu, akammarufuku: “Ah! Ah! Huwezi ukavuta sigara humu. Rudisha!” . . Malaya akarudisha sigara akibinua mdomo. . . “Isiwe kesi.” . . . Baada ya muda kidogo wa safari, Miranda akawashusha maeneo ya Kijitonyama Sayansi mbele ya nyumba ndogo yenye uzio. Wakateta kidogo na Kinoo. . . “Hakikisha kila kitu kinaenda sawa,” alisema Miranda akikaza macho. “Si kila kitu unacho?” . . “Ndio, kila kitu kipo,” akajibu Kinoo. . . “Sasa usije ukanogewa ukasahau kazi.” “Haiwezi ikatokea. Kama lini?” . . “Poa. Kesho! Kama kuna lolote, utanchek kwa phone.” . . “Usikonde.” . . “Enjoy!” . . Gari likahepa. Kinoo akatazama kushoto na kulia. Kulikuwa kimya hamna mtu. Akazama na malaya ndani baada ya kufungua geti.
Wakaekea moja kwa moja ndani ya chumba, milango ikifungwa. Wakapata maji na kujilaza kitandani kwa ajili ya kupeana raha.
Walifanya tendo kwa muda wa lisaa. Kila mtu akawa hoi na mwenye kuhitaji kupumzika. Mwanamke akalala usingizi mzito akiwa tayari ameshapokea chake na kukiweka begini. Ila Kinoo alijitahidi sana kuepuka hilo swahibu. Akakaza macho.
Alijua fika akilala itakula kwake. Hawa malaya huwa wanaondoka majira ya saa kumi na moja asubuhi na sasa ilikuwa saa kumi na madakika yake.
Alipohakikisha mwanamke amelala vizuri, akatoka kitandani na kwenda kabatini.
Kulikuwa kuna makabati mawili moja lilikaa karibu na kitanda na lingine karibu na mlango. Lililo karibu na mlango lilikuwa la ukubwa wa kati lenye milango miwili.
Ila lililokaribu na kitanda lilikuwa kubwa na pana. Milango mitatu na kioo kikubwa. Lilikuwa ni la nguo.
Kinoo alifuata hili la mlangoni akapenyeza mkono wake kwa nyuma, akatoka na ufunguo. Akalifungua kabati. Lilikuwa limegawanyika katika vipengele vitano. Cha kwanza kilikuwa kina vitu vilivyokuwa vimefunikwa na makaratasi magumu meusi.
Vingine vilikuwa vina umbo la mstatili, vingine pembe tatu na hata zisizoeleweka. Kwenye makaratasi kulikuwa kuna maandishi madogo ya lugha ya kirusi. Maandishi hayakuwa mengi, yaliandikwa na kupigiwa mstari.
Kipengele cha pili cha kabati kilikuwa kina matambara ya rangi mbalimbali. Hakikuonekana kama kina zaidi ya hapo, labda kama kingepekuliwa.
Cha tatu kilikuwa kina kitambaa kimoja kikubwa cheusi pamoja na chupa moja kubwa ya plastiki yenye kifuniko kama cha pafyumu.
Cha nne hakikuwa na kitu. Kitupu. Vichengachenga tu vya tembe za vidonge ndivyo vilizagaa.
Cha tano kilikuwa kina chupa tatu za kioo. Chupa moja ilikuwa na shingo nyembamba, umbo la pembe tatu na kalio flat. Chupa nyingine ilikuwa na umbo la mstatili na shingo nyembamba kama ile ya kwanza. Na ya tatu vilevile kama hii ya pili.
Zote zilikuwa zina vifuniko vya vyupa.
Chupa hizi zilikuwa zimebandikwa vikaratasi vya rangi visivyo na maneno. Chupa ya kwanza ilikuwa na karatasi ya rangi ya nyeupe. Ya pili rangi ya chungwa. Na ya tatu rangi nyekundu.
Lakini kile kilichomo ndani ya chupa zote hizi, kilikuwa cheupe kama maji. Kwa macho usingeona utofauti.
Kinoo alinyanyua chupa moja baada ya moja, akaitikisa na kuitazama. Baada ya hapo akachukua kitambaa kilichopo kwenye kipengele cha tatu. Akafungua chupa yenye kikaratasi chekundu na kumiminia kwenye kitambaa kimiminika kidogo kilichomo ndani.
Akarudisha chupa na kufunga kabati. Akazima taa na kwenda kitandani. “Hicho kitambaa cha nini?” Akashtuka kusikia hilo swali. Kumbe mwanamke alikuwa macho na alimuona.
Hakuwa sasa na cha kueleza wala muda wa kupoteza, akamdaka mwanamke na kumziba mdomo na pua kwa kitambaa.
Mwanamke akatapatapa kutafuta hewa. Alijaribu kujichoropoa, lakini hakufanikiwa abadani. Hakuweza kupambana na nguvu za mwanaume Kinoo.
Baada ya dakika tatu akawa kimya tuli akiwa amefumba macho. Kinoo akammwagia pembeni. “Shenzi!” Akasonya. Alirudisha kitambaa kabatini na kulifunga. Akaunyanyua mwili wa malaya yule na kuupeleka kwenye chumba fulani kidogo alipoulaza chini kisha akatoka.
Chumba hichi kilikuwa cheupe kisafi. Hakikuwa na kitu chochote kile. Kilikuwa kina dirisha dogo lililokuwa juu kabisa.
Kinoo alirejea akiwa amebebelea kamera yenye miguu mirefu mitatu. Akaisimamisha na kuiwasha, akaielekezea kwa mwanamke yule chini.
Alipoona inamchukua vema, akatoka na kwenda zake chumbani alipozima taa na kujifunika shuka akalala.
Asubuhi, kwenye majira ya saa nne, akaamshwa na honi kali huko nje. Akakurupuka. Macho yake yalikuwa mekundu kwa kulewa usingizi.
Alijinyanyua akaenda nje. Alijua atakuwa Miranda, na kweli. Akafungua geti Miranda akaingia ndani. “Vipi? Kila kitu kipo shwari?” Aliuliza Miranda wakitembea kuelekea ndani ya sebule. . . “Kila kitu kipo poa. Nimefanya kama maagizo yanavyosema,” akaeleza Kinoo. . . “Enhe, ikawaje?” Miranda akauliza kwa shauku. Walishafika sasa sebuleni wakaketi kwenye sofa. . . “Sijatazama imekuaje. Unajua nilikuwa nimechoka sana. Hapa unavyoniona ndiyo umeniamsha wewe. Nimelala saa kumi na mbili kasoro!” Miranda akanyanyuka. . . “Twende ukanionyeshe,” akaamuru. Akaongozana na Kinoo mpaka kwenye kile chumba kutazama.
Walifungua wakapokelewa na harufu kali. Walikunja nyuso wakaziba pua. . . “Imefanya kazi.” Alisema Miranda akitikisa kichwa. Sauti yake haikusikika vema kwasababu ya kujiziba.
Mbele yao kulikuwa kuna kitu cheusi kisichoeleweka. Ni palepale alipowekwa yule malaya masaa kadhaa nyuma, sasa hivi palikuwa pana chembechembe nyeusi nyingi mno.
Huwezi ukadhani kama binadamu alikuwa hivyo. Ni ngumu kuamini.
Chembechembe hizo zilikuwa zinatoa harufu mithili ya pafyumu kali iliyooza ama kuchacha. Harufu hiyo ilikuwa nyepesi na kali kiasi cha kukutoa machozi ukiivuta mara mbili tu.
Kinoo aliitwaa kamera wakatoka ndani ya chumba kwenda sebuleni. Wakaketi, Miranda akaanza kutazama nini kilichotukia. Kinoo alijitahidi kutazama, ila usingizi ulimmeza ndani ya muda mfupi. Hakuweza kudumu kuendelea kukodoa. Alikuwa na usingizi mzito. Aliachama mdomo wakati Miranda akifuatilia video kwa umakini. Mara nyingine akiipeleka mbele ama kuirudisha nyuma asipitwe na mambo muhimu.
Alipomaliza kuitazama akajikuta anatabasamu. . . “Kinoo, hii ni kabambe!” Akasema akitikisa kichwa. “Imechukua dakika kumi tu, mwili wote umebadilika na kusahaulika! Hakika mkuu ataifurahia.” . . Kimya. Alitazama akamuona Kinoo amelala. Akasonya akisimama. Akaaga kana kwamba Kinoo anamsikia kisha akaenda zake.
Alijiweka kwenye gari akarudi kwenye makazi yake, Kawe. Alikuwa amebebelea kamera aliyokuwa anaitumia kutazamia video.
Alipoingia ndani akanyanyua simu ya mezani akatia namba na kupiga. . . . “Hello, I’ve got good news to tell!” (Helo, nimepata taarifa nzuri za kuongelea) . . Alisema kisha akatabasamu. . . “Yes, it’s about the chemical. The red one’s proved its worth.” (Ndio, ni kuhusu kemikali. Nyekundu imethibithisha thamani yake.) . . “Really. I am going to write a report about it. Expect my email at night.” (Kweli. Naenda kuiandikia taarifa. Tegemea barua pepe yangu usiku.) . . “Ok, later then.” (Sawa, baadae basi.) . . . Akakata simu kisha akashusha pumzi ndefu. Akaenda chumbani akiacha kila kitu sebuleni. Hakukaa muda mrefu chumbani akarejea akiwa amevalia bukta nyeusi na blauzi nyeupe. Akaangaza mezani, hakuona kamera. Moyo ukamlipuka! Hakukaa vizuri akaona mlango wa sebuleni upo wazi. Akili ikamtonya, nimevamiwa!
Haraka akakimbia kufuata meza ya kulia chakula, chiniye akanyofoa bunduki ndogo. Macho yake yakaanza kuambaa ambaa huku masikio yake yakifanya kazi ya kushurutisha sauti ya kila kitu.
Taratibu alikuwa anaufuta mlango wa sebule kwa tahadhari ya kiwango cha juu. . Aliufungua kwa mguu wake wa kushoto akanyooshea bunduki nje, mara mkono wake ukapigwa teke, bunduki ikaponyoka mkono na kurukia mbali. Alikuwa ni mwanaume mrefu aliyevalia suti na kinyago cheusi cha fuvu la kichwa cha binadamu. Mkono wake wa kushoto alikuwa ameshikilia kamera, ile aliyoweka Miranda mezani, huku akiwa hana silaha yoyote. Kwa tahadhari aliweka kamera chini kisha akajipanga kwa ajili ya pambano, Miranda pia. Wakakunja ngumi kila mmoja akimvizia mwenzake awe wa kwanza kufungua mchezo.
Miranda aliitazama kamera kiwizi. Alikokotoa na umbali wa silaha yake ilipo. Aliwaza namna gani ya kufanya avipate vyote kwa pamoja. Adui yake alikuwa anawaza namna gani ya kufanya apate mwanya wa kuhepa na kamera.
Hilo ndilo lilikuwa lengo lake, kamera tu! Hakuwa na haja na kingine chochote. Alijua fika kamera ile itakuwa na jambo muhimu, jambo ambalo litakuwa na soko huko anapotaka kuipeleka.
Ila je, mkono wa mwanamke Miranda, utamruhusu?
Akapima zogo kwa kurusha ngumi, Miranda akakwepa na kutupa yake, ikapanguliwa. Akatupa tena nyingine na nyingine, zote zikapanguliwa na mwanaume mvamizi kisha kukawa tena kimya. Wakitegeana.
Mara hii Miranda hakungoja tena kwa muda, akarusha mateke mfululizo. Alijitupa hewani na kufungua nyonga zake. Mvamizi akajituma kukwepa kwa ustadi, kisha akautafuta mwanya na kumpatia Miranda teke la mgongoni lililomtupia chini. Miranda akanyanyuka upesi. Akakunja ngumi na kumjongea mvamizi. Alishajua sasa anapambana na mtu wa aina gani, mtu mtaalamu mwenye uwezo, hivyo ilibidi awe mwangalifu zaidi.
Hakurusha ngumi wala teke, akangoja. Mvamizi akautuma mwili kwa ngumi mbili, kisha teke, ngumi tatu na teke la kujifungua, vyote Miranda akakwepa kana kwamba alikuwa na miadi navyo.
Mvamizi aliporusha teke la kujikusanya, Miranda akaona sasa fursa ya kushambulia, upesi akainama kukwepa na kuufyeka mguu uliokuwa umemsimamisha mvamizi. Mvamizi akadondoka chini. Ila upesi akajifyatua na mikono yake akasimama.
Akanguruma kwa hasira. Alikuwa amechukia. Pasipo kujua huo ukawa mtaji wa mafanikio kwa Miranda. Alitupa ngumi na mateke kwa fujo. Miranda akakwepa kwa kasi. Takribani ngumi na mateke ishirini yakavuka yakipita pembeni ya masikio ya mwanamke huyo aliyekuwa mwepesi kuepusha kichwa chake, wakati huo kichwani akitafakari namna ya kushambulia. Muda ulipowadia, mvamizi akajaa kwenye rada. Alirusha teke la mguu wake wa kushoto, Miranda akalidaka kwa mikono yake miwili. Mvamizi akataka kutuma teke la kulia kwa kutumia balansi ya mguu wa kushoto ulioshikwa na Miranda, akaula wa chuya.
Akiwa hewani amejifyatua, Miranda akamsukuma, alafu kufumba na kufumbua akajituma hewani na kumpa teke kali alilolituma kwa nguvu zake zote, mwanaume akajikuta yupo chini akiugulia maumivu makali.
Haraka Miranda akachumpa samasoti kuifuata bunduki. Akaiokota na kumnyooshea mvamizi, ajabu mvamizi naye alikuwa tayari ameshainyaka kamera na kuitia mkononi. “Ukifyatua tu, naiachia ipasuke! Ni wewe ndiye utakuwa na hasara ikiharibika.” Mvamizi akatishia. Alikuwa amenyoosha mkono wake wa kushoto akiishikilia kamera kwa kidole kimoja.
Miranda akatulia kwanza akifikiria cha kwanza. Hakuharakisha kufyatua risasi, maana aliona anaweza akakosa anachokipigania japokuwa uwezekano ulikuwa mdogo. “Weka bunduki chini!” Mvamizi akaamuru. “Nimesema weka bunduki chini kabla sijaitupa kamera!” akarudia akitishia kwa kuchezesha kamera kidoleni. Miranda akamwomba asifanye hivyo kwani anatii agizo.
Taratibu akainama akijifanya anataka weka silaha chini, ila akilini mwake alikuwa amepanga jambo. Kabla hajapata mwanya wa kulifanya, honi ikaita huko nje ya uzio! Wote wakatazama getini upesi kana kwamba wataona kitu. Mvamizi akajua sasa usalama wake unazidi kuwa finyu ya wembamba wa nyufa, na alitakiwa afanye jambo upesi kujing’amua. Hakuwa na budi bali kuituma kamera. Uhai wake ulikuwa muhimu kuliko kanda ya kifaa hicho.
Akairushia mbali ya kulia mwa Miranda. Upande wa mkono ule ule ambao mwanamke huyo alikuwa amebebelea bunduki. Haraka Miranda akaikimbilia na kuinyaka mithili ya kipa mashuhuri. Mpaka chini akadondoka nayo akijigeuzia mgongo. Kurusha macho kwa mvamizi, akastaajabu kumuona yupo hewani anavuka ukuta! Akarusha risasi tatu haraka. Ila hazikufanikiwa, mvamizi akatua upande wa pili akakimbia.
Punde, loki ya geti dogo ikavunjwa kwa teke kali akaingia Kinoo akiwa amebebelea bunduki ndogo. Aliangaza macho yake huku na huko, akamuona Miranda chini akiwa na kamera na bunduki. Haraka akamfuata. “Vipi, kuna nini?” “Ninyanyue twende ndani,” Miranda akasema akikunja sura kwa hisia za maumivu.
Kinoo akambeba na kwenda naye ndani, akamuweka kwenye kochi. Miranda akamueleza yale yote yaliyotukia. “Miranda, si salama tena kukaa hapa,” alisema Kinoo akitikisa kichwa. “Kama wameshapajua, basi hili halitakuwa tukio la mwisho!” “Kinoo,” Miranda akaita. “Unadhani walikuwa hawajui hapo kabla kama naishi hapa?” “Ndio! Mbona hayakutukia haya?” “Hapana, mimi siamini.” Miranda akabinua mdomo. “Walikuwa wanajua, ila hawakuwa na sababu.” “Umemsahau yule jamaa aliyekuwa anatufuatilia kwenye bodaboda?” Kinoo akakumbushia akinyooshea kidole hewa. “Huoni kama haya matukio yanafuatana? Yule aliyekuwa kwenye boda ndiye huyu ambaye amekuja kutuvamia. Na itakuwa siku ile alijua haya makazi. Yani hatukufanikiwa kumpoteza maboya,” Kinoo akafafanua.
Miranda akakaa kimya kwanza akitafakari. Alimuomba Kinoo amletee kinywaji, Kinoo akatii kwa kumletea chupa moja kubwa ya mvinyo. Mwanamke akaidaka na kuanza kuinywa kama samaki. Alipopumzika, akasema: “Kinoo, hawa watu wanatupanda kichwani. Kitu kinachonipa presha ni kwamba wanapataje taarifa, ina maanisha wanatufuatilia. Tena kwa ukaribu.
Huyu mvamizi amejuaje kama nina kamera. Kuja kwake hapa ilikuwa ni sababu ya kamera tu, ndiyo maana alipoikwapua, alikuwa anahangaika kuondoka.
Ina maana alituona tukitoka na yule mwanamke kule klabu? Ina maana aliniona nikitoka na kamera kule kwako?
Hivi umeshajiuliza haya maswali?” “Nilikuambia mapema, Miranda. Tunahitaji kumwambia mkuu. Si mpaka maji yakomee shingoni,” akasema Kinoo. “Sijakataa kumwambia mkuu, Kinoo. Ila basi tuwe na maelezo ya kueleweka. Anyway, leo nitamwambia yaliyotukia. Bila shaka tunahitaji ulinzi zaidi.” “Utamwambia saa ngapi?” “Nikimtumia mrejesho wa zile kemikali.” “Inabidi tujiandae.” “Na nini?” “Kazi! Unajua tukituma taarifa kama hiyo kazi huja.” “Hujazoea tu kazi, Kinoo?” Kinoo akatabasamu. “N’taachaje kuzoea sasa,” akasema. Naye akachukua chupa ya mvinyo na kugida. . . . . *** . . . . Isingekuwa simu kuita, Jona asingeshtuka na kutoa macho yake kwenye kibao kikavu alichokuwa anapaka rangi.
Alikunja ndita akikodoa macho ndani ya miwani yake. Aliikwapua simu na kuitazama. Nade! Akasonya na kuiweka simu pembeni kisha akaendelea na kazi zake kama kawaida.
Simu ikaendelea kuita na kuita. Aliipuzia akaendelea na kazi zake kama kawaida.
Siku hiyo alikuwa ametingwa na kazi na tangu asubuhi na hakuwa na muda wa kupumzika. Alikuwa na kazi kama tatu hivi, kama si za kuzimaliza basi za kuzifikisha mahala fulani. Kazi hizo zilikuwa ni za michoro ya kawaida, michoro ambayo anaweza kuifanya, kama ingelikuwa ni ya tingatinga basi Jumanne angelimsaidia.
Sasa ilikuwa ni majira ya saa sita mchana na ni kazi moja tu ndiyo alikuwa ameshaichorea ramani.
Siku yake ilikuwa imebanwa kiasi kwamba hata simu hakushika, wala hakutaka kuishika.
Jumbe kadhaa zilikuwa zimeingia, za kawaida na za mtandao wa Facebook ila hakupata wasaa wa kuzisoma.
Ilipofika majira ya saa nane mchana, akiwa hata hajala, mgeni akaingia ndani ya fremu yake. Ila haraka akadakwa na Jumanne. Alikuwa ni mwanamke. Jona alijua hilo kwa sauti kwani hakuwa na muda wa kutazama.
Ila punde akiendelea kusikia sauti hiyo ikiendelea kuongea na Jumanne, akaing’amua si ngeni.
Akatazama, akamuona Nade. Alistaajabu amepajuaje hapo. Aliacha shughuli yake akamtazama mwanamke huyo aliyekuwa amevalia taiti ya zambarau na tisheti nyeusi.
Miguuni alikuwa amevalia raba nyeusi na kama kawaida alikuwa amevalia miwani yenye fremu kubwa nyeusi, nywele zake ndefu zikiwa zimelala. . . . “Habari, Jona!” Akasalimu. Jona akashusha kwanza pumzi ndefu. . . “Njema, karibu,” . . “Ni mgeni wako?” Jumanne akauliza. . . “Ndio, wa kwangu,” Jona akajibu upesi. . . “Duh! Haya bana. Acha mie mtazamaji nikae kando.” Jumanne akatania, Jona akatabasamu. Alienda zake banda lingine na kumwacha Nade na Jona peke yao. . . “Karibu.” . . “Ahsante, samahani kwa usumbufu Jona.” . . “Pasipo samahani.” “Nilijaribu sana kukutafuta kwa simu lakini haukuwa unapokea, ndiyo maana nikaja hapa.” . . “Umepajuaje hapa?” . . Nade akatabasamu. . . “Ni mtafuta cha uvunguni tu,” akajibu akiminya macho yake kana kwamba anakonyeza. . . “Enhe, kuna kipya?”Jona akauliza. Uso wake haukuwa na tembe ya masikhara. Hakutaka kupoteza muda kwa kazi alizonazo.
Nade akaguna. . . “Sina. Nimekuja kutafuta hilo jipya kwako.” Jona akatikisa kichwa. Akiwa ameshika brashi yake ya rangi akaendelea kuchora kwa sekunde ishirini kana kwamba hana mgeni.
Alikuwa anafikiria jambo kichwani. Japokuwa macho yake yalikuwa juu ya ubao, akili yake ilikuwa inahangaika. . . Akaita: . . “Nade!” pasipo kung’oa macho yake kwenye kibao. . . “Abee!” Nade akaitika. . . “Kuna kitu wewe na Mheshimiwa mnanificha.” . . Nade akanyamaza kwanza asiwahi kujibu. . . “Kitu gani, Jona?” . . “Mnajua wewe na mheshimiwa. Ni kipi hicho?” . . “Mbona hamna!” . . “Una uhakika na usemalo?” . . “Ndio. Nina uhakika.” . . “Ni nini kinawasumbua hivi? Ni kitu gani hamtaki nijue?” . . “Hamna kitu, Jona. Kwanini unawaza hivyo?” . . “Kwanini unanifuatilia hivyo?” . . “Nakuf … kivipi?” . . “Nade, embu tuache kufanyana watoto. Kuna jambo kati yako na mheshimiwa.” Jona akaacha kuchora, akamtazama Nade machoni. . . “Kuna jambo mnanificha. Kuna jambo mnaepuka nisilijue. Ni bora mkaniambia mapema. “
Nade akawa kimya akimtazama Jona. Mara akanyanyuka. . . “Naona leo haupo kwenye mood. Naomba niende.” Jona akatikisa kichwa kisha akaendelea na kazi yake ya kuchora. “Nitakapokigundua mtakuwa mmechelewa.” . . Nade asiseme jambo, akatoka ndani. Akaenda kwenye gari, Toyota Harrier, nyeusi alipojiweka na kufunga mlango.
Ndani ya gari alikuwa mwenyewe. Alijilaza kwenye kiti kabla hajatoa simu yake mfukoni na kupiga.
Fanzhèng wo yào ta si!” (Nataka afe kwa njia yoyote ile!) Mwanaume mezani akasisitizia.
Mwanaume ndani ya suti akaitikia tena kwa kutikisa kichwa. . . . “Shì de xiansheng!” (Ndio, mkuu!) . . . Haraka akatoka ndani ya chumba akiwa haamini kama ametoka na pumzi yake. Alihema kwanguvu jasho likimchuruza. . . . ENDELEA… .
Aliendea gari lake akajiweka na kutoka ndani ya eneo hilo mpaka kwenye bangaloo iliyokuwa umbali wa kama kilomita tatu toka kwenye yale makazi alipofikishia taarifa.
Huko akakutana na wenzake wanne ambao alijumuika nao kwenye kunywa ulabu na kuvuta shisha iliyopo katikati ikiwa imezungukwa na kochi kubwa rangi nyekundu lililokuwa limejikunja kutengeneza umbo la ‘c’. Mwanaume mmoja alikuwa mwenye asili ya Uchina; nywele nyeusi, macho madogo na umbo dogo pia, alikuwa anajulikana kwa jina la Lee. Alikuwa mchangamfu na akiongea lugha ya Kiswahili kwa ufasaha kasoro tu lafudhi. Wengine watatu walikuwa weusi ila wenye maumbo makubwa. Mmoja aliyekuwa amenyoa panki, pia akiwa na ndevu za duara, alikuwa anaitwa Mombo. Macho yake yalikuwa makubwa na sauti yake nzito.
Mwingine alikuwa ana nywele hafifu kichwani, vichengachenga vya ndevu vya hapa na pale kidevuni. Mdomo wake ulikuwa mpana, sauti yake ikikwaruza kana kwamba amekula chokaa. Jina lake Devi.
Wa mwisho yeye hakuwa na ndevu bali afro kubwa nyeusi ti! Alikuwa mwembamba mwenye macho mekundu malegevu. Mdomo wake mkavu mweusi kama kunguru. Aliitwa Nigaa. Alikuwa ndiye anayeshikilia bomba la shisha mara nyingi kuliko wenzake. Walipeana salamu kwa kugusanisha mabega yao kabla mwanaume huyu aliyevalia suti nyeusi kuketi na kuanza kuwapasha wenzake habari namna mambo yalivyotukia. Kwenye haya maongezi, alitambulishwa kwa jina la Bigo. . . “Una kazi nyepesi sana, Bigo,” akasema Devi na sauti yake inayotesa masikio. “Yani unahangaika na mchoraji?! Raha iliyoje. Si unammaliza ndani ya sekunde moja tu!” Wenzake wakamuunga mkono. . . “Yani kama ungeuawa kwasababu ya kushindwa kumuua mchoraji, kingekuwa ni kifo cha kizembe sana. Au una mpango wa kwenda mbinguni, Bigo?” Alisema Nigaa. Lee akaangua kicheko kikali wakati wenzake wakiishia kutabasamu.
Mchina huyu ungeweza kumdhania kama mtu mpole wa pendo, na asiye na tatizo na watu. Mkarimu, mtulivu na mwenye kupenda kufurahi. Ila kiuhalisia, hayo yote yangekuwa uongo kupitiliza.
Mwanaume huyu mwenye asili ya huko mashariki ya mbali mwa dunia, alikuwa ni miongoni mwa watu wauaji wakubwa kabisa kupata kutokea duniani. Alikuwa mkatili na mwenye upungufu wa huruma mwilini pindi awapo eneo la kazi.
Si tu kwa hapa Tanzania, bali hata huko kwao Uchina. Alishaua watu wengi kiasi kwamba hakumbuki tena idadi. Anaweza akamuua mtu lisaa limoja nyuma kisha akasahau hata uso wake!
Miaka ishirini na mitano huko nyuma, mchina huyu aliokotwa akiwa mdogo kabisa katikati ya jiji la Hongkong akiwa anazurura, hana makazi. Akalelewa katika familia ya Wu akichangamana na wenzake ambao nao pia waliokotwa ama kutekwa maeneo mbalimbali ya Uchina. Takribani walikuwa mia mbili, wavulana kwa wasichana. Walihudumiwa vema kwa chakula na sehemu za kupumzikia. Ila walikuwa wanapewa mafunzo ya kupambana, mafunzo ya kufa ama kupona.
Walifundishwa namna ya kuua, na wakapandikiziwa roho mbaya ya unyama. Walifundwa kutokujali wala kutokuwa na rafiki. Ilipogundulikana mtoto mmoja ana urafiki na mwingine, basi alijaribiwa kwa kupewa pambano apambane na mwenzake mpaka pale kifo kitakapo watenganisha.
Japokuwa walikula na kulala mahali pazuri, mazoezi haya yaliwafanya wawe wapweke kwa muda mwingi. Kutokuwa na furaha, wala amani. Ila kwa upande wa familia ya Wu, hiyo ilikuwa sherehe kubwa. Lengo lao lilikuwa linatimia. Walifanikiwa kuwaandaa watoto waliokuja kurithi mikoba ya wauaji waliosambaa ulimwenguni kote wakifanya hili ama lile kwa manufaa ya familia ya Wu. Miongoni mwa watoto mia mbili, ni watoto thelathini tu ndiyo ambao walifanikiwa kukua na kuungana na jeshi, wengine wakienda na maji! Miongoni mwa watoto hao waliofanikiwa, alikuwa ni huyu Lee Sun. Mtambo wa mauti wa familia ya Wu.
Kabla hata hajaenda kwenye uwanja wa mapambano, huko ‘duniani’, alikuwa tayari ameshanyofoa uhai wa binadamu kumi na tano. Wote wakiwa watoto wenzake ndani ya mafunzo.
Kazi yake ya kwanza ilikuwa ndani ya jiji la Hongkong, baadaye Bangkok, Thailand na kisha Rabat, Morocco. Kote huko akifanya kazi moja tu, kuua pasipo mjadala. Alikuwa anakabidhiwa picha ya mlengwa na makazi yake, kisha yeye anaenda kumaliza kazi. Baada ya mafanikio ya shughuli zake hizo, ndipo akahamishiwa Dar es salaam kuipa nguvu makao yao mapya yaliyoanza kumea ndani ya Afrika ya mashariki. . . . “Si kwamba nimeshindwa kumuua, ila majira ya kumuua. Unadhani ningemmaliza pale mgahawani polisi alipokuwapo ingekuaje?” aliuliza Bigo, kisha akaendeleza soga: “Hata tuseme ningemmaliza na polisi pia, huoni kama ingekuwa msala mkubwa – kuchoma utambi mapema hivyo?” . . Lee akatikisa kichwa. . . “Ndiyo maana umeachwa hai la sivyo ungeshakuwa historia sasa, Bigo. Ila ndani ya siku hizo mbili hakikisha unamaliza hiyo kazi. Kama utakwama, usisite kututaarifu. Twaweza kutoa msaada.” . . “Msijali,” Bigo akasema akitikisa kichwa. “Ni kazi ya mkono mmoja tu, sidhani kama nahitaji mkono mwingine wa ziada.”
*** Kwa mujibu wa saa ya mkononi ya Jona, ilikuwa ni saa moja na dakika nane jioni. Kwa kiasi kikubwa alikuwa amesogeza kazi zake ‘lukuki’ na sasa alikuwa akifunga ajirudishe nyumbani kwa ajili ya mapumziko.
Jumanne alikuwa tayari ameshaondoka, hivyo alikuwa mwenyewe. Kwenye mkono wake wa kuume alikuwa amebebelea mfuko mweupe wa Rambo wenye chapa nyekundu, ndani ukiwa umejazwa na baadhi ya vitu.
Alipanda bodaboda, kama ilivyo kawaida yake mara kwa mara, akaenda moja kwa moja mpaka kwenye bar karibu na makazi yake alipojiweka na kuagiza kinywaji laini kisicho na kilevi.
Akiwa anangojea kinywaji, alichomoa simu yake mfukoni akaitazama. Kulikuwa kuna ujumbe kwenye mtandao wa Facebook toka kwa mwanamke fulani ambaye hakumtambua kwa haraka. Mwanamke huyo alikuwa anampa salamu akiambatanisha na vimdoli vitatu vinavyotabasamu. Kabla hajamjibu mwanamke huyo, akaenda kutembelea kwanza ‘profile’ yake. Kwa mujibu wa maelezo aliyoyakuta huko, mwanamke huyu alikuwa ni raia wa Afrika ya kusini. Mjasiriamali anayejihusisha na mauzo ya nguo akimiliki maduka kadhaa ndani ya jiji la Pretoria.
Hakufanikiwa kuona uso wake kwakuwa hakuwa ametuma picha yake hata moja, bali bidhaa zake anazoziuza. Kilichomfanya akajua kuwa ni mwanamke ni jina la mtu huyo na uchaguzi wa jinsia aliouteua kwenye ‘setting’ yake, ‘Female’. Akamjibu salamu yake kwa ufupi, kisha akaacha aone ni nini kitatokea. Punde kinywaji nacho kikaja akakinyaka na kuanza kunywa. Akaagiza pia na chakula ale hapo hapo ili amalize kila kitu kabla hajaenda zake nyumbani ambapo alilenga atajipumzisha moja kwa moja kutokana na uchovu aliokuwa nao.
Alikula na kunywa akisahau kabisa kuhusu simu. Alipomaliza akalipia chakula na kwenda zake nyumbani. Alioga kisha akaendea jokofu kuchomoa chupa kubwa ya kilevi na kuketi kitandani. Hakuwa na mawazo mazito kichwani, alijitahidi kujipuuzisha. Alikunywa kileo chake taratibu macho yake yakiwanda wanda ndani ya nyumba yake pweke.
Haikupita muda mrefu, simu yake ikaita. Alikuwa ni mheshimiwa. Alisita kupokea akijiuliza. Ila akaamua kukata shauri na kuiweka sikioni. . . “Kesho, majira ya saa tano asubuhi naomba tuonane nyumbani kwangu,” sauti ya mheshimiwa ilinguruma. Kabla Jona hajaongea, simu ikakata. Jona akajikuta anatabasamu akitikisa kichwa chake. Akanywa mafundo matatu, kisha akajilaza kitandani. . . “Mheshimiwa, bila shaka bado hatujafahamiana vizuri,” aliongea mwenyewe. “Tumeshayavulia nguo haya maji, hatuna budi kuyakoga.” . . Kama maneno hayo angeliyasikia bwana Eliakimu Mtaja, basi bila shaka angezidi kuchochea hofu. Kwa muda huu tu, akiwa ndani ya sebule yake mkononi akiwa amebebelea glasi yenye kiywaji chekundu, alikuwa tayari amepaliwa na mashaka.
Mkono wake uliobebelea kinywaji ulikuwa unatetemeka. Alikuwa ameubinua mdomowe kama upinde wa mshale. Uso wake ulikuwa mweusi, macho yake yakizama ndani ya fikira.
Pembeni yake alikuwa ameketi Nade akiwa amekunja nne, mapaja yake meupe yakiachwa wazi na kimini cheusi alichokuwa amevaa. Naye mkononi alikuwa amebebelea glasi kubwa ya kinywaji.
Mazingira yalikuwa tulivu. Watu hawa wawili walikuwa wametekwa na mawazo. Walikuwa kimya ila sura zikiwa nzito. Kwa muda kidogo, tendo lililokuwa linafanyika ni kupeleka tu glasi ya kinywaji mdomoni kabla Nade hajauvunja ukimya kwa kuuliza: . . “Kwahiyo sasa? – Kuna haja ya kummaliza?” . . Mheshimiwa akashusha pumzi ndefu. Akanywa kwanza fundo moja. . . “Hapana, Nade. Si haraka kiasi hiko.” . . “Vipi sasa kama akiligundua ya chini ya zulia? Huoni tutakuwa tumeshachelewa?” Nade akauliza. . . “Hapana,” mheshimiwa akajibu akitikisa kichwa. “Jona ni mtu mdogo sana kumhofia. Ataenda kush’taki wapi?” “Mheshimiwa, ishu si wapi atashtakia, ila mambo yetu ya siri yataanza kuwa wazi. Inaweza ikakamata atensheni ya watu na mwishowe chombo kikaenda mrama. Tone moja la chumvi laweza kuharibu chakula.” . . Mheshimiwa akanywa kwanza kinywaji. Fundo moja tena. “Ila Nade, tukimmaliza sasa hivi, hatutampata Mariam. Tutampatia wapi yule mwanamke mzandiki? Mimi namhofia sana Mariam kuliko Jona. Mariam anajua vyetu vingi vya uvunguni. Kadiri anavyoendelea kuwa mbali ya mikono yetu, ndivyo mambo yanavyozidi kuchacha. Mariam anajua mikataba, nyaraka, mipango, watu na mpaka washirika wangu.
Huko alipo hatujui anafanya nini, na yupo na nani. Nilitamani sana kumuagiza Jona ammalize mwanamke huyu pindi tu atakapomuona, ila niliona litazalisha maswali kichwani mwake. Nakosa usingizi kumuwaza mwanamke huyu. Sina raha kabisa! Lengo langu la kwanza ni kumpata huyu mwanamke. Kuhusu Jona, sijali. Nataka tu kumtumia kwasababu najua ana uwezo wa kumpata huyo mwanamke.
Punde tu akapompata, ummalize upesi kabla hajaanza fyoko fyoko yoyote!” . . “Mheshimiwa,” Nade akaita. “N’tajitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu, ila inabidi sasa niwe namfuatilia Jona kwa siri maana naona hatakuwa na mpango wa kunishirikisha kwenye mambo yake tangu aone namfuatilia kupitiliza.” . . “Hakikisha haumtoi machoni mwako, sawa?” . . “Bila shaka.” . . Dakika tano mbele, mlango unagongwa. Mheshimiwa anatabasamu kidogo, ana habari na ujio huu. Anampa Nade ishara ya kichwa, Nade ananyanyuka na kuuendea mlango. Mgeni alikuwa Miranda. Alikuwa amevalia koti dogo jeusi la ngozi, suruali ya jeans ya kumbana na viatu rangi ya kahawia vyenye visigino virefu.
“Karibu sana, Miranda,” Nade alisema kwa bashasha la tabasamu, akiutanua mlango zaidi na kunyooshea mkono wake ndani.
“Ahsante, nimekaribia. Mnaendeleaje?”
“Tupo poa. Kitambo kweli umetususa!”
“Sema tumesusana, Nade. Hata nanyi mmekaa kimya kama maji ya mtungini.”
“Bila shaka kuna jambo kubwa limekuleta!”
Miranda akatabasamu pasipo majibu. Aliketi akamtazama mheshimiwa, wakapeana salamu.
“Najua umeshatambua nini kimenileta mheshimiwa.”
“Hapana. Pengine unikumbushe si unajua mambo mengi, Miranda.”
“Ni kuhusu ile ishu tuliyojadili siku ile kule Mango garden.”
“Hivi tuliongelea kitu gaaa …” Mheshimiwa alikuna kichwa kwa kidole akijaribu kukumbuka pasipo mafanikio. Alimtazama Miranda, Miranda akampa ishara ya macho kwa kumtazama Nade. Basi Mheshimiwa akamtoa Nade sebuleni kwa ishara ya kumtikisia kichwa.
Sasa wakawa wamebakia wenyewe sebuleni.
“Ni kuhusu yale madawa tuliyokuwa tumeyagiza toka Uswizi.”
“Ndio, upo tayari kabisa na umeshapakiwa kwenye makontena kwa ajili ya usafirishaji.”
“Makontena? – mmepanga kutumia njia ya maji?”
“Ndio. Ndiyo njia ya kubeba mzigo mingi zaidi.”
“Ni sawa, pia ndiyo salama zaidi ukilinganisha na njia ya anga. Kwahiyo jumla kuna makontena mangapi?”
“Hamsini na mbili.”
“Ni mengi mno. Haiwezekani yakasafirishwa yote kwa siku moja.”
“Una mpango gani, mheshimiwa?”
“Kuna mwanya wa kusafirisha manne tu kwa sasa, na ni juma lijalo. Mnaweza mkafanya hivyo?”
Miranda akasita kwanza kujibu apate kutafakari.
“Siwezi nikatoa jibu la moja kwa moja mheshimiwa, kama unavyojua ni lazima nipeleke taarifa hizi kwa mkuu wa kitengo kisha yeye ndiyo anipe maagizo.”
“Basi mtaarifu hivyo. Juma lijalo kuna mpango wa kuleta kontena ishirini zilizobebelea vifaa vya kujengea uwanja wa kisasa kama ule wa taifa. Kama unavyojua vifaa hivi havitozwi kodi, na hata upekuzi wake unakuwa hafifu kwakuwa ni vya serikali.”
“Ni kweli mheshimiwa. Ila vipi na kuhusu hiyo mzigo mingine itakayokuwa imebakia? – nayo inabidi ije kwa namna yoyote ile ili kukamilisha pakeji nzima.”
Mheshimiwa akafichama mdomo wake kwa kiganja akitafakari. Aliangazia mianya anayoweza kuenenda afanikishe zoezi hilo. Wazo likamjia.
“Ok, tutafanya hivi. Kadhaa zitabebwa kama nilivyokuambia – kwa kutumia makontena ya vifaa vya uwanja wa mpira. Na hayo mengine, yote, tutapitishia kwa kutumia mgongo wa shirika la madawa nchini.
Tutafanya kama malighafi za kutengenezea madawa ya kutulizia maumivu na nusu kaputi. Unaonaje?”
Miranda akatikisa kichwa kuafki.
“Ni sawa, ila napata shaka kidogo.”
“Gani hilo?”
“Kuhusu usalama wa hiyo mizigo na pia ka …”
“Miranda, hilo ni jukumu langu. Nimeshawahi kuwaangusha?”
“Hapana, mheshimiwa.”
“Basi unaweza kwenda kumfikishia taarifa mkuu wako. Mashaka yangu yapo kwenye muda wa shirika la madawa maana bado sijaongea na mtu wa huko nikajua. Ila … n’tawataarifu kesho I think.”
“Sawa. Ada?”
“Miranda, sasa mnaniangusha. Ndiyo tumeanza kufanya hii kazi leo kiasi cha kutokujua ada?”
“Hapana, mheshimiwa. Kusema ukweli kwa sasa hali yetu imetetereka kiuchumi haswa baada ya sera za mambo ya nje za baadhi ya nchi kubadilika. Tuwiane radhi mheshimiwa na utuzingatie.”
“Nenda, nitaongea na mkuu wako.”
Miranda akanyanyuka na kwenda. Mheshimiwa akamuita Nade aliyekuja sebuleni upesi na kuketi.
“Sorry kwa kukutoa hapa, Nade.”
“Usijali, mheshimiwa. I understand.”
“Thanks. Sasa kuna kazi imeibuka hapa na inabidi ifanywe haraka. Kesho, asubuhi na mapema, nitakuagiza kwenda kuonana na Maxwell Ndoja. Unamkumbuka?”
“Ndio.”
“Kuna mambo machache nataka umfikishie mdomo kwa mdomo. Hak…”
“Hakikisha hamtumii simu, mtandao wala njia yoyote itakayoacha ushahidi!” Nade alimalizia kauli ya Mheshimiwa.
Mheshimiwa akajikuta anatabasamu.
“Sitakuambia tena hayo maneno kumbe umeyashika kiasi hicho. Anyway, baada ya Ndoja itabidi uonane pia na Nassoro Mauje.”
Baada ya kusema hayo, akafunguka kumwambia Nade mambo gani ya kwenda kujadiliana na hao watu. Alipomaliza akafungia mjadala kwa kusema:
“Kuwa makini. Hakikisha unatumia kila njia kuhakikisha hili jambo linafanikiwa, sina haja ya kukueleza ni kiasi gani cha pesa tutakivuna endapo dili hii ikitiki, unajua mwenyewe.”
“Ndio,” Nade akajibu kwa kutikisa kichwa.
***
Saa 04:35 asubuhi, ndani ya nyumba ya marehemu Bite.
Sebuleni kuna watu watano, wanne wageni machoni, mmoja bwana Kinoo. Katika hao wanne ambao ni wageni mbele ya mboni, mmoja alikuwa mwanaume mzee kuliko wote akiwa amevalia suti rangi ya nyekundu na tai nyeusi yenye vidotidoti vyeupe. Aitwa Brokoli.
Mwingine alikuwa mwanaume mwenye makamo ya miaka thelathini mpaka na tano. Alikuwa mweusi mwenye kichwa cha duara, uso mtulivu na macho ya kistaarabu. Alivalia ‘body’ nyeusi na suruali ya jeans. Aitwa Mudy.
Wengine wawili walikuwa mapacha wa kike, Sara na Sasha. Wasichana warembo warefu wenye nywele nyekundu, macho makali makubwa na ‘lips’ pana nyekundu.
Sara alikuwa amevalia gauni jeupe lenye madoa madoa ya maua, Sasha akivalia blauzi ya kijani na suruali pana nyeusi inayobana juu na kumwaga chini. Kwa makadirio, warembo hawa wana miaka isiyozidi ishirini na nane, wala kupungua ishirini na tano.
Mzee Brokoli ndiye aliyekuwa anaongoza kikao hichi ambacho kiliita wajumbe wanaohusika na kampuni ya magari ya marehemu Bite. Lengo lilikuwa ni kujadili mustakabali wa kampuni hiyo lakini pia kumwongelea marehemu Bite kwa ujumla.
Kwenye meza ya kioo, hapo sebuleni, palikuwa pamejazwa vinywaji vilaini; sharubati takribani tatu; ya embe, pasheni na machungwa zikiwa zimetapakazwa kwenye glasi kubwa tano kulingana na idadi ya wajumbe.
Watu hawa walikuwa tayari wameshaanza kikao, na walikuwa katikati ya maongezi ambayo yalikuwa yanapokelewa kwa umakini na utulivu mkubwa.
Brokoli alikuwa ananguruma.
“Hatuelewi nini chanzo cha mauaji haya. Mpaka sasa polisi hawajampata wala kumshikilia mtuhumiwa yeyote yule, inashangaza kwakweli lakini pia inatia hofu. Inatuweka kwenye njia panda kujua kama mauaji haya yanahusiana na kampuni ama la!
Lakini kampuni inabidi iendelee. Si kwamba kifo cha Bite basi ndiyo kiwe kifo cha kampuni. Ni mapema sana kuamua hivyo. Ila kama nilivyosema hapo awali, ni lazima sasa kampuni hii ibadilike. Tufanye mambo mengine mbali na haya mambo ya magari.”
Hoja hii ikachukua muda kujadiliwa. Muda wote huo Kinoo alikuwa kimya kwani hili halikuwa linamhusu. Yeye alihudhuria hichi kikao kama mdau tu wa mbali, mwakilishi wa kampuni moja mteja wa kampuni ya magari ya Bite.
Hapa kikaoni yeye alikuwepo kwa lengo la kupata taarifa tu, kama kutakuwa kuna mpya, kumhusu Bite. Pengine akapata jambo likamjuza aliyehusika na kifo cha mwanamke huyo.
Hilo lilikuwa muhimu sana kwao. Kumjua aliyehusika na mauaji kungewafanya wachukue hatua kujilinda na kufuatilia kwanini mwanamke huyo ambaye alikuwa amebebelea siri kubwa, siri ya mafanikio, akapata kadhia kama hiyo.
Basi hitaji lake hili likamvuta mpaka ukingoni mwa kikao hichi, ambapo huko kuna kauli ya Mudy ilimshtua na kumfanya afikirishe zaidi akili yake.
“Kuna taarifa niliiwasilisha kwa mpelelezi wa kesi hii ya Bite, ni muda mrefu sasa, nikitegemea ingesaidia kwa namna moja kubwa kumpata muuaji. Ila ajabu haikufuatiliwa, ikapuuzwa!
Hata pale nilipokuwa nampigia simu mpelelezi na kumkumbushia, sikuwa Napata majibu ya maana. Kwakweli nikakata tamaa.”
Kiu ya Kinoo ikakua. Alitaka kujua zaidi kuhusu taarifa hiyo, basi akawahi kuuliza:
“Ni taarifa gani hiyo?”
“Sidhani kama kuna haja ya kujadili tena mambo hayo!” Brokoli akaingilia kati. “Hayo yameshapita, na hata tukiyateta hapa hayatabadili chochote. Tuendelee na mengine.”
“Mkuu Brokoli, huoni tukilitilia mkazo linaweza kuleta angalau haki kwa dada yetu aliyeuawa kinyama?” Mudy akauliza.
Brokoli akamkazia macho na ndita. Akamuuliza:
“Mudy, wewe ni nani kwenye kampuni?”
“Accountant,” Mudy akajibu akitazama chini.
“Na mimi ni nani?”
“Mkurugenzi.”
“Basi sina haja ya kuongea tena. Tugange yajayo, si ya nyuma. Ina maana kuna kitu haukuelewa huko nyuma tulivyokuwa tunaongea?”
“Nilielewa, mkuu. Samahani.”
Kikao kikaendelea na kukoma punde fupi. Watu wakanyanyuka na kuondoka zao.
Lakini kifuani mwa Kinoo mulikuwa mna jambo. Jambo mtambuka kumhusu Brokoli. Alimtazama mzee huyo katika namna ya pekee, namna ya tofauti na alivyokuwa anamtazama mwanzoni.
Aliridhia na akili yake mzee huyu anahitaji kufanyiwa upembuzi zaidi, tena wa kina. Kuna jambo analijua kuhusu Bite.
Kwanza, alitaka kujua kwanini alikuwa anasimamia sana hoja yake ya kubadili biashara, akikataa abadani kuendelea na biashara ya magari. Pili, kwanini hakutaka kugusia swala la taarifa ya Mudy juu ya Bite, ilhali mwanzoni alisema amefadhaishwa na ukimya wa polisi.
Aliamini kabisa endapo akiyapata majibu ya maswali hayo, basi hatotoka mtupu. Kuna kitu atapata, muhimu, chenye faida.
Taratibu akiwa ndani ya gari lake akatazama uelekeo wa gari la Mudy ambalo ndani yake lilikuwa pia limewabebelea Sara na Sasha. Gari hilo lilipotoka ndani ya eneo la nyumba, Kinoo akatia moto injini na kulifuatilia taratibu.
Alikuwa yupo ndani ya Range Rover sport wanayoitumia kwenye kazi zao.
Lengo lake lilikuwa ni kujua makazi ya Mudy, kwani watamuhitaji mtu huyo muda si mrefu. Kama taarifa yake ilipuuzwa na Brokoli, basi wao walikuwa wanaitaka. Tena kwa udi na uvumba!
“Pole sana, Mudy, ndiyo boss huyo!” alisema Sara akitikisa kichwa na kutabasamu. Mudy akasonya. Alikuwa anatazama mbele aelekeapo. Mkono wake wa kushoto akiwa ameketi Sara, na Sasha amekaa nyuma peke yake. Ni ndani ya Rav4 nyeupe.
Mudy akatikisa kichwa na kutahamaki:
“Mpumbavu kweli yule. Sasa alikuwa analalamika nini kuhusu polisi kama hataki tuchangie mawazo?”
Sara na Sasha wakaangua kicheko.
“Sasa na hivi Bite amefariki, yule mzee si ndo’ atatupelekesha mpaka basi!” Sasha akapayuka.
“Nakwambia!” Sara akadakia. “Tutapelekwa kama gari bovu maana mzee yule hataki kushauriwa wala nini!”
“Tatizo mkoloni sana!” Mudy akaunga mkono hoja. “Sijui ametuitia nini kwenye hicho kikao chake kama kila kitu tayari ana majibu nacho. Si angetutumia tu ujumbe!”
“Kwakweli. Lakini Mudy, ulikuwa na taarifa gani kuhusu Bite? Mbona hujawahi hata kun’tonya siku zote hizo?” Sara aliuliza.
“Tatizo mambo mengi,” Mudy akajibu. “Huwezi kuamini nilikuwa nimesahau kabisa mpaka pale niliposikia tena kuhusu Bite pale kwenye kikao.”
“Tuambie basi nasi tujue,” Sasha akashupaza masikio, Mudy akatabasamu.
“Mnapenda sana umbea na nyie.”
“Tuambie bana, Mudy,” Sara naye akashadadia. “We hujui umbea kwa mwanamke ni sunna!”
Kabla Mudy hajasema neno, hamaki dereva bodaboda akakatiza upesi mbele yake! Alijitahidi kukwepa bodaboda kwa kupeleka gari kando ambapo napo huko kulikuwa kuna gari iliyokuwa inakuja nyuma kwa kasi, hivyo akaishia kubamizwa ubavuni na kusababisha tafrani barabarani!
Sara na Sasha walipiga kelele kali za hofu. Mudy alifanikiwa kulimudu gari akilipakia pembezoni mwa barabara.
“Shit!” Akalaani akisaga meno. Dereva bodaboda alitokomea asionekane wapi alipoelekea. Hakuna hata aliyenakili pleti namba yake.
“Ahsante, Mungu!” Sara alisema akihema kwanguvu. Vifua vyao vilikuwa vinapwita kwa hofu pana. Sasha yeye alikuwa ameishiwa nguvu kabisa.
Hawakuamini kama wametoka salama katika sekeseke hilo. Walikuwa wazima wa afya ila shepu ya mbele ya gari ikiwa imeharibika kiasi.
Punde alitokea dereva wa gari lile lililoparamiwa wakati Mudy anamkwepa bodaboda. Akaongea na Mudy kwa muda mchache kabla Mudy hajatoleshwa pesa, noti nyekundu kadhaa, dereva huyo akaondoka zake.
Hwakuhitaji trafiki polisi, waliona ni vema wakamalizana wenyewe.
“Pole sana, Mudy. Sasa?” Sara aliuliza.
“Siku yangu ishaharibika. Sina pesa yoyote hapa, yote nimetoa sababu ya yule bodaboda fala!”
“Pole sana, Mudy. Ila bora una uhai, hayo mengine ni ziada tu, na yanatafutwa.” Sasha alimfariji. Mudy akashusha pumzi ndefu.
“Tatizo gari yenyewe ilikuwa ina mafuta kiduchu, nilikuwa nimepanga nipitie sheli hapo mbele nitie mafuta, sasa pesa imeshaenda … anyway, nyie pandeni tu daladala muende, mie n’tajua cha kufanya.”
Sara na Sasha wakaondoka zao. Mudy akasema na yake kifuani: kweli wanawake si wa kuwategemea kwenye shida, hapa ningekuwa na wash’kaji zangu chap tatizo lingekuwa limeisha.
Akiwa hapo bado hajajua cha kufanya, mara Range Rover sport inatokea na kupaki kandokando yake, Kinoo anashuka na kumsalimu. Anamjulia hali na anapendekeza kumsaidia.
“Pole sana, ndiyo mambo ya barabarani hayo. Sasa inabidi uipeleke gereji ifanyiwe matengenezo.”
Mudy akaomba apelekwe kwanza ATM apate kutoa pesa kwa ajili ya mahitaji yake. Kinoo akambeba kumpeleka huko. Safari ikasindikizwa na soga ambazo Kinoo alikuwa amelenga kupatia majibu maswali yake.
“Nyumbani ni mbali sana?”
“Kiasi, naishi Mbweni.”
“Mmh … ni mbali!”
“Basi mie kwakuwa nimeshapazoea, naona si mbali sana. Ila kila mtu ninapomwambia naishi Mbweni husema ni mbali.”
Kinoo akatabasamu pasipo kuonyesha meno.
“In fact, ni mbali … Ila inabidi upunguze mawazo usije ukapata maswahibu mengine barabarani, Mudy. Mambo kama yale hutokea tu.”
Mudy hakuelewa, kabla hajapata mwanya wa kunena, Kinoo akaendelea kujazia nyama simulizi yake.
“Kiukweli Brokoli hakutakiwa kukukrash namna ile, alifanya makosa. Sikupendezwa naye kabisa. Na naanza kupata mashaka kama tutawezana naye kwenye biashara.” Mudy akaguna na kutikisa kichwa pasipo kutia neno.
“Kama kuna watu ambao wamezaliwa kwa ajili ya biashara duniani, Bite alikuwa mmojawao. Mwanamke yule alikuwa smart sana. Anajua kuongea, kupanga na kusimamia. Alikuwa mhimili mkubwa wa kampuni yenu. Pengo lake gumu kulijaza.”
“Ni kweli,” Mudy akaunga mkono hoja. “Zaidi ya yote alikuwa anaishi vizuri sana na wafanyakazi wake, kila mtu alikuwa anampenda. Kifo chake kilitushtua mno. Ametuacha kwenye mikono migumu.”
“Kwakweli. Ni jukumu letu kuhakikisha angalau kifo chake kinaheshimiwa kwa kupata haki na kuwatia nguvuni wauaji.”
“Kivipi sasa na wakati polisi na mkurugenzi hawaeleweki? Naona kama Bite ameenda na hamna lolote litakalokuja kufanyika.”
“Wewe unataka iwe hivyo?”
“Hapana, ila sina la kufanya sasa.”
“La kufanya halikosekani Mudy. Mimi pia sitaki iwe hivyo kama wewe, sasa watu wawili ni wachache kufanya jambo?”
Mudy akasita kujibu.
“Ulisema ni Barclays?” Kinoo aliuliza. Mbele yao umbali mfupi kulikuwa kuna ATM ya Barclays. Yalikuwa ni maeneo ya Sinza, Kijiweni.
“Yah! Ni Barclays,” Mudy akalipuka kujibu. Gari likatafuta mahali pa kuegeshwa, akashuka na kwenda kwenye ATM kutoa pesa. Kinoo akampeleka tena sheli alipochukua mafuta kwa kutumia kidumu kisha akamrejesha mpaka kwenye gari lake.
Wakaagana, Kinoo akahepa zake wakipeana miadi ya kukutana karibuni wapate kutazamia namna gani ya kujadili na kufufua kesi ya Bite. Walibadilishana namba za simu kwa ajili ya mawasiliano zaidi.
***
Majira ya saa nane mchana, maeneo ya Mwenge.
Kwa kiasi kikubwa sasa Jona alikuwa amesogeza kazi zake zilizokuwa zimemtinga. Mgongo ulikuwa unamuuma kwasababu ya kuukunja kwa muda mrefu. Alijinyanyua akaunyoosha akipiga mihayo.
Alimtazama Jumanne aliyekuwa amelala kitini, akamshtua na kumuuliza:
“Vipi, hatwendi kula?”
Jumanne akatikisa kichwa na kufumba macho yake mazito mekundu.
“Unaendekeza usingizi enh?”
“Hamna … sina njaa.”
“Njaa unayo sema usingizi kwako ndiyo bora zaidi. Haya mimi naenda.”
Jumanne akatikisa kichwa akiwa amefumba macho yake.
“Nikisikia tu miguu, naamka,” Jumanne akajibu akiwa bado amefumba macho. Jona akatikisa kichwa na kwenda zake kwa mama K wa mgahawani.
Kama kawaida aliketi na kutoa simu yake wakati anangojea chakula na kuanza kuiperuzi. Alizama mtandaoni Facebook, akakuta jumbe tano, nne toka kwa mwanamke yule wa Afrika ya kusini.
Alikuwa anamjulia hali na pia amemtumia picha kadhaa za bidhaa zake, nguo na mikoba akiulizia kuhusu mrejesho wa fasheni. Jona akampuuzia. Akaenda moja kwa moja kwenye ujumbe mmoja uliosalia, ulikuwa pia wa mtu mgeni – mwanaume mmoja toka Uarabuni.
Nayo akapuuzia.
Hakuona kama kuna la maana huko mtandaoni. Akakagua akaunti ya Mariam – mke wa mheshimiwa, hakupata jambo. Basi akaamua kuacha simu na kufikiri mambo yake mengine.
Chakula kikaja, akala taratibu. Alimfikiria Nade kidogo, akaachana naye. Alimfikiria Mheshimiwa, hapo akakumbuka kwamba ana miadi naye siku hiyo. La haula! Alikuwa amesahau kabisa.
Alitazama saa yake mkononi. Aliwaza ni muda gani anaweza akaenda kumuona Mheshimiwa, akaona kuna haja ya kumuuliza. Akanyanyua simu na kumpigia. Simu ikaita pasipo majibu.
Alirudia kwa mara nne lakini hakukuwa na mabadiliko. Akapata mkanganyiko.
“Pengine akikuta missed calls zangu atan’tafuta,” alihitimisha kwa kusema hivyo kabla hajaweka simu chini, akamalizia chakula.
Akalipia na kutoka ndani.
Akiwa hana hili wala lile akashika barabara kufuata njia mbili kubwa za lami apate kuvuka na kwenda ofisini. Alivuka njia ya kwanza. Akiisogelea ya pili, kuna gari moja ndogo Mark 2 nyeusi, ikahamia upande wa pili wa barabara.
Upande huu ndiyo ambao Jona alikuwepo akiangaza avuke barabara.
Baada ya kuona kuna mwanya wa magari, Jona akashusha miguu yake juu ya lami na kupiga hatua za haraka haraka avuke salama.
Ajabu ile Mark 2, upesi nayo ikahama upande, ila sasa ikiwa imeongeza kasi maradufu! Mlio wake mkali uliokuwa unanguruma ulimshtua Jona, akarusha macho yake kutazama.
Hatua kama tano tu mbele yake, gari hilo, Mark 2, lilikuwa linakuja kwa kasi kubwa. Kwa mahesabu tu ya haraka ni kwamba asingeweza kumaliza barabara kwa kasi ya hatua zake.
Haraka aliwaza. Akarusha hatua zake kukimbia, ila napo hakuweza kumaliza kuvuka, gari lilikuwa tayari limeshamfikia karibu mno kumpindua na kumvunjavunja.
Hapo sasa ikabidia atumie ujuzi wake kujiokoa maisha. Kwa kutumia mguu wake mmoja akajirusha juu, kufumba na kufumbua, mgongo wake ukatua kwenye bodi la gari, akabiringita mara mbili kabla hajamwagikia kando gari likipita!
Alitua akiweka mkono wa kulia chini, mguu wa kushoto ukinyookea nyuma na wa kulia ukiwa umejisimika kwa kuukunja.
Ilikuwa ni ajabu! Walioshuhudia tukio hilo waliachwa kwenye bumbuwazi. Walichozoea kukiona kwenye tamthilia walikiona mbele ya macho yao, tena kamera zikiwa hazipo.
Upesi alisimama kana kwamba hakuna lililotokea, akatafuta miwani yake aliyoiona kando na kuiokota. Ilikuwa imevunjika kioo kimoja na fremu zake zikiwa legelege. Akaikunja na kuiweka mfukoni, akaenda zake ofisini.
Watu walikuwa wanamtazama, wengine wakidhani pengine ameumia pasipo yeye mwenyewe kujua. Aliwaambia yu salama akizidisha hatua apotee hapo.
“Upo sawa, Jona?” Jumanne alimpokea kwa maswali.
“Nipo sawa, usijali J,” Jona akajibu akiketi kitako kwenye kiti. Akachomoa miwani yake mfukoni na kuitazama.
Jumanne alikuwa anamkagua kwa kumuangaza huku na kule kama ataambulia kuona jeraha. Macho yake yalionyesha bado yupo kwenye bumbuwazi la kutoamini kilichotokea.
Kabla Jona hajaanza kuwaza kuhusu lile gari, alikuwa anawaza kuhusu miwani yake kwanza. Alijua fika yeye pasipo miwani ni nusura kipofu. Miwani yake ndiyo macho yake, sasa itakuwaje pasipo nayo?
Ataweza pambana kwenye hii vita akiwa haoni? Alijikuta anajiuliza.
Hakutaka kukaa tena hapo kazini, akaondoka zake. Bila shaka safari hii ilikuwa ni kwenda kutafuta miwani ya macho.
Kwa muda kidogo ni kama kichwa chake kilikuwa kimechina. Hakutaka kukifikirisha zaidi. Alikua anatazamia tu ni wapi atapata miwani nzuri kwa ajili ya macho yake mabovu.
Alikuwa anahitaji miwani haraka iwezekanavyo alafu ndiyo mengine yafuatie. Akanyookea duka moja la mwarabu mzee katikati ya jiji, Kariakoo.
Ilikuwa ni ajabu kwa namna alivyoliteua duka hilo ingali alikuwa mhafifu wa kuona. Aliposhuka tu kwenye gari alijikuta mwili wake ukielekea uelekeo huo ambao haukuwa mgeni kwake.
Ni wazi huko nyuma alishawahi kuja kwenye duka hili kununua miwani.
Muuzaji wake alikuwa mzee wa kiindi mwenye ndevu nyingi rangi ya kahawia na baghalasia nyeupe ya nyavunyavu akivalia kanzu fupi rangi ya maziwa, pamoja na viatu vya wazi.
“Umewezaje kufika hapa pasi na miwani?” muuzaji alimuuliza akiinamisha mgongo wake na kunyoosha mkono kutwaa miwani fulani iliyokuwa imekingwa na zingine, ikipakana na kioo.
“Naenda kwa hisia kama jongoo!” Jona akatania, wakacheka. Alikabidhiwa miwani akaijaribisha kwa kujivesha.
Alikuwa anaona sawia! Bahati kwake alikuwa anajua vipimo vya macho yake na hata aina ya miwani anayotakiwa kuivaa hivyo hakujisumbua wala kumsumbua muuzaji.
Akailipia, ila kabla hajaondoka muuzaji akateka kidogo muda wake. Alikuwa mjawa wa simulizi mwenye maneno mengi japokuwa Kiswahili kilikuwa kinamtatiza hapa na pale.
Wakati Jona anapiga soga na muuzaji huyo, alikuwa anaangaza angaza huku na kule akifurahia uwezo wake wa kuona uliorejea.
Akiwa anaangaza angaza huko, akamuona mtu fulani aliyemtilia shaka. Alikuwa ni mwanamke mrefu aliyekuwa amevalia blauzi nyeupe, suruali nyeusi ya kumbana na viatu vyenye kisigino msawazo.
Hakufanikiwa kuona sura ya mwanamke huyu, ila aliamini kabisa alikuwa anamtazama yeye kwani aliukwepesha uso wake upesi punde tu alipotazama upande alipo – upande wa mashariki.
Alikuwa amevalia nywele ndefu feki ambazo ziliziba shepu ya kichwa chake na masikio. Pengine Jona angeviona hivyo vitu vingemsaidia kumng’amua mwanamke huyo.
Ni nani? Jona akajiuliza. Alipata tu hamu ya kuona sura ya mwanamke japo haikuwa kubwa. Hakuwa na mashaka kiasi cha kumfanya achukue hatua nzito.
“Ahsante,” alijibu upesi akiikwapua risiti kisha akarudisha macho yake kwa yule mwanamke.
Hakumuona! Alikuwa amepotea.
Alitazama huku na huko lakini hakufanikiwa kumpata. Aliamua kupuuzia, akaaga na kwenda zake kujipaki kwenye gari. Akiwa sasa njiani akaanza kudadavua tukio lile la gari mark 2 kutaka kumgonga.
Akili yake yote iliamini tukio lile lilikuwa la kupangwa na si bahati mbaya, lakini ni nani analifanya? Nani yupo nyuma ya tukio hilo? Kwanini anataka kumfanyia hivyo?
Aliamini watakuwa ni wale watu waliokuwa wanamfuatilia mpaka nyumbani kwake, yani Miranda na Kinoo, japokuwa shaka lake lilikuwa sehemu moja – mbona hawakutumia gari lao, Range Rover sport?
Ila hiyo ilikuwa sababu ndogo sana kutia dosari kwenye ubashiri wake. Pengine gari limebadilishwa kuvunja ushahidi, ama basi wana magari mengi. Akili yake iliwaza.
“Nitajua leo,” akajikuta anafanya maamuzi.
Aliona sasa ni wasaa wa kukutana na adui yake uso kwa uso, macho kwa macho. Akashuka na kukwea gari jingine lililompeleka mpaka maeneo ya Kawe alipoteka bodaboda na kwenda moja kwa moja mpaka getini mwa makazi ya Miranda.
Akagonga geti mara tatu.
Mlinzi akafungua na kumtazama. Alikuwa ni mwanaume mrefu mweusi aliyekuwa amevalia sare zenye rangi nyekundu na nyeusi, pamoja na kofia iliyochoka, mkononi akibebelea kirungu.
Mwanaume huyu mlinzi alikuwa mgeni maeneo haya, bila shaka kama si jana yake basi ni juzi ndiyo aliwasili.
“Naweza nikakusaidia?” mlinzi aliuliza kwa sauti ya amri.
“Naomba kuonana na mwenye nyumba.”
“Una miadi naye?”
“Hapana. Ni dharura tu, kuna jambo muhimu nataka kuongea naye.”
“Kama hauna miadi naye siwezi kukuruhusu.”
“Nimekwambia ni dha …”
“Nimekusikia, na bila shaka nawe umenisikia. Siwezi nikakuruhusu kama hauna miadi!” mlinzi akasema akitoa macho yake mekundu.
Jona akasonya. Sasa alilazimishwa kufanya kitu ambacho hakikuwapo kwenye mipango kwakua hakuwa tayari kuona muda wake alioutumia kuja hapo unaenda bure.
Alidaka kichwa cha mlinzi kwa kutumia mkono wake wa kuume, akakizungushia upande wa kisogo na kukikita, mlinzi akazirai. Akamsukumia ndani kabla hajaingia na kufunga mlango mdogo wa geti.
Akagonga sasa mlango wa sebuleni na kusubiria majibu.
Miranda alikuwa chumbani ila aliisikia hodi hiyo. Kabla hajanyanyuka kwenda kuipokea, akafungua dirisha la chumbani na kutazama nje.
Chumba chake kilikuwa kimekaa mahali ambapo alikuwa na uwezo wa kutazama na kuona kibarazani.
Akamuona Jona.
Alishangazwa haswa. Amepajuaje hapa? Hilo ndilo lilikuwa swali la kwanza kuja kichwani. Hodi iliita tena, akanyanyuka na kwenda sebuleni.
Simulizi : Anga La Washenzi (1) Sehemu Ya Pili (2)
Alikuwa amevalia suruali pana ya malighafi laini, kaushi nyeusi pasipo sidiria, miguuni akiwa peku. Nywele zake zilikuwa timu, kinyumbaninyumbani. Nyuma ya kiuno alikuwa amechomeka bunduki ndogo.
Japokuwa alishangazwa na Jona kujua makazi yake, ila hakuwa na wasiwasi sana. ni ‘mchora picha tu, alijiambia moyoni akisogelea mlango.
“Karibu.”
Jona akazama ndani pasipo kusema lolote. Akaketi na kukunja nne. Miranda naye akafuatia nyuma, akaketi kwenye kiti kilichowafanya watizamane vema.
“Najua ujio wangu umekustaajabisha, pengine ulitegemea nisingekuwa hai wakati huu ama basi ni mlemavu, samahani sana,” alisema Jona kwa kujiamini. Miranda akakunja ndita za kukanganyikwa.
Hakupewa muda wa kuuliza, Jona aliendelea kuongea.
“ … Anyway, I am tired of your bullshit. Mnataka nini kwangu? Ile picha? Ni picha ndiyo inawafanya mtake kunitoa roho? Mmeona picha haitoshi sasa mnawinda roho yangu?”
“Usitegemee kama nitajibu swali lolote toka kwako. Sijaja hapa kufanyiwa mahojiano bali kutoa tamko na angalizo. Mosi, hamtapata picha yoyote toka kwangu. Pili, acheni mara moja kunifuatilia, la sivyo …” Hakumalizia, ila macho yake yalisema kila kitu.
Akanyanyuka na kuondoka zake akimwacha Miranda kwenye bumbuwazi.
Mwanamke huyo akamtazama Jona akifungua mlango wa geti na kuufunga kwa kuubamiza. Akagundua mlinzi hayupo. Haraka akanyanyuka na kwenda kutazama.
Akamkuta mlinzi akiwa hana fahamu.
Akampigia simu Kinoo na kumtaka aje nyumbani upesi. Baada ya muda mfupi Kinoo akatia miguu yake eneoni akitumia Range Rover sport nyeupe. Alikuwa amevalia ‘ki body’ cheusi na suruali ya jeans aliyoifunga na mkanda kiunoni, miguuni akila moka nyeusi.
Miranda akamweleza yale yote yaliyotukia kuhusu Jona.
“Si unaona sasa?” Kinoo akatahamaki. “Mi’ ndo’ mana n’likuambia tummalize tu, we ukawa unavunga vunga. Ona sasa!”
“Kinoo, embu uwe unatumia akili hata mara moja moja. Yani we umeona hilo ndo’ la kukimbilia kuropoka?”
“Haya, we endelea kun’zarau.”
“Si kwamba nakudharau, nakwambia ukweli. Kuna maswali ya kuanza kujiuliza na kuyatafutia majibu, na si kuanza kurusha risasi za lawama.”
Kinoo akashusha pumzi ndefu puani na kubinua mdomo wake.
“Haya sema nakus’kiza.”
“Kinoo, huyu mchora picha si tu mchora picha. Nimeshangazwa kwa namna alivyopajua hapa na hata kujiamini kwake.
Kama haitoshi, namna alivyomkabili mlinzi, kunazidi kunifanya nihofie. Pengine mtu huyu anahitaji jicho la pili, ni mtu mwenye ujuzi binafsi ama mafunzo.
Zaidi ya hapo, kwa necha ya maongezi yake kuna watu wanamfuatilia, na hawa watu wanataka kumuua japo hajaweka wazi ni wakina nani na wametumia njia gani. Ila wapo, na ajabu sio sisi! Kwani kwa muda kidogo hatujasumbuka naye, na hatujawahi pia kutishia uhai wake.
Unadhani nini kinaendelea? Ina maana mchora picha huyu naye anataka kumalizwa kama Bite?”
Kinoo akaguna na kubinua lips zake nyeusi.
“Hilo halina shaka. Ina maana tayari wanajua kuhusu mchora picha huyu, na sasa wanataka wamalize ushahidi kabisa kisibakie hata punje. Hii ina maana wanajua kulikuwa kuna mahusiano kati ya Bite na huyu mchora picha.”
“Ndiyo maana yake. Na naona msisitizo ni kumuua mchora picha kuliko kuipata picha yenyewe. Wanataka kummaliza. Ina maana kilichomo kwenye picha hawakihitaji, wanakijua?”
Kinoo akapandisha mabega juu.
“Leo inabidi tupate picha hiyo, Kinoo,” Miranda akasema kwa msisitizo. “Tusipoipata leo, kuna hatihati tukaikosa daima.”
**
Wakati huo upande huu ukiwa unateta, upande mwingine kwenye laini mojawapo ya simu maongezi ya Nade na mheshimiwa waziri, Eliakimu Mtaja, nayo yakawa yanachukua nafasi.
Nade alikuwa amejikobeka mahali fulani alipoegemea ukuta.
Kumbe alikuwa ndiye mwanamke yule Jona aliyemuona kule Kariakoo. Nguoze zilisema hivyo.
Eneo hili alilokuwepo halikujulikana kwa urahisi.
“Nimemshuhudia kwa macho yangu akiingia na kutoka kwa Miranda.”
“Una uhakika?”
“Ndio, mheshimiwa.”
“Ina maana wanajuana na Miranda?”
“Itakuwa wanajuana. Hakukaa kwa muda mrefu ndani.”
“Watakuwa wanafanya ishu gani na Miranda?”
“Sijajua mkuu. Sijajua pia nani aliyejaribu kumuua kwa kumgonga na gari. Inaonekana kuna mambo kadhaa tusiyoyafahamu kuhusu Jona.”
“Mfuatilie kila nyendo,” mheshimiwa akanguruma. “Hakikisha kama anayoyafanya yanahusiana na Mariam, kama ndiyo unipashe habari upesi. Kama sio basi fanya ujue ni jambo gani.”
“Sawa, mkuu,” Nade akajibu na kukata simu.
*** “He’s promised, so very soon things gonna be ok,” (Ameahidi, kwahiyo karibuni vitu vitakuwa sawa) Miranda alisema kwa sura ya uhakika. Alikuwa anaongea na mwanaume mzungu, makadirio ya miaka hamsini na mambo hivi, mwenye ndevu nyeupe zilizochongwa vema, na nywele za wastani kichwani.
Mwanaume huyu alikuwa amevalia shati jeupe lililoziba mikono yake, suruali nyeusi na moka rangi ya kahawia, iking’aa mithili ya kioo. Shingoni alikuwa amejinyonga na tai rangi ya chinikiwiti.
Mkono wake wa kushoto alikuwa ameuvika saa kubwa rangi ya dhahabu, huku mkono wake wa kuume ukiwa umekamatia sigara kubwa ya kaki iliyokuwa inafuka kama gari moshi.
Mkono huu ulikuwa na kazi mbili, moja kupeleka sigara mdomoni, na pili kukung’utia sigara kwenye kisosi kilichokuwapo mezani.
Miranda alikuwa amevalia gauni jeusi linalombana na kumsadifu umbo. Nywele zake zilikuwa zimetengenezwa na kuundwa vema kama nyasi za msonge. Shingoni alikuwa na mkufu wa dhahabu, masikioni hereni za ghali.
Mezani alikuwa ameweka pochi yake ndogo nyekundu yenye zipu kubwa. Alikuwa ananukia kana kwamba ametoka kuoga kwenyee dimbwi la marashi ya Uajemi.
Waliendana na makazi waliyopo – nyumba kubwa ya kisasa iliyozungukwa na bustani ya majani na maua. Mlinzi getini mwenye bunduki na mbwa mkubwa mchanganyiko wa mbegu za Ulaya.
Lakini kwa mujibu wa mavazi yao, usingekosea kubashiri kuwa watu hawa wana safari muda si mrefu ya kwenda mahali fulani. Tena penye taadhima. Haingii akilini kusema wamejikobeka vile kwa ajili ya makutano tu.
Mwanaume huyu mzungu anafahamika kwa jina la Brown Curtis, Ama kwa kifupi BC kama watu wake wa karibu na yeye pia anavyopenda kuitwa. Sauti yake ni nyembamba na ya chini, macho yake ni makali rangi ya bluu.
“But his price goes higher every now and then. It becomes very expensive to afford him,” (Lakini bei yake hupanda kila sasa na baadae. Inakuwa gharama kubwa kummudu,” alisema BC kabla hajapeleka sigara mdomoni na kuinyonya mithili ya mtoto anyonyavyo titi la mama yake.
“But we have no choice. We depend on him so much. Or have you got someone else?” (Lakini hatuna chaguo. Tunamtegemea mno. Au umeshampata mtu mwingine?” Miranda aliuliza.
BC akatikisa kichwa.
“No! And that’s the real problem. I must find a way out.” (Hapana! Na hilo ndilo tatizo haswa. Ni lazima nitafute namna.)
“Be keen. He knows most of our moves, he may spoil the car if we deny him the fare.” (Kuwa makini. Anajua harakati zetu nyingi, anaweza kuharibu gari akijua tumemnyima nauli.)
“Don’t worry, I will be the first one to take action after getting an exit door. He cannot do anything stupid unless I am dead,” (Usijali, nitakuwa wa kwanza kufanya jambo nikishapata mlango wa kutokea. Hawezi akafanya jambo lolote la kijinga labda niwe mfu,) alisema BC uso wake ukiwa umezibwa na moshi wa sigara
Mara akatokea dada wa kazi. Alikuwa amevalia sare rangi nyeusi na nyeupe akibebelea trey yenye glasi kubwa ya sharubati ya Strawberry.
Akaitua mezani na kumkaribisha Miranda, kisha akaenda zake.
“Any suggestion?” (Wazo lolote?) BC aliuliza akimtazama Miranda. Alijua mwanamke huyo hatokosa cha kusema.
Miranda akapandisha mabega juu.
“It’s just ok if you believe things won’t go out of your hands.” (Ni sawa tu kama unaamini vitu vitakuwa poa.)
“Yes. We gat to do something, he takes almost half of the profit. It is dangerous … let us see what will happen.” (Ndio. Inabidi tufanye kitu, anachukua karibia nusu ya faida. Ni hatari … acha tuone nini kitatokea.)
Kukawa kimya kidogo. BC alikuwa anavuta pafu za sigara, Miranda akipiga mafundo ya sharubati yake tamu.
“What about the report I sent? Have you gone through it?” (Vipi kuhusu ripoti niliyokutumia, umeipitia?) Miranda alivunja ukimya. BC akakohoa kwanza mara moja kabla hajajibu.
“I have done so. It’s already sent … and thanks for reminding me, the results are nothing but perfect! You can’t imagine even some governments have already booked them secretly.” (Nimeipitia. Tayari imeshatumwa … na shukrani kwa kunikumbusha, matokeo ni mazuri sana! Huwezi amini hadi baadhi ya serikali wameshaweka oda zao kwa siri.)
“That’s nice! Then we have to produce more!” (Hilo ni jema! Basi inabidi tuzalishe zaidi!)
“Exactly, men are in the laboratories, as we are talking, working day and night. In fact more of it will be here soon special for our enemies.” (Kabisa, watu wapo maabara, hapa tunavyoongea, wakifanya kazi usiku na mchana. Vile vile itatumwa hapa zaidi kwa ajili ya maadui zetu.)
“It’s better! Enemies now are closer than before.” (Ni bora! Maadui sasa wapo karibu kuliko awali.)
“All for the sake of business! Competition is stiff. Chemical and biological weapons are marketable for its effectiveness though they are prohibited in most places. I think it’s time now to put emphasis on this.” (Yote kwasababu ya biashara! Ushindani ni mkubwa. Silaha za kemikali na baiolojia zina soko kwasababu ya ufanisi wake japo zinakatazwa mahali pengi. Nadhani ni muda sasa wa kuweka msisitizo kwenye hili.)
BC alitazama saa yake ya mkononi, kisha akamwambia Miranda.
“It’s time. Let’s go!” (Muda huu. Tuondoke.)
Miranda akamalizia kinywaji chake, BC akaminyia sigara yake kwenye kisosi kuizima. Wakanyanyuka na kwenda kwenye gari, Jeep nyeusi aina ya Cherokee. Wakakwea na kutoka ndani ya jengo.
Mwanaume ndiye alikuwa akiendesha, mwanamke akiwa amekaa pembezoni yake.
Walipoacha tu geti kwa umbali mdogo, Miranda akatoa simu yake kwenye pochi na kumtumia ujumbe Kinoo:
“Naweza nikakawia. Hakikisha unapata ile picha leo hii kama tulivyokubaliana.”
Ujumbe ulipofika, akarejesha simu yake ndani ya pochi.
“I don’t have to tell you about this, you know how important it is. We have to expand our network tonight. We must look for another hand. You are an expert in that and that’s why I go with you.” (Sina haja ya kukuambia kuhusu hili, unajua namna gani lilivyo muhimu. Inabidi tutanue mtandao wetu. Ni lazima tutafute mkono mwingine. Wewe ni mtaalamu kwenye hilo na ndiyo maana naenda nawe.)
“I will do my best,” (Nitajitahidi,) Miranda akasema kwa ufupi, kukawa kimya. *** “Naomba maji makubwa ya Kilimanjaro, ya moto. Na waambie jikoni waniandalie ndizi tano na nyama rosti,” Jona alitoa oda kwa mhudumu. Mhudumu akatikisa kichwa chake na kwenda.
Mwanaume huyu alikuwa ndani ya bar akatizayo kabla ya kwenda nyumbani kwake. Majira yalikuwa ya giza sasa. Alikuwa amechoshwa na uchovu, na mgongo wake ulikuwa unamuuma kwa mbali kutokana na purukushani ile ya ajali.
Akiwa anangojea huduma, akatoa simu yake na kuiangaza. Hakukuwa na ujumbe wala missed call. Akatahamaki Mheshimiwa hajamtafuta mpaka muda ule.
“Hajaona missed calls zangu?”
Alikumbuka maagizo ya Mheshimiwa kwamba akiwa amebanwa basi amtafute Nade na kumwambia shida yake, ila hakutaka kufanya hivyo, akaamua kuachana na jambo hilo.
Kulikuwa kuna jumbe kadhaa toka Facebook ila hakutaka kusumbuka nazo, akazipuuza.
Alipoweka simu yake mezani, macho yake yakatekwa kumtazama mwanaume fulani aliyekuwa anaingia ndani ya eneo ya bar. Mwanaume huyu alikuwa amevaa suti nyeusi na tai nyekundu.
Aliketi karibia na eneo kubwa la kutokea.
Alikuwa ni Bigo! Mwanaume aliyeagizwa kummaliza Jona.
Jona alimtazama mwanaume huyu kwa muda kidogo. Atensheni yake ikaja kuharibiwa na mhudumu akileta maji makubwa aliyoagizwa, akayapokea na kumiminia kiasi ndani ya glasi.
Mhudumu akamfuata Bigo, mwanaume huyo naye akaagiza maji makubwa kama yale ya Jona. Mhudumu akamskiza na kwenda zake.
Mara tatu Jona akakutana macho kwa macho na Bigo. Alikunywa glasi mbili za maji kisha akanyanyuka kabla hajakutana na mhudumu akimletea chakula chake alichoagiza jikoni.
“Kiweke tu hapa mezani, naenda maliwato nakuja,” alisema Jona, kisha akaenda uani kwa ajili ya haja ndogo.
Bigo alitaka kumfuata ila akasita. Hakuwa analijua eneo hilo vizuri, ilimradi alikuwa na uhakika kwamba Jona atarudi kwasababu ameacha mizigo yake mezani, basi akatuama asiwe na mashaka.
“Acha nikamuulie kwake,” alisemea kifuani, akaendelea kunywa maji yake taratibu.
Upande wa pili Jona akamaliza haja yake, akafunga zipu ya suruali na kuanza safari ya kurudi alipokuwepo.
Lakini kabla hajamaliza safari yake, hatua chache tu toka chooni, macho yake yakaona gari Mark 2 nyeusi kwenye kauwanja kadogo ka maegesho ya magari hapo bar. Haraka kumbukumbu yake ikamjuza gari hilo ndilo lile lililotaka kumgonga.
Akataka kuhakikisha.
Kwa tahadhari akalisogelea na kulitazama mbele juu ya bodi, akaona limebonyea. Akaligusa kwa nyuma na mgongo wa kiganja, kama haitoshi akainama na kusogeza kichwa chake uvunguni mwa gari.
Akagundua gari hilo lilikuwa limefika hapo muda si mrefu. Nani ameingia bar muda si mrefu? Hakuna mwingine mbali na mwanaume yule aliyevalia suti, akili yake ikampa majibu haraka.
Basi akajikuta akitabasamu.
“Naona amenifuata kumaliza kazi yake,” alisema kisha akajirudisha kwenye kiti chake. Akaketi na kumtazama Bigo.
Alikunywa maji yake taratibu akiyapanga mambo kichwani. Alipomaliza akamuita mhudumu na kumlipa pesa yake kisha akanyanyuka na kubeba vitu vyake. Taratibu akashika njia ya kwenda nyumbani.
Alitumia njia tofauti na ile kuu. Kadiri alivyokuwa anasonga mbele, basi akawa anaongeza ukubwa wa hatua zake.
Haikupita muda mrefu, akahisi kuna gari linakuja nyuma yake. Pasipo kutazama akajua ni lile Mark 2. Kwa mwendo wake wa ukakamavu akaendelea kukata mbuga. Ndani ya muda mfupi, mbele ya nyumba yake.
Akafungua geti na kuzama ndani.
Hili lilikuwa kosa la kwanza Bigo kulifanya – kumruhusu Jona azame ndani ya nyumba. Hakujua kama amefanya kosa. Alimchukulia Jona kama mchora picha tu. Kwa akili yake akaona Jona amejiingiza kwenye kaburi lake.
Somo la namna mwanaume mwanaume huyo alivyokwepa ajali halikumuingia akilini, au pengine hakulielewa.
Alishuka akaliacha gari ‘on’ kwa minajili kwamba atarejea muda si mrefu na kuhepa zake baada ya tukio. Mkononi alikuwa amebebelea bunduki ndogo, na tayari uso wake ulikuwa umevikwa kinyago cheusi.
Kinyago chenye sura ya fuvu la kichwa cha binadamu.
Akazama ndani kwa kuruka ukuta kama kima. Taratibu akausogelea mlango, akajaribu kuusukuma, ulikuwa umefungwa. Basi hakutaka kuzozana nao kwasababu alitaka mambo yawe kimya kimya.
Alitaka amalize kula pasipo kujaza nzi.
Akazunguka jengo kupitia madirishani, kwa malengo auendee mlango wa uani nao aujaribu, pia amuone Jona yupo pande gani ya nyumba.
Alijuta kwanini hakubebelea kiwamba cha kumezea sauti ya bunduki. Lakini akatafuta ahueni ya juto hilo kwa kujitia hana haja ya kutumia hiyo silaha.
“Nitatumia mikono yangu tu,” akajisemea kifuani. “Huyu si wa kupoteza risasi yangu.”
Akazunguka dirisha la kwanza, hakuona kitu. Dirisha la pili na la tatu pia. Akiwa anasogelea la nne, ambalo ndilo lilikuwa la chumbani kwa Jona, akasikia sauti ya kitu kama karatasi nyuma yake.
Sasa alikuwa karibu na mlango wa uani. Kama hatua tano hivi aukute.
Alipiga hatua tatu, akahisi tena sauti ile ya mwanzoni. Haraka akageuka, saa hii akinyooshea mdomo wa bunduki huko. Hakuona mtu! Aliporejesha uso wake mbele, akakutana na mwanaume amesimama.
Alikuwa Jona.
Kabla hata kichwa cha Bigo hakijajua nini la kufanya, akashangaa kuona Jona yupo juu, kufumba na kufumbua, akala teke lenye kilo nzito lililomtupa chini kama fuko la saruji!
Akanyanyuka upesi kwa kujifyatua na mikono yake. Ila Jona hakumpatia mwanya hata kidogo, akachumpa na kujilaza hewani akijizungusha kama tairi. Akachanua miguu kumzawadia tena teke.
Mara hii Bigo akaliona, akainama kukwepa, kunyanyuka, hajakaa sawa, mkono wenye bunduki ukapigwa, bunduki ikarukia mbali.
Jona akatabasamu. Akatanua miguu yake na kumuita Bigo kwa ishara. Sasa Bigo akajua anapambana na mtu, mwanaume, sio ‘mchora picha’.
Alikuwa ameingia peku kwenye kiwanja chenye mbigiri. Na sasa hakuwa na budi zaidi ya kuonyesha uanaume wake.
Alikunja ngumi akajongea kwa kasi. Akatumikisha kiuno chake kurusha mateke mazito, mateke yakapita kando ya kichwa cha Jona. Akapeleka ngumize, akarudisha viwiko, navyo vikanyimwa mwelekeo.
Baada ya dakika moja, rasmi Jona akaanza kujibu mashambulizi akiwa tayari ameshamsoma adui yake ndani ya muda huo mfupi.
Hakupoteza nguvu, akapiga maeneo dhoofu kwenye mwili wa binaadamu, ambazo kitaalamu kwenye mchezo wa mapigano, martial arts, huitwa pressure points.
Ncha za ngumi yake zilitafuta kingo za kwapa za Bigo, akatia ganzi mikono ya adui. Akampiga pia chini kidogo, katikati ya shingo, penye kashimo kanachotenganisha shingo na kifua, na kummalizia juu ya kitovu kwa hatua moja moja na robo ya vidole.
Bigo akawa hoi.
Jona akamvua kinyago na kumpeleka ndani sebuleni, akamfunga kamba kwenye kiti kisha akachukua kiti kingine na kukisogeza karibu. Akachukua na chupa kubwa ya mvinyo na glasi yake, akamiminia kinywaji humo na kupiga fundo moja akiketi.
“Habari yako? – hatukuwa tumesalimiana,” alisema Jona akimtazama Bigo.
Bigo hakusema kitu. Jicho lake la kushoto lilikuwa jekundu mno. Na kushoto kidogo mwa jicho hilo kulikuwa kuna mfereji mdogo wa damu ukitokea kwenye jeraha la kiasi.
“Haya,” Jona akapandisha mabega yake juu. “Sitajali kama hutaki salamu yangu. Vipi na kinywaji nacho? Hutaki?”
Bigo akaguna kama mtu anayetaka kuangua kicheko. Akasema:
“Siku zako zinahesabika, msanii. Utaenda kuonja udongo muda si mrefu.”
Jona akatabasamu. Akanywa kwanza mafundo matatu ya kinywaji chake.
“Inaonekana unaona kinyume, ndugu yangu. Kwa unavyoona, kati yangu na wewe nani anaenda kuonja udongo muda si mrefu?”
Bigo akaguna kwa kiburi.
“Anyway, sina muda mwingi hapa,” Jona akasema akitazama saa yake ya mkononi. “Muda si mrefu itanibidi nipumzike kwa ajili ya kesho, nina kazi za kufanya na watu wa kuwaona. Hivyo basi ningependa kwenda moja kwa moja.
Wewe ni nani? Na umetumwa na nani?”
Kimya.
“Najua itakuwa ngumu kwako kusema, ila nisingependa tukaumizana na kutiana ukilema alafu ndiyo useme, so tuokoe muda.”
“Okoa muda wako kwa kuniua, msanii,” Bigo akasema, kisha akatabasamu.
Jona akanywa mafundo mawili kwa staili ya tarumbeta kisha akanyanyuka na kumsachi Bigo, akamchomoa funguo za gari.
“Unaenda wapi?” Bigo akawahi kuuliza.
Jona akamtazama na kumpuuza kisha akaenda zake nje mpaka kwenye gari la Bigo. Akafungua mlango na kuanza kupekua chombo hicho akitazama huku na huko huku akisaidiwa na kurunzi.
Akapata simu mbili, risasi nne, leseni na picha nne aina ya pasipoti. Akarejea ndani.
Akaviweka vitu alivyovipata juu ya meza alafu taratibu akaanza kukipitia kimoja baada ya kimoja.
“So unaitwa Alfonce Bigo,” alisema Jona akitazama leseni. Bigo alikuwa kimya akimtazama kwa macho makali, mdomo ameupinda.
Alimaliza kutazama leseni akaiweka juu ya meza, akatazama pasipoti zile nne: zilikuwa za watu tofauti tofauti.
“Na hawa nao umepanga kuwaua ama?” “Achana na vitu vyangu, havikuhusu!” Bigo akafoka. Jona asimjali, akaendelea na kazi yake.
Aligeuza pasipoti akazitazama kwa nyuma, akaona zimeandikwa kwa mbali maneno ya kichina. Kila pasipoti ilikuwa na maneno hayo.
Aliziweka kando akateka simu na kuanza kuzikagua. Moja ilikuwa ni smart phone, Nokia Lumia kubwa nyeusi, nyingine ikiwa ndogo ya kawaida, tekno, nayo nyeusi kwa rangi.
Simu zote zilikuwa zimefungwa kwa namba. Mtu kuingia na kutazama ilikuwa ni mpaka atie namba sahihi.
Bigo alijua Jona hataweza kufungua simu hizo, kwahiyo hapa akawa na amani na taarifa zake zilizomo ndani, zipo salama.
Alitegemea muda si mrefu Jona atamuuliza kuhusu hizo namba. Na aliapa kutozisema hata iweje, atazilinda kwa uhai wake.
Kinyume na matarajio, Jona hakumuuliza chochote, bali akanyanyuka na kwenda chumbani alipotoka na tarakilishi mpakato nyeusi aina ya HP, na waya wa kuhamisha data, USB.
Akaweka tarakilishi mezani na kuiwasha kisha akachomeka waya wa kuhamisha data toka kwenye simu kwenda kwenye tarakilishi.
Sasa hapo akawa huru kufikia mafaili yaliyopo kwenye simu ya Bigo pasipo kutia namba zozote. Mafaili yote akawa anayaona kwenye kioo cha tarakilishi yake.
“Wewe mshenzi acha kupekua simu yangu!’ Bigo aliwaka akitikisa mwili wake kwanguvu. Alitaka kujichopoa toka kwenye kamba. Alijitahidi sana kujing’amua lakini akaishia kupata tu maumivu.
Hakufanikiwa.
Jona, kana kwamba hasikii kelele za Bigo, akaendelea kuperuzi mafaili ya simu. Kuokoa muda akayakopi mafaili hayo na kuyahamishia kwenye tarakilishi yake kwa malengo ya kuyapitia atakapopata muda.
Alipomaliza akachomoa waya, akatoka mezani na kumjongea Bigo.
***
Nje ya nyumba ya Jona kulikua tulivu. Watu walikuwa ndani ya majengo yao na familia zao. Mataa yalikuwa yanamulika, na kelele pekee zilizokuwa zinasikika ni za watoto wakicheka ndani ya uzio.
Kama ungelipita hapo, basi usingeliwaza kama kuna tukio linaendelea ndani ya nyumba ya Jona, japokuwa ndiyo nyumba pekee iliyokuwa imepaki gari kwa nje.
Ndani ya muda mfupi, linatokea gari lingine. Kwa mbali halionekani kutokana na mwanga mkali wa taa. Linaposogea karibu na kufifisha taa, laonekana vema – ni Range Rover sport nyeupe.
Ndaniye alikuwamo bwana Kinoo peke yake. Akalipaki gari nyuma ya Mark 2, kisha akashuka.
Kama kawaida, alikuwa amevalia ‘kibody’ cheusi kilichobana kifua chake kipana pamoja na suruali ya jeans na moka nyeusi kwa chini.
Aliitazama Mark 2 kwa muda kidogo akijiuliza ni la nani. Akarusha macho yake ndani ya jengo la Jona, hakuona kitu.
“Ana mgeni au?”
Akalikagua gari lile Mark 2 kabla hajazama ndani kwa kuruka ukuta baada ya kuona mlango umefungwa. Naye mkononi alikuwa amebebelea bunduki ndogo, na mwendo wake ulikuwa wa tahadhari.
Angalau huyu alikuwa amepewa angalizo na Miranda juu ya Jona.
Alisogelea dirisha la sebule, akachungulia ndani. Hakumuona Jona, ila akamuona mwanaume aliyeketishwa kwenye kiti na kufungwa kamba. Hakumtambua mwanaume huyo kwani alikuwa amezibwa na kinyago usoni.
Lakini kinyago hicho kikamgutua. Kilikuwa ni cheusi chenye umbo la fuvu la binadamu. Alikumbuka Miranda aliwahi kumwambia kukihusu. Ya kwamba mwanaume yule aliyemvamia kuchukua kamera, alikuwa amekivaa.
Ina maana ndo’ huyu? Akajiuliza. Anafanya nini hapa akiwa amefungwa kamba?
Sasa kidogo Kinoo akaanza kuelewa kwanini Miranda alimwambia ‘mchoraji’ yule, ambaye ni Jona, hakuwa mchoraji tu, ni mtu mwenye ngebe za mafunzo na ujuzi. Hakutaka kuingia ndani haraka bali ausome kwanza mchezo, Jona yupo wapi? Na anamfanya nini huyu mtu aliyeonekana dhahiri kuwa mateka? Akatulia kungoja. Kwa dakika kama nne pasipo kuona wala kusikia jambo la kulituhumu. Alikuja kushtuka aliposikia chuma cha baridi kisogoni mwake, na sauti ya Jona ikamuamuru: “Tulia hivyo hivyo! – mikono juu!” Akatii amri. Kwa uzoefu wake alishajua ni mdomo wa bunduki ndiyo ambao upo kisogoni. Ila alikuwa mkaidi kuwa mpole kirahisi. Akaanza kufikiri ni njia gani inaweza kumuokoa akaushika mchezo. Ila kama vile alishtukiwa, akaonywa: “Ukijitia mjanja, nakutoboa kichwa!” Akatulia tuli, macho yake yakiangaza angaza kana kwamba mtu mwenye haraka atafutaye ufunguo wa gari. “Haya ongoza ndani!” Jona akaamuru. Pasipo kubisha, Kinoo akaanza kuchukua hatua kusogelea mlangoni. Kichwani mwake alitafakari ilikuwaje akadakwa kirahisi hivyo? Alijiona mjinga na mzembe pia. Endapo asipofanikisha hili, Miranda ataenda kumlaumu sana. Kumtusi na kumshusha vyeo. Hivyo lazima apate namna. Alipokaribia mlangoni, upesi akakisogeza kichwa chake kukwepa mdomo wa bunduki kabla Jona hajafanya lolote. Kisha akautwaa mkono wa Jona na kujaribu kuupoka silaha. Wakavutana huku na huko nguvu zikitumika. Kinoo akamzidi nguvu Jona, akaiteka silaha akimsukumizia kando mpinzani wake. Ila kabla hajafanya kitu na bunduki hiyo, Jona akautuma mguu wake, haraka sana, kuutengua mkono wa kulia wa Kinoo uliobebelea bunduki. Bunduki ikaangukia chini! Wote wakaitazama kwa macho ya ashki ila wasithubutu kuinamisha migongo yao kwa kumhofia mwenziwe. Kuinama kunamaanisha kumpa fursa adui akutende atakavyo, hilo kosa hakuna aliyetaka kulifanya. Wakaachana na bunduki wakitazamana kama mafahari ya ng’ombe ndani ya zizi. Walikunja ngumi wakitegeana. “Niliwapa onyo, naona hamjataka kulisikia!” Alisema Jona akimkazia macho Kinoo. “Wewe si wa kutupa sisi onyo. Bado huna hadhi hiyo,” Kinoo akajibu kwa dharau kabla hajaguna. Jona akatabasamu asitie neno. Alipanga matendo yake yaongee sasa na si sauti ya mdomoni. Kimwili alikuwa mdogo ukimlinganisha na Kinoo, na alijua hilo lina faida na hasaraze. Endapo akiingia mikononi mwa Kinoo basi itamuwia vigumu kuchoropoka. Faidaye, Kinoo atakuwa mzito kufanya mashanbulizi. Miili mikubwa huchukua hatua kubwa kushurutisha viungo. Basi akajipanga vema kutumia hiyo faida. Akachokoza pambano kwa kurusha ngumi mbili za haraka, Kinoo akazikwepa kisha akatuma ngumi yake nzito. Jona akayeya! Ikapita. Akatuma nyingine na nyingine, Jona akazikwepa kama mchezo wa rede. Kwa nusu dakika, akausoma mchezo, akapata alichokuwa anakitaka. Kinoo hakuwa mzuri kwenye kujilinda, alikuwa mzito kukwepa, na alikuwa akiziacha mbavu zake wazi mara kwa mara. Bila shaka alikuwa anategemea zaidi kushambulia kuliko kujilinda. Jona akaanza kucheza na mbavu za mwanaume huyo, akilenga kumtepetesha na kumminya uwezo wa kuhema. Kinoo akarusha ngumi zake kwa mfululizo, Jona akawa anakwepa kisha anakita mbavu za Kinoo kwa ngumi za upesi. Kila alipopata mwanya, basi akafyatua ngumi tatu ama nne! Ikafikia mahala Kinoo akachoka kwani alikuwa anatumia nguvu nyingi kurusha ngumi zilizokuwa zinaenda patupu. Ukijumlisha na ngumi alizokuwa antekenywa mbavuni, akashindwa kufua dafu. Alikuwa hoi bin taaban. Alikuwa anatamani kuhema kwanguvu, lakini mbavu haizikuruhusu. Ni kama vile alipewa pumu. Ni wazi alikuwa ameshindwa, ila hakutaka kuingia kwenye mikono ya adui, hivyo basi akatoroka kwa kukimbia. Aliruka ukuta akazama ndani ya gari lake na kuhepa kwa kasi! Jona alihofia kufyatua risasi kutoshtua majirani. Hakutaka kuwapa hofu wala makisio na mahisio yoyote juu yake na mambo yake. Basi akamwacha Kinoo aende. Huko akafikishe habari aliyokumbana nayo. Yeye akarudi zake ndani na kumtazama Bigo. Akampuuzia na kuendelea na mambo yake. Akaoga na kisha akajipeleka chumbani alipojilaza akiendelea kunywa. Bigo aliachwa palepale kwenye kiti.
***
Kadiri usiku ulivyokuwa unasonga ndivyo na tafrija ilivyokuwa inanoga. Sasa ilikuwa ni saa tano inayoelekea saa sita usiku na muziki laini ulikuwa unaburuza eneo wageni wakiserebuka. Ndani ya eneo hili lililokuwa limesheheni taa kali zilizogeuza usiku kuwa mchana, kulikuwa kuna walinzi kedekede wakiwalinda wanaume na wanawake waliokuwa humo tafrijani. Watu hawa walikuwa ni ‘vibopa’, watu wazito wenye nyadhfa zao serikalini ama mahala pengine nyeti kiuchumi. Karibia wanaume wote walikuwa wamevalia suti, zikipishana tu rangi. Wanawake ‘wakila’ magauni ya kupendeza na michuchumio ya haja. Nyuso za wanawake hawa zilikuwa zimerembwa kwa ‘make-up’ zilizofiti usoni. Waling’aa kama malaika, ila hawagusa kwa mwanamke Miranda. Alikuwa amependeza haswa. Pia na kujiamini kwake pamoja na kujua kwenda na muda, kulimfanya avutie zaidi. Kila muziki ulipowekwa alijua kwenda na mapigo. Alifanya watu wamtazame na pia kumwongelea wasijue mwanamke huyu alikuwapo kazini, na lengo lake lilikuwa kumtia kimyani mheshimiwa fulani. Muziki ulikata, wakarejea kwenye viti vyao. Miranda alikuwa ameketi na BC meza moja. Meza iliyokuwa imechafuliwa kwa vinywaji. Meza yao ilikuwa inatazamana, kwa umbali kidogo, na meza aliyokuwa ameketi mheshimiwa Boka, waziri wa Afya. Mwanaume mnene mweusi mwenye kitambi kama kiroba cha mihogo. Alikuwa amevalia suti na tai ya bluu. Mezani alikuwa pamoja na mwanamke fulani mnene, pasi shaka mkewe, pia na kijana mmoja wa kiume mwenye kadirio la miaka ishirini na saba – nane – tisa. “You did great!” (Umefanya vizuri!) BC alisema akitazama meza ya mheshimiwa Boka. “He was really impressed, now we’ve to figure the way out to reach him.” (Aliguswa sana, sasa tunatakiwa tutafute njia ya kumpata.) “The problem is his wife,” (shida ni mkewe,) alisema Miranda akikunja shingo kutazama penye lengo. “She’s very close to him as if she knows our intention. But I will get the way out!” (Amemganda sana kana kwamba anajua lengo letu. Lakini nitapata namna!) Miranda aliposema tu hivyo, akanyanyuka akijifanya anatengenezea nguo yake vizuri. Mheshimiwa akamtazama, naye akamtazama kukutanisha macho. Akatabasamu na kutazama kiaibu. Mheshimiwa naye akatabasamu kujibu. Miranda akaketi. Sasa akajua dhahiri mheshimiwa Boka atakuwa anatazama tazama mezani kwake baada ya hilo tukio. Basi hakujiweka mbali. Akawa anampa mheshimiwa macho na kajitabasamu. “The bird’s fallen into the trap!” (Ndege ameangukia mtegoni!) Akasema Miranda kwa tabasamu. “Now take it!” (Sasa mchukue!) BC akashadadia. Punde Miranda akanyanyuka, akamtazama mheshimiwa, kisha akayaelekezea macho yake upande wa maliwatoni. Alafu akaelekea huko akitembea kwa madaha ya walimbwende jukwaani. Mheshimiwa akamsindikiza kwa macho ya ukware. Naye, isichukue muda, akanyanyuka aende huko huko maliwatoni. Basi wakakutana na Miranda kwenye korido. Mwanamke huyo alikuwa anahangaika na zipu ya gauni huko mgongoni, akijinasibu anahangaika kuifunga. “Naweza nikakusaidia?” Mheshimiwa Boka akapaza sauti akitabasamu. ‘Naona umejileta mwenyewe boya wewe!’ Miranda akasema kifuani. Aligeuza uso wake kutazama, akakutana uso kwa uso na waziri. Akaigiza aibu. “Hapana, ahsante mheshimiwa,” akajibu akitabasamu. “Aaaah bwana mrembo kwanini upate shida hivyo na mie nipo?” Miranda hakusema kitu. Alitabasamu tu akaendelea kuhangaika na zipu yake. Basi mheshimiwa akaamua kujisogeza, alichukulia ukimya kama ‘ndio’, akadaka zipu ya Miranda na kuipandisha juu pasi na tabu. “Ahsante sana, mheshimiwa, na samahani kwa usumbufu!” “Usijali, mrembo. Unaitwa nani wewe?” “Flaviana,” Miranda akajibu akitazama chini. “Oooh jina zuri kweli!” “Ahsante.” Mheshimiwa akatazama mazingira, akajiona wapo wenyewe. Ila alijua fika hawatadumu kwa muda mrefu hapo. Aidha mkewe aje, ama watu wengine waliobanwa na haja, basi akaamua afanye mambo upesi. “Sasa mrembo nataka tupate nafasi ya kuongea vizuri na wewe. Vipi sasa nitakupataje? – una simu?” “Ndio ninayo.” “Sawa sawa!” Mheshimiwa akajipekua mfukoni, akatoa kadi ya biashara na kumkabidhi Miranda. “Utan’chek basi, sawa?” Miranda akatikisa kichwa. “Sawa, mheshimiwa, n’tajitahidi.” Mheshimiwa akatabasamu na kujilamba lips, akatoka maeneo ya maliwato na kurudi kwenye meza yake. Baadae kidogo napo Miranda akarudi zake kukutana na BC. Akamwonyeshea kadi aliyopewa na mheshimiwa. “That’s a very big step!” (Hiyo ni hatua kubwa sana!) BC akasema akimpongeza Miranda kwa kumpa mkono. “We have already put him in our store.” (Tayari tumeshamtia kwenye ghala.) Sasa wakanywa kwa furaha wakiendelea kupanga na kusuka mipango yao. Walikuwa na matumaini makubwa ya kumtia mikononi mheshimiwa Boka, na lengo lao kuu ni kumtumia kiongozi huyo wa kitengo cha Afya kusafirisha mizigo yao kwa kutumia kibali chake. Huyu kwake alikuwa na faida kubwa kuliko mheshimiwa Eliakimu kwani yeye anahusika moja kwa moja na mambo ya madawa. Lakini pia gharama yake itakuwa ndogo ama hamna kabisa kwasababu ya kumtumia Miranda kama chambo. Wakiwa wanelekea ukingoni wa tafrija na sasa wakiwa wanajiandaa kuondoka zao,kwa amani kabisa maana hawajaupoteza usiku, mara kwa mbele yao wanamuona mke wa Mheshimiwa Boka akija. Kabla hawajafanya kitu, mwanamke huyo alikuwa mbele yao akishikilia kiuno.
“Marhaba, umenifurahisha sana. Umeufanya usiku wangu kuwa wa kumbukumbu.” Miranda akatabasamu.
“Nashukuru sana mama.”
“Usijali, sasa kuna jambo moja nilikuwa nataka tutete mimi na wewe, ningepata faragha?” Alisema mke wa mheshimiwa akimtazama BC. Miranda naye akamtazama BC kabla hajajibu akipandisha mabega.
“Sina malengo ya kukuvunjia heshima, ila nimependezwa nawe na nikaona nastahili kukushirikisha hili kama utakuwa umevutiwa. Unapendelea mambo ya modeling na ulimbwende?”
“Aaaahmm …kiasi.”
“Nina kampuni ya ulimbwende na modeling ambayo inahusika moja kwa moja na mambo ya vipodozi na marashi. Ningependa kufanya kazi na wewe.”
Kidogo Miranda akabanwa na kigugumizi.
“Sitaki unipe jibu lolote kwa sasa, ni jambo nililokushtukiza. Chukua muda wako na ufikirie, utanipatia jibu.”
Mke wa mheshimiwa akafungua pochi yake, akatoa kadi na kumkabidhi Miranda.
“Unajua sikuwa na wazo lolote lile mpaka pale mume wangu aliponishtua na kunishauri. Ni kweli nilivutiwa nawe sema akili yangu ilikuwa kiparty-party zaidi.” Mke wa mheshimiwa alinena akitabasamu.
“Ahsante sana, mama. N’taona namna itakavyokuwa,” akasema Miranda kisha wakapeana mikono na kuagana. Miranda akamrudia BC wakaondoka zao kuelekea kwenye gari.
Miranda akamueleza BC juu ya yale mke wa mheshimiwa aliyomwambia.
“It might be an opportunity.” (Yaweza kuwa fursa) BC alisema akitazama mbele, kisha akauliza: “Do you have any helpful idea from that?” (Una wazo lolote lenye tija toka kwenye hilo?” Miranda akaminya lips. “Perhaps it may spark later, but for now I take it as a chance for me to be officially closer to Mr. Boka.” (Pengine laweza kutokea baadae, lakini kwa sasa naichukulia kama fursa ya mimi kuwa rasmi karibu na bwana Boka.)
“Yes, but you never know as you will be closer to the wife as well. This game becomes very thrilling, we have to win something out of it!” (Ndio, lakini huwezi jua maana utakuwa karibu na mke vilevile. Huu mchezo unakuwa mzuri zaidi, na tunatakiwa kushinda jambo toka kwenye hilo!”
Miranda hakusema kitu, alikuwa kimya akitafakari.
Gari lilinguruma pasipo watu kuongea mpaka wanafika getini mwa makazi ya Miranda ambapo wanaagana, na Miranda anaingia ndani baada ya kufunguliwa mlango na mlinzi.
“Hajaja na gari?” Miranda aliuliza akiangaza angaza.
“Hapana, alikuja na bodaboda.”
“Alikuwa amebebelea kitu chochote mkononi?”
“Hapana, sijaona zaidi ya simu.”
Miranda akasonya, kisha akanyoosha hatua zake ndefu kuelekea ndani. Alimkuta Kinoo akiwa amejilaza juu ya kiti akijikunyata kana kwamba anahisi baridi kali. Usoni mwake alikuwa na majeraha, na hakuwa nadhifu.
Akamwamsha.
“Vipi, mbona hivi? – umechukua picha?” Akauliza maswali kwa mkupuo. Kinoo akayajibu kwa kutikisa kichwa chake kukataa. Hakutia neno.
“Hujafanikiwa?” Miranda akatahamaki. Alikunja sura yake na kushika kiuno. Akashusha pumzi ndefu kabla hajakaa.
Yalikuwa ni majira ya saa nane usiku sasa. Kulikuwa kimya, kwa mbali kulikuwa kunasikika vijisauti vya vijibwa vikibweka.
“Sijafanikiwa kupata picha,” alisema Kinoo akitazama chini. Alimweleza Miranda namna mambo yalivyotukia ndani ya eneo la tukio. Miranda akashangazwa.
“Nilikuambia Kinoo, na hukutaka kunisikia!”
“Nini sijakusikia?”
“Nilikwambia yule si msanii tu wa kawaida, ni mtu mwenye mafunzo na ujuzi. Ila wewe ukapuuzia, kwa namna ulivyomshambulia ni kana kwamba ulienda kumkamata konda wa daladala!”
Kinoo hakusema kitu, alikuwa anatazama tu chini.
“Huyu mtu ni nani?” Miranda aliuliza akisimama. Aliweka mikono yake nyuma akitambaa na tafakari. “Huyu mtu ni nani haswa? Ni mchoraji tu? Kwanini Bite alimchagua kufanya naye kazi? Kutakuwa kuna sababu yoyote ama ni bahati tu?” Miranda aliteswa na maswali.
Kinoo alimtazama akamwambia:
“Kama ulivyosema hapo awali, mchoraji atakuwa anafuatiliwa na wale watu waliokuja hapa kuteka kamera. Na pasipo na shaka, wao ndiyo watakuwa wanahusika na mipango ya kumuua kwa kutumia gari kama mchoraji alivyokuja kushtaki hapa.”
“Wanataka kumuua,” Miranda alisema akitikisa kichwa. “Wanataka kummaliza, ina maana wanajua mchoraji huyo ana picha hatarishi kwao.”
“Ndio.”
“Sasa tutapataje picha Kinoo? Picha hiyo muhimu sana!”
“Nina wazo – kwanini tusikae meza moja tukaongea na mchoraji yule?”
“Oooh umeona sasa kile nilichokuwa nasema – si kila mara nguvu yatakiwa. Lakini mashaka yangu ni kwa huyo mchoraji, sijui kama atakubali.”
“Nadhani ameshajua sisi hatuhusiki na jaribio la kumuua, anaweza kukubali.”
“Sawa, ila akikubali atataka kujua kuhusu hiyo picha. Atataka kufahamu ina nini na kwanini inatafutwa. Huoni kama hilo ni tishio?”
“Kwani akijua kuna nini?”
“Hapo ndipo mimi naanza kushindwana na wewe. Wewe unajua kilichomo kwenye ile picha?”
“Hapana.”
“Unajua imechorwa nini?”
“Labda…”
“Labda nini? Hatuna uhakika, na pengine tunaweza tukaipata na bado tukashindwa kuing’amua. Endapo kama ina siri kubwa, na ndivyo inavyoonekana kutokana na utafutwaji wake, tutafanyaje? Tutamuua?”
Kinoo kimya.
“Ebu niache nilale. Siku ya leo ilikuwa ndefu sana kwangu,” Miranda alisema akielekea zake ndani ya chumba.
Hakutoka. ***
“Leo unaonekana upo bize kweli ndugu yangu,” Jumanne alimwambia Jona akimshika bega.
Yalikuwa ni majira ya saa mbili asubuhi ndani ya ofisi. Siku ilikuwa imejazwa na shughuli kama kawaida. Magari lukuki yalikuwa yanakatiza huko barabarani kama ilivyo kwenye barabara nyingi ndani ya jiji la Dar es salaam.
“Ni kweli, nimetingwa kidogo,” Jona akamjibu Jumanne pasipo kumtazama. Siku hiyo alikuwa amekuja na tarakilishi yake mpakato na ndiyo alikuwa anahangaika nayo tokea alipokuja.
Pembeni ya tarakilishi hiyo kulikuwa kuna kakibahasha kadogo cheupe, ndani yake kulikuwa kuna picha aina ya pasipoti. Picha moja ilikuwa imetokezea kwa nje.
Jumanne alikuwa anataka kutoka akapate kifungua kinywa, ila akaangaza kidogo alichokuwa anakifanya mwenzake, kile kilichomchukulia muda namna ile.
Akaona Jona yupo mtandaoni, akisoma soma baadhi ya Makala na kupitia baadhi ya picha. Jumanne akapuuzia, ila kabla hajaenda, akaona picha ile iliyokuwa imejitokeza toka kwenye kibahasha.
Aliitazama picha hiyo kwa umakini, haikuwa ngeni. Aliisogelea akaikodolea vema kabla hajamwomba Jona ruhusa ya kuichukua na kuisogeza machoni.
“Unamjua huyo mtu?” Jona akamuuliza Jumanne. Kwa mara ya kwanza aliacha mashine yake akamtazama mwenzake.
“Nahisi kama namjua. Umeitoa wapi?”
“Kuna mtu tu amenipatia. Vipi? – ulimuonea wapi?”
Jumanne alivuta kiti akaketi. Akaendelea kutazama picha hiyo akivuta kumbukumbu.
“Oooh! Sasa nimekumbuka.”
“Ni nani?”
“Huyu ni marehemu Fakiri – aliyewahi kuwa mfanyabiashara mkubwa wa samaki. Alikuwa anasafirisha samaki wa maji chumvi mikoa yote ya Tanzania. Mpaka huko Kongo, Rwanda na Burundi.”
“Mie naenda kunywa chai, mzee. Baadae,” Jumanne aliaga akaenda. Joh akaichukua ile picha aliyokuwa anaitazama Jumanne, akaitazama na yeye.
“Fakiri …” Jona alijikuta anaongea mwenyewe. Alitazama nyuma ya picha, akaona maandishi yale ya kichina ambayo yapo kwenye picha zote.
Akaweka picha pembeni na kurejea mtandaoni kwenye injini ya kusaka majibu. Akaandika: ‘Mauaji ya Fakiri’ alafu akabonyeza kitufe cha ‘ok’. Punde majibu yakaja kibao, akaanza kuyapitia moja baada ya moja.
Fakiri aliuawa kwa kunyongwa siku ya tarehe 12, desemba 2016 maeneo ya nyumbani kwake Masaki. Ameacha mjane na mtoto mmoja, ambaye naye alikuja kuuawa juma moja tu baada ya baba yake, yeye akiuawa kwa risasi.
Mpaka sasa hakuna yeyote anayeshikiliwa na polisi kwa mauaji hayo.
Kama juma moja hapo nyuma kabla ya Fakiri kuuawa, alikuwa akikabiliana na kesi ya ukwepaji kodi. Kesi ambayo ilikuwa inaelekea kumshinda na hivyo basi kutakiwa kulipa limbikizo kubwa la kodi pamoja na faini kubwa. Kwa jumla shilingi za kitanzania milioni mia tano! – nusu bilioni.
Pengine ungweza kudhani Fakiri alijiua kwasababu ya kukwepa fedheha hiyo ya biashara yake kufia mikononi, ila hakujiua! Aliuawa! Ni wazi serikali isingeweza kumuua mtu wanayemdai, tena pesa kubwa hivyo.
Sasa nani alimuua? Na alifanya hivyo kwa malengo gani? Na kwanini mtoto wake naye akauawa? Maswali hayo hayakuwahi kupata majibu toka upande wowote ule.
Ila juu yake hayo, Jona anapata tena swali lingine, mbona picha ya Fakiri ilikuwa ndani ya kibahasha cha Bigo? Ina maana yeye ndiye anahusika na mauaji hayo? Kama ndio, mbona ya mtoto wa Fakiri haipo? Yeye aliuawa na nani?
Akajikuta anashusha pumzi ndefu baada ya kuona ana mlima mkubwa wa kuupanda. Lengo lake lilikuwa ni kumjua tu Bigo ni nani na nani aliyemtuma ila anajikuta anagundua mambo mengine ambayo hakutaraji.
Ayaache? Hapana! Haya mambo yanaweza kumsaidia akaunganisha doti kumjua Bigo hasa ni nani na anamfanyia kazi nani.
Lakini juu ya yote haya, kwanini hawa watu wanataka kumpoteza? Kosa lake ni nini?
Kama angelikuwa bado yu ndani ya jeshi la polisi, basi angesema aliingia kwenye anga zao, ila la hasha! Sasa tabu nini? Alishawahi kuwagusa watu hawa pindi akiwa jeshini? Akajiuliza. Mbona hawakumtafuta muda wote huo?
Masikini hakujua chanzo ni picha. picha tu ndiyo ambayo inataka kumtoa roho. Picha tu ndiyo ambayo inamwingiza kwenye anga la wababe wanaotaka kunyofoa uhai wake kama vile Bite.
Jona anarudishwa ndani ya ulingo wa mapambano pasipo kutarajia. Anarudishwa kazini japokuwa alishakataa hii kazi aendelee na maisha mengine.
Kabla ya kuendelea kuperuzi na kuhangaika juu ya Fakiri, kwanza akapata wazo la kuyatambua yale maneno yaliyokuwepo nyuma ya pasipoti zote za Bigo.
Kwa kutumia alama za kichapio cha tarakilishi zake, anakopi maneno yale kwenye injini ya kusakia majibu mtandaoni kisha anasaka.
Punde yanakuja majibu mengi, anachagua jibu moja na kuliangaza. Anaona maneno matatu: ‘Pumzi ya mwisho’. Kumbe ndiyo maana ya yale maneno.
Moja kwa moja akajihakikishia kumbe wale watu kwenye pasipoti walikuwa kwenye ahadi ya mauaji. Maana yake walikuwa kwenye pumzi zao za mwisho.
Kwanini wauawe? Na ni nani aliyekuwa anataka kuwaua?
Pasipoti zilikuwa mpya mpya. Hilo lilimaanisha orodha hiyo ya mauaji haikuwa ya zamani. Yani kama kwa kukadiria, ina mwaka tu, kama ikizidi ni miezi tu kadhaa.
Kwahiyo wote waliokuwa kwenye pasipoti wameuawa? Au kuna wengine bado wapo hai? Kwanini yeye hayupo kwenye pasipoti ila analengwa kuuawa?
Akili yake ikamwambia yeye alitokea tu kwa dharura, kuna watu waliokuwa kwenye orodha tangu kitambo. Ni nini basi hicho kilichomwingiza kwenye orodha?
Maswali yalizidi kichwa, akaona anahitaji kupumzika. Aliachana na tarakilishi yake kabla hajaidaka simu na kwenda zake nje aliposimama na kuangaza barabarani kana kwamba anahesabu idadi ya magari.
Alitaka kutoka akajipatie kikombe cha chai ila ofisi amwachie nani? Jumanne bado hakuwa amerudi.
Hali hiyo ikamlazimu ang’ae ng’ae macho kabla ya muda kidogo simu yake haijatetemeka kumwashiria ujumbe umeingia. Akaichomoa na kuitazama. Ni ujumbe wa Facebook toka kwa Miriam – mke wa mheshimiwa Eliakimu.
Jona akatabasamu.
‘I think I need your phone number if you don’t mind’ (Nadhani nahitaji namba yako ya simu kama hutojali’
‘It’s just ok, I wanted to ask for it earlier but hesitated.’ (ni sawa, nilitaka kukuomba hapo mapema lakini nikasita.’
Chati yake na Mariam zilionekana hivyo. Yeye alikuwa wa kwanza kutuma ujumbe kuhusu kuomba namba ya simu kabla ya hajajibiwa na Miriam kwamba naye pia alikuwa anataka kuomba.
‘Did you fear to ask?’ (Uliogopa kuomba?)
‘Somehow, you know. You were impressed so I decided to wait.’ (Kiasi, si unajua. Ulikuwa umevutiwa kwahiyo nikaamua kungoja.)
Jona akatuma vimdoli vya kutabasamu, na ndiyo hivyo punde namba ikatumwa na Miriam.
‘At what time am I supposed to find you?’ (Kwa muda gani natakiwa kukutafuta?) Jona akautuma ujumbe kuuliza. Uzuri Mariam alikuwa mtandaoni hivyo akajibu upesi:
‘At any time.’ (Muda wowote.)
‘Really?’ (Kweli?)
‘Yah! Why asking?’ (Ndio! Kwanini unauliza?) Mariam aliambatanisha ujumbe wake na vimdoli vya kushangaa.
‘I didn’t expect that ‘anytime’, aren’t you in relationship? Sorry for asking though.’ (Sikutegemea hiyo ‘muda wowote’, haupo kwenye mahusiano? Samahani kwa kuuliza lakini.)
‘Don’t mind, I am not in relationship that’s why I am free’ (Usijali, sipo kwenye mahusiano ndiyo maana nipo huru.)
‘Better for you! Expect my call n’ messages soon!’ (Ni njema kwako! Tegemea simu na jumbe zangu karibuni!)
‘Wow! Can’t wait.’ (Wow! Nangoja kwa hamu.)
Jona akatoka huko mtandaoni baada ya kuinakili namba ya Bite kichwani, akaitunza kwenye simu yake kwa jina la ‘target no.1’. Kabla hajaendelea zaidi, Jumanne akarejea, basi yeye akaenda kujipatia chai angalau atie joto tumboni.
Akiwa anangoja kikombe cha chai, akaendelea na kazoezi kake.
Akahamishia namba ya Miriam kwenye msako wa lokesheni kwa kutumia GPS. Simu ikaanza kutafuta taratibu. Mara ikaeleza wapi namba ya Miriam inapopatikana.
Jona akajikuta anatabasamu.
“Hadithi imeishia hapa,” akanena mwenyewe.
“Hadithi gani?” mara sauti ikamuuliza na kumfanya atoe macho yake kwenye simu. Alah! Alikuwa mama K akiweka kikombe cha chai mezani. “Masikio yako yapo kazini muda wote mama K!”
“Kama ilivyo mikono yangu,” mama K akajibu kwa tabasamu, kisha akasema: “Jumanne alisema utakuja.”
“Wapi?”
“Kuna mahali pengine zaidi ya hapa?” Alijigamba mama K ndani ya gauni lake la kale lenye mistari hafifu rangi ya kijani. Nywele zake alikuwa amezifumba na kiremba kikubwa cha pande la khanga, miguu yake ndani ya raba za pinki.
Akiwa mgahawani, Jona hupenda kukaa mahali panapoweza kumfanya akaona ofisi yake. Hufanya hivi ili asije akakosa ama kupitwa na taarifa yoyote ile toka upande ule wa pili.
Akiwa anakunywa zake chai taratibu, kichwani akiyapangilia mafaili, kwa mbali alikuwa anatazama ofisi na kushuhudia wageni watatu wazungu wakizama ndani.
Jumanne aliwapokea kwa bashasha na punde akaanza kuwaonyesha bidhaa kwa mikono yake iliyokuwa inapanda na kushuka, ikienda kushoto na kulia.
Mpaka Jona anamaliza kunywa chai, wageni walikuwa tayari wameondoka. Alishika zake njia kurudi ofisini.
Kabla hajafika, ikiwa imebakia takribani kama hatua tatu tu, Jona anamuona mwanamke fulani upande wake wa kushoto hatua kama kumi na tatu kwa umbali.
Mwanamke huyu alikuwa amevalia sketi fupi, topu, koti fupi dogo la kung’aa, viatu virefu vinayokomea magotini, miwani ya jua na wigi refu. Vyote hivi vilikuwa vyeusi kwa rangi!
Mkono wake wa kuume ulikuwa umebebelea simu kubwa. Alikuwa amesimama akichezea hii simu. Ila Jona aliporusha macho yake upande wake, haraka akageuzia sura yake pembeni.
“Nishawahi kumwona huyu mwanamke wapi?” Jona alijiuliza akiingia ndani ya ofisi. Kimo, rangi na shepu ya mwanamke yule kwake havikuwa vigeni. Japokuwa sura hakuwa anaifahamu, ila ‘kapicha’ kalikuwa kyenyeji.
Aliipokutana na Jumanne na kuanza kuongea kuhusu ya mgahawani, akili yake ikampuuzia na kumsahau mwanamke huyo.
*** Kwenye majira ya saa mbili usiku: Mbweni. Mazingira yalikuwa na rasha rasha za vijikelele vya hapa na pale kama mara nyingi inavyokuwa kwenye nyumba za kupanga ambazo zimesongamana pamoja.
Katika eneo hili, kaya nne zilikuwa ndani ya uzio mmoja mkubwa, kila nyumba ikiwa imejitenga mbali kidogo na mwenzake. Nyumba hizi zilikuwa zinafanana kuanzia rangi mpaka mpangilio wake.
Kama mtu ni mgeni wa eneo basi unaweza kupotea ukachanganya milango.
‘Nisubirie hapo hapo nakuja,’ Kinoo aliyekuwa amesimama getini, kwa ndani, aliupokea ujumbe huo simuni. Akangoja.
Alikuwa amevalia ‘kibody’ cheusi, suruali ya jeans na raba nyeupe.
Punde anamwona Mudy, mwanaume yule aliyekuwa anafanya kazi kwenye kampuni ya Bite, akija. Alikuwa amevalia jezi ya mchezo wa mpira ya taifa la Hispania. Mkononi alikuwa ana simu.
Alimpokea Kinoo wakaongozana naye kuelekea nyumba ya upande wa kushoto mwa geti, kwa nje kulipaki Rav4 nyeupe. Wakazama ndani na kujiweka sebuleni. Baada ya maongezi mafupi, Mudy akaenda chumbani na kurejea na faili moja kubwa rangi ya samawati aliloliweka mezani.
“Kuna nyaraka fulani ya malipo, Bite aliniachia wiki moja kabla ya mauaji yake. Nakumbuka alinisisitizia sana niahakikishe natuma pesa kwenda kampuni fulani ya kusambaza umeme wa jua.”
Mudy akaonyesha nyaraka hiyo kwa Kinoo.
“Ilikuwa kiasi kikubwa sana cha pesa. Ila nilikuwa nimetingwa na kazi nyingi na hata kupelekea kupita siku tatu nikiwa sijatuma pesa hiyo. siku ya nne, Bite alikuja akiwa na mashaka na haraka akaniuliza kama nimetuma ile pesa, nikamwambia hapana lakini nikihofia sana huenda atanikaripia kwani alisisitiza.
Ajabu, akafurahi. Akanambia: ‘Ahsante sana Mudy, usitume tena hiyo pesa. Hao watu ni mafedhuli wakubwa, wezi na wauaji. Acha mara moja!’ kisha akaenda zake.
Huoni kampuni hii ndiyo watuhumiwa namba moja na sababu ikawa ile pesa?” Mudy alimalizia taarifa yake na swali. Kinoo akaunga mkono hoja.
“Sijui! Ila nakumbuka walikaa vikao viwili kama si vitatu mfululizo. Hatukuambiwa wanaongelea nini. Wala hatukupashwa habari kama kuna mabadiliko ama mazingatio yoyote kutokana na vikao hivyo!”
Kinoo akaguna kisha akauliza:
“Unajua wapi Brokoli anaishi?”
“Yah! Najua,” Mudy akajibu akitikisa kichwa.
“Na ulishawahi kuiftuatilia hiyo kampuni ya umeme wa jua?”
“Hapana. Sikufanya hilo kwa kutegemea polisi watalivalia njuga.”
“Sawa, na vipi kama hili jambo likabuma tena huko polisi, upo radhi kwenda umbali gani kutafuta haki ya Bite?”
Kidogo Mudy akasita.
“Una maanisha nini?”
“Unajua Mudy, si kila muda mambo yanaenda kama vile tunavyotarajia ama tunavyotaka. Nadhani uliona namna polisi walivyokuangusha ulivyowapelekea hili jambo. Sasa mimi nataka kujua unaweza kwenda kilomita ngapi kutafuta haki ya Bite?”
“Kadiri ya uwezo wangu.”
“Ahsante sana, hicho ndicho nilikuwa nataka. Njia hii inaweza ikawa ngumu na ndefu, inabidi tujiandae. Aidha kupita njia kuu ama nyinginezo ilimradi haki ipatikane.”
Kinoo akasafisha kwanza koo, akaendelea:
“Kikubwa ninachohitaji toka kwao ni taarifa tu, hayo mengine mimi nitayasimamia. Nitahitaji taarifa mbalimbali toka ofisini mwenu kama hutojali, yote kwa ajili ya Bite.”
“Nitajitahidi kadiri ninavyoweza.”
Wakapeana mikono. Kinoo akaaga.
“Ina maana mgeni unaondoka pasipo kupata chochote kitu?”
“Nashukuru sana, usijali. Leo si mwisho wa dunia. Anyway, unaishi mwenyewe?”
“Yah! Nipo mwenyewe.”
“Nyumba yote hii?”
Mudy akatabasamu. “Ndio, nipo mwenyewe.”
“Aisee!” Kinoo akatahamaki akiangaza huku na huko. Akapandisha mabega yake na kupinda mdomo.
“Haya mzee. Ningependa unipatie hizi nyaraka zako nikajaribu kufuatilia baadhi ya mambo. Pengine naweza nikaibuka na jambo.”
Mudy akamkabidhi.
“Kuwa makini, bado zinahitajika na ni muhimu ofisini.”
Kinoo akaitikia kabla hajaenda zake. Cha kwanza alichokifanya ni kumtafuta na kukutana na Miranda. Alikuwa yupo nyumbani kwake akijipatia kinywaji laini na kutazama televisheni. Alikuwa amevalia bukta ya timberland na blauzi nyeusi.
Akamweleza yale yote aliyoyapata huko kwa Mudy.
“Umefanya kazi nzuri!” Miranda akampongeza akipitisha pitisha macho yake kwenye nyaraka alizokuja nazo Kinoo.
“Lakini … Kinoo, kama vile naijua hii kampuni.”
“Serious?”
“Yah! Serious.”
“Ipo wapi?”
“Kama sijakosea, nilishawahi kuiona ikitangazwa kwenye TV. Tena si zamani, jana tu! … ngoja!” Miranda akanyaka rimoti na kubadili alichokuwa anakitazama toka kwenye movie mpaka chaneli ya kawaida.
“Bila shaka niliona hilo tangazo hapa.”
Alipoweka hiyo chaneli, wakaendelea na maongezi mengine. Wakagusia swala la picha ya Bite iliyopo kwa Jona.
“Nimeona ni vema nikaonana naye binafsi,” alisema Bite akikuna kichwa. “Nadhani nikimwelezea vizuri anaweza akanielewa. Hata kama asiponipa hiyo picha basi anipe wasaa mdogo wa kuitazama.”
“Unadhani atakukubalia?” Kinoo akauliza.
“Hayo yote ni matokeo: kunikubalia ama kunikatalia. Ila angalau nimejaribu. Lakini najua sitashindwa.”
Kinoo akaguna.
“Labda … sijui.”
“Kuna utofauti kati yangu na wewe,” Miranda akasema akimtazama Kinoo. “Tofauti moja kubwa mimi ni mwanamke na wewe ni mwanaume.”
Mara simu ya Miranda ikanguruma na kukatisha maongezi. Miranda akaitazama kujua ni nani kabla hajaiweka sikioni. Alikuwa ni waziri wa michezo; Mheshimiwa Eliakimu Mtaja.
“Tunaweza tukaonana, binti?” sauti ya Eliakimu iliuliza.
“Muda gani mheshimiwa?”
“Kesho majira ya jioni hapa nyumbani kwangu.”
“Sawa.”
Simu ikakata. Lakini ilimkumbusha jambo, kuwasiliana na bwana Boka, waziri wa Afya. Alienda chumbani kwake akarejea na kadi ya biashara aliyopewa na mwanaume huyo, akapiga namba iliyokuwa imeanishwa.
Bahati haikuwa kwake, simu haikupokelewa. Alipiga mara tatu kabla hajaamua kusitisha zoezi hilo. *** “Kesho atakuja,” alisema bwana Eliakimu akimwambia Nade. Wote walikuwa sebuleni peke yao. Sauti ya televisheni ilikuwa inanguruma kwa mbali ikikosa shabiki wa kuitazama.
Eliakimu alikuwa amevalia suti ya traki ya michezo rangi ya bluu, Nade akiwa amejivalia suruali nyeusi ya kitambaa iliyoendana na koti lake fupi jeusi lenye kola rangi ya pinki.
“Tangu lini pesa ikatosha?” Aliuliza Eliakimu. “Maxwell anataka kunipanda kichwani sasa. inabidi ajue hichi ni kitabu, hakuna ukurasa mpya kama haupo wa zamani, na ukitoa karatasi moja kwenye riwaya basi riwaya nzima inapoteza maana.”
Aliposema hayo akaulaza mgongo wake kwenye kiti akizama fikirani. Kwa dakika kama moja kukawa kimya kabla Nade hajamuuliza:
“Kwahiyo tunafanya nini, mkuu?”
Bwana Eliakimu akanyaka simu yake, akatafuta jina la Max, akaliita. Baada ya muda mchache ikapokelewa.
“Max, tunaweza tukaonana?” bwana Eliakimu aliuliza. Mzee huyu huwa haongei na mtu kwenye simu kuhusu mambo yake. Kuficha taarifa zake huwa anamwomba mtu wake wakutane. Na hupendelea zaidi nyumba yake kama mahali pa makutano.
“Hapana, hatuwezi kukutana,” ikajibu sauti ndani ya simu.
“Kwanini?”
“Kwasababu sina tena sababu ya kukutana na wewe mheshimiwa. Nadhani kibaraka wako ameshakwambia.”
“Max!”
Simu ikakata. Bwana Eliakimu akaitazama kana kwamba haamini.
“Amekata!” akasema akimtazama Nade. “Hivi huyu ananijua ama ananisikia?”
“Hatuwezi tukamwacha huyu mtu hai,” akasema Bwana Eliakimu. “Anajua siri zetu nyingi mno. Hawezi akatoka tu kienyeji namna hii. Tutapataje uhakiki wa taarifa zetu kwake?”
“Hilo ndiyo jambo kubwa. Siri ziko mashakani sasa. hatuwezi jua nini kimemsukuma akajitoa kwenye duara.”
“Kwanini hukummaliza?”
“Nisingeweza kummaliza pasipo idhini yako.”
Eliakimu akanyanyuka akiweka mikono yake nyuma ya mgongo.
“Hakikisha kesho unammaliza huyu punguani. Usibakize ushahidi wowote nyuma!” alisema bwana Eliakimu kwa macho ya kumaanisha.
“Sawa, mkuu. Nitajitahidi,” Nade akapokea kauli.
Eliakimu akaenda zake chumbani. Alikuwa amekunja uso akibinua mdomo.
*** “Kwanini ulimuua Fakiri?” Jona alimuuliza Bigo aliyekuwa hapo kitini kwa masaa ya kutosha sasa. Bigo hakuwa amekula wala kunywa chochote. Tangu alipofungiwa kwenye kiti hakuwa amesogea wala kwenda popote.
Kuepusha asije akapiga makelele na kuzua tafrani, Jona huwa anamfunga mdomo pale anapotaka kulala ama kuondoka.
Bigo alitabasamu akimtazama Jona kwa kebehi.
“Sijui nini unaongelea,” akajibu kisha akalaza kichwa chake kutazama chini.
“Bigo, unapenda kuhangaika na kuteseka namna hii?” Jona aliuliza. “Mimi sina shida na wewe, najua wewe ni kibaraka tu unayetumwa. Mimi nina shida na bosi wako. Na shida yangu ni kujua kwanini anataka kuniua. Kwanini mnataka kuniua?”
Bigo akatabasamu.
“Ngoja nikwambie kitu kimoja, msanii. Sisi huwa hatumfuati wala kusumbuka na mtu asiye na faida kwetu, tunamfuata yule aliye na chetu, yule ambaye ana kitu tunachokitaka.”
“Mimi nina kipi chenu?”
Bigo akatikisa kichwa kichovu.
“Sina haja ya kukwambia, utakuja kujua mwenyewe. Kwa sasa mimi ni wa kufa tu, aidha nifie kwako ama kwa mkuu wangu. Najua hataniacha hai. Kwahiyo sina cha kupoteza, fanya upendacho.”
“Sina haja ya kukuua. Nipe taarifa ninazozitaka.”
“Alafu?”
“Nitakuacha uwe huru.”
Bigo akajaribu kucheka, ila zoezi likashindikana. Hakukuwa na ushirikiano toka tumboni.
“Huru? … siwezi kuwa huru kamwe maisha yangu yote.”
“Kwanini unasema hivyo?”
“Kwasababu najua. Njia pekee ya mimi kuwa huru ni kifo, la hasha sipo huru kabisa. Kwahiyo kama unataka kuniweka huru, inabidi uniue.”
“Sina haja ya kukuua, Bigo.”
“Basi mimi mwenyewe nitajiweka huru.”
“Kivipi? – huwezi kujiua hapo.”
Katika hali ya kushangaza, Bigo akaanza kuvuja damu nyingi mdomoni. Jona akashangazwa sana na hilo tukio. Alimkagua Bigo na macho yake lakini hakuona kama ana mushkeli popote pale.
Mbele ya macho yake, Bigo akalegeza kichwa, akakata pumzi.
Muda mfupi mbele, bado Jona akiwa ameduwaa, ulimi ukatoka mdomoni mwa Bigo na kudondokea chini!
Bigo alikuwa ameunyofoa ulimi wake kwa kutumia meno!
“Shit!” Jona akaalaani. Alishika kiuno akitafakari. Hakutaka kumuua Bigo ila bado tu msala ulimwangukia. Sasa hakuwa na namna nyingine zaidi ya kwenda kumzika, tena wakati huo huo wa usiku isije ikaleta nongwa.
Aliubeba mwili wa Bigo mpaka uani kisha akachimba shimo na kuuzika. Zoezi hilo lilimchukua nusu saa kulimaliza. Alikuwa ametepeta jasho, akaenda kuoga kabla hajatulia sebuleni kutafakari.
Bigo ameshaenda sasa nini anafanya? Akapata wazo la kufuatilia yale maneno ya kichina ‘pumzi ya mwisho’. Alihisi pengine inaweza kuwa ishara ikamsaidia kugundua vitu vingine muhimu na vikubwa.
Akaunganisha tarakilishi yake na mtandao toka kwenye simu kisha akaanza kuwandawanda mtandaoni. Aliandika maneno yale ya kichina na maana yake kwa kiingereza alafu akaanza kusaka majibu.
Baada ya punde majibu kadhaa yakaja. Akaanza kuyapitia moja baada ya moja.
Taarifa zilikuwa finyu. Na taarifa nyingi katika hizo finyu hazikuwa zile anazozitaka. Lakini asitoke mtupu akakutana na taarifa moja, tena iliyojifichaficha huko mwishoni mwishoni.
Taarifa hii ilikuja kabla ya kidogo hajaghairi. Ilikuwa inawahusu watu wawili huko Shanghai – China waliouawa na polisi.
Jona akapitia taarifa ya tukio hilo ambalo lilitukia mnamo mwaka 2002. Akaja kugundua watu hao wawili walikuwa wametumwa kummaliza mfanyabiashara mmoja wa vipuri ambaye kwa bahati yake alitoa taarifa mapema kwa polisi.
Mfanyabiashara huyo aliwaambia polisi alitumiwa ujumbe mfupi kwenye simu yake: ‘Pumzi ya mwisho’ siku moja kabla hajavamiwa. Hakuuelewa ujumbe huo ila kwa usalama wake maana ana maadui wengi kibiashara akatoa taarifa polisi.
Hapo sasa Jona akajua kumbe ‘Pumzi ya mwisho’ ni kitu ambacho kipo ulimwenguni na si tu Tanzania pekee, ni mtandao mpana, lakini pia ni kitu cha muda mrefu. Na tageti yake kwa kiasi kikubwa ikiwa ni watu wakubwa, haswa wafanyabiashara.
Wauaji hao wa ‘pumzi ya mwisho’ waliuawa na polisi kwenye majibizano ya risasi hivyo haikupatikana taarifa yoyote toka kwao. Haikujulikana nani aliyewatuma na ni kwa malengo gani.
Jona aliamua kutafuta jina la mfanyabiashara huyo aliyenusurika kifo, akapata taarifa aliuawa baada ya juma moja tu tangu aliposalimika. Aliuawa kwa risasi na watu wasiojulikana waliotumia gari lililokuwa kwenye mwendokasi.
Kumbe alikuja kutafutwa na kuuawa! Jona akatahamaki. Alitafuta na kutafuta lakini hakupata kingine zaidi ya hicho.
Hili likamaanisha kwa Jona kwamba wauaji hawa wa ‘Pumzi ya mwisho’ walifanikiwa kutekeleza mauaji yao mengine pasipo kujulikana. Ishu ya mfanyabiashara huyu wa vipuri ilikuwa ndiyo pekee ambayo iliwaweka uchi, angalau ikaacha nyayo juu ya mchanga.
Lakini wapo nyuma ya nani? Nani anawatuma na kwa ajili ya malengo gani? Hayo bado yalimsumbua.
Aliona njia pekee ya kupata majibu ni kwa kutumia udadisi wake kwenye hili jambo la Fakiri. Huo ndiyo moshi pekee ambao unaweza kumwonyesha moto upo wapi.
Akadhamiria kukutana na mjane wa Fakiri, na kama akifanikiwa basi atapata ngazi ya kumpeleka hatua nyingine.
Akazima tarakilishi yake na kwenda kuchomoa chupa ya kileo toka kwenye jokofu. Akaenda nayo mpaka kitandani alipoketi na kunywa taratibu kilevi hicho huku akitafakari na huku akingoja kileo kimkate fikira alale.
Baada ya kama robo saa, chupa ikawa kando wakati yeye akiwa tayari ameshajigeuzia upande mwingine.
***
Majira ya saa kumi na moja na dakika kumi na nane asubuhi, Afrikana: Mbezi beach, Dar es salaam.
“Chai ipo tayari,” alisema mwanamke mmoja mnene mweusi aliyekuwa amevalia gauni la kulalia. Makadirio ya umri wake miaka thelathini na mapema hivi. Alikuwa anamwambia mwanaume mwenye umbo la saizi ya kati, maji ya kunde, akiwa anatengenezea suruali yake akijitazama kwenye kioo.
Kwa makadirio pia, umri wake haukuwa mbali sana na wa mwanamke, ambaye kwa wazi alikuwa mkewe.
“Yah! Wanajiandaa saa hizi, si unajua shool bus lao linavyowahi.” mwanamke akajibu kisha akaenda kitandani alipoketi na kuendelea kumtazama mwanaume ambaye hakukaa muda mrefu sana kabla hajatoka ndani ya chumba kwenda sebuleni kupata kifungua kinywa.
Zoezi hilo likamchukua dakika nane tu, akarejea tena chumbani kuchukua mkoba wake na kumuaga mkewe.
“Usisahau kuja na kile kitu, sawa?” mwanamke alisema akimtazama mume machoni. Mume akatabasamu.
“Nitaomba unikumbushe kwa ujumbe majira ya jioni.”
“Sawa,” mwanamke akaitikia kisha akambusu mumewe kumuaga. Mwanaume akatoka ndani mpaka kwenye gari, Suzuki – vitara nyeupe, akatupia begi lake viti vya nyuma na kuwasha gari.
Ila kabla hajasogeza chombo kwenda popote pale, ghafla akajikuta akibanwa pumzi na kitambaa. Alipapatika kwa muda mchache mno kabla hajalegea akilaza kichwa chake akiachama mdomo wazi.
Anatoka mwanamke ndani ya gari akiwa amevalia suti nyeusi, suruali ya kitambaa na koti, mkono wake wa kuume umeshikilia pochi nyeusi. Alikuwa amevalia wigi kubwa jeusi lililokuwa linaficha uso wake.
Alifuata uzio akaukwea na kujimwagia nje ya nyumba. Alipitia pale ambapo nyaya ya umeme zilikuwa zimekatwa.
Haikujulikana aliingiaje kwenye gari na kufanikisha zoezi lake, hiyo kazi sasa wakaachiwa polisi wahangaike nayo.
Mwanamke huyo aliposonga mbali na nyumba aliyofanya tukio, akatoa simu ndani ya pochi na kutuma ujumbe:
‘Tayari kazi imeisha.’
Alipoona taarifa kwamba ujumbe umefika, akarejesha simu ndani ya pochi. Akapotea akiacha msiba nyuma. ***
Majira ya saa kumi na nusu jioni, ndani ya nyumba ya mheshimiwa Eliakimu.
“Naona umekuja on time!” alisema Eliakimu kwa tabasamu akipeana mkono na Miranda.
“Si unajua ukiitwa na mheshimiwa lazima uzingatie muda,” alisema Miranda akirudisha tabasamu kwa Eliakimu.
“Nyie ndo’ waheshimiwa wenyewe bwana, sio sisi! – karibu sana.”
“Ahsante, nimeshakaribia.”
Alikuja mfanyakazi wa ndani akapewa oda ya kuleta vinywaji laini. Maongezi yakaendelea baina ya Miranda na Mheshimiwa.
“Nimekuita hapa kwa ajili ya ule mpango wetu, nataka nikupatie mrejesho wa hatua ambayo imefikia sasa.”
“Ndio, Mheshimiwa.”
“Kila kitu kipo sawa, mambo yameenda kama ambavyo nilitaka yaende japo kuna kamushkeli kadogo kalijiri ila nimeshakasuluhisha. Nimeshaongea na kuwapanga wahusika. Sasa kinachohitajika ili tumalize hii hatua yetu ni pesa.”
Mfanyakazi akakatisha kidogo maongezi yao kwa ujio wake wa kuleta vinywaji – sharubati ya embe. Kila mtu akateka glasi yake moja toka kwenye trei, mfanyakazi akaenda zake, maongezi yakaendelea:
“Hii pesa ambayo inahitajika hapa si yangu, la hasha. Ni ya kufanikisha tukio kwa kuwapatia mgao hawa vibaraka wadogowadogo angalau ili wafunge midomo yao. Kama unavyojua sisi ni waelekezaji na wasimamiaji ila utendaji upo mikononi mwao.”
“Ndio, mheshimiwa.”
“Sasa nawasikiliza ninyi. Hili jambo la malipo yao mtalikamilisha muda gani?”
Miranda akanywa kwanza kinywaji fundo moja, kisha akauliza:
“Ni kiasi gani, Mheshimiwa?”
“Aaaah mama, kwani haufahamu? Kiasi ni kile kile cha siku zote. Kwani tulishawahi kubadili?”
“Sawa, Mheshimiwa. Lakini siwezi kukupa majibu ya moja kwa moja pasipo kuonana na mkuu wangu kwanza. Inabidi nimfikishie hizi taarifa.”
“Unajua kabla sijakutafuta wewe, nilimtafuta kwanza yeye maana najua yeye ndiye mhusika wa mambo ya fedha. Na nilifanya hivyo kwa siku mbili kabla sijakutafuta wewe. Hakuwa anapokea simu zangu wala kujibu meseji zangu. Sijajua nini shida.”
“Pengine anakuwa ametingwa tu.”
“Kiasi cha kutoweza hata kurejesha ujumbe mfupi? Na ilhali anajua kabisa kuna jambo nyeti lipo mbele yetu?”
Miranda akakosa cha kusema.
“Au mna mpango mwingine wa ziada?” Mheshimiwa akauliza akimtazama Miranda machoni. Miranda akahisi msisimko fulani mwilini.
Swali hili lilifanya sharubati aliyokunywa igome kupita kooni. Alijitahidi kukaza macho yake yasizalishe shaka, akatikisa kichwa.
“Hapana, Mheshimiwa, usiwe na mawazo hayo. Hatuna mpango wowote ule. Hili jambo la mawasiliano si kwako tu, hata kwangu pia. Kwa muda kidogo sijawasiliana na mkuu. Hapatikani kwenye simu yake … ndiyo maana nikasema pengine amebanwa na kazi.”
“Sasa anabanwa na kazi gani kama hizi zake hazifanyi? … Anyway, hili jambo ni la haraka. Kumbukeni huu ni mpango haramu hautakiwi kuvuta muda otherwise utabumburuka.”
“Nimekuelewa mheshimiwa. Nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu kufanikisha hili.”
“Kama kuna tatizo mnaweza mkanishirikisha. It’s ok.”
“Sawa.”
Miranda alishindwa hata kumaliza sharubati yake. Akaweka glasi chini na kuaga.
“Mbona mapema hivyo?”
“Kuna mahali natakiwa kupitia, Mheshimiwa.”
Hakutaka kubakia zaidi hapo. Aliona kadiri anavyokaa hapo basi muda si mwingi anaweza akashtukiwa.
Alipopanda gari na kutoka ndani ya jengo la Mheshimiwa akampigia simu BC na kumpasha habari aliyokumbana nayo. BC akamtaka waonane kesho yake kwani amebanwa na kazi kwa muda huo.
***
Baadae kwenye vyombo vya habari na mitandaoni taarifa ya mauaji ya afisa wa serikali ajulikanaye kwa jina Maxwell Ndoja ikasambaa na kutawala.
Picha za afisa huyo akiwa kwenye gari lake ambalo bado lilikuwa linachemsha injini, ndizo zikawa mjadala huku na huko watu wakishangazwa kwa namna tukio hilo lilivyofanyika kwa ustadi.
Msemaji wa jeshi la polisi alisema tukio hilo lilifanyika majira ya asubuhi ya mapema ambapo mlinzi aliziraishwa na muuaji kabla hajafanikiwa kumnusisha sumu afisa huyo.
Mke wa marehemu ndiye aliyetoa taarifa polisi ya kumkuta mumewe amekufa ndani ya gari baada ya kwenda kumtazama kutokana na kupata mashaka kuliona gari kwenye majira ya saa moja ilhali mumewe aliaga kuondoka muda mrefu nyuma.
Hakuna uharibifu wowote uliotokea zaidi ya ukataji wa nyaya za umeme na hakuna mtuhumiwa yoyote aliyekamatwa. Upelelezi unaendelea.
Nade na bwana Eliakimu wakatazama habari hiyo kwa tabasamu. Kazi si kwamba ilikuwa imeisha bali pia ilikuwa imetendwa vema.
Lengo la kutazama habari hiyo ilikuwa ni kuthibitisha kama tendo limefanikiwa, yani Max amekufa, na hakuna ushahidi wowote ulioachwa nyuma.
Hivyo vyote kwa pamoja vilikuwa vimepatikana. Bwana Eliakimu akampongeza Nade kwa kazi nzuri.
“Nimefanya tu kazi yangu, wala usijali mkuu,” Nade akasema akitabasamu kwa haya.
“Ndio ni kazi yako, ila umeitenda vema. Anayetenda mema siku zote hupongezwa.”
“Ahsante mkuu. “
“Unataka zawadi gani nikupatie?”
“Yoyote tu mkuu unayoona nastahili.”
Eliakimu akajikuna kidevu akitabasamu.
“Sawa, najua nitakupatia zawadi gani. Nipe muda kidogo wa kuitafakari.”
Nade akatikisa kichwa kuafiki. Eliakimu akaendeleza maongezi:
“Vipi alikupatia mushkeli kwenye tendo?”
“Hapana. Hakuweza kufurukuta hata kidogo.”
“Kabisa?”
“Ndio. Alipovuta hewa mara moja tu basi habari yake ikaishia hapo hapo.”
“Aisee! Hizi dawa zina nguvu eenh?”
“Sana! Zinaonekana ni kali mno. Ile glovu niliyovaa kwa ajili ya tukio nimeitazama hivi punde nimeikuta imekatikakatika na kulainika kama bubble gum!”
“Serious?”
“Ndio, mkuu.”
“Unajua haya ndiyo madawa yanayosafirishwa kuingizwa nchini na wakina Miranda?”
“Yah ulinambia.”
“Nilifanya tu kuchomoa chupa moja kwa ajili ya kaudadisi changu, nikagundua ni sumu ila sikuwa makini kwenye kuchambua madhara yake.
Kama ni makubwa hivi, hili jambo linatisha, ni hatari. Itabidi tufuatilie kwa karibu namna mwili wa Max utakavyokuwa baada ya kuingiza sumu hii mwilini.”
“Kwenda hospitali?”
“Hapana, mbona kuhangaika hivyo? Nitaenda tu msibani kutoa pole. Bila shaka mke wake ataeleza yote nayotaka kuyafahamu.”
Nade akatikisa kichwa kuafiki.
“Huenda tukaja tumia pia sumu hizi kummaliza yule mtu wetu baada ya kumaliza kazi,” Mheshimiwa akapendekeza na kuongezea:
“Siku tutakayokata mzizi huo wa fitna, nitafurahi sana na roho yangu itakaa kwa amani. Hilo ndilo jambo pekee lililobakia likininyima usingizi.”
“Usijali, mkuu. Nalo litaisha,” Nade akasema kwa kujiamini.
“Siku litakapoisha, nitahakikisha, kwa uwezo wangu wote, nakutafutia zawadi ambayo hautaisahau maishani mwako daima! Umesikia?”
“Nimesikia, mkuu.”
“Haya nenda kapumzike sasa kesho uendelee na kazi.”
**
Saa mbili asubuhi maeneo ya Masaki, Dar es salaam.
“Karibu!” Sauti ya kiume ilifoka tokea ndani ya uzio, punde geti likafunguliwa na kichwa kikachomoza kutazama nje.
Alikuwa mwanaume mweusi mwenye nywele ndogo pilipili. Amevalia koti kubwa rangi ya bluu na suruali ya kitambaa miguuni akiwa peku.
Alivyotazama nje akakutana na Jona aliyekuwa amevalia shati jeupe la drafti, suruali ya kitambaa na mokasi nyeusi.
“Naweza nikakusaidia?”
“Ndio, bila shaka hapa ni kwa marehemu Fakiri.”
Mwanaume getini akatikisa kichwa kukubali.
“Mimi ni afisa polisi,” Jona akaonyeshea kitambulisho chake bandia. “Nimekuja hapa kuonana na mwenye nyumba.”
“Usijali, lakini sina taarifa yoyote mpya. Zote nilishatoa kwenu polisi.”
“Utaniambia tu hizo hizo ambazo ulizitoa. Kama nilivyosema hapo awali, tunaifufua hii kesi.”
“Karibu.”
Mama huyu hakuonekana mtu mwenye matumaini. Si bure alichoshwa na mahojiano ya aina hiyo, hakuona jipya ama la maana.
Alikuwa anatimiza tu wajibu.
“Kuna adui yoyote wa kibiashara unayemhisi pengine anahusika na mauaji ya mumeo?”
“Hapana.”
“Hamna yeyote?”
“Ndio.”
“Wewe unahisi kwanini mumeo aliuawa?”
“Sijui. Siku zote ukiwa na mafanikio, maadui hawakosekani.”
“Mama, nipo hapa kwa ajili ya kusaidia. Najua umechoshwa na mahojiano ya aina hii na pengine waona yanakupotezea muda.
Tafadhali, naomba unipe ushirikiano wako. Nakuahidi utaona matunda ya hichi utakachokifanya,” Jona alisema kwa kujiamini akimtazama Mama machoni.
Muda mfupi macho ya mama yakawa mekundu.
“Nimeongea na kuongea sana, nimelia na kusaga meno lakini hakuna aliyejali. Alipotokea mtu wa kujali, naye hakuishi wakammaliza!”
Mama akajipangusa machozi kwa vidole vyake.
“Pole mama, najua inaumiza. Nitafanya kadiri ya uwezo wangu kuwaleta wahusika wote mbele ya haki.”
Mama akawa kimya kwa muda kidogo. Ni kama vile alikuwa anavuta kumbukumbu, ila iliyokuwa inamchoma, uso wake ulijieleza kwa ndita za majonzi.
“Nakumbuka kabla mume wangu hajafa, alikuwa ananiambia kila usiku maisha yake yapo mashakani. Nilimuuliza kwanini haendi polisi, akawa ananijibu haitosaidia.
Sikumwelewa anamaanisha nini mpaka pale alipokuja kufariki. Ile kauli yake ya haitosaidia kweli nikaanza kuishuhudia.”
“Alikuwa anakwambia nini kinaweka maisha yake rehani?”
“Ndio. Unajua alikamatwa kwa kosa la kutokulipa kodi. Bishara yake ikayumba sana kwa maana ilikuwa ni kiasi kikubwa sana alichotakiwa kulipa, mbali na msongo wa mawazo.
Akahangaika huku na huko kutafuta pesa hiyo lakini hakuipata kwa wakati.
Alipokuja kupata haikuwa kamili, bali nusu ya ile anayotakiwa kulipa. Alinambia amepewa na mshirika mmoja wa kibiashara anayeitwa Sheng.
Lakini pesa hiyo alipewa kwa masharti ambayo alishindwa kuyatimiza na hatimaye kuuawa.”
“Naomba uniweke wazi kila kitu mama. Masharti gani hayo? Na huyo Sheng wamjua?”
Mama akafuta kwanza machozi kabla hajasema:
“Hakuniweka wazi, alinambia kifupi tu kuwa ameambiwa asafirishe vitu fulani ndani ya mzigo wake wa samaki kwenda Rwanda na Burundi.”
“Na huyo Sheng?”
“Simjui. Yeye mwenyewe mume wangu hakuwa anamjua. Sheng ni mtu wa kutuma watu tu. Walikuwa wanakuja hapa wawakilishi wake kuteta na mume wangu.”
“Kwahiyo ina maana mumeo aligoma kusafirisha mzigo huo?”
“Ndio. Hivyo Sheng hakumalizia kumpatia nusu ya pesa anayodaiwa mpaka kiasi fulani cha mzigo kitakaposafirishwa.
Sasa mume wangu baada ya kupata nusu ile toka kwa Sheng, akaamua kutafuta nusu nyingine ambayo kwakuwa kiasi kilikuwa kishapunguzwa, akaipata kwa urahisi.
Kabla hajalipa, wakamuua.”
Mama akamalizia kwa kulia. Ikabidi Jona apoteze kama dakika nne kumbembeleza kurudia kwenye hali ya kuongea.
“Na kumhusu mwanao? Kifo chake kinahusiana na haya?”
“Ndio. Salim alikuwa anataka kutafuta haki ya baba yake. Unajua Salim alikuwa anashirikiana sana na baba yake kwenye mambo ya biashara. Alikuwa anajua mengi huko kuliko mimi.
Shida yake ilikuwa ni kutafuta haki ya baba yake, ila matokeo yake akapata kifo.”
Jona alinakili yale yote aliyopata kwa mama huyo. Alipomaliza akamuaga na kumpa moyo. Alimwambia:
“Haki itapatikana, hata kama yakawia.”
***
Saa nne usiku: Lorenzo Night club.
Baada ya kugongesha glasi zilizojazwa mvinyo, Lee akanywa fundo moja kubwa kisha akauliza wenzake watatu waliokuwa pamoja naye mezani.
“Bado kimya?”
Wakatazamana kwanza. Wengine hao watatu walikuwa ni Nigaa, Devi na Mombo; kampani yake ya kazi.
Wote walikuwa wamevalia jeans za bluu zilizokuwa zinatofautia kukoza. Juu wakivalia matisheti, isipokuwa Lee peke yake ambaye alivalia jaketi dogo jeusi mtindo wa kizibao.
“Naona bado kimya,” akajibu Mombo na sauti yake nzito baada ya wenzake kuwa kimya kujibu swali.
“Usikute Bigo kamalizwa na sisi tupo hapa tunabung’aa?” Akasema Devi. Sauti yake muda wote ilikuwa inakwaruza kama bati linalosuguliwa na msumari.
“Home kwake hayupo, wala maskani zake. Muda sasa hajatutafuta. Si kawaida!” Nigaa naye akatia neno kisha kukawa kimya.
“Kwa namna bosi anavyomtafuta, akimpata anaweza akamtafuna mbichi,” Devi akasema akitikisa kichwa chake kama mtu anayesikitika.
“Ila mimi nina mashaka,” akasema Lee. “Bigo atakuwa yupo matatizoni. Akili yangu inagoma kabisa kuamini kama yu buheri wa afya.”
“Sasa tutafanyaje?” Akauliza Mombo. Na hilo ndilo lilikuwa la msingi, watafanyaje kama wanatilia mashaka juu ya Bigo?
“Nina wazo,” akasema Nigaa. “Kwanini tusiende kumuuliza mkuu juu ya yule mshkaji ambaye alitakiwa kuuawa na Bigo?”
“Ili?” Devi akauliza.
“Ili tumfuatilie mshkaji wetu. Kama jamaa huyo aliyetakiwa kuuawa bado yupo hai, maana yake Bigo ndiyo atakuwa ameuawa.”
Kukawa kimya kidogo watu wakimeza wazo hilo.
“Naunga mkono hoja,” Lee akasema akitikisa kichwa. “Kama kweli tunataka kujua hatma ya Bigo, hiyo ndiyo njia pekee.”
Basi wakakubaliana wote kufanya vivyo.
“Vipi kama Bigo atakuwa ameuawa?” Akauliza Mombo.
“Sasa kutakuwa na kingine zaidi ya kummaliza huyo aliyemuua?” Akatahamaki Nigaa. “Ni kumuua tu na yeye, moja kulipiza kisasi cha msh’kaji wetu. Na mbili kumaliza kazi ambayo Bigo atakuwa ameishindwa.”
Wakaendelea kunywa. Na baadae wakawaita wanawake kwa mujibu wa idadi yao waendelee kufurahia.
Wakadumu hapo mpaka kwenye majira ya saa tisa usiku, kisha kila mmoja akaelekea upande wake.
Lee akiwa ameongozana na mwanamke mrefu mwembamba mwenye nywele ndefu za bandia wao wakaenda hotelini.
Hoteli kubwa yenye jina la TUMID, hapo wakachukua vyumba na kujiweka ndani.
Wakaenda kuoga kisha wakarejea ndani.
“Naomba pesa yangu kwanza,” akasema mwanamke akisugulisha vidole vyake.
“Shilingi ngapi?”
“Laki moja!”
“Mbona kubwa?”
“Ndiyo bei ya kulala na mimi usiku mzima.”
“Usiku mzima na saa hizi ni saa tisa?”
“Kwani si usiku? Na si nitaondoka asubuhi?”
Lee asibishane, akakubali. Ila akilini mwake alikuwa ameshapanga kumdhulumu mwanamke huyo kwa kumpatia pesa ile anayoona anastahili.
Unajua hawa wanawake wakiona ngozi nyeupe huwa wanawehuka na kudhani wana pesa, aliwaza Lee. Ila nitamkomesha, akaweka nadhiri.
Wakapeana penzi kabla Lee hajachukuliwa na usingizi mzito uliompeleka mpaka asubuhi ya saa moja.
Alifungua jicho moja akaangaza, hakukuwa na mtu kitandani. Haraka akakurupuka na kukagua chumba kizima. Hamna mtu.
Akaenda na bafuni napo, hakuona mtu pia.
Akili yake ikamtaka atizame suruali yake upesi. Akatazama na kukagua mifukoni, mifuko yote ilikuwa meupe!
Hakubakiziwa hata mchanga.
Akalaumu sana. Badala ya kukasirika akajikuta anatabasamu, na mwishowe akacheka. Alijiona fala kabisa, tena yule mtepetevu.
Aliketi juu ya kitanda akashika kichwa akiuchambua usiku mzima namna ulivyokuwa. Akahisi tumbo limekuwa la baridi punde alipokumbuka kuwa ndani ya suruali aliweka pochi.
Macho yakamtoka, mdomo ukamkauka.
Pochi ile ilikuwa na vitu vya msingi na maana sana. Ilikuwa na nyaraka zake za siri! Ni bora mwanamke yule angekomba pesa akamwachia vinginevyo.
Akanyanyuka na kushika kiuno. Tumbo lilinguruma. Alihisi miguu inapoteza nguvu.
Alikuwa amefanya uzembe mkubwa sana ambao hata kuwaeleza marafiki zake ilikuwa ni aibu. Ni kwa namna gani hilo liliwezekana wakati yeye huwa mwangalifu?
Akahisi ametiliwa madawa. Hilo ndilo jibu pekee ambalo lilionekana kusuuza nafsi yake japo hakujuwa ametiliwaje madawa hayo.
Sasa alipata kibarua ambacho hakukitarajia- kibarua cha dharura. Cha kumtafuta mwanamke huyo ampatie pochi yake kulinda nyaraka zilizomo ndani.
Hakuwaza pesa. Lah! Aliwaza nyaraka. Alijikuta anamiminika kijasho chembamba akipepesa pepesa macho chumba kizima kana kwamba kaambiwa na mshenga pochi ipo ndani.
Alihofia endapo pochi hiyo ikikamatwa na mikono isiyo salama. Itakuaje?
Kwani ni nyaraka zipi hizo zi ndani ya pochi?
—
“Huwezi amini, leo nimeangukiwa na embe chini ya mwarobaini!” Alisema mwanamke ambaye ndiye yule aliyemzidi kete bwana Lee.
Hapa alikuwa na mwenzake mfupi mnene ndani ya chumba kimoja kikubwa kipana kilichotandikwa godoro chini.
Chumba hichi kilikuwa kimejazwa vitu lukuki chini mathalan chupa ya chai na beseni dogo jekundu lililokuwa limesheheni vyombo.
Hakukuwa na vitu vingi humo. Na hata vilivyokuwepo havikuwa vya thamani kubwa, wala havikuwa vimepangiliwa vizuri.
Ila ukiwatazama wanawake hawa walivyokuwa wameupara. Loh! Waweza sema makazi yao ni Abu dhabi. Nywele feki za bei, na nguo ambazo si haba.
“Enhe! Nipe mchapo!” Akadakia mwanamke mwingine kwa mdomo wake mpana.
“Bwana wee si nimekutana na mchina si mchina, mjapani si mjapani, sijui mkorea yule jana kule golini.”
“Nilikuona mwenzangu. Nikasema la haulaa! Ushaula shoga maana mie mwenzako nilitoka kapa.”
“Yaani nimeula nimeula! Ila mama mchina mwenyewe anatwanga Kiswahili kama kazaliwa Kigogo!”
Wakaangua kicheko.
“Kwahiyo hakuwa na pesa?”
“Nawe wapenda kuwahi mbele, tuliaa.”
“Haya nafunga bakuli.”
“Pesa alikuwa nazo ila akajifanya anabania. Nikasema hunijui wewe. Chap! Nikafanya mambo yangu yale. Kaingia kichwa kichwa chali! Nikajibebea vyangu.”
“Shing’ngapi?”
“Najua basii? Nimefungua pochi hivi, naona madola dola tu.”
“Weee!”
“Oooh! Nakwambia hivyo.”
Mwanamke yule mwivi akatoa pochi ya Lee toka kwenye mkoba wake akamkabidhi mwenziwe ambaye aliidaka na kuifungua haraka.
“Sasa si bora ungemwachia tu. Umevibeba vya nini?”
“Hivi we unadhani nilipata muda wa kukagua kagua pochi? Mie nilifunua nikaona pesa, basi nikaitupia tu mkobani.”
Yule mwanamke aliyebebelea pochi akatazama na kukagua vitambulisho na karatasi zingine alizokumbana nazo huko.
Alitazama kwa muda kabla hajaamua kuachana nazo kwa maana hakuwa anaelewa. “Naona yameandikwa kwa kichina china na Kiingereza tu.”
Akatupia pochi kando na kuanza kujadili namna watakavyotumbua pesa iliyopatikana.
Laiti kama wangelikuwa wanalijua namna Lee anavyotoka jasho kuitafuta hiyo pochi, wangemrudishia hata kwa kumtuma wakala.
—
“Can I see you?”(Naweza kukuona?) Jona aliuchapa ujumbe huo kwenye simu yake kisha akautuma. Alikuwa ndani ya mtandao wa Facebook akichati na mke wake Eliakimu.
Ni majira ya jioni haya na siku hiyo Jona hakwenda popote pale zaidi ya kuhama toka chumbani kwenda sebuleni, sebuleni chumbani siku nzima.
Alichokifanya punde tu alipoamka ni kumtaarifu Jumanne kwamba hatakuja kazini kisha akalala kwa muda kidogo kabla hajaja kuamka jua likiwa tayari limeshanawiri.
Alipika akala, akateka tarakilishi yake na kuanza kurandaranda mtandaoni. Alianzia huko Facebook ambapo hakupata anachokitaka. Akatoka na kwenda kwenye mambo mengine.
Muda huu sasa ndiyo anarejea baada ya kuona mtu anayemtaka yupo hewani.
“See me? Serious?” (Kuniona? Kweli?) Uliuliza ujumbe wa Miriam, mke wa Eliakimu.
“Yes for sure!” (Ndio kabisa!) Akachapa Jona na kutuma.
“How can you see me while you are so far?” (Unawezaje kuniona ingali upo mbali?)
“I am in Nairobi now for a fashion show.” (Nipo Nairobi sasa kwa ajili ya onyesho la mitindo.)
“Nairobi???”
“Yes. You don’t believe? – I am in Nairobi and I expect to be in Dar es salaam soon.” (Ndio. Huamini? – nipo Nairobi na nategemea kuwa Dar es salaam karibuni.)
“Sure, I would love to see you.” (Kweli, ningependa kukuona.)
“Me as well. Hope to you see soon. Bye!” (Mimi pia. Natumai kukuona karibuni. Kwaheri!)
Jona akaaga na tabasamu. Mbinu yake ilikuwa inaendelea kutimia. Hakutaka kujirahisisha kwa ‘mteja’ wake huyo ili kutompatia doa la shaka.
Alitaka Miriam apate picha kwamba yeye ni mtu ambaye yupo bize, ametingwa na kazi. Ana muda mchache sana wa kuteta na watu mitandaoni.
Alipotoka kwenye mtandao huo wa Facebook, akazima kabisa tarakilishi yake alafu akajiandaa kwa muda mfupi kabla hajatoka ndani akibebelea tarakilishi.
Akaenda internet café, sehemu wanapofanya biashara ya mtandao, akakutana na mhudumu: mwanamke mmoja mweupe, akamuulizia kuhusu huduma ya scanning.
“Ipo,” akajibu mhudumu pasipo kumtazama Jona. Alikuwa yupo bize kutazama tarakilishi yake akichezesha vidole kwenye keyboard.
Jona akatafuta mahali pa kukaa. Punde akaja mhudumu kumsikiliza. Akampatia kibahasha cheupe.
“Humo kuna picha, naomba uziskani na kuzituma kwenye hii kompyuta.”
Mhudumu akatikisa kichwa kisha akaenda. Jona akawasha tarakilishi na baada ya mfupi akaona picha zile zikiwa zimetumwa.
Mhudumu akaja kuulizia muda wa mteja na pesa yake. Jona akalipia kisha akaendelea na shughuli zake.
Akafungua injini ya kusaka majibu alafu akaanza kuchukua picha moja baada ya nyingine na kuanza kuzisakia majibu yake mtandaoni.
Alifanya hivyo kwa picha zote hizo kasoro ya Fakiri. Akajikuta amepata majibu ya picha mbili tu zingine zikiwa hazina mrejesho wowote wa maana.
Picha ya kwanza ilikuwa ni ya mwanaume mwalimu wa shule ya sekondari ya Lamu, Thadeus Malima, na ya pili ni ya aliyekuwa mbunge wa jimbo la Nyamagana, Mwanza, kwa jina Ditto Jigeleka.
Wote hawa walikuwa wameuawa kwa risasi. Na muuaji akiwa bado anaitwa ‘asiyejulikana’. Mauaji ya watu hawa yalitenganishwa na masaa matano tu.
Hapo Jona akapata shaka kidogo juu ya mtendaji wa mauaji haya. Huyu mwalimu alikuwa ni wa shule iliyopo Dar es salaam, wakati mbunge akiwa ni wa Mwanza.
Muuaji alitekelezaje mauaji haya kwa tofauti ya masaa matano tu?
Hata kama alipanda ndege, bado ikamuwia vigumu kuamini kwani mauaji haya yalihitaji mipango thabiti.
Kwahiyo kuna muuaji zaidi ya mmoja? Na wote wanakuwa na hizi picha?
Kabla hajasumbuka sana na hayo maswali akaendelea kuperuzi juu ya marehemu mbunge maana yeye ndiye ambaye taarifa zake zilikuwa zinapatikana kwa wingi ukilinganisha na bwana Thadeus ambaye mtandao ulimtambua kwa taarifa za kifo tu na akaunti ya Facebook.
Akiwa anapekua pekua kuhusu taarifa hizo, akagundua kwamba mauaji ya Jigeleka yalikuwa yalikuwa yanahusishwa na sababu za kisiasa kwakuwa alikuwa chama pinzani akianzisha hoja iliyoonekana kuibana serikali huko bungeni.
Lakini Jona alikuwa mwerevu kung’amua jambo. Muuaji alikuwa ana mipango na malengo fulani. Ukitazama kwa Fakiri na kwa huyu mbunge, utapata kugundua muuaji alikuwa anacheza na matukio na hivyo basi kuacha watu njia panda kwa kusingizia jambo fulani.
Haswa serikali.
Alimaliza muda wake wa kuperuzi akajirudisha nyumbani. Lakini hakuwa amepoteza muda wala pesa kwani kuna kitu alikuwa amepata. Ila basi alitokea kujiuliza sana kuhusu picha ya yule mtu mmoja ambaye hakuwa amepata taarifa zake miongoni mwa zile picha.
Ina maana yeye hajauawa au taarifa zake hazijulikani? Alitamani kujua ili kama basi hajauawa aweze kumwokoa, ila akajikuta hana cha kufanya. Hana pa kuanzia kupata hizo taarifa.
Akiwa anawaza waza na kujiuliza, akakumbuka kuna kitu alitakiwa kupitia kwenye tarakilishi yake. Mojawapo ya faili moja ambalo alilikomba toka kwenye simu ya marehemu Bigo.
Basi haraka akavuta mashine hiyo na kwenda kwenye faili alilolitunza kwa jina la ‘Bigo docs’ akafungua na kwendea faili moja kando ya kioo likiitwa ‘gallery’. Humo akakuta picha nyingi sana.
Hakuona hasara kupitia picha moja baada ya nyingine.
Miongoni mwa picha hizo nyingi zilikuwa zikimwonyesha Bigo akiwa sehemu mbalimbali na watu mbalimbali.
Jona alivutiwa na picha kama tano hivi ambazo alipata kuzitenga kadiri alivyokuwa anazitazama. Picha tatu zilikuwa zinamwonyesha Bigo akiwa na marafiki zake: Lee na wenza. Na mbili zingine akiwa na mwanamke fulani hivi na watoto ambao Jona alihisi wanaweza kuwa familia ya Bigo.
Akazitazama picha hizo kwa umakini. Mojawapo akagundua mandhari yake kutokana na uwenyeji wake ndani ya jiji. Picha hii ilikuwa imepigwa Mango garden, Bigo akiwa na marafiki zake.
Hizo zingine kidogo ikawa ngumu kutambua wapi zilipigwa. Akaziweka kapuni.
Lilikuwa ni swala la muda tu. alijua atapata kujua kadiri hatua zitakavyosonga mbele. Acha apumzike kwanza. *** Usiku wa saa tatu, ndani ya nyumba ya BC.
Miranda akiwa amevalia suruali ya jeans rangi bluu, na tisheti nyeupe. BC alikuwa amevalia suti ya udongo pasipo kuweka kikolombwezo kingine chochote zaidi ya saa kwenye mkono uliokuwa umebebelea sigara kubwa.
Mezani kuna chupa kubwa ya champagne na glasi mbili.
“The guy might sense something fishy,” (Jamaa huenda akahisi jambo mrama.) alisema Miranda akimtazama BC. “You know he’s in this dirty game for long. He has that nose to smell when things turn awkward.” (Unajua yupo kwenye huu mchezo kwa muda mrefu. Ana pua ya kumfanya anuse pale mambo yanapoenda kombo.)
Miranda alikuwa anahofia. Kwa namna ambavyo Eliakimu alikuwa anamtazama mara yake ya mwisho wakiongea naye, kulimfanya ahisi jambo fulani halipo sawa.
Hakuwa anamchukulia Eliakimu kiwepesi hata kidogo.
“Have you told him about his price being high?” (Umemwambia kuhusu bei yake kuwa juu?) BC akauliza.
“That’s of you to tell him.” (Hilo ni lako kumwambia.) Akajibu Rhoda kabla hajanywa kinywaji chake. Jibu hilo likaonekana ni kali kwa mkuu. BC alisafisha koo lake lake asitie neno. Akanyanyua glasi ya kinywaji na kunywa.
Walikuwa njia panda haswa. Walihitaji muda zaidi wa kumsubirisha Eliakimu, ila hilo jambo likaonekana ni gumu kutokea.
Miranda aliona hamna njia nyingine bali kukubali tu kuhusu Eliakimu kwani kuhusu upande huu mwingine wa Boka na mkewe, wanaofuatilia hauwezi kuzaa matunda kwa wepesi hivyo.
Kidogo hilo likawa gumu kwa BC kulipokea. Alijaribu kulisindikiza na kinywaji lishuke ila bado likang’ang’ania koo.
“Wait, I shall talk to him seriously this time and address him about our offer. It’s up for him to decide either to dig in or out. I don’t mind waiting but loss.” (Ngoja, nitaongea naye kuhusu hili swala kwa umakini muda huu na kumwambia kuhusu ofa yetu. Ni juu yake sasa kukubali aidha kuwa ndani ama nje. Sijali kungojea bali hasara.)
Ungeona sura ya Miranda, haikuwa sawa. Alipuuza akanywa glasi mbili za kinywaji kwa pupa kabla hajanyanyuka na kuaga, kuna kazi inamngojea nyumbani.
Alitoka akaenda kwenye makazi ya Kinoo, wakateta kwa kama dakika tatu kabla hawajaachana.
—
Asubuhi ya saa kumi na moja, Miranda akadamka akajitia kwenye gari lake kuanza safari mpaka maeneo ya Makumbusho, si mbali sana na kituo cha mabasi. Hapo akapaki mahali anapostahili na kutulia ndani ya gari akiangaza.
Punde akawaona watu kadhaa wakiingia ndani ya jengo. Akangojea mpaka majira ya saa mbili ndipo akashuka na kuzama ndani ya jengo.
Jengo hilo lilikuwa limebebelea bango kubwa likisomeka: ROADAR SOLAR COMPANY. Pembeni ya bango hilo kulikuwa kuna mabango mengine ya ofisi zingine zilizokuwa zinapatikana ndani ya jengo hilo.
Miranda aliekea kwenye ofisi hii ya solar – umeme wa jua, akaomba kuonana na mkurugenzi wa kampuni. Pasipo kuzungushwa, akapewa nafasi hiyo. Aliingia ndani ya ofisi akamkuta mwanaume mmoja mnene mweusi mwenye kiwaraza.
Alikaribishwa kwa ukarimu akaketi na kueleza shida yake ni kuunganishiwa umeme wa jua kwenye jengo lake zima, jengo kubwa la biashara.
“Huduma hiyo inatolewa,” akajibu mkurugenzi. “Kwani haujapewa maelekezo huko ulipotoka?”
“Nimepewa, sema nikaona ni uwekezaji mkubwa na hivyo natakiwa kuongea nawe. Nahitaji mradi huo utekelezeke sio tu kwenye ofisi zangu hapa bali pia na huko mikoani.”
Wakaongea kwa muda wa dakika kumi na tano kisha wakaagana.
Lengo la Miranda halikuwa biashara bali upelelezi. Macho yake yalikuwa yanatambaa tambaa huku na huko kukagua na kuchambua. Mpaka anaondoka alikuwa ameshapata anachokitaka.
Aliwasiliana na Kinoo wakakutana na kumpasha habari.
“Ile kampuni ya umeme wa jua, ni ya wale wachina.”
“Umejuaje?”
“Nimeona mojawapo ya picha ya mkuu wao ukutani.”
“Kweli?”
“Ndio, ni kampuni mtoto ya wale wachina.”
Kinoo akatikisa kichwa. Sasa alikuwa ameshaunganisha dots za uthibitisho, ya kwamba aliyemuua Bite ni wachina, mahasimu wao. Ndiyo hao wanaoitafuta ile picha. Picha ambayo na wao wanaitaka.
Picha ambayo wanaamini wakiipata itakuwa ndiyo mwanzo wa wao kuwamaliza mahasimu hao. Walitokea kuamini picha hiyo ina ujumbe. Ina neno ambalo Bite alitaka kulisema.
Bite hakuwepo katika upande wowote ule: aidha wa wachina ama wakina Miranda. Daraja hili lilikuwa muhimu. Haswa kwa wakina Miranda ambao wanaamini kwa kiasi kidogo ambacho Bite alikuwa na wale wachina, basi kuna kitu alivuna.
Wakakubalia na Miranda kwamba inabidi baadae wakaonane na Jona. Tena wote kwa pamoja.
“Inabidi ajue kwamba yupo hatarini,” alisema Miranda. “Kama alifanikiwa kumkamata moja wa memba wao, basi inabidi ajue yupo kwenye orodha na hawataacha kumfuata.”
***
Saa mbili usiku, Lorenzo Night club.
Lee alitoka kwenye gari, Noah ya kijivu yenye vioo vyeusi, akanyookea moja kwa moja ndani. Bado muda haukuwa umeanza kuiva ndani ya eneo hili hivyo hakukuwa na watu wengi. Hata hao aliowakuta ni kwasababu tu ilikuwa ni mwisho wa wiki.
Klabu hii ni ya usiku, si usiku wa saa mbili kama huu, bali usiku mzito.
Lee alitembea klabu nzima akipekua mazingira kwa macho yake madogo. Mashaka yalikuwa yameshika uso wake kana kwamba mpangaji aliyepoteza ufunguo pekee uliobakia.
Aliongea na mlinzi wa eneo hilo akijaribu kumfafanulia umbo la mwanamke yule aliyemkwapulia vitu na kumuuliza kama amemwona eneoni hapo. Mlinzi akatikisa kichwa. Hakumwona.
“Tafadhali ukimwona, naomba umshikilie na unipashe habari,” alisema Lee akimkabidhi mlinzi namba yake ya simu na shilingi elfu kumi. “Ukifanya hivyo n’takupatia zaidi.”
Alifanya hivyo kwa watu watatu kabla hajatoka ndani ya klabu na kurudi ndani ya gari. Ndani alikuwepo Nigaa akiwa amekaa pembeni ya kiti cha dereva ambacho ndicho Lee alikalia.
“Umempata?” Nigaa akauliza.
“Hapana,” Lee akajibu akitikisa kichwa.
“Nilikwambia, ila ukashindwa kuelewa. Huu siyo muda wao. Tatizo lako una haraka mno.”
“Siwezi nikangoja zaidi,” Lee akajibu. Alikuwa amechanganyikiwa.
“Brother, huna haja ya kuhofia. Yule malaya atakuja tu hapa na tutampata kiurahisi. Ulikuwa huna hata haja ya kupoteza pesa yako.”
Wakangoja na masaa yakazidi kwenda mpaka saa saba usiku, mwanamke yule hakuonekana. Saa nane … saa tisa, kimya.
“Imekula kwetu,” Nigaa akasema.
“Sasa nafanyaje?” Lee akauliza.
“Inaonekana hili zoezi litatuchukua zaidi ya leo hii.”
Walikaa hapo mpaka kwenye mishale ya kukaribia asubuhi pasipo kumwona mtu wanayemngoja. Waliamua kutia moto chombo na kwenda zao. Lee akiwa na mawazo na majuto.
Akitafakari na kudadavua kichwani. Akitanabahi ni njia gani ya kuenenda pasipo kupata majibu yoyote yale. Aliwaza endapo mkuu wake akipata habari hizi, nini kitatokea. Hakuna kingine zaidi ya kifo.
“Usiwaze sana, Lee. Huyo malaya tutampata tu,” Nigaa alimpa Lee moyo. “Shida si kumpata, Nigaa. Bali yale yaliyomo mule kwenye pochi kama yatakuwepo salama. Sijawahi kufanya uzembe wa aina hii.”
Nigaa alichukua usukani wakaendelea na safari mpaka kwenye makazi yao ambapo waliamua kupumzika kwanza kabla ya baadae kuendelea na kazi zingine. Haswa ya kwenda kuonana na mkuu wao awaeleze kumhusu mtu yule ambaye Bigo alitumwa akammalize.
Kwenye majira ya saa nane mchana wakawa tayari wameshaamka na kujumuika na mwenzao aitwaye Mombo wakaenda kuonana na mkuu wao.
Wakamweleza haja ya mioyo yao. Mkuu akawataka watulie kwani tayari hilo jambo ashalichukulia hatua.
“Wo yijing fale lìng yigè rén,” (Tayari nimeshamtuma mtu mwingine,) alisema mkuu akikuna kidevu chake chongofu. “Ràng women kàn kàn hui fasheng shènme.” (Acha tuone nini kitatokea.) Kwahiyo hapo wakawa hawana tena kauli mpaka pale yule aliyetumwa arejeshe taarifa ama naye atokomee ndipo mkuu achukue hatua nzito.
Kwasababu Jona ni mchoraji tu, hamna haja ya kuhofia sana mpaka kutuma kikosi kamili.
Mwanaume aliyetumwa alijulikana kwa jina la Panky. Mwanaume fulani mwembamba urefu saizi ya kati. Kichwani mwake alikuwa ana nywele zilizochongwa kama mtaro zikiwa zimesimama kama moja.
Kwa shingo upande Lee na wenzake wakaridhia. Ila kabla hawajaondoka, mkuu akauliza:
“Lee, ni hái hao ma?” (Lee, upo sawa?) Akimtazama Lee machoni. upesi Lee akatazama chini na kutikisa kichwa chake kuridhia ya kwamba alikuwa sawa. Wakatoka nje.
***
Saa nane mchana …
“Vipi upo poa now?” “Ndiyo, nadhani nina muda sasa. Tunaweza tukaenda.” “Saa hii?” “Ndio. Au wewe ulikuwa unataka twenda muda gani?” “Usiku. Bila shaka ndiyo muda atakaokuwa nyumbani.” “Unajua usiku nina miadi na Boka. Siwezi kwenda, kama unavyojua kuna ishu nataka nichonge naye.” “Lakini sidhani kama muda huu atakuwepo nyumbani. Mchana huu.” “Basi fanya hivi, si upo town, pitia pale ofisini kwake umcheki.” “Nipe kama robo saa.” “Iwe kweli. Baada ya robo saa … “Hayupo!” “Pamefungwa?” “Hapana. Yupo yupo mshkaji mwingine.” “Muulize basi.”
Punde, Kinoo anashuka kwenye gari na kufuata ofisi ya Jona. Alimkuta Jumanne pekee ambaye alimsalimu na kumuulizia Jona.
“Atakuwa yupo kwake, jana na leo hajafika job. Ila naweza nikakusaidia.” “Usijali,” akajibu Kinoo. “Nilikuwa namhitaji yeye mwenyewe.”
Jona alikuwa amevalia bukta na kaushi nyeupe. Kuna baadhi ya michoro alikuwa anaiweka sawa kwenye ubao wake wa karatasi, michoro ambayo kwa kuitazama upesi huwezi jua alikuwa anachora nini hasa.
Alisikia hodi getini, akaacha shughuli yake na kuangaza dirishani. Akaona Range Rover sport nyeupe. Akashtuka kidogo. Alijua usafiri huo ni wakina nani. Basi akaenda chumbani na kukwapua bunduki yake aliyofichia nyuma ya kiuno akiijaladia na shati jeusi.
Kwa kujiamini akalifuata geti na kuwaruhusu wageni waingie ndani. “Hatujaja kwa shari, bali maongezi,” alisema Miranda. Mwanamke ndani ya sketi fupi nyeusi na topu ya pinki. Akiongozana na Kinoo mwenye nguo zijulikanazo kila uchwao.
Jona akawakaribisha sebuleni akiketi kwenye kiti cha kando kilichoruhusu kila mmoja kumtazama mwenzake.
“Karibuni japo ujio wenu haukuwa na taarifa. Natumai mlikuwa mnajua kama nipo nyumbani.”
“Ndio, tulipitia kazini kwako.” Pasipo kupoteza muda Miranda akaeleza kilichowaleta. Ya kwamba ni picha na baadhi ya taarifa ambazo wanataka kumfikishia Jona.
Wakamwambia kuhusu msako ule wa picha, haswa wakiuhusisha na kundi la kihalifu la kichina ambalo lipo nyuma yake. Ya kwamba picha ile ni mali yao, wanaitafuta na kwa gharama yoyote ile wataipata.
“Uhai wako upo hatarini. Watu hawa hawatakoma kutuma watu wao mpaka pale watakapohakikisha wameitia hiyo picha mkononi. Japokuwa hatujawahi kuiona hiyo picha, tunaamini itakuwa na nyaraka muhimu sana kwao. Na ndiyo maana nasi twaisaka.”
Huu ukawa muda muafaka kwa Jona kuuganisha tarifa zake kichwani na kupata mantiki. Ina maana wageni wake hawa wanawafahamu hawa wachina ambao alikuwa anahangaika kufumbua fumbo?
Hawa wachina ambao wamefanya mauaji ya watu kadhaa!
Kabla hajaongelea picha, akawauliza wakina Miranda kama wanafahamu lolote juu ya kifo cha bwana Fakiri na Jigeleka. Wakasema hawafahamu. Jona akawaambia ni kwa namna gani amepata taarifa za hao marehemu.
“Nilikuta picha zao kwenye hifadhi ya mtumishi wao.”
“Bila shaka walikuwa kwenye pumzi zao za mwisho,” akasema Miranda. Jona akakumbuka neno hilo ‘pumzi ya mwisho’. Ni neno la kichina lililoandikwa kwenye picha za watu wale aliowaona kwenye paspot.
“Unajua lolote kuhusu pumzi ya mwisho?” Akauliza.
“Ndio, najua. Ni kikosi cha mauaji kinachohusika na mauaji ya wale wote wanaoleta kizingiti mbele ya kazi yao. Kikosi hichi kinaundwa na watu stadi wa kazi. Wenye uwezo wa kuua pasipo kubakiza ushahidi wala kielelezo.”
“Na unajua kilichomuua bwana Jigeleka?”
“Hapana, sijajua. Wanaua watu wengi, siwezi nikajua haswa kwanini kila mmoja huuawa.”
Baada ya Jona kuuliza maswali ya kutosha, akataka kujua kwa undani juu ya wakina Miranda, wao ni wa kina nani haswa na wanajishughulisha na nini. Miranda akajibu kwa ufupi kwamba wao ni wafanyabiashara, wakihusika na biashara za kuingiza madawa nchini, madawa ya afya wakiwa na ubia na MSD. “Makajuanaje na hawa wachina?” Jona akauliza.
“Kwasababu walikuwa ndiyo wapinzani wetu kibiasara. Siku zote rafiki huwa karibu, ila adui karibu zaidi.”
“Sasa picha itawasaidia nini?”
“Kama tulivyosema ni adui zetu. Tunataka kujua kila nyendo yao.”
“Basi?”
“Basi. Hicho pekee ndicho kinatuhusu.”
Jona akakereketwa rohoni. Kwanini watu hawa wanafanya uhalifu nab ado wanadunda mtaani? Kwanini wanaua watu nab ado hawachukuliwi hatua? Alijaribu kuwauliza wakina Miranda, akajibiwa kwa ufupi.
“Mikono na miguu yao ina mafunzo. Akili zao zina ujuzi. Mifuko yao ina pesa.”
Wakateta kwa ufupi kabla Jona hajaenda kuwaletea picha ambayo aliwakabidhi na kuwaambia:
“Mnaweza mkanishrikisha kama kuna jambo mtaling’amua kwenye picha hiyo. samahani sitawapa mwende nayo.” Miranda na Kinoo wakaridhia.
Wakaitazama picha kwa umakini sana wakila dakika kama kumi na tano. Lakini wakatoka patupu!
“Una uhakika picha yenyewe ni hii?” akauliza Kinoo.
“Ndiyo yenyewe. Sina zaidi.”
Mbona ni picha ya kawaida tu? visiwa na ndege! Wakatahamaki. Hawakujua nini haswa dhamira ya picha ile. Waliona ni kama urembo.
Ila kama isingelikuwa na maana kwanini itafutwe? Kwanini Jona alengwe kuuawa?
“Hamna chochote ulichokipata pichani?” Miranda akamuuliza Jona. Jona akatikisa kichwa.
“Hapana. Nikadhani pengine nyie mwajua.”
Wote walitota. Hakuna aliyeona cha maana. Ila Jona akasisitizia lazima picha hiyo itakuwa na maana, hawana budi kufuatilia.
“Nakumbuka wakati Bite ananiambia nimchoree hii picha alinipa maelezo very simple, ila alitaka niyafuate na kuyazingatia haswa. Nilirudia kuchora picha hii mara tatu, tena kwasababu ndogo ndogo sana, mara ndege wamekaa mbali, niwasogeze, ama visiwa ni virefu sana na kadhalika. Bila shaka alikuwa na maana yake.”
Mwishowe Jona akawakabidhi wakina Miranda picha nyingine, kopi ya ile orijino ambayo aliichora kwa penseli na karatasi, wakakubaliana yeye abakie na ile orijino.
“Jona,” Miranda akaita. “Wewe ni nani?” Akauliza. Jona akatabasamu kwanza kabla ya kujibu kwa kuuliza: “Kwanini wauliza?” “Kwasababu wewe si mchoraji pekee. Wewe ni nani?” Jona hakutaka kusema mambo mengi, akawaambia hayo mengine yatakuja kadiri na muda. “Kuwa makini sana,” Miranda akamsisitizia Jona. “Usijali,” Jona akamjibu. “Naweza kujitazama vema.”
_____
Robo saa mbele…
“Mkuu, kuna jambo lipo katikati ya Jona na na wakina Miranda,”Nade akatoa taarifa. Wakati huo alikuwa amejiweka kando kidogo ya nyumba ya Jona macho yake ndani ya miwani yakiwa yanaangaza kutazama gari, Range Rover sport nyeupe, ikiishilia.
“Ndio, nimewaona wakiingia ndani ya nyumba ya Jona,” akasema Nade sasa akianza kuchukua hatua kusonga mbali na nyumba ya Joana.
“Wametoka muda si mrefu. Wamedumu kwa muda wa kasoro lisaa.”
Akasikilizia kidogo, kisha akasema: “Sawa, mkuu. Ila inakuwa ngumu kujua wanachokiongelea. Nahofu isije ikawa ni kuhusu Miriam.”
Kimya kidogo akisikilizia. Kisha akasema: “Sawa, mkuu. Jicho halitafunga.” Akakata simu. Ila mara akasikia mkono wa mtu begani. Haraka akageuka. Kutazama alikuwa ni Jona! .
Nade alishtuka, ila kumeza mshtuko huo akatabasamu kana kwamba hakuna kilichotokea. Akamtazama Jona na macho ya wenza, akiuliza:
“Kuna tatizo?”
Jona akatikisa kichwa kukataa. Lakini akamtaka Nade wakapate maongezi kidogo ndani kama hatojali. Nada akatazama kwanza saa yake kabla hajabinua mdomo na kupandisha mabega.
“Ts ok!”
Wakati wanageuka, mara Nade akaona gari fulani kwa mbele yao. Haikuwa umbeli mrefu sana na gari hili lilikuwa limewapa ubapa.
Lilikuwa ni Altezza moja nyeusi, vioo vyake vyote vilikuwa vimezibwa isipokuwa cha dereva pekee.
Kufumba na kufumbua, dereva huyo akatoa mkono wenye bunduki ambayo mdomowe aliuelekezea kule alipo Nade na Jona. Nade akatoa macho kwa mshangao. Katika kasi ya ajabu, akamsukuma Jona waangukie chini.
Sauti ya risasi ikavuma, paah!
Risasi ikatoboa bega la Nade, na mara gari ikachomoka mbio kupotea. Jona akamkarimu Nade kwa kubana mkono wake kwenye jeraha. Huku akimwambia kwamba wana haja ya kumuona daktari haraka iwezekanavyo.
“Sitaki kwenda hospitali,” Nade akasema.
Basi Jona akambeba begani na kwenda naye mpaka nyumbani. Akamlaza chini na kisha akaleta pamba na kopo kubwa la spirit. Kisha akaleta na vifaa fulani ambavyo Nade alistaajabu Jona amevitolea wapi.
Akagundua kwamba ndani ya nyumba ya Nade kulikuwa kuna vitu karibia vyote. Wakati Nade anahangaika kumtibia, yeye alikuwa anapekua pekua, japokuwa hakuona kila jambo, alifanikiwa kuona angalau vichache.
Jona akatoa chuma cha risasi begani mwa Nade, na kisha akampakaa spirit.
“Upo tayari nikushone.”
“Ndio,” Nade akajibu.
Jibu hilo likamshangaza sana Jona maana hakulitegemea kama lingetoka hivyo haraka tena pasipo kusita. Hapo akajua namna gani mwanamke huyo alivyo jasiri. Alivyo mgumu na roho ya kijeshi.
Kuthibitisha hilo zaidi, Jona akachukua uzi na kumshona Nade. Nyuzi si chini ya tano zikaenda begani. Nade akiwa ameng’ata kipande cha mti ambacho Jona alikuwa amemkabidhi apate kupotezea maumivu.
“Ulijifunzia wapi haya?” Nade akauliza.
“Sehemu mbalimbali tu. Nilikuwa napenda sana kuwa daktari ningali mtoto.”
Wakamaliza zoezi lao na kuketi. Jona akamhudumia Nade pombe kali kwenye glasi kisha maongezi mafupi yakachukua nafasi.
“Umekuwa ukinifuatilia toka muda gani?” Jona akauliza. Nade akajitahidi kukanusha ila mwishowe akakubali kwamba alikuwa anamfuatilia Jona kisiri kwa mujibu wa amri ya mheshimiwa Eliakimu.
“Unajua anakuwa na presha kama kazi yake itafanyika au lah.”
Sababu hiyo ikagoma kuiingia ndani ya kichwa cha Jona. Akauliza:
Nade akakanusha yote hayo akimsisitizia Jona kwamba wao shida yao ni Miriam tu. na hapohapo akaulizia harakati za Jona kumtafuta mwanamke huyo zimeishia wapi.
“Bado naendelea, msijali nitawataarifu.”
Maongezi hayo hayakudumu muda mrefu kwasababu kila upande ulikuwa mwangalifu kupitiliza kutamka lolote. Mwishowe wakajikuta wanajadili mengine ambayo yalionekana kusisimua kila upande.
“Ilikuaje ukakutana na Eliakimu?”
Nade akashusha kwanza pumzi. Akasema hapendi kuongelea sana mambo yake ya kale. Ila basi kwakuwa ametaka kujua, hana budi kumjuza.
Watu wengi wamekuwa wakiamini kwamba Nade ni ndugu yake Eliakimu kwa uaminifu wake na uchapakazi wake. Lakini pia kujitolea kwake kumfanyia kazi mheshimiwa huyo, ila kiuhalisia ni kinyume.
“Mimi nilikuwa mfanyakazi wa ndani wa bwana Eliakimu. Tokea kipindi hicho akiwa anagombea ubunge tu na hana hili wala lile kuhusu uwaziri. Alinitoa kwetu Tanga, kwa wazazi wangu maskini.
Akanilelea kama mtoto wake, nikishiriki naye meza moja … si kama mfanyakazi, bali kama mwanafamilia mwenzao.”
“Ikawaje mpaka kukupa nafasi hii?” Jona akakatiza kuuliza. Nade akatabasamu. Alijua fika huko ndipo ambapo Jona alikuwa anapataka.
“Ni siku moja tu ndiyo ambayo mambo yalibadilika. Siku hiyo nakumbuka ilikuwa ni jumapili jioni, mheshimiwa akiwa ameshatoka huko bungeni, alifanikiwa kuupata ubunge.
Siku hiyo alipoingia ndani, kumbe kulikuwa kuna mtu alikuwa amepanga kumuua, na mtu huyo hakuwa mwingine isipokuwa bodyguard wake. Kwa kutumia bunduki. Na alitaka kummaliza ndani ya nyumba yake.
Kama Mungu, wakati nipo jikoni, kwa kupitia kioo cha dirisha la sehemu ya kulia chakula, nikaona bodyguard akichomoa bunduki kiunoni. Basi haraka nikanyaka birika la chai, nikatoka na kulirusha, likamkita bodyguard na kumlaza chali.
Mheshimiwa akfurahi sana kwa kumwokoa maisha. Tangu hapo hakuamini bodyguard, na akataka mimi ndiye niwe bodyguard wake, kwahiyo akamwita mtu na kuanza kunifunda martial arts.”
Jona akamuuliza kama walijua kwanini Mheshimiwa alilengwa kuuawa, Nade akamwambia ulikuwa ni upinzani wa kisiasa tu. Hamna cha ziada.
Ila Nade kabla hajaondoka, akataka kujua kwanini mtu yule ndani ya gari alikuwa anataka kummaliza Jona. Kufupisha habari, Jona akamwambia hafahamu. Ila kichwani kwake tayari alishajua, si wengine bali wale wachina wanaodai picha.
Na aliapa kuwashikisha adabu.
***
“Nakuja, nakuja!” sauti ya Mudy ilisikika kwa ndanii. Nje ya nyumba yake, mlangoni alikuwa amesimama mwanaume mmoja aliyevalia suti na kubebelea mkoba wa rangi ya kahawia.
Kutazama usoni, hakuwa mwingine bali Brokoli. Nywele zake alikuwa amezifumisha vema kuficha uzee. Macho yake alikuwa ameyavesha miwani mepesi ya jua.
Punde mlango unafunguliwa, na Mudy anatokea akiwa ameshikilia kipande cha mkate mkononi. Amevalia bukta nyeusi ya mpira. Akatoa macho kumwona Brokoli mbele yake.
Yalikuwa ni majira ya saa kumi hivi, ila iliyoelemewa na dakika kuifuata saa kumi na moja.
“Mkuu!” Mudy akastaajabu na mkate wake mdomoni. “Karibu, karibu.”
Brokoli akatabasamu akiingia. Akaketi kabla Mudy hajamuuliza angependelea kitu gani. Brokoli akasema maji tu yanamtosha. Na pasipo kupoteza muda, akasema nini kimemleta pale.
“Kuna nyaraka fulani sizioni kule ofisini. Zipo wapi?”
Kauli hiyo ikashtua moyo wa Mudy. Alijikuta anasisimkwa vinyweleo na kupigwa bumbuwazi.
“Hakuna nyaraka ambazo nimechukua mkuu!”
“Sijasema kwamba umechukua, nimeuliza zipo wapi.”
“Sijajua. Ni nyaraka gani hizo unazoziongelea?”
Naye Brokoli hakusema ni nyaraka hizo anazoziongelea. Basi akafungua mkoba wake na kutoa bunduki yenye kiwamba cha kumezea sauti. Akaikoki bunduki hiyo na kumwonyeshea Mudy pasipo kusema kitu.
Mudy akaanza kuropoka. Ya kwamba nyaraka hizo amempatia Kinoo kwani alikuwa anazihitaji, na pia amepanga kuchuku hatua kuhusu kifo cha Bite.
Brokoli akatikisa kichwa na kusema:
“Ahsante. Hicho ndicho nilikuwa nataka.” Kisha akaminya kitufe cha bunduki, bunduki ikakohoa na kumwangusha Mudy chini. Paji lake la uso lilikuwa limetobolewa likivujisha damu.
Brokoli akasafisha bunduki yake vema na kitambaa alichokitoa ndani ya mkoba alafu akarejesha bunduki yake mkobani baada ya kuhakikisha amebebea simu ya Mudy.
Akatoka ndani ya uzio, na kujiweka kwenye gari lake VX ya grey, akatimka akiweka simu sikioni.
Punde simu ikapokelewa, akasema:
“Ameuza taarifa … kwa jamaa yule jamaa, Kinoo.” Akakata simu na kuendelea na safari.
Simulizi : Anga La Washenzi (1) Sehemu Ya Tatu (3)
***
Rrrrrrrrrrrrnng! Rrrrrrrrrnnngg! Lee akashtuka na kutazama simu yake. Alikuwa maeneo ya nyumbani kwake na majira yalikuwa ni ya saa nne usiku,
Jina kwenye kioo halikutokea, bali namna mpya. Aksita kidogo kupokea, ila akapuuza na kuweka simu sikioni. Akanyamaza amsikie kwanza sauti ya aliyempigia. Alikuwa ni mwanaume mwenye sauti nzito.
“Yes, Lee anaongea.”
“Wewe ndiye yule mchina, si ndio?”
Lee hapendi kuitwa hivyo. Ila hakujali, alihisi kuna habari njema inafuata. Akawahi kujibu na kutega sikio.
“Mimi ni baunsa wa hapa klabu ulipoacha namba yako. Nimemwona yule msichana uliyekuwa unamtafuta.”
“Una uhakika?”
“Ndio. Kwa mujibu wa maelezo yako.”
Lee akanyanyuka upesi. Hakumuaga yeyote yule, akajipaki kwenye gari na kwenda moja kwa moja klabu. Alipofika akapiga namba ile iliyompigia, akaongea na kuelekezwa aende wapi.
Akakutana na baunsa aliyevalia ‘kibodi’ cheupe aliyemdai pesa yake kwanza kabla hajamuonyesha mlengwa.
“Tulipane kwanza, vipi ukin’toroka.”
Lee asifanye ajizi, akazama mfukoni na kumpatia baunsa ‘wekundu’ watatu. Baunsa akatabasamu, akamnyakua Lee mpaka ndani. Akamnyooshea kidole mwanamke fulani kwenye kona ya klabu.
Alikuwa amekaa na wenzake akifunikwa na nywele ndefu za badia. Alikuwa amevalia gauni fupi, pamoja na wenzake pia. Taa za rangii rangi zilikuwa zinamulika mulika watu wakipata ‘kilaji’ kungoja usiku uwe mzito zaidi.
Mdundo mzito wa muziki ulikuwa unakita.
Lee akamsogelea mwanamke yule na kumshika bega kwanguvu. Mwanamke huyo alipomtazama, akagundua siye yule aliyekuwa anamtaka. Akaomba radhi na kurejea kwa bodyguard haraka.
“Sio yule!” akang’aka. Bodyguard akashadadia kwamba maelezo yake yaliendana na mwanamke huyo. Lee akataka pesa yake, bodyguard hakuwa tayari kumpatia.
Ugomvi ukazuka.
Wakavutana nje wapate kuonyeshana. Nyama za bodyguard zikamfanya aamini kwamba anaweza kumdhibiti Lee mwenye mwili wa sisimizi.
Bahati kabla hawajaanza pambano, Lee akamshuhudia mwanamke yule aliyekuwa anamtaka. Alikuwa yupo na mwanaume fulani hivi wakifuata mlango wa kuzamia klabu. Lee akaachana na baunsa yule, akakimbilia kwa yule mwanamke.
Akamdaka mkono na kumvuta.
“Unanikumbuka?”
Mwanamke akaigiza hamjui Lee. Alimtaka mwanaume huyo amwachie mkono wake kabla hajamuitia mwizi. Lee akajikuta anatabasamu. Wakati huo na yule mwanaume aliyeongozana na mwanamke huyo anataka kuchukua hatua dhidi ya Lee.
“Sitaki ukorofi wowote. Ninachotaka ni pochi yangu na vile vilivyomo ndani tu. Sina shida na pesa bali nyaraka.”
Bado mwanamke akang’ang’ania msimamo kwamba hana chochote cha Lee. Yule ‘bwana’ aliyekuwa ameambatana na mwanamke huyo akamtaka Lee aondoke na awaache waendelee na mambo yao.
“Tumekuja hapa kustarehe, si kupigana.”
Lee akashindwa kuzuia hasira zake, akamvuta kwanguvu yule mwanamke upande wake kisha akamchakaza mwanaume yule mwambatanizi kwa muda usiozidi dakika moja! Mikono na miguu yake ilikuwa mepesi kana kwamba inaendeshwa na mota.
Alijikuta anashikilia shingo yake kwa maumivu makali, mbavu zikiwa zimetepeta na yupo chini! Kama ungemuuliza ni kwa muda gani amepigwa hivyo, asingekuwa na jibu moja.
Lee akahepa zake kufuata gari watu wakimtazama kwa mshangao. Hakuna aliyethubutu kuhangaika naye.
Akapeleka gari mpaka nyumbani kwa huyo mwanamke akiamuru apewe pochi haraka iwezekanavyo. Hakuwa na hata tone la utani!
Mwanamke akiwa analia kwa hofu, akatafuta pochi ndani lakini hakuikuta. Akahisi anauawa. Mbona pochi ilikuwepo jana? Alijiuliza akihangaika na mikono yake inayotetemeka.
Hakuona kitu.
Macho yake yakiwa mekundu, akamwambia Lee ya kwamba hajapata kitu.
“Sitaki ujinga na tusipotezeane muda. Naomba pochi!”
Katika kuchambua fikira zake, mwanamke akakumbuka jana alimleta mgeni chumbani hapo. Pengine yeye ndiye atakuwa kaichukua.
“Twende kwake,” Lee akasema haraka. Na pasipo kupoteza muda wakaenda mpaka kwa mwanaume huyo. Uzuri mwanamke alikuwa anapafahamu. Ni mwanaume mteja wake wa enzi, mara zingine huwa anaenda kwake huduma ikiwa inahitajika.
“Naomba niende kuongea naye,” mwanamke akasema walipofika kwenye chumba cha mlengwa wao. Lee akakataa na kutaka waende pamoja kwa kuogopa kutiwa mchanga wa macho.
Akiwa yupo nyuma, akaongozana na mwanamke huyo mpaka mlangoni, akagonga na uzuri kuna mtu akawapokea, japokuwa hakuwa mlengwa wao. Alikuwa ni mwanamke mnene mweupe aliyevalia khanga.
Alitoka usingizini na ugeni ule ulimshtua. Lee akaeleza haja yake, lakini mwanamke yule akamwambia hawezi kumsaidia kwani mwenyewe hayupo.
Lee hakutaka kungoja, akazama ndani kwa mabavu. Akasaka chumba na kukuta pochi yake mezani. Akaipekua, akakuta hamna kitu! Basi asipoteze muda hapo, akachukua picha moja ya mwanaume aliyoikuta mezani, pasipoti, kisha akamrudia yule mwanamke mnene na kumuuliza:
“Atakuwa ameenda wapi?”
“Sijui!”
“Mimi najua atakapokuwa mida hii,” akadakia mwanamke aliyekuja na Lee. Basi pasipo kukawiza, wakaenda kwenye gari na safari ikaanza.
“Anapenda kwenda sana viwanja. Kama hayupo Ambiance, basi atakuwa Billicanas.”
Wakaanzia Ambiance, wakahaha klabu nzima. Hapo ndiyo yule mwanamke akajua namna gani Lee alikuwa anamaanisha kutafuta kile kilichomo ndani ya pochi. Alijiuliza ni nini hicho na thamani yake.
Mungu alikuwa upande wao, wakampata. Mwanamke alimnyooshea Lee kidole na kumnong’oneza kuwa ndiye wanayemtafuta.
“Naomba vitu vilivyokuwemo kwenye hii pochi,” Lee alienda moja kwa moja kwenye mada akiwa anamtazama mlengwa wake: mwanaume mwenye mwili kiasi, mweusi na nywele nyingi zilizo hovyo.
Mwanaume yule akaleta nyodo. Akasema vyote vilivyokuwemo amevitupa maana hakuona kama vina umuhimu. Lee akakasirika sana, lakini mwanamke yule akamvutia kando na kumsihi:
“Usianzishe ukorofi hapa. Niachie hiyo kazi n’takufanyia pasipo kutoa jasho.”
“Ndani ya muda gani?”
“Nipe siku moja tu.”
Lee pasipo kuaga, akaondoka zake baada ya kumkata jicho mwanaume yule ambaye alikuwa tayari ameshaita jamaa zake kwa ajili ya shari. Alimwacha mwanamke aliyekuja naye hapo asionekane kama aliyepotea.
Akasonya kabla hajakanyaga pedeli ya mafuta. *** Saa mbili asubuhi …
“Nitakuchek baadae,” Jona alituma ujumbe mfupi kwenda kwenye namba aliyoitunza kwa jina la Jumanne. Akaweka simu kando na kupasulia mayai mawili kwenye frampeni.
Alikuwa amevalia bukta ya bluu akiwa kifua wazi. Akili yake ilikuwa inawaza mambo kadhaa, la kwanza juu ya usalama wake. Na pia juu ya Miriam wa mheshimiwa Eliakimu.
Alikuwa ametenga siku hiyo mahususi kwa ajili ya kupembua, kupanga na kuamua juu ya hatma ya maisha yake kutokana na yanayoendelea kwani hata kipofu angelijua ya kwamba kwa sasa yupo vitani.
Alikaanga mayai yake akayala pamoja na sharubati. Bado akiendelea kutafakari. Akatathmini maisha yake na tathmini hiyo akaenda kuirejelea kwenye makaratasi yake meupe anayotumia kuchora. Hapo akaandika na kuchora kila ambalo lilikuwa linazingira maisha yake.
Kuanzia sakata la kifo cha mke na mtoto wake, biashara yake kufa, picha, Eliakimu, Miranda na Kinoo, Bigo, na mauaji yale yote aliyopata kukumbana nayo. Je vitu hivyo vitakuwa vina mahusiano? Akajiuliza na nafsi yake.
Akachoropoa chupa kubwa ya mvinyo alafu akagida akiendelea kutafakari. Mwishowe alipomaliza chupa nzima, akapitiwa na usingizi baada ya kichwa kuwa kizito.
Alipokuja kuamka yalikuwa majira ya jioni, na simu yake ilikuwa na jumbe nne, tatu toka kwa Miriam na moja toka kwa Jumanne. Kabla ya kusoma jumbe hizo akaoga, alafu akavaa na kutoka ndani mpaka baa iliyokuwepo karibu.
Akaagiza maji makubwa tu, alafu ndipo akatoa simu na kuanza kuhangaika nayo.
“Am in Dar,” (Nipo Dar) alituma ujumbe kwenda kwa Miriam. “Where are you now? When shall we meet?” (Upo wapi saa hii? Lini tutakutana?”)
Hakutaka kungoja. Alitaka sasa kufanya mambo haraka aone matokeo yatakuwaje. Hakuona haja ya kungoja ngoja kuumiza tumbo.
Alipotuma ujumbe huo, akaufungua na ujumbe wa Jumanne.
“Mbona kimya? Kuna mtu amekuja kukuulizia hapa?”
“Nani huyo?” Jona akatuma ujumbe kuuliza.
“Hajajitambulisha,” Jumanne akajibu. “Ni jamaa fulani hivi mwembamba.”
“Alikuja na usafiri?”
“Sijajua. Sikumwona na usafir”
Jona akajiuliza juu ya mtu huyo. Inawezekana akawa ndiye yule anayetaka kummaliza? Akajikuta anatikisa kichwa. Wa kwanza alikuwa Bigo, na sasa huyu.
Suluhisho siyo kummaliza, bali kuukata mzizi kabisa. Endapo akifanikiwa kummaliza huyo anayemtafuta, bado atatumwa mwingine … na mwingine na mwingine. Basi kwakuwa Miranda na Kinoo wanafahamu kuhusu hawa watu, hana budi kuwawahisha kaburini upesi.
Akanywa maji yake. Muda si mrefu, akapokea ujumbe toka kwa Miriam. Alikuwa amefurahi sana kusikia taarifa ya ‘mtu’ wake kuwapo Dar es salaam. Wakaongea kidogo na akajieleza wapi alipo, wakapanga pia pa kukutania.
“I think tomorrow I’ll be free.” (Nadhani kesho nitakuwa huru.) aliandika Jona. Akapata uhakika wa kuonana Miriam.
Baada ya hapo akampigia simu Miranda na kumtaka waonane kesho yake jioni kwani kuna jambo la kuliongelea na kuliweka sawa. —– Siku iliyofuata, Lamada hotel, majira ya saa sita mchana.
Jona alikuwa tayari ameshampanga Miriam kwamba wakutane hapo. Miriam alifika hapo hotelini na gari nyeupe Nissan Murano akiwa amevalia suruali ya kitenge. Karibu na mabwawa ya kuogelea, akaketi hapo na kuanza kuteta na Jona kwa kupitia simu.
Hakufahamu kwamba Jona alikuwa tayari ameshafika eneo hilo, na alikuwa anamtazama.
Baada ya muda mchache Jona akajitokeza na kusogea papo baada ya kuhakikisha kwamba Miriam alikuwa mwenyewe, hamna kampani. Akaketi na kujitambulisha kwa jina la Roden, na kitambulisho cha polisi akatoa kotini.
“Usijali, na wala usihofu. Sina haja wala nia ya kukuumiza,” akasema Jona akimtazama Miriam ambaye uso wake ulikuwa mweusi kwa hofu. Hata mwili wake ukitetemeka.
Jona akasema ametumwa na Eliakimu na yupo pale kwa lengo moja tu, la kumtwaa na kumpeleka huko. Miriam akatikisa kichwa upesi, akamwomba Jona kumwachia huru kwani kumpeleka kwa Eliakimu ni sawa na kumpeleka kwenye domo la simba mwenye njaa.
“Nipo radhi kwa lolote ila si kunipeleka huko. Nakuomba, nipo chini ya miguu yako.”
Hii ikawa fursa adhimu sana kwa Jona kutimiza malengo yake. Akaanza kumpeleleza na kumdadavua Miriam kwa undani. Akahakikisha anapata kile ambacho Eliakimu anamficha.
Alimtaka Miriam afungue simu yake na kumkabidhi. Miriam akafanya hivyo na kinyume na matarajio yake kwamba Jona ataenda kwenye uwanja wa ujumbe, mwanaume huyo akaenda mtandaoni na kupakua kitu fulani na kukitunza kwenye simu ya Miriam. Kisha akairejesha simu na kuendelea na maongezi.
Tukio hilo lilichukua sekunde ishirini tu kisha akaendelea na maongezi.
Lakini wakiwa katikati ya maongezi hayo, Jona akasikia sauti ya kike nyuma yake ikinong’oneza kumwamuru asimame akiwa amenyoosha mikono juu! Haikujulikana ni wapi mwanamke huyo ametokea.
Kwa ustadi mwanamke huyo aliambaa na ukuta na kuhakikisha hagundulikani na yeyote yule. Nywele zake ndefu za bandia zilizozonga uso wake ukijumlisha pia na miwani ya macho, haikuwa rahisi kumng’amua.
Miriam alimwona mwanamke huyo ila alidhani ni mpita njia. Kumbe alikuwa Nade, na ndani ya koti la zambarau alilolivaa alikuwa ameweka bunduki yake ndogo ambayo kwa sasa mdomo wake ameuminyia kwenye mbavu za Jona. Bado bunduki akiwa ameifichia ndani ya koti.
Haraka akampekua Jona na kubeba bunduki yake kisha akamtaka asogee mbali na Miriam asogee upande wake haraka. Matukio hayo yakafanikiwa ndani ya muda mchache mno! Nade akatoka na Miriam ndani ya hoteli.
Wakajipaki ndani ya gari, wakayoyoma! Jona akawatazama namna wanavyoishilia. Akatabasamu na kusema:
“Kama ilivyopangwa.”
Nade pasipo kujua alikuwa ametanguliwa hatua mbili mbele.
Jona alishatambua mpango wa Nade na alifahamu fika mwanamke huyo atakuwa karibu kwani amekuwa akimfuatilia kisirisiri kwa muda sasa.
Hivyo kila kitu alichokifanya alifanya akiwa amejiandaa na uvamizi ndani ya muda wowote ule. Na akajipanga kunufaika na uvamizi huo kwa kupandikiza ‘application’ katika simu ya Miriam itakayomsaidia kutambua wapi mwanamke huyo yupo na pia vile vile kumwezesha kusikia angalau sauti!
Kwahiyo kuondoka kwa Nade akiwa ameongozana na Miriam, kwa Jona ilikuwa ni mpango ulio kamilika.
Jona akiwa hapo amesimama na macho yake yakishuhudia gari la Nade likiyoyoma kwenda kujichoma, haraka ya punde toka upande wake wa kulia, nje ya uzio, akaona gari aina ya Altezza, ile ile ambayo ilihusika na tukio la kujaribu kummaliza, ikikatiza kwa mwendo pole na kioo cha upande wa dereva kikiwa kimefunguliwa.
Akatazama kwa ustadi na karibu zaidi, akamwona dereva akifichamua mkono wake wa kulia! Mara akatoa bunduki na kuonyeshea kule alipo Jona!
Haraka Jona akachumpa na kujikinga kwenye mojawapo ya magari yaliyokuwa yameegeshwa hapo uwanjani. Risasi tatu zikavuma! zikamkosa na kuishia kutoboa magari ya gharama kubwa yasiyo kuwa na makosa. Kisha gari la yule adui, ambaye ni wazi alikuwa ni Panky, likaongeza mwendo maradufu lipate kupotea tukioni!
Upesi Jona akakimbia kufuata uzio, akauruka kama kiunzi! Akasimama katikati ya barabara na kuzuia gari moja, Toyota Corola nyeupe, kwa ishara ya kunyanyua mkono, akaonyesha kitambulisho chake bandia cha polisi na kumwambia dereva:
“Nitahitaji gari lako kusaidia jeshi la polisi.”
Akachumpa ndani ya gari na kulitimua mno kukimbiza gari lile Altezza. Mwendo wake ulikuwa mkubwa mno na hata akatanua kando ya barabara ili apate mwanya wa kujiachia zaidi.
Dereva wa hilo gari akahofia maisha yake. Aliogopa hata kutazama namna gari inavyoendeshwa kwa kushindwa kustahimili. Alitetemeka kwa kukutana na kifo uso kwa uso. Muda wote alikuwa analia gari ipunguzwe mwendo, huku Jona akimwambia hana haja ya kupata shaka!
Ndani ya muda mfupi, Jona akawa amejiweka usawa mzuri na lile Altezza anayoikimbiza. Sasa walikuwa wamefika Afrikana kuikuta barabara ya kutokea Bagamoyo kwenda katikati ya jiji.
Panky akakata kona kushika njia kuelekea Bagamoyo. Naye Jona akaunga mkia! Akamzidi maarifa Panky na kumsogelea karibu zaidi na zaidi. Sasa wakawa wamepeana ubapa.
Ila kichwani mwa Jona hakuwa amelenga kummaliza Panky. Alikuwa na uwezo kamili wa kupindua gari lake ila alimhitaji akiwa hai. Kifo chake kwake pia ingekuwa hasara.
Hivyo nini alichokuwa anakifanya? Kumpa presha zaidi Panky wamalize njia hii kukaribia kuitafuta Bagamoyo, kule ambapo magari si mengi. Yaani mbele kidogo, katikati ya Bunju na Bagamoyo.
Akafanikiwa janja hiyo lakini geji ya mafuta ya gari alilokuwa anatumia ikaonyesha mafuta yanaenda kukauka hivyo muda si mrefu sana chombo hicho kitakuwa na kiu ya kushindwa kufanya kazi!
Sasa ikabidi atumie nafasi hiyo kabla hajawa amepoteza muda wake bure.
Huu ukawa ni muda wa kumwonyesha na kumfunda Panky ujuzi wake kwenye uendeshaji wa vyombo vya moto. Akawasha ‘full lights’ kisha akakanyaga mafuta zaidi. Na kutokana na uhodari wake wa kukwepa magari, punde akawa beneti na adui!
Ndani ya muda mfupi, Jona akafanikiwa kumtoa Panky kwenye barabara ya lami kwa kumtishia kumparamia na gari. Kisha akageuza gari upesi na kukita mti fulani wa wastani kwa kutumia bodi ya nyuma ya gari, mti ukaangukia Altezza na kuibonyeza paa!
Panky akapoteza mwelekeo na kujikita kwenye chaka la miti. Akajeruhiwa kichwa na miguu. Alivuta hewa mara moja tu na mara Jona akawa amewasili!
Akamalizia kupasua kioo akafungua loki na kumtwaa Panky. Alikuwa hajiwezi, hoi asiyejitambua. Kichwa kilikuwa kinachuruzika damu. Macho yamemlegea!
Jona akamlaza chini baada ya kuhakikisha ameshabeba silaha ya adui, akafanya upekuzi wa haraka ndani ya Altezza alafu akayoyoma na Panky.
***
“Kuna kitu umeelewa?” Akauliza Miranda akimtazama Kinoo aliyekuwa ameketi kando yake. Wote mkononi walikuwa wamebebelea karatasi inayofanana. Ile yenye mchoro wa Bite ambao Jona aliwakabidhi.
Kinoo akatikisa kichwa. Hakuwa amepata kitu! Ni masaa sasa wamekuwa wakiichambua picha hiyo pasipo mafanikio. Sasa wakaona wanafanya kazi ya ubuyu.
“Tunafanyaje sasa?” Kinoo akauliza. Miranda akashusha kwanza pumzi na kuiweka kando karatasi apate kunywa sharubati yake ya embe. Akafikiri na akaona kuna haja ya kumshirikisha BC katika hilo, pengine anaweza akawa na maarifa.
Lakini Kinoo akamtaka awe mwangalifu.
“Hatujamshirikisha hili tangu mwanzo, huoni linaweza likatusababishia tafrani?”
Miranda akaona hoja ndani ya kauli ya Kinoo. Lakini wasipofanya hivyo itakuaje na ilhali vichwa vishagoma? Kinoo akapendekeza wajaribu zaidi na zaidi hata kama ikiwachukua mwezi.
Kwa sasa hakuna habari itakayokuwa njema kwa BC isipokuwa ya wao kufungua fumbo hilo.
“Nahofia yule mchoraji anaweza akang’amua hili kabla yetu,” alisema Kinoo.
“Unadhani akigundua atafanya nini?” Miranda akawahi kuuliza, lakini kabla Kinoo hajajibu, mwenyewe akajipa maelezo.
“Alichokipata kinamtosha. Hatakiwi ajue zaidi ya hapo. Inabidi tukumbuke kwamba yule si mshirika wala mtu wetu.”
Wakaona kuna haja ya kummaliza Jona punde tu watakapopata mchanganuo wa picha ile. Aidha utoke kwao ama kwa Jona mwenyewe.
Hakutakiwa kuwa hai baada ya hapo!
“Hakikisha leo unawasiliana naye kumuuliza kama amepata chochote,” alisema Miranda.
“Unajua mimi siendani na yule lofa. Kwanini usifanye hiyo kazi wewe?” Kinoo akarusha mpira.
“Ningekuwa nina muda huo, nisingekusumbua. Ila nina appointment. Sidhani kama n’takuwa huru.”
Ulikuwa umebakia muda mchache kwa Miranda kwenda kukutana na Boka – waziri wa Afya. Muda si mrefu aliwasiliana na mheshimiwa huyo wakapanga miadi ndani ya Kempinski hotel ndani ya majira ya jioni.
Alishamtaarifu BC na huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa wao kutengeneza daraja la pili baada ya la sasa kupiga nyufa.
“I have already arrived,” (tayari nimeshawasili) alisema Miranda kwa sauti ya puani. Alikuwa amejivika gauni moja matata sana! Rangi nyekundu lisilo na mabega likijishikiza kifuani mwake.
Hapo kifuani gauni hilo lilikuwa linametameta. likaenda moja kwa moja na mwili wake uliosimamisha nyonga na kudaka mapaja mpaka chini miguuni lilipojiachia.
Nywele zake zilikuwa zinawaka zikitiririkia mgongoni. Juu kidogo ya sikio la kushoto alikuwa amepachika ua dogo jekundu. Uso wake ulikuwa umekwatuliwa vizuri kwa viwango vya kimataifa!
Katika kijiwanja hicho cha kupata chochote kitu kilichomo ndani ya hoteli, hakuna aliyekuwa amependeza kama yeye.
Punde Boka akatokea. Hakupata shida kuangaza kwani Miranda alikuwa anang’aa. Akajisogeza taratibu akiwa anatabasamu. Nyuma yake alikuwa akiongozana na mlinzi.
Alikuwa amekula suti moja matata nyeusi toka Italia.
Akaomba radhi kwa kuchelewa. Akahisi moyo wake unakuwa wa baridi kila alimpotazama Miranda ambaye alijua kucheza na macho na tabasamu lake kumzizima mwanaume.
Boka akajikuta anatabasamu mara kwa mara. Akisisimkwa vinyweleo!
“Unajua mke wangu hajui juu ya hili kutano letu, na siku ukikutana naye usithubutu kumwambia,” alisem Boka akitabasamu.
“Usijali, sijawa mjinga kiasi hicho,” Miranda akamtoa hofu. Mhudumu akaja na kuwahudumia glasi mbili kubwa za juisi ya Raspberry.
Wakateta kidogo kukumbushiana ya tafrija ile iliyowakutanisha. Ila Boka akapata hamu ya kumjua yule mwanaume aliyekuwa ameongozana na Miranda siku ile, yani BC.
Miranda asifanye makosa akamwambia yule ni mlezi wake. Alimuasili na kumlelea tangu mtoto kwahiyo kwake anamuita baba.
Boka akafurahi na kushukuru kwa taarifa asijue Miranda alikuwa anatengeneza ‘makao’. Akaanza kumpeleleza Miranda juu ya maisha yake ya mahusiano. Na Miranda kumridhisha akampatia majibu ambayo mwanaume huyo alikuwa anataka kuyasikia.
“Mpenzi wangu wa kwanza alikuwa ni mtu toka France, lakini nilishindwana naye tabia. Ni mlevi sana na mtu asiye na ‘future’. Nikapata mwingine lakini naye hayupo ‘serious’ so nikaona inabidi nitulie kwanza kabla ya kuzama tena uwanjani.”
Basi Boka akafurahi mpaka jino la mwisho. Na pasipo kukawia akamtongoza Miranda. Kwanza Miranda akaigiza mshtuko ya kwamba hakuwahi kudhani kama kuna siku anaweza akapendwa na mtu ‘mkubwa’ vile.
Pili akaigiza uoga juu ya usalama wake kwa mke wa Boka ambaye anaonekana ni mjawa wa wivu. Boka akamtoa shaka.
“Hilo niachie mimi. Nikubalie uonje matunda ya nchi, mrembo.”
Miranda, akiwa anaminyaminya lips na kuzimumunya, akaomba apewe muda kwani moyo wake uliojeruhiwa huko nyuma unahitaji kushirikisha akili yake kwanza.
“Kwahiyo mpaka lini mpenzi?”
“Nitakutaarifu.”
Baada ya hapo wakateta kidogo juu ya mkewe Boka, Boka akimtaarifu Miranda kwamba mkewe anaweza kumtafuta muda si mrefu kwani alikuwaanamwongelea hivi karibuni.
Hawakukaa tena sana, wakaagana na kila mtu akaenda zake. Miranda akampigia simu BC na kumtaarifu vile mpango ulivyokwenda.
Yote yalikuwa mema!
***
Simu iliita kwanguvu! Ilikuwa ni alarm ambayo ilimkurupusha Lee toka kitandani akaangaza. Lah! Ilikuwa ni saa kumi na mbili jioni. Akanyanyuka upesi na kwenda kujiandaa pasipo kuoga.
Akajipaki kwenye gari lake na moja kwa moja akanyookea mpaka nyumbani kwa yule mwanamke ambaye alimuahidi kumtafutia nyaraka yake toka kwa yule mwanaume aliyelala naye.
Uzuri akafika na kumkuta akiwa ndani nay u maandalizini akikaribia kuruka viwanja. Mwanamke huyu ni kama popo kwani hulala mchana na usiku kwake ni kazini.
Alikuwa pamoja na marafiki zake watatu ambao walijikuta wanamwonea wivu mwenzao baada ya kumwona akiitwa na mchina. Hawakujua alikuwa matatizoni.
“Vipi ile ishu?” Lee akauliza. Alikuwa ameegemea ukuta akimtazama mwanamke kama vile maelekezo ya mtihani.
“Bado hajanipatia,” Mwanamke akajibu. Lee akajikuta akipandwa na hasira! Akauliza shida ni nini, mwanamke akamwambia wale wanaume wamesema wana hizo nyaraka lakini wanataka pesa kwanza.
Kama kweli ni za muhimu basi na wao wanataka angalau ‘kamgao’. Lee akastaajabu. Yani kamgao na nyaraka ni zangu! Akamkwida mwanamke shingo na kumkazia macho.
“Nipeleke kwa hao mabazazi!”
Mwanamke akamwambia si kwa sasa kwani ana mtoko. Lee akacheka na kumwambia hakutakuwa na mtoko wowote ule mpaka pale atakapohakikisha amepata karatasi zake.
“Twende ama nikuvunje taya saa hii!”
Basi kwanguvu Lee akampaki mwanamke ndani ya gari na kwenda mpaka kule kwenye yale makazi ya yule mwanaume. Wakagonga lakini hakukuwa na majibu. Wakauliza pia hata kwa majirani pasipo mafanikio.
“Sijaona mtu leo hii,” alisema jirani mmoja, mmama mnene mweusi aliyekuwa amevalia khanga aliyoifungia kifuani. Mdomo wake mwekundu akiupindua.
Siku hiyo ndiyo Lee akatambua jina la mwanamke yule anayesumbuka naye kutafuta vilivyo vyake. Alikuwa anaitwa Glady! Akamtaka ampeleke kwenye viwanja anavyoenda huyo mwanaume akamkute huko. Hapo akiwa anajilaumu kwanini ile jana aliimwacha salama.
“Nadhani alikuwa anahitaji funzo, na mbaya sikumpatia.”
Kwahiyo Glady na Lee wakaongozana mpaka viwanja. Lakini Glady alikuwa anasisitizia kwamba ule muda sio. Hawawezi kumkuta huyo mlengwa wao huko labda mpaka baadae, usiku ukiwa umevunja ungo.
Lakini kwa hamu aliyokuwa nayo Lee, hakuelewa! Bado alitaka kwenda akashuhudie na macho. Kweli wakafika kiwanja cha kwanza, hawakupata kitu. Cha pili vilevile hakukuwa na kitu. Mpaka cha tatu!
Glady akamwambia:
“Unaona? Hapa inawezekana bado akawa kwenye mihangaiko yake.”
Lee akauliza: “Na yule mwanamke tuliyemwona jana kule nyumbani?”
Glady akaangua kwanza kicheko. Akamjibu kuwa yule alikuwa ni malaya tu kama yeye. Mwanaume yule huwa anabadili wanawake, kwahiyo itakuwa hajaleta malaya siku hiyo.
Lee akachoka. Kichwa kikagoma kuzalisha mawazo kwa muda. Asikae muda, akasikia simu yake inaita. Haraka akaichoropoa mfukoni na kutazama. Alikuwa mkuu! Alimtunza kwa jina la ‘The Big.”
Akasita kupokea simu akifikiria. Ila mwishowe akapokea na kuongea kwa sauti ya chini.
Maongezi yakadumu sekunde tatu tu! Akakata simu. Sura yake ilikuwa imenyong’onyea. Na macho yake yalifumbwa kwa mawazo.
Ujumbe ukaingia kwenye simu yake. Akautazama. Ulikuwa unatoka kwa Nigaa akimuuliza yupo wapi. Hakujibu akairudisha simu mfukoni na kulalia usukani.
Glady akamuuliza nini kimejiri. Baada ya muda kidogo akamtazama tena Glady na kumuuliza:
“Ina maana hamna namna nyingine tunayoweza kumpata?”
Glady akabinua mdomo na kutikisa kichwa. Lee akawasha gari na kutimka! Akamrejesha Glady nyumbani kwake akimuahidi anaweza kuja baadae, alafu akanyookea mpaka yalipo makao yao kwenda kuonana na mkuu.
“Vipi, ulikuwa wapi?” Nigaa akamuuliza. Lee, kwa sauti ya unyong’onyevu, akamwambia alipotoka.
“Mkuu alikuwa anakuulizia kweli. Bado hujapata ile ishu?”
Lee akamwambia namna mambo yalivyo. Nigaa akafunika mdomo kwa kiganja.
“Sasa utamwambiaje mkuu?” Akauliza.
“Nitajua huko huko,” Lee akajibu akaminya lips. Nigaa akapendekeza waende wote, ila Lee akakataa. Ule ulikuwa ni wito wake na ilibidi autimize. Kwahiyo akaenda zake, lakini Nigaa akabaki na moyo mzito, basi akasonga karibu na mlango apate kusikia.
Maongezi yakachukua kama dakika nane. Mara Nigaa akasikia sauti ya risasi! Pah – pah! Kukawa kimya.
Lee ameuawa? Nigaa akatoa macho. **
“Katika siku ambazo umefanya kazi za kiume, basi ndiyo hii!” alisema mheshimiwa Eliakimu alafu akaangua cheko pana. Macho yake yalikuwa mekundu. Mkononi alikuwa amebebelea chupa kubwa ya mvinyo akiipeleka mdomoni kupiga tarumbeta.
Alikuwa amevalia bukta kaki ya ‘timberland’. Kifua chake kilikuwa wazi na miguuni peku. Pembeni yake tu hapo, alikuwa amesimama Nade akiwa amevalia ‘vest’ ya bluu na suruali ya jeans. Mkononi alikuwa amebebelea bunduki.
Ndani ya chumba hichohicho, alikuwapo pia Miriam. Yeye peke yake ndiyo alikuwa amekaa. Kiti kilikuwa kimoja tu chumba kizima, Miriam alikuwa amefungiwa hapo na kamba ya katani rangi ya manjano.
“Unastahili zawadi, tena nono!” alisema Mheshimiwa akimtazama Nade. “Na nitakupatia zawadi hiyo kwa kuniletea kichwa huyu mbwa koko hapa ngomeni.”
Akanyooshea kidole kwa Miriam aliyekuwa amekaa akimtazama kwa uso wa ghadhabu kali.
Akamwambia Nade kwamba hakuamini pale alipopokea taarifa ya kukamatwa kwa mkewe. Alimfanya asifanye kazi kabisa na kutazamani kutoka ofisini papo hapo. Amekimbiza sana gari mpaka kufika hapo. Hakutaka hata dereva aangaike.
Alipomaliza kusema hayo, akamtazama Miriam na kumuuliza alikuwapo wapi siku zote hizo. Na huko alikuwa anafanya nini. Miriam akacheka kwanza. Akimtazama mumewe, akasema:
“Bwana, nilikuwa kwetu. sikutaka kabisa kuwa na wewe, si uligoma kunipa talaka?”
Mheshimiwa akabana pua na kurudia maneno ya mkewe. Akamzaba kofi kali na kufoka:
“Unadhani mimi ni mjinga, sio?”
Eliakimu alikuwa anaamini kuwa mwanamke huyo alikuwepo mahali na anafanya jambo. anahofia siri zake anaweza akawa ameziweka wazi. Hivyo akamlazimisha sana Miriam aongee kwa kutumia mabavu.
Miriam akachakaa kwa kipigo asiseme kitu. Alitema meno matatu nje lakini bado akisema alikuwa kwa ndugu ambao Eliakimu alishawauliza na wakasema mwanamke huyo hakuwako.
“Utasema tu … utajua namna gani nilivyo mafia!”
Wakiendelea na zoezi hilo, mara simu ya Miriam ikanguruma. Ilikuwa ndani ya mfuko wa bukta ya mheshimiwa Eliakimu. Kabla mheshimiwa hajapokea, akamtazama kwa Nade. Alafu akatoa simu hiyo na kutazama.
‘My heart’ Pale’ alikuwa anapiga.
Eliakimu akasonya. Bila shaka huyo ndiye anayemchukulia na kumzuzua mkewe, akasema. Akamtazama Nade na kumkabizi simu apokee ajifanye Miriam.
Miriam akatamani kupiga kelele, lakini mdomo ulikuwa hautamaniki. Ulikuwa umevuja damu na kupasukapasuka. Ajabu hata Eliakimu alikuwa anangojea mwanamke huyo aongee. Kwa namna gani sasa!
“Hallow!” akasema Nade kwa sauti ya utulivu.
“Vipi, mbona sauti imekuwa hivyo?” sauti nzito ya kiume ikauliza.
“Nipo kwa shangazi,” ndilo jibu lililokuja kichwani.
“Unafanya nini huko? Ina maana hujui kwamba huko ni hatari kwa usalama wako?!” Sauti ikafoka.
“Nitatoka muda si mrefu,” akajibu Nade na kisha akauliza: “Kwani wewe upo wapi saa hii?”
Sauti ikaelekeza makazi. Alikuwa hoteli ipi na chumba namba ngapi, kisha simu ikakata. Eliakimu akafurahi sana kwani aliona sasa anaenda kumpata na huyo mwanaume amalize kazi.
Wakaachana na Miriam kwa muda wapange namna ya kumtia nguvuni ‘mwanahizaya’ huyo. Nade akasema yeye mwenyewe atosha kufanya hiyo kazi, ahitaji msaada. Eliakimu akahofia kidogo kutokana na jeraha alilo nalo mwanamke huyo begani.
Kama isingelikuwa Jona alikuwa hotelini, mahali ambapo kuna watu wengi na ulinzi pia, mwanamke huyu angemdungua risasi Jona. Na Jona alilifahamu hilo hapo kabla na ndiyo maana hakutaka kukutana na Miriam mahali pa kimya zaidi.
Na pia alifahamu Eliakimu na Nade wataenda kubwabwaja maneno lukuki mbele ya Miriam, ndiyo maana akaishurutisha simu ya Miriam kumletea mrejesho wa sauti zote zilizokuwa zinasikika karibu kwa kupitia ‘application’ aliyokuwa ameipakua.
Hawakujua Jona alikuwa ‘amewapelekea’ Miriam, ila wampelekee taarifa pasipo jasho. Na alikuwa anafanikiwa hilo!
Akiwa ametulia chumbani kwake, alikuwa anasikiliza yatukiayo kwa njia ya ‘earphone’. Akajiuliza, je na yeye azuke eneo ambalo Nade ataenda kukutana na mwanaume yule anayedaiwa ndiye kipenzi cha Miriam kwa sasa?
Hakupata jibu haraka. ** Ujumbe ukaingia kwenye simu ya Kinoo – kweng! kweng! – kweng! kweng!
Mwanaume huyo alikuwa amejilaza kitandani akiwa amevaa nguo ya ndani tu. kwa mujibu wa saa yake ya mkononi ambayo alikuwa ameiweka juu ya meza, ilikuwa inasema ni saa nne na robo.
Na ama kwa hakika, hii ilikuwa ni mojawapo ya siku nadra sana kumwona Kinoo hajavalia kibodi chake cheusi. Kifua chake kilikuwa kipo nje kinahema akiwa amelowea usingizi.
Hakusikia sauti ya mlio wa ujumbe. Ila ujumbe huo ukajirudia mara mbili, na baada ya muda kidogo simu ikaanza kuita. Kinoo akamka na kutazama. Namba ngeni! Akajivuta kupokea akijiuliza ni nani huyo amsumbuaye.
“Hallow!”
“Hallo, Sarah hapa. Unanikumbuka?” sauti ya kike iliuliza kwa pupa. Kinoo akaguna akijaribu kuvuta kumbukumbu. Sarah? … Saraaah…
“Yule mfanyakazi wa marehemu Bite!” Sarah akamkubusha. Sasa Kinoo akamkumbuka. Alikuwa ni mmoja wa wale mapacha wawili aliwaona kwenye kikao cha siku ile.
Amepata wapi namba yake na alikuwa anataka kumwambia nini? Akajiuliza upesi akijtengenezea kitako. Sarah akamwambia juu ya mauaji ya Mudy. Kinoo akashtuka sana! Sarah akamwambia na mpaka kuzikwa alishazikwa. Kilichomfanya akampigia ni kutomuona msibani.
Kisha simu ikakata! Kinoo akafanya mpango wa kuongeza salio alafu akamtafuta tena Sarah na kumuuliza juu ya makazi yake. Sarah akamwelekeza na Kinoo akamuahidi kwenda kumtembelea muda si mrefu. Haitazidi lisaa.
Kinoo akajiandaa, kwa kutinga kibodi chake cheusi na suruali ya jeans, akabebelea bunduki ndogo na kisha kujipaki kwenye pikipiki yake kubwa na safari ikaanza. Huko barabarani kulikuwa kuna magari machache, muda wa foleni ulikuwa umeshapita.
Hakuchukua muda mrefu sana mpaka kuwasili alipoelekezwa na Sarah, maeneo ya Sinza Palestina. Akakuta gari, VX ya grey, nje ya makazi hayo.
Gari hili halikuwa jipya machoni. Akatafakari kwa muda mfupi na jibu akalipata, aliliona siku ile ya kikao! La nani?
Lilikuwa ni gari la Brokoli! Akili yake ikalipuka. Haraka akaficha pikipiki yake ubavni mwa nyumba na kulifuata gari lile karibu. Akatambua limekuja hapo muda si mrefu. Lilikuwa na joto kubwa.
Basi akasogelea dirishani ambapo angeweza kusikia chochote kitu toka ndani. Alikuwa na hamu ya kujua nini kimemleta Brokoli hapo. Walikuwa na ajenda gani wanayojadili?
Kwa akili ya Kinoo akafahamu fika kuwa ujio ule wa Brokoli ulikuwa ni wa ghafla. Laiti kama Sarah angelikuwa anaufahamu, basi angelimtaarifu.
Akatazama ndani asione kitu, ila akasikia sauti ya Brokoli ikinguruma. Maneno mengi hayakuwa anayasikia vizuri. Ila kwa sauti na namna yalivyokuwa yanatamkwa, yalikuwa ni maagizo ama matisho. Akili ya Kinoo ikasema vivyo.
Kwa dakika kama tano mbele, akasikia sauti ya vishindo vya miguu inasogea. Haraka akajificha na kuchngulia. Akamwona Brokoli aliyekuwa amevalia Kaunda suti ya kahawia akiingia kwenye gari na kuhepa.
Akatoka mafichoni na kwenda kukutana na Sarah. Alikuwa ameketi sebuleni akilia. Macho yake yalikuwa mekundu na nywele zake hazikuwa mpangilioni. Sasha hakuwepo, yeye alisafiri.
Kinoo akamuuliza kwanza juu ya ujio wa Brokoli hapo, haswa muda huo na kwanini analia. Sarah akamwambia ya kwamba ameacha kazi, na hataki tena! Akiwa anapaliwa na kilio hakuwa anaongea vema.
Kinoo akawa ana kibarua cha kumbembeleza.
“Amesema hataki kuona yeyote yule anasumbuka wala kusema chochote kuhusu kifo cha Mudy. Amefuatilia polisi na amewaachia kesi huko. Nimemwambia naacha kazi, akaniambia niache na kila kitu. Asije akasikia nimesema chochote kinachohusu ofisi. Nikithubutu, nitakiona cha mtema kuni!”
Kinoo akastaajabu. Na pamoja na Sarah wakamshuku Brokoli kuhusika na kifo cha Mudy. Na hata vile vile mkono wake utakuwemo kwenye kifo cha Bite.
“Vifo vyao vinafanana. Nahofia nisije nikawa anayefuata,” alisema Sarah akilowanisha macho yake kwa machozi.
Akamwonya na Kinoo kuwa hayupo salama, inabidi awe mwangalifu sana.
“Kuna taarifa amesema Mudy alizichukua kule ofisini na kumkabidhi mtu mwingine, jina hakumtaja. Na taarifa hizo ni nyeti. Bila shaka mtu huyo atakuwa ni wewe.”
Kinoo akakiri. Na akamwambia wamefuatilia nyaraka hizo na kugundua zina mahusiano na shirika fulani, tawi la kampuni kubwa ya kichina. Hapo Sarah akagutuka na jambo.
“Wachina?” Akauliza.
“Ndio, wachina. Unawajua?” Kinoo akatia swali.
Sarah akasema hawajui ila alikuwa anawaona mara kadhaa pale ofisini wakija kuteta na Bite. Na hata kwenye baadhi ya vikao walikuwa wanahudhuria. Ila hawakuwahi kujua wanahusika na nini.
“Hatujawahi kupewa mrejesho wa vikao vyao. Walikuwa wakivifanya kwa siri,” alisema Sarah. “Kikao cha mwisho wachina hao walikaa pamoja na Bite na Brokoli, ndipo likapita juma moja na Bite akauawa.”
Kinoo akamuuliza Sarah kama kuna chochote anachokijua baina ya pande hizi mbili, wachina na Bite. Walikuwa wana mahusiano gani na nini kiliwaunganisha. Sarah akasema hajui lolote zaidi ya wachina hao kuwa ‘partners’ wa mbali.
Kwa usalama, Kinoo akamshauri aondoe makazi yake hapo maana hawezi jua nini Brokoli amelenga kumfanyia. Sarah akasema hana pa kuelekea. Hana makazi mengine mbali na hayo na ndiyo hivyo kazi ameshaikataa.
Kinoo akapendekeza akakae kwake kama hatojali. Sarah akakubali baada ya mafikirio kidogo. Akabeba nguo zake chache alafu wakaondoka na Kinoo. *** Baada ya Jona kutoka mezani kwake, alikwapua ndoo moja ya bati iliyojaa maji, akaongozana nayo mpaka stoo iliyopo nje. Akafungua mlango na kuwasha taa, kukawa na mwanga!
Ndani ya stoo hiyo iliyokuwa na vitu vichache, alikuwa amelala Panky humo akiwa amefungwa miguu na mikono. Kichwani mwake alikuwa na majeraha yaliyoacha kutoa damu.
Jona akammwagia maji kumwamsha. Panky akakurupuka na kutoa macho kumtazama Jona.
“Muda wa kulala umeisha,” Jona akasema akichuchumaa na kumtazama Panky kwa ukaribu. Mwanaume huyo alikuwa amevimba upande wake wa kushoto wa uso.
Jona pasipo kupoteza muda akamuliza ni nini alikuwa anataka kwake na nani amemtuma. Aliyauliza hayo kwa kujua mtu huyo hatasema, na hata mwishowe anaweza akafanya jaribio la kujimaliza kwa kuunyofoa ulimi.
Kama ilivyotarajiwa, Panky akaleta ubishi. Hakuwa radhi kusema chochote kile na yuko radhi kufa. Jona akaendea kidumu cha maji cha lita tano, alafu akachomoa leso ya kufutia jasho mfukoni na kuifungia usoni mwa Panky.
Taratibu akaanza kumwagia maji juu ya leso hiyo, akihakikisha maeneo ya pua na mdomo yanapata maji ya kutosha. Panky akahangaika kuhema. Kila alipovuta pumzi akawa anavuta maji puani na mdomoni.
Akapaliwa na kupata shida mno!
Jona akabandua leso usoni mwa Panky na kumuliza kama yupo tayari kuongea ama lah. Kabla Panky hajajibu akakohoa sana na kuhaha kutafuta pumzi. Lakini akasema hayupo tayari kusema kitu!
Jona asiongee sana, akarudia zoezi lake mara tatu. Panky akashindwa kuvumilia na mara akaanza kuhororoja. Akasema ametumwa na mkuu wake kuja kummaliza.
“Kwasababu gani minimalize?”
Panky akasema hakuambiwa kwa sabab gani amalizwe, ila agizo tu ya kwamba amalizwe. Zaidi ya hapo hakuna anachojua. Yeye ni mtu wa kuagizwa tu na kwenda kutenda.
Jona akamuuliza juu ya makao ya mkuu wake na anajishughulisha na nini. Panky akamtaja mkuu wake kwa jina moja la Sheng’ akisema ni mfanyabiashara wa vipuri vya magari.
Jona akakumbuka jina hilo la Sheng’. Alikuwa ndiye yule mshirika ambaye mke wa Fakiri alimweleza. Akamuuliza Panky juu ya mauaji hayo, Panky akasema hayafahamu. Hapa Jona akapata maswali, Sheng’ anajihusisha na biashara ngapi? Na imekuaje Panky akasema mambo hayo kwa wepesi hivyo tofauti na Bigo ambaye aliamua kujiua?
Mfukoni akatoa kitambulisho cha kura cha Panky, leseni na makaratasi kadhaa. Akayatazama kwa muda kidogo, kabla hajamuuliza Panky kama anajua lolote kuhusu ‘Pumzi ya mwisho’.
Panky akasema hajui kitu. Jona akahisi anamdanganya. Akamwambia juu ya Bigo na kumgusia juu ya kikundi hicho kuhusika na mauaji. Panky akakiri, lakini akasema yeye afahamu kitengo hicho japokuwa inawezekana kikawa kipo.
“Kuna vikundi vingi ndani yetu, na kila kikundi kina majukmu yake ya kuyatimiza,” alisema Panky ndani ya kamba.
“Na wewe upo kikundi gani kati ya hivyo?” Jona akauliza. Panky akamwambia yupo kwenye kikundi cha ‘Space button’. Kikundi kinachohusika na mambo ya teknolojia, haswa udukuzi.
“Sasa ikawaje ukatumwa kummaliza mtu na ingali si kazi yako?” Jona akauliza.
“Hii ni adhabu nimepewa kwasababu ya kufeli kufanya vema kazi yangu iliyopita. Punde unapokosea, huwa unauawa. Nimetumwa kukumaliza kama namna ya kusahihisha makosa yangu. Ikishindikana basi nifie huko huko kama adhabu yangu inavyosema.”
Jona akafahamu kwanini mateka hyo ameongea kwa urahisi tofauti na Bigo. Hakuwa mtu anayehusika na mauaji bali wa kukaa mbele ya kioo cha tarakilishi. Hata mafunzo ya kujilinda hakuwa nayo na ndiyo maana hakumpatia changamoto pindi anamtia nguvuni.
Lakini Jona akataka kujua ni kosa gani ambalo Panky amelifanya kupelekea kupewa adhabu kama hiyo. Panky akamweleza ni upotevu wa faili moja muhimu sana kwenye mtindo data wao. Faili ambalo hajajua limepoteaje mpaka muda huo.
“Kwanini unaniambia yote haya?” Jona akauliza. Panky akashusha kwanza pumzi yake, na kusema kwa huzuni.
“Najua naenda kufa tu. Angalau nimpe mtu mwanga ama mahali pa kuanzia kuukata mbuyu huu … kama si na wewe, basi nitamalizwa na mkuu wangu. Sina haja ya kufa na taarifa hizi.”
Jona akamwambia hana tatizo naye, atakapopata anachokihitaji, yupo radhi kumwachia. Panky akatabasamu na kutikisa kichwa chake.
“Hata kama ukiniacha hai, sitadumu. Hamna namna ya kumkimbia Sheng’. Hata uwe wapi atakutia tu mikononi na kukumaliza.”
Panky akaongezea ya kwamba pindi unapoingia ndani ya mfumo wa Sheng’, familia yako yote anakuwa anaijua. Watu wako wa karibu na marafiki zako. Ni labda ajue umekufa, na si hai akakukosa!
“Watu kadhaa walishawahi kutoroka, wengine wakitaka kuacha kazi kwa hiyari. Hakuna aliyebakiziwa uhai hata mmoja! Kwa Sheng’ kuna kuingia tu, mlango wa kutokea haupo. Na utakapoulazimisha kuujenga ukutani, basi utalipia gharama zake.” . Jona hakuona haja ya kuendelea kumweka Panky mule stoo kwa ushirikiano wake alioutoa. Akamfungua kamba na kwenda naye ndani alipomkabidhia nguo kavu na nadhifu. Wakaendelea kuongea kwa muda kidogo Jona akipeleleza baadhi ya taarifa.
Panky pasipo kumficha akampatia Jona zile azijuazo. Namna gani alikuwa anatenda na kumsaidia Sheng’ kukamata Tanzania nzima, Afriika Mashariki, na hatimaye Afrika nzima. Namna gani wanavyokusanya data toka sehemu nyeti mbali mbali na kumkabidhi Sheng’ kwa ajili ya kazi zake binafsi atakazogawia vitengo vingine.
Kwa maelezo hayo, Jona akapata uelewa namna gani Panky alivyokuwa na uwezo wa kucheza na tarakilishi kwenye kila kona. Namna gani ujuzi wake ulivyokuwa mkubwa kwenye kunyambulisha taarifa, kutengeneza na kuzipoteza.
“Kama kuna taarifa ama data hatari kwa Sheng’, na taarifa hiyo ipo kwenye mashine ama tarakilishi ya mtu yeyote yule, basi ni jukumu letu kuipoteza. Tunatengeneza virusi na kuvituma kwa mtandao kama mashine ipo mbali. Virusi hao watakula mafaili yote watakayokuta humo na kiacha mashine tupu!”
Kitengo hicho hicho cha Space Button ndicho kinahusika na ukusanyaji wa taarifa popote pale ilipo kwa njia za kisasa aidha mwenye taarifa anataka ama hataki. Kama kuna mkataba ambao Sheng’ anautaka, na upo mtandaoni ama kwenye tarakilishi ya mhusika yeyote ule. Wakimtambua wataupata!
“Sheng’ ana mikataba yote ya ujenzi, madini, ardhi na kila kitu. Ana taarifa za mawaziri, na wabunge. Ana taarifa za taasisi kubwa kubwa, yote hayo yakiwezekana kwa kupitia kitengo hichi cha Space Button.”
Pia kwa kupitia mkono wa kitengo hicho, huwa wanabambikizia watu kesi kwa kuwawekea vitu ndani ya tarakilishi zao ama kwenye tovuti zao. Kutengeneza ‘application’ mbalimbali kwa ajili ya kufanyia kazi za Sheng’.
Jona akamuuliza kama kuna uwezekano wowote wa kupata data na taarifa zilizopo kwenye ‘vault’ ya Sheng’. Panky akamwambia kitu hicho hakiwezekani na hakiwezi kufanywa na mhsika yeyote yule wa Space Button kwasababu imewekwa katika usala sana.
“Kufungua Vault ya Sheng’ utahitaji alama za vidole gumba vya wahusika wote wa Space Button, na utahitaji code nne ambazo ni Sheng’ peke yake anazifahamu.”
Maelezo hayo yakamvutia sana Jona. Kichwani kwake haraka akapata wazo la kumtumia Panky katika kazi zake. Alitafakari ni kwa namna gani ujuzi wa mwanaume huyo utakavyoweza kukamilisha kazi zake kwa ufanisi zaidi.
Lakini akahofia, bado Panky hakuwa mtu wa kumwamini kiasi hicho. Bado alihitaji kumpekua na kumsoma zaidi. Na pia kama ataridhia kufanya naye kazi, maana ni jambo la hiari, si lazima.
“Unaona picha hii?” Jona alimwonyeshea Panky picha ile aliyochora kwa ajili ya Bite. Akamwambia hiyo ndiyo sababu anatafutwa na uhai wake unawindwa. Je ana ufahamu nayo?
Panky akaiteka picha hiyo kwa mikono yake na kuitazama kwa makini. Kuna jambo alikuwa analifikiria, wapi aliona picha ile. Kumbukumbu ikamjia, alishawahi iona siku moja kule ofisini kwao, mwenzake akiwa anaishughulikia.
“Sijui ina maanisha nini lakini nakumbuka siku moja niliwahi kuiona picha hii ofisini, na ndiyo ilikuwa inatengenezwa. Sikuwahi kuifuatilia wala kuiona tena.”
Jona akamuuliza kama anamfaham mtu huyo aliyekuwa anaitengeneza, Panky akasema anamfahamu mpaka na makazi yake. Jona akapanga waende kumtafuta mtu huyo ambaye alitambulishwa kwa jina la Marwa. Lakini kabla ya kwenda huko inabidi akakutane kwanza na yule mwanaume ambaye Nade anataka kwenda kumdhibiti kwa kuhusiana na Miriam – mke wa mheshimiwa. Kazi hiyo ilikuwa ni ya kufanywa kesho yake kwenye majira ya mchana mpevu.
***
Saa tatu asubuhi…
“Huwezi amini yule mzee ameshammaliza yule jamaa!” Alisema Kinoo aliyekuwa amebebelea kikombe cheupe cha chai. Akiwa amekaa na Miranda ambaye mkononi alikuwa ameshikilia simu yake kubwa akiperuzi.
Ni ndani ya nyumba ya Miranda, Kinoo akiwa amewasili hapo muda si mwingi. Miranda alikuwa amevalia dera, nywele zake zikifungashwa na kiremba cheusi.
Kinoo alikwa hapo kumhabarisha juu ya kifo cha Mudy, mwanaume ambaye amewapatia nyaraka zile za kampuni ya umeme wa jua.
Miranda akashangazwa na taarifa hizo. Kifo cha Mudy kilikuwa ni ishara kwamba na wao, ambao wanamiliki nyaraka hizo, wanaweza wakawa ndiyo ‘tageti’ inayofuatia.
“Ni kweli,” Kinoo akamwambia. “Inabidi tuwe makini, la sivyo tutaenda na maji.”
Miranda akasonya na kubinua mdomo. Akamtazama Kinoo kwa macho ya bumbuwazi na kumwambia hawana haja ya kuishi kama digidigi sababu ya Brokoli. Kama ameanzisha vita, basi hawana budi kupambana kabla haijatoka nje ya mikono yao.
“Tuchunge ngamia huyu asije akawa mkubwa kuliko banda. Endapo tukimwacha Brokoli akaendeleza saga hili, linaweza kuwaamsha majabali yaliyolala. Akuanzae mmalize.”
Kinoo akasita kiaina. Lakini Miranda hakuona haja yay eye kufanya hivyo kwani aliamini hayo maamuzi ya yeye kumuua Mudy yametoka mikononi mwake. Na kama amemuua Mudy, sababu ya nyaraka, hatakomea hapo.
Je wapo radhi kuuawa?
“Lakini sifahamu makazi yake,” akasema Kinoo. Miranda akamuuliza:
“Umetafuta ukakosa? Mbona unakuwa kama mgeni kazini.”
Kinoo akakumbuka numbani anaishi na Sarah, pengine atakuwa anafahamu. Akaacha kuulizwa maswali ya ‘kijinga’ kama asemavyo Miranda.
“Kwahiyo kwa muda gani utakuwa umemaliza hiyo kazi?” Miranda akauliza akimtazama Kinoo na macho yake aliyoyatoa kwenye kioo cha simu.
“Nahitaji siku moja tu,” akajibu Kinoo na mjadala huo ukaisha. Miranda akamwambia Kinoo kwamba baadae jioni ana miadi ya kwenda kukutana na mke wa Boka nyumbani kwake Upanga kwa ajili ya majadiliano.
Hivyo atamtaka ampeleke huko kama atakuwa na muda. Ajabu Kinoo akakataa, akimwambia ya kwamba ana kazi ya kufanya usiku. Miranda akataka kjua kazi hiyo.
“Tangu lini ukawa na kazi usiku nisijue?”
Kinoo akatabasamu kwanza kabla hajamtaarifu Miranda ya kwamba anaishi na Sarah – aliyekuwa mfanyakazi wa Bite kwasababu za usalama. Miranda akastaajabu. Alihofia juu ya usalama wao.
“Vipi kama huyo binti akakuchota taarifa?”
Kinoo akamtoa hofu. Anajua mwanamke huyo hatakuwa na lolote kmdhuru. Miranda akamtaka awe makini na macho muda wote.
“Najua umewahi kumpa hifadhi kwasababu ni mwanamke. Huna lolote!”
Kinoo akatabasamu na kukanusha pasipo kumaanisha. *** Saa nane mchana…
Gari aina ya Harrier rangi ya fedha inapaki kwenye uwanja wa hoteli, na baada ya punde Nade anashuka. Amevalia miwani meupe ya urembo. Koti dogo jeusi linalobana mwili wake. Suruali ya jeans na raba nyeupe.
Mkono wake wa kulia umebebelea simu ya Miriam. Na kama ukimtazama vizuri nyuma ya koti lake, utaona amefichama bunduki ndogo. Ila mpaka utazame kwa makini! Kitu ambacho ni kigmu kidogo kutokana na mwanamke huyo anavyovutia, utatazama vingine.
Akatazama kushoto na kulia. Akaridhia kila kitu kipo sawa. Akanyookea mapokezi, ambapo aliteta kidogo kabla ya kuelekezwa kwenda chumba namba fulani ambacho ndipo mtu anayemhitaji yupo.
Akabisha hodi.
Hakukuwa na majibu. Akabisha tena na tena, pasipo majibu. Akatazama simu kwa malengo ya kupiga kumtaarifu ‘mwenyeji’ kuwa ameshafika, yupo nje. Inabidi amfungulie.
Kwenye simu akakuta ujumbe. Kwasababu simu ilikuwa ‘silent’ hakujua ujumbe umeingia saa ngapi. Ilikuwa ni kama dakika kumi na tano zilizopita. Ina maana akiwa njiani kuja.
Na ujumbe huu ulikuwa umetokea kwa ‘My Heart Pale’, yaani yule mwanaume mtuhumiwa wa mahusiano na Miriam.
‘Jipangeni upya. Sipatikani kwa wepesi kiasi hicho. Mnapolala ndipo mimi naamkia.’
Shabash! Amejuaje? Nade akajiuliza. Akatazama kushoto na kulia kana kwamba labda mtu huyo anamtazama. Hakuona mtu. Akatoka eneo hilo na kwenda mapokezi kuulizia.
“Sijui, labda kweli kaondoka maana mie nimeingia zamu muda si mrefu,” alijibu mdada wa mapokezi. Nade akasonya. Itakuwa mwanaume huyo amegutuka na sauti yake, akawaza.
Lakini mwanaume huyo akampatia mawazo Nade. Atakuwa ni mtu mwerevu, ama mwenye uzoefu na mambo haya. Anajihusisha na nini?
Akatoka nje ya hoteli akiendelea kutazamatazama na kuwaza kichwani. Akafungua gari na kuzama ndani. Lakini kabla hajawasha chombo, akahisi kitu cha baridi shingoni, na amri:
“Tulia hivyo hivyo!”
Sauti hiyo ya kiume ilikuwa ngeni kwa Nade. Hakujua ni nani huyo, akapapaswa na woga. Alikuwa amezidiwa ujanja, akawa mpole kama maji mtungini.
“Haya washa gari na twende ntakapokuelekeza,” sauti ikaamuru. Nade akawasha gari na kutoka eneo la hotelini akipewa maelekezo na mwanaume aliyekuwa amemteka.
Sura ya mwanaume huyu ilikuwa mpya! Alikuwa ni mbaba mweusi mwenye nywele fupi zilizochanjwa ‘ways’ nne. Macho yake yalikuwa mekundu na madogo.
Mikono yake ilikuwa imepitiwa pitiwa na michirizi ya mishipa lukuki. Alikuwa amevalia shati ‘beach boy’ na suruali ya jeans iliyokoza.
Mwanaume huyu anajulikana kwa jina la Nyokaa! ‘Chalii’ wa Arusha maarufu kwa pesa za madini. Kazi ambayo aliianza tokea akiwa mtoto mdogo, ‘nyokaa’ lakini mpaka leo hii amekuwa mtu mzima, jibaba, bado anajulikana kwa jina hilo hilo maarufu.
Alimwongoza Nade mpaka nje ya jiji akiwa amenyamaza asiseme lolote. Akamwamuru asimamishe gari na kuanza kumuuliza maswali.
Akataka kujua Miriam yupo wapi na yupo na nani. Yeye ni nani na ametumwa kuja kufanya nini? Nade akalaghai Miriam yupo polisi, na yeye ni polisi pia.
Nyokaa akajua janja hiyo. Akamtishia Nade kuwa atamnyofoa uhai wake kama akiendelea na michezo yake ya kitoto!
“Sina muda wa kupoteza we malaya! Sawa? Najua Miriam atakuwa kwa Eliakimu. Na wewe utakuwa kibaraka wake. Usinifanye mimi mtoto mdogo, najua kila kinachoendelea!”
“Sasa kwanini unaniuliza kama unajua kila kitu?” Nade akauliza. Nyokaa akamzaba kofi zito lililomchana Nade lips. Akavuja damu.
“Unifahamu vizuri, mwanamke! Ngoja utanijua vema muda si mwingi na utanipa kila ninachokitaka.”
Baada ya Nyokaa kusema hivyo akamziraisha Nade kwa kumpiga na kitako cha bunduki kisogoni. Kisha akampigia simu mtu aliyemtunza kwa jina la Ninjaa.
Akamwelekeza mahali alipo na kumtaka afike hapo muda si mrefu kuna kazi wanatakiwa kuifanya. Lakini pia akamtaka ajiweke sawa kwa kuwapasha habari wengineo ya kwamba vita inaweza kuzuka muda wowote.
Basi haikuchukua muda mrefu, gari moja kubwa Hammer nyekundu ikasogea eneo la tukio. Wakashuka njemba tatu, mmoja wao akiwa ndiyo yule Ninjaa.
Watu hawa walikuwa wanafanana kwa rangi, weusi, na wenye sura angama za kazi. Miili yao ilikuwa mirefu na iliyojaa.
Wakateta na Nyokaa kwa muda kidogo, wakamchukua Nade na kumtia kwenye Hammer kisha wakalipua gari ya Nade na kuhepa!
Kitu ambacho hawakuwa wanajua ni kwamba kuna mtu upande mwingine aliyekuwa anasikiliza kila jambo. Mtu huyu aliona wakati Nade akitekwa na hakufanya jambo lolote.
Mtu huyu aliachwa kule hotelini, ila bado alikuwa anawafuatilia kwa ukaribu akitumia kifaa cha simu cha Miriam ambacho Nade alikuwa nacho mfukoni.
Mtu huyu ndiye pekee aliyekuwa anajua kama Nade ametekwa na wapi anapelekwa. Hakuwa mwingine bali Jona!
Mambo yalikuwa yanazidi kupamba moto, na hakutaka kujishughulisha kuuzima moto huu upesi mpaka aone haswa kina cha maji haya ambayo hayatakiwi kupimwa kwa mguu!
Baada ya muda mfupi Nade kuziraishwa, Jona akatimka toka mazingirani mwa hoteli kichwani mwake akiwaza mambo kadhaa ambayo hakika hakuwa na majibu nayo.
Akawaza kama kuna namna zaidi ambayo anaweza akatumia kupata zaidi mambo toka kwenye ile application ambayo ameipakua na kuitunza kwenye simu ya Nade.
Hapo akapata wazo la kumshirikisha Panky. Huenda mwanaume huyo akawa na mawazo zaidi. Ila kwanza akapitia kazini kwake kuhakikisha kila jambo lipo sawa kabla ya kunyookea nyumbani.
Huko ambapo alikuwa amemfungia Panky. *** “Sasa?” Nigaa akauliza baada ya kuchomoa sigara yake mdomoni. Macho yake yalikuwa yanamtazama Lee ambaye alikuwa ameshika tama. Walikuwa ndani ya makazi yao, Nigaa amekunja nne, pakti mbili za sigara zikiwa zimekaa pembeni.
Lee alikuwa anatazama televisheni ila macho yake yakizama fikirani.
“Inabidi leo twende. For once and for all, nijue moja!” Akasema Lee.
“Kazi ndogo sana hiyo Lee. Siyo ya kuumiza kichwa kabisa. Si unajua huyo manzi anapoishi?”
“Ndio.”
“Na huyo famba?”
“Ndio.”
“Sasa kuna nini hapo? Tukiwapata tunawanyonya macho! Hawaweza wakatuletea pigo za kifala fala!” Akasema Nigaa alafu akapiga pafu nne za sigara na kuchafua chumba kwa moshi.
“Kwanini tusiende sasa hivi? Naona kama tunakawia,” Nigaa alisema akitabasamu. Lee akatikisa kichwa na kumwambia wavute vute kidogo. Wakiwahi sana wataenda kukawia huko.
Ulikuwa ni muda wa majira ya saa tatu na nusu hivi, Lee alitaka wavute mpaka majira ya saa nne nne, angalau viwanja vinakuwa vimefunguliwa ama kujaa jaa watu.
Lee alimtaka Nigaa wanywe na kuvuta kwani hakutarajia kama angalikuwepo hai kwa muda huo. Hakutegemea kama angelitoka salama toka chumba cha mkuu.
“Sikuamini alipopiga risasi zile pembeni. Niliposikia mlio wa silaha nikajua nimeshakwesha. Niliposikia kauli ya kupewa nafasi ya mwisho ndipo nikajua bado nipo duniani, na ninahema.”
“Una bahati sana, Lee,” akasema Nigaa. “Mkuu anajua fika akikumaliza basi naye hatapata karatasi hiyo. Wewe ndiyo njia pekee na kuu ya kupata hiyo karatasi.”
“Sidhani,” Lee akasema akitikisa kichwa. “Ni mara ngapi anamaliza watu wakiwa kwenye misheni kubwa na nzito kisha anawaweka wengine? Nadhani siku yangu haikuwa imewadia.”
“Unajua ni mara chache sana Mkuu anampatia mtu nafasi ya pili?” Akasema Nigaa. Lee akakubaliana na kauli hiyo. Kwake ilikuwa kama ngekewa!
Basi muda ule ambao walikuwa wanaungojea, ukawadia. Muda wa kwenda kufanya tukio. Wakajikusanya na kwenda kwenye gari mpaka kwa yule mwanamke, Glady. Ila hawakumkuta!
Walikuta mashoga zake wawili ambao walisema Glady ametoka muda si mrefu. Kwahiyo ikabidi Lee aongoze mpaka kule klabu alipomkuta mwanamke huyo.
Huko napo hawakumkuta. Lee asife moyo akanyooshea usukani kuelekea viwanja vile ambavyo Glady alimpeleka kumtazama yule mwanaume wakianzia na Maisha.
Bahati huko wakamwona mlengwa wao. Alikuwa na mwanaume fulani hivi mrefu katika mazingira ya kimahaba wakiketi kochini. Lee akasonga na kumnyaka bega mwanamke huyo, akamtaka atimize kazi yake.
Alah! Kumbe yule mwanaume aliyekuwepo naye ndiye yule yule wanayemtafuta. Lee akajikuta anatabasamu na kuangua kicheko kabla hajamwambia Nigaa kwamba siku hiyo imekuwa nzuri maana wamewakuta walengwa wao wote kwa mkupuo.
Mwanaume yule kutaka kuonyesha umwamba, akanyanyua chupa ambamizd nayo Lee kichwani. Haki hakuamini kilichotokea! Mkono wake ulidakwa upesi na mguu wa Lee, alafu ukakunjwa na kuvunjwa. Chupa ikadondokea chini!
Mwanaume yule akapiga sana kelele za maumivu. Na kumbe wenzake hawakuwa mbali. Haraka wakasogea karibu. Wanaume wawili warefu, wakijiandaa kwa kubebelea chupa mikononi.
Kwa namba ambavyo wanaume hawa walivyokuwa wanaogopeka, hata mabaunsa hawakuthubutu kuwazuia zaidi ya kuwaomba waachane na huyo mchina na mwenzake kabla hawajaaribu mambo.
Ila hawakusikia. Walitaka kuonyesha ubavu wao. Hawakutaka kudharaulika! Kila mmoja akajigawa kumfuata wake, mmoja akienda kwa Lee na mwingine Nigaa.
Watu wakapisha uwanja hapo klabu na kubakia wakitazama pambano. Ikiwemo hata na mabaunsa wenyewe wanaohusika na ulinzi.
Bwana we! Wale wanaume wakaonjeshwa joto ya jiwe! Hawakufurukuta wala kufanya kitu, teke na ngumi zao zilikuwa kama mvua za vuli zikapita! Chupa walizokuja nazo zikawakata wenyewe na kuwaacha wakivujilia damu lukuki!
Lee akamfuata yule mwanaume kochini na kumuuliza juu ya karatasi yake. Mwanaume yule akiwa bado ameshikilia mkono wake uliokunja nne, akasema ipo nyumbani!
Lee na Nigaa wakambeba na kwenda naye nyumbani. Wakapata nyaraka yao.
“Kuna yeyote uliyempatia hii karatasi?” Lee akauliza.
Mwanaume akatikisa kichwa upesi.
“Hapana hapana … hakuna!” Lee na Nigaa wakaondoka zao. Lee asipoteze muda akanyookea kwa mkuu na kumkabidhi karatasi ile. Mkuu akaikagua na kuridhika. Ila naye akaguswa na swala la usiri wa nyaraka ile.
Akaulizia. Lee akamwambia bado ni ya siri. Ila bado mkuu akataka akahakikishe jambo hilo kwa ufasaha zaidi. Lee akakubali na kisha akaenda.
***
“Umependeza sana,” alisema Mke wa Boka akimtazama Miranda kwa matamanio.
“Ahsante sana!” Miranda akapokea sifa kwa tabasamu pana huku akijitazama tazama.
Akakaribishwa kwenye sebule kubwa kama ukumbi. Hapo kulikuwa kuna viti virefu vikiambaa ambaa na sebule. Viti hivi vilikuwa vina rangi ya kupendeza viking’arisha sebule.
Sebule ilikuwa inametameta kwa samani za bei ya juu! Palikuwa panavutia kuvunja shingo ya mgeni kuangaza angaza.
Miranda asidhulumu macho yake akatazama na kupekua.
Kinywaji kikaja na hata chakula cha usiku. Wakiwa wanakula wakaendelea na kuteta mambo yao kuhusu urembo na ulimwende. Wakajadili kwa muda wa kama lisaa limoja.
Wakakubaliana Miranda kuwa balozi wa kampuni ya urembo ya mama huyo. Atakuwa ndiye msemaji mkuu na atahusika na kuwakilisha kampuni hiyo maeneo mbalimbali.
“Kesho ama keshokutwa tunaweza tukawa na utambulisho mbele ya vyombo vya habari. Utakuwa na muda na utayari?” Akauliza Mama Boka.
Kabla Miranda hajajibu, akasita kwanza. Alihofia endapo akijianika kwenye mtandao na kwenye televisheni inaweza ikamletea tatizo. Maadui zake watajua na itakuwa kana kwamba amewachokoza.
Hapa palihitaji hekima. Na hekima kwasababu ya asili ya kazi zake. *** Akamwambia mama Boka ampatie muda kidogo. Ila kumbuka interview ilitakiwa kuwa kesho ama keshokutwa. Basi ikalazimika isogezwe mbele kukidhi haja ya Miranda.
“Kwahiyo itakuwa lini?” Akauliza mama Boka. Miranda napo akakosa jibu la kusema. Bado akarejea kule kule. Nitakwambia.
Mama Boka akampatia mwanya ila akamtaka awahishe maana hamna muda zaidi. Miranda akaafiki kichwani akipanga kwenda kumwambia BC hilo jambo aone atasemaje.
Basi wakahitimisha hilo jambo na kwendelea kuongea zaidi na zaidi. Usiku ulikuwa unakua, na kwa Miranda hakuwa na presha kwani nje usafiri ulikuwa unangoja.
Kwenye majira ya saa tano, waziri akarejea nyumbani. Akastaajabu kumkuta Miranda hapo mpaka muda huo, akamsalimu na kumkonyeza.
Akatamani sana aupate muda binafsi na mwanamke huyo ila haikuwezekana maana mkewe alikuwa hapo kila sekunde akitazama kila jambo. Ikabidi Waziri awe anamtumia ujumbe binti huyo wakati wakiendelea kuongea.
Chating zao:
“Umependeza love.”
“Kweli? Asante…”
“Karibu. Mpaka nikasisimka.”
“Lol acha uongo bana..”
“Kweli nakuambia, sasa vipi lile jibu langu mrembo?”
“Mmmm umeanza nawee…”
“Niambie bas na mie nile vitamu. Mwenzako nangoja na hutaki kunijibu.”
“Ntakujib usjali.”
“Lini sasa?”
Kimya kidogo.
“Kesho tunaweza tukakutana?” Ujumbe wa Boka ukauliza. Ila mara hii Miranda hakutaka kujibu, akajifanya amaeupotezea. Akaaga aende.
Boka na mkewe wakamsindikiza akajipaki garini na kwenda. Akiwa anatembea barabarani akawa anasoma jumbe za Boka ambazo bado hazikukoma kuingia.
Akatabasamu na kuzipuuza. Si kwamba hakuwa anaziona, la hasha, bali alikuwa anatengeneza mazingira ya kuonekana si mtu wa ‘bei chee’.
Mpaka anafika kulikuwa kuna jumbe kama nane za Boka. Ujumbe wa mwisho ukiwa ni wa kuingiziwa pesa, Boka akiwa ametuma shilingi elfu hamsini!
“Nakutumia nauli ya kesho basi tukutane mida ile ile kule kule sawa?”
Ulisema ujumbe wa pili tokea mwishoni.
Miranda akajikuta akitabasamu. Napo hakujibu ujumbe huo. ***
Saa saba kasoro, usiku…
Sauti ya vibofyeo vya tarakilishi inagonga gonga na kuacha. Kutokana na ukimya uliokuwepo ndani ya chumba na majira haya ya usiku, sauti hiyo inasikika vema.
Mbele ya tarakilishi alikuwapo Jona na Panky.
Panky alikuwa mbele akikodolea kioo cha tarakilishi kana kwamba anatafuta jambo. Jona yeye alikuwa amesimama kwa nyuma mkononi akiwa amebebelea kikombe cheupe cha chai.
Hii kazi wameanza tangu muda. Jona alikuwa amechoka, akipiga piga mihayo, ila Panky yeye alikuwa fiti. Uzoefu wake kukaa kwenye viti muda mrefu, mbele ya tarakilishi, ulikuwa unamsaidia.
Mara Panky akatabasamu na kusema:
“Tayari! Kila kitu kipo sawa sasa!”
Akamweleza Jona kwamba kuanzia muda ule wanaweza wakai – trace ile simu ya Miriam na kujua wapi ilipo. Kama haitoshi hata mawimbi ya sauti yatakuwa bora zaidi.
Na punde ataweza hata kuiwajibisha kuchukua picha ama video!
Jona akafurahi sana na kumpongeza. Na kuhakikisha hilo akaanza kusoma ramani ya wapi Nade alipo. Akapaona! Akaweka earphone masikioni, mawimbi yalikuwa yametulia kiasi kwamba akawa anasikia kitu kilichokuwa kinafanyika kwa mbali!
“Itakuwa wana party,” alisema Jona.
“Yah! Kwa nje ya nyumba huko,” Panky akajazia taarifa. Mbali na muziki huo uliokuwa unasikika kwa mbali hakukuwa na sauti nyingine mbadala.
Mazingira yalikuwa yametulia mno.
“Usijali, hauna haja ya kusikiliza muda wote. Pindi kutakapokuwa na sauti yoyote karibu, itataarifu simu yako kwa njia ya vibration, kwahiyo utasikiliza.”
Utaalamu huo ukamsisimua sana Jona. Alivutiwa nao na akataka kujua historia ya Panky. Ametokea wapi na ilikuaje akajiunga na Sheng’.
Panky akamjibu kifupi, tamaa ya pesa. Alikuwa ametoka mafunzoni na hakuwa na fedha ya kulelea familia yake maskini. Sheng’ akamuahidi mshahara mnono, lakini pia masomo zaidi.
“Ila hapo mwanzoni sikujua kama Sheng’ anajihusisha na biashara haramu. Hata serikali haifahamu. Ni mtu mkubwa na mfanyabiashara wa mambo mengi, mambo ambayo anayatumia kama mwamvuli kukingia biashara zake zimwingiazo pesa zaidi …
Hata pale nilipokuja kugundua, nilikuwa tayari nimeshachelewa. Sikuweza kutoka tena.”
Jona akamuuliza kama angelipendelea kupata fursa ya kutoka, Panky akatabasamu na kujibu, haijalishi namna gani anataka kutoka huko, hilo jambo haliwezekani.
Kwa sasa anamfanyia kazi Sheng’ kwasababu ya uhai wake na wa familia yake tu. Isingelikuwa hivyo angeshalifanya mambo mengine ya maana.
“Hakuna jambo lisilo na kikomo,” Jona akamwambia. “Na pengine haukujaribu vya kutosha kuupata mlango. Mimi naamini inawezekana wewe kutoka.”
Panky akataka kujua ni kwa namna gani hilo linawezekana. Akatega masikio na macho. Jona akamwambia wao ndiyo watu wa kufanikisha hilo na si wengine.
Lakini Panky alikuwa anahofia. Alichokuwa anahofia si yeye, bali mke na mwanaye Nasra.
“Ndiyo kwanza anatimiza miaka minne. Nisingependa afe kwasababu yangu.”
Jona akamhakikishia hakuna atakayekufa. Lakini inatakiwa wawe werevu mno kufanikisha hilo. Jambo kubwa ni kwamba inawezekana kama wakitia nia.
“Mimi nina mpango,” Jona akasema. “Ili kumdhibiti na kummaliza Sheng’ inabidi mtu fulani awepo ndani ya system yake. Mtu huyu ajue yanayoendelea huko. Kila kinachofanyika. Alafu awepo na mtu wa nje, ambaye atakuwa anachanga karata kutengua mipango.”
“Ni hatari,” akasema Panky. Alihofia sana lakini Jona akamwambia hiyo ndiyo njia pekee la sivyo atakuwa mtumwa milele, na misha yake na ya familia yake yakiwa rehani.
“Umetumwa kunimaliza. Wakijua mimi sijafa, watakumaliza wewe. Inabidi uende kwa Sheng’ na umwambie umenimaliza. Nami nitapotea kwa muda fulani. Wakati huo wewe ukiendelea kufanya kazi.”
Jona alimwambia Panky kwamba hiyo ndiyo njia pekee ya yeye kuishi na kuwa salama tangu hajamaliza kazi aliyoagizwa. Lakini pia ndiyo fursa ya wao kufanya jambo kwa urahisi kwasababu mosi, Panky atakuwa amerudi ndani ya system, pili, Sheng’ hatahangaika na Jona kwa kujua amemmaliza.
“Ngoja tuone,” Akasema Panky.
“Kumbuka muda unaenda, inatakiwa urejeshe ripoti kwa Sheng’,” Jona akakumbusha.
Panky akashusha pumzi ndefu.
***
Saa kumi na moja asubuhi …
Kinoo anarejelea ujumbe alioundika na kuutunza kwenye simu jana yake wakati anaongea na Sarah.
‘Nyumba moja kubwa nyeupe yenye geti jekundu. Ukuta wake una sinyenge kwa juu zilizosokotwa sokotwa.’
Aliposoma ujumbe huo akatazama nyumba iliyo mbele yake. Akaona vigezo vilivyomo ndani ya ujumbe vinafanana.
Mwanaume huyu alikuwa juu ya pikipiki yake kubwa. Kichwani amevalia kofia ngumu, mwilini kibodi cheusi na suruali ya jeans na raba – All star.
Jana yake usiku, pasipo Sarah kutambua, Kinoo akamchunguza juu ya makazi ya Brokoli. Mwanamke huyo akabwabwaja na kumjaza Kinoo taarifa. Kinoo akarekodi kwenye ujumbe kana kwamba alikuwa anachat na mtu.
Sasa alikuwa mbele ya nyumba ambayo alihisi wazi ni ya Brokoli kwa mujibu wa maelezo. Akazima pikipiki na kuijongea.
Kwanini wanapenda majira haya ya asubuhi?
Majira haya yana uhakika zaidi kumkuta mtu nyumbani. Muda wa kurudi usiku huwa hautabiriki, na muda wa mchana ni ngekewa!
Lakini asubuhi ya mapema, kwa wafanya kazi huwa ndiyo wanaamka kwenda makazini, wengi wao. Na bado hakujawa zogo.
Mara kaap! Kinoo akatua ndani ya uzio wa nyumba ya Brokoli. Alikuwa hapo kutekeleza jambo moja tu, mauaji! Akuanzaye mmalize.
Kabla hajafanya kingine chochote akasoma kwanza mazingira. Akagundua kuna mbwa wawili wakubwa karibia na chumba cha mlinzi!
Mbwa hao wakampatia ishara ya kwamba pale hapakuwa pa kukaa muda mrefu kwani harufu yake yaweza kusababisha zogo
Basi mfukoni akatoa mfuko mmoja soseji. Akauchanja na meno na kuuweka chini, alafu haraka akaizunguka nyumba.
Punde mbwa wakasikia harufu hiyo. Ikawapuuzisha wasisikie ya Kinoo. Wakafakamia soseji zile. Mlinzi akagutuka na kusonga karibu na mbwa apate kuona nini hicho wanatafuna.
Akaona soseji!
Kutazama vema akaona alama za viatu juu ya sakafu! Akajua wameshavamiwa. Ila haikusaidia kitu, kwani kabla hajafanya lolote, akajikuta amedakwa shingo na kuvunjwa!
Chini akadondoka akifuatiwa na mbwa wake. Kinoo sasa akaachiwa mwanya wa kufanya mambo yake taratibu pasipo papara. Akatega kumwona Brokoli akitoka nje.
Dakika kama kumi mwanaume huyo akatoka nje akiwa amevalia taulo na mswaki upo mdomoni. Kuna kitu alikuwa anaenda kuchukua kwenye gari lake, VX la grey.
Lakini wasaa huo ukawa wa mwisho kwake! Akajikuta amekabwa na mkono mzito. Pua na mdomo vikabanwa na kitambaa kizito chenye malighafi kama taulo.
Kuvuta kwake hewa kukawa kosa. Alivuta mara moja tu na mara mapigo yake ya moyo yakasimama! Habari yake ikaishia hapo hapo!
Kinoo akayoyoma zake akifunga mahesabu… Kwa mbali sauti za majogoo ungeweza kuzisikia zikitangaza asubuhi. Kama ilivyo ada, ndani ya jiji la Dar es salaam, magari yalikuwa yamesongamana barabarani watu wakienda makazini. Wale walioamka na kujiandaa saa kumi na moja, wao walikuwa wameshafika na huenda wameshaanza na kazi. Lakini kwa Jona haikuwa hivyo. Yeye alikuwa yupo ndani, tofauti kabisa na desturi yake ya kudamka asubuhi na kuwahi kazini. ni siku kadhaa sasa amekuwa akifanya hivyo, na sababu kubwa ikiwa ni kazi za hapa na pale ambazo zimekuwa zikitokea na kumuibia muda. Kuna muda anajikuta amerejea kwenye kazi yake ya upelelezi, maana amekuwa akiumiza kichwa kweli.
Anachofanya akiamka, ni ‘kumchek’ Jumanne na kumjulia hali, kisha anaendelea na kazi zake zingine alizozikubalia kuzivulia nguo. Kazi ambazo anajitahidi kuzikimbia na kuziepuka pasipo mafanikio.
Akiwa ameketi na tarakilishi yake, mwenyewe sebule nzima, kwenye majira ya saa mbili asubuhi, akasikia hodi inabishwa getini. Akachungulia kupitia dirisha lake, akaona uso wa mtu mmoja anayemfahamu.
Alikuwa ni Inspekta Norbert Mlanje, mwanaume polisi aliyeonana na Jona miezi kadhaa iliyopita. Mwanaume huyu akiwa ametumwa na uongozi kwa dhumuni la kumshawishi Jona arejee kazini.
Kwahiyo Jona akawa ameshabashiri kinachofuatia. Ila si vema kumwacha mgeni mlangoni, basi akaenda kuwafungulia na kuwakaribisha ndani. Walikuwa wamevalia makoti marefu ya kaki na suti za kaunda kwa ndani. Kama kawaida uso wa Inspekta Norbert ulikuwa umekatwa na mustachi mpana mweusi. Macho yake ya kijanja yalikuwa yanapekuapekua eneo la nyumba ya Jona akiwa anasonga ndani.
Wakajitambulisha, yule mpya machoni mwa Jona alikuwa anaitwa Bwire. Ni afisa wa polisi kwa cheo cha koplo. “Karibuni, bila shaka mtakuwa mna jipya.”
Norbert akasema hana jipya bali ni lile lile, ila kwa sasa ameagizwa na Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam. Anahitaji kumwona haraka iwezekanavyo, ana maongezi nyeti naye. Jona akasema ana kazi za kufanya kwa muda huo. Bwana Norbert akamsihi sana aende kuonana na mkuu muda huo kwani wametumwa kuja kumchukua. Hakukuwa na muda wa kutafakari. Kwa ustaarabu Jona akaridhia. Akajiandaa na kwenda ofisini kwa kamanda baada ya kumuaga Panky ambaye alikuwa amefungiwa ndani ya chumba. Akajipaki kwenye gari la maafisa hao na kuanza safari.
Wakiwa njiani, Norbert akawa anampeleleza Jona juu ya maisha yake. Alikuwa anataka kujua ni kwanini Jona aliamua kuachana na kazi hiyo aliyokuwa akiitenda vema, ila Jona akawa mfinyu wa taarifa. Hakutaka kujiweka bayana kiasi hicho.
Akasema ni maamuzi, na maisha aliyoyachagua.
“Bila shaka utakuwa unafanya vema huko kwenye mambo mengine. Ni wapi ulipojishkiza?” Norbert aliuliza. “Kwenye kazi mbalimbali,” akajibu Jona kisha akafunga mdomo wake. Mpaka wanafika Norbert hakuwa amekipata anachokitaka. Moja kwa moja, Jona akaingizwa ofisini kwa kamanda na kuketi, kamanda alikuwa akiongea na simu ya mezani.
Alipomaliza akamkaribisha Jona na kumjuia hali ya muda mrefu. Akamwambia amemuita hapo kwasababu kuu moja, ya kumtaka arejee kazini kwani wanamhitaji kuliko muda mwingine wowote.
“Jona, unajua serikali ilitoa pesa yake ukapate mafunzo ili uje kusaidia taifa. Tunaomba urejee na uendelee kutimiza majukumu yako. Huu ni muda ambao Taifa linahitaji ujuzi, juhudi na nguvu yako.”
Jona akaendelea kushikilia msimamo wake, hapana. Kamanda akashindwa kumshawishi kabisa, na sasa ikabidi ahamie upande wa pili wa kumpa vitisho Jona. Uso wake ulibadilika akiwa anasisitizia kile anachosema. “Jona, maisha yako kamwe hayatakuwa sawa ukiwa nje ya jeshi. Huu ndiyo wito wako na hauwezi kuukwepa. Na sisi tutakukumbusha hilo kila uchwao.” “Ahsante, Kamanda,” akasema Jona, na kuongezea: “Nitarejea jeshini siku n’takapopata maelezo ya kutosha toka jeshi la polisi juu ya kifo cha mke wangu na mtoto wangu. Siku n’takayopewa maelezo ya kina kwanini biashara yangu ilifungiwa kwasababu sizizo na mantiki. Siku ntakapopewa majibu ya kueleweka, pengine ntashawishika kulamba matapishi yangu.” Kamanda akaangua kicheko kabla hajaanza kukohoa mara kadhaa. Akatulia na kumwambia tena Jona kauli yake aliyoisema hapo awali ya kwamba maisha yake hayawezi yakawa sawa akiwa nje ya jeshi. Hakutoa maelezo zaidi, akamwambia Jona amehitimisha na siku moja atakuja kukumbuka hicho anachokisema. Jona akaaga na kwenda zake. Lakini kauli ya Kamanda juu ya maisha yake haikumwacha upesi.
Akawa anaifikiria akiwa garini na mpaka alipofika nyumbani. Kuna mawazo mabovu yalimjia kichwani, ila akayapuuzia kwa kuona muda utaongea.
Akajikuta anamkumbuka sana mkewe na mwanae kana kwamba wamefariki jana. Alipofika nyumbani, akaendea karatasi zile ambazo amemchora mkewe na mwanae. Akazitazama sana akikumbuka ‘memory’ kadhaa. Machozi yakasonga machoni. Panky akamkuta hapo, na asimsumbue akaachana naye akienda kuketi na kutumia tarakilishi. Punde Panky akamshtua na kumwambia kuna jambo la kulisikiliza. Kuna sauti ilikuwa inasikika toka eneo la tukio, kule ambapo Nade alikuwa amefungiwa. ***
“Haloo!” Mh. Eliakimu aliongea na simu akiwa amekunja sura. “Nade?” Mara akasikia sauti ya kiume. “Malaya wako uliyemtuma, tunaye hapa.” “Wewe nani?” Mheshimiwa akawahi kuuliza.
“Mimi ni yule uliyedhani ni fala kwa kumtuma Malaya wako aje kunimaliza.” Mheshimiwa akapandwa na hasira. Maneno mabovu na makali yakamtoka.
Ila aliyeongea naye akiwa ametulia, akamngojea amalize, kisha akamuuliza: “Unamtaka malaya wako hai ama lah?” Mheshimiwa akanyamaza kwanza. Swali likarudiwa. Akatishishia kummaliza mwanaume huyo endapo akifanya lolote kwa Nade. Vitisho ambavyo havikusaidia lolote lile, kwani mwishowe alinywea na kwenda sawia na mtekaji. Hakuwa na namna.
“Tutabadilishana na Miriam. Utamleta Miriam, nawe utampata mtu wako. Deal?”
Hapa pakawa pagumu kwa Mheshimiwa. Ila akajikuta hana machaguzi mengine zaidi ya kuridhia, japo kwa shingo upande. Simu ikakata.
Akabakia akiwaza haswa juu ya namna ya kufanya. Akabakia akiwaza namna gani ya kumkomboa mwanamke pekee anayemuamini.
Kazi haikwenda kabisa, na kichwa kiligoma. Akaaga na kurudi zake nyumbani. Akamkuta Miriam akiwa ameketi sebuleni anatazama televisheni. Ulinzi ulikuwa mkubwa kuhakikisha mwanamke huyo haendi popote pale.
Mwanamke huyo alikuwa amechafuka kwa majeraha. Uso wake ulikuwa umevimba, macho yake yakiwa mekundu usijue kama analia ama ameumia.
Akamuuliza juu ya yule mwanaume ambaye amemteka Nade. Miriam asiseme kitu, akamtazama na kunyamaza akiangalia televisheni. Baada ya Mh. Kurudia swali mara kadhaa akiambatanisha na vitisho, Miriam akamwambia kwa ufupi, akihangaika kuongea: “Eli, umeingia kwenye anga la wenyewe.”
Baada ya hapo hakusema tena lolote. ***
Kang! Kang! Kang!
Sauti ya chuma kilichopo mlangoni ilisikika ikilia. Mara sauti ya kichina ikatoa ruhusa na mtu akazama ndani, alikuwa Panky. Akasimama kiukakamavu akimtazama mkuu wake aliyekuwa amejaa kwenye kiti kirefu cheusi nyamanyama.
Juu mezani kulikuwa tarakilishi kubwa iliyokuwa ipo on na kunguruma. Panky aliposalimu akakaribishwa kuketi na kisha mwenyeji wake akampatia atensheni yote. Akamtazama na macho yake nyuma ya miwani.
“Nimemaliza kazi,” akasema Panky. Mkuu huyu alikuwa hawezi kuongea Kiswahili vema ila alikuwa anakisikia na kukielewa. Aliposikia kauli ya Panky, akapandisha nyusi zake kwa mshangao. Kisha akauliza kazi hiyo imemalizwa lini akitumia lugha ya kichina.
Uzuri Panky alikuwa anaelewa lugha hiyo, japokuwa naye matamshi yalikuwa yanamshinda. Ana kichwa chepesi cha kujifunza ila lugha ya kichina iligoma kunasa mdomoni.
Akaweka bahasha ya kaki mezani alafu akamsogezea mkuu wake kwa kuiburuza. Mkuu akaipokea na kufungua kutazama yaliyomo ndani.
Akaona picha tatu alizozitoa na kuziangaza kwa macho yake. Akamwona Jona akiwa amelala chini akielea kwenye dimbwi la damu. Paji lake la uso lilikuwa linachuruza damu na macho yake yakiwa yametoka nje!
Picha zilikuwa zinatisha na kusisimua kutazama.
Mkuu akatabasamu na kisha akamtazama Panky. Akampongeza kwa kazi aliyoifanya huku akiweka bayana kwamba hakutegemea kama angefanikisha hilo. Panky akamwambia alijitahidi ili kufuta makosa aliyoyafanya.
Mkuu akampongeza tena na kisha akampatia kibali cha kwenda kuendelea na kazi akimsihi Panky abakize picha zile palepale na yeye. Panky akaridhia na kwenda. Mkuu akamwita Nigaa na kumpatia kazi.
Akamwonyesha picha zile ambazo Panky alimpatia, akamwambia neno moja alilolisema kwa lafudhi ya kichina: “Hakikisha.”
Nigaa akajua nini cha kufanya na pasipo kuuliza akatoka zake nje. Mkuu akalalia kiti na kushusha pumzi. Akatafakari zile picha, ila kwa macho yake zilikuwa sahihi na si za kubandikwa kiteknolojia. Ila hakuamini uwezo wa Panky kiasi hicho. Amewezaje kitu ambacho Bigo ameshindwa?
Alitamani kujua.
“Tayari, nimefanikiwa.” Ujumbe ulifika kwenye simu ya Jona toka kwa Panky. Jona akaupokea na tabasamu alafu akaujibu ujumbe huo.
“Basi fanya kama vile tulivyopanga.”
Panky akaupokea ujumbe huo, na kisha akaujibu:
“Hamna shida,” huku akielekea eneo lao la kazi. Mbele yake kulikuwa kuna mlango mkubwa wa chuma ukiwa umepachikwa bandiko jeupe lililosomeka ‘SPACE BUTTON’. Pembezoni mwa mlango huo kulikuwa kuna kifaa cha kuandikia ‘password’.
Panky akabofya hapo mara kadhaa na mara mlango ukafunguka. Akazama ndani na kupokelewa na wenzake ambao walimkumbatia na kumkaribisha kwa bashasha. Hawakutegemea kama Panky angerejea salama.
Baada ya muda kidogo, na hali kutulia, Panky akamtafuta Marwa ndani ya eneo lao. Eneo lilikuwa kubwa lililotapakaa mashine na tarakilishi. Kwa mbali kwenye kona akamwona mlengwa wake.
Ndani ya ofisi hiyo kuna vitengo kadhaa: ukarani, graphics, hacking na coding, na Marwa alikuwa kwenye kitengo cha graphics. Yeye na jamaa wawili.
Marwa alikuwa ni mwanaume mweusi mwenye nywele nyingi na chunusi kadha wa kadha usoni. Vidole vyake vilikuwa katika keyboard akichapa jambo. Macho yake yalikuwa yamezama kwenye kioo cha tarakilishi.
Kwa kumtazama tu, alionekana yupo bize. Panky akamjongea na kumsalimu. Akajibiwa pasipo kutazamwa. Marwa alikuwa anafanyia kazi picha fulani ambayo Panky aliona inapendeza sana ikikaa ukutani.
Marwa akasimamisha shughuli yake na kumtazama Panky. Alikuwa anamwona anampotezea muda ingali ana kazi lukuki za kufanya. Akauliza:
“Una shida gani?”
Panky akatabasamu. Kisha akamwambia Marwa kuna picha fulani aliiona akiifanyia kazi, ilimvutia na angependa kuiona.
“Nafanyia kazi picha nyingi Panky, unamaanisha ipi?”
Panky akajitahidi kuielezea picha yake iliyokichwani. Marwa akamwelewa, ila akamuuliza pasipo kumtazama:
“Unajua miiko ya kazi?”
“Najua, Marwa. Usijali, Moderator hatajua,” Panky akajibu.
Moderator ni msimamizi wa mule ndani. Ni mchina kwa utaifa na kazi yake ni kuhakikisha kila mtu anafanya kazi yake pasipo kuingiliana. Kuhakikisha wafanyakazi hawapangi jambo lolote kwa pamoja mule ndani, aidha kugoma, kuharibu mashine kwa kudhamiria, ama kupanga jambo la kitaaluma likaathiri kampuni.
Macho ya Moderator yanakuwa yanaambaa muda kwa muda, mahali kwa mahali, na masikio yake yanasikiza muda wote. Ujuzi wake pia kwenye mambo ya tarakilishi na mifumo yake yote, upo juu.
Kabla Marwa hajasema jambo, akasikia vishindo vya miguu. Na mara vikakoma na sauti ikauliza:
“Kuna tatizo hapa?” sauti nyembamba yenye lafudhi ya ki-mandarin. Alikuwa ni Moderator, mwanaume mfupi mwenye nywele za wastani. Macho yake yakisaidiwa na miwani maana yameshaharibiwa na mwanga wa tarakilishi kupitiliza.
Alikuwa amevalia shati jeusi kama vile sweta likimbana mpaka koo. Pamoja na suruali pana ya kitambaa cha rangi ya fedha, na mokasin nyeusi.
“Hamna tatizo,” Panky akawahi kujibu akitabasamu. “Nilikuwa namuuliza kama angeweza kuhudhuria sherehe ya mdogo wangu.” Akasema kwa haraka akijua fika Moderator hakuwa mzuri kwenye lugha hiyo.
Kisha akanyanyuka na kurejea tarakilishi yake. Kuna kazi akawa anazifanya ila akifikiria ni kwa namna gani anaweza kumuingia Marwa. *** Baada ya maongezi yaliyokuwa yanafanyika kwa sauti ya chini chini, Mkuu, ama Sheng’ kama aitwavyo na wachache, akiwa anaongea na mwaname fulani mweusi mwenye nywele ndefu na macho madogo akiwa amevalia suti, akatikisa kichwa na kusema:
“This must be a plot.” (Huu lazima utakuwa ni mpango.) alisema kwa sauti yake ya kichina kiasi usijue kama ameongea lugha ya kiingereza. Mwanamke naye akatikisa kichwa kwa kukubali. Watu hawa walikuwa wanaongelea mauaji ya kushtukuza ya Brokoli. Nani aliyeshiriki, na pia sababu iliyopelekea tukio hilo.
Mwanamke huyu mweusi ambaye yupo hapa, alikuwa ndiye yule ambaye Brokoli alikuwa akiwasiliana naye wakati akifanya tukio la mauaji ya Mudy na hata akiwa njia kumtafuta yule ambaye Mudy amemkabidhi nyaraka, yaani Kinoo.
“The document should be fetched! Otherwise we may awake the dead demon.” (Nyaraka lazima ipatikane! La sivyo tunaweza tukaamsha jinni lililolala.) alisema Sheng’ kwa msisitizo akimwambia yule mwanamke.
Punde mwanamke huyu akasimama na kuinamisha kichwa chake. Alafu akaondoka akitembea kikakamavu. Chini alikuwa amevalia viatu vya visigino virefu lakini akitembea kana kwamba amevaa raba.
Mwanamke huyu akaendea gari lake alilolipaki nje, IST nyeupe new Model, akazama ndani na kuondoa chombo.
Kwa jina waweza kumwita Gee. *** Saa moja usiku …
Simu ilinguruma … ggrrrrrmmmm! Mara mbili kabla Glady hajaipokea na kuweka sikioni. Alikuwa amejilaza kitandani akiwa na mashoga zake wawili wote wakiwa wamevalia nguo za ndani tu.
“Vipi?” akauliza .
“Njoo hapa nje,” sauti ya kiume ikamjibu na mara simu ikakata. Wenzake wakawahi kumuuliza kama ni mteja, Glady akatikisa kichwa chake na kusema ni fala fulani aitwaye Mustapha.
Akajiveka khanga na kutoka nje. Akamkuta huko mwanaume aliyevalia ‘form six’ ya bluu na suruali nyeusi ya kadeti. Mkono wake wa kulia ulikuwa upo ndani ya POP, ameuning’iniza ukibembeshwa na kamba uliyodaka shingo.
Mwanaume huyu alikuwa ndiye yule aliyezama matatizoni na Lee kwa kushikilia nyaraka isiyo ya kwake. Glady akamtazama mkono wake uliovunjwa, alafu akamuuliza:
“Unataka nini?”
Mustapha akamwambia yupo pale kwa ajili ya kupata taarifa za yule mchina, Lee. Kwa alimchofanyia, kamwe hawezi kumwacha salama!
“Vita aliyoianzisha, kamwe haitaisha. Nitahakikisha ananijua mimi ni nani, na si kila mtu ni wa kumchezea!”
Glady akaangua kicheko.
“Mustapa, ulishindwa siku ile. Au unataka uuawe kabisa?”
Mustapha akamsisitizia apewe taarifa za huyo mchina alafu atakuja kumpatia taarifa baadae juu ya nini alichomfanyia. Glady akamwambia hana taarifa yoyote ya Lee. Alikutana naye klabuni na kuachana huko huko.
Mustapha hakuamini. Na kwa kutaka taarifa hiyo ya Lee, akamwambia Glady kwamba ile nyaraka ambayo Lee alikuwa anaitaka na kuichukua, wanayo. Na muda si mrefu watajua kuna nini ndani yake.
Glady akaagua tena kicheko. Alijua Mustapha anaongopa.
“Unatolea wapi na uliitoa?” akauliza. Mustapha akatoa simu yake kubwa na kumwonyesha Glady picha. Kumbe mwanaume huyo alikuwa amepiga picha ile nyaraka ya Lee, picha zimetunzwa kwenye gallery!
Glady akashangazwa.
“Ila we Mustapha una hatari!”
“Hii lazima itakuwa dili. Kwa namna alivyokuwa anaitafuta vile, itakuwa dili tu!”
“Sasa utaelewa nini humo na kimeandikwa kichina?”
“Aaaggh! Unadhani hakuna watu wanaojua kichina? Wachina wapo wangapi Kariakoo?”
Mustapha akamtaka sasa Glady amsaidie kupata taarifa za Lee, ili na yeye aweze kunufaika na chochote kitu kitakachopatikana humo. Taarifa hizo za Lee si tu kwamba zitamsaidia Mustapha kulipiza kisasi, bali pia zitawasaidia kujua namna gani watanufaika na nyaraka ile endapo wakiona kuna mhitaji wa yule ‘mchina’.
Jona amesimama mbele ya karatasi zake za kuchorea, anatazama jambo.
Anafungua karatasi ya kwanza na kisha ya pili. karatasi hizo zina picha ya mkewe na mwanae. Anazitazama kwa muda kabla hajapindua karatasi nyingine mpya na kuanza kuchora mchoro mpya akitengeneza msingi kwa penseli ya kawaida.
Ilikuwa ni picha ya mtoto anachora. Na hakuwa anarejelea popote pale isipokuwa kichwani kwake.
Akiwa anaendelea kuchora mchoro huo, akili yake ipo kwenye amani na macho yake yakizingatia kazi anayoifanya, mara anasikia sauti ya honi huko nje. Anasita na kujiuliza ni nani huyo. Hakuwa na miadi na yoyote, na ule ulikuwa ni muda wa usiku.
Akaendea dirisha na kuchungulia. Akaona gari kubwa, VX rangi ya fedha. Akiwa hapo hapo anatathmini, akaona kuna mtu mmoja ameshuka toka kwenye gari hilo. Macho yake nyuma ya miwani yakatambuo umbo la mgeni huyo.
Alikuwa ni Mh. Eliakimu!
Muda huo! Akastaajabu. Akateka bunduki ndogo na kuikobeka nyuma ya kiuno, alafu akaendea geti na kumkarimu mgeni. Alikuwa amebeba tahadhari zote akiwa tayari kwa lolote linaloweza kutokea.
Mheshimiwa alikuwa ameongozana na bodyguard, mwanaume mrefu mweusi mwenye misuli mipana. Bodyguard huyo akaamriwa abakie nje wakati Mheshimiwa akiingia ndani na kuketi kochini.
“Sikutegemea ujio wako, vipi mheshimiwa?”
Mh. Eliakimu akashusha kwanza pumzi ndefu. Hakuwa anajua wapi pa kuanzia. Kujileta kwake kwa Jona kulikuwa hatari kwake na kwa siri zake, ila ndiyo hivyo hakuwa na namna! Maji yalikuwa yamemfika shingoni.
“Jona,” Mheshimiwa akaita. “Achana na yote yaliyopita. Najua kuna mambo ambayo yalitokea hapa kati, nisingependa kuyaongelea kwa sasa maana si muda muafaka. Nimekuja hapa maana nina shida na ninahitaji tena msaada wako.”
Jona alikuwa kimya akimtazama. Mheshimiwa akameza kwanza mate, alafu akasema:
“Nade ametekwa, naomba unisaidie kumuokoa.”
Ni kama vile Jona alikuwa anategemea kauli hiyo kwani hakushangazwa hata kidogo. Alikunywa fundo moja la mvinyo ndani ya glasi alafu akaendelea kumpatia atensheni mgeni wake.
“Utahitaji kiasi gani?” mheshimiwa akauliza akichojoa pochi yake mfukoni.
“Sitahitaji pesa yoyote toka kwako,” akasema Jona. Na kisha akaongezea: “Ninachohitaji toka kwako ni taarifa tu ya yale unayonificha.”
“Yapi hayo?”
“Kwanza kwanini unataka kuniua?” Jona akauliza akimkazia macho Mh. Eliakimu. Swali hilo likamshtua muulizwaji, akajitahidi kulimudu akiwa tayari amechelewa kwani Jona alimshasoma.
Kama haitoshi, Jona akataka kujua kwanini Nade alikuwa anamfuatilia na kwasababu gani haswa alikuwa anamtafuta mkewe. Maswali hayo yakamfanya mheshimiwa akose cha kunena.
Hakuwa amejiandaa nayo, na kutafuta ahueni akamwambia Jona kwamba watatafuta siku waongee vizuri kila kitu. Kauli ambayo kwa Jona haikuwa na uzito, ila akaridhia kwa kuona hamna haja ya kulumbana. Mheshimiwa alikuwa ni ndege wake, ahitaji kumshikia manati.
“Sawa, hamna shida,” Jona akajibu. “Nitafanya.” Ndani ya moyo wake alikuwa ana nia ya kumsaidia Nade, lakini pasipo kumsahau na Miriam kwa wakati huo huo.
“Na vipi kuhusu Miriam?” akauliza. Mheshimiwa akamjibu kuwa watu waliomteka Nade wanamtaka Miriam kubadilishana na Nade. Jona akataka kujua zaidi juu ya hao watu, ila Mheshimiwa hakuwa na majibu ya kumpa. Yeye mwenyewe hakuwa anajua lolote kuwahusu.
Kwahiyo Jona akawa amepata kibarua kingine, kuwachambua na kuwajua hao watu. Kutopoteza muda zaidi, akakubali kufanya kazi na kumtaka mheshimiwa akapumzike.
“Una hakika auhitaji chochote toka kwangu?” Mheshimiwa akauliza tena. Hakuwa anajua ni namna gani Jona atawapata hao watu ukizingatia hajamuuliza chochote, wala kutilia shaka lolote.
Na akasita kuuliza. Kifuani akizoza kwani yeye shida yake nini wakati ameambiwa kazi itafanywa? Akajikusanya na kuondoka zake akitingwa kichwani. Akajiweka kwenye gari na kuondoka toka eneo hilo.
“Ni lazima nimpate huyu jamaa,” akajisemea peke yake kifuani. “Endapo nikiwa naye hakika mambo yangu yataenda vema.”
Safari nzima akawa anawazia kwa namna gani angekuwa na Jona, jinsi mambo yake yangemalizika kwa wepesi na kwa uhakika. Vipi kama akiwa na Nade na Jona kwa wakati mmoja? Hatakuwa na haja ya kumiliki jeshi. Maadui zake wataona cha mtemakuni.
Basi akajikuta anatabasamu kwa taswira yake hiyo ambayo alitamani iwe uhalisia. *** Saa mbili asubuhi…
Bodaboda ilisimama nyuma kidogo ya fremu, akashuka Jona na kuvua kofia ngumu na kumpatia dereva kisha akamlipa. Akaenda zake ofisini na kumkuta Jumanne akamsalimu na kumwambia hayupo hapo kwa muda mrefu, amepita maana ameona ana haja ya kumpasha habari.
“Sitakuwepo hapa kazini kwa muda, kuna ishu fulani nafuatilia. Sawa?” Jona alisema. Jumanne akastaajabu kidogo, haikuwa kawaida. Akauliza nini shida.
Jona akasisitizia tu kwamba kuna ishu anafanya ila haitakuwa milele. Atarejea.
“Hakikisha kila kitu kinakuwa sawa. Tutakuwa tunawasiliana. Sawa?”
“Poa.” Jumanne akajibu kishingo upande. Alikuwa anawazia ni kwa namna gani atakavyokuwa mpweke. Japokuwa hapa karibuni hakuwa pamoja na Jona ila kitendo cha kupewa taarifa rasmi kuwa hatakuwepo tena kwa muda usiojulikana, Jumanne akafadhaishwa.
Jona asipoteze muda, akayeya! Sasa alikuwa yupo katika hatua nzuri ya kupotea kwenye mazingira yake zoefu. Yote haya kwasababu ya kutengeneza mazingira bandia ya kifo chake.
Lakini pia kujipa muda wa kutenda mambo yake kwa ufanisi zaidi. Alishatafuta mahali pia pa kuishi tofauti na makazi yake ya kila siku. Kila kitu kilikuwa kinaenda kwa mujibu wa mipango karatasini.
Alikuwa amevalia suti ya kahawia iliyomzidi ukubwa kidogo. Alimtazama Jumanne na kisha akazama ndani baada ya kuhakikisha yupo mwenyewe.
Mwanaume huyu ni nani? Akatazama bidhaa ya kwanza na ya pili, kisha akatazama tena nje. Akasogea akizama ndani ya duka. Jumanne alikuwa pembeni yake akisubiria kutoa maelezo pale yatakapohitajika.
Lakini mteja huyu hakuuliza kitu! Akaendelea kukagua bidhaa. Alipomalizikia ndani ya duka, akamnyaka Jumanne na kumminyia kwenye mikono yake minene meusi kumkaba!
Jumanne akafurukuta kutetea uhai wake kwa hali na mali, ila hakufua dafu! Mwanaume huyu aliyemkaba alikuwa mkufunzi wa hili tukio haswa!
Alikuwa amejawa na nguvu na sanaa ya mauaji. Jumanne akaishiwa na nguvu na mwisho wa siku akatulia tulii kukubali sheria!
Mwanaume huyo akahakikisha kama amefanikiwa kisha akahepa zake mara moja kupotea eneo hilo. Alijipaki kwenye pikipiki ambayo ni wazi ilikuwa inamngojea yeye.
Wakayeya!
***
Saa kumi jioni…
“So what did yo do?” (Kwahiyo ulifanyaje?) BC aliuliza.
“I did nothing. I asked her to wait,” (sikufanya kitu. Nilimwomba angoje,) akajibu Miranda.
“Thats good of you! But dear, we have nothing to do here except accepting it.” (Hilo ni jema! Lakini mpenzi, hatuna cha kufanya hapa zaidi ya kukubali.)
“And what about th….” (Na vipi kuhusu ….)
“**** those excuses! Jus do it.” (Acha hizo sababu! We fanya tu.) BC akasema kisha akakamata kinywaji chake, John Walker, na kumiminia kinywani.
“Go do that commercial. I will handle the rest.” (We nenda fanya hilo tangazo. Nitashughulikia mengine.) Akasema kwa kujiamini.
Miranda akatikisa kichwa chake alafu akashika simu yake na kuitazama. Swala hilo lilikuwa limeshaisha. Ilibidi afanye ile interview kama ambavyo mke wa Boka atakavyo. Ilibidi akajianike mbele ya kamera na yote hayo kwasababu tu ya kuhakikisha hiyo dili yake na mke wa Boka inatimia.
Kukawa kimya kidogo. Mazingira ya ufukweni walipokuwepo yalikuwa tulivu. Upepo ulikuwa unapuliza na hakuna kingine chochote kinachosikika.
Ukimya huo ukavunjwa na sauti ya BC punde baada ya kunywa kidogo kinywaji chake glasini.
Alimuuliza Miranda kama amesumbuliwa na Eliakimu hapa karibuni. Miranda akatikisa kichwa chake kukataa. Hakuwa na mawasiliano na mwanaume huyo tangu siku wakutane.
Habari hizo zikamfanya BC awaze kidogo. Eliakimu atakuwa anapanga nini na ukimya wake huu? Akanywa mafundo kadhaa ya Walker akiwa anawaza. Aliona kuna hitaji la kujua Eliakimu ana mpango gani, akamshirikisha Miranda.
“We don’t need to bother. Let us wait for his step first,” (Hatuhitaji kusumbuka. Ngoja tuone hatua yake kwanza.) Akasema mwanamke huyo.
Lakini vipi kama hatua hiyo ikawa na hatari kwao? Swali lilikuja hapo. Tahadhari ikaonekana kuhitajika. Miranda asirefushe mada, akapendekeza kuwasiliana na Eliakimu kama njia ya kumchokonoa.
Ila swala hilo akapendekeza lifanywe na BC.
BC akakaa kimya kwa muda. Akaendelea kunywa na kunywa akiyapanga kichwani.
Fikra zake zilienda mbali sana akiwazia na mzigo wao wa kemikali ambao upo tayari, unangoja tu amri ili upate kuja. Kukaa kwake bandarini kunazidi kuchojosha pesa, na huku bado hakujaeleweka. Afanye nini?
Akakuna kidevu chake akiendelea kuyapanga. Hamna namna BC, ni kurudi kwa Eliakimu tu! Hapana, sirudi huko kwani gharama zake zinawiana na gharama za mzigo kabisa! Sasa tufanyeje na huku Boka bado hajawekwa kwenye mstari?
Akaendelea kuyapanga akizoza na nafsi yake.
Boka lazima akalishwe. Lazima ajaribiwe kama mkono wake utakuwa mwepesi kuenenda na kutenda. Na udhaifu wake ni Miranda.
Miranda inabidi atumie mwili na akili yake kufyatua bomu hili mara moja! Ila pia na hekima yake ni jambo la msingi hapa.
“Miranda,” BC akaita. “Accept the man, Boka, and tell him that I wana see him,” (Mkubalie huyo mwanaume, Boka, na umwambie nataka kumwona.)
Mchezo ukapangwa namna ya kwenda. Miranda amwambie Boka kwamba amemkubalia ila ‘baba’ yake angenda amwone na wajadili mambo kadhaa juu ya mahusiano yao.
Na hapo ndipo BC atakapotumia ‘ubaba’ wake kumminya na kumkamua Boka kama kweli anamhitaji ‘mtoto’ wake kama mpenziwe.
Hapo ndipo Boka ataelezwa juu ya shida za ‘mkwe’ wake na kuzitimiza iwe ndiyo kama mahari. Kama kipimo cha upendo wake kwa mwanamke huyo mrembo, Miranda.
Waliamini tamaa ya kimwili ya Boka, itazima uwezo wake wa akili. Hatafikiria kwa kichwa chake cha juu, bali kile cha chini.
Na hapo, ndipo mcchezo utakapokuwa umeishia.
***
Saa moja jioni…
“Una uhakika ndiyo hapa?” Akauliza Mustapha akinyooshea kidole getini. Alikuwa ameongozana na mwenzake aitwaye Bilali, mwanaume mfupi ambaye uso wake umejawa na majeraha.
Mwanaume huyu alikuwa ni miongoni mwa wale waliopokea vichapo toka kwa Nigaa na Lee. Sasa wote walikuwa wamesimama mbele ya nyumba ndogo iliyozungushiwa uzio, yenye rangi nyeupe na kupendezeshwa na bustani.
“Ndio, ndiyo hapa!” Akasema Bilali akitikisa kichwa. Alafu wakagonga na kutulia hapo. Baada ya muda akafungua mwanaume fulani aliyekuwa amevalia bukta na kaushi ya zambarau. Alikuwa amesokota nywele zake zikisimama kama miba.
Akawauliza wageniwe namna gani angewasaidia.
“Tunahitaji kumwona bosi wako,” akasema Bilali.
“Bosi ametoka,” wakajibiwa kwa ufupi.
“Ametoka?” Bilali akastaajabu. “Mbona aliniambia atakuwepo mida hii mzee?”
“Sijui, ila hayupo. Ametoka,” akasisitizia mwenyeji.
Lakini kabla wakina Mustapha hawajaondoka, ikaja gari hapo, Alphard nyeupe yenye vioo vyeusi. Wakasimama na kutazama. Kioo kikashushwa na akaonekana mchina mmoja mwanaume. Akawasalimu kwa kuwapungia mkono.
“Ndiyo huyo hapo sasa!” Balali akamwambia Mustapha. Wote wakajikuta wanatabasamu.
“You are welcome!” (Karibuni!) Mchina huyo ndani ya gari akasema na kisha akazama ndani ya uzio. Nyuma Mustapha na Bilali nao wakaingia na punde wakajikuta wapo sebuleni, na yule mchina akiwa anatazama ile picha ya nyaraka iliyokuwepo ndani ya simu ya Mustapha.
Kwa umakini akaikagua kwanzia mwanzo mpaka mwisho. Akairudia tena kwa mara ya pili na kisha akauliza:
“Mmeitoa wapi?” kwa sauti ya puani.
Bilali akataka kujibu, lakini Mustapha akamuwahi na kumzuia. Akauliza:
“Kuna ujumbe gani?”
Mchina yule akashusha pumzi ndefu. Alafu akasema ile nyaraka ilikuwa ina taarifa fulani za koo iliyopo huko China. Koo yenye nguvu na ushawishi. Na kwenye hiyo nyaraka kulikuwa kina kipande kidogo tu cha taarifa yao.
Yaani kuna taarifa ambayo imekosekana ili ipate kutimia. Na inaonekana taarifa hiyo ni ya siri, na koo hiyo wanaitafuta ipate kutimiza mahesabu.
“Hapana,” akajibu yule mchina upesi. “Hii ni mali, mali kubwa sana hii, lakini pia ni damu!”
“Damu? Kivipi?” Mustapha akauliza.
“Kwanza ni mali kwasababu kuwa nacho ni pesa. Endapo ikijulikana kama mnacho, mnaweza mkavuta pesa yoyote ile kwasababu tu ya kuifanya ikawa siri…”
“Na damu kivipi?” akauliza tena Mustapha.
“Ni damu kwasababu wanaweza kuitafuta nyaraka yao pasipo kuamua kutoa pesa. Yani kwa lazima na hapo ndipo kuna shida!”
Kukawa kimya kidogo. Kila mtu alikuwa anafikiria lake kichwani. Lakini mchina yule akawatoa hofu akisema:
“Kuna namna lakini ya kutengeneza pesa kama tukikubaliana.”
Mustapha na Balali wakatenga masikio yao.
“Huyu mwenye hii nyaraka anajua makazi yenu? Au mahali anapoweza kuwapata?” mchina akauliza.
Mustapha akatikisa kichwa chake kuafiki.
“Ndio anapajua kwangu.”
“Basi hama,” mchina akashauri. “Tafuta mahali unapojua utakuwa salama, ndipo tufanye hii njia.”
“Kwanini nihame?” Mustapha akauliza.
“Kwasababu watakutafuta,” mchina akamjibu. “Kabla hawajatoa pesa watahakikisha kama kuna njia ya kufanyika kukwepesha mfuko wao. Hawawezi wakatoa pesa kirahisi. Watatoa pesa ambapo wameona hamna namna ya ziada – hamna njia nyingine!”
Mustapha akanyamaza kwa muda. Bilali naye hakuwa na cha kusema. Kukawa kimya wakitazamana. Mchina akaendelea kuongea.
“Ni hatari lakini ni pesa kubwa sana tunaweza tukaitengeneza. Pesa ambayo kila mmoja wetu ataipata na kuifurahia. Mtanunua majumba na magari. Ila ndiyo hivyo, ina gharama yake. Inabidi tuwe radhi kuilipa.”
Mustapha akamtazama Bilali, alafu akamtazama mchina na kumwambia:
“Tupo tayari,” akipandisha kichwa.
Basi mchina yule akaanza kuwaambia namna ambayo wanaweza wakatengeneza pesa kwa kupitia nyaraka ile. Kwanza wahakikishe wanaipata katika nyaraka ngumu, yani waiprint na kuihifadhi. Alafu wataituma mtandaoni moja kwa moja kwenye tovuti ya watu wao na kuwataka walipie pesa wakiwa wameshaainisha na akaunti yao ya benki.
“Hakuna kukutana nao bali kuwasiliana tu mtandaoni. Kila kitu kitafanywa mtandaoni na watainunua nyaraka yao mtandaoni. Ni kama vile unavyofanya manunuzi mtandao wa ebay ama amazon.”
Mustapha na Bilali wakakubaliana na hilo, ila sasa wakawa na kazi ya kwenda kufungua akaunti ya benki na wapate master card. Wakamshukuru mwenyeji wao kwa kuwafungua macho, wakaaga waende.
Ila kabla hawajenda, mchina yule akawaomba:
“Mnaweza mkanitumia nyaraka hiyo kwenye simu?”
Mustapha akakataa. Bado hawakuwa wanamwamini mchina huyo kiasi hicho. Vipi kama akiwazunguka?
“Its ok, hamna shida. Naelewa,” akasema mchina kwa kutabasamu. akawasindikiza wageni wake mpaka nje ya nyumba, akawaomba awabebe kuwapeleka nyumbani maana hana kazi ya kufanya kwa sasa na angependa kuwasaidia.
Mustapha na mwenzake wakaona hamna shida katika hilo, wakajipaki ndani ya Alphard na safari ikashika hatamu.
Wakadumu kwenye gari kwa kama dakika arobaini na tano kabla hawajafika kwa Mustapha ambapo wote walishukia.
“Nashukuru sana,”
“Msijali, tutawasiliana,” mchina akasema na kisha akaondoka zake.
Hili ndilo lilikuwa kosa kubwa alilolifanya Mustapha. Aliweza kuruka viunzi kote huko ila hichi akakisahau. Mchina huyu hakuwa mjinga kuchoma mafuta yake kuwaleta hapa. Kuna kitu alikuwa amekipanga na kukitaka, na alishakipata!
Akiwa ndani ya gari yake, anawasiliana na mwanaume fulani wakiteta kwa lugha yao ya nyumbani. Mchongo ukawekwa bayana wa kumuua Mustapha pamoja na mwenzake na kisha nyaraka ile ndani ya simu iwe mali yao.
Kumbuka huna rafiki wa kweli ndani ya dunia hii ya washenzi! Anamalizia kwa kusema kwa Kiswahili:
“Usibakize hata tone la ushahidi.” ***
Saa nne usiku…
Akiwa anatengeneza juice, simu yake inaita. Jona anaitazama na kuona jina la ‘Beka’ kwenye kioo. Anaguna na kuivuta simu, kisha anapokea.
Beka ni nani? Ni mwanaume jirani na fremu na ya Jona huko Mwenge. Sehemu yake ya biashara inafuatia baada ya pale kwa Jona. Kabla Jona hajapokea simu hiyo, anajiuliza kutakuwa kuna nini. Na akili yake inamwambia si salama.
Si mara kwa mara Beka humpigia.
“Niambie Beka.”
Pasipo kupoteza muda Beka anamwambia juu ya kifo cha Jumanne. Wamemkuta amejifia ndani ya fremu wasijue nani anahusika. Wametambua hilo muda si mrefu wakiwa wanafunga maeneo ya kazi, wakastaajabu kuona Jumanne hafungi na muda ushaenda.
Walipoenda kutazama, wakakutana na kisanga hicho.
“Beka, ni utani au?” Jona akauliza kwa kuchanganyikiwa.
“Si utani, brother. Tupo hapa pamoja na mwili.”
Haraka Jona akajiveka shati na kukimbilia eneo la tukio. Kichwa chake hakikuwa salama kabisa kwa mawazo. Kuna muda akajiuliza kama siku hiyo ilikuwa ya wajinga, ama? La hasha haikuwa!
Aliona dereva bodaboda anabembeleza pikipiki akamhasa aongeze mwendokasi. Alipofika, akajitupa toka kwenye bodaboda akimkabidhi dereva pesa yake. Moja kwa moja akenda eneo la tukio.
Hapo akakuta wanaume wanne wakiwa wamejikusanya na kuteta. Akawasalimu akizama ndani alipoonyeshewa mkono na Beka. Akaukuta mwili wa Jumanne ukiwa umejilaza.
Akatazama mapigo ya moyo, hayakuwa yanapiga. Akahakikisha na pumzi pia, kote hola! Akaamini sasa ni kweli Jumanne alikuwa ameenda. Alikuwa amekufa!
“Hatujui alikufa muda gani, na nani amemuua. Sijui ni nini kilichotokea!” Alisema Beka. “Lakini Chaz anasema ….” Beka akamtazama Chaz, mwanaume mrefu mwenye mwili, akampatia kijiti cha kutia neno.
“Mida ya asubuhi asubuhi hivi nilimwona njemba fulani akitoka ndani huku. Alikuwa amevalia suti, mara nikamwona anatembea fasta fasta, akadandia boda na kusepa! … nahisi anaweza akawa anahusika.”
Jona akaulizia rangi ya suti na mwonekano wa mwanaume huyo, Chaz akamjibu. Akameza taarifa hizo, na kwasababu ule ulikuwa ni mzigo wake, siku hiyo hakulala akaimaliza kwa kuhangaika huku na kule kwa ajili ya marehemu Jumanne.
Akaenda polisi kutoa taarifa na kisha kufanya utaratibu wa kusafirisha maiti mpaka mochwari, kuwasiliana na familia ya Jumanne na kadhalika.
Mpaka kwenye majira ya saa sita usiku ndiyo akawa ametulia, tena akiwa kibarazani mwa nyumba ya Jumanne. Alikuwa pamoja na mke wa marehemu aliyekuwa analia pasipo kupumzika.
Muda si mrefu, majirani wawili nao wakafika hapo kujumuika nao.
Japokuwa kulikuwa kuna maongezi kadhaa na kilio, Jona hakuwa mwenye habari. Kichwa chake alikuwa amekiegemesha ukutani akielemewa na mawazo mazito sana. Ni nani amemuua Jumanne na amefanya hivyo kwasababu gani?
Huyo mwanaume ndani ya suti, ni nani? Hakupata usingizi kabisa wala kujihisi njaa. Alishiba mawazo.
Uwanda wake wa mawazo ukapanuka zaidi, na kuna jambo alipolifikiri likamuwashia taa za hatari kichwani.
Nini kinafuata baada ya kifo cha Jumanne? Kufunga biashara … ndio … maana hataweza kukaa hapo na huku zile msheni zake zinamtaka asionekane. Hii itakuwa ni biashara ya ngapi anafunga sasa?
Kwa namna moja kubwa, Jona akajikuta anatilia mashaka ile kauli ya Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Dar es salaam:
“Jona, maisha yako kamwe hayatakuwa sawa ukiwa nje ya jeshi. Huu ndiyo wito wako na hauwezi kuukwepa. Na sisi tutakukumbusha hilo kila uchwao.”
Alikumbuka maneno yote hayo kana kwamba ametoka kuambiwa muda si mrefu. Akawaza je yatakuwa yanahusika na kifo cha Jumanne? Na hapo tena akajiuliza, je kauli ile itakuwa ina mahusiano na kufa kwa biashara yake?
Jona akajikuta anapata mawazo ambayo hakuwahi kuyawaza hapo kabla.
Je kauli ile ya kamanda itakuwa ina mahusiano na kifo cha utata cha familia yake?
Ya kwamba maisha yake hayatakuwa salama wala ya amani akiwa nje ya jeshi?
Akaona ana haja ya kunywa. Akanyanyuka na kuondoka zake akienda kutafuta bar. Alipopata akanunua mvinyo na kunywa kwa pupa. Akanywa kwa pupa … akanywa kwa pupa.
Aliomba pombe imsaidie kupumzika japo kwa muda. Impeleke mahali ambapo atakuwa salama na mbali na uhalisia.
***
Saa nne asubuhi…
“Amesemaje ulipochonga naye?” aliuliza mwanaume fulani mweupe. Mrefu na mwenye mwili wa mazoezi. Swali hili akilielekezea kwa Nyokaa aliyekuwa ameketi kwenye kochi akivuta sigara.
“Atajua mwenyewe atakavyosema, ila najua atamleta tu yule manzi.”
“Una uhakika?”
“Asilimia mia nane, nina uhakika. Inaonekana anamzimia sana huyu malaya wake. Atajileta tu.”
Kukawa kimya kidogo.
“Ila unajua nini Nyokaa, tukimpata tena yule manzi, tujitahidi kumaliza ile ishu mazee. Unajua yule manzi anaweza akawa ametoboa gunia letu la mchele huko kama alivyotoboa la yule boya?”
“Sidhani asee. Namwamini sana yule manzi.”
“Hapo ndipo unapofeli sasa, unamwanijie manzi kiasi hicho Arif?” .
“Najua Miriam ananipenda na yupo radhi kufanya jambo lolote kwa ajili yangu. We unajua ni mangapi yule manzi amefanya kwa ajili yangu?” akauliza Nyokaa. Kabla hajangoja majibu, akaendelea kumwaga sera: “Amenifanyia mbishe mingi sana asee kabla haya mafyoko hayajatokea hapa kati. Unadhani angekuwa manzi mwingine akithubutu?” Mwanaume yule mweupe, kwa jina Roba, akatikisa kichwa alafu akashusha pumzi yake akitazama kando. Kuna jambo alikuwa analifikiria, na punde akamshirikisha Nyokaa. “Unajua mishe zetu, mwanangu. Za hatari kinoma, inabidi tuwe macho sana kuangaza kama kuna snitch, la sivyo tutaharibu kila kitu.” “Najua,” akajibu Nyokaa kwa ufupi. Na hakutia tena neno lingine kukiwa kimya kwa muda wa kama dakika tatu. “Umeshandaa kila kitu lakini?” Nyokaa akauliza. “Kila kitu kipo tayari yani, ni huyo mgeni tu aje.” Baada ya hapo kimya kikawa kingi.
***
Saa sita mchana. Chumba SPACE BUTTON
“Naweza nikapata kikombe cha kahawa?” alisema Panky akimtazama Moderator. “Cha ngapi sasa?” Moderator akauliza kwa lafudhi yake ya kichina. “Sijui idadi,” akajibu Panky. “Naomba tu uniletee kama hutojali.” Moderator akasita kwanza na kumtazama Panky. Panky akatabasamu kabla hajageukia tarakilishi yake na kuendelea na kazi aliyokuwa anafanya. Moderator akatoka nje. Basi haraka Panky akamtazama Marwa. Mwanaume huyo alikuwa yupo mbali naye sana, kitu ambacho kilikuwa kinamkera si kidogo. Alinyanyuka upesi akamfuata na kumsabahi, na pasipo kupoteza muda akamwambia asome jumbe zake ambazo amemtumia kwenye mashine. Kuepusha kukutwa na Moderator, upesi akarejea kwenye kiti na kuendelea na kazi yake. Na kweli, punde Moderator akatokea akiwa amebebelea chupa kubwa rangi ya bluu. Akaiweka mezani mwa Panky. “Hiyo hapo, hautasumbua tena sasa!” Panky akashukuru kwa tabasamu, akajimiminia kinywaji na kunywa akiendelea na kazi. lakini akili yake ikiwa inamuwaza Marwa kama kweli ameelewa kile alichomwambia. “Kile kichwa kigumu nacho,” alisemea kifuani. Akavizia pale Moderator aliposogea kando, akashusha kazi zake zote chini, alafu akafungua application fulani iliyokuwa na kialama chenye rangi nyekundu, akaandika: “Unanipata?” alafu akatuma kwenye tarakilishi aliyoitunza kwa jina la M-Spy. Alipotuma ujumbe huo, akamtazama Marwa kwa wizi, punde naye Marwa akamtazama. Alafu akabofya keyboard. “Ndio, nakupata. Unataka nini Panky?” Ujumbe ukaingia kwenye tarakilishi ya Panky. Panky akatabasamu kwanza kabla ya kujibu. Alifurahi sasa maana alikuwa amepata ‘chobingo’ ya kuteta na mtu wake. Nafasi adhimu hii. Panky: sina ishu mpya, ni kuhusu tu ile picha. M-Spy: Imefanyaje? Kwani hukunielewa? Panky: Unajua nini Marwa, niliipenda sana ile picha. na nilivyoenda kufanya ile misheni niliyoagizwa, nikajikuta nakumbana nayo. Sidhani kama ni vibaya nikajua maana yake. M-Spy: Panky, acha ujinga. Panky: Kivipi? Nataka kuuondoa huo ujinga kwa kujua. M-Spy: Nikukumbushe mara ngapi kwamba hatutakiwi kushirikiana kwa vyovyote tukiwa kazini mpaka pale Mode atakapokuwa anajua? Panky: Marwa, acha kujifanya bingwa wa kufuata sheria. Ni mara ngapi huwa nakusaidia mambo yako? Huwa unamuita Mode? Kimya. Panky akatazama upande aliopo Marwa, akamwona Moderator akiwa amesimama kandokando ya mwanaume huyo. Moyo ukamlipuka kwa kudhani huenda pamebumburuka. Lakini alivyotazama vema akagundua, Marwa alikuwa tayari ameshatoa yale maongezi yao na yupo bize kufanya kazi. Basi naye kwa muda akazama kazini mpaka baada ya dakika kama tano alipopata ujumbe toka kwa Marwa. M-Spy: Tukutane wakati wa chakula! Panky: Poa. Kazi zikadumu mpaka majira ya saa nane, watu wakafunga kila kitu kwa ajili ya kwenda kutia kitu tumboni. Huko Marwa na Panky wakakutana na kuteta mambo kadhaa kuhusu ile picha. Cha kushangaza ni kwamba, hata Marwa mwenyewe hakuwa anajua nini kimo pichani! Lakini data alizokuwa amepewa kuzitumia kufuma ile picha zilikuwa ni za kushangaza na zenye kuhitaji mafikira kung’amua. “Nashukuru sana, Marwa. Nadhani ingekuwa vema kama ungelinitumia picha hiyo kwenye tarakilishi yangu,” alisema Panky akijua wazi pale hawana muda mrefu wa kujadili. Marwa akatabasamu. “Unajua hilo jambo haliwezekani, Panky.” “Inawezekana.” Panky akamkatiza. “Nimetengeneza code ya kuniwezesha kuwasiliana na kila tarakilishi mule ndani. Nina application za kuniwezesha kutengua security na kupokea ama kutuma faili kwa yeyote ndani ya chumba.” Marwa akastaajabu. “Umewezaje kufanya hivyo?” Panky akatabasamu. “Huu si muda wa kujadiliana, Marwa. Unajua muda wetu hapa.” “Sawa, ila unajua tarakilishi yangu haina uwezo huo kama wako. Sasa natumaje?” “Ngoja n’takuonyesha. Wewe kuwa karibu na messenger tu, sawa?” Wakamaliza kula na kuondoka. Wakafanya kama vile walivyoelekezana, na Panky akafanikiwa kupata picha na maelekezo yote ambayo Marwa aliyatumia kufuma picha hiyo. Basi tabasamu likajaa usoni. Ila muda si mrefu, akashikwa bega na Moderator, akatazamwa na uso mgumu na kisha akaamriwa: “Simama!” Utumbo ukamtetemeka na kichwa kikaanza kumgonga! Watu wote ndani ya chumba wakamtazama. Ila Marwa akiwa anatamazama kwa woga zaidi! Bila shaka alijua sasa kila kitu kimeanikwa wazi! Mwisho wao ulikuwa umewasili, kifo kinawaita. Marwa akajuta kwanini alifanya ujinga ule. Moderator akakaa kwenye kiti cha Panky na kuanza kupekua tarakilishi hiyo. akachukua muda wa dakika tano kabla hajanyanyuka na kumtaka Panky aketi chini. Hakuna alichokigundua! “Unaweza ukaendelea na kazi yako!” akasema Moderator. Panky akaketi akiwa haamini. Lakini baadae akajiona ‘jembe’ kwa namna alivyotengeneza mfumo wake madhubuti kiasi cha kumfanya mtaalamu asipate chochote ndani ya mashine yake. Akajikuta anatabasamu akipekua pekua tena tarakilishi yake. Kila jambo lilikuwapo kama alivyoyaweka. —- Saa kumi jioni:
Panky anachomoa simu yake mfukoni na kumtafuta Jona. Simu ikaita mara tatu pasipo majibu. Akasonya na kujiuliza atakuwa wapi. Alikuwa ameshatoka kazini na akiwa tayari amebebelea flashi ambayo ina faili nyeti la ile picha. Alikuwa ameketi nyumbani kwake, sebuleni, akitafakari. Mkewe akaja akitokea dukani. “Vipi mbona una mawazo hivyo?” Akauliza mwanamke huyu mweupe mwembamba aliyevalia kofia ya kuziba nywele pamoja na dera la njano lenye maua mekundu mekundu. Panky akamlaghai mkewe kwamba yupo sawa na angependa apate muda kidogo wa kutafakari peke yake. “Unataka nikuache, sio?” Mke akauliza kwa shari. “Yani hapa nyuma uliniacha peke yangu, sikujua wapi ulipo na unafanya nini, leo upo hapa nakaa na wewe unataka nikuache?!” “Si hivyo mpenzi!” “Ni vipi? – haya kaa basi mwenyewe!” Mwanamke akanyanyuka na kwenda zake. Panky akabakia kumtazama. Ila mara na simu ikaita, kutazama alikuwa ni Jona. “Nimekutafuta sana mzee vipi? … ishu gani hiyo? … serious? … pole sana kaka, sasa inakuaje? … yah! Nimepata ile kitu sasa ndo nikawa nataka tukutane uione kama vipi … poa, basi utanshtua au sio? … haya baadae!” Simu ikakata. Panky akachomoa flash mfukoni mwake na kuitazama. Akanyanyuka na kwendaze chumbani.
***
Saa moja jioni.
Ngo! Ngo! Ngo! “Naona ameshafika, acha nikachonge naye!” Glady aliwaambia wenzake wawili aliokuwa nao chumbani kabla hajanyanyuka na kwenda mlangoni. Alikuwa amevalia gauni fupi la njano lililoacha miguu yake uchi. Nywele zake alikuwa amezikusanyia ndani ya kiremba cheusi cha kulalia. Alitoka nje akamkuta Mustapha. Alikuwa amevalia shati la buluu, suruali ya kaki na raba nyeupe. Mwanaume huyo akamtaka wakaongelee ndani. “Kuna watu, tuongelee tu hapa hapa!” Glady akasisitiza. Mustapha akatazama kushoto na kulia kwake kama kuna usalama. Uso wake ulikuwa una mashaka. “Mustapha, kuna nini?” Glady akauliza. Alihisi kuna mambo hayapo sawia. “Naomba niingie ndani!” Akasisitiza Mustapha. “Tafadhali!” Kabla hata Glady hajajibu, Mustapha akazama ndani na akaurudishia mlango yeye mwenyewe. Akashika kiuno na kushusha pumzi. Glady akamtazama na kumuuliza nini shida mbona anamtia woga! Mustapha akamwambia hayupo salama, kuna mtu anataka kummaliza! “Nani huyo?” Glady akawahi kuuliza. “Yule mchina?” Mustapha akatikisa kichwa. Akasema muuaji huyu hamjui, amemkosa kosa na risasi akijaribu kujiepusha kwa kupitia mlango wa nyuma! “Mustapha, upo serious?” “Kabisa! Na hapa ninavyoongea na wewe, Bilali ameuawa tayari!” Glady akatoa macho ya mshangao. Na hapo akawa amevaa hofu nyeusi kiasi kwamba akamshangaa Mustapha kuja hapo ilhali ana songombingo la kumwaga damu! Vipi kama akiwaambukiza tatizo? “Sikuwa na kwengine pa kwenda, Glady. Naomba unisaidie hifadhi,” alisema Mustapha kwa huruma. Haraka Glady akaenda dirishani na kutazama huko nje. Akateta na wenzake wakiwa katika hali ya taharuki. “Mustapha, utakuwa umefanya nini saa hii?” “Sijafanya kitu, ila nahisi atakuwa ni yule mchina tuliyempelekea ile nyaraka atutafsrie. Anatuzunguka, anataka kuichukua!” Alisema Mustapha. Jasho lilikuwa linamtiririka. Akamweleza Glady kinaga ubaga walivyoenda kuomba msaada kwa yule mchina ambaye aliwapa lifti kuwarejesha nyumbani. Wakiwa taharukini, wanasikia mlango unagongwa! Glady anamtazama Mustapha, kisha anawatazama wenzake waliokuwa kitandani.
Kila mtu akajawa na hofu. Habari zile za Mustapha ziliwatisha na sasa wakadhani mambo yameanza kutiwa chumvi kunoga. Roho ya mtu imeshafuatwa.
Basi kwa tahadhari, Glady akachungulia dirishani kutazama aliyemlangoni. Akamwona mwanaume fulani mrefu mweusi akiwa amevalia suruali ya kijani na tisheti nyeupe. Mwanaume huyu alikuwa amepachika hereni kwenye sikio lake la kushoto akitafuna jojo kwa mapozi.
Glady akaguna na kisha akamweleza Mustapha juu ya mwonekano wa mwanaume huyo ili ajue kama ndiye yeye anayemtafuta. Kwa kuhakikisha, Mustapha naye akachungulia na akaona si yule ambaye anamuwinda. Ila bado akawa na hofu.
“Embu msikilize anataka nini,” akamwambia Glady. Glady akatoka na kwenda kukutana na mwanaume huyo. Alisimama mlangoni mkono wake wa kushoto ukiwa umeshikilia mlango ambao hakuwa ameufunga ili lolote litakapotokea, ajue namna ya kujikomboa.
“Habari, dada,” akasema mwanaume huyo akimtazama Glady kuanzia juu mpaka chini. Glady akaitikia salamu na kisha akamtaka aeleze shida yake ni nini. Mwanaume akalamba lips zake, akashika kidevu na kumwambia anataka kuonana na Rose.
Angalau hapo Glady akashusha pumzi ya hofu na kuona mambo yapo sawa. Rose ni rafiki yake na yupo ndani. Basi aklichofanya ni kumuita Rose akutane na mgeni wake, alafu yeye akaenda kuteta na Mustapha.
“Najuta kwanini nimejiingiza kwenye janga hili,” akasema Mustapha. “Naona kuna haja ya kuonana na yule mchina na kumweleza yote haya, pengine anaweza kunisaidia.” Glady hakuafiki, wakazoza kwa muda kidogo pasipo kufikia makubaliano.
***
Saa tatu usiku, Mbezi beach: Afrikana ya chini. Ndani ya nyumba kubwa rangi ya kijani yenye uzio mweupe.
Kamanda akasafisha koo lake, akauliza:
“Kwahiyo mpaka sasa umejua yupo na move gani?”
Akiwa ameketi kibarazani kwenye kiti kikubwa kilichofumwa na kambakamba za mbao na kujazwa sponji. Kando yake akiwa ameketi yule mwanaume muuaji wa Jumanne, akiwa amevalia suti rangi nyeusi, ila nayo ikiwa imemzidi umbo. Mbele yao kukiwa kumeketi stuli ndogo nyeusi inayong’aa kama kioo.
Juu ya stuli hiyo kulikuwa kuna chupa kubwa ya maji ya Kilimanjaro na glasi mbili pembeni.
“Bado yupo msibani, ni ngumu kujua amepanga kufanya nini, lakini kwasababu msiba utaisha leo, nitapata kujua,” akasema muuaji. Jina lake ni Alphonce Ndebali – afisa wa polisi, mwanaume huyu akihusika na kitengo nyeti cha mateso.
Kamanda akamhusia:
“Kuwa makini, hakikisha kila jambo linaenda kama lilivyopangwa. Unamjua vema Jona.”
“Usijali, mkuu. Sijawahi kukuangusha na wala haitakuja kutokea,” akasema Alphonce. Hii haikuwa kazi yake ya kwanza kwa Jona kwani alishafanikisha kumuua mke na mtoto wake kwa kuchoma nyumba.
Alishafanikisha pia kufuatilia na kuharibu mipango ya biashara ya Jona. Kwa ujumla, alifanikisha mengi kumfanya Jona aishi maisha ya tabu na dhiki. Na kama haitoshi alikuwa anawinda zaidi na zaidi.
Kazi yake ilikuwa ni kumfanya Jona arejee jeshini kama sehemu yake ya mwisho ya kupata msaada. Akose mkono wa kumsaidia wala mlango wa kutokea. Na alipewa kazi hii kwakuwa anaiweza na kuimudu ipasavyo.
Alphonce Ndebali ama Jabali kama wamuitavyo wenzake hakuwa mtu wa mchezo hata kidogo. Alikuwa ni mtu asiye na chembe ya huruma. Anamuua mtu huku akimtazama machoni na kutabasamu! Anapata raha kila anapomwaga damu na kukatisha pumzi ya mtu.
Hana roho ya binadamu, mishipa yake ya utu ilishakatika muda mrefu sana huko nyuma!
Na japokuwa ni afisa wa polisi, amekuwa akijihusisha na ‘michongo’ mbalimbali ya biashara haramu. Ni muuza madawa ya kulevya, lakini pia amekuwa akikodishwa na watu mbalimbali kufanya mauaji ama kutishia uhai watu kwasababu binafsi.
Huo ulikuwa ni upande wake ambao jeshi haufahamu. Huo ulikuwa ni upande wake ambao unamwingizia kipato kikubwa kuliko kile anachopewa kila mwisho wa mwezi na jeshi la polisi.
“Unajua kuna kitu nawaza,” Kamanda alisema akikuna kidevu chake. Alphonce akamwazima macho na masikio yake. Kamanda akamwambia kama ikishindikana kumrejesha Jona kwa haya yote watakayoyafanya, basi wammalize. Hakuna haja ya kumwacha awe hai kwani itakuwa dharau na ishara ya kufeli.
Alphonce akatabasamu na kuuliza: hilo tu mkuu? Huo ni mfupa mdomoni mwa fisi.
***
Saa sita mchana, Koko bar …
Mezani kuna Smirnoff moja pweke, na Jona ameketi akiwa amelaza kichwa chake juu ya tama. Anawaza mambo kadhaa na hana furaha. Jumanne ameshazikwa na kaenda zake, ila kamwachia maswali mengi sana. Anahisi kichwa chake kimevurugika.
Anachomoa simu yake mfukoni na kutazama, anapiga na kuiweka sikioni. Anaongea na mtu anayemuelekeza mahali alipo na isichukue muda mrefu, mtu huyo anafika. Alikuwa ni Panky akiwa amebebelea begi jeusi, amevalia shati jeupe na suruali ya jeans.
Baada ya kusalimiana na kujuliana hali, Panky anafungua begi lake na kutoa tarakilishi mpakato, anaiwasha na kuchomeka flash disk. Punde inasoma, anamwonyesha Jona kile ambacho alikipata toka kwa Marwa.
Kwenye kioo cha tarakilishi kulikuwa kuna mahesabu kadhaa na drafti ya kwanza ya mchoro. Kupata maana vema, Jona aliona kuna haja ya kuwa na mchoro ule pale pale kwa ajili ya kulinganisha. Hivyo basi akanywa kinywaji chake kwa mkupuo alafu wakaenda nyumbani kwake.
Hapakuwa kule pa zamani, la hasha, bali nyumba nyingine ndogo tu isiyo na uzio. Ina vyumba vitatu na sebule. Humo Jona akatoa picha ile chumbani na kuanza kuirejelea na yale mahesabu ya Marwa na drafti yake ya kwanza.
Wakaja kugundua kumbe kila kilichochorwa mule kilikuwa kimepangwa kisanii na kimahesabu. Vipimo umbali na upana vilikuwa vinafanana. Kuanzia umbali wa kila ndege aliyekuwa anaruka angani, visiwa pichani, na hata mawimbi baharini.
Lakini maana yake nini? Walishindwa kuipata. Lakini hata hivyo, akili ya Jona bado haikuwa imetulia. Hakuwa anawaza vema. Akamwomba Panky amwachie picha hiyo, ataifanyia kazi akitulia na kufanya mambo taratibu.
Panky akaridhia na haikuchukua muda mrefu akaenda zake akimwacha Jona peke yake. Jona akaongeza kinywaji cha pili kisha akalala kwa muda kidogo. Aliikuja kukurupuka akatazama simu yake, saa kumi jioni! Akaoga na kisha kuketi sebuleni.
Akaendelea kupekua pekua picha ile kwa macho yake mekundu. Lakini hakupata kitu. Akaghafirika. Aliona anapoteza muda na kichwa kinazidi kumuuma. Akaifunga picha ile na kwenda kuificha kabatini.
Mara simu yake ikaita, alikuwa ni Mheshimiwa Eliakimu. Akapokea na kuiweka sikioni. Mheshimiwa alikuwa anamuulizia lile jambo la kumuokoa Nade. Wale wanaume watekaji wamempigia simu na wamempatia masaa matano tu awe amatekeleza, la sivyo wasitafutane!
“Hamna haja ya kuhofia,” Jona akamhusia. “Hakuna lolote watakaolifanya kwa Nade kwasababu nao pia wanamhitaji Miriam kwa hali na mali. Ni vitisho tu!”
“Umejuaje? Na unafahamu wanamhitaji kwasababu gani?”
“Nitafahamu karibuni, pamoja na wewe kwanini hutaki wampate Miriam.”
Baada ya kusema hivyo, Jona akamwambia Mheshimiwa kwamba ataifanya kazi yake usiku. Na kabla ya kupambazuka, Nade atakuwa kwenye mikono salama. Kisha akakata simu na kuanza kujipanga kwa ajili ya kazi hiyo.
—
‘Ukithubutu kuleta ujanja wowote, utajuta!’ Ulisomeka ujumbe ndani ya simu ya Mheshimiwa Eliakimu, ujumbe huo ukitokea kwa watekaji, na ukiingia punde tu Mheshimiwa alipotoka kuongea na Jona.
Mheshimiwa akaagiza kwanza maji ya kunywa. Aliogopa kwa kudhani huenda watekaji hao wamejua janja yake ya kumwokoa Nade. Ila hapana! Akatikisa kichwa. Watakuwa wanahisi tu, akawaza. Hakuwa na budi kumwamini Jona. Hakuwa na mlango mwingine wa kutokea.
Mambo yalikuwa tafrani.
***
Saa mbili jioni…
‘Napitia hapo, basi nikukute,’ Boka akatuma ujumbe kwenda kwa Miranda. Mwanamke huyo akaupokea kwa tabasamu kabla hajarudisha majibu:
‘Sawa, utanikuta nakungoja.’
Boka akatabasamu mwenyewe nyuma ya gari kama mwehu. Akampatia maelekezo dereva wake apitie nyumbani kwa Miranda, maeneo ya Kawe.
Miranda naye akaweka mazingira yake safi kwa ajili ya kumpokea mgeni. Aliandaa mvinyo na glasi zake, pamoja na chakula kitamu cha kumfanya mgeni ajilambe na kwenda kusimulia.
Alafu akajivesha nguo maridadi na kufanya hali ya hewa inukie. Akaketi kumngoja mgeni wake kwa hamu.
Dakika chache kupita, akasikia sauti ya honi huko getini. Akatabasamu na kujitengenezea vema gauni lake jekundu. Akamwita mlinzi na kumuagiza afungue geti upesi kwani kuna mgeni wake wa maana.
Geti likafunguliwa, na akastaajabu kuona gari aina ya Murrano nyeupe ikiingia ndani. Kutazama, akamwona mke wa Boka akishuka toka kwenye gari hilo, akamtazama kwa tabasamu akimpungia mkono.
Kichwani akajiuliza mwanamke huyu ametokea wapi? Kwa namna moja akahisi pengine ndiye aliyekuwa anatumia simu ya mumewe, Boka, kumtumia ujumbe. Basi akawa na hofu.
Lakini wakati mama huyo anamjongea akiwa anatabasamu, simu yake ikaingia ujumbe. Akatazama upesi. Ulikuwa unatoka kwa Boka.
‘Nakaribia kufika.’
Moyo wa Miranda ukapasuka pah!
Kwahiyo Boka na mkewe hawakuwa wanajua kama wanakutana sehemu moja! Miranda akajua hilo. Sasa afanyaje? Japokuwa alimpokea mke wa Boka na kumkarimu kwa tabasamu matata, akili yake haikuwa pale kabisa.
Haraka alitumikisha vidole vyake kuandika ujumbe na kuutuma. Akimtaarifu Boka juu ya ujio wa mumewe eneo hilo. Kama haitoshi, pengine kwa kuhofia Boka anaweza akawa hajaupata ujumbe huo, akaibipu simu yake kumtaarifu.
Boka akatazama simu yake akikunja uso. Kiooni akaona ujumbe toka kwa Miranda. Ila kabla hajaufungua ujumbe huo, dereva akawa tayari ameshapiga honi mara tatu getini! Na kwakuwa mlinzi alikuwa na taarifa juu ya ujio huo, haraka akafungua geti.
“Simama!” Boka akampiga dereva begani. “Rudi haraka, tuondoke hapa!” Dereva hakuelewa kinachoendelea. Alipigwa na butwaa, ila kutii amri ya bosi akarudisha gari nyuma upesi, na kuligeuza. Alidhani pengine itakuwa ni kuhusu mambo ya usalama. Wakayoyoma.
Lakini mama Boka akahisi jambo. Akauliza:
“Nimeona kama gari ya mume wangu,” alisema akitazama nje kupitia dirishani. Miranda akaigiza kushtukiza. Mama akanyanyuka na kwenda nje. Akaangaza pasipo mafanikio kwani geti lilikuwa limefungwa.
“Hamna kitu, mama! Utakuwa umeona vibaya,” akasema Miranda akitabasamu kiuongo.
“Hapana, sidhani. Nimefikia uzee huo!”
Basi Miranda kumaliza zogo akamwita mlinzi aliyemkonyeza tayari kwa ishara. Akamuuliza eti ni nani yule aliyekuja na kuondoka, kwanini ameondoka, na alikuwa anataka nini?
“Aaah Madam, ni Kinoo yule!” Mlinzi akasema akijichekesha. “Amesema kuna kitu alikuwa anakuletea ila sasa bahati mbaya amekisahau?”
“Kwahiyo ndo’ ameenda kukichukua?”
“Eeeenh! Ndo maana nikaona hamna hata haja ya kuja kukwambia huku … anaweza akarudi muda si mrefu.”
Angalau Mama Boka akawa ametuliza kifua. Wakarejea ndani na kueleza lile lililonyanyua mguu wake kumleta hapo.
“Samahani sana, najua nimekuja kwa kukushtukiza. Nilikuwa njiani kuelekea City mall, nikaona kuna haja kama nikikatiza hapa maana nina habari za kupasua kifua.”
Akaweka kituo akimeza mate.
“Kuna kampuni kubwa sana ya usambazaji ya huko nchini Kenya, wamevutiwa na kazi zetu na hivyo basi wanataka tuwe na ubia. Maana yake ni kwamba, bidhaa zetu sasa zitavuka mipaka na kwenda Kenya kwa uhakika!”
“Habari nzuri sana hizo!” Miranda akatahamaki. Ila kinafki. Hakuna wazo lake lolote lililokuwa pale. Alikuwa anamuwaza Boka. Namna alivyomkosa. Akijipa moyo ni kukuwe na hana haja ya kumshikia manati.
Ila alikuwa anataka kumaliza kazi. Huyu kuku atakaa nje ya banda kwa muda gani? Basi mawazo hayo yakapeleka mbali kichwa chake, yale aliyokuwa anayaongea Mama Boka kwake yakawa kama kelele za chura. Alichokuja kusikia mwishoni ni kile cha kuambiwa lazima interview yake ifanyike kesho kutwa.
“… Tutakapofanya hicho kitu, hapo ndo’ tutaeleza pia umma kwamba kampuni yetu imetanuka na sasa imefika Kenya.”
Akaitikia: “Sawa.”
Na hata hivyo vingine vyote vilivyofuatia, akamkubalia pasipo shida. Alikuwa anataka mama huyo aondoke amwache huru, haikupita muda akaaga na kwenda. Kitu cha kwanza ambacho Miranda alifanya ni kuchukua simu yake na kumtumia ujumbe Boka.
‘Ameondoka.’
Boka akamjibu baada ya muda mfupi:
‘Tutaonana siku nyingine mpenzi. Usijali.’
***
Saa tano usiku …
“Sasa Mustapha? – nataka kuondoka,” akasema Glady. Alikuwa amevalia bukta fupi rangi ya pinki na kaushi nyeupe nyepesi. Hakuwa amevalia sidiria, na hivyo basi chuchu zake zilikuwa zinaonekana vema zikitoboa kaushi. Miguuni alikuwa amevalia raba nyeupe – converse, mkononi akibebelea mkoba mkubwa mweusi.
“Sawa, we nenda tu,” Mustapha akajibu. Alikuwa ameketi kitandani nyayo zake zikigusa sakafu. Glady akacheka.
“Unajua unachekesha we Mustapha. Niende wapi na wewe umetuama humu? Au mpaka nikuambie amka uende mie nataka kufunga chumba?”
Mustapha akawa kimya kwanza. Sijui akitafakari nini, akamtazama Glady kwa huruma akisema:
“Unajua mikasa yangu ndugu yangu, unadhani n’taenda wapi? Huko nje si salama kwangu,”
“Leo nimekuwa ndugu yako, Mustapha?” Glady akapiga kofi akiangua kicheko. “Kweli shida kirusi. Sasa na mimi chumba changu hakipo salama nikikuacha humu. Umesikia? Mie n’takufuga humu mpaka lini labda?”
“Naomba unihifadhi kwa leo tu,” Mustapha akanyenyekea. “Kesho n’tajua mie pa kuelekea.”
“Sasa Mustaphaa …” Glady akakaa kitandani na kumtazama Mustapha. “Mie nikienda nikapata danga langu huko, n’talipeleka wapi? Mfano halina chumba, au anataka tufanyie kwangu? Ntafanyaje?”
“Kwa leo tu, Glady.”
“Mustapha mie n’takula nini?”
Mustapha akazamisha mkono wake mfukoni, “Basi lala na mimi leo.” Akatoa shilingi alfu kumi na kumwonyeshea Glady. Glady akaangua kicheko kikali. Akakohoa mara kadhaa kabla hajatulia na kumtazama Mustapha kwa macho yake mekundu.
“Mustapha, yani ulale na mimi kwa shing’ efu kumi!”
“Ntakupatia zingine bana, Glady. Mbona unakuwa kama hunijui? Unajua kabisa tukipiga ile hela na wewe utapata mgao au umesahau?”
“Mustapha, mie sio mtoto, sawa?” alisema Glady akiweka pesa yake kwenye mkoba. “Kwanza sasa hivi hakuna cha dili wala nini, ona unavyohangaika hangaika hapa kama digidigi. Pili, hii … hii pesa hii … haiwezi kun’tosha kabisaa! Hii ni pesa niliyolipwa kwa busu tu, upo? … cha kukusaidia, ntakuacha ulale humu, ila haiwezi kun’fanya nikabakia nyumbani.”
Hata hivyo Mustapha akashukuru, Glady akahepa. Alichukua bodaboda mpaka maeneo ya klabu ya usiku, Maasai, akaanza kufanya doria huko akichangamana na wenzake.
Baada ya robo saa …
“Shosti, yule siyo mchina wako uliyeenda naye siku ile?” alisema mwanamke mmoja kandokando ya Glady. Mwanamke huyu alikuwa amevalia topu na sketi fupi. Ilikuwa ngumu kujua rangi ya nguo hizo kwasababu ya ufinyu wa mwanga wa wingi wa taa za rangi rangi zilizokuwa zinakatiza zikienda huku na huko kwa kukimbizana.
Glady alitazama kule alipoelekezwa, kaunta, akamwona Lee! Mwanga uliokuwepo maeneo hayo ya kaunta uliwawezesha kuona vema.
“Au nimekosea?”
“Wala! Ndiye yeye. Acha niende,” akasema Glady akichukua hatua kwa mwendo wake wa madaha.
Lee alikuwa ameketi na marafiki zake, wakina Nigaa, wakipata kinywaji. Kila mtu alikuwa ameshikilia glasi ama chupa yenye kileo. Walikuwa wanasindikizia vinywaji vyao na soga za hapa na pale pamoja na cheko.
Mara Lee akasikia mkono begani, kutazama akamwona mwanamke ambaye kwa haraka alimtambua kama malaya. Akampuuzia akimshukuru na kumwambia ahitaji huduma.
“Ni mimi, unanikumbuka?” Glady alisema kwa sauti ya kubana pua. Hapo ndiyo Lee akatazama na kumgundua sasa Glady. Akamuuliza anataka nini?
“Naweza nikaongea na wewe kidogo?” Glady alisema kwa unyenyekevu.
“Glady, sihitaji usumbufu, sawa?”
“Ni jambo la muhimu, naomba unisikilize.”
Lee akageuka na kumtazama.
“Enhe, nini unataka kunambia?”
Glady akamwambia kumhusu Mustapha na matatizo yake. Yote yakisababishwa na ile nyaraka. Namna Mustapha alivyotaka kuitumia kupata pesa lakini mwisho wa siku ikamdumbukiza matatizoni, anawindwa anyofolewe roho!
Habari hizo zikamshtua Lee. Hakutegemea kama saga hili la nyaraka lilikuwa linaendelea katika ulimwengu huo ambao alidhani ameuacha. Lakini akajiuliza ni mchina gani huyo aliyepokea nyaraka hiyo na kuanza kumsaka?
Akamuuliza Glady:
“Unamjua mchina huyo? Unajua anakaa wapi?”
“Hapana, sijui lolote lile kumhusu.”
Lee akamtaka Glady waongozane mpaka kwa Mustapha. Lakini Glady akamuuliza: “Sasa ukinitoa hapa, maana yake sitaingiza pesa yoyote. Vipi, utan’lipa?”
Lee akaukwapua mkono wa mwanamke huyo na kumswaga baada ya kuwatonya wenzake kwa ufupi ya kwamba anatoka.
“Taratibu basi jamaniii!” alisikika Glady akilalamika.
Kuna makelele makali ya muziki. Wanaume kadhaa pamoja na wanawake wapo ndani ya mahali hapa ambapo unaweza ukapaita klabu ya usiku, lakini ilikuwa ndani ya nyumba ya mtu! Ndani ya eneo hilo kulikuwa kuna kaunta, na eneo kubwa tu la watu kujimwaya kucheza muziki uliokuwa unapigwa.
Vinywaji vilikuwa vingi na vya kumwaga. Kila mtu aliyekuwa eneo hili alikuwa amebebelea kinywaji chake, haswa mvinyo ama whisky, katika mtindo wa chupa ama glasi. Na kila mtu alionekana akiwa na mtu wake.
Mwanga ulikuwa hafifu. Taa zilikuwa mbili tu, nyekundu na ya kijani. Wakati taa moja ikiwa inamulika kushoto, nyingine ilikuwa inamulika kulia. Kwahiyo ilikuwa ngumu kujua watu waliokuwemo humo kwa uso. Labda kwa maumbo.
Kulikuwa kuna milango miwili maeneo hayo, milango yote hii ikiwa ni ya kioo. Ukutani kulikuwa kumechorwa picha kadhaa za wanawake, maua na silaha.
Muziki ukiwa unaendelea kukonga nyoyo za watu, kama si vichwa, mlango mmoja ukafunguliwa na mwanaume fulani aliyekuwa amejaza mwili. Mwanaume huyu alitembea kwa kasi kuelekea meza fulani ukutani. Hapo akamnong’oneza mwenziwe sikioni.
Ghafla huyo aliyenong’onezwa akanyanyuka. Aliangaza kule kaunta akatoa ishara ya mkono, mara muziki ukakata! Akapaza sauti kusema wamevamiwa!
Haraka wanaume wote wakatoka nje, na hapo ndiyo ikaonekana kumbe mwanaume yule aliyepewa taarifa alikuwa ni Nyokaa, na hayo yalikuwa ni makazi yake. Haraka walielekea kwenye chumba walichokuwa wamemfungia Nade, hawakukuta mtu zaidi ya kiti kitupu na kamba zilizokatwa!
Nyokaa akatukana na kusaga meno. Akapiga ngumi kiganja chake na kuwatazama wenzake kwa macho mekundu.
Basi isijulikane na hata wanaume wengine walitokea wapi, jumla wakawa ishirini! Wengi wao walikuwa wamebebelea bunduki, na wachache, watatu kwa idadi wakiwa hawana silaha yoyote ile. Msako ukaanza!
Wakasambaa huku na huko. Wakibeba tochi na wengine wakiyakodoa macho yao kana kwamba matonge ya ugali ili wapate kuona wanachokitafuta. Hawakujua mvamizi ameelekea upande gani, ilikuwa ni kubashiri tu wakiwa wanaamini hatakuwa yupo mbali.
Uzuri kwao, eneo hili lilikuwa ni kubwa, kwa mtu kuvamia na kutoka, haikuwa rahisi. Ingemchukua muda mrefu, na akili pia kwani eneo lilikuwa limezingirwa na msitu mkubwa na njia fupi fupi zilizokomea mitini!
Lazima Nade apatikane. Na si hivyo tu, na huyo mvamizi pia apatikane kwa ajili ya adhabu na kueleza ametumwa na nani.
“Ananitania, hanijui vizuri!” alisema Nyokaa. Pembeni yake alikuwa amesimama Roba. Mkononi mwa Nyokaa kulikuwa kuna chupa kubwa ya kinywaji cha Ciroc, kikihudumia kinywa chake mara kwa mara.
“Ameuchokoza moto uliokuwa umezima, sasa ataona cha mtemakuni!” aliendelea kunena Nyokaa, alafu akajipooza na kinywaji chake.
“Tulifanya makosa sana kumwamini yule mshenzi,” alisema Roba. “Hatukuwa na haja ya kufanya naye mazungumzo yoyote yale, bali vitendo.”
“Nilimpatia nafasi ya kuyamaliza kwa amani,” akasema Nyokaa akitikisa kichwa. “Lakini kaniona fala. Sasa kichwa cha huyu malaya wake, pamoja na huyo mbwa aliyemtuma vitakuwa ni salamu zake tosha. Na kama hatamleta Miriam hapa, tutamfuata mwenyewe huko alipo!”
Wakati maongezi haya yanaendelea, Jona alikuwa anatazama. Alikuwa amejificha kwa kujibanza kando ya jengo akiusoma mchezo mzima. Kumbe wakati wanaume wametapakaa huku na huko kwenda kumtafuta, yeye alikuwepo pale walipopaacha.
Mtihani wake ulikuwa ni kutoka ndani ya eneo hilo akikwepa watu waliozagaa huko. Hili halikuwa gumu kwake kabisa kama angelikuwa mwenyewe, ila shida ni kwamba mgongoni mwake alikuwa amembebelea Nade aliyekuwa hoi.
Macho ya mwanamke huyo yalikuwa yanarembua kwa kuchoka. Mwili wake ulikuwa unanuka damu ukijawa na majeraha. Kama Jona angelimwacha pale, asingeliweza kwenda popote pale kwa maana hakuwa na nguvu hizo.
Jona akapiga mahesabu, kushoto ama kulia, kaskazini ama kusini. Kwa kuhofia kupotea ndani ya eneo hilo alikuwa ameikariri ramani ya eneo zima kichwani kabla hajafanya kazi yake hiyo. Alikuwa anajua wazi wapi kuna njia na wapi kuna kupotelea msituni.
Na basi kwa akili zake timamu akaamua kuenenda upande anaoujua hamna njia. Akifanya hivyo kwasababu za kiusalama zaidi akiamini ya kwamba wanaume wale waliotapakaa huko, watakuwa wamejijaza mahala penye njia wakidhani amezitumia.
Akihema taratibu na akikanyaga hatua fupi fupi za haraka, akasonga. Ndani ya ‘mamiti’ hali ya hewa ilikuwa ni ya ubaridi. Udongo ulikuwa ni wa kutitia ukilowanishwa na unyevunyevu. Kulikuwa ni giza, taa za makazi ndizo zikisaidia kwa mbali.
Wakati Jona akisonga, Roba akasikia sauti ya kukatika kwa kipande cha mti kaskazini mwake upande wa kushoto. Upesi akatazama eneo hilo. Alilitilia mashaka, ila akapuuzia. Hili likawa kosa lake kubwa mno!
Baada ya sekunde chache, roho yake ikiwa haijaridhika, akamwomba Nyokaa kurunzi na kumulika kule alipokuwa amepatilia shaka. Kurunzi ilikuwa kubwa yenye mwanga mkali mweupe. Aliipeleka mbele na nyuma akiangaza, lakini hakuona kitu!
Jona alikuwapo wapi?
Bada ya kurunzi hiyo kuzima na kiza kurudi ndani ya miti, sauti ya Jona inanong’oneza ndani ya msitu:
“Amka, twende!”
Kumbe alikuwa amelala chini, yeye pamoja na Nade. Anamnyanyua Nade na kisha anamuweka tena mgongoni. Wakaendelea na safari.
Lakini Roba hakukaa na amani tangu pale aliposikia mlio ule wa mti. Hakuchukua muda mrefu sana, akamuaga Nyokaa anataka kwenda kutazama hali kule alipomulikia kurunzi.
“Twende wote!” Nyokaa akaropoka akisimama kwa shida.
“Hapana,” akasema Roba. “We kaa hapa, nakuja muda si mrefu.”
Nyokaa akaleta ubishi kidogo, alikuwa chakari kwa kulewa. Hata kusimama likuwa tabu, Roba akamsaidia kwa kumshikilia. Akamtuliza kitako na kisha haraka akapandisha kwenda kutazama.
Ndani ya dakika mbili, Roba akaona alama za viatu kwenye udongo. Akachuchumaa na kuzitazama alama hizo vema, kwa kuusoma ulaini wa udongo akagundua adui alipita hapo ndani ya muda mfupi. Na kwa kusoma kina cha alama hizo, akajua adui alikuwa amembembelea mateka wao.
Basi akatabasamu maana aliona kazi imeshakwisha. Endapo adui huyo amembebelea mateka, basi hatakuwa na kasi ya kutembea wala kukimbia. Na alama zake za miguu zitaonekana kwa urahisi udongoni.
Akaona hamna haja ya kuita watu wengine, kazi ataimaliza kwa mkono wake mwenyewe. Haraka akaanza kusonga kwenda mbele. Alitumia macho yake kama kurunzi na alijitahidi kwa kadiri ya uwezo wake kutembea kimya kimya japo kwa upesi ili asimgutue adui mapema.
Macho yake yalitazama chini, na akitumia alama za miguu kama ramani. Akafikia mahali ambapo alama hizo zilikata. Akasimama na kumulika na kurunzi aone.
Mahali hapo ndiyo palikuwa sehemu ambapo Jona alilala punde baada ya kuona mwanga wa kurunzi kwahiyo Roba alipomulika kwa mbele kidogo, akafanikiwa kuona alama za viatu vya Jona vikiendelea, naye akaendelea kuvifuatilia.
Lakini pasipo kufahamu, akawa ametenda kosa lingine la pili ndani ya usiku huu. Kitendo cha kumulika kurunzi msituni kwa mara nyingine, kikamshtua Jona na kumtaarifu kuwa anafuatwa kwa ukaribu. Anapaswa kuchukua hatua!
Dakika tano mbele, Roba akafika tena mahali ambapo hakuona alama za miguu. Akasimama na kuangaza. Pembeni yake akaona mwili wa binaadamu. Haraka akawasha kurunzi kumulika. Akamwona Nade amejilaza!
Kwa tahadhari akasogea. Akamulika kushoto, kulia, mbele na nyuma. Hakukuwa na mtu wala alama za viatu. Alipotaka kumulika juu ya mti, mara vuuup! Jona akashuka kama radi akamparamia na kumwagusha chini!
Kurunzi ikarukia kando.
Jona akang’ang’ania shingo ya Roba wakishindana nguvu. Roba akamtupia mwanaume huyo mbali kwa kutumia miguu yake, alafu haraka akasimama. Naye Jona upesi akasimama kwa kujifyatua kama mtego wa panya.
“Huu ndiyo mwisho wako!” Roba akasema kwa msisitizo kisha akafikicha pua yake kama mtu mwenye mafua. Akamjongea Jona akijiandaa kwa pambano.
Ngumi na mateke yakarushwa kwa fujo! Kila mtu alikuwa stadi kwenye kukwepa mashambulizi ya mwenzake. Ngumi na mateke ya Roba yalikuwa mazito zaidi, lakini hazikufanikiwa. Jona alikuwa mwepesi mno kukwepa kana kwamba anacheza gemu la nyoka.
Kwa sekunde chache akausoma mchezo wa Roba, na sasa akaanza kucheza faulo za kuleta ushindi. Kila Roba aliporusha ngumi yake nzito, Jona akawa anaipisha na kuisukumia mbali kuharibu balansi ya adui.
Akafanya hivyo mara tano. Roba akajaribu kurusha teke, Jona akalikwepa na kugusa kidogo mguu ulioleta shambulizi , Roba akaenda kombo. Kuja kukaa sawa akamkuta Jona yupo hewani. Kabla hajavuta pumzi, akala teke la kibabe, likamnyanyua na kumtupia chini! Hoi!
Mdomo ulimwaga damu. Macho hayakuona vema, kichwa kikaita kwa miale ya maumivu makali. Lakini hakutaka kushindwa, akajikokota kunyanyuka. Akakunja ngumi apambane tena.
Lakini kwa mara hii haikumuwia vigumu Jona. Alijua adui yake hakuwa sawa, na basi akamruhusu arushe shambulizi lake yeye awe wa mwisho. Roba akaingia mkenge. Aliruhusu hasira zikamtawala. Akairusha ngumi yake kwa pupa, Jona akaiyeya kama amefungiwa ‘springi’, Roba akakatiza hatua mbili mbele, Jona akamrusiha nyuma kwa teke la kukunjuka lililomkita kifuani. Roba akalala tuli asionekane mwenye dalili ya kuamka!
Jona akamuweka Nade mgongoni, wakaendelea na safari. Wakatembea kwa hatua kumi na tano, mara wakamulikwa na kurunzi!
Watatoboa? Jona akageuka na kuangaza mwanga huo watokea wapi na kwa nani, hakuona! Mwanga ulimpiga usoni na kumuumiza macho. Hakuwa na cha kufanya zaidi ya kukazana kukimbia. Alidhani aliyemnyoshea kurunzi ni adui, na yupo karibu.
Alikimbia kwa muda mrefu pasipo kusikia ama kuona chochote. Alifanikiwa kuchoropoka ndani ya ngome ya Nyokaa salama, mgongoni akiwa amembebelea Nade aliyekuwa hajiwezi kwa lolote.
Alikuja kugundua mbeleni ya kuwa kurunzi ile iliyommulika, ilikuwa ni ya Roba aliyemlaza chini, akifanya hivyo kuwapa ishara wenzake baada ya yeye kunoa nanga.
Baada ya nusu saa wafuasi wote wa Nyokaa wanakutana na kutoa taarifa kwamba hawajafanikiwa kumtia mikononi mvamizi wala mateka. Nyokaa ananghafirika, anapasua chupa alikuwa ameibebelea mkononi kisha alaani kwa matusi.
“Yani himaya hii ilivyo kubwa, mtu anatokaje kirahisi namna hiyo? Ni uzembe mkubwa kiasi gani? … Roba!” akaita. Roba akampatia macho na masikio. Alikuwa ameumia mdomo na upande wake mmoja wa uso ukiwa taabani.
“Unaweza ukaniambia ni kwa namna gani huyo ms** ametoka humu?!” Nyokaa akafoka. Akaongea na kuongea lakini hakuna hata mtu mmoja aliyesema neno. Wote walibakia kusikiliza kana kwamba mwalimu mkuu yupo ‘asembo’.
Nyokaa alikuwa ameudhika sana. aliona ni kama vile amevuliwa nguo mbele ya umati. Aliona amedharauliwa na kushushwa kiwango haswa. Inakuaje mtu azame ndani ya nyumba yake na kutawala meza?
Akachojoa sigara kubwa ndani ya mfuko wake, alafu akaiwasha akipepesuka. Akavuta pafu moja zito kabla hajautema moshi nje kana kwamba treni ya makaa. Akanyamaza kwa muda akiwaza kwa kutumia kichwa chake cha pombe, watu wote wakimtazama na kumngojea atasema nini.
“Nataka kichwa cha Eliakimu hapa. Namtaka na Miriam hapa … Utajua mwenyewe cha kufanya. Anayelikoroga sharti alinywe.”
Aliposema hayo akaondoka zake kwenda kujipumzisha, akimwachia jukumu zito Roba, ambaye alishusha pumzi ndefu na kuketi chini kwanza kabla hajafungua kinywa.
Saa tatu asubuhi …
Baada ya usingizi kukoma, Nade anaunguzwa na mwanga wa jua usoni. Alikuwa juu ya kitanda kidogo kilichotandikwa vema, ndani ya chumba cha ukubwa wa kati. Pembeni ya kitanda hicho kulikuwa kuna taa ya mwamvuli, na bado ilikuwa inawaka.
Alipepesa macho yake kukagua chumba kizima kabla hajafanya lolote. Mpaka muda huo hakuwa anajua chumba hicho ni cha nani na amefikaje hapo. Alichokuwa anajua ni kwamba yeye ni mateka, na mara ya mwisho akiwa fahamuni alikuwa amefungiwa kwenye kiti na amegoma kula wala kunywa.
Mbona yupo kitandani?
Akatupia shuka lake kando na kujaribu kuketi kitako. Mwili ulikuwa unamuuma sana. uso wake ulikuwa mwekundu, maungio ya mikono yake yalikuwa mekundu. Mgongo wake ulikuwa unatoa jasho la damu.
Kwa maumivu hayo lakini akamudu kusimama na kutembea kwa hatua chache kwenda ukutani. Aliona picha ya mwanamke hapo na mtoto mdogo wa kiume. Akaitazama picha hiyo kwa umakini akijaribu kushirikisha akili yake. Lakini hakupata kitu!
Akiwa anachechemea kwa maumivu, akauendea mlango na kuusukuma. Ulikuwa wazi, usifungwe na komeo. Hakuusukuma kwanguvu, akiwa na lengo la kuchungulia, ili basi kama ni adui ajue ni namna gani atakabiliana naye.
Alivyotupa macho, akaona taswira ya Jona. Mwanaume huyo alikuwa amekaa kwenye kiti akipitia karatasi ya mchoro, ule ambao aliletewa na Panky toka kwa Marwa. Macho yake nyuma ya miwani yalikuwa yanaenda huku na huko. Juu ya meza kulikuwa kuna kikombe cha chai, karatasi tatu nyeupe, kalamu ya risasi na rula ndefu.
Nade akasimama kwa sekunde kumi na tano akimkagua mwanaume huyo aliyekuwa kifua wazi, ndani ya bukta fupi ‘timberland’.
“Karibu na pole,” Jona akasema akiwa anaendelea kutazama karatasi yake. Nade akajikuta anatabasamu baada ya kugundua ameonekana, akiwa anajivuta kwa maumivu, akasonga na kuketi kwenye kiti.
“Kumbe ni wewe,” Nade akasema akimtazama Jona.
“Nikupatie chai?” Jona akamkarimu Nade.
“Hapana, nashukuru. Nipo sawa.”
“Haupo sawa. Najua haujala kwa muda wa siku tatu. kila chakula ulicholetewa ulikuwa unafanya kukimwaga kwa kukipiga teke. Tumbo lako linahitaji kinywaji cha moto kwa sasa kabla ya chakula … unajua kwanini? Kwasababu unaweza ukajikunja na kukusababishia matatizo.”
“Umejuaje kama nilikuwa sili?”
“Sidhani kama ni siri hiyo, Nade.”
Jona akaamka na kuifuata chupa ya chai akamimina kiasi kwenye kikombe na kumkabidhi Nade. Alafu kwa ukimya, akaendelea kufanya kazi yake ya kupekua ile karatasi, na muda mwingine akiwa anachorachora vitu vyake ambavyo Nade hakuwa anavielewa.
“Ile picha ni ya mkeo na mtoto wako?”
Jona akamtazama Nade kama mtu ambaye hakuamini kusikia swali hilo.
“Picha ipi?”
“Kule chumbani ukutani.”
“Ndio,” akajibu kwa ufupi.
“Wako wapi? Sijawahi kuwaona.”
“Chai itapoa, hakikisha unamaliza upesi,” Jona akasisitiza. Nade akatabasamu na kupiga mafundo mawili ya chai. Macho yake hayakukoma kuendelea kutazama huku na huko.
“Najua mpaka umekuja kuniokoa kuna makubaliano mliyoyaweka. Unaweza ukanishirikisha?”
Jona hakujibu kitu, akaendelea kufanya kazi yake. Nade naye akalipuuzia hilo swali, akaendelea kunywa chai lakini sasa hivi akiwa anazingatia kile ambacho Jona alikuwa anafanya. Kukawa kimya kwa muda.
Kama dakika kumi na tano hivi mbele, Jona akapokea simu yake. Akaongea maneno machache tu akiahidi kufika ndani ya muda. Akanyanyuka toka sebuleni na kwenda chumbani.
Nade akanyakua makaratasi ya mwanaume huyo upesi na kuyatazama. Jona aliporejea, akawa tayari ameshamaliza haja yake.
“Twende kwa bosi wako,” Jona alisema akimwonyeshea Nade mlango. Nade akanyanyuka kwa taabu kabla ya Jona hajamshika mkono na kutoka naye ndani, Huko nje taksi ilikuwa tayari inawangoja, wakajiweka ndani na safari ya kwenda kwa Mheshimiwa ikaanza.
Ndani ya gari kulikuwa kimya. Jona alikuwa anatazama nje ya dirisha lililokuwa limezibwa na kioo. Pembeni yake Nade alikuwa ametulia tuli kama maji ya mtungi. Mbali na mlio wa gari, kwa mbali sana ndiyo ungeweza kusikia sauti ya redio.
Redio hii ilikuwa inaimba nyimbo za zamani, miaka ya themanini huko, na kwa uchache miaka ya tisini kipindi hicho muziki ukiwa muziki. Nyimbo hizi zilikuwa zinaendana na dereva wa taksi hii: mwanaume mweusi aliyepambwa na mvi kadha kwa kadha kichwani.
Derava huyu ndiye pekee anayeaminika na mheshimiwa Eliakimu kwenye mambo ya usafiri, ukimtoa dereva wake anayempeleka ofisini na kumrudisha nyumbani.
“Jona,” Nade akaita na kumshtua Jona. Jona akamtazama pasipo kusema jambo.
“Ule mchoro uliokuwa unautazama pale sebuleni, umeutoa wapi?” akauliza. Jona akampuuza, akaendelea kutazama nje.
“Naujua … naujua ule mchoro,” Nade akasema. Jona akurudisha upesi uso wake kumtazama.
“Umeujulia wapi?”
Hapo Nade akawa amekamata atensheni yote ya Jona. Mwanaume huyo alimtazama akiwa na kiu kubwa ya kujua.
“Nilishawahi kuuona mahali kama sijakosea. Kwenye mojawapo ya vipeperushi ama barua ya mheshimiwa.”
Jona akashangazwa. Mchoro huo ulikuwa na mahusiano gani na mheshimiwa? Alitaka kujua zaidi lakini hakupata majibu kwani Nade naye alikuwa mtupu asiyefahamu kwa kina.
“Nakumbuka siku moja niliuona. Sikuuliza kwa kuwa sikuona kama una maana ya kufanya hivyo,” alisema Nade. Akamuuliza Jona kama ana lolote la kumwambia kuhusu mchoro huo, Jona akamwambia pengine majibu yao watapewa na Mheshimiwa.
Baada ya hapo kukawa kimya tena. Lakini kichwani mwa Jona kukiwa na vurugu kwasababu ya mawazo mapya aliyopewa na Nade. Alijiona ana maswali mengi ya kujibiwa na mheshimiwa. Alijiuliza Eliakimu ni nani haswa asipate jibu.
Akiwa humo fikirani, anashtuliwa na sauti kubwa! Gari lao linayumba vibaya mno! Dereva anajitahidi sana kulimudu na kuliweka sawa. Jona anakuja kusoma mchezo, walikuwa wamepushiwa na gari moja kubwa jeusi, Toyota Prado. Na halikuwa mbali.
Bado dereva akihangaika kuweka matairi sawa, prado inashusha vioo, mkono mweupe uliobebelea bunduki aina ya SMG unatoka. Haraka Jona akapiga kelele:
“Lala chini!”
Mara risasi zinaanza kumwagwa kama njugu kushambulia taksi waliyomo Jona na wenzake. Dereva anakula risasi nne na kufa papo hapo. Taksi inaacha njia na kufuata fremu za maduka kwa kasi.
Sasa hakukuwa na namna la sivyo wanaenda kufa wote. Jona akajirusha upesi toka kwenye viti vya nyuma na kuudaka usukani tena huku akipambana na mwili mfu wa dereva. Akajitahidi kuwakwepa watu na mali zao japo hakufanikiwa kwa kiasi kikubwa, akapasua na kubinua nyungo za karanga na kadhalika.
Lakini hatimaye akafanikiwa kurejesha gari barabarani. Taharuki na makelele yakiwa yametamalaki, magari mengine yakiwa yamesimama ama kuhepa kujiepusha na hasara ama vifo!
Akiwa mtulivu, macho yake yakatazama gari lile lililokuwa linawashambulia, Prado nyeusi, basi akadhamiria kufanya jambo. Taratibu akaanza kuutafuta mwanya wa kuisogelea gari hilo ambalo kwa muda huo tayari yule mshambuliaji alikuwa ameurejesha mkono wake wenye silaha ndani.
Akayekwepa magari ya mbele na pembeni yake kwa ustadi. Kufanikisha adhma yake ikamlazimu atumie barabara ya wanaokuja, si wanaoenda kama yeye. Na hivyo basi ikamlazimu tena awe makini kupitiliza. Akifanya hayo Nade akajawa na hofu kubwa, hata akapiga kelele kumtaka Jona asitishe zoezi.
“Jona, are you crazy!” (Jona, umewehuka!) akawaka akiwa amejishikiza kwenye viti. “Stop the car! Simamisha gari!”
Lakini Jona hakujali, akaendelea kusaka lengo lake. Si kuwaua wale waliokuwa wanamshambulia, lah! Hakuwa na silaha pamoja naye ila alitaka kulitambua gari hilo vema na hata wale waliomo ndani.
Akajitengenezea vema kwenye kiti cha dereva baada ya kumsukumia dereva yule mfu kando. Akakanyaga mafuta na kuendesha atakavyo. Lakini bado muda ukawa haupo upande wake, chombo chake hakikuweza kufua dafu kupambana mwendokasi na Prado, akaachwa.
“Damn it!” akalaani akisaga meno. Akabadili mwelekeo akirejea nyuma kidogo na kisha akachukua njia ya kushoto. Mwendo ukabadilika, akawa anasukuma magurudumu kwa mwendo kati.
“Watakuwa ni wale watu! – wakina Nyokaa!” Akasema Nade. Bado moyo wake ulikuwa unaenda mbio asiamini kama ametoka salama kwenye yale mashindano.
“Hapana!” Jona akatikisa kichwa. “Sio hao unaowadhani.”
“Ni wakina nani basi kama si wao ambao wangefuata roho yetu?” Nade akauliza.
“Sijajua ni wakina nani ila sio hao unawafikiri. Mosi, hakuna mtu anayenijua kama mimi ndiye nahusika na kukuokoa isipokuwa mheshimiwa peke yake. Niliyatenda yote sura yangu ikiwa nyuma ya kinyago.
Pili, kabla sijafanya zoezi la kukuokoa nilifanya upekuzi wa mazingira yote, hamna mahali niliona lile gari. Haitaleta maana kusema wao wanahusika, labda tu kama tungekuwa tumetokea nyumbani kwa mheshimiwa, hapo tungesema walianza kutufuatilia tokea huko, maana makazi yake watakuwa wanayajua.”
“Sasa atakuwa ni nani?” Nade akashupaa kuuliza.
“Sijui ni nani,” akajibu Jona. “Ila atakuwa anawinda roho yangu, si yako!”
Baada ya nusu saa …
“Kwahiyo mwili wake upo wapi?” akauliza Mheshimiwa akiwa ameshikilia kiuno. Alikuwa amevalia kaushi nyeupe nyepesi na bukta iliyokomea juu ya magoti. Usoni akiwa amevalia miwani ya kusomea. Mkono wake wa kuume umebebelea gazeti.
“Upo ndani ya gari!” akajibu Jona.
“Kwahiyo hamjafanikiwa kabisa kugundua hao watu? Kabisa yani!”
“Sijafanikiwa, ila najua muda si mrefu ukweli utajiweka bayana.”
“Ebu twendeni kwanza ndani … tuingie ndani …” mheshimiwa aliwasukumizia Jona na Nade ndani huku akiperuzi macho yake huku na kule. Baada ya muda mfupi mezani kwao kukawa kumependezeshwa na vinywaji vilaini. Nade alikuwa ameketi kando ya Mheshimiwa, Jona akiwa amejitenga kwa umbali mdogo akiketi kwenye kiti cha kuwatazama.
“Hapa hapatakuwa mahali salama tena, ni kheri ukachukua tahadhari mapema,” Jona akashauri.
“Najua hilo na bila shaka umeshaliona. Nimeongeza walinzi sasa maradufu!”
“Sidhani kama watatosha, bado ni wachache. Adui yako ana jeshi kubwa, kwa idadi na hata nyenzo,” Jona akanguruma. “Nakushauri uwe makini zaidi.”
“Sasa Jona na ndiyo hapo sasa nami ninapokuja kwenye ombi langu. Najua endapo nikiwa na wewe basi nitakuwa salama salmini, mkishirikiana na Nade hapa. Walionaje hilo?” Mheshimiwa akatia nadhiri.
Kukawa kimya kidogo.
“Miriam yupo wapi?” Jona akauliza. Mheshimiwa akamtazama Nade kwanza kisha akaurejesha uso wake kwa Jona na kujibu:
“Yupo ndani.”
“Naweza nikamwona?”
“Ya .. yah! Unaweza ukamwona,” Mheshimiwa akajibu. Kukawa kimya kidogo.
“Ila si kwa sasa, Jona,” Mheshimiwa akapendekeza.
“Kwanini si sasa?” Jona akauliza. Mheshimiwa akawa kimya kidogo. Kisha akanyanyuka na kwenda ndani, baada ya dakika mbili akarejea akiongozana na Miriam aliyekuwa mchovu na mwenye huzuni. Alikuwa amevalia dera akitembea kama mwanamke aliyetoka leba.
Jona akamsalimu, hakuitikia. Akamrushia macho yake makali akiwa ameuvuta mdomo. Hakujalisha Jona ameongea kitu gani, yeye hakutia neno hata moja. Macho yake ndiyo yalibadilika rangi kuwa mekundu, na ndani ya kinywa chake akisaga meno.
Baada ya muda huo usiokuwa na matunda, mheshimiwa akamnyanyua mwanamke huyo kumrejesha ndani. Hapo sasa akaufungua mdomo wake akimtazama Jona. Akamlaani vikali akimrushia matusi.
“Sitakusamehe maisha yangu yote kwa kunileta jehanamu!”
Mheshimiwa akampeleka ndani ya chumba na kumfungia.
“Naweza nikaambiwa sasa nini kinaendelea hapa?” Jona akauliza akimtazama Mheshimiwa ndani ya mboni zake. Mheshimiwa akashusha pumzi, kisha akashushia na juisi yake ya komamanga.
“Jona, ni simulizi ndefu sana hii. Ni simulizi ambayo isingependeza kabisa kusikika kwenye masikio ya yeyote yule, haswa mtanzania. Ni simulizi ya kutisha ambayo yaweza kukufanya ukashindwa kulala kwa ndoto za jinamizi!”
“Nipo tayari kuisikia simulizi hiyo,” akasema Jona. Basi Mheshimiwa akamtazama Nade na kumpandishia kichwa pasipo kutia neno. Nade akanyanyuka, na kwa mwendo wake wa majeruhi, akasonga kuondoka zake.
“Jona,” Mheshimiwa akaita. “Mimi si kiongozi mzuri, si mfano wa kuigwa wala sistahili kuwepo kwenye kiti hiki. Ni mambo mengi nimefanya, na yote hayo ni kwa ajili yangu si kwa taifa wala wananchi. Kuna muda nafsi yangu inanisuta sana, lakini sina namna maana yaliyopita hayawezi tena kubadilika.
Nimeshaingia kwenye anga la wenyewe, nikavinjari ninavyotaka, kutua chini ni ngumu …”
Nade akarejea akiwa amebebelea kiboksi kidogo cha chuma. Akamkabidhi Mheshimiwa aliyekipokea kwa mikono miwili na kisha akakiweka mapajani. Akaendelea kunena akiwa anafungua kiboksi hicho.
“… maana nimeshazoea hewa ya huko juu kiasi kwamba naona nikitoa naweza nikafa kwa kukosa pumzi. Kutua chini kutaninyima uhuru niliozoea kwenye anga hilo … kwahiyo siwezi, siwezi tena kutua. Siwezi kurudi tena ardhini.”
Alipomaliza kusema hivyo, mara mkono wake ukatoka ndani ya kiboksi ukiwa umebebelea bunduki ndogo nyeusi. Akamnyooshea Jona.
“Na hivyo basi, haitakiwi mtu yeyote kujua kama nami ni rubani kwenye anga hilo. Ni siri inayotakiwa kudumu milele, na milele, amin,”
Akafyatua risasi mbili kutoboa kifua cha Jona. Kisha akaangua kicheko akirejesha bunduki yake ndani ya kiboksi.
“Kwaheri Jona, kwaheri katuandalie makao.”
Akamuita mmoja wa walinzi wake waliokuwepo nje, akaunyooshea mkono mwili wa Jona.
“Beba hiyo na nyingine ndani ya taksi, kaitupie mbali!”
“Sawa mkuu!”
“Hakikisha hakuna mtu anayekuona, wala anayekufuatilia. Sawa?”
“Sawa!”
Mwanaume huyo mpana na mrefu, akaubeba mwili wa Jona na kutoka nao nje, akautupia ndani ya gari kisha akaubeba na ule wa dereva taksi, alafu akatimka akienda anapopajua yeye kichwani. Kwenda kuitupa miili hiyo isiwahi kuja kujulikana!
Huko nje ya jiji la Dar akaishusha na kuitelekeza baada ya kuhakikisha yupo mwenyewe, na kweli alikuwa mwenyewe. Akajipaki kwenye chombo na upesi akatimka.
“Ndio, mkuu. Kazi imeshakwisha!” akaongea mtumishi huyo mwadilifu.
Baada ya lisaa limoja …
Mtumishi huyo akafungua mlango wa sebuleni na kuangaza macho. Sura yake imebeba hofu na mazingira yalikuwa tulivu mno. Mkononi mwake alikuwa amebebelea bunduki ndogo. Haikuchukua muda, akaona mwili wa mheshimiwa pamoja na wa Nade ukiwa umelala kwenye kochi, damu zinawatiririka vichwani! Akatahamaki. Akawatazama watu hao kwa macho ya bumbuwazi. Akakimbilia napo chumbani kutazama, Miriam hakuwapo! Chumba kilikuwa kitupu, mlango upo wazi.
Hakuamini kilichotokea, akarudi tena sebuleni na kumtazama bosi wake, kwa mbali alikuwa anahema na kumbe alikuwa amejeruhiwa na risasi kifuani na hapo kichwani alikuwa amepasuliwa na kitu chenye ncha kali.
Akamtazama na Nade, mwanamke huyo alikuwa ahemi kabisa. Hakuonyesha dalili yoyote ya uhai! Mara akasikia sauti ya kuguguma toka kwa mheshimiwa, upesi akamtazama. “Haaaammm … “
“Unasemaje mheshimiwa? …” akasema mlinzi yule akiweka sikio lake mdomoni mwa Eliakimu. Lakini hakusikia tena kitu, mheshimiwa akanyamaza na kutulia tuli.
Amekufa? mlinzi akajiuliza. Akamtikisatikisa mheshimiwa lakini hakufanikiwa abadani. Pengine alikuwa ameenda na maji!
Baada ya muda mchache mbele, waandishi wa habari na vyombo vya usalama vikajaa hapo kila mmoja akitenda kazi yake. Ikabainika wanaume watatu waliovalia vinyago usoni ndiyo walihusika ma mauaji hayo.
“Sijajua ni wakina nani na kwanini wamefanya haya mauaji!” Akasema Alphonce akimwambia Kamanda wa polisi mkoa.
“Hivi mtu huyu alikuwa na adui yoyote kisiasa?” Akauliza kamanda.
“Hapana! Labda pengine, huwezi jua.” Akasema Alphonce akiwa anatazama waandishi wa habari wakiwa wanajitahidi kurusha matangazo yao moja kwa moja. “Lakini mkuu …” Alphonce akataka sema kitu. Akamtazama Kamanda kwa uso wa ‘kumtonya’, wakaelekea ndani ya gari la kamanda huyo wapate kuteta. “Unaiona ile gari pale?” Alphonce akasema akinyooshea kidole taksi iliyokuwa imepaki kwenye ndani ya nyumba ya Eliakimu.
“Ndio, naiona. Ndiyo iliyobeba wauaji?”
“Hapana, ila ndiyo iliyombeba yule kasuku!”
“Kasuku? Una uhakika?” Kamanda akatahamaki.
“Ndio! nina uhakika asilimia mia saba. Ile kazi uliyotupa ya kummaliza ilikuwa inafanyika ndani ya lile gari!” “Alphonce, embu acha ngonjera. Nyoosha maelezo!”
“Lile gari ndilo lilimbebelea Kasuku leo, na kumbe lilimleta hapa. Wakati unahojiwa na vyombo vya habari nikachukua muda wangu na kulipekua. Lina matundu ya risasi na hata damu!” “Sasa huyo Kasuku hamkumuua?”
“Hapana, mkuu! Bila shaka atakuwa hajafa. Asingeweza fika hapa.”
“Na huyo Kasuku mule ndani hayupo?”
“Hayupo! Yupo mheshimiwa na mwanamke fulani ambaye alikuwa na Kasuku yule ndani ya hilo gari!”
“Sasa Kasuku atakiwa ameenda wapi? Au unataka kunambia yeye ndo atakuwa anahusika na haya mauaji? “Sijajua! Lakini atakuwa ana cha kueleza kuhusu haya mauaji.”
“Lakini Alphonce, unajua unaniangusha sana kwenye hili! Kwanini huyo mtu unashindwa kummaliza? Na kila kitu unacho!”
“Mkuu, Kasuku ni mjanja mno. Ila itafikia mwisho akaingia tegoni tu.” “Hakikisha hiyo siku na sisi tutakuwa bado tupo hai.”
“Usijali, mkuu!”
“Najali. Unadhani Kasuku huyu akija kutambua tumemuweka kwenye rada, huoni tutakuwa tupo hatarini? Kasuku yule ni mwekundu, na wa kijani! Anabadilika rangi kwa mujibu wa miale ya jua!” Kukawa kimya kidogo. Mara, Alphonce akashika kitasa cha mlango wa gari. “Nakuja!”
“Unaenda wapi?”
“Nimemwona mtu ambaye anaweza kutusaidia kumpata Kasuku!”
Kabla Kamanda hajasema neno, Alphonce akatoka ndani ya gari. Kamanda akabaki akimtazama wapi anaenda. Akamwona mwanaume huyo akienda kuongea na yule mlinzi aliyesalimika kwa kwenda kumtupa Jona. Akakodoa macho akifuatilia kila nyendo, punde akamwona Alphonce akimtaka mlinzi yule aelekee kwenye gari alilomo. Mlinzi huyo akatikisa kichwa ishara ya kukataa, Alphonce akamlazimisha kwa sura ya msisitizo. Mlinzi akaridhia, japo kishingo upande. Wakazama ndani ya gari wakiketi kwenye viti vya nyuma.
“Haya mwambie huyo!” Alphonce akamwamuru mlinzi yule. Alikuwa amejawa na woga, na macho yake yalikuwa mekundu.
“Tuliamriwa na mheshimiwa. Alikuwa tayari ameshakufa kwasababu ya majeraha ya ajali! Alifika hapa akiwa hoi sana. Hakuchukua muda,” mlinzi akalaghai. Mheshimiwa akatabasamu na kumtazama Alphonce kwa macho ya furaha.
“Mheshimiwa, ni mpaka tukihakikisha,” akashauri Alphonce.
Basi muda mchache tu, gari la Kamanda likatoka kuelekea kule ambapo Jona alitupwa wakielekezwa na mlinzi wa mheshimiwa. Ikawachukua kama dakika ishirini wakawasili.
“Ndipo hapa!”
Wakashuka na kusonga kwa ndani, wakauona mwili mmoja, haraka Alphonce akaukimbilia na kuchuchumaa kuutazama. Haukuwa wenyewe! “Nilijua tu! Huyu mbwa hawezi akafa kirahisi hivi!” Akasema Alphonce akisimamama.
“Una uhakika ilikuwa hapa?” Kamanda akamuuliza yule mlinzi.
“Ndiyo, ni hapa kabisa!” Akajibu mlinzi akipepesa macho yake huku na huko. “Nakumbuka nilimtupia hapa!” Akanyooshea kidole.
“Basi atakuwa ameondoka,” akajibu Alphonce, “ila nadhani hatakuwa mbali!” Wakatafuta pasipo majibu. Jona hakuonekana wapi ameenda. Kumaliza ushahidi, Alphonce akammaliza Mlinzi kwa kumnyonga na kumtupia ndani ya msitu!
“Hakikisha mtu huyu anapatikana na kuuawa! Hakikisha hilo Alphonce!” Alisema Kamanda aking’ata meno. Usiku wa saa sita, La Palma Pub
“Nataka kuhama pale!” Akasema Glady baada ya kupulizia moshi wa sigara kando. “Unaenda wapi sasa na kama unavyojua kodi ya pale angalau unaweza kumudu? Au umepata danga jipya mwenzetu?” Mwenzake akauliza. Wote walikuwa wamesimama nje ya pub wakiwa wanavuta sigara. Glady alikuwa amevalia sketi fupi nyeusi na topu nyeupe yenye maneno ya kichina. Mwenzake akiwa amevalia sketi nyekundu yenye mpasuo mpaka kwenye nyonga. “Hamna si mambo ya madanga wala nini, sema nataka kubadili mazingira tu!” “Umeanza lini hiyo tabia Glady?” “Nitaanza hivi karibuni.”
Mara mwenzake na Glady akatazama barabarani na kisha akajinyooshea kidole kifuani. Mara akamtazama Glady na kumwambia kwa sura ya kinyonge: “Unaitwa kule!”
Glady kutazama akaona prado nyeusi. Kioo cha dereva kikashushwa vema, Alphonce akaonekana vema, akamfanyia ishara ya kumwita.
“Kwaheri shost, baadae!” Glady akaaga na kwendaze. Akapanda gari na kuondoka hilo eneo, mwenzake akimtazama.
Ndani ya muda mfupi, mwenzake huyo akasikia simu yake ikinguruma. Akaitoa na kutazama:
“Shosti lazima nipige mshindo kesho tukatumbue!” Ilikuwa ni ujumbe toka kwa Glady. Mwenzake akatabasamu na kuviweka vidole kwenye kioo cha simu, akaandika na kutuma:
“Kamua haswa shoga angu, nakuaminia!” Akausindikiza ujumbe huo na tabasamu. Akatazama na mambo mengine ndani ya simu yake kabla hajairudisha kwenye mkoba na kuendelea kusimama. Saa tisa usiku … Kwachu Best Lodge, Kimara. “Mimi siwezi kutumia kondom kabisa,” alisema Alphonce. Alikuwa amekaa juu ya kitanda akiwa amevalia bukta fupi na yu kifua wazi. Glady alikuwa amebakia na sidiria na kufuli tu, vyote rangize ya pink. Yeye alikuwa amejilaza kitandani. “Hatujakubaliana kavu!” Akaropoka Glady. “Ukitaka kavu basi ongeza pesa!” Alphonce akacheka.
“Na vipi kama nisipokupa hiyo pesa? Utafanya nini?” Akauliza kisha akawasha sigareti yake aliyoiweka mdomoni na kuanza kuifyonza. Macho yake yamelegea ila imara. Mdomo wake ulikuwa mkavu ukipinda mithili ya wa samaki.
“Kwanini usinipe?” Glady akauliza. “Si naamua tu,” Alphonce akajibu. Glady akamtazama kwa macho ya hasira pasipo kusema kitu. Ndani yake alishaanza kutengeneza hofu juu ya mwanaume yule. Hakuwa mtu mzuri.
Lakini kwa mujibu wa fikra zake, ni kama vile aliona kitambulisho cha polisi ndani ya gari la mwanaume huyo. Mwanzoni alijihisi salama, kumbe alikosea.
Akili yake ikaanza kurukaruka na kutambalia mazingirani. Akiwa anawaza, mara Alphonce akanyananyuka na kumwambia: “Nakuja, jiandae!”
Akaelekea chooni kukojoa baada ya kuweka kipisi chake cha sigara kwenye kisosi cha kioo kilichokuwa kipo juu ya kistuli. Aliporejea, akadaka kwanza sigara yake na kupiga pafu mbili za kumalizia.
Lakini kabla hajajimwaga kitandani, akaanza kupoteza uwezo wake wa kuona. Alikuwa anaona kama ukungu mbele yake na kichwa kikawa kinamzumguka, akachukua dakika mbili tu, akadondoka chini kama mzigo! “Ms*nge wewe!” Glady akasema kwa kebehi kisha akanyanyuka toka kitandani na kumtazama Alphonce.
Alikuwa anavuja damu sakafuni. Haraka Glady akavaa na kisha akatoa chupa ya mafuta na kitambaa.
Akalowanisha kitambaa mafuta kisha akapaka kwenye nyayo ya kushoto ya Alphonce na mafuta kidogo akayamiminia chini.
Alafu akaenda zake akiwa kabebelea kila kitu cha Alphonce!
Saa saba mchana, Tikko Hotel ghorofa ya nne.
“Niliona hii sehemu itatufaa sana,” akasema Boka akitazama huku na huko ingali akiketi. Alikuwa amevalia suti nyeusi ya kujichana ikirandana na mwili wake. Kwenye kamfuko ka koti mkewe alikuwa ameweka kijiua kidogo rangi nyekundu, kikivutia na kunogesha vazi.
Mbele yake alikuwa ameketi mwanamke mrembo Miranda. Nywele zake akiwa ameritachi na kuzimwagia kushoto. Kope za macho yake zilikuwa zimesimama dede akirembua. Lips zake zilikuwa rangi ya pink akinukia kama bustani ya kando ya mto.
“Una uhakika?” Akauliza Miranda.
“Aaaah! Unadhani nakutania?” Boka akajoki, “Hapa pametulia sana na hapana macho ya watu wengi si unajua bana siku hizi kila mtu ni mwandishi wa habari wa kujitegemea!”
Wakacheka, kabla hawajamaliza mhudumu akawa amefika. Akawauliza ni nini wanataka, wakaagiza chakula na vinywaji.
“Hivi kuna siku ulisahau kupendeza kweli? Umependeza haswa!” Boka akamsifia Miranda kisha akashushia na kinywaji.
“Ahsante, ila sijakuzidi wewe,” Miranda akapokea sifa kwa sauti ya deko huku akipambana na kisu cha chakula.
Wakapiga stori kwa muda kidogo kabla hawajazama kwenye lengo la kijikao chao. Boka akasafisha koo na kusema:
“Bila shaka umeshaingia ubia na mke wangu. Nilipata kuwaona juzi mkiwa mnajinasibu mbele ya vyombo vya habari. Ni hatua nzuri.”
“Ahsante, vipi ulinionaje? Nilikuwa sawa? Maana sikuwa comfortable kabisa!” Akalalama Miranda akiwa ameacha kula na kumkodolea Boka.
“You were fine! Sikuona tatizo, nilikuwa nawatazama nikiwa ofisini kwangu and felt very proud.”
Miranda akashukuru akitafuna.
“Nataka kukuoa, Miranda. Nataka uwe mke wangu wa pili,” Boka akasema huku anamtazama Miranda kwa jicho lisilo na utani.
“You must be joking, Boka!” (Utakuwa unatania Boka) akajibaraguza Miranda. “Mie niwe mkeo?”
“Kwani haiwezekani?”
“Haiwezekani!”
“Kwanini?” Boka akaacha kula.
“Kwasababu siwezi kugombania pakuo na mwanamke mwenzangu,” akasema Miranda.
“Una maanisha nini?” Boka akauliza.
“Boka,” Miranda akaita. “Mafahari wawili hawakai zizi moja. Unadhani msemo huu ulikosewa?”
“Sasa wataka nifanyaje Miranda na mie ilhali nishazama kwako. Mguu hautaki chomoka kabisa.”
Miranda hakusema kitu. Akatafuna kwanza na kisha akanywa kinywaji chake rangi nyekundu ndani ya glasi yake yenye kiuno chembamba. Kisha akamtazama Boka kwa jicho la kike.
“You want to have me?” (Unataka kuwa nami?) “Yes, I really do.” (Ndio, nataka haswa.)
“But are you ready to do what it takes to have me?” (Lakini uko tayari kufanya namna ukanipata?)
“Yes, I am. But please don’t tell me to abandon my wife.” (Ndio, ni tayari. Lakini tafadhali usiniambie nimwache mke wangu.)
Miranda akacheka.
“Usijali, ila nikuweke wazi nashindwa kukupa jibu la moja kwa moja.”
“Tena?”
“Nop! Si hivyo, I mean unajua kama nina mlezi. Nisingependa kufanya jambo hili siri. Ningependa tukamshirikisha.”
Boka akaguna. Akala na kunywa kwanza kabla hajatia neno.
“It’s ok! Ila huoni kama italeta matatizo na wewe hujaafiki kuwa mke kwangu?”
“Let us give it a try,” akasema Miranda. “Mlezi wangu ni mzungu, huwezi jua.” Akaongezea: “kama wanipenda kweli, kweli, basi nitajua kwa hatua zako.”
Muda si mrefu, ujumbe ukaingia kwenye simu ya Miranda toka kwa BC. Alikuwa anataka kuonana naye hivi punde. Lakini kabla hajasema dhamira yake ya kuondoka, Boka akapigiwa simu na akamtaka waende maana yampasa afike ofisini.
“Basi twaweza tumia gari langu hamna shida,” Boka akapendekeza. Wakapanda gari na kumpitisha Miranda nyumbani kwa BC.
“Ndipo hapa?” Boka akauliza.
“”Ndio, karibu.”
“Ningeingia na kusalimu, sema nahitajika kwa haraka ofisini.”
“Sawa, usijali. Hamna shida,” Miranda akasema na kisha akaaga na kujiendea zake ndani. Akamkuta BC akiwa amelisimama ghorofani akiwa anaangaza macho. Mkononi, mzungu huyo alikuwa amekamatia glasi ya mvinyo. Mwili wake akiuhifadhi kwa shati la “beach boy” alilolichomeka ndani ya suruali yake nyeusi ya kitambaa.
“Hellow, is that the man?” (Habari, yule ndiye yule jamaa?) Akauliza BC akitazama barabara.
“Yah! He is the one. Very soon he will be here talking to you.” (Ndiye mwenyewe, muda si mrefu atakuwa hapa kuongea nawe.)
“That’s nice! You know I called you here to talk about Eliakimu. Have you heard news about him?” (Hilo ni jema! Unajua nimekuita hapa kumuongelea Eliakimu. Umesikia habarize?)
“No! What is it?” (Hapana! Kuna nini?)
“He’s passed away! Some people ambushed and killed him!” (Amefariki! Watu fulani wamemvamia na kumuua!)
Miranda akashangazwa. Akauliza zaidi kuhusu hiyo habari, BC akampatia ‘full mkanda’.
“So from now on we’ll be free to move on.” (Kwahiyo kuanzia sasa tutakuwa huru kuendelea,) akasema Miranda akionyesha kuvutiwa.
“Yes, but I wonder who killed him. I know he had been involving in several crimes, but his killing will leave us safe?” (Ndio, lakini najiuliza nani kamuua. Najua alikuwa akijihusisha na uhalifu kadhaa, lakini kifo chake kitatuacha salama?”
Miranda hakuwa na jibu. Akaguna na kuhema akifikirisha kichwa chake. Mara akakurupuka na swali:
“About the news … where was he killed?” (Kuhusu hiyo taarifa … wapi ameuawa?)
“At his home!” (Nyumbani kwake!)
“All alone?” (Peke yake?)
“Yes. Heard only about him.” (Ndio. Nimesikia kumhusu yeye tu.)
“Sure?” (Hakika?)
“Yes. What’s wrong?” (Ndio. Nini shida?) BC akauliza akimtazama Miranda kwa macho ya kina.
“No – no nothing!” (Hamna kitu!) “Are you sure you don’t have anything to share?” (Una uhakika hauna kitu cha kushirikisha?)
“I think somebody may have the answers,” (Nadhani kuna mtu anaweza kuwa na majibu,) akasema Miranda akitazama kando kwa mawazo.
“Who is it?” (Nani huyo?) BC akawahi kuuliza.
“The girl whom Eliakimu lived with,” (mwanamke aliyekuwa anaishi na Eliakimu.) Kisha akaongezea:
“I think we should look for her.” (Nadhani tuna haja ya kumtafuta.)
“But where? I went there, the house is empty!” (Lakini wapi? Nilienda kule, nyumba ni tupu!)
“There must be a way. We must find Nade where she is. And if we wont find her, then I will be convinced that she is the one who is responsible.” (Kutakuwa na namna. Ni lazima tumtafute Nade alipo. Na kama tusipompata, basi nitaamini kwamba yeye ndiye mhusika.)
BC akanywa kinywaji chake, akatazama barabarani akiwa amekunja mdomo.
***
“Bosi, una mgeni,” akasema mlinzi akimwambia mwanaume wa kichina aliyekuwa ameketi kwenye kochi akisoma gazeti.
Mwanaume huyu wa kichina kwa jina lake halisi anaitwa Foang. Ni mfanyabiashara mkubwa wa vyombo maeneo ya Kariakoo. Ana miliki maduka matatu makubwa akiwa ameajiri watu kadhaa.
Mwanaume huyu ndiye yule aliyeletewa nyaraka na wakina Mustapha kwa dhumuni la kuwasaidia tafsiri. Tangu siku ile amekuwa akisaka nyaraka hiyo pasipo mafanikio. Hivyo moyoni amekuwa na kama donda sugu ambalo lilishapewa dawa kisha ikashaisha. Sasa anaisaka kwa udi na vumba!
Anataka nyaraka hiyo kwa gharama yoyote ile. Kwani ni pesa! Pesa kubwa ambayo inazidi hata mara hamsini ya mtaji wake. Unalalaje sasa? Vipele vya baridi humtoka kila anapofikiria nyaraka hiyo.
Anafahamu ni kwa namna gani atafanya biashara safi ndani ya mji wa Hongkong. Pasi na shaka alikuwa anajiona karibu kabisa na tajiri namba moja barani Asia – Alibaba!
“Mwambie aingie!” Akasema Foang pasipo kumtazama. Macho yake yaling’ang’ania kwenye maandishi ya gazeti, ila alikwishajua ni nani mgeni wake huyo. Hakuwa na haja ya kuhangaika.
Punde, mlango unafunguliwa akaingia mwanaume aliyeshiba. Alikuwa amevalia suti rangi ya brown, koti kubwa kidogo kuvuka mwili wake. Mwendo wake ni wa hatua nzito, akaketi kwa kishindo na kusalimu.
Alikuwa ni Alphonce! Alikuwa ana bandeji kubwa kichwani kwake kwa nyuma. Uso wake ulikuwa umefuma kwa hasira na pembeni ya jicho lake la kushoto alikuwa amevimba. Macho yake yalikuwa mekundu akitengeneza ndita.
Foang akaweka gazeti lake pembeni, akamtazama Alphonce. Kwa dakika kama moja hakunena kitu. Bila shaka alishangazwa na muonekano wa Alphonce, ila hakutaka kujisumbua nao akamuuliza:
“What have you brought on the table?” (Umeleta nini mezani?)
Alphonce akasafisha koo lake kisha akazamisha mkono wake ndani ya koti na kutoa simu. Akailaza mezani. Foang akatabasamu kabla hajainyaka simu hiyo na kuikagua kwa kuigeuzageuza.
“Is this the one?” (Hii ndiyo yenyewe?) Akauliza Foang.
“Yes it is. I got it from the man who was left. I’ve already finished him!” (Ndio yenyewe. Nimeipata kwa yule jamaa aliyebaki. Tayari nimeshammaliza!)
Foang akatabasamu zaidi. Ila akakunja sura yake na kuuliza:
“Are you sure you’ve finished?” (Una uhakika umemaliza?)
“He doesn’t breath anymore,” (Ahemi tena) Alphonce akasema kwa uhakika.
“And about the police?” (Na kuhusu polisi?)
“Told you before. I am the only police whom you should worry about.” (Nishakuambia hapo kabla. Mimi ndiye polisi pekee wa kumhofia.) Kisha akauliza:
“Where my money at?” (Pesa yangu ipo wapi?)
“Where are you rushing at?” (Unakimbilia wapi?) Foang akauliza.
“Let me inspect the phone first!” (Acha niikague simu kwanza!)
Kabla hajaifungua simu, Alphonce akamdaka mkono wake na kumwambia:
“Till I see my money first!” (Mpaka nione pesa yangu kwanza!)
Macho ya Alphonce yalikuwa hayana utani hata kidogo. Hakuwahi na utani kwenye pesa tangu azaliwe. Kwake pesa ndiyo kitu cha thamani maishani. Amezaliwa atafute pesa! Na kutumia pesa! Kuhusu kiapo cha kazi ya upolisi, uzalendo na mambo ya ujamaa, hayo unaweza ukabaki nayo. Yeye mpe pesa! Kama unataka uendelee kuvuta pumzi ama kuishi kwa amani.
Foang akamtazama mwanaume huyo machoni. Akajifunza kweli hana utani. Hata akaogopa. Akatabasamu na kupandisha mabega yake:
“I still depend on you, Alphonce. I can not cheat on you.” (Bado nakutegemea, Alphonce. Siwezi kukulaghai.)
Alphonce hakusema kitu, akaendelea kumtazama na macho yaliyotoa ujumbe tosha. Foang akanyanyuka na kwendaze chumbani, muda si mrefu akarejea na bahasha ya kaki aliyomkabidhi Alphonce.
Alphonce akatupia macho yake ndani ya bahasha, akatabasamu na kunyanyuka akimpatia mkono Foang.
“I think I should go.” (Nadhani napaswa kwenda.)
“But I have not yet inspected the phone!” (Lakini bado sijaipekua simu!) Akalalama Foang.
“Just do it then you will inform me. You know my contacts, right?” (We fanya alafu utanitaarifu. Unajua namba zangu, sio?)
Hakungoja Foang aseme neno, akaenda zake Foang akimsindikiza kwa macho. Mchina huyo hakuwa anajua cha kufanya, akaishia kumtazama Alphonce akiyoyoma.
Alphonce akaweka bahasha yake kwenye kiti cha pembeni, akatekenya funguo na kutoka ndani ya nyumba ya Foang kwa kasi. Haikupita punde, simu yake ikaita. Ilikuwa ndani ya mfuko wa koti, akaichomoa na kuitazama kwa kuibia. Alikuwa ni kamanda.
“Ndio, mkuu … muda si mrefu sana n’takuwa hapo … serious? … sijatazama na wala sijasikia kabisa! … sawa! … sawa.”
Simu ikamuacha ameachama mdomo. Alikuwa amekunja sura, macho yake yakiwa yametambaliwa na utashi wa fikra. Habari alizozipokea zilimshangaza, na kumpatia mawazo. Zilimfanya kwa muda asahau kwamba alikuwa ameweka ‘manoti’ kadhaa kwenye kiti cha pembeni yake akiwa ameziingiza kwa ‘kazi ndogo’.
Akashusha pumzi ndefu. Akasonya na kutikisa kichwa. Lakini ajabu, ghafla akasikia kitu cha baridi shingoni kwake! Akatazama kupitia ‘sight mirror’ akamwona mchina akiwa amemuwekea ‘chuma’, macho ameyakaza wakitazamana kiooni.
Alikiwa ni Lee!
“Habari za muda mrefu, Alphonce.”
“Hivyo ndiyo namna ya kumsalimu rafiki yako ambaye hamjaonana kwa muda mrefu?”
“Si hivi, bali kwa kutoboa shingo yake na risasi! Rafiki hawi tena rafiki anapouarua mgongo wa rafiki yake aliyemkabidhi aukune.”
“Una maanisha nini Lee?”
“Unajua ninachomaanisha. Peleka gari makaoni kabla sijakugeuza nyakati iliyopita … na unafahamu vizuri kwamba sitanii.”
Alphonce akamtazama Lee kiooni. Lee akamtazama Alphonce kiooni. Macho yao yalikuwa yanasema mengi zaidi ya maneno waliyoyatamka na vinywa. Macho haya yalikuwa ya janja janja! Macho ya kizandiki!
Macho ya njama!
Akilini mwa Alphonce kulikuwa kuna mafikirio, kama ilivyokuwa kwenye bongo ya Lee. Alphonce hakuwa tayari kwenda popote pale akiongozana na Lee. Mosi, kamanda anamngojea ofisini. Pili, ilikuwa ni ombwe kwake juu ya anachoenda kukutana nacho huko apelekwapo.
Akili yake ikabidi ifikirie namna ya kujinasua. Hakuwa na budi kumzidi akili Lee kisha atokomee zake! Basi akakaza mkono kwenye usukani wa gari. Akiwa katika mwendo wake wa kasi, akaanza kuhesabu kimoyomoyo, mdomo wake ukiwa unachezacheza kwa mbali.
1 … 2 … 3 … 4 …
… 5!
Akakanyaga breki kwanguvu! Lakini asifahamu kilichotokea, akajikuta hana fahamu baada ya kuhisi amegongwa kwanguvu chini ya kisogo.
Akazama kizani!
—
Robo saa mbele …
Gazeti linatupiwa juu ya meza ya kioo, Kamanda akasonya na kunyanyuka akifuata kabati. Anatazama saa yake alafu anasonya tena. Anachukua faili rangi ya samawati, nalo analirushia mezani.
Anasimama na kufikiri jambo. Akajirejesha kwenye kiti chake na kunyakua simu yake nyeusi, SONY toleo jipya, akapiga. Simu ikaita pasipo kupokelewa. Akapiga tena, haikupokelewa!
Akaweka simu mezani na kulaza kichwa chake kwenye kiti. Akazunguka kwenda kushoto na kulia, kulia na kushoto akitazama feni yake darini.
Lile faili alilolitoa kabatini, hakuonekana kuligusa wala kuwa na mpango nalo. Mezani, kwa mbele yake, ungeweza kuliona gazeti la Habari Leo likiwa na picha ya wanaume wawili waliokuwa wamelala chini, wamejeruhiwa na kutapakazwa damu.
Kwa juu ya picha hiyo ikisomeka kichwa cha habari chenye maneno meusi:
*”WATU WAWILI WAMEUAWA KINYAMA NA MTU ASIYEJULIKANA.”*
Chini ya maneno hayo, kwa mtu mwenye macho ‘mepesi’ angelisoma tena maneno yenye ukubwa wa saizi ya kati yaliyoandikwa kwa wino wa kijani:
“Watu hao watuhumiwa kuwa majambazi, na wameuawa kwa mkono wa siri.”
Chini ya kichwa hicho, kulikuwa na habari kamili sasa ikiwa imeandikwa kwa maneno madogomadogo, ngumu kuonekana kwa macho ya wazi yaliyo mbali. Na mbele kidogo ya taarifa hiyo ikalekezwa kuendelea ukurasa wa tatu.
***
Usiku wa saa mbili …
Baada ya sauti ya vishindo vya miguu, inafuata ya mlio wa mlango kisha Jona anaingia ndani ya makazi yake akiwa anachechemea.
Anawasha taa na kujitupia kwenye kochi kama mzigo. Akahema kwa mafundo makubwa makubwa mara tano kabla hajavua nguo yake ya juu na kubaki na kaushi ya kuzuilia risasi.
Akafungua kaushi hiyo kwa nyuma kisha akaiweka mezani. Kifuani kwake kulikuwa kuna majeraha, kwa mbali kulikuwa kuna rangi nyekundu ya kuvilia damu.
Kabla hajafanya kitu kingine chochote, akanyanyuka na kwenda chumbani akiwa anapepesuka. Alipofika mlangoni, akadondoka chini kama mzigo, akapoteza fahamu!
Baada ya kama dakika tano akiwa hapo chini, taratibu, kwa mbali akaanza kupata taswira ambazo hakuzielewa. Taswira hizi zilikuwa zinakatiza upesi kichwani kwake mithili ya mwanga wa radi!
Kulikuwa na sauti ambazo hazikueleweka. Mayowe na nderemo za kifo. Na mara sauti za watu waliomezwa na giza wakiwa wamebebelea maginga ya moto!
“Amepita wapi?” Sauti moja ya mwanaume ikauliza. Giza lilikuwa pana kiasi cha ginga la moto kutofua dafu!
“Huku! … Amepita huku!” Akasema mwanaume mwingine upesi!
Mara tih! Tih! Tih! Vishindo vikaenda huko na kupotelea gizani.
Jona hakutikisika. Na hakuonyesha dalili ya kuamka karibuni. Masikioni hakusikia tena kitu, na machoni akawa mpofu.
***
Saa sita usiku.
“Bosi nadhani kuna mtu getini,” akasema mlinzi baada ya kugonga mara mbili mlangoni, Foang akatoka akiwa amevalia taulo.
“Who is it?” (Nani?) Foang akauliza. Macho yake madogo ya kichina yalikodoa, mkono wake wa kuume ulikuwa umeshikilia taulo lake lisianguke.
“Bwana mi sielewi! Spiki kiswahili” akalalama mlinzi.
“Nani? Nani huyo?” Foang akafoka kwa lafudhi ya puani.
“Sijui nani? Hauna appointment na mtu?”
“No! No! No appointment!” Foang akatikisa kichwa, kisha akamtaka mlinzi aende, akafunga zake mlango!
Akiwa ndani ya chumba akasimamisha masikio yake apate kusikia kila jambo linalotukia huko nje. Lakini hakusikia hata lepe. Zikapita mpaka dakika nne … tano … sita …
Akaulaza mwili wake kwa amani. Akazima taa, na bunduki yake ndogo ambayo alikuwa ameshaisogeza karibu akaisokomezea chini ya mto.
Kabla hajabebwa na usingizi, akasikia hodi mlangoni. Akalalama na kutusi. Aliona sasa huyu mlinzi ameshindwa kazi, na akaapa kumfunda adabu huko mlangoni aendapo.
Akajikwamua kitandani na kupiga hatua tatu ndefu. Akafungua mlango kwa hasira na kuangaza. Uso kwa uso akakutana na bomba la bunduki!
Alikuwa ni Lee!
Akamwamuru atoke na kumpatia simu aliyopewa na Alphonce. Na akitumia lugha ya kichina, akamuuliza kama amefanya lolote na ile nyaraka. Foang akatikisa kichwa chake upesi, akakana katukatu!
Kuhakiki, Lee akapekua simu ile kwa haraka. Alipomaliza, akamuaga Foang na kisha akamzamishia chuma cha risasi kichwani! Akatoka zake ndani ya jengo kwa kuchumpa ukuta.
Dakika kumi na tatumbele …
“Ndiyo hii?” Akauliza Lee akimwonyeshea simu Alphonce aliyekuwa amefungwa kamba kitini. Walikuwa ndani ya chumba kidogo ndani ya makazi ya Lee. Kulikuwa kimya sana, kama si maongezi haya ungeliweza dhani hapana mtu.
“Ndiyo yenyewe!” Alphonce akajibu kwa kiburi. “Nifungilie basi niende!”
“Bado sijamalizana na wewe,” Lee akananga akitikisa kichwa. Akaketi na kumuuliza Alphonce:
“Niambie ni nani aliyekuwa anawasiliana naye?”
“Mzee!” Alphonce akaita. “Hilo mimi silijui. Kazi yangu ilikuwa ni kutafuta hiyo simu tu!”
Kabla Lee hajaongeza kauli ujumbe ukaingia kwenye ile simu, haraka akatazama. Ilikuwa ni barua pepe toka kwa mtu aliyetunzwa kwa jina la Chen Zi. Lee akalazimika kufungua barua hiyo na kuitazama.
Asiamini macho yake, aliona nyaraka ile, anayoipambania iwe siri, ikiwa imeshatumwa kwenye historia ya maongezi. Na huyu bwana Chen Zi alikuwa yupo huko Hong Kong, China!
Akahisi kuishiwa nguvu. Akapiga moyo konde na kusoma maongezi ya barua pepe ile mwanzo mpaka mwisho. Alipomaliza, akaiweka simu chini akisaga meno. Alipandwa na hasira mno. Alikunja ngumi yake kubwa akifuma ndita.
Akamtazama Alphonce kwa hasira, na mara akanyanyuka na kuchomoa bunduki yake akamuwekea kwenye paji la uso. Hakusema kitu, macho yake yalikuwa tayari mekundu. Akabinua mdomo na kufyatua kitufe cha bunduki!
Klick! Hakuna kitu. Klick! Klick! Klick! Hamna kitu, risasi zilikuwa zimeisha. Kwa hasira akaitupia bunduki mbali Alphonce akishusha pumzi ndefu ya neema.
Akatoka ndani ya chumba na kwenda kuketi sebuleni akiwa ametingwa na mawazo lukuki. Aliwaza, je kuna haja ya kumshirikisha Sheng kwenye mkasa huu?
Vipi kama Sheng akijua hizi habari, ambazo amejitahidi kuziweka chini ya kapeti akashindwa, atafanya nini na atamfanya nini?
Akajikuta akitetemeka mikono.
Kama kuna usiku ambao uliwahi kuwa mgumu kwake, basi ni huu. Hakupata usingizi kabisa. Kichwa chake kilikuwa kinatepeta mawazo. Alijazwa na hofu moyoni.
Baada ya kufikiria kwa muda, aliona kuna haja ya kushirikisha wenzake, pengine wanaweza kumpatia mawazo mbadala maana aliona kichwa chake hakifanyi kazi tena.
Akawatafuta kwa kuwapigia simu lakini hakuwapata. Pengine walikuwa wamepumzika vitandani mwao. Akaona afanye kazi hiyo asubuhi na mapema, japo kishingo upande maana aliona kama anapoteza muda.
Akaendelea kugaragara kitandani, akaichukua ile simu na kuitazama tena. Akapitia zile jumbe za barua pepe kati ya Foang na Chen Zi. Akahisi moyo wampasuka.
Alitamani kurudisha hali lakini haikuwa inawezekana. Akawaza sana kuhusu yule Chen Zi. Alikuwa ni nani, na kwanini Foang amtumie ujumbe kama mtu wa kwanza.
Kwakuwa hakuwa na usingizi, akaona si mbaya akautumia muda wake huo kusaka taarifa za Chen Zi ndani ya mtandao.
Akiwa amekodoa akatafuta jina hilo huku akiwa ameliambatanisha na Hong Kong, punde chache Chen Zi ikaja ikiwa na majibu kadha wa kadha, lakini haswa lililotamalaki lilikuwa ni jina la Chen Zi aliyetambulishwa kama msanii maarufu wa miondoko ya pop nchini China, Hong Kong.
Lee akafuatilia taarifa za msanii huyo akiwa ameshavunjika moyo kuwa si mtu anayemhitaji. Na kama haitoshi, alipochekechua taarifa za mtu huyo akaja gundua Chen Zi alikwishafariki, tena mwaka jana kwa kuzidisha dozi ya madawa ya kulevya!
*”CHEN ZI ‘THE ROCKER’ DOPPED TILL DEATH” (CHEN ZI ‘MTUMBUIZAJI’ AMEZIDISHA DAWA MPAKA KIFO)*
Mojawapo ya kichwa cha habari kilisema vivyo. Akatazama na majibu mengine ya Chen Zi akapata kuona watu wa mitandaoni haswa Facebook. Akasonya na kutoka mtandaoni.
Kitu alichotokea kuamini ni kuwa Chen Zi atakuwa si mtu maarufu mitandaoni. Akawaza sana asilale mpaka asubuhi. Akadhamiria kuwasiliana na Bigo ampe ushauri.
***
Macho ya Jona yalikuja kufunguka akiwa kitandani. Amechoka na mwili ukiwa mzito. Akakohoa na kukunja shingo kutazama kando.
Hakuelewa nani aliyemuweka hapo kitandani, alipatwa na hofu lakini mwili wake haukumruhusu kunyanyuka.
Hakumwona mtu kwa muda wa dakika kama mbili. Hatimaye akamwona mwanaume akiingia, akakaza macho kumtazama akagundua ni Panky. Angalau akawa na amani.
“Unaendeleaje?” Panky akamuuliza akitabasamu kwa mbali. “Ni kama bahati kuja hapa, nilikukuta chini ukiwa hujitambui.”
Jona akamshukuru kwa msaada wake. Akajitahidi sana kuketi wakati Panky akimuuliza nini kilijiri akawa kwenye hali ile. Kabla Jona hajamjibu, akamuuliza kwanza kama kuna habari yoyote kumhusu mheshimiwa Eliakimu.
Panky akahamaki. Akatikisa kichwa chake na kuanza kueleza juu ya habari ya kuvamiwa na kuuawa kwa mheshimiwa huyo. Habari yake imesambaa jiji zima na kuzua taharuki.
“Ninavyokuambia mpaka sasa, hakuna mtu aliyekamatwa.”
Jona akatulia kwanza. Alikuwa anawaza juu ya hayo aliyoambiwa akichambua kwanini mheshimiwa aliuawa. Na tena ndani ya muda mfupi tangu aondolewe pale.
Kichwani akayapata majibu kuwa ahusikaye hapo si mwingine bali wale waliomteka Nade. Kutoonekana kwa mke wa mheshimiwa, kulithibitisha mawazo yake hayo.
Baada ya muda mfupi wa kuwaza, kwa akili yake timamu, Jona akamwambia Panky kuwa anahitaji kurejea jeshini. Panky akashangazwa na maamuzi hayo, lakini Jona akajitetea kuwa hiyo ndiyo njia sahihi ya kukamilisha anachokitaka.
“Panky, nahitaji covering. Nahitaji authority kwenye mikono yangu. Nahisi kuna haja ya kurejea kukamilisha mambo kadhaa.”
Aliposema hayo akaendelea kuwaza. Panky akamhitaji apumzike kwani amechoka sana. Lakini kabla ya kupumzika, Jona akamuuliza kuhusu ile picha. Ni wapi amefikia.
Panky akatabasamu kwanza kabla hajajibu. Akamshika Jona bega na kumweleza kuwa hicho ndicho kilimleta hapo. Na anashukuru kwa maana kama asingelikuja basi angelimpoteza.
“Nimeshapata zile code. Huwezi amini! Na mpaka sasa nashawishika kuamini kuwa ile picha ni siri kubwa ya Sheng! Si bure alikuwa anaitafuta.”
Panky alisema kwamba Marwa ndiye aliyemsaidia kung’amua code za picha hiyo baada ya kumshawishi sana na kumuahidi usalama wake kwa gharama yoyote ile. Akampatia “x-ray pictures” ambazo alimtaka azihifadhi sana, akiwa ameziiba toka kwenye tarakilishi ya ‘administator’ wa kitengo chao.
“Ni kwanini Marwa amekuamini kiasi hicho?” Jona akataka kujua.
“Marwa, ni zaidi yangu. Ni mjuzi wa mambo makubwa sana na ni mtaalamu sana wa mambo haya, lakini hafanyi kazi ile kwa kupenda bali kulazimishwa. Kila mwisho wa mwezi, mbali na kulipwa pesa, hupewa ‘antidote’ kwa ajili ya kuwapatia wazazi wake ambao walidungwa sindano na Sheng.
Kama Sheng asipompatia antidote hiyo wazazi wake hawatachukua hata dakika tano, watafariki dunia!”
Jona akasisimkwa na hiyo simulizi. Akatamani hata kuonana na Marwa, lakini Panky akamwambia watalifanya hilo taratibu mbeleni kwani hakumwambia Marwa juu yake.
“Nilichomwambia ni kwamba hii inaweza ikawa namna ya sisi kujikomboa. Kama unavyojua, hatukuwa na muda mrefu sana wa kuteta. Tunapokuwa kazini huwa tunatazamwa kila saa.”
Baada ya maongezi hayo machache, Panky akamwachia Jona bahasha ya kaki ambayo ilikuwa na taarifa zile alizomweleza. Akamwambia anapaswa kwenda kwani kuna mahali anatakiwa kupitia.
***
Saa kumi na moja jioni, Monduli, Arusha.
“Anapoelekea, atakufa,” Roba alisema akiketi chini. Akamtazama Nyokaa aliyekuwa anavuta bangi akitazama zake bustani. Ni ndani ya nyumba ya wastani yenye bati la bluu.
“Amekula?” Nyokaa akauliza.
“Hajala, analia tu anataka unga,” Roba akajibu kisha akapokea kipisi cha bangi toka kwa Nyokaa naye akawa anakipiga pafu.
Wakawa wanateta juu ya Miriam – mke wa mheshimiwa. Mwanamke huyo alikuwa hoi chumbani akiwa hataki kula wala kunywa chochote isipokuwa heroine. Amekuwa akitetemeka mwili na kuharisha.
“Unadhani ni muda wa kuachana naye sasa?” Akauliza Roba.
Nyokaa akatikisa kichwa chake akikakataa. Akasema hata kama kazi yake ya kuwachomesha ‘ma-broker’ wa madini, ambao ni majamaa wa Eliakimu imeshafanyika, bado wanamhitaji mwanamke huyo. Watamtumia hata kujaribishia madawa.
“Akifa tutamtupia huko mtoni!” Akahitimisha Nyokaa kabla ya kumuuliza Roba juu ya kazi yake aliyoifanya kwa mheshimiwa.
“Roba, yule mwanamke haikupasa umuache hai kabisa. Siwezi nikakaa kwa amani chali’angu. Anaweza akatuchoma.”
Nyokaa akataka Roba amtafute Nade na kuhakikisha anakufa kwa njia yoyote ile. Mara ya mwisho alisikia amelazwa Aga khan kwa mujibu wa vyanzo vyake vya habari.
Alipomsisitizia hilo, akanyanyuka kwenda kumuona Miriam. Akamkuta akiwa amejikunyata. Nywele zake zilikuwa vurugu mwili wake aliokunyata ukiwa ndani ya dera la njano.
“Miriam, mbona hutaki kula?” Akauliza akichuchumaa. Miriam hakujibu zaidi ya kumtazama kwa jicho la husda.
“Inabidi ule, sawa?” Nyokaa akamshika Miriam. Mara Miriam akaanza kububujikwa na machozi yasiyo na kikomo. Kifuani mwake alikuwa anaumia. Maisha yake yalikuwa yameharibika na hakuwa na namna tena kuyarejesha kama hapo awali.
Leo amekuwa mtu wa kuvuta unga! Pua yake haikuwa kawaida asipotia kitu hicho mwilini. Amekuwa mdhoofu na asiyevutia tena. Zaidi ya yote, mwanaume aliyemuingiza huko akiwa ni yule aliyempenda na kumtumaini.
“Nyokaa,” akaita kwa sauti ya chini, kisha akasema:
“Sitakusahau maishani mwangu. Na Mungu wangu aliye juu atakulipia.”
Nyokaa hakujali hayo maneno. Kwake hilo lilikuwa ni dua la kuku kwa mwewe. Akatabasamu na kunyanyuka akisema:
“Utakapojisikia kula, utasema sawa? Sina muda wa ngonjera hapa.” Kisha akaondoka zake akimwacha Miriam akiendelea kumwaga machozi akimshuhudia mwanaume huyo akiyoyoma.
Saa nne asubuhi, ofisini kwa Kamanda wa mkoa.
“Mkuu, una ugeni,” alisema mwanaume mkakamavu ndani ya sare ya jeshi la polisi. Kamanda pasipo kumtazama, akamtikisia kichwa kama ishara huku macho yake yakiwa yameganda kwenye gazeti la MAMBOSASA alilolijaza mkononi.
Punde kidogo, Kamanda akasikia sauti ikimsalimu. Sauti hii ikamfanya abandue macho yake gazetini na kumtazama mgeni huyo nje ya miwani yake ya kusomea. Akastaajabu ni yule mwanaume aliyekuwa anamtafuta.
“Ooh Jona! Karibu sana!”
Jona akashukuru na kuketi. Wakasalimiana, Kamanda akijawa na tabasamu. Lakini haikuchukua muda kwa Kamanda kujua kuwa Jona hakuwa sawa kiafya.
“Vipi, upo sawa?” Akauliza. Jona akalazimisha tabasamu akijibu:
“Nipo sawa.” Kisha akaeleza haja yake iliyomleta pale pasipo kupoteza muda. Kuwa anataka kurejea kwenye jeshi kama alivyokuwa akisisitiziwa.
Kamanda akastaajabu kwanza kabla ya kulipuka kwa cheko la furaha. Kwake hizi habari zilikuwa za kufurahisha ambazo hakuzitarajia kabisa! Hatimaye mbuyu ulikuwa umeangushwa chini.
Akamkabidhi Jona mkono wa pongezi na kusifia maamuzi yake hayo.
“Hapo sasa, umeamua kiume, Jona!”
Lakini pia akataka kujua sababu iliyomfanya Jona arejee jeshini ingali alipingana na hoja hiyo kwa muda mrefu.
“Nimerudi kumalizia kazi zangu nilizoziacha kiporo,” hilo likawa jibu la Jona kabla Kamanda hajampatia tena mkono na kumuahidi ushirikiano kwenye kutimiza adhma yake hiyo.
“We unaweza kwenda sasa, kesho ukarejea hapa majira ya asubuhi. Kuna mambo machache yanipasa kuyakamilisha ili kuweka vitu sawa,” alisema Kamanda. Jona akaenda zake.
Kabla ya kurejea gazetini, Kamanda akatambaliwa na mawazo kichwani. Akalaza kichwa chake kwenye kiti akizunguka kwenda kushoto na kulia huku akitafakari jambo lile la Jona.
Ingawa alifurahishwa nalo, lilimpatia walakini kwa kiasi chake. Ni ‘kiporo’ gani hicho Jona anachotaka kuja kumalizia ndani ya jeshi?
Pengine akawaza Jona atakuwa ameng’amua hila zake za kumtesa ili arejee jeshini na hivyo basi amekuja kumuadhibu? Akawaza. Alitamani sana kufahamu nyuma ya ‘kiporo’ cha Jona, na basi kujiweka salama kwenye bandari hii, akaona ni vema kumtaarifu Alphonce. Wanatakiwa kuwa makini na nyendo za Jona. Lakini mwanaume huyo hakuwa anapatikana tokea jana yake alivyomuita ofisini!
Basi akajikuta hana namna zaidi ya kungoja akiwa amedhamiria kama leo hatomwona Alphonce, inabidi juhudi za makusudi zifanyike kumtafuta.
Akashika gazeti lake, lakini kabla hajaanza kulisoma, akasikia mtu akiingia.
“Samahani sana, mkuu!” Alikuwa ni Alphonce! Alikuwa amevalia suti rangi ya kahawia, koti limemzidi kipimo. Akasimama kwa ukakamavu kutoa salamu kisha akaketi.
Kabla ya kuulizwa, akaanza kujitetea kwa Kamanda ni kwanini alishindwa kutimiza agizo lake la kufika ofisini jana yake.
“Nilipata ajali, mkuu. Sikuwa na uwezo wa kuwasiliana nawe pia kwani simu yangu iliibiwa.”
Kamanda hakuwa na muda wa kupeleleza maelezo hayo ya Alphonce, donge lilikuwa limemkaba shingoni kungoja, akamwambia kuhusu habari za Jona kurejea jeshini.
Kamanda akavuta kwanza pumzi akiweka kituo. Alafu akamwambia Alphonce juu ya hofu yake.
“Unadhani mkono wake utatuacha salama?”
Alphonce akaangua kicheko. Hakuona sababu ya kuhofia. Akamwambia Kamanda wake kama Jona angekuwa anataka kuwamaliza wala hakuwa na sababu ya kurudi jeshini kwani angeweza kutimiza haja yake hiyo hata huko nje.
“Tujipongeze maana hila zetu zimefanikiwa,” akasema Alphonce na kuongezea: “ametambua kuwa maisha yake hayawezi kuwa sawa akiwa nje ya jeshi.”
Lakini bado Kamanda hakujiona mjinga. Bado aliona kuna haja ya kumtazama Jona kwa darubini ya pekee hivyo akamuagiza Alphonce kutenda hilo.
Alphonce aliyekuwa hana shaka akalipokea hilo jukumu.
… lakini hakujua uzito wake kamili.
Akiwa ndani ya daladala kurudi kwenye makazi yake, Jona aliyekuwa ameketi kwenye viti vya nyuma kabisa, alikuwa anawaza juu ya kile alichokiona kule ofisini.
Macho yake yalikuwa nje ya gari lakini ndani ya mawazo. Kichwani kwake taswira ya gari aina ya Prado nyeusi ilikuwa inamjia. Gari lililomwagia risasi nyingi akiwa anaelekea nyumbani kwa Eliakimu ndani ya taksi.
Mbona ameliona gari hilo pale ofisini kwa Kamanda? Akakumbuka pia na taswira ya mwanaume anayemtambua akishuka toka kwenye gari hilo. Alikuwa amevalia suti kubwa ya kahawia – suti inayofanana na ya yule aliyeambiwa na shuhuda kuwa ndiye muuaji wa Jumanne, mshirika wake kwenye biashara ya kuchora na kuuza picha!
Taswira hizo mbili zikamnyima raha. Zikampa ukweli mchungu kuwa Kamanda anahusika na jaribio lake la kumuua, vilevile la kuharibu biashara yake. Haswa kwanini?
Akakumbuka kauli aliyoambiwa na Kamanda kwa mara ya mwisho alipoonana naye ofisini kwake. MAISHA YAKE KAMWE HAYATAKUWA SAWA NJE YA JESHI. Hatomtafuta tena, bali ni yeye atakayemtafuta.
Akashtuliwa na kondakta akidai nauli. Akatoa nauli hiyo na muda si mrefu akashuka toka chomboni, akishkuru kondakta kumshtua kwani hakuwa anafahamu kama alikaribia, kisa mawazo.
“Umeshampatia chakula?” Akauliza Nyokaa akiwa anamtazama kijakazi wake – mwanaume mrefu mweusi aliyevalia nguo iliyombana kifua chake kipana.
“Bado, mkuu!” Akajibu kijakazi kwa ukakamavu.
Nyokaa akamtazama kwa ukali na kufoka kwanini kijakazi huyo hajampatia Miriam chakula mpaka muda huo? Kijakazi akajibu kwa unyenyekevu kuwa mwanamke huyo hali hata pale anapompatia.
“Kutokula siyo kazi yako, bali kumpatia chakula!” Nyokaa akafoka na kumtaka mwanaume huyo haraka iwezekanavyo kwenda kumpatia Miriam chakula, naye akaenda pasipo kupoteza muda.
Nyokaa akisonya, akaketi chini na kumpigia simu Roba.
Roba alikuwa yupo Dar es salaam. Kazi yake kama alivyoagizwa ilikuwa ni kumtafuta na kumuangamiza Nade ili kumaliza chembe ya ushahidi iliyobakia. Punde simu ilipokelewa, Nyokaa akaulizia ni wapi Roba amefikia.
“Nimeshafika hospitali. Ni kitendo cha muda tu kumaliza kazi.”
Nyokaa akamwambia afanikishe hilo upesi arudi Monduli kwani kuna kazi za kufanya. Roba akamuahidi ushindi.
Alipokata simu, Roba akashusha pumzi na kutazama hospitali iliyokuwa imesimama mbele yake. Alikuwa ndani ya taksi, akalipa pesa ya nauli kisha akashuka.
Mwanaume huyu alikuwa amevalia tisheti nyeusi yenye alama ya fuvu jeupe, na chini akijisitiri na suruali ya jeans na moka nyeusi.
Alikuwa na muda mchache wa kumalizana na kazi yake hapo. Alizama ndani ya hospitali na ndani ya muda mfupi akawa ameshafika stoo ya hospitali.
Mwendo wake akifanya kitu moja kwa moja kilithibitisha kwamba ana ramani ya hospitali kichwani mwake, na alishapanga jambo hilo mapema kichwani mwake.
Ndani ya muda mfupi, akawa ameshavalia koti jeupe la daktari, shingoni amezungushia kipima mapigo ya moyo, akiwa anatembea kwa kujiamini.
Akaelekea kwenye wodi za gharama, zikiwa zimegawanywa kwa vyumba vyumba vya wagonjwa binafsi.
Akafungua mlango wa chumba cha kwanza kabisa kukutana nacho, akazama ndani na kumkuta Nade akiwa amejilaza anasaidiwa na mashine kupumua.
Akahakikisha mlango umefungwa vema, alafu akachomoa sindano yenye kimiminika rangi ya ‘green’ na kukidungia ndani ya mfuko wa dripu. Haraka alipofanya hivyo, akatoka ndani ya chumba hicho na kupotea!
Baada ya muda wa kama dakika kumi, dripu ile ikaishilia mwilini mwa Nade. Zikapita dakika kama tano, mwili wa Nade ukaanza kubadili rangi kuwa wa njano!
***
“Tayari, nimeshakamilisha!” Sauti ya Roba ikavuma kwa simu.
“Sawa sawa. Rudi sasa nyumbani na ndege ya jioni,” Nyokaa akanena na kisha akakata simu kabla hajaja kupokelewa na sauti ya kupaza ya kijakaziwe.
“Mkuu, yule mwanamke ametoroka!”
“Mwanamke?” Akastaajabu Nyokaa. “Mwanamke yupi?” Akawahi kuuliza akisimama upesi toka kwenye kiti chake cha kuvinjari.
Kijakazi akasema ni Miriam. Nyokaa kwa hasira akakimbia mpaka kule Miriam alipokuwa amehifadhiwa, hakumkuta!
Akalalama na kutusi. Akaamuru Miriam atafutwe akitishia hakuna mtu atakayebaki hai kama asiporudi na mwanamke huyo.
Wanaume wakazagaa kumtafuta ‘teja’ huyo kwa udi na uvumba.
***
Saa kumi na mbili jioni.
“Ameshafika!” Miranda alisema kwa tabasamu pana akiangaza getini. Alikuwa ndani ya nyumba ya BC kwa juu kabisa akiwa anaangaza kama atamwona mgeni wake akiwa anakuja.
Alikuwa amependeza kwa kuvalia gauni safi linalometameta dhidi ya giza jepesi la jioni. Nywele zake zilikuwa zimerembwa na uso wake ameupara.
Alikuwa ana hamu sana ya kumwona Boka. Alipoona gari la mwanaume huyo likiwa limefika, moyo wake ukawa wa baridi kwani ‘alishampanga’ BC vya kutosha.
Boka anakuja kama alivyomuahidi.
“He is here!” (Yupo hapa!) Rhoda alimwambia BC aliyekuwa ameketi kwenye kiti cha kaunta ndani ya nyumba yake akiwa anakunywa wiski.
BC naye kwa kujiandaa na kikao na Boka, alikuwa ‘amekula’ suti nyekundu na tai nyeusi. Japokuwa kupendeza ni kawaida yake, leo alikuwa zaidi.
Alimtaka Miranda akampokee mgeni na baada ya utambulisho aende ndani, kila kitu atakifanya yeye.
“Are you sure you won’t need me?” (Una uhakika hautonihitaji?) Miranda aliuliza kabla BC hajamtikisia kichwa kama ishara ya ndio. Miranda akaendaze.
Lakini kwa kutaka kujua kitakachoongeleka, akajibana mahali ambapo angepata kusikia maongezi.
“Glad to see you. My daughter’s been telling me about you,” (Nimefurahi kukuona. Binti yangu amekuwa akiniambia kuhusu wewe,) alisema BC kwa tabasamu akimpatia mkono Boka.
Wakateta kwa muda kidogo kupeana historia juu ya wapi walikutana na kuanza kutengeneza mahusiano na Miranda. Baada ya hapo BC akaenda kwenye kitovu cha kikao.
Pasipo kupepesa macho akamuuliza Boka kama kweli yu radhi kuwa na Miranda. Boka akakubali kwa kuwahi kujibu. Lakini BC akarudia kumuuliza mara tatu kabla ya kumwambia:
“Then there is a little sacrifice you have to make.” (Basi kuna sadaka ndogo ya kutoa.)
Boka akasimamisha masikio yake asikie. BC akamweleza kuhusu biashara yake, akihitaji msaada wa mheshimiwa huyo kuingiza ‘madawa’ yake nchini.
Kwa mara ya kwanza Boka akadhani ni madawa ya kulevya. Moyo wake ukaenda mbio mno kabla hajapata angalau ahueni baada ya BC kumwambia ni madawa ya kutibia binadamu.
“Where are you taking them to?” (Unayepeleka wapi?) Akauliza Boka. BC akamwambia yeye hufanya biashara ya kuuza hayo madawa huko Msumbiji, Zambia na Zimbabwe kwa bei ya juu.
Lakini Boka alikuwa na hofu na hakuweza kutoa jibu la moja kwa moja kabisa kwa BC. Hata mikono yake ilikuwa inatetemeka akashindwa kubebelea kinywaji. Akaomba aende zake.
“So what about it?” (Kwahiyo vipi?) BC akauliza. Boka akabanwa na kigugumizi. Akaomba apewe muda kwani jambo hilo ni zito mno. Si la kulichukulia kiurahisi hata kidogo.
Hakumkubuka hata Miranda, akaenda zake akijawa na mawazo kedekede kichwani.
“Do you think it will work?” (Unadhani itawezekana?) Miranda akamuuliza BC akiketi.
“I don’t know. Let’s see!” (Sijui. Acha tuone!) BC akajibu alafu akashushia na wiski.
Boka akafika nyumbani akiwa ametingwa na mawazo hata mkewe akafahamu japokuwa hakuwa radhi kumwambia nini kimemsibu.
Akajilaza akiukosa usingizi akiwaza nini afanye. Katikati ya usiku akapokea ujumbe kwenye simu. Mkewe akawa wa kwanza kuinyaka simu.
Moyo wa Boka ulikuwa unapiga mafundo makubwa makubwa pindi mkewe alipokuwa anatazama simu yake. Aliwaza atakuwa ni nani amemtumia ujumbe, na kwa haraka akili yake ikaegemea kwa BC.
Hakutaka mkewe ajue kinachoendelea kati yake na mwanaume huyo, sasa akadhani siri yao imeingia mchanga.
“Ni nani huyu?” Akauliza mwanamke akimkabidhi simu Boka. Boka akaipokea na kutazama, akajikuta anashusha pumzi ndefu baada ya kugundua si kile alichokuwa anakiwaza.
Alikuwa ni mfanyakazi mwenzake akimsihi kesho awahi kazini wapate kupangilia mambo ya kikao.
Lakini haikupita muda, simu yake ikaingia ujumbe. Ilikuwa ni bahati yake kwani kwa sasa ujumbe ulikuwa umetokea kwa Miranda na simu ikiwa kiganjani mwake.
Kwa muda kidogo akachat na Miranda, muda huo mkewe akiwa anadhani anachati na rafiki yake.
Mwanamke huyo, Miranda, alikuwa anamjulia hali na akimtaka amwambie ni wapi amefikia kwenye maongezi na ‘baba mkwe’ wake bwana BC.
Pasipo kusita, Boka akaonyesha hofu yake juu ya kile alichoambiwa na ‘mkwewe’ lakini kwa wakati huo akijitahidi kumwonyesha Miranda kuwa anampenda na si kwamba hafanyi jitihada.
Naye Miranda kwa maringo, akiwa anajua kidonda kipo wapi, akafanya kumtia hamasa Boka kwamba anataka kuwa naye kwa hali na mali.
“Tafadhali, fanya juu chini mpenzi. Tusiishie njiani.”
Boka akiwa ameshikwa na kigugumizi cha vidole akamwomba ampatie muda kidogo. Na pia mazingira hayakuwa mazuri kuteta kwani mkewe anaweza kumpoka simu muda si mrefu.
Hivyo, wakakata maongezi. Tena baada ya Miranda kumtumia mwanaume huyo maneno matamu ya kumpa moyo. Na kisha bwana Boka kufuta chati zao za kidhalimu.
Akaweka simu kando na kumtazama mkewe, alikuwa amelala. Akashusha pumzi ndefu na kutazama paa. Hakujua ni muda gani usingizi ulimnyakua.
***
Saa mbili asubuhi, ofisi ya kamanda polisi mkoa…
Hodi ndogo iliita kisha ikaruhusiwa kuingia ndani. Alikuwa ni Jona akiwa amevalia suti rangi ya udongo, aliketi kisha akamsalimu kamanda.
“Naona umefika on time!” Kamanda akasema akitabasamu. Pasipo kupoteza muda akanyanyuka na kwenda kabatini alipotoa kiboksi cha chuma alichokiweka mezani na kukifungua, alafu akamsogezea Jona.
Ndaniye kulikuwa kuna vitu ambavyo Jona alivikabidhi siku alipoacha kazi.
“Tulijua utarejea, shida hatukujua ni siku gani haswa,” alisema Kamanda akiketi. Akamwambia Jona kuwa kila kitu kipo sawa, na haikuwa shida sana kwani hakuwa amemuondoa kwenye orodha ya watumishi wake, na siku zote hizo alikuwa akihesabu kama anaumwa.
Lakini kabla ya kuendelea na majukumu yake, Kamanda akamsihi Jona kwamba kila atakachokuwa anafanya hatakuwa na budi kueleza kwa mkubwa wake.
Naye hakuwa mwingine bali Alphonce!
Jona akastaajabishwa na hilo, lakini hakuweka bayana. Alifahamu fika, yeye na Alphonce walikuwa sawa kwa cheo, iweje awe chini yake?
Kabla hajanyanyuka, Kamanda akamwambia kuna kazi kedekede za kuzifanya tangu uongozi mpya uingie madarakani. Wamekuwa wakihofia usalama wa nchi kutokana na kulegalega kwa mahusiano ya kidiplomasia na nchi jirani, kwahiyo atakuwa akisafiri mara kwa mara, haswa mikoa ya mipakani, ajiandae kwa hilo.
“Unajua mimi ni kama daraja tu la kukufikia wewe … unahitajika nchi nzima, na kila mtu ndani ya jeshi anatambua mchango wako. Wanategemea makubwa kutoka kwako.”
Baada ya maongezi hayo, Jona akanyanyuka na kwenda zake. Huku nyuma Kamanda akapiga simu na kumtonya Alphonce yaliyoendelea.
Jona alienda kantini akaketi hapo akinywa kikombe cha chai taratibu, akiwaza. Alikuwa aking’amua na kupanga nini aanze kufanya sasa kati ya yale yaliyomrejesha jeshini.
Akaona ni busara akifanya kazi ya mikono misafi kwanza, kisha akamalizana na ile itakayomchafua. Aanze kwanza na maadui wa nje, alafu atarudi nyumbani.
Akiwa hapo anakunywa chai kusindikizia mawazo, akaona gari lile prado nyeusi ikiingia. Kwa macho yake thabiti akafuatilia lile gari, akamwona Alphonce akishuka, amevalia koti refu jeusi akaangaza na kuzama ndani.
Kifuani mwake alikuwa ana jambo la wazi linalomkereketa kumhusu huyu mwanaume. Aliamini siku yake itafika na atajaa mikononi mwake, akiomba msamaha abakiziwe roho yake.
Baada ya Alphonce kupotea, Jona akarejea kwenye mawazo yake ya awali. Akalipia chai na kutoka ndani ya eneo lile la ofisi ya Kamanda, akaelekea Aga Khan hospital kwa lengo la kuonana na Nade.
Alishapata taarifa kuwa mwanamke huyo yupo huko akiwa hajifahamu tangu tukio la mauaji ya Mheshimiwa lipate kutokea. Alikuwa ana machache ya kuongea naye.
Akawaza sana kwanini mwanamke huyo alimgeuka ilhali alimsaidia dhidi ya mikono ya mbwa mwitu wasio na huruma. Ilikuwaje upesi wakamgeuka na kulenga kumuua?
Akakiri na moyo wake kwamba kuna kitu kikubwa ambacho hawakutaka kabisa akifahamu. Na sasa Mheshimiwa ameenda na siri yake kifuani.
Kama Nade asipokuwa hai, basi hakutakua na masalia yoyote sasa.
Aliomba Mungu amkute kama alivyodhamiria.
Akawasili hospitali na basi kwa kutumia kitambulisho chake akapata mwanya wa kumfikia daktari aliyekuwa anahusika ma mlengwa wake.
Daktari huyu alikuwa mwanaume mnene mwenye asili ya India. Alimtazama kwanza Jona kisha akamwambia ana bahati sana, kwani mgonjwa alikuwa amepitia tundu la sindano kubaki kuwa hai.
“Alizidiwa?” Jona akataka kujua.
“Hapana!” Daktari akatikisa kichwa. “Aliwekewa sumu kwenye dripu!”
Wakati huo walikuwa wanatembea kwenda kumwona Nade.
“Nani alimtilia sumu?”
“Hakuna anayejua. Ila kuna videos za CCTV zilizomuonyesha mtu huyo ambaye hatujamtambua mpaka sasa.”
Wakafika kwa mgonjwa, Jona akamtazama kwa ukaribu. Alikuwa ana rangi ya njano kwa mbali ngozini, anahema kwa msaada wa mashine na kucha zake zilikuwa zina michirizi meusi.
“Kama tungekawia hata kwa sekunde tatu, asingekuwa hai!” Daktari akasema kwa kujiamini.
Jona akamwomba ampeleke akaone hizo video za CCTV.
Pasipo kusita daktari akamuongoza mpaka mahala pa kutazamia video alipowakuta wanaume wawili waliomsalimia na kumsaidia kuiona video aitakayo.
Alipotazama vema, akajikuta anatabasamu mwenyewe na kujisemea kifuani.
“Nilijua tu,” baada ya kumwona Roba akiwa anatoka ndani ya chumba.
Sasa alikuwa amethibitisha aliyeshiriki tendo la kumuua Nade ni Roba, yaani Nyokaa. Na wao pasipo shaka ndiyo ambao walifanya tukio lile la kumuua Mheshimiwa Eliakimu!
Akapata mawazo sana alipokuwa hapo. Mosi, wapi Miriam atakuwapo? Wanamfanyia nini na kwanini hao wanaume wanamhitaji kiasi hicho? Pili, wanahusika na biashara gani haswa?
Akajikuta ana kazi ya kwenda tena kule alipomuokolea Nade akawakute wanaume hao. Lakini pia apate mwanya wa kuonana na Nade, akipata ahueni, ili apate kumweleza anachokijua.
Akashusha pumzi ndefu kisha akaandikisha baadhi ya maelezo na kwenda zake baada ya kuahidi atarejea. Lakini akasihi juu ya usalama wa Nade, kwa upande wake atahakikisha anapatikana askari wa kuja kumlinda.
Akatoka ndani ya hospitali na kuangaza magari yakikatiza, akaweka mikono mfukoni na kuambaa akifuata kituo cha magari.
Lakini kuna mtu alikuwa anamtazama. Mtu huyu alikuwa amevalia koti refu na kofia ya kizee iliyomeza kichwa chake.
Baada ya Jona kusonga umbali wa kutosha toka hospitali, mtu huyu akatoka alipokuwa amejibanzia, mstimu, kisha akazama ndani ya hospitali akitembea kwa tahadhari.
Mwanaume huyu alikuwa ni Alphonce!
Kazi yake hapa ilikuwa moja tu, kujua nini Jona amekuja kufanya hapo? Ndani ya muda mfupi, akitumia nafasi yake, akawa amefika mbele ya kitanda cha Nade akimtazama mwanamke huyo kama mtu aliyemfananisha.
Kichwani kwake alikuwa anafikiria mambo kadhaa. Alisonya alafu akatoka kuongea na daktari.
“Kuna kingine?”
“Hapana, yote tumeshaeleza kwa askari aliyekuja awali.”
“Nataka unieleze na mimi pia hayo yote!” Akaamuru Alphonce. Basi ikambidi Daktari arejelee yale aliyomwambia Jona, na tena zaidi kwani Alphonce alikuwa anataka kila ambacho Jona alikifanya.
Alipomaliza akatoka zake ndani mpaka kwenye gari lake alipotulia na kupiga simu kwa Kamanda akampa taarifa.
“Sijajua, ila bado wanamuwinda kumuua!”
“Na picha umeiona?” Akauliza Kamanda.
“Ndio, ila sura ni ngeni. Bila shaka ndiyo hao hao waliomuua Eli! … kuna haja ya kuifuatilia?”
“Hapana! Anayejua ya kesi hii kwa undani ni Jona. Kuna vitu anavifahamu kuliko sisi, na kama alikuja huko ina maana ameamua kuivalia njuga. Mwache aendelee nayo, cha muhimu ni kumfuatilia tu!”
Alipokata simu, akakanyaga mafuta na kuyoyoma toka eneoni.
Ambacho hakukijua ni kwamba, hata wakati anatoka, Jona alikuwa anamuona! Alimwona tangu anaingia ndani ya hospitali na hata pale alipotoka!
Ni vile alikuwa anajua kwamba atafuatiliwa.
Akatikisa kichwa chake akibinua mdomo. Gari la Alphonce lilikuwa linaishia machoni. Akakuna kidevu chake na kushusha pumzi ndefu, kisha akajikuta anatabasamu.
“Keep your friends close, but your enemy closer!” (Waweke marafiki zako karibu, lakini maadui karibu zaidi!) Jona alijisemea kisha akanyanyua mguu kuchukua hatua.
***
“Ameamka!” Mtoto mdogo wa kike alimwambia mama yake. Haraka mama akaamka na kukimbilia ndani kutazama.
Ndani ya nyumba hii iliyochoka, kulikuwa kuna samani mbovu, mazingira yasiyovutia. Joto na pia kiza.
Mwanamke huyu akiwa ameongozana na mtoto wake, walifika ndani ya chumba chao kimoja, wakatazama kitandani. Kulikuwa kuna mwanamke amejilaza hapo kitandani kana kwamba mtu asiyejiweza. Mwanamke huyu hakuwa anaonekana vema kwasababu ya giza. Dirisha lilikuwa moja tu, dogo, na limezibwa magazeti na majarida ya zamani.
Mwanamke aliyeambatana na mwanae akawasha kibatari na kuangaza. Kumbe mwanamke aliyekuwa kitandani alikuwa ni Miriam!
“Habari yako dada?” Akasalimu mwanamke mwenye nyumba akisogeza kibatari chake auone uso wa Miriam. Macho ya mwanamke huyu yalikuwa makubwa na yenye kujali. Miriam alikuwa anamtazama kwa mbali mdomo wake ukiwa wazi.
“Habari yako dada? Naitwa Mili, wewe ni nani?”
Akajitambulisha, kumbe anaitwa Mili. Alikuwa anamtazama Miriam kwa kina akitegemea kusikia lolote toka kwake karibuni. Lakini haikuwa hivyo, Miriam hakuweza kuongea.
“Tulikukuta shambani kwetu ukiwa hujiwezi. Tungekupeleka hospitali lakini hatuna uwezo huo. Unaweza ukatuambia umetoka wapi? Wewe ni nani?” Akauliza Mili. Lakini Miriam hakuweza kutia neno. Alikuwa anasikia pia kuona lakini akishindwa kusema.
Mili akakata tamaa. Akamtazama mwanaye na kumwambia inabidi wakatoe taarifa kwa mwenyekiti wa kijiji. Alikuwa anahofia sasa yule mgeni anaweza kuwafia pale wakakosa la kusema.
Haraka mtoto akaamka, lakini ghafla Miriam akaanza kuguguma kama mtu anayesikia maumivu huku akitoa ishara kwa kutikisa kichwa! Kwa tabu akamtaka Mili asifanye alivyoadhimia.
“Msi … en … de … pop…pote!” Akasema kisha akakusanya pumzi kwanza kana kwamba mwanariadha aliyekata utepe wa mwisho wa marathoni.
Mili akamtaka mwanaye amletee viazi vilivyopo kwenye bakuli kabatini, akamlisha Miriam akimsindikizia na maji ya kunywa. Angalau Miriam akapata nguvu.
Kwa taabu, akipambana na hisia za maumivu, na kwa ufupi akamweleza Mili wapi alipotokea na yeye ni nani kisha akawasisitizia Mili na mwanaye wasije wakamwambia yeyote juu yake.
“Hapa ni mbali sana toka huko!” Akasema Mili. “Siku ya kwanza walikuja wanaume wawili hapa wakatuulizia kumhusu mwanamke mwenye sifa zako, lakini tulihofia, tukakanusha kukuona.”
Miriam akamuuliza kwanini alifanya hivyo. Mili akamjibu ni kwakuwa waliwaona wanaume hao wakiwa wameficha bunduki ndani ya nguo zao, wakafahamu si watu wema.
“Hata jana mwanangu alipata kumwona mmoja wa wanaume wale akirandaranda na kuangaza huku na huko!” Akamalizia Mili, kisha akamtaka Miriam apumzike wataongea zaidi baadae.
****
Alikitazama kioo akatabasamu mwenyewe. Sasa alijiona amependeza na anaweza kutoka. Akajiangalia tena mwili mzima, akajikubali na kujipa ruhusa. Akabeba mkoba wake na kisha akatoka ndani.
Yalikuwa ni majira ya saa kumi na moja jioni. Jua lilikuwa limepoteza nguvu yake likionekana jekundu linaloadhimia kwenda zake na kuuacha ulimwengu kizani.
Ndani ya jioni hii, Glady alikuwa ana mipango kadhaa ya kutekeleza na sehemu kadhaa za kwenda.
Mwendo wake wa madaha na nguo yake ya nusu uchi, zilimfanya awe gumzo barabarani, lakini nani anajali? Sio Glady huyu! Hakuwa anaogopa macho ya watu hata kidogo. Alikuwa anafanya yale yanayopendezesha nafsi yake tu, mengine mtabaki nayo nyie.
Kwa watu waliokuwa wanamfahamu kuwa anajiuza, hawakustaajabishwa naye, pengine walivutiwa. Glady alikata mitaa kwa hatua zake za maringo mpaka alipowasili mbele ya fremu iliyoandikwa; MSUGULI PHONE ACESSORIES
Alipokutana na fundi, mwanaume mfupi mweusi mwenye nywele pilipili. Akamsalimu na kumuulizia kazi aliyompatia. Mwanaume huyo akatabasamu, kisha akauzamisha mkono wake kwenye kabati la kioo alipotoa simu kubwa nyeusi aliyomkabidhi Glady aipekue.
“Ili uiuze sio?” Glady akauliza akiifungua simu aliyokabidhiwa. Akazama kwenye menyu, ikakubali! Huko akakuta kila kitu. Basi akajikuta akitabasamu.
“Safi sana! Aisee! … yani nilikuwa siamini kabisa kama ungeweza!” Glady akalipuka kwa furaha.
“Nilikuambia ni kitu kidogo sana hiko,” fundi akajigamba. “Yani kufungua maloki ya simu ndo kazi yangu, chap tu mbona unafurahi mwenyewe na roho yako.”
Glady akatoa pesa kwenye mkoba wake, shilingi alfu kumi akamkabidhi fundi. Wakazoza kidogo kwani fundi alikuwa anataka zaidi kwa kazi alofanya. Glady akaishia kumwongezea alfu tano alafu akaenda zake.
Njia nzima akawa anatabasamu mwenyewe. Hakuamini kama amefanikiwa kuifungua simu ile aliyoiiba toka kwa Alphonce. Aliona amefanya kazi kubwa na sasa anaweza akaitumia simu hiyo ambayo ipo juu kiteknolojia ukilinganisha na ya kwake.
Akafika nyumbani na kujimwaga kitandani. Akafungua na kuanza kuipekua simu ya Alphonce, aone kama yaliyomo yamo. Cha kwanza kilikuwa ni kamera, akaridhika nayo, ‘akajitwanga’ picha kadhaa kabla hajaendelea na upekuzi wake.
Akawasili sasa kwenye gallery ambako huko ndipo alichukua muda mrefu kuliko mahali pengine. Akatazama kila picha alizoziona huko. Ajabu ni kwamba, akakuta mpaka picha za watu anaowajua!
Na picha hizi hazikuwa za kawaida, lah! Bali za uchi. Za wanawake mbalimbali, ikiwamo wengine wenye nyadhfa kubwa serikalini ama kwenye mashirika ya umma na yale ya binafsi!
Kama haitoshi, akakumbana na picha kadhaa za watu waliouawa. Akaona mpaka picha ya Mustapha! Hapa sasa kifua chake kikaanza kukita kwa mapigo kasi ya moyo. Akaweka simu pembeni kwa hofu, akigongwa na mawazo kichwani.
Ametoa wapi picha za watu hawa? Je, ameshiriki kwenye mauaji? Ni yeye ndiye alikuwa akimfuatilia Mustapha na hatimaye kumuua? Akawaza sana.
Akaogopa mno kwanini alijihusisha na huyo mtu. Kama amewaua wote hao, je yeye atasalimika? Akajihisi joto, damu inakimbia kwa kasi.
Lakini baadae akakumbuka kuwa mtu yule ni polisi. Naam! Aliona kitambulisho chake kwa macho yake kabisa. Inawezekana zile picha za wafu ni kwasababu za kipolisi? – yani za kipelelezi? Akawaza. Japokuwa hakupata jibu, lakini wazo hili lilisaidia kumshusha presha aliyokuwa ameitengeneza.
Lakini vipi kuhusu hizi picha wanawake walio uchi? – nazo zafanya nini?
Akaelekea kwenye mitandao ya kijamii, huko akapita kila sekta asiache jambo. Ilimgharimu masaa mawili kutimiza haja yake kisawasawa, akikagua kila maongezi ambayo Alphonce aliyoyafanya.
Mwishowe akaja kugundua kuwa mwanaume yule hakuwa mtu wa kawaida. Alikuwa ni muuaji! Na amekuwa akifanya hivyo kwa malipo makubwa na ustadi mkubwa. Na amekuwa akitumia kofia yake ya upolisi kumaliza mambo ‘kirahisi’.
Ana miradi kadhaa, na kwenye akaunti yake kuna pesa ya maana anazozipata kwa mkono mchafu! Hapa pakamkamata Glady na kumbadili mawazo. Pesa! Pesa! Pesa!
Hapa akasahau kwamba anaweza akauawa. Hapa hakuona tena hatari ya kifo, bali akijiona yupo Dubai. Akajiona anaendesha magari makubwa na yenye thamani ya hali ya juu!
Alijikuta anataka kupata mgao wa pesa iliyopo kwenye akaunti ya Alphonce. Abadili mfumo wa maisha yake kabisa.
Hivyo basi akajikuta hana budi kucheza mchezo huu na simba. Mchezo wa aidha nipate nitoke, ama nikose nife. Akadhamiria kumtafuta Alphonce kwa namna yoyote alafu amfahamishe kuwa ana siri zake zote kiganjani. Na kama anataka ziendelee kuwa salama, atume mamilioni!
Tabasamu likachipuka usoni. Mara akashtushwa na hodi mlangoni! Haraka akaficha simu na kuuliza: “Nanii?”
“Aaaaah nawe! Embu funguaga hukoo!” Sauti ikamjibu kwa shombo. Akamtambua ni shoga wake katika kazi.
“Alah! Kumbe muda umeenda!” Akastaajabu. Akasimama upesi na kwenda kumfungulia huyo shoga ‘ake – mwanamke aliyekuwa amevalia kikaptula kifupi cha kijani na blauzi nyeupe inayohakisi ya ndani – sidiria rangi nyeusi.
Wasikae muda, wakatoka kwenda kazini.
***
Saa tatu usiku …
Televisheni ilikuwa inaongea yenyewe. Juu ya meza ya kioo kulikuwa kuna chupa ya mvinyo mwekundu na glasi yake kwa pembeni.
Hakukuwa na nuru ya taa, mwanga pekee uliokuwepo hapa ulikuwa ni ule utokao kwenye televisheni. Na mbali na sauti ya televisheni hii, hakukuwa na sauti nyingine iliyosikika.
Kwenye kochi alikuwa ameketi bwana Lee akiwa ameinamishia kichwa chake chini. Alikuwa ameelemewa na mawazo. Na chupa hii ya mvinyo juu ya meza, ilikuwa inaelekea kukatika pasipo kumsaidia kabisa.
Kwanini asiwe na mawazo wakati maisha yake yapo hatihati? Alikuwa amekonda, endapo ukimtazama vema, wala havutii tena. Rafiki yake mkubwa alikuwa ni pombe, na anajifungia ndani.
Mara kwa mara sauti ya marafiki zake, Nigaa na Mombo, zilikuwa zinamrejelea masikioni zikimtaka asitishe mpango wake wa kwenda Chinakumtafuta Chen Zi.
Wao hawakuona kama hilo wazo ni jema kwani kuondoka kwake kutamsababisha bwana Sheng kuanza kumshuku. Walipendekeza Lee aachane na mambo ya hiyo Nyaraka. Lolote litakalotokea, akane kuhusika nalo.
Lakini atawezaje kufanya hilo? Akajiuliza. Sheng anajua kuwa yeye ndiyo alikuwa na nyaraka hiyo, tena ya thamani kubwa, endapo akisikia huko kwengine atamfikiria nani zaidi yake?
Akajikuta anakataa kabisa wazo la kutokwenda China. Ni lazima aende huko akamaliza alichokianzisha. Akamtafute Chen Zi aliyetumiwa nyaraka hiyo na bwana Foang – mchina aliyemrubuni Mustapha.
Ila sasa kazi inakuja, atatolea wapi sababu ya kwenda huko China? Akahisi kuchanganyikiwa.
Akanyanyuka na kwenda kujiandaa, mara akatoka ndani na kujiweka kwenye gari, safari mpaka klabu. Bahati, akiwa huko akamwona Glady. Alikuwa amesimama na marafiki zake mikononi wakiwa wameshikilia bia za kopo.
Akamfuata mwanamke huyo na kumtaka awe naye kwa usiku huo. Kwa kumtazama tu, Glady akajua Lee hakuwa sawa. Alikuwa na msongo wa mawazo. Basi pasipo kusita, akaridhia kwa kumpa tabasamu.
Lakini kabla hawajatoka ndani ya klabu, Alphonce akazama ndani akiwa anaangaza. Alikuwa amamtafuta Glady!
Mwili wake ulivishwa suti nyeusi, lakini kama kawaida yake, haikuwa imemkaa vema. Nguo ilionekana ni kubwa tofauti na umbo lake. Pengine huwa anajiona ana mwili, ama amenenepa kwa ndani, na hivyo basi matatizo ni kwetu sisi tunaomtazama.
Akaelekea kaunta akaoda wiski moja, aliomba iwe ngeni kinywani mwake. Akiwa anasubiri apatiwe, akawa anaangaza macho yake kutafuta. Lakini shida ni kwamba, mwanga uliokuwemo humo ndani, kumeta-meta kwa rangi nyingi kama pinde za mvua, hazikumruhusu aone watu vema.
Kwahiyo basi yeye alikuwa anasachi kwa mujibu wa maumbo. Alikuwa amelikariri umbo la Glady ma endapo tu angeliona basi angeling’amua kwa wepesi kabisa, hata kama kizani.
Ila mpaka muda huo, alikuwa ameshachelewa. Kwa muda huo, tayari Glady alikuwa ndani ya gari la Lee wakiondoka zao.
“Hii hapa!” Akasema mhudumu akisogeza glasi. Alphonce akaitikia kwa kichwa alafu akapiga pafu moja kana kwamba anakunywa juisi ya machungwa!
Akasafisha koo lake na kumtazama mhudumu machoni. Kwa sauti yenye stara ndaniye, akamuuliza endapo kama anamjua Glady. Si kwa kumtajia jina, la hasha! Bali kwa kumdadavulia mwanaume huyo mhudumu namna gani Glady aonekanavyo. Kuanzia umbo, mwendo na hata sauti.
“Hapana, simfahamu!’ Mhudumu akabinua mdomo. Na akiwa mwenye haraka ya kuhudumia wateja wengine wanaomngoja. Akashika shelvu, akafungua jokofu na kuwapatia watu vinywaji, punde alipomtazama Alphonce akakutana naye macho kwa macho. Na mezani Alphonce alikuwa ameweka kitambulisho chake cha kazi.
Ni askari.
“Pengine unaona haja ya kwenda kujadiliana kituoni?” Akamuuliza mhudumu katika sauti ya kutotaka kuwaogofya wengine.
Mhudumu akatazama kando na kando upesi. Hakuona kama kuna haja hiyo. Ni kweli hakuwa anamjua Glady, lakini kutokana na uzoefu wake wa kazi ndani ya eneo hilo, alishafahamu tokea awali kuwa Glady atakuwa ni mwanamke anayejiuza ndani ya eneo hilo. Na huyo mwanaume, yaani Alphonce, atakuwa anamsaka kishari, aidha walikorofishana kihuduma.
Kwahiyo kuepusha zogo, huwa wanajibu sijui. Lakini kesi ya leo haikuwa iliyozoeleka. Alikabwa na hofu. Na kadiri Alphonce alivyokuwa anakaa pale, hakujihisi mwenye amani.
Akanyooshea kidole upande wake wa magharibi ya mbali kisha akamtazama Alphonce.
“Anaweza akawa pale.”
“Na kama hayupo?” Alphonce akauliza akiweka kitambulisho chake ndani ya mfuko wa koti.
“Basi wenzake watakusaidia kumpata … wale wote ni wenzake!… wote wale!”
Alphonce akagida mafundo yasiyo na mwisho kumalizia wiski yake kisha akanyanyuka. Hata hakulipa, akaendaze alipoelekezwa. Lakini hilo halikumshtua mhudumu, bali namna mwanaume huyo alivyoweza kunywa chupa ile ya kinywaji kikali kana kwamba chai baridi!
Akamtazama akiyoyomea mataani. Akaendelea na kazi yake lakini kila dakika akirusha macho kuangaza usalama kule magharibi. Masikio yake hayakuwa yanasikia tena mziki mkubwa uliokuwa unapigwa mule. Muda wowote yalikuwa yamejitenga kusikia yowe ama makelele ya wale madada poa wakimkimbia ‘askari’.
Ila haikuwa hivyo. Baada ya muda kidogo akamwona Alphonce akitoka nje akiongozana na mwanamke ambaye hakumwona vema, japo alifahamu ni miongoni mwa wale wadada wanaojiuza.
Hapo, angalau sasa akashusha fundo la pumzi alilolikabia kifuani kwa muda.
***
Mlango wa Prado nyeusi ulipofungwa, gari haikuwashwa, badala yake Alphonce akatoa bunduki ndogo na kuipuliza kana kwamba ina vumbi. Akaitazama kana kwamba msomaji wa gazeti apekuae kisa alichosimuliwa. Alafu pasipo kufanya nayo jambo, akairudisha alipoitoa. Akatengenezea ‘sight mirror’ vema kisha akamtazama mwanamke yule ‘aliyeloki’ naye ndani ya gari.
Mwanamke huyu alikuwa ni yule ‘shoga’ aliyempitia Glady kwenda naye ‘kazini’ masaa kadhaa nyuma tu. Kama ni upatu, Alphonce alikuwa ameula.
“Sina shida ya kukupeleka popote, bali mambo mawili. Na katika hayo utachagua mwenyewe lipi linalokufaa. Unipatie taarifa ninayoihitaji ukaenda zako salama, mkononi una pesa, ama nikutoe ndani ya gari hii ukiwa mfu.”
Hata kabla Alphonce hajaendelea, mwanamke huyu alikuwa tayari kusema lolote lile atakaloulizwa. Alishafanya chaguzi. Hakuwa na taarifa ya muhimu kuzidi uhai wake, na wala chungu kutia doa utamu wa pesa.
Alikuwa anatetemeka mno na kama milango ya gari isingekuwa ‘imelokiwa’ basi ni wazi angeshachumpa nje kukimbia kadiri ya urefu na uwezo wa miguu yake.
Bunduki haikuwa kitu alichozoea kukiona.
Kwa utaratibu kabisa, Alphonce akampembua mwanamke huyo, na akapata alichokuwa anakitaka. Akazamisha mkono mfukoni, akatoa noti kadhaa nyekundu, pasipo kuhesabu, akamtupia yule mwanamke mapajani kisha aka’unlock’ milango pasipo kusema kitu.
Mwanamke akashuka upesi. Hapo ndo’ akagundua kumbe alikuwa ameshalowana mapajani na nguo yake ya ndani ilikuwa mbichi. Haraka akakimbilia ndani ya klabu usidhani amevalia viatu vya visigino virefu!
Akaingia ndani kwa pupa, na kusababisha tahamaki kwa waliomuona. Haswa yule mhudumu wa kaunta!
***
Saaa nne asubuhi ….
‘nitakuwa hapo ndani ya dakika kumi,’ Jona alituma ujumbe kisha akaizamisha simu yake mfukoni. Akatazama kando, kando tena, alafu akanyanyuka toka kwenye kituo cha basi na kuanza kutembea kwa ukakamavu.
Alikuwa amevalia shati jeupe, tai nyembamba nyeusi, suruali nyeusi ya kitambaa na moka. Mabegani mwake alikuwa ametundika koti kubwa la mvua lilikomea magotini.
Kwa mtu mwenye macho ya ‘chujio’ ungemtambua huyu mtu hakuwa raia wa kawaida. Alikuwa mtu mwenye mafunzo. Kisigino chake kilikuwa kinaanza kukanyaga chini kwanza kabla ya nyayo, tena kwa ustadi na sare.
Macho yake yalikuwa hayajatulia, yanakwenda huku na kule kuangaza usalama. Alijua anafuatiliwa. Ilipangwa afuatiliwe. Na anatakiwa afuatiliwe!
Hiyo ndiyo maana anatakiwa kuripoti asubuhi na mapema kwa Kamanda mkuu wa mkoa, badala ya kituoni kama ilivyo utaratibu wa kazi, kabla ya kutimiza majukumu yake.
Kufika huku kwa Kamanda kulikuwa ni kwa lengo moja tu, nalo ni kumpachikia ‘mkia’, na si lingine. Jona alitakiwa kuwa chini ya ‘jicho la tai’ kwa muda fulani kuhakikisha mienendo yake si ‘hatari kwa afya’ kwa walioshika mpini.
Alizidi kutembea na huku nyuma yake, hatua kama kumi na nane akiwa anasindikizwa na mwanaume mpana mweusi aliyevalia kaunda suti ya kijivu.
Hatua za mwanaume huyu zilikuwa za kiutu uzima. Suruali yake pana ilikuwa inarushwa rushwa kwa hatua zake za nguvu. Alimjaza Jona kwenye mboni na hakusumbuliwa na kingine chochote kilichokuwa kinakatiza machoni.
Lakini dakika moja ni kubwa sana! Ndani ya dakika moja, yaani sekunde sitini, jambo kubwa linaweza kupangwa, liketekelezeka na kuacha pengo!
Wakavuka kona ya kwanza … pili … tatu … ndani ya dakika moja tu. Mwanaume yule aliyekuwa anamfuatilia Jona akatambua ameshaachwa solemba!
Mbele yake bado alikuwa analiona lile koti alilojivika Jona, halikuwa limebadilika, ni lilelile! Lakini suruali haikuwa nyeusi tena, bali rangi ya udongo! Haraka akakimbia na kumnyaka bega mwanaume mwenye koti hilo, kugeuka alikuwa ni mwanafunzi!
Hakugundua tangu kona ya kwanza, Jona alikuwa ameshamwacha akiendelea kumalizana na kona ya tatu.
“mkuu, amenipotea,” akavuma kwa fedheha akiongea na simu.
***
‘Nipo nje ya mlango’ Ujumbe uliingia ndani ya simu ya Marwa. Akanyanyuka toka kochini alipokuwa ameketi akauendea mlango na kuufungua. Akakutana na Jona. Hakuwa na koti.
Wakasalimiana na kumkaribisha kitini.
“Ungependelea kinywaji gani, mkuu?”
“Hapana, nashukuru … umewasiliana na Panky?” Jona akaenda moja kwa moja kwenye ‘biashara’.
“Ndio, amesema anakaribia,” Marwa akajibu kwa kujiamini akiketi.
Nyumba ilikuwa kimya. Hakukuwa na dalili yotote ya kuwa na mtu mbali na wao walioketi sebuleni. Na kwa Jona, kwa muda mfupi alioketi hapo, akagundua Marwa amekuwa akiishi maisha ya kipweke. Nyumba haikonekana kama ina ‘mguso wa kike’ wala shurba za mtoto.
Alipokuwa amekaa aliweza kuona jiko, ukuta wa korido, samani, sakafu na kadhalika. Havikuwa katika namna ambavyo vingekuwa endapo Marwa angekuwa anaishi na mtu mwingine mule ndani.
Hakujali, ila hakukuwa na kingine cha kufanya wakiwa hapo wanamngojea Panky zaidi ya kuperuzi peruzi. Hakutaka kuanza kumpekenyua Marwa kwa kumrushia maswali mapema yote hiyo, kwani hakuonekana kama mtu aliye ‘comfortable’ mbele ya uwepo wake.
Akaendelea kutazama tazama pasipo kutia neno, mpaka macho yake yalipotua mezani kulipokuwa na tarakilishi nyeusi HP modeli ya kisasa, makaratasi kadhaa, mengine meupe, mengine ya grafu, zaidi kalamu tatu, penseli nne na rula moja.
Kwenye makaratasi hayo kulikuwa kuna michoro michoro mingi, na mengine mahesabu mahesabu yakiwa yametapanywa. Bila shaka Marwa alikuwa anayatumia kufanyia zoezi analoendelea nalo kwenye tarakilishi, akawaza Jona.
Akasafisha koo lake, na kuvunja ukimya.
“Hata leo haupo off?” Akauliza akitabasamu kwa mbali. Marwa akatabasamu zaidi.
“Sijawahi kuwa off. In fact, nafanya kazi overtime mara kwa mara. Nadhani n’shazoea!” Marwa alimalizia kwa kupandisha mabega yake.
“Basi pasi na shaka, mshahara wako ni mnono,” Jona akaendelea kuchokoza mada. Macho yake yalikuwa makini kutazama kila kitu toka kwa Marwa.
“Lah! Nafanya kazi si kwa ajili ya pesa, bali maisha.”
“Pesa ni maisha.”
“Hapana. Pesa si maisha … pesa haiwezi nunua maisha.”
Hapa Jona akaona kuna cha zaidi Marwa alikuwa anataka kusema lakini aidha anakosa namna bora ya kukisema, ama anajitahidi kuzuia kutokukisema.
Lilikuwa ni jukumu lake kukijua hiko kitu.
“Kama pesa kwako si kitu. Unafanyiaje kazi maisha? Wafanya kazi kwa kuwa umezoea?”
Marwa hakujibu upesi. Alitulia kwanza. Jona hakuona haja ya kumshinikiza ajibu kwani uso wa mwanaume huyo ulimwonyesha jibu lipo karibuni. Ni vile anapanga namna ya kulitamka.
Marwa akashusha pumzi ndefu. Pasipo kumtazama Jona, akasema kwa sauti iliyotoka chini ya vungu la moyo wake.
“Output ya kazi yangu, ndiyo pumzi ya wazazi wangu.”
Jona hakupata wasaa wa kuendelea kumdadisi, Panky akawasili. Sasa wakaanza kujadili kuhusu ile picha.
_Picha ya siri._
_Picha ya Bite inayotia rehani roho zao wote._
***
Kama vile uonavyo watahiniwa wakiwa kwenye hall la mtihani, ndivyo ilivyokuwa hapa. Palikuwa tulivu, macho yote yakitazama kioo cha tarakilishi ya Marwa.
Marwa akaelezea kila anachokijua. Tangu alipopewa kazi hiyo na mpaka pale alipoikamilisha kwa Moderator wao. Akaeleza ni kwa namna gani kazi hiyo ilivyofanyika kwa siri, ustadi na mazingatio makubwa.
Kila ‘detail’ ilikuwa imepimwa kwa umbali wa sentimita za kuwiana. Na japokuwa hakuambiwa vitu vile vilimaanisha nini, alishatambua zitakuwa ‘codes’. Na kwa wakati huo akatokea kuamini aidha ni codes za kufungulia tarakilishi tawala – yani ile ‘inayomoderate’ tarakilishi zote hizo ndani ya jengo.
Alipomaliza kuifanya kazi hiyo, akaikabidhi kwa moderator, lakini baada ya muda akiwa amesahau kabisa picha hiyo , Moderator akamrudishia akimwambia kuna mambo alitakiwa kurekebisha. Idadi ya mawimbi baharini!
“Kitu hichi kikanishangaza, si kwamba zilikuwa ni taarifa ndogo ndogo, lah! Bali kwa sasa aliponipatia alikuwa strict mara tatu ya awali akitazama kila nyendo za mkono wangu, macho yangu.
Nilipomaliza, akaniagiza nimrushie. Na hapo ndipo ikawa mwisho wa mimi kukutana na hiyo picha mpaka pale Panky alipoiibua na kunishtua.”
“Unamfahamu Bite?” Jona akauliza. “Bite? … “Marwa akatengua macho kwa kufikiri. “Bite Mayanja?” Akauliza.
“Sijui jina lake la ubini, namjua kwa jina la Bite tu. Kuna mtu yeyote unayemfahamu, ama wamjua anaitwa Bite?”
Marwa akafikiri kwa dakika.
“Sidhani … ila, ebu ngoja. Bitee? … Bitee … Bitee…” akameza lips zake akiendelea kuwazua. Punde akamuuliza Jona juu ya mwonekano wa mwanamke huyo, Bite. Jona akajipambanua kutumia kumbukumbu zake zote kuelezea. Hapa Marwa akapata kitu.
“Unamwongelea marehemu Bite?”
“Exactly! Atakuwa ndiye huyo. Unamjua?”
“Ndio … ila tuseme kiasi chake … namjua kiasi.”
“Ulimjulia wapi?”
“Kazini. Bite alikuwa ni miongoni mwa wafanyakazi wachache niliowakuta. Hakuwa mwanamke muongeaji sana, wala mwepesi kumzoea. Kwa kipindi hicho alikuwa ndiye mwanamke pekee ndani ya chumba cha IT. Lakini hali hiyo haikudumu kwa muda mrefu, akaacha kazi!”
“Alikuambia ameacha? Au ulijuaje?”
“Najua tu aliacha kazi, hata kama hakuniambia. Sheng huwa hafuti mtu kazi, anafuta uhai. Unakumbuka nilivyokuambia Bite ni miongoni mwa wafanyakazi wachache niliowakuta? … wenzake wote niliowakuta hapo, watatu kwa idadi, waliuawa.”
“Umejuaje?”
“Natazama taarifa ya habari. Najua walitaka kuacha kazi, haswa baada ya Bite kufanya hivyo ila hawakufanikiwa.”
“Na kwanini Bite akafanikiwa?”
“Akafanikiwa!” Marwa akastaajabu. Akatabasamu kisha akatikisa kichwa. “Bite alichofanikiwa ni kudumu kwa muda mrefu tu, tofauti na wenzake. Yeye aliweza kukaa miaka na miaka akiwa huru!”
“Lakini iliwezekaje hili?” Jona akauliza. Hapo Marwa hakuwa na majibu. Kila mtu akawa kana kwamba yupo hewani kutafuta tofali hili moja kumalizia nyumba.
Jona akatabasamu. Akatabasamu kwa upana zaidi. Na mara akacheka.
“Bite aliweza kudumu muda mrefu kwasababu ya hii picha,” akajibu akionyeshea kidole kwenye kioo cha tarakilishi.
“Ni wazi Bite alikuwa anajua risk ya yeye kuacha kazi. Basi akaondoka na kitu cha thamani toka kwa Sheng. Kitu atakachokitumia kama dhamana ya uhai wake. Nacho ni hii picha!”
“Sheng alimmaliza baada ya kupata mbadala wa kile alichokuwa nacho Bite mkononi. Ukiachilia mbali bado Bite alikuwa na pandikizi la Sheng ndani ya kila shughuli aliyokuwa akiifanya. Na kwa akili tu ya kitoto, maana yake ni kwamba Sheng alikuwa anajiandaa kuzipokea shughuli hizi punde atakapomwondoa Bite duniani,” Jona akadadavua.
Marwa akakunja usowe kwa kuchanganyikiwa. Akauliza: “Umejuaje Sheng alipata mbadala wa picha aliyokuwa nayo Bite mpaka akaamua kumuua?”
Jona naye akamuuliza: “Ilichukua muda gani kati ya wewe kubadili picha na Bite kuuawa?”
Marwa akajaribu kufikiri. Haraka akainamisha mgongo wake kutazama chini ya meza, kulikuwa kuna magazeti lukuki huko, akapekua pekua magazeti hayo na kuibuka na mojawapo.
Lilikuwa na taarifa ya mauaji ya Bite.
Akalisoma tarehe. Kisha akazama kwenye tarakilishi yake alipopekua mambo kwa muda wa dakika mbili, kisha akasema: “Tofauti ya siku mbili tu!”
Jona akatabasam kwa mbali.
“Umeona enh?”
“Lakini,” Panky akazuka. “Kama ingelikuwa ni rahisi hivyo, kubadili tu picha mchezo ukaisha, kwanini ilichukua muda mrefu Bite kuwa hai?”
“Na hapo ndipo tunaporudi pichani,” Jona akamjibu. “Hizi zilizopo kwenye picha ni codes. Ni kitu kikubwa. Kuongeza tu mawimbi pichani, si tu kupendezesha mambo bali kumaanisha jambo. Jambo ambalo lilimchukua Sheng muda wote huo akichezewa sharubu na Bite!”
Sasa mambo yakaanza ku’ make sense’. Kuhakiki zaidi mambo, Jona akatoa simu yake mfukoni na kutazama picha ya picha ile aliyoichora toka kwa Bite.
Kweli ilikuwa na upungufu wa idadi ya mawimbi ukiilinganisha na ile kopi ya Marwa! Upungufu wa mawimbi mawili tu! Lakini ungeliona hili endapo ungeamua kuua muda wako wa kutosha kuchunguza.
“Wamekuamini sana kukuachia hii kopi,” Jona alisema akimtazama Marwa.
“Hawana hofu kuu nami,” Marwa akajibu. “Maana wanajua sina janja kwao. Nikapofanya lolote lile, watakatisha dozi ya antidote kwa baba na mama yangu, nao watakufa ndani ya sekunde thelathini tu!”
Jona aliona ni namna gani Marwa anaumizwa na hilo jambo. Macho yake yalitamka namna gani anaumia kila akilikiri hilo. Hakutaka kumumiza zaidi, akakengeusha mawazo.
“Hii picha tukiikokotoa. Sheng atakuwa amejaa kiganjani.”
“Hakika!” Panky akaliunga mkono hilo. Lakini kabla hawajaendelea kuumiza vichwa zaidi, Marwa akapendekeza wapate kifungua kinywa kwanza kwani tumbo limeanza kudai chake kwa fujo.
“Hli tumbo limetifuliwa na kuumiza kichwa,” akasema Marwa akienenda jikoni. Pengine alikuwa sahihi kwani mara hii Jona hakumzuia.
Alihisi naye anahitaji kitu kujaza utupu wa tumbo lake.
Chai na vitafunwa kadhaa vikiwa vimewekwa kwenye sinia ya plastiki, nadhifu jeupe lenye nakshi za maua maua, vikawasilishwa mezani. Vikafuatiwa na maji ya kunawa na ya kunywa pia. Marwa akawanawisha wageni wake mikono na kuwakaribisha.
“Umepika mwenyewe hivi?” Jona akauliza baada ya kung’ata kitafunwa kimoja na kukitafuna. Ladha ilikuwa tamu. Na zaidi, aliona ilikuwa ni fursa adhimu kwake kujua machache toka kwa Marwa.
“Hapana, sijapika mie … siwezi kupika hivi!” Marwa akasema akitabasamu. “Si kwamba siwezi, hapana! Ningepika hapa mngejing’ata lakini sina huo muda. Nabanwa sana na kazi.”
“Hakuna wa kukusaidia?” Jona akaendelea kudadisi akitafuna.
“Atolee wapi?” Panky akawahi kumjibu, kisha akacheka kidogo. “Unavyomuona huyu alivyo ndiyo yupo hivyo hivyo!”
Kukawa kimya kidogo. Wote walikuwa wametabasamu midomo yao ikicheza kwa kutafuna.
“Nimechagua haya maisha,” Marwa akavunja barafu la ukimya. “Ni ngumu, najua … lakini sina namna.”
Jona akamtazama kwa macho ya maulizo pasipo kusema kitu. Alitumai Marwa hataishia hapo. Marwa akanywa mafundo mawili ya chai na kufuta mdomo wake kwa mgongo wa kiganja.
“Kazi yangu ya hatari sana,” Marwa akasema kabla hajatia kitafunwa kingine mdomoni. “Kumpata mwanamke siyo shida. Ila nitaweka maisha yake rehani, na huenda akatumika, kama ilivyo kwa wazazi wangu, kunifanya niwe mdhaifu.”
Wote wakaunga mkono hoja yake. Wakaendelea kutafuna kwa muda kidogo kabla Jona hajairudisha tena mada mezani.
“Lakini unajitahidi… indeed unajitahidi sana kukeep nyumba vizuri.”
“Kiasi chake!” Marwa akapokea pongezi kwa aina yake. “Nikipatapata muda unashika hiki na kile, hapa na pale, nidumishe rangi za vitu, angalau hata mgeni akija asipate picha mbaya ya kusimulia.”
Maongezi hayo yakawasha taa kichwani mwa Jona. Kuna kitu aliwaza. Kuna kitu alikipata. Alitazama sinia ile iliyobeba vitafunwa, ilikuwa ni nyeupe peh.
Kudumisha rangi …
Rangi nyeupe …
Rangi nyeupe huonyesha usafi.
Akilini alikuwa anaonganisha mambo …
Ghafla, akalipuka na kuuliza: “Vipi kama rangi za ile picha zikawa ndiyo codes zenyewe?”
“Kusema kwamba?” Panky akatahamaki. Jona akamtazama kwa macho ya uhakika.
“Kusema kwamba, rangi za vile vitu vilivyopo kwenye picha ndiyo zikawa codes!”
Hawakutaka kupinga hoja ya Jona kabla hajaithibitisha. Wakamaliza kula na kuchangia maoni yao kwenye hilo wakiwa wanatazama picha ile kwa umakini.
Lakini wakagundua walikuwa ni wadhaifu kwenye mambo ya rangi. Lakini kabla hawajakata tamaa, Marwa akataka watumie ‘Techonological interpretation of colors’ – yaani wazichambua zile rangi kwa kuzihusanisha na teknolojia kwani kazi hiyo ilitengenezwa na kitengo cha teknolojia tarakilishi ndani ya mtandao wa Sheng.
Basi, Marwa akafungua ‘application’ yake ya siri aliyoitengeneza kwa mikono yake mwenyewe, inaitwa CODAQ. Akaandika namba za siri kwa vidole vyake vyepesi juu ya keyboard. Mara zikaja namba namba nyingi. Akabofya bofya keyboard kwa haraka mno usijue hata aliandika nini, na mara kioo kikawa cheupe.
“Ni nini hii?” Jona akauliza.
“Ni app yangu ya kutengeneza Techonological logos kwa ajili ya techonological gadgets.”
“Kwani wataka kutengeneza logo?”
Marwa akatabasamu. “Hapana. Nataka ku ‘re-assess’ kila rangi na maana yake kwenye techonology field.”
Akabonya bonya keyboard kwa wepesi. Jona hakusumbuka tena kutazama nini Marwa anabofya kwani macho yake hayakuweza kwenda sambamba na kasi ile.
“Unajua kila rangi ina maana yake kwenye logo …” Alisema Marwa akiwa anaendelea kufanya mambo yake. Hakuna mtu mwingine aliyeongea, wote walikuwa wanangojea aweke mambo bayana.
Punde,
“All right!” Akasema Marwaa akitabasamu. Alikuwa amefika mahali alipokuwa anapahitaji, akashirikisha wenzake kwa kile alichokuwa nacho.
Mosi, kwenye ile picha kuna rangi ya blue – ambayo ndiyo ilitumika kupambia bahari. Pili, kuna rangi ya kijani kilichoshamiri kisiwani. Tatu, kuna rangi nyekundu na nyeupe iliyotumika kupambia ndege warukao juu.
Hizo ndo zilikuwa rangi ‘dominative’ pichani. Sasa wakazianisha kimaana.
– Blue = security/strength/dependable. (Ulinzi/ nguvu/cha kutegemewa)
– Nyeupe = purity/reliable (kisafi ama kitakatifu/kuaminika.)
Kwahiyo basi kwa maana hiyo, kisiwa kile (kijani) kilikuwa kinamaanisha uhai wa Sheng, ukuaji wa Sheng, hali nzuri ya Sheng. Lakini hicho kisiwa kikiwa kimezingirwa na blue (maji), kumaanisha ulinzi, nguvu na kutegemewa.
Mpaka hapo, maana yake ni kwamba hakuna ukuaji wala uhai wa Sheng kama hamna ulinzi na nguvu kuzunguka uhai huo. Na kwa tafsiri ya picha, bahari ama rangi blue ndiyo iliyochukua sehemu kubwa.
Na wale ndege waliopo juu ya kisiwa, wakimaansha utakatifu wa mawasiliano kama moja ya nguzo ya kupendezesha mandhari!
Nusu ya kazi ikawa imeisha. Sasa mkia uliobakia ukawa ni kujua maana ya idadi ya kila kilichomo ndani ya picha. Kwanini ndege watano? Mawimbi manne? Kwa maana kama yasingekuwa na maana basi Marwa asingepewa kazi ya kuyarudia kuyaongeza.
“Nguvu ya bahari ni mawimbi yake, sio?” Jona akauliza. Asisubiri majibu akaendelea kuteta: “basi haya mawimbi manne yaliyopo kwenye bahari hii, ndiyo nguvu ya ulinzi wa Sheng. Aidha ni watu ama vitengo.”
“Na basi kama ni hivyo,” Marwa akadakia lain. “Nguvu ya mawasiliano ya Sheng ni watu ama vitengo vitano pia!”
***
Saa kumi na mbili jioni, Whitesand Hotel.
“Nimefurahi sana sana!” Sauti ya kike ya Miranda ilivuma wakati mwanamke huyo akiagana na mheshimiwa Boka kwa kumpatia kumbatio la joto na busu mubashara shavuni.
“Usijali, nimefanya yote haya kwasababu nakupenda. Nimedhamiria haswa kuwa nawe,” Mheshimiwa Boka akajivuna kabla hajatoka zake eneo hilo na kujipaki ndani ya VX yake nyeusi. Akahepa.
Miranda akarudi ndani ya hotel akiwa anatuma ujumbe simuni. Alipoketi, ndani ya muda mfupi BC akatokea nyuma yake na kuketi. Mwanaume huyo alikuwa anatabasamu usoni.
Akampongeza Miranda kwa kukamilisha kazi, kisha akamsikiliza amwambie cha ziada.
“From next month, he will be on trip in South Africa.” (Kuanzia mwezi ujao, atakuwa safarini Afrika ya kusini) Miranda akajipambanua. BC akatoa macho ya mshangao.
“What a coincidence!” (Bahati iliyoje!) Akamsihi Miranda ahakikishe hiyo safari anakwenda na Boka kwani kuna baadhi ya mzigo wao utatua huko, na atakuwa na jukumu la kuuleta hapa nchini.
Kidogo Miranda akaonyesha hofu.
“Never mind, it’s just small one. It will never get you in trouble,” (Usijali, ni mdogo tu. Kamwe hauwezi kukuingiza matatizoni,) BC akampoza akiwa anamkanda bega kwa kiganja chake kipana.
Hawakukaa hapo sana, wakatimka zao.
***
Wivu ndiyo mapenzi. Lakini pia wivu ni kidonda, ukishiriki utakonda. Walisema waswahili. Na hakika hawakukosea kwa neno hilo, ulikuwa ni ukweli mtupu ulio uchi.
Punde baada ya mumewe kuingia bafuni, akaiteka simu ya mumewe na kuanza kuiperuzi. Boka mule bafuni asiwe na hofu yoyote, alikuwa anaimba huku akiusugua mwili wake mpana mweusi kwa ujazo wa sabuni.
Alikuwa anabadili nyimbo hii kwa hii. Wakati mwingine akiwa anagugumia kutengeneza ‘beat’. Alikuwa ana furaha moyoni, ungelijua kwa kumtazama tu. Kama mwili wake ungelikuwa unamruhusu kucheza, basi angelijimwayamwaya.
Lakini laiti angelijua mkewe anaperuzi simuye, nakuhakikishia asingekumbuka hata taulo. Angekimbia upesi kwenda kumpokonya.
Alipomaliza kuoga, akatoka bafuni akiwa amejifunga taulo jeupe kiunoni. Bado akiwa anaimba, akaketi kitandani na kumtazama mkewe. Alikuwa ameigiza kulala.
Akajaribu kumuita mara mbili kwa sauti ya chini. Mama hakuitika. Basi asimsumbue, akaenda zake kabatini na kuteka nguo ya ndani apate kulala.
Bila shaka akijua usiku umeenda salama. Lakini kumbe kifuani mwa mkewe kukiwa kuna vita hatari. Vita inayomtafuna zaidi ya kirusi.
Akazima taa na kisha kujimwaga kwenye kitanda kipana, maridadi kabisa, apate kulala. Kwa ‘kajoto’ kalichokuwepo, hakuhitaki kujifunika shuka.
Alikuwa amechoka mno kwa ‘shughuli pevu’ aliyopewa na Miranda. Hakudumu macho kwa muda mrefu, akapotelea usingizini akiwa anakumbuka raha alizopewa.
Raha za karne.
Lakini mkewe hakuwa amelala. Muda huo alikuwa anatiririsha machozi bujibuji. Alikuwa akisaga meno, kichwa kinamuwaka moto. Likapita lisaa limoja. Akashindwa kuvumilia.
Akanyanyuka na kutoka ndani ya chumba. Baada ya dakika tatu, akarejea akiwa ameshikilia kisu mkononi.
***
Alikuwa amejawa na hasira kedekede. Hakuwaza tena kama ana watoto aliozaa na huyo mwanaume. Hakuwaza kama ana familia inayomtegemea, wala mambo lukuki waliyoyapanga na kuadhimia na huyo mwanaume. Hakuwaza kifungo cha maisha.
Aliwaza kuua tu kuridhisha nafsi yake kwa kuua.
Lakini anawezaje kufanya hili wakati hata kuchinja kuku hajawahi?
Akamsogelea mumewe aliyekuwa hajitambui, kazamia usingizini. Kifuani moyo wake ukimdunda haswa! Na jasho likiwa tayari limelowanisha gauni lake jepesi la usiku.
Mikono yake ilikuwa inatetemeka. Kisu kikienda huku na kule, akijitahidi kukituliza.
“Nitamkita tu tumboni … hapana, anaweza akapona … namkita kifuani. Si atakufa? … Atakufa ndio!” Alikuwa anazoza mwenyewe na nafsi yake.
Lakini ghafla mwanga wa simu ukammulika usoni. Akashtuka mno! Kama isingelikuwa mbavu, moyo wake angeliukutia nje.
Ilikuwa ni simu ya mumewe. Kuna mtu alikuwa anapiga. Baada ya simu kutoa mwanga, punde sasa ikaanza kuita kwa wimbo kwanguvu. Mwanamke akachanganyikiwa. Hakujua cha kufanya kwa haraka.
Alitupia kisu chini kwa kupagawa, alafu upesi akaketi kwenye kingo ya kitanda. Akasikiliza simu ya mumewe ikiita … ikiita … ikiita.
Ikakata!
Ikaita tena. Lakini ikakata pasipo kupokelewa. Mara hii haikuita tena kwa muda mrefu kama hapo awali. Kwa muda wote huo Boka hakusikia chochote kile. Alikuwa akiendelea kukoroma kana kwamba hakuna kilichojiri.
Simu ilikata na kunyamaza kwa muda wa dakika kadhaa. Chumba kikarejea katika hali ya kiza, lakini mama hakukifuata tena kisu chake. Akaendelea kuketi kingoni mwa kitanda akifikiria mambo kadhaa kichwani.
Mara akanyanyuka na kwenda kutazama aliyepiga simu. Alikuwa ni mfanyakazi mwenziwe na mumewe. Akapuuza. Akaelekea kule kwenye jumbe, akainakili namba ya mtu aliyekuwa anachat na mumewe na kuihamishia kwenye simu yake.
Mara namba hiyo ikatokea na jina! Kumbe alikuwa nayo simuni.
Alikuwa ni Miranda.
“Malaya mkubwa!” Akajikuta akitusi. Amekunja ndita na ngumi kwa hasira. “Kumbe ni wewe! … kumbe ni wewe unanizunguka?”
Akajiona mpuuzi sana. Kumbe mwanamke aliyeingia naye kwenye mahusiano ya kibiashara, alikuwa anamzonga nyuma ya mgongo!
Kichwa chake kikampitishia picha za kumbukumbu akiwa na mwanamke huyo, tangu siku ya kwanza kuonana naye. Siku wakiteta na kucheka.
Akaghafirika mno.
Akarejesha kisu jikoni kisha akajilaza kitandani akiwa sasa anapiga mahesabu ya kumpata Miranda. Hakujua atamfanya nini. Ila hakika hakitakuwa kizuri, hiko ndicho alikijua na kuwa na uhakika nacho.
Hakitakuwa kizuri.
Hakulala usiku wote huo.
***
Saa mbili na nusu asubuhi; ndani ya ofisi ya Kamanda mkuu wa polisi mkoa.
Kamanda akamtazama Alphonce kwa macho ya nje ya miwani akiwa ameshikilia gazeti la The Guardian mkononi. Kofia yake ilikuwa juu ya meza, amejilaza kuegemea kiti chake cha kunesa na kuzunguka.
Akamkagua Alphonce aliyekuwa amevalia suti kubwa rangi ya kahawia na mwenye sura ya ukakamavu, alafu akarudisha macho yake gazetini.
Kwa muda kidogo kukawa kimya kana kwamba hamna mtu ndani ya ofisi.
Kamanda akashusha pumzi ndefu puani, alafu akasonya kama mtu aliyesikitishwa na jambo. Akatoa macho yake gazetini na kumtazama Alphonce tena.
Kwa utaratibu akamuuliza: “Tumeshindwana?”
“Hapana mkuu!” Alphonce akajibu kwa ukakamavu. Kamanda akawela gazeti lake mezani kisha akaendea kabati lake akitembea kwa uchovu. Akalifungua na kutoa faili kubwa zito jeusi alilolipekua karatasi kadhaa ndaniye.
Akaita,
“Alphonce,” akiwa anaendelea kuliperuzi faili lake.
“Afande!” Alphonce akaitikia.
“Unajua nina kazi nyingi mno za kuzifuatilia. Kazi lukuki lukuki. Lakini sasa nashindwa kufanya kazi zangu hizo kwa ajili yako, uzembe wako, ubishi na ukaidi wako …”
“Hapana, mkuu si ka –“
“Nyamaza!” Kamanda akageuka na kumtazama Alphonce kwa jicho la bundi. “Sitaki kusikia lolote toka kwako. Lolote! Unajua jana alikwenda wapi? Kufanya nini? Unachukulia haya mambo mepesi, sio?”
Kamanda akarejesha faili kabatini, akamsogelea Alphonce na kuketi juu ya meza akimtazama.
“Unajuwa wazi, tulimaliza familia yake. Tulichoma nyumba yake. Tuliharibu biashara yake. Tukaua washirika wake. Kwako ni mepesi hayo?”
“Lakini mkuu, kwanini tulimrejesha jeshini? Hukuona itakuwa salama yeye ang —“
Twaaah! Kamanda akamzaba kofi zito Alphonce!
“Pumbavu wewe!” Akalaani. “Unadhani nilikuwa siyajui hayo? Jona alikuwa anahitajika kurudi jeshini kwa namna yotote ile. Huo ulikuwa ni msalaba wangu. Jukumu nililopewa kutimiza na IGP. Sikutia sahihi barua yake ya kujiuzulu mpaka leo hii. Jona anahitajika taifa zima. Haswa kipindi kama hiki!”
Kamanda akashusha pumzi ndefu. Akanyaka chupa yake ya maji makubwa ya Kilimanjaro yaliyokuwa mezani akagida mafundo kadhaa kujipoza.
“Ni jambo la muda mfupi tu. Nilikuambia umtazame kwa muda mfupi tu maana naamini wewe ndiye unayeweza hilo jukumu. Shida yangu ni kujua nyendo zake. Kujua kama anafuatilia nyayo zetu za damu. Basi!”
Akanywa tena mafundo kadhaa ya maji. Akamaliza chupa nzima.
“Ni wewe tu ndiye wa kumfuatilia Jona. Kila hatua … kila muda … kila saa!”
Punde Alphonce akatoka ndani ya ofisi na kwenda kukaa ndani ya gari lake. Macho yake yalkuwa mekundu. Uso wake ulikuwa umevimba kwa hasira. Si kwasababu ya kuzabwa kofi, hapana. Moyo wake ulikuwa umejawa na wivu.
Wivu juu ya Jona.
Aliona Jona anathaminiwa kuliko yeye. Jona ni nani haswa? Kwani yeye ndiye jeshi lote la polisi nchini. Hili jambo lilimuuma sana. Lilikuwa linautoboa moyo wake.
Akiwa humo garini, punde akamwona Jona akizama ndani ya ofisi ya Kamanda kuripoti. Alikuwa amevalia suruali jeans na shati nyeupe aliyoichomekea.
Baada ya dakika kama tano, akatoka ndani ya ofisi na kwenda zake.
Alphonce akawasha gari.
Baada ya nusu saa … Ocean road hospital
“Anaendelea vizuri, anaweza akaongea,” alisema nesi kwa tabasamu huku akimtazama Jona.
Walikuwa wamesimama nje kidogo ya chumba alicholazwa mwanamke huyo.
“Kwahiyo naweza nikamwona?” Jona akauliza akiwa anatarajia kuruhusiwa. Mguu wake ulikuwa tayari umeshajiseti kwendaze.
“Mmmmh kwa sasa hapana,” akasema Nesi. “Nimetoka kumdunga sindano ya usingizi muda si mrefu. Amekuwa halali, kuna mambo anayawaza sana bila shaka.”
Jona akajitengenezea vizuri kumtazama Nesi.
“Kwahiyo usiku mzima hakulala?”
“Ndio. Alikuwa anamimina machozi tu na kuvuta makamasi. Sasa anakosa muda wa kupumzika kitu ambacho kinaweza kumpa shida. daktari akaniagiza nimpumzishe kabla sijaondoka maana shift yangu ishakwisha.”
“Oooh!” Jona akatazama kushoto na kulia. “Naweza kuonana na daktari?”
“Bila shaka,” Nesi akamjibu na kuanza kutembea. Jona akamfuata kwa nyuma mpaka ndani ya ofisi ya daktari, kisha Nesi akaenda zake. Jona akaendeleza maongezi na daktari.
Daktari akampatia maelezo ya kutosha juu ya hali ya maendeleo ya Nade.
“Anaonekana mwenye mawazo. Tungepata ndugu au wanafamilia wake nadhani wangetusaidia,” daktari alisema akimtazama Jona kwa macho ya uhakika. Kisha akatazama tarakilishi yake ya mezani.
“Kwa ile dawa mliyompatia, atarudi kwenye fahamu zake muda gani?” Jona akauliza.
“Si muda mrefu in such kwani atahitaji kula chakula chake cha mchana,” daktari akamjibu.
“Ok, then ntangoja,” Jona akasema. Kisha kukawa kimya. Daktari alikuwa anatarajia Jona atatoka ndani ya ofisi yake muda si mrefu, ila haikuwa hivyo.
Akamtazama Jona. Wakakutana macho kwa macho.
“Dokta,” Jona akaita. “Kuna mtu mwingine alikuja baada ya mimi kuondoka siku ile?”
Dokta akamtazama Jona kwa kukodoa. Jona akatambua swali lake hilo limemshtua mwanaume huyo muhindi. Hakukwepesha macho yake, akamtazama.
Dokta akahamishia macho yake kwa kioo cha tarakilishi.
“Watu wanakuja wengi afisa, kila saa na kila muda. Siwezi nikawakumbuka wote waliokuja baada yako,” daktari akajielezea. Jona akiwa anaendelea kumtazama machoni, akamuuliza tena: “Hakuna mwanaume uliyeonana naye muda mfupi baada ya mimi kutoka? … Ni polisi.”
“Hapana.” Daktari akatikisa kichwa. “Hamna!”
“Una uhakika?” Jona akauliza.
“Ndio, hamna polisi aliyekuja hapa baada yako.”
“Nikithibitisha alikuja, sitakuwa na soni nawe. Nitaenda kukulaza ndani kwa juma zima upate akili.”
Daktari akawa kimya. Akamtazama Jona, akamwona ni mtu anayeongea kwa uhakika. Akahofia.
“Afande, nina kazi nyingi za kufanya muda huu. Tafadhali naomba unipatie nafasi,” daktari akajitetea akijikaza kumtazama Jona.
Jona akatoa pingu ubavu wake wa kulia kisha akasimama.
“No! You dont have to do that, kaa chini tuongee,” daktari akamwomba.
“Umekataa maongezi, sina tena huo muda wa kupoteza na wewe hapa,” Jona akakaza.
“Si kwamba sitaki, nimeambiwa nisiseme!” Daktari akaropoka. Jona akaketi chini, akarudishia pingu yake.
“Mnaniweka kwenye wakati mgumu!” Daktari akalalama. “Huyu anakuja ananiambia hivi, mwingine naye anakuja ananiambia hivi. I am confused!”
Kwa utulivu, Jona akaanza kumdadisi. Daktari akamwambia alikuja polisi aliyemtaka aeleze kila kitu alichofanya pamoja na Jona. Baada ya kuambiwa kila kitu, akatoa kitisho kwa nesi na yeye, wasiseme kama alikuja hapo hospitali!
Jona alipopata taarifa hizo akashukuru sana, akamuaga daktari na kumwambia anaenda zake nje kupata chakula. Atakuwapo hapo mpaka pale Nade atakaporejea fahamuni wapate kuteta mambo kadhaa.
Akaenda kantini kula, akiwa hapo akawa anatazama saa yake na huku akitazama njia endapo atabahatisha kumwona Alphonce. Alijua wazi mwanaume huyo anamfuatilia.
Akawa anakula taratibu kuvuta muda.
*** Saa sita mchana … ndani ya nyumba ya Miranda.
Dada wa kazi alimkaribisha Kinoo akiwa ameongozana na wanawake mapacha: Sara na Sasha, wanawake waliowahi kuwa wafanyakazi wa Bite kipindi yu hai.
Wanawake hawa kwa muda walikuwa wametengana ambapo Sasha alikuwa amesafiri akimwacha dada yake Sara aliyejipeleka mikononi mwa Kinoo kwasababu ya hofu. Sasa Sasha alikuwa amerejea, na jana yake tu wakawa na kikao pamoja na Kinoo juu ya mustakabali wao.
“Wewe ni mgeni hapa enh?” Kinoo akamuuliza yule dada wa kazi. Dada akatabasamu,
‘”Ndio, nimekuja hapa wiki iliyopita tu.”
“Oooh! Karibu sana,” Kinoo akamkarimu kisha akajitambulisha kama rafiki mkubwa wa bosi wake. “Ukiniita Kinoo hutokuwa umekosea.”
Dada akashukuru, kisha akawauliza wangependelea vinywaji gani wakati wakingojea Miranda aje. Wote wakaagiza maji ya kunywa. Dada akawapatia, na punde Miranda akatokea.
“Kinoo, umenikumbuka sasa! Yani wewe kama huna dili, hun’tafuti sio?” Miranda alisema akitabasamu. Wakakumbatiana na Kinoo na kusalimiana.
“Nakuona una ugeni.”
“Yah! Huyu anaitwa Sarah na huyu Sasha.”
Wakapeana mikono ya kutambulishana. Kinoo akamtambulisha Miranda na kisha wakateta habari za masiku ya kutokuonana.
Baada ya habari hizo, Kinoo akaeleza lililo kuu. Akamwambia Miranda kwamba Sara na Sasha wameazimia kuungana nao.
Jambo hili likamshtua Miranda, lakini hakufanikiwa kulionyesha. Akaomba apate faragha kidogo na Kinoo.
“Nina akili zangu timamu, Miranda,” Kinoo akajipambanua. “Najua ninachokifanya. Mimi sio mwehu mpaka kukuambia hivyo. Ninawaamini kwa asilimia zote. Hawana la kufanya kwa sasa. Wanaweza wakawa asset nzuri sana kutusaidia.”
“Unadhani BC atatuelewa kirahisi hivyo?” Miranda akauliza. Kinoo akamsogelea mwanamke huyo na kumshika bega.
“Lakini, Kinoo,” Miranda akatia shaka. “Mbona ni haraka hivyo? Mbona ghafla ghafla hivyo? Kuna nini?”
Kinoo akashusha pumzi ndefu na kutazama chini. Akarudisha macho yake kwa Miranda na kumwambia: “Sarah ana mimba yangu.”
Miranda akakodoa. “Wasema?”
“Sarah ana mimba yangu,” Kinoo akasisitizia. Miranda akashusha pumzi ndefu na kuulaza mgongo wake kitini.
Akatikisa kichwa chake akimtazama Kinoo. Akamlaumu kwa jambo hilo la kipumbavu, kamwe hakulitegemea kwa mtu kama yeye.
“Unajua wazi situation yetu. And blindly you are about to make a family!” Miranda akalalama. Hawakuongea sana na Kinoo, akamtaka mwanaume huyo aende, amwache peke yake.
Kinoo akaendaze akiongozana na wanawake wake aliokuja nao. Walijipaki kwenye gari, Escudo ya grey, wakatimka.
“Umefanikiwa?” Sasha akamuuliza Kinoo baada ya kuacha makazi ya Miranda kwa hatua kadhaa. Kinoo akashusha pumzi ndefu. Macho yake yalikuwa yanatazama mbele lakini akiwa amezama fikirani.
“Ni jambo la kuchukua muda,” Kinoo akajibu. “Lakini litakuwa sawa tu,” akawatoa hofu.
Hawakuongea tena kwa muda. Sauti ya gari tu ndiyo ikawa inavuma na kuita.
**
Jona akatazama saa yake mkononi. Muda ulikuwa umeenda sasa. Alishamaliza kula na sasa akaona ni vema akienda kumwona Nade kama vile daktari alivyomwambia kwamba atakuwa macho kipindi cha kula chakula cha mchana.
Akanyanyuka na kulipia bili yake ya chakula, na kwa hatua nzito akajongea mpaka kwa daktari moja kwa moja. Yeye hakuwa anangojea msururu wa wagonjwa kwa kutumia kofia yake ya kazi.
Akiongozana na nesi, akaenda mpaka alipolazwa Nade, akamkuta mwanamke huyo akiwa anakula.
Nade akatabasamu kwa mbali kumtia Jona machoni. Ni kama vile alikuwa anataraji ujio wa mwanaume huyo. Alionekana bado hana nguvu, ila ilikuwa kheri. Akamkaribisha Jona kula.
“Nashukuru,” Jona akasema kwa tabasamu la bati. Kisha “Nimefurahi kukuona,” akasema akimtazama Nade machoni.
Nade akatabasamu kimaumivu. Jona hakumwongelesha tena, akamwacha amalize kwanza kula.
“Daktari kaniambia umekuwa na mawazo sana hapa karibuni, nini shida?” lilikuwa swali la kwanza Jona kuuliza.
Nade akajilaza kwanza kitandani. Akawa kimya kwa muda. Mara macho yake yakaanza kulowana na hatimaye kuvujisha machozi.
Kuna kitu kilikuwa kinamsumbua kifuani. Jona aliliona hilo. Hakutaka kumlazimisha kuongea, akamngojea kwa wakati wake sahihi.
“Nisamehe sana, Jona,” Nade akasema akitazama dari. Macho yake bado yakiendelea kuvuja kama mto.
“Nimekukosea sana, najua hilo. Umekuwa ukinipa mkono wakati mimi nikikukabidhi kisu. Umetetea uhai wangu lakini mimi nikifanya jitihada kuupokonya wa kwako. Nisamehe sana. Sistahili hata msaada wako.”
Uso wake ukawa mwekundu. Mafua yakaanza kumtambalia, na kwikwi za kilio zikampalia.
Akamwomba sana Jona msamaha. Jona akamsihi hana haja ya kufanya hivyo kwani alishamsamehe, hata hivyo alifanya hayo kwasababu za ushawishi wa bosi wake, marehemu Eliakimu.
“Nataka tu uniweke bayana kile ambacho bosi wako alikuwa ananificha. Naomba unisadie kwenye hilo,” Jona akampendekezea, lakini hakutaka kumpa presha mwanamke huyo kutokana na hali yake, akamtaka apumzike, na utakapofika muda basi wataongea kwa urefu na mapana.
Lakini Nade akakataa.
“Tuongee tu hata sasa,” akateta kwa sauti ya chini ya msisitizo. Uso wake ulikuwa mzito ukizongwa na majuto ya kujiona mkosefu. “Huna haja ya kungoja, Jona, ntakwambia hata sasa.”
Kisha akakaa kimya. Bado macho yake yakimwaga machozi.
Kwa uchungu mkubwa, akaanza kufunguka kinagaubaga. Akamweleza Jona ni kwa namna gani Eliakimu alivyokuwa anacheza mchezo wa damu kwa kutumia mkono wa serikali.
Namna gani alivyokuwa anashiriki magendo na biashara haramu na vitu hivyo vikamvunisha pesa nyingi mno. Namna alivyokuwa akishirikiana na magenge ya wauaji, madawa ya kulevya, utakatishaji wa fedha na kadhalika na kadhalika nyuma ya pazia.
Na ni kivipi alivyokuwa anatumkika kama mkono wa kushoto wa bwana Eliakimu akitumwa kuwamaliza maadui zake, na hata wale washirika wake waliomzulumu baada ya kupiga dili.
Akamweleza Jona yote kumhusu BC na Sheng. Namna anavyowafahamu, na jinsi walivyoshirikiana na hao watu kutimiza kazi kadhaa za kimagendo, ikiwamo kuingiza nchini makemikali yaliyokatazwa, pia hata madawa ya kulevya.
“Tulifanya hivyo kwa siri sana tukitambua wazi BC na Sheng walikuwa ni maadui wakubwa kibiashara, lakini tukafanikiwa kula na vipofu.”
Akamwambia pia Jona ni kwasababu gani walikuwa wanamuwinda Miriam, na kwanini basi mwanamke huyo alikuwa anatakiwa kuuawa japokuwa ni mke wa Eliakimu.
“Kwanza Miriam hakuwa anampenda Eliakimu hata kidogo. Eliakimu alikuwa analijua hilo, lengo la mkewe lilikuwa ni kurithi tu mali zake pindi atakapofariki ama kumuua. Ilifikia kipindi Miriam akawa anatembea na mshirika mmoja wa kibiashara wa Eliakimu, mwanaume huyu akiitwa Nyokaa, mfanyabiashara wa madini Arusha.
Nyokaa alikuwa amekorofishana na Eliakimu kwasababu za kibiashara. Kila mmoja akawa anataka kulipa kisasi kwa mwenzake kwa kutuhumiana kurudishana nyuma, lakini kiuhalisia ni Eliakimu ndiye alikuwa na makosa. Aliingia dili na Nyokaa, mwisho wa siku akamsaliti kwa kuchukua kiasi fulani cha mzigo wake na kumdanganya ulipotelea njiani kwasababu za kiusalama.
Kulipiza kisasi na kurejesha fedha yake nyingi, akafanikiwa kumlaghai Miriam ili amtumie kunyooshea biashara zake kwa mtandao wa Eliakimu.”
Jona akakuna kidevu chake. Akajikuta anapata kiu ya kutaka kujua zaidi na zaidi kadiri alivyokuwa anaelezwa.
Akataka kujua kwanini Nade hakutumwa kummaliza Nyokaa baada ya kuyatambua hayo. Nade akamwambia asingeliweza hilo kwani Nyokaa ana jeshi kubwa la watu.
Si rahisi kumkamata kama kutamka.
“Tulikuwa tunataka kumrejesha tu Miriam kwani alikuwa anajua mengi kumhusu Eliakimu, kwahiyo kuwa mikononi mwa adui, ilikuwa ni hatari sana.”
Lakini zaidi, Eliakimu asingeweza kutekeleza mipango na mambo yake yote haya akiwa peke yake. Hilo lilikuwa bayana.
Ni lazima kuna watu vitengo na maeneo mbalimbali aliokuwa anasaidiana nao.
“Ni watu wengi mno,” akasema Miranda. “Kila mtu na eneo lake, kila mtu na kitengo chake. Kila mtu akicheza nafasi yake kutimiza maagizo ya Eliakimu. Na kwasababu alikuwa anatoa pesa nono, haikumuwia vigumu kuwakamata.”
Sasa Jona akaona kuna haja ya kutia nguvuni watu hao wote, lakini ushahidi ni muhimu sana kwenye hili. Ataupataje? Na atawapatia wapi watu wote hawa waliokuwa wanashirikiana na Eliakimu?
“Usijali,” Nade akamtoa hofu. “Eliakimu alikuwa ana orodha ya watu wake wote aliokuwa anafanya nao kazi, pamoja pia na mawasiliano yao.”
Akamwelekeza Jona wapi atavipata. “Chumbani kwake, kwenye droo za kitanda, utakuta nyaraka zake zote humo. Ufunguo wa droo hizo huwa anauweka ndani ya moka zake ndefu nyeusi kwenye stendi ya viatu.”
Jona akashukuru kwa taarifa hizo. Lakini kabla hajaondoka, akamsihi mwanamke huyo asimweleze mtu mwingine yoyote juu ya habari alizoongea naye. Nade akamhakikishia hilo kwa kuapia na maisha yake.
“Sitakusailiti tena kwa sasa.”
Jona akaenda zake.
Lakini kama ilivyo ada, nje ya hospitali Jona akaonekana na Alphonce aliyekuwa ameketi ndani ya gari lake. Mwanaume huyu akamtazama Jona akiishilia, kisha akashuka garini na kuzama ndani ya hospitali.
Moja kwa moja akaonana na daktari na kumtaka afanye vile alivyokuwa anataka, amweleze yale yote Jona aliyoyafanya hapo. Kama haitoshi, akambana pia na nesi, ila bahati si kwake nesi wa zamu, yule aliyekuwa na Jona, alikuwa tayari ameshaondoka.
Akaagiza aonane na Nade.
Akaongozwa na nesi kupelekwa huko chumbani. Akamkuta Nade akiwa amelala. Akamwamsha.
“Naweza nikaongea na wewe machache?” Alisema kwa sura ya bati kisha akamtazama Nesi kwa uso wa kumwomba nafasi. Nesi akaenda zake.
Nade akamtazama Alphonce kwa macho makali akinyanyuka. Akakunja ndita zake na kuuliza:
“Kumbe ni wewe?”
Mwanamke huyu alikuwa anamtambua vilivyo Alphonce! Tayari kichwani kwake akajua mambo si shwari.
Alphonce akatabasamu. Akatoa leso kwenye koti lake la suti kisha akajifuta viganja vyake.
“Ndiyo ni mimi. Bila shaka ni muda mrefu umepita,” akasema kwa sauti nzito.
“Unajua nataka nini, Nade. Mimi ni polisi, umesahau?”
“Polisi gani wewe?” Nade akastahamaki. “Wewe ni muuaji tu uliyevaa sare za polisi. Hujawahi kuwa polisi hata siku moja!”
Alphonce akaguna. Na mara akatabasamu.
“Sijaja hapa kulumbana na wewe, Nade. Nina mambo mengi ya kufanya, kwahiyo tafadhali jali muda wangu nia–“
“Sitakuambia kitu!” Nade akamkatiza. “Usitarajie nitakwambia lolote lile, Alphonce. Kwa hilo sahau.”
“Utakuwa unatania!” Alphonce akastaajabu. “Unajua wazi mimi na wewe tupo behewa moja. Unadhani kutokuniambia kitu kutakuweka wewe salama? Embu acha ujinga. Hii ni kwa ajili yetu wote. Niambie nini Jona alikuwa anataka toka kwako na kwanini alikuwapo nyumbani kwa Eliakimu siku ya tukio?”
Nade akatabasamu. Akatabasamu tena zaidi.
“Alphonce, naona hunielewi. Nimechoka na haya mambo, nipo tayari kufa lakini siyo kuendelea kufanya makosa yaleyale. Niliyofanya yanatosha, usidhani ntakusaidia wewe ukayaendeleze. Enough is enough!”
“Acha upumbavu Nade!” Alphonce akafoka. Sura yake sasa ilibadilika na lile tabasamu la mwanzoni halikuwapo tena. “Acha ujinga wewe mwanamke! Unataka kwenda kuozea jela? Do you know how serious this matter is?”
Nade akatabasamu akimtazama mwanaume huyo. Akamshika mkono na kumwambia kwa upole:
“Yamekwisha, Alphonce. Kila zama zina mwisho wake. Umeshachelewa. Jiandae kwa anguko lako.”
Alphonce akapandwa na hasira kali. Akamkaba mwanamke huyo mpaka alipohakikisha amekufa. Akawaza nini cha kufanya, akawaza ni nini Nade atakuwa amemwambia Jona.
Kichwa chake kikazunguka kwa msongo wa mawazo. Akanyanyuka na upesi akatoka ndani ya chumba. Hakuonana na daktari wala nesi, akanyookea moja kwa moja ndani ya gari lake..
Akaliwasha na gari lilivyoanza kwenda ndipo akapata akili juu ya nini cha kufanya. Aliamini Jona atakuwa ameelekea nyumbani kwa Eliakimu. Maneno ya Nade yalimshawishi aamini hivyo.
Simulizi : Anga La Washenzi (1) Sehemu Ya Tano (5)
***
Klak! Klak! – Klak! Klak! Kitasa kikalia pasipo mlango kufunguka. Jona akajaribu kuupush kwa uzito wake, akashindwa. Mlango ulikuwa mgumu na mzito.
Basi akarudi nyuma na kuukita teke, ukavunjika! Akazama ndani ya chumba hiki cha Eliakimu na kuanza kupekuapekua kwa macho yake.
Kitanda kilikuwa hovyo. Na kulikuwa kuna nguo kadhaa juu yake. Kabati la nguo lilikuwa limefungwa nusu, dirisha nalo likiwa limesukumwa kidogo.
Haraka Jona akatazama droo za kitanda. Akazisogelea na kujaribu kuzifungua kama zipo wazi. Akaona zimefungwa. Akapata tumaini.
Akachukua ufunguo kule alipoelekezwa na Nade kisha akafungua droo hizo. Ndani akakuta mafaili kadhaa, akayapekua kwa haraka haraka na kuyakusanya. Akatoka ndani ya chumba.
Kushika korido, akakutana uso kwa uso na Alphonce aliyekuwa amesimama mlangoni.
“Habari yako?” Alphonce akasalimu kinafki. Kisha akatabasamu na kuuliza:
“Nimekushtua, unh?”
Jona akasonga mpaka sebuleni akitembea kwa kujiamini.
“Kivuli changu kitawezaje kunishtua?” Akauliza akisimama. Kati yao kulikuwa na hatua kama nne tu zikiwatenganisha. “Najua umekuwa kivuli changu ukinifuata kila ninapoenda. Nakutarajia kila ninapotoa mguu.”
Kukawa kimya kidogo wakitazamana kwa macho ya tahadhari. Alphonce akatazama mkono wa Jona, kisha akayarudisha macho yake usoni mwa mwanaume huyo.
“Umekuja kufanya nini hapa?” Akauliza.
“Hiyo si kazi yako,” akajibu Jona.
“Nani amekuruhusu kuja hapa?” Alphonce akauliza tena. “Hii kesi haikuwa yako bali ya inspekta Faridi.”
“Najua,” Jona akajibu. “Hii kesi ni yangu pia kwani nami nahusika … actually, nimewasiliana pia na Faridi juu ya hili.”
Kukawa tena kimya. Akili zao zilikuwa zinaongea mengi kuliko midomo.
“Au unadhani sifahamu hilo? Ukamuua na mfanyakazi mwenzangu pia … yote nayafahamu. Usidhani mimi ni mjinga, Alphonce. Nangoja muda wangu ufike,” Jona alisema kwa sauti makini akiwa amezamisha mkono wake wa kushoto mfukoni.
Alphonce akaguna kidharau.
“Wakati gani huo Jona? Unadhani unaweza ukapigana na ukuta?” Kisha akacheka. “Kutaka kujua vingi, kulimuua paka. Kwanini usicheze kwa mujibu wa ala ya muziki?”
Akaongezea:
“Jona, hakuna mtu aliye upande wako. Tambua hilo. Unatakiwa kubaki jeshini, lakini acha kufuata nyayo za wakubwa zako, ikiwemo mimi kwani kamwe hautafanikiwa!”
Jona hakusema kitu ila moyoni alikuwa anapasuka.
“Uliacha jeshi, mbona umerudi? Kwa mwerevu angejifunzia hapo.”
Jona akasaga meno. Alikabwa na hasira kali, lakini akipambana asiionyeshe. Bado kuna kitu alikuwa anakitaka toka kwa Alphonce.
“Mliteketeza familia yangu, mkaharibu kila kitu changu. Niliwakosea nini?”
Alphonce akacheka. “Nimeshakueleza, Jona. Na ukiendeleza ukaidi, mkono huu ulioteketeza familia yako, utakuteketeza na wewe pia!”
“Nani alikutuma, Alphonce?” Jona akauliza. Macho yake yalikuwa mekundu kama bendera.
“Sina muda wa kuzoza tena, Jona,” Alphonce akamjibu. Kisha akamuamuru: “Nipe hayo mafaili au niyachukue kwanguvu?”
Jona akayaweka mafaili mezani.
“Haya hapa. Chukua.”
Alphonce akatabasamu kwa dharau.
“Nilikuwa naingoja sana hii nafasi,” akasema akivua koti lake la suti. “Leo nitakufunda adabu na kuheshimu wakubwa zako.”
“Unaonaje tukitoka nje?” Jona akapendekeza. Alphonce kwa majivuno akaufungua mlango na kutangulia kumbini. Akakunja ngumi na kusimama sawia kwa ajili ya mpambano.
Jona akamtazama mwanaume huyu kwa macho ya kina. Akamkagua kuanzia juu mpaka chini kisha akasema na moyo wake.
Akakunja ngumi, akatanua miguu kupata balansi. Basi haraka Alphonce akamvamia. Akarusha ngumi tano kwa wepesi mno na kwa hasira!
Vuup! – vup! vuup! – vup!
Kinyume na mwili wake ulivyo, alikuwa mwepesi kwenye kufanya maamuzi na kujifyatua. Alikuwa ana haja ya kumpiga Jona kuliko Jona alivyokuwa na haja ya kumpiga yeye.
Alikuwa anatumia nguvu nyingi kushambulia. Lakini mdhaifu kwenye kujikinga, Jona akatambua dhaifu hilo. Lakini hakuwa na haja ya kumuua Alphonce. Hakudhani kama mwanaume huyo anastahili kufa kwa haraka.
Hakustahili kabisa!
Mwanaume huyu alistahili kifo cha taratibu taratibu. Mwanaume huyu alistahili mateso ya kufanya kifo kionekane ni ahueni.
Mwanaume huyu alistahili ahisi angalau robo ya maumivu aliyoyapata mkewe na mtoto wake ndani ya moto mkubwa wa kuteketeza!
“Shit!” Alphonce akalaani. Alikuwa sasa ametimiza idadi za ngumi ishirini pasipo kufanikiwa hata moja! Na wala Jona hakuanza kumshambulia.
Akabadilisha mtindo. Sasa akawa anamshambulia Jona kwa mateke zaidi na ngumi za kushtukiza. Hapa sasa akafanikiwa kumtwanga Jona ngumi moja ya shavu iliyompepesa!
Akatema damu na kujipangusa na mgongo wa kiganja. Akaghafirika mno. Akasahau agano lake juu ya Alphonce, akaanza kumshambulia mithili ya nyuki waliotibuliwa mzingani!
Akapangua ngumi za Alphonce kwa mateke. Na kwa kasi ya radi, kabla Alphonce hajafikisha ngumi juu ya mwili wake, yeye akawa ameshampachika mwanaume huyo mateke matatu!
Alphonce alikuwa mwepesi, ila Jona alikuwa mithili ya umeme. Alikuwa anatambua nyendo za Alphonce kabla hajaamua hata kuzitekeleza.
Alphonce akagugumia maumivu akiwa chini. Kifua kilikuwa kinamuwaka moto. Alimtazama Jona kwa ghadhabu kisha akajikakamua kunyanyuka arudi kwenye pambano.
Akakimbia kumfuata Jona, lakini kabla hajafanya shambulizi lolote, akastaajabu Jona amefyeka miguu yake na yupo hewani kimo cha ndama!
Hajakaa vema, akashindiliwa teke la tumbo lililombamizisha sakafuni na kumcheusha damu lita moja!
Akatulia kwa muda chini. Alikuwa hajielewi kwa maumivu makali aliyoyapata. Kichwa kilikuwa kinamgonga, tumbo lilikuwa linamvuta! Alihisi kiuno pia kimeteguka.
Akamtazama Jona, akamwona mwanaume huyo akiwa amesimama mkono wake wa kushoto upo mfukoni. Akamuuliza;
“Umemaliza?” kisha akacheka akionyesha kinywa chake kilichokuwa chekundu kwa damu. “Wewe mshenzi tu! Mshenzi tu kwangu. Unasikia?”
Jona hakujibu kitu. Alikuwa anamtazama na macho yake mekundu.
“Bado nakumbuka vizuri siku ile,” Alphonce akajinasibu. “Mkeo alikuwa anapiga yowe kukuita. Mwanao alikuwa analia kwa namna moto ulivyokuwa unamtafuna!”
Akacheka.
“Ilikuwa ni siku maridadi sana! … siku maridadi sana. Sitaisahau. Ilikuwa ni siku niliyolipiza kisasi changu cha kwanza dhidi yako. Ilikuwa ni siku niliyokufanya nawe uhisi kile nilichopitia mimi kwa kunipokonya nafasi niliyokuwa nayo jeshini.
Ulinifanya nidharaulike sana. Kila mtu alikuona na kukusifu wewe. Kila mtu alikuona shujaa. Kila mtu akanisahau mimi ni nani. Juhudi zangu zote jeshini zikawa ni bure!”
Akatemea damu pembeni.
“Nilikuchukia sana, na hata sasa pia. Ulinipokonya kile nilichokuwa nacho, lakini …” akaangua kicheko. “Wewe nimekupokonya zaidi!”
Akacheka tena.
“Bado mimi ni mshindi Jona! Bado mimi ni mshindi!”
Jona akachuruza chozi. Akakunja ngumi yake kwa hasira. Moyo wake ulikuwa unavuja damu. Alimkumbuka mkewe. Alimkumbuka mwanae.
Akasaga meno. Mishipa ya damu ikamsimama kichwani.
“Na hata sasa mimi bado ni mshindi!” Alphonce akaropoka akisimama kwa tabu. Akamjongea Jona apate kurusha tena turufu lake la pambano.
Lakini katika namna ambayo hakuielewa ilitokeaje, akastaajabu kujikuta yupo chini! Kitu pekee alichokuwa anakumbuka, ni kusikia kitu kama upepo ukipita masikioni mwake.
Lakini zaidi hakuweza kuusogeza mwili hata kidole! Ni macho tu ndiyo yalikuwa yanasonga huku na kule.
Hakuuhisi mwili wake kabisa.
“Jona!” Akaita. “Jona! Jona umenifanya nini? Umenifanya nini Jona?”
Jona akamtazama pasipo kusema kitu. Macho yake yote yalikuwa yanatiririsha machozi.
“Nisaidie tafadhali!” Alphonce akaomba. Jona akampa mgongo na kwenda zake ndani. Akachukua mafaili yake na kuondoka akimwacha Alphonce anapiga kelele sakafuni.
**
Saa nne usiku…
Kwa mbali muziki laini ulikuwa unaita. Mazingira yalikuwa yametulia kwahiyo basi ungeweza kusikia vizuri sauti tamu ya kukwaruza ya Michael Bolton akiimba kibao chake matata cha Soul Provider cha mnamo mwaka 1989.
Juu ya kochi, alikuwa ameketi Jona akiwa kifua wazi na kibukta chepesi cha kulalia. Juu ya meza ilikuwa imekaa chupa kubwa ya kinywaji kikali, kando yake kulikuwa kuna yale mafaili aliyoyatoa kwa Eliakimu.
Akanyanyua chupa yake ya kinywaji na kuipeleka mdomoni, akagigida mafundo mawili makubwa. Akiwa amekunja uso, akarejesha chupa hiyo mezani akiisoma jina lake.
_Bacardi 151_
Kwenye lebo yake ya kiasi cha ulevi kilikuwa na alcohol 75.5%! Haikuwa mchezo kabisa!
Jona alikinunua kinywaji hiki maana aliona anakihitaji kwa usiku huo. Huwa anakunywa vinywaji vikali ila siku hiyo alihitaji kikali zaidi na zaidi maana alihisi anaweza akashindwa kulala.
Kila saa alipokuwa anatulia alikuwa anasikia maneno ya kebehi ya Alphonce kuhusu familia yake. Kila aliposikia sauti hiyo, akamkumbuka mkewe. Akamkumbuka mtoto wake kuliko kawaida.
Huwa anawakumbuka, lakini leo hii ilikuwa ni kana kwamba ametoka kushuhudia jengo lake likiwa linateketea. Alphonce alimkumbusha kwa kina. Alikitifua kidonda kilichojenga gamba.
Akashindwa hata kupekua mafaili yale, akabaki anakunywa tu. Baada ya kuongeza mafundo matatu tu ya Bacardi, kichwa kikashindwa kuendeleza kazi, fahamu zikakata, akajimwagia kochini!
Jinamizi lililokuwa linamtesa, leo likarudi kwa nguvu zote.
Saa tatu asubuhi, SPACE BUTTON.
Kulikuwa bize kama ilivyo ada. Watu walikuwa wanatazama vioo vya tarakilishi zao huku vidole vikitwangatwanga ‘keyboard’. Watu hawa kwa idadi walikuwa nane, hakukuwa na mwanamke hata mmoja.
Mazingira yalikuwa tulivu ukiachana na sauti za keyboard. Hakukuonekana kama kuna shida yoyote, wala kama inaweza kubashiriwa kwa hapo mbeleni.
Hali ya hewa ilikuwa baridi, viyoyozi vilikuwa moto. Kuna baadhi yao wakawa wanavuta vikamasi na huku pua zao zikiwa nyekundu kwa kuzifikichafikicha mara kwa mara.
Pengine baridi lilikuwa kali kuliko siku zingine. Mmoja akapaza sauti kumuita Moderator na kumtaka apunguze kasi ya viyoyozi hivyo la sivyo watakufa.
Kidogo zogo likatokea hapa watu wakiunga mkono hoja hiyo. Ni kama vile walikuwa wanamngojea ‘shujaa’ ajitokeze kusemea hilo jambo wapate kum ‘mback-up’. Kinyume kabisa na taratibu ndani ya chumba cha SPACE BUTTON watu wakaruruma na kuzoza. Haikuwa inaruhusiwa kufanya hivi.
Moderator alitii haja yao akapunguza kasi ya viyoyozi, kazi zikaendelea tena kwa ukimya. Lakini miongoni mwa watu hao waliopaza sauti zao kuhusu ukali wa viyoyozi, si Marwa wala Panky aliyekuwapo.
Wao walikuwa kimya. Wao walikuwa wakiendelea na kazi zao kana kwamba hakuna kilichojiri, hakuna walichosikia.
Zikapita dakika tano watu wakiendelea na kazi. Kama ilivyo ada ndani ya SPACE BUTTON ni keyboard tu ndiyo zikawa zinasikika. Ilipohitimu dakika ya sita, mara taratibu viyoyozi vikaanza kurudi kwa kasi.
Baridi likawa jingi, watu wakaanza kupata shida. Ni kana kwamba walipelekwa kwenye kilele cha mlima mrefu mno.
Wakaanza kulalamika tena, mada hii Moderator alikuwa ametoka kidogo. Wakazoza na kuzoza, Moderator aliporudi akastaajabishwa na hali hiyo ya ‘soko’. Kabla hajafoka kukemea na kutoa vitisho, akatambua baridi lilikuwa limeongezeka maradufu.
Haraka akatazama tarakilishi yake. Akabofya keyboard mara kadhaa. Akapiga ngumi mezani kisha akatoka ndani. Bila shaka alikuwa anaenda kuangazia mitambo kama ina hitilafu.
Kiwizi, Marwa akamtazama Panky, akatabasamu, alafu akarudisha uso wake kwenye tarakilishi.
“Nimefanikisha!” Ujumbe ukaingia kwenye tarakilishi ya Panky kwa kutumia jina la M-spy.
PANKY: Sure? (Hakika?) M-SPY: Yah sure. (Ndio hakika). PANKY: How did you do that man? (Umewezaje jamaa?) M-SPY: Aaanh! Maswali gani hayo? Nataka nitazame kama naweza pata chochote kwenye mashine yake. Nipe muda kidogo.
Marwa akaanza kuitembelea tarakilishi ya Moderator kwa kutumia ya kwake. Alikuwa anafanya hayo kwa wepesi kwani hakuwa na muda wa kutosha, na usalama ulikuwa finyu mno.
Alijua endapo Moderator angepata muda wa kutulia kwenye mashine yake, angezijua njama zake. Kwahiyo alitakiwa kutumia fursa hiyo upesi kabla mwanaume huyo hajarejea kitini.
Dakika mbili tu, Moderator akawasili. Tayari hali ya hewa ilikuwa imetulia. Akatazama wafanyakazi wake akikagua tarakilishi zao kwa macho, kisha akaketi. Akashusha pumzi ndefu.
Akakagua tarakilishi yake akijiuliza nini shida. Akakagua kila kitu, hakuona tabu. Akakagua na tarakilishi za wafanyakazi wake kwa kutumia ya kwake, kote akaona wakifanya kazi zao.
Akajilazimsha kuamini tatizo lile la viyoyozi litakuwa ni la mitambo.
PANKY: Umefanikiwa? M-SPY: Kiasi chake. Bado nahitaji kuingia tena kwenye mashine yake kuna kitu sijamalizia. PANKY: Utaingiaje? Amesharejea. Ataongeza uangalifu sasa hivi kuliko mwanzoni. M-SPY: Najua. Natazamia namna nitakavyofanya jambo hili kwa usalama. PANKY: Be careful. (Kuwa makini) Kukawa kimya kidogo kwa dakika nne, Ujumbe wa Marwa uka ‘pop-up’ kwenye kioo cha tarakilishi ya Panky. M-SPY: Nimepata wazo.
Akamshirikisha wazo hilo Panky, naye akalikubali. Ikapita dakika moja, mara Panky akadondoka chini akihangaika kuhema kana kwamba koo lake la hewa limesiliba! Mbavu zikamsimama. Mishipa ikamchomoza. Macho akayatoa huku shingo ikishupaa.
Watu wakapigwa na butwaa. Wakaamini Panky atakuwa ameathiriwa na mabadiliko yale ya hewa yaliyokuwa yanatokea ndani ya chumba hicho hapo nyuma.
Haraka wanaume watatu wakafanya kumsaidia wakiwa pamoja na Moderator. Wakampeleka kupata huduma huko nje. Sasa Marwa akatimiza adhma yake upesi.
Baadae wakati wa kupata chakula cha mchana, wakaketi meza moja na Panky kuteta. Walihakikisha hakuna mtu aliyekuwa anawasikia, na wapo salama.
“Ndio, nimefanikiwa. Nadhani nimepata kila tunachokihitaji.”
Panky akatabasamu. Lakini mara kiganja kikagusa bega lake, akageuka na kukutana na uso wa Moderator.
“Njoo,” Moderator akamwambia kwa lafudhi ya ki Mandarin, kisha akaenda zake. Marwa akamtazama Panky kwa hofu. Moyo wake ulikuwa unakimbia kwa kasi. Alimshika mkono Panky akamwomba awafikishie taarifa familia yake endapo hatofanikiwa kutoka hai.
Kwa haraka pia akamwambia Panky taarifa alizozipata atakazikuta chini ya keyboard karatasini, kisha akaenda zake.
Panky akabaki na mawazo. Vipi kama Marwa amegundilikana? Hakupata hamu ya kula tena. Kifua chake kilikuwa kimejawa hofu. Je, watatambua hata kuumwa kwake kulikuwa ni mpango? Akajiuliza.
Alihisi mwili wake umekuwa wa baridi.
Mara kengele ya kurejea kazini ikalia, wote wakanyanyuka toka kantini na kurejea ndani ya SPACE BUTTON. Marwa hakuwapo kwenye kiti chake. Akamtazama na pale kwa Moderator, hakumwona, si yeye wala Moderator.
Basi haraka akanyanyuka na kwenda sehemu ya Marwa, akavuta droo ya keyboard na kutazama kwa chini, akaona kikaratasi kidogo cheupe. Akakibeba na kurudi sehemu yake upesi.
Hakukitazama kikaratasi hicho, alikiweka mfukoni na kuendelea na kazi yake lakini kila saa akawa anatazama kama atamuona Marwa ama Moderator.
Baada ya kama nusu saa, Moderator akarejea ila Marwa hakuonekana. Hapo sasa Panky akapoteza matumaini. Akahisi kweli pengine Marwa ameuawa.
Hakuweza kufanya kazi vizuri kabisa. Kichwani hakukuwa na maelewano kabisa, alikuwa anamuwaza Marwa. Mpaka unafika muda wa kuondoka kazini, Marwa hakuonekana popote pale!
Panky akakosa amani.
“Kuna shida?” Moderator akamuuliza Panky aliyekuwa amebaki mwenyewe kitini. Chumba kizima cha SPACE BUTTON kilikuwa cheupe.
Panky akashtuka sana. Hakuweza kutazamana macho na Moderator. Alizama fikirani na hata hakuwa anawaza kama mule ndani kaachwa na Moderator pekee.
Akaweweseka,
“Hamna shida! -hamna!”
“Sasa mbona upo hapa mpaka muda huu?”
Akakosa jibu. Akatazama kushoto na kulia kwake, hakukuwa na mtu yeyote. Akazima tarakilishi yake na kusimama.
Pasipo kuaga akaenda zake. Moderator akamtazama mpaka mwisho mwanaume huyo akiishilia.
Alipotoka ndani ya jengo hilo, asiamini, akaongeza kasi mpaka kituo cha mabasi. Akashangaa hakuitwa. Akaketi hapo kituoni akitazama barabara, labda anaweza kumwona Marwa.
Akaketi kwa muda mrefu hapo pasipo matunda. Akaamua kupanda zake gari arudi nyumbani. Sasa akawa anafikiria ni kwa namna gani awataarifu wazazi wake Marwa juu ya mtoto wao.
Kwahiyo kama Marwa akiuawa, wazazi wake wataendelea kupewa antidote? Ama ndiyo wataachwa wajifie maana hawana tena umuhimu?
Alilaza kichwa chake juu ya kioo cha dirisha akiwaza.
Watakuwa wamemuuaje Marwa? Na kama kweli wamegundua alidukua tarakilishi ya Moderator, hawatamdadisi kujua kwanini amefanya hivyo? Je, Marwa atawatoa chambo?
Yalikuwa ni mawazo baada ya mawazo. Shukrani tairi la gari lilizama kwenye kabonde kadogo barabarani gari likayumba, Panky akajigonga na kurudi fahamuni. Akatambua alikuwa anakaribia kupitishwa kituo!
“Shushaa! Shusha hapo!” Aliropoka akisimama. Mfukoni akatoa simu na pesa yake akijongea kwenda mbele kushuka. Mara ujumbe ukaingia.
Haraka akausoma.
‘Mbona hujaningoja? Upo wapi?’ Ilikuwa ni ujumbe toka kwa Marwa. Akajikuta anapiga yowe la ushindi. Akampatia konda shilingi alfu mbili na wala chenji hakuchukua.
“Oh no keep change, una mawazo mengi itakufariji weekend!” Alisema kisha akiondoka kibingwa.
Alicheka. Alihisi kifua chake kimekuwa chepesi.
Marwa yupo hai!
*** Saa kumi jioni, Jangwani Sea breeze.
Akiwa amevalia gauni fupi jeusi lililombana na chini viatu vyekundu vyenye kisigino kirefu Miranda alitazama huku na kule baada ya kuingia kwenye hoteli hii ya wastani.
Alikuwa kapendeza na anavutia japokuwa usoni hakuwa amejipara. Alibaki kiasili.
Nywele zake ndefu za bandia zilikuwa zinarukia huku na kule akipepesa kichwa. Mara akamwona mke wake Boka akiwa ameketi kwa juu, kwenye ghorofa moja iliyokuwepo hapo. Akapandisha ngazi kuelekea huko juu kumkuta.
“Usiniambie nimechelewa?” Akasema Miranda kwa tabasamu huku akiketi. Mke wa Boka alikuwa ametulia kitini ndani ya vazi la kitenge. Mezani kulikuwa kuna chupa ya soda ya Cocacola.
“Wala hujachelewa, karibu,” akasema Mama huyu. Macho yake mekundu yalikuwa yameingia kwa ndani.
Wakasilimiana. Miranda akatazama huku na huko kisha akauliza:
“Hao wazungu wako wapi? Hawajafika bado?”
Mke wa Boka akamtazama kwa sekunde tano, alafu akamjibu:
“Yes, serious,” mama akajibu akijitengenezea kitini.
Miranda akaanza kuhisi jambo. Kwa kiasi akawa na hofu moyoni. Aliukagua uso wa mke wa Boka vema, akajua kitumbua kitakuwa kimeingia mchanga.
Akapanga kukana kila jambo hapa endapo ataulizwa kuhusu Boka.
“Miranda, umeanza lini mawasiliano na mume wangu?”
Nilijua tu, Miranda akasemea kifuani. Mawazo yake yalikuwa sahihi. Kitumbua kimeingia mchanga.
“Mawasiliano ya kivipi, mam?” Akauliza kana kwamba hajui kinachoendelea. Mke wa Boka akamjuza anajua kila kitu na hivyo basi asijaribu kumdanganya hata kidogo.
Anajua amekuwa akikutana na mumewe na pia wana mahusiano kati yao hadi kupanga mikakati ya kusafiri pamoja na hata ndoa.
Miranda akabaki amestaajabu. Sasa rangi zake zilikuwa wazi, hakujua kipi cha kusema zaidi ya kuwa kimya na kutazama chini.
“Sikujua kama wewe ni mbweha kiasi hiki!” Mke wa Boka akateta akisaga meno. “Najua humpendi Boka, unataka tu pesa zake ama kumtumia. Unajua nimetoka naye wapi?”
Miranda hakusema kitu.
“Nakuuliza wewe, unajua nimetoka naye wapi?” Mama akasisitizia swali kwa sauti ya kufoka. Bado Miranda alikuwa kimya anatazama chini.
“Nakuuliza wewe malaya una …” Mama akanyanyua chupa ya soda na kumrushia Miranda kwanguvu. “…jua nimetoka naye wapi?”
Ajabu, Miranda akaidaka chupa hiyo kana kwamba kitenesi kisha akaiweka mezani. Akamtazama mke wa Boka na kumwonyeshea ishara ya kidole kikicheza.
“Usijaribu tena huo ujinga.”
Mke wa Boka akastaajabu. Mwanamke wa aina gani huyu? Asiseme kitu, Miranda akanyanyuka na kwenda zake mke wa Boka akimtazama.
Punde kwenye siti ile aliyokuwa amekaa Miranda, akaja kuketi mwanamke mwingine mnene mweupe. Naye alikuwa amevalia kitenge kama kile cha mke wa Boka, sare.
Huyu alikuwa ni rafiki yake mke wa Boka na walikuja naye hapo tukioni lakini wakatengana muda mfupi kabla Miranda hajawasili eneoni.
“Vipi shoga?” Mwanamke huyo akauliza kwa hamu. “Mbona ameondoka anatamba kiasi kile?”
Mke wa Boka akaminya lips zake. Hakutaka kusema kitu. Alisimama na kumwambia shoga yake waende zao.
Macho yake yakaanza kulowana. Hata shoga yake akaogopa kumwongelesha, akaomba tu safari yao iwe salama maana dereva hakuwa sawa hata kidogo.
“Nitaona kama na risasi utaweza kuidaka!” Akasema mke wa Boka kwa ghadhabu.
—
Baada ya robo saa…
Miranda ndani ya gari kwenye foleni la mataa.
‘The woman will spoil the food. She has already known all of our moves’ (Mwanamke atatuharibia chakula. Ameshajua nyendo zetu zote) Miranda aliutuma ujumbe kwa BC.
‘What woman? His wife?’ (Mwanamke gani? Mkewe?) Ujumbe wa BC ukauliza.
‘Yes, it’s her.’ (Ndio, ni yeye) Miranda akajibu.
‘Then take care of her immediately!’ (Basi mzingatie mara moja!)
‘Thanks’ (Ahsante) Miranda akatuma ujumbe huo akitabasamu.
*** Saa mbili asubuhi kwa ofisi ya Kamanda wa polisi mkoa ..
“Umeambiwa uingie,” alisema mwanamke mmoja polisi aliyetoka ndani ya ofisi ya Kamanda. Mwanamke huyu alikuwa amevalia suti ya kike rangi ya kahawia na alikuwa anamwongelesha Jona.
Jona akamshukuru na kisha akanyanyuka kuzama ndani, akamkuta Kamanda akiwa anasoma gazeti lake kama ilivyo ada nyakati hizi za asubuhi. Akampa heshima yake na kuketi.
“Nimekuja mkuu.”
“Karibu,” akajibu Kamanda na kama vile hakuwa anajua kama kuna mtu hapo, akaendelea kusoma gazeti lake. Akamkalisha Jona kwa muda wa dakika sita kukiwa kimya.
“Aaannh!” Akafunga gazeti akizinduka. “Ndo umefika enh?” Akauliza kipuuzi. Jona hakusema jambo. Kamanda akatazama saa yake ya mkononi na kisha simu yake.
Alikuwa anamngoja Alphonce. Mpaka muda huo mwanaume huyo hakuwa ameripoti eneoni. Sasa atamruhusuje Jona akaendelee na kazi wakati mwanaume huyo wa kumfuatilia hajawasili?
“Em ngoja kidogo.”
Akanyanyua simu yake kupiga. Simu ikaita na kuita pasipo kupokelewa. Akasonya akitikisa kichwa.
_Ananijaribu huyu_ akasema kifuani mwake. Ina maana hakunielewa nilichomwambia? Sasa dharau inavuka mipaka.
Hakuwa na namna akamruhusu Jona aende zake akimuagiza amuitie afande Holombe mara moja pindi atakapotoka nje. Jona akatimiza agizo. Mwanaume mrefu mweusi akaingia ndani ya ofisi ya Kamanda na kusimama kwa ukakamavu.
Kamanda akamuagiza akamfuatilie Jona popote pale atakapokwenda. Jicho lake lisibanduke kumuacha abadani.
“Ukishindwa, usirudi hapa,” Kamanda akatoa kitisho. Holombe akaenda zake kutimiza agizo. Akatoka nje ya ofisi hiyo akiangaza kumtafuta Jona, mara akasikia kiganja begani kugeuka akakutana na mlengwa wake.
“Bila shaka unanitafuta mimi,” Jona akajinasibu. Holombe akatabasamu. Akajaribu kukanusha lakini uso wake ukimsaliti.
“Usijali, najua umepewa agizo na kamanda. Ila tu kiukweli, hutaweza kunifuatilia Holombe.”
“Umejuaje jina langu?”
“Nadhani ungejiuliza kwanza nimejuaje kama umetumwa unifuatilie … anyway, naitwa inspekta Jona. Nisingependa kukuchosha, tutakuwa pamoja, lakini itakapofikia mahali nitakuacha.”
“Lakini mkuu ka–” kabla Holombe hajamalizia, Jona alikuwa tayari yupo mbele hatua nne. Hakuongea tena. — Saa nne kasoro robo, Aga khan hospital…
“Karibu,” daktari alimwambia Jona huku akitazama tarakilishi yake. Jona pasipo kupoteza muda akamtaka ampashe maendeleo ya mgonjwa wake, Nade, na kama kuna uwezekano wa kuonana naye.
Hapa sasa daktari akamtazama Jona akiacha kila shughuli yake. Akamwambia Nade amefariki. Jona akashangazwa. Hakutegemea kabisa kupokea habari hizo kwani alimwona Nade akiwa tayari amesharudi kwenye hali yake.
Vipi sasa kufa huku ghafla?
Daktari asimpe Jona maelezo ya kutosha, akasisitizia tu amefariki na mwili wake umeshahifadhiwa mochwari.
“Inaonekana alikuwa ana internal damage iliyokawia kupona na hatimaye kuathiri organ zingine za mwili.” Daktari akapandisha mabega yake na kumalizia: “Kifo ni kwa kila mmoja.”
Jona akahisi kuna jambo halipo sawa hapa, na hakuwahi kuwa na shaka na akili yake pindi awazapo hivyo. Akamwagiza daktari aongozane naye kwenda kuutazama mwili wa Nade huko mochwari.
“Hapana. Nimeba –“
“Sasa hivi!” Jona akaamuru akimtazama daktari kwa macho ya simba. Daktari akahofu. Akanyanyuka na kutii amri, Jona akapata kukagua mwili wa Nade.
Punde akagundua jambo. “Ameuawa,” akasema kwa kujiamini. Alitomasa tomasa shingo ya marehemu Nade akagundua misuli yake ilikuwa imetapanywa, na koo lake lilikuwa lina ufa.
Akamtazama daktari na kumwambia:
“Ameuawa kwa Manual strangulation. Ulikuwa unajua hilo, sio?”
Manual strangulation ni nini? Tendo hili kwa jina lingine hujilikana kama throttling. Ni kitendo cha kuminya shingo ya mlengwa kwa presha kubwa mpaka kupelekea kupoteza fahamu ama kufa kabisa.
Daktari akashtuka kusikia habari hizo. Akabanwa na kigugumizi.
“Unataka kuniambia ulikuwa hulifahamu hili ama ulikuwa unanificha?” Jona akamuuliza. Hakuwa yule Jona umjuaye, alikuwa sasa anatisha. Endapo mtoto amgemtazama, basi angekunywa bilauri lote la uji kwa kauli moja.
“Nani kamuua?”
“Sijui nani kamuua!”
“Nani alikuwa wa mwisho kuingia ndani ya chumba chake?
Daktari akababaika. Jona akamlamba kofi moja zito. Daktari akapepesuka kama kapitiwa kimbunga.
“Alikuwa ni yule … alikuwa yule askari mwingine!” Daktari akaropoka akisugua shavu lake lililozabwa.
“Sasa naenda kukutia ndani kwa kushirikiana na muuaji!” Jona akafoka. Akamwamuru daktari aongoze mpaka chumba cha kusimamia CCTV kamera zilizopo hospitali. Walipofika huko Jona akataka kuchukua tape (tepu) inayomuonyesha Alphonce akitoka katika chumba cha Nade.
Ajabu tape hiyo haikuwapo. Wale wasimamizi wakamwambia Alphonce aliwapokonya. Akaishiwa nguvu. Akatoka hospitali na kwenda kantini akiwa ameketi na Holombe. Kwa muda akawa kimya. Hakuagiza hata chakula, isipokuwa Holombe pekee. Mara akachomoa simu yake mfukoni na kupiga, akaibinyia sikioni.
Alikuwa anampigia yule polisi aliyempatia kazi ya kumlinda Miranda. Punde polisi huyo akapokea na kumweleza Jona kuwa alipewa oda toka kwa mkubwa wake aache kazi hiyo mara moja na kureja kituoni. Ni kwa muda sasa hakuwapo hapo.
Na ni kweli, Jona akajilaumu kutotambua jambo hilo mapema. Ilikuwaje akapitiwa na uzembe kama huo.
“Ni nani huyo?” Akauliza.
“Inspekta Alphonce,” akajibiwa. Akakata simu na kuiweka mfukoni. Akaagiza maji makubwa akawa anakunywa akiwa anawazua.
Sasa ilikuwa wazi Alphonce alikuwa anajaribu kuficha jambo. Kumuua Nade na kung’ang’ania mafaili aliyoyapata kwa Eliakimu vilithibitisha hayo. Lakini vikathibitisha zaidi kuwa Alphonce hakuwa polisi safi. Kwa namna moja ama nyingine atakuwa anahusika na genge la Sheng, BC au pia wakina Nyokaa.
Kuna haja ya kumfikisha mbele ya dola? Akajiuliza. Akatafakari na kubaini hana haja hiyo. Moja, Alphonce alikuwa tayari ni nusu mfu. Atamwacha afe taratibu tu kuonja ladha ya madhalimu yote aliyoyafanya. Pili, inawezekana kabisa kufanya jambo hilo kukawa ni mbio za sakafuni. Alphonce alishasema hapo awali, anajua kulamba mkono wa wakubwa. Je watamwacha aangamie?
Haikuingia akilini mwa Jona.
Lakini vipi kama kibao kikaja kugeuzwa kwake? Napo akajiuliza. Ila hakuwa na hofu sana kwani alikuwa na ushahidi wa kumfanya awe salama.
Simu yake ilikuwa ina sauti za Alphonce alizozirekodi kipindi mwanaume huyo akiwa anaropoka. Kumbe alipokuwa ameweka mkono wake mfukoni alikuwa akifanya kazi hiyo.
Na kama haitoshi, alikuwa ana nyaraka za Eliakimu mkononi.
Akashusha pumzi ndefu. Mara ujumbe ukaingia simuni.
Akautazama, ulikuwa umetoka kwa Panky. Alikuwa anamhitaji afike kwa Marwa mara moja wapate kujadili kile walichokipata. Pasipo kupoteza muda akalipia maji yake na kisha kwenda zake.
“Samahani sitakuhitaji huku,” alimwambia Holombe aliyenyanyuka upesi aongozane naye. Holombe akaketi na kumtazama Jona akiyoyoma.
Ndani ya dakika kadhaa akawa amefika nyumbani kwa Marwa na kuwakuta vijana wake wakiwa wanamngoja mezani.
“Tumefanikiwa,” Marwa akamwambia akitabasamu. Jona naye akajikuta anatabasamu pia.
“Nini mmepata?” Akauliza.
“Kuna links mbili ambazo zinaenda kwa majina ya BIRD 002 na BIRD 003. Zimekuwa ni link ambazo zinatumiwa sana kuwasiliana na link ya SPACE BUTTON ambayo bila shaka itakuwa ndiyo BIRD 001. Kwahiyo tunaamini kabisa hizi links ni mojawapo ya wale ndege wa mawasiliano.”
Kwa Jona jambo hili likaleta mashiko. Na lilithibitishwa na majina ambayo links hizo zilipewa, BIRD yaani kumaanisha ndege. Na kwenye ile picha ni ndege ndiyo walitumika kama ishara.
“Kwahiyo mpaka sasa hizo links mbili kutimiza tano ndizo zimekuwa kitendawili. Hatujajua zipo wapi na zitakuwa zinafanya kazi gani,” Panky akaeleza.
“Hamna shida,” Jona akawatoa hofu. “Naamini kwenye hizi tulizonazo zinaweza kutusaidia kung’amua hizo zilizobaki.”
Marwa akamueleza wame ‘trace’ links hizo mbili na wamegundua mojawapo inapatikana Dodoma na nyingine ikiwa Nairobi, Kenya. Na zaidi ya hapo wamefanikiwa kupata jumbe kadhaa zilizokuwa zinatumwa toka upande mmoja kwenda mwingine.
Jona akavutiwa na habari hizo. Akawapongeza kwa kazi kubwa waliyofanya. Lakini kama haitoshi, Marwa akamwambia zaidi. Bado wanaweza kuzama kwenye links hizo hata sasa, na kudukua mawasiliano hayo kwa kutumia ‘unknown mode’.
Basi kwa haraka Jona akataka kushuhudia jambo hilo. Marwa akazama kwenye links hizo na kuanza kukagua taarifa wakianza na ile ya Dodoma. Huko wakakuta mambo makubwa yaliyowashangaza mno.
Kuna kambi ndogo ya Sheng ndani ya manispaa ya Dodoma. Na kambi hiyo kazi yake ni kupokea maagizo toka kambi kubwa iliyopo Dar es salaam, kuyatekeleza na pia kutuma taarifa kuja kambi kuu juu ya kinachoendelea bungeni.
Kambi hii ya Dodoma ilikuwa inafahamu kila kitu kinachojadiliwa na kitakachojadiliwa bungeni. Ilikuwa inajua maamuzi yote yanayoafikiwa huko na mipango yote ya serikali.
Lakini haswa katika namna zinavyowagusa Wachina. Haswa namna zinavyowaathiri wao katika nchi na ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati.
Kambi hiyo ilikuwa inahusika na mauaji ya wabunge na viongozi wote wa serikali waliokuwa kikwazo kwa matakwa ya Wachina kwa kutoa taarifa za viongozi hao kisha kikosi cha wauaji kinaagizwa toka kambi kubwa.
Kwa ufupi tu,
Sheng hakuwa tu genge hatari. La hasha! Alikuwa pia ni jasusi wa kiuchumi. Alikuwa ni mtu anayehakikisha maslahi na matakwa ya Wachina yanatimia!
Kwenye kila mkataba wanaopata Wachina aidha kwenye ukandarasi, ama shughuli yoyote ya kiuchumi nchini, Sheng alikuwa na kivuli ama mkono wake hapo. Kwa kifupi alikuwa anaisambaza dola ya kichina kusini mwa jangwa la Sahara, akianzia Afrika Mashariki na kati.
Na kwa kufanya hivyo, Sheng anakuwa chini ya serikali ya China. Analindwa na mkono wa serikali hiyo na kupewa nafasi maalum mbele ya macho yao. Anafadhiliwa kifedha, anasikilizwa na kupewa mazingatio ya juu.
Hakufanya haya kwa bahati mbaya ama kwa sababu za faida ya mbuzi, la hasha, bali kujenga ngome itakayomfanya kuwa salama kiuchumi yeye na koo yake.
Sasa akiingiza ama kutoa mizigo nchini China ama Tanzania, anapewa ‘badge’ ya serikali. Anatumia nafasi hiyo kunufaika kwa kupitishia magendo yake. Anatumia nafasi hiyo kujijenga na kuwa tajiri mkubwa mno. Kuifanya koo yake kuwa ‘dons’.
“Hii ishu ni kubwa,” akasema Jona. “Ni mtandao mpana mno ambao una nguvu, yatupasa kuwa waangalifu sana. Lakini kwa wakati huo tukipanga namna ya kuangusha mipango hii kama daudi alivyofanya kwa Goliath.”
“Tupo pamoja na wewe katika kila namna,” Marwa akamueleza na kumpa moyo.
“Knowledge is power,” (Ufahamu ni nguvu,) Jona akaongezea. “Hatuwezi kupigana na mtandao kama huu kwa ngumi. Lazima uwe na taarifa za kutosha kwanza. Ujue unapiga wapi na kwanini.
Sasa basi kutambua base hizi ya Dar, Dodoma na Nairobi, hakutoshi kabisa. Impact yake ni ndogo sana kwani kazi zake ni kusafirisha taarifa haswa haswa huku mtendaji mkuu akiwa kambi kuu ya Dar.
Tunahitaji kujua yale mawimbi matatu. Yale mafiga matatu ya ulinzi. Hayo tukikabiliana nayo na kuyamudu, Sheng atakuwa mdhaifu. Sasa tutafanya vile tunavyotaka.”
Lakini pia akatoa agizo la kuyatunza yale yote waliyoyapata kama ushahidi. Ni muhimu mno. Na hata pale watakapotaka kuyafunua mambo hayo hadharani basi watatuma hizo taarifa kwa vyombo husika kwa kutumia ‘anonymous profile’.
Isijulikane nani ametuma taarifa hizo, wala wapi zimetokea kwasababu kuu mbili. Mosi, kwa usalama wao wakiwa wanaendelea na kazi zao kama kawaida, na pili wapate fursa ya kutambua hatua zitakazochukuliwa juu ya taarifa zao, kama ni kitu kitakachopokelewa ama kufichwa kwanguvu.
***
Saa tano usiku, maeneo ya Msasani.
Sasha akatazama nyuma yake hatua kadhaa baada ya kuacha geti. Hakukuwa na mtu. Akatembea upesi kulifuata gari aina ya Nissan Murano nyeusi, akafungua mlango na kuzama ndani akiketi siti za mbele kabisa.
Mwanamke huyu alikuwa amevalia dira jekundu, kichwani nywele zikiwa timu.Ndani ya gari kulikuwa kuna wanaume wawili vijana wa Sheng: Nigaa na Mombo, Nigaa akiwa ameukamatia usukani na huku mwenziwe akiwa ameketi viti vya nyuma.
“Vipi umefanikiwa?” Nigaa akauliza.
“Bado naskilizia,” Sasha akajibu. “Ila uhakika upo lazima tu ntapata nafasi.”
Kukawa kimya.
“Nadhani unajua cha kufanya, Sasha. Na jambo hili liwe siri hata dada yako Sarah asilifahamu hata kidogo. Na ujue kabisa hakuna nafasi ya wewe kushindwa kwenye hili. Ukishindwa, utaenda kumsalimu Bite mapema sana,” Nigaa akaeleza. Kukawa kimya.
Hakukuwa na maelezo mengine, Sasha akashuka garini, gari likaondoka.
**** Mwanamke huyo akalitazama gari hilo likiishia alafu akarudi zake ndani na kujiweka kochini akiwaza kwa dakika kadhaa.
Alikuwa mtegoni haswa. Mtego wa kifo na uhai. Mtego unukao mauti. Mtego unaosaka pumzi yake kwa vumba.
Sasha masikini mimi … akajisemea mwenyewe kifuani. Alidhani kukimbilia mkoani kungenusuru roho yake dhidi ya mkono wa mauti uliommaliza Mudy kumbe alikuwa amekosea. Alikuwa tayari kwenye rada.
Pasipo kuelewa ni kwa namna gani ilitokea, aliwekwa kati na kupewa fursa ya kuchagua mambo mawili mikononi mwake. Mosi, abakiziwe uhai lakini kwa kuenenda namna watakavyo, au pili wammalize mara moja na kumtupia mtoni akawe chakula cha mamba.
Akajawa na hofu sana.
“Kwani mnataka nini kwangu?” Akauliza akitetemeka. Mbele yake walikuwa wamesimama wanaume wawili waliovalia suti nyeusi, tai nyekundu na vinyago vyeusi.
Wakamwambia wanafahamu kuwa dada yake Sara sasa anaishi na Kinoo chini ya paa moja. Hivyo basi hitaji lao ni moja tu, afanye afanyavyo, kwa juu ama chini, sukari au chumvi, aingie ndani ya genge la BC.
Huko watamuelekeza cha kufanya. Endapo akifanya inavyotakiwa kufanya basi atafaidika kwa kiasi kubwa, na akikaidi ama kuvujisha siri hiyo hatabaki salama.
Tangu siku hiyo akawa anapewa fedha ya kujikimu. Makazi ya kukaa na kila huduma aitakayo.
Lakini ni nini vitu hivi pale unapokosa amani ya moyo?
Sarah hakuwa anajua kama dada yake anaishi makazi haya mapya. Hakuwa anajua kama anaishi maisha mazuri anayoyatamani hata yeye. Muda wote huo alikuwa akidhani dadaye anateseka na kazi hana. Basi akazidi kumpatia presha Kinoo kukamilisha muamala wa Sasha.
Akiwa kifuani mwa Kinoo, Sarah alikuwa ananung’una kupitia puani akimbembeleza mbaba huyo kwa sauti tamu. Alikuwa anamchezea kidevu wakati Kinoo akipapasapapasa tumbo la mwananmke huyo lililokuwa limemhifadhi mtoto wake.
**
Majira ya asubuhi…
Kwa wale watu ambao wakiamka, hata kabla ya kuswaki na kunawa uso, kazi yao ya kwanza ni kuzama na kupekua mitandaoni, walikuwa wa kwanza kupata habari hii.
Ilikuwa imesambaa mitandaoni na kuzua gumzo kidogo miongoni mwa wachangiaji. Polisi akutwa akiwa hajielewi, amepooza viungo kwenye nyumba ya marehemu Eliakimu.
Picha zikamwonyesha Alphonce akiwa amelala chini sakafuni mdomo wazi jua kali likiwa linamchapa.
Taarifa hizo zikaeleza zaidi kuwa polisi huyo amepelekwa hospitali na uchunguzi zaidi unaendelea.
Nini kimemkumba polisi huyu ndani ya nyumba ya marehemu? Alikuwa akifanya nini hapo? Maswali hayo yakashika vinywa vya wanamitandao. Mmoja wao alikuwa Glady!
Alikuwa anatoa macho asiamini kama yule anayemwona pichani ni mtu anayemfahamu. Akajiuliza kila saa, si yule jamaa huyu? Akaendelea kukagua kwa kushuka chini na chini kwa kufyagia kioo chake cha simu kwa kidole chake gumba.
Alipotazama picha kadhaa akaamini kweli ndiye anayemuwaza huyu. Alikuwa kweli ni yule mwanaume. Basi akajikuta anatabasamu.
Hakuishia hapo, akacheka kabisa.
“Amepata kiboko yake!” Akajisemea kifuani. Upesi akakumbuka simu ya mwanaume huyo, akaitazama na kuanza kuwaza yale yaliyomo ndani ya simu hiyo.
Kwahiyo ndiyo hatopata tena ile pesa? Akawaza.
Hapana. Akakataa. Sasa ndiyo itakuwa rahisi kwake kuipata, akawaza. Ndio! Akakubali na nafsi yake.
Kama Alphonce amepooza basi hataweza kumfanya jambo. Hataweza kumdhuru. Akatabasamu. Na hivyo basi atahakikisha anapata mawasiliano na mwanaume huyo kisha amweleze ana siri yake mkononi, amfanyie muamala wa pesa. Tena si kidogo, muamala mzito. Muamala wa kutikisa akaunti.
Na hivi jambo la mwanaume huyo lilikuwa limeshashika moto mitandaoni. Lilikuwa maarufu na lililosomba hisia za watu wengi. Basi palikuwa na ‘ka-mtaji’.
Glady aliendelea kuwaza na kichwa chake kibovu.
Ama kweli, kufa kuna kufaana ndaniye. ** Muhimbili hospital, Dar es salaam.
“Mnaweza mkanipatia faragha kidogo?” Alisema Kamanda kwa sauti ya chini. Punde daktari na nesi wakawapisha ndani ya chumba.
Alphonce alikuwa amelala juu ya kitanda akitazama dari. Alikuwa amefunikwa na shuka jeupe lenye chapa ya MSD.
“Vipi, nini kimetokea Alphonce?” Kamanda akauliza. “Usiniaminishe eti umedondoka tu na kuwa hivyo kama ulivyowaambia hao wengine. Najua kuna kitu. Nani amekufanya hivi?”
Kamanda akaketi kitandani akimtazama Alphonce kwa kustaajabishwa na maswali hayo.
Alphonce akasafisha kwanza koo lake. Akawa kimya kidogo akipangilia cha kunena. Akamtazama Kamanda kwa macho yake mekundu alafu kwa ufupi akamjibu:
“Ni Jona.”
Kamanda akatoa macho.
“Kwanini akakufanya hivi?” Akauliza. Alphonce asitake kuweka mambo bayana, akadanganya kuwa Jona aligundua kwamba anamfuatilia, hivyo akamshambulia vibaya mno.
Kamanda akashangazwa na maelezo hayo. Kwanini Jona afanye hivyo? Akamuuliza alimkuta Jona akifanya nini ndani ya nyumba ya Eliakimu?
“Alikuwa anafanya search,” Alphonce akamjibu. “Nilimkuta akiwa amebebelea vitu kadhaa mkononi mwake na nilipomtaka anionyeshe hakuwa radhi kabisa. Akanikemea kwanini namfuatilia. Ghafla akanishambulia kabla sijajipanga, nikajikuta chini sijiwezi.”
Kamanda akaguna. Habari hii ilimpa tahamaki. Aliunganisha doti siku ile walipoenda nyumbani kwa Eliakimu na kukuta ushahidi wa Jona kuwapo hapo mapema kabla ya kifo cha mheshimiwa.
Baadae wakaambiwa Jona alienda kutupwa kufuatia kupigwa risasi na Eliakimu. Hapa Kamanda akakubaliana na nafsi yake kwamba Jona ana la kuficha kwenye hili. Ni wazi alikuwa na mahusiano na Eliakimu.
“Kamanda, Jona si wa kumpa nafasi tena. Ni wa kumalizwa haraka iwezekanavyo. La sivyo atatupa shida kwani ameshafahamu yote tuliyomtendea,” Alphonce akaongezea.
“Amefahamuje hayo?” Kamanda akashtuka kuuliza.
“Sijajua ameyafahamuje. Ila anafahamu kwani ameniambia mwenyewe kwa kinywa chake.”
Kamanda akahisi tumbo linakoroga. Amani ikampotea. Akasimama na kushika kiuno chake akizunguka ndani ya chumba.
Akapiga kiganja chake kwa ngumi zisizo na idadi. Pasipo kuaga, akatoka ndani ya chumba alicholazwa Alphonce.
Kichwa chake kilikuwa kimeelemewa mawazo. Na hasira kwa pamoja. Akaenda ofisini kwake na kujilaza kwenye kiti chake. Akaendelea kuwaza akizunguka na kiti kila upande.
Mwishowe akaamua kumpigia simu Jona na kumtaka aje ofisini kwake mara moja. Jona akapokea wito. Akamwahidi ndani ya muda mfupi atakuwa hapo.
Kamanda akatoa bunduki yake kwenye droo na kuikoki, kwa lolote litakalotokea, kisha akairudisha na kuliacha droo wazi iwe rahisi kuifikia silaha hiyo punde atakapoihitaji.
Akangoja kidogo kabla ya Jona kufika ofisini akiwa amevalia tisheti nyeupe plain na suruali ya kadeti rangi nyeusi. Mgongoni alikuwa amevalia begi. Wakasilimiana, Kamanda akaenda kwenye lengo la wito wake pasipo kupoteza muda. Akamsomea Jona mashtaka ya kumtendea ndivyo sivyo Alphonce akiwa kazini kutimiza maagizo yake.
Kinyume na Alphonce alivyotaka, Kamanda akampatia Jona nafasi ya kujieleza. Na wakati huo Kamanda akiwa anajaribu kwa kiasi kikubwa kutunza mihemko yake asimwonyeshe Jona.
Na kwa wakati huo huo mkono wake ukiwa karibu drooni kwa lolote litakalotokea.
“Mkuu, sikumshambulia Alphonce kwasababu ya kumzuia kutimiza majukumu yake bali yeye kutimiza yaliyo yangu.”
“Yapi hayo?” Kamanda akamkatisha. “Hujui ile kesi ipo mikononi mwa Faridi?”
“Nafahamu. Si kwamba nimeamua kuibeba kesi hiyo, la hasha. Nafanya haya Faridi akiwa ana ufahamu na kinachoendelea. Nafanya haya kwakuwa nilihusishwa kwenye jaribio la mauaji na marehemu Eliakimu. Sidhani kama ni vibaya kufuatilia sababu iliyomfanya mheshimiwa akajaribu kuniua. Haswa baada ya kutimiza kazi yake aliyonipatia kwa uweledi mkubwa,” Jona akajieleza.
“Kazi gani hiyo? Na ulikuwa mna mahusiano gani na Mheshimiwa?” Kamanda akauliza.
“Hapo nyuma Eliakimu alikuwa akintafuta nimsaidie baadhi ya kazi zake akiamini historia yangu ya kazi na utendaji wangu. Ikumbukwe sikuwa jeshini kwa muda huo. Na malengo yake ya kuntafuta hayakuwa mengine bali mawili akiahidi kunilipa pesa nzuri. Moja, kumtafuta mkewe, nikalifanikisha. Na pili, kumtafuta mfanyakazi wake aliyetekwa, nalo nikalifanikisha.
Lakini nikiwa nafanya kazi hizi, nikagundua Eliakimu hakuwa mtu safi. Alikuwa anajihusisha na biashara kadhaa za magendo zilizopelekea mkewe na hata mfanyakazi wake kutekwa.
Nikiwa nataka kufahamu hayo, siku nampeleka mfanyakazi wake kwake ajabu barabarani nikashambuliwa kwa risasi na vijana kadhaa waliokuwa ndani ya prado nyeusi. Tukafanikiwa kutoka hai isipokuwa dereva.
Nilipowasili kwa Eliakimu nikahitaji kusikia maelezo yake juu ya shutuma zangu. Lakini sikupata maelezo hayo, badala yake akanipiga risasi na kwenda kunitupa porini pamoja na maiti ya dereva yule aliyefia njiani,” Jona akaweka kituo kisha akaendelea:
“Na hilo ndiyo likawa sumbuko langu tangu hapo. Kwanini Eliakimu aliniua ilhali nilitenda kazi zake? Nini anaficha?
Ni kheri nikasikia mfanyakazi wake, aitwaye Nade, alinusurika kifo katika jaribio la kuuawa yeye na bosi wake, Eliakimu, ambayo najua wazi wahusika watakuwa ni wale waliomteka mfanyakazi huyo. Nikaona ni busara kwenda kumtembelea kwani atanipatia majibu ya maswali yangu…”
Baada ya hapo Jona akamweleza Kamanda namna gani Alphonce alivyohusika kwenye mauaji ya mfanyakazi huyo na hata baadae kutaka kumpokonya nyaraka alizozipata kwenye nyumba ya Eliakimu. Alipofikia hapo Jona akatoa nyaraka hizo begini na kuziweka mezani. Alafu akaendelea na maongezi yake huku Kamanda akiwa anapitiapitia nyaraka hizo kwa macho ya wepesi apate kuzimaliza amsikilize Jona vema.
“Sikukubali kumpatia nyaraka hizo kwani sikuona kama ni sahihi. Nilitaka kumkabidhi Faridi anayehusika na kesi hii lakini hakuwa radhi, sikufahamu kwanini lakini baadae nikaja kugundua kumbe naye alikuwa anahusika na madili batili pamoja na bwana Eliakimu na zile zilikuwa ni juhudi za kuhakikisha jambo hilo linabaki kuwa siri.
Kipindi anataka kunipokonya nyaraka hizo, akawa anasema maneno haya,”
Jona akacheza sauti ya Alphonce aliyoirekodi. Kamanda akiwa ametoa macho akaskiza sauti hiyo huku moyo wake ukimdunda mithili ya trekta linalopambana na ardhi ngumu ya shamba.
Mpaka sauti hiyo inakoma, hakusikia kuhusishwa kwake moja kwa moja. Akashusha pumzi ndefu na akajawa na hasira sana juu ya Alphonce. Hakutegemea kama mwanaume huyo angeenda kuropoka upuuzi wa namna hiyo kwa Jona.
Akatikisa kichwa kwa masikitiko akilaza mgongo wake kitini. Akatazama feni, pangaboi, likizunguka akichambua nini cha kufanya kwa dakika kadhaa. Akaona mwanya wa kumwangushia msala huu bwana Alphonce wakati yeye akijinadi kuwa safi.
Na kwakuwa hakuhusika na bwana Eliakimu kwa namna yoyote ile, hili halikuwa gumu kwake kulitenda.
“Alphonce! Alphonce!” Kamanda akabamiza ngumi nzito mezani. “Sikutarajia kama ungekuwa na wivu wa kijinga kiasi hiki!”
Akaendelea kumshtumu Alphonce hewani akimlaani kwanini wivu wake wa kipuuzi unamuingiza kwenye mauaji yake aliyoyatenda kwa mkono wake mwenyewe.
Akakana kabisa kuhusika na mauaji ya familia ya Jona akisema yeye si ‘mkuu’ huyo anayetamkwa sautini. Hiyo ilikuwa ni janja tu ya Alphonce kujisafisha na kutakatisha matendo yake ya kidhalimu.
Mwishowe,
“Nakuomba haya mambo ya Alphonce yaishie hapa Jona, niachie mimi nitamshughulikia huyo fisadi wa maadili! … unaweza kwenda.”
Jona akaenda zake akimwacha Kamanda kichwa kinamuuma kwa mawazo.
Alichambua kila alilolisikia na kuambiwa. Kwa akili yake akaona Alphonce sasa ni tishio kwake kuliko Jona. Mwanaume huyo si tu kwamba atafanya ijulikane alitia mkono kwenye mauaji ya familia ya Jona, ambacho ni uhalisia, bali atamfanya aonekane alikuwa anashirikiana naye kwenye biashara zake za kidhalimu azifanyazo kwa kofia ya polisi.
Kitu ambacho si uhalisia!
Kwa kujilinganisha na Alphonce akajiona yeye ni mtu safi. Na kuwa safi zaidi alitakiwa kufanya namna.
Ipi hiyo?
Akaweka simu sikioni na kuongea maneno machache.
“Kericho, fika ofisini kwangu mara moja.”
Ndani ya dakika chache akaja hapo mwanaume mrefu mzito maji ya kunde ndani ya kaunda suti.
**
Saa moja asubuhi …
“Ameshaondoka,” mke wa Boka aliongea na simu. Haikupita hata lisaa kamili tangu mumewe amuage kwenda kazini. Mama huyu alikuwa ameketi sebuleni akiwa amevalia khanga kifuani.
“Ndio ebu njoo shoga angu maana hapa sielewi kitu yani! … yani nahisi kuchanganyikiwa … njoo bana … kwani hajatoka? … mida gani? … basi nakuja mimi … sawa nikukute hapo ndani ya robo saa.”
Akaacha simu yake na kwenda kujiandaa. Hakupata hata kifungua kinywa. Ndani ya muda mfupi, akawa ameshavalia batiki lake lililomkaa vema. Akajipaki kwenye gari na kuanza safari.
*** Saa nne asubuhi …
“Samahani, Mheshimiwa,” sauti ya kike ilimfanya Boka abandue macho yake kwenye karatasi kadhaa alizokuwa anazipitia. Alikuwa ni sekretari wake, bi Salma, mwanamke mnene aliyevalia shati jeupe, sketi ndefu nyeusi na hijabu ya pinki.
“Kuna barua yako hapa.”
“Toka wapi?”
“TFF.”
“Ooh niwekee hapo,” akaonyeshea mezani kwa kichwa kisha akaendelea na kazi yake. Bila shaka alikuwa ametingwa. Hii ilikuwa ni miongoni mwa siku zake alizo bize.
Alilenga kufanya kazi pasipo kupumzika mpaka majira ya chakula cha mchana amalizie kila kiporo mezani. Lakini hakufanikiwa kwenye hilo. Kwani muda si mrefu akapata taarifa mkewe amefariki kwenye ajali mbaya ya gari iliyotokea maeneo ya Makumbusho.
Akachanganyikiwa!
Akafanya kwenda hospitali alipoambiwa mkewe amekimbiziwa, huko kweli akathibitisha mwanamke huyo amefariki. Mwili wake uliokuwa umeharibika vibaya ulikuwa umeshalazwa mochwari.
Lakini asiamini, akaenda mpaka kuutazama mwili huo mochwari, labda unaweza ukawa si wa mkewe, wameufananisha! Huenda akawa ni mtu mwingine aliyetumia gari la mkewe. Ndio. Inawezekana. Ama kuna mtu aliyeliiba hilo gari na kukimbia nalo, hatimaye akapata ajali!
Alitengeneza kila picha kichwani akijaribu kumnusuru mkewe. Aligeuza kila taarifa aliyoambiwa ili tu amuokoe mkewe kifikra lakini haikubadilisha ukweli. Alikuwa ndiye yeye. Hakuweza kurudisha mikono ya muda nyuma.
Mwili uliokuwa umelala kwenye jokofu za mochwari haukuwa wa mwingine isipokuwa wa mwanamke aliyemzalia watoto.
Haukuwa unatamanika hata kidogo. Paji la uso lilikuwa limechanika. Amevunjikavunjika. Boka akashindwa kujizuia kutoa machozi.
“Alikuwa na mwenzake ndani ya gari. Yeye amenusurika kifo, lakini yu hoi hajiwezi. Taarifa alizozitoa kabla hajaenda kupoteza fahamu ni kwamba walikuwa wanafuatiliwa kwa muda mrefu kabla ajali hiyo haijatokea.
Kwahiyo kwa namna moja ama nyingine hii haikuwa ajali bali tukio lililopangwa,” alisema polisi aliyepewa jukumu la upelelezi, kwa jina inspekta Geof.
“Sasa kama ni hivyo, mnangoja nini kumtia nguvuni huyo mshenzi?!” Boka akafoka kwa hasira. “Au sio kazi yenu hiyo?”
Inspekta akamsihi apunguze jazba, mambo hayapelekwi mrama kiasi hiko. Tukio ni kubwa na linahitaji utulivu mkubwa kumbaini mhusika, la sivyo wataishia kuwabambikia watu kesi.
Lakini akamuahidi kwa dhati jambo hilo halitachukua muda kukaa bayana. Amuamini. Akaendaze.
Akamuacha Boka hospitalini akiwa ameshikilia kichwa kwa mawazo. Ni nani amuue mkewe? Kwasababu gani haswa? Alijiumiza zaidi na hayo maswali asiyokuwa na majibu. Akaishia kuvuja machozi, zaidi akapandwa na hasira maradufu.
**
Kwenye vioo vya simu … whatsapp App.
‘Umehakikisha amekufa?’
Typing…
‘Ndio, nimefika hospitali kama mwandishi wa habari. Yupo mochwari.’
Typing…
‘Na mazingira ya ajali?’
Typing…
‘Hamna mtu anaweza jua. Nimefanya kiustadi.’ Typing…
‘Nimepata taarifa hakuwa mwenyewe ndani ya gari’
‘Ndio alikuwa na mwanamke mwingine yeye hajafa yupo ICU’
Typing … ikaacha … typing tena …
‘Una uhakika huyo mwanamke uliyemwacha hai hakukuona?’
‘Tukio lilitokea kwa kasi sana hakuniona’
Typing …
‘Kama huna uhakika ni kheri ukammaliza. Hatuna muda wa kusumbuana na polisi’
Typing …
‘Nakuhakikishia hakuna haja hiyo’
‘Ok. Stay low. Njoo tuonane.’
Tap … Offline …
Moja wa mtu huyu anayechat alikuwa ndani ya basi la mwendokasi. Akazamisha simu mfukoni. Alikuwa amevalia suruali ya kitambaa rangi ya kijivu na viatu vyeusi ving’aavyo.
**
Muhimbili hospital, Dar.
Mlango ulifunguliwa taratibu akaingia mwanaume ndani ya shati jeupe na suruali nyeusi. Akamtazama Alphonce kitandani, akamwona akiwa amelala.
Huu haukuwa muda wa kutazama wagonjwa. Hakuwa amepewa ruhusa wala kuonana na mtu yeyote yule kabla hajaingia humu ndani.
Alikuwa ni Kericho. Mwanaume mzito mwenye rangi maji ya kunde. Macho yake yalikagua chumba upesi kisha akamsogelea Alphonce na kumbana pumzi kwa mikono yake mipana iliyoshamiri mishipa ya damu.
Alphonce aliyepooza angefanya nini kuukomboa uhai wake? Kericho akatekeleza zoezi lake kwa wepesi sana. Alimuacha Alphonce baada ya kusikia mlio wa kuashiria mapigo ya moyo yamekata.
Hakutoka hata jasho. Alphonce akawa amekufa.
Akatoka ndani ya chumba hicho upesi. Kama alivyoingia, hakuna aliyemuona. Akayeya zake.
“Nilikwambia,” sauti ikamjibu toka simuni. “Haya leta nilione.”
Kericho akakata simu akiiweka Muhimbili mgongoni mwake. Akajipakia kwenye taksi na moja kwa moja akaelekea Mbweni. Akashukia barabarani na kumkabidhi dereva pesa yake alafu akatembea kwa mwendo wa dakika sita kabla hajazama ndani ya nyumba fulani kubwa ambayo bado haikuwa imemaliziwa kupauliwa.
Humo akakutana na Kamanda akiwa amevalia sare ya traksuti nyeusi.
“Umehakikisha kila kitu kipo sawa?”
“Kila kitu kipo kwa mstari,” akasema Kericho akitabasamu. Kamanda naye akatabasamu kujibu.
“Safi sana. Nilikuamini ndo’ mana nikakupatia hiyo kazi.”
Lakini ikatokea upesi sana, Kericho akaona chepeo na jembe kwa umbali wa hatua kadhaa nyuma ya Kamanda. Kabla hajauliza, akajikuta amedidimiziwa kisu tumboni mara tatu!
Chop! Chop! Chop! Akadondoka chini akimimina damu lukuki.
“Hakuna siri ya watu wawili Kericho,” Kamanda akasema akimtazama Kericho akijifia.
Kericho akamnyooshea kidole Kamanda mkono wake mmoja ukiwa tumboni umemezwa na damu. Macho yake yalikuwa mekundu. Akatamani kusema jambo lakini hakuweza. Akamtazama Kamanda mpaka roho yake inaacha mwili.
“Kwaheri afande,” Kamanda akamfunika macho kisha akachimba shimo na kuufukia mwili wa Kericho humo.
Akakung’utia jasho pembeni alafu akaendea gari lake na kujipakia, akayeya.
Njiani …
“Ndio, mheshimiwa,” akasema akibinyia simu sikioni kwa mkono wake wa kushoto wakati wa kuume ukishikilia usukani.
“Ndio, nimesikia mheshimiwa pole sana kwakweli … yah! Ndo nipo njiani nakuja … usijali, nitakuwa hapo muda si mrefu.”
Akakata simu.
Nusu saa baadae akawa ameshafika hospitali, yu ndani ya sare, anateta na Boka juu ya ajali ya mkewe. Akampatia Boka pole za kutosha baada ya kumpa kumbatio na mkono wa kheri.
“Nakuhakikishia, mheshimiwa, lazima atakamatwa!” Kamanda akasema kwa sura ya msisitizo. “Atatafutwa kokote alipo. In fact, nina wapelelezi wazuri sana hawataniangusha.”
Boka akashukuru.
“Lakini nashangazwa sana, bora ingekuwa mimi ningesema nina maadui wa kisiasa. Lakini kwa mke wangu, mke wangu, ana makosa gani?” Boka akateta kwa uchungu.
“Huwezi jua, Mheshimiwa. Hata hao maadui wako wewe wanaweza wakatumia njia hiyo,” Kamanda akamueleza kisha akamuuliza: “kuna yeyote unayemshuku kwenye hili?”
Boka akafikiria kidogo. Akabinua mdomo wake akitikisa kichwa.
“Sidhani.” Akafikiri tena. “Sidhani kwakweli.”
“Tuliza kichwa,” Kamanda akamsihi. “Najua kwa sasa unafikiri mengi lakini baadae utatengemaa kimawazo. Nijulishe.”
“Sawa, nitakubarisha. Ahsante.”
Wakaachana. Baadae kwenye vyombo vya habari majira ya usiku, Kamanda akanguruma akiongelea kifo cha mke wake Boka na inspekta Alphonce.
Kwa upande wa mke wa Boka akasema uchunguzi unaendelea huku akisisitiza watu waache kusambaza maneno yasiyothibitishwa huko mitandaoni, waache polisi wafanye kazi yao. Kwa upande wa Alphonce akasema mwanaume huyo amefariki kwasababu za kiafya.
“Shit!” Jona akalaani. Alikuwa anatazama taarifa ya habari akimwangalia mkuu wake wa kazi. Yeye pekee ndo alikuwa anajua mwanaume huyo anaongopa juu ya Alphonce.
Punde simu yake ikaita. Alikuwa ni Kamanda. Akajiuliza anataka nini? Alipopokea Kamanda akamuuliza kama amesikia ya Boka.
“Ndiyo nimetoka kuona kwenye habari,” Jona akajibu.
“Ok,” Kamanda akaitikia. “Sasa hiyo kazi nimekupatia uifanye. Nataka huyo muuaji apatikane. Sawa?”
Kimya.
“Sawa?”
“Sawa, mkuu!”
** “Utaonana na Inspekta Geof, atakupatia alipofikia.”
Baada ya hapo Kamanda akampatia Jona namna ya kumpata Inspekta Geof, alafu akakata simu.
Jona akaweka simu yake kando na kuanza kuitafakari simu hiyo ya Kamanda. Akatafakari na kazi aliyopewa. Hakuwa na kitu kichwani na hakuwahi kujisumbua na Boka.
Ndio alikuwa anajua mwanaume huyo ni waziri ila hakuwahi kumfuatilia wala kuwa shabiki wake. Kwanini mkewe auliwe? Akabinua mdomo.
“Huwezi jua ya wanasiasa!” Akajipa pumziko kwa kauli hiyo kisha akapuuzia. Lakini hakudumu muda mrefu, akili yake ikamrudisha tena kwenye hilo tukio.
Vipi kama haya yakawa ni mwendelezo wa mauaji ya watu mashuhuri na maarufu kama ilivyokuwa hapo nyuma? Akawaza.
Inawezekana Boka akawa ameingia kwenye Anga lile la Washenzi? Alifikiri sana lakini akajitahidi tena kupuuzia apumzishe kichwa.
Aliamini atakapokutana na Geof atajua wapi pa kuanza kutia mguu wake. Akanyanyuka na kujipatia chakula akishushia na juisi ya embe.
Kabla hajalala akaamua kushika kitabu kikubwa cha riwaya apate kupitia kurasa kadhaa kuhadaa kichwa alale. Alikuwa anasoma riwaya iitwayo THE BIG SLEEP cha mnamo mwaka 1939 kilichoandikwa na mwandishi nguli Raymond Chandler.
Riwaya hii ilikuwa ni ya mambo ya kijasusi. Ndivyo ambavyo Jona anapenda kuvipitia pale apatapo muda. Vitabu vya kufikirisha akili. Vitabu vya kuchemsha ubongo na kupanua mawazo.
Mbali na hiki cha Raymond Chandler, pia kwenye maktaba yake kulikuwa na vitabu vingine maarufu vya kijasusi vilivyoandikwa kwa mkono mtamu na akili zilizopevuka.
Kuvianisha kadhaa vilikuwa kama: THE HOUND OF THE BASKERVILLES cha mwaka 1902 kikiandikwa na Arthur C Doyle, THE MOONSTONE cha mwaka 1868 kikiandikwa na Wilkie Collins na cha bwana Dashiel Hammett kiitwacho THE MALTESE FALCON cha mwaka 1930.
Ingawa vitabu hivi vilikuwa vya kale, ila vilikuwa na thamani ya kusomwa tena na tena. Haswa kwa watu wa kariba ya Jona, wapendao kudadisi, kufuatilia na kupembua.
Kweli, baada ya muda wa dakika kadhaa Jona akiwa amesogeza karatasi kama kumi hivi, akaanza kusinzia. Mwishowe akalala kabisa.
Leo akawa anauendea usiku pasipo kutumia kilevi. Akalala kwa muda wa nusu saa tu, kabla hajakurupushwa na simu. Akalalama sana.
Alikuwa ameshapotelea usingizini. Alikuwa anafahamu ni namna gani atahangaika kupata nafasi hiyo tena. Na kwa mawazo yake yote alijua Kamanda ndiye aliyemtafuta.
Akasonya akiivuta simu na kuitazama. Alikuwa ni Marwa! Akawaza anataka nini muda huo? Akapokea simu.
“Yes,Marwa … niko poa, wewe? … yah nlikuwa nshalala … bila samahani … sasa hivi? …” Jona akatazama saa kwenye simu, ilikuwa saa tatu usiku na dakika kichele, akairudishia simu sikioni. “Ok, basi nakuja.”
Punde akanyanyuka na kuvaa, akaenda zake.
Akiwa njiani kwenda huko, sie twende huku …
“Kwahiyo umeamuaje sasa?” Aliuliza shoga yake Glady akimtazama mwenzake kwa macho ya mtindio wa urembo. Mwanamke huyu hakuwa mwingine bali yule aliyebananishwa siku ile na Alphonce ndani ya gari, akajichafua na mkojo.
Alikuwa amevalia tight nyekundu na blauzi nyeusi isiyo na mikono. Kandokando yake bibie Glady alikuwa bado amevalia taulo anajikwatua kabla ya kwenda kazini.
“Sasa shoga yangu, niamue nini sasa hapo unadhani?” Akauliza Glady akipaka wanja. “Mtu mwenyewe ndo ashakufa hivyo. Sasa mimi si kaniachia mzigo tu hapa!”
Kukawa kimya kidogo. Glady akauvunja:
“Yani mimi hapa ndipo ninapokereka na maisha. Unajikinga na UKIMWI eeeeenh miaka nenda rudi kutumia marambo alafu unakuja kuuawa au kufa ka siku ka moja tu!”
Akasonya.
“Ila mwanamke wewe una bahati sana!” Shoga akamwambia. “Yule jamaa kama asingekufa alikuwa anakuua wewe nakwambia!”
“Aanzie wapi?” Glady akajivuna akipakaa rangi ya mdomo. “Kama alishindwa nilivyokuwa naye chumbani angeniwezea wapi?”
“Haya, bana! Mie sina neno. Niuzie basi hii simu,” Shoga akapendekeza akiitazama simu ya marehemu Alphonce.
“Ishia hapo hapo!” Glady akamkemea. “Huoni choo ukapita?”
“Sasa shosti ya nini na mtu mwenyewe keshajiendea kwa mola wake? We sema hapa nikupatie laki moja unipe!”
“Fala kweli wewe. Laki moja unampa nani labda? Umeona simu ya laki moja hiyo?” Akamtazama Shoga yake. “Eti?”
“Unataka shingapi sasa?”
“Sitaki chochote we bwana we!” Akasema Glady akimalizia kujipara. Akajipulizia marashi na kujiveka nguo, gauni jeusi la lawama mtaani.
Akaketi kitandani.
“Hiyo simu itanipa pesa zaidi ya hiyo, tena mara kumi yake!”
“Wapi sasa?”
“Tatizo wewe akili yako tope. Nishapata wazo hapa mwenzako. Wazo la kupiga pesa ya maana niache kuuza uchi.”
“Wewe hata upate milioni utauza tu. Iko damuni!”
“Ebu skiza nyoko wewe n’kupe mawazo ya maana, acha kuongea mashudu. Hizo picha zilizokuwepo humo ni pesa. Cha kufanya tunawatafuta wanaohusika na picha hizo tunawaambia watoe pesa tukae na siri, la sivyo mambo kweupee mitandaoni.”
“Mh! Wakikataa?”
“Unaona sasa? Tatizo lako wewe unadhani kila mtu ananuka shida kama wewe. Watu wana pesa zao bwana. Unadhan mke wa mbunge, au mke wa waziri atakubali picha zake za uchi zisambazwe?”
Shoga kimya.
“Ohoo!” Glady akasimama. “Ngoja nkuonyeshe nitakavyotajirika mbele ya macho yako.”
Akavaa viatu akamtaka mwenzake anyanyuke waende.
**
Baada tu ya kuketi, Marwa akamwambia usiku huo umekuwa wa kipekee kwani kuna mambo kadhaa muhimu amepata kuyadukua toka kwenye zile links, akaona si mbaya akamshirikisha kwenye taarifa.
Jona akakaa tenge apate kusikia. Marwa akiwa amemsogezea tarakilishi yake, akamwonyesha Jona jumbe kadhaa toka katika hizi pande. Hazikuwa na maana sana, ila moja.
Jona akatabasamu. Ujumbe huu ulikuwa umeanishwa kama ifuatavyo:
*From : Second Wave, Nairobi.*
*To: First Wave, Dar.*
*Content: Help for an ambush for killing and framing*
*Place: Karen and Langata.*
*Aim: Kamau Githeri and Wachuku Otieno.*
*Time: immediately!*
Ujumbe huo ukawapa mawili, mosi wakatambua ‘nguvu moja ya bahari’ ipo Dar na ya pili ipo Nairobi. Hii kumaanisha huko kuna matawi ya ulinzi yanayolinda kisiwa. Je, ya tatu itakuwa Dodoma? Hawakuwa na uhakika bali makisio.
Lakini pili na zito zaidi ni mpango wa kuuawa kwa viongozi wa kiserikali wa huko Kenya, bwana Kamau na Wachuku. Na si kuwaua tu, bali kufanya pia ‘framing’.
Framing ni nini? Kwa kifupi ni zoezi la kutengeneza ushahidi wa uongo dhidi ya mtu asiye na makosa (an innocent person) ili aonekane mkosefu mbele ya watu ama mahakama, ama kote.
Njia hii imekuwa ikitumika sana ulimwenguni na kuwatia watu hatiani kwa makosa ambayo hawajatenda. Kwa ustadi jambo linatengenezwa na kuhusanishwa na fulani huku mtendaji akibaki salama.
Na mtendaji huyu hufanya hivi kwakuwa huyo aliyemfanyia jambo na huyo anayesingiziwa kitaalamu kuwa yeye ndiye ametenda hilo jambo wakiwa wote ni maadui zake.
“Sasa tunafanyaje?” Akauliza Marwa.
“Inabidi tutoe taarifa kwa vyombo vya usalama vya Kenya,” Jona akashauri.
“Kwa namna gani?” Marwa akauliza.
Hapo Jona akasita kidogo. Alifahamu jambo hilo litampatia shida kupata ‘access’. Akafikiria sana namna ya kufanya, lakini kila njia aliyoipata haikumridhisha kwa umakini wake.
Mwishowe Marwa akamuuliza kama viongozi hao wana nyadhifa ya ubunge pia?
“Ndio,” Jona akajibu. “Vipi kuna wazo umepata?”
“Haswa!” Marwa akamshauri waingie kwenye tovuti ya bunge la Kenya kisha kule wakapekue orodha ya wabunge na taarifa zao.
Jona akaafiki hilo wazo, wakazama mtandaoni na isipite muda wakawapata walengwa wao wanaowatafuta. Wakatazama ‘additional info’ wakapata akaunti ya barua pepe ya Kamau Githeri lakini kwa Wachuku Otieno wakaambulia patupu!
Marwa akamtoa hofu, akamwambia atatuma barua pepe hiyo kwa njia ya kirusi bandia. Kama kawaida itafika kwa mlengwa, na kama huko atakuwa ameweka anti-virus itakuwa bora zaidi kwani itapiga kelele kumshtua.
Hivyo akasoma kwa wakati! Na kwa wakati huo bado simu yake ikibakia salama.
Jona akapenda hilo wazo. Na kwa upande wa Wachuku Otieno?
“Acha tuwasiliane na karani wa bunge kwa hizi namba walizozianisha kwenye tovuti,” Marwa akapendekeza.
“Hapana,” Marwa akamjibu. Akamwambia wataweka ‘chip’ kwenye mashine yake alafu atafanya kautundu wapige kwa ‘private number’.
Wakafanya hivyo, ila hawakufanikiwa kumpata karani. Mwishowe wakaamua kutuma ujumbe wa kumtaarifu wakitumai atausoma kwasababu ya zile ‘missed calls’.
***
Walipomaliza kazi hiyo wakatulia sasa na kufanya mambo mengine. Marwa akampata kumkaribisha Jona vitafunwa vya kusogezea muda huku wakipiga soga za hapa na pale.
“Umeonana na Panky leo?” Jona akauliza.
“Kiasi chake,” Marwa akajibu akitafuna. “Ilikuwa ni asubuhi tukasalimiana na kuteta mambo kadhaa kabla hatujaachana.”
“Kuachanaje?” Jona akastaajabu. “Hamfanyi kazi sehemu moja?”
Marwa akameza kwanza kabla ya kutia neno.
“Asubuhi nilipoongea naye aliniambia wanataka kumbadilisha kitengo, wamtoe SPACE BUTTON.”
“Wampeleke wapi?” Jona akauliza.
Marwa akapandisha mabega. “Sijajua. Hatukuwa na muda wa kuongea naye sana kabla hatujaachana.”
Jona akawaza kidogo.
“Haiwezekani wakawa wametambua na kuyatilia shaka mahusiano yenu?”
“Sidhani!” Marwa akawahi kujibu. “Huwa ni taratibu yao kubadilisha watu vitengo kila baada ya muda fulani. Ila ni kwa mara chache sana hutokea kwa SPACE BUTTON.”
“Sasa mbona imetokea kwa Panky?”
Marwa akabinua mdomo. “Sijajua lakini nadhani ni kwasababu ya kifo cha mmoja wa wafanyakazi wa kitengo cha uhasibu kilichotokea hivi karibuni. Panky atakuwa amepelekwa huko kukaimu nafasi yake.”
“Kwanini Panky, si mwingine?” Jona akaendelea kuuliza maswali.
“Unanifanya nijihisi nipo kituoni,” Marwa akasema na kucheka. Jona naye akacheka.
“Anyways, kwa hisia zangu Panky atakuwa amehamishiwa huko kwasababu ya hali ya hewa. Ofisi ya huyo marehemu haikuwa na kiyoyozi kwasababu alikuwa na tatizo la asthma,” Marwa akadadavua.
“Kwani Panky ana asthma?”
Marwa akacheka.
“Hana, ila aliigiza anayo. Imemgharimu sasa.”
“Huyo marehemu ulijuaje ana asthma?”
“Ni mmojawapo wa wafanyakazi wa muda mrefu sana, actually nilimkuta akiwa hapo. Watu hawa wazamani wengi nawafahamu.”
Jona akaridhika na maelezo haya Marwa. Lakini akapata wazo hapa, kama kweli Panky atakuwa amehamishiwa kwenye hiyo ofisi aliyosema Marwa, hamna namna akapata kuwatambua wanaume watakaotumwa Nairobi kusaidia Second wave?
“Kivipi?” Marwa akamuuliza Jona baada ya mwanaume huyo kumshirikisha wazo hilo.
“Watu hao hawaweza wakatumwa pasipo kupewa fedha za usafiri, makazi na kujikimu. Pesa zinatoka wapi?”
Hii ilikuwa hatua tamu sana kwa Jona kuwang’amua baadhi ya wahusika wa ‘the first wave’ na kisha kuwashughulikia.
Wakafanya mpango wa kumtafuta Panky lakini simu ikaita pasipo mafanikio.
“Ana mke, anaweza akawa anahudumia nyumba,” Marwa akapendekeza wasitishe zoezi hilo. Jona akamsihi kesho asubuhi atakapokutana naye ahakikishe anamuuliza na kufanya namna.
Marwa akamtoa shaka Jona. Wakapumzika sasa Marwa akimsihi Jona alale nyumbani kwake kwani muda umeshaenda.
***
Saa nne asubuhi …
Gari Rav4 rangi ya damu ya mzee ilikuwa imepaki pembeni kidogo mwa njia itumiwayo na daladala kuingia ndani ya kituo cha daladala cha Makumbusho.
Ndani ya gari hiyo alikuwamo Inspketa Geof na Jona wakibadilishana ndimi. Geof alikuwa akimweleza Jona yale aliyoyapata toka kwenye ajali ya mke wa Boka, Jona naye akiuliza maswali kadhaa.
“Gari lilitokea kwa kasi huku stendi, Chaser nyeupe, ikikwepa daladala kwa pupa. Ilipofika hapo kwenye maungio ya barabara ya lami, ikasogea kidogo na kuibamiza gari ya marehemu kwa upande wa dereva! Kisha ikayoyoma,” Geof alielezea hayo akitumia mikono yake kuonyeshea uhalisa wa matukio na mahali yalipotukia.
Akamweleza pia Jona kuhusu shoga wa mke wa Boka aliyelazwa hospitali kisha akamkabidhi Jona faili lake.
“Mpaka hapo tutakuwa tumemalizana,” alihitimisha Geof.
Geof akamtimizia haja yake. Jona akashuka mbele ya nyumba ya Boka na kuzama ndani.
Kulikuwa kuna watu kadhaa. Turubai limefungwa likitoa kivuli kwa viti kadhaa vya plastiki vilivyozagaa.
Akafanya mpango wa Kuonana wa Boka. Haikupita muda mrefu akawa ameketi kando na mwanaume huyo. Akajitambulisha yeye ni nani, ametoka wapi na hapo anafanya nini.
Jona akajibu kwa tabasamu kisha akaanza kutekeleza kazi yake. Akamuuliza Boka maswali kadhaa, na kati ya hayo taarifa iliyokamata sikio lake ilikuwa ni hii.
“Siku hizi mbili au tatu za mwishoni, hakuwa sawa. Hakutaka kuongea na mimi na wala hakunieleza nini tatizo hata nilipojaribu kumuomba.”
Jona akahisi hapa patakuwa chemchem yake ya mfanikio.
“Haukuwa umemkwaza au kugombana kwasababu yoyote ile?”
“Hapana. Hatukuwa na ugomvi japo niliona amebadilika ghafla. Lakini sijui, labda nilikuwa nimemuuzi, ila hakunambia.”
Jona alipotoka hapo akazuru pia kazini kwa mwanamke huyo, huko akakutana na mkurugenzi msaidizi, bwana Liundi akiwa hae hae anataka kutoka aende msibani.
Akamwomba muda kidogo watete.
“Imekuwa ni ghafla mno, amefariki akiwa kwenye projekti kubwa ambayo ingejenga jina la Tanzania na hadhi yake kwa ujumla,” alielezea bwana Liundi.
Jona akataka kujua zaidi kuhusu projekti hiyo. Liundi akaeleza kinaga ubaga, akitoa mpaka na mpango kazi na hata hatua waliyokuwa wamefikia kwenye kusambaza vipodozi vyao vya kiasili nchini Kenya.
Wakiwa humo wanaelezeana, Jona akastaajabu kuona picha ya Miranda! Aliitazama picha hiyo kwa umakini kisha akauliza:
“Huyu ni nani?”
“Aaahm … alikuwa kama patna wa mama kwenye hii projekti.”
“Tangu lini alianza kufanya kazi na mama na unafahamu walijuanaje?”
Liundi akajibu swali la kwanza ila la pili akashindwa. Hakujua Miranda alikutana wapi na aliyekuwa bosi wake.
Sasa kichwani akawa anamuwaza Miranda tu. Imani yake yote ilimwangukia mwanamke huyo maana anamjua vema. Alijikuta anakubaliana na nafsi yake kabisa kuwa mwanamke huyo atakuwa mtuhumiwa wake wa kwanza!
Anahitaji kumtafuta haraka iwezekanavyo.
Akampigia simu, ikaita mara mbili kabla haijapokelewa.
“Unaongea na –“
“Jona!” Sauti ya Miranda ikamkatiza.
“Ndio, Jona hapa, nina shida na wewe haraka iwezekanavyo.”
“Nini shida Jona? Mbona upesi hivyo? Ni mambo ya ile picha?”
“Hapana! Ni kuhusu ajali ya mke wa mheshimiwa!”
“Ooh! My God. Jona, I didn’t do it. Honestly!” (Ooh! Mungu wangu. Jona, sijalifanya hilo. Ukweli kabisa!)
****
Jona akamtaka waonane kesho kwa ajili ya maongezi zaidi. Akakata simu na kuendelea kuwaza. Kuna yeyote zaidi Miranda?
Aliamini hata kama kuna yeyote zaidi ya Miranda basi njia ya kumpata mtu huyo ni kwa kupitia Miranda tu. Atampatia namna ya kupiga hatua hiyo.
Akatulia baada ya muda kidogo, akampigia simu Marwa. Simu ikaita pasipo matokeo. Akagundua Marwa atakuwa yupo kazini kwa muda huo, hivyo ni ngumu kupokea!
Akaachana naye avute subira mpaka majira ya mchana, aotee muda mwanaume huyo atakuwa akipata chakula cha mchana.
Muda ukasonga.
Kwenye majira ya mchana, saa saba na robo, Marwa akawa kantini akipata chakula. Alikuwa ameketi mwenyewe akijitenga kidogo na wenzake. Na kwakuwa Marwa hakuwa amezoeana na yeyote, basi hakuna aliyemuwazia.
Lakini mwanaume huyo alikuwa anamngoja Panky. Alitegemea atakuja kula na hivyo basi waketi pamoja kwa hapo pembeni.
Muda ukasonga kidogo mpaka majira ya saa saba na dakika ishirini na tano, Panky akaonekana akichukua chakula. Akatazama huku na kule pa kukaa, Marwa akanyoosha mkono amwone, Panky akaenda huko.
“Nilikuwa nakungoja muda wote huo.”
“Aanh! Kuna kazi kidogo nilikuwa nazimalizia. Yani huko waliponipeleka ni kama mwehu, kazi kazi kila saa simu tu!”
“Wamekupeleka wapi kwani?”
“Uhasibu na mawasiliano.”
Vile vile kama Marwa alivyokuwa anawaza. Ni ngumu sana kwa Sheng kuajiri mtu mpya kwani inakuwa ngumu sana kwa mtu huyo kujua na kuufuata utaratibu wa kazi chini yake hivyo hupendelea kutoa mtu huku na kumweka pale, kama haitaathiri.
“Ila huko hamna kiyoyozi,” Marwa akatania. Wakacheka. Wakawa kimya kidogo wakitafuna.
“Sasa kuna kazi ya kufanya,” Marwa akaingizia. Kabla hajaendelea simu ikaita, alikuwa ni Jona.
“Yah! Ndo nipo naye … poa, baadae.”
Akaweka simu mezani, na kumwambia Panky maagizo toka kwa Jona. Nini anatakiwa kufanya akirejea ofisini kwake.
“Hope tumeelewana!” Marwa akamalizia.
“Usijali, nitalifanyia kazi. Na nadhani hao watu watakuwa wameshaondoka. Taarifa zao zitakuwepo kule kimalipo. Nitatazama.”
Wakamalizia kula, wakarejea kazini. Panky akaanza kukagua nyaraka za risiti na taarifa kadhaa kwenye tarakilishi, pesa zilizotoka hivi karibuni.
Akanoti pembeni na kumtumia ujumbe Marwa kwa kuhofu baadae anaweza akakawia kutoka hivyo hatokutana naye. Alipotuma ujumbe huo, akaendelea na kazi yake kama kawaida.
Lakini baada ya muda kidogo, akaja kuitwa.
“Unahitajika ofisini kwa mkuu,” alisema mwanaume mmoja akisimama mbele ya Panky.
“Mimi?”
Japo hakujua anaitiwa nini, moyo wake ukaanza kumtwanga. Alipaliwa na hofu. Kuitwa na mkuu halikuwa jambo dogo hata kidogo.
“Ndio, wewe!” Akasema mleta wito.
“Sawa, nakuja,” Panky akajibu.
“Nakungoja twende,” mleta wito akamsihi.
“Kwani lazima twende wote?”
“Ndio! Nimeambiwa nikupeleke.”
Hapa Panky akazidi kupata hofu. Ina maana wanahisi anaweza kukimbia? Akaacha kazi zake na kuongozana na mwanaume huyo mpaka ofisini mwa Sheng. Alipofika, yule aliyemsindikiza akaagizwa angoje nje.
“Panky,” Sheng akaita huku akitazama karatasi kadhaa juu ya kashelf kake kadogo ka kioo juu ya meza.
“Naam, mkuu!” Sheng akaitikia. Mikono yake ilikuwa inatetemeka na kujawa jasho.
Sheng akamuuliza juu ya kazi aliyompatia hapo kitambo ya kummaliza Jona. Panky kusikia hivyo akaishiwa nguvu! Sasa akajua mwisho wake umewadia.
Sheng akiongea kwa lafudh yake ya kimandarin, akamwambia Panky kwamba siri yake isingeweza kudumu kwa muda. Alimpatia kazi na kwa kumdharau hakuitenda, akaja kumlaghai.
Na kwa asili ya uongo wake, inaonyesha ana mahusiano na Jona kwani mwanaume huyo alihama mara moja baada ya yeye kuja kusema amemmaliza.
Panky akalia kuomba msamaha. Hakuwa na lingine sasa la kufanya zaidi ya hilo. Akalia abakiziwe uhai wake. Atakuwa mtiifu kwa Sheng na hatorudia tena kufanya kosa.
Lakini kwa Sheng hayo yote yalikuwa makelele. Hakumwelewa Panky hata kidogo. Akafungua droo yake na kuchomoa binduki ndogo, akaitazama ina risasi ngapi.
Nne.
Akaikoki na kumwonyeshea Panky mdomo wa bunduki kwenye paji lake la uso.
“Nina mke na watoto wananitegemea. Pia wazazi huko kijijini. Tafadhali bakiza uhai wangu!” Panky akawaga machozi.
Sheng akabofya kitufe cha bunduki mara nne! Chuma zikatoboa kichwa cha Panky na kumlaza chini akiwa mfu!
Baada ya risasi hizo, yule mwanaume aliyeambiwa angoje nje, akaingia ndani na kubeba mwili wa Panky.
**
“Sasa? Si naweza nikatoka?” Akauliza Miriam. Sasa alikuwa ameboreka zaidi kiafya. Alikuwa anawasiliana na mama aliyempokea ambaye alikuwa mlangoni akitazama huko nje.
Ni majira ya jioni sasa. Jua lilikuwa linaelekea kuzama. Na siku hii Miriam aliona inafaa kwake kutoroka.
Tayari mtoto alishaenda kukagua huko nje mpaka barabarani. Akarejesha taarifa kwamba kupo salama.
“Ndio, njoo,” mama akamruhusu, Miriam akatoka mpaka huko nje, akamkumbatia mwenyeji wake kumuaga akimshukuru sana. Na akamuahidi atarudi kuja kumshukuru siku moja.
“Bado hutaki nikusindikize?” Akauliza mama mwenyeji.
“Hapana, hatari niliyokuweka kwa muda wote huo inatosha. Acha hili nipambane mwenyewe.”
Miriam akaanza kutembea akitazama chini. Kulikuwa na kaumbali kutoka hapo mpaka kituoni. Alikazana kutembea mkononi akiwa amebebelea kamfuko. Na mwili wake ukiwa umehifadhiwa ndani ya dira chakavu alilopewa na mwenyeji wake.
Akiwa amekaribia kituoni, kuna mtu mmoja akamuita.
“We mwanamke!”
Hakugeuka. Akakazana kutembea. Sauti ikamuita tena, we mwanamke we mwanamke. Ila hakugeuka abadani.
Akahisi anafuatwa. Watu walikuwa wengi kiasi chake hivyo kidogo akawa hana woga. Akatembea kwa kasi mpaka akafika kituoni kungoja basi.
“Napanda hilo linalokuja!” Akajisema kifuani. “Hata kama limejaa vipi.”
Akatazama kushoto na kulia kwake, watu wote walikuwa wametulia, lakini akamwona mwanaume aliyemtilia shaka. Mwanaume huyu alikuwa amevalia shati jeusi, mweupe kwa rangi mwenye macho mekundu.
Naye huyu mwanaume akamtazama Miriam, wakakutana macho kwa macho. Moyo wa Miriam ukadunda kwa kasi.
Akatazama barabara. Gari alilokuwa analingojea lilikuwa limekaribia kufika. Akaendelea kuapia moyoni kwamba lazima alipande gari hilo, hata iweje.
Gari likasimama, yalikuwa ni yale mabasi ya zamani sana. Lilikuwa linamwaga moshi mzito mweusi ambao ukiujumlisha na vumbi la barabara, basi kupata mafua ama matatizo ya kifua ilikuwa haiepukiki.
“Arusha town hiyo!” Konda akapaza sauti. Lakini gari lilikuwa limejaa mno. Hakukuwa hata na pa kukanyaga sembuse pa kusimama.
Lakini wanaume wawili wakaliwahi, ikiwemo na Miriam watatu, wakang’ang’ana kulidandia. Wanaume wakafanikiwa, Miriam akaambiwa na konda angoje lijalo, hataweza.
Hakuwa namna akangoja. Akatazama mahali alipomuona mwanaume yule aliyekuwa anamtilia shaka, hakumwona!
Akajiuliza kaenda wapi? Akaangaza macho huku na kule lakini kabla hajamaliza msako wake wa macho, ghafla akasikia sauti ya gari lingine laja.
Akajiweka sawia kung’ang’ana. Sasa gari liliposimama akawa wa kwanza kufika mlangoni, akazama ndani!
Japo alikuwa amebanwa haswa, hakujali. Alichotaka ni kutoka tu eneo hilo. Lakini kuna jambo.
Kuna jambo ambalo hakuwa analifahamu.
Nyuma yake alikuwa amesimama mwanaume yule aliyekuwa anamtilia hofu. Kumbe naye aligombania gari hilo na kuzama humo ndani.
Miriam alikuja kufahamu hilo baadae baada ya kukaribia Arusha town! Lakini ajabu ni kwamba, hakuelewa kuna nini ama nini kilifanyika, akajikuta anapoteza fahamu.
“Ni dada yangu, anaumwa!” Miriam alisikia sauti ya mwanaume ikisema huku yeye akipotelea kwa kudhoofu.
Alihisi kabisa sauti hii itakuwa ni ya mwanaume yule aliyemtilia mashaka, lakini hakuweza hata kupayuka wala kujikomboa.
Pap! Akawa gizani kamili asijue kinachoendelea.
** Akaja kupata fahamu baada ya muda asioujua. Alikuwa begani mwa mwanaume aliyekuwa anatembea kwa miguu akipiga hatua kubwakubwa.
Akaangaza kushoto na kulia, akayaona mazingira batili. Haya hayakuwa mazingira ya Arusha town. Palikuwa pakavu mno, majani yaliyokauka, barabara ngumu iliyojawa vumbi na mawe.
Oh my God! Sasa akatambua alikuwa anarejeshwa kwa Nyokaa.
Hapana! Akasema nafsini. Kamwe sirudi huko nikiwa hai, labda mfu. Lakini atajinasuaje? Ni wazi asingeweza kupimana ubavu na yule jibaba!
Akaazimia kutafuta namna. Kweli, penye nia pana njia, muda mfupi akaipata ya kwake. Aliona alama ya bunduki kiunoni mwa mwanaume aliyembeba. Ilikuwa ni bunduki ndogo iliyofunikwa na shati alilolivaa.
Akawaza kuikwapua imuokoe. Japo hakuwa anajua namna ya kuitumia, itamtisha adui yake mwishowe akapata upenyo.
Ndio, hiyo ilikuwa ni njia yake sahihi kwani njia ya kwanza aliyoifikiria ya kupiga yowe kali isingemsaidia kwa muda huo. Mahali walipokuwa wanapita hapakuwa na ishara ya mtu kabisa.
Angejichomesha.
Sasa, moyo wake ukiwa unaenda mbio, akaanza kuhesabu. Akifika tatu, anasita. Akifika tatu, anasita kwa woga.
‘I have to do this! Miriam you have to!’ (Inanibidi nifanye hivi! Miriam inakubidi!) akajisemea kifuani.
Akafunga macho kwanguvu, akahesabu, ilipofika tatu akavuta shati la yule mwanaume upesi na kuchomoa bunduki. Akamwekea kichwani.
“Nishushe haraka kabla sijakumaliza!” Akaamuru. Yule mwanaume akamshusha akasimama mwenyewe.
“Ulidhani utanipeleka huko nilipotoka?” Akauliza kwa kiburi. “Umekosea sana. Utaenda mwenyewe.”
Akamwamuru mwanaume huyo ageuke nyuma na akimbie kwa nguvu zake zote. Akihesabu mpaka tatu asimwone, la sivyo atamfyatulia risasi.
Miriam hakuwahi kuua maisha yake yote. Tukio la kumuua binadamu mwenzake lilikuwa ni zaidi ya mtihani. Yeye mwenyewe kifuani mwake alikuwa anafahamu hawezi kulifanya.
Lakini katika namna ya ajabu, mwanaume yule akiwa amenyooshewa mdomo wa bunduki, hakutii agizo alilopewa. Badala yake hata mikono aliyokuwa ameiweka juu akaishusha na kisha akatabasamu.
“Simama hapo hapo! … nimesema simama!” Miriam alifoka lakini mwanaume yule hakutii, akafyatua bunduki, ajabu hakikutoka kitu. Akafyatua tena na tena, hola!
Mwanaume yule akampokonya bunduki hiyo.
“Ukitaka kushoot, unakoki kwanza bunduki, sawa?” Akamwambia Miriam huku akikoki bunduki kisha akamwamuru: “Haya sasa geuka twende!” Miriam akanyong’onyea. Akapoteza matumaini ya kutoroka. Lakini akaapia moyoni mwake hatokuwa radhi kurejeshwa tena kule alipotokea.
Labda tu awe maiti.
“Nimekwambia geuka twende!” Akarudia mwanaume akitoa macho ya kutisha lakini Miriam akaendelea kusimama kana kwamba hajasikia.
Kuonyesha hana mchezo, mwanaume akapiga risasi kandokando ya Miriam kisha akarudia sentensi yake akimtaka Miriam waende.
“Siendi, niue!” Miriam akamwambia pasi na hofu. Kabla mwanaume huyo hajafanya kitu akasikia sauti nyuma yake, kilikuwa ni kishindo cha mtu kwa mbali.
Haraka akageuka kutazama. Kweli alikuwa ni mama aliyekuwa amebebelea ndoo ya maji kichwani. Mama huyo alikuwa ametoa macho ya mshangao akiwatazama.
Mwanaume akamgeuzia bunduki na kufyatua risasi moja, heri ikamkosa, mama akadondosha ndoo na kukimbia kama mwehu akipiga ukunga.
Mwanaume huyo alimpogeukia Miriam akakutana na jiwe la uso! Akadondoka chini akiacha bunduki. Akamwaga damu za kutosha akilalama kwa maumivu makali.
Miriam akaokota bunduki.
“Tatizo nikikuacha, bado utanisumbua!”
Akafyatua bunduki pasipo kumtazama mlengwa wake. Hata alipomaliza kumfyatulia hakumtazama akaondoka zake. Alikuwa anaogopa. Alijua ameshamuua mwanaume huyo.
Kumbe hizo risasi zote zilipiga chini!
***
“Honestly I thank God, kwanza shukrani ziende kwake. Na pia kwa huyo malaika aliyemtuma kuniokoa,” alinguruma bwana Kamau Githeri kwenye televisheni ya KTN wasaa wa taarifa ya habari.
“Unaweza kutuambia ilikuwaje hasa?” Akauliza ripota. Kwa wakati huo maandishi yaliyokuwepo chini ya video yakisomeka kama ifuatavyo:
‘MHESHIMIWA K. GITHERI APONA CHUPUCHUPU YA KUCHUNGULIA KABURI’
“Ni ujhumbe tu nilipongeaga kwa email,” akaeleza mheshimiwa Githeri. “ukinitell kwamba nipo about kuwa ambushed na wauajhi. I didn’t ignore it, nikatake steps along with my family immediately!”
Wakaonyesha walinzi wa nyumba ya bwana Githeri, wawili, wote walikuwa wameuawa pamoja na mbwa wao.
“Unadhani ni kwanini walitaka kukuua?” Akauliza ripota.
“I think ni haya tu issues za politics, nothing more,” akajibu mheshimiwa. “Furthermore, nisingependa kuongea sana. Shauri yangu iko kwa polisi hands as we talk.”
Baada ya hapo KTN wakaonyesha na upande wa pili wa mheshimiwa Otieno. Hapa kichwa cha habari kikabadilika na kusomeka ifuatavyo:
‘HON. OTIENO AMIMINIWA RISASI KUUAWA’
Wakahojiwa baadhi ya mashahidi wa tukio hilo na mhusika mmoja wa familia akieleza namna walivyoguswa na msiba huo kwa ndani.
Hata mhusika huyo wa familia hakuweza kueleza kwa muda mrefu, akakabwa na kilio, mahojiano yakakatishwa.
Habari ikaendelea kurushwa. Sasa wakihamia kwa viongozi wa bunge wameupokeaje msiba huo na mashambulizi hayo ya ghafla ndani ya siku moja huku mojawapo likizaa matunda.
Spika akanena kulaani tukio hilo akisema linatishia uhuru wa bunge kama mhimili muhimu wa serikali kufanya kazi yake. Lakini zaidi akatupa lawama za waziwazi kwa karani wa bunge ambaye alipuuzia ujumbe aliotumiwa na msamaria mwema kuhusu shambulizi hilo.
“Somehow, he is responsible for such act!” (Kwa namna fulani, anawajibika na tukio hilo!)
Baada ya hapo ripota akasema uchunguzi wa kipolisi unaendelea, habari hiyo ikapita zikiendelea zingine.
“Shit!” Sheng akasaga meno. “How is this possible?” (Linawezekanaje hili?)
Alikuwa ameketi sebuleni akikodolea televisheni yake kubwa iliyomeza ukuta. Akatetemeka kwa hasira.
Ni nani aliyetuma taarifa za kutaka kuuawa viongozi hao? Ni swali lililomnyima raha. Hakuweza kukaa nalo kifuani akanyanyua simu yake ya mkononi akapiga.
Akaagiza watu wote wa vitengo vya mawasiliano pamoja na heads wa WAVES zote wafike ofisini kwake kesho asubuhi na mapema.
Wanapokuja wahakikishe wana maelezo yanayojitosheleza. La sivyo wataingia hai na kutoka wafu!
**
“Dada, una mgeni,” mfanyakazi alimtaarifu Miranda.
“Nani huyo?” Miranda akauliza kwa hasira. Alikuwa ameketi kitandani kwake akiperuzi kwa kutumia tarakilishi yake mpakato. Mwilini ana gauni la kulalia.
Majira ni saa nne usiku.
“Simjui mimi. Ni mzungu!” Akajibu dada wa kazi. Miranda akashtuka. Moja kwa moja akawaza atakuwa ni BC.
Lakini mbona hakunipa taarifa?
Akanyanyuka upesi na kwenda sebuleni. Kweli akamkuta BC ndani ya suti kama ilivyo ada. Akamkaribisha na kusalimiana.
Pasipo kupoteza muda BC akamuuliza:
“Are you the one who did it?” (Wewe ndiye uliyelifanya?)
Miranda akatikisa kichwa.
“I didn’t do it,” (sijalifanya) akajibu kwa msisitizo.
BC akashusha pumzi ndefu maana sasa alikuwa amechanganyikiwa. Kama si Miranda aliyetekeleza lile agizo, basi ni nani mwingine?
Hofu ilimuingia ukute wamezamishwa mtegoni na ‘wajanja’ kisha waumie huku wakiwanufaisha wengine. Lakini hao ‘wajanja’ ni wakina nani?
BC akamuuliza Miranda yeye alikuwa amepangaje kummaliza yule mwanamke. Miranda akasema hakuwazia njia ya ajali kabisa kwani ni risk sana. Aliwazia kumtwanga tu risasi akiigiza jambazi ili kufinya ulimwengu wa kipepelezi.
Sasa sio tu kwamba walikuwa kwenye rada za polisi, kama vile Miranda alivyosema kuwa anatafutwa na inspekta Jona, bali pia walikuwa na kazi ya kumng’amua mtu aliyewazidi hatua na kulifanya hilo akilenga kuwa ‘frame’ wakamatwe.
BC akamuaga Miranda na kisha akaenda zake. Alimwachia Miranda kazi ya kufanya, ashirikiane na Jona hatua kwa hatua kumjua mtu huyo. Lakini kwa wakati huo akijiweka safi, mwenye mikono isiyo na hatia.
Usiku huo kwa Miranda ukawa mgumu haswa. Alijaribu kuchambua kila mazingira aliyoyapitia kuangaza kama kuna mahali alifanya kauzembe, hakupata!
Huu mtihani ulikuwa mgumu sana.
Lakini mwanamke huyu alisahau jambo moja. Jambo moja lililomtia kwenye mtego wa ngiri. Hakufahamu, aidha tuseme alisahau kuwa ni yeye aliyefanya akajazwa kwenye rada ya adui.
Adui huyu ni mwerevu mno. Hakurupuki na hubonyeza kitufe pale anapoona anatakiwa sasa kufanya hivyo.
Unakumbuka kipindi kile Miranda alipojionyesha runingani akiwa na mke wa Boka akitambulishwa kama balozi wa kampuni hiyo ya urembo na vipodozi na akinadi bidhaa za kampuni hiyo?
Basi kama wakumbuka, mipango miwili ilianzia hapo, mosi ya kumsaka Miranda, pili, kuimaliza kabisa kampuni ya mama huyu.
Lakini yote hayo yatekelezwe katika njia ‘laini’. Mama afe, Miranda afe pia ama akafie jela.
Kila Miranda alipokutana na Boka, hakujua anatazamwa na kufuatiliwa. Na ijapokuwa wanaomfuatilia hawakujua nini Boka na Miranda walikuwa wanaongea, kiutuzima, ukubwa dawa, wakang’amua watu hao wapo kwenye mahusiano.
Sasa kuna nini tena hapo?
Miranda akawa anatafutwa ajae kiganjani. Kwenda kuonana na mke wa Boka hotelini na kugombana huko, kote kulikuwa kunatazamwa.
Sasa je kuna sehemu gani ya kumaliza mchezo kama hii? Endapo tukimmaliza mke wa Boka, polisi watamalizana na Miranda. As simple as that!
Hakikisha mke anakufa, shoga yake anabaki kutoa ushahidi. Shoga huyu lazima atamtuhumu Miranda kwani alikuwapo wakati zogo latukia.
Unadhani atamhisi nani mwingine? Ni Miranda anataka kumuua mke ili abakie na mume wa mtu!
Miranda alikuwa ana fumbo hili kubwa kulifumbua. Yeye pamoja na Jona.
**
Majira ya saa nne asubuhi.
“Uliona wakati akiitwa?” Jona akamuuliza Marwa. Mezani kulikuwa kuna vikombe viwili vya chai. Vikombe hivi vilikuwa vimejaa lakini chai ikiwa imeshapoa. Tangu viwekwe hapo mezani havikuguswa.
“Sikuona akiitwa,” alijibu Marwa. “Tuliachana vizuri tu kila mtu akaenda kufanya kazi yake. Baadae tulipotoka, sikumwona. Nikajua atakuwa ametingwa kwani aliniambia anaweza akawa yupo tight. Kumbe ndo’ alikuwa ashauawa!”
Hizi habari zilikuwa ngumu sana kwa Jona. Alijaribu kujilazimisha aziamini lakini kichwa chake kikagoma kabisa. Kwanini Panky ameuawa?
“Marwa, inabidi uwe makini sana,” Jona akashauri. “Hatuwezi jua pengine Panky ameuawa kwasababu za kipelelezi ambao unaweza ukakuweka hatarini nawe pia.”
Marwa akanyamaza. Alikuwa anatazama chini uso wake ukimezwa na hofu. Aliogopa sana. Kifo cha Panky kilimshtua na kumkumbusha kuwa hayupo salama abadani.
Aliwaza mtu atakayefuata kuuawa atakuwa ni yeye. Si mwingne. Mawazo hayo yakamfanya asimsikilize kabisa Jona alichokuwa anaongea.
Jona akamtikisa.
“Marwa, tupo pamoja!” Marwa akashusha pumzi ndefu alafu akanyaka simu yake mezani na kumkabidhi Jona.
“Alinitumia ujumbe muda mfupi baada ha kuachana toka kula. Akiniambia hao ndo’ watu waliotumiwa pesa muda si mrefu kwa ajili ya malazi, chakula na makazi nchini Kenya.”
Jona akatazama majina hayo, akamuuliza Marwa kama anawafahamu hao watu, anaweza kumsaidia angalau kwa picha.
Marwa akazama ndani ya tarakilishi yake, punde akapata picha na kumwonyesha. Jona akatumia simu yake kudaka picha hizo na kuzitunza.
Watu hao walikuwa ni Lee na wenzake watatu: Devi, Nigaa na Mombo.
“Ahsante sana,” Jona akashukuru. Marwa akamtazama mwanaume huyo na kumwambia pasi na chembe ya masikhara.
“Hapo ndiyo utakuwa mwisho wa kukusaidia. I am out!”
Jona akaduwaa.
“Una maanisha nini Marwa?”
Marwa pasipo kupepesa macho akamwambia hataki tena ushirika. Mpaka hapo alichokifanya inatosha. Anaomba asihusishwe kwa njia yoyote ile tena!
“It is enough. I cant take this risk anymore!” (Inatosha. Siwezi kubeba hii hatari zaidi!)
Haikujalisha Jona aliongea nini, Marwa hakutaka sikia. Alimtaka aende na amwache na maisha yake kama alivyomkuta.
Ni bora maisha yake ya awali kuliko haya ya sasa ambayo anaweza akakosa vyote. Kheri sasa anapata kimoja, wazazi wake kuwa hai. Inatosha!
Marwa alikuwa ame ‘panik’. Alikuwa pia na hasira ndaniye ambayo ilizidi kujionyesha kadiri alivyokuwa anaongea.
Jona akaona huo si wasaa wa busara kwake kukaa hapo, akaondoka zake.
**
Aliegemea kiti cha taksi akiendelea kuwaza. Alifahamu fika kwa mawazo haya kama angelipanda daladala angepitishwa kituo. Application yake ya UBER ikamsaidia kupata usafiri chap!
Alimfikiria Panky na kisha Marwa. Marwa na kisha Panky. Akaja kubanduliwa toka kwenye mawazo hayo na mlio wa simu. Alikuwa ni Kamanda.
“Umefikia wapi?”
“Bado naendelea na upepelezi, mkuu. Nitakufahamisha, sipo maeneo mazuri.”
Simu ikakata. Sasa Jona akatazama mandhari ya nje ya gari. Akapata kuwaza kidogo kuhusu kesi ya mke wake Boka, akapata wazo.
Alikuwa anaelekea hospitali kuonana na rafiki wa mke wa Boka kisha aende kwa Miranda. Lakini akaona ni vema apite kwa Boka kisha aende mawasiliano.
Akapita huko, akachukua simu na namba ya simu ya marehemu kisha akaelekea mawasiliano ambapo alifanya utaratibu wa kupata mawasiliano ya mwisho na marehemu, akaenda kumalizia utaratibu wake huo TIGO.
Akachapiwa jumbe zote na hata akapata ‘access’ ya ‘recorded calls’ za mwisho. Yote hayo yaliwezekana pasipo kuchukua muda sana kwa kujieleza anayahitaji kiupelelezi.
Napo kwa wakati huo …
Mlio wa risasi ukasikika mara mbili toka ofisini mwa Sheng.
Tah! – tah!
Mlango ukafunguliwa ikatolewa maiti ya mtu mwenye asili ya China! Wanaume wawili walimbebelea wakielekea upande wa kushoto mwa jengo.
Marehemu huyu alikuwa ni Moderator! Moderator wa SPACE BUTTON. Tayari roho yake ilishanyofolewa na mkono wa Sheng baada ya kubainika ni yeye ndiye alifanya uzembe.
“I want that traitor alive!” (Namtaka huyo msaliti akiwa hai!) Sheng alisikika akifoka ndani ya ofisi kisha akabamiza meza.
Mara wanaume kadhaa wakatoka ndani. Wakaendelea kuteta kadiri walivyokuwa wanasonga mbali na ofisi ya mkuu.
Sasa wazi, Marwa alikuwa hatiani!
Hati ya hatiani. Uzembe mdogo hauruhusiwi ndani ya ANGA LA WASHENZI – ANGA LA WAUAJI. Ndani ya dakika chache tu kipindi cha usiku, Marwa baada ya kufanya kazi ya udukuzi, akasahau ku ‘log-out’.
Hakujua alisahau na maisha yake hapo, haraka akatambuliwa. Uangalizi ulikuwa mkubwa sana haswa baada ya kubainika kuwa mawasiliano yao yalidukuliwa na kupelekea zoezi la kuokolewa kwa walengwa.
Haraka alipojulikana, akajazwa kwenye GPS na haraka tena akajulikana makazi yake yalipo. Haya makazi yalikuwa ya nani? – Marwa! Toka SPACE BUTTON – BIRD ONE.
Moderator angeachwaje hai?
**
“Miranda, kila kitu kinakuonyeshea ni wewe,” Jona alisema baada ya kunywa maji mafundo kadhaa.
Miranda akasonya akitikisa kichwa.
“Jona, I swear to God. Sijafanya hicho kitu kabisa kabisa!”
“Sasa tatizo ni kwamba inabidi uthibitishe hilo. Si kwa maneno tu,” Jona akasema akimtazama Miranda kana kwamba mwalimu amtazamavyo mwanafunzi mtoro.
Miranda akashika kichwa chake na kukikuna kwanguvu.
“Pengine ni maadui zangu,” Miranda akajitetea kidhaifu. “Huwezi jua?”
Hata mwenyewe alijiona anaongea kitu ambacho haki ‘make sense’. Jona alikunywa maji tena alafu akamtazama. Akamuuliza ni lini walianza ile projekti ya kupeleka bidhaa zao Kenya.
Miranda baada ya kufikiria kidogo, akasema anakumbuka ilikuwa ni punde tu baada ya majadiliano na makubaliano yaliyofanyika nchini Kenya kuwa bidhaa toka nchi za Afrika Mashariki zipewe kipaumbele sokoni, zipunguziwe makato na kufanyiwa wepesi.
Mke wa Boka akaona hiyo ni fursa adhimu kwake kulivamia soko hilo la vipodozi na urembo.
Baada ya maelezo hayo, Jona akamuaga Miranda aende zake lakini akimuahidi atakuwa anamtembelea mara kwa mara.
“Naamini hautaufanya uhuni wako,” alimwonya akiwa ameushikilia mlango.
**
Saa saba usiku …
Gari jeusi lilisimama kwa mbali hivyo halikuonekana vema ni la aina gani. Wakashuka wanaume wawili waliovalia suti nyeusi, tai nyekundu na vinyago vyeusi.
Wanaume hawa walikuwa wakakamavu wakitembea kwa haraka, wazi wakienda kutenda tukio.
Kutokana na giza lililokuwepo na pia mavazi yao, ilikuwa ngumu kuwatambua. Waliufikia ukuta mmoja akatumika kama ngazi mwenzake kukwea mpaka juu, alafu naye aliye juu akamvuta mwenzake wakaingia ndani.
Hakuna hata chembe ya kelele iliyotokea hapa. Na yote haya yalifanyika ndani ya sekunde tu, wala si dakika, kuthibitisha kwamba wanaume hawa walikuwa wana mafunzo.
Walitumia waya kufungulia kufuli za milango, na kwa upande wa magrili, kabla hawajafungua walimiminia mafuta viungoni, basi yakafunguka pasi na tone la makelele!
Mpaka wanafika kitandani mwa Marwa, walikuwa wametumia dakika mbili tu tangu walipotoka kwenye usafiri wao!
Wakamwamsha Marwa kwa kumpiga na kitako cha bunduki kisha wakamtaka aongozane nao kimya kimya!
“Sasa jifanye mjanja uone kilichomfanya fisi awe na miguu mifupi!
Marwa akatetemeka sana. Jasho likamiminika kama nusu ndoo. Alihisi kila aina ya haja. Aliona roho inamtoka mbele yake na hana cha kufanya!
Akasimama na kuswagwa alekee nje.
Kufika huko kabla hawajatoka, wakasikia sauti ya mluzi! Wanaume watekaji wakaangaza kushoto na kulia, hawakuona mtu!
Wakatazamana.
Sauti ya mluzi ikalia tena, mara hii ikifuatisha melodi za muziki.
***
Watekaji wakachanganyikiwa. Ni nani huyo anawafanyia mchezo? Wakaangaza tena wasifanikiwe. Wakawa wamepigwa na bumbuwazi.
Wakatishia kumuua Marwa endapo huyo apigaye mluzi hatajitokeza mwenyewe. Lakini kinyume na matarajio, mpiga mluzi hakujitokeza!
Na sasa hivi badala ya kupiga mluzi akaongea:
“Najua hamuwezi kumuua. Kama mngelikuwa mmepanga hivyo, msingelikuwa na haja ya kumtoa nje.”
Kisha kukawa kimya kidogo.
Kutazama huku na kule, ghafla akatokea mwanaume hewani! Alikuwa ni Jona. Hamaki kutazama, bunduki ikapigwa teke na kisha Jona akajifichia kwenye mwili wa mwanaume mtekaji.
Risasi mbili zikatupwa! Mwanaume mtekaji alimpiga mwenzake kwa pupa na kumuua. Jona akamrusha yule mtekaji marehemu kwa mwenziwe, akamdaka, ikawa kosa.
Kabla hajafanya jambo, Jona akawa amemchapa teke zito, kinyago na bunduki zikarukia kando. Kuja kukaa sawa, tayari ashawekwa chini ya ulinzi.
“Tulia kama maji mtungini!” Jona akamwamuru. Wakamfunga mikono na miguu na kisha kinywa!
Baada ya muda mfupi wakatoka wanaume wawili nje ya uzio. Walikuwa wamevalia suti na vinyago. Wakatembea kwenda kufuata lile gari lililowaleta watekaji.
Walipolifikia wakamuweka dereva chini ya ulinzi na kumwamuru asogeze gari lake kwa nyumba ya Marwa. Naye wakamfunga miguu na mikono na kinywa, wakampakia na yule marehemu kwenye gari wakawapeleka kituoni.
“Nitakuja kuwahoji mwenyewe,” Jona alitoa maelezo kwa polisi kisha wakitumia lile gari la wavamizi, wakayeya.
Marehemu akapelekwa mochwari.
Lakini bado kichwani mwa Marwa kulikuwa na maswali. Jona aliwezaje kufika pale nyumbani kwake kumuokoa? Alijuaje kama wavamizi watakuja kummaliza usiku huo?
Kusema ukweli alimwona Jona kama malaika kwani alishajua amekwisha usiku huo. Kitendo cha mwanaume huyo kutokea na kumwokoa, kulikuwa ni muujiza. Bado hakuamini!
“Ahsante sana, Jona,” akashukuru.
“Usijali,” Jona akamjibu akitazama mbele. “Ni kazi yangu.”
Kukawa kimya kidogo.
“Najua una maswali kichwani,” Jona akasema akili ya Marwa. ” unawaza nilifikaje pale kwako kwa muda muafaka kiasi kile. Ila tambua nilikuwa nakuwaza. Sikuweza kulala nyumbani kwangu kwa amani kabisa. Na akili yangu iliniaminisha haupo salama. Kama Panky ameuawa, basi nawe lazima utakuwa kwenye rada zao.”
Baada ya kusema hayo, Marwa akaomba msamaha kwa Jona. Alitenda kosa kumfukuza kiasi kile na hata amemsaliti kwenye mapambano.
Jona akamwambia asijali, sasa watazame ya mbele. Amelenga kumfundisha mwanaume huyo sanaa ya mapambano, martial arts, ikapate kumsadia kujilinda kwani atahitaji sana mafunzo hayo kwa kipindi hicho.
Marwa akaridhia. Wakaenda nyumbani kwa Jona na kupumzika. Lakini Marwa hakulala kabisa kwa woga. Alihisi wale majamaa wanaweza kurudi tena kumuua.
Kila aliposikia sauti ya kitu akakurupuka na kuangaza. Alipomtazama Jona yeye alikuwa tayari anakoroma baada ya kunywa vinywaji vyake vikali.
Kama haitoshi Marwa alikuwa anawafikiria na wazazi wake. Yeye amenusurika kifo lakini vipi wazazi wake ambao wanategemea kupata antidote toka kwa Sheng? Wataishije?
Ina maana atawaona baba na mama yake wakifa huku hana cha kufanya? Akakosa amani.
Akajigeuza huku na huko. Akajibaraguza kitandani lakini hakupata usingizi kabisa. Akaona kuna haja ya kupumbaza kichwa.
Akanyanyuka na kumalizia kinywaji alichobakiza Jona chupani. Kilikuwa ni kinywaji kikali mno na yeye hakuwa mzoefu wa hayo mambo kabisa.
Sasa hakuchukua dakika akalala usingizi ambao hajawahi kuupata tangu azaliwe. Kama mfu!
Alikuja kuamka saa tatu asubuhi kichwa kikiwa kinamgonga haswa. Kumtazama Jona, hakuwepo! Alishaondoka akimwachia maelekezo kwa njia ya maandishi,
Aikute supu jikoni.
***
Saa ya ukutani ilikuwa inasema ni saa tano asubuhi hivi sasa. Jona hakuwa mtu wa kukaa ofisini mara kwa mara, ila leo hii huu muda ulimkuta akiwa kwenye kiti nyuma ya meza iliyobebelea tarakilishi.
Kuna mambo kadhaa alikuwa anayapitia haswa kuhusu kesi ya ajali ya mke wake Boka. Alikuwa anachambua maelezo ya Miranda akaona kuna kitu mule ndani yake.
Kuna jambo la kulifuatilia!
Mojawapo ya kanuni ya upelelezi ni kwamba kila kitu mbele yako ni mtuhumiwa katika namna yake. Hutakiwi kupuuza chochote kile, wala kukidharau. Kwani yeyote anaweza kufanya lolote kwasababu yoyote.
Jona akazama mtandaoni na kuangazia yale ambayo Miranda alikuwa anayasema kuwa mke wa Boka alianza kupeleka bidhaa zake nchini Kenya baada ya kuona hali ni shwari huko kisera.
Alipopekua kwenye vyanzo mbalimbali akaja gundua kuwa jambo hilo lilikuwa ni ‘hot issue’ huko nchini Kenya. Ambapo lilizua mjadala mkubwa miongoni mwa wachangiaji, hoja ikiwa kwamba soko la Kenya sasa limefurika bidhaa toka China.
Bidhaa za wazawa zimekuwa hafifu mno na kwasababu za ulimbukeni na unafuu mkubwa ambao unawekwa kwenye bidhaa za China, basi bidhaa za wazawa zimekosa soko, si wakulima wala wafanyabiashara wanaohema kwa unafuu.
Sasa mswada uliletwa bungeni kuangazia namna ya kukabili na kubadili hali hii, miswada hii ikiletwa na wabunge wa chama pinzani ambao kwa jina walikuwa ni waheshimiwa Kamau Githeri na W.Otieno.
Sasa haya majina yakamshangaza Jona! Yalikuwa ndio wale waheshimiwa waliolengwa kuuawa. Kumbe kulengwa kwao ilikuwa ni kwasababu ha hili jambo! Sasa akajua.
Kwa kupitia mswada wao waliouleta bungeni, sheria sasa ikatungwa kuweka mipaka kwa bidhaa za nchini China na huku zikiongezewa kodi na makato ili wazawa na hata wale wafanyabiashara toka nchi Afrika Mashariki wapate ahueni.
Alarm ikaita kichwani mwa Jona! Sasa hapa kulikuwa na harufu ya jambo.
“Hata ukitazama vema, most of Chinese products zimekuwa zikiwaharibu wanawake zetu. Sasa wabadilika rangi kama chameleons hata their shapes zimekuwa awkward. Why cant we allow our natural products to take over and ban these Chinese takataka?” Hii ilikuwa mojawapo ya kauli aliyoitoa marehemu W. Otieno punde baada ya kutoka kwenye mzozo mkali bungeni.
Sasa Jona akapata picha kamili. Hivi vitu vilikuwa vina mahusiano, tena ya kindakindaki! Kilichomuua mke wa Boka, hakuwa Miranda bali wachina ambao walimchukulia kama tishio kwa bishara yao ya vipodozi nchini Kenya!
Jona akatafuta clips za video ndani ya mtandao wa YOU TUBE zikionyesha hotuba za waheshimiwa Kamau Githeri na W. Otieno kupinga udhalimu wa China kwenye kudhoofisha uchumi wao wa ndani, baada ya hapo akazipakua pia na video za marehemu mke wa Boka.
Kama haitoshi akapakua na vielelezo kadhaa toka mtandaoni na kuviprint akiviweka kwenye faili. Sasa akijumuisha na vile alivyovipata kwa link kwa msaada wa Marwa, alikuwa kwenye hatua njema kabisa.
Rrrrrrrrnnng! Simu ikaita. Akaipokea na kuiweka sikioni. Kamanda.
“Nakuja, mkuu,” akasema kwa ufupi simu ikakata. Akanyanyuka na kwenda kuonana na Kamanda ofisini kwake.
“Umefikia wapi?” Lilikuwa swali la kwanza la Kamanda.
Jona akamweleza namna gani anavyowashuku wachina kuhusika na kifo cha mke wa Boka, haswa kwasababu za kibiashara huko nchini Kenya. Watu hao wakilenga kummaliza mwanamke huyo ili kuendelea kutawala soko la bidhaa zao za urembo na vipodozi.
Kamanda akashusha pumzi ndefu. Alielewa kila ambacho Jona alieleza lakini ugumu unakuja hapa, kwa kesi hiyo kutimia, wanahitaji msaada toka jeshi la polisi la Kenya kwenye upelelezi na ‘confirmation’. Mahusiano baina ya nchi hizi mbili kwa hapa karibuni yamedidimia, itawawia vigumu kutekeleza hilo.
“Lakini Jona, bado hii simulizi yako inahitaji ushahidi zaidi,” akasema Kamanda. “Utathibitisha vipi muuaji huyo alitumwa na Wachina? pili, mauaji ya viongozi hao wa Kenya hatuwezi kuyatolea tamko bali mamlaka zao za ndani, tutawasemeaje wameuawa na wachina?”
Jona akamwomba Kamanda ampatie muda zaidi, atatafutia ufumbuzi kila swala lililopo mezani. Kwa muda huo akaomba aende ubalozi wa China kwa ajili ya mahojiano.
“Utaenda kuwauliza nini huko? Huoni utateteresha mahusiano baina yetu na wao?” Kamanda akapata hofu.
“Usijali, Kamanda,” akasema Jona. “Najua namna ya kuenenda.”
Jona akatoka ofisini.
Sasa ilikuwa ni majira ya saa saba ya mchana. Akaona ni kheri kama angelipata kitu tumboni. Akasonga kantini na kujipatia chakula.
Akiwa hapo mara ujumbe ukaingia ndani ya simu yake toka kwa namba mpya. Akaufungua:
‘Habari, Jona. Ni Miriam hapa. Tafadhali naweza kuonana na wewe?”
“Miriam?” Jona akatahamaki. Badala ya kujibu ujumbe huo akaamua kupiga simu. Ikapokelewa na sauti ya kike, akajitambulisha ni Miriam, mke wa marehemu Eliakimu.
“Upo wapi?” Jona akauliza.
“Nipo kwa shangazi yangu Kimara,” akajibu Miriam.
“Sawa, basi nitafanya mpango tuonane jioni.”
Simu ikakatwa.
“Miriam!” Jona akajisemea wenyewe. Alikiri ana maswali kadhaa ya kumuuliza mwanamke huyo, kwa upande wa Eliakimu na hata pia wakina Nyokaa.
Aliamini atapata taarifa za maana toka kwa mwanamke huyo akawatie nguvuni wadhalimu.
Alipomaliza kula akalipia na kunyookea ubalozi wa China. Humo ndani hakumkuta balozi bali msaidizi wake. Wakateta kwa lisaa limoja kabla Jona hajatoka ndani ya jengo hilo.
Kitendo cha kutoka tu, ikachukua dakika mbili, Sheng akaarifiwa juu ya ujio wa Jona. Na shuku zake zote alizozileta ubalozini!
***
MWISHO WA SEASON 1,
– JE SHENG ATAMFANYA NINI JONA?
– MARWA ATAPATA MBADALA WA TIBA YA WAZAZI WAKE?
– MIRIAM ANAMTAKIA NINI JONA?
– JONA ATAWEZA VITA HII MWENYEWE?
– MAJIBU YAPO MSIMU WA PILI! SEASON 2 YA ANGA LA WASHENZI
Simulizi : The Holy Sin (Dhambi Takatifu) Sehemu Ya Kwanza (1) Simulizi ya aina yake inayosisimua na kukufurahisha … fuatilia simulizi hii kujifunza mengi na kuburudika.
MLIO wa kengele ulisikika kutoka kwenye mnara wa kanisa kuashiria muda wa sala ya Jumapili, waumini mbalimbali wakawa wanaingia ndani ya kanisa kwa ajili ya kumuomba Mungu wao. Aidan, mtoto mdogo mwenye umri wa miaka sita, aliteremka kwenye gari lao lililokuwa limepaki nje ya kanisa kabla hata wazazi wake hawajateremka, akaanza kukimbia kuingia ndani. “Caro! Caro!” aliita Aidan huku akimkimbilia mtoto mwenzake, Carolina aliyekuwa ameshikwa mkono na mama yake, wakielekea ndani ya kanisa hilo. Wakakumbatiana kwa furaha na kushikana mikono, hakuna aliyekuwa na shida tena na wazazi wake. Urafiki wa watoto hawa waliokuwa wanasoma shule moja ya chekechekea, uliwafanya hata wazazi wao kuwa karibu kama ndugu. Siku nyingine Aidan alikuwa akilala nyumbani kwa akina Caro, Caro naye akifanya hivyohivyo kwani walikuwa wakiishi mtaa mmoja. Misa ilipoanza, watoto hao walitoka nje ya kanisa na kuendelea kucheza kwa furaha bila kujali kitu. Baada ya misa kuisha, wazazi wao walitoka na kuanza kusalimiana kwa furaha huku watoto wao wakiendelea kucheza. Baadaye wakaagana lakini Aidan hakutaka kumuacha Caro peke yake, akamng’ang’ania waondoke pamoja mpaka mama wa mtoto huyo alipokubali. Wakaondoka pamoja kwa kutumia gari la akina Aidan mpaka nyumbani kwao ambapo waliendelea kucheza kwa furaha mpaka jioni. Siku ziliendelea kusonga mbele, watoto hao wakizidi kushibana utafikiri wamezaliwa kwa baba na mama mmoja. Kila siku Aidan hakwenda shuleni bila kumpitia Caro na kwenda kusubiri basi la shule pamoja, vivyo hivyo kwa Caro. Hata walipofikisha umri wa kuanza darasa la kwanza, ilibidi wazazi wao wawatafutie shule moja ya kulipia kwani hakuna aliyekuwa tayari kukaa mbali na mwenzake. Wakaandikishwa pamoja East Africa International School, Mikocheni jijini Dar es Salaam. Maisha yalizidi kusonga mbele huku watoto hao wakizidi kukua kimwili na kiakili, ukaribu wao ukazidi kuimarika hata wakiwa shuleni kiasi cha baadhi ya wanafunzi wenzao kuhisi walikuwa ndugu wa damu. Miaka saba baadaye, wote walihitimu elimu ya msingi shuleni hapo na matokeo yalipotoka, walikuwa wamefaulu kwa kiwango kikubwa na kuchaguliwa kwenda shule mbili tofauti. Ilibidi wazazi wao waitane na kujadili suala hilo kwani hakuna aliyekuwa tayari kwenda kusoma mbali na mwenzake. Kwa kuwa familia zao zilikuwa za kitajiri, waliafikiana kwamba wawatafutie shule moja ya kulipia, wakapelekwa Maritime Secondary School ambako walianza kidato cha kwanza pamoja. “Caro!”?“Abee Aidan.” “Unajua wewe ni mzuri sana.” “Hahaa Aidan, acha utani wako bwana! Hivi umewaza nini mpaka kuniambia hivyo?” “Aah! Hapana, sijawaza chochote, nimekwambia tu.” “Lakini hujawahi kuniambia hata siku moja.” “Si ndiyo nimeanza kukwambia leo, kwa hiyo hutaki kupokea sifa zako?” “Haya basi ahsante,” alisema Caro kwa aibu huku akiinamisha sura yake chini. Wakaendelea kujisomea lakini Aidan alionyesha kukosa utulivu kabisa, muda mwingi akawa anamtazama Carolina usoni utafikiri ndiyo mara yake ya kwanza kumuona. “Aidan mbona unaniangalia sana, mwenzio nasikia aibu bwana,” alisema Caro huku akiinamisha sura yake chini kama kawaida yake, wakacheka kwa pamoja na kuendelea kujisomea. Hata hivyo, Aidan hakuishia hapo, aliendelea kumtazama Caro kwa jicho la wizi bila mwenyewe kujua huku akianza kuhisi hali ambayo haikuwahi kumtokea hata siku moja. Alianza kuhisi hisia za kimapenzi zikizunguka ndani ya kichwa chake na kutaka kuvuka kwenye urafiki wa kushibana waliokuwa nao tangu wakiwa wadogo. “Sijui nikimwambia atanielewaje? Lakini naogopa,” Aidan aliwaza wakati wakiendelea kujisomea. Huo ukawa mwanzo wa mateso ndani ya moyo wake kwani hakuwa na ujasiri wa kumueleza kilichokuwa ndani ya mtima wake. Kila alipotaka kufumbua mdomo wake na kumueleza Caro kilichokuwa ndani ya moyo wake, ulikuwa mzito mno. Siku zikazidi kusonga mbele huku akijitahidi kuonyesha kwa vitendo namna alivyokuwa anampenda na kumhitaji kwenye maisha yake. Hata hivyo, kila alichokuwa anakifanya kwa Caro, msichana huyo alikuwa akichukulia kama ni upendo wa kawaida waliozoeshana tangu wakiwa wadogo. Kwa kadiri alivyokuwa anazidi kuwa mkubwa ndivyo Caro alivyozidi kupendeza. Uzuri wake wa asili, rangi ya ‘keki’ aliyojaliwa, tabasamu pana lililoupamba uso wake kila mara, umbo lake lililojengeka vizuri na ‘vifuu’ vilivyochomoza kifuani kwake kama michongoma, zilikuwa ni sifa zilizofanya karibu kila mtu atamani kuwa karibu na Caro. Hata hivyo, wavulana wengi shuleni pale hawakupata hata nafasi ya kumsogelea kwani kila mara Aidan alikuwa pembeni yake. Kijana huyo naye aliendelea kuteseka ndani ya moyo wake kutokana na kushindwa kueleza kilichokuwa ndani ya moyo wake. Kitu pekee alichoweza kukifanya kila siku ni kuandika katika ‘notebook’ yake jinsi alivyokuwa anampenda Caro, rafiki yake kipenzi tangu wakiwa watoto. Kila alipokuwa anakwenda, notebook hiyo ilikuwa mfukoni. Kila siku akawa anaandika jinsi anavyompenda msichana huyo mpaka kurasa zikakaribia kujaa. Baada ya kukaa shuleni kwa kipindi kirefu, hatimaye muda wa likizo uliwadia kwani walikuwa wakisoma shule ya bweni. Wakaanza kufungasha nguo zao kwenye mabegi yao ya kisasa, kila mmoja akiwa bwenini kwake. Kwa kuwa wazazi wao walikuwa wakielewana sana, walikubaliana kwamba baba yake Aidan, mzee Kenan Twalipo aende kuwachukua wote wawili kwa kutumia gari lake, jambo ambalo alilifanya. Akaendesha gari lake mpaka shuleni, Maritime Secondary School ambapo aliwakuta mwanaye Aidan na Carolina wakimsubiri kwa shauku. Walipomuona, walimkimbilia na aliposhuka kwenye gari walimkumbatia kwa furaha. “Naona maisha ya hapa shuleni yamekuwa mazuri sana, mnakua vizuri kama mapacha,” alisema mzee Kenan na kuwafanya wawili hao wacheke kwa furaha. Aidan akapakiza mizigo kwenye buti la gari na wakati akiendelea kufanya kazi hiyo, alichomoa notebook yake aliyokuwa akitembea nayo mfukoni na kuichomeka kwenye begi la Caro bila mwenyewe kujua. Safari ya kurudi nyumbani ikaanza.
Wakiwa njiani, Mzee Kenan alikuwa akiwatania mambo mbalimbali, hali iliyowafanya njia nzima wawe wanacheka kwa furaha. Baada ya muda, wakawasili mtaani kwao. Ilibidi wampitishe kwanza Carolina nyumbani kwao. Gari liliposimama, Aidan ndiyo alikuwa wa kwanza kuteremka, akaenda kumsaidia Caro kuteremsha mizigo yake na kuiingiza ndani, wazazi wake wakatoka na kuwalaki wote wawili kwa furaha kubwa. Baadaye, Aidan alirudi garini na kuondoka na baba yake mpaka nyumbani kwao ambako alipokelewa kwa furaha na mama yake. Baada ya kutumia muda mrefu kusalimiana na kusimuliana yaliyotokea wakati akiwa shuleni, baadaye Aidan alienda kuoga kisha akaingia chumbani kwake kupumzika. Alipojilaza kitandani kwake, mawazo juu ya namna alivyokuwa akiteseka kwa penzi la Caro yalianza kujirudia ndani ya kichwa chake. Akawa anawaza mbinu nyingine atakayoitumia iwapo ile ya kumuwekea ‘diary’ kwenye begi lake itashindikana. “Nitakunywa pombe ili kutoa aibu kisha nitamueleza ukweli,” aliwaza Aidan akiwa amelala pale kitandani, wazo hilo akaona litafaa zaidi kwani alishawahi kusikia kwamba mtu akinywa pombe, anakuwa hana aibu hivyo anaweza kuzungumza au kufanya chochote bila hofu. Upande wa pili, baada ya Caro kusalimiana na wazazi wake na kusimuliana mambo mbalimbali yaliyotokea wakati akiwa shuleni, aliambiwa akaoge kisha apumzike kwani alionesha kuchoka. Akaenda bafuni kuoga kisha akarudi chumbani kwake ambapo kabla ya kupumzika, aliamua kupanga vitu vyake vizuri. Akafungua begi lake na kuanza kutoa nguo, vitabu, madaftari na vifaa vingine alivyotoka navyo shuleni. Wakati akiendelea na kazi hiyo, alishtuka kuona diary ambayo aliitambua haraka kuwa ni ya Aidan. “Ooh! Amesahau diary yake, ngoja nikipumzika nitampelekea,” Caro alijisemea kisha akaiweka juu ya droo ya kitanda chake, akaendelea kutoa vitu vyote mpaka alipomaliza, akavipanga kila kimoja sehemu yake kisha akarudi kitandani na kujilaza. Japokuwa alikuwa na uchovu, usingizi haukumjia haraka, akaanza kutafakari mambo mbalimbali aliyokutana nayo shuleni kwa kipindi chote alichokuwa masomoni. “Hivi kwa nini siku hizi Aidan ananiangalia sana usoni na kunisifia kwamba mimi ni mzuri? Kwani nimebadilika nini?” alijiuliza Caro huku akisimama na kusogea kwenye ‘dressing table’ kubwa iliyokuwa ndani ya chumba chake, akaanza kujitazama kuanzia juu hadi chini, akawa anajigeuzageuza kama mwanamitindo, mwisho akaishia kutabasamu. “Ana haki ya kunisifia, mimi ni mzuri kwelikweli,” alisema Caro na sura yake kupambwa na tabasamu pana, akawa anatembea taratibu kurudi kitandani kuendelea kupumzika. Macho yake yakatua juu ya diary (kitabu cha kumbukumbu) ya Aidan iliyokuwa juu ya droo ya kitanda chake, akaitazama kwa muda kama anayejishauri kitu, akaamua kuachana nayo na kupanda kitandani, akaukumbatia mto wake na kuendelea kujigeuzageuza huku maneno ya Aidan kumsifia yakijirudiarudia kichwani mwake. “Lakini hata yeye ni mzuri, mwili wake umejengeka vizuri na anavutia sana. Ngoja nimuandikie kwenye diary yake ili ije kuwa kama ‘sapraiz’ kwake siku akiiona,” aliwaza Caro na kuinuka, akachukua kalamu na ile diary ya Aidan, akarudi kitandani huku akiendelea kutabasamu, akaanza kuifungua. “A diary of my love to Caro!” (Kitabu cha kumbukumbu za penzi langu kwa Caro!) ulisomeka ukurasa wa kwanza wa diary hiyo, moyo wa Caro ukalipuka na mapigo yake kuanza kumwenda mbio. Alirudia kuyasoma maandishi hayo zaidi ya mara tatu akihisi kwamba huenda amekosea kusoma lakini bado hali ilikuwa ni ileile. Alishusha pumzi ndefu na kufungua ukurasa wa pili, alichokiona kilimfanya apigwe na butwaa akiwa ni kama hayaamini macho yake. Aidan alikuwa ameandika mambo mengi kuhusu yeye na Caro, akielezea ni jinsi gani alivyokuwa anampenda tangu wakiwa wadogo. “Nilimpenda kama dada yangu na rafiki tangu tukiwa wadogo, lakini sasa nahisi mawazo yangu yanabadilika kwa kasi kila kukicha. Nataka awe mpenzi wangu lakini kumwambia siwezi, nitaendelea kuteseka…” ilisomeka sehemu ya maandishi aliyokuwa ameyaandika Aidan kwenye ukurasa huo. Caro alifikicha macho yake akihisi huenda alikuwa ndotoni, akashusha tena pumzi ndefu na kuendelea kusoma. Alipomaliza alifungua ukurasa mwingine ambapo napo alikutana na maelezo marefu kutoka kwa Aidan akielezea jinsi alivyokuwa anampenda. Aliandika mambo mengi ya kumsifia huku akijiwekea nadhiri kwamba siku atakayopata ujasiri, atamweleza ukweli unaomtesa ndani ya nafsi yake. Caro aliendelea kufunua ukurasa mmoja baada ya mwingine, akakutana na mashairi ya mapenzi, sifa kemkemu na kila aina ya maneno ya kimahaba, yote yakiwa yameandikwa na Aidan maalum kwa ajili yake. Alijikuta akishindwa kujizua, machozi yakaanza kumlengalenga kwani ilionesha dhahiri kwamba moto mkali wa mapenzi ulikuwa ukiwaka ndani ya mtima wake kiasi cha kumfanya ateseke sana. Alijilaza kitandani huku akiendelea kupitia kurasa za diary ile, machozi yakazidi kumtoka. Licha ya kwamba alikuwa akimheshimu kama kaka na rafiki wa tangu utotoni, alijihisi mwenye hatia kubwa kwa kushindwa kuzielewa hisia za Aidan tangu mwanzo kiasi cha kumfanya ateseke kiasi hicho. Aliendelea kuwaza mpaka baadaye usingizi mzito ulipompitia. Alipozinduka, tayari ilikuwa jioni, akili zake zikamtuma kujiandaa haraka na kumfuata Aidan nyumbani kwao kwani hakupenda kuendelea kumuona akiteseka kwa sababu yake. Akaingia bafuni kuoga kisha akarudi na kuanza kujipodoa. Alichagua gauni lake zuri lililomfanya aonekane mrembo mithili ya ndege tausi. Akaongeza bashasha kwa kujipulizia marashi mazuri ya kuvutia. Alipohakikisha amependeza kisawasawa, alitoka kimyakimya bila hata kuaga na kwenda moja kwa moja mpaka nyumbani kwa akina Aidan. “Ooh! Karibu mrembo, karibu sana,” baba yake Aidan, mzee Kenan alimkaribisha Caro kwa bashasha, huku akiwa amevaa taulo tu. Ilionesha kwamba alikuwa ametoka kuoga muda mfupi uliopita. Akamshika mkono na kuingia naye ndani. “Mwenzako bado amepumzika, inaonesha amechoka sana na mama yako ametoka kidogo, jisikie huru,” alisema mzee huyo kwa uchangamfu, huku akiwa amemkazia macho Caro hasa sehemu za usoni na kifuani mpaka msichana huyo mdogo akawa anajisikia aibu. Akawa anamwagia sifa kemkemu huku akijisogeza karibu naye. “VIPI maisha ya shule unayaonaje?” alisema mzee Kenan huku akizidi kujisogeza kwa Caro, kwa kuwa sofa walilokuwa wamekalia lilikuwa ni la watu wawili, Caro hakuwa na ujanja zaidi ya kutulia, mapigo ya moyo wake yakawa yanamuenda kasi kwani alihisi kuna kitu kibaya kinataka kumtokea. “Inabidi mjitahidi kusoma kwa bidii, unajua sisi wazazi wenu tunawategemea sana,” alisema mzee Kenan, safari hii akiwa amemgusa Caro begani, taratibu akaanza kuupitisha mkono wake mgongoni kwa msichana huyo huku akijifanya kuendelea kumpa mawaidha ya kukazania masomo kwani ndiyo ufunguo wa maisha yao. “Kuna zawadi nzuri nilikuwa nimewaandalia, nilitaka mkirudi tu shuleni niwape, twende nikakupe wewe kwa sababu ndiyo umewahi, mwenzako nitampa baadaye,” alisema mzee Kenan huku akimuinua Caro pale kwenye sofa alipokuwa amekaa na kuanza kuelekea naye kwenye chumba cha wageni. Kwa jinsi Caro alivyokuwa anamheshimu mzee Kenan, alimchukulia kama baba yake kiasi kwamba alishindwa kumbishia chochote alichokisema. Huku mapigo yake ya moyo yakimuenda mbio kuliko kawaida, alitii alichoambiwa na mzee Kenan. “Mbona unaonekana unaogopa sana, jisikie huru, unajua tayari umeshakuwa mkubwa wewe, si unajiona mwenyewe,” alisema mzee huyo na kuzigusa nido changa za msichana huyo mbichi, hali iliyomfanya apige ukelele wa mshtuko. “Ooh, samahani, ni bahati mbaya,” mzee Kenan alijibaraguza na kudai kwamba kitendo cha kugusa kifua cha Caro kilikuwa ni cha bahati mbaya. Caro alitingisha kichwa kuonyesha kukubaliana na mzee huyo, akaendelea kumkokota kuelekea chumba cha wageni kama kondoo anayepelekwa machinjioni. *** Aidan aliendelea kuhangaika chumbani kwake, alijitahidi kuutafuta usingizi lakini hakuupata, mawazo juu ya Caro, msichana wa ndoto zake bado yalikuwa yakiendelea kuzunguka kichwani mwake na kumfanya akose utulivu kabisa. Wazo alilolifikiria kwa muda mrefu, lilikuwa ni kutoka na kwenda sehemu yoyote kunakouzwa pombe kisha anywe kidogo kutoa nishai kisha amfuate Caro nyumbani kwao. “Nikifika nitamwambia nina mazungumzo naye, najua lazima atakubali. Tutaenda kwenye bustani ya maua kule nyuma kisha nitajikaza na kumueleza kwamba nampenda sana na nataka awe mpenzi wangu ili baadaye, nimuoe na kujenga naye familia,” aliwaza Aidan na muda huohuo, aliinuka haraka na kusimama nyuma ya kioo kikubwa kilichokuwa chumbani kwake. Akajinyoosha kutoa uchovu kisha akachukua taulo lake na kuanza kuelekea bafuni, alipogusa mlango wa chumba chake tu, alisikia mtu akipiga kelele za kushtuka, kwa kuwa alikuwa anamfahamu vizuri Caro, aliitambua sauti yake. Harakaharaka akarudi chumbani kwake na kuweka taulo sehemu yake, akavaa nguo vizuri na kujitazama kwenye kioo, akachukua marashi mazuri na kujipulizia huku akijitahidi kuvaa uso wa kujiamini. Akatoka akiwa na bashasha ya hali ya juu ya kuzungumza na Caro. Alipofika sebuleni, alishangaa kuuona mkoba mdogo wa Caro ukiwa kwenye sofa, viatu vyake vikiwa pembeni ya mlango. Aligeuka huku na kule lakini hakumuona, ikabidi apaze sauti na kumuita. “Caroo! Caroo!” lakini hakuitikiwa. Sauti hiyo ya Aidan ilimshtua baba yake ambaye ndiyo kwanza alikuwa akifungua mlango ili amuingize Caro kwenye chumba cha wageni, harakaharaka akamuonyeshea ishara Caro ya kutosema chochote kisha akamruhusu arudi sebuleni wakati yeye akinyata kuelekea chumbani kwake, akajifungia mlango huku akijilaumu kwa kushindwa kutimiza alichokuwa anakitaka. Aidan baada ya kutoitikiwa, alifungua mlango na kutoka nje akiamini atamuona Caro lakini hakukuwa na dalili zozote, akarudi ndani. Wakati anaingia, alishtuka kumuona msichana huyo mrembo akitoka upande wa chumba cha wageni, huku akionyesha kuwa na hofu kubwa ndani ya moyo wake. “Nimesikia kama unaniita,” Caro alisema huku akijitahidi kuificha hofu iliyokuwa ndani ya moyo wake.” “Ndiyo, nilikuwa nimepumzika chumbani, natoka naona viatu na mkoba wako ndiyo nikawa nakuita.” “Nilikuwa msalani,” alisema Caro na kukaa palepale alipokuwa amekaa awali. Kwa kuwa Caro alikuwa ameizoea sana nyumba hiyo kiasi cha kuwa mwenyeji, Aidan hakuendelea kumhoji kwani mara kwa mara alikuwa na uwezo wa kuingia ndani hapo hata kama hakuna mtu na akafanya chochote anachokitaka, kama ilivyokuwa kwa Aidan akiwa nyumbani kwa akina Caro. “Nilikuwa nimepumzika kwani bado nahisi uchovu wa kishuleshule,” alisema Aidan huku akikaa vizuri kwenye sofa na kuwasha runinga, wakawa wanatazama muziki huku wakiendelea na mazungumzo ya hapa na pale. Kwa kuwa tayari Aidan alikuwa ameshapanga mipango yake ya namna ya kumfikishia ujumbe Caro, alimuomba watoke nje na kwenda kwenye bustani za maua zilizokuwa nyuma ya nyumba yao, wakatembea taratibu huku Caro akionyesha kuwa na mawazo mengi. “Mbona unaonekana kama haupo sawa Caro,” alisema Aidan huku akimshika begani. Caro alitamani kumweleza kilichokuwa ndani ya moyo wake lakini aliogopa kuwagombanisha Aidan na baba yake, akaamua kuficha siri juu ya tabia mbaya aliyoionyesha baba yake. Akaamua kubadili mazungumzo. “Nimekuletea ‘diary’ yako uliyokuwa umeisahau kwenye begi langu,” alisema Caro huku akimtazama Aidan kwa macho yaliyokuwa na ujumbe, akaitoa diary hiyo na kumkabidhi, Aidan akahisi aibu kubwa ndani ya moyo wake kiasi cha kukwepesha macho yake. “Umeisoma?” “Hapana, wala sijaisoma,” alisema Caro huku akiachia tabasamu pana, akamkumbatia Aidan kwa nguvu, akamnong’oneza: “Pole kwa kuteseka kwa kipindi kirefu kwa ajili yangu.” Aidan alijihisi kama anapaa angani, akazidi kumkumbatia kwa nguvu. Walibaki kwenye hali hiyo kwa dakika kadhaa, Caro aliyekuwa akitazama upande wa nyumba ya akina Aidan, akashtuka baada ya kugundua kuwa kuna mtu alikuwa akiwachungulia kupitia dirishani. Alipomtazama vizuri, aligundua kuwa ni baba yake Aidan, harakaharaka akamuachia huku mapigo ya moyo wake yakienda mbio kuliko kawaida. “Vipi Caro, mbona umeshtuka ghafla?” aliuliza Aidan kwa mshangao lakini Caro hakumjibu kitu. “CARO, si naongea na wewe? Mbona umeshtuka sana?” “Aaah! Samahani akili zangu zilikuwa mbali, unajua nimeondoka nyumbani bila kuaga sasa nahisi mama ananitafuta, ngoja nikamuage kwanza halafu nitakuja tuendelee na mazungumzo yetu,” alisema Caro huku akijitahidi kuvaa tabasamu bandia, harakaharaka akaondoka na kurudi nyumbani kwao. Aidan alibaki amepigwa na butwaa akiwa haelewi nini kilichombadilisha Caro, hata hivyo, alihisi labda ni aibu za kikekike na ugeni katika medani ya mapenzi ndivyo vilivyomsababishia hali ile, akatafuta sehemu nzuri na kukaa huku akiendelea kuangalia mandhari nzuri ya bustani za maua na matunda zilizotunzwa vizuri. ITAENDELEA
Simulizi : The Holy Sin (Dhambi Takatifu) Sehemu Ya Pili (2) Aliendelea kumsubiri kwa hamu Caro arudi kwani hakuna siku aliyokuwa anaisubiri kwa hamu kama siku hiyo. Licha ya kusubiri sana, Caro hakutokea, hali iliyoanza kumpa wasiwasi Aidan. Kwa kuwa nyumbani kwao hakukuwa mbali na hapo, aliinuka na kuchuma waridi jekundu bustanini hapo na kulificha ndani ya shati lake. Akaanza kutembea taratibu kuelekea nyumbani kwa akina Caro. Kwa kuwa urafiki wao ulipitiliza mipaka na kuwa kama ndugu, aliingia kwa uhuru mpaka ndani kwa akina Caro, akakutana na mama yake aliyekuwa akichagua mchele sebuleni. “Mwenzio yupo chumbani kwake amepumzika, anasema anajisikia vibaya,” alisema mama yake Caro huku akiinuka na kwenda kumuamsha Caro chumbani kwake, alipoamka, aliwapisha sebuleni na kuelekea jikoni kuendelea kuandaa chakula cha jioni. “Caro, upo sawa kweli?” Aidan aliuliza kwa sauti ya upole huku akimsogelea pale alipokuwa amekaa, akatoa ua alilomchumia bustanini na kumsogezea puani ili anuse harufu yake nzuri, Caro akaachia tabasamu hafifu na kulipokea ua hilo. “Ahsante kwa kunijali Aidan, najisikia vibaya mwenzio, sijui nimepatwa na nini kwani hali hii imenitokea ghafla,” Caro alisema huku akiinuka na kwenda kulificha ua alilopewa na Aidan chumbani kwake kwani hakutaka wazazi wake walione akihofia kugundulika kwa uhusiano wao wa kimapenzi ambao ndiyo kwanza walikuwa wanataka kuuanzisha. “Niambie kinachokusumbua Caro, nakuona kabisa haupo sawa au nimekukwaza kwa nilichokwambia? Naomba unisamehe kwani hizo ni hisia za moyo wangu tu,” alisema Aidan kwa upole lakini Caro akatingisha kichwa kuashiria kwamba hakuwa amekwazika na alichomweleza wala alichokisoma kwenye ‘diary’ yake bali alikuwa akijisikia vibaya tu. Akamuomba Aidan amuache apumzike kwa maelezo kwamba anahisi maumivu makali ya kichwa, wakakubaliana kuonana siku inayofuatia. Kwa shingo upande, Aidan akaaga na kuondoka huku akiendelea kuwa na mawazo tele ndani ya kichwa chake. Tangu alipofahamiana na Caro, wakiwa wadogo kabisa, hakuwahi hata mara moja kumwambia kitu kama hicho kwamba amuache apumzike. “Au kwa sababu amejua nampenda? Au hanipendi ndiyo maana ananionyeshea haya yote,” Aidan aliendelea kuwaza wakati akitembea taratibu kurudi nyumbani kwao, kichwa akiwa amekiinamisha, mawazo mengi yakiendelea kukisumbua kichwa chake. Alipofika nyumbani kwao, alipitiliza moja kwa moja mpaka chumbani kwake, kabla hajafungua mlango, alisikia baba yake akimuita. Ikabidi arudi sebuleni kumsikiliza. “Unaonekana haupo sawa, nini tatizo?” “Aaah! Hamna kitu baba,” Aidan alijaribu kuficha hisia zilizokuwa zinautesa moyo wake, baba yake akamkazia macho usoni. “Nahisi umeanza kujihusisha na mambo ya mapenzi katika umri mdogo. Nakusihi kwa upole kama ni kweli, bora uache kabisa kwani tumepoteza fedha nyingi kukusomesha, tunategemea utalipa fadhila kwa kuelekeza nguvu zako kwenye masomo na si vinginevyo, nadhani umenielewa,” alisema baba yake Aidan, mzee Kenan kwa msisitizo huku akionyesha kutokuwa na hata chembe ya masihara. Aidan hakujibu kitu zaidi ya kujiinamia, baba yake alipomaliza kumsomea risala yake aliondoka taratibu na kwenda kujifungia chumbani kwake. “Amejuaje kwamba mimi nimeanzisha uhusiano wa kimapenzi na Caro? Au ndiyo sababu Caro amechanganyikiwa?” alijiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu. Ni kweli alichokisema baba yake kilikuwa na maana kubwa kwake lakini moyo wake ulikuwa unazungumza lugha nyingine kabisa. Hakuwa tayari kulipoteza penzi hilo ambalo sasa alikuwa na uhakika nalo, hasa baada ya Caro kufahamu hisia zilizokuwa ndani ya moyo wake. Jioni hiyo ilikuwa ngumu sana kwake, aliwaza mpaka akapoteza hamu ya kula, akalala na njaa. Kwa upande wa Caro, naye alikosa raha kabisa kutokana na mambo yaliyotokea siku hiyo. Awali alikuwa na furaha kubwa ndani ya moyo wake baada ya kugundua kuwa kumbe Aidan alikuwa akimpenda. Alifurahi kwa sababu alikuwa akimjua vizuri na zaidi alivutiwa na tabia zake nzuri alizozionyesha tangu alipokuwa mdogo. Furaha yake ikazidi kwa kuwa walikuwa wakifahamiana mno, kuanzia wao wenyewe mpaka familia zao. Hata hivyo, furaha hiyo ilidumu kwa muda mfupi, kumbukumbu za vitendo vya kidhalilishaji alivyovifanya baba yake Aidan, mzee Kenan ikiwemo kumgusa kifuani na kumkokota mpaka chumbani huku akionyesha waziwazi jinsi alivyokuwa na uchu wa mapenzi, zilimkosesha kabisa raha msichana huyo mdogo. Kila alipotafakari cha kufanya, alikosa majibu, akaendelea kuteseka kwa mawazo mpaka usiku sana. Kama ilivyokuwa kwa Aidan, na yeye hakula chakula cha usiku siku hiyo, akisingizia kuwa anaumwa. Kesho yake kulipopambazuka, alikuja na wazo jipya, akaona njia pekee ya kuondokana na matatizo hayo, ni kusafiri na kwenda kijijini kwa babu na bibi yake ambako alipanga kwenda kumalizia likizo yake. Wazazi wake walishangazwa na safari hiyo ya ghafla aliyoipanga binti yao lakini kutokana na mapenzi ya dhati waliyokuwa nayo kwake, walikubaliana naye. Hakutaka kumuaga Aidan kwani alijua hawezi kukubali kirahisi aende mbali naye, akajiandaa kimyakimya mpaka alipokuwa tayari. Wakati wazazi wake wakiwa wanajiandaa kumsindikiza Ubungo ambako angepanda basi la kumpeleka kwa bibi na babu yake, mzee Kenan alisimamisha gari lake nje ya nyumba yao na kuteremka kwenda kuwasabahi kama ilivyokuwa kawaida yao. Walipomueleza kuwa wanamsindikiza Caro Ubungo anayetaka kusafiri, mzee Kenan aliwaambia imekuwa bahati nzuri kwani na yeye anaelekea Ubungo hivyo badala ya kuchoma mafuta kwenye gari lao, ni bora yeye ndiyo ampeleke. Awali Caro alitaka kukataa lakini akahofia kuonyesha picha mbaya kwa wazazi wake, kwa shingo upande akakubali kuongozana na mzee Kenan. Akaagana na wazazi wake kisha akapanda kwenye gari na kukaa pembeni ya mzee huyo, safari ya kuelekea Ubungo ikaanza huku kila mmoja akiwa kimya. WAKATI safari ikiendelea, licha ya kuwa bize kubadili gia na kunyoosha usukani, baba yake Aidan alikuwa akitumia muda mwingi kumtazama Caro usoni kiasi cha kumfanya msichana huyo mdogo kuanza kuona aibu za kikekike. Macho yao yalipogongana, Mzee Kenan hakusema chochote zaidi ya kuachia tabasamu lililokuwa na ujumbe ndani yake. “Mungu wangu, hata sijui itakuwaje,” aliwaza Caro huku akijifanya kutazama nje kupitia kioo cha pembeni. Muda mwingine, mzee huyo alikuwa akibadili gia kwa nguvu na kusababisha mkono wake uguse mapaja ya msichana huyo ambaye kiumri alikuwa sawa na mwanaye wa kumzaa. “Tutasimama kidogo kwenye lile duka pale kuna zawadi nataka nikakununulie kabla hujaondoka,” alisema mzee huyo huku uso wake ukiwa umejawa na tabasamu. Caro alitingisha kichwa kuashiria kukubaliana na alichoambiwa na mzee huyo aliyekuwa anamheshimu kama baba yake na mtu wa karibu wa familia yao. Mzee huyo alipunguza mwendo na kuwasha ‘indiketa’ upande wa kushoto, akatoka nje ya barabara ya lami na kusimama mbele ya duka moja kubwa lililokuwa linasifika kwa kuuza nguo za kisasa. “Nisubiri nakuja sasa hivi,” alisema mzee Kenan wakati akishuka kwenye gari, harakaharaka akaingia ndani ya duka hilo. Baada ya dakika kadhaa, alitoka akiwa na mfuko mdogo uliokuwa na vitu ndani yake. Akaingia kwenye gari na kumpa Caro. “Utaenda kufungua ukiwa peke yako, hizi ni zawadi zangu kwako, napenda siku moja nikuone ukiwa umependeza,” alisema mzee Kenan. Bila hata kujua kilichokuwa ndani ya mfuko huo, Caro akapokea na kushukuru kwa adabu, akauchanganya kwenye mizigo yake aliyokuwa anasafiri nayo. “Samahani, kabla sijakufikisha Ubungo naomba tupitie kwenye Hoteli ya The Paradise kuna rafiki yangu namdai fedha zangu kaniambia nimpitie anipe, unaweza kupata na wewe kidogo za kukusaidia ukiwa safarini,” alisema mzee Kenan. “Hatutachelewa kweli baba? Maana muda wa basi kuondoka umekaribia.” “Wala usiwe na wasiwasi, wala hatuchelewi,” alisema mzee huyo, Caro akakubaliana naye lakini tayari kengele ya hatari ikianza kulia ndani ya kichwa chake. Mfululizo wa matukio yaliyokuwa yanatokea kati yake na mzee huyo, ulimtia shaka juu ya usalama wake. Hata hivyo alipiga moyo konde na kuendelea kutulia aone mwisho wake. Ukimya ukapita kati yao, walipokaribia Ubungo, mzee huyo kama alivyosema, alikata kona na kutoka kwenye barabara ya lami, akaongeza mwendo kuelekea The Paradise Hotel. Akiwa kwenye kasi kubwa, gari likaanza kuyumbayumba huku likitaka kutoka nje ya barabara hiyo ya vumbi. “Daah! Mkosi gani tena huu.” “Kwani vipi tena baba?” “Sijui nimekanyaga misumari? Matairi yote ya mbele yamepata pancha,” alisema mzee Kenan huku akiendelea kuhangaika kulidhibiti gari lililokuwa linayumbayumba, akapunguza mwendo na kufanikiwa kusimama salama kando ya barabara. “Sasa si nitachelewa baba? Naomba nikodi hata teksi tafadhali,” Caro alisema baada ya kuona huo ndiyo mwanya pekee wa kumkimbia mzee Kenan, baba wa rafiki yake wa tangu utotoni, Aidan. Mzee huyo alifikiria kwa muda, bila kujibu kitu akateremka na kuangalia jinsi matairi ya mbele yalivyoharibika, akajilaumu sana. Hakuwa na cha kufanya zaidi ya kumsimamishia Caro teksi na kumuelekeza dereva ampeleke Ubungo. Wakaagana huku Caro akimshukuru Mungu wake kwani hakujua mzee huyo alikuwa amepanga kufanya jambo gani ndani ya kichwa chake, hasa kutokana na vituko vya kimapenzi alivyokuwa anamfanyia bila kujali kwamba ni sawa na mwanaye wa kumzaa. Harakaharaka Caro akateremsha mizigo yake na kusaidiana na dereva teksi kuipakiza kwenye gari, wakaondoka huku mzee Kenan akimsindikiza Caro kwa macho mpaka teksi ilipopotea kwenye upeo wa macho yake. Akachukua simu na kumpigia fundi wake kwa ajili ya kuja kumbadilishia matairi kwenye gari lake. Caro alifika Ubungo muda mfupi baadaye, alikwenda moja kwenye ofisi za basi alilokata tiketi. Harakaharaka akasaidiwa kupelekwa kwenye basi hilo ambalo lilikuwa limebakiza muda mfupi kabla ya kuondoka. Ni mpaka alipoingia ndani ya basi na kukaa kwenye siti yake ndipo alipoamini kwamba yupo salama, akashusha pumzi ndefu na kumshukuru Mungu wake. Safari ilianza huku kichwani akiwa na mawazo tele juu ya kila kitu kilichokuwa kinaendelea kwenye maisha yake. Safari ya kuelekea Morogoro, nyumbani kwa bibi na babu waliomzaa mama yake ikaendelea. Baada ya saa kadhaa, tayari basi lilikuwa limeshafika Morogoro, akateremka kwenye Kituo cha Mabasi cha Msamvu na kupanda ‘kipanya’ kilichompeleka mpaka Kihonda ndanindani, nyumbani kwa bibi na babu yake. Bibi na babu yake ambao licha ya umri wao mkubwa walikuwa wakiishi maisha ya kisasa, wakiwa karibu na kila muhimu kwenye himaya yao, walimpokea Caro kwa furaha na kumkaribisha nyumbani hapo. Baada ya kusalimiana na kupeana michapo ya hapa na pale, walimuandalia Caro maji ya kuoga kisha akaandaliwa chakula maalum kwa ajili yake mgeni. Baada ya kula, aliomba kupumzika kutokana na uchovu wa safari ambapo alipelekwa kwenye chumba cha wageni. Akajitupa kitandani na kutulia kwa muda, mawazo juu ya Aidan yakaanza kumjia kwa kasi. Akawa anakumbuka mambo mbalimbali waliyoyafanya pamoja tangu wakiwa wadogo, akaishia kutabasamu mwenyewe. Aliendelea kutafakari mambo mbalimbali kuhusu jinsi urafiki wao ulivyokuwa umeshamiri na hatua waliyokuwa wamefikia ya kutaka kuvuka mipaka ya ukaka na udada waliyojijengea tangu wakiwa wadogo na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi. “Nampenda sana Aidan, yeye ndiyo atakuwa mwanaume wangu wa kwanza na wa mwisho, tukimaliza shule nataka anioe nimzalie watoto wazuri kama mimi,” Caro aliwaza huku akijigeuzageuza pale kitandani, uso wake ukiwa umejawa na tabasamu pana. Ghafla alikumbuka kitu kilichoitibua furaha yake; mzee Kenan na vituko vya kimapenzi alivyokuwa anamfanyia. Akakumbuka kuhusu zawadi alizomnunulia muda mfupi kabla hajasafiri, akashikwa na shauku ya kutaka kuziona zawadi zenyewe. Akainuka na kwenda kwenye mizigo yake, akachukua mfuko aliopewa na mzee Kenan, akaenda nao kitandani na kuanza kuufungua. “Haaa! Hivi vitu gani tena?” Caro alipigwa na butwaa baada ya kuanza kuufungua mfuko huo, akiwa ni kama haamini alichokiona. Alirudia kutazama mara mbilimbili huku macho yakiwa yamemtoka kama mjusi aliyebanwa na mlango. Mzee Kenan alikuwa amemnunulia zawadi ya nguo kadhaa za ndani zikiwa na ujumbe wa kimapenzi pamoja na mkufu wa dhahabu ambao ulionekana kuwa tofauti na ile ya kuvaa shingoni. Hakuyaamini macho yake, akajikuta akiuachia mfuko huo, ukadondoka chini kisha akajishika tama akitafakari kwa kina mzee huyo ambaye kwake alikuwa ni sawa na baba yake, alikuwa na maana gani kumfanyia kitendo kama hicho. LIJIKUTA akizama kwenye dimbi la mawazo kwa kipindi kirefu, akitafakari kwa kina afanye nini ili kuukwepa mtego hatari uliokuwa mbele yake. Kuna wakati alipata wazo kwamba ili kumkomoa mzee huyo, dawa yake ni kuwaeleza ukweli wazazi wake juu ya kila kitu kilichokuwa kinaendelea. Hata hivyo, akili nyingine ilimtuma kuwa asifanye hivyo kwani hiyo ingemaanisha kuvunja kabisa urafiki uliovuka mipaka na kuwa kama undugu, baina ya familia hizo mbili. Pia alitamani kumueleza Aidan lakini akili nyingine ikamzuia kwani kufanya hivyo ilikuwa ni kuwagombanisha mtu na baba yake, jambo ambalo hakutaka litokee. Licha ya kufikiria kwa muda mrefu, bado hakupata jibu la moja kwa moja, akaamua kuendelea kukaa na siri hiyo ndani ya kichwa chake. *** Aidan alishtushwa na taarifa za msichana aliyetokea kumpenda tangu wakiwa wadogo, Caro kufunga safari ya ghafla na kuondoka bila hata kumuaga, muda mfupi tu baada ya kumweleza ukweli uliokuwa ukimtesa ndani ya moyo wake. “Kwani hajakuaga?” “Wala hajaniaga ndiyo maana nashangaa, siyo kawaida yake kabisa.” “Hata sisi wenyewe tulishangaa kwani safari ilikuwa ya ghafla mno na aling’ang’ania kweli, ikabidi tumruhusu kwani hatukutaka kumuudhi,” mama mzazi wa Caro alikuwa akizungumza na Aidan ambaye baada ya kusikia taarifa hizo, ilibidi aende kupata uhakika kwa mama yake. “Amesema atarudi nini?” “Mh! Wala hatujui lakini inawezekana likizo yote akakaa hukohuko kwa bibi yake.” Majibu hayo yalimmaliza kabisa nguvu Aidan, akaondoka akiwa mnyonge na kwenda kukaa kwenye bustani ya maua, mawazo mengi yakikisumbua kichwa chake. Alipowaza kwa kina, alihisi lazima kuna tatizo linalomsumbua Caro ingawa alishindwa kuelewa ni tatizo gani kwani alikuwa na mabadiliko ya ghafla. Alijaribu kujikagua matendo yake akihisi huenda yeye ndiye aliyemkwaza Caro lakini hakugundua kosa lolote alilolifanya. Akaendelea kuzama kwenye dimbwi la mawazo machungu mpaka machozi yakawa yanamtoka. “Mbona umejiinamia hapa kwa muda mrefu? Kuna tatizo?” “Hapana baba, hakuna tatizo lolote,” alisema Aidan huku akijifuta machozi, akitaka baba yake ambaye ndiyo alikuwa akirejea muda huo asigundue chochote. “Unanificha? Unajua siku hizi umekuwa na tabia za ajabuajabu sana?” baba yake Aidan, mzee Kenan alianza kufoka. Aidan alishindwa kuelewa kwa nini baba yake anakuwa mkali kwake bila sababu, hata hivyo hakumjibu kitu zaidi ya kuendelea kujiinamia. “Badala ya kujisomea ndani una kazi ya kulialia tu, najua hiyo yote ni kwa sababu unawaza mapenzi badala ya masomo, na kwa taarifa yako lazima nikuhamishe ile shule unayosoma,” alisema mzee huyo na kuondoka, akamuacha Aidan kwenye lindi lingine la mawazo. Kuhamishwa shule kulimaanisha kumtenga mbali na kipenzi cha moyo wake, Caro, jambo ambalo hakuwa tayari kuona linatokea. Akajilazimisha kuchangamka ambapo aliondoka na kwenda kuchukua madaftari yake, akakaa sebuleni na kujifanya anasoma ili kumfurahisha baba yake. Hakutaka kabisa kuhamishwa shule. Siku zilizidi kusonga mbele, hatimaye likizo ikawa inaelekea ukingoni huku Aidan akijitahidi kwa kadiri ya uwezo wake kumfurahisha baba yake ili asimhamishe shule. Jioni moja, Aidan akiwa anajisomea sebuleni kwao, alishtuka baada ya kusikia sauti kama ya Caro mlangoni kwao akibisha hodi. Harakaharaka akaacha kila alichokuwa anakifanya na kwenda kufungua mlango, hakuamini macho yake kumuona Caro, akiwa amenawiri vizuri na kuzidi kuwa mrembo. Kwa jinsi alivyokuwa amemkumbuka, alimkumbatia kwa nguvu na kumbeba juujuu mpaka sebuleni. Wakaangushana kwenye sofa huku kila mmoja akiwa na furaha ya ajabu. Wakaendelea kukumbatiana kwa muda huku wakimwagiana mabusu mfululizo. “Kwa nini uliondoka bila kuniaga mpenzi wangu?”“Nisamehe sana Aidan, kuna jambo lilinilazimisha kufanya hivyo lakini elewa kwamba nilifanya kwa sababu ya upendo wangu kwako,” alisema Caro huku akiwa bado amekumbatiana na Aidan, akaendelea kumuomba msamaha kwa kitendo hicho na kumhakikishia kwamba anampenda sana. “Kweli unanipenda Caro?” “Nakupenda sana Aidan, kutoka ndani ya moyo wangu! Wewe ndiye mume wangu na baba wa wanangu watarajiwa, tukimaliza shule nataka unioe,” alisema Caro huku akimtazama Aidan kimahaba, kauli iliyomfurahisha sana Aidan. Wakaendelea kuzungumza mambo mengi huku kila mmoja akiwa na furaha kubwa ndani ya moyo wake. Wakatoka wakiwa wameshikana mikono na kwenda kwenye bustani za maua, walipozoea kucheza tangu wakiwa wadogo. Wakawa wanacheza kama watoto wadogo, kila mmoja akiwa na furaha. Baadaye wakakaa sehemu tulivu na kuendelea kuzungumza mambo yao. “Aidan! Aidan,” sauti ya mzee Kenan ilisikika kwa nguvu kutokea ndani kwao, harakaharaka akainuka na kumuacha Caro pale bustanini kwa ajili ya kwenda kumsikiliza baba yake. “Umeanza kuingiza wanawake hapa ndani kwangu si ndiyo? Huu mkoba wa kike ni wa nani?” mzee huyo aling’aka huku akimuonyesha mwanaye mkoba alioukuta kwenye sofa. “Ni wa Caro, sijaingiza mwanamke yeyote baba.” “Ni wa Caro? Kwani amesharudi? Yuko wapi? Hebu kamuite,” maneno yalimtoka mfululizo mzee huyo, ile sura ya ukali ikayeyuka ghafla na tabasamu likaanza kuchanua usoni kwake. Harakaharaka alitoka na kwenda mpaka pale bustanini alipomuacha Caro, akamwambia kwamba baba yake anamuita. Tofauti na alivyotegemea, Caro hakuonyesha kufurahia wito huo, akainuka kwa kujilazimisha huku lile tabasamu alilokuwa nalo tangu alipofika likiyeyuka. Walipoingia tu, alimpokea kwa uchangamfu na kuanza kumuuliza habari za alikotoka. “Aidan nenda dukani kaninunulie vocha,” alisema mzee huyo kama gia ya kumtoa Aidan na kumfanya abaki peke yake na Caro. Alipotoka, alisogea kwenye sofa alilokuwa amekaa Caro na kuanza kuzungumza naye kwa upole kwani alionyesha hayupo sawa. “Vipi zawadi zangu nilizokupa siku ile ulizifurahia?” ITAENDELEA
Simulizi : The Holy Sin (Dhambi Takatifu) Sehemu Ya Tatu (3) BADALA ya kujibu, Caro alijiinamia huku aking’atang’ata kucha kwani alikuwa akihisi aibu kubwa kwa mtu anayemheshimu kama baba yake, kumpa zawadi za aina hiyo. “Naongea na wewe Caro! Mbona hunijibu mama,” alisema mzee huyo akijisogeza na kumshika begani msichana huyo, akazidi kujisogeza kiasi cha kuanza kusikia pumzi na mapigo ya moyo ya msichana huyo mbichi. Kwa upande wa Aidan, alipotumwa na baba yake aliona kama amevurugiwa furaha yake ya kukaa jirani na Caro, akatoka mbiombio na kwenda dukani huku akikimbia, muda mfupi baadaye tayari alishapata vocha alizotumwa, akarudi mbio nyumbani kwao kwa lengo la kumuwahi Caro wake. Kwa jinsi alivyokuwa na haraka, aliingia ndani kwa kasi, akakutana na picha ambayo hakuitegemea. Baba yake alikuwa amekaa jirani mno na Caro, mkono mmoja akiwa amemshika begani huku msichana huyo, kipenzi cha moyo wake akiwa amejiinamia, aking’atang’ata kucha zake. “Vipi umepata? Nilikuwa nampa ushauri mwenzako hapa juu ya kukazania masomo, sitaki mje kututia aibu hapo baadaye kama ninavyokwambiaga kila siku,” mzee huyo alijivunga na kusimama, akapokea vocha na kuondoka kuelekea chumbani kwake. Aidan alibaki bado ameduwaa kwani japokuwa familia hizo mbili zilikuwa zimezoeana sana, hakuwahi hata siku moja kuona kitendo kama hicho, maswali mfululizo yakaanza kupita ndani ya kichwa chake kiasi cha kumfanya ajihisi kama amebeba mzigo mzito kichwani mwake. “Kwani baba alikuwa anakwambia nini?” Aidan aliuliza huku bado akiwa ameduwaa, Caro akashindwa cha kujibu zaidi ya kuchukua mkoba wake na kusimama, usoni akionyesha kukosa kabisa raha. Akawa anataka kutoka nje lakini Aidan alimzuia na kumkalisha kwenye sofa akitaka kujua kilichotokea.
Wakiwa katika hali hiyo, mama yake Aidan ambaye muda mwingi alikuwa akiutumia kazini, aliingia na kuwakuta wanaye wamekaa sebuleni. Kwa kuwa zilikuwa zimepita siku nyingi bila kuonana na Caro, alimkumbatia kwa furaha na kumuuliza habari za safari. Ile furaha iliyokuwa imetoweka kwenye moyo wa Caro, ilirejea ghafla, akatabasamu na kuanza kumsimulia mama yake Aidan mambo yote yaliyotokea akiwa safarini. Baada ya kuridhika, mama yake Aidan aliwaacha wanaye sebuleni, akaenda chumbani kuungana na mumewe. Hata hivyo, Caro hakutaka kuendelea kukaa sebuleni hapo, akamtaka Aidan amsindikize nyumbani kwao na kama ni kupiga stori, wakapigie hukohuko. Bado hakuwa tayari kueleza chochote kilichotokea wakati alipobaki peke yake na baba yake Aidan. Siku hiyo ilipita, baada ya siku kadhaa mzee Kenan alikuja na hoja mpya ya kujifanya anataka kuwapeleka Aidan na Caro ufukweni kupunga upepo wa bahari. Awali Caro alikataa kabisa ofa hiyo mpaka mama yake akawa anamshangaa lakini alipohakikishiwa kwamba watakuwa na Aidan, alikubali kwa shingo upande. Hatimaye Jumamosi ikawadia, siku ambayo walipanga kwenda ufukweni. Japokuwa mkewe hakwenda kazini siku hiyo, mzee Kenan hakutaka kuongozana naye ufukweni pamoja na Aidan na Caro kwa madai kuwa siku hiyo ilikuwa maalum kwa ajili ya watoto wao, yeye asubiri siku yake. Kwa kuwa alikuwa akimuamini sana mumewe, alikubali na kushiriki kuwaandalia vitu vyote muhimu. Wakaondoka kwa gari la familia na kwenda mpaka Msasani Beach, sehemu ambayo mzee huyo alikuwa anapendelea kwenda kupumzika. Baada ya kufika ufukweni, mzee Kenan alijifanya ana mambo yake, akawaacha Aidan na Caro wastarehe wanavyotaka, wakaenda kuogelea na kucheza mchangani huku mzee huyo akiwa amekaa pembeni akinywa pombe kali kama kawaida yake. Aidan na Caro waliendelea kufurahi ingawa bado moyo wa Caro haukuwa na furaha kutokana na uwepo wa mzee huyo kwani alijua chochote kinaweza kutokea wakati wowote. “Aidan! Aidan hebu njoo mara moja,” alisema mzee huyo kwa sauti iliyoonyesha kuwa tayari pombe zilishaanza kumkolea kichwani. “Mama yako amenipigia simu anasema amepata dharura inayohitaji fedha na kadi ya benki nimetembea nayo mimi, hebu chukua Bajaj umpelekee mara moja, utatukuta hapahapa,” alisema mzee Kenan kwa sauti ya kilevi, kengele ya hatari ikalia ndani ya kichwa cha Caro. “Nitaenda naye baba, wala hatutakawia,” alisema msichana huyo, wazo lililopingwa vikali na mzee Kenan kwa madai kuwa wakiongozana wote, watachelewa kufika. Mvutano uliendelea lakini mzee huyo aliendelea kushikilia msimamo wake, Aidan na Caro wakawa hawana cha kufanya zaidi ya kukubaliana na maagizo hayo. Akatoa kadi ya benki pamoja na nauli ya Bajaj na kumkabidhi Aidan huku akimsisitiza awahi kurudi, akaondoka kwa shingo upande na kuwaacha na Caro. Muda mfupi baada ya kuondoka, mzee Kenan alisogea pembeni na kumpigia simu mkewe, akamwambia kwamba amemtuma Aidan ampelekee kadi ya benki ili aihifadhi kwani anaogopa kuipoteza kwenye mchanga wa bahari. “Sasa kwa nini usingeiweka kwenye gari? Huoni kama umemsumbua bure mtoto?” alilalamika mama yake Aidan, mzee huyo akamuweka sawa kwa maneno matamu kisha akakata simu. Harakaharaka akaanza kutembea kurudi mahali alikomuacha Caro ambaye bado alikuwa amevaa nguo za kuogelea na kujifunika kwa mtandio mwepesi juu ya nguo hizo. “Umewahi kunywa juisi ya kopo inayoitwa Redds?” “Hapana sijawahi.” “Basi ngoja nikuagizie uionje wakati tunamsubiri Aidan, naamini utaipenda,” alisema mzee huyo huku akimuita mhudumu na kumnong’oneza sikioni. Akaondoka na baada ya muda mfupi, alirudi na sinia lililokuwa na makopo matatu ya Redds pamoja na mzinga mkubwa wa pombe kali aliyokuwa anakunywa mzee huyo. “Yaani ukimaliza hizi zote nitakupa bonge la zawadi, we mwenyewe utafurahi,” alisema mzee huyo wakati akimfungulia Redds moja na kummiminia kwenye glasi, na yeye akafungua mzinga wake na kuanza kunywa taratibu. “Bila kujua kama ile siyo juisi kama alivyoambiwa bali ni bia, Caro aligida glasi ya kwanza mpaka ikaisha huku akiisifia kutokana na ladha yake nzuri. Mzee Aidan akammiminia glasi ya pili na kumpa. Alipoimaliza, tayari alishaanza kubadilika, akawa anachekacheka huku akiyarembua macho yake kama amekula kungu, hali iliyomfurahisha sana mzee huyo. Alipomaliza chupa ya pili, tayari alikuwa tilalila, akamuinua na kuanza kumkokota kuelekea mahali alikopaki gari lake. “Leo ndiyo leo, asemaye kesho mwongo,” alisema mzee huyo huku akijilamba midomo kutokana na uchu aliokuwa nao. ALIPOMFIKISHA kwenye gari, alimpandisha kisha akamfunga mkanda, harakaharaka na yeye akapanda na kuliwasha gari. Akaondoka kwa kasi kuelekea mafichoni kutimiza azma yake. Caro hakuelewa chochote kilichoendelea kwani kutokana na kuzidiwa na kilevi, aliuchapa usingizi mzito. Aidan akiwa ndani ya Bajaj akiwahi nyumbani kumpelekea mama yake kadi ya benki kama alivyoagizwa na baba yake, alishtuka baada ya simu yake kuanza kuita mfululizo. Harakaharaka akaitoa simu yake na alipoangalia namba ya mpigaji, aligundua kuwa ni mama yake. “Haloo mama, nipo njiani nakuja kukuletea kadi ya benki.” “Kwani umefika wapi mwanangu?” “Ndiyo tupo hapa kwenye daraja la Msasani, kuna foleni lakini tutawahi,” Aidan alisema kwa kujihami akidhani mama yake alikuwa akitaka afike haraka nyumbani. Hata hivyo, tofauti na alivyotegemea, mama yake alimwambia kitu tofauti: “Sikia mwanangu, hiyo kadi we itunze utakuja nayo baadaye, rudi ukaendelee kufurahi na mwenzako ufukweni, baba yako akikuuliza mwambie mimi ndiyo nimekwambia urudi.” “Sawa mama, ahsante sana,” alisema Aidan na kumuamuru dereva wa Bajaj apunguze mwendo na kugeuza. Japo dereva alishangazwa na uamuzi wa ghafla wa mteja wake, hakutaka kuhoji sana kwani alichokuwa anakitaka ni fedha tu. Akageuza Bajaj na kuanza kurudi Msasani Beach Club huku Aidan akiwa na furaha ndani ya moyo wake kwani kiukweli japokuwa hakuwa na uwezo wa kubishana na baba yake, hakufurahishwa kabisa na kitendo cha baba yake kumtibulia starehe na kumtuma nyumbani. Akili yake yote ilikuwa kwa Caro, alitamani waendelee kucheza kwenye mchanga na kuogelea baharini, akajikuta akitabasamu wakati Bajaj ikiendelea kupenya kwenye foleni kurudi Msasani. Baada ya kufika kwenye njia panda ya kuelekea ufukweni, wakati dereva wa Bajaj akiiacha barabara ya lami na kuingia ya vumbi, Aidan aliona gari kama la baba yake kwa mbali likielekea upande wa Kawe lakini hakutilia maanani sana akiamini huenda amelifananisha. Baada ya kufika Msasani Beach Club, alimlipa dereva wa Bajaj fedha yake kisha harakaharaka akashuka na kuanza kuelekea upande wa nyuma alikowaacha baba yake na Caro. Cha ajabu, alipofika kwenye meza aliyokuwa amekaa baba yake, alikuta ikiwa tupu, akahisi huenda na yeye ameenda kutembea kwenye mchanga wa bahari. Harakaharaka akatoka kwenye geti na kuelekea baharini lakini Caro hakuwepo pale alipomuacha, akaanza kuangaza macho huku na kule lakini hakumuona Caro wala baba yake. Alirudi ndani na kuendelea kuangaza huku na kule akidhani labda wanaweza kuwa wamehama meza lakini hakufanikiwa kuwaona. “Au lile gari nililoliona kule barabarani kweli lilikuwa la baba? Lakini kwa nini waondoke ghafla wakati tumekubaliana nikirudi nitawakuta hapa?” Aidan alijiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu. Ikabidi aende kwenye meza aliyokuwa amekaa baba yake akiamini wanaweza kuwa hawajaenda mbali, akakaa na kuanza kusubiri huku muda wote akiangaza macho huku na kule. Licha ya kuendelea kusubiri kwa muda mrefu, Aidan hakumuona baba yake wala Caro huku giza nalo likianza kuingia. Hakuwa na cha kufanya zaidi ya kutafuta usafiri wa kumrudisha nyumbani kwao, akili nyingine ikimtuma kuamini kwamba huenda wamepishana na wao wamesharudi nyumbani. Wakati akiondoka, alijaribu kumpigia baba yake simu yake lakini haikuwa ikipatikana hewani, jambo ambalo siyo kawaida yake. Alitamani Caro naye angekuwa na simu ampigie na kumuuliza yuko wapi lakini haikuwezekana kwani msichana huyo alizuiwa na wazazi wake kumiliki simu mpaka atakapokuwa mkubwa. Huku akiwa na mawazo mengi ndani ya kichwa chake, Aidan alienda kupanda Bajaj na kumuelekeza dereva sehemu ya kumpeleka. Furaha yote aliyokuwa nayo siku hiyo iliyeyuka kama theluji iyeyukavyo juani, akaendelea kuwaza kwa muda mrefu mpaka alipowasili nyumbani kwao, akashuka kwenye Bajaj na kumlipa dereva fedha zake, breki ya kwanza ilikuwa nyumbani kwa akina Caro kumuulizia kama amesharudi. “Sasa Aidan, wewe unamuulizia Caro si mliondoka pamoja? Kwani umemuacha wapi mwenzako,” mama yake Caro alimuuliza Aidan huku na yeye akionyesha kupatwa na mshtuko. “Tulipishana kidogo, yeye akaondoka na baba, nadhani watakuwa wamekwama kwenye foleni,” alijibu Aidan kwa kifupi huku akianza kuondoka. Mama yake Caro alimrudisha na kuendelea kumhoji maswali mbalimbali, alipomhakikishia kwamba yupo na baba yake, angalau aliridhika na kumruhusu aondoke. Akatoka na kuelekea nyumbani kwao alikomkuta mama yake akiandaa chakula cha jioni. Nako alikutana na maswali kama yaleyale aliyoulizwa na mama Caro. Mama yake alishangaa kwa nini amerudi peke yake wakati alishamwambia akaendelee kujumuika na Caro na baba yake kisha warudi pamoja. “Tulipishana nao, nafikiri wamekwama kwenye foleni kwa sababu mimi nilipanda Bajaj,” Aidan alijibu kwa kifupi na kwenda chumbani kwake, akajitupa kitandani huku mawazo yakiendelea kukisumbua kichwa chake. Mama yake naye alibaki na mawazo mengi kwani mfululizo wa matukio yaliyokuwa yanatokea tangu jioni, ulimfanya ahisi kuna jambo halipo sawa kati ya Aidan na Caro ingawa hakumuwazia kabisa mabaya mumewe. Muda ulizidi kuyoyoma bila baba Aidan wala Caro kurejea nyumbani, hali iliyoanza kuwapa wasiwasi wazazi wa pande zote mbili. Muda mfupi baadaye, mama na baba Caro wakafika nyumbani kwa akina Aidan kumuulizia binti yao. Kilichowashangaza zaidi ni kwamba wakati Caro alikuwa hafahamiki mahali alipo, Aidan alikuwa chumbani kwake amejifungia, jambo ambalo halikuwa kawaida kwani tangu wakiwa wadogo, walizoea kuongozana popote wanapokwenda na mara zote wazazi wao hawakuwa na wasiwasi wanapokuwa wawili. “Ni saa nne na nusu sasa bado mtoto hajarudi nyumbani, siyo kawaida yake,” alisema mama yake Caro, mumewe naye akakazia lakini mama Aidan aliwatoa wasiwasi kwamba hakuna kitakachoharibika kwa sababu yupo na mzee Kenan. “Au inawezekana wamepata ajali? Foleni gani hiyo muda wote wawe hawajafika nyumbani?” “Hebu ngoja nijaribu kumpigia simu mzee mwenzangu nijue nini kimetokea,” alisema baba yake Caro lakini alipojaribu kumpigia simu mzee Kenan, hakuwa akipatikana hewani, hali iliyozidi kuwachanganya wote. AKAWAAMBIA wazazi wake jinsi alivyopewa juisi za kwenye makopo na mzee Kenan na jinsi alivyoleweshwa na juisi hizo. “Baada ya hapo nini kiliendelea?” “Sikumbuki baba, nilijihisi mwili wote ukiishiwa nguvu na sikuelewa tena kilichoendelea mpaka nilipozinduka na kujikuta nimelala chumbani kwangu.” SASA ENDELEA… “MUNGU wangu, mbona sitaki kuamini macho yangu?” alisema baba yake Caro baada ya kusikia maelezo hayo ya mwanaye, akamgeukia mkewe ambaye alikuwa amejiinamia akilia kwa uchungu. Kwa jinsi walivyokuwa wakiheshimiana na mzee Kenan, hakuna aliyekuwa tayari kuamini kwamba anaweza kumfanyia ukatili huo binti yao ambaye kimsingi ni sawa na mwanaye. Ikabidi wasogee pembeni na kuanza kujadiliana nini cha kufanya, Caro akawa anaendelea kulia.
“Haiwezekani mume wangu, lazima tuchukue hatua, siwezi kukubali mwanangu aharibiwe kirahisi namna hii wakati nimehangaika sana kumlea mpaka amekuwa mkubwa,” alisema mama Caro huku naye akiendelea kulia kwa uchungu.
Uamuzi ambao waliufikia kwa pamoja ilikuwa ni kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi haraka iwezekanavyo. Wakamchukua binti yao na kwenda mpaka kwenye gari lao, wakaingia na kuondoka kuelekea kituo cha polisi. Walipofika waliandikisha maelezo kisha wakapewa fomu maalum kwa ajili ya kwenda hospitali ili Caro akapimwe na daktari ili kuthibitisha kama kweli amebakwa. Wakaondoka pamoja mpaka hospitali. “Baada ya tukio ulienda kuoga?” “Ndiyo dokta.”
“Ulikosea sana kwani umevuruga kabisa ushahidi, itakuwa vigumu kumtia hatiani mbakaji kwani hakuna tena ushahidi, pole sana binti,” alisema daktari wakati akiendelea kumfanyia vipimo Caro. Wazazi wake waliendelea kuhuzunika, kila mmoja macho yakiwa mekundu kutokana na kulia.
Baada ya daktari kumaliza kazi yake, walirudi kituo cha polisi ambapo mipango kwa ajili ya kwenda kumkamata mzee Kenan ilianza. Mkuu wa kituo akatoa gari pamoja na askari watatu kwa ajili ya kwenda kumkamata mzee huyo mwenye roho ya kinyama. *** Mzozo mkubwa uliendelea ndani ya nyumba ya mzee Kenan kati yake na mkewe, wakawa wanalumbana vikali kuhusu tukio lililotokea usiku. Mzee Kenan alikuwa akisisitiza kwamba hakufanya jambo lolote baya zaidi ya kunywa pombe mpaka usiku. “Hujafanya kitu? Hata aibu huna mwanaume wewe.” “Sijafanya kitu kweli mke wangu, mi nilikuwa nakunywa pombe tu.” “Na mtoto wa watu? Yaani umemlewesha mtoto wa watu ili ufanikishe lengo lako, mwanaume muuaji wewe sijapata kuona, nataka talaka yangu,” alisema mama Aidan huku na yeye akianza kulia. Japokuwa hakuwa na uhakika wa kilichotokea, ushahidi wa mazingira ulimfanya aamini kwamba lazima mumewe alimuingilia kimwili Caro. Mzozo ulipoendelea, ilibidi mzee huyo aamke na kuanza kujiandaa kuondoka huku akiwa bado na pombe kichwani. Akatoka na kumuacha mkewe akiwa anaendelea kulalama na kulia kwa uchungu. “Nitauficha wapi uso wangu mimi? Mwanaume umenitia aibu wewe sina hamu. Lazima utatoa talaka yangu,” alisema mama Aidan wakati mumewe akitokomea kusikojulikana. Hakutaka hata kuondoka na gari, akatembea kwa miguu mpaka barabarani alikosimamisha teksi. *** “Sisi ni maafisa wa polisi kutoka kituo cha kati, hivi ni vitambulisho vyetu,” askari watatu wenye silaha walijitambulisha kwa mke wa mzee Kenan, wakamueleza kuwa walikuwa wakimhitaji mumewe. “Amefanya nini tena?” “Ataenda kujua mwenyewe kituoni,” alisema askari mmoja huku akionyesha kutokuwa na hata chembe ya masihara. Wakaingia mpaka ndani lakini hawakumkuta mzee huyo. “Ameenda wapi?” “Wala hajaniaga, ameondoka muda si mrefu,” alisema mama Aidan huku akiwa bado amepigwa na butwaa. Kwa kuwa mtuhumiwa hakuwepo, walimwambia kuwa itabidi wamchukue yeye mpaka kituoni ili iwe rahisi kumpata mzee Kenan. Aidan aliyekuwa bado amelala, alishtuka baada ya kusikia mzozo sebuleni kwao, mama yake akibishana na watu. Harakaharaka akaamka na kuvaa nguo zake, akatoka mpaka sebuleni. “Mungu wangu, kuna nini tena,” alijiuliza huku akiwa amepigwa na mshangao kuwaona askari wenye silaha wakijibizana na mama yake, akasogea kutaka kujua kinachoendelea. “Tunamchukua mama yako mpaka baba yako aje kujisalimisha kituoni,” alisema askari mmoja huku wakimchukua mama Aidan. Wakatoka naye hadi nje na kumpakiza kwenye ‘difenda’, wakaondoka naye kwa kasi kubwa. “Kwani kumetokea nini? Kwa nini baba anatafutwa na polisi?” Aidan alijiuliza bila kupata majibu, ikabidi atoke mbio mpaka nyumbani kwa akina Caro kuwapa taarifa ili kama kuna uwezekano wawasaidie. Alishangaa kukuta mlango umefungwa kuashiria kwamba hakukuwa na mtu yeyote ndani. Hali hiyo ilizidi kumchanganya, akawa anajiuliza wameenda wapi asubuhi yote hiyo? Hakupata majibu. Harakaharaka akarudi mpaka nyumbani kwao, akachukua simu yake na kuanza kutafuta namba ya baba yake.
Alipoipata alianza kupiga lakini iliita bila kupokelewa. Akatoka na kusimama mlangoni, akaendelea kupiga lakini simu ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa. Alipopiga kwa mara ya tatu, aligundua kuwa simu ilikuwa ikiita kutoka ndani ya gari la baba yake. “Kwani baba ameenda wapi mpaka aache simu yake?” alijiuliza lakini bado hakupata majibu, ikabidi aingie ndani na kwenda kuchukua ufunguo wa gari, akatoka na kulifungua kwa lengo la kuchukua simu ya baba yake.
Ghafla aliona kitu kwenye siti ya nyuma kilichomshangaza sana. Akiwa ni kama haamini, alisogea taratibu huku akikichunguza vizuri kitu hicho. Ilikuwa ni nguo ya ndani, tena ya kike ikiwa kwenye siti ya nyuma ya gari hilo la baba yake. Alipoichunguza vizuri, aligundua kuwa ilikuwa imechanwachanwa, akazidi kujiuliza maswali yaliyokosa majibu. “Mungu wangu? Kwani nini kimetokea? Mbona sielewielewi? ITAENDELEA
Simulizi : The Holy Sin (Dhambi Takatifu) Sehemu Ya Nne (4)
“Nitauficha wapi uso wangu mimi? Mwanaume umenitia aibu wewe sina hamu. Lazima utatoa talaka yangu,” alisema mama Aidan wakati mumewe akitokomea kusikojulikana. Hakutaka hata kuondoka na gari, akatembea kwa miguu mpaka barabarani alikosimamisha teksi. “Unaelekea wapi mzee?” “Nipeleke Cross Bar,” alisema baba yake Aidan kwa sauti iliyoonyesha wazi kwamba ameamka na pombe kichwani. “Cross Bar asubuhi huwa hawafungui!”
“Kijana, nipeleke Cross Bar, sitaki maelezo wala hadithi za sungura na fisi,” aling’aka mzee Kenan huku akiyumbayumba, akapanda kwenye bodaboda na safari ya kuelekea Cross Bar ikaanza. Baada ya muda, tayari mzee Kenan alikuwa amefika Cross Bar, japokuwa baa hiyo aliyozoea kunywa pombe ilikuwa imefungwa kwani bado ilikuwa ni asubuhi sana, aliwagongea wahudumu waliokuwa wakilala vyumba vya uani ambapo waliamka na kumsikiliza. “Nataka bia tatu za baridi na mzinga mkubwa wa pombe kali.” “Mh! Leo mbona mapema mzee Kenan, kuna usalama kweli huko utokako?”
“We leta pombe, hayo mengine hayakuhusu,” aling’aka mzee huyo, bila hiyana mhudumu akamletea chupa tatu za bia alizoanza kuzigida kwa fujo. Nusu saa tu baadaye, chupa zote tatu zilikuwa tupu. “Niongeze nyingine kama hizi,” alisema mzee Kenan kwa sauti iliyoonyesha wazi kwamba pombe zilikuwa zimemkolea. Japokuwa ilikuwa ni asubuhi, aliendelea kunywa pombe kwa fujo, ilipofika saa nne za asubuhi, tayari alikuwa tilalila mithili ya mtu aliyeamka na pombe kichwani tangu jana yake. “Una nini leo mzee Kenan, siyo kawaida yao kupiga mitungi asubuhi yote hii, ina maana leo huendi kazini?” “Hivi kwa nini hamnielewi nyie vijana? Nimesema sitaki maswali ya aina yoyote,” alifoka mzee Kenan kwa sauti ya kilevi, wahudumu ambao ndiyo kwanza walikuwa wakitoa viti kwa ajili ya kuanza kufungua baa hiyo, ilibidi wafyate mkia, wakaendelea kumhudumia mzee Kenan ambaye ndani ya muda mfupi tu, alikuwa amelewa chakari.
Licha ya kulewa, bado kumbukumbu za tukio alilolifanya usiku uliopita, ziliendelea kukisumbua kichwa chake, mara kwa mara akawa anaweweseka na kutamka maneno yasiyoeleweka. Akiwa katika hali hiyo, alishtuka baada ya kuona gari la polisi likija na kupaki mbele ya baa hiyo, askari wanne wenye silaha wakateremka na kuanza kuangaza macho huku na kule. “Yule pale,” askari mmoja alisema, kufumba na kufumbua askari hao wakamvamia mzee Kenan ambaye tayari alikuwa amelewa sana, wakamkamata na kumfunga pingu, wakawa wanamkokota kama kondoo anayepelekwa machinjioni. “Kwani nimefanya nini jamani?”
“Utaenda kujua ukifika kituoni, mbakaji mkubwa wewe,” alisema askari mmoja, kauli iliyompa picha mzee Kenan, akaelewa kilichokuwa kinaendelea.
“Mtu mzima naumbuka leo, yaani mimi ni wa kukamatwa na polisi kwa kesi ya ubakaji,” alisema chinichini mzee Kenan wakati akipakizwa kwenye difenda, safari ya kuelekea kituo cha polisi ikaanza huku mikononi akiwa na pingu.
Alipofikishwa kituoni, alishangaa kumkuta mkewe akiwa chini ya ulinzi wa polisi huku baba na mama Caro pamoja na binti yao nao wakiwa wamekaa pembeni, nje kidogo ya kituo hicho. Kwa jinsi alivyojisikia aibu kuwakuta wazazi wa Caro wakiwa na binti yao, nje ya kituo hicho, mzee Kenan alitamani ardhi ipasuke na kummeza, akashushwa msobemsobe kwenye gari la polisi na kuingizwa ndani ya kituo hicho. Wakati akiingizwa mahabusu, mkewe alifunguliwa na kuachiwa huru, wakakutana uso kwa uso kwenye korido ya kituo cha polisi.
“Ukifanikiwa kutoka, nataka talaka yangu, siwezi kuvumilia upuuzi huu, nini ulichokosa kwangu mpaka ukaamua kwenda kubaka, hunifai tena,” alisema mama Aidan huku akilengwalengwa na machozi. Mzee Kenan alishindwa cha kujibu, akaingizwa mahabusu na geti la chuma likabamizwa kwa nguvu kisha likafungwa kwa kufuli kubwa. Huo ukawa mwanzo wa maisha mapya ya mzee Kenan. *** Aidan akiwa bado ameduwaa baada ya kukuta nguo ya ndani ya kike kwenye gari la baba yake, alijiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu. Kitu kingine kilichozidi kumshangaza ni baada ya kukuta hakuna mtu nyumbani kwa akina Caro. Maswali yalikuwa mengi kuliko majibu.
Akiwa amezama kwenye dimbwi la mawazo, alishtuliwa na sauti ya mama yake aliyeingia ndani ya nyumba yao huku akiangua kilio. Harakaharaka aliacha kila alichokuwa anakifanya, akaelekea sebuleni kutaka kujua ni kitu gani kilikuwa kimemsibu mama yake kwani hakuwahi kumsikia akilia hata mara moja tangu apate akili zake. “Mama! Mama kuna nini? Mbona unalia,” alihoji Aidan huku akimsogelea mama yake lakini badala ya kumjibu, alipitiliza moja kwa moja mpaka chumbani kwao alikoanza kufungasha kila kitu chake kwenye mabegi makubwa mawili. “Mama kwani kuna nini? Mbona sielewi? Polisi walikuja kukukamata, sasa hivi unafungasha vitu vyako vyote, mbona sielewi?”
“Aidan, baba yako amenitia aibu sana, siwezi kuendelea kuishi naye, najua atakayeteseka ni wewe lakini sina namna, ni lazima niondoke,” alisema mama yake Aidan huku akiendelea kulia kwa uchungu. Aidan akiwa amebaki njia panda, alisikia muungurumo wa gari la akina Caro, harakaharaka akatoka na kukimbilia nyumbani kwa akina Caro lakini hali aliyokutana nayo, ilimfanya abaki ameduwaa, akiwa ni kama haamini. Wazazi wa Caro walimfukuza kama mbwa na kumpiga marufuku asikanyage tena kwenye nyumba hiyo.
“MAAAMA! Tafadhali niambie kinachoendelea, mbona sielewi?” “Siwezi kusema chochote kwa sasa Aidan, mimi naondoka tutaonana Mungu akipenda.” “Hapana mama usiondoke, nakuomba mama, shule zinaelekea kufunguliwa na hapa nyumbani ndiyo hivyo sielewi kinachoendelea, nyumbani kwa akina Caro nimefukuzwa kama mbwa, nitakuwa mgeni wa nani mimi? Nitakwenda popote na wewe,” alisema Aidan huku akilia kwa uchungu, hali iliyomtia simanzi hata mama yake. Akarudisha mabegi yake ndani na kurudi pale alipokuwa amemuacha mwanaye, akamuinua na kumkumbatia.
“Basi mwanangu, siondoki kwa sababu yako mpaka baba yako atakaporudi uraiani.” “Atakaporudi uraiani? Kwani sasa hivi yuko wapi?” “Amekamatwa, yupo lupango.” “Niniii! Baba amekamatwa? Kwani wewe na baba mmefanya nini?” “Mimi sina kosa, polisi walikuja kunikamata ili iwe rahisi kumpata baba yako.” “Kwani yeye baba amefanya nini?”
“Mwanangu, we elewa tu kwamba baba yako amekamatwa, hayo mengine msubiri akija kutoka lupango ndiyo utakuja kumuuliza,” alisema mama yake Aidan huku akionyesha dhahiri kwamba kuna jambo alikuwa anamficha mwanaye huyo.
Muda mfupi baadaye, wote walisikia mlango wa nyumba yao ukigongwa, Aidan akatoka haraka kwenda kufungua, akakutana uso kwa uso na mchungaji wao, mzee Katavi ambaye mara kwa mara alikuwa akiwatembelea nyumbani hapo.
Mama Aidan alipomuona tu Mchungaji Katavi ambaye alikuwa amevaa mavazi maalum kama wavaayo watumishi wa Mungu, mkononi akiwa na Biblia, alianza kuangua kilio kwa uchungu, hali iliyomshangaza mchungaji huyo.
Akaanza kumtuliza na kumuomba Aidan awapishe kidogo ili aweze kumueleza kilichokuwa kikimsumbua. Mama Aidan alitulia na kukaa kwenye kiti, pembeni ya mchungaji huyo. Ili kuhakikisha kwamba Aidan hasikii chochote, alimuita na kumtuma kwenda kununua soda dukani. Alipoondoka, alianza kumueleza kila kitu kilichomsibu. Mchungaji Katavi alibaki ameduwaa kwani hakuwahi kufikiria kwamba mtu aliyekuwa akimheshimu kama mzee Kenan anaweza kufanya tukio kubwa la aibu kama hilo. “Nataka kurudi kwetu mchungaji, siwezi kuishi na mwanaume huyu, ameuumiza sana mtima wangu,” alisema mama Aidan huku akiendelea kulia. Mchungaji akawa anambembeleza na kumkumbusha juu ya kiapo cha ndoa alichokula siku walipokuwa wakioana. “Uliahidi utakuwa naye katika shida na raha, utakuwa unafanya dhambi kumkimbia mwenzako wakati ana matatizo.”
“Sasa nitafanya nini mchungaji katika hali kama hii? Nahisi nimeibeba dunia nzima kichwani kwangu, sina namna zaidi ya kuondoka,” alisema mama Aidan lakini mchungaji akawa anambembeleza huku akimpa ushauri wa namna ya kumsaidia mumewe.
Kwa pamoja wakakubaliana kwamba waende kwa wazazi wa Caro na kujaribu kuzungumza nao ili kama inawezekana wayamalize mambo hayo nje ya mahakama. “Akishatoka lupango hapo ndiyo utakuwa na uamuzi wa nini cha kufanya kwa sababu utakuwa umetimiza kiapo chako kwa kuwa naye hata katika wakati wa shida,” alisema mchungaji huyo, kidogo mama Aidan akajihisi ahueni kwenye moyo wake.
Hawakutaka kupoteza muda, wakatoka na kuelekea nyumbani kwa akina Caro, wakapishana na Aidan mlangoni akirudi kutoka dukani. Mchungaji akatumia busara kumueleza kuwa awasubiri ndani watarudi baada ya muda mfupi. Alifanya hivyo kwa makusudi kwani mama yake alishamueleza kuwa hakuwa akijua chochote.
Tofauti na walivyotegemea, walipofika nyumbani kwa akina Caro, walipokelewa kishari mno huku baba wa msichana huyo akitishia kufanya kitu kibaya endapo mtu yeyote kutoka familia ya mzee Kenan ataingia ndani ya nyumba yake.
Ilibidi busara zitumike, mchungaji akamuomba mama Aidan arudi nyumbani kwake kwanza wakati yeye akiendelea kuwabembeleza wazazi wa Caro warudishe nyuma mioyo yao. Kazi haikuwa nyepesi kwa jinsi wazazi wa Caro walivyokuwa mbogo kutokana na mtoto wao kuharibiwa na mtu waliyekuwa wakimuamini na kumchukulia kama ndugu yao. “Tumefundishwa kusamehe saba mara sabini, katika Biblia takatifu, Warumi 12:19, neno la Mungu linasema: Msijilipizie kisasi bali ipisheni ghadhabu ya Mungu maana imeandikwa kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa.
“Pia Mithali 20:22, neno la Mungu linasema: Usiseme mimi nitalipa mabaya mngojee Bwana naye atakuokoa,” alisema mchungaji huyo, akaendelea kukemea roho ya kisasi kwa muda mrefu mpaka baba na mama Caro wakaanza kuelewa kwamba walikuwa wakimkosea Mungu wao. Baada ya kuelewa neno la Mungu kutoka kwa Mchungaji Katavi, walikubali kuongozwa katika sala maalum, wote wakapiga magoti, mchungaji akawawekea mikono kwenye vichwa vyao na akaanza kusali kwa nguvu.
Baadaye alipomaliza, wote walikubali mama yake Aidan akaitwe ili kwa pamoja wajadiliane nini cha kufanya kwani hata wangeamua kumfunga mzee Kenan, hiyo isingebadilisha maana kwamba binti yao ameshaharibiwa.
Mama Aidan alifurahi sana kusikia familia hiyo imekubali wakae mezani na kujadiliana nini cha kufanya. Kilichomfurahisha ni kwamba muda mfupi baadaye angeweza kuikwepa aibu iliyokuwa mbele yake kwani alishapanga kwamba mumewe akitoka tu gerezani, cha kwanza ni kudai talaka yake na kuondoka kabisa kwenye mtaa huo kukwepa aibu nzito. Kikao kilikuwa kirefu mno, pande zote mbili zikitoa hoja nzitonzito, Mchungaji Katavi alikuwa makini kuwatuliza kila walipoonekana kupandwa na jazba. Mwisho wakafikia muafaka kwamba wakaifute kesi hiyo na mambo yote yamalizwe nje ya mahakama. Wakakubaliana kuwa asubuhi ya siku ya pili, wote waongozane hadi kituo cha kati cha polisi kwa ajili ya kwenda kufuta kesi hiyo, mama Aidan akiwa tayari kutoa gharama zote za kufuta kesi hiyo.
Kesho yake kulipopambazuka, wazazi wa Caro pamoja na mama yake Aidan waliongozana mpaka kwenye kituo kikuu cha polisi ambapo walipofika, waliomba kuonana na mkuu wa kituo ambaye walimweleza shida yao. Mkuu huyo wa kituo aliwaeleza wazi kwamba kosa alilokuwa amelifanya mzee Kenan halikuwa la kumalizana kienyeji kwani kwa mtu aliyebaka, huwa anashtakiwa na jamhuri kwa hiyo lazima kesi hiyo ifikishwe mahakamani. “Tusaidie baba, mtuhumiwa ni mume wangu na familia nzima tunamtegemea yeye, nipo chini ya miguu yako, naomba msaada wako afande,” alisema mama Aidan lakini mkuu wa kituo alitingisha kichwa kuonesha kutokubaliana na ombi hilo. “Mimi nikisema nimuachie, nitajibu nini kwa viongozi wangu? Ishu kama hii siyo ya kumalizwa kiholela, samahani sana siwezi kuwasaidia,” alisema mkuu wa kituo huku akisimama kuashiria kwamba hataki tena kuendelea kuwasikiliza. Mama Aidan aliangua kilio cha uchungu ndani ya ofisi ya mkuu wa kituo lakini haikusaidia chochote. Mama Caro na mumewe wakamwambia kwamba wao wapo tayari kulimaliza suala hilo kwa hiyo kazi ni kwake kumshawishi mkuu huyo wa kituo kama atakubali. Mama na baba Caro walitoka nje na kwenda kukaa kwenye benchi nje ya kituo hicho, wakamuacha mama Aidan akiendelea kumwaga machozi. “Afande nipo tayari kufanya chochote ilimradi tu hili suala liishe, niambie chochote unachotaka nitakuwa tayari,” alisema mama Aidan huku macho yake yakiwa mekundu kutokana na kulia kwa muda mrefu. Baada ya kauli hiyo, mkuu wa kituo ambaye alikuwa ameshasimama, alirudi kwenye kiti chake na kukaa, akawa anamtazama mama Aidan usoni. “Unajua hili suala limekaa vibaya sana, naogopa kuharibu kazi yangu,” alisema mkuu huyo kwa sauti ya upole tofauti na awali huku akimtazama mama Aidan. Akashusha pumzi ndefu na kunyoosha mkono wake, akawa anampigapiga kama ishara ya kumbembeleza. “Kwani unampenda sana mumeo?” “Nampenda sana, nipo tayari kufanya chochote ilimradi atoke.” “Sasa unampendaje mtu ambaye haziheshimu hisia zako? Yaani mtu ana mke mzuri kama wewe anashindwa kutulia matokeo yake anaenda kukutia aibu? Yaani mimi ningekuwa na mke mzuri kama wewe mbona ningeringa sana,” alisema mkuu huyo wa kituo huku akiwa amemkazia macho mama Aidan. Akaendelea kumbembeleza mama Aidan huku mkono wake ukiwa kwenye bega lake la mkono wa kushoto, akamwambia yupo tayari kumsaidia lakini kwa sharti moja tu. “Sharti gani afande?” “Usijali, ngoja kwanza nishughulikie suala la mumeo halafu akishatoka nitaomba kuonana na wewe jioni ya leo kwa maelekezo zaidi,” alisema mkuu huyo wa kituo, kauli iliyomshtua mno mama Aidan lakini kwa kuwa alikuwa na shida, hakuwa na ujanja zaidi ya kukubali. “Hebu niandikie namba yako ya simu,” alisema mkuu huyo wa kituo huku akitoa simu yake ya mfukoni na kumpa mama Aidan, akaipokea huku akitetemeka na kuandika namba yake, akamrudishia simu yake. Baada ya hapo, mkuu wa kituo alisimama na kutoka, akamuacha mama Aidan ndani ya ofisi yake, akaenda mpaka kwenye ofisi ya wapelelezi ambapo alimuita Inspekta Kiiza, mpelelezi aliyekuwa akishikilia jalada la kesi hiyo. Akazungumza naye na kumpa maagizo ya kulifunga jalada la kesi iliyokuwa ikimkabili mzee Kenan kisha kumtoa nyuma ya nondo. Akarudi ofisini kwake. Baada ya dakika kadhaa, mlango wa ofisi ya mkuu huyo wa kituo uligongwa, akaingia Inspekta Kiiza akiwa na faili mkononi mwake, nyuma yake akiwa ameongozana na mzee Kenan. Muda mfupi tu aliokaa nyuma ya nondo, ulitosha kumbadilisha mno. Alionekana kuchakaa utafikiri amekaa mwezi mzima gerezani, macho yake yakagongana na ya mkewe, akashindwa kujizuia, machozi yakawa yanamtoka kama chemchemi ya maji. “Umshukuru sana mkeo kwa kukuhangaikia lakini hata hivyo bado mambo hayajaisha, hutakiwi kutoka nje ya mji kwa kipindi chote mpaka utakapoambiwa vinginevyo, mke wako atakuwa anakuja mara kwa mara hapa kituoni kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kisheria,” alisema mkuu wa gereza huku akilipitia faili la kesi yake. Mzee Kenan alimshukuru sana mkuu wa kituo, akamshukuru pia na mke wake ambapo mkuu wa kituo aliwaruhusu kuondoka, wakaenda mpaka kaunta ambapo mzee Kenan alirudishiwa vitu vyake kama mkanda, viatu na vitu vingine alivyovuliwa wakati akiingizwa mahabusu. Wakatoka hadi nje walikowakuta wazazi wa Caro wakiwa wamekaa, nyuso zao zikionesha kuwa na majonzi. Hakuna aliyeweza kumsemesha mwenzake, wakatazamana kwa sekunde chache kisha kila mtu akatazama pembeni. *** Baada ya mama yake kuondoka asubuhi akiwa ameongozana na wazazi wa Caro, Aidan aliona huo ndiyo muda muafaka wa kwenda kuzungumza na Caro. Akasubiri wazazi wao walipoondoka kabisa, harakaharaka akatoka nyumbani kwao na kukimbilia nyumbani kwa akina Caro. Akagonga mlango lakini hakuitikiwa, alipousukuma aligundua kuwa haukuwa umefungwa kwa funguo, akaufungua na kuingia mpaka ndani. Kwa kuwa alikuwa akikifahamu chumba alichokuwa analala Caro, alienda moja kwa moja mpaka mlangoni, alipojaribu kuufungua aligundua kuwa ulikuwa umefungwa. “Caro! Caro! Ni mimi Aidan, naomba ufungue mlango,” alisema kwa sauti ya kubembeleza. Caro ambaye alikuwa amejilaza kitandani akiendelea kutafakari juu ya kitendo alichofanyiwa na baba yake Aidan, alishtuka mno kusikia sauti ya Aidan. Tangu alipotokewa na tukio la kubakwa na mzee Kenan, hakuwa akitaka kumuona Aidan kwenye macho yake kutokana na jinsi alivyokuwa akijisikia vibaya ndani ya moyo wake. Harakaharaka aliamka na kuvaa nguo, akaenda kuufunga mlango kwa funguo akiwa hataki kabisa kukutana na Aidan. Aidan aliendelea kubembeleza pale mlangoni lakini Caro hakukubali kumfungulia zaidi ya kuendelea kulia kwa uchungu. Japokuwa alikuwa akimpenda mno Aidan, kitendo alichofanyiwa na baba yake kilimfanya atamani kwenda kuishi kwenye dunia ya peke yake, mahali ambapo hatakutana tena na mtu yeyote. “Siwezi kukufungulia Aidan, we ondoka tu,” alisema Caro huku akilia kwa uchungu, Aidan akazidi kumbembeleza huku akimkumbusha mambo mbalimbali waliyofanya pamoja. Baada ya kutumia ushawishi wa hali ya juu, hatimaye Caro alikubali kumfungulia lakini moyoni akajiapiza kuwa kamwe hatamwambia kitu chochote, ni bora aufahamu mwenyewe ukweli.
“CARO, unaumwa?” “Hapana siumwi.” “Kwani kuna nini kinachoendelea? Mbona sielewi? Hebu nifumbue macho Caro,” alisema Aidan lakini badala ya kumjibu, Caro alianza kuangua kilio, hali iliyozidi kumchanganya Aidan, akamsogelea na kumkumbatia huku akimfuta machozi. “Tafadhali niambie Caro, kwani kuna nini kimetokea?” Aidan alizidi kumbana Caro lakini bado hakutaka kumweleza chochote zaidi ya kuendelea kulia. Walikaa pamoja kwa muda mrefu lakini bado hakuwa tayari kufungua mdomo wake na kumweleza ukweli Aidan. Walikuja kushtuka baada ya kusikia muungurumo wa gari kwa mbali, harakaharaka Aidan akatoka na kukimbilia kwao akikwepa kukutwa na wazazi wa Caro ambao walishampiga marufuku kukanyaga kwenye nyumba hiyo. Hata hivyo, aliondoka akiwa bado na shauku kubwa ndani ya moyo wake ya kuujua ukweli. Muda mfupi baadaye, wazazi wake nao waliwasili wakiwa kwenye Bajaj, akatoka kuwapokea huku akiwa na hamu kubwa ya kujua nini kilisababisha baba yake akamatwe na polisi. “Pole baba,” alisema Aidan, baba yake akatingisha kichwa na kujiinamia kutokana na aibu aliyokuwa anaihisi. “Kwani ulifanya nini mpaka polisi wakakukamata,” alihoji Aidan lakini hakujibiwa swali hilo, mama yake akamshushua na kumwambia aende akajisomee badala ya kujishughulisha na mambo yasiyomhusu. Akaelekea chumbani kwake huku mawazo mengi yakiendelea kukisumbua kichwa chake. Baada ya mzee Kenan kuoga na kuchoma moto nguo alizokuwa nazo lupango, mkewe alimuweka kitimoto na mjadala mkali ukaanza chumbani kwao. “Nilikuwa nakusubiri utoke na kutulia ndiyo nikwambie langu la rohoni,” alisema mama Aidan na kuanza kueleza masikitiko yake kutokana na kitendo cha aibu kilichofanywa na mumewe na mwisho akaeleza alichokuwa anakitaka. “Nataka talaka yangu, nimekusaidia umetoka salama, baki na mwanao na hata ukitaka kuoa mke mwingine ruksa lakini mimi siwezi kuishi na wewe, najihisi aibu kubwa kwa hiyo uamuzi niliofikia ndiyo huo. Kauli hiyo ilikuwa kama mkuki kwenye moyo wa mzee Kenan, tamaa ya muda mfupi iligeuka shubiri kwenye maisha yake. Ilibidi apige magoti na kuanza kumsihi mke wake amsamehe, akaahidi kuwa tayari kumfanyia chochote atakachokitaka ilimradi amsamehe. Hata hivyo, bado mama Aidan alishikilia msimamo wake, mpaka wanamaliza maongezi yao yaliyochukua zaidi ya saa tatu, hawakuwa wamefikia muafaka. Jioni ilipofika, kama mama Aidan alivyokuwa amekubaliana na mkuu wa kituo, alijiandaa na kumuaga mumewe ambaye alimruhusu kwa moyo mkunjufu. Akatoka na safari ya kuelekea kituo cha polisi ikaanza. Alipofika, alipokelewa kwa bashasha na mkuu huyo wa kituo ambaye baadaye alijitambulisha kwamba anaitwa Ibrahim Mdimu. “Kuna mahali nataka tuende pamoja, hapa hapafai kwa mazungumzo,” alisema Kamanda Mdimu, kengele ya hatari ikalia ndani ya kichwa cha mama Aidan. Awali alihisi kuwa mkuu huyo wa kituo alimuita ili wajadiliane kuhusu kesi ya mumewe lakini kwa maelezo mafupi tu aliyompa, ilionyesha kuna jambo lingine la ziada. Hata hivyo, hakutaka kuonyesha wasiwasi wake mapema, akatoka na mkuu huyo wa kituo mpaka mahali alipokuwa amepaki gari lake, akamfungulia mlango mama Aidan kisha na yeye akapanda, wakaondoka kituoni hapo. “Samahani, huwa unakunywa pombe?” “Hapana situmii, labda waini kidogo ambayo huwa nakunywa nikitaka kulala,” alijibu mama Aidan, safari ikaendelea na baada ya muda, Kamanda Mdimu alipaki gari kwenye maegesho ya hoteli nzuri ya Eastern Beach iliyokuwa ufukweni mwa Bahari ya Hindi. “Nimepachagua hapa kwa sababu ya utulivu wake na mandhari nzuri,” alisema Kamanda Mdimu wakati akimuongoza mama Aidan sehemu ya kwenda kukaa. Wakakaa kwenye meza iliyokuwa imejitenga na kuagiza vinywaji, wakawa wanapunga upepo mwanana wa baharini. “Vipi mmefikia wapi na mumeo?” Kamanda Mdimu alimuuliza mama Aidan, akashusha pumzi ndefu na kumtazama. “Bado hatujafikia muafaka lakini siwezi kuendelea kuishi naye.” “Unamaanisha nini?” “Nataka anipe talaka yangu, siwezi kuishi na mtu asiye na hata chembe ya ubinadamu.” “Safi sana, nakupongeza kwa uamuzi uliouchukua, usirudi nyuma kwani amekutia aibu sana,” alisema mkuu huyo wa kituo na kuahidi kumsaidia endapo atahitaji msaada wake. Alionekana kufurahishwa mno na uamuzi huo, jambo lililomshangaza mama Aidan. “Mke wangu alikufa miaka saba iliyopita kwa ajali ya gari, tangu kipindi hicho sijawahi kuoa, wanangu wameshakuwa wakubwa lakini nahisi kuna kitu nakikosa kwenye maisha yangu.” “Pole kwa yaliyokukuta, unahisi unakosa nini?” “Furaha ya moyo wangu, nimeishi mpweke kwa kipindi kirefu sana, sasa nahitaji kubadilisha maisha yangu,” alisema Kamanda Mdimu na kusogeza mkono wake, akamshika mama Aidan mkono na kumtazama usoni. “Siwezi kuficha hisia zangu, tangu mara ya kwanza nilipokuona nimetokea kukupenda sana na ndiyo maana nikakusaidia, naomba wewe ndiyo uzibe pengo la mke wangu, nitakusaidia kumshinikiza mumeo akupe talaka haraka iwezekanavyo,” alisema Kamanda Mdimu huku akiendelea kumtazama mama Aidan kwa macho yaliyobeba ujumbe.
Simulizi : The Holy Sin (Dhambi Takatifu) Sehemu Ya Tano (5)
Kauli hiyo ya Kamanda Mdimu ilimfanya abaki ameduwaa kwa sekunde kadhaa, macho yakiwa yamemtoka pima. Alishindwa kuelewa atoe jibu gani kwani ni kweli mumewe alikuwa amemfanyia kosa kubwa la kumdhalilisha lakini suala alilolizungumzia mkuu huyo wa kituo lilimfanya azidi kuchanganyikiwa. “Niamini, nitakusaidia kuhakikisha unapewa talaka yako, si unakumbuka uliniahidi kuwa utakuwa tayari kwa chochote ilimradi nimsaidie mumeo awe huru na kesi ile tuimalize?” alihoji Kamanda Mdimu. “Ndi…yo nilisema nitakuwa tayari kwa lolote lakini siyo hili,” alisema mama Aidan kwa kubabaika. “Tafadhali nionee huruma mwenzio, nipo chini ya miguu yako, nakuhitaji kwenye maisha yangu, nimechoshwa na huu upweke,” alisema Mdimu kwa hisia huku akilengwalengwa na machozi kwa mbali. “Basi naomba unipe muda wa kufikiria kwa kina, nitakupa majibu tutakapoonana tena.” “Kwa hiyo tutaonana tena lini?” “Nipe muda nitakwambia.” “Jitahidi basi usichelewe sana, yaani ukinikubalia tu hata wiki haitaisha utakuwa umeshapewa talaka yako kisha tutaoana na kuishi kama mume na mke, nimekuandalia vitu vingi sana vizuri,” alisema Kamanda Mdimu na kuinuka, akamuinamia mama Aidan pale alipokuwa amekaa na kumbusu. Japokuwa mwenyewe hakupendezewa na tukio hilo, alishindwa kufanya chochote kulizuia, akakusanya vitu vyake tayari kwa kuondoka, Mdimu akataka kumsaidia kubeba pochi lakini mwenyewe akakataa. Wakaongozana mpaka kwenye gari walilokuja nalo, akamfungulia mlango mama Aidan kisha akarudi upande wake na kukaa nyuma ya usukani, safari ya kuondoka kwenye hoteli hiyo ikaanza huku kila mmoja akiwa kimya ndani ya gari. “Naomba nikupeleke hadi nyumbani.” “Hapana usinifikishe nyumbani, twende ukaniache kituoni halafu nitajua mwenyewe namna ya kufika nyumbani,” alisema mama Aidan lakini bado mkuu huyo wa kituo akawa king’ang’anizi. Mwisho walikubaliana kuwa akamuache karibu na nyumbani kwake. Baada ya dakika kadhaa, walikuwa wameshafika jirani na nyumbani kwa akina Aidan, akapunguza mwendo na kusimama pembeni ya barabara. Kabla mama Aidan hajateremka, alifungua ‘dashboard’ ya gari na kutoa noti kadhaa za shilingi elfu kumikumi. “Hizi zitakusaidia matumizi madogomadogo,” alisema Kamanda Mdimu kisha akambusu tena mama Aidan shavuni. Akamfungulia mlango na kuagana naye. Kila kilichokuwa kinatokea kwenye maisha ya mama Aidan alikifananisha na njozi za mchana. Alitamani awe ndotoni lakini haikuwa hivyo, tukio la mumewe kumbaka Caro lilikuwa limefungua mlango kwa mambo mengi ambayo hakuwahi kudhani kwamba yanaweza kutokea kwenye maisha yake hata mara moja. Hakuwahi kushikwa mwili wake kimahaba na mwanaume mwingine tofauti na mumewe lakini sasa Kamanda Mdimu alifikia hatua ya kumbusu, tena mara mbili bila ridhaa yake mwenyewe. Pia suala la fedha halikuwa tatizo kwenye maisha yake na mumewe hajawahi kupata matatizo yoyote ya kifedha kiasi cha kufikia hatua ya kuhongwa na mtu yeyote lakini sasa Kamanda Mdimu alikuwa amempa fedha nyingi ambazo wala hakuwa na shida nazo ila alishindwa kuzikataa. “Eeeh Mungu wangu, ninusuru na hii mitego iliyopo mbele yangu, nipe busara ya kuamua ninachokitaka bila kutetereka,” aliwaza huku akitembea, machozi yakawa yanamtoka bila mwenyewe kugundua. Alienda moja kwa moja mpaka nyumbani kwake, akapokelewa na mwanaye Aidan aliyekuwa amekaa sebuleni akijisomea. “Mbona unalia mama? Unaumwa?” alihoji Aidan wakati akimpokea mama yake mkoba, akatingisha kichwa kumkatalia kisha akajifuta machozi harakaharaka, akaongoza mpaka chumbani ambako alimkuta mumewe akiwa amelala. “Mbona umechelewa sana?” “Kuna mambo ya kisheria tulikuwa tunakamilisha na mkuu wa kituo,” alijibu mama Aidan huku akikwepa kutazamana na mumewe usoni. “Ooh! Sawa, pole kwa usumbufu ninaokusababishia,” alisema mzee Kenan huku akikaa kitako kwa lengo la kuendelea kumbembeleza mkewe abatilishe uamuzi wake wa kudai talaka. “Naomba unisamehe mke wangu, na mimi ni binadamu wala siyo malaika, kukosea tumeumbiwa. Naomba usiniache,” alisema baba Aidan kwa sauti ya kubembeleza lakini mkewe hakujibu kitu chochote zaidi ya kujiinamia. “Kumbuka wapi tulikotoka mke wangu, wewe ni shahidi kwamba sijawahi hata mara moja kukusaliti tangu tuoane, ni shetani tu alinipitia mke wangu, nipo chini ya miguu yako,” alisema mzee Kenan huku akiteremka kitandani na kumpigia mkewe magoti. Akiwa bado anaendelea kumbembeleza, simu ya mkewe ilianza kuita mfululizo, mama Aidan aliyekuwa amejiinamia aliinua uso wake na kuichukua, akawa anaangalia namba ya mpigaji. Mapigo ya moyo wake yalilipuka na kuanza kwenda mbio baada ya kugundua kuwa Kamanda Mdimu ndiye aliyekuwa akimpigia. Hakujua kama apokee au asipokee simu hiyo, akabaki kubabaika, jambo ambalo mumewe aliligundua. “Nani anakupigia?” aliuliza mzee Kenan huku akisimama.
“NI mkuu wa kituo, kuna maelekezo alisema anataka kunipa kuhusu kesi yako.” “Ooh! Basi hakuna tatizo, ongea naye tu,” alisema mzee Kenan bila kuelewa chochote kilichokuwa kinaendelea. Mkewe akapokea simu ambapo jambo la kwanza ilikuwa ni kumtaarifu Mdimu kama yupo na mumewe kwa kujihami. “Haloo! Eeh za kazi afande, nipo na mume wangu hapa tunajadili kuhusu kile ulichoniambia,” alisema mama Aidan kisha akabonyeza kitufe cha kukatia simu. “Vipi anasemaje?” mzee Kenan alimuuliza mkewe huku akiwa na shauku ya kutaka kujua ni maelekezo gani amepewa. Kwa kuwa hakuwa na maelekezo yoyote, ilibidi atunge uongo kwamba kuna fedha zinatakiwa ili kutuliza kabisa kesi yake ya ubakaji. “Amesema shilingi ngapi?” “Hajasema ila amesema tujiandae, atatupa taarifa muda wowote akishakuwa na jibu kamili,” mama Aidan alizidi kudanganya, mumewe akamjibu kuwa asiwe na wasiwasi kwani fedha siyo tatizo kubwa kwao. Akashusha pumzi ndefu baada ya kufanikiwa kumdanganya mumewe. Japokuwa mumewe aliendelea kuzungumza naye, akili za mama Aidan zilihama kabisa, akawa anawaza namna ya kuutatua mtihani mkubwa uliokuwa mbele yake. Ni kweli mumewe alimsaliti na hakuwa akitaka kuendelea kuishi naye lakini hakutaka mtu mwingine atumie udhaifu huo kwa manufaa yake binafsi. Alimtazama mumewe kwa muda, akajiinamia na kuendelea kutafakari nini cha kufanya, alijikuta akimuonea huruma kwani kwa jinsi Kamanda Mdimu alivyokuwa na hamu ya kuishi naye, alikuwa tayari kufanya chochote ili mradi atimize malengo yake. “Mbona bado unaonekana una mawazo mke wangu? Tafadhali, nipo chini ya miguu yako, naomba usiniache,” alisema mzee Kenan kwa upole, akaendelea kumbembeleza mkewe kwa muda mrefu lakini muda wote alikuwa kimya. Siku ya kwanza ilipita, kesho yake Kamanda Mdimu akampigia simu mama Aidan na kumuuliza kuhusu jibu lake. “Mbona una haraka? Nimekwambia subiri nifikiri, nitakupa majibu usijali,” alisema mama Aidan. Baada ya siku tatu kupita huku akiwa bado hana maelewano na mumewe, aliamua kuchukua uamuzi mgumu wa kumkatalia Afande Mdimu. Alimpigia simu nakumtaarifu wakutane palepale walipokutania mara ya kwanza. “Japokuwa mume wangu amenikosea sana, nimeamua kumsamehe na sitadai tena talaka kwa hiyo ombi lako limeshindikana,” alisema mama Aidan kwa sauti ya utulivu akiwa na Mdimu, kwenye hoteli ileile waliyokutania mwanzo. “Lakini uliniahidi kuwa upo tayari kufanya chochote ili mradi nikusaidie, sasa shida yako imeisha unaniona sina maana tena, unafikiri ni sawa?” “Siyo sawa Mdimu lakini tambua mimi ni mke wa mtu na nimeshakwambia kwamba nimeamua kumsamehe mume wangu.” “Huyo mumeo angekuwa anakupenda kweli angekutia aibu kwa kumbaka mtoto ambaye ni sawa na binti yenu?” “Sawa lakini nimeamua kumsamehe.” “Kwa hiyo vipi kuhusu mimi?” “Sasa nitakusaidiaje Mdimu?” “Hata kama mmeamua kusameheana na mumeo, na mimi nataka uwe mpenzi wangu lakini tutafanya siri mtu yeyote asijue.” “Haa! Hilo haliwezekani kabisa, siwezi kuwatumikia wanaume wawili kwa wakati mmoja, sikulelewa hivyo mimi.” “Kwa hiyo shukrani ya punda imekuwa mateke si ndiyo? Yaani msaada wangu wote niliokufanyia leo unashindwa kulipa fadhila kwa kitu chepesi kama hicho?” “Nipo tayari kulipa fadhila lakini siyo mwili wangu, we sema chochote unachotaka nitajitahidi kukupa lakini siyo mwili wangu.” “Sasa sikia, nakupa muda nenda kajifikirie tena, nataka uwe mpenzi wangu wa siri kama nilivyokwambia na kama utaendelea kushikilia msimamo wako, naifufua upya kesi ya mumeo akafungwe miaka thelathini. Nimemaliza,” alisema Mdimu kwa hasira, akasimama na kuanza kuondoka, mama Aidan akiwa amepigwa na bumbuwazi. “Basi usiondoke kwanza,” alisema mama Aidan kwa sauti iliyoonyesha dhahiri kutishwa na kauli iliyotolewa na Kamanda Mdimu. “Mimi nimeshamaliza, naondoka zangu,” alisema Kamanda Mdimu huku akionyesha kutokuwa na hata chembe ya masihara. Mama Aidan akazidi kumbembeleza, hali iliyomfanya alegeze msimamo wake, akarudi na kukaa palepale alipokuwa amekaa awali. Mama Aidan akawa anang’ata kucha zake kwa aibu huku akishindwa hata pa kuanzia. “Nakusikiliza!” “Basi sawa nipe muda nikafikirie upya ila nakuomba usiwe na hasira na wala usiifufue kesi ya mume wangu, nakuomba nipo chini ya miguu yako,” alisema mama Aidan huku akilengwalengwa na machozi. “Mimi nakushangaa, mbona jambo jepesi unataka kulifanya liwe gumu?” “Naogopa mume wangu atajua, hakuna siri kwenye mapenzi.” “Atajua kwani utamwambia wewe?” “Hapana lakini najua ipo siku atajua tu, isitoshe mimi sijazoea kumsaliti mume wangu. Tangu anioe sijawahi kutoka nje hata mara moja,” alisema mama Aidan huku akitetemeka kwa hofu. “Wala usijali, hawezi kujua chochote na hata kama akijua, mimi nitakulinda,” alisema Kamanda Mdimu na kusogeza kiti chake jirani na mama Aidan, akapitisha mkono wake shingoni na kumkumbatia kisha akambusu shavuni. Japokuwa mama Aidan hakufurahishwa na kitendo hicho, hakuwa na cha kufanya. “Nikubalie uyafaidi maisha, achana na yule bwege wako anayekutia aibu mbele ya jamii, njoo kwangu nikuonyeshe maana ya mapenzi na heshima ya mwanamke,” alisema Kamanda Mdimu huku mkono wake mwingine ukivinjari taratibu kwenye mwili wa mama Aidan. “Ha…ha…pa…na,” mama Aidan alijaribu kujitoa kwenye mikono ya Mdimu lakini haikuwezekana, akaendelea kumfanyia uchokozi wa makusudi huku akimtolea maneno matamu ya kumlainisha.
Mdimu aliendelea kumfanyia vituko vya kimahaba mama Aidan ambaye aliendelea kupambana naye kwani hakuwa tayari kwa wakati ule kufanya kile Mdimu alichokusudia. Baada ya kusumbuana kwa muda mrefu, hatimaye mama Aidan alifanikiwa kujitoa kwenye mikono ya Mdimu ambaye alionyesha kuwa hoi kutokana na kuelemewa na uchu wa penzi haramu. “Sawa nimekuelewa, nipe muda nikajifikirie tena,” alisema mama Aidan huku akichukua mkoba wake na kuanza kuondoka. Kutokana na hali aliyokuwa nayo, Mdimu alishindwa kusimama na kumsindikiza, akamuacha aondoke mwenyewe mpaka nje ya hoteli hiyo ambapo alisimamisha teksi na kumuelekeza dereva sehemu ya kumpeleka. Akiwa ndani ya teksi, mama Aidan alikuwa akitetemeka mwili mzima kutokana na kilichotokea. Hakuwahi kufikiria hata mara moja kama ipo siku anaweza kuingia kwenye mtego mkali kama huo wa kumsaliti mumewe. Japokuwa ni kweli alikuwa amemkosea lakini mwenyewe alikuwa tayari kumsamehe na hakutaka kumlipizia kwa kumsaliti kama Mdimu alivyokuwa akimshawishi. Njia nzima alikuwa amejiinamia, machozi yakimtoka kutokana na ugumu uliokuwa mbele yake. Kitisho alichokitoa Mdimu kwamba endapo atakataa kuwa na uhusiano naye wa siri basi ataifufua kesi iliyokuwa inamkabili mumewe ya kumbaka Caro, kilimkosesha amani kabisa, akabaki njia panda akiwa hajui kama akubali au akatae. “Mama tumefika,” sauti ya dereva teksi ndiyo iliyomzindua kutoka kwenye lindi la mawazo, kwa kupitia vioo vya teksi aliyokuwa amepanda aliangalia pembeni na kugundua kuwa kumbe ni kweli tayari walikuwa wameshafika sehemu aliyomuelekeza dereva teksi. Harakaharaka alifungua mkoba wake na kumlipa fedha zake kisha akashuka huku akijifuta machozi yaliyokuwa yameulowanisha uso wake. Taratibu akaanza kutembea kuelekea nyumbani kwake huku mawazo machungu yakiendelea kukisumbua kichwa chake. Siku hiyo ilipita huku akiwa amekosa raha kabisa, mumewe na mwanaye Aidan walipomuuliza kilichomfanya akawa kwenye hali hiyo, aliwadanganya kwamba anaumwa sana kichwa. Akawaomba wamuache apumzike, ombi ambalo wote walikubaliana nalo. Kamanda Mdimu aliendelea na kazi yake ya kumshawishi mama Aidan akubaliane na alichokuwa anakitaka, kila siku alikuwa akimpigia simu zaidi ya mara nne, asubuhi, mchana na jioni akimuulizia kuhusu majibu yake. Kila siku jibu la mama Aidan lilikuwa ni kumtaka aendelee kuwa na subira mpaka siku atakayokuwa anampeleka mwanaye Aidan shule. Wiki moja ilipita, hatimaye tarehe ya kufunguliwa kwa shule aliyokuwa anasoma Aidan na Caro iliwadia, kama ilivyokuwa kawaida, wazazi wake walianza kumuandaa kwa ajili ya kwenda shule lakini uchangamfu wao haukuwa kama siku za nyuma. Kila mtu alikuwa akiwaza lake. Kwa kipindi chote hicho, bado Aidan aliendelea kubaki gizani akiwa haelewi ni kitu gani kilichokuwa kinaendelea. Ule utaratibu ambao familia hizo mbili zilikuwa zimejiwekea wa kuwaandaa Caro na Aidan pamoja, safari hii haukuwepo tena, jambo lililozidi kumuumiza mvulana huyo. “Lakini mama, kwa nini hamtaki kunieleza ukweli wa kile kilichotokea kati ya familia yetu na ya akina Caro? Siku hizi hataki kuonana na mimi, wazazi wake wamenikataza nisimfuate nyumbani kwao na sasa hata maandalizi ya kwenda shuleni kila mmoja anafanyiwa peke yake, kwani kuna nini?” “Aidan, ipo siku utaufahamu ukweli lakini kwa sasa elekeza nguvu na akili zako kwenye masomo, haya mambo mengine achana nayo mwanangu,” alisema mama yake Aidan akionesha dhahiri kuficha siri kubwa ndani ya moyo wake. Hatimaye siku ya kuondoka kwenda shuleni iliwadia, safari hii hakupelekwa na baba yake ambaye mara kwa mara ndiye aliyekuwa akiwapeleka na Caro na kuwafuata pindi shule zinapofungwa bali alipelekwa na mama yake. Hata hivyo, ndani ya moyo wake alifurahi shule kufunguliwa kwani aliamini atapata muda wa kuwa jirani na Caro na pengine kuufahamu ukweli uliokuwa unamsumbua msichana huyo aliyetokea kumpenda tangu akiwa mdogo. “Najua nikimbembeleza atakubali kuniambia ukweli wa kinachomsumbua na kwa nini wazazi wake wamenibadilikia ghafla wakati hakuna baya lolote nililolifanya,” aliwaza Aidan akiwa njiani kuelekea shuleni pamoja na mama yake. Walipofika kwenye shule yao, mama yake alimpeleka mpaka kwenye jengo la utawala ambapo alimlipia michango yote muhimu iliyokuwa inatakiwa, akampa na fedha za matumizi kama ilivyokuwa kawaida kisha wakaagana. “Zingatia niliyokwambia mwanangu, elekeza nguvu zako zote kwenye masomo, hayo mambo mengine tuachie tutayamaliza sisi wenyewe,” alisema mama yake Aidan, akamkumbatia mwanaye huyo kipenzi kisha wakaagana, akatoa siku yake na kuanza kuzungumza na mtu ambaye Aidan hakumjua. Taratibu Aidan akawa anavuta begi lake kuelekea bwenini kwake huku akiwa na shauku kubwa ya kuonana na Caro kwani aliamini na yeye atawasili shuleni hapo siku hiyohiyo. Alipogeuka nyuma, alimuona mama yake akiishia kwenye geti huku akiendelea kuzungumza na simu. Baada ya kufikisha mizigo yake bwenini, hakukaa sana, akarudi kwenye jengo la utawala kwa lengo la kumsubiri Caro ili akifika, ampokee kwa uchangamfu. Moyo wake bado ulikuwa na simanzi kubwa kwani tangu alipomtamkia Caro kuwa anampenda, mambo yalikuwa yakienda ndivyo sivyo huku akiwa hajui kosa lake ni nini. Alikaa eneo la utawala kwa muda mrefu lakini hakumuona Caro zaidi ya wanafunzi wengine ambao walikuwa wakiletwa na wazazi wao. Aliendelea kusubiri kwa muda mrefu lakini mpaka giza linaingia, Caro hakuwa ametokea. “Inawezekana leo wamechelewa labda kesho atakuja,” Aidan aalijifariji wakati akisimama pale alipokuwa amekaa kwa muda mrefu akimgoja Caro. Alirudi bwenini kwake ambapo siku hiyo hakupata usingizi akimfikiria Caro mpaka usiku wa manane. Kesho yake aliwahi kuamka na kwenda tena eneo la utawala kumsubiria Caro. Aliamini lazima siku hiyo atamuona kwani kesho yake ilikuwa ni Jumatatu, siku ambayo masomo yangeanza rasmi. Alikaa kwa muda mrefu eneo hilo lakini kama ilivyokuwa jana yake, aliendelea kuwaona wanafunzi wengine wakiwasili lakini miongoni mwao, Caro hakuwepo. Alisubiri kwa muda mrefu lakini mpaka giza linaanza kuingia hakumuona Caro wala kivuli chake, jambo lililozidisha huzuni ndani ya moyo wake. Akapoteza hamu ya kufanya kila kitu. Hakutamani kula wala kujiandaa kwa ajili ya kuingia darasani siku iliyokuwa inafuatia, akawa ni mtu wa mawazo muda wote mpaka wenzake wakawa wanamshangaa kwani haikuwa kawaida yake.
Ni kawaida kila ifikapo saa kumi jioni, Goda ni lazima aende katika shule anayosoma mtoto wa bosi wake Mzee Mheshimiwa Anaeitwa Hemedy kwenda kumchukua kutoka shule kumpeleka nyumbani hapo. Sio kwamba hakukuwa na gari la shule, bali Mzee Mheshimiwa alipenda mwanae huyo wa pekee apelekwe na kurudushwa na gari lake binafsi.
Goda alikuwa ndani ya gari akielekea katika shule anayosoma mtoto wa bosi wake huku akitingisha kichwa chake kufuatisha mdundo wa muziki uliokuwa unapigwa katika radio ya hiyo gari. Alifika katika shule hiyo ya English Medium ikiwa bado kama dakika thelathini ili wanafunzi watoke, Alibadilisha Muziki uliokuwa unakita katika spika za gari na kuweka muziki mwengine ilikuzidi kupata mori wa kusubiri muda wa kutoka wanafunzi wa shule hiyo.
Iliskika kengele iliyo kuwa inapigwa ndani ya shule hiyo kuashiria kuwa muda wa kutoka wanafunzi umefika,Goda aliangaza macho yake kuangalia getini ili aweze kumuona mtoto wa bosi wake atakapotoka, Baada kama dakika tano kupita alianza kuwaona wanafunzi wakitoka ndani ya shule hiyo, alizidi kuangaza macho yake getini lakini hakuweza kumuona mtoto wa bosi wake mwanzo alidhani huenda ikawa bado yupo ndani ya shule lakini kadri muda unavyozid kwenda ndivyo wanafunzi walivyozidi kupungua, wengiwao walipanda katika gari la shule na wengine walipanda katika magari yao binafsi.
Hemedy Hakuwa na kawaida kuchelewa kutoka ndani ya shule hiyo ila siku hiyo alichelewa mpaka akampa wasiwasi Goda, Kuna wazo likamjia kwamba huenda ikawa amepanda katika gari la shule ila wazo hilo hakulipa nafasi sana kwasababu alishawahi kupanda gari ya shule kutokana na marafiki zake wote hupanda gari ya shule, alipo rudishwa nyumbani kwao na gari ya shule Mzee Mheshimiwa alimfokea kwa hasira kwa kitendo hicho cha kupanda gari ya shule, huku akimuacha Goda anamsubiria shule bila mafanikio yoyote, yeye alitaka mwanae apelekwe na kurudishwa na gari lake na sio gari la shule, kesho yake alikwenda mpaka shule na kuonana na mwalimu mlezi wa wanafunzi na kumuambia kuwa yeye mwanae hataki apande gari ya shule, Kuanzia siku hiyo Hemedy alipooneka amependa gari ya shule basi alishushwa na kupelekwa kwenye gari iliokuja kumchukua.
Goda alizidi kuwa na wasiwasi baada ya kuona magari yote yameshaondoka halafu bado hajamuona Hemedy akitoka, akapata wazo kwamba ashuke kwenye gari ili aingie ndani ya shule akaulize kunanini mpaka Hemedy asimuone akitoka nje ya shule. Akashika kitasa cha mlango wa gari na mkono wa kulia ili ashuke chini ila ghalfla akahisi ubaridi katika mkono wake wa kushoto uliokuwa bado umeshikilia usukani, Ubaridi huo ulioanzia kwenye mkono wake ukasafiri mpaka kwenye ubongo wake akijaribu kuutasfiri ni wa nini ila ubongo wake ukakataa kabisa kuutasfiri ubaridi huo ni wa nini.
Ikabidi ageuze shingo yake kwa kasi ya umeme na ndipo alipo pigwa na butwaa, hakuelewa Hemedy ameingia vipi ndani ya gari hadi yeye asimsikie licha ya hivyo pia hakuelewa Hemedy amepitia kwenye malango upi ikiwa yeye macho yake yote yalikuwa kwenye geti la shule na hukuweza kumuona akitoka kwenye geti la shule.
“We mtoto umeingiaje humu kwenye gari? Na mbona sijakuona ukitoka kwenye geti la shule na wanafunzi wenzako?” Goda alimuliza kwa mshangao uliochanganyikana na hofu ndani yake, alipotupa macho yake kwenye mkono wake wa kushoto aliuona mkono wa Hemedy ukiwa upo juu ya mkono wake, ndipo hapo alipopata picha kuwa ule ubaridi alio uhisi ulikuwa umetoka kwenye mkon wa Hemedy.
“Hahahaahah kumbe anko muoga hivyo? Mimi sinimeingia muda mrefu na kukuona wewe unashangaa huko nje, ulikuwa unaangalia nini huko hadi mimi naingia hujaniona?Alisema Hemedy huku akiwa anacheka.
“Kwanza kabla ya yote umepitia wapi mbona sijakuona ukitoka na getini? Aliongea Goda huku akimuangalia mtoto huyo kwa macho ya kuuliza.
“Aaaah!! Acha zako bwana anko kwahiyo hukuniona pale getini wakati natoka? “Sikiliza wewe mtoto usinifanye mimi mtoto mwenzako embu niambie umepitia wapi maana mimi nimeangalia vizuri kwa macho yangu sijakuona ukitoka na getini”
“Hahahahah Subiri nikuambie mimi wakati na nataka kutoka nje nilikuona unaangaza macho yako pale getini, nikaona nikufanyie suprise, nikarudi hadi kwenye vyoo ambavyo vipo huko nyuma ya shule, nikaangalia huku na huku sikuona mtu nikaupanda ukuta wa fensi ya shule hadi juu kwa kutumia matofali yaliyo kuwa pembeni kwa ajali ya kujengea vyoo, nilipofika juu kabisa nikaruka hadi nje ya fensi ndo nikazunguka hadi huku barabarani nikaja hadi hapa kwenye gari nikafungua mlango wewe bado unashangaa tu huko nje, nikakaa nakuangalia tu hadi ulipo taka kufungua mlango ndo nikashtua kidogo tu umeshtuukaa” Alimaliza kumuhadithia huku akicheka.
Goda alibaki ametumbua macho yake kumuangalia mtoto huyo ambae umri wake ni mdogo wa miaka kumi na mbili tu, hakuamini kwamba mtoto kama huyo alielelewa katika maisha ha raha na starehe anaweza akafanya mambo kama hayo, alimuangalia akiwa bado haamini, macho yake yakaganda kwenye mkono wa kulia wa Hemedy uliokuwa na mchubuko uliotoa damu kwa mbali.
“Nahapo kwenye mkono umefanya nini? Alimuuliza huku akimuonyeshea na kidole chake sehemu iliokuwa na mchubuko.
Hapo ndipo Hemedy alipo angalia mkono wake na kukuta kweli ulikuwa unatoka damu kwa mbali, alipo acha kuangalia mkono wake akamuangalia Goda kwa macho ya ‘nitafanya’ nini maana alielewa mama yake akimuona katika hali hiyo lazima atamuhoji na kupelekea kufokewa na yeye hakupenda hayo yote yatokee.
“We mtoto sininakuuliza wewe mbona hunijibu unanitumbulia tu mimacho yako”Goda alimuuliza huku akiwa bado anamuangalia machoni.
“Itakuwa nipale nilipo paramia ukuta” Hemedy alijibu kwa unyonge na uwoga uliochanganyikana ndani yake.
“Kwani hauna kitambara hapo ujifute hiyo damu?
Hapo Hemedy akatoa tabasamu la furaha, akachukua kitambara chake ambacho anakiweka mfuko wa nyuma, akajifuta damu yote ila mchubuko haukuweza kuondoka, Baada ya kumaliza kujifuta damu akamuangalia Goda usoni, Goda akamuonyeshea tabasamu tu na kuwasha gari na kuondoka kwa mwendo wa kawaida.
“Ila siku nyengine usirudie tena upumbavu wako, wewe unadhani kama ingekuwa umeoneka na mwalimu unaruka ukuta siungeadhibiwa na taarifa zinge fika kwa baba yako nae pia angekuadhibu??
“Nimekuelewa anko naomba unisamehe sirudii tena naomba halafu usimwambie baba”Alisema Hemedy huku akimuangalia Goda kwa macho ya huruma, Goda akaachia tabasamu na kumnyooshea dole gumba.
Goda aliendesha gari huku akipiga stori na mtoto huyu wa bosi wake ambae yeye alimchukulia kama mdogo wake tu.
Baada ya kufika nje ya geti la nyumba yao, Goda alipiga honi mara mbili ndipo geti likafunguliwa na mlinzi aliekuwa kwa ndani.
Aliendesha gari hadi kwenye paking ya humo ndani na kuliweka gari katika sehemu husika, Alianza kushuka Goda na kuafuatia Hemedy wote wakaelekea ndani ya nyumba hiyo ya kifahari ilio ya gorofa moja.
Wakaingia hadi sebleni na kumkuta Mwanamke wa makamo amekaa kwenye sofa moja wapo yaliyojazana hapo sebleni. Hemedy baada ya kumuona mwanamke huyo alitupa begi lake la shule chini na kuanzakumkimbila mwanamke huyo ambae hadi muda huo alikuwa ameachia tabasamu usoni kwake. Hemedy alienda na kumkumbatia mwanamke huyo ambae na yeye alitanua mikono ya kumpokea Hemedy.
“Good evening my mom”
“Mwanangu nimeshakuambia mimi mama yako sijasoma, sijui kingereza sasa mbona unaniabisha mama ako?Mwanamke huyo alimwambia Hemedy huku akitabasamu.
“Hahahah Mama nawe sasa kwanini hujasoma? Hemedy aliuliza.
“Nyie mliopata bahati ya kusoma someni tu kipindi hichi sio sawa na kile cha zamani, ilikuwa mtoto wakike akifika darasa la saba tu haendelei tena na shule eti kwavile atakuja kuolewa na kuwa mama wa nyumbani, basi ikawa tunaishia darasa la saba tu ila mimi nilikuwa nina akili sana sema ndo hivyo tu sikubahatika kuendelea na shule, yani zile akili potofu sijui walizitolea wapi wale wazee wa zamani?
Baada ya kusalimiana na Mama yake, Hemedy alinyoosha hadi kwenye ngazi na kuzipanda kuelekea juu katika vyumba vya juu ya nyumaba hiyo ya gorofa, huko ndo kilipo chumba chake chakulala, huku nyuma akifuatiwa na Goda akija na begi la Hemedy alilolitupa mlangoni.
“Hivi anko na wewe pia haukusoma eee? “
“Kwanini umeniuliza hivyo anko?”
“Mama sikasema kuwa nyie watu wa zamani hamkusoma?”
“Hahahahah Anko wewe unamatatizo sana, Mama sikasema wanawake ndo walikuwa hawasomeshwi, halfu mimi sio mtu wa zamani”
“Kwani wewe unamiaka mingapi anko?”
“Mimi nina miaka ishirini na nne tu, embu acha kuongea sana vua ngua za shule twende kula, au wewe husikii njaa?” Hemedy alibadilisha nguo za shule na kuingia chooni kwenda na kuoga. Alivyotoka chooni alivalia track suti na jezi ya mpira, baada ya kumaliza kuvaa aliongozana na Goda kuelekea sebleni na kwaajili ya kwenda kula.
Ilikuwa ni kawaida kwamba Goda alishajizoesha kutokula mpaka hemedy atakapo rudi shule ili ale pamoja na Hemedy. Wakati wanashuka kwenye ngazi kuelekea sebleni, Hemedy alisimama na Kumuangalia Goda kwa uso wa wasiwasi.
“Vipi mbona umesimama halafu unaniangalia hivyo?”
“Anko nakuomba usimwambie mama kama nimeruka ukuta shule” aliongea kwa unyonge akiwa bado macho yake ameyagandisha usoni kwa Goda. Hemedi aliogopa sana kufokea na mama yake ndo maana hadi sasa ana wasiwasi kitendo chake alichokifanya shule cha kuruka ukuta kinaweza kujulikana na wazazi wake. Goda alimtolea tu tabasamu na kumshika mkono kwenda nae sebleni.
*******************************
“Ohhhh my only boy how ar….. “
“Aaa aaa!!! Dady kuanzia leo mimi sitaki kuongea tena kuongea kigereza hapa nyumbani”
“Kwanini my boy?”
“Mama hajui kingereza na mimi sitaki tena kuongea kingereza, kwanini hujampeleka kwenda kusoma au wewe hutaki mama akiongea kingereza?”
“Hapana my son mama yako alikataa mwenyewe kwenda kusoma kingereza sasa na mimi sikutaka kumlazimisha, hata umulize mwenyewe atakuambia”.
Mazungumzo hayo yalifanywa na mtoto na baba yake, Majira hayo ya saa moja jioni ndio muda ambao Mzee Mheshimiwa ana rudi nyumbani kwake akitokea kazini. Mzee Mheshiwa alikuwa ni katika matajiri waliopo katika mji huo wa Tanga, anamiliki showroom ya magari na Sheli za mafuta zilizopo ndani ya mji huo wa Tanga. Mzee Mheshimiwa alipandisha ngazi hadi chumbani alipo ingia mke wake wake.
“Za kazi mume wangu?”
“Safi tu”,Alijibu Mzee Mheshimiwa na Kuuliza“sijui za hapa nyumbani”
“Hapa nyumbani tunamshukuru mungu ni wazima”.
Familia ya Mzee Mheshimiwa ilikuwa ni familia yenye furaha kila siku na walimuomba mungu furaha iyendelee kila siku, Mzee Mheshimiwa alifanya kila awezalo ilamradi familia yake iwe na furaha, Halkadhalka pia Mama Hemedy alifanya kila awezalo ili familia yake iwe na furaha.
Kwakila mwenye mafanikio hakosi maadui na huwezi kuishi na furaha siku zote kwasababu kuna watu hawataipenda furaha uliyo nayo watahakikisha wafanye kila wawezalo ilimradi tu usiwe na furaha.
Mzee Mheshimiwa alijiona ni mwenye furaha siku zote kila anapoangalia familia yake na mali zake. Hakujua kuwa kuna watu wanao angalia mafanikio yake kwa jicho la tatu, hawakupenda kumuona akiwa na mafanikio kiasi hicho, na walipanga kumfanyia UHASAMA yeye na familia yake na mali zake alizokuwa nazo.
*****************************
Majira ya usiku ya siku hiyo hiyo, upande wa pili kulikuwa na kikao kizito kilicho usisha watu watatu wenye mpango wa kumuondosha duniana Mzee Mheshimiwa na familia yake na kuchukua kila kilicho chake ili wajinufaishe wao, watu hawa ndiyo waliopanga kumfanyia UHASAMA Mzee Mheshimiwa.
“Kama tulivyo panga kuwa tutamvamia usiku akiwa yupo na familia yake ilituweze kumsainisha mali zote halafu baada ya hapo tunaua yeye na na familia yake, au sivyo Mata”
“Ni thawa kama itakuwa ndo hivyo ilimradi mpango wetu uwende thawa bathi hakuna shaka, ila thatha itabidi Mrutu wewe uthiende eneo la tukio kwathababu yule ni kaka yako anawedha akakujua” Mata hawezi kuongea vizuru kwasababu alikuwa na “Kilimi” kwenye “S” anaweka “Th” akitaka kusema “Sasa” basi atasema “Thatha na kadhalika pia kwenye “Z” anaweka Dh.
“Hahahaha Mata bwana sasa hatakama akinijua atafanya nini wakati tutamuua hapo hapo?”Aliongea Mrutu kumshangaa Mata kwa maneno aliyo ya sema. Mrutu ni mdogo wake na Mzee Mheshimiwa, Wamezaliwa na Baba mmoja ila Mama mbalimbali.
“Hatakama ila inabidi wewe uthionekane kwathababu yule ni ndugu yako unawedha ukaleta huruma halafu katika kadhi kama hii hakutakiwi mtu mwenye huruma, Ila wewe itabidi ubaki tu ndani ya gari ututhubirie, thithi tuna ingia ndani tunaua halafu tunatoka tunaondoka dhetu, au wewe unathemaje Moto?”
“Yeah inabidi iwe hivyo”
“Poa kama ndo mnavyotaka, sasa kwahiyo hii kazi tutaifanya wenyewe watatu?”
“Nyie mthijali mimi kuna vijana nawajua ni watu wa kadhi kadhi, nitawaita watuthaidie hii kadhi”
“Hao vijana wapo wangapi?”
“Tuta chukua vijana wawili tu wanatosha, halafu nina waamini kwathababu nishawahi kufanya nao kadhi nyingi tu”
“Sawa wewe inabidi uwasiliane nao sasa hivi uwapange kwamba kazi inaendaje na malipo yao ni shilingi ngapi, ili kazi ikishakwisha tusisumbuane”. Moto alihitimisha kikao hicho kifupi kilichokuwa na mpango wa kufanya uhasama kwa Mzee Mheshimiwa.
Baada ya kumaliza kikao hicho, waliondoka na kuhaidiana kuwa wakutane siku inayofuata ili waifanye kazi waliyoipanga.
* * * *
Siku iliyofuata. Nyumbani kwa Mzee Mheshimiwa 3:22 Usiku. Akiwa yupo na familia yake wakiwa wapo mezani wanapata chakula cha usiku. Mzee Mheshimiwa alikuwa ni binadamu kama binadamu wengine, hakuweza kujua kuwa siku hiyo kwake yeye na familia yake inaweza kuwa ni siku mbaya. Wahenga hawakukosea walipo sema “Usilo lijua ni sawa na usiku wa giza”.
Mzee Mheshimiwa hakujua kuwa usiku huu kwake unaweza kuwa ni wa giza, na sio yeye tu hata watu aliokuwa nao katika nyumba yake pia hakuweza kujua kuwa usiku wa siku hii unaweza kuwa ni wa giza.
“Hivi baba wewe unasoma ili baadae ujekuwa nani katika huu ulimwengu?” Mzee Mheshimiwa alimuuliza mwanae Hemedy wakiwa wamemaliza kula chakula na wamekaa sebuleni. Ilikuwa ni kawaida yao kwamba wakimaliza kula chakula cha usiku wanakaa sebuleni kabla ya kwenda kulala na kuongea mawili matatu au kuangalia televisheni iliokuwepo hapo sebleni.
“Mimi nataka kuwa mwanasheria” alijibu Hemedy.
“Kwanini unataka kuwa mwanasheria?”
“Nataka kutetea haki kwa wale wanaodhulumiwa mali zao na kwa wale wanao kwenda jela bila hatia kwa kusingiziwa kesi am………” Ghalfa macho yao wote waliyaelekeza mlangoni baada ya kusikia kishindo cha mlango ukiwa umefunguliwa kwa nguvu. Wakiwa bado wamepigwa na butwaa, waliingia wanaume wanne wawili wakiwa na bunduki mikononi na kuwaelekezea wao.
“Hapo hapo mlipo, hakuna mtu yoyote kujigutha wala kufanya chochote kile tofauti na maelekedho yangu, nyote mnatakiwa kufuata kile ninachothema” Mata aliwatisha huku akiwa amewaelekezea bunduki. Mzee Mheshimiwa alikuwa katika hofu kuu kuliko wote waliokuwepo hapo japokuwa na wao pia walikuwa na hofu, hawakuzitambua sura hizo zilizo ingia humo ndani, sura zote zilikuwa ni ngeni kwenye macho yao.
“Nyote pigeni magoti chini” Mzee Mheshimiwa hakuelewa watu hao wanataka kitu gani kwake, maana yeye akifikiria hakuwahi kuwa na UHASAMA na mtu yoyote yule katika ulimwengu huu, alichofikiria yeye kuwa huenda watu hao wanataka pesa na sio kitu kingine, akaamua kuyajaribu mawazo yake kwa kuwauliza wanachokitaka kuwa ndio hicho alicho fikiria yeye.
“Mnataka nini jamani? Au kama mnataka pesa subirini nikazichukue zipo ndani nije niwape mtuach…..”
“Nyamadha wewe, nani aliekupa ruhutha ya kuongea? Thithi hatutaki petha tu, tunataka na nyaraka dhote dha mali dhako ulidhokuwa nadho ndipo tukuachie na familia yako”. Licha ya kuwa Mzee Mheshimiwa anaipenda familia yake, pia alikuwa anazipenda maliza zake, hakutaka masihara linapokuja swala la pesa. Hata hivyo alilinganisha kati ya familia yake na mali zake,kipi bora kwa wakati huo, akafikiria akitoa mali zake zote jinsi atakavyokuwa fukara wa kutupwa akitanga tanga yeye na familia yake, atakavyoomba msaada kwa matajiri wenzake, mwanzo watamsaidia ila mwisho watamchoka, ndipo hapo sasa atakapo tamani kujiua, wazo la kutoa mali zake akaliweka kando kwanza.
Akafikiria kifo kinafanana vipi? Ila akashindwa kupata jibu kwasababu hakuwahi kufa, hata hivyo pia akijifanya mbishi kuwa hataki kutoa mali zake ili kuokoa uhai wake na familia yake, watamuua na kuzichukua vilevile mali zake japokuwa sio zote, yote hayo yalipita ndani ya kichwa chake kwa haraka sana akitafuata uchambuzi kipi afanye kipi aache, akaona ni bora awape wanachokitaka kwasababu hata hivyo mali zinatafutwa.
Akiwa bado anawaza, alishtushwa na sauti ya bunduki iliyopigwa kwenye bega la Goda, Goda aligugumia kwa maumivu kwa risasi iliyo ingia kwenye bega lake la kushoto.
“Huyu tumemuonjesha tu, ukiendelea kutupotezea muda basi ujue tutafumua kichwa cha mke wako”. Aliongea Moto huku akiwa na gadhabu, hapo ndipo Mzee Mheshimiwa alipo jua kuwa hakukuwa na utani kwenye suala hilo, aliinuka taratibu na kuongoza njia kupanda ngazi kuelekea chumbani kwake akifuatiwa na Mata huku akiwa amemuelekezea bunduki kichwani, Mzee Mheshimiwa hakuwa na ujanja mwengine zaidi ya kufuata maelekezo anayopewa, sio kwamba hakuwa na bastola yake, alikuwa nayo ila kwa wakati huo hakuwa na ujanja wa kuichukua kwasababu alikuwa ameelekezewa bunduki kichwani mwake.
Alipelekwa hadi chumbani kwake na kuuendea mokoba wake wenye nyaraka zote za mali zake, aliuchukua na kurudi nao hadi sebleni huku akiongozwa na Mata aliemuelekezea bunduki kichwani, alimuangalia mke wake jinsi anavyolia, alimuangalia mtoto wake jinsi atakavyo kwenda kuteseka kwa njaa, alifikiria mtoto wake atavyoenda kuacha shule kutokana kukosa pesa ya kumlipia ada, alifikiria jinsi mtoto wake atakavyo poteza malengo yake ya kuwa mwanasheria kama mwenyewe alivyopenda kujakuwa mwanasheria na kuwatetea wanyonge wanaodhulumiwa mali zao kama yeye anavyoenda kudhulumiwa muda si mrefu na watu hao yeye aliodhani kuwa ni majambazi, yote hayo yalipita ndani ya kichwa chake.
Hakuwa na jinsi nyengine ya kufanya zaidi ya kufuata kile alichoambiwa, akapiga saini kuwa mali zote alizokuwa nazo kwa wakati huo sio zake na amekubali kuzitoa yeye mwenyewe, aliandika barua na kuweka saini huku akiiangalia familia yake kwa masikitiko sana, alitamani iwe ni ndoto halafu baada ya muda mfupi ainuke akute hakuja tokea kitu kama hicho, ila haikuweza kuwa ni ndoto bali ni tukio linalotokea “Live” huku yeye na familia yake wakishuhudia.
Alipo maliza kuweka saini kila sehemu ya mali zake, aliwapa nyaraka zote, Mata alizipokea na kuanza kuzisoma moja baada ya nyengine, aliachia tabasamu la ushindi na kuwapa ishara wenzake kuwa kazi walioifanya imekamilika, Goda kipindi chote hicho yeye haikujulikana kuwa amekufa au bado ni mzima kwasababu alikuwa yupo chini amelala kimya bila kujitingisha.
Mata aliyoonekana kuwa ndio kiongozi wao, alitoa ishara amabayo Mzee Mheshimiwa na watu wake hawakuiyelewa, walishtuka tu kuona wafanyakazi wao mmoja baada mwengine akianguka sakafuni na kutulia tuli, hapo ndipo Mzee Mheshimiwa alipoona kuwa mambo yamebadilika, haikuwa kama vile walivyo ahidiwa kuwa wakishatoa mali zote basi wataachiwa waende, kuja kushtuka alimuona mke wake na yeye akienda chini na kutulia tuli kama ilivyokuwa kwa wafanyakazi wake.
Haikuwa picha nzuri kushuhudiwa na mtoto wake ambae hadi sasa anamiaka Kumi na mbili tu tangu aanze kuiyona hii dunia iliyojaa makatili kama hao ambao kwao kuua ni jambo dogo sana, kuua mtu kwao ni kama kuua mbu ndani ya chandarua, hadi sasa walibakia wawili tu ambao ni wazima yeye na mwanae mpendwa Hemedy, wakati yote yanatokea alikuwa amezibwa mdomo asiweze kupiga kelele, alishuhudia Anko wake akipigwa risasi ya bega na kuenda chini, alishuhudia wafanyakazi wao walivyopigwa risasi za vifua na kwenda chini mbaya zaidi alishuhudia mama yake mzazi akipigwa risasi ya shingo naye pia akiungana na wenzake akaenda chini, akajua baada ya hao kwenda chini basi ni zamu yao yeye na baba yake, alikuwa na umri mdogo hakuwa na ubavu wa kushindana nahao majitu aliyo ya fananisha na izrael mtoa roho za watu, ikiwa baba yake ameshindwa kushindana nao, vipi yeye mtoto mdogo ataweza kushindana na mijitu hiyo? Hakua na namna nyengine zaid ya kusubiri kifo chake.
Bila kutarajia aliinuka ghalfa na kumfuata mke wake alie kuwa chini kwa wakati huo ameshikilia shingo yake akishindana na malaika mtoa roho almaarufu kama izrael, kabla hajamfikia mke wake, alihisi kama kuna ubaridi katika mbavu zake, alijaribu kuutafsiri ubaridi huo ni wa nini ila akshindwa kupata jibu sahihi, ila ghafla ubardi huo ukabadilika na kuwa umoto wenye maumivu ndani yake, akiwa bado hisia zake hazijampa jibu kuwa ni kitu gani hicho chenye ubaridi na umoto wenye maumivu, akaona asibitishe kwa macho yake mwenyewe kwa vile hisia zake hazija mpa jibu sashihi.
Akayapeleka macho yake kwenye sehemu yenye ubaridi na umoto wenye maumivu, na kukuta damu zinatoka kwa wingi kwenye mbavu zake, hapo akajua kwamba hiyo ni risasi imepenya kwenye mabavu zake. Kabla hajakaa sawa alipigwa tena risasi ya kichwa na kufumuliwa ubongo wake, na yeye akawa ameungana na wenzake chini sakafuni, wakiwa tayari kwa maandalizi ya kupelekwa makaburini kwenye nyumba zao za milele. Walikuwa ni wafu tayari.
“Mshtue MRUTU aweke gari sawa tuondoke kabla nzi hawaja kuja”. Hayo ndo maneno ya mwisho kuyasikia kabla hajazimia, hakuna kitendo kilichomchanganya akili kama kuona Mama yake ameuliwa mbele yake na Baba yake pia ameuliwa mbele yake tena kwa kifo kibaya cha kupigwa risasi mbili moja ya mbavu, nyengine ya kichwa iliyo sababisha sakafu ichafuliwe na ubongo, akajikuta na yeye kimyakimya anapoteza fahamu bila kutarajia.
“Tumemalidha twendeni thatha”
“Na huyu mtoto tunamfanya nini?” aliuliza mmoja wapo katika hawa vijana wawili waliokodiwa.
“Huyu kashakufa kwa mshtuko kwahiyo haina haja tena ya kummalizia, twenzetuni tusipoteze muda” Moto aliongea na kuwafanya wenzake waanze kutoka mmoja mmoja, hawakusahau mkoba uliokuwa na nyaraka za mali, walitoka nao pia.
* * * *
Baada ya nusu saa Hemedy aliinuka kutoka katika ulimwemu mwengine wa kupoteza fahamu, alishangaa kuona Baba, Mama na Wafanyakazi wengine wamelala sakafuni, kitu kilicho mchanganya zaidi baada ya kuona damu sakafuni, alijiuliza imekuaje tena watu wamelala na damu imesambaa sakafuni? Ndipo hapo tukio lililotokea nusu saa kabla lilipo jirudia kichwani mwake, aliinuka kwa haraka sana hadi walipo lala wazazi wake, alilia huku akijaribu kuwaamsha bila mafanikio yoyote, walikuwa wameshakufa alilijua hilo ila hakutaka kukubaliana nalo moja kwa moja, aliendelea kuwaamsha akidhani huenda ikawa kilio chake wanaweza kukisikia ila haikuwa kama alivyotaka iwe, ilikuwa ni kweli usiopingika kuwa wazazi wake wameshaonja umauti kama ilivyosemwa katika vitabu vya dini. “Kila nafsi itaonja umauti”
Goda alihisi maumivu kwenye bega lake, ila hakuweza kujua maumivu hayo yametokana na nini, akajaribu kurudisha kumbukumbu zake nyuma ili aweze kukumbuka ni kitu gani kinachofanya bega lake liume maumivu ambayo hakuwahi kuyahisi kabla, ni kweli alijaribu kuunganisha tukio lililotokea muda si mrefu kabla hajapoteza fahamu iliyosababishwa na maumivu na kutokwa na damu nyingi kwenye bega, alikumbuka kuwa alikuwa wamekaa sebleni baada ya kumaliza kula, wakawa wanapiga stori, kabla stori hazija isha wakaingia wanaume wanne wakiwa wameshika bunduki, wakimlazimisha Bosi wake atoe nyaraka zote alizokuwa nazo, mwisho kabisa akashtuka amepigwa risasi ya bega, baada ya hapo hakuelewa ni nini kilicho endelea, akapoteza fahamu.
Alifumbua macho yake taratibu baada ya kusikia sauti ya kilio, sauti hiyo aliijua kuwa ni ya Hemedy mtoto wa bosi wake, akajaribu kujiinua taratibu akiwa bado na maumivu yasio ya kawaida akiyahisi katika bega lake, alikaa kitako na kushuhudia mabosi zake na wafanyakazi wenzake wakiwa wamelala sakafuni, alielewa moja kwa moja kuwa hakukuwa na mzima hata mmoja kutokana na damu zilizotapakaa katika miili yao, akajivuta taratibu kutokana na maumivu aliyokuwa akiyahisi kwenye bega, na kamfanya atambae kama mtoto mdogo.
Akaanzia kwa wafanyakazi wenzake kuskiiliza mapigo ya mioyo yao na kukuta wote walikuwa wameshakufa, akatupa macho yake kwa mabosi zake, picha aliyoiyona ilimuogopesha hata yeye baada ya kuona ubongo wa Bosi wake Mzee Mheshimiwa ukiwa upo nje, akajivuta tena hadi kwa mabosi zake, hakuwa na haja ya kuhakikisha kuwa wameshakufa kutokana na risasi walizopigwa, zilipigwa katika maeneo ambayo hata angewahi daktari wa aina gani asingeweza kuokoa maisha yao, Mama Hemedy alipigwa risasi ya shingo na Mzee Mheshimiwa alifumuliwa ubongo wake, walikuwa wameshakufa zamani.
Alichofanya ni kumfuata Hemedy aliekuwa amezing’ang’ania maiti za wazazi wake akiwaamsha bila mafanikio yoyote, alilia kwa uchungu sana kilio ambacho hakuwahi kulia tangu azaliwe, Goda alimfuata na kumuondoa karibu na maiti za wazazi wake na kumpeleka pembeni huku akijaribu kumtuliza, Hemedy alikuwa na uchungu mkubwa sana, alilia kwa kuwapoteza wazazi wake wote wawili kwa wakati mmoja, ali huzunika, ali sikitika, kufumba na kufumbua tayari ameshakuwa yatima.
Goda maumivu bado yaliendelea kumtesa akafikiria afanye nini kwa wakati huo, ndipo alipo kumbuka kuwa nyumba hiyo ya kifahari ilikuwa na camara za CCTV za kurikodia matukio yote yanayofanywa katika hiyo nyumba, aliinuka kwa taabu sana na kusimama, akajaribu kutembea hadi kwenye ngazi na kupanda kuelekea juu, alipanda kwa taabu sana huku akijisaidia na mkono wake mwengine, alienda hadi katika chumba cha kuongozea kamera na kuanza kuangalia matukio ya siku hiyo, alilipata tukio lililofanyika muda si mrefu, alichukua flash na kuichomeka kwenye kompyuta na kuanza kulinyonya tukio lote, tokea lilipoanza wakiwa wameka sebleni hadi walipoingia watu wasio wafahamu wakidhani ni majambazi hadi walipoondoka, alipomaliza akaichomoa flash na kutoka kwa tabu sana ikiwa hali yake ndo inazidi kuwa mbaya kutokana na risasi iliyozama ndani kabisa kwenye bega lake. Alishuka nayo hadi chini na kumkuta Hemedy bado anawalilia wazazi wake, alipomfikia akamshika bega, Hemedy aligeuza shingo yake na kumuangalia Goda, Macho ya Hemedy yalikuwa mekundu kwa kulia.
“Hemedy shika hii flash ndiyo ina video yote ya mauaji ya wazazi wako, ishike vizuri na usiipoteze, halafu hakikisha unakuwa nayo wewe mwenyewe” Goda aliongea kwa tabu sana huku akimkabizi Hemedy Flash yenye tukio zima la mauwaji ya wazazi wake. Hemedy akaipokea hiyo flash na kuendelea kulia, Goda alimfuata na kum’bembeleza. Ila Hali yake ilizidi kuwa mbaya sana, baada ya kuanza kuona nyota nyota kwenye macho yake.
“He..medy ondo…ka ha..pa sio sa…lama kwa..ko, na ukumbuke hi..yo fla..sh ndiyo ina tuki…o lote, haya o..ndoka hapa sio sa…la..ma kwa….” Goda hakuweza kuimalizia sentensi yake na yeye akaungana na wenzake walio lala sakafuni. Akawa amekufa.
Hemedy alilia sana baada ya mtu aliebakia hai na yeye kupoteza maisha, hakua na jinsi nyengine, akanyanyuka na kuiangalia familia yake iliyokuwa imelala sakafuni bila uhai wowote, flash aliyopewa na Goda alipo ambiwa kuwa ndo inatukio zima la mauaji ya wazazi wake, aliitia katika mfuko wake wa suruali na kutoka nje, huko napo alishuhudia miili ya walinzi wao ikiwa nayo imelala chini, moja kwa moja akajua na wao wamekufa.
Alifungua geti kwa wasiwasi na kutoka hadi nje ya nyumba yao, hakuelewa aende wapi usiku huo, hakuwahi kulala nje ya nyumba yao hata mara moja, na hiyo ilikuwa ndo mara yake ya kwanza kulala nje ya nyumba yao, aliiangalia kwa masikitiko makubwa, alielewa kuwa yeye hadi muda huo tayari ameshakuwa yatima, alielewa kuwa na yeye muda si mwingi ataenda kuwa chokoraa, alijua na yeye kuanzia hapo ni mtoto wa mtaani, hakuwa na namna ya kufanya aliendelea na safari yake asiyoijua mwisho wake ni wapi.
Akaikata mitaa asijue anapoelekea ni wapi, hadi kwenye kibaraza cha nyumba ambayo haikumaliziwa na kukaa hapo kwa muda mrefu.
*****************************
“Baba lucas hivi huo mlio ni wa nini”
“Sijajua bado ni wa nini ilaa… tuachane nao bwana kwanza mimi nina usingizi acha nilale” Maongezi hayo yalikuwa yanafanyika nyumba ya jirani kabisa na nyumba ya Mzee Mheshimiwa, mlio walio usikia watu hao wa nyumba ya jirani, ulikiwa ni mlio wa kwanza kabisa alipopigwa Goda risasi ya bega baada ya Mzee Mheshimiwa kugoma kutoa nyaraka zake.
“Mhhhh!!!! Mbona umejirudia tena? Mama lucas alizidi kupatwa na hofu maana ilikuwa sio kawaida, Kabla hawajakaa sawa waliendelea kuiskia kama mara tano tena imelia kwa kufuatana, hapo sasa Baba lucas ndipo alipoelewa kuwa hiyo ni milio ya risasi, akainuka na kuiyendea bastola yake iliokuwemo kwenye droo, akachungulia dirishani ila hakuweza kuona kitu kutokana na ukuta wa fensi ya nyumba yake, akatoka hadi sebleni, hakuelewa afanye nini kwa wakati huo, mara ghafla akamuona mke wake akitoka na simu iliyokuwa ina ita.
“Nani anayepiga simu usiku huu?” Baba lucas aliuliza.
“Ni Mzee John” Baba lucas akaichukua simu yake ambayo bado ilikuwa inaita, akaipokea baada ya kugundua kuwa anaepiga simu ni jirani yao.
“Vipi John mbona wapiga simu usiku kuna nini?”
“Kwani wewe hukuisikia hiyo milio ya risasi hapo kwa Mheshimiwa?”
“Nimeisikia, kumbe inatoka hapo kwa Mzee Mheshimiwa?”
“Ndio tena naona kulikuwa kuna gari hapo nje kwake, kuna watu wametoka kwenye nyumba yake na wamepanda kwenye hilo gari na kuondoka, ila mimi ninahisi ni majambazi hao”
“Sasa itabidi tupige simu polisi au wewe unasemaje”
“Eeeeee itabidi iwe hivyo”
“Sasa nani atakae piga simu, mimi au wewe?”
“Piga tu wewe” walihitimisha maongezi hayo yaliyo fanyika katika simu, Baada ya kukata simu Baba lucas akawapigia simu polisi na kuwaambia kila kitu, akaambiwa aelekeze mtaa wa tukio lilipo fanyika, akawaelekeza vizuri na kuambiwa kuwa polisi watafika muda si mrefu.
Baada ya kama dakika kumi na tano wakasikia mlio wa gari nje kwenye nyumba ya Mzee Mheshimiwa, walianza kutoka kwa uoga na kwa uwangalifu mkubwa, maana hawakuwa na uhakika kwamba mlio wa gari waliousikia ni wa polisi au ndo wavamizi wamerudi. Walichungulia kwenye uzio wa nyumba yao na kuona ni kweli gari ya polisi ndio imepaki nje ya nyumba ya Mzee Mheshimiwa, Baba lucas na mkewe walitoka hadi nje na kumkuta John na majirani wengine wameshatoka, wote waliongozana hadi ndani ya nyumba hiyo, kwa picha waliyoiona wenye mioyo mepesi walilia na wengine hawakutaka tena kuangalia, maana ubongo wa Mzee Mheshimiwa ulikuwa nje.
“Jamani tunaombeni nafasi, embu tokeni nje tufanye kazi yetu” Kwakuwa polisi wamekuja na wanafanya kazi yao kama wenyewe walivyosema, hawakuwa na budi zaidi ya kwenda kusubiri nje, polisi walipiga picha maiti zote na kupiga simu hospitali kwajili ya kuomba gari la wagonjwa ili kuja kubeba maiti zilizopo eneo la tukio. Maiti zilitolewa moja baada ya nyengine na kupelekwa katika gari la wagojwa lililopaki nje ya nyumba ya marehemu Mheshimiwa, maiti ziliingizwa zote kwenye gari la wagonjwa.
“Hivi waungwana ni nani aliye piga simu polisi?” askari mmoja anaeitwa Koplo Taure aliwauliza majirani waliokuwa bado wamesimama nje ya nyumba.
“Ni mimi hapa Afande” Baba lucas alijibu na kujipenyeza kwenye kundi la watu, akafika hadi kwa Koplo Taure.
“Hembu njoo maramoja tuongee” Baba lucas hakuwa na pingamizi, walienda hadi pembeni kidogo na kuanza kuongea.
“Mimi nilikuwa nimepumzika nyumbani kwang……….”Baba lucas alielezea tukio zima kama alivyo ambiwa na Mzee John lilivyokuwa.
“Unaweza Ukaniambia Mzee Mheshimiwa alikuwa anaishi na nani?”
“Alikuwa anaishi yeye, Mke wake na Mtoto wao mmoja na wafanya kazi wa tano, watatu walikuwa wa kiume na wawili walikuwa wa kike”
“Huyo mtoto wao anaumri gani?”
“Mtoto wao ni mdogo tu nahisi ana miaka kati ya kumi hadi kumi na mbili hivi”
“Sasa mbona sisi hatukuona mtoto yoyote mule ndani, Na tumeangalia nyumba nzima?”
“Mmmmh! Kwa hapo sasa sijajua, au labda itakuwa wameondoka nae”
“Wakina nani?”
“Si hao wavamizi, itakuwa wameondoka na huyo mtoto”.
“Haya asante kwa ushirikiano, acha sisi tuende kituoni, tutaendelea na uchunguzi wa kina”
“Kwahiyo afande hakuna hata mmoja aliekuwa hai?”
“Wote wamekufa, hakuna mzima hata mmoja”
Koplo Taure akaridhika na maelezo hayo mafupi, wakapeana mikono na kumruhusu Baba lucas kuondoka, Maaskari baada ya kufanya uchunguzi wao waliifunga nyumba kwa usalama zaidi na kuondoka zao.
*************************************
“Mwiziiii mwiziiii mwiziii”
Zilikuwa ni kelele za raia wenye hasira kali, wakimkimbiza mwizi majira hayo ya usiku, walikuwa wamechoshwa na vibaka hao wanao sumbua mtaa wao. Kijana mdogo aliekuwa anakimbia kama Usain Bolt ilikuokoa roho yake zidi ya raia wenye hasira kali, alionekana kukata tamaa, maana kila anapo kunja kona ndipo raia wanapozidi kutoka majumbani mwao, na hivyo ilikuwa ni usiku basi kelele ndo zilizidi kupaa na kuwaamsha watu wengine, hakuelewa atafanya nini ilikuiyokoa nafsi yake, alitubu dhambi zake kimya kimya huku akikimbia na kumuahidi mungu kuwa kama atapona kwenye hilo zahma basi atamrudia mungu wake, pamoja na kuwaza yote hayo bado hakuacha kukimbia.
Hemedy aliziskia hizo kelele za mwizi akiwa bado amekaa kwenye kibaraza cha nyumba hiyo iliyokuwa bado haijamaliziwa, alikuwa na wasiwasi hakuwahi kulala nje hata siku moja, akafikiria afanye nini usiku huo wenye mashaka kwake, ila hakuwa na cha kufanya, alisimama na kuangaza huku na huko, ghafla akamuona mtu akija mbio ule upande aliokuwepo yeye, hakujua akimbie au abaki, kiufupi hakuwa na chaguo sahihi, katika hali ya kuogopesha yule mtu alikuja hadi pale alipo huku akiwa ana hema.
“Vipi wewe hujaskia kelele za mwizi” yule mtu alimuuliza, Hemedy alizidi kupatwa na hofu, wasiwasi, mashaka na uoga vyote vilimjia kwa pamoja, akabaki ameganda asijue afanye nini, akatingisha kichwa kukubali kuwa ameiskia kelele hiyo ya mwizi.
“Basi kimbia maana hao watu wakija huku watakuua watadhani wewe ndo mwizi, sasa mimi nakushauri kimbia” Maskini Hemedy hakuelewa kuwa anataka kuingizwa katika matatizo mengine ikiwa yale ya mwanzo ameyakwepa, na kwavile alikuwa ni mtoto wa kishua mambo ya uswazi hakuyajua vizuri, bila kujifikiria bila kujiuliza akaanza kukimbia sehemu asiyoijua, yule kijana baada kuona mpango wake umekamilika, akaingia kwenye ile nyumba ambayo haikumaliziwa ambapo mwanzo alikuwa Amekaa Hemedy, aliingia ndani yake na kutulia tuli.
Baada ya muda si mrefu alishuhudia kundi la watu wenye silaha kali wakipita mbio mbio kuelekea upande ambao Hemedy ameelekea, walipoisha wote akatabasamu na kujibanza humo humo ndani.
Hemedy alikimbia mpaka akachoka, akaanza kusikia kelele za mwizi zikizidi kumkaribia, hakuelewa atafanya nini, hakuelewa atajinusuru vipi na hilo zahma ambalo sio lake, hakuelewa asimame au aendelee kukimbia, akaona ni bora aendelee tu kukimbia, kwavile hakuijua mitaa hiyo vizuri akajikuta anaingia katika uchochoro ambao mbele yake kulikuwa na kundi la watu wanakuja mbio kwa hasira wakiwa wameshika silaha kali, Hemedy alisimama na kuanza kugeuza, alikimbia lakini watu hao bado walikuwa nyuma yake, kwavile siku ya kufa nyani miti yote inateleza, Hemedy na yeye alikuwa ni nyani na miti yote ili mteleza, uhai wake siku hiyo aliuona ukimtupa mkono.
Mbele yake kulikuwa kuna kundi jengine lina kuja wakiwa wameshika silaha kali, Hemedy hakuelewa afanye nini baada ya kuzungukwa na watu hao wenye hasira kali na waizi waliokuwa wanawasumbua kila siku, Bila kuuliza watu walianza kumpiga mawe bila kujali umri wake, walimpiga bila kujua kuwa huyo wanaempa adhabu hiyo, haikuwa ikimuhusu na wala haiku mstaili, walimpiga vibaya sana, huku wakishangilia wakidai kuwa watawakomesha waizi hao mmoja baada ya mwingine hadi waizi wote waishe.
“Nipisheni, nipisheni”
Zilikuwa ni kelele za raia mmoja, alie jifanya kuwa na hasira kali kuliko wenzake wote waliokuwepo, pengine hata kumzidi huyo aliye ibiwa, akiwa ameshika kidumu cha mafuta ya petrol, akija nacho kwa gadhabu mbio mbio huku akiwapangua watu, bila ya kufikiria kuwa huyo anayetaka kumfanyia hivyo alikuwa ni binadamu kama yeye, ila kwa vile yeye alitaka sifa kuwa yeye ndio alie leta mafuta ya petrol, akaona afanye kile kitakacho mpa sifa, akafika hadi mbele na kuanza kummiminia mafuta Hemedy waliedhani kuwa ndo yule mwizi walietoka nae mbali. Hemedy hali yake ilikuwa ni mbaya sana hakuweza hata kutoa sauti, alikuwa amekata tamaa ya kuishi katika huu ulimwengu, alikuwa anasubiri kifo chake akaungane na wazazi wake huko walipo. Kijana mwenye hasira kali kuliko wote, alipo maliza kummiminia mafuta Hemedy, akatoa kibiriti na kukiwasha akiwa yupo tayari kumuunguza Hemedy.
Polisi baada ya kuhakikisha nyumba ya marehemu Mzee Mheshimiwa, wameiacha katika usalama, maana huo ulikuwa ni usiku halafu nyumba ilikuwa haina mtu, ndo maana wakafunga na kufuli lao na kuanza safari baada ya gari la hospitali lililobeba maiti za wenye nyumba hiyo kuondoka, nao wao wakaanza safari ya kurudi kituoni.
Wakati wakiwa wapo barabarani, waliskia kelele za watu, ila hawakuelewa kelele hizo ni za nini na zinatokea wapi.
“Afande Taure unazisikia kelele hizo” askari mmoja aliuliza.
“Ndio nazisikia ila bado sijajua ni za nini na sijajua pia zinatokea kwa wapi? Embu simamisha gari hapo mbele” Koplo Taure alijibu na kutoa amri ya gari kusimamishwa, dereva akaegesha gari na kutulia, maaskari wote wakawa wapo kimya wakiziskilizia hizo kelele.
“Afande mbona kama ni huko mbele ndo zinapotoka hizo kelele?” Askari aliuliza.
“Ndio ni huko mbele, hembu endesha gari haraka tuziwahi hizo kelele, huenda ikawa ndo hao majambazi wamekamatwa” Afande Taure alitoa amri na gari ikaendeshwa kufuata kelele zinapotokea. Kwa mbali waliona kundi la watu wakiwa kama wanapiga kitu hivi, ikabidi dereva awahishe gari haraka sana ili kuwahi.
“Oyaaaa pira hilo, wazee wanakujaa”
Kijana mmoja aliekuwepo katika kundi la watu waliokuwa wanampiga Hemedy wakidhani ni mwizi, alitoa kauli hiyo ambayo sio watu wote waliiskia, wengine walikuwa bado wanashangilia wakitaka mwizi achomwe moto, kwa wale ambao walisikia, waligeuka nyuma na kuangalia kuwa walichoambiwa kuwa ni chaukweli, ndipo hapo macho yao yalipotua kwenye gari la polisi lililokuwa linakuja kwa kasi huku likimulika taa zote za mbele.
Bila kusubiri hadi lifike mmoja mmoja aliaanza kushika njia yake kwa kasi ya umeme, akijaribu kuokoa nafsi yake zidi ya hao polisi waliokuwa wanakuja kwa kasi, kwa wale ambao hawakuskia onyo walilopewa na mwenzao kuwa polisi wanakuja, walishangaa baada ya kuona wenzao wakitimka mbio mbio kila mmoja akielekea njia yake, walijiuliza kuna nini mbona watu wanakimbia? Ndipo hapo walipo shuhudia gari la polisi likiwa karibu kabisa na eneo walilopo, na wao bila kujifikiria mara mbili, walitupa mawe waliokuwa wameyashika kwaajili ya kumuadhibu mwizi, na kila mmoja kuanza kushika njia yake.
Hakuna ambae alitaka ashikwe na polisi hao, hakuna ambae alitaka akalale kituoni, maana waliujua ule msemo wa kuwa “Polisi kuingia ni bure, kutoka na hela” hakuna hata mmoja alietaka kuingia bure halafu atoke na hela ndo maana kila mmoja akajaribu kuokoa nafsi yake. Kijana mwenye hasira kali kuliko wote, alietaka sifa ya kuwa yeye ndo ameleta mafuta ya petrol kwaajili ya kumgeuza majivu mwizi, na yeye pia aliliona gari la polisi likija kwa kasi, hakutaka kushikwa pekeake, japo kuwa alipenda sifa, ila mbele ya polisi hakupenda asifiwe, akatupa kibiriti, akatupa kidumu kilichokuwa hakina kitu kwa wakati huo baada ya mafuta yote kuenea katika mwili wa Hemedy aliekuwa amelala chini hajiwezi kwa kipigo alichopokea kutoka kwa raia wenye hasira, akashika njia na kupotea gizani. Akatoweka na yeye.
Maaskari walishuka haraka haraka na kuweka ulinzi eneo hilo, Koplo Taure alishuka na yeye kutoka katika viti vya mbele vya gari hilo, akaenda hadi ulipo mwili wa hemedy na kuchuchumaa, alipokelewa na harufu ga mafuta ya petrol yaliyokuwa kwenye mwili wa Hemedy, alimuwekea kidole chake kwenye pua za Hemedy na kugundua kuwa bado alikuwa ni mzima.
“Beka hembu njoeni tumchukue huyu naona bado ni mzima”
Maaskari bila kuuliza walienda hadi ulipo mwili wa hemedy na kum’beba hadi kwenye gari.
“Dah halafu ni mtoto mdogo kabisa huyu, anatakiwa mda huu awe amelele nyumbani kwao” askari mmoja aliongea.
“Hii miji toto ya mtaani yaliyotelekezwa na wazazi wao ndo wanakuja kuwa machokoraa na mwisho yanakuwa mavibaka, yanatusumbua sana, lina bahati halijiwezi ila ningelipiga hadi kulivunja miguu lisitembee tena hasilani” askari anayefahamika kwa jina la Mkwaju, aliongea maneno hayo bila kujua huyo anaemdhania ni kibaka ndo huyo mtoto wa Mzee Mheshimiwa, waliedhani kuwa ametekwa na majambazi waliovamia nyumbani kwao.
Kwakuwa hali yake ni mbaya sana baada ya kupokea kipigo cha mwizi kutoka kwa raia wenye hasira kali, waliamua wampeleke moja kwa moja hadi hospitali ili akapate matibabu. Walipofika hospitali, walimshusha na kupokewa na manesi wa hospitali hiyo na kumpeleka chumba maalumu na kuanza kumpatia matibabu.
Maaskari baada ya kuona kila kitu kimeenda sawa waliaga na kuahidi kesho yake watarudi kuja kujua hali ya muhalifu wao, hawakuwa na sehemu nyengine ya kuenda, kwavile pia muda ulikuwa umeenda sana na kulikuwa kunakaribia kukucha, wakaongoza gari hadi kituoni ili waendelee na mambo mengine.
***************************** Siku iliyofuata. Kituo cha Polisi Mabawa.
“Afande Jesca, nimekuita hapa nataka unipetaarifa kuhusiana na tukio lililotokea jana usiku” Mkubwa wa kituo, anaejukikana kwa jina la Inspekta Ganjo, aliongea maneno hayo akiwa ndani ya ofisi yake mbele yake akiwa amesimama askari wa kike.
“Mkuu, hapo labda nikuitie Koplo Taure maana yeye jana ndie aliongoza msafara huo”
“Ok niitie mara moja” afande jesca alitoka na kwenda hadi kwenye ofisi ya Koplo Taure, alipofika alipiga hodi, ila hakujibiwa akaamua anyonge kitasa na kuzama ndani, ila hakumuona Koplo Taure, alitoka hadi nje kabisa ambapo aliwakuta maaskari wengine wamekaa, akawauliza mahali alipo Koplo Taure na kuambiwa kuwa ametoka kidogo kwenda kununua vitafunwa vya chai, haikupita muda mwingi, Koplo alirudi huko alipoenda huku mkononi akiwa ameshika mfuko mweusi wa nailoni.
“Wewe ulikuwa wapi?Mkuu anakuita huko ofisini kwake” Afande Jesca alimuambia hivyo baada ya kufika karibu yao.
“We nenda utajua huko huko” afande jesca aliongea huku akiondoka kuelekea eneo lake la kazi baada ya kufikisha taarifa..
Koplo Taure baada ya kupewa taarifa hiyo alienda hadi kwenye ofisi yake na kuweka mfuko wake wenye vitafunio alivyotoka kununua mda si mrefu, aliuweka juu ya meza yake na kutoka kuelekea kwenye ofisi ya Mkuu wake, alipiga hodi na kuambiwa kuwa aingie, baada ya kuingia, alipiga salut na kusubiri ambiwe alichoitiwa.
“Jana wewe ndio uliongoza msafara wa kwenda kufuatilia tukio la ujambazi?”
“Ndio Mkuu”
“Sawa, tukio hilo limetokea wapi?”
“Tukio limetokea mtaa wa Donge kwenye nyumba namba 169 na had…….”
“Whaat?” Inspekta Ganjo aling’aka kwa mshtuko na kumfanya Koplo Taure kurudi nyuma kidogo, maana Inspekta aliipigiza mikono yake kwenye meza na kuinuka katika kiti alichokaa mwanzo.
“Ume..ume….umesema mtaa wa Donge nyumba namba ngapi?
“169 Mkuu, walisema anaitwa Mzee nani siju….”
“Mzee Mheshimiwa?” Mzee Mheshimiwa na Mkubwa wa kituo walikuwa ni marafiki tokea wakiwa wanasoma sekondari, ila walipo maliza sekondari kila mmoja akachaguliwa kuendelea na elimu ya kidato cha tano kwa shule tofauti, hata hivyo urafiki wao uliendelea mpaka kila mmoja alipopata kazi, Mzee Mheshimiwa aliajiriwa katika bandari ya Tanga, alifanya kazi hapo kwa miaka kadhaa, akaacha na kujiajiri mwenyewe, ndipo hapo alipoanzisha sheli zake za mafuta akaona pia haitoshi akafungua showroom ya magari. Na kwa upande wa Inspekta Ganjo yeye alipomaliza elimu yake moja kwa moja akaenda kuomba kazi ya upolisi, kutokana aliipenda kutoka moyoni, basi alifanikiwa kuipata, kutokana na utendaji wake wa kazi akapandishwa cheo mpaka kuwa Inspekta.
“Ndio Mkuu”
“Enhee hembu nipe taarifa imekuaje kuaje”
“Mkuu kwa maelezo tuliyopewa kwa…….” alimuelezea yote aliyoambiwa na Baba lucas na aliyoyaona mwenyewe.
“Kwahayo maelezo uliyoyatoa, unahisi huyo mtoto atakuwa ametekwa na hao majambazi au wewe unahisi nini?” Mkubwa wa kituo aliuliza.
“Kwa hapo bado sijajua Mkuu”
“Sawa fuatilia hiyo kesi kwa kina”
“Ndio Mkuu” alisimama na kuanza kupiga hatua ili atoke, ila kuna kitu alikumbuka, akamgeukia Mkubwa wake.
“Mkuu, halafu wakati jana usiku tunarudi kituoni, tuliona mtu akipigwa barabarani, kwa haraka haraka sisi tulijua ni mwizi, kwasababu walikuwa wanataka kumchoma moto”
“Huyo mtu yupo wapi?”
“Tumempeleka hospitali, na nilikuwa leo nataka niende nikamfuatilie nijue anaendeleaje”
“Sawa unaweza kwenda, ila huyo mwizi utamleta hapa kituoni halafu ndio tutajua tunafanya nini”
“Ndio Mkuu” afande Taure alitoka ofisini kwa Mkuu wake na kuelekea katika ofisi yake kuendelea na shuhuli nyengine.
*************************************
“Hahahahahah Dah thiku tegemea kama kadhi itakuwa rahithi namna ile, hembu tusherekeeni kwandha” Mata aliongea kwa furaha baada ya kukamilisha kazi yao walioifanya jana.
“Hata mimi sikutegemea kama itakuwa ni rahisi vile. Vipi mbona Mrutu wewe hauna furaha? Au bado unamuwaza yule marehemu Mzee mheshimiwa? Moto aliongea.
“Hapana sio hivyo” Mrutu alijibu huku akiwa ana wasiwasi wa waziwazi.
“Thatha kama thio hivyo ni nini? Acha dhako bwana tufurahie petha ambadho hatuja dhitolea jasho thithi tunaita petha dha wajinga, furahia bwana” Mata aliongea.
“Mimi simuwazi Mzee Mheshimiwa, kwanza undugu mwenyewe tumekutana kwa baba kila mtu ana mama yake, sasa mimi nimuwaze wa nini?”
“Sasa kinachokufanya uwe na mawazo hivyo ni kipi? Ujue mimi nilikuwa nakuona tu tangia muda una mawazo siju unawaza kitu gani?”
“Nyie hamjui tu, ndo maana mnasema hivyo, ile nyumba ina CCTV Camera, kwahiyo lile tukio lote ambalo mmelifanya mjue limerikodiwa” wote wa wili macho yaliwatoka, wao walidhani wameshapoteza ushahidi kwa kuua familia nzima, kumbe bado wanakimbembe chengine, hawakujua watafanya nini, vijasho vyembaba vilianza kuwatoka, walikuwa na wasiwasi pengine hata kumshinda Mrutu aliewapa tarifa hiyo. Wakabaki wanaangaliana, wasijue wafanye kitu gani, vinywaji vyote vilivyokuwa mezani kwa ajili ya kujipongeza kazi hiyo waliyo ifanya walivisahau kwa muda huo.
“Thatha kwanini hukutumbia tokea mwandho?” Mata alikuwa ni katili sawa, ila mbele ya polisi alikuwa ni muoga sana, halafu pia aliogopa jina lake kuchafuka, maana yeye baada ya miaka kadhaa alipanga kuja kugombania Ubunge.
“Mataa, huu sio muda wa kulaumiana tena, inabidi tukae tupange tunafanya nini, maana hata ukilaumu haitosaidia kitu”
“Ndo hivyo sasa inabidi tujue tunafanya nini kabla mambo hayaja haribika”Mrutu aliongea.
“Nimepata wazo” Moto aliongea na kuwaangalia wenzake na kuwaona kuwa kila mmoja ameweka utayari wa kumskiliza. “Kwani ile nyumba si haikai mtu sasa hivi”
“Ndio hakuna mtu anaekaa” Mrutu alijibu.
“Safi, itabidi mimi niende, nikaingie hadi kwenye ile nyumba, niingie hadi kwenye chumba cha kuongozea kamera, halafu nifute Data zote, au nyie mnasemaje? Moto alieleza na kuuliza swali.
“Thatha Moto unauhakika gani? Je kama polithi wameshachukua hizo Data?” Mata alionyesha wasiwasi wake.
“Hapana haiwezi kuwa hivyo kwasababu kile chumba ni cha siri sana, yani kama sio mtu wapale huwezi kujua, kwanza mlango wenyewe wa kuingilia humo kwenye hicho chumba upo kama ukuta,kwahiyo kwa mtu ambae sio wa pale hawawezi kujua” Mrutu aliwaambia.
“Thatha wewe vitu vyote hivyo umevijuaje”?
“Wakati anaijenga ile nyumba mimi ndie nilimpa ushauri kuwa aweke kamera za ulinzi namna hiyo”
“Thatha tunafanyaje”
“Itabidi Mrutu unielekeze kila kitu kwasababu wewe si ndio unaejua, ili mimi nikienda nisipate tabu”
“Poa usijali”
“Kwahiyo hiyo kadhi utaifanya thaa ngapi?”
“Nitaifanya kesho usiku”
“Hahahahaha tusherekeeni bathi, maana tushapata jibu la jambo lililo tuchanganya”
Waligongesha glas na kuendelea kufurahia mali za dhuluma.
***********************************
Koplo Taure alienda katika hospitali aliyolazwa Hemedy ili kujua hali yake, aliofika aliambiwa na daktari aliewapokea jana kuwa hali yake sio nzuri sana ila matumaini ya kupona yapo, akatoa msisitizo kuwa mgonjwa huyo anahitajika akatoe maelezo kituoni kwa kile kichomkuta jana yake, na kumsisitizia zaidi kuwa amuwekee uangalia asije akafanya kitendo chochote hususani ni kutoroka hospitali hapo, alihakikishiwa atakuwa katika uangalifu mzuri na daktari huyo, akaaga na kuondoka zake kuelekea kituoni.
Mazishi ya Mzee Mheshimiwa na mke wake yalifanyika kijijini kwao Gombero, Inspekta Ganjo alihudhuria pia mazishi hayo, alikuwa akilia kiume baada ya rafiki yake kipenzi kuingizwa katika kaburi makazi yake ya milele, baada ya kumaliza kufukia kaburi, taratibu nyengine zikafuata kama kumsomea marehemu dua, baada ya hapo kila mtu alianza kuondoka mmoja mmoja, Inspekta Ganjo baada ya watu kuondoka, alichuchumaa kwenye kaburi la rafiki yake kipenzi, na kumuombea mungu amlaze mahali pema peponi, alihuzunika, alisikitika ila ikawa ndio tayari imeshatokea hakua na budi na yeye aliondoka makaburini hapo. Mzee Mheshimiwa akawa amebaki mwenyewe katika kaburi lake, alizikwa pembeni ya mke wake.
Baada ya mazishi kuisha, Inspekta Ganjo alirudi mjini kuendelea na shuhuli zake, ila picha ya rafiki yake bado haikumtoka kwenye ubongo wake, hakuamini kuwa ndio anatoka kumuhifadhi rafiki yake katika nyumba yake ya milele, hakua na jinsi akajaribu kusahau na kuendelea na mambo mengine.
********************************
“Ndio Mkuu”
“Nataka kujua hii kesi ya marehemu Mheshimiwa imefikia wapi”
“Mkuu hii kesi bado ngumu, hadi sasa sijajua nianzie wapi”
“Unasemaje Afande? Yani hujajua uanzie wapi? Sasa wewe ni askari wa vipi halafu tena hunaata aibu eti unasema sijui nianzie wapi? Hivi unajua kusema hivyo ni kosa, tena kosa kubwa sana inastaili kupata hata adhabu, ok sitokupa adhabu sasa hivi, ninakupa siku ya leo tu, kesho nataka uniletee taarifa umefikia wapi katika uchunguzi wako, unaweza kwenda”.
Koplo Taure hakujua afanye, ni kweli kesi hii kwake ilikuwa ni ngumu kutokana na uwezo wake, ila hakutakiwa kusema vile mbele ya Mkuu wake, ila yeye hakusema vile kwania mbaya, amesema vile akidhani atapewa njia ya kuanzia, ila matokeo yake amepewa siku moja ya kupata chanzo cha kifo cha Mzee Mheshimiwa na familia yake.
Hakuwa na jinsi alipiga salut na kuanza kuondoka mdogo mdogo, ila kabla hajafungua malango, akasikia anaitwa na mkuu wake, akageuza shingo kitaratibu na kumuangalia Mkuu wake.
“Nenda kaanzie nyumbani kwake leo usiku” alipewa muongoza na kuambiwa aende.
********************************
Majira ya usiku, Moto alifika hadi katika nyumba ya marehemu Mheshimiwa, lengo lake lilikuwa ni kuingia katika nyumba hiyo na kuingi katika chumba cha kuongozea kamera ili afute data zote za tukio walilo lifanya,alifika hadi pembezoni mwa nyumba hiyo na kukutana na ukimya wa hali ya juu kutokana na eneo hilo kuwa na nyumba zenye mageti, pia ukimya hiyo huo umesababishwa na kuwa mtaa huo unakaaa watu wakishua.
Aliangalia mazingira na kuona kupo vizuri, akaliendea geti na kujaribu kulifungua na kukuta limefungwa na kufuli, hakutaka kukata tamaa aliuangalia ukuta wa hiyo nyumba na kuona ni mrefu sana akajua hawezi kuupanda, akazunguka nyuma ya nyumba hiyo, bahati ikawa kwake, aliona mti mrefu wa muarubaini, akaupanda hadi juu, hapo aliweza kupaona ndani vizuri tu,
Akafikiria atafanyaje ili aweze kuingia ndani, akatoa tabasamu baada ya kuona tawi moja limeingia ndani ya uzio wa nyumba hiyo, akaparamia tawi hilo na kujaribu kuingia ndani ya uzio wa nyumba hiyo, akaruka chini kwenye bustani, hakuwa na ujasiri wa kujihakikishia usalama wake moja kwa moja, alitembea kwa tahadhari akielekea mlango wa mbele wa nyumba hiyo, alipofika akajaribu kunyonga kitasa, bahati ikawa kwake mlango ulikuwa upo wazi, akazama ndani kwa uangalifu akifuata maelekezo aliyopewa na Mrutu, akapanda ngazi na kwenda hadi juu, alipofika kwenye kordo alianza kuhesabu vyumba, chumba chapili ndio chenyewe alichoelekezwa, akanyonga kitasa, bahati ikawa kwake tena, mlango ukafunguka akazama ndani, aliwasha shwichi ya taa na mwanga ukajaa chumba kizima.
Kama alivyoelekezwa akaenda hadi kwenye kabati, pembeni yake kuna droo akaifungua na kukutana na makaratasi mengi, akayatoa yote na kukutana na shwichi kama ya mwanzo aliyoiminya na kuwasha taa ya humo kwenye chumba, na hiyo pia aliiminya, ghafla ukuta uliokuwepo pembeni ya kabati ukajifungua taratibu, bila kujiuliza akazama ndani, taa zimewaka kwenye chumba hicho, akaona kuna kompyuta moja, akaiyendea na kuanza kupekua mafaili, akitafuta faili la tarehe 13, akatoa tabasamu baada ya kulipata, akalifungua ndani, macho yalimtoka baada ya kukutana na mandishi yaliyosomeka “empty folder”. Ikimaanisha faili hilo halina kitu, Hakukata tamaa alipekuwa mafaili yote ila hakuona video anayo itafuta.
Alichanganyikiwa akajua tayari video imeshachukuliwa, hakua na jinsi nyengine ya kufanya, akafunga kama alivyokuta na kuanza kutoka chumbani humo.
Koplo Taure alikuwa yupo ndani ya gari lake akielekea nyumbani kwa marehemu Mheshimiwa, aliendesha kwa kasi kwasababu alichelewa sana. Alipo fika akashuka kwenye gari na kuliendea geti, kwakuwa wao ndo walifunga geti hilo kwaajili ya usalama wa mali za nyumba hiyo, kwahiyo funguo alikuwa anazo, akafungua geti na kuzama ndani, akachomoa bastola yake kwajili ya usalama wake, kwa fikra zake alijua hakuwezikuwa na mtu humo ndani, ila alitoa bastola kwajili ya kujihami na chochote kitakacho tokea mbele yake, aliufikia mlango na kushika kitasa akitaka kuufungua ili kuingia ndani.
Moto pia aliufikia malango mkubwa ili aweze kutoka nje aende zake baada ya kukosa alichokifuata…..
Koplo Taure baada ya kunyonga kitasa, mlango ukafunguka, akatulia kama sekunde kumi, alifanya hivyo ili kujihakikishia kama kunachochote kibaya aweze kujihami, alipoona pako kimya, akafungua mlango kabisa na kuingia ndani, alitumia tochi ya simu yake ili kupata mwanga utakao muwezesha kuiyona swichi ya taa ya hapo sebleni, akafanikiwa kuiyona swichi, akawasha taa na kuangaza macho yake hapo sebleni kama ataweza kupata chochote kitakachomsaidia katika upelelezi wake.
Akatafuta sebleni hapo hadi akachoka ila hakuweza kupata chochote, akaamua kupanda ngazi hadi vyumba vya juu, ili akaangalie kama ataweza kupata chochote kitakacho msaidia katika upelelezi wake.
Dakika tano nyuma kabla Koplo Taure kuingia ndani ya sebule ya nyumba hiyo.
Moto wakati anashika kitasa, iliatoke nje akashangaa kuona kitasa kinazungushwa, akaachia haraka na kuruka pembeni hadi kwenye pazia la dirisha lililokuwepo hapo karibu na mlango, akajificha nyuma ya pazia, zoezi hilo alilifanya kwa sekunde zisizo zidi nne, baada ya kama sekunde tano, akaona mtu akiingia humo ndani, taa ikawashwa, hapo ndipo mapigo ya moyo wake yalipoanza kudunda baada ya kuona mtu alieingia ameshika bastola na yeye hakuwa hata na kisu cha kujihami, akajuta kwanini sehemu kama hiyo hakuja na bastola yake.
Akaona kama kuna kitu anakitafuta tafuta hapo sebuleni, baada ya muda akamuona akipanda ngazi na kuelekea juu ya nyumba hiyo. Hapo hapo bila kuchelewa, akatoka nyuma ya pazia alipo jificha na kufungua mlango, akatoka nje na kwenda kuangalia getini na kukuta geti halijafungwa akatokomea zake.
Koplo taure alifika hadi vyumba vya juu, akaingia chumba kimoja baada ya chengine akitafuta kitu kitachomsaidia katika upelelezi wake, ila hakuambulia chochote, hapo sasa ndipo alipoona hiyo kesi aliyopewa imekuwa ngumu kwake, kwavile hakupata chochote kitachomsaidia katika upelelezi wake, akaamua aondoke tu, hakujua atamjibu nini Mkuu wake endapo atamuuliza amefikia wapi, kwa mara ya kwanza akakilani cheo chake alichokuwa nacho, akatamani na yeye angekuwa anacheo kikubwa, huenda na yeye angekuwa anaamrisha tu, ila haikuwa hivyo. Atakuaje na cheo kikubwa wakati kazi zenyewe hazifanyi kwa akili? Akabaki na cheo chake cha Ukoplo.
Moto alipotoka katika nyumba ya Mzee Mheshimiwa, alimpigia simu Mata na kumuliza yupo wapi kwa wakati huo, akaambiwa kuwa yupo nyumbani kwake, akampigia simu Mrutu kuwa wakutane nyumbani kwa Mata ili awaambie alichokikuta nyumbani kwa mzee mheshimiwa.
********************************
“Kwahiyo hukulikuta faili la ile tarehe” Mrutu aliuliza kwa hamaki baada ya kupewa taarifa ya alichokikuta Moto kwenye nyumba ya marehemu Mheshimiwa.
“Faili nimelikuta, ila video hakuna”
“Dah thijui thatha itakuaje, unajua tunawedhaa kujulika mapema hata kabla hatuja faidi mali”. Mata alionyesha wasiwasi wake.
“Hivi mrutu, unaweza kuhisi ni nani aliyeichukua ile video?” Moto aliuliza.
“Au labda itakuwa ni huyo mtu uliyemuona akiingia nyumbani kwa Marehemu Mheshimiwa”. Mata aliongea.
“Mataa, nikuambie mara ngapi, kwamba kile chumba ni cha siri hakijulikani na watu ambao hawa husiki? Au labda itakuwa ni Goda nini? Mrutu aliongea na kuuliza ila katika hao aliowauliza hakuna hata mmoja anaemjua Goda ni nani.
“Huyo Goda ni nani?”
“Goda, alikuwa ni mfanyakazi wake anaemuendesha na gari, kwani nyie wakati mnaingia hamkumuona mvulana mkubwa mkubwa hivi?”
“Ndio tulimuona na yeye ndo wakwanza kumpiga risasi, nilimpiga risasi ya bega” Moto alijibu.
“Itakuwa ni yeye tu hakuna mwengine, kwani nyie mulihakikisha amekufa kabisa? Mrutu aliuliza.
“Hapana, sisi tulivyomuona ameanguka chini katulia, sisi tukajua tayari tumeshamuua” Moto alijibu, kipindi chote hicho Mata alikuwa yupo kimya, anawasiwasi baada ya video ya tukio walilolifanya kutoonekana. Alikuwa anawasiwasi kweli si mchezo.
“Ayaa!! Sasa nyie mmeambiwa na nani kuwa risasi ya bega inaweza ikamuua mtu hapo hapo? Itakuwa alizimia tu, baada yakuinuka akaenda kuichukua tu”
“Lakini mbona taarifa tulizo zipata zinasema wote wamekufa, ila mtoto wao tu ndo hajaonekana?”
“We taarifa umezipata wapi”
“Haaa!! Kwani nyie hamjaangalia taarifa ya habari? Yule ni mtu mkubwa hapa Tanga lazima watangaze tu kifo chake, sasa nyie mnanishangaza mkisema eti hamjapata taarifa”
“Kumbe pia hamkumuua na yule mtoto wake?” Mrutu aliuliza kwa mshangao.
“Hatukumuua kwa risasi, ila alikufa kwa mshtuko baada ya kumuona Baba yake tumemfumua ubongo” Moto alijibu.
“Sasa nyie mbona mnafanya mambo kama vile hii kazi mmeiyanza jana? Mlikuwa na uhakika gani kama alikufa? Haya mbona hajaonekana?”. Mrutu alianza kupaniki na kuongea kwa hasira.
“Mrutu embu pungudha jadhba, hayo ni makotha tu madogo madogo yanawedha kujitokedha katika kadhi yoyote, kwani wewe unahithi nini hadi hapo?” Mata aliyekuwa kimya mda wote aliongea baada ya kuona Mrutu ameanza kupaniki.
“Mimi kwa mawazo yangu ninavyo hisi, itakuwa Goda na Hemedy walizimia tu, kwahiyo baada ya muda, waliamka na ninavyojua risasi ikipigwa sehemu ambayo ni ngumu sumu kufika kwa haraka hadi kwenye ubongo kama nyie mlivyofanya kumpiga risasi ya bega, ninahisi itakuwa Goda alipata nguvu kidogo na kwenda hadi chumba cha kuongozea kamera, na kuinyonya video yote kwenye flash, ili apate kama ushahidi, ila kama inasemekana yeye alikufa, basi itakuwa flash hiyo alimkabidhi Hemedy kabla yeye hajakufa. Hivyo ndo ninavyo hisi”.
“Wewe si umesema kuwa hiko chumba cha kuongozea kamera hakijulikani na watu wasio husika, Sasa huyo Goda ataingiaje ikiwa yeye hausiki? Moto aliuliza.
“Goda alikuwa ndie mafanya kazi wake mkubwa, yani tangu Mzee Mheshimiwa anahamia alikuwa yupo nae, huenda ikawa na yeye anakijua hiko chumba”
“Hapo Mrutu umeongea, huenda ikawa ni kweli kabitha, Thatha tunafanyaje kumpata huyu mtoto?”. Mata aliyaunga mkono mawazo ya Mrutu.
“Hapo inabidi tumtafute tu, na tukimpata tunamuua halafu kama anayo hiyo flash tunaichukua na kuichoma moto tu” Moto alitoa wazo hilo.
“Je tukimpata halafu ikawa hana hiyo flash, tunafanyaje? Maana hapo mimi nimehisi tu ila sina uhakika” Mrutu aliuliza.
“Tuna muua tu, halafu baada ya hapo tutajua tufanye nini” Moto aliongea.
“Kama ni hivyo sawa, tunaanzia wapi kumtafuta?” Mrutu aliuliza.
“Popote pale, mji wa kwetu huu, tutamsaka hadi tumpate” Moto alijibu.
“Je kama ameipeleka hiyo flash polisi? Mrutu aliuliza tena.
“Polisi hawezi kwenda, kwanza mtoto mwenyewe mdogo, hatokuwa na mawazo hayo”.
Maongezi yao waliya hitimisha hapo na kila mmoja akainuka na kwenda nyumbani kwake, baada ya kupata muafaka kuwa wamtafute Hemedy kila kona ya jiji na wakimpata waichukue flash ya video, waliodhani atakuwa anayo yeye baada ya kuichukua wamuue, ili wazidi kupoteza ushahidi. Wakamuacha Mata hapo, maana hapo palikuwa ni nyumbani kwake, nawao wakaenda makwao.
“Sawa hii kesi wewe ishakushinda, vipi kuhusu huyo muhalifu aliekuwepo hospitali, umeenda kumuangalia?”
“Hapana Mkuu, nilipanga nikitoka ndio niende nikamuangalie”
“Sawa, unaweza kwenda, ila kumbuka kazi ya polisi sio ya kilelemama kama wewe unavyofanya, usione watu wana vyeo vikubwa, ukadhani wamevipata kwa kufanya kazi kitoto kama unavyo fanya kazi wewe, nimekupa kazi ndogo tu ya kufuatilia kesi ya mtu wa kawaida ila umeishindwa, je kama ungepewa kesi ya kufuatilia kifo cha mbunge? Si ndo unge omba uache kazi kabisa, siku nyengine inabidi utumie akili kufanya kazi, unaweza kwenda”.
Koplo Taure alipiga salut na kutoka nje ya ofisi ya Mkuu wake na kwenda hadi katika ofisi yake, alipofika alikaa kwenye kiti na kuanza kuwaza, aliona kama vile ameonelewa kupewa kazi kama hiyo ambayo kwake yeye aliiyona ni ngumu maana hakuwa na pakuanzia kwenye kuichunguza hiyo kesi.
******************************
“Ndio dokta, unaweza ukaniambia hali ya mgonjwa wangu inaendeleaje?”
“Amm!!! Mgonjwa wako hali yake sasa hivi, kidogo inaridhisha, jana usiku alizinduka akawa anapiga kelele tu, anaongea vitu vya ajabu ajabu, mara aseme wanakuja kuniua, mara aseme msimuue Mama yangu, mara aseme Msimuue Baba yangu, yani ni vitu ambavyo havieleweki, kwani huyo mtoto ana nini Afande?”
“Dokta kama nilivyokuambia kuwa huyu mtoto sisi tumemkuta akipigwa na kundi la watu, kwahiyo bado hatujajua ana nini? Hapa tunamsubiria apone ndipo tukamuhoji kituoni”.
“Sawa nimekuelewa, tunaweza kwenda kumuona”.
Waliinuka wote na kuelekea hadi katika chumba alicholazwa Hemedy nakumkuta Hemedy akiwa bado amelala, kutokana na sindano za usingizi walizomchoma kipindi ambacho anasumbua, maana ilikuwa kila akiamka anasumbua kwa kupiga kelele, akidai wanataka kumuua kwahiyo anataka kuondoka zake.
“Sasa dokta, ni lini ataruhusiwa kutoka hapa hospitali”
“Kesho, Tutaangalia kama kesho hali yake itakuwa iko vizuri tutamruhusu”
“Sawa hakuna shida, Kesho mimi nitakuja” Baada ya kuagana na daktari anaemtibu muhalifu wake, akaondoka na kulekea katika mizunguko yake anayoijua yeye.
****************************
“Thatha tunafanyaje, maana nyaraka dhote tunadho, kilicho baki thithi ni kujimilikisha Mali dhote”
“Itabidi tutumie mbinu ambayo itatufanya tusijulikane” Mrutu aliongea.
“Thatha mbinu hiyo ni ipi? Embu tuambie mawadho yako Bwana Mrutu”
“Mnajua tunatakiwa tufanyeje?” Mrutu aliongea na kuwaangalia wenzake, akawaona wote wapo makini kumsikiliza yeye. Akaendelea. “ Mata utajifanya kama vile ndie mmiliki wa mali za mzee Mheshimiwa, ila ulimuchia awe mkurugenzi au msimamizi tufanye, wewe ukiwa umeenda nje ya nchi kwajili ya mambo mengine, na kama Mahakama ikitaka ushahidi, basi tuta waonyesha karatasi aliyoiyandika mara ya mwisho kabla ya kifo chake, kwani ile karatasi si aliandika kuwa malizote sio zake na akaweka hadi na saini yake?” Mrutu alitoa maelezo hayo mafupi na kuwauliza swali.
“Ndio alipiga hadi saini” wakajibu wote kwa pamoja.
“Safi, sasa kwa vile watu walikuwa wanajua mimi ni ndugu yake, siku tutakayoenda mahakamani, nitasema kuwa ni kweli, Marehemu Mheshimiwa mali zote zile hazikuwa zake kama watu wengi wanavyodhani, ndio hapo sasa wakitaka ushahidi ndipo mtakapo itoa ile karatasi, tena itabidi ipigwe kopi, halisi muwe nayo nyie na ile kopi nitakuwa nayo mimi, baada ya hapo tunaiyonyesha mahakama, bila shaka mahakama watakubali tu, kwasababu ushahidi upo na pia saini ni ya mwenyewe ipo”. Kicheko cha furaha kilizuka ghafla baada ya ya Mrutu kuhitimisha mbinu watakayo itumia kuzichukua mali za marehemu Mzee Mheshimiwa kiulaini.
“Aitheee nimefurahi thaaaana, dah thiamini kama ungetoa mpango kama huo, hapo thatha ndio ninakubali kwamba familia yenu inaakili thana” Mata aliongea huku akiwa na furaha ya waziwazi.
“Sawa, tuachaneni na hayo kwanza, vipi kuhusu ile nyumba ya Mzee Mheshimiwa? Maana imefungwa na polisi kwajili ya usalama na funguo wanazo wao” Moto aliongea.
“Kuhusu ile nyumba, hakuna tatizo kwasababu mimi ni ndugu yake, nitaenda polisi na kuichukua funguo, si umesema kituo kinachoisimamia hii kesi ni hapo kituo cha polisi mabawa?” Mrutu alimuuliza Moto, maana Moto yeye ndo aliyeiyona taarifa ya habari kuhusu kifo cha Mzee Mheshimiwa na maelezo yote yaliyotolewa aliyaskia pia.
Baada ya kuhitimisha kikao hicho, kila mmoja akaenda kwake, kwaajili ya kuitafuta kesho yake. Wakaenda kulala.
*******************************
Majira ya asubuhi, Koplo Taure alienda hadi hospitalini, akamuulizia dokta anaemuhudumia Hemedy, kwavile ameshazoeleka ma manesi wa hapo, tangu sikuile alipo mleta Hemedy akiwa hajiwezi, manesi walimuambia kuwa dokta yupo afisini kwake, akaongoza njia hadi ofisini kwa dokta, alifungua mlango akamkuta.
“Karibu Afande”
“Nishakaribia, dokta mgonjwa anaendeleaje?”
“Tumshukuru mungu, maana hali yake leo inaridhisha, unaweza pia ukaondoka nae, twende ukamuone” Waliongozana hadi katika chumba alicholazwa hemedy, na kumkuta akiwa yupo macho. Hemedy siku hiyo hakuleta taabu kama siku zote alizokuwepo hapo hospitali anavyofanya, Koplo Taure aliruhusiwa kuondoka nae. Moja kwa moja akaenda nae hadi kituo cha polisi, walipo fika Koplo Taure, kwakuwa ilikuwa ni majira ya saa moja na nusu asubuhi, Inspekta Ganjo hakuwa bado hajafika kituoni hapo, ikabidi amuache hemedy Mapokezi, ili ahojiwe na Afande jesca.
Wakati huo huo nae Mrutu alikuwa anaenda hapo hapo kituo cha polisi kwenda kuchukua funguo za nyumba ya kaka yake marehemu Mzee Mheshimiwa, alikuwa anaenda hapo hapo mapokezi alipokuwa Hemedy akihojiwa.
Hemedy baada ya kuchukuliwa maelezo mafupi na Afande jesca, alichukuliwa na kupelekwa hadi selo, akafungiwa humo. Mrutu alipo fika kituoni, kabla hajafika mapokezi akakutana na Koplo Taure.
“Afande Taure, Vipi?”
“Poa, niambie Mrutu”
“Fresh tu kaka”
“Pole na msiba bwana, sikuwahi kuhudhuria msibani,maana nilikuwa nina kesi niliyopewa niifuatilie, sasa ile ndio imenifanya nisifike msibani”
“Usijali Afande nishapoa, vipi lakini uko poa kabisa?”
“Namshukuru Mungu, niko poa kabisa, sijui wewe?”
“Hata mimi nashukuru Mungu, Tumeshamzika kaka yangu, ila ndio hivyo si unajua kila nafsi itaonja umauti, kwahiyo hakuna budi kumuombea huko alipo, mwenyezimungu amlaze mahali pema peponi kaka yangu” Mrutu alikuwa akiekti mbele ya Afande Taure, alijifanya anahuzuni nyingi kuondokewa na kaka yake, ila kwa vile usilo lijua ni sawa na usiku wa giza, Koplo Taure akamfariji.
“Usijali Mrutu, hiyo yote ni mipango ya mungu, leo kwake kesho kwetu, kila mmoja atakufa, kwahiyo usihuzunike sana”
“Asante Afande”
“Umekuja kuifuatilia kesi ya kaka yako? Au kuna mengine umefuata?”
“Ndio, ila pia nimefuata funguo za nyumba ya marehemu”
“Dah, kichwa kina mambo mengi, funguo zipo ila zipo kwa Mkuu labda tumsubirie kidog…… Basi huyo apo anakuja” Koplo Taure na Mrutu walikuwa wanajuana sana, kujuana kwao kulianzia siku Mzee Mheshimiwa, alipokuja hapo kituoni katika enzi za uhai wake, kuja kufuatilia kesi yake ya madai ya kudhulumiwa kiwanja chake kilichokuwa huko Mwang’ombe, alikuja na Mrutu, Mzee Mheshimiwa aliingia hadi ndani ila Mrutu alibaki nnje, ndipo hapo alipo juana na huyu Afande Taure, baada ya kuanza kupiga stori kujuana.
Inspekta Ganjo alipofika karibu yao, walimsalimia kutokana wote amewazidi umri, baada ya hapo wakaambiwa wamfuate ofisini kwake, wote watatu waliongozana hadi ilipo ofisi ya Inspekta Ganjo, waliingia ndani baada ya mlango kufunguliwa, walipewa ruhusa ya kukaa baada ya Inspekata Ganjo kukaa, na wao walikaa.
“Enhee, namiskiliza”
“Mkuu, huyu ni ndugu yake na marehemu Mzee Mheshimiwa, amekuja hapa kuifuatilia kesi ya kaka yake halafu pia anataka funguo za ile nyumba”
“Sawa, kwani wewe umeshamuambia chochote?”
“Hapana Mkuu”
“Ok, bwana nani vile” Inspekta Ganjo aliongea huku akimuangalia Mrutu usoni, Mrutu alianza kuwa na wasiwasi, hakujua hicho chochote alichotakiwa kuambiwa ni kitu gani, akadhani siri yao imegundulika, hiyo ikampelekea kuanza kutetemeka, akijua amejileta mwenyewe kwenye mdomo wa mamba.
“Mrutu” alijibu kiuwoga.
“Ok, bwana Mrutu, kesi ya kaka yako bado uchunguzi unaendelea, na tutajitahidi kuwasaka popote walipo hao majambazi waliyo fanya hivi, na nina kuhakikishia tutawapata tu kwahiyo usijali kwa hilo. Inspekta Ganjo hakujua akiongea hivyo ndio anazidi kumpa wasiwasi Mrutu, ambae alikuwa anahusika na tukio la kuondoa roho za familia ya kaka yake.
“Muache atetemeke tu, huo ni uchungu wa kuondokewa na Kaka yake na familia nzima, hata kama ingekuwa ni mimi pia ningekuwa katika hali hii, ila usijali Mr Mrutu tutawapata tu wauwaji.
Mrutu alikuwa anatetemeka kweli baada ya mkuu wa kituo kusisitiza kuwa wata watafuta waliyo fanya mauji, ila alizidi kutetemeka baada ya Koplo Taure kumuuliza swali kuwa mbona anatetemeka, hakujua angemjibu nini, ila alimshukuru kimoyo moyo, Inspekta Ganjo baada ya kumjibia.
“Dah, nyie acheni tu, kufiwa na kaka ambae ndie nilikuwa namtegemea kwa kila kitu, inauma sana, yan……” Hakuweza kumalizia sentensi yake, akaangua kilio cha kuigiza mbele ya hao maaskari ili kuzidi kuwapoteza, ni kweli alifanikiwa kuwapoteza maana walianza kumbembeleza, baada ya dakika kadhaa waliwafanikiwa kumyamazisha Mrutu aliekuwa analia kilio cha kuigiza.
“Pole Mr Mtu, funguo hizi hapa” Insepekta Ganjo alimpa funguo Mrutu, baada ya kuzi pokea akaaga, akaondoka zake.
“Mkuu, halafu na yule muhalifu aliekuwepo hospitali, leo ndio ameruhusiwa kutoka”
“Yupo wapi?”
“Yupo selo”
“Umesha muhoji?”
“Hapana Mkuu, ila amechukuliwa maelezo mafupi na Afande jesca”
“Ok, nenda ukamuhoji sasa hivi”
“Sawa Mkuu” Koplo Taure, aliinuka katika kiti achokaa, akapiga salut na kutoka hadi nje ya ofisi ya Mkuu wa kituo.
*****************************
Mrutu, baada ya kutoka kituo cha polisi, alielekea hadi katika nyumba ya marehemu kaka yake, alipofika akafungua geti na kuzama ndani, alifika hadi katika mlango mkubwa wa kuingilia humo ndani ya nyumba, aliufungua na kuingia ndani, alipoiyangalia seble hiyo, akakumbuka vitu vingi, akakumbuka kuwa ni yeye ndo alimshauri kaka yake, anunue kiwanja hicho kichokuwa maeneo hayo ya Donge, akakumbuka kuwa yeye ndo aliemshauri kaka yake, ajenge nyumba ya dizaini hiyo, akakumbuka alivyoambiwa aishi hapo baada ya nyumba kukumilika, akakumbuka walivyokuwa wakiisha kwa furaha, amani na upendo, akakumbuka alivyopewa uhuru na kaka yake wa kufanya chochote kile ndani na nje ya nyumba hiyo, akakumbuka alivyojengewa nyumba yake maeneo ya Mikanjuni, akakumbuka alivyopewa mtaji na kaka yake huyo aliechangia kumfanyia UHASAMA, akakumbuka mtaji aliyopewa na kaka yake ulivyo mpatia maendeleo hadi ikawa na yeye anajitegemea.
Alivyokumba wema wote aliofanyiwa na kaka yake, nafsi yake ilimsuta, ili mdhihaki, akaiyonea aibu nafsi yake, akawalaumu waliomshawishi kumfanyia UHASAMA kaka yake, ila yote kwa yote akailaumu nafsi yake, hatakama alipewa mtaji na kaka yake na kumfanya na yeye ajitegemee, ila hiyo haikuweza kumfanya aombe kitu kwa Mzee Mheshimiwa halafu anyimwe, Mzee Mheshimiwa alimpenda kama mdogo wake, japokuwa walizaliwa na baba mmoja ila mama tofauti, ila Mzee Mheshimiwa alimchukulia kama mdogo wake wa kuzaliwa nae tumbo moja.
Bila kutarajia machozi yalianza kumtoka, safari hii alikuwa analia kweli, alikuwa haigizi kama alivyofanya kituoni mbele ya Inspekta na Koplo Taure, alilia sana, alijuta, alijilaumu, aliilaumu nafsi yake kwa tamaa zilizo muingia, alitamani siku zirudi nyuma ili arekebishe alipokosea, ila haikuwezekana, alitamani iwe ni ndoto ya kusisimua halafu baada ya mda mfupi azinduke kutoka usingizi, akute mambo yote yalikuwa ni njozi tu, ila haikuwa hivyo.
Baada ya kulia sana na kujuta sana, alifuta machozi na kujipa moyo kuwa yaliyotokea yameshatokea, hakuwa na uwezo wa kuyabadilisha, hata hivyo, alipo waza kuwa muda si mrefu na yeye ataenda kuwa tajiri kwa mali za kaka yake watakazo kwenda kugawana, tabasamu la huzuni likamjia usoni mwake.
“Nisijipe mawazo sana, hata hivyo ilipangwa afe ili mimi ni nufaike na mali zake, nadhani hata yeye huko alipo atakuwa na furaha akiona mali zake naziendeleza mimi” Alijifariji kwa mawazo yake potofu, baada ya yote alifunga mlango na kutoka hadi nje, alipofika hadi nje, alitabasamu baada ya kuona magari matano yamepaki sehemu maaulumu ya kwenye hiyo nyumba. “Itabidi nichukue gari moja, nifanye la kutembelea” aliwaza na kuendelea na safari yake hadi kwenye geti, akalifungua, akatoka nje, akafunga geti vizuri na kuondoka zake.
Safari yake iliishia nyumbani kwa Mata, alipo fika akamkuta na Moto pia yupo, akawaelezea kila kitu alichokifanya kwa siku hiyo, kuhusu mpango wao, akaelezea alivyoenda hadi kituo cha polisi, akaelezea hadi alipo lia machozi ya kuigiza mbele ya askari, ila hakuelezea alipo lia machozi ya kweli nyumbani kwa marehemu kaka yake, hilo akalinyamazia, hakutaka kuoneka mnafki. Akanyamaza.
“Hahahhahaha yani wewe unafaa kabitha kuwa muigidhaji, umelia hadi mbele ya athkari, kwa hapo nakupa hongera”Mata aliongea.
“Ilikuwa ni lazima iwe vile ili niwazuge”
“Kwahiyo funguo unayo hapo?”Moto aliuliza.
“Ndio wamenipa”
“Umehakikisha ndio hiyo yenyewe? Thi unajua tena kwamba polithi hawaaminiki”
“Walivyo nipa nimeenda hadi kwenye ile nyumba kuhakikisha, ndio yenyewe” Wakati wanaongea Moto alikuwa yupo kimya, alioneka kama kuna kitu ana waza, ikabidi wamuulize.
“Vipi Moto mbona unaonekana unamawazo, kuna nini?” Mrutu aliuliza.
“Kuna kitu nimekumbuka”
“Kitu gani hicho? Ndo utuambie thatha”
“Ni kuhusu yule mtu niliemuona nyumbani kwa marehemu Mzee Mheshimiwa, wakati naenda kufuata ile video”
“Thatha ndo ana nini” Mata aliuliza kwa wasiwasi.
“Mimi nahisi itakuwa ni Polisi, maana ile siku niliyo enda, nilijaribu kufungua geti ila nikakuta limefungwa na kufuli, ikamilazimu niruke ukuta, ila baada ya kuingia yule mtu, mimi nilipo pata upenyo wakutoka, nikaenda getini na kukuta geti lipo wazi, hicho ndo kilichonifanya nihisi yule atakuwa ni polisi, maana polisi wao ndo walilifunga lile geti kwa kufuli lao”.
“Sasa kinachokufanya uwe na mawazo ni nini? Wakati funguo tunazo sisi”Mrutu aliuliza.
“Hapana sio hvyo, mimi nilikuwa naumiza kichwa kuwa, ni nani yule mtu, ila tayari nishapata jibu, ila mimi nashauri tusitumie tena lile kufuli”
“Kwa hilo usijali”
Walihitimisha maongezi yao, na baada ya hapo Mrutu alitoka na kumuacha Moto akiwa bado yupo nyumbani kwa Mata, yeye aliondoka na kwenda katika shuhuli zake.
*********************************
Koplo Taure, alienda hadi mapokezi na kuchukua funguo za selo aliyomo Hemedy, alipofungua alimtoa hemedy akampeleka hadi katika ofisi yake, kwajili ya kumuhoji maswali.
“Ndio Afande” Hemedy japokuwa alikuwa na umri mdogo, ila aliijua polisi, alijua kuna kuhojiwa, alijuwa pia kuna kupigwa kama hutoenda sawa nao, na yeye kwavile alikuwa hataki kupigwa, akapanga kujibu yote atakayo ulizwa.
“Jina lako ni nani”
“Hemedy”
“Huna baba” Koplo Taure alimuuliza kwa hasira za kuigiza ili kumtisha.
“Mheshimiwa, Afande”
“Nakuuliza kwa mara ya mwisho, sitorudia tena, Jina lako ni nani”
“Hemedy Mheshimiwa”
Koplo Taure baada ya kusikia jina hilo, alishtuka, ila hakutaka kuunyosha mshtuko wake mbele ya Hemedy.
“Dogo, unajua mimi sipo katika utani, na kama nilivyo kuambia mwanzo ukweli wako ndo utakuokoa, Jina lako halisi ni nani? Nimekupa nafasi ya upendeleo kukuuliza kwa mara nyengine, ila mimi sina kawaida ya kuuliza swali moja zaidi ya mara mbili, kwahiyo naomba uniambie ukweli”
“Afande, jina langu halisi ni hilo, na wala sijakudanaganya, kweli afande”
Koplo Taure alichanganyikiwa, hakuelewa amuulize swali gani, kutokana na jina la baba wa huyo mtoto kumchanganya, Mzee Mheshimiwa alimjua vizuri, ila hakuijua familia yake, mawazo mengine yalimtuma kuwa huenda ikawa mtoto huyu aliopo mbele yake ni mtoto wa marehemu Mzee Mheshimiwa aliesemekana ametekwa na majambazi yaliyo vamia nyumbani kwao, ila hakutaka kulipitisha wazo hilo, akadhani majina huenda ikawa yame fanana tu.
“Ok, nisubiri hapa nakuja sasa hivi” Hemedy alishikwa na wasiwasi, akajua Koplo Taure amekasirika na hapo ameenda kuchukua vifaa vya mateso, ila hakuwa na jinsi ikabidi atulie aone mwisho wake.
Koplo Taure baada ya kutoka katika ofisi yake aliyomuacha Hemedy, akaelekea moja kwa moja hadi katika ofisi ya Inspekta Ganjo, alipofika alipiga salut na kutulia.
“Enheee niambie”
“Mkuu, yule mtuhumiwa ameongea kitu ambacho kimenishangaza sana”
“Kitu gani? Embu nieleze”
“Amesema kuwa yeye ni mtoto wa Mheshimiwa”
“Sasa tangu lini, Mzee Mheshimiwa akawa na mtoto mkubwa, mtoto wake ni mdogo bwana, itakuwa umefananisha majina tu”
“Hapana Mkuu, hata huyo pia ni Mtoto mdogo”
“Unasemaje? Embu twende nikamuone” Waliotoka hadi nje ya ofisi, na kwenda kwenye ofisi ya Koplo Taure, walipofika wakanyonga kitasa na kufungua mlango, mlango ulipofunguka wote walipigwa na butwaa, hawakuamini macho yao kwa walichokiona hapo.
Hali ya Hemedy ili badilika ghafla, kifua chake bado kiliendea kumsumbua, bado kilikuwa na itilafu kutokana na kipigo alichopokea kutoka raia wenye hasira kali wakidhani ni mwizi, Koplo Taure na Insepekta Ganjo, walipoingia walimkuta akikohoa sana hadi machozi yalimtoka, Inspekata Ganjo, alimsogelea na kumuinua kichwa ili amuangalie usoni, ndipo hapo alipo pigwa na butwaa jengine, alikuwa ni Hemedy mtoto wa rafiki yake, majeraha yaliyokuwepo usoni mwake, hayakuweza kumfanya asimtambue “Ndio yeye huyu” Inspekta Ganjo alisema hivyo, bila kuhoji chengine, alimbeba Hemedy hadi nje, alimpakia kwenye gari ya polisi, na kumuambia Koplo Taure aendeshe gari kuelekea Hospitali.
Hospotali ya Tumaini.. “Hali ya mgonjwa wenu sio mbaya sana, ila tatizo lipo kwenye kifua chake”
“Sawa dokta, itachukua muda gani hadi kupona?”Insepekta Ganjo aliuliza.
“Hapa hadi kupona kabisa, itachukua kama wiki moja, ila maombi yana hitajika, si unajua sisi tunaweza tukasema hali yake sio mbaya sana, ila pia mungu akamchukua hivyo hivyo, kwahiyo hapo kinacho hitajika sana ni maombi”
“Hadi hiyo wiki atakapo pona kabisa, itagharimu shilingi ngapi”Inspekta Ganjo aliuliza.
“Hadi hiyo siku atakapo ruhusiwa, ndio tutajua imegharimu shilingi ngapi”
“Sawa dokta, ila naomba awe katika uwaangalizi mzuri, maana ni mwanangu huyu”
“Usijali kuhusu hilo, hata kama ingekuwa sio mwanao, sisi tungempa huduma bora, kwasababu sisi tupo kwajili ya wagonjwa, kwahiyo usiwe na shaka”
“Asante dokta, ila naomba nikaongee nae mara moja nimtoe wasiwasi”
“Hakuna shaka, unaweza ukaenda”
Baada ya kutoka katika ofisi ya dokta, walienda katika chumba alicholazwa Hemedy, Inspekta Ganjo aliamua kumpeleka katika hospitali binafsi ili apate matibabu kwa uwangalifu zaidi.
“Baba naomba unisaidie, wataniua na mimi” Hemedy baada ya kumuona Inspekta Ganjo aliongea hivyo na kuanza kulia, alimuita baba kwasababu ndivyo alivyo zoea tangu kipindi cha marehemu baba yake Mzee Mheshimiwa.
“Usijali mwanangu, hawatokudhuru tena, mimi nipo pamoja na wewe”Inspekta Ganjo alimuondoa wasiwasi huku akiwa amekaa kitandani akimshika shika kichwa chake, ili kumfariji.
“Sawa, lakini usiondoke naomba tubaki wote”
“Usijali mimi nitakuja, kwa sasa hivi wewe utabaki na daktari atakulinda pia, hawato kuua, umesikia mwanangu? Sito chelewa, itakuwa kila muda naja kukuangalia, kwa hiyo wewe usiwe na hofu”
“Sawa”
“Subiri niwaagizie wakuletee chai, ule basi maana hizo dawa unazotumia unatakiwa ule sana, ili upone haraka”
“Sawa”
Baada ya kuongea na Hemedy na kumtoa hofu, Inspekta Ganjo alienda hadi kwa daktari na kumuomba nesi mmoja atakae kuwa anamletea chakula mgonjwa wake, maana yeye anakazi nyingi kwahiyo hatoweza kila muda kumletea chakula, Dokta akamuita Nesi mmoja kwajili ya kuongea na Inspekta.
“Maria, embu msikililize huyu mzee” dokta alimuambia nesi wake kwa jina la Maria, na yeye akamgeukia, Inspekta Ganjo.
“Samahani mama, nilikuwa nataka nikuachie maagizo kwamba mwanangu uwe unampelekea chakula wewe, maana mimi sina muda wa kuja kila saa hapa hospitali kwajili ya kuleta chakula, kwahiyo nilikuwa nataka nikuachie hela kidogo kwajili ya kufanya hiyo kazi”
“Hakuna tatizo, wewe nionyeshe mgonjwa wako, mimi nitampa huduma hiyo” baada ya maongezi hayo Inspekta Ganjo alipeana mkono na Daktari, akaongozana na nesi hadi katika chumba alichokuwepo Hemedy, Inspekta Ganjo alimuonyesha nesi na kumuachia shilingi kadhaa, kwajili ya chakula cha Hemedy.
Baada ya kutoka ndani ya hospitali, akanyoosha hadi katika gari la polisi walilokuja nalo, akamuamuru Koplo Taure, aendeshe gari kuelekea kituoni. Baada ya kufika walishuka wote na Inspekta Ganjo alimuambia Koplo Taure amfuate ofisini kwake.
“Unajua kwamba yule mtoto ndio mtoto wa marehemu Mzee Muheshimiwa” Inspekta Ganjo haikujulikana ameuliza au ameongea, ikamfanya hadi Koplo Taure asijue ajibu ama aendelee kuskiliza, akakaa kimya.
“Kwani wewe ulivyo muhoji, alikuambia kitu gani?”
“Sikumuuliza chochote zaidi ya jina lake, alipo nitajia ndio nikashtuka nikaona nije kukuita wewe umsibitishe kama ndie, maana mimi simjui”
“Sawa, basi jua kwamba yule ndio mtoto wa marehemu Mheshimiwa, aliesemekana kuwa ametekwa na majambazi walio vamia nyumbani kwao”
“Ndio mkuu”
“Itabidi tumpe taarifa baba yake mdogo, kuwa mwanae ameonekana au wewe una semaje?”
“Itabidi iwe hivyo”
“Sasa tutampataje?”
“Anapo fanya kazi napajua, alishawahi kunipeleka”
“Sawa, basi itabidi umfuate na kumpa taarifa hizi, maana itakuwa sio vizuri, mwanae yupo hospitali, halafu yeye hajui”
“Ndio Mkuu”
“Mfuate sasa hivi”
Baada ya maongezi hayo, Koplo Taure aliinuka katika kiti alichokaa na kupiga salut na kutoka hadi nje, alipanda gari ya polisi na kwenda moja kwa moja hadi katika Duka la spea za magari, alilomiliki Mrutu, mdogo wake marehemu Mheshimiwa, alipofika alipaki gari pembeni, alishuka na kuenda hadi ndani ya duka hilo.
“Za saa hizi broo?” Koplo Taure Alimsalimia kijana aliemkuta hapo dukani.
“Salama Afande” kijana aliekuwa hapo dukani alijibu, alimuita afande baada ya kumuona ameshuka katika gari ya polisi.
“Ok, nilikuwa namuulizia Mrutu, sijui nimemkuta?”
“Bosi bado hajafika, na leo sijui pia kama atakuja”
“Au nipe namba zake za simu, ili nimtafute kwenye simu”
“Sawa” Alimtajia namba zake, baada ya hapo Koplo Taure akashukuru na kuingia kwenye gari aliyokuja nalo, alipo ingia kwenye gari akajaribu kuzipiga hizo namba alizopewa, na kuambiwa kuwa mteja anaempigia hapatikani kwa sasa labda ajaribu tena baadae, hakuwa na chakufanya akaamua kuondoka zake.
Alipofika kituoni, akaenda hadi kwa Inspekta Ganjo na kumueleza kila kitu na kuambiwa kuwa ajaribu tena kumpigia baadaye, baada ya hapo akatoka na kwenda hadi katika ofisi yake kuendelea na kazi nyengine.
********************************
Mrutu siku hiyo simu yake ilikuwa imekufa berti, tangia asubuhi alikuwa yupo mjini akiingia katika maduka ya simu kutafuta betri jengine, alizunguka sana ila akafanikiwa kupata betri katika duka lililokuwepo katika uwanja mkubwa wa mpira wa Tanga, Mkwakani, linalo itwa G7, alivyopata betri, hakuta kwenda sehemu yoyote zaidi ya nyumbani kwake, alipofika akaliweka kwenye simu na kuiweka chaji, hakua na chengine cha kufanya, akaamua alale tu.
Majira ya jioni aliposhtuka kutoka usingizini, akaenda kuangalia simu yake na kukuta imejaa chaji, akaichomoa chaji na kuiwasha, kitu cha kwanza kukutana nacho ilikuwa ni meseji zilizotumwa na kijana wake wa kazi anaeliangalia duka lake la spea za magari.
Moyo wake ukashtuka baada ya kuisoma meseji hiyo, alianza kupatwa na wasiwasi usio wa kawaida, “Bosi kuna polisi amekuja kukuulizia hapa dukani leo asubuhi”. Meseji hiyo ilimfanya aanze kuloa jasho mgongoni mwake, hakujua polisi huyo ni nani na alikuwa anataka nini.
Akaachana na meseji hiyo na kuifungua nyengine, “ila amesema yeye ni rafiki yako, anaitwa Afande Teure sijui Taure, ila kitu kama hicho” baada ya kusoma meseji hiyo ya pili kutoka kwa kijana wake wa kazi, akashusha punzi ndefu baada ya kugundua kuwa alieenda kumuulizia alikuwa ni Koplo Taure, hapo hapo akampigia simu kijana wake wa kazi, ili kupata maelezo zaidi.
“Hallo Bosi” sauti iliyotoka katika spika za simu iliskika.
“Niambie kolo”
“Shwari tu bosi”
“Sawa, enhee embu niambie, leo amekuja askari kuniulizi hapo dukani?” Mrutu aliuliza swali la kipumbavu, kwasababu meseji aliziona na zilitoka kwa huyo huyo anaemuliza.
“Ndio bosi, alikuja kukuulizia leo asubuhi”
“Wewe ukamuambiaje?”
“Mimi nikamubia kuwa haupo”
“Haja acha maagizo yoyote?
“Hapana hajaacha maagizo yoyote, zaidi tu aliniambia kuwa alikuja kukutembelea”
“Ila kazi leo zimeendaje?”
“Kazi kama kawaida”
“Basi poa baadaye”
“Sawa, ila bosi kwani kuna nini, mbona polisi asubuhi asubuhi?”
“We kolo ni mpumbavu nini, kwani alivyokuja alikuambiaje?”
“Aliniambia kuwa wewe ni rafiki yake na amekuja kukutembelea”
“Sasa kinachokufanya ulize maswali mengi ni nini?”
“Samahani bosi”
Baada ya maongezi hayo Mrutu alikata simu, na kutuliza presha yake aliyokuwa nayo, akaenda kuoga ili kutoa uchovu aliokuwa nao, alipo rudi, akaikuta simu yake ina miskoli mbili, kabla hajajua ni nani aliye piga simu, simu yake ikanza kuita tena, alipoiyangalia akaona ni namba ngeni, akaipokea.
“Halow” sauti nzito iliskika kwenye spika za simu.
“Yes, halow” Mrutu nae akajibu.
“Samahani, naongea na Mrutu hapo?”
“Ndio, nani mwenzangu?”
“Ni mimi Afande Taure”
“Ooooh, kumbe ni wewe? Naskia leo umekuja dukani kwangu kuja kuniulizia, ulikuwa unataka nini? Mrutu aliuliza maswali mfululizo, Koplo Taure hakujua aanze kujibu lipi.
“Ndio ni mimi bwana, nimekuja leo asubuhi dukani kwako nikaambiwa haupo, nilikuwa nataka nikupe taarifa” Moyo wa Mrtu ulipiga Paaaa!!!! Baada ya kuskia neno taarifa, hakujiamini, hakujua taarifa hiyo ni ya nini, akasubiri aambiwe.
“Taarifa yenyewe ni…….” Koplo Taure akamuelezea kila kitu kuhusu kuonekana kwa Hemedy.
“Asante Afande kesho mimi nitaenda hapo hospitali kwenda kumuona”
“Hakuna shaka”
Baada ya kukata simu, mapigo ya moyo wa Mrutu yalikuwa yakienda kasi, akafikiria kuua tu, alijua kuwa Hemedy akipona, atahojiwa ilikuaje na yeye atasema kila kitu na kama kweli Flash ya video ya tukio la mauwaji ya wazazi wake anayo, basi hiyo itakuwa ndio ushahidi, kupelekea kukamatwa kwa wenzake, na wenzake watakapo kamatwa, wataadhibiwa ili wataje wenzao wengine na watamtaja tu na yeye, na hapo ndipo maisha yake yatakopo kwenda kumalizikia gereza la maweni, hakutaka iwe hivyo
Akapanga kesho akifika hospitali, amuulie huko huko, akafikiria atamuua kwa njia gani, “nikifika pale namkaba hadi anakufa, mmmh!!! Ila mbona kama njia hiyo ni hatari? Nishapata wazo, itabidi afe kwa sumu, eeee njia hii ndo nzuri, itabidi nimtilie sumu kwenye chai nitakayo mpelekea asubuhi, hapo sawa”.
Alijiwazia mwenyewe njia ya kumuondoka Hemedy duniani kabla mambo hayaja haribika, alipopata wazo hilo la kutumia sumu atakayo iweka kwenye chai, endapo Hemedy atainywa basi itaondoka na uhai wake, aka lala na hilo wazo.
Majira ya Asubuhi yalimkuta Mrutu akielekea hospitali aliyolazwa Hemedy ili akatekeleze azma yake aliyo ipanga ya kumuondoa Hemedy duniani. Alipofika akaelekea moja kwa moja hadi katika chumba alicho lazwa Hemedy, kwakuwa alishaelekezwa chumba na Koplo Taure, kwahiyo haikumpa shida. Alipofika Hemedy alianza kuangusha chozi, baada ya kumuona baba yake mdogo amekuja, alilia sana kuwa wazazi wake wameuliwa na majambazi, ikabidi Mrutu amnyamazishe, na baada ya muda Hemedy alinyamaza, bila kuchelewa, akampa chai yenye sumu ili anywe afe ili apoteze ushahidi.
Hemedy bila kujua alianza na andazi akalitia mdomoni, baada ya hapo akachukua kikombe cha chai ili anywe……..
“Za saa hizi kaka”
“Nzuri tu”
“Samahani, nilikuwa namuomba huyu mgonjwa anywe hizi dawa, baada ya hapo ndio atakunywa chai”
“Hakuna tatizo, ila si ungemuacha kwanza amalizie kunywa hiyo chai, halafu ndio atakunywa dawa?”
“Hapana kaka yangu, yani hapa pia amechelewa sana, alitakiwa azinywe mapema sana”
“Ok, hakuna tatizo”
“Hemedy, vipi hali yako lakini?”
“Nashukuru mungu, ila bado kifua kina maumivu kwa mbali”
“Usijali mdogo wangu, utapona, haya kunywa dawa”
“Asante nesi, huyo hapo unaemuona ni baba yangu mdogo”
“Ohooo!!! Karibu, mimi ni nesi ninaemuangalia kwa kila kitu mwanao”
“Asante nesi, asante sana”
Hiyo ndo ilikuwa pona ya Hemedy baada ya nesi anae muuguza kutokea na kumtaka asinywe chai kwanza hadi anywe dawa, Mrutu hakuweka sumu kwenye maandazi aliyo ya nunua, ila sumu aliweka kwenye chai, kama Hemedy angeinywa chai iliyoletwa na baba yake mdogo, sidhani kama angeweza kupona. Mrutu alijilaumu kwanini hakuweka sumu na kwenye maandazi, ila hakujilaumu sana, akajua tayari ameshampata kwahiyo hakuwa na wasiwasi nae.
Baada ya kupewa dawa na nesi, alizinywa na kusukumizia na maji. Baada ya kunywa dawa, nesi akamtaka sasa ndio anywe chai, ila kwa bahati mbaya ikawa chai iliyoletwa na Mrutu, ikawa imepoa, hawakuwa budi zaidi ya kuimwaga kwenye sinki la kunawia mikono lililopo humo humo chumbani.
“Usijali, subiri nikamletee nyengine”
Nesi baada ya kuongea hivyo alitoka hadi nje ya chumba alicholazwa Hemedy, kwenda kuchukua chai nyengine, baada ya muda alikuja na chupa na kikombe chengine cha chai.
“Subiri nikuwekee chai unywe maana hizo dawa ulizokunywa zinahitaji ule sana ili ziweze kufanya kazi”
“Sasa nesi si umuwekee tu humu humu kwenye hichi kikombe kilichokuwa na chai mwanzo, huoni kama hivyo itakuwa unachafua vikombe, wakati hiki cha mwanzo kipo?”
“Usijali kaka yangu, hii kazi nimepewa na baba yake nimfanyie, kwahiyo kwangu sio shida”
“Baba yake yupi aliekupa hiyo kazi?”
“Sii huyu aliemleta hapa hospitali”
“Basi hakuna shida”
Baada ya mpango wake wa kutaka kumuondo duniani Hemedy kufeli, hakuwa na njia nyengine ya kufanya kwa hapo, akapanga kutumia njia nyengine, ikiwa hii ya kumpa sumu imeshindikana.
Baada ya kumuona Hemedy, akamuaga na kumuahidi kurudi tena baadaye, akaondoka hospitali hapo na kuelekea kwake, kutafuta njia nyengine ya kumuondoa Hemedy duniani, kabla siri yao haija gundulika.
Majira hayo hayo ya asubuhi, Inspekta Ganjo na yeye alienda hadi hospitalini kwajili ya kumuona Hemedy.
“Shikamoo baba” Hemedy alimsalimia Inpekta Ganjo baada ya kumuona akiingia ndani ya chumba alicholazwa.
“Marhaba mwanangu, hujambo?”
“Sijambo”
“Vipi hali yako inaendeleaje?”
“Nashukuru mungu, maumivu kidogo yamepungua ila kifua bado kinasumbua”
“Usijali mwanangu, utapona kwa uwezo wa mungu”
“Amina, halfu leo bamdogo kaja”
Baada ya salamu walianza kupiga stori za muda mfupi na baada ya hapo, Inspekta Ganjo akamuaga Hemedy akaondoka chumbani humo, alipofika kwenye kordo alikutana na nesi anae muhudumia Hemedy na kumkabidhi kiasi chengine cha hela ili hemedy atakapo taka chochote ampatie, baada ya hapo aliondoka kuelekea kituoni.
*****************************
Mrutu baada ya kufika kwake, alifikiria njia nyengine ya kumuua Hemedy ila alikosa, akaona ni bora kuwashirikisha wenzake watafute njia ya kufanya ilikumuondoa Hemedy duniani haraka sana.
Akachukua simu yake na kuwapigia wenzake ilikuwauliza mahali walipo, akawaambia kuwa wakutane nyumbani kwa Mata ili wapange namna ya kumuua Hemedy, Na yeye akajiandaa na kuianza safari hadi katika nyumba ya Mata, walipo pafanya sehemu yao ya kufanyia mikutano yao.
“Kwahiyo yuko chini ya uwangalidhi wa polithi?”Mata aliuliza kwa hofu, hakika mtu huyu alikuwa anaogopa polisi kuliko kitu chochote..
“Ndio”Mrutu alijbu.
“Thatha itakuaje jamani, mbona kama vile kadhi hii inaenda ndivyo thivyo?”
“Una uhakika kwamba hajawaambia chochote polisi?” Moto aliuliza.
“Uhakika ninao”
“Thatha wewe umehakikisha vipi?”
“Mimi uhakika ninao, bado haja toa maelezo polisi, kwasababu najua tu polisi wangeniambia”
“Thatha kwanini hajatoa maeledho hadi leo?”
“Maelezo hawezi kutoa, kwasababu bado ni mgonjwa”
“Ana nini kwani? Maana thithi thiku ile hatuja mgutha kabitha?”
“Kwa maelezo waliyonipa kwamba, walimkuta akipagwa na kundi la watu wakidhani ni mwizi, kwahiyo hiyo ndio ilimpelekea hadi hali yake kuwa ni mbaya”
“Dah, vipi huja muuliza kwamba flash yenye video kama anayo yeye?”
“Hapana sikumuuliza”
“Kwanini sasa huja fanya hivyo? Inatakiwa tupate uhakika kwamba flash yenye video anayo au hana?”
“Sasa je kama hana? Maana mimi siku ile nilihisi tu ila sikuwa na uhakika”
“Hata kama hana hiyo flash, inabidi afe tu”
“Thawa, inabidi tupange mpango wa kumuulia kule kule hothpital, kabla hali yake haijaimarika”
“Nime liona hilo ndio maana nimekuja hapa, tupange jinsi ya kumuua kule kule hospitali”
“Mimi naona tumpe daktari petha, ili amchome thindano yenye thumu, halafu akiulidhwa atheme hali yake ilibadilika ghafla na kuwa mbaya, ikapelekea hadi kifo chake, au nyie mna themaje?” Mata alitoa wazo lake na kusubiria majibu kutoka kwa wenzake.
“Hapana, hapo Mata mimi sikuungi mkono, hiyo njia yako ni hatari mno”
“Kwanini?” Mata aliuliza
“Je kama ikigundulika kwamba amechomwa sindano ya sumu, si huyo daktari atatafutwa, akipatikana si atatuja, sasa itakuwa ndio tume fanya nini?” Mrutu alionyesha wasiwasi wake.
“Thatha wewe hii njia yangu umeikataa, je ile yako ya kumpelekea chai yenye thumu halafu angekufa, wewe thi ndo ungeshikiliwa, maana wewe ndio wakwandha kumpa kitu ale, bathi moja kwa moja ungekamatwa tu”
“Dah! Hata hivyo pia namshukuru mungu haijatokea, maana sijui ingekueje?”
“Thatha tufanye nini?”
“Mimi nitaenda hospitali kumuua” Moto aliongea, wote wakamtizama yeye kwa mshangao.
“Enhe tuambie utaendaje? ukumbuke yule mtoto anaijua sura yako vizuri, maana sikuile wakati mnavamia pale kwao hamkuvaa hata maksi ili kuziba nyuso zenu”
“Hadi nimesema hivyo basi ujue nimesha fikiria yote hayo”
“Haya tuambie hiyo njia yako uliyoipata” Mata alisema.
“Ni hivi……..” Moto aliwaelezea Mpango mzima atakao enda kuufanya, aliwaelezea mwanzo hadi mwisho.
Wote wakajikuta wanacheka kwa furaha, na kumsifia Moto kuwa anaakili sana.
“Dah! Yani katika thiku uliyoongea na nikakuelewa bathi jua ni leo, yani leo umeongea kitu ambacho kime nifanya nikuone unaakili thana kuliko hata aliegundua petha, dah! umenifurahisha thana”
“Moto sio siri hata mimi huo mpango wako nimeukubali na ninauunga mkono kwa asilimia zote”
“Ndo hivyo sasa”
“Thatha utaifanya lini hiyo kadhi na thaa ngapi, maana nina wahka wa kujua itafikia wapi, dah! thio thiri huyu mtoto ananichanganya thana”
“Yani nyie msijali, cha msingi ni kuomba mungu mpango utiki tu, si mna jua hata mchawi anapoenda kuwanga sehemu na yeye anamuomba mungu asikamatwe”
“Itabidi ikitiki hii ishu, tufuatilie zile mali ili tuzichukue haraka iwezekanavyo”
“Hata mimi niliwadha hivyo hivyo, maana nishachoka kutembelea kile ki Verostha, nataka na mimi nitembelee V8, nataka na mimi nionekane mtu mbele ya watu”
“Yani nyie msijali, chamsingi nikuomba mpango ufanikiwe tu, mbona yote hayo yatatokea”
“Thatha kwahiyo mimi ndio mnaniacha peke yangu?”Mata aliuliza.
“Wewe ulikuwa wataka uwende wapi wakati hapa ndio kwako”
“Hapana mimi thija themea kuondoka, ila nichothemea mimi kwamba mna ondoka nyote thi bora Moto angebaki tupige wote thtori”
“Tunge baki ila mimi nataka nikauanze leo ule mpango”
“Anhaa! Kama ndio hivyo thawa”
Mrutu na Moto waliondoka nyumbani kwa Mata, walipanda kwenye gari alilokuja nalo Mrutu, Mrutu aliamua kuchukua gari moja kama alivyosema, wakaondoka na kuelekea moja kwa moja hadi dukani kwa Mrutu. Baada ya kukaa sana dukani hapo Moto alitaka kuondoka ili kwenda kuanza mpango walio upanga.
“Sasa Mrutu acha mimi nikuache ili niufatilie ule mpango”
“Usijali kwa hilo wewe nenda tu”
“Basi poa acha mimi niwahi” Baada ya kuagana na Mrutu, Moto aliondoka zake kwenda kuanza huo mpango.
Majira hayo hayo ya mchana, Inspekta Ganjo alifunga safari hadi hospitali, kwenda kumjulia hali Hemedy, baada ya kupata muda kidogo, alipofika aliingia hadi katika chumba alicholazwa Hemedy nakumkuta akiwa anakula chakula alicholetewa na nesi.
“Nakuona mwanangu unakula tu, hata unikaribishi”
“Nikukaribishe vipi wakati mimi ni mgonjwa natakiwa nile sana ili dawa zifanye kazi, au unadhani mimi nataka kukaa hapa hospitali kila siku, mimi nishachoka harufu za madawa”
“Nikumshukuru mungu maana hali yako sasa hivi sio mbaya sana, tofauti na mwanzo, hata uchangamfu wako naona pia umerudi tena, naona leo unaongea kama kawaida yako, ila sasa utundu wako usiulete hadi kwenye dawa, unatakiwa dawa uzimnywe, usilete ujanja ujanja kabisa, au wewe hutaki kutoka hapa hospitali?
“Mmh!!!! Mimi nataka kuondoka hata sasa hivi, au kwanini baba usiwaambie nikamalizie dawa nyumbani?”
“Hapana inabidi ukae hapa hapa hadi utakapo ruhusiwa, unataka kuondoka leo je ukifika nyumbani ukizidiwa itakuaje?”
“Ila mimi nishachoka kuchomwa sindano kila muda, yani sasa hivi hata kukaa viziri pia siwezi kwajili ya kuchomwa masindano tu”
“Hahahahah, Usijali utatoka tu hospotali, na hayo masindano yataisha pia”
“Sawa nimekuelewa, ila mama yangu na baba yangu tayari wameshazikwa?”
“Tayari tumeshawazika, chamsimgi sasa hivi ni kuwaombe kwa mungu tu, awaepushe na adhabu zake”
Hemedy baada ya kuambiwa hivyo, aliacha kula chakula na kuanza kulia aliwakumbuka wazazi wake, ili bidi Inspekta Ganjo, aanze kum’bembeleza, ilichukua kama dakika kumi na tano ndipo Hemedy akanyamaza, Inspekta Ganjo hakuwa na muda wa kuendelea kubaki hospitali, akamuaga Hemedy na kuondoka zake.
******************************
Majira ya usiku mishale ya saa Nne, alionekana mwanaume alievalia mavazi ya kidaktari, alikuwa amebeba kisahani kilicho kuwa na bomba la sindano na na kichupa cha dawa, aliingia kwenye chumba alicholazwa Hemed, alipoingia alifunga mlango vizuri na kumsogelea Hemedy hadi karibu yake huku akitabasamu, alipomfikia karibu kabisa, alishusha suruali aliyoivaa Hemedy, upande wa kalio lake la kushoto na kufanya kalio la Hemedy lionekane vizuri.
Alichomoa bomba la sindano na kulikita katika kichupa cha dawa, akainyonya dawa kidogo na kulichomoa bamba kwenye kichupa, baada ya hapo alilipeleka bomba la sindano hadi kwenye kalio la la kushoto la Hemedy, na kulichoma, alihakikisha dawa yote imeingia ndani ya ngozi ya hemedy, akalichomoa na kutabasamu tena, “Nime maliza kazi” Alisema hivyo na kuondoka zake……
Mtu yule alifungua mlango akatoka nje ya chumba alicholazwa Hemedy, kwenye kordo alikutana na nesi anae muuguza Hemedy.
“haiwezi kutokea, mimi nakua nae muda ambao sina kazi”
“Acha mimi niende maana ninausingizi mwingi sana”
“Poa we nenda, acha mimi nimfuate” Baada ya kuagana na Dokta Imamu, alienda hadi katika chumba alichokuwemo Hemedy, nakumkuta amelala kifudi fudi.
“Hemedy huo ndio ulalaji gani?” Nesi Maria alimuuliza huku akicheka.
“Dada maria we acha tu, ili lijamaa lilokuja linaroho mbaya kumshida Iddi Amini”
“Hahahahah, kwanini?” Nesi maria alimuuliza huku akiwa bado anacheka.
“Yani linakuja huku liki tabasamu, lilipoanza kunichoma sindano, likaondoa tabasamu, aisee limenichoma sindano ya tako lakini nimeisikia hadi kwenye moyo”
Hadi hapo Nesi Maria hakuweza kukizui kicheko chake, akacheka kwa sauti ya juu hadi sauti yake ikasambaa chumba kizima.
“Yani siku nyengine akija kunichoma yeye sindano, nitakataa labda nianze kumchoma mimi kwanza ili ajue maumivu yake, mwenyewe nishakuzoea wewe ukija kunichoma unanimbia nyimbo hadi ukinichoma sindano si isikii kabisa”
“Kwenda zako huko, itabidi asaivi nimpe yeye ndo akuchome maana mimi unanisumbua, ila unanifurahisha sana we mtoto, yani ukiondoka sijui itakuaje, maana nishakuzoea na vituko vyako”
“Kwani wewe unapenda niendelee kubaki?”
“Ndio, ila sasa ndio hivyo haitowezekana, maana inabidi uondoke tu”
“Mimi sitaki kubaki hapa hospitali, maana naliogopa lile lijamaa linaweza siku nyengine likanichoma sindano hadi nika paralaizi, halafu lilivyokuwa na sifa, lilivyomaliza kunichoma sindano, likasema eti nimemaliza kazi, likaondoka huku likitabasamu, yani hujui tu ila hapa nahisi kama vile sina matako, mi sitaki linichome tena sindano”
“Usijali hatokuchoma tena”
Nesi maria alikuwa anacheka tu muda wote kwa vituko vya Hemedy, alimfurahia huyo mtoto, alitokea kumpenda ghafla, alitamani kila muda awe nae wanapiga stori kama hivyo, ila muda mwingi alikuwa yupo na wagonjwa, ni muda mchache sana ndio alikuwa yupo frii, na aliutumia kuwa na Hemedy.
* * * *
Siku iliyo fuata. Mwafrika Phamarcy 5:03 asubuhi.
“Za saa hizi dada yangu?” Moto alimsalimia dada aliemkuta mapokezi kwenye duka hilo kubwa la dawa na vifaa vya hospitalini.
“Salamu tu, nikusaidie nini?”
“Kuna vifaa navihitaji”
“Ok, unaweza ukavitaja”
“Nilikuwa nataka, mavazi ya kidaktari na bomba la sindano na kichupa cha dawa kilichokuwa kitupu”
Dada wa mapokezi alimuangalia Moto kwa wasiwasi, hakuelewa mtu huyo anavitaka vitu hivyo ili akavifanyie nini, haikuwahi kutokea hata siku moja mtu wa kawaida kuja kununua vifaa vya hospitali, alishazoea kuona madaktari wa hospitali mbali mbali, kuja kununua vifaa vya hospitali, tena sio kimoja kimoja kama anavyotaka huyu mteja wake mpya, ila kwa vile wao wanataka hela, hakutaka kumuhoji, alichofanya yeye ni kuingia ndani, baada muda alirudi na vitu alivyo vitaka mteja wake.
“Hivi hapa kaka”
“Asanate, vyote hivi ni bei gani?”
Moto alipoambia bei, akalipa na kuondoka zake, kuelekea nyumbani kwa Mata, alipofika akamkuta Mata amekaa sebleni anaangalia tivi.
“Huwezi amini vitu vyote nimevipata, tena kwa urahisi, yani sikutegemea kabisa”
“Embu nivione” Mata aliomba avione vifaa vya hospitali alivyo kuja navyo Moto, baada ya kuviona, waliamua wampigie simu Mrutu ili waje kupanga mpango utakavyoenda, baada kama nusu saa Mrutu alikuja hadi hapo nyumbani kwa Mata.
“Kwahiyo sasa inakuaje” Mrutu na yeye aliongea baada ya kuviona hivyo vifaa.
“Kama tulivyo panga, kuwa mimi nitajifanya mgonjwa wa tumbo, yani tumbo linaniuma sana, halafu wewe Mata utanipeleka hospitali hiyo hiyo aliyolazwa Hemedy, hata kama wasipoona ugonjwa unaonisumbua, Mata utawalazimisha wanipe kitanda ili waendelee kuiyangalia hali yangu, wakishanipa kitanda, itakuwa mpango wetu umeanza kutiki.
Halafu hivi vifaa itabidi tuvitie ndani ya begi dogo, ambalo kwa juu nitaweka nguo zangu za kawaida, ikifika usiku, nitabadilisha nguo na kuvaa nguo za kidaktari, baada ya hapo, mimi nitaingia hadi katika chumba alicholazwa yule mtoto, baada ya kuingia humo, nitamchoma sindano yenye sumu hadi nihakikishe ame kufa, halafu kama kutakuwa na uwezekano wa kutoka usiku huo huo basi mimi nitaondoka zangu ila kama hakutokuwa na uwezekana huo, itabidi ni lale halafu asubuhi naondoka zangu.
“Mbona katika maelezo yako umefanya kila kitu kuwezekana? Mrutu aliuliza.
“Kivipi yani Sijakuelewa”
“Umesema kuwa utajifanya unaumwa na tumbo, halafu wasipoona ugonjwa, itabidi Mata awalazimishe wakupe kitanda, je kama wasipo kupa kitandana? Unajua mimi jana huu mpango sikuuelewa vizuri, embu leo nieleweshe”Mrutu aliuliza.
“Mrutu hakuna kigumu mbele ya hela, kwahiyo kama wakikataa tutawapa hela, mi naamni watakubali tu”
“Sawa,hapo nimekuelewa, je hizo nguo utazibadilisha wapi? Maana unesema utabadilisha nguo ila hukusema utabadilisha wapi, embu nieleweshe na hapo”
“Kwani vyoo si vipo? Nitabadilisha hata chooni”
“Sawa, hapo pia nimekuelewa, umesema utamchoma sindano yenye sumu, je kama ukimkuta yupo macho? Huoni kama hiyo itakuwa ni hatari maana sura yako itakuwa anaikumbuka? Basi tufanye hatoikukumbuka sura yako, je utamshawishi vipi hadi akubali kuchomwa sindano nyengine, maana sindano ya dawa muda huo atakuwa tayari ameshachomwa na daktari” embu nieleweshe na hapo”
“Itabidi nitumie nguvu tu kama atakataa kuchomwa sindano, yule ni mtoto hawezi kunizidi nguvu”
“Sawa kama ndio hivyo mimi namitakia safari njema”
“Embu jaribu hidho nguo tukuone”Mata aliongea. Moto bila hiyana akazivaa nguo za kidaktari alizo nunua kwajili ya kazi, hakika hakuweza kutofautishwa na daktari, kama akitokea mtu asiye mjua Moto, bila shaka atasema ni daktari mzoefu, kumbe elimu yake ni ya form four tu, hakuwa na taaluma ya udaktari wa aina yoyote.
“Dah! Yani hapo kama vile daktari anaemtibu raithi, kuthema ukweli hayo mavadhi yame kupendedha” Mata alisifia.
“Yani nikishapata hizi hela, itabidi nikasomee udaktari, halafu mata wewe si una miwani yako ile kama ya macho?”
“Ndio ipo, tena thubiri nikailete” baada ya kuongea hivyo Mata alienda hadi chumbani kwake baada ya muda alirudi akiwa na miwani inayofanana na ya mgonjwa wa macho, akampatia Moto akaivaa, alikuwa na haki hata ya kujiita Profesa, kwajinsi alivyotoka, hakutofautishwa na daktari.
“Thatha hapo umekamilika, embu tufanye haraka twendhetu huko hothpitali”
Baada ya muda walijianda na kuianza safari ya kuelekea hospitali waka kamilishe mpango wao walio upanga, baada ya muda walikuwa nje ya hospitali aliyolazwa Hemedy.
Kama ingekuwa Moto anaigiza katika Bongo Muvi, basi angejinyakulia umaarufu mkubwa sana, maana alikuwa ana ekti kama vile kweli, kwa mtu ambae hakuujua mpango wao, basi angemuonea huruma sana, alishika tumbo lake huku akilia, machozi yalimtoka katika macho yake. Manesi walimuwahi na kumuweka juu ya kitanda, na kuanza kumpeleka katika chumba cha matibabu, walipofika kwanza walimchukua vipimo, baada ya muda daktari alimuita Mata hadi katika ofisi yake ili aende kumpa majibu ya ndugu yake.
“Mgonjwa wako tumempima na kugundua kuwa hana tatizo lolote”
“Thatha dokta itakuaje athiwe na tatizo wakati mtu anaumwa vile, hata wewe mwenyewe pia umeona”
“Ni kweli hata mimi pia nimemuona, ila vipimo vinaonyesha hana tatizo”
“Thatha dokta itakuaje?”
“Hapa inabidi tumpe dawa zitakazo tuliza maumivu, mimi nahisi itakuwa ni tumbo la kawaida tu na muda wowote linaweza likaacha”
“Kwahiyo dokta unatakawa kumpa dawa tu hivi hivi?”
“Sasa ulikuwa unatakaje labda?”
“Mimi nilikuwa nataka mumpe kitanda hadi kesho muangalie hali yake kama itatulia bathi hakuna tatizo mutamruhuthu”
“Sawa kama ndio unavyotaka, tutampa kitanda”
“Bathi nashkuru daktari kwa mthaada wako”
“Hakuna shaka”
“Ninawedha kuenda kumuona mara moja?”
“Unaweza kwenda”
Baada ya kuagana na daktari, alitoka katika ofisi ya daktari na kuelekea katika chumba alicholazwa Moto.
“Daktari hana lolote, nimempiga kithwahili kakubali ulale hadi kesho”
“Basi haina shaka mimi hii kazi nitaifanya usiku”
“Bathi acha nikuache”
“Poa”
Baada ya kuaga, Moto alilala kwenye kitanda cha hospitali ili kusubiria usiku afanye kazi iliyomleta hapo hospotali.
******************************* 4:30 Usiku. Hospitali ya Tumaini.
Moto aliinuka katika kitanda cha hospitali hiyo, na kwenda chooni na begi lake dogo, alipofika alibadilisha nguo na kuvaa nguo za kidaktari, akachomoa bomba la sindano na kichupa cha dawa chenye sumu, akavitia mfukoni na kwenda hadi katika chumba alicholazwa Hemedy.
Alipofika akafungua mlango na kuzama ndani, bahati ikawa kwake, alimkuta hemedy amelala, akamuendea hadi karibu na kuchomoa sindano iliyokuwa katika mfuko wa koti la kidaktari na kutoa kichupa chenye sumu, bila kuchelewa akakita bomba la sindano kwenye kichupa chenye sumu, alivyochomoa bomba la sindano ilikuwa imejaa sumu iliyokuwa kwenye kichupa, akaushika mkono wa Hemedy ili achome sindano yenye sumu katika bega la Hemedy, bila kuchelewa akaipeleka sindano hadi kwenye bega la Hemedy na kuanza kuchoma……
Kabla hajamchoma sindano, alisikia mlango ukifunguliwa, akaghairisha mpango wake, sindano akaitia haraka kwenye mfuko wa koti la kidaktari.
“Vipi dokta?” Nesi Maria aliuliza, yeye ndio alieingia humo chumbani.
“Sa…safi tu”Moto alijbu kwa kutetemeka, akajua tayari mpango wake umegundulika, akasubiri matokeo.
“Vipi kwani, mbona umeingia chumba hichi, kuna nini?” Nesi Maria hakuweza kumuhisi vibaya, kutokana na kipindi hicho kulikuwa na Madokta wa fildi, kwahiyo akadhani na yeye pia ni mmoja wapo.
“Samahani, nimekosea chumba”
“Kwani wewe ulikuwa unaenda kwenye chumba namba ngapi?”
“Sijui ni Tisa ile, sina uhakika”Akataja chumba alichokuwa yeye.
“Kama ni chumba namba tisa,basi fuata mkono wa kushoto kutoka hapo nje, utanyoosha hadi kwenye kona utaingia mkono wa kulia, basi kuanzia hapo angalia juu ya milango utaziona namba zimeandikwa kila mlango, wewe zisome hizo namba hiko chumba utakiona”
“Asantea dokta acha mimi niende”
“Poa”
Baada ya kutoka hadi nje alianza kwenda hadi katika chumba alicholazwa yeye, ila kabla hajafika, akaingia kwanza chooni na kubadilisha nguo, akavaa nguo zake za mwanzo na zile za kidaktari akazitia kwenye begi aliloliacha hapo hapo chooni.
“Kumbe ulikuwa bado hujalala?” Nesi Maria, alimuuliza Hemedy baada Moto kuondoka.
“Nilikuwa nimelala, ila maongezi yenu ndio yamenishtua”
“Kwa maongezi gani yale mpaka yakakufanya ushtuke usingizini”
“Mimi nikilala silali kama nimekufa, yani hata hatua za sisimizi pia zinaweza zika nishtua”
“Hahahahah, wewe mtoto usinichekeshe, haya sisimizi ana kishindo gani chakufanya ushutke usingizini?”
“We si hujui tu, ila mimi masikio yangu mazima, halafu pia nina hisia kali sana”
“Muongo”
“Huamini?”
“Ndio siamini”
“Haya subiri nifumbe macho, halafu nianze kukuelezea ulivyo”
“Haya fumba macho” Hemedy akafumba macho.
“Kwanza kabisa, upo mbele yangu, halafu umevaa nguo za kidaktari, halafu hapo ulipo unatabasamu,nime kosea?”
“Hahahhah, mtoto mpumbavu kweli, embu fumbua mimacho yako uko”
Siku iliyofuata, Mata alienda hadi hospitali kuulizia maendeleo ya ndugu yake kama walivyo ekti, na kufika hadi kwa daktari.
“Kwahiyo jana uthiku hakuthumbua kabitha?” Mata alimuuliza daktari baada ya kuambiwa hali ya Moto ilivyokuwa.
“Ndio hakusumbua kabisa, inabidi leo uondoke nae maana hali yake ni nzuri, na nitamuandikia dawa za kutuliza maumivu, mkitoka mtapitia katika dirisha la dawa, muzichukue”
“Athante dokta, ninawedha kuondoka nae?”
“Yeah, unaondoka nae”
“Haya dokta kadhi njema” Baada ya kuagana na dokta, alitoka katika ofisi ya dokta na kuelekea hadi katika chumba alicholazwa Moto.
“Vipi, kadhi umekamilisha?” Mata aliuliza kwa pupa huku akitabasamu akijua kazi imekwisha.
“Subiri nitakuelezea tukifika nyumbani”
“Thatha thi uniambie mara moja tu?”
“Mata, mbona una haraka hivyo?”
“Haya twende”
Walianza safari ya kuelekea nyumbani kwa Mata, walipitia kwenye dirisha la dawa na kupewa dawa kama walivyoambiwa na daktari, wakapitia na mapokezi na kulipa gharama zote.
Baada ya kulipa gharama zote, walitoka nje na kupanda kwenye gari, ili waondoke zao, wakati wapo ndani ya gari wakashauriana wampigie simu na Mrutu ili wakutane nyumbani kwa Mata, walipofika wakaingia hadi ndani, na baada ya muda mfupi Mrutu nae akaingia, baada ya kusalimiana wote wakamtaka Moto awaelezee imekuaje huko hospitali.
“Dah! Yani hamuwezi amini yule mtoto nahisi alipangiwa asife pale hospitali”
“Embu acha kuzunguka mbuyu, tuelezee imekuaje”
“Ok, achaniwaelezee ilivyokuwa. Wakati…..” Moto aliwaelezea kila kitu, mwanzo hadi mwisho.
“Kwahiyo huku fanikiwa kumuua?” Mata alimuliza swali la kipumbavu.
“Mata unataka nikuambie mara ngapi?”
“Aaah!!! Nimechanganyikiwa ndugu yangu”
“Eeeee basi ndo hivyo, sasa sijui tunafanya nini tena” Moto aliongea.
“Hapa hakuna chengine cha kufanya dhaidi ya kumuua tu”
“Ndio lazima afe, sasa hiyo njia ya kumuua ndio ipi tena”
“Itabidi tupange mpango mwengine” Mata alisema.
“Sasa huo mpango mwengine ni upi?” Mrutu aliuliza.
“Tutapanga baadae, kwanza sasa hivi mimi nina usingizi, jana usiku sijalala kabisa kwajili ya hofu”
“Hofu ya nini?” Mata aliuliza.
“We unadhani kufumaniwa unataka kumchoma mtu sindano ya sumu ni mchezo?”
“Kwani umegundulika?” Mata aliuliza.
“Hata kama, ila ndio hivyo sijapata usingizi, halafu pia ndio mara yangu ya kwanza kulala hospitali, hata hiyo pia imechangia nisipate usingizi” Moto aliongea huku akielekea katika chumba kimoja wapo cha hiyo nyumba ya Mata.
“Wewe nenda kalale, ila ukiamka uthithahau kutandika kitanda”
“Utatandika mwenyewe bwana” Moto aliongea huku akifunga mlango.
“Sasa Mata, acha na mimi niende dukani kwangu, maana nimemuacha yule kijana wangu mwenyewe, halafu si unajua pale muda mwengine wateja wanajaa Sasa acha basi mimi nikamsaidie”
“Haya bwana we nenda, hata hivyo mimi mwenyewe pia najiandaa kuondoka hapa kuelekea kadhini, maana kuna kadhi dha watu thija dhimalidhia”
******************************
Majira ya mchana, yalimkuta Inspekta Ganjo, akielekea katika hospitali aliyolazwa Hemedy, alienda hadi katika chumba alicholazwa Hemedy, akamkuta akiwa amekaa. Hemedy alimsalimia Inspekta Ganjo, baada ya salamu, Insepekta Ganjo akamuuliza hali yake inaendela vipi, Hemedy akamjibu kuwa sasa hivi ana unafuu, wakati wakiendelea na maongezi, Nesi Maria akaingia na kumuambia Inspekta Ganjo anaitwa na daktari, Inspekta Ganjo aliinuka na kwenda kwa daktari.
“Hali ya mwanao sasa hivi inaendelea vizuri” Daktari alianzisha maongezi baada ya salamu.
“Nashkuru daktari, kwahiyo ni lini mutamruhusu?”
“Nimekuita hapa ili nikuambie kuwa leo ndio tutamruhusu kuondoka, baada ya kuona hali yake kidogo imetengemaa”
“Kwahiyo mutamruhusu sasa hivi au?”
“Sasa hivi itabidi uondoke nae, na nimemuandikia dawa nyengine za kukausha kabisa vile vidonda, chukua hii karatasi(huku akimpa karatasi iliyo andikwa dawa) mtapitia pale kwenye dirisha la dawa”
“Na malipo?”
“Mkifika pale mapokezi mtaambiwa kila kitu”
“Asante dokta, mungu akubariki”
“Amina, na wewe pia”
Baada ya kuagana, Inspekta Ganjo alienda katika chumba alichokuwemo Hemedy, na kumchukua na kuondoka nae, wakati wakiwa kwenye kordo wakielekea katika dirisha la dawa, walikutana na nesi Maria.
“Haaa!!! Kwani ndio umeruhusiwa kuondoka leo?” Nesi Maria aliuliza.
“Ndio nimeruhisiwa, kwani wewe ulitaka ni baki hadi lini?”
“Hapana, nilikuwa nauliza tu, ila kama umeruhusiwa pia sio mbaya”
“Basi ndio hivyo”
“Sawa, ila nitakuona lini tena mdogo wangu, unajua mimi tayari nishakuzoea?”
“Usija dada maria, mi mbona nitakuja kukutembelea siku yoyote tu”
“Haya safari njema” Baada ya kuagana, walienda hadi katika dirisha la dawa na kumalizia mapokezi, baada ya kukamilisha kila kitu, waliondoka hadi kituoni.
Walimuhoji maswali kwamba ilikuaje kuaje. Hemedy aliwaelezea jinsi tukio lilivyotokea hadi yeye kuponea chupuchupu, aliwaelezea hadi alipo bambikiwa zahma la uwizi, na kunusurika kifo kwa mara ya pili, baada ya kutokea kwa polisi.
“Ndio nawajua, tena…(Hemedy ikawa anataka kusema kwamba flash ya tukio zima pia anayo, ila akakumbuka aliambiwa na Goda kuwa hiyo flash asimpe mtu akae nayo yeye mwenyewe, akaghairisha kusema hivyo) Na wajua nikiwaona” akamalizia. “Koplo Taure, inabidi umpigie simu baba yake mdogo aje amchukue mwanae, akakae nae ikiwa sisi tunaendelea na uchunguzi, tena mpigie sasa hivi”Inpekta Ganjo alimuambia Koplo Taure.
Koplo Taure alimpigia simu Mrutu na kumuambia aje kituoni. Baada dakika ishirini, Mrutu alifika hadi kituoni hapo.
“Ndio bwana Mrutu, mwanao huyo hapo, itabidi wewe uwende nae nyumbani, huku sisi tukiendelea na uchunguzi”
Baada ya hapo, Mrutu aliaga na kuondoka na Hemedy kuelekea nae nyumbani kwake. Walipofika Mrutu, akamkaribisha Hemedy nyumbani kwake, akamuonyesha chumba atakacho lala, baada ya kumuonyesha kila kitu, Mrutu alitoka hadi nje ya chumba alichompa Hemedy huku akitabasamu.
“Kazi imekwisha, nammaliza leo leo” Mrutu aliongea hivyo na kutoka hadi nje ya nyumba yake na kwenda kusikojulikana.
“Tobi”
“Mkuu”
“Nenda kaniitie Tito mara moja”
“Sawa Mkuu”
Kijana mwenye mwili mkubwa kutokana na kufanya mazoezi ya kunyanyua vyuma aliejulikana kwa jina la Tobi, alienda alipo agiziwa na Mzee mwenye mvi zilizoanza kuota kwenye nywele zake. Baada ya muda si mrefu alirudi na kijana mwenzie aliekuwa na mwili mkubwa kama yeye, wote wakasimama mbele ya Mzee mwenye nywele zilizo anza kuota mvi.
“Mkuu” wote waliongea neno hilo.
“Tito?” Mzee mwenye nywele zilizoanza kuota mvi aliita.
“Mkuu” Kijana mwenye mwili mkubwa aliejulikana kwa jina la Tito aliitikia.
“Unaweza ukaniambia kwanini mzigo wakati naondoka niliuwacha mwingi, ila sasa nimerudi nakuta mzigo umepungua na nikiangalia mahesabu naona siyaelewi kabisa, kwanini imekuwa hivi?”
“Mkuu, unachoongea ni kweli kabisa, kuna mtu alitaka mzigo nikampa, ila aliniambia kuwa pesa ataniletea baada ya wiki mbili, ila sasa naona ni mwezi na nusu huu hajaleta bado”
“(huku akiinuka na kuipiga meza iliyokuwepo mbele yake kwa gazabu) Nime kukataza mara ngapi kutoa mzigo bila ya kupewa pesa? Wewe unazijua biashara zetu hizi, kutapeliana ni jambo la kawaida, halafu wewe unaenda kutoa mzigo bila ya kupewa pesa?”
“Mkuu, ila nimefanya hivyo kwa mtu ambae tunamuamini sana na hata wewe pia umeruhusu kuwa akija hata kama akiwa hana pesa tumpe mzigo pesa ataleta siku yoyote”
“Sijajua Mkuu, kwasababu pia sio kawaida yake kuchelewa kuleta pesa baada ya kumpa mzigo”
“Nenda kamfuate na umuambie kuwa tunataka pesa yetu, au kama hana pesa, basi mwambie akupe mzigo wetu”
“Sawa Mkuu”
“Ok, Tito nenda nilipo kutuma, na Tobi wewe nenda kaendelee na kazi”
“Mkuu” walisema wote kwa pamoja na kuondoka.
Mazungumzo hayo yalifanyika katika ngome ya Mzee mwenye nywele zilianza kuota mvi, anaejulikana kwa jina la Mr Bakari Haneni.
Mr Bakari Haneni, alikuwa ni muuzaji wa madawa ya kulevya, alichangia sana kuwaharibu vijana wa Tanga kwa kuwauzia madawa hayo hatari ambayo serikali ilipiga vita kila siku.
Kwa wakati huo alikuwa yupo katika jengo la gorofa mbili lililochakaa kwa kuachwa na wakoloni miaka mingi iliyopita, lililokuwa maeneo ya mwambani kando kando ya bahari ya hindi.
Mr Bakari Haneni, alikuwa ni mtu katili sana, kuua kwake ni jambo jepesi kuliko kufumbua na kufumba kope ya jicho lake, alikuwa na walinzi wanao lilinda jengo hilo zaidi ya hamsini, na kila mlinzi mmoja alikuwa na silaha kali, alikuwa akiwakamata vijana wadogo hasahasa wakiume kwajili ya kufanya kazi ya kufanga madawa ya kulevya kwenye vipakti vidogo vidogo.
Alikuwa ni tajiri mkubwa tu katika mkoa huo wa Tanga kupitia biashara hiyo ya madawa ya kulevya, alikuwa anamiliki nyumba moja ya gorofa iliyokuwepo maeneo ya Raskazone, anamiliki Hoteli za nyota tatu, moja ilikuwa maeneo ya kwaminchi na nyengine ilikuwa pangani, alitembelea magari ya kifahari ya kila aina.
Akiwa hadharani alionekana ni mtu mwema sana, alipeleka misaada katika vituo vya kulelea watoto yatima mbalimbali vilivyopo katila mkoa huo wa Tanga, alionekana ni mtu mwema sana mbele ya watu, kuna waliosema kwamba Mzee huyo akiamua kugombe ubunge kwa mkoa wa Tanga kwa chama chochote kile, basi atapita bila pingamizi lolote, kutokana kuwa watu walimpenda kwa kujitolea kwake.
Ila kwa upande mwengine, alikuwa ni katili na aliuwa watu bila sababu yoyote, alikamata vijana wadogo na kwenda kuwatumikisha katika ngome yake kwa kuwafanyisha kazi za kufunga madawa ya kulevya, na ikionekana kati ya hao vijana mmoja wapo akianza kusinzia tu kutokana na kuathiriwa na madawa hayo wanayo yafunga, aliuliwa na kwenda kutupwa katika shimo na mwisho huchomwa moto, ilikuwa sio rahisi kwa mtu wa kawaida kuingia halafu utoke nje ya ngome hiyo, waliokuwa wakipelekwa katika ngome hiyo waliishia kufa na maiti zao huchomwa moto mpaka kuwa majivu, pamoja na yote hayo, serikali ilikuwa haijui chochote kuhusiana na ukatili aliokuwa akiufanya Mzee huyo.
* * * *
“Hallow”
“Niambie Mrutu”
“Shwari, sijui nani mwenzangu?”
“Tito, Mr Tito hapa naongea”
“Ohhhh!!! Tito, samahani ndugu yangu, simu yangu ilpotea na nimenunua simu nyengine na hata laini pia nimenunua nyengine, sikuweza kuirinyuu kwasababu kitambulisho nilicho sajilia nacho pia kili potea”
“Sawa, mbona sasa kimya? Mwezi huu na nusu hujarudisha pesa zetu halafu pia mawasiliano na sisi umekata, eeeh kuna nini?” Tito alimuuliza kwa upole kabisa kilichomkumba Mrutu hadi ikawa harudishi pesa zao.
“Hapana kaka, nilipatwa na msiba wa kaka yangu halafu pia nimekabidhiwa mimi nimlee mwanae aliemuacha ndio maana ukaona nipo kimya ila ningekuja maskani tuje kuyamaliza, ila usijali pia kwa hilo siku si nyingi nitakucheki ili nirudishe pesa zenu”
“Hakuna tatizo ila naomba unitafute wewe usitake hadi nikutafute mimi maana Mkuu alikasirika kweli ila tulivyomuambia kuwa ni wewe ndio umechukua mzigo, kidogo hapo akapunguza hasira zake ila fanya urudishe pesa za watu au rudisha mzigo kabla Mkuu hajatoa amri mbaya juu yako”
“Usijali nitafanya hivyo hivi karibuni tu”
“Hakuna shaka Bwana Mrutu”
Mrutu alipogundua kuwa anaongea na mtu alieamua kupoteza mawasiliano nae kwa makusudi, kutokana na kudaiwa pesa alizo chukua mzigo wa watu wa madawa ya kulevya, alianza kupatwa na hofu, hakuelewa mtu huyo namba yake iliipata vipi.
Mrutu pamoja na kuwa na duka la spea za magari lililo muingizia pesa nyingi, ila pia aliona haitoshi, baada ya kushawishiwa kuwa kazi ya kuuza madawa ya kulevya ina hela sana, akashawishika na biashara hiyo haramu, akaamua na yeye aanze kuuza madawa ya kulevya.
Akakutanishwa na Tito kwa mara ya kwanza, akaomba kuelekezwa biashara inavyoenda, akaelekezwa vizuri na yeye akanunua mzigo mdogo kwajili ya kuanza nao, bahati ikawa kwake akaumaliza wote.
Akazidi kushawishika na biashara hiyo baada ya kuona imemletea faida kubwa, akamtafuta tena Tito akaomba amuongezee tena mzigo, safari hii aliomba apewe mwingi zaidi ya ule wa mwanzo baada ya kuona ule wa mwanzo faida umemletea kubwa.
Baada ya kufanya biashara sana na Tito, akafanikiwa kuwa mteja mkubwa kuliko wote kwasababu yeye alikuwa anachukuwa mzigo mkubwa sana, ilikuwa akichukua karibia nusu ya mzigo unaokuja, ndipo hapo Mr Bakari Haneni akataka kumuona huyo mteja wake anaechukua nusu ya mzigo anawo uleta, akakutanishwa nae katika hiyo ngome yake, na Mrutu ikawa ndio mtu wa kwanza wa kawaida kuingia na kutoka katika ngome hiyo akiwa na uhai wake.
Alipo aminiwa sana ikawa na yeye akija bila pesa anapewa mzigo bila ya wasiwasi wowote na yeye akimaliza mzigo au hata kama hajaumaliza basi anarudisha pesa ya watu ndipo hapo Mr Bakari Hanaeni alipo muamini na yeye.
Ila toka alipo chukua mzigo mara ya mwisho bila ya kutoa pesa kwanza kama kawaida yake, basi tangia siku hiyo hakurudisha tena pesa ya watu na wala hakupatikana tena kwenye simu, ndipo hapo hasara ilipoonekana na Tito alipo ambiwa amfuatilie.
Mrutu alichukua mzigo kama kawaida yake bila ya kutoa pesa kwanza akiahidi kuwa ataleta baada ya kufikisha mzigo katikati ila baada ya kuuchukua mzigo ule yakamkuta makubwa baada ya kumkabidhi kijana wake anaemuamini kuusambaza, akapotea nao na asijue alipo elekea na kujikuta akidaiwa pesa nyingi bila kujua atazitolea wapi, akaamua kupoteza mawasiliano na Tito afikirie atazipata vipi pesa za watu ili alipe mzigo uliopotea na kijana wake.
Ndipo hapo alipo shawishika tena kwa mara ya pili baada ya kuambiwa wamuue kaka yake na familia nzima ili wachukue mali zote halafu wagawane wao, hapo ndipo alipoona anaweza kuokoka na kundi lile hatari la Mr Bakari Haneni, akapanga atakapo pata mgawo wake wa mali za kaka yake walie amua kumuua ili wazichukue, akapanga kurudisha pesa za watu halafu achane na biashara hiyo, aliwa puuza wale waliosema“Muda hamsubiri mtu” akawapuuza na wale waliosema“liwezekanalo leo lisingoje kesho”
Akawa anaingoja kesho ili aache, ikiwa uwezekana wa kuacha leo ukiwa upo, akawa ameshachelewa kwa kuigoja kesho, sasa amepigiwa simu na yule mtu aliemkimbia kwa kupoteza nae mawasiliano ili mpaka mpango wao ukitimia ndipo arudishe pesa za watu, biashara hiyo aliifanya kwa siri sana hata wakina Mata walikuwa pia hawajui kwamba anafanya biashara kama hiyo.
***************************
“Mkuu, kuna kesi nyingi sana za kupotea kwa watoto huko mitaani” Koplo Taure aliongea.
“Hili jambo lipo, na kuna mafaili mengi yenye kesi kama kama hii,(akamuangalia Koplo Taure kwa umakini) nakukabidhi hii kesi uifuatilie wewe na ninakupa wiki tatu uwe umeshanipa majibu ya hao watoto wanaopotea wanakwenda wapi, umenisikia?” Inspekta Ganjo alisema.
“Mkuu” Koplo Taure aliitikia kwa ukakamavu wa kijeshi.
“Kuanzia sasa hii kesi ipo mikononi kwako wewe, chukua mafaili yote yanayo husika na kesi kama hii, ukae nayo wewe ofisini kwako. Unaweza kwenda”
“Mkuu” Koplo Taure alipiga salut na kuondoka katika ofisi ya Inspekta Ganjo.
*******************************
“Ok, Tito nipe taarifa”
“Mkuu, kazi imefanyika kama ilivyopangwa”
“Ndio nataka unieleze sasa”
“Wale vijana walio enda kuupokea mzigo wamekuja nao bila tatizo na ule mzigo uliobakia, pia tume uuza wote, kwahiyo sasa hivi tuna huu mzigo mpya tu”
“Ok, na vipi kuhusu huyu nani huyu…….”
“Mrutu”
“Yeah, yeah, na yeye ulimfuatilia kama nilivyo kuagiza?”
“Ndio mkuu”
“Amekuelezaje kuhusu kupotea kwake na mzigo wetu mwezi mzima”
“Amenieleza mambo mengi, amesema kwamba alipatwa na msiba wa kaka yake na anavyodai kuwa ameachiwa mtoto wa kaka yake amlee yeye ndio maana ikapelekea hadi kutooneka mwezi mzima”
“Kwahiyo hiyo ndio ilimpelekea kutoweza kutoa taarifa?”
“Hapana Mkuu, amesema pia alipoteza simu ndio maana pia hakuwa na mawasiliano na sisi”
“Kwhiyo hakusema kwamba pesa yetu ataileta lini?”
“Hakusema siku maalumu ila alisema siku si nyingi atakuwa tayari ameshaleta”
“Naona tayari ameanza kupoteza uaminifu, ila mimi nampa wiki moja tu, asipoleta pesa yetu, basi mimi nitajua cha kufanya, wewe nenda kaendelee na kazi”
“Sawa Mkuu”
**********************************
Ni majira ya usiku, katika nyumba ya Mrutu, Mrutu alionekana, akiinuka katika kitanda chake, aka kaa hapo hapo kitandani, akawa kama anafikiria kitu, mara akasimama, alikuwa amevaa pensi, juu alikuwa yupo tumbo wazi, akaiyendea droo yake, akaivuta kwa mbele na kuchukua bastola yake, akaenda kwenye mlango wa kutokea katika chumba chake na kuufungua, alipotoka nje ya mlango wa chumba chake, akaenda hadi kwenye mlango wa chumba alicho lala Hemedy, bahati nzuri ikawa kwake, mlango ulikuwa upo wazi, akazama hadi ndani, akamkuta Hemedy akiwa amelala, hakutaka kupoteza muda, akamuendea hadi pale kitandani na kumuwekea bastola ya kifua upande wa moyo, bila kufikiria mara mbili akamfyatulia risasi iliyozama hadi ndani ya kifua changa cha Hemedy….
“Maaamaaaa!!!!”
Hemedy alishtuka kutoka usingizini, kutokana na ndoto alioiyota muda mfupi, alipiga kelele za kumuita mama yake alie kuwa kaburini, alikuwa akihema haraka haraka kama mtu alietoka kukimbia umbali mrefu, huku majasho yakimtoka, kelele zake zilimfikia Mrutu alie kuwa katika chumba chake na kumfanya aje mbio mbio hadi katika chumba alicho lala Hemedy. “Vipi, mbona kelele tena usiku huu, una nini?”
“Ndoto, nimeota ndoto baba”
“Ndoto gani?” Hemedy alishindwa amuelezee vipi Mrutu hiyo ndoto aliyoiyota, ikiwa muhusika mwenyewe ndio huyo huyo, alizidi kuwa na wasiwasi baada ya kumuona alivyo muota ndivyo alivyo kuja, Mrutu alikuwa ameshika bastola na amevaa pensi ile ile aliyo muota nayo na juu alikuwa yupo tumbo wazi, hakujua amuelezeea au asimuelezee, akabaki kimya tu huku akiwa kamkodolea macho baba yake huyo mdogo.
“Wewe si nakuuliza, hiyo ndoto iliyo kufanya hadi ukapiga kelele ni ndoto gani?”
“Nimeiota ile siku wazazi wangu walipo uliwa na wale watu waliotuvamia” Hemedy aliamua kudanganya, ghafla machozi yalianza kumtoka, alianza kulia chini chini, ikabidi Mrutu alimsogelee na kuanza kum’bembeleza.
“Nyamaza mwanangu usilie, kumbuka kuwa kila mtu atakufa katika huu ulimwengu, wazazi wako wametangulia, inabidi uwaombee mungu awalaze mahali pema huko walipo, inabidi usahau ili mambo mengine yaendelee”
“(huku akimkumbatia Mrutu” inaniuma kila nikiwakumbuka wazazi wangu”
“Najua kwamba inauma, ila inabidi ujikaze, kwasababu wewe sio wa kwanza kufiwa na wazazi wote wawili, kuna wenzako wazazi wote wawili wamekufa na sasa hivi wapo mitaani tu huko hawajui pakwenda, ila shukuru mungu kwasababu umepata mtu wa kukulea, kwahiyo usilie sana hadi uka kufuru mungu” Mrutu alimuonea huruma Hemedy, ila hakuwa na jinsi ya kufanya, kwasababu waliyo yataka tayari yameshatokea, alibaki tu akim’bembeleza, alifanya hivyo kama dakika mbili, Hemedy akanyamaza.
“Haya lala mwanangu”
“Sawa baba”
“Halafu kuanzia kesho inabidi nikupeleke shule, ukaendelee kusoma, kwasababu huo muda uliokaa nyumbani ni mwingi sana”
“Sawa” Hemedy alisema huku akijifunika shuka. Baada ya kuhakikisha Hemedy tayari ameanza kupitiwa na usingizi, Mrutu alinyanyuka na kuichukua bastola yake, aliiyangalia na kumuangalia Hemedy.
Ni kweli alipanga siku hiyo amuue Hemedy, ila kuna kitu kama huruma hivi kilimuingia kwenye moyo wake, hapo ndipo alipo amini kuwa damu nzito kuliko maji, lakini kwa upande mwengine hakuwa na jinsi, ilibidi Hemedy afe ili ushahidi upotee kabisa, kwakuwa yeye alishindwa kumuua Hemedy, akapanga kazi hiyo ata waachia wakina Moto ili waitekeleze. Akaondoka chumbani kwa Hemedy, akaenda chumbani kwake ili kuitafuta kesho yake. Akaenda kulala. ************************ Siku iliyofuata Mrutu alimpeleka Hemedy shuleni kwao, akamueleza mwalimu wake yote yaliyo mkuta Hemedy, mwalimu alisikitika sana, alimsikitikia Hemedy ambae kwa wakati huo alikuwa ni yatima, ila na yeye alikuwa kama wengine tu waliosikitishwa na vifo hivyo, sikitiko lake halikuwa na uwezo wa kuwarudisha wazazi wa Hemedy duniani, akamruhusu Hemedy kwenda darasani.
Baada ya kukamilisha kila kitu Mrutu akaondoka shuleni hapo na kwenda dukani kwake, akapanga hatokaa sana dukani ili awapigie simu wakina Moto, wapange ni jinsi gani ya kumuua Hemedy. ****
Koplo Taure siku hii alipanga kuanza upelelezi wa kesi alizopewa na Inspekta Ganjo za kupotea kwa watoto mitaani, baada ya kupewa ruksa ya kutoka kituoni muda huu wa mchana, aliwasha gari yake na kwenda hadi katika nyumba ya mmoja wapo aliye leta kesi ya kupotelewa kwa mtoto wake, alipofika aliteremka kwenye gari na kwenda hadi mlangoni, akapiga hodi, baada ya sekunde kadhaa akasikia michakacho ya hatua za mtu kutokea ndani, akajua mwenyeji ndio anakuja, akasubiri.
“Za saa hizi?” Koplo Taure, alianzisha maongezi baada ya mlango kufunguliwa, alitokea msichana, Koplo Taure alivyo muangalia tu alijua kuwa huyo atakuwa ni mfanyakazi wa humo ndani.
“Nzuli tu” Msichana huyo alijibu kwa lafudhi ya kabila la kisambaa, Koplo Taure alitabasamu na kuendelea.
“Baba au Mama sijui nimewakuta?”
“Yupo Mama tu Baba hayupo”
“Sawa, pia sio mbaya, naomba uniitie”
“Haya subili nikamuite” Yule msichana aliingia ndani na kumuacha Koplo Taure hapo hapo nje, baada ya dakika mbili alirudi tena.
“Anakuambia upite ndani” Koplo Taure aliingia ndani ya nyumba hiyo, akalakiwa na sebule safi iliyopendezeshwa na vitu vya thamani vilivyowekwa kwenye sebule hiyo, akachagua sofa moja kati ya mengi yaliyo kuwepo katika sebule hiyo, akakaa juu yake, alianza kupitisha macho kwenye sebule hiyo huku na huko, ilimradi tu iwe kama wengi wafanyavyo wanapokuwa ugenini kwa mara ya kwanza, baada ya muda alitokea mwanamke mtu mzima kidogo.
“Karibu” Alisema mwanamke huyo huku akikaa katika sofa jengine tofauti na lile alilo kaa Koplo Taure.
“Asante” Koplo Taure alijibu.
“Wewe ni nani na nikusaidie nini?”
“Bilashaka wewe ndio mzazi wa Hassani Dupe?”
“Ndio ni mimi”
“Mimi ni polisi kutoka katika kituo cha polisi Mabawa(Huku akimuonyesha kitambulisho) Nimekuja hapa nataka nikuulize maswali mawili matatu kuhusiana na kupotea kwa mtoto wako na ninaomba unipe ushirikiano wa kutosha ili nipate mwanga wa kujua ni wapi pakuanzia kumtafuta mtoto wako na sio wako tu, hii kesi ya kupotea kwa watoto zipo nyingi sana kituoni kwetu na vituo vyengine vya polisi, kwahiyo naomba unijibu kila nitakalo kuuliza”
“Ndio niko tayari, uliza tu” Koplo Taure alitoa kijidaftari na kalamu ili aanze kuandika maelezo atakayo yatoa mwanamke huyo.
“Mwanao ana umri gani?”
“Ana miaka kumi na saba”
“Tangu mwanao apotee ana muda gani hadi sasa?”
“Ni wiki tu”
“Unaweza ukanieleza alipotea potea vipi?”
“Iyo siku wakati ndio mara ya mwisho kumuona, aliniaga anakwenda uwanjani kwenda kuangalia mpira, basi tokea siku hiyo ndio sikumuona tena mwanangu mimi(akianza kulia) mwanangu sijui wamempeleka wapi jamani, kwani amewakosea nini hadi wakamfanyia hivyo, mwanangu mwenyewe ndio huyo huyo mmoja tu sina mwengine mimi, eeee mungu mlinde mwanangu uko ali….” Hakuweza kuendelea tena kutokana na kilio cha uchungu wa mwana, ikabidi Koplo Taure afanye kazi nyengine ya kum’bembeleza.
“Dada nyamaza basi tuendelee”
“Mwanangu mimiiii, Hassani wewe upo wapi mwananguuuuu”
“Wanawake bwana!!!” Koplo Taure alijisemea kimoyo moyo“aaah!! ila uchungu wa mwana aujuae mzazi muache alie kwanza” ikabidi amsubirie hadi atakapo nyamaza ndipo waendelee na maongezi yao. Baada ya Dakika tano mwanamke yule alinyamaza mwenyewe, akajifuta machozi kwa kutumia kanga yake, na kumuangalia Koplo Taure.
“Wakati unanieleza maelezo yako, kuna sehemu ulisema kwamba hujui aliwakosea nini hadi wakamfanyia hivyo mwanao, ni wakina nani hao?”
“Mimi si wajui”
“Kwani huko uwanjani ana kawaida ya kwenda kila siku kwenda kuangalia mpira?”
“Hapana, wameanza kwenda hivi juzi juzi tu, walikuwa wanasema kwamba wanaenda kuangalia sijui ligi sijui mambo ya mpira mimi, ila walikuwa wanaenda kuiyangalia timu yao ikicheza”
“Kwani alikuwa akienda na wenzake?”
“Ndio wapo wanne, wanaoenda huko uwanjani kwenda kuangalia mpira”
“Kwahiyo amepotea na hoa wenzake?”
“Hapana, mmoja wao aliwakimbia hao watekaji”
“Huyo mmoja wao alie kimbia ninaweza nikampata ili anieleze tukio zima lilivyokuwa?”
“Hapana, wazazi wake wamemuamisha mji na yeye ndio aliekuja kutoa taarifa hizo za kutekwa kwa wenzake”
“Alisemaje, unaweza ukanielezea?”
“Yeye alisema kwamba wakati wanarudi huko mpirani, njiani walikutana na gari iliyopaki pembeni, kwenye hiyo gari kuna mwanaume mmoja aliwaita wote, walipofika pale kwenye ile gari, ghafla milango ikafunguliwa wakatokea wanaume wengine wanne na kuwashikilia kila mmoja wake, ila huyo mmoja ambae kapona kwenye huo utekaji, yeye alifanikiwa kuwatoroka na kukimbia na yeye ndie aliekuja kutupa hizo taarifa”
“Sawa, hiyo gari hajamiambia kuwa niya rangi gani au labda kama namba zake za gari amezishika?”
“Alivyosema yeye, hiyo gari ilikuwa ni ya rangi nyeusi ila namba za gari ndio hakuzishika”
“Unaweza ukanielekeza huo uwanja wa mpira mahali ulipo?”
“Mbona sio mbali sana na hapa nyumbani, ni hapo mbele tu, kuna mtaa mmoja upo hapo mbele kuna nyumba ina fremu za maduka, kwa mbele kidogo tu ndipo utauona huo uwanja”
“Hakukuja watu au labda mtu mwengine kuja kukuhoji kama hivi?”
“Hapana wewe ndio wa kwanza kuja hapa”
“Sawa, asante Dada, acha mimi nikaendelee na kazi, nikiwa na shida na wewe nitakutafuta”
“Haya kaka, lakini naomba unitafutie mwanangu, maana mtoto mwenyewe ndio huyo huyo mmoja tu”
“Usijali Dada, kwavile jeshi la polisi limeamua kufuatilia basi lazima watapatikana tu”
“Haya kaka karibu tena”
Baada ya kutoka katika nyumba ya mhanga mmoja wapo aliepotelewa na mtoto, Koplo Taure alienda hadi hapo uwanjani tukio lilipotokea, alipofika alipaki gari pembeni na kuangalia angalia hapo kama dakika tano, alipoona hakuna cha maana aliwasha gari na kuondoka.
Akiwa yupo kwenye gari yake akitembea tembea mitaani, akapita katika shule anayo soma Hemedy, bahati nzuri ndio akawakuta wanafunzi mida hiyo ndio wanatoka shuleni hapo, kwambali alimuona Hemedy akitoka ndani ya shule hiyo, akapaki gari pembeni na kumuita, Hemedy alipoona kuwa alie muita ni Koplo Taure, akenda hadi kwenye hiyo gari, Koplo Taure akampa ishara apande na yeye bila kubisha, akazunguuka upande wa pili na kupanda kwenye gari. Wakasalimiana na Koplo Taure akaomba kumpeleka Hemedy hadi nyumbani kwao(nyumbani kwa Mrutu) hapakuwa na pingamizi lolote safari ikaanza huku wakiwa wanapiga stori.
*****************************
“Hapana bwana leo zamu yenu kuja kwangu”
“Thawa kama ndio unavyotaka, thatha umemtaarifu na Moto?”
“Moto nimeshampigia simu tayari akasema tukutane huko huko kwangu, yani hapa ilikuwa ndio nakutaarifu wewe tu”
“Bathi thawa, acha mimi nijiandae nije” Baada ya kuongea na Mata, Mrutu alimuachia duka mfanya kazi wake, akafunga safari hadi nyumbani kwake, alipokuwa njiani, gari yake ilipata pancha, hakuwa na jinsi ikabidi aiyache kwa fundi na yeye akanza safari ya kwenda kwa miguu nyumbani kwake, bahati ilikuwa kwake kwasababu hapakuwa mbali sana na nyumbani kwake, baada ya robo saa akawa tayari ameshafika kwake akawakuta Moto Na Mata wanamsubiria.
“Mbona upo kwa miguu, gari yako ipo wapi?” Mata aliuliza.
“Imenipatia pancha nikaona niiyache kwa fundi, na wewe mbona sioni gari yako, ipo wapi?” Mrutu alijibu na yeye akauliza.
“Mimi gari yangu ameondoka nayo mdogo wangu baada ya kunileta hapa kwako”
“Poa basi tuingieni ndani” Wote watatu wakaingia hadi ndani, Moto na Mata wakakaa sebuleni wakimsubiria Mrutu aliengia chumbani kwake mara moja.
Wakati huo huo Koplo Taure na Hemedy walikuwa tayari wamefika nyumbani kwa Mrutu.
“Sasa si unaenda kubadilisha nguo halafu tunaenda nyumbani kwangu au sio?”
“Itabidi iwe hivyo kwasababu sina chakufanya hapa, ngoja nikabadilishe nguo halafu tunaondoka wote”
“Sasa Baba yako akirudi halafu akikuta wewe haupo, utamuambiaje utakapo rudi?”
“Nita muambia nilikuwa na wewe”
“Haya poa basi fanya haraka mimi nakusubiri. au twende wote huko huko ndani”
Koplo Taure akashuka kwenye gari yeye na Hemedy, wakaongoza kuingia ndani ya nyumba ya Mrutu, kwakuwa Mrutu alimuachia Hemedy funguo yake ili atapo wahi kurudi shule asipate tabu ya kumsubiri hadi yeye atakapo rudi, hivyo Hemedy alikuwa na funguo yake, akafungua geti na kuingia hadi ndani ya uzio wa nyumba hiyo, wakawa wanauelekea mlango wa kuingia ndani ya nyumba hiyo, Hemedy akatayarisha funguo ili afungue mlango huo.
“Au twende tu hivi hivi Anko Taure” Hemedy aliacha kufungua mlango na kumgeukia Koplo Taure.
“Kwanini?”
“Nahofia kama akirudi halafu akakuta sipo anaweza akazingua, lakini kama nikirudi na nguo za shule hatoweza kuzingua”
“Akikuuliza mbona umechelewa wewe utamjibu nini?”
“Nitamuambia kuwa leo tumecheleweshwa kutolewa, halafu pia si hatuto kaa sana, kwahiyo wewe usijali”
“Au kama vipi acha mimi nikuache tu, siku nyengine ukipata muda mzuri nitakupeleka nyumbani kwangu”
“Hapana twende wote leo”
“Kwanini unang’ang’ania twende leo, au unadhani sito kupeleka nyumbani kwangu?”
“Hapana sio hivyo, ila sasa mimi nitabaki na nani hapa, nyumba yote hii nikae pekeangu, sitoweza kumsubiria Baba mdogo hadi atakapo rudi” Alisema hivyo kwa kuwa hakuliona gari la Mrutu hapo kwenye maegesho, kwahiyo akadhani labda huenda ikawa bado hajarudi.
“Haya poa twenzetu”
Wakaanza safari ya kuondoka hapo, wakaenda kwenye gari na kuelekea nyumbani kwa Koplo Taure, walipo fika wakaingia ndani kwavile Hemedy bado hajala, ikabidi Koplo Taure atoke nje ya nyumba yake na kwenda katika banda la chipsi lililokuwa karibu na nyumba yake, akanunua chipsi vipimo viwili, baada ya kupatiwa chipsi zake na kulipa, akarudi nyumbani kwake, akampatia Hemedy mfuko mmoja wa chipsi na yeye akabaki na mmoja, wakawa wana kula, baada ya kumaliza kula wakaendelea na stori nyengine.
Raskazoni, Katika nyumba ya Mr Bakari Haneni. 10:20 Jioni. Ilionekana gari aina ya Verosa ikikunja kona ya upande wa kulia kuashiria kuwa inataka kuingia katika jumba hilo linalo milikiwa na Mr Bakari Haneni muuzaji wa madawa ya kulevya, gari hiyo ilipofika karibu na geti la kuingilia humo ndani, geti lilijifungua lenyewe na kufanya gari hiyo kuingia humo ndani, likaenda hadi katika maegesho ya magari kwenye jumba hilo, wakashuka Tito na Tobi kwenye hiyo gari wakiwa mikononi mwao kila mmoja amebeba briefcas nyeusi.
Ghafla wakasikia sauti ya kupigwa kwa mluzi walipo tafuta sauti hiyo inatoka wapi ndipo macho yao yalipotua juu ya nyumba hiyo ya gorofa na kumuona Bosi wao Mr Bakari Haneni akiwa amekaa kwenye kiti cha thamani kilicho tengenezwa kwa mbao huku pembeni kukiwa na wanawake wawili wanao mpepea, akawaonyesha ishara ya kuwaita na wao bila pingamizi walianza kwenda mdogo mdogo, wakatumia ngazi kufika huko juu alipo bosi wao.
“Naona Mkuu upo huku juu unaangalia mandhari ya bahari ya hindi na kupata upepo wake mwanana tu” Tito alianzisha mazungumzo baada ya kufika mbele ya bosi wao.
“Nina wasiwasi gani wakati kila ninacho kitaka nakipata bwana” akanyamaza kidogo na kuwa angalia wale wanawake“tupisheni kidogo ila mmoja kati yenu alete vinywaji hapa”baada ya kuondoka kwa wale wanawake, akawageukia wakina Tito na kuwaambia wakae kwenye viti vyengine vilivyokuwepo hapo hapo, baada ya dakika kadhaa vinywaji vikaletwa ikawa sasa kila mmoja ana kinywaji chake.
“Enhee nipeni habari vijana wangu”
“Kazi imekamilika, walikuwa wanataka kutuchezea mchezo ambao sisi tumeuanza kabla yao, wameushindwa na kukimbia”
“Imekuaje?” Mr Bakari Haneni aliuliza.
“Tumekubaliana tufanye biashara ya kiamani, ila baada ya makabidhiano wao wakajifanya wajuaji, wakataka kutudhulumu, yani wachukue mzigo wetu na pesa zao, ila wakawa wameingia choo cha kike, hawakujua kwamba wanafanya biashara na watu ambao biashara hizi tumezianza kabla hatuja toka kwenye matumbo ya mama zetu, kibao kika wageukia wao, wakakimbia wameacha pesa zao na mzigo wetu na vyote viwili tukaondoka navyo sisi”
“Safi sana, kwahiyo mmeondoka na mzigo wetu na hela zao?” Mr Bakari Haneni akauliza tena kama hajasikia kile alicho ambiwa.
“Ndio, tumeondoka navyo vyote”
“Safi, embu nionyesheni”
Wakafungua briefcas walizo kuja nazo na kumuonyesha bosi wao, alitabasamu na kuwapa ishara ya kuzifunga na wao wakazifunga.
“Safi sana vijana wangu, mnajua kwamba ninawaamini kuliko kijana yoyote nilie wahi kuwa nae, kwasababu kazi zangu mnazifanya kwa umakini mkubwa sana”
“Ila sasa Mkuu, mimi naona kama vile hawatokubali kushindwa, lazima tu walipize” Tobi alisema
“Hahaha mimi najiamini sana, kwanza hawana taarifa zozote kuhusiana na sisi, halafu wao wana mtandao mdogo sana kwahiyo hawawezi kushindana na mimi hata kidogo” Mr Bakari Haneni alijigamba.
“Tuachaneni na hayo, vipi kuhusu pesa zetu kwa Mrutu?” Aliuliza tena.
“Dah!! Mkuu yule mtu bado mimi sija muelewa kabisa yani” Tito alijibu.
“Kwanini?”
“Yani kila nikimpigia simu ananiambia nimvumilie tu, kila siku hilo ndio jibu lake, sasa mimi nashindwa kumuelewa”
“Naona sasa ameamua kuvunja uaminifu kabisa”
“Hapo ndio nashindwa kuelewa Mkuu”
“Halafu si umesema kwamba ana mtoto ambae anamlea?”
“Ndio Mkuu?”
“Basi itabidi huyo mtoto atekwe mara moja halafu tuone sasa kama hatoleta pesa zetu” Mr Bakari Haneni alisema.
“Ila Mkuu je kama asipo mfuatila huyo mtoto, si itakuwa tumefanya kazi ya bure tu, kwanza mtoto mwenyewe sio wake ni wa kaka yake ambae sasa ni marehemu”
“Hilo nyie lisimipe wasiwasi, tukimteka huyo mtoto halafu asipo mfuatilia sisi tunamuua tu huyo mtoto halafu tutajua jinsi gani ya kurudisha pesa yetu, yule ni mtoto mdogo sana kwangu kwanza kazi yenyewe tumefundisha sisi”
“Kama ni hivyo hakuna tabu, sisi tupe amri tu ni lini tuka mchukue, kazi rahisi sana hiyo” Moyo alisema.
“Msijali tumuangalie kwa hizi siku mbili, asipo leta pesa zetu, basi haina budi hiyo kazi kufanyika”
“Sawa Mkuu”
“Kwanza mmenifurahisha baada ya kurudi na mzigo wetu na hizo pesa za wale wapumbavu, sasa chakufanya sasa hivi, chukueni milioni Tano mkagawane, nataka vijana wangu mufurahi na nyie”
Baada ya kuongea hivyo Tito alifungua briefcas moja iliyo kuwa na vibunda vya noti za elfu kumi kumi, akachukua kibunda kimoja, na kuifunga briefcas, wakaaga na kuanza safari ya kwenda kufurahi kama walivyo ambiwa, wakashuka ngazi hadi chini na kuiyendea gari yao waliyokuja nayo na kutoka hadi ya nyumba hiyo, wakashika uwelekeo wa Hospitali ya Bombo, baada ya kuivuka hospitali ya Bombo, mbele kidogo wakakunja kulia kuingia Hobours club, wakaenda kuimalizia siku yao hapo.
Nyuma kidogo, muda ambao Koplo Taure na Hemedy walivyo ghairisha kuingia ndani ya nyumba ya Mrutu..
Mrutu aliengia ndani ya chumba chake, baada ya muda kidogo akatoka hadi sebuleni alipo waacha Moto na Mata.
“Vipi, mbona kama vile mnashangaa shangaa kuna nini?” Mrutu aliwauliza swali hilo baada ya kuwaangalia wakina Mata usoni na kuona wakiwa kama kuna kitu wanakitafakari vichwani mwao.
“Thio hivyo, ila kuna thauti dha watu tume dhithikia wakiongea ongea thatha ndio tuna jiulidha nidha kina nani”
“Hizo sauti mumezisikia wapi?”
“Huko nje”
“(akauwendea mlango wa kutokea nje, akaufungua na kuangaza angaza, akarudi tena ndani) Nyie mna matatizo mbona huku nje hakuna watu?”
“Bathi labda itakuwa tumethikia vibaya, lakini tume dhithikia kabitha yani”
“Eti Moto ni kweli hata wewe umeziskia hizo sauti za watu?”
“Ndio, hata mimi pia nimezskia”
“Walikuwa wanaongea nini?”
“Hatuja sikia vizuri walichozungumza zaidi ya minong’ono tu”
“Basi tuachaneni na hayo, tuendelee na yaliyo nifanya nimiite hapa, ni hivi Hemedy ninae hapa nyumbani” Mrutu alidhani labda akiwaambia taarifa hiyo wenzake watafurahia lakini ndio kwanza kila mmoja akawa yupo katika hali yake ile ile ya kawaida.
“Huyo Hemdy ndio nani?” Mata aliuliza.
“Aaaaaah!!!!!! Kwahiyo mnataka kuniambia hamumjui Hemedy leo hii??
“Tungemjua tunge kuuliza? Embu acha uswahili basi tuambie ni nani? Moto aliongea.
“Sawa, Hemedy si huyu mtoto wa marehemu mzee Mheshimiwa”
“Kwahiyo unaponae hapa nyumbani kwako?” Mata aliuliza kwa mshangao ulio changanyikana na furaha.
“Ndio, nipo nae hapa nyumbani”
“Usha muua…..aaah ushamuuliza kuhusu hiyo flash kama anayo yeye?” Moto aliuliza kwa wahka.
“Hapana bado sijamuuliza”
“Halafu si umesema yupo hapa kwako? Isije ikawa anatusikia tunacho zungumza” Moto alionyesha wasiwasi wake.
“Hapana, ameenda shule bado hajarudi”
“Ila sio yeye kweli aliekuwa anaongea hapoa nje?” Moto alipo sema hivyo Mrutu na Mata wakashtuka, Mrutu akainuka haraka akaenda nje kwenda kuangalia vizuri, akaizunguka nyumba nzima ila hakuona mtu, akatoka hadi nje kabisa ya uzio huko napo pia hakuona mtu, ikabidi arudi tu hadi sebuleni walipo wenzake.
“Tusijitie presha bure kwanza hajarudi shule bado na kama ingekuwa ni yeye aliekuwa akiongea hapo nje sasa itakuwa alikuwa akiongea na nani? na kwanini asiingie ndani?”
“Thatha kama akirudi shule halafu akitukuta je itakuaje?” Mata aliuliza.
“We nawe una muhofia mtoto mdogo yule, si ndio hapo tutakapo muulia hapa hapa” Moto alisema.
“Sasa wewe ulikuwa unataka afie wapi?” Moto aliuliza.
“Afe popote lakini sio hapa kwangu, sitaki kesi mimi”
“Sawa, halafu kwanini huja muuliza kama ile flash yenye video la tukio zima kama anayo yeye?”
“Nitamuuliza vipi, wakati mtoto mwenyewe nimekabidhiwa jana tu”
“Basi tumsubirini hapa hapa akirudi tutamuhoji kama anayo yeye, au nyie mnasemaje?”
“Je kama hiyo flash yeye hana?” Mata aliuliza.
“Hamna jinsi zaidi ya kumuua tu na…”
“Lakini sio hapa kwangu” Mrutu alimkatisha Moto.
“Hafi hapa kwako bwana”
“Haya tumsubirini nahisi muda si mrefu atarudi kutoka shule” Wakakubaliana wamsubirie Hemedy hapo hapo kwa Mrutu. Wakamsubiri.
Muda ambao wana msubiri Hemedy arudi shule ili wamuhoji maswali yao, ndio muda ambao Koplo Taure na Hemedy ndio wapo kwenye gari wanakuja nyumbani kwa Mrutu, baada ya mwendo wa dakika kadhaa, walifika nyumbani kwa Mrutu, wakateremka wote kwenye gari na kuliendea geti, wakazama hadi ndani.
“Mimi nilikuambia atakuwa bado hajarudi, si unaona hata gari yake haipo” Hemedy alimuambia Koplo Taure huku wakiuwelekea mlango wa kuingilia ndani ya nyumba hiyo.
“Kwahiyo ndio unanisuta?” Koplo Taure alimwambia Hemedy huku akicheka.
“Hapana sikusuti ila wewe ulikuwa m’bishi, hukutaka tu nikae nyumbani kwako ndio maana ukani harakisha hivi”
“Hahahahah wewe dogo mpumbavu sana, sasa mimi nikuharakishe kwa kipi hasa, wewe si ulisema tusichelewe kurudi kwa kumuhofia baba yako” Hemedy hakusema kitu, muda huo alikuwa anatia ufunguo kwenye kitasa, mlango ukakubali akaufungua, ulipofunguka, akapigwa na butwaa baada ya kutupa macho yake kwenye masofa yaliyokuwepo hapo sebuleni, akabaki ameganda tu mlangoni, Koplo Taure baada ya kuona Hemedy ameganda mlangoni haingii ndani, akataka kujua ni kipi alichokiona Hemedy humo ndani na yeye akapenyeza kichwa kuchungulia hapo sebuleni……
“Umefika saa ngapi hapa nyumbani?” Hemedy aliuliza.
“Mimi mbona nimefika muda tu, nimekusubiri kweli naona hutokei, kwani shule ndio mnatoka(akaangalia saa iliyokuwepo hapo ukatani) saa kumi na mbili?” Mrutu akajibu na yeye akauliza.
“Hapana nilikuwa kwa anko Taure, ila shule tumetoka tangia saa tisa na nusu” Alijibu na kuondoka hapo mlangoni ambapo alikuwa ameganda akimshangaa Mrutu, aliingia ndani na kumfanya Koplo Taure na yeye kuingia ndani, akaenda kukaa katika sofa moja wapo.
“Mbona gari sijaiona hapo nje?” Hemedy aliuliza huku akielekea mlango wa chumbani kwake.
“Gari nimeiacha kwa fundi, imepata pancha wakati naja hapa nyumbani” Hemedy baada ya kusikia hivyo akafungua mlango wa chumba chake na kuingia humo ndani.
“Niambie Mrutu”
“Shwari, vipi kaka”
“Safi tu, kumbe ulikuwa upo nae huyu tangia muda wote?”
“Ndio, nilikuwa nipo nae tangu anatoka shule”
“Ulienda nae wapi?”
“Nimeenda nae nyumbani kwangu tu, kuna muda tulikuja hapa tukakuta nyumba tupu haina mtu, ndipo hapo aliponiambia tuondoke wote”
“Mliingia hadi humu ndani?”
“Ndio tulifika hadi hapo nje ila hatukuingia ndani, ndipo alipo niambia tuondoke tu, aisee ila huyu dogo ni mjanja sana, unajua alikataa kabisa kubadilisha nguo za shule kwa kuhofia eti akirudi unaweza ukamuuliza alikuwa wapi”
“Hahahah huo sio ujanja ni upumbavu, sasa alicho hofia ni nini, wakati mimi nimempa uhuru wa kufanya chochote ila tu asivuke mipaka” Hemedy alifika hapo sebuleni na kujumuika nao, wakaendelea na maongezi yao hadi pale Koplo Taure alipoaga na kuondoka zake, Hemedy na yeye akaingia chumbani kwake kwenda kujisomea.
Turudi nyuma kidogo muda ambao Hemedy na Koplo Taure ndio wanaingia kwenye nyumba ya Mrutu.
“Nahisi itakuwa ndio huyo hapo ana rudi, maana nasikia sauti ya geti kufunguliwa” Aliongea Mrutu.
“Mbona nasikia kama kuna mtu anaongea nae” Moto alipoongea hivyo, Mrutu akainuka na kwenda hadi dirishani na kumuona Hemedy ameongozana na Koplo Taure, alichanganyikiwa hakujua afanye nini kwa wakati huo, aliwaona wakizidi kuukaribia mlango wa kuingia hapo ndani, akatoka fasta dirishani hapo na kuwaendea wakina Moto ambao walikuwa katika sintofahamu, hawakujua ni kwanini mwezao amechanganyikiwa kiasi hicho, ikawalazimu wasubiri awaambie ni kipi kilicho mchanganya hivyo.
“Askari, polisi” Nyoyo za kina Mata zilipa “Paaaa!!!!!” baada ya kusikia neno Askari, na wao wakachanganyikiwa hawakujua wafanye nini, Mata alichukua mto wa sofa akajifunika nao usoni na kupelekea wenzake wamcheke kimya kimya.
Mrutu akaona akiendelea kupoteza muda hapo watakutwa na itakuwa mambo mengine, wao hawakumuhofia Koplo Taure ila walimuhofia Hemedy anaweza akawataja kwa askari huyo na kusababisha mengine, Mrutu akawachukuwa na kuwapeleka hadi chumbani kwake, akawafungia humo na yeye akawahi kurudi sebuleni na kutulia kwenye sofa, baada ya sekunde kadha ndipo mlango ulipofunguliwa na Hemedy kupigwa na butwaa baada ya kumuona Mrutu yupo ndani ikiwa yeye alidhani labda itakuwa bado hajafika.
Turudi sasa muda huu.
Baada ya Koplo Taure kuondoka na Hemedy kuingia chumbani kwake, Mrutu aliwafuata wakina Moto na kuwatoka nje ya nyumba hiyo.
“Thatha thi tuende tukamuhoji yule dogo kule ndani?” Mata aliuliza.
“Hapana nyie nendeni mimi nitawatafuta tupange jinsi gani ya kukamilisha huu mpango”
“Kwanini tuthiimalidhe hii kadhi thatha hivi?” Mata aliuliza.
“Mbona Mata wewe ni mbishi? Kwani mimi sinimewaambia nyie nendeni halafu tutapanga jinsi gani ya kukamilisha hii ishu”
“Haya kama ndio unavyotaka acha thithi tuende ila uthithahau kumuuliza kama hiyo flash anayo”
“Msijali nitafanya hivyo” Baada ya kuagana na wakina Mata, alirudi ndani na kupitiliza hadi chumbani kwake, akafikiria atumie mbinu gani kumuhoji Hemedy ili ajue kinacho wasumbua“Lakini yule ni mtoto mdogo hawezi kunishinda maarifa, ngoja nikamuite” baada ya kuwaza hivyo aliinuka akenda chumbani kwa Hemedy, akamkuta bado anajisomea“Embu njoo sebuleni mara moja” alivyomuambia hivyo akatoka hadi sebuleni na kumsubiri Hemedy baada ya dakika mbili Hemedy nae akaja pale sebueleni, akaka kwenye sofa jengine tofauti na lile alilo kaa Mrutu.
“Embu naomba unielezee tukio zima lilivyotokea hadi kupelekea vifo vya wazazi wako” Mrutu akanzisha mazungumzo. Hemedy akatulia kama kama sekunde thelathini, akanza kumuelezea.
“Tulikuwa tumekaa sebuleni, mara ghafl……..” akamuelezea tukio zima lilivyokuwa, alipo maliza kumuelezea akanza kulia, ikabidi Mrutu ambembeleze, baada ya muda akatulia.
“Ila si unajua kama ile nyumba ina kamera za ulinzi?” Mrutu akamuuliza swali la kimtego.
“Ndio najua”
“Mbona kunasiku nilienda kwenye kile chumba cha kuongozea kamera ili nichukue ushahidi wa video ya tukio lakini nikakuta ile video haipo?” Mrutu alimuuliza swali jengine la kimtego baada ya lile la kwanza kufanikiwa. Hemedy hakujua amuambie ukweli au amfiche kama alivyoambiwa na Goda, akabaki njia panda asijue amjibu kitu gani.
“Mimi sijui” akajibu kiufupi.
“Sasa nani ambae kaichukua ile video wakati kile chumba ni cha siri, ingekuwa Goda ni mzima ningesema labda ni yeye ndie kaichuku au kuna mtu mwengine ambae Baba yako alimuonuesha kile chumba?”
“Sijui”
“Mbona kila kitu hujui, we mtoto ni mpumbavu nini? Au wewe ndio umeichukua ile video halafu unanificha?” Mrutu aliongea kwa hasira na kumfanya Hemedy aanze kuogopa, baada ya kuona anakaripiwa sana akaanza kulia huku akisema neno moja tu kwamba hajui. Ikabidi Mrutu ashushe sauti yake na kumbembeleza tena Hemedy.
“Usione hivi mwanangu ni hasira tu zile kwahiyo nyamaza tutawapata tu wauwaji wa wazazi wako, ok nenda kaendelee na kusoma acha mimi niandae chakula cha usiku” Hemedy alinyanyuka na kwenda chumbani kwake, akakaa juu ya kitanda na kuanza kufikiria yaliyotokea muda mfupi ulio pita. “Mbona kila kitu hujui, we mototo ni mpumbavu nini? Au wewe ndio umeichukua ile video halafu unanificha?”
Maneno hayo yalijirudia kichwani mwake na kuyafikiria mara mbili mbili“Kwanini anigombeshe namna hii ikiwa tayari nimemuambia kuwa video sinayo mimi? Aaaa! lakini huwenda ikawa anataka kunisaidia kweli kuwatafuta wauwaji wa wazazi wangu, sasa sijui nimpee au nikae nayo tu” akainuka na kwenda kwenye kabati la nguo zake, akafungua kabati na kuitoa flash na kwenda nayo kwenye kitanda, akakaaa“ Sasa mimi hii flash nitaitumia vipi kuwapata wauwaji wa wazazi wangu, acha tu nimpe, siku akiniuliza tena nitampa” baada ya kuwaza hayo, akaiweka flash kwenye meza yake ya kusomea na kuendelea kusoma.
Koplo Taure baada ya kutoka nyumbani kwa Mrutu, akafikiria aende wapi kuimalizia siku hiyo, ndipo alipo pata wazo la kwenda baa ila hakujua ataenda baa gani, baada ya kuwaza kwa muda mfupi, akatoa simu yake na kuingia sehemu ya majina, akatafuta kwa sekunde kumi, alipo lipata jina alilo kuwa analitafuta, akapiga na kusubiri kwa sekunde kadhaa, akaanza kuongea, “Hellow, mimi mzima sijui wewe, ok nataka nikutane na wewe leo hii, sasa hivi ndio, hobours club?, basi poa mimi ndio naelekea hivi, ok” akakata simu baada ya kumaliza kuongea na huyo alie mpigia, akaenda nyumbani kwake, akaoga na kubadilisha nguo, alivaa tisheti nyeupe na jinzi nyeusi, chini akavaa all star nyeupe kumechisha na tishet aliyoivaa, akaenda kwenye kioo na kujiangalia, akatoa tabasamu baada kujigundua amependeza yeye mwenyewe alijisifu“Utafikiri sio Askari vile” akajisemea mwenyewe na kujipigia salut, akacheka na kutoka nje na kupanda kwenye gari yake, akaelekea sheli, akaongezea mafuta kiasi kwenye gari yake, baada ya kutiliwa mafuta akaenda alipo ahidiana na mtu alieongea nae kwenye simu muda mfupi uliopita, akafika hadi hobous club na kukuta baa hiyo imechangamka kwa kuwa na watu wengi siku hiyo, akapaki gari kwenye maegesho, akushuka na kuyaangalia mandhari hayo vizuri, akapiga hatua kuiyendea meza ambayo ilikuwa iko tupu haina watu, akavuta kiti na kutulia hapo.
Baada ya muda kidogo alioneka msichana mrembo alievalia kileo zaidi, akiingia kwenye baa hiyo, karibia wanaume wengi waliokuwemo kwenye baa hiyo walimkodolea macho mnyange huyo na yeye kama alijua vile kwamba anaangaliwa, alitembea kwa mapozi haikujulikana alikuwa anafanya kusudi au ndivyo anavyotembea, maana alitembea kama vile hataki, ila kwambali akasikia sauti ya mluzi ukipigwa, akageuka huku na huko kuangalia ni wapi ulipotokea, akaachia tabasamu baada ya kumuona aliemfuata, akapiga hatua kumuendea Koplo Taure, alipofika Koplo Taure akainuka na kuachia tabasamu huku akimpa mkono mrembo huyo ambae alifanikiwa kuwapumbaza wanaune karibia wote kwenye baa hiyo, bila ajizi aliupokea mkono wa Koplo Taure, Koplo Taure nae bila ya kuongea lolote akauwinua mkono wa mrembo huyo na kuupeleka hadi mdomoni kwake na kuubusu, mrembo huyo aliishia kutabasamu tu.
“Karibu” Koplo Taure baada ya kuuachia mkono wa mwanamke huyo, akavuta kiti chengine na kumkaribisha mwanamke huyo.
“Asante” alijibu akiwa bado tabasamu lipo usoni mwake, kisha akaka kwenye kiti alichokaribishwa. Muhudumu alifika katika meza yao, wote wawili wakaagiza soda aina ya fanta kusindikiza maongezi yao.
“Kwajinsi ulivyo pendeza mtu anaweza akabisha akiambiwa kuwa wewe ni askari” Koplo Taure alianzisha maongezi.
“Mbona hata kwako pia ni hivyo hivyo, nilikusahau kwa muda baada ya kukuona, leo ndio nimeamini kuwa zile gwanda za polisi wala hazikupendezi, ukizivaa zinauficha uzuri wako, wewe ni handsome sana, najivunia kuwa na wewe”
“Hata mimi najivunia kuwa na wewe Jesca, nina sababu zaidi ya milioni za kujivunia kuwa na wewe, unajua kwamba uzuri wako umewafanya wanaume wengi waliokuwepo hapa kukuangalia wewe hadi nikapata kijiwivu kidogo”. Wakaendelea na mazungumzo yao hawa maaskari wawili wanaofanya kazi kituo kimoja.
Tito na Tobi walikuwa bado wapo kwenye baa hiyo hiyo wakiendelea kunywa pombe baada ya kupewa pesa na bosi wao na kuja kuimalizia siku yao hapo, tangia saa kumi na mbili jioni, walikuwa hapo hadi muda huu wa saa tatu usiku bado wanaendelea kunywa.
“Oyaaaaa Tiiitoooo” Tobi alimuita Tito kwa sauti kubwa baada ya pombe kumkaa kichwani.
“Nambieeee Tobiii” Tito nae alijibu kwa sauti ya kilevi.
“Unamuona yule demuu”
“Yuko wapiii?”
“Yulee kulee aliekaa na yuleeee boyaaa”
“Ndio nimewaona, sii wale kule waliokaa kwenye meza ileee paleee”
“Hivyoo hivyoo tu” Tobi aliinuka kwa kupepesuka na kwenda kwenye meza waliyokaa mtu na mpenzi wake, alitaka kwenda kufanya vurugu amchukue msichana alie kaa na mtu wake.
“We boyaaa, mbona umekaaa na demu mzuriiii halafu unaonekana mchomvuu tu, mademu hawa ni wakwetu sisi, wee kapuku utampeleka wapiii mtoto mzuriiii kamaa huyuuu, embuu nipishee nimchukue mimi”
Tobi alianza kuropoka baada ya kuifikia meza ya wapenzi wale, ila katika watu wale wawili hakuna hata mmoja aliemsemesha, wote wakawa kimya wakimuangalia mlevi huyo anavyo ropoka.
“Yaanii mimi naongeaaa na wewe boyaa halafu unajifanya hunisikii, kwanza unanijua mimi ni nani? Eeeeeee si nakuuliza wewe fala, unanijuaa mimi ni nanii?”
Bado watu wale walikaa kimya tu wakimsikiliza anavyoropoka, si kwamba huyo anaeitwa boya alikuwa akimuogopa huyu mlevi, hakuwa akimuogopa bali alikuwa anasubiri afanye kitendo chochote cha kijinga ili amuonyeshe kazi.
“Naona hunijui mimi vizuri shogaa wewe, oyaaa Tito(akamgeukia Tito) mimi namfanyia huyu fala kum*****ke” alivyoongea hivyo akarusha ngumi iliyoenda usawa wa uso wa huyo jamaa, ila jamaa aliyona akaikwepa, Tobi baada ya kuona ngumi yake imekwepwa akarusha kofi lilioenda usawa wa shavu la huyo jamaa, jamaa akarudi nyuma kidogo na kuudaka mkono wa Tobi, akafanya kama vile anakamua nguo, Tobi akapiga kelele za uchungu huku akikunja sura yake, jamaa baada ya kuona ameridhika na adhabu hiyo aliyompatia, akauwachia mkono wake na kutulia pale pale kwenye kiti, akimsubiria afanye kitendo chengine cha kipumbavu amuadhibu tena. Tukio lote hilo lilikuwa likishuhudiwa na Koplo Taure na Afande Jesca, walikuwa kimya wakiuwangalia mchezo mzima.
“Yani wewe mse**** ndio umenifanyia hivi, hujui kama unachezaa na mtu hatariii”
Akachukua chupa ya bia iliyokuwepo hapo mezani na kuivunja chini, akabakiwa na kipande cha chupa, ikawa anamfuata jamaa kwa kasi ili akamchome na hicho kipande cha chupa, Jama baada ya kuona akimlegezea sana huyu mgeni asiekuwa na adabu anaweza akamdhuru kweli, akainuka kwenye kiti tayari kupambana na huyu mgeni asie na adabu, akapanga kumfundisha adabu, Tobi alikuja mbio mbio huku akipepesuka, kipande cha chupa akikielekeza mbele tayari kwa kumchoma nacho cha tumbo jamaa, Jamaa baada ya kuona Tobi anamletea kipande cha chupa usawa wa tumbo lake, akasogea pembeni kidogo na kuupiga teke mkono wa Tobi uliokuwa umeshika kipande cha chupa na kufanya kipande hicho kiruke pembeni, akampiga ngumi mbili za uso za haraka haraka, na kumfanya Tobi mikono yake yote miwili aipeleke usoni mwake, baada ya sekunde kumi na tano, akatoa mikono usoni na kumuangalia jamaa aliekuwa bado kasimama akimsubiria afanye kitendo chengine cha kipumbavu.
“Haaaa!!!! Yani umenipiga ngumi zakooo halafu bado umesimama mbele yanguuu, naona hunijui vizuri, mimi sishindwi kukuua hapa hapa na hakuna atakae nifanya chochote, nakuua halafu naendaa mwenyewe polisi, na ninakuambia nitatokaa tuu, wewee unamjua Mr Bakari Haneniii? sasa yule mimi ndio bosi wangu, nakuua halafu huko polisi najakutolewa usiku huu huu, subiri nikuonyeshe kwamba mimi sitaniii ninapoongea”
Tito muda wote akimuangalia mwenzake anavyoleta vurugu hapo, ila baada ya kumsikia Tobi anamwambie yule jamaa asubiri ili amuonyeshe akajua moja kwa moja anataka kutoa bastola, akainuka ili amuwahi kabla haja haribu, ni kweli kama alivyowaza ndivyo Tobi alivyotaka kufanya, akapeleka mkono wake ubavuni mwake akitaka kuchomoa bastola ila kabla hajaitoa Tito aliwahi kumzuia.
“Tito niachee ni muonyeshe huyu fala, nasemaaa niaacheeeee, niacheeee, hawezi kunipiga halafu mimi nikamuangalia tu”
“Tobi twenzetuuu utaharibu, sio mahala pake hapaa, embu twende achana na huyo boyaa” Tito aliongea hivyo huku akimvuta Tobi watoke nje ili waende zao.
“Nakwambiaje, nitakutafutaaa tuu kum*****ko, yani wewe ni boyaa tuu, nishakumaki sura nitakutafutaaa nakwambiaa” Tobi aliendelea kutukana huku akikokotwa na Tito hadi kwenye gari yao na kuingia humo, Tito alikamatia usukani wa gari hiyo na kuanza safari ya kuondoka hapo.
Koplo Taure na Afande jesca waliliona tukio lote hadi pale Tobi alipotaka kuchomoa bastola pia waliishudia bastola iliyokuwepo kiunoni kwa Tobi baada ya kupandisha shati alilovaa ili aichomoe, wakapanga wakiondoka na wao wa waungie tela ilikujua mwisho wao ni wapi.
“Kila sehemu ninapokuwa, basi ujue nipo kazini, acha tuwafuate” alisema Koplo Taure na kunyanyuka kwenye kiti na kuianza safari ya kuwafuata wakina Tito akifuatiwa na Afande Jesca kwa nyuma, kwa kuwa walishalipia vinywaji walivyotumia, kwahiyo hakukuwa na mtu alie wasumbua, wakaenda kwenye gari aliyokuja nao, wakaingia wote wawili na kuianza safari ya kuwafuata wakina Tito.
“Wale watu mimi nina mashaka nawo, nahisi sio watu wakawaida” Koplo Taure aliongea huku akiendesha gari mbio ili kuwawahi wakina Tito ambao walikuwa wakielekea njia ya Mkwabi Supermakert baada ya kuivuka Toyota.
“Hata mimi pia nimewaza hivyo hivyo”
“Halafu wamenitia wasiwasi baada ya kusema kwamba ni watu wa Mr Bakari Haneni”
“Sasa hapo wasiwasi wako upo wapi, kwani umefikifia nini baada ya kusema wao ni watu wa Mr Bakari Haneni, kumbuka yule ni tajira na ana watu wengi wanaomfanyia kazi yeye?”
“Kuna hali ambayo si ya kawaida nimeiyona ila usijali nitakuambia”
Waliendelea kuwafuta nyuma nyuma mpaka pale walipo lipita jengo la Club Lavida Loca na kukunja kushoto lilopo jengo la Uhamiaji(Migration) na kuelekea ilipo garden ya uhuru park, waliipita uhuru park na kuifuata Hosteli, walinyoosha moja kwa moja wakaipita round about ya mabanda ya papa wakanyoosha moja kwa moja, wakakipita kituo cha polisi mabawa na kunyoosha hadi chuo cha komesho na kukunja kulia kuelekea majengo, mbele kidogo baada ya kuvuka tuta, wakakunja kushoto kabla hawajaufikia msikiti wa majengo, wakaenda mbele kidogo na kusimama nje ya nyumba nyeupe yenye geti jekundu, Tito akashuka na kuliendea geti la nyumba hiyo na kulifungua lote, akarudi tena kwenye gari na kuliingiza ndani ya nyumba hiyo, akaliweka kwenye maegesho na kushuka, akaliendea geti na kulifunga vizuri na kurudi kwenye gari na kumkuta Tobi akiwa bado amesinzi kwa pombe alizo kunywa, akamkokota hadi ndani ya nyumba hiyo na kumpeleka katika chumba kimoja wapo, akamuingiza humo na kumlaza kitandani na yeye akatoka hadi kwenye chumba chengine na kujitupa kitandani, ili aisake kesho yake, Aka lala.
“Ntaendelea kuwafuatilia kesho” Koplo Taure aliongea hivyo huku akigeuza gari baada ya kuikariri nyumba waliyo ingia watu hao, akaendesha gari taratibu akiufuata uelekeo wa nyumbani kwake.
“Si tunaenda kulala wote leo?” Koplo Taure alimuuliza Afande Jesca.
“Ukalale na nani?”
“Si na wewe kipenzi changu”
“Na hivyo videmu vyako vya mtaani kwenu, utavilaza wapi?”
“Aaa!! Jesca unajua kabisa hakuna mwengine anaeweza kumpa furaha Sentaure zaidi yako wewe, sasa ni vipi unizushie kuwa nina wanawake wengine? Mimi nakupenda wewe tu na hilo mwenyewe unajua”
“Kwa hapo sikupingi ni kweli hatuna lolote juu ya wale tunao wapenda kama mimi ilivyo kwako wewe. sasa vipi ombi langu la kulala nawewe usiku wa leo?”
“Kwani lazima?”
“Hapana mimi sikulazimishi ila moyo wangu ndio unanilazimisha nikulazimishe, naomba usikatae, kwasabau ukikataa utanifanya usiku wa leo ni uone mkubwa”
“Na kesho kazini je?”
“Kuhusu kazini usijali, tutatega alamu ili ituamshe asubuhi, lakini kwa sasa nomba uufanyie kazi mwili wangu”
“Kwenda uko(huku akimpiga kofi lisilo uma kwenye bega lake)Eti uufanyie kazi nwili wangu, utanilipa?”
“Usijali kuhusu hilo, nitakupa mshahara mzuuri wa penzi naamini utaufurahia huo mshahara”
“(akaingiwa na aibu za kike) Maneno yako hayo”
“Maneno yangu yana nini?”
“Mmh! Basi tuache”
“Sawa, lakini si umenikubalia ombi langu?”
“Nahofia nitachelewa kazini kama nikiamkia kwako, yani nikitoka kwako niende tena kwangu nikajiandae niende kazini, si nitachelewa jamani”
“Basi usijali, hapa tunapitia kwako, unachukua nguo zako za kazi halafu tunaenda kwangu, asubuhi ukiamka tunajiandaa kisha tunaondoka wote au wewe unasemaje?”
“Mmmmh!!! Mwanaume king’ang’anizi wewe, haya twende” Koplo Taure aliendesha gari huku akitabasamu muda wote“ huna lolote, wakati wewe mwenyewe ulikuwa pia unataka, sema umeamua kuleta viunzi ambavyo nimeweza kuviruka vyote” alijisemea maneno hayo kimoyo moyo.
“Lione uko, linafurahia tu tabia mbaya” Afande Jesca alisema maeno hayo baada ya kumuona Koplo Taure akitabasamu mwenyewe, ila hakujibu kitu akaendelea nasafari hadi kwa Afande Jesca, wakashuka wote na kuingia ndani ya nyumba hiyo ya kupanga anapoishi Afande Jesca, walipofika ndani ya chumba chake, Afande jesca akachukua nguo zake za kazi na kuziweka kwenye mkoba wake, akachukua na vipodozi na kuvitia kwenye mkoba,(“wanawake bwana, huyu ata akiambia aende eneo lililotokea ujambazi, anaweza akachuku wanja akidhani ni bastola. acheni wanawake waitwe wanawake”)Koplo Taure alijisemea baada ya kumuona Afande Jesca akikusanya vipodozi vyake na kuvitia kwenye mkoba.
“Twende” Afande Jesca baada ya kumaliza kila kitu akamuambia Koplo Taure.
“Wapi?”
“Unajua Sentaure usinizingue, nitaghairisha sasa hivi”
(huna uwezo wa kughairisha)alijisemea kimoyo moyo “Tendwe, mpenzi usije ukanuna bure, nikakikosa nilicho kiomba” Wakatoka nje ya nyumba hiyo, wakapanda kwenye gari kuelekea nyumbani kwa Koplo Taure, walipofika nje ya nyumba hiyo, Koplo Taure akashuka kwenye gari na kwenda kufungua geti, baada ya kufungua akarudi tena kwenye gari ili aliingize ndani.
“Jianaume ji bahili hili, kwani kama ungeweka mlinzi ungepungukiwa wapi kwenye mshahara wako?” Afande Jesca alisema hivyo baada ya Koplo Taure kurudi kwenye gari.
“Kuna mlinzi mmoja muda si mrefu nataka nimuweke ndani humu”
“Nani?”
“Wewe”
“Nyooo!!!!! Nani umuweke mlinzi?”
“Sijamaanisha uwe mlinzi wa getini, bali nataka nikuoe kabisa ili uwe mlinzi wa nyumba yangu”
“Nenda uko, wewe ndio muowaji? Labda yesu arudi”
“Kwahiyo huniamini au?” Koplo Taure aliongea hivyo huku akipaki gari kwenye maegesho ya nyumba hiyo, akashuka kwenye gari ili akafunge geti.
“Ndio sikuamini” Baada ya kufunga geti, alirudi hadi upande alipokuwa Afande jesca, akafungua mlango wa gari na kumnyoshea mkono Afande Jesca.
“Karibu nyumbani kwetu mke wangu mtarajiwa” Afande alitabasamu na kuupokea mkono wa Koplo Taure, wakaongozana hadi ndani ya nyumba hiyo, Afande Jesca akabaki kushangaa shangaa mandhari ya sebule hiyo, sio kwamba hakuwahi kuja katika nyumba hiyo, la hasha! Aliwahi kuja karibia mara tatu, ila alishangaa shangaa ilimradi tu iwe basi, wakaongoza hadi chumbani kwa Koplo Taure, walipofika huko, wakaingia bafuni, ambapo lilikuwepo humo humo ndani, walipotoka wakaenda hadi kitandani, Koplo Taure akanza uchokozi wake wa kikubwa.
“Mmh mmh!!! Mbona unaharaka hivyo? Nenda kazime taa kwanza” KoploTaure kusikia hivyo, akachomoka mbio kama Usain Bolt wa kwenye mashindano ya marathon, sekunde moja ilikuwa nyingi, ikawa tayari amezima taa. mpaka hapo mimi mwandishi sikuweza kuona tena nini kiliendelea baada ya giza kutawala humo chumbani, ila nilichoweza kusikia hapo ni sauti ya kama vile mtu anakula muwa hivi, ila sikutaka kujipa imani hiyo moja kwa moja maana sikuona muwa wowote ndani humo, nikaona isiwe tabu, nikaondoka mdogo mdogo hadi gheto kwangu, nikapanga kuwafuatilia tena asubuhi patakapo kucha. Nikaondoka zangu. ********************************* Nyumbani kwa Mrutu. 12:30 Asubuhi.
Mrutu baada ya kuhakikisha Hemedy ameshajiandaa kwaajili ya kwenda shule, wakaongozana hadi kwenye gari na kuianza safari ya kuelekea shule anayosoma Hemedy, walipofika shule, wakashuka kwenye gari na kuelekea moja kwa moja katika ofisi za shule hiyo kwajili ya kuonana na mwalimu anaewasimamia wanafunzi kwa kila kitu.
“Ndio mwalimu, nataka kuanzia leo hii huyu mwanangu na yeye awe analetwa na kurudishwa kwa gari ya shule, maana mimi sina muda wa kumleta na kumrudisha kila siku” Mrutu aliongea hivyo baada ya salamu na kukaribishwa kwenye kiti ofisini humo.
“Kwahilo usijali, maana huyu aliacha kupanda gari ya shule baada ya baba yake kutaka mwanae amlete na kumrudisha kwa gari yake, sasa kwavile wewe mwenyewe ndio umeamua apande gari ya shule, hakuna tabu, chamsingi ni kuelekeza huo mtaa anao kaa kwa sasa ili aletwe na arudishwe”
Mrutu akamuelekeza mtaa anaokaa, baada ya kuona mwalimu ameujua vizuri, akaaga na kuondoka, akarudi nyumbani kwake kwaajili ya kuijianda kwenda dukani kwake, alipofika akajiandaa vizuri, ila kabla hajatoka kwenda dukani kwake, akaenda katika chumba anacho lala Hemedy, sijui ni kipi kilichomfanya aende ila alienda hadi chumbani humo, akaangaza angaza macho yake chumbani humo, ila ghafla macho yake yakatua kwenye meza ya kujisomea ya Hemedy, akaona kijidude flani kipo hapo juu ya meza, akaiyendea hiyo meza hadi karibu yake, akakuta ni flash ndio ipo hapo juu,(flash hii ndio ile wakina Murutu wanayoitaka kutoka kwa Hemedy) akaichukua na kuigeuza geuza“hii flash ya nini?” alijiuliza mwenyewe, baada ya kuona amekosa jibu, akaona isiwe tabu, akatoka nayo hadi sebuleni na kuiyendea tv ya hapo sebuleni, akaiwasha na kuwasha na deki, ili aijaribu hiyo flash ajue ni ya nini……
Ghafla simu yake iliyokuwa mfukoni mwa surualia aliyoivaa iliita, akaacha kuichomeka flash kwenye deki, akaitoa simu kwenye mfuko na kuangalia nani aliepiga, akaona ni mfanya kazi wake ndio anampigia, akaipokea.
“Enhee!! Niambie kolo”
“Bosi, embu njoo dukani mara moja” sauti iliyotoka kwenye simu iliongea hivyo.
“Kuna nini?”
“Kuna watu hapa mimi siwaelewi wanachokizungumza, labda uje mwenyewe ndio unaweza ukawaelewa”
“Wanataka nini hao watu?”
“Bosi wewe njoo ndio utawaelewa, wanadai wanataka kulifunga hili duka”
“Haya poa nakuja” Mrutu baada ya kusikia kuwa watu hao wanataka kulifunga duka lake, kidogo akachanganyikiwa.
“Wanakuambia ufanye haraka”
Mrutu hakujua watu hao wanao mtaka yeye ni wakina nani na wanataka nini, ikabidi aache alichokuwa anataka kufanya ili kuwahi dukani kwake, akaiyacha flash juu ya deki na kuizima tv na deki, na kuondoka hapo ili awahi dukani kwake. Baada ya dakika ishirini, akawa tayari amefika dukani kwake, akapaki gari pembeni na kushuka, akaenda hadi dukani na kukuta kuna sura ngeni za watu wa tatu wamesimama hapo dukani kwake.
“Za saa hizi jamani” alianza na salamu baada ya kuwafikia.
“Nzuri, wewe ndio mmiliki wa duka hili?” Jamaa mmoja kati ya hao watatu alimuuliza Mrutu.
“Ndio, ndio ni mimi”
“Ok, duka lako halija lipiwa kodi ya mapato ya TRA, na kwanini umechelewa kulipa hadi muda huu, au hamkutangaziwa?” Hadi hapo akajua kwamba watu hao ni watu wa TRA.
“Dah!! Nduguzangu mambo mengi ndio yamenifanya nisahau yote, ila mimi sina kawaida ya kuchelewa kulipa kodi”
“Sawa, sasa sisi tunalifunga hili duka hadi hapo utakapo lipa kodi, ndipo tutakapo lifungua tena” Yule jamaa aliongea hivyo huku akielekea kwenye geti la duka hilo ili kulifunga, ila mrutu akamuwahi na kumzuia.
“Sasa jamaa si tuzungumze kwanza?”
“Tuzungumze kitu gani? Wewe hujui umechelewa kwa muda gani kulipia kodi?”
“Najua nimechelewa, ila si nimekuambia kuwa nina mambo mengi ndio yamenifanya nichelewe kulipa kodi”
“Haya zungumza nakusikiliza” Mrutu hakutaka maneno mengi, akaingia dukani na kutoka na kiasi cha pesa na kumpatia, Jamaa akazitia mfukoni pesa alizopewa.
“Na ukalipie kabla hatuja rudi tena” Jamaa akasema hivyo huku akiondoka dukani hapo akifuatiwa na wenzake, wakapanda kwenye gari yao na kutokomea zao. Mrutu akashusha punzi ndefu(huu mkosi wa asubuhi asubuhi)akawaza huku akiingia ndani ya duka lake. ******* Mtaa wa Majengo. 2:30 Asubuhi.
Koplo Taure alikuwa ndani ya gari lake akisubiri lindo lake alilolianza tokea jana usiku, alikuwa amepaki gari yake mbali kidogo na nyumba ya wakina Tito, akiwasubiria watoke ili awafuatilie tena, yeye mwenyewe hakujua kwanini amepatwa na hamu ya kuwafuatilia watu hao aliowaona jana usiku kwa mara ya kwanza, “Duh!! Najipa kazi ambayo haina maana yoyote, sasa kwanini nawafuatilia hawa watu? Ila acha niifuate nafsi yangu inavyotaka, huenda ikawa watu hawa wanalaziada” alijiwazia mwenyewe.
Baada ya dakika kadhaa aliwaona wakitoka na gari yao na yeye akaiwasha ya kwake ili kuwafuatilia, akawaona wakiingiza gari barabarani wakielekea kule kule kwa jana walipo toka, akawa yupo nyuma ya gari mbili zilizofuatana, ila zile gari mbili baada ya kufika Hosteli zikakunja kuelekea chumbageni, sasa akawa yupo nyuma ya gari ya kina Tito, akaona akiendelea kuwafuata hivyo hivyo wanaweza wakamshtukia, akalipita gari lao na kwenda hadi Toyota kuwasubiria, akapaki pembeni kujaribu bahati yake kama kweli na wao watapita na njia hiyo hiyo, bahati ikawa kwake baada ya kuwaona wanatokea na njia ya jengo la Tanesco, akawasubiri hapo hapo Toyota, walivyofika wakampita na kuelekea na njia ya kuelekea Hospitali ya Bombo, akaendelea kuwafuata nyuma hadi walipoipita Hospitali ya Bombo akawa bado yupo nyuma yao.
“Oya Tobi, unaiyona hiyo gari hapo nyuma?” Tito alimuuliza Tobi.
“Aaa!! Mimi basi nimeanza kuiyona tangia tupo Toyota”
“Basi jua kuwa tunafuatiliwa, sasa wewe embu ishike namba zake, halafu tutajua nini chakufanya” Tobi baada ya kusikia hivyo, akageuka nyuma na kuanza kuzisoma namba za gari ya Koplo Taure, alipozikariri, akarudisha shingo yake mbele.
“Sasa skia, hapa tunajifanya kama tunaingia kwa Mkuu halafu tuone yeye atafanya nini” Aliposema hivyo akawasha endiketa za kulia kuashiria kuwa anataka kukunja.
Koplo Taure baada ya kuona lindo lake linataka kuingia katika nyumba ya Mr Bakari Haneni, akalipita gari la kina Tito na kunyoosha moja kwa moja kama anaenda Beach ya Raskazoni. Wakina Tito baada ya kuona ile gari iliyokuwa inawafuata imenyoosha na wao wakaghairisha kuingia kwenye nyumba ya Bosi wao, wakalifuata gari la Koplo Taure kwa kasi baada ya kuliona limekunja mbele kabisa kwenye kituo kidogo cha polisi, kipindi hicho geti la nyumba ya Mr Bakari Haneni lilikuwa tayari limeshajifungua, ila baada ya wakina Tito kughairisha kuingia likajifunga lenyewe.
Wakina Tito waliendesha gari kwa kasi ilikuliwahi gari la Koplo Taure, wakafika na wao kwenye kituo kidogo cha polisi, wakapiga kona kuingia kulia, ila bahati haikuwa kwao baada ya kutoliona gari la Koplo Taure, maana hapo kulikuwa na njia mbili sasa hawakujua gari hiyo imeingilia na njia ipi, wakageuza gari na kurudi walipotoka, wakafika kwenye nyumba ya Bosi wao Mr Bakari Haneni na kuingiza gari ndani baada ya geti kujifungua. Walipeleka gari sehemu ya maegesho na kushuka garini humo, wakaanza kuelekea ndani ya nyumba hiyo, walipofika sebuleni walimkuta bosi wao akiwa amekaa kwenye sofa moja wapo kati ya mengi yaliyopangwa kwa ustadi mzuri uliopendezesha sebule hiyo.
“Mbona vijana wangu, mlikuja hadi getini halafu ghalfa mkaondoka, mlienda wapi?”
“Mkuu, kuna mpumbavu alikuwa anatufuata nyuma”
“Sijakuelewa Tito, embu fafanua vizuri”
“Kuna gari ilikuwa ikitufuatilia”
“Sasa nyie mlijuaje kama hiyo gari ilikuwa ikimifuata nyie, je kama ilikuwa na safari zake?”
“Hapana Mkuu, hiyo gari ilianza kutufuata tangia tunatoka home”
“Imeishia wapi hiyo gari?”
“Wakati tunataka kuingia humu ndani, ndipo ikatupita na sisi tukaghairisha kuingia humu ndani, ilituifuatilie ila mbele kule ikatupotea” “Ila mumewajua ni wakina nani wanaomifuatilia?”
“Hapana Mkuu, ila tumezimaki namba zake”
“Safi, ila hadi sasa hamjawafikiria kuwa ni wakina nani waliokuwa wanamifuatilia?”
“Sina uhakika, Ila mimi nina wasiwasi huenda ikawa ni wale tulio wachukulia pesa zao na mzigo wetu jana baada ya kutaka kutuletea ujanja ujanja” Tobi alisema.
“Huenda ikawa ndio hao, na kama ndio itakuwa mmefanya kosa kubwa sana kupajua hapa na kumijua nyinyi kuwa ni watu wangu”
“Dah!!! Kweli, sasa tufanyeje Mkuu”
“Hakuna namna nyengine zaidi ya kuwatafuta na kuwapoteza wote katika uso wa hii dunia, kabla hawajaleta madhara ya aina yoyote”
“Sawa Mkuu” wote wawili waliitikia.
“Vipi lakini, maskani iko salama kule” Mr Bakari Haneni aliuliza kuhusu jengo lao zinapoendelea shuhuli zao za madawa ya kulevya.
“Mkuu, hatukufika ila tumempiga simu Yuni, anasema kila kitu kipo shwari”.
Wakiwa wanaendelea na maongezi yao, muda huo Koplo Taure ndio alikuwa anaingia kituoni, alivyoshuka kwenye gari akaenda mapokezi na kumkuta Afande Jesca akiendelea na kazi.
“Mbona umechelewa hivyo?” Afande Jesca alimuuliza Koplo Taure baada ya kufika hapo alipo.
“Dah!!! We acha tu, wamenishtukia kwamba nawafuatilia, ila nimejihakikishia kuwa ni watu wa Mr Bakari Haneni”
“Imekuaje kuaje, embu nielezee”
“Hata sijui, ila walivyofika kwenye nyumba ya Mr Bakari Haneni, mimi nikawapita ila nilivyofika mbele nikawaona wakinifuata kwa kasi, nikaiingiza gari yangu kwenye kile kituo kidogo cha polisi, ndipo hapo nilipowaona wakihangaika kunitafuta baada ya kunikosa wakarudi zao na kuingia kwenye nyumba ya Mr Bakari Haneni, ndipo na mimi nikaondoka zangu”
“Duh! Umenifanya niwe na wasiwasi baada ya kuona hutokei kabisa”
“Usijali mamii, ndio nimerudi mume wako” Koplo Taure aliongea hivyo huku akielekea ndani ya kituo hicho ilipo ofisi yake.
Nnje ya jengo la TRA. 8:15 Mchana. Alionekana Mrutu akitoka ndani ya jengo hilo, alikuwa ameenda kulipa deni analo daiwa duka lake, baada ya kufika kwenye maegesho ya magari, akaliendea gari yake nakuingia humo, akatoa simu yake na kumpigia Mata.
“Haloo” aliongea baada ya simu yake kupokelewa.
“Ndio Mrutu, niambie” upande wa pili ulisikika.
“Safi tu, upo kazini kwako sasa hivi?”
“Hapana, nipo nyumbani, leo thijaenda kadhini”
“Basi poa nakuja” Akakata simu na kuingia tena sehemu ya majina, akatafuta kwa sekunde saba, alipolipata hilo jina analotafuta akapiga.
“Ndio Moto, uko wapi wewe?” aliongea baada ya simu kupokelewa.
“Mimi nipo maskani tu, vipi kuna ishu yoyote imetokea?”
“Hapana, ila naomba tukutane kwa Mata sasa hivi”
“Poa” Alipokata simu, akawasha gari na kuelekea nyumbani kwa Mata, alivyofika akashuka kwenye gari na kuingia ndani ya nyumba ya Mata, akamkuta anakata kata matunda hapo sebuleni.
“Naona mzee unataka kuutia mwili wako vitamini kwa matunda”
“Nataka kuutia mwili wangu au miili yetu? Kama ingekuwa nataka kula pekeangu ningeyaficha haya matunda halafu nathubiri mkiondoka ndio nayala, uthinitie uchoyo bwana”
“Sawa basi yakate kate ili tule wote” aliongea hivyo huku akichukua kipande cha chungwa.
“Aaa!! Mrutu mbona unaandha kula kabla mimi thijakula?”
“We kama hujakula acha mimi nianze kula. Hajakuja bado huyu Moto?” alisema hivyo huku akienda kukaa kwenye sofa jengine.
“Bado hajafika, ila nahith…” kabla hajamalizia sentensi yake, mlango ukafunguliwa na Moto akaingia ndani, moja kwa moja akaenda kwenye sahani ya matunda iliyokuwa imewekwa chini mbele ya Mata aliekuwa akiendelea kumenya matunda mengine, akachukua kipande cha nanasi na kurudi nacho hadi kwenye sofa jengine.
“Nyie vipi? Mbona kila anaekuja anachukua tu halafu anakula, mnajua mimi thijakula kituchochote kati ya hivi nilivyo vimenya? Ohooo!!! Hamtokula thatha hivi” Mata aliongea.
“Acha zako wewe embu menya matunda tule”
“Haya nyie nifanyeni bwege tu”
“Ok, tuachaneni na hayo, ni hivi jana yule dogo nilimuhoji vizuri tu kuhusu ile video, akasema yeye hajui ni nani ambae kaichukua”
“Halafu Mrutu bwana, sasa wewe umeongea kiistarabu unadhani anaweza akakuambia ukweli, ulitakiwa umkazie sura” Moto aliongea huku akiikwepesha miguu yake na maji maji yaliyokuwa yanatoka kwenye kipande cha nanasi alicho kishika.
“Nyie hamjui tu, ila nimemkazia sana tu mpaka akalia, lakini akasema yeye hajui. halafu iweje nimkazie sana, kwani yeye anajua kama mimi pia nipo kwenye huu mchezo”
“Dah!!! Thatha tunafanyaje?”
“Inabidi afe tu ili tupoteze ushahidi kabisa, unajua inaweza ikatokea siku tukakutana nae sehemu mbaya halafu akatuletea matatizo, maana sidhani kama itakuwa sura zetu amezisahau”
“Hapo kweli, thatha tutatumia njia gani ya kumuua?”
“Halafu nimekumbuka kitu, wakati asubuhi nataka kutoka nyumbani kuelekea dukani, kuna flash niliiyona chumbani kwa yule dogo kwenye meza yake ya kujisomea, ila sikupata muda wa kuicheki baada ya kupigiwa simu na yule kijana wangu wa kazi”
“Sasa wewe hiyo flash unahisi ina nini au labda unahisi itakuwa ni hiyo flash yenye ile video?”
“Hata mimi nimehisi hivyo. sasa ngoja nikaichukue ili tuje kuiyangalia wote hapa” akanyanyuka kwenye sofa na kuiyendea sahani yenye matunda na kuchukua kipande cha nanasi na kuondoka nacho, akatoka nje na kupanda kwenye gari yake na kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwake, kwenda kuichukua flash yenye video ya tukio zima walilolifanya wakina Mata nyumbani kwa marehemu Mzee Mheshimiwa.
ENDELEA….
Hemedy muda huo alikuwa kwenye basi la shule akirudishwa nyumbani kwao(nyumbani kwa Mrutu) walipofika nje ya geti, akashuka kwenye gari la shule na kufungua geti, akaingia ndani sebuleni, akaaza kupiga hatua kuelekea chumbani kwake, ila kabla hajaufikia mlango wa chumbani kwake, akarudi nyuma kidogo baada ya kuona kitu juu ya deki alichokifananisha, akaiyendea deki, alaipofika akaiyona ile flash yake yenye video “mmh!! hii flash si nimeiyacha ndani, imefuata nini hapa, huyu itakuwa ni bamdogo, sijui tayari ameshaiyona hii video, mamaa sijui itakuaje kama tayari ameshaiona” alijisemea mwenyewe.
Akaona asipotumia ujanja anaweza akaadhibiwa kwa kosa lakudanganya, akaichukua ile flash, akaenda nayo chumbani kwake, akaificha chini ya godoro lake la kulalia, akatoka tena nje ya chumba chake, akakiendea chumba cha Mrutu na kujaribu kufungua mlango akaona mlango umefungwa“hajarudi bado” hivyo hivyo akiwa na nguo zake za shule ba begi lake, akafunga milango yote vile vile alivyokuta na kutoka nje ya nyumba hiyo na kupotelea huko.
Muda si mrefu naye Mrutu, akafika nyumbani hapo na kuingia hadi ndani sebuleni, akaiyendea deki alipoiyacha ile flash asubuhi, ila cha ajabu hakuikuta, akaanza kuitafuta, akainua deki, akaangalia kwenye tv, akaanagalia kwenye masofa, akaliendea kabati la vyombo na kuitafuta kote huko lakini hakuiyona, ikabidi atulize akili kwanza“ hii flash imeenda wapi? mbona kote huko siyoni, ila asubuhi nakumbuka niliiacha hapa hapa kwenye deki, au itakuwa Hemedy kaichukua? lakini hapana Hemedy yeye si yupo shule, sasa ataichukua vipi? au amesharudi” akaanza kumuita Hemedy huku akienda katika chumba chake, alipofika akafungua mlango akaingia ndani, lakini nako hakumkuta Hemedy, ikabidi aanze kuitafuta humo humo chumbani kwa Hemedy akatafuta kila sehemu lakini hakuiyona“ Duh sasa ni nani ambae kaichukua ile flash, au Hemedy kaichukua?” akapata wazo la kuangalia nguo za Hemedy za shule, lakini nazo pia hakuziona, akajua Hemedy bado hajarudi shule, akatoka hadi sebuleni na kukaa hapo akivuka kumbukumbu vuzuri ya wapi aliiweka ile flash.
Hemedy baada ya kuzurura mitaani kwa nusu saa nzima, akaona arudi nyumbani huwenda ikawa tayari baba yake mdogo amerudi kutoka kazini, akapanga kama asipomkuta basi asiingie ndani mpaka atakapo rudi, baada ya kufika karibu na nyumba yao, akaliona gari ya Mrutu imepaki nje ya geti, akajua tayari amesharudi, akaingia ndani na kumkuta Mrutu amekaa sebuleni.
“Shikamoo baba” Hemedy alimsalimia Mrutu.
“Marahaba, ndio unarudi shule sasa hivi?”
“Ndio”
“Nyumbani ulirudi kufuata nini baada ya kukupeleka shule asubuhi?” Mrutu aliuliza swali la kimtego ili kumnasa Hemedy, Hemedy naye kama alijua vile kwamba ana tegwa, akajua akijibu hovyo tu itakuwa tayari ameshanaswa.
“Hapana, mimi sijarudi nyumbani toka unipeleke shule na ndio ninarudi sasa hivi” Hemedy akajibu kiufundi na kumfanya Mrutu ashushe pumzi nyingi.
“Mbona mimi kunawakati nilikuja shuleni kwenu na kuambiwa kuwa umerudi nyumbani” Hemedy alicheka kimoyo moyo baada ya kuona baba yake huyo mdogo ameishiwa maswali ya kimitego.
“(kwa staili hiyo wala huwezi kunitega kamwe)alijiwazia mwenyewe, Hapana bamdogo kweli mimi sijatoka nje ya eneo la shule”
“Kwahiyo walimu wako waongo?”
“Itakuwa, kwasababu mimi sijatoka hata nje ya darasa, muda wote nilikuwa nipo darasani” Mrutu akaishiwa pozi, hakujua am’bane vipi tena, hakuwa na swali jengine la kumuuliza, ikabidi tu amruhusu Hemedy kwenda kubadilisha nguo, baada ya kubadilisha nguo, Hemedy alirudi sebuleni hapo.
“Sasa skia, hapa sebuleni kuna flash yangu imepotea, kwahiyo kama utaiyona naomba unirudishie maana ina taarifa zangu za kikazi”
“Sawa, hakuna shida” hadi hapo Hemedy akajidhihirishia kuwa Mrutu bado hajaiyangalia ile flash.
“Basi chukua hii(akampa noti ya shilingi elfu tano)utanunua chakula ukitakacho, mimi leo sitopika na sasa hivi kuna sehemu naenda mara moja” Baada ya kumuaga Hemedy, akatoka nje na kupanda kwenye gari yake, akaanza safari ya kwenda nyumbani kwa Mata, baada ya ya dakika kumi na tano akawa tayari amefika, akashuka kwenye gari na kuingia ndani.
“Vipi? Mbona umekuja huna furaha?” Moto alimuuliza huku akiwa ana lamba kokwa la embe.
“Kwanza mbona mimi hamjaniwekea matunda, yani mmeyala yote nyie pekeenu?”
“We si umechelewa mwenyewe, ila tumekubakishia, yale pale juu ya friji kwenye ile sahani” Mrutu akaenda hadi kwenye friji na kuichukua sahani yenye matunda na kwenda nayo kwenye sofa na kukaa.
“Enhee!! Hiyo flash iko wapi?” Mata aliuliza.
“Dah!! Yani ile flash imepotea katika mazingira ya kutatanisha, sijaiyona sehemu nilipoiyacha” Mrutu aliongea hivyo huku akila ubale wa embe.
“Au labda yule dogo aliporudi shule aliichukua” Moto aliongea.
“Hapana sio yeye, maana yule dogo alipo rudi shule alinikuta naitafuta”
“Mata, yule dogo nimempeleka mwenyewe hadi shule, na aliporudi pia nikajaribu kum’bana lakini haonyeshi kabisa kama alirudi nyumbani wakati mimi sipo”
“Bathi hapo ndipo ninapo amini kwamba nyumba yako ina majini, na unatakiwa umuite shekh haraka thana, aje kuipigia kithomo kabla mambo hayajazidi kuwa makubwa, maana thiku unawedha ukalala nyumbani kwako na athubuhi ukajikuta ume lala juu ya bahari”
“Hahahahha!!!! Kwanini umesema hivyo Mata?” Mrutu alicheka baada ya Mata kusema hivyo.
“Hili tukio la leo nikiliunganisha na lile la jana ndio napata picha kamili kwamba nyumba yako ina majini”
“Tukio lipi hilo la jana?” Mrutu akauliza huku akianza kuingiwa na wasiwasi.
“Jana thi tulithikia minong’ono ikitokea nje wakati tumekaa pale thebuleni kwako, halafu ulivyo enda kuangalia hukukuta mtu yoyote, thatha wewe udhani kuwa hiyo ni hali ya kawaida”
“Hahahah!!!! Mata bwana, kumbe ndio hivyo? Ile minong’ono ilikuwa ni ya yule dogo na yule Askari aliekuja nae”
“Hapana, mimi thi themei wakati walipokuja wale, ila nathema mwandho kabitha, wakati ndio tuna ingia ingia pale kwako”
“Hata ile mingong’ono ya mwanzo ilikuwa pia ni wao” Mrutu alipoongea hivyo, Mata na Moto macho yao waliyatoa pima, wakabaki wamemkodolea macho Mrutu.
“Vipi mbona mmeganda hivyo?” akawauliza.
“Kwahiyo unataka kutuambia kuwa maongezi yote yale waliyasikia?” Moto aliuliza.
“Hapana, hawakufika karibu na dirishani”
“Thatha kwanini waliondoka na hawakuingia ndani?” Mata aliuliza.
“Walienda nyumbani kwa yule askari, embu tuacheni na mada hii, turudini kwenye mada iliyotufanya tukutane hapa” Mrutu aliwakatisha na kuwarudisha kwenye mada yao ya mwanzo.
“Ok, tunafanyaje thatha?” Mata aliuliza.
“Itabidi tumteke tukamuulie maporini huko” Moto alitoa rai yake.
“Tatizo lako Moto hufafanui, watakiwa utuambie tuna mtekaje tekaje, sio useme tu tunamteka tunamteka, embu fafanua basi” Mrutu aliongea.
“Sawa, acha nifafanue, ni hivi wewe leo itabidi uchelewe kurudi nyumbani kwako, halafu yeye kule si atabaki pekeake, basi mimi na Mata hapa, tutaenda hadi pale kwako na kumchukua halafu tunaondoka nae, tunatafuta msitu wowote kisha tuna maliza kazi huko huko, au nyie mnasemaje?” Moto alihitimisha ufafanuzi wake.
“Hiyo itakuwa ni njia mbaya upande wangu” Mrutu alionyesha wasiwasi wake.
“Kwanini umesema hivyo?” Moto aliuliza.
“Unadhani akishapotea katika mazingira ya kutatanisha kama hayo, mimi si nitaitwa kusaidia polisi upelelezi, aa aa!!! Aise hiyo njia mimi sijaiafiki kabisa”
“Hata mimi pia thijaiafiki kabitha” Mata nae aliongea.
“Sasa basi toeni mawazo yenu” Moto aliongea.
“Subirini mimi apa niwaambie. leo usiku nitatoka nae kwenda popote pale na gari yangu, halafu tutawasiliana kuwa naelekea wapi, tukiwa katika matembezi, nyinyi matakuja na gari yenu na kutuzibia njia kwa mbele, mimi si nitasimama, basi nyie mnakuja na bastola, mnatuteka wote wawili halafu mtamchukua yeye na kuondoka nae ndipo hapo mtakapo enda kumfanya chochote, na mimi huku nyuma ntajifanya kukimbia polisi kwenda kutoa taarifa, huo ndio utakuwa mpango mzuri, ambao utatufanya tusishtukiwe na yoyote” Mrutu alihitimisha mpango wake na kuwaangalia wenzake aone watasema nini.
“Hapo sawa, lakini utakapoenda huko polisi kutoa taarifa hiyo, je wakikuuliza unawajua waliyomiteka wewe utasemaje?” Moto aliuliza.
“Mimi nitawaambia kuwa walijiziba nyuso zao na maksi, kwahiyo sikuweza kuwaona usoni”
“Basi sawa kama mpango ndio huo, mimi binafsi nimeuafiki, sijui Mata yeye ni vipi”
“Hata mimi pia nikopamoja na nyinyi” Mata nae aliunga mkono wazo la Mrutu.
“Sawa kama mpango ndio huo na vipi kuhusu zile mali, maana na mimi nataka nitembelee gari bwana nshachoka kutembea kwa miguu”
“Hilo tutalishuhulikia baada ya kumaliza kwanza hili” Mrutu alijibu.
“Lakini thi zipo thalama kabitha mali dhetu tarajiwa?” Mata aliuliza.
“Ziko salama, leo tu kabla sijaenda TRA nilipitia katika ofisi zote na kukuta kazi zinaendelea kama kawaida, si unajua mimi ndio nazisimamia mali zote za marehemu”
“Basi kama ni hivyo shwari, maana nilivyokuwa na usongo na hela yani nikipata mgawo wangu, naacha kabisa hii shuhuli ya ujambazi, nisije nikajikuta siku naingia kwenye vyombo vya dola na maisha yangu yakamalizikia jela, nataka na mimi niwe raia mwema” Moto aliongea.
“Sasa si bora uingie kwenye vyombo vya dola kuliko kuingia mikononi mwa raia wenye hasira kali” Mrutu aliongea hivyo huku akiinuka na kuuendea mlango wa kutokea.
“Vipi, mbona unaondoka tena Mrutu, unaenda wapi?” Mata alimuuliza.
“Acha mimi niwaache, kuna sehemu nataka kwenda mara moja”
“Poa, lakini uthithahau bathi kuukamilisha mpango tulioupanga”
“Msijali” Mrutu aliongea hivyo huku akiufunga mlango na kuondoka zake nyumbani hapo kwa Mata, akiwaacha Moto na Mata wakiendelea na maongezi mengine, akawasha gari kutokomea zake.
Katika ngome(maskani) ya Mr Bakari Haneni. 11:07 Jioni.
Tito na Tobi waliingiza gari katika lango la jumba hilo la zamani, ililoachwa na wakoloni miaka mingi iliyopita, lilikuwa likilindwa masaa ishirini na nne na watu wenye bunduki, waliokuwa wakitembea tembea huku na huko, jumba hilo lilikuwa limezungukwa miti mingi iliyotengeneza msitu mdogo, walipoingia ndani ya jumba hilo, wakashuka kwenye gari na kunyoosha hadi ndani ya jengo hilo, wapanda ngazi na kufika katika gorofa ya pili, wakaingia kwenye chumba kikubwa kilicho fananiana kama ukumbi flani kilichokuwepo gorofa ya pili ambayo ilikuwa ndio mwisho wa jengo hilo, huko kulikuwa na kundi la watoto wenye umri kati ya miaka kumi na tano hadi ishirini, wakifunga madawa ya kulevya kwenye vipakti vidogo vidogo, wengine walikuwa wamesinzia na kukaa chini kabisa huku udenda ukiwatoka, ulikuwa ni unyanyasaji na udhalilishaji ila kati ya hao wote hakuna aliewajali watoto hao.
Tito na Tobi walitoka katika ukumbi huo na kuelekea kwenye chumba chengine huko huko kwenye gorofa ya pili, walivyoingia wakakuta watu, wanayapanga madawa hayo yaliyokuwa tayari yamefungwa kwenye vipakti vidogo vidogo, walikuwa wakiyapanga kwenye maboksi yaliyokuwemo chumbani humo, wakatoka katika chumba hicho na kushuka chini kwa kutumia ngazi, huko wakaelekea katika ukumbi nwengine na kukuta kundi la vijana wanafanya mazoezi, baada ya kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa, wakatoka nje na kupanda kwenye gari yao na kutokomea zao mjini.
Nyumbani kwa Mrutu. 3:02 Usiku. “Sasa Hemedy embu jiandae mara moja tukatembee” Mrutu alimwambia Hemedy.
“Wapi?” Hemedy aliuliza.
“We kajiandae twenzetu au wewe unaona raha kukaa nyumbani tu kila siku?”
“Hapana”
“Basi kama ni hivyo kajiandae twenzetu. au ujiandae nini? twenzetu tu hivyo hivyo”
“Hivi hivi?”
“Eeeee!!! Hivyo hivyo pia vinatosha, kwanza hatuendi kukaa sana, muda si mrefu tutarudi” Baada ya kuongea hivyo, walitoka nje na kupanda kwenye gari, ili wakatembee kama Hemedy alivyojua, hakujua kuwa baba yake mdogo anania mbaya na yeye, kama angejua nini kimepangwa juu yake, wala asingeitamani hiyo safari, kwavile, usilolijua ni sawa na usiku wa giza, basi kwa hemedy pia kulikuwa ni usiku wa giza, hakuweza kuona mbele hata hatua moja, baada ya yote safari ya kwenda kumuua Hemedy ikaanza.
Nyumbani kwa Inspekta Ganjo. 2:32 Usiku. Nusu saa nyuma. “We Taure, mbona hadi saa hii hujaenda kumchukua Hemedy?” Inspekta Ganjo alimuuliza Koplo Taure.
“Mzee namalizia kupanga hivi viti mara moja” Koplo Taure alimjibu Inspekta Ganjo.
“Nenda bwana mara moja, hivyo viti muachie Jesca avipange yeye” Inspekta Ganjo alimuambia.
“Sawa” Koplo Taure alijibu na kuacha kupanga viti.
“Jesca, embu vipange hivyo viti haraka, muache Taure amfuate Hemedy, aje kusherehekea na watoto wenzake” Nyumbani kwa Inspekta Ganjo, usiku huo kulikuwa na sherehe ya kuzaliwa mjukuu wake wa kike, anaeitwa Hilda. wanafunzi wenzake anaosoma nao walialikwa kuja kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa mwenzao. Koplo Taure baada ya kuambiwa hivyo, akatoka nje akapanda kwenye gari yake na kwenda kumfuata Hemedy nyumbani kwao, dakika ishirini na tano ikawa tayari ameshafika nyumbani kwa Mrutu, bahati nzuri ndio akawakuta wanatoka, akabidi aweke gari pembeni na kushuka, akaipigia mkono gari ya Mrutu, nae akasimama, akawafuata,Mrutu akashusha kioo cha malango wa gari ili kumsikiliza Koplo Taure.
“Niambie Mrutu” Koplo Taure aliongea hivyo huku akimpa tano(salamu iliyozoeleka kwa vijana) kupitia kwenye kwenye kioo cha mlango kilicho shushwa.
“Freshi tu” Mrutu nae alijibu na kugonganisha mkono wake kwenye mkono wa Koplo Taure. Hemedy nae alimsalimia Koplo Taure, baada ya kuijibu salamu ya Hemedy, akaendelea kuongea na Mrutu.
“Mnaelekea wapi sasa hivi?” Koplo Taure aliuliza.
“Tunaenda kutembea tembea tu” Mrutu alijibu.
“Wapi?”Koplo Taure aliuliza.
(huyu vipi, mbona maswali mengi) alijiwazia mwenyewe. “tunaenda kula msosi wa usiku, maana leo nimechoka kupika” Mrutu alijibu tu hiyo basi, lakini alishayachoka maswali ya Koplo Taure.
“Basi kama ndio hivyo, nilikuwa namuomba huyo dogo, maana Inspekta Ganjo anamuita nyumbani kwake”
“Kuna nini usiku huu”
“Kuna sherehe ya kuzaliwa kwa mjukuu wake, sasa alikuwa anamuhitaji akajumuike na wenzake”
“Sasa.. Lakini.. Hajakula bado huyu, subiri kwanza tukale halafu utakuja kumchukua”
“Lakini ni muhimu, Inspekta anamtaka aende kwenye hiyo sherehe, halafu kama hajakula, mbona hata huko pia chakula kipo kingi tu, ataenda kula”
“Baba, acha niaende tu” Hemedy aliongea. Hadi hapo Mrutu hakuwa tena na chakupinga, labda angesingizia kuwa kesho atachelewa shule, lakini kesho yenyewe ilijuwa ni wikiendi, kwahiyo hakukuwa na shule, akabaki hajui aseme kitu gani, hakuwa na jinsi akamkubalia Hemedy aende na Koplo Taure. Hemedy akashuka kwenye gari, akaingia ndani haraka kwenda kubadilisha nguo, baada ya dakika kumi alirudi akiwa tayari ameshapendeza, alikuwa amevaa jinzi nyeusi na juu akavaa tisheti ya njano aliyo iziba na kikoti cheusi alichokifungua zipu kwa mbele na kufanya tisheti aliyoivaa iyonekane kwa mbele na mikono ya kikoti hicho aliipandisha juu kidogo na kichwani akavaa kofia aina ya cape nyusi aliyoigeuza nyuma kupaleta mbele na chini kabisa akavalia raba za rangi ya njano zenye upapi mweusi. sio siri alikuwa amependeza sana, halafu ukiachana na alivyopendeza, pia alikuwa na sura nzuri, sura ambayo mzazi wowote angetamani mwanae wakiume awe na sura kama ya Hemedy, tungekuwa tupo ulaya tungemuita “Handsome boy” ila kwavile tupo Bongo, basi tunamuita “Mtanashati”.
Mrutu mwenyewe baada ya kumuona alikubali, maana hakuwahi kumuona akiwa amependeza namna hiyo, akabaki tu kujisikitikia,(Dah!!! Sasa kwanini nataka kumfanyia ubaya mwanangu mwenyewe, hivi kweli ninaweza nikaruhusu afe ikiwa uwezo wa kumuepusha na hicho kifo ninao? Sijui, lakini tutaona) Mrutu alijiwazia mwenyewe, wakati huo Hemedy alikuwa akipanda kwenye gari ya Koplo Taure.
“Mrutu, kama vipi na wewe tuongozane sote” Koplo Taure aliongea hivyo huku akielekea kwenye gari yake upande wa dereva.
“Hapana nyie nendeni tu, mimi kuna sehemu naenda sasa hivi” Koplo Taure aliingia kwenye gari yake na kuiwasha.
“Dogo kwajinsi leo ulivyopendeza, sidhani kama huko tunapoenda patatosha” Koplo Taure aliongea hivyo huku akiigeuza gari.
“Kwanini?”
“Aiseee!!!! Umependeza sana, yani kama hutoodoka na demu mmoja basi ujue utaondoka nao wote”
“Hahaha!! Anko bwana, sasa kwani itakuwa ndio nimependeza pekeangu, si wapo watu wengi ambao watukuwa wamependeza tena zaidi yangu mimi”
“Wapo waliopendeza, ila wote umewazidi, subiri mwenyewe utaenda kujionea huko, hivi dogo una demu wewe”
“Mmmmh!! Anko mimi hayo mambo wala siyajui kabisa”
“Basi huku lazima ukaondoke na mmoja” Waliendelea stori huku wakielekea nyumbani kwa Inspekta Ganjo, baada ya dakika kadhaa ikawa tayari wameshafika, Koplo Taure akaingiza gari ndani ya nyumba hiyo na kulipaki sehemu ya maegesho, wakashuka kwenye gari na kuanza kuelekea sehemu ilipo pangwa sherehe hiyo ifanyike, sasa hivi kulikuwa kumechangamka baada ya watoto wengi kuhudhuria sherehe hiyo, ni kweli kama Koplo Taure alivyomuambia Hemedy, kulikuwa kuna watoto wengi wa kiume waliopendeza lakini kati ya hao wote hakuna aliemfikia Hemedy kwa kupendeza, watoto hao walikuwa na umri kati ya miaka kumi na mbili hadi kumi na sita, Koplo Taure na Hemedy wakiwa wanapiga hatua kuelekea vilipo viti ili nawao wakakae kama watu wengine walivyofanya, watu wote wakageuza shingo zao kuwaangalia wao, hasa hasa Hemedy ambae alikuwa mgeni machoni mwao, maana hao watoto wote, walikuwa wanasoma shule moja na mjukuu wa Inspekta Ganjo, na Hemedy yeye hakuwa akisoma shule wanayosoma wao, wakabaki wakimshangaa tu hadi alipoenda kukaa kwenye kiti kimoja wapo, sio kwamba walimshangaa kwakuwa ni mgeni machoni mwao, La hasha!! Bali walimshangaa kutokana na jinsi alivyopendeza.
“Dogo si nimekuambia kuwa lazima uwafunike watu wote hapa? Si unaona wanavyokuangalia?” Koplo Taure alimwambia Hemedy.
“Duh!! We acha tu hadi mwenyewe naona aibu” Hemedy alisema.
“Unamuona yule demu kule mbele anavyokuangalia?” Hemedy akaangalia huko alipoelekezwa na kukuta kweli kulikuwa na msichana wa makamo yake anamtolea macho, macho yao yalipogongana, yule msichana akatoa tabasamu lililo mfanya Hemedy kuondoa macho yake haraka na kuangalia pembeni kwa aibu.
“Sasa sio yule tu, unawaona na hao wawili huko pembeni yako wanavyokuangalia” Hemedy akapeleka macho yake huko alipoelekezwa tena na kukuta kuna wasichana wengine wawili wakimwangalia yeye, akarudisha macho yake na kuangalia mbele tu.
“Yani hapa lazima uondoke na demu tu, maana sio poa wanavyo kutolea macho”
Hemedy hakujibu kitu akabaki akitabasamu tu, alivyotabasamu ndipo hapo uzuri wake ulipoongezeka, ama kwa hakika Hemedy alikuwa ni Handsome boy, hata mimi nilitamani angekuwa ni mdogo wangu tu kwajinsi nilivyo mkubali, sio mimi tu hata wewe msomaji ungefanikiwa kumuona nadhani ungekubaliana na mimi, ngoja kwanza nikuelezee kidogo muonekano wake, alikuwa ana sura flani hivi, sio nene sana wala sio nyembamba sana, nikimaanisha alikuwa na sura ya saizi ya kati, sura yake ilibeba pua ilichongoka kwa mbele kidogo na kufananiana kama za wale watu wa Uganda na alikuwa na macho mazuri, hakuwa mweupe sana na wala hakuwa mweusi, bali alikuw na rangi ya chocolate na hakuwa mfupi sana wala hakuwa mrefu sana bali alikuwa na urefu wa wastani na zile nguo alizovaa ndio zikazidi kuongeze uzuri wake, nadhani hadi hapo, itakuwa tayari ushapata picha Hemedy jinsi alivyo, japokuwa kwa uchache sana.
“Sasa skia dogo, acha mimi nimfuate Mzee nikamwambie kwamba tayari umeshakuja, maana alisisitiza lazima na wewe pia uwepo”
“Poa, mimi utanikuta hapa hapa”
“Sawa, lakini angalia usije ukasababisha ungomvi hapa, ukaharibu shuhuli ya watu”
“Hahahaha!!! Anko bwana!” Mrutu aliinuka na kwenda ndani ya nyumba hiyo, akakutana Inspekta Ganjo, akamueleza kwamba ameshakuja na Hemedy, Inspekta Ganjo, akafurahi na kumruhusu akaendelee na shuhuli nyengine, wakati anatoka akakutana na Afande Jesca, wakaongozana wote na kwenda hadi kwenye viti, sehemu ambayo alimuacha Hemedy.
“Mambo mtoto?” Afande jesca, alimsalimia Hemedy baada ya kufika.
“Poa” Hemedy alijibu.
“Heee!!! Huyu mtoto mbona kama vile namjua ila sikumbuki nimemuona wapi?” Afande Jesca aliongea hivyo huku akimwangalia Hemedy usoni.
“Kwani humkumbuki huyu?” Kaplo Taure alimuuliza.
“Hapana, sikumbuki nilimuona wapi?”
“Nilimleta kituoni siku ile…” Kabla hajamalizia sentensi yake, Afande jesca akamkatisha.
“Basi, basi, nishamkumbuka, duh! kumbe ni mzuri hivi? Siku ile wakati unamleta pale kituoni alikuwa usoni ana vidonda vidonda, lakini leo ndio namuona vizuri. Anaitwa nani vile..”
“Hemedy” Koplo Taure akajibu.
“Anhaaaa!!! Kumbe ndio huyu Mkuu aliokuambia ukamchukue?”
“Ndio, embu tulia kwanza naona kama vile shuhuli ndio inataka kuanza” Ni kweli shuhuli ilikuwa ndio inaanza, Msema chochote, alimaarufu kama “MC” alisogea mbele na kuanza kuwaambia watu kuwa shuhuli ndio inaanza na muda huo, mwenye shuhuli ndio anatoka ndani kwahiyo watu wajiandae kumpokea. Baada ya dakika moja, watu waliambiwa wasimame na kumuimbia nyimbo ya kumtakia furaha ya kuzaliwa binti huyo.
“Happy birthday to you, happy birthday to yo, happy birthday ni ya Hilda, happy bithday to youuu” Watu wote waliimba wimbo huo baada ya kutoke binti huyo mdogo, kati ya umri wa miaka kumi na mbili au kumi na tatu, alikuwa amependeza kushinda wote kwa mavazi aliyoyavaa na sio mavazi tu hata kwa sura alikuwa ni mzuri sana, siwezi kumuelezea kwasababu ninaweza nikachukua karibia page tano, nikiwa bado na muelezea tu, ila jua kwamba alikuwa ni mzuri.
Akaenda kukaa kwenye kiti kilicho pambwa na maua mazuri na mbele yake kulikuwa na meza iliyojaa kila aina ya vinywaji ila ni vile ambavyo havileweshi. Watu wakakaa kwenye viti baada ya mwenye sherehe kukaa, zikafuata ratiba nyengine. ******** Baada ya kuchukuliwa Hemedy na Koplo Taure, Mrutu hakuwa na jinsi, akawapigia simu wakina Mata, ili kuwauliza wako wapi na kuambiwa kuwa wote wawili, wapo nyumbani Mata, wanaisubiria taarifa yake ili wakakamilishe kile walichopanga. Ila Mrutu akawaambia wamsubirie hapo hapo nyumbani kwa Mata na yeye anakuja, wakamshangaa na walipomuuliza kwanini yeye aliwajibu wamsubiri tu watajua huko huko, hawakuwa na jinsi ikabidi wamsubiri. Mrutu aliwasha gari yake kwa safari ya kuelekea nyumbani kwa Mata, baada ya dakika kadhaa, ikawa tayari ameshafika, akapaki gari na kuingia ndani ya nyumba hiyo, akawakuta Mata na Moto wamekaa kwenye masofa wanamsubiri.
“Haya vipi tena, mbona tulivyopanga thivyo, thi tulipanga utupigie thimu ili thithi tuje kumalidha kadhi, haya mbona umekuja wewe huku?” Mata alimuuliza.
“Yani nahisi yule dogo umri wake wa kuishi bado ni mrefu” Mrutu aliongea.
“Kivipi sasa, embu tufafanulie” Moto aliongea.
“Yani ni hivi….” akawahadithia ilivyokuwa.
“Dah!!!! Thatha tunafanyaje?” Mata aliuliza.
“Mimi hata sijui pia tunafanyaje” Mrutu alisema.
“Yule dogo, leo ndio siku yake ya mwisho kuvuta pumvi” Moto aliongea.
“Kivipi?” Mrutu aliuliza.
“Inabidi akafe huko huko kwenye hiyo sherehe” Moto aliongea.
“Tutamuuaje, embu fafanua”Mrutu aliongea.
“Tutavamia pale pale kwenye hiyo sherehe na kumuua halafu tunaondoka zetu”
“Mmmh!!! Mbona kama vile hiyo ni njia ngumu?” Mrutu alionyesha wasiwasi wake.
“Nyie kama kwenu hiyo kazi ni ngumu basi niachieni mimi nitaifanya, chamsingi ni kuondoka sasa hivi na kuelekea huko”
“Mimi nitakuwa pamoja na wewe” Mata aliongea.
“Sawa, lakini kuna anaepajua nyumbani kwa yule Inspekta?” Mrutu aliuliza.
“Mimi napajua ndio” Mata alijibu. Baada ya kukubaliana na mpango huo, wote wakainuka na kutoka nje, wakapanga watumie gari ya Mata na dereva awe ni Mrutu ili Mata na Moto, watakapo vamia sherehe hiyo na kufanya mauaji ya Hemedy, watakapo toka waingie kwenye gari na kukimbia. Wakaanza safari ya kuelekea nyumbani kwa Inspekta Ganjo, dakika ishirini ikawa wameshafika, wakapaki gari nje ya geti la nyumba ya Inspekta Ganjo, Moto na Mata wakaweka bastola zao vizuri na kujiandaa kuelekea ndani ya nyumba hiyo ilipo sherehe ya mjukuu wa Inspekta Ganjo, ili kumuua Hemedy na Kutokomea zao.
Ndani ya nyumba ya Inspekta Ganjo, sherehe ilikuwa inaendelea kama kawaida, wakati huo ndio ulikuwa ni wakati wa kula chakula, watu wote walijipanga katika mstari mmoja kulekea sehemu iliyoandaliwa kwajili ya chakula, Hemedy na yeye alikuwa pia katika mstari huo, yeye alikuwa mtu wa mwisho kabisa kwenye huo mstari. Wakati watu wanaendelea kupata chakula, ghafla watu wote wakageuza shingo zao nyuma baada ya kuskia kishindo kama cha mtu alieanguka, walipoangalia nyuma ya mstari huo, wakapigwa na butwaa baada ya kumuona mtu wa mwisho kabisa kwenye mstari huo akigalala chini na kutulia kimya.
ENDELEA….
“Jamani msiogope, hiyo ni hali ya kawaida ambayo huyo mtu anayo, kwahiyo nyie endeleeni kupanga mstari, sisi acha tumuondoe hapo” Inspekta Ganjo aliongea hivyo huku akimfuata yule mtu aliekuwa amevaa nguo za kiulinzi, alikuwa ni mlinzi wa nyumba hiyo, alieenda kupanga mstari nyuma ya Hemedy baada ya kuona watu wote wamepanga mstari kwajili ya chakula, alikuwa ni mgonjwa wa kifafa na ndio huo uliomuangusha hapo, Inspekta Ganjo akifuatiwa na vijana wawili, wakaenda kumtoa pale alipoanguka na kumpeleka kwenye bustani ya nyumba hiyo.
Hemedy kipindi hicho alikuwa yupo mbali kidogo na mstari huo kwa hofu baada ya mtu huyo kuanguka nyuma yake, alitandwa na hofu kuu, hakujua mlinzi huyo alifika saa ngapi nyuma yake, akabaki ameduwaa tu hadi pale alipoondolewa hapo na kupelekwa kwenye bustani ya nyumba hiyo. Watu wakapanga tena mstari kwajili ya kwenda kupata chakula. kila mmoja alipopewa chakula chake, alienda kukaa kwenye kiti na kuendelea kula msosi huo. Hemedy nae ikafika zamu yake ya kupewa chakula, alipopata akaenda nacho kwenye kiti chake na kumkuta Koplo Taure na Afande Jesca wakiendelea kula chakula, naye akaka na kuanza kula.
“Dogo, kumbe uko vizuri” Koplo Taure aliongea huku akila kipaja cha kuku.
“Kwanini?” Hemedy aliuliza.
“Nimekuona pale umeruka kama mcheza kareti baada ya yule mtu kuanguka nyuma yako”
“Yani nyie acheni tu, nimeshtuka pale, almanusura moyo wangu utoke nje kwa hofu, maana kwa kile kishindo nilijua kumetua bomu la nyuklia nyuma yangu” Hemedy alijibu na kumfanya Afande Jesca atabasamu, tabasamu ambalo lilielekea cheko.
“Sasa wewe ni kipi kilichokufanya hadi ukashtuka vile” Koplo Taure alimuuliza.
“Anko wewe unadhani kile kishindo ni cha kawaida? Mimi nilidhani labda malaika mtoa roho za watu kanishukia kuja kuichukua roho yangu” Hadi hapo Afande Jesca na Koplo Taure walikuwa wanacheka kwa sauti kubwa na kufanya watu wengine wawageukie wao ila hilo halikuwafanya waache kucheka.
“Dah!! Kumbe wewe mtoto una vituko namna hii?” Afande Jesca aliongea hivyo huku akimalizia kucheka.
“Hapana sio hivyo, mimi kile kishindo ndio kimenishtua, maana nilikuwa nataka niparamie ukuta nikimbie zangu”
“Kumkimbia haiwezekani, ila ukijaribu unaweza ukafanikiwa” Wakati huku ndani watu wakiendelea na kula, kule nje wakina Moto bado wanafikiria ni jinsi gani ya kuingia humo ndani.
“Mimi nilijua tu kwamba hiii njia itakuwa ni ngumu” Mrutu aliwaambia wenzake.
“Hapana hii njia sio ngumu bali kuingia humo ndani ndio kugumu” Moto aliongea huku akiwa anaangalia ukuta wa nyumba hiyo nyumba.
“Sasa tutafanyaje?” Mrutu aliuliza.
“Subirini mimi nikaruke ukuta niingie humo ndani, maana itakuwa geti limefungwa” Moto aliongea hivyo huku akifungua mlango wa gari ili atoke, ila Mrutu akawahi kumzuia.
“Sikiliza Moto, usitake kufanya mambo ya kitoto, kumbuka hii nyumba ni ya Inspekta sasa hujui humo ndani kuna askari wangapi, usije ukaingia halafu ukashindwa kutoka, kisha ikapelekea upate matatizo wewe au sote” Mrutu alimwambia Moto.
“Sasa tufanyeje?” Moto aliongea huku akiufunga mlango wa gari vizuri.
“Hapa hakuna namna nyengine zaidi ya kuondoka, huyu dogo yupo, tutampata siku yoyote” Mrutu aliongea hivyo huku akiwasha gari.
“Basi poa twendeni” Moto alijibu kiunyonge. Mrutu aliondoa gari mahala hapo kuelekea nyumbani kwa Mata, Mrutu alikuwa bado anasita kumdhuru Hemedy, japokuwa alijua Hemedy ni tatizo kwao lakini hakupenda afe, alitamani kuwaambia wenzake wabadilishe maamuzi lakini hakujua atawanzaje, ikiwa Hemedy amepona kuawa kama hivyo, basi yeye alishukuru sana, alitamani kila siku wamkose kama hivyo ili Hemedy aendelee kuishi. Walimuacha Moto geto kwake na wao kuendelea na safari yao, walipofika nyumbani kwa Mata, Mrutu alichukua gari yake na kuondoka hapo kuelekea kwake maana usiku pia ulishakuwa mkubwa, alipofika kwake akaingiza gari ndani na yeye akaelekea moja kwa moja hadi chumbani kwake na kujitupa kitandani. “bwana eee mi siogi, kwanza nilioga ile saa kumi na mbili, sasa sahii nioge tena ili iweje” alijiwazia mwenyewe na kuvua nguo haraka haraka na kujitupa tena kitandani akiusaka usingizi. Kwa mbali aliskia simu yake ikiita kipindi hicho alikuwa ndio usingizi unamnyemelea, akainuka huku akisonya kwa kukatishwa usingizi wake usiku huo, akaichukua simu yake na kusoma jina la anaempigia“Afande Taure” jina lilosomeka hivyo, akaipokea.
“Niambie Afande” Mrutu aliongea.
“Mrutu, nilikuwa nakujulisha kwamba Hemedy hatorudi huko kwahiyo atalala huku huku”
“Anhaa!!! Basi sawa hakuna shida”
“Haya poa usiku mwema” Simu ikakatwa na Mrutu kurudi tena kitandani kuusaka usingi kwa mara nyengine, baada ya muda, akalala.
Nyumbani kwa Inspekta Ganjo, baada ya sherehe kuisha, watu walianza kuondoka mmoja mmoja kuelekea makwao, ila Hemedy yeye hakuruhusiwa kuondoka na Inspekta Ganjo akamtaka alale hapo hapo, waliobakia waliondoa ondoa viti vyote na vitu vyengine vilivyotumika kwenye sherehe hiyo, baada ya kuondoa kila kitu, wakaingia ndani ya hiyo nyumba na kila mmoja akaenda kulala, sebuleni wakabakia Hemedy, Koplo Taure, Afande Jesca, Inspekta Ganjo na Hilda.
“Hemedy” Inspekta Ganjo aliita.
“Nam! Babu” Hemedy nae aliitikia.
“Aaa!!!! Usiniite babu bwana, mimi na baba yako, baba yako alikuwa ni mkubwa kwangu, alinipita mwaka mmoja, sasa wewe utaniitaje babu, we niite baba tu, anaetakiwa kuniita babu ni huyu Hilda hapa. Unajua mimi na baba yako tulikuwa marafiki sana kipindi hicho tunasoma, tulipomaliza ‘form six’, mimi nikajiunga na jeshi baba yako akaendelea kusoma, wakati anasoma mimi huku nikaajiriwa kwenye jeshi la polisi, sikutaka kupoteza muda nikaoa, baada ya mwaka mmoja nikapata mtoto wa kike, mtoto huyo alipozaliwa, uzao wake ukaondoka na maisha ya mke wangu, nikabakia na mwanangu ambae niliachiwa na mke wangu, sikutaka tena kuoa mke mwengine, nikaamua nimlee mwanangu.
Baba yako alipomaliza chuo, akaajiriwa kwenye bandari, nikamshawishi aowe ila yeye akajifanya m’bishi, mwenyewe alidai hadi ajiajiri mwenyewe, baada ya miaka tisa ya kuajiriwa bandarini ndipo alipofungua miradi yake na yeye ndio akaoa, wakati huo mimi mwanangu alikuwa na miaka kumi na nane. Baada ya miaka miwili mbele, baba yako na mama yako, ndipo walipo kupata wewe, na mimi mwanangu katika kurukaruka kwake, akapata mimba, na yeye baada ya kumzaa huyu(akamuonyeshea kidole Hilda) na yeye akafa kama mama yake baada ya kujifungua, kwahiyo hapa nimebakiwa na huyu mjukuu wangu ndio kila kitu kwangu, nampenda kama ninavyojipenda mimi”
Inspekta Ganjo baada ya kutoa historia fupi ya maisha yake yeye na Mzee Mheshimiwa, akawaambia Hemedy na Hilda kuwa wao ni ndugu japokuwa hawakutoka katika ukoo mmoja yani undugu huo umeunganishwa kwa urafiki wa wazazi wao. Akawaambia wapeane mikono ishara ya kufahamiana, Hemedy na Hilda walipeana mikono kwa sekunde tano na kila mmoja akaachia mkono wa mwenzake, kwakuwa muda ulikuwa umeenda sana, ikabidi Koplo Taure na Afande Jesca waage na kuondoka zao, wakawaacha Inspekta Ganjo, Hemedy na Hilda wakiendelea na stori, Hemedy alipopata nafasi ya kuongea basi aliwachekesha na kuwafanya hata wasahau kama huo ni usiku wanahitajika wakalale, baada ya kukaa sana sebuleni hapo ikabidi Hemedy aonyeshwe chumba cha kulala na kila mmoja akaingia katika chumba chake kwajili ya kwenda kuitafuta kesho yake.
* * * *
Siku iliyofuata Inspekta Ganjo, aliinuka kama kawaida yake saa kumi na mbili na nusu, akajiandaa kwenda kazini, baada ya kumaliza kujiandaa, akaingia chumba alicholala Hemedy na kumkuta bado akiwa amelala, aliishia kutabasamu tu baada ya kukumbuka vituko vya Hemedy, akafunga mlango na kuwaendea wafanya kazi wa nyumba hiyo, akawaachia maagizo flani flani na kuondoka zake.
Kange. 7:17 Mchana.
“Kwa huu muda tulio waacha unatosha kabisa kulipiza kisasi, nahisi wanadhani tumewaogopa kwa kile walicho tufanyia, sasa ni hivi muda wowote ule tutakapo waona popote pale, lazima walipe kwa walicho tufanyia” Kijana mmoja mwenye macho ya paka aliongea kuwaambia wenzake wawili.
“Doze, unajua kwamba wale watu wana kundi kubwa?” Kijana mwengine mwenye mwili mwembamba alimuambia kijana wa mwanzo kuongea mwenye macho ya paka, alietajwa kwa jina la Doze.
“Haaa!! Kwahiyo Tosh na wewe unawaogopa wale wapumbavu?” Doze alimwambia kijana wa pili kuongea alietajwa kwa jina la Tosh.
“Hapana, si maanishi hivyo” Tosh aliongea.
“Sasa maana yako ni ipi? Wakati tayari ushaonyesha uoga juu ya wale wajinga” Doze alisema.
“Mimi nilikuwa namaanisha kwamba, tusiwaingilie hovyo hovyo, tunaweza tukageukiwa sisi kama siku ile” Tosh aliongea.
“Hapo nimekupata, nilidhani na wewe tayari ushaanza kuwaogopa wale wajinga”
“Wale hawatusumbui tena, bora tayari tumepajua sehemu wanayopenda kwenda kunywa, tutawafuata na kuwaulia mbali tu”
“Hapana, wale hatuwaui kwanza, wale tunawateka halafu tunawaambia wampigie simu bosi wao, aturudishie pesa zetu la tunawaua watu wake, sasa akisharudisha pesa zetu ndio tutajua tuwaue au tuwaache” Kijana mwengine wa tatu, aliekuwa kimya muda wote, alienyoa para na kufanya chogo lake litokeze kwa nyuma, nae akaongea.
“Kiku, unauhakika tukiwateka wale watu, yule mzee ataturudishia pesa zetu?” Tosh aliuliza.
“Lazima arudishe, kwasababu yule mzee wale watu ndio watu wake anaowategemea kwa kila kitu, kwahiyo lazima arudishe tu”kija mwenye chogo, alietwa Kiku alijibu.
“Halafu sikutegemea kama yule mzee anafanya biashara zile” Tosh alisema.
“Sasa hivi hakuna kumuamini mtu, watu wengine wanafanya wema kwa watu ili kulinda maovu yao yasigundulike, sasa wewe unadhani ni nani amabe ukimwambia kuwa mzee yule anafanya biashara kama ile ambayo serikali inaipiga vita kila siku, atakubali, hakuna ambae atakae kuamini hata kidogo” Kiku alisema.
“Kwahiyo hii ishu tunaianza lini?” Doze aliuliza.
“Ikiwezekana ianze leo, hamjui tu jinsi gani ninauchungu wa kuchukuliwa pesa zetu na mzigo wao, hawajui zile pesa sisi tumezitoa wapi, halafu wao wanakuja kuzichukua kirahisi rahisi tu” Kiku aliongea kwa uchungu.
“Kama ni hivyo fresh, itabidi leo tukawatege pale kwenye ile club wanayopenda kwenda kunywa, lazima tuwatie mikononi tu” Tosh aliongea.
“Kama ni hivyo hakuna noma, acha kwanza mimi niwaache, kuna demu mmoja naenda kumshuhulikia mara moja, kwahiyo tutakutana baadae” Kiku aliongea huku akiinuka kwenye sofa alilokaa.
“Oya Kiku, angalia lakini huyo demu asije akakulegeza, ukashindwa kuifanya hii ishu baadae” Doze alimwambia hivyo huku akicheka.
“Usijali, naenda kupunguza maji kidogo tu, maana mwili wangu nahisi kuna uzito umeongezeka” Kiku aliongea hivyo huku akiufunga mlango wa nyumba hiyo.
Nyumbani kwa Inspekta Ganjo. 11:09 Jioni.
Hemedy baada ya kushinda kwa kutwa nzima nyumbani kwa Inspekta Ganjo, akataka kuondoka ili aelekee nyumbani kwao, lakini aliekewa pingamizi kubwa na watu waliokuwepo kwenye hiyo nyumba ya Inspekta Ganjo la kuondoka hapo, kila mmoja akataka abaki hapo hapo, kwa jinsi walivyo muhusudu kwa muda waliokaa nae, aliwachekesha, aliwafurahisha kwa kila namna, alifanya wampende ghalfa kutokana na uchesi wake, lakini nae akasimamia msimamo wake kuwa ni lazima aondoke hapo aelekee kwao, baada ya kumlazimisha sana, akakubali kubaki, lakini akawaambia kwamba ni lazima aongee na baba yake mdogo ili nae ajue atasema nini kuhusu kubaki hapo hadi wikiendi itakapo isha. Wakampigia simu Inspekta Ganjo, wakamuambia kuwa wanataka kubaki na Hemedy nyumbani hapo hadi kesho yake ndipo aondoke, Inspekta Ganjo akawakubalia, wakamuambia kuwa Hemedy amesema anataka kupata ruksa ya baba yake mdogo kuhusu kubaki hapo. Inspekta Ganjo nae akamwambia Koplo Taure ampigie simu Mrutu aongee nae kuhusu ombi la Hemedy, Koplo Taure nae akampigia simu Mrutu na kumuambia alivyoambiwa na Inspekta Ganjo, Mrutu hakuwa na pingamizi akamkubalia Hemedy akae hapo hadi kesho yake. Koplo Taure akarudisha majibu kwa Inspekta Ganjo na Inspekta Ganjo nae akamruhusu Hemedy akae nyumbani kwake hadi hapo kesho.
Walifurahi baada ya kuruhusiwa kubaki na Hemedy hadi hapo kesho, ikabidi mfanya kazi mmoja wa kiume anaempeleka na kumrudisha Hilda shule, achukue gari na kuenda na Hemedy hadi nyumbani kwa Mrutu, walipofika Hemedy aliingia ndani chumbani kwake, akaoga na kubadilisha nguo, baada ya hapo alirudi tena kwenye gari na safari ya kurudi nyumbani kwa Inspekta Ganjo ikaanza.
Hobours Club. 4:30 Usiku.
Tito na Tobi, walienda kwenye club hiyo walioyozoea kuenda kunywa hapo, wakaenda kwenye meza iliyokuwepo gizani kidogo na kukaa, waliagiza pombe na kuanza kunywa mdogo mdogo huku wakiendelea na stori zao. Kwenye meza nyengine iliyokuwa mbali na meza waliyokaa wakina Tito, kulikuwa kuna watu watatu wamekaa wakiwaangalia wao.
“Sasa tunafanyaje, windo letu lilepale tayari limeshafika” Tosh aliongea kuwaambia wenzake.
“Tusiwe na wasiwasi, tusubirini kwanza kama lisaa limoja, walewe ndipo tutakapo enda kuwateka” Kiku aliongea. Baada ya kukubaliana hivyo, wakawaacha wakina Tito kwa lisaa limoja ndipo wakawateke. Baada ya kuwasubiri sana, ndipo walipoamua wawafuate na kuwateka. Doze na Kiku, waliinuka na kuwaendea wakina Tito kwenye meza yao, walipofika wakachomoa bastola zao na kila mmoja akamuekea mtu wake bastola ya mbavu, Doze alimuwekea bastola ya mbavu Tito na Kiku alimuwekea bastola Tobi.
“Mnatakiwa mtulie hivyo hivyo, mkifanya ujinga wowote, basi bastola hizi zitatawanya mbavu zenu” Kiku aliwaambia, alipoona wametulia akaendelea.
“Haya wekeni bastola zenu juu ya meza na msifanye ujinga wowote utakao mfanya malaika mtoa roho, aje hapa ikiwa mwenyewe amepumzika huko juu kwa mungu” Kiku aliwaambia hivyo, Tito na Tobi wakazitoa bastola zao na kuziweka juu ya meza, Doza akazichukua na kuzichomeka kiunoni kwenye jinzi yake aliyoivaa.
“Haya inukeni taratibu kabisa, kumbukeni kosa moja la mmoja wenu linaweza likamshababishia na mwenzake kifo, kwahiyo tunaomba mtulie na mfuate tunachotaka, haya inukeni taratibu” wakainuka na kusubiria amri nyengine, kipindi hicho Tito alikuwa anatafuta mbinu ya kujinasua kutoka kwa hao watu wasio wajua.
“Haya, tunaanza kuondoka taratibu, kama vile marafiki kumbe ni maadui wakubwa tu, kumbukeni kosa moja litawagharimu maisha yenu” Kiku aliendelea kuwaonya, wakaanza kutembea taratibu, ila baada ya kupiga hatua mbili mbele, ghafla…..
“Haya, tunaanza kuondoka taratibu, kama vile marafiki kumbe ni maadui wakubwa tu, kumbukeni kosa moja litawagharimu maisha yenu” Kiku aliendelea kuwaonya, wakaanza kutembea taratibu, ila baada ya kupiga hatua mbili mbele, ghafla Tito akajaribu bahati yake ya kutaka kujiokoa, akamsukuma Doze, na kwakuwa Doze hakujiandaa na tukio hilo, akajikuta akipepesuka na kwenda hadi chini na bastola aliyoishika ikaanguka mita chache mbele yake, Tito alivyotaka kuiwahi, akajikuta akitulizwa na ngumi moja ya pua, akanza kuona mawenge, akahisi kama vile kuna kimiminika kikitoka katika pua zake na churuzikia mdomoni mwake, hakujua ni nini hadi pale alipopeleka mkono wake puani akagusa kidogo na kuuangalia, na kukuta ni damu ndio ambayo inatoka katika pua yake, akataka kujua ni nani huyo aliefanya hivyo, ndipo hapo alipotupa macho yake mbele yake na kumuona mtu mwengine tofauti na wale wawili waliowateka. Tosh akaiyokota bastola iliyoanguka na kumpa Doze bastola yake na yeye akaondoka hapo kuelekea nje kwenye gari lao na kuingia humo. Doze na Kiku, waliwaongoza wakina Tito kama vile hakuna kitu kinachoendelea, watu wengine waliokuwepo hapo club wala hawakujua kwamba watu hao wana kitu wanafanyiana, walitoka nje ya club hiyo na kuelekea kwenye gari lao walilokuja nalo, wakatoa kamba ngumu na kuwafunga wakina Tito mikono yao kwa nyuma, kisha wakawaingiza kwenye gari.
“Nyie si mlikuwa mnajifanya wajanja kututapeli pesa zetu na mkaondoka na mzigo wenu? Haya sasa tutauona ujanja wenu, lazima mtalipa tu kwa mlio tufanyia” Kiku aliongea hivyo na kumuambia Tosh aondoe gari kuondoka hapo na kutokomea kuelekea wanapopajua wao, hadi hapo wakina Tito wakawa tayari wameshajua walio wateka ni wakina nani. Baada ya dakika ishirini, wakafika katika jumba moja lililochoka ila lilikuwa na milango na madirisha yake, wakawaingiza humo na kuwafungia kwenye viti vilivyokuwepo humo humo ndani, wakawafunga kwa kamba ngumu kiasi ambacho zile kamba zikawa zinawaumiza kwa jinsi zilivyokazwa.
“Kuanzia sasa nyumbani kwenu patakuwa ni hapa, kwahiyo tunamiomba mufurahie maisha mapya” Tosh aliongea hivyo huku akiwacheka.
“Tosh, embu tuwasachi hawa, huwenda wakawa na kitu chengine cha kujitetea” Doze aliongea hivyo huku akiwafuata, aliwapekuwa kila sehemu na kutoa visu,sigara, pesa na simu zao na kuvitia mfukoni mwake.
“Ok, mnaweza mkapiga stori wenyewe kama mtapenda kufanya hivyo” Kiku aliongea. Baada ya kuhakikisha wamewaweka katika hali ambayo hawezi kujinasua hapo, wakaondoka na kutokomea zao wanapopajua wao.
“Oya Tito, tunafanyaje ili kujiokoa hapa?” Tobi alimuuliza Tito huku akijaribu kujitingisha aone kwamba anaweza kutoka hapo alipo fungwa ila aliishia kujiumiza tu na hizo kamba alizofungwa nazo.
“Hapa hatuwezi kutoka, tusubirie tu tuone watatufanya nini” Tito aliongea hivyo huku akitafuta pozi la kujiweka vizuri, maana alisikia maumivu mara mbili, maumivu ya kukazwa na kamba na maumivu ya pua yake iliyoadhibiwa na Tosh. Kwakuwa hawakuwa na la kufanya, wakabaki wametulia tu.
Siku iliyofuata. Kituo cha Polisi Mabawa. 3:00 Asubuhi.
“Unakumbuka nimekupa muda gani wa kukamilisha ule upelelezi kuhusu kupotea kwa watoto mitaani?” Inspekta Ganjo alimuuliza Koplo Taure.
“Ni wiki tatu Mkuu” Koplo Taure alijibu.
“Umefikia wapi hadi sasa hivi katika upelelezi wako?” Inspekta Ganjo alimuuliza Koplo Taure swali ambalo hakujua alijibu vipi, maana hakuwa amefikia popote katika kupeleleza chanzo cha kupotea kwa watoto mitaani.
“Mkuu, lakini si umenipa muda wa kupeleleza? Subiri muda ukifika halafu ukiona sikuletei majibu ndio uniulize” Koplo Taure alijitutumua na kujibu hivyo, japokuwa hakutakiwa kumjibu hivyo mkuu wake, lakini hakuwa na jibu la kumpa litakalo mridhisha mkuu wake. Inspekta baada ya kusikia jibu Koplo Taure, alitabasamu tu.
“Najua hujafika popote katika upelelezi wako ndio maana ukanijibu hivyo”
“Hapana Mkuu, hukutakiwa kuniuliza sasa hivi, ungeniuliza baada ya ule muda ulionipa kuisha, halafu ikiwa sijakuletea ripoti zozote”
“Nikuulize swali?” Inspekta Ganjo alimdhihaki Koplo Taure kwa kumuuliza hivyo, eeeee!!! alimdhihaki kweli, kwasababu tangia mwanzo alimuuliza maswali pasi na kumuuliza kwamba amuulize swali, ikiwa hilo lenyewe pia lilikuwa ni swali.
“Ndio Mkuu” Koplo Taure alijibu kwa unyenyekevu.
“Niliwahi kukupa kesi ya kupeleleza vifo vya familia ya Mzee Mheshiniwa, baada ya siku mbili, nikakuuliza swali hili hili ambalo leo umejifanya umelitolea sababu, labda nikukumbushe kidogo, nilikuuliza umefikia wapi katika upelelezi wa vifo vya familia ya Mzee Mheshimiwa, wewe kunajibu ukanipa, unaweza kulikumbuka lile jibu ulilonipa?”
“Ndio nalikumbuka” Koplo Taure alijibu.
“Ulini jibu vipi?”
“Nilikuambia kuwa, sijui nianziea wapi”
“Eeeewalaa!!!! Hivyo hivyo hujakosea. Sasa mbona leo hii nakuuliza swali kama lile la siku ile halafu wewe unanijibu kuwa bado muda wa kukuuliza swali hilo?”
“Mkuu, kumbuka lakini siku ile hukunipa muda wa kuukamilisha ule upelelezi, lakini kwenye kesi hii ya kupotea kwa watoto mitaani, umenipa muda” Koplo Taure alijibu kiunyenyekevu, maana alijua kuwa Mkuu wake tayari ameshakasirika kwa lile jibu alilompa.
“Anhaaa!!! Naona leo umetumia akili sana kujibu maswali yangu, ungekuwa hiyo akili unayoitumia kujibu maswali yangu, ungeitumia kwaajili ya upelelezi, naamini ungekuwa unafanikiwa katika kazi zako na pia kama cheo pia ushapandishwa” Inspekta Ganjo alimdhihaki Koplo Taure kwa maneno ya kejeli kama hayo, Koplo Taure alichukia lakini hakuwa na jinsi, kwavile aliemuambia hivyo ni mkuu wake, akabaki kimya tu.
“Ok, acha nikupe mwanga kidogo, mchunguze Mr Bakari Haneni nyendo zake, kuanzia safari zake na kila anachokifanya…. Unaweza kwenda kuendelea na mapumziko yako, nakutakia jumapili njema” Inspekta Ganjo, alivyomuambia hivyo Koplo Taure, akamruhusu aende, Koplo Taure akainuka na kukakamaa kwa heshima kisha akaanza safari ya kuondoka katika ofisi ya mkuu wake, alipoufikia mlango, akaskia ameitwa, akageuka na kumuangalia Inspekta Ganjo.
“Kuwa makini na huyo mtu unaeenda kumfuatilia, ila baada ya muda niliokupa nahitaji ripoti kamili kuhusu kesi niliokupa ya kuifuatilia” Alipo muambia hivyo, akavuta faili lililokuwa mezani kwake na kuanza kulipekuwa pekuwa, Koplo Taure alivyoona hivyo, akafungua mlango na kuondoka kituoni hapo kuelekea nyumbani kwake, alipofika akapitiliza hadi kitandani na kulala chali akiangalia dari la chumba hicho.
“Kwanini ameniambia nimchunguze Mr Bakari Haneni? Na kwanini ameniambia niwe makini… hapo ndipo ninapoamini kuwa Mr Bakari Haneni sio mtu mzuri japokuwa anaoneka ni mtu mzuri, nikiunganisha na tukio la wale watu niliowaona kule club na walipoingia kwenye nyumba ya Mr Bakari Haneni, Hahahah!!! nimetumia akili sana kuwafuatilia wale watu japokuwa mkuu yeye anaona mimi sifanyi kazi kwa ufasaha, acha nisijiumize sana kichwa kwa kufikiria, nitaanza kumchunguza kesho” alijiwazia mwenyewe na kuchukua simu yake, akaingia upande wa majina, alipolipata jina analotaka kulipiga, akapiga.
“Haloo” sauti tamu ya kike ikaskika kwenye spika za simu ya Koplo Taure.
“Duh!!! Hivi kweli kwa sauti hii, inaweza ikamuhoji muhalifu na ikampa majibu yote inayo muuliza?” Koplo Taure aliongea.
“Hahaah! Kwanini?”sauti ya upande wapili ikacheka halafu ikauliza.
“Unataka kujua kwanini nimesema hivyo?” Koplo Taure aliuliza kwenye swali.
“Ndio”sauti ikajibu.
“Basi njoo nyumbani kwetu mara moja” Koplo Taure aliiyambia sauti iliyotoka kwenye simu yake.
“Poa, nakuja sasa hivi” sauti ilijibu na simu ikakatwa, Koplo Taure akaisubiri sauti aliyoongea nayo ije nyumbani kwake. Baada ya nusu saa, sauti ilibisha hodi katika geti la nyumba yake, akatoka nje haraka haraka ili kwenda kuiwahi sauti isije kuondoka, baada ya kulifikia geti lake, akalifungua na kuonekana mtu mwenye sauti iliyoongea kwenye simu. Alaaa!! Kumbe alikuwa ni Afande Jesca ndio mwenye sauti ile nzuri iliyoskika kwenye simu ya Koplo Taure, wakaingia wote hadi chumbani kwa Koplo Taure.
“Mkuu leo kanipa kazi nyengine ya kumfuatilia Mr Bakari Haneni” Koplo Taure aliongea huku akikaa kitandani.
“Ana nini nae?” Afande Jesca aliongea huku akikaa kitandani karibu ya Koplo Taure.
“Sijui, ila kaniambia nimchunguze tu”
“Huenda ikawa kuna kitu amekiona kwake”
“Labda” Koplo Taure aliongea hivyo huku akipitisha mkono kwenye kiuno cha Afande Jesca.
“Unataka kufanya nini wewe mwanaume?” Afande Jesca alimuuliza baada ya kuona mkono wake ameupeleka kwenye kiuno chake.
“Hujui ninachokitaka kukifanya?” Koplo Taure aliongea hivyo huku akimlaza kitandani.
“Aa aa!!! Sentaure kwa leo haitowezekana” Afande Jesca aliongea hivyo huku akimtoa Koplo Taure alieanza kumlalia kwa juu.
“Kwanini?”
“Nipo katika siku” Koplo Taure baada ya kusikia hivyo, aliishiwa pozi na kujiweka kando, akamuangalia Afande Jesca kwa jicho la “una bahati, maana leo nilivyo kupangia” akayapeleka macho yake juu na kuangalia dari la chumba hicho. Alitahayari! ****** Muda wa jioni, nyumbani kwa Inspekta Ganjo, Hemedy alijiandaa kuondoka katika nyumba hiyo ili alelekee nyumbani kwao, lakini bado watu wa hapo walitaka aendelee kuwepo kwajinsi walivyo mzoea kwa muda mfupi, ila ndio hivyo sasa hawakuwa na jinsi ikabidi wamruhusu aondoke, mfanyakazi wa kuendesha gari akajiandaa kumpeleka Hemedy kwao, na kila kitu kilipokamilika Hemedy akaenda kwenye gari na kukaa tayari kwa safari, mara ghafla Hilda nae akaja mbio mbio kutokea ndani akataka na yeye amsindikize Hemedy nyumbani kwao, hakuna ambae alim’bishia, wakamruhusu na yeye kupanda, akakaa siti za nyuma, ikabidi Hemedy na yeye ahamie siti za nyuma alipo kaa Hilda, Hilda akaishia kutabasamu tu baada ya kumuona Hemedy amekuja kukaa siti za nyuma.
Safari ikaanza ya kumpeleka Hemedy nyumbani kwao, huku nyuma aliwaacha wafanyakazi wa Inspekta Ganjo na huzuni nyingi sana kwa kuondoka kwake, walishamzoea kwa muda mfupi waliokaa nae, aliwafurahisha kwa vituko vyake na kufanya watamani kukaa nae pamoja kila siku, ila ndio hivyo hawakuwa na jinsi, walimuacha aende. Baada ya dakika kadhaa walifika nyumbani kwa Mrutu na kumuacha Hemedy akashuka kwenye gari na kumfanya dereva ageuze gari ili warudi nyumbani kwao. Hilda alihuzunika sana kuchana na Hemedy, alitamani hata kumuambia babu yake kuwa amuombe Hemedy waishi wote nyumbani kwao, ila akajua hata akimwambia ombi lake halito kubaliwa, kwasababu Hemedy anaishi na baba yake mdogo, akabaki akimpungia mkono na Hemedy akampungia mkono, wakaagana hivyo na Hemedy akaingia ndani ya nyumba yao.
Katika jumba walilofungia wakina Tito. 3:25 Usiku. Tosh na wenzake, waliingia kwenye hilo jumba baada ya kuwaacha wakina Tito kwa siku nzma bila ya kuwaletea chakula, walipoingia katika chumba hicho, waliwakuta wakiwa wamechoka, shingo zao wamezilaza kwenye mabega yao, haikujulika ni kwaajili ya uchovu wa kutulia sehemu moja au ni njaa. Tosh akawaendea hadi mbele yao na kuwainua shingo zao, akawaangalia kwa sekunde kadhaa halafu akawaachia na kurudi nyuma kidogo waliposimama wenzake.
“Kitakacho miokoa hapa ni kitu kimoja tu, tunataka kuongea na bosi wenu aturudishie pesa zetu ndipo na sisi tutakapo miachia, kwahiyo sasa hivi nataka mnitajie namba za bosi wenu ili tumpigie” Tosh aliongea ivyo huku akitoa simu tayari kuandika namba zitakazo tajwa.
“Haya, mmoja wenu anitajie haraka hizo namba” Tosh aliongea hivyo lakini hakuna hata mmoja kati ya hao wawili alietaja hizo namba, ikabidi arudie tena kuwaambia kuwa wataje namba za bosi wao lakini hakuna hata mmoja aliethubutu kunyanyua mdomo wake kutaja namba za Mr Bakari Haneni.
“Kumbe nyie jeuri eee, basi hiyo jeuri yenu itakwisha sasa hivi” Tosh alipoongea hivyo akachomoa bastola yake na kuwaelekezea. “Paaa!!! Paaaa!!! Milio ya risasi ilisikika na kuwafanya wakina Doze kushtuka, Tito na Tobi wakaachia tabasamu lililo mshangaza Tosh…
“Mnacheka nini nyie wajinga?” Tosh aliwauliza wakina Tito waliotabasamu baada ya kuwaona Doze na Kiku walivyoshtuka baada ya Tosh kupiga risasi pembeni ya kina Tito.
“Sio kwamba nimewakosa kwa bahati mbaya, hapana mimi huwaga sikosagi ninapotaka kutoa uhai wa mtu na risasi, nimefanya hivyo kwa makusudi ili niwaonyeshe kuwa hii bastola niliyoishika ina risasi nyingi tu, kwahiyo kama naamua kumiua nina miua bila tabu, sasa narudia kwa mara ya mwisho, mnataja namba ya bosi wenu ama hamtaki kutaja? Na msipotaja kwa amani basi mjue mtataja kwa maumivu, si shindwi kutumia nguvu bale inapobidi” Tosh aliwachimba mkwara wakina Tito. Bado wakina Tito waliendelea kuweka ngumu, hawakutaka kutaja namba ya Mr Bakari Haneni, haikujulikana kwamba wanategeana kutaja au wameamua wasiitaje kwa ujeuri. Wote wawili walikaa kimya.
“Naona sasa, mmependa nitumie njia nyengine tofauti na ile ya amani niliowapa. Ok sio mbaya kwavile nyie ndio mnavyotaka basi subirini nitumie njia mnayoitaka” Tosh alioongea hivyo, akatoka humo ndani, baada ya dakika mbili akarudi na kifaa flani cha kutobolea mbao za madirisha kwajili ya kuweka nondo, mimi jina lake limenitoka kidogo, nadhani hadi hapo itakuwa ushakijua hicho kifaa.
Akaenda nacho hadi mbele yao na kusimama nacho, wakina Tito hawakujua Tosh anataka kuwafanya nini na wakina Doze pia hawakujua Tosh anataka kuwafanya nini mateka wao, wakakaa kimya waone kitakachoendelea.
“Si mmekataa kutumia njia ya amani? Sasa subiri nitumie njia ambayo mmeichagua nyie” Tosh baada ya kuongea hivyo, akamuita Kiku hapo mbele na kumuambia aushike mkono wa Tobi vizuri sehemu ya kiganja chake. Kiku akakishika kiganja cha mkono wa Tobi kwa nguvu, maana Tobi alikuwa analeta tabu, baada ya kuhakikisha kiganja kimenyooka vizuri, Tosh akasogea karibu na Tobi na kukikita kile kifaa cha kutobolea matundu kwenye mbao za dirisha, akakikita kwenye kiganja cha Tobi.
“Subiri nikutoboe wewe kidogo, maana mwenzako nilimpa adhabu kule club alipotaka kuleta unja wake wa kike, nataka huu mkono wako wa kulia niutoboe tundu katikati ili hatakama utakapotaka kula chakula, basi kitokee kwenye hili tundu” Tosh aliongea hivyo huku akianza kukizungusha kile kifaa kwenye kiganja cha Tobi, mwanzo alivumilia ila baada ya maumivu kukolea, akapiga kelele za kuomba msamaha.
“Hapana usiniombe msamaha mimi, omba msamaha kiburi chako kilichokufanya ukae kimya kutaja namba za bosi wako” Tosh aliongea hivyo huku akiendelea kukizungusha kile kifaa kwenye kiganja cha Tobi hadi damu zikaanza kutoka lakini hilo halikumfanya Tosh aache kukizungusha kile kifaa.
“Basiiiiiiiii, achaaaaaa, natajaaaaa, natajaaaa, achaaaaaa!!” Tobi alipiga kelele baada ya maumivu kumfikia hadi kwenye moyo, ikabidi Tosh aache kukizungusha kile kifaa.
“0652358545, Aaaaaaaahh!!!!” Tobi alitaja namba ya bosi wake haraka haraka huku akiwa bado ana maumivu kwenye kiganja chake.
“We fala hebu rudia tena kuitaja hiyo namba, usiitaje kama vile nimekulazimisha kuitaja” Tosh aliongea hivyo huku akiitoa simu yake mfukoni tayari kuandika namba zitakazo tajwa na Tobi. Tobi akazirudia tena kuzitaja namba za Mr Bakari Haneni kwa utaratibu kabisa huku akigugumia kwa maumivu.
“Huoni sasa namba umezitaja kwa njia ya maumivu, wakati nilikupa njia ya amani kabisa, aah!!! Lakini sikulaumu sana kwasababu hiyo ndio njia ulioipenda” Tosh aliongea hivyo, akawageukia wenzake na kuwaangalia kwa macho ya (tufanye nini sasa maana namba tunazo) wenzake wakamuelewa na kumpa ishara ya kuzipiga hizo namba, Tosh akazipiga hizo namba na simu ilipo anza kuita,akaiweka sauti ya nje.
“Haloo” Sauti nzito ya upande wapili ilinguruma kwenye spika za simu.
“Naongea na tajiri mwenye roho nzuri mbele za watu kumbe ni mmoja wa watu anaechangia kuwaharibu vijana kwa kuwauzia madawa ya kulevya?” Tosh alimuuliza hivyo huyo mtu wa upande wa pili, moja kwa moja akajua kuwa anaongea na Mr Bakari Haneni ndio maana akaongea hivyo, mtu wa upande wa pili alikaa kimya kama sekunde ishirini.
“We ni nani?” mtu wa upande wa pili aliongea.
“Unaongea na mtu mwenye akili nyingi kuliko wewe uliowatuma vijana wako wapumbavu kuja kutupora pesa zetu na kuondoka na mzigo wenu”
“Unataka nini kwangu? Na vijana wangu unao hapo?” Mr Bakari Haneni aliongea kwa hasira.
“Mmh mmh!!!!! Tuliza hasira zako wewe mzee, ninachotaka mimi, uturudishie pesa zetu na mzigo wetu, vitu ambavyo vijana wako waliondoka navyo vyote baada ya kutaka kufanya biashara” Tosh aliongea hivyo.
“Yeah, nipo nao hapa tuna piga stori” Tosh aliongea hivyo huku akiwaangalia wakina Tito walioyokuwa wanayafuatilia maongezi hayo.
“Embu wape simu niongee nao”
“Ohooooo!! Kumbe unataka kuongea na vibaraka wako? haya hawa hapa” Tosh alimpa simu Tobi aliekuwa bado anagugumia kwa maumivu.
“Mkuu, tusaidie kwa njia yoyote, tunateseka huku” Tobi aliongea baada ya kuwekewa simu karibu na mdomo wake.
“Mko wapi, mko sehemu gani?”
“Mkuu, wasikilize wanachotaka, tunateseka huku” Tobi baada ya kuongea hivyo, Tosh akaiondoa simu na kuendelea kuongea yeye.
“Ok, utatupa mizigo yetu au tuwapoteze vijana wako?”
“Hapana, msifanye hivyo, nitamipa pesa zenu” Mr Bakari Haneni aliongea.
“Sio pesa tu na tunataka na yale madawa”
“Sawa, sasa nitamipatia vipi hivyo vitu mniachie vijana wangu?”
“Kesho saa tisa alasiri, njoo pekeako karibu na chuo cha Utumishi kilichopo huku kange, baada ya hapo tutakupa maelekezo ya nini ufanye ili kutupatia mizigo yetu” Tosh alimuambia.
“Hapana mimi sitoweza kuja, kuna safari nataka kwenda, kwahiyo sitopata muda wa kuja huko, ila nitatuma vijana wangu waje” sio kwamba Mr Bakari Haneni ana safari kama alivyosema, laa hashaa!!! Hakuwa na safari ya aina yoyote ila alikuwa na uoga na watu hao asio wajua.
“Pia sio mbaya, ila kama utatuma vijana wako basi wasizidi wawili, tafadhali zingatia maelekezo ninayokupa, ukifanya kinyume na haya maelekezo basi ujue utajuta, na ninakuambia tena utajuta wewe na kundi lako”
“Sawa, hakuna shaka nitafanya kama mnavyotaka, ila nanyie msije mkatugeuka, kwasababu hata mimi sishindwi kufanya chochote kibaya juu yenu, kwahiyo naomba tufanye makabidhiano ya amani” Mr Bakari Haneni na yeye aka kaza ili asionekane kwamba amewaogopa watu hao.
“Hahahahaha!!! Mzee unaoneka unajiamini sana, ok, sio mbaya ndio inavyotakiwa, tumekuelewa na wewe pia usije ukatugeuka kwasababu na sisi hatushindwi kufanya chochote kibaya juu yako na watu wako, sasa utafanya kama tulivyo kuagiza, usiku mwema” Tosh baada ya kuongea hivyo akakata simu na kuwageukia wenzake.
“Tayari tumeshamaliza, kwahiyo tuwapeni chakula hawa mbwa wale, maana inavyooneka wana njaa sana” Doze akafungua begi alilokuja nalo na kutoa mifuko miwili iliyokuwa na chakula ndani, Tosh akawanyooshea bastola na kumuambia Kiku awafungue kamba walizo wafunga ili wapate kula, Kiku akawafungua na kuwafanya wakina Tito wawe huru, mistari ya kukazwa na kamba ilionekana kwenye miili yao sehemu waliyofungwa na kamba hizo, baada ya kufunguliwa kwenye viti hivyo walisimama juu ili kunyoosha miili yao iliyokaa kwa siku nzima bila kujigeuza upande wowote.
Tosh alikuwa bado amewanyooshea bastola kwaajili ya kuwalinda wasifanye kitendo chochote cha kipuuzi, walipojinyoosha wakakaa tena kwenye viti, ndipo Kiku alipo wapa mifuko yenye chakula kila mmoja wake, wakaifungua na kukuta ni wali na nyama ya kuku, walianza kula hata kabla hawaja nawa kwa jinsi walivyokuwa na njaa, Tobi yeye alitumia mkono wa kushoto kula, kwasababu mkono wake wa kulia ulikuwa umeadhibiwa kwa kuchomwa na kile kifaa cha kutobolea mbao za madirisha, walikula haraka haraka kutokana na njaa ilivyo washika.
Kiku akawatolea maji safi na kuwapa kila mmoja chupa yake, walikula hadi wakashiba na kushushia na maji waliyopewa, baada ya kumaliza kula kila kitu, wakafungwa tena kamba ila safari hii hazikukazwa sana kama mwanzo ila zilifungwa kwa uangalifu mkubwa.
“Ok, mtalala kwenye hii nyumba yenu mpya kwa usiku huu wa mwisho halafu kesho ndio mtajua hatma yenu, usiku mwema waungwana” Tosh aliongea hivyo na kutoka na wenzake katika chumba hicho walichowafungia wakina Tito na kutoka nje kwenye jumba hilo.
“Sasa tukishapata mizigo yetu halafu tunafanyeje?” Doze aliuliza huku akifungua mlango wa nyuma wa gari na kuingia ndani.
“Kama watakuja kiwema, itakuwa haina haja ya kuwaletea tabu ila kama wakitaka mapambano itabidi tupambane nao” Kiku aliongea huku akikaa siti za mbele upande wa abiria.
“Itabidi iwe hivyo, hatuto jali kama ana kundi kubwa au laa” Tosh aliongea hivyo huku akiondoa gari kwenye jumba hilo na kutokomea zao walipo pajua wao.
**************************
Siku iliyofuata. Nyumbani kwa Mata 1:30 Asubuhi.
“Mnajua kila siku tunavyomuacha huyu dogo ipo siku anaweza kutuumbua” Moto aliongea na kuwaambia wenzake.
“Thatha njia za kumuulia kila thiku ndio dhina shindikana, yani kila tukipanga vinatokea vikwadho, hadi nashindwa kuelewa tutumie njia gani ambayo haitoshindikana”
“Yani leo lazima iwezekane tu kwasababu mimi nshachoka kila siku kuzungushana na kitoto kidogo kama kile” Moto aliongea kwa gadhabu.
“Kila mmoja kachoka kuzungushana nae, cha mthingi ni kutafuta njia rahithi ya kumuua ili tupotedhe ushahidi kabitha”
“Leo tunaenda kumteka akitoka shule, naamini njia hii itakuwa rahisi sana”
“Tuna mtekaje yani?” Mata alimuuliza.
“Itabidi tumteke akiwa yupo kwenye gari la shule, hiyo itakuwa ni njia rahisi kwasababu hakuna atakae tusumbua wakati tunamteka” Moto aliongea.
“Hakuna atakae tuthumbua kivi yani?” Mata alimuuliza.
“Yani ni hivi, mimi na wewe Mata tutaliteka gari la shule, halafu tunaingia ndani ya gari hiyo na kutoka na mtu wetu moja kwa moja hadi kwenye gari yetu halafu tunaondoka nae tuna enda kumuulia mbali huko” Moto aliwaambia wenzake.
“Na Mrutu nae kwenye gari, yule dogo thi atamuona Mrutu? Mata aliuliza.
“Hapo inabidi tuchague Mrutu avae maksi usoni au yule dogo tukishamtoa kwenye gari la shule ndio tumvishe maksi ili asimuone Mrutu”
“Hapo itakuwa poa thana, au wewe unathemaje Mrutu, maana tangia tuandhe kuongea wewe hukutia neno lolote” Mata aliongea na kumuambia Mrutu.
“Mi sina neno, kama mpango ndio huo basi fresh” Kiukweli Mrutu hakupenda Hemedy afe ndio maana hakuwa na raha kama mwanzo wala pia hakutaka kuchangia chochote katika maongezi hayo.
“Basi sawa, itabidi saa tisa kamili tuwe maeneo ya shule tukimsubiria yule dogo ili tutimize mpango wetu haraka” Moto aliongea hivyo na kufunga kikao hicho na kila mmoja akenda kazini kwake ila Moto yeye hakwenda popote zaidi ya kwenda maskani kwake maana yeye hakuwa na kazi maalumu ya kufanya.
Katika shule anayosoma Hemedy. 9:30 Alasiri.
Walioneka wanafunzi wakitoka katika geti la shule hiyo, wengine walienda katika magari yaliyo wafuata na wengine walienda kwa miguu nyumbani kwao kwakuwa sio mbali na shule hiyo, baada ya dakika kadhaa, gari la shule lilitoka katika geti hilo huku likiwa limewabeba wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo, na Hemdy pia alikuwa ni mmoja wapo aliekuwepo katika gari hilo.
Liliongoza njia kuelekea majumbani kwa watoto hao, ila kabla halijafika mbali, likapungiwa mkono na wakina Moto na dereva wa gari hilo akalisimamisha pembeni ili kuwasikiliza watu hao. Mata alitoa bastola na kumuweka chini ya ulinzi dereva wa gari hilo na Moto yeye akatoa bastola na kuzama ndani ya gari hilo ili akamtoe Hemedy aondoke nae.
Mrutu alibaki kwenye gari akiwasubiri wenzake wakamilishe huo mpango ili waondoke zao. ila ghafla akaona gari ya polisi ikija mbio mbio upande ambao gari ya shule lime paki, gari ya polisi ikawasha endiketa ishara ya kutaka kusimama upande huo huo lilipokuwa gari la shule, Mrutu hakujua afanye nini ili wajiokoe na hilo zahma litakalo wakumba muda mfupi ujao, Mata pia aliliona hilo gari la polisi likija upande huo, Moto nae aliliona hilo gari kupitia katika kioo cha mbele cha gari hiyo ya wanfunzi, gari hilo la polisi lilikuwa likija kwa kasi sana huku likiacha vumbi kwa nyuma…. Mrutu akawapigia honi wenzake kuashiria kuwa waondoke, Moto na Mata waliiyelewa ile honi ina naama gani, wote wawili wakaacha wanachokifanya na kuanza kukimbilia kwenye gari lao, walipofika wakaingia ndani haraka haraka na Mrutu akaigeuza gari na kuiyondoa kuipeleka njia tofauti na ile gari ya polisi inapokuja, aliyondoa kwa kasi sana na alipofika mbele kidogo, akakunja kona almanusura aiangushe gari, baada ya kuiweka sawa, akapotelea huko huko.
Gari ya polisi ilipofika karibu na ile gari ya shule, ilifunga breki za nguzu na kusimama pembeni kidogo na gari ya shule. Akashuka koplo Taure na kumfuata dereva ambae bado hadi muda huo alikuwa ameganda kwa uwoga wa kunyooshewa bastola kwa mara ya kwanza tangu alipotoka katika tumbo la mama yake.
“Za saa hizi kaka?” Koplo Taure alimsalimia baada ya kumfikia. “Sa..safi tu kaka” dereva alijibu.
“Vipi, mbona kama vile haupo kawaida?”
“Majambazi” alijibu kwa ufupi.
“Sijakuelewa, majambazi wana nini?” Koplo Taure alimuuliza.
“Wamenivamia”
“Unajua mimi sikuelewi kabisa unachokizungumza, embu nyoosha maelezo” Koplo Taure alimwambia hivyo, baada ya kumuona hamuelewi.
“Nimevamiwa na majambazi”
“Wapi?”
“Hapa hapa sasa hivi, ndio wale waliondoka na gari mbio kuelekea huko nyuma” Dereva alimwambia Koplo Taure, baada ya kusikia hivyo, akamwambia amsubiri hapo hapo asiondoke, akawahi kwenye gari yake na kuanza kuwafukuzia wakina Mata ambao hadi sasa washatokomea zao wanapopajua, Koplo Taure kwakuwa aliiyona ile gari ilipokunja na yeye alipofika hapo kwenye kona akakunja ila apofika mbele kidogo hakuona hata dalili ya vumbi, akageuza gari na kurudi hadi pale iliposimama gari ya shule.
“Walikuwa wanataka nini?” Koplo Taure alimuuliza dereva baada ya kushuka kwenye gari na kumfuata.
“Sijui, walikuja wawili hapa, mmoja akaniwekea bastola mimi na mwengine akaingia humu ndani ya gari”
“Baada ya hapo?” Koplo Taure alimuuliza dereva baada ya kuona hajamalizia maelezo yake na kujiangalia kwenye suruali yake, ikabidi Koplo Taure aipeleke shingo yake hadi ndani ya gari sehemu alipokaa dereva na kuona kwenye suruali ya dereva huyo kuna maji maji chini ya mkanda“Mkojo”alijisemea mwenyewe na kutabasamu kisha akarudisha shingo yake nyuma.
“Hawakufanya chochote, ila waliondoka baada ya kuona gari ya polisi inakuja”
“Kwahiyo hawakukuambia chochote?”
“Ndio, hawakusema kitu chochote”
“Wewe unahisi walikuwa wana taka nini?”
“Afande, kusema ukweli mi sijui chochote”
“Sawa, ila mimi kuna mdogo wangu namtaka humu kwenye gari” Koplo Taure akabadilisha mada na kuongea kilichomleta hapo.
“Lakini kwanini usimsubiri hadi akifika nyumbani ndio ukamchukue?”
“Hapana, ni muhimu niondoke nae sasa hivi”
“Anaitwa nani?”
“Hemedy, Hemedy Mheshimiwa” Dereva akamgeukia utingo wake na kumuambia amuite Hemedy, baada ya sekunde kadhaa, Hemedy akashuka nje ya gari hilo na kuenda upande wa dereva, upande ambao Koplo Taure alikuwa amesimama, alipofika akamsalimia na kutulia.
“Mkubwa, ni huyu hapa, asanteni, mnaweza kuendelea na safari yenu” Koplo Taure aliongea hivyo huku akiondoka na Hemedy kuelekea kwenye gari alilokuja nalo.
“Sasa, kaka unaenda nae wapi huyo dogo?” Dereva aliuliza huku akichungulia kwenye kioo cha mbele ya gari hilo.
“Nyie, endeleeni na safari yenu, nitampeleka mimi nyumbani kwao” Koplo Taure aliongea hivyo huku akingia kwenye gari baada ya Hemedy kuingia, akawasha gari na safari ya kuelekea kituoni ikaanza.
Muda huo huo, ndio ulikuwa muda ambao, Mr Bakari Haneni, aliahidiana na Tosh, kupeleka pesa na mzigo wa madawa ya kulevya ili apewe watu wake. Mr Bakari Haneni hakuwa mzembe kiasi hicho, eti apeleke pesa na mzigo halafu awachukue watu wake kijinga jinga hivyo, hakutaka kukubali huo upumbavu, akapanga kupeleka kundi lake likakafanye mashambulizi baada ya kukabidhiana mizigo aliyoombwa na watu hao. Akampigia simu Yuni, mmoja kati ya watu wake wanaolinda ngome yake.
“Njoo nyumbani kwangu mara moja, njoo na watu kama kumi hivi wenye silaha, haraka nawasubiria” Alipoongea hivyo akakata simu na kuwasubiria vijana wake aliowaita. Baada ya nusu saa, gari aina ya Hiace iliingia katika nyumba ya Mr Bakari Haneni, ikapaki sehemu maalum ya kupaki magari katika nyumba hiyo, na hao vijana walishuka na kuelekea katika moja ya bustani ya nyumba hiyo alipokuwa amekaa bosi wao, walipofika wakajipanga mstari na kumuangalia bosi wao. Mr Bakari Haneni aliwapitishia macho mmoja baada ya mwengine alipofika kwa wa mwisho, macho yake akayaleta kwa kijana aliesimama katikati ya vijana hao.
“Yuni, nadhani unajua kwamba Tito na Tobi wametekwa kama jana nilivyokuambia” Mr Bakari Haneni aliongea hivyo kumuambia huyo kijana wa katikati, ambae alikuwa mrefu halafu mweupe mwenye macho makubwa na mwili mkubwa.
“Ndio Mkuu” akajibu kiukakamavu.
“Sasa basi, wale wajinga leo ndio ile siku ya kuwakomesha, haiwezekani wacheze na mimi hata kidogo, kwahiyo nataka mukawafunze adabu ikibidi muwauwe pia kama itawezekana, halafu murudi na wenzenu na mizigo yetu. Mmenielewa?”
“Ndio Mkuu” wakaitikia wote.
“Sasa ni hivi, Yuni utapanda na kijana mmoja kwenye gari nyengine tofauti na hiyo gari mliyokuja nayo nyie ndio ambao mtaenda kukabidhiana nao hiyo mizigo, halafu baada ya hapo hawa wengine watawashambulia ghafla baada ya nyinyi kuwa mbali nao, mtajua jinsi gani ya kujipanga wenyewe ila ninachotaka mrudi na mizigo yangu na wenzenu” Mr Bakari Haneni aliwaambia vijana wake.
“Hakuna tatizo mkuu, tutarudi kama ulivyotuagizia” Yuni alijibu.
“Sasa subiri nikupe namba zao ili mkifika muwasiliane” alimpa namba za Tosh. Baada ya hapo akaendelea.
“Sitaki mrudi kama mnavyoondoka, nataka mrudi na wenzenu na mizigo yetu, halafu hakikisheni hamdhuriki hata kidogo, kwasababu nyote bado nawataka” Mr Bakari Haneni alivyoongea hivyo akawaruhusu waende na wao wakapnda kwenye gari walilo kuja nalo. Yuni na kijana mmoja wao wakapanda kwenye toyota mark 11 grand na safari ya kuelekea katika chuo cha utumishi kilichokuwepo kange ikaanza.
Baada ya dakika thelathini, wakawa wamefika mbali kidogo na kilipo chuo cha Utumishi. Wakasimamisha gari pembeni, ili wapange ni jinsi gani ya kufanya.
“Sasa nyie mtaenda mbele kabla yetu sisi, mtakipita kile chuo na kusimama kwa mbali kidogo, halafu sisi tutaenda kusimama pale pale chuoni walipotuelekeza, kwahiyo sisi tukishakabidhiana mizigo, mtatusubiri tukishafika mbali kidogo, ndipo na nyie mtakapo anzisha mapambano, naamini hadi hapo itakuwa tayari tushawazidi, kwasababu wao itakuwa hawaja jiandaa, halafu baada ya hapo sisi tunachukua mizigo yetu, kisha tunapotea haraka sana” Yuni aliwaambia wenzake. Alipoona wote wapo kimya wakimsikiliza yeye, akaendelea.
“Kumbukeni, Mkuu ametuambia kwamba, turudi kama tulivyoondoka upande wetu, akimaanisha asipungue mtu hata mmoja katika hii kazi na tusirudi kama tulivyoondoka, akimaanisha turudi na wenzetu na mizigo yetu” Yuni alipoongea hivyo akawaambia wale waliokuwepo kwenye Hiace watangulie mbele halafu na wao wafuatie. Ikawa kama walivyopanga, baada ya kuondoka kwa ile Hiace baada ya dakika kumi na wao wakafuatia.
Tosh na Doze walikuwa kwenye gari wamekaa wakiwasubiri wageni wao, gari yao waliipaki pembeni kidogo ya chuo hicho. Waliiyona Hiace iliyowapita muda mchache uliopita, ila hawakuitilia maanani sana, hawakuwafikiria kuwa watakuwa ndio hao wageni, kwasababu wageni wao waliwaambia wasimame chuoni hapo na hiyo Hiace ilipapita chuoni hapo. Baada ya dakika kumi na tatu, waliiyona gari aina ya mark 11 grand ikisimama karibu na chuo hicho.
“Oya Tosh nahisi jamaa itakuwa ni hao hapo, embu jaribu kuwapigia simu” Doze alimwambia Tosh awapigie simu hao wageni wao wanaotaka kukutana nao.
“Wao pia namba yangu si wanayo, watatu pigi…” kabla hajamaliza sentensi yake, simu yake iliita, akaipokea.
“Haloo” Tosh aliongea baada ya kupokea simu.
“Tumefika, mko wapi nyie?” sauti ya upande wa pili iliongea.
“Ndio mko kwenye hiyo mark 11 grand?” Tosh aliuliza.
“Ndio”
“Haya, shukeni na mizigo yetu, halafu si manaiyona hii gari hapa pembeni yenu?”
“Ndio, tunaiyona”
“Shukeni, mmje na mizigo yetu hadi kwenye hiyo gari”
“Hapana, hatuwezi kufanya biashara hiyo, kwanini tusishuke wote, sisi na nyie”
“Pia sawa, shukeni na sisi tushuke” Tosh alipoongea hivyo, akasubiri kwanza walioko kwenye ile gari waliposhuka na wao ndipo wakashuka.
“Mbona hatuwaoni watu wetu, wako wapi?” Yuni alionea huku akiangaza angaza upande wa pili waliopo wakina Tosh waliokuwa wameshuka kwenye gari mikono mitupu.
“Msiwe na wasiwasi, leteni mizigo yetu, halafu ndio mtawaona watu wenu, si tumeamua kufanya biashara ya amani, sasa kinachomiogopesha ni nini?” Tosh alimuuliza Yuni.
“Hata kama, ila ni vizuri zaidi tukiwaona watu wetu”
“Ok, watu wenu wapo kwenye gari ya nyuma yetu, kwahiyo mnaweza kuja tufanye makabidhiano”
Baada ya kukata simu, Yuni na kijana aliongozana nae, waliwafuata wakina Tosh waliokuwa wakiliendea gari ya nyuma yao ili wakafanye makabidhiano, walipokutana kwenye hiyo gari iliyodaiwa kuwa Tito na Tobi wamo. Tosh akataka briefcas walizoshika wakina Yuni zifunguliwe, zilipofunguliwa kwenye briefcas ya kwanza kulikuwa na vibunda vya noti za elfu kumi zimepangwa kwa ustadi mzuri. Tosh alipoona alitabasamu na kuamuru ilifunguliwe na hiyo nyengine nayo ilikuwa na vipakti vya madawa ya kulevya vilivyo jaa kwenye hiyo briefcas.
Baada ya kuhakikisha kila kitu ndicho, akawafungulia mlango wa gari hiyo na kuwatoa wakina Tito wakiwa wamefungwa kamba, baada ya kuwatoa wakawafungua kamba na kuwaruhusu waondoke nao baada ya wao kukabidhiwa mizigo yao.
Baada ya makabidhiano kwenda sawa, Tito, Tobi, Yuni na kijana mwengine walianza safari ya kuliendea gari lao ili waondoke na wenzao kwenye ile Hiace wafanye yao. Wakina Tosh wao hawakuwa na habari kwamba ilipangwa wageukwe, zile briefcas wakaziingiza kwenye ile gari nyengine ambayo alikuwa Kiku ndio anaiendesha, na wao wakaanza kuiyendea gari yao ili waondoke zao. Ila ghafla Doze alikoswa koswa na risasi iliyopita sentimita chache kwenye sikio lake, ikabidi ajirushe upande wa nyuma wa gari aliyokuwemo Kiku. Tosh baada ya kuona tukio hilo yeye alikimbia hadi kwenye gari alilokuja nalo huku akikoswa koswa na risasi, alipofika aliingia moja kwa moja upande wa dereva na kuwasha gari ili aondoke zake, risasi bado ziliendelea kupigwa na kufanya vioo vya hiyo gari kuvunjika, ila yeye hakujali alichotaka kwa wakati huo ni kuokoa uhai wake tu, akawasha gari na kuliondoa hapo kwa kasi huku akisindikizwa na risasi zilizopasua kioo cha nyuma.
Wale watu kwenye ile Hiace baada ya kuona gari moja tayari imeondoka, wakaamisha mashambulizi kwenye hii gari iliyobakia, walipiga risasi hiyo gari, inavyooneka watu hao hawakuwa na mafunzo yoyote ya kutumia bunduki maana walijipigia tu bila ya kulenga shabaha, waliipiga risasi gari na kuipelekea kuifanya chujio kwa matundu ya risasi. Doze baada ya kuona Tosh ameondoka na gari walilokuja nalo, akaona akichelewa tena na gari hii ambayo ndani yake yupo Kiku itamuacha, kwavile alikuwa ubavuni mwa gari hiyo, akafungua mlango wa nyuma na kuingia humo, Kiku baada ya kuona Doze ameingia ndani, akaondoa gari kwa kasi kiasi kwamba nusura nusura akauvamie mti uliokuwa mbele yake baada ya kupata upenyo mzuri akatokomea zake.
Wale watu baada ya kuona watu wao wamekimbia na wao wakapanda kwenye gari yao na kuanza kuwakimbiza huko huko walipoelekea. Wanafunzi wachuo hicho waliposikia milio ya risasi hawakujua wakimbile wapi wakabaki wakifukuzana humo humo ndani ya chuo. ili kuwa kama vile wanaangalia muvi jinsi mapigano hayo yalivyokuwa yakiendelea hapo nje ya chuo hicho.
Kituo cha polisi.
Baada ya kufika kituoni, akaweka gari kwenye paking ya hapo, na kushuka, akanza kuelekea ndani huku akifuatiwa na Hemedy kwa nyuma, wakaongozana hadi kwenye ofisi ya Inspekta Ganjo na kuingia humo. Hemedy alipoingia humo akamsalimia Inspekta Ganjo na kukaa kwenye kiti.
“Habari za shule?” Inpekta Ganjo, alimuuliza.
“Nzuri tu” Hemedy alijibu.
“Unasoma lakini?”
“Ndio, nasoma”
“Vizuri, nimemtuma huyu aje kukuchukua kule shule, ngoja kwanza. hivi watu waliofanya mauwaji ya wazazi wako ukiowaona unawakumbuka?” Inspekta Ganjo alimuuliza.
“Ndio, nikiwaona nawakumbuka” Hemedy alijibu.
“Sawa, Koplo Taure mpeleke akawaone” Inspekta Ganjo alipoongea hivyo, Koplo Taure akamchukua Hemedy na kutoka nae nje ya ofisi na kwenda nae kwenye selo walipo hao alioambiwa kuwa akawaangalie kuwa ndio wauwaji wa wazazi wake.
“Wale pale watatu, embu waangalie kama ndiwo” Koplo Taure alipomuambia hivyo, Hemedy akakaza macho baada ya kuangalia vizuri, akapigwa na butwaa, ikabidi afikiche macho yake kwa kutoamini anachokiona mbele yake.
“Haaaaaa!!!!! Na wewe pia upo?” Hemedy aliuliza Kwa hamaki baada ya kumuona mtu alie mshangaza sana kumuoma mahala hapo. “Dogo, sijakuleta hapa uje kuwauliza watu maswali, embu waangalie wale watu watatu kule mwisho, ndio hao au sio?” Koplo Taure alimwambia Hemedy baada ya kuona amemshangaa mtu huyo aliekuwa pembeni ya watu watatu waliokuwa wamekaa mwisho kabisa ya ukuta wa selo hiyo.
“Hapana, wale sio na wala pia siwajui” Hemedy alijibu huku akiwa bado macho yake ameyagandisha kwa yule mtu aliekuwa amekaa pembeni ya wale wengine.
“Una uhakika?” Koplo Taure alimuuliza.
“Ndio”
“Haya twende” Koplo Taure aliondoka na Hemedy hadi katika ofisi ya Insepekta Ganjo.
“Enhee! Kasemaje, ndiwo au?” Inspekta Ganjo aliongea hivyo baada ya watu hao kuingia katika ofisi yake.
“Amesema siwo” Koplo Taure aliongea hivyo huku akikaa kwenye kiti kilichopo humo ofisini.
“Eti Hemedy, wale watu sio waliofanya mauaji ya wazazi wako?” Inspekta Ganjo alimuuliza Hemedy.
“Sawa, nilimtuma huyu aje kukuchukua shuleni kwenu ili uje kuwaona hawa watu kama ndio au sio, kwasababu hawa watu wamefanya tukio la mauwaji kwenye familia flani siku ya leo, sasa ndio tumefanikiwa kuwakamata, sisi tukawashuku kuwa huenda ikawa ndio hawa waliofanya mauwaji ya wazazi wako pia”
“Hapana, sio wale” Hemedy alisema.
“Basi kama sio, hakuna tatizo(akamgeukia Koplo Taure) mpeleke nyumbani kwao huyu” Koplo Taure alitoka na Hemedy nje ya kituo hicho, wakapanda kwenye gari ya polisi na safari ya kwenda nyumbani kwa kina Hemedy ikaanza.
“Anko” Hemedy alimuita Koplo Taure wakiwa ndani ya gari.
“Sema dogo”
“Hivi yule mtu mwengine aliekaa pembeni ya wale mnaosema majambazi kule selo, ana kesi gani yule?” Hemedy aliuliza.
“Kwani unamjua yule mtu?”
“Ndio namjua yule”
“Umemuona wapi?”
“Yule ni daktari aliekuwa katika ile hospitali nilipoenda kulazwa mara ya pili, aliwahi kunichoma sindano ya dawa, aah aliniumiza, yani kanichoma sindano inauma, halafu sasa ananichoma huku anacheka ikiwa mwenzake mimi nime kasirika”
“Anhaa!!! Yule ana kesi yake ya kumpiga mkewe hadi kumjeruhi, kwahiyo ndio ameletwa hapa na majirani zake, maana alikuwa amekunywa pombe zilizompelekea kumpiga mkewe hadi kumzimisha”
“Dah!! Kumbe ana roho mbaya hadi kwa mkewe”
Koplo Taure alipaki gari nje ya nyumba ya Mrutu baada ya kufika. Hemedy akashuka na kumuaga Koplo Taure kisha akaingia ndani ya nyumba hiyo, Koplo Taure akageuza gari na kurudi kituoni.
* * * *
Kundi la Mr Bakari Haneni baada ya kuwafukuza wakina Kiku na Doze, waliwakosa na kuamua kurudi nyumbani kwa Bosi wao, baada ya mwendo mrefu kiasi kutoka Kange hadi Raskazone, wakafika na kuingiza gari zao ndani ya nyumba hiyo, wakashuka na kumfuata Bosi wao aliekuwa bado yupo pale pale kwenye bustani amekaa.
“Vipi? Mbona sura zenu hazina furaha kama siku nyengine ninapo waagiza mkafanye kazi na kufanikiwa, kwanza vijana wangu wapo wapi?”
“Wale pale ndio wanashuka kwenye gari” mtu mmoja katika kundi hilo aliongea huku akiwanyooshea kidole wakina Tito waliokuwa ndio wana shuka katika gari aliloenda nalo Yuni na yule kijana mwengine, na wao wakaongozana na kwenda hadi mbele ya bosi wao na kusimama mstari mmoja kumuangalia bosi kama walivyofanya wenzao.
“Embu njoeni hapa mbele yangu vijana wangu” Mr Bakari Haneni alipoongea hivyo Tito na Tobi walienda mbele yake na kusimama.
“Dah!! Aise!! Hawaja waumiza lakini(aliongea hivyo huku akiwaangalia angalia vijana hao) Tobi wamekutoboa na nini hapa kwenye mkono?”
“Mkuu, wale watu wana roho mbaya sana na ni lazima walipe kwa hili, hapa wamenitoboa na kifaa flani cha kutobolea matundu kwenye mbao za madirisha” Tobi aliongea kwa ghazabu za waziwazi.
“Ila hawaja waumiza sehemu nyengine yoyote?”
“Hapana Mkuu, walitulaza tu na njaa siku moja na kutufunga kwenye viti kiasi kwamba hatukuweza kujitikisa kwenda popote” Tito alijibu.
“Sawa, mmekuja na mizigo yetu?” Mr Bakari Haneni alimgeukia Yuni na kumuuliza swali hilo.
“Hapana Mkuu” Yuni alijibu.
“Kwanini?” Mr Bakari Haneni aliuliza huku hasira zikianza kumpanda.
“Mkuu, wale watu walikuwa pia wamejiandaa, haikuwa kama vile sisi tulivyodhani, baada ya kukabidhiana wao wakanza kuturushia risasi, ikabidi sisi tujifiche na kuanza kurushiana risasi na wao, ila wao baada ya kuona tuna wazidi wakapanda kwenye gari yao na kukimbia na tukawaunganishia ila hatukuweza kuwapata”
Yuni alidanganya maana alimjua mtu huyo hakuwa na masihara pindi akutumapo kazi halafu usiikamilishe kama yeye anavyotaka, ndio maana akatumia uongo huo ili kumpoza hasira na kweli hasira zilipungua na kuwa katika hali ya kawaida.
“Lakini nyote si mmerudi salama?”
“Ndio Mkuu” wakaitikia wote.
“Ok, nyie wengine mnaweza kwenda mkaendelee na kazi, Tito na Tobi bakini hapa kwanza” Alipoongea hivyo lilekundi lote likaondoka na kwenda kwenye ile Hiace na kutoka ndani ya nyumba hiyo kuelekea kwenye ngome yao.
“Hiyo sehemu mlipofungiwa mnapajua?” Mr Bakari Haneni aliwauliza watu hao baada ya lile kundi kuondoka.
“Ndio Mkuu, tunapajua” Tito alijibu.
“Inabidi mkafanye shambulizi la kushtukiza ikiwezekana kuwateka kabisa na kuwapeleka kwenye ngome yetu ili wakalipe kwa walichokifanya”
“Mkuu, ila mimi sidhani kama lile jumba walilotufungia kwamba itakuwa ndio maskani kwao” Tito aliongea.
“Kwanini?”
“Kwasababu pale walikuwa wanakuja na kuondoka tu, nahisi lile jumba walilikodisha au wamelitumia tu kwa muda kutokana na mimi nilivyo wasoma”
“Ok, itakuaje ili kuwapata, maana wameodoka na mzigo wetu na pesa zao, hiyo ni hasara kubwa sana”
“Mkuu, wale tuna kuhakikishia ndani ya wiki hii hii watakuwa mikononi mwetu na kuwaleta mbele yako”
“Nitafurahi kama itakuwa hivyo, nawaamini sana vijana wangu wa kazi”
“Mkuu wewe usijali”
“Sawa, nendeni katika nyumba yenu, atakuja daktari kuja kumitibu baada ya nyie kufika halafu kesho nitawahitaji hapa Asubuhi”
Baada ya kusikia hivyo waliondoka na kwenda katika gari na kupanda na safari ya kuelekea katika nyumba yao iliyokuwa maeneo ya majengo waliyopewa na bosi wao ikaanza.
* * * * “Duh!!! Yani ilikuwa kama vile muvi la kizungu kwajinsi wale wajinga walivyoturushia marisasi yao” Kiku aliongea hivyo kuwaambia wenzake baada ya kufanikiwa kuwatoroka wakina Yuni na kundi lake. Wakati huo walikuwa wapo katika nyumba yao waliyoifanya kama maskani yao ya kufanya na kupanga mambo yao mengi.
“Halafu huyu mjinga aliniacha na gari sijui alitaka waniue wale wajinga wenzie” Doze aliongea kwa utani.
“Asa mimi nakuona hutokei, unadhani mimi ningefanyaje kama sio kuondoka pale” Tosh aliongea.
“Embu tuachaneni na hayo, kwanza tunafanyaje maana yale magari wameyaharibu hasa hasa upande wa vioo na tena ile gari nyengine tumeiazima sio yetu” Kiku aliongea.
“Kwani vioo si vinabadilishwa tu, tuna badilisha halafu tunalitoa gari la watu” Tosh aliongea.
“Hata hivyo pesa tunazo nyingi tu, hata akitaka tumnunulie gari nyengine pia uwezo huo tunao” Doze aliongea.
“Ila kumbukeni wale wajinga hawatokubali lazima watatutafuta tu kwahiyo tunapokuwa sehemu yoyote tuwe makini tusijiachie” Kiku aliongea.
“Au kama ikiwezekana na sisi pia tuwawinde popote pale tutakapo waona tuwauwe tu kabla hawaja tuanza sisi” Tosh aliongea.
“Hapo Tosh umeongea, inabidi tuwawahi kabla hawaja tuwahi” Doze aliongea.
“Embu kwanza fungua hiyo mizigo yetu tuhakikishe kama ni yenyewe isije ikawa tumeuziwa mbuzi kwenye gunia” Kiku alipoongea hivyo, Tosh akazifungua zile briefcacas na wote macho yao yakatua ndani ya mikoba ile, wakahakikisha ni kweli yale yalikuwa ni madawa ya kulevya origino kabisa na pesa halali kwa matumizi zilizokuwepo katika mkoba mwengine, baada ya kuhakikisha wakaifunga mikoba ile na kuendelea na maongezi yao mengine ambayo hayakuwa na ulazima kuyaandika katika hii hadithi yetu.
* * * *
Wakina Mrutu baada ya kukimbia na gari yao wakaenda moja kwa moja nyumbani kwa Mata.
“Dah!!! Aithee yani yule mtoto ana mungu kweli yani” Mata aliongea hivyo baada ya kukaa kwenye sofa ndani ya nyumba hiyo. “We acha tu mimi tayari kashanichosha, yani kila tunapo mpangia mipango basi anaikwepa hata sijui pia tufanyeje” Moto aliongea kwa masikitiko kana kwamba hivyo wanavyotaka kufanya ni sawa tu.
“Kwandha imekuaje lile gari la polithi likaja pale hai hai?” Mata aliwauliza wenzake kama vile kuna ambae anajua lile gari lilifuta nini pale, ikawa ameuliza swali la kipumbavu kwa upande wangu mimi muandishi sijui wewe msomaji.
“Sasa Mata, nani ambae anajua kwamba lile gari limefuata nini pale, au umekosa maneno ya kuongea ndio maana” Moto aliongea.
“Bathi tuachane na hayo, vipi kuhuthu yule dogo, maana kesho kutwa Mrutu anataka kwenda kuchukua barua ili tuende mahakamani tukachukue mali dhetu”
“Yule dogo twendeni tukammalize huko huko nyumbani kwa Mrutu sasa hivi” Moto aliongea.
“Nshasema nyumbani kwangu sitaki afe mtu” Mrutu aliongea kwa gadhabu, si kwamba kachukia Hemedy kufa nyumbani kwake, laa hasaa!! Bali hakutaka kabisa habari hizo za kuuliwa kwa mwanae huyo.
“Hapana hatumuui hapo kwako, bali tuna mteka na kuondoka nae” Moto aliongea hivyo akidhani kuwa mwenzao amekasirika kutokana na sababu hiyo.
“Ok, twendeni bathi thatha hivi tuka ifanye hiyo kadhi maana kesho kutwa tu tunachukua mali dhetu” Kikao hicho kikafungwa na safari ya kwenda kwa Mrutu ikaanza, baada ya dakika kadhaa ikawa tayari wameshafika nje ya nyumba ya Mrutu.
Kipindi hicho Hemedy alikuwa yupo sebuleni anaangalia Tv, kwa mbali alisikia sauti ya geti likifunguliwa, kwakuwa hapo alipokaa kuna dirisha la kuweza kumuonyesha nje ya sebule hiyo, akapanda juu ya sofa na kufungua pazia la dirisha hilo, akawaona watu watatu wakiingia ndani ya nyumba hiyo, wawili kati yao hakuwajua vizuri, ila mmoja wao akamjua kuwa ni baba yake mdogo, ila wapofika karibu na mlango wa kuingilia ndani ndipo hapo alipo pigwa na butwaa baada ya wawili kati ya hao watu kuwajua vizuri na kuwakumbuka haswaaa kuwa ndio hao walio muulia wazazi wake.
Hakujua watu hao wamejuana vipi na baba yake mdogo hadi kufuatana hadi hapo nyumbani, (au itakuwa wamemteka na yeye nini?) alijiuliza mwenyewe lakini akapingana na hilo baada ya kuona watu hao wapo kiurafiki zaidi na baba yake mdogo, akashindwa kuelewa, akabaki ameduwaa tu, baada ya sekunde tano akainuka hapo na kukimbilia chumbani kwake.
“Huyu dogo yupo, si unaona hata Tv inawaka inavyoelekea yupo humu humu ndani” Moto aliongea baada ya kuingia sebuleni hapo.
“Thatha tumthubirie au tumtafute” Mata aliongea.
“Atafutwe tufanye haraka tuondoke, oya Mrutu embu mfuate chumbani kwake ukamuangalie” Moto aliongea hivyo, Mrutu hakuwa na namna ya kupinga, akaenda hadi katika chumba anacholala Hemedy na kuingia humo ndani, alipoingia alipigwa na butwaa kwa alichokikuta humo ndani, hakuelewa imekuaje hadi ikawa hivyo, akabaki na kuduwaa tu asielewe nini afanye.. “Huyu mtoto yupo wapi?” Mrutu alijiuliza mwenyewe baada ya kutomuona Hemedy humo chumbani kwake, akanza kumtafuta kila sehemu ila alimkosa na kuamua kutoka kurudi sebuleni.
“Humo chumbani dogo hayupo bwana na sijui kaelekea wapi” Mrutu aliwaambia wenzake baada ya kufika sebuleni hapo.
“Umemuangalia hadi chooni huko” Moto aliongea huku akiinuka kwenye sofa alilokaa.
“Ndio, kote huko nimemuangalia ila sija muona. we unataka kwenda wapi mbona umeinuka?” Mrutu alijibu na kumuuliza Moto baada ya kumuona ameinuka kwenye sofa.
“Subiri mimi nikamcheki huko nje, nakuja sasa hivi” alipoongea hivyo akafungua mlango na kutoka nje. Mrutu akanza kuwa na wasiwasi hakujua Hemedy yupo wapi, akapatwa na wasiwsi zaidi baada ya kuona Moto anatoka nje kwenda kumtafuta huko uani, alidhani labda huenda Hemedy akawa yupo huko huko uani, akapanga endapo Hemedy akiletwa na Moto kutoka huko uani basi alete pingamizi lolote ili mradi tu Hemedy asife. Baada ya dakika tatu akarudi sebuleni hapo.
“Haya vipi?” Mata alimuuliza.
“Hayupo” alijibu huku akikaa kwenye sofa.
“Nahisi itakuwa ametoka kidogo ila atarudi muda si mrefu kwahiyo tumsubirini” Moto aliongea hivyo huku akiinuka kwenye sofa na kuliendea friji lililo kuwepo hapo hapo sebuleni na kuchukua soda na kurudi nayo kwenye sofa, akaifungua na kuinywa pafu moja.
“Mrutu na wewe unazingua, kwanini huweki hata pombe bwana, we unatuwekea masoda haya ya kunywa wanafunzi” Moto aliongea.
“Mimi siweki pombe, si unajua kuwa mimi ni muislamu, sasa nitawekaje pombe kwenye nyumba yangu”
“Acha zako wewe nani aliekuambia kuwa waislamu hawanywi pombe, halafu pia wewe kama haunywi unatakiwa utuwekee sisi wageni” Moto aliongea.
“Kwanza mimi sinywi pombe halafu sitoweza kuziweka katika nyumba yangu, kwani wewe kama unataka kunywa pombe, si unywe huko unapotoka halafu ukija hapa uwe tayari ushapendeza”
“Unajifanya muislamu safi kumbe huna lolote” Moto aliongea hivyo huku akiipiga pafu kubwa ile soda, ikabakia nusu.
“Sio muislamu safi, ila si unajua kuwa sisi wengine hatukuzoea hivyo vitu” Mrutu alijibu lakini moyoni mwake alikuwa anaombea Hemedy asirudi muda huo huko alipoenda.
“Anakudanganya tu huyo, kwadha tangu lini akanywa pombe” Mata aliongea.
“Mimi huwaga nanywa siku moja moja nikiamua” Moto alijibu.
“Basi hapa kwangu siweki pombe mimi” Waliendelea na mazungumzo yao huku wakivuta muda Hemedy arudi huko alipoenda ili waondoke nae, wawili kati yao wakiombea Hemedy arudi ili watimize azma yao, mmoja wao aliombea Hemedy asirudi ili wasiitimize azma yao.
Baada ya kukaa kwa muda mrefu nyumbani hapo kwa Mrutu, maana walikaa takribani masaa matatu bila Hemedy kutokea hadi muda huo wa saa tatu na nusu usiku wakaamua tu waage ili waondoke zao.
“Subirini niwasindikize hadi hapo nje nika nunue msosi maana leo nimechelewa kupika msosi” Mrutu aliongea.
“Kwahiyo hukutaka kupika kwaajili yetu, ulidhani labda tutakumalizia chakula chako” Moto aliongea hivyo huku akiuelekea mlango wa kutokea nje.
“Hapana sio hivyo, nyie wenyewe mnajua kwamba tulikuwa wote hapa tunapiga stori kiasi kwamba hadi nimesahau kupika” Mrutu aliongea hivyo huku na yeye akitoka nje baada ya Moto kutoka huku akifuatiwa na Mata nyuma yake. Walitoka nje ya nyumba hiyo, Moto na Mata walipanda kwenye gari na kuondoka nyumbani hapo na Mrutu nae alielekea kwenye kibanda cha mgahawa kwenda kuangalia chakula.
Hemedy kule chumbani kwake alitoka ndani ya kabati ambalo halikuwa na kitu chochote ndani yake, alikuwa amejifungia ndani ya kabati ili kujilindia roho yake kwa watu hao walio muulia wazazi wake, alipokuwa ndani ya kabati alikuwa akiskia tu minong’ono hakuskia kile ambacho kina ongelewa kwa ufasaha zaidi, ila baada ya kuona kimya ndipo akaamua atoke ndani ya kabati hilo kutokana na joto alilokuwa akilipata.
Akanyata hadi mlangoni kwake na kutega sikio vizuri ili aweze kusikia chochote kitakachoongelewa sebuleni hapo, kimya. akafungua mlango na kutoa kichwa akachungulia vizuri na kuona sebule ikiwa tupu, akarudi katika chumba cha baba yake mdogo na kujaribu kuufungua mlango ila akaona mlango umefungwa, “atakuwa ametoka nao wale watu” alijiwazia mwenyewe, akatoka nje ya nyumba hiyo na kwenda katika mti uliokuwa mbali kidogo na nyumba hiyo, akatulia hapo.
Baada ya kujibanza hapo kwenye mti kwa dakika tano, akamuona baba yake mdogo akirudi na mifuko miwili, akamsubiria aingie ndani baada ya dakika mbili na yeye akaingia.
“We ulikuwa wapi masaa yote” Mrutu aliekuwa yupo kabatini akitoa sahani, alimuuliza swali hilo Hemedy alieingia humo sebuleni.
“Nilikuwa hapo jirani kwa rafiki yangu” Hemedy alijibu kwa uoga.
“Haaa!!! Yani wewe umekuja mtaa huu hata wiki hujamaliza tayari ushapata rafiki, mbona muongo we dogo”
“Kweli baba mimi nilikuwa hapo jirani tu”
“Sawa, ila siku nyengine usikae kwa watu hadi muda huu, umeniskia?” Mrutu hakuweza kumgombesha sana, kwasababu yeye mwenyewe pia amefurahi baada ya wakina Mata kumkosa mwanae huyo kwa mara nyengine “hahahah!! hapo ndipo ninapo amini kuwa huyu dogo analindwa na mungu asiuawe, eeee mungu mlinde hivi hivi” alijiwazia mwenyewe huku akimpa sahani Hemedy.
“Sawa nimekuelewa” Hemedy alijibu huku akipokea sahani aliyopewa na Mrutu, akachukua mfuko mwengine uliokuwa umebakia juu ya meza baada ya mwengine kuchukuliwa na Mrutu, akamimina chakula hicho ndani ya sahani, kilikuwa ni pilau na nyama za kuku, na yeye akaenda kwenye meza akakaa na kuanza kula, baada ya kumaliza kula alimuaga baba yake huyo na kwenda chumbani kwake, akabadilisha nguo na kuvaa nguo zake alizozoea kulalia nazo ambazo zilikuwa ni track suti, akazima taa na kujitupa kitandani, hapo mawazo yote yalikuwa kwa wale watu waliomuulia wazazi wake. “kumbe bamdogo anajuana nao, au na yeye anashirikia nao? Hapana haiwezi kuwa hivyo. lakini sasa mbona yupo nao, au na yeye wanataka kumuua, mmhh!! itabidi nimuambie kuwa wale watu ndio walio waua wazazi wangu, sijui nika muambie sasa hiviii? Aagh nitamuambia kesho” aliendelea kuwaza hadi pale alipopitiwa na usingizi na kulala. Akalala. * * * * * * * * * *
Siku iliyofuata. Nyumbani kwa Mr Bakari Haneni. 2:45 Asubuhi.
Gari ya kifahari aina ya Jaguar ilitoka katika nyumba hiyo na kuelekea barabara ya hospitali ya Bombo, ikanyoosha moja kwa moja, ikaipita Regal Naivera Hoteli. “kuna nyuki anatufuata nyuma yetu” Mr Bakari Haneni alimwambia hivyo dereva wake ambae pia ni mlinzi wake baada ya kuona gari aina ya Breves lililokuwa likiifuatilia gari hiyo nyuma yake tangia anatoka nyumbani kwake.
“Twende PSPF tukasimame pale, halafu tumuone yeye ataenda wapi” Wakaipita Toyota na kwenda kusimama mbele kidogo katika jengo la PSPF lililokuwa likiangaliana na jengo la Tanesco, gari ikapaki katika maegesho ya jengo hilo, “subiri mimi nizuge kuingia humu ndani, wewe endelea kumuangalia ataishilizia wapi baada ya sisi kusimama hapa” alimwambia hivyo mlinzi wake kisha akashuka kwenge gari na kupotelea ndani ya jengo hilo.
Ile gari iliyokuwa ikiwafuata nyuma, ilikuwa ni gari ya Koplo Taure, baada ya kuona windo lake limesimama katika jengo hilo, yeye akaenda mbele kidogo kwenye Car Wash iliyokuwa karibu na garden, akapaki hapo na kuelekeza macho yake katika jengo aliloingia Mr Bakari Haneni.
Baada ya dakika ishirini, alimuona Mr Haneni akitoka katika jengo hilo na kuingia katika gari alilokuja nalo, aliiyona gari hiyo ikigeuza na kurudi kule kule ilipotoka na yeye akaingiza gari barabarani ili kuendelea kulifuatilia windo lake.
“Hivi hili gari linalo tufuata unaweza ukalijua?” Mr Bakari Haneni alimwambia dereva wake huku akiwa amegeuza shingo yake kuliangalia gari la Koplo Taure kupitia kioo cha nyuma.
“Hapana Mkuu, silijui” dereva alijibu.
“Ok, sio mbaya, muache atufuatilie” Mr Bakari Haneni alipo ongea hivyo, akarudisha shingo yake mbele.
“Subiri nizikariri namba zake za gari” Mr Bakari Haneni aligeuza tena shingo yake na nyuma, akazikariri namba za gari ya Koplo Taure, wakati huo walikuwa tayari wamefika katika nyumba yake, dereva akaingiza gari ndani na kuipeleka katika maegesho na kusimamisha.
Koplo Taure baada ya kuona windo lake limeingia katika nyumba hiyo, yeye akageuza gari na kurudi kituoni..
Mr Haneni, akashuka kwenye gari baada ya kupakiwa sehemu maalumu ya kupaki magari katika nyumba hiyo na kuingia sebuleni mwa nyumba yake na kuwakuta Tito na Tobi tayari wameshafika nyumbani hapo.
“Vijana wangu karibuni, mmefika saa ngapi hapa?” Mr Bakari Haneni aliongea hivyo huku akikaa katika sofa.
“Tumefika kama dakika kumi tu zilizopita” Tobi alijibu.
“Vizuri. wakati natoka hapa nyumbani kuna gari ilikuwa inanifuata nyuma, ili kujipa uhakika zaidi, nikamuambia dereva wangu aipaki gari yetu katika jengo la PSPF halafu mimi nikashuka nakuingia ndani ya jengo hilo ili kuzuga tu, baada ya kutoka nikamuona mfuatiliaji amepaki gari yake pale Car Wash karibu na ile garden, ikabidi tu ni ghairishe safari yangu na kuamua kurudi hapa” Mr Bakari Haneni aliongea.
“Sijui, ila nilikuja nae hadi hapo nje ya geti, sasa sijui ananisubiria au kaamua aondoke zake”
“Kwahiyo huyo mfuatiliaji huju mjua kuwa ni nani?” Tito aliuliza.
“Sijamjua ila namba zake za gari nimezikariri ni T 946 RKK”
“Mkuu, huyo mtu aliekufuatilia wewe ndio huyo huyo alietufuatilia sisi siku ile” Tobi alisema kwakua yeye ndie aliezikariri namba za gari ya Koplo Taure siku ile alipo wafuatilia kutoka Majengo kwenye nyumba yao hadi hapo nyumbani kwa Mr Bakari Haneni.
“Kama ndio huyo huyo mtu mmoja alienifuatili mimi na nyinyi, basi inavyoelekea kuna kitu anataka akichunguze kwetu, sasa nasema hivi, mkiliona popote gari hilo, hakikisheni mtu mwenye gari hilo mna mkamata mnakuja nae mbele yangu au kama ataleta tabu basi mnaweza kumalizana nae huko huko ila vizuri mkija nae hapa ili nimuone”
“Hakuna shaka Mkuu” waliitikia wote kwa pamoja.
“Ok, Tito vipi kuhusu Mrutu na Mzigo wetu, maana tumempa muda wa kutuletea pesa zetu lakini ameamua kuuchezea mwenyewe au unataarifa zozote kuhusu yeye?”
“Hapana Mkuu, sina taarifa zozote kutoka kwake, wala pia hajaleta pesa zetu”
“Safi, watu wakaidi kama hawa ndio nawapenda, sasa sikia si umesema yule mtoto wa kaka yake anaemlea yeye?”
“Ndio mkuu”
“Basi huyo mtoto namtaka leo hii hii akiwa hai, fanya unachoweza”
“Usijali Mkuu, hilo limepita”
“Kwanza naona maskani watoto wakufanya kazi wamepungua kwahiyo namtaka na huyo mtoto nae akasaidiane na wenzake kufanya kazi”
“Hakuna shaka Mkuu”
“Jana daktari niliemuagizia alikuja kwenu?”
“Ndio Mkuu”
“Vipi hali ya mkono wako Tobi?”
“Mkuu, leo kidogo afadhali, viganja ninaweza kuvikunja” Tobi alijibu.
“Hawa washenzi, itabidi walipe kwa walicho kifanya, ila kwanza leo nendeni mkaniletee huyo mtoto halafu hayo mambo mengine yatafuata baadae”
“Sawa Mkuu” Waliitikia wote kwa pamoja na kutoka nje sehemu walipo paki gari yao, wakaingia na kutoa gari nje ya nyumba hiyo.
“Usijali, huyo dogo mimi namjua tangu ana kaa na wazazi wake hadi sasa anakaa na Mrutu, ila kwa Mrutu sipajui inabidi tumfuate shuleni kwao naamini hapo hatuwezi kumkosa” Tito alijibu.
“Anasoma shule gani?”
“Anasoma pale EBEN-ENZER ENGLISH MEDIUM SCHOOL”
“Lakini sasa hivi bado mapema sana, watakuwa bado hawajatoka shule”
“Kwasasa bado hawajatolewa ndio, inabidi sasa hivi tutafute sehemu tuvute muda, kwenye saa nane nane hivi, tunaenda kwenye ile shule, tutamsubiri akitoka na gari ya shule basi hiyo ndio nafasi, tutamchukua humo humo kwenye gari na kuondoka nae”
“Sasa hivi tuna elekea wapi kuuvuta huo muda?”
“Kwasasa twenzetu Mikanjuni Pazuri tukapate maji maana nina siku kama nne hivi sijapata yale mambo halafu pia itakuwa rahisi kwasababu Mikanjui Pazuri na ile shule sio mbali sana kwahiyo hapo itakuwa afadhali kidogo” Tito alipoongea hivyo, aliongeza spidi ya gari ili kuwahi kwenye baa hiyo.
* *
Majira ya saa tisa na nusu alasiri, wanafunzi wanaosoma katika shule ya EBEN-ENZER walitolewa shuleni hapo ili kila mmoja aelekee nyumbani kwako, wale waliokuwa wakiletwa na kurudishwa na gari ya shule wao walipanda katika gari hiyo na walipotimia gari ilianza kutoka shuleni hapo na kuingia barabarani.
Kama siku ya jana alipo simamishwa na watu asiowajua na leo pia ilikuwa ni hivyo hivyo, dereva anaendesha gari ya shule alipigwa mkono na mtu aliesimama katika ya barabara akimtaka asimamishe gari, kwakuwa mtu huyo alisimama katikati ya barabara dereva hakuwa na jinsi zaidi ya kusimamisha gari, hofu, wasiwasi, uoga vyote vilimpata dereva huyu kwa wakati mmoja, maana alijua watu hao ndio wale wale waliokuja jana na kumtaka asimamishe gari bila ya kujua walikuwa wanataka nini.
Tito alishuka kwenye gari walilokuja nalo na kuingia katika gari ya shule, wakati huo Tobi yeye amesimama mbele ya gari hiyo bila ya kuongea chochote, Tito alipoingia ndani ya gari hiyo akaanza kumuangalia mwanafunzi mmoja baada ya mwingine, wanafunzi hao hawakuwa na hofu na mtu huyo kwasababu hawakujua kuwa alifuata nini ndani ya gari hilo, wao wakabaki kumuangalia anatafuta nini. Tito macho yake yalitua katika sura ya Hemedy, Akatabasamu na kuanza kumfuata sehemu alipokuwa amekaa. ENDELEA….
Alipomfikia akamshika mkono na kumuinua, ila Hemedy akagoma kuinuka na kujaribu kuutoa mkono wa mtu huyo asie mjua, Tito alipoona Hemedy anataka kuleta tabu, maana kitendo hicho aliona kama vile ni upotevu wa muda, ni kitendo cha sekunde mbili tu, jikono lenye jiganja jikubwa mithili ya shepe, lilitua katika uso usio na hatia wa hemedy, wanafunzi wote waliokuwemo ndani ya gari hilo walitaharuki kwa kupiga mayowe hafifu ya kuwaita mama zao bila kupenda waliposhuhudia tukio hilo, walianza kupatwa na wasiwasi na mtu huyo alievamia gari yao. Hemedy kipindi hicho viganja vya mikono yake aliviweka juu ya uso wake huku akilia, aliona giza na nyotanyota kutokana na kutohimili uzito wa hilo kofi alilozawadiwa.
“Unafikiri nimekuja kucheza na wewe hapa? Embu inuka tuondoke” Tito aliongea hivyo huku akimuinua tena, safari hii hakuleta tabu maana alihofia kipigo chengine zaidi ya hicho alichopewa.
Akamtoa nje ya gari hiyo na kumpeleka kwenye gari walilokuja nalo, wakati yote yakiendelea, dereva na utingo wake waliwekwa chini ya ulinzi na Tobi kwa kuwanyooshea bastola, kama kawaida yake dereva wa gari hilo na leo pia alijikojolea kama alivyojikojolea jana yake. Tobi baada ya kuona windo lao wameshalitia mikononi, akaacha kuwaweka chini ya ulinzi watu hao na kuelekea kwenye gari yao kwa mwendo wa haraka, alipofika ndani ya gari alimkuta Hemedy akiwa amefungwa kamba za mikono na mdomoni amebandikwa gundi la plastiki liliweza kumdhibiti vizuri kutopiga kelele, akabaki kugugumia huku machozi yakimtoka, hakuelewa watu hao ni wakina nani na wanataka nini kwake, akabaki kusali kimoyo moyo akimuomba mungu wake amnusuru na balaa lolote litakalo enda kumtokea. Gari liliondolewa kwa kasi kubwa na kutokomea pasipojulikana.
Dereva wa gari ya shule baada ya kuganda kwa muda mrefu akiwa bado kaduwaa kwa matukio yanayomtokea, hakuelewa anamkosi gani maana ni mara ya pili hii kufuatwa na watu asio wajua tena wakiwa ni tofauti tofauti, akafikiria kuacha kazi hiyo lakini hapo hapo akakinzana na wazo hilo, hakuwa na kazi nyengine je atakula nini endapo akiachana na kazi hiyo?, umri wake umekwenda hakuwa na uwezo wa kufanya kazi ngumu je atafanya kazi ipi nyepesi zaidi ya hiyo?.
Akachukua simu yake na kupiga polisi, akawataarifu kwa ufupi tukio hilo na kuambiwa asubiri hapo hapo watakuja muda si mrefu, wakati huo watu walioona tukio hilo wakaanza kujisogeza eneo hilo na kumuuliza dereva maswali ya kimbea ili wapate ya kwenda kuwaeleza wasio shuhudia tukio hilo. watu hao wametungwa jina na kuitwa “redio vifua”.
Baada ya dakika kumi, gari ya polisi iliwasili eneo hilo, polisi walishuka kwa mbwembwe nyingi utafikiri walikuwa wanaenda vitani. Askari mmoja almanusura ateguke mguu kama si kuvunjika kabisa baada ya mguu wake kukwama kwenye bodi ya gari hiyo, kama sio mazoezi aliyoyachukua kipindi akiwa depo, leo hii angeaibika mbele ya raia waliokuwa eneo hilo. Koplo Taure alimfuata dereva wa gari la shule na kumsabahi.
“Na leo tumekutana tena sehemu hii hii, enhee, embu nieleze kwa ufupi tukio lilivytokea” Koplo Taure alianzisha maongezi.
“Dah!! Afande hata sijui nikueleze vipi, nahisi nina mkosi mimi sio bure, itabidi niombe ruhusa mara moja ili niende nyumbani kwetu ndipo nije kuendelea na kazi hii” Dereva alijibu kwa masikitiko utadhani ni mwenye kuonewa sana.
“Leo wamekuja watu wengine tofauti na wale wa jana, mmoja akatuweka chini ya ulinzi mimi na utingo wangu, halafu mwengine akaingia humu ndani na kwenda kumchukua yule mtoto uliemfuata jana”
Koplo Taure hakuamini masikio yake baada ya kusikia hivyo, akafikiria kwamba kuwa mtu anaedhania ndie huyo aliechukuliwa na watu hao wasiojulikana, ikabidi aulize vizuri, na kuhakikishiwa kuwa ndie huyo huyo mtoto aliekutana nae katika mazingira ya kifo na kujenga nae urafiki hadi kumchukulia kama mdogo wake wa kuzaliwa nae tumbo moja, mtoto anaemhusudu kuliko mtoto yoyote yule, eti ndio ametekwa na watu hao wasiojulikana.
Ikabidi amuambie dereva awapigie simu uongozi wa shule na kuwataarifu tukio hilo ili walete dereva mwengine kwaajili ya kuwapeleka watoto hao majumbani kwao, halafu yeye aambatane na polisi hao kuelekea kituoni kwaajili ya kutoa maelezo kamili. Dereva alifanya kama alivyoambiwa na baada ya dakika tano akaja dereva mwengine na baadhi ya walimu wa shule hiyo, wakaelezwa kwa ufupi tukio lilivyotokea na baada ya hapo dereva na utingo wakachukiliwa na kuanza safari wakiwa na polisi hadi kituoni.
Walipofika fika wakapelekwa katika chumba maalumu kwajili ya mahojiano. Koplo Taure akatoka humo na kwenda kumpa taarifa Insepekta Ganjo. Inspekta baada ya kusikia taarifa hiyo alichanganyikiwa kwasababu hata yeye pia ana mhusudu sana mtoto huyo wa marehemu rafiki yake, wakatoka wote hadi katika chumba cha mahojiano na kuanza kuwahoji watu hao.
“Mimi nilimuona mtu akiwa amesimama barabarani huku akinipungia mkono, tukio hilo likanikumbusha la jana maana hata jana pia nilifanyiwa hivyo hivyo na watu nisiowajua kama hivi leo ilivyokuwa, na sikua na jinsi ikabidi nipaki gari pembeni ili kumsikiliza shida yake mtu huyo huku nikiwa na wasiwasi huenda ikawa huyu wa leo akawa kama yule wa jana, baada ya kusimamisha gari akaja hadi upande niliopo na kuniamuru nitulie vile vile nilivyokuwa huku akinitishia maisha kuwa nikifanya jambo lolote basi ndio itakuwa ni tiketi yangu ya kuelekea mbinguni, akamuita na na huyu utingo wangu na kutuweka pamoja wote” akameza mate na kuendelea. “walikuwa wawili, huyo mwengine akaingia ndani ya gari letu akatoka na Hemedy na kumuingiza kwenye gari lao, yule alietuweka sisi chini ya ulinzi akaondoka mbio baada ya kumuona mwenzake tayari ameshaingia kwenye gari walilokuja nalo na kutokomea zao” Dereva akamaliza kutoa maelezo yake.
“Walielekea na njia ipi baada ya kufanya tukio?” Koplo Taure alimuuliza.
“Walielekea na njia hii ya Tairi Tatu hadi hapo sikujua tena walipooelekea”
“Unaweza ukaikumbuka gari hiyo ni ya aina gani na namba zake za usajili?” Koplo Taure alimuuliza.
“Ile gari ni Alteza nyeusi na ina namba za usajili zilizosomeka T 196 YRN” Dereva alijibu. Koplo Taure aliposikia maelezo ya hiyo gari alishtuka, ila akajifanya kukausha ili Mkuu wake asijue mshtuko wake, akabaki kujiuliza gari hiyo aliiyona wapi? Maana hizo namba na maelezo ya gari hiyo havikuwa vigeni kwake, ni kama vile alishawahi kuliona hilo gari ila tatizo linakuja aliliona wapi hilo gari?.
“Watu hao walikuwa na silaha wote? na zilikuwa ni zaina gani?” Koplo Taure alimuuliza.
“Sijui kama wote walikuwa na silaha ila mimi nimemuona nayo huyo alietuweka sisi chini ya ulinzi, na pia siijui ni ya aina gani kwasababu mimi sio mzoefu na majina ya bunduki”
“Sawa, ukiwaona unaweza ukawajua kwa sura?”
“Ndio, hata sasa hivi wakija mimi nitawajua” Dereva alijibu kwa kujiamini.
Hadi hapo Koplo Taure hakuwa na swali jengine la kuongeza, akamgeukia mkuu wake na kumkuta akiwa na sura ya mfadhaiko, haikueleweka imesababishwa na mawazo ya kutekwa kwa Hemedy ama ni vipi? Inspekta Ganjo aliinuka bila kusema chochote na kutoka ndani ya chumba hicho akimuacha Koplo Taure asijue afanye nini na watu hao, na yeye hakuwa na jinsi. Akawaruhusu waondoke huku akiwaambia kuwa wakiihitajika kituoni hapo wasisite kuja kwaajili ya kufanya uchunguzi mwengine kama kutahitajika kufanya hivyo, wakaaga na kuondoka zao.
Koplo Taure akakusanya karatasi za maelezo aliyokuwa akiyaandika na kuziweka katika faili, akatoka na kwenda katika ofisi yake ilipo na kukiendea kiti kilichokuwa nyuma ya meza kubwa iliyo kuwa na makabrashi machache yaliyopangiliwa vizuri upande wa kulia juu ya meza hiyo, akakaa kwenye kiti na kuanza kutafakari maelezo aliyopewa na dereva wa gari ya shule.
“Ile gari ni Alteza nyeusi na ina namba za usajili zilizosomeka T 196 YRN” “Hii gari sio ngeni katika fikra zangu, ila sasa sijui nimeiyona wapi?” akapiga kichwa chake kwa kofi hafifu kidogo ili kurejesha kumbukumbu ya kile anachokifikiria, akalaza kichwa chake kwenye meza kwa sekunde kadhaa, alipokuja kukiinua sura ilipambwa kwa tabasamu, “Ni vijana wa Mr Bakari Haneni ndio wenye gari hii” Mawazo yake yalikatika baada ya kuingia mtu humo ndani, mtu huyo alipiga salut na kumuambia kuwa anahitajika na Inspekta katika osifi yake, akatoweka baada ya kufikisha taarifa hiyo akimuacha mtaarifiwa akijizoa zoa kwenye kiti alichokuwa amekaa, akainuka na kuanza kuelekea ilipo ofisi ya mkuu wake.
“Ndio mkuu” Koplo Taure aliongea hivyo huku akiwa amesimama mbele ya mkuu wake. Akapewa ishara ya kukaa na yeye akafanya hivyo.
“Umepata wazo gani kuhusiana na hii kesi ya kutekwa kwa Hemedy?” Inspekta Ganjo alimuulizia huku akimuangalia kwa macho makavu yasio na mzaha hata kidogo.
“Mkuu, naomba uniachie kwa siku ya leo, kesho nitakupa jibu”Koplo Taure aliongea kwa unyenyekevu, maana alishajua kuwa akijibu vibaya huenda yakamkuta makubwa ambayo hakuyatarajia, alijua kuwa mkuu wake ni mwenye kumhusudu sana huyo mtoto.
“Sawa, na vipi kuhusu ule mshtuko wako pindi ukiwa unamuhoji yule dereva wa gari ya shule alipokutajia namba za gari iliyo mteka Hemedy?” Koplo Taure hakutarajia kuwa mkuu wake alimuona pindi akishtuka wakati wa mahojiano yake na dereva, alidhani mshtuko wake aliuficha mbele ya mkuu wake kumbe ulionekana dhahiri. “Mkuu, yale maelezo yake aliyotoa yule dereva wa gari ya shule kuhusu gari iliyomteka Hemedy, ni kwamba hiyo gari mimi naijua na hata watu wake pia nawajua, ila sina uhakika kuwa ndio watu walio mteka Hemedy”
“Watu hao ni wakina nani?”
“Ni vijana wa Mr Bakari Haneni” Koplo Taure alijibu.
“Na kwanini umesema huna uhakika kuwa ndio watu waliomteka Hemedy?”
“Kwavile bado sina usibitisho kwahilo, ila mara nyingi nimewaona wao ndio wanaiendesha hiyo gari”
“Sawa, nadhani umebakisha wiki moja ili unipe ripoti ya uchunguzi wako ulipofikia kuhusu kupotea kwa watoto mitaani. Sasa basi, naomba kesi hizo uziambatanishe na hii ya kutekwa kwa Hemedy, ndani ya wiki hii nataka uniletee majibu yatakayo niridhisha”
“Sawa, Mkuu” Koplo Taure aliruhusiwa kuondoka katika ofisi hiyo ya mkuu wake, akaelekea moja kwa moja katika ofisi yake ama yao na kukiendea kiti chake na kukaa hapo, macho akayaelekeza juu ya dari na kuangalia huko huku akiwaza afanye nini ili apate ufumbuzi wa hilo jambo.
* * * *
Majira hayo, yalimkuta Mrutu akiwa dukani kwake, alikuwa akiongea na simu, akili yake na sikio lake moja, vilikuwa amevipa utulivu ili kusikiliza kile anachoambiwa kwenye simu hiyo, mara ghafla akaanza kubadilika, alionekana kama mtu anaeanza au aliechanganyikiwa, maana aliongea na simu hiyo huku akitetemeka, alipomaliza kuongea na simu, akamuachia duka msaidizi wake na yeye kutoka nje na kuiyendea gari na kuingia humo, akalitoa gari hilo kwa mwendo wa kasi ya wastani, akishika barabara ya mabanda ya papa, akanyoosha na barabara hiyo hadi alipo ipata Duga Mwembeni, akakunja kushoto na kushika barabara ya Tanga Beach, alipofika Mikanjuni Transifoma akakunja kulia na kuitafuta Tairi Tatu, alipofika hapo akakunja kushoto, akatembea kidogo hadi katika shule ya EBENENZER ENGLISH MEDIUM SCHOOL, alipofika hapo akapaki gari pembeni na kuingia ndani ya shule hiyo, akanyoosha moja kwa moja hadi katika ofisi ya mkuu wa shule kwa mwendo wa haraka.
“Karibu Mr Mrutu, karibu ukae” alikaribishwa na sauti ya mwana mama aliekuwa amekaa kwenye kiti cha kuzunguuka, mwili wake ulikuwa upo ndani ya suti ya kike ya gharama, alipachika miwani ya macho huku mkononi akiwa ameshika kalamu anaizungusha zungusha.
“Asante mwalimu” Mrutu alisema hivyo huku akikaa kwenye kiti.
“Habari zako?” Mwalimu alianzisha maongezi kwa salamu.
“Salama tu. Mwalimu naomba unipe hiyo taarifa vizuri, ilikuaje kuaje?” Mrutu alimuuliza mwalimu huyo huku akimtolea macho huku mikono yake iliyokuwa juu ya meza ikitetemeka.
Mwalimu huyo alimuangalia kwa sekunde kadhaa kisha akamuambia“Ni hivi, mtoto wako Hemedy Muheshimiwa Bhachu, ametekwa na watu wasiojulikana akiwa ndani ya gari ya shule wakati akipelekwa nyumbani na wenzake”
“Kwahiyo hamjui amepelekwa wapi?” Mrutu aliuliza swali la kipumbavu. haikujulikana ni kwasababu Hemedy ametekwa au ni uoga wa kutekwa kwa mtoto huyo.
“Kiukweli hadi sasa hivi hatujui lolote, ila tumewaachia polisi wakifanya uchunguzi, naamini kwa vile jambo hili limefika polisi basi tutampata tu mwanao, na….” Alikatisha maneno yake baada ya kuona simu ya Mrutu ikiita. Mrutu baada ya kuitoa simu yake mfukoni,aliangalia ni nani anaempigia, baada ya kulisoma jina akapokea simu huku akitetemeka zaidi. Alisikiliza kwa sekunde kadhaa. Kisha akaropoka kwa sauti kubwa.
“Nooooo!! Msimfanyie hivyoo!!”
Simu ilikatwa na kumuacha Mrutu akitetemeka huku akipambwa na jasho lililokuwa likimtiririka, ni dhahiri kwamba kiyoyozi kilichokuwa kikifanya kazi ndani ya ofisi hiyo, hakikumsaidia kwa lolote, maana jasho lilizidi kumtiririka tu pasi na kukoma.
“Vipi Mr Mrutu?” Mwalimu alimuuliza hivyo baada ya kuiyona hali ya kuchanganyikiwa iliyomtokea ghafla mtu huyo.
“Mwalimu acha mimi niende nitakutafuta baadae” Mrutu aliinuka bila kusubiri jibu lolote kutoka kwa mwalimu huyo, akatoka mbio mbio hadi ndani ya gari na kutulia akimuacha mwalimu akiwa mdomo wazi pasi na kujua nini aongee. Akatoa simu na kuipiga namba aliyotoka kuongea nayo muda si mrefu.
“Haloo” alianza kuongea baada ya kuona simu imepokelewa.
“Sikiliza Mrutu, tulikupa muda mwingi wa kurudisha pesa zetu, ila muda wote huo umeuchezea, kwasasa hivi tupo njiani tukimpeleka mwanao maskani, tukifika huko tutakupigia simu ili uongee na mkuu mwenyewe” sauti ya upande wa pili iliskika ikiongea hayo.
“Jamani, msifanye hivyo mimi pesa zenu nitamirudishia, ila mwanangu muacheni” Ni kweli Mrutu aliongea kwa uchungu mkubwa na alimaanisha alichoongea, kama ingekuwa ana roho ile ile aliyokuwa nayo mwanzo basi angeshukuru maana ingekuwa wamerahisishiwa kazi ya kumpoteza mtoto huyo, ila kwasasa roho yake imebadilika na kujikuta hataki Hemedy adhurike kwa chochote kile.
“Sisi tumetumwa tu kufanya hivi, hatuna maamuzi mengine, kama unapenda huyu dogo asidhurike kwa chochote, subiri tukifika ukiongea na mkuu ndio utajua ni jinsi gani ya kumshawishi ili amuachie huyu dogo” Simu lilikatwa na kumuacha Mrutu akitokwa na chozi kwenye jicho lake moja huku jengine likijiandaa kufanya hivyo maana tayari lilishaanza kutoa ishara hiyo.
Mrutu hakujua afanye nini kwa wakati huo, akabaki akitetemeka na jicho la pili tayari lilishaanza kufanya kama vile lilivyofanya lile jengine, akajikuta bila kupenda akianza kulia, alilia kwa dakika kadhaa kisha hapo akanyamaza na kuchukua simu yake ili ampigie Mata.
Simu ilipopokelewa akamuuliza yupo wapi kwa wakati huo, akaambiwa kuwa ndio anajiandaa kutoka kazini kwake, akamuambia kuwa yeye atamkuta nyumbani kwake, alipomaliza kuongea na mtu huyo, akampigia na Moto na kumuambia wakutane nyumbani kwa Mata, baada ya hapo akakata simu.
Hakujua atawaambia nini, maana watu hao hawakujua kuwa mwenzao anafanya biashara nyengine ya kuuza madawa ya kulevya na hapo ana UHASAMA na tajiri wake anaemuuzia madawa hayo. Akapanga kuificha ishu hiyo, hakutaka wenzake wajue kwamba yeye anafanya biashara hiyo, akapanga kuwaeleza kilichomkuta Hemedy ila atageuza maneno ili aonekane yeye hana hatia hadi kupelekea mtoto huyo kutekwa, ila hata hivyo akajua akiwaelezea hayo, basi wenzake watafurahi kwasababu wao wenyewe walikuwa wanataka wamuue mtoto huyo, kwahiyo hapo itakuwa wamerahisishiwa kazi.
“Nitajua huko huko nini chakufanya, siwezi kuikosa damu yangu”
Alijiwazia mwenyewe huku akiiwasha gari yake, na kuondoka mahala hapo na kuelekea nyumbani kwa Mata. Dakika kumi na tano, zilitosha kabisa kumfikisha sehemu hiyo, akapaki gari lake nje ya nyumba na kushuka humo. Moto nae alikuja dakika hiyo hiyo na kusalimiana, wakatafuta sehemu ya kukaa wakiwa wanamsubiri mwenyeji aje, baada ya dakika kadhaa, Mata nae alifika hadi hapo, akashuka na kuwapa salamu, akaenda kufungua geti na kuingiza gari yake ndani, Mrutu yeye hakufanya hivyo maana alijua hawezi kukaa humo ndani kwa muda mrefu, wakaingia wote hadi subuleni na kukaa kwenye masofa yaliyokuwepo mahali hapo.
“Enhee!! Tuambie unajipya gani mwendhetu?” Mata alianzisha maongezi.
“Hemedy ametekwa” Mrutu alijibu kiufupi.
“Ametekwa na nani?” Moto aliwahi kuuliza.
“Siwajui na ametekwa leo wakati wakiwa ndani ya gari la shule wakirudishwa nyumbani”
“Kwahiyo ametekwa na wendhake?” Mata aliuliza.
“Hapana, wamemteka pekeake, yani walivyosimamisha gari la shule, wakamchukua yeye na kuondoka nae”
“Mimi namuombea wakamuue kabisa huko huko walipompeleka” Moto aliongea hivyo huku akiurudisha mwili wake na nyuma kuegemea sofa alilokalia, Mrutu alimkata jicho la chuki hadi wenzake hao wakamshangaa.
“Vipi kaka, mbona unamuangalia jamaa kwa jicho hilo?” Mata alimuuliza baada ya kuona hajamuelewa kwanini amemkata jicho wakati ameongea kitu ambacho wao wenyewe walikuwa wanataka wakifanye kwa mtoto huyo. Sasa ni vipi mwenzake alipoongea hivyo yeye amemuangalia kwa jicho baya la kuchukizwa na kauli hiyo.
“Tatizo nyie hamjui mnachokiongea ndio maana mnasema hivyo”
“Ndio utuambie thatha ili tujue” Mata aliongea.
“Hao watu waliomteka huyo dogo, wanataka pesa ili wamuachie” Mrutu aliongea kauli ambayo ili wafanya wenzake wacheke sana kwa kumshangaa mwenzao.
“Kwahiyo hicho ndicho kilichokufanya hadi ukaniangalia kwa jicho baya namna hiyo hadi ukanifanya niogope? Sasa hapo tatizo nini, si unawaachia tu wamuulie tu huko huko maana hata hivyo itakuwa wameturahisishia kazi ambayo kila siku sisi tulikuwa tunatamani tuimalize” Moto aliongea hivyo huku akimalizia na kicheko cha furaha. Hakujua tu jinsi gani Mrutu anachukizwa na kauli zake, akatamani hata kumrukia na kumpiga makofi mawili ila akazizuia hasira zake mbele ya mtu huyo anaeongea maneno yanayo mchoma.
“Halafu kuna jambo nataka niwaambie” Mata aliongea hivyo na kuwafanya wenzake wamuangalie, alipoona wote wapo kimya wanamsikiliza yeye akaendelea.
“Ni hivi, leo nimeenda mahakamani kufungua kethi ya madai, ndipo wakanipa karatathi hii hapa(akaitoa kwenye bahasha na kumpa Mrutu) wameniambia wiki ijayo ndio kethi hii itathomwa” Mrutu aliwaambia hivyo wenzake, Moto nae akaichukua karatasi hiyo na kuisoma.
“Mimi niliwaambia kuwa nimekuja kufungua kethi ya kudai mali dhangu, wakaniuliza nadai kwa nani, nikawaeledhea kwa ufupi kuwa namdai marehemu Mheshimiwa Bhachu, walishangaa na kutaka ushahidi, mimi nikawatolea ile kopi ya karatathi aliyoandika marehemu ile siku tuliyomuua, hapo ndipo waliponipa karatathi hiyo na kuniambia watampelekea barua mthimamidhi wa mali hizo ambae ni wewe muda wowote kuanzia muda huo”
“Kwahiyo unataka kuniambia wiki ijayo tunachukua mali zetu” Moto aliongea hivyo huku akiwa na tabasamu lililo karibia kucheka, inavyooneka taarifa hiyo imeusuuza kabisa moyo wake.
“Ndio,(akamgeukia Mrutu na kumuambia) kuhuthu huyo dogo wewe usimuwadhie maana hata thithi tulikuwa tunataka tumuue ila hao watu bila kujua wameturahithishia kadhi, wewe achana na huyo dogo wiki ijayo tunachukua mali dhetu halafu tunagawana na kila mmoja anakuwa tajira maana mali hidho ni nyingi thana”
“Acheni basi mimi niwaage nielekee nyumbani” Mrutu alisema hivyo huku akiinuka.
“Hakuna shaka, wewe nenda tu” Mata alisema hivyo na Mrutu akaondoka.
“Unajua mimi simuelewi kabisa huyu Mrutu” Moto alimwambia hivyo baada ya kuona Mrutu ameshaondoka.
“Achana nae, lile ni wenge tu la kutekwa kwa yule dogo, ila atatulia tu, kwahiyo wewe usiwe na shaka nae”
* * * * Gari ya kina Tito, iliingizwa kwenye lango la ngome ya Mr Bakari Haneni, ngome hiyo ilionekana kulindwa kwa ulinzi mkali, walinzi hao walijua nini wanafanya maana walikuwa makini kuliko umakini wenyewe, walikuwa wameshika silaha kali kali huku wakiranda nazo kila sehemu kwa mtindo wa kupishana, yani huyu akienda huku basi mwingine anaenda kule alipotoka mwenzie.
Gari hiyo ilipakiwa sehemu na kushuka watu hao huku wakiwa wamemshika Hemedy, walimfungua kamba na gundi walilomuweka mdomoni na kumuacha awe huru kutembea mwenyewe, hofu, wasiwasi, uoga na kutetemeka vyote hivyo vilimshika baada ya kuona eneo hilo lilivyo, aliona watu waliokuwa makini muda wote wakitembea huku na huko huku wakiwa wameshika bunduki kubwa kubwa, yeye mambo hayo alizoea kuyaona kwenye picha za video za kizungu.
Aliongozwa kutembea kuelekea ndani ya jengo hilo la zamani, akiwa na uoga mwingi alienda tu bila kupenda maana alihofia kuleta tabu zitakazo sababishia kupokea kipigo kingine kutoka kwa watu hao wasio taka kucheka hata mara moja, hata hivyo alijua hata kama atafanikiwa kuwakimbia watu hao wawili pia asinge weza kutoka ndani ya ngome hiyo inayilindwa kwa ulinzi mkali, akapanga kutii kile atakacho ambiwa ili aone mwisho wake.
Walienda ghorofa ya pili ya jengo hilo na kuingia katika chumba kimoja wapo ambacho Mr Bakari Haneni alikifanya kama ni ofisi yake akiwa sehemu hiyo, waliingia ndani ya chumba hicho na kumkuta bosi wao akiwasubiri, walimuweka Hemedy mbele yao huku wao wakiwa wamesimama nyuma yake.
“Safi sana vijana wangu, mtoto mwenyewe ndio huyu?” Haikueleweka ameuliza hivyo kwa mamlaka aliyokuwa nayo au alitaka uhakika zaidi maana hakukuwa na mtoto mwengine aliyeagiza aletwe zaidi ya huyo.
“Ndio mkuu” walijibu wote kwa pamoja.
“Sawa, mumewasiliana nae yule mjinga?”
“Ndio mkuu, tumempa tu taarifa ya kuwa mwanae tunae sisi kwahiyo yeye asihangaike kumtafuta”
“Sawa, embu mpigie tena uongee nae” Tito akatoa simu na kumpigia Mrutu, alipoona inaita akaiweka sauti kubwa ili wote wasikilize kitakachoongelewa hapo.
“Haloo” ilisikika sauti ya Mrutu kwenye simu, Tito alimuangalia bosi wake na kupewa ishara ya kuendelea kuongea.
“Sikiliza Mrutu, tumekupa muda mwingi wa kurudisha pesa zetu ila wewe umeuchezea kwahiyo tutakuletea maiti ya huyo dogo uizike mwenyewe pindi atakapo kufa kwa kuathiriwa na madawa ya kulevya, maana ataenda kusaidiana na wenzake kufanya kazi ya kuyafunga madawa hayo” Tito aliongea hivyo.
“Hapana jamani msifanye hivyo, mimi pesa zenu nitamirudishia wiki ijayo, haki ya mungu vile naapia, nitazirudisha kweli”
“Mrutu umechelewa sana kwa hilo, subiri tu nikupe uagane na mwanao vya mwisho” Akamuwekea simu Hemedy karibu, Hemedy alianza kulia huku akimtaka baba yake amsaidie kumtoa mikononi mwa watu hao.
“Hemedy usilie mwanangu, nitakutoa tu kwa watu hao, subiri nifanye mpango niwape wanachotaka, utatoka tu”
Ni dhahiri kilio cha Hemedy kilimfanya Mrutu ajione ni mwenye hatia sana kwa jambo hilo ndio maana akaongea kwa uchungu mkubwa, akimpa moyo kuwa ataachiwa muda si mrefu japo kuwa hakuwa na uhakika wa jambo hilo, alijua kuwa ukiingia katika ngome hiyo si rahisi kutoka ukiwa na uhai wako, labda yatoke majivu ya mwili pindi ambapo utakapokuwa mwili umechomwa moto na majivu hayo yatoke kwa njia ya kupeperushwa na upepo. Mr Bakari Haneni alimpaishara Tito aliekuwa bado ameshika simu iliyokuwa ikitoa sauti ya Mrutu, naye aliiyelewa ishara hiyo na kuirudisha simu hiyo karibu yake.
“Tunakupa siku Nne za kurudisha pesa zetu na zikipita hizo siku tutakuletea maita ya mtoto wako hadi mlangoni kwako ikiwa ipo katika hali ya kupendeza machoni mwako, maana tutavibadilisha viungo vyake nikimaanisha miguu tutaishonea sehemu za mikono na mikono tutaishonea sehemu za miguu huku kichwa chake tukikitenganisha na kiwiliwili, naamini hali hiyo utaipenda, na nina kusisitiza tu, ole wako uwaambie polisi chochote, ukifanya kinyume na maagizo tunayokupa basi jiandae kupokea mwili wa huyu dogo kisha utaupokea na mwili wako mwenyewe ukiwa hauna uhai, nikutakie kazi njema” Tito aliongea kauli za kutisha kiasi ambacho Hemedy alikuwa akitetemeka kwa uoga kama simu mbovu iliyoweka mtetemesho pindi ikiita, hakutaka kusubiri atajibu nini alikata simu na kusubiri maelekezo mengine kutoka kwa bosi wake.
“Mpelekeni kwa IBILISI akampumzishe, inavyooneka amechoka sana huyu mtoto”
“Sawa mkuu” walijibu na kumtoa Hemedy kwenye chumba hicho na kumpeleka kwenye chumba kingine kilichofanana na chumba cha kulalia ila humo hakukuwa na kitanda zaidi ya godoro lilowekwa chini ya mkeka huku juu ya godoro hilo kukiwa na mtu alielala juu yake kichwa na kiwiliwili amevielekeza upande wa pili.
“Ibilisi tumekuletea mwanadamu umfundishe maovu ila kwa sasa bosi amesema apumzike kwanza” Tito aliongea hivyo na kufanya huyo mtu alietambulika kwa jina la Ibilisi ageuze shingo yake na kule sauti hiyo ilipotoka. La haulaa!!!! Mtu huyo alifanana kabisa na jina hilo aliloitwa kutokana sura lake jeusi utadhani amepaka oili chafu usoni, alitisha kumtazama kutokana sura lake lilivyobaya, almanusura Hemedy afe kwa mshtuko uliompata baada ya kuona sura la jitu hulo lililofananiana na mazombi yale ya kwenye picha ya WRONG TURN. Kwahakika hata mimi muandishi na kiri hilo kwamba jitu hilo lilikuwa na sura ambayo sikuwahi kuiyona katika ulimwengu huu, naamini kwamba angeamua kuekti muvi za kutisha angepiga hela kuliko kawaida kutoka na jinsi alivyo, subiri nikupe picha kidogo jinsi alivyo, alikuwa na ngozi nyeusi mithili ya giza la kaburini japo kuwa sijawahi kufika huko, sura lake lilikuwa ni baya la kuogofya huku likipambwa na macho mekunde mithili ya nyanya mbivu, kichwani hakuwa na nywele hata moja, naamini mtoto aliezaliwa leo akimuangalia anaweza kupoteza maisha bila ya kutamka neno lolote kwa ubaya wa sura hilo, alitisha, aliogopesha, kwa kumuangalia tu sura yake ilitangaza roho mbaya aliyokuwa nayo.
Baada ya kumleta Hemedy kwenye chumba hicho, wakaondoka huku wakimuacha Hemedy akiwa bado ameganda akimuangalia mtu huyo wa kutisha, sio kwamba alikuwa akimuangalia kwa kupenda, la hasha! Bali alikuwa bado amepigwa na butwaa kwa kuona zombi mtu laivu bila chenga mbele yake, jitu hilo likaanza kumsogelea huku likimtolea tabasamu la karaha lililozidi kuongeza ubaya wa sura lake, tabasamu hilo ndilo lililomgutusha Hemedy aliekuwa bado ameduwaa, tabasamu hilo lilipambwa na meno ya njano kama unga wa binzari, kwahakika hakufaa hata kukaribia kutabasamu maana ndio alizidi kutisha hadi kuwashinda wale walioekti muvi za kutisha za kizungu, akamsogelea Hemedy hadi karibu kabisa, Hemedy alinza kukohoa sana baada ya harufu ya mdomo ya jitu hilo kumuingia puani mwake…
JITU hilo lilicheka sana huku likirudi nyuma kidogo baada ya kuona Hemedy ameshindwa kuvumilia harufu iliyotoka mdomoni mwake, ilielekea alifanya kusudi kabisa kufanya vile maana alirudi nyuma ili kumpa Hemedy apate nafasi ya kupata hewa nzuri.
“Karibu sana dogo, karibu kitandani upumzike” liliongea kwa sauti baya ya kushangaza, sauti yake ilifanana kabisa na zile spika kubwa za muziki zinazowekwa kwenye klabu (Bass) na kufanya Hemedy azidi kuogopa kwa kuhisi kuwa amekutana na malaika mtoa roho.
“Naona unanjaa sana suburi nikakuletee chakula” aliongea hivyo baada ya kumuona mtu anaemuongelesha amekaa kimya pasi na kuongea chochote. Aliinuka pale kwenye lile godoro na kufanya Hemedy aone kitu chengine cha kustaajabisha kwa mtu huyo. Alikuwa ni mrefu kupita kawaida na mwili mkubwa uliyojengeka kimazoezi. Alitoka ndani humo na kumuacha Hemedy pekeake, safari hii alikaa chini kwenye pembe ya ukuta miguu akiwa ameikunja na mikono yake akiwa ameifumbata kwenye magoti yake huku kichwa chake amekilaza juu ya mikono yake, alikuwa analia huku akimuita mama yake mzazi, hakujua amefanya nini hadi kutekwa na watu hao, akaanza kumfikiria baba yake mdogo ana nini na watu hao hadi kudaiwa pesa za watu na kupelekea akachukuliwa yeye, aligutushwa na sauti ya m’buruzo wa kitu chini ya sakafu ya kwenye chumba hicho, akainua kichwa ili ajue ni nini hicho, sura yake ilipambwa na machozi yaliyotiririka mashavuni na kuangukia juu ya sakafu hiyo, mbele yake alikuta sahani ya chakula imewekwa na lile jitu la kutisha, akakiangalia chakula hicho kilikuwa ni ugali na samaki mkubwa aliekaangwa vizuri pembeni pakiwa na mchuzi wa samaki mwingine aliechanganywa humo, macho yake akayapeleka kwa jitu hilo la kutisha na kulikuta likitoa tabasamu la kuogofya Hemedy akayatoa macho yake haraka kwa jitu hilo maana aliiliogopa sana, jitu hilo halikusema kitu likatoka ndani humo na kumuacha Hemedy mwenyewe.
Alibaki akikiangalia hicho chakula, japo kuwa alikuwa na njaa ila hakutaka kula akihofia maisha yake huenda kimewekwa sumu, aliinuka pale alipokaa na kwenda kwenye mlango wa chumba hicho akijaribu kuufungua na kukuta ukiwa umefungwa kwa nje, akarudi pale alipokaa mwanzo na kukaa mtindo ule ule na kuanza kulia akidai anaonewa kwahiyo anataka uhuru wake.
Mrutu alikuwa amekaa sebuleni kwake majira ya usiku, akiwaza ni jinsi gani atafanya ili amtoe mtoto huyo asiye na hatia mikononi mwa wale mabaazazi, hakujua atafanya nini, akapanga kuwashirikisha polisi ila aliogopa vile vitisho alivyopewa, aliogopa kuupokea mwili wake ukiwa hauna uhai kama alivyoambiwa na pia aliogopa kuupokea mwili wa mwanae ukiwa umebadilishwa viungo, vyote hivyo vilimchanganya, akawa amebaki hajui nini chakufanya ili balaa hilo lipite, ‘nitauza duka langu kisha niwarudishie pesa zao’ akawaza afanye hivyo, ‘hapana siuzi duka, ila nitakopa benki kisha niwarudishie pesa zao halafu tukishagawana hizo mali, naenda kuwalipa benki pesa zao, yes, hiyo ndio njia nzuri zaidi’ alitokwa na tabasamu la matumaini lililo fanya ajisikie amani ya moyo.
ila tabasamu lake lilizima ghafla kama mshumaa upulizwapo na upepo, baada ya kukumbuka sehemu ambayo Hemedy amepelekwa.
“Katika ngome hii si rahisi mtu asie husika kuingia na kutoka akiwa na uhai wake, ila kwako imekuwa bahati sana mkuu kukuamini na kuruhusu utoke ukiwa na uhai wako, wote wanaoingia hapa huwa hawatoki na mwisho wao ni kufa kisha miili yao kwenda kuchomwa moto kwenye shimo lile paleee”
Aliyakumbuka maneno hayo aliyowahi kuambiwa na Tito kwa mara ya kwanza kuingia ndani ya maskani(ngome)ya Mr Bakari Haneni, kipindi hicho alikuwa anasindikizwa kutolewa katika ngome hiyo ndipo alipoambiwa maneno hayo.
‘Nitafanya nini?’ ndio swali lililotawala kichwani kwake kwa wakati huo, ile tabasamu lilikuwa tayari limepotea kitambo usoni kwake, uso wake ulipambwa na mashaka yalio changanyikana na uoga, ukweli ni kwamba, Mrutu alikuwa akijuta kwa kila kosa alilowahi kulifanya katika maisha yake, hakuwahi kufikiria kuwa kazi hiyo ingeweza kuja kumuadhibu kwa mawazo kiasi hicho. ‘Nitawarudishia pesa zao halafu ndio nitajua nifanye nini pindi wakigoma kumtoa mwanangu’ alihitimisha mawazo yake na kauli hiyo, akaondoka sebuleni hapo kuelekea chumbani kwake kulala huku akiacha Tv na taa ya hapo vikiwaka vyote kwa pamoja.
Siku iliyofuata. 12:42 Asubuhi. Mtaa wa Majengo Msikitini.
Koplo Taure aliweka kambi kuwinda windo lake, hiyo sehemu aliyokaa hapakuwa mbali na nyumba na kina Tito, aliweza kuona kila kitu kwa nje kwenye nyumba hiyo, alipanga siku hiyo awafuatilie tena ili ajue wanapoenda baada ya kuamka, ila bahati haikuwa kwake, kwasababu alisubiri sana hadi akachoka, akiangalia saa yake ya mkoni ilimuonyesha ni saa tatu na nusa asubuhi na yeye alikuwa hapo tangia saa kumi na mbili asubuhi, akahisi labda watu hao hawakuwa wamelala kwenye nyumba hiyo au watakuwa wamechoka sana kutokana na sababu zao wanazozijua wao wenyewe, akakata tamaa na kuwasha gari lake na kuelekea kituoni, kwa vile mtaa huo na kituoni kwake hapa kuwa mbali, ili mchukua dakika nne tu kufika kituoni.
Muda ambao Koplo Taure anafika kituoni, ndio muda ambao wakina Tito wanatoa gari lao kwenye nyumba yao na kuelekea kwenye mjengo wa bosi wao ulioko mtaa wa Raskazoni, walipofika waliingiza gari ndani ya mjengo huo na kuweka gari kwenye maegesho, wakashuka na kuelekea juu kwenye ghorofa ya pili ya jengo hilo ambapo bosi wao alikuwa amekaa kwenye kibaraza cha sehemu hiyo akiangalia mandhari ya bahari ya hindi.
“Karibuni vijana wangu” aliwakaribisha wakae kwenye viti vyengine vilikuwa sehemu hiyo na kuwagiza wahudumu walete chai ili wanywe kwa pamoja, baada ya dakika kadhaa ililetwa chai ya nguvu iliyo ambatana na vitafunwa ghali, kila mmoja akashika nafasi yake na kuanza kunywa chai hiyo. Baada ya muda walimaliza na wafanyakazi wa nyumba hiyo wakaondoa vyombo vilivyotumika hapo na kuwaletea vinywaji laini ili kusindikiza maongezi ya watu hao.
“Mnjaua muda wote sikunywa chai, nilipanga niwasubiri nyie ili tunywe wote maana sikuwahi kushiriki chakula cha pamoja na nyie hata siku moja” Waliongea maongezi mengi ya kazi yao hiyo ambayo hayakuwa na ulazima kuyaandika hapa. Baada ya kuongea sana Tito akaomba kumuuliza swali bosi wake, akaambiwa aulize tu asiwe na shaka.
“Hivi wewe familia yako iko wapi? Maana sijawahi kumuona mke wako wala mtoto wako humu ndani, kila nikija nakuta wafanya kazi na walinzi tu wajengo hili” Tito aliuliza.
“Aaaa!!! Mimi katika maisha yangu nilibahatika kuoa mwanamke mmoja tu miaka kumi na tatu iliyopita, tuka kaa mwaka mmoja ndipo mke wangu akashika mimba, baada ya miezi tisa mke wangu alijifungua watoto wawili mapacha wa jinsia tofauti, mkubwa alikuwa ni wakiume na mdogo ni wakike, watoto hao tukawapa majina wa kiume tulimuita Ata na wakike tulimuita Atu, baada ya kufikisha miaka saba watoto hao nikawaamisha nchi kwenda kusoma shule na hapo hapo wafunzwe mapigano, na watarudi hapa nchini wakiwa na miaka ishirini na tano, kwa sasa wanamiaka kumi na mbili. Nataka nifanye makubwa sana hapa nchini hapo baadae wanangu wakirudi na ndio maana nimewapeleka Urusi kwenda kusoma na kufundishwa kupambana, najua kwa miaka watakayo kaa huko, wakirudi hapa watakuwa wameiva kwa mapigano ya ngumi na kulenga shabaha, hahahha!!! Tanzania Tanzania, nchi ya kwetu hii, lazima miaka ijayo niwe tajira sana zaidi ya hapa nilipo kupitia watoto wangu” Alihitimisha kutoa historia fupi ya familia yake na mipango yake mibaya ya baadae juu ya nchi hii.
“Na mke wako je? Mbona sijawahi kumuona hata siku moja au ameenda na wanae kuishi nao huko huko Urusi?” Tito aliumuuliza.
“Mke wangu nilimuua mwenyewe kwa mikono yangu nilipokuja kumfumania na mlinzi wangu mmoja wakifanya mapenzi chumbani kwangu, yeye nilimnyonga kwa mikono yangu na huyo mlinzi nilimuua kifo cha kistaarabu sana, yeye nilimkata kata kila kiungo huku akiwa na uhai wake, halafu ndio nikamchinja na nyama zake nikazipika supu nikawapa mbwa wangu wafurahie. et jamani hicho si ni kifo cha kistaarabu kabisa?”
Haaaa!!! Yani kumkatakata mtu kiungo kimoja kimoja akiwa mzima halafu kumchinja na nyama zake kuzipika supu na kuwapa mbwa, hicho ni kifo cha kistaarabu? Nilistaajabu sana na sio mimi tu hata Tito na Tobi pia walistaajabu ila waliitikia tu kwa kuwa bosi wao ndio amewauliza swali hilo.
“Kwahiyo sasa hivi umeamua kuishi mwenyewe tu?” Tobi alimuuliza.
“Ndio sitaki tena kuongeza familia zaidi ya wanangu tu, kwasababu hao ndio najua watakuja kunisaidia baadae”
“Ila lakini watoto wako umewapa miaka mingi sana ya kuishi huko nje, huoni kama wakirudi watakuwa wamekusahau baba yao?” Tobi aliuliza.
“Hapana, tuna wasiliana sana kwenye mtandao wa Skype kwahiyo siwezi kuwasahau wala wao hawawezi kunisahau mimi” Waliendelea na maongezi yao hadi pale wakina Tito walipotaka kuondoka nyumbani hapo kwa bosi wao, wakataka kuelekea baa kwenda kunywa.
“Hakuna shaka nyie nendeni ila mimi sasa hivi naelekea maskani kuna mambo naenda kuyaweka sawa” Mr Bakari Haneni aliongea hivyo huku akipeana mikono na watu wake. Wakatoka na na kuingia kwenye gari yao, wakatoka nje ya nyumba hiyo na kuelekea walipopanga kwenda, walipofika Toyota, wakaona kuna gari nyuma yao ikiwaungia, walipoliangalia vizuri wakaligundua ni gari ambalo sio mara ya kwanza kuwafuatilia.
“Unajua nini Tito, leo tubadilishe baa, tuelekee Tanga Pazuri, kule ni mbali, hapo ndipo tutakapopata uhakika zaidi kwamba ni kweli hili gari linatufuatilia sisi au laa”
Tito aliliunga mkono wazo la Tobi na kuelekea baa ya Tanga Pazuri iliyokuwa maeneo ya Kwaminchi, kuna sehemu walikuwa wakiangalia nyuma kuliangalia hilo gali hawakuliona na sehemu nyengine waliliona, wakajua huyo anaewafuatilia alijua wapi wanaelekea, ndio maana huyo mfuatiliaji alikuwa akiwafuatilia kwa kuwachanganya.
Baada ya mwendo mrefu kiasi walifika kwenye baa hiyo na kupaki gari lao nje ya baa hiyo na wao wakaingia ndani, wakatafuta sehemu iliwawezesha kuona nje ya baa hiyo, waliliona gari iliyokuwa ikiwafuatilia ikipaki mbali kidogo na wao walipopaki gari yao, ila hawakuona mtu yoyote alieshuka kwenye gari hiyo.
“Itakuwa anatutega ili tuondoke aendelee kutufuatilia, si unaona hataki kushuka” Tobi aliongea hivyo huku akiangalia gari hiyo.
“We subiri tu, asiposhuka tuta mfuata pale pale” Tito alisema kwa kujiamini.
“Halafu unajua hili gari sio mara ya kwanza kutufuatilia, si unalikumbuka?”
“Ndio nalikumbuka, hili gari si ndio lile la siku ile lililokuwa likitufuatilia toka kule hom hadi kwa mkuu halafu likatupita mazima kuelekea na Raskazoni Beach, na tulipolifuata likatupotea tena. Nalikumbuka sana na leo lazima tumjue huyu mwenye gari hili”
Wakati wakiwa wanaendelea kulijadili gari la Koplo Taure. Kuna gari jengine lilikuja na kupaki mbali kidogo na lilipo gari lao, na watu wa gari hilo pia hawakushuka kwenye hilo gari, ila wakina Tito hawakulitilia maana sana gari hilo wao wakabaki kulichunguza gari la Koplo Taure.
Baada ya kukaa kwa dakika nyingi bila kushuka mtu yoyote kwenye lile gari lililokuwa likiwafuatilia, wakakata shauri kuwa wamfute pale pale na kumshusha kilazima mtu au watu waliokuwepo kwenye gari hilo, kwavile walishalipia vinywaji walivyotumi japokuwa hawakuvimalizia, wakaanza kuondoka kulifuata gari hilo, kama hatua tano Tobi alirudi hadi kwenye meza waliokuwa wamekaa, akamalizia kinywaji chake na kukimalizia na cha Tito halafu akaondoka kuambatana na Tito aliekuwa akimsubiri, wakaenda hadi katika gari la Koplo Taure na kumgongea kioo cha mbele upande wa dereva.
Koplo Taure hakujua afanye ili kujiepusha na hao watu maana alishajua kuwa wamemgundua, akapanga kuondoa gari kwa ghalfa ila akaona kwenye kioo mdomo wa bastola ukimuangalia yeye, akajua tayari ameshakamatika, hakuwa na jinsi, akafungua mlango wa gari taratibu na kushuka kabisa kwenye gari lake, Tito alikuwa bado amemnyooshea bastola safarii hii alimnyooshea bastola ya kichwa.
“Tulia hivyo hivyo, usijaribu kufanya ujanja wowote, bastola yangu iko tayari kutii kile nitakacho iamrisha, haya niambie wewe ni nani na kwanini unatufuafuatilia?” Tito alimuonya na kumuuliza swali. Koplo Taure hakujua afanye ili kujiokoa na hilo zahma, Tito alipoona Koplo Taure yupo kimya, akaiondoa usalama bastola aliyoishika na kubaki huru kwamba ikiminywa trigger basi ubongo wa Koplo Taure unamwagika sekunde hiyo hiyo.
“Kwahiyo Jamaa ndio umegoma kuongea?”Tito alimuuliza hilo swali huku akiwa ametabasamu. Ila Koplo Taure akabaki kimya pasi na kujibu chochote.
Ghafla kulisikika mlio wa bunduki huku ukiambatana na kumwagika kwa ubongo na kuwafanya watu waliokuwa katika baa hiyo kutaharuki na kuanza kukimbia huku na huko kila mmoja akijaribu kuokoa roho yake…
Ilikuwa ni mshike mshike eneo hilo, watu walikimbia kutoka katika baa hiyo kila mmoja kukimbilia sehemu yake ili kuokoa roho yake. Tito ndie aliekumbwa na taharuki zaidi baada ya kuona mwili wa rafiki yake Tobi upo chini huku kichwa kikiwa mfano wa matapishi ya mgonjwa wa homa ya malaria, kilikuwa kimepasuka na kufanya ubongo uliochanganyikana na damu vyote vikiipamba ardhi ya eneo hilo na kuifanya iwe ni yenye kutisha kuiyangalia. Koplo Taure muda huo alikuwa nyuma ya gari lake amejificha baada ya kutokea shambulizi hilo la kushtukiza.
Tito hakutaka tena kuganda sehemu hiyo, maana alijua kufanya hivyo ni kujihatarishia uhai wake, hakutaka kimtokee kama kilicho mkuta mwenzake, alichofanya yeye ni kujibu mashambulizi huku akikimbia upande ulipo gari lake huku akirusha risasi upande ulipo gari lao, hilo la kujibu mashambulizi kidogo lilimsaidia, maana wavamizi hao walikuwa wakirusha risasi huku wakijificha nyuma ya gari lao. Tito alifika haraka kwenye gari lao na kuingia ndani, akajaribu kuitia funguo kwenye swichi ila akajikuta akipeleka funguo sehemu nyengine, akajaribu tena kwa mara ya pili, mara hii alifanikiwa na kuiwasha gari na kuliondoa sehemu hiyo kwa kasi kubwa almanusura agonge lori la mafuta lililokuwa likija upande huo, aliondoa gari huku akisindikizwa na risasi hafifu za wavamizi hao.
Koplo Taure baada ya kuona windo lake moja limekimbia huku jengine likiwa limebakia mwili dhalili ulio lala chini pasi na uhai, akazunguuuka upande wa pili wa gari lake na kuingia ndani kupitia mlango wa nyuma na kurukia kwenye siti za mbele upande wa dereva na kuwasha gari ili kumfukuzia Tito aliekuwa mbali kwa wakati huo, aliondoa gari mbio kumuungia Tito alipoelekea.
“Shitii!!, tumewakosa wote, ila sio mbaya huyu mmoja tuliemkosa tutampata siku nyengine, hawawezi kutuchezea mchezo wa kifo kutaka kutuua wakati tulikubaliana tufanye makabidhiano ya amani” Tosh aliongea kwa ghadhabu baada ya kuwakosa wakina Tito waliotaka kuwaua kipindi kile walipofanya makabidhiano ya pesa na madawa ya kulevya na watu kule kange.
“Oya Tosh, tusepeni maana wazee hawakawii kuja hapa halafu ikawa kazi nyengine ya kuwakwepa” Kiku aliongea hivyo huku akiingia kwenye gari walilokuja nalo hapo. Gari hili ndio lile wakina Tito ambalo hawakulitilia maanani sana lilivyokuja eneo hilo. Wakaingia wote watatu kwenye gari lao na kutokomea kusikojulikana wakiuacha mwili wa Tobi eneo hilo ukiwa umelala chini.
Polisi walikuja baada ya dakika kumi kutokea tukio hilo, wakachukua maelezo kwa raia walioshuhudia tukio hilo, kisha wakaondoka na mwili wa Tobi kwenda kuufanyia harakati za kuuzika maana haukuwezekana kukaa hata kwa siku moja kwa jinsi ulivyo haribika, baada ya hapo usubirie adhabu au raha za kaburini kama ambavyo viongozi wa kiimani wasemavyo.
Koplo Taure alikuwa yupo nyuma ya gari la Tito alie kuwa akiendesha gari huku akiwa analia kwa kushuhudia kifo cha rafiki yake, hilo lilimpa wepesi Koplo Taure kumfuatilia bila yeye mwenyewe kujua maana hakuwa makini kuangalia nyuma, yeye alikuwa anachotaka kwa wakati huo afike maskani kwao na kumueleza bosi wake mkasa mzima, na hilo ndio lilikuwa ni kosa maana alikuwa akimpeleka Koplo Taure maskani kwao bila yeye kujua.
Aliipita Mwambani Beach na kulitafuta pori ambalo ndani yake ndio kuna ngome yao, kipindi hicho Koplo Taure alikuwa bado akimfuatilia ila sasa aliongeza umakini zaidi, hakuwa karibu nae, maana alihofia kugundulika mapema kupelekea adhma yake kushindwa kutimia, ikiwa yupo mbali nae ila akikunja kona humuwahi na kuendelea kumfuatila taratibu. Kwa mbele kidogo aliweza kuliona jengo kubwa likiwa ndani pori hilo lililozungukwa na miti mikubwa mikubwa, akasimamisha gari na kushuka haraka, akatafuta sehemu ambayo alikuwa akiliona gari la Tito vizuri na kufuatilia kila tukio kwa mbali, aliona gari hilo likiingizwa katika geti kubwa la chuma na geti hilo likafungwa tena, alitembea kwa kunyata hadi karibu na uzio uliozungushia kwenye jengo hilo, akatafuta mti mrefu uliokuwa mbali kidogo na uzio huo na kuupanda, hapo aliweza kushuhudia ulinzi mkali uliokuwa eneo hilo, akayasoma mazingira ya eneo la ndani, aliweza kuwaona watu waliokuwa makini muda wote wakizunguka huku na huko wakiwa wameshika silaha kali ambazo zilipaswa kutumiwa na jeshi ila sio watu wa kawaida kama hao. Aliporidhika kuyasoma mazingira hayo, akaingia kwenye gari lake na kuondoka eneo hilo kuelekea kituoni.
Huku ndani ya jengo hilo, Tito aliposhuka kwenye gari, akaongoza njia ya kuingia ndani ya jengo hilo huku akilia kama mtoto mdogo, walinzi walimshangaa lakini hakukuwa na hata mmoja aliethubutu kumsimamisha na kumuuliza kulikoni, kila mlinzi alikuwa makini na kazi yake. Alifika katika ofisi ya bosi wake na kuingia bila ya hodi, na kumkuta bosi wake huyo akiwa na mwanamke waliokuwa wanafanya wanachokijua wao ndani humo.
“Tito, ni nini unafanya, ni tabia gani hiyo kuingi….” Mr Bakari Haneni aliongea kwa ghazabu huku akipandisha suruali yake, alikatishwa kauli na sauti ya kilio cha Tito, ikabidi amuambie yule mwanamke atoke nje mara moja kisha hapo atamuita pindi akimaliza maongezi na kijana wake, waje kuendelea na kile walichokikatisha.
“Enhe!!, niambie mbona umekuja huku unalia, kuna nini na Tobi yupo wapi?” Mr Bakari Haneni alimuuliza maswali hayo baada ya yule mwanamke kutoka humo ndani.
“Amekufa, Tobi amekufa mkuu” Tito aliongea hivyo huku akilia na kumuacha bosi wake akiwa amegwaya kwa taarifa hiyo.
“U…una..unasemaje?”Aliuliza kwa kigugumizi wakati hakuwa nacho kabla.
“Tobi ameuliwa mkuu”
“Nani kafanya hivyo, nani aliefanya huo upumbavu, niambieeee” Mr Bakari Haneni aliongea kwa ghadhabu huku akimtingisha Tito utadhani yeye ndio amefanya mauwaji ya Tobi.
“Mkuu, siwajui waliofanya hivyo, na sikubahatika kuwaona vizuri”
Mr Haneni akabaki akiwa ametahayari kwa taarifa hiyo, hakujua aulize nini tena, maana alikuwa na maswali ya kuuliza mengi ila hakujua aanze na lipi kati ya hayo mengi, akatuliza kichwa chake na kutaka aelezewe imekuaje Tobi afe wakati wametoka kuagana muda si mrefu, kipindi hicho macho yake yalikuwa mekundu kwa hasira mithili ya taa za gari za nyuma pindi lichunapo breki.
“Tulipoondoka pale kwako, tulipanga tuelekee baa kama tulivyokuaga, ila nyuma yetu kulikuwa kuna gari lililokuwa likitufuata…” akamuhadithia ilivyokuwa hadi kumuweka chini ya ulinzi Koplo Taure, “ndipo hapo niliposhudia Tobi akianguka chini huku kichwa chake kikitawanyishwa kwa risasi, mimi kuona hivyo, nikakimbilia kwenye gari nakuondoka kuja huku” Tito alimaliza kusimulia huku akijifuta kamasi zilizokuwa zikitoka kwenye tundu za pua yake.
“Kwahiyo mwili wake umeuacha hapo hapo?” Alaa!!! Mr Bakari aliuliza swali la kijinga haikueleweka ni kwasababu ya taharuki juu ya kifo cha Tobi au ni hasira alizokuwa nazo.
“Ndio mkuu, unadhani labda ningewezaje kuondoka na mwili wake wakati mashambulizi bado yalikuwa yakiendelea” Tito alijubu kwa ghadhabu kiasi kwa swali hilo la kijinga aliloulizwa.
“Ok, ok, wewe nenda kapumzike halafu mimi nitajua nini chakufanya, ila kesho asubuhi uwe hapa” Baada ya kuambiwa hivyo Tito aliondoka na kuelekea ilipo nyumba yao waliyopewa na bosi ila kwa sasa alikuwa peke yake, hakujua mwili wa rafiki yake itakuwa upo wapi kwa wakati huo, akapanga kurudi kule kule ili akaangalie kama ataweza kuupata mwili huo ila akajua kurudi kule ni kuyafuata matatizo kwa mara nyengine, akalipinga wazo hilo na kuingia nyumbani kwake.
Mr Bakari Haneni hakuwa tena na hamu na yule mwanamke kwa taarifa hiyo aliyopewa punde tu, akaamrisha mwanamke huyo auawe, sio kwamba auawe eti kwakuwa hawakufanya kile walichopanga kukifanya. la hashaa!. Ila ilikuwa ni lazima auliwe hata kama wangefanya kile walichokuwa wanataka kufanya, bila kuhoji wala kuuliza swali, mwanamke huyo aliuliwa kwa kifo cha kidhalili sana ambacho hakikufaa kufanywa na mwanadamu alieumbwa kwa udongo huu dhaifu tunao tembea juu yake kila kukicha, watu hao waliopewa jukumu la kumuua, walimuingilia kimwili hadi kupelekea kifo chake ila hawakukoma kufanya hivyo bali waliendelea hadi pale waliporidhika wenyewe na kuupeleka mwili huo katika shimo tayari kwa kuchomwa moto.
Koplo Taure alipofika kituoni, moja kwa moja alielekea katika ofisi ya mkuu wake na kuingi humo.
“Mkuu, katika uchunguzi wangu, nimefanikiwa kujua wale vibaraka wa Mr Bakari Haneni gari lao lililo tumika kumteka Hemedy, kujua wanapoenda kwenye ngome yao” Koplo Taure aliongea kwa pupa baada ya kuruhusiwa kuongea.
“Mmh mmh!!!, embu jaribu kuongea taratibu na pangilia maneno ili nikuelewe vizuri” Insepekta Ganjo alimuambia hivyo.
“Ni hivi, leo katika uchunguzi wangu wa kulifuatilia lile gari lililomteka Hemedy, nimefanikiwa kujua mahali kwenye ngome yao na nina hisi hapo ndipo Hemedy alipohifadhiwa”
“We si umesema hunipi taarifa yoyote hadi utakapoisha muda niliokupa? Sasa ni vipi uje kunipa taarifa hizo, au tayari ushaikamilisha kazi niliyokupa?” Inspekta Ganjo alimuuliza kwa kumtahariza utafikiri hiyo taarifa aliyoletewa sio nzuri kwenye masikio yake.
“Hapana mkuu, nimekuambia hivi, ili unipe kikosi kitakachonisaidia kwenda kuivamia ile ngome, maana kuna ulinzi mkali na wakimakini, sitoweza kwenda pekeangua pale”
“Sawa, ulikuwa unataka watu wangapi na ni lini utafanya huo uvamizi?”
“Ni kesho mkuu na nilikuwa naomba askari kama ishirini tukasaidiane hiyo kazi”
“Askari ishirini?” Inspekta Ganjo aliuliza kwa tahamaki.
“Ndio mkuu, kwasababu hiyo ngome inalindwa kwa umakini zaidi, sio ya kuiingia kwa mchezo mchezo”
“Ok, nitakupa Askari hao ila muwe makini zaidi”
“Sawa mkuu”
“Unahisi hiyo ngome ni nani mmiliki wake?” Inspekta Ganjo alimuuliza swali la kimtego, kwa akili za kawaida unaweza ukasema swali hilo ni la kawaida lakini haikuwa hivyo.
“Hapana siwezi jua kwasababu sina ushahidi wowote na siwezi kumuhisi mtu yoyote” Koplo Taure ni kama vile alijua kuwa anategwa, maana alilijibu swali hilo kwa ufasaha kama vile ambavyo Inspekta alitaka lijibiwe. Inspekta akatabasamu baada ya kusikia jibu hilo,‘kidogo sasa hivi akili yako inakuwa, na ukiendelea kufanya kazi kwa akili, utakuja kupanda cheo kwa urahisi kabisa’ alijiwazia mwenyewe na kumruhusu aende akapumzike, na yeye akasimama na kupiga salut ya heshima na kutoka ofisini humo kuelekea nyumbani kwake.
* * * *
Siku iliyofuata. 3:26 Asubuhi.
Polisi waliovalia mavazi ya kikazi kazi zaidi walikuwa kwenye magari mawili ya polisi aina ya ‘defender’ wakiwa na silaha kali kali zikiwepo mabomu ya machozi huku vifuani mwao wakiwa wamevalia vazi lisiloweza kuruhusu risasi kupenya likiwa limezunguka hadi mgongoni, vichwani mwao wamevalia makofia magumu yenye vioo kwa mbele yasio ruhusu risasi kupenya kichwani, magotini na viwiko vya mikono walikuwa wamevalia vazi flani la sponji ili hata kama wakitua sehemu ambazo walihitajika kuruka basi wasiumie, huku miguuni wakiwa wamevalia buti kubwa mithili za wale wakata majani ila hizo zilikuwa ni za kijeshi zaidi. Uzito wake mtoto wa miaka kumi hainui. Kiufupi walitisha na walipendeza kwenye vazi hilo, Koplo Taure yeye alikuwa amevaa kama hao askari wengine ila yeye hakuvaa sare za jeshi la polisi, yeye alikuwa amevalia nguo za kiraia.
Walipokamilika wote, safari ikaanza huku wakiukumbuka msemo walio ambiwa na Insepekta Ganjo kuwa umakini katika kazi ndio unahitajika kuliko kutumia nguvu, kwa mwendo waliokuwa wakienda nao, dakika kumi na tano zilitosha kuwafikisha karibu na ngome hiyo, wakashuka kwa haraka na kila mmoja akaangalia upande wake huku wakisikiliza maelekezo kutoka kwa koplo Taure, walikuwa wakisikiliza maelekezo huku wakiwa wamempa mgongo Koplo Taure aliekuwa katika katika yao. “Ina bidi tujigawe watano watano. Watano wa mwanzo wataenda nyuma ya jengo hili na watano wengine wataenda upande wa kushoto na wengine wataenda upande wa kulia na sisi sita tuliobakia tutaenda upande wa mbele wa jengo hili, umakini katika kazi ndio unahitajika, hakikisheni kila mmoja anamlinda mwenzake, kuingia humo ndani, tutapitia kwa kuruka ukuta huo, kupitia kwenye hii miti iliyokuwa karibu na ukuta huo, watu hao wanaolinda ngome hii wapo makini sana, kwahiyo sisi tunatakiwa kuwa makini zaidi yao, sidhani kama wamejua kwamba leo watavamiwa ila nauhakika tutafanya shambulizi la ghafla litakalo waacha wakibabaika, kuingia ndani ya ngome hii tunatakiwa kuingia sawa, nadahini kila mmoja ana saa yake hapa, kwahiyo baada ya dakika tano kuanzia sasa, wote tunatakiwa tuwe ndani ya jengo hili, hawa walinzi wa mwanzo tunatakiwa tuwauwe kwa kutumia visu au roba, hatutakiwi kutumia risasi maana mlio wake utawafanya hao wengine wajiandae na hapo ndio kutakuwa na ugumu wa hii kazi. Narudia tena, umakini katika kazi ndio unahitajika. Go ahead, step by step, make sure you become protecter of your friend”. (Tunaenda hatua kwa hatua, hakikisha unakuwa mlinzi wa mwenzako).
Baada ya maelekezo hayo kila mmoja akashika nafasi aliyopewa, watano wakaenda nyuma ya jengo hilo, watano wakaenda kulia mwa jengo hilo, watano wakaenda kushoto mwa jengo hilo na sita waliobaki wakaenda mbele ya jengo hilo. Walienda kwa mtindo wa kupishana. Wanyuma kabisa anawahi mbele na wanyuma anaefuatia anawahi mbele ya yule wa kwanza halafu anaebaki nyuma pia anafanya hivyo hivyo, walienda kwa mtindo wa miguu ya jongoo. Walipofika karibu na ukuta huo, kila mmoja akapanda katika mti uliokuwa mbali na mwenzake na kuwafanya wafanane na tumbiri wanaovamia shamba la watu la ndizi. Wakiwa huko juu waliweza kuona eneo la ndani na jinsi kulivyokuwa na ulinzi mkali kuliko wao walivyodhani, hapo ndipo kila mmoja akaongeza umakini zaidi kuliko ule wa mwanzo waliokuwa nao, kila mmoja akabaki kuyasoma mazingira ya humo ndani ili muda waliopanga kuingia humo utakapofika ajue anatua sehemu gani.
Muda waliopangiana ulipofika kila mmoja akaruka na kutua juu ya ukuta huo kwa ustadi wa hali ya juu, kiasi kwamba hakukusikika kishindo cha aina yoyote, hapo wakaanza kutambaa ili kuwafikia walinzi waliokuwa wakiranda chini ya ukuta huo, kwa kuwahesabu kila ukuta ulikuwa na walinzi nane na wao waliku watano watano, wakapeana ishara na kuruka kwa pamoja huku kila mmoja akimuwahi mtu wake, wale watatu waliobakia, walikuwa bado wameduwaa kwa tukio hilo hadi wanapata akili ya kushambulia, wakashangaa wakiwa hawana uhai na kubaki chini wakigaagaa na kushika visu viilivyozama shingoni mwao.
Upande wa mbele sehemu walipoingilia wakina koplo taure, walifanya kama walivyofanya wenzao ila kwao mlinzi mmoja alibahatika kukimbilia ndani huku akipiga mayowe ya kuomba msaada, kufika tu ndani jengo hilo, akakutana na Tito aliekuwa anatoka baada ya kusikia kelele hizo, akamtuliza mlinzi huyo na kumuuliza kulikoni, akaambiwa kuwa wamevamiwa, Tito hakuwa na muda wa kuuliza mvamizi ni nani, akatoa simu yake na kumpigia Mr Bakari Haneni kumpa taarifa hizo.
“Sasa nyie chakufanya ni kuwa makini zaidi, hao wavamizi watajuta kuingia kwenye ngome yangu, subirini nafanya kitu sasa hivi, nyie msiwe na wasi kabisa” alijibu hivyo Mr Haneni na kukata simu…
Haikueleweka amesema hivyo kutokana na hasira au uoga wa kuvamiwa kwa ngome yake, maana hakuwa na chakufanya kama alivyosema, akabaki akitetemeka tu, hakujua wavamizi hao ni wakina nani, akaitwaa simu yake na kumpigia Tito ili ajue wavamizi hao ni wakina nani, jibu alilopewa lilimfanya aingiwe na uoga mkubwa kiasi kwamba akitishwa kidogo tu basi ndio utakuwa mwisho wa maisha yake, maana alipewa taarifa kwamba wavamizi hao ni jeshi la polisi ndio lililovamia ngome yake.
Taarifa hiyo ilimchanganya kiasi kwamba kwa mara ya kwanza tangia atengeneze hiyo nyumba yake aiyone ni ndogo, maana hakutulia sehemu moja, mara aende chumbani mara arudi sebuleni mara afungue friji kisha kulifunga tena bila kuchukua chochote ndani humo, alikuwa amechanganyikiwa si masihara, na kilichomfanya kuchanganyikiwa kiasi hicho ni vile jamii ilivyokuwa ikimchukulia ni mtu mwema mwenye kusaidia kila mtu mwenye shida, mwenye kupeleka misaada kila siku kwenye vituo vya kulelea watoto yatima, hadi wengine wakadiriki kusema kwamba mtu huyo kama ataamua kugombea ubunge kwa chama chochote, basi atapita bila pingamizi lolote, sasa iweje leo hii maovu yake yaje kujulikana kwamba yeye ndie anasababisha upotevu wa watoto mitaani kwa kuwateka na kwenda kuwafanyisha kazi za kufunga madawa ya kulevya, jamii itamchukuliaje?, raia wenye hasira kali si wata muua kwa kipigo cha mbwa mdokozi.
Hakutaka yote hayo yamtokee, akapata wazo la ghafla kuwa ahame nchi na kwenda mbali hadi pale zahma hilo litapopita, akapiga simu uwanja wa ndege wa Tanga kwamba anaweza akapata ndege ya kukodisha, jibu alilopewa lilimfurahisha, hakutaka kusubiri, akachukua simu na kumpigia Tito simu kumuuliza hali inaendeleaje huko, na kupewa majibu mabaya kuwa wanazidiwa na jeshi hilo lililofanya shambulizi la kushtukiza, akamuachia maagizo kuwa wajitahidi kupambana nao na mambo yakiwa sawa basi amjulishe kwa njia ya emal, akamdanganya kuwa yeye anajaribu kutafuta namna ya kutoa msaada ila alimuambia kuwa wajitahidi kadri ya uwezo wao, alijiandaa kwa kutaka kuhama nchii hii.
Huku kwenye ngome mambo yalikuwa yamewiva, ilikuwa ni mtafaruku, kila aliekuwepo ndani ya jengo hilo, alikuwa akitafuta jinsi ya kujiokoa mwenyewe. Milio ya risasi ilisikia kila kona ya jengo hilo, ni hivyo tu kwamba jengo hilo liko mbali kabisa na makazi ya watu, lakini ingekuwa ni patashika na kwa raia pia, maana sehemu hiyo haikutofautishwa na uwanja wa vita, japokuwa walinzi wa jengo waliona kabisa wamezidiwa ila hawakutaka kuacha kupambana, walijitolea kufa na kupona hadi mwisho wa mpambano huo. Wale walinzi waoga ndio walikuwa wakiuliwa hovyo hovyo, maana walikuwa wakikimbia huku na huko wakitafuta sehemu ya kutokea, ila bahati haikuwa kwao, kila pande wanayokimbilia walipigwa risasi na kugaagaa chini kama kuku mwenye ugonjwa wa kideri.
Mmoja kati ya hao walinzi waoga waliokuwa wakikimbia pasi na kuelewa waende wapi, aliuparamia ukuta uliozungurushiwa kwenye jengo hilo ili akimbie, ila bahati haikuwa kwake, alitunguliwa na risasi mbili za mgongo, hakuwa na budi kuachia ukuta huo na kujiacha kutoka huko juu kuja chini, akiwa yupo hewani kabla hajua tua chini, hakuwa akiamini macho yake kwamba na yeye leo anakufa, alipotua chini, hakubahatika hata kumuita shangazi yake mahali hapo, ikawa roho na mwili vimeshatenganishwa zamani na risasi zilizo zama kwenye mwili wake.
Wale walinzi waliobakia wote wakawa wapo ndani ya jengo hilo wamejificha kwa tahadhari, huku nje kulibakia na askari waliokuwa nao wamejificha kwenye mapipa ya maji yaliyokuwepo eneo hilo, hadi kipindi hicho hakukuwa na asakari hata mmoja aliedhurika wala kufa kwenye mpambano huo, walikuwa makini na wakilindana wenyewe kwa wenyewe, kipindi hicho hakukuwa na upande uliokuwa ukirusha risasi kwenda popote, kulikuwa kimyaa utafikiri hakukuwa na mpambano uliokuwa umetokea muda si mrefu. Koplo Taure alikuwa akiwapanga askari wake kwa kutumia ishara ili waweze kuingia ndani ya jengo hilo.
Wawili walitoka mbio na kuenda kubana katika mlango mkuu wa kuingilia ndani humo, wakachungulia kwa umakini na kukuta eneo la ndani ya jengo hilo lililokuwa na ukubwa mithili ya uwanja wa mpira wa kikapu likiwa halina mtu yoyote zaidi ya machuma ya kufanyia mazoezi yaliyokuwa eneo hilo, wakawapa ishara wenzao na askari watano wakaenda haraka na kuwapita wale wawili waliokuwa pale mlango, wakazama ndani na kujibanza ukutani, ghafla zilitoka risasi pasipojulikana na kuwafanya askari hao kuuwahi mlango wa kutokea, askari wote watano walijeruhiwa vibaya maeneo mbali mbali ya miili yao, ila walifanikiwa kutoka nje na kupokelewa na wenzao, wakawahifadhi sehemu salama na kupatiwa huduma ya kwanza na askari mwenye utaalamu na tiba.
Koplo Taure akaamrisha kila askari afunike uso wake kwa kofia maalumu za kuzuia sumu yoyote inayosambaa kwa hewa, na askari wakafanya hivyo na Koplo Taure akaamrisha kupigwe mabomu ya machozi ndani humo, ni kitendo cha dakika moja tu, mabomu ya machozi kama ishirini yalikuwa yametapakaa ndani ya jengo hilo na kupiga mabomu mengine sita ya moshi mzito na kufanya eneo hilo kuwa kama vile ni usiku kutokana moshi huo kutanda eneo lote, wakawasha tochi zao walizozifunga kwenye vichwa vyao na kuzama ndani ya jengo hilo, ndani humo kulisikika kelele za vikohozi kila upande, walichofanya askari hao ni kuzifuatilia kelele hizo na kuwashika kama kuku kwenye banda lao, waliwatoa walinzi kumi na moja, na kuwafunga pingu huku wakiwa chini ya ulinzi mkali.
Hiyo ilikuwa ni sehemu ya chini ya jengo hilo, wakahitajika kupanda juu ili kufika juu ya ghorofa ya pili ya jengo hilo, walipanda kwa umakini mkubwa huku moshi ukipungua taratibu na mabomu ya machozi waliyoyapiga mwanzo yakipungua kasi, walipofika sehemu ya juu ya jengo hilo, walikutana na ujia mrefu ulio tenganisha vyumba, ikawa askari hao wana kazi ya kufungua chumba kimoja baada ya chengine kwa tahadhari kuu, walihofia yasije yakawakuta kama yaliyo wakuta wenzao watano, baadhi ya vyumba hawakukuta kitu zaidi ya magodoro yaliyopangwa chini ya sakafu na vyumba vyengine walikuta maboksi ya madawa ya kulevya yamepangwa vizuri.
Walijigawa watatu watatu kwenda upande tofauti tofauti, wakiendelea kusachi vyumba hivyo vilivyokuwa vingi kwenye flow hiyo, askari watatu walikiendea chumba kimoja kwa uangalifu na kujibanza pembeni ya mlango wake, walipeana ishara na mmoja akarudi nyuma kidogo na kuuenda mlango huo kwa kasi kubwa kwa kuupiga teke moja na kupelekea mlango huo ufunguke. Risasi zilirushwa kutokea ndani ya chumba hicho bila mpangilio, bahati yake askari huyo aliwahi kuruka pembeni, na hapo risasi zikaachwa kupigwa na kuwa kimya cha ghafla, askari hao wakapeana ishara na mmoja akatoa kitu mfano wa kiazi na kukirusha ndani humo, dakika hiyo hiyo watu waliokuwa ndani ya chumba hicho wakaanza kukohoa kwa nguvu huku walinzi hao wakiziachia bunduki zao na kufikicha macho yao, askari hao watatu wakazama haraka na bila kuuliza wakaanza kumimina risasi kwa walinzi hao.
Walinzi walikufa huku wakiwa bado wana utamani uhai, walikuwa wapo sita, ndani ya chumba hicho mbele kulikuwa na mlango mwengine ila huu haukuwa umezibwa na kitu chochote, ulikuwa wazi tu, askari hao wakausogelea kwa umakini na kuufika karibu yake na kutulia, ikawa kila mmoja hataki kuchungulia ndani humo akihofia uhai wake, baada ya kutulia kwa sekunde ishirini, mmoja akajitoa kimasomaso na kuchungulia, alikuta kundi la watoto likiwa limejikunyata sehemu moja huku wengine watatu wakiwa wamelala chini hawajiwezi kwa kuathiriwa na madawa ya kulevya, akawaambia wenzake kwamba pako salama waingie tu na wao wakafanya hivyo, wakawapa ishara ya kutopiga kelele watoto hao na kuanza kuwaongoza njia kuwatoa ndani humo huku wale watatu wakiwabeba wao, waliwatoa hadi nje kabisa ya jengo hilo na kukuta gari la hospitali limeashafika hapo kitambo kwaajili ya kutoa msaada kama kutahitajika hivyo, wale watoto walikuwa wapo ishirini na nne, wakaingizwa baadhi yao kwenye gari hilo na wengine wakaingizwa kwenye gari la polisi, kwajili ya kuwapeleka hospitali ili kutibiwa kutokana na kuathiriwa na madawa ya kulevya.
Maiti zilizozagaa huko nje, zilichukuliwa zote na kuwekwa sehemu moja, bunduki zilizokuwa zikitumiwa na watu hao pia zilikusanywa na kuwekwa sehemu moja, na wale waliokutwa ndani ya jengo hilo, walichukuliwa na kupelekwa kituo cha polisi Chumbageni na kuhifadhiwa humo.
Huko ndani ya jengo hilo, Koplo Taure alifika katika chumba kimoja wapo, na kuufungua mlango kwa tahadhari, alipoingia ndani alimkuta Hemedy akiwa amewekwa chini ya ulinzi na jitu la kutisha kiasi kwamba Koplo Taure alihisi jitu hilo ni mzimu.
“Ukifanya ujinga wowote, huyu dogo namuua kwa risasi, unachotakiwa sasa hivi ni kupambana na mimi ili kuokoa uhai wako na wa huyu dogo, najua siwezi kutoka salama humu, kwahiyo nataka nife na wewe, chakufanya ni kutoka ndani ya chumba hiki na kuingia kwenye hiko chumba kinachofuata, chumba hicho kina sehemu nzuri na kubwa tu ya kupambana” Ibilisi kama tumjuavyo, alipomaliza kuongea hivyo, akampa ishara Koplo Taure atoke humo na kuingia kwenye hicho chumba chengine kwajili ya kupambana, na yeye akafanya kama alivyoambiwa, na jitu hilo nalo, likamfunga Hemedy kamba za miguu na mikono na kumuacha humo humo yeye akaelekea katika chumba alichokuwa Koplo Taure, akampa ishara atoe risasi katika bastola alioishika na yeye akafanya hivyo na kuzitupa pembeni, ikawa ni mkono kwa mkono.
Wakabaki wakiangaliana kama majogoo yaliyotoka kupigana vita ya kugombania mtetea. Koplo Taure akapewa ishara ya kumfuata mtu huyo na yeye akamfuta kwa mapigo ya tik taka yaliyotua kifuani mwa jitu hilo, mapigo hayo hayakumuathiri kwa chochote zaidi ya kumrudisha nyuma tu kidogo na kumfanya jitu hilo lijifute vumbi kifuani mwake huku likitoa tabasamu la kuogofya kwa macho ya mwanadamu wa kawaida, Koplo Taure akajitayarisha kwa pigo jengine na kurusha ngumi za haraka haraka zilizo hepwa na jitu hilo kwa ustadi mkubwa.
Akarudi tena nyuma kujipanga, alijua kuwa jitu hilo, likovizuri kwenye mapigano na lilikuwa liko makini sana, aliwaza kuwa akifanya mchezo basi ndio itakuwa ni mwisho wa maisha yake, akajipanga upya na kulifuata tena, safari hii alikuwa akilipiga mateke ya ugoko na buti lake la kijeshi, mbinu hiyo ili msaidia, lakini haikumsaidia hivi hivi, maana jitu hilo lilikuwa likirusha na ngumi nzito zilizokuwa zikimkosa kosa Koplo Taure, jitu lilipoona ngumi zake anazorusha hazifanikiwi lengo, likaanza kitumia nguvu.
Likamshika Koplo Taure na kumuinua juu kisha lika mtupa na ukutani, hakika pigo hilo lilitosha kumnyong’onyeza Koplo, maana hakuweza hata kuinuka kwa maumivu aliyoyapata, likamfuta tena pale alipo huku likitoa sauti ya kukera kama ile ya muungurumo wa radi pindi mvua inyeshapo, likamuinua juu, safari hii alipanga kumvunja kiuno kwa kumpigisha kwenye goti lake, Koplo japokuwa hakuwa na nguvu, ila aliona akifanya mchezo basi pigo hilo kama si kuondoka na maisha yake basi litamfnya atembelee kiti cha walemavu daima, hakutaka yote yamkute, ndio maana akutumia ujanja wa kumng’ata kwenye mshipa wa shingo kwa nguvu.
Jitu lilipiga kelele za maumivu huku likimuachia na kupiga magoti huku likishikilia shingo yake, akaona sasa hiyo ndio nafasi ya kuliua jitu, akalipiga ngumi za kichwa za haraka haraka, likaenda na chini, hapo lilipokea mabuti yenye kilo nyingi, yasiokuwa na idadi ya kichwa, hadi ikawa linatoka damu za pua na mdomo, Koplo alihakikisha tayari jitu hilo limekufa ndipo na yeye alipoacha na kutoka kwenye chumba hicho na kuingia kwenye chumba alichoachwa Hemedy. Alipofika alimkuta Tito amemuweka chini ya ulinzi Hemedy kwa kumnyooshea bastola ya kichwa.
“Hamuwezi mkanichukua hata mara moja, najua kwamba nilazima nife, lakini siwezi kufa pekeangu, ni lazima nife na huyu mtoto, (akamuangalia Hemedy aliekuwa amempigisha magoti chini na kumuambia) dogo sali sala zako za mwisho, maana unaenda kufa muda si mrefu” Tito alimaanisha kusema hivyo, maana muda huo huo aliitoa usalama bastola yake na kusubiri aiamrishe tu ifanye kile anachokitaka.
‘Paaaa!!’ mlio wa risasi ulijirudia rudia ndani ya chumba hicho na kumfanya Koplo Taure apigwe na butwaa kubwa kwa kitendo hicho huku Tito akitoa tabasamu.
Tito alitoa tabasamu la karaha lililochanganyikana na damu iliyokuwa inatoka mdomoni mwake kutokana na kupigwa risasi iliyozama kichwani kwake, Koplo Taure akageuka nyuma na kukuta ni askari ndie aliempiga risasi Tito alietaka kumuua Hemedy, hawakuongea kitu, Koplo Taure alimchukua Hemedy na kutoka nae nje ya jengo hilo.
“Huyu nae ameathiriwa na madawa ya kulevya?” aliuliza hivyo daktari aliekuwa eneo hilo.
“Hapana huyu ni mzima, labda apimwe aangaliwe kama anatatizo lolote” alijibu Koplo Taure na kumkabidhi Hemedy kwa daktari huyo, yeye na askari wengine, wakarudi tena ndani ya jengo na kuanza kupekuwa chumba kimoja baada ya chengine, walitoa maboksi mengi ya madawa na bunduki nyingi zilizohifadhiwa katika chumba kimoja na kuziingiza ndani ya magari yao, wakakusanya na maiti zilizokuwa zimezagaa eneo lote hilo na kuzitia kwenye gari, walipoona hakuna chengine chakufanya, wakalizungushia jengo hilo utepe na kuondoka eneo hilo.
Walipofika kituoni, Koplo Taure akanyoosha hadi katika ofisi ya Mkuu wake na kuingia.
“Koplo, hakuna muda wa kupoteza, chukua askari muwahi uwanja wa ndege, Mr Haneni anataka kutoroka, nimepewa taarifa hizo na askari wa huko nilie muweka kunipa taarifa juu ya safari za mtu huyu atakapotaka kuondoka kwa kutumia ndege, anataka kuondoka na ndege ya kukodi, kwahiyo wahini kabla hajafika uwanjani hapo, maana akifika tutakuwa tayari tumeshamkosa” Insepekta Ganjo alimuambia hivyo baada tu ya kuingia kwenye ofisi yake.
Koplo Taure alitoka mbio na kuwataka askari wapande kwenye gari ili wamfuatilie Mr Bakari Haneni, bila kuuliza wakapanda kwenye magari na safari ya kumfukuzia mtu huyo ikaanza. Magari yaliendeshwa kwa kasi kiasi kwamba ilitisha na iliogopesha kwa kuangalia, yalikuwa yakifika sehemu ya kona, matairi hutoa sauti za malalamiko, dakika kadhaa, wakawa wameshafika eneo la sabasaba, wakaliona gari la Mr Bakari Haneni aina ya Jaguar kwa mbali, likiendeshwa kwa kasi, gari hilo Koplo Taure alilijua vyema kutokana kuna siku aliwahi kulifuatilia, akajua ndani ya gari hilo ndimo alipo Mr Bakari Haneni, wakaongeza mwendo ili kuliwahi.
“Ongeza mwendo, polisi waanakuja” Mr Haneni alimwambia dereva wake baada ya kuona magari ya polisi kwa mbali yakija kwa kasi.
“Sasa mkuu, unadhani tutawakimbia vipi wakati wameshajua kuwa tunaenda uwanja wa ndege, lazima watukamate tu” dereva alimjibu.
“Nimekuambia ongeza mwendo weweee” aliongea kwa ghadhabu huku akiwa bado shingo yake ameigeuza nyuma kuwaangalia polisi hao wanaokuja kwa kasi ya ajabu. Kwavile na yeye alikuwa ni mtumishi tu, hakuwa na jinsi, akaongeza mwendo na kufanya gari hilo likimbie mithili ya mshale ulioachiwa na muwindaji kwenda kumchoma swala wa nyikani.
Polisi nao hawakukubali kuachwa kizembe na gari hilo, na wao wakaongeza mwendo ya magari yao kiasi kwamba magari hayo yakikanyaga hata punje ya mchanga yanaweza kuanguka. Ikawa ni mshikemshike kwenye barabara hiyo, magari yote yalikuwa yapo kasi kupita maelezo. Mr Haneni alipoona magari hayo yana karibia kuwafikia, akachomoa bastola yake na kuanza kushambulia, polisi nao hawakutaka kushambuliwa kizembe wakati na wao pia silaha wanazo, na wao wakaanza kushambulia gari hilo lililokuwa mbali kidogo na wao.
Wakati wa kushambuliana, gari la Mr Haneni likapigwa risasi ya tairi na kupelekea gari hilo likose muelekeo kutokana na kasi lililokuwa nayo, likahama njia na kwenda nje ya barabara na kugonga mti uliokuwa pembeni ya barabara hiyo na kupelekea ajali kubwa iliyoikumba gari hilo baada ya kuugonga mti huo kwa ubavuni na gari hilo kupenduka mara mbili.
Polisi waliwahi mahala hapo na na kukuta damu zimezagaa kwenye gari hilo, walijitahidi kuwatoa watu hao na kufanikiwa, ila dereva akawa hana tena uhai baada ya kipande cha kioo cha mbele kuja kumchoma kwenye shingo. Mr Haneni alikuwa na hali mbaya, alikuwa akitoa mabonge ya damu mdomoni mwake, wakamchuku yeye na dereva wake ambae kwa sasa ni maiti na kuwapeleka hospitali ya Bombo, dereva alipelekwa monchwari huku Mr Haneni akipelekwa chumba cha matibabu kwajili ya kwenda kuwahiwa kabla hali yake kuwa mbaya zaidi na kupelekea kifo, walimuweka kitandani huku akiwa na pingu mkononi iliyo fungwa kwenye kitanda hicho.
Koplo Taure baada ya kufika kituoni, alihitajika kwenye ofisi ya mkuu wake na kuelekea huko.
“Safi sana Afande, naona sasa unaonyesha juhudi katika kazi, na hivyo ndivyo inavyotakiwa askari awe, ukiendelea kufanya kazi kwa kutumia akili kama hivi ulivyofanya naamini utapanda cheo kwa haraka zaidi, enhee, nipe taarifa, kazi imeendaje huko” Inspekta Ganjo aliongea hivyo huku akiwa amepambwa na tabasamu usoni mwake.
“Tumeifanya kazi kwa ukamilifu, sote tumerudi wazima, japokuwa kuna askari watano wamejeruhiwa, ila kwa uwezo wa mungu, watarudi katika hali ya kawaida kwasababu majeraha yenyewe sio makubwa”
“Kuna ambao mmewakamata katika tukio hilo?”
“Ndio mkuu, tumewapeleka kituo cha chumbageni”
“Katika jengo hilo, ni shughuli gani iliyokuwa ikifanywa?”
“Ni kufunga madawa ya kulevya, kulikuwa na watoto wengi waliokuwa wakiifanya kazi hiyo, ila wote tumewapeleka hospitali ya Bombo”
“Na vipi kuhusu Hemedy, nae mmemkuta pia?”
“Ndio mkuu, nae tumempeleka hospitali japo kuwa hakuwa katika watoto hao waliathiriwa na madawa hayo, ila yeye tumempeleka kwa uchunguzi kama anatatizo lolote”
“Huyu Haneni nae, mmemkamatia wapi?”
“Tumemkamata sabasaba kwa mbele kidogo, baada ya gari lake kupata ajali kwa kugonga mti, dereva wake amekufa hapo hapo ila yeye hali yake ni mbaya na tumempeleka hospitali”
“Sawa, sasa hivi chukua askari watano, muende katika nyumba yake mkasachi kila sehemu,(akafungua droo iliyopo hapo katika meza yake na kutoa bahasha) na hiki nikibali cha kusachi nyumba yake, kama ikiwa walinzi wake watahitaji kibali” Akamkabidhi na kumruhusu aende.
Koplo Taure akatoka nje na kuchukua askari watano na kuingia kwenye gari safari ya kwenda kwenye nyumba ya Mr Bakari Hanein ikaanza. Walipofika nje ya jumba hilo, waligonga geti na kufunguliwa na mlinzi wa getini, baada ya kujitambulisha kuwa wao ni askari, wakaruhusiwa kuingia ndani na kuanza kueleza shida yao.
Jumba hilo lilikuwa na ulinzi mkali kutoka katika kampuni flani inayoshuhulika na maswala hayo ya ulinzi, kama walivyotabiri, walinzi hao walitaka kibali na kuonyeshwa, walipo kihakiki vizuri, ndipo waka waruhusu polisi hao kusachi. Walianzia flow ya chini ya jumba hilo, wakaangalia vyumba vyote ila hawakukuta kitu, wakapanda flowa ya juu, pia wakaangalia vyumba vyote pia hawakukuta kitu, ila kuna chumba kimoja kilikuwa kimefungwa, wakawaita walinzi kadhaa wa jumba hilo na kuwauliza chumba hicho kina nini, mbona kimefungwa tofauti na hivi vyengine, wakajibu hawajui chochote kuhusiana na hilo.
Ikabidi watumie nguvu kufungua chumba hicho, wakapanga kuvunja mlango ili waingie ndani humo, baada ya kuminyana na mlango huo kwa dakika kadhaa, ndipo ukatii kufunguka kwa kuvunjwa. Wakaingia ndani ya chumba hicho, kilioneka kama stoo hivi, maana kilikuwa ni kikubwa kilichojaa makorokoro mengi ikiwemo na maboksi kadhaa, wakafungua maboksi hayo na kukuta ni madaya ya kulevya ndio yamehifadhiwa humo, walinzi wenyewe walishangaa, maana hawakuwahi kufikiria kama bosi wao anafanya biashara hiyo haramu inayopingwa duniani kote. Wakayachukua maboksi hayo, kama ushahidi wa kumfungia Mr Haneni mahakamani pindi akipata nafuu, wakaondoka nayo kuyapeleka kituoni.
Mrutu alipewa taarifa ya kupatikana kwa Hemedy na kwenda moja kwa moja hadi hospitali kumuangalia, Kwavile hakukuwa na tatizo lolote alilokutwa nalo, aliruhusiwa kuondoka siku hiyo hiyo akiwaacha wenzake wakiendelea kutibiwa, akaondoka na Mrutu hadi nyumbani kwake, Mrutu muda wote alikuwa na furaha isiyo kifani baada ya kumpata mwanae huyo kirahisi tofauti na vile yeye alivyodhania.
Walipofika nyumbani, alimuuliza maswali mawili matatu kuhusiana na hali yake na kilichomkuta huko, alimuambia kila kitu kilichomtokea hadi kukutana na jitu la kutisha, Mrutu alicheka sana baada ya kusikia hivyo, maana hata yeye pia alimjua huyo mtu wa kutisha kama Hemedy mwenyewe alivyomuita. Mrutu alipata wazo, alijua Hemedy kuishi hapo ni kuendelea kuyaweka maisha yake hatarini kutoka kwa kina Mata wanaotaka afe, akapanga kumuomba Inspekta, Hemedy akaishi kwake kwa kisingizio cha huenda ikawa kuna wengine wanao muwinda huyu mtoto, akampigia simu Koplo Taure ili ampe namba za Insepekta, hilo halikuwa tatizo, akapewa na kuzipiga muda huo huo, akamueleza kama alivyopanga na Inspekta alikubali bila kinyongo Hemedy akaishi nyumbani kwake.
Baada ya kuongea na Inspekta, Mrutu akampa taarifa hiyo Hemedy aliekuwa chumbani kwake akioga, alifurahi sana baada ya kuambiwa akakae kwa Inspekta maana hata yeye pia alipapenda kutokana na kupata watu wa kuongea nao tofauti na hapo kwa baba yake mdogo, alijiandaa haraka haraka na kuchukua nguo zake kwenda kuyaanza maisha upya kwa Inspekta Ganjo, hakusahau flash yake, aliichukua pia. Alipokamilisha kila kitu, wakaanza safari ya kuelekea nyumbani kwa Inspekta, dakika ishirini zilitosha kuwafikisha nyumbani hapo na kuingia ndani ya nyumba hiyo.
“Haaa!! Medy!”
Ilikuwa ni sauti ya Hilda mjukuu wa Inspekta baada ya kumuona Hemedy akiingia nyumbani kwao, alitoka mbio na kuja kumdandia Hemedy mithili ya nyani alieona mgomba wenye ndizi mbivu zenye kutamanisha, bila kumjali Mrutu aliekuwa amesimama akiangalia tukio, hata hivyo Hilda hakujua kwamba mtu huyo ni baba yake mdogo na mtoto huyo, alichojali yeye ni kuidhihirisha furaha yake baada ya kumuona mtu alietokea kumhusudu vibaya mno, baada ya dakika moja ndipo alipomuachia na kuanza kusalimiana nae, Hemedy nae akachukua nafasi hiyo kumtambulisha mtu huyo kuwa ni baba yake mdogo, hapo ndipo Hilda alipozinduka kutoka kwenye ndimbwi la furaha na kuingiwa na aibu kwa tukio alilolifanya mbele ya mtu huyo, akamsalimia na yeye, akapokea begi la nguo alilokuwa analiburuza Hemedy na kuingia ndani ya nyumba hiyo.
Wafanyakazi wa nyumba hiyo, walipomuona Hemedy walifurahi sana kiasi kwamba wakamfanya Mrutu ashangae kwa furaha ya kumuona mwanae, alijilaumu kwa mara nyengine kwa kutaka kumuua mtoto huyo anaependwa na watu kutokana na ucheshi wake, hata yeye mwenyewe pia alikuwa akimpenda sana tu, ila ameamua kumhamisha kwake ili kumlinda na kifo. Watu wa nyumba hiyo walifurahi zaidi baada ya kuambiwa kuwa mtoto huyo amekuja kuishi kabisa kwenye nyumba hiyo, furaha yao ilipelekea hadi kupanga kufanya kijisherehe cha kizushi ili kumkaribisha mgeni walietokea kumhusudu kuliko mgeni yoyote aliewahi kufika nyumbani hapo.
Wakaandaa mazingira ya sherehe hiyo haraka haraka huku wakimsubiria Inspekta arudi kutoka kituoni ili waje kusherehekea wote sherehe hiyo iliyozushwa siku hiyo hiyo, wafanya kazi wa kike walipika vyakula mbali mbali kwa haraka na kwa ustadi mkubwa kuliko walivyowahi kupika kabla, baada ya maandalizi yote kuisha, wakawa wana msuburi Inspekta aje ili waungane wote kwenye sherehe hiyo, muda huo wa kumsubiri Inspetka, Hemedy alikuwa akiwapiga stori ambazo ziliwafanya muda wote meno yao yawe nje kwa vicheko.
Baada ya saa moja kupita, Inspekta aliingia ndani ya nyumba hiyo huku akifuatiwa na Koplo Taure na Afande Jesca, walipewa taarifa ya sherehe hiyo iliyozuka ndio maana wakaja na vinywaji ili sherehe izidi kupamba, Afande Jesca alipoingia sebuleni hapo, alikumbatiana na Hemedy huku akimpa pole kwa maswahibu yaliyo mkuta. Walifurahi wote kwa pamoja huku wakila na kunywa, japokuwa sherehe hiyo haikupangwa kabla ila ilipendeza na kuoneka kama iliyopangwa muda mrefu tu.
Baada ya kufurahi sana hadi usiku wa saa nne, Mrutu aliaga na kutaka kuondoka nyumbani hapo, muda huo huo nae Koplo Taure aliga na kuondoka wakiambatana watatu yani Koplo Taure, Mrutu na Afande Jesca na kila mmoja alielekea kwake, isipokuwa Koplo Taure na Afande Jesca walielekea sehemu moja. Waliobaki waliendelea kupiga stori hadi pale Inspekta alipoenda kulala na kuwaacha wengine wakiendelea na maongezi yaliyonogeshwa na Hemedy hadi majira ya saa tisa usiku, waliondoka mmoja mmoja kwenda kulala japokuwa hawakutaka kufanya hivyo, ila iliwalazimu kufanya hivyo kutokana na siku inayofuta ni wenye kuhitajika kufanya shuhuli za hapo nyumbani.
* * * *
Siku nne zikapita huku Hemedy akiendelea kuishi nyumbani hapo kwa Inspekta, alipewa uhuru wa kufanya chochote hadi akajihisi yupo nyumbani kwao.
Kesi ya Mr Bakari Hanein ilipangwa kusomwa wiki hiyo hiyo kutokana na ushahidi wote kukamilika, watoto walioathiriwa na madawa ya kulevya kiasi fulani walipata ahueni na kukutana na familia zao, wazazi wao walitoa machozi ya furaha kukutana na watoto wao huku wakikilaani kitendo cha Mfahari huyo kuwateka watoto wao na kwenda kuwatumikisha kazi zisizofaa kwa jamii, watoto hao waliruhusiwa kurudi majumbani kwao huku wakisubiria siku ya kusomwa kesi ya Mr Haneni kwenda mahakamani kutoa ushahidi.
Kesi ya Mr Bakari Haneni iliambatana na ya Mata kwenda kudai mali zake kwa marehemu Mheshimiwa Bhachu kama mwenyewe alivyodai. Kipindi hicho Mr Haneni hali yake na yeye iliridhisha kutokana na kuwa hakupata majeraha makubwa mwilini mwake, akatolewa hospitali na kupelekwa kituo cha polisi cha chumbageni kwajili ya kusubiri siku ya hukumu yake.
Siku mbili zilipita na siku hii ilikuwa ndio siku ya kusomwa kesi yake huku ikiwa ndio siku ya Mata kwenda kudai mali zake mahakamani, bahati nzuri au mbaya kesi zote hizo mbili zilihitajiwa kusikilizwa katika mahakama moja, mahakama ya chumbageni. Mata alijiandaa kwajili ya kwenda mahakamani huku Mrutu nae akijiandaa kwenda mahakamani kama msimamizi wa mali hizo, huku nae Mr Haneni akiandaliwa kupelekwa mahakamani kwajili ya kesi yake.
Watu wote hao walikutana mahakamani hapo kwajili ya kesi zao ila kwa Mr Haneni yeye alihifadhiwa katika chumba maalumu kilichopo mahakamani hapo kwajili ya watuhumiwa wanaosubiri kusomewa kesi zao kwa siku hiyo. Umati wa watu ulijaa mahakamani hapo kwajili ya kushuhudia kesi ya Tajiri huyo aliewashangaza wengi baada ya kuisikia kesi yake.
Kesi nyengine ilianza kusomwa mahakamani hapo, baada ya kesi ya kwanza ikafuatia ya Mata, nae akaenda kusimama kizimabani kudai haki yake kama alivyosema, Mrutu alisimama upande wa mdaiwa, na Moto nae alikuwa amekaa kwenye mabenchi yaliyokuwemo ndani ya mahakama hiyo akishuhudia kila kinachoendelea.
Huko nje ya mahakama, Inspekta Ganjo aliongozana na Hemedy kutaka kuingia ndani ya mahakama hiyo, ili kwenda kushuhudia kesi hiyo inayodaiwa kuwa ni kesi ya madai ya mali za baba yake aliekuwa kaburini, hata yeye pia ilimshangaza taarifa hiyo ya kuwa zile mali hazikuwa ni za baba yake wakati yeye alijua fika ni za baba yake, hata hivyo pia alihitajika kuwa kama shahidi yeye akiwa na watoto wengine waliotekwa na kundi la Mr Bakary Hanein kwajili ya kutoa ushahidi.
Wakiwa wapo mlangoni wa kuingilia ndani ya mahakama hiyo, Hemedy alipigwa na bumbuwazi baada ya kumuona mtu alie mshangaza kuwepo humo ndani ya mahakama, akabaki akiwa ameganda mlangoni akimshangaa mtu huyo, hata mtu huyo alipomuona Hemedy, pia alibaki na mshangao akiwa haamini kwamba huyo mtoto anaemshangaa amemfananisha au ndie yeye, Inspekta Ganjo hata yeye pia aliuona mshangao wa Hemedy akijiuliza mtoto huyo ameona nini kinachonfanya kuwa katika mshangao huo…
“Hemedy!! ni wewe kweli?” sauti ya mtu huyo, iliuliza kwa hamaki baada ya kutoamini macho yake, akataka kuamini kwa kuuliza kabisa.
“Nesi. Nesi Maria!!” ni kama vile waliambia watajane majina yao, wote waliuliza kwa hamaki na mshangao wa wazi wazi.
Nesi Maria alienda hadi pale mlangoni ambapo watu hao walikuwa bado wamesimama, akasalimiana na Inspekta maana mtu huyo pia ni mwenye kujuana nae tangia kipindi kile Hemedy alipopelekwa hospitali kwa mara ya pili kwenda kutibiwa baada ya kupokea kipigo kutoka kwa raia wenye hasira kali wakidhani ni mwizi. Nesi huyo ndie aliepewa kazi ya kumhudumia Hemedy kipindi chote alipokuwa hospitali pale, na kutokea kumhusudu sana kutokana na ucheshi wake usio kera na kutamani muda wote awe nae pamoja na leo hii wamekutana tena kwa mara nyengine baada ya kupoteana kwa takribani miezi miwili.
Akamuomba Inspekta atoke na Hemedy nje wakasalimiane vizuri, na yeye bila kipingamizi akawaruhusu waende, hata kilichowafanya watake kuingia ndani ya mahakama hiyo pia walikisahau, akaingia Inspekta pekeake huku Hemedy akitoka na nesi Maria nje, kama angemtilia maanani yule aliekuwa kizimbani amesimama na kumuangalia vizuri, bila shaka pangetokea jambo jengine ambalo lingewashangaza wengi mahakamani hapo, ila ndio hivyo, hakumtilia maana mtu huyo na yeye akatoka na nesi huyo nje ya mahakama hiyo.
“Umekuja kufanya nini hapa?” nesi Maria alimuuliza Hemedy swali hilo baada ya kuongea nae kwa dakika tatu. Hapo ndipo Hemedy alipokumbuka ni kipi kilichomleta mahakamani hapo, hata hivyo akajiambia mwenyewe kuwa, baba yake mdogo yupo, yeye ndie atakae jua nini chakufanya huko ndani.
“Mimi nimekuja kusikiliza kesi, je wewe umekuja kufanya nini?” akajibu na kurudisha swali lile kwa Maria.
“Hahahah!! We Medy umekuja kusikiliza kesi gani wewe, haya lakini, hata mimi pia nimekuja kusikiliza kesi ya huyu tajiri Haneni, na wewe pia umekuja kusikiliza kesi hiyo hiyo?”
“Ndio”
Wakati wakiwa bado wanaendelea kupiga stori. Huko ndani mambo yaliwiva baada ya Mrutu kukubali kuwa mali hizo hazikuwa ni za marehemu kaka yake bali yeye alikuwa ni kama msimamizi tu wa mali hizo, akapigilia msumari kauli yake kusema kwamba, marehemu kaka yake, alishawahi kumuambia hicho kitu kuwa mali hizo sio zake ila kuna tajiri ambae yupo nje ya nchi hii ndio amemuachia kuwa kama msimamizi kwa miaka mingi sana iliyopita, ili ushahidi ukamilike zaidi, wakatoa ile karatasi ambayo walimshurutisha marehemu andike kuwa mali sio zake na kutia saini yake kabisa ambazo kwa sasa ziko mbili baada ya kuzipiga kopi, na kopi alibaki nayo Mrutu na ile halisi aliichukua Mata.
Kutokana na kuwa ushahidi umekamilika na pia Mrutu kukiri hilo jambo kuwa mali hazikuwa ni za kaka yake, basi hapakuwa tena na mlolongo mkubwa zaidi ya kukabidhiwa Mata mali hizo, kwa hakika isingewezekana hata kidogo kuwadhania kuwa walikuwa wakicheza mchezo mchafu mahakamani hapo, kwa jinsi Mata alivyo vaa, bila shaka ungesema ni kama mfanyakazi wa benki kuu ya dunia au ni mkurugenzi wa kampuni fulani kubwa nchi za nje, alikuwa amevaa suti ghali ya rangi ya kijivu ikinogeshwa na tai nyeupe iliyokuwa ikioneka kwa uchache kifuani mwake, huku chini akiwa amevaa viatu vikali vilivyo ng’arishwa kiwi kiasi kwamba viliumiza macho wakati vikipigwa na mwanga wa jua ukiwa unaviangalia na vilikuwa mithili ya kioo kwajinsi vilivyoweza kuonyesha taswira mbalimbali zilizokuwa zikioneka.
Alikabidhiwa mali zote mahakamani hapo na Mrutu akatia saini yake kwenye karatasi fulani aliyopewa na karatasi hiyo hiyo ikapita kwa Mata na yeye apia akatia saini yake, ikawa hadi hapo, Mrutu amekwisha kabidhi mali hizo kwa Mata na kesi yao ikaisha hapo na kila mmoja akaondoka kivyake.
Huku nje ya mahakama hiyo, Maria na Hemedy walikuwa wakihitimisha maongezi yao, baada ya ule muda wa kesi ambayo iliwafanya kuwa mahakamani hapo kufika, nesi Maria alijaribu kumuuliza kuwa Hemedy ana simu ili aweze kupata mawasiliano nae, lakini jibu alilopewa lilimnyong’onyeza baada ya kujibiwa kuwa hana simu, hakutaka tena kupotezana na mtoto huyo tena, ila hakuwa na jinsi ilibidi iwe hivyo maana Hemedy hakuwa na simu kweli, wakachukuana wote kwa pamoja na kuingia ndani ya mahakama hiyo ili kuisikiliza kesi ya Mr Haneni.
Ukafika ule muda uliokuwa ukisubiriwa na wengi mahakamani hapo, muda wa kusomwa kesi ya Mr Bakari Haneni, watu walitulia kimya huku wakisubiri mfahari huyo aletwe kizimbani kusomewa mashtaka yake, baada ya dakika tano, akaingizwa ndani humo, kila mmoja alikuwa akimuangalia kwa chuki kuu huku wakitamani akishasomewa mashtaka yake na hukumu ikipita, basi waachiwe mtu huyo wamfanye kile ambacho kwao kitapunguza machungu kwa kiasi fulani kwenye mioyo yao.
Akapandishwa kizimbani na kuanza kusomewa mashataka yake na kuulizwa kuwa amekubaliana na hilo au anapinga hayo mashtaka? Chaajabu akataka uletwe kwanza ushahidi wa mashtaka hayo, wakaletwa watoto wote waliokuwa wametekwa na vijana wa tajiri huyo na kukiri kwamba tajiri huyo walishawahi kumuona kwenye ngome waliokuwa wametekewa na yeye ndie mkuu wa kikosi kile, pia uliletwa ushahidi uliopatikana nyumbani kwake wa madawa ya kulevya, na kama hiyo haitoshi, pia alishtakiwa kwa kufanya mauwaji ya watu wengi sana kwa siri, baada ya ushahidi wote huo kuletwa mbele yake, akaulizwa tena kama ana chakupinga kutokana na mashtaka hayo.
Chakushangaza, akayakubali mashtaka hayo, ikimaanisha kwamba, amekubali madawa ya kulevya yaliokutwa nyumbani ni yake, amekubali ni kweli yeye ndie aliekuwa akiwateka watoto na kwenda kuwafungia katika ngome yake na kuwafanyisha kazi hatari na mbaya ya kufunga madawa hayo, amekubali kuwa ni kweli alishaua watu wengi sana bila makosa ya aina yoyote, kila mtu aliekuwa mahakamani hapo alishikwa na ghadhabu kwa mtu huyo, watu wote walitamani hata mahakama itoe hukumu ya kuachiwa mtu huyo kwao ili wamfunze adabu kwa kile alichokifanya, watu wote wakasubiri waone hakimu atatoa hukumu gani kwa mfahari huyo.
Hakimu aliwaambia kuwa wawaachie nusu saa ya kwenda kujadili na baraza la mahakama kuhusu hukumu ya mtu huyo, wakachukuana baraza la mahakama na kuingia katika chumba flani kilichopo hapo hapo mahakamani na kwenda kujadili hukumu hiyo. Baada ya nusu saa, walitoka wote na kila mwana baraza alikaa katika sehemu aliyokaa mwanzo wakimuacha hakimu akienda kaa katika sehemu yake.
“Mmm mmm!!” Hakimu alijikohoza kidogo kuweka koo lake vizuri ili aweze kusema hukumu hiyo, kisha akaendelea baada ya kuona mahakama nzima ipo kimyaa kiasi kwamba hata kishindo cha sisimizi kiliweza kusikika pindi atembeapo ndani au nje ya mahakama hiyo kwa muda huo.
“………….baraza la mahakama limekaa na kujadili juu ya hukumu ya Mr Bakari Haneni kwa makosa yanayomkabili, kwakua ushahidi umeonekana na hata yeye mwenyewe pia amekiri ilo, mahakama inampatia adhabu ya kifungo cha maisha na kazi nzito mpaka pale atakapo fikisha umri wa miaka sitini na tano, ndipo adhabu ya kufanya kazi nzito itaisha ila kifungo kitaendelea hadi kifo chake” hakimu alihitimisha adhabu ya mkwasi huyo na kugonga nyundo akimaanisha kwamba adhabu imepita.
Watu wengine walilipuka kwa furaha huku wengine wakishikwa na ghadhabu kutokana na adhabu aliyopewa, wao walitaka mahakama itoe hukumu ya kunyongwa kwa mtu huyo, ikiwa hukumu hiyo kwa nchi ya Tanzania ilishafutwa zamani sana. Watu waliotaka Mr Haneni anyongwe walianzisha vurugu mahakamani hapo na kufanya kusiwe na maelewano tena, watu hao walitaka kumfuata mfahari huyo hapo hapo kizimbani ili wamtoe na kumuadhibu wenyewe, ila kwajitihada za jeshi la polisi lililokuwa mahakamani hapo, waliwazuia watu hao na kumtoa mkwasi huyo huku wakiwa wamewadhibiti watu hao vizuri, pamoja na hayo pia hawakuacha kumzibiti mkwasi ili asiweze kuwatoroka askari.
Askari walifanikiwa kumtoa nje ya mahakama ili wampakize kwenye gari la wafungwa tayari kumpeleka katika gereza la Maweni. Watu ndio walizidi kuchachamaa wakiwataka askari hao wawaachie mtu huyo wamuadhibu wenyewe, kipindi hichi watu ndio waliongezeka zaidi kiasi kwamba asakari waliona dhahiri wanaenda kushindwa na watu hao, ikabidi waombe msaada kwa askari wengine, na kwavile kituo cha polisi hakikuwa mbali na mahakama hiyo, askari walikuja haraka wakiwa wengi kama kumbikumbi kipindi cha mvua, mikononi mwao wakiwa wameshika mabomu ya machozi huku wengine wakiwa wameshika viboko.
Walipofika hapo hawakutaka kuuliza kuna nini wala nani na nani ana nini, walichofanya wao ni kutembeza kipigo huku wakiwazawadia na mabomu ya machozi, hilo lilisaidia, maana kila mmoja alikimbia kwa njia yake huku wakitoka machozi kama mtoto mchanga alieachishwa ziwa na mama yake ingali muda bado wa kufanya hivyo, baada ya sekunde thelathini katika uwanja huo wa mahakama hapakuwa na raia yoyote aliesalia hapo. Wasubiri nini wakati walishapata kile walichokitaka kutoka kwa askari hao? Kipigo ndicho walichokuwa wakikitaka, ni wazi kwamba walijua wakianzisha fujo mahali hapo, basi jeshi la polisi haliwezi kuwachekea tu kwa wanachokifanya, ilikuwa ni lazima watulize ghasia kwa namna yoyote ile. Gari la magereza liliondoka na wafungwa waliotoka kuhukumiwa siku hiyo, kuelekea gereza la maweni kwajili ya kuwapeleka wafungwa hao kuanza maisha mapya sehemu hiyo, Mr Haneni alikuwa ni mmoja wa wafungwa hao wanaopelekwa.
Mata na wenzake walipotoka mahakamani, walielekea moja kwa moja nyumbani kwa Mata, walipofika nyumbani hapo, kila mmoja alichukua nafasi yake sebuleni hapo huku akiwa na uso wenye tabasamu kuu.
“Thiamini, thiamini kabitha kama leo hii nimekuwa tajiri, dah mungu mkubwa thana” Mata aliongea kwa furaha.
“We acha tu, hunishindi mimi, yani hapa natamani tugawane hata sasa hivi, yani nikipata hizi hela, kwanza nanunua nyumba Kwaminchi maana eneo lile nalitamani sana kuishi, halafu nanua gari kali la kutembelea kisha natafuta mtoto mzuriiii nimuweke ndani, maana nishachoka maisha haya ya ubachela” Moto aliongea hivyo kwa furaha hadi jino lake la mwisho lililokuwa bovu likaoneka.
“Ila kumbukeni ile nyumba ya kaka na yale magari yaliokuwepo pale nyumbani havipo katika mgawo, hapa tutagawana zile sheli za mafuta na ile showroom ya magari basi” Mrutu aliongea hivyo.
“Hivyo vitu havina tatizo, tunalijua hilo kuwa zile ni mali za urithi, kwahiyo vile utajua wewe mwenyewe au sivyo Mata” Moto aliongea.
“Ndivyo”
“Halafu wakati natoka pale mahakami, nilimuona yule dogo, kumbe na yeye pia alikuwa ametekwa na kundi la Mr Haneni” Moto haikuelewa aliuliza au aliongea.
“Dogo yupi?” Mata alimuuliza.
“Hemedy, mtoto wa Mrutu hapa, ambae tulitaka tumuue” Moto alijibu, Mrutu roho ikampiga paaa!! Akajua tayari Hemedy ameoneka na kinachofuta hapo ni mipango ya kumuua ndio itakayoongelewa.
“Anhaa!!! Thatha tunamfanyaje huyu mtoto, au tumuache tu maana kama ni mali thithi tayari tumeshazipata haina haja tena ya kumuua, au kuna haja ya kufanya hivyo?” Mata aliongea na kuuliza swali.
“Inabidi afe, kwasababu uhai wake ni hatari kwetu, anazijua sura zetu yule” Moto aliongea, Lakini alimfanya Mrutu achukukie kupita maelezo kwa kauli hiyo.
“Oya, sikilizeni niwaambie, yule dogo hafi, sasa afe kwasababu gani wakati mali tayari tunazo sisi?” Mrutu aliongea kwa ghadhabu kiasi kwamba wenzake pia wakamshangaa.
“Kumbuka yule dogo anazijua sura zetu lakini, anaweza akatuona sehemu mbaya halafu ikawa ni hatari kwetu” Moto aliongea.
“Wewe unasema anazijua sura zenu, una uhakika gani na hilo? Hapana yule dogo hafi na kama akifa labda nisijue nini kimemuua la sivyo tutaleteana Uhasama wenyewe kwa wenyewe” Mrutu alizidi kuongea kwa ghadhabu huku akiwa macho yake ameyatoa kuwaangalia watu hao, aliogopesha, alitishia, yani kama angekuwa akimuangalia mtoto anaekataa kunywa dawa, basi kwa macho hayo angekunywa dozi nzima kwa siku moja, alifanya hivyo kuwaonyesha msisitizo wa kile alichokisema.
“Mmmhh!! Basi kaka hatokufa kama unavyotaka” Moto aliamua kumshusha hasira kwa kumuambia maneno hayo, kwahilo alifanikiwa, maana mrutu alirudi katika hali aliyokuwa nayo mwanzo.
“Ok, thatha vipi, kuhuthu kugawana hidhi mali?” Mata aliwauliza wenzake swali hilo, haikujilikana aliuliza hivyo ili kupotezea mada iliyopita au ni kiherehere cha kutaka wagawane mali hizo.
“Sasa hivi muda umeenda sana, natakiwa niwepo dukani maana yule msaidizi wangu anaumwa, kwahiyo anataka akapumzike, mambo hayo tutayaongelea siku nyengine, ila acheni mimi niende” Mrutu aliaga na kuondoka mahala hapo na kuwaacha wawili.
“Unajua mimi huyu Mrutu simuelewi kabisa yani na sio leo tu tangia muda naona kabadilika sana yani” Moto aliongea.
“Mimi mwenyewe nilikuwa namuona muda tu hadi nikashikwa na hofu kwamba mahakamani anawedha kutubadilikia”
“Ila bwana mimi siwezi kumuacha yule dogo hai, nitamuua kwa njia yoyote ile, tena wala asinitishe kabisa, mimi mwenyewe mtemi vile vile kama yeye anajifanya mtemi, tena asituchimbie biti, ohoooo! mimi nilikuwa namuangalia tu pale anavyoongea kwa kibesi” Moto aliongea sana, nahisi yote hayo kwasababu Mrutu alikuwa hayupo, ila kama angekuwepo sidhani kama angeweza kuongea yote hayo.
“Hata mimi nakubaliana na wewe ni ladhima tumuue tu”
* * * * Inspekta Ganjo na Hemedy baada ya kuondoka mahakamani walielekea moja kwa moja hadi nyumbani kwake, wao waliwahi kuondoka baada ya kuona vurugu linaanza pale mahakamani, Ganjo yeye ni askari polisi, kwahiyo alijua ni nini kitafuta baada ya vurugu lile, ndio maana akawahi kuondoka akiwa na Hemedy mapema. hata kama yeye ni Inspekta, lakina askari wale wasingeweza kumgundua mapema, kwahiyo na yeye kichapo kingemuangukia bila kujali cheo chake.
Siku hiyo ikapita, ikangia siku nyengine na siku hii mpya ilikuja na taarifa ya kuwa Hilda anahitajika Daresalam kwa Mkuu wake(mdogo wake na Inspekta Ganjo) mwanamke huyo alimuhitaji Hilda akaishi nae kutokana yeye hakubahatika kuwa na mtoto, kwasababu hakuwa kizazi kutokana na matatizo ya kiafya. Inspekta hakupinga, akamtaarifu Hilda taarifa hiyo, ila ilipingwa vikali akidai hawezi kuondoka na kumuacha Hemedy hapo, kwahakika mtoto huyu alikuwa ni mwenye kumhusudu mtoto mwenzie kupita maelezo.
Inspekta akamueleza mdogo wake taarifa hizo, kwakuwa mwanamama huyo alitaka sana Hilda akaishi kwake, basi akaomba kama kuna uwezekano Hilda aje na huyo mtu aliedai hawezi kuondoka na kumuacha, taarifa hizo akafikishiwa Hemedy na yeye akakubali kuondoka ila akataka kwanza apewe taarifa hizo baba yake, hilo halikuwa tatizo, Mrutu alifikishiwa taarifa hizo na yeye akazipokea kwa furaha na kuruhusu Hemedy aondoke hata siku hiyo hiyo, alikuwa na furaha kwasababu alijua hiyo itamuweka Hemedy salama na wakina Moto wanaotaka kumuua.
Taratibu zikafanywa haraka haraka pamoja na kuwaombea uhamisho wa shule watoto hao, baada ya kila kitu kukamilika, siku ya safari ilipofika, watoto hao wakasafirishwa kuelekea katika mji huo pendwa wa Daresalam, masaa sita yalitosha kuwafikisha katika mji huo, wakashuka kwenye basi walilopanda, walikuja kupokelewa hapo stendi ya mabasi Ubungo na kijana. Akawapakiza kwenye gari yake na safari ya kuelekea Kinondoni, sehemu ilipokuwa nyumba ya huyo mkuu wake Hilda ikaanza.
Hapo hapo stendi kulikuwa kuna gari aina ya Nisan Murano, iliyopakia mahala hapo, ndani yake kulikuwa na vijana wawili waliokuwa wakimuangalia Hemedy kila alichokuwa anakifanya mahala hapo kabla hajaondoka na kijana huyo aliekuja kuwapokea, baada ya kuondoka gari lililokuja kuwachukua watoto hao, ndipo kijana mmoja akainua simu yake na kupiga namba anazozijua yeye, kisha simu akaiweka sikioni kusikiliza upande wa pili.
“Sawa, endeleeni kumfuatila kila nyendo zake mtoto huyo, msije mkafanya uzembe kama ule mlio ufanya kule Tanga, kuweni makini na mtoto huyo, kiongozi atakasirika kama alivyokasirika mlipofanya uzembe hadi akatekwa na wale vijana wakati yupo katika basi la shule” ilisikika sauti yenye mamlaka upande wa pili.
“Sawa, nawaamini kwahilo, naamini kazi itakuwa rahisi kuliko vile alivyokuwa kule Tanga, kwahiyo namitakia kazi njema” simu ilikatwa na vijana hao wakawasha gari na kuanza kulifuatilia gari lililokuja kuwapokea wakina Hemedy
ENDELEA..
Vijana hao waliendelea kulifuatilia gari lililokuja kuwapokea wakina Hemedy, walilifuatilia hadi lilipoingia katika nyumba moja kubwa ya rangi nyeupe na wao wakapaki gari yao mbele kidogo na nyumba hiyo na kutulia hapo. Huko ndani ya nyumba hiyo, walishuka kwenye gari na kuanza kuingia ndani ya nyumba huku mabegi yao yakiletwa na kijana alieenda kuwapokea stendi, waliingia sebuleni na kukaa hapo baada ya kutomkuta mtu yoyote mahali hapo, baada ya sekunde kadhaa alitokea mwanamke wa makamo, mwanamke huyo alikuwa ni kibonge, mfupi, mwenye rangi ya maji ya kunde, Hilda alipomuona mwanamke huyo, aliinuka kwenye sofa alilokaa na kwenda kumkumbatia kwa furaha.
“Za safari wanangu?” aliwauliza swali hilo baada ya Hilda kumuachia kumkumbatia.
“Salama tu, shikamoo” walijibu wote kwa pamoja.
“Marahaba. Haya niambie za huko” aliongea mama huyo huku akichezea nywele za Hilda aliekuwa amekilaza kichwa chake kwenye mapaja yake wakiwa wamekaa kwenye sofa jengine, tofauti na lile alilokaa Hemedy.
“Nzuri tu, hatujui za hapa” Hilda alijibu, mwanamke huyo alikuwa na furaha ya hali ya juu baada ya Hilda kuwa nyumbani kwake, mtoto huyo alimtaka tangia mama yake alipofariki, ila Inspekta Ganjo, aliweka ngumu kwa kudai asubiri kwanza akue kue, na leo hii yupo nyumbani kwake alikuwa na furaha ya aina yake.
“Baba na wewe unaitwa nani?” Mkuu wake Hilda alimuuliza Hemedy.
“Hemedy, Hemedy Bhachu Mheshimiwa” alijitambulisha Hemedy majina yake yote matatu utafikiri aliambiwa afanye hivyo.
“Karibu baba, karibu jisikie upo nyumbani”
Waliendelea na maongezi hadi pale chakula kilipokuwa tayari na wote watatu wakaelekea mezani kwenda kula. Walipomaliza kula, kila mmoja akaonyeshwa chumba atakachokitumia hapo, na kila mmoja aliingia katika chumba alichopewa kwenda kufanya anayoyajua yeye mwenyewe. Siku mbili mbele, Hilda na Hemedy, walienda kuanza shule, darasa lile lile la tano waliloishia huko Tanga.
Tanga. Nyumbani kwa Mata. Saa 6:00 Mchana.
Siku hii walikutana tena kwajili ya kupanga mipango yao ya kuuza mali zao.
“Inabidi tuziuze hizi mali kama tulivyo kubaliana, kisha tugawane pesa zitakazo patikana” Mrutu aliongea.
“Hilo ndio la muhimu, sasa mtu wa kununua vitu vyote hivyo, atapatikana wapi?” Moto aliongea.
“Mimi kuna tajiri mmoja nimempata, anatokea Arusha, amethema atanunua hizo sheli dha mafuta, ila akathema akija kuziangalia hidho sheli, bathi ataangalia na hiyo showroom ya magari, kama ataikubali, bathi atainunua nayo” Mata aliongea.
“Huyo tajiri umempatia wapi?, asije akawa ni tapeli” Mrutu aliongea.
“Huyo nimempata mtandaoni, baada ya kutoa tangadho kwenye webthite yangu, ndipo akachukua namba yangu na akathema kesho kutwa atakuja huku Tanga kuja kudhicheki hidho kampuni”
“Basi sio mbaya, ili mradi kila kitu kiende sawa”
Wakafunga kikao chao na kila mmoja akaondoka zake kuelekea anapopoajua yeye huku wakiisubiria hiyo siku atakayo kuja huyo tajiri kutoka Arusha kuja kununua hizo kampuni.
Siku mbili hazikuwa nyingi, siku ya siku ikafika na kweli huyo tajiri alikuja na kutaka kuonyeshwa hizo kampuni, safari hii walikuwa wote watatu, wakimtembeza tajiri huyo aliekuwa akitembea na ulinzi wake, walimpeleka kila sehemu zilipo kampuni hizo na kumuonyeasha kila kitu, baada ya kuzunguka masaa kadhaa, wakatafuta sehemu nzuri itakayo wawezesha kuongea kwa kina kuhusu malipo.
Wakaonelea swala hilo wakaliongelee katika hoteli, wakachagua hoteli moja tulivu sana, iliyokuwa pembezoni ya bandari ya Tanga, NYUMBANI HOTELI ndio hoteli waliochagua kuliongelea swala hilo. Wakafika hadi hapo na kuchagua sehemu moja tulivu kwaajili ya maongezi hayo.
“Ndio mabwana, kampuni nimeziona na zote nimezipenda na nipo tayari kuzinunua” Aliongea Tajiri huyo baada ya kukaa sehemu ambayo kwao wameiyona ni nzuri kwa maongezi yao.
“Ndio hivyo, dhote dhipo kamili, hakuna hata kitu kimoja kilichopungudhwa”
“Mmiliki halali wa zile kampuni ni nani?” Tajiri huyo aliwauliza.
“Ni mimi” Mata alijibu.
“Ok, naomba nione hati miliki, ili nijiridhishe nafsi” aliongea tajiri huyo na kumfanya Mata aufungue mkoba aliokuja nao hapo, akatoa makaratasi na kumkabidhi, alipojiridhisha, akayarudisha makatasi yale kwa Mata. Baada ya hapo, wakaelewana bei kuwa kampuni zote wataziuza kwa kiasi gani, baada ya maelewano zikafuta taratibu nyengine za kuuziana kampuni hizo, mambo yalifanywa haraka haraka, wakawekewa pesa zao walizozihitaji kwenye benki waliyoitaka na kuanzia hapo, hawakuwa na chao tena, labda chao kilikuwa ni hizo pesa tu.
Baada ya kila kitu kuenda kikamilifu, wakachukuana wenyewe watatu na kuongozana hadi nyumbani kwa Mata huku nyuso zao zikiwa na bashasha kila muda.
“Zile pesa ni nyingi sana, kwahiyo huo mgawo naomba ufanyike leo leo, kwasababu panaweza kutokea mmoja wetu akaingiwa na tamaa na kutaka kuzichukua pekeake” Mrutu aliongea kuwaambia wenzie.
“Ulichoongea ni chamaana sana, kama vipi hii ishu tuifanye hata sasa” Moto aliongea.
“Haaa!! Yani petha dhimewekwa leo benki halafu dhikatolewe leo leo, kwandha haitowedhekana kutoa petha nyingi kiasi kile kwa wakati mmoja”
“Hilo tunalijua, yani hapa chakufanya ni kupangiana kila mmoja atachukua kiasi gani kwenye zile pesa, kisha tunaenda kuzihamisha tu kila mmoja kwenye akaunti yake, naamini hilo litakuwa jepesi zaidi kuliko kuzitoa halafu tuanze kugawana” Mrutu aliongea.
“Sasa mimi ambae sina akaunti benki nafanyaje?” Moto aliuliza.
“Si unafungua akaunti tu halafu ndio unaziamisha kwenye akaunti hiyo” Mtutu alimjibu.
“Hapo sawa” alikubali na wakaanza kupangiana kila mmoja atachukua kiasi gani kwenye hizo pesa, waligawana sawa sawa, baada ya hapo, wakaongozana hadi benki, huko walifanya kama walivyopanga, kilikuwa ni kitendo cha nusu saa tu, kila kitu kikawa sawa, na kila mmoja akafa kivyake.
Mrutu kipindi hichi alikuwa anaishi katika nyumba ya marehemu kaka yake, ile nyumba yake aliipangisha na kuhamishia makazi kwenye nyumba hiyo ya ghorofa mbili. Alipotoka benki, akanyoosha moja kwa moja hadi katika nyumba hiyo na kuingia ndani, akaenda hadi katika chumba alichokuwa akilala kaka yake na mke wake, chumba hicho ndio alikifanya ni chumba chake kwa wakati huo, alipofika ndani ya chumba hicho, akakaa kitandani na kuangalia mandhari ya chumba hicho utafikiri ndio mara yake ya kwanza kuingia humo, chumba hicho kilikuwa kina vitu vichache ila vilikuwa ni vya thamani ya hali ya juu.
Baada ya kupepesa macho yake kwa muda mrefu, macho yake yakatua katika ukuta wa chumba hicho, kulikuwa na picha moja yenye taswira mbili zilizokuwa na tabasamu kwenye nyuso zao, sura hizo zilikuwa ni Mheshimiwa Bhachu na mke wake wakiwa wapo pamoja kwenye picha hiyo. Mrutu aliiyendea picha hiyo na kuishika ikiwa bado ipo hapo hapo ukutani.
“Pumzikeni kwa amani kaka na shemeji huko mlipo, zile zilikuwa ni tamaa za pesa tu zilizonikumba kipindi kile, japokuwa kaka yangu ulilkuwa unanipa kiasi chochote ninachokitaka kwako, ila sikuridhika nikataka na mimi niwe kama wewe, ndipo niliposhawishika kukufanyia ubaya kaka yangu bila kosa lolote, nikashiriki kuitoa roho yako na ya mke wako, tulipanga tumuue na mwanao ila hilo limeshindikana hadi sasa nipoongea haya, nakiri mbele ya picha yako, nitamtunza mwanao hadi kifo chake au kifo changu, naamini kwa kufanya hivyo, mtanisamehe kwa yote niliyoyafanya juu yenu, pumzikeni kwa amani na mungu amiweke mbali na adhabu zake” aliongea hayo huku machozi ya uchungu yakimtiririka kwenye macho yake, aliigeuza ile picha upande wapili ili kuziziba taswira za watu hao, maana kila akiiangalia picha hiyo, anaona kama vile zile taswira zina msuta na kumlaumu kwa kile alichokifanya, alijitupa kitandani kuusaka usingizi japo kuwa usiku bado haukuingia.
Sekunde zilipishana dakika zikayoyoma siku nazo zikapuputika ukafuata mwaka, Hemedy na Hilda wakaingia darasa la sita, darasa hilo nalo wakalivuka, hivi sasa walikuwa darasa la saba, Mkuu wake na Hilda aliishi na watoto hao kama wanae wa kuwazaa, aliwapenda na kuwapa kila wanachokitaka, Hemedy hakuwahi kubugudhiwa wala kunyanyaswa kwa kitu chochote na mwanamke huyo, nae pia alimchukulia ni mjukuu wake kama alivyomchukulia Hilda, alimpenda na kumfanya kama ni mwenye kuwa na udugu nae, pamoja na yote hakuacha kuwasisitizia kuhusu swala la masomo, aliwachunga sana kwa jambo hilo.
Kipindi chote hicho, Mata na Moto hawakuuacha mpango wao wa kuiyondoa roho ya Hemedy, walijitahidi kujua mahali ambapo mtoto huyo yupo hadi wakafanikiwa kujua, haikujulikana walijua vipi, ila taarifa zote walikuwa nazo juu ya mtoto huyo, wakapanga kutuma watu watakaoenda huko huko alipo ili kuwatimizia adhma yao waliyoipanga, wakawatafuta wale vijana wawili waliofanya nao mauaji ya familia ya Mheshimiwa, haikuwa tabu kuwapata maana Mata alijua ni wapi pakuwapata watu hao.
Aliwaita katika nyumba yake mpya iliyokuwa maeneo ya Makorora Center baada ya ile nyumba yake ya kwanza kuiuza na kununua nyumba maeneo hayo, ilikuwa ni nyumba ya thamani kiasi chake, kipindi hiki alikuwa ameoa na alifanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu, aliwakaribisha katika bustani ya nyumba hiyo na kukaa hapo pamoja.
“Ni mudu mrefu thana hatuja onana” Mata alifungua maongezi.
“Ni kweli, ila yote hayo yamesababishwa na mishe mishe kuwa nyingi” alijibu kijana mmoja huku mwenzake akiwa kimya.
“Ok, kuna kadhi nataka niwape muifanye na ninajua nyinyi mutaifanya kwa uangalifu mkubwa thana”
“Ndio, wewe tuambie hiyo kazi ni kazi gani halafu tujue tutaifanyaje”
“Ni kadhi moja rahithi thana, kuna roho ya mtoto inatakiwa kutenganishwa na mwili wake, na nadhani hata nyie huyo mtoto mnamjua”
“Ni mtoto gani huyo”
“Kama mna kumbukumbu ndhuri, kuna kipindi niliwahi kuwachukua tukafanye mauwaji ya yule Mzee Mheshimiwa, tukawaua wote na kuondoka dhetu, ila haikuwa vile tulivyodhani, kumbe yule mtoto hakufa na ndio huyo ninaetaka muka mtoe roho yake”
“Ni muda sana, sasa sidhani kama sura yake tunaweza kuikumbuka, labda utupe picha yake”
“Hilo thio tatidho, thubirini nakuja thatha hivi” aliongea hivyo na kuingia ndani, baada ya dakika moja akarudi mahala hapo huku mkononi akiwa na picha.
“Mtoto mwenyewe ni huyo hapo, hiyo picha ni yadhamani kidogo ila naamini thura yake haijabadilika thana, mnawedha kumjua mkimuona” aliongea hivyo huku akiwakabidhi hiyo picha, waliipokea na kuiangalia wote kwa pamoja.
“Hakuna shaka, hii ni kazi rahisi sana, chamsingi ni wewe kutupa maelekezo ya wapi anapatikana na ungependa ichukue siku ngapi hadi kifo chake”
“Tuelewane kwandha ni malipo kiasi gani kwa kadhi hii”
Walielewana kiasi watakacho kwa kazi hiyo na kulipwa nusu huku nusu nyengine wakiahidiwa kupewa baada ya kukamilisha kazi hiyo, baada ya hapo walipewa maelekezo ya wapi anapatika mtoto huyo, zaidi Mata akawapa na gari watakayoitumia kipindi chote watakachokuwa wakiifanya kazi hiyo, waliahidi ndani ya wiki tu itakuwa kazi imekamilika.
Daresalam.
Siku moja wakati Hemedy anatoka shule akiwa amechelewa baada ya kufanya kazi walioachiwa yeye na wenzake wa darasa lao, walicheleweshwa kama lisaa limoja hivi, ikiwa kipindi hicho wenzao wamadarasa mengine tayari wamerudi majumbani kwao, Hilda yeye majira hayo, alikuwa yupo nyumbani kwao, yeye alikuwa akisoma na Hemedy darasa moja ila mikondo ilikuwa ni tofauti.
Hemedy akiwa njiani anaelekea nyumbani, ghafla mbele yake ilisimama gari aina ya Mark 11 Grand, ikampigia honi Hemedy aliekuwa bado nyuma ya hiyo gari baada ya kumpita, honi hiyo iliaashiria kuwa atakapofika karibu na hiyo gari, asogee karibu yake maana mmiliki wa hicho chombo ni mwenye kumuhitaji, alilielewa hilo, alifika hadi dirishani upande wa abiria, alipofika pale, alibaki na mshangao baada ya kuziona sura ambazo aliwahi kuziona mahala fulani, swali likabaki, aliwaona wapi watu hao, akiwa bado anashangaa, akajikuta akivutwa ndani ya gari hilo, ni kitendo cha sekunde tatu tu, akawa yupo ndani ya gari hilo, walikuwa ni vijana waliotumwa na Mata wamuue Hemedy, bila kusubiri chochote, gari ilitiwa moto na kuondoka mahali hapo kwa kasi ya ajabu. Watu walioshuhudia tukio hilo, walibaki midomo wazi huku wengine wakiwa wameshika vichwa vyao kwa taharuki, walitaharuki kwa mambo mawili, kwanza ni kutekwa kwa mtoto huyo, pili ni jinsi gari lilivyoondolewa mahali hapo kwa kasi, wakasahau hata kuzisoma namba za hilo gari..
Wakati wakiendelea na safari yao, majira hayo walikuwa wapo mbali na makazi ya watu. Mmoja wapo alimdhibiti Hemedy huku mwengine akiendesha gari. Walipanga wakamuulie mbali huko halafu na wao warudi Tanga siku hiyo hiyo. Wakiwa bado waposafarini kuelekea huko walipopanga wao. Ghalfa mbele yao palitokea gari aina ya Nissan Murano, gari hiyo ilisimama mita chache mbele yao baada ya kuwapita kwa kasi ya ajabu, kama sio kuchuna breki kwa nguvu na kuifanya gari yao iserereke, basi wangeenda kuigonga hiyo gari na kungetokea ajali kubwa sana ambayo ingeacha damu mahali hapo huku ikipambizwa na vipande vya miili ya watu hao.
Bilashaka watu waliokuwepo kwenye gari iliyovamia safari yao, walijitolea kufa na kupona, inamaana wao hawakujua kufanya hivyo ni kusababisha ajali ambayo hata wao ingewadhuru kwa kiasi kikubwa? Wavamizi hao walishuka ndani ya gari lao kwa haraka mno na kuwaweka chini ya ulinzi wale watekaji, wakawaamrisha watoke nje ya gari na wao wakafanya hivyo huku wakiwa mikono yao wameiweka vichwani mwao, Hemedy walimuacha ndani ya gari, walitoka wenyewe wawili tu. Wavamizi hao walipeana ishara na mmoja wapo akatoa simu na kuiminyaminya na kuiweka sikioni mwake, akasubiri kwa sekunde kadhaa kisha akaanza kuongea.
“Mkuu, tumefanikiwa kuwapata na hivi sasa tumewaweka chini ya ulinzi kwahiyo tunasubiri amri yako tu”
“Nyie msiwadhuru kwa chochote, chakufanya ni kuwapa onyo tu kuwa waache kumfuatilia huyo mtoto na waondoke kwenye huu mji haraka iwezekanavyo, halafu muwaambie wakampe salamu huyo aliewatuma kuwa aachane na hayo mawazo yake ya kutaka kumuangamiza huyo mtoto na wakamuambie kuwa, mipango yake yote inajulikana, kwahiyo asije akafikiria tena kufanya hivyo, akijaribu kufanya tena hivyo, itamgharimu yeye na hao atakao watuma” sauti ya kwenye simu iliongea hivyo.
“Sawa mkuu, na huyu mtoto nae?” Jamaa huyo aliuliza.
“Huyo mtoto atarudi mwenyewe alipotoka kwahiyo nyie muacheni” mtu wa upande wa pili alijibu.
“Sasa mkuu, huoni kama hiyo itakuwa ni hatari kwake, maana huku alipo na nyumbani kwao ni mbali sana, halafu isitoshe hizi njia sidhani kama atazijua”
“Kwahiyo unanifundisha kazi?” sauti yenye mamlaka iliunguruma kwenye simu.
“Hapana mkuu sikufundishi kazi” jamaa alijibu kwa uoga.
“Ila?”
“Nilikuwa najaribu kushauri tu mkuu, nisamehe sana”
“Au unadhani mimi sijui kuwa huyo mtoto hapajui huko, au unadhani mimi sijui kama hazijui hizo njia za kurudi nyumbani kwao? Mimi ndio najua kuwa huyo mtoto anatakiwa awe vipi na sio nyie. Ok fanyeni kama nilivyo miagiza, hao wajinga wapeni hizo salamu wakamfikishie aliewatuma halafu huyo mtoto muacheni arudi mwenyewe nyumbani kwao hata pawe na umbali kiasi gani ila nyie hakikisheni anafika salama kwa kumuwekea ulinzi, ila sasa asijue kama kuna watu wapo nyuma yake wanamfuata. Kumbukeni huyo mtoto Kiongozi anamuhitaji kuliko kitu chochote, kwahiyo hakikisheni usalama wake unakuwa ni mkubwa”
“Sawa mkuu tumekuelewa, tutafanya kama ulivyotuagiza” Baada ya hapo alikata simu na kuwaangalia jamaa hao waliomteka Hemedy.
“Oya nyie washkaji, sote hapa ni vijana na ninadhani mnaakili timamu, akili mlizokuwa nazo zinauwezo wa kuzingatia yale ambayo mnayoambiwa, kwahiyo kwa haya ambayo nitakayowaambia sasa hivi, bila shaka mtayazingatia ikiwa mnapenda kuishi, ni hivi, uwezo wa kuwafanya chochote tunao hata kama tukiamua tuweke silaha chini tupigane mkono kwa mkono, tunamihakikishia sekunde tano nyingi, mtakuwa tayari kuvikwa sanda kwaajili ya kupelekwa kupumzishwa makaburini, tunaomba muwe waelewa, chakufanya sasa hivi ni kuondoka katika mji huu na kurudi mlipotoka, mkifika mpeni salamu huyo aliewatuma kuwa, aache na afute kisha asifikirie tena kupanga mipango ya kumdhuru huyu dogo kwanjia yoyote ile, akijaribu hata kuwaza kumdhuru huyu dogo, basi ajue atakufa kifo ambacho hata yeye mwenyewe pia kitamshangaza…..”akamgeukia yule mwenzake “Kanu, nenda kamtoe yule dogo kwenye gari”
Huyo jamaa mwengine aliejulikana kwa jina la Kanu, akaenda kwenye gari na kumtoa Hemedy kwenye siti za nyuma za gari hiyo. Hemedy muda wote huo alikuwa akitetemeka asijue watu hao ni wakina nani na wanataka nini, kibaya zaidi kilichomchanganya ni kuhusu sura za wale watu wamwanzo, alihisi kama vile alishwahi kuziona sehemu flani ila hakuwa na kumbukumbu nzuri kuwa aliwahi kuziona wapi sura hizo.
Nikama vile kuona kwake bastola ni jambo ambalo amelizoea, maana ni mara nyingi sasa aliziona sehemu tofauti tofauti, tena zote zikiwa na malengo na yeye, pamoja na kuziona sana lakini bado woga ulikuwa upo pamoja nae, alijua fika kifaa hicho hakina masihara pale kunapotumwa kuondoa uhai au hata kumjeruhi mlengwa, akabaki ni mwenye kulia tu muda wote huku akiomba msamaha kwa kosa asilolijua.
Wavamizi hao wakawaruhusu watekaji wa Hemedy waondoke huku wakiwakumbusha kuwa wampelekee salamu bosi wao aliewatuma. Watekaji wakaondoka huku wakimshukuru mungu kwa kuokoka katika mikono ya hao wavamizi, walipanga waondoke jioni hiyo hiyo kurudi Tanga kama walivyohusiwa, wakaondoka mahala hapo na kuwaacha watu watatu tu, yani Wale jamaa wawili na Hemedy.
Jamaa hao baada ya kuhakikisha watekaji wamefika mbali na wao wakaingia kwenye gari yao na kumuacha mtoto huyo akiwa amesimama asijue ni nini hatma yake juu ya kutekwa kwake, jamaa hao wakaondoka huku wakimuacha Hemedy akiwa haelewi mambo yanavyoenda akabaki akijiuliza. ‘inamaana watu hao walipanga kuja kumtelekeza mahala hapo au walikuwa na lao ambalo wamelipanga juu yake?’ hapo ndipo uoga ulipomzidi, akawaza kuwa watu hao walipanga kumuua kwa staili hiyo ya kumuacha hapo kisha kumshambulia kwa chochote kile watakachoona kwao kinafaa kumshambulia nacho.
Alitulia kwa dakika kadhaa kishaapo akaanza kurudi na njia ile ile aliyoletwa nayo, aliogopa sana maana barabara nzima alikuwa yupo pekeake, hakukutokea gari ya aina yoyote wala mtu wa aina yoyote njiani hapo, hapo ndipo alipoiyomba msaada zaidi miguu yake imsaidie kukimbia, nayo haikuwa na kiburi eti kwamba igome kufanya kile ambacho mmiliki ametaka, akawa anakimbia huku akiangalia nyuma kila mara, alikimbia hadi akachoka, akawa anatembea nusu, nusu anakimbia.
Majira hayo, jua tayari lilishazama na kufanya giza liitawale dunia, akaanza kukimbia tena safari hii alikimbia huku akilia, maana alishakimbia zaidi ya lisaa limoja na nusu lakini bado hakuweza kufika kule anapopataka. Baada ya kukimbia kwa nusu saa nyengine, ndipo alipopata matumaini ya kuishi pale alipoona magari kadhaa na nyumba kadhaa zilizokuwepo kando ya barabara hiyo huku magari hayo yakiendelea na safari zake.
Majira hayo yalikuwa ni saa moja na nusu usiku, alitembea hadi akafika katika kituo cha daladala, akajisachi mfukoni na kukuta akiwa na elfu moja mfukoni mwake, akapanda daladala iliyompeleka hadi kwao Kinondoni, kisha akatembea kwa miguu tu hadi nje ya nyumba yao, muda huo ilikuwa ni saa mbili za usiku, akaingia ndani ya nyumba hiyo huku akiwa na wasiwasi wa kuulizwa kuwa alikuwa wapi muda wote.
“We Hemedy, tulikuwa tunakusubiri muda wote huo, ulikuwa upo wapi?” alikutana na swali hilo mara baada ya kuingia sebuleni, Hilda ndie alikuwa muulizaji wa swali hilo.
“Nilikuwa nipo shule, ilipofika saa kumi na mbili ndio nikaondoka kuelekea kituoni kupanda gari ila sasa kila gari lililokuja lilikuwa limejaa hadi kuja kupata gari ilikuwa muda ushaenda sana halafu pia foleni imechangia kuchelewa” Hemedy aliongea hivyo huku akiuwelekea mlango wa chumbani Kwake.
“Muongo Hemedy wala haukuwa shule, wewe kuna sehemu zako umetoka huko ndio unanificha mimi” Hilda aliongea kwa hasira kiasi na kumfanya Hemedy aghairishe kuingia ndani ya chumba chake na kumgeukia yeye, hakuelewa imekuaje hadi mtoto huyo wa kike kuwa katika hali hiyo, kwanza alishangaa wakati akiingia hapo sebuleni alipomuona binti huyo alivyovimba kwa hasira, haikuwa mara ya kwanza kumnunia, mara nyingi alifanya hivyo pale alipomuona Hemedy akiwa amekaa au amesimama na mtoto wa kike kwa muda mrefu wakiwa shule, basi binti huyo anakuwa ni mwenye kununa tu kwa siku nzima na kisa kinachomfanya anune kisijulikane.
“Sasa Hilda wewe unahisi mimi nilikuwa nipo wapi, mji wenyewe huu mimi siujui, mimi niwa nyumbani na shuleni tu mwenyewe unajua, asa ni vipi uniambie natoka sehemu zangu ninazozijua halafu nakuficha?”
“Haya umeshinda, chakula kipo kwenye meza, kama unanjaa unaweza kwenda kula” Hilda aliongea hivyo huku akigeukia upande ilipokuwa luninga.
“Sawa, vipi anti amerudi?” Hemedy alimuuliza.
“Hajarudi bado” alijibu huku akiongeza sauti ya redio ambayo imeunganishwa na luninga kuashiria kuwa hataki tena maongezi na kijana huyo. Hemedy alisikitika tu na kuingia chumbani kwake maana alishajua kuwa tayari mtu huyo ameshakasirika. Hilda aligeuza macho yake kuangalia kule alipoingia Hemedy baada ya kusikia sauti ya kufungwa kwa mlango, aliuwangalia kwa sekunde kadhaa kisha akarudisha macho yake kwenye luninga, akapunguza sauti ya redio na kuendelea kuangalia kinachoonekana kwenye luninga hiyo.
Saa 4:20 Usiku. Tanga.
Wale waliotumwa na Mata kwenda kumuangamiza Hemedy, Waliingiza gari ndani ya uzio wa nyumba ya Mata, wakashuka kwenye gari na kumuona Mata akiwa amesimama kwenye kibaraza cha nyumba hiyo, inaelekea aliujua ujio wa watu hao ndio maana akawasubiri hapo. Akawapa ishara ya kuwa waelekee kwenye bustani na wao wakafanya hivyo huku akiwafuata nyuma, walipofika kila mmoja akachukua nafasi yake kwenye viti vilivyokuwa hapo na kukaa.
“Bosi yule mtoto analindwa na ulinzi mkali sana” jamaa mmoja wapo alijibu.
“Analindwa!! Analindwa na nani?” Mata aliuliza kwa tahamaki.
“Wakati tukiwa tupo nae tukitafuta sehemu nzuri ya kumuulia, ghafla mbele yetu palisimama gari, yani gari hilo lilituziba njia, watu hao wakashuka na kuwahi kutuweka chini ya ulinzi, mmoja wa watu hao, akaongea na mtu kwenye simu kama dakika tano hivi, alipomaliza alitupa onyo na kuturuhusu tuondoke halafu wao wakabaki na yule dogo”
“Onyo gani walilomipa, halafu watu hao mnawajua?”
“Hapana hatuwajui, ila tu walituachia maagizo ya kukuletea wewe, walisema kuwa usijaribu tena kumfuatilia yule mtoto na kama ukifanya hivyo basi ndio unaweza ukawa mwisho wa maisha yako na hao utakao watuma tena”
“Hapana, watu hao wanaoneka wanajiweza kimapigano hata hivyo pia walituwahi, kwahiyo hatukuwa na ujanja wowote wa kuwadhibiti”
“Thawa, thubirini nakuja thatha hivi” Mata aliongea hivyo na kuingia ndani ya nyumba na baada ya dakika moja alirudi hapo huku akiwa mkonono ameshika bastola, bila kuuliza chochote, aliwafyatulia risasi mbili mbili kila mmoja na kuwafanya watu hao wasiache hata usia wa mwisho mahala hapo, hakukuskika milio ya risasi kutokana na bastola hiyo kuifunga kiwambo cha kuzuia sauti.
“Washendhi nyie” hilo ndio neno alilomalizia nalo, kisha akarudi tena ndani na kutoka na funguo za gari, akaichukua miili hiyo na kuingiza kwenye buti la gari walilokuja nalo, alipomaliza, akaenda kufungua geti na kulitoa gari hilo nje ya nyumba hiyo, akarudi tena kulifunga geti na kuingia kwenye gari hilo, alipanga miili hiyo akaitupe kwenye daraja la Amboni, daraja ambalo linasifika kwa kuwa na mamba wengi na wakali, akapanga kuitupa miili hiyo hapo ili iliwe na wanyama hao wakali.
Akaanza safari usiku huo huo kwenda kufanya kile alichopanga, wakati akiwa yupo maeneo ya Chumvini, mbele yake aliona gari la polisi limepaki pembeni huku askari wakiwa wamesimama nje ya gari hilo huku wakiwa wameshika bunduki, polisi hao walikuwa kwenye doria usiku huo. Polisi mmoja alilipiga mkono gari la Mata na yeye hakuwa nabudi zaidi ya kulipaki gari hilo pembeni, wasiwasi, uoga na vyengine vifananavyo na hivyo, vili mpata kwa pamoja, hakuelewa atawajibu vipi askari hao pindi wakiziona maiti zilizokuwa ndani ya buti la gari lake.
“Za saa hizi?” askari mmoja alimuuliza baada ya kumfikia kwenye gari lake kilipo kioo cha upande wa dereva.
“Thalama tu afande” Mata alionekana ni mwenye wasiwasi mbele ya askari huyo ambae alianza kumtilia mashaka.
“Unatoka wapi na unaelekea wapi usiku huu?”
“Natoka Tanga mjini naelekea Amboni”
“Kuna nini huko?” swali hilo lilimfanya Mata atulie kwa sekunde kadhaa bila kujibu hapo ndipo askari huyo alipozidisha mashaka yake kwa mtu huyo.
“Nimepigiwa thimu kuwa mwanangu amedhidiwa huko, kwahiyo naenda kumchukua nimpeleke Hothpitali ya Bombo” Alipata ujasiri wa kujibu hivyo na kumfanya askari huyo kumuangalia kwa muda kisha akaanza kutizama ndani ya gari hilo, alipoona hakuna chochote chakutilia mashaka ndani humo, akamuomba atoe loki ya kwenye buti ili aangalie na huko.
“Thatha afande, mimi nachelewa mwanangu anaumwa thana na hivi thatha nimepigiwa thimu kuwa kadhidiwa, naomba tu uniruhuthu niondeke afande” Mata aliongea huku akiwa analia machozi huku mikono yake akiwa ameifumbata kifuani kwake kama mtu anaeomba mungu, haikujulikana kuwa alikuwa akilia kwa uoga au alikuwa anaigiza.
“Aloo nimesema toa loki ya buti, usinililie mimi, Alaaa!!” Afande huyo aliongea kwa ghazabu kiasi kwamba akamtisha hadi Mata, hakuwa na jinsi nyengine, akatoa loki na kubaki akimuomba mungu wake kutokee muujiza maiti hizo zisionekane na afande huyo. Askari bila kuchelewa, alizunguka hadi nyuma ya gari hilo na kuliendea buti la gari kwaajili ya kulifungua..
“AFANDE, muache aende bwana, anachelewa” hiyo ilikuwa ni sauti askari mwengine ikimuambia yule askari aliekuwa akitaka kulifungua buti la gari la Mata. Askari huyo akaghairisha kufungua buti na kumfuata Mata kule mbela na kumruhusu aende, hakika hakuamini hata kidogo kuwa ni kweli dua zake mungu amezikubali. Akamshukuru askari huyo na kuliondoa gari lake kwa mwendo wa kasi maana alihofia kuitwa tena.
Alipofika kwenye daraja la Amboni, akasimamisha gari pembeni na kushuka, akaangalia huku na huko akaona pako sawa, akaliendea buti na kulifungua, akazitoa maiti hizo na kuziburuza hadi karibu na ukingo wa daraja hilo, kisha akazisukumia ndani ya daraja, akarudi tena ndani ya gari na kuchukua chupa ya maji na kwenda kufuta zile damu ambazo zimebaki wakati anaburuza zile maiti, alipoona kila kitu kimekaa sawa, akawasha gari na kwenda kutafuta gesti yoyote ambayo anaweza kulala usiku huo, alihofia kurudi kisha askari wale wamsimamishe tena halafu wasimuone huyo mtoto anaeumwa.
Majira ya asubuhi, alianza tena safari ya Kurudi Tanga mjini, alipofika nyumbani kwake, akampigia simu Moto na kumtaka afike mara moja hapo na baada ya nusu saa Moto alifika nyumbani hapo akiwa yupo ndani ya gari aina ya Prado Tx, kwahakika alibadilika sana kimuonekano, alikuwa yupo kama mtoto wa tajiri flani au ni kijana kati ya vijana wachache wenye maendelea hapo jijini, alikuwa amevaa kileo zaidi kama wale wasanii wa muziki wa kizazi kipya, masikioni mwake alibandika hereni, shingoni mwake kulikuwa na cheni ya gharama iliyoning’inia huku vidoleni kukijazwa mapete na mkononi alikuwa ameshikilia simu ya maana, achilia mbali mavazi aliyoyavaa, yote hayo yalijidhihirisha baada ya yeye kushuka ndani ya hilo gari.
Akanyoosha moja kwa moja mpaka ndani ya nyumba hiyo na kumkuta Mata akiwa amekaa kwenye sofa sebuleni hapo akimsubiri yeye, wakasalimiana salamu za vijana kwa kupeana tano, akaenda moja kwa moja hadi kwenye friji la hapo, akalifungua na kuanza kuangalia humo kwa sekunde kadhaa kisha akamgeukia Mata aliekuwa akimuangalia tu muda wote.
“Vipi wewe mboma sioni vinywaji humu ndani ya friji?” Chaajabu hata uongeaji wake pia ulibadilika na kuwa kama wale mabitozi wa kimarekani weusi.
“Wala hakuna pombe humo, thi unajua mimi huwa thitumii thana vinywaji hivyo, halafu hata mke wangu pia hapendi nikitumia, kwahiyo ndio maana thiweki hivyo vinywaji unavyotaka”
“Kwahiyo unataka na mimi nitumie juisi kama mtoto mdogo, poa acha nitumie kwa dharula” akachukua jagi lenye juisi ya matunda na kumimina kwenye glasi, akaenda kukaa kwenye sofa na kuanza kunywa taratibu kinywaji hicho.
“Ndugu yangu umebadilika thana yani” Mata aliongea.
“Aaa! Kawaida tu mbona, si unajua watu tunaenda na wakati”
“Hata kama lakini thio kwako, unakumbuka kipindi kile ulikuwa unathema, ohooo, nikidhipata hidhi hela, bathi chakwandha naoa, haya uko wapi ule mthemo wako, atha hivi umekuwa mtu wa kubadilisha wathichana tu, akitoka huyu anaingia huyu, angalia ndugu yangu, utakuja kufa kwa magonjwa”
“Bab, kwanza hayo magonjwa tumeumbiwa sisi, kwahiyo mimi sijali kuhusu hilo, halafu hizo habari za kuoa nilikuwa nazisema kipindi kile sina hela, ila hivi sasa mimi ndio bosi, hahahah! Maisha ukiyaotea raha sana, yani mimi sijasoma ila nimeajiri watu waliosoma na ndio wananiita bosi tena kwa unyenyekevu, halafu hata kama nikioa huyo mwanamke atapata tabu tu, maana sijazoea kuwa na mwanamke mmoja, hata hivyo nioe kwani hivi sasa nakosa kitugani kwa hao ambao sijawaoa? Kwanza umenikumbusha kitu, shemu yupo wapi?” Moto aliongea.
“Shemeji yako ameenda kwao kuthalimia”
“Ndio ameondoka na jembe langu(akimaanisha mtoto wa Mata) au jamaa yupo?”
“Wote wameondoka”
“Sawa, niambie mzee nakusikiliza”
“Ni hivi…” Akamuambia yote yaliotokea tangu anawatuma wale watu wakamuue Hemedy jijini Dar na kujakumletea vitisho kisha kuwaua, hakuacha kumuhadithia kilichomkuta wakati akienda kuzitupa zile maiti.
“Haina haja ya kumfuatilia tena yule dogo, kwanza mimi naona hana madhara tena kwetu, kwahiyo tuachane nae tu”
“Thawa kama ndio umeamua tufanye hivyo, pia ni thawa tu”
“Basi mzee acha mimi nikalale maana hapa ninausingizi kibao wa jana usiku, si unajua mimi ni mzee wa kujirusha, jana nilikuwa klabu nainjoi na watoto wazuri tu, acha basi mimi nikalale” Akainuka pale alipokaa na kwenda kugongesha tano na kuanza kuondoka. Chaajabu zaidi, alikuwa akitembea kwa kudunda dunda kama kitenesi kilichokosa muelekeo baaada ya kupigwa shuti na mtoto mdogo aliekuwa akikichezea. Ama kweli wahenga hawakukosea pale waliposema msemo wao ‘Masikini akipata, matako hulia mbwata’ masikini mwenyewe ndio huyo sasa, alikuwa akipeta na mali za dhuluma, huwezi kumdhania kuwa ndie huyu aliekuwa akikaa maskani bila kazi yoyote. Kwa hivi sasa. Alimiliki baa kubwa sana iliyokuwa maeneo ya sahare na supamaketi ndogo(Min SuperMakert)iliyokuwa katikati ya mji.
Mata na yeye alimiliki mabasi mawili yaliyokuwa yakienda safari za Tanga, Dar na mafuso ya mizigo yaliyokuwa yakimletea pesa nyingi. Huku Mrutu nae akiongeza maduka ya spea za magari na alifungua showroom ya magari baada ya kuona biashara hiyo ilikuwa ikimlipa sana marehemu kaka yake. Kwahakika watu hawa kila mmoja alikuwa amejizatiti upande wake, hakuna ambae alitaka arudi nyuma kimaendelea, ndio maana kila mmoja alipambana kutaka kuzikuza mali hizo walizokuwa nazo.
Mrutu majira hayo ya asubuhi, alienda kutembelea maduka yake na kukusanya pesa zote zilizopatikana kwa hiyo wiki na kuzipeleka benki, akaenda kwenye ofisi yake iliyokuwa ndani ya hiyo kampuni yake ya magari na kwenda kupiga mahesabu ya mauzo ya wiki hiyo, yeye alikuwa akipiga mahesabu kila baada ya wiki moja, alipoona pesa ziko sawa, nazo akazipeleka benki kwenda kuzihifadhi, akarudi nyumbani kwake, nyumba ambayo alikuwa akiishi marehemu kaka yake na familia yake, na kwenda kupumzika siku hiyo.
Tabia yake na ya Moto hazikutofautiana sana ila yeye hakuwa mtu wa kwenda klabu, ila alipenda kubadilisha wanawake kila kukicha, hata hapo pia alimpigia simu mwanamke aliempata jana wakati alipoenda kununua gari kwenye kampuni yake, baada ya dakika kadhaa alifika mwanamke huyo na kumkaribisha kwa bashasha zote, walikaa sebuleni hapo na kuanza kupiga stori ambazo hazikuwa na maana yoyote, baada ya kuishiwa na chakuongea, Mrutu ndio aliona sasa huo ndio muda wa kufanya kile alichopanga juu ya mwanamke huyo.
Akanza kumchombeza kwa maneno yake hadi pale mwanamke huyo alipoanza kukaa sawa, hakuwa na ujasiri wa kukataa hata kidogo, sio kwamba Mrutu alikuwa na maneno matamu kiasi kwamba yakamchanganya mwanamke huyo, la hasha! Ila angeanzaje kukataa wakati ikiwa hata bei ya gari alilonunua kwa mwanaume huyo alipunguziwa kwa kiasi kikubwa, hata hivyo hivyo pia alijiziwa mafuta fulutanki kwenye hiyo gari bure kabisa. Baada ya kuingia kwenye kumi na nane zake, wakavutana hadi chumbani ambako sijui ni nini kiliendelea maana walifunga mlango kwa ndani huku ikiwa mimi nimebaki nje ya mlango huo.
Daresalam.
Maandalizi ya mitihani ya kumaliza darasa la saba yalifanyika Tanzania nzima, kila mwanafunzi alikuwa katika mishemishe za kujiandaa kuukabili mtihani huo wa kuhitimu elimu ya msingi, wanafunzi wengi walionekana wakijaa katika vituo vya kufundisha masomo ya ziada(tution), Hilda na Hemedy pia walikuwa katika mkumbo huo wa kujianda kwa mitihani watakayo ifanya siku mbili mbele.
Majira hayo ya saa kumi na mbili jioni, walikuwa wapo njiani kurudi nyumbani kwao wakitokea katika kituo cha kufundishia masomo ya ziada, walikuwa wakiongoe kwa furaha huku wakikumbushiana mambo mbalimbali ambayo yaliwafanya muda wote kufurahi, hata hivyo pia, ilikuwa ni moja ya kufupisha mwendo wa kufika nyumbani kwao, japokuwa hapo wanaposoma na nyumbani kwao sio mbali.
Walifika nyumbani na kila mmoja kufanya kazi zinazomuhusu, kisha wakachukuana na kuelekea kwenye kibaraza kilichokuwa mbele ya nyumba hiyo na kukaa hapo, walitoa madaftari yao na kuyaweka juu ya meza iliyokuwa mahala hapo na kuanza kusoma kile walichoona kitawasaidia katika mitihani yao, walisoma hadi walipochoka na kuingia ndani kwenda kupata chakula cha usiku kisha kila mmoja akaingia katika chumba chake na kwenda kupumzika.
Siku mbili mbele, wao na wanafunzi wengine wa darasa kama lao nchi nzima, walikuwa ndani ya madarasa yaliyo teuliwa kwa kufanyia mitihani hiyo. Mitihani hiyo waliifanya kwa siku mbili tu na baada ya hapo wakawa tayari ni wahitimu wa elimu hiyo ya kwanza, kila mwanafunzi alikuwa nyumbani akisubiri matokeo yake baada ya kumaliza kufanya mitihani hiyo, wengine walienda kujifunza masomo ya awali ya sekondari(Pre form one) ili hata kama wakibahatika kufaulu, basi wasibabaishwe na zile mada za mwanzo mwanzo pindi waingiapo kidato cha kwanza, na wao pia walienda kujifunza masomo hayo huku wengine wakisubiri matokeo wakiwa nyumbani kwasababu zao wazijuazo wenyewe.
Miezi mitatu mbele, matokeo yao yalitoka na kuwafanya wanafunzi wengi kuwa na kiroho cha kutaka kuyaona matokeo hayo, wengi walikusanyika mashuleni mwao walipomalizia elimu zao, kwenda kuangalia kile walichokipanda kwa miaka saba iliyopita. Hemedy na Hilda, wao matokeo yao waliyaangalia kwenye intaneti na kujikuta wakiwa wamefaulu kwa kiwango kizuri tu, tena bahati ilikuwa kwao, walifaulu shule moja.
Bila kuchelewa, Anti yao aliwafanyia maandalizi haraka haraka yakiwemo sare za shule hiyo na vitu vyengine kama hivyo vinavyohitajika shuleni kwa wale wanafunzi wapya. Mwezi mmoja mbele, wakaanza kwenda kwenye shule waliyochaguliwa, shule ya sekondari Benjamini Wiliam Mkapa. Wanafunzi wageni ndio walidhihirika shuleni hapo huku wenyeji wakimalizia likizo yao waliobakisha ya wiki moja.
Wanafunzi hao wageni, wengi walionekana na nguo za shule ya msingi huku wachache ndio walikuwa wamevaa sare za shule hiyo, walikuwa wamezagaa tu ndani ya shule hiyo, baada ya muda wakaitwa wote na kuwekwa sehemu moja na mwalimu aliewapokea akanza kuwakaribisha shuleni hapo kwa kuwasisitizia wafuate sheria walizozisoma kwenye fomu walizopewa kabla.
Baada ya kuwaeleza mengi, aliwataka waongozane hadi katika madarasa kwaajili ya kwenda kupangiwa, waliitwa kwa majina na kila aliesikia jina lake alitakiwa kuingia kwenye darasa aliloelekezwa. Zoezi hilo lilifanyika kwa lisaa limoja hadi kukamilika na kila mwanafunzi akawa yupo kwenye darasa alilopangiwa, baada ya zoezi hilo kuisha, waliambiwa waende kwenye madarasa mengine kwenda kuchukua viti na meza zilizofemea kwenye madarasa hayo. Hemedy na Hilda walipangwa darasa moja, hapo furaha yao ilizidi mara dufu.
“Niaje jamaa” mwanafunzi mmoja alimsalimia Hemedy wakati wakiwa wapo darasani.
“Freshi tu, niambie kaka” Hemedy nae alijibu huku akigongesha viganja vyake vya mkono huku akiwa amevikunja, vijana waliita ‘Tano’.
“Safi tu, mwanangu mimi sijapata kiti wala meza humu ndani, kwahiyo jamaa naomba msaada wako kwenda kuchukua vitu hivyo madarasa mengine”
“Usijali, maana hata mimi pia sijapata kitu hata kimoja humu ndani, kwahiyo tutasaidiana wote kuchukua vitu hivyo”
“Poa kaka, twenzetu tukavichukue” mwanafunzi huyo alipoongea hivyo, wakaanza safari ya kuelekea madarasa mengine kwenda kuchukua viti na meza, walipishana na wanafunzi wenzao ambao nao walikuwa katika harakati za kuchukua vitu hivyo na kuvihamishia kwenye madarasa yao. Walifanikiwa kupata na kurudi navyo kwenye darasa lao walilopangiwa, kisha wakavipanga karibu karibu, Hemedy alikaa mbele na nyuma yake alikaa huo mwanafunzi mwengine, wakawa wamekaa kwa mfuatano.
“Oya jamaa” mwanafunzi huyo alimuita Hemedy na kumfanya amgeukie.
“Naitwa Ramadhani Kaoneka, ukipenda unaweza ukaniita Rama au kiswaga zaidi ukiniita Ramso, sijui wewe unaitwa nani?” mwanafunzi huyo aliejitambulisha kwa majina hayo alimuambia Hemedy huku akimpa mkono.
“Hemedy Mheshimiwa Bhachu” na yeye alijitambulisha huku akiupokea mkono huo.
“Dah! Jamaa jina lako linafanana na Tajiri mmoja hapa dar, sijui una undugu nae” Rama au Ramso aliongea.
“Hapana sina undugu na mtu yoyote hapa dar” Hemedy alijibu.
“Kwani wewe ni mtu wa wapi?” Rama aliuliza.
“Mimi ni zao la Tanga ndugu”
“Dah! Mwanangu hata mimi pia ni zao la huko huko, sema mimi niliondoka kule tangia nikiwa darasa la tatu ndio nikahamia huku”
“Basi tupo pamoja kaka” Hemedy aliongea.
“Hemedy, jina zuri sana, ila mimi ningependa kukuita Medy ile kiswaga zaidi au wewe unasemaje?”
“Iko poa sana, na mimi ningependa kukuita Ramah ile kiswaga zaidi na wewe unasemaje?”
“Hahaha! Jamaa yangu jina zuri sana ulilonipa, Ramah, dah! safi sana kaka nimelikubali” Muda huo huo akaja Hilda hadi hapo walipokaa, Hemedy akamuuliza kuhusu kupata kiti na meza akajibu ndio na tayari ameshavipanga katika mstari, akamuonyesha pale iliposehemu yake atakayo kaa kwenye darasa hilo.
“Oooh! Sista karibu, naitwa Ramadhani au Ramah kama alivyoniita jamaa yangu” Ramah aliongea hivyo huku akipeana mikono na Hilda.
“Naitwa Hilda Ganjo”
“Nawewe umepangwa darasa hili?” Ramah alimuuliza utafikiri hakuona kipindi Hilda akimuonyesha Hemedy sehemu atakayo kaa darasani hapo.
“Yeah, tupo wote humu”
“Basi vizuri, naamini tutashirikiana wote vizuri tu”
Majira hayo wanafunzi hao wageni waliyatumia kuzunguka zunguka shuleni hapo ili kuyasoma mazingira, walitembea sana hadi walipoona wameridhika kuyasoma mazingira hayo, wakatoka nje ya shule hiyo ili kwenda kupata chakula maana ndani ya shule hiyo hakukuwa na chakula chochote kilichopikwa hapo kutokana na shule kutofunguliwa rasmi, siku hiyo waliitumia kupiga stori tu kwasababu hawakuwa ni wenye kufundishwa chochote kwa siku hiyo ya kwanza.
Muda wa kutoka ulipofika, wakaruhisiwa kuondoka huku wakikumbushwa kuwa siku inayofuata wa wahai kufika ili wafanye usafi wa shuleni hapo. Wiki hiyo iliisha, ikafuata nyengine, wiki hii ndio wiki waliokuwa wakifungua wanafunzi wote wa sekondari, wanafunzi wenyeji wakarudi shuleni na kuwakuta wageni, haikuwa tatizo kwao, kwasababu hata wao pia walikuwa hivyo hivyo.
Ikapangwa ifanyike sherehe ya kuwakaribisha wanafunzi hao wageni, siku ya siku ikafika na sherehe hiyo ikafanyika kwenye ukumbi wa shule. Hemedy Tabia yake ya uongeaji na uchekeshaji hakuiacha, hivyo ilifanya ajulikane na wanafunzi wengi kwa haraka kuliko mwanafunzi yoyote, hata hivyo ni kama vile tabia yake na ya huyo rafiki yake wa kwanza shuleni hapo Ramah ziliendana, wote walikuwa ni waongeaji sana pindi wanapokaa na wenzao kikundi, walihakikisha kila baada ya sekunde moja, watu waliowazunguuka wayaache meno yao nje kwa kucheka. tabia yao hiyo ikawafanya waitwe mapacha.
* * * *
Zilianza sekunde, zikafuatia dakika, yakafuata masaa na kumalizikia mwaka, wakawa wapo kidato cha pili, kidato hichi, waliamua wakazane nacho kusoma maana walijua kuna kurudia kama hutofaulu mtihani wa mwisho wa kidato hicho, walikazana kusoma wote watatu nikimaanisha na Hilda pia, ili waweze kufaulu mtihano huo, na hawakuwa haba kufanya vizuri kwenye mitihani.
Pamoja na kusoma sana na kufanya vizuri kwenye mitihani, pia hawakuacha tabia yao ya kuchekesha, na kitu chengine alichokijua Hemedy kwa Ramah ni kuwa kijana huyo ana kipaji cha kuimba, na mara nyingi sana alikuwa akimuimbia kila Hemedy atakapo taka hivyo, pamoja na hivyo, Ramah hakutaka ajulikane na wanafunzi wenzake kuwa ana uwezo mzuri wa kuimba, vijana hao walijulikana shule nzima kwa tabia yao ya kuongea sana hadi kupelekea kuwa komedi kwa wanafunzi wenzao, na sio kwa wanafunzi tu hadi kwa walimu pia waliwajua.
Mwaka huo nao ukapita, ukaingia mwaka mwengine, mwaka huu walikuwa kidato cha tatu baada ya kufaulu vizuri mtihani wa kidato cha pili, kufaulu kwao hakukuwafanya waache kusoma, walisoma sana hadi kuamua kwenda kuanza kusoma na masomo ya ziada ili mradi watakapofika kidato cha nne wafaulu vizuri ili waendelee na masomo ya juu, wote watatu walichagua kusoma masomo ya sanaa, bahati ikawa kwao tena baada ya kupangwa darasa moja.
“Oya jamaa, mbona huyo sisita wako anakununia ukiwa umekaa na gashi(akimaanisha mwanamke) ana nini kwani?” Siku moja wakati wakiwa wamekaa darasani kipindi hicho kilikuwa ni frii yani hakuna mwalimu anaeingia darasani kufundisha, kipindi hicho kiliachwa kwaajili ya kujisomea wenyewe wanafunzi. Ramah alimuuliza Hemedy hivyo.
“Mwanangu hata mimi mwenyewe pia simuelewi, leo hataki kabisa kuzungumza na mimi kisa nimekaa na yule ‘montres’ wa darasa” Hemedy alijibu.
“Sista wako anakupenda, hataki uharibikiwe kwa kujiingiza kwenye masuala ya wanawake” Ramah aliongea.
“Hata kama, ila sio kiivyo, unajua hii tabia aliianza kitambo sana, sasa mimi simuelewi kabisa”
“Enhee! Subiri nikuulize kitu, maana tokea kitambo nikitaka kukuuliza hii ishu nasahau. Hivi mbona majina ya wazazi wenu hayafanani kabisa, wewe mzee wako anaitwa Mheshimiwa na yeye mzee wake anaitwa Ganjo, sasa hapo ni vipi? embu niambie”
“Mimi na yule hatuna undugu kabisa, yani sio ndugu yangu” Hemedy alijibu.
“Kivipi yani, sijakuelewa mzee” Ramah aliongea hivyo huku akikaa vizuri kitini ili apate kumsikia vizuri, maana yeye alidhani Hilda na Hemedy ni ndugu tokea kitambo, asa ni vipi ajekuambiwa kuwa hawana undugu wowote?.
“Ni hivi, mimi nina wazazi wangu na yeye anawazi wake, ila historia zetu zinafanana, yeye wazazi wake wamekufa na mimi pia hivyo hivyo, yeye akawa anaishi na babu yake huko Tanga, na huyo babu yake na baba yangu walikuwa ni marafiki wakubwa sana enzi za uhai wa baba yangu, sasa baba yangu alipofariki, ndipo baba yangu mdogo alipomuomba babu yake Hilda mimi nikaishi kwake maana yeye ana mambo mengi kwahiyo asingeweza kunihudumia vizuri, ndipo hapo mimi nilipoanza kwenda kuishi kwa kina Hilda nyumbani kwa huyo babu yake” Hemedy akamaliza kuelezea.
“Kwahiyo hapo ndio ukakutana na huyu Hilda?” Ramah alimuuliza swali ambalo jibu lake lilikuwa wazi kabisa.
“Ndio, ila mimi sikuanza kukutananae kwa siku hiyo nilipoanza kuishi hapo, kuna siku moja ilikuwa ni sherehe yake ya kuzaliwa ndio tukakutaniana hapo na ndio ukawa mwanzo wa kujuana”
“Duh! Na yule bi mkubwa mnaeishi nae kule hom ni ndugu wa nani kati yenu nyie wawili?” Ramah aliuliza.
“Ni anti yake na Hilda, yule bi mkubwa alimtaka Hilda aje kuishi nae huku ila Hilda alikataa kuja pekeake, akidai hawezi kuondoka na kuniacha mimi kule ndipo nikaambiwa na mimi nije huku, ila nahisi ule ulikuwa ni utoto tu ulimsumbua”
“Jamaa huo sio utoto, kuna kitu chengine anacho” Ramah aliongea hivyo huku akiigamia kwenye hicho kiti alicho kalia.
“Kivipi? Sijakuelewa”
“Yani mimi nikiunganisha matukio, naona kabisa huo haukuwa utoto hata kidogo, unajua huyo unaemuita sista wako, alishawahi kumkunja shati demu flani hivi anasoma sayansi, anaitwa nani sijui, jina lake limenitoka kidogo. aliwahi kumkunja shati kule chooni kisa wewe ulienda kula nae msosi kwenye ‘break‘’, na sio huyo tu, nishawahi kumshuhudia akiwachimbia biti wanawake wenzake wengi tu kisa wewe muuni wangu” Ramah aliongea huku akitabasamu.
“Duh! Mbona yote hayo mimi siyajui?” Hemedy aliuliza hivyo huku akiwa kayatoa macho yake utafikiri amepewa taarifa ya kifo chake na izraili.
“Huwezi kuyajua kwasababu wewe ndio mlengwa, sasa je kama akiwachimbia biti anawapa onyo wasije kukupa taarifa, wewe unadhani hapo utayajuaje? Huwezi kujua mzee”
“Duh! kwanini sasa anafanya hivyo?” Hemedy aliuliza.
“Mi nakuambia yule sista wako anakitu chengine cha zaidi tofauti na huo usista”
“Kitu gani?” Hemedy aliuliza.
“Anakupenda yule” Ramah alisema kiufupi.
“Kivipi mzee mwenzangu hapo sijakuelewa”
“Aaaaa!! Medy wewe mkubwa bwana, miaka kumi na saba uliyonayo inakutosha kujua mengi, kwahiyo usijifanye mtoto mdogo”
“Ila mwanangu hicho kitu hakuna bwana, unajua mimi na yeye tunaheshimiana kama kaka na dada japokuwa hatuitani hivyo, sasa ni vipi alete kitu chengine kama hicho, na kama ni hivyo, mbona hakuwahi kuniambia hata mara moja?”
“Dah! Jamaa yangu uko nyuma sana yani, tangu lini mwanamke akamuambia mwanaume kuwa anampenda? Yani hadi ukiona mwanamke kamfuata mwanaume kisha akamuambia kuwa anampenda, basi jua mwanamke huyo amefikia hatua ya mwisho ya kuvumilia, nikisema hivyo namaanisha kuwa ameshamuonyesha ishara zote huyo mwanaume hadi zile za barabarani na huyo mwanaume akajifanya kuzivalia miwani ya mbao hizo ishara yani hazioni hata kidogo, kwani wewe hajawahi kukuonyesha ishara zozote?” Ramah alifafanua kisha akauliza.
“Hapana, labda tu yeye anapenda kila wakati kuwa na mimi karibu na hivyo kuninunia ikiwa nimekaa na demu yoyote hapa shule kwa muda mrefu”
“Basi mzee mwenzangu hata hizo pia ni ishara tosha kukuonyesha kuwa anakupenda, kwasababu gani ujue, yeye kama ingekuwa hakupendi kiivyo, basi asinge wachimbia biti wale magashi wengine unaopiga piga nao stori, anafanya hivyo akijua wao wanaweza wakakuchana laivu ikiwa yeye hawezi kufanya hivyo, sasa jamaa yangu jiongeze hapo, ohooo! asije akapata wanaojua kutia mavoko wakamteka halafu wewe akupendae akakuacha akijua wewe humpendi” Ramah wakati akiongea hivyo, mwenzake alikuwa yupo mbali kimawazo, akamshangaa kuwa kwenye mawazo wakati mwanzo walikuwa wakiongea vizuri, ikabidi amshutue na kumuuliza ni kipi anakichokiwaza kwa wakati huo.
“Unajua wewe wakati unaongea hivyo, mimi kuna kitu nimekumbuka, kuna siku tulikuwa tumekaa hom baada ya kumaliza kusoma usiku…”
KUMBUKUMBU.
“Hivi Hemedy wewe, labda kimfano ukiwa kuna mtu umempenda, wewe kama wewe utafanya nini ili ajue kama umempenda” Hilda aliongea hivyo huku akiwa amemlalia Hemedy kwenye bega, huku madaftari yao yakiwa yapo juu ya meza waliyoitumia kujisomea wawapo nyumbani.
“Mimi nitamuambia tu ukweli ili nae ajue, maana kama nisipofanya hivyo yeye hatoweza kujua kama mimi nampenda, si unajua hakuna anaejua yaliyojificha ndani ya moyo wa mtu mwengine, kwahiyo maneno yanahitajika”Hemedy aliongea.
“Mmmh! Mimi siwezi kumuambia”Hilda aliongea hivyo huku akiupitisha mkono wake wa kulia kwenye singo ya Hemedy kwenda bega la kushoto.
“Sasa wewe utafanyeje ili ajue kama unampenda?” Hemedy aliuliza.
“Mimi nitamuonyesha ishara tu, ila kumuambia mmh mmh! siwezi”
MWISHO WA KUMBUKUMBU.
“Sasa hadi mtoto ukiongea nae anakukumbatia namna hiyo, hivi wewe ulikuwa unataka ishara za namna gani labda?” Ramah alimuuliza Hemedy baada ya kukisikiliza kitu kilichomfanya Hemedy awaze wakati akiwa yeye anaongea.
“Sasa mwanangu huko kukumbatiwa pia niishara ya mapenzi? Je kama ni ile kiurafiki tu? halafu pia hilo swala la kunikumbatia wakati tukiwa wenyewe hakulianza siku hiyo”
“Sawa, basi tufanye huku kukumbatiwa mkiwa wenyewe ni kiurafiki tu. Je hiyo ya kuwachimbia biti mademu wenzake kisa wewe, nayo ni vipi, au nayo pia ni kiurafiki tu?” Ramah alimuuliza.
“Ila lakini wewe mwanzo si umesema kuwa huenda ikawa akinilinda nisiharibikiwe kujiingiza kwenye masuala ya kuwa na wanawake?” Hemedy aliuliza.
“Jamaa yangu pale nilikuwa natafuta kiki tu yakukuuliza maswali yote haya, ndio maana nikasema vile, ila mimi niliona tokea kitambo kwamba yule demu anakupenda, ila wewe ukajifanya kumvalia miwani ya mbao usiyaone hayo”
“Sasa wewe unanishauri vipi?” Hemedy aliuliza.
“Mi sina cha kukushauri zaidi ya kukuambia umchane tu”
“Duh! Mtihani huu, akini kataa je? si ataenda kumuambia anti halafu hapo ndio itakuwa mwisho wa kuishi pale nyumbani kwao?” Hemedy aliuliza, alionekana dhahiri alikuwa na hofu, haikujilikana kuwa ni hofu ya kutongoza mara ya kwanza au ya kufukuzwa nyumbani kwa anti yake Hilda pindi atakapoenda kumsemea. Akapeleka macho sehemu anapokaa Hilda na kumuona msichana huyo ni mwenye kumuangalia na yeye, wakajikuta wamegonganisha macho yao, Hilda akawahi kuyaondoa macho yake huku akijifanya amevimbisha mashavu yake kwa kukasirika kama maputo ya kwenye ile sherehe yake aliyowahi kufanyiwa kipindi akiwa na miaka kumi na moja. Hemedy akarudisha macho yake huku akiwa natabasamu usoni mwake.
“Aaaa!! Jamaa hawezi kukukataa hata kidogo, kwanza mtoto mwenyewe anakupenda, sasa ataanzaje kukukatalia?”
“Sasa mzee nitamuanzaje anzaje? maana sijawahi kutongoza mwanamke hata kwa bahati mbaya”
“Hapo mzee mwenzangu itabidi tu upambane na hali yako yani ujitafute mwenyewe maana hata mimi sijui huyu mtoto leo nitaanzaje kumchana”
“Haaa!! Kwani jamaa kuna gashi unataka ukamchane leo?” Hemedy alimuuliza.
“Dah!! Kumbe mwanangu sijakuambia. Kuna demu mmoja anasoma ‘business‘ anaitwa Hawa, nataka leo nikamchane laivu maana nishachoka kuumia mwenyewe kila siku”
“Duh!! Ila lazima akuelewa, yani vile ukimchana huku unamuimbia imbia, lazima akuelewe tu, embu kwanza kabla ya yote niimbie kidogo mzee maana kitambo sijaisikia sauti yako wakati ukiwa unaimba”
“Usijali wewe ni mshikiji wangu lazima nikuimbie” alipoongea hivyo, akajikohoza kidogo na kuanza kuimba.
…………………How many times do i have to tell you? Even when you’re crying, you’re beutifull too. The word is beating you down, I’m around Through every mood. You’re my donwfall, you’re my muse. My worst distraction, my rhythm and blues. Ican’t stop singing, it’s ringing in my head for you. Hayo ni baadhi ya maneno yaliokuwepo kwenye nyimbo hiyo aliyoiimba ya msanii mmoja mmarekani mweusi anaeitwa Jonh Legend, nyimbo hiyo iliitwa All of me. Kwahakika Ramah alikuwa na sauti nzuri ya kuimba.
“Mwanangu safi sana, halafu hiyo nyimbo itabidi pia umuimbie ili akuelewa maana hiyo nyimbo inamashairi mazuri kinyama. Hivi jamaa nani aliekufundisha kuimba?”
“Yani we jamaa kila siku lazima uniulize hilo swali, ila poa subiri nikujibu. Hakuna alienifundisha kuimba ni kipaji tu nimebarikiwa na mungu ndugu yangu, ila gitaa ndio nimefundishwa na mzee mmoja wa pale mtaani”
“Ina maana hata gitaa pia unaweza kupiga?” Hemedy aliuliza.
“Ndio ndugu yangu”
“Fanya basi siku nijekukusikia ukiimba huku ukipiga gitaa, dah sipati picha jinsi utakavyoimba”
“Usijali, sasa kaka subiri nimfuate yule demu nikamuambie kabisa kuwa muda wa kutoka shule ninamaongezi naye, yani sikufichi ndugu yangu, nataka nimuambie leo leo ili nijitue huu mzigo nilioubeba moyoni mwangu tangia muda” Ramah aliongea hivyo huku akinyanyuka kwenye kiti alicho kalia.
“Poa poa kaka, nakuaminia” Hemedy alijibu huku akitabasamu. RamAh alipofika kwenye mlango wa hapo darasani, akageuza tena na kurudi mahali alipo Hemedy.
“Dah!! Mwanangu nina hofu kinyama yani, sijui nighairishe leo?” Ramah aliongea hivyo huku akikaa kwenye kiti.
“Jamaa hapo utaharibu, unajua unapoamua kufanya kitu basi kifanye kwa ule wakati ulioupanga, hofu isikufanye ukaghairisha ulichopanga kukifanya, huwezi jua huwenda ikawa leo ndio siku yako ya bahati” Hemedy alimpa moyo mwenzake.
“Dah!! Nina hofu kinyama mzee mwenzangu iliyochanganyikana na uoga wa kutongoza kwa mara ya kwanza”
“Kumbe hujawahi kufanya hivyo hata siku moja? Ila mi nakushauri leo isipite bila kumuambia na kama ikipita leo, basi usimuambie tena siku yoyote, subiri ifike siku kama ya leo, tarehe kama ya leo, mwezi kama wa leo na mwaka kama waleo ndio umuambie”
“Hahaha! Jamaa nani aliekuambia siku hii itajirudia tena?” Ramah aliuliza huku akicheka.
“Ndio hivyo sasa, unatakiwa siku ya leo isipite bila kumuambia kwasababu haitajirudia tena”
“Sawa, ila nawewe siku ya leo isipite bila ya kumchana ukweli yule mama mvimbaji”
“Hahaha!! Usijali ila anza wewe kwanza”
“Basi poa kaka acha mimi nimfuate yule demu nikamuambie kuwa baada ya kengele ya kutoka hapa shule nina maongezi nae” Alipoongea hivyo akanyanyuka kwenye kiti na kutoka darasani humo. Hemedy akabaki akiwa amekaa mwenyewe, ila ghafla mbele yake akasimama Hilda aliekuwa akimuangalia kwa macho yake mazuri, alifanya hivyo kwa sekunde kadhaa kisha akakaa kwenye kiti kilichokuwa karibu na Hemedy, alionekana dhahiri kuna jambo anataka kumuambia.
“Umekula wewe?” Hilda aliuliza.
“Hapana” Hemedy alijibu.
“Kwanini?”
“Nitaanzaje kula ikiwa niliezoea kula nae ameninunia tena bila kujua kosa langu” Hemedy alijibu taratibu kama vile ni mwenye kuonewa kwa jambo hilo.
“Hapana sio asubuhi, ila ni tangia jana usiku nilivyo kula ndio hadi sasa sikula kisa wewe” Hilda aliposikia maneno hayo, aliangalia saa yake ya mkononi na kusema.
“Bado kama dakika ishirini kengele ya kutoka igongwe” akatulia kidogo na kusema. “twenzetu kantini tukale” Alimshika mkono na kunza kutoka nae humo darasani, wakaongozana hadi sehemu panapouzwa vyakula humo humo ndani ya shule, walipofika waliagiza wanachotaka na kuanza kula baada ya kuletewa chakula hicho, ilikuwa ni kesi ukikutwa una kula muda ambao sio rasmi kwa kufanya hivyo, viboko au adhabu yoyote itakuhusu pindi ukikutwa unakula kwa muda ambao haukupangwa kwaajili hiyo.
“Hilda?” Hemedy aliita wakati wakiwa bado wanaendelea kula.
“Abee” Hilda aliitikia huku akinyanyua kikombe cha chai na kukigusanisha na lipsi zake, akavuta ndani kinywaji aina ya chai kilichopo ndani ya hicho kikombe, kisha akakishusha kwa utaratibu juu ya meza.
“Kwanini unaninunia kama sio kunichukia pale ninapokaa au kusimama na mwanamke yoyote hapa shule?” Hemedy aliuliza kwa utaratibu mno swali hilo na nikama swali hilo binti huyo hakulitegemea kuulizwa mahala hapo, akabaki kutafuna kipande cha chapati kilichokuwa ndani ya kinywa chake huku akiwa sura yake ameinamisha chini, haikujulikana ni uzito wa hilo swali au ni aibu zilizomkumba baada ya kuulizwa.
“Kwani hujui?” aliuliza swali hilo baada ya kupata ujasiri wa kuongea.
“Siku zote mwenye kuuliza hakijui aulizacho, ndio maana ameuliza ili ajue, na hata mimi nimeuliza ili nijue” Hemedy aliongea kwa utaratibu.
“Huenda ikawa unakijua unachokiuliza, ila umeuliza ili upate uhakika zaidi” Hilda alijibu vile vile kwa utaratibu.
“Sawa nimekuelewa. Unaweza ukanijibu, maana mimi sijajua ni kipi hasa kinacho kufanya uwe katika hali ile”
“Muda sahihi ukifika nitakuambia, ila now, twenzetu maana tumeshamaliza kula”
Hemedy hakuwa na jengine la kuongeza, wakalipa walichokula na kuanza kuondoka kuelekea darasani, walipofika, kengele nayo ikagongwa na kuwafanya wanafunzi kuanza kukusanya vilivyovyao na kuondoka mahala hapo.
Katika darasa moja lilokuwepo hapo shule, wakati wanafunzi wengi wameshaondoka shuleni hapo, darasa hili lilihifadhi wanafunzi wawili wajinsia tofauti, wakiume alikuwa ni Ramah na wakike bado hatujapata kumjua, wanafunzi hao walikuwa wamekaa kwenye viti vilivyoangaliana na katikati yao kulitenganishwa na meza.
“Hawa” Ramah aliita jina hilo, na hapo ndipo tulipopata kulijua jina la banati huyo.
“Nakusikiliza” banati huyo au Hawa kama Ramah alivyomuita, aliitikia kwa sauti ya upole na yenye kutamanisha kila muda kuisikia. Ramah alimuangalia binti huyo kwa sekunde kadhaa kisha akajikohoza kidogo na kuongea.
“Mungu alipoiumba hii dunia ambayo ndani yake kuna ardhi na mbingu, akaumba majini ili waje kuishi ndani ya sayari hii, ila baada ya kuona viumbe hivyo vinaleta vurugu katika ardhi yake, akaamua kuviondoa kwenye ardhi kwa kuleta gharika ambalo liliwakimbiza baharini na kwenye miti mikubwa viumbe hao. Alipoona ardhi imebaki tupu bila ya kuwa na kiumbe yoyote, akaona aumbe kiumbe chengine ambacho kitakuja kuishi kwenye hii ardhi, ndipo hapo alipomuumba Adamu, ila Adamu kabla ya kuja kuishi huku duniani, alikuwa akiishi pepono kwa muda mrefu, na wakati wote huo alipokuwa akiishi huko, alikuwa ni mpweke sana, na mungu kwavile alikuwa akikipenda kiumbe hicho alichokiumba mwenyewe, akaamua akiumbie kiumbe chengine ambacho kitakuwa ni faraja kwake, ndipo akamuumba na Hawa kwa kutokana na ubavu wa kushoto wa Adamu. Adamu alifurahi sana baada ya kupata mwenza wa kuishi nae sehemu hiyo, waliishi kwa furaha hadi pale walitolewa sehemu hiyo na kuletwa huku duniani baada ya kushawishiwa na shetani wale tunda ambalo wameambiwa na aliewaumba wasilile. Japokuwa walishushwa duniani, ila mungu aliwashusha kila mmoja sehemu yake tena iliyokuwa mbali, inasadikika kuwa Hawa alishushwa katika nchi ya India huku Adamu akishushwa katika moja za nchi za huko uarabuni” Ramah akanyamaza kidogo kisha akauliza. “Unaweza kujua ni kipi kilicho wafanya wakakutana na kuishi pamoja wakati kila mmoja alishushwa sehemu ya mbali na mwenzake?”
“Hapana sijui” Hawa alijibu huku akijiweka vizuri kitini ili kuyaskiliza maneno ya huyo kijana.
“Upendo. Upendo ndio ulisababisha wakakutana tena kwa mara nyengine. Hawa alitoka India kumtafuta Adamu wake mpaka katika nchi moja ya huko uarubuni, kwa nguvu ya upendo aliyonayo alifanikiwa kumpata. Hii haimaanishi kuwa Adamu hakuwa na upendo kwa Hawa, la hasha! Alikuwa akimtafuta sana Hawa, ila hapa tunaonyeshwa ni jinsi gani nyie wanawake mna roho ya huruma na upendo wa dhati juu yetu, kwasababu mmetubeba katika matumbo yenu kwa miezi tisa na mkatulelea hadi hivi sasa tumekuwa. Japokuwa sisi ndio sababu kubwa kupatikana kwa nyie ila nyie ndio sababu kubwa zaidi kupatikana kwa sisi.” Akatulia kidogo ili maneno hayo yamuingie vizuri binti huyo, kisha akaendelea. “Unajua kwanini mungu alitaka viumbe hawa waishi pamoja?” Ramah alimuuliza.
“Ili waijaze dunia, maana dunia kwa wakati ule ilikuwa haina watu, au nimekosea?” Hawa aliongea hivyo huku akitabasamu, bilashaka aliipenda stori hiyo, maana alisahau kuwa muda huo ni mwenye kuhitajika kuwa nyumbani kwao baada ya wanafunzi kutolewa shuleni.
“Hujakosea hata kidogo, ila kuna jengine la zaidi lililomfanya mungu akataka watu hao waishi pamoja. Upweke ndio uliwafanya watu hao waishi pamoja. Kuna msemo unaosema kuwa hakuna mwanaume bila mwanamke na hakuna mwanamke bila mwanaume. Si hata wewe pia unakubaliana nao?” Ramah aliuliza.
“Yeah, nakubaliana nao, kwasababu hata wazazi wetu pia si wako pamoja ili kuukamilisha huo msemo” Hawa alijibu.
“(Huku akitabasamu) nimependa jibu lako” akatulia kidogo, kisha akaendelea. “Hata viatu huvaliwa kwa pea, huwezi kuvaa kiatu kimoja kwasababu itakuwa umeudhulumu mguu mwengine, hata hivyo huwezi kutembea bila viatu, hapo itakuwa umejidhulumu mwenyewe, na pia huwezi kuvaa viatu tofauti itakuwa umeidhulumu miguu yote miwili. Unajua nini nimemaanisha?”
“Hapana sijajua, nasubiri uniambie” Hawa aliongea huku akijiweka vizuri zaidi kitini.
“Nilipokuambia kuwa huwezi kuvaa kiatu kimoja kwasababu utaudhulumu mguu mwengine, nilikuwa namaanisha kuwa, mwanadamu hawezi kuwa pekeake siku zote, kwasababu anahitajika kupata mtu wa kumfariji kwenye huzuni na kufurahia nae kwenye furaha, na niliposema kuwa huwezi kutembea peku kwasababu itakuwa umejidhulumu mwenyewe, nilikuwa namaanisha. Huwezi kuwa na furaha pasi na kuwepo kitu cha kukupa hiyo furaha, ni lazima uitafute furaha yako popote pale ilipo ili nawe ufurahi kama wafurahiavyo wengine. Na niliposema kuwa huwezi kuvaa viatu tofauti, nilikuwa namaanisha, pamoja na kuitafuta hiyo furaha popote ilipo, nilazima kwanza uzingatie ni furaha ipi itakufanya uwe na furaha kila ukiiona au ukiwa nayo, kwasababu usipozingatia kutafuta furaha sahihi juu yako, basi utakuwa upo kama yule mtu alievaa viatu tofauti, kwasababu hatokuwa akijiamini pale anapopita mbele za watu akidhani labda watu watamcheka au watamsema kwa vile alivyovaa. Basi ataona afadhali avue kimoja ili aiepuke ile aibu ya kuvaa viatu tofauti, hata hivyo pia watu watamcheka kwa kuvaa kiatu kimoja huku mguu mwengine ukiwa hauna kitu. Mwisho wa safari ataamua avue tu hicho kimoja atembee peku akidhani hiyo itakuwa ni afdhali kwake, ndio hapo atakapokuwa amejidhulumu mwenyewe kwa kuitembeza miguu yake peku kwenye jua kali. Unadhani labda afanye nini mtu huyo ili aepukane na yote hayo?” Ramah alieleza kisha akauliza.
“Itambidi kutafuta viatu vilivyofanana na avivae ili aepukane na kuchekwa na watu kisha kuvivua kabisa viatu badili alivyo vaa, kwakufanya hivyo ndio ataonekana yupo sahihi mbele za wtu” Hawa alijibu huku akitabasamu.
“Safi sana, nimeyapenda majibu yako. Yote hayo nilikuwa namaanisha kuwa. Binadamu mwenye moyo wa nyama, inahitajika apate mtu wa kuwa nae pamoja, ambae atakuwa nae kwa kila hali, bila kuwa hivyo, basi mtu huyo atakuwa ni mpweke na hatokuwa na furaha kamwe hata awe na utajiri mkubwa, atakuwa ni kama yule mtu alievaa kiatu mguu mmoja. Na ikiwa amemtafuta mtu wa kuwa nae pamoja na mtu huyo asiwe sahihi kwake, basi atakuwa ni kama yule mtu alievaa viatu badili. Na kwavile amepata mtu asie sahihi kwake, basi atamchoka na kuamua amuache abaki mwenyewe, na ndio hapo tutakapo mfananisha na yule mtu alieamua kuvivua vile viatu badili na kuamua kubaki peku huku akidhani hiyo ndio njia sahihi ya kuamua. Ili apate furaha ya milele, basi inambidi apate mtu sahihi wa kuwa nae. Unajua nini namaanisha?”
“Hapana sijajua bado” Hawa alijibu kwa utulivu huku akimuangalia kijana huyo.
Akapeleka macho yake juu ya dari la hilo darasa walilomo na alipoyashusha, moja kwa moja akamtazama mnyange huyo mwenye kila aina ya sifa za kuitwa mrembo, maana alikuwa katika mavazi ya shule ila uzuri wake ulionekana dhahiri, sipati picha akionekana kwenye mavazi ya kawaida.
“Kila mwanadamu ameumbwa kwa moyo wenye upendo ndani yake, na moyo huo hupenda pale unapoona mtu alieuvutia, najua utajiuliza moyo kwani nao unamacho, ila tambua kuwa unapokea taarifa hizo kwenye ubongo zikitokea kwenye mboni za macho pindi pale yanapokuwa yameona kitu kilicho yavutia. Hadi hapo, kinapatikana kitu kinachoitwa Hisia, kuna hisia za aina nyingi, ila ambazo nazizungumzia hapa ni zile hisia zinazompata mtu pale anapompenda mtu.” alipofika hapo akacheka kicheko kidogo, kisha akamuuliza swali. “Unajua kwanini nimetabasamu kama sio kucheka kabisa?”
“Hapana sijajua” Hawa alijibu.
“Sijacheka eti kwavile ni upumbavu, ila hata hivyo ni upumbavu kweli, kwasababu gani nakuambia hivyo. Kuna ambao hawezi kuzikontroo hizia zao kwa wale wawapendao, ndio pale hujikuta wanaenda kuroga ili ampate mtu ambao hisia zake zimemuelewa, huku wakisahau kuwa hata ulimi pia unaweza kuroga pale utakapoutumia vizuri. Ndio maana nikasema huo ni upumbavu ila upande wao wanaona sio upumbavu, kwasababu gani nakuambia hivyo, pale unapomroga mtu ili akupende, ndio inaweza ikatokea hivyo, ila tambua kuwa zile dawa au kizizi kwa lugha rahisi, zinapungua nguvu kila baada ya kuisha kwa siku, na mwisho yule aliemroga mtu kwa kizizi, pale kizizi kile kitakapoisha, basi zawadi yake ni kupokea maumivu kutoka kwa yule mtu aliemroga ili ampende na mwisho wa siku maumivu yanapo mzidi hupelekea kuwa chizi au hata kujiua kabisa. Nikisema hivi simaanishi wale waliochizika Kwajili ya mapenzi au kujiua kwaajili ya mapenzi wote wale wameroga ili wapendwe, la hasha! ila wengine yanawakuta hayo kutokana na kupenda sehemu ambayo sio sahihi kwao, hapo tuna wafananisha na yule mtu alievaa viatu badili bila ya kujua hiyo sio njia sahihi ya kuitafuta suluhu ya miguu yake kwenye jua kali” Akamaliza hivyo na kumuangalia machoni binti huyo, ni kama vile alikuwa akivuta punzi ili aendelee mbele zaidi, maana alijua hadi hapo huyo banati hajajua nini lengo lake la kumuambia maneno yote hayo, akavuta punzi ndani na kuzitoa nje, kisha akaendelea.
“Najua haujajua ni kipi hasa kilichonifanya mimi nikakuweka hadi muda huu ambao wenzetu tayari wameshafika majumbani kwao, ila napenda tu kukuambia kuwa, unaweza ukaishi na kitu moyoni kwa muda mrefu pasi na kujua ni vipi utakitoa nje ili mlengwa wa hicho kitu akijue, kwa muda mrefu nilikuwa nikimuomba mungu anijaalie ujasiri wa kukiwasilisha kile ambacho kipo moyoni mwangu kwa muda mrefu, sina uhakika kwa hichi ambacho nitakiongea hivi punde kitakuudhi ama la, na kama ikiwa ni hivyo basi huna budi kunisamehe kutokana wanadamu hatukuumbwa kwa ukamilifu, nilazima tukoseane kisha tuombane msamaha ili tuzidi kuimarisha urafiki wetu kama sio undugu kabisa”. akatulia kwa sekunde kadhaa, kisha akaendelea kuongea, kipindi hicho binti huyo alikuwa kimya kabisa utafikiri si yeye mwenye kuambiwa maneno hayo.
“Hawa Nakupenda, Nakupenda kumaanisha, sitaki kuwa na wewe eti kwavile na mimi nijivunie kuwa na mwanamke mzuri mwenye kila sifa ya kuitwa mrembo, hapana, ila nakupenda kwasababu moyo wangu ndio umekuchagua wewe, sikukurupuka kukupenda eti kwa vile umeuvutia moyo wangu, bali nilikaa nikafikiri na kuona wewe ndie ambae utakae kamilisha uwepo wa kiatu chapili kwenye maisha yangu ili nisichekwe na kusemwa kuwa nimevaa viatu ambavyo sio sahihi. Hawa narudia tena kukuambia kuwa Nakupenda” Ramah alipofika hapo akatulia na kusikilizia mnyange huyo atasema nini.
“Mmmh!! Ramah” Hawa aliishia kuguna na kuita tu jina la kijana huyo halafu asijue kitu gani aseme, akabaki kimya.
“Hawa” Ramah alimuita na kumfanya binti huyo kuinua uso wake na kumuangalia kijana huyo, macho yao yalipogongana, akawahi kurudisha uso wake chini, Ramah kuona hivyo, akaendelea na alichopanga kusema.
“Najua huamini kuwa mimi ndio nimekuambia maneno hayo, najua kuwa nimekushtukiza kukuambia hivi, ila tambua kuwa sikuanza kukupenda leo wala jana, nilikupenda muda mrefu, unaweza kuniuliza, Kwanini sikukuambia muda wote huo, ila tambua kuwa kila kitu kinatokea kwa wakati, huenda ikawa siku zote hizo haukuwa wakati sahihi wa kukuambia haya na ndio maana nikaja kukuambia leo baada ya kuona wakati sahishi umefika. Hawa naomba niwe Adamu wako kama yule Adamu wa Hawa, naomba niwe ubavu wako wa kulia kama ambavyo Hawa alivyokuwa ubavu wa kushoto wa Adamu” alipofika hapo akaushika mkono laini wa binti huyo na kumuambia. “Naomba uwe huru na jibu lako, maneno yangu yasikulazimishe unipende, japokuwa moyo wangu unataka unipende, sikulazimishi uwe na mimi, japokuwa mimi nataka niwe na wewe, kwahiyo usiumize kichwa kwa kufikiria ni jibu gani unaweza ukanipa, nipo tayari kupokea jibu lolote japokuwa nitaumia nikisikia ombi langu limekataliwa, nikuambie tu kuwa huru na jibu lako” Ramah aliongea kwa sauti ambayo ilikuwa ni ngumu sana kuingia kwenye ngoma za masikio ya mnyange yoyote halafu isimletee msisimko. Labda awe hana haiba za kike.
“Ramah, nikuambie tu kwamba, kama vile ambavyo hukukurupuka kunifuata na kuja kuniambia hivyo, basi na mimi nakuambia kuwa siwezi kukurupuka na kukujibu chochote kwa leo, kwasababu ninaweza nikawa sahihi au sipo sahihi kwa hilo jibu, kwahiyo nahitaji muda wa kufikiria na mimi” Hawa aliongea hivyo huku akiwa macho yake akiyapeleka huku na huko pasi na kujua ni wapi anataka kuangalia.
“Sikatai kukupa muda wa kufikiria, ila jua utaniweka roho juu juu kama mtu anaesubiria majibu ya kupima ukimwi, ok, nadhani siku ya leo inaweza kukutosha kabisa kwaajili ya kulifikiria hili?” Ramah aliongea hivyo huku akimuangalia binti huyo.
“Usijali, hadi kesho nadhani nitakuwa ninajibu sahihi la kuja kukupa” Hawa aliongea.
“Sawa, lakini naomba basi unitoe wasiwasi kwa hilo jibu utakalonipa”
“Usijali Ramah, kwasasa naomba niende nyumbani maana hata muda pia tayari ushakwisha sana” aliongea hivyo huku akiutoa mkono wake kwenye viganja vya Ramah ambavyo muda wote vilikuwa vimeushikila mkono wake.
“Sawa, mimi nakuruhusu uende ila tambua kuwa tangu muda huu, yupo mwanaume anaekupenda dhati kuliko wote duniani, tukiachana na baba yako mzazi”
Hawa aliishia kutabasamu tu, kisha akainuka na kuanza kupiga hatua ndogo ndogo. Hapo ndipo uzuri wake ulipojidhihirisha dhahiri, alikuwa na umbo matata sana lililo jichonga mithili ya namba nane, alibarikiwa miguu ambayo ni wanawake wachache sana hapa afrika walikuwa wamebarikiwa, hakuwa mrefu sana wala hakuwa mfupi, na chaajabu zaidi, ni pale alipoanza kutembea, alikuwa kama vile hataki au ni mwenye kuiyogopa sakafu ambayo alikuwa akitembea juu yake, ilikuwa si rahisi kwa mwanaume rijali kutogeuza shingo yake pindi akipishana nae barabarani.
“Hawa” Ramah muda wote alikuwa akimuangalia binti huyo anavyotembea, ikabidi amuite muda huo alikuwa ameshafika karibu na mlango wa kutokea, banati huyo aligeuka kwa mgeuko wa kipekee sana, aligeuka kwa taratibu sana utafikiri alikuwa akipelekwa “slow”, kisha akasimama huku akimuangalia Ramah.
Ramah baada ya kuona mnyange huyo amesimama, akainuka pale alipokaa na kumfuata hadi pale aliposimama, wakawa wanaangaliana kama majogoo yaliotoka kupigana muda mfupi uliopita wakigombania kuku jike. Ramah akaunyanyua mkono wake wa kulia na kuushika mkono wa kushoto wa Hawa, kisha mkono wa kushoto wa Ramah akaushika mkono wa kulia wa Hawa. Hawa muda wote alikuwa yupo kimya huku sura yake ameinamisha chini. Ramah akamuita tena na kumfanya binti huyo anyanyue sura yake na kumuangalia kijana huyo. Mdomo wa Ramah, taratibu ulisoge ulipo mdomo wa binti huyo na kujikuta midomo yao ikigandana huku ulimi wa Ramah ukiwa ndani ya kinywa chake, hakuwa na jinsi zaidi ya kufumba macho ili kuyakwepa macho ya Ramah aliekuwa akifanya kitendo hicho huku akimuangalia yeye.
Kitendo hicho kilidumu kwa sekunde kumi, baada ya hapo midomo yao ikaachiana na kubaki wametulia tu huku Hawa uso wake akiurudisha chini tena. “Nakupenda” hilo ndio neno la mwisho kutamkwa na Ramah hapo kisha akamuachia binti huyo na kumfanya aondoke haraka humo na kumuacha Ramah mwenyewe huku akitabasamu, tabasamu hilo lilipelekea kuwa ni kicheko, na kicheko hicho kikapelekea kuanza kurukaruka kama mtoto mdogo aliemuona baba yake akiwa anatoka kazini huku mkononi ameshika ‘icecream’ aliyoomba aletewa asubuhi wakati akiwa baba yake anatoka.
Baada ya kuruka ruka sana, akaona anaweza kuitoboa sakafu hiyo ya hapo darasani kwa kufanya hivyo, akaamia kwenye meza, akapanda juu yake na kuanza kurukaruka huku akirusha mikono juu hadi pale alipoanguka na kuuteua mguu wake wa kushoto, aliinuka huku akiwa ameukunja uso wake Kwa maumivu, alianza kutembea kwa kuchechemea kwa maumivu ya mguu huku akiwa amechukia sana, ila uso ukabadilika na kuwa ni wenye tabasamu baada ya kukumbuka kitendo kilichomfanya hadi kuanguka hivyo, akaondoka darasani humo huku akichechemea na kutokomea zake.
Majira ya tatu usiku, Hilda na Hemedy walikuwa wapo sehemu yao waliyoifanya ni pakusomea wawapo nyumbani kwao. Walisoma kwa saa moja nzima baada ya hapo wakafunga madaftari na kuanza kupiga stori za kawaida hadi pale, walipoishiwa na maeneno ya kuongea.
“Hilda” Hemedy aliita na kumfanya binti huyo kumuangalia ishara ya kumtaka aendelee na kile anachotaka kukisema.
“Kwani bado hujachoka tu kukaa hapa?” Hemedy alimuuliza.
“Kuchoka kivipi yani?” Hilda naye aliuliza.
“Mi nishachoka nataka nikalale”Hemedy aliongea.
“Mi sijachoka, ila kama wewe umechoka, basi tuingie ndani” Walikusanya madaftari yao na kuingia nayo ndani, kwa vile walikuwa tayari wameshakula chakula cha usiku, basi kila mmoja aliingia chumbani kwake kwenda kuisaka kesho yake.
Siku iliyofuata, shuleni kwao, Hemedy alikuwa na hamu ya kutaka kuambiwa kuwa Ramah alifanikiwa kwa kile alichokipanga siku ya jana, ila muda wa kufanya hivyo ndio ambao ulikuwa hakuna kutokana na vipindi vya asubuhi darasani kwao, walimu wote waliingia, hakuwa na budi tu kusubiri, akapanga atamuuliza ifikapo muda wa mapumziko.
Muda wa mapumziko ulipofika, walichukuana yeye na Ramah na kuanza safari ya kuelekea kantini, walikuwa na mazoea ya kwenda watatu, ila kwa siku hiyo, Hilda hakuweza kutoka kutokana na kazi za kufanya alizokuwa nazo kumbana, yeye akabaki darasani huku wenzake wakienda kantini.
“Oya mzee, haya nipe habari, ulifanikiwa jana au mtoto kazingua?” Hemedy alimuuliza baada ya kukaa kwenye viti wakisubiri chakula walichoagiza.
“Anaanzaje kuzingua labda kimfano?” Ramah aliongea kwa majigambo huku akitabasamu.
“Mtoto jana nimempiga masaundi halafu nikadai jibu langu pale pale, ila akasema hawezi kukurupuka kunijibu, akaomba nimpe siku ya jana afikirie kisha leo aniletee jibu” Ramah aliongea hivyo wakati huo vyakula walivyoagiza vikiwa mezani tayari.
“Ukimuangalia matumaini ya kukubali anayo?” Hemedy aliuliza huku akikata andazi na kulitia mdomoni.
“Aaaa!! Sidhani kama atakataa, kwasababu vile anataka kuondoka, mtoto nikamuita, nilipofika karibu yake nikamla denda, halafu nikamalizia na neno nakupenda kisha nikamuacha aende” Ramah aliongea hivyo kisha akachukua kikombe cha chai na kunywa.
“Ebwana eeee!! Kwahiyo umemla hadi denda, hajazingua lakini?”
“Azingue wapi? Katulia tu, yani hapa nina asilimia tisini na tisa za kumpata naweka asilimia moja tu za kumkosa”
Majira hayo wakawa tayari wamemaliza kula, wakalipa na kuanza kuondoka hapo kuelekea darasani. Ramah alimuambia Hemedy kuwa muda huo anaenda kumfuata Hawa darasani kwao ili akapewe jibu lake, akaondoka darasani kwao na kwenda kwenye darasa analosoma binti huyo, alipofika akamuulizia na kuambiwa kuwa siku hiyo hakufika shuleni, hakutaka kuamini maneno ya mtu huyo, ikabidi amuulize mwengine na kupewa jibu hilo hilo kuwa binti huyo Hakufika shuleni.
Akaondoka darasani humo kwa unyonge kama kifaranga cha kuku kilicho mwagiwa maji, akarudi darasani kwao na kutulia sehemu yake kisha akamuambia Hemedy kuwa binti hakufika shule leo. Wakaendelea na vipindi hadi pale kilipofika kipindi cha frii, ndipo walipoanza kupiga tena stori.
“Kwahiyo jana hukumuambia chochote?” Ramah aliuliza.
“Ndio jamaa, sasa unadhani ningeanzaje labda” Hemedy alijibu.
“Dah! Jamaa unazingua kinyama yani, asa umeshindwaje kumuambia?” Ramah alimwambia kwa kulalamika utafikiri hilo jambo ni la muhimu kulifanya.
“Uoga kaka, nina hofu nyingi mshkaji, sijui nimuanzaje”
“Kwahiyo unakiri kabisa kwamba umemkosa?”
“Hapana, ila leo nitajitahidi”
Walimaliza maongezi hayo na kupiga stori nyengine, muda huo nae Hilda alikuja hapo na kupiga stori wote watatu hadi pale kengele ilipogongwa ya kutoka, wakaondoka shuleni hapo kuelekea majumbani kwao huku Ramah akimsisitiza mwenzake siku ya leo asifanye makosa.
* *
Kama kawaida yao, majira hayo ya usiku walikuwa kwenye kibaraza cha nyumba yao huku mbele yao kukiwa na meza ambayo juu yake waliweka madaftari wao wenyewe wakiwa wamekaa kwenye viti kuielekea hiyo meza, walisoma kile walichofundishwa kwa siku hiyo, ila siku hii ya leo Hilda aliona mabadiliko kwa Hemedy, hakuwa ni mwenye kuchangamka kama siku zote, ikambidi amuulize ni kipi kilichomfanya hadi kuwa katika hali hiyo?
“We acha tu” Hemedy alijibu hivyo huku akionekana dhahiri ana jambo lililomsibu.
“Sasa niache nini wakati nakuuliza. unaumwa?” Hilda aliongea hivyo huku akiupeleka mkono wake kwenye paji la uso wa Hemedy kupima kama ana joto.
“Hapana siumwi Hilda, ila kuna kazi nimepewa niifanye” Hemedy aliongea kwa utaratibu.
“Kazi gani hiyo?” Hilda aliuliza kwa shauku. “Nimepewa kazi ya kuuokoa moyo wa mtu zidi ya waizi na mabedui wanao utaka moyo huo kwa hali yoyote ile, kisha wakishaupata waufanye vile watakavyo halafu wauwache na kutupilia mbali ukiwa na maumivu makubwa ya kutelekezwa” Hemedy aliongea hivyo, ila Hilda hakuambulia chochote kwenye maneno hayo, akabaki akiyatafakari, mwisho akakosa jibu na kuamua aulize nini maana ya maneno hayo?
“Hilda, jua kwamba nikiuacha huo moyo upotee, basi nina cha kujibu mbele ya alienituma, na mimi sitaki yote hayo yanitokee kwasababu nitakuwa sijamfanyia haki alienituma, kwasababu alinipa kazi hiyo muda mrefu, ila mimi nilikuwa nakosa njia ya kuulinda moyo huo” Hemedy alizidi kumchanganya binti huyo kwa maneno yake ya mafumbo.
“Unajua Hemedy mimi sikuelewi, embu acha kuongea kwa mafumbo basi ili nikuelewe”
“Upo tayari kunisaidia hiyo kazi bila kujali ugumu uliyokuwepo?” Hemedy alimuuliza.
“Ndio Hemedy, kumbuka mimi na wewe tumetoka mbali, langu lako, lako langu, sasa ni vipi nikuache uifanye mwenyewe hiyo kazi wakati huenda uwezo wa kukusaidi ninao?” Hilda aliongea kwa upole.
Hemedy baada ya kusikia hivyo, akamuangalia banati huyo usoni, kisha macho yake akayapeleka kwenye madaftari yaliyokuwa juu ya meza, alipofika hapo aliyagandisha macho yake utafikiri ni mwenye kuyaomba msaada madaftari hayo yamsaidie kuwasilisha kile anachotaka kusema. Akayaondoa macho yake hapo na kumuangalia Hilda aliekuwa muda wote akisubiri kuambiwa kwa ufasaha hiyo kazi aliyopewa Hemedy.
“Hilda kazi hiyo nimepewa na moyo wangu nije kuokoa moyo wako juu ya wale wanaoutaka moyo wako kwa hali yoyote halafu wakishaupata waufanye vile watakavyo kisha waje kuutelekeza ukiwa na maumivu yatakayopambwa kwa chozi lako, na mimi sitaki yote hayo yatokee” Hemedy aliongea.
“Sijakuelewa nini unamaanisha” Hilda sio kwamba hakuelewa maneno hayo, ila alitaka uhakika zaidi ndio maana akauliza hivyo.
“Namaanisha Hilda Nakupenda, sitaki kuona unawakabidhi watu wengine moyo wako, wasiojua ni furaha ipi unaitaka, wasiojua ni kitu gani unapenda, wakati nikiwa mimi ninaeyajua yote hayo nipo” Akatulia kidogo, na kuendelea. “Hilda, nikisema nakupenda basi jua sikuongopei, ninakupenda kweli, naomba uuruhusu moyo wako useme na moyo wangu, naamini ndio utaamini haya niyasemayo, ila kama hutofanya hivyo, ukiruhusu masikio yako tu yasikilize maneno yangu, basi utaona kama vile nikiongeacho sikimaanishi au utafikiria na mimi ni mmoja wa hao mabedui wanaoutaka moyo wako wauchezee kisha wauache pasi na huruma ukiwa na maumivu ya kutendwa. Hilda naomba niwe faraja yako pale utakapo kuwa na huzuni, naomba nikutoe wasiwasi pale utakapokuwa na hofu, naomba nilidake chozi lako pale litakapo dondoka, naomba niwe mlinzi wako wa moyo wako mnyonge. Hilda ruhusu moyo wako useme na wangu basi” Ramah aliongea Kwa upole na kwakulalamika.
“Hemedy unasema unanipenda?” Hilda muda wote huo alikuwa amekumbwa na butwaa asiamini masikio yake kuwa maneno hayo yanatoka kwa mtu aliemhusudu tangia siku ya kwanza anamuona. Haikujulikana ameuliza swali hilo kwa kutoelewa kuwa ameuliza au aliuliza kwa kupata uhakika zaidi, ila ni uhakika gani anaoutaka wakati kila kitu kipo wazi?.
“Yes I love you, I want you to be my mine, and i promise you, I can’t broken you are heart na kukuachia maumivu ambayo kwangu itakuwa ni huzuni, tafadhali naomba unielewe” Hemedy alitumia lugha ya kingereza ili kusisitiza kile akisemacho.
Muda wote huo Hilda alionekana akiwa haamini macho yake kwa anayoyaona na haamini zaidi masikio yake kwa anayoyasikia. Ghalfa aliinuka hapo alipokaa na kuondoka mahali hapo na kuingia ndani amabapo moja kwa moja akaenda chumbani kwake na kujifungia mlango. Huku nje Hemedy alikuwa haelewi kilichotokea, akabaki kujiuliza, amekuaje huyu mwanamke? Mbona ameondoka haraka na kuingia ndani pasipo kusema chochote?
Akajua sasa yale aliyokuwa akiyahofia ndio yameshatokea, akanza kuwaza akifokewa huku akitolewa nje ya nyumba hiyo akifukuzwa arudi kwao Tanga na Anti yake Hilda baada ya kwenda kusemewa, akajiona ni mpumbavu kumuambia Hilda maneno hayo, akajua tayari amemuuzi na kilichobakia hapo ni kumuomba msamaha kabla hayajatokea makubwa, akakusanya madaftari yote na kuondoka nayo kwa unyonge hadi sebuleni, kisha akauendea mlango wa chumbani kwa Hilda na kujaribu kuufungua, ila akaona umefungwa kwa ndani, ikambidi agonge tu ila hakukuwa na matokeo yoyote, akajua Hilda amekasirika ndio maana hakutaka kufungua mlango, ikambidi aanze kumuita, kisha akasema.
“Hilda najua nimekuudhi kwa yale maneno niliyokuambia, ila tambua mimi sina kosa, mwenye kosa ni moyo wangu baada ya kukupenda wewe ambae muda wote tuliishi kama kaka na dada, ila kwaniaba yake, nauombea msamaha na nitaongea nao kuuambia kuwa ulipopenda hapakuwa mahala sahihi kwake, naamini utanielewa na kuacha tena kukufikiria kila wakati na utatulia mpaka pale utakapo pata moyo sahihi wa kuwa nao, na ninakuahidi Hilda nitakuwa na wewe pamoja mpaka pale utakapopata mtu sahihi wa kuwa nae, mwisho naomba unisamehe na mimi kwa kukuambia yaliyokuwa ndani ya moyo wangu, nakutakia usiku mwema” Hemedy aliongea kwa hisia kiasi kwamba hadi chozi la jicho la kushoto lilitoka, akalifuta na kuyaweka madaftari ya Hilda hapo hapo chini ya mlango kisha yeye akaingia chumbani kwake.
Huko ndani ya chumba, Hilda alikuwa yupo nyuma ya mlango alikuwa akisikiliza maneno aliyokuwa akiyasema Hemedy, alikuwa akitabasamu muda wote, aliposikia ametakiwa usiku mwema, na yeye alisema kwa sauti ya chini, ‘Usiku mwema na kwako kipenzi changu’ kisha akaondoka mlangoni hapo na kwenda kujitupa kitandani huku uso wake ukipambwa kwa tabasu muda wote.
“Hemedy kumbe na wewe ulikuwa ukinipenda muda wote? Sasa Kwanini hukuniambia, umeniacha nikidhani ni mimi mwenyewe ndio ninaekupenda, kumbe hata wewe unanipenda, asante mungu kwa kuzifikisha hisia zangu kwa mtu nimpendae tangia muda mrefu, Hemedy nimeuruhusu moyo wangu useme na wako, nimegundua kuwa unanipenda kweli, nikuambie tu kuwa hata mimi nakupenda zaidi yako, huna haja ya kuniomba msamaha kwa kuniambia kuwa unanipenda ukidhani labda nimechukia kwa kile ulichoniambia, bali unahaja ya kuniomba msamaha kwa kuchelewa kuniambia kuwa unanipenda, nakuahidi nitakupenda hadi pale mungu atakapo chukua roho ya mmoja wetu. Nakupenda Hemedy”
Hilda alikuwa katika furaha ya aina yake, alikuwa akiongea maneno hayo huku akiwa mikono yake ameifumbata kifuani kwake, alikuwa akiongea kihisia sana kama vile aliekuwa akiongea nae yupo mbele yake, akajaribu kuutafuta usingizi ila ulimjia baadae sana baada ya kutawaliwa na mawazo juu ya kijana Hemedy.
Asubuhi kulipokucha, walijianda kwenda shule huku Hilda akijifanya kununa kupita maelezo, hali hiyo ilimtesa sana Hemedy, akapanga kumuomba msamaha watakapo kuwa shule muda ambao ulikuwa ni wa ‘Free’, wakaongozana kama kawaida huku Hilda akijifanya kununa, walifika shule katika hali hiyo hiyo na kila mmoja kuchukua nafasi yake kusubiri vipindi vianze.
Muda wa mapumziko ulipofika, Hemedy na Ramah walichukuana hadi kantini kwenda kula huku wakimuacha Hilda akienda na marafiki zake wa kike kwenda sehemu hiyo.
“Haya broo niambie jana ulifanikisha kumuambia?” Ramah alimuuliza hivyo baada ya kukaa kwenye viti wakisubiri waletewe chakula.
“Dah! Mwanangu nimeharibu kila kitu, najuta hata kumuambia” Hemedy aliongea kwa masikitiko.
“Kivipi mbaba?”
“Jana wakati tunasoma hom, nikaamua kumchana, ila akaondoka kwa hasira na kwenda chumbani kwake kujifungia. Mimi nilijua tu kuwa yule demu hanitaki kimapenzi we ukajifanya kulazimisha, sasa yaliyotea ndio kama hayo nasijui nitayaweka vipi sawa”
“Duh! Ila usijali jamaa, mimi nitakuombea msamaha naamini ataelewa tu”
“Ramah usifanye hivyo, utazidi kuharibu, mimi yule leo nitamfuata mwenyewe na kumuomba msamaha, kwahiyo wewe usijali”
“Dah!! Haya bwana, ila pole sana” Ramah alimuambia hivyo huku wakiendelea kula chakula walicholetewa.
“Oya jamaa, mtoto Hawa leo kaja shule, vipi tayari ushaonana nae?” Hemedy aliongea baada ya kumuona Hawa akiwa katika kundi alilokuwa Hilda hapo kantini wakipata chakula. Muda wote huo Hilda na Hemedy walikuwa wakiangaliana kwa jicho pembe, yani walikuwa wakiangaliana halafu kila mmoja anaendelea na shuhuli zake.
Muda wakawa tayari wamemaliza kula wakalipa na kuondoka mahali hapo kuelekea darasani. Ilikuwa ni kawaida kwa madarasa ya sanaa, kuwa vipindi vya mwisho kabisa, vilikuwa ni vipindi vya kujisomea wanafunzi wenyewe, na muda huo ndio alipanga Hemedy amfuate Hilda akamuombe msamaha kwa kile alichokifanya jana. Akatoka sehemu anapokaa na kwenda anapokaa Hilda, alipofika akavuta kiti ambacho hakikuwa na mtu kisha akakaa kumuangalia Hilda. Wakati Hemedy anaondoka kumfuata Hilda, Hawa nae alikuwa akiingia darasani humo na kumfuata Ramah, akamsalimia, kisha akamuambia kuwa baada ya watu kutolewa shuleni hapo, basi wakutane kwenye darasa lilelile walilokutaniana mwanzo, alipomaliza akaondoka huku akimuacha Ramah akimsindikiza kwa macho hadi alipopotelea nje.
“Hilda” Hemedy aliita baada ya kukaa kwenye kiti kilichoangaliana na cha banati huyo, ila binti huyo akabaki kimya ni kama vile hakusikia huo muito, ikambidi Hemedy aendelee tu.
“Najua nimekuudhi kwa nilichokifanya jana, ila tambua haikuwa lengo langu mimi kukuudhi wewe, nilikuwa najaribu kukuelezea hisia zangu, ila wewe ukazipokea katika hali nyengine, ukaona kama vile mimi sikuheshimu, ukaona kama vile nimekukosea adabu, wewe ukaona sio sawa mimi kufanya vile, lakini sivyo, na kama ingekuwa ndivyo,basi mungu asingetuumba na moyo wenye kupenda, ila yote kwa yote, naomba unisamehe na nipo tayari unipe adhabu ya aina yoyote ile ambayo utaona inalingana na lile kosa nililolifanya jana” Hemedy aliongea kwa upole na kwa utaratibu mno, kiasi kwamba Hilda alimuonea huruma mtu huyo kwa kumfanya ajione ni mkosaji wakati hata yeye mwenyewe alikuwa akimpenda.
“Sikiliza Hemedy, kwavile umesema nikupe adhabu yoyote kulingana na hilo kosa lako, basi wewe nenda, baadae nitakupa hiyo adhabu na ole wako uishindwe, naomba uniache mwenyewe kwa sasa” Hilda alipoongea hivyo, akaikunja mikono yake juu ya meza yake na kukiweka kichwa chake juu yake kumaanisha kuwa hakutaka tena mazungumzo na kijana huyo. Hemedy akabaki akimuangalia tu mnyange huyo, akataka kusema kitu, ila akaghairisha, akaamua aondoke na kwenda kwenye sehemu yake.
Nusu saa mbele, kengele ya kutoka ikagongwa na wanafunzi wakaondoka shuleni hapo. Ramah yeye akaelekea kwenye lile darasa alikotakiwa aende, alipofika tu, macho yako yakakutana na ya Hawa, alimuona binti ni kama vile mwenye kumsubiri kwa hamu sana mahala hapo, akapiga hatua za taratibu kumsogolea.
“Sikiliza Ramah nikuambie, sikutaki na sitaki kuwa na wewe, usione kisa juzi umenila ‘romance’ ukadhani eti ndio ushanipata, tambua kuwa sikuile nilichukia ila sikutaka kukuonyesha pale, na ninaomba kuanzia sasa ukiniona unione kama mkweo” Hawa aliongea hivyo huku akiwa mkono wake wa kushoto ukiwa kiunoni mwake na mkono wake wa kulia ukipepea hewani kama bendera iliokumbwa na kimbunga, alikuwa akiufanya kama wale wanawake wa uswahili wanaposutana.
“Lakin…..” Ramah alitaka kuongea ila alikatishwa na sauti ya Hawa.
“Lakini nini? Ndo nshakuambia hivyo, muone kwanza” alipoongea hivyo akamalizia na sonyo refu na lenye sauti mithili ya firimbi ya refa anapotaka kumaliza mpira uwanjani. Kisha akaondoka hapo, ila alipofika mlangoni, akageuka tena na kumfuata Ramah aliekuwa bado amepigwa na bumbuwazi asielewe kinachotokea mahala hapo, hapo akajua kinachofuata ni kupigwa makofi na mwanamke huyo.
ILA alishanga baada ya kumuona akija na tabasamu mwanana usoni mwake, tena safari hii alikuwa akija kwa mwendo ambao Ramah ulikuwa ukimchanganya kila amuonapo akitembea, akabaki akimuangalia binti huyo anavyokuja karibu yake, kisha baada ya kufikiwa karibu, akaona mikono ya mnyange huyo akiitanua na kumkumbatia yeye, kwa tukio hilo, akabaki haelewi nini kinachoendelea, akabaki tu kutoa macho kuangalia mbele huku kichwa chake kikiwa juu ya bega la binti.
“NAKUPENDA Ramah” Hakutaka kuamini masikio yake baada ya kulisikia hilo neno likitoka kwenye kinywa cha banati huyo alietoka kumtupia maneno mabaya muda mfupi uliopita. Akamtoa kwenye kumbato hilo huku akimuangalia usoni mikono yake ikiwa kwenye mikono ya binti. Ni kama vile hakuwa akiamini, akabaki kumuangalia tu usoni kwa macho ya mshangao, ila alikutana na tabasamu ambalo lilimfanya akiri kuwa banati huyo ni mzuri tangu kwa mara ya kwanza kumuona shuleni hapo. Hawa nae ni kama hakutaka kutolewa kwenye kumbato hilo, akajirudisha tena mwilini mwa kijana huyo kisha akarudia tena maneno aliyoyasema mwanzo.
“Hawa ni kweli unanipenda?” Ramah alimuuliza hivyo huku akiwa bado haamini.
“Ndio Ramah nakupenda, nimeamua kukukabidhi moyo wangu kwavile nimekuamini, imani yangu kwako isiwe sababu ya wewe kuyatoa machozi yangu halafu yakakosa wa kuyafuta. Ramah kumbuka mapenzi yanauma pale unaempenda akikusaliti, inaweza ikapelekea hata mtu kujiua au kupata ukichaa kabisa, naomba yote hayo yasinikute, sijataka wala sitaki na sitotaka kulia machozi kwaajili ya mwanaume yoyote, kwahiyo naomba usinilize, usinifanye nijekujuta na kujiona mwenye hatia kwa kukukabidhi moyo wangu” Alipofika hapo, akajitoa kwenye kumbato la kijana huyo kisha akamuangalia usoni na kusema.
“Ramah naomba uniahidi kitu” Hawa aliongea hivyo huku akimuangalia usoni.
“Hawa, kama nilivyokuomba mwanzo kuwa Adamu wako, ndivyo ambavyo nimeufunga moyo wangu kwako, kama ambavyo nilivyoomba unihifadhi kwenye moyo wako, ndivyo nilivyo uhifadhi moyo wako kwangu. Kumbuka Hawa nimeumbwa na moyo mmoja tu, na moyo huo umeumbwa kwajili ya mwanamke mmoja tu katika ulimwengu huu, na huyo si mwengine bali ni wewe. Sitokuacha ulie pekeako pale utakapo patwa na tatizo, bali nitalia na wewe huku tukitafuta ufumbuzi wa hilo tatizo, chengine usitegemee kudondosha chozi kwaajili yangu, labda iwe kwa bahati mbaya tena sitoruhusu chozi lako dhaifu lidondoke ardhini, bali nitalidaka na kulifikicha viganjani mwangu kisha nitapangusa katika uso wangu. Nitakapokosea naomba unisamehe na wewe utakapo nikosea basi tambua nishakusamehe tangu sasa, na la mwisho nakuahidi kuwa, nitakuwa na wewe hadi mwisho wa maisha ya mmoja wetu. Sikuahidi kufa na wewe kwasababu hata nikifa na wewe sitozikwa na wewe. Nakupenda Hawa” Ramah aliongea kwa hisia kali mithili ya sharukhan kwenye muvi yake ya kuch kuch hotahe.
Hawa muda wote alikuwa akitabasamu kusikia maneno hayo yaliyotoka katika kinywa cha Ramah. Ghalfa alikutanisha kinywa chake na cha mwanaume huyo, na kubadilishana kinywaji ambacho hakiuzwi mahali popote zaidi kwa yule umpendae. Hadi muda huo, walikuwa wamejisahau kuwa wapo darasani tena shule ambako muda wowote anaweza akapita mtu na kuwaona kile wanachokifanya.
Kusimama waliona haitoshi, badala yake wakavutana hivyo hivyo kwa kugandana hadi katika ukuta wa hilo darasa, hapo walianza kushikana kila mmoja kwenye mwili wa mwenkaze. Ramah baada ya kuona haitoshi kutalii kwenye mwili wa mnyange huyo akiwa na nguo zake, akapeleka mkono wake chini ya sketi ya binti na kuanza kuinyanyua hiyo sketi kwa kuipandisha juu. Ila kitendo hicho hakikupata bahati ya kutimia baada ya mkono wa binti kuwahi kuzuia.
“Ramah, hapo sio sehemu salama kufanya hivyo” Hawa aliongea kwa sauati ambayo ilikuwa tofauti na ile Ramah aliyowahi kumsikia binti huyo akiongea, sio kama ilikuwa ni sauti mbaya au yenye kuogopesha, la hashah! bali ilikuwa ni sauti ambayo ingemuongezea hashki mwanaume yoyote ambae alikuwa ni mzima yani rijali. Ramah hakuwa na namna, ikabidi waache kile wanachokifanya na kila mmoja akatabasamu kama sio kucheka kabisa, kisha wakashikana mikono ya kuanza kutoka darasani humo na kuelekea wanapopajua wao.
* *
Masaa yalikatika hadi kufikia majira ya usiku. Hemedy na Hilda, walikuwa katika sehemu yao ya kujisomea nyumbani kwao, siku hiyo kila mmoja alikuwa ‘serious‘’ na mwenzake, japokuwa walikuwa wakiulizana maswali, ila hakukusikia kicheko wala tabasamu usoni mwao, walisoma kwa saa nzima kama ambavyo walipanga wajisomee kwa muda huo.
“Hilda, naomba unipe hiyo adhabu nianze kuitumikia kuanzia sasa, maana sipendi tukiwa katika hali hii ya kununiana. Moyo wangu unaniuma ninapoona sisemeshani na wewe, naomba unipe hiyo adhabu niko tayari kuipokea” Hemedy aliongea hivyo baada ya kumaliza kujisomea.
“Hemedy uko tayari kuitumikia hiyo adhabu, maana ni adhabu ya milele” Hilda aliongea.
“Niko tayari kuitumikia ili mradi nione unaongea na mimi tena, sipendi tukawa na Uhasama baina yangu na wewe” Hilda akamuangalia kijana huyo na kusema.
“Adhabu yenyewe ni kuokoa na kuulinda moyo wangu kwa wale wanaotaka kuuharibu na kuupondaponda kisha kuuacha na maumivu yatayosababisha nitoe machozi. Je ukotayari kuitumikia adhabu hiyo?” Hilda alimuuliza Hemedy ambae alikuwa ameyatumbua macho yake kumuangalia Hilda kwa mshangao uliomkumba baada ya kusikia maneno hayo. Hakutaka kuamini moja kwa moja eti Hilda amekubali kuwa mpenzi wake. Akabaki kutulia tu asiseme chochote, sio kwamba hakuwa na lakusema au hakujua aseme nini, hapana, ila alikuwa bado ameganda kwa mshangao uliomkumba.
“Hemedy nakupenda pia. Tangu mara ya kwanza kukuona ulipokuja kwenye sherehe yangu, sikujua kule kukuhusudu namna ile kumbe kulikuwa ndio kukupenda, sikujua kule kutaka kuwa karibu na wewe kumbe ndio kulikuwa ni kuikuza mbegu ya upendo wangu kwako, sikujua kuwa kule kutamani kuisikia sauti yako kila mara kumbe ndio kulikuwa ni kuimwagilia maji mbegu ya upendo wangu kwako, naamini hata wewe ulijua kuwa nilikuwa nakupenda, ila ukajifanya kutotambua chochote kile kuhusu upendo wangu, ukajifanya kutoona chochote pale nilipokuonyesha upendo wangu.” Akatulia kidogo, kisha akamuangalia usoni, akaendelea. “Hemedy mbona hukuuruhusu moyo wako useme na wangu tangu muda mrefu? Mbona hukuruhusu mboni za macho yako zione upendo wangu tangu muda mrefu? Hemedy jua wewe ndio mwanaume wakwanza na wa mwisho kupendwa na moyo wangu, sitoweza kuja kuvumilia hata kidogo maumivu pindi ukiniacha. Sikuahidi kukutendea mabaya pale utakapo niacha, bali nauahidi moyo wangu kuutendea mabaya kwa kukupenda wewe kwasababu huo ndio sababu kuu ya maumivu yatakayo nipata mwili mzima. Hemedy tambua nilikupenda kabla wewe hujaanza kunipenda, naomba usiutumie udhaifu wangu wa kukupenda kama silaha ya kuniumizia. Nipende kama ninavyo kupenda na mimi nitakupenda zaidi ya ninavyo kupenda, kama ikiwa hivyo, naamini hata mungu atalibariki pendo letu lifike mbali zaidi. Nakupenda Hemedy” Hilda alikuwa akiongea kihisia hadi jicho moja lilitoa chozi dogo lililoishia kwenye shavu lake.
Kwa mara ya kwanza tangu kuzaliwa kwao, siku hiyo ndio siku ambayo waliijua ladha ya kinywaji ghali kupatikana madukani au hata sehemu yoyote ile panapouzwa vinywaji, ila kinywaji hicho hupatikana kwa yule umpendae tu, kwa lugha ngeni wanaita ‘romance’ ila kwa kiswahili mnaita ‘denda’,.
“Nakupenda Hemedy” Hilda aliongea hivyo baada ya kutosheka na kinywaji hicho huku akiskilizia utamu huo kwenye kifua kilichoanza kupevuka cha Hemedy.
“Hilda adhabu uliyonipa kwa kile nilichokifanya inastaili kwangu, adhabu ambayo nilipewa na moyo wangu kuokoa moyo wako usipate machungu ya wale ambao wanataka kuuchezea, moyo ambao unathamani kubwa kwangu kuliko kitu chochote kile hapa duniani, sasa ni vipi niupataie machungu yatakayo ishi ndani yake milele? ni vipi niuache usononeke na kulalamika kwa kunipenda mimi? Hilda tambua yote hayo hufanywa na yule asiejua thamani ya pendo kwa yule ampendae. Hufanywa na yule mpumbavu anaependwa kisha ule upendo akaufanya ndio udhaifu wa kumnyanyasa yule ampendae. Ni vipi mimi nimlize alienipenda tokea utotoni wakati sijui hata kuvaa vizuri? sijui kujizuia pale nilipochapwa darasani kulia machozi mbele yake. Kwanza naanzaje kukuacha, naazaje kukusaliti, naazaje kuliacha chozi lako lidondoke ardhini pasi na kulidaka, naazaje kuruhusu kinywa chako kitoe sauti ya kilio kwajili yangu, naazaje Hilda? Labda unililie kipindi ambacho nipo kaburini, labda unililie kipindi ambacho nipo kitandani siwezi hata kuunyanyua mkono wangu kulidaka chozi lako, hata kama nisipoweza kulidaka chozi lako na kulifanya liangukie sakafuni kama sio ardhini kabisa, basi naamini pale litakapo anguka litajichora jina langu kuonyesha ni kiasi gana unanipenda, naomba na mimi usilidake chozi langu, liache liangukie chini kisha lijichore jina lako ili uamini kwamba na mimi nakupenda kama unipendavyo, nakuhitaji kama unihitajivyo”. Alipofika hapo, akapeleka mikono yake kwenye mashavu ya Hilda ambae muda wote alikuwa yupo kimya akitabasamu tu, alifanya kama vile ni mwenye kufuta futa kitu kwenye mashavu hayo, kisha akaendelea. “Nitakuwa mwanaume wa kwanza mpumbavu kuyafanya mashavu yako yalowane kwa machozi kwa kukuacha”. Kisha mikono yake akaipeleka chini kwenye pua ya banati, halafu akasema. “Nitakuwa mwanaume wa kwanza mjinga kuzifanya pua zako zitoe kamasi pindi ukinililia kwa kukusaliti“. Akapeleka mikono yake chini kwenye mdomo wa banati huyo, halafu akasema. “Nitakuwa mwanaume wa kwanza mpumbavu na mjinga kuruhusu kinywa chako kitoe sauti ya kilio kwa maumivu yatakayotoka moyoni mwako chanzo ikiwa ni mimi. Hilda nimekubali kuitumikia adhabu uliyonipa ya kuulinda moyo wako mpaka kifo changu au chako”
Alipomaliza kuongea, wakakumbatiana kwa muda kisha wakakusanya madaftari yao na kuingia ndani ya nyumba. Sebuleni walimkuta Anti yao akiangalia luninga huku akiwa ameshika sahani iliyokuwa na matunda mbalimbali juu yake.
“Nyie wana mbona mnafuraha namna hiyo? nishirikisheni basi na mimi nifurahi” Anti yao aliongea hivyo huku akila kipande cha parachichi.
“Anti wewe ushazeeka tukiamua kukushirikisha itapelekea ucheke halafu ikiwa bandama zenyewe zishazeeka kwahiyo unaweza ukapata matatizo ya kutokucheka kwasababu itakuwa zimeshakufa tayari kwa kucheka sana” Hemedy aliongea hivyo na kuwafanya Hilda na Anti yake wacheke.
“Hilda umemuona huyo anavyoniambia? Embu nipigie kofi hapo hapo alipo” Anti aliongea hivyo huku akicheka na kumfanya Hemedy asogee mbali kidogo na alipo Hilda.
“Niafadhali hata ungekuja mwenyewe kunipiga, lakini huyo unaemtuma ndio hajiwezi kabisaa”
“Haaa!! Hilda umemsikia anavyokuambia, embu mpige basi na wewe ili aamini kuwa upo ngangari” Anti alipoongea hivyo. Hilda alinza kumfukuza Hemedy hapo sebuleni.
“Kione hata kukimbia pia hakiwezi” Hemedy aliongea hivyo huku akikimbia kuizunguka hiyo sebule, walifanya hivyo kwa dakika moja nzima.
“Waone walivyopendezana kama mtu na mtu wake vile” Anti aliongea hivyo huku akicheka na kumfanya Hilda asimame kwa ghafla na kumuangalia yeye.
“Antiii” aliongoea hivyo huku akitabasamu. Tabasamu la aibu.
“Kwani uongo? halafu nimegundua unampenda sana Hemedy hadi umekataa kuja pekeako huku ukililia kuja nae” Anti alizidi kuongea maneno yaliyomfanya Hilda azidi kuona aibu.
“Ndio nini sasa hivyo Anti?” Hilda aliongea kwa kulalamika utafikiri kinachosema ni uongo.
“Nilishangaa sana kaka aliponiambia kuwa umekataa kuja pekeako huku eti ukidai huwezi kuondoka bila huyo. sasa mimi nikawa najiuliza, anti yangu huyo ambae hataki kumuacha ni nani, nikasema sio kesi acha nisubiri akija nitamuona. Dah anti yangu umejua sana kuchagua, unahaki uone wivu kumuacha mkwe wangu Tanga halafu wewe uje pekeako huku” Hilda aliposikia hivyo, akajifanya kulia huku mkono wake mmoja akiupitisha kwenye macho yake, kisha akaondoka hapo sebuleni na kuelekea chumbani kwake akiwaacha Anti yake na Hemedy wakicheka tu.
“Haya nenda kambembeleze mke wako maana tayari amenuna” Anti aliongea hivyo huku akicheka na kumfanya Hemedy aondoke hapo kuelekea chumbani kwake huku na yeye akicheka.
* * * *
Siku iliyofuata, walienda shule kama kawaida, ila siku hii walikuwa na furaha kuliko siku yoyote ile ambayo walikuwa shuleni hapo. Siku hii walitambulishana wote wanne, yani Ramah alimtambulisha Hawa kwa Hemedy na Hilda kwamba ni mpenzi wake na Hemedy nae alifanya vivo hivyo, wakawa wakifurahi tu muda wote, ila vipindi vya darasani viliwanyima uhuru wa kufurahia pamoja, wakapanga wikiendi hiyo waende katika ufukwe maarufu katika mji huo, ufukwe ambao watu wengi hupenda kuenda kutokana hakukuwa na kiingilio ufukweni hapo, yani palikuwa ni free tu.
Coco beach, ndipo walipopanga kwenda kufurahia wote kwa pamoja mwisho wa wiki hiyo. Baada ya muda wa kutoka shuleni hapo kufika, waliongozana kuelekea majumbani mwao. Ramah, Hemedy na Hilda waliachana na Hawa njiani huku wao wakielekea pamoja maana wao walikuwa wakikaa mtaa moja japokuwa nyumba zilikuwa ni tofauti, ila hakukuwa na umbali wowote kutoka wanapokaa wakina Hemedy hadi nyumbani kwakina Ramah.
Hemedy na Hilda, walipofika nyumbani kwao, walikutana na ugeni uliowafanya wafurahi kukutana nao, hasahasa Hemedy ndie alikuwa ni mwenye furaha zaidi. Walimkuta Mrutu akiwa yupo hapo akiwasubiri wao, walisalimiana kwa furaha baada ya kutoonana kwa miaka mingi. Mrutu aliwaletea zawadi ya simu aina ya Samsung J7 kila mmoja yake na kuwafanya wafurahi zaidi, baada ya kufurahi sana, Mrutu akaaga kutaka kurudi Tanga siku hiyo hiyo akidai amekuja mara moja tu kibiashara, ila alikutana na pingamizi kubwa kutoka kwa Hemedy na Hilda waliomtaka alale tu kwa siku hiyo kisha kesho ndio aondoke, wazo hilo liliungwa mkono na Anti yao na kumfanya Mrutu kukosa tena cha kujitetea, akalala kwa siku hiyo.
Sikuiliyofuata, Mrutu aliaga na kuondoka huku akiwaachia kiasi cha pesa Hemedy na Hilda, ambao walifurahia uwepo wake hapo, na wao wakajianda kuelekea shule wakaimalizie siku hiyo ya mwisho kabla ya kuingia wikiendi. Walipofika shule wakakutana tena na Ramah na Hawa, siku hiyo walikuwa wakisisitizana kuwa kesho yake ndio siku ya kwenda kuinjoi ufukweni. Hemedy na Hilda, walichukua namba za Ramah na Hawa baada ya kuwaambia kuwa na wao wanatumia simu, ikawa shangwe nyengine baada ya kupata mawasiliano yatakayoweza kuwaweka karibu zaidi.
* * * *
Siku iliyofuata. 10:45 Jioni. Coco Beach.
Watu hao walikuwa katika furaha ya aina yake siku hiyo waliyoipanga kuja kufurahi hapo, Ramah na Hemedy hawakuishia kufanya mzaha kila muda ili mradi tu watu wao wafurahi, walifanya hiki na kufanya kile na kupelekea vicheko vitawale muda wote, baada ya kuzunguka zunguka sana kwa pamoja, wakatawanyika na kila mmoja akaenda kukaa sehemu yake na mtu wake, yani wakawa wawili wawili.
Wakiwa hawana hili wala lile wao wakiendelea na kufurahi kwao, kwa mbali kuna watu walikuwa wakiwaangalia kwa umakini sana, watu hawa ndio wale tulianza kuwaona wakimfuatilia Hemedy tangu anashuka Ubongo kwa mara ya kwanza katika jiji hilo. Jamaa mmoja kati ya hao wawili, akatoa simu na kubonyeza bonyeza kisha akaiweka sikioni huku akiwaangalia vijana wale wote wanne japokuwa kwasasa walikuwa wamejitenga wapo wawili wawili.
“Mkuu, naona huyu kijana amejiingiza kwenye mapenzi na yule mjukuu wa Inspekta” Kijana huyo akaongea hivyo baada ya simu kupokelewa.
“Mnachotakiwa nyie ni kuwaangalia tu wasidhurike na chochote, hilo swala la kusema wapo katika mapenzi waachieni wao wenyewe, kwanza pia itazidi kumfanya awe kama vile KIONGOZI anavyotaka kwasababu atapitia mambo mengi yatakayo mfanya awe vile sisi tunavyotaka”
“Lakini mkuu huoni kama hiyo itakuwa ni hatari kwake? Mi naona asijiingize kwenye mapenzi kwasasa” Kijana aliongea.
“Asu, sikuhizi tunafundishana kazi sio?” Sauti ya upande wa pili ilinguruma.
“Hapana mkuu, ila nilikuwa najaribu kushauri tu, nisamehe sana mkuu” Jamaa ambae kwa sasa tunamjua kwa jina la Asu baada ya mtu wa upande wa pili kumuita hivyo aliongea.
“Basi fuata kile ninachosema mimi. nawaambia tena, hakikisheni ulinzi kwa huyo kijana unazidi kuongezeka siku hadi siku, kumbukeni kuwa Kiongozi anamhitaji huyo kijana kuliko vile mnavyofikiria nyie”
“Sawa Mkuu. Halafu kuna jengine nataka kukuambia” Asu aliongea.
“Lipi hilo?” Sauti ya upande wa pili uliuliza.
“Ni kwamba, huyo kijana ana urafiki mkubwa na mwanao Ramadhani au Ramah kama ambavyo wanamuita”
“Kwani wapo wapi?” Sauti ya upande wa ilisikika.
“Wapo huku ufukweni Coco Beach” Asu alijibu.
“Wapo wangapi?”
“Wapo wanne mkuu, nikimaanisha kuwa kila mmoja yupo na mtu wake” Asu alijibu.
“Kwahiyo Ramah pia anampenzi? Hahahah! watoto wa siku hizi bwana! haya endeleeni kuwaangalia, hakikisheni ulinzi kwa wote”
“Sawa mkuu tumekuelewa” Asu alikata simu na kumgeukia mwenzake.
“Oya Kanu, mkuu anasema tuimarishe ulinzi kwa wote wanne. Kama vipi twenzetu pale kwa yule mzee tukale madafu, au wewe unasemaje?” Asu aliongea.
“Twenzetu kaka, ila hawa watoto wanafaidi kinyama, embu ona hao mademu waliokuwa nao, Dah! wakali kishenzi yani” Kanu aliongea hivyo akiwa anawatupia macho vijana hao huku wakielekea sehemu ambapo palikuwa kuna mzee amepaki baiskeli yake akiuza madafu na machungwa.
Walipofika wakanunua madafu na kuanza kula hapo hapo huku wakiwatupia macho muda wote vijana hao. Ila muda kidogo waliwaona vijana wale wakiume wakiinuka sehemu walipokaa na kuwaacha wasichana zao huku wao wakija hapo hapo walipokuwa wapo wao.
“Oya Asu, naona hao madogo wanakuja na hapa hapa, halafu si unajua kuwa huyo dogo mmoja tunaemlinda tulishawahi kumuokoa kwa wale waliomteka, sasa huenda ikawa bado sura zetu anazikumbuka, kwahiyo akituona hapa anaweza akajiuliza maswali mengi halafu ikapelekea mpango kuharibika, embu tuwape mgongo” Jamaa anejulikana kwa jina la Kanu alimuambia mwenzake hivyo baada ya kuwaona Ramah na Hemedy wakija sehemu hiyo hiyo waliyokuwa wao.
“Unawasiwasi tu jamaa, miaka ni mingi sana tangu azione sura zetu sidhani kama atazikumbuka, ila kwa tahadhari zaidi tugeuke tu” Asu alisema hivyo huku akigeuka kwapa mgongo watu hao.
Walipofika hapo walinunua kila mmoja anachotaka, Ramah yeye alinunua madafu mawili huku Hemedy akinunua machungwa mawili. Kisha kila mmoja akarudi sehemu ambayo amemuacha mtu wake na kwenda kukaa nae. Hemedy alipofika kwa Hilda, akamkabizi chungwa moja kisha akakaa karibu yake.
“Sweetie” Hemedy alimuita huku akiwa macho yake ameyaelekezea baharini.
“Abe Honey” Hilda aliitikia.
“Unajua Kwanini nimeenda kununua machungwa?”
“Hapana baby sijajua”
“Embu kwanza kula kipande kimoja” Hemedy alipoongea hivyo, Hilda akang’oa kipande kimoja cha chungwa ambalo tayari lilikuwa limeshakatwa, kisha akalila nusu halafu akamuangalia Hemedy kusubiri aambiwe ni kwanini ameenda kununua machungwa. Ila aliambiwa akimalizie kipande chote na yeye akafanya hivyo.
“Ni ladha gani umeipata wakati unakula kipande hicho?” Hemedy alimuuliza.
“Tamu” alijibu.
“Vizuri. Chungwa ni tunda ambalo lina ladha ya kipekee sana tofauti na matunda mengine yote. Mchungwa unatokana na mmea wa mlimao ambao umekatwa na kuunganishwa kiutaalamu na kuufanya utoke katika uhalisia wake wa mlimao hadi kuwa mchungwa” Hemedy alipofika hapo alikatishwa na swali la Hilda.
“Kwahiyo unataka kuniambia michungwa yote inatokana na milimao?” Hilda aliuliza hivyo huku akionekana dhahiri kuwa na mshangao kwa hicho alichokisema Hemedy.
“Hapana, kuna mengine kama ile ya zamani tena sanaa, ile ilikuwa yajitegemea, ila hii ya sasa mengi ni ya kupandikiza miche. Kipindi cha uhai wa baba yangu aliwahi kunipeleka kwenye mashamba yake huko kijijini, alionionyesha vitu vingi sana moja wapo ni hilo la kuubadilisha mlimao kuwa mchungwa, nilishangaa sana kuona hivyo, ila sikuwa na jinsi ya kubisha ikiwa mwenyewe nimeshuhudia kwa macho yangu”
“Kwahiyo ukiuunganisha mlimao unabadilika hapo hapo na kuwa mchungwa?” Hilda aliuliza swali lililomfanya Hemedy acheke.
“Hapana Hilda haubadiliki hapo hapo, ila unaweza ukachuku hata mwezi ila kama ukipata maji unaweza ukachukua hata wiki tatu”
“Mmhu! Nakusikiliza mpenzi” Hilda aliongea hivyo huku mkono wake wa kushoto akiupitisha juu ya shingo ya Hemedy na kwenda kuishia kwenye bega lake la kushoto.
“Wakati ukiunganishwa, unaanza kuchomoza taritibu ila hapo inakuwa ni baada ya wiki mbili na siku kadhaa, baada ya kuchomoza, unakuwa na kubadilika kabisa kuwa ni mchungwa halisi huku shina la chini likiwa ni la mlimao. Baada ya miaka, kunaanza kuchomoza kwenye matawi maua flani hivi na maua hayo ndio yanakuja kuwa ni tunda chungwa, ndio pale sasa unakuta watu wanakula au wengine kuuza kabisa ila hapo ni baada ya kuwa mbivu haliwezi kuliwa likiwa bichi, kwasababu badala ya kupata utamu utapata uchungu. Unajua nini namaanisha?” Hemedy alimuuliza hivyo Hilda. Ila alikataa kwa kichwa kuashiria kuwa hajajua nini amemaanisha.
“Namaanisha kwamba, tunda hili halija kuwa tu hivi hivi na kuwa ni tamu, mmea wake ulianza kumwagiliwa maji baada ya kupandwa, kisha ukachomza na kutunzwa vizuri kwa kupaliliwa kwa kuondoa majani ambayo yameota pembeni yake, yani unaachwa ukiwa upo pekeake. Kisha ukaendelea na kukua na kukua na kukua hadi ukanawiri, ukafikia hatua ambayo hata pawe na kiangazi gani basi haiwezi kutetereshwa na chochote, hadi muda huu ambao wewe unalila na kuliona tamu, basi ujue mmea wake umepitia mambo mengi sana” Hemedy alimaliza kuelezea.
“Nimekuelewa ulivyoelezea ila nataka unifafanulie zaidi maana” Hilda aliongea.
“Maana yangu ni kwamba. Upendo huanzia chini sana, unaanza kwa kuchipua kwenye mioyo miwili iliyopendana, na ili ukue, basi inabidi umwagiliwe maji ya maneno mazuri yenye ladha kwa yule anaetamkiwa. basi mtaona upendo ukikuwa kadri siku zinavyozidi kwenda, lakini kuna watu ambao hawatapenda vile mnavyopendana, watamizongazonga kwa maneno mabaya au hata waongee maneno ya uongo ilimradi tu upendo ufe. Ndio pale kwenye mmea wa mchungwa unapopaliliwa kuondoa majani ambayo yanauzongazonga ule mmea, maana pasipo kufanya hivyo, itasababisha ule mmea kutokukuwa vizuri au hata kufa kabisa. Mapenzi nayo ndivyo yalivyo. ili tuishi vizuri, inatubidi tusisikilize ya watu, au tuwasikilize kwasababu maneno hayakwepeki, ila tusiyape nafasi sana ya kuyamini, inabidi tufanye uchunguzi kwanza, kisha tukibaini yana ukweli ndani yake, basi ndio tuchukue maamuzi” alipofika hapo, akamgeukia Hilda na kumuangalia usoni. “Ila tusichukue maamuzi wakati tunahasira” akageuza shingo yake mbele na kuendelea kuangalia bahari na watu baadhi waliokuwa wakiogelea. “Tukiupalilia upendo wetu basi utakua imara sana kiasi kwamba hakuna ambae ataweza kutetenganisha labda mungu pekee atakapo chukua roho ya mmoja wetu. Hapo tutakuwa kama ule mmea wa mchungwa ambao umepaliliwa na kukua, hata pawe na kiangaza kiasi gani hauwezi ukatetereshwa. Kwa vile itakuwa tumeuimarisha upendo wetu, basi tukakuja kufaidi baadae matunda ya upendo wetu na kuufurahia na kuuona mtamu kama vile ambavyo wewe umekisifia hicho kipande cha chungwa ulichokila. Nikisema hivi simaanishi kuwa kwa sasa hatufaidi upendo wetu, hapana tunafaidi sana, maana hata huo mmea wa mchungwa unatumika kama kivuli kipindi ambacho haujatoa matunda. hata sisi tutakuja kufaidi vizuri baadae tukija kuwa familia moja huku tukiwa na watoto wetu. Kwahiyo mpenzi wangu naomba tuwe kama mmea wa mchungwa, tuumwagilie maji upendo wetu maana tayari ushachipua, kisha tuupalilie kuondoa mabua na majani ambayo yataufanya upendo wetu kutokukuwa vizuri au hata kufa kabisa, tukifanya hivyo, utakua na kukua na kuwa imara hata watu wakiongea maneno yao kuhusu sisi tuwafananishe na kile kiangazi ambacho hakiwezi kuuteteresha mmea hata kidogo, mwisho tutakuja kufaidi upendo wetu baadae kama vile ambavyo tunayafaidi haya machungwa kwa sasa. Mpenzi wangu tuwe kama mmea wa mchungwa” Hemedy alihitimisha hivyo na kumpiga busu la kwenye paji la uso Hilda. Hilda busu hilo akaona kama vile halitoshi kwake, akataka na denda na bila hiyana akapatiwa, walifanya hivyo bila kujali watu waliokuwa wakipitapita mahala hapo.
Turudi nyuma kidogo wakati Ramah anaenda mahali alipokaa Hawa huku mikononi akiwa ameshika madafu mawili, alipofika hapo akampatia Hawa dafu moja kisha akakaa karibu yake.
“Malikia wangu” Ramah aliita.
“Niambie Mfalme wangu” Hawa nae alimuita huku mkono wake wa kulia akiuingiza kwenye mkono wa kushoto wa Ramah kisha akamlalia begani.
“Ni kwavile yana maji matamu na nyama yake ya ndani pia ni laini na tamu” Hawa alijibu huku akitabasamu.
“Safi sana umejibu vizuri hadi nimependa. Embu kunywa kidogo maji yake ili unisibitishie ni kweli ulichokisema?” Ramah alimuambia hivyo na kumfanya Hawa avute maji yaliyokuwa ndani ya dafu kwa kutumia mrija, akavuta kidogo na kuacha kisha akamuambia Ramah kuwa maji hayo ni matamu kama alivyosema. Ramah akasema.
“Dafu ni mwanzo wa kuwa nazi, na nazi imeota kwenye mnazi ambao ulipandwa kwa begu ya nazi iliyokomaa. Katika mimea ambayo huchelewa kukua kuliko mimea yote ninayoijua mimi ni mnazi. Mnazi unaweza ukachukua miaka zaidi ya sita kukua na kutoa nazi, simaanishi hii minazi ya kisasa ambayo ikipandwa mwezi mmoja tu unatoa nazi hata kama haujakua vizuri, minazi ambayo haiwezi kuvumilia dharuba kubwa hata kidogo hadi kupelekea kufa. nazungumzia minazi ambayo babu zetu ndio waliokuwa wakiitumia, hawakuwa na papara kwa kukua kwake kwasababu walijua baadae itakuja kuwa imara zaidi. Walipofukia ardhini mbegu ambazo ni nazi zilizokomaa, wakasubiri baada ya muda mfupi, zikachomoza kutoka ardhini, hapo wakamwagilia maji na kuufanya mmea ule ukue zaidi, ukafikia wakati wa kuupalilia, wakapalilia na ilipofikia wakati wa kuvumilia jua kali na ukame, wakaiiacha ikue yenyewe, maana walijua mimea hiyo inauwezo wa kuvumilia chochote kile ambacho mimea mingine haiwezi kuvumilia na kupelekea kufa kabisa. Ulipofika wakati huo sasa ndio wakaachana nayo kwavile walijua mimea hiyo ni yenye kuvumilia kila hali, hawakuwa na papara kwa kusubiria miaka mingi kwasababu walijua baada ya miaka hiyo watakuja kupata zao lililokuwa bora, na sio zao tu, hata hiyo mimea haiwezi kufa yenyewe kwa hali yoyote ile, labda waamue kuiua kwa kuikata. na wataikataje wakati wameipanda wenyewe na kuimwagilia maji wenyewe na kusubiri kwa muda mrefu hadi kuja kupata faida? watakuwa wapumbavu kwa kufanya hivyo au labda wawe na maana yao kubwa kufanya hivyo. Sijui umenielewa vizuri na kujua kile ninachokimaanisha?” Ramah alielezea kisha akamuuliza.
“Ndio nimekuelewa na nimejua vitu vingi sana ambavyo nilikuwa sivijui kuhusu mnazi, ila sijajua nini umemaanisha”
“Ni kwamba. Mapenzi yanaanzia chini sana kama vile ambavyo mbegu ya mnazi ilivyopandwa chini. Kisha mapenzi huchipua taratibu na kuhitaji kumwagiliwa maji ya upendo ili yakue zaidi, halafu ya yaimarishwe kwa kutosikiliza maneno ya watu wasiyopenda yaimarike kama ambavyo mmea wa mnazi ulipopaliliwa kuondolewa majani yaliyouzunguka ule mmea ukapelekea ukue bila tabu. Naamini tukifanya hivyo haitakuwa na haja ya kuchungana kwenye mapenzi, zaidi kila mmoja atajichunga mwenyewe asiliharibu penzi lake kama ambavyo wale wazee walipoiyacha mimea hiyo ikue yenyewe baada ya kujua kwa hapo ilipofikia haiwezi kutetereshwa na chochote. Kisha tutasubiri japokuwa ni kwa muda mrefu sana hadi kuja kutimia malengo yetu hapo baadae, hadi hapo malikia wangu tutakuja kufaidi mazao ambayo yatakuwa ni imara zaidi na mapenzi yetu hatutaweza kuyaua wenyewe. Na kwanini tuyaue wakati tumepata tabu ya kuyatunza na kuwa imara hadi hapo yalipofikia? Labda mungu tu ndie anaeweza kuyaua tena atayaua kwa kuichukua roho ya mmoja wetu, lakini bado naamini upendo utaendelea kuishi mioyoni mwetu hadi pale tutakapo ingia katika ufalme wa mungu. Malkia wangu tuwe kama mmea wa mnazi” Ramah alimaliza kuongea na kuupitisha mkono wake wa kushoto kwenye kiuno bambataa cha Hawa, kisha ndimi zao wakaziunganisha mithili ya njiwa jike anapolilisha kinda lake.
Majira hayo wakanyanyuka na kuwafuata wenzao waliokuwa mbali kidogo na walipokuwa wao, walipofika pale wakaungana wote kwa pamoja na kupiga stori hadi pale walipoona inatosha kuwa mahala hapo, wakainuka wote na kuanza kuondoka kuelekea yalipo makazi yao.
* * * *
Wikiendi iliisha na kufuatia jumatatu ambayo wanafunzi walitakiwa wawepo mashuleni baada ya kupumzika kwa siku hizo mbili. Shule ya sekondari Benjamini Wiliamu Mkapa, wanafunzi walikuwa wakiendelea na vipindi muda huo wa asubuhi, hadi pale ulipofika muda wa mapumziko, ulipofika, walienda wote kupata chakula, walipomaliza, Hawa alimuomba Ramah ampeleke chooni, wakaongozana kuelekea huko huku wakiwaacha wenzao wakirudi darasani.
“Oya Babeli, si nilikuambia kuwa yule demu anachukuliwa na yule Ramah, haya sasa wale pale shuhudia mwenyewe kwa macho yako” alikuwa ni kijana mmoja aliekuwa amekaa na wenzake watatu kwenye gogo sehemu ambayo ilikuwa ni mbali kidogo na ilipo njia ya kuendea chooni akimwambia kijana mmoja aliekaa mwisho kabisa wa gogo hilo.
“Dah! Yani yule demu mimi kanichomolea halafu kaenda kumkubalia yule boya?” Huyo kijana aliejulikana kwa jina la Babeli aliongea huku akisikitika asiamini macho yake kwa anachokiona, maana alishawahi kuambiwa kuwa Hawa mwanamke ambae alikuwa akimfukuzia kila siku anatoka na mtu mwengine, ni jambo ambalo lilimuuma sana kupita maelezo.
“Jamaa, mimi nilikuwa nakuambia kila siku ila wewe ukawa unabisha, sasa unaona mwenyewe jamaa akimpeleka demu chooni” Kijana wa mwanzo kuongea alisema.
“Hataa!! Mimi wanangu sikubaliani na hili jambo hata kidogo. Subiri nikamuamshie pale pale yulo boya” Babel baada ya kuongea hivyo, alinyanyuka hapo alipokaa na kuanza kupiga hatua kuwafuata Ramah na Hawa waliokuwa wakielekea chooni, alipanga akafanye fujo.
ENDELEA..
“We jamaa acha uboya wewe, sasa ukienda kufanya fujo pale mbele ya yule demu unadhani atakuelewa tena? Si atakuona mduanzi tu huna lolote, unatakiwa umfuate yule jamaa akiwa pekeake ndio umuanzishie ila ukimfanyia fujo mbele ya yule demu basi ujue ndio utamkosa kabisa” Babel alisimama baada ya kusikia maneno ya yule kijana wa mwanzao kuongea, akayapima na kuona yana ukweli ndani yake, akaghairisha alichotaka kwenda kukifanya na kurudi pale walipo wenzake.
“Mwanangu ghadhabu sana yani, yule demu mimi kila nilivyokuwa nampanga anyee kwenye poti yeye alikuwa akijifanya ananyea nje, kapangwa kidogo tu na yule boya anajifanya amekubali, halafu sasa walivyo na dharau wanakuja kujipitisha mbele yangu kwa makusudi kabisa ili mradi tu waniumize moyo, ila mimi yule boya siwezi kumuacha hivi hivi hata kidogo, lazima nimfunze adabu” Babel aliongea kwa hasira hadi mishipa ya shingo ikamtoka, halikuwa swala la ajabu kwa wenzake maana waliijua ndio tabia yake ya kutaka wanawake kilazima hata kama ikiwa wenyewe walikuwa hawataki. Kilichomtia jeuri ni utajiri wa nyumbani kwao.
“Nakukubali mkali unapoamua lako, ila kwa pale unatakiwa uende kistaarabu sana, ukienda hovyo hovyo basi ujue utamkosa” Kijana mwengine aliekuwa pembeni ya yule aliongea mwanzao akaongea.
“Ni hivi, yani unatakiwa umtafute Ramah halafu umkanye kwa maneno, akijifanya kichwa ngumu basi tunamzingua” Shebe aliongea.
“Je kama tukimzingua halafu pia akijifanya haelewi?” Babel aliongea hivyo lakini alionekana dhahiri hakurizika na ushauri wa Shebe.
“Hapo ndio tutajua cha kufanya mzee” Shebe aliongea.
“Aaaa!! Mwanangu yule boya nishaanza kumtamani, yani nataka nikamfunze adabu hata sasa, asa we Shebe unaponiambia habari za kumkanya sijui na nini naona kama vile tunamlea tu”
“Lakini Babel alichoongea Shebe ni cha kweli, tusimletee mtiti kabla hatuja muonya kwanza” Kijana wa mwanzao kuongea alisema kuunga mawazo ya Shebe.
“Mnama mimi sio kama sijamuelewa Shebe, nimemuelewa sana ila naona kama vile habari za kumkanya ni kupoteza muda tu” Babel aliongea.
“Lakini Babel yule gashi si alikukataa, muachie jamaa bahati yake, mimi naona haina haja ya kuwekeana Uhasama na mwaume mwenzetu kisa demu tu” Kijana wa mwisho anaetimiza unne wao aliongea.
“Oya msikilizeni huyu boya anavyoongea? Mimi namiambieni huyu jamaa snichi tu, ona sisi tunapanga mipango ya kumteka demu yeye analeta maneno yake ya ki**nge hapa” Babel aliongea kwa sauti ya kupaniki hadi akamfanya huyo alieongea maneno hayo kuogopa, maana alimjua mtu huyo hakawii kuleta fujo sehemu yoyote hata iwe wapi. Anaikumbuka sana siku ambayo Babel alipo wagomea walimu kuchapwa kisa kuja shule na gari huku akiwa ameifungulia muziki mwanzo mwisho wakati huo ulikuwa ni wa asubuhi wanafunzi wakiwa wapo mstarini, kitendo kilichowafanya wanafunzi wote wageuke nyuma kuliangalia hilo gari linalo piga muziki kiasi hicho wakati wao wakiwa msatarini. ndipo hapo aliposhuka Babel kwa jeuri kubwa utafikiri kitendo alichokifanya ni sahihi, kitendo hicho kilipelekea kupelekwa osifi ya walimu na kutaka kumuadhibu, ila aliwagomea wote huku akiwatishia kuwafanyia kitendo kibaya endapo watamgusa na fimbo zao. kwa nguvu ya pesa za baba yake, kesi hiyo iliisha baada ya mzazi wake kuja shuleni alipopewa barua ya kumleta mzazi wake.
“Oya Lacho unajua sisi hatukuelewi kabisa, yani wewe sio mara ya kwanza kupinga mipango yetu tunayoipanga, sasa wewe kama ushaona hili kundi limekushinda, basi likatae kimya kimya, hatuwezi tukashirikiana na maboya kama wewe” Mnama aliongea kumuambia Lacho kijana wa mwisho kuongea. Walimuita Mnama kutokana na kabila lake la Kichaga.
Majira hayo kengele iligongwa na kuwafanya wainuke hapo walipokaa na kuanza kuondoka kuelekea madarasani mwao, wote hao wanne walikuwa wakisoma mchepuo mmoja wa masomo ya biashara kidato hicho hicho cha tatu. Walingia darasani huku wakipanga kumfuata Ramah baadae ili wamuonye kwa kile kitendo cha kuwa na Hawa kimahusiano.
Muda ambao ulitumika kama mapumziko ya pili au muda wa kwenda kufanya ibada kwa wale wenye imani ya dini ya kislamu, ndio muda huo waliopanga wamtafute Ramah na kumuonya kama walivyopanga. Walifanikiwa kumpata na kumchukua kiurafiki tu hadi lilipo gogo ambalo wao wamelifanya kama ni maskani yao muda wa mapumziko.
“Oya Ramah, unajua sisi sote hapa ni wanaume, na mwanaume siku zote anapoambiwa jambo huwa ni muelewa sana, sasa jamaa kama sote hapa ni wanaume kuna jambo tunataka tukuambie kistarabu kabisa” Mnama alianza kuongea baada ya kufika mahala hapo.
“Nawasikiliza wana, ongeeni” Ramah aliongea.
“Ni hivi, yule demu unaetembea nae ni demu wa mshkaji wetu hapa Babel. Jamaa roho ilimuuma sana baada ya kukuona na demu wake akataka kuja kukufanyia fujo ili tukamtuliza na kumuambia kuwa tukuite halafu tukuambie maana huenda ikawa ulikuwa hujui” Ramah aliposikia maneno hayo alitabasamu na kumuuliza.
“Kwahiyo nyie mlikuwa mnataka nini?” Ramah aliongea huku akiwa anatabasamu, kitendo hicho na swali hilo, Babel alivitasfiri kama dharau, akataka kumuanzishia fujo ila wenzake wakamzuia.
“Mimi niliwaambia kuwa huyu boya ni ms***ge tu, sasa si mnaona majibu yake ya kishoga shoga anayoyaleta hapa? Haikuwa na haja ya kumuonya wala nini, huyu alitakiwa afanyiwe tu kabla ya yote, tena anadharau anapita na demu wangu mbele ya macho yangu halafu nyie mnasema aonywe?” Babel aliongea kwa sauti kubwa kiasi kwamba hadi wanafunzi waliokuwa wakipita hapo walisikia alichokuwa akiongea.
“Tuliza munkari Babel” Shebe akamtuliza, kisha akamgeukia Ramah na kumuambia. “Ramah sisi tulichokuwa tunataka ni kuachana na yule gashi wa mshkaji wetu, vinginevyo utatafuta vita na sisi” Shebe aliongea hivyo, lakini Ramah bado alikuwa na tabasamu usoni mwake, ilionekana hakutishwa na maneno ya Shebe wala kupaniki kwa Babel hata kidogo.
“Sikilizeni majamaa, nadhani hiyo vita itakayokuja ni vita ya tatu ya dunia baada ya pili kuisha, na nimiambie tu kuwa sitishwi na maneo ya nyie washamba msiojua kubembeleza mademu mkitaka wamipende kifosi. Niko tayari kwa hiyo vita” Ramah aliongea kwa kujiamini kiasi kwamba akawafanya vijana hao midomo yao kuwa wazi kwa mshangao, maana hawakuwahi kumchimbia mtu biti halafu alete maneno ya kujiamini kiasi hicho.
Ramah alipoongea hivyo, akanza kuondoka mahala hapo kwa kujiamini huku akimuacha Babel akishikiliwa na wenzake kwa kumzuia asimfuate Ramah aliekuwa akiondoka kwa majivuno sana. Babel baada ya kuona hawezi kuchomoka kwenye mikono ya hao wenzake, akabaki akimtukana Ramah huku akimuahidi kumfanyia kitendo kibaya ambacho hatoweza kukisahau maishani mwake.
“Oya jamaa, wale wajinga leo wameniita hadi kwenye lile gogo lililokuwa njia ya kuendea chooni, mi basi nikadhani wataenda kuniambia maneno ya maana, kumbe wameenda kuniongelea maneno yao kike waliyozoe kuwatishia hao maboya wengine wakidhani na mimi nitakuwa boya” Ramah alimuambia Hemedy baada ya kufika darasani kwao.
“Hao wajinga ni wakina nani na wamekuambia maneno gani?” Hemedy alimuuliza baada ya kuona hajamuelewa vizuri.
“Si hao wanaojiita STAREHE BOYZ” Ramah aliongea na kumfanya Hemedy acheke sana kisha akanyamaza baada ya dakika.
“Si wale mapimbi wanne? Wamekuambiaje?” Hemedy alimuuliza huku akiwa bado anatabasamu lililoelekea kucheka.
“Hao hao Man, eti wameniita hadi pale, mi nikajua wanataka kuniambia ishu ya maana kumbe wananiambia eti niachane na Hawa kwasababu ni demu wa Babel” Ramah aliongea.
“Kwahiyo na wewe ukaamini hicho kitu?” Hemedy alimuuliza.
“Aaaa!! Jamaa naanzaje kuamini maneno yao ya kutolea sanduku kwa mke?”
“Lakini ukanyeta kwa mkwara wao?”
“Kumbe mwanangu na wewe pia unaniona mimi boya?”
“Hapana man nimekuuliza tu, maana wale jamaa wamewachimbia biti watu wengi halafu wote wakanyeta kwa mikwara yao, ila sio kwamba nimekuona boya jamaa”
“Asa mwanangu unadhani na mimi ni boya kama walivyo hao wengine? Mimi nilipofika pale, wakaanza kuniambia maneno yao, nikawa nawasikiliza tu, halafu nikawajibu kidharau na kutangaza vita na wao, kwahiyo mwanagu nina Uhasama na wale makolo, hivi ninavyokuambia muda wowote ninaweza kuwashiana moto na wale wajinga” Ramah aliongea.
“Kumbuka mimi nimeanza kuwa na urafiki na wewe tangu siku ya kwanza kuja hapa shule, hadi hivi sasa tumekuwa marafiki wakubwa sana, tena sio marafiki tu, tumekuwa ni ndugu kabisa, kwahiyo mwanangu sitokubali hiyo vita uipigane mwenyewe, lazima mzee tutakuwa pamoja, hawatuambii chochote wale wajinga” Hemedy alichoongea alikuwa akimaanisha, maana alikuwa akiongea ‘serious’ huku uso wake ukiwa hauna tabasamu kama mwanzo. Kosa alilofanya Ramah ni kutokumuambia hilo jambao Hawa, wakapanga wapambane wenyewe wawili bila ya kujua kwa kutokumuambia Hawa hilo jambo linaweza kuja kuleta matatizo kwenye mapenzi yao baadae. Hawakujua. Na hawatojua kwasababu wametawaliwa hasira bila ya kuchukua hatua juu ya kitendo hicho. Hawakujua kamwe.
* * * *
“Sasa nyie madogo mtatupa kiasi gani kuifanya hiyo kazi”
“Nyie semeni mnataka kiasi gani ili kazi ikamilike” Babel aliongea kuwaambia watu hawo walionekana dhahiri kuwa na vitendo vya kihalifu.
“Kwavile katika hiyo kazi Kutahitajika gari la kukodi, inabidi mtupe laki tano, yani hapo hatupunguzi wala hatuongezi” Jamaa mmoja kati ya wenzake wawili aliongea.
“Msijali ilimradi kazi ikamilike tu” Babel aliongea.
“Msiwaze maninja, si mmesema asife yani tumuadhibu huku tukimkanya aachane na demu wako?”
“Ndio ni hivyo tu” Babel aliongea.
“Basi acheni hela nusu ili tupate kulipia hilo gari la kukodi” Jamaa huyo aliongea hivyo huku akiwasha bangi, wenyewe wanaita ‘sigara kubwa’. Babel aliingiza mkono mfukoni na kutoa kiasi cha pesa, kisha akazihesabu zilipotimia hela anazotaka akampatia Jamaa.
“Nyie maninja wala msijali, hiyo kazi tutaifanya kesho, halafu usiku wa kesho tutawapigia simu kumijulisha kilichoendelea”Jamaa aliongea hivyo huku akizitia hela hizo kwenye mfuko wake wa suruali, kisha akatoa moshi wa bangi kwenye tundu moja ya pua yake, sijui aliweza vipi kuizibiti tundu ya pili isitoe moshi, kitendo hicho nilikifananisha na bomba la pikipiki aina ya YAMAHA inavyotoa moshi wakati ikiwekwa oili mpya.
Babel na wenzake waliondoka kwenye jumba hilo chakavu(Boma) ambalo mmiliki wake alilitelekeza muda mrefu pasi na kulifanyia ukarabati wowote na kulifanya liwe ni jumba la kujihifadhi wahuni hao, waliondoka na kuelekea wanapopajua wao wakiwaacha wahuni hao wakifurahia kupata pesa za bwerere jioni hiyo.
* * * *
Siku iliyofuata majira ya jioni, Hemedy alienda kwa kina Ramah baada ya kijana huyo kuwa ni mwenye kumuhitaji nyumbani kwao kwa siku hiyo, hilo halikuwa tatizo kutokana na umbali uliokuwepo kutoka kwakina Hemedy hadi kwa rafiki yake. Alipofika hapo, wakasalimiana kidogo kisha wakaingia chumbani kwa Ramah, huko hakukuwa na chengine zaidi ya kucheza gemu mchezo ambao huupenda sana wawapo nyumbani hapo, gemu la mpira ndilo ambalo hupendelea sana kulicheza kuliko mchezo wowote kwenye hicho kifaa.
Majira ya saa kumi na mbili kamili za jioni, walichoka kuicheza hiyo gemu na kuhamia sebuleni ambapo waliweka picha ya IP MAN kwenye luninga wakawa wanaangalia, ila hiyo picha haikufika hata robo yake, Hemedy akaaga kutaka kuondoka akidai nyumba yao hakuiacha na ulinzi mkubwa maana siku hiyo hakukuwa na watu zaidi ya yeye na mlinzi. Hilda na Anti yake waliondoka nyumbani hapo kuelekea wanapopajua wao huku mlinzi nae akitarajia kuondoka majira hayo ya jioni kuelekea alipoagizwa aende na Anti yao, kwahiyo nyumba itabaki tupu ikiwa nae mlinzi akiondoka.
Ramah hakuwa na budi kuondoka nae, maana hata kama akisema abaki hapo nyumbani kwao, hatokuwa na kampani yoyote kwahiyo ni bora waende wote huko, halafu baadae kidogo atarudi nyumbani kwao, wakakubaliana hivyo na kuanza kuondoka nyumbani hapo. Wakati wakiwa wapo njiani kuelekea kwakina Hemedy, nyuma yao kulikuwa kuna gari inayowafuata bila wao kujua.
“Hii ishu ishakuwa ngumu, si unaona wapo wawili na sisi tunamtaka yule mmoja” Jamaa ambae jana alitakwa na Babel wamteke Ramah aliongea kuwaambia wenzake wakiwa kwenye hiyo gari inayowafuatilia wakina Ramah bila wao kujua.
“Kwanini wakati sisi tunamtaka huyu mmoja tu” Jamaa mwengine aliekuwa amekaa siti za nyuma aliongea.
“Kwasababu tukimchukua huyu mmoja, huyu atakaebakia anaweza kupiga kelele au hata kuzisoma namba za gari halafu baadae kwetu ikawa shida, kwahiyo ni bora tuwachukue wote wawili halafu tutajua chakufanya mbele ya safari”
Wakakubaliana kufanya hivyo, wakawa wanawasubiri wafike sehemu ambayo haina watu wengi wafanye hilo tukio. Mbele kidogo wakaona sehemu hiyo itafaa kwa hiyo kazi, bila kuchelewa waliwaekea gari ubavuni mwao, kisha kwa haraka zaidi wakawashika kwa kuwavuta hadi ndani na kuwatia humo, walijitahidi kufurukuta ila ndio hivyo hawakuweza, walikuwa wamedhibitiwa na mikono yenye nguvu ya watu hao na kuwafunga kamba za mikono ambayo waliileta kwenye migongo yao, kisha usoni wakawafunga vitambara vyeusi ambavyo viliwadhibiti vizuri kutokuona chochote.
Kitendo hicho kwa Hemedy kilikuwa ni kawaida japokuwa alikuwa na wasiwasi mwingi, maana yeye hayo matukio ya kutekwa kama hivyo hakuyaanza leo wala jana, aliyaanza tangia akiwa yupo Tanga, kwahiyo kwa kiasi fulani akawa ameyazoea. Ila kwa Ramah tangu azaliwe hakuwahi kufanyiwa kitendo cha kutekwa hata kwa bahati mbaya, yeye ndie aliekuwa na wasiwasi mwingi kuliko hata mwenzake, alikuwa akiwaomba sana watu hao wawasamehe bila kujua wamefanya kosa gani, ila alikuja kunyamaza baada ya kutulizwa na kofi moja matata lililotua kwenye mdomo wake, akaona mdomo wake ukimzidi uzito, bila kupenda akaacha mwenyewe kupiga kelele.
Safari hiyo iliishia kwenye lile jumba chakavu ambalo wahuni hao au watekaji hao walilifanya kama ndio masakani kwao, jumba hilo lilikuwa lipo mbali na nyumba nyengine kutokana na sehemu hiyo kutokuwa na nyumba nyingi, kwahiyo hata kama wangesema wapige kelele kiasi gani wasingeweza kusikika. Waliingizwa ndani humo na kuanza kupewa mateso hasahasa Ramah huku akiambiwa kuwa kosa lake ni kuchukua mwanamke wa mtu, alipigwa sana huku akiambiwa akiri kumuacha huyo mwanamke mara atakapo achiwa hapo, ila kama akijifanya kiburi basi hatoweza kutoka salama humo ndani.
Ramah alikataa katakata kukubali kumuacha huyo mwanamke anaeambiwa aachane nae, haikujulikana ni kiburi au ni nguvu ya penzi ndio inayomfanya akatae kusema kuwa amekubali kuachana na huyo mwanamke, lakini hiyo haikuwa ni kiburi kilichomfanya kutokukubali kusema kuwa amekubali kuachana na huyo mwanamke ambae hata kama angesema amekubali kuchana nae, basi asingeweza kusikia chochote kutokana na kuwa hapo hakuwepo. Sasa ni vipi akatae kukiri hata kwa uongo ili tu kuiokoa nafsi yake? Mapenzi bwana!.
Walimpiga hadi sasa wakawa wanaona huko wanapoelekea wanaweza wakamzimisha kama sio kumuua kabisa, ikabidi wampigie simu aliewapa hiyo kazi, wakamuelezea vyote kwamba kijana amekataa kumuacha huyo mwanamke anaedai ni mwanamke wake, kilichowafanya kumpigia simu ni kutaka kujua wafanye nini maana mtu huyo anaoneka hakuwa na hata na dalili za kukubali kile wanachokita, ila jibu walilopewa kuwa wamvunje hata mguu lazima tu atakubali asitake atake, walipopokea agizo hilo, wakakubaliana nalo na kumfuata Ramah aliekuwa chini hajiwezi huku damu zikiupamba mwili wake wote, walipanga wamvunje mguu ama mkono ili tu akubali kile wanachomlazimisha kukikubali.
JAMAA mmoja wakati akijiandaa kuuvunja mkono wa Ramah, alishtuka akipigwa teke la mbavu lililomfanya agugumie kama mbwa mdokozi aliepigwa jiwe wakati akiwa anajaribu kufunua mfuniko uliofunikiwa kwenye sufuri la nyama lililokuwa jikoni. Jamaa wa pili akiwa bado na kiwewe asielewe nini kilichomkuta mwenzake hadi kurushwa pemebeni mithili ya mcheza sarakasi. Alikuja kushtuka akipokea ngumi ya uso yenye uzito usio mithilika iliyomfanya aone kama dunia yote amebebeshwa kichwani huku nyota zikimzomea na kumdhihaki kwa kitendo alichotaka kukifanya, akakosa muelekeo kwa kuyumba yumba kama mlevi wa pombe chafu aina ya mataputapu, akabaki mikono yake kaiweka usoni mwake akishindana na maumivu anayoyasikia.
Jamaa wa tatu na wamwisho alipoona wenzake kila mmoja akigugumia kwa maumivu, akajaribu kutaka kukimbia ili kuiokoa nafsi yake kwa hao watu waliowafanyia uvamizi wa ghafla. Ila alijishangaa kujikuta hewani akielea kama tiara iliyokuwa ikichezewa na mtoto, wakati akiwa huko hewani, alijiuliza ni kipi hasa kilichompeleka huko wakati muda mfupi tu uliopita alikuwa akitembea ardhini, ila kabla hajapata jibu sahihi, alijikuta akitua chini kwa nguvu mithili ya gunia la viazi lililotuliwa chini kwa ghadhabu na mbebaji aliekosa maelewano mazuri na tajiri aliemtaka ambebee alipeleke kwenye gari lake, alikuja kupata jibu ya kilichomfanya kuwa katika hali hiyo baada ya kuona guu la haja likitua chini baada ya kutoka kumuadhibu yeye.
Wote watatu walibaki chini wakigaagaa kama watoto wadogo walionyimwa sufuria la uji walilotaka kulikombeleza baada ya uji kuisha. Waliofanya shambulizi hilo la ghafla walikuwa ni Asu na Kanu vijana ambao walitumwa kuhakikisha ulinzi wa Hemedy kwa masaa ishirini na nne, baada ya kumaliza kufanya tukio hilo, wakaondoka hapo bila ya kutoa msaada wowote kwa vijana hao na kwenda kwenye gari yao na kutimka mahala hapo.
Huko ndani ya jumba, wale wahuni walikuwa bado wapo chini hawajiwezi hata kunyanyua vidole vyao kwa maumivu wanayoyasikia kwenye miili yao. Kipindi chote hicho Hemedy ambae alikuwa anaunafuu kwenye mwili wake kwasababu yeye hakupigwa sana na wahuni hao, alikuwa akisikilizia yote yanayoendelea hapo, hakuweza kuona chochote kutokana na kitambara alichofungwa nacho usoni.
Baada ya purukushani kuisha humo ndani, akaona pako kimya sana, ikambidi aanze kujitahidi kuzifungua hizo kamba alizofungwa nazo mikononi mwake, haikuwa rahisi kuzifungua hizo kamba kutokana na kuwa zimekazwa sana, baada ya kujitahidi sana, akafanikiwa kuzifungua na kukifungua kitamabara alichofungwa nacho kwenye macho. Alipepesa pepesa macho kwa dakika moja baada ya kutoona vizuri kutokana na kufungwa kitambara hicho kwa muda mrefu, baada ya macho yake kupata nuru nzuri, aliwashuhudia watekaji hao wakiwa chini wamelala kila mmoja akishika sehemu yake anayoona inamfaa kwa kupoza maumivu aliyopatiwa na wavamizi waliowavamia kwa ghafla, hakujua ni kipi hasa kilichowakuta watu hao hadi kuwa katika hali hiyo, akapiga jicho pembeni na kumuona Ramah akiwa hajiwezi kwa kipigo alichopokea.
Hemedy hakutaka kupoteza muda, akamuwahi Ramah na kumfungulia kitambara alichofungwa nacho machoni na kumfungulia na kamba alizofungwa nazo mikononi. Kisha akambeba mgongoni na kumtoa nje ya jumba hilo, hakujua aelekee uelekeo upi kwasababu walipoletwa hapo walikuwa wamefungwa vitambara kwenye macho yao, akashika njia iliyoekuwa kulia kwake baada ya kukosa jibu sahihi ya njia ipi aende.
Wakati Hemedy akiwa amembeba Ramah mgongoni mwake huku akikimbia kuelekea njia ambayo hajui atatokea wapi. Mbali kidogo kulikuwa kumepaki gari ambayo tumezoea kuwaona nayo wale waliotumwa kumlinda Hemedy. Watu hao walikuwa wakiwaangalia vijana hao wanavyokimbia kutoka sehemu hiyo waliyotekwa. Asu kama ambavyo tunamjua, alitoa simu yake na kuiminyaminya kisha akaiweka sikioni kwake.
“Ndio mkuu tumefanikiwa kuwasaidia na tumewaacha wenyewe wajisaidie na hapa tunapoongea Hemedy amembeba mwenzake mgongoni wakiondoka sehemu hii” Asu aliongea.
“Vizuri sana, lakini Hemedy si hajaziona sura zenu?” Mtu wa upande wa pili alisifia na kuuliza.
“Hapana mkuu hajaziona kwasababu walikuwa wamefungwa vitambara kwenye macho yao”
“Anatakiwa asizione sura zenu maana hiyo itamfanya ajiulize maswali mengi kuhusu kufuatiliwa kila mara na nyie”
“Sawa mkuu”
“Hakikisheni ulinzi unakuwa mkubwa kwa hao vijana hadi watakapofika majumbani kwao. Kumbukeni Kiongozi anamuhitaji Hemedy kuliko kitu chochote” Mtu wa upande wa pili alisisitiza.
“Sawa mkuu, ila nashauri na huyu kijana wako pia umuingize katika huo mpango maana nae anaonekana ni jasiri sana”
“Huyo hawezi kuwa katika huo mpango, ila mimi nitamfunza mwenyewe kile ambacho tunataka kumfunza huyo mwenzake, kwahiyo huyo atakuwa ni wangu mimi kama mimi”
“Sawa mkuu acha tuwafuatilie maana wameshafika mbali na tulipo sisi” Asu baada ya kuongea hivyo, alikata simu na kuwasha gari kuwafuatilia wakina Hemedy. Hawa watu ni wakina nani? Na wanampango gani na Hemedy? Na huyo Kiongozi ni nani? KIZUNGUMKUTI.
Hemedy alitembea hadi akachoka, maana mgongoni mwake alikuwa amembeba Ramah ambae kidogo hali yake kwasasa inaanza kuwa nzuri kutokana na kipigo alichopokea. Alimbeba hadi alipofika barabarani na kukuta taksi zikiwa zipo nyingi mahala hapo, akaita moja na kuomba iwapeleke hospitali iliyokuwa karibu, kisha akamuingiza garini Ramah na yeye akaingia humo na safari ya kwenda hospital ikaanza.
Walifika katika hospitali hiyo ya binafsi na kumshusha Ramah kwenye gari akisaidiwa na dereva taksi kumuingiza ndani ya hiyo hospital, walipokelewa na manesi waliokuwa eneo hilo na kumuingiza Ramah kwenye chumba maalumu kwajili ya matibabu. Hemedy alimlipa dereva taksi kiasi chake cha pesa alichokitaka na dereva akaondoka akimuacha Hemedy akielekea kwa daktari aliekuwa amemuita osifini kwake mara baada ya kutoka kwenye chumba alicholazwa Ramah.
“Yule mgonjwa ni nani yako?” Daktari alimuuliza hivyo Hemedy baada ya kumkaribisha kukaa kwenye kiti kilichopo humo osifini mwake.
“Ni ndugu yangu yule. Kwani hali yake inaendeleaje Daktari?” Alijubu kisha akauliza.
“Hali yake sio mbaya sana ila inabidi leo alale hapa ili tujue hali yake itaendeleaje baadae. Kwani hakuna mkubwa yoyote uliekuja nae?” Daktari alimuuliza.
“Hapana hatukuja na mtu yoyote Dokta”
“Basi fanya mawasiliano na watu wa nyumbani kwenu ili waje hapa” Daktari alipoongea hivyo, Hemedy akainuka na kutaka kutoka humo ndani, ila sauti ya dokta ndio iliyomfanya akaacha kufungua mlango wa kutokea na kumuangalia usoni.
“Vipi, mbona unaondoka tena?” Daktari alimuuliza baada kuona mtu huyo akitaka kuondoka.
“Naenda kuichukua simu yake, maana hiyo ndio ina namba za watu wa nyumbani” Hemedy aliongea na kumfanya Daktari kumruhusu kwa kichwa. Kisha akaondoka na baada ya dakika moja akarudi na simu ya Ramah, akaingia sehemu ya majina na kutafuta jina litakalo faa kulipigia, akapiga baada ya kupata jina lililoandikwa ‘FATHER’ kisha akamkabidhi simu Dokta baada ya kusikia ikiita.
“Haloo” Sauti ya upande wa pili ilisikika ikongea.
“Ndio. We ndio mzazi wa..” Alipofika hapo akamgeukia Hemedy aliekuwa ametulia kimya akisikiliza, ishara hiyo aliielewa na kulitaja jina la Ramah kisha Daktari akamtajia mtu huyo wa upande wa pili.
“Ndio ni mimi” Sauti ya upande wa pili ilijibu. Sauti hii ndio ile sauti ambayo tunaisikia kila mara Asu anapoongea na simu kuhusu Hemedy. Daktari baada ya kusikia kuwa huyo anaeongea nae ndio mzazi wa mgonjwa, akamuambia aje hapo hospitali kuna tatizo limemkuta mwanae, mtu huyo wa upande wa pili akajifanya kushtuka na kutaka kuambiwa kuwa mwanae nini kimemkuta, ila Daktari akamuambia aje atakuja kujua huku huku.
Baada ya dakika ishirini, ofisini humo kuliingia mtu mzima ambae kwa makadirio alikuwa na miaka arobaini hadi arobaini na tano, alikuwa mfupi na mwenye rangi ya maji ya kunde, hakuwa mnene sana ila alikuwa na mwili kidogo. Alipofika hapo akawasalimia aliowakuta na kuambiwa akae kwenye kiti chengine.
“Niambie Dokta nini tatizo lililomkumba mwanangu” Mzee huyo aliongea kwa hofu utafikiri alikuwa hajui kilichomkumba Ramah.
“Muulize huyu ndugu yake aliemleta ndio atakuelezea kila kitu kisha mimi nitakupa matokeo ya hali ya mwanao” Daktari aliongea.
“Eti Hemedy, ni kipi kilichomkuta mwenzako” Mzee huyo alimgeukia Hemedy na kumuuliza hivyo. Utajiuliza imekuaje hadi mzee huyo kumuita Hemedy jina lake, ila ni kwamba Hemedy sio mara ya kwanza kuenda nyumbani kwakina Ramah, hata yeye alikuwa akifahamiana na huyo mzee kama baba wa rafiki yake.
“Tulivamiwa na watu tusiowajua wakati tunatoka nyumbani kuelekea nyumbani kwetu, wakatuingiza kwenye gari lao na kutupeleka sehemu tusioijua,huko ndio wakatupiga sana ila Ramah ndio wamempiga sana hadi akawa hajiwezi” Hemedy hakutaka kuficha ila alificha kilichowapelekea kutekwa na watu hao.
“Sasa kwanini wamiteke na wakamipigie huko msipopajua?” Baba yake Ramah alimuuliza. Ila swali hilo lilikuwa gumu sana kwa Hemedy kulijibu, akabaki kimya kwa sekunde kadha akifikiria ajibu nini.
“Hatujajua kwasababu wao walikuwa wakitupiga tu bila kutuambia chochote” Hemedy aliamua kuongopa, jibu hilo lilimfanya Mzee huyo atabasamu baada ya kuoma dhahiri amedanganywa.
“Ok, Daktari hali yake sasa hivi inaendeleaje?” Mzee huyo alimgeukia Daktari na kumuuliza swali hilo.
“Hali yake sio mbaya sana, ila leo inabidi alazwe ili tujue ataendeleaje baadae”
“Sawa naweza kwenda kumuona?”
“Yeah, twendeni” Daktari aliongea hivyo na kuinuka na kuwafanya hao wengine nao kuinuka na kuelekea katika chumba alicholazwa Ramah. Walipofika huko wakamjulia hali na kusema kuwa kidogo afadhali ila anahisi maumivu kwenye kifua chake. Baada ya kumjulia hali, Daktari aliwaambia kuwa waje kesho ili kujua hali yake imeendeleaje kwa siku hiyo. Hawakuwa na budi, wakaaga na kuanza kuondoka ndani ya jengo hilo la hospitali na kwenda kupakia kwenye gari alilokuja nalo Baba yake na Ramah.
Baba yake na Ramah alimpeleka Hemedy nyumbani kwao na yeye akaondoka hapo kuelekea anapopajua yeye. Hemedy aliingia ndani ikiwa ni mishale ya saa tatu usiku, alipofika sebuleni, akawakuta Hilda na Anti yao wakiwa wamekaa kwenye masofa huku wakiwa na wasiwasi mwingi, akajua yote hayo ni kwasababu yake.
“Haya wewe ulikuwa wapi muda wote huo na kwanini simu yako umeizima?” Alikutana swali hilo kutoka kwa Anti na kumfanya ajipekuwe mfuko na kuitoa simu yake na kuiangalia, akakuta kweli ilikuwa imezima.
“Tulipatwa na matatizo Anti mimi na Ramah” Hemedy alijibu.
“Matatizo gani hayo yaliyokufanya hadi uzime simu kabisa?” Anti bado aliendelea kumkomalia na maswali. Hemedy alimuelezea yote yaliyo wakuta ila huku pia alificha sababu ya wao kutekwa.
“Na huyo mwenzako vipi hali yake, anaendeleaje?” Anti aliuliza kwa masikitiko baada ya kuisikiliza hiyo taarifa, ila Hilda alioneka kutoamini maneno hayo.
“Hali yake kwasasa iko vizuri ila bado yupo hospitali akichekiwa zaidi na kesho nitaenda kumuangalia”
“Kwahiyo kesho hutoenda shule?”
“Ndio Anti nilazima nikamuangalie”
“Haya mimi nipo ndani huko napumzika” Anti aliongea hivyo huku akinyanyuka na kuingia ndani akiwaacha Hemedy na Hilda wakiangaliana utafikiri ndio mara yao ya kwanza kuonana. Hilda aliinuka hapo alipokaa na kwenda hadi alipo Hemedy, akamshika mkono na kumvutia nje na kusimama nae kwenye mti ambao ulikuwa ndani ya uzio wa hio nyumba.
“Najua pale umemdanganya Anti. Haya nambie ukweli umetoka wapi we mwanaume?” Hilda alimuuliza Hemedy hivyo huku akiwa mikono ameikunja kwenye kifua chake na mguu mmoja akiuweka mbele huku mwengine ukiwa upo sawa. Swali hilo lilimfanya Hemedy akabaki mdomo wazi huku akimuangalia binti huyo. Akabaki akijiuliza, ina maana hakunielewa kile nilichokisema pale ndani au hakuniamini?
“Hilda mbona sikuelewi? Sinime wahadithia yote yaliyotuka mimi na Ramah? Sasa ni kipi kilichokufanya ukanitoa ndani hai hai hadi huku nje halafu unakuja kuniuliza swali hilo? Hemedy alimuuliza.
“Sikiliza Hemedy, nyie kuna sehemu zenu mmetoka mnajifanya kusingizia kutekwa, haya nyie mtekwe na nani? Mnakipi kinachowafanya hadi mtekwe?” Hilda alimuuliza kwa kutahariza. Hemedy alipoona hapo mlolongo unaweza ukawa mrefu, akaamua kutoa simu yake na kumpigia Ramah, baada ya muda mfupi simu ikapokelewa.
“Oya Ramah, embu ongea na Hilda” aliposema hivyo akampa simu Hilda na kuanza kuongea nae.
“Ramah niambie ukweli, mlikuwa mpo wapi? Mwenzako kaja huku nyumbani anajifanya kusingizia eti mlitekwa, kamdanganya Anti anadhani na mimi pia nitaamini huo uongo wake, ‘please’ Ramah usinifiche naomba uniambie ukweli” Hilda aliongea.
“Hilda sikiliza nikuambie, wewe kama humuamini Hemedy anavyosema basi kesho asubuhi njoo nae hospitali, naamini ukija huku hutokuwa tena na swali la kuuliza. Mpe simu Hemedy” Ramah aliongea kwa sauti ya uchovu au kama ametoka usingizini muda mfupi.
“Hemedy, mjulishe na Hawa pia maana mimi simu yangu salio limeisha” Ramah aliongea hivyo. Hilda aliposikia maneno hayo kidogo akaanza kuamini, maana simu hiyo iliwekwa sauti kubwa.
“Usijali kaka, subiri nifanye hicho kitu sasa hivi” Hemedy alikata simu na kumpigia Hawa kisha akamuambia taarifa hiyo, binti huyo alikuwa na wasiwasi na maswali mengi baada ya kuisikia taarifa hiyo, ila Hemedy akamtoa hofu na kumuambia kama kuna uwezekano, kesho asubuhi waongozane wote wakamuangalie hospitali, kisha akakata simu na kumuangalia Hawa aliekuwa ametahayari muda wote.
“Wewe!! Kumbe ni kweli!” Hawa aliuliza kwa taharuki mithili ya mwanafunzi aliepokea taarifa ya matokeo yake ya kidato cha nne na kuambiwa kuwa amefeli.
* * * *
Siku iliyofuata, waliongoza wote wanne yani Hemedy, Hilda, Hawa na Anti yao kwenda hospitali kumuangalia Ramah, walipofika walimkuta Baba yake na Ramah akiwa eneo hilo kilipo kitanda alicholazwa mwanae, Hawa alipofika hapo akangua kilio kilichomshangaza Anti yake na Hilda, kilio hicho hakiku mshangaza Baba yake Ramah kwasababu alijua huyo huenda ikawa ndio huyo mkwe wake alieambiwa na watu wake kuwa mtoto wake na yeye anampenzi siku ile walipokuwa ufukweni.
Hawa aliacha kulia na sasa alikuwa amekilaza kichwa ha Ramah kwenye mapaja yake baada ya kukaa kwenye kitanda alicholazwa kijana huyo, hakujali watu wazima hao waliokuwa wapo mahala hapo, ila alichojali yeye ni mapenzi yake kwa kijana huyo. alikuwa akimuuliza hali yake huku akiwa anakichezeachezea kichwa cha Ramah, ila kijana huyo alimtoa hofu kabisa kwa kumuambia kuwa hali yake kwa sasa iko vizuri sana tofauti na jana, hapo kidogo banati huyo moyo wake ukatulia.
Alikuja daktari na kumjulia hali kijana huyo kisha akamuomba mzazi wake amfuate ofisini, huko walipofika, hakukuwa na chengine zaidi ya kuambiwa maendeleo ya mwanae kuwa ni mazuri na kwa muda huo anaweza kuondoka nae. Akashukuru sana na kuomba kupewa muongozo mzima wa kulipia gharama zilizotumika. Daktari akampatia karatasi flani na kumtaka aende nayo kwenye dirisha la dawa kisha akampa na karatasi nyengine akimtaka aende nayo mapokezi baada ya kutoka kwenye dirisha la dawa.
Mzee huyo alishukuru na kuaga, kisha akatoka na kuingia kwenye chumba alicholazwa Ramah na kuwataka waondoke hapo maana ruhusa ya daktari imeshatoka. Wakachukua kilichochao na kutoka chumbani humo. Baba yake Ramah alikamilisha kila kitu na kutoka nje ya hospotali hiyo, akawakuta wakiwa wanamsubiri nje, wakaondoka wote kuingia kwenye gari huku Anti yake Hilda akiaga na kuondoka kuelekea kwenye shuhuli zake.
Safari yao iliishia nyumbani kwakina Ramah, wakaingia wote subuleni na kukaa hapo, muda wote huo Hawa alikuwa yupo karibu na Ramah kuliko mtu yoyote ndani hapo, Baba yake Ramah aliwaaga na kuondoka hapo huku akimuachia Ramah kiasi cha pesa ambazo zitamsaidia kununua chochote atakacho. Ramah aliingia chumbani kwake kwenda kuoga kisha akarudi tena hapo sebuleni. Hawa na Hilda walichukua jukumu la kuingia jikoni kwajili ya kupika chakula maana siku hiyo walipanga washinde hapo hapo.
Siku iliyofuata, walienda shule baada ya hali ya Ramah kutengemaa, siku hiyo walikuwa na chuki zilizochanganyikana na hasira kwa lile kundi lililo sababisha kitendo cha kutekwa kwao, walipanga wakawafanyie fujo pindi utakapofika muda wa mapumziko.
Muda wa mapumziko ulipofika, wakatoka darasani huku vichwa vyao vitawaliwa na hasira juu ya vijana hao, waliondoka wao wenyewe wawili na kuwafuata sehemu ambayo watu hao wanaifanya kama ndio maskani yao wawapo hapo shule. Hasira ziliwazidi baada ya kuwaona wakiwa wamekaa tena wakiwa na furaha kupitiliza, hapo wakaongeza mwendo kuwafuata.
ENDELEA
WALIWAFUATA palepale walipokaa, hawakujali uwingi wao, walichojali wao ni kutimiza adhma yao waliyoipanga. Ramah alipofika, hakutaka salamu wala salama, alichofanya yeye ni kumzawadia Bebel ngumi moja iliyoenda kutua kwenye mwamba wa pua na kumfanya kijana huyo kuishikilia pua yake na kuinamisha uso wake chini kwa maumivu aliyoyapata. Akarusha ngumi nyengine iliyokuwa na lengo la kupiga kwenye sikio la Babel, ila kabla ngumi hiyo haijatua sehemu lengwa, alijikuta akipokea ngumi iliyotua sawia kabisa kwenye mbavu zake za kulia na kumfanya ahisi maumivu ya aina yake, ila maumivu hayo hayakuifanya ngumi yake isifikie lengo, ngumi yake ilituwa kwenye sikio la Babel na kumfanya kijana huyo aone kuendelea kukaa hapo ni kujitafutia maumivu kama sio kujeruhiwa kabisa.
Hemedy naye, alirusha teke kumuendea Shebe ambae ndie alimpiga Ramah ngumi ya mbavu, teke hilo lilienda kumpata mtu huyo la kifua na kumfanya arudishwe nyuma huku akiachiwa alama ya kiatu kwenye shati lake jeupe maeneo ya kifua. Hemedy wakati akirudisha guu lake chini baada ya kutoka kumuadhibu Shebe ambae kwa sasa alikuwa chini mbali na yeye kutokana na msukumo wa teke lake, ila kabla guu lake halijatua chini, alijikuta akichotwa mtama maridadi uliyomfanya na yeye kuenda chini bila kupenda. Mtama huo alipigwa na kijana wanaemuita Mnama.
Wakati Ramah akizubaa kumuangalia Hemedy aliekuwa akijizoazoa pale chini baada ya kuchotwa mtama, naye alikuja kushtuka akipokea ngumi ya shingo iliyomfanya kukunja sura kwa maumivu ya sehemu hiyo huku mikono yake yote miwili akiipelekea sehemu hiyo kuishika, kabla hajajiuliza vizuri, alijikuta akipokea ngumi ngengine ya sikio iliyomfanya aone kama yuko njiani halafu mbele yake kuna njia mbili, moja ya kwenda peponi nyengine ya kwenda motoni huku akilazimishwa na viumbe asiovijua aende ile njia ya kwenda motoni, ngumi hizo alizipokea kutoka kwa Babel aliekuwa na hasira nae baada ya kutoka kusikilizia maumivu.
Hemedy muda huo alishainuka na kumfuata Mnama ambae aliekuwa akimsubiri ainuke ili waendeleze mpambano. Alipoinuka akakaa sawa kimapigano kumuangalia hasimu wake kwa hasira, Mnama alipoona adui yake kainuka kwaajili ya pambano, akarusha ngumi ya kizembe sana, ngumi ambayo hurushwa kwa kuuzungusha mkono mithili ya feni. Hemedy ngumi hiyo aliiyona na kubonyea chini kidogo, ikapita na yeye hakutaka kumuacha hivihivi adui yake, alimzawadia ngumi nzito ya tumbo iliyomfanya kijana huyo agugumie kwa maumivu huku mikono yake ikilishikilia tumbo lake huku akirudi nyuma akiwa ameukunja mwili wake kama mgonjwa wa tumbo la kuhara, kitendo hicho kiliufanya uso wake kuwa mbele huku mwili wote ukiwa nyuma, bila kuchelewa Hemedy alipeleka tena ngumi kwenye uso huo chini ya kidevu na kumfanya uso wake kuinuliwa kwa ghafla kwa msukumo wa hiyo ngumi. Ngumi hiyo inaitwa ‘kata funua’ Mnama alirudi nyuma na kwenda kutafuta sehemu ya kukaa, alighairisha kabisa mpambano huo baada kuona anaweza akajeruhiwa au kuvunjwa kiungo, hapo alipokuwa amekaa hakuelewa ashike tumbo au akishike kidevu chake, akabaki kuipa kazi mikono yote miwili, huu akiupeleka tumboni na huu akiupeleka kidevuni kwake, alikaa hapo huku akitema damu huku akijutia kitendo cha yeye kujiingiza kwenye ugomvi ambao hata kama Babel angefanikiwa kumpata huyo mwanamke anaemgombania, basi yeye asingefaidika kwa chochote kile, labda kama angefaidika kumuita mwanamke huyo shemeji tu.
Shebe alikuja kwa kasi kuja kumvaa Hemedy na kumshushia ngumi zisizokuwa na idadi huku Ramah yeye akichezea kipigo kutoka kwa Babel. Dakika hiyo hiyo wanafunzi wa kiume walikuja wengi sehemu hiyo baada ya Lacho kwenda kuwaita waje kuamua huo ugomvi, walifanikiwa kuwaachanisha lakini Babel kama kawaida yake, wakati akiwa kashikiliwa na wanafunzi watatu wakimdhibiti asiende kule aliposhikiliwa Ramah, alitukana huku akidai achiliwe akamfunze adabu kijana huyo. Waliendelea kuwa katika hali hiyo hadi pale Hemedy na Ramah walipoondolewa Sehemu hiyo.
Kengele iligongwa kuashira kwamba mapumziko yamekwisha na muda huo wanafunzi wanatakiwa waende madarasani, ndipo kundi hilo la watu wanne lilipoondoka hapo kuelekea darasani huku wakimalumu Lacho kwanini ameenda kuwaita watu waje kuwaamulia.
Walipofika darasani kwao, walienda kukaa sehemu zao za nyuma kabisa ya darasa na kuanza kupanga mpango mwengine wa jinsi gani ya kuwakomesha mahasimu zao.
“Yani wale was**ge leo nilikuwa nataka niwauwe pale pale, sijui huyu Lacho katumwa na nani kwenda kuwaita wale maboya wengine waje kuamulia wakati mchezo ulikuwa tayari ushanoga” Babel alilalamika.
“Lakini jamaa huoni kama hapa ni shule, je kama angepita kiongozi yoyote au mwalimu, huoni kama ingekuwa soo upande wetu na wao, hapo tungeadhibiwa sana huku tukiulizwa tatizo nini hadi tukapigana, halafu tatizo lije kugundulika ni mwanamke ndie amesababisha tukapigana shuleni, huoni kama hiyo itakuwa ni aibu sana kwa wanafunzi wenzetu na hata kwa wazazi wetu?” Lacho aliongea.
“Majamaa, mimi kwenye hiyo mipango yenu naombeni mnitoe, siwezi kupigana kisa demu, tena demu mwenyewe hatokuwa na faida kwangu hata kama tukimpata. Aloo kama hakuna mpango mwengine zaidi ya kupigana basi mimi najitoa tu siwezi hicho kitu” huku akipeleka mkono wake kwenye meno yake ya chini. “Dah! yule boya kanipiga ngumi kali sana, utafikiri ni ngumi za kieletroniki vile jinsi zilivyoniacha na maumivu” Mnama aliongea hivyo na kupelekea wenzake wacheke kwa hiyo kauli yake ya mwisho.
“Mnama mimi pia nakuunga mkono, siwezi kupigana kisa demu wa mtu. Hemedy alinipiga teke la kifua hadi sasa kifua naona kinawaka moto ndani kwa ndani, yani nikitoka hapa moja kwa moja hadi Muhimbili nikapigwe X-ray, maana sio kwa teke lile, lile pushi kama nimegongwa na fuso la mchanga?” Shebe nae aliongea na kuwafanya wenzake wacheke sana.
“Kwenye mapambano tumekusaliti ndio, labda tupange mpango mwengine lakini sio kupigana, hujui tu ni maumivu kiasi gani ninayoyasikia kwenye tumbo langu kwa ile ngumi niliopigwa, yani jamaa kanifanya nihisi njaa ya ghalfa kama nimezaa pacha” Mnama aliongea hivyo na kuwafanya wenzake wacheke.
“Ila majamaa hata mimi pia sitaki tena kupigana, japokuwa tumewapiga sana ila nawao kuna sehemu zao wametuotea. Kama Ramah pale aliponipiga ngumi ya pua hadi sasa nahisi natakiwa nitumie mipira ya hewa ya oksjeni kuhemea nayo, na pale aliponipiga ngumi ya sikio, nilidhani kanipiga na nondo kama sio nyundo kabisa hadi sasa nasikia nyuki tu kwenye sikio langu wakivuma” Babel aliongea hivyo na kuwafanya wenzake wacheke. Ama kweli mabaya ndio yanayo chekwa, yani wao badala ya kuwa na hasira kwa kile walichofanyiwa, lakini ndio wanacheka kila wakikumbushiana kilicho wakumba.
“Sasa mimi subirini niwape mpango rahisi na mwepesi utakaofanya tumchukue yule demu” Lacho aliongea hivyo na kuwafanya wenzake wote wamuangalie yeye na kusubiri wasikie huo mpango atakao usema.
“Ili waachane wale watu inabidi tuwagombanishe, na kuwagombanisha huko ni kumtafuta mwanamke yoyote tutakae mpa hela ili tumfanyie mchezo Ramah ambao Hawa akiuona huo mchezo lazima atakasiraka na kuamua kuachana na yule jamaa. hiyo ndio njia rahisi na nzuri ya kumpata yule demu, lakini sio kwa kupigana, hivyo hatuwezi kumpata”Lacho aliongea.
“Huo mchezo ni upi?” Babel aliuliza.
“Tukishampata huyo demu, tutamuambia mchongo mzima halafu tutamtaka siku moja hapa hapa shule amuite Ramah kule nyuma ya majengo ya choo, afanye kila awezalo ili mradi waonekane kama vile kunakitu wanataka kukifanya, halafu wewe Babel kwa vile unamtaka yule Hawa, wewe ndie ambae utakaeenda kumchukua halafu utamuambia kuwa Ramah yupo nyuma ya majengo ya choo akifanya mapenzi na mwanamke mwengine, lazima tu atataka kwenda kushuhudia, sasa akifika pale halafu kweli akiona mazingira yapo kama vile ulivyomuambia, basi hapo ujue ndio itakuwa mwisho wa mapenzi yao na wewe utajichukukia mtoto kiulani kabisa” Lacho alimaliza kuongea.
“Dah!! Mwanangu bonge moja la plani hilo apo, sasa mchongo kumpata huyo mwanamke atakae fanya hivyo, mimi niko tayari kumpa pesa” Babel aliongea.
“Kuhusu mwanamke wa kufanya hivyo nyie wala msijali, kuna mwanamke mmoja anaitwa Shamsa, anasoma huko sayansi, yule demu alikuwa kila siku akiniambia kuwa nimfanyie mpango kwa Ramah akidai kuwa anampenda sana, ila mimi siwezi kumfanyia mchongo demu kumpata mwanaume mwenzangu, alikuwa akiniambia hivyo kipindi hicho mimi na Ramah zinaenda sana kabla haijatokea hii vita, sasa mimi nikawa namkwepa kila siku sitaki kumfikishia ujumbe jamaa. asa huyo demu tukimpa huu mchongo lazima tu atakubali kwasababu yeye mwenyewe pia anampenda jamaa” Shebe aliongea.
“Shamsa mwenyewe si ndio yule mwenye rangi flani hivi ‘blackbeuty’ halafu ana umbo moja matata sana?” Mnama aliuliza.
“Mnama undhani hapa ‘form three’ kuna Shamsa wangapi zaidi ya huyo huyo mmoja tu?” Shebe aliongea.
“Sikilizeni majamaa, kama kuna uwezekano huyo demu akaitwe basi tuje kumpa huo mchongo ili hiyo kazi aifanye haraka maana mimi namtaka yule demu hata sasa” Babel aliongea.
“Subirini wana mimi nikamuite” Shebe aliongea hivyo na kutoka hapo darasani, baada ya dakika tatu alirudi akiwa ameongozana na mwanamke mmoja ambae alikuwa ni mzuri kupita kawaida, alikuwa na umbo matata lililoenda hewani, sura yake nyembamba mithili ya wasomali ili mfanya azidi kuonekana ni mzuri kwenye macho ya wanaojua ku‘point’ watoto wazuri, alikuwa na rangi nyeusi isiyotisha, rangi yake ilikuwa ni mithili ya ‘chocolate’. Alitembea kwa mwendo wa madaha kuja huko nyuma ya darasa utafikiri ni mwenye kulazimishwa kutembea, alipofika akawasalimia na kukaribishwa kwenye kiti, muda wote huo Babel alikuwa akimtazama sana mwanamke huyo.
“Sasa wanangu mtoto mwenyewe huyu hapa” Shebe aliongea hivyo huku na yeye akikaa kwenye kiti chengine. Walimuambia mpango mzima utakavyoenda na kumuuliza yupo tayari kwa hiyo kazi, binti nae bila ajizi alikubali kuifanya hiyo kwasababu hata yeye ni mwenye kumpenda sasa huyo kijana.
“Ok, unataka kiasi gani kuifanya hii kazi?” Babel alimuuliza.
“Wala sitaki hela kwasababu hata mimi nampenda sana Ramah, na hivyo mlivyoniambia kwamba anatoka na Hawa, moyo wangu umeniuma sana. mi niko tayari kuifanya hiyo kazi ili mradi nimpate Ramah” Shamsa alisema.
“Safi. Hii ishu wewe utaifanya lini maana mimi nataka kuwa na yule mwanamke hata leo” Babel aliongea.
“Kama ambavyo wewe unataka kuwa na huyo mwanamke, ndivyo na mimi ambavyo nataka hata sasa kuwa na Ramah. Nipo tayari kuifanya hii ishu hata leo” Shamsa aliongea.
“Kwa leo haitowezekana, tufanyeni kesho” Shebe alitoa wazo.
“Pia hakuna tatizo” Shamsa aliongea na kutaka kuondoka hapo akidai kuna kazi anataka kwenda kuimalizia darasani, wakamruhusu akaondoka, ila macho ya Babel yote yalikuwa kwa huyo binti hadi anapotelea mlangoni.
“Mzee vipi, mbona unamuangalia sana yule demu” Shebe aliongea hivyo huku akitabasamu.
“Dah! Mwanangu huyu mtoto ni mgeni au? Maana ndio kwanza leo namuona” Babel aliongea.
“Duh! Jamaa wewe ni mzee wa totozi sana, lakini nashangaa ukiniambia eti humjui huyu mtoto, huyu mbona tumeanza nae hapa hapa tangia ‘form one’?” Shebe aliongea.
“Nikimalizana na Hawa, naruka na huyu” Babel aliongea hivyo huku akikuna kidevu chake kilichoanza kuota ndevu.
* *
Majira ya usiku Hilda alikuwa chumbani kwa Hemedy, walikuwa wakiongea huku wakikumbatiana kumbatiana, muda huo ulikuwa ni muda ambao Anti yao alikuwa amejipumzisha chumbani kwake akiisaka kesho yake. Kumbatiana hiyo ilipelekea wahisi hali ya utofauti kwenye miili yao, wakataka kufanya kile ambacho hawakuwahi kukifanya kabla. Sijui walitaka kufanya nini, ila walionekana wakigaragazana juu ya kitanda huku Hemedy akionekana ndio mchokozi zaidi kwa mwenzake.
“Hapana Hemedy, mi naogopa sijawahi kufanya” Hilda aliongea hivyo huku akim‘push’ Hemedy aliekuwa kamlalia kwa juu.
“Hata mimi naogopa wala pia sijawahi kufanya, lakini leo tufanye tu” Hemedy aliongea kwa masikitiko utafikiri alichotaka kufanya kilikuwa ni sahihi kukifanya.
“Hapana bwana mimi naogopa, tutafanya siku nyengine” Hilda aliongea hivyo huku akinyanyuka hapo kitandani na kutoka chumbani humo, akimuacha Hemedy akimuangalia kwa macho ya ‘mbona umeniacha, umeniacha na nini, embu rudi tufanye kwa mara moja tu’. Hemedy akabaki ametahayari, akajilaza kitandani huku mikono yake akiinyoosha huku na huko huku uso wake ukiangalia dari ya hiyo nyumba, akatabasamu na kufumba macho yake.
* * * *
Siku iliyofuata ndio siku iliyopangwa kuwagombanisha Ramah na Hawa kwa staili ya kufumania fumanizi la kupangwa. Siku hii asubuhi hakukuwa na mwalimu alieingia darasani kutokana na walimu wote kuwa katika kikao cha shule kwenye ofisi ya walimu. Wanafunzi wasiopenda kujisomea walikuwa wapo nje ya madarasa wakiranda huku na huko ili maradi tu wasiwepo madarasani, muda huu ndio waliuona ni muda mzuri wa kufanya kile walichopanga.
Shamsa alitoka darasani kwake na kuenda darasa analosoma Ramah, alipofika alimuomba kijana huyo amfuate kuna jambo anataka kumuambia, Ramah bila kujua chochote, akafuatana na banati huyo hadi huko alipotakiwa kufika, ilimshangaza baada ya kumuona banati huyo akimpeleka uelekeo wa vilipo vyoo, ila hakutaka kujali sana akawa ni mwenye kufuata tu. Walipofika nyuma vyoo, hakumuelewa binti huyo ni kipi hasa anachokitaka, maana hakuwa na maneno yenye kueleweka, mara amuulize kuhusu masomo, mara amuulize alifaulu kwa kiwango kipi ‘form two’, mara amuulize anamalengo gani baadae, ili mradi tu kupoteza muda.
Babel baada ya kuona Ramah amepelekwa eneo la tukio, hakutaka kupoteza muda, pale pale alimuafuata Hawa na kumuita pembeni.
“Hawa nadhani leo ndio utaamini kwamba huyo unaemuona anakupende wala hakupendi, ila mimi unaeniona sikupendi ndio ninae kupenda” Babel aliongea.
“Babel nini, mbona sikuelewi unachokizungumza?” Hawa alimuuliza hivyo baada kuona hajamuelewa mtu huyo.
“Utanielewa pale utakapoenda kwenye majengo ya vyoo nyuma kule, nenda kashushudie mwenyewe kwa macho yako huyo unaemuona anakupenda anavyofanya” Babel aliongea na kumfanya Hawa roho yake kuenda mbio mbio asiamini kile alichokisikia. Masikini bila kujua kwamba huo ni mpango, akanza kutoka mbio mbio mahala hapo kuelekea huko alipoambiwa aende akashuhudie mwenyewe kwa macho yake.
Ramah baada ya kuona mwanamke huyo hamuelewi anachokizunguamza, akataka kuondoka mahala hapo kuenda zake, ila alijikuta akivutwa shati kwa mbele na kumfanya Ramah akose stamina, bila kupenda akaenda kumkumbatia huyo mwanamke, na muda huo huo ndio Hawa anafika mahala hapo na kushuhudia kile kilichoonekana na macho yake. Akabaki kuachama mdomo wake huku mkono wake wa kushoto ukiwa umeuziba mdomo huo, na mkono wa kulia ukiwa upo kifuani mwake sehemu ulipo moyo, bila kutarajia macho yake yalitoa machozi huku asiamini anachokiona hapo, akabaki kutikisa kichwa kushoto kwenda kulia na kulia kwenda kushoto, kisha akageuka nyuma na kuanza kukimbia kuondoka mahala hapo.
HAWA kukimbia kwake alienda kuishia nyuma ya madarasa, alipofika huko, akaegemea ukuta na kushuka nao taratibu mithili ya maji yamwagiwavyo ukutani. Alipofika chini kabisa, akaikunja miguu yake, mikono yake akaiweka juu ya magoti huku kichwa chake akikiweka juu ya mikono. Kitendo hicho kilichagizwa na kilio cha kwikwi huku macho yake yakimwaga machozi mithili ya mbomba la mvua, akawa analia huku akiijutia nasfi yake kumkabidhi moyo wake mtu asiekuwa muaminifu kwake kama alivyoaminishwa na macho yake.
Ramah alimuona vizuri Hawa alipokuja hapo, ila kujinasua kwenye kumbato hilo la ghafla ndio ikawa hawezi, maana kitendo hicho kilikuwa ni cha kushtukiza sana. Ramah baada ya kuona amefumaniwa kwa kitendo ambacho si cha kweli kwenye macho ya mchunguzi, ila kwa macho ya Hawa ni lazima aone ni cha kweli tena cha makusudi kabisa. Akataka kuondoka tena amuwahi Hawa huko alikokimbilia, ila alijikuta akivutwa tena shati lake, safari hii alivutiwa kwa nyuma baada ya kuwa ameshapiga hatua mbili. Aligeuka na kofi lililoenda sambamba kwenge shavu la binti huyo na kumfanya aliachie haraka shati la Ramah na mkono wake mmoja kuupeleka kwenye shavu hilo huku mwengine akiupeleka kuyaziba macho yake, akawa analia chini chini, akitegemea kuombwa msamaha kama si kubembelezwa kabisa kwa hicho alichofanyiwa, alilia kwa dakika nzima ila hakuona mrejesho wa aina yoyote, ikambidi afumbue macho kumuangalia kijana huyo. Alaaa!! Ramah hakuwepo mahala hapo, akaangalia huku na huko kumtafuta kwa macho lakini hakuihisi hata harufu yake mahala hapo. Akabaki akijiuliza, inamaana Ramah hajui kwamba amenipiga kofi na inahitajika animbembeleze?….
Ramah baada ya kuondoka kwa banati yule aliemfanyia mchezo wa kuigiza, alikimbilia kumtafuta Hawa, akaenda darasani kwao kumuangalia, ila hakumkuta, akaenda darasani kwake nako pia hakumkuta, ikabidi aingie madarasa ya ‘form three’ yote, nako pia hakumkuta, akachoka, hakujua binti huyo amekimbilia wapi. Kuna wazo likamjia kuwa mtu akiwa na mawazo sana au kama akiwa na jambo linalomsibu, basi hawezi kukaa sehemu yenye watu wengi, ni lazima atatafufa sehemu iliyotulivu na kukaa hapo kufikiria ni jinsi gani atalitatua hilo jambo linalomsibu. Alipofikiria hivyo, akapata wazo la kumtafuta sehemu zilizojificha, katika tafuta yake, akaenda nyuma ya madarasa, huko alimuona binti akiwa amechuchumaa kama sio kukaa kabisa nyuma ya ukuta akiwa ameuigamia, alimsogelea mpaka pale baada ya kujua kuwa yule anaemtafuta ndie huyo mwenyewe.
“Siwezi kuyalaumu macho yako kwa kile yalichokiona, bali nitaulamu ubongo wako kupokea picha iliyotoka kwenye macho yako bila kuitafsiri kuihakiki kwa kile kilichoonekana. Hawa tambua ule ni mpango, mpango ambao unataka kutuachanisha mimi na wewe kwenye mapenzi yetu, kumbuka nilipokuambia tuwe kama mmea wa mnazi na wewe ukakubali tuwe namna hiyo. Sasa ni vipi umekuja kutetereshwa na jambo dogo namna hii? tena jambo lenyewe wala si kweli na halina uhakika kabisa kwenye fikra zako. Hawa kumbuka nilipokuambia kuwa katika ulimwengu huu hakuna mwanaume yoyote anaekupenda zaidi yangu tukimtoa baba yako, na ndivyo ilivyo kwenye moyo wangu hakuna mwanamke mwengine zaidi yako Hawa. Jua kwamba zile ni hila tu za wasiotaka mapenzi yetu yaendelee” Ramah aliongea hivyo baada ya kumfikia karibu.
Akainua kichwa na kumuangalia“Unasema sina uhakika na nilichokiona? Unasema ubongo wangu hauja kifikiria nilichokiona? Baada ya kunifanyia ule ushenzi unaona sasa uje kunitukana kabisa si ndio?” akainuka na kumuangalia Ramah huku uso wake ukipambwa kwa machozi. “Ramah tambua mimi sio mtoto mdogo, tambua kwamba mimi ni mtu mzima na nina akili zangu timamu. Ramah kwanini umefanya nijione mwenye hatia kwa kukukabidhi moyo wangu? Kwanini umeifanya nafsi yangu iulaumu moyo wangu kwa kukupenda wewe? Kumbe Ramah yale maneno yote uliokuwa ukiniambia yalikuwa ni ya uongo? Siwezi kusema sitopenda tena kwasababu nitakuwa nimeudhulumu moyo wangu haki yake ya msingi, ila nitajutia kukupenda wewe ambae hukua na mapenzi ya kweli kwangu. Ramah kwanini umenifanya nikupende, kwaniniiiii” Hawa alikuwa akiongea maneno hayo huku akilia, aliondoka hapo aliposimama na kumpita Ramah karibu kabisa na yeye, alipofika nyuma kidogo na Ramah akageuka.
“Ramah uliniahidi hutoruhusu macho yangu yatoe machozi, ile ahadi yako leo ndio inajidhihirisha kwamba ni uongo tu ule uliokuwa ukiongea. Ramah najuta kukukabidhi moyo wangu, najuta kukupenda, najutia kuwa na wewe, jua kwamba kuanzia sasa sikupendi, sikuhitaji wala sina haja na wewe. Nakuomba usinifuate, usinisogelee, wala usiniguse. Sikupendi na nina KUCHUKIA Ramah” Hawa alipoongea hivyo, akaondoka hapo huku akijaribu kushindana na mchozi yaliokuwa yakitoka kwenye macho yake kwa kuyafuta na mkono wake. Ramah akabaki kutumbua macho kama ameona wanyama aina ya paka wakifanya mapenzi hadharani.
Hakujua afanye nini ili amrudishie mnyange huyo imani na yeye, akabaki kusimama hapo bila ya kuwa na cha maana kufanya, baada ya kusimama kwa muda kidogo hapo, akaondoka huku kichwa chake akikitwisha mikono yake, akaenda darasani kwao na kutulia kwenye kiti chake. Hemedy hali hiyo aliyoingia nayo rafiki yake hakuiyelewa, ikambidi aondoke hapo alipokuwa amekaa na Hilda kumfuata pale alipokuwa Ramah.
“Kaka vipi mbona katika hali hiyo tena, unanini?” Hemedy alimuuliza huku na yeye akikaa kwenye kiti.
“Hawa kaka, tumeachana” Ramah aliongea kwa huzuni na masikitiko, ni dhahiri kwamba alikuwa akishindana kiume na machozi yanayotaka kumtoka muda wowote kwenye macho yake.
“Kaka embu nifafanulie, sijakuelewa kabisa, mmeachana kivipi?” Hemedy aliongea hivyo huku akivuta kiti karibu kabisa na alipo Ramah. Ikambidi Ramah amuhadithie kila kitu kilichotokea.
“Dah! Ila naamini ni hasira tu zile, akiwa sawa ukimfuata tena atakuelewa tu” Hemedy alimpa moyo mwenzake.
“Hawezi tena kunielewa yule, kaniambia nisijaribu hata kumsogelea, tena kilichoniuma zadi aliponiambia kwamba ananichukia. Hemedy sio siri ndugu yangu, roho inaniuma sana kuona Hawa amekubali maneno ya kuambiwa na kushuhudia kile kisichokuwa kweli na kukiamnini moja kwa moja. Hawa hanipendi tena mimi. Hawa ananichukia mimi, aagh!!” Ramah alishindwa kuyazuia machozi yake yasimtoke kwenye macho yake, ikambidi alaze kichwa chake kwenye meza yake na kulia chini chini, Hemedy alimfariji kwa kumuambia kuwa ataenda kuongea nae, anaamini maneno yale ameyaongea kwasababu ya hasira tu. Hilda nae alikuja baada ya kuwashuhudia watu hao wakiwa katika hali hiyo, alipokuja na yeye akaambiwa kila kitu, hata yeye pia alimuonea huruma sana Ramah kwa kile kilichomkuta. Ila yote kwa yote wa kulaumiwa ni Ramah, kama angemuambia Hawa tangu mwanzo vitendo na maneno aliyoambiwa na Babel, naamini ingekuwa ni kazi rahisi sana ya kumuelewasha Hawa hata kama angekuwa na hasira kwa kile alichokiona. Ila sijui tuseme usilolijua ama ni uzembe, ndio kitu kilichomkuta Ramah hadi sasa analia na moyo wake.
* * * *
Siku zilipita na sasa ikawa imepita wiki tangu Ramah asiwe na maelewano mazuri na Hawa. Kipindi hichi Hawa alionekana akiwa karibu zaidi na Babel, tena walionekana ni wapenzi kama wa muda mrefu kwa jinsi walivyo. Hawa alipelekwa kila sehemu aitakayo na huyo kijana, alipelekwa sehemu nyingi za kujidai, alikula kila anachokitaka, hata wakiwa shule pia walionekana pamoja. Haikujilikana Hawa alikuwa na Babel ili kuyapoza machungu aliyopewa na Ramah au alifanya hivyo ili kumuumiza moyo Ramah. Na kama ni hivyo basi alifanikiwa kwa asilimia zote maana kijana huyo alikuwa na machungu kila akiwaona, faraja yake ikawa ni Hemedy na Hilda pindi aliapo, kuna muda alitamani hata kuacha shule kwajinsi anavyoumia.
“Hemedy acha tu niache shule, siwezi kuvumilia kuwaona wakipita karibu yangu, tena wakionekana wakifanya makusudi kabisa”
Ramah siku moja aligoma kabisa kutoka kwenda kula ulipofika wakati wa mapumziko baada ya kuwaona Hawa na Babel wakipita nje ya darasa lao, ikambidi Hemedy amlazimishe sana waende kula, lakini alikataa katakata na kumfanya Hemedy akose namna nyengine na kuamua na yeye akae tu hapo hapo na rafiki yake.
* *
Siku moja darasani kwao darasa la sanaa, walichanganywa na darasa la biashara alilokuwa akisoma Hawa na kundi la Babel na mwalima wa soma la uraia ‘Civics’ walifundishwa wote kutokana na vipindi hivyo kufanana madarasa hayo mawili, ikambidi mwalimu huyo awachanganye wote pamoja na kuwafundisha somo hilo, baada ya kuwafundisha hadi pale alipoona panatosha kwa siku hiyo, akaamua kubadilisha mada.
“Wiki chache zijazo kidato cha nne watafanya mtihani wao wa kumaliza elimu ya sekondari, baada ya mitihani hiyo kuisha kutakuwa na sherehe ya kuwaaga wanafunzi hao shuleni hapa ambayo itafanyika hapa hapa kwenye ukumbi wa shule, nimezunguka madarasa ya kidato cha kwanza na cha pili kutafuta wanafunzi ambao siku hiyo watatoa burudani ya aina yoyote ile ili mradi isivunje maadili ya shule” alipofika hapo, akatulia kidogo na kuwaangalia wanafunzi hao waliokuwa kimya wakimsikiliza yeye. Wanafunzi na burudani tena!! “Huko nimepata wanafunzi waliojitolea kuigiza igizo ambalo wamelibuni wao wenyewe na wamenipa uhondo kidogo nimeona linaafaa kuigizwa mbele za watu. Sasa nipo hapa kujua na nyinyi mtataka kutoa burudani ya aina gani siku hiyo. Jamani, hiyo sherehe ni ya kwenu nyote japokuwa wahusika wakuu ni hao kidato cha nne, kwahiyo inabidi muwape ushirikiano ili nawao wajihisi walikuwa na thamani ya uwepo wao hapa shuleni kwetu. Kwahiyo nipo hapa kujua nani na nani atataka kutoa burudani siku hiyo, iwe ya kuigiza, kuimba, kuchekesha au hata kuonyesha kipaji chochote kile ambacho unacho” mwalimu huyo wa somo la uraia na akiwa wa michezo pia, aliongea na kusubiri majibu kutoka kwa hao wanafunzi.
Hemedy aliekuwa karibu na Ramah, alimgusa kidogo kumuashiria kuwa asimame. Ramah alikuwa na hofu uliochanganyikana na uoga wa kuimba mbele za watu wengi. Ni kweli kipaji cha kuimba alikuwa nacho tena kwa sauti nzuri tu, ila kipaji cha kuimba mbele za watu hakuwa nacho, ikabidi Hemedy amlazimishe sana kusimama, kutokana na heshima aliyokuwa nayo kwa rafiki yake, hakuwa na budi zaidi ya kusimama. Watu wote darasani walikuwa kimya wakimuangalia yeye aliesimama.
“Enhee! huyo ndio mwanaume bwana, sio nyie wengine mnaambiwa muonyeshe vipaji vyenu mnaogopa mtafikiri mmeambiwa msimame uchi mbele za wakwe zenu. Enhe! Ramah wewe unataka kutuonyesha kipaji gani siku hiyo?” Mwalimu aliongea na kuuliza.
“Kuimba” Ramah aliongea hivyo na kuwafanya wanafunzi darasani humo kucheka kutokana na alichokisema, wengi walimjua mtu huyo ni mwenye masihara mengi hata sehemu isiyo hitaji kitu hicho, hata hapo pia wakadhani ni masihara yake tu.
“Sasa mnacheka nini?” Mwalimu huyo aliongea kwa ghazabu huku akichapa fimbo yake juu ya meza iliyopo mbele ya wanafunzi wawili wa kike waliokaa kwenye kiti kimoja baada ya viti humo ndani kuisha kutokana na kuchanganywa madarasa mawili na kuwafanya wanafunzi hao kushtuka. “Nimemiambia muonyeshe vipaji vyenu, mnajifanya kudengua, mwenzenu kasimama nyie mnacheka. Waone kwanza vimeno vyao vibaya kama punje za mahindi” mwalimu huyo alipomalizia na hilo bezo, aliwafanya wanafunzi hao washindwe kujizuia kwa kucheka, ila safari hii walichekea chinichini wakihofia kudhibiwa na mwalimu huyo.
“Haya Ramah, embu imba kidogo tukusikie” mwalimu huyo aliongea hivyo na kumfanya Ramah kuanza kwa kujikohoza kidogo, kisha macho yake akayatupa sehemu alipokuwa amekaa Hawa na kuyarudusha mbele, kisha akaanza.
Sauti na tabasamu lako, ndio linafanya nikukumbuke. Kinachoniumiza mwenzako, unapolia chozi nsifute. Mapenze sidhaani mimi, kilichobaki ni uadui. Kuniona hutamani kwanini, kwenye maziwa nimegeuka tui. Nami nina mooyo, yapita siku nyingi sijakuona. Nami nina moyo mama, upate siku moja ujeniona. Nami nina moyoo, yapita siku nyingi sijakuona. Nami nina moyo mama, ungalisema neno moja ningepona. Mwenzako sura yangu, nitaiweka wapi, oooh sura yangu, nitaiweka wapi. Ama moyo wangu, nitauweka wapi, oooh moyo wangu, nitauweka wapi. ×2
Alipofika hapo, Hemedy ndio wakwanza kupiga makofi mengi huku wanafunzi wengine wakifuatia. Mwalimu alifurahi sana na kujikuta na yeye akipiga makofi baada ya wanafunzi kumaliza kupiga makofi, kitendo hicho kiliwafanya warudie tena kupiga makofi. Walikuwa na haki ya kufanya hivyo maana hawakuwa ni wenye kujua kuwa mwanafunzi huyo mwenzao kama alikuwa na kipaji hicho. Hawa macho yalimtoka asiamini alichokiona na kusikia hapo, hakuwahi kujua hata siku moja kuwa kijana huyo anakipaji hicho, tena kilicho pambwa na sauti yake nzuri mithili ya waimbaji wale wa ‘bend’ inayoongozwa na Justin Timbelake huko ulaya. Akajua moja kwa moja hata kama Ramah alionyeasha kipaji chake, lakini pia hiyo nyimbo ilikuwa ni dongo kwake. ni kweli Ramah aliimba nyimbo hiyo kwajili yake, ndio maana akabadilisha baadhi ya maneno kwenye ‘verse’ ya hiyo nyimbo aliyoiimba. Nyimbo hiyo ilikuwa ni ya msanii mmoja maarufu hapa nchini anaejulikana kwa jina la Richard Mavoko alieimba na kijana mmoja kutokea Nigeria alieitwa Patoranking, wimbo huo uliitwa ‘Rudi’.
“Safi sana Ramah, naamini sio mimi tu hata hawa wanafunzi wenzako hawakujua kwamba unakipaji hicho ndio maana mwanzo wakacheka uliposema unaimba, ila baada ya kuwaimbia wenyewe wamekubali na kukupigia makofi. Ok kuna mwengine ambae atatuimbia?”
Mwalimu baada ya kumsifia Ramah, aliwauliza tena wanafunzi swali hilo na kumfanya binti mmoja kutoka darasa la biashara kusimama, na yeye akapewa ruhusa, akaimba kwa sauti nzuri mno na kuwafanya wanafunzi wenzake wampigie makofi baada ya kumaliza kuimba. Mwalimu aliuliza kama kuna mwengine, ila kimya ndicho kilichomjibu kuwa hakukuwa na mwengine mwenye kipaji cha kuimba. Akaomba wasimame wengine wenye vipaji tofauti na hicho na kusimama wanafunzi wawili ambao hawa walikuwa ni mapacha wanaofanana kwa kila kitu, walikuwa ni wakiume na waliotoka kwenye darasa la biashara. Wanafunzi hao waliposimama, vicheko na shangwe ndivyo vitu vilivyosikika kwa wanafunzi wengine. Mapacha hao walijulikana kuwa wachekeshaji. Wanafunzi wa darasa la sanaa, walipiga kelele kwa kumtaka Hemedy ainuke aungane na hao wenzake, na yeye hakuwa na jinsi, akaiunka huku wanafuzi wakiendelea kupiga mbinja na makofi.
Mapacha hao na Hemedy wao walichukua nafasi ya kuchekesha hiyo siku ya sherehe huku Ramah na huyo binti wakichukua nafasi ya kuimba. Mwalimu huyo aliwaomba waongozane wote kuelekea kwenye ofisi yake kwajili ya kuwapa utaratibu kabla siku ya sherehe haijafika.
“Kumbe Ramah anajua kuimba kiasi kile?” hiyo ilikuwa ni sauti ya mwanafunzi mmoja wa kike akiongea pekeake baada ya vijana hao kuongozana na mwalimu.
Majira ya usiku nyumbani kwakina Hilda. Baada ya kumaliza kula, Anti yao aliwaaga na kwenda kulala huku akiwaacha vijana hao wakiangalia luninga iliyokuwa hapo sebuleni. Hemedy nae alimuaga Hilda na kuingia chumbani kwake kwajili ya kwenda kulala na yeye, alipofika, akavua nguo na kubakiwa na bukta tu, akaingia chooni, choo ambacho kilikuwa humo humo chumbani, alipotoka huko alikuwa akijifuta maji kuashiria alitoka kuoga. Ila ghalfa aliganda kama anataka kupigwa picha baada ya kumuona Hilda akiwa kitandani kwake amekaa huku akimuangalia yeye kwa tabasamu pana usoni mwake.
“Wewee! Umefuata nini chumbani kwangu?” Hemedy alimuuliza huku akiwa bado ameganda vile vile na taulo lake mkononi.
“Mbona muoga hivyo? Embu njoo tulale bwana” Hilda aliongea hivyo huku Akitabasamu, akajilaza kitandani na kumfanya Hemedy akose cha kusema, akapiga hatua na kuiendea henga, kisha akaliweka taulo juu yake na kubakiwa na bukta na kwenda kitandani alipolala Hilda, akamuangalia kwa muda, kisha na yeye akajiweka juu ya kitanda hicho, wakawa wanaangaliana bila kujua ni kipi kinachowafanya waangaliane hivyo.
Katika kuangaliana hiyo, ikapekea hisia flani ziwakumbe kwenye miili yao na kujikuta wakianza kushikana shikana baada ya kusogeleana. Walifanya hivyo hadi pale Hemedy alipo panda juu ya banati huyo na kujikuta akitaka kufanya kitu ambacho sio akili yake iliyomtuma kufanya hivyo, alianza kutalii kwenye mwili wa binti hadi alipofika sehemu ambayo binti hakuruhusu kirahisi Hemedy ainyemelee. Nilipoona hivyo, nikageuza macho yangu kuangalia pembeni huku nikiwaacha wenyewe wakiendelea kuminyana, huyu akitaka kufanya kitu falani na huyu akikataa kitu hicho kisifanyike.
Baada ya dakika thelathini, nikageuka kule walipo baada ya kusikia sauti ya kilio cha Hilda, hapo nilishuhudia mashuka yakiwa yamepambwa kwa damu huku Hilda akiwa analia ameegamia kwenye ukuta ambao umeachiana na kitanda kwa milimita moja, akiwa amejifunika shuka kuanzia kwenye kifua kuja chini.
“Hemedy ndio umenifanya nini hivi? Kumbe unaroho mbaya kiasi hichi? Hujui kama mwenzako nilikuwa naumia? Haya ona sasa umenitoa ushichana wangu bila ridhaa yangu, umenimwaga damu yangu pasi na huruma halafu eti unajifanya unanipenda. muongo hunipendi wewe hihihiiii”Haa!! Ilishangaza Hilda kusema eti ametolewa usichana wake bila ridhaa yake, kama ni hivyo, sasa ni kipi kilichomfanya hadi akataka kulala kitanda kimoja na rijali Hemedy, sijui alitaka wachekeane tu hapo kama matahira? Aaa!! Lakini hayakuwa yakinihusu hayo.
“Hilda nisamehe, sikujua kama nitakuumiza kiasi hichi, hayakuwa malengo yangu kukutoa damu kiasi hichi” Hemedy aliongea hivyo huku akiwa amekunja mikono yake ishara ya kuomba msamaha. Wakati huo alikuwa amekaa mwisho kwenye ukingo wa kitanda huku mguu mmoja akiwa ameuning’iniza chini huku mwengine ukiwa juu ya kitanda akiwa ameukunja.
“Muongo, muongo Hemedy. Mimi si nilikuambia kuwa unaniumiza lakini wewe ukajifanya hunisikii. Haya sasa umenisababishia tatizo ambalo sijui pia nitalisovu vipi” Hilda aliongea huku akiwa anaendelea kulia, ila safari hii hakuwa akilia kama mwanzo, sasa hivi alikuwa akilia kilio cha chini chini.
“Tatizo gani hilo?” Hemedy aliuliza kwa wahka.
“Leo nipo katika siku za hatari Hemedy!” La haula!! Hemedy macho yalimtoka pima mithili ya mtu aliekutana na mala
“Leo nipo katika siku za hatari Hemedy!” Hemedy macho yalimtoka pima mithili ya mtu aliekutana na malaika mtoa roho uso kwa uso.
“La…la…lakini mimi sijamwagia ndani” Hemedy aliongea hivyo huku dhahiri akionekana akiwa na aibu ilichanganyikana na uoga.
“Hujamwagia ndani kitu gani……..? Sina nakuuliza?” Hilda aliongea kwa kufoka na kumfanya Hemedy akose cha kusema na kubaki kimya tu utafikiri hakusikia hilo swali aliloulizwa.
“Subiri tuone, kwani mwezi ni mbali, na sijui kama ikiwa hivyo itakuaje jamani. Ila yote umeyataka wewe Hemedy, sijui nitatembeaje masikini mimi. Hemedy umeniumiza sana yani” Hilda aliongea kwa malalamiko, ila muda huu hakuwa akilia.
Akamsogelea pale alipo“ Hilda kama ambavyo damu yako imemwagika mbele ya macho yangu, ndivyo ambavyo nitakavyo utunza upendo wangu kwako, sitoruhusu hata kwa sekunde utoe chozi lako eti kisa nimekuacha au nimekusaliti. Nakupenda Hilda na wewe huna haja ya kunijibu kwamba unanipenda pia, hii damu ambayo imetoka limelijibu hilo neno” Akamfuta machozi kwa kutumia vidole vyake kisha akampiga busu moja la kwenye paji la uso. Bilashaka Hilda yale maumivu yote aliyasahau hapo hapo, maana alikuwa ni mwenye kutabasamu tu baada ya kuyasikia maneno hayo.
“Nipishe huko niende zangu” Hilda aliongea hivyo, akajinyanyua hapo alipo huku akiwa bado ameshikilia shuka lisimdondoke mwilini mwake. Hemedy alikuwa akimuangalia tu muda wote huku akitabasamu.
“Fumba macho yako nivae nguo zangu. Lione linatabia mbaya tu kuchungulia wenzake” Hilda aliongea hivyo baada ya kushuka kitandani na kumuona Hemedy anamuangalia tu muda wote. Akageukia ukutani na kumfanya binti huyo aliachie shuka alilojiziba nalo na kuvaa nguo zake, baada ya hapo alianza kupiga hatua za kudema dema kama mtoto mdogo anaefundishwa kutembea huku akigugumia kwa sauti za puani. Sauti hizo zilimfanya Hemedy ageuke na kumkuta ndio anataka kufungua mlango wa kutoka.
“Sasa Hilda na haya mashuka je?” Hemedy aliongea hivyo huku akiyasontea mashuka kidole. Hilda akageuka na kumuangalia yeye.
“Yatandike halafu ulale hivyo hivyo” kisha akafungua mlango na kuondoka zake. Hemedy aliyatoa mashuka hayo na kuyaweka kwenye deli lake la nguo chafu, akachukua mengine na kuyatandika, kisha akajibwaga hapo kitandani chali. Ila ghafla alikurupuka baada ya kukumbuka kitendo alichotoka kukifanya muda mfupi, moja kwa moja akaelekea chooni.
* * * *
“Kwanini lakini unanichukia kwa kosa ambalo si la kweli? Hutaki hata kuniona kwa kosa la kupangwa ili mimi na wewe tuachane Hawa? Mwenzako najihisi furaha pale ninapokuona hata kama unanichukia. Hawa lile tukio usingelipa maamuzi ya papo kwa hapo bila hata ya kulifikiria na kuniuliza ilikuaje. hukutakiwa kuchukua maamuzi ya haraka namna ile, tena kwa kutaka kuniumiza, ukaamua ukaanzishe mapenzi na Babel kwa haraka ili tu nafsi yangu iume, nakupa pongezi kwa hilo kwasababu umefanikiwa kwa asilimia mia kuumiza moyo wangu dhaifu, nakupa hongera kwa kunifanya nitoe machozi kila mara ninapokufikiria, nakupa pongezi kwa kunifanya hata nisahau kula au kuoga pale inaponijia picha yako usoni kwangu. Laiti ungejua kwamba huyo ulieamua kuwa nae kwasasa hana nia nzuri na wewe, wallah usingejaribu hata kumuita jina lake achana na kuwa nae karibu tu. Hawa tambua hakuna mwanaume akupendae kwa dhati zaidi yangu mimi, hao wote wanataka kuuchezea tu moyo wako na kuuacha ukibubujikwa na machozi ambayo kwangu itakuwa ni mfadhaiko mkubwa kwenye mtima wangu. Hawa naomba niwe muokozi wa moyo wako, naomba urudishe imani yako kwangu. Bado Nakupenda Hawa wangu” Ramah alikuwa akilalamika mbele ya mnyange huyo wakati wakiwa shule kwenye eneo la kutupa takataka asubuhi hiyo walipokutana wote wakiwa na vindoo vilivyokuwa na mataka baada ya kuyamwaga kwenye shimo.
“Ramah tambua kwamba mapenzi yetu yaliisha siku ile ile nilipokufumania ukiwa na yule mwanamke wako mkitaka kufanya uchafu wenu kule nyuma ya vyoo. Ramah umenifanya nilie zaidi yako wewe unaelia kilio cha kuigiza mbele yangu eti ukitegemea utairudisha imani yangu kwako, moyo wangu ni mgumu sana kumsamehe mtu alienitenda kimapenzi, nenda kawafuate hao hao wazindaki wenzako wamapenzi, hao ndio ambao utakao endana nao ila sio mimi tena” Hawa aliongea huku akimuangalia kijana huyo kwa nyodo huku mdomo wake akiwa ameupindisha mthili ya mgonjwa wa kifafa.
“Hawa tambua hujui ukijuacho, siku ukija kujua kuwa ukijuacho ulikuwa hukijui, utakuwa umeshachelewa, ila hata kama utakuwa umechelewa, basi tambua akupendae kwa dhati yupo na anakusubiri na kukukaribisha muda wowote” Ramah alipoongea hivyo, akaondoka huku akimuacha banati huyo akiyafikiria maneno hayo ya mwisho.
“Aaa!! Hana lolote kaishiwa na maneno” Aliongea mwenyewe kwa sauti ya chini na kuondoka hapo kuelekea huko anakotakiwa awe. Sio kwamba Hawa hakuwa akimpenda tena Ramah, la hasha! Bali alitaka na yeye apate maumivu kama yale aliyoyapata yeye kipindi anamfumania.
Hilda alijitahidi kumbembeleza rafiki yake aachane na Babel arudiane na Ramah huku akimkumbusha kuwa Babel ni pendapenda wala hana mapenzi ya kweli naye, ila yeye aling’ang’ania msimamo wake kuwa hatoweza kumsamehe Ramah kwa kile alichomfanyia.
“Lakini mboma Hilda unanilazimisha nirudiane na Ramah wakati amenitenda nikiwa naona kabisa?” Hawa alimuuiza hivyo Hilda wakati wakiwa kantini wakipata chakula.
“Wewe hujui Hawa, ule ulikuwa ni mchezo tu wa kuwaachanisha wewe na Ramah. Lakini hakuna ukweli wa aina yoyote kwa unachokifikiria” Hilda aliongea.
“Hilda wewe unasema hivyo kwa vile hujawaona walichokuwa wanafanya kule nyuma ya vyoo na yule mwanamke wake, naamini kama ingekuwa umeona wala usingethubutu kuniambia maneno hayo”
“Sikiliza Hawa nikuambie. Ule ulikuwa ni mpang…..” Hilda alikatishwa na sauti kali ya Hawa.
“Hawa tutagombana sasa hivi, maana naona unapenda unione nikilia kila muda. Ohooo, we endelea tu kuniambia hayo mambo” Hawa alionekana dhahiri akiwa amekasirishwa na maneno ya Hilda aliekuwa akimtaka aachane na Babel arudiane na Ramah.
“Mmh! Basi shosti tusije kugombana bure kwa mambo ambayo hayana ulazima kwangu” Hilda aliongea hivyo huku akijifuta mdomo wake kwa kitambara baada ya kumaliza kula. Wakachukuana kuondoka hapo kuelekea darasani.
* *
Siku hiyo Babel alimchukua Hawa na kwenda nae Mikadi Beach kwenda kufurahia nae. Ndio, alikuwa na haki ya kumfanyia binti huyo chochote anachokitaka ili mradi na yeye apate anachokitaka. Hakuanzia kwa binti huyu tu kufanya hivyo, bali ni kwakila binti ambae ataingia kwenye mikono yake, lazima amfanyie vitu vingi ilimradi apate kile anachokitaka kisha hapo amtelekeze na kumuacha akilia pekeake. Hiyo ndio ilikuwa tabia yake, yupo radhi apoteze kiasi kikubwa cha pesa lakini na yeye apate kile akitakacho. Na alikuwa na msemo wake kuwa akipita mara moja basi harudii tena. Kinachomtia ujeuri ni mali za baba yake ambae kwake alikuwa na mtoto huyo huyo mmoja tu, alikuwa akimpenda kupita maelezo, alimuachia gari atembelee nalo kila sehemu anayotaka kuenda na sio kumuachia gari tu, hata kiasi cha pesa atakachoomba pia hupewa.
Na siku hii alikuwa na Hawa kwenye ufukwe huo wakifurahia, sio kwamba alikuwa akimpenda sana mnyange huyo, laa! Alikuwa na lake aliatakalo na akishalipata basi humuacha akimlilia pasi na kumuonea huruma.
“Hawa unajua mimi nakupenda sana” Babel aliongea hivyo wakati wakiwa wamekaa kwenye viti katikakati yao pakiwa na meza iliyochafuliwa kwa vyakula na vinywaji mbalimbali.
“Najua baby kuwa unanipenda na ndio maana unafanya kila uwezalo ili kunifurahisha” Hawa aliongea hivyo huku aking’ata paja la kuku aliekaangwa kwa ustadi mkuu.
“Sasa kwanini wewe hunipendi?” Babel aliuliza swali liliomfanya Hawa aache kutafuna nyama hiyo na kumuangalia yeye.
“Kwanini?” Hawa alimuuliza.
“Kwasababu kila ninapokuambia tufanye mapenzi wewe unanizungusha” Haa!! Inamaana kufanya mapenzi ndio kipimo cha kumpenda mtu? Sio mimi tu nilie jiuliza hilo swali, hata Hawa na yeye pia alijiuliza lakini akakosa jibu sahihi la swali hilo.
“Baby wala usijali, ipo siku tu utakuwa na mimi kitanda kimoja” Hawa aliongea hivyo huku akiwa na mashaka na mtu huyo.
“We kila siku ni mtu wa kuniambia hivyo hivyo tu nisijali, hujui kama mwenzako nashindwa kuvumilia, sasa kama usiponipa wewe unadhani nani mwengine atanipa. acha zako bwana we kama hunipendi niambie” Babel aliongea kwa ghadhabu kiasi kwamba hata Hawa pia alishangaa, kisha akainuka hapo na kuanza kuondoka.
“Jamani mpenzi unaenda wapi sasa?” Hawa nae alipoongea hivyo, akachukua pochi yake iliyokuwa juu ya meza na kuondoka kumfuata mwanaume huyo anapoelekea huku wakiviacha vyakula vikiwa vingi juu ya meza.
* *
Siku zilipita na kidato cha nne wakamaliza kufanya mitihani yao, wakawa sasa wakijiandaa kusherekea mahafali yao siku moja inayofuata. Siku ya jumamosi ndio siku ambayo ilipangwa mahafali hayo, walikuwa na shamrashamra za maandalizi hayo. Wahenga hawakukosea kuusema ule msemo wa ‘siku hazigandi’ na nikweli siku hiyo haikuganda. Siku hiyo ikapita na kuingia siku iliyosubiriwa na wanafunzi wengi wa shule hiyo. Siku ya mahafali ya kidato cha nne.
Shamrashamra ziliendelea ndani ya ukumbi, wanafunzi walioteuliwa kwaajili ya kuhakikisha ukumbi unakuwa wa kupendeza, waliifanya kazi yao ipasavyo, hadi majira ya saa nane mchana, ikawa kila kitu kipo kama kilivyopangwa, ikawa unasubiriwa muda tu wa shuhuli hiyo kuanza na muda wenyewe ulikuwa ni saa kumi za jioni. Wanafunzi hao wakarudi nyumbani kwaajili ya kujiandaa ili muda utakapofika warudi wakiwa wamependeza.
Majira ya saa kumi, wanafunzi wengi walionekana wakiingia shuleni hapo wakiwa wamependeza kuliko kawaida, kila mmoja hakutaka kuwa nyuma siku hiyo kwa kutokelezea, kila mmoja alivaa vile alivyoona kuwa vitampendeza siku hiyo, hawakuwa wanafunzi tu, hata wazazi pia walihudhuria kwenye mahafali hayo. Wanafunzi waliowekwa kwaajili ya kuwapokea na kuwaelekeza sehemu inapofanyika sherehe hiyo, walikuwa wakipishana kuwapeleka wazazi sehemu husika.
Muda ulipofika, wanafunzi wote na wazazi walikaa sehemu iliyopangwa kwajili yao huku walimu na mgeni rasmi wakikaa sehemu yao. Mahafali yalianza kwa kusomwa sala fupi kisha ikafuatiwa na risala iliyosomwa na huyo huyo mwanafunzi. Baada ya hapo ratiba nyengine zikaendelea. Wanafunzi wa kidato cha nne walioyofanya vizuri kwenye mtihani uliopita kabla wa taifa, walipewa zawadi mbalimbali kulingana ufaulu wao.
Baada ya zoezi hilo lililochukua saa nzima kuisha. Ikafutia burudani zilizopangwa kutolewa na wanafunzi, walianza wao kidato cha nne kutoa burudani zao za mashari ya kuwaaga wenzao, kisha likafuatia igizo la vijana wa kidato cha pili na cha kwanza. Baada ya wao kutoka, wakafuatia mapacha nao wakawachekesha watu waliohudhuria hapo kwa nafasi yao, na wao wakamaliza na kuingia Hemedy. Wanafunzi wote walilipuka kwa shangwa na makofi yalichagizwa na vifijo na mbinja baada ya kijana huyo kupanda kwenye jukwaa.
Alipofika hapo, akakamata kipaza sauti na kuanza na salamu. Kisha akatoa hadithi iliyowafanya watu wazisahau kama sio kutozikumbuka kabisa shida zao na matatizo kwa kucheka kila anapoweka kituo. Hadithi hiyo ilichukua dakika kumi na tano akamaliza na kushuka kwenye jukwaa huku akisindikizwa na makofi ya pongezi.
Ilibakia burudani ya mwisho, burudani ya kuimba, walianza vijana wawili, wakaimba wote kwa pamoja na akafuatia na yule binti nae pia akaimba kisha akashuka baada ya kumaliza. Akawa bado Ramah kupanda kwenda kuimba. Akanyanyuka sehemu aliyokuwa amekaa na kuanza kupiga hatua kuelekea juu ya jukwaa. Wanafunzi waliokuwepo darasani siku ile wao ndio waliompigia makofi huku wengine wakishangwaza na kitendo hicho cha kusikia kuwa Ramah na yeye pia ni muimbaji. Alipofika juu ya jukwaa na yeye akatoa salamu kama walivyofanya wenzake kisha akaliweka koo lake sawa tayari kwa kuimba.
“Baby kama ujana yote nilokupa, tayari nilikupa moyo wangu ili ukae naoo. Leo upendo unanifanya nilie, machozi yafunga mboni zangu nashindwa kutazama. Pendo langu umelizima kamshumaa, umenidharau, umeninyima hata heshima. ×2. Kama wamekuambiaa, mi nakuzinguaa, amini na siku moja ukweli utaujua. Hutofurahiaa, penzi bandiaa, lakweli lipo kwangu na we hujaridhiaaa aaaa.
Bado naamini, nitakuwa na wewee, japo thamini, ila chagua langu wee. Bado naamini, nitakuwa na wewe, japo thamini, ila nitakuwa na wewee, one day.
Kama ni kosa mi kukupenda wewe semaga unanichukiaaa, marafiki wanasemaga, alifichiki pendo mamiyoo, nikikuona mwenzioo, najawa na furaha nakufikiria sanaa aaaa. Pendo langu umelizima kamshumaa, umenidharau, umeninyima hata heshima. ×2. Kama wamekuambiaa, mi nakuzinguaa, amini na siku moja ukweli utaujua. Hutofurahiaa, penzi bandiaa, lakweli lipo kwangu na we hujaridhiaaa aaaa.
Bado naamini, nitakuwa na wewee, japo thamini, ila chagua langu wee. Bado naamini, nitakuwa na wewe, japo thamini, ila nitakuwa na wewee, one day”.
Ramah aiimba kwa ustadi mkubwa na kwa hisia kali sana, akifuatisha biti ya nyimbo hiyo iliyowekwa kwenye muziki uliokuwa humo ndani ya ukumbi. Watu wote walimpigia makofi huku wengine wakidiriki kwenda kumtunza kabisa kwa jinsi alivyoiimba nyimbo hiyo ya msanii maarufu hapa nchini anaeitwa Ibrahnation nyimbo hiyo aliita NAAMINI. Ilikuwa ni nyimbo nzuri iliyowafanya watu wanaoijua kuenda nae sawa wakati akiwa akiimba huku wakitingisha vichwa taratibu kwenda kulia na kushoto.
Watu wote walilipuka kwa shangwa huku wakimpigia makofi wakati akiwa anashuka. Akaitwa na mgeni rasmi na kuenda kupeana nae mkono huku wakipiga picha ya pomoja, hapo akapeana mikono na walimu wote waliokuwa kwenye meza hiyo huku wakipambwa na matabasamu usoni mwao, kisha akarudi sehemu alipokuwa amekaa yeye Hemedy na Hilda.
Hawa nyimbo hiyo ilimfanya aingiwe na ubaridi wa ghafla mwilimi mwake, kwa mara ya kwanza alijutia uamuzi wake wa kuachana na kijana huyo. Sio kwamba eti kwavile alikuwa na kipaji cha kuimba ama kwavile alipongezwa na watu wote hapo ukumbini? Laa hasha! Bali ni kutokana na mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo kwa kijana huyo, aliamua kuachana nae ili tu na yeye apate maumivu kama aliyoyapata yeye wakati akiwa anamfumania.
Kama wamekuambiaa, mi nakuzinguaa, amini na siku moja ukweli utaujua. Hutofurahiaa, penzi bandiaa, lakweli lipo kwangu na we hujaridhiaaa aaaa……..
Maneno hayo kwenye hiyo nyimbo aliyoiimbaa Ramah, yalijirudia kwenye ubongo wake na kumfanya moyo wake uzidi kumuuma.
Kama ni kosa mi kukupenda wewe semaga, unanichukiaaa, marafiki wanasemaga, alifichiki pendo mamiyoo, nikikuona mwenzioo, najawa na furaha nakufikiria sanaa aaaa.
Alipo yakumbuka na maneno hayo, akashindwa kuvumilia kukaa hapo ndani, akatoka nje ya ukumbi mbio mbio huku akiwa ameweka kitambara chake usoni ili kuyazuia machozi yanayomtoka yasionekana na watu wengine. Babel nae baada ya kumuona Hawa ametoka nje akiwa kwenye hali hiyo na yeye akatoka kumfuata huko huko.
ENDELEA
“VIPI MPENZI, mboma umetoka ukumbini haraka namna hii huku unalia? Au ni yule boya ndi…..” Babel alimfuata Hawa aliekuwa yupo nje ya ukumbi kwenye mti ameuigamia. Ila alikatishwa na sauti kali ya Hawa.
“Niache usinishike. Nani mpenzi wako?” Hawa aliongea kwa hasira na kumfanya kijana huyo amshangae sana.
“Nini Hawa kimekukuta? Mbona sikuelewi?” Babel aliongea huku akijaribu kumshika mkono, ila mkono wake ulipangulia kwa hasira.
“Nimekuambia usiniguse. Kahaba wa kiume wewe” Hawa aliongea hivyo na kumfanya Babel ashikwe na hasira za ghafla kwa kutukanwa tusi hilo na mwanamke huyo. Akainua kono lake la kushoto na kulivutia kasi kutaka kulipeleka kwenye shavu la mnyange huyo, ila kono lake liliishia kati baada ya kuzuia na mtu alietokea hapo ghafla.
“Mmh mmh!! Umeona wapi mwanamke akapigwa namna hii? We kama hakutaki usimlazimishe, nenda kawapige hao hao makahaba wenzako uliozoea kuwapiga lakini sio huyu” Hemedy ndie aliezuia kono la Babel lisitue kwenye shavu la Hawa. Aliongea hivyo huku akilirusha kwa pembeni kono hilo. Kitendo hicho Babel alikitasfiri ni dharau kama sio udhalilishaji mbele ya mwanamke.
Hemedy alimfuata Hawa aliekuwa yupo pembeni akilia na kumyanyua. Babel alishindwa kuzizuia hasira zake, akataka kwenda kumvaa pale pale alipo Hemedy, ila alijikuta akizuiwa na kundi la wenzake lililokuwa limefika hapo baada ya kumuona mwenzao ametoka nje kumfuata Hawa huku Hemedy nae akitoka nje. Wakajua tu huko hakutakuwa na usalama kama ikiwa na Hemedy ametoka nje, ikabidi na wao watoke.
Babel alikuwa aking’ang’ania kuchomoka kwenda kumvaa Hemedy kwenye mikono ya wenzake waliomshika barabara huku wakimsihi atulize munkari maana walimjua kijana huyo hakawii kufanya fujo sehemu yoyote ile.
Hemedy baada ya kufanikiwa kumnyamazisha Hawa aliekuwa akilia muda wote. Alimuongoza kuingia nae ndani ya ukumbi, alimpeleka hadi kwenye meza waliyokuwa wamekaa wao watatu na kumuunganisha na yeye akawa wanne. Kipindi chote hicho, Ramah wala hakuwa na habari nae, alikuwa akichezea simu tu hakuangalia sehemu yoyote, hata pale Hawa alipotoa salamu, yeye alijifanya kutoisikia salamu hiyo. Alikuwa ‘busy’ na simu yake.
Hawa akawa hana raha hata tangu afike hapo, japokuwa Hemedy na Hilda wajitahidi kumsemesha na kumfurahisha, lakini kama alikuwa akitabasamu, basi hazizidi hata sekunde tano anakuwa amenyamaza na kuwa vile vile uso wa mashaka. Walijitahidi kuongea stori ambazo walimshirikisha na Ramah, lakini yeye alikuwa akiwajibu kwa kichwa tu na kuendelea na kucheza na simu yake. Hawakuwa na jinsi zaidi ya kutulia na kuendelea kuangalia shuhuli inavyoendelea. Wanafunzi wengi hasa wa kike walikuja wakitaka picha na Ramah na yeye alipiga nao bila ajizi, kitendo hicho kilimuuma sana Hawa, akatamani angekuwa na uwezo wa kuwakataza watu hao wasipige na Ramah picha, lakini angeanzia wapi ikiwa yeye na huyo kijana wamenuniana? Asingeweza kamwe!.
Tena kibaya zaidi alipokuja Shamsa kupiga picha nae, hapo nafsi ilizidi kumuuma huku akimkata jicho kali huyo binti. Ukafika muda wa chakula, watu wote walienda kuchukua chakula na kuenda kukaa kwenye meza zao wakiendelea kula. Ramah hakutaka hata kuinuka hapo alipokaa, ikambidi Hemedy ndio afanye kazi ya kumletea chakula Rafiki yake maana alijua dhahiri amechukizwa na kitendo cha yeye kumleta Hawa kwenye meza yao, lakini yeye lengo lake halikuwa baya, alichotaka yeye ni kuwafanya watu hao wawe karibu tena.
Baada ya kumaliza kula, mgeni rasmi aliondoka, na muda huo ukawa ni muda wa kucheza muziki kuimalizia sherehe hiyo. Wanafunzi waliinuka na kuanza kucheza vile ambavyo kila mmoja ametaka kucheza, wengine walicheza wawili wawili huku wengine wakicheza pekeyao, kuna wengine walicheza chibe chibe wakati huo muziki wala haukuruhusu kucheza hivyo ili mradi kila mmoja aifurahishe nafsi yake tu. Kuifurahisha nafsi kucheza chibe chibe wakati muziki hauendani na staili hiyo! Mmmh!
Hemedy na Hilda waliinuka kwenye viti walipokaa na kwenda mbele kuungana na wenzao kucheza muziki huo. Kwenye meza wakabakia Ramah na Hawa ambapo kila mmoja alikuwa kimya. Hawa kila akitaka kuliita jina la Ramah alijikuta akishindwa kufanya hivyo, akabaki kimya na kumuangalia kijana huyo akiendelea kuichezea simu yake. Ni kama vile Ramah alijua kuwa banati huyo atataka kumuita, akachomeka visikiliza muziki masikioni mwake na kuendelea kuichezea simu yake. Ajabu hii! Ni dhahiri hakuwa akitaka maongezi yoyote na binti huyo ndio maana alichomeka visikilizia muziki masikioni mwake.
Ilikuwa ni jambo la ajabu kusikiliza muziki kwa staili hiyo wakati humo ndani kulikuwa kukipigwa muziki kwa sauti kubwa. Ila yeye alifanya hivyo kuashiria kuwa hataki maongezi na binti huyo. Walikaa hivyo hadi pale Hilda na Hemedy waliporudi na kuungana nao tena huku wakiwaacha wengine wakiendelea kucheza muziki.
“Jamaa mbona umetulia tu hutaki kwenda kucheza hata kidogo rumba” Hemedy aliongea hivyo huku akikivuta kiti kwa mbele baada ya kukaa.
“Jamani twenzetuni mi nishachoka kukaa hapa” Ramah aliongea hivyo huku akianza kunyanyuka kwenye kiti alichokaa.
“Mbona mapema hivyo kaka” akaangalia saa yake ya mkononi. “Saa moja hii na nusu, mapema sana mzee” Hemedy aliongea.
“Kichwa kinaniuma, kwahiyo nataka kuwahi nyumbani” Ramah aliongea hivyo, kipindi hichi alikuwa tayari amesimama kando ya kiti akiwaangalia hao wenzake.
“Sawa, twenzetuni” akamuangalia Hawa kisha akasema. “Vipi Hawa na wewe unabaki au tunaenda wote?” Hemedy alimuuliza hivyo na kumfanya Hawa aitikie kwa kichwa kuashiria na yeye pia anaondoka. Wote wanne wakaondoka na kuenda nje ya ukumbi huo. Hawa alishangaa sana baada ya kumuona Ramah akielekea kwenye gari moja wapo kati ya mengi yaliyokuwa yamepaki hapo. Ilikuwa ni gari aina ya Harrie yenye rangi nyeusi, ilionekana bado mpya kabisa.
Ramah akatoa funguo na kufungua milango ya hiyo gari, kisha akaingia upande wa dereva akiwaacha Hilda na Hemedy wakiingia siti za nyuma. Kitendo hicho kilimfanya Hawa agande nje asijue aingie au arudi tu ukumbini. Hemedy kuona hivyo, akashuka kwenye gari na kumfungulia Hawa mlango wa mbele, kisha Hawa akaingia na kutulia kwenye siti kimya na safari ikaanza baada ya Hemedy kuingia kwenye gari.
Ramah akaweka muziki wa Justin Baby ulioitwa Sorry kwa sauti ya kawaida na kuwafanya Hilda na Hemedy kule nyuma kuufuatisha huku wakikumbatiana na kupigana mabusu kabisa huku wakionekana wakiwa na furaha kupita maelezo. Ramah muda wote alikuwa akitabasamu baada ya kuwaona watu hao kupitia kioo kilichokuwa mbele yake kwa juu. Wakamuacha Hawa nyumbani kwao na wao wakaelekea nyumbani kwakina Hilda. walipofika wakashuka wote na kuingia ndani ya hiyo nyumba, wakamkuta Anti yao akiwa yupo sebuleni amekaa akibadilisha chaneli kwenye luninga. Walimsalimia wote na kukaa nae hapo kwa muda, kisha Ramah akaaga na kuondoka zake akiwaacha wenzake kila mmoja akiingia kwenye chumba chake.
* * * *
Jumatatu ilifika na wanafunzi wa kidato cha tatu hadi cha kwanza walienda shule huku wa kidato cha nne baadhi yao sana wakiwa wameenda shule kukamilisha yale ambayo hawakuyakamilisha kabla. Hemedy na Hilda walipanga siku hii wawapatanishe Ramah na Hawa kivyovyote vile, walijua wote wanapendana lakini hawawezi kusameheana hivi hivi pasi na kupata mtu wa kuwapatanisha. Wakafikiria wakaona kwa hapo shule haitokuwa vizuri kufanya hivyo, wakapanga wawakutanishe kiujanja sehemu nyengine tofauti na hiyo. Coco Beach wakaona sehemu hiyo itafaa sana kuwakutanisha watu hao kiujanja.
“Jamaa leo nataka tuende Coco tukainjoi, ila leo inabidi uwende na gitaa, nataka nikusikie ukiimba huku ukipiga gitaa. Si unakumbuka kuna siku nilikuambia hicho kitu?” Hemedy alimuuliza Ramah.
“Basi mida flani ya jioni jioni tutakupitia hom kwenu tuelekee huko” Hemedy aliongea.
“Mtanipitia wewe na nani?” Ramah aliuliza.
“Jamaa si mimi na Hilda?”
“Sawa”
Hemedy alimaliza kuyaweka sawa Kwa Ramah na kumuachia kazi Hilda nae kumshawishi Hawa hadi akubali kuenda huko. Haikuwa kazi kubwa sana kwa Hilda kumshawishi Hawa, alikubali na kuahidi atatokea huo muda uliopangwa. Wakamaliza hivyo huku wakiwa na furaha ya kufanikiwa kuwashawishi watu hao bila wenyewe kujua.
Majira ya saa kumi na nusu jioni, Hemedy na Hilda walienda kwakina Ramah kwaajili ya kuelekea huko walipopanga, wakamkuta Ramah akiwa tayari ameshajiandaa, kilichofuatia hapo ni kuchukua ufunguo wa gari na wote kuingia humo safari ya kwenda huko walipopanga ikaanza. Baada ya muda wakawa wamefika na leo hii walienda kwenye miamba ya mawe mwisho kuenda kuweka kambi. Wakashuka kwenye gari na kukaa kwenye miamba hiyo au tuseme mawe makubwa mbali kidogo na yanapoishia mawimbi ya maji ya bahari, Wakakaa hapo. baada ya kupiga stori kwa muda mfupi, wakataka Ramah awaimbie huku akipiga gitaa, na yeye bila ajizi akaanza kufanya hivyo. Muda wote Hilda alionekana akichezeachezea simu yake huku akiangalia huku na huko, ni kama vile kulikuwa kuna kitu anakitafuta hivi.
Baada ya dakika tano, alioneka Hawa akija mahala hapo akiwa amependeza kupita kawaida. Ramah baada ya kumuona aliacha kupiga gitaa na kumtazama yeye kwa mshangao. Sio kwamba alikuwa akimtazama kwa jinsi alivyopendeza, hapana, alikuwa akimtazama kwa kujiuliza mtu huyo amefuata nini hapo? Hata kwa Hawa pia ilikuwa ndio hivyo hivyo, akabaki amesimama tu akimuangalia kijana huyo anavyomkodolea macho.
Hilda baada ya kuona amesimama tu pasi na kuja hapo walipo, akamuita na kumfanya binti huyo kupiga hatua za kinyonge kuenda mahala hapo, alipofika alikaribishwa na kukaa sehemu hiyo akiwa hana amani kabisa, akawasalimia wote na safari hii Ramah pia aliitikia salamu hiyo. Wakasitisha zoezi la kuimba wakawa wanapiga stori za kawaida, muda kidogo, Hemedy na Hilda waliaga na kusema wanaenda kununua chochote kitakacho sindikiza maongezi yao. Wakabaki wenyewe wawili hapo, wakawa hawajui waongeleshane au wakae kimya tu hivyo hivyo. Kimya kikavunjwa!.
“Hilda” Ramah aliita baada ya kukaa kwa muda mrefu bila ya kuongea chochote.
“Naam” Hilda nae aliitikia.
“Bado tu unanichukia?” Ramah aliongea hivyo na kumfanya ashindwe kulijibu hilo swali kwa mdomo, badala yake akalijibu kwa kutikisa kichwa kulia kwenda kushoto na kushoto kwenda kulia akimaanisha hapana.
“Kwanini uliamua kunichukia pasi na kunisikiliza nilichokuwa nataka kukuambia?”
“Nisamehe mpenzi. Ni hasira tu zile ndo zilinifanya niwe vile”
“Umeamua nini kuhusu mimi?”
“Ramah mi bado nakupenda, naomba tuweke tofauti zetu pembeni na tuendeleze mapenzi yetu, yale yaliyopita tuyaache, tuangalie yajayo” Hawa aliongea kwa upole.
“Sasa ni vipi utakuwa na mimi wakati umenifumania kwa macho yako?”
“Hapana Ramah mi bado nakupenda. Shamsa alinifuata leo akaniambia kila kitu na nimejuta sana baada ya kusikia kuwa kumbe ulikuwa tu ni mpango wa Babel kunipata mimi. Ila naomba unisamehe kwa yale maneno niliokuwa nakuambia” Hawa aliongea hivyo huku machozi yakimtoka. Ramah alimvutia karibu yake na kuanza kumfuta machozi.
“Hawa niliwahi kukuambia sitoruhusu machozi yako yatoke ikiwa mimi nipo karibu na wewe. Nakupenda Hawa, karibu tena katika himaya ya moyo wangu” Akampiga busu la mdomoni na kumuangalia usoni, hapo kila mmoja alitabasamu na kukumbatiana tena. Baada ya kuachiana, Hawa akaomba aimbiwe nyimbo, Ramah akachukua gitaa na kuanza kuvuta nyuzi moja moja kwa ustadi mzuri huku akimuangalia Hawa usoni.
“…………labda nyayo zako zimekutana na mengi. Ukasema tena kupenda sipendi, sipendi. Ni mimi swahiba wako, fundi mjenzi, nitalinda na kutunza penzi, penzi. Kudhulumiwa na kutangatangaa, kwa kilio na machozi. Mi jahazi na nshatia nangaa, sing’atuki hata waje kwa ndumba. Baby tembea naomba uje, ooh na penzi langu uje uonje……”
Hiyo ilikuwa ni baadhi ya mistari aliyokuwa Ramah akimuimbia Hawa. Hakika Hawa alijiskia faraja sana na kukiri kimoyomoyo kuwa Ramah alikuwa akimpenda kweli tofauti na alivyokuwa na Babel. Kwa Ramah alikuwa nae zaidi ya miezi miwili sasa lakini hakuwahi kumgusia chochote kuhusu kufanya mapenzi. Ila kwa Babel hata wiki haijaisha lakini kijana yule alikuwa ni mwenye kuhitaji kufanya tendo hilo.
Majira hayo Hemedy na Hilda walikuja hapo huku Hilda akiwa ameshika mifuko miwili ya nailoni mikononi mwake. Walimkuta Hawa akiwa amemuigamia Ramah huku akiimbiwa nyimbo. Hemedy alipiga makofi mengi huku Hilda yeye akipiga vigelegele. Kitendo hicho kilifanya watu hao wageuke nyuma na kuwaona wenzao wakiwa na furaha ya ajabu.
“Sasa je, mlikuwa mnachukiana bure, halafu kumbe nyote mnapendana, waone vile walivyo tahayari, Kama mmefumaniwa kichochoroni mkifanya niniliu” Hemedy aliongea hivyo huku na yeye akikaa. Aliposema hivyo wote wakawa ni wenye kucheka tu. Hilda akaifungua ile mifuko na kutoa vichupa vya plastiki vilivyokuwa na juisi ya embe ndani yake. Akampa kila mmoja cha kwake na yeye akakaa hapo na kuendelea na stori nyengine.
* *
Siku za mitihani zilipowadia, wakafanya mitihani hadi pale walipomaliza yote na kufunga shule kwa mwezi mmoja na wiki moja. Hapo wakawa huru zaidi, likizo hiyo waliitumia kufurahia mapenzi yao, lakini hawakusahau kusoma sana kwajili ya kidato cha nne. Likizo hiyo ikaisha na kufungua tena shule, sasa walikuwa kidato cha nne, hawakutaka kufanya mchezo hata kidogo na darasa hilo, wakapunguza mitoko na kuwa ni wenye kujisomea kila mara.
* * * *
Zilianza sekunde, zikafuata dakika, yakafuata masaa na kuenda kwenye miezi. Wakawa sasa wamebakiza mwezi mmoja kufanya mtihani wa mwisho, hapo ikawabidi wayasahau mapenzi yao na kuamua kukazana na kusoma. Mwezi nao ukaisha na siku za mitihani zikafuata. Wakafanya mitihani yao kwa wiki moja tu kutokana na wao kuwa kwenye masomo ya sanaa huku wakimuacha Hawa akiendelea na mitihani kwasababu yeye masomo yake ni ya biashara.
Walimaliza mitihani yao na kufanya mahafali hapo shule, siku hiyo ilikuwa ni huzuni sana kwao kuachana na marafiki zao walizoeana nao sana, walipiga picha nyingi za ukumbusho. Lacho, Shebe na Mnama, majira hayo walikuwa wameacha bifu na watu hao baada ya kuwafuata kipindi kirefu na kutaka waache tofauti zao na kutaka kushirikiana pamoja kama wanafunzi. Ramah na Hemedy walikubali na kuanzia hiyo siku hiyo wakawa wapo pamoja huku bifu lao wakilisahau. Lakini Babel yeye hakutaka suluhisho hata kidogo na watu hao, alichokuwa akitaka yeye bifu liendelee hadi pale afe yeye au wafe wao.
Wakapiga picha za pamoja kama ukumbusho, mahafali yalipoisha, wakawa na wao wameondoka shuleni hapo kabisa kabisa.
Baada ya wiki moja kupita tangu wamalize shule. Ramah akawajia wenzake na taarifa iliyowafanya wanyong’onyee na kuingiwa na mfadhaiko mkubwa kwa taarifa hiyo. Taarifa iliyomfanya Hawa kulia kila muda huku akiwa haamini hata hiyo taarifa. Akaomba iwe ni ndoto au iweni mzaha tu wa Ramah kutaka kuwainjoi wenzake, lakini aliwahakikishia hivyo baada ya kuwatolea kitu kilicho wafanya waamini.
Taarifa yenyewe ni kwamba, Ramah anahitajika akasomee nchi za nje elimu yake iliyobakia. Kwahakika taarifa hiyo ili wafanya marafiki zake waingiwe na ubaridi wa ghafla kwenye miili yao. Mwanzo walidhani ni mzaha tu wa rafiki yao, ila aliwahakikishia kwa kuwatolea tiketi ya ndege inayotakiwa asafiri siku mbili zijazo. Hapo Hawa hakuweza kujizuia kulia, alilia sana huku akisema kuwa Ramah anamuacha mwenye hajui ataishije baada ya yeye kuondoka.
Ikabidi wachukue wasaa huo kumfariji na kumbembeleza mwenzao hadi pale alipotulia kabisa. Kuanzia muda huo hakutaka kabisa kuwa mbali na Ramah akifurahia uwepo wake mwisho mwisho.
Siku ya safari ilifika, wakamsindikiza uwanja wa ndege huku wakiongozana na baba yake Ramah. Walipofika wakashuka wote na kumsindikiza hadi sehemu ambapo walitakiwa waishie hapo maana huko mbele ni kwaajili ya wasafiri tu. Hapo Ramah aliwakumbatia wote ishara ya kuwaaga, alipofika kwa Hawa, hakutaka kumuachia hata kidogo huku bado akiendelea kulalamika akisema haamimi kama kweli anaondoka huku akimuacha yeye pekeake.
Ukafika muda ambao wasafiri wanatakiwa waingie kwenye ukaguzi kwaajili ya safari. Ramah akaondoka huku akitembea kinyume nyume akiwapungia mkono. Ghafla Hawa alichomoka hapo alipo na kumfuata Ramah na kwenda kumrukia kwa kumkumbatia, nusura waanguke. Hapo wakajikuta wote wanalia na kuahidiana kuonana tena mungu akipenda. Waliachiana na Ramah akaondoka na kuingia ndani ya chumba cha ukaguzi. Hemedy jicho moja lilimtoka chozi na kumfanya alifute kabla halijafika chini. Hawa alikuja na kumkumbatia Hemedy huku akilalamika kuwa Ramah amemuacha mwenyewe.
Walikaa hapo hadi pale ndege ilipoiacha anga ya Tanzania na kuingia katika anga ya kimataifa. Kisha na wao wakaondoka uwanjani hapo kuelekea walipotoka. Hawa hakuwa na furaha hata kidogo, kuondoka kwa kipenzi chake kuenda kusomea nchi za nje, tena hata yeye mwenye pia hajui kuwa anaenda kusomea nini wala anaenda kusomea wapi. Lilimuuma sana ila hakuwa jinsi kwasababu ilikuwa ni lazima watengane tu kivyovyote hata kama isingekuwa kwa safari.
* *
Majibu yao ya kidato cha nne yakatoka baada ya miezi mitatu kupita, wote walifaulu vizuri kuendelea na masomo yao, hata Ramah pia alifaulu, ila ndio hivyo hakuwepo nchini. Kibaya zaidi Hawa yeye alifaulu mbeya huku wenzake wakifaulu hapo hapo Dar. Wakatengana kwa mara ya pili, Hawa alizidi kushikwa na uchungu, akajiona hivi hivi wenzake wanamtenga, ila kwa vile masomo ndio yanayo watenganisha, hawakuwa na budi zaidi ya kutengana.
Hawa akaenda mbeya huku Hemedy na Hilda wakibaki Daresalam. Walifaulu shule ya sekondari Tambaza na kuendelea na masomo yao ya kidato cha tano na cha sita hapo. Japokuwa maisha ya kusoma wakiwa wapweke bila ya wenzao yaliwagubika, ila ndio hivyo sasa hawakuwa na jinsi zaidi ya kusoma tu wakiwa wenyewe. Walianza kusoma katika shule hiyo wakiwa wageni kama wenzao. Miezi mitatu mbele, walipata marafiki wapya shuleni hapo japokuwa hawakuwa na ladha kama za wale waliotoka nao katika elimu ya upili. Walisoma kwa bidii huku kila mmoja akiwa na ndoto zake.
Mwaka huo ukaisha, ukaingia mwaka wa pili na sasa walikuwa wakimalizia mwaka wa mwisho shuleni hapo, walikuwa wapo kidato cha sita. Mwaka huo nao ukaisha wakiwa wamemaliza kidato hicho cha mwisho. Wakawa sasa wanasubiri matokeo yao baada ya kumaliza elimu hiyo.
* * * *
“Dah! Mwanangu hii kazi hata sijui itaisha lini, nishachoka kuifanya mimi” Kanu aliongea hivyo kumuambia Asu wakati wakiwa kwenye Cafe moja maeneo ya Msimbazi wakipata staftah asubuhi hiyo.
“We acha tu! Ila sasa tutafanyaje wakati sisi ni vibaraka tu” Asu aliongea.
“Hata kama, lakini na sisi pia tunahitaji mapumziko jamaa. Nina muda mrefu nalala usingizi wa mashaka mashaka tu”
“Inabidi tumuombe mkuu aweke vijana wengine wa zamu wa kuifanya hii kazi, maana ni muda mrefu sana tunaifanya pekeetu”
“Hivi Asu unaweza ukaniambia kuwa Mkuu anampango gani na yule dogo? Na huyo anaesema kila siku Kiongozi ni nani?” MAAJABU! Ina maana hata hawa vijana hawajui wanamlinda Hemedy kwasababu gani? Na hata huyo anaesemwa ni Kiongozi hata wao pia hawamjui?” UTATA!.
“Ndugu yangu hata sijui, ila nahisi ni……” Asu alikatishwa sentensi yake na simu yake iliyokuwa ikiita. Akaitoa mfukoni na kuingalia juu ya kioo ilisomeka jina Mr Kaoneka. “Mkuu” alitamka kwa sauti ndogo kisha akaipokea.
“Sawa Mkuu” alitamka neno hilo moja na kuitoa simu sikioni mwake ikiwa tayari ishakatwa.
“Mkuu anatuita” Alisema neno hilo, kisha akanywa chai iliyokuwa kwenye kikombe.
“Duh! Nishachoka mimi” Kanu alitamka kwa ghadhabu kiasi.
Walipomaliza kula. Wakalipa na kutoka nje ya hiyo Cafe. Wakapanda kwenye gari lao na safari kuelekea huko Mkuu wao alipowahitaji. Walitumia nusu saa tu, kisha wakapaki gari lao nje ya jengo moja refu, wakashuka kwenye gari na kuanza kupiga hatua kuingia humo. Walipofika ndani ya jengo hilo, wakapanda lifti iliyowapeleka flow ya juu ya jengo hilo, huko wakatoka kwenye chumba cha lifti baada ya kujifungua na kuanza kuifuata korido ndefu iliyokuwa mbele yao. Mwisho kabisa wa hiyo korido. Wakaingia kwenye chumba kimoja na kumkuta Mkuu wao (Baba yake na Ramah) akiwa amekaa kwenye kiti chake cha kuzunguuka akiwatazama wao. Akawapa ishara ya kukakaa na wao wakafanya hivyo.
“Nimekuiteni hapa kuna jambo nataka niwaambie” Akatulia baada ya simu yake ya mezani kuita, akaiangalia kwa muda halafu akainyanyua na kuiweka sikioni mwake, kisha baada ya dakika, akaitoa sikioni na kuiweka mahala pake. Kisha akawa anawaangalia tu machoni vijana hao pasi na kusema chochote. Kitendo hicho kilidumu kwa dakika moja, simu yake ya mkononi ikaita, akaichukua na kuipokea kisha akaiweka sauti kubwa na kuiweka juu ya meza akiwa ameilaza upande wa spika ukiwa juu.
“Mr Kaoneka” Sauti ya kwenye simu iliita, lakini muitwaji wala hakunyanyua mdomo wake kujibu. Akakaa kimya, kisha sauti hiyo ikaendelea.
“Nadhani wale vijana sasa wamemaliza shule, ila kinachotakiwa, waishie hapo hapo kidato cha sita, yani wasiendelee tena na elimu yoyote. Unachotakiwa sasa hivi ni kufanya mpango kivyovyote vile waingie JKT na baada ya kumaliza mafunzo hayo, moja kwa moja waingie jeshi la polisi” Mtu wa upande wa pili aliongea.
“Kiongozi sijakuelewa. Kwani wapo wangapi wanaotakiwa? Naona kwenye maelezo yako umeingiza ‘uingi’ wakati mimi namjua mmoja tu” Mr Kaoneka aliongea.
“Aaah! Samahani Mr Sijakuambia kitu. Ni kwamba nimeona hata yule binti anafaa kuwepo kwenye huo mpango, kwahiyo ndio maana nikasema unatakiwa kufanya kila uwezalo waingie JKT kisha hapo wakimaliza mafunzo, moja kwa moja waingie kwenye jeshi la polisi” Akatulia kidogo ili kusubiri maneno hayo yamuingie vizuri Mr Kaoneka. Kisha akaendelea. “Fanya hicho kitu haraka iwezekanavyo. Halafu wakimaliza mafunzo wanatakiwa wakalitumikie jeshi la polisi mkoa wao, mkoa wa Tanga. Baada ya hapo kazi itakuwa ni nyepesi sana kwasababu kwa miaka hiyo, yule kijana atakuwa pia hana tena kisasi na mtu yoyote. Kwasababu hiyo kazi iliyoko mbele yake haihitaji mtu nwenye kisasi”
“Sawa Kiongozi nimekuelewa, hilo jambo ni dogo sana kwa upande wangu, nilazima likamilike”Mr Kaoneka aliongea.
“Mr, tambua nakutegemea sana kwenye jambo hili, na ndio maana ulipotoa wazo hili miaka nane iliyopita viongozi wote waliopita waliliunga mkono na kukuachia wewe hii kazi kwasababu umeaminika sana. Sasa pasije pakatokea uzembe wa aina yoyote na kusababisha mpango ulioanzia kwa viongozi wenzangu waliopita ukaja kuharibika kwangu. Utanifanya nionekane mzembe sana kwenye uongozi wangu na mimi sitaki hicho kitu kije kunitokea.
“Ondoa shaka. Nitahakikisha kila kitu kinaenda sawa” Mr kaoneka alipoongea hivyo, simu ikakatwa na kuwaangalia vijana wake.
“Najua hamjui ni kwasababu gani mnamuwekea ulinzi yule kijana. Hata hivyo hampaswi kujua, mnachotakiwa nyie ni kufanya kama vile ambavyo nawatuma basi. Aaa, nadhani nyote mmemsikia Kiongozi alivyosema japokuwa hamumjui na hampaswi kumjua kwa sasa. Amesema kuwa ulinzi kuanzia sasa muuweke kwa wote wawili, yani yule kijana na yule binti. Tumeelewana?” Mr Kaoneka aliongea kisha akawauliza.
“Ndio mkuu tumekuelewa” walijibu wote kwa pamoja.
“Najua mmeichoka hii kazi, lakini sasa hamna budi kuifanya na pia tu niwaambie kitu, muda si mrefu mtapumzika kwa muda kwasababu wale vijana wanatakiwa waende JKT, kwahiyo huko watakuwa chini ya ulinzi wa wakufunzi wao. Wakishatoka huko moja kwa moja wataenda kulitumikia jeshi la polisi, sasa hapo nyie hamtokuwa na kazi sana ya kuwalinda kwasababu watakuwa wanaweza kujilinda wao wenyewe ila nyie mtakuwa mkihakikisha usalama wao kwa uchache sana. Yule kijana akimaliza kisasi chake kwa wale watu waliomuulia familia yake, basi hapo ndio itakuwa mwisho wa kazi yenu na kuanzia hapo mtakuwa mkilipwa mshahara pasi na kufanya kazi yoyote hadi vifo vyenu, Kwsababu mmefanya kazi kubwa sana. Najua mtajiuliza nimejuaje kwamba ni lazima alipize kisasi cha vifo vya familia yake, na hilo pia hampaswi kujua…. Mnaweza kwenda” Mr Kaoneka alipoongea hivyo, akachukua faili lililokuwa juu ya meza yake na kuanza kulifunuafunua hapo pasi na kuwatazama hao vijana walioko mbele yake.
Vijana hao baada ya kuona mkuu wao ameshika kazi nyengine, wakajinyanyua hapo na kuanza kuondoka humo ndani na kutokomea wanapopajua wao.
* *
Wiki mbili mbele. Hemedy na Hilda walienda JKT kwaajili ya mafunzo. Kwa fikra zao walijua wamechaguliwa kwenda huko, ila haikuwa hivyo, hawakujua kuwa huo ulikuwa ni mpango uliopangwa wao kwenda huko. Baada ya miezi kadhaa mbele. Walihitimisha mafunzo hayo na kutakiwa wachukue mafunzo mengine kwaajili ya jeshi la polisi. Walishangaa sana ila hawakuwa na la kupinga kutokana na kulazimishwa sana na mkufunzi wao.
“Mpenzi unajua hichi kitu kinanishangaza sana. Eti tupelekwe JKT muda ambao wenzetu tayari wameanza kama mwezi mmoja nyuma, halafu na sisi nasi tuchaguliwe kuenda. Halafu kilichonishangaza zaidi tulipo lazimishwa kuchukua mafunzo ya jeshi la polisi” Hemedy alikuwa akimuambia Hilda.
“Hata mimi pia hili jambo limenishangaza sana ila ndio hivyo sasa hakuna budi, inabidi tufuate tu”
“Duh! Ila mimi nahisi kuna namna hapa” Hemedy aliongea.
“Kwanini unahisi hivyo?”
“Haiwezekani kila kitu tulazimishwe lazimishwe tu”
“Mmmh!!”
Baada ya kumaliza mafunzo ya JKT. Walienda kwenye mafunzo mengine ya jeshi la polisi kwa miezi sita, baada ya hapo wakaambiwa wajiandae kuenda kulitumikia jeshi la polisi mwezi mmoja unaofuata.
“Kwahiyo na nyie mnaenda kuwa askari?” Anti yao aliwauliza huku akijiweka vizuri hapo sebuleni kwenye sofa.
“Ndio hivyo Anti. Hata hatujui imekuajekuaje hadi tukafikia huko” Hemedy aliongea.
“Lakini huenda ikawa juhudi zenu mazoezini ndio zimemifanya mkapelekwa huko” Anti aliongea.
“Lakini mimi hayakuwa malengo yangu kuwa askari” Hemedy aliongea.
“Hata kama, huenda ikawa juhudi zenu zimewafanya wakuu wenu wamione mnafaa ndio maana wakamichukua, kwahiyo msilalamike sana”
“Lakini mimi Anti siwezi hizo kazi za vurugu vurugu” Hilda aliongea.
“Unaziweza ndio maana ukachaguliwa, au unadhani hao wenzako walioweza wameanzaje?” Anti aliongea.
“Lakini hii sio ha….” Hemedy alikatisha sentensi yake baada ya simu yake iliyokuwa pembeni ya sofa alilokalia kuita, akapeleka macho kwenye kioo na kuichukua ile simu, akawa anaiyangalia tu bila kuipokea.
“Mbona hupokei simu?” Hilda aliuliza, ni dhahiri alishaanza kushikwa na wivu baada ya kuona Hemedy haipokei ile simu na badala yake anaiangalia tu, akainuka pale alipokaa na kuenda kuipokonya ile simu na kuingalia kwenye kioo kwa muda, huku akiwa ameitumbulia macho kama vile Hemedy alipokuwa ameitumbulia macho.
“I.G.P!” Hilda alisema kwa sauti ndogo huku akiiangalia hiyo simu.
“Anataka nini tena huyo babu yenu?” Anti aliwauliza.
“Hatujajua. Subiri niipokee” Hemedy aliongea hivyo na kuichukua simu kwenye mkono wa Hilda na kuipokea. Akaongea nae kidogo, kisha simu ikakatwa na wenzake wakabaki wakimtazama yeye awaambie ni kipi mtu huyo alikuwa anataka.
“Anasema amepewa taarifa za sisi kuwa askari wa Tanga, akapongeza tu na kusema anatusubiri Tanga” Hemedy alisema.
“Mbona kapewa taarifa mapema hivyo? Au ndio taratibu za kijeshi hizo?” Anti aliuliza.
“Siwezi jua, lakini amesema pia tumepangiwa kwenye kituo chake” Hemedy aliongea.
“Haya jitahidini wanangu, msiikatae hiyo kazi” Anti yao aliongea hivyo huku akiinuka na kuingia chumbani kwake.
* *
“Jamani umebadilika Hawa hadi nakuonea wivu” Hilda aliongea kumuambia Hawa wakati wakiwa Hotelini siku ya pili baada ya Hawa kurudi kutoka shule.
“Mbona hata nyie pia mmebadilika, tena ndio mmezidi kupendeza jamani” Hawa aliongea.
“Vipi lakini masomo huko ulipoenda?” Hemedy alimuuliza.
“Hivyo hivyo tu shemu tumesoma, halafu si unajua tena ugenini kule, nilikuwa nimeboreka kweli yani” Hawa aliongea.
“Unaenda chuo gani kusoma?” Hemedy alimuuliza.
“Namikimbia tena ndugu zangu naenda huko Kenya Nairobi kusoma. Na nyie nanyi?”
“Sisi kwetu kumetokea magumashi ambayo hatuyaelewi, ambiwa na sisi tumekuwa askari” Hemedy aliongea na kumfanya Hawa ashangae.
“Nyote wawili au?” Hawa aliuliza.
“Ndio sote, yani hapa tunapokuambia, baada ya siku ngapi tu tunaenda Tanga” Hemedy aliongea.
“Lakini sio mbaya, hiyo ni bahati sana, yani kumaliza ‘form six’ tu mmepata kazi, kuna wenzanu wamefika hadi chuo lakini bado hawajapata kazi” Hawa aliwaambia.
“Mi mbona nishakubaliana nayo, ila kimbembe kipo kwa huyo rafiki yako hapo” Hemedy aliongea.
Huku akimsukuma begani “Nani aliekuambia kuwa mimi nimeikataa hiyo kazi?” Hilda aliongea.
“Kwahiyo hapa nimekaa na maaskari? Afadhali mmeniambia mapema, ninaweza nikafanya kosa hapa mkanichukua bila huruma” Hawa aliongea na kuwafanya wenzake wacheke.
“Hapana bwana, bado hatujawa askari rasmi ila mafunzo tunayo, sasa usije ukashangaa tutakuadhibu bila ya kukupeleka kituoni” Hemedy aliongea.
“Hivi jamani Ramah mnamawasiliano nae?” Hawa aliwauliza.
“Mmmh! Ramah tangu aondoke sijawahi kuwasiliana nae kwa njia yoyote ile” Hemedy aliongea na kumfanya Hawa anyongee.
“Kwani wewe unaenda lini chuo?” Hilda alimuuliza.
“Kesho kutwa ndio naenda”
* *
Tanga. Uwanja wa ndege majani mapana. 6:30 Mchana.
Hemedy na Hilda kwa mara ya kwanza tangia waondoke katika mji huo ndio wanarudi leo. Walitoka hapo uwanjani na kuanza kupiga hatua ndogo ndogo huku wakiwa wanashangaa shangaa mandhari ya hapo. Hilda aliachia begi lake alilokuwa akiliburuza na kumkimbilia babu yake aliekuja kuwapokea hapo, alipofika akamkumbatia huku wote wakiwa na furaha ya aina yake kukutana tena baada ya kuondoka kwa miaka mingi.
Hemedy alilichukua begi la Hilda akalivuta pamoja na lakwake kuelekea kule walipo. Alipofika akamsalimia na kuwaongoza kwenye gari alilokuja nalo.
“Yani huyu mjukuu wako hajaacha tu kudeka kwako. Tangu tupo Dar alikuwa akikusema sana utafikiri hatutofika” Hemedy aliongea hivyo wakiwa ndani ya gari kuelekea nyumbani.
“Sasa jamani Hemedy hujui kama huyu ni babu yangu na nina muda mrefu sijamuona, kwahiyo lazima ni deke kwake” Hilda nae aliongea.
“Hata kama lakini ushakuwa wewe” Hemedy aliongea.
“Umeona wapi mtoto kwa mzazi akikuwa?”
Waliendelea na maongezi kwenye gari hadi pale walipofika nyumbani. Ikawa shangwe nyengine kwa wale wafanyakazi ambao walikuwa ni wazamani nyumbani hapo huku wale wapya wakiwa ndio kwanza sura hizo wanaziona. Ikaandaliwa sherehe ya kuwakaribisha tena watu hao nyumbani. Maandalizi yalifanywa haraka haraka na kuwaalika baadhi ya watu waliokuwa wakiwajua vijana hao.
Koplo Taure ambae kwa sasa amepanda cheo hadi kuwa Inspekta huku Inspekta Ganjo akiwa ni I.G.P (Inspekta Generalal wa Polisi) na Afande Jesca akipanda cheo hadi kuwa Sajenti. Watu hao walihudhuria hapo na ikawa ni furaha nyengine ya kuonana tena baada ya kupoteana kwa miaka tisa. Mrutu nae alikuja na kuungana na wenzake kuwakaribisha wageni hao. Ikawa ni furaha tu muda wote, wakala wakanywa hadi kufikia majira ya usiku sherehe hiyo ndio ikaisha na kila mmoja kurudi alipotoka huku Hemedy akiondoka na Mrutu.
Walipofika nyumbani kwao Hemedy akawa ni mwenye kuyashangaa mazingira ya hiyo nyumba. Alikumbuka mambo mengi sana ya nyuma. Aliwakumbuka wazazi wake, alimkumbuka na mfanyakazi wao ambae yeye alimchukulia kama kaka yake, akabaki ameganda hapo ndani ya uzio wa nyumba hiyo.
“Anko na mimi nataka uniogesha na hayo maji kama unavyo yaogesha haya maua” Hemedy alimuambia Goda kipindi hicho alikuwa akimwagilia maji bustani za hapo nyumbani.
“Na wewe unataka kuoga kama ninavyo yaogesha haya maua?” Goda alimuuliza huku akiwa anaendelea kumwagilia maji bustani hiyo.
“Ndio Anko” Hapo Goda alimuelekezea mbomba wa maji Hemedy na kuanza kumwagia maji yeye, Hemedy akawa anapiga kelele huku akielekea ndani ya nyumba hiyo, alipofika mlangoni akampamia mama yake aliekuwa anatoka nje baada ya kusikia kelele zake.
“Goda nini tena mbona nasikia kelele?” Mama yake alimuuliza Goda huku akiwa amekishika kichwa cha Hemedy aliekuwa amemkumbatia yeye.
“Muulize huyo mwanao kilichomfanya hadi akawa anapiga kelele ni nini” Goda aliongea huku akicheka na kuendelea kumwagilia maji bustani.
“Eti Hemedy ni kipi kilichokufanya ukapiga kelele?” Mama yake alimuuliza huku akiwa anamuangalia usoni.
“Anko mchokozi” Hemedy aliongea hivyo na kumfanya mama yake acheke na kumvuta kuingia nae ndani. Ila ghafla alichomoka kwenye mkono wa mama yake aliekuwa kamshika na kukimbilia kule alipo Goda, kisha akampiga kofi na kuanza kukimbia kuelekea kule aliposimama mama yake. Ila Goda aliwahi kumkimbilia na kunyanyua juu na kufanya Hemedy apige kelele kumuita mama yake huku akiwa anacheka.
Kumbukumbu hiyo ilimrejea kichwani mwake baada ya kuiona hiyo bustani, bila kutarajia machozi yalianza kumtoka pasi na kilio cha mdomo. Mrutu alipomuona hivyo, akamfuata na kuingia nae ndani huku akiwa anambembeleza. Waliingia sebuleni na kukaa kwenye masofa. Hemedy akawa anapitisha pitisha macho kwenye hiyo sebule na kuona kuna baadhi ya vitu vimebadilishwa ikiwemo masofa. Hapo Mrutu alimuuliza za huko atokako na stori nyengine kama hizo. Baada ya hapo kila mmoja aliingia kwenye chumba chake kwenda kupumzika, hawakuwa na haja ya kula tena kwasababu kule kwa IGP Ganjo wamekula.
Siku mbili mbele, walikuwa wameanza kazi rasmi kwenye kituo ambacho IGP Ganjo anafanya kazi. Siku hiyo ndio walikuwa wakikabidhiwa mavazi na kila kitu cha jeshi ili kuwa askari rasmi. Cheo cha Ukonstebo ndio cheo walichokuwa nacho wao. Cheo cha mwanzo kabisa katika jeshi la polisi. Walianza kazi rasmi hapo.
Mwaka mmoja kupita. Hemedy alipandishwa cheo kiajabu ajabu pasi na yeye kuelewa. Akawa sasa ni Koplo Hemedy huku Hilda akiwa katika cheo chake kile kile cha Ukonstebo. Ilimshangaza kila askari aliesikia hicho kitu lakini ndio hivyo hawakuwa na cha kupinga.
“Unajua Hilda mimi sielewi kabisa nimepandaje cheo kwa mwaka mmoja tu, wakati mimi najua kutoka cheo kimoja hadi kwenda chengine inachukua miaka mitatu, tena hadi uwe na bidii katika kazi ndio unapandishwa cheo. Sasa mimi kwangu hata sijui imekuaje yani” Koplo Hemedy alimuambia Konstebo Hilda wakati wakiwa katika ofisi ya Koplo Hemedy.
“Niajabu kweli lakini inabidi ushukuru kwasababu kupanda cheo kila askari anatamani”
“This is ‘wonder’!” Koplo Hemedy aliongea hivyo huku akiinuka kwenye kiti alichokaa na kuanza kupiga hatua kutoka ndani ya ofisi hiyo.
“Naelekea hom, kwani hujui kama muda ushaisha hapa!”
“Oooh! Basi subiri tuongozane wote ukani ‘drop’ nyumbani”
Wakatoka nje wote na kuingia kwenye gari la Koplo Hemedy alilopewa na Mrutu. Wakaanza safari ya kutoka hapo kituoni kuelekea nyumbani kwakina Konstebo Hilda, walipofika akashuka na kuingia ndani kwao akimuacha Koplo Hemedy akielekea kwenye nyumba yake aliyopanga. Hakutaka kuishi na Mrutu nyumba moja, alihofia anaweza akabanwa banwa kwenye mambo yake ndio maana akaamua apangishe nyumba nzima aishi yeye mwenyewe. Hata pale alipotaka kuishi mwenyewe, Mrutu alitaka kumpa ile nyumba yake aliyokuwa akiishi zamani yeye na ikiwa imepengishwa, lakini pia alikataa na kudai anataka kuanza maisha yake yeye kama yeye.
Alipofika kwenye hiyo nyumba anayoishi iliyoko maeneo ya Msambweni, akaingiza gari ndani na yeye kuingia ndani ya nyumba hiyo. Ilikuwa ni nyumba yenye hadhi kiasi ambayo kijana yoyote angetamani kuishi hapo. Akaingia chumbani kwake na kuliendea kabati na kulifungua, huko alionekana akichangua changua nguo zilizomo humo ndani. Alifanya hivyo kwa dakika kumi na alipokosa alichokuwa anakitafuta, akakaa kitandani na kuanza kufikiria.
Akainuka tena na kuliendea begi lake la nguo na kulifungua, kisha akaanza kutoa nguo moja baada ya nyengine na kuziweka chini. Begi lilipokuwa tupu, akaanza kufungua zipu moja baada ya nyengine kwenye begi hilo. Wakati akiwa anafungua zipu na kutia mkono wake kwenye sehemu hizo, akawa kama kuna kitu amekishika kwa ndani, akakivuta na nje na alipokiangilia, aliachia tabasamu baada ya kuipata flash aliokuwa akiitafuta. Akaiendea ‘laptop’ yake, akaichukua na kuenda kukaa nayo kitandani. Akaiwasha na baada ya dakika moja ikawa tayari imewaka.
Akaichomeka flash na iliposoma akaifungua kwenye mafaili yake na kuliendea faili moja lililoandikwa 13/06, akalifungua. Kwa mara ya kwanza tangu apewe flash hiyo na marehemu Goda ndio anaifungua siku hiyo. Hapo akakutana na video moja tu na kuifungua. Hapo ilianza kumuonyesha video wakati kipindi hicho wakiwa sebuleni wakipiga stori na familia yake hadi pale walipoingia watu wasiowajua na kuiteketeza familia yake huku wakiondoka na briefcase iliyokuwa na nyaraka za mali za baba yake…
Machozi yalikuwa yakimtoka alipomaliza kuiangalia hiyo video. Akaifunga ‘laptop’ yake bila ya kuizima na kuanza kulia tu pasi na kupata wakumbembeleza, alilia sana hadi pale alipoona panatosha. Akachukua simu yake na kumpigia baba yake mdogo.
“Niambie Afande, hahaha!!” Sauti ya Mrutu ilisikaka kwenye spika za simu ya Koplo Hemedy baada ya simu kupokelewa.
“Baba kesho nataka unipeleke yalipo makaburi ya wazazi wangu” Koplo Hemedy wala hakupokea heshima hiyo aliyopewa kwa furaha kama ambavyo Mrutu amefanya.
“Kuna nini tena?” Mrutu aliuliza swali la kibwege huku ikionekana dhahiri amehamanika huko alipo.
“Nataka nikayaone” Koplo Hemedy alijibu kwa ufupi.
“Sawa. Kesho nikipata muda mzuri nitakucheki halafu tutaelekea huko” Mrutu aliongea.
“Sawa” alijibu na kukata simu.
* *
Siku iliyofuata Mrutu na Koplo Hemedy walikuwa ndani ya gari wakielekea huko walipozikwa wazazi wake. Kwavile walikuwa kwenye gari lao binafsi, walitumia saa moja na nusu kufika huko. Walipofika kwanza waliwasalimia baadhi ya ndugu zao huku Mrutu akiwa ndie anaemtambulisha Koplo Hemedy, maana yeye hakuwa akiwajua hata mmoja. Baada ya kuwasalimia hao ndugu zao, walienda moja kwa moja hadi kwenye shamba lao ambalo ndipo makaburi hayo yapo.
Koplo Hemedy alilia sana mbele ya makaburi hayo ya wazazi wake yaliyokuwa yamepekana, alilia sana kiasi kwamba Mrutu na yeye akajikuta akidondosha chozi. Hakutaka kumbembeleza wala kumsogelea pale alipopiga magoti kwenye hayo makaburi, alichofanya yeye ni kumuacha tu hadi pale aliponyamaza mwenyewe na kutulia vile vile akiwa amepiga magoti.
“Baba na Mama yangu huko mlipo mungu awalaze mahali pema. Najua hamkufa kwa mipango ya mungu, ila mmekufa kwa mipango ya wanadamu wenye mioyo dhalimu waliotaka kuchukua mali zenu. Kwa hilo wamefanikiwa, wameniacha sijarithi chochote kutoka kwenu. Labda nilichorithi ni kisasi ambacho kimeishi ndani ya moyo wangu tangu mlipotoweka kwenye ulimwengu huu. Naahidi mbele yenu kulipa kisasi kwa kuwaondoa mmoja baada ya mwengine kwa mikono yangu kama vile ambavyo wameziondoa roho zenu. Nawajua na ushahidi ninao”
Mrutu alishtuka baada ya kusikia maneno hayo ya mwisho aliyoyatamka Koplo Hemedy. Hakuelewa mtu huyo aliongea hivyo kutokana na uchungu alionao au amemaanisha aliochoongea. “Ina maana anawajua hadi sasa waliowaua wazazi wake?…. Lakini hapana hawezi kuzikumbuka zile sura, alikuwa ni mdogo sana. Sasa ni vipi aseme anawajua?… Mrutu alijiwazia mwenyewe bila ya kupata majibu ya hicho anachokiwaza. Ikabidi amuulize.
“Hemedy u..u…unawajuaje waliowaua wazazi wako wakati tukio hilo limetokea zamani sana?” Mrutu alimuuliza huku akiwa na hofu nyingi iliyomkumba ghafla.
“Flash yenye ile video ninayo” Koplo Hemedy aliongea hivyo huku akimuangalia Mrutu usoni. Mrutu baada ya kusikia hivyo, alijikuta akipigwa na butwaa lililoonekana waziwazi na Koplo Hemedy..
“Ile video si nilikuuliza ukasema haunayo wewe?” Mrutu alimuuliza huku akioneka dhahiri anawasiwasi mwingi kupita maelezo.
“Nilikuwa nataka nije kuwatafuta mwenyewe, sikutaka mtu yoyote anisaidie kwa hili”Koplo Hemedy aliongea hivyo huku akiinuka pale chini.
“Sa..sasa mimi baba yako mdogo si nipo? Nitakusaidi kwa hilo. Chamsingi ni kunionyesha hiyo flash na mimi ili niwajue hao watu” Mrutu aliongea.
“Hapana, wewe tulia hii kazi nitaifanya mwenyewe na nitawapata tu kivyovyote” Koplo Hemedy aliongea hivyo huku akianza kupiga hatua kuondoka hapo makaburini.
“Lakini mimi baba yako nipo, nitakusaidia kwa hilo, kwasababu huwezi jua hao watu wana hatari kiasi gani” Mrutu aliongea hivyo huku akimfuata Koplo Hemedy kule anakoelekea.
“Baba kumbuka wale waliouliwa ni wazazi wangu, mimi ndio nina uchungu kuliko mtu yoyote yule, ninapokuambia uniachie mimi naomba ufanye hivyo maana sihitaji mtu wa kunisaidia katika hili” Koplo Hemedy aliongea hivyo huku akiwa kamgeukia.
“Sawa, lakini naomba na mimi pia niwaone” Mrutu aliongea kwa kulalamika.
“Sawa” aliongea hivyo na kugeukia mbele na safari ya kuondoka hapo ikaanza. Walirudi tena kijijini na kuwaaga wenyeji wao na wao wakaondoka. Njiani Mrutu alikuwa na mawazo mengi kupita maelezo, hakujua afanye nini ili kuliepuka hilo balaa lililopo mbele yao. Hapo ndio akajua kwamba siku zao za kufurahi uraiani zinakaribia kuisha kama sio kufika kabisa. Akawaza kama ikiwa hiyo flash ndiyo yenyewe basi aongee na wenzake waone watafanya nini.
Safari yao iliishia nyumbani kwa Koplo Hemedy na wote wakashuka kwenye gari na kuingia ndani ya nyumba hiyo. Koplo Hemedy alimletea ‘laptop’ na flash, kisha akamuekea ile video na kumfanya Mrutu ashtuke tena baada ya kuzishuhudia sura za wenzake zikionekana waziwazi kwenye hiyo video, akabaki kutetemeka tu na kumfanya Koplo Hemedy asimuelewe hata kidogo kwa hicho kitendo. Mrutu aliirudia tena kwa mara ya pili ile video kisha akaaga na kuondoka hapo.
Safari yake iliishia nyumbani kwa Moto na kumkuta mtu huyo akiwa ndio anaamka muda huo kutoka usingizini. Wakachukuana na kukaa sebuleni.
“Kaka kuna tatizo kubwa sana limejitokeza na tusipoliwahi basi litatuwahi sisi” Mrutu aliongea hivyo na kumfanya Moto asimuelewe alichoongea.
“Sijakuelewa mimi hata kidogo. Tatizo lenyewe ni lipi?” Moto alimuuliza.
“Hemedy karudi na sasa anataka kulipa kisasi” Mrutu aliongea.
“Hemedy yupi na hicho kisasi ni kipi?” Moto aliongea hivyo akionekana dhahiri kutomkumbuka mtu huyo kama sio kutomjua kabisa.
“Hemedy yule mtoto wa marehemu Mheshimiwa mulie muulia wazazi wake”
“Karudi vipi, na anataka kulipa kisasi kwani bado anatukumbuka?” Moto aliongea kikawaida sana, alijua huo ni wasiwasi wa Mrutu, alijua kwamba sura zao hadi kwa wakati huo zitakuwa zimefutika katika kumbukumbu ya yule mtoto waliemuulia wazazi wake.
“Ile flash yenye ile video anayo na leo akanionyesha na sura zenu zimeonekana bila chenga” Mrutu alipoongea hivyo. Moto akashtuka mithili ya mtu alieletewa taarifa za kifo cha mtu anaemjua.
“Eeee!! Kaka uko ‘serious’ au unatania?” Moto aliuliza huku akiwa macho kayatoa kama mtu alieona kitu cha kutisha.
“Wala sipo katika matani na ninavyokuambia yule mtu sasa hivi ni askari polisi, na kwavile amesema atawatafuta wauwaji wa wazazi wake, basi ujue lazima afanye hivyo na lazima atamipata tu”
“Ni askari?” Moto alizidi kuchanganyikiwa.
“Ndio ni askari na ana cheo cha Ukoplo”
“Sasa tutafanyaje?” Moto aliuliza, dhahiri alionekana kuchanganywa na hiyo taarifa.
“Ndio nimekuja kwako hapa tujue tunafanyaje”
“Inabidi tumuue, tumtumie watu watakao muua tu” Moto aliongea.
“Kwani hakuna njia nyengine zaidi ya hiyo ya kumuua?” Mrutu alimuuliza.
“Sasa unadhani tutufanya njia gani nyengine? Inabidi afe tu hakuna namna nyengine hapo”
“Tutafute njia nyengine bwana lakini sio kumuua” Mrutu alipinga.
“Basi iseme hiyo njia, sio unasema tutafute njia nyengine halafu hujui pia hiyo njia ni ipi”
“Acha mimi niende, halafu baadae nitakutafuta tujue tunafanyaje” Mrutu aliongea hivyo huku akinyanyuka kwenye sofa alilokaa.
“Sawa wewe nenda ila jua hakuna njia nyengine salama zaidi ya hiyo” Moto aliongea hivyo huku akiigamiza mgongo wake kwenye sofa.
“Kwani Mata hajarudi bado huko alipoenda?” Mrutu aliuliza hivyo huku akiwa ameshika kitasa cha mlango akitaka kuufungua atoke nje.
“Hajarudi bado, ila jana nimeongea nae akasema kesho ndio anarudi”
Mrutu aliposikia hivyo, akafungua mlango na kutoka nje ya nyumba hiyo na kuelekea anapopajua yeye.
“Huyu jamaa ndie alieleta pingamizi hadi yule mtoto hatukumuua tangia kitambo, sidhani kama yote yangetokea haya kama angekufa muda ule” Moto aliongea pekeake baada ya Mrutu kuondoka nyumbani kwake. Akachukua simu na kupigia namba anayoijua yeye na kuiweka sikioni.
“Safi… leo nataka tukutane kwenye ile baa yangu kuna kazi nataka niwape, saa mbili usiku” Alipoongea hivyo, akakata simu na kujiinua kwenye hilo sofa na kuingia ndani.
“Watu tunatiana presha tu saa hizi” Alimalizia maneno hayo akiwa anaufunga mlango wa chumbani kwake.
Majira ya usiku kwenye baa ya Moto ilioko maeneo ya Sahare, palionekana pamechangamka kwa mishemishe za walevi na wasiokuwa walevi waliojumuika kwenye baa hiyo. Kwenye meza iliyokuwa mbali kidogo na zilipo meza nyengine, kulikuwa kuna watu watatu wamekaa kuizunguka meza hiyo, mmoja wao alikuwa ni Moto huku wale wawili hatujapata bado kuwaja.
“Sasa wazee wa kazi nimemiita hapa kuna kazi nataka niwape” Moto aliongea kuwaambia hao watu aliowaita wazee wa kazi.
“Tunakusikiliza mkubwa” Jamaa mmoja wapo aliongea.
“Kuna mtu nataka katika hizi siku mbili awe yupo tayari kwa mazishi na ninaamini hilo nyie mnaliweza” Moto aliongea.
“Ni mwanaume au mwanamke?” Jamaa aliuliza.
“Ni mwanaume, tena kijana mdogo tu” Moto aliongea.
“Kazi rahisi sana hiyo, tulidhani ni mwanamke, kidogo angechelewa kufa” Jamaa aliongea.
“Kwanini?” Moto aliuliza.
“Kwasababu tusingemuacha hivi hivi kabla ya kifo chake, ila kwavile ni mwanaume, basi itakuwa ni rahisi tu. Chamuhimu ni wewe kutupa ‘information’ ya huyo mtu halafu utuambie unataka kwa muda gani awe tayari kwa mazishi basi” Jamaa aliongea.
Moto alitoa simu yake na kuiminyaminya kisha akawapa watu hao hiyo simu. “Mtu mwenyewe ndio huyo hapo” Mrutu aliongea.
“Hahahah!! Mtoto mwenyewe kumbe ni mzuri namna hii?” Jamaa mwengine ambae alikuwa kimya muda wote, aliongea hivyo baada ya kuiona picha ya Koplo Hemedy.
“Ni askari huyo” Moto aliwaambia.
“Huyu hatakama angekuwa komandoo wala sisi asingetupa shida kamwe” Jamaa wa mwanzo aliongea.
“Tuambie anapatikana wapi ili hiyo kazi tuifanye kesho” Jamaa wa pili aliongea.
Mrutu aliwaelekeza sehemu anapopatikana Koplo Hemedy na na kila kitu kuhusiana na yeye, yani muda anaorudi nyumbani na vitu vyengine kama hivyo. Haikujulikana vyote amevijulia wapi, ila ndio hivyo aliwaambia watu hao. Baada ya kumaliza kuwaelekeza, wakaelewana kiasi cha pesa kutokana na hiyo kazi, kisha jamaa hao wakaondoka wakimuacha Moto akitafuta viwanja vyengine vya kuenda kujirusha usiku huo maana alijua kazi imefika mikono salama.
* * * *
Siku iliyofuata. Koplo Hemedy alitoka kwenye nyumba yake na kupanda kwenye gari lake. Akalitoa nje na kushika njia ya panda ya msambweni na kutokea mabanda ya papa. Akaachana na ‘round about’ na kushika uelekea wa njia ya mkuu wa mkoa. Akanyoosha na njia hiyo hadi pale alipoiona Nyinda Hotel mbele kidogo akapaki gari kwenye jengo moja liliokaribu na Hotel hiyo kisha akashuka kwenye gari na kuanza kupiga hatua kuelekea ndani ya jengo hilo.
“Mambo mrembo” Koplo Hemedy alimsalimia binti aliemkuta mapokezi baada ya kufika hapo. Usoni mwake alipambwa na tabasamu huku akiwa funguo yake ya gari akiizungusha zungusha kwenye kidole chake cha shahada.
“Poa. Nikusaidie nini?” Binti huyo alijibu na kuuliza akiwa na yeye amepambwa na tabasamu usoni mwake.
“Kuna shida mbili nataka unisaidie, ila moja utanisaidia baada ya kuimaliza nyengine” Koplo Hemedy aliongea huku akiwa bado na tabasamu usoni mwake.
“Ok, nakusikiliza” Binti huyo alijibu huku akiwa ameweka pozi la kusikiliza hizo shida.
“Kwanza Mr Mata nimemkuta?” Koplo Hemedy aliuliza.
“Bosi hayupo amesafiri ila leo ndio anakuja”
“Sawa, asante kwa ushirikiano wako. Nikutakie kazi njema, acha mimi niende nitarudi kesho kuja kumuona” Koplo Hemedy alipoongea hivyo, akaanza kupiga hatua kuondoka hapo, ila alipofika mbele kidogo kama hatua tano, akageuza na kurudi pale mapokeza.
“Samahani, nilikuambia nina shida mbili lakini nimekutajia moja, ila pia nilikuambia nitakuambia shida ya pili baada ya kuimaliza ya kwanza. Lakini ya kwanza sikuifanikisha ila kesho nitakaporudi tena ‘ofcourse’ nitakuambia” Alipoongea hivyo akaanza tena kupiga hatua kutoka humo akimuacha binti huyo akimuangalia mpaka pale alipopotea kwenye upeo wa macho yake.
Koplo Hemedy baada ya kutoka nje ya jengo hilo, akapanda kwenye gari lake na kurudi na njia ile ile aliyokuja nayo, ila sasa alipofika njia panda ya Msambweni, alinyoosha moja kwa moja hadi kituo cha polisi Mabawa. Alipofika kituoni hapo, akashuka kwenye gari na kuingia ndani hadi kwenye ofisi yake ilipo.
Majira ya saa nane mchana, alitoka kituoni hapo na kuingia kwenye gari lake na safari ya kurudi nyumbani kwake ikaanza. Wakati akiwa barabarani kuelekea nyumbani kwake, kuna pikipiki kubwa juu yake wakiwa wamepanda watu wawili lilikuwa likimfuata nyuma pasi na yeye kujua. Aliongozana nalo hadi alipofika nje ya geti la nyumba yake, akashuka kwenye gari na kwenda kufungua geti kisha akarudi tena garini na kuliingiza ndani, akarudi tena kufunga geti na akaelekea moja kwa moja ndani ya nyumba hiyo.
Huku nje wale wale watu waliokuwa wamevaa ‘Helment’ vichwani mwao, walikuwa wapo mbali kidogo na ilipo nyumba ya Koplo Hemedy, wakaonekana kama wanashauriana kitu, kisha wakawasha pikipiki lao na kuja hadi nje ya geti la nyumba ya Koplo Hemedy. Wakashuka na kuvua makofia hayo, hapo ndipo sura zao zilipoonekana, walikuwa ni wale watu waliokuwa jana wakipewa kazi ya kumuua Koplo Hemedy na Moto.
Mmoja akagonga geti kipindi hicho Koplo Hemedy alikuwa yupo sebuleni amevua fulana na kubaki tumbo wazi huku akiwa anamenya matunda. Sauti ya kugongwa kwa geti aliisikia, akaipuuzia kwa mara ya kwanza ila ikajirudia tena. Ikambidi aache alichokuwa anafanya na kuinuka hapo hivyo hivyo tumbo wazi na kwenda getini kujua ni nani anaegonga. Alipofika akafungua geti dogo na kukutana na ngumi nzito ya uso ilimfanya kurudi nyuma huku mikono yake akiwa ameiweka usoni mwake.
Jamaa hao wakaingia ndani haraka na kumpiga teke la tumbo na kumfanya Koplo Hemedy agugumie kwa maumivu hayo. Jamaa mmoja akachomoa bastola na kumnyooshea yeye. Koplo Hemedy kuja kuitoa mikono yake usoni aangalie ni wakina nani hao waliomvamia. Alikutana na domo la bastola likimuangalia yeye. Akapatwa na hofu, hakuzijua hizo sura na wala hakuwahi kuziona sehemu yoyote ile. Akabaki akiwa anatetemeka kwa hofu maana alijua vyema kazi ya kifaa hicho hakina mas’hara hata kidogo.
“Ongoza njia ukafie ndani ya nyumba yako” Jamaa huyo aliemnyooshea bastola, alimuambia hivyo na kumfanya Koplo Hemedy kurudi ndani huku akiwa mikono ameiweka juu. Waliingia kwa staili hiyo hiyo hadi sebuleni.
“Geuka nyuma ushuhudie kifo chako kinavyoenda kukukuta punde tu” Jamaa alimuamrisha Koplo Hemedy na kumfanya ageuke nyuma kitaratibu kabisa. Jamaa huyo baada ya kuona Koplo Hemedy ameguka kuwaangalia wao. Akamuangalia mwenzake usoni na mwenzake akampa ishara iliyomfanya jamaa huyo kuiondoa usalama bastola aliyoishika huku akianza kuminya ‘triger’ tayari kuruhusu risasi itoke kwenye tundu la bastola hiyo.
.
“Usipige risasi, utajaza nzi, hiyo haina kiwambo cha kuzuia sauti” Jamaa mwengine alimuambia yule mwenzake alieshika bastola. Ikabidi wamuamrishe Koplo Hemedy akae kwenye sofa, sofa lilelile ambalo mwanzo alikuwa amekaa juu yake akimenya matunda kabla haijagongwa hodi. Hilo likawa ni kosa pasi na wao kujua. Akarudi kinyume nyume na kukaa, miguu yake akaibananisha kwa chini kuificha ile sahani ambayo ina matunda na kisu kwa juu.
Wale jamaa mmoja wapo yule ambae hakushika bastola akaanza kupiga hatua kuelekea kwenye kordo inayotenganisha vyumba vya hiyo nyumba, walitaka kabla hawajamuua Koplo Hemedy, waisachi hiyo nyumba na kuchukua chochote kinachobebeka kwa urahisi halafu waondoke nacho. Yule jamaa aliekuwa akienda vyumbani, alipofika kwenye kona ya kuenda kwenye kordo ya kuingia vyumbani, yule mwenzake huku nyuma alikuwa akimuangalia yeye huku akiwa amemnyooshe bastola Koplo Hemedy.
Koplo Hemedy akaona hiyo ndio bahati ya mtende, hakutaka kuichezea hata kidogo. Pale pale akapeleka mkono wake wa kulia chini akakivuta kile kisu na kukirusha kwa ustadi mkubwa hadi kwenye mkono wa yule alieshika bastola. Jamaa alitoa ukelele wa maumivu huku bastola ikimdondoka chini, ukelele huo ulimfanya yule mwenzake kuchungulia haraka kutaka kujua ni kipi kilichomfanya mwenzake akapiga kelele namna hiyo. Alipochungulia alikutana na kipande cha chungwa lilichomenywa na kukatwa katikati. Kipande hicho kilimpiga kwenye macho na kumfanya jamaa aanze kulia kama mtoto mdogo kwa macho yake kupata uchungu wa maji maji yenye ladha ya ugwadu ya chungwa.
Koplo Hemedy haraka akainuka pale na kuiwahi bastola iliyokuwa chini, kisha akampiga yule jamaa aliekuwa kaishika ngumi ya taya na kumfanya jamaa akunje sura na kumfanya afananiane na nyani mzee. Kabla hajakaa sawa, akampiga na ngumi nyengine mbili zaa mbavu. Yule jamaa kule aliepigwa kipande cha chungwa cha macho. Alikuja mbio huku akiwa bado anapepesa pepesa macho, akawa anarusha ngumi za kibwege kumuendea Koplo Hemedy. Ila zote alizihepa na kumpiga ngumi moja ya mdomo, Jamaa akainama kwa maumivu, hapo akampiga dochi moja la kidevu na kumfanya atoe mguno kama wa mbuzi aliepigwa kigongo cha kichwa wakati akila mahindi ya watu.
Dochi hilo alilopigwa lilimfanya aende kutua chini chali. Jamaa mwengine akampiga Koplo Hemedy teke la mgongo na kumfanya aende mbele kidogo huku ile bastola alioishika ikimtoka na kuangukia pembeni, akageuka na teke aina ya ‘yoko’ alilolipiga kwa kuuzungusha mguu na kuja kumpiga jamaa huyo la shingo na kwenda kujipigiza kwenye ukuta. Yule jamaa alielala chini baada ya kupigwa dochi la kidevu, pale alipoangukia ndio pale kile kisu kilipoanguakia, akakiokota na kuinuka nacho kwa kummendea Koplo Hemedy aliekuwa akidili na yule mwenzake.
Koplo Hemedy alikuwa akimuona kupita kioo cha kabati la vyombo lililokuwa mbele yake, akawa anamsubiri afike karibu yake amuonyeshe kazi. Yule jamaa baada ya kudhani hajaonekana kwa hilo analotaka kulifanya, akachomoka kwa kasi huku kisu akikiweka mbele kwajili ya kumchoma nacho Koplo Hemedy cha mgongo. Hapo Koplo akasogea pembeni na kumfanya jamaa apite mazima kisha Koplo akamsindikiza na teke la mgongo na kumfanya jamaa kwenda kuingiza uso wake kwenye kioo cha kabati la vyombo.
Akapiga kelele kwa maumivu huku kisu akikiachia bila kupenda na kuanza kurusha mikono yake kwa kiwewe huku kichwa chake kikiwa ndani ya kabati baada ya kupenyeza kwenye kioo. Yule jamaa mwengine, akainuka pale ukutani na kuchomoa mchuma wa pazia na kwenda nao mbio mbio huku akipiga kelele kama mwehu domo likimtoka udenda ulichanganyika na damu, dhamira yake ilikuwa ni kumpiga na huo mchuma Koplo Hemedy aliekuwa nyuma ya yule mwenzake aliezamisha kichwa kwenye kioo cha kabati pasi na kukitoa. Yule jamaa alieshika mchuma aliuvuta kwa nguvu zake zote kutaka kumpiga nao Koplo wa kichwa, ila Koplo aliinama na kuufanya mchuma huo upite kwa kasi na kwenda kumpiga mwenzake wa mgongo.
Yule jamaa aliezamisha kichwa kwenye kioo cha kabati, baada ya kupigwa mchuma huo kwenye mgongo wake kwa nguvu. Alijikuta akikichomoa kichwa chake bila kupenda kwenye vioo hivyo kwa maumivu ya huo mchuma uliotua kwenye mgongo wake. Lahaula!! Sura yake ilitisha kwa kuingalia kama una moyo mwepesi, sura nzima ilikuwa na vipande vipande vya vioo, akabaki akipiga kelele kama mwehu huku mikono yake akiirusha rusha hewani. Yule jamaa mwengine baada ya kumuona mwenzake akiwa katika hali hiyo, alijikuta kwa mshtuko akiuachia ule mchuma na kumsogelea mwenzake pale alipo. Koplo aliuokota ule mchuma na kumpiga nao wa mgongo na kumfanya jama huyo ajikunje na kukaa chini bila kupenda. Kisha hapo akaiokota bastola iliyokuwa chini yake na kuwaelekezea watu hao.
“Haya inukeni taratibu hapo mlipo na mkae pale mbele” Koplo Hemedy aliwaamrisha hivyo na kuwafanya watu hao wakae sehemu walipoelekezwa huku kila mmoja akiugulia maumivu yake hasahasa yule aliechomwa na vipande vya vioo usoni mwake.
“Wewe kichwa, haya mtoe mwenzako hivyo vioo usoni mwake, na umtoe taratibu” Jamaa huyo aliebatizwa jina la ‘kichwa’ alifanya kama alivyoambiwa. Wakati akimtoa hivyo vipande vya vioo mwenzake, yule jamaa mwengine alikuwa akipiga kelele za nguvu kwa maumivu, zoezi hilo lilichukua dakika moja na kuisha. Kisha Koplo Hemedy akaliendea kabati hilo hilo lililovunjwa, akatoa kichupa ambacho ndani yake kilikuwa na dawa aina ya spiriti, akakifungua na kuenda kumiminia yule jamaa yote usoni mwake. Jamaa alipiga kelele ambazo sidhani kwamba katika maisha yake alishawahi kupiga kelele kiasi hicho. Alikuwa akipiga kelele huku mikono yake ikiwa karibu kabisa na uso wake, hakuelewa aushike uso wake au auache tu. Mikono ilikuwa ikimtetemeka mithili ya kifaranga kilichomwagiwa maji ya baridi.
Baada ya dakika tano, jamaa akatulia huku akiwa bado analia chini chini. Koplo Hemedy muda wote alikuwa akiwaangalia tu pasi na kuwafanya chochote. Alipoona jamaa katulia huku akiugulia maumivu yake chini chini. Akachukua simu yake na kuipiga namba anayoijua yeye kisha akaiweka sikioni.
“Njoo nyumbani kwangu na askari wawili, sasa hivi” alikata simu na kuwaangalia jamaa hao walivyogwaya kwa kusikia habari za askari, wakajua tayari jela inawahusu, hawakuwa na namna ya kufanya. Wakabaki hapo chini wametulia kimya na hofu imewatanda mioyoni mwao kama watoto wakiume wanao subiria kutairiwa. Walionywa kuwa huyo wanaetaka kuenda kumuua ni askari lakini wao wakajibu jeuri baada ya kuonyeshwa picha ya kijana mwenye sura nzuri na ya upole, wakajua ni lelemama tu kama walivyo vijana wengine wenye sura kama hizo.
Baada ya dakika kumi, kuliingia askari watatu ndani humo, walipofungua mlango wa hapo sebuleni, walipigwa na butwaa baada ya kuwaona watu wawili wakiwa wamekaa chini na kwenye miili yao hakutamaniki kwa damu huku mmoja sura yake ikiwa nyekunde mithili ya nyama ya kitimoto.
“Afande vipi tena, mbona hali hii?” Askari mmoja alimuuliza Koplo Hemedy baada ya kutoielewa hali hio.
“Hao jamaa kuna kitu walikitaka kutoka kwangu, lakini sasa kimewageukia wao. Embu wakusanyeni tuondoke nao” Koplo Hemedy aliongea hivyo huku akiingia chumbani kwake, aliporudi alikuwa amevaa fulana tayari na kuwakuta watu hao wakiwa tayari wanapingu mikononi mwao. Wakawatoa humo ndani na kuwapeleka kwenye gari la polisi lililopaki nje ya nyumba hiyo. Wakawatia kwenye gari hilo wao na pikipiki lao na safari ya kuenda kituoni ikaanza huku Koplo Hemedy akienda na gari lake.
Walipofika walishushwa mzega mzega hadi katika chumba cha mahojiano na kufungwa kamba ngumu kwenye viti. Koplo Hemedy alikaa kwenye kiti kilichokuwa kimewaangalia wao. Akawatazama kwa muda huku akiwatolea tabasamu, tabasamu la kejeli kisha akaanza kuwauliza maswali.
“Wewe kichwa, unaitwa nani jina lako halisi?” Koplo Hemedy alimuuliza. Ila jamaa akabaki kumuangalia tu kwa kiburi. Koplo Hemedy akatabasamu na kumuuliza swali hilo hilo yule mwengine ambao alipata maswahibu ya kuchomwa na vioo vya kabati. Ila jamaa na yeye akajifanya kiburi kama vile alivyokuwa mwenzake. Koplo kuona hivyo, akaona akiendelea kuwachekea watazidi kumletea kiburi. Bila kutarajia, jamaa yule aliepata maswahibu ya kuchomwa na vioo. domo lilimlegea mithili ya chupi saizi sitini na tisa kwa kimbaumbau baada ya kupokea ngumi nzito juu ya domo hilo. Akapiga kelele kama kichaa alieona fuko la makande jalalani likiokotwa na mbwa yatima mwenye njaa.
“Sudi….sudi. Naitwa Sudi Afande, nisamehe sana” Jamaa alibwabwaja huku domo likitoa damu iliyochanganyikana na ute kama misekure ya kwenye muvi ya ‘Uwanja wa Dhambi’ wale wahenga kama mimi ndio watakuwa wanaijua hii muvi.
“Huna baba wewe?” Koplo Hemedy alimuuliza huku akitabasamu.
“Khalfani. Masudi Khalfani” Jamaa lilitaja huku likilia kama mtoto mdogo alienyang’anywa puto na mwenzake.
“Nyumbani kwangu mmefuata nini?”
“Kukuua Afande, tusamehe sana, nisamehe sana”
“Nani aliemituma?”
“Moto. Mtu mmoja anaitwa Moto Afande” Koplo Hemedy hakuwahi kulisikia hilo jina wala hakujua mmiliki wa hilo jina ni nani.
“Ni nani na anaishi wapi?”
“Ni kijana mmoja anaemiliki baa inayoitwa Fire iliyoko kule Sahare Afande na anapoishi sipajui” Jamaa alijibu huku udenda ukimtoka mdomoni mwake. Alitia huruma kumtazama!
Akamgeukia na yule mwengine, akamuuliza jina lake, lakini akaonekana bado kiburi kimemjaa. Koplo Hemedy akatoka humo huku akiwa ametabasamu na aliporudi alikuwa ameongozana na askari mmoja wapo aliemuita kule nyumbani kwake. Mkononi alikuwa ameshika rungu kubwa kama la yule mchekeshaji wa bongo anaeitwa ‘Pembe’ ila rungu hili lilionekana kushiba kilo nyingi tofauti na lile. Alipofika hapo, akamfungua pingu yule jamaa kiburi na kumuamuru yule askari mwengine aishike mikono ya jamaa huku akiwa ameilaza juu ya meza iliyokuwa mbele yake. Askari huyo alishika mikono hiyo barabara na kuilazisha juu ya meza kwa nguvu.
Kisha hapo Koplo Hemedy alianza kuvipiga viganja vya mikono vya huyo jamaa. Mbona kiburi kiliisha? Alikuwa akilia kama mtoto huku akiomba asamehewe, lakini ndio kwanza Koplo Hemedy wala hakujali hizo kelele, yeye aliendelea kuliinua juu hilo rungu na kulitulisha juu ya viganja vya huyo jamaa kiburi hadi pale alipotaja jina lake ndio Koplo akaacha kufanya hivyo.
“Mwinyiheri Afande. Mwinyiheri Mbwana” Jamaa alitaja majina yake huku akiwa mikono ameining’iniza kwa mbele mithili ya yale mazombi ya kwenye muvi ya ‘Wrong Turn’ viganja vilikuwa havitamaniki kwa kupondwa na hilo rungu. Akajutia ubishi wake, akajutia kumvamia mtu aliedhani ni nyoronyoro baada ya kumuona kwenye picha, zaidi ya yote, akajutia kuifanya hiyo kazi.
“Anhaa!! Kumbe unaweza kuongea bila tabu. Sasa kwanini umetaka yakukute yote hayo wakati kumbe uwezo wa kujibu ulikuwa unao?” Koplo Hemedy alimuuliza maswali kama yale aliyomuuliza yule mwenzake na kujibu vilevile. Baada ya kuridhika na kuwahoji kwa siku hiyo. Akawachukua na kuwapeleka sero kisha yeye akaondoka kuelekea nyumbani kwake.
Alipfika alimkuta Konstebo Hilda akiwa na yeye ndio anafika hapo. Akamuelezea kila kitu kilichomkuta na kumfanya Konstebo Hilda kushangaa sana huku akimpapole mpenzi wake. Wakaingia wote sebuleni na Konstebo Hilda akashangaa mazingira ya hapo yalivyokuwa hovyo. Ikambidi achukue jukumu la kuisafisha sebule hiyo huku Koplo Hemedy akiingia chumbani kwake. Alipotoka alikuwa ameshika ‘laptop’ mkononi mwake na kwenda kukaa nayo kwenye sofa, kipindi hicho sebule hiyo ilikuwa ishamaliza kufanyia usafi. Konstebo Hilda akaenda kukaa kwenye sofa alilokaa Koplo Hemedy. Hapo Koplo Hemedy kabla hajaiwasha hiyo ‘laptop’, akamuambia mpango wake wa kuwasaka wauwaji wa wazazi wake. Kisha akaiwasha na kuiangalia wote ile video. Sasa alikuwa ameikopi humo humo ndani ya ‘laptop’.
Wakati wakiwa wanaiangalia hiyo video. Koplo Hemedy aliona kitu chengine kilichomshitua kwenye hiyo video. Akawa anairudia rudia mara nyingi sehemu moja hadi pale alipoulizwa kunanini na mpenzi wake.
“Hembu muangalie huyu mtu kwa umakini anavyolitamka hili neno” Koplo Hemedy alimjibu. Video hiyo haikuwa na sauti bali ni picha mjongeo tu. Na sehemu hiyo ni ile baada ya kumuua baba yake na Koplo Hemedy, Moto alipomuambia Mata amuambie Mrutu aweke gari vizuri ili waondoke pale. Hapo Hemedy alianza kuvuta kumbukumbuka kabla ya yeye kuzimia baada ya kushuhudia kifo cha baba yake.
“Mshtue MRUTU aweke gari sawa tuondoke kabla nzi hawaja kuja”. Hayo ndo maneno ya mwisho kuyasikia kabla hajazimia. Na nikweli baada ya kuyakumbuka akafananisha maneno hayo na huo mdomo wa Moto unavyoongea akakuta vikiendana sawa kabisa, tena bila kurefusha wala kufupisha.
“Ina maana Baba mdogo pia alishiriki katika kifo cha wazazi wangu?” Alijiuliza swali hilo na kumfanya Konstebo Hilda asimuelewe hata kidogo.
“Hapana, haiwezekani” Koplo Hemedy aliongea hivyo huku akiwa amebananisha meno yake kwa gadhabu ya hali ya juu.
“Mpenzi nini, mbona sikuelewi? Baba yako mdogo ameshiriki vipi kwenye kifo cha wazazi wako?” Konstebo Hilda alimuuliza hivyo huku akiwa anamuangalia usoni.
“Ameshiriki ndio, ameshiriki na uhakika ninao” Akamgeukia usoni na kumuambia. “Kama unataka kuamini haya, embu fuatiliza maneno haya na huu mdomo wa huyu mtu kwenye hii video ndio utaamini”
“Mshtue MRUTU aweke gari sawa tuondoke kabla nzi hawaja kuja” Koplo Hemedy aliongea kwa sauti maneno hayo na kumfanya Konstebo Hilda kuyafuatiliza na kwa kuuangalia mdomo wa huyo mtu kwenye hiyo video na kukuta yameendana sawa kabisa. “Mmmh!” akaishia kuguna tu na kumuangalia mpenzi wake usoni.
“Hilda siamini hata kidogo. Yani bamdogo Mrutu anaweza kushiriki kumuondoa kaka yake duniani kisa mali tu. Halafu eti mahakamani akadai eti kuwa mali hazikuwa ni za baba” Alipofika hapo kuna kumbukumbu nyengine ikamjia kichwani mwake. Akakumbuka siku ile alipomuona baba yake huyo mdogo akiwa ameongozana na wauwaji wa wazazi wake wakiingia kwenye nyumba yake. Siku ile alidhani watu hao wanampango wa kumuua baba yake mdogo pia ila leo amejidhihirishia mwenyewe kuwa baba yake mdogo alikuwa yupo kwenye mapango na wauwaji hao.
“Subiri niende huko huko kwake” aliongea hivyo huku akinyanyuka hapo. Konstebo Hilda akataka kuungana nae, ila alikatishwa na simu iliyotoka kwa IGP Ganjo akimtaka kituoni kwa muda huo. Hakuwa na la kupinga, akaondoka hapo huku akimuacha Koplo Hemedy akiondoka kuelekea kwa Mrutu.
Nyumbani kwa Mrutu. Mrutu alimuita Moto hapo nyumbani kwake baada ya kupata njia nzuri ya kumdhibiti Koplo Hemedy, asiwagundue au asifanikiwe kwa kuwapata wao. Moto alifika hapo baada ya nusu saa kuitwa na kuingia ndani ya nyumba hiyo. Akaenda kukaa kwenye sofa sebuleni alipokuwa amekaa Mrutu akimsubiri yeye.
“Kaka naona unatembea na basotla kila sehemu?” Mrutu alimuuliza hivyo Moto aliekuwa ameitoa bastola yake kiunoni na kuiweka juu ya sofa baada ya kumsumbua pale alipokaa.
“Si unajua tena ulinzi popote. Duniani hakuna wema kaka” Moto aliongea huku akiiangalia bastola yake utafikiri ndio anaiyona kwa mara ya kwanza.
“Duh! Ni Kweli”
“Niambie kaka umepata mpango gani wa kumdhibiti huyo dogo” Moto aliongea hivyo huku akijua anamzuga Mrutu tu maana alishatuma watu kumuua Koplo Hemedy.
“Njia nimeipata baada ya kufikiria sana na ninzu…..” Wote walishtuka baada ya mlango wa sebuleni kufunguliwa kigadhabu. Macho yao wakayapeleka hapo na kumkuta Koplo Hemedy akiwaangalia kwa hasira kuu. Macho yaliwatoka pima mithili ya mjusi kafiri aliebanwa na mlango baada ya kujua hasimu wao ndie alieingia hapo. Moto akawahi kuichukua bastola yake na kumuelekezea Koplo Hemedy.
Koplo Hemedy alipigwa na taharuki baada ya kumshuhudia baba yake mdogo akiwa na muuwaji wa wazazi wake. Ndio lazima sura aikumbuke si ametoka kuiona kwenye ile video muda si mrefu? Akabaki akiwa hajui afanye nini. Machozi yalianza kumtoka taratibu huku akiwa bado amesimama hapo hapo mlangoni haamini macho yake kama baba yake mdogo angeweza kumuua kaka yake kisa mali tu, akajikuta akianza kupiga hatua za taratibu akiwaendea wao. Ila alisimamishwa na ukelele wa Moto aliekuwa amemnyooshea bastola yeye.
“Simama hapo hapo mbwa wewe na leo nakuua mbele ya baba yako mdogo” Moto aliongea hivyo huku akiwa kasimama macho akiwa kayakaza kumuangalia Koplo Hemedy.
“Moto unataka kufanya nini tena nyumbani kwangu? Hujui kama hiyo ni kesi, tena itaniangukia mimi mwenye nyumba, acha hizo bwana!” Mrutu aliongea hivyo huku akiwa na yeye amesimama. Hapo Koplo Hemedy alivyosikia jina la mtu huyo alieitwa ‘Moto’ akajua ndio huyo huyo aliewatuma wale watu kuja kumuua nyumbani kwake, akazidi kupandwa na hasira na mtu huyo.
“Mimi nataka nipoteze ushahidi kabisa, huyu mtu alitakiwa afe tangu zamani ila wewe ukajifanya kumkingia kifua, sasa leo namuua mbele ya macho yako” Moto aliongea huku bado bastola amemuelekezea Koplo Hemedy.
“Usitake kuchukua maamuzi ya haraka haraka, embu subiri tuyaongee tuyamalize kaka” aliongea hivyo huku akimfuata Koplo Hemedy pale aliposimama. “Mwanangu embu kaa chin…”
“Nani mwanao, tena toka mbele yangu muuaji mkubwa wewe” Koplo Hemedy aliongea hivyo huku akimsukuma Mrutu. Msukumo huo ulimfanya akampamie Moto aliekuwa nyuma yake na Moto bila kutarajia, aliminya ‘trigger’ na risasi ikaenda kupiga kwenye bega la Mrutu. Hapo hapo Koplo Hemedy akamuwahi kwa teke la mkono na bastola ile ikaenda hewani. Moto akabaki kuiangalia bastola ile kule juu na kuisubiria ishuke ili aidake. Koplo Hemedy baada ya kumuona mtu huyo ameinua shingo yake kuangalia juu ilipo bastola. Akampiga ngumi mbili za haraka haraka za kwenye koromelo na kumfanya Moto arudi nyuma huku akiwa ameishika shingo yake. Jambo la kuvuta punzi na kumeza mate akiona kabisa hivi hivi vikimsaliti.
Wakati akirudi nyuma alimpamia Mrutu aliekuwa amelala chini kwa maumivu ya bega lake na kujikuta na yeye akienda chini. Koplo alimruka Mrutu na kumfuata Moto aliekuwa chini akigaagaa huku akiwa ameishika shingo yake. Alipofika pale alipo, alimshika kola ya shati alilovaa na kumuinua juu, kisha akampiga vichwa vitatu vya pua na kuifanya pua hiyo ipinde kwenda kushoto huku ikitoa damu kwenye tundu zote mbili. Akamuinua tena na kumpiga ngumi zisizo na idadi za kifua na kumfanya acheue damu kama sio kutapika kabisa.
Akamuinua tena huku akiwa analia kwa hasira na kumpiga ngumi nyingi za uso, na alipokuja kumuachia uso wote ulikuwa hautamaniki kwa damu kama nyama ya kuku buchani. Akamfuata pale chini alipolala na kumpiga ngumi moja ya nguvu ya mdomo. Halikuwa swala la kubisha au kupinga kwamba bwana huyo hata kama akipona hapo basi atakuwa ni kibogoyo. Meno yalipukusutika kama punje za mahindi kwenye gunzi huku domo likitoa damu iliyochanganikana na ute kama ng’ombe alierogwa.
Koplo Hemedy aliiende bastola iliyokuwa chini kwa hasira na kumuelekezea Moto kwa wakati huo alikuwa amepiga magoti akiomba msamaha pasi na kuongea. Ataongeoaje wakati domo linavuja damu mithili ya bomba la mvua? Tena sehemu hii ndio ile ile alipompigia mama yake na Koplo bastola ya shingo. Koplo Hemedy alipokumbuka hilo, wala hakuna mshauri nahasa wa kumshauri hilo lililoko kichwani mwake na yeye akashaurika. Hapo hapo akampiga risasi ya shingo na kumfanya Moto atoe macho kwa taharuki ya kukutana na malaika mtoa roho kwa mara ya kwanza tangu azaliwe.
Akamuongezea risasi nyengine mbili za kifua, na Moto akabaki mdomo wazi huku akionekana kama vile kuna kitu anataka kusema, lakini alijikuta akifumbwa mdomo na risasi aliyopigwa mdomoni, akaenda chini na kutulia kimya akiwa hawezi tena kunyanyuka. Atanyanyukaje wakati roho yake imeshaagana na mwili muda mfupi uliopita? Koplo Hemedy akabaki kulia tu kwa uchungu huku akiwataja wazazi wake akiwa amepiga magoti chini.
Mrutu muda wote alikuwa ameshika bega lake sehemu lilipo jeraha alilopigwa risasi na hayati Moto huku akiwa haamini hata kidogo kwa anayoyaona, alikuwa ameacha mdomo wazi huku akimuangalia Moto pale chini alipolala pasi na kuwa na roho yake kwa jinsi mwili wake ulivyo chafuliwa. Muda huo huo Konstebo Hilda aliingia humo ndani huku akiwa ameongozana na askari watano wenye silaha mikononi mwao.
Konstebo Hilda alimkimbilia Koplo Hemedy pale alipo na kumuangalia kama yupo salama huku wale askari wengine wakiitoa maiti ya Moto huku wengine wakimchukua Mrutu mzega mzega hadi kwenye gari la polisi. Konstebo alimuinua Koplo Hemedy pale chini alipo na kutoka nae nje, huko walikuta gari la polisi limeshaondoka hapo na wao wakaingia kwenye gari alilokuja nalo Koplo Hemedy hapo na kuondoka kuelekea kituoni.
“Koplo, unauhakika kwamba yule marehemu ndie alieuwa wazazi wako akishirikiana na wenzake akiwemo baba yako mdogo?” IGP Ganjo alimuuliza hivyo baada ya kuwa nae ofisini kwake.
“Mkuu uhakika ninao na ushahidi pia ninao” Koplo Hemedy alimuambia IGP Ganjo hivyo wakati huo alikuwa ameshanyamaza kulia.
“Unaweza ukanipa huo ushahidi, maana hii kesi ya mauwaji itakuhusu kama ukiwa hauna ushahidi kwa hicho unachosema” IGP aliongea na kumfanya Koplo Hemedy kumtolea flash yenye video kisha IGP akaichomeka kwenye Kompyuta yake na kuiangalia kwa umakini hiyo video.
“Hapa kidogo ninayo njia ya kukusaidia kwa kukuokoa na hilo zahma mahakamani…. Unajua Koplo kama usingekuwa na huu ushahidi, basi hii kesi ingekuangukia wewe na wala usinge weza kuchomoka mikononi mwa sheria” akamrudishia flash yake na kumuambia.
“Umesema bado wangapi?” IGP alimuuliza.
“Bado watatu mkuu na mmoja nimeshapajua ofisini kwake” Koplo Hemedy alijibu.
“Embu ngoja kwanza mara moja” IGP aliongea hivyo, kisha akasimama na kuliendea kabati la kuhifadhia mafaili, akachangua changua na kurudi na faili moja, akaliweka juu ya meza na kulifunua, humo ndani kulikuwa na picha nyingi nyengine za kutisha zilizojaa damu na majeraha mengi kwenye miili hiyo ya kwenye hizo picha. Akaanza kuangalia picha moja baada ya nyengine hadi pale alipopata picha mbili zenye taswira zilizokuwa zimechafuka kwa damu na majeraha. Akaziangalia vizuri na kumuomba Koplo Hemedy ile flash tena na kuichomeka kwenye kompyuta yake, kisha akasema.
“Hawa watu wawili kwenye hii video yako ndio hawaapa kwenye hizi picha. Walikutwa wamekufa kwenye daraja la Amboni miaka sita iliyopita” Akamuangalia usoni Koplo Hemedy huku akitabasamu.
“Najua unajiuliza nimewakumbukaje hawa watu baada ya kuwaona kwenye hii video. Ila iposiku na wewe utakuja kujua mimi nimewakumbukaje kama sio kuwajua hawa watu kwenye hii video yako… Hawa watu wameshakufa zamani na muuwaji hajapatikana hadi leo, sasa kumebakia mtu mmoja tu na ndio huyo mwengine kwenye hii video, na bilashaka ndio huyo uliesema unapajua anapofanyia kazi. Nitatuma askari wakamkamate na wamlete hapa kituoni” IGP aliongea.
“Lakini mkuu naomba nikamchukue mwenyewe huyu” Koplo Hemedy aliongea.
“Hapana Koplo, ukienda wewe unaweza hata kumuua kwa hasira ulizokuwa nazo kwa mtu huyo, ni bora waende askari wengine wamlete halafu atahukumiwa na mahakama lakini sio kumuua” IGP aliongea.
“Mkuu nakuahidi sitomfanya chochote hadi namleta hapa kituoni, kwahiyo nakuomba nimfuate mwenyewe Mkuu” Koplo Hemedy aliongea kwa kulalamika na kumfanya IGP Ganjo kumuangalia usoni kwa muda, kisha akasema.
“Unajua Koplo hiyo ni kesi ya mauwaji ikiwa utamuua. Lakini kwa vile wewe ni askari na unazijua sheria, basi mimi nakuruhusu uwende ila chunga sana usije ukaingia pabaya”
“Sawa mkuu” aliongea hivyo kisha akainuka na kupiga salut.
“Unaenda wapi?”
“Naenda kuongea na yule mtuhumiwa alieshiriki kwenye mauwaji ya wazazi wangu” Koplo Hemedy aliongea hivyo na kumfanya IGP kumruhusu aende. Akatoka na kwenda kwenye sero aliyomo Mrutu na kumchukua hadi kwenye chumba cha mahojiano.
“Hivi ni kweli bamdogo umeshiriki kwenye mauwaji ya wazazi wangu. Umeshiriki kuiondoa roho ya kaka yako kisa mali tu?” Koplo Hemedy aliongea hivyo huku dhahiri akionekana anaweza kulia muda wowote kuanzia hapo.
“Nisamehe sana mwanangu ni tamaa tu zile ndio zimeniponza na ninajuta sanaa” Mrutu aliongea huku akilia, kipindi hichi kwenye bega lake kulifungwa bendeji kwenye lile jeraha lake.
“Tamaaa, tamaa wakati baba yangu nakumbuka alikuwa akikupa chochote unachotaka hadi nikadhani mmelazaliwa tumbo moja kumbe mama tofauti. Au nikwavile hujazaliwa na mama nae?” Koplo Hemedy aliongea kwa hasira huku akimuangalia Mrutu kwa macho ya gadhabu.
“Hapana sio hivyo mwanangu, zile zilikuwa ni tamaa tu na ushawishi, lakini sikuwa na uwezo wa kufanya hivyo” Mrutu aliongea huku akilia sasa.
“Ok, ok. Na vipi kuhusu siku ile mahakamani ukasema kuwa zile mali hazikuwa ni za baba, kuna ukweli wowote hapo?” Koplo Hemedy alimuuliza.
“Hapana zile zilikuwa ni ‘trick’ tu kutaka kuzichukua zile mali, lakini hakuna ukweli wowote kwa kile kilichoongelewa pale mahakamani siku ile”
“Mko wa ngapi katika ule mpango wenu?”
“Tulikuwa watatu na mmoja ndio huyo uliemuua. Nisamehe sana Hemedy niko tayari kutoa ushahidi wote mahakamani mali zote zirudi mikononi mwako”
“Nasikitika kukuambia dhalimu wewe kuwa kifungo cha maisha kina kuhusu, subiri apatikane na huyo mwenzako, mtaenda kujibu mahakamani” Koplo Hemedy aliongea hivyo huku akiinuka kwenye kiti na kuondoka hapo huku akimuacha Mrutu akimuomba msamaha bila kikomo.
Majira ya usiku nyumbani kwa Koplo Hemedy, alikuwa yupo sebuleni kwake akiwa amekaa akiminyaminya ‘laptop’ yake. Hapo alionekana Konstebo Hilda akitokea jikoni na kuja kukaa karibu na Koplo Hemedy.
“Mume wangu chakula tayari, twende mezani tukale” Konstebo Hilda pamoja na kuwa ni askari, lakini sauti yake nzuri haikubadilika, ilikuwa ni ileile iliyochagizwa na mirindimo ya kipwani.
“Subiri kwanza nimalizie hapa nakuja sasa hivi” Koplo Hemedy aliongea hivyo pasi na kumuangalia mwanamke huyo usoni. Hapo Konstebo Hilda alionyesha kukasirika akabaki kuvimbisha mashavu yake kama chura mwenye mimba huku akiwa kageukia pembeni. Koplo Hemedy baada ya kumuangalia kwa jicho pembe na kumuona katika hali hiyo. Akaacha anachokifanya na kupitisha mkono wake kwenye kiuno laini cha mnyange huyo mdogo kabisa mwenye kumiliki miaka ishirini na moja tu hadi sasa.
“Ukinuna wewe kwenye moyo wangu ni msiba. Haijalishi ni kwa kiasi gani lakini na kuahidi kukupa mahaba. Yale ya wazee wa zamani naamini utashiba. Nakupenda mke wangu wewe ndio mama mimi baba”.
Koplo Hemedy alipoongea hivyo, Konstebo Hilda kule alipoelekezea uso wake akajikuta akitabasamu, tabasamu ambalo limetoka chini ya uvungu wa moyo wake kwa maneno hayo. Koplo Hemedy baada ya kuona mpenzi wake hajageuka huku upande wake. Akaendelea.
Hapo Koplo Hemedy alimbeba kwa kupitisha mkono wake wa kushoto kwenye shingo ya mnyange huyo huku wakulia ukikamata nyuma ya magoti na kumfanya binti huyo arushe rushe miguu huku akicheka. Alimbeba na kwenda nae kwenye meza ya chakula na kumuweka kwenye kiti na yeye akikaa kwenye kiti chengine. Muda wote Konstebo Hilda alikuwa na tabasamu usoni mwake huku akimuangalia kijana huyo kwa jicho ambalo lilionyesha akihitaji kitu fulani.
Waliendelea kula huku kila mmoja akiwa kimya huku wakiangaliana kwa zamu, ni vijiko tu ndo vilisikika hapo vikipigana vikumbo na sahani. Walipomaliza kula waliingia chumbani baada ya kuhakikisha kila kitu wamekiweka sawa huko nje.
* * * *
Siku iliyofuata wakajianda wote na kuelekea kituo chao cha kazi, walipofika Koplo Hemedy alimuacha Konstebo Hilda hapo na yeye kuondoka hapo baada ya kusaini na kuelekea kwenye kampuni ya Mata. Dakika kumi na tano zilitosha kumfikisha. Alipofika akapaki gari nje na yeye akaingia ndani na mapokezi akamkuta mwanamke yule yule aliekuweko jana.
“Habari ya leo mrembo?” Alisabahi huku usoni tabasamu likimjaa.
“Safi tu, za tangu jana?” Mwanamke huyo alijibu na kuuliza akiwa na yeye anatabasamu usoni mwake.
“Nzuri tu, sijui huyu jamaa nimemkuta?”
“Aaa bosi bado hajakuja, ila hii ndio mida yake ya kuja. Unaweza ukamsubiri hapo kwenye hilo sofa” Mwanamke huyo aliongea hivyo na Koplo Hemedy akaenda kukaa kwenye sofa lililokuwa hapo. Baada ya nusu saa baadae, aliingia Mata alionekana mwili wake kuridhika na hela. Alifika hapo mapokezi na kumsalimia ‘secretary’ wake.
“Bosi halafu kuna mgeni huyo hapo alikuwa anakusubiri” mwanamke huyo aliongea huku akimsontea kidole Koplo Hemedy. Muda wote huo Koplo Hemedy alikuwa akitabasamu tu baada ya kujidhihirishia kuwa mtu aliemfuata ndio huyo hapo mbele yake.
“Karibu ofithini huku” Mata aliongea hivyo kumuambia Koplo Hemedy. Ilionekana dhahiri hakumjua hata kidogo. Hata hivyo atamjuaje wakati alivyomuacha na sasa hivi alivyo ni tofauti? Wakaongozana wote hadi ofisini kwake, alipofika akamkaribisha kwenye viti vya wageni huku yeye akikaa kwenye kiti chake cha kuzunguuka.
“Karibu bwana nani kumbe…?” Mata aliongea hivyo huku akimuangalia mgeni huyo machoni mwake.
“Hemedy… Hemedy Muheshimiwa Bhachu au kwenye kazi yangu wananiita Koplo Hemedy” Koplo Hemedy alikuwa akiongea kwa tabasamu huku huyo anaeongea nae akiwa macho kayatumbua kama mtu aliekutana na mzuka wa Nsyuka macho kwa macho baada ya kusikia jina la mtu huyo. Aligwaya kwa si kitoto!!.
“U…umethema unaitwa nani?” Mata alimuuliza huku hofu, woga, wasiwasi na hamaniko vikiwa pamoja nae.
“Haina haja ya kurudia jina, nadhani hadi hapo ushanijua mimi ni nani” Koplo Hemedy aliongea.
“Unataka nini hapa ofithini kwangu?” Mata alijifanya kukaza wakati dhahiri uoga ulionekana waziwazi usoni mwake.
“Nimekuja kukuchukua tuende kituoni kisha mahakamani ukajibu mashtaka uliyodhani umeyakimbia miaka kadhaa nyuma”
“Sikilidha kijana, nitakupa petha kiathi chochote ukitakacho halafu uniache” Mata alijaribu kumshawishi.
“Hicho kiasi chochote cha pesa unachotaka kunipa nitakipata endepo utasimama pale kizimbani ukisomewa mashtaka yako, utakapo hukumiwa basi itapitishwa na hukumu ya kurudishiwa mali zangu zote ambazo mmezidhulumu”
“Kijana nitakupigia kelele dha mwidhi thatha hivi” Mata aliongea huku akiinua simu ya ofisini kwaajili ya kuita walinzi waje kumtoa Koplo Hemedy. Ila mkono wake ukagandamizwa hapo hapo juu ya hiyo simu na mkono ngangari wa Koplo Hemedy, akabaki akigugumia kwa maumivu huku akijaribu kujinasua, ila hakuweza.
“Sikuja kukuua na usinilazimishe kufanya hivyo kama ambavyo nimefanya kwa yule mwenzenu mnaemuita Moto” Macho ya Mata yalitoka nje sentimita tano na kurudi tena ndani kwa mshtuko alioupata kusikia taarifa hiyo.
“Una…unathema umemuua Moto?” Mata aliuliza huku uoga ukiongezeka mara dufu.
“Ndio nimemuua na sasa yuko monchwari akisubiria ndugu zake waje kuuchukua mwili wake na nitafanya hivyo na kwako kama utaleta ubishi wa aina yoyote… Au sijui nikuue tu na wewe ilinitimize roho mbili kuziondoa duniani…. Unajua kuua raha sana, acha kwanza nikuue halafu nikupeleke kituoni ukahifadhiwe huko kisha mwili wako upelekwe mahakamani kwenda kujibu mashtaka, naamini hiyo itakaa poa sana au wewe unasemaje?”
“Hapana kijana wangu uthiniue, nitakupa hata mali dhote, nithamehe thana” Mata aliongea huku akilia, ukumbuke wakati huo mkono wake bado unaadhibiwa kwa kuminyizwa juu ya simu ya mezani sijui ndio ya ofisini.
“Wewe mbona uliwauwa wazazi wangu huku unacheka, si inaonekana kitendo kile kilikufurahisha, acha na mimi leo nifurahi kwa kuitoa roho yako hapa ofisini kwako, hata hivyo litakuwa ni jambo zuri kwasababu nitakuwa naitoa roho yako kukiwa hakuna mtu yoyote anaeshuhudia kitendo hicho zaidi ya mimi na wewe tu”
“Nithamehe kijana, thirudii tena, mwendhio nina familia, nina mke na mtoto mmoja, sasa unadhani ukiniua mimi familia yangu itaishije” Maneno hayo yalimtia gadhabu Koplo Hemedy na kumfanya auachie ule mkono wake aliougandamiza kwenye simu na kumpiga ngumi mbili za jicho la kulia. Jicho hilo lilivimba kwa juu kidogo huku kwa ndani likibadilika rangi na kuwa jekundu kama limepakwa ‘lipstick’. Kisha akaivuta kwa mbele tai yake na kuufanya uso wake uje mzima mzima kwa mbele, hapo akampiga ngumi nyingi za uso na uso huo ukawa umevimba huku unatoa damu kama maji ya shukayo kwenye maporomoko.
“Mlivyoniulia wazazi wangu mlitegemea mimi niishije, niishi wapi? Au unaongea tu kwavile wewe ndio umefanya vile. Mmenifanya ninusurike kifo kwa kutaka kuchomwa moto bila hatia na raia waliodhani mimi ni mwizi kwa kutanga tanga usiku pasi na kujua nielekee wapi. Halafu unakuja kuniambia eti nikuonee huruma unafamilia, kwani mimi niliishije bila familia baada ya kuniulia wazazi wangu? nataka huyo mwanao na yeye ajekuishi bila familia kama vile ambavyo mimi nimeishi” Alikuwa akiongea kwa uchungu mkubwa sana huku chozi likimdondoka. Akakishika kichwa cha Mata na kukipigiza kwenye meza mara nyingi na alipokiachia……! Ajuae ni mungu na mimi nilieshuhudia.
Akamuinua na kuanza kumtoa nje huku akiwa ameishika tai aliyoivaa akawa anaivuta kwa mbele na kumfanya Mata afananiane na mbuzi anaegoma kupelekwa machinjioni. Akamvuta hivyo hivyo na kumtoa ndani ya hiyo ofisi. Wafanyakazi wote walipigwa na butwaa huku wafanyakazi wakike wakipiga kelele za hofu baada ya kuiona hali hiyo aliyonayo bosi wao. Yule ‘secretary’ wake alizidi kuchanganyikiwa baada ya kuishuhudia sura aliyonayo Koplo Hemedy sio ile aliyokuwa nayo hapo wakati anaingia. Aliingia kwa sura nzuri yenye tabasamu zuri, lakini sasa liletabasamu halikuwepo wala ule uzuri pia haupo.
Alikuwa sura ameikunja kama mtu akunjavyo nguo akitaka kuziweka kabatini huku akimvuta Mata tai yake kumtoa nje. Alijua kabisa kuwa hiyo sio sheria na hata huyo anaemfanya hivyo akiamua kumshtaki basi anakesi ya kujibu, wafanyakazi walitoka nje kumshuhudia bosi wao anavyotolewa nje mkukumkuku na mtu wasiemjua. Ikabidi mfanyakazi mmoja wa kiume ajitoe kimasomaso kumfuata Koplo Hemedy.
“Kaka vipi, mbona huyu mtu hivi tena, kuna nini?” Jamaa huyo aliongea. Koplo Hemedy kwa ghazabu alizokuwa nazo hakutaka hata kuongea, akamtolea kitambulisho cha kazi na kumuonyesha.
“Hata kama ni askari, lakini sio haki kumchukua mtuhumiwa hivi hai hai namna hii” Jamaa aliongea.
“Huyu nimekuja kumchukua kistaarabu, ila yeye akataka kuniitia mimi mwizi, sasa ndio nikaona nimfunze adabu kwanza” Koplo Hemedy alivyoongea hivyo, akamfunga pingu na kumtia kwenye gari lake, safari ya kuelekea kituoni ikaanza. Njia nzima Mata alikuwa akilia huku akiomba msamaha, lakini Koplo wala hakutaka kumsikiliza. Walifika kituoni, akamshusha na kumuingiza ndani, huko akamkabidhi kwa askari mwengine amuhoji maana anaweza akamuulia hapo hapo kituoni kwa ghadhabu alizokuwa nazo, akaenda ofisini kwa IGP.
“Mkuu tayari nimemleta” aliongea hivyo baada ya kukakamaa kwa heshima.
“Yupo wapi?” IGP alimuuliza.
“Yupo chumba cha mahojiano na Koplo Kindo”
“Sawa, nenda kaendelee na kazi na inabidi kesi zao tuzipeleke mahakamani haraka iwezekanavyo kwa sababu ushahidi upo”
“Sawa Mkuu” akakakamaa na kuondoka hapo ofisini.
Siku nne mbele walipelekwa mahakamani kwenda kujibu mashtaka yao. Muda wote huo Mata alikuwa haamini kwamba ndio wanaenda mahakamani na alijua kuchomoka haiwezekani kwasababu ushahidi wa kueleweka upo, tena video bora hata kama ingekuwa ni maelezo angeweza kupinga. Lakini ilikuwa ni sura yake ile ile, ataanzaje kuikataa, labda aseme wapo mapacha au autumie ule msemo kuwa duniani wawili wawili. Lakini ndio afanane kila kitu na yeye?
Mahakama ile ile waliyotumia kudhulumu mali za watu, ndio hiyo hiyo wanayoenda kuhukumiwa. Mahakama ya Chumbageni, ndio mahakama wanayoenda kusomewa mashtaka yao. Walifikishwa na kuingizwa katika chumba cha washtakiwa wanaosubiri muda wao wa kupanda kizimbani ufike waende. Walikaa hapo kwa nusu saa ndio muda wao ukafika. Waliingizwa ndani ya mahakama na kupandishwa vizimbani na kuanza kusomewa mashtaka yao.
Wakaulizwa kwamba wanayapinga au laa! Hawakuwa na namna ya kupinga wakati ushahidi upo wa kujitosheleza. Hapo wakasomewa tena mashtaka ya kudhulumu mali na hapo pia hawakupinga. Ukafika muda wa kutoa hukumu. Hakimu akasoma vifungu vya sheria na kutoa hukumu kwa watu hao.
“…………wana hukumiwa na mahakama kifungo cha maisha kwa kosa la kuua kwa kukusudia na kudhulumu mali za watu kwenye mahakama tukufu bila mahakama kujua. Mali zote walizokuwa wakizimiliki, zitataifishwa na kurudishwa kwa mshtaka bwana Hemedy Muheshiwa Bhachu kuanzi hivi sasa” Hakimu akagonga nyundo kuashiria Hakuna tena la mjadala. Zilisikaka sauti za vilio kutoka kwenye mabenchi ya watu waliokuja kusikiliza hizo kesi. Alikuwa ni mwanamke wa makamo na mtoto mmoja wa kiume ndio walikuwa wenye sauti hizo za vilio baada ya hukumu hiyo kupita.
Mke na mtoto wa Mata ndio waliokuwa wakilia kwa uchungu baada ya kichwa cha familia kuhukumiwa kifungo hicho. Koplo Hemedy pamoja na kuwa na tabasamu kwa hukumu hiyo, lakini aliingiwa na roho ya huruma baada ya kuwaona watu hao wakilia, akajua moja kwa moja ndio hiyo familia ya Mata maana baba yake mdogo hakuoa wala hakuwa na mtoto. Akatamka mbele ya mahakama kuwa ameiachia familia ya Mata nyumba wanayokaa na fuso mbili za kazi ili kujikimu kipindi hicho ambacho Mata atakuwa yupo gerezani akitumikia kifungo chake.
Mahakama haikupinga hivyo kutokana na yeye ndie mwenye hizo mali. Kesi hiyo ikaisha na watu hao wakapelekwa gerezani huku wakimuacha Koplo Hemedy uraiani akiwa na mali nyingi sanaaa. Baada ya siku mbili walipewa taarifa kuwa Mata alikufa huko jela kwa ugonjwa wa moyo. Ikawa ndio mwisho wake huku familia yake ikihuzunika.
Koplo Hemedy baada ya kukabidhiwa mali zake zote zilizokuwa zikimilikiwa na wale watu watatu, yani Mata, Moto na Mrutu. Akaziuza zote ila alibakisha ile showroom ya magari na kuiongezea kuwa kubwa zaidi. Akafungua na kampuni kubwa ya kusafirisha mizigo mikubwa kutoka hapo Tanga kwenda kwenye mikoa mengine na nchi jirani. Akawa sasa anaishi kwenye nyumba iliyoachwa na wazazi wake huku akiwa na Konstebo Hilda.
* *
Siku moja wakati IGP Ganjo akiwa ofisini kwake. Simu yake ya mezani iliita, aliitazama kwa sekunde kadhaa na kuipokea.
“Bilashaka naongea na IGP Makame Ganjo kutoka mkoa wa Tanga kituo cha polisi Mabawa?” Sauti nzito ya upande wa pili iliongea. IGP akajiuliza hii sauti ni ya nani? Maana hakuwahi kuisikia hata siku moja, ila hakupata jibu.
“Ndio ni mimi ila sijajua naongea na nani?” IGP aliuliza.
“Ok, hii ni simu kutoka Ikulu Daresalam” Mtu wa upande wa pili alijibu na kumfanya IGP kuchoka ghafla. Alichoka ndio. Akajiuliza inakuaje simu kutoka ikulu ije kwake wakati kuna wakubwa zake, sasa ni vipi ije kwake? Kwanza alidhani ni masihara, akaitoa hiyo simu sikioni na kuiangalia, akidhani itampa jibu lolote kwa hayo aliyokuwa akijiuliza. Akairudisha tena sikioni na kusikiliza pasi na kusema kitu.
“Kesho asubuhi unatakiwa uende uwanja wa ndege wewe na wale wajukuu zako, yani Hemedy na Hilda. Mkifika hapo mtakuta kuna ndege inawasubiri kuwaleta huku. Najua huamini ila sasa hivi atakuja mtu hapo ofisini kwako kukuletea barua. Asante kwa kunisikiliza. Fanya kama barua itakavyo kuelekeza” Simu ikakatwa na kumuacha IGP Ganjo asielewe ni kipi kilichotokea hadi kuwa hivyo? Na ni kwanini aitwe yeye na Koplo Hemedy na Konstebo Hilda? Baada ya dakika ishirini za kujiuliza maswali. Mlango wake ukagongwa na kumruhusu huyo mgongaji aingie. Aliingia kijana nadhifu alievaa suti safi, ilikuwa ni sura ngeni kwake hakuwahi kuiona hata mara moja. Akamruhusu akae na yeye akakaa. Wakasalimiana kidogo na mtu huyo akatoa bahasha na kumkabidhi IGP. Kisha akaaga na kuondoka.
IGP mikono ilikuwa ikimtetemeka kwa hofu baada ya kushuhudi nembo ya uhuru ikiwa juu kwenye hiyo bahasha pembeni yake pakiandikwa jina lake. Akaifungua na kuanza kusoma, kilichoandikwa humo ndani hakikuwa na tofauti yoyote na vile alivyoambiwa, ila huku msisitizo ulitumika zaidi, chini kabisa kulikuwa na saini ya Raisi. Hapo ndipo alipoamini kuwa ni kweli. Hapo hapo akawaita Koplo Hemedy na Konstebo Hilda ofisini kwake, walipofika hakutaka kuwaambia chochote, aliwakabidhi hiyo barua na kukaa kimya akisubiri wamalize kuisoma.
Iliwachukua dakika moja tu kuisoma na askari hao wakabaki kumuangalia mkuu wao kwa macho ya mshangao na ya kuuliza. Kunanini mbona hivi? Ila walipata jibu kupitia macho ya IGP kuwa. Sijui hata mimi pia nipo kwenye koma.
Siku iliyofuata asubuhi. Walienda uwanja wa ndege na kupokelewa na yule kijana alieleta barua jana, akawaongoza hadi kwenye ndege moja ndogo na kuwaingiza humo na safari ya kuelekea huko wanakotakiwa ikaanza. Walitumia saa moja kufika katika uwanja wa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere. Ndege hiyo ikapaki sehemu maalumu na watu hao wakashuka na kuongozwa kupelekwa kwenye gari mbili za Ikulu zilizokuwa zikiwasubiri hapo uwanjani.
Muda wote walikuwa bado na maswali mengi vichwani mwao. Hawakujua huko wanaenda kufanya au kufanywa nini? Maana sio rahisi kwa askari wa kawaida kupelekwa tu Ikulu kirahisi rahisi. Walifunguliwa geti baada ya kufika na gari hizo zikaenda kupaki sehemu maalumu. Wakashuka huku wakishangaa shangaa mazingira ya humo ndani jinsi yalivyokuwa ya kupendeza. Hapo akaja mtu mwengie aliewataka wamfuate huko anapoelekea yeye, huyu alikuwa ni mwanamke alikuwa ndani ya suti safi ya kike.
Akawaongoza hadi katika mlango mmoja kati ya mingi waliyoipita huko nyuma. Walipofika hapo akawaambia wasubiri muda si mrefu mlango utafunguliwa na wao waingie humo. Kisha yeye akaondoka akiwaacha watu hao wakimuangalia pasi na kuelewa chochote hadi muda huo… Mlango ulifunguka na wakaingia ndani kama walivyoambiwa. Hapo Konstebo Hilda na Koplo Hemedy walipata mshtuko baada ya kumuona Baba yake na Ramah akiwa amekaa na Raisi wa nchi wakiwaangalia wao. Wakakaribishwa wakae kwenye viti wakiwa na mshangao wao hivyo hivyo na wao wakafanya hivyo.
“Najua bado mnajiuliza kwanini mmeitwa hapa. Ila tambueni kuna kazi maalumu mnayotakiwa kuifanya baada ya nyie vijana kutoka mafunzoni” Mr Kaoneka alipoongea hivyo, akamgeukia Raisi na akatakiwa aendelee. Kisha akasema…
“Hemedy wewe tulikuwa tunakufuatilia tangia ukiwa mdogo mwenye umri wa miaka saba baada ya kukaa kikao na Raisi wa nchi wa kipindi hicho na kuona kuna ulazima wa kuunda kitengo cha siri kitakacho fanyia kazi taifa hili baada ya kuona matukio mengi makubwa ya kiuhalifu na ugaidi kushamiri hapa nchini. Tukakaa kikao cha watu watatu tu, ikiwa ni pamoja na mimi na mshauri wa Raisi wa kipindi hicho ambae kwa sasa ni marehemu na Raisi wa kipindi hicho ambae kwa sasa ameshastaafu. Kikao hicho kilikuwa kikizungumzia juu ya usalama wa taifa hili. Tukaona kuna umuhimu wa kutengeneza ama kuunda kitengo cha siri sana kitakacho fanyia kazi taifa hili hapo baadae. Ndipo ikatubidi kutafuta vijana wadogo wenye akili nyingi na uelewa wa haraka na ukakamavu na ujasiri ambao tutawatengeneza waje kukitumikia kitengo hicho. Tukaona tutafute vijana hao katika mikoa tofauti. Tukaanzia hapa Dar, tukaenda na Arusha, tukafuata Mwanza, Tukaenda Tanga na kumalizia na Zanzibar. Huko kote tumetafuta kijana mmoja mmoja. Tukafanikiwa kupata wanaume watatu na wakike wawili. Wakike tumewapata Dar na Mwanza, ila huyo wa mwanza alifariki muda tu, ndipo tukaamua tumeweke huyu Hilda akakave sehemu ya huyo aliekufa. Nadhani mlishangaa sana baada ya kumaliza ‘form six’ mkatakiwa kuenda JKT kisha mkapelekwa jeshini moja kwa moja bila kuelewa. Hiyo yote ilikuwa ni mipango yetu na hata pale wewe Hemedy ulipopandishwa cheo kwa mwaka mmoja tu pia ilikuwa katika mipango yetu…” Akatulia kidogo kuwaangalia watu hao na kuwaona wapo katika usikivu mkubwa. Kisha akaendelea. “Nadhani hapo mshaelewa ni kwanini mmeitwa Ikulu. Hamna budi kukubali kwenda kwenye mafunzo ya ujasusi miaka sita nchi za mbali, hata hivyo mtakuwa mnatetea Taifa lenu na watu wake zidi ya wahujumu wanaotaka kuihujumu nchi hii. Je mko tayari kwa hilo? Kwasababu hatuwezi kuwalazimisha” Mr Kaonekana aliwafafanulia sababu ya wao kuitwa Ikulu kisha akawauliza swali.
Koplo Hemedy na Konstebo Hilda walimuangalia babu yao na kukuta akiwa na tabasamu kuu usoni mwake, kisha akainua kichwa juu chini ishara ya kuwaambia wakubali. Na vijana hao wakakubali kuwa wapo tayari kulitumikia taifa lao kwa njia hiyo. Hapo Mkuu wa nchi na Mr Kaoneka waliachia tabasamu usoni mwao. Kisha Mr Kaoneka akasema.
“Napenda sana vijana wenye kujitolea kwa taifa lao bila kulazimishwa. Wenzenu wawili wameshatangulia kwenda mafunzoni jana. Na kesho ndio mtaondoka nyie halafu kesho kutwa ataondoka huyo mmoja aliebakia. Huko mafunzo yataanzia Korea, halafu mtaenda na Japan, mtamalizia na China kwa bara la Asia. Kisha Mtaenda Marekani na Urusi kisha Mtamalizia na Cuba. Hadi hapo mtakuwa mmeiva kwa kila sekta ya ujasusi. Mafunzo hayo yata chukua miaka sita hadi kumalizika kisha hapo ndio mtarudi Tanzania mkiwa tayari mpo vizuri kukitumikia kitengo tulichokipa jina la TSSI yani Tanzania Secret Service Investigation. Mtakaporudi ndio mtapangwa kutokana na juhudi na umakini mtaouonyesha huko ndio mtapangwa wa kwanza ni nani hadi watano. Yani atapatikana TSSI 01 hadi TSSI 05, hadi hapo mimi sina tena chakusema, labda nimuachie Kiongozi hapa kama analolote la kusema amiambie” Alimaliza Mr Kaoneka.
“Mimi namiambia tu juhudi na umakini ndio vitu vinavyo hitajika huko ili ufaulu vizuri. Huku kuandaliwa nyie hakukuanza leo wala jana. Mpango huu ulianzi kwa Raisi wa awamu ya pili Dr. Hussein Molito. Yeye ndie alikaa chini na huyu Mr Kaoneka na kujadiliana ni vipi watalilinda taifa lao wakiwa pamoja na mshauri mkuu wake ambae kwa sasa ni marehemu. Mpango huo ukaendelea hadi kwa Raisi wa awamu ya tatu naye akajulishwa hadi wanne na wa tano sasa niko mimi wa awamu ya sita. Hata mimi pia nimefurahi kuona vijana mnakuwa wazalendo na nchi yenu pasipo kulazimishwa. Nashkuru sana na ninawatakia safari njema na mafunzo mema” Alimaliza kuongea Mheshimiwa Raisi Alex Kileo na wakaitiwa mtu wa kuwapeleka hotelini kwenda kupumzika.
Siku iliyofuata, walitolewa hotelini na kupelekwa moja kwa moja uwanja wa ndege kwa safari ya kwenda huko mafunzoni. Ilikuwa ni furaha kwa wote kwa kuajiriwa katika kitengo hicho cha siri serikalini. Njia nzima IGP Ganjo alikuwa akiwaasa sana huko wanapoenda wasifanye mchezo na wawe makini sana na mafunzo hadi pale yatakapo kamilika.
Walifika uwanja wa ndege na kufanya taratibu zote. Kisha wakasubiri muda wa kuondoka hiyo ndege ufike. Muda ulipofika waliingia ndegeni na kumuacha IGP Ganjo na Mr Kaoneka kuwanyooshea mkono wa kwaheri na ndege ikapotelea mawinguni. IGP Ganjo na Mr Kaoneka walipeana mikono na IGP akapanda ndege kwaajili ya kurudi Tanga….
Donald Mbeto,akiwa amevalia koti jeupe la kidaktari, machoni alivalia miwani, huku ndevu za bandia zikikipamba kidevu chake. Alitembea kufuata korido ndefu, alikata kona kushoto, kisha akakunja kulia, uso kwa uso akakutana na chumba kikubwa chenye mlango wa vioo. “pharmaceutical room”(Chumba cha madawa), chumba kile kilisomeka kwa lugha ya kizungu,Donald aliingiza mkono wake wa kulia mfukoni, huku akiangaza upande wa kulia na kushoto kwa umakini wa hali ya juu, alitoa mkono wake mfukoni, huku akiwa ameshika funguo yake ndogo iliyokuwa na uwezo wa kufungua mlango wowote ule.
“Ooooh shit! kuna kamera!, hapa nikusambaratisha upumbavu wao, watawakamata wengine sio mimi ……”,Donald Mbeto alizungumza, aliruka teke la kinyume nyume, sekunde tu kamera iliyokuwa juu ya mlango ilisambaratika vipande vipande.
Umeme ulianza kuwaka na kuzima, haraka haraka alifungua mlango wa chumba, ukagoma,akafungua tena ukagoma!,ikabidi abadili mbinu maana funguo ilimcheleweshea kazi.
“Hapa tayali shoti imetokea, ndani ya sekunde ishirini walinzi watakua mahali hapa, sikubali! lazima nikamilishe kazi! “,Donald Mbeto, muuaji wa kimataifa aliongea, huku akitazama taa ambazo ziliwaka na kuzima.
“Yes, yes! kazi imekwisha! “!”,Donald alizungumza, akiwa na tabasamu usoni mwake. Alivuta waya wa kamera uliokuwa ukining’inia na kutoa cheche, akagusisha kwenye kitasa,vioo vikamcheka, mlango ukaachia.
Bila kuchelewa, moja kwa moja akaingia stoo ya kuhifadhia madawa, akaingiza kwenye koti lake mkono wa kushoto,akatoa sindano yake iliyojaa sumu.
“Sodium pentobarbital…!, kesho ni kilio na msiba mzito kwa taifa la Ufilipino, poleni wafiwa “,Donald Mbeto aliongea kwa kejeli huku akitabasamu kwa furaha, alichomeka sindano kwenye dawa zote aina ya kimiminika, na kuweka sumu hiyo hatari kwa maisha ya binadamu!
“,done!, kazi imekwisha! “,alizungumza, akaangalia saa yake ya mkononi, sekunde tano tu zilitumika kukamilisha zoezi la kuweka sumu kwenye madawa.
Alitoka nje, akarudisha mlango,na kuubana vizuri kama ulivyokuwa awali. Alipotazama huku na kule, hakuona mtu, zaidi ya taa ambazo ziliwaka na kuzima,kutokana na shoti ya umeme iliyosababishwa na kamera iliyopigwa teke na Donald.
“Hawa walinzi wazembe kweli, anyway! ngoja nipotee mahala hapa …”,Donald Mbeto alizungumza, huku akipiga hatua kadhaa,ghafla rundo la walinzi walikua mbele yake, hakuwa na wasiwasi,aliweka koti lake vizuri kama daktari.
“Hey doctor, what is the problem? “,(Hey daktari, kuna tatizo gani,?) ,mlinzi mmoja alimuuliza swali Donald Mbeto kwa kutumia lugha ya kizungu, baada ya kugundua alikuwa daktari wa kizungu na sio Mfilipini, kutokana na ndevu za kizungu, ndevu za bandia kidevuni mwake.
“I don’t know anything”,(Sifahamu chochote kile …) ,Donald Mbeto aliwajibu kwa kifupi, akaendelea na safari yake, alinyosha korido aliyoingia nayo, akakunja kulia,moja kwa moja mpaka kwenye lifti,harakaharaka alibonyeza batani ukutani, lifti ikaanza safari ya kupandisha ghorofa za juu zaidi.
………………………………
“Aim not sure if that person is a doctor of this hospital, let’s go back and look for him, aim sure is the one who did this ……”,(Sina uhakika kama mtu yule ni daktari wa hospitali hii, turudi tukamtafute ,nina uhakika ndiye aliyefanya hivi …”,mmoja wa walinzi aliongea, huku wakitazama kamera ambayo ilisambaratika vipande vipande.
Ili kupata maswali ya majibu yao, kundi la walinzi lilirudi haraka sana huku kila mmoja akiwa amekamatilia silaha yake kikamilifu, tayali kwa ajili ya kumkabili bwana Donald Mbeto.
Sekunde tano baadae, walikuwa katika eneo la lifti, walipotaka kuingia tu, ghafla mlio wa helikopta uliwashtua, kwa mbali waliona helikopta iliyokuwa ikiwaka taa mbalimbali, nyeupe na nyekundu, ikipotea kutoka juu ya jengo..
“That bastard has gone…”,(Yule mwanaharamu ameondoka) “,mlinzi mmoja alizungumza, huku akitazama helikopta ambayo ilikuwa ikipotea machoni, kupitia vioo vya jengo ambavyo viliwawezesha kuona nje.
“,Yes, but who is that person? “,(Ndio, lakini mtu yule ni nani? ),mlinzi mwingine alizungumza.
“We don’t know, “(Hatufahamu) ,wote waliitikia. “We have to be careful,anything can happen at any time “,(Tunapaswa kuwa makini, kitu chochote kinaweza kutokea muda wowote), mlinzi mmoja aliongea, kisha walipanda lifti kushuka chini kwenye wodi za wagonjwa kuendelea na majukumu ya ulinzi usiku huu uliojaa utata.
…………………………………
11;20am
Uongozi wa hospitali ya mjii mkuu wa Manila, hospitali kubwa nchini Ufilipino, “Manila international hospital “,wanatangaza vifo vya watu zaidi ya elfu mbili, huku chanzo kikitajwa ni sumu aina ya Sodium pentobarbital iliyowekwa katika dawa zote aina ya kimiminika.
Wagonjwa wote waliotumia dawa hizo, walikufa baada ya dakika moja tu. Waandishi wa habari, maafisa wa jeshi la polisi walizagaa pembe zote za hospitali kukusanya habari, huku walinzi wa usiku uliopita wakiwa washtakiwa namba mbili kwenye sakata hili,tayali wakiwa mahabusu kusubili kusomewa mashtaka yao ya kula njama na muuaji.
“We are so sad to announce, more than two thousand people have died this morning,so ……”,(Tuna huzuni kubwa kutangaza, zaidi ya watu elfu mbili wamefariki dunia asubuhi hii, kwahiyo ……”,
Kabla hata sentesi haijamalizika, kamanda Kendrick alishindwa kuvumilia, alizima tv yake, alichukua koti lake na kuanza safari kuelekea katika hospitali ya Manila, kwa ajili ya kujua ukweli kuhusu vifo vya zaidi ya watu elfu mbili ghafla kiasi kile.
“Nina siku mbili tu tangu nitoke Tanzania, sijapata chochote kile kuhusu muuaji tunayemtafuta, lakini mbona matukio yanafanana, bila shaka ninaweza kugundua jambo fulani. ” ,kamanda Kendrick, askari mpelelezi namba moja wa kuaminika, miongoni mwa askari watatu wa “The super three Soldiers ” kutoka Tanzania, aliongea huku akishuka ngazi kutoka katika jengo la hoteli alilofikia mjini Manila, akiwa na shauku ya kutaka kujua chanzo cha mauaji ya wagonjwa zaidi ya elfu mbili katika hospitali ya kimataifa ya mji wa Manila.
…………………………………
01: 00pm
“Kamanda Philipo,!, kamanda namba mbili ovaaa…!”,Kamanda Kendrick alizungumza kwenye simu, huku akiwa katika chumba cha mawasiliano katika hospitali ya Manila, kwa ajili ya ukaguzi wa kamera za siri zilizofungwa hospitalini bila kuonekana kwa urahisi.
“,Kamanda Kendrick, kamanda namba moja, nakupata ovaaaa! “,upande wa pili wa simu uliongea.
“,Muuaji aliyeweka sumu, katumia mbinu zilizotumika Tanzania, kichwani kaficha uhalisia kwa kutumia ndevu za bandia,nakuomba uje unisaidie kumtambua kama ndiye mtuhumiwa tunaye mtafuta au siye!”Kendrick alizungumza, huku askari wa Ufilipino wakimtazama bila kuelewa chochote kile, walichosubili ni taarifa tu watakayopewa na Kendrick kupitia lugha ya kingereza.
“Sawa kamanda namba moja, dakika ishirini nitakua hapo! “,upande wa pili wa simu ulizungumza.
“,Sawa ovaaa!, nakusubili “,Kamanda Kendrick alizungumza na kukata simu, akimsubili kwa hamu mpelelezi mwenzake aliyefikia hoteli nyingine, kamanda namba mbili, mtaalamu wa kompyuta wa kutegemewa katika kikundi cha “The super three Soldiers ” kutoka Tanzania, wakiwa na siku mbili tu tangu wafike nchini Ufilipino kwa lengo la kumtafuta muuaji, muuaji aliyeua watu kwa sumu nchini Tanzania.
“Inspector, can you tell us what is going on? (Inspecta, unaweza kutwambia nini kinaendelea? “,),askari mmoja wa Kifilipini, askari mwenye cheo kikubwa kuzidi wenzake alimuuliza Kendrick.
“,don’t wory boss, Few minutes to come, we will identify the killer …”,(Usjali mkubwa, dakika chache zijazo, tutamtambua muuaji,”) ,Kamanda Kendrick alizungumza, huku askari wa Kifilipini aliyeuliza swali akitikisa kichwa kuashiria kukubaliana naye
…………………………………
01:30pm
“,What! kwanini anafanya hivi, kwanini anaua bila hatia? anataka nini?,ameua Tanzania, amekuja tena huku kaua, anataka nini? “,Kamanda Philipo aliongea kwa hasira, huku akitazama sura halisi ya muuaji akiwa na nywele zake za mnvi zilizomtapakaa kichwani pamoja na kidevuni, baada ya kuondolewa ndevu bandia, kwa kutumia kompyuta na kumtambua muuaji maarufu anayetafutwa kila kona, bwana Donald Bento aliyependa kujiita Jini mweupe.
“,Tutamkamata tu, lazima tufahamu ukweli! “,Kamanda Kendrick aliongea huku akitazama kioo cha Kompyuta, baada ya Kamanda Philipo kutumia utalamu wake wa kompyuta ipasavyo.
“,Is Donald Bento the one who killed people? “,(Donad Bento ndiye aliyeua watu? “,)askari wa Kifilipino aliyeuliza swali awali, aliuliza swali kwa mara nyingine huku wote wakiwa bize kutazama kioo cha kompyuta kilichopambwa na picha ya Donald Bento, pamoja na jina lake lililiondikwa kwa herufi kubwa, “DONALD MBETO”(JINI MWEUPE)
“Yes boss, “(Ndio mkubwa), kamanda Kendrick alimjibu mkuu wa upelelezi kutoka Ufilipino, kamanda aliyekuwa nao bega kwa bega tangu waanze upelelezi wao nchini Ufilipino.
Kamanda Kendrick alichoka, kamanda Philipo alichoka, jenerali pamoja na askari wote wa Kifilipino walichoka ,hawakujua waanzie wapi kumtia nguvuni Donald Mbeto maarufu kama jini mweupe.
“,Jambo la kwanza tunapaswa kujua Donald Mbeto yupo nchini, au ametorokea nchi zingine, tukitatua swala hili, kazi itakua rahisi kwetu ” ,Kamanda Kendrick aliongea, wote wakisubili taarifa kutoka kwa wataalamu wa rada uwanja wa ndege wa Manila, kuhusu ndege yoyote iliyotoka masaa kumi yaliyopita wakati wa usiku.
“,Hapo umenena ,hujawahi kuniangusha kamanda namba moja! “,kamanda Philipo aliongea, vidole vyake vikichezea bastola yake, akafungua magazini, akapachika risasi, akafunga tena, akawa tayali kusubili amli kutoka kwa jenerali wa Kifilipini.
“,Helikopta aina ya SH-60B Seahawk iliingia Ufilipino siku tano zilizopita, ikaweka kambi katika msitu wa Kijani kaskazini mwa Ufilipini,ilifika majira ya saa sita usiku katika hospitali ya Manila,baada ya kutua ghorofa ya mwisho, muuaji alipokamilisha kazi, ilitoweka nchini kupitia bahari ya hindi “,Kamanda Kendrick alisoma ujumbe mfupi, ujumbe ulioingia kwa lugha ya kifilipini na kutafsiriwa kwa Kiswahili, taarifa iliyotumwa na viongozi wa rada ya Ufilipini iliyo ongoza ndege zote zinazoingia na kutoka, baada ya kukamilisha uchunguzi wao.
“,Inspector Kendrick and your fellow, go to look for the killer, i will help you if you need assistance, good luck! “,lkamanda Kendrick na mwenzako, nendeni mkamtafute Muuaji, nitawasaidia kama mtahitaji msaada, kila laheri! )”,jenerali Fernando alizungumza, kisha akasimama, akapigiwa saluti, akatoka katika chumba cha mawasiliano ndani ya hospitali ya Manila, baada ya kumtambua muhusika wa mauji, kupitia kamera za ziri zilizonasa zura ya bandia ya Donald Mbeto.
“,Ok salute! “,kamanda Kendrick alizungumza, wote pamoja na kamanda Philipo wakapiga saluti kukubali amli, kazi waliyotumwa na taifa la Tanzania, pamoja na nchi ya Ufilipino kama heshima kubwa kwao.
…………………………………
Masaa kumi nyuma;
Helikopta aina ya SH -60B Seahawk iliondoka usawa wa ghorofa ya mwisho, katika hospitali ya Manila saa kumi usiku, ikapaa usawa wa mita mia mbili za jengo kwa umbali wa kilomita mbili, ikapaa juu umbali wa mita mia mbili kumi na tano kutoka usawa wa bahari, ikapotelea angani.
“,Hongera komandoo! kazi nzuri! pesa zako tumekuwekea katika akaunti yako ya siri katika benki ya dunia, ukikamilisha kazi hii ya mwisho, katika hospitali ya Gano, tutakupatia pesa zako zote trilioni moja, kisha utaenda kuishi mafichoni Amerika “,Paresh Kumar, bosi wa Kihindi alimpongeza Donald Mbeto, helikopta ikichanja anga kuvuka mipaka ya nchi kabla jua halijachomoza.
“,Usjali bosi, omba Mungu nisife mapema kazi zako zikalala “,Donald Mbeto aliongea, sura yake halisi ikaonekana, alivua sura na ndevu zake za bandia, akabaki na mnvi zake kidevuni pamoja na rasta nyingi za mnvi kichwani zilizotoa tafsiri ya jina lake, jini mweupe.
“,Hahahaaa, kweli wewe jini Mweupe, kiumbe hatari sana “,Paresh Kumar alikimudu kiswahili ipasavyo, alicheka kwa furaha huku akishika rasta nyeupe za Donald Mbeto kumpongeza.
…………………………………
Gano; 04;20pm
Helikopta aina ya Seahawk ilitua bahari ya Hindi, katika meli kubwa aina ya MD47 Faaraquat inayomilikiwa na kundi kubwa la D47 ,kundi la kigaidi tajiri zaidi duniani.
Donald Mbeto alishuka, akapokelewa kwa furaha na washirika wote wa kundi D47, kundi ambalo lilijishughulisha na kuuza madawa ya kulevya, silaha, pamoja na madini.
“,Karibu White house! karibu makao makuu, pole na kazi, jiandae kwa kazi nyingine dakika kumi zijazo “,daktari mkuu wa kundi la D47 alimpokea Donald Mbeto, akamuongoza mpaka kwenye chumba cha upasuaji, huku akishangiliwa kwa furaha na wafuasi wa kundi hili waliokuwa katika mazoezi ya karate katika uwanja mkubwa melini.
“,Umbo la kike litakua poa zaidi! ,meza dawa hizi, zinaitwa “voice changer “,zingatia, wakati wa kazi usinywe kinywaji chochote kile, sauti yako itarejea kuwa ya kiume “,dokta Govinda, daktari wa Kihindi, alifanikiwa kubadili mwonekano wa Donald Mbeto kwa dakika tano tu.
Akiwa na makalio ya kike yaliyofungwa mwilini, chuchu za bandia pamoja na uso wa mwanamke wa kijapani aliovaa usoni, Donald Mbeto alikabidhiwa sindano ya sumu ile ile ya Sodium pentobarbital, sumu hatari iliyotumiwa na Donald Mbeto kufanya mauaji. Alitoka chumba cha upasuaji,akapigiwa magoti ya heshima na saluti, akapakiwa kwenye nyambizi,safari ikaanza kuelekea nchi ya Gano,kisiwa cha bahari ya Hindi Afrika ya Mashariki.
Nyambizi ilizama futi ishirini kwenda chini, isije ikagundulika na kushambuliwa na helikopta za umoja wa mataifa, zilizofanya doria usiku na mchana katika bahari ya hindi kupinga ugaidi.
“,Nyambizi itasimama kilomita tano kutoka nchi kavu, utachukua mitungi ya gesi, utaogelea baharini kama samaki! dakika kumi zinakutosha kukamilisha misheni hii, utarudi kwa kutumia spidi boti ya mvuvi ambaye ni mshirika wetu”,Kepteni wa Nyambizi alitoa maelekezo kwa Donald Mbeto.
“,Haina shida! “,kwa sauti ya kike,baada ya kunywa vidonge aina ya “voice changer “,Donald Mbeto aliongea, huku akitikisa kichwa kuashiria kukubaliana na maelekezo aliyopewa. Nyambizi ikaendelea kupiga mbizi chini ya bahari.
…………………………………
Tanzania; 6:00 pm
Kamanda Catherine, kamanda namba tatu wa kundi la wapelelezi watatu, “the super three soldiers “kutoka Tanzania, alihisi hali ya hatari katika bahari ya hindi na nchi zote za Afrika mashariki zilizopakana na bahari hii iliyojaa magaidi na maharamia.
“Nyambizi hii mbona imeibuka ghafla tu! kwanini mwanzoni haikusafiri usawa unaoruhusiwa na umoja wa mataifa, nina wasiwasi! bila shaka imebeba magendo …”,kamanda Catherine aliongea, alinyenyua mkonga wa simu yake ya mezani, akabonyeza namba kadhaa kisha akaweka sikioni.
“,Halloo kamanda, nakupata ovaa! “,upande wa pili wa simu uliongea.
“,Kamanda namba tatu, nakupata ovaa! “,kamanda Catherine aliitikia kupitia simu yake ya mezani.
“,Nikusaidie nini TSTS namba tatu …”,sauti ilisikika upande wa pili wa simu.
“,Tuma ndege za kijeshi, kilomita kumi kuelekea kisiwa cha Gano, kuna Nyambizi imevuka usawa wa kimataifa, inaelekea Gano au huku Tanzania, nendeni mkaichunguze ……”,Kamanda Catherine, TSTS namba tatu alitoa maelekezo kwa jeshi la majini.
“,Tumekupata mkuu, dakika ishirini tutakua eneo hilo “,sauti ilisikika upande wa pili, simu ikakatwa.
Kamanda Catherine akabonyeza namba kadhaa za kimataifa, akampigia kamanda Philipo, namba haipatikani, akabonyeza tena, akampigia kamanda Kendrick, namba haipatikani, akatuma ujumbe kupitia saa zao maalumu za mkononi, “Network error “,(Mtandao unashida),saa ya kijeshi iliwaka taa nyejundu, huku ujumbe wa meseji ukionekana kwenye kioo chake.
“,Kuna shida! sio bure, kuna shida! idara ya ulinzi haiko salama, “Kamanda Catherine alinyanyuka, alichukua bastola yake, akafunga kiatu chake pamoja na mkanda wa kijeshi, akafunga mlango wa ofisi yao ya siri kwa kutumia namba maalumu, akatoweka alikokujua yeye ……
…………………………………
Gano; 7;00pm
Donald Mbeto alishuka ufukwe wa bahari nchini Gano, akavua mavazi na mitungi ya gesi akaitelekeza, akavaa nguo za kazi, suti ya kike,akavaa begi lake, akatokomea.
“,Sista wapi? lakini umependeza, “dereva taksi eneo la bandari, alimuuliza Donald Mbeto.
“,Hospitali ya taifa Gano! “!Donald Mbeto kwa sauti ya kike, alijibu kwa kifupi.
“,Ohooo! lakini umependeza, ingekua vizuri ungenipatia namba yako, hata pesa zako sihitaji …”,dereva taksi alichombeza, huku akiliondoa gari kwa fujo eneo la bandari, kufuata barabara kuu ya jiji kuu la Gano.
“,Mbona hunijibu, acha kulinga!”,dereva yule aliyekuwa amebabuka midomo, bila shaka alibugia unga kama sio bangi, alichombeza bila kujua uhalisia wa mtu anayemchombeza.
Donald Mbeto alichomoa bastola, akaikoki, kisha akairudisha kiunoni. Akachukua kisu chake kidogo, akajichana kwenye kidole, damu zikatoka, akalamba, yote ni kumtisha dereva taksi.
“,Basi inatosha, nisamehe tu dada, nilikua sijui! “,bila hata kuguswa, dereva taksi alijitetea, alishuhudia kila kitu Donald Mbeto alichokifanya.
“,Ole wako useme uliyoyaona, nitakuua!Kwa sauti ya kike, Donald Mbeto alitoa onyo, akakunja nne, amani na ukimya ukatawala ndani ya gari.
Masaa manne yaliyopita;
TSTS (the super three soldier) namba moja, kamanda Kendrick, akiwa ameongozana na kamanda Philipo, TSTS namba mbili, walitoka katika hospitali ya manila, kichwani waliwaza kuelekea haraka sana kaskazini mwa jiji la Manila, helikopta aina ya Seahawk ilipotua mara ya kwanza, kabla ya kufika hospitalini kutekeleza tukio la kuweka sumu na kuua maelfu ya watu. Waliamini wangegundua jambo lolote, ambalo lingewasaidia kugundua mahali ambapo Donald Mbeto alitorokea.
Wakawasha gari, wakatoweka eneo la hospitali, wakiwa ndani ya gari, ni muda mrefu walikuwa wamezima simu zao,wakaamua kuziwasha, mlio wa meseji nyingi ukawapokea, meseji zilizotoka kwa “the super three soldier ” namba tatu, kamanda Catherine.
“,Mipaka haiko salama, kuna nyambizi imeibuka ghafla na kuanza kuonekana usawa wa umoja wa mataifa baharini, kilomita kumi kutoka ufukweni, hatujui inaelekea wapi, Tanzania au Gano, isitoshe hatujui imebeba nini! “,meseji ilisomeka, ujumbe kutoka kwa kamanda mtata na mtaalamu wa tehama jeshini, kamanda wa kuaminika na serikali ya Tanzania, Catherine Obadia.
“,Paki gari pambeni tufanye mawasiliano naye, kisha tutaendelea na safari! “,Kamanda Kendrick aliongea, kamanda Philipo akatii amri, akapaki difenda ya polisi pembeni. Kamanda Kendrick akabonyeza namba namba za kimataifa, akaweka simu sikioni, bila shaka alikuwa anampigia kamanda Catherine.
…………………………………
Tanzania;610pm, bandarini
Jeshi la majini walikuwa bize, waliogopeshwa na taarifa waliyo ipokea muda mfupi uliopita, kuhusu usalama hafifu kilomita kumi eneo la bahari.
“,Askari sita ndani ya nyambizi, sita ndani ya chopa, sita ndani ya spidi boti, hakikisheni nyambizi ya maadui haiwaponyoki!! mkuu wa jeshi la majini aliongea, akageuka ghafla, akakutana na sura asiyoitegemea, “Karibu bosi, saluti! “,akaongea, akapiga saluti, vijana wake wakafuatia, wakapiga saluti.
“,Nikitoa kazi staki uzembe!,ndiyo maana nimekuja mwenyewe”,akaangalia saa, akaona nusu saa ilikuwa imepita tangu atoe taarifa.Akazidi kuvimba kwa hasira.
“,Hapana bosi, nilikuwa na ……”,mkuu wa jeshi la majini aliongea.
“,Hapana nini! staki uzembe kwenye kazi, nchi ikivamiwa sisi ndio wa kwanza kuulizwa, hebu kila mmoja apande kwenye usafiri wake tuondoke, haijalishi una nyota, una V mbili au praiveti, wote kazini! “,kamanda Catherine aliongea, licha ya kuwa na nyota tatu begani, hakuwa mzembe na kazi, aliweka vyeo vyake chini, akatanguliza kazi mbele, jambo ambalo lilipelekea kutunukiwa medali tano na umoja wa mataifa, kama mwanamke pekee wa wa Afrika mashariki kuingia vitani akiwa na kundi lake la the super three soldiers nchini Kongo, akafanikiwa kurudi salama.
“,Sawa mkuu, saluti! “,askari wote wa majini waliitikia,ndege ya majini yenye askari sita pamoja na rubani akiwa wa saba, ilitembea kwenye maji kisha ikapaa angani, ikapaa futi hamsini kwenda juu., spidi boti ikafuatia ikaingia baharini na kupotea, kamanda Catherine akiongoza askari saba, akiwemo mkuu wa majeshi ya majini mwenye nyota moja begani, waliingia ndani ya nyambizi, nyambizi ikatembea baada ya dakika tano, kisha ikazama futi kumi kwenda chini, ikapotea kwenye uso wa bahari. Makundi yote yalivaa hedifoni masikioni, simu kubwa za kipolisi (redio call) zilikua mikononi, wakiwasiliana na kujulishana kila hatua.
“,Haloo, haloo, yoyote usawa wa helikopta, pokea simu ovaa! “,simu ilisikika kwenye helikopta, ikapokelewa, kisha ikasogezwa karibu na mdomo.
“,Usawa wa nyambizi, nakupata ovaa! “,mmoja kati ya makamanda sita kwenye helikopta aliongea.
“,baada ya kilomita kumi, simameni eneo hilo, makombola ya ndege yachomoeni kuangaza baharini, kuweni makini msishambuliwe! “,upande wa pili wa simu ulizungumza.
“,Sawa kamanda, tumekupata ovaa! “,usawa wa helikopta ukajibu, kisha simu ikakatwa, tayali kifaa cha kupimia umbali, kilianza kuonyesha kilomita tisa zikiwa zimemalizwa,helikopta ikapunguza mwendo, makombola mawili kama mapembe yakachomoza kwa mbele, tayali kuishambulia nyambizi yoyote eneo hilo.
…………………………………
“,Sogeza karibu na Nyambizi hiyo, kilomita nne kutoka hapa! “,kamanda Catherine aliamua kuubeba mzigo mwenyewe, mtungi wa gesi ulikuwa mgongoni, miguuni na mikononi alivaa vifaa vya kumsaidia kuogelea, usoni alivaa helmenti iliyounganishwa na mtungi wa gesi, alitoa maelekezo huku akijiweka sawa.
Dakika tano mbele, nyambizi ilifika eneo la tukio, wakaiona nyambizi kilomita tano mbele kwa kifaa maalumu, Nyambizi ya jeshi ikapandisha kidogo usawa wa bahari, mlango ukatokeza juu ya usawa wa bahari, Catherine akazima saa yake ili asinaswe na mawasiliano upande wa pili wa maadui, akatoka nje ya nyambizi yao, kisha ikazama tena, yeye akajitupa baharini na kuogelea kama samaki.
…………………………………
Tuko hatarini, nyambizi yetu imeshanaswa na jeshi la ulinzi, japo sijajua kama jeshi hilo ni la umoja wa mataifa, au jeshi la nchi ya Tanzania,au Gano, sijajua kabisa! “,Kepteni aliongea, akiwa na vijana wawili tu ndani ya nyambizi inayomilikiwa na kundi la kigaidi la D47.
“,Hamna jinsi, wakitufikia lazima watuzidi nguvu, cha msingi ni kuwashambulia na makombola wakijaribu kutusogelea ili kuepuka kukamatwa……!”,gaidi kati ya wawili, akiwa na sura nyeusi, kipara chenye mafuta mengi kichwani, alitoa maoni yake kwa kepteni wa nyambizi.
“,Sawa kabisa, ndege inayotutafuta imesimama juu eneo moja, hatuwezi kuchomoza usawa wa bahari, nyambizi yao pia iko kilomita tano kutoka hapa, imesimama pia inatunga sheria, hatuwezi kuondoka na kumwacha Donald Mbeto, lazima tumsubili, hawa wapuuzi wakitusogelea tunawashambulia kwa nyukilia zetu hawata amini macho yao! “,kepteni wa Nyambizi ya D47,aliendelea kujisifia, bila kujua mtego ambao waliwekewa, Catherine alikuwa anawasogelea bila kifaa chochote cha mawasiliano, asionekane katika mitambo yao na kuwanasa kirahisi.
…………………………………
Kamanda Catherine aliifikia Nyambizi, akatoboa kwenye injini, hakutosheka, akatafuta sehemu ya imejensi( imejensi chemba),sehemu ya kutokea kama kuna hatari yoyote, akabana mahala pale, huku akiwa na visu viwili mikononi, alibana, akisubili yoyote yule atakayetoka, aweze kumshughulikia.
Aliendelea kusubilia, maji yakizidi kuingia ndani ya nyambizi,hakukata tamaa, hakukuwa na sehemu nyingine yakutokea kwa urahisi zaidi ya “emergency chamber “,aliendelea kusubili.
…………………………………
Ghafla hewa ilikuwa nzito ndani ya meli,injini ikazima, umeme ukazima,hofu ikamtawala kepteni pamoja na magaidi wawili waliokuwa ndani ya Nyambizi, wakashika bastola mikononi mwao, walitambua tayali walikuwa wamevamiwa,wakaanza kutembea kwa makini ndani ya Nyambizi,ghafla mawimbi yaliwasomba hakuna aliyekumbuka kuwahi boya wala mitungi ya kuogelea,kepteni akabamizwa na mawimbi kwenye chuma cha mlango wa kuelekea chooni akapasuka kichwa, akafa palepale, gaidi mmoja akajigonga huku na kule, akajitahidi kujitetea, maji yalimzidi nguvu, akazimia, gaidi wa tatu maji yalimsomba mpaka karibu na mlango, akaukamatilia vizuri, akaufungua, ukashindikana, ulikuwa umefungwa na komeo, akasogelea chemba ya kutokea kama kuna hatari, chemba karibu na mlango, akaipiga kwa nguvu na mguu, ikafunguka, akaanza kujitahidi kutoka, akishandana na maji yaliyokuwa yanaingia ndani ya nyambizi, akavutwa kwa nje, bila kujua mtu aliyemvuta.
…………………………………
Catherine baada ya kusubili kwa muda mrefu alitaka kukata tamaa, akataka kubadili mbinu,akiwa anatafakari, alishangaa mlango kusukumwa na mguu, akamvutia adui yake nje, akatupa bomu ndani ya nyambizi, likasaidiwa na maji mpaka ndani.
Akamchoma visu vya miguu gaidi yule, akajuta kusaidiwa msaada wa kinafiki kwa kilio kikuu,nguvu hakua nazo tena, ujanja hakua nao tena, akaanza kupandishwa juu na mtu aliyemsaidia na kumshambulia akiwa hajitambui vizuri, Catherine aliogelea kama samaki aina ya papa kwa kasi ya ajabu, kabla bomu alilotupia ndani ya nyambizi ya D47 halijaripuka.
…………………………………
Nusu saa baadae;
Mtuhumiwa alikuwa amepakizwa juu ya ndege,pembeni akiwa ameketi Catherine akimuhoji taratibu,”,Puuuu, puuuu!! “,bomu liliripuka, nyambizi ya D47 ikasambaratika vipande vipande baharini, hakuna chochote kilichosalia.
“,Nitasema, nitasema! “,gaidi lilipiga kelele kwa maumivu. Catherine alimuunguza na sigara jichoni, alilia kama mtoto, Catherine hakua na huruma kazini.
“,Sema, wewe ni nani, mmekuja kufanya nini? “,Catherine alifoka.
“,Tumemleta Donald Mbeto, amekuja kukamilisha kazi ya mauaji nchini Gano, baada ya kutoka Ufilipino masaa kadhaa yaliyopita!! ” ,gaidi lile lilieleza kila kitu kwa huzuni. “, Unasemaje, mmemleta Donald Mbeto kufanya mauji,?”,Catherine aliuliza akiwa haamini, alikuwa amechanganyikiwa, akachana kwa kisu shati la gaidi yule, akatazama mgongoni, kuna kitu alikua anahakikisha kama aliyo ambiwa ni kweli, “D47”,chata kubwa iliyozungushiwa duara ilikuwa mgongoni, aliamini kile alichoambiwa, askari wote ndani ya helikopta wakachanganyikiwa.
Simu iliita, ikaita tena ikazima, hakuweza kuisikia, mawazo yalikua mbali, “mkuu pokea simu “,aliambiwa na askari pembeni yake, kamanda Catherine akashtuka, alipoangalia kwenye kioo akapokea haraka, “Kamanda kendrick “,kioo cha simu, jina la mtu aliyepiga simu ilionekana kwenye skrini.
…………………………………
Manila; Ufilipino.;
“,Donard Mbeto yuko huku, rudini haraka, hapa tuko na gaidi tuliyemkamata, wamemleta na Nyambizi nchini Gano kufanya mauaji mengine, rudini haraka sana! “,kamanda Catherine aliongea.
“,Rudini huku usiku huu, Donald Mbeto yuko huku Afrika Mashariki, njoeni kabla hajaua wengine! “,kamanda Catherine alimalizia,Kamanda Kendrick pamoja pamoja na Philipo hawakua na haja ya kuuliza tena, walijipakia kwenye gari na kutoweka walikokujua wao, kichwani walichanganyikiwa.
Gano; 8:00
Gari dogo ya abiria, ikiwa na bango dogo la prastiki rangi ya njano, lililosomeka “TAXI ” kwa herufi kubwa, ilipaki nje ya hospitali kuu ya taifa nchini Gano, “tumefika bosi! “,kwa heshima, akiwa amejawa na wasiwasi, dereva taksi aliongea. Akafungua mlango wa taksi kwa rimoti ndogo iliyokuwa mikononi mwake, milango ikafunguka, Donald Mbeto akachomoa dola kumi, sawa na shilingi elfu ishirini, akampatia dereva taksi yule.
“,Sina chenji bosi, “dereva taksi aliongea.
“,Usjali, sihitaji chenji yako, naomba unisubili hapa hapa, “kwa sauti ya kike, Donald Mbeto aliongea, dereva taxi akiwa na tabasamu,akatikisa kichwa kukubali, alifurahi kupokea dili kubwa la pesa nyingi jioni hii, Donald Mbeto akaondoka zake, akapanda ngazi kuelekea Hospitalini.
…………………………………
Alikuwa mwanamke mrembo, hakuna aliyemfikiria vibaya,madaktari, manesi, pamoja na wagonjwa waligeuza shingo zao kumtazama, mwanamke huyu wa kijapani aliyetembea kwa maringo,chuchu zake, makalio yake, yalisababisha vidume wenye uchu wa ngono kummezea mate, hawakujua kuwa mwanamke yule alikuwa na makalio pamoja na matiti ya bandia yaliyofungwa kwa ustadi mkubwa,isitoshe hakuwa mwanamke, bali alikuwa mwanaume rijali kabisa.
Nywele zake nyeupe za mnvi hazikuonekana tena, alivaa wigi kuzizuia,usoni alivalishwa sura ya bandia ya mwanamke wa kijapani, kazi iliyofanywa na daktari wa kundi la magaidi D47.
Donald Mbeto alikata kushoto, akapandisha ngazi, alikuwa anaelekea katika choo cha kike, akafika, ramani yote ya jengo ilikuwa kichwani mwake, haikua mara ya kwanza kutekeleza mauaji yenye taswira ya kufanana katika hospitali hii. “,Nina dakika kumi tu, ninapaswa kukamilisha kazi na kutoweka eneo hili, ” Donald Mbeto aliongea, alifunga mlango wa choo kwa ndani, hakutaka mtu yoyote kumgundua.
Akapanda juu, akakanyaga choo, akaufikia mfuniko juu kwenye dali, akaufungua, ukafunguka, akachomoa tochi yake, akapanda na kutumbukia ndani ya dali.
Giza lilikuwa kali, popo walizunguka huku na kule, akachomoa tochi yake kubwa,akaangaza, popo wakakwepa mwanga, wakakimbia mbali”,chumba cha madawa kiko mbele, “aliongea, akaanza kutembelea tumbo polepole, akijivuta taratibu, dakika kumi baadae, akafikia mfuniko alioutarajia, akasogeza sikio karibu na mfuniko, akasikiliza kwa sekunde mbili, hakusikia sauti yoyote ile, “Hakuna mtu yoyote kwenye chumba cha madawa, “Donald Mbeto aliongea, akausogeza mfuniko pembeni, chumba cha kuhifadhia madawa kikaonekana, hakukuwa na mtu yoyote yule, Donald Mbeto akapenya kwenye tundu, akatumbukia ndani..
Bila roho ya huruma, akachomoa sindano yake, sindano iliyojaa sumu aina ya Sodium pentobarbital, sumu Kali inayoua binadamu kwa dakika moja tu. Akaiingiza sumu katika dawa zote za maji, akachanganya, hakutaka mtu yoyote kuhisi dawa hizo, akasogea karibu na drip za maji,akaingiza sumu kwenye chupa takribani hamsini za drip ya maji, akasogelea chupa za drip ya quinine, dawa ya malaria, akaweka sumu ndani ya chupa takribani mia mbili, akazichanganya vizuri…
Masaa mawili nyuma; Chopa ya jeshi la Tanzania, ilishuka makao makuu ya Jeshi, askari wakashuka, huku kamanda Catherine Obadia akishuka akiwa na mtuhumiwa wa ugaidi, mtuhumiwa ambae sura yake ilikuwa imefunikwa na kitambaa cheusi.
“,Songa mbele mpuuzi wewe, lazima utuambie makao makuu yenu yako wapi, haiwezekani mtusumbue kila siku, kila matukio ni nyinyi ndio mnahusika, why? “,kamanda Catherine aliongea, huku akimsindikiza na mateke mtuhumiwa, mateke mawili yaliyomrushia ndani ya chumba cha mahabusu, akagagaa bila msaada wowote. Alimuacha akiwa na kitambaa chake usoni, akafunga mlango, akatokomea na funguo mahali alikokufahamu yeye …
Kamanda Catherine alipaki gari lake dogo aina ya escudo, akatoka, akalisogelea jengo la China plaza, huku akiwa makini. “,Niangalizie gari langu, baada ya dakika kumi nitarejea, “alichomoa shilingi elfu kumi, akampatia mlinzi wa kimasai,kisha akausogelea mlango wa jengo la China plaza, akaufungua, akaanza kupandisha ngazi kuelekea juu.
“,Paaaaa! “,mlio ulisikika, akapepesuka huku na kule, akaanguka chini kama mzigo.
“,Samahani sana dada, samahani …”,raia aliyeonekana kuwa wa kigeni alimuomba samahani Catherine, wote walikuwa wameanguka chini baada ya kugongana, kijana yule alinyanyuka harakaharaka, akatoka nje.
“,Someone tried to unlock the door “,(kuna mtu alijaribu kufungua mlango) “,kamanda Catherine alijaribu kufungua mlango, akaingiza neno siri ikagoma, akaingiza tena ikagoma, ilikua imeshavurugwa, akabonyeza batani nyekundu iliyoandikwa “RESET KEY “,baada ya kubonyeza akaingiza neno siri ikakubali,maandishi mekundu yakaonekana kwenye mlango uliyotengezwa kwa teknolojia ya hali ya juu …
“,Nani alijaribu kufungua mlango? “,kamanda Catherine aliongea, akasubili kidogo, ujumbe ukarudi kwa mara nyingine kwenye kifaa kidogo karibu na mlango, kifaa cha kuingizia neno siri ili mlango kufunguka.
“,Someone tried to unlock your door “,(Kuna mtu alijaribu kufungua mlango wako …)”,ujumbe ulisomeka, picha ya muhusika ikaonekana, sura haikua ngeni katika macho yake, akajishika kichwa, akaitafakari, akaikumbuka,hakuwa na haja ya kuingia ndani ya ofisi tena, alifunga mlango kwa mara nyingine tena,akashuka ngazi harakahara kwa kasi ya ajabu …
dakika kumi baadae, tayali alikuwa nje ya jengo la China plaza,aka angaza barabara ya Karume hakuona mtu zaidi ya walinzi pamoja na watu waliokuwa wamejifunika mashuka na kulala kandokando ya magorofa.
“,Samahani mlinzi, kuna kaka mweupe,ana sura ya kisomali, kichwani kafuga rasta,kaelekea wapi? “,kamanda Catherine aliongea, huku akitoa noti mbili za elfu kumi kumi akampatia mlinzi yule wa kimasai, kama ujuavyo mjini kuuliza pesa, usipotoa pesa basi utapotezwa.
“,Alikuja na gari dakika kumi kabla ya wewe hujafika, akapanda juu ghorofani, lakini wewe ulipoingia tu, nilishangaa akitoka nje akihema kwa kasi, akapanda gari, akatoweka,bila shaka wame elekea mitaa ya mabibo…”,mlinzi yule aliongea. Kamanda Catherine akaisogelea gari lake,alipotaka kuingia,akashtuka!,akatazama kwa makini gari lake,lilikuwa limetolewa upepo,akakasirika,akamsogelea mlinzi wa kimasai aliyemuachia gari alinde…
Akachomoa bastola,akamuwekea kichwani,”Niambie,nani katoa upepo kwenye gari langu,nazani unajua kila kitu,nambie kabla sijasambaratisha ubongo wako!”,kamanda Catherine alifoka.
“,Nisamehe,nitasema,usiniue,nipesa tu mwanangu ndio zimesababisha nishindwe kulinda gari yako kikamilifu.”,mzee yule wa kimasai alilia,kelele zilizowaamsha raia waliokuwa wamelala nje,wengine walitimua mbio baada ya kuona silaha,walizani ni majambazi.
“,Walinipatia laki moja,niwaruhusu watoe upepo kwenye gari lako,nikawaruhusu,pia waliniambia ukiniuliza nikudanganye,hawajaelekea mabibo,wameelekea makao makuu ya jeshi la polisi,kuna mfungwa wao!”,mzee yule alinyosha maelezo,kamanda Catherine akafurahia ukweli wa mzee yule,aliona shida nyingi katika macho ya mzee yule,akamuonea huruma,akafungua pochi yake,akampatia laki mbili taslimu,pesa halali za Kitanzania,mzee akashukuru.
“,Siku nyingine kuwa mwaminifu,”Kamanda Catherine aliongea,akasogelea kando ya barabara,akaita bodaboda,hakuna aliyeweza kumsogelea,wote walimwogopa,wengi walishuhudia alipokuwa anamchimba mkwala kwa kutumia bastola mzee yule,waliogopa kumsogelea,wengine walihama vituo vyao vya maegesho…
“,Nikupeleke wapi kamanda,”bodaboda mmoja aliongea,huku akiisogeza pikipiki yake karibu na kamanda Catherine Obadia,bodaboda huyu hakuwa muoga kama wenzake.
“,Nipeleke makao makuu ya polisi,”kamanda Catherine aliongea.
“,Makao makuu ya mbezi au Temeke?”,bodaboda yule aliongea.
“,Temeke,endesha haraka sana,usiogope trafiki yoyote yule…”,kamanda Catherine aliongea,kichwani akitafakari watu waliokuwa wakimnyemelea muda mfupi uliopita…
“,Hawa ni D47,hakuna wengine,hawatuwezi,lazima tuwatie nguvuni…”,aliongea kwa sauti.
“,Kamanda kuna shida?”,bodaboda aliuliza,baada ya kusikia Catherine akiongea peke yake kama mwendawazimu.
“,Aaaah,hakuna shida usjali,endelea kukanyaga mafuta…”,Catherine aliongea,huku akijishangaa,hakuwa anatambua kama aliongea kwa sauti ikiyosikika kwa mtu asiyestahili,mawazo yake yalikuwa mbali sana.
…………………………………
Gano;
Donald Mbeto akiwa amepanda spidi boti,alivua sura yake ya bandia, sura ya kike,akavua sura ya bandia,akanywa maji kwa wingi,sauti ikaanza kurudi taratibu,huku safari ya kuelekea katikati ya bahari,kilomita kumi kutoka ufukwe wa nchi ya Gano ikiendelea…
…
Baada ya kutembea takribani kilomita sita,machale yalianza kuwacheza,maji yalikuwa yamechafuka yakiwa yamebadirika rangi na kuwa meusi,wakapunguza mwendo wa boti yao,wakaisogeza taratibu eneo la tukio.
“,Yap,imeshambuliwa na askari wa Tanzania,wamemkamata D47 namba sabini,kapelekwa Tanzania,tumeshawapatia maelekezo aweze kuuawa haraka sana kabla hajatoa siri za kutuangamiza…”,upande wa pili wa simu ulizungumza.
“,Hapo sawa,sasa sisi tunarudije?niko na D47 namba kumi,hawezi kurudi Gano lazima atatiwa nguvuni kwa mikasa hii,hali haijatulia huko……”,Donald Mbeto aliongea.
“Sogeeni mpaka kilomita ishirini mbele,rada zisiweze kuisoma kwa urahisi helikopta yetu,inakuja kuwachukua”,upande wa pili wa simu uliongea.
“,Sawa bosi,”Donald Mbeto aliongea,akakata simu.
…………………………………
Makao makuu;.
Helikopta ya jeshi la Tanzania ilitua katika uwanja wa jeshi la upelelezi na kupambana na ugaidi nchini Tanzania. Askari walipanga foleni, huku silaha zao zikiwa begani, walisimama wima, hawakutikisika.
Kamanda Kendrick, akiwa na nyota tatu begani,pamoja na mwenzake kamanda Philipo walishuka ndani ya helikopta, wakapigiwa saluti, risasi tatu za heshima kulingana na idadi ya nyota zao zikapigwa hewani, walipokelewa kwa heshima kubwa, kwani wali iwakilisha vema nchi katika medani ya Kimataifa.
“,Kamanda Catherine yuko wapi?, mtuhumiwa wa ugaidi aliyekamatwa yuko mahali gani? “,kamanda Kendrick aliongea baada ya kusogelea ofisi za jeshi.
“,Ameelekea katika ofisi yenu, ofisi ya ukombozi saa moja iliyopita ,mtuhumiwa yuko mahabusu, mnaweza kwenda kumuona! “,
Kabla hata hawajapumzika na kupeleka mabegi yao nyumbani kwao, walianza kazi usiku huu, hali ya nchi haikua shwari, huku mabegi yao yakipelekwa na askari wadogo wenye vyeo vya chini.
“,Huyo hapo amefika, mmh mbona anakuja anakimbia? “,kabla hata mazungumzo hayajaendelea zaidi, askari wa zamu aliongea, wote wakageuka, walimshangaa kamanda Catherine.
“,Ulinzi uimarishwe mahali hapa, bora mmefika, askari yoyote yule asiende kulala ,nimetoka ofisi ya ukombozi nimekoswa kifo, kundi la mtuhumiwa wa ugaidi wanatutafuta watuue, wanamtafuta pia mtuhumiwa wamuue, tunapaswa kumuhoji, inaonekana anafahamu mambo mengi zaidi. “,kamanda Catherine aliongea, akaeleweka, askari walinzi wakachukua bunduki zao na kukaa lindoni, huku the super three soldiers wakielekea mahabusu kumuhoji mtuhumiwa, kwa upande wa masaa, ilikuwa takribani saa saba usiku.
Mahabusu.;
Hawakuamini walichokiona,walimgusa kidogo mtuhumiwa alipokuwa ameketi na kuegemea ukuta, akadondoka chini,povu lilikuwa linatoka mdomoni kwa wingi, alikufa muda mrefu uliopita..
“,Nani kauwa? bila shaka amekufa kwa sumu, aliyeleta chakula au maji kwa mtuhumiwa akamatwe, atatueleza ukweli “,Kamanda Kendrick aliongea, alikuwa sahihi, wote wakakubaliana naye, wakatoka katika chumba cha mtuhumiwa wa ugaidi, huku vichwa vyao vikijiuliza maswali mengi bila majibu.
Bahari ya hindi; masaa matano yaliyopita …
Harakati ziliendelea makao makuu ya kundi la kigaidi D47,katikati ya bahari. Baadhi ya askari walifanya kazi ya kupakia madawa , kupakia silaha kwenye maboksi, makundi mengine yaliendelea na mazoezi, huku chumba cha mawasiliano kikiendelea kuifuatilia nyambizi yao iliyokuwa safarini kumpeleka Donald Mbeto nchini Gano, kisha imrudishe tena baada ya kazi kukamilika.
“,hapana,yeye bado yuko kazini nchini Gano,walikuwa bado wanamsubili akamilishe kazi warudi naye…”,
“,ok,sasa angalia kwa kutumia kompyuta yako,tujue ni jeshi gani limemkamata mtu wetu,”
“,sawa bosi.”,
Yalikuwa ni mazungumzo kati ya kiongozi wa kundi la kigaidi la D47,bwana Paresh Kumar,pamoja na mtaalamu wake aliyehusika na idara ya mawasiliano na teknolojia,Paresh Kumar alipomaliza kumpatia maelekezo,mtaalamu wake akaendelea kuchezea kompyuta yake,baada ya dakika mbili akamgeukia tena.
“,bosi!”,
“,yes Benard,nambie”,
“,jeshi la Tanzania ndio limemkamata…”,
“,ok sawa,ngoja niwajulishe wenzetu wa Tanzania wamuokoe,ikishindikana wamuue…”,
“,ameshatoa siri zetu,haina haja ya kubakia mzima…”,
“,oooh,kumbe katoa siri zetu,basi ngoja wamuue…”,
Paresh Kumar alimaliza kuzungumza na mtaalamu wake wa teknolojia aliyeitwa Benard,akachomoa simu yake,akabonyeza namba kadhaa,akaweka simu sikioni,simu ikaita,sekunde mbili tu ikapokelewa.
“,haloo D47 namba sitini,Dar es salaam.,Tanzania,
“,nambie mkuu,kuna jipya?”,
“,ndiyo,mwenzetu,D47 namba sabini kakamatwa ,ameletwa Tanzania,hakikisha halioni jua la kesho,”
“,sawa bosi,saa moja tu linatosha,atakua amekata kamba…”,
“,ok,ok,pesa za kazi nawaingizia benki…”,
“,ok mkuu…”,
Mazungumzo kati ya Paresh Kumar,bilionea katili wa kihindi,mmiliki wa kundi la kigaidi la D47 pamoja na kijana wake kutoka Tanzania yalimalizika,akakata simu,akarudisha simu yake mfukoni,sekunde mbili tu,simu ikaita tena,akaichukua katika mfuko wake wa suruali,akaitazama,Donald Mbeto alikuwa amepiga,wote waliokuwa karibu naye wakatazamana,walitaka kujua nini kinaendelea,akapokea simu harakaharaka,akaiweka sikioni.
“,Haloo Donald, kazi inaendeleaje? “,Paresh Kumar aliuliza swali baada Ya kupokea simu ya Donald Mbeto, akajibiwa swali alilouliza.
“,Yap, imeshambuliwa na askari wa Tanzania, wamemkamata D47 namba sabini, kapelekwa Tanzania, tumeshawapatia maelekezo aweze kuuawa haraka sana kabla hajatoa siri za kutuangamiza …”,Paresh Kumar aliendelea kukuongea na Donald Mbeto kwa kutumia simu, kisha akakaa kimya, alikua akisikiliza maelezo kutoka kwa kijana wake mtata Donald Mbeto.
“,Sogeeni mpaka kilomita ishirini mbele, rada zisiweze kuisoma kwa urahisi helikopta yetu, inakuja kuwachukua …”,Paresh Kumar aliongea, kisha akakata simu.
“,Chukueni helikopta, seahawk, nendeni mkamchukue Donald Mbeto na mwenzake, kuweni makini …”,Paresh Kumar alitoa maelekezo kwa vijana wake, wakatoweka mbele yake, akabaki peke yake akiwa na Benard, katika chumba cha mawasiliano ,makao makuu ya kundi lake, katikati ya bahari ya hindi.
…………………………………
Dar es salaam;
“,Wawili waende makao makuu ya polisi, wengine waende Kariakoo kwenye ofisi ya hawa washenzi, lazima tutajua chochote kuhusu mahali alipo mwenzetu “D47 namba sitini aliongea. “,Sawa bosi, tuondoke “,wenzake wakaitikia, kisha wakasambaratika, wakaondoka katika makazi yao yaliyoko kimara, ndani ya jengo la kifahari, lisilo na panya wala mende ndani yake.
…………………………………
Temeke; Makao makuu
Kundi la kwanza lilipaki gari lao karibu kabisa na kituo cha polisi, makao makuu ya askari wapelelezi nchini Tanzania.Mmoja akabaki ndani ya gari, mwingine akatoka,akaangaza huku na kule hakuona kitu, akaanza kutembea kusogelea ofisi za jeshi, uso kwa uso akakutana na mtu aliyemkusudia, askari mamluki.Siku zote alichukua taarifa za serikali na kuwapatia magaidi,ili kujipatia donge nono na kukidhi njaa zake.
“,Mwenzetu amekamatwa,hatujui kapelekwa mahali gani, sijui unaweza kutusaidia …”,
“,yupo mahali hapa, kaletwa muda sio mrefu, kuwasaidia naweza lakini nyinyi hamuwezi kwenda, ulinzi ni mkali mno”,
D47 namba sitini aliagana na askari wa zamu,wakapeana sumu kwa siri, hakuna aliyewaona, kisha kila mtu akachukua hamsini zake, askari wa zamu akarudi kituoni, gaidi akatoka eneo la kituo cha polisi, akavuka barabara, akapanda gari lao, wakaondoka zao …
………………… ………………
Kariakoo;
Gari ya kifahari aina ya BMW ilipaki pembeni mwa barabara ya Karume, nje ya jengo la China plaza. Gaidi mwenye sura ya kisomali, rasta ndefu kichwani mwake, alishuka ndani ya gari, alionekana kuwa na haraka sana, akaingia ndani ya jengo, akapanda juu harakaharaka, ndani ya dakika kumi, alifika ghorofa ya tano, nje ya ofisi ya Ukombozi, ofisi ya kundi la wapelelezi wa Tanzania, maarufu kama the super three soldiers.
Gaidi D47 namba ishirini, akaanza kufungua mlango kwa kutumia utundu wake, aliingiza neno siri katika mlango ukagoma kufunguka, akakadilia tena, akaingiza ukagoma, akatafakari, akaingiza tena mlango ukagoma kufunguka, ghafla simu yake ikaanza kuita, akaichukua, alikuwa ni mkuu wake wa kazi, akaipokea.
“,Njooni kambini haraka, kazi tayali imekamilika, “sauti ilisikika upande wa pili wa simu, akakata simu, akairudisha mfukoni, akaanza kushuka ghorofani bila kutambua tayali alipigwa picha naa kifaa cha kuingizia neno siri mlangoni, baada ya kukosea neno siri mara tatu mfululizo.
“,puuuu, “kishindo kilisikika, walipamiana na mwanamke ambaye alimtambua vizuri sana,alitwa kamanda Catherine, alimanusura amkute ndani ya ofisi yake, wakatupiana maneno, akasimama na kutoweka zake, akafika nje, akampatia maelezo kazaa mlinzi, akampatia pesa, akatoa upepo wa gari, kisha akarudi makao makuu ya kundi lao nchini Tanzania.Huku wakimdanganya mlinzi kuwa akiulizwa aseme walielekea Mabibo au makao makuu ya polisi.
…………………………………
Makao makuu ya polisi;
Askari wa zamu alichukua chakula kama kawaida yake,kuwapatia mahabusu chakula, akaweka sumu kwenye chakula cha mfungwa wa ugaidi,kisha akamuita askari ambaye alikuwa lindo, bila shaka alimzidi cheo.
Afande aliitikia kwa mbwembwe, bila kujua kuwa tayali aliuziwa kesi, akachukua chakula kimoja baada ya kingine, akawepelekea mahabusu, akiwemo gaidi D47,mshatakiwa wa kesi ya ugaidi anayetafutwa kuuawa kwa udi na uvumba.
…………………………………
Gano; 8;20am
Hospitali ya jiji la Gano ilikuwa imejaa watu kama kawaida, wagonjwa, madaktari pamoja na watu mbalimbali hospitalini walijaa na taharuki kubwa, wengine walijadiri kuhusu mripuko wa gari uliotokea usiku uliopita bandarini, wengine wakijadirinana kuhusu karatasi iliyokutwa imebandikwa katika vyoo vya kike hospitalini, ikiwa na maneno yaliyojaa utata,maandishi yaliyoandikwa kwa wino wa damu, neno JINI MWEUPE.
“,naitwa Efreza, mwandishi wa Gano tv,unalizungumziaje swala la karatasi hii iliyobandikwa hospitalini…?”,
“,hii karatasi ilibandikwa mwaka 2008 mahali hapa, baada ya muda vifo vingi vikatokea hospitalini, mwaka 2016,karatasi yenye neno hili ilibandikwa katika hospitali ya taifa la Tanzania, baada ya masaa kadhaa, watu wakafa kama nzige hospitalini, mpaka leo mtuhumiwa anatafutwa bila mafanikio ,kwahiyo naiomba serikali ifanye uchunguzi bila hivyo tutakufaa……”,
Watu walimcheka mwanaume mwenye mavazi yaliyolaruka na kujaa viraka, hawakutafakari maneno yake aliyozungumza wakati wa kuhojiwa, siku zote maskini hawana sauti na maneno yao hupuuziwa, baada ya kumaliza kuhojiwa, aliondoka zake, mwandishi wa habari akaendelea kuhoji watu wengine, nusu saa baadae vifo vikaanza kutokea hospitalini, idadi ya vifo ikaongezeka kila baada ya nusu saa, hawakujua chanzo ni nini, madaktari walikimbia huku na kule, waandishi wa habari wakaanza kujaa hospitalini, polisi wakazagaa kila kona ya hospitali, haikusaidia chochote kile, wagonjwa waliendelea kufa, huku miili yao ikifanyiwa uchunguzi ili kujua chanzo cha vifo vyao, maneno ya tahadhari kutoka kwa masikini aliyehojiwa masaa mawili yaliyopita yakawa na mashiko ndani yake.
Makao makuu ya polisi; masaa sita yaliyopita;
The super three sordiers, walitoka mahabusu, wakiwa na maswali mengi kichwani, maswali ambayo yalipaswa kujibiwa na askari wa zamu, pamoja na askari wa lindo …
“,Kamanda wa zamu, mtuhumiwa wa ugaidi amepoteza maisha, bila shaka yoyote amekufa kwa sumu, maana povu jingi linamtoka mdomoni, unaweza kutwambia nani kauwa? “,kamanda Catherine aliuliza,akiwa amesimama sambamba na wenzake, kamanda Philipo pamoja na kamanda Kendrick.
“,Mtuhumiwa amekufa!, sijui chochote, ndiyo taarifa hii ninaisikia kutoka kwenu “,askari wa zamu alijitetea, alikuwa ameketi kwenye meza yake, karibu kabisa na mlango wa kuingilia kituoni.
“,Uongo kabisa, uongo huo, wewe ndiye uko hapa mezani, mapokezi, yoyote yule anayeingia kituoni au mahabusu lazima aombe kibali kutoka kwako, wewe kama askari wa zamu, kwanini unasema hujui?, “kama Kendrick aliuliza.
“,Mambo mengi bosi, muda mwingine nitatoka kwenda toileti,wakati mwingine nakuwa bize napekua mafaili ya kesi mbalimbali kabatini, kwahyo inawezekana walitumia fursa hiyo, wakapenya, wakasababisha mauaji! “,askari wa zamu aliendelea kujitetea.
“,Ok sawa, sawa kabisa, umejitetea vizuri, lakini ,wewe kama askari wa zamu, unahusika pia na kuwapelekea chakula wagonjwa?, ulionja chakula hicho ?,…”,Kamanda Kendrick aliuliza, askari wa zamu akasita kujibu, akakaa kimya kwa takribani dakika tano, kisha akafungua mdomo wake,bila shaka alitaka kunena jambo.
“,Nilikuwa bize na kazi?, kamanda Agrey, askari wa zamu kulinda mahabusu, nilimuomba anisaidie kuwapa chakula badala yangu …”,askari wa zamu alijitetea.
“,What!, wewe unahusika, unahusika na mauaji, tangu lini ukawa bize mpaka ukakosa dakika tano za kuwapatia chakula mahabusu, tena watatu tu? ,anyway! tuyaache hayo, namuomba kamanda Agrey aje hapa! “,kamanda Catherine aliongea,alikuwa na hasira kupita kiasi, dakika mbili tu kamanda Agrey alifika mbele yao, akapiga saluti …
“,Nimeitikia wito Afande “,kamanda Agrey aliongea, akiwa amesimama wima kwa heshima, bila kutikisika …
“,Ulipeleka chakula mahabusu? “,kamanda Catherine aliuliza …
“,Ndiyo, nilipeleka? “,kamanda Agrey alijibu
“,Ulionja chakula ?”,Catherine aliuliza tena.
“,Hapana, askari wa zamu aliniambia kiko salama, alikuwa tayali ameonja …”,alijibu kwa ufasaha.
“,Unaaminije kama alionja, ulimuona? “,Catherine aliuliza.
“,Ulimuona wakati anatoa vyombo, kwanini atoe vyombo,hakua bize kama alivyosema awali? wakati chakula cha Wafungwa kinaliwa kwa dakika tano tu? “,kamanda Catherine aliuliza.
“,Sijui afande, swali hilo labda umuulize yeye mwenyewe …”,Agrey alijibu.
“,Unajua sababu ya kukuuliza maswali haya yote? “,Catherine aliongea.
“,Hapana!, sijui Afande! “,Agrey alijibu.
“,mshatakiwa wa Ugaidi, aliyeletwa usiku huu amekufa kwa sumu? “,kamanda Catherine aliongea.
“,Unasemaje?, amekufa! “,kamanda Agrey aliongea,alishangaa sana kwa taarifa aliyopatiwa, hakujua chochote kile kilichokuwa kinaendelea.
“,Najua haujaua, lakini utawekwa rumande kwa uzembe, naomba uvue mkanda, pamoja na kofia,haiwezekani uwe zamu kulinda mahabusu, harafu mahabusu afe bila wewe kujua chochote kile, that is nonsense! “,kamanda Catherine aliongea kwa hasira,siku zote akiongea, ameongea, habadili msimamo hata siku moja …
“,Ukikaa rumande kwa wiki moja, i hope next time utakua makini, lakini kwa huyu askari wa zamu, awekwe chumba cha mateso, asulubiwe mpaka aseme nani kauwa? ,maelezo yake yanaonesha anajua kila kitu …”,kamanda Kendrick aliongea, huku askari baadhi wakiitwa, wakawakamata askari wote wawili, kila mmoja akapelekwa katika chumba chake,kadri amri zilivyotolewa na the super three soldiers …
…………………………………
Masaa manne yaliyopita; Bahari ya Hindi
The seahawk, helikopta ya kivita, helikopta ya kutegemewa na kundi la magaidi la D47,ilitua kwa mara nyingine tena, katika meli kubwa inayoitwa D47paraquat, meli yenye uwezo wa kubeba ndege za kivita mia moja, vifalu hamsini,isitoshe ilikuwa na uwezo wa kujigeuza kama nyambizi ikazama chini ya bahari, sifa kubwa kuliko zote, ilikuwa na uwezo wa kupaa angani kama ndege zingine zozote zile …
“,Karibu sana, welcome my hero! kazi imekwisha, kilichobakia ni kusikia tu vifo kesho asubuhi ……”,
bosi wa kihindi, mmiliki wa kundi la D47 maarufu kama Paresh Kumar, alimpokea Donald Mbeto kwa heshima, mara baada ya helikopta kurejea, ilipowafuata kilomita therathini ,katikati ya bahari, kutoka kisiwa cha Gano, baada ya Nyambizi aliyokwenda nayo awali kuripuliwa.
“,Kweli bosi, nimefanikiwa kukamilisha kazi,nitazidi kutikisa dunia, watanitafuta mpaka wanazeeka, hawatanipata!! “,Donald Mbeto alishuka kwenye helikopta, akashikana mikono na bosi wake, huku akiongea maneno ya kejeli kwa mataifa yote duniani yaliyomtafuta kila kukicha.
“,Hahahaa, “wote wakacheka, meno yote yakaonekana kwa nje, walijawa na furaha, kwa kukamilisha kazi kubwa kwa muda mfupi tu.
“,Sasa hapo lazima wajute,lazima wajute kwanini walinikataza nisimiliki migodi ya almasi katika nchi zao, nikapoteza pesa nyingi kuhonga viongozi wakubwa katika serikali zao, lazima wajute kula pesa zangu, harafu nikose migodi ya dhahabu, ok kijana wangu, unatorokea Amerika au wapi! “,Paresh Kumar aliongea, akaeleza sababu ya kijana wake kufanya mauaji Tanzania, Ufilipino,Gano pamoja na nchi zingine, huku baadhi ya nchi Donald Mbeto akiwa amefanya mauaji mara mbili mfululizo.
“,Siendi popote pale, wewe ni mama na pia ni baba yangu!! “,Donald Mbeto aliongea, licha ya umri wake wa miaka sitini, umri uliopelekea awe na mnvi nyingi kichwani na kidevuni, mnvi zilizosababisha ajiite Jini Mweupe, sababu ya mwonekano wake,alimuheshimu sana bosi wake, bosi kijana wa kihindi, bilionea Paresh Kumar mwenye umri wa miaka arobaini tu …
“,Sawa kijana, nafurahi kuskia hivyo, twende ukaburudike …”,bosi Paresh Kumar aliongea, akamchukua Donald Mbeto, wakaelekea katika vyumba vyao vya starehe, vyumba vilivyojaa starehe zote, bila kusahau wanawake wa kila aina, wazungu, waafrika, wachina na wajapan …
Kamanda Catherine, kiongozi mkuu wa idara ya mawasiliano na teknolojia, katika kundi lake la wapelelezi watatu, maarufu kama the super three soldiers, alikuwa amechanganyikiwa, taarifa aliyoipokea kwa mfumo wa barua pepe ya ofisi yao, pamoja na radio na televisheni zilizidi kumchanganya kupita maelezo. Alijizungusha kwenye kiti chake, ndani ya ofisi yao maarufu kama ofisi ya Ukombozi, kabla ya kuelekea kituoni itakapofika saa sita mchana, kwenda kujua nini kinaendelea …
“,We have to go, tunapaswa kwenda,gaidi aliyeuawa alisema ukweli mtupu, tungemuhoji kabla hajafa tungejua mambo mengi zaidi, lakini ndo hivyo, they have killed him, wamemuua, hakijaharibika kitu, tukienda Gano, tutapata mahali pa kuanzia, tujue alipotoka Gano alielekea wapi tena, na kwanini anaua? Mauaji ya kufanana, sio bure, kuna kitu! “,kamanda Catherine, akiwa peke yake ofisini, ilikuwa kawaida yake kuwahi kazini siku zote, aliongea, akatafakari, akanyenyua simu yake, akampigia kamanda Kendrick, mkuu wake wa kazi …
“,Yes kamanda, mzima? “,kamanda Kendrick aliongea, baada ya kupokea simu.
“,Mimi mzima, vipi umefuatilia habari zilizopamba mtaani, Donald Mbeto ameshafanya yake nchini Gano, taifa letu linatutaka kwende haraka sana kisiwa cha Gano tukamtafute muuaji wetu, serikali ya Gano na wenyewe wametutumia ujumbe twende tukawasaidie uchunguzi wa mauaji yaliyofanyika! “,kamanda Catherine alieleza kwa kirefu zaidi.
“,Nimeshapata taarifa hizo, ndiyo taarifa ambazo zimenichelewesha kufika ofisini mpaka sasa hivi, lakini tayali nimeshapata majibu, namna ya kumpata Donald Mbeto, nakuja sasa hivi ofisini, mpatie taarifa kamanda Philipo tukutane hapo ofisini, ndani ya nusu saa ijayo, “kamanda Kendrick aliongea.
“,Sawa bosi, “kamanda Catherine aliongea, akakata simu, kisha akabonyeza tena simu yake, akaitafuta namba ya simu ya kamanda Philipo, akaipata, akapiga, kisha akaisogeza simu yake sikioni.
“,Haloo Cathe,umesikia kuhusu Donald Mbeto huko Gano, yani huko ni kilio na kusaga meno kama jehanamu vile, niko njiani nakuja ofisini, tujue nini cha kufanya! kamanda Kendrick ameshafika ofisini? “,
“,Yani simu hii ni kwa ajili ya huyu mshenzi,tumekubaliana tukutane hapa ndani ya nusu saa ijayo, kamanda Kendrick hajafika ofisini, lakini yuko njiani anakuja, usichelewe, usinywe bia yoyote, najua vizuri matatizo yako, usipo nisikiliza, utakwamisha kila kitu ……”,
“,Hahahaa, sawa, nakuja, siwezi kulewa,nitalewa mpaka Donald Mbeto, huyu jini mweupe awe katika mikono yetu, “
Yalikuwa ni maongezi ya simu kati ya kamanda Philipo, pamoja na Kamanda Catherine, kisha simu zilikatwa.
Ofisi ya ukombozi; 10:02
Kikao kifupi kiliendelea, kamanda Kendrick aliongoza majadiriano, kila mmoja alichangia maoni yake, akatoa mbinu mbalimbali za kumkamata Donald Mbeto.
“,Kabla hatujafika mbali, kamanda Kendrick, hebu tueleze! nilipokupigia ulinambia kuna mbinu ambayo umeipata, hebu tuelezee na sisi tuitambue kama mbinu hiyo inafaa au haifai! “,kamanda Catherine aliongea,wenzake wakimsikiliza kwa makini.
“,Usjali kuhusu hilo, vipi kuhusu ujumbe kutoka Gano,unasemaje, hebu tuusome halafu nitawaeleza mbinu hiyo ya kumkamata huyu Mwanaharamu. “,kamanda Kendrick aliongea, akijizungusha kwenye kiti chake huku na kule,wenzake wakimsikiliza kwa umakini wa hali ya juu.
“,Mauaji yametokea tena kwa mara ya pili sasa, mauaji yanayofanana, kila tukio muuaji katumia sumu, sumu ambayo imetumika kwenye mauji huko nchini kwenu Tanzania, Ufilipino na nchi kadhaa za Afrika, Asia na Ulaya, tunahitaji msaada wenu, mje mara moja kushirikiana na vijana wetu kumsaka adui huyu! “,kamanda Catherine alimaliza kuusoma ujumbe wa barua pepe kutoka nchini Gano, akainua kichwa chake,wote watatu wakatazamana.
“,Haya sasa, nazani umesikia, tueleze hiyo mbinu kisha tuanze kazi haraka sana…”,kamanda Philipo alichangia mawazo yake.
“,Ok! kabla ya kuelekea nchini Gano, tunapaswa kulifumbua fumbo la kifo cha gaidi mshirika wa Donald Mbeto, gaidi aliyeuawa mahabusu, tukifanikiwa! lazima tujue mahali alipojificha Donald Mbeto, hata tukienda Gano, yatatokea kama yaliyotokea Ufilipino. “,kamanda Kendrick aliongea kwa hisia kali,wote wakatikisa vichwa vyao,bila shaka walikubaliana na mawazo yake.
“,Kweli kabisa, kama vile ulikua kichwani mwangu,hata mimi niliwaza hivyo hivyo! mimi ninaona tukamuhoji vizuri askari aliyekuwa zamu, maana mpaka sasa hatujamuhoji kwa kipigo, lazima atasema ukweli,kuna kitu anajua tu yule, maana usiku wakati tunamuhoji hakujiamini hata kidogo “,kamanda Catherine aliongea,akanyenyuka kwenye kiti chake.
“,Twendeni, twendeni kituoni haraka sana, tusipoteze muda, nazani tayali tumefikia muafaka! ,askari yule ahojiwe kwa kipigo, kama siyo yeye muuaji basi nitalipa kila kitu kwa ajili yake”,kamanda Kendrick aliongea, na yeye akanyenyuka kwenye kiti, akaweka tai yake vizuri,akajiandaa kwa ajili ya kutoka nje ya ofisi ya ukombozi. Kamanda Philipo alichukua kompyuta ya ofisi, akaiweka kwenye begi lake, akanyenyuka kwenye kiti,kamanda Kendrick akatoka nje, kamanda Catherine akafuatia, kisha kamanda Philipo akafuata, akasimama nje ya mlango wa ofisi yao, akabonyeza bonyeza mashine pembeni ya mlango,akaingiza nywila (neno siri), mlango ukajiloki. Wakatoweka, wakaelekea kituoni.
…………………………………
Makao makuu ya polisi; 11:02
Kamanda Catherine alikuwa amesimama, mkononi alikuwa ameshika plaizi,kamanda Philipo alikuwa amesimama pembeni ya Catherine, mkononi mwake alishika bakola, fimbo kubwa ya chuma isiyo katika, kamanda Kendrick yeye alikuwa amechuchumaa,mkononi alishika mjeledi, akamtazama askari wa zamu aliyelala chini kama mzigo, akiwa amefungwa mikono na miguu.
“,Ukweli wako ndiyo utakuweka huru, jana tulikuhoji kwa upole, ukazani tunatania, hatujawahi kutania kazini hata siku moja, ndiyo maana tunategemewa na taifa letu, tuko hapa kwa ajili yako! “,kamanda Kendrick aliongea, kamanda Catherine akachuchumaa, akasogeza plaizi yake kwenye masikio ya askari yule, akayabana kwa nguvu bila huruma.
“,yalaaaa! nakufa…a …”,kelele za uchungu zilisikika,askari yule alilia kama mtoto,damu ilichuruzika katika sikio lake,alitamani ajikune lakini hakuweza, mikono yake ilifungwa kwa pingu za chuma.
“,Kufaaa! si hautaki kusema ukweli? “,kamanda Catherine alifoka.
“,Sisemi, nasema sihusiki na chochote! “,askari yule aliongea kwa jeuli.
“,Pyaaa! pyaaa! “,
“,Yalaaaa! mama…aa”,
Sauti za bakola zilisikika, kamanda Philipo alimchapa bakola mbili askari yule kwenye unyayo wa miguu yake,unyayo ukaacha mistali miwili iliyovuja damu,askari yule akaikunja na kuinyosha miguu yake, alitamani kujikuna lakini hakuweza.
“,Nitasema, nitasema! msiniuee ……!”,askari yule alipiga kelele,maumivu yalimzidi nguvu, mwili wake ukashindwa kustahimili mateso ya kipigo ambacho nd’o kwanza kilikua kinaanza.
“,Sema! semaa kabla sijakuchalaza na mjeledi wangu! “,kamanda Kendrick alifoka, akiwa amenyenyua mkono wake wa kulia juu, akijiandaa kumtandika nao askari yule.
“,Nitasema mkuu, msinipigee! “,askari yule mamluki alililia, akaomba msamaha,alikuwa tayali kusema ukweli, wote wakaweka silaha zao za mateso pembeni, wakakaa tayali kwa ajili ya kumsikiliza.
“,Mimi ndiye niliye muua gaidi yule, nilipewa sumu na kundi la D47 niweze kummaliza, kwa muda mrefu nashirikiana nao, nawapatia habari za upelelezi kisha wananipatia pesa, ndiyo maana imekua vigumu hata kumkamata Donald Mbeto”,askari yule aliongea, akaeleza kila kitu, hasira zikampanda kamanda Catherine, akamsogelea askari yule, akamkaba shingoni..
“,Muachee, utamuua! Catherine utamuuaaa! “,kamanda Kendrick aliongea kwa taharuki, akiwa anafanya kazi ya ziada kutoa mkono wa Catherine katika shingo ya askari yule, huku kamanda Philipo akishirikiana naye kufanya shughuli hiyo.
“,Haiwezekani kila siku tuhangaike kumsaka mtuhumiwa kumbe mchawi tunaye ndani,stupid comrade! hautufai katika jeshi letu, lazima sheria ichukue mkondo wake …”,kamanda Catherine alifoka,huku akiiweka vizuri suti yake, baada ya mkono wake kufanikiwa kutolewa na makamanda wenzake katika shingo ya askari yule msaliti.
“,Sawa! tumesikia,makazi ya D47 yako wapi? ,Donald Mbeto na yeye tunampata wapi?”,kamanda Kendrick aliuliza swali jingine,akimtazama askari yule msaliti,akijaribu kuinyosha shingo yake bila mafanikio,alimanusura kamanda Catherine amtoe koromeo.
“,D47 wanapatikana katikati ya Bahari ya hindi,wana meli yao kubwa aneo hilo,hata Donald Mbeto hurudi eneo hilo kila anapomaliza kutekeleza tukio,huenda kupumzika kabla ya kupewa kazi nyingine…,ni hayo tu nayofahamu bosi!”,askari yule aliongea,kamanda Catherine akachana shati la askari yule,akamgeuza,uso ukalamba vumbi,mgongo wake ukabaki wazi,”D47 namba mia moja,”kamanda Philipo aliongea,alisoma chata kubwa iliyozungushiwa duara katika mgongo wa askari yule.Askari yule hakuwa mamluki tu,bali alikuwa mwanachama halisi wa D47.
“,Ndio maana Tanzania hatuendelei,China watu kama hawa wanapigwa risasi mbele ya umma…”,kamanda Kendrick aliongea,akaanza kutoka mahabusu,wenzake wakamfuata.
“,Mahabusu yake iongezewe ulinzi, asiingie wala kutoka mtu yoyote, kamanda Petro andaa helikopta ya kivita! tunapaswa kuelekea nchini Gano, kisha tutaelekea moja kwa moja katikati ya bahari ……” ,kamanda Kendrick alitoa maagizo,kisha wote watatu wakaelekea stoo ya silaha (Amala),wakachukua silaha zote zilizowafaa kwenye mapambano,visu, bastola, kamba, saa zao za kipelelezi pamoja na miwani ya mionzi mikali.
………………………………
01:20
Helikopta ya jeshi iliacha ardhi ya Dar es salaam Tanzania, siku ya ijumaa, saa saba mchana, ilipaa futi sitini kwenda juu, ikaelekea mashariki mwa mji wa Dar es salaam, katikati ya bahari.Askari wa the super three soldiers wote walivalia mavazi maalumu meusi, rangi ya shaba, yasiyo pitisha risasi(bullet proof), machoni walivaa miwani ya mionzi, mkono wa kushoto walivaa saa zao za kipelelezi kwa ajili ya mawasiliano.
“,Kaa tayali kwa misheni, kushindwa ni dhambi, tuna dakika kumi za kufika eneo la tukio nchini Gano, tuna saa moja la kutekeleza misheni na kumpata Donald Mbeto, tunaelewana? “,kamanda Kendrick aliongea, akauliza swali askari wake.
“,Ndiyo afande, tumeelewana! “,wote waliitikia,walikubaliana na maelekezo kutoka kwa mkuu wa kikundi, kamanda Kendrick, safari ikaendelea, helikopta ikaendelea kukata mawimbi.
Gano:02:02pm
Pilikapilika ziliendelea katika hospitali ya jiji la Gano,watu waliingia kuchukua miili ya ndugu zao,waliopoteza maisha kwa sumu hospitalini hapo,waandishi wa habari hawakuchoka, waliendelea kutimiza majukumu ya kuchukua taarifa mbalimbali kama kawaida yao. Polisi waliendelea kufanya uchunguzi wao, wakiongozwa na kamanda wao mkuu wa upelelezi kisiwani Gano.
“,Jiandaeni kupokea wapelelezi kutoka Tanzania, watafanya uchunguzi kwa dakika kumi tu, kisha tutaongozana nao kwenye misheni katikati ya bahari …”,kamanda mkuu wa upelelezi kisiwa cha Gano aliongea,vijana wake ishirini wakapanga mstali, uwanja wa hospitali ya Gano,macho yao yalitazama anga, kaskazini, mashariki na magharibi.Kila mmoja akisimama wima kwa ushupavu, kupokea askari watatu wenye sifa kubwa dunia nzima, kwa upelelezi wao wa kishujaa.
“,Simama wima, heshima toa! “,kamanda yule alitoa amri, helikopta ilipita katika anga la hospitali kwa spidi ya ajabu,ikapigiwa saluti za heshima, ikakunja kona ,kaskazini, kisha ikarudi tena magharibi, ikapunguza kasi, ikaanza kushuka chini iweze kutua.
“,Makamanda wakishuka, piga saluti za heshima, kisha tutawaongoza mpaka eneo la tukio …”,kamanda yule aliongea kwa sauti kubwa, kisha akavuta pumzi ndefu. Macho yake yakiitazama helikopta kubwa ya kijeshi yenye chapa ya Tanzania, ikitua na kutimua vumbi zito eneo lote la uwanja wa hospitali ya Gano.
Helikopta ya jeshi la Tanzania ilitembea kilomita takribani ishirini,ikafika anga la kisiwa cha Gano,ikaanza kushuka taratibu, futi hamsini, arobaini, therathini, mpaka ishirini, ikaanza kufuata ramani mpaka mahali pa tukio, hospitali ya jiji la Gano, kisiwa kinachopatikana bahari ya hindi, jirani kabisa na nchi ya Tanzania.
“,Tumefika, hakuna muda wa kupoteza, kila mtu atimize majukumu yake …”,kamanda Kendrick aliongea,akawakumbusha tena askari wenzake.
“,Ndiyo afande! “,waliitikia, helikopta ikazunguka eneo la hospitali,ikakata kona, kisha ikatua katika uwanja wa hospitali, wakashuka wakitembea harakaharaka,huku wakipigiwa saluti za heshima, kisha askari wenyeji wakawaongoza mpaka eneo la tukio.
“,Eneo lenyewe ndiyo hili, kama unavyoliona, aliingia kupitia choo hiki, akatoa mfuniko wa dali,akapita ndani kwa ndani mpaka chumba cha madawa, akaweka sumu kwenye madawa yote ya kimiminika, hivyo basi yoyote yule aliyetumia dawa hizo asubuhi ya leo aliweza kufa, mpaka sasa wamefariki dunia wananchi elfu tatu! “,kamanda mkuu wa upelelezi nchini Gano alitoa maelezo ya upelelezi wa awali,kamanda Kendrick akatikisa kichwa, akakagua choo chini na juu, kisha akatoka nje, akaangaza huku na kule.
“,Hiyo karatasi vipi?”,kamanda Kendrick aliuliza swali, akasogea ukutani, mahali kulipokuwa na karatasi yenye wino mwekundu.
“,Hiyo ndo karatasi iliyotuongezea taharuki, imeandikwa Jini mweupe, maandishi ya damu …!”,kamanda yule aliendelea kutoa maelezo yake.
“,Sawa nilishapata jibu, huyu ni Donald Mbeto, hakuna mwingine, tuachieni kazi hii, tunaenda kuifanyia kazi, tukihitaji msaada tutawajulisha! “,kamanda Kendrick aliongea,aliona kazi hiyo aifanye yeye mwenyewe pamoja na vijana wake alio wazoea,ombi lake likakubaliwa, askari wa nchini Gano wakapiga saluti, wakaanza kutoka nje,waandishi wa habari wakitimiza majukumu yao kupiga picha na kurekodi kila tukio.
“,Kwa niaba ya waziri wa ulinzi, tunawatakia safari njema na misheni njema, tulitamani sana kuongozana na nyinyi maana tuna hasira na huyu muuaji, kwa msaada wowote msisite kutufahamisha …”,kamanda mkuu wa upelelezi kisiwani Gano aliongea,wakapigiana saluti, the super three soldiers wakaingia ndani ya helikopta,baada ya dakika tano, helikopta ilikua futi sitini juu angani, ikaanza kuelekea kaskazini, kukiacha kisiwa cha Gano, kuelekea katikati ya bahari, kutekeleza misheni ngumu kuliko zote katika maisha yao ya kipelelezi, achilia mbali oparesheni ya kumsaka muuaji hatari Yuan Liang nchini Gano mwaka mmoja uliopita, hii ya Donald Mbeto iliwaumiza kichwa kila siku.
…………………………………
Mbezi, Dar es salaam :2:00
Magaidi wa D47 kanda ya Dar es salaam, walikuwa wameketi kikao cha dharula, wakibadilishana mawazo,askari wa serikali,aliyewapatia taarifa kutoka serikalini na kufanikisha shughuli zao mbalimbali alikua hapatikani kwa simu tofauti na siku zote,tangu usiku wa saa nane walimtafuta wajue nini kinaendelea serikalini, lakini hakupatikana, simu yake haikuwa hewani kabisa, kadri muda ulivyozidi kwenda ndivyo hofu ilizidi kutanda.
“,Hapa kuna kitu,sio kawaida yake kabisa,mimi nashauri twendeni kituoni,mmoja aingie mpaka kituoni,kama kuna lolote baya limemkuta,tumsaidie,bila hivyo kila kitu kitaharibika…”,gaidi D47 namba sitini aliongea,wenzake watatu wakiwa makini kumsikiliza.
“,kweli kabisa,yule ana siri nyingi kama mwenzetu,akiwa pabaya hata sisi tuko pabaya,tuchukue silaha,mmoja ajifanye ameenda kushtaki,apeleleze kisha atuletee taarifa nje tujue mwenzetu yuko salama,au kagundulika,”gaidi D47 namba ishirini aliongea,wote wakanyenyuka,wakasogelea stoo yao ya silaha,wakachukua bunduki zao,mikanda ya risasi,wakatoka kwenye nyumba yao ya kifahari,wakaingia kwenye BMW nyeusi,wakatoweka katika makazi yao haraka sana kwa kasi ya ajabu.
…………………………………
Bahari ya Hindi:
Burudani ziliendelea katikati ya bahari,kila mmoja aliyekuwa katika meli ya D47paraquaat aliburudika kwa starehe aliyohitaji,wengine walikunywa pombe,wengine walijidunga madawa ya kokeini,huku wengine wakizini,kila mmoja alifanya starehe aliyohitaji kufurahia ushindi wa Donald Mbeto,alifanikiwa kukamilisha kazi aliyotumwa na bosi kwa mataifa yote matano aliyotumwa kuua kwa sumu,akaitikisa dunia,jina lake likaenea duniani kote.
“,Danger!danger!our kingdom is in danger!dange!danger!”,(Hatari!hatari!ufalme wetu uko hatarini!hatari!hatari!)
Sauti ya hatari ilisikika,ikapenya katika masikio ya kila gaidi,kifaa maalumu kilitoa taarifa ya hatari, katika kila chumba,pamoja na kumbi za starehe ndani ya meli, magaidi wakaanza kukimbia huku na kule, kila mmoja alitambua jambo la kufanya anaposikia kengele hii, anaacha shughuli zake, anaenda kupanga mstali katika uwanja wa mazoezi.
“,Kuna ndege imeonekana katika rada zetu, kuna ndege kubwa inasogea eneo letu, kutokea mashariki, bila shaka nchini Gano, mahali Donald Mbeto alipotekeleza mauaji muda mfupi uliopita, meli yetu itazama baharini, futi kumi kwenda chini kama nyambizi, lakini lolote linaweza kutokea, jiandaeni! “,bilionea wa kihindi, Paresh Kumar, aliongea kwa kiswahili,alikuwa na miaka mingi pwani hii ya waswahili,alikifahamu kiswahili vizuri sana, baada ya kutoa amri kila gaidi alikimbilia eneo lake, kutimiza majukumu yake,waliamini helikopta hiyo ilikuja ukanda wao kwa vita na wala sio kitu kingine, walikua sahihi kabisa. Bahari ya hindi; 2;40pm
Donald Mbeto alikuwa amezungukwa na wanawake sita wa kizungu,hakuna aliyekuwa na akili zake,kila mmoja alikuwa amelewa chakali, akiwa uchi wa mnyama,chupa za pombe ya ya kizungu, “queen elizabeth”,zilizagaa kila kona ya chumba hiki chenye mwonekano wa kifahari zaidi, godoro la plastiki lillilojaa hewa ndani lilikuwa kitandani, Donald Mbeto alicheza mchezo mchafu na mwanamke mmoja baada ya mwingine, wanawake ambao walitekwa kutoka nchi mbalimbali za dunia, kumbukumbu zao zikafutwa kwa kutumia kompyuta, wakatumikishwa bila kujitambua, huku wakiingiziwa madawa ya kulevya mwilini ili kudumaza akili zao, wakatumika katika kila kazi, uzinzi, kusafirisha madawa(drugs) pamoja na kuua.
“,Ngo! ngo! ngo hodiii! “,licha ya kengele ya hatari kupigwa kwenye chumba cha Donald Mbeto hakuweza kusikia, ikabidi atumwe mtu kumgongea, maana alitegemewa sana kwenye kazi mbalimbali, mawazo yake siku zote yalileta matokeo chanya kwenye kazi za D47.
“,Donald! Donald! kuna hatariii …!”,gaidi mwenye cheo cha chini sana aliita, akaongea kwa sauti kubwaa! .
“,Kwichi, kwichii, kwichiii ………”,sauti ilisikika, sauti ambayo haikua ya Donald Mbeto, bali kelele za kitanda kilichokuwa kimezidiwa nguvu, gaidi yule hakuendelea kuita tena,alirudi kwa unyonge, kumpatia jibu mtu aliyemtuma, maana hakua na njia nyingine ya kufanya.
“,Bosi! amelewa sana, nasikia sauti za walevi ndani ya chumba, nimeita sana hakuna aliyenijali …”,gaidi D47 namba arobaini na mbili aliongea, Paresh Kumar akakasirika, ujumbe alioupokea ulikuwa kinyume na matarajio yake.
“,Ina maana mpaka sasa bado yuko chumbani na wanawake zake? “,bilionea wa kihindi, mmiliki wa kundi la kigaidi la D47 ,Paresh Kumar ,aliuliza swali kwa mshangao.
“,Ndio bosi! “,gaidi yule aliitikia kinyonge, kwa heshima iliyojaa uoga mwingi ndani yake.
Paresh Kumar alinyenyuka ofisini kwake,akatembea kwa haraka,kuelekea katika chumba cha kijana wake machachali, aliyemtegemea kwa kila jambo, mzee wa miaka sitini bwana Donald Mbeto.
“,Paaaaa! “,alipiga kitasa na bastola kikaachia, akaingia ndani, uso kwa uso na wanawake sita wakivunja amri ya sita na kizee wa miaka sitini, mwenye damu mbichi kama kijana wa miaka ishirini tu, bilionea Paresh Kumar hakushtuka,hakuona cha ajabu chochote kile.
“,boosi, ninini tatizo, mbonaaaa umekujaa mbioo?,”Donald Mbeto akiwa uchi wa mnyama, alijitoa mikononi mwa wanawake wale wa kizungu, akasogelea mavazi yake, akaanza kuvaa nguo moja baada ya nyingine, huku akimuuliza maswali bosi wake.
“,Kengele ya hatari imepigwa, haujasikia! nimetuma watu kukuita haujasikia!, kuna tatizo kubwa, tena kubwa kabisaa! “,Paresh Kumar aliongea, mikono yake ikizungusha bastola yake kwenye kidole chake cha kati, mkono wa kulia.
“,Tatizo gani hilo bosi?, na nyie malaya, ondokeni hapa, mnasubili nini? “,pombe zilimuishia Donald Mbeto,akauliza swali kwa mshangao, sura yake akaikunja kwa hasira, akawafukuza wanawake aliokuwa anakula nao raha, kwani walikuwa bado wanasubili kuendelea na starehe zao.
“,Kuna ndege ya kivita inakuja kwenye ukanda wetu baharini,bila shaka imekuja kwa ubaya. “,Paresh Kumar aliongea.
“,Unasemaje bosi? “,Donald Mbeto aliongea kwa mshangao.
“,Ndiyo, twende ukaone …!”,Paresh Kumar aliongea, akaweka bastola yake kwenye koti lake,akaongozana na bosi wake, mpaka chumba cha mawasiliano na teknolojia katika kundi la D47.
“,Banard! “,
“,Yes bosi! “,
“,Vipi,bado ndege hiyo inakuja eneo tulilopo…”,
” „Ndio bosi,kama unavyo ona,”
“,Hawa ni watu wabaya kwetu,Donald nazani umeona ndege hiyo ?”,
“,Ndio bosi,waambie makepteni wazamishe meli kwenda chini kama nyambizi,tusionekane kwenye uso wa bahari,wakifika kwenye anga zetu tuwashambulie kwa makombola…”,
“,Kweli kabisa Donald,hiyo ndiyo mipango yangu,tayali meli yetu imezama kama nyambizi,nenda kashirikiane na askari wa makombola,wapatia maelekezo,ndege ikifika usawa wa bahari yetu tulipue ndege yao,”
“,Sawa bosi!”,
Donald Mbeto aliitikia amri ya bosi wake,akatoka chumba cha mawasiliano,akamuacha Benard akiendelea na majukumu yake,kufuatilia mitambo ya ulinzi katika meli yao yenye uwezo wa kujigeuza kama ndege au nyambizi.
“,Unazani watatumia dakika ngapi hawa washenzi mpaka kufika hapa?”,Paresh Kumar alimuuliza Benard,mkuu wa kitengo cha mawasiliano katika kundi la D47.
“,Dakika kumi zijazo,watakua katika anga letu…”,Benard aliongea.
Kamanda Philipo alichukua kompyuta yake, akabonyeza kitufe,akafanya utundu wake, alibonyeza huku na kule, akapata alichokihitaji.
“,Tumefika, meli yao inatakiwa iwe mahali hapa, lakini mbona hatuioni ,iko wapi? “,kamanda Philipo aliongea kwa mshangao, wote wakashangaa.
“,Ina maana tumefika! “,kamanda Catherine aliuliza kwa mshangao.
“,Ndio Cathe, tumefika, meli inaonekana iko hapa lakini hatuioni, nikisachi mtandao uneonesha hiyo meli ya Paraquat iko hapa ……!”,kamanda Philipo alitoa maelezo.
“,Nimekumbuka kitu, kepteni! Kepteni! ondoa ndege yetu mahali hapa, meli yao inauwezo wa kujigeuza kama nyambizi, kama wametuona bila shakaa wametutega watushambulie ……”,kamanda Kendrick aliongea.
“,Unasemaje?? “,wote waliuliza kwa mshangao, wote wakamgeukia kamanda Kendrick, walitaka afafanue vizuri kile alichozungumza.
“,Puuuuuuu, puuuuu …”,
“,Tumeshambuliwa, luka baharini …!”,
“,Puuuuuuh puuuuuh!
“,Nakufaaa…a……”,..
Ghafla mripuko ulisikika,kabla hata kamanda Kendrick hajamaliza kuongea,helikopta ya the super three soldiers ilipasuka vipande vipande,kelele za kilio zilisikika ,kila mmoja aliipigania roho yake.
…………………………………
Makao makuu ya polisi; 4;02pm
BMW ilipaki pembeni ya barabara, gaidi D47 namba sitini alishuka, akavuka barabara,akazisogelea ofisi za kituo cha polisi.
“,Tukusaidie nini kijana! “,askari wa zamu mapokezi aliuliza.
“,Nataka kuonana na polisi aliyekuwa zamu jana, kuna kesi niliandikisha kwake jana? “,gaidi D47 namba sitini aliongea..
“,Yule mshenzi, msaliti wa serikali yetu, yuko mahabusu, hawezi kushirikiana na wauaji, niambie kesi hiyo inaitwaje, niangalie faili lake kabatini …”,askari wa zamu aliongea. Hakujibiwa,tayali alipata alichohitaji, gaidi alitoka nje haraka sana, aliona ulinzi ulikuwa dhaifu, akawajulisha wenzake.
“,Twendeni,shambulia washenzi wote, asipone hata mbwa mmoja, mwenzetu yuko mahabusu, anapaswa kuuawa, kasema siri zetu …”,D47 namba sitini aliongea kwa hasira, akachukua bunduki, akavaa mkanda wa risasi begani, wenzake wakafanya vivyo hivyo, kila mmoja alichukua bunduki yake pamoja na mkanda begani, wakavuka barabara bila kuogopa kitu chochote kile, wakatembea kikomando kusogelea kituo cha polisi. Makao makuu ya polisi:
Shambulio la kushtukiza lilipelekea askari wengi kupoteza maisha,magaidi wanne wa D47 walikuwa moto wa kuotea mbali, walifyatua risasi kama mashine, wakaua askari wote waliowasogelea kizembe,hawakuogopa chochote kile, walijiamini na kuendelea kushambulia huku wakiingia ndani kabisa ya kituo cha polisi.
“,Mmoja aingie mahabusu, akamilishe kazi kisha tutoweke eneo hili,sisi tuko hapa nje tunadumisha ulinzi”,sauti ilisikika, gaidi D47 namba sitini alitoa amri,magaidi wawili wakaelekea mahabusu, huku wakisafisha njia kwa kuwafyekelea mbali askari ambao walikutana nao.
“,Paaaaa, paaaaa! “,risasi mbili zilisikika, walimfyatulia risasi askari aliyekuwa gaidi mwenzao na kutoa siri zao, wakamuua, kisha wakarudi haraka sana.
“,Tuondoke! tuondokee! “,
“,Tubadirishe nguo, tuvae nguo zao, tutatoroka kwa urahisi, “
“,Vipi kuhusu gari letu? “,
“,Haina haja, tutaliacha palepale, tuchukue moja kati ya magari yao, itakua rahisi hata kupita barabarani ……”,
“,Sawa mkuu …”,
Magaidi wa D47 walijadiriana, wakakubaliana, wakawavua askari watano waliowaua, wakavaa sare zao za polisi, wakatoka nje haraka sana, wakajipakia katika difenda ya polisi yenye king’ora juu, wakatoweka eneo hilo, wakiwa wameua askari takribani ishirini, askari wengine haijulikani walikuwa wapi.
…………………………………
Nusu saa iliyopita;
Donald Mbeto aliwaongoza magaidi wenzake, kitengo cha makombola,wote walikuwa makini kuitazama helikopta ya jeshi, helikopta ambayo ilitokea kisiwani Gano, ikafika katika ukanda wao,ikaonekana vizuri kupitia kompyuta na sattelite zao.
“,Ni watanzania, washambulieni haraka sana, hawa ni watu hatari sana kwetu …!”,Donald Mbeto alitoa amri,magaidi wenzake wakabonyeza vitufe vya makombola, makombola mawili yakafyatuka baharini, moja likaipiga helikopta kwenye mkia, ikapepesuka na kupoteza mwelekeo, kombola la pili likaipiga kwenye kichwa na kuisambaratisha vipande vipande.
“,Yeeeeeee!,wamekwishaa “,
Magaidi wote walipiga kelele za shangwe, wakiongozwa na Donald Mbeto,aliyejiita jini mweupe kutokana na mnvi nyingi zilizomtapakaa kidevuni na kichwani,siku zote alitekeleza matukio hatari sana ya mauji, na kijifananisha kama jini asiye onekana, alijiamini na kujikubali kuliko kiumbe yoyote yule.
“,Hapa kazi imekwisha, ngoja nikale zangu kuku bwanaaa wewe, wametukatishia starehe zetu hawa maboya, wakamsalimie shetani kuzimu ……”,Donald Mbeto alitukana,akaondoka zake, uso wake ulijaa tabasamu licha ya sura yake yenye mikunjo kwa mbali,kutokana na kula chumvi nyingi sana.
…………………………………
Kamanda Kendrick alitoa amri,vijana wake wajitupe kwenye maji, helikopta yao ililipuliwa kwenye mkia, ikaanza kuzunguka zunguka, rubani akashindwa kuiongoza, ikalipuliwa tena, kichwa kikasambaratika, wote watatu wakaruka, isipokuwa rubani aliyepasuka na kuchanika vipande vipande, akalia kwa uchungu na kufa palepale.
Kila mmoja alijitupa kwenye maji na kuangukia upande wake, walikua wamepoteana,hawakuangukia sehemu moja.
“,Kendrick! Kendrick! Philipo mko wapi? “,Catherine aliita,mikono yake akiitupa nyuma na mbele kuogelea, uso wake ulijaa huzuni, macho yake yakadondosha chozi, kelele alizozisikia kipindi ndege inalipuliwa zilimchanganya, hakujua nani amekufa, hakujua kama wenzake walifanikiwa kuluka, kila mmoja alijitupa kwenye maji bila kutambua kama mwenzake aliluka na kujiokoa.
“,Kendrick don’t die please, usife kabla sijakuambia ukweli wa moyo wangu! “,Catherine aliendelea kuogelea kama samaki, huku akiongea maneno ya huzuni moyoni mwake, alizani kamanda Kendrick pamoja na kamanda Philipo walikuwa wamepoteza maisha, kumbe sivyo.
…………………………………
Kisiwa cha Comoro; 4;20pm
Mtumbwi ulisogea mpaka ufukweni, mvuvi mwenye umri wa miaka hamsini alishangazwa na binadamu aliyemuokota baharini, akiwa amepoteza fahamu, akamkandamiza tumboni,akatapika takribani lita tatu za maji, akaendelea kumkandamiza tumboni, akatapika maji, macho yake yalifumba, pumzi yake ilikua kwa mbali sana, akamnyenyua mpaka kwenye kibanda chake cha makuti, kilomita moja kutoka baharini, samaki aliziacha palepale. “,Babaa! huyu ni nani?, halafu mbona ana sura ya kitanzania, au ni mwenzetu? “,binti mrembo, mweupe, mwenye macho meupe ya duara, aliongea, akimshanga mwanaume aliyevutia, akiwa amevaa mavazi ya ajabu sana, usoni akiwa na miwani, mkononi alivaa saa ya dhahabu.
“,Nimemuokota akiwa anahangaika kuogelea, nilipofika tu mahali alipokuwa, aliishiwa nguvu na kupoteza fahamu, nikamchukua na mtumbwi wangu mpaka mahali hapa! kabla ya yote, kachukue samaki ,nimeziacha kwenye mtumbwi, halafu njoo nazo, tuchemshe mgeni ale atakapopata fahamu …”,mzee yule aliongea, akamlaza kamanda Kendrick kwenye magome ya miti, apigwe na upepo, chini ya mti. Akimsubili aweze kuamka, awasimulie yaliyomkuta.
…………………………………
Kisiwa cha Mafia;
Boti ya Mv Mafia ikiwa na abiria hamsini, ilitia nanga katika bandari ya mjini Mafia, abiria walijaa taharuki, mabaharia nao walijaa taharuki,mavazi aliyoyavaa mtu waliyemuokota katikati ya bahari akinywa maji na kuhangaika kujiokoa yalizidi kuwachanganya,abiria walishuka kwenye meli, walikuwa wamefika mwisho wa safari, akabaki nahodha na mabaharia wakimpatia huduma ya kwanza kamanda Philipo,alitema maji mengi takribani lita tano.
“,Watokea wapi yahee,watoka Unguja au Pemba,wewe raia wa wapi?”,kamanda Philipo aliyafumbua macho yake,uso kwa uso na watu wanne wenye sare nyeupe zilizofanana,begani zilifanana na sare za polisi.
“,Nyie polisi wa wapi?”,kamanda Philipo aliuliza.
“,Hahaaaa,kachanganyikiwa huyu,lakini atakua mtanzania wa bara,anaongea kiswahili…!”,walicheka sana,kamanda Philipo alishindwa kujibu alichoulizwa,wakamuona kama amepagawa,wakaendelea kumpatia huduma ya kwanza ili akili yake irudi katika hali yake ya kawaida.
…………………………………
“,Hapo hapo ulipo we malaya,ukijitikisa tunakumaliza……!”,kamanda Catherine aliangukia mikononi mwa magaidi takribani ishirini wa kisomali, walimzunguka na spidi boti, huku wakimtaka ajisalimishe.
“,Nyie ni wakina nani? “,kamanda Catherine aliuliza, mikono yake ikiwa imekamatwa na magaidi kwa nguvu, wakamtupia ndani,katika boti zao.
“,Alshabaab! huuu ni ukanda wetu wa Afrika mashariki, yoyote anayekatiza eneo hili ni mali yetu …!”,gaidi moja lenye rasta ndefu zilizosokotana liliongea, Catherine akashtuka, akaanza kuwaangaza kwa umakini, akitafuta mbinu ya kujiokoa. “,Mkamateni, mfungeni pingu, tuondokee naye! “,gaidi yule alitoa amri, magaidi wawili wakamsogelea kamanda Catherine, hapo ndipo walikipata cha mtema kuni, wakajuta kumsogelea, aliluka mateke mawili hewani, yakawapiga usoni magaidi wale, wakadondokea ndani ya maji, akachomoa bomu dogo,akachomoa pini akalitupa ndani ya boti,akajitupa ndani ya maji kama samaki.
“,Puuuuuu! puuuuu! “,mlipuko ulisikika, boti moja ya magaidi ikalipuka,kiongozi wao aliunguzwa na mlipuko, akafa palepale pamoja na vijana wake wawili, magaidi wengine wakashindwa kuendelea kumtafuta Catherine, wakasogeza boti zao karibu, wakiwa hawaamini kilichotokea, bosi wao alikuwa amekufa palepale, machozi yakawatoka kwa uchungu,shambulio la sekunde moja tu kutoka kwa Catherine liliwachanganya sana na kuharibu kila kitu katika kundi lao.
Kendrick aliyafumbua macho yake,akapapasa mikono yake huku na kule, akashika magome ya miti, akashtuka, akanyenyuka na kuketi, uso kwa uso na mzee mwenye umri sawa na marehemu baba yake, alipoyageuza macho yake upande wa pili, pembeni na mzee yule, alikutanisha macho yake na msichana mweupe,akiwa amevalia magome ya miti yaliyozuia sehemu zake za siri pamoja na matiti yake, macho yake yakashindwa kuvumilia,kope zake zikayaachia uhuru macho yake, yakatazama uzuri wa msichana huyu juu mpaka chini, akatabasamu, akamshukuru Mungu kwa uumbaji wake wa ajabu.
“,Hapa ni wapi?,nyie ni akina nani? “,Kendrick aliuliza, akasimama, akaangaza huku na kule, aliona nyumba moja ya makuti iliyozungukwa na minazi mingi.
“,Huu ni ufukwe wa kisiwa cha Komoro! “,mzee yule alimjibu Kendrick, akazidi kumpatia maswali mengi kichwani mwake yasiyokuwa na majibu.
“,Nimefikaje hapa? “,Kendrick aliuliza tena.
“,Nilikuokota baharini ukiogelea katikati ya bahari,nilikua navua samaki, nikasogeza mtumbwi wangu karibu nawe, ulikuwa umeishiwa nguvu, ukapoteza fahamu, kabla hujazama nilikuokoa na kukuweka katika mtumbwi wangu, nikakuleta mpaka hapa, naitwa mzee Fedinand, huyu ni binti yangu, anaitwa Upendo ………”,mzee yule alimaliza kumwelezea Kendrick, akajitambulisha, akamtambulisha na binti yake wa kike, wote wakatabasamu, walifurahi sana kukutana na mswahili mwenzao kwa takribani miaka kumi sasa, wakiishi peke yao ufukweni, wakivua samaki, kula matunda na kuwinda wanyama.
“,Kabla sijajitambulisha,kwanini mko hapa, makazi haya yanaonekana yako mbali na binadamu, hamuogopi kuishi peke yenu?, hamuogopi maharamia, vipi kuhusu wanyama wakali, hamuwaogopi? “,Kendrick aliongea kwa mshangao, macho yake yakiangaza umbali wa mita kadhaa mbele yake, akaona bahari, kushoto aliona msitu mkubwa wa minazi, akageuza shingo yake mkono wa kulia, aliona minazi mingi sana, nyuma yake vivyo hivyo, kulikuwa na msitu mkubwa wa minazi, akapigwa na butwaa!
“,Huyu ni binti yangu, ana miaka ishirini na mbili kwa sasa, akiwa na miaka kumi na mbili, tulisafiri naye kwenda Zanzibar kwa mapumziko mafupi, tukapata ajari na Mv Spice,tulifanikiwa kuwahi maboya mimi na mwanangu, nikaogelea naye, nikiwa nimemshika ipasavyo mpaka tukafika hapa, tumeishi naye mpaka leo hii, sijawahi kuona binadamu yoyote, leo ndio nimekuona wewe eneo hili ……”,mzee yule alitoa maelezo marefu, kamanda Kendrick akamuangalia machoni, macho ya mzee yule yalisema ukweli, hayakudanganya chochote kile, Kendrick akamuamini mzee yule.
“,Naitwa kamanda Kendrick, askari mkuu wa kikundi cha upelelezi cha the super three soldiers kutoka Tanzania, tukiwa katika majukumu yetu, ndege yetu ililipuliwa na maharamia, mpaka sasa sijui wenzangu wako hai au wamekufa! “,kamanda Kendrick alijitambulisha,mzee Fedinand na binti yake wakatazamana, kisha wakamtazama tena Kendrick.
“,Mzee, haukuona mtu yoyote eneo hilo la bahari tofauti na mimi? “,Kendrick aliuliza tena.
“,Hapana, sikuona chochote kile! “,mzee yule aliongea, binti yake akanyenyuka, akaenda ndani ya kibanda cha makuti, akarejea tena, mkononi alishika samaki waliochomwa,wakiwa wamefungwa vizuri kwenye majani ya miti, akasogea karibu na Kendrick, akapiga magoti kwa heshima, akamnawisha, akampatia samaki, akaanza kula.
“,Sasa itakuaje?, natamani sana mwanangu kurudi Tanzania, nazani nyumbani mke wangu na watoto wanne wanazani tumeshapoteza maisha, isitoshe kwa sasa wamekua, natamani sana kuwaona! “,mzee yule aliongea kwa hisia kali, akadondosha chozi, binti yake na yeye uvumilivu ulimshinda,akamfuta machozi baba yake, huku na yeye chozi likimtiririka.
“,Msijali ondoeni shaka, mko mikono salama, mshukuruni Mungu kuwalinda kwa miaka kumi,kama mko salama mpaka leo hii, basi hamtapatwa na kitu chochote kile katika mikono yangu ……”,Kendrick aliongea, akitafuna samaki wazima wazima, njaa aliyokuwa nayo haikuwa ya kawaida, akamaliza kutafuna samaki watano, akatosheka, akanawa, akaifutafuta saa yake, akaiwasha, ilikua imezima baada ya kuingiliwa na maji, ikawaka kwa mara nyingine tena, akatabasamu, ghafla tabasamu lake likatoweka, saa yake iliwaka taa mbili tu za kijani badala ya tatu,akajiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu, mmoja kati yao hakuwa salama.
…………………………………
Kisiwa cha Mafia :
Kamanda Philipo alikasirika, kicheko cha kejeli kutoka kwa watu waliomsaidia ndicho kilichomkasilisha,akajitoa mikononi mwao kwa nguvu, akasimama.
“,Asanteni kwa msaada wenu, niacheni niondokee! “,kamanda Philipo aliongea, akaondoka zake, nahodha na mabaharia waliokuwa wanamuhudumia wakabaki midomo wazi,wakaachana naye,wakaendelea na shughuli zao, huku wakijiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu.
“,Mimi niliwambia, ameshakua kichaa, kupona kifo baharini lazima uwe na kiwewe, ona sasa, yuko kama mwendawazimu! “,mmoja kati ya mabaharia wa mv Mafia aliongea, wote wakiwa makini kumsikiliza.
“,Kweli kabisa, lakini asikuumize kichwa, achana naye, cha muhimu tumeshampatia msaada! “,baharia mwingine alizungumza, akatoa mawazo yake, wote wakaelekea kwenye majukumu yao.
“,Mungu wangu wee! wote saa zao hazifanyi kazi,taa hata moja ya kwao haiwaki, yes! imewaka, yes nyingine labda itawaka bado moja! “,Philipo aliongea kama kichaa, akiwa bize kuitazama saa yake mara tu baada ya kuiwasha, akaandika ujumbe kwa kupitia saa, akaituma, ili ajue wenzake wako mahali gani.
“,Anyone online! Comrade Philipo, available in Mafia ……”,(Yoyote yule aliyeko hewani!, kamanda Philipo napatikana Mafia …”,)
Alituma ujumbe kupitia saa yake, saa iliyounganishwa na saa za wenzake, akasimama kusubili majibu,wapita njia wakimshangaa kwa mavazi yake, mavazi ambayo yalikuwa maalumu kwa ajili ya kutekeleza misheni ambayo haikufanikiwa, misheni ya kuivamia meli ya D47.
…………………………………
“,Help me! Help me! nisaidieniii, nisaidieenii! “,kamanda Catherine alipiga kelele kuomba msaada, mikono yake ilichoka kuogelea, muda wowote angeweza kuzama,boti kubwa ikaanza kumsogelea, “Bakhresa “, ilisomeka, akaitambua, ilikua boti ya abiria kutoka Dar es salaam kwenda Zanzibar, mabaharia wawili wakajitupa ndani ya maji, wakampatia msaada, akaponea chupuchupu kufa maji.
“,kulikoni kamanda, imekuaje? “,mabaharia wale walimuuliza swali Catherine, walimtambua, alikua maarufu sana jijini Dar es salaam yeye pamoja na kundi lake.
“,Ndege yetu ilipata hitilafu, ikaanguka baharini, asanteni kwa msaada wenu! “,Catherine aliongea, akashukuru, akaiwasha saa yake, ajue kama wenzake wako hai au wamekufa, akatoa tabasamu zuri sana, saa iliwaka taa tatu za kijani,makamanda wote walikuwa wazima.
“,Wenzako wako wapi, tuambie mlipoangukia tukawatafute, nyie ndio mnailinda nchi yetu, bila nyie sisi sio kitu! “,mabaharia wawili waliongea, huku abiria wakitikisa vichwa, walikubaliana na wazo hili, wakasubili majibu kutoka kwa Catherine.
“,Msiwe na hofu, wote tayali ni wazima, asanteni kwa upendo wenu …”,Catherine aliongea,wakakubaliana naye, boti ikaendelea na safari ya kuelekea Dar es salaam Tanzania.
“,Anyone online! Philipo available in Mafia …”,(Yoyote yule aliyeko hewani!, Philipo anapatikana Mafia …),meseji iliingia kwenye saa maalumu ya Catherine, akaisoma, akaandika ujumbe kujibu ujumbe ulioingia katika saa yake.
“,Anyone online! Catherine is on the way to Dar es salaam, via mv Bakhresa …”,(Yoyote yule aliyeko hewani, Catherine yuko njiani anaelekea Dar es salaam Tanzania, kwa kutumia mv Bakhresa) “,alimaliza kuandika ujumbe mfupi, akatuma.
………………………………
Kisiwa cha Comoro :
Mzee Fedinand aliongoza njia, binti yake Upendo akafuatia, wakaongoza njia, kumtembeza Kendrick katika maeneo mbalimbali ya kisiwa hiki. Kendrick aliwaza mbali sana, alikua na hasira ya misheni kuharibika, isitoshe mwenzao mmoja saa yake ya mawasiliano haikuwa hewani.
Ghafla ujumbe ukaingia, alikuwa ni Philipo, akausoma, Philipo alikuwa katika kisiwa cha Mafia, hofu ikazidi kumtanda, mtu aliyempenda, Catherine hakuwa hewani,ghafla taa nyingine ya saa yake ikawaka, taa zikawa tatu, wote walikua hai, ujumbe mwingine ukaingia katika saa yake, akaufungua, akausoma, Catherine alikua njiani anaelekea Tanzania, akafikiria, akajua nini cha kufanya, akaandika ujumbe.
“,Kendrick is online, aim available in Comoro islands, Catherine just go to take helikopter, then come back to pick us ……”,(Kendrick yuko hewani, napatikana katika visiwa vya Komoro, Catherine nenda kachukue helikopta, kisha uje kutuchukua …”,)Kendrick alimaliza kuandika ujumbe, akautuma, moyo wake ukawa na amani.
“,Hapa ndipo tunachukua minazi kwa ajili ya kutumia nyumbani. “,mzee Fedinand aliongea.
“,Unasema? “,Kendrick hakuelewa, mawazo yake yalikua mbali, akauliza tena.
“,Inaonekana hauko sawa, kuna tatizo lolote? “,mzee Fedinand aliuliza swali kwa Kendrick.
“,Nilikua nashughulikia usafiri, muda wowote helikopta itakuja kutuchukua, kwa sasa niko ok kabisaa “,Kendrick aliongea, tabasamu zikaipamba sura ya mzee Fedinand pamoja na binti yake, wakamkumbatia Kendrick kwa furaha, hawakuamini kama muda mfupi ujao wangerejea tena Dar es salaam, baada ya kuishi miaka kumi katika kisiwa cha Komoro, Upendo akiwa binti mdogo, mpaka akawa mtu mzima.
Makao makuu ya polisi :
Catherine alichanganyikiwa, kituo cha polisi kitengo cha upelelezi kilikuwa kimevurugika, maiti nyingi zilitapakaa kila kona,watu wa huduma ya kwanza wakitimiza wajibu wao kubeba maiti na kuzipelekea mochwali, Catherine nguvu zilimuishia, akadondoka chini, akapiga magoti, alikuwa anatazama moja ya maiti iliypopigwa risasi nyingi sana tumboni, machozi yakamchuruzika kama maji bombani.
“,D47 inatoshaa! nasema inatoshaa! mwisho wenu umekalibia,mmetuzidi ujanja lakini hamtatuzidi ujanja milele ……!Catherine alizungumza kwa uchungu, akaguswa begani, akageuka.
“,Imekuaje! mlikuwa wapi mpaka tunaaibika kiasi hiki, shambulio hili limetuaibisha, lakini nimeshajua wakina nani wamefanya hivi…!”,kamanda Catherine alifoka kwa hasira, jasho jembamba likimtoka, mikono yake ilitetemeka, waziri wa ulinzi akaogopa,alizitambua hasira za Catherine.
“,Askari wote leo wako bize na ulinzi,raisi ameingia bara, ana ziara huko kila mkoa,ndio maana ilikua rahisi kutekeleza shambulio hili,magaidi wameondoka na gari letu pamoja na sare za vijana wetu! “,waziri wa ulinzi aliongea,akajikuna kichwani, akaweka miwani yake vizuri, kisha akajiandaa kuzungumza kitu.
“,wenzako wako wapi?, imekuaje ?,ndege yenu ilipotea kwenye rada zetu, tumeitafuta bila mafanikio, nikataka kutuma vijana waje kuwatafuta, ghafla nikapewa taarifa umerejea, nilikua njiani nakuja hapa, ghafla ndio tumekutana, hebu nieleze!! “,waziri wa ulinzi aliongea.
“,Tulishambuliwa na magaidi, wengine nimewaponyoka,kundi limesambaratika, kila mtu yuko eneo lake, Philipo yuko Mafia, Kendrick yuko Komoro ,naomba muheshimiwa fanya jambo kwa ajili yao, tuma helikopta ikawachukue, ulinzi haujakaa vizuri kwa sasa ……” Catherine alitoa maelezo mafupi, akijifuta machozi kwa kutumia kitambaa chake.
“,ok nafanya hivyo,helikopta itaenda kuwachukua nusu. saa kuanzia sasa, kabla jua halijazama, unachotakiwa kufanya, chunguza undani wa tukio hili, kisha nitumie taarifa ofisini kwangu …”,waziri wa ulinzi alizungumza, Catherine akatikisa kichwa, akapiga saluti,waziri akapanda kwenye gari lake, akaondoka zake,waandishi wa habari wakijitahidi kufanya mahojiano naye bila mafanikio, alikataa kuzungumzia chochote kile kuhusu tukio hili la kuvamiwa kwa kituo cha polisi kitengo cha upelelezi.
…………………………………
Helikopta ndogo yenye uwezo wa kubeba abiria sita, iliacha ardhi ya jeshi la anga,Dar es salaam,Tanzania, rubani wa helikopta alitimiza majukumu aliyoelekezwa,alipaswa kuwachukua makamanda wawili wa kitengo cha upelelezi, mmoja akiwa katika kisiwa cha Mafia, mwingine akiwa kisiwa cha Komoro.
“,Usawa wa kisiwa, usawa wa kisiwa,unanipataa ovaaa! “,rubani wa helikopta alizungumza kupitia simu yake kubwa ya mkonga. “,Halooo, halooo! ,oooh shiit! watakua hawana mawasiliano ya simu, hawapatikani hewani,”,aliendelea kuzungumza, akabonyeza tena simu yake ya mkonga, akaiunganisha na saa za kijeshi, saa za upelelezi.
“,Haloo, halooo, niko Mafia, mko wapi ovaaa? “,aliuliza, akasubili jibu. Akiwa katika anga, usawa wa kisiwa cha Mafia.
“,Niko Mafia, sogea bandarini, utaniona …”,sauti ilisikika upande wa pili.
“,Nashuka sasa hivi,hakuna kupoteza hata sekunde, nimepewa nusu saa tu ya kuwachukua! “,rubani wa helikopta aliongea, akakata mawasiliano, akaiweka simu yake kwenye mifuko ya suti yake ya kijeshi. Baada ya dakika tano tu, alianza kuishusha ndege bandarini, ikatua juu ya meli moja, kamanda Philipo akaiona, akasogea karibu na meli hiyo, akaingia, moja kwa moja mpaka usawa wa helikopta, akapanda na kutokomea, wavuvi, mabaharia na abiria waliokuwa eneo hili la bandari wakabaki midomo wazi, wakijiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu.
“,tunaelekea Komoro, kumchukua Kendrick, kisha tutarudi tena Dar es salaam Tanzania …”,rubani yule aliongea, helikopta ikipaa juu futi sitini, ikakunja kona na kuelekea upande wa kusini,bahari ya hindi.
…………………………………
6;02pm
Kamanda Kendrick alisubili helikopta kwa hamu sana, alikuwa na shauku kubwa ya kutaka kufika Dar es salaam,taarifa za kituo chao cha polisi kushambuliwa, askari wakauawa kinyama zilimshtua na kumsikitisha sana.
“,Mbona hauna raha, nini tatizo Kendrick?, japo ni masaa kumi tu tumeweza kukutana, lakini nimetokea kukuzoea, unaonekana kijana mwenye huruma na hekima, sipendi uwe na majonzi ……”,mtoto wa mzee Fedinand aliongea, akamsogelea Kendrick, akakaa pembeni yake.
“,Kuna taarifa mbaya kutoka serikalini, lakini usjali ni majukumu tu ya kikazi ……”,Kendrick aliongea, hakutaka kueleza kile ambacho kilikua kinamsumbua, akaficha,hakupaswa kumwamini mtu yoyote katika shughuli za kiserikali na kuziweka wazi.
“,Papapapapapapapa! …”,muungurumo wa helikopta ulisikika, helikopta ndogo yenye rangi za kijeshi ilipita mita kadhaa usawa wa eneo lao, Kendrick akatazama juu, akaitambua ndege hii, ilikuwa helikopta ya Tanzania, akamshika mkono msichana wa mzee Fedinand.
“,Twendeni wamekuja kutuchukua,baba, babaa, njoo twendee! “,Kendrick aliita, mzee Fedinand akatoka nje ya kibanda, mwilini akiwa amevaa magome ya miti, kwa miaka kumi sasa walitumia magome ya miti kama mavazi, nguo walizopotea nazo miaka kumi iliyopita walizivaa mpaka zikaisha. Hawakupata zingine, wakaamua watumie magome ya miti kusitiri miili yao.
“,Hao ni wa kina nani,wanajua kiswahili?”,Philipo aliuliza.
“,Yes wanajua,salimiana nao,mambo mengine tutazungumza baadae!”,Kendrick aliongea,akamsogelea mzee ambaye alikuwa amesimama sambamba na binti yake.
“,Shikamoo mzee!”,Philipo alisalimia,akampatia mkono wa kulia,wakashikana kama salamu ya heshima.
“,Marhaba!”,mzee yule aliitikia.
“,Habari yako dada!”,alisalimia tena.
“,Salama,asanteni sana kuja kutu……”,kabla Upendo hajamalizia kuongea, sauti ilisikika,sauti iliyomshitua na kumfanya ageuke haraka.
“,Kamanda,tuondokeni!nilipewa nusu saa tu,nikichelewa nitaadhibiwa!”,rubani wa helikopta aliongea,Kendrick na Philipo wakamuelewa,walizitambua vizuri sana sheria za.kijeshi,wakajipakia ndani ya helikopta,helikopta ikapaa na kutokomea angani.
…………………………………
Bahari ya Hindi :6:30
Mkuu wa kikundi cha magaidi wa D47,bilionea Paresh Kumar, alipata taarifa kutoka Tanzania,zilizidi kumfurahisha, akawa na furaha zilizopitiliza, tofauti na siku zote.
“,Wale walikuwa askari wa Tanzania hatari wanaotutafuta kila siku, hasa Donald Mbeto ndiye muhusika mkuu,ndugu zetu kutoka Dar es salaam ndio wamenipatia taarifa hizi,wamemuua D47 namba mia moja, maana aligundulika kushirikiana na sisi, akapewa adhabu kama askari na kusema siri zetu zote, wameshambulia kituo cha polisi, wameua askari wote, ni shangwe na nderemo kwetu sisi, tunachopaswa kufanya ni kuwa makini, lazima watarudi kututafuta!! “,bilionea Paresh Kumar aliongea,mguu wake mmoja alikunja nne, kushoto aliketi mrembo wa kihindi, kulia aliketi mrembo wa kichina, wote walimpapasa na kumshika shika mwilini, alipenda sana wanawake, aliwateka kutoka pembe zote za dunia, akafuta kumbukumbu zao kichwani, wakamtumikia katika kundi lake katika shughuli mbalimbali.
“,Kwa kuwa wameshajua eneo tulilopo,meli yetu ipae angani kama ndege, usawa wa mawingu, watahangaika kututafuta mpaka wanazeeka! “,Paresh Kumar alitoa amri, vijana wake wakaluka juu kwa shangwe, burudani zikaendelea, mziki ukapigwa, kila mtu akaendelea na starehe yake aliyoipenda, kufurahia ushindi, meli yao ikajigeuza, bawa likachomoza upande wa kulia, bawa lingine likachomoza upande wa kushoto, ikaanza kupaa hewani, ikaiacha bahari, haikuwa meli ya paraquat tena, bali ndege kubwa yenye uwezo wa ajabu.Makombola ya nyukilia yakachomoza kila upande wa ndege hii, kwa ajili ya ulinzi.
Ofisi ya ukombozi: 7:00
Catherine alianza upelelezi,aweze kuwapata washirika wa D47 waliofanya shambulio,akiwa anatafakari, akapata jibu, akaondoka haraka sana, kutoka katika kituo cha polisi kilichoshambuliwa, mpaka katika ofisi yao ya ukombozi, ndani ya jengo la China plaza, Kariakoo.
“,This bastard kahusika! picha zake zisambazwe kila kona, tukimpata huyu, tutafahamu mengi ……”,Catherine aliongea, alimkumbuka raia wa kisomali waliyegongana vikumbo siku moja iliyopita,kijana aliyejaribu kufungua ofisi yao bila mafanikio na kuambulia kupigwa picha alipokosea neno siri la kufungulia mlango, Catherine akamkimbiza bila mafanikio, alitaka kumuhoji ajue nini alichotaka katika ofisi yao.
“,Work done, kazi imekwisha,ngoja nikapige picha na eneo la tukio,ni attach kwenye picha yake,kisha nitume kwa waziri,vyombo vya habari viripoti taarifa hii…”,Catherine aliongea,akiitazama sura ya gaidi aliyetaka kuingia ndani ya ofisi yao siku moja iliyopita,akiwa ndani ya suti nyeusi,akiwa ameyavua mavazi yake ya kazi,akatoka nje ya ofisi ya ukombozi,akatokomea.
…………………………………
7:10pm
Kendrick na Philipo walitaka kushushiwa katika eneo la tukio,mahali ambao kitengo chao cha cha upelelezi kilipatikana,kabla ya kushambuliwa,rubani wa helikopta akafanya hivyo,akashusha helikopta,ikatua ardhini na kuikanyaga ardhi ya Dar es salaam kwa mara nyingine tena,Kendrick akashuka,mkono wake wa kulia ulimshika Upendo,mtoto wa mzee Fedinand,Philipo akashuka,akiwa ameongozana na mzee Fedinand,uso kwa uso wakakutana na maiki nyingi za waandishi wa habari,wakitaka kuzungumza nao. “,Naripoti kutoka ITV the super brand Afrika mashariki,naitwa Abdalah Said Abdulah,wewe kama mkuu wa kitengo hiki,unaweza kutueleza chochote kuhusu shambulio hili……”,mwandishi wa habari aliuliza,mwilini alivaa suti nyeusi iliyofiti mwili wake ipasavyo.
“,Sijui chochote,ndiyo narejea baada ya helikopta yetu kupotea baharini,tukiwa katika majukumu yetu,lakini naahidi, tutawakamata watu hawa ndani masaa ishirini na nne yajayo!”,Kendrick aliongea,mwandishi wa habari akimtazama Upendo kuanzia chini hadi juu,alishangazwa sana na mavazi yake.
“,Huyu naye umemtoa wapi?, amevaa mavazi tofauti na asili ya mtanzania,”mwandishi aliendelea kuhoji.
“,Huyu anaitwa Upendo,baba yake anaitwa mzee Fedinad,walipotea na meli ya mv spice miaka kumi iliyopita,walifanikiwa kupona kifo cha maji,baada ya kuogelea mpaka pwani ya kisiwa cha Komoro, eneo lisilo na watu,wakaishi huko wakila matunda na samaki,wameniokoa mimi leo hii,pengine bila wao nisingekuwa hai,popote walipo ndugu zao,wafike nyumbani kwangu,mtoni kijichi,wakiulizia kamanda Kendrick,watafikishwa mpaka mlangoni…”,kamanda Kendrick alitoa maelezo,akamshika mkono Upendo,wakasogea kabisa eneo la tukio.
“,Sasa,unaweza,ukaa……”,mwandishi yule alitaka kuendelea kuhoji,Kendrick alichoka mahojiano,akaondoka zake,akafika eneo la tukio,akatazama kila kona,damu zilikuwa zimeganda na kutapakaa eneo lote.
“,Kendrick uko salama,na huyu ni nani?”,Catherine alifika,akauliza swali.
“,Nitakueleza kila kitu,endelea kuchukua taarifa za upelelezi wa mwanzo,sisi tunaelekea nyumbani na kamanda Philipo,baada ya upelelezi,mpatie waziri majibu taarifa za upelelezi kama sheria zinavyosema, kisha fika haraka nyumbani kwangu,tuzungumze suala hili.”Kendrick aliongea,akatoa maelezo mafupi,wakaongozana na Philipo,pamoja na mzee Fedinand,wakapanda gari ya polisi, wakatokomea.
…………………………………
Kendrick aliishi nyumba moja na mama yake mzazi,kaka zake wawili walipoteza maishi kwa mshituko, waliposikia taarifa za meli ya mv spice kuzama, meli ikiwa imembeba baba yao ambaye alikuwa ni tegemeo kubwa katika familia yao,mama yao alichanganyikiwa,akaugua ugonjwa wa akili kutokana na kupata pigo kubwa kwa wakati mmoja, mme wake na mtoto wake wa mwisho, walipoteza maisha kwa ajari ya meli, watoto wake wakafa kwa mshituko wa moyo,mara baada ya kupokea taarifa za kifo cha baba yao, pamoja na mdogo wao.
Kendrick akiwa kidato cha nne, aliamua kumpeleka mama yake hospitali kuu ya vichaa mkoani Dodoma, hospitali ya Mirembe. Akatibiwa, huku Kendrick akijiunga na jeshi la kujenga taifa, akamaliza mafunzo ya miezi sita, akajiunga na jeshi la polisi, kutokana na utendaji wake, akapandishwa cheo kila kukicha, huku mama yake akipona ugonjwa wake wa akili, akamrudisha nyumbani, wakaishi tena pamoja.Kendrick alifikili baba yake, pamoja na mdogo wake walikuwa wamepoteza maisha katika ajali ya mv spice,kumbe sivyo, Mungu aliwakutanisha tena pamoja.
“,Baba Josephat! “,mama yake Kendrick alipigwa na butwaa,hakuwahi kuisahau sura ya mume wake hata siku moja, aliitambua vizuri sana,alipigwa na butwaa baada ya Kendrick kurudi nyumbani na wageni,mmoja kati ya wageni akiwa ni mume wake wa ndoa.
“,Mamaaa Josephat, ni wewe?,nyumba yetu imebadilika! “,mzee Fedinand aliita kwa mshango, akamkimbilia mke wake, wakakumbatiana.
“,Mbona sielewiii, ina maana, wewe ndiye baba yangu ……?”,Kendrick aliuliza swali kwa mshangao, chozi la furaha likaanza kumtoka.
“,Ndiyo kendrick, huyu ndiye baba yako,sijui umemtoa wapi? “,mama yake Kendrick aliongea, machozi yakimtiririka.
“,Mama Josephat, huyu ndiye mtoto wetu wa mwisho Jacline, huyu ndiye nilisafiri naye kwenda Zanzibar,”mzee Fedinand aliongea.
“,Mamaaa! “,Upendo aliita.
“,Mwanangu! “,mama Kendrick aliitika.
“,Mamaaaa! “,Upendo akaita tena.
“,Jamani mwananguuu …”,mama Kendrick akaita tena, akamkimbilia mwanae, wakakumbatiana, kila mmoja akiona kama ndoto.
“,Kendrick mwanangu, najua unajiuliza maswali mengi, mimi sio Fedinand, naitwa Steward, siwezi kukwambia ukweli katika hali kama ambayo umetukata nayo kule, tulikuwa hatujui wewe ni mtu mwema au mbaya kwetu, ndiyo maana nilikuficha majina yetu halisi, na huyo siyo Upendo, bali ni mdogo wako Jacline, wahenga walisema usimtendee mema binadamu unayemfahamu peke yake, leo hii nimekuokoa baharini, kumbe namuokoa mtoto wangu, Mungu katumia njia ya ajabu kutukutanisha. “,mzee Fedinand alitoa maelezo marefu, kumbe jina lake sio Fedinand, alidanganya,jina lake halisi aliitwa Steward, Kendrick akamsogelea baba yake na kumkumbatia, furaha ikazaliwa upya katika familia ya kamanda Kendrick.
Kamanda Philipo alijifuta chozi ambalo lilikuwa linamdondoka, alishuhudia kila kitu,Catherine alikuwa amesimama mlangoni, alikuwa tayali ameshafika muda mrefu, akajikuta anasimama mlangoni kama sanamu, alishindwa kuendelea mbele, nguvu zilimuishia, historia ya kustaajabisha aliyoisikia ilimchanganya sana, hakuamini kama Kendrick alipitia mkasa wa kutisha kiasi hicho, hakuwahi kumweleza hata siku moja, alikua msiri sana.
“,Catherine! umefika, kumbe uko hapa, karibu ndani, nilitaka nikueleze kuhusu kukutana na watu hawa,tujue namna ya kuwasaidia kuwapata ndugu zao, lakini kumbe tayali wameshafika nyumbani! “,Kendrick aliongea kwa furaha, Catherine akatabasamu, akasogea sebureni, akakaa kwenye sofa.
“„Josephat na Yohana wako wapi? ,au wameshaoa, wako na familia zao? “,mzee Steward, baba yake Kendrick aliuliza, mama yake Kendrick akanyongonyea, tabasamu ikatoweka usoni mwake, vivyo hivyo kwa Kendrick, akapoteza furaha kabisa, akapiga moyo konde, akajikaza kiume na kuongea ukweli. “,Kwa sasa ni marehemu, tuliwazika siku moja tu baada ya kupokea taarifa za meli kuzama na abiria wote kupoteza maisha, walipatwa na mshituko, wakafa palepale, mama naye akachanganyikiwa, lakini namshukuru Mungu, mama alipatiwa matibabu, kwa sasa ni mzima ……”,Kendrick aliongea,baba yake akadondosha chozi, haikusaidia chochote kile,watoto wake walikuwa tayali wameshapoteza maisha, wasingerudi tena.
“,Wapumzikee kwa amani wanangu! “,mzee Steward alizungumza, mke wake akamkumbatia, akambembeleza, akajikaza kiume, akajaribu kuificha huzuni yake lakini hakuweza, machozi yake yaliendelea kutoka, alihuzunika sana kuwapoteza watoto wake.
Mbezi :8:02
Magaidi wa D47,kanda ya Dar es salaam, walikuwa wameketi katika nyumba yao ya kifahari,chupa za bia zilikua mezani, walikunywa mpaka wakatapika,walikamilisha kazi kama walivyopanga, bosi wao akafurahishwa zaidi na kitendo hicho, akamuingizia kila mtu dola elfu moja kwenye akaunti yake. Akawapatia kazi nyingine kubwa, kuhakikisha wanawaua maaskari watatu wanaolifuatilia kundi lao.
“,Kesho asubuhi na mapema tunaanza kazi, hawa watu lazima tuwauee, tusipo waua sisi, watatuua! “,D47 namba sitini alizungumza, wenzake watatu wakiwa. pembeni yake,kila mmoja alikuwa ameshika chupa ya bia mkononi.
“,Kweli kabisa,mimi nina plani,nina mipango ambayo itaifanya kazi hii kuwa rahisi kabisa……”,gaidi mwembamba,mrefu,mweupe,alizungumza,akawatazama wenzake usoni.Wote wakaweka bia zao,wakatulia kusikiliza mbinu hiyo,walikuwa na shauku ya kupata pesa nyingi kama wakifanikiwa kuwaua wapelelezi watatu hatari wa kundi la the super three soldiers.
“,Mbinu gani hiyo chuma cha puaa?”,gaidi mwingine aliuliza,mweusi,mfupi,kichwani alikua na kipara.
“,Tuteke familia zao,hasa ya kiongozi wao wa kundi,lazima watajileta wenyewe,wote watatu,kutaka kuwakomboa,sisi tutaacha eneo hili likiwa limetegwa mabomu,wakifika eneo hili kukomboa ndugu zao,tunalilipua,wanakufa woteeee!”,gaidi yule aliyejulikana kwa jina la chuma cha pua aliongea,licha ya wembamba pamoja na urefu wake,alikuwa amekomaa kama chuma,ngumi yake ilikuwa na uwezo wa kupasua matofauli kumi ya bloko,aliwahi kumuua gaidi mwenzake,allimpiga na kichwa chake,akampasua fuvu la kichwa,wote wakiwa mazoezini,wakamubatiza jina hilo,mwili wake ulikomaa kwelikweli.
” ,Yeeeeeeh!,”waligonga chupa zao kwa furaha,walikubaliana na plani ya mwenzao,kilichobakia ni utekelezaji,wakanywa bia kwa fujo, wakalewa chakali,usingizi ukawachukua,wakalaliana kama mizigo,wakiwa hawajitambui.
…………………………………
Ofisi ya Ukombozi:9:00pm
Makamanda watatu walikutana tena,mara baada ya kutoka nyumbani kwa kamanda Kendrick.Kila mmoja aliketi katika kiti chake,ndani ya ofisi ya ukombozi.
“,Catherine nipe ripoti!”,Kendrick aliongea,akijizungusha zungusha kwenye kiti chake.
“,Kila kitu kiko sawa,picha za mmoja kati ya magaidi anayetuhumiwa kuhusika na shambulio,zimefika katika vyombo vya habari,kesho asubuhi taarifa zitaenea na kutangazwa kila kona.”,Catherine alimaliza kutoa ripoti yake.
“,Ok sawa,sasa nazani mnafahamu magaidi walipo,mahali tuliposhambuliwa,walitugundua mapema,meli yao ikajibadirisha kama nyambizi,ikawa rahisi kutushambulia,hivyo basi,kabla ya mapambano tuelewe,meli yao ni ulinzi tosha kwao,ina uwezo kujigeuza katika maumbo mbalimbali,ikawa kama meli,nyambizi au hata ndege ,ikapaa angani kama ndege zingine!”,Kendrick alitoa maelezo mafupi.
“,Nafahamu nini cha kufanya,nikipata uhakika wa eneo walilopo,iwe baharini au angani,nitaweza kudukua(kuhack) mifumo yote ya mawasiliano kwenye chombo chao,itakua rahisi kuwavamia,hawatatuona wakati wa kukivamia chombo chao.
“,Sawa,naona tukiwakamata hawa magaidi walioko Dar es salaam,watatusaidia kujua wenzao wako wapi,itakua rahisi kufanya udukuzi!”,Catherine aliongea.
“,Wazo zuri,tukutane hapa saa kumi na mbili asubuhi,tuanze kazi,kila mmoja awe makini kujilinda,kila tunapopiga hatua,maadui zetu wako nyuma,zingatieni suala hili……”,Kendrick alizungumza.
“,Sawa afandee!”,wote waliitikia,wakapigiana saluti za heshima,kila mmoja akatoka nje, kuelekea nyumbani kwake kupumzika..
…………………………………
Hisia za kimapenzi ziliusumbua moyo wake, kadri siku zilivyozidi kwenda, Kendrick hakuonesha hisia zozote za mapenzi juu yake,uvumilivu ukamshinda kabisa, moyo wake ulichoka kuteseka na mapenzi,akafikiria, akapata wazo, wazo aliliona sahihi.…
“,Kendrick,nimepoteza funguo za nyumba yangu, sijui hata nafanya nini, hotelini siyo salama, siwezi kulala kabisa ……”,Catherine alidanganya, akiwa pembeni ya gari lake, sura yake ilikuwa siliasi, haikuonesha hata chembe ya uongo, alijiamini kwa yale aliyoyazungumza.
“,Kwa nini usije kulala nyumbani kwangu, kuna vyumba vya kutosha, kesho tutatafuta funguo zako au kuchongesha zinginee! “,Kendrick aliongea.
“,Hapo utakua umenisaidia saanaa, lakini ujue sasa hivi familia yako imeongezeka, mzee wako, mama yako pamoja na mdogo wako, hawawezi kukufikilia vibaya,wakafikili umeleta mwanamke ndani? “,Catherine alifurahi plani yake kufanikiwa kama alivyo panga,akajifanya kama hakupanga jambo hilo, akaendelea kuuliza maswali ya uchokozi.
“,Hapana,wewe ni rafiki yangu,tunafanya kazi pamoja, hawezi kuwaza chochote kile, japo mama yangu kila siku ananiuliza kuhusu suala la kuoa, mimi bado sijawa tayali, nitamlisha nini mie? “,Kendrick alimjibu Catherine, uso wake ukaachia tabasamu kwa mbali. .
“,Hahaaa, “wote wakacheka, wakajipakia kwenye magari yao, nje ya jengo la ofisi ya ukombozi, wakatokomea, kamanda Philipo alikuwa tayali ameshaondoka zake dakika takribani kumi zilizopita.
…………………………………
Mtoni Kijichi :
Catherine na Kendrick walifika nyumbani, mama yake Kendrick, baba yake, pamoja na mdogo wake Jacline walikuwa tayali wamelala.
“,Tutaonana kesho,kalale chumba cha wageni, pita korido hii, chumba cha kwanza mkono wa kushoto! “,Kendrick aliongea, baada ya kumaliza kula, yeye pamoja na Catherine.Kendrick alinyanyuka, akataka kwenda kuchukua maji ya kunywa kwenye friji.
“,Subili nikuletee! “,Catherine aliongea, akanyanyuka kwenye sofa, akaisogelea friji, akachukua chupa ya maji ndani ya friji, akamimina kwenye grasi. Akageuka nyuma, Kendrick alikuwa anasinzia sinzia, usingizi ulikuwa unamzidi nguvu, hakutambua chochote kile kilichokuwa kinaendelea, catherine akaingiza mkono ndani ya koti lake la suti, akachukua kidonge cha usingizi, vidonge ambavyo walivitumia katika oparesheni mbalimbali za kijeshi. Baada ya kuweka kidonge kile ndani ya maji, akatikisa vizuri kiweze kuyeyuka, kisha akampelekea Kendrick.
“,Kendrick, Kendrick! “,Catherine aliita.
“,Yeeees, nanambiee! “,Aliitika kwa kigugumizi, usingizi ulimzidi nguvu, isitoshe alichoka sana, tangu asubuhi alizunguka huku na kule bila kupumzika.
“,Kunywa maji, haya hapa! “,Catherine aliongea, Kendrick akachukua glasi ya maji, akanywa maji yote,akaweka glasi mezani, ndani ya sekunde mbili tu, akalala fofo.
“,Hahaaa, leo unalala na mimi, kila siku nikigusia suala la mapenzi unaona kama natania, sasa leo tunalala wote, kesho wakitukuta, lazima tufunge ndoa ya mkeka, unasema huoi askari kama wewe, sasa utaoa kwa lazima…”,Catherine alisahau vita kubwa mbele yao kwa muda mfupi tu, hisia za mapenzi zilikuwa zimemtawala, akamnyenyua Kendrick, akampeleka katika chumba cha wageni, chumba ambacho alielekezwa akalale, wote wakalala huko.
Mtoni kijichi :7:30am
Magaidi wanne wa kundi la D47,walipaki gari nyeusi aina Toyota Hallier, pembeni, nje ya jumba la kamanda Kendrick, jumba ambalo lilizungushiwa geti kubwa.
“,Hapa ndipo nyumbani kwake,waliotuelekeza hawajadanganya, kama unavyo ona, kuna askari getini, anatimiza majukumu yake ya ulinzi
……”,gaidi D47 alioongea.
“,’Nazani mwenyewe ameshaelekea ofisini,chuma cha pua, toka kaongee na mlinzi, fanya lolote tuweze kuingia ndani! “,gaidi D47 aliendelea kuongea.
“,Sawa bosi”,chuma cha pua aliitikia, akatoka nje, akalisogelea geti,mpaka mahali alipokuwa amesimama mlinzi.
“,Karibu muheshimiwa, sijui nikusaidie nini? “,askari mwenye kirungu mkononi aliuliza,akamkaribisha kwa heshima zote gaidi, kutokana na suti nyeusi ya heshima aliyokuwa amevaa.
“,Nina mazungumzo na bosi wako, tulisoma naye, ni muda mrefu hatujaonana, naomba kuzungumza naye…”,gaidi aliyejulikana kwa jina la chuma cha pua aliongea,askari yule akaonekana kuyaamini maneno ya mgeni huyu.
“,Japo bosi hayupo, ameshaenda kazini, unaitwa nani? “,askari yule aliuliza swali tena,huku akidanganya kuwa Kendrick hayupo, alielekezwa kusema hivyo kwa mtu yoyote asiyemfahamu.
“,Acha maswali yako kijana, au nimpigie simu uongee naye, utamwaga unga sasa hivi …”,chuma cha pua aliongea, akaingiza mikono yake mfukoni, akatoa simu, akajifanya kama anataka kupiga, askari yule akaanza kutetemeka kwa hofu.
“,basi baba! basii, yaishee, ingia ndani ,lakini bosi hayupo……,”askari yule aliongea,akadanganya, hakuna aliyemsikiliza, akafungua mlango, chuma cha pua aliangalia kulia, akaangalia tena kushoto, hakuona mtu yoyote yule, alimpiga kabali askari yule, akaivunja shingo yake, ulimi wa askari yule ukatokeza kwa nje, akafa palepale. Chuma cha pua akambeba, akamuweka kwenye buti la gari,walitaka mauaji yafanyike kimya kimya, asigundue mtu yoyote yule, baada ya kumfyekelea mbali, magaidi wote watatu wakatoka ndani ya gari, wakaingia ndani ya jengo la kamanda Kendrick, wakafunga geti kwa ndani, asije akaingia mtu yoyote yuke, akaharibu mipango yao.
“,Yuko na wifi yako,nimeona viatu vya kike mlangoni tofauti na vyangu wala vyako,leo amechelewa kwenda kazini,muache apumzikee…”,mama yake Kendrick aliongea,huku akitabasamu.
“,Hapo hapo mlipo,asijitikise mtu yoyote,mkijitikisa tunawaua!……”,sauti ya kutisha ilisikika,walipogeuza shingo zao,wakatazama mlangoni,uso kwa uso na wanaume wanne wenye bastola mkononi,usoni walivaa miwani rangi nyeusi,rangi ambayo ilifanana na suti zao pamoja na mabuti yao meusi. “,Nyie ni wakina nani?mnataka nini?”,mama yake Kendrick aliuliza swali.
“,paaaaaaa!”,alichapwa kibao,akadondokea upande wa pili wa sofa.
“,Mamaaaaaaa!”,Jacline alipiga kelele,hasira za mama yake kupigwa mbele yake zikampanda,akakosa cha kufanya.
“,Malaya mwenyewe!”,Jackline hakuogopa chochote kile,akawatukana magaidi.wale,akamtemea makohozi usoni,gaidi ambaye alikuwa amemchapa kibao mama yake,huku akimwita Jackline malaya.
“,Tunakubaka sote wanne sasa hivi,mbele ya baba yako,pamoja na mama yako,halafu tuone sisi na wewe nani malaya……”,chuma cha pua alizungumza,wakamfunga kamba mama yake Kendrick mkononi na miguuni,wakamfunga na baba yake.Wakajiandaa kumubaka Jackline,chuma.cha pua alianza kuifungua zipu yake.
…………………………………
Kamanda Catherine alikuwa amechoka sana,alilala na mtu aliyempenda kwa mara ya kwanza, lakini hakufanya naye chochote kile, alitaka kutimiza malengo yake, Kendrick aweze kufungishwa ndoa ya mkeka pamoja naye, watakapokutwa wamelala pamoja asubuhi. Usingizi hauna ndugu, alilala fofofo tofauti na siku zote, Kendrick ndiyo kabisaa, dawa ya usingizi aliyopatiwa usiku uliopita, iliendelea kutimiza majukumu yake, akauchapa usingizi bila hata kushtuka.
Ghafla Catherine alikurupuka usingizi, mapigo ya moyo wake yalienda kasi sana,akageuka upande wa pili, akamgusa gusa Kendrick begani, hakushtuka! alikuwa bado amelala. Catherine akaitazama saa yake ya kijeshi, “8:00am”,saa yake ilisomeka.
“,Saa mbili kamilii! “,aliongea peke yake kwa mshangao, akachukua viatu vyake, akavaa suti yake, akaziweka vizuri nywele zake, kwa mbali akasikia vitisho sebureni, akasikiliza kwa makini, mapigo ya moyo wake yakapiga kwa kasi sana,walikuwa wamevamiwa, akasogea kitandani, akampiga piga Kendrick aweze kushtuka,Kendrick hakushtuka, aliendelea kukoroma kama kawaida.
“,Kendrick, Kendrick, tumevamiwa, najuta mimi! amka tukapambane! “,Catherine aliita, bila mafanikio,hakua na budi kuubeba mzigo yeye mwenyewe, bila hivyo chochote kile kingeweza kutokea, wazazi wa Kendrick wasije wakauawa, akalaumiwa,akakosa mume pamoja na kuharibu kazi yake.
“,Kakaa, nabakwaa, kaka nabakwaaa, njooo unisaidiee ……”,Jackline alipiga kelele,kelele zikapenya katika matundu mawili ya masikio ya Catherine, akakasirika.
“,Hahaaahaaa, hakuna atakayekuja kukusaidia, hahaa……”,magaidi yale yalizungumza, yakacheka kwa kejeli, Catherine akazidi kukasirika,alisikia kila kitu.
“,nimelala kwa Kendrick, najua uko ofisini, njoo, tumevamiwa …”,Catherine alituma ujumbe kwa kamanda Philipo kupitia saa yake iliyotumika kama simu,akapiga mahesabu namna ya kuwavamia magaidi, awashambulie kabla hawajafanya ubakaji. Akafungua mlango taratibu, akachungulia,akamuona jambazi aliyegongana naye uso kwa uso, alimtambua vizuri sana.
“,Wamejileta wenyewe, watakufa, “Catherine aliongea, akaifunga bastola yake mfumo wa sauti, akalala chini, hakuweza kuonekana, sofa zilimzuia. Chuma cha pua akachomoa uume wake uliosimama kwa njaa kali, bila aibu akamsogelea Jacline.
“,Yalaaaaaa ……”,uume wa chuma cha pua ulisambaratika, damu zikaruka, akapiga kelele za uchungu, hawakutambua risasi imetokea wapi. Wakaanza kupiga hovyo risasi, kwenye sofa, ukutani, dirishani, milangoni, walikuwa kama wamechanganyikiwa.
“,Mtafuteni tumuue! jitokeze kabla hatujaua familia yako ……”,kiongozi wa kundi hili aliongea, alikuwa D47 namba sitini, bastola yake aliinyosha kuelekea juu, akafyatua risasi, zikapiga juu ya dali.
“,Nasema jitokeze tutawauaa wazazi wako! “,gaidi alitoa amri kwa mara nyingine tena.
Milio ya risasi ikamkulupua usingizini kamanda Kendrick,akavaa suruali, akachukua bastola yake, akafungua mlango taratibu, huku akijiuliza maswali mengi, hakujua amefikaje katika chumba hiki cha wageni, chumba ambacho alipaswa kulala kamanda Catherine.
“,Jitokeze kabla sijawaua wazazi wako, moja, mbili tatu ……”,gaidi lile lilianza kuhesabu, Kendrick hakuwa tayali kuwapoteza ndugu zake, akajibanza ukutani, uso kwa uso na kamanda Catherine akiwa amelala chini.
“,Chuchumaa chini, watakuona, vipi tunafanyaje hapa?,nimefikilia mbinu ya kutumia nimeshindwa”,Catherine alimuuliza Kendrick.
“,Piga kule mlangoni, wakiwa bize kuangaza mlangoni risasi hizo, tutaruka na kuwashambulia ,kwanza wako bize wanamuhudumia mwenzao, amefanya nini?……”,Kendrick aliuliza.
“,Nimempiga risasi kwenye dudu lake, alitaka kumubaka mdogo wako, “Catherine aliongea.
“,Sita, saba, nikifika kumi nauwa familia yako yote, nane, “gaidi aliendelea kuhesabu, akatoa onyo, akaendelea tena kuhesabu, Catherine na Kendrick wakasitisha mazungumzo yao, Catherine akapiga bastola kwenye mlango wa kutokea ndani ya nyumba, wote wakageuka, wakautazama.
“,Vuuuup, kwaaacha……”,Kendrick aliluka mateke mawili yaliyosindikizwa na ngumi, akamtandika ngumi gaidi D47 namba sitini ,mateke mawili yakawapata magaidi wawili waliokuwa wanampatia huduma mwenzao, wote wakagagaa. Catherine akawanyoshea bastola, akawateka, Kendrick na yeye akawanyoshea bastola yake.
“,Paaaa! “,alipiga risasi chini, magaidi yakarudisha mikono yao, yalitaka kuzichuka bastola zao zilizodondoka mita kadhaa na mahali yalipodondokea.
“,Mmejileta wenyewe, tulikuwa tumepanga leo tuwasake kona zote za mji huu wa makonda, karibuni sana nyumbani kwangu, “Kendrick aliongea, mkono wake wa kulia ulishika bastola, mkono wake mwingine alikuwa akiwafungua kamba wazazi wake, ghafla mlango ukafunguliwa, kamanda Philipo alikuwa amefika.
“,Ewalaaa! asante sana Mungu, leo sitalala kama maiti ,jana nimechoka sana sababu yenu, kazi ya leo imeisha asubuhi tu, sasa mtakipata cha mtema kuni! “,Kamanda Philipo aliongea, akayafunga kamba magaidi haya manne, huku Jackline akiyapiga teke kwa hasira na kuyatemea mate.
“,Asante wifi, umeyaokoa maisha yangu! “,Catherine alilia kwa furaha akamkumbatia Catherine.
“,Usjali wifi yangu, ni kazi yangu …”,Catherine alijibu.
“,Huyu ndiyo mkwe sasa, Kendrick unajua kuchagua ……”,mzee Steward na mke wake waliongea, wote wakamkumbatia Catherine, walishuhudia ushujaa wake, Kendrick yeye alikuwa amepigwa na butwaa, hakujua chochote kile, Catherine akakonyezana macho na kamanda Philipo, kamanda Philipo alifahamu kila kitu, wote wakatabasamu.
“,Saluti afandee! “,askari watano wenye virungu waliingia ndani, wakapiga saluti.
“,Salutiii, chukueni washenzi hawa, pakieni kwenye karandinga, mpaka chumba cha mateso, tutafika huko kufanya nao mahojiano, “Kendrick aliongea.
“Sawa mkuu, tumefika na kukagua gari lao, tumekuta maiti ya askari wetu anayelinda geti lako, “,askari wale waliendelea kuripoti.
“,Kwahyo wameuaa?”,aliuliza kwa hasira.
“,Ndiyo bosi,maiti iko kwenye gari lao”askari wale waliitikia.
“,Andika kwenye faili, jana wameua watu ishirini na moja, wakateketeza na kituo chetu, huyu ni mtu wa ishirini na mbili, toa taarifa kwa waziri pamoja na vyombo vya habari wapate taarifa hii ……”,Kendrick aliongea.
“,Kabla ya yote,usiku mmelala pamoja, sisi kama wazazi tumeshuhudia, kulingana na mila yetu ya , tunapaswa kuwafungisha ndoa na kuwapatia baraka zote, tukiwa tunasubili ndoa rasmi, tucheze ngoma na kuburudika, “mama yake Kendrick aliongea, Catherine akatabasamu, Philipo akatabasamu, Kendrick akatabasamu japo kwa shingo upande. “,Mama mimi sikulala naye chumba kimoja, sasa sijui nitamlisha nini! “,Kendrick aliongea, hofu ya majukumu ilimuandama moyoni.Isitoshe hakutambua chochote kile, Philipo na Catherine wakiwa wanachekelea kwa furaha, sio Philipo tu, Jackline alikuwa anafurahi kwa kile ambacho kilikuwa kinafanyika.
“,umelala naye hujalala naye sisi haituhusu, mpatie mkono mwenzako! “,mama Kendrick aliongea, alichoka kusubili mkwe kila siku,akiishia kuambulia ahadi zisizotimia kutoka kwa mtoto wake, leo alimkamatisha.
Catherine akamshika mkono Kendrick, akafunga na kanga mikono yao, akaongea maneno ya kimila, akatoa baraka zake zote yeye na mume wake, wote wakapiga kelele za shangwe. Mama Kendrick akapiga meza kama ngoma, mdundiko ukapigwa, Catherine akacheza, Phipo akacheza, wote uvumilivu ukawashinda, wakaanza kucheza ngoma kwa furaha.
Mtoni Kijichi :08:40am
Nyumba ya Kendrick ilijawa na furaha tele, kila mmoja alicheza kadiri alivyoweza, walisahau kabisa kuwa ilikuwa ni muda wa kazi, burudani iliwafanya wasahau kila kitu, walisahau majukumu mazito yaliyokuwa mbele yao.
“,Kendrick! saa tatu kasoro! “,Catherine aliitazama saa yake, akashtuka sana, muda ulikuwa unazidi kwenda mbele, walikuwa hawajafika ofisini.
“,What!twendeni,bila shaka wanatusubili…”,Philipo aliongea,kila mtu akachukua kilicho chake,Kendrick akaenda kuvaa suti yake nyeusi,wote wakaondoka kuelekea kazini
“,Oooh sitaki kuoa, ooh sijajipanga, utajipanga mpaka lini, utaoa kwa lazima ,mimi ndiyo mama Kendrick ……”,yalikuwa maneno ya mama Kendrick, akiwa amebaki nyumbani, yeye, mume wake pamoja na mwanae wa kike.
“,Kweli kabisa, lakini mimi bado nawafikilia wale majambazi, mimi naona kaka abadilishe kazi, kazi yake ni ya hatari watakuja kufa siku moja! “,Jacline aliongea.
“,Sasa askari wote wakiacha kazi, nani atakulinda?, acha watimize majukumu yao, kila mmoja atakufa, hakuna mtu yoyote atakayeishi milele …”,baba yake Kendrick, mzee Steward aliongea, binti yake akakaa kimya.
“,Haya sasa, mwanangu na mkwe wangu wote askari, nikiguswa tu na majirani,cha moto watakiona! “,mama yake Kendrick aliongea,licha ya kula chumvi nyingi, tabia za uswahilini alikua bado anazo. Waswahili husema ng’ombe hazeeki maini.
“,Sawa mke wangu, ngoja mi nijiandaee,nikazulule mtaani, maana muda mrefu sijaona magari, “mzee Steward aliongea.
“,weweee naye, tabia zako hujaziacha tu,bila shaka umekumbuka wanawake zako,haya kila laheri, uwasalimie wake wenza ……!”,mama Kendrick alizungumza.
“,Mama Kendrick, maneno gani unazungumza mbele ya binti yako, unamfundisha nini huyu mtoto! ……”,baba Kendrick aliongea, hasira zilimjaa usoni, sura yake ikakunjamana.
Kendrick, Catherine pamoja na Philipo, walifika chumba cha mateso, chumba ambacho kilipatikana katika gereza kuu la Segerea.Ulinzi uliimarishwa, kila aliyeingia na kutoka, alikaguliwa kwa mashine maalumu ya umeme,hakuna aliyeruhusiwa kuingia na silaha isipokuwa kwa kibali maalumu.
“,You are not allowed to get in, unless you put down your guns ……”,(Hamruhusiwi kuingia ndani, mpaka tu mtakapo weka bunduki zenu chini …).
Mashine ya ukaguzi pembeni ya mlango iliongea kwa sauti, Kendrick, Catherine pamoja na Philipo, wote walikuwa na bastola katika miili yao, Kendrick alikuwa ameipachika kwenye kiatu chake, Philipo alikuwa ameipachika katika koti la suti yake, Catherine alikuwa ameipachika katikati ya mkanda wake.
“,Haina jinsi, milango hii ni ya umeme, msipo weka silaha zenu, milango haitafunguka ……”,askari magereza aliyekuwa anawaongoza aliongea, wote wakachomoa bastola zao, wakampatia mmoja kati ya askari magereza, akazihifadhi kisha wakarudi tena, mashine ikawakagua, walikuwa hawana silaha, mlango ukafunguka, wakaingia ndani, askari mkuu wa magereza alikuwa mbele akiongoza msafara, Kendrick alifuatia, kisha Catherine pamoja na Philipo walifata kwa nyuma.
“,Hawa ndiyo walifanya shambulio la kigaidi, wakateketeza kituo chenu? “,askari magereza aliuliza.
“,Ndio mkuu, tunapaswa kuwahoji tujue Donald Mbeto yuko wapi kwa sasa, ikiwezekana wafanye mawasiliano nao, tukawakamate! “,Catherine aliongea.
“,Magaidi wana roho ngumu, huwa hawasemi kirahisi namna hiyo, mmejipangaje? “,askari magereza aliongea.
“,Watasema tu, twende ukaone! “,kamanda Philipo aliongea, askari magereza aliwaamini sana vijana hawa, siku zote kazi yao ilikua ya uhakika.
Wakatembea korido ndefu, wakapita gereza la kwanza lililojaa wafungwa takribani elfu moja, wakiwa wamelaliana kama ndizi,baada ya dakika tano wakalivuka gereza hili, wakakata kona mkono wa kulia, wakakata kushoto, uso kwa uso na chumba kikubwa kilichozungushiwa nyavu kila kona. Mlangoni kilifungwa na kufuli kubwa la kilo tano, ndani ya chumba hiki kulikuwa na viti vitano, viti ambavyo vilikuwa maalumu kwa ajili ya kutoa mateso pamoja na kunyonga. “,Karibuni sana, naona mmefurahi sana, lakini tambueni kuwa, wenzetu wakitambua jambo hili, watakuja kutukomboa ……”,chuma cha pua aliongea, alikuwa na roho ngumu sana, nyeti zake zilikuwa zimefungwa bandeji,haja ndogo alitumia mpira maalumu, lakini hakukoma, aliendelea kuwa katili kama kawaida.Mara tu baada ya kundi la the super three soldiers kuingia ndani ya chumba walichokuwa wamefungwa, aliwakaribisha kwa kejeli.
“,Hahaaaaa, mmekuja na malaya humu ndani! “,magaidi wote watatu walicheka, wakamkejeli Catherine. Catherine akataka kuwasogelea awatandike makonde, Kendrick akamzuia.
“,Nilitaka wote mtumie mipira kukojoa kama mwenzenu, muda mfupi ujao mtalia machozi, chekeni mara ya mwisho! “,Catherine alifoka, ngumi yake alikuwa ameikunja, akachomoa sindano za kibanio chake cha nywele, akajiandaa kutoa mateso wakati utakapofika.
Kendrick alijua nini cha kufanya,akasogelea meza yenye batani nyekundu,akafika, akakaa juu yake. Catherine pamoja na Philipo wakasimama katikati ya magaidi wanne.
“,Mnaweza kutwambia uwezo wa meli yenu ya D47paraquaat ……?”,Kendrick aliuliza swali la kwanza.
“,Hahaaaaa!,kirahisi rahisi hivyo, hata ufanye nini, kuingia ndani ya meli yetu hutaweza dunia yote imeshindwa, sembuse wewe sisimizi mdogo tu ……”,Chuma cha pua alicheka sana, akaongea kwa kejeli, akawaponza wenzake.
“,Yalaaa…aaaa, yalaa…aaa …”,Kendrick alibonyeza batani nyekundu iliyokuwa mezani, kelele za magaidi zikasikika, walipigwa na shoti ya umeme kutoka kwenye viti vya chuma walivyokalia, jasho likawatoka kama maji kwa sekunde moja tu. Baada ya dakika mbili Kendrick akabonyeza tena, shoti ikakata, zingezidi dakika mbili basi angewaua kabisa magaidi hawa.
“,Hehee…ee, bola utuue tu …”,chuma cha pua alicheka tena, Kendrick akakasilika, akabonyeza tena mtambo wa shoti ya umeme.
“,Yaaala…aa, uwiiii…ii! “,,yalipiga kelele, yakalia kwa uchungu.Catherine akayachoma na sindano zake mgongoni, kila mmoja, yakaugulia maumivu.
“,Sikilizeni, tuyapatie nafasi yawasiliane na wenzao,sisi tujifanye wajinga,yatumie simu yetu kuwasiliana ,kisha tutaunganisha simu yetu pamoja na kompyuta tutajua imepigwa kutoka wapi,hawa wana roho ya paka hawawezi kusema.’ ,Catherine aliongea wenzake wakamuelewa.
“,Ndiyo,sasa hivi mnajifanya wajanja kwa vile hawana taarifa,Donald Mbeto atawaua nyoteee…”,magaidi haya manne yalijitamba na kuchimba mkwala.
“,Sasa sisi tunataka tuwapige mbele yenu hao mnaowategemea,simu inaletwa,muwapigie,waambieni mmekamatwa,waje wawaokoe……” Kendrick aliongea, yakatikisa kichwa, yakakonyezana.Dakika mbili tu, askari magereza alileta simu, akawakabidhi,chuma cha pua akafunguliwa mkono mmoja, akapatiwa simu,simu ilikuwa imewekwa raudi spika.Akabonyeza namba alizozifahamu yeye, akapiga.
“,Vipi imekuaje, mbona kimya? “,upande wa pili wa simu ulipokea.
“,Njoeni mtuokoe, tumekamatwa,tumebahatisha simu tuwapatie taarifa, “Chuma cha pua aliongea.
“,Hao mbwa wanajiamini nini, ndani ya nusu saa ijayo vijana watakuja kuwakomboa, “upande wa pili wa simu uliongea, simu ikakatwa, Philipo akachukua kompyuta yake, akaunganisha na simu ambayo imetumika,akabonyeza bonyeza, kisha akatoa jibu.
“,simu imepigwa kutoka katika ndege yao, iko futi sitini angani, tayali nimedukua (hack) mifumo yao ya mawasiliano,tuwafuateni huko huko,nyie maboya mmefeli ,hawatatambua mahali mlipo tena……”,Philipo aliongea,akatoka nje,yeye na wenzake,wakaondoka zao.
“,Shiit,roho yangu ilisita,sijui ilikuaje mpaka tukaingia mtegoni…”,magaidi walibaki wanalalamika,hakuna akiyewasikia,chumba chao kilifungwa kwa kufuli kubwa,huku wao wakiwa wamefungwa katika viti maalumu,miguu na mikono.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano, katika kundi la D47,alipokea taarifa iliyomshitua sana,baada ya sekunde tu simu ikakatwa, ghafla mifumo yote ya mawasiliano ikazima.
“,Banard kuna nini?, “mmoja wa magaidi alimuuliza Bernard, mkuu na mtaalamu wa mitambo ya mawasiliano katika meli ya magaidi wa D47.
“,Wenzetu wanne ,kitengo cha Dar es salaam, Tanzania wamekamatwa! inatakiwa wakombolewe kabla hawajauawa, lakini ghafla simu imekatwa,nilipojaribu kutafuta mahali ilipotokea, mifumo yote imezima ……”,Benard aliongea.
“,Ina maana mifumo yetu ya ulinzi imedukuliwa? “,mmoja kati ya magaidi, chumba cha mawasiliano aliuliza.
“,Itakua hivyo, kampatie taarifa bosi haraka sana! “,Benard aliongea, akajaribu kurekebisha mitambo ikagoma, kompyuta zote zilikuwa zimezima. Ndani ya dakika tano tu, bilionea Paresh Kumar alifika katika ofisi hii, akiwa ameongozana na Donald Mbeto.
“,Bosi nimepokea taarifa, wenzetu wa Dar es salaam wamekamatwa! nilipojaribu kutaka kujua eneo walilopo, kompyuta zote zikazima, mifumo yetu imedukuliwa, ndiyo narekebisha, mpaka turudi hewani, saa moja litakua limepita tayali! “,Benard alitoa maelezo kwa bosi wake.
“,Sawa, weka mambo sawa, kisha fanya utundu wako tujue eneo walilopo,tutume vijana waende kuwakomboa! “,Paresh Kumar aliongea, Benard akatikisa kichwa, aliyaelewa maelekezo aliyopewa, akaanza kutekeleza kama alivyoelekezwa. Paresh Kumar akaondoka zake, akiwa pamoja na rafiki yake kipenzi, kijana wake wa kazi, jini mweupe au Donald Mbeto.
…………………………………
Kamanda Kendrick, Catherine, pamoja na Philipo walikuwa katika mavazi yaleyale ya kazi,usoni walivalia miwani yao ya mionzi,bastola zao zilikuwa kiunoni. Helikopta ya kivita iliiacha ardhi ya jiji la Dar es salaam saa tano kamili asubuhi, siku ya jumamosi.
“,ndege yao iko futi sitini juu,upande wa kaskazini,tunapaswa kuingia ndani ya ndege yao kabla mifumo yao ya mawasiliano haijawa activated ndani ya saa moja!”,kamanda Philipo alitoa maelekezo,akaeleweka,rubani akaendelea kutimiza majukumu yake.Makamanda watatu walijiandaa,walikuwa tayali kwa lolote lile,Catherine alikuwa bize akichukua silaha za kumfaa,silaha moja baada nyingine,katika sanduku kubwa ambalo walilipakia katika ndege,silaha za kila aina,silaha kubwa na ndogo.
“,Mabomu haya yatanifaa,visu hivi vitanifaa kufyeka shingo zao,bunduki kubwaa sitaki,bastola yangu inanitosha……”,Catherine aliongea,alikuwa amekamilika.
“,Mimi sichukui chochote kile,kisu changu,bastola yangu,pamoja na miwani yetu ya mionzi inatosha,……”,Kendrick aliongea,akatazama saa yake,ilikua saa tano na dakika kumi na tano,walikuwa wamekalibia,mahali ndege ya magaidi ilipoweka kambi angani.
“,Haloo,haloo ovaa,usawa wa ndege,usawa wa ndege mnatupata ovaa!”,simu ya mkonga ilisikika,upande wa pili wa simu uliongea.
“,Mmekalibia,angalieni mbele yenu,kazi ianze mara moja…”,kitengo cha mawasiliano cha jeshi walifatilia kila hatua za ndege yao,hawakutaka ishambuliwe kwa mara nyingine tena.Wakampatia maelekezo rubani wa ndege yao,kisha simu ikakatwa.
“,Tumefika,nazani ndiyo ndege hiyo kubwa mnayoiona mbelee yenuu……”,rubani aliongea,huku akishangaa,hakuwahi kuona ndege kubwa na ya ajabu kiasi kile.
“,Whaaat!ndege nzuri sana na kubwaa,Kendrick,tusitumie milipuko yoyote,tunapaswa kuilinda iwe salama,tukishinda vita hii,ndege itaifishwe iwe mali ya serikali ……”,Catherine aliongea, alishangazwa na ndege iliyonekana mbele yao.
“,Kweli kabisa, wazo zuri sana, ina maana hii ndiyo ilitushambulia? “,Philipo aliongea, akauliza swali, macho yake yalitazama mita mia mbili mbele yake, helikopta yao ikasogea karibu kabisa na ndege hii, ili wapate nafasi ya kuikamata kwa mikono sehemu yoyote ile, waweze kuingia ndani.
“,Ndiyo hii, kazi ianze mara moja! “,Kendrick aliongea kwa kifupi, akakamata bawa la ndege ya maadui wakapanda juu yake, alilikamatilia bawa kwa nguvu, akishindana na upepo mkali. Wenzake wakafanya kama yeye, wote wakakamatilia bawa la ndege ya magaidi wakaanza kuisogelea taratibu, upepo mkali ukivuma, lakini walikua imara, hawakutikisika, miwani ya mionzi ilifanya kazi yake ipasavyo, ikawakinga na upepo mkali machoni.
“,tumia emergency exit! kioo hicho hapo mbele, kisogeze chini juu, tuingie wote haraka sana kabla upepo haujaingia ndani ya ndege na kutuzidi nguvu …”,kamanda Philipo alitoa maelekezo,Kamanda Kendrick akafanya kama alivyoelekezwa, dirisha likafunguka, akaingia ndani, Catherine akafuatia, Philipo akawa wa mwisho, akarudisha kioo cha dirisha mahala pake, wote wakatokea ndani ya chumba cha choo.Huku ndege ikitikisika kwa sekunde kadhaa kisha ikarudi mahala pake.
…………………………………
“,Mbona ndege imetikisika kiasi hiki, ina maana kuna sehemu ya ndege yetu iko wazii, au tumevamiwa? “,rubani wa ndege hii ya magaidi alizungumza, machale yakamcheza,akamtuma msaidizi wake,kepteni ambaye alifanya kazi ya kuongoza ndege hii inaposafiri kama meli baharini, alikuwa na wasiwasi uliopitiliza. “,Mwambie bosi,walinzi wakague kila sehemu, ulinzi uimalishwe, kila mtu achukue pozisheni yake,dirisha la dharula bila shaka lilikuwa wazi”rubani wa magaidi aliongea.
“,Sawa, hata mimi nimewaza jambo hilo! “,kepteni wa magaidi aliongea, akatoka chumba cha kuongoza ndege hii ya D47paraquaat, akaondoka zake.
…………………………………
“,bosi, bosi! “,kepteni alifika katika ofisi ya Paresh Kumar, bosi akashtuka, alikuwa ananyonyana ndimi na wanawake zake wa kizungu, wakakurupuka, walishtukizwa.
“,Mbona unaingia ofisi ya bosi wako bila taarifa, kuna tatizo gani? “,Paresh Kumar alifoka kwa hasira.
“,Bosi, dirisha la dharula lilifunguliwa muda mfupi uliopita, kisha likafungwa tena, hatujui kama aliyefanya hivyo ni mtu wetu au adui yetu, nimetumwa kuleta ripoti, ulinzi unapaswa kuimalishwa “,kepteni aliongea,maneno yakapenya vizuri katika kichwa chake, akawasukumia mbali wanawake zake, akafunga vifungo vya shati lake, akaondoka zake, akawaacha wanawake zake wa kizungu wakiwa na hasira, mmoja alikuwa na sindilia, mwingne alikuwa amebaki na bikini yake, ofisi ya Paresh Kumar ilikua zaidi ya kasino,uovu mwingi ulifanyika masaa yote. Akatoka nje ya ofisi yake, uso kwa uso na Donald Mbeto.
“,Kila mtu achukue pozisheni yake, hakikisheni aliyeingia ndani ya ngome yetu hatoki salama, maraisi wao waliowatuma, watajuta!!nitafanya mauaji mpaka nikabidhiwe migodi ninayohitaji, haiwezekani waingie madarakani kwa msaada wangu harafu waninyime ninachohitaji, walizani pesa zangu za kampeni ninawapa bure, kijani wangu utaendelea kufanya mauaji mpaka niseme basi, haya ondoka mara moja,kafanye kama nilivyokuagiza! “,Donald Mbeto alipokea maelezo kutoka kwa bosi wake, akaanza kazi, bosi wake alikuwa amekasirika, kengele ya hatari ikapigwa.
“,danger! danger! everyone should take his position (hatari! hatari!, kila mtu achukue nafasi yake…) ,Donald Mbeto maarufu kama jini mweupe alipiga kelele, magaidi wakakimbia huku na kule, kila mmoja akikamata silaha inayomfaa kwa mapambano.
Catherine, Kendrick pamoja na Philipo, walichungulia kupitia matundu madogo, katikati ya mlango, hawakuona mtu yoyote yule,Wote wakiwa na miwani yao ya mionzi mikali yenye lenzi, wakakitazama kitasa cha mlango kwa sekunde mbili, kitasa kikayeyushwa na mionzi mikali kutoka kwenye miwani, kitasa kikayeyuka,mlango ukafunguka. Wakatoka nje, uso kwa uso na bunduki nane, kulia na kushoto, mbele yao, kote kulikuwa na bunduki, waliwekwa chini ya ulinzi na magaidi waliovalia suti za bluu, zenye nembo ya D47.
“,Tumewakamata! hahaaa, tuwapeleke kwa bosi! “,magaidi yale yalicheka, the super three soldiers hawakuongea kitu chochote kile, walizitazama bunduki walizowekewa kichwani, sekunde mbili tu, bunduki za magaidi wale zilipigwa na mionzi kutoka kwenye miwani, bunduki zikayeyuka,zikawa kama uji.
“,What! nini hiki, maajabu haya! “,magaidi wale walishangaa,kitendo cha bunduki zao kuyeyuka kiliwashangaza sana, wakasahau kama walikuwa wamewaweka watu chini ya ulinzi.
“,Vuuuup, vuuuup, vuuup …”,Kendrick alipiga ngumi tatu, zikawapata magaidi watatu kichwani,wakadondoka chini, Catherine akaluka mateke mawili, magaidi wawili wakandoka chini, wakabaki wawili, wakiwa wamesimama, walikuwa hawajielewi, kitendo cha bunduki zao kuyeyuka mbele yao walikiona cha ajabu sana, wakawa kama vichaa, wakataka kukimbia, Kamanda Philipo alichomoa visu viwili, akavirusha, vikawapata mguuni, wakadondoka chini.
“,Yala…aaa, mmetuumiza washenzii nyie ……”,magaidi yale yalitukana,lakini haikubadirisha kitu chochote kile, Kendrick, Catherine pamoja na Philipo walichomoa bastola zao wakayanyoshea magaidi yale.
“„Nyote ingieni humo chooni haraka sana, nasema ingieeni! “,Kendrick aliyakalipia, magaidi sita yakiwa yameweka mikono kichwani yakaingia, kamanda Philipo akayaburuta magaidi ambayo yalichomwa na visu mguuni, yalikuw hayawezi kutembea, wote wakawekwa chooni.
“,Catherine akachomoa bomu lake dogo, akachomoa pini, akalitupilia ndani ya chumba cha choo.
“,Puuuuuu, puuuuuu! “,mlipuko ukasikika, ndege ikatikisika tena, kisha ikarudi katika hali yake ya kawaida, Kendrick na wenzake walilukia upande wa pili, wakalala chini, hawakujeluhiwa popote pale.
“,Umefanya nini, tulikubaliana vipi? situlisema hakuna kutumia milipuko …”,Kendrick alilamika.
“,Haina jinsi, hiyo ndiyo mbinu ya kuwaua kwa urahisi, muda mfupi ujao, wote watafika eneo hili, utaona watakavyo kufa,”Catherine aliongea, akachomoa mabomu yake mawili madogo, akayaseti yalipuke ndani ya dakika tano, wote wakatembea harakaharaka, mpaka mahali kulipokuwa na magari pamoja na ndege za kivita nyingi sana.
“,Waooooh! “,Philipo hakusita kuonesha furaha yake,alitazama ndege,magari pamoja na vifalu vya kivita,ghafla kundi kubwa la magaidi lilisikika,wakija mahali kuliposikika mlipuko,Catherine na kundi lake wakaingia chini ya magari,wakajificha,hawakuonekana,magaidi yakapita bila kukagua kona zote,lilikuwa kundi la magaidi takribani mia moja.
“,Hawa wehu,wametuchokoza,wameua wenzetu,mimi ndiye Donald Mbeto mwenyewe,nasema hivi,hawatoki salama mahali hapa……”,Donald Mbeto aliongea,alikuwa hana silaha yoyote ile mkononi,tofauti na wenzake ambao kila mmoja alikuwa ameshika bunduki yake.Alizigeuza geuza maiti za wenzao,moshi ukiwa unaishia na kubaki kweupe,mlipuko huu haukuhalibu ndege hii,bali iliwasambaratisha vipande vipande magaidi nane.
“,Kuna mabomu!kuna mtego”,Donald Mbeto aliongea,akaluka serekasi,akatua upande wa pili,akalala chini.
“,Puuuuu,puuuuu,puuuu,”mlipuko ulisikika tena,mabomu ambayo Catherine aliyatega,akayaweka chini ya maiti,yalililipuka,magaidi mia moja ambao waliongozwa na Donald Mbeto walijeruhiwa vibaya sana,wengine wakafa palepale.Isipokuwa Donald Mbeto ambaye hakujeruhiwa mahali popote pale.Akanyenyuka ,vijana wake walikuwa wameumia vibaya,wengine walivunjika shingo,miguu na wengine walikatika viuno.
“,Huo ni uzembe katika kazi,hunifaaii……”,Donald Mbeto aliongea,akammalizia gaidi mwenzake ambaye alivunjika miguu yote miwili,lakini alikuwa bado mzima,akilia na kuhitaji msaada.
“,Twendeni,twendeni tukaone,watakua wamekufa!,huo mlipuko sio wa kawaida…”,Philipo alitoa wazo lake.
“,Hajafa,unamsikia anavyotukana,muda ukifika tutajitokeza,asiwe na shaka……”,Catherine alizungumza,mkono wake wa kulia alikuwa ameshika bastola mkono wa kushoto ulishika mabomu mawili.Aliona ndio silaha pekee ya kuua watu wengi kwa muda mfupi tu.
Ghafla sauti za watu kukimbia zilisikika,wote wakageuza shingo zao,wakatazama mahali sauti za vishindo zilikuwa zinatokea,jeshi kubwa lilikiongozwa na mwanaume wa kihindi lilisogea mahali mlipuko ulikuwa umetokea,mikononi walishika bunduki zao,walijiamini sana.
“,Kendrick tunafanya nini!”,Catherine aliomba ushauri kwa Kendrick,huku akifikilia mbinu ya kufanya.
“,Wote hawajui mahali tulipo,pembeni yetu kuna ndege nyingi kubwa,ndege zenye makombola,tukipanda ndege moja,shambulio moja tu tunawatekeza woteee!”,kamanda Philipo alitoa mawazo yake.
“,Wazo zuri sana,lakini vipi kuhusu mtuhumiwa wetu,tunapaswa kuondoka na Donald Mbeto kutoka mahali hapa,lazima akaonje joto la jiwe,asife kirahisi tu,anapaswa kufa kama alivyotesa raia wasio na hatia…”,Kendrick aliongea.
“,Nimewapata hilo niachieni mimi,pandeni ndani ya ndege,lakini msifanye chochote mpaka niwajulishe……”,Catherine alizungumza,kamanda Kendrick aliangalia kushoto na kulia,hakuna aliyewaona,akaingia ndani ya ndege ya kivita,kamanda Philipo akafuatia,wakasubili amri kutoka kwa Catherine,Catherine alipita chini ya magari,hakuonekana,jeshi la magaidi liliendelea kusogea mahali mlipuko ulikuwa umesikika,akarusha mabomu mawili,katikati ya miguu ya magaidi,kisha akarudi ,akipenyeza chini ya uvungu wa mataili ya gari pamoja na ndege.
“,Ukisikia mlipuko,washeni ndege,watakua bize na kujihami,nyie mtatumia upenyo huo kuwasogelea na kuwashambulia,hakikisheni mtu yoyote hapati upenyo kusogelea eneo hili,akaingia ndani ya vifaru,mtakua mmekwisha…”,Catherine aliongea.
“,Puuuu,puuu,puuuu,”mlipuko ukasikika,magaidi wengi wakafyekelewa mbali,bilionea Paresh Kumar alikufa palepale,magaidi wengine walizitupa silaha zao,wakalala chini kuepuka mlipuko huu,Kendrick akatumia mwanya huu,akawasha helikopta kubwa ya kivita,kamanda Philipo akachomoa makombola,yakatokeza pembe zote,mbele makombola mawili,nyuma makombola mawili,wakaanza kupaa hewani,ndani ya ndege hii kubwa yenye vioo kwa juu,kiasi kwamba anga lote lilionekana,ndege ya magaidi ikitaka kujigeuza umbo la meli,vioo ambavyo vimeifunika ndege vinajifunua,mabawa yanarudi kwa ndani.
Kendrick alipaa,hakutaka kupaa juu zaidi,angegonga vioo ,upepo ukaingia ndani ya ndege kubwa ya magaidi,akahatarisha maisha yao,alipofika usawa wa kufanya mashambulizi,futi kumi kwenda juu,akaisogeza helikopta eneo la magaidi,akafyatua makombola mawili,yakatekeza kundi lotee.
“,Bosiiiiiii ,bosiiii!”,Donald Mbeto alishuhudia kitendo cha bosi wake kushambuliwa,akakimbia mpaka eneo la tukio,kila kiungo cha bosi wake kilikuwa mahali pake,akakasirika.
Catherine alitabasamu,ushindi ulikuwa umekalibia,akaanza kusogea taratibu,kwa mara ya kwanza alikutana uso kwa uso na Donald Mbeto.Catherine alitazama juu,Kendrick alikuwa ameelekeza makombola kwa Donald Mbeto,alitaka kummalizia palepale.
“,Hapana,usimuue,nataka nimvunje miguu,mimi mwenyewe!”,Catherine aliongea kwa sauti,akawakataza wasimuue,kisha akakunja ngumi,Donald Mbeto akazifunga rasta zake nyeupe,akajikuna kidevu chake,akakunja ngumi.
11:40am
Donald Mbeto alimtazama Catherine juu mpaka chini,akamtazama usoni, kisha akaitazama miguu yake,alikuwa anafikilia mbinu ya kumshambulia, aivunje miguu yake. Donald Mbeto aliluka mateke mawili hewani, Catherine akazuia mateke yote kwa mikono yake,hajakaa sawa alipigwa ngwala akadondoka chini, Donald Mbeto akaluka hewani, akarudi chini kwa kasi akiwa amekunja kifuti cha mkono wake, akafika juu ya mguu wa Catherine, akaupiga na kifuti.
“,Kachwaaaaa!!, “mguu wa Catherine uliitikia.
“,Yalaa…aa! “,Catherine alipiga kelele, akajigeuza upande wa pili, akampiga Donald Mbeto na teke usoni, akadondokea upande wa pili, damu zikimvuja mapuani.
“,Shiiit! amemuumiza, atamuua, tushuke chini
……”,Kendrick akiwa juu ya helikopta, aliona kila kitu kilichokuwa kinaendelea,hisia za mapenzi zikamsumbua, alikuwa na hofu ya kumpoteza Catherine.
“,Usiwe na hofu, naona sasa mapenzi yameshakuingia, umeshapenda tayali ,usjali Catherine ni komandoo……”,kamanda Philipo alimuondoa shaka Kendrick.
“,Hapana, mwanamke ni mwanamke siku zote, isitoshe mtu anayepambana naye ni hatari sana,ameshamtemgua mguu ……”,kamanda Kendrick aliongea.
Catherine alijaribu kusimama,alishindwa,mguu wake wa kushoto ulikuwa na maumivu makali, aliteguliwa, alimanusura avunjwe mguu, akajaribu kusimama tena, akadondoka chini, mguu wake ulimuuma sana, alikuwa hananguvu kabisa.
“,Lazima ufe,huwezi kutoka salama, huwezi kumuuwa bosi wangu halafu uwe salama,mimi ndiyo jini mweupe,shujaa wa dunia”Donald Mbeto aliongea, akazishika rasta zake nyeup, akazifunga vizuri, akajikuna kidevu chake, akaanza kumsogelea Catherine aweze kummalizia.
Catherine alimuona Donald Mbeto akimsogelea, alimuangalia usoni, akayatazama macho yake kwa makini, akazitambua hisia zake, alikuwa anakuja kumshambulia, Catherine akajiandaa, japo alishindwa kusimama, lakini alijiamini, Donald Mbeto alipofika mahali Catherine alipokuwa, aliluka tena juu, akashuka chini kwa kasi na pigo lile lile, alitaka kuvunja mguu mwingine wa Catherine, Catherine alinyanyuka juu kama mzuka, akaluka hewani,mkononi alishika kisu chake, wote wakakutana hewani, alilipangua teke la Donald Mbeto akamsindikiza na visu viwili, alichoma visu viwili Donald Mbeto miguu yote ,kulia na kushoto,haikutosha, akampiga na teke, akadondokea mita kadhaa kama mzigo. Donald Mbeto akalia kwa uchungu,hakuwa na uwezo wa kusimama tena. “,Haya sasa, wote viwete! “,Catherine aliongea,akatazama helikopta juu yake, akawanyoshea mkono Kendrick na Philipo, wakaishusha helikopta,Kendrick akachomoa pingu, akamfunga Donald Mbeto, wakamnyenyua na kumuweka kwenye helikopta,Kendrick akaipaisha juu, ikapasua vioo vya ndege kubwa ya magaidi hawa,ikatokomea hewani.
“,Bado kuna magaidi, wamejificha, lipua ndege yoteee! “,Kendrick aliongea,kamanda Philipo akafanya kama alivyoelekezwa, akaruhusu makombola mawili, yakaipiga ndege, ikapepesuka, ikapoteza mwelekeo, akaipiga tena na makombola mengine mawili, ikalipuka na kuungua moto, Kendrick akageuza helikopta, akaanza kurudi kusini,kisha akakunja tena kona, akaelekea mashariki, akaanza kuishusha chini helikopta, futi arobaini mpaka therathini,akaanza kurudi Dar es salaam,Tanzania
“,Tujikomboe sisi wenyewe, bila hivyo tutakufa, kifo chetu ni kunyongwa, hakuna hukumu nyingine tofauti na hiyo ambayo tunaweza kupewa …”,chuma cha pua aliongea.
“,Kweli kabisa, lakini gereza hili lina ulinzi mkali, hatuwezi kutoka kirahisi kama unavyofikilia ……”,gaidi D47 namba sitini aliongea.
“,Ngoja niwaoneshe,askari atakaye tuletea chakula, akitufungua tu mahali hapa,mimi naan.……”,chuma cha pua kabla hajamaliza kuongea,Catherine, Kendrick pamoja na Philipo walitokeza, Kendrick alikuwa anamburuta mtu hatari sana ambaye hawakutegemea kama angeweza kukamatwa.
“,Mliyekuwa mnategemea atakuja kuwakomboa huyu hapa, huu ndiyo mwisho wenu, chombo chenu tumekilipua,hakuna aliyetoka mzima zaidi ya huyu mtuhumiwa wetu, tunataka afe mbele ya raia ……”,Catherine aliongea, akiwa anatembea kwa kuchechemea, akamnyenyua Donald Mbeto, akamkalisha kwenye kiti cha mateso kilichokuwa wazi, wakamfunga mikono na miguu.
“,Hapa hamuwezi kutoroka kamwe! hata mfanye nini hamtaweza, subilini hukumu yenu ya kunyongwa hapohapo kwenye viti vyenu ……”,Kendrick aliongea,akamshika mkono Catherine, akambusu, akamsaidia kutoka ndani ya chumba cha mateso, walikuwa wamekamilisha kazi, kama ilivyotakiwa. Taarifa za kukamatwa kwa Donald Mbeto zikasambaa duniani kote,waandishi wa habari kutoka mataifa mbalimbali duniani walifika nchini Tanzania, walitaka kufanya mahojiano na Donald Mbeto, wampige picha na kuitambua sura yake,hawakutaka kupitwa na taarifa za mtu huyu,lakini ulinzi ulikuwa mkali,wengi walizuiliwa,vyombo vya habari kutoka Tanzania vikaifanya kazi hiyo.Huku hukumu ya magaidi hawa watano ikisubiliwa kwa hamu na watu wote duniani.
…MWISHO…………………
The super three soldiers walizawadiwa tuzo za heshima, kutoka mataifa yote ambayo Donald Mbeto maarufu kama jini mweupe alitekeleza mauaji ya sumu, Kendrick na Catherine wakafunga ndoa, huku kamanda philipo akiwa Mc wa ndoa yao.…
Lango kuu la gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam lilifunguliwa na mtu mmoja mrefu alitoka nje ya lango lile kwa hatua za kujiamini na kusimama kiasi cha hatua zipatazo tano nje gereza lile. Nyuma yake, lile lango lilifungwa, na hivyo kufungia historia ya miaka miwili ya taabu, mateso, kazi ngumu na uchungu mwingi ambayo mtu huyu alipitia alipokuwa upande wa pili wa lango lile. Ilikuwa ni saa tatu na robo asubuhi siku ya jumatano.
Jamaa aliangaza kulia na kushoto pale nje huku akivuta pumzi ndefu zilizoingiza hewa nyingi mapafuni mwake, kisha akashusha pumzi zile zikiambatana na mguno wa faraja, iliyotokana na kuvuta hewa ile ya ulimwengu huru, akiwa mtu huru. Hili ni jambo alilokuwa akilisubiri kwa hamu katika muda wote ule aliokuwa akitumikia kile kifungo chake cha miaka miwili.
Pamoja na kimo chake kirefu, mtu huyu alikuwa na mwili ulioshiba pamoja na kuwa alikuwa kifungoni. Hii ni kutokana na mazoezi mazito aliyokuwa akijilazimisha kufanya akiwa kule gerezani kwa lengo maalum. Misuli yake ya mikono iliyojaa vizuri ilijidhihirisha wazi kwa kututumka na kufanya mikono ya fulana yake ya mikono mifupi ionekane kumbana. Vivyo hivyo, misuli yake ya mapaja ilionekana kututumka na kuifanya ile suruali yake ya jeans nayo ionekane kuwa inambana.
Bila kugeuka nyuma, jamaa alianza kutembea kwa hatua moja moja zilizokuwa zikivutwa bila ya haraka yoyote kuelekea barabara kuu iliyokuwa mbele yake, akiliacha lile jengo la gereza nyuma yake akiwa na azma ya kutorejea tena ndani ya kuta za jengo lile maishani mwake.Bora kufa, kuliko kurudi tena gerezani. Alishaazimia hivyo muda mrefu, na bado alibaki na azma hiyo.
Kwake yeye mji aliuona ukiwa umebadilika sana ndani ya miaka ile miwili, lakini hilo halikuwa na maana yoyote kwake, kwani alijua kitambo kuwa pindi atakapotoka gerezani angekuta mabadiliko mengi sana jijini. Alikuwa akitembea huku akijaribu kutazama mambo yote yaliyokuwa mbele yake kwa jicho la kudadisi. Aliona kuwa magari ya usafirishaji wa abiria yalikuwa yamechorwa mistari ya rangi, tofauti na hali aliyoiacha wakati anaingia gerezani. Kidogo hili lilimpa taabu, kwani alianza kujiuliza ni jinsi gani ataweza kujua ni rangi ipi ndio ilikuwa ikiwakilisha basi la kuelekea sehemu ambayo alikuwa ameazimia kwenda baada ya kutoka gerezani.
Aliweka sawa mkoba wake mdogo alioupitisha begani kwake na kuuacha ukining’inia mgongoni na kuzidi kuikurubia ile barabara ambayo juu yake, magari yalikuwa yakipita kwa kasi sana kiasi cha kumkosesha amani.
Jamaa alikuwa na sura ya kuvutia ambayo baada ya miaka miwili gerezani, ilikuwa imeingia ukomavu fulani ambao haukuwepo hapo kabla, na ambao kwa namna yake uliongezea mvuto kwenye sura ile.
Lakini wakati akitembea taratibu kwa mwendo wake wa hatua moja moja kukiendea kituo cha mabasi yaelekeayo katikati ya jiji kilichokuwa upande wa pili wa barabara, uso wake ule wenye mvuto ulionekana wazi kuwa ulikuwa una dhamira thabiti juu ya nini alikuwa anataka kufanya baada ya kutoka gerezani, kwani baada ya miaka miwili ya kupanga na kupangua akiwa kule gerezani, hakika alikuwa anajua ni nini haswa alichotakiwa kukifanya.
Kwenye kituo cha mabasi yaliyokuwa yakielekea maeneo ya Kariakoo na katikati ya jiji kilichokuwa upande wa pili wa ile barabara kuu, mmoja wa watu waliokuwa wakisubiri mabasi pale kituoni alikuwa akifuatilia kila hatua ya yule mtu mrefu aliyetoka kule gerezani, ambaye sasa alikuwa akisubiri nafasi muafaka ya kuvuka barabara ili naye aende pale kituoni.
Alikuwa ni mwanamke aliyejitanda khanga mwili mzima hadi kichwani, kama jinsi wanawake wengi wa pwani wapendavyo kujitanda, na usoni alikuwa amevaa miwani myeusi iliyoficha kabisa sura yake. Ingawa alionekana kuwa ni msafiri miongoni mwa wale wasafiri wengi waliokuwa wakisubiri daladala pale kituoni, ukweli ni kwamba mwanadada yule aliyejitanda khanga, alikuwa akimsubiri yule mtu mrefu aliyetoka gerezani asubuhi ile!
Jamaa alivuka barabara na alikuwa akikiendea kile kituo cha mabasi, wakati mlango wa mbele wa gari dogo aina ya Hyundai nyeupe yenye namba za serikali ulipofunguka na msichana mmoja mwenye kimo cha kawaida alipoteremka na kusimama nje ya lile gari huku mkono mmoja bado ukiwa umeshikilia mlango wa gari lake.
Huyu naye alikuwa amevaa miwani ya jua, ingawa yeye alikuwa amevaa gauni refu la kitambaa laini chenye maua madogo madogo lililokuwa na mpasuo mpana upande mmoja. Kichwani alikuwa amebana nywele zake ndefu zilizotiwa dawa za kulainisha na kupendezesha nywele katika ile staili ya Pony Tail , ambapo kile kimkia cha nywele kilichokuwa kikining’inia kisogoni mwake kilikuwa kimechomoza kutokea kwenye sehemu ya nyuma ya kofia aina ya kapelo aliyokuwa ameivaa. Aliweka mkono wale wa pili juu ya paa la gari na kumtazama yule jamaa akipita upande wa pili wa lile gari akielekea kule kituoni. “Roman!” Aliita.
Jamaa alisimama katikati ya hatua na kugeuka taratibu ule upande ilipotokea sauti iliyoita jina lake. Alimtazama yule dada mwenye kapelo na miwani ya jua huku akikunja uso kujaribu kumtambua. Yule dada aliendelea kumtazama bila ya kusema neno zaidi, akimpa muda yule mtu aliyemwita kwa jina la Roman amtambue.
Kule kituoni yule mwanamke aliyejitanda khanga naye alianza kupata waiswasi baada ya kuona yule jamaa aliyekuwa akimvizia akisimama na kumgeukia yule dada aliyetoka kwenye lile gari lenye namba za serikali. Ni nini tena pale?
Jamaa alimtazama kwa makini zaidi yule dada na alihisi kuwa alishapata kuiona ile sura wakati fulani huko nyuma, ingawa bado hakuweza kuioanisha sura ile na kumbukumbu zake za miaka miwili iliyopita.
“Miaka miwili ni mingi kiasi cha kukufanya unisahau Roman?” Hatimaye yule dada alimuuliza yule jamaa huku akitoa miwani usoni kwake, na hapo jamaa akaachia mdomo kwa mshangao.”Afande Fatma…?” Yule dada alirudisha tena miwani yake usoni. “Sasa nimekuwa Inspekta…Inspekta Fatma.”
Jamaa alikunja uso, safari hii ikiwa ni kwa kukereka, na kubetua midomo kwa namna ambayo ilionesha kuwa hakufurahishwa na hali ile.”Unataka nini Inspekta?” Roman aliuliza, huku akitilia mkazo wa kebehi lile neno “Inspekta.”
“We need to talk Roman…you and me! (Tunahitaji kuzungumza Roman…mimi na wewe!)” Inspekta Fatma alimwambia yule jamaa bila ya kujali kebehi na kukereka kwake kwa wazi. Roman alitikisa kichwa kwa masikitiko.
“Yaani siku yangu ya kwanza nikiwa mtu huru! Halafu mtu wa kwanza kukutana na kuongea naye ni askari! What’s this (Nini maana yake hii)?” Roman alisema kwa hasira.”We need to talk Roman, and we need to talk now!(Tunahitaji kuzungumza Roman, na tunahitaji kuzunguza wakati huu!)”
“About what (Kuhusu nini)? Nimetumikia kifungo changu, nimemaliza. Sasa mimi ni raia huru…” “Ingia kwenye gari Roman!” Inspekta Fatma alimkatisha. Na sauti yake ilikuwa imebeba mamlaka yote aliyokabidhiwa na jamhuri kama afisa wa jeshi la polisi mwenye jukumu juu ya usalama wa raia wote wa Tanzania.
Kule kituoni yule mwanamke aliyejitanda khanga alizidi kujichanganya katikati ya kundi la watu waliokuwepo pale kituoni huku akizidi kufuatilia kwa makini kila kilichokuwa kikiendelea kule kwenye lile gari dogo lenye namba za serikali. Na kwa kadiri ilivyokuwa, ni wazi kuwa kile kitendo cha yule mtu aliyeitwa Roman kusimama na kuongea na yule dada aliyetoka kwenye lile gari lenye namba za serikali kilimchanganya sana.
Ni nini kinaendelea pale? Roman alibetua mabega na kuuliza kwa kukereka kwa hali ya juu. “Ili iweje afande? Ni lazima niingie kwenye hilo g-” “Sio lazima. Lakini ni muhimu tuongee. Nataka kukupa lifti…” Mtu aliyeitwa Roman alimtazama yule askari wa kike kwa muda, na yule askari aliendelea kumtazama bila ya kutetereka. Kisha, bila ya kusema neno zaidi, Roman alipiga hatua moja kubwa na kufungua mlango wa upande wa abiria wa lile gari na kuingia. Inspekta Fatma aliingia nyuma ya usukani na kuliondoa lile gari kutoka eneo lile kwa ustadi mkubwa.
Huku kituoni, mwanamke aliyejitanda khanga alichanganyikiwa vibaya sana. Alilitazama lile gari likiondoka kutoka eneo lile kwa fadhaa iliyochanganyika na hasira.
***
“Unaelekea wapi?” Inspekta Fatma aliuliza huku akiwa amekaza macho yake barabarani. Roman alikuwa amegeuzia uso wake nje ya dirisha akiangalia mandhari ya jiji alilolikosa kwa muda wa miaka miwili. Hakufanya juhudi yoyote kuficha jinsi alivyokereka na hali ya kuwa na yule askari ndani ya lile gari. “Umesema unataka kuongea. Ongea nami nakusikiliza.
Unaweza kuzunguka jiji lote hili wakati tunaongea…sio lazima ujue niendako!” Alimjibu kwa hasira huku bado akitazama nje ya dirisha. “Nimesema tunahitaji kuongea…mimi na wewe. Hivyo natarajia na wewe uwe unaongea. Na ndio maana nimekuuliza swali ambalo naomba unijibu. Unaelekea wapi Roman?””Hiyo inakuhusu nini? Wewe si ndugu yangu, si jamaa yangu, na wala si mke wangu! Sasa sioni swala la mimi ninaelekea wapi linaingiaje kwako.
Mimi ni mtu huru bwana!” Roman alimjibu kwa jazba. Inspekta Fatma alimtupia jicho la pembeni halafu akabaki kimya kwa muda, akijishughulisha na kuendesha gari, ingawa uso wake ulionesha kuwa na mawazo mazito. Roman alifumbata mikono yake kifuani na kuendelea kutazama nje ya dirisha la lile gari. Safari iliendelea katika hali ile kwa muda mrefu, na katika muda ule walikuwa wameanza kuingia katikati ya jiji.
Walipita uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es Salaam, na mwendo mfupi baadaye, Inspekta Fatma alipunguza mwendo wa gari na kuingia kulia ambapo aliliegesha kwa ufundi mkubwa nje ya mgahawa maarufu wa Best Bite katika lile tawi lake lililopo barabara ya Nyerere, zamani Pugu Road. “Okay, Roman, nadhani hapa tunaweza kuongea kwa kituo zaidi.”
Inspekta Fatma alimwambia yule mtu mrefu mwenye mwili ulioshiba huku akiteremka kutoka kwenye gari. Bila ya kuongea neno, lakini akionesha wazi kuwa alikuwa amechukia, Roman aliteremka na mkoba wake kutoka kwenye lile gari na kumfuata yule afisa wa polisi mrembo ndani ya ule mgahawa mzuri. Baada ya kuagiza soda aina ya Coca Cola kwa ajili yake na bilauri ya juisi ya nanasi kwa ajili ya Roman kwa mujibu wa utashi wake, Inspekta Fatma alianzisha tena maongezi. “Roman, najua kuwa utakuwa unanichukia sana hivi sasa kwa kufanya haya niyafanyayo, lakini naomba uelewe kuwa hii ni kwa faida yako na si vinginevyo…”
Roman alimtazama yule binti bila ya kusema neno, na Fatma aliendelea.”…najua kuwa baada ya kumaliza kifungo chako utakuwa tayari una mipango uliyojipangia katika maisha yako mapya. Basi na iwe ya kheri Roman, vinginevyo itakuwa mbaya sana kwako.”
Roman alizidi kumtazama tu yule dada bila ya kusema neno. “Mimi nimeamua kuja kukusubiri pale Ukonga leo hii kwa sababu najali maisha yako, na kwa jinsi ninavyohisi, naona una hatari ya kurudi tena gerezani kama hutaamua kusahau yaliyopita na kutazama mbele.”
Inspekta Fatma alizidi kumueleza kwa upole na msisitizo wa hali ya juu. Bado Roman alikuwa akimtazama kwa macho makavu bila ya kusema neno lolote wala kupitisha hisia yoyote usoni mwake ambayo ingeweza kusomwa na macho makini ya yule askari wa kike. Lakini Inspekta Fatma alikuwa anajua ni nini alichokuwa anataka Roman aelewe, hivyo hali ile haikumkatisha tamaa hata kidogo.
“Sahau yaliyopita Roman, na uanze maisha mapya sasa. Kama utahitaji msaada mimi niko tayari kukusaidia kwa kadiri nitakavyoweza, lakini achana kabisa na mawazo uliyonayo Roman, hayatakusaidia kitu…” Hapo Roman hakuweza kuendelea kubaki kimya.
“Mnhu! Yaani we’ unataka kuniambia kuwa unajua mi’ n’na mawazo gani? Achana na mimi kabisa afande!”
“Sahau yaliyopita Roman, na uanze maisha mapya sasa. Kama utahitaji msaada mimi niko tayari kukusaidia kwa kadiri nitakavyoweza, lakini achana kabisa na mawazo uliyonayo Roman, hayatakusaidia kitu…” Hapo Roman hakuweza kuendelea kubaki kimya. “Mnhu! Yaani we’ unataka kuniambia kuwa unajua mi’ n’na mawazo gani? Achana na mimi kabisa afande!” Inspekta Fatma alitikisa kichwa taratibu. “Huwezi kunidanganya Roman. Nimekuwa nikikutazama tangu unasubiri kuvuka ile barabara pale nje ya gereza hadi ulipokuwa ukipita mbele ya gari langu pale jirani na kituo cha basi. Katika sura yako kulikuwa kuna kusudio la wazi kabisa ambalo lilithibitisha hofu yangu juu ya mambo utakayotaka kuyafanya muda huu ukiwa umemaliza kifungo chako. Achana na mawazo hayo kabisa Roman…” “Hujui usemalo Fatma…na kama huna la zaidi naomba niende zangu!” Roman alimjibu kwa hasira. Lakini Inspekta Fatma alikuwa na msimamo. “Mimi najua, Roman. Na usidhani utanilaghai na huo ukimya wako au utanipoteza lengo kwa hayo maneno yako ya hasira. Najua! Na ndio maana nimekuja kukuasa mapema Roman. Acha yaliyopita yawe yamepita. Angalia mbele…!” Roman alitikisa kichwa kwa kustaajabia upotofu wa mawazo ya yule askari. Lakini Fatma hakuwa mjinga. “I am telling you Roman, let it go!(Nakuambia Roman, achana nayo kabisa!)” “Let what go, Fatma?(Niachane na nini, Fatma?)” Roman alimuuliza kwa kukereka huku akimkunjia uso. Fatma alitomasa hewa mbele ya uso wa Roman kwa kidole chake cha shahada kutilia msisitizo maneno yake. “You know what!(Unajua!). Mi’ najua miaka miwili uliyokaa gerezani ulikuwa ukisubiri tu siku hii ya leo ifike…na sasa imefika, unataka kutimiza yote yale uliyodhamiria wakati ukiwa kifungoni. Niamini mimi Roman, asilimia tisini ya mambo watu wanayodhamiria kufanya baada ya kutoka huko ulikotoka wewe leo hii huwa ni juu ya uovu, udhalimu zaidi na visasi! You can’t be any different! (Wewe huwezi kuwa tofauti na hao)” Roman aliguna na kutikisa kichwa. “Kwa hiyo unataka kuniambia kuwa jela haisaidii kurekebisha tabia? Sasa kwa nini basi huwa mnatupeleka huko?” Alimuuliza kwa kejeli ya wazi. Sasa ilikuwa zamu ya Inspekta Fatma kutikisa kichwa. “You are a good guy Roman…(U-mtu mzuri Roman…)” “Good guys do not get sent to prison, do they? (Watu wazuri huwa hawapelekwi gerezani, au sivyo?)” Roman alidakia kwa jazba na huku akipiga meza waliyokuwa wamekalia kwa kiganja cha mkono wake. Baadhi ya watu waliokuwamo mle ndani waliwageukia na kuwakodolea macho na mhudumu mmoja alisogea na kuuliza iwapo kulikuwa kuna tatizo lolote. Ilibidi Inspekta Fatma afanye kazi ya ziada kumhakikishia kuwa hakukuwa na tatizo lolote wakati Roman akibaki akiwa amekunja uso kwa ghadhabu. Inspekta Fatma alimtazama kwa upole uliochanganyika na simanzi yule jamaa. “You used to be a good guy Roman!(Kabla ya kupelekwa gerezani ulikuwa mtu mzuri Roman!). Nataka uendelee kuwa hivyo sasa baada ya kutoka gerezani. Usiiache hii hali…haya mambo yaliyotokea, yakuharibu. Let it go!(Achana nayo!)” Inspekta Fatma alimjibu kwa hisia kali. Kidogo macho yalimtembea Roman na alitazama pembeni. Hakutaka kabisa kumtazama yule dada usoni. “Lakini bado hiyo haikutosha kunifanya nisipelekwe gerezani Inspekta!” Roman alisema kwa uchungu. “Ndio, lakini…You don’t belong there Roman! (gerezani si mahala pako Roman!) Ndio maana sitaki ufanye kosa litakalosababisha urudi tena gerezani, kwani ikitokea hivyo Roman, ujue huko ndiko kutakuwa makazi yako for good (milele)! Yaani hukutakiwa kabisa kwenda huko…” Roman alitikisa kichwa taratibu na kumuuliza. “Una maana sheria ilikosea iliponipeleka gerezani?” “No! Lakini mazingira yaliiwezesha sheria ikupeleke gerezani. Ndio maana nakuasa usifanye jambo litakalokufanya uje ujute maisha yako yote Roman!” “Aanhaa! Kwa hiyo na wewe unakubali kuwa hii tunayoiita sheria ina upungufu? Kwamba inaweza ikatengenezewa mazingira fulani, kisha ikatumika kuwaadhibu wasio na kosa na kuweka huru waliokosa?” Inspekta Fatma alipepesa macho kidogo. Ilikuwa ni hoja ngumu kwake kuiafiki. “Aa…sometimes, but…(mara nyingine, lakini…) “Kwa hiyo unakubaliana na mimi?” Inspekta Fatma alimtazama Roman kwa macho makali. “This does not apply to your case Roman, and you know it!(Hali hiyo haipo kwenye swala lako Roman, nawe walijua hilo!)” Roman alibetua mabega. “Sawa. So what do you want from me now?(Kwa hiyo sasa unataka nini kutoka kwangu?). Inspekta Fatma alijibu moja kwa moja bila kusita. “Achana na yote yaliyopita Roman. Just Forget it! (Yaani sahau tu!)” Roman hakumjibu na badala yake alitazama pembeni. Inspekta Fatma alimtazama kwa makini, na kwa muda mrefu. “Hunipi ushirikiano mzuri Roman.” Hatimaye alimwambia. “Kwa sababu sitaki kushirikiana nawe afande!” Alimjibu huku akiendelea kutazama pembeni, kisha akaongezea; “…na nisingependa kuendelea kukuona maishani mwangu, if you don’t mind (kama hutajali)” Jibu hili lilionekana wazi kuwa lilimuumiza sana Inspekta Fatma. “Naamini kama utafuata ushauri wangu hutaniona tena maishani mwako Roman. Lakini ukipuuzia na kufuata mambo ambayo nadhani ndio unataka kuyafanya…” Afande Fatma alimjibu kwa upole, huku akiiachia ile sentesi yake ielee hewani bila kuimalizia. Roman alisoma kitisho kilichokuwa ndani ya kauli ile, na alimkazia macho ghafla. “Nikipuuzia…then what?(kisha nini?) Alimuuliza kwa jazba huku akimtolea macho ya ghadhabu ambayo yangeweza kumtisha mtu mwingine yeyote, lakini sio Inspekta Fatma. Inspekta Fatma hakufanya haraka kumjibu, badala yake alimtazama kwa muda, kisha huku bado akimtazama moja kwa moja machoni, alimjibu kwa sauti ya upole lakini iliyojaa yale mamlaka yake yote iliyokabidhiwa na jamhuri. “Basi nasikitika kuwa itakubidi uwe unaendelea kuniona tu kwa muda wote utakaohitajika ili kukutupa tena jela rafiki yangu!” Jibu hili lilikuwa nje kabisa ya matarajio ya Roman na alifinya macho yake kumtazama vizuri yule askari wa kike mwenye msimamo. Walitazamana kwa muda na katika muda ule hakuna mmoja kati yao aliyekubali kushusha chini macho yake. “Unanitishia afande?” Hatimaye Roman alimuuliza kwa sauti kavu huku akiendelea kumtazama kwa makini yule askari. Badala ya kumjibu, Inspekta Fatma alimuita mhudumu kwa ishara ya vidole vyake, na kulipia vile vinywaji walivyoagiza. Alibandika miwani yake ya jua usoni na kuinuka kutoka kwenye kiti alichokuwa amekalia. “Good Luck in your new life Roman!(Kila la kheri katika maisha yako mapya Roman!)” Aligeuka na kuondoka eneo lile kwa mwendo wa madaha ya kike lakini ukionesha kuwa alikuwa akijiamini na asiyetishika na lolote hapa duniani. Kwa muda mrefu Roman alibaki akiwa amekaa pale kwenye ule mgahawa nadhifu huku uso wake ukionekana kuwa na mawazo mazito. Hatimaye aliinuka na kutoka nje ya mgahawa ule kuendelea na safari yake aliyokuwa ameidhamiria wakati alipotoka kule gerezani, akiiacha ile bilauri ya juisi aliyonunuliwa na Inspekta Fatma pale juu ya meza ikiwa haijaguswa hata kidogo. ****** Kate aliingia ndani ya sebule ghali na kuubamiza mlango nyuma yake kwa ghadhabu. Alirusha funguo za gari alilokuwa akiendesha aina ya Toyota Prado Metallic, Short Chasis, juu ya meza ndogo na nzuri sana iliyokuwa ndani ya ile sebule iliyojitosheleza kwa kila kitu. Alirusha miguu yake mbele mmoja baada ya mwingine huku akisonya na kuviacha viatu vyake vizuri vya kuchomeka vikiruka kila kimoja upande wake na kubaki vikigaa gaa juu ya zulia zito lililotandikwa pale sebuleni. Alisonya tena na kutupa pembeni zile khanga aliyokuwa amejitanda kichwani na sehemu ya juu ya kiwiliwili chake, na hivyo kuachia nywele zake nzuri zilizokuwa zimewekwa katika ule mtindo wa ‘utajiju’, na kudhihirisha fulana nyeupe kubwa iliyoonesha mwinuko mdogo wa matiti yake mazuri ambayo yalionekana wazi kuwa hayakuwa yamebanwa na sidiria na wala hayakuonesha kuwa yalikuwa yanahitaji kubanwa na sidiria yoyote. Alitoa na ile khanga nyingine aliyokuwa amejitanda kiunoni na kuitupia juu ya sofa jingine lililokuwa karibu yake na kudhihirisha suruali ya jeans iliyoukamata mwili wake kwa namna ya kutamanisha haswa, ikionyesha jinsi makalio yake yalivyochongwa kwa mvuto wa kipekee. Aliinua uso wake na kutoa ile miwani yake ya jua aliyokuwa ameivaa na kuiweka taratibu juu ya meza ya Runinga kubwa aina ya Sony Plasma. Aliliendea jokofu lililokuwa kwenye kona moja ya sebule ile na kulifungua huku akiinama na kuchungulia ndani ya jokofu lile ambalo nalo lilikuwa la bei mbaya na ambalo daima lilikuwa halikauki mahitaji muhimu ndani yake. Kwenye sofa lililokuwa kwenye kona moja ya sebule ile, mtu mmoja wa makamu aliyepata umri wa miaka ipatayo arobaini na minane hivi ambaye muda wote huo alikuwa akitazama nyendo zote za yule binti kwa utulivu mkubwa tangu aingie mle ndani, aliitazama ile sehemu ya nyuma ya yule binti mrembo akiwa ameinama namna ile kwa macho yaliyoonesha kuwa yalikuwa yanavutiwa na yalichokuwa yakikiona. Kate aliinuka akiwa na juisi ya boksi aina ya Ceres mkononi na kugeuka huku akiinua lile boksi ambalo lilikuwa limeshafunguliwa na kulipeleka kinywani. Wakati huo huo yule mwanaume aliyekuwa akimtazama kwa utulivu tangu aingie mle ndani alionesha umakini na kumtupia swali. “Kwani imekuwaje huko…?” Alikuwa ni mtu aliyevaa mavazi ghali na shingoni alikuwa amening’iniza cheni moja ya dhahabu kinyume na jinsi ambavyo wengi wangetarajia kutoka kwa mtu wa umri wake. Alionekana wazi kuwa ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa pesa na yule binti angeweza kabisa kuwa mwanawe wa kumzaa. Kate alibugia ile juisi kwa mfululizo huku akiwa ameinua juu kichwa chake ili ile juisi ishuke vizuri kooni mwake huku akimtupia jicho la pembeni yule mwanaume mtu mzima mwenye mwili mnene wa wastani na mvi chache kila upande wa kichwa chake. Alishusha lile boksi la juisi kutoka kinywani mwake. “Sikuweza kuongea naye chochote bwana!” (Akasonya). Kisha aliinua tena lile boksi la juisi na kupiga funda jingine dogo la kile kinywaji alichokipenda sana huku akiliendea sofa lililokuwa karibu yake kwa mwendo wa pozi. “Lakini umemuona? Ni yeye hasa? Ametoka leo?” Yule mzee aliuliza kwa bashasha. Kate aliafiki kwa kichwa kabla ya kumthibitishia kwa maneno. “Yep! Ndiye haswa!” Jibu hili lilionesha kumfurahisha yule bwana, lakini alitaka kujua vije amuone mtu aliyemkusudia halafu asiongee naye. “Ah!(Aliguna) Kwa taarifa yako sio mimi peke yangu niliyekuwa nikimsubiri Roman pale nje ya gereza leo hii…” Kate alimjibu kwa kushutumu huku akiwa amembetulia midomo na yule bwana alionekana kushitushwa na habari ile huku akijisogeza mbele kwenye lile kochi alilokuwa amekalia kwa kiherehere. “Eti Whaat?” Aliuliza kwa kutoamini. “Kabisaaa!” Kate alimjibu na kuendelea kumuelezea mambo yote jinsi yalivyotokea hadi pale yule mtu aliyeitwa Roman alipoondoka na lile gari lenye namba za serikali. Yule bwana alibaki mdomo wazi huku akiwa amekunja uso wake katika jitihada ya kujaribu kuelewa undani wa maelezo ya Kate. “Yaani yule mwanamke ameniboa! Laiti angejua kuwa kuna wanawake wanaoendesha gari za bei mbaya kuliko kile kimkebe chake cha serikali wala asingejitia kumchukua yule jamaa pale. Yaani nimepoteza muda wangu bure…!” Kate aliponda kwa hasira huku akiwa amekunja uso. Lakini yule mwenzake alikuwa na wasiwasi na mambo mengine kabisa kutoka katika yale maelezo yake “Umesema Roman amechukuliwa na gari yenye namba za serikali…?” Yule mzee aliuliza tena, na kwa mara nyingine Kate alimthibitishia kuwa hivyo ndivyo. Jamaa aliguna na kutikisa kichwa. “Sasa hii itakuwa nini…?” Aliuliza kwa sauti ya chini, ni kama alikuwa anajisemea mwenyewe tu. “Sa’ mi’ n’tajuaje, Master D? Labda yule ni demu wake….” Kate alimjibu huku akijilaza kwenye lile sofa alilokuwa amekalia. Yule mtu alimtupia jicho la pembeni kisha akaendelea kutazama ukutani alipokuwa akitazama hapo awali. “Hapana, Kate. Demu wake aje na gari la serikali? Sivyo. Hii ni issue kubwa kuliko unavyodhani…” “Aaah, kwani si kuna mademu wengi tu humu mjini wanaofanya kazi serikalini na kupewa magari ya kutembelea? Kwa nini asiwe demu wake? Jamaa anaonekana handsome kwa kiasi chake, ingawa nilimuona kwa mbali…” Kate alimbishia. Yule bwana aliinuka na kwenda kusimama nyuma ya dirisha na kutazama nje ya sebule ile. “Hapana. Nadhani hao ni askari…itabidi kuwa makini sana katika hili jambo.” Kate aliinua macho na kumtazama yule bwana mtu mzima kwa muda, lakini hakusema kitu zaidi. Aliamua kuziweka safi kucha zake kwa kuzichokoa-chokoa kwa kijiti cha kuchokolea meno alichokiokota sehemu fulani ndani ya sebule ile. Muda mrefu ulipita bila yeyote kati yao kusema lolote, yule mtu mzima akiwa kwenye dimbwi la mawazo, wakati yule mrembo mwenye deko aliyeitwa Kate akiendelea kucheza na kucha zake. “Sasa tutampataje tena huyu mtu…” Yule jamaa wa makamu aliyeitwa Dan alijisemea mwenyewe. Dan Dihenga ndilo jina lake halisi, ingawa marafiki zake wa karibu walizoea kumkatisha na kumuita Master D. Kate alimtazama yule bwana kwa muda, kisha akamjibu huku akiendelea kucheza na kucha zake. “Mi’ kazi yangu nilishaifanya ila nd’o hivyo imeingiliwa na huyo mwanamke. We’ ndiye unayejua…toa maelekezo, mi’ n’tafuata.” Sasa ilikuwa zamu ya Master D kumtazama yule binti mrembo aliyekuwa akiendelea kuchezea kucha zake, ila sasa alikuwa ameziingilia za miguuni. Muda mrefu ulipita bila yeyote kati yao kusema neno, hatimaye Master D alirudi kwenye sofa alilokuwa amekalia hapo mwanzo na kukunja nne. “Nadhani sasa kuna sehemu moja tu ambayo tunaweza kubahatisha kumpata. Na nadhani itatubidi tuelekee huko haraka.” *** Sasa ilikuwa zamu ya Master D kumtazama yule binti mrembo aliyekuwa akiendelea kuchezea kucha zake, ila sasa alikuwa ameziingilia za miguuni. Muda mrefu ulipita bila yeyote kati yao kusema neno, hatimaye Master D alirudi kwenye sofa alilokuwa amekalia hapo mwanzo na kukunja nne. “Nadhani sasa kuna sehemu moja tu ambayo tunaweza kubahatisha kumpata. Na nadhani itatubidi tuelekee huko haraka.” *** Roman aliusogelea ule mwinuko mdogo wa udongo kwa hatua za pole pole mno, na kadiri alivyozidi kuusogelea ndivyo miguu ilivyozidi kumuwia mizito, na moyo ulivyozidi kumuuma. Ingawa alijua fika tangu alipotoka gerezani asubuhi ile kuwa mahala pale ndipo alipokuwa amedhamiria kuja kabla ya kwenda mahala pengine popote, lakini baada ya kufika alitamani kuwa asingekuja kabisa. Lakini isingewezekana kuwa vinginevyo. Kwa vyovyote ilimbidi afike mahala pale. Na kama si yule askari wa kike kuingilia utaratibu wake, muda huu angekuwa ameshahudhuria eneo hili na kuwa mahala pengine kabisa. Alisimama mbele ya ule mwinuko na kumbukumbu ya mara ya mwisho aliposimama mbele ya sehemu hii kabla haijawa na mwinuko kama ilivyo sasa ilimrudia na hapo alitoa sauti ya uchungu na macho yakamchonyota kwa machozi huku donge kubwa likamkaba kooni. Wakati aliposimama mbele ya sehemu hii kwa mara ya mwisho palikuwa na shimo badala ya mwinuko… Roman alipiga goti moja mbele ya ule mwinuko uliokuwa mithili ya tuta na kuinamisha uso wake kwa uchungu, paji la uso wake likiwa limelalia juu ya mkono wake uliolazwa juu ya goti lake. Machozi yalimbubujika na uchungu mwingi uliutawala moyo wake. Alijaribu kumuomba Mungu lakini hakuna neno takatifu hata moja lililomjia akilini mwake wakati ule. Kichwa kilimrindima kwa ghadhabu na moyo ulimtetema kwa uchungu. Aliinua uso wake na kuuangalia msalaba uliochomekwa mbele ya lile kaburi, na moyo wake uliingia mlipuko mpya wa simanzi iliyochanganyika na uchungu pale aliposoma jina lililoandikwa kwenye ule msalaba.
Rachel Koga.
Ilimuwia vigumu kuamini kuwa alikuwa akilisoma jina lile kwenye msalaba…hakika hakuwa ametegemea kabisa kitu kama hicho maishani mwake. Chini ya jina lile la marehemu aliyelala chini ya ule mwinuko wa udongo kulikuwa kuna tarehe yake ya kuzaliwa na ile aliyoaga dunia, tarehe ya kuaga kwake dunia ikiwa ni miaka miwili iliyopita. Kwa mujibu wa zile tarehe zilizoandikwa kwenye msalaba ule, ilionesha kuwa yule marehemu aliyekuwa akiitwa Rachel, aliiaga dunia hii akiwa na umri wa miaka kumi na tisa. Miaka kumi na tisa tu! Roman alilia! Alilia akiwa amepiga goti pale mbele ya lile kaburi bila ya kujizuia. Alilia kwa uchungu na hasira na majonzi. Hatimaye alipata maneno ya kuongea na Mungu wake akiwa pale mbele ya lile kaburi, hivyo huku machozi yakimbubujika kwa wingi, Roman aliinua uso wake na kutazama mbinguni na maneno yakamtoka kinywani mwake huku bado kilio kikiwa kimemkabili. “Mungu wangu! Natumai utanisamehe kwa nitakalolifanya. Ni wewe pekee ndiye mwenye uwezo wa kusamehe hata wale waliokukosea kwa namna kubwa kabisa…lakini mimi ni mwanadamu tu Mungu wangu, na ni kiumbe dhaifu sana. Sina uwezo wa kusamehe kama ulio nao wewe…na sina namna ya kutofanya makosa kwani hiyo ni ada yangu kama mja wako. Sina ninalotumainia isipokuwa msamaha wako, kwa hiyo naomba msamaha kabisa mola wangu kwa sababu jambo nililodhamiria kulifanya kwa hakika linahitaji msamaha wako…” Hakuweza kuendelea. Aliinamisha kichwa kwa simanzi huku machozi yakimtiririka kwa wingi na sauti ndogo za uchungu zikimtoka ilhali mabega yakimpanda na kumshuka kwa kila kwikwi ya kilio iliyomtoka. Kwa hakika alikuwa ni mtu mwenye uchungu wa hali ya juu. Alilia mpaka akaishiwa machozi, ndipo alipoinuka kutoka pale alipokuwa amepiga goti na kuanza kujishughulisha na kuling’olea majani lile kaburi na kuuweka sawa ule msalaba ambao kidogo ulilalia upande mmoja kutokana na kumong’onyoka kwa udongo upande mmoja wa lile kaburi. Alijazia udongo sehemu zilizokuwa zimemong’onyoka kwa mikono yake bila kujali kujichafua. Alipomaliza alijipangusia mikono yake kwenye suruali yake ya jeans na kurudi nyuma hatua chache na kutazama kazi yake. Ilimridhisha. Alilitazama lile kaburi kwa muda mrefu, kisha aligeuka na kuondoka eneo lile la makaburi kwa unyonge mkubwa. Bila ya yeye kujua, watu wawilli waliokuwa ndani ya gari lililokuwa limeegeshwa hatua kadhaa kutoka kwenye yale makaburi ambayo hayakuwa yamejengewa uzio, walikuwa wakishuhudia mambo yote aliyokuwa akiyafanya pale kaburini kwa utulivu mkubwa. Alipotoka na kuanza kuelekea kituo cha basi kilichokuwa karibu kabisa na makaburi yale, alipita karibu na lile gari bila hata ya kuliangalia. Muda huo Kate alianza kufungua mlango ili amfuate, lakini Master D alimzuia huku akiendelea kumtazama yule mtu mwenye majonzi akijikongoja kutoka eneo lile. Kate alimgeukia Master D kwa mshangao huku akitoa sauti ya kukereka na kumuuliza kulikoni anamzuia asimwendee yule mtu ambaye walikuwa wanamhitaji sana na hawajui kuwa wakimkosa wakati ule wangempata wapi tena. “Huu sio muda muafaka Kate…” Dan alimjibu kwa sauti ya upole huku uso wake ukionesha mawazo mazito wakati akimtazama yule mtu aliyetoka gerezani asubuhi ile. “Sasa tutampata vipi tena Master D?” Kate aliuliza wakati akimshuhudia Roman akipanda daladala mbele yao. Bila ya kujibu, Dan aliingiza ile Prado Short Chasis barabarani na kuanza kulifuata lile daladala aina ya kipanya.Kazi yako ni kuangalia Roman anateremka kituo gani baby…mengine niachie mimi!” Alimwambia yule binti. Badala ya kumjibu Kate alijiegemeza vizuri kwenye kiti chake na kuikazia macho ile daladala iliyokuwa mbele yao. Safari ya Roman iliishia maeneo ya Kawe ambako alienda moja kwa moja hadi kwenye eneo kubwa kidogo la biashara ambalo lilikuwa limezungukwa na milango mingi ya maduka ya biashara mbali mbali, zikiwamo saluni za kike na za kiume, maduka ya bidhaa mbalimbali za rejareja, maduka ya mavazi, simu za mikononi, huduma za kupigisha simu na mauzo ya vocha za simu mbalimbali na vitu kama hivyo. Nje ya eneo lile alimuulizia mtu aliyekuwa akimtaka na alielekezwa kwenye mlango mdogo wa chuma ambao alipoingia ndani yake alitokezea nyuma ya maduka yale ambako kulikuwa kuna baa iliyojificha. Kwa muda ule ile baa haikuwa na wateja isipokuwa walevi wachache sana waliobobea. Pale aliulizia tena na kijana aliyekuwa akifanya usafi pale baa alimuelekeza kwa kidole upande mmoja wa ile baa ambako kulikuwa kuna ukuta uliokuwa na mlango mpana wa chuma. Roman aliusukuma ule mlango na kuingia ndani. Alitokea kwenye eneo pana lililozungukwa na mabenchi na viti vya namna mbali mbali katika kila kona ya eneo lile, ilhali eneo la katikati ya ukumbi ule kukiwa kuna ulingo wa ndondi uliokamilika. Roman alitembeza macho mle ndani na kushuhudia vijana wengi wakiwa katika harakati za mazoezi mbali mbali ya viungo na kujenga miili yao kama mabondia wanavyotakiwa kufanya, na ile taswira ilimrejeshea kumbukumbu za siku nyingi za nyuma na akahisi mwili ukimsisimka na moyo ukimlipuka kwa matarajio na kuanza kumuenda mbio. Alibaki akiwa amesimama pembeni ndani ya ukumbi ule kwa muda akitazama zile harakati zilizokuwa zikiendelea mle ndani kwa namna ya kuvutiwa sana. Kwenye ukuta uliokuwa mbele yake upande wa pilli wa ukumbi ule kulikuwa kuna maadishi makubwa yaliyosomeka KAWE BOXING CLUB. Hapo alijua kuwa hakuwa amepotea, kwani ndipo haswa mahala alipokuwa amekusudia kufika baada ya kutoka kule makaburini. Wale vijana waliendelea na harakati zao bila ya kumtilia maanani, naye alilisogelea benchi moja lililokuwa kwenye kona moja ya ukumbi ule na kuketi akitazama zile harakati huku akijaribu kuangaza huku na huko mle ndani akimtafuta mtu aliyekuwa amemkusudia, lakini ilikuwa wazi kuwa hakuwepo. Hilo halikumtia wasiwasi wowote. Alijua kuwa angetokea tu, naye aliamua kusubiri huku akiwatazama wale vijana wakitokwa jasho kwa harakati zao za kujiweka sawa kimazoezi. Muda mfupi baadaye mtu mmoja mfupi mwenye upara na aliyeonekana kuwa na umri wa kati miaka arobaini na saba na hamsini aliingia mle ndani kwa mwendo wa haraka akitokea kwenye mlango mwingine mdogo uliokuwa upande wa pili wa eneo lile, kando ya yale maandishi yaliyosomeka “Kawe Boxing Club”. “Alright! Alrght! Alright….! Hey!” Yule mtu alisema kwa sauti ya juu huku akipiga makofi na wale vijana waliacha mazoezi yao na kujipanga pamoja kumsikiliza. Roman aliachia tabasamu kubwa baada ya kumuona yule mtu ambaye haikuwa na shaka kabisa kuwa ndiye mkufunzi au kocha wa wale vijana. Alikuwa amevaa suti ya mazoezi (Track Suit) iliyomkaa vizuri sana, na viatu vya raba aina ya Reebok. Alipendeza sana, na Roman alikumbuka nyakati za siku za nyuma alipokuwa pamoja na mtu yule mzee mwenye roho ya kipekee. Yeye na mwenzake mwingine… Alijitikisa kichwa kwa namna ya kuyafuta mawazo yale kichwani mwake na kurejesha akili yake kule kwa bwana mwenye upara na vijana wake. “Okay! Tuna mechi ya kugombea ubingwa wa wilaya kesho kutwa na wote tunawajua wapinzani wetu tulionao hapa wilayani ni akina nani. Lengo letu ni kuchukua ubingwa wa taifa, lakini hatuwezi kufanya hivyo kama hatujashinda ngazi ya wilaya na mkoa. Mko tayari?” “Ndiyoooo!” Wale vijana walijibu kwa sauti ya juu huku wengine wakipiga mbinja na kurukaruka huku na huko, wakitupa mgumi hewani kiufundi kwa jazba na kujijaza hamasa. Roman alizidi kuachia tabasamu kufurahishwa na hali ile. “Okay! Dulla!” Bondia aliyeitwa Dulla alichomoka mbele kwa mbwembwe kali za kibondia, akitupa ngumi nyingi za mfululizo hewani kwa nguvu na kasi ya kuvutia, huku akibonyea mara kwa mara kama anayekwepa masumbwi ya mpinzani na kujiinua tena na kutupa ngumi nyingine kwa mitindo ya hook na upper cut, kisha akatulia mbele ya kocha wake akiwa ameinua ngumi zake usoni mwake kama jinsi mabondia wanavyosimama wakiwa wanasubiri amri ya mwamuzi kabla ya kuanza kwa pambano. Yule kocha alimtazama mpiganaji wake kwa namna ya kuridhishwa na makeke yake, kisha akamueleza. “Utapanda ulingoni na Chumbi wa timu ya Wandava Boxing katika uzito wa Bantam! Chumbi ni moto wa kuotea mbali na sina haja ya kukumbusha juu ya hilo, tatizo lako kubwa ni kujiamini kuliko kawaida Dulla, na usipoangalia, hilo ndilo litakuwa kaburi lako katika ndondi…” Hapo macho ya yule mtu mwenye upara yalimuona Roman akiwa ameketi kwenye benchi kando kabisa ya ukumbi ule na hapo hapo alikatisha maelezo yake. Badala yake uso wake ulijaa mshangao huku akifinya macho kumtazama vizuri yule mtu aliyetoka gerezani asubuhi ile. Wale vijana wote nao wakafuata macho ya kocha wao na kumgeukia Roman. “Roman…!?” Yule mzee alisema kwa sauti ya chini iliyojaa mshangao na maswali ya kutoamini. Taratibu yule bwana aliyejengeka kimazoezi aliwasogeza pembeni wale vijana waliokuwa mbele yake na kumuendea Roman kwa mwendo wa taratibu. Roman aliinuka kutoka kwenye lile benchi alilokuwa amekalia na kuanza kumsogelea yule mzee. Walitazamana kwa muda huku wakisogeleana, na hatimaye yule mzee alijihakikishia kuwa ni kweli macho yake yalichokuwa yakimuonesha, kwamba kwa hakika yule aliyekuwa akimuona alikuwa ni mtu aliyemtambua kwa jina la Roman. “Roman! Roman…! Umetoka…?” Walikimbiliana na kukumbatiana kwa nguvu na upendo wa hali ya juu kwa muda mrefu. Hatimaye yule mzee alimsukuma nyuma kidogo Roman na kumtazama usoni huku akiwa amemshika mabega. “Ah! Roman! Umetoka lini? Mbona sikuwa na taarifa…? Unaonekana uko fiti sana!” Aliuliza. “Leo, Kocha! Nimetoka leo…asubuhi hii hii…” Roman alimjibu yule mzee ambaye kufikia pale hakuweza kuyazuia machozi yasimtiririke. “Ah, Roman my boy! Miaka miwili sio mingi kumbe afterall eenh?” Alisema huku akiachia machozi yamtiririke bila ya kufanya bidii yoyote ya kuyafuta. “Yeah, Coach…sio mingi kama ilivyoonekana hapo mwanzo.” Roman alimjibu huku akimpangusa machozi yule mzee aliyemwita ‘Coach’ kwa kiganja cha mkono wake. Wale vijana waliokuwa wakifanya mazoezi pale ukumbini walikuwa wakitazama tukio lile kwa udadisi wa hali ya juu. Yule bwana mwenye upara alimshika mkono Roman na kumuongoza kuelekea kule kwenye mlango aliotokea hapo awali na kuwakuta wale vijana wake wakifanya mazoezi pale ukumbini. “Come on! Twende tukaongee ofisini kwangu!’ Alimwambia bila kujali mshangao ulioonekana wazi kwenye nyuso za wale wanafunzi wake. Waliingia ndani ya ile ofisi na yule bwana alifunga mlango na kumuelekeza Roman aketi kwenye kiti kilichokuwa mbele ya meza yake mle ofisini naye akaketi juu ya meza, akikiacha kiti chake kilichokuwa nyuma ya ile meza. Walitazamana kwa muda, kisha Roman aliongea kwa upole. “I am out now Mark (Nimetoka sasa Mark). Umeniwekea vitu vyote nilivyokuagiza?” Makongoro “Mark Tonto” Tondolo, kocha wa ndondi wa muda mrefu, na bingwa wa zamani wa taifa wa ngumi za ridhaa katika uzito wa juu (Heavy Weight) alimtazama Roman kwa muda bila ya kusema neno. Kisha aliinuka na kuzunguka nyuma ya ile meza aliyokuwa ameikalia na kutoa faili jembamba kutoka kwenye droo ya meza ile na kumkabidhi. “Kila kitu kimo humo ndani Roman, kama jinsi ulivyoagiza!” Alimwambia.
Yule kocha alimtazama mpiganaji wake kwa namna ya kuridhishwa na makeke yake, kisha akamueleza. ?Utapanda ulingoni na Chumbi wa timu ya Wandava Boxing katika uzito wa Bantam! Chumbi ni moto wa kuotea mbali na sina haja ya kukumbusha juu ya hilo, tatizo lako kubwa ni kujiamini kuliko kawaida Dulla, na usipoangalia, hilo ndilo litakuwa kaburi lako katika ndondi?? Hapo macho ya yule mtu mwenye upara yalimuona Roman akiwa ameketi kwenye benchi kando kabisa ya ukumbi ule na hapo hapo alikatisha maelezo yake. Badala yake uso wake ulijaa mshangao huku akifinya macho kumtazama vizuri yule mtu aliyetoka gerezani asubuhi ile. Wale vijana wote nao wakafuata macho ya kocha wao na kumgeukia Roman. ?Roman?!?? Yule mzee alisema kwa sauti ya chini iliyojaa mshangao na maswali ya kutoamini. Taratibu yule bwana aliyejengeka kimazoezi aliwasogeza pembeni wale vijana waliokuwa mbele yake na kumuendea Roman kwa mwendo wa taratibu. Roman aliinuka kutoka kwenye lile benchi alilokuwa amekalia na kuanza kumsogelea yule mzee. Walitazamana kwa muda huku wakisogeleana, na hatimaye yule mzee alijihakikishia kuwa ni kweli macho yake yalichokuwa yakimuonesha, kwamba kwa hakika yule aliyekuwa akimuona alikuwa ni mtu aliyemtambua kwa jina la Roman. ?Roman! Roman?! Umetoka??? Walikimbiliana na kukumbatiana kwa nguvu na upendo wa hali ya juu kwa muda mrefu. Hatimaye yule mzee alimsukuma nyuma kidogo Roman na kumtazama usoni huku akiwa amemshika mabega. ?Ah! Roman! Umetoka lini? Mbona sikuwa na taarifa?? Unaonekana uko fiti sana!? Aliuliza. ?Leo, Kocha! Nimetoka leo?asubuhi hii hii?? Roman alimjibu yule mzee ambaye kufikia pale hakuweza kuyazuia machozi yasimtiririke. ?Ah, Roman my boy! Miaka miwili sio mingi kumbe afterall eenh?? Alisema huku akiachia machozi yamtiririke bila ya kufanya bidii yoyote ya kuyafuta. ?Yeah, Coach?sio mingi kama ilivyoonekana hapo mwanzo.? Roman alimjibu huku akimpangusa machozi yule mzee aliyemwita ?Coach? kwa kiganja cha mkono wake. Wale vijana waliokuwa wakifanya mazoezi pale ukumbini walikuwa wakitazama tukio lile kwa udadisi wa hali ya juu. Yule bwana mwenye upara alimshika mkono Roman na kumuongoza kuelekea kule kwenye mlango aliotokea hapo awali na kuwakuta wale vijana wake wakifanya mazoezi pale ukumbini. ?Come on! Twende tukaongee ofisini kwangu!? Alimwambia bila kujali mshangao ulioonekana wazi kwenye nyuso za wale wanafunzi wake. Waliingia ndani ya ile ofisi na yule bwana alifunga mlango na kumuelekeza Roman aketi kwenye kiti kilichokuwa mbele ya meza yake mle ofisini naye akaketi juu ya meza, akikiacha kiti chake kilichokuwa nyuma ya ile meza. Walitazamana kwa muda, kisha Roman aliongea kwa upole. ?I am out now Mark (Nimetoka sasa Mark). Umeniwekea vitu vyote nilivyokuagiza?? Makongoro ?Mark Tonto? Tondolo, kocha wa ndondi wa muda mrefu, na bingwa wa zamani wa taifa wa ngumi za ridhaa katika uzito wa juu (Heavy Weight) alimtazama Roman kwa muda bila ya kusema neno. Kisha aliinuka na kuzunguka nyuma ya ile meza aliyokuwa ameikalia na kutoa faili jembamba kutoka kwenye droo ya meza ile na kumkabidhi. ?Kila kitu kimo humo ndani Roman, kama jinsi ulivyoagiza!? Alimwambia. Roman alilipokea lile faili na kulifungua kidogo kisha akaliweka juu ya mapaja yake, na kumtazama tena yule mtu mzima aliyependa kumwita kwa jina la utani ?Mark Tonto?. Walitazamana. ?Una uhakika na unalotaka kulifanya Roman?? Mark alimuuliza huku akimtazama machoni. Roman hakufanya haraka kumjibu. Na alipomjibu, alikuwa na asilimia mia moja za kujiamini katika jibu lake. ?Kwa mwaka mzima nimekuwa nikijiandaa kwa jambo hili Mark. Sasa ndio wakati wa kuanza kutekeleza azma yangu, na Mwenyezi Mungu ni shahidi juu ya hilo!? Makongoro Tondolo alimtazama Roman kwa muda mrefu bila ya kusema lolote. Na katika muda huo, Roman naye alikuwa akimtazama yule mzee bila ya kusema neno kwa muda, kisha akamuuliza huku akiendelea kumtazama kwa macho makavu. ?Uko tayari kunisaidia kama tulivyokubaliana mara ya mwisho uliponitembelea gerezani? Au umebadili mawazo?? Makongoro Tondolo aliendelea kumtazama kwa makini huku akionekana wazi kuwa kichwani mwake alikuwa na mawazo mengi. ?Kama umebadili mawazo mi? n?taelewa Mark. Lakini sitorudi nyuma. Nitaendelea na azma yangu, na wewe au bila wewe!? Roman alimwambia kwa msisitizo. Mark Tonto aliinuka kutoka kwenye meza aliyokuwa amekalia na kwenda kusimama hatua chache kutoka pale alipokuwa ameketi Roman, bado uso wake ulionekana kuwa na mawazo mengi. Kisha alirudi tena pale alipokuwako Roman na kusimama mbele yake. ?Mimi niko tayari kukusaidia Roman. Unajua kuwa siwezi kukukatalia. Ila kusema kweli nigefurahi na ningekuwa na amani zaidi kama ungeamua kuachana kabisa na jambo hili Roman?? ?No! God Damn it, No! We? unajua nimepitia wapi kabla ya kuja hapa kwako Mark?? Roman alifoka huku akipiga kiganja cha mkono wake juu ya ile meza naye akisimama, akiwa amelibana lile faili kwapani kwake. ?I come straight from the cemetery Mark (Nimekuja moja kwa moja kutoka makaburini Mark)! Rachel yuko chini ya rundo la udongo kule Mark! Na huko amelala milele, Damn shit! Milele!? Alimalizia kwa hasira huku akinyooshea mkono wake kule alipotokea. Mark alinyanyua juu mikono yake kwa ishara ya kutaka amani na kumsogelea kwa mwendo wa haraka. ?Okay, Okay, Okay, Roman, Okay! Usiwe na jazba?nilikuwa nakupa mawazo yangu tu!? ?Lakini utawezaje kufanya hivyo Mark? Baada ya yote yaliyotokea?baada ya yote unayojua kuwa nimelazimika kukabiliana nayo!? ?Okay Roman, tuyaache hayo! Nilikuwa natoa rai hiyo kutokana na kujali maslahi yako mwenyewe na si kwa sababu ya kutojali yaliyokukuta. I am sorry, Okay?? Mark alimjibu kwa upole. Roman alimtazama yule mzee kwa muda, kisha akaketi taratibu kwenye kile kiti alichokuwa amekalia hapo awali. Kwa muda mrefu walibaki kimya mle ndani. ?Kwa hiyo utanisaidia au vipi?? Hatimaye Roman alimuuliza huku akitazama sakafuni bila ya kumtazama. ?Of Course I will help you Roman, why not?? Mark Tonto alimjibu kwa uhakika wa hali ya juu. Roman alimtazama kwa muda, kisha aliinuka na kumkumbatia kwa mara nyingine yule mzee. ?Ahsante sana, Mark! Ahsante sana.? Mark Tonto alimsukuma nyuma kwa upole na kumtazama usoni kwa upendo sawia kabisa na ule wa baba kwa mwanaye ampendaye kwa dhati akiwa amemshika mabega kwa mikono yake miwili. ?Sasa unahitaji kupata josho la nguvu, utoe kabisa jasho na harufu ya Ukonga, Roman. Halafu ukakate hizo nywele?upumzike, tukatembee mjini ujikumbushe jiji ulilolikosa kwa muda mrefu,au siyo?? Alimwambia. Roman alitabasamu ?Ni kweli Mark, nahitaji kutoa hii minywele ya gerezani na kuoga maji yaliyostaarabika. Lakini sina muda wa kupumzika wala kutembea hovyo mjini. Nina lengo la kutimiza, na wewe sasa hivi umetoka kuniahidi kuwa utanisaidia kwalo?? Roman alimjibu huku akipitisha mkono wake kichwani. Mark alimtazama kwa muda. ?Okay, Roman, naona umedhamiria?basi nadhani ungeanza kukata nywele kwanza, halafu ndio ukaoge?? Alimwambia. Mark alimpeleka Roman kwenye moja ya saluni zilizokuwa nje ya ile klabu ya ndondi ambayo alikuwa akiimiliki. Kisha waliingia kwenye moja ya maduka ya nguo za kileo yaliyokuwa yameizunguka ile klabu ambamo Roman alichagua nguo safi zilizoonekana kumtosha na kumkaa vyema. Bila ya wao kujua, Dihenga na Kate walikuwa wakifuatilia nyendo zao zote wakiwa ndani ya gari lao waliloliegesha mbele ya yale maduka mengi yaliyoizunguka ile klabu. Waliporudi tena ndani ya ile klabu, Roman aliingia bafuni kuoga kwa mara ya kwanza akiwa mtu huru. Alitumia muda mrefu sana kule bafuni, akijisugua kwa nguvu, kama kwamba kwa kufanya vile angekuwa anafuta kabisa ukweli kuwa alikuwa ametoka gerezani na mambo yote yaliyotokea huko nyuma yangefutika katika maisha yake kama jinsi ambavyo taka na jasho vilivyokuwa vikiutoka mwili wake wakati akioga. Na wakati akioga, kumbukumbu ya marehemu Rachel Koga ilimjia kichwani mwake na aliljikuta akibubujikwa upya na machozi, na kwa mara nyingine tena alijithibitishia kutekeleza azma aliyotoka nayo gerezani. Azma ambayo ilionekana sio tu kumtia shaka yule askari wa kike aitwaye Fatma, bali pia rafiki yake na mwalimu wake Makongoro?Mark Tonto? Tondolo, ingawa alikuwa amekubali kumsaidia. Baada ya kumaliza kuoga na kuvaa nguo zake mpya, Mark alimtaka aende naye nyumbani kwake, ambako hapakuwa mbali na ile klabu, ili ampatie chumba cha kulala na awe anaishi naye, kwani baada ya kutoka gerezani, Roman hakuwa na mahala pa kuishi. ?Hapana Mark. Mimi ningependa kulala hapa hapa klabuni?humu ofisini kwako kama hutajali. Nitahitaji godoro tu, labda na chandarua kama haitakuwa usumbufu?? Roman alimwambia. ?Nini? Roman unachekesha! Yaani utoke gerezani halafu uje huku uraiani tena ulale chini? Yaani ulale humu wakati mi? n?na nyumba yenye nafasi ya kutosha? No way bwana! No way! Unakuja kuishi kwangu Roman, na kwa hili hakuna mjadala!? Mark alimjia juu. Lakini Roman alikuwa ameshaamua. ?Hebu fikiri hali ya nyumbani itakuwaje Mark. Mkeo, wanao?watajisikiaje kuwa wanaishi na mtu aliyetoka gerezani nyumbani mwao?? Alimuuliza kwa upole. Mark alianza kupingana naye, lakini Roman alimkatisha. ?Wacha Mark! Msaada ulionipatia mpaka sasa, na ambao uko tayari kunipatia, ni mkubwa sana. Mimi nitakuwa radhi kabisa kulala humu ofisini Mark. Kama nikiwa na godoro dogo sitakuwa na wasiwasi hata kidogo. Gerezani nilikuwa nalala sakafuni kabisa bwana!? Mark alizidi kupingana naye. ?Lakini hapa sio gerezani Roman. Kwa nini unataka kujitesa bila ya sababu? Nakuhakikishia kuwa familia yangu haitakuwa na tatizo lolote na wewe kuwepo nyumbani kwangu?? ?Sio rahisi Mark, mimi naelewa! Najua una nia nzuri sana na mimi, lakini haitakuwa vyema. Hata mimi mwenyewe sitajisikia vizuri kuwa nyumba moja na watu watakaokuwa wakinong?onezana kila ninapotokea kuwa ?huyo ndiye jamaa aliyetoka jela?? Sio freshi kabisa!? ?Aaah. Lakini hiyo si itakuwa kwa muda tu? Hatimaye itazoeleka na kuisha kabisa. Unanitia unyonge sana Roman?? ?Usikonde juu ya hilo kocha wangu. Nadhani hii itakuwa ni njia nzuri na salama zaidi. Hasa ukizingatia juu ya mpango nilionao kichwani mwangu hivi sasa. Haitachukua muda kabla polisi hawajaanza kupiga-piga hodi nyumbani kwako na kuanza kuuliza maswali kwa mkeo na wanao juu yangu kama nikiishi nawe, hujafikiria juu ya hilo?? Roman alimuuliza. ?Khah! Polisi? Kwa nini polisi waje kuwauliza maswali wanangu? What are you talking about Roman (Ni nini unachoongea Roman)?? Mark Tonto alimuuliza kwa mshangao mkubwa. Roman alitikisa kichwa kwa masikitiko, kisha akamuelezea tukio zima lililotokea siku ile mara baada ya yeye kutia mguu nje ya gereza. Mark alichoka! ?Inspekta Fatma? Ni nini tena anachotaka yule mwanamke lakini? Yaani amediriki kuja kukusubiri nje ya gereza na kuanza kukutishia?(alisonya) Ana wazimu nini?? Mark alikasirika kupita kiasi. Alibaki akihema kwa hasira. Kisha akajijibu mwenyewe. ?Ana wazimu sana yule mwanamke!? Akasonya tena. Roman alimtazama kwa utulivu. ?No Mark. Hana wazimu. Na nadhani wewe mwenyewe unaona ni jinsi gani isivyokuwa salama kwa mimi kuja kuishi nyumbani kwako sasa hivi.? Alimwambia. Mark hakuwa na jibu. Ni wazi kuwa Roman alikuwa sahihi. Hatimaye walitoka nje ya ile ofisi na Mark alimtambulisha Roman kwa wale mabondia wengine wa ile klabu yake ya ndondi. ?Tumepata bondia mwingine katika timu yetu, anaitwa Roman. Tutaanza naye mazoezi kesho. Na sasa sote tutaenda kupata soda hapo baa kwa ajili ya kumpokea mpiganaji mpya katika timu yetu, kwani sasa tuna uhakika zaidi wa kuchukua sio tu ubingwa wa wilaya, bali hata wa taifa.? Kocha Makongoro Tondolo aliwaambia wanafunzi wake. Wale vijana walilipuka kwa vifijo, hoi hoi na mbinja nyingi kumshangilia bondia mpya miongoni mwao, hususan ule mwaliko wa kupata soda. Kundi zima lilielekea baa na kila mmoja aliagiza soda aliyoipenda. Kocha Makongoro Tondolo alikaa na bondia wake mpya, pamoja na mabondia wake wengine na kunywa soda pamoja nao. Ilikuwa ni furaha kubwa kwa wale vijana, kwani waliuona ubingwa wa taifa ukiwa mikononi mwao. Lakini kwa kocha Mark Tonto na Roman, ule kwao ulikuwa ni mwanzo wa kutekeleza mpango mkali na wa hatari sana kwao iwapo utagundulika. Na kwenye kona moja pembeni kabisa ya baa ile, Dan na Kate walikuwa wakishuhudia mkusanyiko ule kwa udadisi mkubwa, huku wakipata vinywaji taratibu. ?Mmnh! Master D, unadhani ni nini kinaendelea pale sasa?? Kate alimuuliza Dihenga huku akimkodolea macho Roman. Dan alipeleka bilauri yake ya bia kinywani na kupiga funda kubwa kabla ya kuishusha ile bilauri mezani na kuachia mbwewe kubwa. Mdomo wake ulifanya tabasamu dogo la upande mmoja na kumjibu huku naye akitazama kule walipokuwapo akina Roman. ?Sijui. Lakini nadhani kinachotokea pale ndicho kile haswa nilichokuwa nikikitaka. Na nadhani kazi yetu haitakuwa ngumu sana?? Kate alimtazama kwa mshangao, ni wazi kuwa hakuwa amemuelewa. Halafu akatazama tena kule walipokuwa akina Roman, na kumgeukia tena yule mtu aliyependa kumwita Master D. ?Sijaelewa?? Alimwambia. Lakini Master D alitoa pesa ya kulipia vinywaji vyao na kuiweka juu ya meza huku akimwita mhudumu kwa ishara ya mkono wake naye akiinuka. ?Utaelewa kadiri tunavyoendelea mrembo. Twen?zetu.? Alimjibu huku akianza kuondoka eneo lile. Kate alimtazama kwa mshangao huku naye akiinuka na kumfuata. Saa moja baadaye Roman alikuwa ameketi kwenye kiti cha Mark Tonto lile faili likiwa wazi mbele yake pale mezani. Alilitazama kwa muda lile faili, juu yake kukiwa kumeandikwa kwa kalamu ya rangi yenye ncha nene:
……..Deusdelity Macha, a.k.a. ?Deus-deadly? Macha.
……..WBA Champion, Super Middle.
(Deusdelity Macha, a.k.a. ?Deus-wa mauaji? Macha. Bingwa wa dunia katika uzito wa Super Middle ,anayetambuliwa na shirikisho la ndondi duniani, WBA.) Roman alilitazama lile jina kwa muda mrefu. Kisha alilifungua lile faili na kuanza kulisoma.
Kate alimtazama kwa mshangao, ni wazi kuwa hakuwa amemuelewa. Halafu akatazama tena kule walipokuwa akina Roman, na kumgeukia tena yule mtu aliyependa kumwita Master D. “Sijaelewa…” Alimwambia. Lakini Master D alitoa pesa ya kulipia vinywaji vyao na kuiweka juu ya meza huku akimwita mhudumu kwa ishara ya mkono wake naye akiinuka. “Utaelewa kadiri tunavyoendelea mrembo. Twen’zetu.” Alimjibu huku akianza kuondoka eneo lile. Kate alimtazama kwa mshangao huku naye akiinuka na kumfuata. Saa moja baadaye Roman alikuwa ameketi kwenye kiti cha Mark Tonto lile faili likiwa wazi mbele yake pale mezani. Alilitazama kwa muda lile faili, juu yake kukiwa kumeandikwa kwa kalamu ya rangi yenye ncha nene:
Deusdelity Macha, a.k.a. “Deus-deadly” Macha. WBA Champion, Super Middle.
(Deusdelity Macha, a.k.a. “Deus-wa mauaji” Macha. Bingwa wa dunia katika uzito wa Super Middle ,anayetambuliwa na shirikisho la ndondi duniani, WBA.) Roman alilitazama lile jina kwa muda mrefu. Kisha alilifugua lile faili na kuanza kulisoma.
Ndani ya lile faili kulikuwa vipande vya magazeti vilivyokatwa vizuri kutoka kwenye kurasa za magazeti mbali mbali ya hapa nchini, ya kiswahili na ya kiingereza, na vilikuwa vimepangwa kutokana na tarehe za matukio yaliyokuwa yakiripotiwa katika magazeti yale. Vipande vyote vile vya magazeti vilikuwa vikiripoti juu ya habari za bondia Deusdelity Macha, bingwa wa dunia uzito wa Super Middle anayetambuliwa na WBA.
Na kutokana na habari zilizokusanywa kwa uangalifu na umakini wa hali ya juu katika faili lile ndani ya mwaka mmoja na nusu, Roman aliweza kusoma na kuelewa kila kitu juu ya bingwa huyu wa dunia katika uzito wa Super Middle aitwaye Deusdelity Macha. Ambaye mashabiki wa ndondi nchini walimbatiza jina la Deus-deadly, yaani “Deus-wa mauaji”. Aidha, katika faili lile kulikuwa kuna picha mbali mbali za bondia Deusdelity Macha akiwa katika mapambano mbali mbali ya ngumi zilizomuonesha akiwasulubu vibaya wapinzani wake. Habari zilizokusanywa na Mark Tonto katika faili lile zilieleza kwamba Deusdelity Macha aliingia katika ulimwengu wa ngumi za kulipwa (Professional Boxing) kiasi cha mwaka mmoja na nusu uliopita, akitokea kwenye ngumi za ridhaa (Amateur Boxing) ambako alikuwa akipigana katika timu ya vikosi vya majeshi, yeye akiwa mwanajeshi wa jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Uwezo wake mkubwa wa kuzipiga ulionekana kwa kiasi kidogo sana wakati alipokuwa katika michezo ya majeshi, ambapo vikosi vyote vya majeshi ya ulinzi na usalama nchini huwa vinashiriki katika michezo mbalimbali, ikiwemo ndondi. Huko, Deusdelity, aliingia kwenye ndondi tangu akiwa katika chuo cha maafisa wa jeshi Monduli, ambako yeye pamoja na wenzake wachache walijiunga mara baada ya kumaliza elimu ya juu ya sekondari. Baada kupigana ngumi za ridhaa kwa muda mrefu akiwa mhasibu wa jeshi la wananchi wa Tanzania, promota maarufu wa ngumi nchini alimuona na kuvutiwa naye. Aliamua kumshawishi ajiunge na ngumi za kulipwa ili ajiendeleze zaidi katika ndondi na wote wanufaike zaidi katika mchezo ule uliokuwa ukijipatia wapenzi wengi nchini. Deusdelity alilikubaliana naye mara moja. Swala la Deus kujiunga na ngumi za kulipwa halikuwa jepesi kutokana na kazi yake, kwani ngumi za kulipwa zilihitaji awe anakuwa nje ya kituo chake cha kazi katika nyakati ambazo muajiri wake, JWTZ, pia alikuwa akimhitaji. Alitakiwa aandaliwe mapambano mbali mbali ya kimataifa ambapo pamoja na yeye kulazimika kuletewa wapinzani kutoka nje ya nchi, pia alitakiwa asafiri nje ya mipaka ya nchi kwa ajili ya mapambano; jambo ambalo lilikuwa gumu kwake, akiwa kama askari wa jeshi la wananchi wa Tanzania.
Ni katika mazingira kama haya, ndipo Deusdelity Macha alipolazimika kuacha kazi yake ya uanajeshi ili aweze kujiingiza kikamilifu katika ngumi za kulipwa. Mwandishi wa habari ile alikiita kitendo cha Deus kuamua kuacha kazi yake ya kulitumikia taifa, ili aweze kushiriki kikamilifu katika ndondi za kulipwa kuwa ni “uanamichezo halisi” na kuwa ni kitendo kilichostahili sifa kubwa. (Kufikia hapa Roman aliachia tabasamu dogo la dharau huku akitikisa kichwa kuonesha kutokubaliana kabisa na hoja ile). Baada ya hapo Deus aliweza kuandaliwa mapambano kadhaa na promota wake tajiri yaliyofanyika humu humu nchini dhidi ya mabondia wengine wa hapa nchini. Kutokana na uzito wake, Deus aliingia katika ndondi kwa uzito wa Super Middle, ambao ulihitaji mpiganaji awe na uzito wa kati ya kilo 51.1 hadi 51.5. Na ni hapa ndipo alipojipatia sifa kem kem katika upiganaji wake na jinsi alivyoweza kuwasulubu wapinzani wake.
Katika kipindi hiki, akiwa na miezi minne tu tangu aingie katika ngumi za kulipwa, Deus alipambanishwa na bingwa wa dunia wa uzito wa Super Middle kwa wakati ule, katika pambano lisilokuwa la kugombea ubingwa wowote. Katika pambano hilo, Deus alifanikiwa kumshinda bingwa huyo wa dunia kwa Knock Out! Pamoja na kuwa pambano halikuwa la ubingwa au mkanda wowote, ushindi huu ulitosha kabisa kumuweka Deus katika ramani ya ndondi sio tu hapa nchini, bali duniani kwa ujumla. Na baada ya hapo Deus hakuzuilika tena.
Alifanikiwa kuwatwanga vibaya wapinzani wake wa hapa nchini, kiasi promota wake akafikia hatua ya kumnadi kuwa Deus hakuwa na mpinzani yoyote nchini. Hivyo alikuwa anamtafutia wapinzani kutoka nchi za jirani za Afrika ili angalau apambane na mabondia wenye uwezo sawa na wake. Pambano lake la kwanza la kimataifa alipambanishwa na bondia kutoka Uganda, na Deus alimdondosha chini kunako raundi ya kumi na kuondoka mshindi kwa Knock Out. Watanzania wakawa wameanza kumtazama Deus kwa matumaini zaidi. Wakati huo malumbano baina ya kambi yake na ile ya yule bingwa wa dunia aliyempiga kwa Knock Out yakawa yameshamiri. Yule bingwa akidai kurudiwa pambano, wakati Deus na promota wake wakisisitiza kuwa hakukuwa na bondia yoyote wa kushindana naye hapa nchini, akiwemo huyo aliyekuwa “akisemekana” kuwa ni bingwa wa dunia. Hali hii ilizidisha ushindani baina yao na wakati huo huo mashabiki wakaongezeka. Watanzania wakawa na hamu ya kurudiwa kwa mpambano ule. Deus na promota wake wakawa wameshikilia msimamo wao, na upinzani ukazidi mara dufu. Bondia wa pili wa kimataifa kupambanishwa na Deus alikuwa kutoka Zambia. Huyu alisulubiwa vibaya zaidi, na mnamo raundi ya nane ya mchezo refa alilazimika kusimamisha pambano baada ya Mzambia kuchanika vibaya juu ya jicho na kuvuja damu nyingi. Pambano liliisha na Deusdelity Macha aliibuka mshindi kwa Technical Knock Out (TKO). Na ndipo hapo alipopachikwa jina la “Deus-deadly”, yaani Deus wa mauaji.
Katika pambano hilo na Mzambia, bingwa wa dunia wa wakati ule katika uzito ule wa Super Middle alikuwamo ukumbini akishuhudia pambano, na baada ya kumsambaratisha mzambia, Deus alisogelea upande ambao mpinzani wake mkubwa alikuwa ameketi na kumnyooshea ngumi huku akimpigia kelele, “Sasa nautaka huo mkanda wako!” Ukumbi ulilipuka kwa hoi hoi na vifijo vya ushabiki, wakati yule bingwa, akiwa ameghadhibishwa na kauli ya Deus, alipoparamia jukwaa na kutaka kuweka naye mpambano pale pale. Ilikuwa hekaheka si kidogo! Lakini Hatimaye hali ilidhibitiwa na hakuna lolote lililotokea, zaidi ya uhasama baina yao kuongezeka. (Roman alikunja uso alipokuwa akisoma sehemu hii, dhahiri kuwa hakupendezewa na tabia ile). Bondia Deus alipambanishwa na bondia mwingine wa kimataifa, safari hii alikuwa ni mzungu kutoka Hungary. Huyu alikuwa na historia ya kuua mtu ulingoni, na watanzania waliofurika ukumbini kushuhudia pambano hilo walikuwa wamekuja kumshuhudia Deus akiaga dunia ulingoni. Mpaka kufikia raundi ya kumi na mbili mabondia wote wawili walikuwa hoi ulingoni, lakini hakuna aliyekubali kwenda chini. Pambano lilitangazwa kuwa suluhu. Alipoongea na waandishi wa habari baada ya pambano, mzungu alimsifia sana Deus, akisema kuwa hajawahi kupambana na bondia mwenye uwezo mkubwa na mwenye ngumi nzito kama yule tangu aanze ndondi, na kwa upande wake alishukuru sana kwa pambano lao kuisha suluhu, kwani kama kungetokea mshindi katika pambano lile, yeye alijipa nafasi ndogo sana. Hii ilizidi kumpa chati Deus, ambaye kwa upande wake aliongea na waandishi wa habari na kusema kuwa hakuwa ameridhika na matokeo yale, lakini alikiri kuwa kwa mara ya kwanza tangu aingie kwenye ngumi za kulipwa alikuwa amepata mpinzani wa kweli. Alibainisha kuwa alikuwa tayari kurudiana naye baadaye na aliahidi kuwa pindi yule mzungu atakapofanya kosa la kukubali kurudiana naye tu, basi huo ndio utakuwa mwisho wake. Huyo ndiye bondia Deusdelity Macha.
Roman alishusha pumzi ndefu na kufikicha macho. Aliinuka kutoka kwenye kiti alichokuwa amekalia na kutembea mle ndani huku akijinyoosha na akiendelea kufikicha macho. Uso wake ulionekana kuwa na mawazo mengi. Alitoka nje na kwenda kuketi pale kwenye baa akitafakari yale mambo aliyoyasoma kuhusu bondia Deusdelity Macha. Muda huo Mark Tonto aliingia eneo lile akiongozana na mmoja wa mabondia wake wakiwa wamebeba godoro dogo, na begi dogo lililokuwa na vifaa muhimu kama shuka, taulo, chandarua, dawa ya meno na vitu kama hivyo. Kwa muda wa zaidi ya nusu saa iliyofuata, akili ya Roman alihamia katika kujishughulisha kusaidiana na Mark na yule kijana kuweka mazingira ya malazi yake pale ofisini kuwa mazuri. Baada ya hapo muda wa chakula cha mchana ulikuwa umewadia na Mark alimkaribisha Roman nyumbani kwake kwa ajili ya mlo wa mchana. Roman alianza kusita, lakini kwa hili Mark hakuwa na majadiliano zaidi.
“Nazungumzia mlo wako wa kwanza wa maana baada ya miaka miwili ya kubugia maharage ya kuchemsha na ugali usioiva Roman! Sio mchezo bwana! Huko kuna pilau la kuku na juisi za kila fani….mke wangu amepika maalum kwa ajili yako! Lazima uje ule Roman, na lazima uje ule sasa hivi!” Mark Tonto alimwambia kwa msisitizo, na pamoja na kusita kwake, Roman aliuhisi mdomo ukimjaa mate. Akilini mwake alivuta picha iliyokuwa ikizungumzwa na Mark na akajihisi matumbo yakiunguruma kwa hamu ya kuingiza vile vyakula vilivyokuwa vikitajwa na Mark. “Mmmnh! Kwa hapo naona umefanikiwa kunishawishi Mark. Twen’zetu…Fasta!” Alimwambia. Mark alicheka kwa furaha na kumuongoza Roman kuelekea nyumbani kwake ambapo hapakuwa mbali na pale. Huko Roman alipigwa na butwaa baada ya kuona maandalizi yaliyofanywa kwa ajili yake. Walipoingia tu ndani ya sebule ya nyumba ile, alikuta maandishi makubwa yaliyowekwa kwa marembo mazuri kama yale yanayowekwa kwenye sherehe za siku za kuzaliwa au katika sikukuu mbalimbali. KARIBU NYUMBANI ROMAN. Ni maneno yaliyokuwa yamebandikwa ukutani kwa nakshi maalum, huku yakiwa yamezungushiwa maua mbalimbali na maputo. Mke wa Mark Tonto alimkimbilia na kumkumbatia kwa nguvu huku akimkaribisha pale nyumbani kwao. “Oooh Roman shemeji yangu! Pole sana baba’angu! Karibu tena uraiani…karibu nyumbani!” Alisema kwa hisia kubwa huku akibubujikwa na machozi yule mama mwenye moyo mkunjufu kama wa mumewe. Hii ilikuwa ni hali ambayo Roman hakuitarajia kabisa. Alimkumbatia yule mwanamke kwa shukurani ya hali ya juu na machozi yalimbubujika kwa furaha lakini pia kutokana na uchungu aliouhisi moyoni mwake kwa mapokezi yale. “Oooh, Ahsante sana shemeji….” Alijibu huku akibubujikwa na machozi, akilini mwake akijua kuwa kama si Mark na mkewe kumfanyia mambo haya, hakuna mtu yeyote ambaye angejali wala kukumbuka kumfanyia mambo kama yale. Kwani sasa baada ya kutoka gerezani, Roman hakuwa na ndugu wala jamaa yoyote wa damu hapa duniani…zaidi ya urafiki na ukaribu wake na Mark Tonto. Kwa hiyo mambo yale aliyoyakuta pale nyumbani kwa sahibu yake Makongoro “Mark Tonto” Tondolo yalimfariji kupita kiasi.
Ni maneno yaliyokuwa yamebandikwa ukutani kwa nakshi maalum, huku yakiwa yamezungushiwa maua mbalimbali na maputo. Mke wa Mark Tonto alimkimbilia na kumkumbatia kwa nguvu huku akimkaribisha pale nyumbani kwao. “Oooh Roman shemeji yangu! Pole sana baba’angu! Karibu tena uraiani…karibu nyumbani!” Alisema kwa hisia kubwa huku akibubujikwa na machozi yule mama mwenye moyo mkunjufu kama wa mumewe. Hii ilikuwa ni hali ambayo Roman hakuitarajia kabisa. Alimkumbatia yule mwanamke kwa shukurani ya hali ya juu na machozi yalimbubujika kwa furaha lakini pia kutokana na uchungu aliouhisi moyoni mwake kwa mapokezi yale. “Oooh, Ahsante sana shemeji….” Alijibu huku akibubujikwa na machozi, akilini mwake akijua kuwa kama si Mark na mkewe kumfanyia mambo haya, hakuna mtu yeyote ambaye angejali wala kukumbuka kumfanyia mambo kama yale. Kwani sasa baada ya kutoka gerezani, Roman hakuwa na ndugu wala jamaa yoyote wa damu hapa duniani…zaidi ya urafiki na ukaribu wake na Mark Tonto. Kwa hiyo mambo yale aliyoyakuta pale nyumbani kwa sahibu yake Makongoro “Mark Tonto” Tondolo yalimfariji kupita kiasi.
Mark Tonto hakuwa amezidisha chumvi alipoongelea juu ya maandalizi yaliyofanywa na mkewe juu ya ujio wa Roman. Pilau ya kuku ilikuwa imetulia na kupendeza kabisa mezani pamoja na aina zipatazo tatu za juisi, na Roman aliushambulia ule msosi kwa nguvu sana. Alikumbuka vyakula duni alivyokuwa akila wakati akiwa gerezani na akashindwa kuelewa aliwezaje kula vyakula vile kwa miaka miwili mfululizo bila kuathirika kiafya. Baada ya kupata chakula kile kizuri, Roman alimshukuru mke wa Mark na wote wakaketi sebuleni na kuongelea mambo mbalimbali hususan kuhusiana na maisha ya Roman alipokuwa gerezani. “Nina masikitiko sana shemeji kuwa hukutaka kuja kuishi nasi hapa nyumbani…kwani najua kuwa sasa huna mahala pa kulala…” Mke wa Mark alimwambia Roman kwa ile lafudhi yake ya ki-Tanga ambayo Roman hupenda sana kumtania kwayo. Roman alimtupia jicho la haraka Mark, kisha akajibalaguza kidogo kwa shemeji yake kabla ya kumjibu.
“Aaah…hapana shemeji. Sio kuwa sikutaka kuishi nanyi hapa nyumbani, ila tu kwa sasa ningependelea niwe peke yangu kwa muda. Unajua mambo yaliyotokea kabla ya kupelekwa kwangu gerezani, na…”
“Aaah. Roman mimi sio mtoto bwana! Muda wa kuwa peke yako ulikua nao wa kutosha sana wakati uko gerezani. Sasa unahitaji kuwa karibu na watu wanaokujali na kukupenda bwana! Unahitaji kuwa na sisi! Na ndivyo nilivyomueleza Mark vilevile, lakini inaonekana tayari nyie mmeshakubaliana nami siwezi kubadili lolote katika hilo.” Tandi, mke wa Mark Tonto, alimjibu Roman kwa hamasa, huku akimtupia jicho la shutuma mumewe. Mark na Roman walitazamana, kisha wote wakatazama pembeni huku Mark akibwabwaja utetezi wao.
“Ooh Come On, Tandi! Hebu muache Roman afanye anavyojisikia bwana! Ye’ anajua kuwa hapa kwetu ni kwake na yuko huru kuja wakati wowote. Lakini sasa anahitaji kuwa peke yake kwa muda…and so be it (basi na iwe hivyo)!” Mark Tonto alidakia na kumkatisha mkewe. “Eeeh, kwani ugomvi babu? Mtu n’na hamu na shemeji yangu, na n’najua kuwa siwezi kumpata hapa nyumbani kwangu kama ambavyo ningependa, sasa basi hata mawazo yangu nisiyaweke wazi?” Tandi alimjibu mumewe, na hapo Roman aliamua kuingilia kati.
“Hey, shem…hamna muvi nzuri humu jamani? Sijaangalia muvi kwa miaka miwili! Si unajua jinsi nilivyokuwa mpenzi wa muvi?” Alimwambia Tandi huku akimtupia Mark jicho la pembeni. Wazo hilo lilielekea kumpendeza Mark vilevile, lakini lilimpendeza Tandi zaidi. Baada ya kuchagua mikanda na CD za video kadhaa, hatimaye waliishia kutazama kitu ambacho Roman alikuwa akitaka kukitazama kwa muda mrefu. CD za ndondi, ambazo Mark alikuwa nazo kwa wingi mle ndani mwake.
“Nataka kuona tena jinsi Mike Tyson alivyopigwa!” Roman aliwaambia. Kwa muda wote uliobakia katika siku ile walibaki wakitazama video za ndondi huku Tandi akimdekeza Roman kwa vinywaji mbalimbali na mapochopocho ya kila aina. Ilikuwa ni siku ya furaha sana, lakini pamoja na yote hayo,Roman alikuwa akingalia ile mikanda kwa umakini wa hali ya juu, na mara kadhaa alikuwa akijadili na Mark ni namna gani bondia mmoja angeweza kumkwepa mwingine, au ni wapi bondia mmoja alipotea stepu kiasi cha kumpa mpinzani wake nafasi ya kumshinda. Na wakati akiangalia ile mikanda, msisimko wa ajabu ulimuingia na akajihisi kama aliyezaliwa upya.
“Shemeji una mpango wa kuingia kwenye ndondi nini?” Tandi alimuuliza kwa utani, na Roman alicheka sana, lakini hakutoa jibu lolote. Ilikuwa ni saa moja ya usiku wakati Roman aliporudi kwenye makazi yake mapya pale kwenye klabu ya ndondi ya Mark. “Unaona ilivyokuwa hatari mimi kuja-kuja kwako Mark? Tayari Tandi alishaanza kuuliza maswali ya kipolisi! It’s very dangerous, Mark! Very dangerous I tell you!(Ni hatari sana nakwambia!)” Roman alimwambia Mark wakati wakisindikizana kurudi kule kwenye klabu yao ya ngumi. “Kweli Roman. Nadhani tunahitaji kuwa makini sana tunapokuwa na shemeji yako…” “Nadhani njia ya salama zaidi ni mimi kuwa bidhaa adimu nyumbani kwako Mark.” Roman alisema na wakaendelea na safari yao wakiwa kimya hadi walipoagana. ***** Roman alipitiliza moja kwa moja hadi kwenye ule mlango wa chuma uliotokea kwenye ule ukumbi wa ngumi wa ile klabu ya ngumi ya Mark Tonto. Alikuwa akiingia kwenye mlango ule huku akiingiza mkono wake mfukoni kutoa ufunguo wa mlango wa ofisi ya Mark, wakati ghafla alipopamiana na mtu aliyekuwa akitokea kule kwenye ukumbi wa ngumi kwa mwendo wa haraka. Yule mtu alijigeuza upesi kuficha uso wake na kutaka kutoka nje, lakini Roman alimkamata na kumsukumia ndani kwa nguvu huku akiusukuma ule mlango kwa kisigino cha mguu wake.
“Heeey! We’ vipi?” Sauti ya kike ilimkemea kwa ukali, na haraka sana Roman alipeleka mkono wake kando ya ule mlango na kuwasha taa za mle ukumbini, ambapo taa zaidi ya sita za mianzi ziliwaka kwa pamoja na kukawa kweupe kama mchana. Na hapo alijikuta akitazamana uso kwa uso na binti mmoja mrembo sana aliyekuwa amevaa suruali ya jeans iliyombana na kuonesha miinuko muhimu ya sehemu ya chini ya mwili wake, na juu alikuwa amevaa fulana kubwa nyeupe iliyoonesha miinuko midogo ya matiti yake.
“We’ vipi kivipi? Unatafuta nini humu wewe saa hizi?” Roman alimchachamalia yule mrembo. Woga ulimtawala Kate na akabaki akimkodolea macho yule mtu ambaye asubuhi tu ya siku ile alikwenda kumvizia nje ya gereza la Ukonga, sasa akiwa naye uso kwa uso. Mate yalimkauka ghafla na akajikuta akijaribu kukohoa ili angalau apate kuongea vizuri, akilini mwake akijilaumu kwa kuruhusu yule jamaa amkute mle ndani muda ule.
“Nakuuliza wewe mwanamke! Unatafuta nini humu?” Roman alimuuliza tena huku akimsogezea uso wake kwa kumshutumu. Kate alirudi nyuma kwa woga.
“Aam…Ni…nilikukwa natafuta choo! Nimepotea tu,samahani…!” Alimjibu kwa kitetemeshi kikubwa. Roman alimtazama yule binti kwa muda, na yule binti alijaribu kumzunguka na kuuendea mlango wa kutokea nje ya ukumbi ule lakini Roman alisogea mbele yake na kumzuia huku bado akiendelea kumtazama. “We! Unataka kujitia mbakaji sio? N’tapiga kelele sasa hivi nikujazie watu hapa!” Kate alimwambia kwa sauti ya kitetemeshi huku akimnyooshea kidole.
“Hebu acha ujinga weweee! Sasa kama hutaki kubakwa humu ndani umefuata nini,eenh?” Roman alizidi kumchachamalia. Kate alimtazama kwa woga. Moyoni akilaani kiherehere chake cha kutaka kujitia kuja huku peke yake muda ule. “Nimekwambia kuwa nilikuwa nataka kwenda chooni nikapotea njia! Mi’ mgeni katika baa hii…” “Kwa hiyo na kusoma pia hujui?” Roman alimuuliza. Kate alimtazama kwa mshangao na kumuuliza alikuwa anamaanisha nini kwa swali lile. “Yaani unataka kuniambia kuwa hujaona kuwa hapo nje ya huu mlango kumeandikwa “Kawe Boxing Club”? Au ndio hujui kusoma?” Kate hakuwa na ujanja. Alimtazama na kuinamisha kichwa chake chini, kisha akamtazma tena. “Okay…Nilikuwa nakutafuta wewe Roman.” Alimjibu huku akimtazama usoni, na Roman alibaki mdomo wazi kwa mshangao. Yaani ulikuwa ni mshangao wa mwaka kwake, na alibaki akimkodolea macho yule binti mzuri kama kwamba alikuwa ameona jini. “U…nini? We’ umenijuaje mimi?” Aliropoka kwa jazba huku akiukamata mkono wa yule binti kwa nguvu kama kwamba alijua kuwa muda wowote yule msichana angeanza kutimua mbio. Kate alitoa mguno wa maumivu na kujaribu kuuchomoa mkono wake bila mafanikio. “Aaah! Sasa…unaniumiza wewe!!” Kate alilalamika kwa uchungu
“Nimekwambia kuwa nilikuwa nataka kwenda chooni nikapotea njia! Mi’ mgeni katika baa hii…” “Kwa hiyo na kusoma pia hujui?” Roman alimuuliza. Kate alimtazama kwa mshangao na kumuuliza alikuwa anamaanisha nini kwa swali lile. “Yaani unataka kuniambia kuwa hujaona kuwa hapo nje ya huu mlango kumeandikwa “Kawe Boxing Club”? Au ndio hujui kusoma?” Kate hakuwa na ujanja. Alimtazama na kuinamisha kichwa chake chini, kisha akamtazma tena. “Okay…Nilikuwa nakutafuta wewe Roman.” Alimjibu huku akimtazama usoni, na Roman alibaki mdomo wazi kwa mshangao. Yaani ulikuwa ni mshangao wa mwaka kwake, na alibaki akimkodolea macho yule binti mzuri kama kwamba alikuwa ameona jini. “U…nini? We’ umenijuaje mimi?” Aliropoka kwa jazba huku akiukamata mkono wa yule binti kwa nguvu kama kwamba alijua kuwa muda wowote yule msichana angeanza kutimua mbio. Kate alitoa mguno wa maumivu na kujaribu kuuchomoa mkono wake bila mafanikio. “Aaah! Sasa…unaniumiza wewe!!” Kate alilalamika kwa uchungu. “Na hapo bado hata sijaanza mrembo! Nikianza kukuumiza wala hutakuwa na uwezo wa kuongea namna hiyo! Wewe ni nani, na unataka nini kwangu? Umelijuaje jina langu na umewezaje kunifuata mpaka hapa…?” Roman alimvurumishia maswali kwa hasira huku akimtikisa-tikisa kutilia msisitizo maswali yake. “Sasa….sasa si ungoje basi nikueleze….!” Kate alimwambia kwa kulalamika, woga mkubwa ukiutawala moyo wake. “Na unanitafuta kwa nia gani?” Roman bado alizidi kuvurumisha maswali kama kwamba hakusikia utetezi wa yule binti. “Ndio nakwambia ngoja nikueleze basiii! Aah! Unaniumiza bwana!” Kate alizidi kujitetea huku akimtazama kwa uso uliojikunja kwa maumivu, kwani ni kweli kuwa Roman alikuwa amembana kwa nguvu sana. Kufikia hapa alikuwa akitetemeka kwa woga na alitamani Master D angekuwa pamoja naye. Roman alimtazama kwa muda, na aliona kuwa ni kweli alikuwa akimuumiza yule binti. Alilegeza kidogo vidole vyake lakini bado aliendelea kumshika mkono, sehemu iliyokuwa juu kidogo ya kiwiko. “Haya…nieleze. Umesema ulikuwa unanitafuta…anza kwa kunieleza wewe ni nani!” Roman alimwambia yule binti huku akilini mwake akipitiwa na maswali mengine mengi aliyotaka kumuuliza yule binti,kubwa miongoni mwayo likiwa iwapo yule binti alikuwa ni askari aliyetumwa na Inspekta Fatma. Wazo hili lilipopita kichwani mwake ghadhabu zilimpanda kwa namna ya ajabu na akajikuta akiubinya tena mkono wa yule binti kwa nguvu kiasi kumfanya binti aachie yowe la uchungu, na Roman aliona kuwa alikuwa amezidi kumuumiza bila sababu. “Oh! Pole…Lakini..n’na ghadhabu sana na wewe ujue! Hivyo fanya hima kutoa maelezo!” Alimkemea huku akimsogezea uso wake uliojaa jazba. Kate alimtazama kwa muda huku moyo ukimwenda mbio. Alimeza funda la mate na kujitutumua kumuuliza, akijitahidi kuifanya sauti yake isidhihirishe woga uliomtawala. “Una ghadhabu na mtu usiyemjua Roman? Hebu twende tukaketi hapo baa basi ili tuongee vizuri…” Roman alimtazama yule binti kwa mashaka huku akili ikimtembea. Alitaka kuugomea ushauri ule, lakini hakuwa na sababu ya kulazimisha kuwa na yule binti ndani ya ule ukumbi wakiwa wawili tu, na tayari alianza kupata hisia za ajabu-ajabu, kwani kwa miaka miwili aliyokuwa gerezani hakuwa amepata kuwa na mwanamke kwa ukaribu namna ile, achilia mbali kule kumtia mikononi kama vile halafu akiwa mrembo namna ile. Akili yake ilirudi kwenye lile faili alilopewa na Mark Tonto saa kadhaa zilizopita. Je, huyu mwanamke amefanikiwa kuingia mle ndani na kuliona? Kama ni hivyo basi itakuwa mbaya sana kwake! Lakini hili halikuwa rahisi, kwani ule mlango ulikuwa umefungwa kwa ufunguo na ufunguo alikuwa nao yeye. Lakini pia kulikuwa na uwezekano wa yule binti kuufungua ule mlango kwa kutumia funguo malaya, hasa kama angekuwa kweli ni askari. Haraka sana alimbana yule binti na kumpapasa mwili wake haraka haraka akijaribu kumsachi uwapo alikuwa amelificha lile faili chini ya ile fulana yake kubwa, na kukuta kuwa hakuwa amevaa sidiria chini ya ile fulana na hisia zake za kimapenzi zikamchachamaa ghafla na kumkosesha utulivu wa moyo. Kate alitoa sauti za kulalamikia tendo lile huku akijaribu kujitoa mikononi mwa yule mwanamume mwenye misuli, akilini akijua kuwa ndio alikuwa anabakwa na alitaka kuanza kupiga kelele, lakini kilikuwa ni kitendo cha haraka sana na kilikuwa kimeshafanyika kabla hata hajaweza kusema neno zaidi. “We…! Ume…ulitaka kunifanya nini, eenh?” Alimuuliza kwa ukali huku moyo ukimtetema kwa woga. Roman alimeza funda kubwa la mate, ile hisia aliyoihisi wakati mkono wake ukipita juu ya titi la yule binti lililosimama vizuri likiwa chini ya ile fulana bado ilikuwa hai kichwani mwake. “Ni…(alijikohoza kidogo) nilikuwa nakusachi…” Alimwambia kwa mkato. Kate alifumbua mdomo na kutaka kusema neno, lakini akaghairi. Alimtazama kwa jicho la udadisi na aliona kuwa tayari alikuwa ameleta athari katika hisia za yule mwanamume mwenye mwili uliojaa kimichezo na sura ya kuvutia. Aliuma mdomo wake wa chini na akilini mwake akajiuliza itakuwaje iwapo yule jamaa akiamua kumbaka mle ndani, hasa akizingatia kuwa ndio kwanza alikuwa ametoka gerezani, na kwa mara nyingine tena akajilaani kwa ujinga na kiherehere chake cha kuja kumsaka huyu mtu peke yake. “Okay…twende huko baa…na usiniletee ujanja wowote huko!” Sauti ya Roman, iliyotoka kwa mkwaruzo ambao hapo awali haukuwepo, ilikatisha mawazo yake, na hapo hapo alijikuta akiongozwa kutoka ndani ya ule ukumbi wa ndondi na kuelekezwa kule kwenye baa, akiwa ameshikwa mkono kwa nguvu. Roman alichagua meza iliyojificha pembeni kabisa ya ukumbi ule na wote wakaketi taratibu. “Wewe ni nani?” Roman alimuuliza yule binti mara walipoketi. “Nahitaji kinywaji tafadhali…” Kate alisema huku akimtazama Roman machoni. Hapo hapo Roman alikunja uso kwa hasira, na Kate akadakia haraka;”…aamm, n’talipia mwenyewe! Usiwe na wasiwasi…” Roman alijitahidi kustahamili wakati Kate akijiagizia kinywaji aina ya Sparleta, akakataa kununuliwa kinywaji chochote na yule binti, na kurudia tena lile swali lake. “Mi’ naitwa Kate. Ni mfanyabiashara wa kawaida tu hapa jijini.” Yule binti alimjibu swali lake kwa utulivu uliomtia wasiwasi Roman. Alimtazama kwa muda, na yule binti aliinua bilauri ya kinywaji chake na kuipeleka kinywani, akimtazama Roman kutokea juu ya ukingo wa ile bilauri kwa macho yaliyotulia. Roman hakuwa na namna ya kujua iwapo alikuwa anasema kweli au vinginevyo. Aliamua kuliacha hilo kwanza. “Okay, Kate. Umelijuaje jina langu na unanitafutia nini?” Alimuuliza. Kate alirejesha ile bilauri mezani taratibu, kisha akaachia tabasamu moja pana na zuri sana. “Hapo ndipo haswa ulipokuwa ukipataka, sio?” Alimuuliza huku akimchekea. Khah! Huyu demu vipi? Yaani… Roman alikuja juu vibaya sana. Alimsogezea uso wake kwa hasira na kupiga meza kwa kiganja cha mkono wake huku akimkemea kwa ukali. “Hebu usinichezee mimi wewe, Ebbo! Unataka kun’letea nyodo wakati…” Kate aliruka kwa mshituko na kuigonga ile bilauri iliyokuwa na soda ambayo ilimmwagikia kifuani na kumlowesha hadi kwenye suruali yake, kabla ya kuanguka sakafuni na kuvunjika kwa kelele kubwa. Hapo hapo zilisikika sauti za wanywaji wengine zikishangilia kitendo kile, kila mmoja kwa namna yake. Kate aliruka kutoka kwenye kiti chake na kusimama huku akitoa yowe la mshituko na akijitazama jinsi alivyolowana kwa kile kinywaji. Roman alisimama haraka na kumtazama kwa ukali. “Nini sasa wewe!” Alimfokea “Umenishitua mpaka nimejimwagia! Angalia sasa!” Kate alilalama kwa sauti iliyojaa deko, na Roman hakuamini kabisa kuwa jambo alilofanya lingeweza kumshitua yule binti namna ile. “Wacha ufala wewe! Umeshitushwa na nini sasa!?” Alizidi kumkemea huku akiketi kwenye kiti chake na akitembeza macho mle kwenye ile baa kuona kama watu walikuwa wakiwatazama. Na kweli walikuwa wakiwatazama, kwani kile kilikuwa ni kituko kisichoweza kupita bila watu kutaka kushuhudia. Kate alimtazama kwa macho ya ghadhabu na kutaka kumjibu, lakini muda huo mhudumu alifika na kuuliza iwapo anaweza kusaidia. “Nipeleke chooni Anti. Itanibidi niivue hii fulana na niikamue sasa!” Kate alimwambia yule mhudumu huku akikung’uta mikono yake na akielekea usawa wa vyoo vya akina mama. Roman alianza kupinga swala lile, lakini wakati huo huo Kate alimgeukia kama aliyekumbuka kitu na kumrushia pochi yake ndogo. “Aaah, nishikie pochi yangu…I’ll be back soon (Nitarudi baada ya muda mfupi)”. Alimwambia na kugeuka kumfuata yule mhudumu wa kike kuelekea sehemu iliyokuwa na choo cha akina mama kabla Roman hajaweza kusema lolote. Roman alibaki akiwa amefura kwa hasira akisubiri. Lakini angalau alikuwa na ile pochi ya yule dada ambayo hakuwa na shaka kuwa ilikuwa na pesa, hivyo alijua kuwa yule binti angerudi tu. Kate hakurudi. Hakurudi na wala hakumuona akitoka nje ya ile baa pamoja na kuwa alikuwa makini sana. Baada ya nusu saa kupita alijua kuwa alikuwa ameingizwa mjini. Alimuita yule mhudumu na kumuuliza juu ya yule binti aliyemsindikiza chooni. “Khah! Kwani hajarudi mpaka sasa?” Yule mhudumu aliuliza kwa mshangao. Badala ya kumjibu, Roman aliinuka kwa hasira na kutoka haraka nje ya ile baa, akimwacha yule mhudumu akiwa amepigwa na butwaa. Kule nje aliangaza huku na huko akijaribu kumtafuta yule binti, lakini aliambulia patupu. Alipiga ngumi ndani ya kiganja chake kwa hasira na kutoa tusi zito la nguoni. Yule binti amemtoka kipumbavu sana! Alijua tu kuna ujanja ulikuwa unafanyika pale alipojitia kushituka na kujimwagia soda. Kumbe ilikuwa ndio mbinu yake ya kumtoroka! Alipiga tena ngumi kwenye kiganja chake kwa hasira kabla ya kurudi tena ndani ya ile baa. Bila ya yeye kujua, Kate alikuwa ametulia tuli ndani ya ile gari yake aina ya Toyota Prado, Short Chasis Metallic akimuangalia. Kutokana na vioo vya ile gari kuwa tinted, Roman hakumuona kabisa na wala hakuwa na namna ya kuhisi kuwa angekuwa ndani ya ile gari kwani kulikuwa kuna magari mengi tu pale nje ya ile baa. Roman alipita moja kwa moja hadi ofisini kwa Mark Tonto, ambako alifungua ule mlango na kujifungia kwa ndani akiwa amekasirika vibaya sana. “Tutaonana tena tu Kate, kama hilo ni jina lako kweli. Na tutakapoonana tena ndipo kweli utapata kitu cha kukushitua!” Alijisemea peke yake kwa hasira, kisha akatoa msonyo mkali na kujibwaga kwenye godoro lake huku akiwa na ile pochi ndogo ya Kate mkononi mwake. Aliitazama kwa muda kisha akaifungua na kuangalia vilivyokuwamo ndani yake. Ndani ya ile pochi kulikuwa kuna fedha kiasi cha shilingi elfu arobaini, na chenji ndogo ndogo, vipodozi vya kike vilivyojumuisha kijichupa kidogo cha uturi, rangi ya mdomo, na kishubaka cha poda. Pia kulikuwa kuna picha ndogo yenye ukubwa wa pasi ya kusafiria (passport size). Roman aliichukua kwa pupa ile picha na kuitazama, uso wake ukifanya mikunjo ya ghadhabu na tafakuri nzito. Alijibwaga kwenye kiti kilichokuwa nyuma ya meza iliyokuwa mle ofisini na kuitupia ile picha juu ya ile meza, uso wa picha ile ukiwa juu. Kwa muda mrefu Roman alikaa pale ofisini akiitazama ile picha iliyokuwa juu ya ile meza. Alikuwa akiitazama sura yake mwenyewe ikiwa pale juu ya meza. “Wewe ni nani mwanamke…? Na kwa nini unatembea na picha yangu kwenye pochi yako, eenh? Umetumwa, au…?” Hatimaye Roman alisema peke yake kwa sauti ya kunong’ona, kisha akainuka na kwenda kujilaza kwenye godoro aliloletewa na Mark Tonto huku bado akiwa na mawazo juu ya yule mwanadada aliyemtoroka usiku ule. Alibaki katika hali ile mpaka usingizi ulipompitia. Asubuhi ya siku iliyofuata Roman aliungana na Mark Tonto pamoja na mabondia wengine wa ile klabu ya ndodi kwenye mazoezi ya kukimbia, viungo na ngumi kidogo. “Kuna jambo limetokea jana ambalo nitahitaji kuongea nawe Mark…baadae.” Roman alimwambia rafiki yake baada ya mazoezi. Mark alimtazama kwa makini, uso wake ukiwa na mashaka kidogo. “Baadaye Mark…okay?” Roman alimwambia. “Okay, basi mi’ naenda home kwanza… n’takuja baadaye kidogo…!” Mark alimwambia na Roman akaafikiana naye kwa kichwa. Baada ya kuoga na kupata kifungua kinywa aliendelea kusoma lile faili lililokuwa na habari za bondia Deusdelity Macha. Kutokana na habari zilizokusanywa kwenye lile faili, Roman alizidi kupata undani wa bondia Deus-deadly Macha, kwamba “Deus-deadly” alisifika kwa mtindo wake wa upiganaji ambao ulifananishwa sana na ule wa bingwa wa ndondi wa zamani Muhammad Ali, wa kupiga wapinzani wake kidogo kidogo, hasa ile namna yake ya kuwachezeshea uso mbele yao na kuwakwepa huku akichezesha miguu yake kibondia. “Hah! Hao hawakujui kama nikujuavyo mimi Deus!” Roman alijikuta akiyasemesha yale maandishi aliyokuwa akiyasoma kwenye lile faili kwa sauti, kisha akatikisa kichwa huku uso wake ukiachia tabasamu, “…eti Muhammad Ali! (Aliguna) Laiti wangejua siri yako hao hata wasingethubutu kukupa jina kubwa namna hiyo rafiki yangu!” Alisema tena huku akiitomasa picha ya Deus iliyokuwa ndani ya lile faili.
Baada ya lile pambano lake na mzungu kutoka Hungary, Macha alipambana na bondia kutoka Afrika ya Kusini mjini Johannesburg, ambako alimtawanya taya msauzi huyo na kuondoka mshindi. Sifa za bondia “Deus-deadly” Macha sasa zilikuwa zimeenea duniani kote, na Tanzania ikawa moja ya nchi za kutazamika katika ulimwengu wa ndondi. Kwenye faili kulikuwa kuna habari juu ya mzozo baina ya Deus na promota wake, mzozo ambao kwa mujibu habari za magazeti, ulitokana na Deus kutoridhika na mapambano anayoandaliwa na promota wake huyo. Mwisho wa habari ile ilielezwa kuwa Deus alivunja mkataba na promota huyo na kujiunga na promota mwingine ambaye alionekana kuwa na mtazamao wa maendeleo zaidi kwa Deus kuliko yule promota wake wa awali aliyemtoa jeshini. (Roman alitikisa kichwa tena kwa masikitko, kisha akendelea kusoma). Ndipo, miezi sita baada ya lile tukio la kutishiana baina yake na yule bingwa wa dunia wa wakati ule, promota mpya wa Deus alipokubali pambano baina ya bondia wake na bingwa yule, pambano likiwa ni la kugombea mkanda ule wa dunia. Kufikia hapa Roman alikuwa anasoma kwa hamasa, akiwa amejawa udadisi wa kujua kilichojiri kwenye pambano lile baina ya Bondia Deusdelity Macha na yule bingwa wa dunia wa wakati ule… Lilikuwa ni pambano lililotangazwa na kunadiwa sana, na siku ya tukio ukumbi ulifurika kuliko ilivyowahi kutokea. Kengele ya kuanza pambano ilipogongwa, wapinzani wale waliendeana kwa bashasha na azma ya pambano la kukata na shoka. Na hapa ndipo Deus alipoonesha kuwa kweli yeye alikuwa muuaji kwani kufikia raundi ya kumi na moja bingwa wa dunia aliyekuwa akitetea ubingwa wake alikuwa ameshavunjwa mwamba wa pua na akitokwa damu kama maji. Refa alilazimika kusimamisha pambano na Deus akatawazwa ubingwa wa dunia katika uzito wa Super Middle kwa Technical Knock Out. Picha ya mwisho ndani ya faili lile ilimuonesha Deus akimvugumizia konde la kulia katikati ya uso mpinzani wake, ngumi ambayo ndiyo iliyomvunja mwamba wa pua na kumvua ubingwa. Hii ilikuwa ni miezi sita iliyopita… Roman alishusha pumzi ndefu huku akilifunika lile faili. Aliketi kwa muda mrefu pale kwenye kiti akiwa amejawa na tafakuri nzito, kisha akainuka na kutoka nje. Alienda kuketi kwenye kona moja ndani ya ile baa iliyokuwa nje ya ile klabu na kuagiza kinywaji. Uso wake ulikuwa umekunjamana kwa mawazo mazito. Muda mfupi baadaye, Makongoro “Mark Tonto” Tondolo aliingia eneo lile na kuanza kuelekea kule kwenye klabu yake ya ndondi. Roman alimpigia mbinja, na Mark alipogeuka, alimpungua mkono. “Haya niambie nini kilitokea jana Roman…Inspekta Fatma alikuibukia hadi huku?” Mark alisema huku akiketi kwenye kiti mbele ya Roman. Roman aliita muhudumu na Mark akaagiza kinywaji. “Bora ingekua Inspekta Fatma Mark, angalau yeye najua ni nini kinachomsumbua” “Ama! Ni nani kumbe?” Roman akamsimulia juu ya tukio baina yake na yule mwanadada aliyejitambulisha kwa jina la Kate. Mark alichanganyikiwa. “Mnh!Kate? Kate huyu wa wapi? Na alikuwa anataka nini hasa?” Alijikuta akiuliza maswali ambayo tayari Roman alishajiuliza. Roman alimbetulia mabega na kubaki akimtazama tu. Kimya kilichukua nafasi baina yao kwa muda, kisha Mark akaongea. “Okay, sasa unadhani tufanyaje juu ya hii hali?” “Tusifanye kitu…tuendelee na mipango yetu kama tulivyopanga.” “Khah! Sasa na huyu Kate…?” “Kate hatuzuii kufanya lolote. Yeye atakuja tena tu, na safari hiyo hatonitoka kirahisi…” Roman alisema kwa utulivu. Lakini Mark hakuwa na utulivu hata kidogo katika swala lile. “Hii ni mbaya sana Roman…mbaya sana!” Alisema kwa hamasa. Roman alibaki akimtazama akiwa kimya. “Sasa unajuaje iwapo huyu…huyu…Kate, si askari aliyetumwa na Inspekta Fatma Roman? Unajua huyu Fatma mi’ hanipi amani kabisa?” Alizidi kusema kwa wasiwasi. Roman alimtazama yule rafiki yake wa makamu na kumpiga ngumi ya maskhara begani. “Relax kocha, okay? Haitusaidii kuumiza kichwa kwa jambo ambalo hatuna hakika nalo kwa sasa bwana. Lolote ambalo yule dada alikuwa analitaka kwangu, hakulipata, hivyo lazima atarudi tena, na hapo ndipo tutajua. Kwa sasa tunaendelea na mambo yetu kama kawaida.” Alimwambia kwa kirefu. Mark alimtazama kwa muda, kisha huku bado uso wake ukiwa makini, alimwambia; “Tutaendelea na mipango yetu kama kawaida, lakini hatutakiwi ku-relax hata kidogo juu ya swala la huyu Kate, Roman…mpaka tujue ni nini hasa anataka kutoka kwako, okay?” “Okay, kocha wangu…” Kimya kilichukua nafasi kwa muda wakati watu wale wawili wakiendelea kunywa vinywaji vyao, kila mmoja akiwa na mawazo yake. “Kesho ndio mnaanza mechi za kugombea ubingwa wa wilaya, sio?” Hatimaye Roman aliuliza. “Yeah Roman. Naona vijana wako katika hali na ari nzuri, natumai tutashinda tu…” Kimya kilitawala tena. “Jina langu limo kwenye orodha ya mabondia waliosajiliwa kwenye timu yako?” Roman aliuliza tena.
“Kama tulivyopanga Roman. Nilikusajili tangu wakati uko gerezani, na kama bado una nia ya kuendelea na azma uliyoweka, basi nawe utapanda ulingoni pindi ukiwa tayari…” “Azma iko pale pale Makongoro. Ila itabidi vijana wako wafanye kazi ya kuvuka katika ngazi hii ya wilaya, mimi nitaingia kwenye ngazi ya mkoa…nahitaji mazoezi zaidi…” Roman alimjibu, kisha akaendelea, “…unadhani wanaweza kutuvusha?” “Ninajua kuwa wanaweza kutuvusha…” Mark alijibu kwa kujiamini.
****
Kwa wiki mbili mfululizo baada ya siku ile, Roman alijishughulisha katika mazoezi mazito sana ya ndondi. Akikimbia umbali mrefu kila alfajiri na kurudi kwenye ile klabu yao ya ndondi kwa ajili ya mazoezi zaidi ya viungo na ya ulingoni chini ya usimamizi makini wa kocha wake wa muda mrefu, Mark Tonto. Timu yao ya ndondi haikufanikiwa kuchukua ubingwa wa wilaya, lakini ilifanikiwa kusonga hadi ngazi ya mkoa kwa kutoka washindi wa pili katika ngazi ile ya wilaya. Na katika wiki mbili zile, pamoja na kuweka umakini wa hali ya juu kila alipokuwa, Roman hakuonana tena na Kate wala Inspekta Fatma. Mazoezi yaliendelea kwa nguvu, na kadiri alivyokuwa akiendelea na mazoezi, ndivyo alivyozidi kujihisi akirudia kwenye uwezo wake wa ngumi aliokuwa nao hapo awali…kabla hajapigwa marufuku kushiriki katika mchezo ule aliokuwa akiupenda sana, na kujikuta akikaa nje na ulingo kwa miaka mingi, miwili kati ya hiyo akiwa gerezani. Kadiri siku zilivyosogea, ndivyo alivyozidi kuhisi msisimko wa ajabu wakati utashi wa mchezo ule ukimtambaa ndani ya mishipa yake ya damu. Mchezo wa ngumi…ndondi…mchezo wa mabondia. Naye sasa alikuwa anajiandaa kuingia tena ulingoni kushiriki mchezo ule. Wengi walikuwa wakishiriki mchezo ule kwa ajili ya kutaka sifa na umaarufu, wakati wengine walikuwa wakishiriki kwa ajili ya pesa tu, ilhali wengine ilikuwa ni kwa ajili ya pesa na umaarufu na sifa. Na wachache miongoni mwa mabondia walikuwa wakishiriki mchezo ule kwa upenzi tu wa michezo kama ilivyokuwa kwake kabla hajapigwa marufuku… na kabla ya kifungo chake. Lakini safari hii Roman alikuwa anarudi ulingoni kwa ajili ya kutimiza azma. Azma ya hatari. Azma iliyokuwa ikifumfukuta moyoni kwa miaka miwili. Azma iliyogubikwa usiri mkubwa. ***
Roman alikuwa akikimbia huku akitupa ngumi mbele yake na kuruka huku na huko kibondia kando ya barabara. Alikuwa amevaa suruali ya mazoezi na fulana nchinjo ya mazoezi ambayo ilikuwa na kofia iliyofunika kichwa chake. Usoni alikuwa amevaa miwani maalum ya kumkinga na upepo na vumbi. Mark Tonto alikuwa akimfuta nyuma taratibu akiwa kwenye baiskeli. Walikuwa kwenye mazoezi makali, ikiwa ni siku tatu tu kabla ya kuanza kwa mashindano ya ndondi za ridhaa kugombea ubingwa wa mkoa, safari hii Roman naye akiwa miongoni mwa mabondia wa Kawe Boxing Club watakaopanda ulingoni. Wakiwa katika harakati zao zile za mazoezi, hawakuitilia maanani kabisa Toyota Prado short chasis yenye rangi ya metallic iliyokuwa imeegeshwa kando ya barabara ile waliyozoea kuitumia kila asubuhi kwa ajili ya mazoezi yao makali. Ndani ya ile gari, Master D na Kate walikuwa wakiwatazama kwa utulivu wawili wale wakiendelea na mazoezi yao. Kate alimtazama yule jamaa aliyetoka gerezani siku kadhaa zilizopita jinsi akitupa masumbwi hewani namna ile huku akiranda kulia na kushoto kistadi wakati akikimbia kando ya ile barabara, na uso wake ukafanya tabasamu dogo. “Enhe? Nini kinafuata sasa Master D?” Alimuuliza yule mtu mzima aliyekuwa naye ndani ile gari huku bado akiwaangalia akina Roman. Ilikuwa ni zamu ya Dan kuachia tabasamu dogo, kisha akaliondoa gari kando ya barabara, akawapita akina Roman na kuondoka eneo lile. “Kinachofuata ni kukabiliana na Roman sasa…nadhani mambo yanaenda kama tutakavyo…” Master D alimjibu. “Okay…lini sasa?” Kate alihoji. “Soon…very soon…(muda mfupi sana ujao) mrembo wangu!”
*** Mashindano ya ndondi kugombea ubingwa wa mkoa wa Dar es Salaam yalichukua muda wa wiki tatu. Katika wiki ya kwanza Kawe boxing club ilipandisha mabondia wanne ulingoni, watatu wakishinda na mmoja akipoteza pambano. Roman alikuwa miongoni mwa watatu walioshinda kwa kumuangusha mpinzani wake katika raundi pili tu ya pambano, na hapo hapo kujipatia mashabiki kwa jinsi alivyokuwa akipigana. Wakiwa mazoezini ndani ya ile klabu yao mwisho wa ile wiki ya kwanza,Roman alipata ugeni asioutarajia. Siku hiyo alikuwa ulingoni akipigana na bondia mwenzake ikiwa ni sehemu ya mazoezi, mkufunzi wao Mark Tonto akiwa kama muamuzi na wakati huo huo akitoa mafunzo. Mabondia wengine wa timu ile ya ndondi walikuwa nje ya ulingo wakifuatilia pambano lile la mazoezi kwa makini, wote sasa wakiwa wamemkubali Roman kama mwenzao na kama bondia mwenye uwezo mkubwa miongoni mwao. Yule bondia alikuwa akimjia kwa ngumi kali za mfululizo, na Roman alikuwa akiruka huku na kule, akitupatupa miguu yake mbele na nyuma kiufundi huku akimsogezea uso mpinzani wake na kuurudisha nyuma kila jamaa alipojaribu kumtupia konde, hoi hoi na vifijo vikirindima kutoka kwa mabondia wenzao waliokuwa nje ya ulingo. Jamaa alikuwa akimjia kwa kasi, Roman aliyumba kushoto na kubonyea kidogo huku akimsogelea, wakati jamaa alipotupa konde kali la kushoto lililopita hewani, na Roman aliibuka na upper cut iliyotua sawia kidevuni kwa mpinzani wake na kumpeleka chini kama mzigo. Shangwe ziliibuka kutoka kwa mabondia wenzao, wakati Roman akimsaidia bondia mwenzake kuinuka kutoka pale chini. “Pole partner…sikuipa nguvu zangu zote hata hivyo…kwa hiyo hutadhurika sana!” Alimwambia yule bondia huku akimsaidia kusimama. “Sasa huo ndio upiganaji Roman!” Mark alisema kwa hamasa huku akiwasogelea wale wapiganaji wake, na kumgeukia yule kijana aliyepelekwa chini kwa konde la Roman, “…na ule si upiganaji! We’ umenaswa kwenye mtego wa Roman, Chumbi… anakuchezeshea uso nawe unautamani uso, unasahau kujikinga…” Mark alikuwa akisema, lakini hapo macho yake yaliangukia nje ya ulingo, na kutulia huko kwa muda, sentensi yake ikibaki ikielea hewani. Alimtupia jicho la haraka Roman, na kuyarudisha tena macho yake kule nje ya ulingo. Roman aligeuka kufuata ulelekeo wa macho ya Mark, kama jinsi ambavyo na wale mabondia wengine walikuwepo pale walivyofanya. Inspekta Fatma alikuwa amesimama nyuma kabisa ya ule ukmbi wao wa mazoezi, akiwa amevaa mavazi yake ya kiaskari, kofia yake akiwa ameikumbatia chini ya kwapa lake la kushoto. Kwa mkono wake wa kulia alikuwa ameshika fimbo yake ya kiaskari ambayo alikuwa akiipiga-piga taratibu kwenye tumbo la kiganja chake cha kushoto. Uso wake uliokuwa umefunikwa kwa miwani myeusi ulikuwa ukimtazama Roman moja kwa moja kule ulingoni. “Sasa huyu anataka nini tena hapa?” Mark Tonto alisema kwa sauti ya chini huku akimtazama yule askari wa kike. Roman alimuacha Chumbi na kuusogelea ukingo wa ule ulingo na kusimama akiwa ameshika kamba ya ulingo ule huku akimtazama Inspekta Fatma. Walibaki wakitazamana kwa muda, kisha Inspekta Fatma aliweka kofia yake kichwani taratibu, na bila ya kusema neno lolote, aligeuka na kuondoka. Hivyo tu! Roman na Mark walitazamana, lakini hakuna yeyote kati yao aliyesema neno, kisha Mark akawageukia wale mabondia wake. “Alrigh, alright, alright, Hey! Haya tunaendelea, tumeshaona jinsi Roman na Chumbi walivyojifua…sasa nataka niwaone Dulla na Kibwe ulingoni…” Alisema huku akipiga makofi kuwahamasisha wachezaji wake. Roman aliteremka ulingoni, na taratibu aliondoka eneo lile kuelekea ofisini kwa Mark, ambako ndiko kilikuwa chumba chake cha kulala. Uso wake ulikuwa umekunjamana kwa tafakuri nzito. “Sasa ndio nini vile?” Mark Tonto alimuuliza Roman saa moja baadaye wakiwa wamekaa kwenye ile baa iliyokuwa nje ya klabu yao ya ndondi pale Kawe, kisha akaendelea, “…yule askari ana maana gani kuja hapa na kuondoka bila kusema neno?” Roman aliuma mdomo wake kwa hasira. “Alikuwa anajaribu kunipa ujumbe Mark…” “Ujumbe gani sasa?” “Kwamba bado ananifuatilia na kwamba nisisahau onyo alilonipa siku ile nilipotoka gerezani.” Mark alitikisa kichwa kwa mastaajabu. “Ama hakika huyu mwanamke majinuni…sasa tufanyaje Roman?” “Sisi tunaendelea na harakati zetu kama kawaida, hakuna kinachobadilika.Hii mikwara ya Inspekta Fatma hainitishi hata kidogo mimi.” Wiki ya pili ya mashindano ya ubingwa wa mkoa wa ndondi za ridhaa, Kawe boxing club ilipoteza bondia mmoja, na Roman na Chumbi wakasonga mbele kwenye fainali, safari hii Roman akimuangusha mpinzani wake katika dakika ya kwanza tu ya raundi ya nne na ya mwisho. Lilikuwa ni pambano lililojaa hoi hoi na nderemo kwa jinsi Roman alivyokuwa akimchezea yule mpinzani wake, na hatimaye kumuangusha kwenye ile raundi ya mwisho. Sasa Roman alikuwa ni miongoni mwa mabondia wenye mashabiki wengi kabisa katika mashindano yale. Jioni ile Mark aliandaa sherehe fupi pamoja na mabondia wake kuwapongeza Roman na Chumbi kwa kufikia fainali ambayo ingefanyika katika wiki ifuatayo. Wakiwa katikati ya sherehe zao pale kwenye ile baa iliyokuwa nje ya klabu yao, Mark alinunua gazeti la jioni lililokuwa likipitishwa na mchuuzi pale baa na kumuonesha Roman habari iliyokuwa kwenye ukurasa wa michezo wa gazeti lile. Deus wa mauaji kukabiliana na Mswazi. Kichwa cha habari ile kilinadi, na mara moja Roman akawa makini na habari ile, ambayo ilieleza kuwa bingwa wa dunia wa uzito wa Super Middle Deus “deadly” Macha alikuwa akitarajia kuzipiga na bondia kutoka Swaziland katika pambano la kimataifa kutetea ubingwa wake alioupata miezi sita iliyopita. Pambano lile lilipangwa kufanyika mwisho wa wiki ile, siku ya jumamosi katika ukumbi wa PTA jijini. Habari ile ilileta mjadala baina ya wale mabondia wa ile timu ya Kawe, baadhi ya wale mabondia wakimsifia Deus jinsi alivyo mahiri katika masumbwi, na jinsi alivyokuwa akiwaangusha wapinzani wake, wengine wakitamani siku moja kuwa kama yeye. Roman na Mark Tonto walitulia kimya akiwasikiliza wale vijana wakimjadili Deus. “Okay boys, mnaonaje sote tukienda kushuhudia pambano hilo jumamosi hii, eenh?” Hatimaye Mark aliuliza. Mayowe na shangwe vililipuka kutoka kwa vijana wale, wakiiafiki hoja ile ya Mark kwa mbinja na hoi hoi, wengine wakirukaruka huku wakitupa ngumi hewani na kucheza kibondia kufurahia swala lile. “Aaah, acheni fujo sasa, ebbo!” Mark aliwaasa wale vijana wake kwa ukali huku akiona wateja wengine pale baa wakionekana kuwashangaa na kukereka kwa mayowe yale. Roman aliinuka na kuondoka na lile gazeti kuelekea chumbani kwake bila ya kuaga. Mwili ulikuwa ukimtetemeka kwa mchanganyiko wa hamasa na jazba.
***
Siku ya pambano ukumbi wa PTA ulifurika mashabiki wa kitaifa na kimataifa. Baada ya mapambano ya utangulizi hatimaye ulifika wakati ambao hasa watu wote waliofurika pale walikuwa wakiusubiri. Bondia kutoka Swaziland alipanda ulingoni akisindikizwa na kocha na wapambe wake wachache, shangwe kidogo zilisikika,lakini zaidi ilikuwa ni sauti za kuzomea kutoka kwa mashabiki wa Deus. Kisha akaingia Deus mwenyewe akiongozana na kocha na promota wake pamoja na msururu wa wapambe, muziki wa bongo flava maalum wa kumsindikiza ukirindima kutoka kwenye maspika makubwa yaliyotandazwa kila kona ya ukumbi ule, mayowe, vifijo na mbinja vilirindima kila upande, na kadiri zile shangwe zilivyozidi, ndivyo Roman, akiwa miongoni mwa watazamaji waliohudhuria pambano lile pamoja na mabondia wenzake wa Kawe Boxing Club na kocha wao Mark Tonto, alivyoweza kusikia muitiko wa pamoja kutoka pale ukumbini. “Deus…Deadly…Deus…Deadly…Deus…Deadly…!” Roman alitulia kimya akitazama kila tukio kwa makini, na kengele ya kuanza pambano ilipogongwa, alishuhudia jinsi Deus akimsulubu mpinzani wake kutoka uswazi kwa namna ambayo ilimfanya aelewe ni kwa nini alifikia hatua ya kuitwa “Deus wa mauaji”. Mswazi alienda chini mara mbili, kwenye raudi ya nne na ya tisa, na alipoenda chini kwa mara ya tatu kwenye raundi ya kumi hakuinuka tena. Kwisha kazi. Deus alikuwa amefanya “mauaji’ kwa mara nyingine. Ukumbi ulipagawa kwa vifijo. Mashabiki walijaribu kuvamia ulingo, kabla ya kutulizwa na Deus akatangazwa mshindi rasmi. Hapo ukumbi ulilipuka upya, Deus aliinuliwa juu huku akizungusha ngumi hewani kushangalia ushindi wake. Roman alisimama na kuanza kusogea karibu na ule ulingo, Mark Tonto akiwa sambamba naye. “Vipi Roman…” Mark aliuliza. “Nataka nimuone vizuri…” Roman alijibu huku akijisukuma mbele na kusimama hatua chache kando ya ule ulingo, akiwa amefumbata mikono kifuani kwake akimtazama yule bingwa wa dunia mtanzania akifurahia ushindi wake. Na ndipo ghafla, katika kuzunguka kwake huku na huko akishangilia ushindi wake ilhali uso wake ukiwa na tabasamu pana, macho ya “Deusdeadly” Macha yalipoangukia kwa Roman akiwa amesimama kando ya ule ulingo akimtazama. Walionana…uso kwa uso. Ghafla uso wa bingwa wa dunia Deus ulibadilika, na lile tabasamu likafutika, nafasi yake ikichukuliwa na mshangao, kisha kitu kama woga mkubwa, na haraka ule woga ukachukuliwa na ghadhabu. Alijikurupusha na kuteremka kutoka mabegani kwa yule shabiki aliyekuwa amembeba. Katika kufanya hivyo,aliinamisha kichwa chake kuangalia asianguke, na wakati alivyofanya vile, Roman aliweza kumuona Inspekta Fatma akiwa upande wa pili wa ule ulingo. Yule askari hakuwa akiangalia yale yaliyokuwa yakitendeka ndani ya ule ulingo, bali alikuwa akimtazama Roman kutokea kule alipokuwa amesimama! “Shit! Inspekta Fatma!” Roman alinong’ona kwa hasira na kujirudisha nyuma akijichanganya kwenye umati wa mashabiki waliokuwepo pale. “Wapi…wapi?” Mark Tonto alinong’ona kwa wahka, lakini Roman alimshika mkono na kumvutia kule alipokuwa akitowekea, akizidi kujichanganya katikati ya kundi la watu. “Deusdeadly” Macha, bingwa anayeendelea kutamba na mkanda wake wa dunia katika uzito wa Super Middle, alitoka mbio hadi kwenye ukingo wa ulingo katika ule upande ambao alimuona Roman akiwa amesimama hapo awali, na kuangaza macho yake yaliyojaa wahka eneo lile. Patupu! Roman hakuwepo! Badala yake aliona kundi la mashabiki tu wakimshagilia na kumpungia mikono huku nyuso zao zikiwa zimejawa tabasamu. Deus hakuwatilia maanani. Alikuwa akimtafuta Roman katika kundi lile lakini hakumuona tena. Aligeukia upande wa pili wa ulingo ule hali ikawa vilevile, aliranda huku na huko ndani ya ulingo ule akijaribu kumtafuta tena Roman, lakini Roman hakuonekana kabisa machoni mwake. Ilikuwa kama kwamba yule aliyemuona hakuwa Roman bali ni taswira tu iliyojijenga kichwani mwake! Kwenye kona moja ya ukumbi ule, Master D alimgeukia Kate na kumwambia huku akiinuka kutoka kwenye kiti chake. “Okay, tunaweza kwenda sasa mrembo wangu…tumeona mengi kwa leo au sivyo?” “Sana anko…sana tu. Si umeona jinsi uso wake ulivyohamanika alipomuaona Roman? E bwana we! Leo mbona tumeona mambo!” Kate alisema huku naye akiinuka.
*****
Roman alikuwa akikimbia kando ya barabara asubuhi huku akitupa-tupa ngumi hewani mbele yake kama kawaida yake. Asubuhi hii alikuwa peke yake. Ilikuwa ni asubuhi ya siku ya pili baada ya lile pambano la Deus na mswazi. Yeye pambano lake lilikuwa siku ile jioni, ambapo angepanda ulingoni na bondia kutoka timu ya wilaya ya Ilala, kugombea ubingwa wa mkoa katika ndondi za ridhaa. Alikuwa akikimbia katika upande wa barabara ambao ulimuwezesha kuona magari yaliyokuwa yakimjia mbele yake. Hata hivyo alfajiri ile barabara ile haikuwa na magari mengi, na ndio maana alipenda kukimbia alfajiri. Mbele yake, kiasi cha mita ishirini hivi, gari aina ya Toyota Prado Short Chasis Metallic lilikuwa limeegeshwa kando ya barabara likiwa limeelekea kule alipokuwa akielekea yeye, lakini upande wa pili wa barabara. Kutokea nyuma yake alisikia mvumo wa gari likielekea kule alipokuwa akikimbilia yeye, lakini hakutilia maanani, alikuwa akiendelea na mazoezi yake tu kama kawaida. Mvumo wa lile gari lililokuwa likitokea nyuma yake uliongezeka na akahisi kama lile gari lilikuwa likiongeza kasi, na hata wakati wazo lile lilipokuwa likipita kichwani mwake, aliona mlango wa ile Prado iliyokuwa imeegeshwa mbele yake, ambayo sasa ilikuwa umbali wa kama mita tano tu kutoka pale alipokuwa, ukifunguka ghafla na mtu mmoja aliyekuwa amevaa suruali na fulana ya mazoezi akiruka nje na kumpungia mikono kwa wahka huku akipiga kelele, na hapo hapo alilisikia lile gari liliyokuwa nyuma yake likimkaribia huku likizidisha kasi. Oh, my God! Nagongwa…! Bila ya kugeuka nyuma, Roman alizidisha kasi ya mbio na hapo hapo alijirusha kwa nguvu kulia kwake na kuangukia kwenye kichaka kilichokuwa kando ya ile barabara. Muda huo huo aliliona gari ndogo likimpita kwa kasi sana usawa wa pale alipokuwa akikimbilia sekunde moja tu iliyopita, alijibiringisha na kusimama wima akilitazama lile gari likiyumba kidogo baada ya kumkosa na kurudi barabarani, likimkosakosa na yule mtu aliyeruka kutoka kwenye ile Prado, ambaye alijirusha upande wa pili wa gari lake lile gari lililomkosa kumgonga likitokomea kwa kasi eneo lile. Yaani lile gari ilihama kutoka upande wake na kumfuata kule alipokuwapo! Tusi zito lilimtoka Roman, na kutimua mbio kukimbilia pale kwenye ile Prado na kuzunguka upande wa pili huku akitweta. Moyo ulimlipuka na kujikuta akibwata huku akiwa amekodoa macho. “Wewe!!” Kate alikuwa amekaa chini kando ya lile gari huku akiwa amejishika mguu wake. “Unajua kwenye pochi yangu kulikuwa kuna hela mle?” Kate alimwambia huku akitabasamu, ingawa alionekana kama kwamba alikuwa kwenye maumivu makali. “Ama?” Roman alimshangaa yule binti na kubaki akimkodolea macho, kisha akamtupia swali, “Unasemaje wewe?” “Jamaa zako walikuwa wanataka kukugonga wale! Na kwa kasi ile wangekuua tu!” Kate alisema tena, akipuuzia lile swali la Roman. Roman alizidi kuchanganyikiwa. “Jamaa zangu? We’ umewaona waliokuwa kwenye lile gari?” “Kulikuwa kuna watu wawili, ila sijawaona sura…walikuwa wamekudhamiria wewe haswa!” “Sasa we’ ulikuwa unafanya nini huku. Na usiniambie kuwa ulikuwa unanitafuta mimi tena!” Roman alimwambia kwa jazba. “Ndio haswa. Nilikuwa nakuvizia wewe. Na ni bora nilivyofanya hivyo kwani nimekuokoa, kwani kama si mimi kukupigia kelele za kukutahadharisha jamaa wangekugonga wale!” “Mnh! Kweli…ahsante sana. Lakini…kwa nini ulikuwa unanivizia huku saa hizi?” “Si nikudai pesa zangu!” Kate alimjibu kwa maskhara huku bado akiwa amefinya uso kwa maumivu. Roman alibaki akimtazama kwa mastaajabu. “We’ unafanya maskhara kwenye kila kitu, eenh?Hebu inuka hapo unieleze vizuri ni nini kinachoendelea hapa?” “Siwezi…nadhani nimetegua mguu! Nisaidie tafadhali…!” Kate alimwambia huku uso wake ukionesha kuwa alikuwa kwenye maumivu makali. Roman alimsaidia kuinuka, na alipojaribu kutembea tu yule msichana aliachia kiyowe kidogo cha maumivu na kuanza kuanguka tena chini, lakini Roman aliwahi kumdaka kiuno. “Dah! Nimeumia sana…naomba unisaidie kuingia kwenye gari…” Kate alisema kwa uchungu. Roman alimsaidia na kumuweka nyuma ya usukani. “Oh, Roman samahani, lakini itabidi uniendeshe, mimi sitaweza, kwani mguu niutumiao kuendeshea ndio ulioumia…” Kate alisema akiwa kwenye maumivu makali. Roman alimtazama yule dada kwa muda na akaona kuwa hakuwa akifanya maskhara. “Sasa unajuaje kama mi’ naweza kuendesha?” Alimuuliza. “Oh, come on Roman, mi najua mengi juu yako bwana, kwa hiyo najua kwamba unaweza kuendesha gari…hebu nisaidie tafdhali, nipeleke nyumbani!” “Nikikusaidia utanieleza kinachokufanya unifuate-fuate namna hii?” “Of course nitakueleza…leo nd’o nilikuwa nataka tupange siku ya kuonana, lakini ndio yametokea haya…twende tafadhali!” Kate alimjibu huku akijisukumia kwenye kiti cha abiria kule mbele. Roman aliangaza huku na huko, kisha akaingia nyuma ya usukani na kuliondoa lile gari kutoka eneo lile. Njiani Roman alijaribu kuwaza juu ya tukio lile la kukoswa kugongwa, lakini hakuweza kuwaza kitu cha msingi juu ya tukio lile kwani Kate alikuwa akimuongelesha. “Inaelekea una maadui wengi Roman…mpaka wengine wanataka kukugonga na magari!” “Hilo halinipi taabu.Linalonipa taabu ni wewe uko upande gani Kate, na unataka nini kwangu?” “Mnhu! Kuhusu mimi usiwe na taabu. Mi’ niko upande wako, na nd’o maana nikakupigia kelele nilipoona kuwa lile gari lilikuwa linaelekea kukugonga…” “Na ndo maana siku ile ukaja kupekua ofisini kwetu na kunitoroka?” Roman alidakia. Kate alicheka. “Siku ile ulinishtukiza Roman, sikuwa na namna zaidi ya kukutoroka…I am so sorry…” Kate alimjibu, na kuendelea, “…lakini pesa zangu nazitaka ujue, nilijua siku tukikutana n’takudai tu!” “Pesa zako zipo na wala sijazitumia, ila sinazo hapa. Sasa je unaweza kuniambia ni nini unachotaka kwangu Kate…kama hilo ni jina lako kweli?” “Okay…kwanza Kate ni jina langu kweli…kama jinsi Roman lilivyo jina lako la kweli. Na pili…ninachotaka kutoka kwako ni muda wako tu…kuna mtu nataka nikukutanishe naye Roman. Ni muhimu sana kwako na kwake pia!” Kate alimjibu, safari hii uso wake ukiwa umepoteza kabisa maskhara. “Ni nani huyo unayetaka nikutane naye? Na ana nini ambacho ni muhimu kwangu na kwake?” “Mimi kazi yangu ni kukutanisha naye tu Roman. Najua leo una pambano la ngumi jioni, unaonaje tukija kuonana nawe baada ya pambano leo usiku pale kwenye ile baa ya pale kwenye klabu yenu?” Kate alisema. Roman alitikisa kichwa kwa mastaajabu. “Inaelekea unajua mambo mengi juu yangu Kate…why?” “Labda leo usiku utajua, nikimleta huyo mtu anayetaka kukutana nawe.” Kate alimjibu. Baada ya hapo Roman hakuongea tena. Aliendesha kimya mpaka alipomfikisha Kate nyumbani kwake. Kate alipomkaribisha ndani hakukubali. “Sasa utarudi vipi? Ngoja basi nikupe pesa ya teksi…” Kate alimwambia. “Usijali…n’tarudi kwa mbio tu…si unajua bado nilikua mazoezini?” Roman alimjibu. Kate alichanganyikiwa kidogo, lakini Roman hakumpa muda wa kuongea zaidi. Aliruka nyuma hatua mbili, akageuka, na kuanza kukimbia kimazoezi kurejea kwenye klabu yake ya ndondi. “Basi sisi tutakuja huko leo usiku, okay?” Kate alimpigia kelele. Roman alimpungia mkono bila ya kugeuka wala kupunguza kasi…
***
Jioni le Roman alipanda ulingoni akiwa na ghadhabu kubwa, ghadhabu ambayo alikuwa ameielekeza kwa yule mtu asiye sura aliyetaka kumgonga makusudi asubuhi ile. “Nakupa asilimia tisini na tisa Deus anahusika na tukio hilo Roman!” Mark alisema baada ya Roman kumsimulia tukio lile asubuhi ya siku ile. “Kwa nini unasema hivyo Mark…? Angeweza kuwa mtu mwingine yoyote…” Roman aliuliza, ingawa hata yeye alikuwa na hisia kama alizokuwa nazo Mark. “Acha hizo Roman! Huyu ni yeye tu! Kwanza jiulize…iweje siku zote jambo hili lisitokee lije kutokea leo baada ya yeye kukuona kwa mara ya kwanza tangu urudi uraiani? Ni yeye bloody swine…ni yeye!” Mark alimjibu kwa jazba. Ghadhabu zake zilimuishia mpinzani wake pale ulingoni jioni ile, kwani kwa mara ya kwanza tangu arudi tena kwenye ngumi za ridhaa, Roman alitupa makonde mazito kabisa yaliyosukumwa na ghadhabu iliyokuwa ikimchemka mwili mzima. Alisukuma makonde ya nguvu na hasira kiasi kwamba katika raundi ya kwanza tu alishamdondosha chini mpinzani wake mara mbili, na alipomdondosha mara ya tatu katika raundi ile, muamuzi akatangaza Technical Knock-Out, na Roman akaipatia timu yake ya Kawe Boxing Club ubingwa wa wilaya! Ndani ya dakika tatu tu! Ukumbi ulilipuka kwa hoi hoi na vifijo, mabondia wenzake walivamia ulingo kwa furaha, naye akajikuta akiinuliwa juu juu, akiwa ameinua juu ngumi kuashiria ushindi wake ilhali sura yake bado ikiwa imefura kwa hasira…
***
“Hongera kwa kunyakua ubingwa Roman…hakika leo umepigana kwa namna tofauti kabisa na mapambano yako yaliyopita…” Dan Dihenga alimwambia mara baada ya kutambulishana na kusalimiana jioni ile. “Oh, ahsante…kwani ni mapambano yangu gani mengine uliyowahi kuyaona?” Roman alimjibu na kumuuliza huku akimtupia jicho Mark Tonto aliyekuwa pamoja nao pale kwenye meza iliyokuwa kweye kona kabisa ya ile baa iliyokuwa nje ya klabu yao ya ndondi. “Oh, tumekuwa tukihudhuria mapambano yako yote Roman…” . Master D alimjibu huku akitabsamu, na kuendelea, “…na nd’o maana nakwambia leo umepigana kwa namna tofauti kabisa na mapambano yako yote hayo niliyowahi kuyashuhudia.” “Mnhu! Ukiniuliza mimi n’takwambia kuwa leo amepigana kwa ghadhabu zaidi kuliko vinginevyo!” Kate alisema huku akimtazama Roman kwa macho ya uchokozi. Muda ulikuwa ni saa mbili za usiku. Kate na Master D walifika pale klabuni kiasi cha saa moja na nusu za jioni na kutulia pale kwenye baa kwa muda, wakisikia shangwe na hoi hoi zilizokuwa zikirindima pale kwenye ile klabu ya ndondi ya akina Roman mpaka wale mabondia wengne walipoondoka na kuwaacha Roman na Mark Tonto pale klabuni. Ndipo Kate, huku akichechemea,alipokwenda kuwabishia hodi na kuwaarifu kuwa walikuwa wameshafika. Ndipo wapojumuika nao pale kwenye ile meza waliyokuwa wamekalia. “Okay, mnaonaje mkitueleza dhamira ya ujio wenu?” Mark Tonto aliuliza huku akiielekeza kauli yake kwa Master D. Roman alitikisa kichwa kuafiki kauli ya Mark. “Sawa kabisa…” Dan alisema na kujiweka sawa, kisha akaendelea, “…kama nilivyojitambulisha hapo awali, mi’ naitwa Dan Dihenga…na huyu ni mpwa wangu Kate…” “Na kama nilivyosema hapo awali, jina lako si geni masikioni mwangu Mr. Dihenga…” Mark alisema. “Yeah, na kama ungekumbuka ni katika mazingira gani ulipata kulisikia jina langu, moja kwa moja ungejua dhima ya ujio wetu huu…” “Sasa unaonaje ukituweka wazi Mr. Dihenga, maana mi’ nahitaji kujipumzisha…” Roman, bingwa mpya wa ngumi za ridhaa wa uzito wa Super Middle kwa mkoa wa Dar es Salaam, alisema. “Very well Roman. Nitaenda moja kwa moja kwenye swala lililo kichwani mwangu…” Master D alisema na kumtazama Roman kwa muda, kisha akamgeukia Mark Tonto, na kumrudia tena Roman, “…nataka nikuingize kwenye ndondi za kulipwa Roman…nataka niwe promota wako…” Moyo ulimpasuka Roman kwa kauli ile, na akafinya macho kidogo kwa umakini huku akimtazama yule mtu aliyeketi mbele yake, kisha akamtupia jicho Mark, moyo ukimwenda mbio. Hapo hapo Dan akamgeukia Mark haraka. “Eenh, sina nia ya kukuvua nafasi yako kwa Roman Mark…la hasha, najua wewe ndiye umekuwa promota na kocha wake, lakini…” “Nimeshakukumbuka sasa!” Mark alisema kwa hamasa, akimwangalia kwa mtazamo mpya yule mtu huku akimuoneshea kidole. Dan Dihenga alimuinulia nyusi na kutamtazama kama kwamba akimwambia “alaa?” “Wewe ni Dan Dihenga!” Mark alisema huku bado akiwa na hali ya mshangao. Roman aliachia mguno huku akimtazama Dan kwa makini. “Hilo hata mimi nalijua Mr. Tondolo…” Master D alimjibu huku akitabasamu, lakini Mark alikuwa kama kwamba hajamsikia, akaendelea,“Wewe ni promota mkubwa wa ndondi nchini…!” Master D alibetua mabega yake tu bila ya kusema neno. Bado Mark alikuwa akimtazama kwa ule ung’amuzi mpya uliomshukia baada ya kumkumbuka yule mtu. “Wewe…wewe…ndiye promota wa zamani wa Deusdelity Macha!” Mark alimalizia, na hata pale alipomalizia kauli ile, Roman alitoa mguno mkubwa wa mshangao na kumtumbulia macho yule jamaa aliye mbele yao, na kumtupia jicho Kate, ambaye alimtawanyia tabasamu pana ambalo kama kwamba lilikuwa likimwambia “…sasa ulikuwa unatarajia nini?” “There you are!” Dan Dihenga alisema huku akitupa mikono hewani kumaanisha kuwa sasa Mark alikuwa amesema hasa kilichokuwa ndicho. Kimya kilichukua nafasi wakati wale watu wakitazamana, kila mmoja akiuweka sawa akilini mwake ufahamu ule mpya uliotokana na ung’amuzi wa uhalisia wa Dan Dihenga. “Kwa nini?” Hatimaye Roman aliuliza taratibu. “Ndio kazi yangu Roman!” Dan alimjibu, na kuendelea, “Mimi kama promota wa ndondi, ni kazi yangu kutafuta mabondia wazuri na kuwapromoti katika mchezo huu mpaka wafikie mafanikio yanayohitajika kwao, kwangu na kwa mchezo huu wa ndondi hapa nchini na duniani kote. Hiyo ndio azma yangu kubwa katika ku-promoti ndondi…” “Kwa nini umtake Roman…?” Mark aliuliza. Dan alimtazama kama kwamba alikuwa ameuliza swali la kijinga. “Roman ni bondia mzuri! Promota yeyote ajuaye kazi yake akimuona tu Roman apiganavyo, hatosita kum-promoti. Nami ni promota nijuaye kazi yangu Mr. Tondolo…naijua vizuri sana!” Alimjibu. Muda wote huu Kate alikuwa kimya tu akifuatilia mazungumzo yale. “Come on Mr. Dihenga! Kuna mabondia wengi tu wazuri hapa nchini ambao wana uwezo wa kufanya makubwa kama watapata promota kama wewe. Unataka kuniambia kuwa hao wote hukuwaona ila Roman tu?” Mark alimuuliza kwa hamasa. Dihenga alimtazama, kisha akamtupia macho Roman. “Jibu swali bwana Dihenga…why me…and why now?” Roman alimsisitizia swali la Mark, akimaanisha kwa nini amteue yeye na kwa nini amteue wakati ule. Dan aliachia cheko hafifu na kutikisa kichwa kwa mastaajabu.
“Mbona napata picha kama kwamba mnaniona adui ndugu zangu?” Hatimaye aliuliza. “Nadhani hapo mwanzo ulisema kuwa utaenda moja kwa moja kwenye swala lililo kichwani mwako Mr. Dihenga, sasa mbona tena unaaza kusua-sua? Nimesema mapema kuwa mi’ nataka kwenda kujipumzisha. Kwa hiyo kama mtaniwia radhi ndugu zangu, mi’ naenda kulala!” Roman alisema na kuanza kuinuka. Haraka sana Kate ulimdaka mkono na kumzuia. “Hatuendi hivyo mzee!” Alimwambia huku akimtazama usoni. Roman alibaki akimtazama yule binti kwa mshangao, na kabla hajauliza Kate akamwambia, “Hapa huondoki mpaka unirejeshee pesa zangu!” “Ati nini wewe?” Roman alimaka huku akiuchomoa mkono wake kwa nguvu kutoka kwenye himaya ya yule binti. “Achana na Kate Roman, tuongee mambo ya maana. Kaa kitini tafadhali!” Dan alimwambia kwa utulivu. Roman alimtazama Kate kwa muda, kisha akamgeukia Dan. “Nimekuuliza swali jepesi sana Mr. Dihenga…why me? Umeshindwa kujibu kwa hiyo mi’ naona…” “Kwa sababu ni wewe pekee ndiye unayeweza kumvua ubingwa Deusdelity Macha, Roman!” Dan Dihenga alimkatisha kwa kumjibu kwa utulivu ilhali bado akimtazama moja kwa moja usoni. “Atii???” Mark Tonto alimaka huku akiinuka kutoka kwenye kiti alichokuwa amekalia, wakati huo huo, Roman akajikuta akiketi kitini huku akiacha kinywa wazi na akimtazama yule mtu kama kwamba ndio kwanza alikuwa anamuona. “Ndio!” Dihenga alithibitisha jibu lake huku akimtulizia macho Mark kwa muda kkabla ya kuyarudisha tena kwa Roman. “Ni kweli kuwa kuna mabondia wengi wazuri hapa nchini. Lakini nakuhakikishia kuwa hakuna hata mmoja kati yao anayeweza kumuangusha Deus…” Dihenga aliendelea kutetea hoja yake. Mark na Roman walitazamana. Wazi hili halikuwa kabisa miongoni mwa matarajio yao. “Isipokuwa wewe Roman!” Dan alimalizia huku akimuoneshea kidole Roman. Kimya kilichukua nafasi kwenye ile meza. “Kwa nini unataka Deus aangushwe Mr. Dihenga?” Hatimaye Mark alimuuliza, ingawa tayari jibu alikuwa nalo. Dan Dihenga alibadilika kidogo, uso wake ukionesha ghadhabu yenye kufukuta. “Mimi ndiye niliyemfikisha mahala pa kutambulika kimataifa kwenye ndondi mshenzi yule…lakini akathubutu kunigeuka na kunitolea kebehi na kashfa. Nataka nimuoneshe kuwa kama mimi ndiye niliyemfikisha hapo alipo mpaka hao anaowaona ndio mapromota wanaomfaa wakamuona, basi mimi ndiye nitakayemporomosha!” Dan Dihenga alisema. “Na unataka kunitumia mimi katika hicho kisasi chako binafsi?” Roman alimuuliza. “Hapana Roman. Mimi na wewe tunahitajiana katika kumfikisha Deus mahala panapomstahili…” “Nini kinachokufanya uamini kuwa mi’ nataka kushirikiana nawe katika hilo?” Roman aliuliza. Dan alitabasamu kidogo. “Najua mengi juu yako na Deus, Roman…mengi. Hivyo najua kuwa kwa namna moja au nyingine nawe unahitaji kumfikisha Deus mahala panapomsatahili…na pale alipo sasa sipo panapomstahili. Sote twalijua hilo!” Duh! Roman na Mark walichoka. “Unaelewa nini juu yangu na Deus wewe?” Roman alikuja juu. Dan hakufanya haraka kumjibu. Badala yake alimuita mhudumu na kumuomba bili ya vinywaji waliyoagiza pale mezani. Alipewa bili naye akalipa. “Najua kiasi cha kutosha kunihakikishia kuwa mimi na wewe hivi sasa tuna lengo moja kuhusu Deus, nalo ni kumtia adabu. Sababu zetu za kutaka kufanya hivyo zinaweza kuwa tofauti, lakini hakika lengo letu laweza kuwa moja…na…naamini sote tunahitajiana katika hili!” Dan alimjibu baada ya yule mhudumu kuondoka. “Si kweli. Sikuhitaji…hatuhitaji mtu yeyote. Tunajitosheleza kama tulivyo. Naona mkutano huu umekwisha!” Roman alisema. “Kwa hiyo hukatai kuwa nawe una kisasi na Deus?” “Sijui unaongelea nini…” Roman alianza, lakini Dan Dihenga alimkatisha. “Wazee, hilo ndilo nililokuja nalo kwenu. Kitu ninachosema ni kwamba iwapo tutakubaliana, mimi nataka niwe promota wako katika ngumi za kulipwa. Nitakulipa pesa nzuri, nitakupatia vifaa vyote na mahitaji yote muhimu kwa professional boxer, nitakupatia nyumba nzuri ya kuishi, na nitakupa nafasi ya kuuchukua ubingwa ulio mikononi mwa Deus mbabaishaji hivi sasa…” akamgeukia Mark Tonto, “…na kwako, nitakuajiri kama kocha wa bondia wangu Roman, na nitakulipa kwa kadiri ya makubaliano tutakayoafikiana…ambayo nakuhakikishia kuwa yatakuwa ni makubaliano mazuri sana Mark. Wewe ni kocha mzuri, na najua kuwa unajua upiganaji wa mabondia wote wawili hawa.” Alimalizia na kubaki akiwatazama wale watu wawili wenye azma ya siri. Si Roman wala Mark aliyeongea, hivyo Dan akamalizia, “Hiyo ndiyo kete yangu kwenu. Naomba muifikirie kwa makini sana, na baada ya siku tatu nitamtuma mpwa wangu kuja kupata jibu lenu la mwisho. Kama bado hamtakubaliana nami basi nitawaacha na hamsini zenu nami nitaendelea na hamsini zangu. Usiku mwema!” Dan na Kate waliinuka kwa pamoja na kuanza kuondoka, wakiwaacha Roman na Mark wakiwa vinywa wazi. “Kate!” Roman aliita. Kate na Dan walisimama na kugeuka. Roman alitoa ile pochi ya yule dada ambayo ilikuwa mfukoni mwake muda wote, na kuiweka juu ya meza huku akimtazama kwa hasira. Kwisha kufanya hivyo alimuashiria Mark na kwa pamoja waliinuka na kuondoka, ile pochi ikibaki pale mezani. Kate aliirudia pochi yake kwa mwendo wa kuchechemea…
*** Usiku ule Roman na Mark walichelewa sana kulala. Walibaki pale ofisini wakijadili juu ya ule ujio wa promota Dan Dihenga kwa undani. Hofu kubwa ya Roman ilikuwa ni iwapo Dan alikuwa ametumwa na Deus aje kumchimba undani wake, au iwapo atakuwa ametumwa na Inspekta Fatma. “Kwa hayo yote mawili mimi nakataa Roman. Ni kweli kuwa Dan Dihenga ni promota wa ndondi, na ni kweli kuwa alikuwa promota wa Deus…na ni kweli kuwa Deus alimsaliti…hivyo ana kila sababu ya kuwa na kinyongo naye.” Mark alisema. “Kwa hiyo…?” “Kwa hiyo hawezi kuwa kibaraka wa Deus…yule mtu ana kinyongo kikubwa na Deus…si umesoma makala nilizokukusanyia kwenye lile faili? Walifikia hadi hatua ya kutaka kupelekana mahakamani bwana!” “Ni kweli…na sasa nakumbuka kuwa hata jina lake nililisoma kwenye lile faili…” Roman aliafiki, kisha hapo hapo akauliza, “…na vipi kuhusu Inspekta Fatma…hawezi kumtumia?” “Kwa lengo gani? Hali ilivyo, Dihenga ndiye ambaye anaweza kuwa kwenye nafasi ya kumtumia Inspekta Fatma na si vinginevyo. Nadhani nia ya Dihenga ni hiyo hiyo aliyotueleza…anataka akupromoti wewe ili umnyang’anye Deus ubingwa…hiyo ni njia yake ya kumlipizia kisasi. Swala ni je, sisi…wewe…uko tayari kushirikiana naye?” Kimya kilitawala, kisha Roman akarudia tena kauli ambayo tayari alikuwa ameshaitumia zaidi ya mara tatu mle ndani tangu akina Kate waondoke. “Lakini…inaelekea hawa akina Kate wanajua sana habari zangu…hii mimi hainipi amani kabisa Mark!” “Sasa basi ni bora tuwe nao sambamba Roman…!” Mark alisema. “Ili?” “Ili tuweze kujua ni nini hasa wajuacho kuhusu wewe… na sisi tuweze kuwajua wao zaidi…nadhani tukubaliane na wazo la Mr. Dihenga Roman. Kwani sisi hatutapoteza lolote zaidi ya kunufaika…kwanza tutaweza kutimiza azma yetu, pili tutaweza kuitimiza azma hiyo katika mazingira yaliyo bora zaidi…sasa hivi Roman huna kipato chochote, kujiunga na Dihenga kutakupatia makazi bora, vifaa bora zaidi vya mazoezi, na pesa nzuri…nami pia nitanufaika kama kocha wako. Hii ni nafasi nzuri kwetu Roman…ni sawa na nyota ya jaha!” Mark alisema na kubaki akimtazama Roman kwa muda, kisha akamalizia kwa sauti ya chini, “Hiyo ni kama bado una nia ya kuendelea na ile azma yako Roman.” “Azma iko pale pale Mark…iko pale pale!” Roman alimjibu haraka bila hata ya kusita. “Basi na tukubaliane na ofa ya Dihenga…we have nothing to lose (hatuna cha kupoteza) kwa hii ofa Roman!” Mark alimwambia. Siku tatu baadaye, Kate alifuata jibu. “Mwambie Dihenga tumekubali…no problem!” Roman alimwambia bila kupoteza muda. Hii ilikuwa ni taarifa tamu sana kwa Kate na Dan Dihenga.
*****
Maisha ya Roman yalibadilika ghafla. Dan alitimiza kila aliloahidi. Kwa kuhofia jaribio jingine la kumuua Roman, Dan alimhamishia Roman Bagamoyo, ambako alimpangia nyumba ndogo lakini nzuri na yenye kujitosheleza. Mark Tonto kama kocha wake alilazimika awe anaishi baina ya Bagamoyo na Dar. Kila siku akifanya safari za Bagamoyo asubuhi na kurudi jioni, baadhi ya siku akilala huko huko. Huko kazi ilikuwa ni moja tu, nayo ilikuwa ni mazoezi makali. Dan alimpatia Roman vifaa vyote muhimu vya mazoezi, na pale kwenye nyumba aliyompangia alimtengea chumba maalum cha mazoezi (Gym) ambacho kilikuwa na kila kitu. Kwa miezi mitatu mfululizo Roman alijichimbia Bagamoyo akijijenga kibondia. Mark Tonto alikuwa naye muda wote huo ingawa siku nyingine alikuwa akirejea Dar kuwa na familia yake. Kate na Dan nao walikuwa wakimtembelea na kumtazama akifanya mazoezi, wakitumia sehemu ya muda wao kutazama mapambano ya Deusdelity Macha kwenye mikanda ya video. Na katika miezi mitatu ile, Roman na Kate waliondokea kujenga ukaribu, na hata siku nyingine Kate alikuwa akienda kule Bagamoyo peke yake na kukutana na Roman, wakitembea pwani na kuongea mambo mengi na kujuana zaidi. Ndani ya miezi mitatu ile, hakuonana kabisa na Inspekta Fatma, isipokuwa siku moja tu alipoletewa salamu na Mark kuwa Inspekta Fatma alifika pale kwenye klabu yao ya Kawe na kumuulizia. Kwa kuwa hata wale mabondia wa Mark pale klabuni hawakujua Roman alipo, hawakuwa na msaada wowote kwake. Roman aliendelea na mazoezi yake, na Dan hakuishia hapo katika kumjenga zaidi. Pamoja na kuwa na Mark kama kocha, pia alimletea makocha kutoka nje ya nchi ambao walikuja kumuongezea mbinu zaidi za ndondi, ikiwa ni pamoja na namna ya kubadili namna ya upiganaji akiwa ulingoni kutokana na aina ya upiganaji wa mpinzani wake. Na baada ya miezi hii mitatu ya mazoezi makali na ya nguvu, Roman alikuwa tayari kuingia katika ulingo wa ndondi za kulipwa, kama professional boxer.
***
Dan Dihenga alimuandalia Roman pambano lake la kwanza kama bondia wa kulipwa mwezi mmoja baada ya Roman kujinadi kuwa yuko tayari kuingia rasmi ulingoni, ambapo alimpatia mpinzani kutoka afrika kusini. Katika pambano hili Roman alikuwa na nafasi ya kujivunia milioni tano za kitanzania akishinda, na milioni mbili akishindwa. Dan hakutaka kulinadi sana pambano hili kwenye vyombo vya habari, na waliondoka kimya kimya kwenda Afrika Kusini, msafara wao ukimjumuisha Dan, Roman, Mark, Kate na tabibu mmoja. Pamoja nao alikuwamo mwandishi wa habari mmoja. Mark alimuuliza Dan sababu ya kutolinadi ipasavyo pambano lile la kwanza la Roman. “Roman hahitaji kunadiwa Mark…Roman atajinadi mwenyewe baada ya kufanya mauaji huko sauzi…we’ subiri tu, utaona!” Dan alimjibu wakiwa angani kuelekea Johannesburg. Usiku wa pambano jijini Johannesburg, Roman alitoa kipigo cha mbwa mwizi kwa mwenyeji wake, na mnamo raundi ya nane, kocha wa mpinzani wake alilazimika kutupa taulo ulingoni kumnusuru bondia wake! Ukumbi ulilipuka kwa hoi hoi kutoka kwa watanzania wachache waishio Afrika Kusini waliokuwapo pale ukumbini, Roman akiinuliwa juu juu na watanzania wale. Ilikuwa ni furaha isiyo kifani kwa kambi ya Roman kule ugenini. Mara moja habari zilirudi nyumbani, mwandishi wa habari aliyesafiri na akina Roman akituma habari nyumbani usiku ule ule kwa simu, na akituma picha kadhaa za jinsi Roman alivyokuwa akimsulubu mwenyeji wake kwa mtandao wa intaneti. Usiku ule ulikuwa ni usiku wa tafrija kwa kambi ya Roman jijini Johannesburg. Walirejea Tanzania siku iliyofuata, na kukuta habari za pambano la Roman nchini Afrika kusini zikiwa zimetapakaa jijini,na waandishi zaidi wa habari wakiwasubiri uwanja wa ndege. Na ndipo hapa ambapo Dan Dihenga alimpomnadi Roman kuwa ndiye bondia wake mpya. Waandishi walimtupia maswali kadhaa naye kama promota mzoefu alitumia nafasi hiyo kumnadi vizuri sana bondia wake. Alipohojiwa na waandishi juu ya ushindi wake ule, Roman alisema kwa utulivu kabisa kuwa ushindi ule haukuwa ajabu kwake, kwani alijua kuwa atashinda. Ndipo mwandishi mmoja alipomtupia swali Dan. “Bwana Dihenga, je ndio unataka kutuambia kuwa Roman amekuja kuchukua nafasi ya Deusdelity Macha, bondia wako wa zamani na ambaye ndiye bingwa wa dunia hivi sasa?” Bila ya kusita, Dan Dihenga alimjibu yule muandishi, “Nijuavyo mimi Roman ni bondia bora kuliko bondia mwingine yeyote hapa nchini katika uzito wake…hivyo siwezi kusema kuwa kaja kuchukua nafasi ya mtu yeyote hapa, labda tu niseme kuwa amekuja kuchukua nafasi yake inayomstahili!” “Una maana gani kwa kauli hiyo bwana Dihenga?” Waandishi kadhaa walimrukia kwa swali hilo. Dan hakujibu kitu zaidi ya hapo. Alimuongoza bondia wake kwenye gari na kuondoka eneo lile, akiwaacha wale waandishi wakijijazia majibu yao wenyewe. Habari ya pambano lake la afrika kusini ilimfanya Roman awe gumzo kwa wengi nchini. Lakini pia ilimrejesha tena Inspekta Fatma katika maisha yake.
*** Siku mbili baadaye alikuwa amekaa kwenye mgahawa maarufu wa Brake Point akijisomea kitabu cha historia ya bondia Mohammad Ali huku akimsubiri Kate ambaye alikuwa na miadi naye. Mara alishtukia gazeti likitupwa mbele yake pale mezani, na alipoinua uso wake alimuona Inspekta Fatma, ndani ya sare zake za kiaskari, akiwa amesimama mbele yake. Alishusha macho yake na kulitazama lile gazeti. Ukurasa wa michezo wa lile gazeti ulikuwa umebeba kichwa cha habari kilichomnadi: “Roman: Bondia aliyekuja kuchukua nafasi yake katika ndondi”. Chini ya habari ile kulikuwa kuna picha yake akiwa ameinua ngumi juu ilhali bondia msauzi aliyemsambaratisha kule afrika kusini akiwa amechutama kando yake ulingoni. Roman aliachia tabasamu pana na kumtazama tena yule askari wa kike ambaye sasa alikuwa ameshaketi kwenye kiti kilichokuwa mbele yake. “Vipi afande, ina maana sasa unanifuatilia kila niendapo?” “What’s this Roman, eenh?” Fatma alimuuliza kwa jazba huku akiioneshea kidole ile habari iliyokuwa pale gazetini, akilipuuzia lile swali la Roman. “What’s what Fatma? Mi’ sikuelewi! Unataka kuniambia kuwa we’ hujui kuwa hilo ni gazeti?” Roman alimuuliza kwa kebehi. Fatma alifunua kinywa lakini hakusema kitu, akabaki akimtazama kwa huzuni yenye ghadhabu ndani yake. Kisha akashusha pumzi ndefu na kujitahidi kudhibiti jazba zake, kabla ya kumuuliza kwa upole. “Kwa nini unafanya hivi Roman?” “Kwa nini nafanya nini Fatma? Mbona sikuelewi?” Inspekta Fatma alimtazama kwa muda, kisha akatikisa kichwa kwa masikitiko, kabla ya kufafanua zaidi swali lake. “Kwa nini unajiingiza kwenye hii michezo ya ndondi namna hii, eenh? Na kwa nini sasa hivi…una lengo gani wewe?”
“Kwa sababu ni nchi huru Inspekta, na kwa sababu kila mtu yuko huru kucheza mchezo autakao na auwezao…infact, hata wewe unaweza kucheza kama unaweza, ila nadhani kwako “marede” ndio ungekuwa mchezo muafaka!” “Roman!” Inspekta Fatma alimaka kwa mshangao kwa jibu lile. “Nini?” “Ndio majibu unayonijibu hayo? Unanikosea adabu mimi wewe?” Roman hakumjibu, badala yake alirudisha macho yake kwenye kitabu chake. Inspekta Fatma alimtazama kwa muda, kisha akamwambia kwa upole. “Roman, hili ndilo nililokuwa nikikuasa siku kwanza kabisa ulipotoka gerezani…” “Sikumbuki kabisa kukusikia ukiniambia kuwa nisicheze ndondi afande!” Roman alimjibu huku akifunua-funua kurasa za kitabu chake. “Sina maana hiyo Roman, nawe unajua! We unataka kupambana na Deus!” “Sasa hilo kwako ni tatizo?” Roman alimuuliza huku bado akiendelea kufunua-funua kurasa za kitabu chake. Inspekta Fatma alikikwapua kile kitabu kutoka mikononi mwake, na Roman aliinua uso wake huku akitoa sauti ya kukereka. “Nitazame ninapoongea nawe Roman!” Fatma alimkemea, na kubaki akimkodolea macho huku akitweta kwa ghadhabu. Roman alibaki akimtazama kwa hasira. Hali ya hewa pale mezani ilikuwa ikinuka ghadhabu tupu. “Sikiliza Roman…wewe na mimi tunajua kuwa we’ umezuiwa kushiriki mchezo huu Roman…” “Sijazuiwa…nilizuiwa… ni wakati uliopita huo afande…past tense!” “…na sote tunajua ni kwa nini umezuiwa kushiriki mchezo huu Roman…!” Inspekta Fatma alimwambia kama kwamba Roman hakuingilia kati ile kauli yake ya hapo mwanzo. “Hiyo ilikuwa zamani sana afande, na ilikuwa amri ya kijeshi! Amri ambayo niliitii kwa miaka yote niliyokuwa nje ya ulingo. Na niliitii kwa kuwa ilikuwa ni amri halali ya kijeshi nami nilikuwa mwanajeshi ninayewajibika kutii amri zote za kijeshi! Lakini sasa mimi si mwanajeshi tena! Sasa mimi ni raia tu kama raia wengine hapa nchini na hivyo hiyo amri uisemayo hainihusu tena!” Roman alimjibu kwa hamasa. Inspekta Fatma alibaki mdomo wazi akimkodolea macho kwa mshangao,hatimaye alipata jibu. “Sawa Roman, inawezekana kuwa hiyo amri isiwe na nguvu tena kwako hivi sasa…” “Sio inawezekana…ndivyo ilivyo! Hiyo amri haina nguvu kabisa kwangu hivi sasa!” “…lakini sababu na mazingira ya amri ile kutolewa bado hayajabadilika Roman, kwa hivyo acha kujifanya mjinga…achana na hili swala Roman, tafuta jambo jingine ufanye…uishi kwa amani!” “Kwa hiyo unataka kuniajiri niwe karani wako sasa Inspekta?” Roman alimuuliza kwa kebehi, kisha akaendelea kwa hisia kali, “Mimi ni raia niliyemaliza kutumikia kifungo changu Inspekta. Sina namna yoyote ya kupata kazi popote pale, kwani hakuna mtu anayetaka kuajiri mtu aliyetoka gerezani, sina ujuzi wowote wa kujiajiri na sina mtaji wowote kusema labda nianzishe biashara hata ya karanga! Sasa nimeamua kuendesha maisha yangu kwa kutumia michezo ili nami nijipatie rizki halali kama wengine. Si kosa langu kuwa mchezo pekee niuwezao ni ndondi Fatma, sijui ni kipi kigumu kwako kuelewa hapo, eenh? Acha kunifuata fuata bwana!” Roman alimjia juu. Inspekta Fatma alifunua mdomo kutaka kumjibu lakini hapo hapo alikatishwa na sauti kutoka nyuma yake. “Hey, vipi…nimechelewa sana nini?” Kate alisema huku akimtazama Roman akiwa amesimama kando ya ile meza waliyokuwako, macho yake yakahamia kwa Inspekta Fatma, yakarudi kwa Roman na kuyarudisha tena kwa Inspekta Fatma, na mara moja akamtambua. Wale wanamama walitazamana kwa muda, kisha Kate akamtupia Fatma salamu. Lakini inaelekea Fatma hakuwa na muda wa kusalimiana, na badala yake alimgeukia tena Roman kwa ghadhabu. Lakini kabla hajasema alichotaka kusema, Roman akamgeukia Kate. “Ah, Kate! Wala hujachelewa. Tena ndio umefika katika muda muafaka haswa, kwani Inspekta Fatma hapa nd’o alikuwa anaaga.” Roman alisema, kisha hapo hapo akamgeukia Inspekta Fatma, “Kwa heri Inspekta, na…usikose kuhudhuria mapambano yangu yajayo, okay?” Kate akavuta kiti kingine kilichokuwa pale mezani na kuketi. Inspekta Fatma alimtupia Roman jicho la ghadhabu, kisha akainuka huku bado akiwa amemkazia macho Roman. “Huu mjadala haujaisha Roman!” Alisema kwa hasira, kisha akapachika kofia yake ya kiaskari kichwani, akageuka na kuondoka kikakamavu. Kwa muda Kate na Roman walibaki wakiukodolea macho mgongo wa yule askari wakati akiondoka eneo lile, kisha Kate akamgeukia Roman. “Inahusu nini hii Roman?” Roman alibaki akitabasamu huku akiendelea kumtazama Inspekta Fatma akiondoka eneo lile. “Inahusu askari aliyeshindwa kupata akitakacho kutoka kwangu!” Roman alimjibu huku bado akitabasamu.
***
Siku zilizofuatia mkabala ule baina yaje na Inspekta Fatma zilikuwa za mishughuliko sana kwa Roman na bondia Deus “deadly” Macha. Baada ya waandishi wa habari kuzidi kuandika habari za Roman magazetini, wengi wao wakipewa motisha wa kufanya hivyo na Dan Dihenga, promota wa bingwa wa dunia Deusdelity Macha alimuandalia pambano jingine dhidi ya bondia kutoka Kenya, ambaye alipigwa kwa Knock-out mnamo raundi ya sita. Magazeti yakaandika sana kuhusu ushindi ule wa Deus na kidogo akarudi tena kwenye vyombo vya habari. Dihenga naye akamuandalia Roman pambano jingine la kimataifa, safari hii akipata mpinzani kutoka Zimbabwe. Ilipofika raundi ya nne kwenda ya tano Mzimbabwe akagoma kurudi ulingoni, kipigo alichokuwa akipokea kutoka kwa Roman kilikuwa kizito sana, na refa akasitisha pambano, Roman akatoka mshindi! Ushindi wa Roman nao ukaandikwa kwa sana na vyombo vya habari, ukielezewa kuwa ni ushindi wa aina yake katika historia ya ndondi, kwani haijawahi kutokea bondia kugoma kurudi ulingoni akihofia kipigo kutoka kwa mpinzani wake. Sasa ikawa Deus anapambana, anashinda. Roman naye anapamana, anashinda. Ilikuwa kama kwamba kila mmoja anamtumia ujumbe mwenzake kwa kumpiga mpinzani anayepambana naye. Ikiwa ni pambano la Roman, Deus naye hakosi kwenda ukumbini kushuhudia. Na Roman naye ikawa hivyo hivyo, siku Deus akipambana naye hakosi ukumbini. Hali hii iliendelea hata kwa mapambano yaliyokuwa yakifanyika nje ya nchi, ambapo Roman na Dan walisafiri hadi nje ya nchi kushuhudia mapambano ya Deus. Kutokana na umahiri wake ulingoni, Roman akapachikwa jina la bondia asiye na mpinzani. Jambo hili lilimkera sana Promota wa Deus kiasi cha kuita mkutano na waandishi wa habari, akisema kuwa anashangaa kuwa mabondia wasio na ubingwa wowote wasemekane kuwa hawana wapinzani wakati mabingwa wapo. Deus pia alikuwapo kwenye mkutano ule wa waandishi wa habari, na alipoulizwa juu ya hilo, alisema kwa dharau na kujiamini. “Dunia nzima inajua kuwa mimi ndiye bingwa wa dunia…hakuna mwingine katika uzito wangu. Sasa kama kuna mabondia wasio na wapinzani, basi ni wazi hao hawana hadhi ya kuwa mabondia, watafute michezo mingine tu wacheze…kuna netiboli, marede…kuruka kamba, kombolela au mdako…yaani michezo ni mingi tu sio lazima ndondi.” Sasa ikawa ni uhasama wa wazi baina ya mabondia Deus na Roman. Waandishi wa habari hawakufanya ajizi, walimfuata Roman mazoezini kwake na kumuuliza ana kauli gani juu ya yale maneno ya Deus. “Mimi huwa sipigani kwa maneno…napigana ngumi ulingoni. Sasa kama kuna mtu anayetaka kujua iwapo mimi nina hadhi ya kuwa bondia au vinginevyo, apande nami ulingoni tu. Hapo ndipo kila kitu kitakuwa wazi, au unaonaje mwandishi?” Loh, jibu la Roman likaleta mjadala mzito miongoni mwa wapenzi wa michezo, hususan ndondi. Swala kubwa sasa likiwa ni nani mbabe kati ya Deus na Roman. “Naona sasa mambo yanaenda kama tulivyokuwa tukiyatarajia Roman…wananchi wanataka mpambano baina yako na Deus sasa!” Mark Tonto alimwambia Roman. “Yeah…na ndicho nilichokuwa nikikitaka…mambo yanaelekea kule tulipotaka yaelekee Mark…muda si mrefu azma itatimia…muda si mrefu!” Roman alijibu huku uso wake ukionesha azma ya wazi. Mwezi mmoja baadaye Roman akaandaliwa pambano jingine la kirafiki na bondia wa hapa hapa nchini. Pambano lilifanyika ndani ya ukumbi wa hoteli marufu ya Ubungo Plaza, ambapo ulingo wa kisasa uliwekwa maalum kwa pambano lile. Kutokana na ushabiki wa mchezo ule, ukumbi ulifurika kweli kweli siku ya pambano, na kama kawaida yake, Deus na promota wake walifika ukumbini. Pambano lilikuwa kali sana, na bondia mpinzani alitoa upinzani wa hali ya juu kwa Roman, huku mashabiki wake wakimshagilia kwa nguvu. Mpaka raundi ya sita wote walikuwa nguvu sawa. Kutokea kule ulingoni Roman alimuona Deus akiwa na tabasamu la kejeli, akiona kuwa Roman alikuwa amewekwa katika wakati mgumu na yule bondia asiye na jina hata kidogo. Ghadhabu zilimpanda. Raundi ya saba Roman aliingia kwa nguvu na akitumia mtindo tofauti kabisa wa upiganaji na ule alioanza nao. Yule bondia ambaye tayari alishajiona kuwa ameusoma mchezo wa Roman alichanganyikiwa vibaya sana, na ndipo Roman alipomporomoshea masumbwi mazito na ya mfululizo ambayo hakuweza kuyahimili. Akawa anatupa ngumi ovyo, ngumi ambazo Roman alizipisha kirahisi sana huku akizidi kumtandika ipasavyo. Ndani ya ile raundi ya saba, Roman aliyumba kushoto na kumgusa mpinzani wake kwa ngumi nyepesi ya kulia, jamaa akayumba kushoto kuikwepa, na hapo ndipo Roman aliyejawa ghadhabu sio kwa mpinzani wake bali kwa Deus aliyekuwa akijichekesha kwa dharau nje ya ulingo, alipomvutia ngumi ya kushoto aliyokuwa inaenda kuua. Nje ya ulingo Mark Tonto aliona kile ambacho Roman alikuwa anataka kukifanya, na aliinuka huku akimpigia bondia wake ukelele, “Roman Noooo!” Ngumi ya kushoto ya Roman ilikuwa ikimshukia yule mpinzani wake aliyeleweshwa masumbwi, na katika sekunde ya mwisho kabisa, Roman aliirudisha nyuma ngumi ya kushoto, na hapo hapo alimchimbua yule mpinzani kwa upper cut ya mkono wa kulia. Jamaa alienda chini kama mzigo na kutulia huko huko. Ukumbi ulilipuka kwa hoi hoi na shangwe. Nje ya ukumbi Mark Tonto alishusha pumzi za faraja na kuketi kitini akishuhudia jinsi watu walivyokuwa wakishangilia ushindi mwingine wa Roman. Kule ulingoni Roman wala hakuwa akizisikia zile shangwe, mishipa ilikuwa imemtutumka kwa ghadhabu wakati akienda kutulia kenye kona muafaka, wakati refa akimtangaza mshindi kwa knock-out. Hoi hoi na vifijo vilirindima huku na huko. Roman alienda hadi ule upande ambao Deus na promota wake walikuwa wameketi na kumnyooshea ngumi Deus, kisha akajiashiria alama ya mkanda wa ubingwa kiunoni mwake na kujipiga-piga kifuani kibabe. E bwana we! Deusdelity Macha alichachamaa na kusimama kutoka pale alipokuwa ameketi. “Nini wewe! Unataka mkanda wangu? Unadhani unaweza kuchukua mkanda wangu wewe?” Alipiga kelele huku akijaribu kuparamia ulingoni, wapambe wake wakimzuia na kumrudisha pale alipokuwa amekaa. Roman alibaki akimtazama huku akimcheka kwa dharau. “Wewe huna ubavu wa kuchagama na mimi wewe!” Deus alibwata kwa hasira akiwa nje ya ulingo. “Mimi ndio bingwa wa dunia na hakuna anayeweza kunivua ubingwa huu!” Deus alizidi kujigamba kwa jazba. Roman alimcheka sana, kisha akamnyooshea kidole na kumfanyia ishara ya kuonesha kuwa alikuwa akiongea sana. Ukumbi ulilipuka kwa shangwe na hoi hoi mpya, jina la Roman likirindima kila kona. Wakati Deus aliondolewa ukumbini kwa kubururwa na wapambe wake, mwenyewe akitaka kupanda ulingoni kukabiliana na Roman, mwenzake aliondoka akiwa amebebwa juu juu na wapambe wake. Kutokea kwenye kona moja ya ukumbi ule, Inspekta Fatma alikuwa akifuatilia kila kilichokuwa kikitokea pale ukumbini kwa umakini wa hali ya juu, uso wake ukionesha kusikitishwa na kile alichokuwa akikiona. “Sasa kwa nini pale ulipiga kelele kumwambia Roman No? Yaani hukutaka ashinde… au…? Sikuelewa kabisa pale!” Kate alimuuliza Mark Tonto baadaye usiku ule wakiwa kwenye kambi yao baada ya pambano. Mark alimtupia jicho la wizi Roman, ambaye aligeuza uso wake pembeni. “Yeah…hata mimi sikukuelewa pale coach…nini ilihusu ile?” Dan Dihenga alisaili. Mark Tonto aliguna kidogo na kukaa kimya kwa muda. “Unajua pale niliona kabisa kuwa Roman alikuwa akipigana kwa hasira zaidi kuliko busara…ni hatari sana namna ile…na mabondia wengi hupoteza mapambano kwa kuruhusu hasira ziwatawale ulingoni…lakini nashukuru nilipompigia kelele alinielewa na akajirekebisha, na tukashinda pambano!” Hatimaye Mark alifafanua, muda wote alipokuwa akitoa maelezo yale, macho yake yalikuwa yamefungana na yale ya Roman. “Sasa unaona Roman? Jazba itakuja kutuaibisha bwana!” Dan Dihenga alidakia. Roman alimtazama kidogo, kisha bila ya kujibu kitu, alirudisha macho yake kwa Mark na kubaki wakitazamana kwa muda. Baina yao, walijua kuwa ile sio sababu iliyomfanya Mark apige ule ukelele wakati Roman alipokuwa akipigana pale ulingoni usiku ule.
***
Siku mbili baadaye, Dan Dihenga aliitisha mkutano wa waandishi wa habari, na katika mkutano huo, alitangaza rasmi nia ya bondia wake asiye na mpinzani, Roman, kuwania mkanda wa ubingwa wa dunia katika uzito wa Super Middle. Mkanda ambao ulikuwa ukishikiliwa na bondia Deusdelity “deadly” Macha. Kilichofuatia hapo ni malumbano makali kupitia vyombo vya habari baina ya Deus na Roman, Deus akijitamba kuwa Roman hana uwezo wa kupambana naye hata kidogo, Roman akiendelea kusisitizia kauli yake kuwa yeye ni bondia anayepigana kwa ngumi ulingoni na si kwa maneno redioni na magazetini. Na katika malumbano haya, kila mmoja alijikusanyia mashabiki lukuki, wale waliokuwa wakimshabikia Deus hapo awali, sasa walipata wapinzani waliokuwa wakimshabikia Roman. Sasa na malumbano yakahamia kwa mashabiki, na homa ya mpambano baina ya Roman na Deus ikazidi kupanda. Swala kubwa likiwa ni je itatokea siku wawili hawa wakapambana uso kwa uso ulingoni? Hii ilitokana na ukweli kwamba si Roman pekee aliyekuwa akiuwania ule mkanda wa Deus. Kulikuwa kuna mabondia wengine waliokuwa wakiutaka ule mkanda wa Deus duniani. Ndipo hatimaye, shirikisho la mchezo wa ngumi duniani, lilipopitisha uamuzi wa kumpambanisha Roman na bondia Sergoyev “the hulk” Sucuchev kutoka Serbia, ambaye naye pia alikuwa akiuwania mkanda ule. Mpambano ulipangwa kufanyika katika ukumbi wa hoteli kubwa na maarufu ya The Conrad, kandokando ya mto Nile, ndani ya jiji la Kairo, nchini Misri. Pambano lilipangwa kufanyika miezi miwili baada ya Roman kutangazwa kuwania mkanda wa Deus. Mshindi katika pambano hili angeondoka na kiasi cha dola za kimarekani zipatazo elfu kumi na saba, na ndiye ambaye angepambana na bingwa wa dunia Deus “deadly” Macha kutoka Tanzania.
*** Sergoyev Sucuchev, kama jinsi ambavyo jina lake la kimichezo “the hulk” lilivyomnadi, alikuwa ni bondia mwenye mwili mkubwa, akimzidi urefu Roman kwa inchi tatu, na alikuwa amejichora tojo, au tatoo, nyingi mwilini. Alikuwa na historia ya mapambano kumi na saba ya kimataifa, kumi kati ya hayo akiwa ameshinda kwa knock-out, manne kwa pointi, mawili suluhu na kupoteza moja. Siku ya pambano, The Conrad ilifurika mashuhuda kutoka kila pembe ya dunia, na kutoka Tanzania, Dan aliweza kutumia uwezo wake kama promota kupata ufadhili wa makampuni maarufu na makubwa nchini ambayo yalidhamini safari ya watanzania wapatao hamsini kwenda Kairo kushuhudia pambano lile, wakiwemo waandishi wa habari. Na kwa upande wake, promota mpinzani wa Dan Dihenga,alitumia wadhamini wake kugharamia safari yake na bondia wake Deus kwenda Kairo kushuhudia jinsi ndoto ya Roman ya kumvua ubingwa Deus ikisambaratishwa na bondia yule hatari sana kutoka Serbia. Kwa Roman lile lilikuwa ni pambano kali kabisa miongoni mwa mapambano aliyowahi kushiriki tangu aingie kwenye ndondi za kulipwa. Sergoyev “the hulk” Sucuchev alikuwa na ngumi kali na nzito, na kwa mara ya kwanza Roman alijikuta akipokea masumbwi yaliyomletea kizunguzungu ulingoni. Tangu raundi ya kwanza ya pambano,mabondia wale hawakuwapa nafasi ya kutulia vitini watazamaji wa pambano lile. Ilikuwa ni piga nikupige, na kufikia raundi ya tano mabondia wote wawili walikuwa wakivujwa damu, lakini si kwa kiasi cha kumlazimisha mwamuzi kusimamaisha pambano. “Roman vipi…naona sasa ubadili mtindo wa upiganaji…huyu jamaa ni mzuri kweli kweli!” Mark Tonto alimwambia bondia wake wakati wa mapumziko kabla ya raundi ya sita. Roman aliafiki kwa kichwa huku akitweta. Kengele ikagonga, na mabondia wakaingia tena ulingoni kuanza raundi ya sita, lakini Roman hakubadili mtindo wa upiganaji ingawa pambano lilikuwa kali zaidi, mabondia wote wawili wakitupiana makonde mazito. Kengele ilipogonga kumaliza raundi, ilikuwa wazi kuwa raundi ya sita ilikuwa nguvu sawa baina ya mabondia wale wawili. “What’s the matter with you Roman? Nimekwambia ubadili mtindo wa upiganaji! Una nini leo? Huyu Mserbia mjinga sana! Unataka atuadhiri hapa? Sisi tumekuja huku ili…” “Relax Mark! Hana ubavu wa kuniadhiri yule!” “Usipobadili huo mtindo wako atatuadhiri…” “Sibadili mtindo Mark!” “Why, for God’s sakes Roman, why?” Mark alipandwa wahka. Kengele ya kurudi ulingoni kwa raundi ya saba iligonga. “Kwa sababu sitaki Deus aone mtindo wangu mwingine wa upiganaji Mark!” Roman alimjibu, kisha akainuka na kurudi ulingoni. Raudi ya saba ilikuwa na msisimko wa aina yake, na ukumbi wa hoteli ile maarufu jijini Kairo ulirindima kwa hoi hoi na vifijo kutoka kwa watazamaji. Sergoyev “the hulk” sasa alikuwa amepandwa jazba, kwani naye alimuona Roman kuwa ni mpinzani tata kwake. Alikuwa akimuendea kwa ngumi kali na za mfululizo, wakati Roman aliendelea kumkwepa na kumtandika ngumi za hapa na pale. Ndipo ilipotokea nafasi ambayo Sergoyev “the hulk” asingeweza kuipoteza hata kidogo, pale alipotupa konde zito lililomsukuma Roman mpaka kwenye kamba, kisha akasukumwa tena ulingoni na zile kamba akionekana kabisa kuwa alikuwa amepoteza uelekeo, mkono wake wa kulia ukiwa chini na ule wa kushoto ukiwa umeinuliwa juu. Na hapo, uso wa Roman ukibaki bila kinga yoyote. Ni nafasi ambayo bondia yoyote duniani huwa akiiombea, na Sergoyev hakufanya ajizi. Alikwenda mzima mzima, akimtupia Roman konde la kulia lililokuwa limebeba nguvu zake zote nyuma yake. Ukumbi uliachia mguno wa fadhaa ilhali watazamaji wengine, akiwemo Deusdeadly Macha, wakiinuka vitini kwa midadi huku wakiwa vinywa wazi. Kila mtu alijua kuwa sasa Sergoyev alikuwa anamaliza mchezo. Roman aliliona konde la m-serbia likimjia wazi wazi usoni, na katika nukta ya mwisho kabisa alijipindua haraka kutokea sehemu ya kiuno kwenda juu akilalia kulia kwake, na kwa namna isiyotegemewa, ngumi nzito ya m-serbia ilimkosa kwa kupita kiasi cha milimeta chache sana mbele ya uso wake. Sergoyev Sucuchev aliachia mguno wa mshangao na wakati huo huo akageuza uso wake kumtazama Roman bila ya kuamini kuwa ngumi yake ilikuwa imemkosa mtanzania yule, na wakati huo huo akipoteza muelekeo na kupepesuka kama mlevi. Sasa Roman alikuwa akiutazama uso wa m-serbia ukiwa hauna kinga yoyote, na hii ndiyo nafasi ambayo yeye alikuwa akiitarajia. Mkono wake wa kushoto uliokuwa juu muda wote ulishuka na pigo moja lililotukuka, na kushuka kama nyundo usoni kwa m-serbia. Sergoyev Sucuchev alienda chini kama gogo lililooza. E Bwana we! Hakika ile ilikuwa ni sucker punch ya hali ya juu na m-serbia hakuiona kabisa ilipotokea. Ukumbi ulilipuka kwa hoi hoi. Haraka sana yule m-serbia, ambaye hakuamini kama kweli alipokea pigo kwa mtindo wa ajabu namna ile, aliinuka tena, lakini miguu ikamkatalia na akaenda tena chini kwa kishindo. Ukumbi ukaachia ukulele mwingine mkubwa. Sergoyev bado alijitahidi kuinuka tena huku akishikilia kamba za ulingo na kupiga hatua moja… Refa akamkibilia huku akiumuashiria kuwa atulie. M-serbia akapiga hatua ya pili… Sasa ukumbi ulikuwa kimya kabisa, ukifuatilia kile kilichokuwa kikitokea pale ukumbini. M-serbia akanyanyua mguu kupiga hatua ya tatu…kisha macho yake yakapinduka na kubaki weupe tu, na akapiga mweleka mwingine mzito sana, akisambaratika chali kwenye sakafu ya ulingo. Kwisha kazi! Ukumbi ulirindima kwa mayowe yenye mchanganyiko wa hisia wakati refa alipomtazama Sergoyev na hapo hapo kuamua kuwa hawezi tena kuendelea na pambano. Roman akainuliwa mkono juu na kutangazwa mshindi kwa Knock-Out! Si mchezo! Hoi hoi, nderemo na vifijio vilitawala pale ukumbini kutoka kwa watanzania na wananchi wa nchi nyingine waliokuja kushuhudia mpambanao ule wa kukata na shoka. Hoi hoi pia zilikuwa zikirindima sehemu mbali mbali nchini Tanzania kutoka kwa watanzania waliokuwa wakiufuatilia mpambano ule wa kimataifa kupitia kwenye chaneli za Supersport na ESPN kupitia kwente runinga zao. Sergoyev Sucuchev aliyepoteza fahamu alitolewa ulingoni akiwa kwenye machela, wakati Roman alibebwa juu juu huku akiwa ameinua ngumi yake hewani, macho yake yakimtafuta Deusdelity Macha pale ukumbini bila mafanikio. Waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali vya kimataifa walimzonga Roman kwa maswali kem kem juu ya ushindi wake ule. Aliongea kwa kifupi tu kuwa kwake lile ndilo lilikuwa pambano la kugombea mkanda wa ubingwa wa dunia katika uzito wa Super Middle, na kwa ushindi ule ni kwamba tayari yeye alikuwa ndiye bingwa wa dunia. “Lakini tunavyofahamu sisi ni kwamba mpaka sasa bingwa wa dunia bado ni mtanzania mwenzako Deusdelity Macha, Roman, sasa una maana gani kwa kauli yako hiyo?” Mwandishi wa shirika la habari la Reuters ya uingereza alimuuliza kwa kimombo. “Ndio Roman… una maana gani? Kwani tujuavyo ni kwamba sasa unatakiwa upambane na bingwa aliyepo, Deusdeadly Macha, na mshindi wa hapo ndiye atakayekuwa bingwa!” Mwandishi mwingine alidakia. “Kwangu mimi pambano langu na Deus si la kugombea ubingwa!” Roman alijibu kwa kimombo fasaha, kisha akafafanua; “…Kwangu lile ni pambano la sherehe tu ya kunikabidhi mkanda wangu niliojinyakulia leo hii!” “Hatujakuelewa Roman…” Mwandishi wa chanel ya televisheni ya Al-Jazeera aliuliza. Roman alitulia kwa muda akiwaangalia waandishi wale, kisha akajibu. “Namaanisha kwamba Sergoyev Sucuchev…the hulk…ni bondia mzuri mara tano zaidi ya huyo Deus…na nyote mmeona jinsi nilivyomfanya hapa!” Kisha akageuka na kuwaacha waandishi wakitupa maswali zaidi ambayo hakujishughulisha kuyajibu. Sasa azma yake ilikuwa inaelekea kutimia.
*** Siku mbili tu baada ya pambano la kule Kairo, Deus “deadly” Macha alitupa gazeti kwa hasira huku akiachia tusi zito la nguoni, na kusimama kutoka kwenye kiti alichokuwa amekalia na kubaki akitweta huku amejishika kiuno. Promota wake aliyekuwa naye mle ndani alimtupia jicho la mshangao na kuyarudisha macho yake kwenye lile gazeti lililotupwa kwa ghadhabu na yule bondia wake. “Nini sasa Deus?” “Ujinga mtupu! Mimi nimuogope Roman mimi?” Deus alimaka kubisha kile kilichokuwa kimeandikwa gazetini. “Ah, hayo si magazeti tu? Sioni sababu ya kujijaza upepo kwa habari kama hiyo, hao wanataka kuuza magazeti tu!” Promota alimwambia. Walikuwa sebuleni nyumbani kwa Deus. Deus alibaki akiwa amekunja uso bila ya kujibu kitu. Lile gazeti lilikuwa limeandika kuhusu kauli ya Roman aliyoitoa siku ile aliyomuangusha m-serbia Sergoyev Sucuchev kuwa pambano lake na Deus lilikuwa ni la sherehe za kumkabidhi Roman mkanda wa ubingwa ule. Tangu kauli ile itolewe, Deus hakujibu kitu, na ndio maana gazeti liliandika namna ile. “Sasa kwani ni kweli kuwa we’ unamuogopa Roman Deus…?” Promota alimuuliza kwa mashaka. Deus alimgeukia yule promota na kumtazama kwa hasira, kisha akarudi na kuketi kitini. “Mi’ siwezi kumuogopa Roman hata siku moja…haniwezi!” “Sasa ya nini kujijaza jazba?” “Kwa sababu we’ hutaki nimjibu kashfa zake gazetini bwana! Mi sipendi namna hii…!” “Kama nilivyokwambia Deus…sasa maneno basi. Tutapambana naye ulingoni tu, kwisha!” Promota alisisitiza. Dakika kumi baadaye promota alitoka na kumuacha Deus peke yake pale nyumbani kwake. Alikaa kimya kwa muda akiwa amejawa na mawazo mazito, akilini kwake akikumbuka siku alipopambana na Roman miaka kadhaa iliyopita… wakati huo wote wawili wakiwa wanajeshi katika jeshi la wananchi wa Tanzania, wote wakiwa mabondia wa ridhaa katika michezo ya majeshi…. Mwili ulimsisimka. Alikaa vile kwa muda mrefu, kisha akachukua simu yake ya mkononi na kupiga namba ambayo alikuwa akiijua kwa kichwa. “Ni mimi…” Alijitambulisha kwa yule mtu aliyepokea ile simu, kisha akaendelea, “…sasa nataka nikupe tena ile kazi uliyoshindwa kuitekeleza wakati ule…” Alisikiliza kwa muda, kisha akaongea tena, “…si tatizo pesa yako utapata, ila nataka safari hii kusiwe na makosa bwana…Roman apatwe na ajali mbaya…!” Alisikiliza kwa muda kisha akasema neno moja tu kabla ya kukata simu. “Okay!” Wiki moja baadaye shirikisho la ndondi duniani lilitangaza kuwa pambano kati ya Roman na Deus lingefanyika miezi mitatu baadaye, jijini Dar es Salaam.
*** Maisha ya Roman yalibadilika sana baada ya yale mapambano yake mawili ya kulipwa. Aliweza kununua gari zuri la kutembelea na kiwanja ambacho alipanga kuanza kukijenga taratibu. Dan Dihenga naye kama promota wake na Mark Tonto kama mwalimu na rafiki yake nao walinufaika na mamilioni yale aliyoyakumba baada ya kumuangusha m-serbia kule Kairo. Lakini vyote hivi, bado havikuwa lengo la Roman kuingia kwenye ndondi za kulipwa. Lengo lake kuu bado lilikuwa halijatimia, ingawa sasa lilikuwa limekaribia sana. Baada ya kurejea kutoka Kairo, Roman alipokelewa kwa shangwe sana uwanja wa ndege na mashabiki wa ndondi. Ushabiki baina ya kambi ya Roman na Deus ukapamba moto maradufu, mashabiki wakiisubiri kwa hamu siku ambayo mabondia wale wawili wenye upinzani mkali nchini wangekutana ana kwa ana ulingoni. Bondia Deusdelity Macha alikuwa na mkataba wa udhamini na kampuni moja kubwa ya simu za viganjani nchini, ambayo ilisimamia mapambano yake yote, na kumdhamini kwa namna mbalimbali katika vifaa vya mazoezi, mavazi na hata safari zake za kimataifa. Deus kwa upande wake naye alitokea kwenye matangazo mengi ya biashara ya kampuni ile. Sasa ilijitokeza kampuni nyingine ya simu za viganjani ambayo nayo ilikuwa ikigombea soko la watanzania katika uteja wa huduma zake za simu. Matokeo yake makampuni haya mawili yakawa kwenye ushindani mkali wa kibiashara. Dan Dihenga aliona nafasi ya kuwanufaisha yeye na bondia wake katika hili, na hivyo aliweza kuishawishi ile kampuni ya simu pinzani kumdhamini Roman kama sehemu ya upinzani wake na ile kampuni iliyokuwa ikimdhamini Deus. Hoja yake ilipita bila kupingwa. Na ndipo bila ya yeye mwenyewe kujua, alipofanikiwa kuyaokoa maisha ya Roman kutokana na ajali ya kupangwa ya kugongwa na gari akiwa mazoezini, pale alipoishawishi ile kampuni kudhamini maandalizi ya Roman kwa pambano lake na Deus kwa kumuweka kambini nje ya nchi, kwenye visiwa vya ushelisheli, kwa siku zote mpaka siku ya pambano lake na Deus. Siku ilipotangazwa kuwa Roman hatokuwapo nchini kwa muda wote hadi siku ya pambano lake na Deus, bingwa wa dunia Deus “deadly” Macha alipokea simu kutoka kwa mtu wake. “Sorry boss, naona zoezi halitawezekana tena…Roman anaondoka nchini ndani ya siku mbili, nami sina uhakika wa kumpata akiwa mazoezini barabarani ndani ya siku mbili hizi!” Alimueleza. Deus alifura kwa hasira. “Si bado yuko nchini ndani ya siku mbili? Mtafute, mfuatilie mpaka umpate! Hakikisha jambo linamtokea kabla hajaondoka bloody fool!” Deus alifoka, kisha akakata simu. Alibaki akiwa amefura kwa hasira.
***
Mark Tonto alingia sebuleni kwa Roman pale kwenye nyumba aliyopangiwa na Dan Dihenga kule bagamoyo, na kushusha pumzi ndefu. “Wheew! Si joto hilo! Nijaalieni maji ya kunywa tafadhali jamani.” Alisema. Roman, aliyekuwa amejilaza kwenye kochi aliachia tabasamu pana wakati, Kate aliyekuwa kwenye kochi lile lile alilokuwa amelalia Roman, alijiinua na kwenda kumletea maji Mark. “Pole sana mzee…vipi za Dar?” Roman alimuuliza. “Huko shwari tu…” Mark alijibu huku akipokea gilasi ya maji baridi kutoka kwa Kate. Muda huo ulisikika muungurumo wa gari lililokuwa likiegeshwa nje ya nyumba na muda si muda hodi ikabishwa pale mlangoni. Roman na Mark walitazamana. “Vipi, unatarajia mgeni nini?” Mark aliuliza. Roman alitikisa kichwa. “Hapana. Dan hatokuja leo, na zaidi yake na sisi tuliomo humu ndani, hakuna mtu mwingine apajuaye hapa!” Kate alienda kufungua mlango, na mara alipoufungua tu, Roman na Mark walimsikia akiachia mguno wa mshangao. Walitazamana, kisha wote wakakurupuka kuelekea kule mlangoni…
***
“Vipi Kate…hujawahi kuona askari akibisha hodi mlangoni?” Inspekta Fatma, akiwa ndani ya sare zake za kiaskari, alimuuliza huku akiachia tabasamu la upande mmoja. Kate alibaki akimkodolea macho ya kutoamini. Aliishia kujiona sura yake kwenye miwani myeusi ya jua iliyokuwa usoni kwa yule askari. Roman na Mark walifika pale mlangoni, nao wakabaki wakishangaa. “Mark…unaendesha gari kwa kasi sana wewe. Hujui kuwa ni hatari kwa usalama wa barabarani?” Fatma alimwambia Mark, kisha akamgeukia Roman, “…siku nyingine ukimuachia kocha wako hili gari lako jipya hakikisha umelifunga kidhibiti mwendo Roman, ama si hivyo utalikuta mtaroni siku moja!” Roman alimtazama kwa kutoamini yule dada. Mark alikunja uso. “Khah! Ina maana…” alianza kusema, lakini Fatma alimkatisha. “Ndio hivyo Mark…nimekufuata kwa gari tangu Dar mpaka hapa…vinginevyo ningepajuaje huku?”
“Na kwa nini umepata taabu yote hiyo afande, kama naruhusiwa kuuliza?” Roman alimuuliza kwa hasira. Fatma alimtazama kwa muda. “Kwa hiyo sikaribishwi ndani?” Akamuuliza. Roman alimtazama kwa muda kisha akageuka na kurudi ndani kwake, wengine wote wakimfuata ndani. Roman alisimama katikati ya sebule na kumuuliza. “Okay Fatma, unataka nini tena kwangu?” “Nahitaji kuongea nawe Roman.” “Ongea nakusikiliza…!” “Naomba tuongee peke yetu…mimi na wewe.” “Hilo halitawezekana…” Roman alianza kujibu, lakini hapo hapo Mark Tonto akaingilia. “Eh, mi’ na Kate tutakuwa nje kwa muda…” Roman na Fatma walibaki peke yao pale sebuleni. “Hongera kwa ushindi wa Kairo Roman…” Fatma alianza. “Fatma usinipotezee muda. Hukuja mpaka huku eti kunipongeza. Sema lililo kuleta uende zako!” Fatma alimtazama kwa huzuni, kisha akatikisha kichwa kwa masikitiko. “Roman, nadhani bado nina wajibu wa kukuasa juu ya pambano lako na Deus…najua utaondoka ndani ya siku mbili kwenda ushelisheli kwa maandalizi, lakini…bado mi’ nilikuwa nadhani kuwa hutakiwi kufanya hivyo Roman…bado una nafasi ya kubadili mawazo!” “Kwa hiyo unachoniambia ni kwamba niite waandishi wa habari halafu niwaambie kuwa nimeamua kujitoa kwenye pambano langu na Deus? You must be crazy Fatma. Mi’ sirudi nyuma!” “Kuna namna nyingi za kulimaliza hili Roman, sio lazima iwe hivyo…unaweza kujitoa kutokana na sababu za kiafya…achana na…” “No! Sina tatizo la kiafya Fatma…” Roman alimjia juu, kisha akamwambia, “Lakini Fatma, kwa nini unanifuata fuata mimi tu? Kwa nini usiupeleke ushauri huu kwa mtu ambaye atanufaika nao zaidi?” “Mtu gani sasa?” “Deus!” Roman alimjibu mara moja, na kuendelea, “Deus ndiye haswa ambaye ungepaswa umpe ushauri huu Fatma, sio mimi. In fact, sasa naomba nikutume rasmi kwa Deus…kamwambie kuwa mimi niko tayari kusahau yote yaliyopita iwapo atatangaza kujitoa kwenye pambano na kuusalimisha mkanda wake kwangu. Akiweza kufanya hivyo, kila kitu kitakuwa sawa!” Fatma alibaki akimtazama kwa muda mrefu kabla hajaongea. “Naona umeamua kutimiza ahadi uliyoitoa miaka miwili iliyopita Roman.” “Khah! Mbona sikuelewi…mi’ nimekupa ufumbuzi wa hili tatizo halafu…” “Unajua kabisa kuwa Deus hawezi kukubali hiyo hoja Roman…” “Ila kwa kuwa mimi bwege, tena bwege mtozeni, ndiye ninayetakiwa nikubaliane na huo upuuzi wako? Toka nyumbani kwangu Fatma. Peleka ujumbe niliokutuma kwa Deus, ama si hivyo sitaki nikuone tena mbele ya uso wangu!” Roman alimjia juu. Fatma alimtazama kwa muda mrefu, kisha aliinuka taratibu na kuelekea mlangoni. Alifungua mlango, lakini kabla ya kutoka, alimgeukia tena. “Okay, Roman. Mi’ nimejitahidi kadiri ya uwezo wangu kuokoa ubinaadamu wako Roman…” “Nashukuru kwa hilo. Sasa naomba uende!” “…ila tu nataka uelewe kuwa ni ile kauli yako ya mwisho wakati unapelekwa gerezani, na azma niliyoiona wazi machoni mwako wakati ukitoa kauli ile, ndivyo vilivyonifanya nipate taabu yote hii kwa ajili yako…kwa sababu mi’ bado naamini kuwa ndani kabisa ya huo moyo wako uliozongwa na chuki, kuna binadamu mwema na mstaarabu. Nahofia kuwa binaadamu huyo yuko mbioni kupotezwa kabisa na ile kauli yako Roman…usiruhusu hilo litokee!” Fatma alimweleza kwa kirefu. Na baada ya maelezo yale, alibaki akimtazama Roman usoni kwa macho makavu. Roman alifunua kinywa kutaka kumjibu, lakini hakupata neno muafaka la kumwambia. Walibaki wakitazamana tu, kisha Fatma akatoka nje, akiufunga mlango taratibu nyuma yake. Mark na Kate walirudi mle ndani na kumkuta Roman akiwa ameketi ilhali uso wake ukiwa na mawazo mazito. “Haya, leo amekuja na lipi tena yule askari?” Kate alimuuliza. “Yale yale tu ndugu zangu…Inspekta Fatma anadhani nitakuwa binaadamu na mstaarabu zaidi kama nikijitoa kwenye kugombea mkanda wa Deus…” “Ana wazimu…!” Kate alimaka kwa hasira. “Tena sana…” Roman aliafikiana na Kate, bado uso wake ukiwa na mawazo mazito. Mark alimtazama kwa mashaka, lakini hakusema kitu. …ni ile kauli yako ya mwisho wakati unapelekwa gerezani, na azma niliyoiona wazi machoni mwako wakati ukitoa kauli ile, ndivyo vilivyonifanya nipate taabu yote hii kwa ajili yako… “Sasa mmemalizana vipi?” Kate alihoji zaidi. “Nimemtuma kwa Deus…akamwambie ajitoe kwenye mpambano na asalimishe mkanda wake kwangu…” “Wacha bwana!” Mark alimaka. “Ndiyo…! Na akishindwa kufanya hivyo, basi asirudi tena kwangu na ule upuuzi wake!” Roman alimalizia, lakini bado alionekana kuwa kuna kitu kilikuwa kikimsumbua akilini mwake. Nahofia kuwa binaadamu huyo yuko mbioni kupotezwa kabisa na ile kauli yako Roman… “Roman, uko sawa lakini…? Mbona nakuona kama kwamba una kitu kinakusumbua?” Kate alimuuliza kwa wasiwasi. Roman alimtazama kwa muda, kisha akamgeukia Mark, halafu akatazama ukutani kwa muda. …usiruhusu hilo litokee… “Aam…nadhani nahitaji kuwa peke yangu kwa muda jamani…samahani…” Hatimaye aliwaambia wenzake, na bila kusubiri kauli yao, aliinuka na kuelekea chumbani kwake. Mark na Kate walibaki wakitazamana. “Usijali…mpe muda atulie kwanza…bila shaka Inspekta Fatma amemkumbusha mambo mengi mazito, lakini atakuwa sawa tu.” Mark alimwambia Kate. Kate aliafiki kwa kichwa bila ya kusema kitu. Chumbani kwake Roman alivuta droo na kutoa picha ya msichana aliyekuwa amesimama kwenye bustani huku akiwa ameachia tabasamu mororo, furaha iliyokuwa moyoni mwake ilikuwa wazi machoni mwake, na ikanaswa sawasawa na kamera. Alikuwa ni binti mrembo aliyepata umri wa miaka kama kumi na minane hivi wakati picha ile inapigwa. Aliketi kitandani taratibu huku akiitazama ile picha ilhali uso wake ukiwa na simanzi kali, na hapo kwikwi ya kilio ilimtoka bila kutarajia, tone la chozi likiangukia kwenye ile picha. “Oh, Rachel mdogo wangu! Nisamehe malkia wangu…nilikuacha mikononi mwa shetani mdogo wangu, na sasa haupo tena duniani…” Alibwabwaja huku akilia kwa uchungu. Alilia kwa muda mrefu, kisha alijitahidi kujifuta machozi, na kuitazama tena ile picha, sasa uso wake ukiwa na ghadhabu zaidi kuliko huzuni. “…lakini nakuahidi mdogo wangu…nakuahidi, kama jinsi nilivyokuahidi hapo awali Rachel…nitahakikisha kuwa nalipiza kifo chako, nitalipiza kisasi…na muda si mrefu azma hiyo itatimia Rachel…!” Aliiambia ile picha huku akibubujikwa na machozi. …kwa sababu mi’ bado naamini kuwa ndani kabisa ya huo moyo wako uliozongwa na chuki, kuna binadamu mwema na mstaarabu… “Inspekta Fatma anadai kuwa nikilipiza kisasi nitapoteza moyo wangu wa ubinaadamu na ustaarabu…” Roman alizidi kuongea na picha ya hayati mdogo wake, akaachia mguno wa dharau, kisha akaendelea, “…kitu ambacho haelewi ni kwamba huo moyo wa ustaarabu na ubinadamu ndio uliosabaisha nikuache mikononi mwa shetani, nikiamini kuwa naye ni binadamu na mstaarabu kama mimi Rachel…shetani aliyekuja kukuangamiza mdogo wangu. Hapana Rachel, ni bora nipoteze ubinaadamu na ustaarabu, kuliko kuacha kifo chako kipite bila kulipizwa! Nitalipiza…nitalipiza…na nitalipiza kwa namna ambayo ninaiweza! Hiyo ni azma yangu!” Roman Kogga aliongea kwa uchungu na ile picha ya hayati mdogo wake, Rachel Kogga. Na ndani ya muda huo, matukio ya miaka kadhaa iliyopita yalimrudia kichwani mwake kama kwamba yalikuwa yametokea jana tu…
******
MIAKA KADHAA ILIYOPITA…..
Roman Kogga alikuwa ni miongoni mwa vijana waliojiunga na jeshi la wananchi wa Tanzania baada ya kumaliza masomo yake ya kidato cha sita. Baba yake, ambaye naye alikuwa ni afisa katika jeshi la wananchi wa Tanzania, ndiye aliyekuwa kishawishi kikubwa cha yeye kujiunga na jeshi. Akiwa jeshini, alijiunga na chuo cha usimamizi wa fedha, akisomea shahada ya uhasibu, chini ya udhamini wa jeshi la wananchi. Na wakati akiwa anakamilisha masomo yake, wazazi wake wote wawili walipata ajali mbaya ya gari na kufariki dunia. Ndipo Roman alipojikuta akikabiliwa na jukumu la kumlea Rachel, mdogo wake wa pekee ambaye muda huo alikuwa kidato cha pili. Lakini kwa kuwa tayari yeye alikuwa ana kazi ya uhasibu katika jeshi la wananchi, na wazazi wao waliwaachia nyumba na mali kadhaa, hawakutetereka kimaisha. Roman alimchukua mdogo wake na kuishi naye kwenye nyumba aliyopewa na jeshi, na ile nyumba waliyoachiwa na wazazi wao wakaipangisha. Hivyo maisha hayakuwa na tatizo. Tangu akiwa shuleni, Roman alikuwa akipenda sana mchezo wa ngumi, na alikuwa akihudhuria mazoezi ya vikundi mbali mbali vya ngumi. Lakini alipata nafasi ya kujiingiza zaidi kwenye ndondi wakati alipojiunga na jeshi. Na huko ndipo alipokutana na Sajini Meja Makongoro “Mark Tonto” Tondolo, ambaye alikuwa ni mwalimu wa ndondi katika jeshi la wananchi wa Tanzania. Roman aliondokea kuwa bondia mzuri sana katika timu ya jeshi, na katika maandalizi ya michezo ya majeshi, Sajini Meja Mark Tonto alimchagua kwenye timu ya kikosi chake. Na hapa ndipo Roman alipokutana na bondia mwingine aliyekuwa akija juu sana katika mchezo ule jeshini, Desudelity Macha. Baada ya uteuzi wa timu, Sajini Meja Makongoro TAondolo aliinoa timu yake kwa mazoezi makali, na hapa akajionea uwezo mkubwa wa mabondia Roman Kogga na Deusdelity Macha. Moja kwa moja Mark akajua kuwa wawili wale ndio ambao wangekuwa vinara wa timu yake. Kwa upande wao, Roman na Deus walijenga urafiki haraka sana. Wote walikuwa wakiupenda mchezo ule, na walikuwa wakikutana kila siku kwenye mazoezi. Na katika siku ambazo hakukuwa na mazoezi ya timu yao, wao wenyewe walikuwa wakikutana na kupeana mazoezi mbali mbali. Lakini nyota ya Roman katika ndondi za ridhaa ilianza kuzimika pale ambapo siku moja, wakiwa katika mazoezi ya maandalizi, alipopanda ulingoni na bondia mwenzake katika timu ya kikosi chao, na katikati ya pambano, Roman alichomoa sumbwi la mkono wa kushoto kwa mtindo wa upper-cut, sumbwi lililotua sawia kidevuni kwa mpinzani wake na kumpeleka chini kama puto lililotobolewa. Jamaa aliaga dunia pale pale! Heh! Lilikuwa ni tukio la kushtua sana, ingawa mwisho wa yote lilionekana kuwa ni ajali tu ya kimichezo. Lakini kuanzia wakati ule kocha Mark Tonto alianza kumtazama Roman kwa makini sana. Siku zilipita, mashindano ya michezo ya majeshi yalikaribia, lile tukio likasahaulika, na Roman akapambanishwa na Deusdelity Macha katika mazoezi. Mark Tonto alikuwa makini sana na pambano lile, kwani wapiganaji wale ndio walikuwa vinara wa timu yake, na pambano lao lilikuwa kali sana. Deusdelity alikuwa mpiganaji mzuri sana aliyetoa upinzani mkali kwa Roman. Pambano lilikuwa linaelekea kuwa nguvu sawa, lakini ilipokuwa imebaki raundi moja pambano liishe, Deus alitupa konde kali sana lililokuwa linaelekea usoni kwa Roman. Roman aliyumba, konde likamkosa, na hapo hapo mkono wake wa kushoto ulichomoka na hook iliyotua kwenye taya la Deus, na hapo hapo aliona macho ya mpinzani wake yakitumbukia ndani huku akienda chini kama mzigo! E bwana we! Roman alibaki akimshangaa Deus akiwa chini wakati kocha Mark Tonto na wauguzi wakiwahi ulingoni. Dakika chache baadaye Deus alitolewa ulingoni akiwa kwenye machela akiwa hana fahamu. Si mchezo! Deus alipona, lakini hakuweza tena kushiriki mashindano ya majeshi ya mwaka ule, kwani alikaa hospitali wiki mbili akitibiwa taya lililovunjika, na baada ya hapo alitakiwa awe nje ya ulingo kwa miezi sita. “Roman, nadhani unabidi uwe makini sana na hiyo ngumi yako ya kushoto…ningeshauri utumie zaidi ngumi ya kulia, na utumie mkono wa kushoto kujikingia na kutupa ngumi ndogo ndogo tu…inaonekana ni ngumi hatari sana!” Kocha Mark Tonto alimwambia Roman baada ya tukio lile. “Ah, coach…sasa ndio n’takuwa bondia gani wa kutumia mkono mmoja tu bwana? Mi’ naona hili shoto ndio turufu yangu ulingoni bwana…” “Hapana Roman, hiyo ngumi ni hatari sana…inaua!” “Aaw, come on coach…ile ilikuwa bahati mbaya tu bwana…” “No Roman, hii si maskhara. Ona jinsi ulivyomfanya Deus…bahati ile ngumi imemshukia kwenye taya, ingempata juu kidogo tu kichwa, juu ya sikio, nakuhakikishia naye tungemzika!” Kocha Mark Tonto alimwambia kwa hamasa. Roman alibaki akishangaa. “Kwa hiyo basi unaniambia kuwa niache ndondi kocha!” “Hapana…ila nataka nikuulize swali moja Roman…je unajua iwapo utotoni mwako ulipata kuchanjiwa mkono wako wa kushoto?” Roman alimshangaa zaidi yule mkufunzi wake. “Kuchanjiwa?” “Ndio Roman…kuchanjiwa! Nasikia kuna makabila ambayo huwa yanachanjia vitu kama hivi…mtu anakuwa na ngumi nzito yenye uwezo wa kuua…je nawe ulifanyiwa kitu hicho Roman?” Mark alimuuliza. Roman alidhani kuwa mwalimu wake alikuwa akimtania, lakini alipomtazama aliona kuwa hakuwa akitania hata kidogo. “Hapana coach…sina habari ya kitu kama hicho…kama kipo basi wazazi wangu hawakuniambia…” Roman alimjibu kocha wake. “Basi zingatia ushauri wangu.” Mark alimwambia na mjadala ukaishia pale. Roman hakuyatilia maanani kabisa yale mazungumzo, kwani kwake kitu cha mtu kuchanjiwa kuwa na ngumi ya kuua hakikumuingia akilini hata kidogo. Kwa hiyo timu ya kikosi cha Mark Tonto iliendelea na mashindano yale bila ya Deus. Na katika mashindano yale, ambayo ndio yalikuwa ya kwanza kabisa makubwa kwake kushiriki, Roman aliua mtu mwingine ulingoni kwa sumbwi la mkono wa kushoto! *** *** Waraka aliopokea kutoka makao makuu ya jeshi ulikuwa unajitosheleza. Kufuatia matukio mawili ya kuua wapinzani wake ulingoni, na moja la kumjeruhi vibaya mpinzani mwingine katika mchezo wa ndondi, Kapteni Roman Kogga, kuanzia tarehe ya waraka ule, alikuwa amezuiliwa kushiriki katika mchezo wa ndondi popote pale ndani ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Ni amri. Imezuiliwa. Ndoto za Roman kuwa bondia bora wa ngumi za ridhaa ndani ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania zilikatikia hapo. ** Roman Kogga aliachana kabisa na ndondi, na kuendelea na utumishi wake ndani ya jeshi kama mhasibu. Lakini muda wote huo urafiki wake na Deus haukutetereka. Alikuwa akienda kumtembelea hospitali na hata alipotoka na kulazimika kukaa nje ya ulingo kwa miezi sita, Roman na Deus walikuwa wakiendelea na urafiki wao. Baada ya kupona Deus alirudi tena ulingoni na kuwa bondia mzuri sana ndani ya jeshi. Walikuwa wakitembeleana na siku za mwisho wa wiki, walikuwa wakienda kwenye kumbi za starehe na kujifurahisha kwa starehe mbali mbali. Miezi sita baada ya Deus kupona na kurejea ulingoni ndani ya jeshi,Kepteni Roman Kogga alipata udhamini wa jeshi la wananchi kwenda kusomea shahada ya pili ya uhasibu nchini Uingereza. Ilikuwa ni habari ya furaha sana kwake, lakini pia ilikuwa na wingi wa huzuni, kwani ilimaanisha yeye kuwa mbali na mdogo wa pekee wa kike, Rachel, kwa miaka miwili! Roman aliongea na rafiki yake mpenzi, Deus juu ya hatima ya Rachel wakati yeye akiwa nje ya nchi. Akamuomba amuangalie mdogo wake wakati yeye yuko nje ya nchi. “Usijali partner…Rachel ni mdogo wetu sote bwana, kwa hiyo hatokuwa peke yake. Mimi nitachukua jukumu la kumuangalia katika muda wote ambao hutakuwepo…nenda ukasome salama rafiki yangu, na mungu akujaalie!” Deus alimwambia. “Loh, ahsante sana partner…ahsante sana. Nilijua kuwa ninaweza kukutumainia rafiki yangu.” Roman alimjibu kwa shukurani. Kufikia wakati huu Rachel alikuwa ameshamaliza kidato cha nne na alikuwa amefaulu kuendelea na kidato cha tano. Kabla hajaondoka, Roman alihakikisha kuwa dada yake ameshapata nafasi kwenye bweni la shule aliyoteuliwa kujiunga nayo jijini Dar, na hivyo Rachel hakulazimika kuishi peke yake nyumbani kwa Roman. Pia alimfungulia akaunti na kuweka maelekezo maalum ya kukatwa sehemu ya mshahara wake kila mwezi na kuingizwa moja kwa moja kwenye akaunti ya Rachel. Siku ya safari ilipowadia, kaka na dada waliagana kwa huzuni. “Usiwe na wasiwasi Rachel, tutakuwa tukiwasisliana kwa mtandao mara kwa mara…na kama kuna tatizo lolote litakalokuwa nje ya uwezo wako, muone kaka yako Deusdelity…atakusaidia”. Roman alimwambia mdogo wake wakiwa uwanja wa ndege. “Sawa kaka…uende salama…” Rachel alijibu huku akibubujikwa machozi. “Come on Rachel…sio kwamba Roman anaenda kuuawa huko bwana…anaenda kuongeza elimu kwa faida yenu nyote. Usilie namna hiyo…tumuombee mungu tu huko aendako arudi salama, au sio?” Deusdelity Macha, aliyekuwa pamoja nao pale uwanja wa ndege alimfariji Rachel. “Najua kaka Deus…lakini…” Rachel alijitahidi kujibu lakini hakuweza kumalizia, alizidi kulia. Roman alimkumbatia mdogo wake kwa muda mrefu, kabla ya kumtazama usoni kwa muda, machozi yakimlenga-lenga, na kumbusu kwenye paji la uso. Aligeuka na kuingia ndani ya uwanja ule bila kugeuka nyuma. Akiwa ndani ya uwanja, ambapo alijua hawataweza kuona jinsi alivyokuwa akitiririkwa na machozi, aligeuka na kuwapungia mkono. Deus na Rachel walimpungia, naye akapotelea ndani ya eneo la kusubiria ndani ya uwanja ule. Ndio ilikuwa mara yake ya mwisho kumuona mdogo wake akiwa hai… *** Ndani ya mwaka wake wa kwanza alikuwa akiwasiliana mara kwa mara na Rachel na Deus, na mara moja moja sana alikuwa akiwasiliana na Sajini Meja Makongoro Tondolo. Na katika moja ya mawasiliano yao adimu na kocha wake wa zamani wa ndondi, Mark alimfahamisha Roman kuwa alikuwa ameamua kustaafu jeshi ili aweze kusimamia miradi yake binafsi na apate muda zaidi wa kuinua mchezo wa ndondi. Roman alimtakia kila la kheri, naye akaendelea na masomo yake. Siku moja, akiwa ameanza mwaka wake wa pili wa masomo yake kule uingereza, Roman alipokea simu usiku wa manane kutoka Tanzania. “Eh…hallo…” “Roman…this is Mark…Mark Tondolo!” “Mark…? Coach…? vipi za huko, kwema?” “Huku si kwema Roman…ni Rachel…” “Rachel…?” “Amekunjwa sumu…ana hali mbaya sana…” “Whaaaat? Ame…Deus yuko wapi…?” Roman alihamanika, usingizi wote ukimkauka ghafla, moyo ukimuenda mbio. “Sijui Roman…Deus hapatikani…mi’ nimepigiwa simu na wanafunzi wenzake waliomfikisha hapa hospitali…walipewa namba na Rachel mwenyewe kabla hajaingizwa ICU…!” Mark alijibu. Saa tano baadaye, Roman alikuwa kwenye ndege akirejea Tanzania. Akili ilikuwa ikimzunguka muda wote alipokuwa angani, machozi yakimbubujika, donge kubwa likiwa limemkaba kooni.
***
Mark Tonto alikuwa akimsubiri uwanja wa ndege. Alipomuona tu alijua kuwa kuna kitu hakikuwa sawa. Alitupa chini begi lake na kumkimbilia pale alipokuwa amesimama. “Mark! Coach…vipi Rachel…yuko hospitali gani….? Deus je…?” Roman alimvurumishia maswali ya wahka, lakini Mark alikuwa amesimama kimya akimtazama kwa huzuni, midomo ikimtetemeka. Roman alimshika mabega na kumtazama kwa woga mkubwa. Macho ya Mark yalimthibitishia kile alichokuwa akikihofia tangu anapanda ndege kurudi nyumbani. “No, Mark…No!” Alisema kwa maombolezo. “…usiniambie kuwa Rachel ame…ame…” “She is dead Roman…Rachel is dead!” Mark alimjibu kwa huzuni huku akimkumbatia. Maneno yale yaliuchoma moyo wake kama kwamba yalikuwa ni msumari wa moto. “Ah! Coach…imekuwaje? Kwa nini lakini…?” Roman aliuliza huku akilia kama mtoto. “Twende nyumbani Roman…ni hadithi ndefu kidogo…” “No! Nipeleke nikamuone mdogo wangu bwana! Na Deus yuko wapi lakini?” Roman alibwabwaja wakati Mark akimuongoza kwenye teksi. “Tutamtafuta Deus baadae Roman, sasa tushughulikie msiba uliopo mbele yetu…” Mark alimjibu. Alipouona mwili wa mdogo wake Roman alipoteza fahamu pale pale hospitali. Alipozinduka, alikuwa amelazwa kitandani pale hospitali. Mark Tonto alikuwa ameketi kwenye kiti kando yake. “Oh, Mark…Rachel ametutoka Mark…” Roman alibwabwaja huku akiinuka na kuketi pale kitandani. Mark aliinuka na kuketi pamoja naye pale kitandani. “Ni amri ya mungu Roman…kuwa jasiri ndugu yangu…” “Si amri ya Mungu hii Mark…ndugu yangu amekunywa sumu. Ina maana aidha amejiua, au ameuawa…sijui kipi ni kipi, lakini lolote litakalokuwa kati ya hayo mawili, jibu linabaki kuwa hii si amri ya Mungu!” Roman alisema kwa uchungu. Mark alimkumbatia rafikiye kwa kumfariji. “Usikufuru Roman…hakuna litokealo bila mapenzi ya Mungu bwana. Wewe ni mpiganaji, pigana na hili kijasiri Roman…” Roman alianza kulia upya. Muda mfupi baadaye tabibu aliyempokea Rachel pale hospitali alifika kuonana na Roman. “Pole sana Kepten Kogga…pole sana.” Yule tabibu alimwambia, na Roman alimtazama na kuitika kwa kichwa. “Okay, sasa…nadhani unahitaji kujua mazingira ya kifo cha mdogo wako Kepten…” Tabibu alimwambia. “Najua…amekunywa sumu…” Roman alisema taratibu. “Yeah…ilikuwani sumu kali na nyingi, kiasi kwamba pamoja na jitihada zetu zote, hatukuweza kuokoa maisha yake wala ya kiumbe kilichokuwa tumboni kwake…” “Whaaat?” Roman alimaka na kumtazama kwa makini yule tabibu. “…ki…kiumbe? kiumbe gani tumbon…oh, My God, yaani Rachel alikuwa mjazito?” “Oh, hukuwa na habari…? Ndiyo, Rachel alikuwa na ujauzito wa miezi minne…” Roman aliona kuwa dunia yote ilikuwa imeamua kumsaliti na kumzonga. Alimtazama yule tabibu kwa uchungu, kisha akamgeukia Mark. “Ni nini hiki kinachotokea kwangu jamani, enh? Ni nini lakini…?” Aliuliza kwa uchungu huku akilia. Mark alibaki akitikisa kichwa tu. “Sasa…sasa…huyu mwenye ujauzito huo…aliyembebesha ujauzito mdogo wangu…anafahamika? Mark, we unamfahamu?” Alimuuliza Mark kwa hamaniko kubwa kabisa. Mark aliuma midomo yake kwa uchungu. “Hata mimi hii habari imenijia kwa mshituko mkubwa Roman…” “Oooh, Mark….!” Roman alisema kwa masikitiko, machozi yakimbubujika. *** Mark aliandaa taratibu zote za mazishi. Msiba uliwekwa nyumbani kwake, na maziko yalifanyika siku iliyofuata, bila ya Deusdelity Macha kuhudhuria. Baada ya maziko, watu wachache walioshiriki kwenye msiba ule walibaki pale nyumbani kwa Mark, wakiwemo wananfunzi na walimu wa shule aliyokuwa akisoma marehemu. Roman alimfuta Mark na kumwambia, “Mark, sasa nimekubali kuwa Rachel amekwenda na hatorudi tena. Ila bado nina mambo matatu yanayosumbua kichwa changu Mark, na haya sitatulia mpaka niyapatie majibu…” Mark Tonto alimtazama tu rafiki yake bila ya kusema kitu, na Roman aliendelea, “Kwanza, ilikuwaje hata Rachel akanywa sumu…” alitulia kidogo, na kuendelea, “…pili, ni kwa nini Deus, ambaye ndiye niliyemkabidhi jukumu la kumuangalia Rachel wakati mimi sipo, hajaonekana kabisa katika msiba huu…” kisha akamalizia, “na tatu, ni nani huyu aliyempa ujauzito mdogo wangu…?” Mark alitikisa kichwa kuafiki umuhimu wa mambo yale huku uso wake ukiwa umefanya tafakuri zito. Alikaa kimya kwa muda mrefu, kisha taratibu aliinua uso wake na kumtazama Roman. “Majibu ya maswali hayo yapo Roman, ila ni machungu sana rafiki yangu…” “Hayawezi kuwa machungu kuliko uchungu wa kifo cha mdogo wangu Makongoro…” Kimya kilitawala kwa muda baina yao, kisha Mark akasema. “Basi itabidi nikukutanishe na binti aitwaye Sada, Roman, yeye ana majibu ya maswali yote hayo…” Roman alishikwa wahka mkubwa. “Ni nani huyu Sada, na…yuko wapi?” “Huyu ni rafiki mkubwa wa marehemu…na yupo hapa hapa msibani.” Maelezo ya Sada yalibadili kabisa muelekeo wa maisha ya Roman… ***** Sada alikuwa rika moja na Rachel, na alipoonana uso kwa uso na Roman hakuweza kujizuia kuangua kilio upya. Mark na Roman walijitahidi kumtuliza, na baada ya muda, alijifuta machozi kwa upande wa khanga yake, akapenga kamasi laini kwa khanga ile ile na kuwaangalia wale watu wawili waliokuwa mbele yake. “Sa…samahani sana…” “Usijali, ni msiba mkubwa kwetu sote Sada.” Mark alisema kwa upole, kisha akaendelea, “Sasa naomba umueleze Kapten Roman hapa, yale uliyonieleza mimi juu ya Rachel, na mazingira ya kifo chake.” Mark alimwambia. “Okay…kaka zangu…” Sada alisema na kupenga tena kamasi. “Na…naweza kusema kuwa mimi ndiye nilikuwa rafiki wa karibu sana wa mar…wa Rachel. Alikuwa akikuongelea sana kaka Roman. Kwake wewe ulikuwa ni shujaa asiyeshindwa na lolote…” Roman aliuma midomo kwa uchungu, lakini alijitahidi kujizuia, alitaka kujua ukweli wa kifo cha ndugu yake. “…pia alinieleza kuhusu Deus, ya kwamba ni rafiki yako mkubwa na kwamba ndiye angekuwa anamsaidia iwapo atakutwa na tatizo lolote kubwa. Kiujumla tuliishi bila matatizo pale shuleni, na kaka Deus alikuwa akija kumtembelea Rachel mara kwa mara na mara nyingine, siku za mwisho wa wiki alikuwa akija kutuchukua na kutupeleka kula Ice Cream au sinema na kuturudisha shuleni…” Roman alizidi kusikiliza kwa makini. “Sa’ siku moja, tukiwa kwenye likizo ya katikati ya muhula, Rachel alienda mjini na Deus, na aliporudi aliniambia kuwa …kuwa…kaka Deus alim…alimtaka kimapenzi!” “Whaat??” Roman alimaka kwa kutoamini, macho yakimtoka pima. “Deus???” “Ndio kaka Roman…nilishituka sana. Rachel alilia sana siku ile, hakuamini kuwa kaka Deus angeweza kumtamkia jambo kama lile…” “Mwanaharamu…! Yani Deus anaweza kunifanyia hivi?” Roman alisema kwa uchungu. “Hujasikia habari yote Roman…muache binti aendelee, kisha tutajadili kwa undani swala hili.” Mark alimwambia. “Kwa hiyo unataka kuniambia kuwa ni Deus ndiye aliyembebesha mimba Rachel?” Roman aliuliza kwa jazba, mishipa ya shingo ikiwa imemtutumka. Sada alitikisa kichwa kwa masikitiko. “Mnhu! Dunia ina mambo kaka zangu…hali ilienda mpaka Rachel akajikuta akikubaliana na hoja za Deus…nadhani Deus alikuwa na nguvu ya kubwa ya ushawishi. Wakawa wapenzi…” Sada alisema na kuanza kulia. “Ah!” Roman aliguna, na kubaki akitikisa kichwa, macho yake yakitoa mng’aro wa ghadhabu isiyo kifani. Sada aliendelea kueleza kuwa Rachel alimwambia kwamba Deus alimuahidi kumuoa “…alimwambia kuwa…kuwa hata wewe, kaka Roman, ungefurahia kuwa shemeji yake…” “Ah, sasa mbona sikuambiwa juu ya uchumba huo? Uongo mtupu!” Roman alimaka. “Walikubaliana kuwa wakusubiri mpaka urudi…Deus ndio angeongea nawe kwanza…ilionekana ni utaratibu mzuri tu kwa wakati ule…” “Mzuri? Ni utaratibu mzuri huo? Mtu namkabidhi mdogo wangu yeye anaenda kumtongoza?” “Namaanisha huo utaratibu wa kukusubiri urudi na Deus aongee nawe…lakini mambo yaliharibika pale Rachel aliposhika ujauzito…” “Deus akamkana…!” Roman alidakia kwa jazba, sasa machozi yakimtiririka waziwazi. Sada alitikisa kichwa kwa simanzi. “Hapana. Akamtaka atoe ile mimba…!” “Ama!?” Roman alimaka kwa mshangao, “Yaani…kwa nini?” “Kuna sheria kali sana dhidi ya wanaume wanaowatia mimba wanafunzi kaka Roman. Deus alikuwa akiogopa hilo, lakini Rachel hakutaka kutoa mimba. Alimwambia akupigie simu huko uliko akueleze kila kitu…Deus hakuwa tayari, alisisitiza msimamo wake kuwa Rachel atoe mimba. Ikawa mizozo na majibizano. Rachel akaanza kukosa kuhudhuria masomo, kutwa barabarani akimtafuta Deus. Hali ilipozidi kuwa mbaya, Rachel akamtishia kumshitaki kwa wakuu zake wa kazi. Deus alikuja juu, na hapo ndipo alipomtakia kuwa haujui ule ujauzito…” “Hah!” “Ndiyo kaka…Rachel alichanganyikiwa!” Kufikia hapa Roman alikuwa akilia waziwazi. Uchungu aliokuwa nao haukuwa na mfano. “Kwa…kwa…kwa hiyo nd’o mdogo wangu akanywa sumu kwa hilo…? Why Rachel…? Why…?” Roman alisema huku akizongwa na kwikwi za kilio. Sasa na Sada naye alikuwa akilia pamoja naye. Mark alitikisa kichwa huku naye akitiririkwa na machozi. Ilikuwa ni hali ya kutia uchungu sana. Lakini uchungu bado ulikuwa haujatimia. “Hapana kaka Roman…hilo silo lililosababisha Rachel achukue uamuzi aliochukua…” Hatimaye Sada alimjibu. Roman alimtazama kwa mshangao. “Sio hilo…?” Aliuliza kwa kutoamini, akitembeza macho baina ya Mark na Sada. “Sasa kuna ubaya gani tena zaidi ya huu ambao mdogo wangu amefanyiwa jamani? Hebu niambie Sada…ni nini tena Deus alichomfanya mdogo wangu…?” “Ah, kaka Roman…we’ acha tu…” Sada alisema na kuangua kilio upya. “No! Nieleze tafadhali…niambie tu mdogo wangu…ni nini kilichosababisha Rachel ajiue?” Sada alilia kwa muda, kisha akajilazimisha kumueleza. “Siku hiyo…kiasi cha wiki moja baada ya Deus kuukana ujauzito wake, Rachel aliniomba nimsindikeze nyumbani kwa Deus ili ajaribu kuzungumza naye…” Sada alitulia kidogo, akipenga kamasi na kujifuta machozi, “…huko tulimkuta Deus akiwa na mwanamke mwingine!” Sada alimalizia kauli yake na kuangua kilio kizito. Duh! Mark na Roman walitazamana, uchungu aliokuwa nao Roman ukijiweka wazi machoni mwake. “Ilikuwa ni vurugu kubwa…Rachel akilia na kumshutumu Deus kwa kumlaghai, yule mwanamke mwingine naye akimshutumu Deus kwa kumlaghai, Deus naye akimkana Rachel na kumuita malaya….”
“Ah, jamani…hivi ni Deus huyu huyu nimjuaye ndiye aliyefanya mambo hayo?” Roman alisema kwa mshangao na uchungu. “Ndiye kaka…ndiye.” Sada alimjibu huku akishindana na kwikwi za kilio, kisha akaendelea, “…na kitendo alichomfanyia Rachel pale nyumbani kwake siku ile ndicho kilichogongelea msumari wa mwisho…pamoja na kuwa nilikuwa naye muda wote siku ile baada ya kutoka kule kwa Deus…Rachel aliamka usiku wakati wote tumelala, na kunywa sumu…nilikuja kuamshwa na sauti zake akikoroma na kugumia…nilipogundua alichofanya, niliwaarifu waalimu na tukamkimbiza hospitali…” Sada alimalizia na kuangua kilio. Hakuweza tena kuendelea. Alikuwa akilia kwa uchungu mkubwa. “Mimi nilipigiwa simu na mmoja wa waalimu wao…Rachel aliandika namba yangu na ya Deus pale shuleni kwa ajili ya dharura yoyote itakayotokea…walisema namba ya Deus ilikuwa haipatikani. Nilipofika hospitali na kukuta hali ilivyo, ndipo nilipokupigia simu. Baada ya hapo nimekuwa nikijaribu kumafuta Deus kwenye simu bila mafanikio. Jamaa hakuwa hewani kabisa…nadhani aliamua kubadilisha namba kabisa.” Mark aliingilia kati na kufahamisha zaidi. “Lakini mi’ nilimpata…wakati Rachel anahangaika usiku ule, kabla hata sijawaita waalimu nilimpigia na nikampata…nikamwambia kuwa amesababisha Rachel anywe sumu…na kwamba nitahakikisha namfikisha mbele ya sheria…nadhani baada ya hapo ndio akaamua kufunga kabisa simu yake!” Sada alisema huku akilia. Roman alilia! Alilia sana.Alilia kwa uchungu, majuto na hasira pia.Alilia kweli kweli. “Kwa hiyo…Rachel hakuacha ujumbe wowote kueleza sababu za uamuzi wake ule?” Hatimaye Roman aliuliza. “Hapana…hakuacha chochote…” Sada alisema. Roman alibaki akitikisa kichwa kwa masikitiko. “Na ndio maana tunashindwa kumchukulia Deus hatua yoyote sasa Roman…mimi nilishindwa kwenda polisi…nigekuwa na ushahidi gani? Ni ushuhuda wa Sada tu, ambao unakanika kirahisi sana…” Mark alisema kwa uchungu. “Dah! Ni kweli Mark…hakuna ushahidi wa kushikika na kuukabidhi kwa polisi…lakini ushahidi wa kuwa Rachel…mdogo wangu, amekufa upo…she is dead Mark!Dead! Bado binti mbichi kabisa!” Roman alisema kwa uchungu, “…na Deus ndiye anayehusika…lazima alipe! Hii haina mjadala kabisa, lakini kwanza nataka nisikie kutoka kwake mwenyewe…anasemaje kuhusu kifo cha mdogo wangu niliyemkabidhi kwake?” Hatimaye alisema. “Mimi nilikwenda kumuona Deus jana kabla sijaenda uwanja wa ndege kukupokea Roman…” Mark alisema, na kuendelea, “… hakukana kabisa kuwa alikuwa na uhusiano na Rachel…alisema ni jambo la bahati mbaya naye hakulitegemea…hakutegemea kuwa Rachel angechukua uamuzi ule…na hakika alikuwa na majuto makubwa…” “Sasa mbona hakuja hata kwenye maziko Mark…?” “Alisema hataweza kuja…hataweza kukutazama tena usoni baada ya yote yaliyotokea…” Roman alilia sana. Alilia kwa muda mrefu. “Basi ana bahati mbaya sana… kwa sababu mimi nataka nimtazame yeye usoni…” Hatimaye Roman alisema huku akijifuta machozi.
*** Kapten Deusdelity Macha aliteremka kutoka kwenye gari la jeshi na kutembea kiaskari kuuelekea mlango wa nyumba yake. Upande wa pili wa barabara, Roman alijiinua kutoka kwenye benchi alililokuwa amekalia lililokuwa mbele ya kibanda cha mkaanga chipsi na kumfuata taratibu. Usoni alikuwa amevaa miwani ya jua na ndani ya kifua chake alikuwa akihisi mfukuto wa ghadhabu wakati akimtazama Deus akifungua mlango wa nyumba yake na kuanza kuingia ndani. “Hallo Deus…!” Aliita taratibu, sasa akiwa hatua si zaidi ya tano kutoka mlangoni kwa Deus. Deus aligeuka, na mara tu alipomuona uso ulimbadilika na kusajili mshituko mkubwa sana. “Roh…Roman!” Alisema kwa kitetemeshi na kubaki akimtazama. Walitazamana. “Un…nataka nini…umekuja lini…?” Deus alijikuta akiuliza bila kufikiri. Roman alibaki akimtazama, chuki isiyo kifani ikijijenga moyoni mwake. “Rachel is dead Deus.” Deus alitazama chini. “Na…naomba uende Roman…nasikitika kwa msiba uliotokea, lakini…” “Sijakuona msibani hata kidogo Deus…sasa najiuliza, kwa mtu ambaye ndiye niliyekukabidhi mdogo wangu wakati naondoka nchini, kwa nini usitokee msibani?” Roman alimwambia kwa sauti ya utulivu. Deus alianza kufunga mlango, akimuacha Roman nje. Haraka sana Roman aliweka kiatu chake mlangoni na kuuzuia ule mlangokufunga. Deus aliinua uso wake na kumtazama Roman kwa mshangao. “Toka bwana!” Alisema huku akimsukuma kwa ule mlango. Roman hakutetereka. “Umemuua Rachel Deus….” “No! Amejiua mwenyewe Roman, na naomba usinilaumu kwa hilo…mi’ sikuwa na nia mbaya kwake, nilimpenda kikweli kabisa, lakini…” Hapo Roman alishindwa kuzuia ghadhabu zake. Aliukamata mlango kwa nguvu na kumsukumia ndani Deus huku naye akimfuata nyuma yake. “Kelele wewe! Ulimpenda mdogo wangu wewe? Mi’ nilikukabidhi ili umrubuni na kumtelekeza?” Alimfokea huku akimsukuma kwa mikono yake yote miwili kifuani. Hapo hapo Deus alimtandika ngumi kali ya uso, na Roman akayumba hadi ukutani huku akiachia mguno wa maumivu. Deus aligeuka na kukimbilia ndani zaidi ya nyumba yake na kujifungia chumbani kwake, ambako alienda moja kwa moja hadi kwenye simu iliyokuwa kando ya kitanda chake. “Hallo Polisi? Mimi ni kapteni Desudelity Macha! Nahitaji msaada haraka sana nimevamiwa nyumbani kwangu…haraka!” Nyuma yake Roman alikuwa akibamiza mlango wa kile chumba. “Fungua mwanaharamu, fungua!” Roman alifoka huku akiubamiza mlango ule kwa hasira. “Ondoka Roman, ondoka! Mi’ nimeita polisi…yatakayokukuta tusilaumiane!” Deus alimpgia kelele kutokea chumbani kwake. “Umemuua mdogo wangu Deus! Nimekukabidhi nikiamini kuwa u-binaadamu kumbe ni shetani usiye haya?” “Sikudhamiria Roman! Hebu ondoka upesi Roman…ondoka nyumbani kwangu!” Roman alipandwa na ghadhabu. Alirudi nyuma na kuurukia kwa nguvu ule mlango. Lakini ule mlango ulikuwa mgumu sana naye aliishia kuanguka chini kwa kishindo. “N’takuua mwanaharamu! N’takuua kama ulivyomuua mdogo wangu shenzi wee!” Roman alipiga kelele kwa hasira. Nje ya nyumba ile majirani walisikia mayowe na wakaanza kukimbilia kwenye ile nyumba kujua kulikoni. Roman aliubamiza mlango kwa nguvu bila mafanikio. Alitoka mbio na kuingia jikoni. Akachukua chupa ya mafuta ya taa na kuitupia pale mlangoni, chupa ikapasuka na mafuta ya taa yakiilowesha pazia iliyokuwa imetundikwa mbele ya ule mlango. Akaliwasha moto lile pazia. “Utatoka humo ndani paka we! Utatoka! Kama hutoki basi utaangamia humo humo ndani kwa moto baradhuli mkubwa we!” Alimtupia maneno ya ghadhabu. Moto ukapamba kwa kasi, mlango ukaanza kuugua, moshi ukatanda kila mahali. Kule chumbani Deus alianza kukohoa kwa taabu, moshi ukimuelemea. “Roman! Roman…acha ujinga…acha…” Alipayuka kwa taabu. Sasa moto ulikuwa umetawala mlango wote, na bila kufikiri Roman aliurukia ule mlango na kupita nao mzima mzima mpaka ndani, huku nyuma akisikia mayowe ya majirani na ving’ora vya magari ya polisi. Deus alimshitukia Roman akitua ndani ya chumba kile kwa kishindo. Alijitupa pembeni na kujaribu kumzunguka Roman ili akimbilie nje ya ya chumba kile, lakini Roman alimrukia na kumdaka kiuno na wote wawili wakaenda chini. Deus alimsukumia Roman teke lililomtupa pembeni. Wote waliinuka kwa wakati mmoja na Roman akamsukumia konde kali la uso, lakini Deus aliliona, akabonyea likapita hewani naye akamtandika ngumi nzito ya tumbo. Roman aliguna kwa maumivu na hasira huku akiyumba. Sasa ule moto uliokuwa mlangoni alitambaa mpaka ndani na kupamba kwenye shuka la kitanda. Roman akamrukia Deus mzima mzima na kumshidilia kichwa cha mwamba wa pua, na Deus alipelekwa mpaka ukutani, akiachia kilio cha maumivu huku akijishika pua iliyokuwa ikibubujika damu. Roman alimuendea na kumchapa konde kali la mbavu na Deus alijipinda huku akigumia kwa uchungu. Roman akamshindilia konde jingine la ubavu wa pili, Roman akajipindia upande wa pili. Roman akampa konde jingine zito la tumbo, Deus akajipinda kwa mbele. Roman akamkamata kichwa na kumsihdilia kwa goti usoni na Deus alienda chini kama mzigo. Sasa chumba chote kilikuwa kimetanda moto, kitanda chote kilikuwa kikiwaka moto, na ndimi za moto ule zilirukia kwenye pazia za madirisha, nayo yakashika moto. “Acha Roman…acha!” Deus alikuwa akibwabwaja huku akijitahidi kuinuka. Sasa Roman alikuwa amepandwa wazimu wa ghadhabu. Alimdaka ukosi wa gwanda lake la jeshi na kumuinua, kisha akamshindilia kichwa kingine kilichotua sawia mdomoni. Deus alichia yowe kubwa huku akienda tena chini. “Umemuua mdogo wangu, Deus! Umemuua mdogo wagu halafu unaniambia nitoke nyumbani kwako? Nyama we, sasa nawe utaenda kuzimu kunakokustahili!” “Roman, I am sorry…! Nisa…me…he…brother!” Deus alibwabwaja, lakini Roman alikuwa ameshapanda mzuka wa kulipa kisasi. Huku wakiwa wamezongwa na moshi kila upande, alimkamata na kuunyofoa kwa nguvu mkanda wa gwanda la kijeshi alilokuwa amelivaa Deus na kumzingira nao shingoni. “Roman Nooookkhhhh!” Deus alipiga kelele lakini hapo hapo Roman alianza kumkaba kwa kutumia ule mkanda, akimkata mayowe yake na kumuacha akikoroma. “Utamfuata Rachel alipo ili ukamuombe msamaha nyau we!” Roman alisema huku akitweta na akizidi kumkaba kwa ule mkanda. Macho yalimtoka pima Deus, alianza kutupa mikono huku na huko, akijitahidi kufurukuta bila mafanikio kutoka kwenye kifo dhahiri kilichokuwa mbele yake. “Polisi! Jisalimishe sasa hivi!” Sauti kali ya kiaskari ilifoka kutokea mlangoni. Roman aliinua macho yake yaliyowiva kwa ghadhabu na moshi uliotanda mle ndani, na aliona kivuli cha mtu akiwa amesimama pale mlangoni. “Sijisalimishi mimi! Naua! Namuua bazazi huyu! Niacheni nimmalize halafu nanyi mkaninyonge!” Aifoka huku akizidi kumkaba. Mara hiyo mlio wa bastola ulisikika, na kabla hajatanabahi, Roman alishuhudia kiumbe kikijitupa mle ndani na kujibiringisha sakafuni, kisha akajikuta akiwa amewekewa kabali shingoni kwake na mdomo wa bastola ukiwa umekandamizwa kwenye upande wa kichwa chake. “Uko chini ya ulinzi mwanaume! Muachie huyo mtu sasa hivi, ama si hivyo napasua bichwa lako kwa risasi!” Ilikuwa ni sauti kali ya kike. Roman alizidi kumkaba Deus kwa ule mkanda, pua zikimtutumka, akitweta kwa ghadhabu. “Niue nami nakufa naye afande!” Alisema kwa hasira, kisha akamalizia, “…huyu mwanaharamu kasabaisha kifo cha mdogo wangu gaddemitt, afande!” “Utakufa wewe kwanza, naye utamuacha akitapatapa kutafuta pumzi, lakini akiwa hai. Muachie huyo askari sasa hivi!” Fatma, wakati huo akiwa koplo, alisema kwa msisitizo, bastola yake ikiwa kichwani kwa Roman. Na hata alipokuwa akisikia maneno yale, Roman alishuhudia askari wengine watatu wakivamia mle ndani, bunduki aina ya SMG zikiwa mikononi mwao, zote zikiwa zimemuelekea yeye, huku moto ukizidi kupamba mle ndani. Alihema kwa pumzi za haraka haraka, na huku bado akizidi kumkaba Deus kwa ule mkanda, alisogeza mdomo wake sikioni kwa yule rafiki yake aliyebadilika na kuwa adui yake mkubwa, na kumnong’oneza kwa sauti nzito ya kongofya. “Umeokolewa na askari safari hii Deus, lakini ujue kuwa bado kifo chako kiko mikononi mwangu…I will kill you one day Deus…that’s a promise (nitakuua tu siku moja Deus…nakuahidi hilo)!” Kwisha kusema hivyo, alimsukuma mbele kwa nguvu, akimuacha Deus akisambaratika ovyo sakafuni, naye akijikuta akisukwasukwa kwa nguvu na wale askari, mikono yake ikivutwa nyuma na akipachikwa pingu. “Ita gari la kuzima moto hapa…upesi!” Koplo Fatma alibwata huku akimburura Roman nje ya kile chumba kilichokuwa kikiwaka moto mtindo mmoja. Nje ya nyumba ile kundi la watu waliojaa udadisi lilikuwa limetanda, wengi kati yao wakiwa ni majirani wa Deus pale mtaani. Akiwa ndani ya gari la polisi kabla ya kuondolewa eneo lile, Roman aliiona nyumba ya Deusdelity Macha, ikiteketea kwa moto kuanzia ule upande kilipokuwa chumba chake cha kulala kuelekea nyuma ya nyumba ile. Kate alikuwa ni miongoni mwa majirani waliojazana pale nje siku ile, wakimshuhudia Roman akiingizwa kwenye gari la polisi akiwa na pingu mikononi, na jirani yao Deus akiingizwa kwenye gari jingine la polisi huku akivujwa damu. Na wakati akimtazama yule mtu aliyempa kipigo cha haja jirani yao, Kate hakutegemea kabisa kuwa kiasi cha miaka miwili baadaye angekutana na mtu yule uso kwa uso…
***
Roman alishitakiwa kwa kosa la shambulio baya na kusababisha hasara ya mamilioni baada ya kuiteketeza nyumba ya Deus kwa moto. Aliwekwa rumande wakati Deus na jamhuri wakiandaa ushahidi wa kumtia hatiani kwa kosa lile zito alilotuhumiwa kwalo. Mark alijitahidi kumtafutia dhamana, lakini haikuwezekana. Roman alionekana ni mtu hatari sana kuachiwa huru mitaani hivyo aliwekwa ndani. Mara moja Mark Tonto alitafuta wakili wa kumtetea. Kesi iliendeshwa kwa miezi mitatu, Koplo Fatma akiongoza upande wa upelelezi. Na ni katika miezi mitatu ile, ndipo Koplo Fatma alipopata kuufahamu kwa undani uhasama uliojengeka baina ya Roman na Deus. Lakini mambo mabaya ndio kwanza yalikuwa yanaanza kwa Roman. Kutokana na kuhusishwa na kesi ya kiraia, Roman alijikuta akisimamishwa kazi jeshini, wakuu wake wa kazi wakiweka wazi kuwa iwapo atapatikana na hatia, basi na ajira yake jeshini nayo itakuwa imekwisha. Kesi ya Deusdelity Macha dhidi ya Roman Kogga ilivutia watu wengi hususan majirani wa Kapten Deusdelity Macha walioshuhudia siku ile Roman alipotiwa nguvuni baada ya kumporomoshea kipigo Deus na kuiteketeza nyumba yake kwa moto. Miongoni mwa wale waliokuwa wakiifuatilia kesi ile kwa karibu sana kila ilipotajwa alikuwamo Kate, jirani wa Deus. Na ni katika kuendelea kwa kesi ile, ndipo mambo yote ya jinsi Deus alivyomrubuni Rachel, mdogo wa rafikiye Roman yalipoweka hadharani, Sada akitoa ushahidi wa matukio yote hayo. Siri ya Deus ikawa wazi kwa majirani na wakuu wake wa kazi pia. Hata hivyo, upande wa mashitaka ulifanya kazi nzuri ya kuusambaratisha ushahidi wa Sada kuwa hauna vithibitisho na badala yake ulikuwa ni simulizi tu miongoni mwa masimulizi ya kubuni. Aidha, upande wa mashitaka, uliweza kutumia historia ya nyuma baina ya Roman na Deus kuonesha kuwa Roman alikuwa na chuki binafsi na Deus kwa muda mrefu, pale muendesha mashitaka wa serikali alipompandisha Deus kizimbani kutoa ushuhuda wa jinsi Roman alipompiga kwa nguvu wakati wakifanya mazoezi ya ndondi wakiwa michezoni jeshini, na kumvunja taya. Kwa jinsi Deus alivyoielezea hali ile, ilionekana kama kwamba wakati walitakiwa wapigane kimichezo, Roman aliingia ulingoni kwa lengo la makusudi la kumuumiza. Ushahidi huu ulimuweka Roman kwenye wakati mgumu sana pale ulipooanishwa na lile tukio la kumvamia Deus nyumbani kwake, kumpiga na hatimaye kumchomea moto nyumba yake. Mwisho wa kesi, mahakama ilimtia Roman hatiani. Hukumu ikawa ni kifungo cha miaka miwili pamoja na kumfidia Deus kwa hasara aliyomsababishia alipomteketezea nyumba yake kwa moto. Hivyo alitakiwa atumikie kifungo, na baada ya kifungo, alipe fidia ya ile nyumba aliyoiteketeza.Au atekeleze yote mawili kwa pamoja, lolote litakalokuwa rahisi zaidi. Muda wote wakati hakimu akimsomea hukumu ile, Roman alikuwa amemkazia macho Deus huku akiwa ameuma midomo yake kwa hasira. Baada ya kusomewa hukumu yake Roman alitiwa pingu pale pale mahakamani, na Koplo Fatma akisaidiwa na askari wengine watatu walimuongoza kuelekea chumba cha mahabusu pale mahakamani ili asubiri gari la kumpeleka gerezani, na wakati akiongozwa kutoka pale kwenye chumba cha mahakama, Roman alipitishwa karibu na alipokuwa amesimama Deus na muedesha mashitaka wake. Roman alisimama na kumtazama kwa muda mrefu yule adui yake, kisha kwa sauti iliyojaa utulivu mkubwa alimwambia; “Mimi nakwenda gerezani Deus. Lakini nataka nikuhakikishie kuwa miaka miwili si mingi…nitatoka. Na nikitoka, nakuja kukuua Deus, hilo ni hakika kabisa!” Ilikuwa ni kauli ya kuogofya kuliko zote ambazo Deus alipata kuzisikia. Na wakati akiongea maneno yale, sauti na macho yake vyote vilionesha kuwa Roman alikuwa amedhamiria kulitekeleza lile alilokuwa akilisema. Kwa muda karibu mahakama yote ilikuwa kimya kabisa. Watu walitazamana, kila mmoja aliyesikia kauli ile asijue achukue hatua gani. Deus alibaki akimtazama Roman kwa woga uliokithiri, akishindwa kusema lolote. “Twende Roman…acha mambo hayo sasa!” Koplo Fatma alimwambia huku akimsukuma mbele. Roman alimgeukia na kumtazama kwa jicho kali sana, kisha bila ya kusema neno, aligeuka na kuelekea kule alipokuwa akiongozwa. Kutoka kwenye kona moja ya mahakama ile, Mark Tonto na Sada walikuwa wakimtazama Roman akiondolewa eneo lile huku wakibubujikwa na machozi. Kwa hukumu ile, Roman Kogga akawa amepoteza rasmi kazi yake jeshini…
***
Wiki mbili baada ya hukumu, wakili wa Roman alifanikiwa kufikia muafaka na wakili wa Deus, wa namna ya kumfidia hasara ya kumuunguzia nyumba yake. Ilikubaliwa kuwa nyumba ya Roman aliyoachiwa urithi na wazazi wake iuzwe kwa usimamizi wa mahakama, na pesa zitakazopatikana zilipe gharama za ukarabati wa nyumba ya Deus. Swala likafikiwa muafaka. Hivyo, ndani ya muda mfupi sana, Roman alipoteza mdogo wake wa damu, kazi yake iliyokuwa ikimpatia riziki hapa duniani, na nyumba yake ya urithi. Na yote ni sababu ya mtu mmoja tu…Deusdelity Macha.
*** Miezi miwili baadaye, Mark Tonto alienda kumtembelea kule gerezani. “Mark…” Roman alimsalimu rafiki yake huku akitabasamu. Mark Tonto alifanya jitihada za hali ya juu kujizuia asiangue kilio. “Roman…vipi hali yako bwana…?” Alimuuliza kupitia kwenye dirisha la wavu lililowatenganisha. “Sio mbaya…nahesabu siku tu…” Roman alimwambia. Mark aliuma midomo na kutikisa kichwa. “Jamaa yetu ameacha kazi…ametoa notisi ya saa ishirini na nne…” Mark alimwambia. Roman alimtazama kwa macho ya kuuliza. “Deus…amecha kazi?” “Yap! Taarifa nilizozipata zinasema kuwa jeshi lilikuwa linajiandaa kumuachisha kazi kutokana na mazingira ya kujihusisha kwake na kifo cha Rachel…inasemekana ingawa mahakama haikumtia hatiani kwa kuwa hakushitakiwa kwa kifo kile, tayari alikuwa ameshalitia doa jeshi…” “Kwa hiyo yeye akawahi kujitia kuacha kazi kabla hajafukuzwa?” Mark akaafiki kwa kichwa. Roman akatikisa kichwa kwa masikitiko, uso wake ukionesha kukereka na tabia ile. “Na sasa ameingia kwenye ngumi za kulipwa…eti ameamua kuwa professional boxer…” Mark alisema kwa dharau. Lakini Roman alikuwa akimtazama kwa makini, ilhali akionekana kuwa na mawazo mazito, akili yake ikiichambua kwa kasi sana habari ile iliyoletwa na Mark. “Unasema kaamua kuwa bondia…wa kulipwa?” Roman alimuuliza tena kwa sauti iliyojaa udadisi. Mark alimtazama kwa mshangao kidogo. “Ndio…kwa nini?” Roman alikaa kimya kwa muda, akiwa kwenye mawazo mazito. “Okay, naomba kuanzia sasa unikusanyie habari zake zote.Najua atakuwa anaandikwa sana magazetini, naomba unikusanyie makala zote…nitakapotoka nitataka kuziona…” Hatimaye alisema. Mark akamtazama kwa muda. “Kwa nini unataka habari zake…kuna kitu hujaniweka wazi Roman?” “Usijali. Naomba unifanyie hivyo nikuombavyo Mark…na…mengine nitakueleza kadiri siku zinavyokwenda. Kuna wazo limepita kichwani mwangu, ila nahitaji kulichekecha vizuri kwanza…kisha nitakueleza…” Roman alimjibu. Mark Tonto alimtazama yule rafiki na mwanafunzi wake kwa muda, kabla ya kukubaliana naye. “Okay, Roman…unajua nitafanya lolote kwa ajili yako…” “Thanks buddy!” Hiyo ilikuwa ni kiasi cha miaka miwili na miezi kadhaa iliyopita…
******
Siku mbili baada ya ujio wa Inspekta Fatma pale nyumbani kwake Bagamoyo, Roman, alipanda ndege kuelekea visiwa vya ushelisheli kwa ajili ya maandalizi ya pambano lake na Deusdelity Macha. Pamoja naye walikuwako Kate, Mark na Dan Dihenga. Ilikuwa ni miezi mitatu ya mazoezi mazito kwa Roman kuliko wakati wowote maishani mwake tangu aanze kucheza ndondi. Wakati wote akiwa kwenye mazoezi yake kule ushelisheli, huku nyumbani matangazo ya redio, televisheni na hata magazeti, yalizidi kulinadi pambano lile lililokuwa likisubiriwa kwa hamu. Kambi za ushabiki baina ya mabondia wale wawili zilizidi kukua, watu wakiwekeana madau makubwa na madogo. Vipindi maalum vya michezo viliwasiliana naye moja kwa moja kwa simu akiwa kule ushelisheli na kumhoji juu ya maandalizi yake kwa mpambano ule wa kihistoria, kama jinsi alivyokuwa akihojiwa Deus aliyekuwa Tanzania. Kila bondia alikuwa akijigamba kumuonesha kazi mwenzake. Na kwa upande mwingine, wadhamini wao pia walikuwa wakiwatumia mabondia wale kushindanisha biashara zao. Picha za Roman akiwa ushelisheli akiongea kwa simu ya kampuni iliyomdhamini zilionekana kwenye matangazo ya televisheni na magazeti, na wakati huo huo, picha za Deus akizinadi huduma za simu za kampuni inayomdhamini nazo zilionekana kwenye televisheni, magazeti na mabango ya barabarani. Ndani ya miezi mitatu ile, Roman Kogga na Deusdelity Macha, walikuwa watu maarufu sana miongoni mwa watanzania na duniani kote.Lakini ukweli ulibaki kuwa mshindi wa pambano lao, ndiye ambaye angekuwa maarufu zaidi ya mwenzie. Hatimaye siku ya pambano iliwadia. Pambano lilipangwa kufanyikia kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar.
***
Roman, Kate na Mark waliingia nchini saa nne asubuhi siku moja kabla ya pambano. Dan Dihenga alitangulia siku moja kabla yao ili kufanya maandalizi ya muhimu. Akiwa uwanja wa ndege, kundi la waandishi wa habari lilimzonga Roman kwa maswali juu ya matarajio yake katika pambano lililokuwa mbele yake. “Kama nilivyosema kule Kairo, pambano la kesho ni la kusherehekea kukabidhiwa kwangu ule mkanda niliounyakua kule Kairo…kwa hiyo nawaomba watanzania waje kwa wingi kushuhudia nikikabidhiwa mkanda wangu hiyo kesho. Ahsanteni sana.” Roman aliwajibu waandishi huku akipigwa picha za magazeti, televisheni na kurekodiwa na wanahabari wa vyombo mbalimbali vya redio. Kwisha kusema hivyo, Dihenga alimuongoza Roman na msafara wake kwenye gari la kifahari alilowaandalia na kuondoka eneo lile. Siku ile Dan hakuwapeleka Bagamoyo, badala yake msafara wao uliishia kwenye hoteli ya kifahari ya Movenpick, jijini. “Leo tutalala hapa Roman…” Dan alisema, “…na tutaondokea hapa kwenda ukumbini hiyo kesho.” “Wow! Yaani tayari mmeshaanza kunipa huduma za kibingwa? Safi sana!” Roman alisema huku akitabasamu, na wote walicheka. “Hizo ni fadhila za wafadhili wetu Roman…kwa hiyo hatuhitaji kuwaangusha kesho, au sio?” Dan alimwambia. “Ah, kuangushwa kesho ni lazima, hakuna ujanja…” Roman alijibu akiwa hana utani hata kidogo. Wote waliokuwemo mle ndani walimshangaa. “Ati…?” Mark Tonto aliuliza kwa mshangao. “Nini…?” Dan alimaka, wakati Kate akimtazama Roman kwa macho yaliyojaa maswali. “…ila tu atakayeanguka hiyo kesho ni Deus!” Roman alimalizia kauli yake huku bado akiwa makini sana. Pumzi za ahueni ziliwashuka wenzake aliokuwa nao mle chumbani, Mark akiangua kicheko kikubwa. “Ah, Roman ulitupa ugonjwa wa moyo kidogo pale…” “Mwenye ugonjwa wa moyo saa hizi ni Deus tu…” Roman alimjibu. Saa sita mchana siku ile walienda kwenye zoezi la kupima uzito kwenye ukumbi wa habari maelezo. Waandishi wa habari kutoka katika kila chombo cha habari nchini na nje ya nchi walikusanyika. Mabondia wote wawili walifika na makocha na ma-paromota wao. Kwa mara ya kwanza baada ya miaka miwili na miezi kadhaa, Roman alikutana tena uso kwa uso na hasimu wake Deusdelity Macha. Walipoonana tu, mabondia wale walisogeleana na kutunishiana vifua huku wakitazamana usoni kwa ghadhabu, wapiga picha za televisheni na magazeti wakipiga picha tukio lile kwa bashasha. “Nilipata ujumbe wako kutoka kwa Inspekta Fatma, Roman…na nilimwambia kuwa nitakujibu ulingoni siku ya tukio…na sasa siku imewadia!” Deus alimwambia kwa sauti iliyojaa uchokozi. Roman alibaki akimtazama kwa ghadhabu, akiwa amebetua midomo yake kwa kukereka, lakini hakumjibu kitu. “Vipi, leo huna la kusema Roman? Hakuna macho ya watu ya kukupa kiburi cha kuropoka utumbo wako?” Deus alimsaili kichokozi. Roman alizidi kumtazama kwa ghadhabu, sasa midomo ikimcheza kwa hasira, misuli ikiwa imememtutumka, mishipa ya shingo ikiwa imemsimama. “Nilipokuwa napelekwa gerezani nilikuahidi jambo Deus…” Hatimaye Roman alimjibu kwa sauti iliyojaa ghadhabu na dhamira halisi, “…kesho nitakutimizia hiyo ahadi, kwa hiyo usiniharakishe…vumilia kidogo tu, ahadi itatimia!” Uso wa Deus ulimbadilika, na akafunua kinywa kutaka kusema kitu, lakini muda huo huo walinda usalama wakaja kuwatenganisha. Zoezi la kupimana uzito lilipokamilika, waandishi wa habari waliwahoji wale mabondia kwa muda, na Deus akajigamba kuwa yeye ndiye bingwa na ataendelea kuwa bingwa baada ya pambano lake na Roman. Kwa upande wake Roman alirudia ile ile kauli yake aliyoitoa kule Kairo, na pale uwanja wa ndege wa JK Nyerere. Alikuwa anaenda ukumbini kuchukua mkanda wake alioushinda kule Kairo. Magazeti yakaandika, redio an televisheni zikanadi, na homa ya ushabiki juu ya nani atamshinda mwenzake kati ya Roman Kogga na Deusdelity Macha ilipanda mara dufu…
***
*** Ulingo wa kimataifa ulitengenezwa ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee jijini. Ukumbi ule ulibadilika kwa kupambwa kimataifa. Watazamaji na majaji walioteuliwa na shirikisho la ndondi duniani walikuwa wameshaingia ukumbini saa kumi na mbili za jioni. Mapambano kadhaa ya utangulizi,au exhibition, yalifanyika, lakini ilikuwa wazi kuwa wote waliofurika ukumbini usiku ule walikuwa wamekuja kushudia pambano kati ya bingwa wa dunia Desudelity Macha, na mpinzani wake mkubwa kabisa, Roman Kogga. Ndipo muda ulipowadia, ukumbi ukiwa umejaa wahka, mtangazaji maarufu alipanda ulingoni na kutangaza kuwa muda wa pambano kuu la usiku ule, au main card, ulikuwa umewadia. Ukumbi ulilipuka kwa hoi hoi na vifijo. Mwamuzi wa pambano lile kutoka Caracas, Venezuela, alipanda ulingoni na kuwaita mabondia. Ndipo kwa mbwembwe za hali ya juu, mtangazaji alianza kwa kumuita mpinzani, Roman Kogga ulingoni. Roman aliingia ukumbini kutokea mwenye chumba cha mapumziko akiwa kidari wazi na chini amevaa bukta yake nyeusi ikiwa na mkanda mpana kiunoni, jina lake la kwanza likiwa limeandikwa kwenye mkanda wa bukta ile kwa maadishi makubwa ya rangi nyeupe. Ukumbi ulilipuka kwa hoi hoi wakati alipokuwa akikimbia kibondia kuelekea ulingoni akisindikizwa na second wake, ambaye pia ndio alikuwa kocha wake, Mark Tonto. Roman alipanda ulingoni na kukimbia huku na huko, akitupa ngumi hewani kwa kasi ya ajabu kisha akajipigapiga kifuani na kuinua ngumi yake juu kwa ishara ya ushindi. Ukumbi ulipagawa kwa vifijo. Kwenye viti vya watazamaji, Dan Dihenga alimgeukia Kate kwa jazba. “That’s my boxer! Leo ndio Deus atajuta kunisaliti mwanaharamu!” Alimwambia. Kate alibaki akitazama kwa wasiwasi. “Naomba mungu amsaidie Roman ashinde Dan…naomba sana!” “Ooh! Atashinda tu Kate…atashinda..tena kwa kishindo!” Kule ulingoni, mtangazaji alimnadi bingwa Deus“deadly” Macha, na muda huo Deus naye alitoka chumbani kwake na kuelekea pale ulingoni, akiwa kifua wazi, na chini akiwa ameva bukta nyekundu, jina lake likiwa limeandikwa kwa maadishi makubwa meusi kwenye mkanda mpana wa bukta ile, mkanda wake wa ubingwa wa dunia akiwa ameuning’iniza begani kwake. Ukumbi ulimpokea kwa shangwe na mayowe mengi, naye akawa anatembea taratibu kuelekea ulingoni akisindikizwa na kocha wake huku akiwa ameinua juu ngumi yake. Lakini ilionekana wazi kuwa Deus alikuwa anaenda ulingoni kama ng’ombe anayepelekwa machinjoni. Hakuonesha bashasha ambayo mashabiki wake waliitarajia. Alipanda ulingoni, na hapo alibadilika ghafla. Alianza kurukaruka huku na huko, na kutupa ngumi za haraka haraka hewani huku ukumbi ukimshangilia kwa jazba, kisha akageuka kila upande wa ulingo akiuonesha juu ule mkanda wake aliokuwa anaushikilia. Baada ya kila bondia kufanya majigambo yake ulingoni, mwamuzi aliwatuliza na kuwaita ili kuwapa nasaha za maadili ya pambano. Kisha kila bondia akarudi kwenye kona yake.Mwamuzi aliwaita kati ya ulingo na wale wapinzani wawili wakaziacha kona zao na kwenda kusimamiana kibondia katika ile pozi ya honour stance, wakisubiri amri ya kuanza pambano.Hatimaye kengele ya kuanza pambano ikagongwa, na mwamuzi akaruhusu pambano. Deus alianza raundi ya kwanza kwa kasi. Akimshambulia Roman kwa ngumi za haraka haraka na zenye uzito wa kumpeleka mtu chini, lakini Roman alikuwa mtulivu, akimkwepa na kumtandika ngumi za kudokoa na mara moja moja akimtupia ngumi kali za ghafla ambazo hazikuleta madhara yoyote kwa Deus. Na sekunde chache kabla ya raundi ya kwanza kuisha, mabondia wale wawili walijikuta wakiwa wamekumbatiana. “Umemuua mdogo wangu Deus…sasa leo ndio nami nakutimizia ahadi niliyokupa siku ile nilipokuwa napelekwa gerezani, mshenzi we!” Roman alimnong’oneza kwa hasira. Deus alifurukuta kujichomoa mikononi mwa Roman, lakini Roman alizidi kumbana mpaka refa alipokuja kuwatenganisha. Wote walirudi kwenye kona zao na kuanza kurudiana tena kwa pambano wakati kengele ya kumaliza raundi ilipogonga. “Unamchezea Roman!” Mark alimkemea Roman wakati wa mapumziko. Roman alibaki akimkodolea macho yaliyojaa vitisho Deus, ambaye alibaki akimtupia macho huku akitweta kutokea kule kwenye kona yake. “Nampiga taratibu…mpaka ajute kujiingiza kwenye ndondi!” Roman alimjibu kocha wake na kuinuka kurudi ulingoni baada ya kengele ya raundi ya pili kugongwa. Raudi ya pili, Deus aliingia kwa kasi kali zaidi, sasa akionesha hasira za wazi wakati Roman alikuwa mtulivu zaidi, akimtupia makonde ya kushtukiza huku akimcheka mpinzani wake. Lilikuwa ni pambano kali, na kwa dakika moja nzima, Deus alimbana Roman kwenye kona na kumvurumishia makonde makali ya mfululizo huku ukumbi ukirindima kwa hoi hoi, lakini Roman alifanikiwa kuyakwepa masumbwi yale akiwa pale pale kwenye kona, mengine akiyakinga na machache yakimpata, ndipo akiwa pale pale kwenye kona alipojikunja na kujikunjua kwa sumbwi kali la upper cut lililojikita sawia kidevuni kwa Deus na kumyumbisha vibaya, naye akajichomoa kutoka kwenye ile kona na kurudi kati kati ya ulingo. Lakini sasa Deus alikuwa ameshapata matumaini ya kumuangusha mpinzani wake hivyo akamuendea tena kwa kasi, Roman akampisha kidogo na wakati huo huo akimzungushia ngumi ya kushoto, Deus aliiona na kujikinga haraka, na kushitukia akipokea cross nzito ya mkono wa kulia lililotua sawia kwenye upande wa uso wake. Deus aliyumba mpaka kwenye kamba na ukumbi ulichangamka kwa vifijo. Roman alibaki akirukaruka katikati ya ulingo akimsubiri mpinzani wake, ingawa ile ilikuwa ni nafasi nzuri ya kumbana Deus pale kwenye kamba na kumsulubu atakavyo. Deus alirudi kwa hasira na kujaribu kumtupia makonde ya nguvu. Roman alimpisha tena kidogo na kumtandika konde la tumbo, na Deus alijikunja huku akimkumbatia Roman. “Unamkumbuka Rachel Deus…?” Roman alimnong’oneza wakiwa wamekumbatiana pale ukumbini. Deus alijikurupusha kujinasua kutoka mikononi mwa Roman, wazi kuwa yale maneno ya Roman yalikuwa yakimchanganya, na Roman alitumia nafasi hiyo kumuachia ghafla na hapo hapo akampa upper-cut nyingine ya kulia iliyotua tena kidevuni. Deus alitupwa nyuma na kuangukia goti pale ulingoni. Ukumbi ulilipuka kwa shangwe, na Roman alikuwa anamuendea wakati kengele ya kumaliza raundi ulipogonga, na ukumbi ukaachia mguno wa fadhaa. Pambano liliendelea kwa raundi nyingine mbili, na waliposhikana tena kwenye raundi ya tano, Roman alimnong’oneza, “Unakumbuka jinsi nilivyokuvunja taya Deus…? Unakumbuka jinsi nilivyoua mabondia wawili ulingoni…?” Deus alipiga ukelele za hasira na kumsukuma nyuma kwa nguvu Roman. Mara moja refa aliingilia kati na kuweka nidhamu pale ulingoni. Deus alibaki akimkodolea macho ya ghadhabu Roman huku akitweta, wakati Roman akimtazama huku akimcheka. Sasa Deus alionekana wazi kuwa alikuwa akipigana huku akiwa makini sana na ngumi ya kushoto ya Roman, lakini kufikia raundi ya saba, mabondia wote walionekana kama kwamba walikuwa wametoshana nguvu. Lakini ilipofikia raundi ya nane, Roman aliingia na mtindo tofauti kabisa wa upiganaji. Badala ya kusimama kwa mtindo aliokuwa akiutumia tangu mwanzo wa pambano wa orthodox, yaani kusimamia kulia, ambao ndio ungempa nafasi nzuri zaidi ya kumpiga mpinzani wake kwa mkono wa kushoto, yeye sasa alitumia mtindo wa kusimamia kushoto, yaani southpaw. Deus alichanganyikiwa, kwani kwa kutumia msimamo huu, Roman hangeweza kutupa konde la kushoto. Deus akahisi Roman amejisahau, na kuingia kwa makonde ya nguvu na ya mfululizo. Katikati ya raundi ile, ghafla bila ya Deus kutaraji, Roman alirudisha tena mtindo wa orthodox na kumtupia konde kali la kushoto lililomkosa kichwani Deus kwa umbali mdogo sana. Deus akajibu kwa konde la kulia la mtindo wa jab, lililompata Roman tumboni. Roman akayumba, Deus akaingia mzima mzima kwa sumbwi la cross, ambalo linapigwa kwa karibu huku mpigaji akienda na mwili wake wote kwa mpinzani wake. Roman alikuwa ametarajia jambo hili, hivyo alijikunja huku akilalia kulia na kumpisha na wakati huo huo akijikunjua huku akiachia right hook iliyotua upande wa kushoto wa kichwa wa Deus, Deus aliyumba, na hapo hapo Roman akalalia kushoto na kujikunjua haraka huku akiachia left hook iliyompata Deus upande wa kulia wa kichwa. Deus akapoteza mwelekeo, sasa Roman alikuwa upande wake wa kushoto na sio mbele yake tena, ukumbi ulikuwa umepagawa kwa shangwe. Deus akageuka haraka kushoto kwake, lakini Roman akaruka hatua moja mbele na kumtupia ngumi sita za mfululizo za usoni kwa mtindo wa one-two, yaani kulia na kushoto kama mara tatu hivi, kila ngumi iliyoingia ilikuwa ikipokelewa na ukelele wa pamoja kutoka kwa watazamaji. Deus akayumba nyuma na kuangukia kwenye kamba, Roman aliingia pale pale kwenye kamba kwa upper cut ya kulia, na kwenye nukta ya mwisho kabisa akabadili mkono na kumshindilia Deus kwa upper cut ya kushoto iliyompata sawia kidevuni, na hapo Roman aliona macho ya Deus yakipinduka, weusi wa mboni ukipotelea ndani ya macho, na bila kusubiri zaidi alimmalizia na hook ya kulia iliyompata Deus kichwani na kumpeleka moja kwa moja sakafuni kama mzigo. E bwana we! Ukumbi ulilipuka kwa hoi hoi, Dan Dihenga na Kate waliruka wima na kushangilia huku wakikumbatiana, Mark Tonto akifuatilia kwa makini wakati Roman akirudi kwenye kona yake na mwamuzi akianza kumhesabia Deus. Huku nje ya ukumbi, Inspekta Fatma akiwa katika mavazi ya fulana na suruali ya jeans na kofia yake ya kepu kichwani alijipenyeza hadi kwa kocha wa Deus. “Simamisha pambano hili…simamisha sasa hivi kocha uokoe maisha ya bondia wako!” Alimwambia kwa wahka huku akimvuta mkono. Kocha wa Deus alimgeukia kwa mshangao. “Khah, we’ mwanamke vipi…? Hebu toka hapa…!” “No! Mimi ni afisa wa polisi na najua kinachoelekea kutokea…” “Hebu toka hapa, ebbo!” Kocha alimkemea na kugeukia kule ulingoni. Wakati askari wa usalama pale ukumbini walipokuja kumvuta kando Inspekta Fatma. Kule ulingoni Deus aliwahi kusimama ilipofikia nne na kujiweka tayari kwa pambano. Refa alimuuliza iwapo yuko sawa, akaafiki kwa kichwa, akamuwekea vidole viwili mbele ya uso wake na kumuuliza anaona vingapi, Deus akamjibu anaona viwili, refa akaruhusu pambano liendelee.Kutokea upande wa pili wa ulingo Mark Tonto, Kate na Dihenga waliona kile kilichokuwa kikitokea baina ya Inspekta Fatma na kocha wa Deus, ingawa hawakuweza kuelewa ni kwa nini kilikuwa kinaongelewa. Sasa ukumbi ulikuwa hauna utulivu hata kidogo. Deus aliingia kwa kasi ya ajabu, akiwa na ghadhabu za kupelekwa chini na mpinzani wake wakati Roman akiwa amedhamiria kumaliza mchezo na kumuweka Deus mahala pake. Deus alikuja na ngumi ndefu-ndefu za mfululizo, na kwa muda walikuwa wakizungukana bila ya madhara kwa yeyote, wakati ghafla sana Roman alipomuendea kwa kasi mpinzani wake na kusita kama kwamba alikuwa amejigonga miguu na kupoteza uelekeo, akijikunja kutokea kwenye magoti kama anayetaka kuanguka. Deus aliiona nafasi ile na hakuifanyia ajizi. Alimuendea kwa left hook iliyobeba nguvu zake zote, na hapo, bila kutarajiwa, Roman aliruka mbele huku bado ameinama, na kujiinua wima akiwa moja kwa mojambele ya Deus. Deus akajikuta yuko karibu sana na Roman kiasi cha kutoweza kumpiga kama alivyokusudia, haraka alijitahidi kurudi nyuma lakini alikuwa amechelewa kwani alikuwa ameingia kwenye mtego wa Roman kama inzi aingiavyo kwenye utando wa buibui, na wakati alipojiinua wima namna ile, Roman aliinuka na upper cutnzito ya kulia na hapo hapo akaifuatishia na upper cut nyingine ya kushoto. Yaani ilikuwa ni one-two ya upper cut! Si mabondia wengi wanaoweza kupiga namna ile, mara lipigwapo pigo la namna ile, basi huwa ni pigo la kumaliza mchezo. Ukumbi ulipayuka kwa mayowe, wakati kwa mara nyingine katika raundi ile, Deus alipojiona akinyong’onyezwa nguvu za magoti na mikono kwa mapigo ya Roman. Roman alimuona mpinzani wake akilegea, na ndipo kwa nguvu zake zote, alipomshushia konde la mkono wake wa kushoto kwa mtindo wa left hook. Deus aliiona ngumi ikimwendea kakini hakuwa na nguvu tena ya kuikwepa wala kujikinga. Ngumi ilimpata Deus juu kidogo ya sikio na kumpeleka kiubavu-ubavu mpaka chini, akisambaratika sakafuni na kubiringika vibaya. Ukumbi uliachia shangwe za ajabu… “Kwisha kazi bloody kenges! Roman kamaliza mchezo bloody bastard!” Dihenga akamgeukia Kate na kumwambia kwa bashasha. Lakini kwa namna ambayo haikutegemewa,Deus alijiinua haraka na kusimama, akayumba kinyuma-nyuma na kusimamia kamba. Mashabiki wake waliamsha hoi hoi za kumtia moyo, wakitaja jina lake kwa pamoja. Deeee-us…deadly! Deeee-us…deadly! Deee-us…deadly…. Inspekta Fatma alimfuata kocha wa Deus kwa mara nyingine.
“Inabidi usimamishe hili pambano sasa hivi kocha! Please…!” Alimwambia kwa jazba. Lakini kocha alikuwa makini na kile kilichokuwa kikiendelea kule ulingoni. “No! Anaendelea na pambano bado mwanamke! Hebu tok…” Fatma alilikwapua taulo jeupe kutoka mabegani kwa yule kocha na kurukia kamba za ule ulingo huku akilitupia ndani ya ulingo lile taulo. “No Dan…look…!” Kate alipayuka huku akioneshea kule ulingoni, ambako Inspekta Fatma akiwa ameshikilia kamba za ulingo huku akipayuka maneno ya wahka. Mwamuzi alishangaa kuona taulo likitupiwa ulingoni na mtu asiye kocha wa yeyote kati ya wale mabondia wawili. Ukumbi mzima uliachia mguno wa fadhaa uliofuatiwa na kelele za kuchanganyikiwa. Roman alimtazama yule askari mtukutu kwa hasira, wakati Deus akimgeukia kwa mchanganyiko wa mshangao na kutoelewa. “Achana na hili jambo Deus! Huwezi kushinda hili pambano…okoa maisha yako!” Inspekta Fatma alimpigia kelele yule bondia aliyeelemewa. Hapohapo Fatma akamgeukia Roman. “Haina haja ya kuendelea na pambano Roman, tayari umeshaonesha uwezo wako…achana na visasi!” “Toa nje huyo mwanamke!’ Mwamuzi alipiga kelele wakati askari wa jeshi la polisi waliokuwa kwenye sare rasmi za kazi wakimkamata Fatma na kumvuta kutoka ulingoni Fatma alizing’ang’ania zile kamba huku akipiga kelele. “No, niacheni! Deus achana na pambano hili tafadhali! Kubali kushindwa tu…there is no way utashinda hili pambano! Mwenzio hakuja ulingoni kwa nia ya mchezo kama wote hapa wanavyodhani, nawe walijua hilo! Get out now wakati bado uko hai Deus…PLEASE!” Deus alimtazama yule mwanadada akitolewa pale kwenye kingo za ulingo huku akitweta. Alimgeukia Roman aliyekuwa amesimama katika ile honour stance akisubiri uamuzi kutoka kwake huku akimtazama kwa macho ya ghadhabu iliyokithiri. “Achana na hili jambo Deus! Huwezi kushinda hili pambano…okoa maisha yako!” Inspekta Fatma alimpigia kelele yule bondia aliyeelemewa. Hapohapo Fatma akamgeukia Roman. “Haina haja ya kuendelea na pambano Roman, tayari umeshaonesha uwezo wako…achana na visasi!” “Toa nje huyo mwanamke!’ Mwamuzi alipiga kelele wakati askari wa jeshi la polisi waliokuwa kwenye sare rasmi za kazi wakimkamata Fatma na kumvuta kutoka ulingoni Fatma alizing’ang’ania zile kamba huku akipiga kelele. “No, niacheni! Deus achana na pambano hili tafadhali! Kubali kushindwa tu…there is no way utashinda hili pambano! Mwenzio hakuja ulingoni kwa nia ya mchezo kama wote hapa wanavyodhani, nawe walijua hilo! Get out now wakati bado uko hai Deus…PLEASE!” Deus alimtazama yule mwanadada akitolewa pale kwenye kingo za ulingo huku akitweta. Alimgeukia Roman aliyekuwa amesimama katika ile honour stance akisubiri uamuzi kutoka kwake huku akimtazama kwa macho ya ghadhabu iliyokithiri. “Yuko sahihi Deus! Kubali kushindwa…huu mkanda hauna thamani ya maisha yako!” Alimwambia, na akaona Deus akikunja uso kwa ghadhabu maradufu. Kule nje kocha wa Deus alikuwa akiruka huku na huko kwa hasira, akipinga kitendo cha yule mwanadada kurusha taulo ndani ya ukumbi bila ya ridhaa yake. Kule kwenye meza ya majaji nako kulikuwa kuna mtafaruku mkubwa, baadhi wakisema pambano liendelee wakati wengine wakishauri lisimamishwe. Huku ulingoni, Deus alilitazama lile taulo lililokuwa mbele yake pale chini, kisha kwa mguu wake wa kulia alilisukumia nje ya ulingo na kusima katika ile honour stance tayari kuendelea na pambano huku akimtazama Roman kwa ghadhabu. “Sikuja hapa kushindwa Roman! Kama unadhani maisha ni bora zaidi ya mkanda, jitoe wewe kwenye pambano!” Alimwambia kwa hasira, na Romana akaona kuwa yule jamaa alikuwa amedhamiria. Ukumbi uliamka kwa hoi hoi mpya, wakati Inspekta Fatma akijishika kichwa na kuangukia magoni sakafuni huku akitazama kile kilichokuwa kikitokea kule ulingoni kwa fadhaa kubwa. Kabla mwamuzi hajapitisha uamuzi, Deus alijiengemeza kwenye kamba na kuziacha zimsukume mbele kwa kasi naye akaenda mzima mzima huku akiachia ukelele wa ghadhabu ilhali akimsukumia Roman konde la mkono wa kulia. Roman alimuona Deus akimjia na ngumi ya mkono wa kulia huku miguu ikimuishia nguvu, na ndipo aliporuka mbele haraka kumfuata mpinzani wake yule bazazi, mkono wake wa kushoto ukiwa juu kabisa hewani, kisha akaushusha na kuuzungusha kutokea chini na kumshindilia konde zito sana kwenye upande wa kichwa chake chini kidogo ya jicho lake la kulia. Deus alienda chini kama mzigo, kinga ya meno iliyokuwa kinywani mwake ikimtoka na kusambaratika mpaka nje ya ulingo. Roman alirudi nyuma na kusimama kwenye kona ya neutral, akiiacha kona yake, huku akimtazama mpinzani wake kwa makini. Deus alijiinua na kubaki akiwa amepiga magoti na ameshika sakafu kwa mikono yake, akajiinua wima, akayumba kulia na kushoto, kisha akaenda chini mzima mzima na kuanguka chali kwa kishindo. Ukumbi ulilipuka kwa shangwe na hoi hoi zisizo kifani. Roman alibaki akimtazama mpinzani wake akiwa ametulia chali pale sakafuni, damu ikimtoka puani na mdomoni. Mwamuzi alimsogelea Deus na kuanza kumhesabia na ilipofika tano bila ya Deus kutikisika, watazamaji nao wakawa wanahesabu pamoja naye. “SITA…SABA…NANE…TISA…KUMIIIIII….!” Ukumbi ulilipuka kwa hoi hoi na nderemo, jina la Roman likitamkwa kila kona ya ukumbi ule. Mwamuzi ulimuinua Roman mkono juu kumtangaza mshindi, na mara baada ya kufanya hivyo alimgeukia Deus aliyelala pale chini, kisha akawaashiria wahudumu walete machela. Roman alibaki akiwa anatweta huku ameinua juu mkono wake wa kushoto kwa ishara ya ushindi huku akimtazama adui yake aliyelala pale chini. Machozi yalikuwa yakimtiririka na alikuwa akigeuka huku na huko akiwa akiwatafuta Dan, Mark na Kate, lakini kwa namna ya ajabu alikuwa hawaoni. Sasa ulingo ulikuwa umevamiwa na baadhi ya watu wa kambi ya Deus walioenda kumtazama mtu wao aliyelala taabani pale chini. Walimvua glovu na mikono yake ikabaki na zile bandeji mabondia wanazozifunga mikononi mwao kabla ya kuvaa glovu za kupigania. Macho ya Roman yakaangukia kwa Inspekta Fatma aliyekuwa amepiga magoti nje ya ulingo huku akimtazama kwa fadhaa na masikitiko makubwa. Walitazamana… Huku nyuma Deus alijaribu kujiinua lakini alishindwa. Watu wachache walikuwa wamemzonga pale chini lakini bado akili yake iligoma kabisa kukubali kuwa alikuwa amebwagwa chini na Roman. Aligeuza uso wake uliomvimba na kumuona Roman akiranda kibabe pale ulingoni huku akiwa ameinua juu mkono wake, na ghadhabu zikamzonga. Alihisi maumivu yasiyo ya kawaida kichwani…ndani ya kichwa chake, na kwa mara ya kwanza akabaini kuwa amekuwa akisikia mvumo mzito masikioni mwake tangu alipojigundua kuwa alikuwa ameagushwa chini na Roman. Ina maana huu ndio mwisho wangu kweli? Alijisukuma na kuinuka kwa kujishikilia kwenye kamba za pale ulingoni na baadhi ya watu wake wakamsaidia kuinuka. Nimevuliwa ubingwa na Roman! “Tulia tu Deus, tulia. Pambano limeisha hili…tumeshindwa kaka!” Mmoja wa watu wa kambi yake alimwambia, bila ya kujua kuwa Deus hakuwa akisikia lolote zaidi ya ule mvumo mzito masikioni mwake. Alijishikilia kwenye stuli iliyowekwa pale kwenye kona yake kwa ajili ya kupumzikia mwisho wa raundi, na hata pale alipojishikilia kwenye stuli ile, aliona tone la damu nzito kutoka puani kwake likiangukia pale kwenye ile stuli. Yaani Roman ndio amenifanya hivi kweli? Aligeuka kule alipokuwa Roman na kuona kuwa alikuwa hatua chache kutoka pale alipokuwa, akiwa amemgeuzia mgongo na amezibwa kidogo na watu. Kwa nguvu alizobakiwa nazo zilizosukumwa na ghadhabu ya hali ya juu aliikwapua ile stuli na kuwasukuma wale watu waliomkinga Roman huku akimwendea kwa hasira… Roman alikuwa anaanza kuhamisha macho yake kutoka kwa Inspekta Fatma ili awasake akina Kate, wakati alipoona uso wa yule Inspekta ukibadilika na kuwa wa taharuki, macho yakimtumbuka na kinywa kikimtanuka bila ya sauti kumtoka. Pamoja na badiliko lile alilolishuhudia katika uso wa Inspekta Fatma alisikia sauti ya Kate ikiita kwa wahka kutoka nyuma yake. “Roomaaaaaan!” Wito wa Kate ulikuja nukta moja tu kabla ya ule wa Inspekta Fatma ambaye hapo naye alipiga ukelele wa hamaniko huku akimuoneshea kwa mkono wake nyuma yake. “Angaliaaaaaaa!” Haraka Roman aligeuka nyuma yake… La Haula! Alijikuta uso kwa uso na Deus aliyekuwa amefinyanga uso kwa ghadhabu huku akiwa ameinua juu ile stuli kwa mkono wake wa kulia, na aliona wazi kuwa ile stuli ilikuwa inamshukia kichwani… Deus hakuwa akisikia mayowe ya watu waliokuwa wakipiga kelele kutahadharisha juu ya kile alichokuwa akikifanya, na aliishusha kwa nguvu sana ile stuli kichwani kwa Roman aliyekuwa ameegemea kamba pale ulingoni bila ya namna yoyote ya kujiokoa… Kate, Dan na Mark Tonto waliokuwa upande wa pili wa ulingo waliachia vilio vya fadhaa huku wakishuhudia kiwetewete kilichokuwa kinatokea. Bila ya kuhama hata kidogo kutoka pale alipokuwa amesimama, Roman alijipindua kutokea kiunoni kwenda juu na kulalia kulia kwake huku akiwa ameegemea kamba za ulingo, na pigo baya la Deus likakikosa kichwa chale na kumpunyua kidogo juu kidogo ya unyusi wake wa kushoto, na hapohapo, bila ya kufikiri wala kupanga, Roman akajigeuza kulalia kushoto huku sumbwi lake la kushoto likichomoka kwa nguvu yenye msukumo wa ajabu na kumshindilia Deus kwa upper cut nzito sana iliyojikita sawia chini ya kidevu na kumnyanyua hewani mzima mzima kabla ya kumbwaga tena sakafuni kama mgomba. E Bwana we! Ukumbi sasa ulilipuka kwa yowe moja kubwa la pamoja, ambalo halikuwa la kushangilia bali na la mshituko, au mastaajabu, au mshangao. Kisha kimya kikatanda ukumbi mzima wakati Kate, Dan na Mark wakivamia ulingo na kwenda kumzingira Roman aliyebaki akiwa ameegemea kamba huku mikono yake ameiinua kibondia katika ile honour stance, tayari kuendelea na pambano kama lipo. Kate alishindwa kujizuia na kumkumbatia Roman pale pale ulingoni. Roman naye akamkumbatia huku ukweli wa kile kilichotokea pale ukimfunukia wazi akilini mwake. “Oh, Roman! Alitaka kukuua yule Roman!” Kate alibwabwaja, na Roman ahakuwa na jibu, kwani alihisi donge kubwa likimkaba kooni. Watu wengine pamoja na watoaji huduma ya kwanza walimkibilia Deus aliyekuwa amelala chali pale kwenye sakafu ya ulingo ule huku damu ikitambaa taratibu pale sakafuni kutokea sehemu kwenye kichwa cgake. Wale wahudumu wa huduma ya kwanza waliweka machela kando ya Deus pale ulingoni na kumchunguza kwa muda, kisha mmoja akamgeukia mwamuzi kwa macho yaliyohamanika. “Amekufa huyu refa!” Alisema kwa wahka mkubwa. Mwamuzi alibaki akiwa amekodoa macho. Roman aliyeisikia kauli ile alifumba macho huku akimeza funda kubwa la mate kondoa donge lililomkaa kooni. “Nimelipiza kifo chako Rachel…sasa unaweza kutulia kwa amani huko uliko mdogo wangu…rest in peace.” Alinong’ona peke yake huku akiwa amemkumbatia Kate kwa mkono mmoja, ilhali kwa ule mwingine akiwa amenyoosha ngumi yake juu, jina lake likitajwa kwa shangwe ukumbi wote ule. Rooman…Koooga! Rooman…Kooogga! Roooman…Kooogga! Hatua chahe pale ulingoni, Mark Tonto alikuwa akimtazama yule rafiki yake aliyetimiza azma aliyojiwekea tangu akiwa gerezani, na hakuweza kuzuia machozi kumtiririka. Moja kwa moja alikutana na macho ya Inspekta Fatma aliyekuwa akimtazama kwa macho yenye mchanganyiko wa fadhaa na kutoamini, naye akakwepesha macho yake na kujichanganya na akina Dihenga na Kate, pamoja na kundi la mashabiki waliovamia ulingo na kumbeba Roman juu juu. Roman aliinua juu ngumi yake huku akibubujikwa na machozi. “Nimelipiza kifo chako Rachel…nimelipiza…kama nilivyokuahidi!” Alijisemea mwenyewe wakati akimshuhudia bingwa wa zamani Deusdelity Macha akitolewa ulingoni akiwa kwenye machela. Saa moja baadaye dunia na umma wa watanzania walitangaziwa kuwa bondia Deusdelity Macha alifariki dunia akiwa ulingoni baada ya kupigwa na mpinzani wake wakati akitetea ubingwa wake wa dunia katika uzito wa Super Middle, dhidi ya bingwa mpya wa dunia wa uzito ule, Roman Kogga.
*** Kaburi lilikuwa limejengewa vizuri kwa marumaru ghali, na msalaba uliokuwa kwenye kichwa cha naburi lile ulikuwa umesimama wima, nao ukiwa umetengenezwa kwa marumaru. Kwenye kichwa cha kaburi lile, kibati cha shaba kilichojengewa pale kaburini na kuwekea kioo juu yake kilimnadi wazi yule marehemu aliyelala usingizi wa milele ndani ya kaburi lile.
Rachel Kogga Dada uliyependwa kwa dhati. Uliishi, ukadhulumiwa, ukalipiziwa. Pumzika kwa amani. Chini ya maneno yale, paliandikwa tarehe ambayo marehemu Rachel Kogga alizaliwa na ile ambayo aliiaga dunia .
Wanaume nane walikuwa wakichimba shimo katika eneo la makabuli ya isevya mkoani tabora,. naam ilikuwa ni shimo siwezi kusema ni kabuli kwakuwa namna ya uchimbambaji wa shimo lile haukuwa vile kabuli linavyo takiwa kuchimbwa,.kwa haraka haraka pengine ungeweza kuhisi labda ni kwa ajili ya kufukia mzoga wa mnyama aliyekufa siku nyingi na kutoa harufu kali,. lakini swali, Je mzoga wa mnyama hufukukiwa katika makabuli? jibu ni no,. Ama labda hawa jamaa walikuwa na matambiko yao kama zilivyo desturi za jamii nyingi za kiafrika?. Sijui.,. ilikuwa ni kati ya saa moja kasorobo za jioni, kando kidogo kulikuwa na mwili wa mwanamke,.mwili ulio kuwa tayari ni maiti, mwili ule ulifunikwa kanga moja tu iliyo ishia magotini kutokea kichwani. Kulikuwa na mtoto mdogo wa kiume kati ya miaka tisa pekee ndiye aliye onekana kuguswa na msiba ule,alikuwa akilia mno alitamani kufunua uso wa ile maiti uliyo kuwa umefunikwa kwa khanga japo amtie machoni kwa mara ya mwisho lakini alishindwa, aliogopa mkwara mzito alio chimbwa na wale watu walio kuwa wakichimba shimo kwa ajili ya kuufukia ule mwili,. Mtoto alizidi kulia hakutaka kabisa mama yake azikwe akiwa hajamtia jicho la mwisho,.mahaba ya kumtizama mama yake yalizidi kumzonga,.mtoto alikuwa akihaha, Alisimama,akaketi,alipiga piga miguu yake katika ardhi kama kwamba haja ndogo imembana, mikono yake ikiwa kichwani,sauti ndogo ya kilio cha uchungu ilimtoka,akiwa mwingi wa wahka,. “liwalo na liwe” hatimaye mtoto alipata ujasiri, akavuta kanga kutoka kichwani mwa maiti ile ya ‘mamae’ Naam!! Harufu kali na mbaya ikatapakaa eneo lote!. Uso wa yule mwanamke ulikuwa una majeraha makubwa ya moto yalionekana katika macho ya mtoto,. mwili ulikuwa umeungua vibaya mno nyama nyekundu yenye kuvuja maji maji ilijidhihirisha katika macho ya mtoto., majeraha yale yalitoa harufu kali ya mnuko,.mtoto alipata uchungu usio mithilika. “Wewe mshenzi hebu funika huo mzoga unataka tupate kipindu pindu sasa hivi, mwana haramu mkubwa wewe, na uwe mpole vinginevyo tuta kuua sasa hivi kama tulivyo muua huyu MCHAWI mwenzio,. haya funika upesi huo mzoga ” alisema kwa ukali jamaa mfupi mwenye kitambi kikubwa, akiwa amekamata sime yenye makali kote kote,. Mtoto alipatwa na joto la tumbo,hofu na huzuni vikamkamata aliinama karibu na sikio la kulia la mama yake kisha kwa sauti ya chini yenye kitetemeshi akawa anamwita mama yake amke, lakini wapi. alimtingisha kwa nguvu akimwita kwa sauti ya chini yenye mchanganyiko wa kwikwi za kilio, Yule binadamu hakuamka,tayari alikuwa ni maiti, “mama amkaa” nzi walio kuwa wakijipatia chakula chao wengi wakaruka kutoka katika kichwa cha ile maiti, Harufu kali ilizidi kusambaa,. “mamaaa uuuiwii mamaa,.mamaaa amka mamaa amkaa” mtoto alilia,. “keleleee we mbwa kelelee!.alaaa! kelele” yule jamaa mwenye kitambi alimkalipia kwa ukali huku macho yake makali akiyatumbua vibaya kwa kile kitoto kisicho elewa lolote katika hii dunia. Mtoto alinyamaza ghafura,. lile jitu katili lilimkazia macho huku mashavu yake mabaya yakiwa yamevimba kama kwamba kanyweshwa mkojo wa mlevi wa gongo,. “oyaa sogezeni huo mzoga ufukiwe hili shimo linatosha, haya mazingira ya makaburini ikifika saa moja na nusu huwa siyo pazuri huku” alisema mtu mwingie maarufu kwa jina la utani la Kibonde, “Haya wewe mchawi mtoto sogea huko” lile jitu baya la mashavu lilisema kwa dhihaka akimsukuma yule mtoto mfiwa, Mwili ile maiti ulibebwa na watu wanne wawili walishika mikono na wengine wawili walishika miguu kisha ukapelekwa katika shimo dogo na jembamba,. “moja,.mbili,.tatu., twendeeeee” walihesabu kisha ile maiti ya mwanamke ikatupiwa katika shimo kama mzoga wa mbwa, mwili ule ulijibamiza katika kuta za shimo lile kisha ukakaa kihasara hasara., mkono huku mguu kule huku baadhi ya nyama zikimenyeka vibaya,. Mtoto alizidi kulia. Baada ya hapo wakaanza kufukia kwa makoleo na majembe, ndani ya dakika kumi badae zoezi la kufukia ile maiti ya mwanamke likawa limekamilika., “Haya ulale mahala pema motoni mshenzi mkubwa wewe kaloge na huko KUZIMU shetani wewe” alisema yule mtu mwenye sura mbaya na mashavu kama mimba ya panya,.mtoto mdogo aliendaelea kupata donge rohoni mwake,alilia akiwa juu ya tuta la kabuli la mama yake,. Hakuna mtu aliye kuwa na chembe ya huruma kwa yule mtoto,. walimwacha eneo lile wao haoo wakaondoka zoa,. Maumivu makubwa yalitanda ndani yan moyo ya mtoto mdogo, Mwanamke aliye kuwa amefukiwa ndiye alikuwa kila kitu kwenye maisha yake,historia ya kile kitoto inaonyesha hakuwahi kumjua baba, mjombo bibi,wala shangazi,siku zote mama yake alikuwa ndiye baba ndiye mjomba ndiye bibi na ndiye rafiki mkuu katika huu ulimwengu, Waliishi kwa mapenzi yeye na mamaye katika nyumba ndogo ya udongo na makuti katika vitongoji vya isevya,. Hakuwahi kuona jirani ama mtu yeyote akija katika nyumba yao kuwatembelea,.hapakuwepo na ushirikiano wa aina yoyote kati yao na jamii ya watu wa Isevya,. walitengwa katika kila jambo, mama yake ailishutumiwa kwa imani za kishirikina,walimsema ni mchawi,. Kwa mika mingi tangu akiwa mtoto yeye pia hakupata nafasi ya kucheza na watoto wezake, mtaani watoto wote walimkwepa,. sumu ilipandikizwa vichwani mwa watoto wa mtaani kumwepuka kabisa yeye kwa imani kuwa yeye na mama yake ni walozi, siku zote alikuwa katika mazingira ya upweke,ni mama yake peke yake ndiye alikuwa rafikiye,. tangu anapata ufahamu ule uvumi ulikuwa kama kiitikoa cha wimbo mtaani kwamba wao ni wachawi,.katika kipindi cha miaka kadhaa alizoea uvumi ule aliishi kwa furaha yeye na mama yake tu,. “Wewe ndiyo furaha yangu na mimi ndiyo furaha yako kama watu hawatupendi mungu wetu yeye anatupenda siku zote amini hivyo,. na hawezi kutuacha peke yetu,. daima yupo nasi” ni maneno ambayo yaliyo zungumzwa na mama yake kila siku,. Leo mama yake hayupo kauwawa kikatili kwa mapanga kwa tuhuma kuwa ni mchawi kisa tu macho yake ni mekundu. looh! Ujinga gani huu! Mtoto alilia kiasi sauti ikamkauka,wakati huo ilikuwa ni saa mbili kasorobo za jioni giza lilikuwa limekwisha tanda eneo lile la makabuli ya isevya,. hakuonekana mtu yeyote kabisa eneo lile palikuwa kimyaaa! Ni sauti za wadudu na kilio cha mtoto mdogo ndicho kilicho lindima peke yake,. Pamoja na kuwepo kwa hadithi za kuwepo kwa mizimu na ushetani katika mazingira yale ya makabuli lakini Mtoto hakuogopa aliendelea kulala juu ya kabuli la mamaye kwikwi za kilio zikomtoka,. Saa nne usiku ilitimu mtoto aliendelea kuwepo makabulini hakutamani kabisa kuondoka eneo lile alilo fukiwa mama yake,. Baridi na upepo vilianza kushika hatamu,.mwili wa mtoto ulitetemeka, epepo ukaongeza kasi ya kuvuma,mvumo ukawa mkubwa hata masikioni na machoni mwa mtoto,. lakini mtoto akaendelea kuwepo pale hakuhitaji kabisa kuondoka eneo lile,hakuihitaji,. giza likiwa limetanda,. Ni kiasi cha kama robo saa tangu majira ya saa nne kutimu, Mazingira yale yalitisha,.kulikuwa na vivuli vya vitu visvyo eleweka mita kadhaa kutoka mahala mtoto alipo kuwepo,. Ila mtoto hakubanduka wala kuogopa, Miale ya radi ikamyeka ikamwezesha mtoto kuona kitu umbali wa mita mbili kutoke alipo,.akapata utulivu wa nukta kadhaa akiwa makini na kile alicho kiona kama ni sahihi ama laa! Miale ikamyeka tena huku ikiambatana na ngurumo ndogo,naam! alipata kuona barabala nyoka aina ya chatu mkubwa kwelikweli akimnyatia mahala pale taratibu,. Alikurupuka na kusimama wima yule chatu nae akasimamisha kichwa chake akijiandaa kukabiliana na kitoweo kile alicho kuwa akikinyatia!. Mtoto alianza kurudi nyuma taratibu mashaka makubwa yakiwa maoyoni mwake aliogopa lile joka kubwa,.nyoka alizidi kumkaribia akijianda kurusha mate kama siraha yake ya kwanza kwa chakula kile,. Ghafla mtoto alitimua mbio kali nyoka yule alirusha mate yake yenye sumu,. yakampata vema lakini yakiangukia katika shati la mtoto yule,ikawa bahati kwa mtoto lakini ikawa mkosi kwa nyoka yule kukosa kitoweo,. Mtoto alikimbia huku akipiga kelele lakini kelele yake haikusikika umbali japo wa mita hamsini sauti yote ilikaukia katika kilio cha msiba wa mama yake,. “puuuuuu” alipiga mweleka baada ya kujikwaa kidoleni na kutoa ukucha,.mtoto alipata maumivu makali kidoleni lakini haikuwa mwisho wa mbio zake alisimama akaendelea kujisukuma kwa mbele. mbio kali akiwa ametapakaa vumbi mwilini mwake,. Alitokea katika barabara kubwa ya kuelekea mjini hapo moyo wake ukapata ahueni,. Akatembea kwa kuchechemea maumivu yakiwa makali katika dole gumba lake lililo kuwa likivuja damu huku ukucha ukiwa unaning’inia,. alikuwa peku,.baridi na upepo iliongeza maumivu yake kisawa sawa,. Aliona ulimwengu haumtaki, aliona mungu amemsahau,alijiona mdogo zaidi ya nukta,alikosa mwelekeo,dunia ilikuwa kubwa mno kwake., Huyu ndiye Raymond Fambo Mwakabuku,. Unaweza kumwita Ray. Usiku huo Ray alitembea katika mitaaa akichechemea,kidole chake kilicho kuwa kikining’iniza ukucha kilizidi kutoa maumivu makali,.alitembea pasina kujua anako elekea,. Angefanya nini hali ya kuwa hata makazi yao yalikwisha tiwa kiberiti siku ile ile ya kusurubiwa kwa mama yake,.*******************************
MIAKA ISHRINI NA TANO BADAE Mauji ya kutisha tena ya aina moja yalikuwa yakizidi kushika kasi siku hadi siku katika vitongoji vya mitaa ya isevya,.watu wengi hususani wazee walikuwa wakipoteza maisha yao katika mtindo wa aina moja.walichinjwa vichwa kwa kutenganishwa na kiwiliwili,. Hali ya sinto fahamu ilikugubika mji wa tabora,.mauji yale yalikuwa ni gumzo nchi nzima,.hakuna aliye jua anaye fanya mauwaji yale ni nani,.kila siku ziendazo kwa mungu aliokotwa mwili wa mtu ukiwa hauna kichwa,.cha kushangaza zaidi muuaji aliondoka na kichwa na kuacha mwili,. Hali ilikuwa tete, lakini hakuna aliye jua kama Raymond Fambo ndiye muhusika wa ule uhalifu,. Hofu kubwa ilitawala mji wa tabora,.homa ya matukio ya mauwaji ilivyozidi kuwa kubwa ndivyo takwimu za mauaji zilivyozidi kuongezeka siku hadi siku,. Afisa wa polisi mkoa wa tabora hakupata usingizi hata tone,alikuwa na kazi kubwa kuhakikisha anatoa msukumo wa ziada kwa watendaji wake wa chini kuhakikisha muuaji anakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria,. lakini wapi. Hakuna aliyejua sababu za matukio yale ni nini, kila mtu alisema lake,.hisia za watu wengi ziliwapeleka katika imani za kishirikina,.pamoja na hisia hizo kwa mamia ya wananchi bado lawama nyingi zilielekezwa kwa jeshi la polisi kwa kushindwa kuzuia matukio yale,. Ndani ya jeshi la polisi hali ilikuwa tete mabosi hawakukaa maofisini mwao kimuhemuhe cha kumsaka muawaji kilipamba moto kila kukicha,. Raymond Fambo,aliendelea kufanya mauaji kwa wazee kwa siri kubwa, hakuna watu aliowachukia mkoani tabora kama rika hilo la wazee,.ilikuwa ni kisasi,tena kisasi alicho jiapiza muda mrefu kukifanya,.kisasi dhidi ya mauaji ya mama yake mpendwa aliye uawawa kwa mapanga kwa imani za kishirikina wakati akiwa angali mtoto,.aliamini wazee aliowaua ndio kizazi kilicho husika na mauwaji ya mama yake,.shida na mateso aliyoyapata utotoni mwake aliapa kuteketeza vijana hao wa zamani mpaka pale ubongo wake utakapo sema basi!. Kwa zaidi ya wiki tatu bado hakukamatwa wala kuhisiwa mtu hata mmoja dhidi ya matukio yale yaliyo kuwa yanendelea,. Jijini Dar es salama,wizara ya mambo ya ndani Ispekta jeneral wa polisi{I.G.P} Ernest Kamkuru azidi kuchanganyikwa pale taarifa za matukio ya mauwaji zilivyo zidi kushika kasi pasi na taarifa yeyote ya kukamatwa kwa muuwaji wa vifo vile, Siku hii akiwa katika ofisi yake nadhifu,macho yamemwiva,huku mishipa ya kichwa ikiwa imemsimamaa mwili wake ulikuwa umefura kwa hasira za nyati, pamoja na uwepo wa feni iliyokuwa ikizunguka kwa kasi lakini bado jasho jingi lilimtoka mwilini mwake. Kila baada ya dakika mbili alinyanyua mkono wake wa kushoto na kuitazama saa yake ya mkononi na kadiri muda ulivyo zidi kuyoyoma ndivyo hasira yake ilivyo zidi kuongezeka mara dufu, Alinyanyua mkonga wa simu ya mezani na kupiga namba Fulani kisha akaiweka simu sikioni, Simu iliita upande wa pili kwa sekunde chache kisha ikapokelewa kwa nidhamu na sauti nyembamba ya kike,. “koplo anna kutok….” “KEEP QUIAT MWANAMKE!.” Ispekta Ernest alimkatisha kwa sauti ya ukali yenye mikwaruzo mizito kooni kama kwamba alikuwa anakohozi katika koo lake “hao watu nilio waita wako wapi mpaka dakika hii.?” alisema Ernest kwa ukali. “Samahani afande taarifa zilizopo ni kwamba afande kilanga yupo njiani anakuja akitokea gongo la mboto, lakini kwa bahati mbaya barabarani kuna foleni ndefu hali inayo pelekea kuto wasiri kwa wakati hadi dakika hii, ila afande Babra yeye kisha wasiri ndio kwanza kapandisha ngazi kuja ofisini kwako muda mfupi uliopita”. alijibu yule dada kupitia simu,. Dakika hiyohiyo Kabla Ispekta Ernest hajatia neno mlango wa ofisi yake ulisukumwa na ispekta Babra akatokeza. alikuwa ni mwanamke mrefu mweusi mwenye matiti makubwa na mwili wenye nguvu zile za kiafrika,alisimama kikakamavu na kusaluti huku akiwa anatiririkwa jasho mwili mzima, I.G.P Ernest alimtizama kwa ghadhabu kuu zaidi kisha akasema, “Hivi ninyi mnadhani mimi ni mjomba wenu!. Yanii mimi nawaita,mpaka mjishaue shaue ‘ndo’ mje siyo? Haya, hilo jenzako liko wapi?” Alisema ispekta Ernest,lakini kabla hata Babra hajajibu mlango wa ofisi ile ulisukumwa taratibu na mara Kilanga akatokeza, “Heee! hivi ninyi ni majini watu!., I.G.P alizidi kuhamanika kwa hasira, “mara gongo la mboto, mara katika foleni mara,..ninyi vipi? mmenizoea kiasi cha kuniona mimi mjomba wenu siyo?,. Alibwata kwa sauti ya ukali kwelikweli, Si kilanga wala Babra aliye mjibu, I.G.P aliwatizama kwa zamu wale askari wake huku akihema kwa kasi na kufanya kifua chake kipande na kushuka wakati akivuta pumzi na kuzitoa nje.“Abubakar Kiranga” I.G.P aliita kwa sauti yenye kiburi huku akiwa kisha hamisha macho yake kwa wale askari wake alio waamini, sasa alikuwa akitizama pembeni midomo yake ikiwa imenuna kama kwamba amenyweshwa mkojo wa mlevi, “Ndiyo afande” aljibu Kilanga kwa heshima na sauti ya kikakamavu, “Babra frances” “Ndiyo afande” “Nawatuma tabora mkaniletee muuwaji wa vikongwe” Alisema I.G.P kisha akatulia macho yake madogo yakiwa yanatizama pembeni. Kilanga na Babra wakatazamana kwa mshangao huku kilanga akimeza funda la mate, ubaridi Fulani ukapenya katika maungo yake. Msinitumbulie macho ninyi viumbe.! Kati yenu hakuna asiye jua juu ya matukio ya mauwaji ya kuchinjwa shingo dhidi ya wazee yanayo endelea kule tabora!. Alisema kwa sauti ya ukali huku akihamisha macho yake kwa kasi na kuwatizama askari wale wawili, Nimekwisha ongea na kamanda wa polisi mkoa wa tabora juu ya ujio wenu na nimemweleza file lote la mauwaji ya vikongwe kuanzia kesho litakuwa chini yenu,namaanisha kesho asubuhi sitaki kusikia harufu yenu hapa jijini,alisema tena kibabe huku akiwa kawatumbulia macho yake makali, “Kuna swali” aliuliza baada ya kuzungumza, “Kwanini umetuteuwa sisi na siyo c.i.d wengine afande” Babra aliuliza swali la kipuuzi!. Come on askari!! Wewe ulitaka nimteuwe nani? Nimekuteuweni kwakuwa nimejisikia kukuteuwa,shenzi taipu,sifa tu!. miaka yote hujui kama ninyi ndio chaguo langu nambari moja katika kazi nyeti kama hizi. Alisema I.G.P huku macho yake madogo yakitoka katika hali ya ukali na kuwa katika mshangao. Ukimya wa nukta kadhaa ulichukua nafasi kabla ya I.G.P kuwaruhusu kwa mara nyingine kuondoka. Babra na Kilanga waliondoka katika ofisi ya I.G.P wakiwa na mori kubwa ya kazi kutokana na sababu mbili ama tatu,kwanza ni kule kuaminika mbele ya bosi wao ambae ndiye mkuu wa jeshi la polisi nchini pili ni kule wao kuonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kutatua kesi ambazo mara nyingi huwa ngumu na kuwashinda askari wengi, sasa leo jukumu lililokuwa mbele yao ni kumtafuta muuwaji wa mauwaji ya vikongwe yanayo endelea kule tabora, Katu hakuna mtu kati yao aliyejua kama ile kesi ingepelekea kuharibu kabisa muelekeo wa maisha yao kwa miaka mingi!. ******************************************** Wakati tume ya kipelelezi ikiundwa kibabe jijini dar es salam,.upande wa pili mkoani tabora Raymond Fambo alikuwa akijianda chumbani kwake kwa ajili ya kutoka, Kiharisia ilikuwa ni mvao wa mtoko wa kazi,.kazi maalum yenye kuupoza hasira yake na donge lake la moyo.,kazi aliyo ifanya pasina shaka kuwa ni kisasi cha mauwaji ya mama yake,. Basi Alivaa jinsi yake ya blue, shati la langi jekundu lililo mkaa vema,kofia kubwa ya pama na groves za mikono., Alijitazama mala mbili katika kioo cha kabati leke la nguo,.alipo lidhika na muonekano wake aliinama chini ya uvungu wa kitanda na kutoa viatu vukubwa buti za rangi ya kaki kisha akatia miguu yake ndani ya viatu,. naaaam!. hapo muenekano wake wa kazi ukawa umekamilika,. Alitoka chumbani kwake na kuingia katika moja ya chumba alicho kifanya kama stoo katika nyumba yake..ilikuwa ni stoo isiyo kua na vitu vingi ndani zaidi ya jokofu kubwa na godoro jipya la tanform,. Raymond alichukua kisu kikubwa chenye makali ya uhakika kilicho kuwa juu ya jokofu ile na kukichomeka katika ala yake kisha akakipachika kiunoni kisha taratibu pasina haraka taratibu akauendea mlango,. “kumekucha muda wa kazi” alijisemea moyoni akifungua malango na kutoka nje,. Alitembea kwa mguu kutokea mtaa ule wa nyumbani kwake mpaka stendi ya mabasi ya mkoani,hapo madereva baiskeli walikuwa wengi, kimwenekano alikuwa ni mtu aliyehitaji usafiri,. wale madereva wakamzonga,. “kweli nahitaji usafiri lakini siyo wa baiskeli,mimi si wakupanda baiskeli” alisema Raymond huku akiwasha sigara yake kwa kibiriti cha gesi na kuvuta kwa mkupuo na kutoa moshi mwingi puani na mdomoni mwake,. Wale madereva waliondoka wakinung’unika moyoni kwa kukosa rizki kwa kukataliwa na mtu yule mwenye muonekano wa majivuno sijui kwa umaridadi aliokuwa nao ama ni nini!!. Dakika kumi na mbili badae alikuja dereva pikipiki iliyo kuwa inaendeshwa na kijana mrefu mweupe akiwa amevaa suruali ya jinsi na tshert nyeusi na shuka jekundu la kimasai, “oyaaa twendzaoo” alisema yule dereva aliyeitwa Richard,. Raymond alipanda kisha safari ikaanza,. Walipita katika shule ya sekondari ya uyui na kukatisha kushoto wakashika njia ndogo ya vumbi wakazidi kuvuta mafuta,. “vipi kwa hapa” Rchard aliuliza,.baada ya kwenda mwendo wa kilomita takribani mbili na nusu,. “Hapa hapa panatosha” Alijibu Raymond,. Usikawie basi sisi unajua washenzi hawa sasa hivi wameweka ulinzi kila kona”alisema Richard; Sikawii mzee mwenyewe,. huyu wa leo mrembo sana” alijibu Raymond huku akitelemka katika pikipiki na kutembea kwa mguu umbali wa nusu kilomita,. ilionekana safari yake imefika mwisho mbele ya nyumba ndogo ya udongo na makuti,wakati huo ilikuwa ni saa mbili na dakika mbili usiku,.
. Ilikuwa ni nyumba ya mzee mganga wa jadi aliyejulikana kama babu mwana Malunde,alikuwa ni mganga kiboko,. Ndani ya nyumba Zilisikika nyimbo za kinyamwezi zilizo kuwa zikiimbwa na Mwana Malunde,. wakati nje palikuwa hapana mtu mwingine zaidi ya Raymond aliyekuwa akinyatia taratibu kuingia ndani mkononi akiwa kakamatilia kisu kikubwa,. Taratibu Raymond alinyatia na kujitoma ndani kwa kasi,.alimvaa mzee Mwanamalunde na kumkaba koo kwa nguvu zake zote huku akiachia ngumi nzito za mbavu Mwanamalunde mzee wa watu akatepeta,kulia alishindwa kuzungumza pia alishindwa pumzi zilikuwa zimebana kwa zile ngumi za mbavu,. “Leo ni zamu yako kuondoka na kichwa chako mshenzi mkubwa wewe” alisema Raymond kwa hasira huku akiweka kisu chake vizuri mkononi,. “Ko-sa—la—ngu nini?” aliuliza Mwanamalunde kwa sauti yenye kugumia maumivu ndani kwa ndani., Badala ya kujibu Raymond aliachia konde zito lilipasua mdomo wa Mwanamalunde na hata kuzidi kupunguza idadi ya meno mdomoni mwa mzee yule,. Mzee aliachia kilio kikali cha maumivu hapohapo Raymond alimkamata na kupitisha kisu kwa nguvu katika shingo ya Mwanamalunde,.ilikuwa ni kama kama vile anachinja mbuzi wa iddi,. Damu ziliruka hovyo, mzee macho yalimtoka pima, ulimi nao ukiwa toka zaidi nje,.mh! ilikuwa hatari,. Raymond alichinja kabisa kichwa cha Mwanamarunde kisha kile kichwa akakitia katika mfuko wa Rambo akiacha kiwiliwili kikiwa kimelala kihasara hasara katikati ya vibuyu na hirizi pale chini,.kwa mala nyingine Raymond alijisijika raha moyoni mwake, aliona anajitendea haki kabisa,. Baada ya kupachika vema kichwa kile katika mfuko wa Rambo sasa alitoka nje ili apotee mazingira yale, wakati huo tayari giza lilikuwa limefunika kabisa sura ya nchi,. Lakini ghafla!!. Sauti kali ilisikia hatua chache kutoka nyuma yake,. “Hapo hapo ulipo nyoosha mikono yako juu na usifurukute wala kukohoa,. nitamwaga ubongo wako!.,upo chini ya ulinzi,. Raymond Fambo muuwaji!!,. leo kwisha habari yako” ilikuwa ni sauti kali` yenye amri ya vitisho ikitokea hatua tano nyuma ya Raymond punde baada ya kuuwa mkononi akiwa na mfuko wa Rambo aliobeba kichwa cha mtu,. Raymond Fambo tumbo lilimchemka,akili yake ilizunguka,.aliona habari yake ‘kushnei’ na kiama chake kimefika,. kibaya zaidi mtu yule alimjua hata mpaka jina lake, “Ray nimesema nyoosha mikono yoko juu ukiwa huna chochote mkononi sitanii nitafumua kichwa chako sasa hivi kwa risasi” alisema tena yule mtu kwa sauti kali yenye mikwaruzo,. Raymond alinywea kama maji ya mtungini, alitupa chini mfuko wake wa Rambo uliokuwa na kichwa cha mtu,.! Bado akili yake ilikuwa ikishindana na moyo wake kunyoa ama kusuka,.sauti mbili tofauti zilipenya katika kichwa chake,.moja ilimwambia anyooshe mikono juu na ajisalimishe ili kuepukana na kifo cha risasi,.sauti ya pili ilimwambia asikubali kujisalimisha kwa yule mtu aliye nyuma yake mwenye bunduki badala yake ni bora kufa kuliko kukamatwa na kupelekwa mbele ya mkono wa sheria ambapo huko hukumu yake haitakuwa nyingine tofauti na kifo,. “Tafadhali Ray usinilazimishe kufanya maamuzi ya kukusafirisha kuzimu sasa hivi,. fanya ninavyo kulekeza upesi” yule mtu alizidi kumpa wakati mgumu Raymond,. “Just going on guy…,I don fear any thing” Ray alijibu kwa kimombo akiwa ni mwenye kutokuwa na shaka tena,. “heee!. unajifanya majinuni sasa nahesabu hadi tatu usipo tii amri haki ya mama nitakuonyesha jinsi niivyo jeuli” alisema yule mtu huku akikoki bunduki yake na kumlenga vema Raymond,. Hapo Raymond akageuka taratibu kumtizama yule mtu aliye mvamia kwa mara ya kwanza tangu harakati zake za mauaji zianze,.hakuogopa kifo kwa kujiamini kabisa aligeuka na kutizamana uso kwa uso na mtu yule,. Balaa!! Alikuwa ni koplo Frances Kidogori kutoka kituo cha kati cha stesheni,. Alikuwa ni askari mwenye umri kati ya miaka arobaini na mitano ama sita,. alikondeana mno pengine labda kwa mshahara kiduchu aliolipwa huku majukumu yakiwa chungu nzima,.ni mzee waliyekuwa wakifahamina vizuri kutokana na ushabiki wa kandanda kule katika majumba ya sinema ambako Ray na koplo Kidogori walijuana kutokana na ushabiki wa timu za aina tofauti za kule wingereza Ray akiwa mshabiki mzuri wa riverpool huku koplo Kidogori akiwa mshabiki nambari moja wa Man u,. ubishi wa hoja na uchambuzi yakinifu ndio ulio fanya watu wale kuwa marafiki wapinzani kila inapo fika wakati wa mechi,.sasa siku hii walikutana katika ukinzani mwingine hatari,. “Haki ya mama nakulipuaa!” alisema koplo kidogori kwa wahka mikono yake ikiwa ina mtetemeka! Sijui kwanini,. “Lipua” alijibu Ray kwa sauti yenye kisirani,. “heee! Ibirisi wewe unadhani nashindwa!!. Naweza kufanya hivyo sekunde yoyote,. Huwezi kufanya mauwaji ya kikatili kiasi hiki halafu utegemee nitakuacha, eti kisa tu wewe ni mtu ninae kufahamu!,. haiwezekani hata tone…!, yanii umechukua rikizo kwa ajili ya kufanya udhalimu huu!!,kwanini lakini Ray kwanini??,.” Alisema koplo Kidogori kwa sauti yake nzito isiyo endana na mwili wake, “Ndio nishafanya sasa,. amua unalo taka” Ray alijibu huku akimtizama koplo kidogori kwa jicho la dharau,. “Paaaaaaaaaaaa!!.” Risasi alitoka katika bunduki ya afande kidogori na kumpata barabala Raymond mwana wa Fambo,. Fambo alitoa sauti kali ya maumivu na kuanguka chini huku damu nyingi zikiruka,.. Hali ilikuwa tete!. “Kwisha habari yako mwanaharamu mkubwa wewe,.nisha kueleza kama wewe kiburi mimi jeuri” alijigamba koplo Kidogori huku akisogea mahala alipo angukia Raymond huku damu zikimvuja kwa wingi ktk mwili na kumwagika ardhini,. Raymond aligumia maumivu makali ya risasi ya mguu wa kushoto aliyotandikwa na koplo Kidogori,. Koplo kidogori baada ya kuona hasimu wake hajiwezi alitoa simu yake ya upepo katika mfuko wake wa suruali tayari kwa kutoa taarifa kwa askari polisi wenzake walio kuwa wametanda kona zote za mji wa tabora kufanya doria,… Ghafla!!!.sauti ya kishindo ikasikika “Puuuuu”ilikuwa ni sauti pigo,. pigo zito na la ghafla alilokutana nalo koplo kidogori,. Alianguka chini huku akigumia maumivu makali katika kichwa chake,. Haruna hakumpa nafasi ya kujihami kwa kutumia kofia ile ile ngumu ya pikipiki aliyo itumia kumpigia, aliinyanyua tena kwa nguvu na kumwezeka nayo katika paji lake la uso,.koplo kidogori aliona nyota,.hakuweza tena kunyanyuka,lakini Richard hakuishia hapo aliendelea kuponda ponda kwa nguvu kichwa cha koplo Kidogori,.damu ziliruka na kutapakaa katika kofia ile ngumu ya pikipiki,.habari ya koplo kidogori ikabaki kuwa innalillahii,. Baada ya kumsafirisha koplo kidogori kwa sir god Richard alimgeukia Ray aliye kuwa akigumia maumivu ya risasi ya mguu pale chini,. “Amka kaka, hapafai tena hapa, amka jikaze twende” alisema haruna Huku akimshika bega na kumnyanyua juu,. “aiseeee! Si..we..zi ku..simama Haruna, siwezi ndugu,hebu nifunge kwanza kitambaa katika jeraha damu inavuja kwa kasi huyu mshenzi{akamtukania mama yake} kanipasua vibaya” alisema Ray huku mishipa ya kichwa ikiwa imemkakamaa., upesi Richard alichana ukingo wa shati lake na kisha kumfunga katika tundu lililokuwa likimwaga damu kwa kasi,. “haya jikaze twende” alisema haruna na kumnyanyua kwa nguvu,.Ray aliachia miguno ya maumivu makali akiwa kisha simama, hata mfuko wa Rambo wenye kichwa cha mwana Malunde haukukumbukwa tena,. taratibu walijikongoja kuingia gizani kuitafuta pikipiki yao.,*******************
Siku hii ya juma tatu ilikuwa ni siku yenye kimuhemuhe katika mji wa tabora mauwaji yaliyo tokea ndio ilikuwa habari ya mjini, wapi ungepita usikute watu wanazungumzia matukio mawili ya mauwaji moja likiwa la askari polisi na lapili likiwa ni lile la mganga maarufu wa kienyeji mjini tabora, Mwana Malunde?. Saa moja na nusu Kilanga na Babra walitoka katika ofisi ya R.P.C mkoa wa tabora wakiwa wamekabidhiwa file la mauwaji ya vikongwe pamoja na taarifa nyingine zote zenye kuhusu kesi ile, Walingia katika tenga la polisi wakiongozana na askari wanne kwa maana ya wao wawili dereva wa tenga la polisi, na C.I.D mwingine ambaye awali alikuwa akifuatilia ile kesi kabla ya kuwekwa kando. Walielekea katika vitongoji vya Isevya walikoishi watu masikini, Ilikuwa ni nyumbani kwa mwana Malunde ambako maiti zote mbili zilikutwa, Moja ikiwa imetenganishwa kichwa na kiwiliwili huku nyingine ikiwa imebondeka vibaya katika kichwa.
Robo saa ilitosha kuwafikisha katika eneo la tukio,walikutana na mlundo wa watu walio kuwa mazingira yale,huku nyuso zao zikionekana kuwa ni zenye mahamaniko makubwa, bila shaka ni kutokana na namna macho yao yalivyo shuhudia miili isiyo kuwa na uhai ya binadamu wenzao namna ilivyo uwawa kinyama. Kilanga na timu yake walishuka kwa mbwembwe katika tenga la polisi huku macho ya watu yakiwazonga, Walisogea mahala maiti ya koplo kidogori Ilipo lala huku kichwa chake kikiwa kimepasuliwa vibaya na kufanya jeraha kubwa kudhihirika,damu zilionekana kumtapakaa mwili mzima,sentimita chache kulikuwa na bunduki ya SMG iliyokuwa imetelekezwa kihasara., Kutoka mahala bunduki ilitelekezwa kulikuwa na fuko la Rambo lililokuwa limelowa kwa damu huku ndani yake kukiwa na kichwa cha mtu!. hali ilitisha!. Kilanga na Babra waliendelea kutizama na kudadafua mazingira yale katika bongo zao., “Ispekta Kilanga” Babra aliita kwa wahaka akiwa makini kutizama kifaa kidogo kilicho kuwa chini hatua chache kutoka mahala ilipo lala maiti ya koplo kidogori,. “ganda la risasi” alisema Babra akimwonyenyea Kilanga kile kifaa chenye rangi ya shaba, “Hii risasi bila shaka ilitumiwa na huyu askari kukabiliana na muuwaji,..lakini!.. sasa ilikuwaje..mpaka muuwaji akamshinda”? alisema kilanga “Kwanini unaseama muuwaji? pengine si muuwaji ila ni wauwaji” hawezi kuwa muuwaji mmoja akashindana na watu wawili tena wenye bunduki akawashinda ispekta” “Kisio lako ni sahihi Babra lakini hawa wauwaji inawezekana wakawa wanabunduki”. “Sina uhakika ispekta kilanga, kwasababu maiti ya huyu askari inaonekana imepondwa pondwa kichwa mpaka kufa, na si kifo cha risasi, sina uhakika wa asilimia mia kama wauwaji wana siraha,na hata kama wanazo silaha basi katika tukio hili hawakuzitumia.” “Ona hii tena Babra” alisema kilanga akiwa makini zaidi, “damu ispekta!.” Babra alisema huku akitizama damu iliyokuwa imekauka sentimita sabini kutoka kichwa cha mtu kilipokuwa kimetelekezwa, Kilanga alitizama kwa makini umbali kutoka kichwa cha mtu kilipokuwa akalinganisha kutoka umbali maiti ya koplo kidogori ilipolala akang’amua kitu.sura yake ikajaa muonekano wa viulizo kibao, “Taarifa zinaonyesha kila muuwaji anapofanya mauwaji anaondoka na kichwa cha mtu! Iweje hiki hajaondoka nacho!!. Kuna kitu hapa.” Kilanga aliwaza akilini, Alitoka hapo na kuingia ndani kuliko kuwa kunasadikika kulikuwa na mwili wa mzee mwana Malunde, walikuta mwili wa mwana malunde usio kuwa na kichwa ukiwa umelala bila uhai huku vitu vya kiganga vikiwa shabarabaghala mule ndani,. “Humu ndani kulikuwa na mvutano wa makabiliano baina ya muuwaji na marehemu” alisema kilanga huku akipachika sigara mdomoni na kuiwasha kwa kiberiti cha gesi kisha akavuta mkupuo mmoja na kutoa moshi mwembamba kupitia mdomoni na puani,. Babra alitikisa kichwa kukubaliana na kisio la Kilanga huku jasho la pua likijidhihirisha usoni mwake,. “Mpaka sasa sijajua yule askari kule nje ilikuwaje hadi akafika eneo hili kabla ya kukutana na umauti?” alisema Babra huku akipangusa jasho usoni mwake kwa kiganja chake cha mkono wa kushoto,. “Fanya mahojiano na familia ya huyu askari pengine tunaweza kupata lolote” alisema Kilanga. “Afande yule ni askari anae tokea katika out post ya railway station” askari waliye ongazana nae alisema,. “Vizuri sana”, kilanga alisema kwa wahka “sasa ni wewe ndiye utakae fuatilia huko kituoni kwake na uje na taarifa zinazo husu uwepo wake eneo hili akiwa na silaha” alisema Kilanga huku macho yake yakiendelea kusaili maiti ya yule mganga wa kienyeji udadisi ukiongezeka mara dufu zaidi kwa kila dakika iliyo pita wasaa ule,. Aliingiza mkono mfukoni na kutoa kamera ndogo ya Samsung kisha akapiga picha kadhaa maiti ya mwanamalunde, Wakati huo huo kulikuwa na vilio tofauti vilivyo sindikizwa na maneno lukuki yenye kuwataja wapendwa wao na kufanya mchanganyiko ule wa sauti kuwa makelele,. ilikuwa ni familia ya marehemu mzee malunde na ile ya koplo kidogori, Babra alisogea mahala ambako mke wa koplo kidogori alikuwa akibugujikwa na machozi, kisha akatoa kitambaa katika mkoba wake na kumpa mke wa marehemu koplo kidogori kwa kujifutia machozi yaliyo kuwa yakimmiminika kwa kasi,alikuwa ni mwanamke mnene aliyeshiba kwelikweli, Utulivu ukapita baina ya Babra na mke wa marehemu koplo kidogori kabla ya kuanza kufanya mahojiano,. Dakika nne badae mahojiano yalianza kufanyika baina yao,hapo kwa kila sentesi aliyo izungumza mke wa koplo kidogori iliibua hisia hatari kwa Babra mapigo yake ya moyo yalienda kasi mpaka ujasiri wa kiaskari ukapotea, akaogopa na nguvu zikamwishia,.***************** **************** Ray alikuwa katika usingizi mzito katika sofa alilo kuwa amejilaza huku mguu wake uliokuwa na bandeji kubwa pajani ukiwa umelazwa kihasara hasara pale sofani,. Pembeni katika sofa dogo, alikaa Richard aliyekuwa katika hali ya kuchanganyikiwa, wasiwasi ulimwenea moyoni mwake, leso yake iliyo kuwa mkononi mwake ililowa kwa jasho la viganjani,.mwanaume mwingine aliyekuwa amesimama pembeni ya mahala alipo lala Ray alikuwa akivuta dawa katika kichupa kidogo kwa kutumia sindano iliyo kuwa imeunganishwa na bomba lake,.aliingiza ujazo aliona unatosha kisha akaminya kidogo,. matone ya dawa yaliruka kwa kasi, kisha akainama akielekeza ile sindano katika paja la Ray, taratibu alimdunga sindano ile na kuhakikisha ameingiza dawa yote iliyokuwa katika bomba la sindano,.kisha akachukua pamba iliyo lowanishwa na dawa maalumu ya kuzui damu na kuipachika mahala pale alipo mdunga sindano,. “hii itapunguza maumivu aliyo nayo kwa muda kadhaa ni bahati hakuna madhala katika mfupa wa mguu wake,.imekuwa bahati kwake hiyo risasi ilipenya katika nyama na kutokea upande wa pili wa mguu,. haikubaki mwilini mwake” Alisema dokta yule aiyekuwa ikimtibia Ray huku akiweka sawa miwani yake midogo ya macho iliyo pendezesha muonekano wake,. Richard alishusha pumzi ndefu kifua chake kikipanda na kushuka pindi alipo vuta pumzi kwa ndani na kuzitoa nje,mikono yake ikiwa kiunoni,.alisogea karibu na mahala alipo simama yule dokta akaingiza mkono mfukoni na kutoa burungutu la pesa kisha pasina kuhesabu wala kuzungumza akamkabidhi yule dokta,. “thanks mr small fish, well done” alisema kwa kimombo yule daktari huku akizipokea zile pesa na kuzitumbukiza katika mfuko wake wa koti la suti., “nitakuja tena jioni kumcheki” aliendelea kusema yule dokta,. Richard hakutia neno,. Ikawa anakusanya vifaa vyake vya kitabibu na kuvipachika katika mkoba wenye ukubwa wa wastani kisha taratibu akauendea mlango na kutokomea nje,. Richard alibaki amesimama mahala pale macho yake yakiwa kwa Ray,.huruma iliyo changanyikana na hofu iligubika ndani ya moyo wake, alimtizama Ray vile alivyo fumba kope za macho yake akiwa katika usingizi mzito wa dawa za usingizi alizo pewa, kumbukumbu za maisha ya nyuma zilipenya katika ubongo wake,.alikumbuka miaka mingi iliyopita namna walivyo kutana na mtu huyo wakiwa watoto wadogo wa miaka kumi.,**************** APRIL. 6 .1994 /KIGALI RWANDA, Ilikuwa ni usiku wa saa tano na nusu,Zilisikika sauti nyingi za vilio kila kona ya mtaa katika jiji la Kigali nchini Rwanda, Vishindo vya sauti za mabomu na risasi ziliugubika mji wa Kigali, ukimya uliokuwa umezoeleka hasa nyakati za usiku katika mji wa kigali siku hii ulipotea,miale mikubwa ya mioto ilitanda katika anga, moshi mzito ulifuka, nyumba za watu zilichomwa kwa moto! vilio na mayowe ya maumivu yalisikika kila mahali, watu waliuwana! Damu za watu wasio na hatia zilimwagika!, wanawake walibakwa kabla ya kuuwawa kwa panga, watoto walichomwa moto katika nyumba,.wakati wanaume walikatwa vichwa mala moja kwa upanga,. Yote haya yalitokea Ikiwa ni punde baada ya usiku huo vyombo vya habari kutangaza mauwaji ya rais Juvenal Habyarimana, Matokeo ya siasa za kikabila sasa zikaanza kuonekana,. Watu walichinjana kama kuku,watusi waliuwawa mithili ya nzige dhidi ya wanamgambo wa kihutu{interahamwe} kutoka chama cha MRND. Wao waliita opalesheni safisha Mende, Watusi walikuwa mende mbele ya wahutu, Kigali iligeuka machinjio ya watu, makelele yalilindima masikioni mwa wakazi walio kuwa wamejifungia milango kwa makomeo imara miyoni mwao wakitetemeka kwa mashaka makubwa,. watoto walijificha uvunguni,. hali ilikuwa tete! Laiti kama watu wangejua kitendo cha kujifungia majumbani mwao ni hatari zaidi kwa maisha yao katu wasinge endelea kukaa katika majumba yao wakiwa wamejifungia kwa ndani kwa makufuri mazito,wakiiamini milango yao kuwa ngoa ya kuwatenganisha na madhalimu wauwaji,. Sebastiani na mkewe Sophia walikuwa wakifanya maombi makubwa, waliamini yesu ndiye mwenye kuweza kubadilisha hali ile ya machafuko,na hata kuweza kuikinga nyumba yao dhidi ya kiama kile,. mtoto wao mdogo wa pekee Richard,. alikuwa amejikunyata uvunguni akitetemeka kwa hofu,. Sauti za mayowe za watoto wenziwe waliokuwa wakilia kwa kuomba msaada kutoka nyumba za jirani zilizidi kujenga hofu kubwa kwa Richard,. Magdalena mtumishi wa ndani ya nyumba ya Sebastiani pia alikuwa kajificha katika sinki la jikoni moyo ukimdunda kwa hofu mithili ya ngoma za kihehe,. Kadri muda ulivyo jongea ndivyo Sauti za Wanamgambo wa interahamwe zilivyozidi kukaribia nyumba ya Sebastiani,. Waliimba nyimbo za kuhamasisha oparesheni safisha mende!.
“NGO,NGO NGO HAYA, HAYA HAYA WAFANYA USAFI TUMEFIKA FUNGUA MLANGO” mlango wa nyumba ya Sebastini uligongwa huku sauti kali ikisika ikikoroma kwa amri kali,. Kimya.., “Ninyi mbwa humo ndani hamtusikii fungua huu mlango upesi”,.kamanda wa interahamwe alisema tena kwa ukali huku wanamgambo wengine wakiwa na mori kubwa ya kuuwa. Kimya kingine,.! Ndani kwa Sebastiani,Sophia alisimama wima akiwa anatetemeka, jasho lilimtoka, hakuna aliyeweza kuendelea na maombi tena. Sophia alielekea chumbani kwake na kuinama chini ya uvungu wa kitanda na kumchomoa Richard aliyekuwa amejikunyata akitetemeka mwili mzima,. “Njoo mwanangu,haya njoo baba kwa mama hakuna baya lolote litakalo kukuta” “mimi naogopa nimewasikia interahamwe wamefika, wako mlangoni” “shiiiiiii..!!, nyamaza interahamwe hawawezi kukuuwa mimi nipo, baba yupo, na yesu yupo, wote tuna kulinda wewe, unatakiwa utulie,.baba anakuja kukuficha mahala pazuri” alisemaSophia akimpa matumaini mtoto wake japo ukweli hata yeye aliujua moyoni kuwa kifo chao dakika chache zijazo kitawafikia,. “Haya haya haya!.hakuna kushangaa upesi tunatokea mlango wa nyuma tunatimka tokeni upesi mwiteni na huyo Magdalena naye sijui yuko wapi,..!!!” sauti kali ya Sebastiani alizungumza akitokea sebureni,. Kabla hajamaliza sauti nyingine kali ya kishindo kikubwa ilisikika mlangoni,. Wanamgambo wa interahamwe alivunja mlango kwa kombora zito wakaingia ndani kwa kasi,. Sebastiani na Sophia walibaki wamebung’aa ulikuwa ni uvamizi wa ghafla wakiwa hawajafanya jambo lolote la kujikomboa,. “Ingia kabatini Richard utulie kimya usipige kelele wala kutoka nje” alisema Sophia kwa wahka huku macho kayatoa pima,. Richard aliingia katika kabati la nguo na kujikunyata kimya,. Ninyi mende ninyi,. haya kuja hapa,. yanii muda wote sisi tunawataka mfungue hili lango la bangaluu lenu mnaleta mishauo!. Sasa leo mtajua kuwa maharagwe ni mboga na mchuzi wake ni mtamu!. mafisadi wakubwa ninyi,.” alisema kamanda wa intarahamwe wakijichoma ndani zaidi kuwatafuta wenyeji wa nyumba ile “Haya kuja hapa mende ninyi” alisema kamanda baada ya kuwaona “Jamani sisi hatuna kosa lolote”alisema Sebastiani, kauli hiyo ilitosha kumpeleka akhera mbele ya macho ya mke wake na mtoto wake Richard aliyekuwa akishuhudia kupitia nyufa za mlango wa kabati, mauwaji mmoja alinyanyua juu upanga mkubwa na wenye makali na kutwisha nao Richard kichwani,. Taharuki!. Uwiiiiii jamani mumemuuwa mume wangu!., uwiiiiii Sebastiani wanguuuuuuu!. Sophia alilia, aliruka ruka juu kwa kupagawa,alipatwa na kimuhemuhe,. Damu zilimiminika katika kichwa cha Sebastiani kama koki ya bomba iliyo ng’olewa,. Sebastian alitulia kimyaaa! Panga moja la kichwa lilitosha kukamilisha safari yake hapa duniani,. uhai wake iliishia hapo!,. “Haya wanaume nyonyeni maziwa ya huyo mwanamke, mkimaliza UA” amri alitolewa,.wanamgambo wanne walimvaa Sophia,. Wakamdhibiti,wakamvua nguo akiwa ameelekezewa mitutu ya bunduki na panga,..wakamalazimisha kulala chali kisha wakambaka kwa zamu,. Walikuwa kumi na nne walimbaka wote kiasi cha kwamba Sophia alipoteza fahamu,haikuwa kigezo cha walio kuwa hawajabaka, kutobaka,walibaka mpaka miili yao iliposema basi, “Haya UA” amri alitolewa, Sophia alichomwa singe ya bunduki tumboni ikatokezea mgongoni,. mguno hafifu wa maumivu ulimtoka,. macho akayafumbua kwa mbali huku midomo yake ikimcheza,.hakuwa na nguvu kabisa katika mwili wake na wakati huohuo kifo kibaya kilikuwa kinamkabili,. Mchomaji alichomoa singe kwa nguvu damu zilitapakaa katika singe ya bunduki, kisha kwa nguvu akamdunga tena kifuani mwa mwanamke yule asiye kuwa na hatia,. singe ilitokezea tena upande wa pili wa mgongo.,.aiseee!,. Hali ilitisha!. “Kosa lako ni kuzaliwa mtusi!.” alisema kiongozi kisha akatoa tusi kali kumtukania mama yake,. Hapo nyimbo za kisiasa za kabila la kihutu zikaimbwa kwa shangwe nderemo na hoihoi,. “Hivi mmetafuta mende wengine humu ndani mmekosa kabisa?” kiongozi aliuliza kwa ukali. “Hakuna mende” “Haya mwagieni petroli nyumba nzima kisha tia kibiriti kusafisha vema,.tunataka Kigali ibaki nyeupee peeeee! pasina mende wa aina yeyote” alisema kiongozi kisha mafuta yaliyo kuwa katika madumu yakaanza kumwagwa katika nyumba ya Sebastiani,. Richard alishuhudia kila kitu alitamani awe Rambo apambane na watu wale, lakini ukweli haukubadilika,.yeye ni Richard na hawezi kuwa Rambo kamwe. Kwa macho yake alishuuhudia namna wazazi wake walivyo kufa kikatili, sasa zamu hii, ilikuwa ni zamu yake kufa kwa moto akiwa ndani ya kabati la nguo lililo fungwa kwa nje na kufuli,. Akiwa ndani ya kabati tumbo lilimchemka,mashaka makubwa yaligubika nafsi yake, maumivu ya kuungua na moto mpaka kufa yalimtia hofu kubwa alitamani apige kelele lakini kitendo kile ilikuwa si salama kwake badala yake kama interahamwe wangegundua uwepo wake angebadilishiwa staili nyingine tu ya kifo, kutoka kuunguzwa kwa moto kwenda kuchinjwa shingo kwa panga. Alitulia tuli!,. Baada ya interahamwe kumwaga petroli nyumba nzima wote walitoka nje ya nyumba, kisha ikatiwa kibiriti!. Moto mkubwa ulilipuka, nyumba ya Sebastiani ikaanza kuungua kwa kasi kubwa. Kwa mara nyingine wakashangilia kwa kitendo hicho huku risasi nyingi zikitoka katika bunduki zao. Looh! Ujinga gani huu!. Magdalena alikurupuka mafichoni baada ya joto kuwa kali na moshi kumwelemea, moto ulikuwa ukiwaka kwa kasi kubwa,alipiga kelele nyingi za kuomba msaada,. Lakini wapi!. Akili yake ikamwongoza kujaribu kujinasua katika moto mkubwa uliokuwa ndani ya nyumba ile badala ya kuendelea kumaliza nguvu zake kwa kupiga kelele za kuomba msaada,. Alipiga hatua kubwa akiwa makini kuukwepa moto ulio kuwa ukiwaka kwa kasi na kunguza vitu, Alinyata mpaka usawa wa chumba cha Sebastian mlango ulikuwa wazi,hapo mianga ya mioto ikamwezesha kuona maiti mbili zikiwa zimelala zikiwa zimeuwawa kikatili,.alipata mshutuko mkubwa hofu kubwa ikazidi kumjaa, Maiti ya Richard hakuiona!. Akazidi kuingia ndani zaidi,ni vile mungu alimwongoza tu kuingia ndani zaidi pasina kujua kwanini anazidi kuzubaa mule ndani badala ya kutimka,.hapo sauti ya Richard aliye kuwa ndani ya kabati ikapenya katika masikio yake,. Magdalena hakutaka kujiuliza mara mbili zaidi alikwisha elewa fika Richard alifichwa humo kabatini na wazazi wake kabla ya wao kuuwawa,. Upande wa kulia chumba hicho aliona pasi ya mkaa iliyo tumiwa kunyooshea nguo, upesi aliichukua ile pasi na kuikamatilia vizuri kwa mbele kisha pigo moja la nguvu lilitosha kusambaratisha kufuli dogo la kabati, Richard alitoka upesi akamrukia Magdalena na kumkumbatia huku akilia kilio cha huzuni kubwa,. Moto ulizidi kupamba moto,. “Twende nifuate huku hatuna muda wa kupoteza humu ndani vinginevyo tutateketea kwa moto” alisema Magdalena kwa sauti kali., kilichofuata ilikuwa ni kutimua mbio kupitia mlango wa uwani ambako huko moto ulikuwa hauja kolea, wakatokea katika geti dogo kisha wakatokomea nje gizani wakiwa salama salimini,. Wakati huo ulikwisha timu saa saba kasoro za usiku ama kwa hakika ulikuwa ni usiku usio sahaulika katika vichwa vya wananchi wa Rwanda,usiku wa mauwaji,usiku wa maumivu, usiku uliopeteza ndoto za maelfu ya watu, haya ndio mauwaji ya kimbari,. Basi ikawa Magdalena na Richard wanatembea kwa tahadhali kubwa wakipita pembezoni mwa barabara hata wasijue wanakoelekea!. watu kadhaa walipishana nao wakiwa na kimuhemuhe cha kuwa mbali na mji wa Kigali,. Walitembea umbali wa kiometa nne kwa mguu wakawa mbali kabisa na makazi yao, Walifika katika eneo la keiza katika kanisa kubwa la katholiki watu wengi walionekana kuingia humo ni eneo kidogo lililo onekana kuwa salama., Watu walikuwa wengi katika kanisa lile kubwa kwikwi za kilio zilisikia kwa kila mtu, Kwa namna nyingine huduma ya kwanza dhidi ya watu walio jeruhiwa na mapigano ilikuwa ikitolewa na watumishi wa kanisa lile,******************** Richard alistushwa katikati ya kumbukumbu ya maisha yake na mtu aliye kuwa akigonga mlango kwa kasi,. Alijinyanyua kivivu huku akipiaga miayo akajinyoosha, mifupa ikalia “ka,kaa,ka” kisha akauendelea mlango na kufungua akatoa shingo nje huku robo tatu ya mwili ikibaki ndani na kutizima mgongaji wa ule mlango,. Macho yake yakakutana na macho ya msichana aliyekuwa amebeba beseni la mboga za majani mwenye urembo uliofichika kutokana na aidha hali ngumu ya kimaisha ama adha nyingine za kimaisha., “Nauza Mbogamboga kaka” alisema yule dada huku akimtupia Richard jicho lenye utafiti fulani wa siri,. “Huwa sina desturi ya kupika dada,simply mboga sihitaji” alisema Richard huku akionekana kutopenda hali ile ya kutembelewa na mgeni wa dizaini ile hasa katika nyakati zile ngumu kwake,. “Heee! Samahani kaka!, kumbe wewe bado msimbee!! Hahahaha,.. sikujua hilo!…” alisema kibwege yule dada muuza mbogo huku akijichekesha pasina sababu ya msingi,. Richard hakujibu kitu alitikisa kichwa huku akiludi kwa ndani akimuaacha yule muuza mboga mwenye ugonjwa wa ‘chekelea’ pale nje,. Yule dada alikamatilia vizuri beseni lake la mbogamboga akipiga hatua kuiacha nyumba ile ya yule msimbe mwenye kupenda kula hotelini,. Alipita katika mitaa miwili mitatu akaingia vichochoroni akiwa na beseni lake la mboga kichwani,. hapo aliangaza macho huku na kule kisha akalitua beseni na kumwaga mboga zote ardhini na kuzifunika kwa beseni lake, Haraka haraka akajiweka vema, akavuta kifaa kidogo cha mawasiliano kilicho unganishwa na waya mwembamba uliopita katika nywele zake ukitokea ndani ya ukingo wa gauni lake chakavu, kisha akasogeza mkabala na mdomo wake akasema.; “one step remain is over,. muwaji amepatiaka mpaka kufikia kesho atakuwa mikononi mwa serikali ya Rwanda,.alisema yule dada muuza mboga,. Tobaaa!! Kumbe alikuwa ni shushushu kutoka serikali ya nchi ya Rwanda,..************
Machallo anajiunga na chuo kikuu cha Mt. Agustino kilichopo jijini Mwanza, jiji mashuhuri katika Afrika ya Mashariki lenye miamba mingi. Anaanza kufanya udahili pale chuo. Zoezi la udahili linakamilika, anapata ratiba na utaratibu mzima wa pale chuo ambao alipashwa kuufuata kwa kipindi chote anapokuwa pale chuo. Anajitahidi kuuzoea na kuendana nao kisha anaanza kuuuzoea taratibu kadri siku zinavyokwenda.
Muda unayoyoma, masomo yanazidi kuchanganya na mambo mengi ya pale chuoni yanadhihirika kwa Machallo. Anajikuta katika wakati mgumu kwani anaona kuna mambo mengi yanayoendelea pale chuo, yanayompelekea katika mazingira ambayo siyo rafiki mzuri kwake. Anajiuliza kama anaweza kujitawala na kuyashinda mambo yaliyo kinyume na maadili yaliyomjenga kutokana na mazingira aliyoishi muda mrefu. Anakumbuka shule ya sekondari ambako alisoma, shule yenye wanafunzi wa jinsia moja (wavulana). Hakuwa amezowea kusoma na kujichanganya karibu na wasichana, jambo lililokuwa tayari limemjengea woga kwa jinsia tofauti na yake na kujikuta mwenye aibu anapokuwa karibu na viumbe hao.
Pale Hosteli anaishi na wenzake watatu akiwemo Selike, Gibsoni na Gamba, lakini wanajikuta wana matabaka yaliyojengeka kulingana na vitivo wanavyosoma. Machallo na Selike wako kitivo kimoja (kitivo cha elimu) ambao wanajikuta wako karibu zaidi wakishirikiana mambo mengi na kujenga urafiki mkubwa sana. Gamba pamoja na Gibsoni wako vitivo tofauti, Gamba anasoma kitivo cha Sheria wakati Gibsoni akisoma kitivo cha Uongozi wa Biashara. Hawa wawili hawakuwa karibu sana wala haukuwepo ukaribu kati yao na akina Machallo na Selike. Kila mmoja aliona kitivo anachosoma ni bora kuliko kitivo anachosoma mwingine jambo linalowafanya Machallo na Selike wadharaulike mbele ya Gamba na Gibsoni kwa ajili ya dhana kwamba kitivo wanachosoma ni duni. Jambo hilo halina nguvu kiasi cha kuwasumbua hawa waalimu walioko mafunzoni.
Selike anakuwa maarufu kiasi pale chuoni, hasa katika kozi anayosoma tofauti na Machallo ambaye alikuwa hafahamiki. Selike anachaguliwa kuwa mwakilishi wa darasa jambo linalomfanya afahamike kwa kila mtu anayesoma katika lile darasa ambalo lilikuwa na watu ‘utitiri’ Machallo anaamua kutoa hisia zake wakati wamekaa chumbani akiwa na Selike mida ya jioni baada ya vipindi kumalizika. ‘umetokea kuwa maarufu sana ndani ya kipindi hiki kifupi’ anaeleza machallo huku akiendelea ‘..yaelekea una nyota ya kupendwa na watu’. Anaeleza Selike. ‘Nahisi uongeaji ndio unaochangia, si unajua tena mi mtoto wa uswazi, tantalila za kutosha!’ anajibu Selike huku akitabasamu na kuinuka kuelekea kabatini kuchukua kompyuta mpakato yake kuiweka ipate chaji. Mazungumzo yanaendelea hadi unafika wakati muafaka kwa ajili ya kupata chakula cha usiku. Wanatoka kuelekea ‘Canteen’ ambako huwa wanapata chakula.
Wanafika sehemu ya chakula pale canteen, Selike anaitwa na mwanadada ambaye anafahamika kwa jina la Maunda aliyekaa na rafiki zake wawili. Selike anafika, anaketi katika moja ya kiti kilichokuwa wazi pale kando ya meza. Baada ya salamu Maunda anafanya utambulisho kuhakikisha Machallo anawafahamu wale rafiki aliokaa nao bila kuacha kumtambulisha Machallo kwa rafiki hao. Wakati zoezi la utambulisho likiendelea, Joyce anamwita muhudumu kwa ishara akimtaka aje pale alipokaa. Muhudumu anafika na kusimama kando ya Joyce. ‘Msikilize kaka hapa chakula anachohitaji umhudumie’. Joyce anamweleza yule muhudumu. ‘Wali samaki’ anajiongeza Machallo kabla hajaulizwa na mhudumu. Mhudumu anaondoka kwenda kumletea chakula Selike. ‘Mlikuja wawili, mbona mwenzio ameenda kukaa peke yake?’ Ni sauti ya Joyce akimuuliza Selike. Kabla Selike hajajibu swali hilo, Maunda anarudisha chakula kwenye sahani ambacho alikuwa amechota kwa kijiko kwa ajili ya kubugia, anafuta mdomo wake kwa tishu kisha anaeleza jambo kuhusiana na swali la Joyce. Anaeleza kuwa anamfahamu huyo kaka aliyeambatana na Selike. Mara nyingi huwa anajitenga, usipomkuta peke yake basi atakuwa na Selike. Mara chache sana utamkuta amekaa na watu tena ni wavulana tuu. Anaweka bayana kuwa hajawahi kumwona akiwa amekaa na wasichana au akiongozana na msichana.
‘Au domo zege?’ anachomekea Joyce, kauli inayowafanya waangue kicheko huku Msope, Joyce na Maunda wakigeuka kumwangalia Machallo katika kona aliyokuwa amekaa. ‘Hivi ana ‘girlfriend’?’. Anauliza Msope ambaye amekuwa kimya kwa muda huku akimtazama Selike kwa makini. ‘Vipi unataka awe boyfriend wako nini?’ Ni Selike anamjibu kwa mtindo wa swali kwa lengo la kumtaka Msope afunguke ‘Inaelekea anapenda wanaume wapole huyu… kama yeye alivyo’ anadakia Joyce kabla Msope hajajibu, huku akimsonda. Maunda anaeleza wazi kuwa Msope sio mpole kama wanavyomdhania. Yeye anamfahamu, anaongea kama chiriku kwani amekuwa rafiki yake kwa muda mrefu. ‘Msope anaongea sana, hata hivyo leo nashangaa amekuwa sio mwongeaji kama siku zingine’. Anaeleza Maunda.
Wakati huo wakipiga soga huku wakipata chakula, Machallo anawatazama kwa macho ya wizi-wizi toka katika kona aliyokaa. Japo yuko mbali kiidogo kiasi cha kutosikia mazungumzo yao, anahisi kuna kitu wanamzungumzia hasa pale walipogeuka na kumwangalia alipokaa wakati wa majadiliana yao. Anajisikia vibaya, sio kwa sababu anahisi amezungumziwa bali kwa kile kilichowafanya wamzungumzie. Anajua dhahiri kuwa walimzungumza kutokana na yeye kujitenga na kukaa peke yake. Anataka aweze kuyashinda mazoea hayo mabaya yaliyomjengea tabia ambayo haimpi uhuru, kwani kukaa na wasichana sehemu moja ulikuwa ni mtihani uliomfelisha mara nyingi sana, jambo ambalo halipendi hata kidogo. Anatamani awe aina ya mwanaume bora anayejiamini na mwenye umaarufu kwa watu wengi zaidi badala ya kuwa duni asiye na mvuto wala thamani kwa wengine kama fikra zake zilivyompelekea.
Anamaliza kula chakula. Anaingiza mkono wake katika mfuko wa suruali yake na kutoa simu yake ya mkononi. Anafungua sehemu ya ujumbe mfupi wa maneno kisha anamtumia ujumbe rafiki yake Machallo ‘natangulia room’. Anaondoka kwenda chumbani huku kichwani akiwa na mawazo mazito akiwaza namna ya kushinda hulka yake iliyojenga tabia ambayo inamnyima uhuru na furaha kwa ujumla. Anafika chumbani, anasimama mbele ya kioo kikubwa kilichopo pale chumbani kuanza kujitathmini. Anajiona kuwa ni mwanaume bora, mwenye umbo zuri lenye mvuto na kila sifa inayomfanya kuwa bora kuliko vile alivyo. Anavuta taswira ya rafiki yake Selike na wanaume wengine pale chuoni ambao wana umaarufu mkubwa kuliko yeye, anagundua kuwa wengi wao hawana sifa kama zile anazozishuhudia katika taswira yake mbele ya kioo anachotazama. Uzuri wa umbo la kiume lililojengeka na kumfanya kuwa na mvuto kwa baadhi ya wanawake ambao mara kadhaa walishamsifia kwa nyakati tofauti linamfanya ajione anastahili kuwa aina ya mwanaume anayotaka. Lakini bado anajua iko kazi kubwa na ngumu ya kujenga fikra za kujiamini na kubomoa zile za kutojiamini, aibu na woga.
Anaketi na kuchukua simu yake ya mkononi ambayo ina huduma ya mtandao wa intaneti, anafungua ajifunze mambo yatayomfanya awe mwenye kujiamini na kuondoa hofu kwa watoto wa kike. Anafungua katika mtandao wa google na kuandika kile anachokikusudia kujifunza. Yanakuja matokea mengi, anachagua yale anayoona yanaelekeza vizuri kile anachokusudia kujifunza. Katika kuperuzi anakutana na mbinu zinazomfurahisha na kumfanya ajifunze kwa makini kuwa aina bora ya mtu anayohitaji. Maelezo yanaenda mbali zaidi kiasi cha kugusa uhalisia wa maisha yake anaona kuwa mwandishi wa ule mtandao alidhamiria kuandika kwa ajili yake kutokana na kuainisha sababu zinazomfanya awe vile, ambazo zina uhalisia mkubwa kwake.
Anadhamiria kuanza kuyafanyia kazi mashauri aliyosoma katika wavuti ile ambayo aliamini yatakuwa ni msaada mkubwa kwake kuweza kuondokana na kuishinda kabisa ile hali duni aliyokuwa nayo kisaikolojia. Anajua haitakuwa kazi ndogo wala haiwezi kutokea kwa siku moja, ila ingechukua muda na kuhitaji uvumilivu mkubwa. Lakini anajihakikishia, ‘lazima nifanikiwe kwani maisha ni mapambano kujenga kile ninachokikusudia maishani, kukitunza na kukilinda. nisipopambana, kujenga wala kukilinda ninachokikusudia, kile nisichokusudia kitachukua nafasi kama silka na kutawala maishani’
Selike anamaliza kula wakati ambao akina Maunda na wale rafiki wengine walishamaliza. Anaamua kuaga na kuondoka huku akiwaacha akina Maunda pale wakisuburi waletewe bili. Anafika chumbani na kumkuta Machallo akiwa ‘bize’ na simu yake ya mkononi. Anamuuliza kama anawasiliana na watu kupitia mitandao ya kijamii, Machallo anamweleza kwamba alikuwa akiperuzi habari katika mtandao. Hakutaka kumweka bayana kwa wakati ule kuhusiana na jambo linalomsumbua akilini kutaka kuzishinda fikra zake zinazomwangusha.
Selike anamweleza Machallo kuwa waende darasani kwa ajili ya kujisomea. ‘Najisikia ovyo leo’. Machallo anatoa udhuru ‘……….haina shaka, pumzika’. Anaeleza Selike huku akikusanya vitabu vyake vya rejea na kumuaga rafiki yake, kwenda darasani. Anapotoka, kabla hajamaliza kufunga mlango anakumbuka kumweleza Machallo jambo ambalo alipaswa amwambie. Anarudi ndani kumweleza Machallo kuwa, walipokuwa ‘canteen’ kupata chakula yule aliyemwita alikuwa ni Maunda. Alijua siyo mgeni machoni mwa Machallo hivyo alijua bila shaka Machallo anamfahamu japo alikuwa na wasiwasi huenda hawafahamu wale rafiki wengine waliokuwa wameambatana naye. Hivyo anaamua kumfahamisha Machallo kuwa, aliyekaa jirani naye (Selike) anaitwa Joyce, anasoma kitiivo cha Mawasiliano ya Umma, wakati yule aliyekaa jirani na Maunda anaitwa Msope, yuko kitivo cha Elimu. Wote ni mwaka wa kwanza. ‘Kuna kitu nimekisikia kwa masikio yangu mawili toka kwa Msope, ngoja nikupe mchapo huenda ni zali la mentali!’ anaeleza Selike. ‘lipi hilo kaka?’ anauliza Machallo kwa hamaki akitaka kujua kilichojiri. ‘Msope amekusifia sana, anasema wewe ni mwanaume wa kipekee ambaye uko tofauti sana na wengine. Mpole, mwenye kujiamini, pia uko ‘serious’ na mambo. Anapenda sana awe karibu nawe ila anasema tatizo anakosa namna ambayo anaweza kukuweka karibu’. Ndivyo anavyomalizia Selike na akifungua mlango kuondoka kwenda kujisomea huku akisisitiza ‘mi nimefikisha ujumbe kama nilivyosikia’.
Maneno yale yanapokelewa kwa furaha moyoni mwa Machallo. Anagundua kuwa, yeye siyo duni machoni mwa akina dada warembo kama alivyokuwa akidhania awali. Suala linarudi pale pale alipokuwa anafikiria, ‘kujiamini na kuondoa woga’.
Lakini maneno yale yalitoka kinywani mwa Selike ili kupoza mambo. Alihisi huenda machallo alijisikia vibaya alipokaa peke yake ‘canteen’ kitu kilichommbadili ‘mudi’ na kumfanya ashindwe kujumuika naye kujisomea jambo ambalo halijazoeleka kwa marafiki hao. Aliamini maneno yale yangemfanya ajione wa thamani mbele ya wengine, hasa akina dada ambao huwakwepa kama ukoma!
Machallo anaendelea kutafakari huku akifungua mtandao wa intaneti kuendelea kujifunza zaidi baada ya kusitisha kwa muda wakati akisikiliza maongezi toka kwa rafiki yake Machallo kabla hajaondoka kwenda kijisomea. Anafungua historia ya mwigizaji mkubwa na mashuhuri sana duniani ambaye alikuwa ‘bongo lala’ almaarufu kama ‘kilaza’ darasani wakati akisoma. Anavutiwa sana pale anaposoma kuwa alikuwa ni mtu wa aibu sana na mwoga asiyejiamini. Alipoingia katika tasnia ya uigizaji, mwalimu wake alimfundisha na kumsaidia jinsi ya kujiamini na kuificha hofu aonekane shujaa pale anapoigiza. Machallo anajikuta akitokea kuvipenda vipengele vinavyoelezea jinsi ya kuwa mtu unayejiamini vilivyoainishwa pale na kudhamilia kuvifanyia kazi ili abadilishe mazoea yake ambayo tayari yalishajenga tabia iliyokomaa. Anamaliza kujisomea katika wavuti ile, anafunga huduma ya mtandao na kuchukua filamu inayoitwa ‘Famous’ iliyoigizwa na muigizaji huyo nguli ambaye ametoka kusoma habari zake kwenye mtandao kisha anaanza kuitazama Baada ya kuitazama filamu hiyo iliyodumu kwa takribani saa 2, Machallo anajikuta akitokea kuipenda sana na kutamani awe na tabia iliyojengwa katika uhusika aliouvaa Elvin, mwigizaji mashuhuri ambaye ndiye nyota katika ile filamu. Anazima televisheni kisha anajipumzisha kitandani huku akitafakari hili na lile yote yakiwa yanalenga kumfanya awe mtu bora. Wakati akiendelea kutafakati, taratiiibu usingizi unamnyemele na kumpitia. Anashtuka usiku wa manane, kutazama saa, inamuonesha ni saa nane usiku. Ukimya umetawala sio tu pale chumbani ambapo kila mtu alishalala, bali hata nje ambako palikuwa na utulivu kuashiria kila kiumbe alikuwa tayari ameshalala isipokuwa bundi na popo ambao ndiyo mida yao ‘kuvinjari’
Usingizi unapaa kwa muda, anaamua kuchukua simu yake na kufungua sehemu ya mtandao wa intaneti ili aendelee kujisomea zaidi na kukazia maarifa juu ya kile alichojifunza. Hizi zilikuwa ni jitihada katika harakati zake za kuitawala akili yake na kuiongoza kufanya yale anayokusudia bila kukatishwa na fikra dhaifu. Dakika zaidi ya arobaini za kuperuzi mtandao wa intaneti zinakoma pale anapochoka na kuamua kuiweka simu yake pembeni na kuvuta shuka tayari kwa ‘kuuchapa’ usingizi.
Anaamka asubuhi na mapema. Anaenda kufanya mazoezi ya viungo kama ilivyo desturi yake na kurudi kwa maandalizi ya kuanza ratiba ya masomo katika siku ile. Anapoingia chumbani anamkuta Selike akinyoosha nguo zake yakiwa ni maandalizi ya kuingia darasani. Anamueleza jinsi alivyofurahishwa na ujumbe wa Msope siku iliyopita huku akiulizia zaidi habari za Msope. Selike anaahidi kumweleza kinagaubaga baadaye, kwa wakati huo anamtaka akaoge haraka ili waweze kuwahi vipindi kwani muda umeenda sana, wamebakiza dakika chache kabla vipindi havijaanza.
Wanamaliza maandalizi na kuingia darasani mahsusi kuanza vipindi. Awamu hii Machallo anaamua kuvaa moyo wa ujasiri na kujitahidi kuficha aibu zake mfukoni ukiwa ni mwanzo wa jitihada zake za awali kuhakikisha anajenga aina ya tabia anayoikusudia. Darasani katika ukumbi wa mihadhara anakaa karibu na mabinti. Jirani upande wa kushoto amekaa na binti ambaye anaonekana yuko tayari kwa ajili ya mhadhara. Machallo anaamua kutumia sekunde chache zilizobaki kabla ya mhadhara kuanza, awasiliane na yule binti. Anamsalimu, dada anaitikia. Machallo anaenda mbali zaidi ya salamu kwa kumuuliza maswali ya udadisi kutaka kujua A B C D kuhusu huyo dada. Dada anakuwa mzito kujibu, jambo linalomjengea Machallo dhana ya kukata tamaa na kutaka kuachana na maongezi yale. Anahisi huenda yule dada anamchukulia Machallo sio wa hadhi yake. Wazo lingine linamjia kuitikia sauti inayotoka ndani inayomtia moyo kwa kumwambia yeye ni mwanaume hodari mwenye hadhi ya kimataifa hivyo asijenge fikra za kukataliwa.
Anaamua kuanza upya au kama vijana wa siku hizi wanavyosema ‘kupanga swagga’. “…..unanukia vizuri!” Anamsifia yule dada. ‘Asante’ dada anajibu kwa bashasha tele!. Chezea Machallo wewe…..!!??’ Machallo anadhamiria kumuuliza swali yule mrembo, anapofumbua mdomo wake kuanza kuzungumza, anakatishwa na sauti ya Mhadhiri ambaye alikuwa tayari kwa ajili ya kuanza Mhadhara unaodumu kwa saa moja. Saa moja la mhadhara linaisha, machallo anaamua kutafuta fursa ya kupiga soga na yule kigoli. Bahati mbaya yule dada alishaondoka mapema bila yeye kujua hivyo mpango mzima unakwama.
:: Unavyodhani nini kitaendelea hapo?
:: Huu ni mwanzo tu wa simulizi hii kali na ya kuvutia
Saa moja la mhadhara linaisha, machallo anaamua kutafuta fursa ya kupiga soga na yule kigoli. Bahati mbaya yule dada alishaondoka mapema bila yeye kujua hivyo mpango mzima unakwama.
Songa nayo sasa… ********************** Sekunde, saa, siku, juma na miezi ilisonga. Jitihada za makusudi zinazidi kufanywa na Machallo kuhakikisha anapambana na hali yake duni kifikra. Matokeo yanaonekana, anajikuta tayari ameanza kupiga hatua na kujenga uwezo kidogo wa kujiamini na kupambana na hali yake licha ya vikwazo lukuki anavyokumbana navyo. Anagundua kuwa zile wavuti alizotembelea na vitabu mbalimbali alivyosoma vimemfanya awe bora zaidi na aimarike kifikra. Anatokea kukipenda sana kitabu chenye kichwa ‘Saikolojia ya Kujitambua’ kilichoandikwa na Habel Samida ambacho kimekuwa na msaada mkubwa sana kumfanya ajitambue zaidi ya awali na kutambua nguvu, vipaji, uwezo na uimara ulioko ndani yake na namna ya kuviendeleza.
Inafika siku ya jumamosi, mwisho wa juma. Siku ambayo kila mtu huwa na pilika za mambo yake binafsi kwani huwa hakuna ratiba ya masomo. Machallo anashinda chumbani akiwa peke yake. Anasimama mbele ya kioo kilichopo pale chumbani na kujaribu kufanya ‘reharsal’ ya kila aina ya tabia anayotaka kuijenga. Anasimama akiwa amevaa vizuri, mbele ya kioo akitamka maneno na kuonesha ishara kwa mikono yake akijaribu mambo mengi anayotaka kushindana nayo. Anavuta taswira yuko kwenye ukumbi wenye maelfu ya watu, yeye ndiye mtu maalumu anayetoa hotuba pale. Anafanya hivyo huku akijitazama kwenye kioo kilicho mbele yake. Anagundua amekuwa bora zaidi, anajiona imara kama chuma cha pua mwenye uwezo wa kusimama popote bila aibu wala hofu.
Baada ya majaribio mengi, anahamia katika suala lingine ambalo ni nyeti sana moyoni mwake. Suala hilo sio jingine, ni mahusiano yake ya kimapenzi na binti ambaye macho yake yamemwona na moyo ukamchagua. Ni mzuri wa sura, umbo hata tabia. Wanaume wengi hutokea kuvutiwa naye kwa sifa lukuki alizonazo ila suala la kumweleza bayana huwa zito kwani wengi wao hujikuta midomo imejaa maji!
Anaamini akimpata mlimbwe huyo, atakuwa ametimiza ndoto yake kubwa ‘kuwa maarufu’ iliyojengeka tangu akiwa mdogo. Aliamini kuwa na yule dada kungemfanya aikamilishe hiyo ndoto yake kulingana na hadhi na nafasi aliyonayo huyo dada katika jamii. Anainuka kusimama mbele ya kioo kujaribu ‘staili’ ambayo inaweza kuwa nzuri kwake, jinsi atakavyokwenda kumweleza mwanadada wa ndoto yake yanayotoka moyoni. Anajaribu kwa mara ya kwanza, anahisi hiyo siyo namna nzuri, anajaribu tena. Awamu hii anaona ameboresha maneno ni mazuri ila tatizo mavazi aliyovaa hayana hadhi ya kusimama mbele ya ‘mchumba’. Anaamua kufungua begi lake ambalo hulitumia kutunza nguo. Anachagua nguo ambazo anaona ni nzuri zaidi ya zingine na akivaa anahisi anapendeza. Nguo zimejikunja, hivyo anaamua kuzinyoosha ili avae aweze ‘kutokelezea’ tayari kwa kuanza mazoezi ya kumvutia kasi mwanadada ambaye ametokea kumpenda. Anamaliza kuzinyoosha, anavaa na kuhakikisha amechomekea vizuri kwa ustadi. Anasimama vizuri ajitazame kwenye kioo huku akiachia tabasamu matata na kuvuta picha yuko na yule mlimbwende ambaye ametokea kumfanya teja wa mapenzi. “Flaviana, Wewe ni mwanamke ambaye una sifa lukuki, za kipekee ambazo siwezi kuuelezea ulimwengu na kuzimaliza kwa dakika hizi chache….
Kwa sifa hizo, unastahilii kuwa na aina ya mwanaume ambaye atajali nafasi uliyonayo na kukufanya bora zaidi siku zote ujione umependelewa na Mwenyezi Mungu. Mimi ni chaguo sahihi kwako. Najua hunifahamu kwa karibu, ila naomba unipe nafasi uone mimi ni mtu wa namna gani!
Usije kunifikiria na kunichukulia kama maleghuni ambao siku zote wao hubananga”.
Anajisemea Machallo huku anashuhudia kijasho chembamba kikimtoka anapomaliza kutamka yale maneno, kitendo kinachoashiria kuwa ile siyo shughuli ndogo hata mara moja. Anapanga mikakati kabambe kuhusu namna atakavyokutana na huyo kiumbe adhimu na ‘kumtemea madini’ ambayo anaamini ni Tanzanite. Wakati amekaa na kutafakari hayo, anafika Selike pale ndani. Anagundua, kuwa kuna jambo zito linalomkabiri rafiki yake kipenzi. Kwakuwa alijua, lolote linalomgusa Machallo linamgusa hata yeye, anaamua kumuuliza kinachomsibu hadi awe anatapatapa katika bwawa la mawazo kiasi kile. Bila kusita, Machallo anafunguka kueleza lile lililoko moyoni mwake na dhamira yake ya dhati. Anaeleza kuwa, anafikiria jinsi atakavyompata yule ampendaye awe sehemu ya maisha yake. Jambo ambalo linamfanya Selike aulize kwa shauku kubwa kutaka kujua moyo wa rafiki yake umetua wapi!
Machallo anabainisha kuwa anampenda msichana ambaye amedhamilia kumpata awe naye maishani. Furaha yake itakamilika pindi atakapofanikiwa kwani akili yake, moyo, mwili, damu, maji na mifupa yake ilikuwa inamshuhudia umuhimu wa kiumbe huyo maishani mwake. Hapati picha mateso atakayopata akimkosa.
Wakati akieleza hayo Selike yuko makini anasubiri afahamishwe ni nani hasa ambaye anaunyanyasa moyo wa rafiki yake ili aone namna ya kumsaidia rafiki yake ahakikishe anapata shemeji mwema.
‘Flaviana ni chaguo langu sahihi’ anasema Machallo huku akishusha pumzi ndefu. “ni Flaviana yupi?” Selike anajiuliza. Maana yeye anamfahamu Flaviana mmoja tu pale chuo. Ni dada maarufu sana sio tu pale chuo, bali katika jiji la Mwanza, Tanzania bara na visiwani, pamoja na Afrika Mashariki na kati kwa ujumla. Hadhani kama anaweza kuwa Flaviana huyo anayemfahamu yeye, anajua huenda ni Flaviana mwingine. Kuondoa mkanganyiko anaamua kumuuliza Machallo ili apate uhakika. Selike anashindwa kujizuia, anacheka kwa dharau baada ya kuambiwa kuwa ni Flaviana huyohuyo anayemfahamu. Kicheko hicho kinatosha kumfanya Machallo agundue kuwa rafiki yake anaamini kwamba hizo ni ndoto za Alinacha, kwani hawezi kumpata mrembo huyo kutokana na mafanikio makubwa na umaarufu alionao katika tasnia ya Filamu (Bongo Movie), kuwa mwanamitindo anayefanya vizuri, pia kuwahi kutwaa taji la ‘Miss Tanzania’.
Selike anaweka bayana kuwa huyo dada sio wa hadhi yake! ‘…not your stuff, anyway!’ Anaamua kumweleza Machallo asijisumbue kumfikiria mwanadada huyo, anaweza kuumia na kuambulia maradhi ya moyo bure! Ni bora atulize moyo wake amtafute wa hadhi yake. Kauli hiyo haina nguvu kiasi cha kumkatisha tamaa Machallo. ‘Naamini kitu chochote ambacho mtu atakidhamiria kwa dhati na kufanya jitihada za makusudi bila kukata tamaa kinawezekana. Ndivyo ninavyoamini itatokea…’ Anasisitiza Machallo. Anamuhakikishia rafiki yake kuwa lazima ampate. ‘Yangu macho….., ila nakuahidi, kama utaweza kumpata Flaviana, siku hiyo mi ntavua nguo na kutembea uchi chuo kizima! Tena mchana kweupeee…’ anaongea Selike kwa kebehi, Kauli inayomfanya Machallo amwambie Selike ‘wapinge’ (njia ya kuweka makubaliano) ili siku ikitokea, avue nguo kweli na kutembea uchi.
Wanamaliza kupinga, Selike anaenda kabatini na kuchukua glasi. Anamimina juisi na kumpa Machallo huku naye akichukua glasi nyingine na kujiwekea. Anatafuta filamu nzuri ambayo anaweza kuangalia. Anamuuliza Machallo filamu ambayo angependa waangalie. Machallo anamweleza kuwa aweke filamu yoyote nzuri ila iwe ‘love story’. Anaangalia katika ‘droo’, anapata filamu inayoitwa ‘Gharama ya penzi’
Wanaangalia ile filamu nzuri yenye mikasa ya kimapenzi inayosisimua wakati Machallo akiwa amekaa chini huku akikodolea macho TV, lakini mawazo yake hayako pale. Alikuwa akimfikiria Malkia wake mwenye hadhi kuwa malkia wa ulimwengu ambaye ametokea kumkaa akilini kuliko kitu chochote.
Anajisikia vibaya kuwa ‘dissappointed’ na rafiki yake ambaye hayuko upande wake kumtia moyo. Potelea mbali…. Anakusidia kusonga mbele bila kukatishwa tama na maneno ya rafiki yake. ‘lazima azma yangu itimie bila kujali vikwazo’ anajisemea moyoni.
********************
Kadri siku zinavyokwenda ndivyo njaa ya umaarufu inamzidia kiasi cha kuwaza sana kile anachoweza kufanya apate kukidhi njaa yake. Hilo ndilo lengo lake kubwa linalomfanya amfikirie sana Flaviana. Alijua akimpata huyo manzi, umaarufu utakuwa ni ‘wakufikia’. Maneno ya kumkatisha tama yaliyotolewa na rafiki yake Selike yanajirudia akilini mwake. Anafikiria sifa alizonazo yule ‘mamiito’ anakubaliana na kauli ya Selike kuwa sio wa hadhi yake. Lakini bado dhamiri yake inamtuma arushe nyavu ili aweze kumnasa kiumbe huyo.
Ni jumatatu, ratiba ya chuo inaendelea kama ilivyo ada. Akili ya Machallo imetawaliwa na fikra za kuwa maarufu na kumpata Flaviana. Anadhamiria kujitutumua amfuate kumweleza hisia zake. Alifahamu kuwa Flaviana huwa anapenda kwenda kupata chakula ‘canteen’ maalumu kwa ajili ya wahadhiri na wanachuo wenye uwezo mkubwa kifedha kwani bei ya vyakula na vinywaji pale ni kubwa kuliko sehemu zinigine. Anatambua uwezo wake kifedha sio mkubwa. Kiasi cha fedha alichonacho ni kidogo hivyo alitambua akienda pale kupata huduma ya chakula na kinywaji wakati akimsubiria Flaviana, atakuwa ametumia kiasi kikubwa cha fedha, ambacho kitamharibia bajeti yake siku za usoni ataishiwa pesa. Anaamua kutojali hilo huku akiwa tayari hata kula mlo mmoja ilimradi afanikiwe mpango wake mahususi. Anaangalia muda, anagundua bado haujafika ule muda muafaka ambao Flaviana hufika pale ‘canteen’ kupata chakula cha mchana. Anaendelea na masuala mengine huku akisubiria muda muafaka ufike. Muda unafika, anataka kughairi kwenda lakini anajipa moyo. Anarudi chumbani kwanza kujiangalia kwenye kioo. ‘you are so great’ anajisemea wakati akijiangalia kwenye kioo kushuhudia ‘alivyotupia’ suti yake nyeusi ambayo ni moja tu aliyonayo. Anakumbuka kuwa alipewa na shangazi yake katika sherehe aliyofanyiwa na familia yake ikiwa ni kumpongeza kupata nafasi ya kujiunga na chuo kikuu, kitendo kilichoipa heshima kubwa sana ile familia kwani, katika ukoo mzima yeye ni mtu wa kwanza kugusa elimu ya chuo kikuu. Anakumbuka asubuhi alipulizia manukato ‘pafyumu’ lakini anaamua kufungua kabati tena kuchukua manukatu na kujipulizia kwa mara nyingine kisha anaamua kuelekea uwanja wa mawindo. Anapotoka, kufika nje anakumbuka hakutengeneza nywele zake vizuri. Anaamua kurudi ndani na kuchukua ‘brashi’ anazitengeneza vizuri nywele zake zilizonyolewa na kuachwa fupi zikipendeza. Sasa anajiamini baada ya kujiridhisha, anatoka kwenda kuianza shughuli. Kufika ‘VIP canteen’ anaangaza macho huku na kule kuona kama Flaviana ameketi mahali, bila kumwona. Wakati akifanya zoezi hilo alikuwa makini asije kuonekana mshamba kwa jinsi anavyoshangaa. Anaamua kwenda sehemu ya mbele , ambako anakaa karibu na TV kubwa iliyowekwa ukutani. Kumaliza kuketi tayari muhudumu ameshafika na kuanza kumuuliza anachohitaji. Wakati muhudumu anauliza, tayari Machallo amemuona mwanadada ambaye anajua ni Flaviana akiingia mule ndani kwa mwendo wa madaha!. Jambo hilo linamfanya atumbue macho huku mawazo yote ameyahamishia kule anakotazama. Anashituka kidogo anapoguswa begani huku akisikia sauti inamuuliza ‘kaka nikuhudumie nini nakuuliza?, ni muhudumu akiuliza. Anageuka na kumwangalia mhudumu usoni huku macho yake akiyapepesa kwa haraka ‘Juisi ya parachichi’ anajibu kwa haraka huku akijibaraguza baada ya kugundua kuwa muhudumu amekuwa akimuuliza mara kadhaa bila kujibu baada ya kuwa ‘amepitiwa’ pindi alipomwona yule kigoli wakati anaingia. Muhudumua anaondoka ili akamletee mteja wake kile alichoagiza. Machallo anatupa jicho tena kuangalia yule mrembo ameketi maeneo gani baada ya kukatishwa na muhudumu zoezi lake la kumsindikiza kwa macho kuona pale atakapokaa. Kuangalia kule alikokuwa anaelekea kuketi yule mrembo, anamuona, loh! Kumbe amemfananisha ‘bhana’. Mawazo yanamtawala, huku shauku ya kumwona Flaviana na kupata nafasi ya kuongea naye inatanda. Anamwangalia tena yule dada ili ajiridhishe kama sio Flaviana kweli. Anagundua siyo kwa mara nyingine. Saa yake inamuonesha ni saa saba na nusu mchana, ikiwa imebaki nusu saa kufika saa nane muda ambao ana kipindi. Anaamua kujitoa ‘muhanga’ hata kama atakosa kipindi lakini lazima amsubiri Flavana hadi amwone. Anaendelea kunywa juisi huku akiwaza na kuangaza macho yake yashuhudie tukio muhimu, pindi Flaviana anapoingia ‘mjengoni’. Muda unazidi kwenda bila kumtia machoni Flaviana. Anawaza huenda alishafika pale kupata chakula na kuondoka kabla yeye hajafika. Au pengine siku hiyo Flaviana hajafika chuo. Lakini anakumbuka alipoangalia ratiba kozi anayosoma Flaviana, aliona ana kipindi kuanzia saa sita mchana hadi saa saba kamili, hivyo alijirishisha kuwa atakuwa bado hajafika pale kula chakula kabla yeye hajafika. Anawaza mengi, mwishowe anakata tama kumsubiri. Anaamua kuondoka. Anaenda ‘kaunta’ kulipa bili. Anatoa noti ya shilingi elfu kumi anamkabidhi mhasibu. Wakati akisubiria chenji akaangaza katika lango kuu la kuingilia ‘kantini’, anamuona kiumbe aliyekua akimsubiria kwa takribani saa moja na dakika zipatazo arobaini na saba anaigia. Kumwona, moyo ‘unampasuka’ kiasi cha mapigo ya moyo kuongezeka kwa kasi. Anamsindikiza kwa macho hadi alipokwenda kuketi. Anaamua kumfuata ili apate nafasi ya kuongea naye amweleza lililomo ‘uvunguni’ mwa moyo wake. Anasahau kuwa amekuwa akisubiria chenji anaondoka. ‘kaka chukua chenji yako’ ni mhasibu aliyekuwa akimweleza Machallo ambaye alikuwa ameanza kuondoka. Machallo anarudi, anachukua chenji na kuelekea alipokaa yule malaika. Anafika na kumsalimia huku akimtolea tabasamu zito linalochimba ‘vijisima’ vidogo mashavuni mwake. Flaviana anaitikia kwa uchangamfu bila hiyana. Anaomba aketi pamoja naye kwa maongezi mafupi, Flaviana anakubali na kumruhusu. Machallo anashukuru kwa ukubali ule, anakaa huku akitafakari wakati mgumu alionao kueleza hisia zake kwa yule mwanadada. Alijua kitendo kile kilihitaji ujasiri wa hali ya juu. Anajua kuwa hakuna jambo lingine muhimu zaidi ya jitihada za kuvaa moyo wa ujasiri ili aanze kumtemea madini yule manzi.
*************
::: Je machallo ataweza kutupa kete kwa flaviana?? itakuwaje sasa atakubaliwa?? nini hatma ya Machallo?
:: Safari ndio kwanza imeanza, hapo ndipo utajua maana ya ‘SHETANI MSALABANI’ hakika si ya kukosa endelea kufuatilia kujua.
Machallo anashukuru kwa ukubali ule, anakaa huku akitafakari wakati mgumu alionao kueleza hisia zake kwa yule mwanadada. Alijua kitendo kile kilihitaji ujasiri wa hali ya juu. Anajua kuwa hakuna jambo lingine
Songa nayo sasa…
Japo anavaa moyo wa ujasiri, tayari ameshasahau maneno yote aliyopangilia kumwambia mwanadada yule ambayo amekuwa akiyarudiarudia kwa wakati Fulani ili yamkae vizuri akilini kwani aliamini yalikuwa ni silaha tosha ya kufanya mashambulizi ya hatari ambayo yangemletea ushindi kwa asilimia zaidi ya tisini na tisa nukta tisa. ‘Flaviana’ Machallo anamwita yule mrembo jina. ‘Aabe!’ anaitika Flaviana huku akimtazama na kumkazia macho tayari kwa kusikiliza kile Machallo anachotaka kumwelezea. ‘Naitwa Machallo, ni mfuatiliaji mzuri sana wa filamu zako. Hakika unajua kukitendea haki kipaji ulichopewa’ ni maneno toka kwa Machallo. ‘Nafurahi kukufahamu Machello’ anajibu Flaviana. ‘ni Machallo sio Machello’ anamsahihisha Machallo. ‘Nashukuru kukufahamu Machallo, pia asante kwa kufuatilia kazi zangu. Mi naamini bila wewe mimi sio kitu’ anaendelea kuelezea zaidi Flaviana kuwa anaamini kipaji cha uigizaji alipewa na Mungu ili aweze kugusa maisha ya watu wengi. Furaha yake kubwa siyo mafanikio makubwa ya kiuchumi aliyoyapata na anayoendelea kuyapata katika tasnia ya filamu, bali ni aina ya mtu anayetaka kuwa na jinsi anavyogusa maisha ya watu kwa namna tofauti. Machallo anagundua kuwa Flaviana ni mtu wa watu, anawathamini sana watu wanaothamini kile anachofanya. Jambo kubwa linalomfurahisha ni ule ukarimu na uchangamfu ambao ameuonesha Flaviana tofauti na mawazo yake yalivyompelekea awali kulingana na hadhi na mafanikio aliyonayo Flaviana. Wakati wakiongea maongezi ya hapa na pale, kabla Machallo hajafunguka, anakuja mwanadada mrembo ambaye sio mgeni sana machoni mwa Machallo kwa jinsi anavyomtazama na kuvuta kumbukumbu. Anafika pale walipokaa, anampatia Flaviana ufunguo wa gari na kumweleza kuwa amesumbuka kidogo kupata sehemu nzuri ya kupaki gari ndiyo maana amechelewa kufika tangu Flaviana alipomwacha ‘garini’. Anakaa na kumsalimia Machallo, bila kumfahamu huku akiwa na shauku kutaka kumfahamu. Kabla hajauliza, Flaviana anamtambulisha Machallo kuwa huyo dada ni rafiki yake kipenzi anaitwa Lightness. Kisha anamgeukia Lightness na kumwambia kuwa yule kaka anaitwa Machallo, ni shabiki wake mkubwa sana wa filamu zake. Ameamua kujumuika nao ili wapate fursa ya kuongea machache. Machallo anaamua kueleza kile anachokifahamu kuwa anakumbuka alishawahi kumwona Lightness katika moja ya filamu alizowahi kuangalia ila hakumbuki haswa jina la ile filamu inaitwaje! ‘Sijawahi kucheza filamu hata moja’ anabainisha Lightness huku akiongeza kuwa, huyo Machallo aliyemwona ni dada yake ambaye ni mwigizaji maarufu sana. ‘Watu wengi hushindwa kututofautisha wanapotuona, jinsi tunavyofanana’ anaongezea Light huku akieleza kuwa yeye alishawahi kushiriki kuwania taji la Miss Tanzania japo hakunyakua, ila alifarijika taji hilo liliponyakuliwa na rafiki yake kipenzi Flaviana. ‘Niliamini ushindi wa Flaviana ni ushindi wangu’ ni kauli ya Light. Wanaagiza chakula, Machallo anapata bahati ya kuambiwa na Flaviana aagize chakula anachopenda. Anaagiza, baada ya muda chakula kinaletwa wanaanza kula huku wakiiendelea na mazungumzo. Fursa ile ilikuwa ni adhimu sana maishani mwa Machallo, anajiona tayari ameshakubaliwa na kupewa nafasi ndani ya moyo wa yule mwanadada wa ndoto yake. Anaenda mbali zaidi kifikra na kujiona ameshakuwa ‘nyota’ kwa bahati ile iliyomtembelea siku ile.
Kibarua bado hajakikamilisha. Suala ambalo linamfanya afikirie jinsi anavyoweza kufunguka, somo lipate kueleweka kwa mwanadada huyo ambaye hachoki kumwangalia huku akimshusha na kumpandisha bila kuona dosari. Anapanga mashambulizi kimoyo-moyo ‘Moja… mbili.. tatu…’ mmmh!, eeeh!. Maneno yanakwama kutoka. Anaamua kuanza kwa swali kwa Light huku akivuta kasi na kupanga gia ya kumwingilia malaika Flaviana. ‘Lightness, una ‘boyfriend’?’ anauliza huku akimtazama macho ya aibu iliyochanganyikana na woga kwa mbali. ‘Sina, nina marafiki tuu. Bado sijafikiria wala kuamua kufanya uchaguzi sahihi kwa sasa japo wanaokuja ni wengi’. Anafafanua Lightness. Anakaa kimya kidogo, kisha anafikiria jinsi ya kuanza kutema ‘swagga’ kwa Flaviana. Kabla hajafikia muafaka aanzie wapi, anapata swali la uchokozi toka kwa Flaviana. ‘Mbona mimi hujaniuliza kama nina ‘boyfriend’ au sina?’. Machallo anajibu ‘najua lazima utakuwa naye, msichana mzuri kama wewe ukose boyfriend?’ jibu hilo lilitolewa na Machallo makusudi akimtaka Flaviana abainishe ukweli kama anaye au hana. Kabla hajatamka neno lolote, simu yake ya kiganjani inaita hivyo anaamua kuipokea. Wakati Flaviana akiendelea na maongezi ya simu, Lightness anarudisha swali kwa Machallo akitaka kujua kama ana ‘girlfriend’. Anabainisha kuwa hana, ila kwa muda mrefu amekuwa akimsaka msichana mwenye sifa za kipekee azipendazo bila mafanikio. Anaendelea kufafanua kuwa, ameshamwona mwenye sifa anazohitaji. Kilichobaki ni kumweleza hisia zake toka moyoni ili naye asikilize moyo wake kama anaweza kutoa nafasi. Maongezi hayo yanakatizwa na Flaviana ambaye amemaliza kuongea kwa simu, anamtaka Light waondoke kwenda mahali ambapo kuna mtu walikuwa wamepanga miadi wakutane mida ile. Wanamuaga Machallo na kuondoka kitendo kinachomfanya Machallo ajilaumu na kutoamini kile anachokishuhudia. Anashindwa kuamini kama ni kweli Flaviana anaondoka au ni mauza-uza anayoyaona. Machallo anabaki kimya huku akiwasindikiza marafiki hao kwa macho hadi anahakikisha wametokomea mbele yake. Anaamua kuondoka pale alipokaa huku akiwa na furaha kidogo iliyochanganyika na huzuni tele kwa kushindwa kuitumia fursa ile kukamilisha mpango wake.
Lightness na Flaviana wanafika mahali lilipo pakiwa gari lao. Wakati wakifungua gari na kuingia Light anamuuliza Flaviana kama anafahamiana na yule kaka (Machallo) kwa muda mrefu. Flaviana anamwambia kuwa hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kuonana naye ‘Nilipofika ‘canteen’ nikamwona kaja na kuomba akae pale nilipokaa. Nikamkubalia, hapo ndipo akaanza kujitambulisha kwangu ndiyo nikamfahamu. si unajua tena ukiwa maarufu……………?’ ni maneno ya Flaviana
Machallo anajiona ni mwanaume asiye na maarifa, hilo ni suala jingine ambalo anaahidi ndani ya moyo wake kuwa atapambana nalo kwa nguvu kuhakikisha analikabiri hadi anashinda. Anafika chumbani, anavua suti yake na kuitundika katika ‘stendi’ maalumu ya kutundikia nguo iliyopo pale chumbani. Anaketi kitandani akiwa na bukta ndogo. Anatafakari yaliyotokea pale uwanja wa mawindo na kujiona ameshindwa kumfyatua risasi swala aliyenona! Anafungua simu yake ya mkononi kuangalia sehemu alipohifadhi picha. Anaangalia picha ya mwanadada huyo ambaye amepata bahati kukutana naye. Licha ya kushindwa kutimiza kusudi lake anaamua kujipongeza kwa jitihada zile alizofanya kwani anagundua haikuwa rahisi kujivisha ujasiri ule kukutana na mlimbwende yule ambaye alipokuwa akimtazama toka chini hadi juu hakuona dosari.
************* Ni semista ya pili baada ya kufunga chuo kwa mapumziko. Maisha ya Machallo yanabadilika. Anakuwa mtu wa kujiweka katika hadhi ya juu na kupenda kusalimiana na kila anayekutana naye, pengine kujitambulisha ili kusudi lake kuwa maarufu lipate kutimia. Ameshakwaruzana na Selike kutokana na kupishana mienendo kufuatia mabadiliko ya tabia yaliyojitokeza kwa Machallo. Hilo linamfanya asijali, hadi ahakikishe anatimiza azma yake. Alitumia fursa kutumia mitandao ya kijamii ya facebook, twitter, instagram na mingine akitafuta umaarufu. Kama hiyo haitoshi, alitumia muda wake kufungua wavuti (blog) yake ili kuhakikisha watu wengi wanaitembelea na kusoma habari zake ili atii kiu yake. Kujenga ukaribu na watu maarufu lilikuwa ni jambo alilotamani sana, aliitumia vizuri fursa alipoipata. Alihakikisha anapokutana na mtu maarufu, lazima ajitambulishe kwake. Jitihada za kumuweka karibu mwanadada Fllavi bado ziliendelea japo zilikabiri changamoto ‘kibao’
Unafika wakati ambao wanachuo wanapata fursa ya kuchagua viongozi wao katika serikali ya chuo. Machallo anaona ni fursa nzuri kwake kuingia katika kinyang’anyiro hicho ambacho kitamfanya awe maarufu pindi atakapopata madaraka. Anachukua fomu na kugombea miongoni mwa nafasi nyeti pale chuo.
Kampeni zilianza, anajitahidi kujinadi kwa sera ambazo anaamini zitamweka katika nafasi ile anayowania. Bahati inakuwa mbaya kwake, anashindwa kupata ile nafasi baada ya kushindwa wingi wa kura na hashimu wake ambaye alikuwa na nguvu kubwa katika sera zenye mvuto. Jambo hilo linamnyima furaha, anajiona ana bahati mbaya kama ‘analala na bundi’ jambo linamchelewesha kufika katika kilele cha ‘umaarufu’.
Mtiririko wa mambo hayo yote yanamfanya atumie gharama kubwa sana katika mavazi, vyakula pamoja na vitu vingi alivyohitaji ambavyo alijua vingemweka katika tabaka la juu. Anajikuta katika wakati mgumu ambapo anataka kuishi maisha ya juu huku uwezo wake kifedha ni mdogo. Suala la kumpata Flaviana amweleze la moyoni limekuwa shughuli pevu kushinda awali. Jitihada za kutafuta namba yake ya simu zinaendelea, anabahatika kupata namba ambayo anajaribu kupiga, inaita bila kupokelewa. Jaribio la kupiga ile namba linaendelea mara kwa mara bila mafanikio.
Unafika wakati ambao hawezi kuendelea kungoja kwani njaa na kiu ya mafanikio inazidi. Anapata wazo, kujichanganya katika makundi pindi watu wanapokuwa ‘wakipiga stori’ ili kuhakikisha anayateka mazungumzo na kujijengea jina. Zoezi halikuwa rahisi kwani ni mara chache watu walikuwa wavumilivu kusikiliza mazungumzo yale jinsi alivyokuwa akijipeperushia bendera. Katika harakati, siku ya siku anafumania kundi la wanachuo waliokaa katika ‘vimbweta’ wakijadili habari za mpira kuhusiana na watani wa jadi Simba na Yanga. Anajichanganya katika lile kundi kuanza kuchangia mada. Wakati maongezi yakiendelea, linapita gari aina ya prado. Ambalo linaonekana kama gari analopenda kulitumia Flaviana mara nyingi. Mmoja wao anauliza kama lile gari sio la Flaviana. Machallo anadakia ‘siyo lenyewe’ Anaona hiyo haitoshi anaamua kujifagilia ‘Flaviana ni demu wangu, popote alipo lazima anitaarifu’ maneno yale yalimsababisha Machallo ashambuliwe kwa vicheko vya dharau na kejeli huku maneno ya kashfa yakimfuata. Anashindwa kuvumilia kwa fedheha anayopata, anaondoka eneo lile huku akiendelea kuzomewa na kutaniwa. Kitendo kile kinamkosesha amani kwa muda na kumvunja moyo kuendelea kuvamia makundi. Anaanza kufikiria jinsi anavyoweza kufanya ili akamilishe ndoto yake. Jitihada zinashindwa kuzaa matunda hadi mitihani inapoanza, wakati ambao anakuwa ‘bize’ kiasi cha kukosa muda wa kufanya jitihada zozote zinazoweza kumkutanisha na Flaviana wala kumfanya maarufu. Semista ya pili inaisha baada ya mitihani kumalizika na chuo kinafungwa tayari kwa likizo ndefu.
Wakati wa likizo ulikuwa ni muda mzuri kwake kujipanga ili chuo kinapofunguliwa aweze kuwa na mafanikio katika ndoto yake kubwa. Anatambua kuwa hawezi kumpata Flaviana katika kipindi hicho cha likizo, kwani husafiri kwenda Daresalaam katika kipindi chote cha likizo.
Anapata nafasi ya kufanya ‘field’ katika shule maarufu sana isiyokuwa ya serikali ya Knowledge Springs iliiyoko jijini Mwanza. Field yake inakuwa na mafanikio makubwa kuanzia majuma machache tangu aanze, kutokana na kutokea kupendwa sana sio tu na wanafunzi, bali waalimu pamoja na baadhi ya wazazi waliosikia sifa zake.
Kadri siku zinavyoyoyoma, anajikuta maarufu sana katika mazingira yake ya kazi kutokana na tabia njema na mwenendo uliotukuka wa maadili mazuri ya ualimu. Jambo hili linamtofautisha na vijana wengine ambao huonesha utovu wa nidhamu pindi wanapokuja kufanya field pale shule, huanzisha mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi.
Kutokana na uwezo wake mzuri kufundisha darasani, wanafunzi waliweza kuelewa sana somo la baiolojia alilokuwa akifundisha. Somo lilitokea kupendwa hata na wanafunzi ambao walilichukia na kuliona gumu. Uongozi wa shule unaamua kuweka makubaliano ya kumlipa Machallo ilii aweze kufundisha vipindi vya ziada na kumpangia kufundisha madarasa mengi. Anakubali na kujituma. Kiasi cha pesa anachopata kinamsaidia kwa kiasi kikubwa sana katika kumudu gharama za maisha.
‘Anajibana’ na kutumia sehemu kubwa ya fedha anayopata kuanzisha kipindi cha redio mara moja kwa juma, kila siku ya jumamosi kuanzia saa nne asubuhi. Kipindi kinachodumu kwa muda wa dakika 45 akifundisha somo la baiolojia. Kipindi kilikuwa na mafanikio makubwa sana baada ya kupata wasikilizaji wengi ambao asillimia kubwa walikuwa ni wanafunzi ambao walikuwa wakituma barua pepe, ujumbe mfupi wa maneno na kupata fursa ya kupiga simu wakati wa kipindi kuuliza maswali na kutoa maoni.
Bahati inakuwa nzuri upande wake pale anapopata udhamini toka kwa kampuni kubwa inayojihusisha na uchapaji wa vitabu. Anaingia nao mkata, wanamchapia kitabu cha baiolojia ambacho alikuwa ameshamaliza kukiandika, alichoanza kukiandika mwaka mmoja uliopita. Kitabu kinakamilika, anaanza kukinadi kwa wanafunzi shuleni anakofundisha na shule nyingine za jirani pamoja na redioni anapofanya kipindi. Wengi wanatokea kukipenda sana kile kitabu kwa jinsi kilivyo ‘nondo’ jambo linalomfanya Machallo afanikiwe kuuza nakala nyingi ndani ya majuma machache. Mauzo yanapelekea akaunti yake ya benki kuanza ‘inapumua’ baada ya kutengeneza na kuendelea kutengeneza kiasi kikubwa cha pesa kutokana na ujasiriamali huo. Kwakuwa pesa ipo sasa, anatafuta nyumba yenye nafasi na kuondoka kwenye chumba kimoja allichokuwa amepanga. Maisha yake yanabadilika kiuchumi, japo bado anatafuta wigo wa soko la kubwa zaidi la kitabu chake ili kiuzwe katika mikoa yote Tanzania jambo litalomletea manufaa makubwa zaidi. Kwa mafanikio aliyopata anawakumbuka ndugu zake kwa kuwalipia ada wanaosoma, kumwongezea mama yake pesa kwa ajili ya kulima shamba pamoja na mambo mengine ya msingi.
Wakati akiendelea na mambo hayo yote, bado suala lake la kujipanga kuhakikisha chuo kikifunguliwa hafanyi makosa lilikuwa endelevu. Awamu hii anadhamiria lazima awe na mahusiano ya kimapenzi na mwanadada Flaviana jambo litalomfanya apate nafasi ya kuonekana katika mitandao mbalimbali inayotembelewa na watu duniani kote, pia vituo vya redio, televisheni hata magazeti jambo ambalo lingempa umaarufu wa kufumba na kufumbua.
Anajihahidi kuangalia filamu, kusoma vitabu mbalimbali pamoja na kutembelea mitandao mbalimbali ya intaneti ili kupata uelewa na maarifa ya kutosha na mbinu zitakazofanikisha mpango wake. Anajikuta anatokea kuipenda filamu inayoitwa ‘love doesn’t cost a thing’. Anagundua muhusika katika filamu ile alikuwa na shauku ya kuwa maarufu akaona jinsi alivyofanya akafanikiwa kujizolea umaarufu, jambo lililompa moyo na kumfanya aamini kuwa anaweza bila kujali changamoto na misukosuko atayokumbana nayo.
Anakuja mdogo wake wa mwisho wa kiume anayeitwa Babuu toka nyumbani kwao kuishi naye hapo jijini Mwanza wakati akitafuta fursa ya ajira, kwani alikuwa amemaliza kidato cha nne na kusomea kozi inayohusiana na ‘graphics designing’, uandaaji wa picha za video pamoja na ufundi wa kompyuta.
Machallo anadhamiria kununua gari la kutembelea. Jambo ambalo aliamini lingemfanya awe tabaka la juu, japo hakuwa na uhakika sana kama angeweze kulijaza mafuta na kuhakikisha analifanyia matengenezo siku za mbeleni. Anaamua kumshirikisha mdogo wake wazo hilo, Babuu anaona ni jambo zuri ila alishauri kuwa lingekuwa jambo zuri zaidi endapo kiasi hicho cha pesa kingewekezwa katika biashara ambayo ingeingiza faida kuliko gari kwa wakati ule ambalo llingehitaji gharama nyingi za mafuta na matengenezo.
‘Unafikiri tunaweza kufanya biashara gani nzuri hapa mjini?’ anauliza Machallo. Babuu amshauri afungue ofisi itayohusika na kutoa huduma ambazo amezisomea jambo litalompa fursa ya ajira badala ya kukaa tu pale kwa kaka yake.
Machallo anaona ni jambo jema, japo anatamani sana kumiliki gari. Anakubaliana na wazo la mdogo wake na kuamua kufungua ofisi maeneo ya Malimbe~Nyegezi, jirani na chuo cha Mt. Agustino anakosoma.
Ofisi inaendelea vizuri, pesa ya kuendeshea maisha inapatikana bila wasiwasi. Babuu anajituma sana na kuonesha uaminifu mkubwa, jambo linamfanya Machallo azidi kumpenda na kumwamini sana mdogo wake. Anaamua kumweleza mambo yake mengi bila kuacha kumweleza shauku yake kumpata Flaviana.
Likizo imeisha, chuo tayari kimefunguliwa. Ni nafasi nzuri sasa kwa Machallo kuanza zoezi lake la kumpata Flaviana. Anadhamiria kumuwinda kwa nguvu ili kuhakikisha anapata nafasi ya kumweleza hisia zake.
Siku hazigandi, ila ugumu wa kumpata Flaviana unazidi kwani Flaviana yuko ‘busy’ sana semista hii kuliko iliyopita. Mara kadhaa aidha baada ya Machallo kumvizia Flaviana anapotoka katika mhadhara, maktaba au anapotoka sehemu moja kwenda nyingine huomba nafasi kumtaka Flaviana ampe nafasi dakika chache ili amwambie jambo lakini mara zote Flaviana amekuwa akimwambia kuwa hana muda kwa wakati ule.
Masomo yanazidi kushika kasi kiasi cha kumfanya Machallo akose nafasi. Ndoto yake inakuwa mbali sana kiasi cha kujiona anakosa kutimiza `dhamira yake maishani.
Inafika siku ya Jumapili, Machallo anakutana na Flaviana ‘super~market’ kubwa na maarufu sana jijini Mwanza iliyoko jirani na kipitashoto chenye sanamu ya samaki. Hii imetokea kama bahati kwa Machallo, ambaye amesubiri pale kwa takribani saa tatu tangu alipofika maeneo ya jirani na eneo la tukio tangu saa tatu asubuhi. Alifahamu ratiba, katika siku za jumapili mrembo huyo hufika pale kununua mahitaji yake.
Wakati akiwa mle ndani akinunua mahitaji, Machallo anamsogelea huku akitabasamu. ‘Mambo mrembo?’ anatoa salamu Machallo. Flaviana anaitikia ile salamu kwa uchangamfu huku akitaja jina la Machallo kwa ufasaha. Anashangaa kidogo kuwa mrembo alikuwa akimkumbuka jina. ‘nakumbuka tulionana……. Wapi vile? Anajaribu kukumbuka bila mafanikio, anaamua kuuliza. Bila kuchelewa Machallo anajibu kwa kujiamini ‘Chuo, St. Augustine. Tulikutana kwa mara ya kwanza canteen tukala chakula pamoja, ulikuwa na rafiki yako Lightness’. Flaviana anakumbushwa.
‘nambie… za siku?’ anauliza Flaviana. ‘njema’ anajibu Machallo, anaendelea kumweleza kuwa amekuwa akihitaji fursa ya kuongea naye kwa muda mrefu ila Flaviana amekuwa ‘busy’ sana kiasi cha kumfanya akose nafasi hiyo.
Flaviana anafafanua kuwa amekuwa na mambo mengi sana tangu miezi kadhaa iliyopita, kuna mambo mengi anayofanya huku akiendelea na masomo kwa wakati mmoja jambo linalomfanya awe bize kiasi kile.
Machallo anaamua kupiga moyo konde na kueleza lililoko moyoni mwake bila kumung’unya maneno kwani alijua ile ni nafasi adhimu ambayo ameipata kwa bahati wala isingeweza kujirudia.
‘Sina sababu ya kuficha mambo wala kuishi na maumivu moyoni mwangu. Napenda niweke bayana jambo ambalo limekuwa likinitesa kwa muda mrefu sasa’ Anamweleza Flaviana. ‘Eleza nakusikiliza’ ni sauti ya Flaviana baada ya kuona ukimya kidogo.
************ :: Machallo atafanikiwa kusema ya moyoni?? vipi kuhusiana na Flaviana atakubaliana kweli na machalo?? nini hatma ya Machalo katika simulizi hii??
Napenda niweke bayana jambo ambalo limekuwa likinitesa kwa muda mrefu sasa’ Anamweleza Flaviana. ‘Eleza nakusikiliza’ ni sauti ya Flaviana baada ya kuona ukimya kidogo.
Songa nayo sasa…
‘Nimekuwa nikifikiria kuwa na mpenzi mwenye sifa na vigezo stahiki ninazohitaji nikagundua kuwa wewe ndiye mwanamke wa pekee ambaye unakidhi vigezo hivyo. Naomba nafasi ndani ya moyo wako nikuoneshe penzi la dhati nililonalo’ anaongea Machallo kwa hisia kali huku akimwangalia Flaviana machoni. Flaviana anabaki kimya, akiwa anayaangalia macho ya Machallo ambayo yanamshuhudia mateso anayoyapata Machallo kumkosa mtu muhimu maishani mwake.
Machallo anaendelea kumweleza Flaviana kuwa, lengo lake sio kumchezea wala kumpotezea muda. ‘napenda tujenge penzi bora, tuwe vielelezo ili ulimwengu ushuhudie tukio hili takatifu ambalo litaleta amani, furaha na upendo mioyoni mwetu kwa kipindi chote kiliichobaki cha maisha yetu pindi tutakapokuwa pamoja’ anahitimisha Machallo.
‘Nimekuelewa Machallo. Naheshimu sana hisia zako, napenda nikueleze ukweli ambao utakuweka huru. Tayari nina mpenzi, nampenda sio taratibu na tayari nimeshampa roho yangu, ninaishi ndani yake naye anaishi ndani yangu hivyo nafasi ni moja, wala sina nyingine’. Anaeleza Flaviana huku akiendelea na zoezi la kuchagua mahitaji.
Kauli ile inaupasua moyo wa Machallo, anajiona ‘amepoteza’. Japo anajifariji kuwa ana nafasi ya mwisho kujaribu bahati yake. Anambembeleza Flaviana ampe nafasi moyoni mwake, jitihada zinazogonga mwamba kwa kukutana na msimamo wa Flaviana asiyetaka kuyumbishwa katika penzi lake kwa mtu anayempenda.
‘Naomba nafasi niwe rafiki yako, unijue mimi ni mtu wa namna gani na nia yangu kwako. Pengine inaweza kusaidia kubadili maamuzi na kukusaidia kukupeleka katika chaguo bora zaidi’. Anasema Machallo zikiwa ni jitihada zake za mwisho.
Ombi lake linasubirishwa, kwani Flaviana ameshaanza maongezi, akiwasiliana na mtu kwa simu huku zoezi lake la kuchagua mahitaji likiendelea. Alikuwa akichagua mahitaji kwa mkono mmoja huku mwingine umeshika simu aliyoweka sikioni huku kuwasiliana na mtu. Mahitaji aliyohitaji alikuwa akiweka katika kitoroli ambacho Machallo alijikuta akimsaidia kukisukuma huku akimfuata kule anakoelekea kama ‘bodu gurd’. Flaviana anamaliza kuchagua mahitaji , anaelekea sehemu ya kufanya malipo iliyoko jirani na mlango wa kutokea huku machallo akimfuata nyuma na toroli lenye mahitaji aliyochukua.
Flaviana anatoa kadi na kuichanja katika mashine maalumu iliyopo pale ili kufanya malipo kisha anapewa risiti. Baada ya kukamilisha, anatoka nje kuelekea kwenye gari alilopaki nje ya ‘supermarket’ wakati mtu maalumu kwa kusaidia wateja kubeba mizigo anampokea Machallo toroli, anaipanga mizigo vizuri katika boksi na kuipeleka kwenye gari, Flaviana anafungua ‘buti’ yule kaka anauweka mzigo kwenye buti kisha anafunga ule mlango wa buti.
Wakati huo Machallo amesimama hapo pembeni akishuhudia kinachoendelea huku shauku yake kubwa ikiwa ni kuona Flaviana anamaliza kuongea kwa simu ili asikie jibu la ombi lake. Anahamaki na kubaki mdomo wazi pale anaposhuhudia Flaviana anaingia kwenye gari, na kumpungia mkono ishara ya kumwambia kwaheri kisha anawasha gari na kuendesha akiwa ameshika usukani kwa mkono mmoja wakati mkono mwingine ukiwa umeshika simu ambayo ilikuwa bado iko sikioni akiendelea na mazungumzo na mtu.
Maumivu makali ya moyo yanamtesa Machallo, anaamua kuondoka pale kuelekea katika kituo zinapopaki bodaboda. Anakodi kupelekwa nyumbani, akiwa mnyonge mwenye mawazo mengi. Anaona tayari ndoto yake imekufa, wala hana nafasi tena ya kuishi aina ya maisha ya ndoto yake ambayo imejengeka akilini mwake kwa muda mrefu. Anapatwa wazo, afikirie namna nyingine inayoweza kumpa umaarufu.
Siku zinaenda bado jawabu halijapatikana. Mitihani nayo inaanza, anakuwa bize na masomo na kushindwa kujua njia sahihi atayomfanya akamilishe ndoto yake kwa wakati ule.
Ni semista ya pili katika ule mwaka wa pili wa masomo pale chuo. Ofisi ya Machallo inazidi kupata umaarufu kwa kazi nzuri zinazofanyika. Wanachuo, wahadhiri na watu wengine hupenda kupeleka kazi zao pale ofisini ili zifanyike. Kazi zilifanywa kwa uaminifu na kwa wakati uliopangwa bila usumbufu.
Inafika siku ya ijumaa, mida ya mchana, Babuu yuko bize sana pale ofisini. Anakuja mteja, mwanadada, anatoa compyuta mpakato yake na kuelezea tatizo ili irekebishwe.
Babuu anatoa daftari maalumu kwa ajili ya wateja ambao huandika taarifa zao wanapoleta kazi zifanywe pale ofisini. Anamaliza na kumweleza kiasi cha pesa ambacho atalipia, yule dada analipa kiasi kile cha pesa na kuuliza muda ambao kazi itakuwa imekamilika. ‘Uje kesho mida ya saa nne asubuhi itakuwa tayari’ anamjibu Babuu.
Dada anaondoka zake, Babuu anaendelea na kazi aliyokuwa anaifanya. Baada ya kumaliza ile kazi aliyokuwa akiifanya anagundua tayari muda ulikuwa umeenda sana zikiwa zimebaki dakika chache ufike muda wa kufunga ofisi hivyo anaamua kuondoka na ile kompyuta aliyoleta yule dada ili akifika nyumbani apate nafasi ya kuifanyia matengenezo.
Muda wa kufunga unafika, anafunga na kuondoka. Anafika nyumbani, baada ya kupumzika na kupata chakula cha usiku anaamua kuianza kazi ya kuitengeneza ile kompyuta ya mteja ili siku inayofuata apate nafasi ya kufanya kazi zingine na pindi yule dada akifika akute iko tayari kwa wakati waliokubaliana.
Anaifungua ile kompyuta na kuiwasha. Anaona picha ya Flaviana mwanadada ambaye anausumbua sana moyo wa kaka yake. Anafungua mafaili yaliyomo mle ndani anaona yanamhusu Flaviana. Anakuta picha za Flaviana pamoja na mambo mengi yanayomhusu mwanadada huyo.
‘Hii laptop itakuwa ya Flaviana bila shaka’ anajisemea. Kabla hajaanza zoezi la kuitengeneza ile kompyuta, anamwita kaka yake ambaye yuko chumbani kisha anamweleza kuwa anahisi ile kompyuta ni mali ya Flaviana kutokana na mambo aliyoyaona mule ndani yanamuhusu Flaviana. Machallo anaangalia ili kujiridhisha kama anachoambiwa kina ukweli au Babuu ameamua kumtania kwa kujua anampenda Flaviana. Anagundua kuwa ni kweli, ile kompyuta itakuwa mali ya mwanadada huyo bila shaka.
Anaona mambo mengi yanayomhusu Flaviana na maisha yake kwa ujumla, familia, chuo, Marafiki pamoja na tasnia za Mitindo, filamu na urembo. Anaziona filamu anazozipenda Flaviana ambazo amezihifadhi pamoja na zile alizowahi kuigiza. Anachukua ‘external hard disk’ yake na kuhamishia baadhi ya vitu toka katika kompyuta ya Flaviana. Zoezi linakamilika kisha anachukua ‘moderm’ na kutumia kompyuta ya Flaviana kuingia kwenye huduma ya mtandao wa intaneti.
Anaona orodha ya wavuti mbalimbali alizotembelea Flaviana. Anafungua sehemu ya barua pepe na kugundua ilikuwa iko wazi. Anasoma barua pepe za Flaviana, anasoma barua pepe ambazo ametuma mpenzi wake Flaviana pamoja na picha. Katika kuendelea kupekua, anaiona barua pepe ambayo alimtumia Flaviana kama majuma mawili yaliyopita.
Wakati akiendelea kusoma barua pepe moja baada ya nyingine, anakutana na barua pepe inayomfanya ashindwe kuzuia hisia zake. ‘Enheeee….!!!’ Anaonesha kufurahishwa na kile anachokiona. Anachukua kalamu na karatasi kisha ananakiri kitu toka katika ile barua pepe anayosoma. ‘nini hicho kaka?’ anauliza Babuu kwa shauku ya kutaka kujua. Machallo anamweleza kuwa ameliona neno la siri la wavuti ya Flaviana toka kwenye ile barua pepe, lililotumwa wakati Flaviana alipokuwa akibadili neno la siri.
Machallo anamweleza Babuu kuwa, amedhamiria kumpata Flaviana. Hivyo alipanga atumie kila njia ili ampate kwakuwa jitihada nyingi zilifanyika bila kuzaa matunda, aliona ile ni fursa nyingine ambayo inaweza kuleta matokeo chanya kama akiitumia kikamilifu. Anamshauri mdogo wake amsaidie ili atume ‘post’ kwenye wavuti ya Flaviana kuelezea kuwa wao ni wapenzi. Babuu anashauri bora wabadili neno la siri ili Flaviana asiweze kuingia tena katika ile wavuti. Babuu anaingia katika wavuti, anaenda sehemu ya kubadili neno la siri, anaweka neno la siri la awali kisha anaweka neno la siri jipya na kuthibitisha. Neno la siri linatumwa katika anwani ya barua pepe ya Flaviana. Anafungua kisha anaifuta hiyo barua pepe yenye neno jipya la siri katika kikasha cha ujumbe ili Flaviana asiweze kuisoma na kulipata neno la siri jipya.
************
Machallo anamwambia mdogo wake achukue picha ya Flaviana katika kompyuta ya Flaviana aunganishe na picha yake (Machallo) kwenye kompyuta yake kwa kutumia majo ya ‘program’ ya kompyuta mahususi kwa ajili ya kazi hiyo ili ionekane kama wamepiga hiyo picha pamoja. Babuu anafanya zoezi hilo huku Machallo anabuni maneno ya kuandika watakayoyatuma kwenye wavuti hiyo. Baada ya muda mfupi Babuu anamaliza kazi wakati ambao Machallo anamaliza kazi yake pia.
Machallo anachukua kompyuta mpakato yake, anahakikisha ile picha imehifadhiwa tayari kwenye kompyuta hiyo kisha anaingia nayo chumbani wakati akimwacha Babuu akianza zoezi la kuitengeneza kompyuta ya Flaviana. Machallo anafika chumbani na kukaa kitandani huku akiiweka kompyuta yake tayari kwa zoezi lake. Anaingia katika mtandao wa intaneti, anaingia kwenye wavuti ya Flaviana na kuiweka ile picha na yale maneno aliyobuni.
Anajua sasa adhma yake inaenda kutimia kufuatia tukio hilo litakaloleta taswira mpya katika maisha yake. Anamaliza kutuma kisha anayapitia yale maneno aliyobuni na kuyaweka katika mtandao kwa mara nyingine;
“Halloo Dunia.., Leo nafungua ukurasa mpya ambao unaleta taswira mpya katika maisha yangu.
Napenda kuweka wazi tukio hili maalumu ambalo linagusa maisha yangu na kuyafanya yawe na maana sana kwa wakati huu kuliko kipindi kingine chochote cha maisha yangu.
Namtambulisha kwenu Machallo Mussa (niliyepiga naye picha hapo juu) kuwa ndiye chaguo la moyo wangu. Ni tukio ambalo pengine, linaweza kuchukuliwa kwa hisia tofauti ila ninachojua kwa sasa, kuna kitu special ninachopata toka kwake ambacho sitarajii kukikosa katika kipindi chchote cha maisha yangu.
Najiona nimekamilika sasa, maisha yamekuwa na maana zaidi ya vile ninavyoweza kueleza. Naahidi kumpenda leo, kesho na hata milele.
Mwenyezi Mungu bariki PENZI hili linalomea katika mioyo yenye rutuba”.
Ni usiku wa manane, macho ya Machallo ni makavu. Hana hata chembe ya usingizi, anawaza jinsi tukio hili litakavyo leta taswira mpya. Anawaza umaarufu ambao unaenda kupatikana kupitia njia ya panya aliyoigundua ili azima yake ipate kutimia. Tafakuli zinafikia ukingoni pale anapoianza ku~abiri kuelekea katika bandari ya asubuhi njema.
Asubuhi kunapambazuka, siku mpya ya jumamosi. Babuu anakuwa wakwanza kuamka kabla ya Machallo, anaanza kufanya maandalizi kuelekea kazini zoezi linaloendelea hadi majira ya saa mbili asubuhi. Machallo bado amelala, Babuu anaamua kumwamsha ili amuage tayari kwa kuondoka. Baada ya Babuu kumuaga Kaka yake anaamua kuondoka kuelekea kazini aweze kufungua ofisi tayari kuanza kazi huku nyuma akiwa amemuacha Machallo bado anaendelea kulala kutokana na usingizi mwingi. Simu ya Machallo inaita mara kadhaa lakini kutokana na usingizi alionao anashindwa kuisikia.
Ni majira ya saa nne na dakika ishirini na mbili asubuhi, Machallo anaamka, anajinyoosha na kufikicha macho yake huku anapiga miayo!. Anatandika kitanda na kwenda ‘uani’ kupunguza maji mwilini. Baada ya muda mfupi anarudi chumbani. Anaanza kufanya usafi wa jumla kama ilivyo desturi yake katika siku za jumamosi. Mara simu yake inaita, kuangalia ni namba ya Babuu. ‘Nambie dogo’ anaiipokea ile simu, na kuelezwa kuwa afungue redio Vibes Fm kuna habari inarushwa hewani mida ile ataisikia. Anafungua redio na kukuta habari inaisha. Anagundua ni habari ya mahusiano yake na Flaviana aliyoandika kwenye mtandao. Anafungua kituo kingine maaruufu kinachorusha matangazo yake toka jijini Mwanza na kusikika Tanzania pamoja na nchi jirani. Kipindi ni dondoo za magazeti na Mitandao. Anasikia muhtasari wa habari zitakazosomwa, miongoni mwa habari hizo anasikia habari ya Flaviana kufunguka juu ya mahusiano yake na mpenzi wake wa sasa, aliyoituma katika wavuti yake.
Habari ile inamdhihirishia Machallo kuwa amefanya kazi nzuri ambayo itakamilisha kusudi lake kubwa la kuwa mtu maarufu kwa kupata nafasi kuandikwa katika mitandao na kuonekana katika televisheni pamoja na vyombo vingine vya habari.
Anafungua mtandao wa facebook kupiitia simu yake ya mkononi ambako aliweka ile picha yake akiwa na Flaviana katika ukurasa wake na kuandika maneno yanayoonesha kuwa wawili hao ni wapenzi. Anakuta ‘comments’ nyingi pamoja na ‘likes’ pia wengine wame ‘share’. Ni habari ambayo imegusa sana hisia za watu, kila mmoja alisema alilojisikia kusema.
Wakati akifanya zoezi la kufungua intaneti alikuwa akiendelea kuitegea sikio ile habari iliyokuwa ikitangazwa redioni. Mtangazaji akabainisha kuwa amejaribu kupiga simu ya Flaviana ili aweze kufanya naye mahojianao kidogo kwa njia ya simu aelezee kuhusiana na tukio hilo bila kupokelewa. Habari anaisha, anaendelea na shughuli za usafi ambazo alikuwa amekatisha kwa muda wakati akisikiliza ile habari.
Ikiwa ni mida ya saa sita mchana Babuu akiwa ofisini akiendelea na kazi, anafika yule dada aliyeacha kompyuta yake siku iliyopita. ‘kaka mambo?’ anamsalimia Babuu. ‘poa dada, mzima? Anajibu Babuu na kutaka kumjulia hali. ‘sijambo’ anaitikia yule dada. Babuu anaitoa ile kompyuta kisha anampa yule dada, ambaye anaikagua na kugundua imesha tengemaa. Anairudishia katika begi kisha anaanza kuondoka ‘asante’ anashukuru huku akiondoka. ‘karibu tena’ anajibu Babuu.
Yule dada anaingia katika gari yake aliyokuwa amepaki pale pembeni, anachukua simu yake ya kiganjani na kubofya akitafuta namba ya simu ya rafiki yake Flaviana. Anaipata na kupiga ambapo simu inaita bila kupokelewa.
Anaamua kwenda nyumbani kwake ambako anaamini atamkuta. Anaendesha gari kwa muda wa robo saa tayari anafika nyumbani kwa Flaviana.` ‘Wooow! Lightness…karibu mpenzi’ ni sauti ya Flaviana akimkaribisha rafiki yake ndani. ‘yaelekea umetoka kuamka muda simrefu’ anauliza Lightness. ‘jana nilichelewa kulala baada ya kutoka kushoot ile movie, nikaanza kuangalia movie mpya iliyotoka’. Anajibu Flaviana. Lightness anamkabidhi rafiki yake ile kompyuta. ‘asante mwaya’ nataka niingie kwenye mtandao ili nipost trailer ya filamu mpya iliyotoka’ ni maneno ya Flaviana akimwambia Lightness.
Wanaendelea na mazungumzo, baada ya muda mfupi simu ya Lightness inaita. Ni dada yake amempigia akimtaka arudi nyumbani mara moja kuna dharula imejitokeza bila kumwambia suala lenyewe. Anamuaga Lightness na kumuahidi atarudi baadaye akipata nafasi.
Wakati yuko kwenye gari kuelekea nyumbani, simu yake inaita. Ni Bosco, mpenzi wake Flaviana. ‘hallo shem’ anaitikia Lightness. ‘mbona Flaviana hapokei simu yangu?’ anauliza Bosco kwa ukali. Lightness anahisi kitendo cha kutokupokea simu alichokifanya Flaviana kimemkwaza Bosco, japo anajua kuwa Flaviana hawezi kuacha kupokea simu ya kipenzi chake. Anamwambia huenda Flaviana alikuwa bafuni anaoga wakati Bosco akimpigia simu, sababu ambayo haimwingii akilini Bosco. ‘Wewe na huyo msaliti mwenzio lenu moja’ anafoka Bosco. ‘Mbona sikuelewi shem?’ anauliza Lightness kwa mshangao. ‘sawa jifanye hunielewi, ila mwambie huyo shetani wa kike nashukuru sana kwa alichonifanyia’ anahitimisha Bosco na kukata simu.
Lightness anajiuliza maswali mengi bila majibu. Anashangaa shemeji yake kumtolea maneno makali vile bila kuelewa sababu. Furaha inakwenda likizo, anajikuta mwenya huzuni mithili ya mtu ‘aliyetendwa’.
Anafika nyumbani. ‘una tatizo gani mamii?’ Anauliza Zawadi, dada yake Lightness alipomwona Laghtness anaingia sebuleni akiwa hana furaha. Lightness anakuwa kimya huku akipitiliza chumbani kwake. Zawadi anahisi huenda kitendo cha kumwita Lightness arudi nyumbani wakati akiwa na mambo yake kimemkwaza. Anaamua kumuacha kwa muda ili baadaye kidogo aende kuongea naye, kwani anampenda sana mdogo wake na hapendi kumkwaza wala kumwona akiwa katika hali ya huzuni. Alipenda kumfanya mdogo wake mwenye furaha na amani muda wote kwani amemlea tangu mdogo tangu wazazi wao walipofariki.
Lightness anafika chumbani na kujitupa kitandani huku ana msongo wa mawazo. Anaamua kumpigia simu rafiki yake Flaviana ili amuulize kama kuna tatizo kati yake na Bosco na amwambie kile kilichojiri, jambo linalokwama baada ya simu ya Flaviana kutopokelewa. Wakati akitafakari, simu yake inaita. Anaangalia namba inaonekana ni namba asiyoifahamu. Anapokea na kusikia sauti ya mtu aliyejitambulisha kwa jina la Madadi akijitambulisha kuwa ni mwandishi wa habari katika gazeti la kila siku la ‘mwanahabari; akimtaka kufahamu kuhusiana na tukio jipya linaloendelea la mahusiano mapya kati ya rafiki yake Kipenzi Flaviana na mpenzi wake wa sasa. ‘sielewi unachoniuliza’ anajibu Lightness kwa jazba huku akikata simu.
Zawadi anaingia chumbani kwa Lightness, anamkuta akiwa bado katika hali ya huzuni. ‘Naomba unisamehe mdogo wangu, sikujua kama nIngekukwaza kukuita wakati una mambo yako ya msingi’ ni maneno ya Zawadi akiomba radhi kwa mdogo wake huku akipaza sauti ya upole. ‘Hapana dada, siyo hilo. Kuna jambo jingine…’ anajibu Lightness. ‘lipi hilo?’ anauliza Zawadi akitaka kujua. Lightness anamweleza dada yake jinsi alivyoambiwa maneno ya utata toka kwa Bosco akimshutumu kwa mambo asiyoyajua. ‘Kwani hujuwi chochote kuhusiana na suala la usaliti alioufanya rafiki yako kwa Bosco?’ anauliza Zawadi . ‘Sijuwi, ila sidhani kama kuna jambo Flaviana anaweza kunificha’ anafafanua Lightness.
Zawadi anamfungulia Lightness wavuti, anaangalia na kusoma zile habari ambazo zinamshitua Lightness. ‘Mbona Flaviana hajawahi kunidokeza kuhusiana na suala hili?’ anauliza Lightness kwa mshangao. Zawadi anamuuliza Lightness kama anamfahamu huyo mpenzi mpya wa Flaviana, anakiri kuwa hadhani kama alishawahi hata kumwona. Kutokana na kumbukumbu kufutika kama alishawahi kukutana naye, kwani kwa kawaida hukutana na watu wengi sana hivyo inamuwia vigumu kuwakumbuka wote.
Hali ya sitofahamu inaendelea kumkumba Lightness ambaye anashindwa kuelewa kwanini rafiki yake amekuwa msiri kwake kiasi kile kwa jambo lile wakati huwa wanawekana wazi kwa kila kitu. Flaviana anafungua tovuti yake, anakutana na kitu kipya ambacho kimepokelewa kwa ‘comments’ nyingi kuliko kitu chochote alichowahi kuandika tangu afungue tovuti ile.
Anaisoma ile habari na kujikuta akipiga mayowe bila kujizuia asiamini kile anachoona katika mtandao wake. Anaangalia simu yake pale alipokaa anaikosa, anaangalia kabatini bila mafanikio. Anachukua mkoba wake kuangalia, anaiona. Anaona ‘missed calls’ nyingi pamoja na ujumbe mfupi wa maneno. Anaamua kumpigia simu Lightness kwanza kabla hajaangalia missed calls na kusoma ujumbe mfupi wa maneno. Simu ya Lightness inaita bila kupokelewa kwani alikuwa ameingia ‘uani’ hivyo simu aliiacha kitandani pale chumbani.
‘Anajua upuuzi alioufanya ndiyo maana hataki kupokea simu yangu, atanitambua leo’. Anajisemea Flaviana huku akikaa kwa ajili ya kuingia kwenye mtandao kwa ajili ya kufanya jitihada za kufuta ile habari ambayo anaona sio kwamba imemfedhehesha tu, bali imemchafua vilivyo. Anaingiza neno la siri, anaona ujumbe ukieleza kuwa amekosea neno la siri. Anaamua kuingiza neno la siri kwa mara nyingine, matokeo anayopata ni yaleyale jambo linalomshangaza na kumfanya asielewe kile kinachoendelea. Anaamua kuingiza neno la siri alilokuwa akitumia awali kabla hajabadilisha lakini bado anagonga mwamba. Anagundua kuwa kuna mchezo mchafu uliofanywa na rafiki yake Lightness.
Hasira na chuki juu ya Lightness vinampanda Flaviana kiasi cha kulia mithili ya mfiwa. Anaamua kumfuata Lightness nyumbani kwao ili amtambue! Kwani anadhamiria kupambana naye iwe kwa heri ama shari kutokana na kile anachojua ni ubazazi aliofanyiwa na rafiki yake Lightness ambaye tayari amegeuka kuwa adui.
************ :: Machallo atafanyaje kukabiliana na mchezo aliokwishaufanya?? nini hatma yake baada ya kutafuta umaarufu kwa njia ya mkato?? Atajulikana kama yeye ndio aliofanya hivyo??
Anaamua kumfuata Lightness nyumbani kwao ili amtambue! Kwani anadhamiria kupambana naye iwe kwa heri ama shari kutokana na kile anachojua ni ubazazi aliofanyiwa na rafiki yake Lightness ambaye tayari amegeuka kuwa adui. CHANZO: Songa nayo sasa…
Anatoka chumbani ili aondoke kwenda kwa adui yake. Anapofika sebuleni anakutana na sura ya Lightness ambaye anaingia sebuleni kwa rafiki yake akiwa na shauku ya kutaka kujua kile kinachoendelea ambacho anashindwa kuelewa kwanini rafiki yake kipenzi ambaye wameshibana ameamua kumficha mahusiano mapya jambo lililosababisha kupokea lawama toka kwa shemeji yake Bosco. Flaviana anashindwa kuzitawala hisia zake na kijikuta akimpokea Lightness kwa matusi na maneno makali ya kuumiza. Lightness anaduwaa bila kujua rafiki yake amepandwa na pepo wa aina gani!.
‘Mnafiki mkubwa we, unajifanya rafiki kumbe ‘snichi’. Leo utanitambua nakwambia’. Yalikuwa ni maneno ya Flaviana huku akiwa na hasira kama simba jike aliyejeruhiwa, anamfuata Lightness ‘amvagae’ kitendo kinachomfanya Lightness amuulize swahiba yake amepandwa na wazimu gani.
Ugomvi mkubwa sana unazuka pale ndani huku matusi yakimfyatuka Flaviana bila kizuizi. Lightness anashushiwa kichapo kikali kinachomfanya aanze kulia huku akipiga mayowe kuomba msaada. Kipigo kinazidi, Lightness anashindwa kujizuia hivyo anaamua kutoka ‘nduki’ ili aepuke makonde mazito toka kwa bondia mpya wa uzito wa juu mwenye hasira za mbogo.
Flaviana anammkimbiza Lightness ili ahakikishe anamshikisha adabu hadi amkome. Lightness hakumbuki kama alikuja na gari ila anachoona ni njia ya uchochoro yenye kona nyingi.
Wakati riadha ile ya mbiyo ndefu ikiendelea, breki ya matusi kinywani mwa Flaviana ilikuwa imekatika, hivyo maneno yalitoka bila ‘gonga’. Tukio lile linashuhudiwa ‘laivu’ bila chenga na majirani pamoja na wapita njia ambao wanalipokea kwa hisia tofauti. Wengine wanaamua kuacha shughuli zao na kufuatilia mkasa huo ili waone mkanda mzima.
Vita vile vya panzi ikawa sherehe kwa kunguru. Waandishi wa habari nao tayari wameshaanza kufanya yao bila makosa wakifuatilia na kuona jinsi jitihada za Flaviana kumtia mikononi adui yake zikikwama pale anapoteleza na kuangukia katika kidimbwi kidogo cha maji machafu. Flaviana anainuka kwa haraka na kukuta tayari adui yake alishatokomea.
Kuangaza anakutana na umati wa watu wakishuhudia igizo hilo ambalo unaweza kuliita ‘komedi’ lakini utakuwa hujakosea kama ukiliita ‘tragedy’. Wakati huo wengine walijua Flaviana yuko kazini katika tasnia yake ya filamu, wakati wengine wakijua lile sio igizo bali ni shughuli pevu.
Flaviana anajisikia vibaya kuuona umati wote ule ukimshuhudia kile anachofanya. Anaamua kuangaza huku na kule kama anaweza kuona ‘taxi’ ili apande kuepuka kuzongwa na mapaparazi pamoja na mashuhuda kibao jambo linalogonga mwamba kwani hakuna taxi maeneo yale. Anaamua kupanda bodaboda iliyokuwa jirani na kumuamuru dereva ampeleke kwake. Bila kupoteza muda dereva anaendesha kwa mwendo wa kasi hadi nyumbani kwa Flaviana huku akiacha watu wakimsindikiza kwa macho hadi anatokomea.
Flaviana anafika kwake, anaingia ndani huku akihema kwa nguvu. Anapitiliza moja kwa moja chumbani ambapo anasimama mbele ya kioo. Anashangaa kuona jinsi ‘make~up’ ya tope ilivyokolea wakati akifanya zile ”aksheni’. Mbaya zaidi anagundua kuwa ‘kisketi’ chake kifupi alichokuwa amevaa kimechanika vibaya kiasi cha ‘kufuli’ kuonekana wazi~wazi. Anagundua kuwa amefanya kituko ambacho kimeharibu taswira ya maisha yake na kuleta tafsiri mbaya ambayo haitafutika akilini mwa watu. Anatamani angekuwa na uwezo wa kurudisha nyuma gurudumu la wakati ili asahihishe makosa aliyofanya, lakini anagundua kuwa hana nafasi hiyo.
Anaamua kwenda bafuni kuoga, kisha anarudi chumbani. Anachukua simu yake ya mkononi na kupanda kitandani. Anafungua sehemu ya ujumbe mfupi wa maneno, anakutana na ujumbe toka kwa Bosco akimweleza kuwa anashukuru kwa maamuzi mapya aliyoamua kufanya, ya kuanzisha mahusiano na mwanaume mwingine. Anamtakia kila la kheri katika mahusiano yake mapya. Ujumbe ule unamuumiza sana moyo Flaviana kiasi cha kuanza kulia kwa huzuni huku akimpigia simu Bosco amweleze ukweli jambo linalokwama baada ya kupiga simu ya Bosco mara kadhaa bila kupokelewa. Mara simu yake inaita, anaangalia kutaka kujua kama ni Bosco ndiyo anapiga ile simu, kuangalia ile simu anaona ni namba asiyoifahamu. Anaacha kupokea kutokana na kutokuwa na furaha.
Mawazo yanamwelemea kiasi cha kujikuta anapata maumivu makali ya kichwa. Anaangalia mahali ambapo huwa anaweka dawa, anachukua dawa za kutuliza maumivu na kumeza kisha anapanda kitandani ajaribu kama anaweza kubahatisha kupitiwa na usingilizi atulize akiili yake iliyovurugika. Licha ya kuhangaika kwa muda mrefu, usingizi unagoma jambo linalomkwaza mwanadada huyo na kusababisha atamani …kuleeewa…kuleeewaaa ili apunguze mawazo ila anaogopa kwani hajawahi kutumia pombe aina yoyote katika maisha yake. Anafikiria pia anaweza kunywa pombe na kulewa halafu akajikuta analeta ‘majanga’ yanayoweza kuongeza tatizo badala ya kuleta suluhu.
Anaangalia saa yake kubwa ya ukutani iliyoko pale chumbani ili kujua muda. Saa inamuonesha ni saa kumi na mbili na dakika tano jioni. Anakumbuka kuwa hakula chochote zaidi ya kifungua kinywa alichopata asubuhi, japo hajisikii njaa wala hana hamu ya kula kitu chochote zaidi ya kuhisi kiu ya maji inayomfanya aamke kuyafuata maji ya kunywa yalipo na kuikata kiu yake na kurudi pale kitandani. Anawaza jinsi atakavyoweza kuipata faraja katika wakati ule ambao aliihitaji kuliko wakati mwingine wowote. Anaamua kuwasha redio na kuweka nyimbo ‘laini’ zinazomfanya aanze kumkumbuka mpenzi wake Bosco ambaye amekuwa mtu muhimu sana kwake katika kipindi chote tangu wamekuwa pamoja. Hafikirii kama itakuja kutokea siku moja wanaweza kutengana kutokana na jinsi ambavyo wamekuwa wakipendana.
Anaamua kufungua sehemu ya barua pepe, anakutana na barua pepe aliyotumiwa na Bosco akieleza jinsi alivyohuzunishwa ha kitendo cha usaliti alioufanya Flaviana kwa kujiingiza katika mahusiano na mwanaume mwingine, ujumbe unaomfanya Flaviana atoe machozi kwa vile anavyohukumiwa kwa kosa ambalo hakufanya yeye. Anajibu ile barua pepe kwa kumweleza Bosco ukweli wote ili aweze kunusuru penzi lake ambalo linaonekana kuyumbishwa na dhoruba kali. Anamaliza kutuma ule ujumbe na kufungua mtandao wa twitter kisha anamtumia Bosco ujumbe kueleza masikitiko yake kwa tukio baya lililojitokeza ambalo limemchafua sana.
Anamaliza kumtumia ujumbe Bosco katika mtandao wa twitter kisha anaanza kusoma ujumbe aliowahi kumtumia Bosco katika ukurasa wake. Anasoma ujumbe mmoja baada ya mwingine, huku akitafakari maneno yale matamu ambayo Bosco alimwandikia. Anaendelea kupitia ujumbe ili angalau moyo wake upate kufarijika na maneno matamu ya upendo toka kwa Bosco ambayo. Anajua jinsi mpenzi wake anavyojua kutoa maneno ambayo yenye mvuto hasa pale anapoelezea mapenzi yao na kumsifia.
Anafika katika ujumbe ambao ulitumwa takribani miezi miwili iliyopita ambao amekuwa akiusoma mara nyingi tangu ulipotumwa, kwani alikuwa akiusoma alimkumbuka sana Bosco na kumfanya azidi kutambua umuhiu wake maishani mwake.
Anausoma ujumbe na kurudia mara kadhaa. Ujumbe unasomeka hivi;-
Flaviana My love, You are so great. You are among those great women in the world. Nafasi yako ni kubwa hakuna wa kubeza. Utu wenye heshima, hekima na busara ni miongoni mwa sifa lukuki zinazokufanya kuwa mwanamama imara wa Kiafrika kama chuma cha pua!, ambapo siku zote umekuwa ukiueleza ulimwengu jinsi ya kupenda, tambua kuwa wewe ni kile kitu bora na cha thamani sana ambacho nilikusudia kutokukikosa maishani japo ni bahati kubwa, kwani wema na sifa zako zitanichukua maisha yangu yote kuuelezea ulimwengu unielewe ninachoelezea.
Wakati huu ambao uko mbali nami, ukiwa maelfu ya maili toka hapa nilipo huku tukiwa tumetenganishwa na bahari, maziwa, milima, mabonde, tambarare na miamba, navuta taswira ya mke wangu mtarajiwa ambaye umekuwa TUNU maishani. Siwezi tu kueleza upweke uliopo moyoni mwangu kwa wakati huu bali pia jinsi gani inavyonigharimu missing the smell of your skin`………………………………
Mbele yetu naona taswira kubwa sana ya maisha yetu ya siku za usoni na zijazo hapo baadaye sana, naamini hiyo ndiyo picha ya uhalisia wa maisha ambayo tunayahitaji na kuyaandaa. Nakuombea sana kwa Mwenyezi Mungu akusaidie uweze kujitinza hadi pale ahadi yetu itakapokamilika ili tufunge pingu za maisha, tukio takatifu litakaloleta furaha ya dhati katika maisha yetu na kufanya tushuhudie mibaraka ya pekee ambayo Mungu ameamua kutumiminia, na kuleta furaha sio kwetu tu, bali kwa jamaa, ndugu na marafiki na kutufanya tuwe wenye shukrani za dhati kwa hayo yote. By the way, nimekuandalia zawadi very special. Hii ni zawadi ya maisha ambayo pia itakuwa kumbukumbu ya milele milele na milele……
Tuzidi kumuomba Mungu azidi kutulinda na kututunza na azidi kutupatia hekima. Tambua NAKUPENDA MOYO WANGU, kamwe huwezi kutengana na mwili huu isipokuwa mauti pekee………………………………………………………………..
‘Hope we are going to have another very happy moment in our live, even more than before.’ JITUNZE.
************ Flaviana anamaliza kusoma maneno hayo yanayomchoma sana kutokana na kile anachokipitia kwa wakati ule kisha anafunga kompyuta yake. Anaangalia muda na kugundua kuwa muda umeenda na tofauti na alivyodhani. Saa inamuonesha kuwa sasa yapata saa tatu na nusu usiku. Anaamka na kuamua kumimina chai, anachukua na vipande vichache vya mkate kisha anakula na kukaa sebuleni kwaajili ya kuangalia filamu kama alivyozoea. Anaangalia filamu inafika katikati, filamu inakosa mvuto kwake kutokana na msongo alionao. Anazima televisheni na kwenda kulala.
Anajikuta yuko juu ya kinara kirefu sana. Akiangalia chini anoana nyumba zinaonekana ndogo kutokana na umbali toka pale alipo hadi chini. Anashangaa na kujiuliza amefikaje pale. Akiangalia haoni ngazi ambayo anaweza kuitumia kushuka chini. Anajaribu kuangalia mbele, nyuma, kushoto, na kulia huenda atapata msaada lakini matumaini hayaonekani kwani anaona mawingu tu ambayo yako umbali wa sentimeta chache sana toka pale alipo.
Wakati akitafakari bila kupata jibu, mbele yake anaona ndege ya abiria ikipita kwa mbali sana. Kwa umbali ule alijua hata angepaza sauti yake kuita aombe msaada wala sauti yake isingeweza kusikika. Anaamua kuita kwa nguvu japo anajua zoezi lake haliwezi kufanikiwa. Anasitisha zoezi la kuita pale anapoona ile ndege tayari imefika mbali sana na kutokomea machoni mwake. Anaanza kuangua kilio cha huzuni kubwa kinachodumu kwa muda mrefu.
Baadaye ananyamaza na kufuta machozi kwa kutumia kiganja chake cha mkono na kuanza kutafakari maisha yake tangu alipokuwa na umri mdogo ambao tayari alikuwa anajitambua. Anakumbuka mambo mengi aliyojifunza toka kwa wazazi wake katika umri ule. Anakumbuka jinsi mama yake alivyokuwa akImweleza kuwa anapaswa kumwomba msaada Mwenyezi Mungu anapokuwa na tatizo ili Mwenyezi Mungu amsaidie. Anakumbuka pia jinsi walivyokuwa wakipata shida pale nyumbani, walimwomba Mungu akaonesha njia.
Wazo linamjia amwombe Mungu ili amsaidie kwa njia ya kipekee huku akifikiria kuwa, Mwenyezi Mungu atatuma malaika waje wamshushe katika kinara kile. Kabla hajaomba wakati akifikiria jinsi Malaika watakavyokuja kumnyakua, anasikia muungurumo wa ndege. Sauti ya muungurumo ilikuwa inasikika kwa mbali lakini kadri muda unavyokwenda, ndivyo sauti hiyo ilivyosikika kwa karibu zaidi hatimaye inatokeza helikopta upande wa kushoto ikija pale alipo Flaviana. Tukio hilo linaleta matumaini makubwa sana kwa Flaviana ambaye anaanza kutabasamu huku akiishuhudia ile chopa jinsi inavyokaribia.
Anaanza kupunga mikono ishara ya kuomba msaada baada ya kuona chopa hiyo imekaribia sana maeneo yale. Punde chopa inafika karibu kabisa, kutazama vizuri anamuona Bosco ndiye aliyekuwa rubani. Furaha isiyo kifani inamjaa moyoni mwake na kujiona yuko salama. Anaanza kuita kwa nguvu ; ‘Boscoo…. Boscoo, mpenzi wango Bosco’. Bosco anageuka kumwangalia Flaviana ambaye uso wake umejaa furaha. Furaha ya Flaviana inatoweka ghafla anaposhuhudia ille chopa ikimpita huku ikiongeza mwendo bila kuonesha dalili zozote za uokozi. Haamini kama Bosco anaweza kumpita hivihivi bila kumuokoa wakati akiwa amechoka na mwenye njaa bila matumaini yoyote. Anaanza kulia huku akiitazama ile helikopta ikipotelea kwenye mawingu. Anaona haimpasi tena kuendelea kuishi kwani hana msaada. Alitegemea Bosco amsaidie lakini amemuacha solemba. ‘Yanipasa nini mimi kuendelea kuishi wakati niliyetegemea anisaidie amenicha….’ Ni manung’uniko ya Flaviana huku akilia kwa uchungu. Dakika ziliendelea kusonga, Flaviana bado anaendelea kulia na kuzidi kupoteza matumaini. Anaangalia chini anaona ni mbali sana, akiandalia juu anaona mbalamwezi na nyota ziking’aa. Akiangalia pande zote haoni msaada. Baridi kali inaanza, anakunja mikono yake na kujikunyata huku akitetemeka. Nguvu zinamwishia na hewa inakuwa nzito hivyo anapumua kwa taabu. Anajua tayari huo ndiyo mwisho wake umefika kwani anaona jinsi hali ile inavyomuelemea.
Anajua kuwa hana dakika nyingi za kuendelea kuishi. Anatamani aache ujumbe lakini haoni sehemu ya kuuandika. Mara wazo linamjia aandike pale juu ya mnara ili hata kama akifa, ujumbe ule ubaki pale. Anajaribu kufikiria kitu cha kuandikia kwa dakika zile chache za maisha yake zilizobaki. Anachukua pini aliyokuwa nayo na kuamua kujitoboa ili damu itoke aitumie kuandika asije kuondoka duniani wakati bado hajaacha ujumbe ambao alikuwa anaukusudia kwa mpenzi wake Bosco. Damu hazitoki licha ya kujitoboa mara kadhaa. Anaamua kuikandamiza ile pini kwa nguvu pajani mwake huku akilia sana kwa maumivu makali anayoyapata. Anaichomoa pini na kuiichomeka tena katika paja lake kisha kuitoa tena. Anaina damu zinatoka kidogo sana jambo linalomfanya aamue kujikwaruza kwa nguvu huku akutoboa sehemu ilipo mishipa ya damu katika mkono wake wa kushoto. Awamu hii anafanikiwa, damu zinaanza kutoka kwa wingi. Anaanza kuchovya ile damu kwa kidole chake kisha anaanza kuandika ujumbe kwa shida sana huku hali yake ikiwa ni mbaya sana. Mara anashindwa kuendelea kupiga magoti wakati akiendelea kuandika ule ijumbe, anajikuta anaisiwa nguvu na kuanguka kifudifudi.
Anajua tayari safari imewadia kwani tayari ameanza kuhisi hali ambayo siyo ya kawaida. Anajaribu kunyoosha mkono wake ili aendelee kuandika huku akiwa amelala pale chini, jitihada zinakwama. Ghafla kaupepo mwanana kanavuma hivyo kanampatia nguvu kidogo angalau za kujivuta. Anaanza kufanya jitihada za kunyanyuka ili angalau apate kukaa wakati akimalizia dakika zake za upendeleo alizopewa.
Wakati akifanya zile jitihada za kujisgeza apate kujinyanyua pale chini, ghafla anafika sehemu iliyoinama na kuanza kubingilita akielekea kuanguka chini. Anafanya jitihada za kujizuia lakini inashindikana anajikuta akiwa hewani toka juu kwenye kinara kuitafuta ardhi. Hapati picha chini palivyo mbali aliposhuhudia wakati ule yuko pale juu ya kinara. Anajua anakufa kifo kibaya sana ambacho anaona hakikumstahili, aliona bora angefia pale juu ya kinnara kuliko kwenda kugawanyika kama glasi iliyopasuliwa sakafuni na kuvunjika vipande vipande.
Anaamua kusali dua ya mwisho, ili ikiwezekana basi Malaika waje kumdaka na kama itashindikana ikiwa malaika wako mbali sana, basi Mwenyezi Mungu amsamehe dhambi zake na kumuweka mahali pema peponi. Anaposema amina, anajikuta ametua kwenye turubai kubwa ambalo lilikuwa limekingwa ili asianguke chini. Haamini macho yake kujiona yuko salama. Anaamka na kuangaza anaona watu wengi washika pembeni mwa lile turubai. Wale watu wanashusha lile turubai, mmoja anamkaribia na kumshika mkono akinyanyua. Kuinua macho yake anamwona ni mpenzi wake Bosco. Anaanza kulia kilio cha furaha huku haamini yale yote yaliyomkuta. Bosco anamfuta machozi kisha anambeba kumpeleka nyumbani. Wakati Bosco amembeba akiwa njiani kuelekea nyumbani, ghafla anateleza wanaanguka chini kama magunia ya mihogo. Anapotua pale chini, Flaviana anashtuka na kugundua alikuwa anaota. Usingizi unapaa kwa muda mrefu. Akipata usingizi unakuwa wa mang’amung’amu. Hali hiyo inaendelea kusumbua sana usiku ule hadi inafika mida ya asubuhi kunapambazuka. Anaamka akiwa na njaa kuliko kawaida. Anaandaa kifungua kinywa na kuketi mezani kuanza kula. Wakati akiendelea kula, anasikia mlango wa sebuleni ukigongwa, anaingia Lightness, akifuatiwa na Zawadi pamoja na watu wengine wawili mmoja amevaa sare za jeshi la polisi wakati mwingine za kawaida. Wanajitambulisha wale watu wawili kuwa ni maafisa wa jeshi la polisi na kueleza kilichowaleta ni kumchukua ili aende kituo cha polisi cha kati kwa ajili ya kutoa maelezo kuhusiana na tukio la kumshambulia Lightness alilolifanya.
Anaongozana nao hadi kituo cha polisi ambako ‘anatupwa ndani’ kwa kosa la kumtishia maisha Lightness na kumshambulia kwa kumpiga na kumtukana. Habari zinazagaa kuhusiana na tukio la Flaviana kuswekwa ‘lupango’ kiasi cha kutawala vichwa vya habari katika vyombo mbalimbali vya habari.
Machallo anapata habari kuwa Flaviana yuko kituo cha polisi. Anavaa vizuri kuhakikisha amependeza, kisha anaamua kwenda kituoni kumuona huyo mpenzi wake wa kughushi. Kwakuwa tayari anajua ameshakuwa maarufu, anaona hapaswi kupanda matatu, wala bodaboda. Anaamua kwenda kukodi gari katika kampuni ambalo hukodisha magari. Anakodi gari aina ya lexus na kuanza safari hadi kutuoni ambako anafikia kudakwa na mapaparazi ambao wanamhoji kuhusiana ma mahusiano yake na mwanadada Flaviana. Anajifanya kama hataki kuongea lakini mwishowe anaamua kufunguka. ‘Nimekuja kumwona mpenzi wangu na kufanya taratibu za kumwekea dhamana’ anaeleza Machallo wakati kamera za waandishi wa wa habari zikimulika tukio na vinasa sautii vikiwa vimewekwa sambamba na mdomo wa Machallo.
Maswali yanaulizwa na mapaparazi hao kuhusiana na mahusiano ya wawili hao ambayo yaliwekwa wazi na Flaviana, pia wanamuuliza kuhusiana na sekeseke lililotokea kati ya Flaviana na rafiki yake Lightness. ‘Inasemekana, ugomvi kati ya Flaviana na Lightness ulisababishwa na kitendo cha wewe kuwa na uhusiano na Lightness huku mkimzunguka Flaviana, unalisemeaje hili?’ anauliza mmoja wa mapaparazi huku akisogeza kinasa sauti jirani na mdomo wa Machallo.
************ :: Je nini kitaendelea hapo? nini hatma ya Machallo?
:: Safari ndio kwanza imeanza, hapo ndipo utajua maana ya ‘SHETANI MSALABANI’ hakika si ya kukosa endelea kufuatilia kujua.
Simulizi : Queen Of Gorillas ( Malkia Wa Masokwe ) Sehemu Ya Kwanza (1)
Septemba 9, 1990 Monrovia – Liberia Hali ilikuwa imetulia, hakuwepo mtu hata mmoja aliyefikiria kwamba saa chache zijazo zingebadili kabisa maisha ya familia ya bwana na bibi Davis Kanyon na mkewe Christine Steven pamoja na watoto wao wawili, Dorah mwenye umri wa miaka kumi na tisa na kaka yake, Harvey, mwenye umri wa miaka kumi na saba. Jioni hiyo, walikuwa wameketi sebuleni wakipata chakula cha jioni huku mzee huyo akisimulia jinsi familia yake ilivyohamishwa kutoka Marekani mpaka Liberia. Ni historia hiyo ndiyo iliyoonekana kuwavutia zaidi watoto hao, wakataka kupata simulizi yote juu ya nini kilitokea mpaka wakawa hapo.
“Huo ndiyo ukweli wanangu, asili yetu sisi ni Marekani.” “Nini kilitokea baba?” Harvey aliuliza akijiweka vyema kitini. “Ni historia ndefu sana kuisimulia hapo nimeeleza kwa ufupi?” “Mh!” watoto wakaguna. “Kwa hiyo ina maana tungekuwa Wamarekani?” Dorah aliuliza. “Huo ndiyo ukweli wanangu.” “Baba kwa nini tusirudi huko?” Harvey aliuliza. “Haa! Haa! Haaa!” mzee Kanyon akaachia kicheko kikali. “Mbona sasa unacheka?” “Nimefurahi lakini ukweli ni kwamba hatuwezi kurejea tena huko,” alimaliza mzee huyo.
Vijiko vikaendelea kuingia mdomo kwa kasi wakicheka na kutaniana na mara kadhaa wakiongea mambo mengi kuhusu maisha ya baadaye lakini ghafla mzee Davis akatupa macho yake kwenye televisheni iliyokuwa pembeni kidogo, habari ya kushtusha ilikuwa ikisomwa, taratibu bila kusema kitu akaweka kijiko chake chini na kunyanyuka kitini kisha kuisogelea televisheni.
“Mungu wangu!” ndiyo kelele pekee iliyosikika. Mke na watoto nao wakasogea karibu kuangalia ni kitu gani kilikuwa kimetokea.
Kwa masikio yao yote huku wakisikia na kuona ilikuwa ni habari juu ya machafuko yaliyoikumba Liberia, rais wao Samuel Doe, alikuwa amepinduliwa na kundi la waasi la Independent Nationa Patriotic Front lililoongozwa na Prince Johnson kisha kukatwa kichwa chake na kuzungushwa mtaani. “Tumekwisha! Liberia imeingia katika machafuko makubwa,” Davis aliongea huku machozi yakimbubujika. “Kimetokea nini?” mkewe alihoji, yeye pia alikuwa akilia.
“Hata mimi sijui, ndiyo kwanza habari hii naiona hapa sasa hivi.” “Tufanye nini sasa?” “Haraka tuondoke vinginevyo…” aliongea Davis na haraka bila kusema tena neno akatoka mbio kuelekea chumbani huku akiwataka watoto wake nao pia wafanye maandalizi na kuchukua vitu vilivyokuwa muhimu. Wakakubaliana na baba yao, wao pia wakaingia kwenye vyumba vyao na haikuchukua hata dakika tatu wakatoka mbio sebuleni hapo wakimkuta mama na baba wakiwasubiri. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Tuombe Mungu wanangu, tunatoroka kukimbilia…” aliongea Davis lakini kabla hajamalizia sentensi yake mlango ukasukumwa na kundi la watu waliovalia kijeshi likaingia, mitutu ya bunduki, mapanga na mashoka vikiwa vimetangulia mbele. Ishara tosha ya kuonesha hatari. “We are going to die!” (Tutakufa) alisema Davis huku akiwa katika hali ya kutaharuki. Kwa macho yake, bila watu hao kusema kitu, alishuhudia panga likitua kichwani kwa mtoto wake mpendwa Dorah na kuanguka chini huku akivuja damu nyingi kupita maelezo.
Akatupa kila kitu kilichokuwa mikononi mwake ili aingie kazini kupambana lakini tayari alishachelewa wauaji walishamkata mkewe Christine na kumpiga kwa panga kama walivyofanya kwa mtoto wake, akashuhudia kelele moja tu ya mkewe akilalama kwa maumivu kisha kuanguka chini na kukata roho.
Davis akaelewa hivyo vilikuwa ni vita vya kuangamiza familia yake hivyo akajitoa mhanga kama ni kufa basi naye aifuate familia yake. Akiwa na hasira nyingi, akapigana kiume kufa na kupona huku mapanga kadhaa yakiendelea kupita ndani ya mwili wake na akisikia maneno kutoka kwa waasi kwamba ilikuwa ni lazima afe kwani yeye pia alikuwa ni mmoja wa wafuasi wa Samuel Doe.
“Lazima afe huyu hakuna kumwacha akiwa hai, ni mmoja wao!” alisema mmoja wa waasi. “Ua! Ua! Piga panga !” zilikuwa ni sauti za waasi na sauti ya panga likitua juu mwili wa mtu ikasikika. “ Paaa ! ” ilikuwa sauti ya kipigo ikiambatana na kilio kikali. Mwili wa Davis ulijaa majeraha makubwa na damu nyingi kuvuja lakini bado aliendelea kujikaza kiume akipambana na kundi la watu wasiopungua kumi lakini mwisho akaonekana kuzidiwa nguvu kwa kushushiwa panga moja kwenye paji lake la uso, ni jambo hilo ndilo lililompeleka chini na kupoteza uhai wake.
“Hureee! Hureeee! Hapa kazi tumemaliza twendeni mbele !” zilikuwa ni sauti za waasi ndani ya nyumba wakishangilia ushindi kwa kufanya mauaji ya familia ya David Kanyon. Wakati waasi hao wakifurahia ushindi kwa mauaji ya kikatili Harvey pekee ndiye aliyekuwa amesalia ndani ya nyumba hiyo kwa kujificha nyuma ya mlango huku akishuhudia ukatili na unyama wote jinsi waasi walivyoitendea familia yake. Moyo wake ukauma kupita kiasi, akalia na kuomboleza huku akimwomba Mungu amnusuru na balaa hilo baya, akailaani siku hiyo kutokea katika maisha yake huku akiapa kutosahau mpaka siku atakapoingia kaburini.
Mara kadhaa taswira ya ndugu zake ilimjia hasa wakati baba yake akisimulia kwamba wao walikuwa ni Wamarekani waliohamishwa kwa nguvu kuja nchini Liberia. Akiwa katika mawazo hayo ghafla akaisikia sauti ya baba yake ndani ya kichwa chake ikijirudia. “Huo ndiyo ukweli wanangu, asili yetu sisi ni Marekani.”
Harvey akalia machozi ya uchungu. Walipohakikisha kwamba kila kitu kimekwenda kama walivyopanga, bila kufahamu kwamba kulikuwepo na mtu mwingine ndani ya nyumba hiyo, waasi wakashangilia na kuanza kutembea kutoka ndani kuelekea nje huku wakiimba nyimbo za ushindi, vishindo vyao vikasikika vikipotea, ishara kwamba walikuwa wakitokomea kuondoka eneo hilo.
Taratibu alipohakikisha kwamba waasi wameondoka eneo hilo, akatoka sehemu aliyokuwa huku akinyata na kusogea karibu na mahali baba yake alipoangukia, akainama na kumtingisha huku akimwita kwa sauti ya kunong’ona lakini hakuonyesha kuwa na majibu, kwikwi ya kulia ikiwa imemkaba Harvey, akainama na kumbusu baba yake juu ya paji lake la uso huku akitamka maneno.
“Shujaa wangu umekwenda, najua umetangulia nami nitafuata muda si mrefu,” aliongea kwa uchungu na akafanya vivyo hivyo kwa mama na dada yake na alipomaliza akatembea kuuelekea mlango huku akigeuka nyuma kuangalia maiti zilizokuwa chini, akaishia kuangua kilio. Moyo wake ukiwa umejawa na hofu kubwa, akatoka mpaka nje ya nyumba na kuangaza huku na kule bila kumwona mtu yeyote, hapo akapiga moyo konde na kuanza kutembea taratibu huku akinyata kuingia barabarani kukiwa na ukimya wa ajabu.
Huku akilia, Harvey hakufanikiwa hata kupita hatua tano mbele, akakutana na maiti za watu zikiwa zimetapakaa njia nzima, hofu ikazidi kuugubika moyo wake, akashindwa kuelewa hatima ya maisha yake lakini akajipa moyo na kuendelea kukimbia kutokomea kusikojulikana. Ukimya aliokutana nao ndiyo uliozidi kusumbua ubongo wake. Eneo lote alilofanikiwa kupita hakukutana na mtu yeyote, hata alipojaribu kutupa macho yake kuangalia ndani ya nyumba hizo hakuambulia kitu zaidi ya maiti nyingi zilizokuwa zimezagaa chini.
Kwa mwendo wa nusu saa nzima bado aliendelea kukimbia peke yake lakini ghafla akiwa amekata tamaa kabisa, kwa mbali alimwona mtu ambaye naye pia alionekana kukimbia kitu fulani. Kwa ishara akamwita na alipogeuka aligundua alikuwa ni kijana ambaye hawakutofautiana naye umri, hivyo bila kuongea kitu chochote wote kwa pamoja wakaanza kukimbia kusonga mbele. Waliendelea kusonga mbele wakikutana na vijana wengine zaidi, hatimaye kufanya idadi yao kufikia watano lakini bado waliendelea kukuta maiti nyingi zaidi, jambo lililozidi kuwatia hofu ndani ya mioyo yao. Hatimaye mbio hizo ziliwafikisha pembezoni mwa bahari huku hali zao wote zikiwa mbaya.
WAKATI wanalifikia jahazi tayari watu wengine walishaanza kupanda ndani yake, muda mfupi baadaye nao wakalipa fedha zilizohitajika kisha wakaanza kuingia mmoja baada ya mwingine. Ndani yake wakapanda vijana wanne, mmoja
waliyeongozana naye akakosa nafasi kutokana na fedha zake kuwa kidogo. Ni hapo ndipo walipolazimika kumwombea msaada kwa mmiliki ambaye alisita kwa muda lakini walipombembeleza sana hatimaye akawa amekubali, akaungana na wenzake huku furaha ikitawala kati yao.
Safari ikawa imeanzia hapo, ndani ya mioyo yao wote walifikiria kufika walikokuwa wanakwenda na walipozungusha macho yao huku na kule ndani ya jahazi walishuhudia watu wengi wakiwa katika hali kama zao, wao pia walikuwa wamekutwa na matatizo kama ya kwao japo hakuna mtu aliyeongea na mwenzake.
Jahazi likaanza kukatisha bahari na kutokomea, hatimaye wakawa wameondoka. Ndani ya moyo kwa Harvey hali ilikuwa ni tofauti kabisa, muda wote machozi yalionekana kububujika mashavuni mwake, taswira ya familia yake ikiuawa kinyama mbele ya macho yake ikawa inajirudia, moyoni akajilaumu kwa kutoweza kufanya jambo lolote kuokoa maisha yao.
“Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi. Mimi nimenusurika na mauaji, nimeondoka Liberia kuingia nchini Marekani nikiwa ndani ya jahazi lakini sina uhakika na huko niendako kama nitafika salama. Ikitokea hivyo basi nitamshukuru Mungu wangu lakini nikiri wazi kwenu ndugu zangu kama kweli kuna sehemu nyingine tutaonana basi na iwe hivyo…” kwikwi ya kulia ikamkaba Harvey, akashindwa kujizuia na kuangua kilio kikali kilichowafanya watu wote ndani ya jahazi kugeuka na kumwangalia. “Harvey wewe sasa umeshakuwa mkubwa unatakiwa uwe na moyo wa uvumilivu, jikaze bwana wewe ni mwanaume wa shoka…” mmoja wa vijana aliosafiri nao ndani ya jahazi aliongea akijaribu kumtuliza.
“Inauma! Hapa nilipo nimempoteza mama, baba na dada, wote wamekufa nimebaki mimi peke yangu, nimebaki yatima nikiwa sina msaada wowote, ninaichukia hii dunia kwa ukatili wake…” “Harvey hii ndiyo dunia, sote tumepata majeraha kama yako lakini tunavumilia.”
Hakujibu kitu tena, akainamisha kichwa chake chini na kutulia kimya, alionekana kuwa na mawazo mengi kichwani mwake na hata wenzake walipomwangalia waliligundua jambo hilo, wao pia pamoja na kuwa na maumivu ndani ya mioyo yao wakamgeukia Harvey na kumfariji, hakika dunia ilikuwa imemtenda kitu kibaya.
SAFARI ya kuingia nchini Marekani ilikuwa imeanza, watu wote ndani ya jahazi pamoja na kwamba walikuwa na huzuni walikuwa na furaha ya kuondoka nchini Liberia kukimbia vita. Wakalishuhudia jahazi likiyakata maji na kutokomea lakini kwa Harvey hali ilikuwa tofauti kabisa. Muda mwingi alikuwa ameinama chini akigugumia kwa maumivu na kuilaumu dunia kwa unyama iliomtendea. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Taswira za baba, mama na dada yake wakiuawa kinyama mbele ya macho yake ilikuwa ikijirudia mara nyingi ndani ya kichwa chake. Ni hali hiyo ndiyo iliyouumiza zaidi ubongo wake, akayaona maisha kwake hayana maana tena kwani alipoteza nguzo muhimu. Jahazi lilizidi kupasua mawimbi na kusonga mbele.
“Wote wamekufa, wameniacha peke yangu! Hivi ni kwa nini dunia haina usawa?” alijiuliza swali hilo mara kadhaa ndani ya kichwa chake bila kupata majibu. Aliponyanyua uso wake na kuzungusha macho yake huku na kule ndani ya jahazi, hakumfahamu mtu hata mmoja zaidi ya vijana wanne aliokutana nao njiani wakati wakikimbia kunusuru roho zao, hao ndiyo walikuwa ndugu zake kwa wakati huo.
Siku ya kwanza ilikatika wakiwa bado ndani ya maji, watu wengi walionekana kuchoka na wengine kulalamika njaa lakini hiyo ndiyo ilikuwa safari, nahodha wa jahazi hilo aliwataka kuwa wavumilivu kwani safari ingechukua muda mrefu. Kama nahodha wa jahazi alivyokuwa amewaeleza mwanzo kwamba safari yao ilikuwa ngumu na iliyohitaji uvumilivu, ndivyo
ilivyotokea. Wiki ya kwanza ilikatika, hatimaye ikaja ya pili wakiwa bado ndani ya bahari. Walipojaribu kudadisi ni lini safari yao ingefika mwisho, walipewa jibu moja tu, kwamba bado safari ilikuwa ni ndefu.
Ikatimu wiki ya tatu na siku nne, watu ndani ya jahazi wakaanza kuchoka. Njaa na kiu viliwasumbua huku wengi wakiugua maradhi mbalimbali, vyakula vilivyokuwa vimechukuliwa ili kukidhi mahitaji ya safari zao vilikuwa vimekwisha. Si hilo tu, hata dawa za huduma ya kwanza nazo zilikuwa zimekwisha, watu wakaanza kupata hofu kama watafika salama, wengi afya zao zilikuwa mbaya kwa kukosa huduma muhimu.
“Nakiona kifo mbele yetu, sijui kama tutafika salama huko tuendako?” alisema Harvey kwa sauti ya chini. “Mungu ni mkubwa, ukimwomba kitu hawezi kukunyima.” “Najua hilo lakini…,” Harvey alijibu mbele yake aliiona hatari kubwa. “Kwa nini unasisitiza jambo hilo kila mara?” rafiki yake mmoja aliuliza. “Mimi mwenyewe nashindwa kuelewa ni kwa nini lakini hivyo ndivyo moyo wangu unavyonieleza.” “Hebu achana na hayo mawazo mabaya, unajiumiza moyo bure.”
Kwa muda waliendelea na mazungumzo yao, hatimaye usiku ukaingia wakiwa bado safarini. Ni hapo ndipo usingizi ulipowapitia wote, wakalala fofofo huku kelele za watu wachache waliokuwa macho muda huo zikiendelea kusikika, hizo ndizo zilizowaamsha. “Nini kinataka kutokea?” aliuliza Harvey akiyafikicha vyema macho yake ili aone vizuri. “”Dhoruba!” “Dhoruba?” “Mh!” “Mungu wangu, yametimia.”
Kelele nyingi zilitawala ndani ya jahazi, watu wakawa wanalia na kuomba msaada ili kunusuru maisha yao kwani kwa jinsi hali ilivyokuwa, hatari kubwa ilikuwa mbele yao na ingewakumba ndani ya muda mfupi. Bahari ilikuwa imechafuka, upepo na mawimbi makubwa ulikuwa ukivuma kutoka pande kuu nne za dunia, hali ilikuwa imebadilika kabisa.
Abiria wote wakaanza kumwomba Mungu awasaidie kwani kama jahazi lingepinduka tu, basi asingesalia mtu hata mmoja. Watu wote mia moja na ishirini wangekufa maji na miili yao kuliwa na samaki wakubwa baharini. “Mungu ninakuomba unisamehe kwa kila dhambi niliyoitenda na uipokee roho yangu na kuilaza mahali pema peponi, amina!” alisema Harvey huku akishuhudia dhoruba hiyo.
Kwa muda wa saa nzima watu wote walishaamka na walionekana kufanya jitihada kubwa ili kujiokoa lakini dhoruba ilikuwa imewashinda. Tayari ndani ya jahazi kulishaanza kuingia maji na taratibu lilianza kupoteza mawasiliano.
Wakati wakifikiria nini wafanye, sauti ya nahodha ikasikika ikiwatangazia kwamba jahazi lilikuwa katika hali ya hatari hivyo kungeweza kutokea kitu chochote, akawataka watu wavae makoti maalum (life jackets) ambayo yangewasaidia wasizame ili kuokoa maisha yao mara jahazi litakapozama.
Hali ya hewa ilishachafuka, hakukuwa na mawasiliano tena ndani ya jahazi, kila mtu alikuwa akifikiria kuokoa nafsi yake na si vinginevyo. Wengi walilia na kujilaumu kwa kuamua kuchukua uamuzi wa kuondoka nchini kwao kukimbia mauaji. Waligundua kuwa kumbe walikuwa wameruka majivu na kukanyaga moto na sasa walikuwa wakifa kwa maumivu.
Harvey alikuwa kimya kabisa, taswira za ndugu zake zilikuwa zikijirudia ndani ya akili zake, akaamini kwamba muda si mrefu angeungana nao huko walikokuwa.
“Ninakuja kuungana nanyi muda si mrefu…” alisema maneno hayo na akashuhudia wimbi kubwa likilipiga jahazi huku watu wakipiga kelele nyingi bila mafanikio. Akiwa hapo akashuhudia wimbi la pili nalo likija kwa nguvu na kulipiga jahazi lao, maji mengi yakaingia ndani. Watu wakaanza kutapatapa huku na kule, wengi wakionekana kuzimia.
Akashuhudia pia watu wakijirusha kutoka jahazini na hadi baharini huku wakizidi kupiga kelele za kuomba msaada bila mafanikio. Harvey akauona mwisho wake, hakutaka kuamini kuwa atakufa kifo cha uchungu cha kuzama bahari na mwili wake kuliwa na samaki wakubwa. Machozi yakawa yanambubujika, pamoja na maumivu hayo alifurahi kwamba alikuwa anakwenda kuungana na baba, mama na dada yake, akajikuta akiachia kicheko.
Wimbi la tatu likapiga tena, safari hii kwa nguvu zaidi. Harvey akashuhudia jahazi likipinduka na hatimaye kuzama huku kelele za watu zikisikika. Ghafla ukimya wa ajabu ukatanda eneo lote.
KELELE nyingi zilitawala ndani ya jahazi, watu wakawa wanalia na kuomba msaada ili kunusuru maisha yao kwani kwa jinsi hali ilivyokuwa, hatari kubwa ilikuwa mbele yao na ingewakumba ndani ya muda mfupi. Bahari ilikuwa imechafuka, upepo ulioandamana na mawimbi makubwa ulikuwa ukivuma kutoka pande kuu nne za dunia, hali ilikuwa imebadilika kabisa. Abiria wote wakaanza kumwomba Mungu awasaidie kwani kama jahazi lingepinduka tu, basi asingesalia mtu hata mmoja. Watu wote mia moja na ishirini wangekufa maji na miili yao kuliwa na samaki wakubwa baharini. “Mungu ninakuomba unisamehe kwa kila dhambi niliyoitenda na uipokee roho yangu na kuilaza mahali pema peponi, amina!” alisema Harvey huku akishuhudia dhoruba hiyo. Kwa muda wa saa nzima watu wote walishaamka na walionekana kufanya jitihada kubwa ili kujiokoa lakini dhoruba ilikuwa imewashinda. Tayari ndani ya jahazi kulishaanza kuingia maji na taratibu lilianza kupoteza mawasiliano.
Wakati wakifikiria nini wafanye, sauti ya nahodha ikasikika ikiwatangazia kwamba jahazi lilikuwa katika hali ya hatari hivyo kungeweza kutokea kitu chochote, akawataka watu wavae makoti maalum (life jackets) ambayo yangewasaidia wasizame ili kuokoa maisha yao mara jahazi litakapozama.
Hali ya hewa ilishachafuka, hakukuwa na mawasiliano tena ndani ya jahazi, kila mtu alikuwa akifikiria kuokoa nafsi yake na si vinginevyo. Wengi walilia na kujilaumu kwa kuamua kuchukua uamuzi wa kuondoka nchini kwao kukimbia mauaji. Waligundua kuwa kumbe walikuwa wameruka majivu na kukanyaga moto na sasa walikuwa wakifa kwa maumivu.
Harvey alikuwa kimya kabisa, taswira za ndugu zake zilikuwa zikijirudia ndani ya akili zake, akaamini kwamba muda si mrefu angeungana nao huko walikokuwa. “Ninakuja kuungana nanyi muda si mrefu…,” alisema maneno hayo na akashuhudia wimbi kubwa likilipiga jahazi huku
watu wakipiga mayowe bila mafanikio. Akiwa hapo akashuhudia wimbi la pili nalo likija kwa nguvu na kulipiga jahazi lao, maji mengi yakaingia ndani. Watu wakaanza kutapatapa huku na kule, wengi wakionekana kuzimia. Akashuhudia pia watu wakijirusha kutoka jahazini hadi baharini huku wakizidi kupiga mayowe ya kuomba msaada bila
mafanikio. Harvey akauona mwisho wake, hakutaka kuamini kuwa atakufa kifo cha uchungu cha kuzama bahari na mwili wake kuliwa na samaki wakubwa. Machozi yakawa yanambubujika, pamoja na maumivu hayo alifurahi kwamba alikuwa anakwenda kuungana na baba, mama na dada yake, akajikuta akiachia kicheko.
WIMBI la tatu likapiga tena, safari hii kwa nguvu zaidi. Harvey akashuhudia jahazi likipinduka na hatimaye kuzama huku kelele za watu zikisikika. Ghafla ukimya wa ajabu ukatanda eneo lote. Ilikuwa ni ajali mbaya katika jahazi hilo lililokuwa na watu mia moja na ishirini. Hakika lilikuwa tukio la kuhuzunisha kupita maelezo.
Ni wakati wimbi la tatu linapiga na Harvey kulishuhudia kwa macho yake likija kwa kasi, akasogea karibu na kijana mmoja kati ya wale waliofanikiwa kukimbia vita pamoja na kumshika mkono huku akimweleza maneno ya uchungu.
“Sasa ni wakati wa sisi kufa lakini kabla hatujafa ni lazima tujaribu kufanya kitu, sogea karibu yangu na wote tushikane mikono kwa nguvu,” aliongea Harvey na kwa pamoja huku wakitetemeka wakaruka na kuliacha jahazi likizama. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Walizama na kuibuka mara kadhaa baharini na walipojaribu kutupa macho yao kuona kama wangepata msaada hawakufanikiwa kuona kitu zaidi ya giza nene lililokuwa limetanda kila upande, wakalia machozi ya uchungu kwamba nao pia wangekufa muda si mrefu. “Harvey?” “Mh!” “Sidhani kama tutapona. “Tutapona nishike mkono vizuri usiniachie.” “Siwezi nimechoka naona nguvu zinaniishia.” “Hapana usifanye hivyo kamata vizuri tutapata msaada muda si mrefu.” Akaushika vyema mkono wa Harvey na kwa pamoja wakaanza kusonga kwenda mbele wakijaribu kuokoa maisha yao. Ni juhudi za Harvey akimfariji mwenzake ndizo ziliwafikisha juu ya mgongo wa jahazi wakapanda kwa pamoja na kumshukuru Mungu. “Ahsante Mungu kwa ukombozi wako, hakika huu ni muujiza!” aliongea Harvey huku jahazi likisukumwa taratibu na upepo kwenda mbele. “Tunayo kazi kubwa mpaka kufika tunakokwenda.” “Kwa neema za Mungu tutafika tu.” Harvey alizidi kumpa moyo mwenzake ambaye alionekana kukata tamaa waziwazi. Wakati jahazi likisukumwa na upepo taratibu walijaribu kuangaza huku na kule kuona kama wangefanikiwa kuona mtu mwingine lakini haikuwa hivyo, wakatoka eneo moja kwenda jingine bila mafanikio.
Wakiwa hawajui muelekeo wa maisha na hatima yao, njaa, kiu na baridi kali viliendelea kuwasumbua lakini hawakupoteza tumaini. “Nasikia homa,” aliongea rafiki wa Harvey. “Pole lakini huna budi kuvumilia rafiki yangu, tunachotaka sisi ni kufika Marekani basi,” Harvey alizidi kuongea akimpa moyo rafiki yake.
“Unachozungumza ni kweli tupu rafiki yangu lakini sijui…” Waliongea wakiwa juu ya jahazi hatimaye mchana ukaisha na usiku ukaingia bila kupata msaada wowote ule huku bado wakiendelea kuteseka kwa njaa na baridi kali ambayo ilizidi kudhoofisha miili yao.
Wakiwa juu ya jahazi, bado waliendelea kuona machafuko ya bahari, upepo mkali ukivuma na kulisukuma jahazi. Wakiwa juu yake, waliendelea kumwomba Mungu anusuru maisha yao. Hakika kwao ilikuwa ni safari ndefu na yenye machungu mengi lakini
hawakuwa na jinsi, ilibidi waikubali kwani huko walikokuwa wakitoka hakukuwa na amani, vita ndivyo vilivyotawala na kupoteza ndugu, jamaa na marafiki. Walitaka wafike Marekani, kuanza maisha upya na kutafuta ndugu wengine. Huko ndiko yangekuwa maisha yao yote kama wangefanikiwa kufika wakiwa hai.
Wiki ya kwanza ikakatika, ya pili, hatimaye ya tatu wakiwa bado wako juu ya jahazi bila msaada wowote na hatimaye nao wakaanza kuchoka na kukata tamaa ya kufika Marekani salama, wakakiona kifo mbele yao, afya zao zilikuwa mbaya, wakakonda kupita maelezo na nguvu nazo zikaisha, tumaini la kufika salama likapotea, wakati huo wakakitamani kifo zaidi kuliko uhai. “Harvey!” “Unasemaje?” “Mimi ninakufa muda si mrefu, nimevumilia vya kutosha naona sasa niachie na kuzama baharini.” “Usiniache peke yangu bado nakuhitaji ni wewe ndiye ndugu yangu tafadhali jitahidi.” “Siwezi, hali ni mbaya, njaa inanisumbua.” “Sikiliza! Piga moyo konde amini kwamba Marekani tutafika.” “Lini? Wakati hakuna hata dalili ya kisiwa wala meli baharini ambayo itaweza kutuokoa?” “Mungu ataleta muujiza,” Harvey aliongea. Jahazi likazidi kusukumwa na upepo kadiri siku zilivyozidi kusonga mbele ambapo hali ikazidi kuwa mbaya. “Harvey acha mimi nitangulie, hakika siwezi kuendelea tena nimechoka, Mungu akipenda tutaonana.” “Nasema hapana, huwezi kufa nitakulinda.” “Najua unanipenda kweli lakini si mimi, ni moyo ndiyo umetamani kuwa hivyo, hakika siwezi kuendelea na safari hii ninakufa.” Harvey akageuka na kumshika vyema rafiki yake huku akiongea maneno ya faraja lakini bado hayakuonekana kumwingia kichwani mwake kwani bado aliendelea kusisitiza kwamba ni bora afe. Akajitahidi kwa nguvu zake zote mwisho naye akachoka kubembeleza na kumwachia Mungu aamue. Akiwa pembeni tu akashuhudia rafiki yake mpendwa, ndugu pekee aliyebaki naye akilegea taratibu na mikono yake kuachia sehemu aliyokuwa amejishikilia, mwisho akasikia kilio kikali kikiambatana na mlio. “Dubwi!” Harvey akalia huku akimwomba Mungu amnusuru rafiki yake na kifo, akiwa juu ya jahazi akashuhudia kwa macho yake akizama mara ya kwanza na kuibuka, mara ya pili ya tatu pamoja na kwamba giza lilishaanza kuingia hakumwona tena akiinuka juu akajua tayari ameshakufa maji. Akaangua kilio kwani tayari alikuwa amebaki peke yake bila mtu yeyote, kwake tumaini la kufika alikokuwa akielekea lilishaanza kutoweka ndani ya moyo wake. Nguvu zikiwa zimemwishia taratibu akajilaza juu ya jahazi akiendelea kumwomba Mungu amtendee muujiza. Mara kadhaa alikumbuka familia yake akaziona taswira za baba, mama na dada yake zikimwita awafuate, akashindwa kujizuia na kwikwi ya kulia ikamkaba. Akaliona giza nene machoni mwake, mwili wake pia ulikuwa ukichemka kwa homa kali, mwisho wake naye ulikuwa umekaribia taratibu akashuka na kujilaza juu ya jahazi akayafumba macho yake na kumwomba Mungu amsamehe dhambi zake zote na ikiwezekana amkaribishe kwenye ufalme wake. Alipomaliza tu salama hiyo usingizi mzito ukamchukua.
Ilikuwa ni ajali mbaya mno ambayo ilichukua maisha ya watu wengi katika kipindi hicho na kuyavuruga kabisa maisha ya kijana Harvey ambaye alikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa wakisafiri na jahazi hilo lililopinduka likiwa safarini kuelekea Marekani ambako angeanza upya maisha yake akiwa hana ndugu, jamaa wala rafiki. Alikuwa amebaki yatima asiyejua nini kingetokea mbele ya maisha yake, akakiona kifo waziwazi mbele yake.
Kwa muda wa saa tatu mfululizo alilala juu ya boti akiwa kati hali ya kutojitambua, hatimaye saa ya nne upepo mkali ukaanza kuvuma. Huo ndiyo uliomuamsha kutoka katika usingizi mzito aliokuwa amelala, akanyanyua kichwa chake na kuangaza huku na kule akijaribu kuvuta kumbukumbu. Taswira za mauaji pamoja na ajali ya jahazi vikamwijia kichwani mwake, uchungu mkali ukamgubika ndani ya moyo wake. Hakika dunia ilikuwa imetenda kitu kibaya sana maishani mwake, akaapa kutosahau maumivu hayo mpaka mwisho wa uhai wake.
Kadiri muda ulivyozidi kusonga ndivyo hali ya Harvey ilivyozidi kuwa mbaya zaidi huku akijitahidi kwa nguvu kidogo zilizokuwa zimebaki kuendelea kukaa juu ya jahazi. Akawa anamwomba Mungu amtendee muujiza pengine hata wa meli au boti ambayo ingekatisha baharini hapo na kumpa msaada lakini haikuwa hivyo, usiku ukaingia na hatimaye mchana bila kupata msaada Harvey akachoka kabisa.
Homa kali ilizidi kumsumbua, baridi na njaa navyo vilichangia kumweka katika hali mbaya. Akiwa hapo akapata wazo ndani ya kichwa chake la kumkumbuka Muumba wake. Alitaka kufanya sala ya toba pengine kama ikitokea akafa basi aende mahali pema, taratibu akajiweka vizuri na kuanza kusali.
“Mungu wa Mbi .nguni tege meo pekee amba lo ninalo ni wewe, na omba usiniache na ka ma ita to kea basi yata kuwa ni ma takwa yako pu mzisha roho yangu mahali pema lakini pia nitafu .rahi zaidi ni..kiku tana na wape ndwa wangu walio tangulia ahsa nte kwa sababu utanijibu sawa sawa na maombi yangu Ami n…” alisali Harvey. Kabla hajamalizia sentensi hiyo, nguvu zikamuishia kabisa, pamoja na kwamba muda huo kulikuwa na baridi kali akahisi jasho mwili mzima, mapigo yake ya moyo nayo yalizidi kupotea, kibaya zaidi macho yakaingia kiza, akawa anakiona kifo mbele yake. Akajaribu kufungua mdomo wake angalau kupaza sauti ili kama kuna mtu anapita karibu na eneo hilo aweze kumpa msaada lakini haikuwa hivyo, taratibu akalegea na mwisho akalala juu ya jahazi na kutulia kimya. *** Madaktari na wauguzi walikuwa katika hekaheka nzito, wakikimbia huku na kule ndani ya wodi, kila mmoja akitumia uwezo wake wote kuhakikisha wanafanikiwa kuokoa maisha ya kijana aliyeletwa hapo muda mfupi akiwa katika hali ya kufa. Baada ya uchunguzi, madaktari wakashauri kwamba ni vyema mgonjwa huyo akapelekwa chumba cha wagonjwa mahututi kwani hali yake haikuwa nzuri.
“Mtundikieni dripu haraka imsaidie kuongeza maji mwilini mwake, halafu pamoja na kuwa katika hali ya kuzimia anaonekana yu katika njaa kali, asaidiwe haraka, mmenisikia?” “Ndiyo daktari,” muuguzi mmoja aliitikia na haraka dripu ikaletwa na mgonjwa akawekewa. “Mkimaliza hapo apelekwe chumba cha wagonjwa mahututi kwanza mengine yatafuata baadaye” “Mh!”
Machela ikasukumwa kuelekea chumba cha wagonjwa mahututi, juu yake kijana mzuri alilazwa akionekana kuwa katika hali ya kuzimia, hakuwa akijitambua hata kidogo. “Masikini wa Mungu, sijui ni nani, ametokea wapi na amekutwa na balaa gani?” muuguzi aliyekuwa anasukuma machela kupeleka chumba cha wagonjwa mahututi alijiuliza maswali kichwani mwake. Baada ya muda yule muuguzi alifika wodi ya wagonjwa mahututi, mlango ukafunguliwa kisha mgonjwa akaingizwa ndani ambako madaktari wengine walikuwa tayari wameshafika wakimsubiri. “Tunaweza kuwafahamu ndugu zake?” daktari mmoja aliuliza.
“Kuna mtu amemleta hapa.” “Yuko wapi?” “Hapo nje?” “Haraka tunamhitaji hapa ili atusaidie zaidi,” alisema daktari na muuguzi akatoka mbio kuelekea nje ya wodi na kumwita mwanaume ambaye ndiye haswa alikuja na kijana huyo. “Tafadhali tunakuomba wodini,” muuguzi alisema na wote kwa pamoja wakatoka eneo hilo huku wakikimbia kuingia ndani.
“Karibu sana” “Ahsante,” alijibu mwanaume huyo huku akionekana kutweta kwa hofu. “Ah! Tunahitaji jambo moja tu kutoka kwako juu ya mgonjwa.” “Amefariki?” aliuliza mwanaume huyo. “Hapana” ” Hali yake ni mbaya!”
“Mh! Sina cha kueleza, mimi ni msamaria mwema tu niliyemsaidia na kumleta hapa?’ “Si ndugu yako?” “Simfahamu hata kidogo, nikiwa baharini katika kazi zangu za uvuvi ndipo nilipomwona akiwa katika hali ya kupoteza fahamu,” alijieleza mwanaume huyo kwa ujasiri. “Inamaana hana ndugu huyu?” “Ndiyo.”
“Basi tunakushukuru kwa msaada wako, unaweza kuondoka sasa.” Kazi ikabaki mikononi mwa hospitali, kwa ushirikiano madaktari na wauguzi wakaapa kufanya kila walichoweza kuhakikisha maisha ya kijana huyo yananusurika na kifo. “Tutajitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kuhakikisha anapona, pengine anaweza kueleza historia ya maisha yake nini kilimpata.”
“Kweli kabisa.” Wakati wakiongea hayo, dripu bado ilionekana kuingia mwilini mwa mgonjwa huku muuguzi maalum akiwepo pembeni ya kitanda chake kumwangalia. Ghafla wakiwa katika majadiliano, sauti ikasikika. “Daktari dripu yake imesimama kabisa, haiingii tena mwilini.” “Unasema?” tayari walikifikia kitanda cha mgonjwa na daktari mmoja akajaribu kutingisha ili kuangalia kama ilikuwa inatembea au la!
“Ni kweli imesimama kabisa.” “Sasa?” “Hebu angalieni mapigo yake ya moyo yanakwenda au yamesimama?” Wakafanya kama alivyoshauri, mapigo ya moyo nayo hayakusikika kabisa. “Hili ni tatizo, tafadhali mashine ya hewa ya oksijeni iletwe hapa haraka huku tukisubiri jambo hilo apewe msaada wa kushtua moyo “
USHIRIKIANO mkubwa ulikuwa ukionyeshwa ndani ya wodi ya wagonjwa mahututi, kijana ambaye hakufahamika alikuwa ameletwa na msamaria mwema baada ya kumwokota baharini hali yake ilikuwa mbaya, na madaktari walitakiwa kufanya kila walichoweza kuhakikisha wanaokoa maisha yake. “Hebu pimeni mapigo ya moyo yanakwenda sawa hivi sasa?” CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Mh! Hebu tuangalie tena,” alijibu muuguzi na ukimya wa takriban sekunde mbili nzima ndani ya wodi ukajitokeza. “Majibu tayari?” daktari aliuliza. “Sasa nayasikia japo kwa mbali.” “Vizuri nitapenda kupewa majibu kila baada ya dakika kadhaa kuhusu mapigo hayo ya moyo.” “Sawa daktari hakuna shida,” muuguzi aliyekuwa ameketi pembeni alijibu, huyo ndiye alikuwa amepewa jukumu la kumwangalia mgonjwa huyo.
Kila kitu kilikwenda sawa kabisa na jinsi walivyopanga, mashine ikafungwa na kuendelea kufanya kazi, dripu nazo zilikuwa zikishuka kwa kasi kuingia mwilini, zote hizo zilikuwa ni harakati za kuokoa maisha ya kijana aliyekuwa katika hali ya kufa. “Kama kutakuwa na tatizo lolote basi nipewe taarifa, sawa?”
“Tutafanya hivyo daktari,” muuguzi akajibu na kushuhudia mlango ukifunguliwa na daktari kuondoka ndani ya wodi. Kazi ya muuguzi ikawa ni moja tu, kupima na kuandika ripoti ya mapigo ya moyo ya mgonjwa kama kumbukumbu ili daktari atakapoingia aweze kumpatia na kuiangalia. Saa zikazidi kusonga hatimaye jioni ikawadia hali ya mgonjwa ikiwa bado tete madaktari wakibadilishana zamu huyu akitoka mwingine anaingia, lilikuwa ni zoezi gumu mno lakini liliwalazimu kulifanya kwani hiyo ndiyo ilikuwa kazi yao.
“Tiiii! Tiiiii! Tiiii!” sauti ilisikika ndani ya chumba, ni hiyo ndiyo iliyomzindua muuguzi aliyekuwa pembeni mwa kitanda ambaye alionekana kupitiwa na usingizi.
“Nini?” aliuliza akinyanyua kichwa chake, akazungusha shingo yake huku na kule ndani ya chumba akijaribu kutafuta ni wapi sauti hiyo ilitokea, ghafla akatupa macho yake kwenye mashine ya hewa ya oksijeni iliyokuwa imefungwa kumsaidia kupumua mgonjwa. “Mungu wangu!” alitamka maneno hayo akisogea karibu, akiwa hajui nini cha kufanya akaishuhudia mashine hiyo ikielekea kusimama akapata wazo la kupiga kelele kuomba msaada.
“Daktari! Daktari!” aliongea muuguzi huyo akifungua mlango na kutoka nje mbio kuelekea ofisini. “Nini tatizo?” “Mashine imesimama tafadhali njoo!”
“Unasema?” muuguzi mwingine aliuliza akiwa haamini kama alichokisikia kilikuwa ni sawa. “Naona huna msaada wewe, tafadhali mwite daktari haraka aje, vinginevyo tutamko…” aliongea muuguzi huyo na kabla hajamalizia
sentensi yake tayari alishaufikia mlango wa chumba cha daktari, akausukuma na kuingia ndani. “Tafadhali twende ukaokoe maisha ya mgonjwa, mashine inayomsaidia kupumua inaonekana kusimama.”
“Mh!” Daktari akaguna tayari naye ndani ya kichwa chake taa nyekundu ilishawaka kuashiria hatari. Wote wawili wakatoka mbio kueleka chumba cha wagonjwa mahututi hofu nyingi ikitawala ndani ya mioyo yao.
“Kimetokea nini kwani?” ”Kwa kweli sijui daktari, nimeshtuka tu na kukuta hali hiyo.” “Hujagusa kitu kweli wewe?” “Naapa kwa Mungu imegoma tu yenyewe.” “Lakini lazima kutakuwa na tatizo,” tayari walishaufikia mlango wa wodi na wote wakaingia ndani huku daktari akitupa macho yake kuangalia mashine. “Hebu tujaribu kushtua tena mapigo yake,” aliongea daktari na zoezi hili likaanza mara moja. “Moja…mbili…tatu…” zilikuwa ni harakati za kuushtua tena moyo wa kijana aliyekuwa amelala juu ya kitanda akiwa hana fahamu kabisa. Kwa ushrikiano mkubwa waliendelea kumpa mgonjwa huduma ya kuushtua moyo wake kwa muda wa saa moja bila mafanikio nao pia kama madaktari wakaanza kuingiwa na hofu na kuhisi pengine alikuwa ameshaaga dunia. “Hapana daktari hebu tuendelee kwa muda tuone,” muuguzi alitoa wazo ambalo lilikubaliwa na kuanza kufanyiwa kazi. Zoezi hilo likaendelea madaktari wote wakiwa ndani ya chumba kila mmoja akihakikisha anachangia ipasavyo lakini haikuwa hivyo, mwisho wake wakaanza kukata tamaa kwani walikuwa wamefanya zoezi hilo bila mafanikio yoyote. “Ameshakufa.” “Hapana mimi ninaamini ataamka.” “Kwa nini unasema hivyo daktari?” “Ninazo hisia zote kwamba ataamka hata kama si leo basi kesho.” Jambo la mgonjwa kufa likazua mtafaruku mkubwa ndani ya chumba, makundi mawili yakagawanyika, baadhi wakisema amekwishafariki na wengine wakisema alikuwa katika hali ya kuzimia na muda si mrefu angezinduka. Wakajipa moyo na kusubiri kwa muda kadhaa wakiamini muujiza ungetokea na mgonjwa angeamka lakini haikuwa hivyo. Uchunguzi wa mwisho ukaonyesha wazi kwamba tayari alishaaga dunia na hakukuwa na haja tena ya kuendelea kumweka ndani ya chumba hicho hivyo daktari akaandika ripoti ya kifo na kuikabidhi kwa wauguzi ambao wangechukua mwili na kwenda kuuhifadhi chumba cha maiti. “Muuguzi!” “Ndiyo daktari!” “Mfunikeni vizuri na kumwondoa hapa kumpeleka chumba cha maiti, sawa?” “Sawa daktari,” wauguzi wakaitika na bila kuchelewa huku wakiwa na sura za majonzi wakafanya kama walivyopewa maelezo na bosi wao. Wakafanya maandalizi na walipohakikisha kwamba kila kitu kilikuwa sawa wakaubeba mwili na kuulaza juu ya kitanda maalum ambacho kingesukumwa mpaka chumba cha kuhifadhia maiti. Kwa mwendo wa pole wakaisukuma, hawakuwa na uhakika kama kweli mgonjwa wao alikuwa ameaga dunia lakini wakalazimika kukubaliana na ripoti ya daktari kwani huyo ndiye alikuwa msemaji wa mwisho. “Maskini wa Mungu kijana mzuri kama huyu amekufa kweli?” “Ni kweli daktari hawezi kukosea.” “Mh!” “Lakini wamejitahidi kadiri ya uwezo wao wote nadhani ilikuwa imepangwa hivyo.” “Ni kweli kabisa, kibaya zaidi hana ndugu sijui itakuwaje?” “Atazikwa na serikali,” yalikuwa ni maongezi ya wauguzi wawili wakisukuma machela kuelekea chumba cha kuhifadhia maiti, wao pia walikuwa wakilengwalengwa na machozi.
“KHO!Kho!Kho!” “Mh!” “Marehemu amekohoa” “Nini?” Tayari wauguzi waliokuwa wakiisukuma machela kuelekea chumba cha kuhifadhia maiti walishaiachia na kutimua mbio huku wakipiga kelele. “Kimetokea nini?” “Yule mtu amekohoa wakati ameshafariki kitambo.” “Mnasema kweli?” “Hakika daktari sisi wenyewe jambo hilo limetustaabisha.” “Hebu twendeni.” Wauguzi wakamtaka daktari atangulie mbele kisha wao wangefuata nyuma kwani bado walikuwa na hofu ya jambo walilolishuhudia muda mfupi uliopita. Kwa mwendo wa haraka daktari alitembea na kuifikia machela ambayo juu yake alionekana kulala mtu akiwa amefunikwa na shuka kuanzia kichwani hadi miguuni. Huku akionesha hofu machoni mwake, haraka akalivuta shuka na kulifunua huku macho yake yote yakikodoa kumwangalia mtu ambaye aliaminika kufa na sasa alikuwa ameonyesha ishara ya uhai kwa kukohoa. Kwa takriban dakika tano nzima aliendelea kusimama hapo kuchunguza mwili huo lakini hakufanikiwa kuona kitu, kwa ishara akawaita wauguzi waliokuwa pembeni kidogo na kuwaeleza kwamba mtu huyo alikuwa amekufa kwani hakukuwa na dalili yoyote ya uhai kwake. “Daktari sisi tunakuambia amekohoa huyu!” “Hapana, pengine mlikuwa na mawazo vichwani mwenu.” “Tulichokisikia ndicho daktari wala hatujakosea.” “Haraka pelekeni maiti ikahifadhiwe vizuri.” Wakati wakiongea hivyo umati mkubwa ulishafurika eneo hilo, wengi walishapata taarifa kwamba kulikuwa na kijana aliyefariki dunia muda mfupi uliopita na alikuwa akipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti lakini akiwa mlangoni alikohoa. “Pengine ni kweli jamani labda hajafa!” “Wewe mtu akishafariki harudi tena.” “Na hao waliosema kakohoa?” “Ah! Mbona daktari kaja na kumwangalia amethibitisha tena kwamba amekufa kitambo.” Yalikuwa ni majibishano ya wagonjwa waliokuwa eneo hilo la hospitali wakionyesha kushangazwa na tukio lililotokea. Baada tu ya daktari kutoa kauli, wauguzi walisogea tena karibu na machela huku wakitetemeka wakaanza kuisukuma kuiingiza ndani ya chumba lakini hawakufanikiwa kutembea hata hatua mbili, sauti ikasikika kutoka ndani ya shuka. “Chafya! Chafyaaa!” “Daktari! Daktari huyu mtu hajafa vizuri hebu mpimeni tena jamani safari hii amepiga chafya tumesikia kwa masikio yetu…” aliongea muuguzi mmoja huku akipaza sauti kumwita daktari. Ni tukio hilo ndilo lililofanya madaktari wote waliokuwa ndani ya ofisi zao, wengine wodini kutoka mbio kuelekea eneo la tukio kujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea hapo. “Nini kimetokea tena?” “Amepiga chafya” “Mnasema kweli” “Hakika daktari” “Mh!” Nao pia wakapigwa na butwaa iweje mtu aliyekufa apige chafya? Hilo likabaki kuwa swali ndani ya vichwa vyao. “Hebu mrudisheni chumba cha wagonjwa mahututi haraka tukamwangalie kwa ukaribu pengine hajafa amezimia tu!” daktari mmoja alitoa wazo ambalo lilipokelewa na kufanyiwa kazi bila kuchelewa. Machela ikageuzwa haraka na kurejeshwa chumba cha wagonjwa mahututi, madaktari wote wakifuata kwa nyuma huku kila mmoja ndani ya kichwa chake akijiuliza maswali mengi bila majibu. Dakika tatu tu tayari machela ilishafikishwa chumba cha wagonjwa mahututi ikaingizwa ndani na mtu aliyeaminika kufariki dunia akateremshwa na kulazwa juu ya kitanda ambacho alikuwa awali, bila kuchelewa madaktari wakakizunguka na kuanza kumchunguza upya. “Hebu pimeni mapigo yake ya moyo,” daktari mmoja aliongea na haraka zoezi hilo lifanyika. “Mh!” “Vipi?” “Mapigo yake nayasikia kwa mbali sana,” “Hebu mwingine apime naye tusikie atasemaje?” Daktari mwingine akasogea karibu na kupima mapigo ya moyo naye alitoka na jibu kama la daktari wa kwanza. “Kama hivyo ndivyo basi leteni mashine ya oksijeni ifungwe tena kisha tuangalie tuone.” “Sawa”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi kila kitu kikafanyika kama ilivyotakiwa na jopo la madaktari na wauguzi wote walikuwa hapo kutoa msaada ambao ungehitajika. Kadiri muda ulivyozidi kusonga ndivyo hali ya mgonjwa aliyeaminika kufa ilivyoendelea kuwa nzuri, mapigo yake ya moyo yakaendelea kuongezeka na hewa ya oksijeni nayo aliyoyofungiwa ikisaidia kumpa hewa safi. “Tumwangalie kwa muda wa siku nzima leo tukimchunguza kwa ukaribu ili tuone ataendeleaje lakini kikubwa ni kupima mapigo yake ya moyo kila mara na muuguzi atakayefanya kazi hii ashirikiane na daktari kwa ukaribu tusije tukafanya kosa kama tulilolifanya mwanzo la kumuua mtu wakati bado yuko hai, hili lisitokee tena madaktari wenzangu, sawa?” aliongea daktari mkuu wa hospitali. “Tutakuwa makini daktari,” kwa pamoja walijibu na wakaanza kutoka ndani ya wodi wakimwacha daktari mmoja na wauguzi wawilia ambao wangekuwa hapo kumsaidia mgonjwa muda wote. Kwa muda wa wiki nzima mfululizo madaktari waliendelea kumhudumia mgonjwa ambaye hali yake ilionekana kuwaridhisha wengi, kikubwa walichotamani kitokee kwa wakati huo ni mgonjwa huyo kuamka na kueleza historia yake kwamba alikuwa nani na alitokea wapi ili kama kungekua na uwezekano basi ndugu zake watafutwe na kupewa taarifa juu ya ndugu yao huyo. Muda ukazidi kusonga mgonjwa akiwa bado kitandani, kibaya zaidi bila fahamu kama hali yake ilionekana kubadilika siku hadi siku. “Akiamka tu aeleze ni wapi walipo ndugu zake ili tuwape taarifa haraka.” “Hilo ndilo suala la muhimu kwetu tunamwombea uzima,” yalikuwa ni maongezi ya madaktari ndani ya wodi asubuhi ya wiki ya pili walipokuwa wakifanya mzunguko wao wa kila siku. *** Miezi miwili ilishakatika na mgonjwa alikuwa akiendelea vizuri kabisa, mashine ya hewa ya oksijeni ilishaondolewa na alikuwa akipumua kwa njia ya kawaida jambo lililowafurahisha madaktari waliokuwa wakimpatia matibabu, pamoja na hayo yote tatizo moja kubwa lilikuwa limebaki ambalo lilileta hofu na shaka kwa madaktari, mgonjwa hakuweza kuongea kitu chochote hata walipojaribu kumuuliza wakimdadisi kwamba alikuwa nani na alitokea wapi hawakupata ushirikiano ni kama vile hakuwa na kumbukumbu ya kitu chochote. “Hili ni tatizo.” “Pengine ni bubu?” “Hapana inawezekana hii ajali aliyoipata ndiyo imesababisha kuwa hivi” “Sasa tufanye nini?” “Mimi naona tumwangalie kwa muda huku tukijaribu kuongea naye kwa upole na upendo ataongea tu,” ulikuwa ni ushauri wa Dk. Lewis ambaye alijitolea kuwa karibu na kijana huyo kwa kila kitu. Hali hiyo iliendelea hivyo siku nazo zikizidi kwenda mbele tumaini la madaktari kuona kijana huyo akifungua mdomo kuongea kitu chochote zaidi sana alipoletewa chakula alikipokea na kula kisha kurejea tena kitandani bila kusema kitu chochote.
alikufa na uamuzi wa kumpeleka chumba cha kuhifadhia maiti ukafikiwa, alikuwa amezinduka baada ya kukohoa na kupiga chafya. Akarejeshwa tena wodini, kwenye chumba cha wagonjwa mahututi kuendelea na matibabu, watu wengi wakifika kumwangalia ili kuthibitisha kama habari zilizokuwa zimezunguka kila pembe ni za kweli. Pamoja na kuzinduka, kijana huyo hakuwa na uwezo wa kuongea chochote, walijitahidi kumsemesha lakini hakuitika wala kujibu maswali yao, ikadhaniwa yawezekana alikuwa ni bubu. Hakuna aliyefahamu kijana huyo alikuwa nani, alitokea wapi zaidi ya kujua tu kwamba baharia mmoja aliyemwokota majini wakati meli yake ikikata maji kuelekea Marekani ndiye aliyempeleka kwenye hospitali hiyo kubwa.
JACKSON Memorial Hospital, ndiyo ilikuwa hospitali kubwa kabisa katika Jiji la Miami, ilitibu watu wote wa maeneo hayo na wengine waliletwa kutoka hata Jacksonville kwa sababu ya huduma zake kuwa nzuri hasa kwa wagonjwa wa majeraha.
Ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi cha hospitali hii ndimo alimokuwa amelazwa kijana huyu, kitanda chake kilikuwa kimezungukwa na madaktari saa moja na nusu asubuhi wakijadili juu ya hali yake.
“Do you think he is dumb?” (Je, mnadhani ni bubu?) Dk. Lewis ….. bingwa wa magonjwa ya wanadamu au kwa Kiingereza taaluma yake huitwa physician, aliwauliza wenzake katika mjadala huo.
“I don’t think so!” aliitikia Dk. Clara Thomas, akimaanisha hakufikiria hivyo kama mgonjwa huyo alikuwa bubu. “Why?” (Kwa nini?) “One of the nurses told me yesterday that, he had some hallucinations and spoke some words in the African language.” (Mmoja wa wauguzi aliniambia jana kwamba, mgonjwa alipatwa na maluweluwe na kujikuta anasema maneno katika lugha moja ya Kiafrika.) “Sure?” (Ni kweli?) “Yeah!” (Ndiyo). “Then, he might probably had hit his head somewhere and caused a concussion to his brain, which resulted into memory
loss.” (Basi inawezekana alipiga kichwa chake sehemu fulani na kusababisha mtikisiko wa ubongo ambao matokeo yake yakawa kupoteza kumbukumbu.) Dk. Lewis alifafanua akijaribu kutafuta chanzo cha mgonjwa huyo kutoongea.
“Or he is just probably depressed!” (Au inawezekana ana mfadhaiko wa akili tu.) “May be, we need a CT Scan of the brain urgently.” (Tunahitaji kupiga picha ya ubongo haraka.) Wote wakakubaliana na jambo hilo, Dk. Lewis katika hali isiyo ya kawaida alikuwa ametokea kumpenda sana mgonjwa huyo
mpaka wauguzi na madaktari wengine wote wakagundua kilichokuwa kikiendelea. Hisia zao ziliwatuma kuamini pengine ni kwa sababu alikuwa ni mtu mwenye asili ya Afrika kama yeye.
“He is tall, you never know, he might play for the Miami Heat basketball team when he recovers!” (Ni mrefu, huwezi kujua, pengine anaweza kupona na kuchezea timu ya mpira wa kikapu ya Miami Heat!)
Wote wakacheka wakiondoka kuelekea ofisini, huku machela ikisogezwa ili mgonjwa abebwe na kupelekwa chumba cha kupigia picha ya ubongo. Hawakwenda hata hatua kumi wakasikia kelele, haraka wakarudi wakikimbia mpaka kando ya kitanda tena na kuwakuta wauguzi wakiwa wamejawa na tabasamu badala ya huzuni.
“What happened?” (Kimetokea nini?) “He has spoken some few words!” (Amezungumza maneno machache.) “Really?” (Kweli?) Dk. Clara aliuliza kwa mshangao huku Dk. Lewis akimsogelea mgonjwa kwa karibu kama vile alikuwa hakusikia kilichosemwa. “What is your name?” (Jina lako nani?) “Ha…rve…y!” “How old are you?” (Una miaka mingapi?) Kijana huyo hakujibu, alibakia kimya akiangalia tu, ndipo Dk. Lewis akionyesha furaha akaongeza swali jingine la ni wapi alikotokea, akitaka kufahamu historia ya mgonjwa wake ambaye mpaka wakati huo alikuwa hafahamiki vizuri asili yake. “Liberia!” “Liberiaaaa!?” “Yes.” “How?” “I am hungry, give me some food then I will be able to narrate my entire story.” (Nina njaa, nipe chakula baada ya hapo nitakuwa na uwezo wa kuwasimulia historia yangu yote.)
Hapakuwa na chakula wodini wakati ule, kwani ilikuwa bado ni asubuhi, alichokifanya Dk. Lewis ni kutoka akikimbia hadi nje ambako aliingia ndani ya gari lake na kuendesha kwa kasi hadi kwenye mgahawa wa KFC, uliokuwa umbali wa kama
kilomita tatu kutoka hospitali ya Jackson Memorial. Hapo alinunua chips, baga na vipapatio vya kuku kisha kurejea haraka hadi wodini, ndani ya dakika ishirini, tayari Harvey alikuwa akila na kuendelea kwa takriban saa nzima ndipo akamaliza. “Tueleze sasa.”
Kwanza machozi yalianza kumtoka alipokumbuka namna wazazi na dada yake walivyouawa kinyama, picha yote ilionekana akilini mwake, akalazimika kuihamisha kutoka humo na kuiingiza masikioni kwa watu waliokuwa wakimsikiliza. Ilikuwa ni simulizi ya kutisha, ni kweli wote waliona kwenye vyombo vya habari namna ambavyo mauaji yalifanyika huko Liberia lakini kumbe hawakuwa wamepata picha halisi mpaka walipomsikia Harvey.
Hakukomea hapo, akaendelea jinsi yeye na wenzake walivyojaribu kutoroka kuelekea Marekani nchi ambayo baba yake mzazi alimwambia ndiko walikotokea, mateso ya njiani yaliwasikitisha wote waliosikiliza. Harvey akaendelea kuongea huku machozi yakimtoka, namna wenzake wote walivyokufa na yeye kupoteza fahamu kisha kujikuta akiwa hospitalini hapo.
“Nani alinileta hapa?” “Baharia mmoja.” “Anaitwa nani?” “Tutaliangalia jina lake na kukuambia baadaye.” Dk. Lewis alijibu akijifuta machozi, kwa mara ya kwanza tangu aanze kazi hospitalini, siku hiyo alilia mbele ya mgonjwa jambo ambalo kitaaluma lilikuwa halitakiwi. “Ni muujiza, Mungu alipanga nisife.” “Mshukuru sana Mungu, Harvey.” “Mungu ni mwema.”
Kila mtu alikuwa amefurahishwa na kilichotokea, habari za Harvey zikazidi kuenea, mpaka waandishi wa habari wakawa wanafika wodini kumpiga picha na kuzungumza naye juu ya namna alivyonusurika kifo kimaajabu. Hata hivyo, wiki mbili baadaye, aliruhusiwa kutoka hospitali, akiwa hajui mahali pa kuelekea.
Watu karibu wote waliokuwa ndani ya chombo hicho wanapoteza maisha lakini Harvey kwa mara nyingine tena ananusurika kimiujiza. Anaokotwa akiwa na hali mbaya baharini na msamaria mwema aliyekuwa akijishughulisha na shughuli za uvuvi. Anapelekwa mpaka Miami, kwenye Hospitali ya Jackson Memorial. Kutokana na hali yake ilivyokuwa mbaya, kila mtu anamkatia tamaa akidhani atapoteza maisha muda wowote, lakini haiwi hivyo. Roho yake inapambana na roho ya mauti na hatimaye anazinduka akiwa wodini na kueleza yeye ni nani, ametoka wapi na nini kilichomsibu. Historia ya maisha yake inawasisimua wengi, akiwemo Dk. Lewis. Anaendelea kupatiwa tiba ya hali ya juu na hatimaye afya yake inaimarika.
BAADA ya hali ya Harvey kuwa ya kuridhisha, madaktari wa Hospitali ya Jackson Memorial, Miami walikubaliana kuwa wamruhusu aondoke hospitali. Cheti maalum cha kumruhusu kutoka hospitali (Discharge Form) kikaandaliwa na kusainiwa na daktari aliyekuwa akisimamia matibabu ya Harvey tangu alipofikishwa hospitalini pale, Dk. Lewis.
“Unatarajia kuelekea wapi baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali?” Dk. Lewis alimuuliza Harvey wakati akimsindikiza kutoka wodini alikokuwa amelazwa. Katika hali ambayo ilimshangaza Dk. Lewis, Harvey alimueleza ukweli kuwa japokuwa anatoka hospitalini, hajui wapi kwa kwenda kwa sababu hakuwa na ndugu wala mtu yeyote anayefahamiana naye katika Jiji la Miami, CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ akamwambia kuwa alikuwa akisali kimoyomoyo kuwa angalau madaktari wachelewe kumruhusu kutoka hospitali kutokana na hali ile.
“Sina mtu hata mmoja anayenifahamu kama nilivyokueleza, ni mgeni kabisa hapa Miami na Marekani kwa jumla, natamani Mungu aichukue roho yangu ili nikapumzike na wazazi wangu ahera kuliko haya mateso ninayoyapata,” alisema Harvey huku akilengwalengwa na machozi.
Kauli ile iliuchoma sana moyo wa Dk. Lewis, ikabidi amchukue Harvey mpaka kwenye bustani ya maua, jirani na lango la hospitali ile, wakakaa kwenye viti vya kisasa vilivyokuwa vimepangiliwa kinadhifu eneo hilo, wakaanza kuzungumza kwa kirefu. Dk. Lewis alimhoji maswali mengi Harvey, akataka kufahamu kwa kina historia ya maisha yake na mambo yote
aliyokutana nayo maishani mwake. Harvey alizungumza kama alivyoongea mara ya kwanza akiwa wodini. Hakupindisha neno.
Alisimulia kila kitu kuanzia jinsi alivyokuwa akiishi na wazazi wake nchini Liberia kabla hali ya amani haijachafuka na kusababisha mapigano makubwa yaliyozigharimu roho za ndugu zake wote na maelfu ya wananchi. “Nimebaki peke yangu,
mimi peke yangu! Nguzo zangu zote zimeanguka hata sijui wapi pa kukimbilia, eeh Mungu, kwa nini mimi?” “Usilalamike sana Harvey, umri wako bado ni mdogo na una nafasi ya kuyaanza upya maisha yako kwa kufungua ukurasa mpya, ukiendelea kulalamika mwisho utamkufuru Mungu, amini kila jambo huja kwa sababu limepangwa, jifunze
kumshukuru Mungu kwa kila jambo,” alisema Dk. Lewis huku naye akilengwalengwa na machozi. Hali ya maisha aliyokuwa nayo Harvey ilimsikitisha sana, akaamua kwa moyo mmoja kumchukua na kwenda kuishi naye nyumbani kwake.
“Kuanzia leo utakuwa ukiishi na mimi, nitakupeleka nyumbani kwangu ambapo nitakutambulisha kwa mke na motto wangu na kuanzia hapo na wewe utakuwa sehemu ya familia yangu. Nimeamua kuyabadili maisha yako na naamini hilo litawezekana,” alisema Dk. Lewis huku akiinuka na kumkumbatia Harvey ambaye bado alikuwa akibubujikwa na machozi.
Taarifa ile ilimfanya Harvey apigwe na butwaa kwa muda, masikio yake yakawa kama hayaamini kile alichokisikia kutoka kwenye mdomo wa daktari yule. Hakutaka kuamini kuwa kumbe duniani kuna watu wenye roho nzuri, wenye upendo na wanaoyachukulia matatizo ya wengine kama ilivyokuwa kwa Dk. Lewis. Alimkumbatia kwa nguvu, akazidi kulia kwa
kwikwi, safari hii kwa furaha kwani hatimaye aliamini maisha yake yatabadilika. Baada ya kusimama wakiwa wamekumbatiana kwa muda, hatimaye walianza kuondoka eneo lile hadi nje, Dk. Lewis akamuongoza mpaka eneo alipokuwa amepaki gari lake, wakaingia na safari ya kuelekea nyumbani ikaanza.
Njia nzima hakuna aliyemsemesha mwenzake, Dk. Lewis alikuwa akifikiria namna ya kumfanya Harvey kuwa kijana mwenye
furaha tena kwani ilivyoonesha matukio aliyoyapitia maishani mwake yalimfanya aathirike kabisa kisaikolojia. “Lazima nitampeleka shule na kumhudumia kama mwanangu, nahitaji kuwa chanzo cha furaha yake,” aliwaza Dk. Lewis wakati gari likizidi kukata mitaa kuelekea nyumbani kwake.
Wakati Dk. Lewis akiwaza hayo, Harvey alikuwa akifikiria yake. Bado kumbukumbu za matukio ya kutisha yaliyozigharimu roho za wazazi wake zilikuwa zikimtesa akilini mwake. Kuna wakati alisikia sauti ikimwambia ndani ya moyo wake kuwa ni
lazima siku moja arejee kwao Liberia na kulipa kisasi kwa wote waliohusika. Hakutaka kuipa nafasi sauti hiyo, nasaha za Dk. Lewis kuwa kila kitu amwachie Mungu zikawa zinamfariji. Akawa anaisanifu mitaa ya Jiji la Miami kupitia dirisha la gari lile. Baada ya takribani dakika 20, gari liliwasili mbele ya nyumba kubwa ya kifahari, Dk. Lewis akapiga honi ambapo mlinzi
alitoka kufungua geti haraka, gari likaingia hadi eneo la maegesho, wakashuka huku Dk. Lewis akimtaka Harvey kujisikia yupo nyumbani.
“Hapa ndipo ninapoishi na familia yangu na ndipo yatakapokuwa makazi yako kuanzia leo, tafadhali kuwa huru kunieleza jambo lolote, nitakuwa pembeni yako kukupa msaada kila utakapohitaji,” alisema Dk. Lewis huku akimpigapiga mgongoni
Harvey, wakaelekea kwenye ngazi za kuingilia ndani na kuongoza moja kwa moja mpaka sebuleni. Kila kitu kilikuwa kama miujiza kwa Harvey. Maisha aliyozoea kuishi kwao Liberia yalikuwa tofauti kabisa na pale Miami. Mandhari nzuri kuanzia nje hadi ndani ya nyumba ile, vilimfanya ajihisi anaingia peponi hapahapa duniani. Dk. Lewis
alilitambua hilo, akawa na kazi ya ziada ya kumchangamsha na kumfanya aone kila kitu ni cha kawaida. “Unatumia kinywaji gani?” “Maji tu yanatosha,” alisema Harvey kwa sauti ya kubabaika, Dk Lewis akamwambia kuwa kwa sababu ametoka hospitali, ni bora anywe juisi ya matunda, wazo ambalo aliliunga mkono. Akainuka na kuelekea kwenye friji, akatoa juisi na kuimimina kwenye glasi mbili, wakaanza kunywa taratibu huku wakibadilishana mawazo.
Muda mfupi baadaye, honi zilisikika nje ya geti la nyumba ile, mlinzi akaenda kufungua haraka. Kwa kupitia dirisha la vioo, Harvey aliliona gari la kifahari aina ya Range Rover jekundu likiingia na kwenda kupaki. Mwanamke mrefu wa Kizungu, mwenye nywele ndefu zilizofika mpaka mabegani akateremka na kwenda kufungua mlango upande wa pili, akamteremsha mtoto mdogo aliyekuwa na mchanganyiko wa baba na mama (chotara), akamshika mkono, wakawa wanaelekea ndani huku nyuso zao zikionesha kuwa walikuwa na furaha.
“Huyo anayeingia ndiyo mke wangu, ametoka kumchukua mwanangu wa kipekee shuleni, nitakutambulisha vizuri usiwe na wasiwasi,” alisema Dk. Lewis, wale watu wakawa wanaelekea pale walipokuwa wamekaa. “Dadiiii! I miss u,” alisema yule mtoto wa kike, akamkimbilia baba yake na kumrukia, wakakumbatiana kwa muda huku kila mmoja akifurahi, yule
mwanamke akawa anamkazia macho Harvey kama anayejiuliza huyu ni nani? Baada ya hapo, Dk. Lewis alikumbatiana na mkewe na kupigana mabusu, akaanza kumtambulisha mgeni.
“Anaitwa Harvey, amekuja kuungana na sisi hapa nyumbani.” “Oooh! Ndiyo yule kijana uliyekuwa ukinisimulia habari zake, karibu sana na jisikie upo nyumbani,” alisema yule mwanamke kwa uchangamfu, akapeana mikono na Harvey.
“Harvey, huyu ni mke wangu, anaitwa Suzan Lewis na huyu ni mwanangu wa kipekee, anaitwa Skyler,” alisema Dk. Lewis, Harvey akailazimisha furaha machoni mwake, akapeana mikono na Skyler kisha wakaketi. Mke wa Dk. Lewis akaanza kumpa pole upya kwa yaliyomsibu na kumsihi amuachie Mungu kwani yeye ndiye anayepanga hatima ya kila mwanadamu
hapa duniani. Kwa mara nyingine, Harvey alijikuta akishindwa kuyazuia machozi, yakawa yanatiririka kwa wingi na kuyalowanisha mashavu yake.
Licha ya ukweli kwamba karibu watu wote waliokuwa ndani ya chombo hicho kilichopata ajali baharini wanapoteza maisha, Harvey kwa mara nyingine ananusurika kimiujiza na kuokotwa na msamaria mwema akiwa hajitambui. Anapelekwa mpaka Miami, nchini Marekani kwenye Hospitali ya Jackson Memorial.
Baada ya kutibiwa kwa muda mrefu, hatimaye anarejewa na fahamu zake akiwa wodini ambapo anaeleza yeye ni nani, ametoka wapi na nini kilichomsibu. Historia ya maisha yake inawasisimua wengi, akiwemo Dk. Lewis. Baada ya kupata ahueni, anaruhusiwa kutoka
hospitalini lakini anakosa mahali pa kwenda. Hali hiyo inamfanya daktari aliyekuwa akisimamia matibabu yake, Dk. Lewis kujitolea kumchukua na kwenda kuishi naye nyumbani kwake. Anamtambulisha kwa mkewe, Suzan na mwanaye Skyler ambapo wanampokea kwa mikono miwili. Anayaanza maisha mapya akiwa na familia ya Dk. Lewis.
DK. Lewis na mkewe, walikuwa na kazi ya ziada kumfariji Harvey kwani kuna wakati alishindwa hata kuendelea kula nao chakula cha usiku, kilio cha kwikwi kikawa kinambana mara kwa mara. Kilichomliza zaidi, ni kuona Skyler amekaa katikati ya wazazi wake, huku wote wakiwa na furaha.
Kumbukumbu za wazazi wake zikawa zinamjia, akatamani yeye ndiyo awe amekaa katikati ya baba na mama yake huku ndugu zake wengine wakiwa pembeni, lakini hilo halikuwezekana. Taswira za jinsi wapiganaji walivyoivamia nyumba yao na kuwatoa roho kikatili wazazi na ndugu zake, zilikuwa zikiendelea kupita ndani ya mawazo yake kila baada ya muda mfupi, akawa mtu wa machozi muda wote.
Baada ya kumbembeleza sana, hatimaye Harvey alitulia, wakamalizia kula chakula kisha mke wa Dk Lewis, akawaongoza katika sala maalum. Wote walifumba macho, Suzan akaanza kumuomba Mungu wao. Baada ya kumaliza kumuomba Mungu wao, wote waliweka mikono yao juu ya kichwa cha Harvey, wakafumba macho na kuendelea kumuombea kwa Mungu amsahaulishe matatizo yote katika maisha yake na kumwezesha kufungua ukurasa mpya.
Skyler, licha ya umri mdogo wa miaka tisa tu aliokuwa nao, alionekana kuimarika sana kiroho kwani alikuwa akisali na kumuombea Harvey kama mtu mzima. Angalau maombi yale yalisaidia kwani walipomaliza, Harvey alitulia, wakawa wanaangalia runinga kubwa iliyokuwa sebuleni pale. Akili zao zikachukuliwa na mechi ya Ligi Kuu ya Mpira wa Kikapu ya Marekani (NBA) kati ya Miami Heats na Memphis
Grizzlers iliyokuwa inaoneshwa runingani. Mechi hiyo ilipoisha, wote walienda kulala, Harvey akasindikizwa na Dk. Lewis mpaka kwenye chumba chake.
Alimpa nasaha chache, akamuuliza kama atapenda kuendelea na masomo au la, Harvey akajibu kwa shauku kubwa kuwa yupo tayari. Japokuwa mfumo wa elimu kati ya nchi aliyotoka, Liberia na Marekani ilikuwa tofauti sana, Harvey alimhakikishia Dk. Lewis kuwa atajitahidi kukazania masomo ili hatimaye ndoto zake zitimie. Kwa kuwa ilikuwa ni Ijumaa, Dk. Lewis alimwambia kuwa atasimamia mambo yote ili aanze masomo Jumatatu.
Kesho yake kulipopambazuka, Dk. Lewis alienda kumuamsha Harvey asubuhi na mapema, akampa nguo za mazoezi na kutoka naye, wakawa wanafanya mazoezi mepesi kwa kukimbia huku na kule kwenye barabara safi za Jiji la Miami. “Unapenda mchezo gani Harvey?” “Napenda sana basketball ila kule kwetu Liberia hakuna viwanja vizuri wala mashabiki wengi wa mchezo huo.”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Hapa Marekani ndiyo penyewe, kuna viwanja karibu kila mtaa, wengine wamejijengea viwanja ndani ya nyumba zao… hata mashabiki wengi wanapenda basketball kuliko hata soka au rugby.” “Natamani sana kuwa mchezaji hodari wa mchezo huo, naamini Mungu atanisaidia.” “Yaah! Kila mwomba Mola hupata. Mtangulize Mungu kwa kila jambo naamini utafanikiwa. Hata umbo lako limekaa ki-
basketball, si unaona ulivyo mrefu… ukikazana unaweza kuja kuwa staa kuliko hata Kobe Bryant,” Dk. Lewis na Harvey walikuwa wakizungumza huku wakikimbia taratibu pembeni ya barabara kupasha misuli ya miili yao. *** Jumatatu ilipofika, Dk. Lewis kama alivyokuwa amemuahidi Harvey, aliongozana naye hadi katika shule ya sekondari ya Miami Elementary School, akaingia naye katika jengo la utawala na kwenda kumsajili kwa mkuu wa shule. Kwa kuwa Dk.
Lewis alikuwa akifahamika shuleni pale, hasa ukizingatia kuwa mwanaye Skyler naye alikuwa akisoma palepale, zoezi la kumsajili Harvey halikuwa gumu. Akapokelewa na kusajiliwa rasmi kama mwanafunzi halali wa shule ile. Ilikuwa ni siku nyingine ya miujiza kwa Harvey. Alishindwa kuzificha hisia za moyo wake, akadondosha chozi la furaha wakati Dk. Lewis akimkabidhi kwa mkuu wa shule, akawa anajiandaa kuondoka kuelekea kazini.
“Usilie Harvey, jikaze wewe ni mtoto wa kiume, jitahidi kuishi vizuri na wanafunzi wenzako… kama utakuwa na tatizo lolote mtafute Skyler, anasoma hapahapa ila yeye bado yupo shule ya msingi, madarasa yao yapo upande wa kule juu, naamini atakusaidia,” alisema Dk. Lewis huku akimpigapiga mgongoni Harvey. Akaondoka na kumuacha shuleni pale ambapo Mkuu wa shule alimuita mwalimu wa darasa wa kidato cha kwanza na kumkabidhi Harvey.
“Umekuja na vifaa vyako vyote?” aliuliza mwalimu Wisconsin Myler, mwanaume mrefu mwenye upara. “Ndiyo mwalimu,” alijibu Harvey kwa nidhamu huku akijitahidi kuyaficha machozi yake. “Haya twende darasani,” alisema mwalimu huku akimshika mkono Harvey, akamuongoza mpaka darasani ambapo alimpanga mkondo C. Akayaanza masomo rasmi. Kila kitu kilikuwa kigeni kwake. Mazingira aliyokulia kwao Liberia, shule aliyosoma,
marafiki zake, majengo, nyenzo za kufundishia na vinginevyo, vyote vilikuwa tofauti sana kwa Harvey. Akawa na kazi ya ziada kujitahidi kuendana na maisha mapya pale shuleni.
Jambo ambalo liliwashangaza wanafunzi wenzake na walimu, Harvey muda wote alikuwa kimya kabisa, huku akionekana kuwaza mambo mazito ambayo hakuna aliyeyajua. Hali ile ilifanya wanafunzi wenzake washindwe kujenga naye urafiki kwa urahisi, akawa ni mtu wa kujitenga muda wote huku uso wake ukipambwa na huzuni.
“This black dude seems to be so strict like a guerrilla, many students are scared of him,” (Huyu jamaa mweusi anaonekana kuwa siriasi kama mpiganaji wa vita vya msituni, wanafunzi wengi wanamuogopa) “Im scared of him too! He might be with weary historical background and wounded soul.
(Hata mimi namuogopa. Lazima atakuwa na historia mbaya ya maisha ya zamani na nafsi iliyoumizwa).
Wanafunzi wawili walikuwa wakimjadili Harvey bila mwenyewe kujua, muda wa mapumziko baada ya kumuona akiwa amekaa peke yake kwenye bustani za maua, akionekana kuzongwa na mawazo. Akiwa amekaa katika hali ya huzuni, Harvey alishtukia mikono laini ikimziba macho kutokea upande wa nyuma. Alishtuka
kwani hakutarajia kuna mwanafunzi anaweza kuwa amemzoea kiasi cha kumfanyia masihara kiasi kile. Alimwachia, akageuka kumtazama, macho yake yakagongana na ya Skyler aliyekuwa amejawa na tabasamu pana usoni mwake.
“Jamani kaka Harvey! Mbona umekaa peke yako kinyonge namna hii? Nimekutafuta sana, nimeingia madarasa yote sijakuona kumbe umetulia huku? Vipi unayaonaje maisha mapya ya hapa shuleni,” alihoji Skyler kwa bashasha za hali ya juu huku akikaa pembeni ya Harvey.
“Kwa kiasi fulani, Harvey alichangamka baada ya kumuona Skyler, akainuka pale alipokuwa amekaa na wakaanza kutembea taratibu huku wakibadilishana mawazo. “Maisha mapya ni mazuri, shule nzuri, wanafunzi wazuri na kila kitu kizuri, nafurahi kusoma hapa kwani hapafanani kabisa na shule niliyokuwa nasoma kule kwetu Liberia.”
“Sasa kama ni hivyo mbona bado unaonekana kuwa na mawazo na muda mwingi umejiinamia kwa huzuni?” “Usijali dada’angu, unajua matukio niliyoyashuhudia maishani mwangu yamenifanya niwachukie binadamu wote. Roho inaniuma sana nikiwakumbuka wazazi wangu, ningekuwa na uwezo ningewafuata huko waliko… ili… na…mi…” Harvey alishindwa kumalizia sentensi yake, kilio cha kwikwi kikambana.
BAADA ya chombo alichokuwa anasafiria Harvey pamoja na maelfu ya watu wengine waliokuwa wanakimbia vita nchini Liberia kupinduka, watu karibu wote waliokuwa ndani ya chombo hicho wanapoteza maisha lakini Harvey kwa mara nyingine ananusurika kimiujiza na kuokotwa na msamaria mwema akiwa hajitambui. Continued after the jump ….
Anapelekwa mpaka Miami, nchini Marekani kwenye Hospitali ya Jackson Memorial ambapo baada ya kutibiwa kwa muda mrefu, hatimaye anarejewa na fahamu zake na kueleza historia ya maisha yake ambayo inamsisimua kila mtu, akiwemo Dk. Lewis. Baada ya kupata ahueni, anaruhusiwa kutoka hospitalini lakini anakosa mahali pa kwenda. Dk. Lewis anajitolea kumchukua na kwenda kuishi naye nyumbani kwake, Miami nchini Marekani. Anamtambulisha kwa mkewe na
mwanaye na anayaanza maisha mapya akiwa kama mwanafamilia kwenye familia hiyo. Anafanyiwa mpango wa kurejea shuleni na siku chache baadaye anaanza rasmi masomo ya sekondari kwenye shule ya Miami Elementary School. Hata hivyo, bado jinamizi la huzuni kali linamshambulia.
WAKATI Harvey na Skyler wakiendelea kuzungumza, kengele ya kuingia madarasani iligonga, ikabidi waachane kwani madarasa waliyokuwa wanasoma yalikuwa sehemu mbili tofauti. Harvey aliyekuwa kidato cha kwanza, majengo yao yalikuwa upande wa Kusini wakati Skyler aliyekuwa anasoma shule ya msingi, madarasa yao yalikuwa upande wa Kaskazini wa shule ile ya Miami Elementary School.
“Muda wa kurudi nyumbani ukifika unisubiri getini, mama atakuja kutuchukua,” alisema Skyler huku akimpungia mkono Harvey, kila mmoja akaelekea darasani kwake. Harvey akawa anajifuta machozi kwa kutumia kitambaa cha mkononi akikwepa kujulikana kuwa alikuwa akilia. Vipindi vilipoanza, somo lililokuwa la kwanza lilikuwa ni Baiolojia lililokuwa linafundishwa na mwalimu Wisconsin Myler ambaye pia alikuwa ndiyo mwalimu wao wa darasa.
“Ok guys, today we are going to discuss about human endocrine system. First of all let us start to discuss a hormone known as Adrenaline. Adrenaline is a natural stimulant made in the adrenal gland of the kidney. Adrenaline is carried in the bloodstream and affects the autonomous nervous system, which controls functions such as the heart rate and secretion of sweat and saliva.”
(Leo tutajadili kuhusu mfumo wa homoni wa mwili wa binadamu. Kwa kuanzia tutajadili homoni iitwayo Adrenaline. Hiki ni kichocheo cha asili ambacho kinazalishwa na tezi ya Adrenal kwenye figo. Adrenaline husafirishwa kwenye mkondo wa damu na kuathiri mfumowa neva za fahamu, zinazodhibiti kazi mbalimbali kama mapigo ya moyo,uzalishwaji wa jasho na mate)
Mwalimu Wisconsin alikuwa akifundisha mbele ya wanafunzi wa kidato cha kwanza, akawa anatumia mfumo wa maswali na majibu ili kuwafanya wanafunzi wazingatie alichokuwa anawafundisha. Aliendelea na somo kwa zaidi ya nusu saa, kabla ya kugundua kuwa kuna mwanafunzi ambaye kimawazo hakuwa pamoja na wenzake.
“Harvey, what is Adrenaline?” alimuuliza Harvey kwa sauti kubwa, wanafunzi wote wakageuka na kumtazama Harvey ambaye licha ya kuulizwa, alionekana kujiinamia kama ambaye hajasikia kile alichoulizwa.
“Harvey?” alisema mwalimu Wisconsin kwa sauti kubwa, safari hii akiwa amemsogelea kabisa Harvey. Kwa mshtuko mkubwa, aliruka pale alipokuwa amekaa, almanusra aanguke lakini mwalimu wake akamuwahi na kumkalisha vizuri. Akachukua karatasi aliyokuwa ameishika na kuanza kuiangalia.
Kumbe wakati mwalimu Wisconsin akifundisha, yeye alikuwa akichora picha za mauaji ya watu wengi vitani na wengine waliokuwa wanazama baharini. Licha ya kuwa hakuwa mchoraji mzuri, kile alichokuwa anakimaanisha kilijidhihirisha kwenye karatasi lile.
“Why are you drawing massacre pictures while I’m teaching?” (Kwa nini unachora picha za mauaji ya halaiki wakati mimi nafundisha?” “That is the only memory I have in my brain, im sorry.” (Hiyo ndiyo kumbukumbu pekee niliyonayo ndani ya kichwa changu, samahani). “What’s is your home country?” (Unatokea nchi gani?) mwalimu Wisconsin alimuuliza Harvey kwa sauti ya chini kiasi kwamba hakuna mwanafunzi aliyesikia.” “Liberia,” alijibu Harvey. “Go and wait for me at my office,”
(Nenda kanisubiri ofisini kwangu) alisema mwalimu Wisconsin baada ya kumuona Harvey ameanza kulengwalengwa na machozi. Alitii maelezo aliyopewa, akakusanya vifaa vyake na kwenda kumsubiri mwalimu yule kwenye ofisi yake. Baada ya kumaliza kipindi, mwalimu Harvey alifanya mazungumzo marefu na Harvey na kujaribu kumdadisi kwa undani juu ya matatizo yaliyokuwa yanamsumbua. Historia ya maisha yake ilimhuzunisha hata mwalimu yule, lakini akamsisitiza kuwa kwa sababu kilichompeleka pale
shuleni ni masomo, hakukuwa na maana ya kuendelea kukumbuka na kuumia moyoni kwa sababu ya matukio ambayo yalishapita. Muda mfupi baadaye, kengele ya kuhitimisha muda wa vipindi vya darasani iligonga, wanafunzi wakakusanyika kwenye eneo la mkusanyiko (assembly) na kupewa matangazo machache kabla ya kuruhusiwa kila mmoja kurejea nyumbani kwao.
“Harvey! Harvey! Im here (Nipo hapa) alisema Skyler kwa sauti huku akimkimbilia Harvey, akamuongoza mpaka sehemu ambayo mama yake huwa anakuja kumchukua na gari. Muda mfupi baadaye, Range Rover nyekundu iliwasili eneo lile la maegesho, mama yake Skyler akateremka na kwenda kuwachukua Skyler na Harvey. Aliwashika mikono kwa upendo, akawaongoza hadi kwenye gari ambapo safari ya kuelekea nyumbani ikaanza.
Licha ya kila mmoja kuendelea kujitahidi kumfariji Harvey aone kila kilichotokea ni cha kawaida, bado aliendelea kuwa vilevile. Muda mwingi akawa anajitenga na kukaa peke yake akiomboleza vifo vya wazazi na ndugu zake.
Siku ziliendelea kusonga, akafanya mtihani wake wa kwanza ambapo alikuwa mwanafunzi wa mwisho kati ya 45 waliokuwa wanasoma kidato cha kwanza. Matokeo yale yaliwasononesha sana Dk. Lewis, mkewe na mtoto wao Skyler sambamba na walimu wake. “Labda ni kwa sababu ya tofauti kubwa ya mazingira kati ya kwao Liberia na hapa Marekani.” “Wala tatizo siyo hilo. Bado anasumbuliwa na msongo wa mawazo na huzuni kali.” “Mimi nina wazo, labda tuanze kumpeleka kanisani huenda neno la Mungu likamsahaulisha matatizo yake.” “Nilishawahi kuzungumza naye kuhusu suala hilo, akasema hayupo tayari kwenda kanisani kwa sasa kwa sababu haamini kama Mungu yupo. Anasema kama kweli Mungu angekuwepo asingeruhusu wazazi wake wauawe na binadamu waendelee kuteseka kama anavyoteseka yeye.
“Mh, kama ndiyo hivyo basi tatizo lake ni kubwa zaidi,” alisema mama Skyler, wakabaki kutazamana na mumewe wakiwa hawajui namna ya kumsaidia. Muhula wa kwanza ulipomalizika, maendeleo ya Harvey shuleni yakawa bado hayaridhishi. Akawa anapata alama za chini katika mitihani kuliko mwanafunzi yeyote. Mwalimu wake wa darasa akawa na kazi ya ziada kuhakikisha anamrejesha Harvey kwenye mstari. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Unaona? Nilikwambia sahau hayo matatizo yako na elekeza nguvu kwenye masomo ukawa huelewi, matokeo yake kila siku unashika nafasi ya mwisho kwenye mtihani, una nini Harvey kisichoisha?” mwalimu Wisconsin alikuwa akizungumza na Harvey ofisini kwake. Alianza upya kazi ya kumshauri lakini wakati akiendelea na zoezi hilo, Harvey alikuwa akitiririkwa na machozi, hali iliyosababisha akatishe mazungumzo naye. Akamwambia aende darasani atazungumza naye siku nyingine.
Siku zilizidi kusonga mbele, Harvey akawa anazidi kuboronga kwenye masomo mpaka wanafunzi wenzake wakawa wanamtania kwa kumuita jina la Bogus. Akaingia kidato cha pili, hali bado ikawa ileile, muda wote akawa ni mtu wa machozi na maombolezo. Furaha ikaendelea kuwa msamiati mgumu kwake.
LICHA ya matatizo anayoyapitia kijana mdogo Harvey, bado Mungu yupo upande wake. Licha ya chombo alichokuwa anasafiria pamoja na maelfu ya watu wengine waliokuwa wanakimbia vita nchini Liberia kupinduka na watu karibu wote waliokuwa ndani ya chombo hicho kupoteza maisha, Mungu anamnusuru, anaokolewa na msamaria mwema anayempeleka Jijini Miami, nchini Marekani kwenye Hospitali ya Jackson Memorial. Continued after the jump ….
Baada ya kutibiwa kwa muda mrefu, hatimaye anarejewa na fahamu zake na kueleza historia ya maisha yake ambayo inamsisimua kila mtu, akiwemo Dk. Lewis. Baada ya kupata ahueni, anaruhusiwa kutoka hospitalini lakini anakosa mahali pa kwenda. Dk. Lewis anajitolea kumchukua na kwenda kuishi naye nyumbani kwake, Miami nchini Marekani. Licha ya kuyaanza maisha mapya na kutafutiwa shule, bado huzuni kali inamsumbua Harvey kila anapokumbuka jinsi wazazi wake na ndugu zake walivyouawa kikatili, jambo linalosababisha hata maendeleo yake shuleni kuwa ya kusuasua. Muda mwingi anajitenga na kujiinamia kwa huzuni.
SIKU zilizidi kusonga mbele, maisha ya Harvey shuleni pale yakawa yanazidi kudorora kila siku. Hakuwa na marafiki zaidi ya Skyler, muda wote akawa ni mtu wa kujiinamia huku akionekana kuwa na huzuni kali na majonzi. Mwaka ulipoisha, aliingia kidato cha pili, bado akawa anafanya vibaya kwenye mitihani yake, jambo lililozidi kuwakatisha tamaa Dk Lewis na mkewe.
Mara kwa mara, Dk Lewis alilazimika kuwa anamtembelea shuleni pale na kumfariji, akimtaka ajitahidi kusahau yote yaliyopita na nguvu zake zote kuzielekeza kwenye masomo. Dk Lewis alizungumza pia na mwalimu wake aliyempokea siku ya kwanza, Wisconsin na kumweleza kuwa kijana wake huyo anahitaji uangalizi wa karibu kwa sababu ya tatizo la msongo na huzuni kali lililokuwa linamkabili.
“Najitahidi sana kumuweka sawa lakini haelewi, inaonekana ameathirika kwa kiasi kikubwa sana. Hapendi kuzungumza na mtu zaidi ya Skyler na wenzake wanapomtania, amekuwa akitishia kuwaua.” “Sasa unafikiri tutafanya nini mwalimu?”
“Hatuna cha kufanya zaidi ya kuendelea kumsisitiza akazanie masomo. Muda husahaulisha hata yale ambayo katika hali ya kawaida ni vigumu kuyasahau.”
Baada ya mazungumzo yale kati ya Dk. Lewis na mwalimu Wisconsin, alizungumza kidogo na Harvey, akaendelea kumpa ushauri nasaha, kisha akaondoka na kurejea kazini kwake.
Matokeo ya nusu muhula wa mwaka wa pili yalipotoka, bado Harvey aliendelea kuburuza mkia, akashika tena nafasi ya mwisho. Hali iliendelea hivyo hata mwishoni mwa mwaka wa pili, akaingia kidato cha tatu na hatimaye, akaingia kidato cha nne huku historia ya maendeleo yake darasani ikizidi kudorora.
“Harvey mwanangu, huu ni mwaka wako wa mwisho, inabidi ujitahidi baba ili angalau upate alama zitakazokuruhusu kuendelea na masomo ya juu,” Suzan Lewis, Mke wa Dk Lewis alikuwa akimpa ushauri mwanaye huyo wa hiyari.
“Nitajitahidi mama ingawa bado kumbukumbu mbaya zinanisumbua ndani ya kichwa changu.”
“Kumbukumbu gani zisizoisha Harvey? Kumbuka wewe ni mwanaume, miaka michache baadaye utakuwa na familia yako na itabidi wewe ndiyo uwe kiongozi wa kila kitu. Utaweza vipi kuimudu familia kama hujiamini na badala yake unaumizwa sana na mambo ambayo yalishapita miaka mingi?”
“Anachokisema mama ni kweli Harvey, jitahidi kakaangu,” alidakia Skyler, akaenda kukaa kiti kimoja na Harvey na kumlalia miguuni.
Muda mfupi baadaye, mama Skyler alitoka na kwenda kuandaa chakula cha jioni, akawaacha wakiwa wawili tu sebuleni. “Unajua kaka Harvey wewe ni mzuri sana, yaani kama ungekuwa unazingatia masomo na kuachana kabisa na mawazo juu ya mambo ambayo yalikutokea miaka mingi iliyopita maishani mwako, tayari ungeshakuwa na mchumba mzuri pale shuleni kwani kila siku wasichana unaosoma nao wananiuliza kuhusu habari zako.”
“Siyo kwamba napenda kuwa hivi Skyler, hata mimi nina moyo, hebu vuta picha kama ndiyo ungekuwa wewe umewapoteza wazazi wako wote wawili pamoja na ndugu zako huku ukishuhudia, ungeweza kusahau kweli?”
“Ningejitahidi kusahau kaka Harvey, lakini wewe umezidi, yaani kuna kipindi hata mimi naogopa kukaa jirani na wewe. Jitahidi kaka’angu,” alisema skyler huku akijilaza vizuri miguuni kwa Harvey.
Siku zilizidi kusonga kwa kasi na hatimaye siku ya kufanya mtihani wa mwisho wa kuhitimu elimu ya sekondari iliwadia, Harvey na wanafunzi wenzake waliokuwa wanasoma kidato cha nne, wakaingia chumba cha mtihani. Kwa kuwa walikuwa wakisoma masomo tisa, iliwachukua wiki nzima kumaliza mitihani yote, walipomaliza, ikabidi Harvey arudi nyumbani kwenda kusubiria matokeo.
Miezi miwili baadaye, matokeo ya mtihani wa kidato cha nne, yalitoka. Katika hali ambayo kila mmoja aliitegemea, Harvey alipata divisheni ziro baada ya kupata alama F katika masomo yote.
“Si nilikuambia mwanangu? Unaona sasa umevuna ulichokipanda!” alisema Dk Lewis kwa masikitiko.
“Mimi mwenyewe kila siku nilikuwa namwambia kuwa elimu ndiyo itakayoziba mapengo ya wazazi wake lakini hakuwa akitilia maanani, sasa wazazi kawakosa na elimu kaikosa pia,” aliongezea mkewe.
“Unanihuzunisha sana Harvey, sasa unafikiri tutakupeleka wapi ikiwa umeshindwa kufanya vizuri kwenye mtihani?” “Nataka kurudi nyumbani kwetu Liberia, lazima nikalipe visasi kwa wote waliohusika kuwapoteza wazazi na ndugu zangu,” alijibu Harvey huku akilengwalengwa na machozi.
“Yaani mpaka leo bado unafikiria kulipa kisasi? Wewe ni binadamu wa namna gani usiyesahau?” alihoji kwa jazba Dk Lewis. “Huyu bwana anajiendekeza, mi nishamchoka, tumtafutie tu nauli aondoke zake,” alisema mke wa Dk Lewis.
“Hapana mke wangu, tusifanye hivyo, tulishakula yamini ya kuhakikisha tunafanya kila liwezekanalo kuyabadilisha maisha yake, hatutakiwi kukata tamaa.”
“Mama usimuache kaka Harvey akaondoka, mi nimeshamzoea na nampenda sana kaka’angu, mpe nafasi nyingine atajirekebisha,” alisema Skyler katika kikao maalum cha wanafamilia kilichowakutanisha Harvey, Dk Lewis, mkewe na Skyler.
Kwa jinsi ilivyoonesha, mama Skyler alishachoka na hali aliyokuwa nayo Harvey lakini bado Dk Lewis na mwanaye Skyler walikuwa na matumaini makubwa kuwa ipo siku atabadilika. “Mimi nina wazo lakini sijui kama Harvey mwenyewe atalikubali.” “Wazo gani mume wangu?” “Kwa kuwa ameshindwa kufanya vyema katika masomo ya darasani, nafikiri itakuwa busara kama tukimpeleka katika chuo cha ufundi.” “Wazo zuri sana mume wangu, hata mimi naliunga mkono.”
“Hata mimi baba naliunga mkono,” alisema Skyler, kwa pamoja wakamtazama Harvey kusikia atasema nini. “Harvey, baba yako ametoa wazo kuwa uende kusomea masomo ya ufundi, mbona unanyamaza kimya bila kujibu chochote? Au hutaki?” alihoji mama Skyler, Harvey akafikiria kwa muda mrefu bila kusema kitu chochote, baada ya ukimya wa zaidi ya dakika tatu, akafumbua mdomo wake na kusema kuwa yupo tayari.”
“Mbona umefikiria kwa muda mrefu kiasi hicho? Kama haupo tayari ni bora useme mapema, tusije tukaharibu fedha zetu ukaishia kufeli kama ulivyofanya kwenye masomo ya sekondari,” alisema mama Skyler, Harvey akawahakikishia kuwa yupo tayari kwa moyo wake wote na kwamba atajitahidi kwa kadiri ya uwezo wake wote
Baada ya mazungumzo yale yaliyochukua zaidi ya saa tatu, walimshukuru Mungu wao kisha kila mmoja akaelekea chumbani kwake kulala.
Kulipopambazuka, Dk Lewis alianza kufanya taratibu za kumtafutia Harvey chuo cha ufundi kama walivyokuwa wamekubaliana. Akaenda kuulizia nafasi katika Chuo cha Miami Engineering College kilichokuwa ndani ya Jiji la Miami, nchini Marekani. Kutokana na kufahamika kwake, Dk. Lewis alipata nafasi haraka katika kitivo cha Mechanical Engineering (Ufundi Makenika).
Kwa kuwa alitembea na kiwango cha fedha kilichokuwa kinatosha kulipia karo, alimaliza kila kitu. Akalipa ada ya mwaka mzima na kurudi nyumbani akiwa na furaha. Akamuita mkewe, Harvey na mwanaye Skyler ambapo walikaa tena kikao cha familia na kuwaeleza alipokuwa amefikia.
Kila mmoja alifurahi sana, hata Harvey mwenyewe kwa mbali alionesha kutabasamu ikiwa ni ishara ya kufurahishwa na jinsi familia ya Dk. Lewis ilivyokuwa inamjali.
MCHUMA janga hula na wa kwao! Tabia ya kuendekeza huzuni na kumbukumbu zenye kuumiza inamfanya Harvey ashindwe kuzingatia masomo yake. Hali hiyo inasababisha apate matokeo mabaya kwenye mitihani yote, tangu akiwa kidato cha kwanza hadi cha tatu. Hatimaye anaingia kidato cha nne, licha ya ushauri anaopewa na walezi na walimu wake mara kwa mara , bado anashindwa kuzingatia masomo na matokeo yake anapata divisheni ziro kwenye mtihani wa kuhitimu elimu ya sekondari. Continued after the jump ….
Matokeo hayo yanawasikitisha sana Dk Lewis na mkewe, wanajadiliana nini cha kufanya kwenye kikao cha familia lakini Harvey anang’ang’ania kuwa anataka kurejea kwao Liberia na kulipiza kisasi kwa wote waliohusika kuwaua wazazi na ndugu zake. Hata hivyo, baadaye anabadili msimamo ambapo anakubaliana na wazo la kupelekwa kwenye chuo cha ufundi. Ari mpya inaamka ndani ya moyo wake, anajiapiza kuwa atafanya kila liwezekanalo kushindana na huzuni kali na mawazo mabaya yaliyokuwa yanamtesa, anaweka nadhiri ya kuhakikisha anasoma kwa bidii na kuwafuta machozi walezi wake ambao matokeo yake ya kidato cha nne yaliwavunja sana nguvu. Dk Lewis anaanza taratibu za kumtafutia chuo, anaenda kumuandikisha Miami Polytechnic and Engineering College ambapo anamtafutia nafasi katika kitengo cha Mechanical Engineering.
HARVEY alifarijika sana kwa namna Dk Lewis na familia yake walivyoendelea kuwa naye katika hali zote. Kitendo cha wao kuanza kufikiria nini watamfanyia baada ya kufeli mtihani wa kidato cha nne, kuliamsha ari mpya iliyokuwa imepotea ndani ya moyo wake. Akatambua fika kuwa walikuwa na nia ya kweli ya kumsaidia hivyo hakutaka kuendelea kuwavunja moyo.
Akaahidi kufanya kila linalowezekana ili afaulu masomo yake ikiwa kama malipo ya fadhila alizokuwa anafanyiwa. Kwa kuwa chuo kile kilikuwa na nafasi za bweni pekee, maandalizi ya vifaa vyote muhimu vilivyokuwa vinahitajika, yalianza kufanyika. Dk Lewis akamchukua Harvey na kwenda kufanya ‘shopping’ ya vitu mbalimbali vilivyokuwa vikihitajika shuleni.
Baada ya kuzunguka kwenye maduka mbalimbali kwa siku mbili mfululizo, vifaa vyote muhimu kwa ajili ya Harvey vilipatikana, akawa anafanya maandalizi ya mwisho kabla ya kuondoka kuelekea chuoni. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Jamani kaka Harvey, unaondoka unaniacha na nani? Mi nishakuzoea jamani,” alisema Skyler huku akifungua mlango wa chumba cha Harvey, akaingia na kwenda kujitupa kitandani kwa Harvey. Alimjibu kwa kifupi kuwa atakuwa akienda kuwatembelea pale nyumbani kwao mara kwa mara kwa kuwa chuo hakikuwa mbali, akaendelea kupanga vitu vyake.
Licha ya kumwambia vile, Skyler hakuridhika, akainuka pale kitandani alipokuwa amelala na kusimama, akamsogelea Harvey huku machozi yakimlengalenga. Harvey alizitambua hisia zake, naye akamsogelea na kumkumbatia kwa nguvu, Skyler akajilaza kifuani kwake kama mtoto afanyavyo anapobebwa na mama yake huku machozi yakiulowanisha uso wake mzuri.
“Usijali dada’angu, kimwili tutakuwa mbali lakini kiakili tutaendelea kuwa pamoja, wala usiwe na wasiwasi.” “Hapana kaka Harvey, mi najisikia wivu mwenzio… najua huko unakoenda utakutana na wasichana wazuri watakaokushawishi uanzishe nao uhusiano wa kimapenzi.”
“Hapana Skyler, mimi sipo hivyo, we mwenyewe unanijua. Lakini hata hivyo, kwani we hupendi kaka yako nikuletee wifi mzuri?” “Sitaki, sitaki kabisa kusikia hizo habari… kumbe hunipendi kaka Harvey.” “Basi nisamehe dadaangu, nakupenda sana na sitaki kukuudhi! Si unajua we ndiyo dadaangu wa ukweli?” alisema Harvey, lakini
katika hali ambayo hata yeye ilimshangaza, Skyler hakutaka kumuachia, aliendelea kumkumbatia kwa nguvu kifuani kwake huku machozi yakiendelea kumtoka. “Basi usilie Skyler, nenda chumbani kwako kalale si unajua tayari ni usiku na kesho unatakiwa kuwahi shuleni?” alisema Harvey lakini Skyler akawa ni kama hasikii. Aliendelea kumkumbatia kwa muda mrefu mpaka aliporidhika, akamuachia huku macho yake yakizungumza lugha ambayo hakuielewa.
Baada ya Skyler kuondoka, Harvey aliendelea na maandalizi yake, alipomaliza akaenda kuoga na kurudi chumbani kwake kulala. Vitendo alivyofanyiwa na Skyler vilimfanya ajiulize maswali mengi kichwani mwake bila majibu. Akajipa moyo kuwa hakuna chochote kibaya alichokuwa anakiwaza kwani alimchukulia kama mdogo wake waliyezaliwa tumbo moja.
Kulipopambazuka, familia nzima ilimsindikiza Harvey mpaka chuoni. Saa moja za asubuhi juu ya alama, Range Rover nyekundu iliyokuwa inaendeshwa na mke wa Dk. Lewis, Suzan iliwasili kwenye lango la kuingilia kwenye Chuo cha Miami Polytechnic and
Engineering College, pembeni yake akiwa amekaa mumewe na siti ya nyuma wakiwa wamekaa Harvey na Skyler. Baada ya kukamilisha taratibu za pale langoni, waliruhusiwa kuingia mpaka ndani, gari likaenda kusimama mbele ya jengo lililokuwa na maandishi makubwa yaliyosomeka ‘Adminstration Block’, wakateremka na kuanza kushusha mizigo. Baada ya kukabidhiwa kwa wakufunzi wa chuo kile, waliagana tayari kwa kuondoka.
“Kaka Harvey nakuomba uniweke mimi kwenye kumbukumbu zako muda wote. Usinisahau jamani, nakupenda sana kakaangu,” alisema Skyler huku akiwa amemkumbatia Harvey wakati wakiagana. Skyler alimkumbatia Harvey kwa muda mrefu huku akionekana kuvuta hisia nzito, mpaka mama yake alipopiga honi na kumwambia kuwa atachelewa shule, akamuachia huku akijifuta machozi.
“Mwanao kamzoea sana Harvey, atajisikia vibaya sana kuishi naye mbali, hebu mtazame anavyolia,” Dk Lewis alikuwa akiongea na mkewe wakati Skyler akitembea kinyonge na kuingia ndani ya gari. Gari likaanza kuondoka huku wakipungiana mikono na Harvey. Skyler alishindwa kujizuia, akawa analia kwa kwikwi.
Walimfikisha mpaka shuleni kwao, akateremka na kuelekea darasani huku akionekana kuwa mnyonge kuliko siku zote. Baada ya hapo, mama Skyler alimpitisha mumewe kazini kisha na yeye akaelekea ofisini kwake.
Harvey akawa ameyaanza maisha mapya chuoni kwani muda mfupi baada ya familia yake kuondoka, alipelekwa kwenye bweni walilokuwa wanaishi wanachuo wenzake wa mwaka wa kwanza, akapewa chumba ambacho tayari kulikuwa na wanachuo wengine watatu, yeye akawa wa nne.
Alipoanza rasmi masomo, kidogo alijitahidi kujirekebisha, akawa siyo mtu wa kukaa na kujiinamia peke yake, nguvu zake zote alizielekeza kwenye masomo ingawa bado hakupenda kujichanganya na wenzake, muda mwingi akawa anautumia darasani baada ya masomo akawa anapenda kwenda kufanya mazoezi ya mpira wa kikapu kwenye uwanja wa chuo.
Taratibu akaanza kuuelewa mchezo huo kuliko mwanzo, siku zikawa zinazidi kusonga mbele, akayazoea maisha ya chuo na wanachuo wenzake wakaanza kumfahamu na kupenda kufanya naye mazoezi ya mpira huo.
“Ebwana kuna yule mwanafunzi mgeni wa mwaka wa kwanza anaitwa nani sijui, mweusi hivi halafu mrefu, anacheza basketball huyo, sijapata kuona.”
“Anaitwa Harvey lakini tatizo lake huwa hapendi kabisa kujichanganya na wenzake, hata mazoezi huwa anafanya peke yake.” “Nasikia hata alipokuwa anasoma sekondari alikuwa anapenda kujitenga hivyohivyo, sijui ana matatizo gani?”
“Lakini licha ya kujitenga kwake, mi namkubali sana kutokana na jinsi alivyo na kiwango kikubwa, akibadili tabia zake anaweza kuja kuwa mtu maarufu sana hapa Marekani na duniani kote.” wanafunzi wawili, Mike na Angelus waliokuwa wanasoma chuo kimoja na Harvey, walikuwa wakimjadili.
Si hao tu, uwezo mkubwa wa Harvey kwenye mchezo wa basketball ulimfanya awe gumzo chuo kizima, kila mahali akawa anazungumziwa yeye ingawa wengi walikuwa wakishangazwa na tabia yake ya kupenda kujitenga. Mabinti nao walichanganywa sana na jinsi Harvey alivyokuwa na umbo zuri la kimazoezi. Kifua chake kilikuwa kimejengeka vizuri kimazoezi, mikono yenye
nguvu na urefu wake, vilikuwa ni miongoni mwa vitu vilivyowachanganya sana wanachuo wa kike. Japokuwa Harvey alikuwa akiishi chuoni hukohuko, karibu kila mwisho wa wiki Skyler alikuwa akienda kumtembelea na kumpelekea zawadi mbalimbali yakiwemo maua, kadi, chokleti na vitu vingine vizuri kwa lengo la kumfariji na kumsahaulisha matatizo aliyokuwa nayo.
Kila mwisho wa wiki hakukosa kufika chuoni pale mpaka wanachuo wengine hasa wa kike wakaanza kumchukia kwani waliona kama anawanyima nafasi ya kuongea na Harvey. Wachache waliufahamu ukweli kuwa alikuwa mdogo wake ingawa wengine walikuwa wakihisi kuwa huenda wana uhusiano mzito wa kimahaba.
“HARVEY! Harvey! Tafadhali simama nahitaji kuongea na wewe, nipe nafasi ya dakika tano tu zitatosha kabisa,” ilikuwa ni sauti nyororo ya msichana mrembo aliyeitwa Suzan ambaye walisoma darasa moja na Harvey. “Sawa,” Harvey alijibu. “Tunaweza kusogea pembeni kidogo?” “Bila shaka” Taratibu wakajikongoja na kusogea pembeni.
“Harvey tafadhali nipe muda wako kidogo, ni siku nyingi nimehitaji kuongea na wewe jambo fulani lakini moyo wangu umekuwa na kigugumizi.” “Nieleze tu wala usiogope.” “Kwanza kabisa nahitaji kujua hivi kweli Skyler ni dada yako?” Ukimya wa dakika kama tatu ukatokea, wote wawili ni kama vile walishikwa na vigugumizi. “Suzan!” Harvey aliita. “Mh!” “Niwie radhi kwa swali langu nahitaji kujua tu.” “Uliza tu usijali.”
“Unajua ukweli kutoka moyoni mwangu wewe kama mwanaume umeshasoma macho yangu ukaelewa nini nataka kutoka kwako, Harvey ni siku nyingi tu nimekupenda na mara nyingi joto la penzi limekuwa likinitesa ndani ya moyo wangu…” aliongea Suzan.
Harvey akanyanyua macho yake na kumkodolea Suzan akijaribu kuyasoma macho yake kwa umakini wa hali ya juu, alitaka kuona dalili zilizokuwa ndani ya macho yake kwamba kweli alimpenda kama alivyomaanisha.
Akayashuhudia machozi yakitiririka mashavuni mwa msichana huyo mrembo, akashawishika kunyoosha mikono yake na kumkumbatia kisha kumsihi aache kulia na amjibu swali alilokuwa amemuuliza. “Sikiliza Suzan, mimi na Skayler ni mtu na dada yake huo ndiyo ukweli wangu na ninaomba uupokee. “Ni kweli?” “Hakika.” “Lakini watu wanasema ninyi ni wapenzi?’ “Si kweli hata kidogo, ninachokueleza mimi ndicho hicho.” “Mh!” Suzan akaguna huku akimwangalia Harvey .
“Basi naomba mimi niwe mpenzi wako kama kweli Sklayer ni dada yako?” “Suzan sijawaza wala kufikiria kuwa na mpenzi ingawa umri wangu unaniruhusu kufanya hivyo nataka nisome mpaka nitimize
malengo na ndoto zangu zote ndipo mapenzi yafuate,” aliongea Harvey machozi yakimbubujika. Alikuwa katika kipindi kigumu katika maisha yake, mara kadhaa alipoikumbuka familia yake na maisha aliyowahi kuishi huko nyuma yalikuwa yakimuumiza sana, alitamani kuwa na wazazi wake wote pamoja na dada yake lakini bahati mbaya walikuwa wametangulia mbele ya haki.
“Harvey kwa nini unalia? Nimekuudhi? Basi naomba unisamehe halikuwa kusudio langu ni mapenzi ndiyo yamenipeleka huko, Harvey ninakupenda tangu siku ya kwanza nilipokuona na ningependa uwe wangu.” “Hapana Suzan kwa sasa siko tayari nipe muda kwanza nitakujibu.” “Mpaka lini?” “Sijui ila ninaomba muda…ahsante na naomba sasa tuagane mimi niende bwenini kupumzika.” “Basi sawa lakini weka jambo hili kichwani mwako kwamba mimi Suzan ninakupenda ningependa siku moja niwe wako,” alimaliza Suzan na kila mmoja akashika njia yake.
Ni kweli kabisa tangu Harvey aingie chuoni hapo siku ya kwanza tu Suzan alipomwona alihisi mapigo yake ya moyo yakienda kasi, alimpenda kijana huyo kupita maelezo na alikuwa akitafuta ni namna gani angeweza kumwingia kijana huyo ampate na kuwa wake
lakini maneno ya watu wengi chuoni humo yalimvunja moyo kwamba kijana huyo asingekubali kuwa mpenzi wake kwa sababu tayari alishakuwa na wake tangu mwanzo na hata yeye mwenyewe Suzan pamoja na kusikia aliona kwa macho yake jinsi Harvey alivyopendwa na Skayler ndiyo maana baada tu ya kupata wasaa wa kuongea naye alijaribu kutupa ndoano yake bila woga wowote. ***
“Nitaendelea kumpatia zawadi mfululizo bila kuchoka na mwisho nitamwingiza kwenye mtego wangu, siko tayari kumkosa Harvey, nataka awe wangu kwa gharama yoyote ile, eti kaka nani kasema, hiyo ni danganya toto tu nadhani hata yeye mwenyewe hajagundua kwamba ninahisi penzi ndani ya moyo wangu, nitahakikisha ninampata…” aliwaza Skyaler siku moja akiwa chumbani
kwake akitazama albamu ya picha na kuiona picha ya mwanaume aliyempenda na kuapa kumpata. Alipoingia ndani ya nyumba yao na kutambulishwa kwake kama kaka yake, Skyaler alimpokea lakini kadiri siku zilivyozidi kusonga
alihisi hali ya tofauti, uzuri wa kijana huyo uliichanganya akili yake pamoja na kwamba alikuwa katika hali ya ugonjwa lakini uzuri wake hakika haukujificha hata kidogo, moyoni mwake akaapa kumfanya mpenzi wake wa maisha pamoja na kufahamu kwamba hilo lilikuwa ni kosa la jinai kwani wazazi wake wasingekuwa tayari kukubali jambo hilo.
“Najua itakuwa ngumu lakini nitaufanya kwa siri kubwa uhusiano wangu mimi na Harvey na nitamweleza wazi kwamba muda mwingi nimekuwa nikimtaka mapenzi najua hata yeye hatakataa, atakubali kwa uzuri nilionao,” aliwaza Skyaler akivuta shuka lake na kujifunika gubigubi. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Ndani ya kichwa chake alifahamu wazi kwamba alikuwa akicheza mchezo hatari lakini ambao pengine ungeleta shida au matatizo katika maisha yake lakini alitaka kujaribu bahati yake kwa kuwa na kijana mzuri kama Harvey.
“Nitasubiri akirudi tu likizo nimweleze ukweli naye nitamtaka afanye siri kubwa sihitaji baba wala mama afahamu uhusiano wetu, lakini pia nitahakikisha anapata mahitaji yote muhimu kama ilivyo kwangu…ninampenda kuliko maelezo…”
Wanakaa kikao cha familia kujadili nini cha kufanya baada ya Harvey kufeli, mwenyewe anasisitiza kuwa anataka kurejeshwa nchini kwao Liberia kwa ajili ya kazi moja tu, kulipa kisasi kwa wote waliohusika kuiangamiza familia yao. Dk Lewis, mkewe na mtoto wao, Skyler wanajaribu kumbadilisha mtazamo ambapo baadaye wanafikia muafaka kuwa apelekwe kwenye chuo cha ufundi. Anaandikishwa katika Chuo cha Miami Polytechnic and Engineering, katika kitengo cha Mechanical Engineering. Anayaanza masomo huku akiahidi kurekebisha makosa aliyoyafanya awali. Anaelekeza nguvu zake zote kwenye masomo huku akiutumia muda wa ziada kufanya mazoezi ya basketball. Kadiri siku zinavyozidi kwenda mbele, anazidi kung’ara katika mchezo huo, hali inayosababisha wanachuo wengi wa kike waanze kumtamani kimapenzi. Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…
“KAKA Harvey mbona siku hizi nikija kukusalimia nakukuta unazungumza na wasichana… unajua mi sipendi Harvey, sipendi nasema,” alilalamika Skyler na kumfanya Harvey awe na kazi ya ziada kujitetea mbele yake. “Lakini Skyler nilishakwambia kuwa sihitaji kuwa nao kimapenzi kwa sasa, naomba uniamini, usimwambie baba au mama, sina uhusiano wowote nao, ” alisema Harvey kwa kujitetea, akiamini anafanya yale mbele ya mdogo wake, kumbe haikuwa hivyo kwa upande wa Skyler, kichwani mwake alikuwa akiwaza mapenzi.
Wivu wa kimapenzi ulikuwa ukimsumbua ndani ya mtima wake. Japokuwa hakuwahi kumtamkia jambo lolote la kumtaka kimapenzi, aliamini ishara alizokuwa anamuoneshea zinatosha kufikisha ujumbe aliokusudia. Jambo hilo lilimfanya ajisikie vibaya kila alipokuwa anaona wasichana wanamshangilia Harvey anapokuwa kwenye mazoezi ya basketball.
Baada ya Harvey kutumia muda mwingi kumbembeleza, hatimaye Skyler alitulia, wakawa wanapiga stori na kukumbushana mambo mbalimbali ya nyumbani.”
“Yaani siku hizi hadi najiona kama nakonda, nilikuzoea sana kaka Harvey… napata sana shida kwa kuwa muda mwingi upo mbali nami.” “Usijali Skyler, bila shaka utafurahi sana kusikia kaka yako nimefaulu masomo ya chuo, nakumbuka jinsi ulivyoumizwa na matokeo yangu ya kidato cha nne, jikaze bado miezi michache nitarudi nyumbani kwa likizo fupi,” alisema Harvey huku akimpigapiga Skyler mgongoni kumbembeleza.
Baada ya kukaa pamoja kwa saa zaidi ya mbili, Harvey alimsisitiza Skyler umuhimu wa kuwahi nyumbani. Kwa shingo upande Skyler akakubali kuondoka kwa ajili ya kwenda kufanya maandalizi ya shule siku inayofuatia kwani siku ile ilikuwa ni Jumapili. “Kwani mimi nina kasoro gani mpaka Harvey hanitamkii kuwa ananipenda? Kwa nini anavutiwa na kina Suzan na wanachuo wengine wa kike kuliko mimi,” alijisemea Skyler muda mfupi baada ya kuwasili nyumbani kwao, akiwa nyuma ya kioo kikubwa chumbani kwake.
“Akavua nguo moja baada ya nyingine na kubaki na ‘skin-tight’ pekee, akawa anageuka na kujishika kiuno kama wafanyavyo warembo wanapokuwa kwenye mashindano ya umiss. Alifanya vile kwa muda mrefu, akawa anajikagua kila kiungo katika mwili wake kuona kama hana kasoro.
“Sura yangu nzuri na inawavutia wengi, hata mama huwa ananiambia kila siku kuwa mimi ni mzuri sana… kifua changu bado kichanga, rangi ya ngozi yangu inafanana na chokleti… kwa nini Harvey hanipendi lakini? Kwa nini? Roho yangu inauma sanaaa,” alisema Skyler huku akilengwalengwa na machozi, akazibana vizuri nywele zake ndefu na nyeusi, zilizokuwa zinakaribia kufika kiunoni.
“Harvey… I love you baby, please be mine, come and show me the meaning of love… come and teach me how to love…” (Harvey… nakupenda mpenzi, nakuomba uwe wangu, njoo unioneshe maana ya mapenzi… njoo unifundishe namna ya kupenda…)
alisema Skyler kwa sauti ya kunongo’na huku ameikumbatia picha ya Harvey kwenye kifua chake kilichokuwa na vifuu vyenye ukubwa wa wastani na ngozi laini kama sufi, akajilaza chali taratibu akiwa bado ameikumbatia picha ile, machozi yakawa yanatiririka kupitia kona za macho yake na kulowanisha shuka. *** Harvey alizidi kupata umaarufu pale chuoni kwao, idadi ya marafiki zake ikaanza kuongezeka kwa kasi. Japokuwa hakuwa mwepesi wa kuwachangamkia watu wengine, kutokana na jinsi alivyokuwa anacheza vizuri mchezo wa basketball, alijikuta wanachuo wenzake wakianza kumchangamkia kila wanapomuona, jambo lililomfanya taratibu aanze kuachana na tabia ya kujitenga.
“Siamini kama Harvey mimi naweza kuheshimika kiasi hiki, tazama kila ninapopita nasikia wanachuo wenzangu wakilitaja jina langu… siamini kabisa. Hata darasani kila mtu anapenda kukaa karibu na mimi, naona kama muujiza mkubwa…eeh Mungu nisimamie, bado safari yangu ni ndefu,” Harvey alijisemea akiwa amejilaza juu ya kitanda cha ‘double decker’, ndani ya bweni
kwenye chuo cha Miami Polytechnic and Engineering College alipokuwa anasoma. Kumbukumbu za mambo yaliyomtokea zamani zikawa zinamezwa kwa kasi na faraja na sifa alizokuwa anazipata kutoka kwa wanafunzi wenzake kwa sababu ya kiwango kikubwa cha mchezo wa basketball alichokuwa nacho.
“Harvey, tunakuomba uwe unafanya mazoezi na timu ya chuo ya basketball kwani siku chache zijazo mashindano ya NCCA yataanza na hatutaki chuo chetu kipate aibu… tunaamini utakuwa mchango mzuri kwetu,” nahodha wa timu ya mpira wa kikapu ya chuoni pale, Cazzard Emmert alikuwa akimwambia Harvey.
Harvey alikubali, habari ambazo zilipokelewa kwa furaha na wanachuo wengi, kila mmoja aliamini ataibeba timu yao kutokana na kipaji kikubwa alichokuwa nacho.
Kama alivyoahidi, siku iliyofuatia Harvey akaanza rasmi mazoezi na timu ya chuo ikiwa ni maandalizi ya michuano mikubwa ya mpira wa kikapu kwa wanafunzi wa vyuo nchini Marekani iliyopewa jina la National Collegiate Athletic Association au kwa kifupi NCAA. Michuano ya NCAA, kwa kawaida ilikuwa ikizishirikisha timu za mpira wa kikapu kutoka vyuo zaidi ya 68 ambapo kwa miaka mingi, Vyuo Vikuu vya UCLA, Kentucky, Indiana, North Carolina na Duke ndivyo vilivyokuwa vikibadilishana ushindi na kushika nafasi za juu.
“Mwaka huu ni zamu ya Miami Polytechnic and Engineering College kuchukua ubingwa, tumejifua vya kutosha na nawaomba wapenzi wa mchezo huu wa basketball waishangilie timu yetu kwani tuna wachezaji wenye ari, nguvu na kila sababu ya kuchukua ubingwa kama Harvey,” nahodha wa timu ya mpira wa kikapu ya chuo kile, Cazzard alikuwa akitoa tambo kwenye runinga wakati
akihojiwa na kituo maarufu cha CBS kilichokuwa kinasifika kwa kuonesha vizuri mechi zote za mashindano hayo. Shamrashamra za maandalizi ya mashindano hayo ambayo yalipangwa kuzinduliwa rasmi kwenye makao makuu ya NCCA yaliyopo White River State Park, Indianapolis katika Jimbo la Indiana nchini Marekani ziliendelea kwa nguvu, Harvey akazidisha
kasi ya kufanya mazoezi ambapo kila baada ya kumaliza ratiba ya mazoezi na timu ya chuo alikuwa akitenga muda wa mazoezi binafsi.
“Harvey bwana mi sipendi uwe unafanya mazoezi kifua wazi, si unaona wale wasichana wanavyokuangalia kichokozi, umbo lako limejengeka vizuri sana, usilioneshe ovyo, cheki kifua kilivyotanuka,” alisema Skyler jioni moja baada ya kumtembelea Harvey chuoni pale na kumkuta akifanya mazoezi na timu ya shule huku wasichana wengi wakiwa wamekaa makundi-makundi pembeni ya uwanja.
Wote walionekana kumkazia macho Harvey na alipokuwa anafunga magoli walikuwa wakimshangilia kwa nguvu. Harvey alimjibu Skyler kuwa amemuelewa alichokisema, akaahidi kuwa hatakaa kifua wazi tena.
Siku zikawa zinasonga kwa kasi, hatimaye siku ya ufunguzi wa mashindano hayo ikawadia. Harvey na wanachuo wengine wakasafiri kwa basi la shule hadi Indianapolis, mahali ufunguzi wa mashindano hayo ulipokuwa ukifanyika. Timu yao ikawa miongoni mwa ambazo zilipanga kuanza mechi siku ya ufunguzi.
Licha ya kupata matokeo mabaya kwenye mtihani wa mwisho wa kuhitimu kidato cha nne, Dk Lewis na familia yake bado wanaahidi kumsaidia Harvey kwa uwezo wao wote. Hali hiyo inamfanya aamue kuwatoa kimasomaso kwa kukazana kwenye masomo na kuendelea na mazoezi ya mpira huo wa kikapu. Nyota ya umaarufu inaanza kumuwakia kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza mpira wa kikapu. Anaanza kuwa gumzo miongoni mwa wanachuo wenzake na anaitwa kuichezea timu ya chuo kwenye mashindano makubwa ya mchezo wa mpira wa kikapu kwa wanafunzi wa vyuo nchini Marekani (NCAA). Upande wa pili, Skyler anaanza kuonesha dalili za mapenzi kwa kaka yake huyo wa hiyari lakini Harvey anakuwa mgumu wa kumuelewa kwani anamchukulia kama mdogo wake. Wanachuo wa kike nao wanazidi kuchanganywa na uzuri na kipaji alichokuwa nacho Harvey.
Michuano mikubwa ya mpira wa kikapu kwa wanafunzi wa vyuo nchini Marekani iliyopewa jina la National Collegiate Athletic Association au kwa kifupi NCAA, ilizinduliwa rasmi katika makao makuu ya NCAA yaliyopo White River State Park, Indianapolis katika Jimbo la Indiana nchini Marekani.
Wanafunzi kutoka kwenye vyuo vipatavyo 68 vikiwemo UCLA, Kentucky, Indiana, North Carolina na Duke walifurika kwa wingi kwenye uzinduzi huo. Chuo cha Miami Polytechnic an Engineering nacho hakikuwa nyuma.
Ratiba ikaonesha kuwa timu ya chuo alichokuwa anasomea Harvey kitafungua mashindano hayo kwa kucheza na timu ya UCLA, mechi ambayo ndiyo ilikuwa ya kwanza kabisa. Vuguvugu la sintofahamu likatanda miongoni mwao kwani UCLA ndiyo walikuwa mabingwa watetezi.
Muda mfupi baadaye, wachezaji waliokuwa katika kikosi cha kwanza na wale wa ;reserve’ wa Chuo cha Miami Polytechnic Engineering and College walishabadilika kimavazi ndani ya chumba cha kubadilishia mavazi, wakatoka wakikimbia mpaka kwenye
uwanja, wakaanza kufanya mazoezi mepesi mepesi ya kupasha misuli moto huku wakishangiliwa na mashabiki wao. Muda mfupi baadaye, pambano lilianza rasmi ambapo Harvey alikuwa ni miongoni mwa wachezaji walioanzia benchi. Mtifuano mkali uliendelea huku wanafunzi wa vyuo hivyo wakishangilia kwa nguvu kila mchezaji wa timu yao alipokuwa akigusa mpira.
Baada ya muda, chuo cha akina Harvey kikawa kimeelemewa kimchezo, hali iliyosababisha wafungwe vikapu vingi mfululizo. “Kocha muingize Harvey,” alisikika Cazzard akimwambia kocha wao ambaye alikuwa ni mwalimu wa michezo pale chuoni kwao. Bila kupoteza muda, Harvey akasimama na kuanza kupasha misuli yake, mabadiliko yakafanyika haraka, Harvey akaenda kuongeza nguvu kwenye timu yake ambayo sasa ilikuwa ikifungwa pointi nyingi.
Kama wengi walivyotarajia, Baada ya Harvey kuingia, alianza kuonesha uwezo wake kwa kuwakimbiza sana wachezaji wa timu pinzani na ;ku-score’ mfululizo kuisawazishia timu yake. Dakika chache baadaye, timu yao ambayo ilikuwa nyuma kwa pointi nyingi, ikaanza kuwakaribia wapinzani wao na hatimaye matokeo yakawa sawa.
Harvey akawa anajitahidi kuwachezesha wenzake kwa kasi, hali ya mchezo ikabadilika mara moja, wakawazidi wapinzani wao kimchezo na kuanza kuwaelemea. Wanachuo wa Miami Polytechinic, wakawa wanashangilia kwa nguvu huku wakilitaja jina la Harvey kama shujaa wao.
Hali hiyo ilizidi kumpa morali Harvey, akazidi kuwachangamsha wenzake na baada ya muda kupita, timu yao ikawa inaongoza kwa pointi nyingi. Waandishi mbalimbali wa habari za michezo wakawa wanasubiri kwa hamu mchezo uishe ili wapate kumfanyia mahojiano Harvey, ambaye kwa hakika alionekana kuwa nyota wa mchezo.
Mchezo ulipoisha, Harvey alizungukwa na waandishi wa habari kutoka vituo mbalimbali vya runinga na redio, akawa anaulizwa historia fupi ya maisha yake, wazazi wake na namna alivyojiingiza kwenye mchezo. Licha ya furaha aliyokuwa nayo Harvey kwa kuweza kupigana kiume kuiokoa timu yake, bado hakufurahishwa na maswali ya waandishi wa habari
“Natokea Miami Polytechnic and Engineering College, ” alikuwa akijibu kwa ufupi Harvey huku akiondoka na kuelekea chumba cha kubadilishia nguo. Waandishi wengi wa habari walipigwa na butwaa kwani Harvey hakuwapa ushirikiano kama walioutegemea, wakahisi kuwa huenda ni mara yake ya kwanza kufuatwa na vyombo vya habari kwa wingi namna ile.
“Mbona unalia Harvey! Wenzako tunafurahi wewe umejiinamia unalia, nini tatizo?” nahodha wa timu yao, Cazzard alikuwa akimuuliza kwa upole Harvey, baada ya kumuona anatokwa na machozi ndani ya chumba cha kubadilishia nguo. Wenzake karibu wote hawakuwa na habari naye, wakawa wanaendelea kusherehekea ushindi mnono walioupata.
Baada ya Cazzard kujaribu kumbembeleza, Harvey alinyamaza, akabadilisha jezi na kuvaa nguo zake alizokuwa amezivaa awali, akavaa na miwani ya jua kuficha macho yake ambayo yalishabadilika na kuwa mekundu kutokana na kulia.
Baada ya mchezo ule, jina la Harvey likapaa maradufu, kila mmoja akawa anamzungumzia yeye. Hata wanafunzi wa vyuo vingine walishangazwa na uwezo mkubwa aliouonesha siku ya kwanza tu ya michuano hiyo. Baada ya mechi nyingine za ufunguzi kuisha, CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Harvey na wanachuo wenzake waliingia ndani ya basi lao la shule na safari ya kuelekea chuoni kwao ikaanza. Walipofika chuoni, Harvey alipitiliza bwenini kwao na kwenda kulala. Maswali aliyoulizwa na waandishi wa habari kuhusu historia yake yakawa yanajirudiarudia kichwani mwake. Akaona ni kama wamemtonesha donda ambalo lilikuwa bado halijapona. Baada ya muda usingizi ukampitia, akalala na kuwaacha wanachuo wenzake wakizidi kusherehekea ushindi mnono walioupata siku ya kwanza tu ya michuano ile. *** “Anaitwa nani?” “Harvey.” “Urefu wake ukoje?”
“Unafaa sana kwa mchezo wa mpira wa kikapu, hebu angalia hii video ya mechi ya ufunguzi, mhusika ni huyu mwenye kitambaa mkononi,” maafisa wa timu ya mpira wa kikapu ya Miami Heat walikuwa wakijadiliana jioni ya siku ile, baada ya kurejea kwa wawakilishi wao waliowatuma kwenda kufuatilia michuano ya NCAA na kujaribu kutafuta vipaji vipya vya mchezo huo kwa ajili ya timu yao.
“Tunatakiwa kutafuta vijana wenye uwezo na vipaji vikubwa kama huyu Harvey, si mnaona wapinzani wetu wa Chicago Bulls wanavyotishia kutupokonya ubingwa wetu msimu huu?”
“Ni kweli meneja… huyu kijana atatufaa sana, nashauri mazungumzo ya awali yaanze kufanywa kati yetu na uongozi wa chuo anachosoma.”
Kikao kilimalizika, viongozi wakakubaliana kuendelea kumuangalia kwa karibu mchezaji huyo huku wengine wakianza mchakato wa mazungumzo na chuo alichokuwa anakisomea.
Siku ya mechi ya pili ya Chuo cha Miami Polytechnic dhidi ya Chuo cha Arkansas iliwadia. Watu wakawa wanasubiri kwa shauku kumuona Harvey kwani habari zake zilizotangazwa na vyombo vya habari baada ya mechi ya ufunguzi, ziliwashtua wengi. Kama kawaida, Harvey na wanachuo wengine wakasafiri kwa basi la chuo mpaka kwenye Chuo cha Arkansas kwani walipangiwa mechi ya ugenini.
Tofauti na mechi ya awali, Harvey alipangiwa kuanza katika kikosi cha kwanza, Cazzard akamkabidhi ukapteni wa timu, jambo ambalo angalau lilimpa faraja Harvey. Akapania kuhakikisha anafanya maajabu kwa mara nyingine.
Mchezo ulipoanza tu, Harvey alifunga kikapu cha kwanza ndani ya sekunde chache na kuipa timu yake ushindi wa mapema, akaongeza kasi na kuwachezesha vilivyo wenzake, jambo lililofanya wapate pointi nyingi ndani ya dakika tatu za mwanzo. Uwanja mzima ukawa unalipuka kulitaja jina la Harvey kila alipopata mpira.
“Harvey! Harvey! Harvey!” uwanja mzima ulilipuka, mpaka mashabiki wa timu pinzani ambayo ndiyo ilikuwa mwenyeji wakawa wanamshangilia.
Skyler alikuwa akimalizia kufanya ;homework’ aliyopewa shuleni kwao. Akaamua kuwasha runinga kuangalia kilichokuwa kinajiri, macho yake yakatua kwenye mechi ya mpira wa kikapu ambapo alimuona mtu kama Harvey akiruka na ;kudank’ kwenye goli la wapinzani, akakimbilia chumbani kwa baba na mama yake ambapo aliwaita harakaharaka, wote wakakimbilia sebuleni kumuangalia.
MAISHA ya Harvey, kijana mdogo kutoka nchini Liberia aliyekimbia mauaji ya halaiki yaliyozigharimu roho za wazazi na ndugu zake, yanaanza kubadilika akiwa katika Chuo cha Miami Polytechnic and Engineering College nchini Marekani ambapo taratibu anaanza kusahau maumivu ya kuwapoteza wazazi wake na yote yaliyotokea akiwa njiani kukimbia mapigano nchini kwao.
Licha ya kupata matokeo mabaya kwenye mtihani wa mwisho wa kuhitimu kidato cha nne, Dk Lewis na familia yake bado wanaahidi kumsaidia Harvey kwa uwezo wao wote. Hali hiyo inamfanya aamue kuwatoa kimasomaso kwa kukazana kwenye masomo na kuendelea na mazoezi ya mpira huo wa kikapu.
Nyota ya umaarufu inaanza kumuwakia kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza mpira wa kikapu. Anaanza kuwa gumzo miongoni mwa wanachuo wenzake na anaitwa kuichezea timu ya chuo kwenye mashindano makubwa ya mchezo wa mpira wa kikapu kwa wanafunzi wa vyuo nchini Marekani (NCAA).
Upande wa pili, Skyler anaanza kuonesha dalili za mapenzi kwa kaka yake huyo wa hiyari lakini Harvey anakuwa mgumu wa kumuelewa kwani anamchukulia kama mdogo wake. Wanachuo wa kike nao wanazidi kuchanganywa na uzuri na kipaji alichokuwa nacho Harvey
Ingawa Harvey alipata matokeo mabaya kwenye mtihani wa mwisho wa kuhitimu kidato cha nne, Dk Lewis na familia yake bado wanaahidi kumsaidia kwa uwezo wao wote kumjengea maisha bora. Anaandikishwa katika Chuo cha Miami Polytechnic and Engineering College nchini Marekani. Taratibu anaanza kusahau maumivu ya kuwapoteza wazazi wake na yote yaliyotokea akiwa njiani kukimbia mapigano nchini kwao na anaelekeza nguvu zake zote kwenye masomo na mazoezi ya mpira wa kikapu. Nyota ya umaarufu inaanza kumuwakia kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza basketball. Anakuwa gumzo kwenye mashindano makubwa ya mchezo wa mpira wa kikapu kwa wanafunzi wa vyuo nchini Marekani (NCAA) ambapo anaiongoza timu yake kupata mafanikio makubwa. Timu kubwa ya mpira wa kikapu nchini humo, Miami Heat inavutiwa na uwezo wake na sasa imeshaanza taratibu za kumshawishi ajiunge nayo. Fungu kubwa la fedha linatengwa kwa ajili ya usajili wake.
“Mama… ona…ona, yule si kaka Harvey yule?” “Ni yeye… jamani hata siamini macho yangu.” “Mi nilijua tu huyu Harvey ana kitu kikubwa alichojaaliwa na Mungu ila bado hajaanza kujitambua,” alisema Dk Lewis na kukumbatiana na mkewe na Skyler. “Ni fahari kubwa kwetu, ila bado kuna jambo anatakiwa kusaidiwa… sitakata tamaa kumtafutia washauri wa kisaikolojia ili kumsahaulisha kabisa yote aliyowahi kuyapitia maishani mwake,” alisema Dk. Lewis, wakakaa kwenye viti na kukodolea macho runinga. Kila mmoja alinyamaza kwa muda, lakini baadaye Skyler alishindwa kuvumilia, akawa anashangilia kwa nguvu na kurukaruka mbele ya baba na mama yake. Furaha aliyokuwa nao iliwazidi wote, akajikuta akizidi kumpenda ndani ya moyo wake na kumfanya muda wote achekecheke mwenyewe. Waliangalia runinga mpaka kipindi kile cha michezo kilipoisha, kila mmoja akaondoka kuelekea chumbani kulala huku wakiwa na furaha tele. Skyler alipofika chumbani kwake, alichukua picha ya Harvey na kuikumbatia, akawa anakimbiakimbia mle chumbani huku akiwa na furaha ambayo sasa ilionekana kupitiliza. “We Skyler si ulale, furaha gani isiyo na mwisho?” “Hapana mama, niache nifurahie mafanikio ya kaka’angu mpendwa Harvey, nampenda sana,” alisema Skyler akiwa chumbani kwake, akaendelea kufurahi kwa muda mrefu mpaka usingizi ulipompitia. Akawa anaweweseka na kuzungumza maneno asiyoyaelewa akiwa usingizini. “Mwanao ana nini leo? Mbona mpaka muda huu anaongea peke yake na kucheka?” “Atakuwa anaweweseka huyu, ni kawaida yake kuweweseka kila anapolifikiria jambo moja kwa muda mrefu.” “Hebu nenda kamlaze vizuri, anaweza kupata madhara usiku,” alisema Dk Lewis, mkewe akaamka na kuelekea chumbani kwa mwanaye ambapo alimkuta akiwa amelala huku amekumbatia picha ya Harvey, jambo lililomfanya ajiulize maswali mengi kichwani. Hata hivyo aliamua kupuuzia, akaichukua ile picha na kuiweka mahali pake, akamlaza vizuri Skyler na kumfunika, akazima taa na kurejea chumbani kulala. “Unajua mume wangu lazima tuwe makini sana na uhusiano wa Skyler na Harvey, wanazidi kukua na kama unavyomuona mwanao Skyler ameshakuwa mwali sasa.” “Ni kweli mke wangu, lakini kwa namna tunavyowalea watakuwa wanachukuliana kama kaka na dada na si zaidi ya hapo.” “Ni sawa lakini si unajua akili za vijana wanaovuka kipindi cha mpito na kuingia utu uzima? Mi nafikiri itabidi nitafute siku ya kukaa na Skyler na kuzungumza naye mambo kadhaa… nampenda sana mwanangu na sipo tayari kuona maisha yake yanaingia dosari kwa namna yoyote ile,” alisema mama Skyler huku akijifunika vizuri, wakaendelea kulala. *** Wakati kila mtu akiendelea kuyafurahia mafanikio makubwa aliyoyapata Harvey, kwa upande wake bado hakuwa na furaha kama ile waliyokuwa nayo wanachuo wengine. “Hivi nitaendelea kuteswa mpaka lini na historia ya maisha yangu? Nafikiri ni muda wa kuwa mkweli kwa nafsi yangu na waandishi wa habari ili kila mtu ajue historia halisi ya maisha yangu, nitaeleza kila kitu kilichonitokea,” alijisemea Harvey akiwa amelala chali na kutazama juu ya dari la bweni. Licha ya kuwa ilikuwa ni usiku sana, bado Harvey hakuwa amepata usingizi hata chembe. Alidhamiria kueleza kwa waandishi wa habari kila kitu kuanzia jinsi alivyokimbia mapigano nchini kwao Liberia mpaka alivyopokelewa na Dk Lewis. Siku iliyofuatia, kama kawaida Harvey aliwahi kuamka na kwenda kufanya mazoezi kwenye viwanja vya mpira wa kikapu shuleni pale. Baada ya kumaliza, alianza kujiandaa kuingia darasani kwani siku hiyo alikuwa na kipindi cha kwanza kinachoanza asubuhi na mapema. “Nakuomba ukimaliza kipindi chako cha kwanza uje kwenye ofisi ya Dean of Students, kuna jambo la muhimu nahitaji kuongea na wewe,” mlezi wa wanachuo au maarufu kama dean, alimwambia Harvey asubuhi na mapema wakati akiingia kwenye kipindi cha kwanza. Harvey alimjibu lakini akawa anajiuliza maswali mengi juu ya sababu za kuitwa kwa dean asubuhi yote ile. Hata wakati profesa wa kipindi cha kwanza akiendelea kufundisha, Harvey hakuwepo kabisa kimawazo, akawa anafikiria kwa kina bila kupata majibu juu ya alichoitiwa. Kipindi kilipoisha, wanachuo walianza kutoka, Harvey bila kuchelewa akaongoza moja kwa moja kwenye ofisi ya mlezi wa wanachuo. “Kuna ujumbe wako kutoka kwa uongozi wa Miami Heat, wanahitaji kuja kuzungumza na wewe ana kwa ana kuhusu kuingia nao mkataba wa kuichezea timu yao nje ya muda wa masomo.” “Whaaat? Miami Heat? Mbona mimi ndiyo kwanza nimeanza kucheza mpira siku mbili hizi, nitawezaje kumudu kuwa na timu kubwa kama ya Miami Heat?” “Jiamini kijana, una sifa zote anazotakiwa kuwa nazo mchezaji bora wa mpira wa kikapu, ukiona mpaka viongozi wa Miami Heat wamekuja hapa kukufuata, ujue neema ipo jirani kukufikia. “Hakuna timu inayolipa vizuri wachezaji kama Miami Heat, ukifanikiwa usinisahau na mimi kwenye ufalme wako,” alisema yule mlezi wa wanachuo na kumtoa wasiwasi Harvey, wakawa wanacheka kwa furaha huku akimtaka ajenge moyo wa kujiamini. Habari ile ilimfanya Harvey ajihisi kama yupo kwenye njozi tamu, akawa anaomba kimoyomoyo kuwa kile alichoambiwa na mlezi wao kisiwe ndoto bali ukweli utakayoyabadilisha kabisa maisha yake. Mechi mbili tu za mpira wa kikapu alizoiongoza timu yake ya Miami Polytechnic and Engineering College dhidi ya timu za Vyuo vya UCLA na Arkansas zilimfanya ageuke gumzo kila mahali. Hakutaka kuamini kuwa uwezo ule wa siku mbili tu aliouonesha unaweza kuwachanganya watu kiasi cha kuwaniwa na timu kubwa kama Miami Heat. Kutwa nzima ya siku ile alishinda akichekacheka mwenyewe, akawa anavuta picha kichwani mwake akiwa amevaa jezi za timu kubwa kabisa ya mpira wa kikapu nchini Marekani, Miami Heat iliyokuwa inatetea ubingwa wa Ligi ya NBA. Mechi yao ya tatu walipangiwa kuchezea pale chuoni kwao dhidi ya timu ya Chuo Kikuu cha Duke. Baada ya kusikia habari juu ya kuwaniwa na timu ya Miami Heat, alipania kwa moyo wote kuonesha kuwa hawakuwa wamekosea kumchagua ajiunge na kikosi hicho. Mazoezi makali aliyokuwa anayafanya yalisababisha awe na nguvu nyingi na pumzi za kutosha kama faru dume, mchezo ulipoanza tu, akaanza kucheza kwa kasi kubwa na nguvu. Kwa mara nyingine alifanikiwa kuonesha uwezo mkubwa kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mchezo huo, tena akiwa katika uwanja wao wa chuo. Kwa muda wote wa mchezo, Harvey alikuwa akishangiliwa kwa nguvu huku baadhi ya wanachuo wakiwa wamebeba mabango makubwa yaliyokuwa na ujumbe wa kumhusu. Akazidisha juhudi na kuiwezesha timu yake kuibuka na ushindi mnono dhidi ya wapinzani wao wa Duke. Baada ya mechi ile ambayo ilikuwa ya tatu kwa mzunguko, wanaume wawili waliokuwa wamevalia suti nadhifu, mikononi wakiwa na briefcase, walimfuata na kujitambulisha kuwa wao ni maafisa kutoka timu ya Miami Heat, wakamwambia wana mazungumzo naye hivyo watafute sehemu ya kukaa na kuzungumza kwa kina.
Michuano ya mpira wa kikapu kwa wanafunzi wa vyuo nchini Marekani, almaarufu NCAA yanayovikutanisha vyuo vingi vya elimu ya juu, ndiyo yaliyofanya uwezo na kipaji kikubwa alichokuwa nacho Harvey kijulikane. Mechi za awali alizoshiriki akikichezea chuo chake cha Miami Polytechinic and Engineering College, zinamtangaza vyema kutokana na jinsi alivyoonesha uwezo mkubwa kwenye mchezo huo.
Uwezo mkubwa anaouonesha unawavutia viongozi wa timu kubwa mbalimbali zilizokuwa zinashiriki ligi kuu ya mpira wa kikapu nchini Marekani, NBA ikiwemo Miami Heat. Timu hiyo kubwa iliyokuwa inatetea ubingwa wa ligi hiyo, inaanza kumuwania Harvey. Taarifa zinatumwa chuoni kwao na mipango ya kumsajili inaanza kufanywa mara moja.
Upande wa pili, tamaa ya mapenzi kwa Harvey inazidi kumuwakia Skyler lakini anashindwa kumwambia moja kwa moja kwani wanaishi kwenye familia moja kama kaka na dada. Mafanikio anayoyapata yanamfanya Skyler azidi kumpenda Harvey na anajiapiza kuwa lazima atakuja kuwa na uhusiano naye.
“BILA shaka wewe ni Harvey?” aliuliza mmoja kati ya wanaume wale ambao walijitambulisha kama maafisa kutoka timu ya mpira wa kikapu ya Miami Heat. Harvey aliwapa ushirikiano mzuri kwani tayari alishakuwa na taarifa za ujio wao, alizozipata kutoka kwa mlezi wa wanachuo (dean of students) pale chuoni kwao.
Waliingia katika chumba maalum kilichokuwa katika jengo la utawala, wakaenda kukaa kwenye meza ya duara iliyotengenezwa kwa vioo na wale wanaume wakaweka briefcase zao mezani na kutoa ujumbe waliotumwa na timu yao ya Miami Heat.
“Vipi kuhusu masomo yangu ya chuo?”
“Utaruhusiwa kuendelea na masomo kama kawaida lakini pale tutakapokuwa tunakuhitaji hususani jioni baada ya muda wa masomo, utakuwa unakuja kuchukuliwa kisha kurejeshwa chuoni mapema, tutayapa kipaumbele masomo yako,” alisema mmoja kati ya wale wanaume, mwenzake akawa anamuunga mkono kwa kutingisha kichwa.
Waliendelea kuzungumza mambo kadha wa kadha, wakamfafanulia kila kipengele kilichokuwa katika mkataba ambao Harvey alitakiwa asaini. Baada ya kusaini angepewa kiwango kikubwa cha fedha kama malipo ya usajili wake na mishahara yake ya miezi mitatu. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Nahitaji kwenda kujadili na familia yangu kwanza, wao ndiyo wenye mamlaka ya kusema cha kufanya,” alijibu Harvey, wakakubaliana na wazo lake, wakaahidi kurejea tena siku inayofuata.
Walipoondoka tu, Harvey alienda kumpa taarifa mlezi wao (dean of students), akamweleza kila kitu walichozungumza na maafisa wale wa Miami Heat, akamuonesha na nakala ya mkataba waliokuwa wanataka ausaini na fedha ambazo angelipwa. Dean akawa anaupitia juujuu, akakutana na kipengele kilichokuwa kinasomeka ‘$45 million as per advance salary of three month’. (Dola milioni 45 kwa ajili ya malipo ya awali ya mshahara wa miezi mitatu).
“Duuh! Watakuwa wanakulipa dola milioni 15 kwa mwezi? Yaah wamemaanisha hivyo kwa sababu hapa wanasema watakupa kianzio cha mishahara ya miezi mitatu ambayo ni dola milioni 45… achilia mbali mamilioni ya kusaini mkataba mnono kama huu… ama kweli Mungu yu mwema,” alisema Dean na kumshika mkono Harvey.
“Bila shaka Dk Lewis atafurahi sana, inatakiwa uende nyumbani sasa hivi kumfikishia taarifa,” alisema. Bila kupoteza muda, Harvey akaenda hostel kujiandaa haraka kisha akaianza safari ya kuelekea nyumbani kwao. Dakika 30 baadaye tayari alishawasili nje ya geti, akasalimiana na mlinzi na kuingia mpaka ndani.
“Kwa kuwa muda ule ilikuwa bado ni mapema, Dk Lewis na mkewe walikuwa kazini huku Skyler akiwa shuleni. Nyumba ilikuwa imepoa kwa ukimya. Harvey akapata wazo kuwa ni bora amfuate Dk Lewis kazini na kumfikishia taarifa zile, wakubaliane nini cha kufanya mapema. Akiwa anajiandaa kutoka alisikia sauti ya mtu kama Skyler akizungumza na mlinzi getini.
“Mh hapa leo kazi ipo,” alijisemea Harvey huku akichungulia dirishani kuangalia upande wa mbele kwenye geti. Alitambua fika kuwa Skyler alikuwa na hisia za mapenzi lakini hakutaka kuruhusu hilo litokee.
Baada ya muda alimuona Skyler akiingia huku akiwa amebeba begi lake la shule mgongoni, akiwa amejishika mikono tumboni. Kwa jinsi alivyokuwa anaonesha, Skyler alikuwa akihisi maumivu makali ya tumbo. Harvey akatoka nje kumsaidia kuingia ndani.
“Whaooo! Harvey kumbe umekuja? Kwa nini hujanitaarifu? Mbona mlinzi hajaniambia kama upo ndani… oooh come on!” alisema Skyler na kuchangamka ghafla, akamkimbilia Harvey na kumkumbatia kwa nguvu. “Kwa nini umewahi kurudi shule?”
“Naumwa Harvey, tumbo linaniuma sana,” alisema Skyler kwa kudeka, wakaingia ndani na kwenda kukaa sebuleni. Kwa jinsi Skyler alivyokuwa na bashasha baada ya kumuona Harvey, hata maradhi ya tumbo aliyokuwa nayo yaliisha ghafla. Akawasha runinga na kuanza kumsimulia jinsi walivyomuona akicheza mpira wa kikapu usiku uliopita.
“Nilirekodi kwenye VCD, nilifurahi sana,” alisema Skyler na kuuchukua mkoba wake wa DVD, akaanza kuitafuta kwa lengo la kumuonesha Harvey. Muda mfupi baadaye, runinga kubwa ya kisasa iliyokuwa pale sebuleni ilikuwa ikionesha kipande cha mchezo kati ya chuo alichokuwa anasoma Harvey na timu nyingine.
“Umeshakuwa superstar Harvey… im so proud of you (najivunia sana kuwa na wewe) alisema Skyler, akajilaza kwenye miguu ya Harvey aliyekuwa ametulia juu ya sofa, akiendelea kukodolea macho kwenye runinga. Kwake kila kitu kilikuwa kama miujiza, hakuwahi kudhani anaweza kupata umaarufu mkubwa kiasi kile.
“Kaka Harvey naomba unikumbatie kifuani kwangu,” alisema Skyler kwa sauti ya kudeka huku akimsogelea Harvey pale juu ya kochi.
“No Skyler… tumeshakuwa wakubwa sasa, hatuwezi kukumbatiana mwilini kama zamani, lazima tutaingia kwenye vishawishi tu,” alisema Harvey lakini Skyler hakutaka kumuelewa.
Harvey hakuwa na ujanja tena, akaamua kutulia na kufanya kile dada yake alikuwa anakitaka. Walikumbatiana kwa nguvu, kwa kuwa Harvey alikuwa akifanya mazoezi, hakupata shida, wakakaa pale juu ya sofa kwa dakika kadhaa.
“Kaka Harvey mi nasikia usingizi, nataka unipeleke chumbani nikalale,” alisema Skyler huku akimtazama Harvey kwa macho yaliyokuwa na ujumbe mzito.
Harvey aliamua kujikaza na kuonesha uvumilivu hadi hatua ya a. Akamuinua Skyler pale kwenye sofa na kumsindikiza mpaka chumbani kwake, akamlaza kitandani na kumfunika.
“Utapona usijali umesikia Skyler!”
“Ahsante Harvey, naomba ukae hapa pembeni ya kitanda changu,” alisema Skyler huku akiupitisha mkono wake mmoja na kumgusa Harvey kiunoni, akamganda kama ruba. Walikaa katika hali ile kwa muda mrefu, Skyler akaanza vituko vingine, akawa anamwambia Harvey kuwa anasikia joto kali. “Nikuwashie feni?”
“Hapana… nataka unisaidie kuvua nguo za shule,” alisema Skyler na kujilegeza mwilini mwa Harvey. Hali ile ilimpa wakati mgumu sana Harvey lakini akaamua kujikaza kiume, akamvua shati na kumuacha akiwa amevaa blauzi nyepesi ndani, akamwambia hataweza kumvua sketi bali afanye vile mwenyewe na yeye atamsaidia kuzitundika ukutani.
Kwa makusudi Skyler alisimama na kuanza kutaka kuvua sketi mbele ya macho ya Harvey, hali iliyomfanya afungue mlango na kutoka nje. Akamuacha Skyler kule chumbani.
“Hivi huyu Skyler kwa nini ananifanyia hivi? Si ameshakuwa kama dada yangu wa kuzaliwa tumbo moja huyu? Kwa nini anataka kuleta hisia za kimapenzi?” alijiuliza Harvey bila kupata majibu, akaamua kutoka nje kabisa ili kuepusha kile kilichokuwa kinataka kutokea.
Kwa bahati nzuri, muda mfupi baadaye mama Skyker aliwasili nyumbani pale akitokea kazini. Harvey akampokea na kumweleza kwa kifupi kilichomfanya arudi nyumbani.
“Skyler naye yupo chumbani kwake anasema tumbo linamuuma,” alisema Harvey, mama yao akapitiliza moja kwa moja mpaka chumbani kwa mwanaye na kumuacha Harvey akiteremsha baadhi ya vitu kwenye gari. “Mum im sick, my stomach is aching,”
(Mama naumwa) alisema Skyler huku akijigalagaza huku na kule. Baada ya kubaini kuwa ni tumbo ndiyo lilikuwa likimsumbua mwanaye, alienda chumbani kwake na kutoka na sanduku maalum la huduma ya kwanza. Akaanza kumtafutia dawa za kutuliza maumivu ya tumbo. Baada ya kupewa dawa, Skyler alitulia, akalala na kuwaacha mama’ke na Harvey wakiendelea kuupitia ule mkataba. Waliendela kupitia kifungu kimoja baada ya kingine na kutafuta tafsiri ya kila kilichokuwa kimeandikwa. Baada ya saa kadhaa kupita, Dk Lewis alirejea nyumbani na kuwakuta wakiendelea na zoezi lile.
Akiwa na watu wengine wengi, wanatoroka nchini kwao kukimbia machafuko na kuelekea nchini Marekani. Wakiwa njiani, balaa jingine linatokea ambapo chombo walichokuwa wanasafiria baharini kinapinduka. Harvey anakuja kurejewa na fahamu na kujikuta akiwa hospitali, jijini Miami nchini Marekani. Baada ya kueleza kilichomsibu, Dk Lewis anajitolea kumsaidia, anamchukua na kwenda kuishi naye nyumbani kwake. Anayaanza maisha mapya nchini Marekani ambapo anapelekwa shule ya sekondari lakini anashindwa kufanya vizuri kutokana na msongo wa mawazo. Dk Lewis na familia yake wanaamua kumtafutia chuo cha ufundi na hapo ndipo nyota yake ya mafanikio inapoanza kung’ara kupitia uwezo mkubwa wa kucheza mpira wa kikapu aliokuwa nao. Ligi ya mpira wa kikapu kwa wanafunzi wa vyuo nchini humo maarufu kama NCAA inamfanya apate fursa ya kuonesha kipaji chake na sasa anageuka gumzo nchi nzima huku timu kubwa ya Miami Heat ikiwania kumsajili.
Viongozi wa timu hiyo maarufu wanaenda kuonana na Harvey chuoni pale na kumpa mkataba ambao wanamwambia aupitie kwa makini na akiridhika asaini. Harvey anaamua kurejea nyumbani kwenda kuomba ushauri kwa walezi wake, Dk Lewis na mkewe.
BAADA ya Dk Lewis kuwasili, ilibidi Harvey aanze kuelezea kila kitu kilivyokuwa, kuanzia jinsi alivyopewa taarifa na mlezi wao pale chuoni, jinsi alivyokutana na maafisa wa ngazi za juu wa timu ya mpira wa kikapu ya Miami Heat na mazungumzo yote waliyoyafanya pamoja.
Kwa Dk Lewis, ile ilikuwa ni zaidi ya habari njema. Japokuwa alitoka kazini akiwa na uchovu sana, aliposikia habari ile, moyo wake ulifurahi kupita kawaida. Mkewe hakuwa na tofauti naye. Mara kwa mara walikumbatiana kwa furaha, wakawa wanamshukuru Mungu wao kwa kumfungulia Harvey njia ya mafanikio.
Waliendelea kuupitia mkataba ule kifungu kimoja baada ya kingine na walipojiridhisha kuwa kila kilichokuwa kimeandikwa kina manufaa kwa Harvey, walimsaidia kuujaza. Dk Lewis akaweka sahihi sehemu ya mzazi au mlezi pamoja na anuani yake ya makazi.
Baada ya kumaliza kazi ile, waliagana na kutakiana usiku mwema, Dk Lewis akatoka na mkewe hadi chumbani kwa mtoto wao, Skyler kumjulia hali kwani alikuwa akilalamikia maumivu ya tumbo. Harvey alienda chumbani kwake huku akiwa na furaha ya ajabu moyoni mwake.
Kilichomfurahisha zaidi ni kwamba Dk Lewis na mkewe waliyafurahia sana mafanikio yake na kuahidi kuwa naye bega kwa bega. Wakamfanya asione pengo la wazazi wake kwa muda ule. Kwa furaha aliyokuwa nayo, alipoingia chumbani kwake hakukumbuka hata kufunga mlango, akaenda kufungulia muziki na kujitupa kitandani, hisia za furaha zikawa zinapita ndani ya kichwa chake, hali iliyomfanya muda wote uso wake ujawe na tabasamu pana.
Hakuelewa usingizi ulimpitia saa ngapi lakini alikuja kushtuka baadaye baada ya kusikia kitu kikimpapasa mwilini. Alifumbua macho na kutulia, akawa anataka kujua ni kitu gani. Kilichomshtua, wakati anapitiwa na usingizi hakuwa amezima taa, kufunga mlango wala kujifunika lakini aliposhtuka kutoka usingizini, alijikuta akiwa amefunikwa na shuka huku taa ikiwa imezimwa na mlango kufungwa.
“Harvey!” alisikia sauti ya mtu akinong’ona jirani kabisa na sikio lake la upande wa kushoto. Mshtuko alioupata ulimfanya akurupuke pale kitandani na kukimbilia kwenye swichi, akawasha taa na kukodolea macho pale kitandani. Alipatwa na mshangao mkubwa kumuona Skyler akiwa pale juu ya kitanda chake, tena akiwa amevaa ‘night dress’ pekee.
Mapigo ya moyo yalianza kumwenda mbio kuliko kawaida kwani alijua endapo wazazi wake wangeamka ghafla na kuwakuta wakiwa katika hali ile, wangehisi tayari wameanza kushiriki mchezo haramu.
“Kumetokea nini Skyler… kwa nini upo hapa muda huu,” aliuliza Harvey kwa sauti ya chini akiogopa asije kusababisha kelele ambazo zitawaamsha Dk Lewis na mkewe. Skyler hakujibu kitu zaidi ya kumuoneshea ishara kuwa asipige kelele, akainuka kutoka pale kitandani alipokuwa amelala na kumsogelea Harvey mwilini. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Akiwa bado haelewi cha kufanya, Harvey alishtukia Skyler amemkumbatia kwa nguvu na kumganda kama ruba, akawa analalamika kuwa ameshindwa kulala chumbani kwake kutokana na baridi aliyokuwa anaisikia, hasa ukizingatia kuwa bado tumbo lilikuwa linamuuma.
“Huoni kama utanisababishia matatizo makubwa? Hivi ikitokea baba na mama wametukuta huku chumbani tukiwa katika hali kama hii unafikiri watatuelewaje?” aliuliza Harvey kwa sauti ya chini huku akijaribu kujinasua kutoka mwilini mwa Skyler bila mafanikio.
“Harvey please… nasikia baridi sana nahitaji unikumbatie,” alisema Skyler huku akizidi kumganda. Alijaribu kutumia ujanja wake wote kumuweka sawa ili amuachie lakini haikuwezekana.
“Hata baba na mama wakitukuta mi nitawaambia nakupenda na nataka unioe.”
“Skyler… hujui tunaishi kama kaka na dada, unafikiri nani atatuelewa? Utanisababishia matatizo makubwa, tafadhali nakuomba rudi chumbani kwako ukalale.”
“Sirudi… nimeshakwambia nasikia baridi, hunionei huruma wakati mwenzio naumwa?” alilalama Skyler huku akijikamua ili machozi yamtoke. Alipoona Harvey hataki kumuelewa, ikabidi amtolee vitisho:
“Ukikataa kufanya ninavyotaka nitapiga kelele niseme ulikuwa unataka kunibaka,” alisema Skyler na kubenua midomo yake mizuri kwa jeuri. Harvey alimsihi sana asifanye vile, akamwambia kuwa yupo tayari kufanya kila alichokuwa anakitaka lakini asifanye kile alichokusudia.
“Basi nakukumbatia kidogo, ukiacha kusikia baridi utarudi chumbani kwako,” alisema Harvey huku akivua shati lake na kumsogeza Skyler kifuani kwake. Wakakumbatiana kwa dakika kadhaa wakiwa wamesimama wima katikati ya chumba cha Harvey.
“Kwa nini tusisogee kitandani? Nimechoka kusimama,” alisema Skyler huku akimsukumia Harvey kitandani. Harvey akaona atakuwa amevuka mipaka ya maadili, akamkatalia kufanya vile alivyotaka. Wakiwa bado wanavutana, walisikia mlango wa chumba cha baba na mama yao ukifunguliwa, Skyler akamuachia Harvey haraka na kukimbia kwa kunyata kuelekea chumbani kwake.
Harvey alishindwa kuificha hofu iliyokuwa ndani ya moyo wake, moyo ukawa unadunda kwa nguvu. Aliyajua madhara ambayo angeyapata endapo baba au mama yake wangegundua kuwa alikuwa na Skyler chumbani kwake usiku ule. “Eeeh Mungu nisaidie,” alisema Harvey huku akiurudishia mlango wake taratibu, akazima taa na kurudi kitandani kimyakimya huku masikio yake yakiwa makini kusikiliza kilichokuwa kinaendelea.
Alisikia mlango wa maliwatoni ukifunguliwa, akashusha pumzi ndefu na kutulia, angalau akawa na imani kuwa hakuna anayeweza kugundua kilichotokea muda ule. Baada ya muda, alisikia mlango ukifunguliwa tena, akasikia hatua za mtu akitembea kuelekea chumbani kwa Skyler. “Mbona unatetemeka sana mwanangu halafu jasho linakutoka,” alisema mama Skyler baada ya kumkuta mwanaye katika hali ile. Skyler alijibu
kwa sauti ya kuigiza kuwa alikuwa anahisi baridi kali na ndiyo iliyomfanya awe katika hali ile. Harvey alikuwa akisikiliza kwa makini kila kilichokuwa kinaendelea.
“Basi ngoja nikamuage baba yake nije tulale wote,” alisema mama Skyler huku akitoka. Muda mfupi baadaye alirejea na kulala na mwanaye, hiyo ndiyo ikawa ahueni kwa Harvey. Akaenda kuufunga mlango wake kwa ndani na kujilaza taratibu kitandani. Hata ile furaha aliyokuwa nayo kwa mafanikio aliyoyapata, ilitoweka na sasa akawa analifikiria tukio lile.
Baada ya muda akapitiwa na usingizi. Kulipopambazuka, Harvey ndiyo alikuwa wa kwanza kuamka, akajiandaa tayari kwa kuondoka. “Mbona umewahi sana kuamka?” aliuliza Dk Lewis baada ya kumkuta Harvey sebuleni akiwa ameshajiandaa. “Leo tuna kipindi cha asubuhi, inabidi niwahi sana,” alisema Harvey, Dk Lewis akamuunga mkono. Wakakubaliana kuwa ampeleke kwa kutumia
gari lao la familia mpaka chuoni kisha ndiyo arudi kwa ajili ya ratiba nyingine. Harvey akaondoka kabla Skyler hajaamka. Wakiwa njiani, akawa anaendelea kufikiria kwa kina juu ya kile kilichotokea usiku uliopita.
Kipaji kikubwa cha kucheza mpira wa kikapu alichojaaliwa na Mungu wake, kinamfanya awe maarufu ndani ya muda mfupi, akiwa ni mwanafunzi katika Chuo cha Miami Polytechnic and Engineering College. Dk Lewis na familia yake ndiyo waliompeleka kwenye chuo hicho, baada ya kushindwa kufanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa kidato cha nne aliofanya.
Mafanikio yake yanamfanya angalau aanze kusahau machungu aliyopitia maishani mwake. Ule msongo wa mawazo uliomtesa kwa kipindi kirefu, sasa umekwisha na kipaji chake cha kucheza mpira wa kikapu kinazidi kujidhihirisha kwenye michuano ya NCAA, iliyokuwa inawahusisha wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali nchini Marekani.
Kutokana na kipaji kikubwa alichokionesha kwenye michuano ya NCAA, timu kubwa ya mpira wa kikapu ya Miami Heat inavutiwa naye na sasa viongozi wake wanafanya mipango ya kumsajili. Upande wa pili, Skyler anachanganywa na hisia kali za mapenzi alizokuwa nazo kwa Harvey. Anaanza kumtega akitaka awe mpenzi wake bila kujali kuwa wanaishi kama kaka na dada.
BAADA ya kuona mbinu yake ya kumnasa Harvey imeshindikana kwa usiku ule, Skyler alianza kuandaa mtego mwingine. Kwa hatua aliyokuwa amefikia, alikuwa tayari kufanya jambo lolote kuhakikisha anamnasa Harvey kimapenzi. Ile heshima aliyokuwa anampa kama kaka yake tangu wakiwa wadogo, sasa iliisha na jambo pekee lililokuwa ndani ya kichwa chake, lilikuwa ni mapenzi.
“Cheki alivyo na kifua kizuri cha mazoezi, itazame mikono yake ilivyojazia vizuri, sura yake ya kitanashati, urefu wake… oooh! Lazima awe mpenzi wangu,” Skyer alikuwa akijisemesha mwenyewe wakati akiitazama picha ya Harvey chumbani kwake.
Wakati akiendelea kuitazama ile picha, alisikia mlango wa chumba chake ukigongwa, akaificha ile picha haraka chini ya mto na kwenda kufungua mlango. Alikuwa ni mama yake, Suzan. “Unaendeleaje mwanangu,” alisema Suzan huku akimbusu Skyler kwenye paji la uso. “Bado tumbo linaniuma sana mama, naona zile dawa za jana hazijanisaidia.” “Utaweza kwenda shule kweli?”
“Hapana, nataka nipumzike tu nyumbani, nikizidiwa kaka Harvey atanipeleka hospitali.” “Mwenzio ameshaondoka kurejea chuoni, kwani hakukuaga? Labda aliogopa kukusumbua mgonjwa, ameondoka alfajiri na mapema,” alisema Suzan, kauli ambayo ilipenya kwenye mtima wa Skyler na kumfanya aduwae kwa muda.
“Basi pumzika mwanangu, sisi tunaenda kazini, ukiona hali inazidi kuwa mbaya utanipigia simu kunitaarifu,” alisema mama Skyler huku akitoka na kuufunga mlango wa chumba cha Skyler. Kauli ya mama yake kuwa Harvey tayari alishaondoka, ilimmaliza kabisa nguvu Skyler.
Mpango kabambe aliokuwa ameupanga ndani ya kichwa chake, ambao alitaka kuutumia kwa Harvey muda mfupi baada ya wazazi wao kuondoka kwenda kazini, ulivurugika… akawa anajilaumu kwa kushindwa kuitumia vizuri nafasi aliyoipata usiku uliopita. Alipohakikisha wazazi wake wameshaondoka kwenda kazini, harakaharaka aliinuka pale kitandani, akaenda kujimwagia maji
bafuni na kuanza kujiandaa kutoka. Alipanga kwenda kumfanyia Harvey ‘shopping’ ya vitu vidogovidogo ambavyo angevitumia kuwasilisha ujumbe wake wa mapenzi kwa Harvey. Alipokuwa tayari, alitoka na kuingia mtaani. Aliongoza moja kwa moja mpaka kwenye ‘supermarket’ kubwa ya Miami Mall iliyokuwa mtaa wa tatu kutoka pale nyumbani
kwao. Akanunua kadi nzuri iliyokuwa na ujumbe mzito wa kimahaba, chokleti, vanilla, nguo za ndani za kiume, pafyumu nzuri na maua mazuri, akaomba kufungiwa vitu vyote katika boksi la zawadi. Wahudumu wa ile supermarket wakafanya kama alivyotaka. Alipohakikisha kila kitu kipo safi, alilipa fedha na kutoka kurejea nyumbani kwao. Alipofika alipitiliza mpaka chumbani kwake,
akaingia tena bafuni kwa mara ya pili na kuoga. Alipomaliza, akaanza kujipamba na kujipodoa mwili mzima. Alitumia zaidi ya nusu saa akiwa kwenye ‘dressing table’ yake.
Aliporidhishwa na namna alivyopendeza, alisimama na kuelekea kwenye kabati la nguo. Akawa anachagua nguo nzuri ambazo aliamini zitamvutia Harvey. Baada ya kuchagua nguo karibu kabati zima, hatimaye aliipata iliyompendeza zaidi.
Alichagua gauni la kisasa la rangi ya pinki alilonunuliwa na mama yake kwenye siku yake ya kuzaliwa, wakati akitimiza miaka 19. Alipolivaa alijipitisha mara kadhaa mbele ya kioo, akawa anageuka huku na kule kama wafanyavyo mamisi, alipohakikisha amependeza vya kutosha, alichukua boksi lake la zawadi na safari ya kuelekea chuoni kwa akina Harvey ikaanza. *** Baada ya kufikishwa chuoni na Dk Lewis, Harvey alipitiliza moja kwa moja mpaka bwenini kwao. Kwa kuwa ilikuwa bado ni asubuhi sana, aliungana na wanachuo wenzake waliokuwa wanajiandaa kwa ajili ya kuhudhuria kipindi cha asubuhi ile. “Ulilala wapi Harvey? Usiku tulikuwa na wasiwasi kweli baada ya kuona hutokei, tukahisi labda umepatwa na tatizo.” “Dah! Mtanisamehe kwa sababu niliondoka bila kuwaaga, nilikuwa nimeenda nyumbani kujadiliana na familia yangu kuhusu mkataba wa kuichezea Miami Heat.”
“Mkataba wa kuichezea Miami Heat? Kwani wanataka kukusajili?”
“Ndiyo, na tayari wameshanipa mkataba wao, nilienda nyumbani kuwaonesha ili wanisaidie kuujaza. Leo wakija tena nitawapa halafu nitasubiri kuona hatua inayofuata.”
“Daaah! Hongera sana mtu wangu, watu wengine mna bahati zenu bwana! Umepata dili la kucheza kikapu kwenye Timu ya Miami Heat? Basi siku chache zijazo utakuwa bonge la milionea, kumzidi hata Lebron James.”
“Kweli kaka, lakini nahitaji dua zenu zaidi, si unajua wewe ndiyo umekuwa mshauri wangu mkubwa kwenye haya mambo,” Harvey alikuwa akizungumza na mwanachuo mwenzake, Cazzard huku wakiendelea kujiandaa kwa ajili ya masomo.
Muda wa masomo ulipowadia, Harvey na wanachuo wenzake waliingia katika ukumbi maalum wa kufundishia wanachuo (Lecture Hall). Kipindi kikaanza kama kawaida. Wakati mhadhiri akiendelea kufundisha, kila mtu akiwa kimya kumsikiliza, Harvey aliona kitu kilichomshtua. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Kwa kupitia madirisha ya vioo ya ukumbi ule, alimuona Skyler akija huku mkononi akiwa amebeba boksi lililoonekana kuwa na mzigo ndani yake.
“Huyu Skyler si alisema anaumwa tumbo jamani… halafu mbona leo amenifuata asubuhi namna hii? Nisipokuwa makini shetani atanizidi nguvu kwani simuelewi kabisa anachotaka kutoka kwangu,” alijisema Harvey huku akili zake zikiwa zimeshahama darasani. Akawa anawaza atakavyokabiliana naye bila kumuudhi, huku kumbukumbu za tukio lililotokea usiku uliopita zikipita kwa kasi akilini mwake.
Aliendelea kumtazama Skyler kwa mbali mpaka alipopotelea kwenye majengo mengine ya chuo kile. Bila kusubiri kuja kutafutwa, aliinuka mwenyewe na kukusanya kila kilichokuwa chake, akatoka kwa kupitia mlango wa nyuma bila mtu yeyote kugundua.
Aliongoza moja kwa moja mpaka kwenye jengo la utawala, akamkuta Skyler akiwa amekaa kwenye sehemu ya wageni, huku usoni akiwa amejawa na tabasamu pana. Alipomuona Harvey tu, aliinuka haraka na kumkimbilia, akamkumbatia kwa nguvu huku akimmwagia mvua ya mabusu usoni.
“Nimependeza eti eeeh! Mbona hunisifii?” alisema Skyler huku akizidi kumkumbatia Harvey kwa nguvu.
“Umependeza sana dadaangu, nimekuona tangu nikiwa darasani,” alisema Harvey huku akijilazimisha kuchangamka. “Sitaki unite dada Harvey, niite jina zuri kama darling, honey, sweet, dear au lolote zuri utakalolipenda,” alisema Skyler huku akizidi
kumkumbatia Harvey kifuani. Baada ya Skyler kumkumbatia Harvey kwa dakika kadhaa, aliporidhika alimuachia na kumshika mkono, akamwambia kuwa amemletea zawadi nzuri ambazo anataka akazifungue chumbani kwake na yeye akiwepo.
“Twende ukafungulie kwenye chumba unacholala, wenzako si wapo madarasani muda huu,” alisema Skyler na kumkabidhi Harvey lile boksi la zawadi. Wakawa wanatembea taratibu kuelekea kwenye chumba alichokuwa analala Harvey.
Walipofika na kuingia ndani, Skyler aliufunga mlango kwa ndani, akaenda kujitupa kitandani huku akiuficha uso wake kwa aibu za kikekike. Harvey akaanza kulifungua boksi la zawadi.
Mtoto wa Dk Lewis, mwanaume wa makamo aliyempokea Harvey na kujitolea kuyabadilisha maisha yake aitwaye Skyler, anaanza kuonesha hisia za mapenzi kwa kaka yake huyo wa hiyari. Anatumia mbinu mbalimbali kuwasilisha
ujumbe wake wa kimapenzi kwa Harvey lakini anakuwa mjanja na kujitahidi kuvishinda vishawishi. Bado Skyler hakati tamaa na anajiapiza kuwa atafanya kila linalowezekana kuhakikisha analipata penzi la Harvey, ambaye sasa umaarufu wake ulikuwa ukizidi kuongezeka siku baada ya siku, kutokana na kiwango kikubwa cha
kucheza mpira wa kikapu alichokionesha kwenye mashindano ya NCAA, yaliyokuwa yanawahusisha wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali nchini Marekani.
HARVEY alifungua boksi la zawadi, akakutana na harufu nzuri ya manukato yaliyokuwa yamepuliziwa vizuri. Akaanza kutoa zawadi moja baada ya nyingine. Kwa kiasi fulani alifurahishwa na zawadi zile, akajilazimisha kuamini kuwa kwa sababu zimetoka kwa dada yake, hakutakuwa na tatizo lolote.
“Umezipenda?” “Nimezipenda sana Skyler, nashukuru kwa kunijali.” “Hizo zinakutosha? Hebu ijaribu hata moja nione inavyokupendeza,” alisema Skyler huku akinyoosha kidole kwenye nguo za ndani alizokuwa amemletea Harvey kama zawadi.
“Nitazijaribu nikiwa peke yangu… naamini zitanipendeza sana,” alisema Harvey akiwa tayari ameshaugundua mtego wa Skyler. “Hapana bwana, mi’ nataka uzijaribu sasa hivi ili nione kama nimechagua nzuri,” alisema Skyler na kusimama, akamsogelea Harvey na kuushika mkanda wa suruali yake, akawa anajaribu kuufungua lakini Harvey akatumia ujanja wa hali ya juu.
“Subiri kwanza nikazibadilishie bafuni halafu nitakuita uje unione nilivyopendeza,” alisema Harvey na kuzichukua, akaelekea kwenye bafu lililokuwa ndani. Alipofika aliingia na kujifungia mlango kwa ndani, akawa anahema juujuu huku akifikiria namna ya kumkwepa Skyler.
“Kwani akiniona nitapungua nini, potelea mbali, liwalo na liwe,” alisema Harvey huku akianza kuivua suruali yake na kuzijaribu zile nguo za ndani alizoletewa na Skyler. Wakati akiendelea kubadilisha, alisikia sauti ya mwanachuo mwenzake, Cazzard akimuita na kugonga mlango.
“Nipo huku bafuni, nakuja,” alisema Harvey huku moyoni akishukuru kwa kitendo cha rafiki yake huyo kumfuata. Harakaharaka alivaa suruali yake na kutoka, akamfungulia mlango. Alipomtazama Skyler, alimuona akikunja sura kuashiria kuwa hakufurahishwa na ujio wa Cazzard.
“Nimetumwa kuja kukuita, kuna wageni wako pale utawala,” alisema Cazzard, Harvey akaweka vitu vyake vizuri na kuzifungia zile zawadi zake kwenye kabati.
“Twende mara moja halafu tutarudi kuja kuendelea,” alisema Harvey huku akimshika mkono Skyler na kumuinua, kwa shingo upande akakubali kuongozana naye. Walikwenda mpaka kwenye ofisi za utawala wa chuo kile ambapo Harvey aliwaona wanaume wawili waliokuwa wamevalia suti nadhifu na kubeba ‘briefcase’ mikononi mwao. Aliwakumbuka vizuri kuwa ni wale maofisa wa timu ya Miami Heat, akatabasamu.
Aliwasalimu kwa heshima, wakaenda kukaa kwenye chumba cha mazungumzo ambapo walianza kumuuliza juu ya hatua aliyofikia kuhusu mkataba waliomuachia siku iliyopita. Aliwajibu kuwa kila kitu kilienda vizuri, akawaomba wamsubiri kidogo akaulete ukiwa tayari umeshajazwa. Skyler naye alisimama, wakaongozana hadi kwenye hosteli ya akina Harvey.
“Nina furaha sana Skyler, wale ndiyo mameneja wa Miami Heat walioleta ule mkataba niliokuja nao jana nyumbani, naamini siku chache zijazo na mimi nitakuwa mchezaji maarufu sana duniani,” alisema Harvey kwa furaha akitegemea Skyler atamuunga mkono lakini haikuwa vile.
“Wee ukishakuwa maarufu si utatafuta wanawake wengine maarufu kama wewe? Mi’ sitaki uwe maarufu,” alisema Skyler huku akijikamua machozi, Harvey akamsogelea na kuanza kumbembeleza. Skyler aliitumia vyema nafasi ile kwani alijilaza kwenye kifua cha Harvey kwa kudeka, mikono yake akaipitisha kijanja na kuanza kumpapasa mgongoni.
“Harvey… nifanye nini ili uelewe hisia za moyo wangu? Nakupenda sana na nakuhitaji uwe wangu wa maisha,” alisema Skyler huku akizidi kumpapasa Harvey mgongoni.
“Nakupenda pia Skyler lakini hatuwezi kuwa wapenzi, sisi ni ndugu… tafadhali naomba unielewe dada’angu.”
“Ndugu? Kwani mimi na wewe tumezaliwa tumbo moja? Halafu si nilishakukataza kuniita dada? Harvey nakuomba utibu maradhi ya moyo wangu, naomba unielewe… Nakupenda sana,” alisema Skyler kwa sauti iliyojaa huba, akamsogezea mdomo wake na kutaka kumbusu lakini Harvey akamkwepa na kumwambia kuwa wafanye haraka kwa sababu wanasubiriwa na watu muhimu kule nje.
“Kwa hiyo hao mameneja wa Miami Heat ni muhimu kuliko mimi? Kwa nini hutaki kunielewa Harvey? Nifanye na mimi nijione ni mwanamke niliyekamilika, naomba niwe mpenzi wako,” alilalama Skyler huku akizidi kumkumbatia Harvey kwa nguvu.
Harvey aliamua kutumia nguvu kumtoa Skyler mwilini mwake. Akaenda kwenye kabati lake la kuhifadhia vitu na kuutoa ule mkataba ambao tayari ulishajazwa. Akamuinua Skyler ambaye alikuwa amejiinamia huku akilia, akampa moyo kuwa suala lile watalijadili kwa kina baada ya kumaliza taratibu za kukabidhiana ule mkataba na maafisa wa Miami Heat.
Skyler alikubali kwa shingo upande, wakatoka na kurudi kule utawala ambapo waliwakuta wale maafisa wa Miami Heat wakiwasubiri. Alipowapa mkataba uliojazwa, walimpa kitabu maalum cha kusaini kisha mmoja akafungua briefcase yake na kutoa hundi.
“This cheque worth ten thousand dollar for you! Registration allowance,” (Hundi hii ina thamani ya dola elfu kumi kwa ajili yako! Posho ya usajili)
alisema afisa mmoja huku akiigeuza na kuisaini upande wa nyuma. Kwa Harvey, ule ulikuwa kama muujiza. Dola elfu kumi kama posho, nje ya malipo ya mkataba na mshahara wake, hakutaka kuamini haraka. Baada ya makabidhiano yale, wale maafisa waliaga na kuondoka, wakamuahidi kuwa watawasiliana naye na kumpa maelekezo ya nini cha kufanya baada ya kusaini mkataba.
Kwa furaha aliyokuwa nayo Harvey, alijikuta akimkumbatia Skyler kwa nguvu, akambusu kwenye paji la uso wake na kumnyanyua juujuu. Kitendo kile angalau kilirejesha furaha kwenye mtima wa Skyler. Wakakubaliana kuwa waondoke asubuhi ileile mpaka benki kwa ajili ya kwenda kuzitoa fedha zile.
“Nisubiri hapahapa nikajiandae, nakuja muda si mrefu,” alisema Harvey, akaondoka mbiombio hadi chumbani kwake ambapo alibadilisha nguo tayari kwa kutoka kwenda kuchukua fedha zake benki. Muda mfupi baadaye, tayari alishakuwa amejiandaa.
Wakaondoka na Skyler mpaka kwenye benki kubwa ya Miami Corporate, Harvey akatoa ile hundi na taratibu za kibenki zikaendelea. Baada ya muda mfupi, noti mpya za dola miamia zilipangwa mbele ya Harvey, akazichukua na kuzihakiki kisha wakaondoka na Skyler mpaka nyumbani kwao. “Si umefurahi sana Harvey.”
“Nimefurahi mno Skyler, yaani hata sijui niseme nini,” alijibu Harvey bila kuelewa sababu za Skyler kumuuliza vile, akamshika mkono na kumwambia amfuate. “Unataka kunipeleka wapi?”
“Wee nifuate bwana, unaogopa nini,” alisema Skyler huku akizidi kumvuta Harvey mkono, akampeleka mpaka chumbani kwake na kumsukumia kitandani, akafunga mlango kwa funguo kisha akazitupia chini ya kitanda.
“Kwa kuwa leo umefurahi nataka na mimi unifurahishe, nimechoka kuteseka kwa ajili yako,” alisema Skyler huku akianza kutupa nguo mojamoja mwilini mwake. Akavua gauni lake zuri alilokuwa amelivaa na kubakia na nguo za ndani. Umbo lake changa likajionesha vizuri mbele ya Harvey.
“Sijawahi kumruhusu mwanaume yeyote kuujua mwili wangu, nilikutunzia wewe hii zawadi, naomba uitumie na mimi nijione ni mwanamke niliyekamilika,” alisema Skyler huku akijinyonganyonga kiuno chake kama dondora na kurembua macho yake kimahaba. Harvey alikuwa ameduwaa pale kitandani akiwa ni kama hayaamini macho yake. Taratibu uzalendo ukaanza kumshinda, hisia za mapenzi zikaanza kumpanda. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“LAKINI Dk Lewis akigundua kuwa natembea na mwanaye wa kipekee si nitakuwa matatizoni sana? Mama Skyler naye…” aliwaza Harvey ndani ya kichwa chake, mawazo yale yakamfanya hisia za kimahaba ambazo sasa zilikuwa zimeshapanda, zikatike ghafla. Akaamka na kwenda kujaribu kuufungua mlango lakini hakuweza kwani Skyler aliufunga kwa funguo walipoingia.
“Niache niende Skyler, leo sijisikii vizuri, nitakutafuta mwenyewe siku nyingine na kukupa hicho unachokitaka mpaka utosheke.” “No Harvey, huwezi kuondoka humu ndani bila kunitimizia haja zangu.”
“Please Skyler, nimekwambia sijisikii vizuri leo, tumbo limejaa gesi na linauma sana, naomba nielewe tafadhali, haraka za nini?” “Nimeshasema, kama hutaki tutakaa humuhumu chumbani kwangu mpaka mama arudi, na akiuliza nitasema unataka kunibaka.”
“Mungu wangu! Skyler kwa nini unataka kuniharibia maisha kiasi hicho? Nimekukosea nini? Hupendi kuniona nikiwa na furaha,” alisema Harvey huku machozi yakianza kumlengalenga lakini Skyler hakuelewa kitu.
“Sasa sikiliza, kama unanilazimisha hatuwezi kufaidi raha ya mapenzi, kwa leo niache lakini nakuahidi siku nyingine yoyote tutakayokutana, nitatii kila utakachoniambia? Kwa nini hutaki kunielewa Skyler?” alilalama Harvey, safari hii michirizi ya machozi ikianza kuulowanisha uso wake.
Skyler, baada ya kumuona Harvey anatokwa na machozi, alienda kumkumbatia kwa nguvu, akamwambia kwa sauti ya kunong’ona kuwa amemuelewa alichokisema lakini akamuomba siku nyingine wakikutana asikatae tena kama siku ile.
Harvey alishukuru Mungu kuona Skyler amemuelewa, naye akamkumbatia huku akijifuta machozi, akavaa vizuri nguo zake na kumuomba Skyler afungue mlango. Alipofanya hivyo, alitoka harakaharaka huku akimuahidi kuwa atarudi siku nyingine. Bila hata kugeuka nyuma, Harvey aliondoka kasi hadi nje, akapanda basi hadi chuoni kwao huku mawazo tele yakiendelea kukisumbua kichwa chake.
Alimuona Skyler kama kikwazo kingine maishani mwake, akajiapiza kuwa atafanya kila awezalo kumkwepa binti yule kwani kiukweli hata yeye alishaanza kuingia kwenye mtego wa kutaka kuvunja naye amri ya sita, jambo ambalo hakutaka kabisa litokee. Baada ya muda, aliwasili chuoni kwao huku akiwa na kiwango kikubwa cha fedha kwenye begi lake. Akapitiliza moja kwa moja mpaka hostel ambapo alienda kuzihifadhi zile fedha kwenye kabati lake. Kwa jinsi kichwa chake kilivyokuwa kimezongwa na mawazo, alijitupa kitandani na muda mfupi baadaye, usingizi mzito ukampitia. ***
“Oyaaa amka twende mazoezini, si unajua kesho tuna mechi ngumu dhidi ya wanafunzi wa chuo cha New Hampshire,” Cazzard alimuamsha Harvey aliyekuwa amezama kwenye dimbwi la usingizi wa pono. Harvey alishtuka kutoka usingizini, harakaharaka akaamka na kuanza kutafuta nguo zake za mazoezi. Muda mfupi baadaye akajumuika na wanafunzi wenzake kwenye mazoezi ya mpira wa kikapu.
“Leo unaonekana kuwa na mawazo sana, kuna tatizo nyumbani ulikoenda?” “Hapana Cazzard, nipo sawa lakini si unajua nimetoka kulala. Uchovu wa usingizi ndiyo umenifanya niwe hivi,” Harvey alijaribu kudanganya baada ya mwanachuo mwenzake kumuuliza swali lile. Ukweli ni kwamba kichwa chake kilikuwa kimezongwa na
mawazo kutokana na tukio lililotokea nyumbani kwao ambapo Skyler alikuwa akimlazimisha kufanya jambo ambalo hakutaka kabisa litokee. Baada ya muda wa mazoezi kuisha, Harvey alirejea hostel na baada ya kuoga, hakutaka hata kula chakula cha jioni wala kwenda kujisomea, akapitiliza kulala. Muda uliyoyoma hatimaye siku ya pili ikawadia. Kwa kuwa siku hiyo chuo chao kilikuwa kikishiriki kwenye mzunguko wa pili wa ligi ya NCAA, pilikapilika zilianza tangu asubuhi, hali iliyomfanya Harvey angalau asahau matatizo ya Skyler.
Wanachuo wengi walikuwa wakimpa moyo Harvey kuwa wanamtegemea sana siku hiyo kwani bila yeye, wasingeingia kwenye mzunguko wa pili wa ligi hiyo. Muda ulipowadia, wanachuo wengi akiwemo Harvey, walisafiri kwa basi la shule hadi katika Mji wa Hampshire, wakanyoosha moja kwa moja mpaka kwenye chuo kikuu cha mji huo, mahali ambapo pambano la mpira wa kikapu lingefanyika.
Kama kawaida yake, Harvey alijiandaa vya kutosha na muda wa mechi kuanza ulipowadia, aliwapanga wachezaji wenzake vizuri, kazi ikaanza. Ndani ya dakika chache za mwanzo, Harvey alifanikiwa kufunga pointi nyingi mfululizo, wanachuo wenzake wakawa wanamshangilia kwa nguvu huku waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nao wakimzungumzia kama mchezaji nyota aliyeng’ara siku ile.
Mpaka mchezo unafikia mwisho, timu ya chuo chao ilikuwa inaongoza kwa pointi nyingi, shangwe zikaendelea ambapo wanachuo wenzake walimbeba Harvey juujuu kama shujaa wao. Waandishi wa habari nao wakawa na kiu ya kumfanyia mahojiano lakini walishindwa kutokana na wanachuo wenzake kumshangilia kwa nguvu na kumbeba hadi kwenye basi walilokuja nalo. Muda mfupi baadaye wakaondoka na kurejea chuoni kwao.
Timu yao ikawa imefuzu kuingia hatua ya robo fainali kwa juhudi kubwa za Harvey. Kila mmoja alimuona kama shujaa anayestahili kushangiliwa, wanachuo wenzake wakambatiza jina la Lebron, mchezaji nyota aliyekuwa anaichezea timu kubwa ya Miami Heat.
Siku mbili baadaye, timu yao ilijitupa tena uwanjani kupambana na chuo cha Illinois kilichokuwa na historia ya kuchukua ubingwa wa ligi hiyo mara kadhaa. Pambano lilikuwa la kukata na shoka kwani chuo hicho nacho kilikuwa na wachezaji nyota ambao walimsumbua sana Harvey, wakawa wanamkaba watatuwatatu ili asipate nafasi ya kufunga magoli.
Kwa kiasi fulani, walifanikiwa kumpunguza kasi lakini mpaka mwisho wa mchezo, timu yao ilikuwa imewazidi wapinzani wao kwa pointi chache. Wakaibuka washindi ingawa Harvey alipata majeraha kadhaa kutokana na kubanwa sana na wachezaji wa timu pinzani.
“Leo walikukamia sana, si unaona walikuwa wanakukaba watatu watatu, lakini bado wameshindwa kukuzuia, we jamaa ni hatari sana, yaani chuo chetu hakijawahi kufuzu kuingia nusu fainali ya NCAA hata mara moja, leo ndiyo mara ya kwanza,” mwanachuo mmoja alimwambia Harvey wakiwa njiani kurejea chuoni kwao. Wote wakacheka na kushangilia kwa nguvu wakati daktari wa timu akiendelea kumpatia Harvey huduma ya kwanza.
Timu ya chuo cha Miami Polytechnic and Engineering College, kwa mara ya kwanza ilivuka hatua zote hadi ikafanikiwa kuingia katika hatua ya mwisho ya fainali, ambapo ilipangwa kucheza na timu ya Chuo Kikuu cha York College cha jijini New York.
Hatimaye siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa ya fainali ya michuano hiyo iliwadia. Akina Harvey na wenzake wakasafiri hadi jijini New York wakiwa na matumaini makubwa ya kunyakua ubingwa. Pambano hilo lilivuta hisia za watu wengi, kila mmoja akawa na hamu kubwa ya kuiona timu mpya ya Miami Polytechnic and Engineering College ikichukua kombe kwa mara ya kwanza, chini ya kiongozi wake, Harvey.
Kilichotabiriwa na wengi ndicho kilichotokea kwani pambano lilikuwa kali na la kusisimua. Mpaka mwisho wa mchezo, Harvey kama kawaida yake akafanikiwa kufunga magoli mengi peke yake, na kuvunja rekodi ya mchezaji aliyepachika vikapu vingi kuliko wote tangu ligi hiyo ianze.
Furaha waliyokuwa nayo wanachuo wenzake ilikuwa haielezeki, muda wa kutolewa kwa zawadi ulipowadia, chuo hicho kikakabidhiwa kombe pamoja na fedha taslimu, huku Harvey akichukua tuzo tatu kwa mpigo. Tuzo ya kwanza ilikuwa ni ya mchezaji bora aliyechipukia kwenye mashindano hayo, tuzo ya pili ikawa ni mfungaji bora wakati tuzo ya tatu ikawa ni mchezaji bora.
Alikabidhiwa tuzo tatu pamoja na fedha taslimu, tukio lililorushwa na vituo karibu vyote vya runinga nchini humo. Jina la Harvey likaingia katika orodha ya wachezaji bora kabisa wa mchezo wa kikapu kwa wanachuo kuwahi kutokea.
“Unajisikiaje kunyakua tuzo tatu kwa mpigo na kukiwezesha chuo chako kwa mara ya kwanza kunyakua kombe la NCAA?” Larry Clarkson, mtangazaji wa michezo wa runinga ya CNN alikuwa akimhoji Harvey, muda mfupi baada ya shamrashamra za fainali hiyo kumalizika jijini New York.
“Najisikia fahari sana, sikuwahi kutegemea kuwa ipo siku nitakuwa na uwezo mkubwa kiasi hiki kwenye mchezo wa mpira wa kikapu. Namshukuru Dk Lewis na familia yao kwani bila hivyo nisingekuwa hapa nilipo. Zaidi namshukuru Mungu wangu kwa kuninusuru na yote yaliyotokea mpaka leo nimefika hapa nilipo,” alisema Harvey huku akijifuta machozi ya furaha.
Licha ya ugumu aliokumbana nao mwanzo kutokana na kuzongwa na msongo mkali uliosababishwa na kumbukumbu za kuhuzunisha za jinsi wazazi wake walivyouawa mbele ya macho yake kisha kunusurika kufa baharini wakati akitoroka na wenzake, nyota ya jaha inaanza kung’aa maishani mwake.
Kipaji kikubwa cha mchezo wa mpira wa kikapu alichojaaliwa kinamfanya awe maarufu haraka nchini Marekani. Michuano ya mpira wa kikapu ya NCAA iliyokuwa maalum kwa wanafunzi wa vyuo nchini humo, inamtangaza na sasa kipaji chake kinaonekana na kila mtu.
Wakati akianza kusahau machungu aliyopitia maishani mwake, kikwazo kingine kinaanza kuibuka. Mtoto wa Dk. Lewis, Skyler anaonesha hisia nzito za mapenzi kwa Harvey na kuanza kumtega ili akubali kuvunja naye amri ya sita lakini anakuwa makini na kumzidi shetani nguvu. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ HARVEY aliendelea kupamba vyombo mbalimbali vya habari nchini Marekani na sehemu nyingine kwa wiki kadhaa huku kila mmoja akimtabiria kuja kuwa mtu mwenye mafanikio makubwa kupitia kipaji kikubwa cha mpira wa kikapu alichokuwa nacho.
Siku zilizidi kusonga mbele huku jina lake likizidi kuwa gumzo kila mahali. Akaendelea na masomo huku safari hii akipewa heshima ya kipekee kutoka kwa wanachuo wenzake, wakufunzi na watu wa kila aina, akawa anaishi kama waishivyo watu maarufu nchini humo.
Licha ya yote aliyokuwa anayapitia, kwake heshima kwa wakubwa na wadogo ilibaki kuwa nguzo yake muhimu. Kamwe hakujisikia wala kuwadharau wengine, akaendelea na masomo yake huku kila mwisho wa muhula, matokeo yake ya mitihani chuoni hapo yakizidi kuwa mazuri.
Hakuacha kuwaheshimu Dk Lewis na mkewe ingawa alipunguza sana safari za kwenda kuwatembelea nyumbani kwao akihofia kukutana na Skyler. Alitambua fika kuwa itakapotokea akakutana na Skyler wakiwa wawili tu, lazima shetani atamzidi nguvu na kumsukuma kufanya jambo ambalo mwisho wake utakuja kuwa mbaya.
Badala ya kuwatembelea nyumbani kwao, akabadili utaratibu ambapo alikuwa akimfuata Dk Lewis kazini kwake na kufanya naye mazungumzo hukohuko kisha kurejea chuoni. Hata alipohitaji kuzungumza na mama Skyler, alikuwa akimfuata kazini kwake na kumalizana naye.
Kila Skyler alipokuwa anamtembelea chuoni, alikuwa akiwaita marafiki zake wawili au watatu na kumfanya ashindwe kumfanyia vituko vya kimapenzi, jambo lililoonekana kumchukiza Skyler, akapunguza safari za kumfuatafuata huku moyoni akiweka nadhiri kuwa ipo siku yale aliyokuwa anayataka yatatimia.
Hatimaye Harvey alimaliza mwaka wa pili chuoni pale kwa mafanikio makubwa, kipindi cha likizo hakurudi nyumbani kama ilivyokuwa kawaida, badala yake akaomba ruhusa kwa walezi wake ya kwenda kuimalizia likizo yake (vacation) kwenye Jiji
la Bridgetown kwenye Visiwa vya Barabados kujipongeza kwa mafanikio makubwa aliyoyapata. Alihitaji muda wa kukaa mbali na watu wote ili apate fursa ya kuyatazama upya maisha yake na kuangalia alipotoka, alipo na anapolekea. Wazo lile liliungwa mkono na Dk Lewis na mkewe kwani hata washauri wa kisaikolojia waliokuwa wanamtibu Harvey siku za mwanzoni, walishauri jambo kama lile.
Hakuongozana na mtu yeyote katika safari ile, akachukua vitu vichache zikiwemo nguo na baadhi ya vitabu vyake. Akasafiri kwa ndege mpaka kwenye Jiji la Bridgetown. Kwa kuwa fedha hazikuwa tatizo tena kwake, alifikia kwenye hoteli yenye hadhi ya nyota tano ya Bajan Grenadines iliyokuwa kwenye ufukwe wa Bahari ya Atlantic iliyokuwa inakizunguka kisiwa hicho.
Alikaa kisiwani humo kwa siku 28 huku kila siku asubuhi na jioni akitumia muda mwingi kufanya mazoezi ya mpira wa kikapu, ikiwa ni maandalizi kabla hajaenda kuripoti rasmi kwenye timu ya Miami Heat. Kwa siku zote alikuwa bize kiasi cha kumfanya asihisi upweke wa aina yoyote. Baada ya wiki nne kuisha, alijiandaa kwa safari ya kurejea Miami, Florida nchini Marekani.
Baada ya maandalizi yote kukamilika, alisafiri kwa ndege ya American Airline hadi Marekani na bila kupitia nyumbani kwa Dk Lewis alipitiliza moja kwa moja chuoni japokuwa bado muhula wa masomo ulikuwa haujaanza. Kilichomfanya apaone nyumbani kwa Dk. Lewis kama kituo cha polisi ni vituko vya Skyler. Aliona njia pekee ya kuepusha shari iliyokuwa inataka kutokea ni kujiweka mbali na binti huyo.
Siku chache tangu arejee kutoka Barbados, alipigiwa simu na viongozi wa timu ya Miami Heat wakimtaarifu kuwa siku inayofuata, viongozi wa juu wa timu hiyo walikuwa wakihitaji kuzungumza naye.
Alijiandaa na siku iliyofuatia akafunga safari mpaka kwenye makao makuu ya timu hiyo yaliyokuwa katika Mtaa wa Miami Chini (Downtown) kwenye Jimbo la Florida. Alipofika, alipokelewa kama shujaa na watu ambao tayari walikuwa wameandaliwa kwa kazi ile bila mwenyewe kujua. Ikawa ni kama ‘sapraizi’ kwake ambapo alibebwa juujuu hadi kwenye chumba cha mikutano katika jengo la American Airways Arena lililokuwa linatumika kama ofisi za timu hiyo.
“Harvey, karibu sana Miami Heat, kutana na Micky Arison, huyu ndiye mmiliki wa timu hii, utamfahamu zaidi ukianza kushiriki mazoezi na timu yetu,” alisema meneja wa timu hiyo, Pat Riley, Harvey na Arison wakapeana mikono huku kila mmoja akiwa na furaha ya kukutana na mwenzake.
Akatambulishwa pia kwa kocha mkuu wa timu hiyo, Erik Spoelstra ambaye walipopeana mikono alijaribu kumpima nguvu kwa kuusukuma mkono wake kwa kushtukiza.
“Safi sana, hapa nilikuwa nakufanyia jaribio jepesi, unaonekana una nguvu za kutosha kwenye mikono yako, jambo ambalo ni muhimu sana kwa wachezaji wa mpira wa kikapu,” alisema kocha Spoelstra huku akicheka, ukumbi mzima uliokuwa umejaa maafisa wa juu wa timu hiyo, ukalipuka kwa vicheko.
Utambulisho uliendelea ambapo alikutanishwa na maafisa wengine waliokuwa wanaunda menejimenti ya timu hiyo. Baada ya kumaliza utambulisho huo, Harvey alielekezwa sehemu ya kukaa ambapo mmiliki wa timu hiyo alianza kutoa hotuba fupi ya kumkaribisha Harvey kwenye timu yake.
“Tutakulipa mshahara mnono kila wiki na utakapomaliza chuo tutakupa nyumba ya kuishi pamoja na usafiri. Tunataka uitumikie timu yetu kwa uwezo wako wote kuhakikisha tunatetea kombe la NBA tunalolishikilia na kunyakua mengine zaidi,” alisema Arison kwenye sehemu ya hotuba yake na kupigiwa makofi na wote waliokuwa ukumbini mle.
Akakabidhiwa jezi namba yenye namba 11 mgongoni ambayo aliambiwa ndiyo atakuwa akiitumia awapo na timu hiyo. Wakafuatia viongozi wengine ambao kila mmoja alitoa hotuba fupi akionesha matumaini makubwa kwa mchezaji huyo.
Kwa Harvey bado alikuwa anaona kama yupo ndotoni, hata alipopewa nafasi ya kusema chochote, aliishia kumwaga machozi ya furaha na kuahidi kuitumikia timu ile kwa moyo mkunjufu. Baada ya kikao kile kumalizika, Harvey alienda kutambulishwa kwa wachezaji wenzake waliokuwa wanaendelea na mazoezi kwenye viwanja vya timu hiyo.
Akakutanishwa na mchezaji nyota wa timu hiyo, Lebron James ambaye alianza kumtambulisha kwa wachezaji wengine kama Ray Allen, Joel Anthony, Shane Battier, Chris Bosh, Mario Chalmers, Norris Cole, Eddy Curry, Justin Hamilton, Terrel Harris na wengine wengi.
Ilikuwa siku ya kipekee sana kwa Harvey kwani alizoea kuwaona wachezaji hao kwenye runinga na vyombo vya habari lakini siku hiyo alipeana nao mikono laivu na kuzungumza nao mawili matatu. Baada ya muda, akaambiwa abadilishe nguo zake na kuvaa jezi mpya alizokabidhiwa kisha aungane na wenzake kwenye mazoezi.
Waandishi mbalimbali wa habari wakiwemo wapiga picha na watangazaji wa redio na runinga walishaataarifiwa kuwa Harvey atatambulishwa rasmi siku hiyo, hivyo wakamiminika kwa wingi kwenye viwanja vya timu hiyo. Baada ya Harvey kuvaa jezi nadhifu za timu hiyo, aliingia uwanjani huku akishangiliwa kwa nguvu, akaanza kufanya mazoezi huku kila mtu akiwa makini kumtazama.
“Aisee hatujakosea kumsajili huyu kijana, hebu cheki anavyowakimbiza wenzake na ku-dunk, yaani hata Lebron James hapa itabidi afanye kazi ya ziada kulinda namba yake,” alisema mmiliki wa timu hiyo, Arison na kuungwa mkono na wenzake. Mazoezi yakaendelea ambapo kwa mara nyingine Harvey alifanikiwa kuthibisha uwezo wake kwa vitendo.
Baada ya kukaa na kupambana na ugumu aliokumbana nao mwanzo kutokana na kuzongwa na msongo mkali uliosababishwa na kumbukumbu za kuhuzunisha za jinsi wazazi wake walivyouawa mbele ya macho yake, Harvey anaanza kusahau yote na mafanikio yanaanza kuelekea upande wake.
Kipaji kikubwa cha mchezo wa mpira wa kikapu alichojaaliwa, kinamfanya awe maarufu haraka nchini Marekani na kusajiliwa na timu kubwa ya Miami Heat, iliyokuwa inashikilia ubingwa wa NBA nchini Marekani. Harvey ambaye aliibukia kutoka kwenue michuano ya mpira wa kikapu ya NCAA iliyokuwa maalum kwa wanafunzi wa vyuo nchini humo, anakuwa gumzo kila sehemu.
Wakati maisha yakimnyookea, kikwazo kingine kinaanza kuibuka. Mtoto wa Dk. Lewis, Skyler anaonesha hisia nzito za mapenzi kwa Harvey na kuanza kumtega ili akubali kuvunja naye amri ya sita lakini anakuwa makini na kumzidi shetani nguvu.
HARVEY aliendelea kufanya mazoezi na wachezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya Miami Heat, huku benchi la ufundi la timu hiyo, likiangalia mambo kadhaa kwa mchezaji huyo waliyekuwa tayari wamesaini naye mkataba mnono.
Viongozi wa juu wa timu hiyo, akiwemo mmiliki, meneja, kocha na maafisa wengine wa ngazi za juu, wote walikuwa uwanjani huku wachezaji wote wakiendelea na mazoezi kwa nguvu. Kwa kuwa Harvey alikuwa na mazoea ya kufanya
mazoezi magumu kila siku, kwake ile ilikuwa nafasi ya kuonesha uwezo wake mwingine. Akaendelea kujitahidi kwa uwezo wake wote, huku akishangiliwa kwa nguvu. “He was born to succeed through basketball,” (alizaliwa ili afanikiwe kupitia mpira wa kikapu)
alisema meneja wa timu hiyo, wakati akibadilishana mawazo na mmiliki pamoja na maafisa wengine. Waandishi wa habari nao waliendelea kufanya kazi yao, Harvey akapigwa picha nyingi kuanzia zile za kawaida (still) mpaka za video. Kwa kipindi chote alichocheza, hakuna hata dakika moja ambayo alionekana kupunguza kasi, akawa anawachangamsha wenzake na
kuwaonesha ufundi wa kila aina, kila mmoja alimpigia makofi huku wengine wakiendelea kumshangilia kwa nguvu. Mpaka muda wa mazoezi unamalizika, jina la Harvey lilikuwa mdomoni mwa kila mtu, watu wakawa wanaulizana alikuwa wapi siku zote kujitokeza.
“Safi sana, naamini hapa ndipo ulipopangiwa kuja kufanikiwa maishani mwako. Nimefurahishwa na uwezo wako, na nakuahidi utakapoendelea kuongeza juhudi kila siku na malipo yako yatakuwa yanaongezeka,” alisema mmiliki wa timu ile, Micky Arison. Wakazungumza mambo mengi ambapo pia walikubaliana Harvey aendelee kubaki na timu ile kwa siku chache ambazo zilikuwa zimesalia kabla ya muhula wa masomo kuanza. Kwa kuwa Harvey bado alikuwa na siku chache kabla ya kuanza masomo, alikubaliana na wazo lile, akaendelea kukaa kwenye makao makuu ya timu hiyo, Miami Downtown akifanya mazoezi ya asubuhi, mchana na jioni kulingana na ratiba ilivyokuwa inaeleza.
Aliendelea kuonesha kipaji chake muda wote huku wenzake wengi wakitamani nao wangekuwa na uwezo kama wa Harvey. Siku moja kabla ya tarehe ya kuanza rasmi kwa masomo chuoni ilipowadia, Harvey akiwa tayari ameshafanya mambo mengi na wachezaji wenzake na angalau kuanza kuzoeana nao, alianza kujiandaa kwa ajili ya kurejea chuoni siku inayofuatia “Usiondoke Harvey, endelea kufanya mazoezi na sisi, ukiondoka tutapooza kabisa, tumeanza kukuzoea,” alisema Lebron James, nahodha wa timu hiyo iliyokuwa inashikilia ubingwa wa kombe la ligi kuu ya mpira wa kikapu nchini Marekani (NBA). Hakutaka kabisa kusikia taarifa za Harvey kurejea chuoni. “Ahsante kaka, najua mnavyojisikia , lakini ni lazima nihitimu kwanza masomo yangu, tupo pamoja wala msijali,” alijibu Harvey huku akiwa ameshikana mkono na Lebron, wakaendelea kuzungumza mambo kadhaa yaliyowafanya wazidi kuzoeana.
Wachezaji wengi hawakutaka Harvey aondoke kwani mbinu, nguvu, ubunifu na kasi alivyovionesha kwa muda mfupi aliokuwa amekaa na timu ile, viliwafanya wachangamke sana, tofauti na walivyokuwa mwanzo. Nguvu ya kujiamini ikaongezeka kwa kila mmoja. Hata hivyo, Harvey ilikuwa ni lazima arejee chuoni kumalizia mwaka wa mwisho kama mkataba ulivyokuwa unaeleza. Akawaahidi kuwa angeendelea kushirikiana nao siku za mwisho wa wiki au baada ya muda wa masomo.
Ikabidi iandaliwe hafla nyingine fupi ya saa zisizozidi tatu, ambapo wachezaji na viongozi wote, walimshukuru Harvey kwa kujumuika nao kwa siku zile chache, wakakubali kuwa uwezo na kipaji alivyokuwa navyo, ni hazina kubwa kwa timu ile. Walimsihi asikubali kurubuniwa na timu nyingine kwani pale ndiyo kwao na mkombozi waliyekuwa wanamsubiri kwa muda mrefu kwenye mpira wa kikapu, alikuwa amewadia. Baada ya hafla ile fupi iliyojumuisha watu kula, kunywa na kucheza muziki kumalizika, Harvey alisindikizwa na msafara mkubwa wa wachezaji na viongozi wa timu ya Miami Heat mpaka chuoni kwao, shamrashamra za kujiunga kwake na timu hiyo zikalitikisa jiji lote la Miami na Jimbo la Florida kwa jumla. Shangwe zikapamba moto kwenye mitaa yote msafara wa kumsindikiza chuoni ulipopita. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Mpaka wanawasili chuoni kwao, Miami Polytechnic and Engineering College, wanachuo wenzake walikuwa wameshajipanga, wakampokea kwa shangwe na kupitiliza mpaka kwenye ukumbi mkubwa wa Hall 7, uliokuwa unatumika kufanyia sherehe na matamasha ya wanachuo, burudani kubwa ikaendelea chuoni pale. “Najisikia fahari sana, mafanikio haya niliyoyapata ni yenu na nayatoa kwa ajili yenu, namshukuru Mungu wangu na wote mnaoniunga mkono, naheshimu sana wema wa Dk Lewis na familia yake kwangu, sina cha kusema zaidi ya ahsanteni sana,” alisema Harvey huku akishangiliwa kwa nguvu. ***
Siku ile ya kipekee kwenye maisha ya Harvey ikapita, usiku akalala usingizi wa ajabu, ambao hakuwahi kuulala tangu azaliwe, akawa anajiona anaelea kwenye mbingu ya saba kwa mafanikio yale. Kesho yake, alfajiri na mapema aliamka kama kawaida, akavaa nguo zake za mazoezi na kwenda kwenye ‘gym’ ya chuo kwa ajili ya kujifua.
Siku zote hakutaka kubweteka, japokuwa kila mtu alikuwa akiukubali uwezo wake awapo uwanjani, mwenyewe bado hakuwa akiridhishwa na kiwango chake, akapania kufanya mazoezi ya nguvu mara kwa mara ili kuongeza uwezo wake maradufu. Aliendelea na mazoezi mpaka saa moja kasoro za asubuhi, akaenda kujiandaa na wenzake kwa ajili ya kuhudhuria masomo kulingana na ratiba yao ya chuo ilivyokuwa.
Wakati akiendelea kujiandaa, mwanachuo mwenzake, Cazzard alimfuata na kumweleza kuwa jana yake, wakati yeye akiwa bado hajarejea kutoka kwenye utambulisho wa timu ya Miami Heat, mdogo wake, Skyler alifika chuoni pale na kumkosa. “Alikusubiri kidogo, baadaye akaondoka na kuahidi kuwa leo atakuja tena kwa sababu ana ujumbe muhimu sana kwako.” “Aaah! Huyu dada’angu naye… anataka kuniharibia ‘future’ hivihivi.” “Kwa nini unasema hivyo Harvey?” “Mh! Najisikia aibu kusema lakini ndiyo ukweli… dada’angu huyu anataka tuwe na uhusiano wa kimapenzi.” “Whaaaat? Mapenzi? Huyu si mdogo wako kabisa huyu, halioni hilo?” “Yaani mi sina la kusema, amenikosesha raha kwa kipindi kirefu sana.” “Ndiyo maana siku ile nilipokuja kukugongea mlango mkiwa naye ndani alinitazama kwa jicho baya sana? Una msala
mwanangu… lakini mtoto mzuri kama yule siku moja unafumba macho na kuuweka undugu pembeni ‘then’ unaonja asali lakini mara moja tu teh teh teh! Im just kidding! (natania tu),” alisema Cazzard na kumfanya Harvey amkazie macho. “Sipendi utani huo, be serious Cazzard, hili ni tatizo lingine kwenye maisha yangu,” alisema Harvey, ikabidi rafiki yake abadili mazungumzo haraka akikwepa kumkasirisha zaidi.
Muda mfupi baadaye, wakati vipindi ndiyo vikikaribia kuanza, Harvey alishtuka kumuona Skyler akija mbiombio. Kwa kuwa safari hii alikuwa anapafahamu mpaka kwenye chumba alichokuwa analala Harvey pale chuoni, aliongoza moja kwa moja.
Harvey akaishiwa nguvu, ikabidi akubali kumpokea, wanafunzi wengine wakaanza kuelekea kwenye vipindi vya masomo yao, kila mmoja kulingana na ratiba yake ilivyokuwa inasema. “Skyler, naomba niende darasani tutazungumza baadaye.” “Noo Harvey, naomba uahirishe vipindi vya asubuhi, nina ujumbe mzito kwa ajili yako, please, fanya hivyo kwa ajili yangu,” alisema Skyler kwa kubembeleza. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ ITAENDELEA
Simulizi : Queen Of Gorillas ( Malkia Wa Masokwe ) Sehemu Ya Pili (2)
WAHENGA walinena kuwa ukiona giza linaongezeka, ujue mapambazuko yamekaribia. Usemi huu unaonekana kuwa kweli kwa Harvey, kijana kutoka nchini Liberia, aliyekimbia machafuko ya wenyewe kwa wenyewe nchini kwao na kunusurika kufa baharini kabla hajaokolewa na wasamaria wema waliompeleka hospitali kisha kupewa hifadhi na Dk Lewis, Miami nchini Marekani. Continued after the jump ….
Anapambana na tatizo la msongo wa mawazo na huzuni kali lililompata kila alipokuwa anawakumbuka wazazi wake. Dk Lewis na familia yake wanakuwa msaada mkubwa kwake mpaka anasahau kila kitu.
Baada ya muda, kipaji kikubwa cha mchezo wa mpira wa kikapu alichojaaliwa, kinamfanya awe maarufu haraka nchini Marekani, anasajiliwa na timu kubwa ya Miami Heat lakini kikwazo kingine kinaanza kuibuka. Mtoto wa Dk. Lewis, Skyler anaonesha hisia nzito za mapenzi kwa Harvey na kuanza kumtega ili akubali kuvunja naye amri ya sita.
BASI tuzungumze haraka maana kipindi hiki cha asubuhi ni muhimu sana, naomba unielewe tafadhali.” “Harvey! Ina maana masomo yako ni muhimu kuliko mimi? Kwa nini hutaki kunielewa?” “Wewe ni muhimu Skyler, lakini masomo yangu ni muhimu pia. Hukujisikia vizuri nilipofeli mtihani wangu wa kidato cha nne, unataka nifeli tena?”
“Huwezi kufeli Harvey kwa kukosa kuingia kwenye kipindi kimoja, hebu nisikilize vinginevyo tutakorofishana,” alisema Skyler huku akianza kubadilika usoni.
“Basi Skyler, siendi darasani kwa ajili yako,” alisema Harvey, Skyler akamsogelea palepale alipokuwa amekaa, akapitisha mkono wake begani na kuanza kumpapasa Harvey mgongoni huku akimtazama kwa macho yake mazuri ya mviringo.
“Nisamehe kwa kuvuruga ratiba zako, hata mimi nina haki ya kukaa na wewe na kufurahi,” alisema Skyler huku akijichekelesha. Harvey hakujibu kitu, akawa anamhimiza amwambie kile kilichompeleka chuoni kwao asubuhi ile. “Wala sina tatizo au ishu kubwa kama unavyodhani isipokuwa nataka unikubalie jambo moja tu Harvey. Ukikubali nitafurahi sana na utayafanya maisha yangu kubadilika kabisa,” alisema Skyler huku akizidi kumtazama Harvey kwa macho yaliyokuwa yamebeba ujumbe.
Skyler akamwambia kuwa alikuwa amemfuata chuoni pale kwa lengo la kumchukua na kwenda naye nyumbani kwao. Akamwambia kuwa kuna jambo alikuwa anataka kwenda kumuonesha na kwamba hawatachelewa kurudi. Kutokana na ushawishi alioutumia, Harvey ilibidi akubali lakini akampa sharti moja kuwa ni lazima waende haraka kwani hakuwa tayari kukosa na kipindi cha pili.
Skyler alimkubalia na kumuahidi kuwa hatamchelewesha, wakaondoka huku akionekana kufurahia sana ushindi aliokuwa ameupata. Kwa kuwa Skyler alikuwa amejiandaa kikamilifu, walipotoka chuoni pale hakutaka wapoteze muda, akakodi taxi iliyowachukua moja kwa moja hadi nyumbani kwao.
Walipofika, waliingia moja kwa moja hadi sebuleni, Skyler akamwambia Harvey amsubiri palepale. Akaenda mpaka chumbani kwake na baada ya dakika zisizozidi tatu, alitoka akiwa amebadilisha nguo, safari hii akiwa amevaa kigauni chepesi kilichoachia sehemu kubwa ya mwili wake ikiwa wazi. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Usoni alikuwa amejipodoa na kumfanya abadilike kabisa na kuwa na mvuto mithili ya malaika. Alijinyunyizia marashi yaliyokuwa na harufu nzuri kiasi cha kufanya mapigo ya moyo ya Harvey yaanze kwenda mbio. “Simama na ufumbe macho,” alisema Skyler huku akimsogelea kwa mwendo wa madaha, akaenda kumfunga kitambaa machoni mwake ili kumzuia kuona, akamshika mkono na kuanza kumkokota kuelekea chumbani kwake mithili ya kondoo anayepelekwa machinjioni.
Baada ya kuingia chumbani, Skyler aliufunga mlango kwa kufuli kisha akaenda kumfungua Harvey kitambaa alichokuwa amemfunga machoni, kisha akamwambia afumbue macho.
“Whaoooo! Chumba chako kimebadilika, umekipamba vizuri sana,” alisema Harvey baada ya kufumbua macho. Japokuwa ilikuwa bado ni asubuhi, mandhari ya chumbani mle yalifanya kuonekane kama usiku. Madirisha yote yalikuwa yamefungwa na kufunikwa kwa mapazia mekundu, taa yenye mwanga hafifu wa rangi nyekundu, ikawa inawaka na kukiongezea nakshi chumba kizima.
Manukato mazuri yalikuwa yamepuliziwa chumba kizima huku kitanda kikiwa kimetandikwa kwa mashuka masafi meupe, yaliyokuwa na maua mekundu. Kulikuwa na kadi kadhaa za mapenzi pale kitandani, zote zikiwa na jina la Harvey huku kukiwa pia na waridi ambayo yaliwekwa vizuri mle chumbani.
Skyler alikuwa amedhamiria kweli kulipata penzi la Harvey kwani kwa jinsi ilivyoonesha, alitumia muda mrefu kukibadilisha chumba chake ili kiwe na mwonekano wa kimahaba. Mpangilio nadhifu wa chumba kile, ukichanganya na jinsi Skyler alivyokuwa amevaa kihasara, vilitosha kumuamsha shetani wa mahaba wa Harvey.
Wakawa wanatazamana usoni kama majogoo yanayotaka kupigana, Skyler akamsogelea Harvey kwa hatua za taratibu kisha akamkumbatia kimahaba na kujilaza kifuani kwake.
“Nakupenda sana Harvey ndiyo maana nafanya yote haya kwa ajili yako. Japokuwa unanichukia, bado sitachoka kulipigania penzi lako wala sitachoka kukutamkia kuwa nakupenda kwa dhati kutoka ndani ya moyo wangu,” alisema Skyler huku akianza kulengwalengwa na machozi.
Kwa kuwa shetani wa Harvey alishaanza kupanda kichwani, alianza kumbembeleza Skyler huku akimpapasa taratibu mgongoni, akamwambia yeye hamchukii lakini anadhani siyo busara kujiingiza kwenye uhusiano wa kimapenzi kwani wao ni kama kaka na dada.
“Wazazi wako wamenilea kwa ukarimu kama mtoto wao tangu siku ya kwanza waliponiokota hospitalini nikiwa sina mbele wala nyuma. Unafikiri baba’ako atajisikiaje siku akigundua kuwa mimi na wewe tuna uhusiano wa kimapenzi?
“Huoni litakuwa ni tatizo kubwa sana linaloweza hata kuyavuruga maisha yangu?” alisema Harvey, Skyler akawa anahema kwa nguvu na kutoa miguno ya kimahaba huku viungo vya mwili wake vikianza kuishiwa nguvu. Hakutakakuelewa chochote.
“Nitakulinda Harvey, najua namna ya kuwatuliza wazazi wangu, nakupenda sana na nipo tayari kufanya lolote kwa ajili yako,” alisema Skyler huku akianza kufungua vifungo vya shati la Harvey.
Alijitahidi kumzuia lakini shetani wa mahaba ambaye alikuwa tayari ameshakolea kichwani mwake, alimshawishi Harvey kulimenya tunda lile bivu na kulitia kinywani. Dakika chache baadaye, Harvey na Skyler walikuwa kama walivyoletwa duniani, wakawa wanaendelea kupashana moto miili yao, huku mtoto wa kike akiyarembua macho yake na kutoa miguno ya raha.
“Taratibu Harvey… si unajua mwenzio sijawa..hi… uuuh!” alilalama Skyler wakati Harvey akijiandaa kuanza kukimbia mbio za mita mia moja, sekunde chache baadaye, Skyler alipiga yowe kubwa baada ya Harvey kufanikiwa kuutoboa ukuta mgumu wa ngome ya Skyler na kuivunja glasi yake kwa nguvu.
Shuka jeupe na nadhifu alilokuwa ametandika kitandani, likabadilika rangi na kuwa na madoa makubwa ya rangi nyekundu… glasi ya Skyler ilikuwa imevunjika!
Kutokana na maumivu makali aliyokuwa anayasikia Skyler, aliendelea kupiga mayowe kwa nguvu huku akilitaja jina la Harvey.
Harvey aliyekuwa anaendelea kutimua mbio kwa kasi kwenye uwanja wa Skyler, alishtuka baada ya kusikia mlango wa nje unagongwa kwa nguvu, akamziba Skyler mdomo huku akianza kuhaha kutafuta sehemu ya kujificha.
“Kuna mtu anagonga mlango, hebu sikiliza,” alisema Harvey huku akijifuta kijasho chembamba. Skyler alitulia na kusikiliza, wote wakaanza kuhaha kutafuta njia ya kujificha wasigundulike.
Skyler akajizoazoa na kusimama huku akisikia maumivu makali katikati ya miguu yake, akajifuta damu ambazo sasa zilikuwa zinachuruzika kwa wingi na kuanza kuelekea mlangoni kufungua mlango.
“Kaa hukuhuku chumbani wala usiogope, kila kitu kitakuwa sawa,” alisema Skyler huku akiukunja uso wake kuonesha kuwa alikuwa akihisi maumivu makali. Harvey akaingia chini ya kitanda na kujificha huku akitetemeka kupita kiasi.
Baada ya sekunde chache, Harvey alitoka kule chini ya kitanda baada ya kuhisi kuwa lazima ataonekana, akajaribu kupanda juu ya dari akajifiche lakini haikuwezekana. Akajaribu kuingia kwenye kabati la nguo za Skyler lakini napo alishindwa, akabaki ameduwaa kama mnyama aliyenaswa mtegoni.BASI tuzungumze haraka maana kipindi hiki cha asubuhi ni muhimu sana, naomba unielewe tafadhali.” “Harvey! Ina maana masomo yako ni muhimu kuliko mimi? Kwa nini hutaki kunielewa?” “Wewe ni muhimu Skyler, lakini masomo yangu ni muhimu pia. Hukujisikia vizuri nilipofeli mtihani wangu wa kidato cha nne, unataka nifeli tena?”
“Huwezi kufeli Harvey kwa kukosa kuingia kwenye kipindi kimoja, hebu nisikilize vinginevyo tutakorofishana,” alisema Skyler huku akianza kubadilika usoni.
“Basi Skyler, siendi darasani kwa ajili yako,” alisema Harvey, Skyler akamsogelea palepale alipokuwa amekaa, akapitisha mkono wake begani na kuanza kumpapasa Harvey mgongoni huku akimtazama kwa macho yake mazuri ya mviringo.
“Nisamehe kwa kuvuruga ratiba zako, hata mimi nina haki ya kukaa na wewe na kufurahi,” alisema Skyler huku akijichekelesha. Harvey hakujibu kitu, akawa anamhimiza amwambie kile kilichompeleka chuoni kwao asubuhi ile. “Wala sina tatizo au ishu kubwa kama unavyodhani isipokuwa nataka unikubalie jambo moja tu Harvey. Ukikubali nitafurahi sana na utayafanya maisha yangu kubadilika kabisa,” alisema Skyler huku akizidi kumtazama Harvey kwa macho yaliyokuwa yamebeba ujumbe.
Skyler akamwambia kuwa alikuwa amemfuata chuoni pale kwa lengo la kumchukua na kwenda naye nyumbani kwao. Akamwambia kuwa kuna jambo alikuwa anataka kwenda kumuonesha na kwamba hawatachelewa kurudi. Kutokana na ushawishi alioutumia, Harvey ilibidi akubali lakini akampa sharti moja kuwa ni lazima waende haraka kwani hakuwa tayari kukosa na kipindi cha pili.
Skyler alimkubalia na kumuahidi kuwa hatamchelewesha, wakaondoka huku akionekana kufurahia sana ushindi aliokuwa ameupata. Kwa kuwa Skyler alikuwa amejiandaa kikamilifu, walipotoka chuoni pale hakutaka wapoteze muda, akakodi taxi iliyowachukua moja kwa moja hadi nyumbani kwao.
Walipofika, waliingia moja kwa moja hadi sebuleni, Skyler akamwambia Harvey amsubiri palepale. Akaenda mpaka chumbani kwake na baada ya dakika zisizozidi tatu, alitoka akiwa amebadilisha nguo, safari hii akiwa amevaa kigauni chepesi kilichoachia sehemu kubwa ya mwili wake ikiwa wazi. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Usoni alikuwa amejipodoa na kumfanya abadilike kabisa na kuwa na mvuto mithili ya malaika. Alijinyunyizia marashi yaliyokuwa na harufu nzuri kiasi cha kufanya mapigo ya moyo ya Harvey yaanze kwenda mbio. “Simama na ufumbe macho,” alisema Skyler huku akimsogelea kwa mwendo wa madaha, akaenda kumfunga kitambaa machoni mwake ili kumzuia kuona, akamshika mkono na kuanza kumkokota kuelekea chumbani kwake mithili ya kondoo anayepelekwa machinjioni.
Baada ya kuingia chumbani, Skyler aliufunga mlango kwa kufuli kisha akaenda kumfungua Harvey kitambaa alichokuwa amemfunga machoni, kisha akamwambia afumbue macho.
“Whaoooo! Chumba chako kimebadilika, umekipamba vizuri sana,” alisema Harvey baada ya kufumbua macho. Japokuwa ilikuwa bado ni asubuhi, mandhari ya chumbani mle yalifanya kuonekane kama usiku. Madirisha yote yalikuwa yamefungwa na kufunikwa kwa mapazia mekundu, taa yenye mwanga hafifu wa rangi nyekundu, ikawa inawaka na kukiongezea nakshi chumba kizima.
Manukato mazuri yalikuwa yamepuliziwa chumba kizima huku kitanda kikiwa kimetandikwa kwa mashuka masafi meupe, yaliyokuwa na maua mekundu. Kulikuwa na kadi kadhaa za mapenzi pale kitandani, zote zikiwa na jina la Harvey huku kukiwa pia na waridi ambayo yaliwekwa vizuri mle chumbani.
Skyler alikuwa amedhamiria kweli kulipata penzi la Harvey kwani kwa jinsi ilivyoonesha, alitumia muda mrefu kukibadilisha chumba chake ili kiwe na mwonekano wa kimahaba. Mpangilio nadhifu wa chumba kile, ukichanganya na jinsi Skyler alivyokuwa amevaa kihasara, vilitosha kumuamsha shetani wa mahaba wa Harvey.
Wakawa wanatazamana usoni kama majogoo yanayotaka kupigana, Skyler akamsogelea Harvey kwa hatua za taratibu kisha akamkumbatia kimahaba na kujilaza kifuani kwake.
“Nakupenda sana Harvey ndiyo maana nafanya yote haya kwa ajili yako. Japokuwa unanichukia, bado sitachoka kulipigania penzi lako wala sitachoka kukutamkia kuwa nakupenda kwa dhati kutoka ndani ya moyo wangu,” alisema Skyler huku akianza kulengwalengwa na machozi.
Kwa kuwa shetani wa Harvey alishaanza kupanda kichwani, alianza kumbembeleza Skyler huku akimpapasa taratibu mgongoni, akamwambia yeye hamchukii lakini anadhani siyo busara kujiingiza kwenye uhusiano wa kimapenzi kwani wao ni kama kaka na dada.
“Wazazi wako wamenilea kwa ukarimu kama mtoto wao tangu siku ya kwanza waliponiokota hospitalini nikiwa sina mbele wala nyuma. Unafikiri baba’ako atajisikiaje siku akigundua kuwa mimi na wewe tuna uhusiano wa kimapenzi?
“Huoni litakuwa ni tatizo kubwa sana linaloweza hata kuyavuruga maisha yangu?” alisema Harvey, Skyler akawa anahema kwa nguvu na kutoa miguno ya kimahaba huku viungo vya mwili wake vikianza kuishiwa nguvu. Hakutakakuelewa chochote.
“Nitakulinda Harvey, najua namna ya kuwatuliza wazazi wangu, nakupenda sana na nipo tayari kufanya lolote kwa ajili yako,” alisema Skyler huku akianza kufungua vifungo vya shati la Harvey.
Alijitahidi kumzuia lakini shetani wa mahaba ambaye alikuwa tayari ameshakolea kichwani mwake, alimshawishi Harvey kulimenya tunda lile bivu na kulitia kinywani. Dakika chache baadaye, Harvey na Skyler walikuwa kama walivyoletwa duniani, wakawa wanaendelea kupashana moto miili yao, huku mtoto wa kike akiyarembua macho yake na kutoa miguno ya raha.
“Taratibu Harvey… si unajua mwenzio sijawa..hi… uuuh!” alilalama Skyler wakati Harvey akijiandaa kuanza kukimbia mbio za mita mia moja, sekunde chache baadaye, Skyler alipiga yowe kubwa baada ya Harvey kufanikiwa kuutoboa ukuta mgumu wa ngome ya Skyler na kuivunja glasi yake kwa nguvu.
Shuka jeupe na nadhifu alilokuwa ametandika kitandani, likabadilika rangi na kuwa na madoa makubwa ya rangi nyekundu… glasi ya Skyler ilikuwa imevunjika!
Kutokana na maumivu makali aliyokuwa anayasikia Skyler, aliendelea kupiga mayowe kwa nguvu huku akilitaja jina la Harvey.
Harvey aliyekuwa anaendelea kutimua mbio kwa kasi kwenye uwanja wa Skyler, alishtuka baada ya kusikia mlango wa nje unagongwa kwa nguvu, akamziba Skyler mdomo huku akianza kuhaha kutafuta sehemu ya kujificha.
“Kuna mtu anagonga mlango, hebu sikiliza,” alisema Harvey huku akijifuta kijasho chembamba. Skyler alitulia na kusikiliza, wote wakaanza kuhaha kutafuta njia ya kujificha wasigundulike.
Skyler akajizoazoa na kusimama huku akisikia maumivu makali katikati ya miguu yake, akajifuta damu ambazo sasa zilikuwa zinachuruzika kwa wingi na kuanza kuelekea mlangoni kufungua mlango.
“Kaa hukuhuku chumbani wala usiogope, kila kitu kitakuwa sawa,” alisema Skyler huku akiukunja uso wake kuonesha kuwa alikuwa akihisi maumivu makali. Harvey akaingia chini ya kitanda na kujificha huku akitetemeka kupita kiasi.
Baada ya sekunde chache, Harvey alitoka kule chini ya kitanda baada ya kuhisi kuwa lazima ataonekana, akajaribu kupanda juu ya dari akajifiche lakini haikuwezekana. Akajaribu kuingia kwenye kabati la nguo za Skyler lakini napo alishindwa, akabaki ameduwaa kama mnyama aliyenaswa mtegoni.
HARVEY, kijana kutoka nchini Liberia aliyekimbia machafuko ya wenyewe kwa wenyewe nchini kwao na kunusurika kufa baharini kabla hajaokolewa na wasamaria wema waliompeleka hospitali
kisha kupewa hifadhi na Dk Lewis, Miami nchini Marekani, anaanza kupata mafanikio kutokana na kipaji kikubwa cha kucheza mpira wa kikapu alichokuwa nacho. Kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao, anaiwezesha timu ya chuo chake kunyakua ubingwa wa kombe la mpira wa kikapu kwa wanafunzi wa vyuo, NCAA. Baadaye anasajiliwa na timu kubwa ya
mpira wa kikapu nchini Marekani, Miami Heat ambapo anaenda kutambulishwa rasmi kwenye makao makuu ya timu hiyo. Wakati hayo yakiendelea, upande wa pili mambo yanaanza kumwendea kombo Harvey. Mtoto wa
Dk. Lewis, Skyler anaonesha hisia nzito za mapenzi juu yake na kuanza kumtega ili akubali kuvunja naye amri ya sita. Licha ya kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wake wote kujizuia, Harvey anajikuta akinasa kwenye mtego wa binti Skyler na kushiriki naye mchezo wa kikubwa.Wakati wakiendelea na
walichokuwa wanakifanya,wanasikia mtu akigonga mlango kwa nguvu. “MBONA unagonga mlango kwa nguvu? Unasemaje?” “Nimesikia unapiga kelele za kuomba msaada, nikahisi umepatwa na tatizo kubwa ndiyo maana nimekuja kutoa msaada.” “Mh! Umenisikia mimi napiga kelele? Are you out of your mind?” (Umechanganyikiwa?) “Basi nisamehe kama nimekosea, lakini lengo langu halikuwa baya.” “Mimi sijapiga kelele zozote na wala sina tatizo, waweza kwenda na kuendelea na kazi yako.” “Sawa Skyler, lakini mbona unachuruzika damu miguuni? Umeumia?” aliuliza mlinzi huku akikodolea macho miguu ya Skyler ambayo kweli ilikuwa inachuruzika damu.
“Mungu wangu? Nitakuwa nimeingia kwenye siku zangu bila kujijua,” alisema Skyler kwa aibu iliyochanganyikana na mshtuko, akabamiza mlango na kumuacha yule mlinzi akiwa ameduwaa pale mlangoni. Alishahisi kuna kitu kilikuwa kinaendelea ndani lakini akaamua kujikausha na kuendelea na kazi zake kama kawaida.
“Aaah! Watu wengine bwana, kazi kufuatilia mambo yasiyowahusu,” alisema Skyler huku akijivuta kurudi chumbani kwake . Akawa anajifuta damu ambazo sasa zilikuwa zinachuruzika na kuchafua zulia la sebuleni.
Alipoingia chumbani kwake, alimkuta Harvey akiwa anababaika mithili ya mwendawazimu. Akamtuliza na kumwambia kuwa hawakuwa wazazi wao kama walivyohisi awali. “Niambie ukweli, sio baba’ako huyo?” “Wala siyo baba… ni mlinzi, eti anasema amenisikia nikipiga kelele za kuomba msaada,” alisema Skyler huku akitafuta taulo lake. Kutokana na jinsi alivyokuwa amechafuka, alilazimika kwenda bafuni kujimwagia maji na kujisafisha. Alipomaliza, alirudi chumbani kwake ambapo alimkuta Harvey ameshavaa nguo zake. “Umevaa nguo unaenda wapi?” “Si tulikubaliana kuwa sitachelewa kurudi chuoni?”
“Mh! Kuhusu kurudi chuoni sahau tu Harvey, leo ni siku yangu, lazima nijidai na wewe,” alisema Skyler huku akibadilisha shuka lililokuwa halitamaniki. Akatandika lingine kisha akamsogelea Harvey na kumvutia tena kwenye uwanja wa fundi seremala.
Wakaanza maandalizi ya safari ya pili, Harvey akaonekana kuishiwa na woga uliokuwa unamtesa awali. Muda mfupi baadaye, walikuwa dimbani wakiendelea kulisakata kabumbu kwa fujo. Japokuwa wote ilikuwa ndiyo mara yao ya kwanza kushiriki mchezo ule, walioneshana ufundi mithili ya wataalamu waliobobea kwenye sanaa za kikubwa.
Nusu saa baadaye, kila mtu alikuwa hoi bin taaban kwa uchovu. Mwili wa Harvey ulikuwa umelowa chapachapa kwa jasho, huku Skyler naye akiwa hatamaniki. “Harvey!” “Mmmh!”
“Hakika wewe ni mwanaume wa shoka, nashukuru sana kwani hatimaye umenitimizia kitu kilichokuwa kinautesa moyo wangu kwa siku nyingi sana. Nakuahidi kukupenda kwa moyo wangu wote.” “Nashukuru Skyler, mimi pia nimefurahi kwa raha ulizonipa, siku zote nilikuwa nakuona bado mdogo kumbe nilikuwa nachelewa! Nakuomba uniahidi kitu kimoja cha msingi…” “Kitu gani tena mpenzi?”
“Naomba iwe siri yetu, najua siku wazazi wako wakijua wanaweza hata kuniua, wewe pekee ndiye unayeweza kuniokoa kwa kutunza siri.”
“Usijali, nitahakikisha hakuna anayejua kinachoendelea kati yetu.” “Sasa vipi kuhusu mlinzi, si lazima atashtukia mchezo na kumwambia baba?”
“Mpuuzi tu yule, kwanza baba akirudi nitamtafutia zengwe mpaka afukuzwe kazi, ukija tena hapa utakuta kuna mlinzi mwingine kwani akiendelea kukaa hapa, ipo siku atavujisha siri,” alisema Skyler huku akikichezea kifua cha Harvey kilichojazia vizuri kutokana na mazoezi. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Baada ya kupumzika vya kutosha, Harvey na Skyler walielekea bafuni pamoja, wakaanza kuogeshana huku wakifanyiana vituko vya kimahaba vya hapa na pale. Walijisahau kabisa na kujiona wapo kwenye ulimwengu tofauti.
Baada ya kumaliza kuoga, walienda kuvaa nguo zao na kufuta ushahidi wa kimazingira mle ndani, walipohakikisha kila kitu kipo sawa, walitoka kuelekea chuoni kwa akina Harvey.
“Haa! Kumbe na wewe ulikuwepo ndani?” aliuliza mlinzi huku akionekana kushangaa sana, Harvey ikabidi aanze kujiumauma na kumwambia kuwa aliingia muda mfupi uliopita. “Mh! Mbona muda wote mimi nipo hapa lakini sijakuona ukiingia?” “We mlinzi vipi? Huyu amekuja sasa hivi, labda ulikuwa umelala. Na kama ndiyo tabia yako baba akija nitamwambia kuwa badala ya kulinda nyumba una kazi ya kulala,” aliingilia kati Skyler na kumtolea maneno makali yule mlinzi, ikabidi aufyate mkia kulinda kibarua chake. Wakatoka na safari ye kuelekea chuoni kwa akina Harvey ikaanza. “Skyler!” “Abee mpenzi wangu.”
“Unajua bado nina wasiwasi sana, si umemsikia yule mlinzi alivyokuwa anasema, lazima atawaambia wazazi wako.” “Wala usijali, mimi nitamuwahi kabla hajafanya chochote, nakuhakikishia leo ndiyo siku yake ya mwisho kufanya kazi hapa. Baba’angu anavyonipenda nikimwambia amfukuze kazi lazima atekeleze,” alisema Skyler na kumtoa Harvey wasiwasi.
Mpaka wanafika chuoni, tayari ilikuwa ni saa tisa alasiri, wakapitiliza mpaka kwenye bustani nzuri ya maua iliyokuwa chuoni pale, wakakaa sehemu iliyotulia na kuendelea kucheza michezo ya kimahaba.
“Unajua nimelihangaikia sana penzi lako, siku nikisikia una mwanamke mwingine… nitawaua wote wawili.” “Wala hata usiwe na wasiwasi Skyler, wewe ndiyo mwanamke wangu wa kwanza na wa mwisho, sitathubutu kukusaliti wala kukuuumiza hata mara moja.” “We unasema tu, kwa mfano ukianza kuichezea Miami Heat moja kwa moja, hutanisahau kweli na kuhamia kwa mastaa wenzako?”
“Siwezi Skyler, nitatulia na wewe kwa siku zote, wala umaarufu hautanichanganya,” alisema Harvey na kumbusu Skyler mdomoni. Wakaendelea kukaa eneo lile mpaka giza lilipoanza kuingia. Ikabidi Harvey amhimize Skyler kuwahi nyumbani kwani kwa jinsi ilivyoonesha, alishasahau hata kurudi kwao. Akamsindikiza mpaka nje ya geti la chuo na kumtafutia usafiri. *** “Harvey leo umeshinda wapi?” “Nilitoka mara moja Cazzard, vipi kwani kuna tatizo?” “Hapana, baba’ako alikuja kukujulia hali muda wa mchana lakini akakukosa.” “Baba? Dk Lewis?” “Yap, huyohuyo, kwani wewe una baba mwingine?” “Mungu wangu? Alipokuja amesemaje?”
“Hajasema kitu, alienda kukuulizia pale utawala, nikaitwa kuja kukutafuta lakini nilipokukosa, nikamdanganya kuwa huenda umeenda kufanya mazoezi na timu yako mpya ya Miami Heat. Vipi mbona umeshtuka?”
“Hapana sijashtuka… nipo kawaida tu,” alisema Harvey huku akianza kuondoka na kuelekea hosteli. Japokuwa hakutaka kusema ukweli, Cazzard alishahisi kuwa huenda alipoondoka na Skyler asubuhi ile, walienda kufanya mambo yasiyostahili na ndiyo maana alishtuka kusikia baba yake alifika kumtafuta chuoni pale.
“Nimefanya nini sasa?” alijilaumu kimoyomoyo Harvey huku akiwa amejilaza chali kitandani kwake. Kumbukumbu za matukio yote yaliyotokea siku ile, kuanzia asubuhi mpaka muda ule yakawa yanajirudia akilini mwake mithili ya mkanda wa video.
Aliendelea kujilaumu kwa kumruhusu shetani amzidi nguvu na kuangukia kwenye dhambi ya kushiriki mchezo wa kikubwa na Skyler. Alijiuliza maswali mengi kichwani mwake ambayo yote hakuyapatia majibu.
Alitambua fika kuwa endapo Dk Lewis na mkewe wakishtukia kilichokuwa kinaendelea, basi maisha yake yatakuwa mashakani sana. Aliendelea kuwaza kwa muda mrefu bila kupata majibu, usingizi ukaanza kumchukua taratibu. Alikuja kushtuka baada ya kusikia simu yake ya mkononi inaita, akaichukua harakaharaka na kuangalia namba ya mpigaji.
“Mungu wangu, lazima watakuwa wameshagundua kilichoendelea,” alijisemea Harvey huku akianza kujishauri kama apokee simu ile au la. Kwenye kioo cha simu, lilisomeka jina la Dk Lewis kumaanisha kuwa ndiyo aliyekuwa anampigia simu . Aliangalia saa yake na kugundua kuwa ilikuwa tayari ni saa nne za usiku. Haikuwahi kutokea hata siku moja Dk Lewis akampigia simu usiku.
Mtoto wa Dk Lewis, mtu aliyejitolea kumpa hifadhi Harvey aitwaye Skyler, anaanza kuonesha dalili za kumtaka kimapenzi kaka yake huyo wa hiyari. Licha ya Harvey kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wake wote kuvishinda vishawishi, hatimaye anajikuta akiangukia dhambini. Mtego mkali aliouandaa Skyler, unafanikiwa kumnasa Harvey na kwa mara ya kwanza wanafanya mapenzi ndani ya chumba cha binti huyo, nyumbani kwa Dk Lewis wakati wazazi wao wakiwa kazini.
BAADA ya kubabaika kwa muda, aliamua kujikaza na kupokea simu ile. Tofauti na alivyotegemea, alikutana na sauti ya kike… alikuwa ni Skyler.
“Mambo mpenzi, nimekumiss yaani mpaka nimeshindwa kulala,” alisema Skyler kwa sauti ya kimahaba, Harvey akashusha pumzi ndefu na kuanza kumjia juu kwa kumshtua usiku ule.
“Kwa nini utumie namba ya simu ya baba? Unajua mwenzio nilishaanza kutetemeka hapa.” “Mh! Wewe nawe, wasiwasi wako tu, kwani ulihisi nini?” “Nilihisi wamekubana huko nyumbani na umeeleza ukweli wa kilichotokea mchana, yaani bado mapigo ya moyo yananienda kasi
mithili ya injini ya jet,” alisema Harvey, Skyler akacheka sana na kumpa pole kwa kilichotokea. “Baba yupo sebuleni anaangalia TV, nimechukua simu yake bila mwenyewe kujua na hapa nimejifungia chumbani kwangu,” alisema Skyler huku akiendelea kucheka, wakaendelea kuzungumza mambo mbalimbali huku mara kwa mara Skyler akieleza jinsi alivyofurahi kwa walichokifanya asubuhi. “Vipi mlinzi mmefikia naye wapi?”
“Nimeshamwambia baba kuwa mlinzi hafanyi kazi yake na badala yake analala kazini, kama hiyo haitoshi nimemwambia kuwa ananitaka kimapenzi. “Baba amechukia sana, anasema anamtafuta mlinzi mwingine kimyakimya na akimpata tu, hata kesho anamfukuza huyu. Mi nilikwambia baba’angu anavyonipenda lazima anisikilize,” alisema Skyler, kauli iliyomshangaza sana Harvey.
“Sasa kama Dk Lewis anampenda mwanaye kiasi hiki, siku akisikia kuwa natoka naye kimapenzi si ataniua?” aliwaza Harvey lakini akaamua kuuweka woga pembeni kwani kama ni maji, tayari yalishamwagika. Walizungumza kwa muda mrefu usiku ule, mpaka Harvey akamkatisha Skyler na kumweleza kuwa alikuwa anataka kulala. ***
Uwezo aliouonesha Harvey kwa siku kadhaa alizokaa na wachezaji wenzake wa Miami Heat, uliendelea kuwa gumzo miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu wa timu ile pamoja na wachezaji wenyewe. Kila mmoja alikuwa akimsifia na kuuomba uongozi ufanye kila linalowezekana kuhakikisha Harvey anajumuika na timu ile angalau mara tatu kwa kila wiki. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Anatuongezea morali ya ushindi na kutufundisha namna ya kupambana bila kukata tamaa, tunamhitaji awe anakuja hapa mazoezini mara kwa mara, si unajua ligi inakaribia kuanza,” alisema Lebron James wakati akizungumza na kocha wa timu yake ya Miami Heat, Erik Spoelstra.
“Mkataba wake unaeleza kuwa kwa kipindi hiki anachoendelea na masomo, atakuwa akijumuika nasi pale atakapopata muda tu, hatuwezi kumlazimisha kuwa anakuja mara kwa mara mazoezini, tutakuwa tunakiuka masharti,” alijibu kocha Erik na kuahidi kuwa atajaribu kuzungumza na wenzake ili kama inawezekana, Harvey ahamie pale makao makuu na awe akienda chuoni na kurudi kutokea makao makuu ya Miami Heat.
Wazo lile liliungwa mkono na kila mmoja, wakaomba uongozi wao ufanye haraka kulishughulikia suala lile hasa ukizingatia kuwa Ligi Kuu ya Mpira wa Kikapu nchini Marekani ilikuwa mbioni kuanza.
Walitumwa tena viongozi wa juu wa timu ile kwenda kuzungumza na uongozi wa chuo cha Miami Polytechinic and Engineering College ili wamruhusu Harvey ahame kutoka kwenye hosteli za chuo na kuhamia kwenye makao makuu ya timu ya Miami Heat ili apate muda mwingi wa kukaa pamoja na wachezaji wenzake na kujenga timu imara.
Baada ya mazungumzo yaliyochukua zaidi ya saa mbili baina ya uongozi wa Miami Heat na uongozi wa chuo, hatimaye waliamua kumuita Harvey ili yeye ndiyo aseme kama atakuwa tayari kufanya kama viongozi wa Miami Heat walivyopendekeza.
Harvey alikubali kwa moyo mkunjufu, hasa baada ya kuhakikishiwa kuwa atapewa gari ambalo atakuwa analitumia kusafiria kwenda chuoni kila asubuhi na kurudi nalo baada ya kumaliza vipindi. Utaratibu maalum ukaandaliwa ili kuhakikisha anaweza
kumudu mambo yote kwa wakati mmoja. Viongozi wa Miami Heat wakaondoka wakiwa na furaha tele kwenye mioyo yao.
Harvey naye alifurahia sana kile walichokubaliana, hasa alipofikiria jinsi atakavyokuwa anakata mitaa akiwa anaendesha mwenyewe gari la kifahari. Aliendelea kumshukuru Mungu wake kwa miujiza aliyokuwa anaitenda kwenye maisha yake.
Akamfuata Dk. Lewis kazini kwake na kumpa taarifa juu ya walichokuwa wamekubaliana.
“Mi sina kipingamizi chochote mwanangu, nakutakia kila la heri, nakuomba sana uzingatie kilichokupeleka kule. Jitume zaidi kwenye mazoezi pamoja na wachezaji wenzako na umheshimu kila mtu.
“Nidhamu uliyoionesha kwa siku zote ulipokuwa chuoni kaiendeleze na huko uendako, nakutakia kila la heri ila usisahau masomo. Kazana chuoni ili upate cheti ambacho kitakusaidia siku za mbele kwenye maisha yako,” alisema Dk Lewis huku akionesha kufurahishwa sana na mafanikio aliyoyapata Harvey.
Moyoni alifurahi sana kwani lengo la kumfanya Harvey asahau yote aliyopitia maishani na kuwa na maisha yake mwenyewe, lilikuwa likielekea kutimia. Akampa baraka zote na kumtakia kila la heri. Wakaagana ambapo Harvey alirudi chuoni.
Kama walivyokuwa wamekubaliana, siku tatu baadaye wale viongozi wa Miami Heat walirejea tena pale chuoni, safari hii wakiwa wamekuja kumhamisha Harvey. Baada ya kusainishana nyaraka kadhaa na uongozi wa chuo, Harvey alikusanya kila kilichokuwa chake, wenzake wakamsaidia kumpakiza kwenye gari walilokuja nao wale viongozi na safari ya kuelekea Miami Downtown, yalipokuwa makao makuu ya timu ya Miami Heat ikaanza.
Harvey akapewa vyumba vitatu kwenye ghorofa ya saba ya jengo la American Airways Arena lililokuwa linatumiwa na timu hiyo kama makao makuu yao. Alipewa chumba cha kulala, sebule na jiko, huku kukiwa na samani za gharama ndani.
“Hapa ndiyo utakuwa unaishi, kila kitu kilichomo humu ndani ni mali yako na jisikie huru. Ukipata tatizo lolote wasiliana na uongozi, tutakuwepo karibu yako kukupa msaada wowote utakaouhitaji,” alisema meneja wa Miami Heat wakati akimkabidhi funguo
Harvey. Wote wakatoka na kumuacha mwenyewe akiendelea kushangaa mandhari ya mle ndani. “Sijawahi kuota hata siku moja kuwa naweza kuja kuishi kwenye ghorofa, tena kukiwa na kila kitu ndani, kweli Mungu hashindwi kitu, inabidi nianze kwenda kanisani kila Jumapili,” alisema Harvey huku akiangalia mandhari ya nje ya jengo lile kupitia madirisha makubwa ya vioo.
Baada ya kushangaashangaa kwa muda mrefu, alienda sebuleni na kukaa kwenye masofa ya kisasa, akawasha runinga ya muundo mpya (flat screen) iliyokuwa imetundikwa ukutani na kuanza kuchagua chaneli ya kuangalia. Akiwa bado anaendelea kumshukuru Mungu wake, simu yake ya mkononi iliita, alipoitazama namba ya mpigaji alikuwa ni rafiki yake wanayesoma pamoja chuoni, Cazzard.
“Ebwana mdogo wako Skyler amekuja huku chuoni anakutafuta, tumemwambia kuwa umehamia huko anasema anataka kukufuata, nimwambieje?” aliuliza Cazzard, Harvey akamwambia ampe simu ili aongee naye mwenyewe, alipopewa simu akaanza kumuelekeza mahali alipohamia, kwenye makao makuu ya Miami Heat ambapo alimwambia apande taxi na yeye atamlipa dereva wakifika.
“Ukifika utanikuta nakusubiri kwenye lango la kuingilia, nakusubiri mpenzi wangu,” alisema Harvey, akionesha dhahiri kunogewa na asali aliyoilamba kwa kutumia ncha ya kisu. Kila alipokumbuka raha alizozipata siku waliposhiriki mchezo haramu kwa mara ya kwanza, alijikuta akiingiwa na hamu ya kurudia tena.
MUONJA asali haonji mara moja. Harvey na Skyler baada ya kuonja asali, sasa wanataka kuchonga mzinga. Baada ya kushiriki kwenye mchezo wa kikubwa na Skyler, Harvey, kijana kutoka nchini
Liberia aliyekimbia machafuko ya wenyewe kwa wenyewe nchini kwao na kubahatika kupata mafanikio makubwa nchini Marekani kutokana na kipaji kikubwa cha kucheza mpira wa kikapu, ananogewa na sasa hasikii la mwadhini wala la mnadi swala.
Wakati hayo yakitokea, upande wa pili mambo yanazidi kumnyookea Harvey ambapo timu yake mpya ya Miami Heat inaenda kuzungumza na uongozi wa chuo alichokuwa anasoma na
wanakubaliana kuwa ahamishiwe makao makuu ya timu hiyo ili aendelee kujumuika na wachezaji wenzake mazoezini kujiandaa na ligi ya NBA iliyokuwa mbioni kuanza.
Anakabidhiwa funguo ya sehemu ya kuishi yenye kila kitu ndani, kuanzia samani za bei ghali na vifaa vingine muhimu vya ndani. Anaahidiwa pia kupewa gari ambalo atakuwa analitumia kuendea
chuoni kila siku. Anayaanza maisha mapya huku akimshukuru Mungu wake kwa miujiza aliyokuwa anamfanyia maishani. DAKIKA ishirini baadaye, gari dogo lililokuwa na maandishi makubwa ubavuni yaliyosomeka ‘taxi’ liliwasili kwenye lango kuu la kuingilia kwenye Makao Makuu ya Timu ya Miami Heat. Harvey aliyekuwa amejibanza kwenye kona ya geti, alipoiona ile taxi,
harakaharaka alitoka nje na kupunga mkono, Skyler aliyekuwa ndani ya lile gari, akamuelekeza dereva sehemu ya kusimama. “Simama hapo pembeni, mtu mwenyewe ninayemfuata yule pale anayepunga mkono,” alisema Skyler, dereva akapunguza mwendo na kufunga breki pembeni ya geti lile, Harvey akatoka mbiombio mpaka pale gari liliposimama.
“Habari zenu?” alisema huku akifungua pochi yake na kutoa noti ya dola kumi, akampatia yule dereva na bila hata kusubiri chenji, alifungua mlango wa pili na kumtoa Skyler aliyekuwa amevalia kigauni kifupi kilichoyaacha mapaja yake wazi. Mwilini alikuwa amejipulizia manukato mazuri na kujipodoa kisawasawa, alionekana kama malaika. Harvey akamkumbatia kimahaba palepale, wakaanza kupigana mabusu motomoto.
“Nilikumisi sana mpenzi wangu, sikutegemea kama naweza kukukuta unanisubiri getini, kumbe unanipenda eeeh?”
“Nakupenda sana Skyler, sijawahi kupenda kama ninavyokupenda wewe,” alisema Harvey huku akimuongoza Skyler kuelekea mahali zilipokuwa lifti za ghorofa lile.
“Harvey, yaani ndiyo wamekuhamishia huku? Jumba zuri na mazingira yake ni mazuri utafikiri tupo ikulu!” alisema Skyler na kujilaza kwenye bega la Harvey, akiwa anaendelea kuangalia mandhari ya eneo lile.
Baada ya muda mfupi, tayari walikuwa ndani ya lifti, Harvey akabonyeza kitufe kilichokuwa na namba ukutani kisha lifti ikaanza kupanda juu taratibu. Ilipowafikisha ghorofa ya saba, milango ilifunguka, wakateremka na kuelekea moja kwa moja kwenye chumba alichokabidhiwa Harvey na uongozi wa Timu ya Miami Heat.
“Karibu, hapa ndipo makazi yangu yalipo kuanzia leo na kuendelea,” alisema Harvey wakati akifungua mlango, Skyler akaingia na kupitiliza moja kwa moja mpaka kwenye masofa ya kisasa yaliyokuwa pale sebuleni, akajitupa na kulifanya gauni lake fupi lizidi kupanda juu. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Yaani nyumba yote unaishi peke yako? Halafu nzuri, sijapata kuona samani nzuri kama hizi zilizopo humu ndani,” alisema Skyler huku akizungusha macho huku na kule kutazama vyote vilivyokuwepo mle ndani. “Na kule ni wapi?” aliuliza Skyler akionesha kwa kidole mahali kulipokuwa na mlango mwingine. “Kule ndiyo kwenye chumba cha kulala, unataka ukakione?”
“Ndiyo,” alijibu Skyler huku akiyazungusha macho yake makubwa kimahaba. Harvey akamshika mkono na kumuongoza, akasukuma mlango na kuingia chumbani.
“Waoooo! What a beautiful apartment! (Nyumba nzuri sana hii) alisema Skyler huku akionesha furaha ya waziwazi. Kitanda kikubwa kilichotengenezwa kisasa, kabati la nguo la vioo na samani nyingine za bei mbaya, vilizidi kukipendezesha chumba kile.
“Mwenzio mi nimechoka nataka nilale kidogo,” alisema Skyler huku akionesha dhahiri kuanza kupandwa na shetani wake wa mahaba. Bila hata kueleza alichokuwa anakitaka, tayari Harvey alimuelewa, akamvutia kifuani kwake na kumkumbatia, wakagusanisha ndimi zao na kuanza kuelea kwenye ulimwengu tofauti. “Harvey, utanioa kweli?”
“Nitakuoa Skyler, ninavyokupenda sipo tayari kukupoteza, nitafanya kila linalowezekana, hata ikibidi kuihama hii nchi ilimradi niishi na wewe,” alisema Harvey huku akianza kulivua gauni la Skyler, naye akawa anafungua vifungo vya shati lake. Muda mfupi baadaye, wote walikuwa kama walivyotoka kwenye matumbo ya mama zao.
Wakaendelea kuipasha miili yao tayari kwa safari ndefu huku Skyler akionesha kuwa na haraka kuliko kawaida. Muda mfupi baadaye, tayari walishaingia dimbani, wakawa wanalisakata kabumbu huku kila mmoja akijitahidi kumuonesha mwenzake uwezo wa kuumiliki mpira.
Kwa raha alizokuwa anazipata Skyler, alijikuta akipiga kelele na kutoa miguno iliyoambaa na kusikika mpaka kwenye korido ya ghorofa lile. Akawa analitaja jina la Harvey kwa sauti ya juu huku akisisitiza kuwa siku akigundua ana uhusiano na mwanamke mwingine, atajiua.
Mechi yao ya kirafiki iliendelea kwa kasi, huku timu zote mbili zikishambuliana kwa zamu, ikafika kipindi, wote wakawa hawajielewi wapo sehemu gani, wakawa wanahisi kama wanaelea kwenye sayari ya peke yao. *** Kocha Mkuu wa Timu ya Miami Heat, Erik Spoelstra na nahodha wa timu hiyo, Lebron James sambamba na meneja, walikuwa wakipita kwenye chumba cha mchezaji mmojammoja ili kuhakiki kama wote walikuwepo kambini. Zoezi hilo lilifanyika baada ya siku kadhaa zilizopita baadhi ya wachezaji kuanza tabia ya kutoroka kambini na kwenda sehemu za starehe, jambo ambalo lilikuwa kinyume na sheria za timu hiyo. “ Unajua katika kipindi hiki kigumu tunapoelekea kuianza ligi, lazima tuhakikishe vijana wetu wanaachana kabisa na mambo ya anasa. Lazima muda wote wawepo kambini na kupumzika vya kutosha kabla ya kwenda mazoezini,” alisema kocha Spoelstra wakati wakiendelea kukagua vyumba vya wachezaji.
“Ni kweli, hawa vijana bila kuwasimamia kwa karibu, unaweza kujikuta timu inashindwa kunyakua ubingwa kwa sababu wanapenda sana starehe. Pombe na wanawake ndiyo ugonjwa wa wengi.”
“Lakini siyo wote, mbona sisi wengine tunafahamu kilichotuleta na tunazingatia kila tunachoambiwa?” alijitetea Lebron, wakaendelea na ukaguzi na sasa wakafika kwenye ghorofa namba saba.
“Hizo kelele zinazosikika ni za nini? Halafu mbona kama nasikia sauti ya mwanamke? Kuna watu wanaingia na wanawake huku?” aliuliza kocha Spoelstra huku akitega masikio kwa makini kutaka kujua sauti zile walizokuwa wakizisikia zilikuwa zinatoka wapi.
“Mh! Mbona inaonesha zinatoka kwenye chumba cha huyu mchezaji mgeni aliyewasili leo?” “Nani? Harvey? Hawezi kuwa yeye… hebu tusogeeni karibu na mlango,” alitoa wazo meneja wa timu ile, wote watatu wakausogelea mlango wa chumba cha Harvey na kutega masikio yao kwa umakini. Katika hali ambayo hakuna aliyeitegemea, waligundua kuwa ni kweli sauti zile zilikuwa zinatoka ndani ya chumba cha Harvey.
Wote walipigwa na butwaa kwani bila hata kuuliza, walitambua kilichokuwa kinaendelea ndani. Ile sauti ya mwanamke ikawa inazidi kupaa huku ikitamka maneno ya mapenzi na kutoa miguno ya kimahaba, wakashauriana nini cha kufanya palepale mlangoni, wakakubaliana kugonga mlango. Walipougusa mlango, waligundua kuwa haukuwa umefungwa, wakausukuma na kuingia sebuleni. Sauti zile zikawa zinasikika kutoka kwenye chumba cha kulala.
Wakasogea mpaka kwenye mlango wa chumbani na kujaribu kugonga lakini waligundua kuwa nao haukuwa umefungwa, wakausukuma na kuingia, Lebron akiwa mbele. Maisha yanazidi kumnyookea Harvey ambapo timu yake mpya ya Miami Heat inaenda kuzungumza na uongozi wa chuo alichokuwa anasoma na wanakubaliana kuwa ahamishiwe makao makuu ya timu hiyo ili aendelee kujumuika na wachezaji wenzake mazoezini kujiandaa na ligi ya NBA iliyokuwa mbioni kuanza.
Wakati hayo yakiendelea, upande wa pili tatizo kubwa linaanza kufuka moshi. Mtoto wa Dk Lewis, Skyler anaonesha hisia nzito za mapenzi kwa Harvey na kuanza kumuwekea mitego mingi ya kimapenzi. Licha ya kujitahidi kumkwepa, Harvey anajikuta akiangukia dhambini na Skyler na wanavunja amri ya sita.
BAADA ya kusukuma mlango na kuingia, Lebron akiwa mbele, wote walipigwa na butwaa kwa walichokiona. “Ooh! My God, I can’t believe this! Harveeeey! What are you doing? (Ooh Mungu wangu, siwezi kuamini! Harveeeey! Unafanya nini) alipiga kelele Lebron huku akiwa haamini kile alichokuwa anakiona mbele yake. Hali ilikuwa hivyohivyo kwa kocha na meneja
wa timu, wakabaki wamepigwa na butwaa. Harvey alikuwa akimshughulikia Skyler kisawasawa.
Harvey na Skyler walikurupuka na kuanza kutafuta nguo zao, wakajiziba nyuso zao kwa kutumia mashuka huku wakitetemeka kupita kiasi. Bila kusema neno lolote, Lebron, kocha na meneja waligeuza na kutoka ndani ya chumba kile mpaka nje. Wakawa wanajadiliana nini cha kufanya.
“Mi nashauri tumuite huyu kijana ofisini sasa hivi! Hatuwezi kukubaliana na utovu wa nidhamu wa kiasi hiki,” alisema meneja wa timu hiyo.
“Nafikiri hakuna haja ya kukaa kikao, moja kwa moja huyu hatufai tena. Mchezaji yeyote hata kama ana kipaji kikubwa namna gani, kama hana nidhamu hawezi kuwa msaada kwetu,” alisema kocha, wakashuka mpaka kwenye ofisi za chini na kuitisha kikao cha dharura.
“Akaitwe sasa hivi, Lebron panda juu kamwite Harvey haraka,” alifoka mmiliki wa timu ile, utekelezaji ukafuatia mara moja.
Harvey na Skyler walianza kulaumiana kwa kilichotokea, kila mmoja akimlaumu mwenzake kuwa ndiyo sababu. Wakiwa bado hawajui nini cha kufanya, Harvey alisikia akiitwa na kepteni wa timu yao, Lebron.
“Unaitwa utawala sasa hivi, wamesema tuongozane wote,” alisema Lebron huku akionesha kukasirishwa sana na kitendo alichokifanya Harvey, tena ikiwa ni siku ya kwanza kukaa kambini pale.
Harvey alijiandaa harakaharaka, akavaa nguo zake na kumwambia Skyler naye avae na kuondoka lakini katika hali ya kushangaza, Skyler alikataa kuvaa nguo wala kuondoka, akamwambia atamsubiri chumbani mpaka arudi, hali iliyozidi kumchanganya Harvey. “Twende bwana tunachelewa,” alisema Lebron huku akimvuta mkono Harvey, wakatoka na kumuacha Skyler mle ndani.
Harakaharaka waliingia kwenye lifti na kushuka mpaka chini ya ghorofa lile kulipokuwa na ofisi za utawala. Kwa muda wote huo, Harvey alikuwa hajitambui kwa hofu. Alikuwa akitetemeka na kutokwa na kijasho chembamba
kilichomfanya alowe mwili mzima. Waliingia mpaka kwenye chumba cha mikutano ya siri ambapo tayari maafisa kadhaa wa ngazi za juu wa Miami Heat walikuwa wamekaa.
Harvey alipowatazama, alijikuta miguu ikiishiwa nguvu na kizunguzungu kikaanza kumzonga lakini akajikaza. Akaelekezwa sehemu ya kusimama ambapo aliambiwa ajieleze juu ya kilichotokea. “Naomba mnisamehe, ni shetani alinipitia,” alisema Harvey huku akianza kulengwalengwa na machozi lakini hiyo haikusaidia chochote. Aliambiwa ajieleze kwa sababu kuna maafisa wengine walikuwa hawajui chochote hivyo wasingeweza kumsamehe wakati hawajui kosa lake. Harvey akazidi kuwa katika wakati mgumu.
Hakuwa na namna zaidi ya kueleza ukweli kua alifumwa akifanya mapenzi na Skyler kwenye chumba chake. Alijitetea na kueleza kuwa wakati hayo yanatokea, alikuwa hajielewi kutokana na furaha aliyokuwa nayo kuhamia kwenye jengo la makao makuu ya timu hiyo. Akaongeza kuwa hakuwa akijua kuwa sheria za timu hiyo haziruhusu kufanya vitendo kama vile.
Baada ya kumaliza kujieleza, aliambiwa atoke nje na kusubiri majibu ya watakachoamua maafisa wale. Akatoka na kwenda kusimama nje ya ukumbi ule wa mikutano, huku akionesha kabisa. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Mi nafikiri kwa sababu wote tumemsikia alivyojitetea, tuanze kuchangia hoja juu ya adhabu inayomfaa kwa sababu kufanya kosa ukiwa unajua au hujui hakuzuii sheria kufuata mkondo wake.”
“Unachokisema ni kweli, wachezaji ambao waliwahi kufanya makosa kama hili alilolifanya Harvey leo, tuliwafukuza kwenye timu yetu licha ya uwezo mkubwa waliokuwa nao uwanjani. Sheria hiyohiyo itumike.” “Akiendelea kuishi hapa kwa miezi michache na wenzake atawaambukiza tabia mbaya ya kupenda ngono na timu haitaweza kutetea ubingwa.”
“Samahani viongozi wangu, mimi nina mawazo tofauti kidogo, naomba nisimame ili nisikike vizuri,” alisema Lebron James, nahodha wa timu ya Miami Heat, akasimama na kuanza kuongea kwa busara.
“Ni kweli Harvey amefanya makosa makubwa. Kwa niaba yake na wachezaji wote naomba radhi kwa kitendo alichokifanya kwani kimevuruga uaminifu na uhusiano mzuri uliokuwepo baina ya viongozi na wachezaji. Nawaomba mumchukulie kama mtoto wenu anayehitaji kufundishwa, kuonywa na kurekebishwa anapokosea.
“Kwa kuwa leo ndiyo mara yake ya kwanza, nawaomba sana mumsamehe na kusahau yote yaliyopita. Naamini atakuwa amejifunza kitu kupitia hiki kilichotokea na kama akirudia tena basi sheria ichukue mkondo wake,” alisema Lebron kwa kubembeleza, viongozi wakaanza kutazamana usoni huku wakionesha kuunga mkono kile alichokisema.
Mjadala uliendelea kwa muda mrefu, mwisho wakakubaliana kumsamehe na kumpa nafasi nyingine ya kurekebisha makosa yake. Baada ya muafaka kufikiwa, Harvey aliitwa na kuingia tena mle ukumbini. Meneja mkuu wa timu akaanza kuzungumza namna walivyokasirishwa na kitendo alichokifanya na uamuzi waliofikia.
Akamwambia wazi kuwa amshukuru sana kepteni wao, Lebron kwani ndiye aliyemkingia kifua vinginevyo huo ndiyo ungekuwa mwisho wake. Akapewa onyo kali na kuambiwa kuwa waliamua kumsamehe na kumpa nafasi ya mwisho.
Harvey alishindwa kujizuia, akawa anabubujikwa na machozi kama mtu aliyepokea taarifa za msiba. Akapiga magoti chini na kuinua mikono juu kama ishara ya kushukuru, akaendelea kumwaga machozi pale chini wakati maafisa wale wakikusanya vitu vyao na kuondoka mle ukumbini.
“Usirudie tena Harvey, ukiwa hapa nidhamu ndiyo kitu cha kwanza,” alisema Lebron huku akimuinua pale alipokuwa amepiga magoti, akamsindikiza mpaka kwenye chumba chake na kumsaidia kumtoa Skyler ambaye bado alikuwa anang’ang’ania kulala palepale na Harvey.
“Binti, umemsababishia matatizo makubwa mwenzako, kama kweli unampenda ondoka na usirudie kuja hapa kwani ameshapewa onyo kali, anaweza hata kufukuzwa kambini,” alisema Lebron, Skyler akaanza kujiandaa kuondoka kwa shingo upande.
Kwa muda wote huo, Harvey alikuwa amejiinamia huku akijifuta machozi yaliyokuwa yanaendelea kuulowanisha uso wake. Skyler akaondoka kwa kususa na kumuacha Harvey na Lebron wakiwa bado mlemle ndani. Lebron alipohakikisha Skyler ameondoka, alizungumza na Harvey mambo kadhaa na kumwelekeza namna ya kuishi bila kukwaruzana na uongozi wa timu hiyo.
Alipomaliza aliaga na kuondoka, Harvey akamshukuru sana kwa msaada wake na kuahidi kujirekebisha. Akajifungia milango na kuendelea kutafakari kwa kina juu ya kilichotokea.
“Leo ndiyo mwisho wa kuendelea na uhusiano na Skyler, anaweza kuniharibia maisha yangu,” alijisemea Harvey kimoyomoyo.
TUKIO la aibu linamkumba Harvey, kijana mwenye asili ya nchini Liberia anayeishi Marekani, katika siku ya kwanza tangu ahamie kwenye kambi ya
wachezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya Miami Heat. Anabambwa na viongozi wa timu hiyo akivunja amri ya sita ndani ya nyumba ambayo alikabidhiwa muda mfupi uliopita.
Anaitwa mbele ya kikao cha dharura na kuambiwa ajieleze kisha viongozi wa timu hiyo wanaanza kujadili juu ya adhabu ya kumpa. Kosa alilolifanya linawavunja nguvu wengi kwani hawakutegemea kama mchezaji
waliyemsajili kwa gharama kubwa anaweza kuonesha utovu wa nidhamu ndani ya muda mfupi namna ile.
Kwa bahati nzuri, wanaamua kumsamehe na kumpa nafasi ya kujirekebisha. Harvey anamshukuru sana Mungu wake na anajiapiza kuwa huo ndiyo mwisho wa uhusiano wake na Skyler. Anaweka nadhiri kuwa kamwe
hatarudia kitendo kama kile. Kepteni wa timu hiyo, Cazzard anakuwa msaada mkubwa kwake kwani anamjenga upya kisaikolojia.
BAADA ya tukio lile, Harvey alikuwa ni kama ametoneshwa mtima wake, huzuni iliyokuwa imetawala maisha yake kipindi cha nyuma alipotoroka mauaji nchini kwao Liberia, zilikuwa ni kama zimerudi upya. Muda wote akawa anajilaumu kwa kushindwa kukishinda kishawishi cha Skyler na kujikuta akivunja naye amri ya sita. Kilichomuuma zaidi ni kuona jinsi uhusiano haramu kati yake na Skyler ulivyomchafulia heshima katika timu yake mpya ya
Miami Heat, tena ikiwa ni siku chache tu tangu asaini mkataba mnono wa kuichezea timu hiyo. Maneno yaliyozungumzwa katika kikao cha kujadili tukio lile, yalikuwa yakijirudiarudia kichwani mwake kama mkanda wa video na kumfanya muda wote awe amejiinamia kwa huzuni. Hakuna jambo ambalo tangu awali alikuwa analiogopa kama kuonekana ana tabia mbaya mbele ya jamii.
Alishinda ndani siku nzima mpaka giza lilipoanza kuingia, hata muda wa chakula cha jioni ulipowadia, hakutaka kwenda kujumuika na wenzake, akajifungia chumbani kwake huku mawazo tele yakiendelea kukisumbua kichwa chake.
Hata muda wa kulala ulipofika, Harvey hakupata usingizi mapema, alijilaza kitandani kwa muda mrefu lakini usingizi ulimpaa kabisa, mawazo machungu yakaendelea kukizonga kichwa chake na kumfanya aumie sana ndani ya moyo wake.
Hata hivyo, kwa upande mwingine alishukuru tukio ile kutokea kule kambini kwani kama lingetokea nyumbani, Dk Lewis asingekubaliana na kilichotokea na huenda madhara makubwa zaidi yangetokea.
Aliendelea kutazama hatari zilizokuwa zinamkabili endapo mzee huyo ambaye kwa kiasi kikubwa ndiye aliyemsaidia kuamsha ari mpya ya kuishi kwa mafanikio na kumjengea maisha bora, angegundua kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na binti yake kipenzi.
“I won’t repeat this I swear,” (sitarudia tena naapa) alijisemea Harvey huku akionesha ishara ya kujiapiza. Akaendelea kulisanifu dari la chumba chake cha kulala mpaka usiku sana. Hata hakuelewa usingizi ulimpitia muda gani, akaja kushtuka ikiwa tayari ni alfajiri. Akaamka kinyonge na kuchukua nguo zake za mazoezi, akaelekea kwenye uwanja wa mazoezi, akiwa ni mtu wa kwanza kabisa kufika. “Dah! Umewahi sana leo, hukulala nini?” kepteni wa timu ya Miami Heat, Cazzard alikuwa akizungumza na Harvey. Kwa
jinsi alivyomtazama tu, alitambua kuwa bado hakuwa katika hali yake ya kawaida, akautumia muda ule kuendelea kumpa ushauri. “Ukiwa na stress hutaweza kucheza vizuri uwanjani, chukulia yote yaliyotokea kama upepo mbaya ambao umeshapita, kuwa imara Harvey, wewe ni mwanaume,” alisema Cazzard huku akimvuta Harvey na kuingia naye uwanjani, wakaanza kufanya mazoezi mepesimepesi.
Wachezaji wengine waliendelea kuongezeka mmoja baada ya mwingine mpaka wote wakatimia. Mazoezi yakaendelea lakini Harvey hakuwa kama yule ambaye wachezaji wenzake walimzoea. Alipooza sana na hata kasi yake ilipungua. Baada ya muda wa mazoezi ya asubuhi kuisha, wachezaji waliendelea na ratiba nyingine. Taratibu Harvey akaanza kuyasahau yote yaliyotokea na kuelekeza nguvu zake nyingi kwenye mazoezi.
Siku zikawa zinasogea mbele kwa kasi huku Harvey akimudu vizuri kuchanganya michezo na masomo. Akawa anahudhuria vizuri mazoezi ili kurekebisha makosa na wakati huohuo akawa anahudhuria pia masomo chuoni kwao, Miami Polytechnic and Engineering College kwa kutumia gari alilopewa na uongozi wa timu hiyo.
*** “Huyu Skyler Lewis siku hizi ana matatizo gani? Mbona mahudhurio yake yanazidi kudorora na hata uwezo wake wa masomo unashuka?”
“Mh! Mbona anaonekana mtulivu sana? Kama hizo tabia amezianza basi itakuwa ni katika siku za hivi karibuni. Namfahamu kwa kipindi kirefu lakini sikuwahi kumuona akivunja sheria za shule.”
“Usimtetee, njoo uangalie ‘attendance’ kwa macho yako mwenyewe,” walimu wawili wa Shule ya Sekondari ya Miami, alipokuwa anasoma Skyler walikuwa wakijadili jambo wakiwa peke yao ndani ya ofisi ya nidhamu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Mwalimu wa Nidhamu, Keith Amstrong ambaye ndiye aliyekuwa na jukumu la kufuatilia maendeleo ya kila mwanafunzi, alionesha
kushtushwa sana na mabadiliko aliyokuwa nayo mwanafunzi huyo kwa siku za hivi karibuni. Alimuonesha mwenzake daftari la mahudhurio ambapo ilionekana Skyler ameanza kulegalega katika uhudhuriaji wa vipindi shuleni hapo.
Mara kwa mara alikuwa akitoa udhuru kuwa anaumwa lakini alipotakiwa kupeleka ‘sick sheet’ kama ulivyokuwa utaratibu wa shule ile, alikuwa akipiga chenga. Walimu wake waliendelea kujadiliana kwa kina juu ya mabadiliko ya Skyler, wakafikia uamuzi
wa kumuita mzazi wake wa kike ili atoe maelezo kama anafahamu chochote kuhusu binti yake. Mke wa Dk Lewis, Suzan alipigiwa simu na mwalimu wa malezi wa shule ya sekondari aliyokuwa anasoma mwanaye, akaambiwa anatakiwa kufika shuleni hapo asubuhi ya siku inayofuatia. “Kuna nini?”
“Ni mambo ya kawaida kuhusu maendeleo ya mwanao, ukifika kesho utaelezwa kwa kina,” alisema mwalimu Armstrong, mama Skyler akakubaliana naye kuwa angefika shuleni kesho yake kama walivyopanga. “Walimu wako wamenipigia simu kuwa kesho natakiwa niende shuleni kwenu, kwani kuna nini?” “Mh, sijui, labda wanataka wakuulize kuhusu michango.”
“Mbona hatudaiwi chochote? Ngoja tutaenda kujua hiyo kesho hukohuko shuleni,” alisema mama Skyler wakati akizungumza na binti yake wakiwa wanaandaa chakula cha jioni. Taarifa ile kwa Skyler haikumfurahisha kabisa kwani alijua lazima mama yake atakuwa anaitiwa suala la mahudhurio yake.
Alitambua kuwa ni kweli kwa siku kadhaa zilizopita, hakuwa akienda shuleni ingawa asubuhi alikuwa akijiandaa vizuri kisha kutoka na wazazi wake lakini muda mfupi baadaye alikuwa akirudi na kujifungia chumbani kwake.
Hata ratiba yake ya kulala nayo ilibadilika, muda mwingi akawa anapenda kulala chumbani kwake huku Harvey akichukua sehemu kubwa katika kichwa chake. Siku iliyofuatia iliwadia, Suzan akaongozana na mwanaye mpaka shuleni, wakaelekea moja kwa moja kwenye ofisi ya mwalimu wa nidhamu kama alivyomuelekeza kupitia simu.
“He! Skyler, mambo? Za siku shosti? Ulikuwa unaumwa nini?” mwanafunzi mmoja wa kike alimkimbilia Skyler na kumkumbatia, akawa anamuuliza maswali yale mbele ya mama yake. Suzan alibaki kushangaa kwani ilionesha kuwa mwanaye hajahudhuria masomo kwa siku kadhaa na ndiyo maana hata wanafunzi wenzake walikuwa wakimshangaa.
Akaamua kunyamaza kimya na kupuuzia, Skyler akamjibu kwa mkato yule mwanafunzi mwenzake kisha akamuongoza mama yake mpaka kwenye ofisi ya mwalimu wa nidhamu.
Taarifa aliyoipata mama Skyler na ushahidi wa daftari la mahudhurio, vilimduwaza sana, akamgeukia mwanaye na kutaka aeleze siku zote alikuwa akienda wapi kwani wao walikuwa wanajua anakwenda shuleni na kila siku walikuwa wakiamka pamoja na kujiandaa kisha kuondoka. “Ina maana alikuwa hafiki shuleni?” alijiuliza huku akimkazia macho mwanaye aliyekuwa anajiumauma.
MAMBO yanaanza kumwendea mrama Harvey, kijana mwenye asili ya nchini Liberia anayeishi Marekani ambapo katika siku ya kwanza tangu ahamie kwenye kambi ya wachezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya
Miami Heat, anakumbwa na tukio la aibu. Anafumwa na viongozi wa timu hiyo akivunja amri ya sita na Skyler ndani ya nyumba ambayo alikabidhiwa muda mfupi uliopita.
Kikao cha kumjadili kinafanyika lakini kwa bahati nzuri, anasamehewa na kutakiwa abadilike kitabia. Upande wa pili, Skyler anaanza kuonesha tabia ya uvivu shuleni, hali inayowashtua walimu wake. Mama yake anaitwa shuleni kwa ajili ya kujadili jambo hilo na anagundua uozo wa mwanaye.
MAMA Skyler alimtazama binti yake kwa dakika kadhaa mfululizo huku akijiuliza maswali mengi ambayo hakuyapatia majibu. Tangu mwanaye aanze shule, hakuwahi hata mara moja kumuona akitega kwenda shule wala kusikia taarifa zozote mbaya kutoka kwa walimu wake. Hata siku ambazo alikuwa anaumwa, kwa jinsi alivyokuwa anapenda shule, alikuwa akijilazimisha kwenda hivyohivyo. Hakujua nini kimemsibu mwanaye. “Kwani siku zote hizo ulikuwa unakwenda wapi?” “Nilikuwa nakuja shuleni lakini nilikuwa nawahi kuondoka.” “Kama kweli ulikuwa unakuja si walimu wako wangekuwa wanakuona? Na kama ulikuwa unawahi kuondoka, mbona hukuwahi kunipa taarifa hata siku moja kama una tatizo linalokufanya ushindwe kukaa shuleni muda wote?” “Nisamehe mama, sitarudia tena,” alisema Skyler huku akijikamua machozi ya uongo, mwalimu wa nidhamu, Armstrong akaingilia kati na kumuamuru Skyler atoke nje ili apate muda wa kujadiliana na mzazi wake. “Umemsikia mwenyewe? Hapa alikuwa anakwepesha maneno tu lakini ukweli ni kwamba alikuwa haji kabisa shuleni, lazima kuna tatizo hapa, ngoja nimuite matron wao,” alisema mwalimu Armstrong huku akiinua mkonga wa simu ya mezani, akabonyeza namba fulani kisha akawa anaisikiliza simu masikioni. “Matron, nakuomba mara moja kwenye ofisi ya nidhamu,” alisema mwalimu Armstrong kisha akakata simu. Muda mfupi baadaye, mwanamke wa makamo, mnene wastani, mrefu na mwenye nywele nyeusi, alisimama mbele ya meza ya mwalimu wa nidhamu. “Kutana na Suzan Lewis, mama wa mwanafunzi Skyler, keti chini tujadiliane jambo, kuna tatizo linalomhusu Skyler,” alisema mwalimu Armstrong, yule mwanamke ambaye baadaye alitambulishwa kuwa anaitwa madam Nicole, mlezi wa wanafunzi wa kike wa shule ile, aliketi pembeni ya mama Skyler huku akionesha kuwa na shauku kubwa ya kutaka kujua alichoitiwa. Mwalimu Armstrong alianza kueleza juu ya tatizo lililokuwa linamhusu Skyler, kisha kwa pamoja wakawa wanajadili juu ya hatua za kuchukua ili kuufahamu ukweli wa nini kilichokuwa kinamsumbua Skyler. “Mi nafikiri jambo la kwanza ni kwenda kumpima ujauzito, wanafunzi wengi wa kike hushawishiwa na wanaume na kujiingiza kwenye suala la mapenzi ambapo matokeo yake hushindwa kuzingatia masomo na kuanza utoro,” alisema Madam Nicole, wazo lililoungwa mkono na wote. Utaratibu ukaandaliwa harakaharaka ambapo Skyler aliambiwa arudi darasani kisha mwalimu Armstrong na Madam Nicole wakaanza kupanga namna ya kwenda kuwapima wanafunzi wote wa kidato alichokuwa anasoma Skyler. “Mh! Mbona mnawahangaisha na wanafunzi wengine wasiohusika, kwa nini asichukuliwe peke yake na kupelekwa kupimwa harakaharaka,” alisema mama Skyler lakini mwalimu Armstrong akamfafanulia kuwa lazima mbinu za hali ya juu zitumike ili kukwepa kumuumiza kisaikolojia Skyler ikibainika kuwa kinachomsumbua siyo ujauzito kama wanavyodhani. Mama Skyler alikubaliana nao na taratibu za kwenda kuwapima wasichana wote wa darasa alilokuwa anasoma Skyler zikafanyika mara moja. Kwa jinsi mbinu za kisaikolojia zilivyotumika, hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyeshtukia kilichokuwa kinaendelea zaidi ya Skyler mwenyewe. Wote wakashtukia wanaingizwa kwenye zahanati ya shule na kuanza kuitwa majina mmoja baada ya mwingine na kupewa vichupa maalum ambavyo walitakiwa kila mmoja kwenda kuweka haja ndogo na kuvirudisha haraka kwa ajili ya kupimwa ujauzito. *** “Sikia Sandra, mwenzio nina wasiwasi sana, hivi nikikutwa na ujauzito si baba’angu ataniua?” “Skyler na wewe kwa woga? Hiyo mimba itakuwa imeingilia wapi wakati bado humjui mwanaume?” “Mh! Shosti we acha tu, mwenzio tayari nimeshayaanza mambo ya kikubwa na siku chache zilizopita nilishiriki mchezo wa kikubwa bila kuchukua tahadhari yoyote, naomba unisaidie jambo moja la muhimu, ukiweza nitakupa bonge la zawadi.” “Mbona sikuelewi Skyler? Anyway… niambie unachotaka nikusaidie kwa sasa kisha mengine tutaongea baadaye,” alisema mwanafunzi aliyekuwa anasoma darasa moja na Skyler, akiwa haelezi kilichokuwa kinamsibu mwenzake. “Nataka ikifika zamu yetu ya kuingia kwenda kutoa haja ndogo kwa ajili ya kupimwa, wewe ndiyo utoe na kuweka kwenye vichupa viwili, cha kwangu na chako,” alisema Skyler huku akimsisitiza kuwa atampa kiwango kikubwa cha fedha kama ujira kwa ajili ya kazi ile. Kwa kuwa Sandra alikuwa na shida ya fedha, alikubaliana na Skyler ambapo alizidi kumsisitiza kuwa asimwambie mtu yeyote kuhusu siri hiyo. Waliendelea kusubiri pale nje na ilipofika zamu yao, Skyler na Sandra waliingia na kupewa vichupa maalum. Kila mmoja akaelekea chooni huku kichwani wakiwa tayari wanaelewa walichokusudia kukifanya. Sandra alifanya kama alivyoambiwa, akaweka haja kwenye vichupa vyote viwili kisha akamrudishia Skyler na kumkabidhi kwa siri kiasi kwamba hakuna aliyeshtukia mchezo huo. Skyler aliporejesha kichupa kile, matron wake alimkazia macho kama aliyekuwa na uhakika kuwa hayupo salama, Skyler akatoka mbiombio na kurejea darasani. Baada ya wanafunzi wote kuacha sampuli za haja ndogo, manesi walianza kazi ambapo walikuwa wakirekodi majibu katika jina la kila mwanafunzi. Kilichowashangaza wengi ni kwamba baada ya zoezi lile kukamilika, hakuna mwanafunzi aliyekutwa na ujauzito kama walivyotegemea. “Sasa kama hana ujauzito tatizo litakuwa ni nini?” “Mh! Hata mimi sielewi, itabidi tuendelee kumchunguza kwa makini. Na wewe kama mzazi inabidi ukae chini na binti yako na kujaribu kumdadisi kwa kina, naamini anaweza kukwambia kinachomsumbua.” “Sawa, nashukuru kwa msaada wenu na nawaahidi kuanzia kesho nitakuwa namleta Skyler mpaka hapa shuleni na nitakuwa nakuja kumchukua kila baada ya muda wa masomo kuisha, naomba ushirikiano wenu zaidi kwani nampenda sana mwanangu na sitaki atokewe na jambo lolote baya,” alisema mama Skyler, akaagana na walimu kisha akaondoka huku kichwani akiwa na mawazo tele. *** “Nimetoka shuleni kwa akina Skyler, nilichokikuta yaani nimechanganyikiwa kabisa.” “Nini tena mke wangu? Kuna tatizo?” “Mwanao hajafika shuleni kwa siku kibao, walimu wamechachamaa ndiyo walikuwa wananihoji kama nafahamu chochote.”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Hajaenda shule kwa siku kibao? Mbona sikuelewi mke wangu? Kila siku Skyler si tunaondoka naye nyumbani akiwa amevaa nguo za shule, kwani huwa anakwenda wapi?” “Hata mimi sielewi mume wangu, nimejaribu kumuuliza mbele za walimu wake akaniambia huwa anarudi nyumbani kwani anaumwa.” “Lazima wewe na mwanao mtakuwa mnaelewa kinachoendelea. Inawezekanaje mwanao awe anafanya upuuzi kama huo bila ya wewe mama yake kugundua?” “Mume wangu ukinitupia lawama utakuwa unanionea, mimi mwenyewe nashinda kazini kama wewe… wala hutakiwa kuwa mkali. Subiri jioni tukirudi tutamuita Skyler na ataeleza kila kitu kinachoendelea,” alisema mama Skyler wakati akiongea na mumewe, Dk Lewis katika bustani za hospitali aliyokuwa anafanyia kazi. Taarifa zile zilionekana kumchanganya sana Dk Lewis kwani hakuna kitu alichokuwa anakithamini maishani mwake kama mwanaye wa kipekee, Skyler. “Lazima aseme ukweli, hata ikibidi kutumia nguvu nitafanya hivyo,” alisema Dk Lewis kwa jazba.
BAADA ya Harvey kusajiliwa na timu ya Miami Heat, mambo yake yanaanza kwenda vizuri. Akiwa hajafika mbali anajikuta ndani ya tatizo lingine ambapo mtoto wa Dk Lewis, Skyler anamshawishi na kujikuta wakivunja amri ya sita. Wote wanaonekana kunogewa na kamchezo hako kachafu na baadaye wanafumwa ndani ya vyumba vya wachezaji wa Miami Heat. Upande wa pili, Skyler anaanza kuonesha dalili ambazo zinawashtua walimu na wazazi wake. Wanafunzi wote wa darasa lake wanapimwa ujauzito lakini hakuna anayebainika kuwa nao. Walimu na wazazi wake wanaanza kumfuatilia kwa karibu baada ya kuhisi jambo.
JIONI ilipofika, mama Skyler alimpitia mwanaye na kurudi naye nyumbani. Tofauti na siku zote, hakuna aliyekuwa anamsemesha mwenzake garini, kila mmoja alikuwa kimya. Walipofika nyumbani, walimkuta Dk Lewis akiwa tayari
amesharejea nyumbani, akawa amekaa sebuleni akitazama taarifa ya habari kwenye runinga. “Mbona umewahi sana mume wangu?” “Uliponipa taarifa zile mchana nimeshindwa kuendelea kufanya kazi, nimeona bora nije kupumzisha kichwa,” alisema Dk Lewis huku akimkazia macho mwanaye Skyler. Kwa kuwa alikuwa anajua makosa yake, Skyler hakutaka kutazamana na baba
yake, akawa anakwepesha macho. Dk Lewis hakutaka kusema neno lolote kwa muda ule, kila mmoja akaenda kubadilisha nguo kisha majukumu ya kawaida ya pale nyumbani yakaendelea kama kawaida. Skyler alisaidiana na mama yake kuandaa chakula cha usiku na baada ya kumaliza, walitayarisha mezani kisha wakajumuika pamoja kupata ‘dinner’. Baada ya kumaliza kula, Dk Lewis aliwataka wote kuhamia chumbani kwake kwa ajili ya kikao cha
familia na kuanza kujadili suala la Skyler. Alipotakiwa kueleza ukweli juu ya kilichokuwa kinasababisha ashindwe kuhudhuria shuleni kwa siku zote hizo, bado Skyler aliendelea kung’ang’ania jibu lake kuwa alikuwa akijisikia vibaya kila baada ya kufika shuleni hivyo kurudi nyumbani kulala. Dk Lewis alijitahidi kuwa mkali ili mwanaye aseme ukweli, lakini kutokana na mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo kwa binti yake huyo, alipoanza kujiliza na kutokwa machozi, Dk Lewis alikuwa mpole ghafla na kusitisha maswali yote, akaanza kumbembeleza.
“Sasa kama mnabembelezana namna hiyo si ndiyo tatizo litazidi kuwa kubwa, wewe unasema mimi nachangia mwanao kuharibika, mbona na wewe unashindwa kuwa mkali?” mama Skyler alianza kulumbana na mumewe, Skyler akawa anaendelea kulia huku akilalamika kuwa anaonewa. Suluhu ilishindwa kupatikana, ikabidi Skyler atoke na kwenda chumbani kwake kulala.Huku nyuma Dk Lewis na mkewe wakawa wanaendelea kulaumiana.
“Tatizo mwanao umemdekeza sana kiasi kwamba hata akifanya makosa huwezi kumkaripia wala kumhoji kwa ukali, malezi gani hayo?” alisema mama Skyler kwa hasira, mumewe akawa anamtetea Skyler kuwa hata kama amefanya makosa, anapaswa kupewa nafasi ya kuwa peke yake na kutafakari kilichotokea.
Siku ya kwanza ilipita, kesho yake, kama alivyokuwa ameahidi, mama Skyler akampeleka mwanaye shuleni ambapo alihakikisha ameingia kwenye geti la shule, ndipo akageuza gari na kuendelea na safari ya kuelekea kazini kwake. Jioni ilipofika, alipokuwa anatoka kazini alimpitia na kurudi naye nyumbani. Siku zikawa zinasonga mbele na lile tatizo lililotokea likaanza kusahaulika kwenye vichwa vyao. Wiki ya kwanza ilipita, ya pili, hatimaye ya tatu ikawadia.
“Mwalimu Armstrong, nimepata taarifa kutoka kwa wanafunzi wanaosoma darasa moja na Skyler kwamba siku hizi ameanza tabia ya kupenda kulala-lala darasani, wanasema mwalimu akitoka tu, yeye anajilaza kwenye dawati lake na kuuchapa usingizi, inabidi tumfuatilie kwa makini huyu binti.” “Hata mwonekano wake nao unabadilika haraka, ameanza kunawiri na ngozi yake inapendeza sana, au ndiyo adolescence?” “Tungekuwa hatujawapima ujauzito tungesema tayari amenasa, lakini haipo hivyo.”
“Haya tusubiri tuone, wateue ma-prefect (viranja) wawili wa kike kwa ajili ya kumfuatilia nyendo zake,” alisema mwalimu wa nidhamu, Armstrong, matron akaitika na kutoka kwenda kuendelea na shughuli zake. Jioni moja, Dk Lewis, mkewe na mtoto wao walikuwa wakipata chakula cha usiku huku wakitazama tamthiliya kwenye runinga. Walikuwa wakipiga stori na kufurahi, mama Skyler akiwa ndiyo msimuliaji mkuu. Wakati wakiendelea kula, ghafla Skyler aliinuka na kukimbia kwenye sinki dogo lililokuwa kwenye korido.
Akaanza kutapika chakula chote alichokula. Dk Lewis na mkewe, walitazamana kisha wakageuka kumuangalia Skyler ambaye alikuwa akiendelea kutapika. Harakaharaka wote waliinuka na kukimbilia pale kwenye sinki mtoto wao alipokuwa akitapikia. “Umepatwa na nini?” alisema mama Skyler huku akimsaidia mwanaye. ’’Nimesikia kichefuchefu ghafla, nahisi ni malaria,” alisema Skyler kwa tabu. Wakamshika huku na huku na kumpeleka chumbani kwake, mama Skyler alikimbilia kwenye kisanduku chake cha huduma ya kwanza, kwa kusaidiana na mumewe wakawa wanampa dawa Skyler za kuzuia kuendelea kutapika.
Baada ya kunywa dawa, walimlaza kitandani kwake na muda mfupi baadaye usingizi ukampitia. “Mke wangu unajua hii hali ya Skyler mimi siielewi kabisa!” “Hata mimi mume wangu, inaweza kuwa tayari amenasa ujauzito.” “Lakini si shuleni kwao walimpima na kuona hana?”
“Ndiyo, inawezekana pale ilikuwa bado ndogo kiasi cha kutoonekana kwenye vipimo, mi nafikiri itakuwa busara kama tukienda kumpima tena.” “Sasa tukimpeleka hospitali na ikaonekana hana, si ataona tunamnyanyasa kisaikolojia?” “Hapa tutumie akili tu, huyu ni mtoto wetu na sisi ndiyo tulimzaa, tumdanganye kwa jambo lolote ilimradi kesho asubuhi tuondoke naye mguu kwa mguu mpaka hospitali.”
“Haiwezi kuwa ni ujauzito, mwanangu bado hajaanza kuwajua wanaume, siku zote si anashinda hapa ndani?” alisema Dk Lewis, mkewe akamwambia kuwa vyovyote itakavyokuwa, lazima akapimwe ujauzito. Baada ya kulala kwa saa kadhaa, Skyler alizinduka usingizini na kutazama saa ya kwenye simu ya baba yake ambayo ilikuwa pembeni ya droo ya kitanda chake. Ilikuwa ni saa nane na nusu za usiku, akaanza kutafakari kwa kina juu ya kilichotokea usiku ule wakati alipokuwa anakula chakula cha usiku na wazazi wake.
“Hivi inawezekana ikawa ni mimba? Kwani Harvey siku ile nilipofanya naye mapenzi alinipa ujauzito? Hapana,” Skyler alikuwa akijiuliza na kujijibu mwenyewe kichwani mwake, akapata wazo la kujaribu kumpigia simu Harvey na kumwambia alichokuwa anakihisi.” Aliichukua ile simu ya baba yake ambayo tayari alishajenga mazoea ya kulala nayo chubani kwake, akaingia sehemu ya majina na kutafuta namba ya Harvey. Alipojaribu kuipiga namba ya Harvey, haikuwa ikipatikana.
Kwa wiki kadhaa, tangu walipofumwa wakivunja amri ya sita kule kambini kwa akina Harvey, mawasiliano yao hayakuwa mazuri. Kila Skyler alipopiga namba ya Harvey, haikuwa ikipatikana. Akahisi huenda atakuwa amebadilisha namba anayoitumia. Aliendelea kuwaza pale kitandani, akafikia uamuzi kuwa alfajiri na mapema ya siku inayofuatia, ajifanye anaumwa sana ili wazazi wake wakiondoka, amfuate Harvey kambini au chuoni na kumpa taarifa juu ya mabadiliko ya afya yake.
Kulipopambazuka tu, mama Skyler ndiyo alikuwa wa kwanza kuamka, akaenda kumuamsha mwanaye ambaye kama alivyokuwa amepanga tangu awali, alijifanyisha kama anaumwa sana na hawezi hata kuinuka.
‘Twende hospitai ukapime, inawezekana una tatizo la minyoo au amiba tumboni mwako,” alisema mama Skyler lakini binti yake akawa mbishi na kueleza kuwa atatumia dawa tu. Ilibidi mama Skyler awe mkali, akamwambia mwanaye kuwa ni lazima waende hospitali kisha ndiyo aandikiwe dawa za kutumia.
Alipoona mama yake amekazania, Skyler hakuwa na namna ya kufanya zaidi ya kukubali, wakajiandaa na kwa kutumia gari la familia, Dk Lewis, mkewe na Skyler wakaongozana mpaka kwenye hospitai ya Miami aliyokuwa akifanyia kazi. Harakaharaka Dk Lewis alizungumza na wasaidizi wake, akawaambia wamchukue vipimo vyote binti yake. Akaingizwa kwenye wodi maalum na kuchukuliwa vipimo vyote kama baba yake aivyokuwa ameagiza.
‘Sasa mimi naumwa tumbo nyie mnachukua haja ndogo, vinahusianaje?” aliuliza Skyler huku akianza kuwa na hofu. Manesi walimtoa wasiwasi kuwa wanaenda kuangalia kama mkojo wake ulichafuka kwani hiyo nayo ni sababu inayoweza kusababisha maumivu ya tumbo na kumfanya mgonjwa awe anatapika.
Baada ya vipimo, Dk Lewis alishauri binti yake arudishwe nyumbani kupumzika na majibu ya vipimo atayachukua yeye mwenyewe. Walikubaliana, mama Skyler akaondoka na binti yake kurudi nyumbani. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ WAKATI Harvey akianza kuyafaidi matunda ya kipaji chake cha kucheza mpira wa kikapu alichojaaliwa na Mungu, jinamizi lingine linaingia kwenye
maisha yake baada ya kushawishiwa mpaka akalainika na kushiriki mchezo mchafu na Skyler, mtoto wa mtu pekee aliyembadilisha na kumjengea upya misingi ya maisha bora nchini Marekani, Dk Lewis.
Baada ya kunusurika kutimuliwa kwenye kambi ya timu ya mpira wa kikapu ya Miami Heat kufuatiwa kufumwa akivunja amri ya sita ndani ya chumba
alichokabidhiwa muda mfupi baada ya kuripoti rasmi kambini hapo, Harvey anajiapiza kuwa kamwe hatarudia tena kufanya kosa kama hilo na kuamua kuuvunjilia mbali uhusiano wa kimapenzi na Skyler, anafungua ukurasa mpya wa maisha yake na kujiapiza kudumisha nidhamu muda wote.
Hata hivyo, upande wa pili hali ya mambo inazidi kuwa tete kutokana na Skyler kuanza kuonesha mabadiliko yanayowashtua wazazi na walimu wake,
anaonesha dalili kama aliyenasa ujauzito ingawa vipimo vya awali vinashindwa kubaini tatizo hilo kutokana na Skyler kutumia ujanja kuuficha ukweli akishirikiana na rafiki yake, Sandra.
BAADA ya majibu ya vipimo vya mara ya pili alivyochukuliwa Skyler kutoka, ilibainika kuwa tayari binti huyo aliyekuwa na umri wa miaka kumi na tisa tu, alikuwa na ujauzito wa mwezi mmoja, taarifa ambayo almanusra imtoe roho Dk Lewis kwa mshtuko alioupata.
“Hapana nesi, utakuwa umekosea vipimo, mwanangu hana ujauzito. Rudia tena tafadhali.” “Dokta Lewis kwani vipi? Tafadhali tulia, hayo ni mambo ya kawaida kwa watoto wa kike, hili nalo litapita.” “Hapana, mwanangu hawezi kuharibika kirahisi namna hii akiwa mikononi mwangu, bado ni mdogo sana kubeba ujauzito, haiwezekani… nasema haiwezekani!”
Dk Lewis hakuweza kuendelea kufanya kazi, aliingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo na kuvua koti lake jeupe la kidaktari, akatupatupa vifaa vyake vya kazi na kutoka bila kumuaga mtu yeyote, akawa anatembea kuelekea nyumbani kwake kwa miguu, jambo ambalo halikuwa kawaida yake.
Njia nzima, kila aliyekuwa akikutana naye alikuwa akimshangaa Dk Lewis kwa jinsi alivyobadilika kwani alikuwa akizungumza peke yake kama mwendawazimu huku muda mwingine akishindwa kujizuia na kumwaga machozi barabarani, alitia huruma.
“Dokta umepatwa na nini? Ingia kwenye gari nikupeleke nyumbani,” mfanyakazi mwenzake aliyekuwa akielekea kazini, alishangazwa na hali aliyomuona nayo Dk Lewis, ikabidi ageuze gari na kumfungulia mlango wa mbele. “Ingia twende, nitakupeleka mpaka nyumbani kwako,” alisema yule mfanyakazi mwenzake, Dk Lewis akasitasita kwa muda lakini baadaye akakubali, safari ya kuelekea nyumbani kwake ikaanza.
“Kwani una tatizo gani bosi?” “Mwanangu… mwanangu Skyler!”
“Kafanya nini ambacho kimekuchanganya kiasi hicho?” “Wamempa ujauzito, najisikia hamu ya kuua, nitamuua yeyote aliyehusika na kuniharibia mwanangu… oooh shit,” alisema Dk Lewis huku akijifuta machozi na kamasi ambavyo vilikuwa vikimtoka kwa wingi.
“Ujauzito? Skyler ana ujauzito? Mungu wangu, mbona bado mdogo?” yule mfanyakazi mwenzake alishtuka sana, akaelewa ni kwa nini Dk Lewis alikuwa amechanganyikiwa kiasi kile, akawa na kazi ya ziada kumtuliza lakini hakufanikiwa.
Yule mfanyakazi mwenzake alipohakikisha Dk Lewis ameteremka na kuingia ndani ya geti, aligeuza gari na kuendelea na majukumu yake kama kawaida. Alitambua ni kwa kiasi gani suala la mwanaye kupata ujauzito lilimchanganya Dk Lewis, akawa anamsikitikia kimoyomoyo.
Baada ya kuingia ndani, Dk Lewis alianza kuzunguka huku na kule akiwa haelewi hata alichokuwa anakitafuta. Mlinzi alilitambua hilo, akamfuata kwa upole na kuanza kumuuliza kama kuna tatizo.
Tangu alipomkaripia vikali wiki kadhaa zilizopita na kutishia kumfukuza kazi kwa kile alichoelezwa na Skyler kuwa ni uzembe kazini, mlinzi yule hakuwa na amani kabisa, akawa anamuogopa bosi wake kama simba. Licha ya hayo yote, aliamua kuweka
tofauti zao pembeni na kumnyenyekea bosi wake ili amwambie kilichokuwa kinamsumbua, akamuuliza kwa upole lakini akakutana na majibu makali.
“Unaacha kufanya kazi yako ya ulinzi matokeo yake unasababisha mpaka mwanangu anapewa ujauzito halafu eti unaniuliza kama nina tatizo, lazima nikufukuze kazi.” “Ujauzito?” mlinzi naye alionekana kushtushwa na kauli ile, akili zake zikamrudisha haraka siku aliyomsikia Skyler akilia kimahaba chumbani kwake akiwa na Harvey.
Alikumbuka kila kitu kilichotokea siku hiyo mpaka wakati Harvey anaondoka, alitamani kufungua mdomo wake na kueleza kilichokuwa ndani ya mtima wake lakini akajikuta amebanwa na kigugumizi cha ghafla, akaondoka haraka na kurudi kwenye kibanda chake cha kazi huku akiwa haamini kile alichokisikia.
Ilibidi Dk Lewis ampigie simu mkewe na kumweleza hali halisi, naye akapatwa na mshtuko mkubwa uliomfanya ashindwe kuendelea na kazi, harakaharaka akaomba ruhusa na kuondoka kazini kurudi nyumbani. Kwa jinsi alivyokuwa anaendesha gari kwa kasi, dakika kumi baadaye tayari alikuwa mbele ya geti la nyumba yao, akapiga honi
ambapo mlinzi alifungua geti haraka, akaingiza gari mpaka eneo la maegesho na kutoka mbiombio mpaka ndani ambapo alimkuta mumewe akiwa bado anazungukazunguka nyumba nzima.
Kama ilivyokuwa kwa mumewe, mama Skyler naye alichanganyikiwa kupita maelezo, wakawa wanatupiana lawama kila mmoja akimshtumu mwenzake kuwa ndiyo chanzo cha matatizo ya Skyler, amani ikatoweka kabisa ndani ya nyumba. ***
Baada ya kushinikizwa na wazazi wake kwenda hospitali kupima ujauzito bila ridhaa yake, Skyler alijua mambo yameshaharibika, akajua lazima siri aliyokuwa anataka kuificha itafichuka na kumuingiza yeye pamoja na Harvey kwenye matatizo makubwa, jambo ambalo hakutaka litokee.
Kitu pekee alichoona kinafaa kwa wakati ule ilikuwa ni kutafuta njia ya kumfikishia ujumbe Harvey ili kwa pamoja waamue nini cha kufanya.
Kila alipojaribu kumpigia simu Harvey, namba yake haikuwa ikipatikana hewani, akaendelea kujaribu mara nyingi kwa kadiri ya uwezo wake lakini bado hakufanikiwa. Akaona njia bora ni kumfuata kule kwenye kambi ya Miami Heat na kumtafuta mpaka ampate ili wazungumze ana kwa ana juu ya tatizo lile.
Baada ya muda wa masomo kumalizika, Skyler alifanya haraka na kutoka kupitia mlango wa nyuma akikwepa kukutana na mama yake ambapo aliamini atamkuta akimsubiri na gari nje ya geti kama ilivyokuwa kawaida yake.
Akaongeza mwendo na kutokomea mitaani, alipofika mahali ambapo aliamini hakuna mtu anayeweza kumshtukia, alibadili nguo za shule na kuvaa nguo nyingine alizokuwa amezibeba kwenye mkoba wake wa madaftari, akapanda taxi na kumwelekeza dereva sehemu ya kumpeleka.
Nusu saa baadaye alikuwa ameshawasili mbele ya jengo la makao makuu ya Timu ya Miami Heat, American Airways Arena, mahali alipokuwa anaishi Harvey. Kwa kuwa ilikuwa ni jioni, aliwakuta wachezaji wakiendelea na mazoezi kama kawaida,
alipojaribu kuingia ndani kumfuata Harvey, walinzi wawili wenye silaha walimzuia na kumwambia kuwa uongozi wa timu hiyo ulipiga marufuku wageni wa kike kuwatembelea wachezaji kambini. “Lakini mimi nimekuja kumtembelea kaka yangu, napo siruhusiwi?” “ Binti kuwa mwelewa, hata angekuwa ni mumeo, sheria mpya inazuia, subiri mpaka VD (Visiting Day) ifike, hatuwezi kukuruhusu,” alisema mlinzi mmoja huku akimuelekeza Skyler kwa ishara kuwa aondoke eneo lile.
Licha ya kuendelea kuwabembeleza kwa muda mrefu, Skyler hakusikilizwa kabisa na hata alipotaka apewe nafasi ya kuacha ujumbe wa maandishi ili Harvey akimaliza mazoezi apewe, bado hakuna aliyemjali. Ilibidi arudi nyumbani kwao huku kichwani akiwa na mawazo mengi juu ya nini kitakachotokea akifika nyumbani, alitambua fika
kuwa lazima baba yake atakuwa amerejea na majibu ya vipimo vya ujauzito vilivyochukuliwa asubuhi ya siku hiyo. Hakuwa na ujanja, ikabidi ajikaze hivyohivyo na kurejea mpaka nyumbani kwao.
“Nataka uniambie nani aliyekupa ujauzito, vinginevyo leo nitakuchinja kwa mikono yangu,” alifoka Dk Lewis kwa hasira muda mfupi baada ya Skyler kuwasili, hali iliyomfanya aanze kutetemeka mithili ya mtu aliyemwagiwa maji ya baridi. Tangu awe na akili, CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ hakuwahi kumuona baba yake akiwa amekasirika kiasi kile, akajua asipoeleza ukweli anaweza kumdhuru au hata kumuua kama alivyokuwa anatishia. Mchuma janga hula na wa kwao, walinena wahenga. Harvey, kijana mdogo kutoka nchini Liberia aliyekimbia mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na
kupewa hifadhi na Dk. Lewis nchini Marekani, analichuma janga kwa kuthubutu kuvunja amri ya sita na Skyler na sasa balaa kubwa linamnyemelea.
Baada ya kushiriki kwenye mchezo mchafu na Harvey, Skyler ananasa ujauzito na baada ya muda mfupi, wazazi pamoja na walimu wake wanaanza
kuona dalili zisizo za kawaida wanaamua kumfanyia uchunguzi wa kina kubaini tatizo lililokuwa linamsumbua.
Baada ya kugundua kuwa mwanaye amepewa ujauzito, Dk. Lewis anachanganyikiwa kuliko kawaida na sasa anamshinikiza Skyler amtaje
mhusika wa mzigo ule. Anajiapiza kuyakatisha maisha ya yeyote atakayegundua kuwa ndiye aliyehusika kumharibia mwanaye maisha.
“Usinidhuru baba, ngoja niseme ukweli mwenyewe.” “Sitaki unipotezee muda, sema haraka.” “Sawa baba, ni… ni…,” Skyler alishindwa kumalizia alichokuwa anataka kukisema, akatoka mbio mpaka kwenye sinki na kuanza tena kutapika mfululizo.
Dk. Lewis hakujali kitu, akamsogelea palepale kwenye sinki alipokuwa anatapika, akamsubiri mpaka alipomaliza, aliendelea kumshinikiza aseme ukweli haraka vinginevyo atamdhuru. “Skyler mwanangu, kwa nini unamsumbua baba yako? Si useme ukweli tu?” “Namtaja mama, ni… ni kaka Harvey?” “Whaaaaat? Harvey? Sitaki kuamini, muongo wewe,” alisema mama Skyler huku mumewe akidakia: “We mtoto usinitanie? Harvey hawezi kufanya ujinga kama huo, sema ukweli.” “Huo ndiyo ukweli, Harvey ndiye mhusika,” alisema Skyler huku akiangua kilio, baba na mama yake wakatazamana kwa dakika kadhaa wakiwa kama hawaaamini walichokisikia, wakamgeukia mtoto wao. “Skyler, sema ukweli mwanangu, Harvey si ni kaka yako? Iweje afanye kitendo kama hiki kwako wewe mdogo wake? Namuamini sana, hawezi… nasema hawezi!”
“Ni kweli mama, kama hamuamini muulizeni,” alisema Skyler huku kwa mara nyingine tena akikimbilia kwenye sinki na kuendelea kutapika. Dk. Lewis bado alikuwa kama yupo ndotoni, hakutaka kuamini alichokisikia kutoka kwa binti yake. “Harvey? Hapana, sitaki kuamini… haiwezekani,” alisema Dk. Lewis na kuondoka kwa hasira kuelekea chumbani kwake,
akapitiliza mpaka kwenye droo iliyokuwa pembeni ya kitanda chake ambapo aliifungua kwa nguvu, akaingiza mkono na kutoa bastola yake ya kisasa aina ya revolver, akachukua kiboksi kilichokuwa na risasi na kuanza kuzijaza. “Harvey! Harvey! Yaani umesahau wema wangu wote niliokutendea mpaka unafikia hatua ya kuniharibia binti yangu? Kama
ulikuwa unampenda kwa nini usisubiri akue? Unastahili kifo,” alijisemea Dk. Lewis kwa hasira. “Mume wangu mbona unaongea peke yako? Hutakiwi kuwa na hasira kiasi hicho, halafu hiyo bastola unaenda nayo wapi?” “Niache, niache mke wangu… naomba usiniulize kitu chochote, najua ninachotaka kukifanya,” alisema Dk. Lewis huku akijifuta
machozi yaliyokuwa yanamchuruzika na kuulowanisha uso wake. Akatoka harakaharaka mpaka nje ya nyumba yake, akawa anazunguka huku na kule akiongea peke yake kama mwendawazimu.
“Bosi kuna tatizo lingine?” Mlinzi aliuliza baada ya kumuona Dk. Lewis akizidi kuchanganyikiwa, hakumjibu kitu zaidi ya kuendelea kulitaja jina la Harvey huku bastola ikiwa mkononi mwake.
Aliondoka pale jirani na mlinzi na kuzunguka upande wa nyuma huku akiendelea kuongea peke yake, baada ya muda mfupi akarudi pale kwa mlinzi, safari hii akionekana kufura kwa hasira kama nyoka kifutu. “Unajua nini kuhusu uhusiano wa kimapenzi kati ya binti yangu Skyler na Harvey?” “Sijui chochote bosi.”
“Lazima unajua, sasa sikia, kama hutaki kusema ukweli nitaumwaga ubongo wako, sema ukweli.” “Ni kweli bosi, Harvey na Skyler walikuwa na uhusiano wa kimapenzi, niliwasikia siku wakifanya mapenzi chumbani kwa Skyler.” “Kwa nini hukuniambia? Nakulipa mshahara mkubwa kumbe na wewe unashiriki kuniharibia nyumba yangu.”
“Nilitaka kukuambia bosi lakini Skyler aliwahi kuja kukufikishia maneno ya uongo kuhusu mimi, ukawa mkali kwangu kiasi kwamba nilishindwa kukueleza ukweli, nisamehe,” alijitetea mlinzi huku akitetemeka kupita kawaida.
Tangu azaliwe, hakuwahi kunyooshewa bastola hata mara moja kama alivyokuwa amefanya Dk. Lewis muda ule mbele yake, akawa anasikia harufu ya kifo, akawa anamuomba Mungu wake Dk. Lewis asimpige risasi.
Bila hata kusema neno, Dk. Lewis aliondoka na kuelekea mahali alipokuwa amepaki gari, akaingia na kuliwasha. Bila kumuaga mtu yeyote akaendesha gari na kuondoka kwa kasi kuelekea kusikojulikana.
“Skyler mwanangu, tazama unavyoleta balaa ndani ya nyumba yetu, yaani umediriki kuvunja amri ya sita na kaka yako? Aibu gani hii uliyotuletea? Tutaficha wapi sura zetu?”
“Nisamehe mama lakini naomba umwambie baba kuwa nampenda sana Harvey na nataka anioe.” “Akuoe? We mtoto una wazimu nini? Yaani hufikirii tatizo lililopo mbele yako bado unazidi kutibua mambo? Una akili kweli wewe?”
“Ni kweli mama, nampenda sana Harvey na nipo tayari kumzalia mtoto,” alisema Skyler huku akikimbilia kwenye sinki na kutapika tena. *** “ Nimekumbuka sana kwenda nyumbani, siku nyingi zimepita sijamuona Dk. Lewis wala mama… lakini naogopa nikienda nitakutana na Skyler na atataka tena turudie mchezo ule wa hatari jambo ambalo sitaki litokee, potelea mbali ngoja leo niende nikawasalimu hata kwa dakika chache roho yangu itulie,” aliwaza Harvey muda mfupi baada ya kumaliza mazoezi ya jioni akiwa na wachezaji wenzake wa Timu ya Miami Heat.
“Cazzard, natoka kidogo rafiki yangu, naenda nyumbani lakini nitarudi baada ya muda mfupi.” “Muda umeshaenda sana Harvey, isitoshe umechoka baada ya mazoezi mazito, kwa nini usisubiri wikiendi ndiyo uende?”
“Kwa sababu natumia gari langu wala sitachelewa, nusu saa inanitosha kabisa,” alisema Harvey, akaingia ndani ya chumba chake na kujiandaa, harakaharaka akaelekea mahali alipokuwa amepaki gari lake na kuliwasha. Taratibu akaanza kulirudisha nyuma na kulitoa eneo la maegesho, akapiga honi ambapo walinzi walimfungulia geti, akatoka na safari
ya kuelekea kwa Dk. Lewis ikaanza. Kwa kuwa alikuwa na haraka, aliamua kutumia njia ya mkato tofauti na ile aliyozoea kuitumia siku zote, dakika kumi baadaye akawa tayari amewasili nje ya nyumba ya Dk. Lewis.
Mlinzi ambaye bado alikuwa akiendelea kutetemeka ndani ya kibanda chake, alishtushwa na honi mfululizo, akainuka haraka akidhani Dk. Lewis alikuwa amerejea lakini katika hali iliyomshtua zaidi, alikutana na Harvey aliyekuwa ndani ya gari dogo la kisasa.
“Nifungulie geti,” alisema Harvey lakini mlinzi alikataa akihofia kuzidi kumuudhi bosi wake, ikabidi Harvey apaki gari nje kabisa, pembeni ya barabara na kuteremka, akawa anatembea kwa miguu kuelekea pale getini.
“Kwa nini unakataa kunifungulia geti?” Aliuliza Harvey kwa hasira, bila hata kusubiri kujibiwa akaingia kwa nguvu mpaka ndani na kuelekea moja kwa moja kwenye mlango mkubwa wa kuingilia ndani. Akiwa anapandisha ngazi ili aingie, alisikia Skyler akizungumza na mama yake huku jina lake likitajwa mara kadhaa.
Akabisha hodi na kuingia ndani ambapo alimkuta mama Skyler akiwa na macho mekundu huku mwanaye akitiririkwa na machozi kuashiria kuwa amani haikuwepo ndani ya nyumba ile. Wote walipomuona akiingia walishtuka sana, wakapigwa na butwaa na kuanza kutazamana, Harvey akabaki njia panda akiwa haelewi kinachoendelea.
BALAA kubwa linaanza kumnyemelea Harvey, kijana mdogo kutoka nchini Liberia aliyekimbia mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na kupewa hifadhi nchini Marekani, baada ya kuanza kujiingiza kwenye uhusiano wa kimapenzi na Skyler, mtoto wa Dk Lewis. Hali ya hewa inachafuka nyumbani kwa Dk Lewis baada ya kugundua kuwa mwanaye ni mjamzito na sasa anamshinikiza amtaje mhusika vinginevyo atamuua. Baada ya kubanwa sana, Skyler anaeleza ukweli kuwa mhusika wa ujauzito ule ni Harvey, jambo linalowashangaza wazazi wake kuliko kawaida. Dk Lewis ndiyo anaonekana kuchanganyikiwa zaidi. Baadaye anachukua bastola yake na kutoka nje kuelekea kusikojulikana.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “UMEFUATA nini Harvey? Umefuata nini nakuuliza? Ondoka haraka,” alifoka mama Skyler kwa hasira zilizochanganyikana na uchungu.
“Mama, Harvey hana makosa, kama unamfukuza basi na mimi naondoka, nampenda sana,” alidakia Skyler, Harvey akabaki amepigwa na butwaa kwani hakuwa akielewa kinachoendelea. “Kwani kumetokea nini jamani, mbona sielewi?”
“Huelewi? Shetani mkubwa wewe… yaani wema wote tuliokufanyia unaishia kutuharibia binti yetu kwa kumpa ujauzito?” “Whaaaat? Ujauzito?” Harvey alishtuka kupita kiasi baada ya kusikia maneno yale, akamgeukia Skyler akiwa ni kama asiyeamini kile alichokisikia. “Eti ni kweli una ujauzito wangu?” “Ni kweli na nipo tayari kukuzalia mtoto,” alijibu Skyler.
Harvey alishindwa kuficha hisia zake za hofu kubwa iliyochanganyikana na kukata tamaa, akajua huo ndiyo mwisho wa kila kitu kwenye maisha yake, akainamisha kichwa na kuanza kutokwa na machozi. “Mnafiki mkubwa wewe, unajifanya kulia kwani ulikuwa hujui ulichokuwa unakifanya,” alizidi kufoka mama Skyler huku naye akiangua kilio cha kwikwi.
Harvey bado alikuwa haamini kama kile alichokisikia kilikuwa ni kweli lakini alipojaribu kuvuta kumbukumbu, aligundua kuwa mara zote alizoshiriki kuvunja amri ya sita na Skyler hakutumia kinga, akahisi uzito wa dunia nzima ukimuelemea kichwani.
Mama Skyler alizidi kufoka huku akilia, akawa anamlaumu Harvey kwa kushindwa kuwa na fadhila na kufikia hatua ya kumharibia maisha binti yao ambaye kiumri bado alikuwa mdogo. Wakiwa katika hali ile, kwa mbali walisikia muungurumo wa gari likija kwa kasi kisha likasimama mbele ya geti la nyumba yao, honi ikapigwa na mlinzi akaenda kufungua.
Wote waliokuwa ndani walikimbilia dirishani kuchungulia ni nani aliyeingia kwa kasi namna ile, wakagundua kuwa ni Dk Lewis. Harvey hakuwahi kumuona Dk Lewis akiwa katika hali kama ile hata siku moja, akajua asipofanya jambo la kuokoa maisha yake kwa haraka, anaweza hata kupoteza maisha yake. “Kimbia kaka Harvey, kimbia! Baba ameshika bastola, atakuua,” alisema Skyler kwa sauti, Harvey akatimua mbio kuelekea
kwenye mlango wa nyuma, akaufungua na kutoka hadi nje kwa kasi, akazidi kutimua mbio mpaka kwenye kona ya uzio mrefu wa nyumba ile, akaanza kupanda kwa kasi na kufanikiwa kurukia upande wa nje. “Yupo wapi? Yupo wapi huyu mwanaharamu? Mmemficha siyo?” alifoka Dk Lewis baada ya kuingia ndani na kumkosa Harvey wakati tayari alishaliona gari lake kule nje. Kuepusha shari, mama Skyler alimwambia kuwa amekimbia na kutoka kupitia
mlango wa nyuma, Dk Lewis akiwa amevimba kwa hasira, bastola ikiwa mkononi, alikimbia mpaka kwenye mlango wa nyuma, akakuta upo wazi ambapo alitoka na kuanza kuangaza macho huku na kule. Mara alisikia gari la Harvey likiwashwa upande wa nje wa fensi, akajua anataka kumkimbia. Harakaharaka na yeye alitimua mbio huku bastola ikiwa mkononi, akaingia ndani ya gari lake huku akimpigia kelele mlinzi ili afungue geti. Sekunde chache
baadaye tayari alishalitoa gari lake nje, kwa mbali akamuona Harvey akitokomea akiwa ndani ya gari lake. Hakutaka kumpa nafasi ya kutoroka, akakanyaga mafuta mpaka mwisho na kuanza kulifukuzia lile gari kwa nyuma. “Lazima afe, lazima,” alisema Dk Lewis huku akizidi kukanyaga mafuta na kuikoki bastola yake, gari likawa linakimbia kwa spidi ya kilometa 120 kwa saa.
Harvey aliyekuwa na imani kubwa kuwa tayari amefanikiwa kumkimbia Dk Lewis na kukikwepa kifo cha kupigwa na risasi, aliendelea kujilaumu kutokana na kitendo alichokifanya na kuangukia dhambini na Skyler. Mawazo mengi yakiwa yanaendelea kukizonga kichwa chake, alishtuka kupita kiasi baada ya kuliona gari la Dk Lewis kupitia kioo cha pembeni (sight mirror) likija kwa kasi ya ajabu nyuma yake.
“Mungu wangu, nimekwisha,” alisema Harvey na kukata kona ya ghafla, gari lake likaserereka na kutoka nje ya barabara, hali iliyomfanya Dk Lewis apitilize na gari lake. Harakaharaka Harvey aligeuza gari na kuanza kurudi kule alikotoka, safari hii kwa kasi kubwa kama anashiriki mbio za magari za Formula One.
“Shiiit!” alisema Dk Lewis baada ya kuona Harvey amemzidi akili na kugeuza gari lake na kuanza kurudi kule walikotoka. Harakaharaka na yeye aligeuza la kwake na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara, alipofanikiwa akaongeza kasi na kuanza kumfuata tena Harvey lakini safari hii haikuwa rahisi kumuona kwani tayari alishapotea kwenye upeo wa macho yake.
Breki ya kwanza ya Harvey ilikuwa ni chuoni kwao, akateremka kwenye gari huku akitetemeka mwili mzima, akakimbia mpaka kwenye bustani za maua za chuo hicho, akakaa na kuanza kutafakari kilichotokea. Kila kitu alikiona kama ndoto ya mchana au filamu ya kusisimua.
“Eeeh Mungu niokoe kutoka kwenye hili janga,” alijisemea Harvey huku akitokwa na machozi, akawa amejiinamia huku mawazo mengi yakiendelea kukizonga kichwa chake. Akiwa katika hali ile, alisikia muungurumo wa gari likija kwa kasi chuoni pale,
akasimama juu ya ukuta na kutazama kwenye lango kuu la kuingilia, akaliona Range Rover jekundu la Dk Lewis likiingia kwa kasi na kwenda kupaki nyuma ya gari lake alilokuwa amelipaki sehemu ya maegesho.
“Mungu wangu, leo nimekwisha,” alisema Harvey kimoyomoyo huku hofu ikizidi kuutesa mwili wake. Alishuka juu ya ule ukuta na kujificha kwenye maua, akawa anamchungulia Dk Lewis kila alichokuwa anakifanya, akamuona akiteremka kwenye gari na kuichomeka bastola yake kiunoni kisha akajifunika na koti, akawa anatembea kwa kasi kuelekea kwenye ofisi za utawala.
Harvey alimsubiri mpaka alipoingia ndani, akatoka kwa kasi pale alipokuwa amejificha na kukimbia hadi pale alipokuwa amelipaki gari lake, akaliwasha na kuligeuza kisha akaondoka kwa kasi eneo lile.
Kabla hata hajafika mbali, alimuona Dk Lewis akitoka kwenye ofisi za utawala huku akikimbia. Aliingia kwenye gari lake na kuliwasha, akaligeuza kwa vurugu kisha akaondoka kwa spidi kubwa, hali iliyowaacha wanachuo na wakufunzi wakiwa wamepigwa na butwaa. Hakuna aliyeelewa kilichokuwa kinaendelea.
Harvey baada ya kufanikiwa kutoka eneo lile la chuo, aliingia kwenye Barabara ya Dolphin Exyp, akahama sehemu aliyokuwa anatakiwa kuendesha gari na kuingia katikati ya barabara kwenye eneo la mabasi yaendayo kwa kasi, akazidi kukanyaga mafuta na kuongeza kasi.
Akazidi kuchochea gari kuelekea upande wa Kaskazini, akiwa haelewi anakoenda, akakatiza kwenye ufukwe wa Miami na kuzidi kuchanja mbuga. Licha ya kujitahidi kukimbiza gari, Dk Lewis hakutaka kumuachia, naye akawa anazidi kuongeza kasi na kwa kuwa gari lake lilikuwa kubwa na lenye nguvu kuliko lile alilokuwa anaendesha Harvey, baada ya kilometa kadhaa alimkaribia kabisa.
Harvey alipotazama tena nyuma kwa kutumia sight mirror, aliliona Range Rover jekundu likija wanguwangu, nalo likipita sehemu ya magari yaendayo kwa kasi, hali iliyozidi kumchanganya.
Ukarabati wa njia za kurukia (run ways) za Uwanja wa Ndege wa Miami ulikuwa ukiendelea kwa kasi, magari makubwa yakawa yanasomba mawe, kokoto, mchanga na vifaa vingine vya ujenzi kutoka kwenye machimbo ya Melreese yaliyokuwa upande wa
Magharibi wa uwanja ule na kuvuka barabara kisha kuyapeleka kwenye uwanja huo. Kutokana na shughuli hizo za ujenzi zilizokuwa zinaendelea kwenye uwanja huo, kulikuwa na alama za barabarani nyingi zikiwatahadharisha madereva kupunguza mwendo ili kuepusha ajali.
Licha ya tahadhari hizo, Harvey hakujali kitu. Akili yake ilikuwa ikiwaza jambo moja tu, kumkimbia Dk Lewis. Alipofika kwenye makutano ya Barabara za Dolphin Exyp na Le Jeune, mbele ya Uwanja wa Ndege wa Miami, Harvey alitaka
kuvuka bila kuzingatia taa nyekundu iliyokuwa imewaka, alipofika katikati, alishtukia roli kubwa lililokuwa limebeba mawe likija kwa kasi kubwa ubavuni mwake, kufumba na kufumbua, likaligonga gari la Harvey na kulirusha mita kadhaa pembeni kabla ya kwenda kulipanda juu na kulifanya libondeke kama chapati.
BAADA ya Dk Lewis kugundua kuwa Harvey ndiyo aliyempa mwanaye ujauzito, anapandwa na hasira kuliko kawaida na kujiapiza kuwa lazima ampige risasi na kumtoa roho yake. Anachukua bastola yake na kutoka kwa hasira nyumbani kwake, anamfuata Harvey kwenye kambi ya timu ya Miami Heat.
Baada ya kufika kambini, anagundua amepishana naye ambapo anaambiwa kuwa ameondoka muda mfupi uliopita kuelekea nyumbani kwa Dk Lewis, anageuza gari haraka na kuondoka kwa kasi kuelekea nyumbani kwake kwa lengo la kumuwahi.
Upande wa pili, baada ya kuwasili nyumbani kwa akina Skyler, Harvey anashtushwa sana na mazingira aliyoyakuta. Mama Skyler anampokea juujuu na kuanza kumshambulia kwa kumpa ujauzito Skyler. Dk Lewis
anarudi na kumkuta Harvey ambapo anaanza kumfukuza kwa lengo la kumpiga risasi lakini baadaye Harvey anapatwa na ajali mbaya ya gari baada ya kugongwa na lori lililobeba mawe.
UMATI wa watu ulianza kukimbilia eneo la tukio huku kila mtu akionekana kushtushwa sana na ajali ile ya kutisha iliyosababisha barabara zote zifungwe kwa muda kwani mawe makubwa yalimwagika eneo lote. Askari wa usalama barabarani na wale wa kikosi cha msalaba mwekundu walifika eneo la tukio kujaribu kutoa msaada. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Amekufa? Masikini kijana wa watu? Lakini kwa nini alikuwa anaendesha gari kwa mwendo kasi kiasi hiki?” “Mwenzangu hata mimi sielewi, ametupita kule nyuma kama anashiriki mbio za magari za Formula One, kumbe anakiwahi kifo!” wasamaria wema wawili waliokuwa pembeni ya eneo la tukio walikuwa wakijadiliana wakati polisi wakiendelea kufanya jitihada za kulichomoa gari lake kutoka kwenye uvungu wa lile lori kubwa.
Dk Lewis aliyekuwa akimfukuzia Harvey kwa nyuma, aliposhuhudia ajali mbaya iliyotokea mita chache mbele yake ikilihusisha gari la Harvey, naye alishtuka na kubaki ameduwaa akiwa ni kama haamini kile kilichotokea. Alitambua fika kuwa watu wakigundua kuwa yeye ndiyo aliyekuwa akimfukuza Harvey kwa nyuma na kumsababishia ajali ile, atakuwa na kesi ya mauaji ya kujibu.
Kwa kasi kubwa akaligeuza gari na kuingia barabara ya upande wa pili, akakanyaga mafuta mpaka mwisho na kurudi kule alikotokea huku akitetemeka mwili mzima. Hakuna aliyemhusisha na tukio lile, akaongoza moja kwa moja mpaka nyumbani kwake huku akitweta kwa woga. Baada ya kuhangaika sana, askari wa usalama wa barabarani na wale wa kikosi cha msalaba mwekundu, walifanikiwa kulitoa gari la Harvey kutoka chini ya lile lori, likiwa limebondekabondeka kiasi cha kutotamanika. Kitu cha kwanza ilikuwa ni kuitafuta mashine ya kukatia vyuma ambapo walikata mabati ya lile gari na kuutoa nje mwili wa Harvey ambao ulikuwa hautamaniki.
Damu zilitapakaa eneo lote na kulifanya lionekane kama machinjioni. Mwili ulikuwa umeharibika vibaya sehemu za usoni na kichwani, hali iliyofanya iwe vigumu kwa polisi kuutambua. Gari la msalaba mwekundu liliwasili ambapo mwili ule uliingizwa na kupelekwa hadi katika Hospitali ya Coral Gables iliyokuwa jirani na eneo la tukio.
Wakati mwili wa Harvey ukipelekwa hospitali, maafisa wa polisi walikuwa wakiendelea na kazi ya kulivuta lile lori na kulitoa barabarani sambamba na kufanya kazi ya kuyakusanya mawe makubwa yaliyokuwa yametapakaa eneo lote la ajali. Baada ya kuhangaika sana, hatimaye walifanikiwa kulitoa lile lori, barabara zikafunguliwa tena na shughuli zikaendelea kama kawaida. *** “Vipi mume wangu? Uliondoka ukiwa umechanganyikiwa lakini naona umerudi ukiwa umechanganyikiwa zaidi, nini tatizo?” “Mke wangu hebu niache kwanza, kichwa changu hakipo sawa kabisa.” “Najua mume wangu, mwanao naye anatishia kuwa endapo jambo lolote baya litampata Harvey atajinyonga au kunywa sumu.” “Achana naye mshenzi sana huyo mtoto, anazidi kutusababishia matatizo tu hapa nyumbani,” alisema Dk Lewis huku akipitiliza
kujitupa kitandani kwake. Mkewe alimfuata lakini aligundua kuwa hayupo sawa. Alikuwa akitetemeka sana mwili mzima, jambo lililozidi kumtia wasiwasi mkewe.
Kichwani mwake alihisi huenda mumewe amempiga risasi Harvey kama alivyojiapiza muda mfupi uliopita, akaichukua bastola ya mumewe na kuikagua lakini haikuonesha dalili za kutoka kutumika muda mfupi uliopita, akawa anazidi kujiuliza kilichomfanya mumewe awe katika hali ile.
“Kwani kuna nini mume wangu? Mimi ndiyo mtu pekee unayeweza kuniambia siri zako na nikazitunza, hata kama Harvey amepatwa na jambo baya we niambie tu,” alisema mama Skyler kwa sauti ya kubembeleza, Dk Lewis akawa anajiumauma tu. Baada ya kumbana sana, hatimaye aliamua kumueleza mkewe kila kilichotokea mpaka ajali mbaya aliyoipata Harvey, jambo
lililomshtua sana mama Skyler. “Whaaat? Harvey amapata ajali? Mungu wangu.” “Usiseme kwa sauti mke wangu na wala usimwambie mwanao kwani siri hii ikivuja na ikabainika kuwa mimi ndiyo niliyekuwa namfukuza, nitakabiliwa na kesi ya mauaji.” “Jamani mume wangu, roho inaniuma sana! Amepona kweli?” “Sielewi chochote mke wangu lakini ni ajali mbaya sana.” “Basi twende tukatoe taarifa polisi.” “Hivi una akili kweli mke wangu? Kwa hiyo unafurahia mumeo nikafungwe kwa kosa la mauaji?” “Sasa tutafanya nini mume wangu?” alihoji mama Skyler huku akianza kutiririkwa na machozi kwenye mashavu yake. Japokuwa Harvey alikuwa amewafanyia kitendo kibaya sana, bado aliona hakustahili kufa kikatili namna ile. “Nimeshakwambia usimwambie mtu yeyote kuhusu suala hili, hata huyo mwanao hatakiwi kujua chochote kwa sasa,” alisema Dk
Lewis na kugeukia upande wa pili kuonesha kuwa hakutaka mazungumzo yale yaendelee. Mama Skyler alijikuta akiishiwa na nguvu kabisa, akakaa pembezoni mwa kitanda na kujishika tama, akazama kwenye dimbwi kubwa la mawazo na kushindwa kujua nini cha kufanya.
Skyler baada ya kumuona baba yake amerejea nyumbani, aliamini lazima alishindwa kumpata Harvey hivyo kuamua kumsamehe. Hakutaka kumuuliza kitu chochote akiogopa kuamsha upya hasira zake ambazo sasa zilionekana kutulia.
Siku ya kwanza ilipita, ikawadia ya pili na hatimaye ikafika siku ya tatu tangu kutokea kwa ajali ile. Si Dk Lewis wala mkewe aliyekuwa anafahamu nini kilichoendelea kwa Harvey, hali ilikuwa mbaya zaidi kwa Skyler ambaye karibu kila siku alikuwa akihangaika kumpigia simu bila mafanikio.
Wakati akihangaika na simu, mama yake alikuwa akimwangalia kwa huruma bila kumwambia kitu chochote. Akawa anatamani kumwambia kilichotokea lakini kila alipokumbuka maneno ya mumewe, akawa anajitahidi kuificha siri.
“Mama mbona unaniangalia halafu unatoka na machozi? Au kuna kitu kingine kinachokuliza?” aliuliza Skyler, mama yake akajaribu kuuficha ukweli na kukimbilia chumbani kwake.
Skyler alihisi lazima kuna jambo zito ambalo mama yake anamficha, akamfuata chumbani kwake na kuanza kumbembeleza kama kuna tatizo lolote basi amweleze. “Hakuna tatizo lolote mwanangu.”
“Hapana mama, sijawahi kukuona ukiwa na hali kama hiyo hata siku moja, lazima kuna kitu unanificha, halafu mbona baba siku mbili hizi simuelewi?” alisema Skyler huku naye akianza kulengwalengwa na machozi.
Baada ya kumuona mwanaye anaanza kulia, mama Skyler alipiga moyo konde na kuamua kumweleza mwanaye kila kitu, lakini akamsisitiza kutoonesha dalili yoyote kuwa anaujua ukweli. “Niniiiiii? Hapana mama haiwezekani!
YAMETIMIA kwa Harvey, kijana mwenye asili ya nchini Liberia ambaye dhambi ya kuvunja amri ya sita na mtoto wa Dk Lewis aliyempokea na kumpa hifadhi nchini Marekani, imekomaa na sasa inamsababishia mauti. Baada ya Dk Lewis kugundua kuwa Harvey ndiyo aliyempa mwanaye ujauzito, anaanza kumsaka kwa udi na uvumba akitaka kumuua. Wakiwa wanafukuzana kwenye magari, Harvey anajikuta akivunja sheria za barabarani na kugongwa na lori kubwa lililokuwa limebeba mawe, jirani na Uwanja wa Ndege wa Miami. Gari lake linaharibika vibaya.
“Niniiiiii? Hapana mama haiwezekani, nasema haiwezekanii,” alipiga kelele Skyler baada ya kuambiwa Harvey amepata ajali mbaya, akatoka chumbani kwa mama yake hadi sebuleni, akawa anazunguka huku na kule akiwa ni kama haamini kile alichokisikia kutoka kwa mama yake. Mama Skyler alipomuona mwanaye amechanganyikiwa, alimuita na kuanza kumtuliza lakini haikusaidia kitu. “Lazima baba ndiyo atakuwa amemuua na kwenda kumtupa barabarani,” alisema Skyler huku akianza kuangua kilio cha
huzuni. Mama yake alimbishia na kumweleza kuwa baba yake hawezi kuwa katili kiasi kile. Akasisitiza kuwa hata bastola yake aliikagua aliporejea lakini hakugundua kitu.
“Hapana mama siyo kweli, unamtetea baba, maskini Harvey wangu, nitamlea mwanangu na nani?” alisema Skyler na kukimbilia chumbani kwake ambapo alijifungia mlango kwa ndani na kuendelea kuomboleza. Hata hivyo, bado alikuwa hataki kuamini kama kweli alichokisikia kutoka kwa mama yake kimetokea kweli.
Kwa kuwa alikuwa na namba ya simu ya rafiki yake Harvey aitwaye Cazzard, aliona njia pekee ya kuthibitisha kile alichokisema mama yake ni kumpigia simu, ambapo alipomuuliza kama amemuona Harvey au ana taarifa zake, alimjibu kuwa hajafika chuoni kwa siku tatu na kwamba hana taarifa zozote zinazomhusu.
Skyler alizidi kuangua kilio, akatoka chumbani kwake mbiombio na kuanza kukimbilia nje. Mama yake alipomuona, alijaribu kumzuia lakini haikusaidia kitu, akatoka hadi barabarani na kuanza kuongea mwenyewe kama mwendawazimu.
Akiwa pale nje, alisimamisha taxi na kumwelekeza dereva ampeleke chuoni kwa akina Harvey, akawa bado haamini kama kile alichokisikia ni kweli, akilini mwake akahisi huenda mama yake alimwambia vile kwa lengo la kuuvunja uhusiano wao wa kimapenzi. “Siamini kabisa mpaka nikahakikishe mwenyewe,” alisema Skyler akiwa ndani ya taxi, dereva akageuka kumwangalia na kumuuliza kama alikuwa na tatizo, akatingisha kichwa kisha safari ikaendelea.
Baada ya takribani dakika ishirini, waliwasili chuoni pale, akamlipa dereva fedha yake na kuteremka, akawa anatembea harakaharaka kuelekea upande zilipokuwa hosteli za wavulana ambapo alimkuta rafiki mkubwa wa Harvey, Cazzard akiwa anafua. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Tafadhali Cazzard niambie ukweli, Harvey yuko wapi?” alisema Skyler huku akianza kuangua kilio, hali ile ilimshangaza sana Cazzard, akaacha kila alichokuwa anakifanya na kumsogelea Skyler. “Kwani kumetokea nini? Mbona sielewi?” “Harvey! Namtaka Harvey,” alisema Skyler huku akizidi kuangua kilio, ilibidi aanze kumbembeleza ambapo alipotulia, alimweleza ukweli wa kila kitu kilichotokea nyumbani kwao mpaka Harvey akatoweka na taarifa alizopewa na mama yake. “Basi tulia shemeji yangu, hapa cha kufanya twende kwanza makao makuu ya Timu ya Miami Heat, naamini kule ndiyo tutapata majibu kamili kwa sababu mara ya mwisho alikuwa kule, nyamaza kila kitu kitakuwa sawa,” alisema Cazzard wakati akimbembeleza Skyler.
Haraka haraka walitoka na Skyler mpaka nje ya geti la shule na kukodi taxi nyingine iliyowapeleka moja kwa moja mpaka kwenye jengo la British Airways Arena, mahali yalipokuwa makao makuu ya timu ya mpira wa kikapu ya Miami Heat aliyokuwa anaichezea Harvey.
Walipofika waliomba kuonana na uongozi wa timu ile, wakaelekezwa kwenye ofisi ya meneja wa timu ambapo Cazzard alieleza kilichowapeleka pale. Meneja wa timu alipiga simu haraka na kuagiza kepteni wa timu, Lebron James aende haraka ofisini kwake, alipofika jambo la kwanza aliloulizwa ni kama ana taarifa zozote zinazomhusu Harvey.
“Aliondoka juzi jioni na kuniaga kuwa anaenda kuwasalimia wazazi wake nyumbani kwao, baada ya hapo hajarejea tena kambini na kila ninapopiga simu yake ya mkononi haipatikani,” alisema Lebron.
“Hawa wageni unaowaona hapa mbele yako ni ndugu zake na wanasema hayupo nyumbani kwao wala chuoni, inawezekana amepatwa na tatizo, hebu tufuatilie haraka,” alisema meneja wa timu ile, wakaanza kupiga simu kwenye vituo vya polisi na hospitali zote za Miami kuulizia taarifa zake.
“Kuna mtu alipata ajali juzi kwenye makutano ya Barabara za Dolphin Exyp na Le Jeune, alipelekwa kwenye Hospitali ya Coral Gables, fuatilieni kama mnaweza kumtambua, gari lake limeharibika vibaya na limehifadhiwa kwenye kituo cha polisi cha uwanja wa ndege,” Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Miami, Hector Bauer alisema kwa msisitizo.
Kwa kuwa meneja alikuwa ameiweka simu ‘loud speaker’, wote walisikia vizuri alichokisema, Skyler akajaribu kuunganisha maelezo yale na aliyoambiwa na mama yake, akazidi kuangua kilio. “Binti huna haja ya kulia, nendeni kwanza mkamuangalie kama ni yeye, hutakiwi kukata tamaa,” alisema meneja yule, harakaharaka
Cazzard, Lebron na Skyler wakatoka nje ya ofisi ile na kuelekea sehemu ya maegesho ya magari ambapo Lebron aliwaambia kuwa yupo tayari kuwasindikiza mpaka eneo la tukio kwa kutumia gari lake.
Wote watatu wakaingia ndani ya gari na safari ya kuelekea kwenye kituo cha polisi cha Uwanja wa Ndege wa Miami kisha Hospitali ya Coral Gables ikaanza. Kutokana na umbali uliokuwepo, iliwachukua zaidi ya dakika arobaini kufika kwenye kituo hicho cha polisi ambapo jambo la kwanza walitaka kwanza wakalione gari lililopata ajali.
Baada ya kujitambulisha na kueleza kilichowapeleka kituoni pale, askari mmoja alitoka na kuwapeleka mahali ambapo magari yaliyopata ajali huwa yanahifadhiwa. Yule askari aliongoza moja kwa moja mpaka kwenye gari lililokuwa limeharibika vibaya na kuwaeleza kuwa lile ndiyo lililopata ajali siku mbili zilizopita kwenye makutano ya Barabara za Dolphin Exyp na Le Jeune.
“Oooh! Mungu wangu, Harvey… Harvey jamani! Hili ndiyo gari lake,” Skyler alipiga kelele kwa nguvu huku akikimbilia pale lile gari lilipokuwa limehifadhiwa, hakuweza kufika kwani ghafla alianza kuhisi kizunguzungu kikali, akapepesuka na kutaka kuanguka, Cazzard na Lebron wakawahi kumdaka na kumlaza chini. Akapoteza fahamu kwa muda.
Cazard na Lebron nao walikuwa ni kama wamepigwa na butwaa kwani kweli lile gari walilokuwa wanaliona mbele yao ndiyo alilokuwa anaendesha Harvey, wakatazamana wakiwa ni kama hawaamini kilichotokea. Hata hivyo ilibidi wajikaze kiume na kusaidiana kumbeba Skyler mpaka ndani ya gari la Lebron, wakamuingiza na kuondoka eneo lile kuelekea kwenye Hospitali ya Coral Gables.
Wakiwa njiani, Skyler alizinduka na kurejewa na fahamu zake, akawa anapiga kelele kwa nguvu akitaka apelekwe akamuone Harvey wake. Cazzard alimtuliza na kumwambia kuwa inabidi ajikaze kwani walikuwa wamekaribia kufika kwenye hospitali aliyopelekwa baada ya kupata ajali. Dakika kadhaa baadaye, gari lao lilipaki kwenye maegesho ya magari ya hospitali ile.
Wakateremka harakaharaka na kumsaidia Skyler kuteremka garini kwani hakuwa na nguvu za kusimama mwenyewe, wakamshika huku na kule na kuanza kutembea kuelekea sehemu ya mapokezi ambapo walipofika walijitambulisha na kueleza kilichowapeleka eneo lile. Kwa muda wote huo Skyler alikuwa akiomboleza kwa uchungu akiwa ni kama asiyeamini kilichotokea.
Mhudumu wa afya waliyemkuta, aliwaeleza kuwa mhusika alifariki eneo la ajali na kwamba mwili wake ulikaa hospitalini pale kwa siku tatu bila kutambuliwa na ndugu zake, jambo lililowalazimu waende kuuzika asubuhi ya siku ile. Kusikia vile, Skyler alipiga
mayowe kwa nguvu, akadondoka chini kama mzigo na kuanza kutokwa na povu mdomoni na puani kabla ya kupoteza fahamu kwa mara nyingine.
Baada ya Dk Lewis kugundua kuwa Harvey ndiyo aliyempa mwanaye ujauzito, anaanza kumsaka kwa udi na uvumba akitaka kumuua. Wakiwa wanafukuzana kwenye magari, Harvey anajikuta akivunja sheria za barabarani na kugongwa na lori kubwa lililokuwa limebeba mawe, jirani na Uwanja wa Ndege wa Miami. Gari lake linaharibika vibaya.
TAARIFA za kifo cha Harvey zilianza kusambaa kwa kasi, mamia ya wanafunzi cha Chuo cha Miami Polytechnic and Engineering College, wachezaji na mashabiki wa Timu ya Miami Heats wakaanza kumiminika kwa wingi kwenye Hospitali ya Coral Gables, kila mmoja akiwa haamini kama taarifa zile zilikuwa za kweli.
“Mnamzungumzia Harvey huyu ninayemfahamu mimi au yupi?” “Harvey mcheza basketball, huyo huyo unayemfahamu,kwani kuna Harvey gani mwingine.” “Noo! Haiwezekani kijana mzuri mwenye kipaji cha hali ya juu kama yule akafa kirahisi namna hiyo.” “Hutakiwi kubisha sana Beatrice, nani awezaye kuipinga kazi ya Mungu?” “Twendeni tukawaulize vizuri wale madaktari.” “Hakuna haja, majibu waliyoyatoa mara ya kwanza ndiyo hayohayo, wamesema hawatakuwa tayari kuzungumzia jambo lolote kwa sababu suala
hilo lipo kwenye mikono ya uongozi wa hospitali hiyo na idara ya polisi ya Home Security na LADP,” watu walikuwa wakibishana na kueleweshana nje ya Hospitali ya Coral Gables, wakawafuata tena madaktari na kuanza kuwahoji kwa jazba.
“Tutaaminije kama kweli amekufa na mmemzika bila kutuonesha kidhibiti chochote?” “Inatakiwa muamini tu kwani huo ndiyo ukweli na hakuna anayeweza kuubadilisha.” “Hakuna kitu kama hicho, katuonesheni kaburi lake.”
“Hospitali yetu haina utaratibu huo kwa sababu ndugu wakishashindwa kuja kuutambua mwili wa marehemu kwa muda wa saa 72 ambazo ni siku tatu, huwa tunachukua uamuzi wa kumzika katika makaburi maalum ambayo yapo kwenye karantini ya kuzuia watu wa kawaida wasiyasogelee bila kuwa na tahadhari za kiafya.”
“Lakini kwa nini hamkutangaza kwenye vyombo vya habari? Yaani kweli watu walishindwa kumtambua mtu maarufu kama Harvey? Nani asiyemjua hapa Miami? Lazima una kitu kinafichwa hapa. Kwa nini haya yote yatokee?”
“Kijana hayo maswali yako anayeweza kuyajibu ni msemaji wa Hospitali ya Coral Gables, kwa hiyo kama unataka maelezo zaidi kaonane na uongozi wa hospitali, acha sisi tufanye kazi yetu, huoni kama tuna wagonjwa wengine wanaohitaji huduma yetu?” Malumbano yaliendelea, wanafunzi wa Miami Polytechnic wakaendelea kupandishiana na madaktari wa hospitali ile, hakuna aliyekuwa tayari CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ kuamini kama kweli aliyekufa ni Harvey, kila mmoja akawa anataka kuoneshwa ushahidi, jambo ambalo lilikuwa gumu. Skyler alikuwa hajitambui, akawa amelazwa ndani ya wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum wa madaktari tangu alipozimia alipopewa taarifa za uthibitisho wa kifo cha Harvey. Wakati umati wa watu ukiendelea kujazana mbele ya hospitali hiyo, Skyler alikuwa wodini madaktari wakihangaika kumsaidia. *** “Mke wangu, huyo mwanao Skyler mpaka muda huu yuko wapi? Kwa nini amechelewa kurudi nyumbani namna hii?” “Nilipompa taarifa za ukweli wa kilichompata Harvey, alitoka akiwa amechanganyikiwa sana, nikashindwa kumzuia kwani alikuwa akikimbia kutoka nje. Hataki kuamini kama kweli umesababisha kifo cha Harvey.” “Tuachane na hayo, yeye bado ni mtoto wetu na tuna wajibu wa kumlinda na kuhakikisha yupo salama kwenye mikono yetu bila kujali hali aliyonayo.”
“Ungekuwa unayajua hayo, ungetumia busara tangu mwanzo na wala haya yote yasingetokea. Kibaya zaidi hukutaka kumweleza ukweli wewe mwenyewe, unafikiri atakuelewaje? Si anakuona muuaji hatari?” “Huu siyo muda wa kunilaumu mke wangu, damu ya Harvey ipo mikononi mwangu na sijui nini kitanipata.” “Nataka uende ukamtafute mwenyewe kwani siku zote tatizo moja huzaa lingine, la kwanza la Harvey limetokea na sasa hatujui Skyler yupo wapi. Ondoka kamtafute mwanangu,” alisema mama Skyler kwa hasira na uchungu, Dk Lewis akabaki amejiinamia pembeni ya kitanda akiwa ameshika tama.
Sasa akili zake zilikuwa zikifanya kazi vizuri na haikumuwia rahisi kuamini kuwa yeye ndiye aliyesababisha kifo cha Harvey. Kila kilichokuwa kinatokea alikuwa akikifananisha na ndoto za mchana ambazo aliamini muda si mrefu zitaisha.
Picha za tukio la ajali zikawa zinajirudia kichwani mwake mara kwa mara na kumfanya muda wote awe anaweweseka mwenyewe. “Nooo! Nooo! Harvey don’t go!” (Hapanaaa! Hapanaaa! Harvey usiende?” mwangwi wa sauti yake aliyoitoa muda mfupi baada ya ajali ile, ulikuwa ukijirudia kichwani mwake kama mkanda wa video, aliendelea kuteseka ndani kwa ndani kwa saa nyingi mfululizo.
“Nimefanya makosa makubwa sana, sijui kama Mungu wangu atakuja kunisamehe, kwa nini lakini?” alijiuliza Dk Lewis huku akianza kubanwa na kilio cha kwikwi, mke wake ambaye hakutaka hata kumuangalia usoni, naye alizidi kuumizwa na hali ile, nyumba nzima ikazizima kwa huzuni.”
“Wewe ndiyo baba wa familia, badala ya kujenga nyumba yako unaibomoa kwa mikono yako mwenyewe, unadhani nani atakuelewa? Wewe ni mwanaume wa aina gani?”
“Nisamehe mke wangu na nakuomba katika kipindi hiki kigumu uwe na mimi, uliniahidi kuwa watu wote watakaposhindwa kuwa na mimi, wewe pekee ndiye utakuwa pembeni yangu, mbona huoneshi hivyo?”
“Hapana mume wangu, siwezi kuwa na wewe kirahisi namna hii wakati umefanya dhambi kubwa ya kukatisha uhai wa binadamu mwenzio, tena kijana ambaye wewe mwenyewe ulimuokota akiwa katika hali mbaya na kumkuza mpaka hapa alipofikia.”
“Kwa hiyo na wewe mke wangu unashiriki kunikandamiza, unataka na mimi nife?” “Siyo hivyo mume wangu.”
Wakiwa wanaendelea kuzungumza, simu ya mkononi ya mama Skyler iliita mfululizo, alipotazama kwenye kioo, ilikuwa ni namba ngeni. Alipopokea akapewa taarifa kuwa Skyler amepoteza fahamu na amelazwa kwenyeHospitali ya Coral Gables.
HAKUNA marefu yasiyo na ncha, Harvey, kijana mwenye asili ya nchini Liberia anaonja umauti baada ya dhambi ya kuvunja amri ya sita na mtoto wa Dk Lewis aliyempokea na kumpa hifadhi nchini Marekani, kukomaa.
Baada ya Dk Lewis kugundua kuwa Harvey ndiyo aliyempa mwanaye ujauzito, anaanza kumsaka kwa udi na uvumba akitaka kumuua na kwa bahati mbaya, Harvey anapata ajali wakati akimkimbia Dk Lewis.
Ajali hiyo mbaya inayagharimu maisha yake ambapo mwili wake unatolewa ukiwa umeharibika vibaya na kupelekwa kwenye Hospitali ya Coral Gables ambapo baada ya siku tatu unazikwa kwenye makaburi ya
hospitali baada ya ndugu zake kushindwa kufika kuutambua. Skyler anapoteza fahamu baada ya kuhakikisha kuwa ni kweli Harvey amekufa.
HARAKAHARAKA mama Skyler na mumewe walianza kujiandaa tayari kwa safari ye kuelekea Hospitali ya Coral Gables kumuangalia mtoto wao. Wakiwa tayari wameshajiandaa, ghafla Dk Lewis alibadilisha uamuzi na kumtaka mkewe aende mwenyewe.
“We nenda tu mke wangu, mimi kwa hali niliyonayo siwezi kutoka humu ndani, niache tu,?” alisema Dk Lewis huku akionekana kujutia sana kitendo alichokifanya ambacho ndicho kilichoyakatisha maisha ya Harvey. “Lakini kwa nini unakuwa hivyo mume wangu? Unapenda kuendelea kuniona nikilia?” “Hapana mke wangu lakini ndiyo hivyo nimeshakwambia.”
“Unakosea sana mume wangu, kwa hiyo dhambi moja iendelee kuzaa dhambi nyingine? Skyler si mwanao? Kwa nini unakuwa katili kiasi hicho,” alisema mama Skyler lakini Dk Lewis aliendelea kushikilia msimamo wake. Mama Skyler alipoona mumewe anaendelea kushikilia msimamo wake, aliamua kumuacha.
Akatoka hadi nje ambapo aliingia ndani ya gari na safari ya kuelekea Coral Gables ikaanza mara moja. Njia nzima mama Skyler alikuwa akiteswa na mawazo machungu ndani ya kichwa chake. Japokuwa Harvey alikuwa na makosa, lakini alijiambia
mwenyewe kuwa hakustahili adhabu kali kiasi kile. Kimoyomoyo akawa anamuomba Mungu mwanaye Skyler naye asije akaamua kujidhuru kama alivyokuwa ameahidi.
Safari haikuwa nyepesi, baada ya kuendesha gari kwa muda mrefu, hatimaye mama Skyler aliwasili kwenye Hospitali ya Coral Gables na kushtushwa na umati wa vijana wa kiume na wa kike waliokuwa wamejaa nje ya hospitali ile. Alipowatazama, alitambua
fika kuwa walikuwa ni wanachuo waliokuwa wanasoma na marehemu Harvey na wachezaji wenzake wa Miami Heat, akazidi kujisikia uchungu kiasi cha kuanza kutokwa na machozi upya.
Baada ya baadhi ya watu waliokuwa pale nje kumtambua mama Skyler, walianza kuangua vilio huku wengine wakimpa pole kwa kuondokewa na mwanaye, Harvey. Mama Skyler alizidiwa na huzuni lakini akajitahidi kujikaza, akaenda moja kwa moja mpaka sehemu ya maulizo pale hospitali na kujitambulisha.
Alipewa maelezo yaleyale kama waliyopewa watu wote waliokuwa wanaulizia habari za kilichomkuta Harvey. Akaomba kwenda kumuona mwanaye Skyler ambapo alielekezwa wodi aliyokuwa amelazwa huku akiendelea kupatiwa huduma kwa karibu.
Alipoingia wodini, mama Skyler alizidi kububujikwa na machozi kutokana na hali aliyomkuta nayo mwanaye huku madaktari wakiendelea kumhudumia. Alipewa muda mfupi wa kumuona ambapo bado alikuwa hajarejewa na fahamu zake, baada ya hapo akaambiwa akamsubiri nje ili madaktari wapate nafasi ya kufanya kazi yao.
“Yaani baba Skyler na wewe daktari mzima unakubali Harvey azikwe kienyeji namna hii? Hebu fanya jambo uwapunguze watu majonzi, ungekuja kuona hali ilivyo hapa sijui ungejisikiaje?” alisema mama Skyler huku akilia kwenye simu wakati akizungumza na mumewe.
Kutokana na jinsi mkewe alivyokuwa anazungumza kwa uchungu, Dk Lewis aliamua kufanya jambo ili angalau mwili wa Harvey, japokuwa tayari ulishakuwa umezikwa, ufukuliwe na kupewa heshima zote zinazostahili. Aliamka kinyonge pale kitandani alipokuwa amelala na kwenda kuvaa nguo zake za kazini, akatoka na kuelekea kwenye Hospitali ya Miami aliyokuwa anafanyia kazi.
Alipofika alimweleza daktari mkuu wa hospitali ile hali halisi ya kilichotokea ingawa hakutaka kabisa kueleza namna alivyohusika na kifo kile, akamuomba amuandikie kibali maalum cha kwenda kuufukua mwili wa Harvey kutoka kwenye makaburi ya Hospitali ya Coral Gables kisha uhifadhiwe hospitali pale wakati taratibu za mazishi zikipangwa upya.
Alimweleza umuhimu wa kufanya vile kwani kulikuwa na utata mkubwa kuhusu kifo chake, wengi wakiamini aliyefariki hakuwa yeye, akataka watu wote wapate japo nafasi ya kwenda kuuaga mwili huo na kutoa salamu za mwisho.
Daktari mkuu alimkubalia, akaandika hati maalum kwenda Hospitali ya Coral Gables na kumpa gari moja la kubebea maiti sambamba na watu wanne wa kuifanya kazi ile kitaalam. Harakaharaka wakaondoka na kuelekea mahali ilipokuwa hospitali ile. Wakiwa jirani kufika, Dk Lewis alishtushwa na umati wa watu uliokuwa nje ya hospitali ile, akaelewa kwa nini mkewe alimwambia vile. Gari likaingizwa mpaka sehemu maalum ya maegesho ambapo Dk Lewis na wale watu waliteremka na kwenda kuonana na daktari mkuu wa hospitali ile. Alipooneshwa hati ile maalum, naye alitoa wafanyakazi wanne ambao waliungana na wale wengine, wakaenda kuufukua mwili wa Harvey na kuurudisha katika jokofu lililokuwa ndani ya chumba cha maiti cha hospitali ile.
Kwa kuwa haukuwa umekaa muda mrefu ndani ya kaburi lile, bado ulikuwa haujaanza kuharibika, ukasafishwa tena kwa dawa maalum za kuzuia maiti isiharibike (embalm) kisha ukaingizwa ndani ya gari maalum la kubebea maiti tayari kwa safari ya kuelekea CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ kwenye Hospitali ya Miami kwa ajili ya kuhifadhiwa kwenye mazingira bora zaidi. “Jamani naomba tusikilizane, kama mlivyoshuhudia wenyewe wazazi wa Harvey nao hawakuwa na taarifa ya kilichotokea na baada ya kuugundua ukweli, wamefanya taratibu zinazostahili kupongezwa.
“Mwili umefukuliwa kutoka kwenye makaburi ya hospitali hii na sasa umepelekwa kwenye hospitali kubwa kwa ajili ya kuhifadhiwa kisha kuzikwa kwa heshima zote.
“Msiba utakuwa nyumbani kwa Dk Lewis, Miami, twendeni tukashiriki kumuaga mpendwa wetu Harvey. Kwa sasa wote tunaombwa kuondoka hapa hospitalini na kutawanyika,” alisema Cazzard kwa niaba ya familia ya Dk Lewis nje ya hospitali ile. Eneo zima lilizizima kwa huzuni ya hali ya juu.
Muda mfupi baada ya watu wote kuondoka hospitalini pale na maiti ya Harvey kuhamishiwa Hospitali ya Miami, Skyler alirejewa na fahamu zake na kuanza upya kuomboleza. Mama yake ambaye kwa muda wote bado alikuwa pembeni ya kitanda cha mwanaye, alianza kumbembeleza na kumweleza kuwa mwili wa Harvey ulifukuliwa na kupelekwa hospitali kuhifadhiwa ili azikwe upya kwa heshima zote.
Baada ya madaktari kuridhishwa na hali ya afya ya Skyler, walimruhusu mama yake kuondoka naye, wakatoka mpaka sehemu ya maegesho, mahali mama Skyler alipokuwa ameacha gari lake, akamsaidia mwanaye kuingia ambapo waliondoka na kurejea nyumbani kwao kuendelea na msiba wa Harvey.
Walipofika walikuta tayari umati wa watu umeanza kuwasili nyumbani pale, taratibu za kawaida za msiba zikaendelea ambapo maelfu ya watu kutoka sehemu mbalimbali walifika kuhakikisha kama kweli Harvey ameaga dunia. Taratibu za mazishi ziliendelea kama kawaida huku suala la uhusika wa Dk Lewis kwenye kifo cha Harvey likibaki kuwa siri ya wanafamilia wenyewe.
Kesho yake mwili wa Harvey ukatolewa na kupelekwa nyumbani ambapo uliagwa na maelfu ya waombolezaji kisha safari ya kuelekea kwenye makaburi ya watu mashuhuri ya Miami Graveyards ikaanza. Umati mkubwa wa watu waliohudhuria kwenye mazishi yale ulitosha kuthibitisha jinsi Harvey alivyokuwa akikubalika mbele ya jamii.
Vyombo karibu vyote vya habari nchini Marekani viliripoti habari ile, nchi nzima ikazizima kwa simanzi wakati jeneza la kisasa lililokuwa na mwili wa Harvey likiingizwa kaburini. Huo ndiyo ukawa maisha ya Harvey hapa duniani.
“Sitaki kuendelea kukaa hapa, nataka kwenda sehemu ya mbali ambapo hakuna atakayejua mahali nilipo mpaka kumbukumbu za kuhuzunisha zitakapoisha ndani ya kichwa changu, sitaki mtu yeyote anitafute,” alisema Skyler kwa uchungu, mama yake akawa anamtaka abadilishe uamuzi wake.
MAISHA ya Harvey, kijana mwenye asili ya nchini Liberia ambaye nyota yake ilikuwa inang’ara sana kutokana na kipaji kikubwa cha kucheza mpira wa kikapu alichojaaliwa na Mungu wake, yanafikia tamati baada ya kupata ajali mbaya ya gari wakati akimkimbia baba yake Skyler kutokana na kesi ya kumjaza ujauzito binti yake.
Kifo hicho kinawashtua watu wengi, awali wanakuwa hawaamini na kudhani aliyekufa siyo Harvey lakini baada ya mwili wake kufukuliwa na kuzikwa kwa mara ya pili kwa heshima zote, watu ndiyo wanaamini. Msiba unaitingisha Marekani kwani umaarufu wake ndiyo kwanza ulikuwa umeanza kukolea kwenye medani ya mpira wa kikapu.
Hatimaye Harvey anazikwa kwa majonzi makubwa huku siri ya kifo chake ikibakia kwa watu watatu tu, baba Skyler, mkewe na binti yake. Kufuatia tukio hilo, Skyler anaanza kumchukia sana baba yake na anajiapiza kuodoka nyubani kwao na kwenda kuishi mbali naye.
SKYLER aliondoka nyumbani kwao kama alivyokuwa, hakuchukua kitu chochote zaidi ya nguo alizokuwa amezivaa. Fedha na utajiri wote wa wazazi wake havikuwa na maana yoyote kwake. Aliamini baada ya kumpoteza Harvey, kila kitu katika maisha yake kilipoteza maana, akawa anamlaani baba yake kwani aliamini bila yeye, yale yote yasingetokea.
“Ni bora na mimi nife, siwezi kuendelea kuishi bila Harvey, naichukia dunia nzima,” alisema Skyler huku akitembea pembeni ya barabara, mbali kabisa na nyumbani kwao. Hakuwa anaelewa alikokuwa anaelekea, kitu pekee alichokuwa anakitaka ilikuwa ni kuishi mbali na wazazi wake.
Baada ya kutembea kwa umbali mrefu, Skyler alianza kuhisi uchovu wa hali ya juu, miguu yake nayo ilianza kuvimba, akawa hana namna zaidi ya kutafuta sehemu ya kupumzika. Alienda kukaa chini ya mti mkubwa uliokuwa mita kadhaa kutoka barabarani. Alivua kitenge kimoja alichokuwa amekivaa kuficha tumbo lake ambalo sasa lilianza kuwa kubwa, akatandika chini na kujilaza.
Mawazo mengi yakawa yanaendelea kupita ndani ya kichwa chake na kumfanya muda wote awe anabubujikwa na machozi. “Nimekukosea nini Mungu mpaka umchukue kipenzi changu Harvey wakati bado namhitaji? Nitaishi na nani mimi,” alisema Skyler huku akizidi kuomboleza, muda mfupi baadaye usingizi mzito ukampitia akiwa palepale chini ya mti.
Alipokuja kuzinduka, tayari ilikuwa ni jioni, jua likawa limeshaanza kuzama. Skyer alijishangaa kwajinsi alivyoweza kulala saa nyingi katika eneo kama lile, aliamka na kujiegemeza kwenye mti, akawa anaendelea kuwaza.
“Haya ndiyo yatakuwa makazi yangu kwa siku zote, sitaki kuishi jirani na binadamu yeyote,” alisema Skyler, akaendelea kukaa pale kwa muda mrefu mpaka giza lilipoanza kuingia. Japokuwa wadudu kama mbu na papasi walikuwa wakimng’ata mara kwa mara, hakujali kitu, akajilaza na kujifunika mwili mzima kwa kutumia kitenge, akalala.
Dk Lewis na mkewe walianza kulumbana baada ya kuona muda unazidi kwenda bila Skyler kurejea. “Ulianzaje kumruhusu aondoke wakati unaona hali yake siyo nzuri?” “Sasa mimi ningefanya nini mume wangu? Nilijaribu kumzuia lakini haikusaida kitu.” “Sasa ndiyo utakapoelewa kwamba umefanya uzembe wa hali ya juu, yule ni mwanao na wewe ndiye uliyemtoa tumboni kwako, iweje useme umeshindwa kumzuia?”
“Mume wangu huu siyo muda wa kuanza kulaumiana, hata ungekuwa ni wewe angekushinda, hujui kwamba kwa sasa anatuchukia sana kwa kuona kwamba wewe ndiyo chanzo cha matatizo yote haya?” “Hayo yameshapita mke wangu, hakuna kinachoweza kumrejesha tena Harvey duniani, hapa cha msingi ni kuhakikisha binti yetu
anatulia katika kipindi hiki cha ujauzito wake. Twende kumtafuta,” alisema Dk Lewis, wakatoka na mkewe jioni hiyo na kuanza kumtafuta Skyer katika sehemu zozote ambazo walihisi anaweza kuwepo. Walijaribu kuzunguka kwa marafiki zake wote walikodhani anaweza kuwepo lakini waliambulia patupu, ikabidi wakatoe taarifa kituo cha polisi na kuanza kuzunguka kwenye hospitali mbalimbali. Mpaka kunapambazuka, bado Skyler hakuwa amepatikana.
Kesho yake alfajiri na mapema, Dk Lewis na mkewe walianza tena kazi ya kumtafuta binti yao, walizunguka mitaa mingi bila mafanikio, saa zikawa zinazidi kuyoyoma bila kupata habari zozote za kuwatia matumaini. Jioni ilipoanza kuingia, Dk Lewis na mkewe, wakazidi kuchanganyikiwa, wakajiapiza kuwa siku hiyo hawatalala mpaka kunapambazuka ilimradi binti yao apatikane.
“Kuna binti mdogo ameonekana kwenye dampo la Miami County Sanitation, Barabara ya 2200 N. County, 25-A, Troy, tunajaribu kumhoji lakini hasemi chochote, fikeni kwenye kituo cha polisi cha kati haraka kuja kumtambua,” simu ilipigwa kutoka kituo cha polisi kuwataarifu Dk Lewis na mkewe juu ya upotevu wa binti yao walioenda kuuripoti jana yake.
Bila kupoteza muda, Dk Lewis na mkewe walilifuata gari lao mahali walipokuwa wameliegesha wakati wakiendelea na kazi ya kumtafuta Skyer, wakaingia na safari ya kuelekea kituo kikuu cha plisi ikaanza haraka. Baada ya takriban nusu saa, tayari waliwasili kituoni hapo, wakaenda sehemu ya maulizo ambapo walijieleza na kueleza kilichowapeleka.
Walielekezwa sehemu binti huyo alipokuwa amehifadhiwa, kwenye vyumba vya kupumzikia kituoni pale. Waliongoza mpaka sehemu hiyo, Dk Lewis aliyekuwa mbele ndiyo alikuwa wa kwanza kumtambua Skyler aliyekuwa amekaa kwa kujiinamia. “Ooh Skyler, nisamehe mwanangu kwa yote yaliyotokea, nakuomba urudi nyumbani, tuna nafasi kubwa ya kurekebisha makosa yetu,” alisema Dk Lewis kwa sauti ya kubembeleza lakini Skyler hakutaka kabisa kuelewa. Ilibidi mama yake aingilie kati, kwa kiasi fulani akafanikiwa kumtuliza, akakubali kurudi nyumbani.
Taratibu zote za kiusalama zilifanyika kituoni pale, Skyler akakabidhiwa kwa wazazi wake na kuondoka kurejea nyumbani kwao. Siku ya kwanza ilipita huku Skyler akizidi kuonesha namna alivyokuwa anamchukia baba yake, hatimaye siku ya pili na ya tatu. Skyler alianza kutulia, kila mmoja akawa anaamini tayari msongo wa mawazo uliokuwa unamsumbua umeanza kuisha kumbe haikuwa hivyo.
Alikuwa akiwafanya geresha wazazi wake ili watakapoanza kwenda kazini, aitumie nafasi hiyo kutoroka tena. Hakutaka kabisa kuendelea kukaa jirani na baba yake kwani kila alipokuwa anamuona ndiyo hasira zilivyokuwa zinazidi kumpanda. Baada ya takriban siku saba kuisha, wakati Dk Lewis na mkewe wakiwa kazini, Skyler aliondoka nyumbani kwao bila mtu yeyote kugundua.
Akawa anaelekea upande wa magharibi kulikokuwa na msitu mkubwa wa Miami Conservative Forest. Alitembea kwa muda mrefu, hatimaye akafika kwenye msitu huo. Kama kawaida yake, hakuwa amechukua kitu chochote zaidi ya shuka la kujifunka na nguo alizokuwa amevaa tu. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Alitafuta sehemu yenye kivuli kikubwa, akasafisha chini na kuchomeka miti huku na huku, akaezeka juu mithili ya kibanda cha kuamia ndege kwenye shamba la mpunga, hayo ndiyo yakawa makazi yake mapya. Kwa kuwa msitu wenyewe ulikuwa pembeni kabisa ya makazi ya watu, hakuna mtu yeyote aliyeelewa mahali Skyler alipoelekea.
Akayaanza maisha mapya porini huku ujauzito wake ukizidi kuwa mkubwa. Kwa kuwa hakubeba chakula cha aina yoyote, ilibidi awe anaishi kwa kula matunda ya porini na kunywa maji yaliyokuwa yanapatikana kwenye chemchemi iliyokuwa upande wa chini wa msitu ule.
Hakuogopa baridi kali wakati wa usiku, mvua iliyokua inanyesha mara kwa mara wala wanyama wakali, kila kitu alikiona kipo sawa, akawa anaendelea kumkumbuka Harvey na kila kitu walichofanya pamoja. Upande wa pili, wazazi wake waliendelea kumtafuta lakini safari hii hawakufanikiwa. Ujumbe wa maandishi walioukuta kwenye
kitanda cha Skyler siku aliyotoroka kwa mara ya pili,ukawa unawatoa machozi kila walipokuwa wanausoma. Siku zilizidi kuyoyoma bila kupata taarifa zozote zilizokuwa zinamhusu Skyler, wazazi wake wakawa wanaamini huenda na yeye aliamua kujiua kama alivyoandika kwenye ujumbe wake wa mwisho aliouacha.
MAZISHI ya Harvey yanafanyika na kuhudhuriwa na maelfu ya waombolezaji kutoka chuo alichokuwa anasoma cha Miami Polytechnic and Engineering College, timu ya mpira wa kikapu ya Miami Heat na
mashabiki zake kutoka sehemu mbalimbali nchini humo na kuhitimisha safari yake ya mwisho hapa duniani. Siku kadhaa baadaye, Skyler anatoweka nyumbani kwao na anajiapiza kuwa hatakuja kumsamehe baba
yake kamwe kutokana na kusababisha kifo cha Harvey. Jitihada za kumtafuta zinafanywa ambapo anakutwa jirani na dampo na kwenda kuhifadhiwa kituo cha polisi kabla ya kukabidhiwa kwa wazazi wake. Hata hivyo,
anatoroka kwa mara nyingine na safari hii, wanamtafuta bila mafanikio.
SIKU zilizidi kusonga mbele, ujauzito wa Skyler ukawa unazidi kuongezeka na kufanya tumbo lake liwe kubwa huku wazazi wake nao wakiendelea kumsaka kwa udi na uvumba. Walimtafuta kila sehemu lakini hawakupata taarifa zozote zenye kutia matumaini, wakawa wanaendelea kumuomba Mungu wao amnusuru mtoto wao.
“Jamani mwanangu, huu ndiyo kwanza ujauzito wake wa kwanza, haelewi chochote… nani atamsaidia jamani,” alisema mama Skyler huku akibubujikwa na machozi.
“Tulia mke wangu, ukilia sana utakufuru, amini mwanao yupo salama na kila kitu kitakuwa sawa.” “Hapana, siwezi! Roho inaniuma sana kuona mwanangu anaenda kuteseka kama mtoto yatima, haya yote umeyasababisha wewe… tazama tumekosa vyote kwa pupa.”
“Ilikuwa ni lazima haya yatokee mke wangu, kila jambo huja kwa sababu maalum, kwa hiyo ulitaka nimchekelee Harvey hata kama ameniharibia binti yangu?”
“Kwani yeye ndiyo wa kwanza? Ina maana wote ambao binti zao waliharibiwa kama Skyler waliwaua wahusika? Umekuwa katili sana mume wangu na damu ya Harvey itakuandama popote uendapo.”
“Kwa hiyo na wewe unashiriki kunikandamiza siyo? Nani atakuwa faraja kwangu katika kipindi kigumu kama hiki ambacho dunia nzima imenielemea kichwani?”
“Sijawahi kukudharau wala kukupinga hata mara moja mume wangu lakini kuhusu hili la Skyler, maelewano hayatapatikana humu ndani mpaka mwanangu apatikane.”
“Sasa kwani mimi ndiyo niliyemtorosha? Unanionea bure mke wangu. Wewe mwenyewe ni shahidi wa jinsi nilivyojitahidi kumtafuta Skyler, tazama wiki ya tatu sasa siendi kazini, kutwa tunazurura mitaani kama wendawazimu, usinihukumu mke wangu,” alijitetea Dk Lewis huku naye akilengwalengwa na machozi.
Dunia ilikuwa ikimuelemea kiasi cha kushindwa kuelewa hatima ya familia yake, akawa anamuomba Mungu wake afanye miujiza kurejesha amani. Alikuwa akisali usiku na mchana ili Skyler apatikane kwani alijua ikitokea naye akapatwa na tatizo litakalogharimu uhai wake, huo ndiyo utakuwa mwisho wa maelewano kati yake na mkewe. ***
Maumivu makali ya tumbo yalimfanya Skyler awe analia kwa kugugumia pale chini ya mti alipokuwa amehamishia makazi yake. Kwa siku kadhaa sasa, tumbo lilikuwa likimuuma kupita kiasi, huku mguu mmoja wa kushoto ukivimba na kubadilika kabisa. “Oooh! Mungu wangu, kwa nini usiuchukue uhai wangu na mimi ili nikaungane na kipenzi cha roho yangu, Harvey huko aliko?
Tazama mateso ninayoyapata,” alisema Skyler huku akilia kwa uchungu. Japokuwa nyumbani kwao kulikuwa na kila kitu na familia yao iliishi maisha bora, chuki iliyojengeka ndani ya mtima wake kwa baba yake baada ya kusababisha kifo cha Harvey, ilimfanya achukie sana kuishi nyumbani kwao.
Kimoyomoyo alijiapiza kuwa hata iweje, kamwe hayupo tayari kurudi na kuendelea kuishi na familia yao, akaona ni bora afe kwa njaa, magonjwa, maumivu au kuliwa na wanyama wakali kule porini lakini siyo kurudi kwa wazazi wake.
Akiwa bado anaendelea kuugulia kwa maumivu makali, akiwa hana hata uwezo wa kusimama mwenyewe, alisikia hatua za kitu kikitembea kwa kunyata kusogea pale alipokuwa. Akili zake zilimtuma kuamini kuwa huenda ni mnyama mkali alikuwa akimsogelea ili amgeuze kitoweo.
Hakuogopa kitu, akafumba macho yake na kuanza kuvuta pumzi ndefu na kuzitoa, akawa anasubiri kuona kitakachotokea. “Wewe ni nani?” sauti kavu ya mwanamke mzee ilisikika kutoka ndani ya kichaka, akashtuka sana kwani hakutarajia kukutana na binadamu wa aina yoyote porini kule, akageuka na kutazama kule sauti ile ilipokuwa inatokea. “Nakuuliza wewe ni nani na umefuata nini huku?”
“Naitwa Skyler, naomba msaada wako, tumbo linaniuma sana,” alisema Skyler huku akimtazama vizuri yule mtu. Alikuwa ni mwanamke mzee mwenye mvi kichwa kizima, ngozi yake ya uso ikiwa imekunjamana sana kuonesha kuwa alikula chumvi ya kutosha. Mgongo wake ulikuwa umepinda kiasi cha kutembelea mkongojo.
Alitembea taratibu na kusogea hadi pale alipokuwa amelala Skyler, akaanza kumhoji vizuri yeye ni nani na amefikaje kwenye msitu ule hatari ambao ni nadra sana kukutana na binadamu.
“Baba yangu amesababisha kifo cha mpenzi wangu, namchukia sana na ndiyo maana nimeamua kuja kuishi huku peke yangu.” “Pole sana lakini ni hatari sana kuishi huku, kuna wanyama wakali, nyoka wenye sumu, wadudu waenezao magonjwa na kila aina ya hatari.”
“Ni bora nife, nataka nimfuate Harvey wangu huko aliko,” alisema Skyler huku akibubujikwa na machozi, yule bibi kizee akatambua namna binti huyo mdogo alivyoathirika kisaikolojia kutokana na kifo cha mtu aliyekuwa anampenda. “Mh! Hiki ni nini?” yule bibi alishtuka baada ya kugusa kitumbo cha Skyler ambacho kilionesha dhahiri kuwa na mtoto ndani. “Mimi ni mjamzito.”
“Mjamzito? Masikini weee! Mbona unaonekana bado mdogo kabisa… kwani ulikuwa umeolewa?” “Hapana, na sidhani kama nitaolewa tena kwani mchumba wangu aliyenipa mimba ndiyo huyo ameshatangulia mbele za haki,” alisema Skyler, akaanza upya kuangua kilio, yule bibi kizee akawa anaendelea kumbembeleza huku akimsihi atulie kwani hali aliyokuwa nayo ya ujauzito hakutakiwa kukaa na majonzi kiasi kile.
Baada ya muda, yule bibi kizee alimuinua Skyler pale chini, akamwambia kuwa ataenda kuishi naye kwenye kibanda chake kilichokuwa ndani ya msitu huo mpaka atakapojisikia kurudi kwa ndugu zake. Akamshika mkono na kuanza kumuongoza njia ya kuelekea alipokuwa anaishi.
Baada ya kutembea kwa dakika kadhaa, wakijipenyeza kwenye vichaka vikubwa na kupishana na wanyama wa mwituni, hatimaye walifika chini ya mti mkubwa, palipokuwa na kibanda kilichojengwa kwa ustadi mkubwa kutumia miti na udongo. “Hapa ndiyo ninapoishi, tutakaa wote hapa kwa siku zote utakazotaka wewe, nitakusaidia kuulea huo mzigo wako,” alisema yule bibi ambaye baadaye alijitambulisha kuwa anaitwa Chloe Salem. “Unaishi na nani huku porini bibi?” “ Naishi peke yangu mjukuu wangu, ni stori ndefu ambayo kila nikiikumbuka huwa inanitoa machozi, ipo siku nitakusimulia kila kitu,” alisema yule bibi kizee huku akitafuta kiberiti na kuwasha moto. Akamkalisha Skyler pembeni ya moto kwani alikuwa akitetemeka kutokana na kuloa na umande wakati wakitembea porini. “Na huu mguu wako mbona umevimba kiasi hiki?”
“Sijui bibi, ulianza wenyewe tu, halafu nasikia maumivu makali sana hapa kiunoni,” alisema Skyler huku akimuonesha eneo la chini ya kitovu upande wa mguu wa kushoto uliokuwa unamuuma.
“Mh! Hii ni dalili ya hatari sana kwa mama mjamzito, inawezekana mimba imetunga nje ya mfuko wa uzazi, hebu jinyooshe nikuangalie vizuri,” alisema bibi Chloe, akamlaza Skyler kwenye jamvi na kuanza kumpapasa eneo la tumboni.
“Inabidi nikuanzishie dawa haraka iwezekanavyo, mimba yako imetunga nje ya kizazi kama nilivyokuwa nimehisi,” alisema bibi yule aliyeonekana kubobea katika mambo ya tiba za asili, akainuka na kuanza kutafuta dawa alizokuwa amezihifadhi kwenye vikapu vingi alivyokuwa amevitundika ukutani.
KIFO cha ghafla cha Harvey kinabaki kuwa fumbo gumu kwenye vichwa vya wengi, kuanzia katika chuo alichokuwa anasoma cha Miami Polytechnic and Engineering College mpaka kwenye kambi ya timu ya mpira wa kikapu ya Miami Heat. Wengi wanafananisha kifo hicho na tukio la kufikirika kwani ameondoka duniani ghafla mno akiwa bado anahitajika.
Nyumbani kwa Dk Lewis nako hali inakuwa tete kwani siku kadhaa baada ya kifo cha Harvey, Skyler anatoweka nyumbani kwao na kuelekea kusikojulikana, anajiapiza kuwa hatakuja kumsamehe baba yake kamwe kutokana na kusababisha kifo cha Harvey.
Upande wa pili, Skyler anaokotwa kwenye msitu mkubwa na bibi kizee Chloe, anamchukua mpaka kwenye kibanda chake kilichopo katikati ya msitu mkubwa na kuanza kumhoji. Baadaye anagundua kuwa ujauzito wake umetunga nje ya kizazi, anaanza kumtafutia dawa za kumsaidia ajifungue salama. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ SIKU zilizidi kusonga mbele, hata wale ambao awali walikuwa wakifananisha kifo cha Harvey na filamu ya kutisha au simulizi ya kusisimua, wakaanza kuamini kuwa kumbe ni kweli hawatamuona tena duniani. Ulikuwa ni ukweli wenye kuuma sana. Baada ya siku arobaini kupita, kulifanyika kumbukumbu maalum ya kumuombea marehemu katika sehemu tatu tofauti, chuoni alikokuwa anasoma,
Miami Polytechnic and Engineering College, Makao Makuu ya Timu ya Miami Heat na nyumbani kwa Dk Lewis. Misa maalum ilisomwa kumuombea marehemu apumzike kwa amani, waombolezaji wakaenda kwenye kaburi lake na kuweka mashada ya maua pamoja na kuwasha mishumaa ya zambarau. Hali ilikuwa mbaya zaidi nyumbani kwa Dk Lewis kwani tangu Skyler atoweke, amani ilikosekana kabisa.
Suzan Lewis, mama mzazi wa Skyler alimuwekea mumewe mgomo baridi, akawa hataki kufanya kitu chochote kwa sharti la mumewe kufanya kila linalowezekana kumtafuta binti yake Skyler na kumrudisha nyumbani. Mumewe aliposhindwa kufanya hivyo, migogoro ilipamba moto ndani ya nyumba hiyo, muda wote akawa anashinda kuomboleza huku akitishia kudai talaka yake endapo Dk Lewis atashindwa kumrejesha Skyler nyumbani.
Hakutaka kuendelea kufanya kazi, akaomba likizo isiyo na malipo kwa muda usiojulikana, muda wote akawa anashinda ndani kuomboleza kifo cha Harvey na kutoweka kwa binti yake Skyler katika mazingira ya kutatanisha.
Dk Lewis alijitahidi kwa kadiri ya uwezo wake kumtuliza mkewe lakini haikusaidia kitu, aliwatumia wazee wenye busara na viongozi wa dini lakini haikusaidia kitu, msimamo wa mama Skyler ulikuwa uleule, binti yake atafutwe popote alipo na kurejeshwa nyumbani. ***
“Amka unywe dawa mjukuu wangu,” alisema bibi Chloe wakati akimtingisha Skyler aliyekuwa amejilaza kwenye jamvi, ndani ya kibanda alichokuwa anaishi mwanamke huyo mzee katikati ya msitu wenye miti iliyoshonana sana. Skyler aliamka na kujiegamiza kwenye ukuta wa miti wa kile kibanda, bibi Chloe akaanza kumnywesha dawa za mitishamba alizomuandalia.
“Hizi zitasaidia mtoto kukaa vizuri tumboni, mimba ikitunga nje ya kizazi ni hatari sana kwa usalama wako na wa mtoto,” alisema yule bibi kizee, Skyler akajikaza na kuanza kunywa dawa ile chungu.
Alikunywa kikombe cha kwanza, akaongezewa cha pili kisha akampa mizizi ya kutafuna. Baada ya kunywa, Skyler alipitiwa na usingizi mzito, akalala fofofo. Bibi Chloe alitoka na kwenda kutafuta dawa nyingine kwa ajili ya kuendelea kumtibu tatizo lake la ujauzito kutunga nje ya kizazi.
Siku ziliendelea kusonga mbele, Skyler akawa anazidi kumzoea bibi Chloe ambaye ndiyo msaada pekee uliokuwa umebakia maishani mwake. Ujauzito wake nao ulizidi kuongezeka, tumbo likawa kubwa huku matatizo ya kuvimba miguu nayo yakimsumbua mara kwa mara. “Bibi, uliniambia kuwa utanisimulia kilichofanya mpaka ukaja kuishi huku porini peke yako, niambie sasa.”
“Nitakwambia mjukuu wangu lakini siyo hivi sasa, hali uliyonayo hutakiwi kusikia vitu vya kuhuzunisha wala kupata taarifa mbaya. Historia ya maisha yangu iliharibika sana kiasi kwamba nilipoteza kabisa matumaini ya kuishi. Namshukuru Mungu kwa kuweza kunisimamia na kunipa nguvu ya kuishi mwenyewe katika mazingira ambayo dunia nzima imenitenga.
“Rafiki na ndugu zangu wamekuwa wanyama wa mwituni wakiwemo masokwe na nyani, hakuna mtu yeyote anayejua kuwa nipo hai mpaka leo,” alisema bibi Chloe huku akijilazimisha tabasamu usoni mwake wakati ukweli ni kwamba alikuwa akiumia moyoni. Alibadilisha mada haraka na kuanza kuzungumzia mambo mengine, akamwambia Skyler kuwa ipo siku atamweleza kwa kina kilichomtokea lakini akampa ujasiri kuwa hata dunia nzima ikijitenga mbali naye, bado maisha yanaendelea.
Baada ya kuzungumza kwa muda mrefu, bibi Chloe alitoka na kwenda kutafuta dawa nyingine kama ilivyokuwa kawaida yake kila jioni. Kutokana na hali aliyokuwa nayo Skyler, ilikuwa ni lazima amuache peke yake pale nyumbani wakati yeye akielekea porini kutafuta dawa. Skyler akajilaza kwenye jamvi kusubiri bibi Chloe arudi lakini tofauti na siku zote, muda ulizidi kuyoyoma bila bibi kizee huyo kurejea pale kwenye kibanda chao, hali iliyoanza kumtia wasiwasi.
“Siyo kawaida yake kuchelewa kurudi namna hii, amepatwa na nini?” alijiuliza Skyler wakati akijikongoja kuamka pale alipokuwa amelala na kutoka nje ya kibanda kile. Aliangaza macho huku na kule lakini hakumuona mtu yeyote zaidi ya nyani na masokwe yaliyokuwa yanaruka kutoka mti mmoja hadi mwingine huku yakipiga kelele kwa nguvu.
Muda ulizidi kuyoyoma na hatimaye giza likaanza kuingia, hofu ikazidi kutanda kwenye moyo wa Skyler, akahisi huenda amepatwa na tatizo kubwa porini alikoenda kumtafutia dawa kwa ajili ya tatizo lake lililokuwa linamtesa la ujauzito kutunga nje ya kizazi. Alitamani kutoka na kwenda kumtafuta lakini hali yake ilimzuia, akabaki kuomba dua ili muujiza wowote utokee na kumnusuru bibi kizee huyo. Giza lilizidi kutanda, macho na masikio ya Skyler yakawa makini kusikiliza kama atasikia bibi Chloe akigonga mlango lakini haikuwa hivyo.
Muda ulizidi kuyoyoma kwa kasi, mpaka ndege wa porini wanaanza kupiga kelele kuashiria mapambazuko ya siku mpya, bibi Chloe hakuwa amerejea, Skyler akaanza kulia na kuomboleza. Akaamka mahali alipokuwa amelala na kutafuta gongo la kutembelea, akajikongoja na kutoka nje, akaanza kutembea kwa tabu kufuata ile njia aliyoelekea bibi Chloe wakati anaondoka.
Sirudi nyuma mpaka nifahamu kilichompata, yeye ndiyo mtu pekee anayeweza kunisaidia katika hali kama hii,” alisema Skyler huku akizidi kujikongoja. Tumbo lake tayari lilikuwa kubwa sana kiasi cha kumfanya awe mzito kufanya kila kitu.
Baada ya kutembea kwa umbali mrefu, alifika mahali palipokuwa na kichuguu kilichoinuka, akakisogelea na kupanda juu yake kwa lengo la kutazama pande zote kama anaweza kumuona bibi Chloe.
“Mungu wangu, hiki nini tena,” alisema Skyler baada ya kuwaona tai wakubwa wakiruka na kutua jirani na pale kwenye kichuguu. Alikumbuka jinsi mwalimu wao wa somo la Baiolojia alivyowahi kuwafundisha kuwa ukiwa porini na ukawaona ndege hao, uwezekano mkubwa ni kwamba kuna mtu au mnyama amekufa kwani tai hula nyama kama walivyo wanyama wakali wa porini.
Hakutaka kusadiki haraka kile alichokuwa anakihisi, akajilazimisha kuamini kuwa huenda kuna mnyama wa porini amekufa lakini akili yake ikawa inamlazimisha kujikongoja mpaka eneo lile kwenda kujionea mwenyewe.
Alitembea huku mwili mzima ukimtetemeka mpaka alipofika jirani na pale walipokuwa wamekusanyika wale tai, akalitumia gongo lake la kutembelea kuwakurupusha ndege hao ambao waliruka na kutua juu ya miti iliyokuwa jirani. Akatupia macho pale walipokuwa wamekusanyika muda mfupi uliopita. “Mungu wangu,” alisema huku akizidi kusogea eneo lile, mwili mzima ulikuwa ukitetemeka kwa hofu.
MABALAA yanazidi kumuandama Skyler, bahati mbaya, mikosi na kila aina ya nuksi vinayapamba maisha yake. Baada ya kifo cha Harvey, anatoroka nyumbani kwao na kukimbilia kusikojulikana kutokana na chuki kali aliyokuwa nayo moyoni mwake. Anajiapiza kuwa kamwe hatarudi nyumbani kwa wazazi wake.
Baada ya kutoroka kwao, Skyler anakimbilia kwenye msitu mkubwa na kuweka makazi yake huko. Baadaye anakuja kuokotwa na bibi kizee Chloe anayemchukua mpaka kwenye kibanda chake kilichokuwa ndani kabisa ya msitu huo. Wanayaanza maisha lakini muda mfupi baadaye, bibi huyo anafariki porini na kugeuka chakula cha tai.
Nyumbani kwa Dk Lewis nako amani inatoweka kabisa, mkewe anamshinikiza kuwa ahakikishe mtoto wao, Skyler anapatikana vinginevyo atadai talaka yake. Dk Lewis anajitahidi kwa kadiri ya uwezo wake wote lakini jitihada zake zinagonga mwamba, hali inayoiyumbisha kabisa ndoa yao.
SKYLER alishindwa kuamini kile alichokuwa anakiona mbele ya macho yake kama ni kweli, mwili wa bibi Chloe ambaye tayari alikuwa amefariki, ulikuwa umeshambuliwa na tai na kuharibiwa vibaya. Kitu pekee kilichofanya amtambue kuwa ni yeye, ni nguo alizokuwa amezivaa mara ya mwisho wakati anaondoka kule kwenye kibanda chake.
Skyler alishindwa kujizuia, akaangua kilio kwa sauti kubwa kuomboleza kifo cha Chloe ambaye ama kwa hakika aliondoka na kumuacha akiwa hajui nini hatma yake. Alipiga magoti na kusali sala maalum kumuombea marehemu, alipomaliza alinyanyuka na kuanza kujikongoja kurudi kule kwenye kile kibanda.
Njia nzima alikuwa akilia kutokana na uchungu wa kumpoteza mtu pekee aliyedhani angekuwa mkombozi wake katika maisha, bibi Chloe. Hata hivyo, alilazimika kuukubali ukweli, akaendelea kujikongoja kwa tabu mpaka kwenye kile kibanda cha bibi Chloe.
Kila alipokuwa akivitazama vitu vilivyokuwa mle ndani, alikuwa akiiona taswira ya bibi Chloe mbele ya macho yake, akaendelea kuomboleza siku nzima. Hakula wala kunywa kitu chochote, jambo pekee aliloweza kulifanya ilikuwa ni kulia tu.
Baada ya siku ya kwanza kupita, Skyler aliendelea kutafakari juu ya hatima ya maisha yake na hali aliyokuwa nayo. “Kama ujauzito wenyewe umekaa nje ya kizazi na huku porini nipo peke yangu, nitaweza kujifungua salama kweli?” alijiuliza Skyler huku akijishika tumbo lake ambalo lilikuwa linazidi kuwa kubwa kila siku. Japokuwa awali alikuwa hataki kukutana na mtu yeyote zaidi ya bibi Chloe, baada ya kifo chake aliona kuna haja ya kubadilisha uamuzi wake.
“Ngoja nitoke huku msituni lakini naapa sitarudi nyumbani, bora nikazalie barabarani kuliko kurudi nyumbani, namchukia sana baba na sidhani kama ipo siku nitakuja kumsamehe,” alisema Skyler. Siku ya tatu tangu kifo cha Bibi Chloe kitokee, Skyler alianza kujiandaa kwa safari ya kuondoka ndani ya msitu ule. Alihakikisha ameweka vizuri kila kitu ndani kibanda kile, nguo zote za bibi Chloe akazifunga kwenye kitenge na kuziweka vizuri, akapanga vyombo na kusafisha mle ndani ya kibanda.
Alipomaliza, alichukua kila kilichokuwa chake, akafunga mlango wa miti kwa kutumia kamba kama alivyokuwa anafanya bibi kizee huyo wakati akiwa hai, taratibu akaanza kujikongoja kufuata njia ile waliyoitumia siku wakati wanafika eneo lile na bibi Chloe. Alipofika mita kadhaa mbele, aligeuka na kutazama kile kibanda, machozi yakazidi kummiminika kwa wingi.
“Pumzika kwa amani bibi Chloe, Mungu akulipe mema kwa moyo wa upendo uliouonesha kwa kipindi kifupi tulichokaa pamoja, hakika wewe ni mwanamke jasiri, kalale mahali pema peponi, aamen!” alisema Skyler huku akizidi kububujikwa na machozi, akageuka na kuendelea na safari yake huku akiwa hajui anaelekea wapi.
Baada ya kutembea kwa saa nyingi porini, akipishana na wanyama wa mwituni wakiwemo sokwe, swala, tumbili, nyani na pundamilia, huku akitumia gongo kama msaada wake, alitokeza sehemu ambapo kulikuwa na vichaka vidogovidogo vilivyoachana.
Alitazama huku na kule lakini bado hakuona dalili za kuwepo kwa makazi ya watu jirani na eneo lile. Kwa mbali alianza kusikia sauti za magari yakipita barabarani, akaendelea kujikongoja na kusonga mbele. Baada ya muda, alitokezea kwenye barabara ambayo hata hakuelewa inatoka wapi na kuelekea wapi.
“Ooh! Ahsante Mungu kwa kunifikisha salama,” alisema huku akitafuta sehemu nzuri ya kukaa. Akaweka kifurushi chake kidogo na gongo lake pembeni, akakaa chini na kujiegamiza kwenye mti, akawa anayatazama magari yaliyokuwa yanapita kwa kasi.
“Siwezi kurudi nyumbani, siwezi… namchukia sana baba,” alisema huku akilia. Bado kumbukumbu mbaya zilikuwa zikimtesa ndani ya kichwa chake. Ilifika mahali akawa anamkufuru Mungu wake kwa kumpitisha kwenye majaribu makubwa kiasi kile. Tukio la mwisho aliloshuhudia mwili wa bibi Chloe ukiliwa na tai wakubwa, lilienda kutonesha kidonda ambacho bado kilikuwa hakijapona.
“Mke wangu, yule mtu anafanya nini huku porini peke yake?” “Mtu? Hakuna mtu anayeweza kukaa huku, lazima utakuwa umeona nyani au sokwe mkubwa.” “Hapana mke wangu, ni binadamu… nimemuona mwenyewe kwa macho yangu.” “Siyo binadamu, twende tunachelewa bwana, hujui tuna safari ndefu ya kurudi nyumbani? Kuna umbali mrefu sana kutoka hapa mpaka Orlando.” CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Ina maana huniamini mke wangu? Kwani mimi sifahamu tofauti kati ya binadamu na nyani au sokwe?” Watu wawili, Bill Jones na mkewe Scolastica walikuwa wakibishana ndani ya gari lao dogo baada ya Bill kudai kuwa amemuona mtu kando ya barabara. Kufuatia ubishi huo, Bill aliyekuwa nyuma ya usukani, alisimamisha gari mita kadhaa mbele na kuteremka.
Akaanza kurudi pale alipomuona yule mtu, mkewe naye aliteremka, akawa anamfuata mumewe kwa nyuma. “Mungu wangu, kumbe kweli ni binadamu?” alisema Scolastica, mumewe akaongeza mwendo kumfuata yule mtu. Muda mfupi baadaye walifika na kumkuta binti akiwa amekaa kichovu na kuegamia mti, machozi yakichuruzika kutoka kwenye pembe za macho yake na kulowanisha uso wake.
“Binti, unaitwa nani na kwa nini upo porini muda huu?” alihoji Bill, yule mtu akashtuka kuonesha kuwa alikuwa amezama kwenye dimbwi la mawazo machungu.
“Naitwa Skyler, ni stori ndefu lakini siwezi kumsimulia mtu yeyote mpaka nitakapojifungua.” “Sasa huoni ni hatari kukaa sehemu ya hatari kama hii? Kila siku watu wanaliwa na wanyama wakali au kugongwa na nyoka wenye sumu eneo hili, tafadhali tunaomba uongozane nasi mpaka kwenye gari letu.”
“Siendi popote, nimeamua maisha yangu yawe hivi,” alisema Skyler huku akijichomoa kutoka kwenye mikono ya Bill na mkewe ambao walishaanza kusaidiana kumuinua kutoka pale alipokuwa amekaa. Ilibidi waanze kumbembeleza taratibu huku wakimtaka awaeleze tatizo lililokuwa linamsumbua kiasi cha kushindwa kutambua thamani yake kiasi kile. Wakati wanaendelea kumbembeleza, ndipo walipogundua kuwa kumbe alikuwa mjamzito, tumbo lake likiwa tayari limeshakuwa kubwa kabisa.
“Kumbe una ujauzito? Uchungu ukikushika peke yako huku porini huoni utahatarisha sana maisha yako?” alisema Scolastica huku akianza kuingiwa na huruma ndani ya mtima wake, Skyler hakujibu kitu zaidi ya kuendelea kutiririkwa na machozi.
Baada ya kumbembeleza sana, hatimaye Skyler alikubali kuongozana na wale watu, wakamsaidia kuinuka na kumpeleka kwenye gari lao walilokuwa wamelipaki pembeni ya barabara, taratibu wakawa wanatembea mpaka kwenye gari, wakamsaidia kuingia ndani ya gari. Safari ikaanza kuelekea nyumbani kwa wanandoa wale.
Baada ya safari ndefu iliyowachukua takribani saa mbili, wakawa tayari wamewasili kwenye Mtaa wa Orlovista, Orlando, yalipo makazi yao. Wakamsaidia Skyler kuteremka kwenye gari, wakamuingiza ndani ya nyumba yao waliyokuwa wanaishi. “Hapa ndiyo nyumbani kwetu, bado hatujabahatika kupata mtoto kwenye ndoa yetu, tunaishi peke yetu na mfanyakazi wa ndani, jisikie kama upo kwenu,” alisema Scolastica wakati akimuongoza Skyler kuingia ndani. Moja kwa moja akampeleka bafuni kuoga.
BAADA ya kuteseka porini kwa kipindi kirefu na kumpoteza mtu pekee aliyekuwa msaada kwake, Bibi Chloe, Skyler anakata tamaa ya kuishi na sasa anatamani kufa. Anaomboleza kwa kipindi kirefu kiasi cha kumkufuru Mungu wake, baadaye anapiga moyo konde na kuamua kutoka katikati ya msitu alikokuwa anaishi.
Anajikongoja na ujauzito wake na kuanza kukatiza vichaka, mabonde na milima ndani ya msitu ule, hatimaye anatokezea sehemu yenye uwazi. Anaendelea kutembea na baadaye anafika barabarani, anatafuta sehemu yenye kivuli pembeni ya barabara na kukaa huku akiwa amepoteza kabisa matumaini ya kuendelea kuishi.
Bill na Scolastica, wanandoa waliokuwa wanatoka kwenye matembezi ya jioni, wanashtuka baada ya kuhisi kuwa kuna mtu wamempita akiwa amekaa pembeni ya barabara jirani na msitu mkubwa. Wanabishana kwa muda kisha Bill anateremka na kuelekea pale alipomuona mtu huyo huku mkewe akifuatia kwa nyuma.
Wanagundua kuwa kweli ni binadamu, wanamchukua na kwenda naye nyumbani kwao na hiyo ndiyo inakuwa ponapona ya Skyler. Baada ya kuoga, Skyler alipelekwa kwenye chumba cha wageni na kuambiwa hapo ndiyo atakapokuwa anaishi kwa siku zote atakazokaa nyumbani pale. Alimshukuru mwenyeji wake, Scolastica na kujiegamiza kitandani. “Utakula chakula gani nikakuandalie?” aliuliza Scolastica, Skyler akajibu kuwa chakula chochote watakachopika, na yeye atakula hichohicho.
Alitoka na kuelekea jikoni, akamuacha Skyler amejilaza kitandani huku akijishikashika tumbo lake ambalo sasa lilishakuwa kubwa kabisa, mawazo machungu yakawa yanaendelea kupita ndani ya kichwa chake kama filamu ya kuhuzunisha. “Nitajifungua salama kweli? Ooh! Mungu, onesha miujiza yako,” alisema Skyler huku akiendelea kujishikashika tumbo.
Baada ya kumaliza kuandaa chakula, Scolastica alienda kumuamsha mumewe Bill aliyekuwa amepumzika chumbani kwao, akaenda kumuamsha na Skyler, wote watatu wakaenda kujumuika kupata chakula cha usiku. “Jisikie huru kufanya jambo lolote wakati wowote, jisikie kama upo nyumbani kwenu Skyler,” alisema Bill wakati wakiendelea kupata chakula.
“Ujauzito wako una umri gani?” aliuliza Scolastica, Skyler akajibu kuwa hafahamu na wala hakumbuki chochote.” “Sasa unaishije na ujauzito ikiwa hujui hata siku ya makadirio ya kujifungua? Huoni ni hatari sana?” “Inabidi kesho uende naye kliniki, ni hatari sana kuishi namna hii,” alisema Bill, wakakubaliana kuwa asubuhi waende kliniki.
Waliendelea kula na baada ya kila mmoja kutosheka, walienda kutazama runinga sebuleni kwa muda kisha baadaye wakaagana na kwenda kulala.
“Ukumbuke kumuomba Mungu wako kabla hujalala, huo ndiyo utaratibu wetu hapa nyumbani,” alisema Scolastica, Skyler akaitikia kwa kutingisha kichwa, akaelekea kwenye chumba alichopewa.
Kulipopambazuka, kama walivyokuwa wamekubaliana, Scolastica aliwahi kuamka na kumuandaa mumewe kwa ajili ya kwenda kazini, akamuamsha na Skyler, kwa pamoja wakaanza kujiandaa kwenda kliniki.
“Kwa nini mmechelewa kumleta hospitali kiasi hiki? Hili ni tatizo kubwa,” alisema daktari mkunga waliyemkuta, akawa anaendelea kumfanyia vipimo Skyler akitaka kujua kuhusu ujauzito wake. “Ujauzito wake umetunga nje ya kizazi, ni hatari sana kwake na kwa kiumbe kilichopo ndani ya tumbo lake, mngewahi kumleta tungejua mapema nini cha kufanya.”
“Mungu wangu? Mimba ipo nje ya kizazi? Ataweza kujifungua salama kweli,” Scolastica alishtuka kupita kiasi baada ya kupewa taarifa ile na daktari. Kwa jinsi alivyokuwa anafahamu, ujauzito unaotunga nje ya kizazi humsababishia matatizo makubwa mama na wengi hupoteza maisha wakati wa kujifungua.
Akamtazama Skyler kwa macho ya huruma na kumgeukia daktari. “Tafadhali fanya chochote kinachowezekana ili muda ukifika ajifungue salama, hata ukitaka fedha za ziada tutakuongeza na mume wangu,” alisema Scolastica, yule daktari akazidi kumfafanulia mambo kadhaa ya kitaalamu.
“Angekuja siku za kwanza wakati ndiyo ujauzito wake umeanza, tungejua namna ya kumsaidia lakini kwa sasa mmechelewa sana, inabidi mjiandae kukubaliana na hali yoyote itakayotokea,” alisema daktari, Scolastica akazidi kukata tamaa.
Hali ilikuwa mbaya zaidi kwa Skyler kwani hata yeye alishasikia kuwa ujauzito ukitunga nje ya kizazi, kama mhusika hakupata matibabu ya kitaalamu katika hatua za mwanzo, uwezekano mkubwa ni kupoteza maisha wakati wa kujifungua au kuzaa mtoto aliyekufa. Baada ya daktari kumaliza kuchukua vipimo, aliwaacha Skyler na Scolastica na kuingia maabara, baada ya muda akarudi na majibu kuwa ujauzito wa Skyler ulikuwa na umri wa wiki ishirini na nne (miezi sita). Akawapa ushauri kuwa Skyler anatakiwa kula vyakula vya kuongeza damu kwa wingi zikiwemo mboga za majani na matunda.
Akawaambia kuwa wawe wanampeleka kliniki kila baada ya wiki mbili ili kuangalia maendeleo ya mtoto ambaye vipimo vilionesha amejishikiza kwenye nyonga. Scolastica na Skyler walitoka hadi nje ya hospitali ile, mahali walipokuwa wamepaki gari walilokuja nalo. Wakaingia na kuanza kuondoka, hakuna aliyemsemesha mwenzake ndani ya gari mpaka wanafika.
Baada ya kuteremka kwenye gari, Skyler alipitiliza moja kwa moja mpaka chumbani, akajifungia na kujitupa kitandani. Akaanza kulia kiasi cha kufikia hatua ya kumkufuru Mungu wake.
Alimlaumu sana kwa kumleta kwenye dunia hii iliyojaa mateso na kila aina ya dhiki, akazidi kumlaumu kwa kuruhusu yale yote yamtokee akiwa bado na umri mdogo kabisa.
“Why me? Why always me?” alisema Skyler huku akijipigapiga kifuani. Baadaye usingizi mzito ukampitia. Akalala vilevile alivyokuwa, bila hata kuvua viatu. Mume wa Scolastica aliporudi, alielezwa majibu ya daktari, naye akajikuta akiingiwa na hofu kubwa ndani ya moyo wake kuhusu usalama wa Skyler.
Walikubaliana kufuata maelekezo ya daktari na kumpeleka hospitali kila baada ya wiki mbili kama walivyokuwa wameshauriwa. Siku zikawa zinasonga mbele kwa kasi, ujauzito wa Skyler nao ukazidi kuongezeka ukubwa.
MIEZI MITATU BAADAYE
Mvua kubwa ilikuwa ikinyesha na kuifanya mitaa mbalimbali ya Orlando, Marekani hasa Mtaa wa Orlovista uliokuwa bondeni kuanza kufurika maji. Barabara zote zilijaa maji kiasi cha kufanya wenye magari wawe wanasafiri kwa mwendo wa taratibu wakihofia kusombwa na maji au kuingia kwenye mitaro.
Bill na mkewe Scolastica, walikuwa wakirejea nyumbani kutoka kwenye matembezi ya mwisho wa wiki. Kwa kawaida, kila Jumapili walipokuwa wanatoka ‘out’, walikuwa wakiongozana na Skyler lakini kutokana na ujauzito wake kuzidi kuwa mkubwa, walilazimika kuanza kumuacha nyumbani akiwa amejipumzisha.
“Unajua mwenzio sina amani kabisa, hii mvua inavyonyesha na nyumbani tumemuacha Skyler peke yake, sijui kukitokea dharura itakuwaje?”
“Hamna chochote kinachoweza kutokea, si unakumbuka wakati tunaondoka tulimuacha akiwa amechangamka kabisa, tena yeye mwenyewe ndiyo aliyetusindikiza mpaka tunatoka!”
“Ni kweli lakini maumivu ya uchungu wa kujifungua hayatabiriki, mtu anaweza kuwa anacheka muda huu lakini dakika mbili mbele hali ikawa tofauti kabisa. Ongeza mwendo tuwahi nyumbani.”
“Hatuwezi kuongeza mwendo zaidi ya hapa, si unaona mwenyewe barabara zilivyojaa maji, tunaweza kuingia kwenye mtaro na haraka zote zikaishia hapohapo, hakuna tatizo lolote,” alisema Bill lakini bado akili ya mkewe ilikuwa haijatulia. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Baada ya kukaa dakika kadhaa kwenye foleni, hatimaye walivuka sehemu yenye maji na kuingia kwenye barabara nzuri, wakaharakisha kuelekea nyumbani kwao. Walipofika, Scolastica aliteremka haraka kwenye gari na kukimbilia mpaka kwenye chumba alichokuwa analala Skyler.
“Mungu wangu, kumbe nilichokuwa nakihisi ni kweli,” alisema Scolastica baada ya kumkuta Skyler akiwa amelala sakafuni, huku damu nyingi zikimtoka sehemu zake za siri. Ilivyoonesha, alikuwa amekaa kwenye hali ile kwa muda mrefu kiasi cha kumfanya
apoteze fahamu. Scolastica akamuita mumewe kwa sauti ya juu, wakasaidiana kumbeba Skyler hadi kwenye gari, wakatoka kwa kasi na kumkimbiza hospitali.
GIZA linazidi kutanda kwenye maisha ya Skyler ambapo baada ya kupata pigo kubwa la kwanza la Harvey kufa katika mazingira ya kutatanisha, anaamua kuondoka nyumbani kwao kwa hasira na kukimbilia porini huku ujauzito wake ukiendelea kukua.
Anakutana na bibi kizee, Chloe ambaye anajitolea kumsaidia na kuishi naye katikati ya msitu mkubwa lakini jioni moja, bibi huyo anakumbwa na balaa na kupoteza maisha wakati akiwa anamtafutia dawa Skyler. Hilo linakuwa pigo lingine kwenye maisha yake na sasa anapoteza dira.
Baadaye anaamua kutoka ndani ya msitu huo na kwenda kutafuta msaada ambapo anafika jirani na barabara na kukaa. Muda mfupi baadaye anakutwa na wasamaria wema, Bill na Scolastica ambao
wanamchukua hadi nyumbani kwao, Orlando. Anayaanza maisha mapya akiwa na familia hiyo na baadaye anashikwa na uchungu. WALIPOMALIZA mtaa wa kwanza, walifika upande wa bondeni ambako maji bado yalikuwa yakiendelea kuvuka kwa kasi barabarani, safari hii yakiwa na nguvu kubwa kiasi cha magari kulazimika kusimama mpaka yapungue. “Endesha gari mume wangu, hali ya mgonjwa ni mbaya sana, atatufia mikononi huku tunamuona.”
“Sasa mke wangu we mwenyewe unaona magari hayapiti kabisa kutokana na maji yanayovuka, unataka gari letu likazolewe?” “Basi geuza gari tuangalie njia nyingine ya kupita, hali ya mgonjwa ni mbaya sana.”
“Papara hazitasaidia jambo lolote, tumeshachelewa sana na hapa cha kufanya ni kumuomba Mungu tu, tukiwa na papara tunaweza kujikuta na sisi tumepata ajali bure,” alisema Bill, hali iliyofanya washindwe kuelewana na mkewe.
Baada ya kupigizana sana kelele na mkewe, Bill alilazimika kugeuza gari na kupita barabara nyingine kwa lengo la kumuwahisha Skyler hospitalini. Njia waliyopita iliwasaidia kwa kiasi kikubwa kutoka kwenye Mtaa wa Orlovista uliokuwa
umekumbwa na mafuriko, wakaingia kwenye barabara nzuri na safari ya kumkimbiza hospitali ikapamba moto. Dakika thelathini baadaye, gari lao liliwasili kwenye jengo la kisasa lililokuwa na maandishi makubwa yaliyosomeka
Orlando Maternity Hospital, gari likapitiliza mpaka mapokezi huku likiwa limewasha taa za mbele. Wauguzi wa hospitali ile waliokuwa wamevalia kinadhifu, walipoliona tu gari lile, walitoka na kitanda cha kusukuma kwa magurudumu.
Muda mfupi baadaye, Skyler alipandishwa kwenye kitanda cha magurudumu, manesi wakawa wanamkimbiza kuelekea wodini huku Bill na mkewe Scolastica wakiandikisha maelekezo kwenye daftari la wagonjwa.
“Jina lake anaitwa nani?” “Skyler Lewis.” “Ana umri wa miaka mingapi?” “Miaka kumi na tisa.”
“Kumi na tisa? Kwa nini mmemruhusu abebe ujauzito akiwa na umri mdogo kiasi hicho? Kwani hamjui sheria za nchi zinavyosema?”
Bill na mkewe walipoona maswali yameanza kuwaelemea, ilibidi waseme ukweli kuwa wao ni wasamaria wema tu waliomkuta binti huyo tayari akiwa mjamzito. Yule nesi aliondoka na kuwaacha palepale mapokezi, akakimbilia wodini alikoingizwa Skyler.
“She needs special care during her labour, she is under twenty,” (Anahitaji uangalizi maalum wakati wa kujifungua, ana umri wa chini ya miaka ishirini) Alisema yule muuguzi, madaktari wakunga na manesi wakawa wanaendelea kumhangaikia ili kuhakikisha anajifungua salama.
“Wamechelewa sana kumfikisha hospitali, inavyoonesha amekaa na uchungu kwa zaidi ya saa nne, ni hatari sana,” alisema daktari aliyekuwa anamchunguza. Kutokana na hali aliyokuwa nayo, ilibidi daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake aende kuitwa, harakaharaka akaingia wodini na kwenda hadi pale Skyler alipokuwa amelazwa. “Connect her to Oxygen Cardio- Pulmonary bypass as quick as possible, she is suffocating,”
(Muunganisheni kwenye mashine ya kumsaidia kupumua haraka iwezekanavyo, anashindwa kupumua) alisema daktari mkuu, Matilda Heinneman, wauguzi waliokuwa chini yake wakatekeleza haraka, muda mfupi baadaye mashine ya kisasa ya kumsaidia kupumua ikaunganishwa na kuanza kufanya kazi.
Hata hivyo, kwa kuwa alikuwa amekaa kwa muda mrefu katika hali ya uchungu, bado hakuwa na uwezo wa kumsukuma mtoto wala kufanya kitu chochote, madaktari wakafikia muafaka kuwa ni lazima afanyiwe upasuaji. “We must send her to theatre ready for Caesarean Section,”
(Tumpelekeni chumba cha upasuaji kwa ajili ya kufanyiwa oparesheni ya uzazi) alisema Daktari Matilda, harakaharaka milango ya wodi ikafunguliwa na jopo la madaktari na wauguzi zaidi ya nane wakawa wanasaidiana kukisukuma kitanda cha Skyler kuelekea chumba cha upasuaji huku mashine ya kumsaidia kupumua ikiendelea kufanya kazi.
Bill na mkewe Scolastica ambao tayari walishafika nje ya wodi ile aliyoingizwa Skyler, wakiwa wanasubiri kusikia kitakachojiri, walishtuka sana baada ya kuona mlango unafunguliwa na jopo la madaktari na wauguzi wanakimbizana kumuwahisha Skyler wodini.
“Dokta, dokta, anaendeleaje? Mgonjwa wetu anaendeleaje?” aliuliza Scolastica huku naye akikimbia kuwafuata madaktari lakini hakujibiwa chochote, akazuiwa mlangoni na walinzi waliokuwa wamevalia sare za kiaskari, akaambiwa asubiri nje ili kuwapisha madaktari wafanye kazi yao.
Harakaharaka alirudi pale alipokuwa amemuacha mumewe, akakaa pembeni yake huku machozi yakimtiririka, akamuegamia huku akizidi kububujikwa na machozi.
“Usilie mke wangu, huo utakuwa ni uchuro… inabidi tumuombee Skyler kwa Mungu,” alisema Bill na kumkumbatia mkewe, wakashikana mikono na kufumba macho, wakawa wanamuomba Mungu wao.
Madaktari ndani ya chumba cha upasuaji waliendelea kuhangaika kwa kadiri ya uwezo wao wote kuokoa maisha ya Skyler lakini vikwazo navyo vilizidi kuongezeka. Wakati maandalizi ya kufanyiwa upasuaji yakiwa yamekamilika, Daktari Matilda alibaini tatizo lingine ambalo lilizidi kufanya kazi iwe ngumu.
Ilibainika kuwa Skyler alipoteza damu nyingi wakati wa uchungu hivyo isingewezekana kufanyiwa upasuaji mpaka aongezwe damu na kupewa muda wa kupumzika. Kwa kuwa benki ya damu ya hospitali ile ilikuwa na akiba ya kutosha, nesi mmoja alitumwa na baada ya muda mfupi, alirejea akiwa na chupa mbili za damu, ikabidi Skyler achomwe sindano ya kuchelewesha uchungu kisha akatundikiwa dripu ya damu.
Wakati damu ikiendelea kutiririka kwenye mishipa yake kwa kasi, madaktari walikuwa wakiendelea kumchunguza mtoto jinsi alivyokaa tumboni. Vipimo vya Ultra Sound na X Ray vikawa vinaonesha kuwa amejiegamiza kwenye nyonga, upande wa kushoto. Kitaalam, mama mjamzito ambaye mimba yake imetunga nje ya mfuko wa kizazi, upasuaji wake hutofautiana na yule ambaye ujauzito wake umekaa kwenye kizazi.
“Itabidi kazi ya kumfanyia upasuaji ifanyike kwa umakini wa hali ya juu sana, mtoto amejiegamiza mahali penye mishipa mingi ya fahamu, kosa dogo linaweza kusababisha madhara makubwa kwa mama au mtoto,” alisema Daktari Matilda wakati
akizungumza na madaktari wenzake, dripu ya damu ikaendelea kutiririka kwenye mishipa ya Skyler. “Tatizo hawa vijana wetu siku hizi wanayawahi sana mambo ya kikubwa, mtazame kama huyu, bado mbichi kabisa lakini
tayari muda si mrefu atakuwa anaitwa mama, ameruka kutoka hatua ya utoto mpaka umama, anatia huruma sana,” alisema daktari mwingine, wote wakatulia kimya, wakawa wanamtazama Skyler ambaye bado fahamu zake zilikuwa hazijamrudia.
Chupa ya kwanza iliisha, akatundikiwa nyingine ambayo nayo iliendelea kutiririka kwa kasi kuingia kwenye mishipa yake. Dakika arobaini baadaye, tayari ile chupa ya pili nayo ilikuwa imemalizika. Ikabidi wamuache apumzike kwa muda kuruhusu ile damu iingie vizuri mwilini, akachomwa na sindano za dawa za kuongeza nguvu mwilini ili kurahisisha zoezi la kumfanyia upasuaji.
Bill na mkewe Scolastica bado walikuwa wakisubiri sehemu maalum ya kupumzikia huku wakiwa na shauku kubwa ya kutaka kujua maendeleo ya mgonjwa wao. Kila mlango wa chumba cha upasuaji ulipokuwa unafunguliwa, walikuwa wakisimama na kusogea wakitarajia kusikia chochote kutoka kwa madaktari lakini mara zote hawakuwa wakijibiwa kitu zaidi ya kuambiwa waendelee kusubiri.
Saa mbili baadaye tangu Skyler aongezewe damu, mapigo yake ya moyo yalirudi sehemu yake ya kawaida na sasa akawa anapumua vizuri. Vifaa vya upasuaji vikasogezwa pembeni ya kitanda alichokuwa amelala, madaktari na manesi wakavaa mavazi maalum yaliyoziba nyuso zao isipokuwa macho tu, Dokta Matilda akaongoza zoezi la kumfanyia upasuaji Skyler.
Wakati upasuaji ukiendelea, Dokta Matilda aliwageukia wenzake na kuanza kujadiliana nao kutokana na hali iliyokuwa imejitokeza. “Kuna tatizo kubwa sana, inabidi tuamue jambo moja haraka iwezekanavyo,” alisema Dokta Matilda huku akionesha kuchanganyikiwa.
HALI ya sintofahamu imetanda kwenye chumba cha upasuaji cha Hospitali ya Orlando Maternity ambapo Skyler anafanyiwa upasuaji wa kumsaidia kujifungua. Awali upasuaji huo ulilazimika kusogezwa mbele kid ogo kutokana na Skyler kubainika kuwa na upungufu mkubwa wa damu, akatundikiwa chupa mbili za damu na kupewa muda wa kupumzika kisha zoezi hilo likaendelea.
Wakati upasuaji ukiendelea, Daktari Mkuu, Matilda anagundua tatizo kubwa na anasimamisha zoezi hilo na kuanza kujadili na madaktari wenzake na kuwataka wachangie mawazo juu ya nini cha kufanya kwani ilitakiwa wachague kuokoa mmoja kati ya mama (Skyler) au mtoto kutokana na tatizo lililojitokeza.
Wasamaria wema waliokuwa wanaishi na Skyler kwa kipindi kile, Bill na mkewe Scolastica wapo nje ya wodi hiyo huku kila mmoja akiwa na hofu kubwa ndani ya moyo wake juu ya hatima ya Harvey. Kwa pamoja wanamuomba Mungu amnusuru binti huyo mdogo.
“Tatizo gani tena daktari?” “Inaonesha kuwa mgonjwa ana tatizo la kifafa cha mimba na mkondo wa umeme kichwani mwake unaongezeka kwa kasi, muda mfupi baadaye ataanguka kifafa tukiwa bado hatujamaliza kumfanyia upasuaji, jambo linaloweza kusababisha kifo chake.”
“Sasa tufanye nini dokta? Wote ni muhimu.” “Kwani nyie wote si mmefuzu mafunzo ya udaktari? Mlifundishwa nini mkiwa vyuoni kukitokea jambo kama hili?” CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Kuna mbinu tatu za muhimu ambazo inabidi daktari anayeongoza oparesheni aamue moja. Ya kwanza ni kuhakikisha anaokoa maisha ya mama na mtoto, ikishindikana inabidi mbinu ya pili ya kuokoa maisha ya mama itumike lakini hiyo nayo ikishindikana, inabidi daktari aokoe maisha ya mtoto.” “Ungekuwa wewe ndiyo unaongoza oparesheni hapa ungeshauri mbinu gani itumike?” “Ningeshauri ya kwanza lakini kama ikishindikana basi itumike ya pili.”
“Wengine mnasemaje?” “Tunaunga mkono alichokisema mwenzetu, tujitahidi kwenye hiyohiyo mbinu ya kwanza kwani maisha ya wote ni muhimu,” walijibu madaktari waliokuwa chumba cha upasuaji, Dokta Matilda akawataka kila mmoja atimize wajibu
wake kisawasawa kuhakikisha wanaokoa maisha ya Skyler na kiumbe kilichokuwa ndani ya tumbo lake. “Inject her with Anti- Epileptic Drug (AED), 2.5cc of Phenobarbital Serum and Oxcarbazepine,”
(Mchomeni sindano za dawa za kuzuia kifafa cha mimba (AED), 2.5cc ya dawa ya Phenobarbital na Oxcarbazepine) alisema daktari Matilda, manesi wakaanza kuhangaika huku na kule, muda mfupi baadaye Skyler
akachomwa mchanganyiko wa dawa za AED ili kuzuia asianguke kifafa wakati upasuaji unaendelea. Baada ya kuchomwa sindano ya dawa ya AED, mkondo wa umeme kwenye kichwa chake uliokuwa unaoneshwa
kupitia kompyuta iliyokuwa pembeni ya kitanda alicholazwa, ulianza kupungua na mapigo yake ya moyo yakarudi kwenye hali yake ya kawaida, upasuaji ukaendelea.
Baada ya kuhangaika kwa zaidi ya saa tatu, hatimaye zoezi la kumsaidia Skyler kujifungua lilifanikiwa, mtoto akatolewa salama na kupelekwa kwenye chumba maalum, Skyler akaanza kushonwa jeraha alilofanyiwa upasuaji na kuongezewa damu kwani alipoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.
Akaongezewa dawa za kumzuia kuanguka kifafa akiwa katika hali ile kisha akatolewa kwenye chumba cha upasuaji na kupelekwa kwenye wodi ya akina mama. Bill na mkewe Scolastica ambao kwa muda wote walikuwa wamekumbatiana kwa kukata tamaa, walishtuka kupita kiasi baada ya kuona milango ya wodi ya upasuaji
ikifunguliwa, wakasimama na kukimbilia kwenye kile kitanda huku wakitaka kujua kilichoendelea. “Dokta, dokta, mgonjwa wetu anaendeleaje, dokta… tunataka kujua hali ya mgonjwa wetu,” alisema Bill huku mapigo yake ya moyo yakimwenda kasi kuliko kawaida.
“Mbona hamtujibu? Au amekufa? Tuambieni,” alisema Scolastica huku akianza kuangua kilio, dokta Matilda aliyekuwa nyuma kidogo akawaita na kuwataka waongozane naye hadi ofisini kwake. “Msiwe na wasiwasi, tumefanikiwa kumzalisha salama binti yenu ingawa kazi haikuwa nyepesi. Amejifungua
mtoto wa kiume kwa njia ya upasuaji ila bado anahitajika kuendelea kukaa hapa hospitalini chini ya uangalizi maalum.”
“Mtoto wa kiume? Ooh! Kumbe ndiyo maana ujauzito wake umekuwa na misukosuko mingi kiasi hiki! Ahsante Mungu,” alisema Scolastica huku akimkumbatia mumewe, machozi ya furaha yakawa yanawatoka wote wawili.
Dokta Matilda aliwapeleka kwenye chumba maalum wanachohifadhiwa watoto waliotoka kuzaliwa, akawaonesha mtoto wa Skyler, nao wakamuangalia na kuhakikisha kuwa kweli alikuwa wa kiume.
“Amezaliwa akiwa na kilo tatu na afya njema, inabidi mkamfanyie sherehe maalum kwani mama yake alichungulia kaburi tukiwa chumba cha upasuaji,” alisema Dokta Matilda.
“Lazima tumfanyie sherehe! Tena ameleta dume la shoka… inaonekana amefanana na baba yake maana hii sura siyo ya mama yake kabisa, labda kidogo macho ndiyo amefanana na mama yake,” alisema Bill huku akiwa amembeba mtoto yule mchanga.
Baada ya kuridhika, walimrudisha mtoto na kwenda wodini ambapo walimkuta Skyler akiwa bado hajarejewa na fahamu zake, chupa ya damu ikiendelea kutiririka kuingia kwenye mishipa yake ya damu.
“Inabidi wewe urudi nyumbani kwenda kuandaa mahitaji yote muhimu yanayohitajika, ngoja mimi nibaki hapa na mgonjwa,” alisema Bill huku akitoa funguo za gari na kumkabidhi mkewe. Bila hiyana akatoka na kwenda
kuandaa mahitaji muhimu zikiwemo nguo za mtoto, dishi la kuogea, chakula cha mfyele na vitu vingine vinavyohitajika.
Skyler aliendelea kulala akiwa hajitambui kwa muda mrefu, huku manesi wakipishana kwenye kitanda chake kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa. Scolastica baada ya kupata vifaa vyote muhimu, alirudi haraka hospitali na kumkuta mumewe akiwa bado anaendelea kumuangalia Skyler pembeni ya kitanda chake.
“Manesi wamesema karibu atazinduka, walikuwa wanakusubiri ili wakakukabidhi mtoto,” alisema Bill, mkewe akaweka vizuri vifaa alivyokuja navyo na kuelekea kwenye ofisi ya daktari mkuu ambapo alipewa fomu maalum ya kujaza. Baada ya taratibu zote kukamilika alienda kukabidhiwa mtoto, akambeba mpaka kwenye wodi aliyokuwa amelazwa Skyler.
Kwa umakini wa hali ya juu akamlaza pembeni ya Skyler na kumfunika na nguo laini alizokuwa amekuja nazo. Baada ya muda, Skyler alianza kupiga chafya mfululizo, Scolastica akainuka haraka na kwenda kuwaita manesi ambao walifika pale
kitandani mbiombio na kuanza kumsaidia Skyler aliyekuwa anarejewa na fahamu zake taratibu. Ilibidi Bill na mkewe watolewe nje kwa muda, manesi wakafanya kazi yao ipasavyo ambapo baada ya muda, Skyler
alirejewa na fahamu zake ingawa alikuwa akizungumza mambo yasiyoeleweka kutokana na kuleweshwa na dawa za ganzi na usingizi alizochomwa kwa wingi wakati akifanyiwa upasuaji.
“Maziwa yamejaa vizuri, bila shaka atakuwa na uwezo wa kunyonyesha vizuri bila matatizo.” “Ndiyo, nilikuwa na wasiwasi sana mwanzo kama kweli ataweza kunyonyesha,” manesi walikuwa wakijadiliana pembeni ya kitanda cha Skyler wakati wakimuandaa tayari kwa kuanza kumnyonyesha mwanaye.
Baada ya muda, walifanikiwa kumuweka mtoto kwenye ziwa, akaanza kunyonya kwa fujo. Hali ile ilimshtua sana Skyler, akawa analalamika kwa manesi kuwa mwanaye anamtekenya, wakamwambia kuwa atazoea tu kunyonyesha. “Kwani ni mtoto gani?” aliuliza Skyler kwa sauti ya chini.
“Umezaa dume, tena dume la shoka,” alisema nesi mmoja, wenzake wakamuunga mkono na kuanza kucheka, Skyler akatabasamu kwa furaha.
“Hebu muwekeni vizuri nimuangalie usoni,” alisema Skyler, manesi wakafanya kama alivyokuwa anataka. “Haaa! Harvey mtupu… ahsante Mungu kwa kuniletea mtu wa kunifuta machozi na kunifariji,” alisema Skyler huku akianza kulengwalengwa na machozi. Manesi wakamuuliza huyo Harvey anayemsema ni nani ambapo aliwaeleza kuwa ndiyo baba wa mtoto yule lakini kwa bahati mbaya tayari alikuwa ameshatangulia mbele za haki.
“Ooh! Pole mwaya… kila jambo linakuja kwa sababu ambazo Mungu pekee ndiye anayejua. Mshukuru kwa sababu amekuletea zawadi ya kipekee,” alisema nesi mmoja, wakaanza kumfariji Skyler na kumwambia kuwa asilie kwani anaweza kujiumiza kwenye mshono ambao bado ulikuwa haujapona. Mwanaye akawekwa vizuri na kuendelea kunyonya, Bill na Scolastica wakaenda kuitwa.
BAADA ya kulichungulia kaburi wakati wa kujifungua kutokana na ujauzito wake kutunga nje ya kizazi pamoja na kukumbwa na tatizo la kifafa cha mimba, hatimaye Skyler anafanikiwa kujifungua salama mtoto wa kiume mwenye afya njema akiwa amefanana kwa kiasi kikubwa na baba yake, marehemu Harvey. Baada ya kuzinduka kutoka kwenye usingizi wa kifo, Skyler anafurahi sana kugundua kuwa alikuwa amejifungua mtoto wa kiume, aliyekuwa amefanana kwa kiasi kikubwa na kipenzi cha moyo wake, Harvey… anajiapiza kumtunza kwa kadiri ya uwezo wake wote. Bill na mkewe Scolastica, nao wanaahidi kumtunza Skyler na mwanaye kwa kadiri ya uwezo wao wote, Skyler anaendelea kutibiwa na afya yake na ya mtoto zinazidi kuimarika siku baada ya siku.
“WHAOO! Hongera Skyler, Mungu anakupenda sana ndiyo maana akakuvusha salama kwenye haya mapito,” alisema Scolastica huku akimbusu Skyler kwenye paji la uso. Bill naye alifanya vilevile, Skyler akaachia tabasamu pana na kupokea pongezi zile, wakawa wanamtazama anavyoendelea kunyonyesha. “Unajisikiaje kunyonyesha?”
“Mtoto ananitekenya kwenye maziwa yangu,” alisema Skyler, wote waliokuwa pale wakaangua vicheko na kumwambia kuwa ataizoea hali ile. Ilikuwa ni siku ya furaha kupindukia kwa Skyler, Bill na Scolastica, wakaendelea kuzungumza mambo mbalimbali huku wote wakiwa na nyuso za furaha.
Siku ya kwanza ilipita, ya pili hatimaye ya tatu ikawadia. Afya ya Skyler na mwanaye zilizidi kuimarika, mtoto akawa anabadilika kila siku na kuzidi kuwa na afya njema huku kidonda cha oparesheni cha Skyler nacho kikizidi
kupona. Scolastica na Bill walikuwa na kazi ya ziada ya kuwahudumia Skyler na mwanaye kwa kila kitu. Siku ya saba ilipowadia, Skyler alitolewa wodini na kupelekwa chumba cha upasuaji kwa ajili ya kufumuliwa nyuzi alizoshonwa tumboni na kusafishwa kidonda chake.
“Anarejewa na nguvu zake haraka na kidonda kinapona kwa kasi,” alisema Dokta Matilda wakati wakiendelea kufumua nyuzi kwenye kidonda cha Skyler. Kila mmoja alifurahishwa na namna Skyler alivyokuwa akipona haraka.
Wakamsafisha kidonda na kumfunga bandeji safi, kisha akarejeshwa wodini ambapo alipumzishwa kwa muda mpaka dawa za usingizi alizochomwa zilipopungua nguvu. Hali yake iliendelea kuimarika na baada ya siku kumi akaanza kufanyishwa mazoezi mepesi.
Aliendelea kufanyishwa mazoezi kwa wiki nzima, asubuhi na jioni kila siku mpaka alipopona kabisa. Akaruhusiwa kutoka hospitali na mwanaye huku Scolastica na mumewe Bill wakipewa maelekezo ya namna ya kumhudumia na kupewa ushauri wa kumrudisha hospitali kila baada ya wiki mbili kuangalia maendeleo ya afya yake na mwanaye. “Utampa mwanao jina gani?” CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Bado sijaamua, nataka nikae naye kwa siku arobaini bila kumpa jina na siku atakayokuwa anatoka ndiyo nitamchagulia jina zuuuri!” alisema Skyler wakati wakiwa ndani ya gari kurejea nyumbani kwa Bill na mkewe. “Sasa kwa nini ukae siku arobaini bila kumpa mtoto jina? Mbona huo siyo utaratibu wa kawaida?” aliuliza Scolastica aliyekuwa amembeba mtoto, wakiwa wamekaa siti ya nyuma ya gari lile.
“Kwa mateso na majaribu niliyopitia tangu siku ya kwanza niliyopata ujauzito wa huyu mtoto, hakuna tofauti na mtu aliyekuwa akiteseka jangwani kwa siku arobaini. Nataka mwanangu naye ashiriki kuomboleza kifo cha baba yake aliyemuacha akiwa bado tumboni mwangu, kamwe sitamsahau Harvey katika maisha yangu na nitaendelea kumuenzi milele,” alisema Skyler huku akianza kulengwalengwa na machozi.
Baada ya kugundua kuwa alikuwa amezitonesha hisia za Skyler, Scolastica alibadilisha mada haraka na kuanza kuzungumza jambo lingine tofauti, safari ikaendelea huku kila mmoja akiwa kimya ndani ya gari. Hatimaye wakawasili yalipokuwa makazi ya Bill na mkewe.
“Karibu nyumbani mama, tunamshukuru Mungu tumerejea salama kwani siku tuliyokuwa tunakutoa kukupeleka hospitali, hakika kila mmoja alikuwa amekata tamaa… yaani ni Mungu tu,” alisema Scolastica wakati wakimsaidia Skyler kuteremka kwenye gari na kushusha vitu vyote vilivyokuwa vinatumika hospitalini. “Inabidi tukufanyie sherehe maalum ya kumshukuru Mungu kwa kukunusuru na kumleta salama duniani huyo malaika,” aliongezea Bill, wakawa wanatembea taratibu kuingia ndani.
Skyler alipelekwa kwenye chumba chake ambacho kilikuwa kimekarabatiwa vizuri na kuongezwa vitu vingi vipya, jambo lililomfariji sana. Akayaanza maisha mapya, safari hii akiwa na mwanaye aliyekuwa amefanana kwa kiasi kikubwa na marehemu Harvey.
Siku zilianza kusonga mbele, afya za Skyler na mwanaye zikawa zinazidi kutengemaa huku mtoto akizidi kuchangamka siku baada ya siku. *** Abdulkarim Charwe, alikuwa ni Mtanzania aliyezaliwa Bukoba na kukulia mjini humo kabla ya kuhamia jijini Dar es Salaam alikosomea masomo yake ya sekondari na kuhitimu kidato cha sita. Baada ya kuhitimu masomo yake ya sekondari, Charwe alijiunga na Chuo Kikuu Kishirikishi cha Tiba, Muhimbili (MUCHS) jijini Dar es Salaam, Kitivo cha Udaktari (Faculty of Medicine).
Baada ya kusoma kwa zaidi ya miaka mitano na kuhitimu shahada ya kwanza ya udaktari, Charwe alienda kufanya kazi kwenye Hospitali ya Wazazi, Meta jijini Mbeya ambako alikutana na binti wa Kinyakyusa, Anganile aliyekuwa akisomea uuguzi katika hospitali hiyo. Charwe na Anganile walitokea kuwa marafiki wakubwa,
wakazoeana sana na baadaye wakajikuta wakianzisha uhusiano wa kimapenzi. Uhusiano wao ulidumu kwa kipindi cha mwaka mmoja, baada ya kila mmoja kuridhika na tabia ya mwenzake, waliamua kuchumbiana na miezi sita baadaye, Charwe alienda kujitambulisha nyumbani kwa wazazi wa Anganile, Kiwira-Tukuyu mkoani Mbeya.
Baada ya kupata Baraka zote kutoka kwa wazazi wa binti huyo aliyekuwa na uzuri wa asili, mrefu wastani, maji ya kunde mwenye umbo lililogawanyika vizuri, Charwe aliamua kumpeleka nyumbani kwa wazazi wake, Bukoba mkoani Kagera alikoenda kumtambulisha rasmi.
Baada ya taratibu zote kukamilika, Charwe na Anganile walifunga ndoa ya kimila na kuhalalishwa kuwa mke na mume, wakarejea jijini Mbeya ambapo walienda tena kufunga ndoa ya kidini na kuwaalika ndugu, jamaa, marafiki na wafanyakazi wenzao.
Wakayaanza maisha mapya ya ndoa. Miezi kadhaa tangu waanze kazi, Charwe alipata nafasi ya kwenda kusomea Shahada ya Pili ya Udaktari (Masters in Medicine) nchini Cuba, akalazimika kusafiri na mkewe ambaye naye alimtafutia nafasi ya kusoma kwenye chuo cha Havanna School of Medicine nchini humo, wakaishi nchini humo kwa muda wa miaka mitatu.
Baada ya kuhitimu masomo, Charwe na mkewe walirejea Tanzania ambapo baada ya kufanya kazi kwa miezi miwili jijini Mbeya, alipandishwa cheo na kupewa nafasi ya kuwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Bugando jijini Mwanza. Kutokana na jinsi alivyokuwa anaipenda kazi yake, Charwe aligeuka na kuwa tegemeo la wagonjwa kutoka sehemu mbalimbali za Kanda ya Ziwa.
Hakuwa akijali uwezo wa kiuchumi wa watu aliokuwa anawatibu, kwake watu wote walikuwa na thamani inayofanana na mara kwa mara alikuwa akigombana na wafanyakazi wake waliokuwa wanawabagua watu masikini na kutoa huduma za upendeleo kwa wenye nazo.
Jina lake likaanza kuwa maarufu jijini Mwanza na maeneo ya jirani. Miezi saba tangu aanze kazi kwenye hospitali hiyo, mkewe kipenzi, Anganile alishika ujauzito, furaha ikazidi kuongezeka kwenye familia yao. Wakati ujauzito wa mkewe ukizidi kukua, alipokea barua kutoka Wizara ya Afya iliyomtaarifu kuwa ameteuliwa kwenda kufanya kazi kwenye Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani, jijini Geneva, Uswisi.
Kwa Charwe, ule ulikuwa ni zaidi ya muujiza kwani hakutegemea kuwa ipo siku juhudi zake kazini zinaweza kuonekana kiasi cha kupewa heshima kubwa kama hiyo. Kama barua ile ilivyomtaarifu, alitakiwa kusafiri mpaka jijini Dar es Salaam kukamilisha taratibu za vibali vya kufanyia kazi na nyaraka nyingine muhimu za utambulisho. Baada ya wiki moja, taratibu zote zikawa zimeshakamilika.
Charwe na mkewe pamoja na vitu vyao vyote muhimu vikasafirishwa kwa ndege ya Shirika la ATCL kutoka Mwanza hadi jijini Dar es Salaam ambapo walibadili ndege na kupanda kwenye ndege kubwa ya kisasa, Airbus 380 mali ya Shirika la Ndege la Uswisi, Swiss Airways na safari ya kuelekea Geneva ikaanza.
HATIMAYE Skyler anajifungua salama mtoto wa kiume akiwa chini ya uangalizi wa Bill na mkewe Scolastica. Jitihada za madaktari na manesi wa Hospitali ya Orlando Maternity zinafanikisha zoezi hilo kufanyika salama licha ya matatizo makubwa yaliyokuwa yanamuandama Skyler.
Baada ya kujifungua salama, hali ya Skyler na mwanaye inakuwa ya kuridhisha na kwa kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele, hali yake inazidi kuwa nzuri, hatimaye wanaruhusiwa kutoka hospitali. Bill na mkewe Scolastica wanamchukua Skyler na mwanaye na wanaahidi kuwalea kwa kadiri ya uwezo wao.
Upande wa pili, Mtanzania Abdulkarim Charwe, mzaliwa wa Bukoba, anasomea udaktari na kupata kazi jijini Mbeya. Miezi michache baadaye anaenda tena kusomea udaktari nje ya nchi na kurudi nchini baada ya miaka mitatu. Ufanisi wake katika kazi unamfanya ateuliwe kwenda jijini Geneva, Uswisi kufanya kazi kwenye makao makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO).
BAADA ya kufika jijini Geneva, Charwe na mkewe walipokelewa vizuri na Afisa Uhusiano wa Shirika la Afya Duniani, Ludovic Chappelle ambaye aliwachukua kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Geneva (zamani Cointrin Airport) hadi makao makuu.
“Karibuni sana Uswisi, jina langu ni Ludovick Chappelle.” “Ahsante sana, naitwa Abdulkarim Charwe na huyu ni mke wangu, anaitwa Anganile.”
“Nimefurahi sana kuwafahamu, nimetumwa na bosi kuja kuwapokea na kuwapeleka mpaka ofisini.” “Ahsante sana,” Chappelle alikuwa akizungumza na Charwe na mkewe kwenye uwanja wa ndege wa Geneva, baada ya utambulisho mfupi, Chappelle aliwasaidia kupakiza mizigo yao kwenye gari maalum alilokuwa amekuja nalo, alipomaliza
wote wakaingia ndani ya gari na safari ya kuelekea yalipokuwa makao makuu ya shirika hilo ikaanza. “Kwani makao makuu ya WHO yapo mtaa gani hapa Geneva?” aliuliza Charwe, Chappelle akamjibu: “Yapo Avenue Appia 20, 1211 Geneva, siyo mbali sana, baada ya dakika ishirini tutakuwa tumeshafika.”
Safari iliendelea huku Charwe na mkewe wakishangaa mandhari nzuri ya Jiji la Geneva lililopambwa na milima iliyofunikwa na theluji nyeupe, huku mashamba ya maua na bustani nzuri vikiupendezesha mji wote. “Duh! Kuna sehemu nyingine duniani zina uzuri wa kustaajabisha, utafikiri tupo kwenye bustani ya Eden,” alisema Anganile, mumewe na Chappelle wakamtazama na kuangua vicheko.
“Wala msijali, kuna vivutio vingi sana vya utalii hapa Geneva, nafikiri kwa wiki nzima ya kwanza tutakuwa na kazi ya kuvitembelea kimoja baada ya kingine, naamini mtafurahi sana kuona vitu kama Ziwa Geneva, Victoria Hall, Makumbusho ya Patek Philippe, Makumbusho ya Histoire Naturelle, Jet d’Eau, Cathedrale de St-Pierre (St Peter Cathedral) na vingine
vingi, mtafurahi sana kufika Geneva,” alisema Chappelle, Charwe na mkewe wakawa wanamsikiliza kwa makini. “Kule kwetu Tanzania kuna mji huwa unaitwa Geneva ya Afrika, umewahi kuusikia?”
“Arusha? Ndiyo, nimewahi kufika miaka kadhaa iliyopita, nimepanda mpaka Mlima Kilimanjaro. Si upo Kenya eeeh!” “Hapana, watu wengi wanafikiri hivyo lakini Mlima Kilimanjaro upo Tanzania.” “Mh! Lakini mume wangu hivi kweli unaweza kuifananisha Arusha na Geneva?”
“Kuna baadhi ya vitu vinafanana kwa mfano hali ya hewa na wingi wa vivutio vya kitalii kama mbuga za wanyama na vinginevyo.” CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Lakini Geneva kuzuri jamani, tusifanye masihara… natamani maisha yangu yote niishi hapa,” alisema Anganile, mumewe na Chappelle wakacheka tena. Wakati wakiendelea kuzungumza, kumbe tayari walikuwa wameshawasili makao makuu. Chappelle akakata kona upande wa kushoto na kuingia kwenye geti kubwa la kisasa, akaingiza gari ndani na kuegesha nje ya jengo kubwa la kisasa la ghorofa sabini, akawageukia wageni wake.
“Jamani hapa ndiyo makao makuu ya WHO, jisikieni mpo nyumbani na nitakuwa nanyi kwa kipindi chote mpaka mtakapozoea mazingira. Kuweni huru kuniuliza jambo lolote,” alisema Chappele, Charwe na mkewe ambaye ujauzito wake ulikuwa unazidi kuwa mkubwa, wakatingisha vichwa kama ishara ya kukubaliana naye. Akawafungulia milango na kwa pamoja wakateremka.
“Nifuateni,” alisema Chappelle, Charwe akamshika mkono mkewe na kuanza kutembea taratibu kumfuata Chappelle. Walienda mpaka kwenye lifti za kisasa, wakaingia kisha Chappelle akabonyeza kitufe cha namba ukutani, lifti ikaanza kupanda juu.
Baada ya muda, wakawa tayari wamefika ghorofa ya 33, Chappelle akateremka na kuwaongoza mpaka kwenye ofisi iliyokuwa na kibao juu ya mlango kilichosomeka C.E.O (Chief Executive Officer), Chappelle akabonyeza kitufe cha ‘alarm’ mlangoni, sekunde chache baadaye mlango ukafunguka, wakaingia na kwenda mpaka ndani ambapo mwanamke wa makamo aliyekuwa amevaa miwani na kuiteremsha kidogo, aliwapokea kwa bashasha.
“Naitwa Margareth Palmer, kiongozi wa Shirika la Afya Duniani, bila shaka wewe ni Abdulkarim Charwe.” “Naam! Hujakosea, na huyu ni mke wangu, anaitwa Anganile,” alisema Charwe huku akipeana mkono na mwanamke yule wa makamo. Baada ya utambulisho, kiongozi yule alianza kuzungumza na Charwe na kumueleza kilichowafanya mpaka wamteue kwenda kuungana nao pale makao makuu.
Alimweleza kuwa wamekuwa wakisikia mara kwa mara juu ya sifa na utendaji wake wa kazi uliotukuka na ndiyo maana wameamua kumchukua. Charwe alifurahi sana, akaahidi kuendelea kufanya kazi kwa uwezo wake wote kuwasaidia watu wenye uhitaji.
Baada ya mazungumzo yale, Bi Margareth alimueleza Charwe kuwa gharama zote za maisha zitakuwa juu yao ambapo alimwambia kuna nyumba ya kisasa, gari na vitu vingine kadhaa vimetolewa na ofisi kwa ajili yake. Akainua mkonga wa simu na kumpigia Chappelle ambaye muda mfupi baadaye aiingia. Akamwambia awapeleke wageni kwenye makazi yao mapya.
Wiki ya kwanza ilipita wakiwa jijini Geneva, kila kitu kilikuwa kigeni kwao, Chappelle akawa anaendelea kuwatembeza sehemu mbalimbali za jiji hilo la kisasa. Wiki ya pili ilipowadia, Charwe alianza kazi rasmi kwenye ofisi za makao makuu ya Shirika la Afya Duniani. *** “Nilishakwambia kama umeshindwa kumpata mwanangu na mimi nataka talaka yangu.” “Jamani mke wangu, wewe ni shahidi wa jinsi ninavyohangaika usiku na mchana kuhakikisha mtoto wetu anarejea nyumbani. Tumeshatoa taarifa kila sehemu hapa Miami lakini hatujafanikiwa. Unataka nifanye nini?” “Wewe si ndiyo ulisababisha yote haya… nimeshasema namtaka mwanangu na kwa sababu umeshindwa kumpata, niandikie talaka yangu.” “Siwezi kukupa talaka mke wangu kwa sababu bado nakupenda.”
“Mnafiki mkubwa wewe, ungekuwa unanipenda ungekubali kuniondolea furaha maishani mwangu? Wewe mwenyewe ni shahidi wa jinsi nilivyoteseka kuanzia siku namzaa Skyler, nilivyomlea mpaka amekuwa, leo kirahisirahisi unamfanya apachukie nyumbani kiasi hicho?”
“Lakini nilifanya yote haya kwa lengo la kumlinda mwanangu.” “Kumlinda? Hivi una akili timamu wewe? Mtoto ameondoka hapa akiwa mjamzito na tayari miezi tisa imeshatimia… hata hujiulizi nini kilichompata wakati wa kujifungua? Hujui kwamba alikuwa bado mdogo na alihitaji uangalizi mkubwa ili ajifungue salama?
“Nakuchukia sana mwanaume wewe… utatoa talaka yangu utake usitake,” Suzan Lewis alikuwa akirushiana maneno na mumewe, Dk Lewis chanzo kikuu kikiwa ni kupotea kwa binti yao wa kipekee Skyler. Licha ya kujitahidi kumbembeleza mkewe kwa kipindi chote hicho, jitihada za Dk Lewis ziligonga mwamba kwani mkewe hakutaka kusikia la mwadhini wala mchota maji.
Alipoona mumewe hataki kutoa talaka kwa hiyari yake, alimpeleka mahakamani, kesi ikanguruma kwa miezi miwili kabla ya mahakama kutoa amri ya Dk Lewis kumpa talaka mkewe.
Vitu vyote walivyochuma pamoja vikauzwa na wakagawana nusu kwa nusu, huo ukawa mwisho wa maisha ya ndoa kati ya wawili hao.
SKYLER baada ya kujifungua salama, Bill na mkewe Scolastica wanamchukua na kurudi naye nyumbani kwao huku wakimuahidi kumtunza yeye na mwanaye kwa kadiri ya uwezo wao wote. Hata hivyo, amani inatoweka kabisa nyumbani kwa wazazi wake na wanafikia hatua mbaya ya kupeana talaka.
Upande wa pili, familia mpya ya Charwe na mkewe Anganile, inajaliwa kupata mtoto mzuri wa kike na wakati mwanamke huyo wa Kitanzania akijiandaa kusafiri na mwanaye mchanga mpaka Geneva, Uswisi, anapokea
barua kutoa Wizara ya Afya ikimtaka akaripoti kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kuanza kazi. MAISHA ya kukaa mbali na mumewe yalikuwa magumu sana kwa Anganile, akawa muda mwingi anautumia kuzungumza kwa simu na mumewe ambaye alikuwa akiendelea na kazi kwenye Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO), Geneva, Uswisi. Siku zilizidi kusonga mbele, mtoto Charlotte akawa anazidi kukua na kubadilika, urembo aliozaliwa nao ukawa unazidi kuchanua
kila kukicha. Ili kurahisisha kazi, Anganile alitafuta msichana wa kumsaidia kumlea mwanaye, Mwanaisha. Akawa anaendelea na kazi huku msichana huyo akimsaidia kwa kiasi kikubwa malezi ya mwanaye.
Ilipofika mwezi Desemba, Charlotte akiwa ndiyo kwanza anatimiza umri wa miezi minne, Anganile alipewa likizo fupi aliyoomba kwa ajili ya kwenda kumtembelea mumewe jijini Geneva, Uswisi.
Maandalizi ya safari yalianza kufanyika, Charwe akamtumia mkewe tiketi ya ndege na fedha nyingine za matumizi ya dharula. Anganile akamuandaa mwanaye vizuri na safari ya kuelekea Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere ikaanza. Ilibidi amuachie Mwanaisha kazi ya kulinda nyumba na vitu vyote alivyoviacha.
Alisafiri na mwanaye mpaka Geneva, Uswisi ambapo alimkuta mumewe akiwa anamsubiri Uwanja wa Ndege wa Geneva. Aliwapokea kwa bashasha na furaha tele na kuwapeleka mpaka nyumbani kwake. Wakaishi kwa furaha kwa siku zote za likizo na ilipoisha, Anganile na mwanaye Charlotte walianza kujiandaa kwa safari ya kurejea Tanzania.
“Natamani siku zirudi nyuma ili tuendelee kuishi pamoja, nimejisikia vizuri sana kwa kipindi chote nilichoishi nanyi,” alisema Charwe, mkewe akatabasamu na kumjibu kuwa na yeye anatamani iwe hivyo lakini hawana budi kurejea Tanzania kwa ajili ya kazi.
Aliwasindikiza mpaka uwanja wa ndege, wakaagana kwa huzuni, Charwe akawa anatokwa na machozi wakati mkewe akiwa na mwanaye Charlotte wakipanda ngazi na kuingia ndani ya ndege, tayari kwa safari ya kurejea Tanzania.
Walisafiri salama hadi Tanzania na baada ya siku kadhaa, Anganile aliripoti kazini na kuendelea na majukumu yake katika Hospitali ya Muhimbili huku mfanyakazi wake, Mwanaisha akiendelea kumhudumia Charlotte kwa kila kitu wakati mama yake akiwa kazini.
Siku zilizidi kuyoyoma, Charlotte akawa anazidi kukua na kupendeza. Ikawa kila inapotokea likizo fupi, Anganile na mwanaye wanasafiri mpaka Geneva, Uswisi kumtembelea mumewe. Safari za mara kwa mara kwenye ndege zikawa ni kitu cha kawaida kwa Anganile na mwanaye.
Wakati mwingine, Charwe naye alikuwa akisafiri kuja kuitembelea familia yake Tanzania na kukagua maendeleo ya miradi yao mbalimbali, ikiwemo ujenzi wa nyumba yao ya kifahari eneo la Mbezi Beach. Furaha iliendelea kutawala kwenye familia hiyo huku Charwe na Anganile wakizidi kuoneshana mapenzi motomoto licha ya kuishi sehemu mbili tofauti. *** Baada ya kukaa siku arobaini za uzazi, Skyler kwa kushirikiana na walezi wake, Bill na Scolastica, waliandaa sherehe maalum kumshukuru Mungu kwa kuwezesha Skyler kujifungua salama mtoto wa kiume. Kama alivyokuwa ameahidi, Skyler alichagua jina zuri kwa ajili ya mwanaye.
“Kwa heshima na kumbukumbu ya kipenzi cha roho yangu Harvey, mwanangu ataitwa Harrison, kila nitakapokuwa naliita jina hilo, nitakuwa namkumbuka marehemu baba yake,” alisema Skyler huku akilengwalengwa na machozi.
Bill na mkewe walijitahidi kumchangamsha, majirani na marafiki kadhaa waliokuwa wamealikwa kwenye sherehe ile nao wakawa wanashangilia na kupiga vigelegele kwa wingi, Skyler akaanza kuchukulia yote yaliyotokea kama kitu cha kawaida. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo kwa kipenzi cha roho yake Harvey, sasa aliyahamishia kwa mwanaye Harrison, sherehe ikaendelea ambapo watu walioalikwa walikunywa, kula, kucheza muziki na kufurahi pamoja.
“Nashukuru sana kwa upendo wa dhati mlionionesha, sijui nitawalipa nini, Mungu atanilipia, mmechukua nafasi ya wazazi wangu.” “Wala usijali, ni wajibu wetu kukufanya uwe na furaha, tutahakikisha upo salama wewe na mwanao kwa siku zote za maisha yenu.
Mungu ametunyima watoto katika ndoa yetu kwa hiyo tunakuchukulia wewe kama mtoto wetu na Harrison kama mjukuu wetu. Kuweni na amani kabisa,” alisema Bill akiwa amekumbatiana na mkewe Scolastica.
“Mungu alipanga kutukutanisha pamoja ili haya yote yatimie,” alisema Scolastica huku akizidi kujilaza kwenye kifua cha mumewe. Siku zilizidi kusonga mbele, Skyler akazidi kuchangamka sambamba na mwanaye ambaye alikuwa akizidi kuchangamka huku afya yake ikizidi kuwa bora, hali iliyozidi kuleta furaha katika familia ya Bill.
Harrison alipotimiza mwaka mmoja, aliandaliwa sherehe kubwa ya kumpongeza, Bill na mkewe wakagharamia kila kitu katika sherehe hiyo ambayo waliwaalika ndugu, majirani na marafiki kadhaa.
Tayari Harrison alikuwa na uwezo wa kusimama mwenyewe kwa kujishikilia kwenye vitu mbalimbali kama ukuta na viti, akawa pia na uwezo wa kuzungumza maneno machache, ikiwemo kuita mama na vitu vingine vidogovidogo. Hali ile ilimfariji sana Skyler, akawa muda mwingi anautumia kucheza na mwanaye huku akimuangalia jinsi alivyokuwa anafanya mambo mbalimbali.
“Mtoto mtundu sana huyu, sijui amerithi kwa nani? Kwani na wewe ulipokuwa mtoto ulikuwa mtundu hivi?” aliuliza Scolastica wakati Harrison akicheza kwenye vyombo.
“Wala mimi sikuwa mtundu, labda baba yake,” alijibu Skyler, wote wakacheka kwa furaha. Siku zilizidi kuyoyoma, mtoto akazidi kukua na hatimaye alitimiza umri wa miaka mitatu ambao ulikuwa ukitosha kumuanzisha shule ya chekechekea (Nursery School). Harrison akaenda kuandikishwa katika Shule ya Orlando Kindergarten iliyokuwa jirani na pale walipokuwa wanaishi.
Siku za mwanzo Harrison alipata shida kuzoea mazingira kwani alishazoea kuishi mikononi mwa mama yake lakini kwa kadiri siku zilivyokuwa zinasonga mbele, alianza kuzoea kucheza na watoto wenzake.
“Mama, leo tumejifunza kuhesabu… moja… mbili… tatuu,” alisema Harrison kwa lafudhi ya kitoto baada ya kurudi shuleni. Skyler alikuwa akifarijika sana kumuona mwanaye ameanza kuelewa baadhi ya mambo, yeye mwenyewe akawa haamini kwani kila kitu kilikuwa kikitokea kwa haraka sana.
“Mama, leo Tony amekuja kutembelewa na bibi yake shuleni, kwani mimi bibi yangu yuko wapi?” “We mtoto wewe, maswali gani hayo? Bibi yako ni Scolastica na babu yako ni Bill.” alijibu Skyler huku akionesha kushtushwa na jinsi mwanaye alivyokuwa na uelewa mkubwa wa kufahamu mambo licha ya umri wake mdogo aliokuwa nao.
Licha ya kumjibu vile na kufanikiwa kumtuliza, Skyler alionekana kuzama kwenye dimbwi la mawazo. Ni kweli wazazi wake hususan baba yake alikuwa amemkosea lakini kwa kadiri alivyoishi nao mbali, alijikuta hata ile chuki aliyokuwa nayo awali ikianza kuyeyuka.
“Kila siku kanisani tunafundishwa kuwasamehe waliotukosea, lazima siku moja nimpeleke Harrison kwa babu na bibi yake halisi,” aliwaza Skyler wakati akimbadilisha mwanaye nguo za shule. Siku zilizidi kusonga mbele, Harrison akazidi kuwa mtundu huku uelewa wake nao ukizidi kupevuka siku baada ya siku.
Simulizi : Queen Of Gorillas ( Malkia Wa Masokwe ) Sehemu Ya Tatu (3)
MTOTO wa Skyler, Harrison anazidi kukua vizuri licha ya kwamba alizaliwa katika mazingira magumu. Kwa kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele, ndivyo mtoto huyo
anavyozidi kuwa mkubwa, huku utundu ukiwa umemtawala. Anapotimiza miaka mitatu, anaandikishwa shule ya chekechekea.
Ile huzuni iliyokuwa imetanda kwenye maisha ya Skyler, sasa inaanza kupungua kwa jinsi alivyokuwa anafarijika akimtazama mwanaye huyo. Mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo kwa Harvey, sasa anayahamishia kwa Harrison.
Kumbukumbu juu ya wazazi wake, Dk Lewis na Suzan zinaanza kukisumbua kichwa chake. Anajiambia kuwa ameshawasamehe kwa yote yaliyotokea na anaanza kufikiria kurudi nyumbani kwao na kuwapelekea mjukuu wao, Harrison.
Upande wa pili, familia mpya ya Charwe na mkewe Anganile, inajaliwa kupata mtoto mzuri wa kike, Charlotte. Mwanaume anaendelea kufanya kazi Geneva, Uswisi na mwanamke anafanya kazi kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Hali hiyo inafanya
wawe wanasafiri kwa ndege mara kwa mara kwa ajili ya kutembeleana, hasa kipindi cha likizo au sikukuu.
MSIMU mwingine wa sikukuu uliwadia, Anganile akawa anajiandaa kwa safari ya kuelekea Geneva kwa mumewe, akiwa na mwanaye kipenzi, Charlotte ambaye alikuwa akizidi kukua, huku urembo na shani alivyojaliwa na Mungu vikizidi kujidhihirisha. Baada ya maandalizi yote kukamilika, Anganile aliwasiliana na mumewe, akamtumia tiketi ya ndege. Anganile akamchukua mwanaye pamoja na
zawadi nyingine walizomuandalia baba Charlotte, wakafunga safari mpaka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Walipofika kwenye ofisi za Shirika la Ndege la Uswisi (Swiss Airways), mhudumu aliyekuwepo aliwapa taarifa juu ya mabadiliko ya ratiba za ndege yaliyosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyozikumba nchi za Ulaya.
“Ukungu mwingi umetanda kwenye anga la nchi mbalimbali za Ulaya hususan Ufaransa, Sweden, Uholanzi na Uswisi mnakotaka kwenda. Kuepusha ajali za ndege zinazoweza kuzuilika, safari zote kuelekea Ulaya moja kwa moja kutoka Afrika zimesitishwa.
“Kampuni yetu imeamua wateja wote wanaosafiri kuelekea nchi za Ulaya waende mpaka New York, Marekani na baada ya hapo watahamishiwa kwenye ndege nyingine itakayowapeleka mpaka barani Ulaya. Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza,” alisema yule mhudumu, Anganile akashusha pumzi ndefu na kusogea pembeni na mwanaye.
Habari zile zikawa zinaendelea kutangazwa pale uwanja wa ndege kwa kutumia vipaza sauti vilivyokuwa kwenye kila kona. Abiria wengi walikumbwa na taharuki, wakawa na wasiwasi mkubwa juu ya usalama wao na mali zao CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Taarifa zile zilimchanganya sana Anganile, ikabidi awasiliane na mumewe Charwe kwa njia ya simu na kumueleza hali halisi. “Ni kweli kuna ukungu mzito huku, ndege nyingi zimesimamisha safari zake, ningeweza kusema muahirishe safari mpaka wakati mwingine lakini kwa kuwa nimewakumbuka sana na sikukuu zimekaribia, fuateni mlivyoambiwa na wahudumu wa ndege, kampuni yao ndiyo itakayogharamia kila kitu,” alisema Charwe.
Mkewe alienda kubadilisha tiketi ya ndege kama walivyoambiwa na baada ya kusubiri kwa saa moja, ndege kubwa ya Swiss Airways iliyokuwa inaelekea Marekani, ilianza kupakia abiria. Anganile na mwanaye wakawa ni miongoni mwa abiria walioingia kwenye ndege ile. Baada ya muda, safari ikaanza.
Baada ya safari ndefu iliyochukua takribani saa kumi angani, ndege ile iliwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa John F. Kennedy jijini New York, Marekani. Abiria wakaanza kuteremka mmoja baada ya mwingine, Anganile na mwanaye nao wakawa miongoni mwao.
Kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya zaidi kwenye nchi za Ulaya, ukungu ukiendelea kuwa tishio, ilibidi abiria wote waliokuwa wanaendelea na safari wapelekwe kwenye hoteli walizokuwa wanazitaka kwa gharama ya Kampuni ya Swiss Airways mpaka asubuhi ya siku ya pili.
Anganile na mwanaye walienda kupumzika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, New York ambapo asubuhi walikuja kuchukuliwa na kupelekwa tena uwanja wa ndege. Wakapandishwa kwenye ndege kubwa ya kisasa, Herpa Lufthansa Premium, toleo jipya namba C-47B-DK 1:200 iliyokuwa na uwezo wa kusafiri hata kwenye ukungu mzito.
Kwa kuwa kulikuwa na abiria wengine kutoka sehemu mbalimbali za dunia ambao nao walikuwa wamekwama kwenda nchi za Ulaya kutokana na hali ya hewa, ndege ilijaa yote. Ghorofa zote mbili, ya juu na ya chini zilishona abiria, muda mfupi baadaye safari ya kuelekea Geneva ikaanza. Ndege ikaanza kujongea taratibu na kugeuka kuelekea kwenye njia za kurukia (run ways), ikaanza kuongeza kasi huku injini zikizidi kuchanganya, sekunde chache baadaye ikapaa na kuiacha ardhi ya Marekani.
Muda mfupi baada ya ndege hiyo kuruka, marubani walianza kuhangaika kwani ukungu ulikuwa mzito kuliko walivyotegemea, hali iliyosababisha mawasiliano yawe magumu. Ndege ile, licha ya kuwa ilikuwa ni toleo jipya, ikiwa na taa maalum za kumulika kwenye ukungu na uwezo mkubwa wa kuhimili hali mbaya ya hewa, ilianza kuyumbayumba.
Abiria wakakumbwa na hofu kubwa, hali ya sintofahamu ikatanda kila mahali huku wakianza kusali kwa imani zao wakimuomba Mungu awanusuru na janga kubwa lililokuwa mbele yao.
Hali iliendelea vile kwa muda mrefu, hatimaye ndege ile ikapoteza mwelekeo na kuanza kuzunguka angani. Maafisa wa Uwanja wa Ndege wa John F. Kennedy kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Marekani, walipokea taarifa za ndege hiyo kupoteza mwelekeo, haraka wakaanza kuhangaika kuitafuta angani.
Mitambo iliyokuwa inaongozwa na satellite sambamba na wataalamu wa usafiri wa anga na wale wa vikosi vya uokoaji, walisaidiana na baada ya kuhangaika sana, walifanikiwa kutambua mahali ndege hiyo ilipokuwepo.
“Tunaiona ikiwa inazunguka kwenye ukungu mzito, juu ya msitu mkubwa wa Tongass, Kusini Mashariki mwa Jimbo la Alaska karibu na mpaka wa Marekani na Canada lakini tumepoteza kabisa mawasiliano na marubani,” alisema Kamanda wa Kikosi cha Uokoaji, Russel Winans, harakaharaka ndege za kijeshi za uokoaji zikaanza kuondoka kwa kasi kubwa kuelekea kwenye Msitu wa Tongass kuiokoa ndege ile kabla haijaanguka. ***
Harrison alizidi kuwa mkubwa, masomo ya shule ya awali aliyokuwa anasoma yakamfungua upeo wake wa kuelewa mambo kwa kiasi kikubwa. Akawa anaweza kuhesabu vizuri, kuwatambua wanyama na vitu mbalimbali. “Huyu mtoto anapenda sana kucheza na wanyama, atakuja kuwa daktari wa wanyama akiwa mkubwa.” “Akuu, mwanangu awe daktari wa wanyama? Mi nataka aje kuwa mtaalam mwenye kazi yake ya maana, siyo hiyo,” alisema Skyler wakati akizungumza na Scolastica.
Scolastica alimwambia Skyler ni vizuri kumtazama mtoto mapema na kumuongoza katika kipaji au karama aliyokuwa nayo. Waliendelea kuzungumza mambo mengi kuhusu mtoto yule. Kila Skyler alipokuwa akimtazama mwanaye, alikuwa akifarijika sana ndani ya moyo wake. Ile furaha iliyokuwa imetoweka kwa kipindi kirefu, ikawa inarejea na kumfanya ajione shujaa.
Siku zilizidi kusonga mbele, mawazo ya Skyler juu ya wazazi wake yakawa yanazidi kumsumbua kichwani. “Inabidi nirudi nyumbani,” aliwaza Skyler, akazungumza na Scolastica ambapo alimueleza mambo mengi kuhusu familia yao ambayo awali hakuwahi kuyasema. Scolastica alimsubiri mumewe Bill ambapo alimueleza kila kitu alichozungumza na Skyler. Wakakubaliana kuwa watamsindikiza ili nao wakafahamiane na wazazi wake kwani tayari walishakuwa kama ndugu.
“Kesho tunaenda kwa bibi na babu wengine, si kila siku unanisumbua,” Skyler alimwambia mwanaye wakati wakijiandaa kulala. Harrison alichekelea sana, japokuwa alikuwa mdogo, alikuwa akiweza kutofautisha na kuelewa mambo mengi.
Asubuhi na mapema, Skyler na mwanaye sambamba na walezi wake, Bill na Scolastica waliingia ndani ya gari la familia, safari ya kuelekea Miami ikaanza. Walisafiri kwa muda mrefu, hatimaye wakaanza kukaribia kufika.
“Hii ndiyo shule niliyokuwa nasoma,” alisema Skyler huku akiwaonesha Bill na Scolastica majengo ya shule iliyokuwa pembeni ya barabara. Aliwaelekeza njia za kupita na baada ya muda, wakawa tayari wameshaingia kwenye mtaa aliokuwa anaishi Skyler na wazazi wake. “Simama kwenye hilo geti hapo mbele,” Skyler alimuelekeza Bill aliyekuwa akiendesha gari. Gari likasimama ambapo Skyler ndiyo alikuwa wa kwanza kufika. Mazingira aliyoyakuta, yalimshtua kuliko kawaida.
Nyumba ilikuwa imechakaa, madirisha na milango vikiwa wazi kuonesha kuwa hakukuwa na watu waliokuwa wanaishi kwenye nyumba hiyo. Majani yalikuwa yameota karibu kila sehemu kuzunguka nyumba. Zile bustani za maua ambazo kipindi cha nyuma zilikuwa zikihudumiwa na kutunzwa vizuri, sasa ziligeuka na kuwa vichaka vya kutisha. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ FAMILIA mpya ya Charwe na mkewe Anganile inaingia kwenye msukosuko mkubwa baada ya ndege waliyokuwa wanasafiria Anganile na mwanaye Charlotte, Herpa Lufthansa Premium wakati wakiwa njiani
kwenda Geneva, kupoteza uelekeo ikiwa angani kutokana na ukungu mzito uliokuwa umetanda. Licha ya vikosi vya uokoaji kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wao wote kuiokoa ndege hiyo kabla haijapata ajali, ukungu unafanya zoezi liwe gumu. Inazidi kupoteza uelekeo, ikiwa kwenye anga la Msitu Mkubwa wa Tongass, kwenye Jimbo la Alaska nchini Marekani.
Upande wa pili, Skyler, mwanaye Harrison na walezi wake, Bill na Scolastica wanasafiri mpaka nyumbani kwa akina Skyler, Miami lakini wanapofika, wanakuta eneo lote likiwa kimya kabisa na kutawaliwa na upweke, hali inayoonesha kuwa hakuna mtu aliyekuwa akiishi ndani ya jengo hilo.
LICHA ya marubani wa ndege ile kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wao wote kupambana na hali mbaya ya hewa, bado hawakufanikiwa kuirudisha ndege kwenye mstari. Walizidi kusukumwa na upepo mkali ulioambatana na ukungu juu ya Msitu wa Tongass, Kusini Mashariki mwa Jimbo la Alaska karibu na mpaka wa Marekani na Canada.
“Injini moja ya kushoto imepoteza uwezo wake wa kufanya kazi. Lazima itakuwa imeingia maji kutokana na ukungu.” “Mungu wangu, sasa itakuwaje? Mi’ nashauri tutafute sehemu yenye uwazi tutue.” “Hatuwezi kutua, kuna ukungu mzito sana, tukiteremka mita chache kutoka hapa tulipo injini nyingine zote zitazima.” “Hebu tujaribu kuongeza joto kwenye injini ili kukausha ukungu unaosababisha maji kujaa,” marubani wa ndege ya Herpa Lufthansa Premium, toleo
jipya namba C-47B-DK 1:200 walikuwa wakijadiliana cha kufanya ili kuiokoa ndege ile ambayo sasa ilipoteza kabisa uelekeo. Muda mfupi baada ya injini ya kwanza kuzima, nyingine ilizima na kusababisha ndege nzima iwe inaendeshwa kwa injini mbili zilizosalia, tena zote zikiwa upande mmoja wa kushoto.
Vikosi vya uokoaji vikiongozwa na Kamanda wa Kikosi cha Uokoaji wa Anga, Russel Winans, vilikuwa vikiendelea kuhaha huku na kule kuitafuta ndege ile. Ndege za kijeshi zilizotumwa eneo la tukio kujaribu kuiokoa ndege ile, nazo zilimezwa na ukungu mzito, zikashindwa kuendelea na safari ya kuifuata ndege ile.
Mawasiliano pekee yaliyokuwa yamesalia, yakiwa yanaongozwa na satellite, nayo yalianza kusuasua, hali ya sintofahamu ikazidi kutawala kila sehemu. Baadhi ya vyombo vya habari vilianza kurusha habari ile, wananchi wengi wa Marekani na nchi jirani ambao ndugu zao walikuwa kwenye ndege ile wakazidi kuchanganyikiwa.
Charwe, akiwa ofisini kwake, alishtushwa na habari iliyokuwa inarushwa na kituo cha runinga cha CNN iliyoeleza juu ya ndege kubwa ya Herpa Lufthansa Premium iliyokuwa na zaidi ya abiria mia mbili, wakiwemo mkewe Anganile na mwanaye wa kipekee, Charlotte. “Mungu wangu, balaa gani tena hili,” alisema Charwe huku akiongeza sauti kwa kutumia rimoti, akasogea kwenye runinga huku akijishika mikono kichwani.
“No! Haiwezekani, haiwezekani,” alisema Charwe huku akizidi kuitumbulia macho runinga iliyokuwa ofisini kwake. Habari ile iliendelea kurushwa mara kwa mara, watu wengi wakawa wanaelewa kilichokuwa kinaendelea, huku kila mmoja akimuomba Mungu kwa imani yake ili kuzuia janga lile lisitokee.
“Tunawaomba watu wote watulie, kikosi cha uokoaji wa anga kinajitahidi kufanya kila linalowezekana ili kuiokoa ndege kabla haijapatwa na tatizo lolote. Tunaendelea kushughulika na bado abiria wote wapo salama ndani ya ndege,” alinukuliwa Kamanda wa Kikosi cha Uokoaji wa Anga, Winans wakati akizungumza na mtangazaji wa runinga ya CNN.
Licha ya kujaribu kuwapa moyo watu waliokuwa na ndugu zao ndani ya ndege hiyo, bado hali ya taharuki ilizidi kutawala, watu wakaanza kujikusanya kwenye vikundi mitaani, huku wakiwa makini kusikiliza kilichokuwa kinaendelea.
“Tangazo! Tangazo! Tangazo! Abiria wote tunaomba usikivu wenu. Ndege yetu imepatwa na hitilafu na hivi sasa inapita kwenye mkondo wa hewa unaokwenda kasi kutokana na ukungu. Tunaomba kila mmoja akae kwenye kiti chake na kujifunga mkanda ili kuipa ndege uzito unaotakiwa. Tunaomba kila mmoja afunge mkanda na kutulia,” mhudumu wa ndege ile alikuwa akijaribu kuwatuliza abiria.
“Mwanangu Charlotte, nakupenda sana mwanangu… sipo tayari kuona unapoteza maisha yako ukiwa na umri mdogo kiasi hicho. Ni bora nife mimi lakini nikuokoe wewe,” alisema Anganile huku akilengwalengwa na machozi. Alishakata tamaa ya kusalimika kwenye ajali ile, akajua kifo kipo mbele yake.
Muda mfupi baadaye, wahudumu wa ndege ile walianza kupita kwa abiria na kuwagawia maparachuti maalum ambayo wangeyatumia kutoka ndani ya ndege baada ya kukaribia kufika ardhini. “Tumelazimika kutua kwenye msitu wa Tongass kwa dharura, tukikaribia kufika ardhini milango itafunguliwa na abiria wote mtaruka na kutoka nje mkiwa kwenye maparachuti yenu,” alisikika rubani wa ndege ile akitoa maelekezo. Abiria wakayashika maparachuti yao na kusubiri maelekezo mengine.
Anganile aliamua kumvalisha mwanaye parachuti lile na kumfunga vizuri, Charlotte ambaye hakuwa akielewa chochote kutokana na umri wake mdogo, alikuwa akichekelea kuvalishwa parachuti na mama yake. Kufumba na kufumbua, ndege iligeuka kwa kasi kubwa na kuanza kulalia upande mmoja.
“Ooh shit! Injini zote zimezima, hatuna ujanja… eeeh Mungu onesha miujiza yako,” rubani mmoja alisema baada ya kugundua kuwa zile injini mbili zilizokuwa zimesalia, nazo zilikuwa zimeingia maji na kuzima. Ndege ikaanza kujigeuzageuza huku abiria wakichomoka kwenye viti vyao na kuanza kugongana wao kwa wao.
Kufumba na kufumbua, Anganile alikanyaga kioo kilichokuwa jirani na pale alipokuwa amekaa na mwanaye, alirudia kukanyaga kwa nguvu, kioo kikachomoka na kuachia nafasi, kwa ujasiri wa hali ya juu akalishika parachuti alilokuwa amemvalisha mwanaye Charlotte na kulisukumia pale kwenye uwazi, likatoka nje na kufunguka, akamsukumia mwanaye nje, akawa anaelea kwenye ukungu mzito. Charlotte akiwa ananing’inia kwenye parachuti, alisukumwa na upepo mkali kuelekea Magharibi mwa msitu huo.
Alipomaliza tu kufanya vile, Anganile alijaribu kusimama ili atafute parachuti lingine na kuvaa ili na yeye aruke nje ya ndege kama mwanaye lakini alichelewa kwani kufumba na kufumbua moto mkubwa ulianza kuwaka kutokea kwenye vyumba vya marubani, abiria wakawa wanakimbia huku na kule, ndege ikazidi kubiringika angani.
Moshi mzito ukatanda ndani ya ndege yote, abiria wakawa wanakohoa huku wengine wakianza kuzirai na kupoteza fahamu. Muda mfupi baadaye ndege yote ikalipuka, moto mkubwa ukawa unaonekana juu ya anga la Msitu wa Tongass. “Oooh Mungu wangu, ule moshi kule ni wa nini?” alisema Kamanda Winans aliyekuwa ndani ya ndege ya kijeshi iliyokuwa jirani na pale ndege ile kubwa ilipokuwepo. Alipotoa darubini yake iliyokuwa na uwezo wa kupenya hata kwenye ukungu, alishuhudia ndege hiyo ikiteketea kwa moto mkubwa.
“Herpa Lufthansa Premium inateketea kwa moto, hatuna la kufanya kwani ipo kwenye mkondo wa hewa inayosafiri kwa kasi, moto mkubwa umetanda angani,” alisema Kamanda Winans wakati akitoa taarifa kwa wenzake waliokuwa ardhini. Habari zikasambaa kwa kasi, taifa la Marekani likaingia kwenye maombolezo makubwa. Hakukuwa na uwezekano wa abiria hata mmoja kuokolewa kutoka kwenye ndege ile.
Ndege iliendelea kuteketea kwa moto mkubwa, baadhi ya vyuma vya ndege vikaanza kujiachia na kudondoka mpaka kwenye msitu mnene wa Tongass. Baada ya kuungua yote, vyuma na majivu viliendelea kudondoka ardhini. Hapakuwahi kutokea ajali mbaya ya ndege kama ile nchini Marekani.
Vyombo vya habari viliendelea kuripoti habari ile ambayo ilitangazwa kama janga la kitaifa, bendera zote za Marekani zikashushwa nusu mlingoti kama ishara ya maombolezo.
Charwe alishindwa kuamini macho yake wakati Kituo cha Runinga cha CNN kilipokuwa kikirusha picha zilizopigwa kutoka ardhini, zikiionesha ndege ile wakati ikiteketea kabla haijageuka kuwa majivu. “Nooo! Haiwezekaniii, mke wangu na mwanangu jamaniii!” alipiga kelele Charwe, akadondoka na kupoteza fahamu.
AJALI mbaya ya ndege ya Herpa Lufthansa Premium iliyosababishwa na ukungu mzito uliokuwa umetanda angani, inasababisha pigo kubwa kwa Charwe kwani anampoteza mkewe kipenzi na mwanaye, Charlotte waliokuwa njiani kuelekea Geneva kumfuata Charwe.
Jitihada za vikosi vya uokoaji zinashindwa kuzaa matunda na watu wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo, wanapoteza maisha na kuteketea ndani ya ndege hiyo. Upande wa pili, Skyler anaamua kurejea nyumbani kwao akiwa na walezi wake, Bill na Scolastica na
mwanaye Harrison lakini tofauti na alivyotegemea, anakuta nyumba yao ikiwa imetawaliwa na upweke wa hali ya juu. Inavyoonesha, hakuna mtu aliyekuwa akiishi ndani ya nyumba ile.
LICHA ya vikosi vya uokoaji kufika eneo la tukio, hakuna mtu wala kitu chochote kilichookolewa kutoka kwenye ndege ile, vyuma, mafuvu ya binadamu na mifupa vikawa vinadondoka kutoka angani na kuangukia kwenye msitu mkubwa wa Tongass. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Tangu nianze kazi ya uokoaji wa anga sijawahi kuona ajali mbaya kama hii. Yaani abiria wote wameteketea kwa moto wakiwa angani? Hii imevunja rekodi,” Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Uokoaji wa Angani, Russell Winans alisema wakati akitembea kwa miguu na kikosi cha askari waliokuwa wa kwanza kufika eneo la ajali, ndani kabisa ya msitu wa Tongass.
Vyombo vya habari viliendelea kuripoti hatua kwa hatua juu ya kilichokuwa kinaendelea, maombolezo yakaendelea huku watu waliopoteza ndugu zao wakielekezwa kuelekea kwenye Ukumbi wa Madison Square ambapo mabaki yaliyokuwa yanaendelea kuokotwa eneo la tukio yalipelekwa.
Maelfu ya waombolezaji wakiwa wamevalia mavazi meusi wakawa wanaongozana kuelekea katikati ya Mtaa wa Manhattan jijini New York. Maombolezo yakaendelea, bendera zote zikawa zinapepea nusu mlingoti.
Baada ya kurejewa na fahamu, Charwe alijikuta akiwa kwenye chumba chenye mashuka meupe, huku pembeni yake akiwa amezungukwa na wafanyakazi wenzake. “Hapa ni wapi na nimefikaje?” “Upo hospitalini Charwe, umekutwa ukiwa umedondoka na kuzimia nyumbani kwako.” “Ahaaa,” alisema Charwe huku akionekana kuanza kuvuta kumbukumbu ya kilichotokea. “Kwani umepatwa na tatizo gani?” “Mke wangu na mwanangu, oooh! Mungu wangu, kwani haya yanitokee mimi?” “Unamaanisha nini Charwe? Tuambie ili kama ni msaada tujue tunaanzia wapi.” “Mke wangu na mwanangu ni miongoni mwa abiria waliopata ajali na ndege ya Herpa Lufthansa Premium, wote wamekufaaaaa,” alisema Charwe huku akilia kwa uchungu, wafanyakazi wenzake wakawa na kazi ya ziada kumtuliza.
Ilibidi taratibu za kiofisi zifanyike haraka, Charwe akakatiwa tiketi ya ndege kutoka Geneva mpaka jijini New York kuungana na waombolezaji wengine kwenye Ukumbi wa Madison Square. Akasindikizwa na wafanyakazi wenzake wawili mpaka New York, wakaungana na maelfu ya waombolezaji waliokuwa wanaendelea kumiminika kuangalia mabaki ya ndugu zao Madison Square.
Baada ya mabaki karibu yote yaliyokuwa yametapakaa kwenye eneo la tukio kukusanywa, makaburi ya halaiki yalianza kuchimbwa nje kidogo ya Jiji la New York. Siku tatu baadaye, mazishi ya pamoja yakafanyika, majina ya watu wote waliokuwepo ndani ya ndege yakaandikwa na kubandikwa kwenye kuta zilizojengwa kuzunguka makaburi yale.
Baada ya taratibu zote za mazishi kukamilika jijini New York, Charwe alilazimika kusafirisha msiba mpaka Tanzania na kwenda moja kwa moja mkoani Mbeya, nyumbani kwa mkewe Anganile. Kwa kuwa tayari alishawasiliana nao kwa njia ya simu, msiba ulikuwa ukiendelea.
Alipofika, alipokelewa kwa vilio na maombolezo na ndugu wa mwanamke sambamba na ndugu zake waliosafiri kutoka Bukoba, msiba ukawa ndiyo kama umeanza upya. Pigo lilikuwa kubwa sana kwa Charwe kwani mbali na mke, alimpoteza mwanaye kipenzi Charlotte kwenye ajali hiyo.
Kwa jinsi alivyokuwa akimpenda mkewe na mwanaye, Charwe aliweka nadhiri ya kukaa siku arobaini nyumbani kwa marehemu mkewe. Alitimiza nadhiri yake na baada ya siku arobaini kuisha, walimsomea marehemu dua kisha akasafiri mpaka nyumbani kwao Bukoba alikokaa siku tatu kisha akapanda ndege kurejea kazini kwake, Geneva nchini Uswisi. *** Baada ya kuona mazingira ya pale nyumbani kwao jinsi yalivyokuwa, Skyler aliwashauri Bill na mkewe wajaribu kwenda kazini kwa baba yake ili kujua kama kuna taarifa zozote zilizokuwa zinamhusu Dk Lewis na mkewe.
“Watakuwa wamepatwa na nini?” alijiuliza Skyler wakati gari walilokuwa wanasafiria likikatiza mitaa kuelekea Miami Hospital, alipokuwa anafanya kazi Dk Lewis. Walipofika, Bill na mkewe walibaki ndani ya gari pamoja na mtoto wa Skyler, Harrison. Akateremka na kuanza kutembea harakaharaka kuelekea mapokezi.
Kila mtu aliyekuwa anakutana naye, alikuwa akimshangaa Skyler, akajikaza na kutoonesha mshtuko wowote. Alipofika mapokezi, alimkuta msichana ambaye ilionesha kuwa ndiyo kwanza anaanza kazi. Skyler akashusha pumzi ndefu kwani alijua kuwa endapo angemkuta mtu anayemjua, angeanza kumhoji maswali ya mahali alipokuwa siku zote hizo, jambo ambalo lingemkasirisha. “Namuulizia Dokta Lewis.” “Wewe ni nani?”
“Mwambie naitwa Skyler,” alijibu huku akikwepesha sura yake. Hakutaka yule dada aendelee kumtazama usoni. Alinyanyua mkonga wa simu na kuzungumza na upande wa pili kisha akakata. “Mbona ameshtuka sana nilipomtajia jina lako?” “Sijaonana naye siku nyingi.”
“Anasema anakuja sasa hivi,” alijibu yule dada, Skyler akasogea pembeni na kukaa huku muda mwingi akiwa amejiinamia chini. Sekunde chache baadaye, mwanaume wa makamo aliyekuwa amevalia kidaktari alikuja huku akiwa anakimbia. Alikuwa ni Dokta Lewis ambaye taarifa za uwepo wa Skyler hospitalini pale alizipokea kama muujiza.
“Yuko wapi? Yuko wapi Skyler wangu?” Dokta Lewis alimuuliza yule dada wa mapokezi huku akigeuka huku na kule. “Babaaaaaa,” alisema Skyler baada ya kumuona baba yake, akasimama na kumkimbilia. Dokta Lewis aligeuka, akakutana na Skyler aliyekuwa anakuja mbio, wakakimbiliana na kukumbatiana kwa nguvu. Kila mmoja akawa anatokwa na machozi.
“Nisamehe mwanangu, nisamehe kwa yote, nakupenda sana Skyler,” alisema Dk Lewis huku akiwa bado amemkumbatia mwanaye Skyler. “Nilishakusamehe baba na wewe naomba unisamehe kwa yote.”
“Nilishakusamehe mwanangu… vipi mjukuu wangu yuko wapi? Au hukujifungua?” aliuliza Dk Lewis huku akimtazama mwanaye tumboni.
“Sikwambii chochote mpaka uniambie mama yuko wapi na siku hizi mnaishi wapi kwani nimepita nyumbani nimekuta hali ya ajabu sana,” alisema Skyler huku akijifuta machozi yaliyokuwa yanaulowanisha uso wake.
Dokta Lewis alishusha pumzi ndefu, akamtazama mwanaye na kurudia kumkumbatia, wakashikana kwa muda mrefu bila kuzungumza chochote. Dokta Lewis alimshika mwanaye mkono, akamuongoza kwenda kwenye bustani za maua zilizokuwa jirani na pale walipokuwa wamesimama, ndani ya Hospitali ya Miami.
“Ni stori ndefu mwanangu, kutoweka kwako kulisababisha matatizo makubwa kwenye familia yetu. Namshukuru sana Mungu kwamba umerejea, naamini bado nina nafasi ya kuisimamisha upya familia yangu.” “Unamaanisha nini baba? Mbona sikuelewi?”
“Mimi na mama yako tumetengana, ilibidi nimpe talaka mahakamani. Mama yako alikuwa anakupenda sana hivyo ulipoondoka, alinichukia mno akiamini mimi ndiyo chanzo cha matatizo. Alinipa masharti ya kuhakikisha nakupata na hilo liliposhindikana akanipeleka mahakamani na kudai talaka.
“Vitu vyote tulivyochuma pamoja maishani ilibidi tugawane, vingine tukauza na kubakiza kitu kimoja tu, nyumba ambapo hata hivyo tulikuwa kwenye mipango ya kuiuza lakini tukakosa mteja kutokana na bei yake kuwa kubwa. Hivi sasa mimi naishi mwenyewe na mama yako alirudi nyumbani kwao,” alisema Dokta Lewis huku naye akibubujikwa na machozi.
Skyler hakujibu wala kuchangia kitu, akampeleka baba yake kwenye gari la Bill na mkewe lililokuwa limepaki nje ya hospitali ile. “Hawa ndiyo walezi wangu walioniokota nikiwa kwenye hatua za mwisho za maisha yangu na kunitunza mpaka leo,” alisema Skyler
lakini kabla hajamaliza kumtambulisha, macho ya Dokta Lewis yalitua kwa mtoto aliyekuwa amekaa siti ya nyuma. “Mh! Hii sura mbona imefanana sana na Harvey? Huyu ndiyo mjukuu wangu nini?” “Mbona una haraka baba? Tulia nikutambulishe mwenyewe. Huyo ndiyo mjukuu wako, anaitwa Harrison.
“Mbona amekuwa mkubwa hivi? alisema Dokta Lewis, Skyler akafungua mlango wa gari na kumtoa mwanaye, na kumtambulisha kwa babu yake.
“Harvey ‘copyright’! Kweli Mungu ana miujiza yake… naamini bibi yake akimuona hasira zake zote zitaisha na atakubali kurudiana na mimi,” alisema Dokta Lewis huku akimrusharusha Harrison. Lile tabasamu ambalo lilipotea kwa kipindi kirefu kwenye maisha yake, sasa lilichanua upya kama lichanuavyo waridi.
AJALI mbaya ya ndege ya Herpa Lufthansa Premium iliyolipuka angani baada ya kupoteza mwelekeo kutokana na ukungu mzito uliokuwa umetanda, inasababisha pigo kubwa kwa Charwe aliyewapoteza mke na mwanaye waliokuwa njiani kumfuata jijini Geneva ili washerehekee pamoja Sikukuu ya Krismasi.
Abiria wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo wanapoteza maisha na hakuna kinachookolewa zaidi ya mabati na vyuma vya ndege sambamba na mafuvu ya binadamu yaliyokuwa yanaangukia kwenye Msitu wa Tongass. Msiba mkubwa unalikumba taifa la Marekani na nchi nyingine ambazo raia wake walipoteza maisha kwenye ndege hiyo. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Upande wa pili, Skyler, mwanaye Harrison na walezi wake, Bill na Scolastica, baada ya kukuta mazingira yasiyoeleweka nyumbani kwa akina Skyler, wanafunga safari mpaka kwenye Hospitali ya Miami, alikokuwa anafanyia kazi Dk Lewis na wanafanikiwa kukutana naye. Haamini macho yake kama kweli amekutana tena na Skyler, tena akiwa amemletea mjukuu wa kiume aliyefanana kwa kiasi kikubwa na Harvey.
BAADA ya kuzungumza mambo kadhaa, Dk Lewis alirudi ofisini kwake na kuomba ruhusa, akatoka hadi pale nje alipokuwa amewaacha Skyler, Harrison, Bill na mkewe Scolastica. Akawachukua Skyler na mwanaye na kuwapakiza kwenye gari lake, akawataka Bill na mkewe Scolastica nao waingie kwenye gari lao na wamfuate.
Msafara wa magari mawili ukatoka kwenye lango kuu la Hospitali ya Miami na kukata kona upande wa kushoto. Wakaingia kwenye barabara na kusafiri umbali wa takriban kilometa tano, Kaskazini mwa Jiji la Miami. Ndani ya gari, Dk Lewis aliendelea kuchekacheka mwenyewe akiwa kama haamini kilichotokea.
Mara kwa mara alikuwa akimtazama mwanaye na mjukuu wake huku akiwa na tabasamu pana kwenye uso wake. “Naitwa babu sasa! Hongera sana mwanangu kwa kumleta upya Harvey! Nisamehe kwa yote yaliyotokea, naamini Mungu alikuwa na makusudi yake kuacha haya yote yatokee,” alisema Dk Lewis huku akikata kona na kuingia upande wa kulia, akazipita nyumba kadhaa kabla ya kuegesha gari mbele ya nyumba ndogo iliyokuwa na rangi ya bluu.
“Hapa ndipo ninapoishi tangu nilipotengana na mama yako, nimepanga,” alisema Dk Lewis wakati akipaki gari vizuri, akateremka na kuwaelekeza Bill na mkewe Scolastica namna ya kupaki gari lao. Alipomaliza, aliwafungulia mlango Skyler na mjukuu wake Harrison, akambeba juujuu huku akiendelea kumrusharusha.
“Karibuni sana, hapa ndiyo ninapoishi,” alisema Dk Lewis wakati akiwakaribisha Bill na mkewe, akafungua mlango mkubwa na wote wakaingia. Ilikuwa ni nyumba ndogo lakini yenye kila kitu muhimu. Wakaingia na kukaa sebuleni, Dk Lewis akafungua friji na kutoa jagi lililokuwa na juisi, akawatolea glasi na kuwamiminia kila mtu ya kwake. “Baba nani kakutengenezea juisi?”
“Nimetengeneza mwenyewe, mbona hata chakula huwa napika mwenyewe na kuosha vyombo!” alisema Dk Lewis huku akiendelea kucheza na mjukuu wake Harrison, wote wakacheka kwa furaha na kumsifia kutokana na kutengeneza juisi nzuri kiasi kile. Waliendelea na mazungumzo, Dk Lewis akisimulia jinsi alivyohangaika baada ya mwanaye kutoweka bila kutoa taarifa.
Baada ya mazungumzo marefu, Bill na mkewe Scolastica waliaga na kuondoka, wakaahidi kuendelea kuwatembelea mara kwa mara. Waliwasindikiza mpaka getini kisha Dk Lewis, mwanaye Skyler na mjukuu wake Harrison wakarudi ndani. “Hapa kazi kubwa iliyobaki ni kumfuata mama yako nyumbani kwao, naamini akikuona atabadilisha uamuzi wake na kukubali kuishi tena na mimi,” alisema Dk Lewis, bila kupoteza muda wakaanza kujiandaa tayari kwa safari ya kuelekea Wisconsin, nyumbani kwa wazazi wa Suzan.
Walitoka hadi nje na kuingia ndani ya gari la Dk Lewis, safari ikaanza. Dk Lewis alikuwa makini kwenye usukani, kila mmoja akawa kimya ndani ya gari isipokuwa Harrison ambaye alikuwa akiendelea kucheza na midoli iliyokuwa ndani ya gari lile. Baada ya muda, waliwasili nyumbani kwa wazazi wa mama Skyler, wakapokelewa kwa ukarimu huku kila mmoja akimshangaa
Skyler na mwanaye. Waliambiwa kuwa mama Skyler alikuwa bado hajarudi kutoka kazini ingawa huo ndiyo ulikuwa muda wake. “Sasa hivi atakuja, wala msiwe na wasiwasi, alisema mama mwenye nyumba na kuungwa mkono na mumewe ambao kwa pamoja umri ulikuwa umewatupa. Dk Lewis akaanza kueleza kilichomkuta Skyler na jinsi walivyokutana upya baada ya kupotezana kwa kipindi kirefu. Akiwa anaendelea kusimulia, wote walisikia honi ya gari kutoka getini.
“Huyo anakuja,” alisema bibi yake Skyler huku akitoka mbiombio kwenda kumfungulia mwanaye. Geti lilipofunguliwa, Suzan aliingiza gari mpaka eneo la maegesho na kulipaki, akatoka na mkoba wake na kwenda kusalimiana na mama yake. “Kuna wageni ndani, sikwambii ni akina nani nataka ukajionee mwenyewe,” alisema huku akimshika mkono Suzan, akaingia naye ndani.
“Whaaat? Naota au ni kweli? Nooooooo!” alipiga kelele Suzan baada ya kumuona Skyler amembeba mtoto, huku pembeni yake akiwa amekaa mtalaka wake, Dk Lewis. Kutokana na mshtuko mkubwa alioupata, mama Skyler alianguka chini kama mzigo na kupoteza fahamu, wote wakainuka na kukimbilia pale alipokuwa ameangukia, wakaanza kumpepea ili azinduke.
Licha ya kumpepea kwa muda mrefu, bado hakuzinduka, Skyler na bibi yake wakawa wanalia huku Dk Lewis na babu yake Skyler wakihangaika kumuinua na kumpeleka kwenye gari, tayari kwa safari ya kuelekea hospitali iliyokuwa jirani. Muda mfupi baadaye, tayari wote walikuwa ndani ya gari wakielekea hospitali. Dk Lewis ndiyo alikuwa akiendesha huku mkwe wake akiwa amekaa pembeni. Skyler na bibi yake walikuwa wamekaa na mgonjwa wakiendelea kumpepea.
Baada ya kuwasili hospitali, walipokelewa na wahudumu wachangamfu, Suzan akapandishwa kwenye kitanda cha magurudumu na kukimbizwa wodini.
“Hana tatizo kubwa, vipimo vinaonesha amepatwa na mshtuko, msijali atakuwa sawa,” alisema daktari aliyekuwa anamhudumia. Akalazwa wodini huku dripu za maji na dawa zikiendelea kutiririka mishipani mwake. Baada ya kulazwa kwa zaidi ya saa tatu, Suzan alipiga chafya na kuzinduka, akawa anapepesa macho huku na kule kama anayejiuliza pale ni wapi na amefikaje. Ilibidi watu wote watolewe wodini wakihofia anaweza kupata mshtuko mwingine, akabakia mtu mmoja tu, mama yake.
“Pole mwanangu, usijali, utapona tu,” alisema mama yake huku akimpapasa shingoni kwa upendo, Suzan akawa bado anavuta kumbukumbu na kujaribu kukumbuka kilichotokea mpaka akawa na hali kama ile. “Mama, ni kweli nimemuona Skyler akiwa na mtoto au nilikuwa naota?” “Ni kweli mwanangu, mwanao hakufa kama ulivyokuwa unahisi, ni stori ndefu lakini ukweli ni kwamba Skyler amerudi, tena akiwa na mtoto wa kiume.”
“Ooh! Ahsante Mungu, nilishamhukumu mume wangu bureee! Ningesikiliza ushauri wako huenda mpaka leo tungekuwa tunaishi pamoja.”
“Wala hakijaharibika kitu, talaka iliyotolewa mahakamani inaweza kubatilishwa kwa wahusika kula viapo na kuthibitisha mahakamani kama mmemaliza tofauti zilizofanya mpeane talaka. Kama upo tayari nitalisimamia hili.” “Mi siwezi kusema kitu kwa sababu sijazungumza chochote na mume wangu na sijui kama hakuoa tena baada ya kuachana na mimi.”
“Mumeo kasema bado anakupenda na ndiyo maana ameamua kumleta Skyler na mwanaye ili uwaone na kubatilisha uamuzi wako. Ukipona utamsikia mwenyewe akisema kuwa bado anakuhitaji,” alisema mama Suzan huku akiendelea kumpapasa mwanaye shingoni. ***
Baada ya kurushwa dirishani na mama yake, muda mfupi kabla ajali haijatokea, huku akiwa amevaa parachuti, Charlotte alipulizwa na upepo mkali na kupelekwa upande wa Magharibi ya msitu wa Tongass, mbali kabisa kutoka eneo ilipotokea ajali ya ndege ya Herpa Lufthansa Premium.
Aliendelea kuelea angani kwa saa nyingi, sauti ikamkauka kutokana na kulia kwa muda mrefu na kupulizwa na upepo mkali ulioambatana na ukungu mzito. Kutokana na umri wake mdogo, tena akiwa hajazoea kukaa kwenye baridi kali, Charlotte alipoteza fahamu akiwa angani, hakuelewa tena kilichoendelea.
Alikuja kushtuka saa nyingi baadaye na kujikuta akiwa amelala kwenye nyasi ndefu, huku parachuti lake likiwa limeanguka mita chache kutoka pale alipokuwa. Licha ya umri wake mdogo, Charlotte alisimama na kujifikicha macho, akajivua kamba za parachuti na kukaa pembeni, akawa analia huku akimtaja mama yake.
Akiwa anaendelea kulia, alisikia sauti za wanyama wa porini ambao hakuwatambua, zile sauti zikawa zinazidi kusogea huku nyasi na vichaka vilivyokuwa jirani na pale alipokuwa amesimama, vikitingishika. Alijaribu kuinua shingo yake ili aone ni wanyama gani
lakini hakufanikiwa kuona chochote kutokana na ufupi wake. Zile sauti zilizidi kusogea, vichaka vikawa vinazidi kutingishika, mara akajikuta amezungukwa na wanyama ambao kutokana na umri wake mdogo, hakuweza kuwatambua.
BAADA ya kutengana kwa miaka kadhaa kutokana na kupotea kwa mtoto wao wa kipekee, Skyler, hatimaye Dk Lewis na Suzan wanakutana na kuanza kupanga mikakati ya kuijenga upya familia yao. Kupatikana kwa
Skyler, tena akiwa na mtoto aliyekuwa akifanana kwa kiasi kikubwa na marehemu baba yake, Harvey kunaonekana kuwa faraja kubwa kwa wote.
Mama Skyler ambaye awali alipatwa na mshtuko uliosababisha apoteze fahamu baada ya kumuona mwanaye katika mazingira ambayo hakuyategemea, anapelekwa hospitali na baada ya muda anapata CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ nafuu na kurudishwa nyumbani. Mwanaye anamsimulia kila kitu kilichotokea baada ya kuondoka nyumbani. Wanaombana radhi na sasa wanakubaliana kufungua ukurasa mpya wa maisha yao. Suzan anakubaliana na Dk Lewis kwenda kuvunja talaka mahakamani na kula kiapo kipya cha kuishi pamoja kama mume na mke.
KWA kutumia gari la Dk Lewis, walisafiri mpaka kwenye Mahakama ya Miami County High Court na kwenda moja kwa moja kwenye kitengo cha viapo. Wakaeleza shida yao ambapo karani waliyemkuta aliwaelekeza kwenda chumba namba 7113.
“Karibuni sana, niwasaidie nini?”aliuliza mwanamke wa makamo aliyekuwa amekaa nyuma ya meza kubwa ya mapokezi. “Mimi na mwenzangu tulipeana talaka lakini sasa tumeamua kurudiana,” alisema Dk Lewis huku akimpapasa Suzan mgongoni kimahaba.
Yule mwanamke aliwatazama mmoja baada ya mwingine kisha akawaelekeza kwenye ofisi ya Jaji Valentine Powell aliyekuwa akishughulika na viapo vya ndoa, talaka na kadhalika. Waliongozana na baada ya muda mfupi waliingia ndani ya ofisi hiyo, wakapokelewa na mwanaume mzee mwenye mvi nyingi kichwani. Dk Lewis akaanza kueleza kilichowapeleka.
“Kitu gani kilichosababisha muachane na sasa kitu gani kinachowafanya mtake kurudiana?” “Tulikuwa na matatizo ya kifamilia lakini tayari tumeshayamaliza na hayawezi kujirudia tena,” alisema Dk Lewis kwa kujiamini. “Kwa kawaida ili kuvunja talaka inabidi mle kiapo mbele ya mashahidi halafu baada ya hapo mtakula kiapo kingine cha ndoa ya mkataba.” “Ndoa ya mkataba?”aliuliza Suzan kwa mshangao.
“Ndiyo, mkishapeana talaka sheria ya ndoa inasema mkirudiana inabidi ndoa yenu iwe ya mkataba na mtakuwa mkiuongeza kwa kadiri mtakavyokuwa mnaishi kwa maelewano,” alijibu Jaji Powell, Suzan na Dk Lewis wakatazamana kwa sekunde kadhaa kisha wakatingisha vichwa vyao kuonesha kuwa wameridhia.
Walitoka kwenda kutafuta wadhamini na baada ya muda wakarudi na kula kiapo cha kuvunja talaka, wakapewa fomu maalum ya kusaini wao na wadhamini wao. Walipomaliza walipewa fomu nyingine ya ndoa ya mkataba, Jaji Powell akawaongoza kula kiapo kisha wakasaini kwenye zile fomu.
“Sasa mmehalalishwa kuwa mke na mume kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1972, kipengele kidogo cha 3b,” alisema Jaji Powell.
Baada ya shughuli ile, Suzan alimrukia Dk Lewis, wakagonganisha ndimi zao na kuanza kuelea kwenye ulimwengu wa mahaba. Walikaa kwenye hali ile kwa zaidi ya dakika mbili, wakaachiana na kuanza kutazamana kama majogoo yanayotaka kupigana.
“Siamini macho yangu kama umerudi kwenye mikono yangu,”alisema Dk Lewis huku akilengwalengwa na machozi. “Mimi mwenyewe siamini, naahidi nitalilinda penzi lako mpaka siku nafukiwa kaburini, tusahau yote yaliyopita na tufungue ukurasa mpya,” alijibu Suzan huku naye akitokwa na machozi ya furaha. Akatoka huku wakiwa wamekumbatiana mpaka kwenye gari lao.
Safari ya kurudi nyumbani kwa Dk Lewis ilianza na baada ya muda wakawa tayari wameshawasili. Walipitiliza moja kwa moja mpaka chumbani wakajifungia.
Baada ya kukaa chumbani kwa saa nyingi wakiwa peke yao, baadaye walitoka wakiwa wamechoka na kuingia ndani ya gari, wakaondoka na kurejea nyumbani kwa wazazi wa Suzan ambapo waliwakuta wote wakiwasubiri kwa hamu.
“Vipi mmefikia wapi?” aliuliza mama Suzan, mwanaye akamjibu kuwa kila kitu kimeenda kama kilivyopangwa na tayari wameshakuwa mume na mke halali. Kila mmoja akashangilia kwa nguvu, wakawakumbatia na kuanza kuimba nyimbo za furaha. Shangwe ziliendelea mpaka usiku sana.
Wakaruhusiwa kuondoka pamoja lakini Skyler na mwanaye Harrison wakalazimika kubaki palepale. Kesho yake kulifanyika sherehe ndogo ya kuwapongeza, wakafungua ukurasa mpya wa maisha ya ndoa.
Sherehe ilipoisha, waliwachukua Skyler na mwanaye Harrison na kurudi nao mpaka pale Dk Lewis alipokuwa anaishi. Kwa kuwa nyumba ilikuwa ndogo, walikubaliana kwenda kuikarabati nyumba yao waliyokuwa wanaishi kabla hawajatengana. Mafundi wakatafutwa ambapo kazi ya ukarabati ilianza haraka. Madirisha na milango ambavyo vilikuwa vimeharibika vikarudishiwa upya, kuta za ndani na nje zikapakwa rangi na kuifanya nyumba ionekane mpya.
Dk Lewis aliomba likizo ya dharura kazini kwao, mama Skyler naye akafanya hivyohivyo, siku chache baadaye wakahamia kwenye makazi mapya na kuyaanza maisha ya kifamilia, safari hii wakiwa na mtu aliyeongezeka, Harrison.
Kwa kuwa Harrison tayari alikuwa ameanza masomo ya chekechea wakiwa nyumbani kwa Bill na mkewe, ilibidi taratibu zifanyike za kumhamishia jirani na pale nyumbani kwao, akaendelea na masomo kwenye shule ya Miami Kindergaten.
“Sikuwahi kutegemea kuwa familia yangu inaweza kurudi na kuungana pamoja kama hivi, namuomba Mungu hii furaha tuliyonayo iendelee miaka yote,” alisema Dk Lewis jioni moja wakati wakipata chakula cha usiku.
“Hata mimi sikutegemea mume wangu, naamini sote tumejifunza jambo kwa haya yaliyotokea,” alisema Suzan, wakaendelea kula chakula cha usiku.
Siku zilizidi kusonga mbele, maisha yao yakazidi kutawaliwa na amani, upendo na furaha. Baada ya muda, likizo zao ziliisha, wakalazimika kurudi kazini huku Skyler akibaki nyumbani. Harrison akawa anazidi kukua huku akili yake nayo ikipevuka kutokana na masomo ya chekechea aliyokuwa anafundishwa. “Mume wangu, mi nilikuwa na wazo.” “Wazo gani mke wangu kipenzi?”
“Huyu Skyler mi sifurahishwi na yeye kuendelea kukaa nyumbani. Kwa nini tusimtafutie shule ili aendelee na masomo yake?” “Hata mimi nilikuwa nawaza hivyo mke wangu, nafikiri ni jambo la msingi sana. Ila umeshazungumza naye na kumsikia anasemaje?” “Hapana, lakini kwa sababu wote tupo, nafikiri huu ndiyo muda muafaka wa kumuita na kumuuliza,” alisema Suzan, akainuka na
kwenda kumuita Skyler aliyekuwa akiendelea kucheza na mwanaye Harrison. Walikaa naye na kumweleza walichokuwa wamekiamua, naye akaonesha kufurahishwa sana na uamuzi ule wa wazazi wake.
“Nataka niendelee na masomo ya sekondari kuanzia pale nilipokuwa nimeishia, bado nina ndoto kubwa kwenye maisha yangu na elimu pekee ndiyo itakayonifanya niweze kuzitimiza,” alisema Skyler huku akionesha kufurahishwa sana na uamuzi ule.
Taratibu za kumrudisha shuleni zilifanyika, akatafutiwa shule ya kulipia, tofauti na ile aliyokuwa anasoma awali. Baada ya wiki kadhaa, akaendelea na masomo ya sekondari, safari hii akiwa na uchungu na elimu kuliko kawaida. Harrison naye aliendelea na masomo na baada ya miezi kadhaa, aliandikishwa kuanza darasa la kwanza. ***
Charlotte aliendelea kupiga kelele na kumuita mama yake lakini hakuna mtu aliyemsikiliza, wale wanyama wakamzunguka na kuanza kumshangaa. Waliendelea kumzunguka lakini hawakumdhuru, baada ya kumshangaa kwa muda mrefu, mnyama mmoja aliyeonekana kuwa mkubwa kuliko wengine alimshika Charlotte kama afanyavyo mama kwa mwanaye na kumuweka mgongoni.
Wakaondoka kundi zima na kutokomea ndani kabisa ya Msitu wa Tongass, wakawa wanaruka kwenye matawi ya miti huku mnyama yule mkubwa akiwa makini kuzuia Charlotte asidondoke.
Licha ya awali kujawa na hofu juu ya usalama wake, taratibu Charlotte alianza kuwazoea wale wanyama, ile hofu aliyokuwa nayo ikaisha hasa baada ya kugundua kuwa wanyama wale hawakuwa na lengo la kumdhuru. Akaanza kuzoea kushinda nao, siku zote akiwekwa katikati yao, akilishwa mizizi na matunda ya porini kama wao walivyokuwa wanakula.
Kilichomtesa ni kwamba hawakuwa na nyumba au pango la kujisitiri wakati wa mvua au baridi kali, akawa anateseka lakini taratibu alianza pia kuzoea hali ile. Akaanza kujifunza kuruka kwenye matawi ya miti kama viumbe wale, akaanza kujiona kama hana tofauti yoyote. Hayo ndiyo yakawa maisha yake mapya.
Siku zilizidi kusonga mbele, Charlotte akawa anazidi kukua huku haiba na tabia za kibinadamu zikitoweka kwenye maisha yake na kuishi kama wale wanyama. Kilichompa faraja ni kwamba kila kulipotokea hatari yoyote, wale wanyama walikuwa wakimthamini yeye kuliko kitu kingine chochote. Akawa anazidi kuwa mkubwa.
HAKUNA marefu yasiyo na ncha, walinena wahenga. Baada ya familia ya Dk Lewis kuvurugika hadi kufikia hatua ya daktari huyo kupeana talaka na mkewe kutokana na kupotea katika mazingira ya kutatanisha kwa
mtoto wao wa kipekee, Skyler, hatimaye mambo yanatulia. Baada ya Skyler kupatikana, tena akiwa na mtoto Harrison aliyefanana kwa kiasi kikubwa na marehemu CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ baba yake, Harvey, Dk Lewis anamfuata Suzan aliyekuwa anaishi na wazazi wake baada ya kupeana talaka. Suzan anashtuka mno baada ya kumuona Skyler na anapoteza fahamu kwa muda. Baada ya kupewa huduma ya kwanza anarejea kwenye hali yake ya kawaida.
Baadaye wanaenda mahakamani na Dk Lewis kuvunja talaka waliyopeana. Zoezi hilo linakamilika ambapo familia inaungana upya na kufungua ukurasa mpya.
MAISHA yalizidi kusonga mbele, Skyler akaendelea na masomo huku akizidisha juhudi kuliko ilivyokuwa awali. Mwanaye naye alizidi kukua, akawa
mchangamfu, hali iliyozidi kuleta faraja ndani ya nyumba ya Dk Lewis. “Unataka ukiwa mkubwa usomee nini mwanangu?” “Nataka kusomea tabia za wanyama.” “Kuna somo linaitwa tabia za wanyama?”
“Aah, nimekosea mama, nataka kuwa mtaalam wa Bailojia, kipengele cha Zoology, mwalimu ametufundisha kuwa Zoology ni sehemu ya Bailojia lakini yenyewe inazungumzia zaidi wanyama.”
“Mh! Yaani wewe ndiyo huna akili kabisa, badala ya kuchagua masomo yanayoendana na ulimwengu wa kisasa kama Teknolojia ya Mawasiliano (IT) au ufundi wa kompyuta (Computer Science) kama mimi mama yako wewe unataka kusomea mambo ya wanyama, kwa hiyo utakuwa unaishi porini?”
Unakosea Skyler, hata wewe tulikupa nafasi ya kuchagua masomo unayoyataka na ndiyo maana muda si mrefu utakuwa mtaalam wa IT mwenye sifa na vigezo vyote, usimlazimishe mjukuu wangu awe kama wewe, mpe anachokitaka,” mama Skyler alilazimika kuingilia kati mazungumzo ya mwanaye na mjukuu wake, Harrison.
“Mama, yaani na wewe unakubali mjukuu wako aje kuwa daktari wa wanyama? Nimemzaa ili aje kuwa shujaa hapa duniani, siyo mtaalam wa wanyama!”
“Anaweza kuwa shujaa hata kwa kusomea Ethology (somo la tabia za wanyama), cha msingi ni kumsikiliza anachokitaka na kumsaidia atimize malengo yake, tena anaonesha somo la Baiolojia analiweza sana, si unaona matokeo yake yanavyoridhisha?” “Hapana mama, sipo tayari kuona hilo linatokea, lazima asomee masomo ambayo atapata kazi na mafanikio kwa urahisi,” alisema Skyler, kauli ambayo haikuwafurahisha mwanaye Harrison na bibi yake.
Licha ya Skyler kuonekana kumpinga, bado Harrison ambaye alikuwa akizidi kukua kwa kasi, alishikilia msimamo wake kuwa anataka kusomea masomo hayo.
Maisha yalizidi kusonga mbele, miaka miwili baadaye Skyler akahitimu masomo ya sekondari na kuendelea na elimu ya juu ambapo alijiunga na Chuo cha Teknolojia cha Oregon alikosomea Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Information and Communication Technology). Harrison naye aliendelea na masomo ya shule ya msingi, akazidi kukua kimwili na kiakili huku malezi mazuri aliyoyapata kutoka kwa mama yake pamoja na bibi na babu yake, yakimjengea uwezo mkubwa wa kujiamini.
Japokuwa awali mama yake, Skyler alikuwa hataki Harrison asomee elimu ya viumbe hai na tabia za wanyama, baada ya kuona mwanaye anazidi kuyakazania masomo hayo, huku matokeo ya kila mtihani akifaulu kwa alama za juu, ilibidi akubaliane na hali halisi. Akamruhusu kwa moyo mkunjufu aendelee huku akimpa msaada wa kila alichokuwa anakihitaji.
Skyler baada ya kumaliza masomo yake, alipata ajira kwenye Kampuni ya Microsoft Limited, tawi la Miami ambapo alikuwa akifanya kazi kwenye kitengo cha ICT. Akawa analipwa mshahara mzuri uliomfanya auchukue mzigo wa kugharamia masomo ya mwanaye Harrison kutoka kwa wazazi wake.
Akawa anamlipia ada mwanaye na kumnunulia vitabu ikiwa ni pamoja na kumtafutia twisheni ya masomo aliyokuwa anayapenda. Fedha nyingine alimfungulia akaunti benki, ikawa kila mwisho wa mwezi anaenda kumuwekea akiba ya kumsaidia siku za baadaye. *** MIAKA 15 BAADAYE Harrison aliendelea vizuri na masomo yake, akahitimu shule ya msingi na kujiunga na Shule ya Sekondari ya Miami Academy, akasoma kwa miaka minne akiwa amechagua mchepuo wa masomo ya sayansi na kuhitimu kwa mafanikio, akapata alama za juu na kuwa miongoni mwa wanafunzi kumi bora.
Kutokana na kufaulu vizuri, hususan masomo ya Botany na Zoology, Harrison alipata nafasi ya kuendelea na masomo ya juu, akajiunga na chuo cha Michigan State University, School of Ethology. Akiwa chuoni hapo, alisomea Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Zoolojia (Bachelor Degree of Science in Zoology).
Mwaka wa kwanza uliisha, matokeo ya mwisho wa mwaka yalipotoka, Harrison alifaulu vizuri, hali iliyofanya wanachuo wenzake pamoja na wakufunzi kuanza kuulizana juu ya mwanachuo huyo kwani wengi walikuwa hawamjui.
“Unamjua bwana, ni mkimya sana na anapenda kukaa nyuma kabisa. Ukimuona utasema haongei lakini ana utundu wa chinichini huyo!” “Mpenzi wake ni nani?”
“Mh! Sijawahi kumuona na msichana, muda mwingi yupo bize na masomo, anapenda kubeba vitabu vikubwavikubwa vya Baiolojia,” wanachuo wawili walikuwa wakijadiliana pembeni ya ubao wa matangazo, baada ya kuona jina la Harrison Harvey likiwa la kwanza kwenye matokeo ya mtihani wa mwisho wa mwaka chuoni pale.
Habari zake ziliendelea kusambaa, watu wengi wakawa na hamu ya kumjua na kwa kadiri siku zilivyozidi kusonga mbele, akapata marafiki wengi, wa kike na wa kiume. Likizo alirudi nyumbani kwao, akapokelewa kwa shangwe na mama yake, babu na bibi yake ambao walimuandalia sherehe ndogo ya kumpongeza kwa kufaulu vizuri masomo yake.
“Umeamini sasa kwamba kila mtu na kipaji chake? Ungemlazimisha asomee masomo kama ya kwako, ungempoteza Harrison, tazama anaongoza chuo kizima.”
“Mh! Unayoyasema mama ni ya kweli, siamini kama mwanangu anaweza kuongoza kwa matokeo ya mwaka mzima, tena kwa chuo kama Michigan State kilichojaa watu wenye vipaji kutoka sehemu mbalimbali!” Skyler na mama yake walikuwa wakijadiliana wakati wakiwa jikoni kuandaa chakula cha jioni.
Harrison na babu yake walikuwa wakitazama runinga sebuleni, wakawa wanaelekezana mambo kadhaa yaliyokuwa yanaoneshwa kwenye kituo cha runinga cha Discovery walichokuwa wanatazama.
“Mto Amazon ni wa pili kwa urefu duniani, umeanzia Brazil na unakatiza nchi nyingi mpaka kwenye Bahari ya Pacific unakomwaga maji, unafahamu nini kuhusu Amazon?” aliuliza Dk Lewis.
“Karibu theluthi moja ya viumbe vyote duniani, wanyama wa porini, ndege, samaki na wengineo, wanaishi kwenye misitu minene inayozunguka mtu huo.”
“Ni kweli kabisa, inaoesha upo makini sana na masomo yako. Unafahamu kuhusu nyoka wakubwa waitwao Anaconda wanaopatikana kwenye mto huo?”
“Ndiyo babu, Anaconda ndiyo nyoka wakubwa kuliko wote duniani na wanapatikana kwenye Mto Amazon pekee. Maisha yao yote huishi kwenye maji na huacha vichwa vyao vikielea juu ya maji wanapowinda.” “Vipi kuhusu pomboo wakubwa wa Amazon?”
“Ahaaa, unazungumzia kuhusu samaki aina ya dolphin? Wapo tena wakubwa haswaa! Tofauti na dolphin wa baharini, wale wa Amazon huwa wanabadilika rangi, wakiwa wadogo huwa na rangi ya kijivu, baadaye huwa na rangi ya pinki na wakikomaa hubadilika na kuwa weupe.
“Pia naujua msitu wa Tongass na viumbe wote waliomo ndani yake, kuna sokwe wakubwa, ndege, swala na wanyama kibao,” alijibu Harrison, babu yake akawa anakuna kipara chake kwani mjukuu wake alikuwa na uelewa mkubwa sana wa viumbe hai na mazingira.
BAADA ya kutengana kwa miaka kadhaa kutokana na kupotea kwa mtoto wao wa kipekee, Skyler, hatimaye Dk Lewis na Suzan wanakutana na kuanza kupanga mikakati ya kuijenga upya familia yao.
Kupatikana kwa Skyler, tena akiwa na mtoto aliyekuwa akifanana kwa kiasi kikubwa na marehemu baba yake, Harvey kunaonekana kuwa faraja kubwa kwa wote. Mama Skyler ambaye awali alipatwa na mshtuko uliosababisha apoteze fahamu baada ya kumuona
mwanaye katika mazingira ambayo hakuyategemea, anapelekwa hospitali na baada ya muda anapata nafuu na kurudishwa nyumbani. Mwanaye anamsimulia kila kitu kilichotokea baada ya kuondoka nyumbani.
Wanaombana radhi na sasa wanakubaliana kufungua ukurasa mpya wa maisha yao. Suzan anakubaliana na Dk Lewis kwenda kuvunja talaka mahakamani na kula kiapo kipya cha kuishi pamoja kama mume na mke.
KWA kutumia gari la Dk Lewis, walisafiri mpaka kwenye Mahakama ya Miami County High Court na kwenda moja kwa moja kwenye kitengo cha viapo. Wakaeleza shida yao ambapo karani waliyemkuta aliwaelekeza kwenda chumba namba 7113. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Karibuni sana, niwasaidie nini?”aliuliza mwanamke wa makamo aliyekuwa amekaa nyuma ya meza kubwa ya mapokezi. “Mimi na mwenzangu tulipeana talaka lakini sasa tumeamua kurudiana,” alisema Dk Lewis huku akimpapasa Suzan mgongoni kimahaba.
Yule mwanamke aliwatazama mmoja baada ya mwingine kisha akawaelekeza kwenye ofisi ya Jaji Valentine Powell aliyekuwa akishughulika na viapo vya ndoa, talaka na kadhalika.
Waliongozana na baada ya muda mfupi waliingia ndani ya ofisi hiyo, wakapokelewa na mwanaume mzee mwenye mvi nyingi kichwani. Dk Lewis akaanza kueleza kilichowapeleka.
“Kitu gani kilichosababisha muachane na sasa kitu gani kinachowafanya mtake kurudiana?” “Tulikuwa na matatizo ya kifamilia lakini tayari tumeshayamaliza na hayawezi kujirudia tena,” alisema Dk Lewis kwa kujiamini.
“Kwa kawaida ili kuvunja talaka inabidi mle kiapo mbele ya mashahidi halafu baada ya hapo mtakula kiapo kingine cha ndoa ya mkataba.” “Ndoa ya mkataba?”aliuliza Suzan kwa mshangao.
“Ndiyo, mkishapeana talaka sheria ya ndoa inasema mkirudiana inabidi ndoa yenu iwe ya mkataba na mtakuwa mkiuongeza kwa kadiri mtakavyokuwa mnaishi kwa maelewano,” alijibu Jaji Powell, Suzan na Dk Lewis wakatazamana kwa sekunde kadhaa kisha wakatingisha vichwa vyao kuonesha kuwa wameridhia.
Walitoka kwenda kutafuta wadhamini na baada ya muda wakarudi na kula kiapo cha kuvunja talaka, wakapewa fomu maalum ya kusaini wao na wadhamini wao. Walipomaliza walipewa fomu nyingine ya ndoa ya mkataba, Jaji Powell akawaongoza kula kiapo kisha wakasaini kwenye zile fomu.
“Sasa mmehalalishwa kuwa mke na mume kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1972, kipengele kidogo cha 3b,” alisema Jaji Powell.
Baada ya shughuli ile, Suzan alimrukia Dk Lewis, wakagonganisha ndimi zao na kuanza kuelea kwenye ulimwengu wa mahaba. Walikaa kwenye hali ile kwa zaidi ya dakika mbili, wakaachiana na kuanza kutazamana kama majogoo yanayotaka kupigana.
“Siamini macho yangu kama umerudi kwenye mikono yangu,”alisema Dk Lewis huku akilengwalengwa na machozi. “Mimi mwenyewe siamini, naahidi nitalilinda penzi lako mpaka siku nafukiwa kaburini, tusahau yote yaliyopita na tufungue ukurasa mpya,” alijibu Suzan huku naye akitokwa na machozi ya furaha. Akatoka huku wakiwa wamekumbatiana mpaka kwenye gari lao.
Safari ya kurudi nyumbani kwa Dk Lewis ilianza na baada ya muda wakawa tayari wameshawasili. Walipitiliza moja kwa moja mpaka chumbani wakajifungia.
Baada ya kukaa chumbani kwa saa nyingi wakiwa peke yao, baadaye walitoka wakiwa wamechoka na kuingia ndani ya gari, wakaondoka na kurejea nyumbani kwa wazazi wa Suzan ambapo waliwakuta wote wakiwasubiri kwa hamu.
“Vipi mmefikia wapi?” aliuliza mama Suzan, mwanaye akamjibu kuwa kila kitu kimeenda kama kilivyopangwa na tayari wameshakuwa mume na mke halali. Kila mmoja akashangilia kwa nguvu, wakawakumbatia na kuanza kuimba nyimbo za furaha. Shangwe ziliendelea mpaka usiku sana.
Wakaruhusiwa kuondoka pamoja lakini Skyler na mwanaye Harrison wakalazimika kubaki palepale. Kesho yake kulifanyika sherehe ndogo ya kuwapongeza, wakafungua ukurasa mpya wa maisha ya ndoa.
Sherehe ilipoisha, waliwachukua Skyler na mwanaye Harrison na kurudi nao mpaka pale Dk Lewis alipokuwa anaishi. Kwa kuwa nyumba ilikuwa ndogo, walikubaliana kwenda kuikarabati nyumba yao waliyokuwa wanaishi kabla
hawajatengana. Mafundi wakatafutwa ambapo kazi ya ukarabati ilianza haraka. Madirisha na milango ambavyo vilikuwa vimeharibika vikarudishiwa upya, kuta za ndani na nje zikapakwa rangi na kuifanya nyumba ionekane mpya.
Dk Lewis aliomba likizo ya dharura kazini kwao, mama Skyler naye akafanya hivyohivyo, siku chache baadaye wakahamia kwenye makazi mapya na kuyaanza maisha ya kifamilia, safari hii wakiwa na mtu aliyeongezeka, Harrison.
Kwa kuwa Harrison tayari alikuwa ameanza masomo ya chekechea wakiwa nyumbani kwa Bill na mkewe, ilibidi taratibu zifanyike za kumhamishia jirani na pale nyumbani kwao, akaendelea na masomo kwenye shule ya Miami Kindergaten.
“Sikuwahi kutegemea kuwa familia yangu inaweza kurudi na kuungana pamoja kama hivi, namuomba Mungu hii furaha tuliyonayo iendelee miaka yote,” alisema Dk Lewis jioni moja wakati wakipata chakula cha usiku.
“Hata mimi sikutegemea mume wangu, naamini sote tumejifunza jambo kwa haya yaliyotokea,” alisema Suzan, wakaendelea kula chakula cha usiku.
Siku zilizidi kusonga mbele, maisha yao yakazidi kutawaliwa na amani, upendo na furaha. Baada ya muda, likizo zao ziliisha, wakalazimika kurudi kazini huku Skyler akibaki nyumbani. Harrison akawa anazidi kukua huku akili yake nayo ikipevuka kutokana na masomo ya chekechea aliyokuwa anafundishwa.
“Mume wangu, mi nilikuwa na wazo.” “Wazo gani mke wangu kipenzi?”
“Huyu Skyler mi sifurahishwi na yeye kuendelea kukaa nyumbani. Kwa nini tusimtafutie shule ili aendelee na masomo yake?”
“Hata mimi nilikuwa nawaza hivyo mke wangu, nafikiri ni jambo la msingi sana. Ila umeshazungumza naye na kumsikia anasemaje?”
“Hapana, lakini kwa sababu wote tupo, nafikiri huu ndiyo muda muafaka wa kumuita na kumuuliza,” alisema Suzan, akainuka na kwenda kumuita Skyler aliyekuwa akiendelea kucheza na mwanaye Harrison. Walikaa naye na kumweleza walichokuwa wamekiamua, naye akaonesha kufurahishwa sana na uamuzi ule wa wazazi wake.
“Nataka niendelee na masomo ya sekondari kuanzia pale nilipokuwa nimeishia, bado nina ndoto kubwa kwenye maisha yangu na elimu pekee ndiyo itakayonifanya niweze kuzitimiza,” alisema Skyler huku akionesha kufurahishwa sana na uamuzi ule.
Taratibu za kumrudisha shuleni zilifanyika, akatafutiwa shule ya kulipia, tofauti na ile aliyokuwa anasoma awali. Baada ya wiki kadhaa, akaendelea na masomo ya sekondari, safari hii akiwa na uchungu na elimu kuliko kawaida. Harrison naye aliendelea na masomo na baada ya miezi kadhaa, aliandikishwa kuanza darasa la kwanza. ***
Charlotte aliendelea kupiga kelele na kumuita mama yake lakini hakuna mtu aliyemsikiliza, wale wanyama wakamzunguka na kuanza kumshangaa. Waliendelea kumzunguka lakini hawakumdhuru, baada ya kumshangaa kwa muda mrefu, mnyama mmoja aliyeonekana kuwa mkubwa kuliko wengine alimshika Charlotte kama afanyavyo mama kwa mwanaye na kumuweka mgongoni.
Wakaondoka kundi zima na kutokomea ndani kabisa ya Msitu wa Tongass, wakawa wanaruka kwenye matawi ya miti huku mnyama yule mkubwa akiwa makini kuzuia Charlotte asidondoke.
Licha ya awali kujawa na hofu juu ya usalama wake, taratibu Charlotte alianza kuwazoea wale wanyama, ile hofu aliyokuwa nayo ikaisha hasa baada ya kugundua kuwa wanyama wale hawakuwa na lengo la kumdhuru. Akaanza kuzoea kushinda nao, siku zote akiwekwa katikati yao, akilishwa mizizi na matunda ya porini kama wao walivyokuwa wanakula.
Kilichomtesa ni kwamba hawakuwa na nyumba au pango la kujisitiri wakati wa mvua au baridi kali, akawa anateseka lakini taratibu alianza pia kuzoea hali ile. Akaanza kujifunza kuruka kwenye matawi ya miti kama viumbe wale, akaanza kujiona kama hana tofauti yoyote. Hayo ndiyo yakawa maisha yake mapya.
Siku zilizidi kusonga mbele, Charlotte akawa anazidi kukua huku haiba na tabia za kibinadamu zikitoweka kwenye maisha yake na kuishi kama wale wanyama. Kilichompa faraja ni kwamba kila kulipotokea hatari yoyote, wale wanyama walikuwa wakimthamini yeye kuliko kitu kingine chochote. Akawa anazidi kuwa mkubwa.
MAISHA ya familia ya Dk Lewis yanarudi kwenye mstari na anafanikiwa kuiunganisha upya familia yake kufuatia kupatikana kwa mtoto wake wa kipekee, Skyler ambaye alitoweka kipindi kirefu kilichopita. Skyler
anakuja na mtoto wa kiume, Harrison ambaye amefanana vitu vingi na marehemu baba yake. Siku zinasonga mbele kwa kasi na Harrison anazidi kuwa mkubwa. Anamaliza elimu ya msingi na kuanza shule ya sekondari anakohitimu kidato cha nne. Baadaye anajiunga na chuo cha Michigan State University
anakosomea masomo ya tabia za wanyama, Ethology. Anahitimu masomo yake na kuwa mtaalamu wa tabia za wanyama. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Baada ya kuhitimu masomo, anaenda kufanya utafiti kwenye msitu wa Tongass, lengo lake likiwa ni kujua mambo mbalimbali yahusuyo wanyama, hususan sokwe wengi wanaopatikana kwenye msitu huo mkubwa.
ILIBIDI akajibanze kwenye mti mkubwa na kuangalia ni wanyama gani, macho yake yakatua kwenye kundi kubwa la sokwe wakubwa waliokuwa wanaruka kutoka tawi moja kwenda jingine kwa kasi kubwa, wakawa wanaelekea pale alipokuwa amejibanza.
Kelele zilizidi kuongezeka, utulivu uliokuwepo ndani ya msitu ule ukatoweka, Harrison akazidi kujibanza pale kwenye mti huku bastola yake iliyokuwa inatumia risasi za mpira ikiwa mkononi, tayari kwa kujihami endapo lolote lingetokea.
“Mungu wangu, mbona wakubwa hivi? Halafu mbona wengi kiasi hiki?” alijiuliza Harrison huku akiichukua kamera yake kwenye begi kwa mkono mmoja, akakaa vizuri na kuanza kupiga picha kwa mbali. Alipiga picha kadhaa, akawa anaendelea kushangaa jinsi sokwe wale walivyokuwa wakubwa na wengi.
Kundi lile la masokwe lilipotoweka, alishusha pumzi ndefu na kuweka vifaa vyake vizuri. Ilibidi arudi kwenye hema lake, akaenda kuweka kumbukumbu za alichokiona. Akawa anaandika baadhi ya mambo kwenye kijitabu chake cha kumbukumbu.
Siku zilizidi kuyoyoma Harrison akiwa bado ndani ya msitu wa Tongass, kila siku akawa anaendelea na kazi ya utafiti juu ya tabia za masokwe na viumbe wengine katika msitu ule, pamoja na kuchunguza uoto wa asili. Taratibu alianza kuwazoea masokwe wale wakubwa na wa kutisha.
Tofauti na wanyama wengine, sokwe wa msitu wa Tongass walikuwa wakitembea kwa makundi makubwamakubwa, huku moja likionekana kuwa kubwa zaidi. Kila alipobahatika kuwaona, walikuwa kwenye makundi, wakiruka juu ya matawi ya miti kwa namna ambayo ilimshangaza sana Harrison.
Baada ya kukaa kwa muda wa wiki mbili ndani ya msitu ule, Harrison aliamua kuondoka na kurejea nyumbani kwao kwenda kufanyia kazi taarifa mbalimbali za kiuchunguzi juu ya tabia za wanyama hususan masokwe wa Msitu wa Tongass alizozipata.
Alijiandaa kwa kufungasha vitu vyake vyote, akalikunjua hema na kulibana kwa namna ambayo ilikuwa rahisi kubebeka, alipohakikisha amechukua kila kitu, aliianza safari ya kuelekea kwenye ofisi za msitu ule kwa ajili ya kukabidhi baadhi ya vifaa alivyokuwa amepewa.
“Umefanikiwa?” “Nimefanikiwa kwa kiasi kikubwa na namshukuru Mungu sijapata madhara yoyote.” “Unawaonaje masokwe wa Msitu wa Tongass?”
“Mh! Sijawahi kuona sokwe wakubwa kama hawa, halafu wanatembea kwa makundi makubwa sana, lazima nitarudi tena kwani nadhani ndani ya msitu huu nitajifunza vitu vingi ambavyo awali sikuwa navifahamu.
“Ngoja nikafanyie kazi hizi data nilizozipata,” alisema Harrison wakati akizungumza na askari wa wanyama pori aliyemkuta kwenye ofisi za msitu ule.
Baada ya makabidhiano, Harrison alitembea kwa miguu kwa kilometa chache kabla ya kuifikia barabara kuu. Akasimamisha gari na safari ya kurejea nyumbani kwao, Miami ikaanza.
”Ooh! Karibu baba, umekuwa mweusi kweli, inaonesha kuna baridi sana huko ulikotoka.” “Ahsante sana, kuna baridi kali kwenye Msitu wa Tongass lakini namshukuru Mungu nimefanikiwa kwa kiasi kikubwa,” alisema Harrison wakati akipokelewa na bibi yake. “Mama yupo wapi?” “Ameenda kazini lakini muda si mrefu atarudi. Mh! Habari za huko?”
“Nzuri kabisa mama, nimeifurahia sana safari yangu kwenye Msitu wa Tongass, nimewaona sokwe wakubwa haooo! Yaani hata wewe nikikuonesha picha utashangaa,” alisema Harrison.
Baada ya kuingia ndani na kupumzika kwa muda, Harrison alienda kuoga na kubadilisha nguo, akachukua kamera zake mbili alizokuwa anazitumia kupigia picha na kwenda kuziunganisha kwenye kompyuta kwa lengo la kuzitoa zile picha na kuzihifadhi vizuri.
Alichomeka waya maalum kutoka kwenye kamera na kuunganisha kwenye kompyuta, akaanza kutoa picha, zoezi lililomchukua zaidi ya nusu saa. Alipomaliza alianza kuzichunguza vizuri moja baada ya nyingine. Aliendelea na zoezi lile
huku akizitenganisha katika mafaili mbalimbali, kuanzia zile za mazingira, za uoto wa asili mpaka zile za makundi ya sokwe. Wakati akiendelea kuzifuatilia, aligundua jambo ambalo lilimshangaza. Kila alipokuwa akizichunguza kwa makini picha alizopiga makundi yale ya sokwe, aligundua kama kuna kitu katikati yao ambacho hakikuwa kikionekana vizuri.
Alibaini pia kuwa sokwe wale walikuwa wakitembea kwa mtindo wa kuweka duara, hata walipokuwa wanaruka kutoka mti mmoja kwenda mwingine, katikati kulikuwa na kitu ambacho walionekana kukilinda kwa nguvu kubwa. “Hiki ni nini?” alisema Harrison huku akijaribu kuivuta picha karibu kwenye kompyuta, ‘akai-zoom’ mpaka mwisho, hali
iliyomsaidia kuona vizuri, akagundua kuna kitu kilikuwa katikati ya sokwe wale ingawa hakuelewa mara moja ni kitu gani. Aliendelea kufuatilia picha zile kwa muda, akajikuta akisisimka mwili mzima kutokana na kitu alichokuwa anakiona. “Lazima nirudi Tongass, nitaenda kufuatilia kwa makini ili nijue ni kitu gani,” alijisemea Harrison huku akiendelea kuzitazama zile picha. Aliifanya kazi ile kwa muda mrefu mpaka muda wa kulala ulipowadia.
Kesho yake, alfajiri na mapema Harrison aliamka na kuaga kuwa anarudi tena kwenye msitu wa Tongass kuendelea na kazi. “Wewe si ulisema utapumzika kidogo? Kinachokufanya uwahi kurudi bila kukaa nasi hata kidogo ni nini?” “Mama kuna kazi ya muhimu nilikuwa sijaimalizia, ni muhimu sana,” alisema Harrison bila kutaka kufafanua ni kazi gani.
Mama yake hakuwa na hiyana, alimruhusu lakini akawa anajiuliza maswali mengi ambayo hayakupata majibu. Harrison akasafiri kwa mara nyingine kurudi kwenye msitu wa Tongass. Safari hii hakupanda treni bali alisafiri kwa mabasi, akaunganisha safari mpaka alipofika Tongass.
“Mbona umerudi tena? Kuna kitu umesahau?” askari wa wanyama pori aliyemuacha jana yake, alimuuliza Harrison, akamweleza kuwa kuna jambo la muhimu alisahau kulifanyia kazi. Hata hivyo, hakumueleza ni jambo gani, akapewa vifaa na kurudi msituni, akaenda kuweka kambi pembeni kidogo ya pale alipokuwa amesimamisha hema lake.
Kwa kuwa tayari muda ulikuwa umeenda huku uchovu wa kuunganisha safari ukimsumbua, Harrison aliamua kupumzika mpaka kesho yake. Kulipopambazuka tu, aliwahi kuamka na kwenda nje ya hema, akawa anaangaza macho huku na kule akitegemea kuliona tena lile kundi la sokwe.
Muda ulianza kwenda lakini masokwe hawakutokea, ikabidi aanze kuwatafuta sehemu mbalimbali za msitu ule. Kuna wakati alisikia kelele, akahisi watakuwa ni wenyewe lakini alipofuatilia, alikuta kundi la tai likiufaidi mzoga wa mnyama aliyekuwa amejifia.
Akaendelea kuzunguka huku na kule, akijipenyeza katikati ya miti iliyokuwa imefungamana ndani ya msitu huo. Baada ya kuhangaika sana bila mafanikio, Harrison aliamua kurudi kwenye hema lake kupumzika. Akiwa mita chache kutoka kwenye hema, alianza kusikia kelele upya, alipoangaza macho yake juu ya miti, aliwaona sokwe wakiruka kwa kasi, akatafuta sehemu na kujibanza, akawa anaangalia kwa makini katikati ya lile kundi.
Kamera yake nayo ilikuwa mkononi, akiwa tayari kupiga picha endapo angekiona kile kitu alichokuwa anakisubiri. Hata hivyo, kazi haikuwa nyepesi, kila sokwe wale walipokuwa wanaruka, walikuwa wameweka duara huku wakiwa makini kuziba kitu kilichokuwa katikati yao.
HARRISON aliendelea kusubiri ili aone ni kitu gani kilichokuwa katikati ya kundi lile la masokwe kwa muda mrefu lakini hakufanikiwa. Akiwa bado amejibanza pale pembeni ya mti, alishtukia akipigwa na jiwe mgongoni, akadondoka na kuangusha kamera yake. Ghafla alishtukia sokwe mkubwa akiruka kutoka kwenye tawi la mti huku mkononi akiwa ameshika fimbo ndefu, akaanza kumcharaza Harrison
aliyekuwa bado amelala pale chini. Masokwe wengine wakubwa nao wakawa wanaporomoka kutoka kwenye matawi ya mti na kumzunguka Harrison pale chini huku wakitoa milio ya kutisha.
Kwa kasi ya ajabu aliiokota kamera yake na kuanza kutimua mbio lakini wale masokwe waliendelea kumkimbiza kwa kasi huku lile kundi lingine likizidi kutokomea ndani kabisa ya Msitu wa Tongass. Alipoona wale masokwe wakubwa wanakaribia kumdhuru alikumbuka kuwa mfukoni alikuwa na bastola inayotumia risasi za mpira.
Harakaharaka alichomoa ile bastola na kufyatua risasi moja hewani, wale masokwe wakatawanyika na kuanza kukimbilia mahali lile kundi lingine lilipoelekea hiyo ndiyo ikawa ponapona yake. Alitafuta sehemu ya kukaa akawa anajitazama alama za fimbo na jiwe alilopigwa mgongoni. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Hawa wanyama ni hatari sana, nisipokuwa makini naweza nikafia huku porini,” alisema Harrison huku akiugulia maumivu aliyokuwa anayapata. Aliikagua kamera yake na kugundua kuwa haikuwa imeharibika, akamshukuru Mungu kimyakimya na kurudi kwenye hema lake kupumzika. *** “Mume wangu, Harrison ameshakuwa mkubwa sasa. Aina ya kazi aliyoichagua inamfanya ajitenge na binadamu wengine, jambo ambalo linaweza kumsababishia matatizo hapo baadaye.” “Ni kweli mke wangu, wataalamu wengi wa mambo ya wanyama pori hujikuta wakiutumia ujana wao mwingi porini wakifanya tafiti mbalimbali matokeo yake hujikuta wanazeeka bila ya kuoa wala kuwa na watoto. Sitaki hali hii imtokee mjukuu wangu.” “Kwa mtazamo wako unataka tumsaidiaje?” “Mimi nashauri tumtafutie mke wa kuoa.” “Hata mimi nilikuwa nawaza hivyohivyo.”
“Hayo mawazo yenu ya kizee mtayaacha lini? Hakuna mtu mwenye haki ya kumchagulia mume au mke mtu mwingine. Ndoa ni jambo la hiyari, nataka mwanangu aamue mwenyewe,” Skyler aliingilia kati mazungumzo ya wazazi wake.
Dk Lewis na mkewe walitazamana kwa sekunde kadhaa kisha wakamgeukia Skyler, mama yake akawa anazungumza: “Mwanangu Skyler, wewe umeshakuwa mtu mzima, hata kama hujaolewa najua unafurahi sana kumzaa Harrison na kumlea mpaka hapo alipofikia. Hutaki na yeye aje kuwa na watoto?”
“Isitoshe mjukuu wangu huyu sijawahi kumuona hata akiwa na rafiki wa kike, akiendelea hivi anaweza asione umuhimu wa kuoa. Ni wajibu wetu kumsaidia,” alikazia Dk Lewis lakini bado Skyler aliendelea kushikilia msimamo wake.
Mazungumzo yaliendelea kwa muda mrefu, Skyler akawa anasisitiza kuwa mwanaye apewe uhuru wa kujiamulia mambo yake mwenyewe lakini wazazi wake hawakuafikiana naye. Wakajiapiza kuwa ni lazima wamtafutie mjukuu wao mke hasa kwa kuzingatia kuwa alishamaliza masomo yake. Skyler alipoona wanang’ang’ania msimamo wao, aliamua kuondoka na kuwaacha peke yao sebuleni. ***
Baada ya siku ile ya kwanza kupita, kesho yake Harrison aliwahi kuamka na kujiandaa kuendelea na kazi yake na akachukua vifaa vyake vyote muhimu na kuingia porini. Alipanga kuendelea kulifuatilia kundi lile la masokwe mpaka ajue ni kitu gani kilichokuwa katikati yao.
Alielekea upande wa Magharibi mwa msitu ule lilipoelekea kundi lile jana yake. Akiwa anaendelea na kazi yake, mara alishtukia miti ikianza kutingishika huku kelele za ajabu zikisikika, akajua ni lile kundi kubwa la masokwe, akajibanza kwenye mti mkubwa na akaanza kujipanga tayari kwa kupiga picha.
Ugumu alioupata jana yake uliendelea kuwa vilevile kwani hakupata hata upenyo wa kutazama vizuri kilichokuwa katikati ya kundi lile, ikabidi abadilishe lenzi ya kamera na kutumia yenye uwezo wa kuona mbali, akawa analifuatilia wakati likiruka kutoka tawi moja hadi lingine. Bahati mbaya mvua ilianza kunyesha na kumfanya airudishe kamera yake kwenye mkoba akihofia kuiharibu kwa maji ya mvua, akakubali kuendelea kuloana na mvua mpaka atakapojua ni kitu gani kilichokuwa katikati ya masokwe wale.
Mvua iliendelea kunyesha kwa muda mrefu lile kundi likawa linatafuta sehemu ya kujibanza ili lisinyeshewe na mvua, likakimbia mpaka mahali palikuwa na pango kubwa. Masokwe wote wakaingia ndani ya pango lile.
“Hapahapa, nitakaa mpaka nione mwisho wao,” alisema Harrison huku akitafuta sehemu nzuri ya kujibanza. Akasubiri mpaka mvua ilipoanza kupungua, wale masokwe wakaanza kutoka mmoja baada ya mwingine. Baada ya dakika kadhaa kupita, Harrison hakuamini alichokiona mbele ya macho yake.
Kiumbe ambaye alikuwa tofauti kabisa na wale sokwe alitoka kwenye lile pango,Harrison akaiweka vizuri kamera yake na kupiga picha kadhaa mfululizo. Akamuona yule kiumbe akiingia katikati ya kundi la wale sokwe na kuanza kuparamia matawi ya miti kama wanyama wale.
“Mungu wangu mbona amefanana na binadamu lakini mbona anaruka kwenye miti kama sokwe? Kwa nini analindwa kiasi hicho,”Harrison alibaki amepigwa na butwaa kwa sekunde kadhaa kabla ya kushtukia akidondokewa na kitu kizito kutoka juu ya mti.
Alikuwa ni sokwe mkubwa ambaye kumbe alimuona Harrison akipiga picha. Akaanza kumrarua kwa meno na kucha huku akipiga kelele zilizo washtua wenzake. Ikabidi Harrison atumie uwezo wake wote kujinasua kutoka kwenye makucha ya yule sokwe, akatimua mbio huku akijitahidi kuweka vizuri kamera yake.
Kundi lote lilianza kumfukuza kwa kasi akatimua mbio mpaka kwenye hema lake na kuingia ndani na kujifungia. Lakini katika hali ambayo hakuitegemea, sokwe wakubwa wakaanza kuchanachana lile hema hali iliyomfanya atokee upande wa pili na kutokomea vichakani huku akijitahidi kuiweka vizuri kamera yake .
Kutokana na kuhofia usalama wake hakutaka kurudi nyuma alikimbia mpaka kwenye ofisi za msitu huo na kukabidhi vifaa alivyopewa, akaaga na kuondoka huku askari wa wanyama pori aliyekuwa zamu akawa anamshangaa kutokana na hali aliyokuwa nayo. “Vipi kuna tatizo?” “Hapana afande,nimeamua kurudi nyumbani.”
“Na hizo alama za kucha mwilini ni za nini? Umevamiwa na chui? Mbona mizigo yako hujachukua?” aliuliza yule askari lakini Harrison hakumjibu chochote akaondoka zake kwa kasi.
MWILI wake wote ulijaa majeraha yaliyotokana na mashambulizi ya sokwe lakini Harrison hakujali, alitaka kurejea zake Marekani haraka iwezekanavyo ili akautangazie ulimwengu juu ya kiumbe cha ajabu alichokiona katikati ya pori kikilindwa na sokwe kama malkia wao. Hakuwahi hata mara moja kusikia kama kulikuwa na sokwe aliyefanana na binadamu kiasi hicho.
Akiwa amechoka baada ya kutembea umbali mrefu katikati ya pori aliamua kuketi kando ya njia na kutoa kamera yake kwenye mfuko, akaiwasha na kuanza kubonyeza huku akiangalia picha moja baada ya nyingine, mpaka akazifikia alizozipiga kabla ya mapambano yake na sokwe.
“Mungu wangu, sijapata kuona mwanamke mrembo kama huyu maishani mwangu, ona nywele zake, matiti yake, hips zake, makalio yake na hata urefu wake. Rangi yake ya ngozi ndiyo kabisaa inavutia mno, ni nani huyu? Aliyeamua kuja kuishi porini na sokwe na akaelewana nao kiasi cha wao kumlinda? Nahitaji kumjua, bila shaka sitakiwi kurejea Marekani bila kuikamilisha kazi hii ambayo ninajua siku moja nikiichapisha
itanijengea heshima kubwa sana duniani, hili si jambo la kawaida hata kidogo,” aliwaza Harrison akiendelea kuitazama picha ya msichana huyo, tayari alikuwa na uhakika wa asilimia mia moja kuwa be huyo hakuwa sokwe. Baada ya kutuliza mawazo yake vizuri, aliiweka kamera yake kwenye begi, akaitoa bastola yake kiunoni na kuhakikisha iko sawa, ndipo akaamua kugeuza kurejea tena porini, alipofika kwenye eneo la ofisi za msitu, askari wa wanyamapori yuleyule alikuwepo.
“Vipi tena?” “Ninarudi porini.” “Kufanya nini?” “Kazi yangu haijakamilika.” “Kibali chako hakijaisha?” “Bado.” “Hebu.” Harrison akaingiza mkono mfukoni na kukitoa kibali kisha kunyoosha mkono wake kumkabidhi askari ambaye alikisoma na kuthibitisha kilikuwa na mwezi mmoja na nusu mbele, hivyo kilifaa kutumika, hata hivyo alimweleza Harrison kuhusu usalama wa porini, kuwa sokwe walikuwa wamekasirishwa na jambo ambalo hakuna mtu aliyelijua mpaka wakati huo askari wengi wa wanyamapori walikuwa wamejeruhiwa vibaya. “Nakushauri usiende!” “Niache tu.” “Lakini kumbuka ukipatwa na matatizo sisi hatuwajibiki!” “Hakuna tatizo. Najua jinsi ya kujilinda.” “Una silaha?” “Ndiyo.” “Iko wapi?” “Hii hapa,” aliongea Harrison akionesha bastola yake. “Ha! Ha! Ha!” badala ya kufurahi, askari alicheka kwa dharau. “Mbona unacheka?”
“Huwajui sokwe wakikasirika? hiyo siyo silaha, watakunyang’anya halafu watakuchomoa hiyo shingo mwilini.” “Bwana litakalokuwa na liwe, lazima niikamilishe kazi niliyoianzisha, aliyesema ‘Never start something you can’t finish’ (Kamwe usianzishe
jambo ambalo huwezi kulikamilisha) hakuwa mjinga,” Harrison aliongea akianza kuchapa mwendo kurejea porini; kamera mkononi. Masaa mawili baadaye alikuwa katikati ya pori akitembea kwa uangalifu, macho yakiwa chini kutafuta nyayo za sokwe na wakati mwingine
kusikiliza milio yao, hakwenda umbali mrefu sana kabla hajasikia mlio wa sokwe uliomaanisha kutoa taarifa kwamba kulikuwa na adui ili sokwe wote wa kiume wakusanyike, aliuelewa mlio huo ulikuwa na maana gani kwa sababu ndiyo elimu aliyoisomea.
“Mungu wangu!” alisema maneno hayo baada ya kushuhudia sokwe wakikusanyika makundi kwa makundi na kumuweka katikati huku wakitoa milio iliyomaanisha “ ua” moyo ulimdunda, jasho likamtoka na akahisi nguo ya ndani ikilowana, hakuhitaji elimu kubwa sana kutaka kufahamu kama huo ulikuwa ni mkojo.
Baada ya kama nusu saa hivi, zaidi ya sokwe wasiopungua elfu mbili walikuwa wamemuweka katikati, wakionekana kama walikuwa wakisubiri amri kutoka mahali fulani ili waweze kumaliza kazi iliyokuwa mbele yao. Harrison akawa mwenye uhakika kabisa kuwa huo ulikuwa mwisho wake, hakuwa na namna yoyote ya kujiondoa eneo hilo, risasi za plastiki alizokuwa nazo kwenye bastola yake zisingeweza kumsaidia, akaamua kuachana nayo.
“Ningejua ningemsikiliza yule askari wa wanyamapo…” hakumalizia sauti yake baada ya kusikia sauti nyembamba ya kike ikiwaamuru sokwe wavamie na kuua adui, sauti ilitokea kwa nyuma na sokwe wote waliokuwa na ukubwa kama wa ng’ombe wakaanza kukimbia kwenda mbele kwa kasi lakini kabla hawajamfikia alisikia tena sauti ileile ikiwaamuru waache kuua, sokwe wote wakafunga breki na kuanza kurudi kinyumenyume kumpisha aliyetoa sauti.
Huku akitetemeka Harrison alimshuhudia msichana yuleyule aliyemuona katikati ya sokwe akitokea, usoni amejawa na tabasamu, mashavuni kukiwa na vishimo vilivyoitwa dimpoz. Chini ya pua yake, mkono wa kushoto kulikuwa na kidoti cheusi kilichomfanya azidi kuonekana mzuri. “My God, what a chick! Am I dreaming? What is she doing in this thick forest?” (Mungu wangu, msichana mrembo ajabu! Ninaota? Anafanya nini kwenye msitu huu wa kutisha?) aliwaza Harrison akinyanyuka. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Cha kwanza alichokifanya ni kuikamata kamera yake na kuanza kupiga picha za mfululizo, sokwe wakataka kumvamia lakini msichana akanyosha mkono wake juu, sokwe wote wakatulia kabisa na kulala chini wakionesha utiifu wa hali ya juu, Harrison akazidi kupiga picha.
“Who are you?” (Wewe ni nani?) aliuliza. “What are you doing here?” (Unafanya nini hapa?) “Tell me.” (Niambie.)
Harrison alizidi kuuliza maswali mfululizo lakini hakuna hata moja lililojibiwa, msichana huyo aliendelea kutabasamu tu huku akimpapasa Harrison mwili wake kama vile alikuwa akishangaa. Ilionekana wazi ilikuwa ni mara yake ya kwanza kukutana na kiumbe cha aina hiyo, Harrison aliligundua hilo kutokana na mshangao ulioonekana machoni mwake, alipoanza kuzungumza alizungumza kwa lugha ya sokwe, Harrison akashangaa lakini hakuweza kumjibu chochote.
Akatoa mlio fulani, sokwe wakanyanyuka na kusimama wima kisha kuanza kutembea wote wakiwa wamemuweka katikati, Harrison alizidi kupiga picha, kichwani mwake akijisemea maneno; Yes, she is the queen of the gorillas, too beautiful to live here though. I am going to do
whatever I can to bring her to civilization.” (Ndiyo, ni malkia wa masokwe, ingawa ni mzuri mno kuishi hapa. Nitafanya kila linalowezekana kumuondoa hapa na kumpeleka kwenye maisha ya ustaarabu.) aliwaza Harrison akishuhudia kundi kubwa la sokwe likiondoka mbele yake, haikuwa rahisi kuamini kama alikuwa amenusurika kuchanwachanwa.
HARRISON, mtafiti wa wanyama ambaye mara baada tu ya kumaliza masomo yake ya chuo kikuu aliamua kuzama kwenye msitu wa Tongass kuwafanyia utafiti sokwe na maisha yao, amefanikiwa kupiga picha ya ajabu ambayo hakutarajia kabisa kukutana nayo kwenye msitu huo.
Ni picha ya msichana mrembo mno, ambaye yeye amembandika jina la Queen of the Gorillas kwa sababu msichana huyo aliishi na sokwe porini na walimlinda kama malkia wao, uzuri wake ulitisha, alikuwa mrefu, mwenye umbile zuri, nywele ndefu alizozivuta kwa nyuma, ngozi laini ya mwili wake na miguu minene yenye kuvutia.
Picha hiyo imemchanganya kabisa akili Harrison, mara ya kwanza aliamua kuondoka kuokoa maisha yake baada ya kupokea kichapo kutoka kwa sokwe ambao hawakutaka kupigwa picha lakini akiwa njiani alikata shauri kurejea ili akamilishe vizuri uchunguzi wake kwa msichana aliyempiga picha.
Safari ya pili alijikuta amezingirwa na kundi kubwa la sokwe waliokuwa tayari kumuua, bila msichana huyo kujitokeza na kuwazuia sokwe wasitekeleze amri aliyokuwa ametoa, ni wazi Harrison angechanwachanwa kiasi kwamba hakuna kipande cha nyama yake kingeonekana.
Baada ya sokwe kuzuiliwa, aliwashuhudia wakiondoka na malkia wao na kumwacha yeye akiendelea kuwapiga picha. Hakika alikuwa amepigwa na butwaa, akabaki eneo hilohilo akiwashuhudia sokwe wakipotea porini.
“OH, Mungu wangu, lazima niondoke, nimepata kitu nilichokuwa nakitafuta, nitarudi tena siku nyingine kumfuata huyu msichana niende naye Marekani, hafai kuishi hapa! Acha kwanza nirejee nyumbani nikaueleze ulimwengu juu yake, najua hakuna atayenianimi lakini kwa ushahidi nilio nao kila mtu atakubali na lazima nitapata hata tuzo ya upiga picha, kwani hakuna mtu amewahi kufanya kazi ya aina hii, ningekwishaiona
mtandaoni!” aliwaza Harrison akibeba mabegi yake na taratibu akaanza kuondoka kuelekea kwenye kituo cha maaskari wa wanyamapori.
Hapo alibahatisha ndege iliyoleta watalii kutoka Marekani, akaomba msaada wa usafiri na hakuna aliyemkatalia. Saa moja baadaye alikuwa angani na kuruka kwa masaa matano mpaka San Francisco ambako ndiko ulikuwa mwisho wa safari ya ndege hiyo. Akashuka na kutaka kulipa l
akini pesa yake ilikataliwa na kuambiwa alichopewa ulikuwa ni msaada, Harrison akashukuru akaondoka hadi stesheni ya treni huko alipanda treni iliyoondoka San Francisco kuelekea Los Angeles, akaingia saa tano za usiku na kutafuta nyumba ya wageni ya bei rahisi maeneo ya Pasadena na kupumzika mpaka siku iliyofuata asubuhi. “Sasa ndiyo wakati wa kutengeneza pesa maishani mwangu,” aliwaza akiziangalia picha alizokuwa nazo na kuipitia upya taswira ya mambo yote aliyokutana nayo.
Siku hiyohiyo alitafuta kampuni ya uchapishaji wa vitabu iitwayo Modern World Publishing na kuzungumza nao juu ya kuchapisha kitabu chake ambacho alitarajia kukiandika juu ya maisha ya malkia wa sokwe. Wote walionyesha mshangao, wakishindwa kuelewa ni nani angetaka kununua kitabu cha namna hiyo.
“Najua ninachokiongea.” “Tuelezee kidogo.”
“Nitawaelezea kwa mdomo lakini sitawaonyesha picha.” “Hakuna shida.” Akasimulia kila kitu juu ya msichana aliyemwona bila kutaja msitu alikokuwa na hata kuwaonyesha picha, kila mtu alivutiwa na wote wakakubaliana naye kuhusu kukichapisha kitabu hicho, wakimtaka haraka sana aandike muswada na kuwapelekea ofisini kwao ili waanze kuupitia. “Itakuchukua muda gani?” “Mwezi mmoja, si maneno mengi sana, zaidi itakuwa ni picha.” “Sawa.”
Mkataba ukasainiwa na Harrison akaondoka kwenye ofisi za kampuni hiyo akiwa mwenye furaha kupindukia, tangu siku hiyo alianza kazi ya kuandika kitabu na mwisho alipomaliza, wiki tatu baadaye badala ya mwezi mzima alikwenda kwenye ofisi za kampuni ya uchapishaji, wote
wakashangazwa na kasi yake lakini wakashangazwa zaidi na picha alizokuwa nazo, hawakuwahi kuona picha za aina hiyo, wote waliamini kitabu hicho kingeuzwa kuliko kingine chochote ambacho kimewahi kuchapishwa katika historia. “Mwanzoni nilifikiri ni uongo, lakini kwa picha hizi nimekuamini. Huyu msichana yupo?”
“Ndiyo.” “Wapi?” “Kwenye msitu wa Tongass, nitakueleza kwa sababu nimesaini mkataba na wewe, vinginevyo nisingesema.” “Alifikaje huko?” “Hata mimi sijui, hakunieleza chochote zaidi ya kutabasamu, tabia zake ni za sokwe kabisa.” “Du!” *** Dk. Charwe Rwegoshora hakuipenda kabisa Geneva tena, kifo cha mke na mtoto wake kwenye ajali mbaya ya ndege iliyolipuka kilimwumiza mno. Kifupi maisha yake hayakuwa sawa baada ya tukio hilo, kazi ilimshinda, akawa ni mtu wa kunywa pombe masaa ishirini na nne akiamini alikuwa anapoteza mawazo kumbe alikuwa anazidi kujididimiza.
Aliishi kwa msaada wa serikali ya Uswisi na hakutaka kurejea nyumbani Buzilayombo ambako aliamini moyo wake ungemuuma zaidi, mara mbili alishajaribu kukatisha maisha yake lakini akaokolewa.
Kwake msiba ulikuwa haujaisha, alimlilia mke na mtoto wake kila siku na kutamani angalao kungekuwa na makaburi ambako wangezikwa na yeye angewatembelea na kuzungumza nao, lakini haikuwa hivyo.
Kila mwezi wa kumi na mbili alisafiri hadi mahali ambako ndege iliangukia na kufanya ibada maalum peke yake akiwaombea mke na mtoto wake, hakuna mtu wa kumweleza kwamba miaka mingi baadaye mtoto wake alikuwa yu hai, akiishi na sokwe katikati ya msitu wa Tongass na sokwe waliomwokoa wala hakuwa na taarifa kabisa kwamba eti alikuwa na familia sehemu fulani.
Charwe alishakata tamaa kabisa, wala hakutaka kuoa tena na kupata mtoto mwingine. Kifupi hakuhitaji mke maishani mwake, kwake kufanya hivyo ilikuwa ni sawa na kumsaliti mkewe, jambo ambalo hakutaka kabisa kulifanya. Watu wengi walimwona kama mtu asiye na akili timamu
kwa jinsi alivyotembea na kuongea peke yake njiani, bila kufahamu kila alikokwenda alisikia sauti za mwanaye Charlotte na mke wake Anganile zikimsemesha. NDEGE aina ya Air Bus iliyokuwa na abiria zaidi ya 415 inaanguka karibu kabisa na Msitu wa Tongass na watu wote waliokuwemo ndani yake wanaaminika kufa bila kufahamu kwamba mwanamke mmoja
aliyekuwa na mtoto wake (Charlotte) alivunja kioo cha dirisha na kumpitisha mtoto wake hapo kabla ndege haijajatua chini, kwa msaada wa parachuti mtoto huyo alifanikiwa kutua porini na sokwe wakamuokota, kisha kutokomea naye porini.
Baadaye taarifa zilitangazwa kwamba watu wote wamekufa! Ndipo Dk. Charwe Rwegoshora, aliyekuwa akimsubiri mke na mtoto wake Charlotte katika Uwanja wa ndege wa Geneva alikokuwa akiishi kuchanganyikiwa na kuvurugikiwa kabisa na maisha yake kuharibika, kwani familia yake ndiyo ilikuwa kitu muhimu kuliko kazi na fedha zote alizopata.
Sokwe wakamchukua mtoto yule na kuishi naye msituni kama mtoto wao hadi akakua akijiona ni sehemu yao na wakamfanya kuwa malkia wao, hakujua alikotokea na aliishi na kuwa na tabia za kisokwe. Hakuwahi kuwa na mawasiliano na binadamu mwingine yeyote mpaka mpiga picha mmoja (Harrison)
ambaye pia alikuwa mtafiti wa wanyama alipompiga picha msituni, siku hiyo ndiyo binti huyo alipogundua tofauti aliyokuwa nayo kati yake na sokwe. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Picha alizozipiga Harrison alisafiri nazo hadi Los Angeles ambako lengo lake lilikuwa ni kuzichapisha katika kitabu na kuelezea maisha ya msichana wa ajabu aliyemuona msituni, akasaini mkataba na kampuni ya uchapishaji ya Modern World Publishing ili wakachapishe na kukisambaza kitabu hicho duniani kote.
KWA Dk. Charwe maisha hayakuwa na maana tena, simanzi ilimsumbua, hakuna mtu aliyemuona ambaye aliamini alikuwa ni daktari. Uchafu ulimfunika na burudani yake kubwa ikabadilika na kuwa pombe ambazo baada ya muda zilionekana kutompa furaha aliyoitafuta, hapo ndipo akavamia dawa za kulevya aina ya cocaine, akazidi kudidimia na hakuwa na mtu yeyote wa kumgeuza.
Ndugu zake walishajitahidi kadiri ya uwezo wao kumshawishi arejee Tanzania lakini hakuwa tayari, jibu lake liliendelea kuwa moja tu; “Haya ni maisha yangu, niachiwe mwenyewe.” Hakuna siku iliyopita bila kutumia pombe au madawa ya kulevya kwenye damu yake, alitisha na hakuna
aliyemuamini kwani alifikia mpaka hatua ya kuiba vitu ndani ya nyumba za rafiki zake ili tu aweze kupata fedha za kunywea pombe au kununua cocaine, hili lilifanya azidi kutengwa.
Baada ya kuuza kila kitu ndani ya nyumba yake na kodi ya nyumba kuwa tatizo, hatimaye aliamua kuingia mitaani ambako aliishi na mateja wengine wa madawa ya kulevya wasio na makazi, juhudi za kumuondoa huko kumpekeka kwenye vituo vya kuwasaidia waathirika wa madawa ya kulevya mara kadhaa zilishindwa kuzaa matunda, kwani alitoroka huko na kurejea mitaani ambako aliendelea kubwia unga.
“Mungu wangu ajali ile,” dereva wa gari moja alisikika akisema baada ya kushuhudia mkusanyiko wa watu katikati ya barabara, kukiwa na msongamano mkubwa wa magari, taratibu akashuka na kutembea hadi eneo hilo. “Amegongwa tena vibaya sana!” Mtu mwingine alisema akitokea eneo hilo.
“Kagongwa na nini?” “Gari la kuzoa taka!” “Duh! Imekuwaje mpaka akagongwa?” dereva aliuliza. “Nimeshuhudia kwa macho yangu.” “Umeshuhudia nini?” “Aliyegongwa nadhani ni mteja wa unga, alikuwa anabembea barabarani bila ya kuangalia kushoto wala kulia kwenye ile kona, si akaja yule dereva wa gari la taka akiwa mwendo wa kasi, wakati anakata kona ndiyo yule mteja naye akawa amefika, pale pale …..” “Hebu na miye nikaone.” “Hutaweza kuangalia, kaumia sana.” “Ngoja…”
Dereva alisogea mbele akipita katikati ya watu mpaka akafika mahali alipolala mtu aliyegongwa, hakuonekana kuwa mzima, akazidi kumuangalia kwa umakini ili aone kama angeweza kumtambua. Ghafla akapiga kelele alipoviangalia viatu vyake, akatamka kwa sauti kwamba huyu alikuwa ni daktari Mwafrika aliyeamua kuingia kwenye matumizi ya haramu ya madawa ya kulevya.
“Mungu wangu! Huyu si Dk Charwe?” Alipouliza hivyo tu watu wote walifumbuka macho kwani Dk. Charwe alikuwa maarufu katika Jiji la Geneva kwa kuwa alishaandikwa sana na Magazeti ya Udaku kutokana na tabia yake ya ulevi wa kupindukia ambayo madaktari wengi walidai, bila kujua tatizo lililokuwa likimsumbua, kwamba aliidhalilisha taaluma yao.
Wakati Dk. Charwe ananyanyuliwa na kupakiwa kwenye gari la wagonjwa, watu wote walikuwa na uhakika kwamba alishakata roho lakini alipofikishwa hospitali na kupimwa, aligundulika kwamba moyo wake ulikuwa bado ukipiga kwa mbali, hivyo akakimbizwa chumba ha upasuaji
ambako alishonwa sehemu zote zilizokuwa zikivuja damu, kisha akapigwa picha za X-Ray, MRI na CT- Scan ili kuona kama alikuwa na maumivu kwa ndani, majibu yalipotoka, kila mtu alisikitika.
“Kwa hali ilivyo, inawezekana akanusurika kifo lakini maisha yake yote atakuwa mtu wa kitandani, maana ameumia mgongo na uti wa mgongo kuanzia shingoni, sehemu yote ya chini kuanzia mikono hadi miguuni hazifanyi kazi.”
“Atarejewa na fahamu kama kawaida?” Muuguzi aliuliza. “Zitarejea baada ya muda ila kitu ambacho hakiwezi kurejea ni fahamu za kwenye miguu.” “Basi tena, ataishi maisha ya shida sana.” “Ana ndugu?” Daktari aliuliza. “Hapa Uswisi?” “Ndiyo”
“Hana ndugu, nasikia tu mke na mtoto wake walikufa katika ajali ya ndege wakisafiri kutoka Afrika kuja hapa, hicho ndicho chanzo cha yeye kuvurugikiwa na akili na kuamua kunywa pombe na hatimaye madawa ya kulevya.”
“Namkumbuka sana huyu daktari, itabidi muwasiliane na watu wa kitengo cha Ustawi wa Jamii ili waweze kuwapigia simu ndugu zake huko Afrika juu ya tatizo lililomtokea.” “Sawa daktari tutafanya hivyo.”
Daktari akaondoka na matibabu ya Dk. Charwe yakaendelea huku mawasiliano ya ndugu zake waliokuwa Tanzania yakiendelea kwa kutumia anuani za barua pepe ambazo walizipata kwenye ofisi aliyokuwa akifanyia kazi kabla mambo hayajamharibikia.
Mwezi mmoja baadaye, fahamu zikiwa zimemrejea, ndugu zake walifika na taratibu zikafanyika, Dk. Charwe akasafirishwa hadi Tanzania ambako safari iliendelea hadi kijijini kwao Muleba, Bukoba kwenye nyumba aliyoijenga na kuanza maisha akiwa na bibi yake tu, kila mtu alijua hakuwa na muda mrefu wa kuishi duniani.
“Ogu Omwana owo mwandetela ndamkolaki?.” (Nitamfanya nini mtoto huyu, mmeniletea mimi?) Alisema bibi yake baada ya kumpokea.
*** “Sifanani nao, nafanana na yule waliyetaka kumuua!” aliwaza msichana huyo akiwa katikati ya kundi la sokwe waliokuwa wakimlinda. Kulikuwa na tofauti kubwa sana kati yake na viumbe aliokuwa akiishi nao, hakufanana nao kwa kitu chochote, aliowaona ni wazazi wake ambao alijitambua akiwa mikononi mwao walikuwa ni wanyama wenye sura mbaya na miili iliyojaa manyoya, vivyo hivyo ndugu zake wawili waliomfuatia nao pia walikuwa na sura hizohizo tofauti na ya kwake.
“Hapa lazima kuna tatizo! Haiwezekani mimi peke yangu ndiye niwe tofauti na wengine wote, ningependa kujua.”
Mawazo haya yalimfikisha Charlotte kwenye hali ya kutaka kuufahamu ukweli, mtu pekee wa kumuambia ukweli huo hakuwa mwingine bali ni yule aliyefanana naye, hivyo ndivyo alivyoamini baada ya kuwauliza sokwe wote mpaka wazazi wake bila kupata ukweli. Akaamuru mtu huyo atafutwe na Sokwe, kama angepatikana basi aletwe kwake mara moja, kazi ikaanza.
Hayo yakitokea porini Tongass, tayari kitabu cha Harrison chenye sura na historia ya msichana mrembo wa ajabu aliyeishi na sokwe kilikuwa kimetoka chini ya kichwa cha habari “THE QUEEN OF THE GORILLAS” yaani Malkia wa Masokwe na watu dunia nzima walikuwa
wakikigombania kwa dola ishirini kwa kitabu kimoja, hii ilikuwa ni dalili kuwa kitabu hiki kingemtajirisha Harrison ndani ya muda mfupi na ndivyo ilivyotokea, kwani katika kipindi cha miezi mitatu tu, nakala milioni kumi zilishauzwa kila pande ya dunia na kilikuwa kikitafsiriwa
katika lugha nyingine mia moja na moja (101), wataalamu wa mambo walianza kusema hapakuwa na kitabu kilichowahi kuuza nakala nyingi kiasi hicho.
MAISHA ya Dk. Charwe, baba wa Charlotte (msichana aliyeko msituni akiishi na sokwe) yanaharibika baada ya kuamini mke na mtoto wake walikufa katika ajali ya ndege iliyoanguka na kuua abiria wote waliokuwemo ndani yake, hakuna aliyejua kwamba mtoto alinusurika na
kuokotwa na sokwe ambao waliishi naye msituni na kumfanya kuwa malkia wao. Harrison, ni kijana wa Kimarekani mtafiti wa wanyama ambaye alifika kwenye msitu wa Tongass na kufanikiwa kupiga picha za msichana huyo
akiwa katikati ya kundi la sokwe wengi waliomlinda na kumheshimu. Picha hizo anazitumia kuandika kitabu kiitwacho The Queen of Gorillas ambacho baadaye alikichapisha na kupata mamilioni ya dola kilipouzwa dunia nzima. Maisha yake yakabadilika kabisa.
Tayari Harrison alikuwa maarufu kuliko alivyowahi kufikiria maishani mwake, utajiri wake ulitisha, kitabu kimoja tu, The Queen of Gorillas kilikuwa kimebadilisha kabisa maisha yake, mamilioni ya dola yalikuwa yakimiminika kwenye akaunti yake, akiwa na umri wa miaka ishirini na nane tu.
Karibu kila chombo cha habari cha Ulaya na Marekani kiliandika habari zake, alifanya mahojiano katika vipindi mbalimbali vya televesheni, vikiwemo vya Oprah Winfrey Show, Larry King, Friday Night Show na vingine vingi tu, kifupi ndani ya miezi sita alikuwa maarufu sawasawa kabisa na wachezaji sinema wa Hollywood, jambo lililomfanya aalikwe sehemu mbalimbali ambako watu maarufu walikutana.
“Hi! Are you Harrison?” (Salama! Wewe ni Harrison?) aliuliza msichana mmoja wakati Harrison akiingia kwenye Ukumbi wa MGM Grand, siku ya utoaji wa tuzo ya Cliff Edom’s New American Award, ambayo inawahusu watu waliofanya mambo ya kuheshimika nchini Marekani. “Yeah! Can I know who is this friend of mine?” (Ndiyo! Naweza kujua huyu rafiki yangu ni nani?) “I am Linda Morris!”(Naitwa Linda Morris) “You look good in that dress!”( Gauni ulilovaa limekupendeza sana) “Thank you, you look handsome too in that black suit and red tie!”(Ahsante, unaonekana mzuri pia ndani ya hiyo suti nyeusi!) “Thank you!”(Ahsante) “Are you here alone?”(Uko peke yako?) “Yeah!”(Ndiyo) “I am alone too, can we give each other some company?”(Niko peke yangu pia, tunaweza kuwa pamoja?) “No problem!”(Hakuna tatizo)
Wakashikana mikono na kuanza kutembea kuingia ndani huku wakikanyaga zulia jekundu, kamera zote ziliwafuata wao. Hivyo ndivyo ilikuwa katika maisha ya Harrison tangu apate umaarufu, pati zote alizoalikwa, wasichana wa kila aina walimtaka kimapenzi, hisia zake zilimfanya ealewe walichokipenda si yeye bali fedha na umaarufu wake.
Wakaketi kwenye kiti cha watu wanne, muda mfupi baadaye mcheza sinema maarufu Chuck Norris na mkewe walifika na kuketi kwenye meza hiyohiyo, Harrison hakuamini kwamba hatimaye siku moja alikuwa ameketi meza moja na mtu aliyemuona kwenye sinema tu. Wakasalimiana na mazungumzo yakaendelea. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Linda alijaribu kadiri ya uwezo wake wote kuwa karibu na Harrison, akimtega kwa kila mbinu ili aingie kwenye mstari wake, jambo ambalo Harrison aliligundua mapema. Isitoshe hakuwa tayari hata kidogo kuwa na uhusiano na msichana mwingine kwa wakati huo, mwanamke pekee aliyemuwaza kichwani mwake ambaye alimtaka ampate kwa udi na uvumba na kumuoa hakuwa mwingine bali ni yule aliyemuona msituni.
“Nampenda sana yule msichana, laiti ningefanikiwa kumpata kutoka porini, basi ningefunga naye ndoa ya ajabu. Sijui kama nitafanikiwa lakini lazima nirudi tena msituni kumsaka na kujaribu kumuondoa katika mazingira hayo, watu watashangaa sana na pengine anaweza kuja kukutana na familia yake,” aliendelea kuwaza Harrison bila kujua kilichoendelea ukumbini kwa jinsi alivyokuwa amezama kwa mawazo.
“And the winner of this year’s Cliff Edom’s New American Award is Harrison Harvey for his book the Queen of the Gorillas which has transformed many people’s lives!”(Na mshindi wa tuzo ya mwaka huu ya Cliff Edom’s NewAmerican Award ni Harrison Harvey kwa kitabu chake kiitwacho Malkia wa Masokwe ambacho kimebadilisha maisha ya watu wengi.)
Ukumbi wote ukalipuka kwa shangwe na nderemo watu wakimshangilia Harrison ambaye alipigwa na butwaa baada ya kusikia jina lake likitajwa, ilikuwa ni heshima kubwa mno kwake kupata tuzo hiyo ambayo kwa kawaida ilichukuliwa na watu waliofanya mambo makubwa hata katika masuala ya vita n.k.
Taratibu alinyanyuka mahali alipoketi na kuanza kutembea akiongozana na Linda, watu waliowaona walidhani alikuwa mpenzi wake, ingawa hakufurahia tabia hiyo, Harrison hakuwa na jinsi ikabidi amuache Linda afanye kilichomfurahisha. Akapokea tuzo kisha akapewa muda mfupi wa kuongea kutoa shukrani.
“Thank you very much, this award goes to my mom and dad wherever he is, my grandparents, for their support and lastly, thanks to all Americans and the girl I love…” (Ahsanteni sana, tuzo hii iende kwa mama na baba yangu popote alipo, babu na bibi yangu kwa kuniunga mkono na mwisho ni kwa Wamarekani wote na msichana nimpendaye…) Harrison akasita na kumwangalia Linda
ambaye sura yake ilijaa tabasamu, meno karibu yote yakiwa nje, kama jinsi ambavyo watu wote ukumbini walivyodhani aliyekuwa akiongelewa hapo ni Linda, ndivyo msichana huyo pia alivyowaza. Alibaki kimya akisubiri tu jina lake litajwe ili ashangilie. “…who is in the forest living with gorillas, without her photographs, I wouldn’t be here today. She is pretty and beautiful, hope one
day she will be my wife living here with us.” (aliyeko porini, akiishi na masokwe, bila picha zake mimi nisingekuwa hapa. Msichana mzuri wa kuvutia, tumaini langu ni kwamba siku moja awe mke wangu na aishi hapa mjini pamoja na sisi) alimaliza Harrison akimsifia malkia wa masokwe, Linda akainamisha kichwa chake kwa aibu.
Sherehe ilipomalizika kwenye majira ya saa sita usiku hivi, watu walisambaa kila mmoja kwenye gari lake na kuondoka, Harrison alikuwa akiendesha gari aina ya Audi New Model yenye thamani kubwa, nyuma yake alikuwepo Linda ndani ya Escarade mpya,
akiangalia kupitia kioo cha pembeni, Harrison alishindwa kuelewa msichana huyo alikuwa ni nani hasa mpaka kuendesha gari la kifahari kiasi hicho. Badala ya kuendelea na safari yake msichana huyo alimfuata Harrison kwa nyuma mpaka nyumbani kwake maeneo ya matajiri yaitwayo Bel Air, gari likaingizwa ndani na ya Linda ikafuata nyuma. Alipoegesha Harrison alishuka na kumfuata Linda kwenye gari lake.
“What’s up?”(Vipi?) “I wanna talk to you.”(Nataka kuongea na wewe) “About what? It is midnight baby, we all need to go to bed, call me tomorrow!”(Juu ya nini? Ni katikati ya usiku, wote tunahitaji kupumzika, nipigie kesho.) “It is important!”(Ni muhimu) “What is it about?”(Juu ya nini?) “It about us!”(Ni juu yetu) “I don’t have any deal with you.”(Sina biashara yoyote na wewe) “You just don’t know, give me time to explain!”(Hujui tu, nipe muda nikueleze) “Meeen! I need to go to bed, get the hell out of here!”(Hapana! Nahitaji kupumzika, ondoa upuuzi hapa!) “Let me be open!”(Acha niwe muwazi) “About what?”(Juu ya nini?) “I love you so much, please accept me in your life!”(Nakupenda sana, tafadhali kubali niwe maishani mwako) “You know what?”(Unajua nini?) “I don’t know!”(Sijui) “I hear that word ‘I love you’ about one hundred times a day, so you better go home, this is a wrong number.” (Nalisikia hilo ‘nakupenda’ karibu mara mia moja kwa siku, hivyo nakuomba tu uondoke, hapa siyo mahali sahihi.)
WAKATI Malkia wa Sokwe (Charlotte, binti anayeishi Msituni na Sokwe, ambaye baba yake anaamini alikufa ndege ilipoanguka miaka mingi kabla lakini kumbe alinusurika na kuingia kwenye himaya ya Sokwe) akiwa amewaagiza Sokwe wamtafute mvulana aliyempiga picha porini
(Harrison) baada ya kugundua hakufanana na wanyama hao ila kijana huyo, tayari Harrison yupo Los Angeles, amekwishachapisha kitabu chake kiitwacho Queen of the Gorillas na kujipatia mamilioni ya dola kutokana na mauzo dunia nzima.
Hivi sasa Harrison si yule wa zamani tena, ni mtu maarufu sawasawa na wacheza sinema wa Hollywood, akiishi Beverly Hills, maeneo ya watu matajiri, hajaoa na siku zote anatamani kurudi porini kwenda kumtafuta msichana mrembo aliyemwona, akiamini huyo ndiye alitakiwa kuwa mke wake.
Akiwa katika fikra hizo, amejitokeza msichana aitwaye Linda Morris, ambaye walikutana kwenye pati ambayo Harrison alipokea tuzo Cliff Edom’s New American Award kutokana na kitabu chake. Msichana huyu anamng’ang’ania Harrison hadi nyumbani kwake baada ya sherehe hiyo kuisha ingawa Harrison hataki kabisa uhusiano naye, alishaapa kutokuwa na uhusiano na msichana mwingine yeyote kabla hajamuoa Malkia wa Sokwe.
“I don’t care how many times you do hear the word ‘I love you’, all I know is I love you truly, please accept me!” (Sijali unalisikia neno ‘nakupenda’ mara ngapi kwa siku, ninachojua mimi ni kwamba ninakupenda mapenzi ya kweli. Tafadhali nikubali.) aliongea Linda tena akilengwalengwa na machozi, jambo lililoashiria wazi kuwa alimaanisha alichokisema. Harrison alimwonea huruma lakini hakuwa na cha kufanya, kwani moyo wake ulikuwa kwa mtu mwingine kabisa na mtu huyo alikuwa ni Charlotte, Malkia wa Sokwe.
“I can read your eyes and understand your heart, but…” (Naweza kuyasoma macho yako na kuuelewa moyo wako, lakini…) “But, what darling… I love you.” (Lakini, kitu gani tena mpenzi…nakupenda.) “I am committed to someone else and I promised my heart to love only one woman!”(Nimekwishajiweka kwa mtu mwingine na niliuahidi moyo wangu kumpenda mwanamke mmoja tu!) “Who is that luck woman?” (Huyo mwanamke mwenye bahati ni nani?) “Do you wanna know?”(Unataka kujua?) “Yeah!”(Ndiyo) “Won’t you be hurt?”(Hutaumia?) “Just tell me, whether I will be hurt or not is non of your business!”(Wewe niambie tu, nitaumia sitaumia, siyo shughuli yako!) “Why are you so fierce?” (Kwanini ni mkali hivyo?) “I love you and for really I don’t want loose you.”(Nakupenda na kwa hakika sitaki kukupoteza.) “So I shouldn’t tell you?”(Kwa hiyo nisikuambie?) “Ok, go ahead and tell me.”(Sawa, niambie tu.) “I don’t know her name, but she is the Queen of the Gorillas!”(Simjui jina lake, lakini ni Malkia wa Sokwe.) “The one in your book?”(Uliyemwandika kwenye kitabu chako?) “Yeah!?”(Ndiyo) “Oh my God! That sucks!” (Mungu wangu! Hiyo ni mbaya) “Why?”(Kwa nini?) “She is too dirty and shabby!” (Ni mchafu na shaghalabaghala!) “Don’t say that, do not call my girl that name.”(Usiseme hivyo, usimwite msichana wangu jina hilo.) Harrison aliongea machoni
akionyesha kukerwa, Linda hakuwa na namna zaidi ya kuomba msamaha. Waliendelea na maongezi mpaka saa tisa na nusu usiku, Linda akibembeleza na Harrison akiwa ameweka msimamo, hatimaye
usingizi ukawashika. Alichokifanya Harrison ni kumchukua Linda hadi nje ya nyumba kulikokuwa na nyumba ya wageni, akafungua mlango na kumkaribisha ndani ambako alimpeleka hadi chumbani na kumwonyesha bafu pamoja na choo kisha kumtakia usiku mwema.
“Why can’t I sleep in your room?”(Kwanini nisilale chumbani kwako?) “No! We might fall into temptations! Good night Linda” (Hapana! Tunaweza kuingia majaribuni usiku mwema Linda)
“Ok!”(Sawa!) Linda aliitikia kwa shingo upande na Harrison akaondoka kuelekea nyumbani kubwa ambako aliingia chumbani na kuanza kusoma kitabu chaQueen of the Gorillas akiangalia picha za Malkia wa Masokwe, alimpenda mno, hakuamini kama kungekuwa na mwanamke mwingine wa kumchanganya akili yake kama ilivyotokea.
Baadaye alipitiwa usingizi bila hata kuoga wala kuvua nguo alizokuwa nazo, aligutushwa usingizini na kengele ya mtu akitaka kufunguliwa mlango, alipotupa macho kwenye saa yake aligundua tayari ilikuwa ni saa kumi na nusu usiku, karibu kabisa na asubuhi. Haraka akanyanyuka na kufungua mlango kisha kuanza kushuka ngazi hadi chini.
“What’s up?”(Vipi tena?) Aliuliza baada ya kufungua mlango na kukutana na Linda. “I can’t sleep!”(Siwezi kulala) “Why?”(Kwa nini?) “There are so many ants inside there!”(Kuna wadudu wengi sana huko ndani.) “Ants? In my compound? No way! We do fumigate every week, please Lind stop your funny jokes!(Wadudu? Ndani ya eneo langu? Hapana! Tunapuliza dawa ya kuua wadudu kila wiki, Linda acha utani wako!)
“Yeah!”(Ndiyo!) aliitikia Linda akiwa tayari amekwishaingia ndani na kumwacha Harrison amesimama nje. Hakuwa na jinsi zaidi ya yeye pia kuingia ndani na kufunga mlango.
“So what do you want us to do?”(Kwa hiyo unataka tufanye nini?) “Let’s just go and sleep in your room.”(Twende tu tukalale chumbani kwako) “I have told you that can’t happen!”(Nimekwishakuambia hilo haliwezi kutokea)
“Please!”(Tafadhali!) Linda alizidi kubembeleza, huku akilia tena kwa uchungu kabisa, taswira hiyo ilimwingia Harrison moja kwa moja moyoni mwake na kujikuta akimwonea huruma. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Linda what do you want from me?”(Linda unataka nini kutoka kwangu?) “I don’t need anything, I am Linda Morris Ford, descendant of the Ford family, I so rich Harrison, I do not need a single penny
from you, all I need is your love, period!”(Sihitaji kitu chochote, acha nikuambie, ninaitwa Linda Morris Ford, kitukuu cha familia ya Ford, sihitaji hata senti yako, ninachohitaji ni penzi lako tu!) alisisitiza Linda huku akimsogelea Harrison na kumkumbatia.
Kilichotokea baada ya hapo ni watu wawili kupandisha ngazi hadi ghorofa ya kwanza ambako walinyoosha moja kwa moja hadi chumbani kwa Harrison, uso wa Linda ukiwa umeanza kurejewa na tabasamu, sehemu fulani ndani ya moyo wake alijisikia mshindi na kuamini kweli hakuna mwanamume alikuwa mjanja mbele ya mwanamke kama mitego ikiwekwa sawasawa.
“You are in this room under one condition.”(Uko ndani ya chumba hiki kwa sharti moja tu.) “What is that condition?”(Sharti hilo ni lipi?) “NO SEX!”(hakuna ngono) “I don’t need it either.”(Hata mimi sihitaji pia.) “Ok! Let get in bed now.”(Haya tulale.)
Harrison akajitupa kitandani na nguo zake vivyo hivyo Linda na gauni lake refu kama la bibi harusi, wakategana migongo na kuanza kutafuta usingizi, jambo ambalo lilikuwa gumu sana kutekelezeka. Kila mmoja alifikiria kimya akifikiria mambo yaliyokuwa
yakitokea, Harrison akimfikiria Malkia wa Sokwe na Linda akiwaza namna ambavyo angelifanikisha zoezi la kumfanya Harrison amvue nguo na wafanye tendo la ndoa.
“Kwa shepu yangu lazima atalegea tu, acha nicheze mchezo wa sitaki nataka kwanza asije akaniona rahisi.” Aliwaza Linda akiwa kimya.
Nusu saa baadaye alianza kumsikia Harrison akikoroma, akagundua kweli mwanaume huyo alikuwa mgumu na alidhamiria kutofanya tendo hilo.Akamsogelea karibu na kumwekea paja lake kubwa kwa juu kisha kusogeza mdomo wake karibu kabisa na sikio la Harrison, taratibu akaanza kumhemea sikioni akiamini kitendo hicho lazima kingemsisimua, lakini Harrison aliendelea kukoroma kama vile hapakuwa na kilichokuwa kikiendelea.
“Harrison!Harrison!” aliita akimtingisha baada ya kuona kile alichofanya kilikuwa hakiwezekani. “Vipi tena?” “Hebu nifungulie zipu mgongoni, hili gauni linanipa joto sana!” “Lakini kuna kiyoyozi? Tena mimi nasikia baridi sana.” “Nataka kwenda kuoga.” “Sawa!”
Harrison alimfungua zipu, akiwa amefumba na kufumbua macho yake nusu sababu ya usingizi, kisha kurejea kitandani na Linda akanyoosha moja kwa moja ambako alivua gauni lake na kuoga.Haukupita muda mrefu sana akaibuka na gauni lake mkononi, akiwa kama alivyozaliwa, shepu yote nje! Harrison alikuwa usingizini akasogea hadi karibu yake kabisa na kumgusa. “Harrison! Harrison!” “Naam.” “Niweke wapi hili gauni?” “Kwenye kabati!” “Liko wapi?” “Hapo kushoto.” “Sioni.”
Harrison aliketi kitako na kumwangalia Linda, ilikuwa ni kama ndoto kwa alichokuwa akikiona mbele ya macho yake, hakuwa na uhakika kama katika maisha yake yote aliwahi kukutana na mwanamke mwenye umbile la namna hiyo. “Mungu wangu!”Ndilo neno pekee alilosema wala hakukumbuka swali ambalo Linda alikuwa ameuliza.
KIJANA maarufu Harrison ambaye umaarufu wake umetokana na kuandika kitabu kiitwacho Queen of the Gorillas ambacho kimeuzwa mamilioni ya kopi duniani na kumfanya awe miongoni mwa matajiri anajikuta katika mapenzi mazito na msichana wa msituni ambaye aliandika kitabu juu yake.
Msichana huyu ni Charlotte, ambaye miaka mingi kabla alikuwa akisafiri na mama yake kwenye ndege kuelekea Uswizi, ndege ikaanguka na watu wote kufa isipokuwa yeye, akaokotwa na Sokwe ambao walimlea mpaka akakulia msituni akiwa hajui chochote na sokwe walimfanya Malkia wao.
Harrison alipomwona msichana huyu alikuwa akifanya utafiti wa Sokwe porini na baada ya kuuza kitabu chake alitamani kurejea porini kwenda kumtafuta, akijiandaa kufanya hivyo, anakutana na msichana mwingine mrembo aitwaye Linda ambaye amedhamiria kumpata kwa gharama yoyote.
Pamoja na kukataa, Harrison anajikuta amemkaribisha Linda nyumbani kwake na wanakubaliana kulala na nguo ili wasifanye mapenzi lakini usiku wa manane Linda ameanza vituko, yupo kama alivyozaliwa na Harrison anashuhudia.
MACHO ya Harrison yalitua moja kwa moja kwenye maumbile ya Linda, akamwangalia kutoka kichwani, akaridhika kabisa kwamba sura ya Linda haikuwa ya kuvutia sana lakini kilichompa pointi ni ile ambayo vijana wengi huiita ‘Figa’. Hakika Linda aliumbika.
Kifuani alikuwa na vilima viwili vilivyonyanyuka vyenye ncha kali, kushuka tumboni hakuwa na tumbo kabisa, wala yale ambayo huiitwa ‘sanamu la michelini’ chini ya tumbo kulikuwa na kiuno chembamba ambacho chini yake kidogo tu mtoto alipanuka mithili ya mtungi wa maji, halafu chini ya hapo akaanza kupungua na mwisho kabisa kulikuwa na mguu mzito.
Huyo ndiye alikuwa Linda, hakika Harrison alihitaji nguvu ya ziada ili kuweza kukishinda kishawishi kilichokuwa mbele yake, kwani kila dalili ilishaonekana kwamba alichohitaji msichana huyo ni tendo la ndoa na alikuwa amedhamiria. Bila kutarajia Harrison alianza kusikia suruali yake ikimbana kwa mbele chini ya mkanda.
“Nitaweza? Mimi mwanaume bwana lazima nionyeshe uwezo, nilishaahidi sitatembea na mwanamke kabla ya ndoa na mwanamke pekee ninayemtaka maishani mwangu ambaye atatakiwa kunibikiri kama hata wanaume huwa wanabikiriwa ni Malkia wa Sokwe, basi! Ee Mungu nisaidie,” aliwaza Harrison akimwangalia Linda mbele yake.
Alichokifanya ni kufumba macho na kumwelekeza Linda mahali pa kutundika nguo yake, kisha msichana huyo akaja moja kwa moja na kupanda kitandani akiwa kama alivyozaliwa. Harrison alivuta shuka na kujifunika, kisha kuzihamisha kumbukumbu zake kwa msichana huyo na kuzipeleka msituni; akaanza kumfikiria Malkia wake wa Sokwe.
Hakuchukua muda mrefu sana, fahamu zikampotea, alikuwa katikati ya usingizi, wala hakukumbuka kwamba kando yake alikuwepo Linda akihema kwa nguvu sababu ya tamaa za mwili wake. Kilichomshtua usingizi ni kitu kizito kikimgandamiza ubavuni. “Nini tena Linda?” “Siwezi!” “Huwezi nini?” “Kuvumilia.”
“Lakini tumekubaliana hakuna tendo la ndoa kati yetu.” “Naelewa, lakini nimezidiwa sana, nihurumie Harrison, leo tu, wala haitatokea tena siku nyingine.” “Haiwezekani Linda, nilishaweka kiapo.”
Linda akaanza kulia akimbembeleza Harrison akubali lakini haikuwezekana mwisho akaanza kujieleza kuhusu lengo lake, kwamba hakuwa na nia yoyote ya mali alizokuwa nazo, wala alikuwa havutiwi na umaarufu wake isipokuwa alimpenda kutoka moyoni. “Harrison” “Naam.” “Hivi unajua mimi natoka familia gani?” “Ndiyo, familia ya Ford.” “Kwa hiyo sina shida na pesa, tunazo nyingi za kutumia mpaka wajukuu zetu.” “Najua.”
“Kwa hiyo sikufuati kwa sababu ya fedha zako bali ninakupenda kutoka moyoni!” “Najua lakini hatuwezi kufanya tendo la ndoa, nakubali tuwe marafiki.”
Linda akajibwaga pembeni kwa hasira na kuanza kulia, Harrison alimbembeleza lakini haikusaidia ikabidi aendelee mpaka asubuhi akililia penzi.Harrison alidamka asubuhi na kuandaa kifungua kinywa, wakanywa pamoja baada ya kuamka na kuoga, kilichofuata
hapo ikawa ni mazungumzo, Harrison akijaribu kumpa mwenzake ushauri juu ya maisha na kufanya maamuzi sahihi. Saa nne kamili Linda aliondoka, wakiwa wamekubaliana kuendelea na urafiki wa kawaida badala ya mapenzi na hivyo ndivyo
ilivyotokea, kila mwisho wa wiki walikuwa pamoja kiasi cha watu kufikiri kulikuwa na uhusiano zaidi ya kawaida kati yao. Harrison alitambulishwa kwenye familia ya Ford na Linda akatambulishwa kwenye familia ya Harrison, wote walifurahia na
waliwashawishi hata wafikirie kufunga ndoa ili kuimarisha zaidi uhusiano wao lakini kwa Harrison jambo hilo lilionekana haliwezekani.
“When is your birthday?”(Siku yako ya kuzaliwa ni lini?) Linda alimuuliza Harrison wakiwa wameketi ufukweni maeneo ya Santa Monica wakipunga upepo. “Tenth August every year!”(Tarehe kumi mwezi wa nane kila mwaka.) “Do you celebrate?”(Huwa unasherehekea?) “Yeah, but not too much! And when is yours?”(Ndiyo, lakini siyo sana na yako ni lini?) “April twenty eighth! ”(Tarehe ishirini na nane mwezi wa nne.) “Do you celebrate?”(Huwa unasherehekea?) “So much.”(Sana.)
Linda alikuwa amefahamu siku ya kuzaliwa Harrison mwanzoni tu mwa urafiki wao baada ya kuchunguza mtandaoni, hakumwambia Harrison chochote na siku hiyo wakiwa wameketi ufukweni ilikuwa ni tarehe kumi mwezi wa nane, kwa sababu ya shughuli nyingi alizokuwa nazo Harrison alikuwa hakumbuki chochote. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Baada ya mazungumzo yao yaliyoisha kwenye saa nne hivi usiku, ndipo Linda alishauri wahame kutoka mahali walipokuwa na kuingia ndani sababu ya baridi kali. Wakanyanyuka na kuingia ukumbini ambako Harrison alishangazwa na idadi ya watu kuwa kubwa, jina lake likiwa limeandikwa ukutani na watu wote wakanyanyuka na kushangilia huku wakiimba wimbo wa ‘Happy
Birthday’ Harrison akapigwa na butwaa, kumbe Linda alishaandaa kila kitu na familia zote mbili zilikuwepo. Hakuamini alipomwona mama yake katikati ya watu, akasogea karibu na kumkumbatia kwa furaha huku mama yake akimtamkia maneno ya kumtakia afya njema na maisha marefu. Baadaye watu wote walifika na kumkumbatia wa mwisho kabisa akawa ni
Linda ambaye alipata nafasi ya kuzungumza ili kuanza rasmi sherehe. “Nakupenda Harrison, sikupendi kawaida tu, nakupenda isivyo kawaida na ningefurahi mambo yangekuwa tofauti na yalivyo sasa!
Hongera kwa kutumiza miaka ishirini na sita.” Alimaliza Linda na kumsogelea Harrison, akampiga busu usoni.
“Ahsante Linda, nakupe…” Harrison alishindwa kumalizia maneno hayo, machozi yakamlengalenga, upande fulani wa moyo wake ulikuwa unaanza kumpenda Linda lakini alikuwa akipambana nao kwa nguvu zote kwani hakutaka kumsaliti mwanamke aliyempenda ambaye wala hakuwa na habari juu ya penzi hilo.
“Kuna kitu kidogo kama zawadi yako, ningependa nikupe sasa hivi kabla ya chakula rafiki yangu mpendwa, mabibi na mabwana, wazazi wangu, ndugu na marafiki nimejitahidi kutunza fedha kidogo kidogo kwa muda mrefu ambazo nimezitumia kumnunulia
Harrison zawadi yake ya siku ya kuzaliwa…” Linda aliongea akiwa amejawa na tabasamu watu wote uwanjani wakageukia upande alikoelekeza mkono wake. Pazia likafunguka.
Lilikuwa ni gari jeusi, lenye matairi makubwa na likiwa limepambwa vyema ambalo liliendeshwa taratibu kuingizwa katikati ya ukumbi, kila mmoja wao akayasoma maandishi ubavuni “Ranger Rover” mpyaaaaa! Harrison hakuamini, akiwa katika mshangao, Linda alimsogelea na kumkumbatia, kisha kuusogeza uso wake karibu kabisa na wa Harrison.
HARRISON amepata mafanikio makubwa sana baada ya kuchapisha kitabu kiitwacho Queen of Gorillas ambacho kinamhusu msichana mrembo aliyempiga picha katikati ya pori akiwa amezungukwa na sokwe, alionekana ni kama mnyama wa porini kwa tabia zake zilivyokuwa, hakika msichana huyo alifanana na sokwe kwa kila kitu isipokuwa maumbile.
Harrison hivi sasa ni milionea wa dola za Kimarekani, anaweza kulinganishwa kabisa na wacheza sinema wa Hollywood. Ameingia kwenye orodha ya watu maarufu wa nchi hiyo na hivi sasa kinachomsumbua sana ni mabinti ambao wengi wanampenda na wanataka kuwa wapenzi wake ili baadaye waolewe naye.
Akili yake yote ipo kwa msichana aliyemwona porini ambaye ndiye alimwandikia kitabu na kujipatia utajiri, huyu ndiye anataka kurudi porini kwenda kumtafuta ili baadaye aweze kuwa mke wake. Anamuota kila siku, kumuwaza kila mara na anaamini ndoto yake itatimia. Akiwa katika fikra hizo anaibuka Linda, msichana kutoka familia tajiri ya akina Ford ambao utajiri wao hauwezi kuisha mpaka kwa wajukuu.
Msichana huyu anampenda Harrison na amedhamiria kumpata kwa gharama yoyote, anaamini huyu ndiye atakuwa mume wake. Harrison hataki sababu ya mwanamke wake wa msituni.
Linda anabembeleza kwa muda mrefu lakini anakataliwa na kuombwa awe rafiki wa kawaida, akakubali, ukaribu ukaongezeka siku hadi siku na mwisho wakajikuta wamekuwa kama wapenzi huku Linda akiingia moyoni mwa Harrison taratibu.
Ni siku ya sikukuu ya kuzaliwa Harrison, Linda anampa zawadi ya ajabu ya gari aina ya Ranger Rover Sport, ya thamani kubwa. Harrison haamini anachokishuhudia na ghafla moyo wake unaanza kumpenda Linda ambaye sasa amemkumbatia, amemsogezea uso, pua zimegusana na baadaye midomo tena mbele za watu, Harrison anakielewa kinachotaka kutokea lakini hana jinsi, ameanza kumpenda Linda.
“NO!”(hapana) ilikuwa ni sauti ya Harrison kabla ndimi zao hazijagusana, akili yake ilikuwa imerejea tena msituni kwa Malkia wa Masokwe, bado alimpenda msichana huyo kuliko alivyompenda Linda pamoja na utajiri wa familia yake. “Why?”(Kwa nini?) “We can’t do that before our parents.”(Hatuwezi kufanya hivyo mbele ya wazazi wetu.) Hilo ndilo lilikuwa jibu la Harrison ambalo kwa Linda lilimaanisha kulainika kidogo, kwani tafsiri yake ilikuwa kama wazazi wasingekuwepo walichotaka kufanya kingetendeka. “Can we go outside?”(Tunaweza kwenda nje?) “Not now, may be later!”(Siyo sasa! Labda baadaye.)
Linda akasinyaa, hata hivyo alijikaza na kumshika Harrison mkono ili watu wasigundue na kwenda naye moja kwa moja hadi kwenye gari ambako alitamka maneno: “Hii ndiyo zawadi yako” kisha wote wawili wakaingia ndani ya gari, watu wakishangilia na kurudi kinyumenyume wakitoka ukumbini huku MC akiendelea.
Nje ya ukumbi, kwenye giza kidogo, alichokifanya Linda ni kumwambia Harrison asimamishe gari, akajinyoosha hadi upande wa dereva na kumshika mabegani huku gia ikimuumiza kiunoni lakini hakujali, akamvuta karibu yake na hatimaye midomo yao ikagusana, kilichofuata baada ya hapo ni ambacho Harrison kwa kipindi kirefu alikuwa amekipinga; mabusu.
“I love you Harrison!”(Nakupenda Harrison.) “Nakupenda pia Linda.” “Kweli?” “Kabisa.” “Vipi juu ya yule mwanamke wa msituni?” “Nimebadilisha mawazo.”
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa penzi lao, Linda akawa amemzidi Harrison ujanja na kumwingiza mtegoni. Alifahamu kabisa alikuwa hapendwi lakini moyoni aliamini kwamba penzi kama ulivyo mmea mwingine wowote, hukua iwapo litaendelea kumwagiliwa na kuwekewa mbolea.
Kazi ya Harrison sasa ilishakuwa ni utunzi wa vitabu, maana hivyo ndivyo vilikuwa vimempa jina na kipato ambacho hakuwahi kutarajia kuwa nacho, akaanzisha kampuni iitwayo Upgraded Publishing Company Ltd yeye akiwa mkurugenzi. Pamoja na kuandika vitabu pia aliwasaidia waandishi wengine wachanga waliokuwa na miswada yao ambayo ilikuwa haijachapishwa, kuiandaa na hatimaye kuichapisha.
Linda alifanya kazi kwenye kampuni ya magari ya familia yao, lakini kila siku jioni ilikuwa ni lazima waonane na mara nyingi alilala nyumbani kwa Harrison hasa siku za mwisho wa wiki, mapenzi yalizidi kupamba moto na kila mmoja akamtambulisha mwenzake kwa familia yake, watu wote waliwafurahia na kuwataka wafunge ndoa haraka iwezekanavyo.
“Lini mnatarajia kufunga ndoa?” Baba wa Linda alimuuliza Harrison siku moja. “Bado kidogo.” “Fanyeni haraka, kwa muda mrefu nimesubiri sana harusi ya Linda.” “Haitapita miezi sita!” “Eti Linda ni kweli?” “Ni kweli baba.”
Nusu ya mawazo ya Harrison yalianza kutawaliwa na Linda, lakini nusu yalibaki msituni, karibu kila siku alimfikiria Malkia wa Masokwe akiwa na uhakika kabisa kwamba wala msichana huyo alikuwa hamkumbuki. Ni kweli alitaka kumuoa Linda lakini
upande mwingine bado alitaka kumuoa Malkia wa Masokwe, mawazo hayo yakamweka njia panda akiwa ameshindwa kabisa kuelewa nini cha kufanya.
Wakati huohuo, Linda alikuwa taaban kimapenzi, hakuwa tayari kusikia habari ya mwanaume mwingine yeyote, akili yake alishaihamishia kwa Harrison. Hakuwa msichana mwenye tabia mbaya, alijiheshimu na wanaume wengi walitaka kumuoa lakini aligundua kilichowafanya wengi wachukue uamuzi huo ilikuwa ni utajiri wa familia yake, walifikiria mali zaidi kuliko yeye ndiyo maana alipokutana na Harrison alizama moja kwa moja.
“Sijui nitafanya nini siku ukiniambia unaniacha.” “Siwezi kukuacha Linda.” “Unasema kweli?” “Kabisa.” “Mwanamke wako wa msituni je?” “Huyo…” “Huyo nini?”
“Tuachane naye!” alijibu Harrison ingawa ukweli wa mambo ni kwamba bado msichana huyo alimtesa, kuna wakati hata alifikiria kumkimbia Linda lakini alishindwa akijua lazima msichana huyo angejiua na familia ya Ford isingemwacha Harrison hai kama tukio hilo lingetokea.
Miezi saba baadaye, Harrison akiwa katikati ya fikra kati ya wanawake hao wawili, maandalizi ya harusi yalianza, michango kutoka kwa marafiki na familia ikafanyika. Maelfu ya dola yalikusanywa, kampuni maalum ya kuandaa na kusimamia harusi iliyoitwa Los Angeles Wedding Planners ndiyo ilipewa tenda ya kusimamia harusi hiyo haraka ambayo watu wote maarufu nchini Marekani walitarajiwa kuhudhuria ikiwa ni pamoja na rais wa taifa hilo kubwa na lenye nguvu duniani.
Kwa Linda ilikuwa furaha kubwa lakini kwa Harrison ilikuwa nusu furaha ingawa hakutaka kuonesha wazi akiwa hataki kumvunja moyo mke wake mtarajiwa, bado akili ilikuwa msituni lakini alikosa jinsi ya kujinasua kwa jinsi mambo yalivyokuwa yamepelekwa maana harusi hiyo ilikuwa gumzo kwenye vyombo vya habari, hasa taarifa ziliposambaa kwamba hata mwana wa Mfalme wa Uingereza ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa familia ya Ford alihudhuria.
“Hivi nampenda kiasi cha kumuoa kweli? Nitaishije maisha ya taabu miaka yote? Kwa nini nisiachane na hili jambo nikaingia msituni kumtafuta mwanamke nimpendaye?” aliwaza Harrison.
Hakuwa na uwezo wa kuchukua hatua hiyo kwa kuhofia Linda angejidhuru na hilo lingemletea matatizo, hivyo akaendelea kutulia na kuacha mambo yaendelee mpaka siku ikawadia ambayo watu zaidi ya elfu tatu walijaa ndani ya Kanisa la Los Angeles Baptist
Church kushuhudia harusi hiyo kubwa na ya kifahari ikifungwa. Linda aliingia akiwa na msafara wa magari ya kifahari zaidi ya kumi na kuongozwa moja kwa moja kuingia kanisani, Harrison alikuwa hajafika, mpaka nusu saa kabla ya muda wa kufunga ndoa hakuwa ameonekana kanisani. Linda na watu wengine wakaanza kuingiwa na wasiwasi, wazazi wakachanganyikiwa na watu mbalimbali walimfuata mama yake aliyekuwepo kanisani kumuuliza. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Anakuja, nimemwacha nyumbani.” “Kweli?” “Kabisa.”
Hali iliendelea kuwa hivyo mpaka zilipobaki dakika tano ndipo muungurumo mkubwa wa pikipiki ukasikika, alikuwa ni Harrison na suti yake nyeusi, jasho likimtoka. Maelezo yake yakawa ni kwamba alikutana na foleni, hivyo kuamua kukodisha pikipiki. Linda alipomwona kanisani, alifuta machozi na furaha ikamjaa.
Watu wakaanza kuimba nyimbo za sherehe ya ndoa, walinyamaza mchungaji alipoingia na kuanza kuiendesha sherehe hiyo mpaka sehemu ambapo wawili hao walitakiwa kula kiapo na kuvishana pete. Kwanza aliuliza kama kulikuwa na mtu mwenye pingamizi, hakuna aliyejitokeza, hapo ndipo mchungaji akamgeukia Linda.
“Linda unakubali kuolewa na Harrison awe mume wako katika shida na raha, katika mateso na chuki, umpende na kumheshimu siku zote za…” “Ndiyo nakubali.”
Kanisa likalipuka kwa shangwe na nderemo pia vifijo, kabla mchungaji hajamgeukia Harrison na kumuuliza swali lilelile, badala ya kujibu ili watu washangilie, alibaki kimya kwa kama dakika tatu, ikabidi mchungaji aulize tena huku kanisa zima likiwa kimya. “Sikubali!” Linda akaanguka chini, Harrison akatoka mbio hadi nje ambako muungurumo wa pikipiki ulisikika akiondoka kwa kasi.
HARRISON, mtoto wa marehemu Harvey na Skyler, amepata mafanikio makubwa sana baada ya kuchapisha kitabu kiitwacho Queen of Gorillas kinachomhusu msichana mrembo anayeishi na masokwe ndani ya msitu mkubwa wa Tongass.
Alifanikiwa kumpiga picha msichana huyo mrembo katikati ya pori akiwa amezungukwa na sokwe, akiwa na haiba zote kama mnyama wa porini, hakika msichana huyo alifanana na sokwe kwa kila kitu isipokuwa maumbile.
Baada ya kuupata utajiri huo, Harrison anaingia kwenye orodha ya watu maarufu wa nchi hiyo na hivi sasa kinachomsumbua sana ni mabinti ambao wengi wanampenda na wanataka kuwa wapenzi wake ili baadaye waolewe naye.
Miongoni mwa mabinti hao ni Linda, msichana kutoka familia ya kitajiri anayetokea kumpenda sana Harrison na kutaka awe mume wake. Licha ya kumweleza mara kadhaa kuwa hampendi, Linda anamng’ang’ania mpaka baadaye wanakubaliana kufunga ndoa kanisani.
Siku ya harusi inafika, Linda anatangulia kanisani akiwa amerembwa kama bibi harusi, watu mashuhuri kutoka sehemu mbalimbali wanamiminika kanisani kushuhudia ndoa hiyo lakini mambo yanageuka na kuanza kwenda mrama baada ya Harrison kumkataa binti huyo madhabahuni.
WAPAMBE wa bwana na bibi harusi pamoja na wazazi wa pande zote mbili walikuwa na kazi ya ziada ya kumpepelea Linda ili arejewe na fahamu huku taratibu za kutafuta gari la kumkimbiza hospitalini zikifanywa kwa kasi.
“Mlegezeni mkanda wa gauni, mvueni viatu na vitu vyote vinavyombana,” alisema mchungaji, wapambe na wazazi wake wakafanya kama walivyoelekezwa. Kila mmoja alikuwa akihaha kuokoa maisha ya Linda.
Wakati hayo yakiendelea, kanisa zima lilikumbwa na hali ya sintofahamu, kila mtu akiwa haamini kilichotokea. Minong’ono na sauti za watu wakilia chinichini zilisikika kutoka kila kona ya kanisa, wengine wakilifananisha tukio hilo na filamu ya kusisimua.
Muda mfupi baadaye, ving’ora vya gari la kubebea wagonjwa (ambulance) vilianza kusikika nje ya kanisa. Manesi wanne waliokuwa na kitanda cha kubebea wagonjwa, walipandisha ngazi za kanisa na kuingia ndani haraka baada ya kupigiwa simu na wazazi wa Linda, waumini wakawapisha wafanye kazi yao ambapo walipitiliza mbiombio mpaka madhabahuni, eneo Linda alipodondokea na kupoteza fahamu.
Wakasaidiana kumuinua Linda na kumlaza kwenye kitanda cha magurudumu, sekunde chache baadaye wakawa wanakisukuma kitanda kile kwa kasi, Linda akiwa amelala katika hali ya kupoteza fahamu. Walitoka mpaka nje, milango ya ambulance ikafunguliwa, mpambe wa bibi harusi na mama mzazi wa Linda pamoja na wale manesi, wakaingia na safari ya kuelekea hospitali ikaanza kwa kasi kubwa.
Waumini waliosalia kanisani walitoka nje na kulisindikiza gari lile kwa macho mpaka lilipopotea kabisa, wakajikusanya vikundivikundi na kuanza kujadili kilichotokea.
“Huyu si juzijuzi tu alimtunukia zawadi ya gari la kifahari aina ya Range Rover mumewe mtarajiwa siku ya ‘birthday’ yake?” “Ndiyo! Bibi harusi kwao mambo safi, si unamjua vizuri baba yake? Anatisha kwa utajiri.” “Sasa kwa nini amemkimbia bibi harusi? Si bora angekataa tangu mapema?” “Inawezekana Linda ndiyo alikuwa analazimisha mapenzi.” “Hamna kitu kama hicho, yule bwana harusi atakuwa amerogwa, siyo bure.” “Wanaume wabaya sana, sasa kama alikuwa hamtaki kwa nini alikubali kuja kanisani?”
Kila mtu alikuwa akizungumza lake kanisani pale lakini hakuna aliyeweza kuubadili ukweli kuwa Harrison alimkimbia Linda madhabahuni. *** Muungurumo wa pikipiki kubwa ulisikika nje ya nyumba ya Rogers Presley, kijana wa Kimarekani aliyekuwa akifanya kazi kwenye Hospitali ya Oklahoma Medics.
“Nani tena huyo anayekuja kwa kasi kama yupo kwenye mashindano ya pikipiki?” alijiuliza Rogers wakati akifunua pazia la sebuleni kwake na kuchungulia nje. “Haaa! Harrison? Ni wewe?” “Ni mimi Rogers, yaani hapa sijielewi kabisa.” “Kwani vipi? Leo si ndiyo siku yako ya kufunga ndoa na Linda?” “Ndiyo Rogers lakini mambo yamekuwa ndivyo sivyo, ngoja nitakusimulia kila kitu,” alisema Harrison huku akihema kwa nguvu. Rogers akamshika mkono na kuingia naye hadi ndani, wakakaa sebuleni huku Rogers akiwa na hamu kubwa ya kutaka kujua kilichotokea.
Harrison na Rogers walikuwa ni marafiki tangu wakiwa watoto wadogo, walisoma pamoja shule ya msingi na baadaye sekondari ingawa baadaye walitengana baada ya Rogers kwenda kusomea uuguzi katika Chuo Kikuu cha Havard nchini humo. Urafiki wao uliendelea hata baada ya kila mmoja kumaliza masomo na kuanza kazi.
“Rogers! Wewe ni rafiki yangu mkubwa sana.” “Ndiyo najua Harrison.” “Nadhani unafahamu kila kinachoendelea kati yangu na Linda.” “Ndiyo najua Harrison lakini niliposikia unafunga naye ndoa, nilijua umeamua kurudisha moyo wako nyuma.” “Nimejitahidi sana kuulazimisha moyo wangu lakini kiukweli simpendi kabisa Linda.” “Ni sawa Harrison, lakini bado hujaniambia nini kilichotokea.” “Nimefanya dhambi kubwa sana leo, ooh! Linda nisamehe,” alisema Harrison huku akianza kutokwa na machozi. Ilibidi Rogers amsogelee na kuanza kumtuliza huku akimsihi amueleze kilichotokea ili wajue nini cha kufanya. “Nimemkana Linda madhabahuni na kumkimbia.” “Whaaaaat? Are you out of your mind?” (Niniiii? Umechanganyikiwa?) aliuliza Rogers huku akiwa amemtumbulia macho Harrison. “Nimefanya kosa kubwa sana, najua kila mmoja atanichukia lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kufanya hivi nilivyofanya,” alisema Harrison huku akizidi kububujikwa na machozi. “Sasa kwa nini umefanya hivyo Harrison?” “Rogers, nampenda sana malkia wa masokwe, nadhani hata wewe unalijua hilo. Sipo tayari kumpoteza na kumuoa mwanamke mwingine yeyote. Naomba msaada wako.”
Rogers alikaa kimya kwa zaidi ya dakika mbili, akawa anatafakari kwa kina kile alichokisikia, mwisho akashusha pumzi ndefu na kumgeukia Harrison.
“Najua jinsi unavyojisikia Harrison lakini kwa kuwa wewe ni rafiki yangu, nipo tayari kukusaidia.” “Utanisaidiaje Rogers? Nataka kwenda kuishi na malkia wa masokwe.” “Najua familia ya akina Linda haiwezi kukubali jinsi ulivyomdhalilisha binti yao. Baba yake anaweza hata kutuma watu waje kukuua. Namjua vizuri yule mzee. Sasa hapa inabidi tucheze mchezo wa kimafia.” “Nipo tayari kwa lolote utakalolisema Rogers, nakutegemea wewe.”
“Inabidi tupate maiti moja ya kiume inayoshabihiana na wewe kisha nitakuelekeza nini cha kufanya.” “Maiti? Halafu itakuwaje?”
“Nitakuelekeza cha kufanya, ngoja niende kuzungumza na mtu wa mochwari pale hospitalini ninapofanyia kazi kisha nitakuelekeza nini cha kufanya,” alisema Rogers na kusimama, akamuaga Harrison na kutoka nje mpaka mahali anapopaki gari lake. Akaliwasha na kuondoka kwa kasi.
Harrison alibaki ameduwaa akiwa hajui rafiki yake huyo alikuwa amefikiria mpango gani kichwani mwake. Baada ya takriban dakika thelathini, Rogers alirejea na kuliingiza gari lake mpaka sehemu ya maegesho, akatoka na kumuita Harrison wasaidiane kubeba maiti iliyokuwa kwenye buti. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Baada ya kuiingiza ndani, Rogers alimwambia Harrison avue kila kitu, kuanzia suti yake ya harusi iliyonunuliwa kwa bei mbaya mpaka viatu. Akapewa nguo nyingine za kuvaa kisha wakaanza kusaidiana kuivalisha maiti ile zile nguo za Harrison. Baada ya muda wakawa wameshamaliza.
UTAJIRI mkubwa alioupata Harrison, mtoto wa marehemu Harvey na Skyler, umekuja baada ya kijana huyo kuchapisha kitabu kiitwacho Queen of Gorillas kinachomhusu msichana mrembo anayeishi na masokwe ndani ya msitu mkubwa wa Tongass.
Harrison anafanikiwa kumpiga picha msichana huyo mrembo katikati ya msitu wa Tongass akiwa amezungukwa na masokwe, akiwa na haiba zote kama mnyama wa porini.
Hata hivyo, licha ya kuwa na tabia kama mnyama, Harrison ambaye sasa ameshaingia kwenye orodha ya watu maarufu wa nchi hiyo, anatokea kumpenda sana kiasi cha kuwakataa wasichana wote waliokuwa wanataka kuolewa naye.
Penzi alilonalo Harrison kwa malkia wa masokwe, linamfanya amkatae Linda, msichana kutoka familia tajiri aliyetokea kumpenda sana. Anamkana madhabahuni siku ya harusi yao kisha kukimbia kuelekea kusikojulikana kwa kutumia pikipiki kubwa.
“NIWEKE wazi Rogers, unataka kufanya nini?” “Tulia Harrison, si unataka msaada kutoka kwangu?” “Ndiyo.” “Basi tulia uone nitafanya nini, wasiwasi wa nini?” “Inatakiwa tufanye haraka, ndugu zake Linda wanaweza kuja hapa ikawa balaa,” alisema Harrison kwa hofu, Rogers akaendelea kushikilia msimamo wake wa kumtaka atulie. Baada ya kumaliza kuivalisha maiti ile nguo alizokuwa amevaa Harrison, Rogers alimwambia kuwa inatakiwa lipatikane gari la kununua au la kukodi haraka iwezekanavyo. “Sasa tutapata wapi gari?” “Kwani wewe huna fedha za akiba?” “Ninazo lakini kadi zangu za benki na nyaraka zote nimeviacha nyumbani na siwezi kurudi.” “Basi usijali, kwa kuwa nimeamua kukusaidia nitakupa lile gari langu ambalo silitumii.” “Halafu nini kitafuata?” “Nataka tutengeneze ajali ambayo itawafanya watu wote waamini kwamba umekufa.” “Nimekufa? Rogers! Huoni kama ni hatari?” “Hiyo ndiyo mbinu pekee itakayokufanya uendelee na maisha ambayo umeyachagua wewe mwenyewe.” “Sasa mbona sura yangu na hii maiti hazifanani?” “Hiyo mbona kazi ndogo sana,” alisema Rogers huku akivaa ‘gloves’ mikononi mwake. Akafungua kabati lililokuwa ukutani na kutoa chupa kubwa iliyokuwa na maandishi yaliyosomeka Concentrated Hydrochloric Acid. Rogers alisogea mpaka pale kwenye ile maiti, akafungua mfuniko wa chupa iliyokuwa na tindikali na kuimwagia ile maiti usoni. Katika hali ambayo Harrison hakuitegemea, ndani ya sekunde chache alishangaa kuona sura ya ile maiti ikiharibika kiasi cha kutotambulika. Rogers alipomaliza, alimwelekeza kuwa wasaidiane kuibeba ile maiti mpaka kwenye gari. Harrison alifanya kama alivyoelekezwa, wakaibeba na kuitoa mpaka sehemu ya maegesho ya magari, wakaiingiza na kuikalisha ndani ya gari dogo aina ya Corolla lililokuwa na vioo vyenye rangi nyeusi (tinted). Wakaipakiza na pikipiki ya Harrison. “Tutakwenda mpaka kwenye daraja la Miami, pale nitakuelekeza cha kufanya,” alisema Rogers huku akikanyaga mafuta na kuingiza gia, gari lao likawa linasafiri kwa kasi kubwa kuelekea Miami. Safari haikuwa nyepesi kutokana na umbali uliokuwepo kutoka Oklahoma mpaka Miami. Baada ya kusafiri kwa saa nyingi, hatimaye walifika kwenye daraja kubwa la Miami lililokuwa likipita juu ya bahari na kuunganisha upande mmoja na mwingine. Rogers alitafuta sehemu nzuri, akapunguza mwendo na kusimamisha gari. Akamuelekeza Harrison nini cha kufanya. “Inabidi tusaidiane kuiteremsha pikipiki na kuiweka katikati ya barabara, kisha tutapita na gari juu yake ili ionekane umegongwa na gari ukiwa unaendesha pikipiki.” “Halafu hii maiti tutaifanyaje?” “Tutaiburuza kidogo barabarani kisha tutaitupia baharini.” “Watu wakituona si itakuwa balaa?” “Muda huu hakuna watu wengi wanaoitumia hii barabara.” Baada ya kusema vile, waliteremka haraka garini na kuishusha pikipiki. Rogers akarudi ndani ya gari na kukanyaga mafuta kwa nguvu, akaenda kuigonga ile pikipiki na kuifanyaiharibike vibaya. “Zoezi la kwanza limekamilika, bado la pili,” alisema Rogers huku akifungua mlango wa nyuma wa gari. Wakasaidiana kuitoa ile maiti, wakaiburuza kwenye kingo za barabara na kuifanya ipate majeraha mengine, walipomaliza wakasaidiana kuitosa baharini. Kishindo kikubwa kikasikika; chubwii! Harakahara walirejea kwenye gari, wakaingia na kuondoka kwa kasi kubwa bila kuonekana na mtu yeyote. *** “Hapa ni wapi?” aliuliza Linda baada ya kurejewa na fahamu zake na kujikuta akiwa ametundikiwa dripu ndani ya chumba kilichokuwa na rangi nyeupe, akiwa amefunikwa mashuka meupe. “Hapa ni wapi na nimefikaje?” aliuliza tena Linda, mama yake aliyekuwa amekaa pembeni yake akitokwa na machozi, alimsogelea na kumshika shavuni kwa upendo. “Upo hospitalini mwanangu. Ulipatwa na mshtuko ukiwa kanisani.” Baada ya kusikia kauli ile, Linda alianza kuvuta kumbukumbu, akakumbuka vizuri kuwa siku hiyo alikuwa kanisani akijiandaa kufunga ndoa na Harrison. “Mama, mume wangu Harrison yuko wapi? Leo si ndiyo siku ya harusi yetu?” aliuliza Linda huku akionekana kama asiyekumbuka vizuri kilichotokea. Mama yake alishindwa cha kumjibu, akawa anajifuta machozi kwa uchungu. Hali ile ilimfanya Linda atulie kwa dakika kadhaa, akakumbuka vizuri kilichotokea. “Harrison! Harrison kipenzi changu, kwa nini umenikimbia kanisani? Kwa niniii?” alisema Linda huku akianza kuangua kilio upya kama mtu aliyeletewa taarifa za msiba. Licha ya mama yake kujitahidi kumbembeleza, Linda hakutulia, aliendelea kulia kwa nguvu, mara akachomoa sindano ya dripu aliyokuwa amechomwa mkononi, akasimama wima kama mwendawazimu. “Namtaka Harrison wangu, nataka anioe! Bila hivyo naenda kujiua,” alisema Linda huku akianza kutimua mbio kuelekea upande kulipokuwa na lifti ya kupandia ghorofani. “Simama Linda, bado haujapona mwanangu, utapata matatizo zaidi,” alisema mama yake Linda lakini binti yake huyo hakumsikia. Alilishika gauni lake la harusi kwa mkono mmoja ili apate uhuru wa kukimbia vizuri. Kelele alizokuwa anapiga mama yake, ziliwashtua manesi na madaktari, wote wakaanza kutimua mbio kuelekea kule Linda alikokuwa anakimbilia. Walichelewa kwani Linda alishaingia kwenye lifti na kujifungia, akabonyeza kitufe ukutani, lifti ikaanza kupanda kuelekea juu. Ilimpeleka mpaka kwenye ghorofa ya 33, juu kabisa ya jengo lile la hospitali. Alipoteremka kwenye lifti, alipanda ngazi chache na kutokezea upande wa juu kabisa, kwenye paa la ghorofa lile refu. Baada ya dakika chache, mama yake akiwa ameongozana na manesi na wauguzi, nao walipanda mpaka kule Linda alikokimbilia. “Ishieni hapohapo, mkisogea hata hatua moja mbele najirusha mpaka chini nife,” alisema Linda kwa sauti ambayo haikuwa na masihara hata kidogo. Ilibidi wote wasimame huku wakiwa hawaamini walichokuwa wanakiona mbele ya macho yao. Linda alikuwa amesimama ukingoni kabisa mwa ghorofa lile, mahali ambapo hata upepo wenye nguvu ukipiga, ungeweza kumuangusha mpaka chini. “Noo! Noo Linda, tupo tayari kufanya chochote unachokitaka,” alisema mama yake huku akipiga magoti. “Namtaka Harrison wangu, nataka mkamtafute mahali popote alipo na kumleta hapa, vinginevyo najirusha mpaka chini.” “Harrison atapatikana mwanangu lakini nakuomba usogee huku tulipo, hapo ni hatari sana mwanangu, nakuomba Linda,” alisema mama Linda huku akizidi kulia kama mtoto mdogo. Linda hakutaka kuelewa chochote, alishikilia msimamo wake kuwa Harrison atafutwe mahali popote alipo na kuletwa pale juu ya ghorofa, vinginevyo atajirusha hadi chini. Muda mfupi baadaye, wanausalama na madaktari wengine walifika kule juu ya ghorofa, wakawa wanamsikiliza Linda anachokitaka. “Kwa hiyo tukimleta Harrison utakubali kurudi huku tulipo na kuteremka hadi chini kwa usalama?” “Ndiyo! Nampenda sana Harrison, sipo tayari kuishi bila yeye,” alisema Linda huku akilia kwa uchungu.
HALI ya sintofahamu imetanda kwenye Hospitali ya Oklahoma Medics baada ya Linda, mtoto wa tajiri maarufu nchini Marekani kutishia kujiua kwa kujirusha kutoka juu ya ghorofa refu akishinikiza Harrison, mchumba wake aliyemkimbia kanisani wakati wakitaka kufunga ndoa, atafutwe.
Linda amedhamiria kujiua na haoneshi masihara hata kidogo, jambo linalozidi kuwatia hofu mama yake, manesi, madaktari na watu waliofika eneo la tukio. Anataka kitu kimoja tu, Harrison atafutwe na kuletwa pale alipo ili wafunge naye ndoa, sharti linaloonekana kuwa gumu kwani mwanaume huyo alishaonesha kwamba hamhitaji na ndiyo maana alimkimbia kanisani muda mfupi kabla ya kufunga ndoa.
Upande wa pili, Harrison kwa kushirikiana na rafiki yake Rogers, wanatumia mbinu za hali ya juu na kutengeza ajali ili ionekane kwamba mtunzi huyo wa kitabu cha malkia wa masokwe amefariki kwenye ajali wakati akimkimbia Linda. Akili ya Harrison ipo kwa msichana mrembo anayeishi na masokwe ndani ya msitu mkubwa wa Tongass.
Kwa mara ya kwanza alifanikiwa kumpiga picha msichana huyo mrembo katikati ya msitu wa Tongass akiwa amezungukwa na masokwe, akiwa na haiba zote kama mnyama wa porini. Moyo wake ukatokea kumpenda licha ya hali aliyokuwa nayo na sasa anawakataa wasichana wote wanaotaka kuolewa naye, akiwemo Linda. Ndoto zake ni kumuoa malkia wa masokwe.
“HAPA tukitaka kutumia nguvu tutaharibu kila kitu.” “Sasa tutafanyaje?” “Mimi nafikiri tumtimizie anachokitaka. Inawezekana kabisa Harrison akapatikana na kuletwa hapa,” maafisa wawili wa usalama wa Hospitali ya Oklahoma Medics walikuwa wakijadiliana wakiwa eneo la tukio, juu kabisa ya ghorofa. Bado Linda alikuwa amesimama kwenye ukingo wa ghorofa lile, akiwa sentimeta chache kutoka mwisho wa ghorofa. Wakati wakiendelea kujadiliana, waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, zikiwemo runinga na redio waliwasili juu ya ghorofa lile baada ya kupata taarifa juu ya tukio lililokuwa linataka kutokea. Wakati waandishi hao wakianza kuandaa vifaa vyao zikiwemo kamera na vinasa sauti kwa ajili ya kunasa tukio lile, baba mzazi wa Linda, mzee Ford naye aliwasili huku akitiririkwa na jasho mwili mzima. Mkewe alipomuona alimkimbilia na kuanza kulia kwa sauti. “Linda anataka kujiua, fanya chochote kumuokoa mwanangu,” alisema mama Linda huku akiwa amekumbatiana na mumewe. Ilibidi mzee huyo aliyekuwa anasifika kwa kumiliki utajiri mkubwa ajaribu kuzungumza na mwanaye. “Nakuomba mwanangu, rudisha moyo nyuma. Maisha yanawezekana hata bila Harrison, chondechonde Linda.” “Siwezi baba, nataka Harrison akatafutwe haraka iwezekanavyo, bila hivyo nitajirusha mpaka chini,” alisema Linda huku naye akibubujikwa na machozi. Baba yake alipojaribu kupiga hatua moja kumsogelea, Linda alizidi kusogea ukingoni mwa ghorofa, hali iliyofanya wote waliokuwa eneo lile kupiga kelele kwa woga huku wakiwa wameshika vichwa vyao. “Linda!” “Abee baba.” “Harrison akipatikana hutajiua?” “Nakuahidi baba, nataka japo nimuone tu na anitamkie kwamba ananipenda, bila hivyo maisha yangu hayana maana yoyote.”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Wakati akisema hivyo, tayari waandishi wa habari walikuwa wakimrekodi huku picha nyingi zikipigwa. Lilikuwa ni tukio la aina yake lililozigusa hisia za wengi nchini Marekani. “Harrison! Harrison! Mahali popote ulipo, nakuomba uje haraka kwenye Hospitali ya Oklahoma, mwanangu anataka kujirusha kwenye ghorofa kwa ajili yako, nakuomba sana uyanusuru maisha ya binti yangu, nipo tayari kukupa chochote unachokitaka,” alisema baba Linda mbele ya kamera za waandishi wa habari kutoka vituo mbalimbali vya runinga. Mkewe naye alipewa nafasi ya kuzungumza lakini kutokana na uchungu aliokuwa anauhisi, alishindwa kuongea na kuishia kulia kwa kwikwi. Habari zile zikasambaa kama moto wa kifuu, runinga ya CNN ikawa ya kwanza kuirusha habari ile moja kwa moja kutoka eneo la tukio. Hali ya sintofahamu ikatawala kila sehemu. Baba Linda aliendelea kuzungumza kwenye vyombo vya habari huku akiahidi donge nono la dola za Kimarekani milioni hamsini kwa yeyote atakayefanikiwa kumshawishi Harrison afike eneo lile. Watu katika mitaa mbalimbali walijikusanya kwenye vikundi vidogovidogo wakijadiliana juu ya tukio lile. “Kuna watu wengine wana mapenzi mpaka shetani anayaogopa. Yaani huyu binti yupo tayari kufa kwa sababu ya mwanaume?” “Alimpenda sana lakini bahati yake mbaya. Unajua jamaa amemkimbia kanisani?” “Kamkimbia kanisani kivipi?” “Walikuwa wafunge ndoa leo, si unamuona huyu binti amevaa gauni la harusi? Sijui kumetokea nini jamaa kamuacha kwenye mataa.” “Sasa amefikaje juu ya ghorofa la hospitali?” “Baada ya kukimbiwa kanisani alipoteza fahamu ndiyo akaletwa hapa, alipozinduka ndiyo akakimbilia huku juu ya ghorofa.” “Aisee! Tukio linasisimua sana hili, utafikiri filamu?” “Wasipokuwa makini anaweza kweli kujiua huyu, ameshachanganyikiwa,” watu waliokuwa wanatazama runinga walikuwa wakijadiliana wakati wakiendelea kutazama tukio la Linda kutaka kujirusha kwenye ghorofa. *** Einsten Duke, mwanaume wa makamo aliyekuwa akiyaendesha maisha yake kupitia kazi ya uvuvi kwenye Bahari ya Atlantic, alikuwa akitegesha nyavu kwenye bahari tayari kwa kazi ya uvuvi. Kwa kuwa ilikuwa ni majira ya joto, hakuwa akienda mbali na ufukwe kwani samaki walikuwa wengi sana pembezoni mwa bahari. Wakati akiendelea na kazi ya kutega nyavu jirani na daraja la Miami, alishtuka baada ya kuona kitu kinaelea kwenye maji. “Yule siyo mtu kweli? Hebu nisogee,” alisema Duke huku akigeuza boti ndogo ya uvuvi na kusogea jirani na pale alipoona kile kitu mithili ya mtu kikielea. “Mungu wangu! Ni binadamu! Inaonesha amepata ajali na kuangukia huku,” alisema huku akiuchunguza mwili ule. Haraka alitoa simu yake na kupiga namba 911! Aliwaeleza polisi kila kitu alichokiona ambapo baada ya dakika chache ving’ora vya magari ya polisi vilianza kusikika sambamba na boti za uokoaji. Wakiwa juu ya daraja, polisi walistuka baada ya kuona pikipiki kubwa ikiwa imeharibika vibaya katikati ya barabara. Haraka walisimamisha magari yao na kuteremka, wakaanza kuangalia kilichotokea. “Inaonesha kuna mwendesha pikipiki amegongwa na gari,” alisema askari mmoja akiwaambia wenzake, harakaharaka eneo lote la ajali likazungushiwa utepe maalum wa kuzuia watu wasiohusika kusogea. “Msamaria mwema aliyepiga simu ameelekeza kuwa ameona mwili wa mwanaume ukielea baharini jirani na daraja hili.” Wakati wakiendelea kujadiliana, walisogea kwenye kingo za daraja na kuchungulia chini ambapo waliwaona wenzao wa kikosi cha uokoaji majini wakisaidiana na yule msamaria mwema, Duke kuopoa mwili uliokuwa unaelea baharini. Waandishi wa habari nao tayari walishapata taarifa zile, wakafika eneo la tukio haraka na kuanza kurekodi kila kilichotokea. Kilichowashangaza wengi, mwili wa mwanaume yule ulikutwa ukiwa umevaa suti ya harusi, harakaharaka watu wakaanza kuunganisha matukio. Kilichofanya kazi ya kuutambua mwili ule iwe ngumu ni kuharibika vibaya kwa sura ya marehemu. Hata hivyo, pikipiki iliyokutwa barabarani ilisaidia kupata mwanga wa taarifa za marehemu yule. “Haaa! Ile si ndiyo pikipiki aliyokuwa anaitumia Harrison?” “Mh! Mi mwenyewe nahisi ndiyo aliyoitumia kumkimbia bibi harusi kanisani.” “Unataka kusema Harrison amepata ajali na kufa?” CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ ITAENDELEA
Simulizi : Queen Of Gorillas ( Malkia Wa Masokwe ) Sehemu Ya Nne (4)
LINDA, mtoto kutoka familia ya kitajiri, yupo juu ya ghorofa refu la Hospitali ya Oklahoma Medics na anataka kujirusha hadi chini ili afe baada ya kipenzi cha moyo wake, Harrison kumkana kanisani siku ya ndoa
yao. Linda anatoa sharti moja kuwa mpaka Harrison atakapokubali kumuoa ndiyo atabatilisha uamuzi wake wa kujiua.
Upande wa pili, vyombo mbalimbali vya habari vinaripoti tukio la ajali mbaya iliyotokea kwenye Daraja la Miami. Mtu anayesadikiwa kuwa ni Harrison, anapata ajali mbaya akiwa anaendesha pikipiki na mwili wake unaokotwa ukielea baharini.
Habari hizo zinawashtua watu wote waliokuwa wanamfahamu Harrison, wanakimbilia eneo la tukio ambapo ushahidi wa pikipiki aliyokimbia nayo Harrison pamoja na mavazi ya harusi aliyokuwa ameyavaa, unafanya kila mmoja aamini kuwa Harrison amekufa.
Hakuna anayejua kuwa kila kitu kimetengenezwa na Harrison kwa kushirikiana na rafiki yake Rogers, ambao wanatumia mbinu za hali ya juu kucheza na akili za watu. Akili ya Harrison ipo kwa msichana
mrembo anayeishi na masokwe ndani ya msitu mkubwa wa Tongass. Ndoto zake ni kumuoa msichana huyo.
“LINDA, Linda! Kuna habari tumezipata muda si mrefu kumhusu Harrison.” “Sitaki habari zozote, namtaka Harrison aje hapa.” “Tusikilize kwanza, ni muhimu ukajua kinachoendelea kwani tunaamini ulikuwa unampenda sana Harrison.” “Bado nampenda, nimesema hapa siondoki mpaka aletwe,” alisema Linda na kuwakata kauli maafisa usalama wa hospitali ile ambao walikuwa wanataka kumfikishia habari za ajali aliyoipata Harrison. “Jamani tufanyeje? Inaonekana hataki kuelewa chochote.” “Mi nashauri runinga moja iletwe huku juu haraka iwezekanavyo kabla habari za ajali aliyopata Harrison hazijaisha,” alisema mmoja kati yao, utekelezaji ukafanyika mara moja. Runinga ndogo ikaenda kuchukuliwa kutoka kwenye chumba kimoja cha ghorofa ile na kupandishwa mpaka kule juu kabisa alikokuwepo Linda na watu wengine. Waya mrefu ukatumika kuiunganisha kwenye umeme kisha ikawashwa na kuwekwa Kituo cha CNN. “Tunaomba uangalie mwenyewe kinachotangazwa,” alisema mmoja kati ya wale maafisa huku akimgeuzia Linda runinga. Kwa muda wote huo, wazazi wake walikuwa wameshapata taarifa za kifo cha Harrison na walikuwa njiani kuelekea eneo la tukio kwenda kuthibitisha kama kweli walichokisikia ni sahihi. Baada ya kugeuziwa runinga ile, Linda alishtuka kuliko kawaida kwa alichokuwa anakiona. Ilibidi mwenyewe asogee kutoka kule kwenye ukingo wa ghorofa mpaka jirani na ile runinga, akawa anatazama kilichokuwa kinatangazwa kama asiyeamini macho yake. “Whaaat? Harrison amefanya nini? Noooooo!” alisema Linda kwa sauti kubwa huku akianza kuangua kilio kama mtoto mdogo. Maafisa usalama waliitumia nafasi hiyo kikamilifu, wakamzunguka pale alipokuwa amesimama ili asipate tena upenyo wa kukimbilia kwenye ukingo wa lile ghorofa. “Noooooo! Harrison hajafa, hap…a…a…a…n,” Linda alishindwa kumalizia kauli yake, akadondoka chini na kupoteza fahamu kwa mara nyingine. Wale maafisa usalama na manesi wakambeba juujuu mpaka kwenye ngazi na kuanza kuteremka naye, wakaingia kwenye lifti na kushuka hadi chini ya jengo lile ambapo alianza kupewa huduma ya kwanza haraka. *** “Jamani hivi ni kweli Harrison amekufa? Mbona mi siamini?” “Yaani inasikitisha sana jamani kwani ndiyo kwanza alikuwa ameanza kupata mafanikio, roho inauma sana.” “Au kuna mkono wa mtu? Mbona mi sielewi jinsi haya matukio yanavyotokea?” “Mi mwenyewe nahisi kuna mkono wa mtu, haiwezekani bwana harusi amkimbie bibi harusi kanisani halafu akapate ajali mbaya na kufa, lazima kuna jambo hapa,” watu waliokuwa wamekusanyika wakitazama taarifa ya habari kwenye runinga, walikuwa wakijadiliana, kila mmoja akizungumza la kwake. Baada ya mwili kuopolewa baharini, ulipelekwa mpaka kwenye Hospitali ya Miami ambapo ulifanyiwa vipimo kadhaa kisha kwenda kuhifadhiwa kwenye chumba cha maiti kusubiri ndugu wa marehemu wawasili. Kila aliyeisikia habari ile alipatwa na uchungu usioelezeka kwani ndiyo kwanza nyota ya mafanikio ya Harrison ilikuwa imeanza kung’ara baada ya kuchapisha kitabu cha Malkia wa Masokwe, kilichouza mamilioni ya nakala nchini Marekani na nje ya nchi. Ndugu wa Harrison wakiongozwa na mama mzazi wa kijana huyo, Skyler, babu yake, Dk Lewis na mkewe, waliwasili kwenye Hospitali ya Miami wakiwa hawaamini kilichotokea. Skyler ndiyo alikuwa katika hali mbaya zaidi kwani hakuwa na mtoto mwingine yeyote zaidi ya Harrison na hakutaka kuolewa baada ya kipenzi cha moyo wake, Harvey kufariki dunia. “Nina mkosi gani mimi mama? Furaha pekee ya maisha yangu nayo imetoweka, nitaishi maisha gani mimiiii?” alilia Skyler kwa huzuni wakati wakiwasili kwenye Hospitali ya Miami. “Jikaze mwanangu, yote kazi ya Mungu! Tulimpenda Harrison lakini Mungu kampenda zaidi, ukilia sana utakufuru,” mama Skyler alikuwa akimbembeleza mwanaye. Wakati wakiendelea kuomboleza, wazazi wa Linda nao waliwasili hospitalini pale, mama yake akawa analia kama mwendawazimu. Huzuni kuu ilitanda kila mahali.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Baada ya Linda kurejewa na fahamu, alipelekwa mpaka msibani, akawa anaendelea kuomboleza kwa uchungu kuliko watu wote waliofika msibani. Baada ya taratibu za kuchukua maiti kukamilika hospitalini pale, mwili ulichukuliwa mpaka nyumbani kwa Dk Lewis ambapo ndipo ndugu walipokubaliana msiba uwekwe. Kampuni ya Oklahoma Funerals iliyopewa kazi ya kusimamia msiba ule, ikapeleka gari la kubebea maiti pamoja na mengine ya kuwabeba ndugu na jamaa wa marehemu. Maelfu ya watu walifurika nyumbani kwa Dk Lewis kwenye msiba ule wa kihistoria, idadi ya waliokuwa wanapoteza fahamu kutokana na kumlilia Harrison ikawa inaongezeka kwa kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele. Vyombo mbalimbali vya habari zikiwemo runinga na redio, vikawa vinatangaza moja kwa moja kila kilichokuwa kinaendelea msibani. *** Baada ya kushirikiana na rafiki yake, Rogers kutengeneza ajali feki ya kuonesha kwamba amekufa, Harrison alisafiri kwa siri hadi kwenye Msitu wa Tongass akiwa na lengo moja tu, kumpata malkia wa masokwe. Tofauti na zamani ambapo kila alipokuwa anawasili Tongass alikuwa akienda kuomba kibali cha kuingia kwenye msitu huo mkubwa, safari hii Harrison aliingia bila kutoa taarifa sehemu yoyote. Mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo kwa malkia wa masokwe yalimchanganya kiasi cha kutoiona hatari iliyokuwa mbele yake iwapo ataingia kichwakichwa ndani ya msitu huo. “Samahani sana Linda, najua ulinipenda kwa moyo wako wote lakini ukweli ni kwamba yupo ninayempenda zaidi yako. Najua kumbukumbu za kitendo cha kukukimbia kanisani hazitafutika maishani mwako lakini ilibidi iwe hivyo, samahani kwa yote! Nampenda malkia wa masokwe kuliko wewe,” alijisemea Harisson kimoyomoyo wakati akikatiza kwenye vichaka kuingia ndani ya msitu wa Tongass. Kumbukumbu za tukio la ajali waliyoitengeneza na rafiki yake, Rogers bado zilikuwa zikijirudiarudia ndani ya kichwa chake kama filamu ya kutisha. Alikuwa akijiuliza maswali mengi ambayo hakuyapatia majibu lakini kwa kuwa alishaamua kumtafuta malkia wa masokwe kwa nguvu zote, alipiga moyo konde. Akiwa anaendelea kujipenyeza kwenye vichaka, Harrison alishtuka kupita kiasi baada ya kusikia matawi ya miti yakitingishika kwa nguvu huku sauti za ajabu zikisikika. Akiwa bado ameduwaa, alishtukia kitu kizito kikimuangukia mgongoni na kumuangusha chini. HABARI za ajali mbaya iliyotokea kwenye Daraja la Miami ikimhusisha mwendesha pikipiki aliyegongwa na gari kisha kurushwa hadi baharini, zinasambaa kwa kasi kubwa na kuwafikia watu wengi. Vikosi vya uokoaji wakiwemo askari wa usalama barabarani wanawasili eneo la tukio na baada ya muda, mwili wa mtu aliyepoteza maisha kwenye ajali ile unapatikana.
Uchunguzi wa awali unawafanya watu wote waamini kuwa aliyekufa kwenye ajali ile ni Harrison kwani mwili wake unakutwa na suti ya harusi huku pikipiki aliyokuwa anaitumia muda mfupi kabla ya ajali ikikutwa eneo la tukio ikiwa haitamaniki. Habari zinaenea kuwa aliyefariki ni Harrison, jambo linalozidi kuzua simanzi kubwa.
Upande wa pili, Linda, mtoto kutoka familia ya kitajiri, aliyekuwa juu ya ghorofa refu la Hospitali ya Oklahoma Medics akitishia kujirusha mpaka chini ikiwa Harrison hatatafutwa na kuletwa mbele yake, anafikishiwa habari juu ya kifo cha mtu anayedhaniwa kuwa ni Harrison.
Anapatwa na mshtuko mkubwa na kujikuta akiahirisha alichokuwa anataka kukifanya, anateremshwa kutoka juu ya ghorofa na maafisa usalama waliokuwa wanamlinda asijirushe na kupelekwa hadi nyumbani kwa Dk Lewis, kulipokuwa na msiba wa Harrison. Simanzi kubwa inatawala nchi nzima kutokana na umaarufu aliokuwa nao Harrison baada ya kuchapisha kitabu kilichokuwa kinaitwa Malkia wa Masokwe.
“MUNGU wangu, sokwe!” alisema Harrison huku akianza kupambana na sokwe mkubwa aliyekuwa amemuangusha chini. Kila alipojaribu kutafuta upenyo wa kukimbia, Harrison alizidi kubanwa pale chini na yule sokwe aliyeonekana kuwa na hasira, ikabidi
apambane kiume, akaokota gongo kubwa lililokuwa pembeni, akampiga yule sokwe mgongoni na kufanikiwa kupata upenyo wa kutoroka.
“Kumbe nimeumia?” alisema Harrison huku akizidi kutimua mbio kuelekea ndani kabisa ya msitu. Mkono wake wa kulia ulikuwa ukivuja damu baada ya sokwe yule kumng’ata kwa hasira. Alizidi kutimua mbio huku akijifunga jeraha lake kwa kutumia kitambaa cha mkononi alichokitoa mfukoni mwake.
Kwa kuwa alikuwa akifahamu uelekeo ambao masokwe waliokuwa wanamlinda malkia wao walizoea kushinda, Harrison alizidi kuchanja mbuga kuelekea upande ule. Safari haikuwa nyepesi kwani aliingilia upande tofauti na ule aliozoea, jambo lililomfanya atumie muda mrefu kujipenyeza kwenye miti iliyokuwa imefungamana.
Baada ya kutembea kwa miguu kwa takribani saa nne, Harrison alitokezea mahali ambapo alizoea kuweka kambi alipokuwa akifanya utafiti ndani ya Msitu wa Tongass.
“Sijabeba hema, chakula wala maji, sijui nitaishi vipi huku msituni,” alijisemea Harrison wakati akitafuta sehemu ya kupumzikia. Akakaa chini ya mti mkubwa na kujiegamiza, akawa anahisi uchovu wa hali ya juu. Alipumzika kwa dakika kadhaa kabla ya kuamka na kuanza kutafakari nini cha kufanya.
“Nisamehe Linda, najua bado unaomboleza kifo changu! Mungu akipenda ipo siku utaujua ukweli kuwa sikufa. Nisamehe kwa yote, nimejaribu kuulazimisha moyo wangu ukupende lakini imeshindikana, nampenda zaidi malkia wa masokwe,” alisema Harrison huku akilengwalengwa na machozi.
Akawa anazunguka huku na kule kujaribu bahati yake kama atamuona malkia wa masokwe. Alizunguka kwa muda mrefu lakini eneo lote lilikuwa kimya kabisa, giza likaanza kuingia taratibu. Akatafuta sehemu nzuri na kuanza kuisafisha kwa ajili ya kulala.
Akakusanya kuni kavu na kuwasha moto kwa kutumia kiberiti alichokinunua wakati akikimbilia msituni.
“Naamini nikiwasha moto hakuna mnyama yeyote mkali anayeweza kunidhuru, hata simba hawawezi kusogea,” alijisemea Harrison huku akihangaika kuwasha moto. Baada ya muda akafanikiwa, akatafuta jiwe kubwa na kulisogeza jirani na moto, akalitumia kama kiti chake. ***
“Harrison mpenzi wangu! Umeniachia kovu ambalo halitafutika kirahisi kwenye moyo wangu, kwa nini usingenioa kwanza ndiyo ufe? Ooh Mungu, kwa nini mimi?”
“Usilie sana Linda kwani utakuwa unamkufuru Mungu. Yeye ndiyo mwamuzi wa yote, mshukuru kwa kila jambo,” mama mzazi wa Linda alikuwa akimbembeleza mwanaye ambaye alikuwa akilia kwa huzuni kali. Maneno aliyokuwa anayatamka Linda yalizidisha huzuni msibani, akina mama wakawa wanaomboleza kwa huzuni huku wengine wakiwafariji wafiwa.
Hali ilikuwa mbaya zaidi kwa mama yake Harrison, Skyler ambaye naye alikuwa akizimia mara kwa mara na kuzinduka. Hakutaka kuamini kama mwanaye wa pekee, kipenzi cha moyo wake alikuwa amefariki dunia. “Atazikwa lini?” “Kesho mchana.” “Sasa mwili wake si utaharibika?” “Hauwezi kuharibika, umehifadhiwa kwenye mochwari jirani na hapa nyumbani.” “Ataagwa saa ngapi?”
“Hayo tutajua hiyo kesho lakini kuna uwezekano mkubwa asiagwe kwani sura yake imeharibika vibaya, anatisha.”
“Daah! Inasikitisha sana, ameondoka akiwa bado kijana mdogo sana,” mzee mmoja wa makamo aliyekuwa akiishi jirani na Dk Lewis, alikuwa akizungumza na mzee mwenzake juu ya taratibu za mazishi ya Harrison. Babu wa marehemu, Dk Lewis akawa anamuelewesha juu ya mipango ya mazishi.
Habari zilizidi kuenea nchini Marekani kutokana na umaarufu ambao Harrison alikuwa ameanza kuupata. Watu wengi ambao walimfahamu baada ya kusoma kitabu chake cha Malkia wa Masokwe, wakawa wanamiminika kwa wingi kutoka pande mbalimbali za Marekani kushiriki katika msiba ule. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Vyombo mbalimbali vya habari navyo havikuwa nyuma, vikawa vinaripoti hatua kwa hatua juu ya kila kitu kilichokuwa kinaendelea msibani pale. Kama ilivyokuwa imepangwa na wanandugu, kesho yake ilipowadia, taratibu za mazishi zilianza kufanyika.
Watu wote waliokuwepo msibani wakatengenezewa fulana maalum zilizokuwa na picha na jina la Harrison, akina mama wakatengenezewa kanga maalum zilizokuwa na maandishi yaliyosomeka; Buriani Harrison.
Ilipofika saa sita za mchana, maiti ilienda kuchukuliwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti kilichokuwa jirani na nyumbani kwa Dk Lewis kwa gari maalum, mali ya Kampuni ya Oklahoma Funerals iliyopewa kazi ya kusimamia msiba ule.
Wakati maiti ikiteremshwa kwa ajili ya kusomewa misa maalum, watu wengi walikuwa wakiendelea kupoteza fahamu kutokana na huzuni waliyokuwa nayo. Kikosi cha Msalaba Mwekundu kilichokuwepo eneo hilo, kilionekana kuanza kuzidiwa uwezo, wafanyakazi wake wakawa wanajituma kwa uwezo wao wote kuwapa huduma ya kwanza watu waliokuwa wanaanguka na kupoteza fahamu.
Mchungaji Calagher Powel ndiye aliyeongoza misa maalum ya kuuombea mwili wa marehemu. Baada ya misa kuisha, mwili wa marehemu na waombolezaji walisafirishwa kwa magari maalum ya Kampuni ya Oklahoma Funerals mpaka kwenye Makaburi ya Miami Cemetery.
Mwili ambao kila mmoja aliamini ni wa Harrison, uliwekwa pembeni ya kaburi na taratibu za kawaida za mazishi zikafanyika kisha ukazikwa kwa heshima zote. Baada ya mazishi, waombolezaji walirudishwa nyumbani kwa Dk Lewis, wakaendelea na maombolezo huku wengine wakianza kuondoka mmoja mmoja.
“Naapa sitaolewa na mwanaume mwingine yeyote kwa ajili ya kumuenzi marehemu Harrison,” alisema Linda akiwa amejilaza miguuni mwa mama yake. “Mh! Kwa nini umesema hivyo mwanangu?”
“ Naamini Harrison alikuwa ananipenda sana lakini alichanganyikiwa dakika za mwisho kabla ya kufunga ndoa. Nimemsamehe kwa yote kwani naamini ni mauti yalikuwa yanamuita ndiyo maana akanikimbiakanisani. Sitaolewa maisha yangu yote.”
“Usiseme hivyo mwanangu, wewe bado ni msichana mdogo, lazima itafika wakati utahitaji kuwa na mume na watoto, usijiapize.”
“Nimeshasema mama, hatatokea mtu mwingine yeyote akaziba nafasi ya Harrison kwenye moyo wangu,” Linda alizidi kushikilia msimamo wake. Siku zikawa zinazidi kusonga mbele, waombolezaji wakawa wanazidi kupungua nyumbani kwa Dk Lewis kwa kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele.
PENZI la dhati alilokuwa nalo kijana Harrison kwa malkia wa masokwe linamfanya amkimbie mchumba wake, Linda kanisani kwa kutumia pikipiki kubwa na kwenda kwa rafiki yake, Rogers ambapo wanapanga mbinu kabambe ya kuandaa ajali feki.
Rogers anamsaidia Harrison kutafuta maiti ambayo wanaivalisha nguo za kijana huyo kisha wanaenda mpaka kwenye daraja kubwa la Miami ambapo wanatengeneza mazingira yanayowafanya watu waamini kuwa Harrison amepata ajali mbaya na kufa kisha kutumbukia baharini.
Hakuna anayeshtukia mchezo huo na habari zinasambaa kwa kasi kubwa zikieleza kuwa Harrison amekufa kwenye ajali hiyo, jambo linaloamsha huzuni kubwa kwa familia yake, ya mchumba wake Linda na kwa mashabiki wake nchini Marekani.
Wakati taratibu za mazishi zikifanywa, upande wa pili Harrison anakimbilia mpaka kwenye Msitu wa Tongass kwa ajili ya kazi moja tu, kuhakikisha anampata malkia wa masokwe.
HATIMAYE, baada ya siku saba tangu kutokea kwa kile watu walichoamini kuwa ni kifo cha Harrison, watu wote waliondoka nyumbani kwa Dk Lewis kulipokuwa na msiba isipokuwa ndugu zake wa karibu, Linda na wazazi wake ambao waliendelea kukaa msibani hapo mpaka baada ya wiki mbili.
Watu wote walipoondoka na kwenda kuendelea na maisha yao, Linda aling’ang’ania kubaki msibani kwa maelezo kuwa ataondoka baada ya siku arobaini.
“Mbona kila kukicha unazidi kukonda Linda, nini tatizo?” “Hamna tatizo, naona ni mabadiliko ya mwili tu.” “Mh! Kweli?” “Ndiyo mama.” “Mimi ni mtu mzima, naelewa jinsi mapenzi yanavyotesa. Najua ulimpenda sana mwanangu Harrison lakini lazima tukubaliane na ukweli kuwa Mungu kampenda zaidi.” “Ni kweli mama, yaani mpaka leo bado siamini kama sitamuona tena Harrison kwenye maisha yangu, ameniachia pigo kubwa sana na hiyo ndiyo sababu inayofanya nizidi kudhoofika.” “Pole sana, inabidi ujikaze kisabuni, taratibu utaanza kusahau na utampata ambaye ataziba pengo aliloliacha.” “Mh! Kiukweli sitaweza kumsahau na wala hatapatikana mtu wa kuziba pengo lake, nilimpenda sana Harrison,” Linda alikuwa akizungumza na mama mzazi wa Harrison, Skyler. Mazungumzo yao yaliendelea kwa muda mrefu, wakazungumza mambo mengi mpaka muda wa kulala ulipofika.
Siku zilizidi kusonga mbele na hatimaye arobaini ikawadia. Misa ya kumuombea marehemu ikafanyika ambapo mchungaji Calagher Powel aliwaongoza mamia ya watu kusali juu ya kaburi la marehemu. Baada ya misa ya kuhitimisha msiba kuisha, kaburi lilisafishwa
na kujengewa upya kisha watu wote wakaelekea nyumbani kwa Dk Lewis. Wakiwa nyumbani hapo, walikula chakula maalum kilichoandaliwa na familia kama shukrani kwa ushiriki wao kwenye msiba wa Harrison. Baada ya hapo watu wote wakatawanyika kurejea makwao, akiwemo Linda. ***
Baada ya kukaa pembeni ya moto aliouwasha ndani ya msitu wa Tongass kwa muda mrefu, Harrison alienda kujilaza kwenye eneo maalum alilolitengeneza, usingizi mzito ukampitia bila kujali mbu na wadudu wengine waliokuwa wakimfaidi. Alipokuja kushtuka, tayari ilikuwa ni alfajiri ya siku ya pili, akaamka na kuanza kujinyoosha.
“Lazima nimpate malkia wa masokwe, sitarudi mjini mpaka nihakikishe kimeeleweka, nampenda sana na nipo tayari kumuoa ili aje kuwa mke wangu,” alisema Harrison huku akiendelea kujinyoosha mwili wake ambao karibu kila kiungo kilikuwa kikiuma kutokana na uchovu.
Jua lilianza kuchomoza upande wa Mashariki wa msitu ule mnene wa Tongass na kulikimbiza giza totoro la usiku, ndege nao wakawa wanaimba nyimbo zao nzuri huku wakiruka kutoka tawi moja la mti kwenda jingine.
Jua lilipoanza kuchomoza, Harrison alianza tena kazi yake ya kulitafuta kundi kubwa la masokwe lililokuwa likitembea na malkia wao. Alifuata njia alizokuwa anazitumia akiwa ndani ya msitu ule, akaupata uelekeo ambao kundi kubwa la masokwe hupendelea kupita kila asubuhi. Akatafuta sehemu nzuri na kujibanza, akiwa makini kusikiliza huku akiangaza macho huku na kule.
Baada ya muda, alianza kusikia kelele za matawi ya miti kuvunjika na milio ya masokwe, akakaa mkao wa tahadhari kwani alikuwa akizijua fujo za masokwe wanapogundua kuwa kuna mtu anawafuatilia.
“Leo nitajitahidi kupambana mpaka nimsogelee jirani malkia wa masokwe, sitajali kama nitaumia,” alijisemea Harrison huku akiwa amejibanza kwenye shina la mti mkubwa. Dakika chache baadaye, tayari lile kundi la masokwe lilikuwa limewasili eneo lile, akawa anajaribu kuangalia katikati yao akiwa na matumaini ya kumuona malkia wa masokwe lakini kazi haikuwa nyepesi.
“Mungu wangu, nitasalimika kweli?” alisema Harrison baada ya kushtukia jiwe kubwa likivurumishwa na kutua mita chache kutoka pale alipokuwa amejificha. Kabla hajakaa sawa, alishtukia mvua ya mawe makubwa yaliyokuwa yanarushwa na masokwe wale ikimuandama, ikabidi atoke alipokuwa amejificha na kuanza kutimua mbio kuokoa maisha yake.
Kundi kubwa la masokwe lilianza kumkimbiza, akawa anajaribu kukwepa mawe na fimbo zilizokuwa zinarushwa, ikafika mahali akashindwa kuendelea kukimbia kwani masokwe walikuwa wamemzunguka pande zote, ikabidi asimame akiwa hajui nini hatima yake.
Katika hali ambayo hakuitegemea, alishangaa kuona yule malkia wa masokwe ambaye siku zote alikuwa akimuona kwa mbali, akijitokeza mbele yake huku akitoa ishara kwa wale masokwe kuacha kumshambulia Harrison. Cha ajabu, masokwe wote walitii, wakatulia na kuanza kumkodolea macho Harrison aliyekuwa akitetemeka kupita kawaida.
Malkia wa masokwe ambaye kwa mwonekano alikuwa na nywele ndefu zilizoshuka mpaka kiunoni, kucha ndefu kama mnyama na meno yaliyokuwa yamebadilika rangi na kuwa meusi kutokana na kula matunda ya porini na mizizi, alisogea mita chache kutoka pale Harrison alipokuwa amesimama.
Akawa anamtazama Harrison huku akijifananisha naye, akagundua kuwa alikuwa na tofauti kubwa kati yake na wale masokwe lakini alikuwa akifanana sana na Harrison. Aliendelea kujishangaa huku akimuangalia Harrison, ghafla alianza kukimbia na kupanda juu ya matawi ya miti, wale masokwe wote nao wakamfuata na kuanza kukimbia naye, baada ya muda mfupi, walishatoweka kabisa eneo lile, Harrison akabaki ameduwaa akiwa haelewi kinachoendelea.
“Mbona ameniangalia na kujifananisha kisha akatimua mbio?” alijiuliza Harrison huku akiugulia maumivu makali aliyoyapata kutokana na kushambuliwa kwa mawe na fimbo na masokwe wale. Sura ya malkia wa masokwe ilikuwa ikijirudiarudia kichwani mwake.
Japokuwa alikuwa na haiba kama mnyama, bado uzuri na shani za asili alizokuwa nazo, hazikujificha, Harrison akajikuta akizidi kumpenda kiasi cha kujiapiza kufanya lolote mpaka ampate.
Kutokana na maumivu aliyokuwa akiyahisi, ilibidi arudi mpaka eneo alilolala usiku uliopita, akajilaza chini na kupumzika huku akitafakari atakula nini kwa siku hiyo. Baada ya muda, akili ilimjia kuwa ni lazima akatafute matunda ya porini na maji. Akainuka baada ya kupumzika na kuanza kujikongoja kuelekea ndani kabisa ya Msitu wa Tongass.
Baada ya muda, alifanikiwa kukusanya matunda mengi ambayo mengine hata hakuwa akiyajua. Kilichomuongoza kujua yapi yana sumu na yapi hayana, ilikuwa ni kuliwa na wadudu na ndege. Yale aliyokuta yameliwa, aliyachuma na yale yaliyokuwa hayajaguswa, aliyaacha kama yalivyo. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Baada ya kurudi pale alipoweka makazi yake, alikaa na kuanza kuyala matunda yale. Akiwa katika hali ile, alishtuka baada ya kusikia vishindo vikisogea jirani na pale alipokuwa kutokea vichakani. Akaacha kila alichokuwa anakifanya na kutega masikio kwa makini huku akizungusha kichwa chake huku na kule kutazama ni kitu gani kilichokuwa kinamsogelea.
HARRISON anaaminika kuwa amekufa kwenye ajali mbaya iliyotokea kwenye Daraja la Miami akiwa anaendesha pikipiki na kugongwa na gari kisha kurushwa hadi baharini. Habari zinasambaa kwa kasi kubwa na kuwafikia watu wengi. Kila mmoja anaamini kuwa ni kweli amekufa.
Vikosi vya uokoaji wakiwemo askari wa usalama barabarani wanawasili eneo la tukio na baada ya muda, mwili wake unapatikana. Uchunguzi wa awali unawafanya watu wote waamini kuwa aliyekufa kwenye ajali ile ni Harrison kwani mwili wake unakutwa na suti ya harusi
huku pikipiki aliyokuwa anaitumia muda mfupi kabla ya ajali ikikutwa eneo la tukio ikiwa haitamaniki. Simanzi kubwa inatanda. Taratibu za mazishi zinafanyika na anaenda kuzikwa kwa heshima zote kwenye makaburi ya Miami. Msiba unafanyika nyumbani kwa Dk. Lewis,
babu yake Harrison. Baada ya matanga kuisha, watu wote wanatawanyika lakini Linda anakataa kuondoka, anakaa msibani mpaka baada ya siku arobaini.
Upande wa pili, Harrison ambaye watu wote wanaamini amekufa, yupo kwenye msitu wa Tongass akiendelea na kazi yake ya kumtafuta malkia wa masokwe. Penzi la dhati alilokuwa nalo juu yake, linamfanya awe tayari kwa lolote ilimradi ampate.
BAADA ya kurudi pale alipoweka makazi yake, alikaa na kuanza kuyala matunda yale. Akiwa katika hali ile, alishtuka baada ya kusikia vishindo vikisogea jirani na pale alipokuwa. Akaacha kila alichokuwa anakifanya na kutega masikio kwa makini huku
akizungusha kichwa chake huku na kule kutazama ni kitu gani kilichokuwa kinamsogelea. “Kijana unafanya nini huku porini peke yako?”
“Shikamoo mzee,” alisema Harrison akionesha kushtushwa sana kumuona mtu ndani ya msitu wa Tongass. Alikuwa ni mwanaume mzee, akiwa na nywele ndefu zenye mvi kichwa kizima. Mkononi alikuwa ameshika silaha za kijadi kuonesha kuwa alikuwa ni mwindaji.
“Marahaba, nakuuliza unafanya nini peke yako huku? Hujui kama kuna wanyama wakali wanaoweza kukudhuru? Au wewe ni jangili?” yule mtu alizidi kumhoji Harrison, naye akionesha kushtushwa na kitendo cha kumkuta ndani ya msitu ule akiwa peke yake.
Harrison alimsogelea na kuanza kuzungumza naye kwa upole, akajitambulisha vizuri na kueleza kilichompeleka kule porini. “Kuna msichana nimetokea kumpenda lakini anaishi na masokwe.” “Anaishi na masokwe? Na yeye ni sokwe?” “Hapana, ni binadamu lakini ana tabia kama masokwe.” “Alifikaje huku porini?” “Hata sijui alifikaje lakini ninachojua anaishi huku msituni.” “Sasa ulishawahi kuzungumza naye?” “Hapana, wala sijui kama anafahamu kuzungumza kama sisi.” “Sasa utamfikishiaje ujumbe?” “Nitafanya chochote ilimradi nimpate.” “Utakaa siku ngapi huku?” “Mpaka nitakapohakikisha nimempata, hata kama ni mwaka mzima.” “Unafurahisha sana kijana, yaani huko mjini hakuna wanawake wazuri mpaka uje kuhangaika na viumbe wa ajabu huku porini?” “Mzee, we niache tu! Hujui ni kwa kiasi gani nampenda na kumhitaji malkia wa masokwe, nitafanya chochote ili mradi nimpate.” “Lakini mbona mimi kila siku nawinda kwenye huu msitu sijawahi kumuona huyo malkia wa masokwe?” “Huwezi kumuona kirahisi, analindwa mno na kundi kubwa la masokwe, mi mwenyewe nilimuona kama bahati tu.” “Kwa hiyo utakuwa unaishi wapi?” “Hata sielewi, hivi unavyoniona sina chochote! Sijui nitalala wapi wala nitakula nini, shida yangu ni malkia wa masokwe tu,” alisema
Harrison kwa kujiamini, yule mzee akamtazama na kuanza kumuonea huruma. “Basi mimi nitakusaidia kujenga japo kibanda cha miti na nyasi kikusitiri, ni hatari kukaa huku porini bila kujihadhari, watu wengi wamekufa kwa kuliwa na wanyama wakali,” alisema yule mzee huku akishusha zana zake za kuwindia chini na kuanza kutafuta sehemu ya kujenga kibanda.
Kwa kushirikiana na Harrison, walianza kufyeka majani na kukata miti, wakasafisha eneo dogo kisha wakaanza kuchimba mashimo. Baada ya muda, walikuwa tayari wamesimamisha miti mikubwa minne, kazi ikaendelea kwa nguvu. Baada ya saa nyingi, kibanda kidogo cha nyasi na miti kilikuwa tayari kimekamilika.
“Utakuwa unaendelea kukiboresha taratibu kwa kadiri utakavyokuwa unaishi, nitakuwa nakuja kukutembelea mara kwa mara. “ “Ahsante sana mzee! Sina cha kukulipa, Mungu atanilipia,” alisema Harrison kwa unyenyekevu. “Wala usijali, najua jinsi unavyojisikia na naahidi kuwa msaada kwako mpaka utakapotimiza ndoto zako,” alisema yule mzee huku akichukua zana zake tayari kwa kuondoka. Akamwambia Harrison inabidi naye ajifunze kuwinda kwa ajili ya kupata chakula kwa siku zote ambazo atakaa kule porini.
Wakati anaondoka, alimwachia mkuki mmoja na sime. Akamwambia kuwa hizo ndiyo zitakuwa silaha zake akitaka kuwinda au kujilinda na wanyama wakali. Harrison alishukuru sana, akamsindikiza kidogo yule mzee na kurudi kwenye kibanda chake. Alishusha pumzi ndefu na kuanza kukitazama kile kibanda.
Kutokana na uchovu aliokuwa nao, aliingia ndani na kujilaza kwa muda, akapumzika mpaka alipohisi uchovu umeisha. Akatoka nje na kuanza kuangaza macho huku na kule, wazo likamjia la kwenda kutafuta maji kwani tangu afike kwenye msitu huo, hakunywa hata kidogo.
Alitoka na kuanza kuzunguka huku na kule, baada ya muda akafanikiwa kufika mahali palipokuwa na chemchemi ya maji. Akainama na kuanza kuyanywa kwa fujo kwani alikuwa na kiu kikali. Alipomaliza alirudi kwenye kibanda chake, akalala mpaka kesho yake.
Alfajiri na mapema, Harrison alishtuliwa kutoka usingizini na milio ya ndege waliokuwa wanaruka kutoka tawi moja la mti kwenda jingine, wakifurahia mapambazuko. Aliamka harakaharaka na kutoka hadi nje ya kibanda chake.
Akawa anajinyoosha huku akitafakari wapi pa kuanzia kazi ya kumtafuta malkia wa masokwe. Alichukua mkuki aliopewa na yule mzee jana yake na kuanza kuzunguka huku na kule. Baada ya muda, alianza kusikia matawi ya miti yakivunjikavunjika na kusababisha kelele za ajabu.
Kwa kuwa tayari alishaanza kuzoea, alitambua kuwa ni lile kundi la masokwe linapita. Akajibanza kwenye shina la mti mkubwa na kuanza kutazama kule kundi lile lilipokuwa linatokea.
Baada ya sekunde chache, lile kundi lilifika pale alipokuwa amejibanza. Harrison kwa mara nyingine akafanikiwa kumuona malkia wa masokwe, aliyekuwa anaruka kwenye matawi kama wale masokwe wengine.
Harrison alisubiri lile kundi lipite, akaanza kulifuatilia nyumanyuma. Hakutaka kuwashtua wale masokwe wengine, akawa analifuata kwa mbali akitaka kujua huwa linaelekea wapi kila siku.
Aliendelea kulifuatilia kwa muda mrefu, akawa anapita kwenye majani marefu, vichaka vilivyofungamana na wakati mwingine kupenyeza hadi kwenye miti ya miba. Kazi haikuwa nyepesi lakini kwa kuwa alikuwa na nia ya dhati kufahamu mahali kundi lile lilipokuwa linaelekea, alijikaza.
Baada ya kutembea kwa saa nyingi, wingu zito lilianza kutanda angani, radi zikawa zinapiga kwa nguvu huku ngurumo kali zikisikika. Manyunyu yalianza kudondoka, yakafuatiwa na mvua kubwa iliyokuwa inapiga na upepo mkali. Harrison alianza kulowana, akawa anatetemeka mwili mzima kwa baridi lakini hakukata tamaa, aliendelea kulifuatilia lile kundi ambalo nalo lilionekana kuchanganywa na mvua ile.
BAADA ya watu wote kuamini kuwa Harrison alikuwa amekufa kwenye ajali mbaya ya kugongwa na gari wakati akiendesha pikipiki na kutumbukia baharini kwenye Daraja la Miami, kijana huyo anakimbilia kwenye msitu mkubwa wa Tongass.
Penzi la dhati alilokuwa nalo kwa msichana wa ajabu aliyekuwa anaishi porini na kulindwa na kundi kubwa la masokwe, linasababisha amkatae mchumba wake Linda kanisani muda mfupi kabla ya ndoa yao kufungwa. Ndoa hiyo inayeyuka kama theluji iyeyukavyo juani na Linda anapoteza fahamu kanisani. Anapozinduka
anatishia kujiua lakini baada ya kupata taarifa za kifo cha Harrison, anabadili mawazo yake. Baadaye kila mmoja anakubaliana na ukweli kuwa tayari Harrison ameiaga dunia, msiba unapelekwa nyumbani kwa bibi na babu yake, Dk Lewis na mkewe Suzan ambapo taratibu za kawaida zinaendelea na baadaye mwili unaenda kuzikwa kwenye makaburi ya Miami.
Upande wa pili, Harrison ambaye watu wote wanaamini amekufa, yupo kwenye msitu wa Tongass akiendelea na kazi yake ya kumtafuta malkia wa masokwe. Anajiapiza kuwa hatarudi mjini mpaka atakapofanikisha kumpata malkia wa masokwe.
MVUA kubwa iliendelea kunyesha ikiambatana na upepo na radi kali, Harrison akawa anaendelea kulifuatilia kundi lile la masokwe mpaka aone mwisho wake. Kutokana na mvua ile, mifereji iliyokuwa ndani ya msitu wa Tongass ilifurika maji yaliyokuwa yanakwenda kwa kasi, hali iliyomfanya Harrison apate ugumu kuendelea na kazi yake.
“Nahisi mwili wote kuishiwa nguvu, itakuwa ni homa nini!” alijisemea Harrison huku akitetemeka mwili mzima. Ilibidi atafute sehemu ya kujificha ili asilowane kwani hali yake ilianza kubadilika na kuwa mbaya. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Aliingia kwenye shimo kubwa lililokuwa chini ya mti mkubwa, akajikunyata na kujiinamia chini, mvua kubwa ikaendelea kunyesha kwa saa nyingi huku wingu zito likisababisha giza kutanda kila upande.
Baada ya kunyesha kwa saa nyingi mfululizo, hatimaye mvua ilianza kupungua, lile wingu zito likasambaa angani na kulifukuzia mbali giza lililokuwa limeanza kutanda. Harrison alitoka mahali alipokuwa amejificha na kusimama juu ya kisiki kikubwa cha mti, akawa anatazama huku na kule akiamini ataliona tena lile kundi la masokwe.
Kilichozidi kummaliza nguvu ni kwamba mvua ile ilisababisha maji mengi kutuama na kuweka madimbwi makubwa kwenye msitu huo. Mifereji mikubwa nayo ilikuwa ikiendelea kutiririsha maji mengi kuelekea sehemu za mabondeni.
“Mungu wangu, nitarudije kwenye kibanda changu?” alijisemea Harrison huku akiendelea kuangaza macho huku na kule. Licha ya hali ile, alijitahidi kujikaza na kuanza safari ya kurejea kule kwenye makazi yake ya muda.
Alijipenyeza kwenye vichaka vilivyokuwa vimelowa kwa mvua, akawa anaruka madimbwi makubwa na mifereji kuelekea kwenye makazi yake. Giza nalo likawa limeanza kutanda upya kwani tayari muda ulikuwa umekwenda sana.
Baada ya kuhangaika kwa muda mrefu kutafuta njia ya kurudia kwenye kibanda chake, hatimaye Harrison alifanikiwa kufika. Kibanda chote kilikuwa kimejaa maji, hali iliyomfanya ashindwe hata kuingia ndani, akatafuta sehemu iliyokuwa na mwinuko kidogo na kukaa, akawa anasubiri maji yapungue ili aingie kwenye kibanda chake.
Baridi nayo ilizidi kumtesa, akawa anaendelea kutetemeka huku viungo mbalimbali vya mwili wake navyo vikianza kumuuma. Muda ulizidi kwenda lakini maji hayakupungua, ikabidi apande juu ya mti na kutafuta sehemu ambayo angeitumia kama kitanda mpaka asubuhi.
Usiku hali yake ilizidi kuwa mbaya, akawa anatetemeka mwili mzima huku joto la mwili likianza kupanda kwa kasi. Kutokana na hali ile, hakupata hata lepe la usingizi, mpaka kunapambazuka hali yake ilikuwa ikizidi kuwa mbaya.
Kwa bahati nzuri, kulipopambazuka jua lilianza kuchomoza kwa mbali, Harrison akajikaza na kuteremka mtini, akatafuta sehemu ambapo kijua kilikuwa kinapenya na kumfikia, akakaa. Jua lilizidi kuchomoza, akawa anazidi kujisogeza ili limpate vizuri zaidi.
Kwa kadiri muda ulivyokuwa unazidi kusonga mbele, hali ya Harrison kiafya ilizidi kuwa mbaya, homa kali ikawa imechachamaa na kumfanya muda wote ajikunyate huku akitetemeka sana.
Kutokana na hali ile, Harrison alishindwa hata kuinuka na kuendelea na kazi yake ya kumtafuta malkia wa masokwe. Hata aliposikia kelele za matawi ya miti kuvunjika na milio ya masokwe jirani na pale alipokuwa, alishindwa kusimama zaidi ya kugeuza shingo na kuangalia kwa mbali.
Jioni ilipofika, alijikongoja mpaka ndani ya kibanda chake ambacho sasa hakikuwa na maji, akapanga vitu vyake vizuri na kujilaza juu ya kitanda cha miti na nyasi. Kama ilivyokuwa kwa siku iliyopita, hakupata usingizi hata kidogo, usiku kucha akawa anatetemeka kutokana na maradhi yaliyokuwa yanamsumbua.
Siku ya kwanza ilipita, hali yake ya kiafya ikazidi kuwa mbaya. Kutokana na kukosa dawa, chakula na maji safi ya kunywa, siku ya pili kulipopambazuka Harrison alizidiwa. Akaanza kutapika mfululizo na kuhara, hali iliyoufanya mwili wake kuishiwa na nguvu kabisa.
“Ooh Mungu wangu, niokoe mimi mwanao kutoka kwenye hili janga, nitakufa peke yangu kwa kukosa msaada huku porini, nipe nguvu ooh Yehova Shalom,” Harrison alinong’ona.
Hata hivyo haikusaidia chochote kwani aliendelea kutapika na kuhara mlemle ndani ya kibanda chake mpaka akawa hoi bin taaban, kizunguzungu nacho kikazidi kumbana. Ikafika muda akawa hawezi hata kujitingisha pale juu ya kitanda cha miti alipokuwa amejilaza.
Giza nene likatanda kwenye macho yake na kumfanya apoteze fahamu, akawa haelewi chochote kilichokuwa kinaendelea. ***
“Mamaa! Mamaa!” “Nini tena mwanangu? Mbona unatushtua usiku wote huu?” “Mama nimeota ndoto mbaya sana.” “Ndoto? Kuhusu nini?” “Kuhusu mwanangu Harrison.” “Aaah! Hayo ni maruweruwe ya kawaida, lazima uchungu wa mwanao uendelee kukusumbua.” “Hapana mama, nimemuona kabisa yupo mahali anateseka sana.” “Labda bado hajapata sehemu ya kupumzika huko peponi, njoo tufanye maombi maalum Mungu aipokee roho yake,” Suzan,
alikuwa akizungumza na mwanaye Skyler, mama mzazi wa Harrison usiku wa manane. Licha ya mwanamke huyo ambaye sasa umri wake ulikuwa umekwenda sana, kujitahidi kumbembeleza mwanaye Skyler na
kumfanya aamini kile alichokiota kilikuwa ni ndoto za kawaida tu, bado hakutaka kukubaliana naye. Akashikilia msimamo wake kuwa amemuona Harrison akiteseka mahali. Mama yake alimshika mkono, wakafumba macho na
kuanza kuomba dua maalum kwa ajili ya Harrison. Muda mfupi baadaye, Dk. Lewis naye alishtuka usingizini na kwenda kuungana na mkewe na mtoto wao, Skyler.
Mpaka kunapambazuka, bado walikuwa wanaendelea na maombi. Jua lilipochomoza, Skyler akamuomba mama yake amsindikize kwenye kaburi ambalo wote walikuwa wanaamini kuwa ndiyo alilozikwa Harrison. Walipofika walipiga magoti huku mikononi mwao wakiwa na Biblia, wakaanza kusali upya.
Wakiwa wanaendelea kusali, Skyler alianza kuona mambo ambayo yalimfanya apige mayowe kwa nguvu, akiwa kwenye hali ile mara alidondoka chini na kujipigiza kwenye kaburi, akapoteza fahamu. Mama yake akapiga kelele za kuomba msaada ambapo muda mfupi baadaye walinzi wa makaburi walifika na kuwasaidia.
Wakambeba Skyler juujuu hadi nje, wakasimamisha gari na kumkimbiza hospitali. Baada ya kutundikiwa dripu, Skyler alizinduka, akaanza kupiga kelele kama alivyofanya akiwa kule makaburini. “Kwani tatizoni nini mwanangu? Hebu tulia unieleze.”
“Mama wakati nikiwa nimezama kwenye maombi kule makaburini, nimepata maono kuhusu Harrison. Nimemuona anateseka sana huko aliko, tumbo la uzazi linaniuma sana.”
BAADA ya watu wote kuamini kuwa Harrison alikuwa amekufa kwenye ajali mbaya ya kugongwa na gari wakati akiendesha pikipiki na kutumbukia baharini kwenye Daraja la Miami, kijana huyo anakimbilia kwenye msitu mkubwa wa Tongass. Penzi la dhati alilokuwa nalo kwa msichana wa ajabu aliyekuwa anaishi porini na kulindwa na kundi kubwa la masokwe, linasababisha
amkatae mchumba wake Linda kanisani muda mfupi kabla ya ndoa yao kufungwa. Ndoa hiyo inayeyuka kama theluji iyeyukavyo juani na Linda anapoteza fahamu kanisani. Anapozinduka anatishia kujiua lakini baada ya kupata taarifa za kifo cha Harrison,
anabadili mawazo yake. Baadaye kila mmoja anakubaliana na ukweli kuwa tayari Harrison ameiagadunia, msiba unapelekwa
nyumbani kwa bibi na babu yake, Dk Lewis na mkewe Suzan ambapo taratibu za kawaida zinaendelea na baadaye mwili unaenda kuzikwa kwenye makaburi ya Miami. Upande wa pili, Harrison ambaye watu wote wanaamini amekufa, yupo kwenye
msitu wa Tongass akiendelea na kazi yake ya kumtafuta malkia wa masokwe. Anajiapiza kuwa hatarudi mjini mpaka atakapofanikisha kumpata malkia wa masokwe. Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO… MVUA kubwa iliendelea kunyesha ikiambatana na upepo na radi kali, Harrison akawa anaendelea kulifuatilia kundi lile la masokwe mpaka aone mwisho wake.
Kutokana na mvua ile, mifereji iliyokuwa ndani ya msitu wa Tongass ilifurika maji yaliyokuwa yanakwenda kwa kasi, hali iliyomfanya Harrison apate ugumu kuendelea na kazi yake. “Nahisi mwili wote kuishiwa nguvu, itakuwa ni homa nini!” alijisemea Harrison huku akitetemeka mwili mzima. Ilibidi atafute sehemu ya kujificha ili asilowane kwani hali yake ilianza kubadilika na
kuwa mbaya. Aliingia kwenye shimo kubwa lililokuwa chini ya mti mkubwa, akajikunyata na kujiinamia chini, mvua kubwa ikaendelea kunyesha kwa saa nyingi huku wingu zito likisababisha giza kutanda kila upande. Baada ya kunyesha kwa saa nyingi mfululizo, hatimaye mvua ilianza kupungua, lile wingu zito likasambaa angani na kulifukuzia mbali giza lililokuwa limeanza
kutanda. Harrison alitoka mahali alipokuwa amejifichana kusimama juu ya kisiki kikubwa cha mti, akawa anatazama huku na kule akiamini ataliona tena lile kundi la masokwe. Kilichozidi kummaliza nguvu ni kwamba mvua ile ilisababisha maji mengikutuama na kuweka madimbwi makubwa kwenye msitu huo. Mifereji mikubwa nayo ilikuwa ikiendelea kutiririsha maji
mengi kuelekea sehemu za mabondeni. “Mungu wangu, nitarudije kwenye kibanda changu?” alijisemea Harrison huku akiendelea kuangaza macho huku na kule. Licha ya hali ile, alijitahidi kujikaza na kuanza safari ya kurejea kule kwenye makazi yake ya muda. Alijipenyeza kwenye vichaka vilivyokuwa vimelowa kwa mvua, akawa anaruka madimbwi makubwa na mifereji
kuelekea kwenye makazi yake. Giza nalo likawa limeanza kutanda upya kwani tayari muda ulikuwa umekwenda sana. Baada ya kuhangaika kwa muda mrefu kutafuta njia ya kurudia kwenye kibanda chake, hatimaye Harrison alifanikiwa kufika. Kibanda chote kilikuwa kimejaa maji, hali iliyomfanya ashindwe hata kuingia ndani, akatafuta sehemu iliyokuwa na mwinuko kidogo na kukaa, CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ akawa anasubiri maji yapungue ili aingie kwenye kibanda chake. Baridi nayo ilizidi kumtesa, akawa anaendelea kutetemeka huku viungo mbalimbali vya mwili wake navyo vikianza kumuuma. Muda ulizidi kwenda lakini maji hayakupungua, ikabidi apande juu ya mti na kutafuta sehemu ambayo angeitumia kama kitanda mpaka asubuhi. Usiku hali yake ilizidi kuwa mbaya, akawa
anatetemeka mwili mzima hukujoto la mwili likianza kupanda kwa kasi. Kutokana na hali ile, hakupata hata lepe la usingizi, mpaka kunapambazuka hali yake ilikuwa ikizidi kuwa mbaya. Kwa bahati nzuri, kulipopambazuka jua lilianza kuchomoza kwa mbali, Harrison akajikaza na kuteremka mtini, akatafuta sehemu ambapo kijua kilikuwa kinapenya na kumfikia, akakaa. Jua
lilizidi kuchomoza, akawa anazidi kujisogeza ili limpate vizuri zaidi. Kwa kadiri muda ulivyokuwa unazidi kusonga mbele, hali ya Harrison kiafya ilizidi kuwa mbaya, homa kali ikawa imechachamaa na kumfanya muda wote ajikunyate huku akitetemeka sana. Kutokana na hali ile, Harrison alishindwa hata kuinuka na kuendelea na kazi yake ya kumtafuta malkia wa masokwe. Hata
aliposikia kelele za matawi ya miti kuvunjika na milio ya masokwe jirani na pale alipokuwa, alishindwa kusimama zaidi ya kugeuza shingo na kuangalia kwa mbali. Jioni ilipofika, alijikongoja mpaka ndani ya kibanda chake ambacho sasa hakikuwa na
maji, akapanga vitu vyake vizuri na kujilaza juu ya kitanda cha miti na nyasi. Kama ilivyokuwa kwa siku iliyopita, hakupata usingizi hata kidogo, usiku kucha akawa anatetemeka kutokana na maradhi yaliyokuwa yanamsumbua. Siku ya kwanza ilipita, hali yake
ya kiafya ikazidi kuwa mbaya. Kutokana na kukosa dawa, chakula na maji safi ya kunywa, siku ya pili kulipopambazuka Harrison alizidiwa. Akaanza kutapika mfululizo na kuhara, hali iliyoufanya mwili wake kuishiwa na nguvu kabisa. “Ooh Mungu wangu,
niokoe mimi mwanao kutoka kwenye hili janga, nitakufa peke yangu kwa kukosa msaada huku porini, nipe nguvu ooh Yehova Shalom,” Harrison alinong’ona. Hata hivyo haikusaidia chochote kwani aliendelea kutapika na kuhara mlemle ndani ya kibanda chake mpaka akawa hoi bin taaban, kizunguzungu nacho kikazidi kumbana. Ikafika muda akawa hawezi hata kujitingisha pale juu
ya kitanda cha miti alipokuwa amejilaza. Giza nene likatanda kwenye macho yake na kumfanya apoteze fahamu, akawa haelewi chochote kilichokuwa kinaendelea. *** “Mamaa! Mamaa!” “Nini tena mwanangu? Mbona unatushtua usiku wote huu?” “Mama
nimeota ndoto mbaya sana.” “Ndoto? Kuhusu nini?” “Kuhusu mwanangu Harrison.” “Aaah! Hayo ni maruweruwe ya kawaida, lazima uchungu wa mwanao uendelee kukusumbua.” “Hapana mama, nimemuona kabisa yupo mahali anateseka sana.” “Labda bado hajapata sehemu ya kupumzika huko peponi, njoo tufanye maombi maalum Mungu aipokee roho yake,” Suzan,
alikuwa akizungumzana mwanaye Skyler, mama mzazi wa Harrison usiku wa manane. Licha ya mwanamke huyo ambaye sasa umri wake ulikuwa umekwenda sana, kujitahidi kumbembeleza mwanaye Skyler na kumfanya aamini kile alichokiota kilikuwa ni ndoto za kawaida tu, bado hakutaka kukubaliana naye. Akashikilia msimamo wake kuwa amemuona Harrison akiteseka mahali.
Mama yake alimshika mkono, wakafumba macho na kuanza kuomba dua maalum kwa ajili ya Harrison. Muda mfupi baadaye, Dk. Lewis naye alishtuka usingizini na kwenda kuungana na mkewe na mtoto wao, Skyler. Mpaka kunapambazuka, bado
walikuwa wanaendelea na maombi. Jua lilipochomoza, Skyler akamuomba mama yake amsindikize kwenye kaburiambalo wote walikuwa wanaamini kuwa ndiyo alilozikwa Harrison. Walipofika walipiga magoti huku mikononi mwao wakiwa na Biblia, wakaanza kusali upya. Wakiwa wanaendelea kusali, Skyler alianza kuona mambo ambayo yalimfanya apige mayowe kwa nguvu,
akiwa kwenye hali ile mara alidondoka chini na kujipigiza kwenye kaburi, akapoteza fahamu. Mama yake akapiga kelele za kuomba msaada ambapo muda mfupi baadaye walinzi wa makaburi walifika na kuwasaidia. Wakambeba Skyler juujuu hadi nje, wakasimamisha gari na kumkimbiza hospitali. Baada ya kutundikiwa dripu, Skyler alizinduka, akaanza kupiga kelele kama
alivyofanya akiwa kule makaburini. “Kwani tatizoni nini mwanangu? Hebu tulia unieleze.” “Mama wakati nikiwa nimezama kwenye maombi kule makaburini, nimepata maono kuhusu Harrison. Nimemuona anateseka sana huko aliko,tumbo la uzazi linaniuma sana.”
Akiwa porini, Harrison anaendelea na harakati za kumsaka malkia wa masokwe. Mvua na jua vinamuishia mwilini kila siku lakini mwenyewe hajali. Kwa bahati mbaya, anaanza kuugua akiwa ndani ya msitu huo. Anazidiwa na homa kali inayomfanya aishiwe
nguvu, anakosa msaada na anakata tamaa ya kuendelea kuishi, anabanwa na kizunguzungu kikali na kupoteza fahamu. Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO… Harrison hakuelewa tena kilichoendelea mpaka alipokuja kuzinduka na kujikuta akiwa amelala juu ya kitanda cha ngozi ya mnyama, pembeni yake moto ukiwa unawaka. Alijaribu kukumbuka pale ni wapi lakini hakupata majibu,
alijaribu kunyanyuka lakini bado mwili wake haukuwa na nguvu, akageuza shingo na kuangalia upande ule kulipokuwa na moto, akagundua kuwa alikuwa ndani ya nyumba ya mtu. “Nimefikaje hapa? Nani kanileta?” alizidi kujiuliza maswali mengi, mara
akasikia vishindo vya mtu akitembea kuelekea pale alipokuwa amelala. “Unaendeleaje rafiki? Umeshaamka?” alizungumza mwanaume wa makamo ambaye Harrison aliitambua vyema sura na sauti yake. “Niambie hapa ni wapi na nani kanileta.” “Usiwe
na haraka kijana, nitakuelekeza kila kitu, inuka kwanza unywe dawa mengine yatafuatia baadaye,” alisema yule mwanaume huku akimsaidia Harrison kuinuka pale kitandani na kumuegamiza ukutani. Alikuwa ni yule mwanaume aliyemsaidia kujenga kibanda
cha miti ndani ya msitu wa Tongass, siku kadhaa zilizopita. Baada ya kumkalisha kitandani, alifunua chungu kikubwa kilichokuwa kinachemka jikoni, akachukua kikombe cha chuma na kukoroga dawa za kienyeji zilizokuwa zinachemka kisha akachota na kumsogezea Harrison. “Ni chungu lakini jikaze unywe ili upone haraka,” alisema yule mwanaume huku naye akikaa pembeni ya
Harrison, akawa anamhimiza anywe. Ilibidi Harrison ajikaze na kuanza kunywa, japokuwa dawa ilikuwachungu sana lakini alimaliza kikombe chote, jambo lililomfurahisha sana yule mzee. “Safi sana, utapona haraka kuliko nilivyotegemea, una juhudi za kunywa dawa, homa kali ilikuwa imechachamaa, ningechelewa kidogo ungekufa.” “Kwani ilikuwaje?” “Nilikuwa kwenye shughuli
zangu za uwindaji kama kawaida, si unajua huu msitu kwangu ni kama nyumbani? Nimezaliwa kwenye kijiji hiki na kukulia hapa hivyo kuwinda ni kama jadi yangu.” “Mh! Ikawaje?” “Baada ya kumaliza kuwinda, niliamua kukupitia japo nikuachie na wewe kitoweo kidogo, nikashtushwa na ukimya uliokuwa umetawala kwenye kibanda chako. Nilipofungua mlango ndiyo nikakukuta
umekauka kitandani ukiwa hujiwezi, nikakubeba haraka na kukuleta mpaka hapa kwangu.” “Ooh! Ahsante sana mzee wangu, Mungu atakulipia, nashukuru sana,” alisema Harrison huku akilengwalengwa na machozi. “Usijali kijana, nilikuahidi tangu siku
ya kwanza kuwa nitakusaidia mpakandoto zako za kumpata malkia wa masokwe zitakapotimia, pumzika kidogo nikuandalie supu japo urudishe nguvu,” alisema yule mtu, akainuka na kumsaidia Harrison kulala vizuri kisha akatoka nje ya kibandakile cha miti na udongo ambacho kilikuwa kimeezekwa kwa makuti. Baada ya muda alirudi akiwa na bakuli kubwa la bati lililokuwa limejaa
supu na nyama za porini. “Amka ule,” alisema yule mwanaume ambaye baadaye alijitambulisha kuwa anaitwa Carrick Hondo, raia wa Canada aliyezaliwa pembezoni mwa msitu wa Tongass baada ya wazazi wake kuyakimbia makazi yao miaka mingi iliyopita wakihofia usalama wa maisha yao. Alimsaidia tena Harrison kukaa vizuri, akamsogezea bakuli lililokuwa limejaa supu,
akaanza kumnywesha na kumlisha nyama. “Nyama ya swala hii, inasaidia sana kurudisha nguvu kwa mgonjwa kama wewe, siku nyingine inabidi nikufundishe majani ambayo yanatibu homa, unaweza kufa porini bila mtu yeyote kukujua.” “Nitashukuru sana, sijaumwa siku nyingi sana, homa ilivyochachamaa nikahisi naelekea kufa.” “Vipi umefikia wapi na kazi yako ya kumsaka
malkia wa masokwe?” “Nilifikia sehemu nzuri lakini kwa bahati mbaya mvua ikanikatisha. Nilikuwa nalifuatilia kundi la masokwe linalomlinda nikitaka kujua linapoenda kulala, mvua kubwa ndiyo ikaanza kunyesha na kunivurugia mipango yangu yote.” “Usijali, bado una nafasi ya kurudi tena na kufanikisha malengo yako.” “Kwani hapa ni wapi?” “Hiki kijiji nacho kinaitwa Tongass, watu
wanaoishi hapa wengi ni wawindaji, kipo pembezoni mwa msitu, siyo mbali sana kutoka msituni, ni mwendo wa saa nne tu unakuwa umefika katikati ya msitu.” “Afadhali, nilijua ni sehemu nyingine kabisa, kwa hiyo huku nako ni Marekani?” “Hapana,
huku ni upande wa Canada, ni mpakani kabisa si unajua huu msitu umeingia hadi Canada?” “Nimefurahi sana kufika huku, japo matatizo ndiyo yaliyonileta. Nataka nikimpata malkia wa masokwe nije kuishi naye huku.” “Litakuwa wazo zuri sana, kijiji kina watu wachache sana, na wewe ukija idadi yetu itazidi kuongezeka,” alisema Hondo huku akiendelea kumnywesha supu Harrison.
Bakuli zima liliisha, angalau akapata nguvu hata za kuweza kuinuka na kukaa vizuri mwenyewe. Siku ya kwanza ilipita Harrison akiendelea kunywesha dawa za kienyeji, siku ya pili kulipopambazuka, alikuwa na nafuu kubwa ingawa bado mwilihaukuwa
umerejea kwenye hali ya kawaida. Akawa anaendelea kunywesha dawa na kula vyakula vizuri, zikiwemo nyama za porini. Siku ya tatu alikuwa ameshapona kabisa, akaaga na kuanza safari ya kuelea msituni. Mzee Hondo alimsindikiza na kumuelekeza njia rahisi ambayo itamfikisha moja kwa moja mpaka kwenye kibanda chake. Baada ya kumfikisha mbali, waliagana na Harrison
akaendelea na safari yake. Baada ya kutembea kwa saa zaidi ya nne, akikatiza kwenye milima na mabonde ndani ya msitu ule uliokuwa na miti iliyoshonana, Harrison alifika kwenye kibanda chake. Kazi ya kwanza aliyoanza kuifanya ni kusafisha kibanda chake kwani wakati alipozidiwa alikuwa akimalizia hajazake zote humohumo. Alipomaliza aliwasha moto na kubanika nyama
aliyopewa na mzee Hondo,akala na kupumzika kwa muda akitafakari mambo kadhaa kwenye kichwa chake. “Nikimpata maisha yangu yatakuwa mazuri sana, nitahakikisha nambadilisha kila kitu, nampenda sana malkia wa masokwe mpaka nahisi
kuchanganyikiwa,” alijisemea Harrison akiwa amepumzika pembeni ya moto aliouwasha. Kwa kuwa muda ulikuwa umeenda, ukichanganya na uchovu aliokuwa nao wa kutembea umbali mrefu, aliamua kulala mpaka kesho yake asubuhi. ***
BAADA ya Harrison kwa kushirikiana na rafiki yake wa siku nyingi, kufanikiwa kuudanganya ulimwengu kuwa amekufa kwenye ajali mbaya ya kugongwa na gari wakati akiendesha pikipiki na kutumbukia baharini kwenye Daraja la Miami, Harrison anahamia kwenye Msitu wa Tongass. Kinachompeleka huko ni penzi la dhati alilokuwa nalo kwa msichana wa ajabu aliyekuwa anaishi kwenye msitu huo na kulindwa na kundi kubwa la masokwe.
Penzi lake kwa msichana huyo wa ajabu linasababisha amkatae mchumba wake, Linda kanisani muda mfupi kabla ya ndoa yao kufungwa. Ndoa hiyo inayeyuka kabisa baada ya taarifa za kifo cha Harrison kusambaa kwa kasi.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Akiwa porini, Harrison anaendelea na harakati za kumsaka malkia wa masokwe. Mvua na jua vinamuishia mwilini kila siku lakini mwenyewe hajali. Kwa bahati mbaya, anaanza kuugua akiwa ndani ya msitu huo. Anazidiwa na homa kali inayomfanya aishiwe nguvu, anakosa msaada na anakata tamaa ya kuendelea kuishi, anabanwa na kizunguzungu kikali na kupoteza fahamu. Anakuja kuokolewa na mzee mwindaji, Carrick Hondo anayemnywesha dawa za mitishamba mpaka akapona. Baada ya hapo
anarudi msituni kuendelea na kazi yake.
KULIPOPAMBAZUKA, kama kawaida Harrison aliamka mapema na kufanya mazoezi mepesi ya mwili kisha kijua kilipoanza kuchomoza, alijiandaa tayari kwa kazi ya kumfuatilia malkia wa masokwe. Alisogea mpaka jirani na mahali kundi kubwa la masokwe lilipokuwa linapita, akatafuta sehemu ya kujificha na kutulia kwa muda.
Baada ya muda kupita, alianza kusikia kelele za matawi ya miti kuvunjika na milio ya masokwe ikianza kusikika kutoka mbali. Alijiweka tayari huku mkuki wake ukiwa mkononi kwa ajili ya kujihami endapo kundi la masokwe litamshambulia kama ilivyokuwa kwa siku za nyuma.
Baada ya dakika chache, kundi kubwa la masokwe lilikuwa tayari limeshawasili pale Harrison alipokuwa amejificha, masokwe wakubwa wakawa wanaruka kutoka tawi moja la mti hadi lingine huku wakijitahidi kwa kadiri ya uwezo wao kumkinga malkia wao asidhurike.
Harrison alisubiri mpaka kundi lote lipite kisha kwa kasi kubwa na yeye akaanza kulifuata kwa nyuma. Akawa anakimbia na kujificha kwenye mashina ya miti akilifuata kundi lile kwa karibu.
“Kila ninapomuona nahisi kama uzuri wake unaongezeka! Lazima nimuoe,” alisema Harrison huku akizidi kulifuatilia lile kundi la masokwe wakubwa na wengi. Mara kwa mara alifanikiwa kumuona malkia wa masokwe kwa ukaribu, akawa anazidi kuvutiwa naye kutokana na uzuri wa asili aliokuwa nao.
Wakati akiendelea kulifuatilia lile kundi, masokwe waliokuwa nyuma waligundua kuwa kuna mtu anawafuata kwa lengo la kumdhuru malkia wao, wakaanza kutoa milio ya tahadhari, hali iliyowafanya masokwe wote wasitishe safari yao na kuanza kuangalia kuna jambo gani.
Harrison alishtukia ameshazungukwa na masokwe wakubwa, wakaanza kumshambulia kwa matawi ya miti, magongo na mawe. Malkia wao ambaye bado alikuwa hajagundua kilichokuwa kinaendelea, alipoona anayepigwa ni Harrison, alitoa mlio mkali uliofanya masokwe wote waache kumshambulia Harrison.
Akaruka kwenye matawi ya miti kwa kasi kubwa na kushuka hadi pale alipokuwa amesimama Harrison. Akawa anamsogelea taratibu huku akimtazama kwa macho kama anayemshangaa na kumfananisha naye.
Harrison ambaye tayari alikuwa na majeraha kadhaa mwilini kutokana na kipigo cha masokwe wale, alifurahi sana malkia wa masokwe kumsogelea, akaachia tabasamu pana huku naye akipiga hatua fupifupi kumsogelea.
Malkia wa masokwe alimtazama Harrison kwa muda mrefu, akawa anamuangalia kiungo kimojakimoja na kujifananisha naye. Japokuwa alikuwa amelelewa na masokwe, bado alitambua kuwa kuna tofauti kubwa kati yake na viumbe wale hivyo alipomuona Harrison, aligundua kuwa anafanana naye kwa vitu vingi.
Aliendelea kumshangaa Harrison huku lile kundi la masokwe likiwa limewazunguka, akamzunguka hadi nyuma na kuendelea kumchambua kiungo kimojakimoja. Baada ya muda, malkia wa masokwe alitoa mlio kama mnyama kisha akakimbia na kurukia juu ya tawi la mti kama wafanyavyo masokwe, nao wakamfuata na kurukia juu ya matawi, wakaanza kutimua mbio kutokomea kusipojulikana.
Kwa kuwa Harrison alikuwa amechoka sana, ilibidi akubali kushindwa, akaliacha kundi lile liondoke na yeye akageuza na kuanza kutembea taratibu kurudi kwenye kibanda chake.
Kimoyomoyo alikuwa akijipongeza kwani kwa mara ya pili alifanikiwa kusogeleana na malkia wa masokwe. Akaamini akiongeza juhudi anaweza kufanikisha azma yake ya kumpata malkia wa masokwe. Alitembea taratibu mpaka kwenye kibanda chake, alipofika kitu cha kwanza alichokifanya ilikuwa ni kuwasha moto na kuanza kuchoma nyama aliyopewa na mzee Hondo.
Aliichoma vizuri kisha akala na kushushia na maji, usingizi ukampitia kutokana na uchovu aliokuwa nao. Alikuja kushtuka baada ya kusikia kelele za kundi la masokwe likirudi, akakurupuka pale chini alipokuwa amelala na kusimama wima, kelele zikaongezeka kwa kadiri kundi lile lilivyokuwa linazidi kumsogelea.
Katika hali ambayo hakuitegemea, alimuona malkia wa masokwe akichomoka kutoka katikati ya kundi la masokwe wakubwa na kusogea upande ule aliokuwa amesimama Harrison. Alipomsogelea, alibwaga chini furushi la matunda ya porini jirani na pale alipokuwa amesimama Harrison kisha akakimbia kwa miguu na mikono na kujichanganya tena na kundi la masokwe, muda mfupi baadaye wakawa wametoweka eneo lile.
Harrison hakuamini kile kilichotokea, akasogea mbele taratibu na kuinama pale malkia wa masokwe alipoliacha furushi lile la matunda, akalifungua ambapo alikuta kuna matunda mbalimbali ya porini, mengine akiwa hajawahi hata kuyaona. Kilichomvutia ni kwamba yote yalikuwa yameiva vizuri, akajikuta mate yakimjaa mdomoni. Bila kupoteza muda alianza kuyala moja baada ya jingine huku akiwa na tabasamu pana usoni mwake. Aliamini hayana sumu kwani kama masokwe pamoja na malkia wao walikula bila kudhurika, hata yeye asingeweza kudhurika. Alikula hadi akatosheka, mengine akaenda kuyahifadhi ndani ya kibanda chake.
Muda ulizidi kuyoyoma kwa kasi na hatimaye giza likaanza kuingia. Harrison aliwasha moto kwa kutumia kuni alizokusanya msituni na kujilaza pembeni. Akawa anaendelea kuchoma nyama taratibu huku akimalizia kuyala matunda aliyopewa na malkia wa masokwe.
Akiwa anaendelea kuota moto na kuivisha nyama, alisikia vishindo vikitokea kichakani, akakimbilia ndani ya kibanda na kuchukua mkuki aliopewa na mzee Hondo, akajificha nyuma ya mti huku akiwa tayari kwa lolote.
Katika hali ambayo hakuitegemea, alishtuka kumuona malkia wa masokwe akichomoza kutoka vichakani, safari hii akiwa hajaongozana na masokwe kama ilivyokuwa kawaida yake. Akawa anaangaza macho huku na kule kama anayetafuta kitu.
Harakaharaka Harrison alichomoka vichakani na kujitokeza, akawa anasogea pale alipokuwa amesimama malkia wa masokwe huku akiwa na tabasamu pana usoni. Wakawa wanatazama usoni kama majogoo yanayotaka kupigana. Mara malkia wa masokwe alitimua mbio na kurudi vichakani, akajificha na kuanza kumchungulia Harrison.
Muda mfupi baadaye akajitokeza tena na kuanza kumsogelea Harrison, alipomkaribia alikimbia tena na kurukia juu ya tawi la mti. Ilivyoonesha alikuwa anapenda kucheza na Harrison ingawa michezo yake ilikuwa ya kisokwesokwe.
Kwa kuwa Harrison alikuwa anatafuta namna ya kujenga naye ukaribu, alianza kumuiga alivyokuwa anafanya, naye akawa anakimbia na kujificha kisha kurudi tena, mara akawa anaparamia matawi ya miti kama malkia wa masokwe, jambo lililomfanya aanze kutabasamu.
Wakaendelea kucheza kwa muda mrefu huku moto ukiendelea kuwaka, walipochoka, Harrison alimsogelea malkia wa masokwe, akamkumbatia kwa nguvu. ***
PENZI lina nguvu kuliko mauti, walinena wahenga. Harrison, kijana msomi anajikuta akiangukia kwenye penzi la msichana aliyekuwa akiishi na masokwe ndani ya msitu wa Tongass. Hajali mazingira anayoishi msichana huyo na tabia zake alizonazo zinazofanana na masokwe.
Penzi lake kwa msichana huyo wa ajabu linasababisha amkatae mchumba wake, Linda kanisani muda mfupi kabla ya ndoa yao kufungwa. Anatoroka kanisani kwa kutumia pikipiki kubwa na kuwaacha watu wakiwa hawaamini kilichotokea.
Kwa kushirikiana na rafiki yake wa siku nyingi, wanafanikiwa kuudanganya ulimwengu kuwa Harrison amepata ajali mbaya ya kugongwa na gari wakati akiendesha pikipiki na kutumbukia baharini kwenye Daraja la Miami, na kufa papo hapo. Taarifa hizo zinasambaa kwa kasi na kila mmoja anaamini ni kweli amekufa.
Akiwa porini, Harrison anaendelea na harakati za kumsaka malkia wa masokwe. Mvua na jua vinamuishia mwilini kila siku lakini mwenyewe hajali. Kwa bahati mbaya, anaanza kuugua akiwa ndani ya msitu huo mpaka kuwa taabani, anaokolewa na mzee mwindaji, Carrick Hondo anayemnywesha dawa za mitishamba mpaka akapona.
Baada ya hapo anarudi msituni kuendelea na kazi yake. Anajaribu kujenga mazoea na msichana huyo. Baada ya kuteseka sana, hatimaye ndoto yake inaanza kuelekea kutimia.
MALKIA wa masokwe alijitoa kwa nguvu mikononi mwa Harrison, akakimbilia kichakani na kujificha. Harrison alimfuata kwani tayari alishaanza kujihisi tofauti alipomkumbatia. Malkia wa masokwe alipoona Harrison anamfuata tena kwa lengo la kumkumbatia, aliparamia matawi ya miti na kutokomea gizani.
Harrison alijaribu kumfuatilia lakini hakufanikiwa kumpata, akarudi pembeni ya moto alipokuwa amekaa, akawa anatabasamu kwani kwa mara ya kwanza alifanikiwa kucheza na malkia wa masokwe. Alikaa kwa muda mrefu pembeni ya moto akitegemea kumuona tena msichana yule wa ajabu lakini hakurudi.
Baadaye akaingia ndani ya kibanda chake na kulala. Usingizi haukumchukua haraka, akawa anamuwaza sana malkia wa masokwe na kitendo alichokifanya cha kumfuata pale akiwa peke yake. “Inawezekana na yeye ameanza kunipenda?” alijiuliza kimoyomoyo, akaachia tabasamu pana na kujigeuza juu ya kitanda chake cha miti, baada ya muda usingizi ukampitia.
Kulipopambazuka, aliwahi kuamka na kutoka nje ya kibanda chake, akawa anafanya mazoezi mepesi huku akilisubiri kundi la masokwe lipite. Penzi lake kwa malkia wa masokwe lilikuwa linazidi kuongezeka kila uchao, akawa anamuomba Mungu wake siku moja ndoto zake za kuishi naye zitimie.
Baada ya muda, kundi la masokwe liliwasili eneo lile, malkia wao akiwa katikati kama kawaida. Harrison alitamani malkia wa masokwe amsogelee lakini haikuwezekana. Lilipopita alianza kulifuatilia kwa nyuma. Tofauti na siku zote, malkia wa masokwe alikuwa akigeuka na kumtazama Harrison mara kwa mara. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Baada ya kukimbia kwa muda mrefu, hatimaye kundi lile la masokwe lilifika kwenye miti ya matunda, Harrison akajibanza kwenye mti mkubwa uliokuwa jirani. Alikuwa anaogopa kumsogelea hovyo malkia wa masokwe kwani mara zote alizojaribu kufanya hivyo, aliambulia kipigo kikali kutoka kwa masokwe waliokuwa wanamlinda.
Masokwe waliendelea kula matunda juu ya miti, wakihama kutoka mti mmoja hadi mwingine. Walipotosheka walikusanyana na kuanza safari ya kuondoka huku wakihakikisha malkia wao anapata ulinzi wa kutosha. Harrison alisubiri masokwe waanze kuondoka, na yeye akaanza kuwafuata kwa nyuma huku akikimbia.
Licha ya kujitahidi kukimbia kwa kasi, Harrison alijikuta akizidiwa na uchovu, akaamua kuliacha kundi lile kubwa liondoke, akatafuta sehemu yenye kivuli na kupumzika. Baada ya muda aliinuka na kuanza kujikongoja kurudi kwenye kibanda chake.
Baada ya kutembea umbali mrefu, alifika kwenye kibanda chake, akashtuka baada ya kuona kuna furushi limewekwa jirani na mlango wa kuingilia. “Nani tena aliyeweka mzigo wake mlangoni?” alijiuliza Harrison huku akitembea kwa tahadhari kuusogelea. Katika hali ambayo hakuamini macho yake, aligundua kuwa ni furushi la matunda mchanganyiko kama ambayo aliletewa jana yake na malkia wa masokwe.
“Kumbe ananipenda sana? Kila siku ananiletea matunda?” alijisemea Harrison kimoyomoyo huku akitabasamu. Kwa kuwa alikuwa na njaa, alikaa na kuanza kuyafaidi. Mengine aliyahifadhi kwa ajili ya kuyala jioni, akanywa na maji na kujilaza nje ya kibanda chake.
Muda ulizidi kuyoyoma, jua likawa linazidi kuwa kali. Kwa kuwa nyama aliyopewa na mzee Hondo ilikuwa imeshaisha, alijikuta akipatwa na akili ya kwenda kuwinda ili apate kitoweo. Asingeweza kuendelea kuishi kwa kutegemea kula matunda tu.
Akachukua mkuki na kisu kikubwa alivyopewa na mzee Hondo na kutoka, akaelekea upande kulipokuwa na chemchemi ya maji kwani aliamini muda ule wa jua kali, wanyama wengi hupenda kwenda kunywa maji. Hakuwahi kuwinda hata mara moja katika maisha yake lakini hakuwa na ujanja.
Alitembea umbali mrefu mpaka alipofika kwenye chemchemi ndani ya msitu ule wa Tongass, akatafuta sehemu nzuri na kujiweka tayari kwa mawindo. Baada ya muda, aliona kundi la swala wakielekea kunywa maji, akaushika mkuki wake vizuri na kuanza kunyata kusogea mahali kundi lile lilipokuwepo.
Alipolikaribia, alirusha mkuki wake lakini kwa kuwa hakuwa na uzoefu wa kuwinda, alikosea kulenga shabaha, mkuki ukaenda kuangukia mbali huku wale swala wote wakikimbilia vichakani. Alienda kuuokota mkuki wake, akarudi tena kujificha huku akijipa moyo kuwa lazima atapata kitoweo.
Baada ya muda, kundi lingine la digidigi lilifika kunywa maji kwenye chemchemu ile, Harrison akanyata hadi karibu na kurusha tena mkuki wake kwa nguvu. Kama ilivyokuwa mwanzo, alikosea shabaha na kusababisha wanyama wale wakimbilie vichakani. Akaenda kuuokota mkuki wake na kurudi tena.
Alienda kuwakosakosa wanyama mpaka jua lilipoanza kuzama, akaamua kukubali kushindwa. Akanywa maji na kuanza safari ya kurudi kwenye kibanda chake akiwa mikono mitupu. Alitembea kwa muda mrefu mpaka giza lilipoingia, akafanikiwa kufika salama kwenye kibanda chake.
Kwa kuwa njaa ilikuwa inamuuma, alimalizia matunda aliyokuwa ameyabakiza na kunywa maji, akawasha moto na kukaa pembeni huku mawazo juu ya malkia wa masokwe yakiendelea kukitawala kichwa chake.
“Leo akija nitamfurahisha mpaka akubali kulala na mimi hadi asubuhi,” aliwaza Harrison huku akiendelea kuweka kuni kwenye moto. Muda ulizidi kuyoyoma bila malkia wa masokwe kutokea.
Uchovu ulisababisha aanze kuhisi usingizi mzito, akanyanyuka pale alipokuwa amekaa na kujikongoja kuingia ndani ya kibanda chake. Hakukumbuka hata kuubana vizuri mlango, usingizi mzito ukampitia.
Alikuja kuzinduka usiku wa manane baada ya kuhisi kuna mtu ameingia ndani ya kibanda chake, akatulia kimya akitaka kujua ni nani. Alihisi huenda ni mnyama mkali wa porini anataka kumdhuru, akatulia kimya huku mapigo yake ya moyo yakimwenda mbio kuliko kawaida.
Akiwa katika hali ile, alishtukia akiguswa mgongoni na mkono wa binadamu, mapigo ya moyo yakawa yanazidi kumwenda mbio, akawa anatetemeka mwili mzima. Kwa ujasiri wa hali ya juu alikurupuka na kusimama wima, hakuamini macho yake baada ya kugundua kuwa aliyekuwa ameingia ndani ya kibanda chake ni malkia wa masokwe. ***
HARRISON, kijana msomi anajikuta akiangukia kwenye penzi la msichana aliyekuwa akiishi na masokwe ndani ya msitu wa Tongass. Licha ya kuwa na mwonekano wa kibinadamu, msichana huyo ana haiba kama za masokwe kwani alilelewa msituni tangu alipokuwa mdogo.
Penzi la Harrison kwa msichana huyo wa ajabu linasababisha amkatae mchumba wake, Linda siku ya ndoa yao, muda mfupi kabla hawajafunga ndoa kanisani.
Anamkimbia kanisani kwa kutumia pikipiki kubwa na kuwaacha watu wakiwa hawaamini kilichotokea. Kwa kushirikiana na rafiki yake wa siku nyingi, wanafanikiwa kuudanganya ulimwengu kuwa amepata ajali mbaya ya kugongwa na gari wakati akiendesha pikipiki na kutumbukia baharini kwenye Daraja la Miami, na kufa papo hapo.
Taarifa hizo zinasambaa kwa kasi na kila mmoja anaamini ni kweli amekufa kumbe ukweli ni kwamba amemfuata malkia wa masokwe msituni.
Akiwa msituni, Harrison anaendelea na harakati za kumsaka malkia wa masokwe. Licha ya ugumu anaokutana nao, hakati tamaa na haogopi chochote. Mvua na jua vinamuishia mwilini kila siku lakini mwenyewe hajali. Baada ya kuteseka sana, hatimaye ndoto yake inaanza kuelekea kutimia.
ALIJARIBU kumsemesha maneno mawili matatu lakini aligundua kuwa malkia wa masokwe hakuwa akifahamu kabisa lugha ya kibinadamu, akawa anatoa miguno na sauti kama wafanyavyo masokwe. Alijaribu kumuelekeza kwa vitendo kuwa apande juu ya kitanda cha miti ili walale pamoja lakini malkia wa masokwe alikuwa mgumu kuelewa.
Alipoona Harrison anazidi kumng’ang’aniza walale pamoja, malkia wa masokwe alikimbia na kutoka nje ya kibanda, Harrison naye akatoka. Japokuwa ilikuwa ni usiku wa manane, malkia wa masokwe alionesha kuwa na hamu ya kucheza na Harrison kwani alikuwa akikimbia na kuparamia matawi ya miti.
Harrison hakutaka kuonesha kuwa alikuwa amechoka, na yeye alimfuatisha kila alichokuwa anakifanya, wakawa wanacheza huku mbalamwezi ikiwamulikia. Waliendelea kurukaruka mpaka Harrison akachoka, akafanikiwa kumshika malkia wa masokwe na kumkumbatia kimahaba.
Kutokana na kuzidiwa na hisia za kimapenzi, Harrison alimbusu malkia wa masokwe shavuni bila kujali uchafu wa ngozi yake. Tofauti na alivyotegemea, malkia wa masokwe alimparua kwa kucha zake ndefu, akachoropoka mikononi na kuanza kukimbia.
Hakuelewa kupigwa busu maana yake ni nini, akahisi huenda Harrison alikuwa anataka kumdhuru, jambo lililomfanya ajihami. Harrison alibaki kuugulia maumivu makali, akajikongoja na kurudi ndani ya kibanda chake, akapanda kitandani na kujilaza. Usingizi haukumjia haraka, aliendelea kumuwaza malkia wa masokwe na mbinu ambazo huenda zingefanikisha ndoto yake ya kumuoa kutimia.
“Kesho akija nitahakikisha namkata kucha na nywele, lazima nimbadilishe… nataka ajue kuzungumza kama binadamu na awe na tabia za kibinadamu, nitaweza tu,” aliwaza Harrison wakati akiendelea kuugulia maumivu makali.
Baada ya muda, usingizi ulimpitia. Akalala mpaka asubuhi, akawahi kuamka na kutoka nje ya kibanda chake. Hakuamini macho yake baada ya kumkuta malkia wa masokwe amelala juu ya mti, nje ya kibanda kile. Kwa jinsi ilivyoonesha, alilala usiku mzima palepale juu ya mti.
Taratibu alitembea mpaka chini ya ule mti, akapanda kwa kunyata mpaka alipofika kwenye tawi ambalo malkia wa masokwe alikuwa amelala. Ghafla alizinduka kutoka usingizini, akataka kurukia kwenye tawi lingine lakini Harrison alimuwahi, akamshika na kushuka naye hadi chini.
Kitu cha kwanza alichofanya ilikuwa ni kuanza kumkata kucha kwa kutumia kisu kikali alichopewa na Mzee Hondo. Kazi haikuwa nyepesi kwani alihisi kama Harrison anataka kumdhuru, akawa anajihami kwa kutishia kumng’ata na kumparua mwilini.
Baada ya purukushani kubwa, hatimaye alifanikiwa kumkata kucha za mikono yote ambazo zilikuwa ndefu kama mnyama wa porini. Alipomaliza alimkumbatia tena mwilini, safari hii alishindwa kumjeruhi kwa kucha kwani zote zilikuwa zimekatwa.
“Unaitwa nani?” “Mhhh! Arrrgh! Whuuuu,” alinguruma malkia wa masokwe kwa hasira, ikabidi Harrison amuanzishie michezo aliyokuwa anaipenda, akakimbia na kuparamia tawi la mti, malkia wa masokwe naye akamfuata.
Wakaanza kucheza kwa furaha huku mara kwa mara Harrison akimkumbatia malkia wa masokwe. Wakiwa wanaendelea kucheza, Harrison alishtuka baada ya kusikia kelele kubwa za matawi ya miti kuvunjika na milio ya masokwe.
Kufumba na kufumbua, kundi kubwa la masokwe waliokuwa wamebeba mawe makubwa, fimbo na magongo liliwasili eneo lile na kukizunguka kibanda cha Harrison. Masokwe walikuwa wanamtafuta malkia wao ambaye alitoweka tangu usiku uliopita.
“Mungu wangu, leo nimepatikana… nitatoka salama kweli hapa?” alisema Harrison huku akitafuta upenyo wa kukimbilia. Alishangaa kuona malkia wa masokwe anamfuata mwilini na kumshikilia akionesha kwamba hakutaka masokwe wenye hasira wamdhuru.
Mara malkia wa masokwe alitoa mlio kwa ishara ambayo masokwe waliielewa, wakashusha fimbo na magongo chini huku wale ambao walishajiandaa kuvurumisha mawe makubwa nao wakiyatupa chini. Harakaharaka malkia wa masokwe aliparamia kwenye matawi na kuruka hadi katikati yao, kwa kasi ya ajabu kundi lote likaanza kuondoka eneo lile. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Harrison alishusha pumzi ndefu huku akiwa haamini kilichotokea. Alijiuliza maswali mengi ndani ya kichwa chake ambayo yote hakuyapatia majibu, akajisogeza mahali kijua cha asubuhi kilipokuwa kinapenya, akakaa na kuanza kuota jua.
Muda ulizidi kuyoyoma, baadaye akachukua mkuki wake na kutoka kwenda kuwinda kwani njaa ilikuwa ikimuuma sana na hakuwa na chakula. “Leo lazima nipate kitoweo, nitajitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu,” alisema Harrison wakati akitembea katikati ya vichaka kuelekea mahali kulipokuwa na chemchemi.
Baada ya kutembea kwa umbali mrefu, hatimaye alifika kwenye chemchemi, akatafuta sehemu nzuri na kujificha huku mkuki wake ukiwa mkononi.
Baada ya muda, kundi la paa liliwasili na kukimbilia kunywa maji, taratibu akaanza kunyata na kusogea huku mkuki wake ukiwa mkononi. Baada ya kusogea, aliinua mkuki na kuurusha kwa nguvu zake zote, ukaenda kumchoma paa mmoja shingoni, akajaribu kukimbia lakini alianguka mita chache mbele huku lile kundi lingine likitawanyika. Akakimbia hadi mahali paa yule alipoangukia, akachomoa kisu na kummalizia huku akiwa haamini kama kweli amefanikiwa kupata kitoweo.
Kwa jinsi alivyokuwa na njaa, hakutaka kupoteza muda, alimnyanyua na kumbeba begani, akaanza safari ya kurudi kwenye kibanda chake. Alitembea vichakani huku jasho likimvuja kutokana na uzito wa kitoweo chake, baada ya kutembea kwa umbali mrefu akafika.
Jambo la kwanza lilolifanya ilikuwa ni kuwasha moto kisha akaanza kuandaa kitoweo. Alimchuna ngozi na kumtoa utumbo, akamkatakata na kuanza kumchoma kwenye moto aliouwasha. Akiwa anaendelea kuandaa kitoweo, aliendelea kumfikiria malkia wa masokwe na jinsi alivyofanikiwa kujenga naye ukaribu.
Japokuwa alikuwa akifahamu kabisa kuwa ni dhambi kufanya mapenzi kabla ya kuoana, alijikuta tamaa ya mwili ikimjaa na kuanza kufikiria kukutana kimwili na malkia wa masokwe. Kila alipokuwa anakikumbuka kifua chake kilichonakshiwa na vifuu vya nazi vilivyochongoka sawia na umbo lake la Kibantu lililositiriwa na kipande kidogo cha kitambaa kikuukuu, alijikuta akisisimka kuliko kawaida. “Lazima nimpate, lazima awe mke wangu,” alijisemea Harrison huku akiendelea kuchoma nyama. ***
MVUMILIVU hula mbivu, walinena wahenga. Penzi la malkia wa masokwe, msichana aliyelelewa na masokwe ndani ya msitu wa Tongass linamchanganya kabisa Harrison. Tangu mara ya kwanza alipomuona malkia wa masokwe wakati akiwa kwenye utafiti wake wa tabia za wanyama ndani ya msitu huo, anajikuta akizama penzini kiasi cha kuwa tayari kufanya lolote ilimradi ampate.
Penzi lake kwa msichana huyo wa ajabu linasababisha amkatae mchumba wake, Linda kanisani muda mfupi kabla ya ndoa yao kufungwa. Anatoroka kanisani kwa kutumia pikipiki kubwa na kuwaacha watu wakiwa hawaamini kilichotokea.
Kwa kushirikiana na rafiki yake wa siku nyingi, wanaandaa mpango maalum wa kuwafanya watu waamini kuwa Harrison amekufa. Wanatengeneza ajali feki inayowafanya watu waamini kuwa amepata ajali mbaya ya kugongwa na gari wakati akiendesha pikipiki na kutumbukia baharini kwenye Daraja la Miami.
Kwa jinsi walivyouandaa mpango huo kwa umakini, kila mtu anaamini kuwa ni kweli kijana huyo msomi amekufa, wanaomboleza kisha wanaenda kuuzika mwili ambao kila mmoja alikuwa anaamini kuwa ni wa Harrison.
Baada ya hapo anatorokea porini ambako anaendelea na kazi yake ya kumtafuta malkia wa masokwe. Hajali ugumu anaokutana nao, akili yake inawaza kitu kimoja tu, penzi la malkia wa masokwe. Jitihada zake zinamuwezesha kuanza kujenga mazoea na malkia wa
masokwe kiasi cha kuwa wanacheza pamoja michezo ya kisokwe mara kwa mara.
WAKATI Harrison akiendelea kuchoma nyama pembeni ya kibanda chake, ndani kabisa ya msitu wa Tongass, alisikia vishindo vya mtu akitembea vichakani kuelekea pale alipokuwa. Japokuwa kigiza cha jioni kilikuwa kimeanza kuingia, alipogeuka tu alimtambua malkia wa masokwe mara moja. Akaacha kila alichokuwa anakifanya na kusimama.
Malkia wa masokwe alitembea taratibu mpaka alipomkaribia Harrison, akasimama mita kadhaa kutoka pale alipokuwepo. Harrison alitabasamu kwa furaha, akamuonesha kwa ishara kuwa asogee jirani na moto kisha akae. Malkia wa masokwe alisita kwa muda, kisha akasogea mpaka pale pembeni ya moto na kukaa.
Harrison akawa anaendelea kuchoma nyama huku akitumia muda mwingi kumtazama malkia wa masokwe usoni. Alitamani angekuwa na uwezo wa kuzungumza kama binadamu wengine ili amueleze kilichokuwa ndani ya moyo wake lakini haikuwa hivyo.
Malkia wa masokwe hakuwa akijua lugha yoyote zaidi ya ishara kama wafanyazo masokwe. Akakaa kimya pembeni ya Harrison, akawa anamuangalia jinsi alivyokuwa anachoma nyama. Alipoanza kuivisha, Harrison alikata kipande na kula, kisha akampa na malkia wa masokwe.
Cha ajabu ni kwamba alishindwa kula nyama, akaishia kuinusa kisha akaitupa chini. Harrison alijaribu kumpa tena lakini bado alifanya vilevile, akavuta kumbukumbu juu ya tabia za masokwe alizojifunza alipokuwa chuoni kwamba wanyama hao hawali kabisa nyama zaidi ya mizizi, matunda na majani ya porini.
Alikumbuka kuwa ni aina chache sana za sokwe ndiyo hula wanyama wadogo lakini wanapatikana zaidi barani Afrika. Kwa kuwa alikuwa na njaa, aliendelea kula mwenyewe huku malkia wa masokwe akimtazama. Baada ya kula kiwango kikubwa cha nyama, iliyobakia aliibanika kisha akaiingiza ndani ya kibanda chake.
Akatoka na kuanza kucheza na malkia wa masokwe. Mara kwa mara macho yake yalikuwa yakitua kwenye kifua kibichi cha msichana huyo, hisia za mapenzi zikaanza kumpanda taratibu ingawa alijitahidi kuzizuia. Hakuna kitu ambacho malkia wa masokwe alikuwa anapenda kama kucheza michezo ya kisokwe na Harrison.
Mara kwa mara alikuwa anapenda wafukuzane kwenye miti na kuparuana na kucha lakini Harrison hakuwa na uwezo huo zaidi ya kuwa anakimbiakimbia na kujificha kwenye miti. Waliendelea kucheza kwa muda mrefu, Harrison akachoka sana hasa ukizingatia kuwa siku hiyo alitembea umbali mrefu kwenda kuwinda.
“Ngoja nijaribu kumkumbatia na kumbusu, sijui ataelewa?” aliwaza Harrison wakati akimuangalia malkia wa masokwe aliyekuwa anaendelea kurukia matawi ya miti. Baada ya kurukaruka, alimsogelea Harrison aliyekuwa amekaa chini akitaka waendelee kucheza. Alipomkaribia, Harrison alimrukia na kumkumbatia, akambusu shavuni.
Kama ilivyokuwa kawaida ya malkia wa masokwe, alichoropoka mikononi mwa Harrison na kujaribu kumparua akidhani anataka kumdhuru. Kwa kuwa Harrison alishamkata kucha, hakumjeruhi. Akakimbia na kwenda kwenye tawi la mti, akapanda juu na kuanza kumuangalia Harrison.
Alimfanyia ishara ya kumuita kwa kutumia mikono yake, malkia wa masokwe akateremka kwenye tawi la mti lakini safari hii hakutaka kumsogelea, akasimama mbali huku akimuangalia kwa macho ya woga. Kwa kuwa tayari ilikuwa ni usiku sana, Harrison alimuoneshea ishara kuwa waingie ndani wakalale lakini malkia wa masokwe akakataa kwa kutingisha kichwa na mabega.
“Huyu dawa yake ndogo, atanifuata mwenyewe,” alijisemea Harrison kimoyomoyo, akafungua mlango wa kibanda chake na kuingia ndani, akaenda kujilaza huku hisia za mapenzi zikiendelea kumtesa.
“Angekuwa anaelewa jinsi ninavyoteseka juu yake asingekuwa anakimbia nikimkumbatia na kumbusu,” alijisemea huku akiendelea kuteseka kwa hisia kali za mapenzi alizokuwa nazo. Wakati akiendelea kuwaza, malkia wa masokwe alisukuma mlango, naye akaingia na kusimama kwenye pembe ya kibanda kile.
Harrison alijifanya hajamuona, akaendelea kujilaza vilevile, baada ya kusimama kwa dakika kadhaa, malkia wa masokwe alisogea na kukaa pembeni ya kitanda, kwa msaada wa mbalamwezi iliyokuwa inapenya mpaka ndani ya kibanda kile, Harrison alianza kuusanifu uzuri wake bila mwenyewe kugundua kuwa alikuwa anatazamwa.
Aliendelea kumuangalia kiungo kimoja baada ya kingine, kuanzia usoni mpaka kushuka chini. Kwa hakika malkia wa masokwe alikuwa na uzuri wa kipekee unaoweza kumchanganya mwanaume yeyote aliyekamilika.
Kutokana na kuzidiwa na hisia za kimapenzi, Harrison alijikuta akiinua mkono wake mmoja na kumshika kifuani malkia wa masokwe, akaruka na kusimama, Harrison naye akasimama na kumkumbatia kwa nguvu. Malkia wa masokwe alijaribu kujichoropoa lakini kwa sababu Harrison alimbana ukutani, alishindwa, akabaki anahangaika.
Kwa mara nyingine Harrison alipeleka mkono wake mmoja kifuani na kumgusa upande wa kulia, malkia wa masokwe akashtuka tena na kuanza kuhema kwa nguvu. Harrison alimbusu shavuni na shingoni, akarudiarudia mara kadhaa mpaka malkia wa masokwe akatulia huku akizidi kuhema kwa nguvu.
Kwa kutumia mkono mmoja, Harrison aliteremsha suruali yake na kuivua akiwa bado amembana malkia wa masokwe pale ukutani. Alifungua pia vishikizo vya shati lake huku akiendelea kumbusu sehemu mbalimbali, alipomaliza alimbeba malkia wa masokwe na kumbwaga kitandani.
Kabla hajatimiza alichotaka kukifanya, malkia wa masokwe alipata upenyo, akamsukuma kwa nguvu mpaka ukutani, akainuka na kutoka nje kwa kasi, Harrison alifanikiwa kumdaka mkono, wakawa wanavutana kabla ya malkia wa masokwe kutishia kumng’ata mkono. Harrison alipoona hivyo, alimuachia, akatimua mbio na kutokomea vichakani. Harrison aliokota nguo zake na kuzivaa huku akihema kama ametoka kukimbia riadha.
“Kwanza afadhali amekimbia, kanisani tulifundishwa kuwa ni dhambi kukutana kimwili kabla hamjafunga ndoa na kuhalalishwa mbele za Mungu,” alijisemea Harrison huku akijifuta kijasho chembamba kilichokuwa kinamtoka. Alirudi kitandani na kujilaza, akawa anaendelea kumuwaza malkia wa masokwe.
“Sijui nifanye nini ili anielewe kuwa nampenda, sitakata tamaa mpaka atakapokuja kuwa mke wangu,” alijisema Harrison. Licha ya kujitahidi kuubembeleza usingizi, Harrison hakulala haraka. Mawazo juu ya malkia wa masokwe yaliendelea kumtesa kwa muda mrefu. Akiwa bado anagalagala juu ya kitanda cha miti, alisikia vishindo vya mtu akija, mara akaona mlango ukisukumwa, malkia wa masokwe akaingia tena na kwenda kukaa palepale alipokuwa amekaa awali. ***
LICHA ya aina ya maisha anayoishi msichana wa ajabu ndani ya msitu mkubwa wa Tongass akiwa na tabia kama masokwe, Harrison anajikuta akiangukia kwenye penzi zito la msichana huyo. Hajali watu watamuonaje, anachotaka ni mapenzi tu. Hali hiyo inamfanya amkatae mchumba wake, Linda kanisani muda mfupi kabla ya ndoa yao kufungwa. Anatoroka kanisani kwa
kutumia pikipiki kubwa na kuwaacha watu wakiwa hawaamini kilichotokea. Kwa msaada wa rafiki yake wa siku nyingi, wanaandaa mpango maalum wa kuwafanya watu waamini kuwa Harrison amekufa.
Wanatengeneza ajali feki inayowafanya watu waamini kuwa amegongwa na gari wakati akiendesha pikipiki na kutumbukia baharini kwenye Daraja la Miami nchini Marekani.
Kila mtu anaamini kuwa ni kweli kijana huyo msomi amekufa, wanaomboleza kisha wanaenda kuuzika mwili ambao kila mmoja alikuwa anaamini kuwa ni wa Harrison.
Baada ya hapo anatorokea porini ambako anaendelea na kazi yake ya kumtafuta malkia wa masokwe. Taratibu anaanza kujenga mazoea naye kiasi cha kufikia hatua ya malkia wa masokwe kuwatoroka masokwe na kumfuata Harrison kwenye kibanda chake. Harrison naye anazidi kupandwa na hisia kali za mapenzi. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Harrison alijikausha kama hajamuona malkia wa masokwe kwani alijua kuwa akianza kumfanyia vituko tena, anaweza kukimbia kama awali na asirudi tena. Alitulia kimya kitandani, akajifanya macho yake ameyafumba kumbe alikuwa akimtazama malkia wa masokwe kwa wizi.
“Lazima atapitiwa na usingizi tu,” aliwaza Harrison huku akiendelea kujikausha. Baada ya malkia wa masokwe kukaa pale pembeni ya kitanda kwa muda, alianza kuhisi uchovu mkali, akajisogeza vizuri na kulala kama Harrison alivyokuwa amelala lakini tofauti yao ni kwamba kila mmoja alikuwa amegeukia upande wake huku miguu ya malkia wa masokwe ikiwa kwenye kichwa cha Harrison.
“Yap, lazima ataingia kwenye mtego tu, leo ndiyo leo asemaye kesho mwongo,” alijisemea Harrison huku akizidi kujikausha pale kitandani. Baada ya kukaa kwa zaidi ya dakika arobaini, alianza kumsikia malkia wa masokwe akikoroma kwa mbali kuashiria kuwa usingizi ulikuwa umeanza kumpitia.
Kwa tahadhari kubwa aliinuka huku akijitahidi kutosababisha kelele zozote zinazoweza kumshtua malkia wa masokwe. Aliteremka mpaka chini ya kitanda, taratibu akavua suruali yake na shati, akabaki kama alivyoletwa duniani. Kwa msaada wa mbalamwezi alimsogelea malkia wa masokwe pale alipokuwa amelala, akaanza kumpapasa mwili wake kuanzia kichwani kushuka chini.
Alijitahidi kufanya kila kitu kwa utulivu wa hali ya juu akikwepa kumshitua, alimbusu kwenye mashavu yake huku akizipapasa nywele zake taratibu, akahamia shingoni na kuanza kushuka chini.
“Tazama ulivyoumbika, nikubalie ombi langu tafadhali… nataka uwe mke wangu wa halali, tujenge familia pamoja, niitwe baba na wewe uitwe mama,” alisema Harrison kwa hisia za hali ya juu. Malkia wa masokwe hakuwa akielewa chochote kutokana na kupitiwa na usingizi mzito.
Aliendelea kumpapasa mwili wake taratibu, akafika kwenye kifua chake kichanga kilichonakshiwa na michongoma miwili iliyokuwa imesimama wima. Taratibu akaanza kukisanifu huku mapigo yake ya moyo yakizidi kuongezeka kwa kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele.
Alivinjari kwenye michongoma ile kwa zaidi ya dakika ishirini mpaka aliporidhika, akaendelea kushuka chini hadi kwenye kitovu, akaweka kituo hapo na kuanza kucheza nacho. Hakujali uchafu aliokuwa nao msichana huyo wa ajabu, akawa anatalii huku na kule huku akilibusu tumbo lake lililokuwa limejengeka vizuri.
“Sijawahi kuona msichana mzuri kama huyu, sijui ilikuwaje mpaka akaja kuishi huku porini, angekuwa mjini huyu angewasumbua sana wanaume wakware,” aliendelea kuwaza huku vidole vyake vikiendelea kumpapasa malkia wa masokwe
hapa na pale. Hakuishia hapo, alizidi kushuka chini ambapo sasa alishindwa kuzizuia hisia zake. Akawa anajaribu kumfungua kitambaa kikuukuu alichokuwa amejifunga kiunoni na kujisitiri sehemu muhimu zaidi za mwili
wake. Hakuweza kufanikiwa kirahisi kwani kilifungwa mafundo mengi na kwa ustadi mkubwa. Akaamua kusitisha zoezi lile na kuendelea kwenda chini, akakutana na mapaja yaliyonawiri vizuri, akawa anayabusubusu kwa hisia kali. Alijiuliza maswali mengi ambayo yote hakuyapatia majibu. Alishangaa iweje mtu anayeshindia matunda ya porini na mizizi awe na mwili uliojengeka vizuri kimahaba kiasi kile?
Aliendelea kufanya utundu wake mpaka alipofika kwenye nyayo za miguu yake. Alipozipapasa aligundua kuwa nyayo zimekuwa ngumu sana, akahisi huenda ni kwa sababu ya kutembea bila viatu. Alipozidi kuzipapasa, aligundua kuwa alikuwa na vipande vingi vya miba na vijiti ambavyo vilikuwa vimeng’ang’ania ngozi yake ya miguuni, akajikuta akimuonea huruma.
“Kesho nitamtoa miba yote na kuisafisha miguu yake,” alijisemea huku akiianza upya safari ya kutalii mwili wa malkia wa masokwe, safari hii akianzia chini kwenda juu. Alipofika karibu na kiuno, aliweka kituo na kuanza tena kujaribu kufungua kitambaa alichokuwa amejifunga.
Akiwa anaendelea na zoezi lile, alishtuka kupita kiasi baada ya kusikia kishindo kikubwa juu ya paa la kibanda chake, punde zikaanza kusikika kelele za matawi ya miti kuvunjika na purukushani za hapa na pale kwenye miti iliyokuwa inakizunguka kibanda kile, akajua kundi la masokwe limemfuata malkia wao.
Alitamani masokwe wamuachie japo dakika chache ili amalizie kufanya kile alichokuwa amekikusudia lakini haikuwezekana, masokwe waliokuwa na hasira walianza kukibomoa kibanda chake huku wengine wakirusha mawe makubwa.
Kufumba na kufumbua, masokwe watatu wakubwa walivunja mlango na kuingia ndani ya kibanda ambapo walimkuta Harrison akiwa kama alivyozaliwa na malkia wao akiwa amelala kitandani.
Masokwe wawili walianza kumuadhibu vikali Harrison wakati yule mmoja alimbeba malkia wao. Harrison alijitahidi kujiokoa lakini hakuweza kutokana na nguvu walizokuwa nazo masokwe wale, wakawa wanamtandika makofi mazito huku alama za viganja vyao zikibaki kwenye mwili wa Harrison.
Purukushani zile zilisababisha malkia wa masokwe azinduke kutoka usingizini, akajikuta tayari amebebwa juujuu na sokwe mkubwa. Japokuwa ilikuwa ni usiku wa manane, malkia wa masokwe aliona jinsi Harrison alivyokuwa anasulubiwa, ikabidi apige yowe kubwa kama ishara ya kuwakataza wale masokwe wasiendelee kumdhuru Harrison.
Wale masokwe walimuachia Harrison lakini tayari alikuwa amejeruhiwa vibaya, damu zikawa zinamtoka mdomoni na puani huku uso wote ukiwa na alama za viganja vya makofi aliyokuwa anapigwa na masokwe wale.
Sekunde chache baadaye, kundi lile lilitokomea na malkia wao gizani kwa kasi kubwa, Harrison akatoka nje ya kibanda chake kwa kujikongoja, akapiga magoti na kuanza kulia kwa uchungu kutokana na maumivu aliyokuwa anayahisi. Baada ya hasira kupungua na maumivu kupoa kiasi, alirudi ndani na kujilaza kwenye kitanda ambacho kiliharibiwa upande mmoja na wale masokwe.
Akalala mpaka asubuhi, kulipopambazuka tu aliamka na kuwasha moto, akabandika maji kwa kutumia kigae alichokiokota njiani siku alipokuwa anatoka kwa mzee Hondo, yalipopata moto akaanza kujichua usoni na sehemu mbalimbali zilizokuwa na majeraha.
“Nitavumilia mateso na shida zote mpaka nimpate malkia wa masokwe, sitakata tamaa,” alijisemea Harrison huku akiendelea kujichua kwenye majeraha kwa maji ya moto. ***
HARRISON, kijana mdogo aliyekuwa amebobea kwenye masomo ya tabia za wanyama na mimea, anajikuta akiangukia kwenye penzi la msichana wa ajabu ndani ya msitu mkubwa wa Tongass. Msichana huyo mwenye tabia kama masokwe, anamchanganya Harrison kiasi cha kutojali watu watamuonaje au watasemaje, anachotaka ni mapenzi tu kutoka kwake.
Malkia wa masokwe anamfanya Harrison amkatae mchumba wake, Linda kanisani muda mfupi kabla ya ndoa yao kufungwa. Anatoroka kanisani kwa kutumia pikipiki kubwa na kuwaacha watu wakiwa hawaamini kilichotokea. Kwa msaada wa rafiki yake wa siku nyingi, wanaandaa mpango maalum wa kuwafanya watu waamini kuwa Harrison amekufa. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Wanatengeneza ajali feki inayowafanya watu waamini kuwa amegongwa na gari wakati akiendesha pikipiki na kutumbukia baharini kwenye Daraja la Miami nchini Marekani. Kila mtu anaamini kuwa ni kweli kijana huyo msomi amekufa, wanaomboleza kisha wanaenda kuuzika mwili ambao kila mmoja alikuwa anaamini kuwa ni wa Harrison.
Baada ya hapo anatorokea porini ambako anaendelea na kazi yake ya kumtafuta malkia wa masokwe. Taratibu anaanza kujenga mazoea naye kiasi cha kufikia hatua ya malkia wa masokwe kuwatoroka masokwe na kumfuata Harrison kwenye kibanda chake.
Harrison naye anazidi kupandwa na hisia kali za mapenzi na kujikuta akitamani kuvunja amri ya sita na msichana huyo. Ghafla masokwe wanakivamia kibanda chake na kumchukua malkia wao huku wengine wakimtembezea Harrison kichapo. HARRISON aliendelea kujiuguza majeraha yake kwa siku tatu mfululizo, hatimaye akapona ingawa alibaki na makovu sehemu mbalimbali za mwili wake. Kwa siku zote hizo, malkia wa masokwe hakumtembelea tena mpaka akaanza kuwa na wasiwasi. “Au wale masokwe walimdhuru siku ile?” Harrison aliwaza akiwa amekaa nje ya kibanda chake, akajiapiza kuwa siku inayofuata ataamka mapema na kufuatilia nini kilichomtokea malkia wa masokwe kwani haikuwa kawaida yake. Akiwa anaendelea kuwaza, alisikia vishindo vya mtu vikitokea vichakani, alipotazama vizuri aligundua kuwa ni malkia wa masokwe. Tofauti na siku zote, safari hii alionekana kuwa mnyonge sana. Muda wote alikuwa ameinamisha kichwa chake chini huku mwili wake ukiwa umedhoofika. “Amepatwa na nini?” alisema huku akimsogelea kwa tahadhari. Malkia wa masokwe alisimama pembeni ya mti na kuuegamia, alionesha kuishiwa nguvu. Harakaharaka Harrison alimsogelea, akagundua kuwa alikuwa ametokwa vidonda vingi mdomoni kuashiria kwamba alikuwa anaumwa. “Mungu wangu, nitafanya nini kumsaidia?” aliwaza Harrison huku akijaribu kukumbuka dawa aliyopewa na mzee Hondo siku aliyokuwa anaumwa. Hakukumbuka hata kidogo, akapata wazo kichwani mwake ingawa aligundua kuwa kuna ugumu. Alipata wazo la kumpeleka malkia wa masokwe nyumbani kwa mzee Hondo ili akatibiwe kwani kwa jinsi ilivyoonesha, hali yake ilikuwa mbaya sana. Akawa anajiuliza atawezaje kuondoka naye, isitoshe tayari muda ulikuwa umekwenda sana. Bila kupoteza muda alifunga mlango wa kibanda chake na kumshika mkono malkia wa masokwe. Wakaondoka na kuianza safari ya kuelekea nyumbani kwa mzee Hondo. Harrison hakujali umbali uliokuwepo na kwamba muda ulishaenda sana, kitu pekee alichokuwa anakiwaza kwa wakati ule ilikuwa ni kuhakikisha malkia wa masokwe anapona. Walitembea vichakani kwa muda mrefu, jua likaanza kuzama wakiwa bado ndani ya msitu huo. Mwendo wao ulikuwa wa taratibu sana kwani malkia wa masokwe hakuwa na nguvu kabisa, wakaendelea na safari yao kwa muda mrefu. Jua lilipoanza kuzama, malkia wa masokwe alishindwa kuendelea kutembea, akawa anatetemeka mwili mzima huku akitaka kujitoa kutoka kwenye mkono wa Harrison. Harrison alimuachia, akainama na kumuoneshea ishara kuwa apande mgongoni. Malkia wa masokwe alipanda kwenye mgongo wa Harrison huku akiendelea kutetemeka, akambeba na safari ikaendelea. Japokuwa alikuwa mzito, Harrison alijikaza, akawa anatembea harakaharaka huku jasho likimtoka. Safari iliendelea kwa muda mrefu, giza likaanza kuingia wakiwa bado ndani ya msitu wa Tongass. Ilifika muda Harrison akawa amechoka sana, akatafuta sehemu ya kupumzika, akamshusha malkia wa masokwe na kumkalisha chini. Baada ya kupumzika vya kutosha, akambeba tena na safari ikaendelea. Kutokana na jinsi alivyokuwa anaumwa, malkia wa masokwe alipitiwa na usingizi akiwa mgongoni mwa Harrison, safari ikaendelea. Baada ya kutembea umbali mrefu, ikiwa ni tayari usiku sana, hatimaye Harrison alifika nyumbani kwa mzee Hondo. Akamshusha malkia wa masokwe na kumlaza chini, akaanza kugonga mlango wa nyumba ya mzee huyo mwindaji. Aligonga kwa muda mrefu bila kuitikiwa, baadaye akasikia mtu akitembea kwa kunyata kusogelea mlango. Akachungulia nje kisha ndiyo akafungua mlango. Hiyo ndiyo ilikuwa kawaida ya mzee huyo ambaye muda mwingi alikuwa akijihami. Alipofungua mlango alikutana na Harrison aliyekuwa ameloa jasho mwili mzima. “Vipi? Mbona umekuja usiku namna hii halafu unatokwa na jasho jingi? Unaumwa?” aliuliza mzee Hondo kwa mshangao kwani Harrison hakuwa katika hali ya kawaida. Hakumjibu kitu badala yake alimuoneshea mahali alipokuwa amelala malkia wa masokwe. Mzee Hondo alirudi ndani na kuwasha taa yake ya karabai, akatoka nje na kumulika pale malkia wa masokwe alipokuwa amelala. “Huyu ni nani?” “Ndiyo msichana niliyekuwa nakwambia siku zote.” “Amepatwa na nini? Mbona mwili wake umechemka hivi?” alihoji mzee Hondo huku akimgusa kwenye paji la uso. Ilibidi Harrison amuelezee kila kitu. Wakasaidiana kumbeba na kumuingiza ndani, akaenda kulazwa kwenye kitanda cha kamba akiwa hajitambui. Bila kupoteza muda, mzee Hondo aliwasha moto wa kuni na kubandika chungu kikubwa, akatoka nje na kumwambia Harrison aendelee kuchochea moto. Japokuwa ilikuwa ni usiku sana, baada ya dakika kadhaa mzee Hondo alirudi akiwa na furushi la majani ya porini na mizizi. Akachambua harakaharaka na kuweka kwenye chungu cha maji ambacho sasa kilikuwa kinachemka. Waliendelea kusaidiana kuchochea moto mpaka dawa ikachemka. Wakasaidiana kuanza kumnywesha dawa huku nyingine wakimchua nayo mwili mzima. Kwa kadiri walivyokuwa wanamnywesha na kumkanda mwili mzima ndivyo hali yake ilivyokuwa inabadilika. Baada ya mwili wake kukolea dawa, alianza kupiga chafya mfululizo kisha akafumbua macho. Alianza kuangaza macho huku na kule kama anayejiuliza pale ni wapi, Harrison akamsogelea na kuanza kumpapasa shingoni kwa upole huku mzee Hondo akiendelea na kazi ya kumkanda. “Kijana halali yako kusota porini kwa ajili ya huyu msichana, sijawahi kuona mwanamke mwenye sura nzuri kama huyu, tena anaonekana bado mbichi kabisa,” alisema mzee Hondo, Harrison akacheka kwa furaha. Baada ya mzee Hondo kuridhika na hali yake, aliacha kumkanda, wakakaa pembeni ya kitanda chake na kuanza kumtazama. “Na wewe mbona una makovu mengi? Nini kilikupata?” “Mh! Yaani we acha tu mzee wangu, nilishambuliwa na kundi la masokwe kwa sababu ya huyu mrembo,” alisema Harrison, kauli iliyomfanya mzee Hondo avunjike mbavu kwa kicheko. Wakiwa wanaendelea na mazungumzo ya hapa na pale, walianza kusikia kelele kubwa nje huku matawi ya miti yakivunjikavunjika. “Mungu wangu, tumekwisha,” alisema Harrison kwa hofu huku akijificha nyuma ya mzee Hondo. “Kwani vipi?” “Masokwe wamemfuata malkia wao.” “Sasa wamejuaje kuwa umemleta huku wakati ni usiku?” “Wana tabia ya kunusa, wamegundua kuwa nimemleta huku kwa kufuatisha harufu ya njia niliyopita naye.” “Basi tulia, mimi ndiyo mzee Hondo, nitahakikisha hawatusababishii madhara yoyote,” alisema mzee Hondo, akaingia chumba cha pili na kukusanya zana zake za kuwindia. Akatoka na kumwambia Harrison amfuate, wakafungua mlango na kutoka nje. “Mungu wangu, mbona wengi hivi?” alisema mzee Hondo kwani awali alidhani ni masokwe wachache ndiyo waliokuja lakini haikuwa hivyo. Ikabidi warudi ndani haraka kujipanga upya, Harrison akawa anatetemeka kwa hofu huku mara kwa mara akigeuka na kumuangalia malkia wa masokwe aliyekuwa ametulia kitandani. “Hapa inabidi niwaite mbwa wangu wa kuwindia watusaidie kazi,” alisema mzee Hondo, akaanza kupiga miluzi kwa nguvu. Baada ya sekunde kadhaa, kundi la mbwa wapatao kumi lilikusanyika mbele ya nyumba ya mzee Hondo. Akatoka na kuwaelekeza mbwa wawafukuze masokwe waliokuwa wanazidi kuongezeka. Mbwa wakaanza kubweka kwa sauti kubwa huku wakikimbilia mahali kundi lile la masokwe lilipokuwa. ***
PENZI la Harrison kwa malkia wa masokwe linazidi kuchanua kila uchao. Kijana huyo aliyekuwa amebobea kwenye masomo ya tabia za wanyama na mimea, kwa mara ya kwanza alimuona malkia wa masokwe wakati akifanya utafiti kwenye msitu huo na kujikuta akiangukia kwenye penzi la msichana wa ajabu.
Kikwazo kikubwa ni kwamba msichana huyo, licha ya uzuri wa asili aliojaaliwa, alikuwa na tabia kama za masokwe. Hakuwa akijua kuzungumza kama binadamu wengine wala kufanya chochote, alishazoea kuishi kama masokwe.
Msichana huyo anamfanya Harrison amkatae mchumba wake, Linda kanisani muda mfupi kabla ya ndoa yao kufungwa. Anatoroka kanisani kwa kutumia pikipiki kubwa na kuwaacha watu wakiwa hawaamini kilichotokea. Kwa msaada wa rafiki yake wa siku nyingi, wanaandaa mpango maalum wa kuwafanya watu waamini kuwa Harrison amekufa.
Wanatengeneza ajali feki inayowafanya watu waamini kuwa amegongwa na gari wakati akiendesha pikipiki na kutumbukia baharini kwenye Daraja la Miami nchini Marekani. Kila mtu anaamini kuwa ni kweli kijana huyo msomi amekufa, wanaomboleza kisha wanaenda kuuzika mwili ambao kila mmoja alikuwa anaamini kuwa ni wa Harrison.
Baada ya hapo anatorokea porini ambako anaendelea na kazi yake ya kumtafuta malkia wa masokwe. Taratibu anaanza kujenga mazoea naye kiasi cha kufikia hatua ya msichana huyo kuwatoroka masokwe na kumfuata Harrison kwenye kibanda chake.
Mazoea yanaongezeka kila uchao, siku moja malkia wa masokwe anamfuata Harrison lakini anaonesha kutokuwa sawa kiafya, mwili wake umechemka na anatetemeka sana. Harrison anaondoka naye hadi nyumbani kwa mzee Hondo anakoanza kupatiwa tiba. Wakiwa wanaendelea, kundi la masokwe linavamia nyumba ya mzee Hondo.
VITA kali kati ya kundi kubwa la masokwe na mbwa wa mzee Hondo iliendelea kwa dakika kadhaa, eneo lote likachafuka na kugeuka kuwa uwanja wa vita. Harrison ambaye alikuwa akizifahamu vyema vurumai za masokwe, alikuwa akitetemeka kwani alijua baada ya muda, masokwe watahamia kwao. Kwa kuwa masokwe walikuwa wengi na wakubwa, waliwashinda mbwa wa mzee Hondo, wakawa wanawarushia mawe makubwa na kuwapiga kwa magongo yaliyowajeruhi vibaya mpaka wote wakakimbia na kutokomea gizani. “Mungu wangu, tumekwisha.” “Hapa hatuna cha kufanya zaidi ya kuanza kuwaua, tukichelewa watatuua sisi,” alisema mzee Hondo huku akiziweka vizuri silaha zake za kuwindia. “Hapana, tusimuue sokwe hata mmoja, tutaanzisha vita kali kwani hawatakubali kuona mwenzao ameuawa.” “Sasa tutafanya nini? Tusipojihami watatuua kweli.” “Mi nashauri tumtoe malkia wa masokwe mimi nitakimbia naye.” “Huwezi kutoka naye, unafikiri utapita wapi wakati wameshatuzunguka,” alisema mzee Hondo huku akimshika mkono Harrison na kumvutia nyuma ya nyumba, kufumba na kufumbua nyumba yote ikavamiwa, masokwe wakavunja milango na kuingia hadi ndani walikomkuta malkia wao amelala kwenye kitanda cha kamba. Malkia wa masokwe alishtuka kuona masokwe wamemfuata, akaamua kuwa mpole kwani alikuwa anajua endapo atapingana nao, watasababisha maafa makubwa. Japokuwa alikuwa bado hajapona, alikubali kuondoka, masokwe wakambeba juu kwa juu na kuanza kutimua naye mbio kurudi msituni. Harrison alishindwa kujizuia, akawa anamwaga machozi kwa uchungu kama mtu aliyepewa taarifa za msiba. “Bado una nafasi ya kumpata, ukipata tena nafasi toroka naye mpaka mjini, huko hawawezi kukufuata,” alisema mzee Hondo huku akimpigapiga Harrison mgongoni kama ishara ya kumbembeleza. Kwa kuwa ilikuwa ni usiku sana, ilibidi Harrison alale palepale kwa mzee Hondo mpaka kulipopambazuka. Mzee Hondo akamfungashia furushi la dawa za mitishamba kwa ajili ya kuendelea kumtibu malkia wa masokwe endapo atakutana naye. Akaianza safari ya kurudi kwenye msitu wa Tongass akiwa na furushi lake la dawa. Alitembea kwa unyonge kwani kwa mara nyingine masokwe walimvunja nguvu na kufanikiwa kumchukua malkia wao mikononi mwake. ***CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Upande wa pili, msichana Linda bado alikuwa na kidonda ndani ya moyo wake ambacho bado kilikuwa hakijapona. Kukimbiwa na Harrison wakiwa kanisani kabla ya kufa katika mazingira ya kutatanisha kama kila mtu alivyokuwa anaamini, kulimfanya muda wote awe kama mgonjwa. Afya yake ikawa inazorota siku hadi siku huku muda mwingi akionesha kuwa na huzuni. Licha ya utajiri wa wazazi wake, bado hawakufanikiwa kumrejeshea furaha yake, baba yake akishirikiana na mama yake walifanya kila linalowezekana kumfurahisha lakini hawakufanikiwa. “Mbona umejiinamia Linda? Una tatizo?” “Roho inaniuma sana baba, bado sijamsahau Harrison.” “Najua namna unavyojisikia Linda lakini huna budi kukubaliana na ukweli, ukiwaza sana mwisho utakufuru.” “Hapana baba, nampenda sana Harrison mpaka inafika muda na mimi natamani bora nife ili nikaungane naye ahera.” “Usifikie huko mwanangu, bila shaka ipo siku utampata mwanaume mwingine atakayekusahaulisha machungu yote.” “Lakini baba mimi bado nina wasiwasi mkubwa sana, huenda Harrison aliuawa na watu waliochukia mimi kutaka kuolewa naye. Nahisi lazima kuna hujuma zilifanyika.” “Mh! Kwa nini unahisi hivyo mwanangu? Si ilikuwa ni ajali kama zilivyo ajali nyingine?” “Roho inaniambia hivyo kwa sababu ya jinsi matukio yalivyoongozana. Najua Harrison alikuwa ananipenda lakini pale aliponikataa kanisani inawezekana kuna kitu kilikuwa nyuma ya pazia. Kwanza alikuja kanisani akiwa amechelewa na inaonesha ni kama alikuwa anafukuzwa na watu.” “Yote yanawezekana mwanangu lakini hata ukifuatilia sasa hivi haitakuwa na maana tena.” “Hapana baba, lazima nifuatilie ili nijue ni akina nani wapo nyuma ya tukio la kumpoteza kipenzi changu niliyekuwa nampenda kuliko kitu chochote chini ya jua,” Linda na baba yake, mzee Ford walikuwa wakizungumza nje kwenye bustani ya maua. Baada ya mazungumzo yale, Linda aliinuka na kwenda chumbani kwake, akajiandaa na baada ya muda akatoka na kuchukua gari lake. Hakumuaga mtu na hata baba yake alipomuuliza mahali alikokuwa anakwenda, Linda alijibu kwa kifupi kwamba anatoka mara moja. Aliendesha gari mpaka eneo Harrison alipopata ajali na kufa kama watu wote walivyokuwa wanaamini. Taratibu Linda aliteremka kwenye gari na kutembea kwa hatua fupifupi mpaka eneo lile. Alikuwa analikumbuka vizuri, akaanza kupatazama mahali Harrison alipopatia ajali mpaka kwenye maji alikodondokea. “Mh! Mbona kina cha maji siyo kirefu kiasi cha kusababisha mtu afe? Halafu mbona hakuna kona wala chochote kinachoweza kusababisha ajali eneo hili?” Linda alikuwa akijiuliza maswali ambayo yote hakuyapatia majibu. Alizunguka eneo lote, mwisho akaingia kwenye maji na kupima kina chake. Kilichozidi kumshangaza ni kwamba hapakuwa na kina kirefu kinachoweza kusababisha kifo cha Harrison. Hata eneo alipopatia ajali bado hapakuonesha alama zozote kwamba mtu anaweza kupata ajali mbaya kiasi kile na kufa. Kengele ya hatari ikalia kwenye kichwa chake. “Lazima kuna mchezo ulichezwa hapa, nitafanya kila linalowezekana kuufahamu ukweli, hata kama itanigharimu kiasi gani lakini lazima nihakikishe waliomuua Harrison wangu wanapatikana. ***
KWA kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele, Harrison anazidi kuzama kwenye penzi la malkia wa masokwe kiasi cha kuwa tayari kufanya lolote ilimradi ampate. Kwa mara ya kwanza, Harrison aliyekuwa amebobea kwenye masomo ya
tabia za wanyama na mimea, alimuona malkia wa masokwe wakati akifanya utafiti kwenye msitu huo na kufanikiwa kumpiga picha akiwa katikati ya kundi la masokwe, akajikuta akiangukia kwenye penzi la msichana huyo wa ajabu.
Kikwazo kikubwa ni kwamba msichana huyo, licha ya uzuri wa asili aliojaaliwa, alikuwa na tabia kama za masokwe. Hakuwa akijua kuzungumza kama binadamu wengine wala kufanya chochote, alishazoea kuishi kama masokwe. Hakuwa na tabia za kibinadamu hata kidogo.
Kutokana na penzi la msichana huyo, Harrison anamkataa mchumba wake, Linda kanisani muda mfupi kabla ya ndoa yao kufungwa. Anatoroka kwa kutumia pikipiki kubwa na kuwaacha watu wakiwa hawaamini kilichotokea. Kwa msaada wa rafiki yake wa siku nyingi, wanaandaa mpango maalum wa kuwafanya watu waamini kuwa Harrison amekufa.
Wanatengeneza ajali feki inayowafanya watu waamini kuwa amegongwa na gari wakati akiendesha pikipiki na kutumbukia baharini kwenye Daraja la Miami nchini Marekani. Baada ya hapo anatorokea porini ambako anaendelea na kazi yake ya kumtafuta malkia wa masokwe.
Purukushani kubwa zinaendelea kati yake na kundi la masokwe waliokuwa wanamlinda, hata pale malkia wa masokwe alipokuwa anaumwa, alipojaribu kumsaidia ili apone alijikuta akizusha vurugu kubwa zilizoleta maafa.
Upande wa pili, Linda bado haamini kama Harrison alikufa kifo cha kawaida na sasa anajiapiza kufanya kila linalowezekana kuujua ukweli.
BAADA ya Linda kutoka eneo la ajali, alikwenda mpaka nyumbani kwao huku akionesha kuwa na huzuni kali. Alipofika alipitiliza moja kwa moja mpaka chumbani kwake, akajifungia mlango na kuchukua ‘diary’ yake nyeusi na kuanza kuandika baadhi ya vitu muhimu. Alipomaliza alitoka nje huku bado akionesha kuwa mnyonge. “Vipi, mbona unaonekana mnyonge mwanangu kipenzi,” aliuliza mzee Ford, baba mzazi wa Linda. Alishindwa cha kumjibu, akamsogelea na kujilaza kifuani kwa baba yake huku akilengwalengwa na machozi. “Niambie mwanangu kinachokusumbua, nitakuwa tayari kukusaidia kwa lolote,” alisema mzee Ford huku akitembea taratibu akiwa amekumbatiana na mwanaye mpaka kwenye bustani ya maua, wakatafuta sehemu tulivu na kukaa, akawa anaendelea kumsisitiza amueleze kinachomsumbua. “Baba roho inaniuma sana kwa sababu nahisi kifo cha Harrison hakikuwa mpango wa Mungu bali kuna watu walifanya njama za kumuua.” “Kwa nini unaamsha vidonda ambavyo vilishapona mwanangu, hiyo ni kazi ya Mungu na tukiendelea kuzungumzia jambo moja kila siku tutakuwa tunakufuru.” “Hapana baba, lazima nifuatilie kwa njia zozote mpaka nifahamu ukweli juu ya watu waliohusika kumuua kipenzi cha roho yangu Harrison.” “Sasa unafikiri tutafanya nini mwanangu?” “Mi nataka kwenda kutoa ripoti polisi ili uchunguzi wa kina ufanyike upya.” “Hiyo itakuwa kazi ngumu mwanangu kwa sababu tayari siku nyingi zimepita tangu ajali ilipotokea. Ingekuwa umehisi hayo kipindi kilekile wakati tukio linatokea, ingekuwa rahisi sana.” “Hapana baba, hata kama hutanisaidia mi nitafanya uchunguzi mwenyewe mpaka nibaini ukweli uliyojificha nyuma ya pazia,” alisema Linda huku akiendelea kububujikwa na machozi. Baba yake alikataa kumuunga mkono kwenye hoja hiyo kwa sababu alijua hata kama akiujua ukweli kuwa kuna watu walimuua Harrison, haitakuwa na msaada wowote kwake kwani Harrison hawezi kufufuka kutoka katika wafu. Linda alirudi chumbani kwake na kujifungia, akawa anawaza mbinu anazoweza kuzitumia ili kuubaini ukweli. Akili yake ilimtuma kwenda mpaka makao makuu ya polisi, Miami na kuomba kuona ripoti ya uchunguzi uliofanywa eneo la ajali na kitengo cha Crime Scene Investigation (CSI). Siku nzima alishinda akiwa hana raha, baba na mama yake wakawa wanajitahidi kumsahaulisha na kumsihi kutoendelea na alichokuwa amekipanga lakini hakutaka kuelewa chochote. Asubuhi ya siku iliyofuatia, Linda aliwahi kuamka na kujiandaa, tayari kwa safari ya kuelekea makao makuu ya polisi. Alichagua gari dogo la kifahari aina ya Porsche na kutoka kwenye geti la nyumba yao, akawa anaendesha taratibu huku mawazo yake yote yakimtuma kuhakikisha anafanya kila linalowezekana kuufahamu ukweli juu ya kifo cha Harrison. Alipofika kwenye jengo kubwa la Makao Makuu ya Polisi, Miami, Linda alienda kueleza shida yake eneo la mapokezi ambapo alielekezwa kupanda mpaka ghorofa ya saba kwenye kitengo cha Crime Scene Investigation. *** Baada ya masokwe kufanikiwa kumkomboa malkia wao na kurudi naye porini, Harrison alishindwa kuzificha hisia zake, akawa anamwaga machozi kwa huzuni, hali iliyomfanya mzee Hondo amuonee huruma. Alimpa moyo kwamba bado anayo nafasi ya kutimiza ndoto zake kwani mpaka hapo alipofikia tayari kulikuwa na matumaini makubwa ya kutimiza alichokuwa anakitaka. Kwa shingo upande akaianza safari ya kurudi kwenye msitu wa Tongass akiwa na furushi lake la dawa pamoja na chakula cha akiba. Alitembea kwa unyonge akiwa hana raha kabisa. Baada ya kutembea kwa saa nyingi, akipanda milima na kushuka mabonde kwenye msitu mnene wa Tongass, hatimaye alifanikiwa kufika kwenye kibanda chake. Alijibwaga chini na kupumzika kwa muda wakati akikitazama kibanda chake ambacho kilikuwa kimeharibiwa na vurugu za masokwe wakati wakimsaka malkia wao. Baada ya kupumzika vya kutosha, alianza kukata miti na nyasi kwa ajili ya kurekebisha sehemu zilizokuwa zimeharibiwa. Alipomaliza kukarabati kibanda chake, aliwasha moto na kuanza kuchoma nyama aliyopewa na mzee Hondo kwani alikuwa akisikia njaa kali. Aliwasha moto mkubwa na kukaa pembeni yake huku akiimba nyimbo za mapenzi kujifariji. Baadaye alienda kujipumzisha ndani ya kibanda chake kwani alikuwa akihisi uchovu kupindukia. Alipojilaza kwenye tu, usingizi mzito ulimpitia, akawa anaota ndoto za kutisha, hali iliyomfanya awe anaweweseka sana. Alikuja kuzinduka alfajiri baada ya kuhisi kuna mtu amelala pembeni yake. Awali alihisi huenda ni mnyama mkali au nyoka mkubwa amelala pembeni yake lakini alipofumbua macho kwa tahadhari kubwa, hakuyaamini macho yake baada ya kumuona malkia wa masokwe akiwa amelala, kijasho chembamba kikiwa kinamtoka. Kwa jinsi ilivyoonekana, bado homa kali ilikuwa ikimsumbua kwani haikuwa kawaida yake kutokwa na jasho kiasi kile, tena ikiwa ndiyo kwanza kunaanza kupambazuka. Harrison aliamka haraka na kumsogelea, akawa anampima joto la mwili wake sehemu mbalimbali za mwili. Aligundua kuwa bado anaumwa. Akaamka na kuanza kuwasha moto. Kazi haikuwa nyepesi kwani kuni zote zilikuwa zimelowanishwa na umande wa usiku kucha. Baada ya kuhangaika sana, hatimaye alifanikiwa kuwasha moto, bila kupoteza muda akaanza kuchemsha dawa alizotoka nazo kwa mzee Hondo kama alivyoelekezwa. Baada ya muda, dawa tayari ilikuwa imechemka vya kutosha, akaanza kumnywesha malkia wa masokwe huku nyingine akimkanda mwili mzima. Baada ya kuendelea kumtibu kwa muda, malkia wa masokwe alianza kupiga chafya mfululizo, joto lake la mwili likaanza kushuka. Angalau alipata nguvu na sasa akawa anaweza kurukaruka, tofauti na alivyokuwa awali. Harrison akawa anamtazama kwa hisia huku akijiapiza kuwa atakapopona kabisa, lazima atoroke naye kwenda mjini. ***
PENZI la msichana wa ajabu linamchanganya kabisa Harrison, kijana msomi aliyekuwa amebobea kwenye fani ya tabia za wanyama na mimea. Tatizo ni kwamba msichana huyo, analindwa na kundi kubwa la masokwe kama malkia.
Kwa mara ya kwanza alimuona malkia wa masokwe wakati akifanya utafiti kwenye msitu huo na kufanikiwa kumpiga picha akiwa katikati ya kundi la masokwe, akaandika kitabu kilichomfanya awe maarufu nchi nzima.
Licha ya kupata fedha nyingi kupitia kitabu hicho, moyo wake unaangukia kwenye penzi la msichana huyo wa ajabu. Uzuri wa asili aliokuwa nao unamchanganya kabisa Harrison lakini kikwazo kikubwa ni kwamba msichana huyo alikuwa na tabia kama za masokwe. Licha ya yote hayo, Harrison anaweka nadhiri kuwa lazima ampate.
Penzi hilo linamfanya Harrison amkatae mchumba wake, Linda kanisani. Anatoroka kanisani kwa kutumia pikipiki kubwa na kuwaacha watu wakiwa hawaamini kilichotokea. Baada ya hapo, anashirikiana na rafiki yake wa siku nyingi kuandaa ajali feki inayofanya kila mtu aamini kuwa amekufa.
Baada ya hapo anatorokea porini ambako anaendelea na kazi yake ya kumtafuta malkia wa masokwe na taratibu ndoto zake zinaanza kuelekea kutimia. Upande wa pili, Linda bado haamini kama Harrison alikufa kifo cha kawaida na sasa anajiapiza kufanya kila linalowezekana kuujua ukweli. Anajaribu kumweleza baba yake hisia zake lakini anakatishwa tamaa. Anaamua kuutafuta ukweli mwenyewe.
ALIPOFIKA kwenye jengo kubwa la Makao Makuu ya Polisi, Miami, Linda alienda kueleza shida yake eneo la mapokezi ambapo alielekezwa kupanda mpaka ghorofa ya saba kwenye kitengo cha Crime Scene Investigation.
“Karibu binti, unaitwa nani na nikusaidie nini?” mzee wa makamo aliyekuwa amekaa kwenye kiti cha kuzunguka, nyuma ya meza kubwa iliyokuwa na kibao kilichosomeka ‘CSI Executive Director’, alimuuliza Linda kwa ukarimu huku akimuonesha sehemu ya kukaa.
“Ahsante, naitwa Linda Ford, nina shida binafsi tafadhali,” alisema huku akikaa kwenye kiti alichoelekezwa. Bila kupoteza muda, Linda alianza kueleza kilichompeleka pale. Alieleza jinsi mazingira ya kifo cha Harrison yalivyokuwa na yote yaliyofuatia baada ya hapo, mwisho akamalizia kwa kueleza wasiwasi wake juu ya kile alichokihisi kama hujuma. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Tukio lilitokea tarehe ngapi?” alihoji yule mzee wa makamo ambaye baadaye Linda aligundua kuwa anaitwa Daniels Wilshere. Linda alitoa kitabu chake cha kumbukumbu na kuanza kukipekua kutafuta tarehe ya siku Harrison aliyoaga dunia. Akamtajia ambapo bila kupoteza muda alinyanyua mkonga wa simu na kutoa maelekezo upande wa pili.
Dakika chache baadaye, msichana wa umri wa kati aliingia akiwa na faili mkononi, akamsabahi Linda na kuliweka faili mezani. Daniels alilifungua na kuanza kukagua ukurasa mmoja mpaka mwingine kisha akateremsha miwani yake na kumtazama Linda.
“Nasikitika kukwambia kuwa jalada la tukio hilo lilishafungwa kwani inaonesha ni ajali ya kawaida hivyo sina cha kukusaidia. Ungewahi kipindi kile kazi ingekuwa rahisi lakini umechelewa sana.”
“Kwani kinachoshindikana na nini mzee wangu? Mi naomba niiangalie tu hiyo ripoti ya ajali, kuanzia mchoro wa ajali yenyewe, vitu vilivyookotwa eneo la tukio na taarifa nyingine muhimu.”
“Binti, hii kazi haiendeshwi kienyeji kama unavyofikiria, kuna taratibu za kisheria na kimaadili ambazo lazima zifuatwe. Nasikitika kukwambia kuwa sitaweza kukusaidia,” alisema Daniels na kunyanyua mkonga wa simu ya mezani, akazungumza na upande wa pili ambapo sekunde chache baadaye yule msichana aliyelileta faili lile aliingia na kukabidhiwa, akalirudisha alikolitoa.
Kwa unyonge Linda alisimama na kuaga, akatoka nje ya ofisi huku kichwa chake akiwa amekiinamisha chini. Alitoka mpaka nje alipokuwa ameegesha gari lake la kifahari aina ya Porsche na kuingia ndani yake, akaliondoa taratibu huku kichwani akiwa na mawazo lukuki.
Aliongoza moja kwa moja mpaka nyumbani kwao, akaegesha gari sehemu yake na kwenda mpaka chumbani kwake, akajifungia na kuanza kulia kwa uchungu. Aliona kama anaonewa kwa kukataliwa alichokuwa anakitaka.
“Nimepata wazo jipya, alisema Linda huku akiinuka haraka kitandani, akajifuta machozi na kutoka mpaka nje, akaenda kwenye bustani za maua alikomkuta baba yake anajisomea gazeti la The Daily Mail, akakaa pembeni yake na kumuomba kuzungumza naye jambo.
“Nataka kwenda kusoma.” “Mh! Kwa nini usifanye kazi kwanza japo mwaka mmoja ndiyo uende kujiendeleza? Umehitimu shahada yako ya kwanza juzijuzi tu.” “Hapana baba, nataka kwenda kusoma, tena haraka iwezekanavyo.” “Sawa mwanangu, nilishaahidi kuwa pamoja na wewe kwa kila kitu. Unataka kwenda kusomea nini?”
“Nataka kwenda kusomea kozi ya upelelezi ya Crime Scene Investigation (CSI).” “Lakini si lazima kwanza upitie jeshini ndiyo ukasomee kozi hiyo? Unataka kuwa mpelelezi?” “Siyo lazima kupitia jeshini baba, siku hizi sheria zimebadilishwa, mbona kuna wenzangu niliokuwa nasoma nao sekondari wameenda kusomea bila kupitia jeshini?”
“Kwani lengo lako hasa la kutaka kusomea Crime Scene Investigation ni nini?” “Nimeamua tu baba, naomba uniunge mkono tafadhali,” alisema Linda huku akijilaza kwenye kifua cha baba yake, mzee Ford akashusha pumzi ndefu na kumtazama mwanaye. Alishajua kilichokuwa kinamsumbua ndani ya moyo wake, penzi la Harrison lilikuwa limeacha kidonda ambacho kisingeweza kupona kirahisi, ikabidi akubaliane naye. *** Baada ya kuhakikisha malkia wa masokwe anaendelea vizuri, Harrison alimuoneshea ishara akimtaka arudi kwa masokwe kabla hawajafika na kuanza kuleta vurugu eneo lile. Malkia wa masokwe hakuwa mwepesi kuondoka, muda wote akawa anataka kukaa jirani na Harrison huku akijilazimisha kukimbia huku na kule na kurukia matawi ya miti.
Tofauti na siku zote, walikaa naye kwa muda mrefu bila kundi la masokwe kumfuata malkia wao, jua lilipokuwa kali, kelele za matawi ya miti kuvunjika na milio ya ajabu ikaanza kusikika. Malkia wa masokwe alipowaona masokwe, hakutaka wamdhuru Harrison, akawakimbilia na kuwazuia kabla hawajakifikia kibanda chake, wakageuza naye na kuanza kurudi walikotoka kwa kasi kubwa.
Harrison aliwasindikiza kwa macho mpaka walipopotea kwenye upeo wa macho yake. Akashusha pumzi ndefu na kukaa chini, mawazo mengi yakawa yanapita kwenye kichwa chake. Akiwa katika hali ile, alikumbuka jambo, harakaharaka akarudi ndani ya kibanda chake na kuanza kupekua kwenye mifuko ya bukta aliyokuwa ameivaa kwa ndani siku alipowasili kwenye msitu huo.
“Whaooo, safi sana,” alisema Harrison kwa furaha baada ya kufanikiwa kuipata kadi yake ya ATM ya Benki ya Barclays. Alikuwa na akaunti kwenye benki hiyo ambayo ilikuwa na fedha zake nyingi alizozipata baada ya kuchapisha na kuuza kitabu cha Queen of Gorillas kilichomfanya awe maarufu sana nchini Marekani na kwingineko.
Aliamini utajiri wake mkubwa bado haujaguswa na mtu yeyote licha ya watu wote kuamini kuwa tayari amekufa. Aliitazama kadi ile ya ATM vizuri, akagundua kuwa haikuwa na tatizo lolote.
“Nitaishi na malkia wa masokwe sehemu yoyote, hakuna kinachoweza kunishinda mbele ya fedha,” alisema Harrison huku akiibusu kadi ile, akaihifadhi sehemu salama na kuendelea kusubiri apate nafasi ya kutoroka na malkia wa masokwe. Muda ulizidi kuyoyoma kwa kasi, hatimaye giza likaanza kuingia. Kama kawaida, Harrison akawasha moto na kuanza kuchoma nyama aliyopewa na mzee Hondo ambayo bado alikuwa nayo ya kutosha. ***
HARRISON bado analihangaikia penzi la malkia wa masokwe. Msichana huyo wa ajabu aliyekuwa anaishi na kulindwa na masokwe kama malkia wao, anamchanganya kabisa Harrison kiasi cha kumfanya awe tayari kufanya lolote ili mradi ampate na kuishi naye kama mkewe.
Kwa mara ya kwanza, Harrison aliyekuwa amebobea kwenye fani ya uchunguzi wa tabia za wanyama na viumbe wengine, alimuona malkia wa masokwe wakati akifanya utafiti kwenye msitu huo na kufanikiwa kumpiga picha akiwa katikati ya kundi la masokwe, akaandika kitabu kilichomfanya awe maarufu nchi nzima.
Licha ya kupata fedha nyingi kupitia kitabu hicho, moyo wake unaangukia kwenye penzi la msichana huyo wa ajabu. Uzuri wa asili aliokuwa nao unamchanganya kabisa Harrison lakini kikwazo kikubwa ni kwamba msichana huyo alikuwa na tabia kama za masokwe. Licha ya yote hayo, Harrison anaweka nadhiri kuwa lazima ampate.
Penzi hilo linamfanya Harrison amkatae mchumba wake, Linda kanisani. Anatoroka kanisani kwa kutumia pikipiki kubwa na kuwaacha watu wakiwa hawaamini kilichotokea. Baada ya hapo, anashirikiana na rafiki yake wa siku nyingi kuandaa ajali feki inayofanya kila mtu aamini kuwa amekufa.
Baada ya hapo anatorokea porini ambako anaendelea na kazi yake ya kumtafuta malkia wa masokwe na taratibu ndoto zake zinaanza kuelekea kutimia. Upande wa pili, Linda bado haamini kama Harrison alikufa kifo cha kawaida, anaanza kufuatilia kwa kina kutaka kuujua ukweli. Anapoona hakuna anayemjali, anaamua kwenda kusomea upelelezi ili aifanye kazi ile yeye mwenyewe.
BAADA ya kukaa pembeni ya moto kwa muda mrefu, Harrison alianza kusikia usingizi, akakusanya vitu vyake vyote na kujikongoja mpaka ndani ya kibanda chake, akajitupa kwenye kitanda cha miti na usingizi ukampitia. Akawa anakoroma kutokana na uchovu wa siku nzima. Alikuja kuzinduka alfajiri baada ya kuanza kusikia milio ya ndege waliokuwa wanarukaruka kwenye matawi ya miti kushangilia mwanzo wa siku mpya. Aliamka na kujinyoosha, akatoka nje na kuanza kufanya mazoezi mepesimepesi. Akiwa anaendelea kukimbiakimbia, alisikia vishindo vikitokea kichakani. Bila hata kuuliza alijua ni malkia wa masokwe, akajikuta akitabasamu. Malkia wa masokwe ambaye sasa alikuwa ameshapona vizuri, alipomuona Harrison, naye aliachia tabasamu pana, akawa anakimbia na kurukia kwenye matawi ya miti kwa furaha. “Leo silazi damu, lazima niondoke naye asubuhi hiihii, mengine nitajua mbele kwa mbele,” alisema Harrison na kurudi ndani ya kibanda chake. Akakusanya kila kitu chake na kuweka vizuri kibanda chake, akapiga magoti na kusali sala fupi akimuomba Mungu wake aifanikishe safari ya kumtorosha malkia wa masokwe kutoka ndani ya Msitu wa Tongass. Alipomaliza alisimama na kutoka nje, akamkuta malkia wa masokwe akiwa bado anachezacheza kwenye matawi ya miti. Alimsogelea kwa upole kisha akamshika mkono. Malkia wa masokwe hakuwa mbishi, akaanza kumfuata, Harrison akawa anampitisha katikati ya vichaka, kuelekea upande tofauti na ule ambao kundi la masokwe hupenda kufika. Alijikagua mifukoni mwake na kuhakikisha kadi yake ya benki ipo mahali pake, safari ikaendelea huku njia nzima malkia wa masokwe akiendelea na michezo ya hapa na pale, akiwa ameshikwa na Harrison. Baada ya kutembea kwa umbali mrefu, Harrison alitafuta mti wenye kivuli kizuri, akakaa chini na malkia wa masokwe na kupumzika. Alikuwa anatamani sana kumweleza nini alichokuwa amekipanga lakini kwa kuwa hakuwa akielewa lugha yoyote ya kibinadamu, ilibidi aendelee kunyamaza. Baada ya kupumzika, safari ikaendelea, wakawa wanakatiza kwenye vichaka vilivyoshonana, wakapanda milima na kushuka mabonde mpaka walipofika eneo lililokuwa na hali ya hewa tofauti na kule walikotoka. Waliingia kwenye ukanda wa baridi ambapo anga lote lilikuwa limetawaliwa na ukungu huku vilele vya milima na miti mirefu vikiwa vimefunikwa na theluji. Bado hakutaka kumuachia malkia wa masokwe, wakaendelea kutembea kwa umbali mrefu mpaka giza likaanza kuingia. Kwa kuhofia kuwa huenda kundi la masokwe likawa linawafuata kwa nyuma kwa lengo la kumkomboa malkia wao, Harrison hakutaka kupumzika, safari ikaendelea usiku kwenye eneo lenye baridi kali. Baada ya kutembea kwa umbali mrefu, malkia wa masokwe alianza kutetemeka kutokana na baridi kali aliyokuwa anaihisi. Ilibidi Harrison avue shati lake na kumvalisha, yeye akabaki kifua wazi. Safari ikaendelea. Ilipofika usiku wa manane, hali ya hewa ilizidi kuwa mbaya zaidi, theluji ikawa inadondoka kwa wingi kutoka angani, hali iliyofanya Harisson atafute sehemu ya kujihifadhi na malkia wa masokwe. Kutokana na uchovu waliokuwa nao baada ya kutembea umbali mrefu, walipopata sehemu kavu ya kupumzika, malkia wa masokwe alikuwa wa kwanza kulala. Kwa tahadhari, Harrison alimfunga kamba malkia wa masokwe mkononi kisha akajifunga na yeye mkononi. Alifanya vile ili hata kama malkia wa masokwe ataamka kabla yake, asimkimbie. Wakalala mpaka alfajiri, Harrison akawa wa kwanza kuamka ambapo alianza kumtingisha malkia wa masokwe ambaye bado alikuwa ameuchapa usingizi. Baada ya kuamka, safari iliendelea huku Harrison akiwa hajui hata upande anaoelekea. Alichoamini ni kwamba lazima msitu ule mkubwa ulikuwa na mwisho, hivyo kitu pekee alichokuwa anataka ni kutoka na malkia wa masokwe nje ya msitu, bila kujali watatokea upande gani. Walitembea kwa umbali mrefu, wakavuka eneo lile lenye theluji na kuingia kwenye eneo lililokuwa na miti mifupimifupi iliyoachana. “Lazima huku kutakuwa ndiyo mwisho wa msitu, mbona hakuna tena miti mirefu!” alijisemea Harrison huku akizidi kukaza mwendo. Kwa muda huo, malkia wa masokwe hakuwa akiendelea na michezo yake tena kutokana na uchovu aliokuwa anauhisi. Mara kwa mara alikuwa akitaka kupumzika lakini Harrison hakumpa nafasi.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Baada ya kutembea mchana kutwa, njaa na kiu vikiwa vimewabana kisawasawa, Harrison aliamua wapumzike. Kwa bahati nzuri, kulikuwa na chemchemi ya maji jirani na mahali walipopumzika, wakanywa maji na mengine kujimwagia kwenye miili yao ili kupunguza uchovu. Wakapumzika kwa dakika kadhaa kisha safari ikaendelea. Giza lilipoanza kuingia, malkia wa masokwe alianza kusumbua akitaka wapumzike palepale, jambo ambalo Harrison hakukubaliana nalo. Ikabidi ambebe mgongoni na safari ikaendelea. Uchovu wa kutembea umbali mrefu ukichanganya na uzito wa kumbeba malkia wa masokwe mgongoni ulimchosha Harrison lakini akapiga moyo konde. Baada ya kutembea kwa umbali mrefu, Harrison alitafuta sehemu ya kupumzika, akamshusha malkia wa masokwe ambaye tayari alishapitiwa na usingizi, akamlaza chini vizuri kisha akawa anajinyoosha mwili ili kupunguza uchovu. Akiwa anajinyoosha, aliona kitu kilichomfanya afikiche macho yake mara mbili akiwa haamini kama ni kweli. Kwa mbali alianza kuona mwanga wa taa za umeme, kuashiria kuwa tayari walikuwa wameukaribia mji, ingawa hakujua ni mji gani. “Ooh! Ahsante Mungu wangu,” alisema Harrison huku akiinua mikono juu kama ishara ya shukrani. Alitamani kuendelea na safari usiku huohuo lakini miguu ilikuwa ikimuuma sana, akaendelea kuangalia upande ule uliokuwa na mji kwa muda mrefu mpaka baadaye alipozidiwa na uchovu. Akarudi pale alipomuacha malkia wa masokwe, akalala pembeni yake huku akiwa na matumaini makubwa ya kuufikia mji ule siku inayofuata. Hata usingizi wake ulikuwa wa mang’amung’amu, akawa anashtuka mara kwa mara kabla hata hakujapambazuka. Alfajiri na mapema, aliwahi kuamka na kumuamsha malkia wa masokwe, wakaendelea na safari kuelekea upande ule uliokuwa na mji. Saa nane mchana, wakawa wametokezea mahali kwenye mji mdogo. “Hapa ni wapi?” Harrison alimuuliza kijana mdogo aliyekuwa anachunga kondoo pembeni kidogo ya mji. “Petersburg, Canada,” alijibu yule kijana huku akimkodolea macho malkia wa masokwe. ***
MVUMILIVU hula mbivu, walinena wahenga. Harrison bado anaendelea kulihangaikia penzi la msichana wa ajabu aliyekuwa anaishi na kulindwa na masokwe kama malkia wao. Harrison anachanganyikiwa kabisa kiasi cha kumfanya awe tayari kwa lolote ili mradi ampate na kuishi naye kama mkewe.
Kwa mara ya kwanza, Harrison aliyekuwa amebobea kwenye fani ya uchunguzi wa tabia za wanyama na viumbe wengine, alimuona malkia wa masokwe wakati akifanya utafiti kwenye msitu huo na kufanikiwa kumpiga picha akiwa katikati ya kundi la masokwe, akaandika kitabu kilichomfanya awe maarufu nchi nzima.
Licha ya kupata fedha nyingi kupitia kitabu hicho, moyo wake unaangukia kwenye penzi la msichana huyo wa ajabu. Uzuri wa asili aliokuwa nao unamchanganya kabisa Harrison lakini kikwazo kikubwa ni kwamba msichana huyo alikuwa na tabia kama za masokwe. Licha ya yote hayo, Harrison anaweka nadhiri kuwa lazima ampate.
Penzi hilo linamfanya Harrison amkatae mchumba wake, Linda kanisani. Anatoroka kanisani kwa kutumia pikipiki kubwa na kuwaacha watu wakiwa hawaamini kilichotokea. Baada ya hapo, anashirikiana na rafiki yake wa siku nyingi kuandaa ajali feki inayofanya kila mtu aamini kuwa amekufa. Baada ya hapo anatorokea porini ambako anaendelea na kazi yake ya kumtafuta malkia wa masokwe.
Baada ya kuhangaika kwa kipindi kirefu, hatimaye anafanikiwa kutoroka na malkia wa masokwe na kutokezea upande wa pili wa msitu huo, kwenye mji mdogo wa Petersburg nchini Canada. Upande wa pili, Linda bado haamini kama Harrison alikufa kifo cha kawaida, anaanza kufuatilia kwa kina kutaka kuujua ukweli.
“HAPA ni wapi?” Harrison alimuuliza kijana mdogo aliyekuwa anachunga kondoo pembeni kidogo ya mji. “Petersburg, Canada,” alijibu yule kijana huku akimkodolea macho malkia wa masokwe. “Hapa kuna benki jirani?” “Hapana, hakuna benki hapa mpaka Abbotsford.” “Kuna umbali gani kutoka hapa?” “Ni mbali lakini kuna treni za umeme. Kituo kipo pale mbele, nyoosha na hii barabara, mpaka mwisho. Mbona huyo hajavaa nguo za heshima?” alisema yule kijana huku akiendelea kumkodolea macho malkia wa masokwe. Harrison hakujali, akamshika mkono malkia wa masokwe na kuendelea na safari yake, sasa wakiwa tayari wameshaingia ndani ya mji mdogo wa wafugaji wa Petersburg, upande wa Canada. Malkia wa masokwe alikuwa akishangaa kila kitu, hakuwahi kuona nyumba, magari wala pikipiki, akawa na kazi moja tu, kushangaa. Japokuwa watu walikuwa wakiwakodolea macho hasa kutokana na mwonekano wa malkia wa masokwe, Harrison hakujali kitu chochote, akatembea kwa kasi akiwa amemshika malkia wa masokwe mkono mpaka walipofika kwenye kituo kidogo cha treni ya umeme cha Petersburg. Kwa bahati nzuri, kituo kile kilikuwa kinapokea kadi za malipo za Mastercard kama ile aliyokuwa nayo Harrison. Akaenda mpaka sehemu ya kukatia tiketi, akamuelekeza mkata tiketi kuwa awape mbili za kuelekea Abbotsford. Shida yake kubwa ilikuwa ni kufika kwenye benki zilizokuwa kwenye mji huo ili atoe fedha kwa ajili ya kumnunulia malkia wa masokwe nguo na kutafuta sehemu ya kujihifadhi. Yule mhudumu wa stesheni ile, aliichukua kadi ya Harrison na kuipitisha (swap) kwenye mashine maalum, akapewa tiketi mbili kisha akarudishiwa kadi yake. Harrison akiwa bado amemshikilia malkia wa masokwe, alisogea pembeni na kukaa sehemu maalum iliyotengwa kwa ajili ya abiria kusubiria usafiri. Kila mtu aliyekuwa anapita alikuwa anamshangaa malkia wa masokwe. Baada ya kusubiri kwa dakika kadhaa, treni liliwasili kituoni pale, milango ikafunguka na abiria wakaanza kuingia. Harrison alikuwa makini mno na malkia wa masokwe, alihakikisha anamdhibiti ipasavyo. Dakika chache baadaye, safari ya kuelekea kwenye Mji wa Abbotsford ikaanza. Ndani ya treni, malkia wa masokwe aliendelea kuwa kituko, kila kitu kilikuwa kigeni kwake. Kwa kuwa ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kusafiri kwa treni ya umeme, njia nzima alikuwa akitapika na kuhangaika, akawa anataka kuruka kupitia dirishani. Harrison hakukata tamaa wala kuchoka, alikuwa akimsaidia malkia wa masokwe kwa kila hatua. Baada ya kusafiri kwa saa kadhaa, hatimaye sauti ya mhudumu wa treni ilisikika kutoka kwenye vipaza sauti ndani ya treni ikiwataarifu abiria kuwa tayari walishawasili kwenye Mji wa Abbotsford. Kwa kuwa malkia wa masokwe alikuwa amejichafua sana baada ya kutapika njia nzima, Harrison alikuwa wa kwanza kuteremka. Akamshika malkia wa masokwe mpaka kwenye vyoo vilivyokuwa pembeni kidogo ya stesheni. Akamuingiza ndani na kumkalisha kwenye bomba, akafungulia maji na kuanza kumsafisha mwili mzima. Baada ya kumaliza, alivua shati lake na kumpa malkia wa masokwe ajisitiri, wakatoka na kujichanganya na abiria wengine kuelekea katikati ya mji. “Ndugu samahani, eti hapa kuna benki yoyote jirani?” “Benki gani?” “Barclays.” “Nyoosha na hii barabara mpaka pale kwenye mataa, kata upande wa kushoto utaona ghorofa refu likiwa na maandishi makubwa yanayosomeka Barclays.” “Ahsante sana,” Harrison alimshukuru kijana aliyewaelekeza, akafuata maelekezo akiwa na malkia wa masokwe. Mara kwa mara malkia wa masokwe alikuwa akitaka kumponyoka na kukimbilia mbali na barabara, hasa alipoona magari makubwa yanapita kwa kasi pembeni yao. Baada ya kutembea umbali wa mita kadhaa, hatimaye Harrison alifika kwenye benki ya Barclays, tawi la Abbotsford. Alipofika mlangoni, askari waliokuwa wanalinda nje ya benki hiyo walimsimamisha kwa muda na kuanza kumhoji. Kwa mwonekano wa haraka, ungeweza kudhani alikuwa ni mwizi au kibaka kwani alikuwa kifua wazi baada ya kumpa malkia wa masokwe shati lake. Alipoonesha kadi yake ya benki, aliruhusiwa kuingia mpaka sehemu maalum kulipokuwa na mashine za ATM (Automatic Teller Machine). Huku kijasho chembamba kikimtoka, Harrison aliisogelea mashine na kuchomeka kadi yake sehemu maalum. Hakupata shida kwani tayari alishakuwa na uzoefu wa namna ya kutumia mashine hizo. Kitu cha kwanza alichofanya ilikuwa ni kuangalia salio, akabonyeza kitufe cha kuangalia salio na kusubiri kwa sekunde kadhaa. “Whaoooo! Ahsante Mungu,” alisema Harrison kwa sauti ya juu na kwenda kumkumbatia malkia wa masokwe baada ya kukuta mamilioni yake aliyoyaacha kwenye akaunti yake bado yapo. Hiyo ndiyo akaunti ambayo aliitumia kuhifadhi fedha alizozipata baada ya kuuza kitabu chake alichokiandika cha Queen of Gorillas kilichompa utajiri wa haraka na umaarufu mkubwa. Bila kupoteza muda, aliisogelea tena mashine ya ATM na kubonyeza namba fulani ili itoe kiwango cha fedha ambacho aliamini kitatosha kununulia nguo mpya, za kwake pamoja na malkia wa masokwe, kununulia chakula, kupangisha chumba hotelini na mahitaji mengine muhimu. Baada ya muda mfupi, tayari alikuwa na burungutu la fedha mkononi. Kwa kuwa dola za Kimarekani zilikuwa zikitumika sehemu nyingi duniani, hakupata shida kufanya manunuzi. Kitu cha kwanza ilikuwa ni kununua nguo nzuri, akabadilisha akiwa na malkia wa masokwe na kuzivaa ndani ya duka hilo. Malkia wa masokwe akawa anachekacheka kwani katika maisha yake hakuwahi kuvaa nguo mpya hata siku moja. Akawa anajitazama kwenye vioo vikubwa ndani ya duka lile. Baada ya kumaliza kununua nguo, Harrison alitoka na malkia wa masokwe hadi kwenye hoteli kubwa iliyokuwa jirani na pale ya Glaciers Peak Motel. Kwa kuwa alikuwa na fedha za kutosha, kila kitu kilienda vizuri. Akapangisha chumba na kulipia kwa muda wa wiki nzima. Harrison na malkia wa masokwe wakaelekea mpaka ndani ya chumba chao, ndani ya hoteli ya kifahari ya Glaciers Peak Motel. ***
JITIHADA za dhati alizozionesha Harrison katika kupigania penzi la malkia wa masokwe, zimeanza kuzaa matunda baada ya kufanikiwa kutoroka na msichana huyo kutoka kwenye msitu mkubwa wa Tongass, uliokuwa kwenye mpaka wa Marekani na Canada. Anatembea naye kwa siku kadhaa porini mpaka wanapokuja kutokezea upande wa pili wa msitu huo, kwenye mji mdogo wa wafugaji wa
Petersburg nchini Canada. Wakiwa kwenye mji huo, Harrison anajaribu kuulizia mahali penye benki, kijana mmoja mdogo anamuelekeza kuwa inabidi asafiri kwa treni mpaka mji wa pili uitwao Abbotsford.
Harrison akiwa amemshika mkono malkia wa masokwe aliyekuwa na mwonekano uliomshangaza kila mtu aliyemuona, anafanikiwa kwenda mpaka stesheni ya treni na kwa bahati nzuri, ananunua tiketi mbili kwa kutumia kadi yake ya benki, muda mfupi baadaye safari ya kuelekea Abbotsford inaanza.
Baada ya kusafiri kwa saa kadhaa, wanawasili kwenye mji huo uliopo nchini Canada ambapo Harrison anakwenda moja kwa moja benki, kwa bahati nzuri, baada ya kuingiza kadi yake kwenye mashine ya ATM, anagundua kuwa bado fedha zake zote zilikuwa salama kwenye akaunti yake.
Akatoa kiasi ambacho kilitosha kununulia mavazi mapya, kupanga chumba kwenye hoteli, kula na nyingine ya akiba kwa ajili ya matumizi madogomadogo. Harrison na malkia wa masokwe wakayaanza maisha mapya kwenye Hoteli ya Glaciers Peak, huku msichana huyo akionekana kushangaa kila kitu.
Upande wa pili, Linda bado haamini kama Harrison alikufa kifo cha kawaida, anaanza kufuatilia kwa kina kutaka kuujua ukweli. Anawaomba wazazi wake apelekwe upya shuleni kusomea masomo ya upelelezi na ujasusi.
BAADA ya kutoa fedha benki na kununua mavazi mapya, Harrison alienda kupangisha chumba na kulipia kwa muda wa wiki nzima. Akaongozana na malkia wa masokwe mpaka ndani ya chumba chao, ndani ya hoteli ya kifahari ya Glaciers Peak Motel. “Nakupenda sana mpenzi wangu, sitaki kukupoteza, nitafanya chochote ilimradi niishi na wewe,” alisema Harrison lakini malkia wa masokwe hakuwa anaelewa chochote. Alikuwa ametulia kimya kwenye kiti, akiendelea kushangaa kila kitu alichokiona ndani ya chumba kile. Kutokana na jinsi mwili wake ulivyokuwa mchafu, Harrison aliamua kuanza kwa kumsafisha, akamshika mkono na kumpeleka bafuni, akamvua nguo na kumkalisha chini, akafungulia bomba la maji, akaanza kumsugua sehemu mbalimbali za mwili wake huku akimpaka sabuni iliyokuwa inanukia vizuri. Kazi haikuwa nyepesi lakini alijitahidi kutumia nguvu zake zote. Alipomaliza kumsafisha mwili mzima, alianza kumsugua meno ambayo yalikuwa yamebadilika rangi kutokana na kula mizizi na matunda ya porini kwa kipindi chote cha maisha yake. Pia kazi haikuwa nyepesi kwani malkia wa masokwe alikuwa akiutafuna mswaki na fizi zake zilikuwa zikitoa damu. Alipomaliza, alimpunguza nywele ambazo zilikuwa zinamfanya aonekane kama mnyama wa porini. Akamsugua na miguu yake iliyokuwa imepasukapasuka kutokana na kutembea bila viatu kwa kipindi kirefu. Alipomaliza alimrudisha chumbani na kumlaza kitandani, akachukua mafuta mazuri yanayonukia, aliyoyanunua maalum kwa ajili ya malkia wa masokwe. Akaanza kumpaka mwili mzima, mwanzoni malkia wa masokwe alikuwa akileta upinzani lakini baadaye akatulia, Harrison akaendelea kumpaka mwili mzima. Alipomaliza alimbadilisha nguo na kumvalisha nyingine ambazo nazo zilikuwa mpya. Wakapumzika kitandani. ***CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Mzee Ford aliamua kumtimizia mwanaye alichokuwa anakitaka, akaenda kumuandikisha katika chuo cha upelelezi cha Scotland College of Crime Scene Investigation (SCCSI) kilichokuwa jijini London, Uingereza. Kila kitu kilikamilishwa haraka, Linda akapanda ndege na kuelekea jijini London. Siku tatu baadaye, alianza masomo huku akijiapiza kufanya juhudi ili aelewe kwa kina namna ya kufanya uchunguzi kitaalamu. Siku zilizidi kusonga mbele, Linda akawa anaendelea na masomo huku akijitahidi kuyazoea mazingira mapya ya nchini Uingereza. Kwa kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kusonga mbele, Linda alizidi kuwa mahiri kwenye masomo, hali iliyomfanya aanze kupata marafiki wengi. Hata hivyo, bado akili yake ilikuwa ikimuwaza Harrison, uchungu ukawa unazidi kumshika ndani ya moyo wake, akawa anajiapiza kuhakikisha anaujua ukweli juu ya kifo chake. Miezi mitatu baadaye, Linda alirudi nyumbani kwao nchini Marekani baada ya chuo chao kufungwa. Akiwa nyumbani kwao, muda mwingi alikuwa akipenda kukaa peke yake huku akionekana kuwa na mawazo mengi. Mara kwa mara wazazi wake hasa baba yake alikuwa akimfariji na kumtaka akubaliane na hali halisi. Hata hivyo, haikusaidia kitu kwani mara nyingi alikuwa anashinda ndani akikataa kuonana na marafiki zake. Baada ya likizo kuisha, Linda alirudi chuoni kuendelea na masomo, ikawa kila baada ya miezi mitatu kuisha anarudi nyumbani kwao na kupumzika kwa siku kadhaa kisha kurudi tena chuoni. Alifanya hivyo kwa sababu alikuwa hajazoea kukaa mbali na wazazi wake. Suala la nauli halikuwa tatizo kwao kwani baba yake alikuwa na uwezo mkubwa kiuchumi. *** Siku ya kwanza iliisha, Harrison na malkia wa masokwe wakiwa hotelini, huku msichana huyo akizidi kumzoea Harrison taratibu. Japokuwa hakuwa amevizoea vyakula vya kawaida malkia wa masokwe alilazimika kuanza kula mikate na vyakula vingine alivyofundishwa na Harrison. Mara mojamoja alikuwa akienda kumnunulia matunda kwenye ‘supermarket’ iliyokuwa jirani na hoteli ile. “Inabidi nimtafutie mwalimu wa kumfundisha lugha, tutaendelea kukaa kama mabubu mpaka lini?” aliwaza Harrison huku akipitia kitabu cha namba za mawasiliano (yellow pages) kilichokuwa ndani ya chumba kile. Akapata jina la mwalimu anayeweza kumsaidia kufanya kazi ile. Alimpigia simu na kuomba kukutana naye siku inayofuatia. Kesho yake asubuhi, mwanaume wa makamo aliyekuwa na kichwa chenye mvi nyingi, alifika kwenye Hoteli ya Glaciers Peak Motel na kuomba kuonana na Harrison. “Naomba unisaidie kumfundisha mpenzi wangu kusoma, kuandika na kuzungumza kama watu wengine.” “Kwani ana matatizo gani? Ana mtindio wa ubongo?” “Hapana, ameishi sehemu ambayo haina watu, amekaa porini kwa muda mrefu.” “Utanilipa shilingi ngapi?” alisema yule mzee huku akijaribu kuwasiliana na malkia wa masokwe kwa lugha ya ishara.” “Nitakupa kiasi chochote utakachohitaji,” alisema Harrison huku akimtazama mzee yule alivyokuwa anawasiliana na malkia wa masokwe. Baada ya kufikia makubaliano, Harrison aliongozana na yule mzee mpaka benki iliyokuwa jirani na hoteli ile, akatoa fedha kiasi benki na kumlipa kama malipo ya awali kwa ajili ya kazi ile. Kesho yake asubuhi, mzee yule wa makamo ambaye baadaye alijitambulisha kwamba anaitwa mwalimu Gallagher, aliwasili akiwa na vifaa vyake vya kufundishia. Kwa kuwa ilikuwa vigumu kwa malkia wa masokwe kukaa peke yake na mtu ambaye hajamzoea, ilibidi Harrison akae naye, mwalimu akaanza kumfundisha kusoma na kuandika. Mwanzo ilikuwa vigumu sana kwani hakuwa anaelewa chochote lakini baada ya kukaa muda mrefu, taratibu alianza kuelewa herufi kadhaa. Akawa anaweza kutamka kama mwalimu Gallagher alivyokuwa anatamka, hali iliyomfanya Harrison afurahi kuliko kawaida. Baada ya kumfundisha kwa zaidi ya saa tano mfululizo, mwalimu Gallagher aliaga na kuondoka, akaahidi kurudi kwa ajili ya masomo ya jioni. Huku nyuma Harrison akawa anacheza na malkia wa masokwe huku akiendelea kumfundisha ustaarabu, ikiwa ni pamoja na namna ya kutumia choo anapobanwa na haja. Jioni ilipofika, mwalimu Gallagher alirudi tena na Harrison akamchukua malkia wa masokwe na kukaa naye kwa utulivu, tayari kwa awamu ya pili ya masomo. Taratibu malkia wa masokwe akaanza kuingiza neno mojamoja kwenye kichwa chake. ***
BAADA ya kulipigania penzi la malkia wa masokwe kwa kadiri ya uwezo wake wote, hatimaye Harrison anafanikiwa kumnasa msichana huyo na kutoroka naye kutoka kwenye msitu mkubwa wa Tongass, uliokuwa kwenye mpaka wa Marekani na Canada. Wanatembea kwa miguu kwa siku kadhaa porini mpaka wanapokuja kutokezea upande wa pili wa msitu huo, kwenye mji mdogo wa wafugaji wa Petersburg nchini Canada. Baada ya hapo, wanasafiri kwa treni ya umeme kuelekea kwenye mji wa pili uitwao Abbotsford. Baada ya kusafiri kwa saa kadhaa, wanawasili kwenye mji huo uliopo nchini Canada ambapo
Harrison anakwenda moja kwa moja benki, kwa bahati nzuri, baada ya kuingiza kadi yake kwenye mashine ya ATM, anagundua kuwa bado fedha zake zote zipo salama kwenye akaunti yake.
Akatoa kiasi ambacho kilitosha kununulia mavazi mapya, kupanga chumba kwenye hoteli, kula na nyingine ya akiba kwa ajili ya matumizi madogomadogo. Harrison na malkia wa masokwe
wanayaanza maisha mapya kwenye Hoteli ya Glaciers Peak, huku msichana huyo akionekana kushangaa kila kitu.
Anamtafuta mwalimu maalum kwa ajili ya kuanza kumfundisha malkia wa masokwe kuzungumza, kusoma na kuandika. Mwalimu Gallagher, anapewa kazi hiyo huku Harrison naye akiendelea kumfundisha ustaarabu msichana huyo.
Upande wa pili, Linda anaendelea na masomo ya Crime Scene Investigation na anajiapiza kuwa lazima afaulu vizuri kisha aingie mwenyewe kazini kuutafuta ukweli wa kifo cha mpenzi wake,
Harrison. Bado haamini kama alikufa kifo cha kawaida, anahisi kuna njama zilikuwa nyuma ya tukio hilo.
JIONI ilipofika, mwalimu Gallagher alirudi tena na Harrison akamchukua malkia wa masokwe na kukaa naye kwa utulivu, tayari kwa awamu ya pili ya masomo. Taratibu malkia wa masokwe akaanza kuingiza neno mojamoja kwenye kichwa chake.
Kwa muda wa wiki nzima, mwalimu Gallagher na Harrison walikuwa na kazi ya ziada ya kumfundisha lugha malkia wa masokwe. Kwa kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kusonga mbele, ndivyo malkia wa masokwe alivyokuwa anazidi kuelewa mambo mbalimbali ya kibinadamu, ikiwemo lugha.
Mara kwa mara Harrison alikuwa akitoka naye na kumtembeza nje ya hoteli ili kumpunguza ushamba. Siku za mwanzo alikuwa akishangaa kila kitu lakini kwa kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kusonga mbele, akaanza kuzoea mazingira. Akapunguza kuwaogopa watu, magari na vitu vingine ambavyo awali vilikuwa vikimtoa ushamba.
Pia Harrison alikuwa na kazi ya ziada ya kumfundisha ustaarabu kuanzia namna ya kuvaa nguo kila anapoamka asubuhi, jinsi ya kula kwa ustaarabu mezani, jinsi ya kutembea kwa miguu miwili bila kushikashika mikono chini kama wafanyavyo masokwe, kuoga na kulala kwa ustaarabu.
Siku saba za kwanza zilikuwa za mafanikio makubwa kwa Harrison, akawa na matumaini makubwa kuwa siku chache zijazo malkia wa masokwe atakuwa binadamu aliyekamilika. Kilichokuwa kinamfurahisha zaidi Harrison ni kwamba kwa kadiri malkia wa masokwe alivyokuwa anaishi maisha mazuri, ndivyo alivyozidi kuwa mrembo.
Ngozi yake ikaanza kuwa nyororo huku yale madoa ya uchafu yaliyokuwa yanaiharibu ngozi yake yakitoweka taratibu, ung’avu wake wa asili ukawa unajionesha dhahiri. Pia nywele zake nazo ziliacha kutoa harufu kama zamani baada ya kuwa anamuosha kwa ‘shampoo’ kila siku. Kucha zake zilizokuwa zimebadilika rangi kwa uchafu nazo zikaanza kupendeza.
Harrison alipata wazo, akaona kuendelea kuishi hotelini kutamgharimu sana kwani alipanga maisha yake yote kuyahamishia katika mji huo uliochangamka wa Abbotsford, akaona njia pekee ambayo inaweza kumpunguzia matumizi yasiyo ya lazima ni kutafuta nyumba ya kupanga.
Kwa kuwa hakuwa na mtu mwingine yeyote aliyekuwa anamfahamu kwenye mji ule, aliamua kumtumia mwalimu Gallagher. Baada ya kumwambia nia yake, mzee huyo alimuahidi kumtafutia madalali ambao ndiyo wanaofahamu wapi kuna nyumba za kupanga.
Kesho yake, kama alivyokuwa amemuahidi, Gallagher alimkutanisha Harrison na dalali wa nyumba, Xavier Simmons. Baada ya mazungumzo na Harrison, Xavier aliomba kupewa muda ili kutafuta nyumba ambayo ingekidhi vigezo alivyovitoa Harrison. Siku mbili baadaye, nyumba ilipatikana katika Mtaa wa Langley, Harrison akapelekwa kwenda kuiona. Ilikuwa ni nyumba nzuri yenye
kila kitu ndani. Wamiliki wa nyumba hiyo walikuwa wamesafiri kwenda nje ya nchi hivyo hawakutaka nyumba yao ikae bila mtu, wakaamua kutafuta mpangaji ambaye angeitunza mpaka watakaporejea. Harrison alifurahi sana, bila hiyana akaenda benki na kutoa kiwango cha fedha kilichokuwa kinatakiwa, akalipa kodi ya mwaka mzima na kuanza kufanya maandalizi ya kuhamia. ***
Linda aliendelea na masomo yake kwa juhudi, hakukosa kuhudhuria vipindi hata siku moja. Hata siku za mwisho wa wiki ambazo wenzake walikuwa wakizitumia kustarehe, yeye alikuwa akishinda maktaba akijisomea. Hakutaka kufanya masihara kwenye masomo hata kidogo, akajiwekea nadhiri kuwa ni lazima afaulu kwa alama za juu.
Siku zilizidi kusonga mbele, akawa anazidi kupata ujuzi wa namna ya kuendesha kesi zilizokuwa zinahitaji upelelezi wa kutosha. Kila alipokuwa akirudi likizo nyumbani kwao, alikuwa akizidi kubadilika. Hakuwa Linda yule ambaye watu wengi walikuwa wanamfahamu, msichana ‘mayaimayai’ aliyelelewa kitajiri na kupata kila alichokitaka kutoka kwa wazazi wake.
Sasa alianza kubadilika huku muda mwingi akipenda kujifungia ndani peke yake, akipitia vitabu mbalimbali vilivyokuwa vinahusiana na masomo yake. Hata alipokuwa akitoka na kutembea kupunga upepo, muda mwingi alikuwa mkimya akionesha kuzama kwenye lindi la mawazo. Mara kwa mara alikuwa akilitembelea eneo ambalo Harrison alipata ajali na kufa.
Wazo pekee lililokuwa ndani ya akili yake, ni kusoma kwa bidii mpaka ahitimu masomo ya Crime Scene Investigation kisha baada ya hapo, alivalie njuga suala la Harrison mpaka aupate ukweli wa nini kilichosababisha kifo chake na utata uliokuwa nyuma ya tukio lile.
Aliamua kufanya hivyo mwenyewe baada ya kuona msaada alioutegemea kutoka jeshi la polisi hususan kitengo cha Crime Scene Investigation umeshindwa kukidhi kile alichokuwa anakitaka. Akaamua kuingia mwenyewe vitani ili kufahamu kilichomsibu Harrison, mwanaume wa maisha yake ambaye alitokea kumpenda kwa moyo wake wote. ***
Baada ya kukamilisha taratibu zote zilizokuwa zinatakiwa, Harrison alihama kwenye Hoteli ya Glaciers Peak aliyokuwa amefikia na kuhamia makazi mapya, kwenye Mtaa wa Langley. Mwalimu Gallagher aliendelea kumfundisha malkia wa masokwe hata baada ya kuhamia makazi mapya, ikawa kila siku anafika mara mbili, asubuhi na jioni kwa ajili ya kuendelea kumfundisha Harrison ambaye kwa kadiri siku zilivyokuwa zinasonga mbele ndivyo alivyokuwa anazidi kuelewa.
Taratibu akaanza kutamka maneno machache, ikiwa ni pamoja na kumudu kulitamka vizuri jina la Harrison. Akaanza kujua kujieleza ingawa bado ilikuwa kwa shida. Alipohisi njaa alisema, alipobanwa na haja ndogo au kubwa vilevile alikuwa akimwambia Harrison ambaye alikuwa akimpeleka sehemu husika.
Baada ya Harrison kuridhika na maendeleo aliyokuwa nayo, alianza kupanga mipango ya ndoa. Hakutaka kuvunja amri ya sita na msichana huyo mrembo kabla hajaingia rasmi kwenye ndoa. Japokuwa hisia za mapenzi zilikuwa zikimtesa sana, hasa ukizingatia walikuwa wakilala kitanda kimoja, wakati mwingine wakiwa wamekumbatiana, Harrison alijikaza kwa kadiri ya uwezo wake. Akawa anasubiri siku ya kuhalalisha rasmi uhusiano madhabahuni. *** CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
MTAFUTAJI hachoki, akichoka ujue amepata. Msemo huu unajidhihirisha kwa Harrison ambaye kwa kipindi kirefu amelipigania penzi la malkia wa masokwe kwa kadiri ya uwezo wake wote hadi akafanikiwa kumnasa msichana huyo
na kutoroka naye kutoka kwenye msitu mkubwa wa Tongass, uliokuwa kwenye mpaka wa Marekani na Canada. Kijana huyo aliyekuwa amebobea kwenye elimu ya viumbe hai, baada ya kumnasa malkia wa masokwe, anatembea
naye kwa miguu kwa siku kadhaa porini mpaka wanapokuja kutokezea upande wa pili wa msitu huo, kwenye mji mdogo wa wafugaji wa Petersburg nchini Canada. Baada ya hapo, wanasafiri kwa treni ya umeme kuelekea kwenye mji wa pili uitwao Abbotsford.
Baada ya kuwasili Abbotsford, Harrison na malkia wa masokwe wanayaanza maisha mapya kwenye Hoteli ya Glaciers Peak, huku msichana huyo akionekana kushangaa kila kitu. Anamtafutia mwalimu maalum kwa ajili ya kuanza kumfundisha kuzungumza, kusoma na kuandika.
Baada ya kukaa hotelini kwa wiki moja huku akifanya kazi ya ziada ya kumfundisha ustaarabu msichana huyo, aliamua kutafuta nyumba ya kupanga, akafanikiwa kuipata na kulipa kodi ya mwaka mzima. Maisha yakawa yanazidi kusonga mbele huku malkia wa masokwe akibadilika taratibu.
Upande wa pili, Linda anaendelea na masomo ya Crime Scene Investigation na anajiapiza kuwa lazima afaulu vizuri kisha aingie mwenyewe kazini kuutafuta ukweli wa kifo cha mpenzi wake, Harrison. Haamini kama mpenzi wake huyo
alikufa kifo cha kawaida, anahisi kuna njama zilikuwa nyuma ya tukio hilo na anajiapiza kufanya kila linalowezekana kuufichua ukweli.
JAPOKUWA hisia za mapenzi zilikuwa zikimtesa sana, hasa ukizingatia walikuwa wakilala kitanda kimoja, wakati mwingine wakiwa wamekumbatiana, Harrison alijikaza kwa kadiri ya uwezo wake. Akawa anasubiri siku ya kuhalalisha rasmi uhusiano wao madhabahuni.
Malkia wa masokwe aliendelea kufundishwa na mwalimu Gallagher kila siku, kwa kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kusonga mbele, akawa anapanuka ufahamu wake, akaanza kuzungumza sentensi fupifupi huku pia akimudu kutaja majina ya vitu mbalimbali kama alivyokuwa anafundishwa.
Pia alikuwa akizidi kustaarabika, yale mambo aliyokuwa anayafanya muda mfupi baada ya kutoka msituni, sasa hakuwa akiyafanya tena, akawa anaweza kufanya kazi ndogondogo za nyumbani kama kufua na kufanya usafi. Kila siku Harrison alikuwa ni mtu wa furaha, kila alipokuwa anamtazama malkia wa masokwe, alikuwa akitabasamu hasa akikumbuka jinsi alivyoteseka porini.
Kwa kuwa mpaka muda huo hakuwa akilifahamu jina halisi la malkia wa masokwe, aliamua kumbatiza jina jipya. Akampa jina la Angel. Akawa anamuita kwa jina hilo mara kwa mara mpaka alipoanza kulizoea. Ikawa mtu yeyote akimuuliza jina lake anamwambia anaitwa Angel.
Siku zilizidi kusonga mbele, Harrison, kwa kuhofia ndugu zake kumtafuta na kugundua ukweli kuwa hakufa, na yeye aliamua kubadilisha jina kwenye nyaraka zake zote. Akajibatiza jina jipya la Alex Wolfgang kisha akaenda kuonana na daktari Albert Stein aliyekuwa anasifika kwa utaalamu wa kuwafanyia watu upasuaji wa kubadilisha sura (plastic surgery).
“Kwa nini unataka kubadilisha sura? Isije kuwa wewe ni mhalifu unatafuta njia ya kuukimbia mkono wa sheria.” “Hapana, kuna sababu binafsi zinazonifanya nibadilishe sura. Nipo tayari kukuelezea lakini niahidi kwamba hutaitoa hii siri yangu,” alisema Harrison huku akijiweka vizuri kwenye kiti.
Alipohakikishiwa kutunziwa siri, Harrison alimueleza Daktari Stein kila kitu ingawa hakutaka kumueleza kwa undani zaidi akihofia kuharibu mambo.
“Msichana mwenyewe ndiyo huyu?” aliuliza Daktari Stein huku akimkazia macho malkia wa masokwe ambaye sasa alikuwa akiitwa Angel. “Ndiyo huyu, nipo tayari kufanya lolote ilimradi nimuoe.” “Lakini hujakosea, msichana mzuri sana huyu, halafu mnapendezana,” alisema Daktari Stein kwa masihara huku akianza kuandaa vifaa vyake tayari kwa kazi.
Kazi haikuwa nyepesi, ilichukua zaidi ya saa tatu Harrison akiwa ndani ya chumba maalum, daktari akiendelea na kazi yake. Malkia wa masokwe naye alikuwa amekaa na kutulia pembeni, akiangalia jinsi Harrison alivyokuwa anabadilishwa sura. Baada ya upasuaji kumalizika, Harrison alisimama na kwenda kujitazama kwenye kioo kikubwa kilichokuwa ukutani, akatabasamu
kwani alibadilika sana. Isingekuwa rahisi kwa mtu yeyote kumtambua kirahisi. Baada ya kazi kumalizika, Harrison na malkia wa masokwe walirudi kwenye makazi yao kwenye Mtaa wa Langley.
Harrison aliendelea na kazi ya kujibadilisha, sasa akahamia kwenye vyeti na nyaraka zake muhimu. Akapanga kwenda kupiga picha za pasipoti ambazo ndiyo angezitumia kwenye nyaraka zake muhimu ikiwa ni pamoja na hati ya kusafiria. Aliamua pia kubadilisha jina ili kuzidi kupoteza ushahidi.
Akajibatiza jina jipya la Alex Wolfgang ambalo ndiyo alipanga kulitumia kwenye nyaraka zake zote. Alipomaliza zoezi hilo, alipumzika na mchumba wake huku mipango ya ndoa ikianza kukisumbua kichwa chake. Baada ya kazi ya kubadilisha jina na sura kukamilika, hakukuwa na kipingamizi chochote cha kufunga ndoa.
Kuonesha jinsi alivyokuwa na mapenzi ya dhati kwake, alipanga kwenda kufunga naye ndoa ya kanisani na kuweka kiapo cha maisha. Kwa utaratibu wa dini ya Kikristo, ndoa zilizokuwa zinafungwa kanisani ilikuwa haziwezi kutenganishwa na chochote zaidi
ya kifo. Hata ikitokea wanandoa wakahitilafiana na kupeana talaka, hakuna aliyekuwa anaruhusiwa kuoa au kuolewa tena.
“Sidhani kama itakuja kutokea siku nikaachana na Angel wangu, kifo pekee ndiyo kitakachotutenganisha,” alisema Harrison huku akianza kufikiria kumpeleka mchumba wake huyo kanisani akaanze kujifunza mambo ya kiroho. Siku kadhaa baadaye, Harrison aliongozana na Angel wake hadi kwenye kanisa lililokuwa jirani na pale walipokuwa wanaishi.
Wakaomba kuonana na mchungaji ambapo Harrison ambaye sasa alikuwa akijitambulisha kwa jila la Alex, alimweleza mchungaji historia ya maisha ya mchumba wake kisha akaomba msaada aweze kuandikishwa kwenye orodha ya watu ambao walikuwa mbioni kubatizwa.
Pia aliomba wote wawili wapewe mafunzo ya ndoa na namna ya kuishi wawili, ikiwa ni maandalizi ya kuingia kwenye ndoa halali. Mchungaji alimkubalia, akawataka wote wawili wawe wanahudhuria vipindi vya dini kanisani hapo kila jioni.
Harrison na mchumba wake wakarudi hadi kwenye makazi yao huku mara kwa mara akijitahidi kumzoesha kuzungumza kwa kawaida. Taratibu wakawa wanaelewana kwenye mazungumzo yao ingawa bado malkia wa masokwe hakuwa na uwezo wa kuzungumza na kuelewa kama watu wengine.
“Mimi nataka kukuoa wewe uwe mke wangu, tuishi pamoja na tuzae watoto wazuri,” Harrison alikuwa akimwambia mchumba wake huku akijitahidi kumuonesha kwa ishara ili waelewane vizuri. Hakumjibu chochote zaidi ya kuwa anachekacheka tu, hali iliyomfanya Harrison ashindwe kuelewa kama amemuelewa au la.
“Nitakuwa namwambia hivi kila siku mpaka anielewe, nahitaji aridhie kutoka ndani ya moyo wake, sitaki kumlazimisha,” alisema Harrison. Ikawa anamtamkia maneno yale mara kwa mara huku akimuonesha upendo wa dhati.
Siku kadhaa baadaye, walianza kuhudhuria vipindi vya dini kanisani. Wakajiwekea ratiba kuwa asubuhi Angel atakuwa anafundishwa na mwalimu Gallagher kama kawaida na jioni wanaongozana kwenda kanisani kuhudhuria mafunzo ya ubatizo na elimu ya ndoa na uhusiano. ***
HARRISON, baada ya kulipigania kwa muda mrefu penzi la malkia wa masokwe, hatimaye anafanikiwa kumnasa na sasa yupo chini ya himaya yake. Amefanikiwa kumtorosha kutoka kwenye mikono ya masokwe kwa tabu kubwa hadi
alipotoka naye kwenye msitu mkubwa wa Tongass, uliokuwa kwenye mpaka wa Marekani na Canada. Baada ya kufanikiwa kumnasa malkia wa masokwe, anatembea naye kwa miguu kwa siku kadhaa porini kisha
wanatokezea upande wa pili wa msitu huo, nchini Canada. Baada ya hapo, wanasafiri kwa treni ya umeme kuelekea kwenye mji wa pili uitwao Abbotsford.
Wakiwa kwenye mji huo, wanayaanza maisha mapya kwenye Hoteli ya Glaciers Peak, huku msichana huyo akionekana kushangaa kila kitu. Baadaye anamtafutia mwalimu maalum kwa ajili ya kuanza kumfundisha
kuzungumza, kusoma na kuandika kisha wanahama hotelini baada ya kupata nyumba ya kupanga. Maisha yanazidi kusonga mbele huku malkia wa masokwe akibadilika taratibu na sasa anafikia hatua ya kuanza
kuzungumza kama binadamu wa kawaida. Anafundishwa ustaarabu na Harrison na kwa kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele, malkia wa masokwe anazidi kuwa mrembo. Baadaye wanaanza kusomea mafundisho ya dini kuhusu ndoa na uhusiano ikiwa ni maandalizi ya kuoana.
Upande wa pili, Linda anaendelea na masomo ya Crime Scene Investigation na anajiapiza kuwa lazima aufahamu ukweli uliokuwa umejificha nyuma ya kifo cha mpenzi wake, Harrison. Haamini kama mpenzi wake huyo alikufa kifo
cha kawaida, anahisi kuna njama zilikuwa nyuma ya tukio hilo na hiyo ndiyo sababu inayomfanya aingie kazini mwenyewe kuhakikisha anaujua ukweli.
Harrison na malkia wa masokwe (Angel) waliendelea kuhudhuria mafunzo ya ubatizo na elimu ya uhusiano na ndoa kila siku. Walishaingiza katika ratiba yao ya kila siku, ikawa asubuhi Angel anafundishwa na mwalimu Gallagher elimu ya kidunia na jioni wanaongozana hadi kanisani kufundishwa elimu ya kiroho. Siku zilizidi kuyoyoma, Angel akawa na utashi na uelewa kama binadamu wengine. Akaanza kuwa na hisia za mapenzi mazito kwa Harrison hasa kutokana na jinsi alivyokuwa anamdekeza. Siku zote, Harrison ambaye sasa alikuwa akitambulika kwa jina la Alex Wolfgang, hakutaka mchumba wake apatwe na matatizo yoyote. Alikuwa akimtunza kama mboni ya jicho lake, muda wote akiwa pembeni yake. Kutokana na kazi kubwa iliyokuwa inafanywa na mwalimu Gallagher, baada ya miezi kadhaa Angel tayari alikuwa na uwezo wa kuzungumza na kuelewa vitu vingi sana. Usingeweza kuamini kwamba huyo ndiye msichana aliyelelewa na masokwe kwa kipindi kirefu katika maisha yake. Alistaarabika na sasa akawa hana tofauti na wasichana wengine, kila siku alikuwa akijifunza mambo mapya na kuzidi kuwa bora. Harrison alimzoesha tabia ya kusoma vitabu vyenye maarifa mbalimbali huku muda mwingine wakitazama mikanda ya video iliyokuwa inafundisha mambo mbalimbali ya maisha. Tayari alishasahau maisha ya porini aliyokuwa anaishi na masokwe. “Nataka nikuvalishe pete ya uchumba mpenzi wangu, nataka mwaka huu ukiisha tufunge ndoa na kuwa mume na mke halali, nakupenda sana Angel.” “Nakupenda pia mpenzi wangu, natamani siku ya kufunga ndoa ifike haraka,” alisema malkia wa masokwe, Harrison akamvutia kifuani kwake na kumkumbatia kimahaba, akawa anambusu sehemu mbalimbali za mwili wake huku Angel naye akimrudishia. Wakaendelea kucheza kimahaba kwa muda mrefu huku kila mmoja akimuonesha mwenzake mapenzi ya dhati. “Nilikuwa naisubiri kwa hamu kubwa siku ambayo Angel wangu atazielewa hisia zangu, namshukuru Mungu hatimaye imewadia,” Harrison alijisemea moyoni huku akizichezea nywele za mchumba wake aliyekuwa amejilaza kifuani kwake. ***CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Linda aliendelea na masomo yake kwa juhudi, akikazania kuelewa kwa vitendo namna ya kufanya upelelezi kwenye maeneo ya matukio ya uhalifu (Crime Scene). Kila mwisho wa muhula, Linda alikuwa akiongoza kwenye wastani wa matokeo ya mitihani na majaribio waliyokuwa wanayafanya. Kila mmoja alikuwa akitamani kuwa na urafiki naye lakini haiba yake ya kuwa kimya muda wote, ilifanya iwe vigumu kuzoeana na wanachuo wenzake. Mwaka wa kwanza uliisha, Linda akawa anaongoza kwa wastani wa matokeo ya mitihani. Mwaka wa pili nao ulienda vizuri, msichana huyo akiweka rekodi kwa kuongoza masomo ambayo siku zote yalikuwa yakiongozwa na wanaume. Mwaka wa tatu kama ilivyo kawaida ya vyuo vingi vya juu, ulikuwa ni mwaka wa kufanya majaribio kwa vitendo (field work). Kutokana na alama za juu alizokuwa anazipata katika mitihani yake, Linda alipata nafasi ya kwenda kufanya majaribio kwa vitendo kwenye mashirika makubwa ya ujasusi ya CIA la Marekani na Scotland Yard la Uingereza. Kote alikopita, Linda alikuwa akiweka historia ya ajabu huku sifa yake ya kuwa mkimya muda wote ikimuongezea alama za juu. Baada ya kumaliza mafunzo kwa vitendo, alirejea nyumbani kwao ambapo jambo la kwanza alilomwambia baba yake ni kwamba akishamalizia muhula wa mwisho, anataka kufungua kampuni yake ya upelelezi. Kwa kuwa suala la fedha halikuwa tatizo kwa wazazi wake, mzee Ford alimhakikishia kumsaidia kila kitu ili afanikishe azma yake. Akawasiliana na wasaidizi wake ambapo maandalizi yalianza kufanyika. Akatafutiwa ofisi, vyeti vya usajili wa kudumu pamoja na nyaraka nyingine zote zilizokuwa zinatakiwa. *** Baada ya Harrison kuridhishwa na maendeleo ya malkia wa masokwe (Angel) katika kuelewa elimu ya kidunia na ile ya kiroho, aliamua kumvalisha pete ya uchumba na kuutangaza rasmi uchumba wao hadharani. Mchungaji aliyekuwa anawafundisha elimu ya kiroho, alimuelekeza kila kitu kilichokuwa kinatakiwa ili kuufanya uchumba wao uwe mtakatifu ikiwa ni maandalizi ya kuingia kwenye ndoa ya halali. Walipokamilisha taratibu zote, Alex (Harrison) na Angel (malkia wa masokwe) walitangazwa rasmi kanisani Jumapili moja mbele ya waumini wengine kuwa wao ni wachumba ambao walikuwa mbioni kufunga ndoa. Kila mtu aliwatakia kila la heri kwani ama kwa hakika walikuwa wakipendana na kupendezana. Walidumu kwenye uchumba wao kwa kipindi kirefu, kila siku ikawa mpya kwao kwani walikuwa wakizidisha kupendana. Ikafika mahali wakawa kama mapacha, usingeweza kumuona mmoja bila mwingine kuwepo. Walikuwa wakifuatana kama kumbikumbi. “Kwa nini hupendi kukivua hicho kidani chako shingoni? Kwani ulikipata wapi?” Harrison alimuuliza mchumba wake, jioni moja wakiwa wanapunga upepo kwenye bustani nzuri ya maua iliyokuwa jirani na pale walipokuwa wanaishi. “Mh! Sikumbuki nilikipata wapi lakini tangu napata akili nilikuwa nacho, huu ndiyo ulinzi wangu ulionifanya nivuke vikwazo vyote maishani mwangu nikiwa salama.” “Ooh! Vizuri sana, nikikununulia kingine kizuri utakipenda? Hicho kimeshachakaa sana na tayari kimeanza kukubana shingoni.” “Hata ukininunulia kingine nitakuwa navivaa vyote viwili shingoni, nakipenda sana,” alijibu Angel huku akitabasamu, wakakumbatiana na Harrison na kuanza kubusiana sehemu mbalimbali za miili yao. Siku zilizidi kusonga mbele, hatimaye siku ya harusi yao ikawa imekaribia. Wakaanza maandalizi ya hapa na pale ikiwa ni pamoja na kununua nguo watakazovaa siku hiyo. Kwa kuhofia watu wasije kuingilia ndoa yao na kukwamisha mpango wao, waliamua kutofanya sherehe zaidi ya kuhalalishwa mbele za Mungu kisha wangesafiri pamoja kwenda sehemu ya mbali kabisa kula fungate pamoja. ***
MIPANGO ya kufunga ndoa kati ya Harrison na mchumba wake, Angel (malkia wa masokwe) imepamba moto. Baada ya kulipigania kwa muda mrefu penzi la msichana huyo mrembo, hatimaye tayari yupo mikononi mwake na sasa anachosubiri ni siku ya kuhalalishwa rasmi madhabahuni. Kazi haikuwa nyepesi mpaka kufikia hapo kwani ilimlazimu Harrison kukaa siku nyingi kwenye msitu mkubwa wa Tongass akitafuta njia ya kumtorosha msichana huyo aliyekuwa analindwa na kundi kubwa la masokwe waliokuwa wanamheshimu kama malkia wao. Baada ya kuhangaika sana, hatimaye anafanikiwa kumtorosha kutoka kwenye mikono ya masokwe na kuelekea upande wa pili wa msitu huo. Wanatembea siku nyingi porini na kutokezea kwenye Mji wa Petersburg, Canada. Baada ya hapo, wanasafiri kwa treni ya umeme kuelekea kwenye mji wa pili uitwao Abbotsford. Wakiwa kwenye mji huo, wanayaanza maisha mapya kwenye Hoteli ya Glaciers Peak, huku msichana huyo akionekana kushangaa kila kitu. Baadaye anamtafutia mwalimu maalum kwa ajili ya kuanza kumfundisha kuzungumza, kusoma na kuandika kisha wanahama hotelini baada ya kupata nyumba ya kupanga. Maisha yanazidi kusonga mbele huku malkia wa masokwe akibadilika taratibu na sasa anafikia hatua ya kuanza kuzungumza kama binadamu wa kawaida. Anafundishwa ustaarabu na Harrison na kwa kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele, malkia wa masokwe anazidi kuwa mrembo. Baadaye wanaanza kusomea mafundisho ya dini kuhusu ndoa na uhusiano ikiwa ni maandalizi ya kuoana. Kwa kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele ndivyo malkia wa masokwe anavyozidi kubadilika na kuwa na tabia zote kama binadamu wengine. Harrison anabadilisha kabisa mwonekano wake akikwepa kugundulika na ndugu zake ambao wote wanaamini kuwa alishakufa kwenye ajali mbaya ya barabarani. Sasa maandalizi ya ndoa yamepamba moto na wanachosubiri ni siku husika kufika.
Siku zilizidi kusonga mbele, hatimaye siku ya harusi yao ikawa imekaribia. Wakaendelea na maandalizi ya hapa na pale ikiwa ni pamoja na kununua nguo watakazovaa siku hiyo. Kwa kuhofia watu wasije kuingilia ndoa yao na kukwamisha mpango wao, waliamua kutofanya sherehe zaidi ya kuhalalishwa mbele za Mungu kisha wangesafiri pamoja kwenda sehemu ya mbali kabisa kula fungate pamoja. Harrison na mchumba wake Angel waliendelea na maandalizi ya harusi, wakanunua shela zuri kwa ajili ya bibi harusi na suti maridadi kwa ajili ya bwana harusi, pamoja na pete za ndoa za dhahabu. Kwa kuwa akaunti ya Harrison bado ilikuwa na fedha za kutosha alizozipata baada ya kuchapisha na kuuza kitabu chake cha Queen of Gorillas, kila kitu kilienda kama kilivyokuwa kimepangwa. Akiwa katika mwonekano mpya wa sura na jina, Harrison alikuwa na matumaini makubwa kuwa hakuna kitu kitakachokwamisha ndoa hiyo. Kilichomfurahisha zaidi ni kwamba alikuwa akimuoa mwanamke aliyekuwa akimpenda kwa dhati kutoka ndani ya moyo wake, akiwa amemhangaikia sana mpaka kufanikiwa kumpata. Maandalizi yalizidi kupamba moto, ndoa yao ikawa inatangazwa kanisani kila wiki ili kama kuna mtu yeyote mwenye pingamizi ajitokeze kama ilivyokuwa kawaida kila ndoa zinapotaka kufungwa. Kwa kuwa hakuna aliyekuwa anamfahamu Harrison wala Angel (malkia wa masokwe) kila kitu kilienda kama kilivyopangwa. Kama alivyokuwa amepanga tangu mwanzo, Harrison hakutaka kufanya sherehe ya aina yoyote. Alipanga kuwa wataenda kanisani kufunga ndoa kisha baada ya hapo watasafiri kwenda kwenye Visiwa vya Barbados ambako wangekula fungate kwa raha zao bila kubughudhiwa na mtu yeyote. Kabla hata hawajafunga ndoa rasmi, tayari Harrison alishafanya ‘booking’ kwenye hoteli yenye hadhi ya nyota tano ya Bajans Legacy Apartment iliyokuwa kwenye mji wa pili kwa ukubwa visiwani humo, Speightstown. Alilipia gharama za kuishi kwenye hoteli hiyo iliyokuwa kwenye ufukwe wa Bahari ya Atlantic kwa muda wa mwezi mzima. Siku ya harusi ikawadia, Harrison akavaa suti yake maridadi na Angel (malkia wa masokwe) akavaa shela lake lenye hadhi ya kipekee. Kama ndiyo ingekuwa mara ya kwanza kuwaona, ungeweza kudhani wanatoka kwenye familia ya kifalme kwa jinsi walivyokuwa wamependeza. Wapambaji waliokodiwa na Harrison, walifanya kazi yao ipasavyo kwani Angel alibadilika mno. Sasa alikuwa malaika kweli kama jina lake lilivyokuwa. Kila Harrison alipokuwa anamtazama, alikuwa akijisikia raha ya ajabu ndani ya moyo wake. Mwalimu Gallagher na mkewe ndiyo waliokuwa wasimamizi wa ndoa hiyo. Baada ya kumaliza kujiandaa, walitoka mpaka nje ambapo magari mawili ya kifahari waliyoyakodi, yalikuwa yakiwasubiri. Bwana harusi akaingia kwenye gari moja na mwalimu Gallagher ambaye naye alikuwa amependeza kisawasawa. Bibi harusi akaingia kwenye gari lingine akiwa na mke wa mwalimu wake, safari ya kuelekea kwenye Kanisa la St. Peter Langley ikaanza. Kwa kuwa hapakuwa mbali sana, baada ya muda mfupi wakawa wamewasili. Wakateremka na kuelekea moja kwa moja ndani ya kanisa hilo, huku bendi ya kanisa ikiwatumbuiza kwa muziki laini. Hakukuwa na watu wengi waliohudhuria zaidi ya viongozi wa kanisa na waumini wachache waliokuwa wanaishi jirani. Wawili hao walienda moja kwa moja mpaka madhabahuni na kusimama wakiwa wanatazamana. Baada ya taratibu za kawaida za kufungisha ndoa, mchungaji alimuongoza Harrison (Alex) kula kiapo cha ndoa baada ya kumhoji maswali kadhaa. “Mimi Alex Wolfgang, nakubali kumuoa Angel kuwa mke wangu wa ndoa, kuanzia leo na kuendelea, katika raha na shida, katika utajiri na umaskini, katika maradhi na uzima mpaka kifo kitakapotutenganisha,” alisema Harrison (Alex) kisha akamvalisha pete ya ndoa, akamsindikiza na busu zito. Watu wote wakashangilia na kupiga makofi. Alipomaliza, mchungaji alimgeukia Angel ambapo alimuuliza maswali kadhaa kisha akamuongoza naye kula kiapo cha ndoa. Alipomaliza, alimvalisha pete Harrison kisha wakashikana mikono kwa upendo na kukumbatiana, wakabusiana kimahaba, hali iliyofanya watu wote wasimame na kushangilia kwa nguvu. Baada ya hapo walijaza cheti cha ndoa, walipomaliza wakashikana mikono na kuanza kutembea kwa hatua za taratibu kushuka madhabahuni, wakatembea kwa hatua za taratibu mpaka kwenye zulia maalum, wakaongoza moja kwa moja mpaka nje ambako waliingia kwenye gari moja. Wakakumbatiana na kugusanisha ndimi zao, kila mmoja akiwa na furaha isiyoelezeka. Kwa kuwa walishajiandaa kwa safari, baada ya kutoka kanisani, walisindikizwa moja kwa moja mpaka Uwanja wa Ndege wa Abbotsford. Wakapanda kwenye ndege kubwa ya Airbus 380 iliyokuwa inaelekea Visiwa vya Barbados. Walitengewa sehemu maalum katika daraja la kwanza (Diplomatic Class). Muda mfupi baadaye, ndege ikaanza kujongea taratibu kuelekea kwenye njia za kurukia (run ways). Mwalimu Gallagher, mkewe na watu wachache waliowasindikiza wakawa wanawapungia mikono huku wakiwatakia kila la heri kwenye fungate yao. Taratibu ndege ikaiacha ardhi na kupaa angani. “Mbona unalia mke wangu,” Harrison alimuuliza Angel aliyekuwa amejiinamia chini machozi yakimtoka. “Nalia kwa furaha mpenzi wangu, sitaki kuamini kama kweli nimekuwa mke wako halali. Umenitoa mbali sana Harrison, yaani hata siamini,” alisema Angel huku akizidi kutokwa na machozi. “Usijali kipenzi changu, nilikuahidi kuwa lazima nikuoe na leo nimetimiza ahadi yangu, nakupenda sana mahabuba na kama nilivyoapa kanisani nitakuwa na wewe mpaka kifo kitakapotutenganisha,” alisema Harrison na kumkumbatia mke wake, akawa anamfuta machozi huku akimbusu sehemu mbalimbali za mwili wake. Safari iliendelea kwa muda mrefu, hatimaye wakamsikia mhudumu wa ndege akiongea kupitia vipaza sauti vilivyokuwa kwenye ndege, akiwataarifu abiria wote wafunge mikanda yao kwani ndege ilikuwa ikijiandaa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Speightstown kwenye Visiwa vya Barbados. Harrison alimsaidia mke wake kumfunga mkanda, na yeye akajifunga na kutulia, ndege ikatua salama uwanjani na baada ya muda, mlango ukafunguliwa na abiria wakaanza kuteremka. Harrison alimbeba mke wake kutoka ndani ya ndege mpaka chini kisha wakaelekea kwenye mlango wa kutokea. Mizigo yao ilipitishwa kwenye mtambo maalum hadi upande wa nje, nao wakatoka hadi sehemu ya mapokezi ambapo walikuta gari maalum kutoka Hoteli ya Bajans Legacy likiwasubiri. Harrison hakujali watu waliokuwa wanamtazama alivyombeba mkewe, akamuingiza mpaka ndani ya gari kisha safari ya kuelekea hotelini ikaanza. Njia nzima alikuwa akimwagia mvua ya mabusu. *** CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
BAADA ya kulihangaikia penzi la malkia wa masokwe kwa kipindi kirefu, Harrison anafanikiwa kumtorosha msichana huyo, chaguo la moyo wake kutoka kwenye himaya ya masokwe na kwenda naye nchini Canada. Akiwa kwenye Mji wa Abbotsford, Harrison anafanya kazi ya ziada ya kumbadilisha msichana huyo. Baada ya kazi kubwa, hatimaye anafanikiwa kumfundisha ustaarabu wa kibinadamu, pia anamtafutia mwalimu anayemfundisha kuongea, kusoma na kuandika. Baada ya muda, malkia wa masokwe anabadilika kabisa na sasa anakuwa na haiba kama binadamu wengine. Kwa pamoja wanaanza kujifunza masomo ya ndoa na mambo ya kiroho na baadaye wanajitambulisha rasmi kama wachumba. Mipango ya ndoa inaanza kupangwa huku kila kitu kikiendeshwa kwa usiri ili ndugu wa Harrison wasishtukie kuwa ndugu yao hakufa. Mwisho Harrison na malkia wa masokwe wanafunga ndoa na kuhalalishwa madhabahuni kuwa mume na mke halali. Muda mfupi baada ya kufunga ndoa, wanaondoka pamoja kuelekea kwenye Visiwa vya Barbados wanakoenda kula fungate. Upande wa pili, msichana ambaye Harrison alimkimbia kanisani muda mfupi kabla ya kufunga naye ndoa, Linda, haamini kama kweli mpenzi wake huyo alikufa kifo cha kawaida. Hali hiyo inamfanya akasomee upelelezi akiwa na dhamira kubwa ya kuingia mwenyewe kazini kufuatilia ni nini kilichotokea siku ya tukio.
Mizigo yao ilipitishwa kwenye mtambo maalum hadi upande wa nje, nao wakatoka hadi sehemu ya mapokezi ambapo walikuta gari maalum kutoka Hoteli ya Bajans Legacy likiwasubiri. Harrison hakujali watu waliokuwa wanamtazama alivyombeba mkewe, akamuingiza mpaka ndani ya gari kisha safari ya kuelekea hotelini ikaanza. Njia nzima alikuwa akimwagia mvua ya mabusu. Baada ya dakika kadhaa, gari lililowabeba Harrison na mkewe liliwasili kwenye hoteli ya kisasa ya Bajans Legacy Apartment iliyokuwa ufukweni mwa Bahari ya Atlantic. Wahudumu wachangamfu wakaenda kuwapokea mizigo mpaka sehemu ya mapokezi. Harrison akajitambulisha pamoja na mkewe, kwa sababu alishafanya ‘booking’ siku kadhaa nyuma, hakupata shida. Wakaongozwa moja kwa moja mpaka kwenye chumba chake kilichokuwa na kila kitu ndani. Wahudumu wakawasaidia kupanga vitu vyao vizuri kisha wakaanza kuwaonesha mazingira ya hoteli ile ambayo ama kwa hakika ilikuwa inavutia. “Tutakaa hapa kwa kipindi cha mwezi mzima, nataka tufurahi na kusherehekea pamoja ushindi tulioupata,” alisema Harrison huku akimkumbatia mkewe, akawa anambusu sehemu mbalimbali za mwili wake. Waliagiza chakula ambacho kililetwa muda mfupi baadaye, wakala pamoja huku kila mmoja akionekana kuwa na furaha kuliko kawaida. Baada ya kula walitoka na kwenda kupumzika ufukweni huku wakipigwa na upepo mwanana. Ilibidi wabadilishe nguo walizokuwa wamevaa na kuvaa mavazi ya kuogelea (swimming costume). “Duh! Mke wangu amejaaliwa uzuri wa asili sijapata kuona. Lazima leo tuingie rasmi kwenye ulimwengu wa mapenzi, najua hajawahi kumjua mwanaume kama nilivyo mimi,” aliwaza Harrison wakati akicheza na mkewe ufukweni. Walikuwa wakikimbia huku na kule na kubebana kama watoto. Kwa kadiri walivyokuwa wanazidi kucheza, ndivyo hisia za mapenzi zilivyokuwa zinazidi kuwapanda wote wawili, wakawa wanabusiana kimahaba huku wakinyonyana ndimi mara kwa mara. Baadaye wakaangushana kwenye mchanga wa bahari, wakawa wanatazamana kama majogoo yanayotaka kupigana. “Angel!” “Abee mume wangu.” “Nakupenda sana kipenzi changu, naahidi kukutunza kwa kadiri ya uwezo wangu wote mpaka kifo kitakapotutenganisha.” “Ahsante mume wangu, mimi pia naahidi kukupenda na kukuheshimu kwa siku zote za uhai wangu,” alisema Angel huku akimpapasa mumewe kifuani kwa mahaba. Hisia za mapenzi zilipowazidia, walinyanyuka pale mchangani na kuanza kukokotana kuelekea kwenye chumba chao. Njia nzima walikuwa wakimwagiana mvua ya mabusu kwa mahaba, wakakokotana mpaka chumbani kwao, Harrison akamuinua mkewe juujuu na kumbwaga juu ya kitanda kikubwa cha kisasa. Wakaanza kupashana miili yao joto kwa ajili ya safari ya kwanza kuelekea kwenye ulimwengu wa mahaba. Baada ya takribani dakika kumi na tano, kila mtu alikuwa hajiwezi kwa hisia za kimapenzi. Angel alikuwa akiguna kimahaba wakati Harrison akivinjari sehemu mbalimbali za mwili wake, hali iliyomfanya azidishe utundu. Wote walipokuwa tayari, waliianza safari kwa mara ya kwanza. Wakiwa safarini, Angel alikuwa akipiga kelele sana wakati Harrison akitumia nguvu kubwa kuuvunja ukuta imara wa ngome yake kwani hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kusafiri kuelekea kwenye ulimwengu wa huba. Huo ukawa mwanzo wa wawili hao kushiriki tendo la ndoa. Mwanzo ulikuwa mgumu sana kwa Angel lakini kwa kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kusonga mbele, akawa anazoea huku yale maumivu makali aliyoyahisi mwanzo wa safari yakiisha kabisa. Fungate ilikuwa tamu sana kwa wote wawili, siku zikawa zinakwenda kwa kasi kuliko kawaida huku upendo ukizidi kushamiri kati ya wanandoa hao. Baada ya kumaliza muda wao wa kukaa fungate, Harrison na mkewe walifunga safari ya kurudi kwenye makazi yao, Abbotsford nchini Canada. Wakasafirishwa kwa gari maalum la hoteli waliyofikia mpaka kwenye Uwanja wa Ndege wa Speightstown kwenye Visiwa vya Barbados. Safari ya kurejea nyumbani kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Trans Atlantic ikaanza. Walifika salama na kuendelea na maisha yao, sasa wakiwa mume na mke halali. Siku zilizidi kusonga mbele, kwa pamoja wakakubaliana kwamba wasifanye haraka kwenye suala zima la kutafuta mtoto mpaka maisha yao yatakapotengemaa. Harrison akaanza kutafuta kazi kwani japokuwa alikuwa na fedha za kutosha, hakutaka kukaa nyumbani siku zote. Japokuwa hakuwa na vyeti vyake, lakini ujuzi aliokuwa nao ulisababisha apate kazi haraka kwenye idara ya uchunguzi wa tabia za wanyama na mimea kwenye Mji wa Abbotsford. Hakutaka mkewe naye awe mama wa nyumbani, akamtafutia chuo cha mafunzo ya kompyuta. Wakawa wanaondoka pamoja asubuhi mpaka kwenye Chuo cha Langley Computer College ambapo Harrison alikuwa akimuacha mkewe kisha yeye kuelekea kazini kwake. Jioni alikuwa akimpitia na kurudi naye nyumbani, maisha yakawa yanazidi kuwa matamu. Kama walivyokuwa wameapa madhabahuni, kila mmoja alizidi kuonesha upendo wa dhati kwa mwenzake, wakawa wanazidi kupendana kwa kadiri siku zilivyokuwa zinasonga mbele na kuwa mfano wa kuigwa kwa watu wote waliokuwa wanawazunguka, kuanzia nyumbani, chuoni kwa Angel mpaka kazini kwa Harrison. *** Baada ya baba yake kukamilisha mahitaji yote aliyokuwa anayataka ili kufungua kampuni yake binafsi ya upelelezi jijini Miami, Florida, Linda alizidi kuongeza juhudi kwenye masomo yake ya ujasusi, safari hii akiwa na matumaini makubwa ya kutimiza ndoto zake. Hatimaye aliingia mwaka wa tatu na wa mwisho wa masomo yake. Kama alivyoanza mwanzo, hakutaka kulegeza kamba hata kidogo, akaendelea kuongeza juhudi mpaka siku ya mwisho aliyohitimu masomo yake. Akatunukiwa shahada ya kwanza ya Crime Scene Investigation. Mahafali yakafanyika chuoni hapo ambapo wazazi wengi ambao vijana wao walikuwa wakihitimu walijumuika nao, wakiwemo mzee Ford (baba yake Linda) na mkewe. Baada ya mahafali kumalizika, walisafiri na binti yao mpaka nyumbani kwao, Miami. Linda hakutaka kupumzika hata kidogo, alifikia moja kwa moja kwenye kampuni yake. Siku chache baadaye, kampuni yake ya American Private Investigation Bureau ikazinduliwa rasmi. *** Nisingependa kumaliza hadithi hii ya leo bila kukumbusha jambo muhimu la kutoa maisha yako kwa Mungu. Maisha tuliyonayo hapa duniani ni mafupi sana, yanapita kama maua yachanuavyo na kunyauka. Wengi unaowafahamu wamekufa lakini wewe unapumua, ni vyema basi kufikiria maisha baada ya kifo. Kila siku jiulize: “Hivi nikifa leo nitakwenda jehanam au peponi?” Kila mmoja wetu analo jibu lake, bila shaka sote tungependa kwenda peponi. Kama hivyo ndivyo, basi tiketi ya kwenda huko ni matendo mema na kujiepusha na uovu. Tukumbuke mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele.
MCHUMIA juani hulia kivulini. Harrison aliyesota kwa kipindi kirefu akilihangaikia penzi la malkia wa masokwe, hatimaye anafanikiwa kupata alichokuwa anakitaka. Anamtorosha msichana huyo aliyekuwa analindwa na kundi
kubwa la masokwe kutoka ndani ya Msitu wa Tongass na kwenda naye nchini Canada. Baada ya kufika nchini Canada, kwenye Mji wa Abbotsford, Harrison anafanya kazi ya ziada ya kumbadilisha
msichana huyo na hatimaye anafanikiwa kumfundisha ustaarabu wa kibinadamu. Pia anamtafutia mwalimu anayemfundisha kuongea, kusoma na kuandika. Baada ya muda, malkia wa masokwe anabadilika kabisa na sasa anakuwa na haiba kama binadamu wengine.
Baada ya kuridhishwa na mabadiliko aliyokuwa nayo, Harrison na msichana huyo wanaanza kujifunza masomo ya ndoa na mambo ya kiroho na baadaye wanajitambulisha rasmi kama wachumba. Mipango ya ndoa inaanza kupangwa huku kila kitu kikiendeshwa kwa usiri, hatimaye wanafunga ndoa halali kanisani iliyohudhuriwa na watu muhimu tu.
Muda mfupi baada ya kufunga ndoa, wanaondoka pamoja kuelekea kwenye Visiwa vya Barbados wanakoenda kula fungate kwa muda wa mwezi mzima. Baada ya kumaliza fungate, wanarejea kwenye makazi yao ambapo Harrison anamuandikisha mkewe kusomea kompyuta na yeye anatafuta kazi.
Upande wa pili, Linda ameshahitimu masomo ya Crime Scene Investigation na kutunukiwa shahada yake. Baba yake ameshamfanyia mipango yote ya kufungua kampuni binafsi ya upelelezi.
BAADA ya mahafali kumalizika, walisafiri na binti yao mpaka nyumbani kwao, Miami. Linda hakutaka kupumzika hata kidogo, alifikia moja kwa moja kwenye kampuni yake. Siku chache baadaye, kampuni yake ya American Private Investigation Bureau ikazinduliwa rasmi. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Linda akiwa ndiyo mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo, aliwaajiri wapelelezi wengine kadhaa pamoja na watu wa kumsaidia kazi, baada ya uzinduzi wa kampuni hiyo uliohudhuriwa na watu wengi mashuhuri nchini Marekani, wakiwemo rafiki za baba yake, Linda alianza rasmi kazi na kama alivyokuwa amejiwekea nadhiri ndani ya moyo wake, jukumu la kwanza lilikuwa ni kufuatilia juu ya kifo cha Harrison.
Kwa kuwa sasa alikuwa ni mpelelezi aliyekamilika, akiwa amesajiliwa katika bodi ya wataalamu wa Crime Scene Investigation, kila kitu kilikuwa rahisi kwake. Jambo la kwanza alilolifanya ilikuwa ni kwenda mpaka kwenye Daraja la Miami, Florida, mahali Harrison alipopatia ajali. Kwa kutumia mbinu za kiintelijensia alizokuwa amejifunza chuoni, alianza kwa kulikagua eneo lote huku akipiga picha kwa kutumia kamera maalum. Alikuwa akichunguza kitu kimoja baada ya kingine, kuanzia urefu wa daraja, kina cha maji chini ya daraja hilo, wingi wa magari yanayopita kwa dakika moja pamoja na taarifa nyingine muhimu.
Kama alivyokuwa amebaini hata kabla hajaenda kusomea mafunzo hayo, kina cha maji chini ya daraja hilo kilikuwa kifupi sana, hali iliyomfanya aamini kama mtu akitumbukia eneo hilo, hawezi kufa kirahisi. Pia hata urefu wa daraja, kutoka juu mpaka kwenye usawa wa bahari, haukuwa mrefu kiasi cha kutisha.
Baada ya kufanya uchunguzi wa kina katika eneo hilo uliochukua zaidi ya saa tatu, alirudi ofisini kwake na kuweka vizuri taarifa zake katika ‘database’ ya kompyuta yake. Aliandika baadhi ya vitu kwenye kitabu chake maalum kisha akatoka na kuelekea kwenye Kituo Kikuu cha Polisi cha Miami County.
Alipofika alijitambulisha ikiwa ni pamoja na kutoa kitambulisho chake, akapokelewa kwa unyenyekevu na kuelekezwa ofisi aliyokuwa anataka kuingia. Shida yake kubwa ilikuwa ni kuonana kwa mara nyingine na afisa mkuu wa upelelezi wa kituo hicho, ambaye kipindi cha nyuma alikataa kumpa ushirikiano alipotaka kujua undani wa ajali iliyomuua kipenzi cha moyo wake, Harrison.
Tofauti na alivyotegemea, alipofika kwenye ofisi iliyokuwa na maandishi makubwa yaliyosomeka Crime Scene Department, alikutana na sura tofauti na ile aliyoikuta miaka kadhaa iliyopita. Safari hii alimkuta kijana ambaye hawakuwa wakipishana naye sana umri, wakasalimiana kisha Linda akajitambulisha. Baada ya utambulisho, Linda alieleza shida iliyompeleka. “Mbona tukio lenyewe lilitokea siku nyingi sana? Kwa nini unataka kujua undani wake leo?”
“Kuna sababu maalum za kiintelijensia, nakuomba unipe msaada ninaouhitaji,” alisema Linda kwa msisitizo, akionesha kutokuwa na hata chembe ya masihara.
Baada ya mazungumzo mafupi, yule afisa alinyanyua mkonga wa simu yake na kupiga namba fulani. Baada ya muda, akaingia msichana nadhifu na kumsabahi Linda kisha akamsogelea bosi wake kumsikiliza. Alimpa maelezo ya kwenda kutafuta faili lililokuwa na maelezo ya ajali hiyo.
Kwa kuwa Linda alikuwa anakumbuka mpaka tarehe ya siku ya ajali, kazi haikuwa ngumu. Yule msichana akaondoka na kuelekea kwenye chumba maalum mafaili hayo yalipokuwa yanahifadhiwa. Baada ya kupekua kwa zaidi ya nusu saa, alifanikiwa kulipata faili na kulipeleka ofisini kwa bosi wake.
Faili limepatikana, niambie unataka kujua kitu gani kutoka humu ndani.” “Kwanza nataka kuona mchoro wa namna ajali ilivyotokea, ramani ya eneo la tukio lilivyokutwa baada ya ajali na kila kitu kilichokuwepo, alama zilizoachwa eneo la tukio, ripoti ya daktari aliyeupima mwili wa marehemu na sehemu alikoenda kuzikwa,” alisema Linda kwa msisitizo.
Kwa kuwa alikuwa akihitaji vitu vingi sana, alikabidhiwa faili zima, akaambiwa kila kitu kilikuwa ndani yake lakini haruhusiwi kuondoka nalo kwa mujibu wa taratibu za kiuchunguzi na kiintelijensia. Bila kupoteza muda, Linda alilipokea faili hilo na kuomba apewe muda wa kukaa peke yake kwa ajili ya kulipitia kwa kina na kuangalia kila kitu alichokuwa anakihitaji.
“Mpeleke chumba cha wageni, nafikiri kuna utulivu wa kutosha,” alisema yule afisa akimpa maelekezo msaidizi wake. Linda akatoka na kuongozana na yule msichana mpaka kwenye chumba maalum kilichokuwa kimetengwa kwa ajili ya wageni. Akakaa na kushusha pumzi ndefu kabla ya kuanza kulipitia, ukurasa mmoja baada ya mwingine. Baada ya kutulia kwa sekunde kadhaa, huku
mapigo ya moyo wake yakimuenda kasi kuliko kawaida, alianza kufunua ukurasa wa kwanza uliokuwa na maelezo ya hali ilivyokuwa eneo la tukio. Alisoma neno moja baada ya jingine kwa umakini mkubwa, huku akiandika vitu muhimu kwenye kitabu chake. Kwa mujibu wa maelezo yaliyokuwa yameandikwa kwenye faili hilo, ilionesha kuwa Harrison akiwa anaendesha pikipiki, aligongwa na gari kwa nyuma na kuburuzwa mita kadhaa kwenye kingo za daraja, kisha akatupwa mpaka baharini.
Alipomaliza kusoma ukurasa wa kwanza, alifunua ukurasa wa pili ambao ulikuwa na picha za marehemu kama alivyokutwa eneo la tukio akiwa anaelea baharini, picha ya pikipiki aliyokuwa anaitumia na maelezo mengine muhimu. Aliitazama picha ya marehemu ya kwanza, akaitazama ya pili na ya tatu. Katika kitu kilichomshangaza, katika picha zote zilizopigwa, hakukuwa na picha iliyokuwa inamuonesha marehemu usoni.
“Ina maana ajali hiyo ilisababisha uso wake uharibike kiasi cha kutotambulika?” alijiuliza Linda huku akiendelea kuzitazama picha zile kwa umakini mkubwa. Aligandisha macho yake juu ya picha hizo kwa muda mrefu, akajikuta amezama kwenye dimbwi la mawazo machungu. Alipozinduka, alianza kuitazama pikipiki aliyokuwa anaitumia marehemu ambayo nayo ilionekana kubondeka vibaya. Akawa anajiuliza kama iligongwa kutokea nyuma, mbona taa zake hazikuwa zimepasuka na wala hakukuwa na dalili zozote za kugongwa kutokea nyuma?
Alishusha pumzi ndefu na kuandika baadhi ya vitu katika kitabu chake cheusi. Akafunua ukurasa mwingine ambao ulikuwa na alama zilizokutwa eneo la tukio. Alianza kufuatilia kwa kina kila kitu, katika hali iliyomuacha mdomo wazi, aligundua uwepo wa alama za viatu vya watu wawili tofauti.
Alizifuatilia kwa makini, zikaonesha kusogea mpaka kwenye kingo za daraja kisha zikageuka na kurudi zilikotokea. “Mbona inaonesha kama kuna watu walitupa kitu baharini,” alijiuliza Linda huku akiziangalia vizuri zile picha. ***
BAADA ya Harrison kusota kwa kipindi kirefu akilihangaikia penzi la malkia wa masokwe, hatimaye anatimiza ndoto zake. Anafanikiwa kumtorosha msichana huyo aliyekuwa akilindwa na kundi kubwa la masokwe kutoka ndani ya Msitu wa Tongass na kwenda naye nchini Canada.
Wakiwa katika Mji wa Abbotsford nchini Canada, Harrison anafanya kazi ya ziada kumbadilisha msichana huyo ambapo anafanikiwa kumfundisha ustaarabu wa kibinadamu. Pia anamtafutia mwalimu wa kumfundisha elimu ya kidunia.
Baada ya muda, malkia wa masokwe anabadilika kabisa na sasa anakuwa na haiba kama binadamu wengine. Baadaye wanaanza kujifunza mafunzo ya ndoa na uhusiano kisha wanatangaza uchumba. Mipango ya ndoa inaanza kupangwa na hatimaye wanafunga ndoa halali kanisani. Baada ya kufunga ndoa, wanaelekea kula fungate katika Visiwa vya Barbados kisha kurejea Abbortsford.
Harrison anamuandikisha mkewe kusomea kompyuta na yeye anatafuta kazi. Wanaendelea na maisha yao wakiwa kama mume na mke halali. Upande wa pili, baada ya Linda kuhitimu masomo ya Crime Scene Investigation anaanza kufanya kazi kwenye kampuni yake binafsi ya upelelezi akiwa na ari kubwa ya kuufahamu ukweli nyuma ya kifo cha kipenzi cha moyo wake, Harrison.
Hatua za awali za upelelezi wake zinamuwezesha kufahamu mambo mengi yaliyokuwa yanaashiria kuwa Harrison hakufa kifo cha kawaida kama watu wengi walivyokuwa wanaelewa. Anajiapiza kuendelea na kazi hiyo mpaka aufahamu ukweli. Anagundua kuwepo kwa alama za viatu za watu wawili tofauti eneo ambalo Harrison alipata ajali.
Linda alizifuatilia kwa makini alama hizo za viatu, zikaonesha kusogea mpaka kwenye kingo za daraja kisha zikageuka na kurudi zilikotokea.
“Mbona inaonesha kama kuna watu walitupa kitu baharini,” alijiuliza Linda huku akizitazama vizuri zile picha. Alichokibaini kilimshangaza sana, akarudia tena na tena kuzitazama zile picha, kweli ilionesha kuwa haikuwa ajali ya kawaida. Ilivyoonekana, kuna kitu kilitupwa baharini na watu wawili waliokuwa wanasaidiana, jambo lililozidisha shauku ndani ya moyo wake ya kutaka kuufahamu ukweli.
Baada ya kugundua jambo hilo, Linda aliendelea kufunua kurasa nyingine za faili lile, akafika kwenye ukurasa uliokuwa na ripoti ya alama za vidole zilizokutwa kwenye pikipiki. Pia katika hali ambayo ilimshangaza, aligundua kuwa pikipiki iliguswa kwenye usukani na zaidi ya mtu mmoja.
“Lazima kuna jambo hapa, haiwezekani,” alisema Linda huku akiendelea kufuatilia taarifa zote zilizokuwa ndani ya faili lile. Kilichomshangaza zaidi ni kukosekana kwa umakini kwa askari waliofika kuchunguza eneo la ajali kwani kuna vitu vya wazi mno hawakuvifanyia kazi.
“Kwa nini maafisa wa polisi waliofanya uchunguzi eneo la tukio hawakubaini vitu hivi muhimu ambavyo mimi naviona? Au hawakuwa na elimu ya kutosha kama mimi?” alijiuliza Linda, mwisho akajipa majibu mwenyewe kuwa huenda hawakutilia mashaka tukio hilo na kuona ni la kawaida ndiyo maana hawakujishughulisha zaidi.
Aliendelea kufunua kurasa nyingine za faili lile ambapo alibaini vitu vingi vilivyozidi kumfanya aamini kuwa lazima kuna njama zilikuwa nyuma ya tukio hilo. Alipomaliza, alishusha pumzi ndefu na kuinuka, akalibeba faili na kulirudisha ofisini ambapo alimshukuru bosi wa kitengo cha Crime Scene Investigation kisha akaagana naye na kuondoka, kichwani akiwa na mawazo lukuki.
Kwa jinsi alivyokuwa anajisikia, hakutaka kurudi kazini, aliongoza moja kwa moja mpaka nyumbani kwao, akaingia chumbani kwake na kujifungia. Akajitupa kitandani huku machozi yakianza kumtoka na kudondokea kwenye shuka. Mawazo mengi yalikuwa yakipita ndani ya kichwa chake, alijiuliza maswali mengi lakini hakupata majibu.
Utata alioubaini ulimfanya aumie sana ndani ya mtima wake, akajua kumbe tukio zima halikuwa mipango ya Mungu kama ambavyo watu wote walikuwa wanaamini bali kulikuwa na mkono wa mtu nyuma yake. Hali hiyo iliamsha majonzi upya, akawa anakumbuka maumivu aliyoyapata kuanzia siku aliyopokea taarifa za kifo cha mpenzi wake huyo mpaka siku hiyo. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Sikubali, sikubali nasema, lazima niujue ukweli,” alisema Linda huku akijifuta machozi. Hakuweza kufanya jambo lolote kwa siku hiyo, hata chakula hakula, akaendelea kujifungia chumbani kwake huku akiomboleza. Mama yake alishtushwa na hali hiyo, akaenda kujaribu kumgongea mlango lakini Linda hakufungua mpaka asubuhi ya siku ya pili.
Kulipopambazuka, Linda aliwahi kuamka kuliko siku zote, akajiandaa na kuchukua vitu vyake muhimu, moja kwa moja akaelekea ofisini kwake ambapo siku hiyo alikuwa wa kwanza kufika. Akaingia na kuanza kupanga namna ya kuendesha oparesheni ngumu na ya hatari ya kutaka kubaini ukweli uliokuwa nyuma ya tukio hilo.
Alianza kwa kuandika jinsi alivyokuwa anataka mpango mzima ufanyike, jambo la kwanza alitaka kuomba kibali cha kwenda kulifukua kaburi alilozikwa Harrison kwa lengo la kupima vinasaba (DNA) kwenye masalia ya mwili wake kutaka kubaini kama kweli aliyezikwa ni Harrison.
Pia akapanga kwenda kuonana na mamlaka iliyokuwa inashughulikia kazi ya kuongoza kamera za usalama barabarani kwa lengo la kuangalia siku ya tukio nani na nani walifika eneo hilo na walichokifanya.
“Naamini nikifanikisha hizi kazi mbili nitapata ukweli wa kinachoendelea,” alisema Linda na kushusha pumzi ndefu. Bila kupoteza muda alienda mpaka makao makuu ya polisi jijini Miami. Akaomba kukutana na mkuu wa kituo kuomba kibali maalum cha kuufukua mwili wa marehemu.
Alitoka hadi kwenye maegesho ya magari, akaingia ndani ya gari lake la kifahari alilonunuliwa na baba yake kama zawadi wakati anahitimu masomo yake ya Crime Scene Investigation. Akawasha na kuondoka kwa mwendo wa taratibu kuelekea kwenye Makao Makuu ya Polisi, Miami County.
Alipofika aliomba kuonana na mkuu wa jeshi la polisi kwenye Jimbo la Florida ambapo alijitambulisha na kuonesha vitambulisho vyake, kisha akaeleza shida yake. Kwa kuwa na yeye alikuwa mtaalamu aliyefuzu, alipewa kibali cha kwenda kufukua kaburi la Harrison lakini akaelekezwa kuwa watu wa mwisho wenye mamlaka ya kumruhusu ni Halmashauri ya Jiji la Miami.
Alipewa fomu maalum ambazo alizijaza kisha zikapigwa mhuri na kuwekwa saini na mkuu wa polisi, akamshukuru na kuaga. Akatoka hadi nje alikokuwa amepaki gari lake na safari ya kuelekea kwenye Ofisi za Halmashauri ya Jiji la Miami ikaanza. Alipofika, alikutana moja kwa moja na Meya wa Jiji la Miami, Collins Duke. Akajitambulisha na kueleza shida yake.
Bila hiyana, meya huyo aliweka saini yake katika ile fomu maalum aliyopewa na polisi, akamuelekeza kwenda kwenye ofisi za daktari mkuu wa jiji ambaye angempa wataalamu wa afya wa kwenda kusaidiana naye. Linda alimshukuru na kutoka nje, akafuata ramani aliyopewa kwenda kwenye ofisi ya daktari mkuu ambayo ilikuwa ghorofa ya chini katika jengo kubwa la Halmashauri ya Jiji la Miami. Aliingia kwenye lifti na kushuka hadi ghorofa ya chini, akakata kona kuelekea upande wa kushoto mpaka alipofika kwenye ofisi ya daktari mkuu.
Kama kawaida yake, alijitambulisha na kuonesha vielelezo vyote muhimu. Daktari mkuu wa jiji naye akaweka saini kwenye sehemu yake lakini kabla ya kuwateua wataalamu watano wa afya ambao wangeongozana naye hadi kwenye Makaburi ya Miami Cemetery, alimuuliza swali. “Ndugu zake wana taarifa ya unachotaka kukifanya?” “Hapana, hawana taarifa.”
“Hatuwezi kukuruhusu mpaka upate idhini kutoka kwa ndugu zake. Fuatilia hilo kwanza ukishakamilisha, uje na mwakilishi yeyote kutoka kwenye familia ya marehemu ndiyo utaongozana na wataalamu kutoka ofisi yangu,” alisema Daktari Adams Phillips, Linda akaahidi kurejea ofisini kwake siku inayofuata akiwa na mwakilishi kutoka familia ya marehemu.
Alipotoka aliongoza moja kwa moja kwa kutumia gari lake mpaka nyumbani kwa akina Harrison, walikokuwa wanaishi mama wa marehemu, Skyler, babu na bibi yake. Kwa bahati mbaya, alipofika hakumkuta mtu, hali iliyomlazimu kusubiri kwa muda mrefu mpaka jioni.
Mtu wa kwanza kurejea nyumbani alikuwa ni mama mzazi wa Harrison ambaye alipomuona Linda, alishtuka sana, akamkaribisha ndani huku akiwa na shauku ya kutaka kujua kilichompeleka. Bila kupoteza muda, Linda akaanza kumueleza alichokibaini juu ya kifo cha Harrison na alichokuwa anataka kukifanya. ***
Harrison tayari amefanikiwa kutimiza ndoto yake ya siku nyingi ya kumpata malkia wa masokwe, baada ya kusota kwa kipindi kirefu akilihangaikia penzi lake kwenye Msitu wa Tongass. Amevumilia mateso ya muda mrefu wakati akilipigania penzi la msichana huyo aliyekuwa akilindwa na kundi kubwa la masokwe.
Baada ya kutoka ndani ya msitu huo, anatoroka naye na kwenda mpaka nchini Canada anakoenda kuishi na msichana huyo katika Mji wa Abbotsford nchini Canada. Harrison anaanza kazi ya kumbadilisha msichana huyo ambapo anafanikiwa kumfundisha ustaarabu wa kibinadamu. Pia anamtafutia mwalimu wa kumfundisha elimu ya kidunia.
Malkia wa masokwe anabadilika kabisa na sasa anakuwa na haiba kama binadamu wengine. Baadaye wanatangaza uchumba na mipango ya ndoa inaanza kupangwa. Hatimaye wanafunga ndoa halali kanisani na kuwa mume na mke halali. Harrison anamuandikisha mkewe kusomea kompyuta na yeye anatafuta kazi. Wanaendelea na maisha yao kama kawaida.
Upande wa pili, baada ya Linda kuhitimu masomo ya Crime Scene Investigation anaanza kufanya kazi kwenye kampuni yake binafsi ya upelelezi akiwa na ari kubwa ya kuufahamu ukweli uliojificha nyuma ya kifo cha kipenzi cha moyo wake, Harrison.
Upelelezi wake unamuwezesha kufahamu mambo mengi yaliyokuwa yanaashiria kuwa Harrison hakufa kifo cha kawaida kama watu wengi walivyokuwa wanaelewa. Anaendelea na upelelezi ambapo anabaini vitu vingi vilivyokuwa na utata wa hali ya juu. Mwisho akaanza kushughulikia kibali cha kufukua kaburi la Harrison akiwa na nia ya kuchukua vipimo vya DNA.
Mtu wa kwanza kurejea nyumbani alikuwa ni mama mzazi wa Harrison ambaye alipomuona Linda, alishtuka sana, akamkaribisha ndani huku akiwa na shauku ya kutaka kujua kilichompeleka. Bila kupoteza muda, Linda akaanza kumueleza alichokibaini juu ya kifo cha Harrison na alichokuwa anataka kukifanya. “Nahisi Harrison hakufa kwa mipango ya Mungu, lazima kuna mkono wa mtu.” “Kwa nini unasema hivyo Linda?” “Nimefanya utafiti wa kitaalamu, nimegundua kuwa lazima kuna njama zilifanyika, nahitaji baraka zenu ili niendelee na upelelezi utakaoibua majibu kamili juu ya nini kilichosababisha Harrison akafa.”
“Hamna shida mama, mimi nakubaliana na wewe kwa roho nyeupe kabisa, nina hamu kubwa ya kuufahamu ukweli,” alisema Skyler huku akilengwalengwa na machozi. Hata alipomueleza kuwa ili kupata kibali cha kufukua mwili wa marehemu (exhumation order) inahitajika aongozane naye hadi kwenye ofisi za Manispaa ya Jiji, Skyler hakuwa na pingamizi.
Wakakubaliana kuwa asubuhi ya siku inayofuatia, atampitia ili waongozane pamoja kwenda kufuatilia kibali hicho. Linda akaondoka huku akiwa na matumaini makubwa ya kufanikisha kazi kubwa iliyokuwa mbele yake. Alipofika nyumbani kwao, Linda aliwaeleza baba na mama yake kila kitu kilichokuwa kinaendelea.
Nao wakaahidi kuwa kesho wataungana naye makaburini watakapoenda kuufukua mwili wa Harrison. Baada ya kula chakula cha usiku, Linda alikuwa anaona kama saa hazisogea haraka, akawa anatamani kupambazuke haraka akakamilishe kazi ya kuufukua mwili wa Harrison na kuchukua vipimo vya DNA.
Kulipopambazuka, Linda ndiyo alikuwa wa kwanza kuamka, akaanza kujiandaa na kuwaamsha wazazi wake ili nao wajiandae. Kila mmoja alipokuwa tayari, waliingia ndani ya gari la familia na kwenda moja kwa moja mpaka nyumbani kwa akina Skyler. Wakamchukua na kwenda moja kwa moja mpaka kwenye ofisi za Halmashauri ya Jiji la Miami.
Baada ya kukamilisha taratibu zote za kiserikali zilizokuwa zinatakiwa, Linda alikabidhiwa kibali cha kufukua kaburi la Harrison. Wakapewa na wafanyakazi wa halmashauri, gari, vifaa pamoja na daktari kwa ajili ya kuzingatia usalama wa afya zao watakapokuwa wanafanya zoezi hilo.
Safari ya kuelekea kwenye Makaburi ya Miami Cemetery ikaanza, gari la halmashauri likawa mbele na gari walilopanda Linda, wazazi wake na Skyler likawa linafuata nyuma. Walipofika, walipaki magari yao na kutembea kuelekea kwenye kaburi la Harrison.
Kazi ya kulifukua ikaanza. Kazi haikuwa nyepesi, ilibidi wafanyakazi hao watumie akili ya ziada kuvunja zege juu ya kaburi hilo, wakafanikiwa kusogeza mfuniko na mmoja kati yao akaingia mpaka ndani ya kaburi na kuchukua mabaki ya mfupa mdogo na nywele.
Wakati zoezi hilo likiendelea, kwa upande wa Linda alikuwa akijisikia vibaya sana. Picha za siku ya mazishi ya Harrison zilikuwa zikijirudia akilini mwake, hali iliyomfanya alie kwa uchungu sana. Hali ilikuwa hivyohivyo kwa Skyler, alikuwa akilia kwa uchungu sana utafikiri siku hiyo ndiyo mwanaye wa kipekee aliiaga dunia.
Baba na mama yake Linda wakawa na kazi ya ziada ya kuwatuliza. Zoezi liliendelea, vitu vilivyochukuliwa kaburini vikawekwa kwenye mfuko maalum na kufungwa kitaalamu, kaburi likajengewa upya na mfuniko ukarudishwa mahali pake.
Baada ya kazi kumalizika, Linda aliwashukuru sana wafanyakazi wale wa halmashauri, wazazi wake pamoja na mama mzazi wa Harrison kwa ushirikiano waliomuonesha. Pia alimuomba Skyler atoe nywele zake kidogo ambazo zingetumika kufananisha vinasaba (DNA) kati ya marehemu na mama yake.
“Lazima niupate ukweli kwa gharama yoyote,” alisema Linda huku akijifuta machozi, akampa maelekezo daktari aliyeongozana naye alichokuwa anakitaka. Alitoa cheki na kuwapa wale wafanyakazi wa halmashauri kama shukrani kwa kazi waliyoifanya kisha wakaondoka eneo hilo la makaburini.
Kwa jinsi alivyokuwa anajisikia uchungu, Linda alishindwa kufanya kitu chochote siku hiyo. Hali hiyo ilimtokea pia Skyler ambaye alikuwa akiomboleza kwa uchungu. Kesho yake, Linda akawahi kuamka na kuanza kujiandaa kwa ajili ya kwenda kukutana na yule daktari waliyeongozana naye makaburini.
“Vipi umefikia wapi?” “Mh! Nimeshachukua vipimo vya DNA lakini majibu yanaonesha utata.” “Utata? Kwani umegundua nini?” “Majibu yanaonesha kutofanana kati ya DNA za mwili tulioufukua kaburini na ya mama yake Harrison.” “Mungu wangu, kwa hiyo unataka kusemaje?” “Mwili uliozikwa kwenye kaburi hilo siyo wa Harrison,” alisema daktari huyo kwa msisitizo huku akimkabidhi Linda majibu ya vipimo vya DNA.
Alijikuta akishindwa kuyazuia machozi ya uchungu, akaagana na daktari na kuondoka na majibu yake huku akiendelea kulia. Akaenda mpaka kwenye gari na kuingia. Aliingia kwenye gari lake na kuegamia usukani, machozi yakawa yanazidi kumtoka.
“Umepatwa na nini Harrison wangu? Kwa nini haya yananitokea mimi? Ina maana hukufa? Kama ni hivyo, uko wapi baba… njoo tutimize ahadi yetu ya kufunga ndoa, njoo Harrison wangu! Sijawahi kuwa na furaha tangu ulipoondoka kwenye maisha yangu, rudi baba…” alisema Linda kwa uchungu huku donge likiwa limemkaba shingoni.
Alilia kwa muda mrefu sana mpaka macho yakavimba na kuwa mekundu. Aliendelea kulia mpaka akapitiwa na usingizi akiwa ndani ya gari. Alikuja kushtuliwa na mlinzi aliyekuwa anagonga kioo cha gari lake, baada ya kumuona amelala kwa muda mrefu. “Una tatizo dada?”
“Ha.. hapana kaka yangu,” alijibu Linda huku akijinyoosha na kujifikicha macho, akawasha gari na kuondoka kwa mwendo wa kasi. Mlinzi alibaki amepigwa na butwaa kwani kwa kasi aliyoondoka nayo Linda, hakujua kama atafika salama huko aendako. Alipoingia kwenye barabara kubwa, Linda alizidi kukanyaga mafuta, gari lake likawa linaenda kwa kasi kubwa iliyowashtua madereva wengine.
Baadhi ya magari yakawa yanasimama kumpisha kwani alionesha kuchanganyikiwa. Majibu ya DNA aliyopewa, yalimfanya awe kama mwendawazimu. ***
NDOTO za Harrison za kuishi na malkia wa masokwe, hatimaye zimetimia. Baada ya kuhangaika kwa kipindi kirefu akitafuta nafasi ya kumtorosha kwenye Msitu wa Tongass, Harrison anafanikiwa kumpata msichana huyo aliyekuwa akilindwa na kundi kubwa la masokwe.
Anatoroka naye kutoka ndani ya msitu huo hadi nchini Canada anakoenda kuishi naye katika Mji wa Abbotsford. Harrison anaanza kazi ya kumbadilisha msichana huyo ambapo anafanikiwa kumfundisha ustaarabu wa kibinadamu. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Msichana huyo anabadilika kabisa na sasa anakuwa na haiba kama binadamu wengine. Baadaye wanafunga ndoa halali kanisani na kuwa mume na mke. Harrison anamuandikisha mkewe kusomea kompyuta na yeye anatafuta kazi. Wanaendelea na maisha yao kama kawaida.
Upande wa pili, baada ya Linda kuhitimu masomo ya Crime Scene Investigation anaanza kufanya kazi kwenye kampuni yake binafsi ya upelelezi akiwa na shauku kubwa ya kuufahamu ukweli uliojificha nyuma ya kifo cha Harrison.
Upelelezi wake unaibua mambo mengi ambapo kuna kila dalili zinazoashiria kuwa Harrison hakufa kifo cha kawaida. Uamuzi wa mwisho anaofikia ni kwenda kulifukua kaburi la Harrison kwa ajili ya kuchukua vipimo vya DNA. Anachokibaini kinamliza sana.
ALIPOINGIA kwenye barabara kubwa, Linda alizidi kukanyaga mafuta, gari lake likawa linaenda kwa kasi kubwa iliyowashtua madereva wengine. Baadhi ya magari yakawa yanasimama kumpisha kwani alionesha kuchanganyikiwa. Majibu ya DNA aliyopewa, yalimfanya awe kama mwendawazimu. Kwa bahati nzuri, hakupata ajali licha ya vurugu alizokuwa anazifanya barabarani, breki ya kwanza ikawa ni nyumbani kwao. Bila hata kulisimamisha gari kwenye eneo maalum la maegesho, Linda aliteremka na kukimbilia ndani kwao huku akiangua kilio kama mtoto mdogo. “Hee! Kuna nini tena mwanangu? Umepatwa na nini?” “Ni bora nife mama, niacheni nife tu, sioni umuhimu wa kuishi.” “Kwani kuna nini Linda?” “Bora nife mimi.” “Mwanangu hebu tulia kwanza utueleze,” mama yake Linda alikuwa akimtuliza mwanaye huku baba yake, mzee Ford naye akionesha kushtushwa na hali aliyokuwa nayo binti yao. Licha ya kubembelezwa sana, Linda hakutaka kusema chochote zaidi ya kuendelea kulia kwa uchungu. Katika purukushani za kumtuliza, Linda alijibamiza ukutani na kudondoka chini kama mzigo, akapoteza fahamu. Hali hiyo ilizidi kuwachanganya wazazi wake, harakaharaka wakamkimbiza mpaka nje, wakampakiza kwenye gari na safari ya kuelekea hospitalini ikaanza. Kutokana na umaarufu wa baba yake, Linda alipofikishwa hospitalini, alipokelewa harakaharaka na kulazwa juu ya kitanda cha magurudumu, wauguzi zaidi ya wanne wakawa wanasaidiana kukisukuma kitanda kumpeleka wodini. “Amepatwa na nini?” “Amejigonga ukutani na kupoteza fahamu.” “Ooh! Poleni sana, atakuwa sawa msijali,” daktari aliyempokea Linda alikuwa akizungumza na wazazi wa binti huyo, nje ya wodi aliyolazwa. Jitihada za haraka zikafanyika ambapo alitundikiwa dripu na kuanza kupewa huduma ya kwanza. Baada ya kutibiwa kwa saa nyingi, hatimaye Linda alizinduka na kujikuta yupo wodini. Akawa anaangaza macho huku na kule akiwa ni kama anajiuliza pale ni wapi na amefikaje. “Mama!” “Abee mwanangu.” “What happened to me?” (Nini kimenitokea?) Mama Linda alimuinamia mwanaye na kumshika kwenye paji la uso, akawa anampa pole na kumsihi atulie. Mara akarejewa na kumbukumbu zake na kuanza kulia upya. “Harrison mama! Harrison!” “Harrison kafanyeje tena mwanangu?” “Harrison hakufa mama…” “Whaaat?” (Niniii?) “Harrison hakufa, kuna mchezo ulifanyika, nimepata ushahidi,” alisema Linda huku akilia kwa kwikwi, mama yake akabaki amepigwa na butwaa kutokana na maelezo yale. Harakaharaka alitoka na kwenda kumuita mumewe, mzee Ford aliyekuwa nje ya wodi, wakaongozana hadi ndani kumsikiliza Linda alichokuwa anakisema. Bado alieleza vilevile kama alivyomwambia mama yake, safari hii akilia kwa nguvu. Ilibidi daktari aje kumchoma sindano ya usingizi kwani kwa hali aliyokuwa nayo, kulikuwa na hatari kubwa ya kuendelea kujidhuru. Akaendelea kulala huku wazazi wake wakitazamana, wakiwa hawaamini walichokisikia. “Unataka kusema Harrison hakufa? Mbona hainiingii akilini?” “Mimi mwenyewe hata sielewi, mbona sote tulihudhuria mazishi yake?” “Mh! Labda tusubiri azinduke, yeye mwenyewe ndiyo mtu pekee anayeweza kueleza kilichotokea,” wazazi wa Linda walikuwa wakijadiliana, wakiwa wamesimama nje ya wodi aliyolazwa mtoto wao. Daktari alitoka na kuwaambia kuwa hawatakiwi kumuuliza mgonjwa maswali yoyote mpaka atakapopona kabisa, ushauri ambao waliupokea kwa mikono miwili. Dawa ya usingizi ilipopungua nguvu, Linda alishtuka lakini safari hii alikuwa haeleweki alichokuwa anazungumza kutokana na dawa hizo kumlevya. Daktari aliwaruhusu wazazi wake wamchukue na kurudi naye nyumbani lakini akawasisitiza kumuacha apumzike mpaka atakapokuwa sawa. Walisaidiana kumshika huku na huku, wakatembea taratibu mpaka nje walikokuwa wamepaki gari lao. Mzee Ford aliwafungulia mlango wa nyuma, Linda na mama yake wakaingia na kukaa na yeye akakaa nyuma ya usukani. Safari ya kuelekea nyumbani kwao ikaanza. Linda alijiegamiza kwenye bega la mama yake, machozi yakawa yanaendelea kumtoka mpaka walipofika kwao. Kama walivyoshauriwa na daktari, hakuna aliyemhoji Linda kitu chochote. Walipofika walisaidiana kumteremsha garini na kumpeleka mpaka chumbani kwake. Akaendelea kulala. Kutokana na hali yake ilivyokuwa, mama yake alilazimika kulala naye chumbani kwake mpaka asubuhi. “Mama!” “Abee mwanangu.” “Harrison hakufa mama, nimepata uthibitisho.” “Tuachane na hayo mwanangu, hali yako bado siyo nzuri, ukipona tutaongea kwa kirefu.” “Nimeshapona mama, nimefanya upelelezi na kugundua kuwa mwili tuliouzika haukuwa wa Harrison, roho inaniuma sana mama.” “Basi mwanangu, jikaze kila kitu kitakuwa sawa.” “Siwezi kuwa sawa mama mpaka nijue Harrison alipo, bado nampenda mama.” “Kwani umejuaje kuwa hakufa,” mama Linda aliuliza swali lililomfanya mwanaye aanze kueleza hatua kwa hatua kilichotokea. Maelezo aliyoyatoa yalimfanya mama yake abaki mdomo wazi kwani alikuwa na uthibitisho wa kutosha. Ilibidi akamuite mume wake, wakawa wanajadiliana kwa pamoja juu ya suala hilo. Linda alishikilia msimamo wake kuwa lazima amtafute Harrison kwa gharama zozote ili ajue mbivu na mbichi. Licha ya wazazi wake kumkataza, bado alishikilia msimamo wake, akala yamini kuwa ni lazima aifanye kazi hiyo. ***
Wakati Harrison akifurahia kutimia kwa ndoto zake za siku nyingi za kuishi na malkia wa masokwe, hali si shwari kwa aliyekuwa mpenzi wake, Linda. Baada ya Harrison kuhangaika kwa kipindi kirefu akitafuta nafasi ya kumtorosha malkia wa masokwe kwenye Msitu wa Tongass, anafanikiwa kumpata na kutoroka naye kutoka ndani ya msitu huo hadi nchini Canada.
Baada ya kufika nchini humo, Harrison anaenda kuishi naye katika Mji wa Abbotsford. Harrison anaanza kazi ya kumbadilisha msichana huyo ambapo anafanikiwa kumfundisha ustaarabu wa kibinadamu. Msichana huyo anabadilika kabisa na sasa anakuwa na haiba kama binadamu wengine. Baadaye wanafunga ndoa halali kanisani na kuwa mume na mke. Harrison anamuandikisha mkewe kusomea kompyuta na yeye anatafuta kazi. Wanaendelea na maisha yao kama kawaida. Kwa upande wa Linda, baada ya kuamua kwenda kusomea upelelezi, anahitimu na kutunukiwa shahada ya kwanza ya Crime Scene Investigation kisha anaanza kufanya kazi kwenye kampuni yake binafsi ya upelelezi akiwa na shauku kubwa ya kuufahamu ukweli uliojificha nyuma ya kifo cha Harrison. Katika upelelezi huo, anagundua mambo mengi ambayo yanaashiria kuwa Harrison hakufa kifo cha kawaida. Uamuzi wa mwisho anaofikia ni kwenda kulifukua kaburi la Harrison kwa ajili ya kuchukua vipimo vya DNA. Anachokibaini kinamliza sana kwani anagundua mwili uliozikwa haukuwa wa Harrison. Anachanganyikiwa kabisa na kuanza kuomboleza tukio hilo upya.
Kwa siku tatu nzima, Linda hakwenda kazini badala yake akawa anashinda chumbani kwake akiwa amejifungia. Aliendelea kuomboleza baada ya kubaini kuwa kumbe kulikuwa na njama kali nyuma ya tukio la kifo ‘feki’ cha Harrison. Aliendelea kuwaza kwa kina mahali pa kuanzia. Siku tatu zilipopita, tayari alikuwa na jibu la nini cha kufanya. Alienda kuwasiliana na jeshi la polisi jimboni Florida na kuomba picha za usalama barabarani zilizochukuliwa na kamera za CCTV kuanzia eneo la tukio. Kutokana na kitengo cha usalama barabarani kuwa na utaratibu maalum wa kuhifadhi picha zote za matukio ya barabarani, kazi haikuwa ngumu kwa Linda. Alipofika alijitambulisha na kueleza shida yake ambapo alihojiwa maswali kadhaa kabla ya kuambiwa akasubiri ndani ya chumba maalum. Baada ya takriban dakika ishirini, Linda aliitwa kwenye maktaba maalum ya picha za video na kazi ikaanza. Alipewa rekodi nzima ya matukio ya barabarani ya eneo la tukio, kuanzia muda ambao ilisemekana Harrison alipata ajali. Kama alivyokuwa amebaini awali, ni kweli alishuhudia magari mawili yakiondoka kwa kasi eneo la tukio baada ya ajali kutokea. Alianza kuyafuatilia, moja baada ya jingine. La kwanza lilionekana kurejea kwenye mitaa ya makazi ya watu jijini Miami na la pili lilionekana kusafiri kwa kasi kubwa kuelekea kaskazini, nje ya jimbo la Florida. “Lazima atakuwa kwenye gari hili,” alisema Linda na kumtaka afisa usalama aliyekuwa anamsaidia kazi ile, kulivuta karibu gari hilo na kufuatilia kwa makini upande lilikoelekea. “Mungu wangu, ni yeye kweli,” alisema Linda huku akiwa amekodoa macho yake kwenye ‘skrini’ kubwa iliyokuwa ukutani. Ni kweli alikuwa ni Harrison lakini safari hii hakuwa amevaa mavazi ya harusi. Alikuwa amebadilika na kuvaa nguo ambazo Linda hakuwahi kumuona nazohata siku moja, kichwani akiwa amevaa kofia kubwa. Linda aliendelea kufuatilia gari hilo kwa makini jinsi lilivyokuwa likichanja mbuga. Alilifuatilia kwa makini mpaka lilipotoka nje ya Jiji la Miami na kuingia kwenye Jiji la Orlando. Akaendelea kulifuatilia kwa makini huku akiandika taarifa muhimu kwenye kitabu chake kidogo. Machozi yalikuwa yakimtoka mara kwa mara, akawa analia na Mungu wake kwa kumsababishia mtihani mgumu kiasi hicho. Picha hizo zilimuonesha Harrison alipoenda hadi kwenye kituo cha treni za umeme cha Orlando Metro ambapo alilitelekeza gari alilokuwa analitumia na kwenda kwenye ofisi za stesheni hiyo. “Lazima nitampata tu,” alisema Linda huku ndita zikijionesha dhahiri kwenye uso wake, akamshukuru afisa huyo wa kitengo cha usalama barabarani kwa msaada aliompatia kisha akaaga na kuondoka, huku akilini akiwa ameshapata wazo la nini cha kufanya. Alipotoka, hakutaka kurudi nyumbani, aliendesha gari lake kwa kasi kubwa kuelekea Jiji la Orlando ambapo alipanga kwenda kufuatilia taarifa za wasafiri wote waliopanda treni, siku ajali feki ya Harrison ilipotokea. Kwa kuwa alitaka kuwahi kwenda na kurudi, alilazimika kusafiri kwa kasi kubwa, njia nzima akawa anamlaumu Harrison kwa kitendo alichomfanyia na kumuachia maumivu makali ya mtima kiasi kile. Baada ya kusafiri kwa muda mrefu, akinusurika kupata ajali mara kadhaa, hatimaye aliwasili jijini Orlando na kwenda moja kwa moja mpaka kwenye ofisi za Stesheni ya Orlando Metro. Akaenda kujitambulisha kwa mkuu wa stesheni hiyo na kueleza kilichompeleka. Kwa kuwa alieleza kuwa kazi aliyoifuata hapo ni kwa ajili ya usalama wa nchi, alikubaliwa bila kipingamizi na kupelekwa kwenye chumba maalum kilichokuwa na kompyuta nyingi zilizotumika kuhifadhi ‘Database’ za safari zote za treni. Linda akaomba kutafutiwa rekodi za wasafiri wote waliosafiri kwa treni, siku Harrison aliyopata ajali feki. Kwa kuwa alikuwa na kumbukumbu nzuri za tarehe na muda Harrison alipowasili kituoni hapo, kazi haikuwa ngumu. Taarifa zote za wasafiri wa muda na siku hiyo zikaanza kuoneshwa ambapo alifuatilia jina moja baada ya jingine kuangalia kama ataliona jina la Harrison. Katika kupekuapekua kwake, akakutana na jina la Harrison Harvey ambapo ilionesha kuwa amesafiri siku hiyo kwa treni kuelekea Kituo cha Tongass ambapo ndiyo ilikuwa mwisho wa safari ya treni hiyo. Akashusha pumzi ndefu na kuanza kuandika taarifa muhimu, ikiwa ni pamoja na muda ambao alitegemewa kufikakwenye kituo hicho. Wakati akiendelea kuandika, alikumbukakitu kilichomfanya aunganishe matukio kwa urahisi. Alikumbuka kuhusu kitabu kilichoandikwa na Harrison cha Queen of Gorrilas ambacho kilimpatia umaarufu mkubwa nchini Marekani. “Aliandika kuwa msichana wa ajabu anayelelewa na masokwe anapatikana kwenye msitu wa Tongass, inamaana aliondoka na kwenda kuendelea na utafiti wake kuhusu msichana huyo? Kwa nini hakutaka kumuaga mtu yeyote,” aliwaza Linda huku machozi yakianza tena kumtoka. Akahisi wivu mkali ndani ya nafsi yake. Baada ya kumaliza kuchukua taarifa zote muhimu, alitoka hadi ndani ya gari lake na kukaa kwa muda kuanza kutafakari tafsiri ya matukio aliyokuwa anayagundua kila kukicha. Kwa bahati nzuri, alikumbuka kuwa ndani nyumbani kwao ana nakala ya kitabu cha Queen of Gorrilas. Japokuwa tayari alishamaliza kukisoma kitabu hicho, alijiapiza kwenda kukirudia, kuanzia ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho kwa lengo la kuchunguza vizuri kitu alichokiandika akiamini lazima atapata taarifa zitakazomsaidia kufahamu mahali Harrison alipo. ***CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Maisha yalizidi kuwanyookea Harrison na mkewe, kila mmoja akawa anaendelea na kazi huku wakioneshana upendo wa dhati kila kukicha. Jioni moja wakati wakilishana chakula cha usiku kwa mahaba, Angel au malkia wa masokwe, alionesha dalili ambazo zilimshtua mumewe. Alianza kulalamika kusikia kichefuchefu kikali kilichosababisha atapike chakula chote alichokula. Harrison akawa na kazi ya ziada ya kumsaidia mkewe ambapo alimpeleka chumbani kulala huku akizoa matapishi yote na kusafisha sakafu. “Inabidi kesho twende hospitali mke wangu, inawezekana unaumwa,” alisema Harrison kwa sauti ya upole, wazo lililoungwa mkono na mkewe. Walilala mpaka asubuhi ambapo kulipopambazuka, Harrison alienda kumuombea mkewe ruhusa kazini na yeye akaomba kazini kwake. Wakaongozana mpaka Hospitali ya Langley ambapo walikutana na daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake. Angel akaeleza dalili alizokuwa anazihisi, akachukuliwa vipimo kisha wakaambiwa wasubiri majibu. ***
MAISHA yanazidi kusonga mbele kati ya Harrison na mkewe ambao wanaendelea kuifurahia ndoa yao. Harrison anafurahia kutimia kwa ndoto zake za siku nyingi za kuishi na malkia wa masokwe kwani baada ya kuhangaika kwa kipindi kirefu akitafuta nafasi ya kumtorosha msichana huyo, hatimaye anafanikiwa.
Anamtorosha hadi nchini Canada ambapo baada ya kufika nchini humo, Harrison anaenda kuishi naye katika Mji wa Abbotsford. Anaanza kazi ya kumbadilisha msichana huyo ambapo anafanikiwa kumfundisha ustaarabu wa kibinadamu.
Malkia wa masokwe anabadilika kabisa na sasa anakuwa na haiba kama binadamu wengine. Baadaye wanafunga ndoa halali kanisani na kuwa mume na mke. Harrison anamuandikisha mkewe kusomea kompyuta na yeye anatafuta kazi. Wanaendelea na maisha yao na baada ya muda, Angel anaanza kuhisi dalili zinazowafanya wakubaliane kwenda hospitali.
Upande wa pili, Linda amechachamaa kutaka kuufahamu ukweli juu ya kifo cha Harrison. Baada ya kuhitimu masomo ya Crime Scene Investigation na kutunukiwa shahada yake, anaanza kufanya kazi kwenye kampuni yake binafsi ya upelelezi akiwa na shauku kubwa ya kuufahamu ukweli uliojificha nyuma ya kifo cha Harrison.
Kwa kadiri anavyoendelea na upelelezi huo, anagundua mambo mengi ambayo yanaashiria kuwa Harrison hakufa kifo cha kawaida. Hata baada ya kuamua kulifukua kaburi lake na kupima DNA, anagundua kuwa mwili uliozikwa haukuwa wa Harrison.
Anachanganyikiwa na kuanza upya kuomboleza huku akijipanga namna ya kuendelea na kazi hiyo mpaka aufahamu ukweli. Anatumia mbinu kali alizojifunza chuoni kuendesha upelelezi huo huku akijiapiza kuwa ni lazima ampate Harrison.
Baada ya vipimo kukamilika, daktari aliwaita Harrison na mkewe ofisini kwake ambapo alianza kwa kuwapa hongera. “Hongera ya nini daktari?” “Mkeo ni mjamzito.” “Kweli? Oooh! Ahsante Mungu,” alisema Harrison kwa furaha huku akiinuka na kumkumbatia mke wake ambaye naye alikuwa amepigwa na butwaa akiwa haamini alichokisikia. Walikumbatiana kwa furaha na kumwagiana mvua ya mabusu, kila mmoja akionesha kufurahishwa sana na majibu yale. Daktari aliwapa maelezo ya namna ya kuilea mimba changa ambapo alitoa ushauri kwa Harrison kuhakikisha mkewe hafanyi kazi ngumu zinazoweza kuleta matatizo kwa ujauzito wake. Pia aliwashauri vyakula bora ambavyo mwanamke mjamzito anatakiwa kula ili kumjenga vizuri mtoto tumboni. Baada ya darasa refu, Harrison na mkewe walitoka na safari ya kurudi nyumbani ikaanza. Njia nzima Harrison alikuwa akifurahi kuliko kawaida huku akilibusu tumbo la mkewe mara kwa mara bila kujali watu waliokuwa wanawatazama. Upendo kwa mkewe uliongezeka maradufu, akawa anamdekeza na kumjali kuliko hata ilivyokuwa mwanzo, hali iliyomfanya Angel awe na furaha kupindukia. Kazi zote za nyumbani sasa alikuwa akizifanya Harrison, kuanzia kufua, kusafisha nyumba na mambo mengine mengi, mkewe alibakia na kazi moja tu, kupika. Siku zilizidi kusonga mbele huku amani na upendo wa dhati vikitawala kwenye maisha ya wanandoa hao, ujauzito ukawa unaendelea kukua vizuri bila matatizo yoyote. Harrison alikuwa na shauku kubwa ya kuitwa baba, akawa anamtunza mkewe kama mboni ya jicho. *** Linda alirudi mpaka nyumbani kwao, kama kawaida yake akapitiliza hadi chumbani kwake ambapo alijifungia na kuanza kutafuta kitabu cha Queen of Gorrilas kilichoandikwa na Harrison. Alipokipata, alianza kusoma ukurasa mmoja baada ya mwingine huku akiandika pembeni vitu vyote muhimu ambavyo aliamini vitamsaidia katika kazi yake ya kumsaka Harrison. Jambo ambalo awali hakuwahi kuligundua ni kwamba ndani ya kitabu hicho, Harrison alitumia muda mwingi kumsifia msichana huyo wa ajabu huku akisisitiza kuwa urembo wake haufanani na wa msichana yeyote aliyewahi kukutana naye maishani mwake. Wivu ukaanza kufurukuta ndani ya moyo wa Linda, alijisikia vibaya sana kwa jinsi Harrison alivyousifia urembo wa malkia wa masokwe ndani ya kitabu hicho. Kibaya zaidi, Harrison alieleza waziwazi kuwa msichana huyo wa ajabu alikuwa mrembo kuliko hata yeye Linda, jambo lililozidi kumnyong’onyeza. “Lazima alikuwa anampenda na ndiyo maana akakataa kuoana na mimi, kwa nini Harrison? Kwani mimi siyo mzuri? Kwani sina mvuto? Mbona niliwakataa wanaume wengi kwa sababu yako Harrison?” alisema Linda huku akibubujikwa na machozi, akasimama na kuanza kujiangalia kwenye kioo huku akiendelea kutokwa na machozi. Alijigeuzageuza huku akijiuliza maswali ambayo hakuyapatia majibu. Alikichukua kitabu cha malkia wa masokwe na kuanza kuitazama picha iliyopigwa kwa mbali ya malkia wa masokwe na kuanza kujifananisha nayo. “Mbona mimi ni mzuri kuliko huyo malkia wa masokwe? Mbona mimi ni msafi, najua kujitunza na pia nimesoma? Huyo malkia wa masokwe amenizidi nini?” alijiuliza Linda huku akiendelea kububujikwa na machozi, akakaa kitandani na kuendelea kusoma kitabu. “Kumbe Msitu wa Tongass upo kwenye mpaka kati ya Marekani na Canada? Lazima niende… nataka Harrison anitamkie mbele ya macho yangu kuwa hanitaki na anampenda huyo nyani wake kuliko mimi,” alisema Linda huku akibubujikwa na machozi. Kuna wakati alishindwa kuendelea kusoma kutokana na macho yake kuzingirwa na machozi, akakitupa kitabu pembeni na kulala, usingizi ukampitia. Akiwa usingizini alianza kuota ndoto za ajabuajabu, hali iliyomfanya ashtuke na kukaa kitandani.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Siku hiyo nayo alishinda vibaya sana, mpaka giza linaingia, hakuwa amefanya kitu chochote zaidi ya kuendelea kulia kwa uchungu. Hakutaka mtu yeyote aingie ndani ya chumba chake, hata chakula hakikulika siku hiyo. Kesho yake asubuhi, aliwaaga wazazi wake kuwa anasafiri kwa siku kadhaa ingawa hakuwa tayari kueleza anakwenda wapi. Jambo pekee alilowaambia ni kwamba anasafiri kikazi akiwa anaendelea na uchunguzi wa suala la Harrison. Wazazi wake hawakuwa na la kufanya zaidi ya kumruhusu kwani tangu alipoanza kufuatilia suala hilo, alikuwa ni kama amechanganyikiwa hivyo alitakiwa kupewa uhuru wa kutosha kufanya kazi yake. Bila kupoteza muda, alisafiri kwa gari lake la kifahari hadi katika Jiji la Orlando ambako alikwenda mpaka kwenye stesheni ya treni iendayo kwa kasi, safari hii akiwa kama abiria. Alipofika, aliomba kuonana na mkuu wa ‘stesheni’ waliyezungumza naye siku moja iliyopita ambapo alimuomba amhifadhie gari lake. Alipopata uhakika wa usalama wa gari lake, alikata tiketi ya treni na kusubiri kwa muda mpaka treni lilipowasili. Akaingia na kwenda kwenye siti yake, safari ikaanza. Linda hakubeba vitu vingi zaidi ya mkoba wake muhimu uliokuwa na vitu vichache. Safari haikuwa nyepesi kama Linda alivyoifikiria kwani walilazimika kupita majimbo mengi kuelekea Tongass. Mpaka inafika saa kumi jioni, Linda alikuwa bado hajafika. Ilipofika saa kumi na mbili jioni, walianza kuuona mji mdogo wa Tongass uliokuwa umezungukwa na misitu minene. Sauti za wahudumu wa treni zikawa zinasikika kwenye vipaza sauti zikiwataarifu abiria kuwa treni lilikuwa limekaribia kuwasili kwenye kituo cha mwisho cha Tongass na kwamba abiria wote walitakiwa kushuka kwani hapo ndiyo mwisho wa safari. Linda akaanza kujiandaa kwa kuteremka. Muda mfupi baadaye, treni lilisimama na abiria wachache waliokuwa wamesalia ndani yake, akiwemo Linda wakaanza kuteremka na kuelekea kwenye lango kuu la kutokea. Mji wa Tongass ulikuwa mdogo wenye wakazi wachache. Linda akaongoza mpaka kwenye lango la kutokea na kuanza kuangaza macho huku na kule. Hakujua aelekee wapi baada ya kufika kwenye mji huo. Akajaribu kuuliza kwa wenyeji mahali anapoweza kupata nyumba ya kulala wageni ambapo alielekezwa. Kwa kuwa hapakuwa mbali sana kutokea kituoni, alitembea kwa miguu mpaka alipofika. Akalipia chumba na kuingia ndani kupumzika wakati akitafakari wapi pa kuanzia. ***
Simulizi : Queen Of Gorillas ( Malkia Wa Masokwe ) Sehemu Ya Tano (5)
Harrison na mkewe, Angel au Malkia wa Masokwe wanazidi kuoneshana mapenzi makubwa, kila mmoja akiwa na furaha kubwa ndani ya mtima wake. Harrison anaonesha kuwa na furaha zaidi kwani ndoto zake za siku nyingi za kuishi na Malkia wa Masokwe zilikuwa zimetimia.
Baada ya kuhangaika sana akitafuta nafasi ya kumtorosha msichana huyo kutoka ndani ya Msitu wa Tongass alikokuwa analindwa na masokwe, hatimaye anafanikiwa na kukimbia naye hadi nchini Canada. Wakiwa nchini Canada wanaenda kuishi katika Mji wa Abbotsford. Harrison anafanya kazi kubwa ya
kumbadilisha msichana huyo, anafanikiwa kumfundisha ustaarabu wa kibinadamu. Baadaye wanafunga ndoa halali kanisani na kuwa mume na mke. Harrison anamuandikisha mkewe kusomea
kompyuta na yeye anatafuta kazi. Wanaendelea na maisha yao na baada ya muda, Angel anaanza kuhisi dalili zinazowafanya wakubaliane kwenda hospitali. Wanapoenda kupima, wanagundua kuwa Angel amenasa ujauzito.
Upande wa pili, Linda amechachamaa kutaka kuufahamu ukweli juu ya kifo cha Harrison. Baada ya kuhitimu masomo ya Crime Scene Investigation na kutunukiwa shahada yake, anaanza kufanya kazi kwenye kampuni yake
binafsi ya upelelezi akiwa na shauku kubwa ya kuufahamu ukweli uliojificha nyuma ya kifo cha Harrison. Upelelezi wake unafanikiwa kubaini kuwa aliyekufa hakuwa Harrison na hata mwili uliozikwa haukuwa wa kwake.
Hali hiyo inamchanganya sana na anaapa kutumia mbinu kali alizojifunza chuoni kuendesha upelelezi huo huku akiweka nadhiri kuwa ni lazima ampate Harrison. Anafuatilia nyendo zote za Harrison kwa karibu.
LINDA hakupata usingizi usiku kucha kwani alikuwa akiwaza njia itakayomuwezesha kumpata Harrison kwa gharama yoyote. Bado penzi lake kwa kijana huyo mtanashati halikuwa limekwisha, kila mara alikuwa akimkumbuka na kujipa moyo kuwa lazima ipo siku atafanikiwa kumpata na kukamilisha tendo la kufunga naye ndoa.
Mawazo kwamba huenda Harrison alimkimbia kwa sababu alimpenda zaidi Malkia wa Masokwe, hakutaka kuyapa nafasi katika kichwa chake ingawa mara kwa mara yalikuwa yakimuandama. Alijipa moyo kuwa yeye ni mrembo na ana sifa zote za kumfanya Harrison amuoe kwa ndoa halali.
Mpaka kunaanza kupambazuka, Linda hakuwa amepata hata lepe la usingizi. Jua lilipoanza kuchomoza, alijilazimisha kuamka na kukaa juu ya kitanda, akachukua kitabu chake alichokuwa anakitumia kuandika mambo mbalimbali na kuanza kupitia ukurasa mmoja baada ya mwingine.
Alikuwa akijaribu kutafakari wapi pa kuanzia ili aikamilishe kazi yake. Licha ya kufikiria kwa muda, bado hakupata jibu la haraka, akakifungua kitabu cha Queen of Gorillas na kuanza kupitia kurasa mbalimbali ambazo aliamini zinaweza kuwa na taarifa muhimu zitakazomfanya ampate Harrison. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Katika ukurasa mmoja, alisoma jinsi Harrison alivyofanikiwa kuingia kwa mara ya kwanza kwenye msitu huo. Akagundua kuwa kumbe kuna ofisi za misitu ambazo ndizo zinazotumika kuulinda msitu huo na kutoa vibali kwa ajili ya watu mbalimbali wanaotaka kuingia ndani.
Wazo pekee aliloliona linafaa likawa ni kwenda moja kwa moja mpaka kwenye ofisi hizo akiamini anaweza kupata taarifa zitakazomsaidia kujua mahali alikoelekea Harrison. Kwa kufuata maelekezo yaliyokuwa yameandikwa na Harrison, aliianza safari ya kuelekea mahali zilipo ofisi hizo, akalazimika kutembea umbali mrefu kwa miguu kwani hakukuwa na usafiri wa aina yoyote eneo hilo.
Baada ya kutembea umbali mrefu, hatimaye alifika kwenye geti kubwa la mbao ambalo ndiyo lililokuwa linatumika kama lango kuu la msitu huo. Alipofika alijitambulisha kwa walinzi aliowakuta getini, akaelekezwa mahali ofisi zilipokuwa. Kwa kuwa hapakuwa mbali, alitembea hatua kadhaa akawasili kwenye ofisi iliyokuwa imejengwa kwa mbao na kuezekwa kwa vigae.
Akapokelewa na mzee wa makamo aliyejitambulisha kuwa ndiye Mkuu wa Hifadhi ya Msitu wa Tongass, Ludovick Pharell. Linda lijitambulisha na kuonesha kitambulisho chake cha kazi. Akaeleza kilichomfanya asafiri kutoka Miami mpaka kwenye msitu huo.
“Umesema anaitwa nani?” “Harrison Harvey,” alijibu Linda na mzee Ludovick akaanza kupitia daftari la wageni waliotembelea msitu huo kwa kipindi cha mwaka mzima. Jambo lililomshangaza Linda ni kwamba hakukupatikana taarifa zozote za Harrison kuutembelea msitu huo kwa mwaka huo.
Kutokana na kuendelea kusisitiza sana, Mzee Ludovick aliamua kutoa vitabu vyote vya wageni kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita. Wakaanza kukagua kitabu kimoja baada ya kingine.
Kwa bahati nzuri, walifanikiwa kulipata jina hilo likionesha kuwa Harrison alitembelea msitu huo karibu miaka minne iliyopita. Linda alipoangalia tarehe, aliishiwa nguvu kwani zilionesha kuwa ni kipindi ambacho alikuwa bado hajapata matatizo. Mara ya mwisho, ilionesha kuwa Harrison alitembelea Msitu wa Tongass miezi mitano kabla ya kupata ajali feki.
“Kwani hapa hakuna uwezekano wa mtu kuingia kinyemela bila kupitia hapa ofisini kupata kibali?” “Uwezekano ni mkubwa na karibu kila mwaka kuna idadi ya watu ambao huingia kinyemela msituni na kufanya mambo yao kisha kutokomea bila sisi kujua. Kama unavyojua huu msitu ni mkubwa sana na umeenda mpaka kwenye mpaka wa Marekani na Canada hivyo inakuwa vigumu kwetu kufuatilia kila kitu,” alisema Mzee Ludovick. “Ina maana huu msitu umeingia hadi Canada?”
“Ndiyo! Na baadhi ya wahamiaji haramu hupitia ndani ya msitu huu kuingia na kutoka nchini Marekani au Canada bila kushtukiwa na maafisa wa uhamiaji.”
Baada ya kujibiwa hivyo, kengele ya hatari ililia ndani ya kichwa cha Linda hasa baada ya kugundua kuwa msitu huo ulikuwa ukiziunganisha nchi hizo mbili. Alibaki amepigwa na bumbuwazi kwa dakika kadhaa, akawa amezama kwenye lindi la mawazo akitafakari mambo mengi kwa wakati mmoja.
Baada ya kuwaza sana, Linda alipata wazo la kurudi hadi nyumbani kwao kwanza na kujipanga upya kwani kwa jinsi ilivyoonesha, Harrison alikuwa ametumia akili za hali ya juu kuusuka mpango huo. Kwa shingo upande aliagana na mzee Ludovick na kutoka kwenye ofisi hizo.
Akaawaaga na wale walinzi waliomuonesha ofisi kisha safari ya kurudi Miami ikaanza, alirudi mpaka kwenye mji mdogo wa Tongass ambapo alikata tiketi ya treni na kukaa stesheni kulisubiri. ***
Ujauzito wa Malkia wa Masokwe ulizidi kukua, muda wa kuanza kuhudhuria kliniki ulipowadia, Harrison hakutaka kumwacha aende peke yake. Ikawa kila siku ya kwenda kliniki anaomba ruhusa kazini na kumsindikiza mkewe. Upendo aliokuwa anaounesha kwa mkewe, ulimfurahisha kila mmoja, wanawake wengi wakawa wanatamani waume zao
wangekuwa na akili kama za Harrison. Njiani alikuwa akimsaidia kubeba mizigo yote ikiwemo mkoba wake. Alikuwa akimdekeza kama mtoto mdogo.
“Mwanao ameanza kucheza, hebu msikilize,” alisema Angel jioni moja akiwa amekaa na mumewe kwenye bustani nzuri ya maua wakipunga upepo. Harrison alimuinamia mkewe na kusogeza sikio lake kwenye tumbo lake ambalo sasa lilishaanza kuwa kubwa.
“Eeeh! Kweli, inaonesha atakuwa mtundu sana huyu,” alisema Harrison huku akimbusu mkewe kwa furaha. Mapenzi yalikuwa yakizidi kuongezeka kila uchao, furaha, amani na upendo vikazidi kushamiri. Ujauzito ulipofikisha miezi minne, Harrison alimuombea ruhusa mkewe ili asimame kufanya kazi mpaka atakapojifungua. Hakutaka mkewe apate shida hata kidogo, ombi hilo lilipokubaliwa, Angel akawa anashinda nyumbani kuendelea kulihudumia tumbo lake. ***
UPENDO, amani, furaha na maelewano vinazidi kushamiri kwenye ndoa ya Harrison na mkewe, Angel au Malkia wa Masokwe. Kila mmoja anafurahia maisha ya ndoa na mapenzi anayoyapata kutoka kwa mwenzake. Harrison
anaonesha kuwa na furaha zaidi kwani ndoto zake za siku nyingi za kuishi na Malkia wa Masokwe zilikuwa zimetimia. Jinsi alivyohangaika wakati akitafuta nafasi ya kumtorosha msichana huyo kutoka ndani ya Msitu wa Tongass
alikokuwa analindwa na masokwe, inabaki kuwa historia. Mara kwa mara wanakumbushana jinsi Harrison alivyohangaika kumtorosha hadi alipofanikiwa kuondoka naye kuelekea nchini Canada. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Baada ya kufunga ndoa, Angel ananasa ujauzito na sasa wanasaidiana kuulea, huku Harrison akimtunza mkewe huyo kama mboni ya jicho lake. Mara kwa mara anampeleka kliniki na baadaye anamsimamisha kazi aliyokuwa anafanya. Siku zinazidi kuyoyoma na ujauzito wa Angel unazidi kukua vizuri.
Upande wa pili, Linda anaendelea na upelelezi wa hali ya juu kutaka kuufahamu ukweli juu ya kifo cha Harrison. Baada ya kuhitimu masomo ya Crime Scene Investigation na kutunukiwa shahada yake, anaanza kufanya kazi kwenye
kampuni yake binafsi ya upelelezi akiwa na shauku kubwa ya kuufahamu ukweli uliojificha nyuma ya kifo cha Harrison.
Kwa kadiri siku zinavyozidi kwenda, ndivyo anavyogundua mambo mengi yaliyokuwa yamejificha kuhusu kifo hicho. Anagundua kuwa Harrison hakufa kwenye ajali kama ambavyo kila mtu alikuwa anaamini. Anaendelea na upelelezi wa kina na sasa anakaribia kuujua ukweli wa mahali Harrison alikojificha.
Baada ya kurudi mpaka Miami, Linda aliendelea kutafakari namna ya kumpata Harrison lakini hakupata jibu la haraka. Alijaribu kwenda kwenye idara ya mawasiliano na kuangalia kama namba ya simu ya mkononi ya Harrison ilikuwa ikiendelea kutumika sehemu nyingine lakini hakufanikiwa kupata taarifa zozote muhimu. Aligundua kuwa siku ya mwisho kwa namba hiyo ya simu kutumika, ilikuwa ni ile ambayo Harrison alipata ajali feki. Linda hakukata tamaa, akaendelea kuumiza kichwa kutafuta njia ambayo itamfanya agundue ukweli wa mahali Harrison alipo. Kutokana na uchovu wa safari, siku hiyo hakutaka kuendelea na kazi, akarudi nyumbani kupumzika huku akiendelea kutafakari kichwani mwake. Baada ya muda, alipata wazo aliloona linaweza kumsaidia kuujua ukweli. Aliamini kama kweli Harrison amevuka mpaka na kuingia nchini Canada, lazima taarifa zake za hati ya kusafiria, tarehe ya siku aliyovuka mpaka na sehemu alikoelekea zitakuwepo kwenye idara ya uhamiaji ya nchi hiyo. Kesho yake akajiandaa na baada ya muda, safari ya kuelekea makao makuu ya idara ya uhamiaji jijini New York ikaanza. Alilazimika kusafiri kwa ndege kutoka jijini Miami mpaka New York. Bila kupoteza muda akaenda moja kwa moja mpaka kwenye ofisi za Idara ya Uhamiaji. Alipofika alijitambulisha na kueleza shida yake, kwa kuwa alisisitiza kuwa anafanya hivyo kwa sababu za usalama wa nchi, alipewa ushirikiano mkubwa kuliko alivyotegemea. Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Russell Isaacs alimuongoza mpaka kwenye chumba maalum kilichokuwa na kompyuta nyingi zilizounganishwa na mtandao wa internet. Wakaanza kuangalia taarifa za watu mbalimbali waliokuwa wanatoka na kuingia ndani ya mipaka ya Marekani lakini jina la Harrison halikuonekana. Walifuatilia kumbukumbu za kipindi chote tangu Harrison atoweke lakini hakukuwa na taarifa zozote zilizoonesha kuwa ameingia au kutoka nje ya Marekani. “Au alibadilisha jina?” “Hata kama amebadilisha jina lazima angeonekana katika taarifa za watu waliobadilisha majina na kula viapo kwani haiwezekani mtu akabadilisha jina kienyeji halafu akapata hati ya kusafiria,” alisema Russell, hali iliyozidi kumchanganya Linda. Baada ya kushindwa kupata taarifa zozote muhimu za kumsaidia, aliaga na kuondoka, akaenda mpaka Uwanja wa Ndege ambapo alikata tiketi na muda mfupi baadaye, safari ya kurudi Miami ikaanza. Licha ya vikwazo alivyokuwa anakutana navyo, bado Linda hakukata tamaa, alijiapiza kuwa atatumia mbinu zote anazozijua mpaka afahamu ukweli wa mahali Harrison alipo. Siku zilizidi kusonga mbele, Linda akawa anaendelea kuumiza kichwa namna atakavyofanikiwa kuufahamu ukweli wa mahali Harrison alipo. Jioni moja wakati akirejea kutoka kazini kwake, alipitia ‘super market’ kwa ajili ya kujipatia mahitaji muhimu. Wakati akiendelea kununua bidhaa mbalimbali, alifika kwenye upande ambao vitabu, majarida na magazeti vinapatikana. Katika hali ambayo ilimshangaza, alishtuka kukiona kitabu cha Queen of Gorillas kikiwa miongoni mwa vitabu vinavyouzwa. Kilichomshtua ni kwamba tangu Harrison atoweke, hakukuwa na mtu aliyekuwa akisimamia kazi zake na kwa kipindi hicho, nakala karibu zote za vitabu zilikuwa zimeshauzwa na kuisha kwenye mzunguko. Alisogea mpaka kwenye kabati la vioo lililokuwa na vitabu, akafungua na kukitoa, akakitazama kwa muda na kugundua kuwa hakikuwa na tofauti na kile alichokuwa nacho nyumbani kwao. Akajiuliza maswali mengi ambayo yote yalikosa majibu. Akakirudisha mahali pake na kumalizia kufanya manunuzi kisha akaondoka na kurudi kwao. Alipofika, alikichukua kitabu chake na kuangalia namba za mawasiliano za kampuni iliyohusika na kazi ya kukichapisha kitabu hicho kwa mara ya kwanza. Aliziandika pembeni kisha akainuka na kuelekea sebuleni. Bila kupoteza muda, alipiga simu kwenye makao makuu ya kampuni ya Planet Link Publishers, wachapishaji na wasambazaji wa kitabu hicho. Baada ya simu kupokelewa, Linda alijitambulisha na kuanza kuhoji maswali kuhusu kukiona kitabu hicho kikiendelea kuuzwa wakati mhusika alishafariki. Pia alitaka kujua fedha za mauzo zinakopelekwa. Majibu aliyoyapata yaliamsha kitu kipya ndani ya akili yake. Alishangaa sana kusikia kuwa mauzo ya kitabu hicho yanaingizwa kwenye akaunti ya Harrison na kwamba wazo la kukichapisha upya kitabu hicho lilitoka kwa ndugu wa marehemu aishiye Canada ambaye aliwasiliana nao kwa barua pepe (e-mail) na kuwapa maelezo hayo. Linda aliomba kupewa namba ya akaunti ambayo fedha hizo zilikuwa zikiingizwa kisha akamuomba mtu aliyezungumza naye kutomwambia yeyote mambo yote waliyozungumza kisha akakata simu. Alishusha pumzi ndefu na kutulia kwa muda, mawazo mengi yakipita ndani ya kichwa chake. Akainuka na kuelekea chumbani kwake ambapo alijifungia mlango na kujitupa kitandani. Wazo pekee alilolipata ni kwenda kwenye makao makuu ya Benki ya Barclays jijini Miami kwa ajili ya kufuatilia taarifa za akaunti ya Harrison. *** Ujauzito wa Angel ulizidi kukua vizuri bila matatizo yoyote, jambo lililoongeza furaha katika ndoa yao. Kazi aliyokuwa anafanya pamoja na fedha za mauzo ya vitabu vyake kwa pamoja vilimfanya awe na uwezo mzuri kiuchumi hivyo suala la kumtunza na kumhudumia mkewe halikumpa shida. Miezi ilizidi kukatika, mwezi wa tano ukapita, ukaja wa sita, wa saba, wa nane hatimaye miezi tisa ikatimia. Maandalizi ya kukipokea kiumbe kipya yakaanza kufanyika huku kila mmoja akiwa na hofu kubwa kwani hakuna aliyekuwa na uzoefu na jambo hilo. “Mume wangu, hivi nitafanikiwa kujifungua salama kweli?” “Usijali mke wangu, utajifungua salama salmini, si unakumbuka mara ya mwisho daktari alisema kila kitu mwilini mwako kipo sawa? Tena ukichanganya na mazoezi ninayokufanyisha naamini kila kitu kitakuwa sawa.”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Nitafurahi sana kukuzalia mtoto, nakupenda sana mume wangu,” alisema Angel na kumkumbatia mumewe, wakawa wanapigana mabusu kwa mahaba mazito. *** Maisha yanazidi kuwanyookea Harrison na mkewe Angel (Malkia wa Masokwe) ambao sasa wanaishi kwenye ndoa halali nchini Canada katika Mji wa Langley. Kwa kadiri siku zinavyosonga mbele ndivyo wanavyozidi kuoneshana mapenzi ya dhati, kila mmoja akifurahia sana kuwa na mwenzake.
Baada ya kukaa kwenye ndoa kwa muda, Angel ananasa ujauzito na sasa wanasaidiana kuulea na mumewe, huku Harrison akimtunza mkewe huyo kama mboni ya jicho lake. Mara kwa mara anampeleka kliniki na baadaye anamsimamisha kazi aliyokuwa anafanya. Siku zinazidi kuyoyoma na ujauzito wa Angel unazidi kukua vizuri na hatimaye unatimiza miezi tisa.
Upande wa pili, Linda hakubali matokeo, anaendelea na upelelezi wa hali ya juu kutaka kuufahamu ukweli juu ya kifo cha Harrison. Kwa kutumia kampuni yake binafsi ya upelelezi, anafanikiwa kugundua mambo mengi yaliyokuwa yamejificha nyuma ya tukio hilo.
Anagundua kuwa Harrison hakufa kwenye ajali kama ambavyo kila mtu alikuwa anaamini. Anaendelea na upelelezi wa kina na sasa anagundua kuwa akaunti ya
Harrison ilikuwa bado inaendelea kutumika. Anajiapiza kuwa ni lazima afahamu mahali Harrison alikojificha.
Angel akiwa anafanya shughuli ndogondogo nyumbani kwake, tumbo lake likiwa limeongezeka ukubwa maradufu, alianza kuhisi hali iliyomfanya apate woga. Tumbo lilianza kumuuma ghafla, akajikokota kutoka jikoni alikokuwa anaandaa chakula na kuelekea chumbani lakini kabla hajafika, akiwa kwenye korido maumivu yalimzidi. Akajishikilia ukutani na kukaa chini huku akiugulia maumivu makali, ghafla akasikia kitu kama kisu kikali kimepita katikati ya miguu yake, maji mengi yakaanza kuvuja na kulowanisha nguo zake. Kwa kuwa hiyo ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza, hakuelewa ni kitu gani kilichokuwa kinamtokea. “Mu…me wa…ngu! Na..ku..faaa!” Angel aliongea na mumewe kwa njia ya simu kisha akajilaza chini na kutulia kimya. Harrison aliyekuwa njiani akitokea kazini, alishtuka kupita kiasi kutokana na alichoambiwa na mkewe. Hata alipojaribu kupiga tena simu, ilikuwa ikiita bila kupokelewa. Akaharakisha kuelekea nyumbani kwake. Alipofika, bila kupoteza muda, moja kwa moja alikimbilia ndani, alichokutana nacho kilimfanya ashikwe na woga kuliko kawaida. Mkewe alikuwa ameanguka chini huku maji mengi yakimchuruzika kutoka katikati ya miguu yake. “Mungu wangu!” alisema Harrison huku akiinama na kujaribu kumtingisha mkewe. Mapigo ya moyo yalikuwa yakisikika kwa mbali lakini hakuwa na fahamu. Akalazimika kutoka nje haraka na kwenda kutafuta msaada wa gari la kubebea wagonjwa (Ambulance). Kwa bahati nzuri, alipopiga namba ya simu ya dharura na kueleza mahali mgonjwa alipo, alipata mwitikio wa haraka, baada ya dakika chache ving’ora vya gari la kubebea wagonjwa vikawa vinasikika jirani na nyumba yao. Muda mfupi baadaye, gari likapaki nje ya nyumba yao, wauguzi waliokuwa na kitanda maalum cha kubebea wagonjwa wakashuka na kumfuata Harrison. “Yupo ndani,” alisema Harrison huku akitangulia kuingia ndani. Wauguzi hao wakamfuata na kwenda moja kwa moja mpaka mahali Angel alipokuwa amelala. “Amebanwa na uchungu na tayari chupa ya uzazi imepasuka,” alisema muuguzi mmoja wakati wakisaidiana kumbeba Angel na kumuweka kwenye kitanda maalum, wakatoka mbiombio na kumpeleka mpaka kwenye ambulance na safari ya kuelekea hospitali ikaanza. Njia nzima Harrison alikuwa akimuomba Mungu wake amsaidie mkewe kujifungua salama kwani hakuna kitu alichokuwa anakisubiri kwa hamu kama mtoto kutoka kwenye tumbo la mwanamke aliyekuwa anampenda kuliko kitu kingine chochote chini ya jua. Baada ya kufikishwa hospitali, Angel aliteremshwa harakaharaka na kuwekwa juu ya kitanda cha magurudumu, akakimbizwa kwa kasi kuelekea kwenye wodi ya wazazi (maternity). “Inject her with pitressin drip!”(Mtundikieni dripu ya maji ya uchungu) alisema daktari mkunga aliyepewa jukumu la kumsaidia Angel kujifungua. Baada ya kutundikiwa dripu hiyo, Angel alizinduka na kuanza kulalamikia maumivu makali aliyokuwa anayasikia mwili mzima baada ya kuingizwa maji ya uchungu mwilini, hasa tumboni. Manesi na wakunga wakamzunguka, Harrison akazuiwa kuingia kwenye wodi ya wazazi na kila mtu akawa anahaha kujaribu kuokoa maisha ya mama na mtoto. Kelele alizokuwa anapiga Angel, zilimfanya Harrison ashindwe kukaa na kutulia, kiti alikiona cha moto, akawa anazunguka huku na kule, mikono ikiwa kichwani. Kila alipomuona daktari au nesi akitoka kwenye wodi aliyokuwa amelazwa mkewe, alikuwa akimfuata na kumuuliza hali ya mgonjwa. “Kuwa na subira kaka, kaa na utulie kila kitu kitakuwa sawa.” “Nitatuliaje wakati namsikia mke wangu analia kwa uchungu? Asije akafa nesi.” “Hawezi kufa, hayo ni mambo ya kawaida na ndiyo maana wanaume huwa hamruhusiwi kusogelea kwenye wodi za wazazi,” nesi alimwambia Harrison huku akimtaka kwenda kukaa sehemu maalum ya kusubiria. Akili za Harrison zilikuwa zimehama kabisa, akawa anamuonea huruma mkewe kutokana na mateso aliyokuwa anayapitia. “Sukuma! Sukuma! Jikaze… ukijilegeza utamuua mwanao, sukuma kwa nguvu…” manesi na wakunga walikuwa wakimuelekeza Angel cha kufanya, baada ya kuhangaika kwa muda, hatimaye Angel alifanikiwa kujifungua salama. Kutokana na kutumia nguvu nyingi, Angel hakuelewa tena kilichoendelea. Alikuja kuzinduka na kujikuta amelazwa kwenye wodi nyingine, manesi wawili wakiwa pembeni yake. Alipojishika tumboni, aligundua kuwa tumbo lake limepungua ukubwa ingawa alikuwa akisikia maumivu makali kupita kiasi. “Hongera dada! Umejifungua mtoto mzuri.” “Nimejifungua mtoto gani? Mwanangu yupo wapi?” “Umejifungua mtoto wa kiume, mzuri kama mama yake. Ngoja tukamlete,” alisema nesi na kuondoka kuelekea kwenye chumba maalum ambapo mtoto alikuwa amehifadhiwa kwa muda. Muda mfupi baadaye, mtoto aliletwa na kulazwa pembeni ya mama yake, Angel hakuyaamini macho yake, mtoto alikuwa mzuri ajabu! Halafu alikuwa na mchanganyiko mzuri wa sura kati ya baba yake na mama yake, akajikuta akitokwa na machozi ya furaha. Manesi wakawa wanamuelekeza namna ya kuanza kumnyonyesha. Angel akawa anacheka wakati akimtazama mwanaye alivyokuwa ananyonya kwa fujo kuonesha kuwa alikuwa na njaa kali. Muda mfupi baadaye, Harrison alifungua mlango wa wodi aliyokuwa amelazwa mkewe na kuanza kuangaza macho huku na kule. Angel aliwaambia kuwa huyo ndiyo baba mtoto wake, wakampa ishara ya kumuonesha mahali mkewe alipokuwa amelazwa. Harrison akawa anatembea kwa hofu kubwa kuelekea pale alipoelekezwa. Alipofika, hakuyaamini macho yake kumuona mkewe amelala huku akiwa anamnyonyesha mtoto mchanga. Tabasamu pana lilikuwa limemjaa mkewe, alipomtazama usoni akajikuta akizidi kufurahi. “Mtoto wetu huyu hapa,” alisema Angel huku akimuweka vizuri mwanaye, Harrison akainama na kumbusu mkewe kisha akambusu na mtoto huku akimkodolea macho mwanaye ambaye alikuwa amefanana naye kwa kiasi kikubwa. Akamkumbatia mkewe kwa furaha huku naye machozi ya furaha yakimtoka. *** Kulipopambazuka, Linda alijiandaa na baada ya kumaliza, safari ya kuelekea Miami ikaanza. Alikwenda moja kwa moja kwenye Makao Makuu ya Benki ya Barclays jijini Miami ambapo aliomba kukutana na meneja mkuu. Baada ya kujitambulisha na kuonesha vitambulisho vyake vya kazi, Linda alieleza kilichompeleka pale. Japokuwa benki hiyo haikuwa na utaratibu wa kutoa taarifa za wateja wake kwa watu wasiohusika, meneja alikubali kumpa taarifa hizo Linda hasa baada ya kusisitiza kuwa anafanya kazi kwa ajili ya taifa la Marekani. Akaomba kupewa ‘bank statement’ ya akaunti hiyo na taarifa nyingine muhimu za kuweka au kutoa fedha kwenye akaunti ya Harrison Harvey. Akaambiwa asubiri wakati wafanyakazi wa benki wanalifanyia kazi ombi lake. ***
Harrison anaendelea kujilia mbivu zake baada ya kufanikiwa kulipata penzi la msichana aliyemsumbua kwa kipindi kirefu, Angel (Malkia wa masokwe) ambaye awali alikuwa akiishi kwenye msitu mkubwa wa Tongass, akilindwa na masokwe wengi. Baada ya CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/- kumtorosha, anaenda naye nchini Canada ambako anamfundisha ustaarabu wa kibinadamu na baada ya kubadilika, anatangaza ndoa. Wanaoana kimyakimya na kuwa mke na mume halali. Wanaishi maisha ya furaha na
upendo mkubwa. Baada ya kukaa kwenye ndoa kwa muda, Angel ananasa ujauzito. Harrison anamlea kama mboni ya jicho lake na hatimaye miezi tisa inatimia. Angel anashikwa na uchungu ambapo Harrison anamkimbiza hospitali ambako
anajifungua salama mtoto wa kiume, akiwa na mchanganyiko mzuri wa sura ya mama na baba yake. Furaha inazidi maradufu kwenye familia yao, Harrison anaongeza upendo kwa mkewe huku akifurahia sana kuitwa baba.
Upande wa pili, Linda anaendelea na upelelezi wa kina kufuatilia ukweli uliokuwa umejificha nyuma ya maisha ya Harrison. Licha ya watu wote kuamini kuwa tayari kijana
huyo alishakufa, upelelezi wa Linda unamuwezesha kugundua kuwa kumbe hakufa bali ilikuwa ni danganya toto.
Jambo hilo linamuumiza sana moyo wake na sasa amechachamaa kutaka kufahamu ukweli wa mahali Harrison alipo. Anajiapiza kuwa ni lazima ampate mahali kokote alikojificha.
“Siamini! Siamini kama na mimi nitakuwa naitwa baba! Natamani mama yangu angelijua hili lakini ndiyo hivyo tena,” alisema Harrison huku akijifuta machozi ya furaha, wakaendelea kukumbatiana na mkewe huku wakipigana mabusu motomoto. Angel na mwanaye waliendelea kupewa huduma chini ya uangalizi wa daktari na manesi kwa muda, jioni wakaruhusiwa kurudi nyumbani.
Harrison akatafuta usafiri wa kuwarudisha mkewe na mwanaye nyumbani huku akiwa na furaha isiyoelezeka. Kwa jinsi alivyokuwa anachekacheka ungeweza kudhani akili zinataka kumruka, mtoto alimchanganya mno. Wakiwa kwenye gari, Harrison alimpakata mtoto na kukaa pembeni ya mkewe aliyekuwa amemuegamia begani.
Walipofika nyumbani kwao, Harrison ndiyo alikuwa wa kwanza kuteremka garini, akampeleka mtoto ndani kisha akarudi na kumsaidia mkewe kuingia ndani. Alipomfikisha chumbani alirudi na kumalizia kuteremsha vitu vyote kwenye gari na kumlipa dereva fedha zake.
“Nimeandaa zawadi ya jogoo mkubwa kwa ajili yako mke wangu, nataka umle na kummaliza,” alisema Harrison huku akianza kuandaa kitoweo cha kuku mkubwa alichokuwa ameandaa maalum kwa ajili ya mkewe. Alishughulikia kila kitu, akawasha moto na kuanza kupika huku mkewe akiendelea kumnyonyesha mtoto wao.
Pilikapilika ziliendelea, Harrison akamuandalia mkewe supu ya kuku mzima na kumuwekea mezani, akamuandalia kila kitu kisha akamsaidia kumbeba mtoto na kumtaka ale.
“Nashukuru kwa kunijali mume wangu, kumbe unajua kupika vizuri namna hii,” alisema Angel huku akila taratibu. Furaha ilizidi kuongezeka zaidi ndani ya nyumba hiyo, muda mfupi baadaye wafanyakazi wenzake Harrison na wale waliokuwa wanafanya kazi na mkewe wakaanza kuwasili nyumbani hapo wakiwa na zawadi mbalimbali.
Kila aliyekuwa anamuona mtoto, aliwasifu kwani kwa hakika alikuwa mzuri sana. Wengine wakawa wanawatania kuwa wajiandae kukabiliana na kesi nyingi za mabinti kupewa ujauzito na mtoto wao kwani alikuwa ‘handsome’ kwelikweli. Vicheko vya furaha vilitawala kila sehemu.
Utaratibu wa maisha ya Harrison ukabadilika, akawa analazimika kuwa wa mwisho kulala kila siku na wa kwanza kuamka. Jambo la kwanza kila asubuhi ilikuwa ni kumuandalia mkewe maji ya moto kwa ajili ya kumchua tumbo lake na kuoga kisha kumuogesha mtoto.
Baada ya hapo alikuwa akimuandalia mkewe supu kisha kufua nguo za mtoto alizochafua usiku kucha. Ratiba yake ya kwenda kazini nayo ikabadilika kwani kwa siku tatu za mwanzo aliomba ruhusa kwa ajili ya kuihudumia familia yake, baada ya hapo akawa anaondoka nyumbani majira ya saa nne baada ya kumaliza kazi zote nyumbani.
Upendo wake kwa Angel ndiyo uliomsukuma kufanya yote hayo na kamwe hakuona ugumu wa kufanya hivyo kama walivyo wanaume wengi ambao huwaachia mzigo huo wake zao bila kujali hali za kiafya wanazokuwa nazo wakitoka kujifungua. Baada ya siku kadhaa, wakampa jina mtoto wao ambapo Harrison alipendekeza aitwe Harvey Junior au kwa kifupi Junior, wazo ambalo Angel alikubaliana nalo.
Watu wengi wakaanza kuwaita Harrison na mkewe kwa jina la mama na baba Junior, wakawa wanajisikia fahari kubwa kwani nao sasa walikuwa wazazi, tena wanaopendana pengine kuliko watu wote kwenye mji huo.
“Mh! Mama Junior mumeo anakujali mpaka naona wivu, natamani na mimi mume wangu angekuwa ananipenda na kunijali kama wewe! Yaani anafua nepi za mtoto na kumuogesha? Mbona mwenzetu una raha!” mwanamke mmoja aliyekuwa anaishi jirani na familia ya Harrison alimwambia Angel asubuhi moja baada ya kumkuta akianika nguo za mwanaye. Angel hakujibu kitu zaidi ya kutabasamu.
Baada ya siku kadhaa,walianza kumpeleka mtoto kliniki ambapo Harrison kama kawaida yake, alikuwa akifanya kazi zote, kuanzia kumbeba mtoto, kumbebea mkewe mkoba wa nguo za mtoto na vitu vingine. Kila walipokuwa wanapita, watu walikuwa
wakimshangaa Harrison huku wengi wakimsifu kwani alikuwa na upendo wa dhati kwa mkewe. Siku zikawa zinazidi kusonga mbele huku Harvey Junior akizidi kukua vizuri na kuchangamka kila uchao. Uwepo wake ukazidi kuichangamsha nyumba yao kwani mara kwa mara mtoto huyo alikuwa akisikika akilia au kucheka kama wafanyavyo watoto wengi wakiwa bado wadogo. ***
Baada ya wafanyakazi wa Benki ya Barclays jijini Miami kulifanyia kazi ombi la Linda, walikuja na majibu yaliyosababisha msichana huyo mrembo atake kupoteza fahamu. Walimpa taarifa kuwa akaunti hiyo inaendelea kutumika kama kawaida nchini Canada na kwa mara ya kwanza, ilitumika kwenye Mji wa Abbotsford kutoa fedha na baada ya hapo, iliendelea kutumika kwenye mji huo na baadaye ikaonesha kuwa ilitumika Langley.
“Mungu wangu! Ina maana Harrison anaendelea na maisha yake kama kawaida? Ooh Lord! Why is this happening to me? (Ooh Mungu! Kwa nini haya yananitokea?) alisema Harrison akiwa ndani ya ofisi ya meneja mkuu wa benki hiyo.
“Kwani vipi afisa?” meneja huyo alimuuliza Linda lakini hakujibu kitu zaidi ya kutoa kitambaa kwenye pochi yake ndogo ya bei mbaya na kuanza kujifuta machozi. Hakutaka kuendelea kukaa ndani ya ofisi hiyo, alishukuru kisha akakusanya karatasi alizopewa
na kuziweka kwenye mkoba wake, akatoka mbio huku akiendelea kumwaga machozi kama mtu aliyepokea taarifa za msiba. Kila aliyemuona alimshangaa kwani haikuwa kawaida kwa msichana mrembo kama yeye, anayeonesha kuwa na kila kitu kwenye
maisha yake kulia hadharani. Alikwenda mpaka kwenye eneo la maegesho na kuingia ndani ya gari lake la kifahari alilokuja nalo. Akajifungia na kulalia kwenye usukani, akawa analia kwa uchungu sana. Alitia huruma.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“My heart is broken! I have never been tired of living like now! Harrison my love, why did you leave me? Why?” (Moyo wangu umevunjika! Sijawahi kuchoka kuishi kama ilivyo sasa! Harrison mpenzi, kwa nini uliniacha? Kwa nini?)
Linda alisema kwa uchungu huku akijipigapiga kichwa kwenye usukani, alilia kwa muda mrefu lakini hakukuwa na mtu wa kumfuta machozi. Kwa unyonge akawasha gari na kuanza kuondoka kurejea nyumbani kwao.
Hata hivyo, licha ya Linda kugundua kuwa Harrison alimkimbia siku ya ndoa yao kwa sababu anazozijua mwenyewe, hakutaka kukata tamaa. Aliamua kupiga moyo konde na kuendelea kumfuatilia ili aujue ukweli. Hakutaka kujali ataumia kiasi gani kuufahamu ukweli, alishakula nadhiri tangu mwanzo kuwa atamfuatilia kwa karibu hadi ajue mwisho wake hivyo hakuwa na la kufanya zaidi ya kuandaa safari ya dharura kwenda Canada. *** Dunia haina siri, licha ya Harrison kuudanganya ulimwengu kuwa amekufa kwenye ajali ya barabarani, ukweli unakaribia kujulikana. Bila kujua kuwa anafuatiliwa kwa karibu,
Harrison anaendelea kujilia mbivu zake baada ya kufanikiwa kulipata penzi la msichana aliyemsumbua kwa kipindi kirefu, Angel (Malkia wa masokwe).
Harrison amefanikiwa kumnasa msichana huyo ambaye awali alikuwa akiishi kwenye msitu mkubwa wa Tongass, akilindwa na masokwe wengi. Baada ya kumtorosha, anaenda naye nchini Canada ambako anamfundisha ustaarabu wa kibinadamu na baada ya kubadilika, anatangaza ndoa.
Wanaoana kimyakimya na kuwa mke na mume halali. Wanaishi maisha ya furaha na upendo mkubwa. Baada ya kukaa kwenye ndoa kwa muda, Angel ananasa ujauzito.
Harrison anamlea kama mboni ya jicho lake na hatimaye miezi tisa inatimia. Angel anashikwa na uchungu ambapo Harrison anamkimbiza hospitali ambako anajifungua salama mtoto wa kiume, akiwa na mchanganyiko mzuri wa sura ya mama na
baba yake. Furaha inazidi maradufu kwenye familia yao, Harrison anaongeza upendo kwa mkewe huku akifurahia sana kuitwa baba. Wanampa mtoto wao jina la Harvey Junior.
Upande wa pili, Linda ameshagundua kuwa akaunti ya benki ya Harrison inaendelea kutumika nchini Canada na sasa anajiandaa kusafiri kwa ndege kuelekea nchini humo. Hakati tamaa mpaka ahakikishe amempata Harrison.
“Baba na mama, nimewaita jioni ya leo ili niwaambie jambo moja tu kwamba nataka kusafiri kwenda Canada na sijui nitarudi lini. Nafikiri mpaka nitakapokamilisha kazi yangu ndipo nitakaporudi, sitajali muda nitakaoutumia lakini cha msingi mpaka nikamilishe kazi yangu.”
“Mbona ghafla hivyo mwanangu? Kwani unaenda kufanya kazi gani?” aliuliza mama mzazi wa Linda huku akionesha wasiwasi ndani ya moyo wake.
“Nakwenda kuendelea na kazi yangu ya upelelezi, kuna jambo moja muhimu sana ambalo inabidi nilifuatilie kwa kina mpaka niujue mwisho wake.”
“Usituambie kuwa bado unamfuatilia Harrison,” alisema mzee Ford huku akiwa na shauku kubwa ya kusikia mwanaye atajibu nini. Japokuwa wote walikuwa wanafahamu jinsi binti yao alivyokuwa anampenda kijana huyo, hawakuwa tayari kuona anazidi kuteseka kumfuatilia mtu asiye na mapenzi kwake.
Linda hakujibu kitu, aliwatazama baba na mama yake kwa zamu kisha akajiinamia chini. Wote walitambua kilichokuwa kinapita ndani ya kichwa chake, wakamsogelea na kumkumbatia kwa pamoja. “Linda mwanangu, hatukukulea uje kuwa hivi, lazima ujifunze kukubaliana na matokeo, haitakuwa na maana yoyote kuendelea kumfuatilia mtu ambaye mara zote amekuwa akiuvunja moyo wako, hayo uliyoyagundua yanatosha, tafadhali usiende.”
“No! Lazima niufahamu mwisho wa Harrison, ukweli ndiyo kitu pekee kitakachonifanya niishi kwa amani, naombeni mniruhusu.” “Lakini Linda, ni ukweli gani tena unaoufuatilia mwanangu? Sote tumeshagundua kuwa Harrison hakufa bali ulikuwa ni mpango wake wa kukwepa kukuoa, hiyo pekee inatosha kukufanya uamini kuwa hakuwa na mapenzi ya dhati kwako, usiendelee kuutesa
moyo wako, utampata tu mwanaume bora,” alisema mama Linda huku akiungwa mkono na mumewe, kwa pamoja wakawa wanambembeleza binti yao.
Licha ya kujaribu kutumia ushawishi wao wote, bado Linda hakutaka kubadilisha msimamo wake, aling’ang’ania kuwa ni lazima asafiri mpaka Canada kuikamilisha kazi yake. Baada ya wazazi wake kuona binti yao ameshikilia msimamo wake, ilibidi wakubaliane naye kwa shingo upande, wakamruhusu kwenda Canada lakini wakamtaka kuwa mwangalifu na kuendelea kuwasiliana nao mara kwa mara.
Siku mbili baadaye, Linda alikwenda kwenye Uwanja wa Ndege wa Miami, akakata tiketi ya kuelekea Ottawa, Canada kisha akakaa sehemu ya abiria kusubiria ndege. Uchungu aliokuwa nao ndani ya moyo wake ulimfanya muda wote awe anatokwa na machozi. Akakaa kwenye kiti kusubiria ndege huku akiendelea kulia kama mtu aliyepokea taarifa za msiba.
Abiria waliokuwa karibu yake walibaki kumshangaa kwani haikuwa kawaida kumuona binti mrembo kama yeye akilia hadharani, tena bila ya kuwa na mtu wa kumbembeleza. Baada ya kusubiri kwa muda, ndege kubwa ya Shirika la Ndege la Nordic Airways ilianza kupakia abiria kwa safari ya kuelekea nchini Canada.
Linda alikuwa miongoni mwa abiria wa kwanza kupanda kwenye ndege hiyo, akaenda moja kwa moja mpaka kwenye siti yake na kutulia kimya, mawazo machungu yakiendelea kupita ndani ya kichwa chake. Baada ya dakika arobaini kupita, sauti kutoka kwenye vipaza sauti ndani ya ndege hiyo ilianza kusikika ikiwataka abiria wote kufunga mikanda.
Muda mfupi baadaye, ndege kubwa ya Airbus 380, mali ya kampuni ya Nordic Airways ikaanza kusogea taratibu kuelekea kwenye njia za kurukia (run ways). Baada ya muda, injini zote zikawashwa na ndege ikaanza kunguruma kwa nguvu, ikaanza kuondoka kwa kasi na hatimaye ikaiacha ardhi ya Marekani na kupaa angani.
“Lazima nimpate Harrison kwa njia yoyote, nataka anitamkie ana kwa ana kwamba hanipendi na hataki kuishi na mimi, najua akiniona lazima atabadilisha msimamo wake kwani bado nampenda sana na naamini na yeye ananipenda ila shetani aliingilia kati tu,” Linda aliwaza huku akijifuta machozi, ndege ikapotelea angani. *** Kwa kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kusonga mbele, mtoto wa Harrison na Angel, Harvey Junior alizidi kuchangamka, akawa anakua vizuri akiwa na afya njema, jambo lililozidisha furaha kwa wote wawili. “Mume wangu!” “Naam mke wangu.” “Kuna jambo nataka kumfanyia mtoto wetu kwa manufaa yake ya baadaye.” “Jambo gani kipenzi changu.”
“Nataka unisaidie kukivua hiki kidani changu shingoni, tukisafishe vizuri kisha tumvalishe ili na yeye kimpe ulinzi kama kilivyofanya kwangu tangu nikiwa mdogo mpaka leo hii nimekuwa mkubwa,” alisema Angel huku akikaa vizuri ili mumewe amvue kidani hicho. Tangu siku ya kwanza Harrison alipomuona Angel kwa karibu, aligundua kuwa alikuwa na kidani hicho shingoni ambacho
kutokana na kuwa na nywele nyingi, hakikuwa kikionekana kwa urahisi. Kuna wakati aliwahi kumhoji alikokipata kidani hicho lakini majibu yake yalionesha kuwa na yeye hakumbuki ila tangu aanze kuwa na akili, alijikuta akiwa amekivaa.
Mara kwa mara Harrison alikuwa akitaka kumvua lakini alikuwa mkali kwa madai kuwa amekuwa akikitumia kama kinga yake kwa kipindi chote cha maisha yake mpaka siku hiyo alipoamua mwenyewe kwa hiyari yake. Harrison alimkubalia, akaanza kazi ya kukifungua.
Kutokana na kukaa miaka mingi mwilini mwake, kazi ya kukivua haikuwa nyepesi mpaka akalazimika kukikata, kikaacha alama kwenye shingo ya Angel. Licha ya kuonekana kuchakaa sana, kidani hicho kwa mbali kilionesha kuwa na maandishi yaliyokuwa yanasomeka kwa shida, Harrison akakishika na kuanza kukichunguza kwa umakini wa hali ya juu. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Wakakubaliana kuwa kabla ya kumvalisha mtoto wao, lazima wakipeleke kwa sonara kikasafishwe na kung’arishwa ili kirudie upya wake, kazi ambayo Harrison alitakiwa kuifanya. Kabla ya kuondoka, Harrison aliendelea kumuuliza mkewe maswali mbalimbali kuhusu kidani hicho lakini kama alivyokuwa akimjibu siku zote, hakuwa akikumbuka chochote jinsi kilivyofika mwilini mwake.
Baada ya muda, Harrison alitoka na kwenda kwenye duka la sonara lililokuwa jirani na pale walipokuwa wanaishi. Jambo la kwanza kabla ya kukisafisha, Harrison alimuomba sonara amsaidie kuyasoma maandishi yaliyokuwa kwenye kidani hicho kwa kutumia kifaa maalum. Akaahidi kumpa malipo ya ziada baada ya kuikamilisha kazi hiyo. Sonara akakichukua na kukiweka kwenye mtambo maalum na kuanza kukipitisha taratibu kwa lengo la kuyasoma maandishi hayo. *** SIRI kubwa iliyokuwa imejificha juu ya maisha ya Harrison ya kuudanganya ulimwengu kuwa amekufa kwenye ajali ya barabarani ili apate muda wa kwenda kuwa na malkia wa masokwe, inakaribia kujulikana. Harrison hajui
kama anafuatiliwa kwa karibu, anaendelea na maisha yake kama kawaida na mkewe kipenzi, wakiwa tayari wamejaliwa kupata mtoto wa kwanza, Harvey Junior.
Kila anapokumbuka jinsi alivyolipigania penzi la msichana huyo ambaye sasa ni mke wake halali, anajikuta akizidi kumpenda na kuahidi kumlinda kwa siku zote za maisha yake. Wanaendeleza maisha yao katika Mji wa Langley nchini Canada.
Upande wa pili, upelelezi wa nguvu unaofanywa na Linda, msichana ambaye Harrison alimkimbia kanisani siku ya harusi yao, amecharuka mno na sasa amekaribia kufahamu mahali Harrison alipo baada ya kugundua kuwa akaunti yake ya benki ilikuwa ikiendelea kutumika kutoka kwenye Mji wa Abbortsford nchini Canada. Anaamua kufunga safari mpaka kwenye mji huo.
“Lazima nimpate Harrison kwa njia yoyote, nataka anitamkie ana kwa ana kwamba hanipendi na hataki kuishi na mimi, najua akiniona lazima atabadilisha msimamo wake kwani bado nampenda sana na naamini na yeye ananipenda ila shetani aliingilia kati tu,” Linda aliwaza huku akijifuta machozi, ndege ikapotelea angani.
Baada ya kusafiri kwa saa nyingi angani, hatimaye ndege aliyopanda Linda, Airbus 380 mali ya Kampuni ya Nordic Airways iliwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ottawa nchini Canada. Mhudumu wa ndege akatoa taarifa kwa abiria wote kuwa kila mmoja afunge mkanda kwani ndege ilikuwa ikijiandaa kutua.
Muda mfupi baadaye, ndege iligusa ardhi ya Canada, ikakimbia kwa kasi mpaka mwisho wa uwanja kisha ikageuza na kuanza kurudi taratibu kuelekea kwenye ofisi za uwanja huo wa kimataifa. Ikasimama kisha ngazi zikateremshwa, abiria wakaanza kushuka mmoja mmoja. Linda alikuwa miongoni mwa abiria hao, akawa anaangaza macho huku na kule kwani hiyo ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kufika nchini humo.
Hakutaka kupoteza muda, alipoteremka kwenye ndege tu, alitoka nje ya uwanja wa ndege na kuulizia usafiri wa kuelekea Abbotsford. Dereva teksi mmoja akamuelekeza kuwa ni lazima asafiri kwa mabasi yaendayo kwa kasi ili kufika huko kwa sababu kulikuwa na umbali mrefu kutoka Ottawa.
Linda alikubaliana naye na kumuomba ampeleke na teksi yake mpaka stendi ya mabasi yaendayo kwa kasi. Akaingia ndani ya gari na safari ikaanza. Alipomfikisha stendi, Linda alimlipa fedha zake kisha akateremka na kuelekea kwenye sehemu ya kukatia tiketi. Kabla ya kutoa fedha, aliuliza mambo mawili matatu kuhusu safari yake, alipojibiwa akakata tiketi kisha akaenda kuungana na abiria wengine kusubiri basi lianze safari.
Takribani dakika kumi na tano baadaye, basi liliwasili stendi, abiria wakapanda na safari ya kuelekea Abbotsford ikaanza. Bado mawazo yaliendelea kukisumbua kichwa cha Linda kiasi cha kuona anachelewa kufika. Japokuwa basi hilo lilikuwa likisafiri kwa spidi kubwa, Linda aliona kama linakwenda taratibu, akatamani angekuwa na uwezo apae angani kama ndege ili awahi kufika.
Safari haikuwa nyepesi kwani kulikuwa na umbali mrefu kutoka Ottawa mpaka Abbortsford, Linda akajikuta akipitiwa na usingizi akiwa ndani ya gari. Akiwa usingizini, alianza kuota ndoto za ajabuajabu, hali iliyomfanya awe anashtukashtuka kila mara.
Baada ya safari ndefu, hatimaye basi likawasili Abbortsford. Kwa kuwa muda ulikuwa umekwenda sana, Linda alitafuta hoteli nzuri ya kitalii na kufikia hapo. Akaenda kujipumzisha wakati akifikiria nini cha kufanya na wapi pa kuanzia. Hakutaka mtu yeyote ajue juu ya uwepo wake eneo hilo.
Usiku hakulala, aliendelea kuwaza mambo mengi ndani ya kichwa chake, kitu ambacho hakuweza kukibadilisha mpaka muda huo ilikuwa ni penzi lake kwa Harrison. Kwa kadiri alivyokuwa anakaribia kufahamu ukweli juu ya Harrison, ndivyo hisia zake za mapenzi zilivyokuwa zinazidi kuamka. Akawa anajiapiza kuwa hawezi kuhangaika kiasi hicho halafu akaishia kulikosa penzi la mwanaume wa maisha yake.
Hakutaka kujali Harrison kwa nini alimkimbia au yupo na nani, kitu pekee alichotaka ilikuwa ni kutimiza ndoto yake iliyoyeyuka miaka kadhaa iliyopita ya kuolewa na Harrison. Aliendelea kuwaza mambo mbalimbali huku akiandika vitu muhimu kwenye kitabu chake cha kumbukumbu. Asubuhi kulipopambazuka, aliwahi kuamka na kujiandaa kisha akatoka na kwenda kwenye kituo cha teksi.
“Naomba unipeleke kwenye Benki ya Barclays, Tawi la Abbortsford,” Linda alimwambia dereva teksi aliyekuwa jirani naye, akaingia ndani ya teksi na safari ikaanza. Iliwachukua dakika kumi tu, wakawa tayari wameshafika. Linda akamlipa dereva fedha zake kisha akaingia ndani ya benki hiyo na kuomba kuonana na meneja mkuu.
“Mimi ni afisa upelelezi kutoka nchini Marekani, kuna taarifa muhimu nazifuatilia kuhusu mtuhumiwa mmoja ambaye alitoroka siku nyingi zilizopita na duru za kiintelijensia zinaonesha yupo kwenye mji huu,” utambulisho alioutoa Linda ulimfanya meneja wa benki hiyo akae vizuri na kumtegea sikio kwa umakini. Akamuonesha vitambulisho vyake na hati maalum ya kufanya kazi ndani ya Canada ambayo aliitafuta kabla hajasafiri.
Alimueleza meneja huyo kuwa taarifa za kibenki zinaonesha kuwa mtuhumiwa anayetafutwa, anaendelea kutumia akaunti yake kupitia tawi hilo. Linda aliamua kutumia jina la ‘mtuhumiwa’ kwa Harrison ili iwe rahisi kwake kupata taarifa muhimu kwani alijua kuwa akimtambulisha kama mpenzi wake aliyemkimbia, suala hilo litapoteza uzito.
Aliendelea kueleza mambo kadhaa ambayo yalizidi kumpa picha meneja huyo kuwa ni kweli mtu anayezungumziwa yupo ndani ya mji huo na anatumia akaunti yake kupitia benki hiyo. Kwa kuwa tayari Linda alishaandika tarehe ambayo akaunti ya Harrison ilitumika kwa mara ya kwanza kwenye tawi hilo, meneja hakupata shida.
Alichokifanya ilikuwa ni kumuita mtaalamu wa IT (Information Technology) wa benki hiyo na kumuomba waongozane mpaka kwenye chumba kilichokuwa na kamera za siri zilizotegeshwa kwenye mashine zote za ATM kwenye benki hiyo. Walipofika ndani ya chumba hicho kikubwa kilichokuwa kimejaa mitambo ya kisasa ya ulinzi, Linda alielekezwa sehemu ya kukaa kisha mtaalamu huyo akaanza kazi akishirikiana na meneja wake.
“Unaikumbuka namba ya akaunti yake?” “Ndiyo, hii hapa,” alisema Linda huku akifunua kitabu chake cha kumbukumbu, wakazitumia namba hizo kufahamu muda ambao ilitumika ili iwe rahisi kunasa picha za mtu aliyeitumia. Mtaalamu wa IT aliendelea kushughulikia mitambo na baada
ya muda, akafanikiwa kuzinasa picha za Harrison zikimuonesha jinsi alivyochukua fedha kwenye mashine ya ATM. “Mungu wangu, ndiyo yeye! Jamani Harrison… ni yeye,” Linda aliyekuwa amekaa, alikurupuka na kuisogelea kompyuta
aliyokuwa anaitumia mtaalamu yule kufuatilia picha za matukio baada ya kuiona taswira ya Harrison. Japokuwa alikuwa amebadilika kidogo kwa kufuga nywele ndefu zilizoonesha kukosa matunzo na ndevu, bado Linda aliweza kumtambua vizuri Harrison, mapigo ya moyo wake yakawa yanaenda kwa kasi akiamini sasa kila kitu kitafahamika na lazima atampata Harrison kama alivyokuwa amejiapiza. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Baada ya kufanikiwa kwa hatua hiyo ya kwanza, Linda aliomba ahamishiwe picha hizo kwenye ‘laptop’ yake kwa ajili ya ushahidi, jambo ambalo lilitekelezwa kisha akaomba kupata ‘bank statement’ na picha za ushahidi za siku zote ambazo Harrison alitumia tawi hilo la benki.
Katika siku za mwanzo, Harrison alionekana akifika benki kwenye mashine ya ATM na kutoa kiwango fulani cha fedha na kuondoka lakini baada ya kufanya hivyo kwa siku kadhaa, alionekana mtu mwingine kabisa, akiwa na sura tofauti akifika benki na kutoa fedha kwa kutumia akaunti ya Harrison. Kilichozidi kumchanganya Linda, mtu huyo alikuwa akifanana na Harrison umbo la mwili wake na jinsi alivyokuwa akitembea. Utata mwingine ukaibuka. *** Nisingependa kumaliza hadithi hii ya leo bila kukumbusha jambo muhimu la kutoa maisha yako kwa Mungu. Maisha tuliyonayo hapa duniani ni mafupi sana, yanapita kama maua yachanuavyo na kunyauka. Wengi unaowafahamu wamekufa lakini wewe unapumua, ni vyema basi kufikiria maisha baada ya kifo.
LINDA amechachamaa kumfuatilia Harrison mpaka aujue mwisho wake. Hataki kukubali kuwa mwanaume huyo aliyemkimbia kanisani siku ya harusi yao anampenda msichana mwingine kuliko
anavyompenda yeye. Anaamini alipitiwa na shetani tu ndiyo maana akafanya yote hayo lakini bado anampenda.
Baada ya kugundua kuwa akaunti ya benki ya Harrison inaendelea kutumika kwenye Mji wa Abbotsford, Canada, msichana huyo kutoka familia ya kitajiri anaamua kufunga safari mpaka nchini humo. Anatumia mbinu zote za upelelezi alizojifunza akiwa chuoni ili kuhakikisha anamrejesha Harrison mikononi mwake.
Anaenda mpaka kwenye benki iliyoonesha kuwa akaunti ya Harrison ilitumika. Kwa kutumia picha zilizopigwa na kamera maalum zilizotegeshwa kwenye mashine za ATM, Linda anafanikiwa
kugundua kuwa kumbe Harrison bado alikuwa hai. Hata hivyo, anashangazwa na watu wawili wanaotumia akaunti hiyo. Anaamua kufuatilia kwa kina. Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…
Kilichozidi kumchanganya Linda, mtu huyo alikuwa akifanana na Harrison umbo la mwili wake na jinsi alivyokuwa akitembea. Utata mwingine ukaibuka. Hata hivyo, hakutaka kuonesha wasiwasi wake mbele ya watu, akatulia na picha zikaendelea
kuhamishiwa kwenye laptop yake mpaka zilipoisha. Akapewa na ‘bank statement’ kama alivyokuwa ameomba. Baada ya taratibu zote kukamilika, aliwashukuru meneja wa benki na mtaalamu wa teknolojia ya mawasiliano (IT) ambao walimsaidia sana kutimiza alichokuwa anakitaka. Alipotoka, alirudi moja kwa moja mpaka kwenye chumba cha hoteli aliyokuwa
amefikia na kujifungia ndani ya chumba chake, akaitoa laptop yake iliyokuwa na picha na taarifa zote muhimu na kuanza kuichunguza kwa jicho la tatu.
Alitaka kufahamu yule mtu mwingine aliyeonekana anaitumia akaunti ya Harrison ni nani na ana uhusiano gani na mpenzi wake huyo. Alizivuta jirani (zoom) picha zote mbili, ile ya Harrison na ile ya mtu mwingine. Picha ya kwanza ilimthibitishia kuwa aliyemuona alikuwa ni Harrison kwani licha ya kuwa na nywele ndefu na ndevu nyingi, bado sura yake haikubadilika.
Kwa uhakika zaidi, alitoa picha yake nyingine aliyokuwa anatembea nayo kwenye mkoba wake, akawa anaifananisha na ile ya kwanza, akajiridhisha kuwa ni kweli alikuwa ni Harrison. Akaanza kuifananisha na ile ya mtu yule ambaye bado alikuwa hajamtambua.
Kila alipojaribu kuvuta kumbukumbu kama alishawahi kumuona wapi, hakupata jibu. Akaanza kumchunguza kiungo kimoja baada ya kingine. Katika hali ambayo hakuitegemea, aligundua kuwa mtu yule alikuwa akifanana kwa kiasi kikubwa na Harrison kwa vitu vingi.
Alifanana naye kuanzia macho, pua, mdomo, masikio na jinsi mwili wake ulivyokuwa umejengeka. “Mbona Harrison hajawahi kuniambia kama ana ndugu yake anayefanana naye kiasi hiki? Yeye alizaliwa peke yake kwa mama yake na hana ndugu yeyote. Huyu ni nani?”
Linda alijiuliza maswali mengi ambayo yote yalikosa majibu. Ikabidi ajipe muda wa kutafakari kilichokuwa kinaendelea, akawa anarudiarudia kuitazama ile picha.
“Au ni yeye ameamua kubadilisha sura kwa kufanyiwa plastic surgery?” wazo jipya liligonga ndani ya kichwa cha Linda, akazidi kuitazama ile picha kwa umakini wa hali ya juu.
Akili zake zikamtuma kuwa lazima yule ni Harrison ila aliamua kubadilisha sura ili iwe vigumu kwa watu waliokuwa wanamfahamu kumtambua.
“Kama aliweza kuudanganya ulimwengu kuwa amekufa, unafikiri anaweza kushindwa kujibadili sura ili aendelee kuishi bila kusumbuliwa?” Linda alijiuliza maswali yaliyozidi kumpa mwanga wa nini cha kufanya.
Alizidi kuumia moyo wake kuona Harrison alikuwa tayari kupoteza ushahidi wa yeye kuwepo duniani kwa sababu ya mapenzi ya mwanamke aliyelelewa na masokwe. Ndani ya nafsi yake alijiapiza kufanya kila linalowezekana kuhakikisha anampata Harrison na kumrudisha mikononi mwake. Kamwe hakutaka kukubali kushindwa kirahisi kumpoteza mwanaume aliyekuwa anampenda kuliko kitu chochote duniani.
Baada ya kupata uhakika kuwa Harrison atakuwa amebadilisha sura, alianza kazi ya kutafuta vituo vya plastic surgery vilivyokuwa ndani ya Mji wa Abbotsford. Aliamini kwa kutumia mafunzo yake ya kipelelezi aliyoyapitia, lazima atafanikiwa kujua alibadilishwa sura kwenye kituo gani. Aliamini akishakijua kituo hicho na kumpata mtu aliyefanya kazi hiyo, itakuwa rahisi kufahamu anuani ya makazi ya Harrison.
Hakutaka kupoteza muda, alianza kutafuta kwenye intaneti orodha ya kliniki zilizokuwa zinatoa huduma ya kubadilishwa sura (plastic surgery). Aligundua kuwa kulikuwa na kliniki tatu pekee ambazo ndiyo zilizokuwa zinatoa huduma hiyo, Abbotsford Clinic, Facial Surgery Clinic na Albert Stein Sanitarium.
Muda huohuo alinyanyuka akiwa ameshanakili anuani za mahali kliniki hizo zilipo, akabeba laptop yake na kutoka hadi nje, akakodi teksi na kumuelekeza dereva kumzungusha kwenye kliniki hizo.
Alianzia Abbotsford Clinic, alipofika alijitambulisha kuwa yeye ni mpelelezi wa kimataifa kutoka Marekani na amefika hapo kwa ajili ya kumsaka mtuhumiwa ambaye alifanya uhalifu nchini kwake na kutoroka.
“Kuna taarifa za kuaminika kuwa amebadilisha sura na sasa ana mwonekano tofauti kabisa. Tafadhali nisaidie kuangalia katika orodha ya watu uliowafanyia ‘plastic surgery’ na ukinisaidia kumpata nitakupa donge nono,” alisema Linda huku akikaa kwenye kiti, mbele ya daktari mzoefu wa kazi hiyo.
“Samahani, siwezi kukusaidia kwa sababu ni mwiko kwa taaluma yetu kutoa taarifa za wateja wetu, utanisamehe kwa hilo.” “Kwani hujui kwamba kuna sheria zinazoisimamia kazi yako? Nimeshakwambia mimi ni mpelelezi wa kimataifa na hiki ni kitambulisho changu.
Ukishindwa kunipa ushirikiano nitatoa maagizo ukamatwe na kutupwa lupango,” alisema Linda huku akionesha kubadilika. Sasa alivaa sura ya kazi na hakutaka masihara hata kidogo.
Baada ya daktari huyo kuona Linda amebadilika, ilibidi atii amri aliyopewa, akafungua kompyuta yake na kuanza kumuonesha Linda orodha ya watu wote waliofanyiwa plastic surgery katika kliniki hiyo. Linda alianza kupitia taarifa za mtu mmoja baada ya mwingine lakini hakuona kama Harrison alikuwepo.
Alipojiridhisha, aliondoka huku akiahidi kuwa atarudi tena endapo atakwama. Akachomoa noti kadhaa na kumpa daktari huyo kisha akaondoka. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Alitoka nje ambapo alimkuta dereva teksi aliyemleta akiwa anamsubiri. Akaingia na safari ikaanza kuelekea kwenye kliniki ya pili, Facial Surgery Clinic ambapo Linda alitumia mbinu kama alizozitumia awali.
Hata hivyo, alipopewa orodha ya watu waliofanyiwa upasuaji wa kubadilishwa sura kwenye kiliniki hiyo, Harrison hakuwa miongoni mwao. Linda akaanza kukata tamaa kwani matumaini yake yalikuwa yakififia kwa kasi.
Hata hivyo, hakutaka kuishia hapo, aliamua kwenda kuhitimisha kazi yake kwenye kliniki ya mwisho.
Alitoka hadi nje na kuingia ndani ya teksi huku akionesha kuwa na mawazo mengi, akamuelekeza dereva kumpeleka kwenye kliniki ya mwisho, Albert Stein Sanitarium. Alipofika, alijitambulisha mapokezi kisha akapelekwa moja kwa moja kwa Dk. Albert Stein aliyekuwa akiimiliki kliniki hiyo. Linda alijitambulisha na kutoa kitambulisho chake kisha akaeleza kilichompeleka.
Tofauti na kliniki mbili alizopitia awali, Dk. Stein alionesha ushirikiano wa hali ya juu, akaanza kumuonesha orodha ya watu wote waliofanyiwa upasuaji huo kwenye kliniki yake. Wakati akiendelea kumuonesha, Linda aliona picha ambayo ilimfanya apige kelele. “Ndiyo mwenyewe! Mungu wangu,” alisema huku akimtaka Dk. Stein kuivuta kwa karibu picha ya Harrison.
MAPENZI kati ya Harrison na mkewe Angel yanazidi kushamiri, upendo wa dhati unaongezeka kati yao baada ya kupata mtoto wa kwanza, Harvey Junior. Wakati hayo yakiendelea, msichana ambaye Harrison alimkimbia siku ya harusi yao, Linda amechachamaa kumfuatilia Harrison mpaka aujue mwisho wake. Hataki kukubali kuwa mwanaume huyo anampenda malkia wa masokwe kuliko anavyompenda yeye na ndiyo maana alikuwa tayari kupata shida kwa kipindi kirefu wakati akipigania penzi lake. Linda anaamini Harrison alipitiwa na shetani tu ndiyo maana akafanya yote hayo lakini bado anampenda kwa dhati. Upelelezi wa kina anaoufanya Linda unamuwezesha kugundua kuwa Harrison yupo kwenye Mji wa Abbotsford, Canada. Msichana huyo kutoka familia ya kitajiri anaamua kufunga safari mpaka nchini humo na baadaye anagundua kuwa kumbe Harrison alibadilisha sura. Baada ya kugundua jambo hilo, Linda anaanza kupita kwenye kliniki za kubadilishia sura akitafuta maelezo ya kina ya Harrison na mahali alikokuwa anaishi kwa muda huo. Anajiapiza kuwa ni lazima ampate mwanaume huyo na kurejesha penzi lake.
Sonara aliyepewa kazi na Harrison ya kuyasoma maandishi yaliyokuwa yameandikwa kwenye kidani cha Angel, alifanya kazi yake kwa bidii hasa baada ya kuahidiwa kuwa angepewa fedha za ziada kwa kuikamilisha kazi hiyo. Kwa kutumia mashine maalum iliyokuwa na lenzi kali, sonara huyo alifanikiwa kuyasoma maandishi hayo. Akachukua kalamu na karatasi na kuyaandika huku akijipongeza kwa kufanikiwa kazi aliyopewa bila kutokwa na jasho. ‘Charlote Abdulkarim Charwe’, sonara aliyaandika maneno hayo kwenye karatasi dogo kisha akaendelea na kazi ya kukisafisha kidani hicho huku kichwani akiwaza dau aliloahidiwa na mteja wake. Baada ya muda, Harrison alimfuata sonara huyo na kumuuliza alikuwa amefikia wapi kwenye kazi aliyompa. “Kazi yako tayari bosi, nipe changu,” alisema sonara huyo huku akimkabidhi Harrison kikaratasi kilichokuwa na maandishi yale pamoja na kidani ambacho baada ya kusafishwa, sasa kilikuwa kiking’aa kama ndiyo kimetoka dukani. “Ahsante sana,” alisema Harrison huku akiingiza mkono mfukoni na kutoa kitita cha fedha, akahesabu kiwango alichokuwa amemuahidi na kumpa. Sonara akachekelea mpaka jino la mwisho likaonekana, akaondoka na kurudi nyumbani kwake huku njia nzima akiwa anakisoma kile kikaratasi na kukirudiarudia. Alishindwa kuelewa majina yale yalikuwa yanamaanisha nini na yalifikaje kwenye kidani cha mkewe kipenzi. Akawa anayatamka huku akiendelea na safari ya kurudi nyumbani. “Charlote Abdulkarim Charwe,” Harrison aliendelea kuyakariri majina hayo huku akipanga kwenda kumuuliza vizuri mkewe kama kuna chochote alichokuwa anakifahamu. Baada ya kufika nyumbani, alipokelewa kwa bashasha na mkewe, wakaingia ndani ambapo Harrison kama kawaida yake, alipitiliza chumbani kwenda kumuangalia mwanaye ambaye alikuwa amelala. “Kuna jambo nataka kukuuliza mke wangu kipenzi.” “Jambo gani baba?” “Kwanza kidani chako hiki hapa, kimeshasafishwa,” alisema Harrison huku akikitoa kidani cha mkewe ambacho sasa kilikuwa kinang’aa. Mkewe akamshukuru na kumbusu shavuni, akataka kwenda kujaribu kumvalisha mwanaye aliyekuwa amelala lakini mumewe akamzuia. “Hicho kidani kina maandishi ambayo nimeshindwa kuyaelewa.” “Maandishi? Yameandikwaje?” aliuliza Angel huku akionesha kushtushwa na kilichosemwa na mumewe. “Harrison akatoa kikaratasi kilichokuwa kimeandikwa; Charlote Abdulkarim Charwe na kumuonesha. Akawa anamuuliza kama anafahamu chochote kuhusu majina hayo. Angel hakuonesha kufahamu chochote, na yeye akawa anashangaa yamefikaje kwenye kidani chake. Waliulizana mambo mengi lakini hakuna aliyekuwa na jibu, Harrison akaamua kuendelea kulifuatilia suala hilo. Kesho yake kulipopambazuka, Harrison aliondoka na kikaratasi kilichokuwa na majina hayo na kwenda kwenye ‘internet cafe’ iliyokuwa jirani na wanapoishi. Alipofika, alilipia na kukaa kwenye kompyuta, akaliandika lile jina na kuanza kulitafuta mtandaoni. Majibu aliyoyapata yalionesha kuwa Abdulkarim Charwe ni daktari anayefanya kazi kwenye Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa jijini Geneva, Uswisi. Aliandika maelezo hayo kwenye karatasi kisha akaondoka na kwenda kazini. Njia nzima akawa anaendelea kujiuliza kuhusu uhusiano uliokuwepo kati ya majina hayo, daktari huyo na mkewe. Jioni aliporudi nyumbani, alimweleza mkewe alichokigundua kuhusu majina hayo, Angel naye akawa anashangaa kwani hakuwa anaelewa chochote. *** Linda alipatwa na mshtuko mkubwa baada ya kuiona picha ya Harrison akiwa miongoni mwa watu waliofanyiwa upasuaji wa kubadilisha sura (Plastic Surgery) kwenye Kliniki ya Albert Stein Sanitarium. Akamwambia daktari huyo aivute picha yake jirani ili aione vizuri. Daktari huyo alitii alichoambiwa, akaivuta na kubonyeza sehemu katika kompyuta ambapo picha mbili zilifunguka, moja ikimuonesha Harrison kabla ya kufanyiwa upasuaji huo na nyingine baada ya kufanyiwa. Alipoifananisha na ile ya kwenye laptop yake, aligundua zinafanana sana, akawa amepata jibu kuwa Harrison alijibadilisha sura, hali iliyomliza sana Linda mpaka daktari akamshangaa. Aliomba kupewa anuani ya makazi ya Harrison ambapo daktari huyo alimpa bila hiyana. Linda akachomoa burungutu la dola za Kimarekani kwenye mkoba wake na kumpa Dk. Stein, akaaga na kurudi hotelini kwake huku akilia kwa uchungu kama mtu aliyefikishiwa taarifa za msiba. Alipofika, alijifungia chumbani kwake na kuanza kuitazama karatasi iliyokuwa na anuani ya mahali Harrison alipokuwa anaishi, mpaka namba ya nyumba. Kulipopambazuka tu, Linda aliwahi kuamka na kwenda moja kwa moja mpaka kwenye mtaa ambao alikuwa anaishi Harrison kwa kutumia maelekezo ambayo aliyapata kwenye kliniki ya Dk. Stein. Kwa kuhofia kuonekana kabla hajamaliza kazi yake, Linda alivaa kofia kubwa iliyoziba sehemu kubwa ya uso wake. Akabadili mpaka mwendo wake, akatafuta sehemu iliyojificha na kukaa huku macho yake akiyaelekeza kwenye nyumba aliyoelekezwa kuwa ndipo Harrison anapoishi. Alitaka kuhakikisha kwa macho yake kama ni kweli Harrison alikuwa akiishi kwenye nyumba hiyo. Pia alitaka kujua alikuwa anaishi na nani. Akiwa amejibanza mahali hapo, Linda alishuhudia mlango ukifunguliwa, mapigo yake ya moyo yakawa yanamuenda kwa kasi kubwa. Alimuona mwanaume ambaye bila wasiwasi alijua kuwa ni Harrison licha ya kubadili sura. Akawa anamtazama kwa makini huku akimfananisha na picha alizotembea nazo, alizochukua kwenye kliniki ya Dk. Stein. Akawa anamuangalia anafanya nini, akamuona akitoka na nguo kwenye beseni na kuanza kuzianika kwenye kamba zilizokuwa nje ya nyumba. Alipozitazama vizuri nguo alizokuwa akizianika, aligundua kuwa ni za mtoto, wivu mkali ukamchoma moyoni kwani hicho kilikuwa ni kiashiria kuwa tayari Harrison alikuwa na mtoto. “Ina maana amezaa na yule sokwe?” Linda alijiuliza huku akijifuta machozi yaliyokuwa yanaulowanisha uso wake. Baada ya kumaliza kuanika nguo, Harrison alirudi ndani. Hakutoka mpaka muda wa kwenda kazini ulipofika ambapo mkewe alimsindikiza. Wakati wanaagana, wakakumbatiana na kumwagiana mvua ya mabusu, huku Linda akishuhudia. Moyo wake ulimchoma sana, akawa analia kwa uchungu mithili ya mtu aliyepewa taarifa za msiba. Alisubiri mpaka walipomaliza kuagana, mwanamke huyo akarudi ndani na Harrison akaondoka kuelekea kazini. Linda alitoka mafichoni na kuanza kumfuatilia kwa nyuma akitaka kujua anakofanyia kazi. Harrison hakuwa na taarifa yoyote kuwa kuna mtu anamfuata kwa nyuma. *** Nisingependa kumaliza hadithi hii ya leo bila kukumbusha jambo muhimu la kutoa maisha yako kwa Mungu. Maisha tuliyonayo hapa duniani ni mafupi sana, yanapita kama maua yachanuavyo na kunyauka. Wengi unaowafahamu wamekufa lakini wewe unapumua, ni vyema basi kufikiria maisha baada ya kifo.
UPENDO wa dhati unazidi kushamiri kwenye ndoa ya Harrison na mkewe Angel baada ya Mungu kuwajalia kupata mtoto wa kwanza, Harvey Junior. Kila mmoja anazidisha mapenzi ya dhati kwa mwenzake. Wakati hayo yakiendelea,
msichana ambaye Harrison alimkimbia siku ya harusi yao, Linda amechachamaa kumfuatilia Harrison mpaka aujue mwisho wake.
Bado anaamini kuwa mwanaume huyo anampenda kwa dhati ila alipitiwa na shetani lakini ipo siku atarudi kwenye maisha yake ili watimize ahadi waliyopeana, ya kufunga ndoa. Hataki kukubali kwamba Harrison anampenda malkia wa masokwe kuliko anavyompenda yeye.
Tayari Linda ameshafika kwenye Mji wa Abbotsford, Canada. Msichana huyo kutoka familia ya kitajiri anagundua kuwa kumbe Harrison alibadilisha sura. Anaanza kumfuatilia kwa karibu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Baada ya Harrison kugundua kuwa kati ya majina yaliyokuwa kwenye kidani cha mkewe, mawili ya Abdulkarim Charwe yalikuwa ni ya daktari aliyekuwa anafanya kazi kwenye Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa jijini Geneva, Uswisi, hakuishia hapo. Aliamua
kuendelea kufanya utafiti kimyakimya akitaka kubaini uhusiano uliokuwepo kati ya mkewe, Angel, jina la Charlote na daktari huyo. Aliamini lazima siri kubwa ya historia ya maisha ya mkewe ilikuwa imejificha kwenye majina hayo kwani kwa siku zote tangu
amfahamu Angel, akiwa kwenye Msitu wa Tongass alikokuwa analindwa na masokwe, hakupata bahati ya kumjua ndugu yake yeyote. Akajiapiza kuwa lazima afuatilie kwa kina, hata ikibidi kusafiri mpaka Geneva, Uswisi na kwenda kuonana na daktari huyo.
Kesho yake, aliendelea kufuatilia taarifa mbalimbali zilizokuwa zinamhusu daktari huyo mtandaoni, akafanikiwa kuipata picha yake, akiwa kwenye kongamano la madaktari wa magonjwa ya saratani kwenye makao makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) jijini
Geneva. Baada ya kuichunguza kwa makini picha hiyo, alishtuka baada ya kubaini kuwa daktari huyo ambaye alikuwa ni mweusi, alikuwa akifanana vitu vingi na mkewe.
“Lazima atakuwa ni ndugu yake, mbona anafanana naye kiasi hiki?” alijisemea Harrison na kumuomba mhudumu wa kituo cha intaneti alichokuwa akiifanyia kazi ile, ‘kui-print’ picha yake kwenye karatasi kwa ajili ya kuondoka nayo. Hakutaka kumshirikisha mkewe kuhusu suala hilo mpaka apate uhakika, akawa anaendelea na uchunguzi wa kimyakimya.
Wakati anatoka kwenye kituo hicho cha intaneti, alishtuka baada ya kumuona msichana aliyevaa kofia kubwa akijificha kwenye magari yaliyokuwa yameegesha nje ya kituo hicho cha intaneti. Alijaribu kumfuatilia lakini hakupata bahati ya kumuona sura kwani alijificha kwenye magari kisha akatokomea kusikojulikana.
Alijiuliza maswali mengi msichana huyo ni nani na kwa nini alikuwa akimfuatilia lakini hakupata majibu. Kilichomshangaza zaidi ni kwamba alikuwa amevaa kofia kubwa iliyomziba sehemu kubwa ya mwili wake. Alibaki na maswali mengi ambayo hayakuwa na majibu.
Baada ya kutoka, alienda kazini kwake kuendelea na ratiba zake kama kawaida. Jioni akarudi moja kwa moja mpaka nyumbani kwake na kumweleza mkewe juu ya mtu huyo ambaye ilionesha kuwa alikuwa akimfuatilia.
“Atakuwa ni nani?” “Hata sijui, yaani hapa nimebaki na maswali mengi kweli kichwani.” “Kuwa makini mume wangu, si unajua wewe ndiyo kila kitu kwenye maisha yetu? Tunakupenda na kukutegemea.” “Usijali mke wangu, nitajitahidi kuwa makini,” alisema Harrison kisha wakaendelea na mazungumzo ya kawaida. Hata hivyo,
Harrison hakumwambia chochote kuhusu hatua aliyokuwa ameifikia kwenye utafiti wake aliokuwa anaendelea kuufanya juu ya majina aliyoyakuta kwenye kidani cha mkewe.
Siku hiyo ilipita, kesho yake akawahi kuamka ambapo alimuandalia mkewe maji ya kuoga pamoja na ya mtoto, pamoja na kupika uji kwa ajili ya mwanaye huyo. Akawaamsha na kumuogesha mtoto kisha akafua nguo alizozichafua mtoto huyo usiku. Baada ya kumaliza kazi hizo, alijiandaa na kuondoka kwenda kazini na kumuacha mkewe na mwanaye wanaendelea kupumzika.
“Mume wangu ananipenda mpaka naogopa. Hivi ni mwanaume gani anaweza kuwa anamfanyia yote haya mkewe?” akija nitamshauri tutafute msichana wa kutusaidia kazi ili siku chache zijazo na mimi nianze kwenda kazini,” aliwaza Angel akiwa amejilaza kitandani, akimnyonyesha mwanaye.
Mumewe aliporudi kutoka kazini, alimuandalia chakula na baada ya kula, alimweleza kuwa anataka kuzungumza naye kuhusu malezi ya mtoto wao. Harrison hakuwa na kipingamizi, akakaa mkao wa kumsikiliza mkewe.
“Mume wangu.” “Naam mke wangu kipenzi.” “Najua unanipenda na unampenda pia mtoto wetu kiasi cha kuwa tayari kufanya chochote. Nafarijika sana lakini kuna jambo nataka nikuombe mume wangu.” “Ongea tu mke wangu, nakusikiliza.”
“Nataka tutafute msichana wa kutusaidia kumlea mtoto wetu kwani nataka mume wangu upumzike, kubwa zaidi na mimi nataka nianze kufanya kazi.”
“Huoni kwamba mtoto wetu bado mdogo? Kwa nini usiendelee kumlea mke wangu?” “Napenda kuendelea kukaa nyumbani lakini hali ya maisha inazidi kuwa ngumu mume wangu. Tafadhali niruhusu,” alisema Angel,
Harrison akafikiria kwa muda kisha akakubaliana na mkewe. Wakakubaliana kuwa Linda ndiyo afanye kazi ya kumtafuta msichana wa kuwasaidia kazi. Alifurahi sana mumewe kukubaliana naye, akamkumbatia na kumbusu kimahaba, wakaendelea kuzungumza mambo yao ya kifamilia mpaka muda wa kulala ulipofika. ***
Baada ya kupata uhakika kuwa aliyemuona alikuwa ni Harrison lakini akiwa amejibadilisha sura, Linda alikaa nje ya kituo cha intaneti alichoingia na kumsubiri mpaka aone mwisho wake. Kikubwa alichotaka kufahamu ni mahali alipokuwa anafanyia kazi ili ajipange vizuri namna ya kumnasa na kumrejesha kwenye mikono yake.
Kwa bahati mbaya, alijisahau alipokuwa amejificha mpaka Harrison alipotoka, ikabidi ageuke nyuma haraka na kwenda kujificha kwenye magari yaliyokuwa yamepaki nje ya kituo hicho. Alipoona anamfuata, ilibidi akimbie kwani hakupenda amtambue wakati bado hajakamilisha kazi yake.
Mpango wake wa kumfuatilia mpaka kazini kwake ukawa umeshindikana kwa muda huo lakini hakutaka kukata tamaa. Jioni alitoka hotelini alikokuwa amefikia na kutembea taratibu mpaka kwenye nyumba aliyokuwa anaishi Harrison. Akajipenyeza kimyakimya mpaka kwenye dirisha la nyumba hiyo na kujificha kwenye maua.
Alikaa hapo mpaka aliposikia Harrison akiingia, akatega sikio na kuanza kusikiliza mazungumzo yao. Roho ilimuuma sana alivyokuwa akisikiliza mazungumzo yao kwani walionesha kuwa walikuwa kwenye mapenzi mazito. Licha ya machozi kumtoka, hakutaka kuondoka, aliendelea kuwasikiliza mpaka walipoanza kuzungumza suala la kumtafuta msichana wa kazi.
Aliposikia kuwa wanatafuta mfanyakazi wa kuwasaidia kumlea mtoto wake, alifurahi sana ndani ya moyo wake, akajua hiyo ndiyo nafasi yake ya pekee ya kumrudisha Harrison kwenye mikono yake. Akaondoka kwa kunyata na kurudi hotelini huku akijipanga kuitumia nafasi hiyo kikamilifu.
Kesho yake asubuhi, aliwahi kwenye Kliniki ya Abbotsford Plastic Surgery kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa kubadilisha sura ili akaombe kufanya kazi ndani ya nyumba ya wanafamilia hao. ***
Nisingependa kumaliza hadithi hii ya leo bila kukumbusha jambo muhimu la kutoa maisha yako kwa Mungu. Maisha tuliyonayo hapa duniani ni mafupi sana, yanapita kama maua yachanuavyo na kunyauka. Wengi unaowafahamu wamekufa lakini wewe unapumua, ni vyema basi kufikiria maisha baada ya kifo.
MAHABA ya dhati yanazidi kushamiri kwenye ndoa ya Harrison na mkewe Angel. Mungu anawajalia kupata mtoto wa kwanza wa CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ kiume, Harvey Junior, jambo linalozidisha mapenzi. Kila mmoja anaifurahia ndoa na hakuna anayejuta kukutana na mwenzake.
Kupitia kidani alichokuwa amekivaa Angel tangu Harrison amfahamu, wanagundua kuwa kuna majina matatu yameandikwa.
Harrison anakipeleka kwa sonara na kugundua kidani kina majina ya Charlote Abdulkarim Charwe. Anaanza kupeleleza ambapo anagundua kuwa ni daktari nchini Uswisi.
Wakati hayo yakiendelea, Linda amechachamaa kumfuatilia Harrison mpaka aujue mwisho wake na sasa ameshajua mpaka anapoishi, anamfuatilia mitaani bila mwenyewe kujua.
Linda akiwa amejificha nyuma ya nyumba ya Harrison na mkewe, aliwasikia wakijadiliana kuhusu kutafuta msichana wa kuwasaidia kazi za ndani ikiwa ni pamoja na kumlea mtoto wao, Harvery Junior. Baada ya kusikia mazungumzo hayo, Linda alianza kushangilia ndani ya moyo wake kwani alijua hiyo ndiyo nafasi pekee ya kupenya na kuingia kwenye familia hiyo. Hakutaka kupoteza muda, aliondoka eneo hilo kwa kunyata hadi alipofika mbali, akatimua mbio kurudi hotelini alikokuwa amefikia na kuanza kutafakari njia pekee itakayomuwezesha kuingia ndani ya familia ya Harrison kwa urahisi. Akili ikamjia kuwa na yeye aende kubadilisha sura kisha akaombe kazi ya uhausigeli ili atimize malengo yake. Kesho yake asubuhi, aliwahi kwenye Kliniki ya Abbotsford Plastic Surgery kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa kubadilisha sura ili akaombe kufanya kazi ndani ya nyumba ya wanafamilia hao. Baada ya kusubiri kwa muda mapokezi, hatimaye Linda alipata nafasi ya kuingia ndani ya chumba cha daktari aliyekuwa anashughulika na kazi ya kufanya upasuaji wa kubadilisha sura. Akazungumza naye na kuahidi kumpa dau nono endapo ataifanya kazi hiyo ndani ya muda mfupi kadiri awezavyo. Kwa kuwa daktari alishatangaziwa dau, alikubaliana naye. Akavunja ahadi za wagonjwa waliokuwa wanamsubiri na kuingia ndani ya chumba cha upasuaji, akaanza kazi ya kumbadilisha Linda kama mwenyewe alivyokuwa anataka. Alichagua kuwa na mwonekano wa sura kama walivyo wasichana wa Canada. Baada ya kazi ngumu iliyochukua zaidi ya saa tatu, upasuaji wa kumbadilisha Linda sura ulikuwa umekamilika. Usingeweza kumtambua kuwa ni yeye kwani alikuwa amebadilika kabisa. Hata hivyo, daktari alimuelewesha kuwa endapo atataka kurejea kwenye mwonekano wake wa zamani, alitakiwa kupaka aina fulani ya mafuta ambayo yangeilainisha plastiki iliyokuwa juu ya ngozi ya uso na kuibandua. Alimshukuru sana na kama alivyokuwa amemuahidi, alimtolea bunda la noti nyingi za Kimarekani. Baada ya taratibu zote kukamilika, Linda alitoka na kuelekea moja kwa moja kwenye maduka ya nguo ambako alichagua mavazi kama waliyokuwa wanavaa wasichana kutoka familia zenye hali duni nchini Canada. Aliamini wasichana wanaofanya kazi za uhausigeli lazima watoke kwenye familia masikini hivyo ili kutowashtua Harrison na mkewe, ilikuwa ni lazima na yeye afanye kila kinachowezekana kujifanyisha kama anatoka kwenye familia masikini. Baada ya kufanya manunuzi ya hapa na pale, alirudi hadi hotelini na kubadilisha nguo zake. Vifaa vyake vyote muhimu akavifungia kwenye kabati, akabeba mfuko mdogo wa plastiki uliokuwa na nguo kadhaa pamoja na vitu vingine vidogovidogo kisha akatoka na kuanza kutembea kwa miguu kuelekea kwenye nyumba aliyokuwa anaishi Harrison na familia yake. Alipokaribia, alianza kupanga mbinu za kuingilia ndani ya nyumba hiyo, akaona ajifanye ana matatizo makubwa kwenye familia yao, hali iliyomlazimu kusafiri mpaka kwenye mji huo kwa ajili ya kutafuta kazi ili apate chochote cha kuisaidia familia yao. “Ngo! Ngo! Ngo! Ngo!” “Karibu,” sauti ya mwanamke ilisikika kutoka ndani sambamba na kilio cha mtoto mdogo. Alikuwa ni Angel ambaye alikuwa akimbadilisha mwanaye nepi baada ya kuzichafua alizokuwa amevaa. Baada ya kusikia mlango ukigongwa, alimalizia kumbadilisha mwanaye haraka kisha akatoka kumuangalia mtu aliyekuwa anabisha hodi. “Karibu! Pita ndani,” alisema Angel huku akimkaribisha mgeni wake kwa uchangamfu. Licha ya kumchangamkia sana, mgeni alionesha kupooza, macho yake yakiwa mekundu kama mtu aliyekuwa amelia kwa muda mrefu. Akaingia naye ndani mpaka sebuleni ambapo alimuuliza kama anaweza kumsaidia. “Samahani dada yangu, nina matatizo makubwa mwenzio. Mama yangu amepooza na inatakiwa fedha nyingi kwa ajili ya kwenda kumtibu. Baba yetu alikufa miaka mingi iliyopita na kutuacha mimi, mdogo wangu mmoja na mama yetu. Naomba unipe kazi yoyote ili nipate fedha za kugharamia matibabu ya mama,” alidanganya Linda huku akijikamua machozi. “Ooh! Pole sana mdogo wangu. Hayo yote ni majaribu ya dunia ambayo inabidi upambane kuyashinda,” alisema Angel na kumsogelea msichana huyo, akawa anambembeleza kwa kumpigapiga mgongoni. “Kwani unaitwa nani?” aliuliza Angel huku akiendelea kumbembeleza msichana huyo. Akilini mwake aliamini kuwa ni kweli alikuwa na shida kubwa iliyohitaji msaada ili kuitatua. Hakufikiria hata kidogo kwamba alikuwa akizungumza na mtu aliyekuwa na lengo moja tu, kumpata Harrison na kumrudisha kwenye himaya yake. “Naitwa Abigail,” Linda alidanganya huku akianza kuchunguza mandhari ya sebule ile. “Kwani unaweza kufanya kazi gani?” “Yoyote, hata kukusaidia kumlea mtoto na kufanya kazi zote za ndani.” “Tena imekuwa bahati nzuri sana kwa sababu nilikuwa natafuta msichana wa kunisaidia kumlea mwanangu, nataka kuendelea na kazi lakini sikuwa na mtu wa kumuachia mtoto,” alisema Angel huku akionesha furaha aliyokuwa nayo kwa kumpata hausigeli kiulaini. Alimhakikishia kuwa asiwe na wasiwasi kwani kama ni kazi basi ameipata. Akamwambia atajadiliana na mumewe atakaporudi ili wawe wanamlipa mshahara mzuri utakaomuwezesha kumudu kugharamia matibabu ya mama yake kama alivyoeleza. Linda ambaye sasa alijitambulisha kwa jina la Abigail, akiwa na mwonekano tofauti kabisa wa sura, alimshukuru Angel mpaka akapiga magoti. Akamuahidi kuwa atakuwa mchapa kazi na atajituma kwa kadiri ya uwezo wake wote. Wawili hao waliendelea na mazungumzo ya hapa na pale, Angel akampa msichana huyo mwanaye ili acheze naye wakati wakimsubiri Harrison arudi kazini. Ilipofika jioni, Harrison alirejea kutoka kazini akiwa na zawadi mbalimbali kwa ajili ya mkewe na mwanaye. Alipoingia ndani tu, mkewe aliinuka na kumvaa mwilini, wakakumbatiana kwa dakika kadhaa huku wakimwagiana mvua ya mabusu kama ilivyokuwa kawaida yao. Baada ya kumaliza kusalimiana na mkewe, Harrison alimbeba mwanaye na kuanza kumrusharusha kwa upendo. Mkewe akautumia muda huo kumtambulisha kwa mgeni aliyekuwa amekaa pembeni akishuhudia kila kilichokuwa kinaendelea. Akamtambulisha kuwa ndiyo atakuwa mfanyakazi wao wa ndani. “Mbona kama una wasiwasi sana?” Harrison alimuuliza msichana huyo wakati akisalimiana naye, muda mfupi baada ya kutambulishwa na mkewe. Alishangaa kumuona akitetemeka huku akilengwalengwa na machozi. Hat hivyo, Harrison alidhani ni hofu ya ugeni ndiyo iliyomfanya awe hivyo. Walikula chakula cha jioni pamoja kisha wakaenda kumuonesha chumba ambacho atakuwa akikitumia. Baada ya hapo wakaagana, Harrison, mkewe na mtoto wao wakaelekea chumbani kwao wakati msichana huyo naye alianza kujiandaa kulala kwenye chumba chake. “Lazima nimpate Harrison wangu, hata ikibidi kuua nipo tayari,” aliwaza Abigail (Linda) akiwa amejilaza kitandani, mawazo mengi yakipita ndani ya kichwa chake. ***
WAKATI mapenzi kati ya Harrison na Angel yakizidi kupamba moto, wakimshukuru Mungu wao kwa kuwaongezea furaha kwa kuwajalia kupata mtoto mzuri wa kiume, Harvey Junior, kumbe Linda anafanya kila liwezekanalo kuingia kwenye maisha yao. Baada ya kufanikiwa kufahamu nyumba waliyokuwa wanaishi Harrison na mkewe, jioni moja Linda anaenda nyuma ya nyumba hiyo na kusikiliza mazungumzo ya wanandoa hao. Anasikia wakizungumzia kuhusu kutafuta hausigeli. Baada ya hapo, Linda anakwenda kujibadilisha sura kisha anarudi hotelini anakoingia bila kuonekana, anachukua baadhi ya vitu vyake na kutoka mpaka nyumbani kwa Harrison. Anaingia kwa gia ya uongo na kufanikiwa kupata kazi ya uhausigeli
Walikula chakula cha jioni pamoja kisha wakaenda kumuonesha chumba ambacho atakuwa akikitumia. Baada ya hapo wakaagana, Harrison, mkewe na mtoto wao wakaelekea chumbani kwao wakati msichana huyo naye alianza kujiandaa kulala kwenye chumba chake. “Lazima nimpate Harrison wangu, hata ikibidi kuua nipo tayari,” aliwaza Abigail (Linda) akiwa amejilaza kitandani, mawazo mengi yakipita ndani ya kichwa chake. Wakiwa chumbani kwao, Angel na Harrison waliendelea na mazungumzo ya hapa na pale huku wakifanyiana michezo ya kimahaba. Harrison akaamua kuutumia muda huo kuwasilisha mpango maalum aliokuwa ameupanga kichwani mwake, akitaka kufahamu ukweli juu ya maisha ya zamani ya mkewe. “Mke wangu, nataka kusafiri kwenda Geneva, Uswisi. Tunakwenda kikazi pamoja na wafanyakazi wenzangu wawili,” alisema Harrison huku akijaribu kumficha mkewe sababu ya safari yake hiyo ya dharura. Angel alishtuka kusikia taarifa hiyo kutoka kwa mumewe kwani tangu waoane, hakuwahi kusafiri na kwenda mbali naye hata kwa siku moja. “Mh! Kama ni hivyo tuondoke wote, kwani utakaa siku ngapi?” “Tunakwenda kukaa siku mbili tu mke wangu, hatuwezi kuondoka wote kwa sababu mtoto wetu bado mdogo, isitoshe tunakwenda kikazi,” Harrison alijaribu kumuweka sawa mkewe. Angel aliendelea kumng’ang’ania mumewe kwani kwa jinsi alivyokuwa amemzoea, kukaa mbali naye kwa siku mbili aliona ni sawa na mwaka mzima. Hata hivyo, baada ya kumbembeleza sana, Angel alikubali kubaki ingawa alilia sana usiku huo mpaka mumewe akamuonea huruma. Mpaka usingizi unampitia, alikuwa akiendelea kulia akiwa kwenye kifua cha mumewe ambacho alikilowanisha kwa machozi na kamasi. Harrison alimuonea sana huruma lakini hakuwa na cha kufanya zaidi ya kushikilia msimamo wake kwani alikuwa akitaka kuufahamu ukweli juu ya asili ya mkewe. Kwa upande wa Linda, baada ya kuwaza kwa muda mrefu, hatimaye usingizi ulimpitia mpaka asubuhi. Kulipopambazuka tu, yeye ndiye alikuwa wa kwanza kuamka, akaanza kufanya usafi nyumba nzima kisha akaandaa kifungua kinywa. Alipomaliza alienda kumuamsha Angel na kumuomba nguo za mtoto alizozichafua ili akazifue. “Huyu msichana ana bidii sana na kazi, akiendelea hivi atatufaa sana,” alisema Harrison baada ya mkewe kumaliza kumtolea nguo za kufua. Mkewe alimuunga mkono ingawa bado hakuwa na furaha kutokana na mumewe kutaka kusafiri.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Walipoamka, kazi zote za ndani zilikuwa tayari zimeshafanywa na Linda ambaye wao walikuwa wakimjua kwa jina la Abigail, Harrison akaenda kuoga na kuwahi kuondoka kwa ajili ya kwenda kujiandaa na safari ambayo ilipangwa iwe siku inayofuatia. Baada ya kumaliza kujiandaa, Harrison alimuaga mkewe kisha akaenda kumuaga Abigail. Wakati wakiagana, Harrison alipatwa na mshtuko wa ajabu baada ya kusikia sauti ya msichana huyo wa kazi kwani aliifananisha na sauti ya mtu aliyekuwa akimfahamu kwa kina ingawa kwa haraka hakuweza kumkumbuka. Licha ya kujitambulisha kuwa yeye ni raia wa nchi hiyo ya Canada, lafudhi ya matamshi yake ilikuwa ikifanana kwa kiasi kikubwa na Wamarekani, jambo lililomfanya Harrison abaki na viulizo vingi kichwani. “Mbona umeshtuka? Kuna nini?” mkewe aliyekuwa nyuma yake, alimuuliza baada ya kumuona mumewe akishtuka baada ya kuisikia sauti ya mfanyakazi wao wa ndani. Linda naye baada ya kugundua kuwa alifanya kosa la kushindwa kuibana sauti yake, alijifanya kuendelea na kazi nyingine, akawaacha Harrison na mkewe wakiendelea kuhojiana. Hata hivyo, Harrison alijivunga na kuonesha kuwa kila kitu kilikuwa sawa. Akaondoka na kumuacha mkewe akiwa na maswali mengi kichwani mwake. Baada ya kufika kazini, Harrison aliomba ruhusa kuwa ana matatizo ya kifamilia hivyo atasafiri kuelekea Geneva kwa siku mbili. Kutokana na uchapakazi wake, alipewa ruhusa kirahisi. Mawazo juu ya sauti aliyoisikia kutoka kwa hausigeli wao ilizidi kumsumbua kichwani. Akatoka na kwenda benki kutoa kiwango cha fedha ambacho kitamtosha kwenye safari yake hiyo. Pia akatafuta hati mpya ya kusafiria akitumia jina na sura mpya. Kutokana na kutumia ushawishi wa fedha, kila kitu kilienda kama alivyopanga, baada ya muda mfupi tayari akawa na hati ya kusafiria iliyomtambulisha kuwa raia wa Canada. Hakutaka kupoteza muda, siku hiyohiyo alianza kutafuta hati ya kusafiria, akaenda mpaka kwenye Ubalozi wa Uswisi. Akafanikiwa kupata viza maalum iitwayo Schengen ambayo ingemuwezesha kusafiri kwa zaidi ya nchi 26 za Jumuiya ya Ulaya na nyinginezo. Alipokamilisha kila kitu, alikwenda mpaka Uwanja wa Ndege wa Abbotsford ambapo alikata tiketi ya kuelekea Geneva siku inayofuata. Akalipia kabisa kisha akaondoka na kurudi nyumbani kwake kuendelea na maandalizi ya safari hiyo. Alipofika alipokelewa na mkewe ambaye bado alionesha kuwa na majonzi kwani hakuzoea kukaa mbali na mumewe kipenzi. Hata hivyo, alijitahidi kumfariji mumewe mpaka akamuelewa. Siku hiyo hawakulala mapema, usiku walikuwa wakizungumza mambo mbalimbali kuhusu mipango yao ya maisha ya baadaye na mtoto wao. Baadaye wakapitiwa na usingizi mpaka kesho yake, kulipokucha tu, Angel alimuandaa mumewe kwa ajili ya safari na alipokuwa tayari, alimsindikiza mpaka uwanja wa ndege. Wakakumbatiana kimahaba kwa muda wa zaidi ya dakika mbili huku Angel akitokwa na machozi, baadaye wakaagana, Harrison akiwa na mkoba wake mdogo, akaanza kuelekea ndani ya uwanja huo ambapo Angel alimsindikiza kwa macho mpaka alipopotea kwenye upeo wa macho yake. Akaondoka na kurudi nyumbani kwake. *** Baada ya kuwa na uhakika kuwa Harrison amesafiri, Linda aliona hiyo ndiyo nafasi yake pekee ya kutimiza kile alichokuwa amekipanga. Akajiapiza kuwa Harrison atakaporejea, atawakuta mkewe na mwanaye wakiwa maiti. Roho ya ukatili ilishamjaa na alijiapiza kufanya kila linalowezekana kumrudisha Harrison kwenye mikono yake. Baada ya Angel kuondoka kuelekea uwanja wa ndege kumsindikiza mumewe, huku nyuma Linda alijiandaa na kuondoka haraka kuelekea kwenye duka la madawa na kemikali lililokuwa jirani. Alipofika kwenye duka lililokuwa jirani, aliomba kuuziwa sumu hatari ya Cyanide. Muuzaji akamwambia kuwa sumu hiyo huwa haiuzwi kiholela mpaka awe na maelekezo maalum yaliyoidhinishwa juu ya matumizi yake. Alipoona anaanza kumuwekea vipingamizi, Linda aliamua kutumia ushawishi wa fedha kama kawaida yake, akatoa noti kadhaa za dola za Kimarekani na kumpa nje ya malipo ya ununuzi wa sumu hiyo. Muuzaji alipoona fedha hizo, alilegeza msimamo wake na kuamua kumuuzia. Alipopewa tu, alirudi haraka akiwa na kopo hilo la sumu, akaenda kumchukua mtoto ambaye bado alikuwa amelala, akambeba huku mkono mmoja akiwa ameshika kopo lenye sumu, akaanza kukoroga uji huku akijiandaa kuichanganya sumu hiyo kwenye uji wa mtoto. ***
NDOA ya Harrison na Angel, msichana aliyemhangaikia sana kabla ya kumpata na kumuoa, inazidi kushamiri huku upendo, heshima na maelewano vikizidi kuongezeka kila kukicha. Upande wa pili, msichana ambaye Harrison alimkimbia siku ya harusi yao, Linda ameamua kulivalia njuga suala la
kutoweka kwa mpenzi wake huyo na baada ya kusomea upelelezi kwa kipindi kirefu na kufuzu, anaanza kumfuatilia hatua kwa hatua akitaka kujua yuko wapi na anafanya nini.
Baada ya kuhangaika sana, hatimaye anaugundua ukweli na sasa amefika hadi mahali Harrison alikokimbilia na msichana wake, malkia wa masokwe. Moyo wake unamuuma sana kugundua kuwa kumbe Harrison alimkimbia kwa sababu ya malkia wa masokwe na hakufa kama alivyoudanganya ulimwengu.
Wakati akiendelea kuwafuatilia wanandoa hao, anawasikia wakizungumzia suala la kutafuta msichana wa kazi. Anaitumia nafasi hiyo kuingia upya kwenye maisha ya Harrison ambapo anaenda kujibadilisha sura kisha anakuja
kuomba kazi. Anakubaliwa bila wenyewe kugundua kuwa wamemkaribisha mtu hatari mno ndani kwao. Baada ya muda anaanza kuandaa mipango ya kulipa kisasi.
Baada ya Angel kumfikisha mumewe uwanja wa ndege, wakiwa kwenye geti la nje walikumbatiana kimahaba kwa muda wa zaidi ya dakika mbili, huku Angel akitokwa na machozi, baadaye wakaagana, Harrison akiwa na mkoba wake mdogo, akaanza kuelekea ndani ya uwanja huo. Angel alimsindikiza kwa macho mpaka alipopotea kwenye upeo wa macho yake.
Harrison alitembea huku akigeukageuka nyuma mpaka alipozamia ndani ya uwanja wa ndege, akajipanga sehemu ya lango la ndani la kuingilia kisha utaratibu wa ukaguzi kwa abiria ukaanza kama kawaida. Ilipofika zamu yake, alikaguliwa na kila kitu kikaonekana kipo sawa, akaruhusiwa kuingia mpaka mahali ndege ilipokuwa imeegeshwa. Akapanda na kwenda kukaa kwenye siti yake. Bado mawazo mengi yalikuwa yakiutesa mtima wake juu ya asili ya Angel. Japokuwa kwa mara ya kwanza alimkuta kwenye Msitu wa Tongass akiwa analelewa na kundi kubwa la masokwe, aliamini hakuna uwezekano wowote wa sokwe kuzaa binadamu hivyo akawa na matumaini makubwa kuwa lazima ataufahamu ukweli wake.
Penzi la dhati alilokuwa nalo kwa Angel ndiyo lililomsukuma kufanya kila linalowezekana ili aijue asili, ndugu na kila kitu kilichokuwa kinamhusu mwanamke huyo ambaye alikuwa akimpenda kuliko kitu kingine chochote kwenye maisha yake.
Aliamini mtu pekee anayeweza kumfumbulia fumbo kubwa lililokuwa limejificha kwenye maisha ya mkewe, ni Abdulkarim Charwe ambaye jina lake alilikuta kwenye kidani cha mkewe ambacho kwa maelezo yake, tangu anapata akili alijikuta tayari anacho mwilini mwake. Aliamini lazima Abdulkarim Charwe anafahamu ukweli wa maisha ya mkewe na hiyo ndiyo sababu kubwa iliyomfanya apige moyo konde na kusafiri kutoka Abbotsford, Canada yalikokuwa makazi yake na familia yake mpaka Geneva, Uswisi.
Kilichomsukuma kuamini kuwa Abdulkarim anaishi Geneva ni baada ya kulitafuta jina lake kwenye mtandao wa intaneti na kugundua kuwa mtu huyo alikuwa ni daktari katika Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) jijini Geneva, Uswisi.
Wakati mawazo mengi yakizidi kupita ndani ya kichwa chake, alisikia sauti kutoka kwenye vipaza sauti vilivyokuwa ndani ya ndege hiyo ikiwataarifu abiria wote kufunga mikanda kwani ndege ilikuwa ikijiandaa kuruka. Yeye pamoja na abiria wengine wote walitii agizo hilo, ndege ikaanza kujongea taratibu kuelekea kwenye njia za kurukia (runways). Ikaanza kuongeza kasi huku muungurumo wa injini nao ukizidi kuwa mkubwa, ikaondoka na kuongeza kasi kwa kadiri ilivyokuwa inasonga mbele mpaka ilipoanza kuinuka upande wa mbele. Akajua tayari ndege ilikuwa angani, akawa anamuomba Mungu wake amuwezeshe kukamilisha kazi kubwa iliyokuwa mbele yake. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Baada ya kusafiri angani kwa saa nyingi, hatimaye ndege ya Swiss Air aliyokuwa ameipanda Harrison ikawasili jijini Geneva, Uswisi. Baada ya kutua uwanjani, Harrison na abiria wengine waliteremka na kufuata taratibu za kawaida kwenye viwanja vya ndege vya kimataifa. Baada ya kukamilisha kila kitu, alitoka na kukodi teksi, akamuelewesha dereva kumpeleka kwenye ofisi za Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani. Safari ikaanza huku Harrison akijaribu kupangilia vizuri maelezo yake ili akifika kwenye ofisi hizo asibabaike. Baada ya muda, teksi iliwasili kwenye jengo refu la kisasa lililokuwa na mandhari ya kuvutia, likiwa limepambwa kwa bustani nzuri za maua pande zote. Dereva teksi akaliingiza gari mpaka kwenye maegesho na kumwambia Harrison kuwa wamefika, akamlipa fedha zake kisha akateremka na kuanza kutembea kwa hofu kuelekea kwenye lango la kuingilia kwenye ofisi hizo. Alipofika getini, alisimamishwa na walinzi na
kukaguliwa kisha akaulizwa shida yake. Baada ya kujieleza, Harrison alielekezwa aende mpaka sehemu ya mapokezi. Alipofika hapo, pia alijitambulisha na kueleza kilichompeleka, akaelekezwa kwenda kwenye ofisi ya Inquiries Department ambayo ndiyo ilikuwa ikihusika na maulizo ya taarifa mbalimbali za watumishi wa shirika hilo. “Umesema anaitwa nani?” “Abdulkarim Charwe,” Harrison alijibu kwa kusitasita wakati akizungumza na mwanamke wa makamo aliyekuwa amekaa nyuma ya
kompyuta ya kisasa. Baada ya kutaja jina hilo, mwanamke huyo wa Kizungu aliandika kitu kwenye kompyuta yake kisha akasubiri kwa sekunde chache. Baada ya kusoma maelezo fulani, aliteremsha miwani yake na kumtazama Harrison kwa kumkazia macho. “Umesema ni nani yako?” “Ni ndugu yangu,” alijibu Harrison huku akionesha kutokuwa na uhakika na majibu yake. *** Baada ya Angel kumsindikiza mumewe mpaka Uwanja wa Ndege, awali alitaka kurudi mpaka nyumbani lakini akiwa njiani alikumbuka
kitu. Alikumbuka kuwa walikubaliana na mumewe kuwa aende kazini kwake na kuzungumza na mabosi wake kuhusu kurejea kazini kabla hata ya kumalizika kwa likizo yake ya uzazi. Aliamini baada ya kumpata msichana wa kazi, Abigail (Linda) sasa atakuwa na uwezo wa kuendelea na kazi bila matatizo.
Alipitia kazini kwake na kuwapa taarifa viongozi wake ambao kwanza walimpongeza kwa kujifungua salama mtoto wa kiume, Harvey Junior lakini pia walimpongeza kwa moyo wa kujituma na kupenda kazi aliokuwa nao kiasi cha kuamua kurejea kazini kabla ya likizo yake ya uzazi kumalizika. Walimkubalia na kuahidi kumuongeza nusu ya mshahara wake kwa moyo wa kujituma aliouonesha.
Baada ya kukamilisha taratibu zote muhimu, alikodi teksi na kurudi mpaka nyumbani kwake. Kabla hata hajaingia ndani, alipokelewa na sauti ya kilio cha mwanaye aliyekuwa akilia kwa nguvu. Hakuna kitu alichokuwa hakipendi kama kumsikia mwanaye huyo akilia bila sababu ya msingi, tena bila kubembelezwa. Akamlipa dereva fedha zake na kuteremka. Akawa anatembea kwa kasi kuelekea ndani. Alipofika mlangoni, alijaribu kuusukuma mlango lakini ulikuwa umefungwa kwa ndani. Akagonga kwa nguvu lakini hakuitikiwa, sauti ya mwanaye akilia ikawa inazidi kuongezeka, hali iliyomuumiza moyo wake kupita kiasi. Akawa anaugonga mlango kwa nguvu huku akiliita jina la hausigeli wake. Alipoona kimya, alitoa simu yake ya kiganjani na kuanza kupiga namba ya mfanyakazi huyo, simu ikawa inaita bila kupokelewa.
Alipoona mtoto anazidi kulia kwa sauti kubwa, alianza kutafuta namna ya kuuvunja mlango, akawa anautingisha kwa nguvu lakini kutokana na uimara wa mlango, hakuweza kufanya chochote. Akajikuta na yeye akianza kutokwa na machozi, akaanza kuomba msaada kwa majirani kumsaidia kuvunja mlango kwani hakujua nini kilichomtokea mtoto wake mpaka afikie hatua ya kulia kwa nguvu kiasi kile. Baada ya kupiga kelele za kuomba msaada, majirani kadhaa walikusanyika na kuanza kumuuliza kulikoni. Wakawa wanamtuliza kuwa asiwe na wasiwasi kwani ni kawaida ya watoto kulia hasa wanapokuwa mbali na mama zao. Licha ya kila mtu kujaribu kumtuliza, bado moyo wake haukutulia, akawaomba majirani wamsaidie kuvunja mlango. ***
WAKATI furaha ya Harrison na mkewe Angel ya kupata mtoto kwenye ndoa yao ikiwa inaendelea, matatizo makubwa yanaanza kuinyemelea familia hiyo. Msichana ambaye Harrison alimkimbia siku ya harusi yao, Linda ameamua kulivalia njuga suala la kutoweka kwa mpenzi wake huyo. Baada ya kusomea upelelezi kwa kipindi kirefu na kufuzu, anaanza kumfuatilia hatua kwa hatua akitaka kujua yuko wapi na anafanya nini. Hatimaye anaugundua ukweli kuwa mwanaume huyo aliyekuwa anampenda kuliko kitu chochote, hakufa bali alimkimbia na kwenda kumuoa malkia wa masokwe ambaye sasa anaishi naye kama mkewe, akiwa amebadilisha sura na jina. Moyo wake unamuuma sana na anajiapiza kuhakikisha analipa kisasi kwa kuwapoteza Angel na mwanaye. Anatumia mbinu kali na kufanikiwa kuingia kwenye familia hiyo akiwa kama hausigeli. Harrison anasafiri kwenda Uswisi kuwafuatilia ndugu wa mkewe bila kumwambia ukweli. Akiwa safarini, huku nyuma Linda anataka kuitumia nafasi hiyo kutimiza lengo lake.
Baada ya Harrison kuwasili kwenye Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO), Geneva, Uswisi alijitambulisha mapokezi na kueleza shida yake. Akaelekezwa aende kwenye Idara ya Maulizo (Inquiries Department) ambayo ndiyo ilikuwa ikihusika na maulizo ya taarifa mbalimbali za watumishi wa shirika hilo. Baada ya kufika kwenye ofisi hiyo, Harrison alijitambulisha tena na kueleza shida yake, mwanamke wa makamo, Mzungu aliyekuwa amekaa nyuma ya kompyuta ya kisasa akajaribu kupekua kompyuta yake na baada ya muda akamgeukia Harrison na kumuuliza uhusiano uliokuwepo kati yake na mtu aliyekuwa anamuulizia. Harrison alijibu kuwa ni ndugu yake, yule mwanamke akashusha pumzi ndefu na kujiweka vizuri kwenye kiti chake. Akaanza kumueleza kuwa ni kweli kwamba Dk. Abdulkarim Charwe amewahi kufanya kazi kwenye ofisi hizo lakini baadaye walilazimika kumsafirisha na kumrudisha kwao Tanzania kutokana na matatizo ya kiafya yaliyokuwa yanamsumbua. “Baada ya mkewe na mwanaye mdogo kupata ajali ya ndege na kufa, Charwe alishindwa kuukubali ukweli, muda wote akawa analia mwenyewe kwa huzuni, hali iliyopunguza ufanisi wake kazini,” alisema mwanamke huyo wa Kizungu. Akaendelea kueleza kuwa kutokana na uchungu wa kuipoteza familia yake, Dk. Charwe alianza ulevi wa kupindukia akiamini kuwa anapunguza mawazo lakini haikumsaidia kitu. Baadaye akaanza kuumwa maradhi ya hapa na pale na baada ya kufanyiwa utafiti wa kina, ikabainika kuwa anasumbuliwa na msongo mkali wa mawazo ambao pia ulimsababishia huzuni kali, ‘mental depression’. “Tulijitahidi kumsaidia kwa kadiri ya uwezo wetu lakini bado alishindwa kuhimili maumivu ya kuipoteza familia yake. Siku moja akiwa chooni, alianguka na kupoteza fahamu. Akakimbizwa hospitali na kutibiwa na madaktari wenye uwezo mkubwa, aliporejewa na fahamu, alipatwa na ‘stroke’, akaparalaizi mwili mzima,” alisema mwanamke huyo wa Kizungu huku akilengwalengwa na machozi. Taarifa ile ilikuwa mbaya kwa Harrison kwani alijikuta akigonga mwamba. Hata hivyo, alipata mwanga fulani katika maelezo hayo. Akaanza kumdadisi mambo mbalimbali mwanamke huyo. Maelezo yote aliyokuwa anapewa alikuwa akiyaandika kwenye kitabu chake maalum. Akatajiwa mpaka kampuni ambayo ndege yake ndiyo waliyosafiria mke wa Dk. Charwe na mwanaye kabla ya kupata ajali na kusababisha wafikwe na mauti. Pia alimuuliza kuhusu sehemu aliyorudishwa daktari huyo baada ya kuparalaizi. Akaambiwa kuwa Charwe alikuwa mwenyeji wa Bukoba, Tanzania na huko ndiko alikorudishwa. Baada ya kuridhishwa na maelezo aliyopewa, Harrison aliaga na kuondoka huku akiendelea kujiuliza maswali mengi ndani ya kichwa chake. Alishaanza kupata picha ya historia ya mkewe. Aliamini endapo ataendelea kulifuatilia suala hilo kwa karibu, siku si nyingi ataugundua ukweli wa historia ya mkewe, jambo alilokuwa analisubiri kwa hamu kubwa. Alirudi mpaka kwenye hoteli aliyokuwa amefikia na kuanza kutafakari namna ya kuendelea na uchunguzi wake. *** Baada ya kufanikiwa kuipata sumu hatari ya Cyanide, Linda ambaye sasa alikuwa akijiita Abigail, alirudi nayo mpaka nyumbani kwa Harrison. Akamchukua mtoto na kuanza kumkorogea uji ambao alipanga kuuchanganya na sumu hiyo. Akiwa anaendelea kukoroga, alikumbuka maelezo ya muuzaji kuwa sumu hiyo ina uwezo wa kuua ndani ya sekunde chache lakini endapo atahitaji sumu nyingine yenye uwezo wa kuua baada ya siku kadhaa, pia ilikuwa ikipatikana. Akili ikamcheza haraka, akaona endapo angemkorogea sumu hiyo mtoto kwenye uji, tafsiri yake ni kwamba angekufa kabla hata mama yake hajarudi. Hata hivyo, malengo yake yalikuwa ni kuwaua wote wawili hivyo akajua endapo atarudi na kumkuta mwanaye amekufa, lazima atachanganyikiwa na kujaza watu nyumbani hapo hivyo kukwamisha mpango wake wa kuwaua wote wawili. Ghafla akapata wazo la kurudi dukani na kwenda kubadilisha sumu ili apewe yenye uwezo wa kuua baada ya siku kadhaa. Baada ya kupata wazo hilo, alienda kumlaza mtoto chumbani kwake, akazima jiko na kuutoa uji jikoni, akatoka mbiombio na kurudi dukani alikouziwa ile sumu. Kwa bahati mbaya kwake, alipofika dukani, muuzaji aliyemuuzia mara ya kwanza alikuwa ametoka kwenda kupata kifungua kinywa na kumuacha msaidizi wake. Linda alipojaribu kumueleza msaidizi wake kile alichokuwa anakitaka akamwambia amsubiri mwenyewe kwani yeye hakuwa na mamlaka ya kumsaidia. Ilimlazimu Linda kukaa na kumsubiri. Hata hivyo, hakurudi haraka kama alivyotegemea. Wakati akiendelea kusubiri, upande wa pili Angel alishamaliza mizunguko yake na kurudi nyumbani. Ndipo alipokutana na hali iliyomtia wasiwasi mkubwa baada ya kusikia mwanaye analia kwa nguvu akiwa ndani. Baada ya kuwakusanya majirani , walisaidiana kuuvunja mlango. Walipofanikiwa tu, Angel ndiyo alikuwa wa kwanza kuingia ndani, akakimbilia mpaka mahali sauti ya mwanaye ilipokuwa inatokea, kwenye chumba cha msichana wao wa kazi. Alipomfikia, alimbeba haraka na kuanza kumuangalia kama yupo salama. Haraka akamtolea ziwa na kuanza kumnyonyesha, mtoto akanyamaza. Majirani waliingia na walipokuta mtoto yupo salama, waliaga na kuanza kuondoka mmojammoja huku wengine wakimcheka Angel kwa jinsi alivyokuwa na presha na mwanaye. “Ni mtoto wake wa kwanza ndiyo maana ana presha kiasi hicho, siyo kosa lake,” mwanamke mmoja alisema na kuungwa mkono na wenzake. Angel hakujali, akawa anaendelea kumnyonyesha mwanaye huku akizunguka kwenye vyumba vyote kukagua usalama. Alijiuliza mahali alipokwenda hausigeli wake, tena bila kuaga na kumuacha mtoto akilia peke yake lakini hakupata majibu. Akapanga kuwa akirudi ampe onyo kali na endapo atarudia tena mchezo huo, atajua namna ya kumuadabisha. Kule dukani, baada ya kusubiri sana, hatimaye muuzaji alirejea na kumkuta Linda akimsubiri. Alipomueleza alichokuwa anakitaka, alimtaka kuongeza fedha kwani sumu aliyokuwa anaitaka yeye ilikuwa ikiuzwa bei kubwa kuliko ile ya awali. Kwa kuwa Linda alidhamiria kweli, alitoa fedha na kuongeza. Akapewa sumu hiyo ambayo tofauti na ile ya awali, ilikuwa kwenye mfumo wa vidonge vidogo vyenye rangi ya dhahabu. Baada ya kupewa, alitoka haraka na kuanza kukimbia kurudi nyumbani kwani alikuwa na wasiwasi kuwa mtoto atakuwa analia sana. Alipokaribia, alishtuka mno kuona mlango umefunguliwa wakati yeye aliufunga na funguo alikuwa nazo mkononi. Akiwa bado ameduwaa, alishtuka kumuona Angel akitoka huku akiwa amembeba mwanaye aliyekuwa anaendelea kunyonya. “Ulikuwa wapi?” Angel aliuliza kwa ukali, Abigail (Linda) akawa anajiumauma na kukosa majibu. ***
HARRISON ameiacha familia yake na kusafiri kwenda jijini Geneva, Uswisi kufanya utafiti wa kina kuhusu asili ya mkewe, Angel. Jina la Charlotte Abdulkarim Charwe alilolikuta kwenye kidani cha mkewe ndiyo lililompa mwanga wa wapi pa kuanzia. Baada ya kutafuta mtandaoni, anagundua kuwa Abdulkarim Charwe ni daktari anayefanya
kazi kwenye Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) jijini Geneva, Uswisi. Baada ya kuondoka, huku nyuma familia yake inaingia kwenye msukosuko mkubwa. Linda ambaye alifanya upasuaji wa kubad
ilisha sura (plastic surgery), anafanikiwa kuingia kwenye familia hiyo akijifanya ni hausigeli. Baada ya kuingia kwenye familia hiyo, Linda anaanza kufanya mipango ya kumuua Angel na mwanaye kwani
aliwaona kama kikwazo kwenye maisha yake, akawa anaamini kuwa akiwaondoa duniani atapata fursa nzuri ya kuwa na mwanaume wa maisha yake, Harrison. Anataka kuwaua wote wawili kwa sumu.
Baada ya kutoka dukani, Abigail (Linda) alishtuka mno kuona mlango umefunguliwa wakati yeye aliufunga na funguo alikuwa nazo mkononi. Akiwa bado ameduwaa, alishtuka kumuona Angel akitoka huku akiwa amembeba mwanaye aliyekuwa anaendelea kunyonya. “Ulikuwa wapi?” Angel aliuliza kwa ukali, Abigail akawa anajiumauma na kukosa majibu. “Nilikuwa nimeenda dukani, najisikia vibaya kwa hiyo niliendaa kununua dawa.” “Unaumwa nini na kwa nini hukunipigia simu kunipa taarifa?” “Samahani bosi, nisamehe sitarudia tena alisema Abigail huku akipiga magoti mbele ya Angel aliyekuwa amefura kwa hasira. Kutokana na roho yake ya upole na huruma, Angel alimsamehe kirahisi, akamwambia siku nyingine akirudia atamfukuza kazi. Abigail alijifanya msikivu, akawa anasikiliza kila kitu na kukiri makosa yake. Aliposamehewa, harakaharaka aliingia mpaka chumbani kwake na kujifungia mlango. Mapigo ya moyo wake yakawa yanamuenda mbio kutokana na hofu aliyokuwa nayo. Alipohakikisha amejifungia na hakuna mtu mwingine anayemuona, alitoa vidonge vya sumu alivyovinunua na kuvificha chini ya godoro, akalala kitandani na kuanza kutafakari nini cha kufanya. “Lazima nikuue Angel! Wewe na mwanao lazima muondoke duniani ili nipate nafasi ya kuishi na mwanaume wa maisha yangu, Harrison! Nampenda sana na nipo tayari kufanya chochote ili nimpate,” Abigail aliwaza akiwa amelala kitandani, akawa anaendelea kupanga mikakati ya namna ya kutekeleza mpango wake. Angel alienda kumtafuta fundi wa kutengeneza mlango, kazi hiyo ilipofanyika akaendelea na shughuli zake za nyumbani huku akiwa amembeba mwanaye. Tayari alishamsamehe Abigail na hakuendelea tena kumfikiria. Muda ukawa unazidi kuyoyoma huku Abigail akiwa bado amejifungia chumbani kwake. “Nikaiweke hii sumu kwenye maji ya kunywa au kwenye vyakula?” Abigail alijiuliza kichwani, akapata wazo la kwenda kuiweka sumu hiyo kwenye mboga zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye jokofu pamoja na kwenye maziwa ya mtoto. Alikuwa na uhakika kuwa vyovyote itakavyokuwa, lazima Angel atapika na kula mboga hiyo na vilevile lazima atampa mwanaye maziwa. Alipopata wazo hilo, harakaharaka aliinuka na kuchukua vidonge viwili vya sumu, akavificha kwenye mfuko wa nguo aliyokuwa ameivaa na kutoka mpaka sebuleni alikomkuta Angel akiendelea na shughuli zake kama kawaida. “Naomba nikusaidie kazi mama.” “We nenda kapumzike tu, nitafanya kila kitu mimi mwenyewe,” Angel alimjibu hausigeli huyo, akaendelea na shughuli zake za kawaida. Abigail hakutaka kurudi chumbani, akakaa kwenye kochi huku akitafuta nafasi ya kufanya alichokuwa amekipanga. Hata hivyo, hakupata nafasi hiyo kwa urahisi kwani Angel hakutoka nje hata mara moja wala kuondoka sebuleni hapo mpaka alipomaliza kuandaa chakula. Alipomaliza, alienda chumbani kwake kumuamsha mtoto wake, Abigail akaona hiyo ndiyo nafasi yake ya kutimiza lengo lake. *** Baada ya Harrison kupata taarifa zote muhimu alizokuwa akizihitaji kuhusu Abdulkarim Charwe, alirudi hotelini na kuanza kutafakari nini cha kufanya. Wazo pekee aliloona linafaa zaidi, ilikuwa ni kwenda mpaka kwenye shirika la ndege ambayo ndiyo mke na mtoto wa Charwe walisafiria kabla ya kupata ajali na kufa. Alihitaji kufahamu vizuri taarifa zao ikiwa ni pamoja na majina yao kamili, eneo ajali ilipotokea na kama kuna taarifa nyingine zozote zinazoweza kumsaidia. Hakutaka kupoteza muda, akafunga safari mpaka kwenye Shirika la Ndege la Lufthansa ambalo aliambiwa kuwa ndiyo lililokuwa linamiliki ndege ya Herpa Lufthansa Premium iliyopata ajali na kusababisha maafa makubwa. Baada ya kufika kwenye ofisi za shirika hilo, Harrison alijitambulisha na kueleza shida yake. Bila hiyana, alielekezwa mpaka kwa meneja wa shirika hilo aliyempokea kwa ukarimu na kumueleza kila kitu kuhusiana na ajali hiyo ambayo bado ilikuwa kwenye vichwa vya wengi kutokana na maafa iliyoyasababisha. Meneja huyo alianza kumueleza upya, akamfafanulia kuwa ndege iliyopata ajali, Herpa Lufthansa Premium ilipoteza uelekeo ikiwa angani baada ya kuzidiwa na ukungu ikiwa safarini kuelekea Geneva, Uswisi. “Kwani ajali yenyewe ilitokea wapi?” “Ilitokea kwenye mpaka kati ya Marekani na Canada, kwenye msitu mkubwa wa Tongass,” alijibu meneja huyo, kauli iliyomshtua mno Harrison. “Kijana mbona umeshtuka sana? Kuna tatizo?” “Ha… hapana,” alijibu Harrison kwa kubabaika, mshangao alioupata haukujificha. Akaomba kupewa orodha ya wasafiri waliokuwa ndani ya ndege siku hiyo. Meneja huyo akatafuta kwenye kompyuta kisha ‘aka-print’ na kumpa karatasi lenye majina ya wasafiri wote Harrison. Wakati anapitia, alikutana na majina mawili ya watu waliokuwa wamekaa siti moja siku hiyo. Macho yake yakaganda hapo, akayatazama majina hayo huku akiwa amekodoa macho, kijasho chembamba kikimtoka. “Anganile Charwe, Charlotte Charwe,” Harrison aliyataja majina hayo kwa sauti ya juu, meneja akamfafanulia kuwa hao walikuwa ni mwanamke na mwanaye mdogo aliyekuwa na umri usiozidi miaka mitatu. Akamfafanulia kuwa wote walikufa kwenye ajali hiyo. Kengele ililia ndani ya kichwa cha Harrison, akajaribu kuunganisha matukio. Kidani alichokikuta kwa mkewe kilikuwa na jina lililosomeka Charlotte Abdulkarim Charwe, jina ambalo ndiyo aliloliona katika orodha ya wasafiri waliokuwa ndani ya ndege siku hiyo. Pia alipotafakari kuwa kwa kipindi hicho Charlotte alikuwa na miaka isiyozidi mitatu, alipatwa na hisia kuwa huenda ndiyo mkewe. “Naweza kupata picha za hawa watu wawili?” “Picha zao zipo lakini hazina ubora kwani zilichukuliwa kutoka kwenye nakala ya hati zao za kusafiria.” “Naomba nizione hivyohivyo,” alisema Harrison akiwa na shauku kubwa ya kuhakikisha kama anachohisi ni cha kweli. Baada ya kupekuapekua kwenye kompyuta yake kwa dakika kadhaa, meneja huyo alizipata na kumuonesha Harrison. Hakuwa amekosea, alichokihisi ndiyo ulikuwa ukweli. Japokuwa Charlotte alikuwa bado mdogo lakini sura yake haikubadilika sana, Harrison hakuhitaji kuvaa miwani kutambua kuwa Charlotte aliyedhaniwa kufa kwenye ajali ndiyo Angel, mkewe kipenzi. Alishusha pumzi ndefu na baada ya kupata uhakika huo, aliaga na kuondoka huku mawazo mengi yakiendelea kupita ndani ya kichwa chake. Jambo aliloona linafaa kwa wakati huo, ilikuwa ni kumtafuta mzee Abdulkarim Charwe kwa udi na uvumba mpaka ampate na kumuunganisha na mwanaye. Alirudi hotelini na kuanza kujiandaa kwa safari ya kurudi nyumbani huku akiwa na shauku kubwa ya kumweleza mkewe juu ya utafiti wake na alichokigundua. Hakutaka kulala siku hiyo, akakabidhi chumba na kuondoka kuelekea uwanja wa ndege. *** BAADA ya Harrison kuiacha familia yake na kusafiri kwenda jijini Geneva, Uswisi kutafuta ukweli juu ya asili ya mkewe, Angel, huku nyuma tatizo kubwa linakaribia kutokea. Linda, msichana aliyekimbiwa na Harrison siku ya harusi yao, anafanya upasuaji wa kubadilisha sura (plastic surgery) na kuwa na mwonekano wa tofauti kisha anafanikiwa kuingia kwenye familia hiyo akijifanya ni hausigeli. Baada ya kuipata nafasi hiyo, anaanza kuumiza kichwa juu ya namna ya kuisambaratisha familia hiyo. Anaenda kununua sumu hatari ya Cyanide kwa ajili ya kumuua Angel na mwanaye lakini baada ya kufikiria sana, anaamua kubadilisha sumu hiyo. Anapewa vidonge maalum vya sumu nyingine ambavyo baada ya kuingia ndani ya mwili, humuua mhusika taratibu. Anarudi na vidonge hivyo vya sumu na kuanza kumtegea Angel akizubaa amchanganyie kwenye chakula na hatimaye anafanikiwa.
Baada ya Harrison kupata vielelezo na uthibitisho aliokuwa anautaka jijini Geneva, Uswisi alijiambia ndani ya nafsi yake kuwa jambo pekee linalofaa baada ya kuyafahamu yote hayo, ni kutafuta muda wa kutosha na kufunga safari mpaka nchini Tanzania kumtafuta mzee Abdulkarim Charwe. Alijiapiza kuwa atafanya kila liwezekanalo mpaka ampate mzee huyo na kumuunganisha na mwanaye. Harakaharaka alirudi Alirudi hotelini na kuanza kujiandaa kwa safari ya kurudi nyumbani huku akiwa na shauku kubwa ya kumweleza mkewe juu ya utafiti wake na alichokigundua. Hakutaka kulala siku hiyo, akakabidhi chumba na kuondoka kuelekea uwanja wa ndege. “Haloo mke wangu!” “Haloo baba!” “Nipo njiani naenda uwanja wa ndege mama, muda si mrefu nitapanda ndege na kurudi nyumbani.” “Oooh! Usiniambie mume wangu? Yaani kwa jinsi nilivyokukumbuka sitakula wala kufanya chochote mpaka utakaporudi mume wangu,” alisema Angel kwa furaha, mumewe alipokata simu, alimbeba mwanaye na kwenda naye sebuleni. Muda huo, tayari Abigail alikuwa ameshafanya alichokikusudia kwa kuchanganya sumu kwenye chakula alichokuwa amekipika Angel na kwenye uji wa mtoto, akawa anasubiri kwa shauku kuona jinsi maadui zake hao wanavyoianza safari ya kifo. Baada ya kufanya ushetani huo, Abigail alirudi kwenye kiti chake na kutulia kimya utadhani hakuna kilichotokea. Akiwa katika hali hiyo, akamuona Angel akitoka chumbani akiwa na mwanaye, usoni akiwa amejawa na tabasamu pana. “Mbona umefurahi sana mama?” aliuliza kwa sauti ya kutetemeka. “Mume wangu kanipigia simu kasema anaelekea uwanja wa ndege, yaani jinsi nilivyommisi sitafanya chochote mpaka atakaporudi,” alisema Angel huku akishindwa kuificha furaha yake. Kauli hiyo ilimshtua mno Abigail, akajikaza na kuuliza tena. “Kwa hiyo hutakula mpaka arudi? Kwa nini usile hata kidogo? Utakaa na njaa kwa muda wote huo?” “Wala usijali, nitamsubiri tu kwani yeye ni muhimu kuliko hata chakula. Isitoshe kwa usafiri wa ndege hatachukua muda mrefu atakuwa tayari ameshafika.” “Basi njoo nikusaidie kumnywesha mtoto uji wake,” alisema Abigail huku akiinuka na kumsogelea Angel ili ampe mtoto lakini akamkatalia. Akamwambia hata yeye hatamnywesha uji wala kufanya chochote mpaka baba yake atakaporudi. Kauli hiyo ilionekana kumvunja nguvu Abigail, akarudi kukaa kwenye kiti chake huku akionesha kuwa na mawazo mengi kichwani. Angel akawasha runinga na kuanza kuangalia kipindi alichokuwa anakipenda kupitia chaneli maarufu nchini humo ya BET. Akawa anatazama runinga huku shauku ya kumsubiri mumewe ikizidi kuongezeka kwa kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele. Mawazo yalizidi kumtesa Abigail, akawa anajiuliza itakuwaje endapo Harrison akirudi na kutaka kula chakula kile alichokitia sumu pamoja na mkewe? Alijikuta akishindwa kuelewa nini cha kufanya, akainuka na kwenda chumbani kwake kutafakari kwa kina. “Harrison naye akila si atakufa? Sasa ndiyo nitakuwa nimefanya nini?” alijiuliza Abigail huku akizungukazunguka chumbani kwake. Alitamani utokee muujiza Harrison aahirishe safari yake lakini hilo halikuwezekana. Pia alitamani angekuwa bado hajaichanganya sumu hiyo kwenye chakula ili asubiri mpaka atakapopata nafasi nzuri lakini pia haikuwezekana. Akawa anaendelea kuzungukazunguka chumbani kwake kama mtu aliyechanganyikiwa. Bado hakupata jibu la nini cha kufanya. Muda ulizidi kuyoyoma akiwa bado anababaika, mara akamsikia Angel akizungumza na simu. Harakaharaka alitoka mpaka sebuleni kwa lengo la kusikiliza alikuwa anazungumza na nani. Alipogundua kuwa Angel hakuwa anazungumza na mumewe, kidogo hofu ilimshuka, akarudi chumbani kwake kuendelea kupanga nini cha kufanya ili kuepusha hatari kubwa iliyokuwa inataka kumpata Harrison. “Abigail! Abigail!” aliita Angel, msichana huyo akatoka na kwenda kumsikiliza. “Pakua chakula uanze kula kwani muda unaenda na kama nilivyokwambia mimi nitamsubiri mume wangu mpaka arudi,” alisema Angel huku akimuonesha msichana huyo mahali alipokuwa amehifadhi chakula. Abigail alijishauri kama akubali au la, akaona njia pekee ni kujifanya kama anapakua chakula ili kutomtia wasiwasi Angel kisha kwenda kukitelekeza chumbani kwake. Harakaharaka akapakua chakula kidogo pamoja na mboga na kwenda nacho chumbani kwake. Kabla hajafika, Angel akamuuliza swali lililomfanya ababaike. “Umeanza lini tabia ya kwenda kulia chakula chumbani?” “Leo najisikia vibaya ndiyo maana nimeamua kuja kulia huku chumbani kwangu,” alisema Abigail huku akitembea harakaharaka kuelekea chumbani kwake kukwepa kuambiwa kuwa aje kulia sebuleni. Angel alijiuliza maswali kadhaa lakini akaamua kulipuuzia jambo hilo, akawa anaendelea kutazama runinga huku akimsubiri mumewe. Kule chumbani, Abigail hakukigusa chakula kile zaidi ya kukisukumia chini ya kitanda, akawa anaendelea kuzungukazunguka huku akiongea peke yake kama mwendawazimu. Baada ya saa kadhaa, Harrison alimpigia simu mkewe na kumtaarifu kuwa tayari alishawasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Abbotsford, Canada. Akamwambia aende kumpokea uwanja wa ndege kwani alikuwa na mizigo ya zawadi mbalimbali alizomnunulia. Harakaharaka Angel akajiandaa pamoja na kumuandaa mtoto wake. Hakutaka kuondoka peke yake, alimwambia Abigail naye ajiandae ili waondoke wote. Awali Abigail alitaka kukataa kwenda ili Angel atakapoondoka aendelee kutafakari nini cha kufanya lakini Angel alipomwambia kuwa kuna mizigo ya kwenda kubeba, hakuwa na cha kufanya zaidi ya kukubali. Muda mfupi baadaye wakajiandaa na kuondoka kuelekea uwanja wa ndege kwa kutumia teksi ya kukodi. Walipofika, tayari Harrison alikuwa ameshashuka kwenye ndege na kwenda sehemu maalum ya kukaa. Alipowaona mkewe, mwanaye na msichana wa kazi, aliinuka na kwenda kumkumbatia mkewe kimahaba akiwa na mwanaye. Akawamwagia mvua ya mabusu huku kila mmoja akionesha dhahiri jinsi alivyofurahi. Abigail alikuwa amesimama pembeni huku akionesha kuzama kwenye dimbwi la mawazo na hofu kuu. Walipomaliza, Harrison alisalimiana pia na Abigail kisha wakasaidiana kubeba mizigo na kuipeleka kwenye teksi. Safari ya kurudi nyumbani ikaanza huku Harrison na mkewe wakiwa wamekumbatiana kimahaba pamoja na mtoto wao. Walipofika nyumbani kwao, Angel alimuandalia mumewe maji ya kuoga na wakati akiendelea kuoga, yeye akaanza kuandaa chakula na kukiweka mezani. Kwa kuwa mwanaye naye alikuwa bado hajanywa uji wake, akamuandalia na kuweka kila kitu mezani. ***
MCHUMA janga hula na wa kwao! Usemi huu wa wahenga unamhusu kijana Harrison. Siku nyingi zilizopita, Harrison alimtoroka Linda kanisani muda mfupi kabla hawajafungishwa ndoa na kutorokea kusikojulikana huku akiudanganya
ulimwengu kwamba amekufa. Sasa siri yake imegundulika kwamba hakufa bali alimkimbia Linda na msichana huyo anajiandaa kulipa kisasi.
Kwa kutumia mbinu za kijasusi, Linda anamfuatilia Harrison hatua kwa hatua mpaka anafanikiwa kujua kuwa kumbe alibadilisha sura na kuishi na malkia wa masokwe kama mume na mke. Linda anaumia sana kuufahamu ukweli huo na kamwe hakubali kushindwa.
Anajibadilisha sura na kuingia kwenye maisha ya Harrison akijifanya hausigeli. Harrison anaposafiri kwenda Geneva, Uswisi, msichana huyo anayetumia jina bandia la Abigail anaamua kukamilisha azma yake ya kumuua Angel pamoja na mwanaye ambao aliwaona kama kikwazo kwenye maisha yake. Anaenda kununua sumu hatari na kuwachanganyia kwenye chakula.
Baada ya kurudi kutoka safari yake ya jijini Geneva, Uswisi, Harrison alilakiwa na mkewe na mwanaye, Harvey Junior pamoja na msichana wao wa kazi, Abigail. Harrison na mkewe wakasalimiana kwa kukumbatiana kimahaba na kumwagiana mvua ya mabusu kisha safari ya kurudi nyumbani ikaanza.
Walipofika nyumbani, harakaharaka Angel alienda kumuandalia mumewe maji ya kuoga na wakati akiendelea kuoga, alianza kuandaa chakula. Baada ya muda mfupi, kila kitu kilikuwa tayari juu ya meza. Kwa kuwa Harvey Junior naye alikuwa bado hajanywa uji wake, mama yake alimuandalia na kwa pamoja wakawa wanasubiri Harrison amalize kuoga ili waungane mezani.
“Mbona wewe unakaa mbali? Sogea tule pamoja,” Angel alimwambia Abigail aliyekuwa amekaa pembeni kwenye kochi huku akiwa amejishika tama. Abigail alitingisha kichwa tu kuashiria kuwa yeye tayari ameshakula. Muda mfupi baadaye, Harrison alishamaliza kuoga, akaenda kuungana na familia yake mezani.
“Tuombe,” alisema Angel huku akimtaka kila mmoja kufumba macho, akaanza kukiombea chakula kama ilivyokuwa kawaida yake kila siku. Wakati wakiwa wamefumba macho, Abigail alisimama na kusogea mezani, machozi yakimtoka kama chemchemi ya maji. Walipomaliza kusali, wote walipigwa na butwaa kumuona Abigail amesimama pembeni ya meza, huku machozi mengi yakiwa yanamtoka.
“Mungu wangu nisamehe,” alisema Abigail huku akizidi kutokwa na machozi kwa wingi. Nafsi yake ambayo awali ilitawaliwa na ushetani wa kutisha, sasa ilibadilika na kutambua kuwa alichokuwa anakifanya ni dhambi kubwa ambayo kamwe asingeweza kusamehewa na Mungu wake.
“Kwani vipi? Abigail… kuna tatizo?” alisema Harrison huku akiwa amepigwa na butwaa, akasimama na kumsogelea Abigail aliyekuwa akiendelea kulia huku akitamka maneno ya kumuomba radhi Mungu wake.
Wote wakiwa bado wamepigwa na butwaa, walishangaa kumuona Abigail akiinyanyua meza iliyokuwa na vyakula na kuiangusha kwa nguvu, kila kitu kikamwagika chini, kuanzia chakula mpaka uji wa mtoto.
“Nakuchukia Angel, nakuchukia sana, nakuchukia malkia wa masokwe,” alisema Abigail na kumrukia Angel mwilini, akamdondosha chini na kumkaba shingoni kwa nguvu. Kila mmoja alibaki amepigwa na butwaa, hakuna aliyeelewa kilichokuwa kinaendelea.
“Sauti aliyoitoa wakati akitamka maneno hayo na jinsi alivyomtaja Angel kama malkia wa masokwe, viliifanya akili ya Harrison ifunguke haraka na kengele ya hatari ikalia kichwani mwake.
“Amejuaje kuwa mke wangu ni malkia wa masokwe? Halafu mbona sauti yake inafanana na ya mtu ninayemfahamu? Harrison alijiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu, akawa anababaika kujaribu kukumbuka sauti ile aliisikia wapi. Alishtuliwa kwenye dimbwi la mawazo na sauti ya mkewe aliyekuwa anakoroma kwa nguvu baada ya kukabwa kisawasawa na Abigail.
Kwa kasi ya ajabu, alitumia uanaume wake kumvaa Abigail pale chini alipokuwa amemkaba Angel, akamshika mikono yake na kumtoa kwa nguvu, akamsukumia pembeni kisha akamuinamia mkewe na kuanza kumpa pole.
“Nakufa mume wangu, naku..fa,” alisema Angel na kukohoa mfululizo, Harrison akawa anamsaidia kupumua huku akimlegeza nguo alizokuwa amezivaa mwilini. Alipogeuza shingo kumtazama Abigail, mapigo ya moyo wake yalimlipuka baada ya kumuona akiwa ameshika kisu kikali cha kukatia mboga, akiwa amemuelekezea mtoto Harvey Junior aliyekuwa akilia kwa sauti kubwa.
“Noooo! Abigail, nipo chini ya miguu yako, naomba usimdhuru mwanangu,” alisema Harrison kwa sauti ya juu huku akiinua mikono yake kama dalili ya kusalimu amri.
“Kwa nini ulinitenda Harrison? Kwa nini? Ulijua sitakupata siyo? Mwanaume muuaji sana wewe,” alisema Abigail huku akilia kwa kwikwi kama mtu aliyepokea taarifa za msiba. Bado Harrison alikuwa gizani kwani hakumtambua kwa haraka Abigail ni nani na kwa nini anafanya yote yale.
“Kama ulikuwa hunipendi si bora ungeniambia kuliko mateso uliyonisababishia Harrison! Nilikukosea nini mpaka kustahili adhabu kali kiasi hiki? Nilikosea kukupenda? Nilikosea kukukabidhi moyo wangu?” alisema Abigail huku akizidi kulia kwa uchungu, kisu akiwa amekielekeza kwenye shingo ya mtoto wa Harrison, Harvey Junior.
Japokuwa Angel alikuwa kwenye maumivu makali baada ya kukabwa kwa nguvu na msichana huyo, alijikakamua na kusimama, naye akapigwa na butwaa kumuona Abigail amemuelekezea kisu mtoto wake huku akizungumza mambo kama mtu aliyekuwa anamfahamu vizuri Harrison. Mtoto Harvey Junior hakuwa akielewa chochote, akawa anawatazama wote kwa zamuzamu.
Angel naye akaanza kulia kumbembeleza Abigail asimdhuru mwanaye, kutokana na jinsi alivyokuwa anamlilia mwanaye kwa uchungu, Abigail aliingiwa na moyo wa huruma. Kwa kasi ya ajabu akakigeuza kisu na kujielekezea tumboni, akawa anataka kujichoma na kujitoa uhai kwani hakuona tena sababu ya kuendelea kuishi.
“Kwani wewe ni nani? Naomba uniweke wazi kwani mpaka sasa sijakujua bado.” “Unajifanya hunijui? Unajifanya hunijui siyo? Harrison wewe ni muuaji na kamwe sitakusamehe! Nilipanga kuiteketeza familia yako kwa sumu lakini sijui malaika gani amebadili mawazo yangu, najuta kukupenda Harrison,” alisema Abigail kwa kilio cha kwikwi,
akaingiza mkono mmoja mfukoni na kutoa kichupa kidogo kilichokuwa na mafuta huku mkono mmoja akiwa bado amejielekezea kisu tumboni.
Akakifungua kile kichupa na kujimimia mafuta kidogo, akaanza kujipaka usoni kwa kutumia mkono mmoja huku ule mwingine ukiwa umekikamata kisu barabaraba. Baada ya kujipaka mafuta yale, alijibandua ngozi ya bandia usoni kwake na kutoa nywele za bandia alizokuwa anazivaa.
“Haaaa! Lindaaaa, ni wewe ni…sa..m..e..h,” Harrison alishindwa kumalizia alichotaka kukisema, kutokana na mshtuko mkubwa alioupata, alidondoka chini kama mzigo, jambo lililoamsha kilio upya kwa mkewe, Angel. Akamkimbilia mumewe pale chini na kuanza kumtingisha.
Kuona hivyo, Abigail alikitupa kisu na kusogea mpaka pale Harrison alipokuwa amenguka, huku machozi mengi yakiendelea kumtoka. Akamsukuma Angel kwa nguvu kisha akamuinamia Harrison mpaka chini na kumlalia kifuani, akawa anaendelea kulia kwa uchungu huku maneno ya kimapenzi yakimtoka.
Kuepusha shari, Angel aliinuka na kwenda kumchukua mwanaye. Alijua endapo ataleta ujeuri na Abigail kuamua kumdhuru, hakuna mtu yeyote anayeweza kumsaidia kwani Harrison alikuwa amepoteza fahamu. Wakati Abigail akiendelea kulia kwa uchungu pale chini, akiwa amejikunyata kwenye kifua cha Harrison, Angel alikimbia mpaka nje na kwenda kuomba msaada kwa majirani.
Akawa anapiga kelele za kuomba msaada, muda mfupi baadaye, watu wakajazana nje ya nyumba ya Harrison. Wanaume wakajitosa na kuingia hadi ndani, wakatumia nguvu kumtoa Abigail kwenye kifua cha Harrison na kumkimbiza kwenye hospitali iliyokuwa jirani huku wengine wakimdhibiti msichana huyo asije akaleta madhara makubwa. Bado hakuna aliyekuwa na maelezo kamili ya kilichotokea. ***
HAKUNA marefu yasiyo na ncha. Siri aliyoificha Harrison siku nyingi zilizopita na kuudanganya ulimwengu kuwa amekufa kwenye ajali, hatimaye inafichuka baada ya Linda kuingia kazini kuhakikisha anaufahamu ukweli.
Linda anajisikia vibaya sana kugundua kuwa kumbe Harrison alimkimbia siku ya harusi yao ili apate muda wa kuishi na malkia wa masokwe. Hali hiyo inamfanya awe na hasira na kuwa tayari kufanya lolote kulipiza kisasi.
Bila ya Harrison wala Angel kujua kuwa kumbe Abigail alikuwa amejibadilisha sura, wanampokea nyumbani kwao akiwa kama hausigeli. Msichana huyo anaanza kupanga kufanya ukatili mkubwa wa kuwaangamiza Angel na mwanaye ili apate muda wa kulifaidi penzi la Harrison.
Hata hivyo, mpango wa kuwaua kwa sumu Angel na mwanaye unaingia dosari baada ya Harrison naye kutaka kula chakula kilichowekwa sumu, jambo ambalo Linda hakuwa tayari kuona linatokea. Anaamua kukimwaga chakula hicho na kusababisha kizaazaa kikubwa na baadaye, anaivua sura yake ya bandia na kubaki na sura yake halisi. Harrison anazimia baada ya kugundua kumbe ni Linda.
Kuepusha shari, Angel aliinuka na kwenda kumchukua mwanaye. Alijua endapo ataleta ujeuri na Abigail kuamua kumdhuru, hakuna mtu yeyote anayeweza kumsaidia kwani Harrison alikuwa amepoteza fahamu. Wakati Abigail akiendelea kulia kwa uchungu pale chini, akiwa amejikunyata kwenye kifua cha Harrison, Angel alikimbia mpaka nje na kwenda kuomba msaada kwa majirani. Akawa anapiga kelele za kuomba msaada, muda mfupi baadaye, watu wakajazana nje ya nyumba ya Harrison. Wanaume wakajitosa na kuingia hadi ndani, wakatumia nguvu kumtoa Abigail kwenye kifua cha Harrison na kumkimbiza kwenye hospitali iliyokuwa jirani huku wengine wakimdhibiti msichana huyo asije akaleta madhara makubwa. Bado hakuna aliyekuwa na maelezo kamili ya kilichotokea. Harrison alifikishwa hospitalini na kupokelewa na manesi wachangamfu, akapakizwa juu ya kitanda chenye magurudumu na kukimbizwa wodini. Muda mfupi baadaye, alianza kupewa huduma ya kwanza, akatundikiwa dripu na kupewa dawa, baada ya muda mrefu kupita, akapiga chafya na kufumbua macho. Akawa anashangaa jinsi dripu ilivyokuwa ikitiririka kwenye mishipa yake ya damu. Akawa anajiuliza pale ni wapi na amefikaje. Nesi aliyekuwa anaendelea kumhudumia, akamwambia kuwa hapo ni hospitalini na amefikishwa baada ya kuanguka na kupoteza fahamu akiwa nyumbani kwake. Dakika chache baadaye, Harrison akiwa anaendelea kutafakari kilichomtokea, mlango wa wodi aliyokuwa amelazwa ulifunguliwa, akamuona mkewe na mwanaye mdogo wakiingia huku Angel akionesha kuchanganyikiwa mno. “Jamani mume wangu, pole baba,” alisema Angel huku akibubujikwa na machozi, akamuinamia mumewe pale kitandani na kumbusu shavuni huku akiendelea kutokwa na machozi. Harrison alimueleza kuwa ana ahueni kubwa, Angel akakaa pembeni ya kitanda chake huku akiwa amembeba mwanaye, huku akiwa na shauku kubwa ya kufahamu kilichokuwa kinaendelea. “Kwani kuna nini kinachoendelea mume wangu, mbona mi sielewi chochote?” alihoji Angel huku akimshika mumewe kwa upole kichwani. Harrison alishusha pumzi ndefu na kumtazama mkewe usoni, akashindwa cha kumjibu zaidi ya kumwambia kuwa anampenda sana. “Najua unanipenda sana mume wangu lakini hebu nitoe wasiwasi.” “Abigail yupo wapi?” “Tumeenda kumhifadhi kwenye kituo cha polisi cha jirani kule nyumbani.” “Ooh! Mmefanya vizuri, polisi walifika nyumbani?” “Ndiyo, pia wamechukua na sampuli za vyakula kwani ilibidi niwaelezee kisa kizima.” “Sawa, umefanya vizuri mke wangu, nikitoka hospitali nitakueleza kila kitu,” alisema Harrison huku akijinyoosha na kulala vizuri. Nesi alimwambia Angel kuwa mgonjwa anahitaji muda zaidi wa kupumzika. Ikabidi atoke na kwenda kukaa nje ya wodi huku akijiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu. Alimtafakari sana Abigail na tukio lililotokea, alijiuliza maswali mengi sana mpaka akaanza kuhisi kichwa chake kinachemka. Alishangaa zaidi baada ya kugundua kuwa kumbe kwa siku zote hizo, Abigail alikuwa amevaa sura ya bandia. “Atakuwa anataka nini? Inaonekana kuna siri kubwa imejificha hapa! Lazima Harrison aniambie ukweli,” aliwaza Angel huku akaikaa vizuri kwenye kiti, nje ya wodi aliyokuwa amelazwa mumewe. Alikaa hapohapo mpaka nesi alipokuja kumwambia kuwa aingie wodini kwani tayari mgonjwa ameshapumzika vya kutosha. Baada ya kuingia wodini, Angel alianza tena kumdadisi mumewe juu ya kilichotokea. Hata hivyo, Harrison alimsisitiza kuwa asiwe na haraka ya kujua kwani atamueleza kila kitu watakapotoka hospitali. “Nesi amesema baada ya saa chache nitaruhusiwa, usiwe na wasiwasi mke wangu, nitakueleza kila kitu,” alisema Harrison, mkewe ikabidi atulie, wakawa wanazungumza mambo mengine. Baada ya muda, kama nesi alivyomwambia Harrison, aliruhusiwa kutoka hospitalini, mkewe akamsaidia kutembea mpaka nje walikoingia kwenye gari na safari ya kurudi nyumbani ikaanza. Walipofika nyumbani, Harrison alimuomba mkewe wakafanye taratibu za kumtoa polisi Abigail, wazo ambalo Angel hakulikubali kirahisi. Akawa anasisitiza kuwa msichana huyo ni hatari sana kwenye maisha yao hivyo hatakiwi kuwasogelea tena. “Hapana mke wangu, nikubalie kisha utagundua kwa nini nimekwambia hivyo,” alisema Harrison lakini mkewe bado akawa anashikilia msimamo wake, akamwambia akitaka akubaliane naye, amueleze kila kitu kwanza kisha ataamua kama wakamtoe au la! Kwa jinsi walivyokuwa wanaishi vizuri, kwa amani na upendo kwa siku zote tangu walipofahamiana, Harrison alikubali kumueleza ukweli wa kila kitu. Akaanza kumsimulia kuanzia jinsi walivyokutana na msichana aitwaye Linda ambaye ndiyo huyo aliyekuwa akijiita Abigail. Akamueleza kila kitu kilivyokuwa mpaka siku aliyomkimbia kanisani. “Sasa kwa nini ulimkimbia mume wangu? Kumbe ndiyo maana ana hasira kiasi hiki.” “Nisamehe mke wangu na naomba Mungu naye anisamehe kwa hili lakini ukweli ni kwamba wewe ndiyo ulisababisha nimkimbie Linda.” “Mimi? Kwa nini?” alihoji Angel huku akiwa amepigwa na mshangao. Harrison akashusha pumzi ndefu na kumsogelea mkewe, akamueleza kuwa hakuwahi kumpenda Linda hata siku moja ila siku aliyomuona yeye (Angel) kwenye Msitu wa Tongass, alijihisi hali ya tofauti na kujikuta akimpenda kuliko maelezo. “Upendo wangu wa dhati kwako ndiyo uliosababisha nimtoroke Linda siku ya harusi yetu! Naomba Mungu anisamehe sana,” alisema Harrison huku akianza kulengwalengwa na machozi, mkewe akaenda kumkumbatia na kuanza kumbembeleza. Akamuuliza jinsi alivyotoroka siku ya ndoa yake na Linda, Harrison akaanza kumuelezea kila kitu. Hakuacha kitu, alieleza jinsi alivyoshirikiana na rafiki yake wa siku nyingi kutengeneza ajali feki ambayo iliwafanya watu wote waamini kama Harrison amekufa kwenye ajali. Alieleza kila kitu, Angel akajikuta akitokwa na machozi kwani hakuwahi kujua kuwa Harrison alilihangaikia penzi lake kiasi hicho. Wakawa wanabembelezana huku wakijadiliana nini cha kufanya. Kwa pamoja walikubaliana kwenda kumtoa Linda kituo cha polisi na kurudi naye nyumbani hapo ili kila kitu kiwekwe hadharani. “Niahidi kuwa utaendelea kuwa mume wangu na hutaonesha udhaifu mbele ya Linda,” alisema Angel huku akionesha kuwa na wasiwasi kwani kwa jinsi alivyomsimulia, ilionesha kuwa Linda alikuwa akimpenda sana Harrison kiasi cha kuwa tayari kufanya lolote kwa ajili yake. ***
MBIO za sakafuni huishia ukingoni! Hatimaye siri aliyoificha Harrison kwa siku nyingi zilizopita na kuudanganya ulimwengu kuwa amekufa kwenye ajali ili apate nafasi ya kulifuatilia penzi la malkia wa masokwe, inafichuka baada ya Linda kuufahamu ukweli. Msichana huyo kutoka familia ya kitajiri anajisikia vibaya sana kugundua kuwa kumbe Harrison hakufa na badala yake alimkimbia siku ya harusi yao kwa sababu ya penzi lake kwa malkia wa masokwe. Anapandwa na hasira kali kiasi cha kuwa tayari kufanya jambo lolote ili kulipiza kisasi. Linda akiwa na mwonekano wa sura na jina tofauti, anaingia kwenye maisha ya Harrison na mkewe akijifanya ni hausigeli bila ya Harrison wala Angel kuujua ukweli. Kutokana na hasira kali, anapanga kuwaua Angel na mwanaye kwa sumu lakini mpango wake unaingia dosari baada ya Harrison naye kutaka kula chakula kilichowekwa sumu. Songombingo kubwa linaibuka.
“Niahidi kuwa utaendelea kuwa mume wangu na hutaonesha udhaifu mbele ya Linda,” alisema Angel huku akionesha kuwa na wasiwasi kwani kwa jinsi alivyomsimulia, ilionesha kuwa Linda alikuwa akimpenda sana Harrison kiasi cha kuwa tayari kufanya lolote kwa ajili yake. “Wala usiwe na wasiwasi mke wangu, mimi ndiyo ninayejua jinsi nilivyolihangaikia penzi lako, sitakuwa tayari kukupoteza,” alisema Harrison kwa sauti ya chini, akamkumbatia mkewe na kumbusu kimahaba. Baada ya hapo, waliondoka pamoja na kuelekea kwenye Kituo cha Polisi cha Langley alikokuwa anashikiliwa Linda. Baada ya kufika kituoni hapo na kueleza shida yao, mkuu wa kituo hicho cha polisi aliwaeleza kuwa majibu kutoka kwa mkemia wa serikali kuhusu sampuli za vyakula vilivyokutwa nyumbani kwa Harrison, zilionesha kuwa na sumu hatari ambayo ingesababisha vifo kwa wote ambao wangekula chakula hicho. “Kisheria ni kosa la jinai kujaribu kuua kwa hiyo mtuhumiwa hataachiwa, lazima aburuzwe mahakamani ili kujibu mashtaka yanayomkabili,” alisema mkuu wa kituo, Bill Curtis, kauli iliyowafanya Harrison na mkewe watazamane. Walishtuka mno kusikia kumbe vyakula walivyokuwa wanataka kula vilikuwa na sumu hatari kiasi hicho. “Ina maana Linda alitaka kutuua? Mwanamke muuaji sana huyu.” “Lakini, kama kweli dhumuni lake lilikuwa ni kutuua, kwa nini aliamua kupindua meza na kumwaga vyakula vyote kabla hata hatujaanza kula?” Harrison na mkewe waliulizana maswali ambayo hakuna aliyekuwa na majibu. Kwa kuwa tayari muda ulikuwa umeenda sana, hawakuwa na la kufanya zaidi ya kuondoka kituoni hapo na kurudi nyumbani kwa ajili ya kutafakari kwa kina kilichotokea. “Mume wangu!” “Abee mke wangu.” “Unajua Linda ametukosea sana lakini kama maandiko matakatifu yanavyosema, inabidi tumsamehe kwa moyo mkunjufu.” “Ni kweli mke wangu, lakini hilo suala limeshafika kwenye mkono wa sheria, unafikiri itakuwa rahisi kiasi hicho?” “Hakuna kisichowezekana mume wangu, mtu pekee anayeweza kumuokoa Linda ni wewe, lazima ukaeleze ukweli wa mlolongo wa matukio yote tangu siku uliyomkimbia kanisani ili kumjengea mazingira kwamba wakati anatenda kosa hilo hakuwa akijielewa,” alisema Angel, akiwa amemkumbatia mumewe na kulala juu ya kifua chake, wakiwa chumbani kwao. Harrison alishangazwa sana na moyo wa huruma aliokuwa nao mkewe. Licha ya ubaya wote aliotaka kuwafanyia, bado Angel hakutaka kabisa kumhukumu Linda na akawa mstari wa mbele kuhakikisha anakuwa huru. Harrison na mkewe walizungumza mambo mengi sana usiku huo, Angel akawa anasisitiza kuwa baada ya kufanikisha kumtoa polisi, inatakiwa wakae pamoja na kuelezana kinagaubaga. “Linda anahitaji kusikia kutoka kwako kama bado unampenda au la! Unafikiri kama ungemweleza tangu mwanzo kuwa humpendi na haupo tayari kuishi naye angehangaika kukufuatilia kiasi hiki? Ukweli ndiyo silaha pekee unayotakiwa kuitumia, nakuamini sana mume wangu,” Angel aliendelea kumwambia mumewe maneno ya busara kwa upole mpaka usingizi ulipowapitia. Kama walivyokubaliana, asubuhi na mapema Harrison alikwenda mpaka kwenye Kituo cha Polisi cha Langley na kuomba kuonana na mkuu wa polisi. Alipoingia ofisini kwake, ilibidi aeleze kinagaubaga juu ya mlolongo wa matukio yaliyotokea mpaka kumsababishia Linda kufanya kitendo hicho. Hata hivyo, katika maelezo yake, Harrison alikwepa sana kutoa maelezo ya jinsi alivyodanganya kifo chake na namna alivyoishi kwa kipindi chote nchini Canada bila kuwa na vibali halali. Baadhi ya maelezo aliyoona yanaweza kumtia hatiani yeye mwenyewe, aliyaruka. Akajieleza kwa muda mrefu huku mkuu wa kituo cha polisi, Bill Curtis akimsikiliza kwa makini. Baada ya kumaliza, mkuu wa kituo aliandika maelezo fulani kwenye jalada la kesi ya Linda kisha akamhakikishia Harrison kuwa ampe muda wa saa chache kushughulikia suala hilo na lazima Linda atatolewa mahabusu kwani maelezo aliyoyatoa Harrison ni mazito sana. Harrison alimshukuru sana na kuondoka, akapitia kwanza kazini kwake kuripoti kwani tangu arejee kutoka Geneva, Uswisi, hakupata muda wa kwenda kutoa taarifa kwamba amesharejea. Baada ya kuripoti kazini, Harrison alirudi nyumbani kwake alikomkuta mkewe anamsubiri kwa shauku. Akamueleza kila kitu kilichoendelea na majibu aliyopewa na mkuu wa kituo cha polisi, Bill Curtis. “Kwa hiyo tutapataje taarifa kuwa ameachiwa? Inabidi akitoka tu, tumchukue na kuja naye mpaka hapa nyumbani,” alisema Angel. “Nimemuachia mkuu wa kituo namba zangu za simu, amesema atanipigia,” Harrison alijibu. Wakawa wanaendelea kucheza na mtoto wao huku wakipanga mipango mingine ya maisha yao, ikiwa ni pamoja na Harrison kurejea nyumbani kwao na kuwaambia watu wote ukweli wa kila kitu kilivyotokea pamoja na kuomba radhi kwa usumbufu, machungu na huzuni alizowasababishia watu wake wa karibu na mashabiki wake. Pia walizungumza kuhusu suala la kusafiri mpaka nchini Tanzania kwenda kumtafuta mzee Abdulkarim Charwe, baba mzazi wa Angel. Wakiwa wanaendelea na mazungumzo hayo, simu ya Harrison iliita na alipotazama kwenye ‘skrini’, alikutana na namba mpya. “Haloow! Nani mwenzangu.” “Bila shaka wewe ni Harrison Harvey.” “Ndiyo, hujakosea.” “Unazungumza na mkuu wa Kituo cha Polisi cha Langley.” “Oooh! Kamanda, habari ya kazi.” “Nzuri, unaombwa kufika hapa kituoni mara moja kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kumtoa Linda, vitu vingi vimeshakamilika,” alisema mkuu huyo wa polisi kisha simu ikakatwa. Bila kupoteza muda, Harrison na mkewe walijiandaa na kutoka wakiwa sambamba na mtoto wao, wakaenda mpaka kituo cha polisi. Harrison akapewa baadhi ya nyaraka azisaini kisha wakaambiwa wasubiri kidogo, baada ya takribani dakika kumi, wote wakashuhudia milango ya chuma ikifunguliwa kisha Linda akatolewa na askari wa kike mpaka kaunta, akaandikisha tena baadhi ya maelezo kisha akaachiwa huru. “Pole sana Linda kwa yaliyokukuta, hizi ni changamoto za maisha,” alisema Angel kwa sauti ya upole lakini katika hali ya kushangaza, Linda hakumjibu chochote, akampita na kutoka hadi nje kabisa ya kituo hicho. Harrison alizungumza na mkewe harakaharaka na kumweleza kuwa yeye abaki kimya, kazi ya kumaliza kila kitu ataifanya mwenyewe. Harrison akamkimbilia Linda na kumuomba amsikilize. Msichana huyo akasimama huku akionesha bado kuwa na kinyongo, akamgeukia Harrison huku akiwa amekunja uso, mwanaume akaanza kumlainisha kwa maneno matamu huku akimsihi arudishe moyo nyuma na kukubali kwenda nao nyumbani ili wakayamalize. ***
Uongo mkubwa alioutumia Harrison na kuwafanya watu wote waamini kwamba amekufa, hatimaye unabainika baada ya Linda kumpeleleza kwa muda mrefu na kufanikiwa kumpata akiwa nchini Canada, akiwa amebadilisha jina na sura.
Msichana huyo kutoka familia ya kitajiri anajisikia vibaya sana kugundua kuwa kumbe Harrison hakufa na badala yake alimkimbia siku ya harusi yao kwa sababu ya penzi lake kwa malkia wa masokwe. Anapandwa na hasira kali kiasi cha kuwa tayari kufanya jambo lolote ili kulipiza kisasi.
Naye anatumia mbinu za hali ya juu kujibadilisha sura na jina kisha anaingia kwenye maisha ya Harrison na mkewe akijifanya ni hausigeli bila mtu yeyote kuujua ukweli. Kutokana na hasira kali, anapanga kuwaua Angel na mwanaye kwa sumu lakini mpango wake unaingia dosari baada ya Harrison naye kutaka kula chakula kilichowekwa sumu.
Vurugu kubwa inaibuka, Linda anamwaga vyakula vyenye sumu na kutaka kumdhuru Angel na mwanaye, Harrison anatumia nguvu kubwa kumdhibiti lakini baadaye anapogundua kuwa ni Linda aliyemkimbia siku ya harusi yao, anapatwa na mshtuko mkubwa unaosababisha aanguke na kupoteza fahamu. Msichana huyo anapelekwa kituo cha polisi lakini baadaye anaachiwa kwa jitihada za Harrison.
Harrison akamkimbilia Linda na kumuomba amsikilize. Msichana huyo akasimama huku akionesha bado kuwa na kinyongo, akamgeukia Harrison huku akiwa amekunja uso, mwanaume akaanza kumlainisha kwa maneno matamu huku akimsihi arudishe moyo nyuma na kukubali kwenda naye nyumbani ili wakayamalize.
“Sitaki! Niache muuaji mkubwa wewe! Nakuchukia, nakuchukia Harrison,” alisema Linda kwa sauti kubwa, hali iliyosababisha watu wawageukie na kuwashangaa. Licha ya kumtoa nishai mbele za watu, Harrison bado aliendelea kumbembeleza Linda. Msichana huyo akaanza kuangua kilio kwa nguvu, Harrison akaona huo ndiyo muda muafaka wa kumshinda.
Akamsogelea na kumshika, akawa anambembeleza kwa maneno laini, hali iliyomfanya Linda apunguze sauti, akaendelea kumlaumu kwa kumtesa moyo wake kiasi hicho. Harrison aliamua kujishusha, akawa anakubali makosa lakini akamsisitiza kuwa hiyo haikuwa sehemu muafaka ya kuzungumzia mambo hayo.
Akamsihi atulize moyo wake na kila kitu kitakuwa sawa, Linda akawa anaendelea kulia kwa kwikwi huku akionesha kukubali kuondoka na Harrison pamoja na mkewe, Angel. Kwa kuwa watu wengi walikuwa wameacha shughuli zao na kuwashangaa, Harrison aliita teksi harakaharaka, akamuingiza Linda na kukaa naye huku mkewe aliyekuwa na mwanaye wakikaa mbele.
Wakaondoka eneo hilo na kuwaacha watu wakiwa wamepigwa na butwaa. Kwa kuwa hapakuwa mbali na wanapoishi, baada ya dakika chache waliwasili nyumbani kwao, wakateremka na kuingia ndani, huku muda wote Harrison akiwa makini na Linda asije kusababisha madhara tena. Wakaingia moja kwa moja mpaka sebuleni na kukaa, Harrison akiwa katikati, kushoto akiwa amekaa mkewe na kulia akiwa amekaa Linda. Harrison akauvunja ukimya:
“Najua nimekukosea sana Linda, najua umelia na kuteseka mno kwa kipindi kirefu chanzo kikiwa ni mimi, nahisi hatia kubwa ndani ya nafsi yangu na jambo pekee litakalonifanya nijisikie amani ni kueleza ukweli wa kila kitu kilichotokea tangu siku nilipokukimbia kanisani mpaka leo hii. Nakuomba ukubali kunisikiliza,” alisema Harrison kwa sauti ya busara, Linda akatingisha kichwa kuashiria kuwa yupo tayari kumsikiliza.
Harrison akashusha pumzi ndefu na kuanza kueleza kila kitu kilivyokuwa. Alianza kwa kueleza kilichotokea siku ya harusi. Alieleza jinsi ambavyo moyo wake ulikuwa haujamkubali kuwa mkewe na jinsi alivyoamua kumkimbia kanisani.
“Nilikuwa kama nimechanganyikiwa, moyo wangu haukuwa tayari kukupokea wewe kuwa mke wangu wa ndoa lakini nilishindwa kukuambia kwa kuhofia kukuumiza. Nilijua kwa jinsi ulivyokuwa unanipenda, ungeweza hata kujiua kwa ajili yangu, ndiyo maana nikaona njia pekee ni kukukimbia,” alisema Harrison huku akilengwalengwa na machozi.
“Baada ya kukukimbia kanisani, nilienda kwa rafiki yangu ambaye alinipa mbinu nyepesi za namna ya kumaliza tatizo hilo, tukaandaa ajali feki na kufanya kila mtu aamini kwamba nimepata ajali na kufa. Nilikuwa sijielewi kwani nilichokuwa nakitaka kwa wakati huo ilikuwa ni kukutana na malkia wa masokwe tu kwani nilikuwa nampenda sana licha ya tofauti kubwa iliyokuwepo kati yangu na yeye.
“Ukweli ni kwamba sikufa kwenye ajali bali tulitafuta maiti na kuivalisha nguo zangu za harusi kisha tukatengeneza mazingira ili ionekane kama kuna ajali mbaya imetokea. Baada ya hapo mimi nikaondoka na kukimbilia kwenye msitu wa Tongass kumfuata kipenzi cha moyo wangu,” alisema
Harrison huku akimgeukia mkewe ambaye naye alikuwa amejiinamia, machozi yakimtoka. Wakakumbatiana huku kila mmoja akitokwa na machozi. Harrison akaendelea kueleza jinsi alivyohangaika na malkia wa masokwe mpaka alipofanikiwa kumtorosha na kukimbilia nchini Canada alikoanza kumfundisha ustaarabu wa kibinadamu mpaka walipofunga ndoa.
“Kwa hiyo mlishafunga ndoa? Ya mkataba au kanisani?” aliuliza Linda kwa sauti ya kilio, akiwa haamini alichokisikia. Harrison alimjibu kuwa walifunga ndoa ya kanisani, Linda akashindwa kujizuia, akawa analia kwa kwikwi huku akisisitiza kuwa bado anampenda.
“Basi na mimi nioe niwe mke wako wa pili, bado nakupenda Harrison nionee huruma. Tangu uliponikimbia sijawahi kuwa na mwanaume mwingine yeyote,” alisema Linda huku akiendelea kulia kwa uchungu, Harrison akawa anambembeleza na kumueleza kuwa suala hilo haliwezekani kwani imani ya dini ya Kikristo hairuhusu mwanaume kuoa mke zaidi ya mmoja.
“Wewe bado ni mrembo sana Linda na umri wako siyo mkubwa, utampata mwanaume mwingine utakayempenda kuliko hata ilivyokuwa kwangu na utasahau yote yaliyotokea. Mimi na mke wangu tunakuombea kila la heri upate mume mzuri lakini tafadhali naomba ukubali kunisamehe na kutuacha tuendelee kuishi kwa amani,” alisema Harrison kwa sauti ya kubembeleza.
Linda hakutaka kukubaliana na alichokuwa anaambiwa, akawa anaendelea kulia mpaka sauti ikamkauka na macho kuwa mekundu sana. Harrison akaendelea kumbembeleza kwa muda mrefu, jibu la mwisho alilolitoa ni kwamba hawezi kukubali kulikosa penzi lake kirahisi namna hiyo.
“Mimi naondoka kurudi nyumbani kwetu, lakini msimamo wangu ndiyo huo. Sipo tayari kukukosa Harrison, nitafanya chochote mpaka ndoto zangu za miaka mingi zitimie,” alisema Linda na kuondoka. “Sasa unaondoka muda huu unakwenda wapi?”
“Nilikuwa nimefikia hotelini kabla ya kuhamia hapa na nilishalipa kila kitu kwa hiyo msiwe na wasiwasi,” alisema Linda huku akiondoka kwa kasi. Harrison na mkewe wakabaki kutazamana huku macho ya kila mmoja yakiwa mekundu kwa kulia. “Sasa tutafanyeje mume wangu?”
“Yaani hata sielewi cha kufanya. Mimi nafikiri kwa hali ilivyo, inabidi turudi Marekani ili nikawaombe radhi watu wote, wakiwemo wazazi wangu na kuwaeleza ukweli wa kila kitu kama nilivyomweleza Linda kisha baada ya hapo nitaenda kuzungumza na wazazi wa Linda ili wao ndiyo wazungumze na binti yao. Naamini atawasikiliza wazazi wake,” alisema Harrison, wazo lililoungwa mkono na Angel.
Kwa kuhofia kuwa Linda anaweza kuwa amechanganya ile sumu kwenye vyakula vingine na maji, Harrison, mkewe na mtoto wao walitoka na kwenda kula hotelini. Walipomaliza kula walirejea ndani kwao na kuendelea na mipango yao ya kurudi Marekani pamoja na safari ya kwenda Tanzania kumfuata baba mzazi wa Angel, Abdulkarim Charwe.
Mipango iliendelea kufanyika mpaka usiku, wakalala huku wakiwa hawana amani kabisa kwani bado walikuwa wa wasiwasi kuwa Linda anaweza kurudi na kufanya lolote ili kutimiza malengo yake. ***
UNAWEZA kuwadanganya watu fulani kwa kipindi fulani lakini huwezi kuwadanganya watu wote kwa kipindi chote, usemi huu wa wanafalsafa wa kale unamhusu Harrison ambaye hatimaye uongo mkubwa alioutumia na kuwafanya watu wote waamini kwamba amekufa, unabainika.
Kijana huyo wa Kimarekani, aliyebobea kwenye masomo ya tabia za wanyama na mimea, aliudanganya ulimwengu kwamba amekufa kwenye ajali mbaya siku ya harusi yake aliyotakiwa kumuoa Linda, msichana ambaye hakuwa chaguo la moyo wake licha ya kwamba alikuwa akitoka kwenye familia ya kitajiri. Baada ya kumkimbia Linda, Harrison alikimbilia kwenye Msitu wa Tongass alikoanza kupigania penzi la malkia wa masokwe mpaka alipofanikiwa kumtorosha na kukimbilia naye nchini Canada walikooana na kuanza maisha mapya wakiwa kama mume na mke. Hata hivyo, Linda anaamua kufanya upelezi wa chini kwa chini na hatimaye anagundua kuwa Harrison hakufa bali alibadilisha jina na sura na sasa anaishi na malkia wa masokwe. Anafanikiwa kuingia kwenye
maisha yake akijifanya ni hausigeli na anataka kulipa kisasi kwa kuwaua mke wa Harrison na mwanaye. Muujiza unatokea na anashindwa kutimiza malengo yake. Utata unaendelea.
Kwa kuhofia kuwa Linda anaweza kuwa amechanganya ile sumu kwenye vyakula vingine na maji, Harrison, mkewe na mtoto wao walitoka na kwenda kula hotelini. Walipomaliza kula walirejea ndani kwao na kuendelea na mipango yao
ya kurudi Marekani pamoja na safari ya kwenda Tanzania kumfuata baba mzazi wa Angel, Abdulkarim Charwe. Mipango iliendelea kufanyika mpaka usiku, wakalala huku wakiwa hawana amani kabisa kwani bado walikuwa na wasiwasi kuwa Linda anaweza kurudi na kufanya lolote ili kutimiza malengo yake ya kulipiza kisasi.
Kulipopambazuka, Harrison na mkewe waliwahi kuamka na kuanza mipango ya kutimiza kila kitu walichokizungumza usiku. Kwa kuwa kila kitu kilikuwa hadharani, Harrison hakuona sababu ya yeye na mkewe kuendelea kuishi kama
wakimbizi nchini Canada, mipango ya kusafiri kurejea nyumbani kwa akina Harrison, Miami nchini Marekani ilianza. Jambo la kwanza, walikubaliana kuwa kila mmoja akaombe likizo ndefu isiyo na malipo kazini kwake. Wakaongozana
pamoja na kuanzia kazini kwa Angel ambapo aliomba likizo hiyo na kuwashtua viongozi wake. Ilibidi awaeleze kuwa kuna matatizo ya kifamilia ambayo inabidi apate muda wa kutosha kuyashughulikia.
Walipokubaliwa, walienda mpaka kazini kwa akina Harrison, akazungumza na viongozi wake na kuwaeleza malengo yake. Naye hakukubaliwa kirahisi kwani uttendaji kazi wake ulimfanya kuwa tegemeo kazini kwao ndani ya muda mfupi hivyo kuondoka kwake kungesababisha kampuni iyumbe. Hata hivyo, hakuwa na cha kufanya zaidi ya kushikilia msimamo wake, akaruhusiwa kwa shingo upande.
Baada ya hapo, waliondoka na kurudi nyumbani ambako waliwaaga baadhi ya majirani na maandalizi ya safari yakapamba moto. Angel alitafutiwa hati ya kusafiria huku Harrison akiendelea kutumia hati iliyokuwa na jina na sura bandia. Baada ya maandalizi kukamilika, Harrison, mkewe na mtoto wao, Harvey Junior walielekea Uwanja wa Ndege wa Abbotsford.
“Abiria mtakaosafiri na ndege aina ya Douglas DC-6 ya kampuni ya Orca Airways mnaombwa kuanza kuelekea ndani ya ndege,” sauti ya mhudumu wa kike ilisikika kwenye vipaza sauti vilivyokuwa kwenye uwanja huo wa kimataifa, abiria wengi waliokuwa ndani ya jengo la uwanja wa ndege, wakainuka na kuanza kusogea kwenye lango la kuingilia sehemu ya ukaguzi kisha kuelekea ndani ya ndege.
Harrison na mkewe nao walikuwa miongoni mwa abiria, wakasaidiana kusogeza mabegi yao makubwa yaliyokuwa na vitu vyao vyote mpaka sehemu ya ukaguzi. Baada ya kukaguliwa, Harrison na mkewe walishikana mikono na kuanza kuelekea mahali ndege ilipokuwa imepaki, wakapanda ngazi na kuingia kwenye ndege hiyo ya kisasa, wakaenda kukaa kwenye siti zao kama tiketi zao zilivyokuwa zinaeleza.
“Kwa heri Canada! Nimekumbuka sana nyumbani, sijui ndugu zangu wakiniona watanipokeaje?” alijiuliza Harrison akiwa amekaa kwenye siti yake na kumsaidia mkewe kumbeba mtoto. Waliendelea kuzungumza mambo mbalimbali na mkewe mpaka waliposikia tangazo la kuwataka kufunga mikanda kuashiria kwamba ndege ilikuwa ikitaka kuondoka.
Muda mfupi baadaye, injini za ndege ziliwashwa na kuanza kutoa muungurumo, ndege ikageuka na kuanza kusogea kuelekea kwenye njia za kurukia, ikawa inaongeza kasi taratibu mpaka ilipokolea mwendo, hatimaye ikapaa na kuiacha ardhi ya Canada.
Baada ya kusafiri kwa saa kadhaa angani, hatimaye ndege aina ya Douglas DC-6 ya kampuni ya Orca Airways iliwasili jijini Miami na kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Miami. Kwa muda wote huo, Harrison alikuwa akitafakari namna ndugu zake watakavyoipokea taarifa kwamba hakufa. Hakutaka kuchelewa mpaka Linda ndiyo akawaambie ukweli, alitaka kuanika kila kitu kwa kinywa chake mwenyewe.
Baada ya kuteremka kwenye Uwanja wa Ndege wa Miami, akiwa na mwonekano tofauti wa sura na umbo, Harrison alimuongoza mkewe mpaka kwenye Hoteli ya Olympia Heights iliyokuwa jirani kabisa na nyumbani kwao, alikokuwa anaishi mama yake mzazi, Skyler. Baada ya kufika kwenye hoteli hiyo, Angel akishangaashangaa mazingira ya Miami, Harrison aliwasiliana na mtaalamu wa upasuaji wa kubadilisha sura (plastic surgery) aliyepata namba zake kutoka kwenye kitabu cha
mawasiliano cha Yellow Pages. Akamuelekeza kufika hotelini hapo kwa ajili ya kumfanyia upasuaji mdogo wa kuondoa sura ya bandia ili abaki na sura yake halisi.
Kwa kuwa alimuahidi fedha za kutosha, Daktari Federer aliyebobea kwenye mambo ya ‘plastic surgery’ aliacha kazi alizokuwa anazifanya na kufunga safari mpaka kwenye Hoteli ya Olympia Heights na kwenda kuonana na Harrison aliyemweleza kuwa anataka kuivua sura ya bandia. “Hiyo mbona kazi rahisi sana! Jipake haya mafuta kisha usubiri kidogo nitakuonesha cha kufanya,” alisema Daktari Federer huku akimpa Harrison kichupa kilichokuwa na mafuta maalum. Baada ya Harrison kujipaka mafuta hayo usoni, aliingizwa kwenye chumba maalum kilichokuwa na baridi na kulazwa juu ya kitanda maalum.
Akaambiwa afumbe macho mpaka atakapoambiwa afumbue, akatii. Baada ya takribani nusu saa, daktari aliingia kwenye chumba hicho akiwa na vifaa mbalimbali kama mikasi, sindano, nyembe na visu vidogo. Akaanza kazi ya kumbandua ngozi ya bandia Harrison pamoja na nywele, zoezi lililochukua karibu dakika thelathini. Alipomaliza, alimsafisha uso kisha akamwambia akajitazame kwenye kioo kikubwa kilichokuwa ndani ya wodi hiyo.
“Whaoooo! Huyu ndiye Harrison wa siku zote, nimekuwa mzuri kama zamani,” alisema Harrison huku akijishika usoni. Akapakwa Mafuta mengine ya kulainisha ngozi kisha akatoka mpaka sehemu ya mapokezi alipomkuta mkewe na mtoto wao wakimsubiri kwa shauku. “He! Umebadilika mume wangu, kumbe ile sura ya bandia ilikuwa inakuzeesha bure! Cheki ulivyo ‘handsome’,” alisema Angel huku akimkumbatia mumewe kimahaba na kumbusu. Harrison alikuwa mwingine kabisa, kama ungemuona saa kadhaa zilizopita, hakika usingeweza kutambua kuwa ni yuleyule kwani alibadilika mno kuanzia nywele mpaka sura.
Baada ya kukamilisha malipo kwa Daktari Federer, wawili hao waliondoka na mtoto wao na safari ya kuelekea nyumbani kwa mama yake Harrison ikaanza. Kwa kadiri walivyokuwa wanakaribia kufika, ndivyo Harrison alivyoanza kubadilika kwani alijisikia uchungu sana kurudi kwenye mazingira aliyokulia baada ya kuwa amemdanganya mpaka mama yake aliyemzaa kwa shida.
Moyoni alijiona mwenye hatia kubwa kwa kuudanganya ulimwengu kwa kipindi chote hicho lakini alipogeuka na kumtazama mkewe aliyekuwa amekaa pembeni yake akimnyonyesha mtoto wao, alijikuta akifarijika na kupiga moyo konde kwamba licha ya kuumiza mioyo ya watu wengi, hatimaye furaha aliyokuwa akiisaka maishani mwake aliipata. Gari walilopanda likawafikisha mpaka nje ya geti la nyumba ya mama yake Harrison, Skyler, Harrison na mkewe wakateremka na kuanza kusogea taratibu kwenye mlango wa kuingilia ndani. ***
Baada ya kulihangaikia penzi la malkia wa masokwe kwa kipindi kirefu kiasi cha kuudanganya ulimwengu kwamba amekufa, hatimaye ukweli unafahamika kwamba Harrison hakufa kama watu wote walivyokuwa wanaamini.
Siri hiyo inagunduliwa na Linda ambaye Harrison alimkimbia siku ya harusi yao kwa ajili ya kumfuata malkia wa masokwe kwenye msitu mkubwa wa Tongass. Msichana huyo anaamua kufuatilia kwa kina kilichotokea siku ya harusi yao mpaka Harrison akamkimbia.
Upelelezi wake unamfikisha kwenye Mji wa Abbotsford, Canada ambako anamkuta Harrison akiwa amebadilisha sura na kuishi kinyumba na malkia wa masokwe ambaye sasa alikuwa amestaarabika na kuwa kama binadamu wa kawaida. Roho yake inamuuma sana kugundua kuwa kumbe Harrison alimkimbia kwa sababu ya
msichana huyo, anapanga kulipiza kisasi kikali huku akijiapiza kuwa ni lazima Harrison arudi kwenye mikono yake. Vurumai kubwa inatokea baada ya Linda kuujua ukweli lakini Harrison anashikilia msimamo wake kwamba mwanamke aliyekuwa anampenda ni Angel. Linda
anaondoka na kutoa vitisho, huku nyuma, Harrison na mkewe wanaamua kurudi nchini Marekani kwani siri yao ilishafichuka. Wanasafiri kwa ndege mpaka Miami, Marekani nyumbani kwa akina Harrison na tayari wapo nje ya nyumba ya mama yake Harrison, Skyler.
Sijui mama yangu yupo? Sijui akiniona atanipokeaje? Sijui jamii itanielewaje kwa hiki nilichokifanya? Eeeh Mungu nisamehe na unipe ujasiri katika kipindi hiki kigumu,” alisema Harrison huku wakizidi kuusogelea mlango wa kuingilia ndani ya nyumba yao, mkewe akiwa nyuma yake pamoja na mtoto wao, Harvey Junior. Walisimama mlangoni, Harrison akabonyeza kitufe cha kengele, akasubiri kwa sekunde kadhaa kisha wakashuhudia mlango mkubwa ukifunguliwa, msichana aliyeonekana dhahiri kuwa mfanyakazi wa ndani akafungua mlango wa ndani kisha akafungua geti. Akawasalimu Harrison na mkewe kisha akawauliza awasaidie nini. “Tunaweza kuonana na mwenye nyumba?” “Nani? Mama? Yupo ndani amepumzika. Nimwambie nyie ni akina nani?” “Mwambie tu kuna wageni wake,” alisema Harrison huku mapigo ya moyo yakizidi kumwenda mbio na miguu yake kuishiwa nguvu. Msichana huyo aliwakaribisha mpaka sebuleni, akaelekea chumbani kwa bosi wake (Skyler) na kumpa taarifa kuwa kuna wageni wake. Skyler aliamka na kuvaa vizuri nguo zake, akatoka mpaka sebuleni, macho yake yakatua kwa msichana aliyekuwa amembeba mtoto. Alipogeuza shingo yake upande wa pili, macho yalimtoka pima baada ya kumuona mtu ambaye hakutegemea kuja kumuona tena maishani mwake. “Harrison! Hapanaaa, haiwezekani, jamani mzimu wa Harri…” Skyler alipiga kelele kwa nguvu zilizosikika mpaka kwa majirani lakini kabla hajamalizia alichotaka kukisema, alianguka chini kama mzigo na kupoteza fahamu. Msichana wa kazi ndiyo aliyekuwa wa kwanza kufika sehemu bosi wake alipoangukia, akifuatiwa na mke wa Harrison, wakainama chini alipoangukia Skyler ambaye sasa alishaanza kuzeeka na kuwa mtu mzima, tofauti na wakati Harrison anamuona kwa mara ya mwisho. Harrison alibaki amepigwa na butwaa huku machozi yakimtoka, hakutegemea kama mama yake anaweza kushtuka kiasi hicho mpaka kupoteza fahamu. Muda mfupi baadaye, majirani kadhaa waliomsikia Skyler akipiga kelele kwamba ameuona mzimu wa mwanaye, walifika nje ya nyumba hiyo kwa lengo la kutoa msaada. Kwa kuwa nao walikuwa wakimfahamu Harrison, walipoingia ndani na kumkuta, kila mtu alikimbia nje wakiamini kwamba ni kweli mzimu wa Harrison ulikuwa umewatokea, Harrison na mkewe wakawa na kazi ya ziada ya kuwaelewesha ingawa kazi haikuwa nyepesi. Baada ya kujieleza sana, baadhi ya majirani wa kiume ambao hawakuwa waoga, waliingia ndani na kusaidiana kumbeba Skyler ambaye hakuwa na fahamu na kumtoa mpaka nje, wakampakiza kwenye gari na kumkimbiza hospitali ili kuokoa maisha yake. Harrison aliongozana nao huku muda wote akiwa amejiinamia, machozi yakimtoka kama chemchemi ya maji. Bado watu waliendelea kumshangaa, wakiwa wanajiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu kwani kila mtu alikuwa anajua Harrison alikufa siku nyingi zilizopita na kuzikwa. Baada ya kufikishwa hospitali, Skyler alilazwa na kuanza kupewa huduma ya kwanza, akatundikiwa dripu iliyoanza kutiririka kwa kasi kuingia kwenye mishipa yake. Muda mfupi baadaye, wazazi wa Skyler, mzee Lewis na mkewe walipewa taarifa kuwa mtoto wao wa kipekee, Skyler alikuwa amelazwa kwenye hospitali aliyokuwa akifanyia kazi mzee huyo kabla ya kustaafu. Harakaharaka, wazee hao waliingia ndani ya gari lao huku kila mmoja akiwa na wasiwasi mkubwa juu ya afya ya mtoto wao. Japokuwa mzee Lewis alikuwa amezeeka, bado alikuwa na uwezo wa kuendesha gari vizuri kwa umakini, wakaelekea mpaka kwenye Hospitali ya Miami na kwenda kuuliza mapokezi. Kwa kuwa wafanyakazi wengi wa hospitali hiyo walikuwa wanamfahamu daktari huyo mstaafu, hakupata shida, muda mfupi baadaye tayari walikuwa kwenye wodi aliyolazwa Skyler. “Dokta kwani kumetokea nini?” aliuliza mzee Lewis akiwa ameshikana mkono na mkewe. Daktari akawajibu kuwa mgonjwa wao alikuwa amepatwa na mshtuko lakini atakuwa sawa baada ya muda mfupi. Wakatazamana na mkewe kisha daktari akawaomba waende sehemu ya kupumzikia ili madaktari wapate nafasi ya kuendelea kumtibu mgonjwa. Mzee Lewis na mkewe wakatoka kuelekea kwenye bustani ya maua iliyokuwa nje ya wodi hiyo na kuelekea kwenye viti maalum vilivyokuwa eneo hilo. Wakati wakitembea taratibu, wakijiandaa kukaa, mzee Lewis aliona kitu kilichomshtua moyo wake kuliko kawaida, akamkonyeza mkewe na kumuoneshea kwa kidole. Mke wa mzee Lewis alipiga kelele kwa nguvu baada ya kuona alichooneshwa na mumewe. “Harrisoooon! Hapana, siyo yeye, ni mzimu wa…ke,” alipiga kelele mama huyo mzee na kujikuta akiishiwa nguvu, mumewe alijaribu kumdaka lakini alishachelewa, mama huyo akaanguka chini kama mzigo na kupoteza fahamu. Manesi waliokuwa jirani, wakakimbilia eneo hilo na kumsaidia kumuinua na kumbeba juu ya kitanda cha magurudumu, akakimbizwa wodini. Kelele alizopiga mwanamke huyo kabla hajaanguka na kupoteza fahamu, ziliwashtua watu wengi, akiwemo Harrison na mkewe waliokuwa wamekaa eneo hilo wakisubiri mgonjwa wao, Skyler azinduke. Kwa kuwa muda wote Harrison alikuwa ameinama, machozi yakimtoka kutokana na hali iliyompata mama yake mzazi baada ya kumuona, hakuwaona bibi na babu yake wakati wakifika eneo hilo. Kilichomshtua ni baada ya kusikia jina lake likitajwa, alipoinua macho yake yaliyotandwa na machozi, alimshuhudia mwanamke mzee akianguka huku mwanaume akijaribu kumsaidia. Alipomtazama vizuri mwanaume huyo, alimkumbuka kwa haraka kuwa ni babu yake, moyo ukamlipuka paah! Harakaharaka aliacha kila alichokuwa anakifanya, akainuka na kuanza kuelekea eneo la tukio, lakini kabla hajafika, manesi tayari walishakuwa wamemuinua mwanamke huyo mzee na kumpakiza kwenye kitanda cha magurudumu. “Harrison! Ni wewe au naota? Mungu wangu,” alisema mzee Lewis huku akitetemeka mwili mzima, akihisi amekutana na mzimu wa mjukuu wake. Harrison alishindwa cha kujibu, machozi yakawa yanamtoka. Akapiga magoti mbele ya babu yake huku akiinua mikono kwa ishara ya kuomba msamaha. Kwa moyo wa ujasiri, mzee Lewis alimsogelea Harrison na kumpa mkono kisha akamuinua, akamsogeza kifuani kwake na kumkumbatia huku akiwa bado haamini kama ni Harrison kweli au ni mzimu wake. Harrison akawa analia kwa kwikwi huku akitamka maneno ya kumuomba msamaha babu yake na watu wengine wote. “Kwani nini kilitokea?” alihoji mzee Lewis huku akimtoa Harrison kifauni kwake na kumfuta machozi. ***
Harrison anasababisha mshtuko mkubwa kwa ndugu zake ambao walikuwa wanaamini kuwa alishakufa siku nyingi zilizopita. Wa kwanza kushtuka hadi kupoteza fahamu ni mama yake mzazi, Skyler ambaye baada ya kumuona, anadhani amekutana na mzimu, anaanguka na kupoteza fahamu.
Majirani wanaofika kumpa msaada Skyler baada ya kusikia akipiga kelele, nao wanatoka mbio baada ya kumkuta Harrison akiwa ndani kwani wote walishaamini kwamba amekufa. Hata hivyo, wachache wenye ujasiri wanamhoji kilichotokea, anawaeleza ukweli kisha wanasaidiana kumkimbiza Skyler hospitali. Mzee Lewis, babu yake Harrison anapopata taarifa za kuanguka kwa mwanaye Skyler, anaondoka na mkewe mpaka hospitali lakini baada ya kufika, anapigwa na butwaa baada ya kumuona Harrison. Anapomuonesha mkewe alichokiona, anapatwa na mshtuko mkubwa, naye anapoteza fahamu. Wote wanalazwa kwenye hospitali hiyo na mzee Lewis anaanza kumhoji Harrison kilichotokea.
KABLA Harrison hajaanza kumueleza mzee Lewis kilichomtokea maishani, alianza kwa kumtambulisha Angel na mwanaye, mzee huyo akazidi kupigwa na butwaa kwani hakutegemea kuwa tayari Harrison anaweza kuwa ameoa na kuzaa. Akiwa bado amepigwa na butwaa, Harrison alimuoneshea ishara kuwa wakakae kwenye viti vilivyokuwa pembeni ili amueleze kinagaubaga. Mzee Lewis akiwa bado amepigwa na bumbuwazi, akimshangaa mke wa Harrison na mtoto wake, alisogea mpaka kwenye viti, wote wakakaa. Harrison alishusha tena pumzi ndefu kisha akaanza kumsimulia mzee Lewis kila kitu kilivyokuwa tangu siku aliyomkimbia Linda kanisani. Mzee huyo alikuwa akishangaa kila kitu, hakuwahi kudhani kwamba Harrison aliyekuwa anamjua, anaweza kudiriki kufanya mambo hayo kwa sababu tu ya mapenzi. Harrison hakuacha kitu, alieleza kuanzia jinsi walivyoshirikiana na rafiki yake kutengeneza ajali feki, jinsi alivyokimbilia kwenye msitu wa Tongass na yote yaliyofuatia mpaka akafanikiwa kumpata malkia wa masokwe na kwenda naye nchini Canada alikofunga naye ndoa ya kanisani. “Ulikosea sana Harrison, vipo vya kudanganya lakini siyo kifo. Sisi tulishakuzika ndiyo maana bibi yako na mama yako wamepoteza fahamu baada ya kukuona. Kila mtu anajua kuwa ulikufa kwa ajali na kuzikwa! Umemkosea Mungu na watu wote hasa mashabiki wako wanaokipenda kitabu chako, ulisababisha huzuni kubwa sana nchi nzima,” alisema mzee Lewis huku akijifuta machozi. “Najua kuwa nimefanya dhambi kubwa lakini mimi pia ni binadamu, niliyafanya yote hayo kwa sababu ya penzi langu kwa Angel, nawaomba sana mnisamehe na nitatubu kwa Mungu wangu,” alisema Harrison huku naye akilengwalengwa na machozi kisha ukimya ukatawala, kila mmoja akazama kwenye dimbwi la mawazo. Walikuja kuzinduliwa na nesi aliyewasogelea na kuwapa taarifa kuwa Skyler amerejewa na fahamu. Harakaharaka wote wakainuka na kutaka kukimbilia wodini lakini nesi akamzuia Harrison kwa maelezo kuwa akienda kumuona mgonjwa anaweza kumsababishia mshtuko mwingine, wazo lililoungwa mkono na mzee Lewis. Wakakubaliana kwamba mzee huyo ndiyo aende kwanza wodini kumjenga mwanaye kisaikolojia kabla ya Harrison kuingia. Harakaharaka akaongozana na nesi hadi kwenye wodi aliyokuwa amelazwa Skyler. Japokuwa Skyler alikuwa amesharejewa na fahamu, bado alikuwa hakumbuki vizuri kilichosababisha mpaka akafikishwa hospitalini hapo. Alipomuona baba yake, alianza kumuuliza kilichompata. Mzee Lewis akakaa pembeni ya kitanda chake na kuanza kumueleza kila kitu. Ni hapo ndipo kumbukumbu zilipomrudia Skyler, akawa anamwambia baba yake kuwa amekutana na mzimu wa Harrison. Ilibidi mzee Lewis amuanzie mbali ili kumfanya aamini kwamba alichokiona hakikuwa mzimu bali ni Harrison mwenyewe. Haikuwa kazi nyepesi kwa Skyler kuamini alichokuwa anaambiwa na baba yake, akawa anasisitiza kuwa Harrison alishakufa. Ilibidi mzee Lewis atoke nje na kwenda kumuita Harrison na mkewe, wakaingia wote wodini na kwenda mpaka kwenye kitanda alichokuwa amelazwa Skyler. “Harrison! Harr…,” alisema Skyler lakini akashindwa kumalizia kauli yake, akawa anaangua kilio kama mtu aliyepewa habari za msiba huku akimng’ang’ania mzee Lewis mwilini kutokana na hofu. Mzee huyo aliendelea kumueleza kwamba alichokiona hakikuwa mzimu kama alivyokuwa akifikiria awali, akazidi kumsisitiza kwamba Harrison hakufa kama watu wote walivyokuwa wanaamini. Kwa muda wote huo, Harrison alikuwa kimya kabisa, kichwa chake akiwa amekiinamisha chini huku machozi yakimtoka. Baada ya Skyler kutulia, Harrison alipiga magoti pembeni ya kitanda chake na kuanza kumuomba msamaha mama yake kwa yote yaliyotokea. Alimweleza kuwa hakufa kama watu wote walivyokuwa wanaamini, akaukumbatia mkono wake huku akitokwa na machozi kama chemchemi ya maji. Skyler bado alikuwa haamini kama ni kweli Harrison hakufa, akawa anamtazama kwa makini huku akijiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu. Alishindwa kuelewa nini kilichotokea mpaka watu wote wakaamini kwamba Harrison amekufa wakati siyo kweli. Hata hivyo, mzee Lewis alimwambia kuwa asiwe na wasiwasi kwani akishatoka hospitali ataelezwa kila kitu jinsi kilivyokuwa. Skyler alishusha pumzi ndefu na kukubali kumsamehe mwanaye, akawageukia Angel na mtoto wake ambao muda wote walikuwa wametulia pembeni ya kitanda. Kabla hata hajauliza, Harrison alimuwahi na kumtambulisha Angel kama mkewe wa ndoa. “Mungu ametujalia tumepata mtoto, anaitwa Harvey Junior,” alisema Harrison huku akimshika mkono mkewe na kumsogeza jirani na mama yake. Japokuwa Skyler alikuwa na hali mbaya kitandani, aliachia tabasamu pana kusikia mtoto wa Harrison amepewa jina kama la kipenzi cha moyo wake, marehemu Harvey. Akataka apewe mtoto ili amshike, Angel akamshusha mgongoni na kumpa Skyler, akajikakamua na kumbeba huku tabasamu likizidi kuchanua usoni kwake. Alipomtazama vizuri usoni, aligundua kuwa mtoto huyo alikuwa akifanana sana na Harrison, akashindwa kujizuia kuonesha furaha yake. Akambusu kwenye paji la uso kisha akamrudisha kwa mama yake. Wakati wote wakiendelea kufurahi, nesi alikuja kuwapa taarifa kuwa mke wa mzee Lewis aliyekuwa amelazwa kwenye wodi nyingine baada ya kuanguka na kupoteza fahamu, ameshazinduka. Harakaharaka Harrison na babu yake, mzee Lewis walitoka na kuelekea kwenye wodi aliyokuwa amelazwa, wakamuacha Angel na mtoto wake pembeni ya Skyler. Walipofika, kama ilivyokuwa awali, Harrison alizuiwa kuingia wodini kwa kuhofia anaweza kusababisha mgonjwa akapatwa na mshtuko kwa mara nyingine. Ikabidi asimame mlangoni wakati mzee Lewis akiingia kumtazama mkewe. Alikwenda moja kwa moja mpaka kwenye kitanda alichokuwa amelazwa, alipomuona tu, alianza kumwambia kuwa amekutana na mzimu wa Harrison. Kama alivyofanya kwa Skyler, mzee Lewis alianza kumuelewesha mkewe kwamba alichokiona siyo mzimu bali ni Harrison. Akajaribu kumjenga kisaikolojia mpaka akaamini kwamba kumbe Harrison hakufa kama kila mtu alivyokuwa anaelewa. Alipohakikisha mkewe yupo kwenye hali nzuri kisaikolojia, alitoka na kwenda kumchukua Harrison aliyekuwa amejiinamia mlangoni, nje ya wodi aliyolazwa bibi yake. Wakaingia wote mpaka pembeni ya kitanda alicholazwa, akawa anamshangaa Harrison kwa macho ya udadisi. Mzee Lewis akamwambia kuwa akisharuhusiwa kutoka hospitalini, atamueleza kwa kina kilichotokea, wazo ambalo mwanamke huyo alilikubali. Akawa anaendelea kumshangaa Harrison kama asiyeamini alichokuwa anakiona. Baada ya kuzungumza kidogo, wote walitoka nje kuwapisha manesi waendelee kumhudumia mgonjwa. Baada ya muda, wagonjwa wote wawili waliruhusiwa kutoka wodini, wakaenda mpaka nyumbani kwa mzee Lewis ambapo Harrison alianza upya kuwaeleza kilichotokea kuanzia siku aliyomkimbia Linda kanisani mpaka siku hiyo. Ilikuwa ni simulizi iliyowatoa wote machozi. ***
KILA anayeufahamu ukweli kwamba kumbe Harrison hakufa kama watu wote walivyokuwa wanaamini, anapatwa na
mshtuko mkubwa na kujiuliza maswali mengi yanayokosa majibu.
Wa kwanza kushtuka hadi kupoteza fahamu ni mama yake mzazi, Skyler ambaye baada ya kumuona Harrison,
anadhani amekutana na mzimu, anaanguka na kupoteza fahamu.
Majirani wanaofika kumpa msaada Skyler baada ya kusikia akipiga kelele, nao wanatoka mbio baada ya kumkuta
Harrison akiwa ndani kwani wote walishaamini kwamba amekufa. Baadaye, bibi yake Harrison naye anapoteza
fahamu baada ya kumuona mjukuu wake. Anaamini amekutana na mzimu.
Wote wanalazwa kwenye hospitali moja na mzee Lewis anaanza kumhoji Harrison kilichotokea. Baada ya kuufahamu
ukweli, anatumia utu uzima wake kuwaelewesha Skyler na mama yake baada ya kurejewa na fahamu. Hali ya taharuki
inaendelea kutanda kila mahali, kila mmoja akiwa haamini anachokisikia.
Baada ya muda, wagonjwa wote wawili, Skyler na mama yake waliruhusiwa kutoka wodini, wakaenda mpaka nyumbani kwa mzee Lewis ambapo Harrison alianza upya kuwaeleza kilichotokea kuanzia siku aliyomkimbia Linda kanisani mpaka siku hiyo. Ilikuwa ni simulizi iliyowatoa wote machozi.
“Ulikosea sana Harrison! Sijui tutazificha wapi sura zetu watu wakiufahamu ukweli, lazima watahisi kwamba ulishirikiana na sisi kwenye mpango huo mchafu,” alisema Skyler huku akitokwa na machozi. Akaungwa mkono na mzee Lewis ambaye aliwaambia
watu wote kwamba anajisikia vibaya sana kugundua kuwa kumbe Harrison aliwadanganya kwa kipindi chote hicho kwamba amekufa wakati haikuwa kweli.
“Nilikwambia hakuna kitu kibaya kama kujichulia kifo, inabidi tumtafute mchungaji ambaye atakuongoza kwenye sala ya toba kisha itabidi uitishe mkutano na waandishi wa habari na kuwaeleza ukweli bila kuficha chochote, watu wote waambiwe ukweli,” alisema mzee Lewis, wote wakakubaliana na wazo hilo.
Wakaanza pia kumhoji kuhusu historia ya mkewe na jinsi walivyofanikiwa kumpata mtoto. Harrison alishusha pumzi ndefu na kuwatazama usoni mmoja baada ya mwingine. Akawaeleza kila kitu kuhusu Angel na jinsi alivyofanikiwa kufahamu kwamba asili yake ni nchini Tanzania.
Pia aliwaeleza kila kitu kuhusu Linda na jinsi alivyomfuatilia kimyakimya mpaka alipofanikiwa kuwakuta nchini Canada. Aliwaeleza jinsi Linda alivyojifanya hausigeli na kufanikiwa kuingia kwenye maisha yao na kitendo alichokifanya cha kujaribu kuwaua Angel na mwanaye kwa sumu.
Kila mmoja alipigwa na butwaa, wakawa wanajiuliza kama muujiza usingetokea na Harrison kuamua kurudi haraka nyumbani, nini kingewapata Angel na mwanaye? Kila mmoja kwa imani yake alimshukuru Mungu kwani muda huo wangekuwa wanazungumza habari nyingine.
“Linda ana roho mbaya sana,” alisema mzee Lewis lakini akapingwa vikali na Skyler na mama yake. Wote walimtetea kwamba hakuwa na roho mbaya kama walivyokuwa wanahisi bali alikuwa akilipigania penzi lake kwa sababu aliamini bado Harrison anampenda.
“Ungemwambia ukweli kwamba humpendi wala asingefikia hatua ya kufanya hivyo, ulikosea sana Harrison, unapaswa kumuomba radhi yeye na watu wote uliowakosea,” Skyler kwa uchungu na kuungwa mkono na mama yake.
Mjadala uliendelea kwa muda mrefu na mwisho wote wakakubaliana kwamba Linda hakuwa na makosa katika suala hilo, muafaka ukafikiwa kwamba wazazi wa Harrison, mama, bibi na babu yake waongozane mpaka nyumbani kwa wazazi wa Linda na kwenda kuzungumza nao kuhusu suala la Linda.
Hawakutaka kupoteza muda, harakaharaka wakajiandaa na safari ya kuelekea nyumbani kwa akina Linda. Harrison na mkewe ilibidi wabaki nyumbani kwao kwa sababu ya usalama wao. ***
Baada ya mzee Lewis, mkewe na Skyler kufika nyumbani kwa wazazi wa Linda, walishtushwa na umati mkubwa wa watu waliowakuta nje ya nyumba hiyo.
“He! Kuna nini tena jamani? Kuna usalama kweli hapa?” aliuliza mzee Lewis baada ya kuteremka kwenye gari na familia yake.
Hakuna mtu aliyewajibu, wakaongoza moja kwa moja mpaka kwenye mlango wa kuingilia ndani. “Karibuni! Karibuni sana,” alisema baba yake Linda, akawapokea wageni na kuingia nao mpaka ndani ambako waliwakuta baadhi ya watu wakiwa wamekaa sebuleni huku wakiwa na nyuso za huzuni.
“Vipi kuna nini mzee mwenzangu,” aliuliza mzee Lewis, baba yake Linda akamvutia pembeni na kuanza kumueleza kilichokuwa kinaendelea. Akamwambia kuwa mtoto wao Linda aliyekuwa amesafiri kwa kipindi kirefu, amerejea lakini amekuja na ujumbe wa ajabu unaowafanya watu wote waamini kwamba amerukwa na akili. “Kwani amekuja na ujumbe gani?”
“Anasema eti Harrison hakufa bali alimkimbia na kwenda kuoana na malkia wa masokwe, nahisi penzi la mjuu wako linamfanya binti yangu awe mwendawazimu, sijui alimpa nini?” alisema baba yake Linda kwa uchungu.
Akaendelea kumueleza kuwa watu wote waliokuwa wamekusanyika siku hiyo hapo nyumbani kwake walikuwa ni ndugu zake ambao waliitana kwa lengo la kujadili mustakabali wa Linda na namna ya kumsaidia kwani tangu afike, aligoma kula wala kufanya kitu chochote zaidi ya kuwa analia usiku na mchana akilitaja jina la Harrison.
Ilibidi mzee Lewis amuombe mzee mwenzake watoke nje na kwenda kuzungumza pembeni kwani alihisi endapo angemweleza ukweli palepale mbele za watu, angepata mshtuko mkubwa ambao ungeongeza matatizo kwenye familia hiyo. Baba yake Linda alikubaliana naye, wakatoka mpaka kwenye bustani ya maua na kukaa kwenye viti.
“Mzee mwenzangu una kifua?” “Kifua ninacho, utu uzima dawa.”
Kauli hiyo ilimshangaza sana baba yake Linda, akakodoa macho kama asiyeamini alichokisikia. Mzee Lewis akaendelea kumueleza kila kitu kama alivyohadithiwa na Harrison mwenyewe kuanzia siku aliyomkimbia Linda kanisani na kila kitu kilichoendelea baada ya hapo.
Kijasho chembamba kikawa kinamtoka baba yake Linda. Alijiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu lakini mwisho hakuwa na cha kufanya zaidi ya kukubaliana na ukweli. Wakawa wanajadiliana nini cha kufanya kwa sababu mpaka muda huo, Linda alikuwa kwenye hali mbaya sana na mara kwa mara alikuwa akitishia kwamba atajiua.
Baada ya kuambiwa maneno hayo, baba yake Linda alitafakari kwa dakika kadhaa kisha akaona jambo muhimu kwa wakati huo, ni kuzikutanisha familia zote mbili na kujadili kwa kina kuhusu suala hilo. Kwa kuwa tayari nyumbani kwa akina Linda kulikuwa na
watu wengi, alishauri kwamba wamchukue Linda pamoja na mama yake kisha wakalijadili suala hilo nyumbani kwa mama yake Harrison, kila mmoja akiwepo. ***
Kuonekana upya kwa Harrison baada ya kutoweka kwa kipindi kirefu, kunasababisha sintofahamu kubwa huku baadhi ya watu waliomuona wakihisi wamekutana na mzimu. Karibu kila mtu alishaamini kwamba kijana huyo alikufa kwenye ajali ya barabarani na kuzikwa kwenye Makaburi ya Miami Cemetery hivyo kuonekana kwake kunazua maswali mengi.
Mama mzazi wa
Harrison, Skyler aliyekuwa wa kwanza kumuona, anaanguka na kupoteza fahamu akidhani amekutana
na mzimu. Hali hiyo inamtokea pia bibi yake Harrison na majirani kadhaa. Babu yake, mzee Lewis
anamkabili Harrison na kumuuliza kilichotokea ambapo anamueleza kila kitu.
Mzee huyo anabeba jukumu la kuwaelewesha watu wote ukweli juu ya Harrison, anafanya kazi hiyo
nzito na baada ya muda, baadhi ya watu wanaanza kuelewa na kuamini maelezo hayo. Upande wa pili, Linda amesharejea nyumbani kwao lakini bado hataki kukubaliana na ukweli kwamba
Harrison hampendi bali anampenda mkewe, Angel. Hali hiyo inasababisha ndugu zake waitane kwa ajili ya kikao cha familia kwani anagoma mpaka kula kisa kikiwa ni penzi la Harrison.
Baada ya kuambiwa maneno hayo, baba yake Linda alitafakari kwa dakika kadhaa kisha akaona jambo muhimu kwa wakati huo, ni kuzikutanisha familia zote mbili na kujadili kwa kina kuhusu suala hilo. Kwa kuwa tayari nyumbani kwa akina Linda kulikuwa na watu wengi, alishauri kwamba wamchukue Linda pamoja na mama yake kisha wakalijadili suala hilo nyumbani kwa mama yake Harrison, kila mmoja akiwepo.
Waliondoka kwa kutumia magari mawili tofauti, Linda alipanda gari moja na baba na mama yake wakati mzee Lewis aliondoka na mkewe na Skyler kwa kutumia gari lingine. Njia nzima, Linda alikuwa akiendelea kulia, akiwa amejilaza kwenye kifua cha mama yake aliyekuwa na kazi ya ziada kumbembeleza.
Mzee Lewis, mkewe na Skyler ndiyo walikuwa wa kwanza kufika, wakawaambia Harrison, mkewe na mtoto wao waingie chumbani kwanza mpaka watakapowaita, harakaharaka wakasaidiana kupanga viti na kuiweka sebule katika hali nzuri, tayari kwa kikao.
Muda mfupi baadaye, Linda na wazazi wake waliwasili, wakapokelewa na kupelekwa moja kwa moja sebuleni. Mzee Lewis, mkewe, Skyler na Harrison nao wakatoka na kuungana na wageni sebuleni. Angel aliendelea kubaki chumbani na mwanaye, kikao kikaanza.
Wa kwanza kuzungumza alikuwa ni mzee Lewis aliyetumia busara za hali ya juu kujaribu kumuweka sawa Linda ili aone kwamba kilichotokea ni jambo la kawaida. Alimlaumu Harrison kwa kitendo alichokifanya na kumtaka kabla hawajaendelea mbele, awaombe radhi watu wote waliokuwa kwenye kikao hicho.
Harrison alikubali kutii agizo hilo na kuwaomba radhi wote kwa kilichotokea, akakiri kwamba ni kweli alikosea sana kumkimbia Linda kanisani na baadaye kudanganya kwamba amekufa. Alijitetea kwamba alikuwa hajielewi ndiyo maana akafanya yote hayo.
Baada ya kuomba radhi kwa takribani dakika kumi na tano, kikao kiliendelea. Linda naye akapewa nafasi ya kueleza yaliyokuwa ndani ya moyo wake. Kazi haikuwa nyepesi kwani kila baada ya kuongea kidogo, Linda alikuwa akishindwa kuendelea kutokana na kubanwa na kilio cha kwikwi. Mama yake akawa na kazi ya ziada ya kumtuliza.
“Licha ya yote aliyonifanyia, ba..do na…mpenda sana Harri…son, nata…ka anioe ni..we….” alisema Linda na kushindwa kumalizia alichotaka kukisema, akawa analia kwa kwikwi kiasi cha kuwatoa machozi wote waliokuwa ndani ya nyumba hiyo.
Hata hivyo, ilibidi busara zitumike kuweka mambo sawa, Linda akafafanuliwa kwamba tayari Harrison alishaoa, tena kwa ndoa ya kanisani hivyo asingeweza kumuacha mkewe ambaye amezaa naye wala asingeweza kuoa mke wa pili.
Awali Linda aling’ang’ania sana msimamo wake lakini kwa kadiri alivyokuwa anazidi kupewa nasaha na kuelezwa kwamba kila jambo lina sababu yake, taratibu alianza kuelewa. Akaendelea kupokea nasaha mfululizo kutoka kwa bibi, babu na mama yake Harrison pamoja na wazazi wake ambao kwa pamoja walimueleza kuwa Harrison hakuwa riziki yake na ndiyo maana hayo yote yalitokea.
“Wewe bado ni msichana mrembo ambaye huwezi kukosa mume mzuri wa kukuoa. Isitoshe umesoma sana, familia yako ina uwezo mkubwa wa kiuchumi! Una kila kitu cha muhimu kwa hiyo usiumie sana ndani ya moyo wako. Ukubali ukweli hata kama unaumiza namna gani kisha songa mbele na maisha yako bila Harrison,” alisema mzee Lewis na kuungwa mkono na baba yake Linda.
Kikao kiliendelea kwa muda mrefu, Linda akakubali kwa shingo upande kumuacha Harrison aendelee na maisha yake na familia yake lakini akaomba waendelee kuwa marafiki wa kawaida. Baada ya kauli hiyo, watu wote walimpigia makofi na kumshangilia kutokana na ukomavu aliouonesha.
Angel akaenda kuitwa na kuelezwa muafaka uliofikiwa. Naye kwa upande wake alionesha kufurahi sana kwani licha ya kwamba alikuwa anamuonea huruma Linda kwa kilichotokea, alitamani kuona amani inarejea kwenye ndoa yake na kumuombea siku moja apate mume mzuri watakayejenga naye familia.
Kwa furaha, Angel aliwashukuru wote kwa kazi kubwa waliyoifanya kisha wakapatanishwa na Linda, wakakumbatiana kwa zaidi ya dakika mbili huku kila mmoja akitokwa na machozi. Baada ya hapo, wote walioshiriki kazi hiyo walianza kupeana mikono kama ishara ya upatanisho, Linda na Harrison nao wakapeana mikono kuashiria kwamba mambo yote yamekwisha.
“Kazi iliyobaki kama tulivyokubaliana awali ni kwa Harrison kuitisha mkutano na waandishi wa habari kisha kuwaeleza ukweli wote na kuwaomba radhi mashabiki wako na watu wote ambao waliguswa na taarifa za uongo juu ya kifo chako,” alisema mzee Lewis, wote wakaliunga mkono wazo hilo.
Waliagana, Linda akaondoka na wazazi wake akiwa kwenye hali tofauti na aliyokuwa nayo wakati akiwasili nyumbani hapo. Huku nyuma, Angel na Harrison walikumbatiana kwa furaha kwani hatimaye, amani ilikuwa imerejea ndani ya ndoa yao baada ya kuhangaika kwa kipindi kirefu.
Harrison alikumbatiana pia na mama yake, Skyler kisha babu na bibi yake ambao wote kwa pamoja walikuwa na furaha ya hali ya juu baada ya Linda kuamua kuukubali ukweli. Mipango ya Harrison kwenda kuzungumza na waandishi wa habari ikaanza kupangwa. Siku mbili baadaye, Harrison akiwa ameongozana na mkewe, mwanaye, mama yake, bibi na babu yake,
alikwenda mpaka kwenye ofisi za shirika la habari la serikali ambako alikuta waandishi wengi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsubiri kwa shauku kwani walishakuwa na taarifa juu ya azma yake ya kuzungumza na vyombo vya habari baada ya ‘kufufuka’.
Muda mfupi baadaye, picha na sauti ya Harrison vikawa vinasikika na kutazamwa na mamilioni ya Wamarekani. Kila aliyesikia habari hiyo kwamba kumbe Harrison hakufa, alipigwa na butwaa na kushindwa kuamini haraka. Hata hivyo, huo ndiyo ulikuwa ukweli.
“Nawaomba watu wote ambao kwa namna moja au nyingine mliguswa na tukio hilo mnisamehe. Nimeshamuomba msamaha Linda lakini narudia tena, nataka watu wote wajue kwamba nilifanya makosa ambayo mpaka leo nayajutia, namuomba Mungu wangu na watu wote mnisamehe kwa hili,” alikaririwa Harrison wakati akiongea na waandishi wa habari.
Kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo, licha ya kuomba msamaha, Harrison na rafiki yake waliyeshirikiana kuandaa ajali feki, walikuwa na kesi ya kujibu mahakamani ambapo pia walitakiwa kueleza mahali walipoipata
maiti waliyoitumia. Baada ya kumaliza kuzungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali, Harrison, familia yake na ndugu zake walitoka kwenye ukumbi wa mikutano. Walipofika nje, wote walishtuka baada ya kuwakuta polisi kadhaa wenye silaha wakiwa wanamsubiri Harrison.
Wakamfunga pingu na kuondoka naye mpaka kwenye Kituo cha Polisi cha Miami alikotakiwa kutoa maelezo ya kutosha juu ya mahali alikoipata maiti waliyoitumia kuandaa ajali feki. Alipomtaja rafiki yake waliyeshirikiana kwenye tukio hilo, naye alienda kukamatwa siku hiyohiyo. ***
SIRI aliyoificha Harrison kwa kipindi kirefu inafichuka. Inabainika kwamba kumbe hakufa bali alimkimbia Linda kabla hawajafunga ndoa, kisha akatengeneza ajali feki ambayo ilionesha kwamba amekufa.Akakimbilia kwenye Msitu wa Tongass kumsaka malkia wa masokwe.
Baada ya miaka mingi kupita, akiwa tayari ameshamuoa malkia wa masokwe, anaamua kurejea nyumbani kwao ambapo ujio wake unasababisha kizaazaa kikubwa.
Baadaye anaeleza ukweli na kuwaomba radhi watu wote kwa kilichotokea. Kikao cha kifamilia kinafanyika na kuombana msamaha.
Baadaye Harrison anaitisha mkutano wa waandishi wa habari na kueleza ukweli lakini muda mfupi baada ya kumaliza kueleza kila kitu, anawekwa chini ya ulinzi na askari wenye silaha.
Askari hao wenye silaha wakamfunga pingu na kuondoka naye mpaka kwenye Kituo cha Polisi cha Miami alikotakiwa kutoa maelezo ya kutosha juu ya mahali alikoipata maiti waliyoitumia kuandaa ajali feki, kama alivyoeleza mbele ya waandishi wa habari.
Alipomtaja rafiki yake waliyeshirikiana kwenye tukio hilo, Daktari Rogers ambaye ndiye aliyefanikisha mpango wa kupatikana kwa maiti, naye alienda kukamatwa siku hiyohiyo na kuunganishwa na Harrison, wakawekwa nyuma ya nondo.
Baada ya wote wawili kukamatwa na kupelekwa mpaka kwenye Kituo Kikuu cha Polisi cha Miami, taratibu za kuwaburuza mahakamani zilianza kufanywa haraka iwezekanavyo. Shinikizo kutoka kwa viongozi wa
jeshi la polisi nchini humo lilikuwa kubwa kwani walijua wakiwaachia bila kuwachukulia hatua yoyote, wananchi watawadharau na hadhi yao mbele ya jamii itashuka sana.
Hata hivyo, kwa kuwa mahojiano aliyokuwa akiyafanya Harrison na waandishi wa habari yalionekana na watu wengi, mawakili wengi kutoka pande mbalimbali za nchi hiyo walijitokeza kutaka kumsaidia. Kila
mmoja alijua wakati anafanya kosa hilo, hakuwa sawa kiakili na ndiyo maana alifikia hatua ya kufanya tukio la ajabu kiasi hicho.
Gumzo nchini Marekani likawa ni habari ya Harrison ambapo kila mtu alikuwa akisema lake. Wanaharakati wa haki za wanawake, walikilaani mno kitendo cha Harrison kumkimbia Linda kanisani wakati kila kitu kilishakamilika. Wakasisitiza kwamba alikuwa na nafasi ya kumweleza ukweli kuliko mateso aliyomsababishia.
Hata hivyo, kwa sababu mwenyewe alikiri kufanya makosa na kuwaomba radhi wote aliowakosea akiwemo Linda, baadhi walimsamehe ingawa kuna kundi dogo bado liliendelea kumsakama kwa kitendo alichokifanya.
Harrison aliendelea kutawala kwenye vyombo vya habari, runinga, redio na magazeti vyote vikawa vinazungumzia kwa kina mazungumzo yake aliyoyafanya na waandishi wa habari na hatua ambazo jeshi la polisi lilimchukulia kutokana na alichokifanya. Wazazi na ndugu zake pamoja na ndugu wa Linda walikuwa pamoja na Harrison kwani walikubali kuupokea msamaha wake kwa dhati.
Angel ndiyo alikuwa na hali mbaya zaidi kutokana na kukamatwa kwa mumewe, akawa analia muda wote, hali iliyowapa kazi ya ziada mama yake Harrison, bibi na babu yake. Alikuwa na wasiwasi mkubwa kuwa
Wakawa wanambembeleza na kumweleza kuwa kila kitu kitapita, wote wakawa wanashinda nje ya Kituo Kikuu cha Polisi cha Miami wakijaribu kutafuta njia ya kumuwekea dhamana. Hata hivyo, kutokana na uzito wa kesi iliyokuwa inamkabili, hakupata dhamana kwa urahisi. Siku ya kwanza ikapita wakiwa nyuma ya nondo.
Siku iliyofuata, kesi yao ilisomwa kwa mara ya kwanza mahakamani ambapo Harrison na mwenzake walikuwa wakikabiliwa na mashtaka matatu; kumuua mtu kisha kutumia maiti yake kuudanganya ulimwengu kwamba ni Harrison, kupanga njama na kufanya udanganyifu.
Timu ya mawakili watano walijipanga kuwatetea Harrison na mwenzake na baada ya kesi hiyo kutajwa, mawakili hao ambao awali walifanya mazungumzo ya kina na Harrison pamoja na mwenzake, Dokta Rogers wakiwa mahabusu.
Kesi ilipoanza kunguruma, mawakili hao walianza kuwatetea wateja wao. Wakaieleza mahakama kwamba hawakumuua mtu yeyote kama mashtaka yao yalivyokuwa yanasema bali maiti waliyoitumia ilichukuliwa kutoka kwenye mochwari ya hospitali ambayo Rogers alikuwa akifanyia kazi.
“Mtukufu hakimu, maiti iliyotumika ilikuwa imekaa zaidi ya siku nne ndani ya mochwari na mipango ilishaanza kufanywa ili ikazikwe na manispaa. Hivi hapa ni vithibisho vyake,” alisema wakili mmoja huku akiweka mezani cheti cha kifo cha maiti iliyotumika.
Wakili mwingine alieleza kuwa wakati mteja wao anafanya yote hayo, hakuwa sawa kiakili kutokana na kushinikizwa kumuoa mwanamke ambaye hakuwa akimpenda kutoka ndani ya moyo wake. Kesi iliendelea
kuunguruma kwa saa kadhaa huku pande mbili za mawakili wa upande wa serikali na wa upande wa Harrison na mwenzake wakivutana.
Mpaka muda wa mahakama unaisha, tayari Harrison na mwenzake walikuwa wameyapangua mashtaka ya mauaji na kubakiza mashtaka mawili ya kupanga njama na udanganyifu ambayo hata hivyo, kisheria yalikuwa na dhamana. Taratibu zikafanywa na ndugu zao kisha wote wawili wakaachiwa kwa dhamana.
Ilikuwa ni furaha iliyoje kwa Angel na familia nzima ya Harrison. Akakumbatiana na ndugu zake kwa furaha na kurudi hadi nyumbani kusubiri siku nyingine ya mashtaka yao kusomwa. Habari hiyo pia
ilitangazwa sana na vyombo vya habari, jina la Harrison likazidi kuwa maarufu midomoni mwa watu huku mauzo ya kitabu chake cha Queen of Gorillas yakizidi kuongezeka.
Kila mtu alikuwa na hamu ya kukisoma kitabu hicho ambacho kilikuwa kinaelezea jinsi Harrison alivyokutana na malkia wa masokwe kwa mara ya kwanza. Mauzo hayo yalizidi kuitunisha akaunti yake na kumfanya apate fedha nyingi.
Siku zilizidi kusonga mbele, hatimaye tarehe ya kutajwa tena kwa kesi iliyokuwa ikimkabili Harrison iliwadia. Wakaenda tena mahakamani ambapo kesi ilianza kunguruma huku umati mkubwa wa watu wakiwa wamehudhuria mahakamani sambamba na waandishi wa vyombo vya habari. Katika hali ambayo wengi hawakuitegemea, hakimu alipoisoma kesi hiyo, mwanasheria mkuu wa serikali aliwasilisha hati maalum kutoka kwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali ya Marekani (DPP), James
Conrad na kuieleza mahakama kuwa baada ya kuupitia mwenendo mzima wa kesi hiyo na mazingira ambayo tukio hilo lilitokea, aliamua kuwafutia mashtaka Harrison na Rogers.
Hakimu akagonga nyundo mezani na shangwe za hapa na pale zikatawala mahakamani, Harrison akawa anakumbatiana na mawakili wake pamoja na ndugu zake na mashabiki wengi waliokuwa wamefurika
mahakamani. Hoihoi, nderemo na vifijo vikatawala eneo lote la mahakama mpaka umati ulipoanza kuondoka kuelekea nyumbani kwa akina Harrison.
“Nakupenda sana mume wangu, narudia tena kukuhakikishia kwamba nitakupenda mpaka mwisho wa maisha yangu,” alisema Angel huku akitokwa na machozi ya furaha, akakumbatiana na Harrison kimahaba. Watu waliokuwa wamewazunguka wakawa wanashangilia kwa nguvu.
Huo ukawa mwanzo wa maisha mapya ya uhuru wa Harrison na familia yake. Waandishi mbalimbali waliendelea kumtembelea nyumbani kwa mama yake na kumhoji maswali mbalimbali kuhusu ugumu alioupata mpaka alipofanikiwa kumpata malkia wa masokwe. Ilikuwa ni simulizi ya mapenzi iliyomsisimua kila aliyeisikia.
Baada ya wiki moja, Harrison na mkewe walianza maandalizi ya safari ya kwenda Tanzania kumtafuta baba mzazi wa Angel na kuijua vyema asili ya msichana huyo ambaye sasa alikuwa ni mke wake halali, akiwa na baraka zote kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki wa Harrison. ***
Baada ya kuficha siri kwa kipindi kirefu juu ya mahali alipokuwa amejificha, hatimaye siri inafichuka kwamba kumbe Harrison hakufa kama watu wote walivyokuwa wanaamini. Linda ndiyo anakuwa wa kwanza kugundua kuwa kumbe Harrison alitengeneza ajali feki kisha akakimbilia kwenye Msitu wa Tongass kumsaka malkia wa masokwe.
Anaumia sana kuujua ukweli huo na anafuatilia nyendo zake kimyakimya mpaka alipofanikiwa kumkuta nchini Canada. Kufichuka kwa siri hiyo kunazusha tafrani ya hali ya juu. Harrison anarejea nyumbani kwao akiwa na mkewe na mtoto wao na kila anayemuona anahisi amekutana na jini.
Baadaye anaeleza ukweli na kuwaomba radhi watu wote kwa kilichotokea. Kikao cha kifamilia kinafanyika na kuombana msamaha na Linda kisha anaenda kuzungumza na waandishi wa habari kueleza ukweli wa tukio lote. Sakata
linakuwa kubwa kwani Harrison na rafiki yake wananaswa na mkono wa sheria ingawa kwa bahati nzuri, wanatetewa na mawakili wazoefu kisha wanaachiwa huru.
Anaungana tena na familia yake na mipango ya kusafiri mpaka Tanzania kumtafuta baba mzazi wa mkewe, Angel inaanza.
Baada ya wiki moja, Harrison na mkewe walianza maandalizi ya safari ya kwenda Tanzania kumtafuta baba mzazi wa Angel na kuijua vyema asili ya msichana huyo ambaye sasa alikuwa ni mke wake halali, akiwa na baraka zote kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki wa Harrison.
Baada ya maandalizi yote kukamilika, Harrison, mkewe na mtoto wao, Harvey Junior walisindikizwa na ndugu jamaa na marafiki mpaka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Miami (MIA). Kwa kuwa tayari walishakata tiketi za ndege, waliingia kwenye ukumbi maalum wa kusubiria ndege. Mzee Lewis, mkewe na Skyler, wao hawakutaka kuondoka mpaka wahakikishe Harrison na mkewe wameshapanda ndege.
Wakakaa nao sehemu ya kusubiria ndege mpaka matangazo yalipoanza kusikikia kupitia vipaza sauti vilivyokuwa uwanjani hapo, yakiwataarifu abiria wa ndege namba 876Q, Airbus 380 mali ya Kampuni ya Travelocity kujiandaa kuingia kwenye ndege.
Harrison alikumbatiana na babu yake, bibi yake kisha mama yake mzazi, Skyler ambaye alimpa baraka zote na kumuombea dua katika safari yake.
“Naamini Mungu atawasimamia, nawaombea muende salama, mfanikiwe kumpata mzee Charwe kisha mrudi salama kuendelea na maisha yenu ya ndoa, nawapenda sana,” alisema Skyler huku akiwakumbatia Harrison na mkewe, Angel. Baada ya kumaliza kuagana na kutakiana heri ya safari, Harrison na mkewe waliingia sehemu ya ukaguzi wa abiria na mizigo uwanjani hapo.
Taratibu zote za kiusalama zilipokamilika, waliruhusiwa kwenda mpaka mahali ndege ilipokuwa imesimama ikisubiri abiria. Harrison akiwa amembeba mwanaye Harvey Junior na kumshika mkono mkewe, Angel, walitembea taratibu mpaka kwenye ngazi, wakapanda na kuingia ndani ya ndege, wakaenda kwenye siti zao na kukaa huku kila mmoja akiwa kimya.
Angel alikuwa akijihisi kama yupo ndotoni kwani tangu alipopata akili zake timamu, hakuwahi kudhani kwamba ana ndugu. Alishaamini kwamba masokwe waliokuwa wakimlea, kumlinda na kumtunza tangu alipokuwa mdogo ndiyo ndugu zake. Mawazo mengi yaliendelea kupita ndani ya kichwa chake, akijiuliza baba yake yukoje, sura yake ikoje na kama anao watoto wengine zaidi yake, wako wapi na wana umri gani.
Wakati mawazo yakiendelea kupita kwenye kichwa cha Angel, Harrison naye alikuwa akiwaza ya kwake. Alimshukuru sana Mungu wake kwa kufanikiwa kulimaliza salama sakata la Linda. Alijiona ni mwenye bahati ya kipekee kwa kufanikiwa kumaliza kila kitu kwa amani.
Sauti laini ya mhudumu wa ndege iliyokuwa ikisikika kupitia vipaza sauti vilivyokuwa ndani ya ndege ikiwahimiza abiria wote kufunga mikanda, ndiyo iliyowazindua wanandoa hao kutoka kwenye dimbwi la mawazo. Harakaharaka Harrison alimsaidia mkewe kumfunga mkanda kisha na yeye akajifunga na kumpakata vizuri mtoto wao, Harvey Junior.
Ndege ikaanza kujongea taratibu kuelekea kwenye njia za kurukia (runways). Baada ya muda mfupi, tayari ilishakuwa imegeuka kuelekea upande wa kurukia, ikawa inaongeza kasi kwa kadiri muda ulivyokuwa unaenda. Ikakimbia kwa kasi mpaka ilipokaribia mwisho wa uwanja, taratibu ikaiacha ardhi ya Miami na kupaa angani, ikapotelea mawinguni.
Harrison na mkewe waliendelea kuzungumza mambo mbalimbali, wakitaniana na kuchekeshana mara kwa mara kama ilivyokuwa kawaida yao. Baada ya takribani saa nane angani, sauti ya mhudumu ilisikika kwa mara nyingine ikiwataka abiria kufunga mikanda kwani ndege ilikuwa ikijiandaa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.
Wote walifunga mikanda kisha kwa kupitia madirisha madogo ya ndege hiyo, wakawa wanaangalia mandhari ya Jiji la Dar es Salaam. Ndege ikaanza kutua, baada ya dakika kadhaa, tayari ilishasimama na milango ikafunguliwa. Abiria wakaanza kuteremka, wakiwemo Harrison, mkewe na mtoto wao.
Kila kitu kilikuwa kigeni kwao kwani hakuna aliyewahi kufika Tanzania kabla, kwa msaada wa kitabu chenye ramani ya Tanzania kilichotengenezwa maalum kwa ajili ya kuwaongoza watalii, Harrison na mkewe waliondoka uwanjani hapo baada ya taratibu zote za kiusalama kukamilika kisha wakaelekea kwenye Hoteli ya The Southern Sun, katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
Dereva teksi aliyewapakiza, alikuwa akiwaelewesha vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na majina ya mitaa na vivutio vingine vilivyopo jijini Dar es Salaam ikiwemo sanamu ya askari iliyopo katikati ya jiji. Wote walifurahia sana kufika Tanzania, nchi ambayo walikuwa wakizisikia sifa zake nzuri kupitia vyombo vya habari.
Siku iliyofuatia, kwa kutumia maelezo yaliyokuwa kwenye kitabu maalum cha watalii, Harrison na mkewe waliwahi kuamka na kukodi teksi iliyowapeleka mpaka Stendi Kuu ya Mabasi ya Mikoani, Ubungo. Kwa kuwa waliwahi, walipouliza kwa wapiga debe kituoni hapo, walielekezwa kwenye basi la Zuberi lililokuwa linakwenda Bukoba. Kwa bahati nzuri, walifanikiwa kupata siti mbili kwenye basi hilo, wakalipa nauli na kuanza kusubiri muda wa basi kuanza safari. Kila kitu kilikuwa kigeni kwao kuanzia utaratibu uliokuwepo kwenye stendi hiyo, mpangilio wa mabasi, wingi wa abiria na mambo mengine mengi ambayo hawakuwahi kuyaona huko walikotoka.
Baada ya takribani dakika arobaini tangu walipopanda basi, safari ya kuelekea Bukoba ilianza. Wakawa wanaendelea kushangaa mambo mbalimbali waliyokuwa wanayaona njiani. Safari ilipamba moto, wakasafiri kwa kilometa nyingi wakikatisha kwenye mapori, misitu, milima na mabonde.
Baada ya kufika Kahama, ikiwa tayari ni usiku sana, kondakta wa basi walilopanda aliwapa taarifa abiria wote kwamba basi halitaendelea na safari hivyo watalazimika kulala hapo Kahama mpaka alfajiri ya siku ya pili, taarifa ambayo iliwashangaza sana Harrison na mkewe.
Walipohoji zaidi, waliambiwa kuwa kulikuwa na tishio la kutekwa na majambazi kwani tayari ilikuwa ni usiku sana na kipande cha barabara kilichobakia kabla ya kufika Bukoba kilikuwa na msitu mnene ambao ulikuwa ukitumika kama maficho ya majambazi.
“Isitoshe barabara ni mbaya sana, hatuwezi kuendelea na safari usiku huu, tusipotekwa na majambazi basi huenda tukapata ajali. Tunafanya hivi kwa sababu ya usalama wa abiria wetu,” kondakta aliwafafanulia, ikabidi wakubaliane naye. Kama ilivyokuwa kwa abiria wengine, walilazimika kuteremka kwenda kutafuta vyakula.
Vyakula vingi vilivyokuwa vinauzwa kwenye mji huo vilikuwa vigeni kwao lakini kwa kuwa walikuwa na njaa na hakukuwa na uwezekano wa kupata vyakula walivyovizoea, iliwalazimu kula hivyohivyo. Baada ya kushiba, walirudi kwenye basi na kulala humohumo kama walivyoelezwa na kondakta.
Kutokana na uchovu waliokuwa nao, walipitiwa na usingizi mpaka alfajiri ya siku ya pili. Kulipopambazuka tu, waliendelea na safari kwa kupitia Barabara ya Runzewe na Nyakanazi. Baada ya safari ngumu, hatimaye waliwasili kwenye mji uliokuwa umetawaliwa na uoto wa asili wa rangi ya kijani, ukipambwa na migomba mingi.
“Haya tumefika Bukoba jamani, kila mmoja achunge mizigo yake wakati wa kuteremka,” kondakta aliwaambia abiria, Harrison na mkewe wakaanza kuweka mizigo yao vizuri huku wakiendelea kushangaa mandhari tulivu na ya kuvutia ya Mji wa Bukoba. Hatimaye basi la Zuberi walilokuwa wamepanda liliwasili kwenye Stendi Kuu ya Bukoba, abiria wote wakateremka, wakiwemo Harrison, mkewe na mtoto wao. *** Nisingependa kumaliza hadithi hii ya leo bila kukumbusha jambo muhimu la kutoa maisha yako kwa Mungu. Maisha tuliyonayo hapa duniani ni mafupi sana, yanapita kama maua yachanuavyo na kunyauka. Wengi unaowafahamu wamekufa lakini wewe unapumua, ni vyema basi kufikiria maisha baada ya kifo.
Kila siku jiulize: “Hivi nikifa leo nitakwenda jehanam au peponi?” Kila mmoja wetu analo jibu lake, bila shaka sote tungependa kwenda peponi. Kama hivyo ndivyo, basi tiketi ya kwenda huko ni matendo mema na kujiepusha na uovu. Tukumbuke mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele.
BAADA ya safari ndefu ya hadithi hii ya Queen of Gorillas (Malkia wa Masokwe), hatimaye leo tumefikia sehemu ya mwisho. Tumeona jinsi siri aliyoificha kijana Harrison kwa kipindi kirefu na kuudanganya ulimwengu kwamba amekufa ilivyofichuka na kuishangaza dunia nzima. Ukweli unafahamika kwamba kijana huyo hakufa bali alimkimbia Linda kanisani kwani hakutaka kufunga naye ndoa kwa sababu hakuwa akimpenda kama alivyokuwa akimpenda malkia wa masokwe. Baada ya kila kitu kuwa hadharani, kijana huyo anaomba radhi kwa kila mtu. Sakata linakuwa kubwa kwani Harrison na rafiki yake wananaswa na mkono wa sheria ingawa kwa bahati nzuri, wanatetewa na mawakili wazoefu kisha wanaachiwa huru. Harrison na mkewe wanasafiri pamoja na mtoto wao, Harvey Junior mpaka nchini Tanzania. Lengo lao ni kwenda kumtafuta mzee Abdulkarim Charwe, baba mzazi wa Angel ambaye waliambiwa kwamba anaishi Bukoba, Tanzania. Tayari wameshawasili nchini Tanzania na kusafiri kwa basi hadi Bukoba.
Baada ya kuwasili mjini Bukoba, Harrison na mkewe walianza kuwauliza wenyeji kama kuna mtu aliyekuwa akimfahamu mzee
Abdulkarim Charwe. Kutokana na umaarufu aliokuwa nao mzee huyo kwa sababu ya historia ya maisha yake aliyokuwa anaipitia, hawakupata shida.
“Mnamuulizia yule mzee Charwe aliyekuwaga Ulaya? Twendeni niwapeleke,” alisema mwanaume mmoja kwa lafudhi ya Kihaya,
akionekana ametoka shambani, begani akiwa na mkungu wa ndizi na jembe. Akaushusha mzigo wake na kuanza kuwaongoza
Harrison na mkewe mpaka nje kidogo ya mji.
“Mnaiona ile nyumba pale? Ndipo anapoishi Charwe lakini sijui kama mtaelewana naye kwani tangu afiwe na mkewe na mwanaye
miaka mingi iliyopita, amekuwa kama kichaa,” alisema mwanaume huyo huku akiwaonesha kwa kidole mahali palipokuwa na
kijumba kidogo cha bati, kilichozungukwa na migomba mingi.
Harrison na mkewe walitazamana kama wasioamini walichokisikia na walichokiona. Ilikuwa vigumu kwao kuamini kwamba daktari
mashuhuri aliyefanya kazi mpaka Makao Makuu ya Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO), jijini Geneva, Uswisi ndiyo
alikuwa akiishi kwenye kibanda hicho.
Hata hivyo, walipiga moyo konde na kusonga mbele, wakasogea mpaka kwenye mlango wa kijumba hicho, wakapokelewa na
harufu nzito ya uvundo kutoka ndani. Kila mmoja akashika pua yake.
Harrison alibisha hodi huku mkewe akiwa nyuma yake lakini hawakuitikiwa, ikabidi asukume mlango kwa tahadhari kubwa na
kuingia ndani, walichokutana nacho kiliwasikitisha mno. Mwanaume mzee aliyekuwa na mvi nyingi, mwili wake ukiwa umedhoofika
mno, alikuwa amelala juu ya kitanda huku akionesha kutokuwa na nguvu hata za kuinuka.
Harrison alipojaribu kumsemesha, alifumbua macho na kuanza kuwatazama mmoja baada ya mwingine huku akishangaa ni akina
nani na wamefikaje hapo. Kwa taabu alifumbua mdomo wake na kuwauliza, Harrison akaanza kwa kujitambulisha kisha
akamueleza kuwa walikuwa wakimtafuta mzee Abdulkarim Charwe. Kwa taabu, mzee huyo aliitikia kwamba ni yeye, akamuomba
amsaidie kuamka kitandani na kuegemea ukutani. “Mnasemaje na mmelijuaje jina langu,” alisema mzee huyo huku akimkazia macho Angel kama anayejaribu kukumbuka kitu
kichwani mwake. Harrison akamuuliza kama alikuwa anamfahamu Charlotte Charwe. Swali hilo lilizidi kumshtua mzee huyo,
akazidi kuwakazia macho wote wawili, akashusha pumzi ndefu kisha akamtazama tena Angel.
Machozi yakaanza kumtoka kama anayekumbuka kitu. Akamjibu Harrison kuwa huyo Charlotte alikuwa ni mwanaye wa kipekee
aliyekufa na mkewe, Anganile kwenye ajali ya ndege iliyotokea eneo la Tongass, kwenye mpaka wa Marekani na Canada miaka
mingi iliyopita. Alilia kwa uchungu sana huku bado akiendelea kumtazama Anganile.
Kabla hata hajasema chochote, Harrison alianza kumueleza kwamba mwanaye Charlotte hakufa kwenye ajali hiyo bali aliangukia
kwenye msitu mkubwa wa Tongass na kulelewa na masokwe mpaka yeye alipokutana naye. Akamueleza kwamba msichana
aliyekuwa anamtazama mbele yake ndiyo alikuwa Charlotte, jambo lililomshtua sana mzee huyo aliyekuwa kwenye hatua za
mwisho za uhai wake.
Kwa kuwatazama sura, kweli Angel na mzee huyo walikuwa wamefanana sana, kuanzia macho, pua, mdomo mpaka jinsi sura zao
zilivyoumbika. Akawa analia kwa uchungu huku akiwa amemkumbatia Angel (Charlotte) kwa nguvu. Akamwambia Harrison
kwamba inawezekana Mungu alimuweka hai mpaka muda huo kwa makusudi ili asife mpaka atakapomuona binti yake huyo.
Harrison akamsimulia kila kitu jinsi alivyomuokota msichana huyo msituni, alivyotoroka naye na kuamua kuishi naye kama mume na
mke kwa uhalali. Mzee huyo alifurahi mno, akawapa baraka zote na kuwatakia maisha mema yenye mafanikio na furaha. Akaomba
amshike mjukuu wake, Harvey Junior. Baada ya kumshika kidogo, aliomba apokewe kisha akaomba maji ya kunywa.
Kwa kuwa Angel (Charlotte) alikuwa na chupa ya maji, alimpa baba yake huku akitokwa na machozi. Alipokunywa tu,
alitabasamu kisha akalala na kufumba macho huku akiwa bado ametabasamu, akatulia kimya. Tayari roho na mwili wake
vilishatengana. Harrison na Charlotte wakaanza kulia kwa sauti, kitendo kilichowakusanya majirani wengi.
Msiba ukafanyika kwa mila za watu wa Bukoba na kesho yake, mzee huyo alizikwa nyuma ya nyumba yake, katikati ya migomba
huku kila mmoja akiliona tukio hilo kama muujiza kwamba baada ya kuteseka kwa kipindi kirefu, mzee huyo alikufa muda mfupi
baada ya kumuona binti yake ambaye aliamini ameshakufa.
Harrison na Charlotte walikaa kwa siku arobaini mjini Bukoba, baada ya hapo walienda kulijengea kaburi la mzee Charwe vizuri
kisha wakasafiri na mtoto wao kurejea Miami, Marekani walikowasimulia watu wote walichokutana nacho. Kila mtu aliyesikia
kilichotokea alisikitika sana, mzee Lewis akaitumia nafasi hiyo kumuelezea Harrison historia ya maisha ya baba yake, Harvey.
Alimueleza jinsi alivyokutana na baba yake aliyekuwa akikimbia machafuko yaliyotokea nchini kwao, Liberia baada ya Rais Samuel
Doe kupinduliwa na waasi na kusababisha wananchi waanze kupigana wao kwa wao. Alimsimulia jinsi baba yake alivyojaribu
kutorokea Marekani lakini akaishia kupata ajali mbaya baharini na kuokolewa na wasamaria wema waliompeleka kwenye hospitali
aliyokuwa akifanyia kazi mzee huyo.
Akaeleza kila kitu kilichoendelea, jinsi walivyoishi pamoja kwa amani na upendo na mwisho jinsi kijana huyo alivyoanzisha uhusiano
wa kimapenzi ambao ndiyo ulisababisha Harrison azaliwe. Akamueleza kila kitu mpaka jinsi alivyosababisha kifo cha kijana huyo
kwa bahati mbaya baada ya kugundua ana uhusiano wa kimapenzi na binti yake, Skyler.
“Nilishamuomba sana Mungu anisamehe na leo nakuomba na wewe unisamehe kwani halikuwa kusudio langu,” alisema mzee huyo
huku akipiga magoti mbele ya Harrison. Kila mmoja aliyekuwa ndani ya nyumba hiyo, alikuwa akilia kwa uchungu kwani ilikuwa ni
historia chungu lakini ambayo ilimsaidia Harrison kuifahamu vyema asili yake.
Kwa moyo mkunjufu, Harrison alikubali kumsamehe mzee huyo na wakakubaliana kufungua ukurasa mpya wa maisha yao.
Wakaanzisha mfuko maalum wa kuwasaidia watu wenye matatizo katika Miji ya Monrovia, Liberia ilipokuwa asili ya baba yake
Harrison, Harvey na mjini Bukoba, ilikokuwa asili ya mkewe, Charlotte.
Wakaendelea kuishi kwa amani, upendo na furaha huku wakisahau yote yaliyopita maishani mwao. Harrison na Charlotte walizidi
kupendana na baada ya miaka mitatu, walibarikiwa kupata mtoto wa pili waliyempa jina la Abdulkarim. *** Ndugu wasomaji wangu, ninawashukuru sana kwa kuwa nami bega kwa bega tangu mwanzo wa hadithi hii, mkinishauri
na kunikosoa pale nilipokwenda tofauti. Niliyachukua mawazo yenu na kuyafanyia kazi na ndiyo maana nikafanikiwa
kuifikisha hadithi hii hapa ilipofika.
Naamini mmejifunza mengi na kuburudika vya kutosha, yale yaliyo mema yachukueni na kuyafanyia kazi lakini yale
yasiyofaa mbele za Mungu na wanadamu, hampaswi kuyatenda. Ninawaalika tena mjiunge nami Jumatatu katika
Msichoke kunipa ushauri kwani kufanya hivyo kunanifanya nizidi kukomaa zaidi siku hadi siku. Niwaeleze jambo moja
muhimu ambalo hakika nitakuwa sijatenda haki mbele yenu na kwa Mungu pia kama sitalisema. Ukweli ni kwamba
NINAWAPENDA SANA. Mungu awabariki sana. Ahsanteni.
James Makabi alishangazwa na kitendo cha mtu mwenye kofia kubwa ya pama kumfuatilia kwa namna ya kuvizia. Mwanzo hakuwa na wazo lolote juu yake lakini akashangazwa na kitendo cha kiumbe huyo mrefu kupita kila anapopita. Wasiwasi ulianza kumuingia baada ya kugundua kuwa jamaa huyo alikuwa makini na hakutaka kabisa James agundue kuwa anafuatwa. Kila alipogeuka nyuma James alimshuhudia yule mtu akijifanya aidha kununua bidhaa, kuongea na simu au hata kujikuna pale alipokosa kisingizio cha haraka. Akaamua kubadili njia na kufuata barabara inayoelekea mtaa wa Kongo. Baada ya kutembea dakika kadhaa bila kumuona yule mtu akaamini kuwa alikuwa na wasiwasi wa bure. Akaamua kupita kichochoro kidogo ambacho kinatokea mtaa wa Lindi. Jua lilikuwa limepoteza ukali pia nuru yake ilianza kufifia, likafanya rangi ya kaa la moto, rangi ile ikaambukiza hata vidimbwi vidogo kwani navyo vilibadilika na kuwa na rangi hiyo. James akapiga hatua zaidi huku akielekea kituo cha daladala kilichoko mtaa wa Lindi. Akasimama pale kwa muda akisubiri gari linaloelekea Kiwalani. Akiwa ameegemea nguzo ya jengo moja ambayo kwa upande mwingine iliegemezwa meza ya kuuzia magazeti mara akaliona gari lenye ufito wa kijani ubavuni. Akaungana na abiria wengine ambao walikuwa wanatimua mbio bila shaka ikiwa ni kwa lengo la kuwahi sehemu ya kuketi. Akiwa miongoni mwa abiria waliokosa siti akashika bomba la juu ambalo watu wote waliosimama walikuwa wamelishika. “Oyaa, kaka mkubwa mwenye shati jeupe hapo geuka upande wa pili,”alipiga kelele konda huku akimnyooshea kidole James ambaye hakusita kugeuka. Alipogeuka ndipo alipopatwa na mshtuko wa mwaka! Yule mtu ambaye dakika kadhaa zilizopita alikuwa anamkimbia alikuwa amekaa siti ya nyuma kabisa akisoma gazeti. Kwa kasi ya aina yake James akajitoa kwenye msitu wa watu na kushuka kwenye gari. “Hawa wengine wezi tu,” alilalamika mmoja wa abiria ambaye alionekana kukerwa na kitendo cha James huku akiungwa mkono na abiria kadhaa, ambao walirusha maneno mawili matatu ya kashfa. “Abiria jikagueni kama kila mmoja simu yake ipo.” Aliongeza konda “Aaa, amechemsha huyo naona anatafuta sehemu nyingine…..” Mjadala ukaendelea zaidi ya hapo kama kawaida ya mijadala ambayo huibuka kwenye daladala. Akatembea haraka haraka akielekea mtaa wa Kipata, mara kwa mara alikuwa anageuka nyuma kuangalia kama bado anafuatwa na yule mtu mwenye kofia ya pama, hakumuona. Hilo la kutomuona bado halikuweza kumuondolea hofu na wasiwasi aliokuwa nao. Lakini nini hasa kilimfanya aingiwe na hofu? Ghafla alijiuliza swali ambalo lilimfanya asitishe mbio zake hizo. Kama gerezani alishaachiwa kwa msamaha wa Rais, haiwezekani aingiwe na hofu wakati hana kosa, akapiga moyo konde na kutafuta kituo kingine cha daladala. Alijidanganya, alijidanganya sana kwani mawazo juu ya mtu yule mwenye kofia ya pama yaliendelea kumtesa. Kwanini anaviziwa? Lazima kuna jambo si la kawaida! Ni jambo gani? Alijikuta akipata wakati mgumu kwa maswali yasiyo na majibu. Huku akiendelea kutafakari akajikuta akikabiliana na giza ambalo lilishatanda maeneo mbalimbali ya jiji. Baada ya kutembea kwa muda mrefu huku akiwa hana uelekeo maalum aliamua kurejea tena eneo la Suwata lililoko mtaa wa Lindi ili apande gari linaloelekea Kiwalani. Akafika eneo hilo na kukuta kukiwa na abiria wachache jambo lililomshangaza. Akatoa simu yake aina ya siemens na kuangalia muda, “Khaa!” Akashtuka baada ya kukuta kuwa ni saa nne kasorobo. “Bila shaka Tamasha atakuwa amechoka kunisubiri, labda ajue nilipouficha funguo,” alijikuta akiwaza kabla hajaingia kwenye daladala. Akaileta tena kichwani picha ya mtu yule mwenye kofia ya pama. Ni mtu mrefu, mpana kiasi mwenye kutembea kwa umadhubuti, hata mwili wake ulionesha kuwa ni mtu madhubuti. Uso wake ambao hata akiwa mbali haukustahimili kuficha weusi ulikuwa umezungukwa na sharubu zilizofuatiwa na ndevu zilizopunguzwa kwa ustadi. Wakati ule anamfuata James na hata pale alipokuwa anasoma gazeti bado hakudiriki kubandua mawani yake nyeusi. Akiwa kwenye siti ya nyuma kabisa ya gari hakuacha kuikagua kila siti kwa macho, pia kila abiria aliyeingia alihakikisha kuwa anamuona. Akaridhika baada ya konda kujitoma ndani ya gari huku akifunga mlango. Gari likaondoka huku akiwa ameondokewa kabisa na hofu ya mtu yule mrefu mwenye kofia ya pama. Akajikuta akirudiwa na furaha yake ambayo ilipotezwa na mtu yule mkakamavu. Saa nne na robo (4.15) daladala likasimama maeneo ya Kijiwe samli. James akateremka huku akijilaumu kwa kuchelewa nyumbani kwa sababu za kipuuzi. Alijiona mjinga baada ya kuona amemuogopa mtu kwa kuhisi anamfuatilia. Hata kama angekuwa anamfuatilia bado alijiona kutokuwa na sababu ya kumuogopa kwani hata macho yalihukumu kuwa yule ni mtu mkwasi. Mavazi yake peke yake yangeweza kuwa mtaji wake wa biashara ndogondogo. Yule mtu alikuwa amevaa suti ya kijivu ambayo ni ya gharama kubwa. James aliwahi kuona suti kama hiyo ikiuzwa kwenye duka fulani mitaa ya samora kwa bei ambayo ni mara nne ya kiwango cha juu cha mshahara wa mwalimu. James akajikuta akijilaumu maradufu kwa kitendo cha kumuogopa mtu yule. “Wakati mwingine woga unaweza kukufanya uipige ngwara bahati bila kutarajia”, aliwaza huku akijihisi kuipiga teke bahati. Akajishangaa mwenyewe baada ya kutanabahi kuwa kwa mara ya kwanza katika maisha yake ameanza kuingiwa na woga. Kwanini amejikuta anamuogopa mtu ambaye hamfahamu? Mbona alipokuwa gerezani alikutana na watu wakorofi na wabaya sana lakini hakuwahofia na mara chache alipambana nao kitu kilichomjengea heshima na kuogopwa ndani ya gereza. Hakuwahi kuogopa kwenye maisha yake kama alivyoogopa ile siku aliyosimama mbele ya jaji kwa kosa la kusababisha ajali ambayo iliua makumi ya watu. Aliikumbuka vema siku hiyo kwani alikuwa anaendesha basi la abiria lililokuwa linatoka Dar es salaam likielekea Handeni huko Tanga. Hakukusudia kusababisha ajali hiyo na wala halikuwa kosa lake, kosa lilikuwa la muheshimiwa waziri wa Nchi, umaskini na majanga ambaye alikuwa anaendesha mwenyewe badala ya dereva wake tena akiwa amelewa chakari. Kesi iliposikilizwa waziri akashinda! Ni kawaida kwa nchi za kiafrika.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Yamepita…….. Akatembea taratibu akiupita ukumbi maarufu wa starehe unaojulikana kama Koyanga. Akaelekea mbele kidogo huku akisindikizwa na muziki nzito uliokuwa unasikika kutoka kwenye ukumbi huo wa starehe. Akakatisha kwenye kichochoro kidogo ambacho kilikuwa kinatenganisha baa ya Koyanga na nyumba iliyopakana na ukumbi huo. Baada ya kumaliza kile kichochoro akatembea hatua kama kumi, akaibukia mtaa mwingine na baada ya kuangalia upande wa kulia aliweza kuiona nyumba yake. Ilikuwa kama hatua thelathini za mtu mrefu kufika kwake. Mwenyewe hakuiita nyumba, alipenda kuita banda. Ilikuwa na chumba kimoja na sebule tu, wakati anakaribia kukamilisha chumba cha pili ndio akapatwa na balaa la kukamatwa baada ya ajali hiyo ya gari. Kwa mbali aliweza kuiona taa ya nje ikiwaka, akafurahi baada ya kubaini kuwa Tamasha atakuwa ameziona funguo pale zilipo. Akaufanya mwendo wake kuwa madhubuti zaidi huku akijisikia furaha moyoni. “Ndiyo maana nampenda huyu binti ana akili sana,” aliwaza James huku akihisi kama umbali wa nyumbani kwake umeongezeka kutokana na shauku ya kuonana na Tamasha. Alimpenda. Tofauti na matarajio yake, Tamasha alikuwa nje akihangaika na mapishi. Hakuna kizuizi kilichozuia macho ya James kuona jinsi kuku mkubwa aliyenona alivyojaa kwenye sufuria akiandaliwa. Hili likamshangaza kiasi kwani ndani hakuacha hata shilingi mia, kama si kuogopa kuonekana mtu aliyekosa ustaarabu angeuliza, “umempata wapi huyu kuku!?” Hakuuliza, alimpenda na kumuamini Tamasha. Alifahamu wazi kuwa lazima ataelezwa wapi alikompata kuku yule wa kienyeji katika wakati huu ambao wakazi wengi wa jiji la Dar es salaam wanakula miguu, utumbo na vichwa vya kuku. “Waooooh, karibu mpenzi,” Tamasha alimlaki mpenzi wake kwa furaha. “Oh, Ahsante dear, yaani ndo unaanza kupika saa hizi si ungepumzika tu!” “Ningeweza kupumzika kama si huyo mjomba aliyeko ndani, kuku kaja naye mwenyewe……..” James akamkatisha kwa swali la haraka. “Mjomba! Mjomba gani?” “Haraka ya nini mpenzi, we ndiye unaetakiwa kunitambulisha kwake. Si uingie ndani ukamuone kakaa muda mrefu sana anakusubiri.” Moyo wake ukapiga mlipuko wa hofu, akasahau kuwa walikuwa hawajasalimiana na Tamasha, hakujali kusalimiana kwani akili yake yote ilikuwa huko ndani kwa mtu aliyejitambulisha kama mjomba. Haraka haraka akajitoma sebuleni ili kumuona mjombake aliyekuja na kuku wa kienyeji. “Paah.” Moyo wake ulilipuka baada ya kumuona mtu mkakamavu mwenye kofia ya pama akiwa amekaa kwenye kochi kama nyumbani kwake. “Ooh! Karibu sana bwana James Makabi!” Aliongea yule mtu kwa sauti ya ujivuni. Alijikuta akishindwa kuongea lolote na kukaa kwenye kiti kilichoelekeana naye. Yule mtu akasimama na kumsogelea James kisha akampa mkono. Kwa moyo uliojaa hofu James akaupokea mkono ule, Jambo jingine! Ulikuwa mkono mgumu uliojaa ukakamavu kwelikweli. “Habari yako bwana James,” alisalimia mtu yule mkakamavu mwenye kofia ya pama. “Aah! Salama mjomba,” alilazimisha tabasamu baada ya kumuona Tamasha anaingia ndani, hakutaka mpenzi wake atambue walakini uliopo. Akaitumia fursa hiyo kuusanifu mwili wa yule jamaa kwa haraka. “Dear, naomba uende hapo Koyanga ukachukue soda kwa ajili ya mjomba…….”akakohoa kidogo kisha akaendelea “……muulize kwanza atakunywa soda gani?” “Aah, mjomba alishakataa soda, tena kakataa hata chakula kasema hata nikiandaa yeye hatakula kwani amekuja kwa ajili ya mazungumzo tu!” Alimaliza Tamasha.
“Ok, basi hakijaharibika kitu.” “Mi naondoka, hiyo mboga nitakuja kumaliza kutengeneza asubuhi.” “Leo hulali hapa?” “Leo ngumu dear si nilishakuambia nataka nimsindikize shangazi stendi kesho anaenda Mwanza?” “Oh, nilisahau dear.” “Kwa heri mjomba.” “Ahsante wasalimie nyumbani.” Baada ya Tamasha kuondoka yule mtu mrefu aliyevaa kofia ya pama akamgeukia James. “Naitwa Mjomba Masharubu……….”
* * * JOHN OSCAR alitembea taratibu kuelekea ofisi ya mhariri mkuu wa gazeti la MUUNGWANA. Alikuwa ni kijana mwenye kimo na mwili wa wastani. Alivaa shati jeupe, suruali nyeusi na viatu vyeusi ambavyo vilikuwa vimeng’arishwa vema kwa dawa. Alikuwa na mwaka mmoja tu kwenye fani ya uandishi wa habari, hii ilikuwa ni baada ya kuachishwa kazi jeshi la polisi ambako alitumikia kwa miaka mitano na kisha kutimuliwa kazi baada ya kutokea kashfa ya kutoroka mahabusu kwenye kituo alichokuwa anafanyia kazi. Hakuhusika na utorokaji huo na wala hakuwa kazini siku ya tukio, lakini msamiati wa dhana ya uwajibikaji ukamfanya yeye pamoja na askari wenzie wa kituo hicho kufukuzwa kazi bila kujali walikuwa kazini au vinginevyo. Panga hilo liliwakuta askari wa vyeo vya chini. Kufukuzwa kwake haukuwa mwisho wa maisha, ndipo akaamua kujiunga na chuo kimoja kinachotoa kozi za jioni za uandishi wa habari. Baada ya kumaliza kozi yake kwa ngazi ya stashahada ndipo akapata ajira ya muda kwenye gazeti hilo ambalo halikuwa na umaarufu mkubwa. Alikuwa mchapakazi nzuri kiasi ambacho alipendwa na mhariri mkuu wa gazeti hilo huku akichukiwa na baadhi ya waandishi ambao waliona wanaanza kupokwa umaarufu na heshima zao. Hata hivyo zilikuwa ni chuki ndogo na za chinichini ambazo hakuzitilia maanani. “Habari Jesca!” Alisalimia huku akiingia ofisi ya mhariri mkuu. “He, kaka John mbona juu juu! Hata hutulii tukasalimiana vizuri?” Alisikika Jesca. Hakujibu badala yake aliingia ndani moja kwa moja. Ofisi ya mhariri mkuu ilikuwa ndogo yenye mandhari ya kuvutia. Ndani kulikuwa na viti vinne kimoja ndani ya mkunjo wa meza ya nusu duara ambacho alikaa mhariri mkuu, kimoja kilikuwa mbele kabisa karibu na meza huku viwili vikiwa nyuma kama hatua tatu kutoka kile kilichotangulia.Pembeni kulikuwa na kabati kubwa la chuma lenye rangi ya fedha lililosheheni vitabu vya aina mbalimbali. Ukutani kulikuwa na kalenda mpya ambayo ilikuwa na picha za viongozi mbalimbali wa chama na serikali. Kama zilivyo ofisi nyingi za wahariri hii nayo ilikuwa na ngamizi ya kisasa aina ya Hp Compaq yenye sikrini bapa huku kukiwa na kicharazio cha rangi ya fedha ‘keyboard’ John alilakiwa na ubaridi mkali uliotokana na kiyoyozi ambacho kiliwekwa namba ya juu kulingana na afya ya mhariri huyo ambaye hupendelea hali hiyo ya hewa. Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuitwa na mhariri mkuu. Haikuwa mara ya kwanza kuingia ofisi hiyo, alikuwa anaingia mara kwa mara siku ambazo nafasi hiyo hukaimiwa na mhariri mkuu msaidizi ndugu Gideon Masatu ambaye alipenda sana kumtumia John kwenye kazi nyingi. Akamsalimia mkuu wake huyo wa kazi kabla ya kukaa kiti kimoja cha nyuma miongoni mwa viti vile viwili. “Oh, karibu ndugu John, keti hapo mbele usiwe na wasiwasi,” aliongea ndugu Kasim Jamali mhariri mkuu kwa sauti iliyojaa uchangamfu. “Ahsante mzee, shikamoo.” “Marahaba, tafadhali keti.” “Ahsante.” Akaketi na kumkazia macho mkuu wake wa kazi. Mzee Kasim alikuwa na kimo cha wastani ingawa unene ulimfanya aonekana kuwa mfupi. Kichwa chake kilikuwa kimesheheni nywele nyingi ambazo zilikuwa na mvi kiasi. Alikuwa anakaribia miaka sitini na mitano lakini bado alikuwa na afya madhubuti tofauti na wazee wa hirimu yake. Alikuwa amevaa kaunda suti nyeusi ambayo ilimkaa vema na kumfanya avutie. John, aliendelea kukaa kwa utulivu huku akisubiri alichoitiwa kwa shauku kubwa. Mhariri aliinua kichwa chake na kumkazia macho John. Kabla ya kuongea chochote akavuta saraka lililokuwa kwenye meza yake, akatoa kalamu na karatasi kisha akaanza kuongea bila kuandika chochote. “Ndugu John Oscar, ninayo furaha kubwa kukufahamisha kuwa ofisi yetu imekuchagua kwenda kwenye mkutano wa chama tawala cha MMD utakaofanyika makao makuu yake yaliyoko Magomeni.” Akatulia kidogo kisha akaendelea “… Hii ni nafasi kubwa na ya kipekee ambayo umepewa kutokana na umahiri wako katika fani hii pia ukiwa na sifa ya ziada ya kuwa mpigapicha nzuri. Nimekuita hapa kutokana na unyeti wa shuguli yenyewe na kile unachotakiwa kukifanya.” Akatulia na kumeza mate kabla ya kundelea tena. “… Kitu cha kwanza kuwa mwangalifu sana na aina ya picha utakazopiga, hakikisha unapata picha za maeneo yenye watu wengi na yasiyo na mianya. Tunapopiga picha za chama tawala hatutakiwi kuonesha nafasi zilizo wazi, hii ni kinyume kwa picha za vyama vya upinzani ambazo unatakiwa kupiga picha maeneo yenye mianya na watu wachache, hii hutuongezea heshima mbele ya serikali.” Akatulia tena na kumkazia macho John. “Nafikiri umenielewa.” “Sawa mkuu nimekuelewa.” “Hicho kipengere cha namna ya kupiga picha za chama tawala ndicho nilichokuitia, maagizo mengine utapewa na ndugu Masatu.” Akainuka kwenye kiti na kupeana mikono na mkuu wake wa kazi kabla hajaondoka ofisini humo. Akafungua mlango na kuingia kwenye chumba kidogo cha katibu muhutasi. “Sorry Jesca unajua nilikuwa na hofu ya kufukuzwa kazi ndiyo maana sikukusalimia vizuri wakati naingia.” “ha ha ha ha!” Akacheka kwa nguvu Jesca ukiwa ni ujanja wa kulazimisha jino lake la dhahabu lionekane. Alifanikiwa, maana Macho ya John yalitua kwenye jino hilo lenye mng’ao wa kipekee. “Vipi kulikuwa na usalama huko ndani?” Aliuliza Jesca. “Aaah, ni mambo ya kawaida tu, ni kuhusu mkutano mkuu wa MMD mwezi ujao.” “Hongera, nasikia kuna posho nzuri kule.” “Inatolewa na ofisi?” “Ofisi inatoa, pia chama nacho kinatoa chochote kwa vyombo vya habari ambavyo ni rafiki wa chama.” “Vyombo vya habari rafiki wa chama!!” Alistaajabu huku akiondoka eneo hilo. ***** II
“….. Huna sababu ya kuniogopa mimi ni mtu mwema, tena mwema sana kwako!” Aliongea Mjomba Masharubu kwa sauti nzito lakini yenye utulivu mkubwa huku akilazimisha upole ambao hakuwa nao. “Pamoja na wema wako kitendo cha kunifuata kwa kunivizia kimenipa hofu sana, pia nimeshangaa kwa jinsi ulivyoweza kupafahamu nyumbani kwangu na hata jina langu wakati mimi ndio mara ya kwanza nakuona!” Kwa sauti nzito Mjomba akacheka kidogo na kumkazia macho James. “Usiwe kama mtoto James, sio kila unayemfahamu anakufahamu na sio kila anayekufahamu unamfahamu, kuna watu wanaweza kukufahamu zaidi ya unavyojifahamu!” Akatulia tena na kufuta uso wake kwa kitambaa hku akibandika sigara mdomoni mwake kabla hajatoa kiberiti kidogo cha gesi. Pamoja na kauli hiyo nzuri ya kusisimua bado hakufanikiwa kuondoa mshangao katika nafsi ya James. Hapo kabla alimuogopa sana Mjomba, lakini muda huo akajikuta akiwa na shauku ya kutaka kujua mengi kuhusu mtu huyo pamoja na huo wema wake ambao amejisifu kuwa nao. “ James, Mimi nafahamu kuwa wewe ni dereva nzuri sana na umetoka gerezani hivi karibuni, kwa msamaha wa Rais kwani kifungo chako kilikuwa ni miaka mitano…..” akakohoa kidogo na kuvuta sigara yake funda tatu kwa utulivu mkubwa zaidi kama anayetafakari neno la kuongea kasha akaendelea,“….. Kutoka kwa msamaha wa Rais si jambo rahisi kama unavyofikiria ni lazima ufanyiwe mipango, mimi ndiye niliyekufanyia mpango mpaka ukapewa msamaha wa Rais.” Akatulia kidogo na kumpa nafasi ya kutafakari ujumbe huo mpya kabla ya kuendelea. Akainua macho na kumtazama Mjomba Masharubu usoni. Akakumbuka kitu! Alimuona siku ya kufunguliwa kwake lakini hakumtilia maanani, Mjomba hakuonesha dalili yoyote ya kuhusika kwake na msamaha huo. “Nafikiri unafahamu kuwa mambo ya hapa mjini ni kusaidiana, hivyo nami pia nimekuja kwako naomba msaada wako.” “Msaada upi ambao unahitaji kutoka kwangu?” Aliuliza James huku akiwa amepungukiwa na hofu iliyomtawala muda mfupi uliopita. “Kuna kijikazi kidogo nataka unisaidie, hata hivyo kutakuwa na bakhshishi nitakupa.” “Nafikiri ni bora unitajie hiyo kazi ili kupunguza dukuduku langu.” “Usijali ni kazi ndogo sana, ukishamaliza hiyo kazi kuna bakshishi ya nyumba, gari, shamba na pesa taslimu milioni mia mbili na hamsini” Akatumbua macho na kumtazama Mjomba Masharubu kwa mshangao huku nafsi yake ikiwa njia panda kama amuamini mtu huyo au vinginevyo. “Mia mbili hamsini milioni?” Aliuliza akitaka uhakika wa alichokisikia. “Usijali ni pesa ndogo sana hiyo, fedha ninazo hata nikitoa hicho kiasi ni kama sijapunguza chochote.” “Kazi gani?” Aliuliza tena James. “Utaifanya?” “Kwa kiasi hicho niko tayari kufanya kazi yoyote isipokuwa ushoga.” “Ha ha ha haaaaaaa..” Kwa mara ya kwanza tabasamu likachanua katika uso wa Mjomba Masharubu. “Unataka kuijua kazi yenyewe?” “Bila shaka, nawe unafahamu hilo” “Ok, kwanza chukua namba yangu ya simu ili ukikamilisha hiyo kazi uweze kunitafuta kwa ajili ya malipo yako,” “Poa, ngoja niisevu kwenye simu yangu.”
*
Ndani ya ukumbi wa KBT viongozi na wajumbe mbalimbali wa chama tawala MMD walikuwa wamekusanyika tayari kwa tukio maarufu ambalo linajulikana kama NATANGAZA NIA. Tukio hili hufanyika baada ya Katibu mkuu wa chama kupokea majina ya wanachama wote wenye nia ya kugombea uraisi. Hutajwa jina moja moja kisha mgombea hupewa nafasi ya kuthibitisha kwa mdomo kuwa ni kweli ameamua kuwania nafasi ya kugombea uraisi kupitia chama hicho, pia hupewa nafasi ya kuzungumza mawili matatu kwa wanachama wao, baada ya hapo huzinduliwa kampeni kwa wagombea ambao hupita mkoa hadi mkoa wakitafuta kuungwa mkono na wajumbe wa mkutano mkuu kwenye hatua ya mwisho . Ukumbi ulikuwa umepambwa kwa bendera za chama zenye rangi nyeupe na nyekundu huku katikati ya bendera kukiwa na alama ya msumeno. Nyimbo mbalimbali za kukisifu chama ziliimbwa, wanachama walionekana kuwa na furaha sana huku wakiwa wameficha hofu nzito katika nyoyo zao kwa kutojua nani atachukua hatamu ya kuongoza nchi na chama. waliita utaratibu huu kuwa mbio za kupokezana vijiti. Ni utaratibu ambao ulileta hofu kubwa kwani kila mmoja alikuwa na chaguo lake huku wengine wakitarajia vyeo iwapo Yule waliyempenda angebahatika kupata uongozi. Mijadala ya hapa na pale iliendelea huku kila mwananchi akijaribu kueleza hisia zake za nani anatamani awe mgombea wa chama hicho kikubwa chenye nguvu. Kuna wale ambao hawakuwa na makundi wao walikuwa wasikilizaji tu, hawa kwa kiasi kikubwa walikuwa ni wale wanaoangalia utendaji bora wa mtu atakayeteuliwa. Pamoja na mijadala hiyo yote hakuna aliyekuwa na uhakika nani na nani watagombea kutokana na usiri mkubwa uliogubika zoezi hilo. Yako baadhi ya majina ambayo yalitajwa tajwa lakini bado uhakika ulikuwa mdogo. Ghafla, lango kuu likafunguliwa
Ghafla, lango kuu likafunguliwa msafara wa viongozi waandamizi wa chama na serikali ukaanza kuingia. Ulinzi mkali ulikuwa umeongozana na msafara huo. Nyimbo za chama zikaanza kuimbwa shangwe na vigeregere vikahanikiza ukumbi, mayowe na mbinja vikachukua nafasi yake. Mwanamuziki maarufu wa bendi ya chama Alex Kilaza akaanza kutumbuiza nyimbo mbali mbali na kuwafanya wanachama walipuke kwa nderemo na vifijo. Baada ya muda kelele zikapungua na watu wakaanza kukaa kwenye nafasi zao. Zikaanza hotuba mbalimbali za viongozi wastaafu wa chama na serikali, nyingi zikisifu kukua kwa uchumi na kuondoka kwa umaskini bila kusahau mikakati ya muhula unaokuja pindi kitakapoingia madarakani,baada ya hapo ikafuata nafasi ya Katibu mkuu kusoma majina ya watu walioweka nia ya kugombea uraisi. “MMD hoyeeee, Ushindi upooooo, Wapinzani kwishaaaa.” “Kwishaaa, kwisha kabisa chinjia baharini….” Walijibu wajumbe kwa maneno ambayo yalionekana kama yanaimeza demokrasia. “Ndugu wanachama, mashabiki, wakereketwa na wafurukutwa; MMD hoyeee!” “Hoyeeeeeeeee.” Sauti iliyochanganyika na mbinja ilirindima ukumbini. Akaanza kwa kuwasalimu kama ilivyo ada kisha akaongea maneno kadhaa ya kujitapa kisiasa, baada ya hapo ukafika wakati ambao wengi walikuwa wanausubiri kwa hamu kubwa. “…………. Na sasa ni ule muda muafaka ambao tulikuwa tunausubiri kwa hamu kubwa.” Makofi, vigeregere na mbinja vikaongezeka, ukumbi ukahanikizwa kwa mbinje na mayowe. Baada ya kutulia katibu akaendelea. “……… waliojitokeza kuwania nafasi hiyo safari hii ni watano.” Ukumbi ukarindima tena kwa kelele na vifijo. “wa kwanza ni Bw.Gideon Kulindwa.” Makofi na vigelegele vikatawala tena kisha kukawa kimya. Tunamuomba asimame na kuthibitisha nia yake huku akiisindikiza kwa maneno mawili matatu, dakika tano tafadhali……” Baada ya kuzungumza na kupigiwa makofi kama yule wa kwanza wakafuata wengine watatu nao hawakuwa na tofauti kubwa na yule aliyetangulia. “……. Watano na wa mwisho ni Mheshimiwa Oscar Ole Nunga.” Hapo ukumbi ukalipuka kwa vifijo na nderemo. Ukumbi ukachangamka zaidi kuliko wakati wowote. Tabasamu likaonekana wazi katika wajihi wa mheshimiwa Ole Nunga. Hata pale alipomaliza kuongea bado shamra shamra ziliendelea. Shamra shamra hazikuishia hapo bali hata majumbani nako kulikuwa na shamrashamra kwani watu wengi walikuwa na imani na mheshimiwa huyo. Wengi walikuwa kando ya viredio vyao wakisikiliza mkutano huo ambao ulikuwa unarushwa moja kwa moja na kituo cha redio cha Taifa na baadhi vya watu binafsi na vile vya chama. Mkutano ukafungwa watu wakatawanyika ili kuwapa nafasi wagombea hao kuanza kampeni kabla ya kupatikana mmoja ambaye atakiwakilisha chama kwenye nafasi ya mgombea urais.
* * * Akiwa amevaa fulana maalum nyeupe iliyokuwa na maandishi ya njano kifuani ikimtambulisha kuwa mwandishi wa gazeti la Muungwana, John Oscar aliamua kutoka ndani ya ukumbi ili apate picha za viongozi watakapokuwa kwenye msafara wa kuondoka. Aliamua kuifanya picha hiyo kuwa ya mwisho, akatembea hadi kituo cha mafuta ambacho hakikuwa mbali sana na eneo la mkutano. “Habari yako dada,” alimsalimia dada ambaye alikuwa amesimama karibu na kisima cha mafuta ya taa kikiwa na ubao mkubwa ulioandikwa KEROSENE. “Nzuri nikusaidie nini kaka.” “Kuna gari hilo hapo,” huku akinyoosha kidole kwenye gari bovu “naomba kukaa hapo juu nataka kupiga picha magari ya viongozi yatakapokuwa yanatoka mkutanoni.” “Ongea na meneja wetu hapo ndani!” Akatembea hadi kwenye ofisi ya kituo kile cha mafuta, ndani kulikuwa na kijana ambaye alikuwa anafuatilia mkutano kupitia runinga ndogo. “Habari mkuu,” alisalimia. “Salama kaka, karibu.” “Ahsante.” “Naitwa John Oscar,” huku akichomoa kitambulisho “ni mwandishi wa gazeti la muungwana. “Oh, karibu bwana John sijui nikusaidie nini?” “Nilikuwa naomba kukaa juu boneti ya hilo gari mbovu hapo nje nataka kuchukua picha za viongozi watakapokuwa wanatoka ukumbini.” “Aaaah, ni hilo tu! Unajua umenitisha sana?” “Kwa nini?” “Nilifikiri umekuja kunihoji juu ya skendo za uchakachuaji mafuta.” “Ha ha ha ha haaaa, kwani nanyi huwa manachakachua?” “Hapana, nilikuwa na hofu tu ya jina langu kuamkia gazetini siku inayofuata.” Wote wakaangua kicheko kisha John akaelekea kwenye lile gari bovu. Akiwa na kamera ya kisasa kabisa yenye mfumo wa dijitali aina ya NIKON D4, Kamera yenye uwezo mkubwa wa kigrafikali wa ‘megapikseli 16’ John Oscar alitulia juu ya boneti ya gari lile huku akiyaona mazingira aliyoyahitaji kwa usahihi mkubwa.
* * *
Upande wa pili wa barabara kulikuwa na mtu mwingine ambaye alikuwa na jukumu maalum. Kijasho chembamba kilikuwa kinamtoka licha ya kuwa na kipoza joto ndani ya gari. Moyo wake ulikuwa unapiga kwa nguvu hasa pale alipokuwa anasikia mlipuko wa shangwe kutoka kwenye ukumbi wa KBT. Mara kwa mara aliinua mkono wake wa kushoto na kuangalia muda. Wakati mwingine ilikuwa inamchukua sekunde thelathini tu kuuinua tena mkono huo na kutizama muda. Kuna wakati alijihisi hata kubanwa na haja ndogo. Kadri muda ulivyokuwa unazidi kuyoyoma ndivyo alivyozidi kutawaliwa na hofu. Ghafla, akasikia mlipuko mkubwa wa vifijo na nderemo. Mwili wake ukasisimka, damu ikachemka na kumfanya ahisi joto kali. Bila kujijua shati lake lilikuwa limelowa jasho kama mtu aliyemwagiwa maji. “Gari, nyumba, shamba na pesa taslimu, potelea mbali….” Aliwaza kwenye nafsi yake akijipa moyo wa kukabiliana na tukio lolote lile. Binafsi alichukulia tukio hilo kama nafasi yake ya mwisho katika maisha, akose ajutie au apate afurahie. Hakuona kama ana cha kupoteza kwani maisha yenyewe kila siku yalizidi kuwa magumu. Bei za vitu zilikuwa zinapanda siku hadi siku. “M.W.R…,M.W.R…M.W…” James Makabi aliyarudia rudia maneno ya windo lake. Aliyakariri maneno hayo kwani ndiyo maelekezo aliyoyapata kutoka kwa Mjomba Masharubu. Maneno ya Mjomba yakajirudia kichwani. Hakuelewa kabisa kirefu cha neno M.W.R, hakuambiwa kama kuna namba zingine baada ya maandishi hayo. “Kuwa makini sana, gari unalotakiwa kuligonga ni lile lenye nambari M.W.R baada ya hapo potea kabisa”
Waaaaa…! Moyo wake ulitoa mlipuko pale aliposikia kwa mbali sauti iliyokuwa inasema mkutano umefungwa. Hakujali kama windo lake ni kiongozi au mwanachama wa kawaida, muhimu kwake ilikuwa ni kuhakikisha anakamilisha kazi aliyotumwa. Kwa upande mwingine aliwaza kuwa kama windo lake ni mwanasiasa basi hakuna kilichoharibika. Aliwachukia wanasiasa, alihisi kuwa ndio waliosababisha awe hapo alipo. Asingeweza kusahau jinsi alivyofaulu masomo ya darasa la saba lakini akakosa fursa ya kuendelea kutokana na serikali kuwazuia wakulima kuuza mazao yao wenyewe kule wanakotaka, badala yake serikali iliweka utaratibu wa kuwakopa wakulima kupitia vyama vya ushirika, kisha baada ya kuuza mazao yao kokote walikouza wakapanga nini wamlipe, ilimuuma sana kwani serikali ilikuwa haijushugulishi kwa namna yoyote kuwasaidia wakulima wakati wa maandalizi ya mashamba yao, badala yake waliwaingilia na kuwafanyia ukatili mkubwa ukifika muda wa mavuno. Jambo baya zaidi serikali ikathubutu hata kuweka askari wenye silaha za kivita barabarani ili kuwazuia watu kuuza mazao yao kwa utaratibu wanaoutaka kana kwamba walitoa msaada wa pembejeo. Bado wimbo wa kilimo kwanza ulikuwa mtaji wao wakati wa kuomba kura, aibu! Akakumbuka vema jinsi baba yake alivyoathiriwa na mfumo huo wa kikatili, kwani ufuta wake ulikopwa jambo lililosababisha akose fedha ya kumsomesha mwanawe. Baada ya baba yake kushindwa kumsomesha ndipo alipoamua kuja kujifunza ufundi magari hatimaye udereva. Mawazo hayo yalipokuwa yanapita kichwani akajikuta akipandwa na hasira na kuwa na dhamira ya dhati ya kutekeleza kazi yake si kwa sababu ya malipo atakayopewa tu bali pia kulipiza kisasi kwa mateso makali anayoyapata. Hofu ilikuwa imemtoka sasa. Alianza kuwaona watu wakiwa wanatawanyika, kisha magari ya viongozi ambayo yalifuata baada ya kutangulia msafara wa pikipiki na magari ya watu wa kawaida. Hapo akakumbuka vema maagizo ya Mjomba Masharubu. Hakuwa mbali sana na jengo la mikutano la chama cha MMD lililopo magomeni mwembe chai. Akapatwa na mshtuko baada ya kuliona windo lake kwa mbali. Aliwasha gari kisha akakaa tayari kwa tukio. Akaliondoa gari kwa kasi huku akiwa hajali kitendo cha askari wa usalama barabarani kusimama katikati ya barabara ile ya vumbi ambayo ilikuwa inaingia barabara ya morogoro, askari yule alikuwa ameliona gari lile lilivyokuwa linakuja kasi akajaribu kulizuia kwa kupunga mkono. Uhai mtamu, askari akajirusha kutoka barabarani na kujikuta akipiga mwereka mkubwa. Tahamaki, alikuwa kwenye mtaro akiwa tayari ameshavunjika mguu huku akikosa uhakika kama kiuno chake ni kizima. “Mungu wangu….!” Alisikika askari wa kike ambaye alikuwa kando ya barabara huku akiwa amepigwa na bumbuwazi kwa tukio lile la ghafla. Buuuuuuuu! Kilisikika kishindo kizito ambacho kilifuatiwa na milio ya risasi. Gari aina ya Toyota Landcruiser yenye namba M.W.R likaacha barabara na kuingia kwenye mtaro huku kioo cha mbele kikipasuka na kutawanyika kabisa. Nissan Patrol iliondoka kwa kasi ya ajabu kisha likaiacha barabara ya morogoro na kufuata ile ya Kawawa. Kasi ilikuwa kubwa na ya kutisha hata magari mengine yalilazimika kukaa pembeni. Gari la polisi Deffender110 lilikuwa linaifuata ile Nissan kwa kasi. Dereva wa Nissan alionekana kuwa hodari zaidi kuliko polisi. Ghafla, akaliona gari lingine la polisi likija kutoka mbele yake. “Oh, Jesus…” alijisemea kwa sauti ndogo baada ya kugundua nyuma anafuatwa na mbele pia si shwari. Akazidi kuongeza kasi ya gari yake kwa kukanyaga kiongeza mwendo. Sasa ilikuwa ni kama anayetaka kuligonga lile gari la polisi. Kwa kasi aliyokuwa nayo alifahamu wazi kuwa baada ya tukio hilo hakuna kingine zaidi ya kifo, tena kifo kibaya ambacho hata sura haitajulikana. Kwa haraka akaangalia upande wa kulia na kushoto, akaziona nyumba za Kigogo bondeni ambazo zilikuwa zinaonekana kana kwamba zimejengwa shimoni. “Ni uamuzi sahihi!” Alijisemea kwa sauti ndogo huku akiuacha upande wake wa barabara na kufuata upande wa kulia. Almanusura asababishe ajali ya gari pale daladala ambalo lilikuwa linakuja kasi lilipofunga breki ya ghafla baada ya kuliona gari lile. Hakujali kitakachotokea akalipeleka gari upande wa kulia na kufuata mporomoko unaolekea nyumba za Kigogo.
Gari likaserereka kuelekea kule bondeni, likagonga kwenye kitu kigumu likapinduka matairi yakawa juu bodi ikawa chini. Likaanza kuporomoka kwa mtindo wa pia. Dakika chache baadae gari likajipiga kwenye kiwambaza cha nyumba moja ambayo ilikuwa inauzwa pombe za kienyeji, ukasikika mlipuko mkubwa, gari likaanza kuwaka moto. Tafrani ikawa kubwa kila mtu akihaha kuyaokoa maisha yake, wako ambao pombe zilikuwa zimewakolea na walitembea kwa kuyumba lakini tukio hilo liliwarudishia fahamu zao na kujikuta wakitimua mbio za mashindano. Moto ulikuwa mkubwa na moshi wenye kutia hofu ukatanda eneo lote. Baadhi ya wakazi wa eneo hilo walilazimika kuyakimbia majumba yao kutokana na kishindo hicho ambacho kila mmoja alikitafsiri kwa namna yake. Dakika chache baadae helikopta ya polisi ilitua ikiwa na viongozi waandamizi wa jeshi hilo. Kama ilivyo ada watu walianza kurudi eneo la tukio, taarifa zilisambaa eneo hilo ni gari ambalo limesababisha ajali ya gari la makamu wa Rais dakika chache zilizopita. Pale lilipolipuka kulikuwa na miili ya watu watatu ambao walikuwa wameungua vibaya. Ilikuwa ni vigumu kumfahamu yeyote kwani waliungua na kuwa weusi kama mkaa. Katika kundi la watu wale alikuwepo yule mtu mrefu ambaye alijitambulisha kwa James Makabi kama Mjomba Masharubu. Kama alivyokuwa siku ya kwanza leo hii pia alikuwa ametinga suti ya bei mbaya na kofia yake ya pama. Tofauti na watu wengine yeye alikuwa anaangalia tukio hili kwa tabasamu na furaha. Ni tabasamu ambalo alilificha ndani ya moyo wake, hata furaha yake aliificha pia, ikafunikwa vema na huzuni na mshtuko wa bandia. Alichokihitaji kilikuwa kimekamilika kama filamu fulani ya kusisimua. Kazi yake ilikuwa imekamlika kwa urahisi zaidi kuliko alivyopanga. “Kwisha!” Alinong’ona kwa sauti ambayo ni yeye mwenyewe tu ndiye aliyeisikia kisha akaliacha kundi lile la watu na kutokomea alikokujua mwenyewe.
* * *
John Oscar alishtuka baada ya kuliona Nissan Patrol lililokuwa linaelekea barabarani kwa kasi. Hisia kali za uaskari zilichukua nafasi yake lakini akajikuta akikumbuka kuwa alishafukuzwa siku nyingi hivyo hakuwa na haja ya kuingilia jambo hilo, yeye sasa ni mwandishi hivyo ni jukumu lake kushuhudia kitakachotokea ili aweze kuripoti kwa ufasaha hasa katika zama hizi ambazo habari ni biashara. Akakumbuka usemi maarufu kuwa bara nyingi habari mbaya ndio habari nzuri kwa mwandishi. Alitegemea kushuhudia ajali ya kawaida lakini haikuwa hivyo, alichokiona ni utaalamu mkubwa wa mauaji ya kukusudia ambao hakuwahi hata kuufikiria hapo kabla. Sambamba na ile ajali mbaya ya kukusudia alishuhudia muheshimiwa Ole Nunga akirushwa juu na kutupwa chini huku kwa masikio yake ya uaskari akisikia kitu kama mlipuko wa bastola ambao kwa kiasi fulani ulifunikwa na kishindo cha ajali ile. Kilichomshtua sio mlipuko wa bastola bali aina ya mlipuko aliousikia, Haukuwa mlipuko wa kawaida wa bastola. Kama sio milipuko miwili kwa pamoja basi ni aina ya bastola au silaha ambayo hapa nchini haifahamiki Mikono yake iliendelea kutetemeka na kuifanya kamera nayo kucheza cheza, akajikuta bila kujijua akipiga picha ovyo ovyo. Mambo yalikuwa yanafanyika kwa haraka sana kiasi cha kushtukia ndani ya muda mfupi ile Nissan patrol ikiwa imepotea machoni pake. Ghafla akajikuta akirejewa na akili zake za kawaida na kutambua kuwa yuko kazini. Alishuka haraka juu ya boneti ya lile gari bovu na kukimbilia eneo la tukio baada ya kuona watu wakianza kuzingira eneo lile. Aliwahi kuchukua mapema picha za marehemu Ole Nunga kabla polisi hawajawahi eneo la tukio na kuwazuia waandishi wa habari. Hakuishia hapo akakodi pikipiki ambayo ilimuwahisha pia eneo ambalo gari la muuaji lilikuwa limeelekea. Hapo akakutana na utata mwingine wa aina yake lile gari nalo lilikuwa limepata ajali, kulikuwa na maiti tatu zote zikiwa zimeungua vibaya. Zaidi ya vimo vyao kwani maiti moja ilionekana kuwa ya mtu mrefu kuliko hizi mbili zilizosalia hakuna kingine kilichoweza kumfanya yeyote kubaini maiti hizo. Baada ya maiti hizo kuondolewa ndipo akatanabahi kuwa fulana aliyovaa ilikuwa imeloa kutokana na jasho. Akapiga picha chache za mwisho kabla ya kuwahoji watu wawili watatu aliowakuta eneo la tukio ambao hawakutofautiana sana maelezo yao.
III
Ilikuwa Jumatatu ya aina yake, gumzo kubwa likiwa mauaji ya makamu wa Rais. Kila kona ya jiji mjadala ulikuwa huo, halikuwa jambo la kawaida kusikia mauaji ya mwanasiasa mkubwa kama huyo katika nchi yenye sifa ya amani na utulivu. Magazeti yote ya siku hiyo yalihanikizwa na habari hizo, hata magazeti ya michezo nayo yalikuwa na habari hiyo. Inspekta Tunu Nzowa wa kituo cha Magomeni alikuwa amejifungia ofisini kwake akiwa na rundo la magazeti mpaka yale ya michezo ambayo kwa kawaida hakupenda kuyasoma. Alikuwa ametoa agizo kwa Koplo Peter Mkwabi kumkusanyia magazeti yote ya siku hiyo. Aliyapitia magazeti yote kwa haraka haraka huku akiwa amekata tamaa ya kupata habari yoyote ambayo itamwongoza kwenye upelelezi wa tukio lile. Lakini alipofika kwenye gazeti la MUUNGWANA akagandisha macho yake hapo. Picha kubwa iliyopamba ukurasa wa mbele wa gazeti hilo ilimfanya awe makini na gazeti hilo. Ilikuwa ni picha yenyewe hasa ambayo aliihitaji kwa wakati huo. Chini kulikuwa na maelezo kuwa habari na picha zaidi ziko ukurasa wa ndani. Akaliweka kando lile gazeti ili akili yake ipate kutulia kwanza ndipo asome vizuri kwani alikuwa hajawahi kushugulikia kesi ambayo ilikuwa nzito kama hiyo. Kwa upande mwingine alishangazwa na uamuzi wa haraka uliofanyika wa kukabidhiwa yeye jukumu hilo. Hakutaka kulifikiria sana hilo kutokana na kanuni za utii wanazofundishwa. Kengele ya simu yake ya mezani ikamtoa kwenye lindi la mawazo. Akanyanyua kiwiko cha simu na kusikiliza amri kutoka upande wa pili kwani namba alizoziona zilimjulisha kuwa anaongea na mkuu wake wa kazi. “Ndiyo afande.” Alijibu baada ya kusikia alichoambiwa. “Nimeamua kushirikiana na Koplo peter Mkwabi na kachero sajenti Dadi Kasweyaga wa kituo cha Buguruni.” Akasikiliza tena kilichoongelewa na mkuu huyo wa kazi kisha akajibu, “Hapana afande nimepitia rekodi za askari wengi nimeona kuwa hawa ndio watakaonifaa.” “Ahsante.” Alijibu kisha akarudisha kiwiko cha simu sehemu yake. Akashusha pumzi na kuitazama simu ile ya mezani kwa hasira, hakuhitaji kuongea na yeyote muda huo. Alihitaji kupitia gazeti lile kwa umakini mkubwa. “Tukio la jana tu leo hata sijafanya chochote naanza kuulizwa maendeleo ya kazi, upuuzi!” Aliongea kwa sauti ndogo kisha akamalizia kwa kusonya akionesha kukerwa na simu ya kamishna wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam. Kwa utulivu na umakini wa hali ya juu akaanza kufunua kurasa za gazeti la MUUNGWANA, ni kana kwamba gazeti hilo liliamua kuwa toleo maalum la mauaji ya Makamu wa Rais . Kulikuwa na picha mbalimbali za marehemu Ole Nunga kuanzia akiwa ukumbini mpaka wakati ule ajali inatokea. Kiasi fulani alishangazwa na umakini wa hali ya juu wa mwandishi au waandishi wa gazeti lile kwa jinsi walivyochukua picha na kutoa maelezo ya tukio zima kana kwamba walikuwa na fununu ya nini kitakachotokea. ‘…….. Wakati viongozi wanatoka ukumbini ndipo gari hilo jipya kabisa aina ya Nissan Patrol jeupe ambalo halijasajiliwa lilipojitokeza ghafla na kusababisha ajali hiyo ambayo ni wazi kuwa ilikusudiwa.’ Ilisomeka sehemu ya gazeti hilo. ***
IV
Kachero Inspekta Tunu Nzowa aliwasili katika viunga vya ofisi ya gazeti la Muungwana vilivyoko maeneo ya Ubungo Maziwa akiwa na wasaidizi wake Koplo Peter Mkwabi na Sajenti Dadi Kasweyaga.Akatembea taratibu hadi kwenye banda dogo la mlinzi ambaye alikuwa amevaa sare za rangi ya dhambarau. “Habari yako kijana!” “Nzuri shikamoo afande!” alijibu kijana yule kutoka kampuni ya KK Security. Inspekta hakujali kuitikia ile salamu badala yake akauliza moja kwa moja. “Naweza kuonana na Mhariri?” “Bila shaka, we nenda tu hapo lango kuu utaona kidirisha kimeandikwa mapokezi, hapo utaelekezwa uende wapi.” “Ok.” Alijibu kwa mkato na kuondoka huku akifuatiwa kwa karibu na sajenti Dadi Kasweyaga. Koplo Peter alibaki kwenye gari akiwa ameegemea usukani. “Habari yako binti.” Alisalimia Inspekta Tunu ambaye alikuwa ameibana kofia yake kwapani na kuruhusu kuonekana nywele zake ambazo zilianza kupigiwa hodi na mvi. “Salama shikamoo.” “Marahaba, naweza kuonana na mhariri?” “Ndiyo, fuata hii Korido chumba cha mwisho kabisa utaona maandishi mlangoni MHARIRI MTENDAJI” Kachero Dadi kasweyaga ambaye tofauti na wenzake alikuwa amevaa nguo za kiraia akakaa kwenye moja ya viti vya mapokezi ambavyo vilikuwa vimepangwa pale kwenye korido huku akimsindikiza bosi wake kwa macho. “Karibu sana.” Mzee Kasim mhariri mkuu wa gazeti la Muungwana alimkaribisha Inspekta Tunu. “Ahsante mzee, bila shaka wewe ndio mhariri mkuu wa hili gazeti” “Ndiyo afande, tafadhali keti nikusikilize.” Aliongea Mzee Kasim kwa sauti yenye furaha. “Naitwa Inspekta Tunu Nzowa,” alijitambulisha huku akitoa kitambulisho chake. “Hakuna haja ya kitambulisho afande kwani tumeshakutana mara kadhaa ingawa hapa ofisini ni mara yako ya kwanza kufika.” Inspekta akakaa vizuri kwenye kiti na kumuelekea Mhariri. “Habari yako Ndugu Kasim!” “Ah tunashukuru Mungu habari ni nzuri!” “Sawa, bila shaka una taarifa juu ya mauaji ya makamu wa rais bwana Ole Nunga.” “Ndiyo, tuna taarifa hizo pengine sisi ndiyo ambao tumeiripoti vizuri zaidi habari hiyo.” “Na ndio sababu ya kuja hapa, kwani nimezisoma kwa kina kabisa taarifa hizi kupitia gazeti lenu.” “Sijui ni kwa vipi tunaweza kukusaidia afande.” “Vizuri, kuna chochote ambacho hakijaelezwa kwenye taarifa yenu?” “Ndiyo kuna mambo kadhaa ambayo yanatakiwa kupangiliwa ipasavyo kisha tutayaweka kwenye toleo linalofuata, kwani wakati ile taarifa inatoka tayari gazeti lilikuwa limekamilika likisubiri kuingia mtamboni” “Vizuri,moja nahitaji kuonana na mwandishi au waandishi ambao mliwatuma kwenye mkutano mkuu wa chama, pili nahitaji taarifa hiyo hata kama haijapangiliwa vizuri yaani naihitaji kama ilivyo tatu naomba kukufahamisha rasmi kuwa nazuia kuendelea kutolewa taarifa hii katika gazeti lako kwani inaweza kuleta usumbufu katika upelelezi wetu.” Akatulia na kumkazia macho mzee Kasim.
“Ok, Mwandishi aliyefanya kazi hii ni mmoja tu na ameomba muda wa kuifanya kazi yake kwa utulivu akiwa nyumbani kwake, ameahidi kutuletea taarifa hiyo saa moja na nusu usiku kabla gazeti halijaenda mtamboni anaitwa John Oscar, Sijui kama utahitaji aje kwako au wewe ndio utaenda nyumbani kwake?” “Kutokana na mazingira jinsi yalivyo nahitaji kuonana naye nyumbani kwake.” “Anaishi kariakoo, mtaa wa Muheza karibu kabisa na makutano ya Muhonda nyumba namba 716.” “Ok Nashukuru kwa maelezo yako.” Wakapeana mikono kisha akainuka na kuondoka mle Ofisini. Safari ya kuelekea nyumbani kwa John ikaanza.
“Nafikiri huyu kijana anaweza kutusaidia” alianzisha maongezi Inspekta huku akimkazia macho Kachero Dadi Kasweyaga. “Ni kweli afande lakini nahisi tunatakiwa kuwa makini sana.” “Umakini unatakiwa kwenye kazi yoyote, Sijui ni umakini gani unauzungumzia hapa?” Aliuliza huku akimkazia macho makali. “Huyu Mwandishi anaonekana kuwa muhimu sana na hawa wauaji wanaweza kuwa watu hatari hivyo lazima watamuua ili kupoteza ushahidi kama hatutamuweka chini ya uangalizi maalumu.” “Wazo zuri ambalo sikulifikiria kabla, nitajadiliana naye ili awe kwenye maficho hadi pale tutakapokamilisha uchunguzi.”
*** Safari yao ikawafikisha makutano ya Muhonda na Muheza. “Ninyi mtanisubiri hapa nje wakati mimi nitakapokuwa nahojiana na jamaa huko ndani.” “Kwanini tusiingie wote afande” aliuliza kachero. “Nataka awe anajibu kwa utulivu kwani anaweza kubabaika atakapojikuta anakabiliana na maafande wawili.” “Huyo si mtuhumiwa afande hivyo hawezi kuwa na wasiwasi wa kuhojiwa tena kubwa zaidi ni mwandishi.” Alisikika kachero Dadi huku akiwa na shauku kubwa ya kwenda kumsaili huyo mtu.
Wakati Inspekta anapiga hatua kuelekea ndani mara simu yake ya mkononi ikaanza kuita. Aliitazama simu ile akaona ni namba ya Kamishna wa polisi wa makosa ya jinai muheshimiwa Kigoda Kanjowe. “Eeh, nakupata afande” “Kazi inaendelea vizuri, na hivi ninavyozungumza niko nyumbani kwa John Oscar Mwandishi wa gazeti la Muungwana nafikiri atatusaidia sana kurahisisha kazi yetu kwani anazo taarifa za kutosha juu ya tukio lile.” Akasikia mtu anashusha pumzi upande wa pili wa simu kisha simu ikakatwa. Kabla hajasonga mbele mara simu yake ikaanza kuita tena. “Ndiyo afande kuna tatizo?” “Unaweza kunielekeza hiyo nyumba iko wapi?” “Ndiyo.” Alijibu Inspekta huku akionesha wazi kukerwa na usumbufu huo wa mkuu wake wa kazi. “Huyu afande Kigoda ni msumbufu sana.” “Anasemaje?” “Anataka kujua eneo iliko nyumba ya huyu mwandishi.” “Anahitaji nini wakati hii kazi tumeshakabidhiwa?” “Ah! Ni usumbufu tu.” Wakati anataka kupiga hatua tena mara simu yake ikaita kwa mara nyingine. “Hallow afande kuna nini tena?” “Hili swala ni nyeti sana na linahitaji usiri mkubwa naomba uwaruhusu hao uliongozana nao halafu ubaki peke yako na usionane nae mpaka nifike hapo.” “Kwa nini afande.” “Ni upelelezi nyeti ambao hautakiwa kufikiwa na kila sikio hivyo waruhusu hao halafu unisubiri baada ya dakika chache nitakuwa hapo na usiwaeleze kuwa mimi nitakuja hapo kwani sitaki yeyote abaini kuwa nachunguza haya mauaji.” Akawaruhusu wale vijana wawili akaamua kumsubiri Kamishna. Baada ya kupita nusu saa akaamua kupiga simu. “Eeeh afande mbona kimya?” “Basi…ah… samahani kwa usumbufu nenda uhojiane naye nitakukuta hapo kabla hujaondoka.” Inspekta alikunja uso kwa hasira baada ya kupata majibu hayo kutoka kwa mkuu wake, kama si nidhamu za kiaskari angeweza hata kumtukana.
Nyumba namba 76 ilikuwa ni miongoni mwa nyumba chache ambazo hazikuwa na hadhi ya kuendelea kuwepo eneo la kariakoo. Kilichosababisha nyumba hiyo kupangishwa kwa bei kubwa ni kutokana na ubora wa eneo lakini si nyumba. Bati zake zilikuwa zimechakaa na kuwa nyekundu kutokana na kutu. Bila shaka kipindi cha mvua nyumba hiyo ilikuwa miongoni mwa nyumba zilizoleta kero kwa wapangaji kutokana na kuvuja. Akagonga mlango kama mara tatu ndipo akasikia mtu akimkaribisha. Mzee ambaye umri ulikuwa unampungia mkono ndiye aliyefungua mlango. Ingawa umri wa Inspekta Tunu ulikuwa umeenda kiasi cha kubakiza miaka mitano tu kustaafu kazi lakini kwa huyu mzee alikuwa sawa kabisa na mjukuu wake. “Shikamoo mzee!” “Marahaba, bila shaka unamuhitaji huyu John.” “Umejuaje?” “Leo amekuwa na wageni wengi sana tena huyu aliyemtembelea mara ya mwisho hata hajatoka huko ndani.” “Wageni wa aina gani?” “Wa mwisho ni askari kama wewe, karibu sana babu, yuko chumba cha uani huko.” Yule babu alimaliza kwa kicheko kikubwa. Inspekta alimkazia macho yule babu ambaye aliendelea kucheka akagundua kuwa akili zake zimeanza kurudi kwenye utoto kutokana na uzee. Akatembea kwa ukakamavu huku akivipita vyumba kadhaa ambavyo wapangaji walikuwa wanasikiliza Redio au kutazama runinga. Yule babu aliendelea kucheka hadi Inspekta alipoibukia uani. Uani kulikuwa na vyumba viwili ambavyo vilikuwa vimefungwa. Huku mlango ambao ulionesha kubeba vyumba viwili na sebule ukiwa wazi. Chumba hiki kilikuwa kimya, hazikusikika sauti za muziki kama vyumba vingine. Alipofika mlangoni akagonga mlango taratibu lakini hakuitikiwa. Akashangaa baada ya kulakiwa na ukimya huo. “Labda kenda kuoga.” Lilipita wazo lililkomfanya agande mlangoni lakini bado ukimya ulichukua zaidi ya muda wa kuoga. Akasukuma mlango na kuingia ndani, kwanza alishtushwa na harufu nzito. Ilikuwa ni harufu ambayo hukutana nayo mara kadhaa kwenye matukio ingawa ilikuwa imepita siku nyingi kabla ya kukabiliana na hali hiyo. DAMU! Mbona mapema? Alijiuliza huku akisonga mbele kwa tahadhali. Vitu vilikuwa vimetawanywa ovyo pale sebuleni. Karatasi zilikuwa zimetawanywa huku na huko. Hisia kali za hatari zikaendelea kumtawala kadri alivyokuwa anasonga mbele, kwanza akaangalia upande wa kulia mlango wa chumba ulikuwa umefungwa, alipoangalia ule wa kushoto ulikuwa umefunguliwa kidogo huku ukiacha nafasi kama ya mtu anayechungulia nje. Akasukuma ule mlango na kujitoma chumbani, kama hisia zake zilivyomtuma kwanza alianza kuona mchirizi wa damu akatembeza macho kwa haraka huku nywele zikimsisimka, mwili wa mtu ambaye alidhania kuwa ni John Oscar ulikuwa umelala chali huku ukiwa na jeraha baya la risasi upande wa kushoto. Moyo wa Inspekta ulikuwa unapiga kwa kasi kwani alihisi kuwa muuaji hayuko mbali kwani damu ilikuwa ni mbichi mno. Haraka haraka akainua Radio call yake, hakuwahi! Mkono wenye nguvu ulimshukia kichwani kwa pigo kali. Inspekta akalegea na kuanguka pale kwenye dimbwi la damu akapoteza fahamu. Kwa utulivu mkubwa muuaji akaondoka huku akikatisha pale kwenye korido bila wasiwasi. Hakuwa muuaji wa kawaida!
*** Watu waliojawa na maswali walikuwa wameizunguka nyumba ile namba 716 wakati maiti zinatolewa ndani. Kamishna wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam alikuwa miongoni mwa askari waliokuwepo eneo la tukio. Miongoni mwa watu walionekana kuwa na mawazo Mazito alikuwa Kachero Dadi Kasweyaga, Saa moja na nusu iliyopita alikuwa anaongea na Inspekta Tunu Nzowa lakini kwa sasa alikuwa nusu kuzimu. Pamoja na kutawaliwa na mawazo mengi ya kutatanisha bado aliendelea kuandika hili na lile, moyoni mwake alikuwa na kitu kizito ambacho alikuwa anawaza lakini akawa na hofu ya kukigusa. Alianza kufikiria upya kuhusu simu iliyopigwa na Kamishna maalum wa makosa ya jinai Kigoda Kanjowe, kwanini baada ya maongezi na mkuu huyo wao wakaambiwa waondoke na mwisho wa yote ni shambulizi kwa In spekta ambalo bila shaka lilikuwa ni kusudio la kumuua? Kuna nini kinaendelea juu ya sakata la kifo cha muheshimiwa makamu wa Rais? Maswali hayo yaliendelea kumtesa kachero huyo ambaye alikuwa na cheo kidogo.
*****
V Luteni Taisamo Alitazama kwa furaha jinsi watu walivyokuwa wanaburudika kwa muziki mtamu katika baa ile ya MASAWE NIGHT PARK iliyoko maeneo ya Vingunguti, kwake kilikuwa ni kichekesho kizuri kwani wengi walikuwa wanacheza bila kufuata utaratibu kutokana na vinywaji kuwakolea vichwani.Furaha yake ilikatika alipokumbuka kuwa ile ilikuwa tarehe 30 mwezi wa saba ambapo alitakiwa kulipa kodi ya nyumba. Akainuka pale kwenye kiti tayari kwa kuondoka. “Mbona unaondoka kaka si uliagiza mchemsho?” Sauti ya kike ikamzindua na kumfanya atahayari. “Nilitaka kununua sigara hapo nje.” Alijitetea. “Mbona hata hapa zipo?” “Aah, Kumbe, nilikuwa sifahamu basi nipe kwanza huo mchemsho pesa yako hii hapa.” Akamkabidhi noti ya shilingi elfu kumi. “Sigara gani unahitaji?” “We lete mchemsho tu nilitaka kununua sigara ili kuvuta muda.” Aliendelea kujitetea kwani hakuwa mvutaji. Wakati analetewa mchemsho mara simu yake ya kiganjani ikaanza kuita. “Hallow zero zero one fifty (00150) ni wewe?” “Ndiyo nani mwenzangu.” Alijibu kwa mshtuko kidogo kwani kutajwa kwa namba kulimaanisha kuwa kuna kazi muhimu anatakiwa kuifanya. “Rose hapa, uko wapi?” “Rose!?” “Ndiyo sitaki maswali zaidi, that’s my code name Liutenant, nisikilize kwa makini tafadhali. Uko wapi?” Ilikuwa ni sauti ya kike lakini iliyojaa amri.
“Vingunguti, MASAWE NIGHT PARK.” “Kaa hapo hapo usiondoke hadi utakapopewa maagizo mengine.” Rose lilikuwa jina geni kwake kikazi na hakutaka kuhoji zaidi kama alivyoonywa kwani alijua wazi kuwa hilo si jina halisi. Tayari aliishiwa na hamu ya kula kutokana na shauku ya kujua alichoitiwa. Hisia zake zilimtuma kuwa huenda kuna safari ya Sudan kusini chini ya vikosi vya umoja wa mataifa kwenda kulinda amani au kutuliza machafuko. Dakika arobaini na tano zilikatika bila kupokea maagizo yoyote, mara simu yake ikaanza kuita tena. “Hallow.” “One fifty, toka hapo ulipo nenda upande wa barabara ndogo inayoungana na barabara ya Nyerere.” Bila kuhoji huku moyo ukienda kasi akainuka pale kwenye kiti na kuongoza kule alikoelekezwa. Kilichomshangaza hapa ni kuwa kama ni kuitwa kwenda kulinda amani basi huu ulikuwa utaratibu mpya. Alijua wazi kuwa kuna jambo zito anatakiwa kufanya. Bado ulikuwa ni utaratibu wa kushangaza mno kwake kwani hajawahi kuusikia. “Hata huagi?” Sauti ya msichana aliyemletea mchemsho haikuyafikia masikio yake wakati anaondoka kwa staili hiyo ya aina yake. Luteni Taisamo kijana mwenye urefu wa wastani, mwili uliojengeka kimazoezi, mweusi lakini mwenye wajihi wa kuvutia kutokana na mng’ao wa weusi wake. Suruali yake ya jeans ya bluu na viatu vyeusi vya ngozi vilimkaa vema, fulana yake nyeusi ambayo ilikuwa na maandishi ya kichina ilimfanya ilimfanya azidi kuvutia katika macho ya yeyote anayemtazama. “Yes, tunakuona one fifty. Simama hapohapo ulipo.” Mpaka hapo alikuwa na maswali mengi kichwani mwake kwani alikuwa hajawahi kuitwa na mkuu wake wa kazi kwa namna ya kustaajabisha kama hiyo. Pia huyo Rose kama alivyojitambulisha alikuwa mpya. “Haraka ingia kwenye Benz jeupe unaloliona mbele yako.” Hapo alisita kidogo kwani alihisi kuwa huenda anakifuata kifo mwenyewe, lakini akili yake ilikataa haraka sana kwani toka aingizwe kwenye kitengo cha Interejensia ndani ya jeshi(CMI) alikuwa hajawahi kufanya kazi yoyote ya hatari ambayo inaingilia maslahi na heshima za watu ambayo ingeweza kumfanya aandamwe kiasi kile. Akafuata lile Benzi, ndani hakuwepo yule mwanamke aliyekuwa anaongea naye kwenye simu.Hakushangaa kwani si jambo la ajabu kwa watu wa aina hiyo kuwasiliana na mtu ambaye hakuoni huku na yeye akipokea maelezo kutoka sehemu nyingine. Ndani ya gari kulikuwa na dereva ambaye pia hakumfahamu. Kwa macho ya haraka mno aliweza kubaini kuwa yule dereva si askari. Wakasalimiana kisha gari likaondoka kwa kasi likifuata barabara ya Nyerere kuelekea Tazara,lilipofika makutano ya Nyerere na Mandela likaacha barabara ya nyerere na kufuata ile ya Mandela. Mpaka kufikia hapo Taisamo aliamua kuacha kuendelea kuwaza, aliamua kutulia ili akili yake ikae vizuri kukabiliana na lililoko mbele yake. Hakutaka kumuuliza swali lolote yule dereva ingawa alishangaa kumuona akiwa hana dalili yoyote ya uaskari. Alikuwa na uwezo mkubwa wa kumtambua hata askari ambaye ana miezi mitatu kazini. Waliongea mambo ya kawaida tu huku yule dereva akishindwa kugusia lolote kuhusu safari yao. “Jamaa akiniachia mpaka kesho ‘nitainjoi’ sana na huu mkoko.” Alisikika dereva na kumfanya Taisamo azidi kupigwa na mshangao. “Ina maana huwa hakuachii siku zote.” Alijifanya kama anayefahamu kuhusu gari hilo. “Thubutu, we unamjua vizuri yule mzee? Vile Vikorona na Korola atakuachieni muende mutakako na mafuta atakuongezeeni lakini hii Benzi sijui ni kwanini huwa anaitumia mara mojamoja, tena leo ajabu kunituma mimi na hii benzi.” Maelezo hayo yalimfanya Taisamo afahamu kuwa aliyemchukua hafahamu lolote. Pia hakutaka kuhoji na kumjua huyo anayemuita ni nani. Aliifahamu vema michezo ya watu wa Intelijensia, ni watu ambao mara nyingine hata wao wenyewe hawaaminiani.
***
Gari lilisimama mbele ya majengo ya Wizara ya ulinzi. “Sasa kaka mkubwa ee, mzee aliniambia nikuache hapa, bila shaka mwenyewe unaelewa zaidi wacha mimi nitanue kidogo maana nikichelewa kidogo tu anaweza kuniambia nirudishe gari nyumbani” Maelezo hayo yaliliendeleza mshangao wa Taisamo ambaye alifahamu kwa taratibu za kazi huwa wanafanya kazi kwa UNIT, yaani kunakuwa na mgawanyo maalum wa vikundi ndani ya wapelelezi vikundi hivyo hufanya kazi kwa kushirikiana na ikitokea kazi huwa kuna UNIT maalum inapewa kazi hiyo na si mtu mmoja mmoja kama ambavyo alianza kuhisi Taisamo kuwa inataka kutokea kwake. Alisimama palepale aliposhushwa akaendelea kusubiri maagizo mengine kutoka kwa Rose. Dakika ilikatika mara akafuatwa na mlinzi aliyekuwa upande ule wa lango kuu la kuingilia ndani. “Habari yako.” Alisalimia mlinzi aliyekuwa analinda jengo lile. “Nzuri, samahani bwana kuna mtu ameniambia tuonane maeneo haya hivyo nasubiri simu yake.” “Ahaa! We ndo mgeni wa mzee, panda ghorofa ya mwisho kabisa fuata hiyo korido chumba cha mwisho upande wa kushoto gonga mara tatu.” Taisamo alimsikiliza yule mlinzi huku akifahamu wazi kuwa haongei na mlinzi wa kawaida. Dalili za ukachero za mtu huyo zisingeweza kujificha katika mboni kali za Taisamo. Uso uliojaa mishuguliko na ujanja wa kujifanya mtu wa kawaida. Akafanya kama alivyoelekezwa, kutokana na shauku aliyokuwa nayo alilazimika kupanda harakaharaka ngazi za jengo lile lenye ghorofa tano huku akisahau kabisa kama kuna lift ambayo ingemrahisishia zoezi lake. Akainua mkono wake wa kushoto na kutazama saa yake. “Saa nne nusu, anahitaji nini huyu Mwaikambo?” Alijiuliza huku akili yake ikimtuma kuwa anaitwa na mkuu wake wa UNIT mwenye cheo cha Meja. Hata hivyo alitatanishwa na staili iliyotumika ili kualikwa kwenye wito huo kwani Meja Mwaikambo alikuwa na namba zote za wale anaowaongoza kwenye UNIT yake, hakuwa na haja ya kumtumia mtu wa kati anayejiita Rose. Alipoufikia ule mlango akagonga mara tatu kama alivyoelekezwa. Simu yake ya mkononi ikaanza kuita tena. “Hallow.” “Hallow one fifty Rose hapa, fungua mlango uingie ndani.” Kidogo alianza kuhisi hasira baada ya kuona anapelekwapelekwa na mtu asiyemfahamu .Hakuwa mgeni sana na jengo hilo alishawahi kufika mara kadhaa lakini aliishia huko chini ambako nje ya kulikuwa na ofisi nyingine ya ziada ya Meja Mwaikambo; hakuwahi kufika ofisi za juu na wala hakujua nini kinaendelea zaidi ya kufahamu kuwa huko juu ndiko iliko ofisi ya waziri wa wizara husika na baadhi ya wakuu wakiwemo makatibu. Jengo hili lilikuwa na mambo mengi zaidi ya kiusalama yaliyokuwa yanaendelea bila kufahamika. Hapa ulifanyika uchujaji wa mambo na kupelekwa kwenye kitengo husika, sio kila kitu kilichogunduliwa na wapelelezi wa polisi CID kilikuwa ndani ya uwezo au majukumu yao, pia hata wale wa usalama wa taifa na wale majasusi wa kijeshi hawakuwa na uwezo wa kutekeleza kila jukumu. Hapa ulifanyika ubadilishanaji mkubwa wa taarifa kwa maslahi ya Taifa. Kila jambo lilipelekwa kwenye kitengo husika. Jengo hili ambalo lilizungukwa na majengo kadhaa ikiwa ni pamoja na benki ya wananchi na majengo kadhaa ya kampuni ya simu, lilikuwa na urefu wa kutosha kiasi kwamba kwa yeyote ambaye angepanda huko juu angeweza kufaidi mandhari nzuri ya bahari ya hindi. Akafungua mlango kama alivyoelekezwa na kuingia ndani, hakuamini macho yake, alipatwa na mshtuko kidogo na kisha akatoa heshima ya kijeshi kwa kupiga saluti. Macho yake yalitua kwa maafisa wale wawili wa juu kabisa katika ngazi za utawala ndani ya jeshi. Huyu mmoja alimfahamu zaidi kwani licha ya kuwa mkuu wake wa kazi pia aliwahi kuwa mwalimu wake alipokua anachukua mafunzo maalum ya usalama katika chuo maalum cha kijeshi ambacho kiko Dar es salaam lakini wengi hawakitambui. Zaidi ya kumuona kwenye runinga na picha alikuwa hajawahi kukutana na mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama nchini Jenerali Othman Nalinga.Aliyatuliza macho kwa mzee yule kisha akayarudisha kwa mnadhimu mkuu wa Jeshi, Luteni Jenerali Robert Ruhumbika. Hakuwahi kufikiria kuwa siku moja angeitwa na maafisa wale wazito, pia alishangaa kwani hata Meja Mwaikambo hakuwajibika moja kwa moja kwa wakuu hao na badala yake alipokea amri kutoka kwa Luteni kanali, Kanali na mara mojamoja sana kutoka kwa Brigedia Jenerari. Hakuna hata jambo moja ambalo alilifikiria katika kichwa chake ambalo linaweza kuwafanya wakuu wale wamuite moja kwa moja kwani mara nyingi aliwajibika kwa Meja ambaye pia alikuwa ni mkuu wa UNIT yao ambayo ilijulikana kwa jina la snake.
Akaituliza akili yake na kuiweka kikazi zaidi ili aweze kupokea majukumu kwa ukamilifu. Wakati akiwa anasubiri alichoitiwa akapata nafasi ya kuisanifu ofisi ile. Chini ilikuwa imetandikwa zulia zito jekundu, pembeni upande wa kulia kulikuwa na kabati kubwa la chuma. Meza ya kubwa ya duara ilikuwa katikati ya ofisi huku ikiwa imezungukwa na viti vipatavyo sita. Ni ofisi ambayo haikuwa na vitu vingi zaidi ya hivyo alivyoviona kwani ilikuwa kama ukumbi wa mikutano tu. Ukutani kulikuwa na picha za maraisi wastaafu na waliowahi kuwa wakuu wa jeshi. Picha ya Raisi wa Kwanza ndiyo iliyokuwa kubwa zaidi huku ikita imezungushiwa taji la maua. “Karibu sana Luteni.” Alianza kuongea Jenerali. Macho maangavu ya Luteni Taisamo yaliweza kumwona Jenerali Nalinga akifunua jalada pekee ambalo lilikuwa pale mezani. Taisamo akalitazama lile jalada kwa shauku kubwa. “Sasa ni muda muafaka wa kuanza kikao chetu.” Alisikika Jenerali huku macho yote akiwa ameyaelekeza kwenye jalada lililoko pale mezani. “Kwa kuwa hiki si kikao cha wanasiasa naona niende moja kwa moja kwenye mada husika, Hali ya nchi kwa sasa si nzuri inaonesha kuna kitu kinafukuta chini kwa chini, hivyo tumeamua kutumia kitengo chetu kutafuta ukweli, kutokana na unyeti wa suala lenyewe na wasiwasi wa kuonekana kuwa huenda kuna maafisa waandamizi wanahusika ndio maana tumekuteua wewe kufanya kazi hiyo. Sababu iliyotufanya tukuteue ni uwezo mkubwa wa mitihani ya kiakili ambao uliuonesha ulipokuwa chuoni Monduli na hata ulipokuwa ukichukua mafunzo maalum hapa Dar.” Akatulia na kumeza mate. “Kifo cha makamu wa Rais pekee kisingetosha kutushawishi kufanya kazi hiyo moja kwa moja, tungewaachia wenzetu wa CID au Usalama wa Taifa. Ni kweli kifo cha makamu wa Rais kimetokana na ajali ya gari, lakini pale polisi walipojaribu kufuatilia wameishia kushuhudia Afisa mwandamizi akinusurika kifo. Kinachotia mashaka zaidi ni jinsi zoezi hili lisivyotiliwa mkazo na wenzetu wa polisi na usalama wa Taifa, tunataka tufahamu nini kimejificha nyuma ya pazia, kwa kuanzia utaanza na hili jalada la maelezo kutoka polisi ingawa nafahamu fika halina kitu cha maana sana lakini siku zote safari ya ghorofani huanzia nyuma ya ngazi na si kwenye ngazi.” Aliongea Jenerali kwa sauti iliyojaa utulivu huku akilisogeza lile faili. “Pia utatakiwa kuripoti matukio yote kwangu au kwa Luteni Jenerali Nalinga pale ambapo nitakuwa sipo. Zingatia utatumia namba yangu ya kiganjani ambayo nitakupatia pale utakaponihitaji, usithubutu kuja ofisini kwangu sitaki afahamu yeyote zaidi yetu kuwa kuna kazi inaendelea. Kuhusu matumizi umeingiziwa kiasi cha fedha kwenye akaunti yako kama utahitaji msaada zaidi tafadhali wasiliana nami au Luteni Jenerali Nalinga.” Kama si ukubwa wa jukumu alilopewa basi hiyo ilikuwa ni siku ya furaha mno kwake, alielewa wazi ugumu wa jukumu alilokabidhiwa hivyo asingeweza kufurahia zile fedha alizoingiziwa. “Jambo la kwanza unatakiwa kutafuta ofisi yako binafsi pale unapoona panafaa kufanya shuguli zako kwa usiri na utulivu, jambo la pili hatakiwi kujua yeyote hususani maafisa wako waandamizi juu ya jambo hili. Hivyo huna sababu ya kuaga kwa mkuu wako wa UNIT,nafikiri hii ndio kazi yako ya kwanza ambayo inaendana na mafunzo yako toka upandishwe cheo, kazi njema.” Aliongea jenerali kwa msisitizo.
MWEZI MMOJA KABLA YA MAUAJI
Saa 8.30 usiku, ndani ya chumba kidogo kilichowekewa ulinzi madhubuti. Hakutakiwa yeyote asiyehusika kunusa kinachoendelea huko ndani, hata walinzi wake hawakutakiwa kujua lolote. Waliridhika na posho nono waliyoahidiwa mara baada ya kikao hicho, hawakuwa na muda zaidi wa kutaka kujua nini kinaendelea huko ndani. Posho ya kulinda chumba hicho usiku mmoja ilikuwa ni zaidi ya mara kumi ya mishahara yao. Haikuwa mara yao ya kwanza kupewa kazi kama hiyo. Meza kubwa ya duara ilikuwa imetawala eneo kubwa la chumba hicho, nafasi iliyobaki ilimezwa na viti ambavyo idadi yake ilikuwa kumi na viwili. Viti vyote vilikuwa vimeenea, hakuna kilichokuwa kitupu. Chumba kilitawaliwa na mwanga hafifu wa bluu kitu kilicholeta ugumu wa kuwatambua walio hudhuria kikao hicho cha aina yake. Mwenyekiti wa kikao akakohoa kidogo na kuwakazia macho wenzake kabla ya kuongea lolote. “Ni matumaini yangu kuwa nyote hamjambo,” alianza mwenyekiti huku akitembeza macho yake kwa wajumbe. Akakohoa tena kabla ya kuendelea. “Kubwa lililotuleta hapa ni juu ya mbio za uraisi.” Akatulia na kuwatazama wajumbe ambao walitulia zaidi huku wakiwa na shauku kubwa. “….Kwa taarifa nilizo nazo ni kwamba Bw.Oscar Ole Nunga atatangaza nia ya kugombea urais mwaka huu na ameshaanza mchakato.” Akatulia na kuwatazama wajumbe huku akijaribu kusoma fikra zao, wapo walioonesha mshtuko na wapo ambao walichukulia kama taarifa ya kawaida ambayo haikustahiki kuitana usiku wa manane. Licha ya kuwa mwenyekiti wa kikao hakutaka kuzungumza zaidi, badala yake aliamua kuwapa nafasi wajumbe ajue wameipokeaje taarifa hiyo. “Kabla sijaendelea naomba kujua kutoka kwenu mmeichukulia vipi taarifa hii?” Akatulia tena huku akiwatazama wajumbe kama kuna ambaye alitaka kuzungumza. Mjumbe mmoja ambaye kama wenzake nae alionekana kushiba madaraka akanyoosha mkono. “Enhe, mheshimiwa hapo nafikiri una mchango!” Ilikuwa ni kanuni ya kikao kutotajana majina. “Ndiyo, mkuu.” “Haya tunakusikiliza.” “Kwa mtazamo wangu hakuna tatizo kwa Bwana Ole Nunga kuwania uraisi kwani ni kada mwenzetu na hana tatizo lolote,” akatulia na kuwatazama wenzake huku akiona wazi jinsi wengine walivyokuwa wanatikisa kichwa kukubaliana nae huku wengine wakipingana naye waziwazi. “Mkono mwingine…” alisikika mwenyekiti ambaye kwenye kikao alitumia jina la mkuu. Mkono ukanyooshwa na mtu aliyekuwa karibu kabisa na mkuu. “Enhe.” “Mi nafikiri hakukuwa na sababu ya kuitisha mkutano huu wa dharura kwa mtu ambaye anafahamika wazi kuwa ni kada nzuri ambaye hana matatizo!” Mkuu ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hakuonekana kuwa na haraka ya kujibu hoja hizo za wajumbe badala yake aliendelea kukusanya mawazo bila kuzungumza lolote. Hata pale wajumbe walipoonekana kupinga kikao kile bado mwenyekiti alionekana kuwa mtulivu na asiye na jazba jambo lililowatisha wajumbe wengine. Baada ya kupita muda bila kutokea hoja yoyote mkuu alianza kutembeza macho kwa mjumbe mmoja baada ya mwingine kisha kwa utulivu zaidi akaanza kuongea. “Nafikiri tunayo haki ya kuzungumza au kufikiri tunavyofikiri kwa kuwa hatuelewi undani wa mambo, Ole Nunga ni mtu hatari tofauti na baadhi yetu mnavyomchukulia. Ana uhusiano mkubwa na baadhi ya wabunge wa upinzani ambao ni matata na tishio kwa mustakabali wa chama, pia ni mfuasi mkubwa wa sera za marehemu Josi Mkulu muasisi wa chama chetu si hivyo tu Ole Nunga ana ushawishi mkubwa sana ndani ya chama…..” akanyamaza kidogo huku akiendelea kuwa mtulivu zaidi, kisha akaendelea. “….Pia taarifa za kiinterijensia zinaonesha kuwa ndiye mtu anayetoa siri za serikali kwa vyama vya upinzani hasa pale unapofanyika uozo, amekuwa na falsafa ya hatari ya Nchi yetu kwanza chama baadae, napenda kuwafahamisha kuwa yeye ndiye aliyetoa siri ya ununuzi wa meli mbovu ya kijeshi jambo ambalo limetupunguzia wapiga kura na kuleta ufa ndani ya chama na kusababisha kukosekana ushindi wa kishindo pia.” Akatulia kwa muda mrefu zaidi na kuongeza shauku ya wasikilizaji ambao sasa walionekana kukubali uzito na umuhimu wa kikao kile. “…..Si hivyo tu kwa masikio yangu mwenyewe nimewahi kumsikia akidai kuwa atapambana na wote ambao wana akaunti katika benki za nje, hebu niambieni zile fedha zetu zilizoko uswiswi kweli tutanusurika?” Akatulia tena na kuwaachia wajumbe muda wa kutafakari. Aliwaona wazi wajumbe wale jinsi walivyokuwa wanatokwa na jasho kutokana na woga mkubwa. Bila shaka walianza kumuelewa kwa kina kile alichokuwa anakusudia. “Kwanini mmempa madaraka makubwa kiasi kile wakati mnatambua wazi kuwa ni mtu hatari?” Aliuliza mmoja miongoni mwa wajumbe. “Jibu lake ni rahisi sana, anafahamu mikataba mingi ya hatari kwa jinsi alivyo na ushawishi angeweza kuanzisha hata chama au kujiunga na upinzani kama angeachwa nje ya serikali na isingewezekana kumfunga mdomo, ingekuwa hatari kwa chama na serikali yetu hivyo hatukuwa na namna bora ya kumfunga mdomo zaidi ya kumpa nafasi ile kubwa, tena uzuri ni kwamba ile nafasi ni ya kisiasa zaidi na si ya kiutendaji, yaani tunachotakiwa kufanya ni kumuwekea boksi la mikasi tu ili akazindue miradi ya barabara na majengo mbalimbali hiyo ndiyo kazi ya makamu wa Raisi.” Akatulia tena na kupisha maswali zaidi. “Kwanini asifungwe mdomo kama tunavyofanya kwa wengine?” Aliuliza mjumbe mwingine. “Hapo ndipo nilipopataka na ndio hasa maana ya kikao hiki, lakini inatupasa kutambua kuwa Ole Nunga si kama hao wengine, anatofautiana nao kwa kiasi kikubwa kama mbingu na ardhi. Ifahamike kuwa Ole Nunga alishawahi kuwa kwenye system, kabla ya hapo ni kapteni mstaafu. Mbaya zaidi ni mtu mwenye akili timamu anayejua nini anakifanya na wakati gani, si hivyo tu pia anajua anaishi dunia gani na aishi vipi! Si mtu wa kumziba mdomo kikawaida kama watu wengine…..” akasita kidogo baada ya kugundua ameongea mfululizo tofauti na kawaida yake ya kuwaachia wajumbe kuchangia.
Baadhi ya wajumbe walionekana kuanza kuingiwa na hofu juu ya Ole Nunga baada ya taarifa hiyo fupi lakini nzito. “Hivi inashindikana vipi kutafuta watu wa kawaida ambao watamnyamazisha kwa risasi moja tu ya kichwa?” “Haishindikani!” Sauti mzito ya mjumbe ambaye alikuwa na nafasi muhimu kwenye kikao hiki lakini muda wote alikuwa kimya ikasikika. Akavuta hisia za wote na kufanya wamgeukia. “Bila shaka wengi tuliopo kwenye kikao hiki tumewahi kuwa kwenye system katika wakati mmoja au mwingine…….” akawatazama wajumbe wale ambao kila mmoja alitikisa kichwa kukubaliana na kauli hiyo. “….. nafikiri hii ndio sababu ya mkuu kutufanya sisi kuwa wajumbe wa kudumu wa vikao hivi ambavyo vina maslahi makubwa kwa chama na serikali.” Utulivu ukatawala tena. “….. Vinginevyo hii kazi ilitakiwa asihusishwe yeyote kati yetu maana kulikuwa hakuna ushauri wa kitaalamu ambao ungetolewa. Nirudi kwenye hoja, kumziba mdomo Ole Nunga kwa mtindo wa kutumia watu wa kawaida kutatuletea shida kubwa sana, Nunga ni mtu wa watu na ana watu kwenye system, CID na jambo la hatari zaidi amewahi kuwa kitengo cha ajira ndani ya idara ya usalama wa Taifa hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kuwepo kwa masalia yake. Kinachotakiwa hapa ni kutumia akili ya ziada katika kummaliza vinginevyo tutaangukia pua.” Akatulia na kuwaacha wajumbe wengine wakiwa na nyuso zenye hisia tofauti, kila mmoja akijaribu kutafakari mbinu bora ya kummaliza Ole Nunga. “Ok, nimepata wazo,” alisikika mmoja kati ya wale wajumbe. “Lazima system itumike, nafikiri mjadala ufungwe.” “Ufungwe vipi bila ufumbuzi?” Aliuliza mjumbe mmoja. “Ufumbuzi upi?” Sauti nyingine ya mjumbe iliuliza. Ile sauti nzito ya mwanzo ikajibu “Jibu ni moja tu… Masharubu..” Ilijibu ile sauti. “Who is he!”(Ni nani?) Mjumbe mwingine ambaye hakuwahi kuzungumza hapo kabla aliuliza. “He is a P.K” mjumbe mwingine akajibu haraka. “P.K?!” Aliuliza mjumbe mwingine kwa mshangao. “Yes, Professional Killer!” Sauti ile nzito ikajibu. “Safi, Uko sahihi.” Kwa mara ya kwanza tabasamu lilionekana kwenye uso wa Mkuu. Kikao kikafungwa.
* * * Muziki mororo uliendelea kurindima kwenye baa maarufu ya Mazda iliyopo maeneo ya Tabata Kimanga. Mtu mrefu mweusi mwenye suti ya nrangi nyeusi ya bei mbaya alikuwa amekaa kwenye moja ya kona ya baa hiyo. Mara kwa mara aliinua mkono wake na kutazama saa huku macho akiwa ameyaelekeza langoni. Alikuwa na miadi na mtu, alikunja sura baada ya kuona muda unayoyoma bila ya kutokea yule mtu waliyeahidiana kukutana hapo. Huyo ndiye mtu aliyekuwa na kivuli cha jina la Mjomba Masharubu, mtu mrefu mwenye sura pana akiwa na mwili wa wastani. Alikuwa na kidevu cha ufuto ambacho kilisheheni ndevu zilizotunzwa vema. Kama lilivyo jina lake mtu huyu alikuwa na masharubu ambayo yalikuwa yanatunzwa vizuri. Rangi yake nyeusi, masharubu, mawani nyeusi na suti nyeusi vilimfanya afanane na giza licha ya mwanga hafifu uliokuwa unatoka kwenye taa zilizozunguka eneo hilo. Akiwa amekata tamaa ya kuonana na yeyote waliyeahidiana kukutana hapo, mara simu yake ya kiganjani ikaanza kuita. Akaitoa simu mfukoni na kutazama namba ya mpigaji. Namba ngeni! Akaipokea ile simu na kuanza kusikiliza. “Hallow P.K, Mr.J hapa naongea.”Sauti nzito ilisikika kwenye simu. Ni watu wachache na muhimu sana ndio waliofahamu jina lile la P.K na wakamjua PK mwenyewe ni nani, hivyo kuitwa kwa jina lile kulimaanisha jambo. “Ndio mkuu, nakusikiliza!” “Njoo namba 3 kuna dharura, tunatakiwa kupunguza mnyama mbugani!” “Twiga au…..” “No, It is a lion, a king of animals!”(Hapana, ni simba mfalme wa wanyama.) Alielewa. Akashusha pumzi, bila kujali kuwa ana miadi na mtu akatembea kwa hatua za haraka kuelekea kwenye lango la kutokea nje ya baa ile. “Wapi sasa mbona unaondoka?” Sauti ya kike ilimshtua alipokua anavuka lango la baa ile. “Oh! Rose, I’m sorry nina dharura kubwa natakiwa mahali saa hizi nina ujumbe wa msiba!” “Mungu wangu, nani tena?” “Secretary wangu, amegongwa na gari huko kwao Moshi, chukua hizi nitakutafuta!” Alitoa kiasi cha noti ambacho hakukihesabu na kumkabidhi. Rose akapokea kile kiasi huku moyo ukimwenda mbio, ni kiasi kikubwa ambacho hakukitarajia tena kwa mtu ambaye ndiyo kwanza walikuwa wamepanga kukutana kwa mara ya kwanza, hakuwa mpenzi wake labda siku hiyo ndio ungekuwa mwanzo wa mapenzi yao. Mjomba Masharubu alitembea kwa hatua za haraka kuliendea gari lake aina ya Toyota etios , akajitoma ndani na kukaa kwa dakika kadhaa kabla ya kuliwasha. Alikuwa ameshikilia usukani kama anayetafakari jambo. Kidogo alipatwa na mshtuko baada ya kuambiwa mnyama anayetakiwa kuuwawa ni simba, tena msemaji akaongeza kuwa ni mfalme wa wanyama. Alishtuka kwa sababu alijua uzito wa kazi iliyoko mbele yake, hakupenda kufanya lolote kabla hofu yake haijapoa, ndio maana aliukumbatia usukani ili akili yake irudi kuwa ya kawaida kabla hajaanza lolote. Baada ya kutulia kwa dakika chache akawasha gari na kuliondoa kwa mwendo wa wastani hadi alipoipata barabara Mandela. Hapo akakanyaga mafuta na kuifanya gari iondoke kwa kasi sana. Mjomba Masharubu ni mwajiriwa wa idara ya usalama wa taifa akijulikana kwa jina la kikazi kama P.K. Si wengi sana waliomfahamu kwa jina hilo, hata wafanyakazi wenzake walikuwa wanajua kama kuna P.K lakini hawakujua ni nani. Walipishana nae hapa na pale bila kufahamu kuwa ndiye P.K mwenyewe. Katika akili zao walijua ni mtu hatari ambaye Idara inamtumia sana kwenye kashikashi nzito ambazo mauaji lazima yafanyike. Wapo waliojaribu kunusa wakitaka kumfahamu huyo P.K ni nani! Lakini gharama ya jambo hilo haikuwa ndogo kama walivyofikiri kwani waliishia kupata barua kali ya karipio na wengine hata kuhamishwa makao makuu. Watu maalum, watu wachache walimjua ni nani P.K. Hata Mjomba Masharubu mwenyewe kuna wakati alijifanya kutafiti mbele ya wenzake akitaka kumjua huyo P.K ni nani, ikabaki kuwa P.K ni mtu hatari ambaye hata watu wa system walimuogopa Kikubwa kilichoongeza usiri wa kumjua huyo P.K ni kutokana na kuwa na mpasuko ndani ya Idara, baadhi ya wafanyakazi walikuwa wanatoa siri nyeti za nchi kwa viongozi au wabunge wa vyama vya upinzani ambao hujichukulia sifa kubwa pale wanapoenda kuweka mambo hadharani. Wafanyakazi hawa huwa wameahidiwa nyadhifa fulani iwapo chama hicho kitaingia madarakani, wengine huvunja viapo vyao vya kutunza siri kwa sababu ya urafiki tu pia wapo wale ambao hufanya hivyo kwa uzalendo wa kuipenda nchi yao kwa kuona nchi inaenda kombo na wengine hufanya kazi hiyo kwa tamaa ya fedha. Idara ilikuwa inajitahidi kwa kiasi kikubwa kuishauri serikali mambo mbalimbali kiuchumi, kisiasa, kijamii na mengineyo mengi lakini ikakutana na kiburi na majivuno ya viongozi ambao walitia pamba masikioni na kufanya mambo kwa matakwa yao. Tabia hiyo ya viongozi ikasababisha wananchi kukosa imani kwa chama tawala cha MMD. Mporomoko huo wa chama ukaonekana kuwa hatari kwa maslahi ya baadhi ya wachache ambao walikuwa wameiweka serikali na chama mkononi. Hatari hiyo ya kuanguka kwa chama ndiyo ikasababisha kuibuliwa kwa mtu huyu Mjomba Masharubu. Ni mtu hatari ambaye alikuwa na mafunzo ya juu ya ujasusi. Kwa mtazamo alionekana kuwa mtu wa kawaida lakini undani wake alikuwa zaidi ya mnyama. wajibu wake kwa mkuu wa kazi ulikuwa ni kutekeleza maagizo bila kuhoji. Kuna wakati alishawahi kusafiri nchi mbali mbali za kiafrika kwenda kukatisha maisha ya watu ambao walionekana kuwa hatari kwa usalama wa nchi hizo. Hizo ni zile zinazoitwa nchi rafiki. P.K alishawahi kukatisha maisha ya baadhi ya wafanyakazi wa idara baada ya kubainika kutoa siri au kuacha kazi na kujiunga na vyama vya upinzani, pia amewahi kukatisha maisha ya viongozi kadhaa wa vyama vya upinzani ambao walionekana kuwa hatari kwa chama tawala. Hii ndio sura ya chama tawala ambayo ilikuwa tayari kwa gharama yoyote kuhakikisha kuwa inabaki madarakani lakini si maendeleo ya wananchi.
*** Namba 3 au ‘kichwa’ ni ofisi maalum inayotumiwa na idara ya usalama wa taifa. Mara nyingi hutumiwa na maafisa waandamizi tena sio wote isipokuwa wale waliochaguliwa na mkurugenzi. Usiri mkubwa wa ofisi hii ulitokana na unyeti wake kwani maamuzi mazito ya idara mara nyingi yalianzia hapo. Ni ofisi hii hii ambayo saa 8 usiku uliopita kulifanyika kikao cha watu kumi na wawili. Mjomba Masharubu aliingia ndani ya Ofisi hiyo iliyoko maeneo kariakoo mtaa wa Livingstone. Baada ya kuingia akakutana na mkurugenzi wa usalama wa taifa ndugu Wahuva Kilale. Baada ya kusalimiana akakaa na kumuelekea mzee huyo ambaye mvi zilikuwa zimetawala kwenye kichwa chake. “Karibu kijana, sijui utapendelea kinywaji gani?” “Sihitaji chochote mzee!” “Ok, nafikiri hatuna mazungumzo marefu zaidi ya kuingia moja kwa moja kwenye point ya msingi!” “Ndiyo mzee.” “Safari hii kuna kazi nzito kidogo tofauti na zilizotangulia!” Akatulia na kufanya kero ya shauku ya kusubiri hilo jina iongezeke kwa Mjomba Masharubu. Hakuna alichohitaji kwa wakati huo kama kumjua huyo mlengwa au windo lake jipya. “Safari hii kamati imeamua kufupisha maisha ya Mheshimiwa Oscar Ole Nunga.” Akainua macho na kumtazama mkuu wake wa kazi kwa mshangao. “Makamu wa Raisi?” Aliuliza akitaka kupata uhakika zaidi kwa alichokisikia. “Ndiyo!” Alijibu kwa mkato. “Kulikoni?” “Umesahau kanuni P.K?” “Kutekeleza majukumu bila kuuliza?” “Ndiyo.” “Napenda nifanye kazi nafsi ikiwa imetulia, maana ninavyofahamu Nunga ni kada mwenzenu!”
“Sawa. Nyati kwenye kundi la ng’ombe. Anautaka uraisi kwa udi na uvumba wakati anajua wazi safari hii ni zamu ya ………” akasita kidogo kisha akaendelea huku akijutia alichotaka kuzungumza. “…………. Ona nataka kutoa siri za ndani kabisa, anyway ni mtu hatari kwa usalama wa chama na serikali pia amekuwa ni chanzo cha kuundwa kamati teule za bunge kwa kuvujisha baadhi ya mambo nyeti. Siwezi kupokea maswali zaidi.” Ilikuwa ni amri hata hivyo aliridhika kwani alifahamu tatizo. “Ok, nimekuelewa mzee.” “Naomba unifahamishe kila unachokihitaji kwenye kazi hii!” “Nahitaji gari mpya ambayo haijasajiliwa!” “Simple aina gani?” Alisikika mkurugenzi. “Nissan Patrol.” Alijibu kwa mkato huku sura yake ikiwa imebadilika kwa kubeba tafakari nzito, bila shaka akijaribu kupanga nini cha kufanya. “Kesho saa 2.30 njoo uchukue hapa!” “Ok.” “Unaweza kunidokeza plan yako?” “Boss umesahau kanuni?” “Ya kutoingilia taratibu zako?” “Sawa kabisa.” “No, sijakuingilia isipokuwa nimeuliza tu maana mwili unasisimka kwa jinsi ulivyoanza haraka hiyo mipango.” “Hapana bado sijaratibu vizuri nahitaji siku nzima ya kutafakari kwa makini ingawa gari mpya isiyosajiliwa tayari ni sehemu ya mpango wangu.” Mzee Wahuva hakuongea kitu zaidi ya kutikisa kichwa kukubaliana na kijana wake. “Ok kazi njema.” Aliongea mkurugenzi huku akimpa mkono Mjomba.
* * *
Taisamo alipofika ofisini kwake, kwenye jengo la Mwalimu house eneo la Ilala boma , ilikuwa yapata saa nne na nusu. Alifungua mlango wa ofisi ile mpya ambayo hakuna yeyote katika watu wake wa karibu aliyeifahamu. Alitabasamu baada ya kukaa kwenye kiti kile ambacho kilikuwa na uwezo wa kuzunguka na hata kusogea sehemu nyingine. Kiujumla ilikuwa ofisi nzuri yenye mahitaji yote muhimu kama computer, printer, kabati kubwa la kuhifadhia mafaili na simu ya mezani. Alitumia siku mbili kuandaa ofisi hii. Jambo la kwanza alilolifanya ni kuanza kusoma taarifa za kifo cha Makamu wa Rais kama alivyopewa na Jenerali Nalinga. Akili yake ilimtuma kuwa ni kazi rahisi tu kwani angeanzia pale walipoishia wenzake. Akalifungua lile faili au jalada la Mauaji akaanza kulisoma. Muheshimiwa aliuwawa muda mfupi baada ya kutoka kwenye mkutano mkuu wa chama. Chanzo cha ajali yake ni ajali ya gari iliyosababishwa na dereva mzembe aliyeingia ghafla barabarani wakati msafara wa viongozi wa chama na serikali ulipokuwa unatoka ukumbini. Alisoma huku akiyakariri maneno yale kwa sauti ndogo. Mwandishi mmoja wa gazeti la Muungwana alilifuatilia kwa karibu tukio lile. Inspekta Tunu Nzowa alipewa jukumu la upelelezi. Alianza kazi kwa kumfuatilia mwandishi wa gazeti la Muungwana ndugu John Oscar. Haijulikani nini kilitokea, kilichoshuhudiwa ni kukutwa Inspekta akiwa amepoteza fahamu kwa kipigo ambacho ni wazi kusudio lake lilikuwa ni kummaliza, mwandishi ambaye alionekana kufahamu vizuri kilichotokea akakutwa ameuwawa kikatili, nukta! Alishangazwa na kile kilichoitwa taarifa kutokuwa na msaada wowote kwake, ilitosha kwake kama angeanza moja kwa moja kuifanyia kazi kutoka katika vyombo vya habari au watu wengine. Aliitazama taarifa ile na kugundua kuwa haina msaada wowote kwake. Akainua kiwiko cha simu yake ya mezani akapiga namba alizozihitaji. Alishanga ile namba kutopokelewa na Jenerali Nalinga kama alivyotarajia. “Hallow one fifty Rose hapa, bila shaka unahitaji msaada!” “Ndiyo naomba unitengenezee kitambulisho chenye jina la Frank Stefano mwajiriwa katika gazeti la serikali la THIS MONTH.” “Ok, baada ya masaa manne kazi yako itakuwa tayari, utakikuta kitambulisho nyumbani kwako una ombi lingine?” “Ndiyo.” Alivuta pumzi huku akitafakari jinsi upande wa pili utakavyopokea ombi lake. “Naomba tuonane!” “Oh, mara ngapi?” “Kwani tulishawahi kuonana?” Kwa mara ya kwanza akamsikia mwanamke yule mwenye amri za kiume akicheka. “Usijali utaniona maana inaelekea hutaki kuzingatia hata maonyo yangu.” “Lini?” “At the end of your mission.(mwisho wa kazi yako)” Simu ikakatwa. Aliamua kutafuta sehemu ambayo angepata chakula kwani alikuwa hajanywa hata chai mpaka kufikia muda huo wa saa nane kasorobo.
* * * Alirejea nyumbani kwake Meneo ya Tandika maghorofani saa moja na nusu. Wakati anafungua mlango wa chumba chake ndipo aliposikia sauti ya mama mwenye nyumba. “Baba samahani kuna mzigo wako hapa.” Alisikika yule mama wa makamo huku akiwa na bahasha kubwa ya kaki mkononi. “Ahsante mama, naweza kumuona mzee saa hizi.” “Hapana mbona toka juzi kasafiri, kaenda Kigoma mazishini kaka yake amefariki kumbe ulikuwa huna taarifa?” “Taarifa nilikuwa nayo lakini aliniambia anasubiri kodi yangu ili aweze kusafiri kwani alisema hana pesa kabisa.” “Kuna mpangaji kahamia chumba hicho……” Huku akimuonesha kwa kidole chumba ambacho kilielekeana na kile cha kwake. “…… Siku nne zilizopita, alipopata tu kodi yake ya miezi sita akaamua kukimbilia msibani ndio akatuachia maagizo kuwa hela ya kula tutaipata kutokana na kodi yako ya miezi miwili nyingine ni ile ambayo ulimkopesha alisema mnakatana juu kwa juu.” “Sawa mama lakini kodi ya miezi miwili itatosha kweli kuendesha maisha ya hapa nyumbani?” “Tutafanyaje mwanangu, tutajibanabana hivyohivyo bora tusukume siku.” Akaingiza mkono mfukoni akachomoa noti za shilingi elfu kumi kumi. “Hizi ni za kodi na hizi zitakusaidia kusukuma siku.” “Ahsante baba lo! Umenifaa kweli maana hata hapo dukani nilikuwa nadaiwa naona deni litakwisha leo.” Yule mama akaondoka huku akiwa na furaha kwani fedha za ziada alizopewa na Taisamo zilikuwa nyingi kuliko kiasi alichokuwa anamdai. “Ah! Samahani mama.” “Bila samahani.” Aligeuka yule mama na kusimama. “Amejitambulisha kwako aliyeleta hii bahasha.” “Hapana baba, ni kijana mmoja ambaye ni dereva teksi kasema mlishawasiliana.” “Ahsante.” Akasikika huku tayari mguu mmoja ukiwa chumbani kwake.
***
2 KUTAFUTA UKWELI
I Asubuhi ya Ijumaa hiyo ilimpambazukia Alex Taisamo kwa ishara tofauti tofauti. Kuku waliopokezana na kutambiana kwa ujasiri wa kuwika walizidi kupoteza usingizi wake. Hisia za jukumu zito alilopewa na hofu ya kufanya vibaya kazi hiyo zilianza kumuandama. ‘This is your first mission Liutenant,Goodluck’ Maneno ya mkuu wa majeshi ya ulinzi yalijirudia kichwani mwake. Kilichomtia hofu zaidi ni kitendo cha Jenerali kufikisha ujumbe yeye mwenyewe ingawa kulikuwa na Mnadhimu wa Majeshi Luteni Jenerali Ruhumbika, kwake hii ilibeba tafsiri ya ukubwa wa jukumu lililoko mbele yake. Akayafutilia mbali mawazo hayo ambayo yalikuwa yanakatisha tamaa na kupunguza morari ya kufanya kazi. Siku hiyo hakujisikia kabisa kufanya mazoezi kama ilivyokuwa kawaida yake, badala yake aliamua kuoga mapema. Ili kujiandaa kwa siku ile ambayo mwenyewe aliona kuwa ndiyo anaanza kazi rasmi. “Mafunzo ya hapa chuoni pekee hayatoshi, hizi ni kazi ambazo wakati mwingine akili yako ya kuzaliwa inahitajika zaidi.” Maneno ya mmoja wa walimu wake alipokuwa chuoni, Meja Mwita yalijirudia kichwani mwake. Wakati anatoka kuoga akapishana na binti mrembo ambaye naye alikuwa anaelekea bafuni akiwa na ndoo yake ya maji. Walipokutanisha macho yao alihisi moyo wake ukilipuka kwa mshtuko. ‘Bila shaka huyu ndiye mgeni aliyenieleza mama’ Aliwaza. Alitamani kugeuka lakini akaamua kupiga moyo konde. ‘Sijui ana mtu huyu?’ Aliendelea kujiuliza huku akifungua mlango wa chumbani kwake. Baada ya kuvaa nguo alikaa dakika kadhaa kitandani kisha akafungua ile bahasha yenye kitambulisho chake. Kilikuwa na mihuri yote muhimu, akatabasamu kwani zoezi lake lilikuwa limeenda jinsi alivyopanga. Dakika chache baadae akatoka na kuelekea kituo cha daladala. Ilikuwa yapata saa kumi na mbili na robo. Baada ya kupiga takribani hatua kumi akageuka na kumuona yule dada mgeni akiwa nyuma yake na mkoba begani. ‘Nimsubiri?’ Alijiuliza huku akiwa amepunguza mwendo. ‘Bila shaka ni vema nikimsubiri, kazi na dawa bwana?’ Alihalalisha kitendo chake hicho kwa kutumbukiza msemo wa mtaani. “Habari yako dada.” Alisalimia baada ya kuona amemsogelea. “Nzuri.” Alijibu kwa mkato huku akionesha kuwa na haraka zaidi ya Taisamo. “Karibu sana maana nimekuona jana lakini nasikia umeingia siku nne zilizopita.” “Ahsante.” “Naitwa Alex Taisamo, sijui mwenzangu…..” “Suzana Lusungu ukipenda niite teacher Suzy au teacher Lusungu.” “Aah, kumbe ni mwalimu nitakuita tu Suzy hilo la teacher mutaitana huko shule.” Akacheka na kuruhusu meno yake yaliyojipanga vema kuonekana. “Sijui unafundisha wapi Suzy.” “Jiandae, ni ya mtu binafsi iko Kinondoni.” “kumbe tunapanda gari moja mimi niko pale Ilala Boma. Ni mwandishi wa gazeti la serikali la THIS MONTH niko tawi la Ilala au unaweza kusema mkoa wa kihabari wa Ilala.” “Mbona mama mwenye nyumba aliniambia chumba hicho ni cha mwanajeshi?” “Hajui kuwa niliacha kazi siku nyingi.” Baada ya hapo kila mmoja alikuwa kimya huku akiwa na fikra zake kichwani. Taisamo aliutumia muda huo kulisanifu umbo zuri la Suzy lakini huku akijiuliza jinsi yule msichana alivyoweza kubaini mapema kazi yake. “Yaani alimuuliza Yule mama kazi yangu?” Alijiuliza huku akionekana wazi kutatanishwa na kitendo hicho. Alikuwa msichana mrembo mwenye uso wa duara, macho yake yalikuwa makubwa yenye kuvutia, kichwa chake kilibeba nywele ndogo ambazo hazikuwekwa dawa yoyote zaidi ya mafuta ya kawaida ya nywele. Kifua chake kilibeba matiti ya wastani ambayo yalimvutia Taisamo. Blauzi yake nyeupe na sketi ya rangi ya kaki yenye mpasuo mdogo ni vitu vilivyomfanya Taisamo ajisahau kwa muda. Miguu yake mizuri iliyojazia vizuri kwa kuumuka kama maandazi ya duara yaliyowekwa hamira ilizifanya fikra za Taisamo zipae mbali zaidi. “Karume..Magomeni…Kinondoni…Mwananyamala.” Mpiga debe aliwazindua viumbe wale wawili. Wakajitoma ndani ya gari huku wakiwa kimya, Suzy alikaa mbele kidogo huku Taisamo akikaa siti ya pili nyuma yake. Moyoni aliwalaumu wanaopenda kukaa siti za dirishani kwani kama si wao pengine angekaa siti moja na Mwalimu Suzy.
* * * Saa 2.30 Taisamo alipiga simu kwa Jenerali, kama kawaida Rose akapokea ile simu. “Habari Luteni.” “Salama Rose, kuna jambo naomba unisaidie kidogo…….” Akakohoa kidogo kisha akaendelea. “Nahitaji kumfahamu daktari aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu.” “Anaitwa Dokta Gabriel Kilonzo, yuko taasisi ya mifupa pale Muhimbili.” “Duh, uko faster binti au umemeza flash?” “Ushaanza vituko vyako.” Alisikika Rose huku akiangua kicheko. “Na lile la kufahamiana?” “Kwani unataka nini zaidi?” “Sura yako mrembo.” “Una matatizo Luteni, mimi ni mkuu wako wa kazi halafu nakaribia kustaafu bado unaniita mrembo?” “Ng’ombe hazeeki maini.” Akasikia kicheko upande wa pili simu ikakatwa. Baada ya kupata staftahi aliamua kwenda kuonana na Dokta Kilonzo. Alifika maeneo hayo ya hospitali saa 5.21. “Vipi bosi nikusubiri?” Aliuliza dereva wa teksi iliyomleta baada ya kupewa pesa yake. “Mpaka saa ngapi?” “ukimaliza shuguli zako.” “Ingawa ninakusudia kutochelewa lakini inaweza kutokea vinginevyo.” “Nitakusubiri bosi wangu kijiweni hakuna dili siku hizi watu wa bodaboda wametuharibia soko……” Hakusikia maneno ya mwisho aliyokuwa anawalani madereva bodaboda. Alipiga hatua za haraka haraka kuelekea kwenye lango la kuingilia hospitali.
***
Ilikuwa yapata saa sita na dakika Ishirini na tano wakati Dokta Kilonzo alipokuwa anakusanya nyaraka zake muhimu ili aondoke akasikia mlango unagongwa. “Fungua.” Mlango ukafunguliwa kijana mtanashati ambaye alikuwa amevaa shati la pinki na suruali ya kijivu akaingia. Alikuwa amevaa viatu vyeusi ambavyo viling’arishwa vema kwa dawa. “Karibu sana.” “Ahsante. Habari za kazi dokta” Alisalimia huku akikaa kwenye kiti kilichomuelekea dokta. “Marahaba, sijui nikusaidie nini maana ninataka kwenda wizarani mara moja.” “Naitwa Frank Stefano, ni mwandishi wa habari za uchunguzi katika gazeti la serikali la THIS MONTH.” “Karibu sana Bwana Frank, sijui nikusaidie nini?” “Ahsante, ujio wangu ni juu ya kifo cha makamu wa Rais mheshimiwa Ole Nunga, Bila shaka wewe ndiye uliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu.” “Labda nirekebishe kauli yako, mimi ni mwenyekiti wa Jopo la madaktari walioufanyia uchunguzi mwili wa marehemu.” “Unaweza kunifahamisha sababu za kifo chake.” “Ripoti yake tuliikabidhi Polisi na tulizuiwa kuzungumzia swala hilo kwa yeyote kwani tutaharibu uchunguzi wa Polisi.” “Ni nani alipokea taarifa hiyo?” “Hata hilo pia lilizuiwa.” “Kwani kuna kitu zaidi ya ajali ya gari kilisababisha kifo chake?” “Naona nimeshakujibu kiasi cha kutosha, hilo swala tulifunge. Nimekwambia tumezuiwa kutoa taarifa kwa yeyote sina la zaidi.” “Labda nikuulize swali la mwisho.” “Lakini lisihusiane na kifo cha Muheshimiwa.” “Sawa. Je! Imewahi kutokea katika maisha yako ya kazi kuwekewa pingamizi namna hii?” Dokta Kilonzo akatulia huku anakuna kichwa. “Kijana, nyakati hubadilika kwani katika maisha yangu ya kazi sijawahi kuufanyia uchunguzi mwili wa kiongozi yeyote hivyo inawezekana kabisa kukawa na utofauti katika uchunguzi wa mwili wa kiongozi mkubwa na kiongozi wa kawaida au raia.” “Tofauti inakujaje wakati tunahubiri haki sawa?” “Kiongozi ni kiongozi kutoa taarifa za kifo chake kunaweza kusababisha maafa hulijui hilo?” “Kwa hiyo kuna watu wakigundua kuwa ameuwawa na si ajali kama wanavyofikiri inaweza kusababisha vurugu.” “Kwa nini isitokee vurugu wakati ana wafuasi wake.” “Kwa hiyo waliomuua ndio ambao wameamua kuzuia hii taarifa kwa kuogopa vurugu?” “Kijana, hayo maswali yako naona umekusudia kuniharibia siku yangu. Inatosha, unaweza kuondoka au ukabaki peke yako hapa ofisini umenifanya niongee nje ya mipaka yangu.” Akachukua vifaa vyake na kunyanyuka huku akimwacha Taisamo kaduwaa.
*** Saa 10.43 alasiri; Alilakiwa na sofa ambalo muda mrefu limekuwa na upweke mkubwa, hakukumbuka hata kuvua viatu akaitawanya miguu yake mmoja juu mwingine chini. Aliaziacha fikra zake zitafakari matukio ya siku ile. Swali kubwa alilojiuliza ni kwanini ripoti ya kifo cha mheshimiwa imegubikwa na usiri mkubwa, kilichomshangaza zaidi ni kuona katika taarifa aliyopewa hakuna taarifa ya kidaktari juu ya kifo cha mheshimiwa Ole Nunga. Kwanini daktari alikuwa mkali sana alipomuuliza juu ya taarifa? Kwanini hakukuwa na Press conferance kama ilivyo ada. Aliliandika jina la daktari Kilonzo kisha akalizungushia alama nyekundu kwa kalamu yake. “Atasema tu” alinong’ona kwa sauti ya chini sana. Wakati akiwa kwenye lindi la mawazo mara akamsikia Suzy yule mpangaji wa chumba cha pili anaongea. “Karibu sana, karibu mpendwa.” Alisikia sauti ya Suzy, moyo ukamlipuka kwa wivu. Moyo wake ukaanza kwenda mbio pale alipokuwa anafikiria kufungua mlango ili amuone huyo mpendwa. Akatoka ili aweze kujionea mwenyewe, mshtuko alioupata ulikuwa ni zaidi ya alivyotarajia. Haraka akageuza sura yake na kuielekeza upande mwingine ili asiweze kuonana na yule mtu, hakutaka kabisa yule mtu afahamu kuwa yuko pale. Akatembea haraka haraka kuelekea nje. “Dokta! Ina maana dokta na Suzy wana uhusiano?” Alijiuliza huku akiwa amesimama kwenye mlango wa kuingilia chooni. Hakuingia, badala yake akarudi ndani kwani alihisi watakuwa wameshaingia chumbani. Dakika kumi na tano baadae aliwasikia tena wakiongea nje ya chumba. Akasimama mlangoni na kuwachungulia kwenye tundu la funguo.
* * *
“Naomba ulifuate lile gari.” Alihimiza Taisamo huku akimwonesha dereva wa teksi gari ambalo aliingia dokta Kilonzo. “Bosi si tuelewane kabisa.” “Unataka ngapi?” “Inategemea na urefu wa safari.” “Una mafuta ya kutosha?” “Full tank.” “Mfwate nitakulipa full tank kwanza halafu nyingine tutaongea.” “Bosi Ishu kama hizi za kufuatilia watu zinakuwa na malipo ya ziada.” “Oyaa anatuacha huyo, au nichukue gari lingine?” “Hawezi kutupotea yule dokta nafahamu mpaka nyumbani kwake nishawahi kumpeleka mara nyingi tu si ana dispensary hapo nyuma? Taisamo akatulia kidogo na kumwangalia yule dereva. “Nyumbani kwake, nikulipe kiasi gani?” Alipomtajia kiasi wakakubaliana kisha wakaanza kuifuata gari ya dokta Kilonzo Starlet nyeupe. “Kama haelekei nyumbani kwake tutafanyaje?” “we mfwate tu.” “Halafu kuhusu malipo!” “Una wasiwasi na mimi?” “Sio wasiwasi bosi ‘some times’ wateja mnakuwa watata.” “Ok, shika hizi.” Galasa yule dereva teksi alitoa macho ya uchu baana ya kuona akichotewa pesa kutoka katika kibunda cha noti. Akazihesabu na kuziweka mfukoni huku akiwa na furaha.Ni pesa nyingi kwa mtu wa kawaida. “Nafikiri hizi zinatosha kufanya kazi zangu za leo na kesho.” “Bila shaka mkuu.” Alijibu huku akikenua meno na kumtazama Taisamo kwa jicho la wizi bila shaka akimjumuisha katika kundi la ‘mapedeshee’ wasiofahamika. “Haya naomba tumfuate dokta sasa.” “Poa.” Alijibu huku akiliwasha gari lake.
* * *
Saa 3.30 usiku.Mlango uligongwa tena, safari hii mgongaji alitumia nguvu kidogo. Dokta Kilonzo ambaye alikuwa sebuleni akitazama Runinga akainuka taratibu kwenda kufungua mlango. “Karibu.” “Ahsante dokta.” “Habari yako.” “Nzuri , shikamoo.” “Marhaba,karibu ukae.” “Ahsante, bila shaka unanikumbuka.” Alianza Taisamo huku akijiweka sawa kwenye kiti. “Hapana, labda unikumbushe maana kazi zetu hizi zinatufanya tukutane na watu wengi sana.” “Naitwa Frank Stefano, ni mwandishi wa haba………” “Oooh, Mungu wangu! Ni nani kakuonesha huku nyumbani kwangu?” “Hukutaka nipafahamu?” “Kabisa, yaani kama suala ulilojia ni kuhusu kifo cha muheshimiwa, nikueleze wazi tu kuwa sina majibu.” “Leo utanijibu dokta.” “Nimekwambia sina majibu na ni hiyari yangu huwezi kunilazimisha.” Dokta alikunja sura wakati anajibu. “Ok, kwanza nataka kujua familia yako iko wapi?” “Kama swali ni hilo nitakujibu, wako Kilolo Iringa, sijui una maana gani kuuliza swali kama hilo.” “Nisingependa washuhudie jinsi nitakavyokisambaratisha kichwa chako kwa kukataa kujibu swali langu.” “Kwani ni lazima?” “Ni lazima sana.” Dokta akashtuka baada ya kauli ile kwani alikuwa anatazamana na mdomo wa bastola. “Sijawahi kusikia waandishi wanatafuta habari kwa mfumo kama huu.” “Sema hujawahi kuona sio lazima usikie kila kitu, ok sina muda wa mjadala utajibu maswali yangu la sivyo…” “Ni hiyari yangu, kwa sababu nikikujibu gharama yake ni kifo na nisipokujibu pia gharama ni kifo.” “Mimi ndiye niliyekuahidi kifo iwapo hutanijibu.” “Hata MKUU kaahidi kifo iwapo siri hii itatoka, tofauti yako na mkuu ni kwamba mkuu ana mkono kila kona wewe mkono wako ni mfupi sana.” “Mkuu ni nani?” “Kumbe umedhamiria kuniua, kwani hata nikikuambia Mheshimiwa alimalizwa kwa risasi itakusaidia nini?” “Kwa hiyo kauwawa kwa Risasi na Mkuu, Ni nani huyo?” Ghafla, akasikia sauti nzito nyuma yake. “Utamjua huyo mkuu muda si mrefu, shusha bastola chini na usithubutu kugeuka….”. Taisamo alisisimka kutokana na hisia kali ya adui aliyeko nyuma yake. Kitu kizito mithili ya chuma kikagusa kisogoni kwake. Kitu kilichomshangaza ni hiyo sauti, licha ya uzito wa kuigiza bado haikuwa ngeni sana kwake. Ameisikia wapi? Hilo ni swali gumu ambalo kwa muda huo hakutaka kulipa nafasi. “Kabla sijakulipua nataka kwanza ujibu maswali yangu.” Sauti hiyo isiyo na mzaha ilipenya kama mwale wa moto kwenye masikio ya Taisamo. “Wewe ni nani, umetoka wapi na umetumwa na nani kwa lengo gani?”. “Naitwa Frank, ni mwandishi wa gazeti la THIS MONTH.” “Usinitanie kijana, waandishi wa Tanzania hawawezi kutumia hata kisu sembuse bastola.” “Si kweli, wengi wamepitia JKT kabla ya kuajiriwa hivyo si jambo la ajabu.” “Usinifanye kuwa mjinga, kwa umri wako JKT ilikuwa imeshafutwa.” “JKT ipo mpaka sasa na inaendelea kuchukua vijana wazalendo.” “Wewe chizi acha kunipotezea muda nataka unieleze ukweli ni nani kakutuma? Pia napenda ufahamu kuwa zimebaki dakika tano tu nitakulipua” II
*** Ubaridi wa alfajiri ndio uliomzindua, alifumbua macho na kushangaa mazingira aliyopo. Wakati anafumbua macho alihisi kuwa yupo kitandani kwake, akatumia mkono wake wa kulia kupapasa akiamini kuwa hicho ni kitanda na pembeni yake yupo Tamasha. ‘Mchanga?’ Alishtuka baada ya kushika kitu ambacho kilikuwa tofauti na godoro lake, akaanza kuhisi ubaridi ambao si wa kawaida, akashtuka na kuendelea kuutembeza mkono wake wa kulia akashika kitu kingine ambacho kiliendelea kumstaajabisha. ‘Majani?!’ Lilikuwa jambo jingine la kushangaza.
Macho yake yalikuwa mazito lakini akalazimisha kufumbua, lilikuwa ni eneo geni kwake, alijihisi kama mtu aliyeko kwenye kilele cha mlima kwani kwa mbali aliweza kuona taa zikiwaka kwenye nyumba ambazo zilionekana kwa chini. Alijaribu kadri alivyoweza kuvuta kumbukumbu ya pale alipo lakini akili yake ilikuwa nzito. Baada ya dakika chache akaanza kurudiwa na fikra juu ya kilichotokea. James Makabi alikiona kifo mbele yake, hakuamini kama anaweza kupona iwapo gari lile litafika mwisho na kugonga vile vijumba vya wauza gongo, akaamua kufungua mlango na kujichomoa ndani ya gari. Alishuhudia vumbi zito ambalo lilitimuliwa na lile gari, kutokana na kasi ya lile gari alijikuta akiyumba na kusukumwa kwa kasi hadi kichakani. Akaangukia hapo kwenye kichaka na kuliona lile gari likizidi kuserereka kuelekea kwenye zile nyumba zilizoko bondeni. Akili yake ilimfanya aone kama kila kitu kinazunguka wakati huo. Dakika chache baadae akasikia kishindo kikubwa na kushuhudia moshi nzito ukipanda angani. “Mungu wangu….” Alitamka dakika chache kabla hajapoteza fahamu, hakukumbuka chochote mpaka muda huo aliozinduka. Fikra za ile ajali zikamkumbusha jina muhimu sana kwake, Mjomba Masharubu. Akajiinua pale kichakani na kujipongeza kimoyomoyo jinsi alivyoweza kufanya mauaji ya mtu ambaye mpaka muda huo hakumfahamu bila kukamatwa na polisi. Akili ya pesa alizo ahidiwa ikajirudia. Akajiinua na kuanza kutembea kwa mwendo wa kuchechemea. Alilikumbuka tukio zima kama sinema Fulani ya kusisimua. Akapapasa mifuko ya suruali yake, akatabasamu baada ya kugundua kuwa simu yake bado ilikuwemo. Akaichomoa na kuikagua. Bado ilikuwa mzima na ilimtambulisha kuwa hiyo ilikuwa ni saa 10.30 Alfajiri. Akatabasamu kwa mara nyingine baada ya kuwasikia wanadi swala kutoka misikiti mbalimbali. ‘Swalaa…swalaaa…swalaaa, saa kumi na nusuuu.’ Sauti hizo kali za spika zilipenya kwenye masikio yake. Na kumfanya asadiki kile alichokiona kwenye simu. Baada ya kujikung’uta vumbi akatembea taratibu kuelekea kule bondeni ambako gari liliangukia. Akayaona mabaki ya lile gari, hakuhitaji uthibitisho kuwa lazima lile gari lilijeruhi au kuua watu kule chini. Nyumba moja ilikuwa imeteketea kwa moto ambao vilevile alifahamu ulitokana na gari. ‘Hivi kulikuwa na haja gani kwa yule mtu kutumia gharama zote zile kumuangamiza mtu mmoja tu? Yule mtu ni nani na ana thamani gani?’ Alianza kujiuliza maswali ambayo yalimtisha hata yeye mwenyewe. ‘Kama yule mtu amethubutu kutumia gharama kubwa kuua hivi kweli hawezi kuniua hata mimi pale nitakapoanza kudai ujira wangu’ Swali hilo lilimshitua na kumfanya aanze kukosa raha. Furaha aliyokuwa nayo ikaanza kutoweka kama giza la usiku lililochomozewa na jua ghafla. “Nitanyaje iwapo polisi waliipata picha yangu wakati wa tukio!” Aliongea kwa sauti ndogo ambayo ni yeye mwenyewe aliyeisikia. Alianza kupishana na watu wawili wachache ambao walikuwa wanawahi kwenye shuguli zao. Fikra zikamfanya atembee mpaka Magomeni Kagera bila kujijua wakati dhamira yake ilikuwa ni kuelekea Magomeni Mikumi. Akatazama tena saa kwenye simu yake, ilikuwa ni saa 11.45. Akasimama kituo cha daladala cha Kagera na kusubiri gari zinazoelekea ubungo. Haukupita muda mrefu kabla gari aina ya DCM halijawasili. “Ubungo, Manzese, Kimaraaa…” Mpiga debe aliendelea kupiga makelele. Akajitoma ndani ya gari na kuchagua siti ambayo haikuwa na mtu. Akashangaa kuona dada mmoja ambaye alikuwa amekaa siti ya kushoto kwake akimwangalia kwa macho ya wizi kila dakika. Akaja kugundua hata mtu aliyekuwa siti iliyofuata naye alikuwa akimtazama kwa jicho lilelile. “Brother vipi mbona umechafuka sana kwa vumbi ulianguka? Halafu upande huu kuna damu kwenye shati inakuwaje?” Swali hilo likamzindua na kumfanya aandae majibu ya haraka. “Nilikuwa najenga huko ‘saiti’, tumekesha hukohuko. Hapa kuna kipande kidogo cha tofali kimeniangukia ndio maana nimeamua kurudi nyumbani kwanza halafu nitarudi tena maana tutakuwa huko kwa siku tatu.” “Dah, pole sana mimi nilishakufikiria vibaya.” Yule dada ambaye alikuwa anamtazama kwa jicho la wizi naye akaongea.
Aliendelea kutafuna nyama taratibu huku akishushia na bia baridi ya Kilimanjaro. Pembeni alikuwa amekaa na binti mrembo ambaye hawakuendana kabisa kiumri. Mara mojamoja aliupeleka mkono wake kunako kifua na kumpapasa mrembo yule. Kama ungebahatika kumuona pale alipokaa basi usingemtambua alikuwa na nani. Ni sauti yake tu ndiyo ingemfanya mtu aliyemzoea afahamu kuwa alikuwa Mjomba Masharubu. Siku kadhaa zilikuwa zimepita toka afanye kazi maalum iliyokuwa mbele yake, kama kawaida mkuu wake alimpa likizo isiyokuwa na muda maalum hadi pale atakapomuhitaji kwa kazi maalum. “Vipi dear mbona uko kimya sana.” Alisikika yule binti alikuwa amekubuhu kwenye mambo ambayo yalimzidi umri. “Usijali, hii ndio aina ya furaha yangu au unapenda kukaa na mtu mwongeaji.” “Inuka basi mi nataka tukacheze.” Aliongea huku akibana pua. “Mi nataka tukalale unasemaje?” “Wewe tu, lakini si tulishakubaliana bei ya kukesha?” “Kwani tutakuwa hatulali mpaka asubuhi,Usijali nitakupa hata zaidi ya ile.” “Ndio maana nakupenda dear, kwanza siku nyingi sijapata mwanaume wa kuninywesha na kunilisha kama wewe. Yaani leo nimeeinjoi si mchezo.” Aliendelea kubwabwaja binti yule ambae umri wake haukuzidi miaka kumi na sita. “Twende nyuma huku kuna guest.” “Unataka nilale Gesti za shilingi elfu tatu?” “Sasa wapi dear.” Pombe ilikuwa inafanya kazi yake na kumfanya aondokewe kabisa na aibu. Kabla hajamjibu simu yake ya mkononi ikaanza kuita. Aliitazama namba ile ngeni akataka kuipuuza lakini akashtuka baada ya kuona ni namba ambayo alikuwa anaifahamu sana. “Hallow nani mwenzangu.” “James naongea, nimekamilisha kazi yako nahitaji malipo yangu.” Sauti hiyo ilipenya kama kitu chenye ncha kali kwenye moyo wake. “Makabi?” “Ndiyo mimi.” Akashusha pumzi na kuganda dakika kadhaa bila kuongea chochote. “Ina maana…” “Niko hai.” “Ulipona?” “Sio nilipona nimepona.” Sauti ya upande wa pili ilimtia hofu. “Ok, nimekuelewa bwana Makabi uko wapi kwa sasa?” “Palepale uliponikabidhi ile kazi.” Kwa mara nyingine akajikuta akiingiwa na hofu na kumsahau kabisa kiumbe ambaye alikuwa amekaa naye muda huo. “Ok naomba unisubiri hapo hapo usiondoke sawa?” “Sawa mkuu nakusubiri.” Akakata simu. Akajishika kichwa dakika kadhaa kabla ya kuanza kupiga namba nyingine. “Hallow mr. Moyo.” “Ndiyo kaka nikusaidie nini?” “Una kazi?” “Sina.” “Kuna Bwege anatakiwa kuharakishiwa safari unaweza kunisaidia?” “Ni bwege kweli, nisijiandae kwa msako wa mbuzi kumbe ni chui.” “Acha woga bwana, nikisema bwege namaanisha kile ninachozungumza au siku hizi hatuaminiani? We fanya hiyo kazi mshiko tukutane palepale.” “Poa Kamanda wangu nakuaminia sana.” “Sasa subiri, nitakutumia maelekezo kwa meseji wapi uende maana muda huu yuko nyumbani kwake ananisubiri.”
*** Baada ya kugundua kuwa kifo alichosababisha kilikuwa cha Muheshimiwa Makamu wa Rais aliamua kuishi kwa tahadhari, hata pale alipokuwa anaongea na yule mtu anayejiita Mjomba Masharubu kuwa anahitaji pesa zake bado hakumwamini. Hili ndilo lililosababisha kumsubiri kwa hadhari kubwa. Akili yake haikumtuma kuwa anaweza kuzipata kiulaini pesa hizo. Alihisi jela ikinukia tena , hakuiona hata dalili ya msamaha wa Rais kama ule alioupata, tena safari hii alihisi kitanzi kikiwa mbele yake. Muda ulizidi kuyoyoma, kadri saa zilivyozidi kusogea ndivyo alivyozidi kuandamwa na hisia za hatari. Alijishangaa kuona amezidiwa na hofu. ‘Si bure!’ Aliwaza huku akiinuka pale alipokaa na kwenda nje, aliamua kujificha nyuma ya ndoo ya maua. Dakika chache baadae akasikia mchakato wa mtu aliyekuwa anatembea taratibu. Moyo wake ukazidi kupiga kwa kasi huku akitiririkwa na jasho kwa wingi. Mtu akaibuka kama kivuli kwa mwendo uleule wa taratibu. Aliendelea kukitazama kivuli kile hadi kilipofika usawa wa mlango ambako kulikuwa na mwanga hafifu wa mshumaa ambao ulitoka nje. Akashusha pumzi, baada ya kugundua kuwa yule ni mpenzi wake Tamasha. “Dear, dear… uko wapi?” Aliita Tamasha. James baada ya kujishauri kwa dakika kadhaa akaamua kujiondoa pale kichakani na kumfuatilia Tamasha. Sekunde chache tu wakati anainuka akaibuka mtu mwingine ambaye kama Tamasha naye huyu alionekana kama kivuli. Tofauti ya huyu na Tamasha ni kwamba alikuwa anatembea kwa tahadhari kama mtu anayevizia windo lake lisishituke. Hofu ambayo ilianza kutoweka ikajirudia tena safari hii akaanza kutetemeka. Alihisi meno yake yakigongana kwa hofu na baridi iliyotokana na woga. Tumbo pia lilimfanya mngurumo huku akihisi kubanwa na haja ndogo,alijihisi kama mtu ambaye amebanwa na pumzi. Yule mtu alitembea kwa mwendo ule ule wa kunyata hadi alipofika mlangoni. Akasita kidogo na kujibanza pembeni ya mlango. James akapatwa na mshituko mkubwa zaidi baada ya kumuona yule mtu akichomoa kisu kutoka kwenye ala ambayo ilikuwa karibu na mfuko wa kulia wa suruali yake. Akaingia ndani na kuurudisha mlango kwa nguvu. “Maskini Tamasha.” Aliongea kwa sauti ndogo huku akiinuka pale kichakani na kuliendea tofali ambalo lilikuwa sentimita chache kutoka pale alipojificha. Hisia za woga zilianza kumtoka na badala yake akatawaliwa na ujasiri mkubwa. Akavua kandambili na kukimbia kwa kasi akisimamia vidole vyake. Alipofika mlangoni akasimama na kutega sikio. “Sema haraka yuko wapi huyu mbwa wako.” Alifoka yule jamaa. Tamasha hakutoa jibu lolote zaidi ya kilio cha kwikwi. James alishindwa kuelewa yule jamaa kasimama upande gani wa mlango jambo lililosababisha ugumu wa dhamira yake ya kumshambulia kipande kile cha tofali. “Kwa kuwa hutaki kusema basi nitaanza na wewe halafu atafuata malaya wako.” “Mmmmmm!” Iliksikika sauti ya mtu aliyezibwa mdomo. Hakutaka kujiuliza tena akausukuma mlango na kujitoma ndani kwa kasi, kitendo hicho kilimshtua yule adui na kumfanya akose umakini. Kabla hajaamua nini cha kufanya akashtukia kipande cha tofali kikitua katikati ya uso wake, akayumba na kuanguka pembe ya kushoto ya sebule. Damu zilikuwa zinachuruzika kutoka usoni, akaanza kutapatapa hatimaye akakata roho. “Mungu wangu,Umeua dear .Kuna nini kinaendelea?” Aliuliza Tamasha. “Kwanza tumuondoe huyu mshenzi hapa mambo mengine baadae.” “Tutampeleka wapi?” “Nafikiri ni bora tuchimbe shimo hapo uani kisha tumfukie.” “Dear kwanini usitoe taarifa Polisi?” “Polisi? We unawajua polisi au unaongea tu! Kama unataka kujitia matatizoni hebu toa taarifa ndio utajua sheria za nchi yetu jinsi zilivyo.” “Kwanza niambie huyu mtu ni nani?” “Dear huyu mimi simjui, ninachofahamu ni kuwa katumwa na mjomba ni mambo mazito nitakusimulia kila kitu lakini kwanza tufanye hiyo kazi.” “Jembe tutalitoa wapi?” “Hapa tuna chepe na vipande vya chuma, vitatusaidia kuifanya kazi hiyo.” “Lakini mi nataka kuondoka dear.” “Unaweza kuondoka lakini ukumbuke kuwa nimeua kwa ajili yako, nilikuwa na fursa nzuri ya kutoroka lakini mapenzi yangu kwako ndiyo yaliyosababisha yote haya.” “Nisamehe dear, kweli leo ninge kufa.” “Hivyo hutakiwi kuondoka mpaka tumaleze jukumu hili kwa ukamilifu.”
*** “Dakika tano za kunilipua kwa kosa lipi?” Aliuliza Taisamo huku akijaribu kuvuta muda na kutafuta fursa ya kujiokoa. Wakati huohuo akamuona dokta akiinuka kutoka pale alipokaa. “Kaa chini dokta, kinywa chako lazima kikuponze umeonekana huwezi kutunza siri zilibaki sekunde chache ungemtaja Mkuu.” Alifoka yule mtu. Ghafla, taa zote zikazimika. Ni wakati huo ambao Taisamo alijikuta akiwapongeza na kuwashukuru Tanesco kwa kuleta mgao wa umeme. Alitumia nukta hiyohiyo kujirusha pembeni na ni wakati huohuo ndipo aliposikia mlipuko wa bastola. Mlipuko huo ulileta patashika hata kwa nyumba za jirani ambao wengi walikimbilia kule ulikotoka mlipuko. Hii ndiyo tabia ya Watanzania ya kupenda kukimbilia tukio hata kama ni la hatari.
Ikafuata milipuko minne ambayo iliwatawanya watu kadhaa ambao walikimbilia nyumbani kwa dokta kushuhudia nini kimetokea. Taisamo akasikia mlango unafunguliwa, akajua jamaa anakimbia. Naye akatoka mbio ili kumfuatilia huyo jamaa ambaye hakubahatika kumuona sura. TKD 2341. Alizisoma namba za gari lile ambazo zilisomeka kwa tabu kisha akaziandika kwenye simu. Akarudi ndani haraka na kuwasha tochi yake ndogo. Dokta alikuwa anagaragara sakafuni ndipo alipobaini kuwa kuna risasi zilikuwa zimempata dokta. “Dokta, dokta……” “Nenda kijana siwezi kupona.” Aliongea kwa ufasaha dokta ambaye alikuwa anavuja damu begani na kifuani. “Wacha nikuwahishe hospitali.” “No… Aaaa.. Nend… aaa ofis..kwangu …. Fung..ua kabat….. kuna rip..ya mauaji na chupa… yeny… Usss…..” Hakuweza kumaliza kauli yake akakilaza kichwa chini na kutoa macho. Alikuwa amekufa. Dakika chache baadae vikaanza kusikika ving’ora vya gari za polisi. Luteni Taisamo akaitumia nafasi hiyo kuchomoka ndani kwa kasi. Alikuwa na bahati kwani sekunde chache baadae nyumba ikazungukwa na Polisi ambao walikuwa wanamulika kurunzi kuzunguka eneo lile. Baada ya kuhakikisha kuwa yuko katika eneo ambalo macho ya Polisi hayawezi kumfikia akaanza kutembea taratibu hadi kituo cha teksi. Alikuwa anasikia njaa lakini maelekezo ya dokta juu ya faili la mauaji yalimfanya apuuze kula. “Nifikishe Muhimbili.” Aliongea baada ya kuingia kwenye teksi iliyokuwa kwenye foleni. “Poa mkubwa.” Alijibu dereva wa teksi.
*** “Haya sasa nieleze yaliyokusibu maana juzi nimekuja mchana we haupo, usiku pia haukuwepo jambo la kushangaza zaidi muda mwingi ulikuwa umezima simu.” “Dear haya yote yamesababishwa na mjomba, si unamkumbuka yule mjomba aliyekuja ile siku niliyochelewa kurudi?” “Ndiyo, sasa yeye anahusika vipi?” James akamsimulia Tamasha kila kitu kilichotokea. “James, ina maana wewe ndiye uliyemuua makamu wa Rais?” Aliuliza Tamasha kwa hamaki huku akiwa ameyatoa macho kwa mshangao. “Sina uhakika Tamasha.” “Huna uhakika vipi wakati umeshaeleza kila kitu hapa!” “Sina uhakika kwa sababu hofu ilinifanya niigonge vibaya ile gari yaani tofauti na vile nilivyoelekezwa na sikuona uwezekano wa Muheshimiwa kupoteza maisha.” “Mbona vyombo vyote vya habari vimeandika kuwa alikufa kutokana na ajali ya gari?” “Unaviamini vyombo vyetu vya habari?” “Unataka kuniambia waandishi ni waongo?” “Sina maana hiyo Tamasha mpenzi, kwa sheria za nchi yetu mwandishi hana ubavu wa kuandika kila anachokiona au kukiamini yeye kuwa ni sahihi.” “Una maana gani?” “Waandishi hawako huru kuandika itakiwavyo hususani wanapogusa maslahi fulani.” “Huoni kama umejitia matatizoni kwa kukubali jukumu hilo?” “Nisingekubali ningeuwawa.” “Mtu mmoja tu anakutisha James?” “Uwe unafikiria Tamasha mpenzi, yule mtu ana jeuri ya pesa na sina uhakika ni nani yuko nyuma yake pia ndiye aliyefanya mpango nikatolewa gerezani kwa msamaha wa Rais!” “Unahisi kuwa kuna watu wako nyuma yake?” “Sio kwamba ninahisi, kuna watu wazito sana nyuma yake.” “lipi linalokufanya uamini hivyo?’ “Lile gari nilipewa wiki moja kabla lakini nimeweza kuzunguka nalo bila kukamatwa, kila trafiki aliyekuwa analiona alikuwa analiheshimu sana, yaani ilikuwa kama kuna trafiki maalumu ambao wanafahamiana na Mjomba wamepangwa barabarani.” “Sasa utafanyaje ili kujinusuru maana naona kama mjomba alikusudia nawe pia ufe lakini Mungu kakunusuru.” “Ni kweli Tamasha na hapa inabidi niondoke, nahitaji kuishi kwa kujificha mpaka mambo yatakapopoa.” “Usithubutu kuendelea kudai zile pesa mpenzi.” “Dear, siwezi kukubali. Nimeingia gerezani, naishi maisha magumu hawezi kunifanya bwege hata kama ni komando, nitapambana naye mpaka tone la mwisho lakini pesa yangu atalipa tu vinginevyo niwe nimekufa.” “Hilo halitakusaidia mpenzi, uhai ni muhimu kwako kuliko chochote. Pesa zinatafutwa lakini si uhai.” “Una maneno mazuri mpenzi, lakini ninaomba kitu kimoja tu kutoka kwako. Kwa yote uliyoyasikia na utakayoyasikia naomba mdomo wako uweke super glue.” “Sawa mimi niko tayari lakini hiyo mipango yako naona unatafuta kifo.” “Dear, maisha yangu yamegubikwa na mikosi kwa hiyo sina cha kupoteza zaidi yako. Nimekaa gerezani kwa kosa ambalo si langu, sasa umefika wakati wa kuingia gerezani kihalali.” “Kwa hiyo umeamua kulitafuta gereza kwa nguvu zote?” “Sina maana hiyo mpenzi, natafuta haki yangu ambayo imepotea, napigania haki yangu ambayo watu wachache walioko madarakani wameimiliki.” “Huoni kama na wewe unahusika kupoteza haki za watu kwa kudhamiria kumuua Muheshimiwa?” “Kweli mwanzo nilikuwa na mawazo hayo, lakini nilipokutanisha macho yangu na sura yake iliyojaa upole na busara moyo wangu ukasita na ndio maana nikamuhurumia na kuligonga gari lake ubavuni.” “Sasa ni nani kamuua?” “Hicho ni kitendawili kingine dear, nashindwa kuamini kama alikufa kwa ajali ile.” “Kwa hiyo utaishi wapi?” “Hii nyumba nitapangisha, yaani kesho nitaanza kuongea na madalali.” “Na huyu uliyemuua hapa atakapoanza kutafutwa itakuwaje?” “Nitamfahamisha mjomba kuwa mtu wake nimemuua.” “Huoni kuwa utakuwa unahatarisha maisha yako.” “Hapana, nafikiri itasaidia kumtia hofu.”
*** Nesi Belinda alikuwa anajaribu kupiga simu bila mafanikio, simu ilikuwa inaita lakini haikupokelewa. Kulikuwa na dharura ambayo ilimuhitaji dokta Kilonzo kuja kuitatua. Ilikuwa ni kawaida yao inapotokea dharura kama hiyo kuitwa madaktari maalum ambao walikuwa zamu. “Hallow Anna, njoo unisaidie najaribu kumpigia dokta lakini hapokei simu na leo ni zamu yake.” Aliongea huku akionesha kuwa na hasira. Hakumuona mtu aliyesimama nyuma yake. “Na inavyoonekana alikuwa hapa ofisini muda mfupi uliopita maana huku kwenye chumba chake amepekuapekua vitu na hata kabati lake amesahau kufunga.” Akakata simu huku akisonya kwa hasira. Ghafla akasikia sauti kutoka nyuma yake. “Hutomuona tena dokta.” Akashtuka na kugeuka, hapo ndipo alipokutanisha macho yake na Taisamo. “Wewe…….” Alishtuka na kutaka kupiga kelele kwa hamaki kabla Taisamo hajamuonya kwa ishara ya kuweka kidole mdomoni. “Shhhhiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, Naomba unisikilize kwa makini nesi, hivi ninavyozungumza Dokta kapigwa risasi na watu wasiofahamika nyumbani kwake Tabata, kuna matatizo mazito sana yamejitokeza hivyo naomba ushirikiano wako.” “Wewe ni nani?” Aliuliza Nesi huku akiwa ametoa macho kwa hofu. Usiwe na hofu, mimi ni askari maalum ambaye nimekuja kufanya kazi muhimu. Dokta kabla ya kifo chake aliniagiza kuja kuchukua nakala ya ripoti ya muheshimiwa Makamu wa Raisi pia alitaja kitu kama chupa sijaelewa bado kuna uhusiano gani kati ya hiyo ripoti na chupa.” “Maskini dokta, sasa ni nani kafungua kabati lake wakati funguo anazo mwenyewe?” “Inaonekana hao waliomuua ndio wamekuja kufungua, naomba unisaidie kama naweza kupata hiyo ripoti.” “Mimi nilikuwepo wakati mwili wa muheshimiwa unafanyiwa uchunguzi, zimetolewa risasi mbili mwilini mwake ambazo alizihifadhi kwenye chupa maalum ambayo iko pamoja na ripoti, lakini mimi nilizuiwa kuzungumza chochote na dokta alisema kufanya hivyo ni hatari kwa usalama wangu.” “Kuna yeyote mwingine anayefahamu kuwa ulikuwepo wakati wa uchunguzi?” “Sio kwamba nilikuwa chumba cha uchunguzi huko sikuruhusiwa, siku hiyo nilikuwa zamu ndipo dokta alipokuja na kunionesha risasi mbili ambazo zimetolewa kwenye mwili wa Muheshimiwa, siku ya pili akaniambia mambo ni mazito kile alichonieleza basi nisimueleze yeyote na lau kama angejua basi hata kunidokeza asingenidokeza akanisimulia mambo mengi ambayo yalinitetemesha na kunionya nisithubutu kuzungumza kwa yeyote.” “Ok, haya uliyonieleza hakikisha unakuwa msiri kama ulivyoelezwa na dokta vinginevyo ni hatari kwa maisha yako. Ok sasa naomba unionesha kabati lake ambalo anahifadhi vitu muhimu, halafu tupange muda wa kukutana ili tuweze kuongea hayo mengine .”
“Kabati ni hilo lililofunguliwa na hilo faili na chupa ya risasi zilizotolewa mwilini ziko chini kabisa, faili lina jalada la rangi nyekundu.” Taisamo akaanza kulitafuta lile faili lakini hakuliona ingawa alikuwa na bahati ya kuiona ile chupa ambayo ilisadikiwa kuwa na hizo risasi zilizotolewa katika mwili wa muheshimiwa. “Ok, inaonesha wameshachukua hilo faili. Kikubwa nitahitaji maelezo kutoka kwako kama ulivyonieleza, kutokana na wakati tulio nao hatuwezi kuongelea hapa hayo mambo naomba upange sehemu ya kukutana.” “Sawa lakini tumefahamiana juujuu sana mimi naitwa Belinda Kagaruki naishi Kinyerezi mtaa wa Kifuru, nyumba no.23, mjumbe wangu anaitwa mzee Mvula, nafahamika sana hapo.” “Umepanga au ni nyumba yako?” “Ni nyumba yangu.” “Hongera sana.” “ahsante.” “Nesi nashukuru kwa maelezo yako mazuri mimi utanifahamu zaidi muda huo tutakaokutana, naondoka kumbuka kuwa msiri kama nilivyokueleza la sivyo utakuwa una hatarisha maisha yako.” “Dokta amekufa!” Nesi alijikuta akiongea kwa sauti ya chini wakati Taisamo anaondoka ndani ya ofisi ile.
*** “Sasa umepata faida gani baada ya kumtisha Mjomba?” Aliuliza Tamasha kwa sauti ya kulaumu kwa kitendo kilichofanywa na James cha kumpigia simu Mjomba Masharubu. “Tamasha, mimi ni mwanaume nimeumbwa ili kuja kupambana. Sasa huu ndio wakati hasa wa kuonesha uanaume wangu.” “Sawa dear lakini tambua kuwa nyuma yako kuna mwanamke ambaye anakutegemea na pengine kitu usichokifahamu ni kuwa nina kiumbe chako tumboni unafikiri tutaishije bila wewe pale utakapokuwa umeuwawa?” “Kwani mimi tu ndio ninayestahili kufa? Hata yeye anaweza kufa kwani huu ni mchezo ambao hauna mwenyewe yeyote anaweza kushinda.” Aliendelea kushikilia msimamo wake. “Umepatwa na nini dear mbona umebadilika sana?” “Nina hasira na mambo mengi, hao hao walionisababishia kifungo ndio walioniachia huru, eti msamaha wakati kosa lilikuwa la waziri. Alipita upande si wake akasababisha ajali na bado mzigo wote wa vifo vile nikabebeshwa mimi, walewale watu wake wamekuja kunitoa ili wanitie kwenye msukosuko mwingine kisha waniue, safari hii ama zangu ama zao.” “Unajiapiza bure kwa hasira wenzio wana silaha wewe una nini?” “Akili pia ni silaha.” “Kuwa makini dear kumbuka hasira ni hasara.” “Sawa, unaweza kuwa sahihi lakini mbona nimepata hasara kabla ya hizo hasira, naomba unielewe Tamasha mpenzi kamwe sitorudi nyuma, nitakutii kwa lolote katika mapenzi yetu lakini si hili la kuachana na hawa jamaa kwani hata nikiachana nao bado watakuwa wananiwinda tu.”
*** Baada ya kuhangaika kwa dakika kadhaa na kuuliza kwa watu kama watatu alifanikiwa kuiona nyumba namba 23 iliyopo mtaa wa kinyerezi eneo la kifuru. Nyumba hiyo ilikuwa imezungukwa na nyumba kadhaa ambazo ujenzi wake ulikuwa haujakamilika, baadhi ya nyumba hizo tayari zilikuwa zimeshahamiwa bila shaka na watu waliochoshwa na maisha ya kupanga. Nyumba nyingine zilikuwa zinaendelezwa ujenzi wake. Nyumba ya Belinda ilikuwa imejengwa kwa mtindo maarufu wa ‘L’ huku ile sehemu iliyotakiwa kuwa na nyumba kubwa ikiwa na mchanga na kokoto ambazo zilionesha kukaa hapo zaidi ya miaka miwili. Kulikuwa na kila dalili ya ujenzi wa nyumba hiyo kwenda kwa mwendo wa kinyonga bila shaka kutokana na maslahi madogo ya manesi ambayo hayakulingana na ukubwa wa majukumu yao. Nyumba nyingi za eneo hili zilikuwa hazijavutiwa umeme. Taisamo alishuhudia kupitia nyufa za mlango mwanga ambao alihisi kuwa ni wa kibatari. “ngo,ngo,ngo” Aligonga mlango kwa dakika kadhaa huku akilakiwa na ukimya. Akaamua kupiga namba ya yule Muuguzi. Hapo akapokelewa na wimbo wa taarabu ambao bila shaka ulikuwa unatoka katika simu ya nesi Belinda huko ndani. Akaamua kuvuta subira huku roho yake ikimtuma kuwa labda nesi yuko na mwanaume huko ndani. Ni wazo hilo ndilo lililomfanya asogee upande wa dirisha ambako alihisi kuwa ni upande wa chumba cha kulala ili aweze kusikia angalau mihemo ya mahaba. Bado ukimya uliendelea kutawala. Aliamua kuerudi tena mlangoni na kuendelea na zoezi la kugonga. Hatimaye alijikuta akichoshwa na zoezi lile na kuamua kujaribu kufungua mlango, mlango ukafunguka. Akaanza kupatwa na hisia kali ambazo zilisababisha msisimko wa mwili, vinyweleo vikasimama na hisia za woga zikamtawala. Mapigo ya moyo wake yalianza kwenda kasi pale alipoona vitu vikiwa vimetawanywa hovyo pale sebuleni, akaona kitu kingine ambacho kilimshtua zaidi na kuvuta hisia zake, akatazama nyuma, kushoto kisha kulia hakumuona yeyote, akachomoa bastola yake aina ya SIG P 228 yenye kiwambo cha kuzuia sauti. Kwa mwendo wa kinyonga huku akiwa na hisia kali za hatari mithili ya mtu anayetembea kwenye kichaka chenye nyoka wengi wenye sumu kali. Hali hiyo iliwahi kumtokea walipokuwa kwenye zoezi maalumu la kutegua mabomu yaliyoachwa wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Angola. Asingeweza kuisahau siku hiyo ambayo waliingia ukanda wenye mabomu mengi zaidi ambayo yalitegwa ardhini. Alikumbuka vema kauli ya Meja mstaafu Silvester Rutakinikwa, “Ukanda tulioingia ni wa hatari, tumeshafanya uzembe wa kuingia eneo hili bila kulifahamu vizuri hivyo kutoka ni hatari na kuendelea kubaki ni hatari jambo la muhimu tuombe Mungu huku tukiendelea na zoezi letu.” Aliongea Meja katika zoezi hillo lililoshirikisha wanajeshi kumi na sita wanne kutoka Tanzania ambao walikuwa wakiongozwa na mtaalamu wa silaha ambaye alitegemewa sana hata na jeshi la umoja wa mataifa meja Rutakinikwa ambaye aliongozana na askari watatu ambao walitolewa maalumu na jeshi ili kuja kupata mafunzo kwani Meja alikuwa anakaribia kustaafu. Pia walikuwepo wanajeshi wanne kutoka Msumbiji ambao waliongozwa na Kapteni Saimon Chavara, huku wale wanne wa angola wakiwa chini ya Luteni kanali Jonas Dosantos pia walikuwepo wanne kutoka kenya ambao walikuwa chini ya Meja Frank Omondi. Hata hivyo kutokana na umahiri wa meja Rutakinikwa ambaye alisomea taaluma ya silaha mbalimbali kutoka vyuo vya kijeshi vya China, Urusi, Marekani, Cuba na Israel walifanikiwa kutoka salama eneo hilo la hatari. Taisamo akapandishwa cheo baada ya zoezi hilo kutoka koplo mdogo ‘lance corporal’ na kuwa Koplo kamili, pia akajikuta akihamishiwa kitengo cha Interejensia yaani Millitary Inteligency akapangiwa UNIT ya 12 ambayo ilikuwa na jina la Snake ikiongozwa na Meja Mwaikambo. Akapewa namba ya utambulisho ya 150, huko alipandishwa vyeo na kujikuta akiwa Luteni. Kikazi alikuwa anafahamika kama Taisamo kwa waliomfahamu kama Taisamo, lakini kikazi zaidi alifahamika kama 150, toka aingie kwenye kitengo hicho alikuwa hajawahi kufanya kazi yoyote kubwa zaidi ya upelelezi wa kawaida wa kukusanya habari hususani kutoka katika makundi ya wanajeshi wenzao, pia hakupewa uzito wowote wa umahiri katika kitengo hicho nyeti zaidi ya kuchukuliwa kama mtu ambaye yuko kwenye mafunzo zaidi. Hii ndiyo sababu alipopewa jukumu la kufuatilia mauaji ya Makamu wa Raisi alipatwa na mshtuko kutokana na udogo wa nafasi na uwezo wake. Alitegemea zaidi kazi hiyo kuongozwa na Kapteni,meja au Luteni kanali.
Wakati kumbukumbu ya yote haya ikijirudia kichwani mwake bado alikuwa ameikamata barabara bastola yake yenye kiwambo cha kuzuia sauti. Licha ya mwanga hafifu wa mshumaa ambao ulikuwa juu ya stuli ambayo haikukumbwa na zahama ya kuangushwa kama stuli na viti vingine, aliweza kuyaona vema matone ya damu ambayo yalishaanza kuganda. Akapiga hatua huku umakini na hisia za hatari zikiongezeka. Akatembea kufuata yalikoelekea matone ya damu, alikuwa anajihisi wazi kukifuata kifo lakini hakutaka kurudi nyuma. Alipoangalia mlango wa kuingilia chumbani ulikuwa umefunguliwa kidogo sana kana kwamba kuna mtu alikuwa anataka kuchungulia kinachoendelea sebuleni. Alipotazama chini ili kujua kilichozuia mlango ule kujifunga au kufungwa moja kwa moja akajikuta akipatwa na mshituko. “My God!” Alitokwa na neno hilo huku macho akiwa ameyaelekeza pale sakafuni.
*** Alishajenga mazoea ya kukusanya magazeti yote ya asubuhi na yale ya jioni na kisha kuanza kupitia moja baada ya jingine ifikapo saa mbili na nusu usiku. Hakuwa na tabia ya kupuuza gazeti lolote, hata yale yaliyoitwa magazeti pendwa au ya udaku hakuacha kuyasoma. Sio kwamba alipenda kusoma habari za wasanii na vituko zilizoandikwa kwenye magazeti hayo ambayo watanzania wengi hupenda kuyasoma, kilichosababisha ni kanuni yake ya kutopuuza na kudharau habari yoyote. Hii ilikuwa ni sehemu ya majukumu yake ya kazi ambayo alijipangia mwenyewe ingawa kimsingi idara ilichagua watu maalum wa kufanya kazi hizo. Mara nyingi alijiuliza kilichowavutia watanzania kusoma magazeti hayo ambayo wengi huyaita ya udaku, lakini mwishowe alipata jibu kuwa watanzania wamechoshwa na habari za siasa zao ambazo mara nyingi zimekuwa zikiwapa msongo wa mawazo. Siasa ambazo hazina matumaini ya kuleta ukombozi wa kweli kiuchumi na kijamii. Ni siasa hizo ambazo ziliwafanya watanzania watumie muda mwingi kwenye mambo ya kuwaburudisha kwani walikuwa wanakatishwa tamaa. Mfano mzuri ni magazeti ya siku hiyo ambayo mengi yalikuwa na vichwa vya habari vyenye kuleta hasira kwa mtanzania. Moja ya magazeti hayo lilikuwa na kichwa cha habari kilichosema KILA MTANZANIA ANADAIWA DOLA LAKI NNE, hiyo ilikuwa imeandikwa kwenye gazeti la chama KIKULACHO, pia alisoma habari nyingine kwenye gazeti lingine lilikuwa na kichwa cha habari, MABILIONI YA WATANZANIA YATUMIKA KUNUNUA MAGARI MABOVU YA SERIKALI akaiona nyingine ambayo bila shaka ilikuwa ni ya kutia hasira kwa mtanzania SERIKALI YAJIANDAA KUTOKOMEZA UMASKINI KATIKA MPANGO WA MIAKA 250 IJAYO. Habari hizi zote bila kujali ni za uchumi, kijamii au vyovyote vile watanzania waliziweka kwenye kundi moja la habari za siasa, muda wao wa kuumiza kichwa kwa habari hizi ulikuwa umekwisha na walichohitaji wao ilikuwa ni burudani tu ili nafsi zao ziweze kutulia. Hii ndio sababu pekee iliyosababisha vijana wengi wa kitanzania kupenda magazeti hayo ambayo yaliwarudishia furaha yao iliyopokonywa na viongozi wabovu wenye uchu wa madaraka na pesa za wavuja jasho, viongozi ambao msamiati uliwapamba kwa kuwapa jina lililojengwa kitafsida zaidi yaani MAFISADI lakini ukweli ukibaki kuwa ni WEZI, MATAPELI au MAJAMBAZI na kama si kuogopa hatua za kisheria ilifaa pia kuitwa WASHENZI. Muheshimiwa Wahuva Kilale mkurugenzi wa Usalama wa Taifa aliyaangalia haya kwa jicho la upofu, sio kwamba hakutambua kwamba mambo yanaenda sivyo ndivyo isipokuwa hata yeye ameingia madarakani kwa njia hizohizo zisizokuwa rasmi. Unaweza kufikiri ‘CV’ yake ndiyo iliyomuingiza madarakani, la hasha! Yeye alikuwa ni mume wa rafiki wa mke wa Rais, kwa mgongo huo naye akawa rafiki wa Rais, kuanzia wakati wa kampeni akawa mstari wa mbele kupambana ili muheshimiwa aingie madarakani, yeye ndiye alikuwa kiunganishi na wahariri wa vyombo vya habari ambao walipokea pesa nyingi ili kulisafisha jina la muheshimiwa na kumfanya aingie Ikulu. Miezi michache baada ya muheshimiwa kuingia Ikulu ndipo akapata zawadi hiyo ya ukurugenzi. Tatizo lililojitokeza ni Idara hiyo nyeti kutoendeshwa kitaalamu, badala ya kuwa na jicho kali la kuwatazama wanasiasa idara hiyo ikajikuta ikiwa inatazamwa kwa jicho kali na wanasiasa. Ikabadilika na kuwa idara maalumu kwa ajili ya usalama wa viongozi maalumu kwa maslahi maalumu. Jicho la kawaida haliwezi kuilaumu idara hii kwa kufikiri inafanya kazi yake sawasawa, jicho linaloona mbali pekee ndilo lingeweza kuyaona makosa ya idara hiyo ambayo yamejenga uzio wa kutotaka kufuatiliwa na kulaumiwa. Lakini kimsingi ilistahili lawama kubwa sana kwani ilitakiwa kujikita hata katika mambo ya kiuchumi na kiteknolojia. Ujasusi ambao hufanywa na nchi kama china, pakistani na nyingi zilizoendelea si wa kiusalama tu, nchi hizi zina ujasusi maalumu wa kiuchumi ‘Economic Inteligency’ na aina nyingine za ujasusi ambazo ni kwa manufaa ya nchi. Lakini hii ya kwetu inaonekana zaidi kwenye ‘Politician security service inteligency’. Akiwa amezungukwa na magazeti hayo ambayo alianza kuyapitia kwa kusoma vichwa habari, mara simu yake ya mkononi ikaanza kuita. Akaitazama namba ya mpigaji. “Halow, habari Mr. Masharubu.” “Habari mbaya mkuu.” “Vipi kila kitu si kimeenda vema?” “Hapana kuna makosa yalijitokeza, yule mtu ambaye nilimtumia kusababisha ajali bado yuko hai na ameshaanza kusumbua, si hivyo tu inaonesha kuna mtu ndani ya system anafuatilia kadhia hii kwa umakini mkubwa sana na amepiga hatua kubwa kiasi kwani ameweza kumfikia hata Dokta na kusababisha tumfunge mdomo, Sijajua ni nani miongoni mwetu umempa kazi hii kwani anajiita Mwandishi wa habari lakini ana kila dalili za ukachero ingawa anaonesha hayuko makini na si mzuri sana au ni mgeni wa kazi.” Akatulia dakika kadhaa bila kujibu. “Ok, huyo dereva anataka nini?” “Anataka pesa zake milioni mia mbili na hamsini, shamba na gari ambavyo tulimuahidi ili aweze kutunza siri.” “Unayo picha yake?” “Ninayo mzee.” “Ok scan hiyo picha kisha uitume kwenye email yangu haraka, mia mbili hamsini milioni atazikosa na badala yake anastahili zaidi risasi ya kichwa au kitanzi. Nipe habari za huyo mwingine.” “Huyo mwingine haeleweki vizuri tumejaribu kufuatilia mfanyakazi mwenye jina lake katika gazeti la THIS MONTH tumegundua kuwa mfanyakazi mwenye jina hilo amekufa siku nyingi, jambo la kutatanisha zaidi kuna mtu mwingine ameonekana kufuatilia nyendo zake yaani inatatanisha mkuu si mchezo yaani anawindwa tena na mtu ambaye si wa kwetu.” “Huyo mfuatilieni taratibu na kwa umakini isije kuwa kuna msaliti miongoni mwetu nahitaji habari na picha zake kabla hatujajua nini cha kufanya.” Simu ikakatwa.
***
Simu yake ikaanza kuita dakika chache baada ya kumaliza maongezi na mkurugenzi. “Ndiyo Makabi unasemaje?” Aliuliza baada ya kuitambua namba ya mpigaji. “Pesa zangu Masharubu, una masaa 48 tu, la sivyo nitaanika kila kitu hadharani.” “Ok lakini nilishafika nyumbani kwako na nimekuta bango, nyumba inapangishwa unategemea ningekupatia vipi huo mzigo wako?” “Mimi sio mpumbavu Masharubu, ninachotaka ni fedha zangu na jinsi ya kukutana unatakiwa kupokea maelekezo kutoka kwangu.” “Ok, unatakaje sasa.” “Nafasi ninayokupa ni ya kuchagua muda tu ndani ya hayo masaa 48, nataka uniambie ni saa ngapi naweza kuzipata hizo fedha?” “Saa nne na nusu asubuhi, kesho.” “Una uhakika?” “Ndiyo.” Sauti ilijibu kwa utulivu uliomtia hofu muulizaji. “Ok, nitakusubiri Buguruni sheli njoo na begi langu la pesa sitaki tena ujanja Masharubu.” “Mbona ni eneo la wazi sana huoni kuwa ni hatari kukabidhiana pesa eneo hilo.” “Masharubu usitake kuzungusha maneno, wewe ni hatari kuliko hilo eneo niletee pesa zikiwa kwenye begi na si briefcase mimi ndo nitajua cha kufanya.” “Sawa Kijana tukutane hiyo kesho.” Alimaliza huku uso wake ukifanya matuta ya hasira yaliyoufanya uso wake utishe kama simba anayejiandaa kushambulia. *** Anaitwa Mary, umri wake unakadiriwa kufikia miaka 25, alitoka Iringa kuja kufanya kazi jijini Dar es salaam, aliahidiwa mambo mengi sana na mwajiri wake aliyemleta. Maskini hakujua kuwa anakuja kuwa mtumwa wa ngono. Mwajiri wake alimtumikisha kwa biashara hiyo inayovunja heshima na utu kwa miaka kadhaa kabla hajaamua kuachana nae na kuifanya biashara hiyo yeye mwenyewe. Amekuwa ni mzoefu kwenye biashara hiyo kwani kwa miaka 11 amekuwa ndani ya biashara hiyo ya kuuza mwili kwa pesa kidogo. Alianza akiwa na miaka 14 tu, yaani muda mfupi baada ya kumaliza darasa la saba. Uzoefu huo umemfanya akutane na watu mbalimbali wenye tabia za aina tofauti tofauti, ni biashara hiyo ambayo mara moja moja imemfanya ajikute akiwa chini ya himaya ya majambazi ambao walimshirikisha katika baadhi ya kazi zao hususani za uporaji wa magari. Pia amewahi kushiriki matukio kadhaa ya kijambazi akitumika kama chambo kwa wanaume dhaifu ambao hukosa umakini pale wanapokuwa mbele ya Mwanamke mrembo wa sura kama Mary. Ni aina ya wanaume ambao hata wanapofanya biashara huweza kukosa umakini kwa sauti au manukato ya warembo ambao huwa ni wateja wao. Mfano mzuri ni wale wanaouza magenge ya nyanya ambao hujikuta wakiongeza zaidi na zaidi pale binti anapomlewesha kwa uzuri au mbwembwe zingine ambazo wakati mwingine hufanywa makusudi. Sio siri alikuwa ameumbika, Uso wa duara ambao ulibeba pua iliyochongoka kama ya msomali ulimfanya mwanaume kumtazama mara mbilimbili, macho yake makubwa ambayo yalikaribia kuwa ya duara yangeweza kubadilisha mapigo ya moyo ya mwanaume yeyote anayetazamwa. Macho hayo pia yangeweza kubadilisha hata mapigo ya moyo ya mwanamke mwingine ambaye angeyatazama kwa wivu. Kifua chake kilibeba matiti ambayo yalisimama vema kwa msaada wa sidiria, kifua chake kilikuwa ni sababu ya uchokozi kwa wanaume wenye uchu. Jumapili hii wateja walikuwa wamepungua sana ndipo alipojikuta akikabiliana na mteja ambaye alionekana kuwa tofauti kidogo. Hisia zilimtuma kuwa ni wateja wake wale wa hatari ambao mara nyingi humtumia kwenye mambo mazito. “Sema basi si unatafuna maneno, unajua unavyonizingua nakuwa sikuelewi?” James Makabi hakuwa na papara bado alihitaji utulivu na umakini kuongea na mwanamke huyo ambaye alizipata simulizi zake kutoka kwa madereva wenzake ambao alikuwa nao kituo kimoja cha daladala. “Haraka ya nini, si tuingie huko ndani tuongee?” “Kunitoa tu hapa na kunipeleka ndani mkono mtupu sio ishu.” “Nani kakwambia ni mikono mitupu?” “Aah, maana ushaanza mara maongezi kidogo na wewe, sijui nini, hii ni sehemu ya kazi na sio kutongozana. Hapa ni biashara yaani kazi tu!” Aliendelea kubwabwaja Mary huku akimalizia kipande cha sigara ambacho kilikuwa mdomoni mwake.
James hakujishugulisha kutazama kitu ambacho kilikuwa kigumu kuita kaptura au kichupi cha jinzi kilichovaliwa na mrembo huyo. Ni kivazi hicho ambacho kiliruhusu maeneo nyeti ya kahaba huyo kuwa nje. Ni kana kwamba kilienda kuziba sehemu nyeti zaidi na kuacha maeneo mengine ambayo ni nyeti kubaki nje. Mapaja yake yaliyojaa vizuri ndiyo yaliyomfanya apate wateja wengi kuliko wenzake. “Mary, punguza kubwabwaja kwani tunataka kuongea ishu ya mamilioni.” Kauli hiyo ilimtuliza Mary ambaye alishazoea kubwabwaja ovyo. “Mamilioni. Duh, mchizi wangu sio ishu ya kuuzana hiyo?” Aliuliza huku akikaa vizuri na kukunja miguu kwa mtindo wa nne pale kitandani. “Ni kazi ndogo sana unatakiwa kufanya.” “Halafu malipo.” “Milioni kumi, ukifanikiwa.” “Nikishindwa.” “Sote tutakuwa tumekosa.” “Enhe nipe mchoro.” “Utatakiwa kusimama hapo Buguruni sheli, Jamaa atakuja na begi lenye noti. Atakukabidhi kisha utafuata maelekezo nitakayokupa.” “Hivyo tu?” “Ndiyo.” “Halafu milioni kumi? Sio tunauzana kweli mchizi wangu.” “Hatuuzani, kuna biashara ya unga tumeifanya, na huo ndio utaratibu wangu wa kupokea pesa.” “Mbona huna dalili ya kuwa Zungu wewe?” “Unataka dalili ipi?” “Huna harufu ya pesa mchizi.” “Nilikuwa gerezani, nimetoka miezi michache iliyopita unatarajia nini?” “Ok, nimekuelewa mchizi, lini sasa hilo dili?” “Kesho saa nne na nusu.” “Poa niache na ya kiroba basi mchizi.” Aliongea kwa sauti iliyojaa dalili ya ulevi lakini akionesha wazi kuelewa mazungumzo yao. Akaingiza mkono mfukoni na kutoa noti tatu za shilingi elfu kumikumi. “Dah, poa mchizi wangu, ngoja nipate kiroba nitulize kichwa maana mchongo huu si mchezo.” Makabi akaondoka kwenye kile chumba na kufuata uchochoro mdogo ambao unatokea kituo cha magari cha Temeke Hospitali. Alikuwa na uhakika wa kufanikisha mpango wake kwa asilimia kubwa zaidi bila kudhurika.
Jumatatu saa 4.30 simu ya James Makabi iliita kwa sekunde chache kabla ya kupokelewa. “Niko eneo la tukio.” “Sikuoni.” “ Unaiona hiyo Rav4 nyeusi inayowekwa mafuta?” “Ndiyo nimeiona.” Alijibu James akiwa na uhakika kuwa alikuwa anazungumza na Mjomba Masharubu. “Ok, we uko wapi?” “Mzigo wangu unao?” “Niko kamili uko wapi? unapoteza muda kijana.” “Rudi nyuma, fuata barabara ya Mandela upande wa kulia ambako hupita watembea kwa miguu.” “Mpaka wapi?” “Utaiona karakana inayoranda mbao. Nimesimama karibu na lango.” Mjomba akapiga jina linguine kwenye simu yake. “Fuata Lumumba Road Kama unaenda Tabata Matumbi, upande wa kulia kuna karakana angalia nani anaongea na simu.” Akakata simu na kupiga tena namba ya James. “Nimefika bado uko hapo karibu na lango la karakana?” “Ndiyo niko karibu na lango si umebeba begi la fedha?” Simu ikakatwa bila kujibiwa swali hilo kisha ile namba iliyopigwa kabla ikapigwa tena. “Vipi umemuona mtu anayeongea na simu?” Baada ya simu kukatwa akakunja uso kwa hasira. “Mbona unaleta usumbufu uko wapi wewe?” “Angalia hapo karibu na lango kuna mwanamke amevaa hijabu nyeusi naomba umkabidi huyo fedha zote.” “Shiiit….” alichukia Masharubu huku akisindikiza hasira zake kwa tusi zito la hifadhini. Akiwa na hasira kali akatembea kwa kasi akiwa na begi lake mkononi.
*** James Makabi alifika eneo la tukio sa 3.00 yaani saa moja na nusu kabla. Alikuwa amempa Mary maelekezo muhimu jinsi ya kuja kupokea fedha hizo. Akili zake zilifanya kazi haraka na hisia za kuwa Masharubu ni mtu hatari ndizo zilizotawala kichwa chake, alipofika eneo hilo la Buguruni sheli akavuka barabara na kukaa upande wa pili ambako kulikuwa na madereva wengi wa magari madogo madogo ambayo yalitumika kubebea mizigo. Akajiunga na madereva wa eneo hilo kwani alifahamiana na wawili kati yao. Hata wale ambao hakufahamiana nao bado hakuwa mgeni kwao kwani walishakutana mara kadhaa na kupelekea kutambuana kwa sura. Simu yake ilipoanza kuita akajitenga kidogo na eneo lile. Aliweza kumuona vema Mjomba Masharubu akiteremka kutoka kwenye Rav4 nyeusi. Baada ya mawasiliano ya dakika kadhaa na makubaliano yao ndipo alipomuona Masharubu akirudi kwenye gari na kuchukua Begi la fedha. Alitabasamu. Tabasamu lililochanganyika na hofu ingawa pia alikuwa na hisia za ushindi ndani yake. Kwenye hisia zake aliweza kujenga nyumba nzuri ya kisasa ambayo ilikuwa na mabanda ya kufugia kuku wa mayai na wale wa nyama. Bustani nzuri ya maua ambayo ilikuwa inamwagiliwa na Tamasha akisaidiwa na mfanyakazi binti wa miaka kumi na minne ilikuwa inapendeza na kuvutia. Yote haya yalipita kwenye akili zake baada ya kuliona begi lile ambalo aliamini kuwa lilikuwa na fedha. “Mia mbili Hamsini milioni!” Alijikuta akitamka kwa sauti ambayo alijisikia mwenyewe. “Eee bwana kuna mshikaji namfuatilia hapo mbele.” Alisikika Makabi akimuaga mmoja wa wenyeji wake pale kijiweni. “Poa kamanda.” Alijibu rafiki yake huyo wa siku nyingi. Akavuka barabara haraka na kwenda kusimama kituo cha daladala zinazoelekea Tabata, Ubungo na Mwenge. Bado Masharubu alikuwa hajapotea kwenye macho yake. Wakati huohuo aliweza kumuona Masharubu akiongea na simu. Kidogo akaanza kuingiwa na mashaka, alitamani sana kujua nini anaongea katika wakati ule nyeti na wa hatari. Umbali uliyawezesha macho kufika aliko Masharubu na kumuona anachokifanya lakini uliyanyima fursa masikio yake kusikia alichokuwa anaongea. “Usalama upo kweli?” Alijiuliza. Aliweza kumuona Mary akiwa amesimama kwa umakini kabisa wakati Masharubu anamuendea. Muda huohuo Makabi akampigia simu. “Ni huyo mrefu mwenye suti nyeupe, tai nyekundu na kofia ya pama.” “Poa mchizi.” Alijibu Mary ambaye alikuwa amevaa headphone upande mmoja wa sikio lake.” Hakujua walikuwa wanaongea nini lakini alimshuhudia Masharubu akikabidhi begi lile la fedha kwa Mary. Kabla hajaondoka Mary akafungua kidogo zipu ya begi na kuchungulia, akatikisa kichwa kukubali. Muda huo huo akamuona Masharubu akirushia kitu fulani ambacho kutokana na umbali hakuweza kukifahamu ndani ya lile begi. Hakujali sana alichoona muhimu ni kitendo cha Mary kutikisa kichwa kwa ishara yakukubali huku akitabasamu.
Hakujali kuwa zitakuwa zimetimia zote milioni mia mbili hamsini, muhimu kwake ni kuwa hizo fedha zilikuwa nyingi hata akiamua kutoroka zitatosha. Ndoto za maisha mazuri zilikuwa zimejikita kwenye nafsi yake. Akili yake ilitawaliwa na harufu ya noti. Alijihisi akikaza mipira kadhaa ya kufungia noti ‘ruberband’’, furaha iliyochanganyika na hofu ilikuwa inarindima kwenye nafsi yake. Wakati Mjomba Masharubu anaondoka eneo la makabidhiano ndipo Makabi aliposhuhudia kitendo ambacho hakukielewa. Mary alitimuka kwa kasi sana na kujitoma kwenye Toyota Corola nyeupe ambayo iliegeshwa karibu na eneo la makabidhiano. Kilichomshtua Makabi ni kuwa ile Corolla ilikuwa nje ya mpango wao. Hisia za kuibiwa na yule mwanamke zikachukua nafasi yake. Wakati akiwa amepigwa na butwaa ghafla akashuhudia tukio lingine la kutisha. Hakuamini macho yake kuwa mambo haya yote yalikuwa yanafanyika ndani ya muda mfupi kwa kasi ya aina yake. Watu walipiga mayowe na kutawanyika ovyo, ni wakati huo ambao Makabi alijikuta akituliza akili yake kwa kiwango cha hali ya juu na kuyatazama matukio yaliyokuwa yanatokea pale kama filamu fulani ya kusisimua. Alitazama kila upande kuanzia kwa watu waliokuwa wanakimbia ovyo mpaka eneo la tukio. Watu walikuwa kwenye taharuki kubwa. Kama si kila mtu kuwa katika hekaheka za kuokoa nafsi yake basi Makabi angekuwa anamshangaza kila mtu kwa hali ya utulivu na ujasiri aliokuwa nao kwenye mazingira magumu kama yale. Hakuwa peke yake, pamoja na tukio hilo la kutisha aliweza kumuona Mjomba Masharubu akiingia kwenye gari kwa utulivu mkubwa kana kwamba hakuna tukio linaloendelea.
*** Ilikuwa saa 4.45, Taisamo alifika nyumbani akiwa amechoka sana. Hakuwa na wazo la kulala pale nyumbani. Akachagua nguo chache na kuziweka kwenye kibegi kidogo ambacho kilifanana na ‘briefcase’ Baada ya kuhakikisha kuwa amekamilisha zoezi hilo fupi akatoka na kufunga mlango wa chumba chake. Alitazama chumba chake kana kwamba anakiambia kwaheri. Akaanza kupiga hatua za haraka kuondoka. “Mbona hatuagani?” Alishitushwa na sauti ya teacher Suzy ambaye alikuwa nyuma yake. “Umekuwa adimu Suzy, huonekani.” Alijitetea Taisamo. “Nimefiwa na mume wa Shangazi yangu, anaitwa Dokta Kilonzo hivi ninavyokuambia najiandaa kwenda huko msibani mazishi yatachelewa kidogo kwani mwili wake unafanyiwa uchunguzi na madaktari.” Kidogo Taisamo akapatwa na mshituko kwa kauli hiyo, akahisi kama imezungumzwa kwa kukusudiwa. Akainua macho yake na kumtazama Suzy. Hayakubeba huzuni ya mfiwa, yalikuwa yameficha kitu cha ziada ambacho kiliufanya moyo wa Taisamo ulipuke kwa mshituko. Alikuwa anatazamana na macho yaleyale, hayakuwa macho ya kawaida, macho ambayo yalificha kitu zaidi ya huzuni. Kisasi? Alishituka baada ya kujiuliza swali hilo. Askari? Hapana, alikataa haraka sana. Mwandishi? Hapana alishanieleza mapema kuwa yeye ni mwalimu. Alishangaa kujikuta akitazamana na macho ya Suzy yasiyo ya kawaida. Halafu mbona kama sura yake sio ngeni sana? Alijiuliza. Sekunde chache zilipita akiwa amekodoleana macho na binti huyo mrembo ambaye aligeuka kuwa kitisho kwa wakati huo. “Suzy, pole sana kwa msiba. Nilikuwa na mengi ya kuongea na wewe lakini nimepata dharura ya safari ya kikazi ambayo itanichukua siku mbili au tatu. Nina mengi ya kuzungumza na wewe tutaonana nikirudi.” Alimaliza Taisamo huku akionesha wazi kuwa na haraka. “Ok, basi niachie hata namba ya simu.” Alibembeleza Suzy. Taisamo akataka kuchomoa business card inayomtambulisha kuwa mwandishi wa habari lakini akasita akaamua kuiandika namba hiyo kwenye kipande cha karatasi na kumpatia. “Kwa heri Suzy.” Aliaga huku akiwa ameshapiga hatua kadhaa. Hakuwa na jibu la kumpa Jenerali, hakuwa na jibu la kumpa Luteni Jenerali. Alikuwa na mambo mawili tu ya kufanya, kutoroka na kujificha huku akitafutwa kila kona na mkono mrefu wa serikali au kutafuta ukweli kwa gharama yoyote ili aweze kujitoa kwenye tuhuma hizo. Njia ya pili ilimsisimua na kumvutia zaidi, kuutafuta ukweli ambao alishaonywa kuwa ni kukitafuta kifo chake mwenyewe. Alijua wazi kuwa ili kuupata ukweli hakutakiwa tena kufuata mpango wa ofisi huku akifuatiliwa kila analolifanya na mtu anayeitwa Rose. Alijihisi kumchukia Rose kwani alipenda afanye kazi kwa uhuru zaidi na sio kila dakika kuulizwa hatua aliyofikia. Dakika arobaini na tano baadae alikuwa eneo la Mtoni kwa Azizi Ali, ndani ya chumba kimoja dhaifu katika nyumba ya kulala wageni ambayo haikuwa na umaarufu zaidi ya kujulikana zaidi kwa wapenda ngono na makahaba. Akiwa na tafakari nzito juu ya matukio yanayomtokea ndipo simu yake ikaanza kuita, ilikuwa ni miongoni mwa namba ambazo zilikuwa zinamkera sana. “150, Rose hapa naomba kukukumbusha kuwa wakuu wanakuhitaji, imebaki saa moja tu, hakikisha unakuwa na ushahidi wa kutosha kwani leo huenda ukakamatwa na Millitary police(MP) kwa uzembe katika kazi na kusababisha mauaji ya daktari pamoja na nesi ambayo inasemekana umemuua saa chache zilizopita.” Alikuwa kama aliyepigwa na shoti ya umeme baada ya kusikia taarifa hizo za kifo cha nesi saa chache zilizopita. Alizidi kuchanganyikiwa kwani alihisi kutembea na mtu asiyemuona. Sasa alikuwa na kitu zaidi ya mshangao, nini? Woga! Hakupenda kuruhusu woga kwenye kazi, alitafakari na kuona huu ni wakati wa Liwalo na liwe. Akiwa bado ameing’ang’ania simu yake akajikuta akitoa jibu ambalo hata mwenyewe alijishangaa. “Rose, please tell your boss .MISSION CANCELLED. (Rose mwambie mkuu wako mpango umefutwa” “150!” “Dont call me 150 or Liutenant (Usiniite 150 au Luteni), napenda nibaki kuwa Taisamo.” “Una maana gani?” “Nimeacha kazi.” “what?” “Hujanielewa? kila kitu kimeharibika mwanamke, mpango umefeli nahisi kuna msaliti hapo kati maisha yangu yako mashakani.” “Unaonaje ukifikisha hayo madai yako kwa Jenerali?” “Mwanamke, usinitafutie balaa. Kwaheri.” “Usiniite kwa dharau kiasi hicho mimi ni mkuu wako wa kazi.” “No, ulikuwa mkuu wangu, kwaheri.” Simu ikakatwa. Alijihisi hatia ndani ya nafsi yake lakini akajikuta hana uwezo wa kukabiliana na maswali ya Wazee wale wawili ambao wako katika nafasi za juu za kiutawala ndani ya jeshi. Alizifahamu vizuri taratibu na sheria za kijeshi ambazo huwa kali kama pilipili machoni pindi unapofanya kosa alilolifanya yeye. Alijua kwa taratibu za jeshi lazima atafutwe kutokana na kuwa na baadhi ya vifaa vyao kama vile silaha na fedha. Aliwaza kitu ambacho alitakiwa kukifanya haraka. Alijua nini aanze nacho kesho. Ukweli ni kwamba alikuwa amechanganyikiwa, kwani dakika chache zilizopita alikuwa akiota heshima na pengine kupandishwa cheo lakini ghafla upepo umebadilika amejikuta akielekea kudhalilika na pengine kuingia gerezani kutokana na mtego ambao hajui nani kautega na kwa lengo gani. Sasa anatakiwa kujibu maswali ambayo kama atashindwa lazima apelekwe kwenye mahakama ya kijeshi. Alishangaa kuona mambo haya yakitokea kama ndoto.
*** Ilikuwa yapata saa 1.30,ndio kwanza Enerst Bigambo Meneja wa Benki ya NMB tawi la kariakoo alikuwa anakaa kwenye kiti. Ulikuwa ni utaratibu wa matawi mengi ya benki hiyo kuanza kazi zao za ndani kuanzia muda huo hadi saa 2.30 ambapo utaratibu wa kawaida wa kibenki wa kuhudumia wateja huanza. Akiwa amevutiwa na tukio la kusisimua la ujambazi lililotokea Buguruni Sheli, alikuwa ni mmoja miongoni mwa wafanyakazi wa benki hiyo ambao walikuwa wamesimamisha utaratibu wa kawaida wa kazi kwa nukta chache na kuelekeza macho yao kwenye tukio hilo ambalo lilikuwa linatangazwa na kuonyeshwa na moja ya vituo vya Runinga. Dakika chache baada ya kumalizika kwa taarifa hiyo simu yake ya mkononi ikaanza kuita. “Bosi, kuna mtu anaomba kuonana na wewe mara moja.” Ilikuwa ni sauti ya Miriam katibu muhutasi wake. “Ananihitaji kibinafsi au…….” “Kikazi Bosi.” “Miriam, mbona unakuwa kama mgeni unashindwa kumueleza taratibu za kazi?” “Nimemueleza kila kitu akanitisha akaniambia mambo yakiharibika nitakuwa Responsible kwani ana kazi muhimu ambayo haitakiwi kusubiri muda wa kawaida kuonana na Meneja.” “Dah, we si unajua wateja jinsi walivyo wasumbufu wakiwa na haraka zao mruhusu.” Sekunde chache baadae mlango wa ofisi yake ukafunguliwa na mtu ambaye kabla ya kukaribishwa alikaa kwenye kiti kilichoelekeana na kile cha meneja. “Habari yako Meneja.” “Nzuri, ndugu yangu, sijui nikusaidie nini maana umekuja mapema mno.” Aliongea meneja huku akilazimisha kicheko ili kuficha karaha yake kwa tukio hilo. “Nina haraka, ninahitaji pesa kama milioni thelathini kutoka kwenye akaunti yangu.” “Lakini muda wetu wa………” “Hapana meneja kuna mambo mengine huwa ni ya dharura, mimi nafanya kazi muhimu ambayo inanitaka ndani ya dakika kumi na tano niwe nimeshachukua fedha na kuianza.” Meneja alianza kuonesha hasira kidogo na kutaka kugeuka mbogo kwa mteja. Mteja alilifahamu hilo na kwa haraka akatoa kitambulisho chake. Kisha yakafuata maelezo mafupi. “Luteni JWTZ!” Alishangaa meneja huku akikitazama kwa umakini kitambulisho kile na kuridhika kuwa kilikuwa chenyewe hasa. “Kuna kazi muhimu sana inatakiwa kukamilishwa ndani ya muda mfupi ujao kama utashindwa kunisaidia ina maana utakuwa ni mmoja wa waliochangia kushindwa kwa kazi hiyo.” Hata kama asingetoa maelezo hayo, kile kitmbulisho kilitosha kumfanya meneja kubadili msimamo wake kwani alifahamu anaongea na nani. Muda huo huo akabonyeza namba fulani kwenye simu yake ya mezani. “Hallow Frank, namleta kwako mteja wetu Alex Taisamo…… naomba umsaidie kutoa fedha anazohitaji kutoka kwenye akaunti yake.” “Nenda kwa cashier namba 3 hapo chini utasaidiwa, pole kwa usumbufu bwana Taisamo.” “Ahasante mkuu usijali…..”
Dakika tano baadae fax ikaingia kwa meneja. Hakuwa na haraka ya kuisoma kwani alitumia kama dakika nne kumaliza chai ambayo ilikuwa kwenye kikombe. Hakuwa mtu mwenye kupenda kuharakisha mambo, alipenda kufanya kila kitu kwa utulivu. Alishtushwa na taarifa aliyoisoma kwenye fax ile, dakika hiyo hiyo akasimama huku akishindwa kujua nini la kufanya kwa muda huo. Taarifa ya dharura Kwa Mameneja wote. Account no. 02042513272432 ya mteja wetu Alex Taisamo imezuiwa, haruhusiwi kuchukua kiasi chochote cha fedha na pindi atakapoonekana, taarifa ifikishwe makao makuu haraka iwezekanavyo. Wataalamu wetu wa IT wanaendelea kufanya kazi ili kuizuia Akaunti hiyo lakini kuna tatizo kidogo kwenye system, Tafadhali wasiliana na Tellers wote walifahamu hili kabla ya kuanza kwa shuguli yoyote ya kibenki, Zingatia system inasumbua lakini kwa sasa tunalazimika kutoa taarifa hii ya dharura. Ilimaliza taarifa hiyo ambayo ilimtoa jasho meneja huyo wa Tawi la kariakoo. Dakika hiyo hiyo akainua simu na kupiga namba ile ile. “Frank, yule mteja bado yupo?” “Ndiyo bosi” Ulijibu upande wa pili. “Mhhhh!” Alishusha pumzi meneja. “Vipi, kuna tatizo bosi?” “Ndiyo, kuna agizo kutoka makao makuu ambalo linatutaka kuzuia akaunti yake, pia tutoe taarifa kuwa yupo hapa umeshampa hizo pesa?” “Ndiyo, anamaliza kuzipanga kwenye begi.” “Mungu wangu mzuie.” “No, Bosi ana bastola, hajatishia maisha yangu lakini anaonekana ni mtu ambaye hana masihara.” “Mungu wangu, ina maana anakusikia unavyoongea?” “No, hapa nilipo hanisikii maana nimejifungia, si unajua sauti haitoki humu ndani ingawa unaweza kumuona aliyeko nje.” Aliongea Frank ambaye alikuwa kwenye kichumba kidogo cha vioo. “Acha maneno mengi Frank, nishauri nifanye nini?” “Toa Taarifa kuwa huyo mtu yuko hapa Benki na ameshachukuwa hizo fedha kabla ya taarifa ya zuio haijaingia, pia usisahau kuwafahamisha kuwa hajafanya vurugu zozote lakini ana bastola mkononi, nasisitiza tena ana bastola mkononi.” “Duh….” Alisikika Meneja kisha akakata simu. “Nasisitiza ana bastola mkononi…..” Yalijirudia maneno hayo katika kichwa cha meneja huyo mwoga ambaye hakuwahi kupitia JKT wakati anarudisha kiwiko cha simu sehemu yake.
*** Ndani ya chumba kidogo ambacho kuta zake zilikuwa zimepambwa kwa picha kubwa za ngono, chumba hiki kilikuwa na harufu ya udi ambayo haikukatika mara zote. Hakikuwa na mvuto mkubwa kutokana na maisha duni ya mmiliki wa chumba hicho kutokuwa na uwezo wa kumiliki samani za gharama, badala yake kulikuwa na ndoo chache, kabati dogo na stuli chakavu ambayo juu yake kulikuwa na boksi ambalo lilikuwa limesheheni kondom ambazo hutolewa bure katika hospitali za serikali. Kitandani alikuwa amekaa mrembo ambaye alikuwa na fikra nzito, siku hiyo hakuhitaji mteja katika biashara yake hiyo ya kuuza mwili; Taarifa za kwenda kupokea Fedha zilimsisimua Mary ambaye alijiona mwenye bahati kwa kuhisi kuwa wakati wa kuachana na ukahaba umefika. Matukio mengi ambayo alishirikishwa alilipwa fedha kidogo sana licha ya ugumu ambao alikumbana nao, hili la kwenda kupokea fedha kwake lilikuwa jukumu jepesi ambalo lina malipo makubwa. Akiwa na fikra nzito juu ya jambo hilo ndipo alipomkumbuka Mudy Guy, hakumfahamu kwa jina lingine zaidi ya jina hilo. Mudy Guy alikuwa rafiki yake mkubwa ambaye alimshauri mambo mbalimbali, hata pale wateja wake walipokataa kumlipa mara nyingi alitaka msaada kutoka kwa kijana huyo mbabe ambaye mara nyingi alikuwa akishinda kwenye kituo cha teksi, mara moja moja akipata kazi za muda mfupi maarufu kama ‘deiwaka’. Alipata kazi hizo pale dereva anapokuwa amechoka au ameenda kula. “Nina mazungumzo muhimu sana Mudy ndio maana nimekuita.” Alianza Mary huku akichezeachezea vidole vya Mudy ambaye hakuonekana kuitilia uzito sana kauli hiyo. “Unajua nimeshtuka sana nilipoambiwa unatafutwa muhimu sana usithubutu kukosa.” “Ni kweli Mudy, kama nisingekuona bila shaka nisingelala leo.” “Kuna mtu kakudhulumu?” “Sio dhulma ni mpango wa pesa mchizi wangu.” “Duh, si ungesema tu maana nimeishiwa yaani sina kitu kabisa.” “Sina maana hiyo, kuna dili la pesa nahitaji ushauri.” “Sasa ushauri gani unahitaji hapo si unachukua tu halafu tunaingia viwanja kunako vinywaji?” “Mudy, sizungumzii pesa ya chai. Nakusudia mamilioni ya shilingi.” Mudy ambaye muda mwingi alikuwa amekaa kivivuvivu akakaa vizuri huku akimkazia macho Mary. Kisha akamsimulia mpango mzima kama alivyoelezwa na Makabi. “Duh, hilo dili si mchezo mtu wangu.” “Ndio maana nikaona ipo haja ya kukutafuta unipe ushauri.” “Hizo pesa ni zetu, nakuambia huyo bwege kaingia choo cha kike, kama yeye zungu launga basi sisi ni wazungu wa pesa.” “Kivipi Mudy.” “Tunakomba zote, hizo haziwezi kuwa chini ya mia.” “Halafu…” “Usiwe mjinga mtoto wa kike, kinachofuata ni kusepa na kwenda kutumbua kuku kwa mrija.” “Tutawezaje?” “We si umeniita nikupe ushauri.” “Ndio maana yake.” “Au unataka kula peke yako?” “Si hivyo Mudy, mi nimetaka kujua nini tufanye si unajua ninavyokutegemea katika mambo yangu mengi?” “Subiri kidogo, nahitaji nusu saa nitarudi na jibu” Akainuka na kutembea kwa haraka akikiacha chumba kile. ******* Baada ya nusu saa akarudi akiwa ameongozana na mtu mwingine jambo ambalo lilionekana kumkera Mary. “Mary, kutana na Cheusi ni rafiki yangu wa siku nyingi nimeamua kumwalika katika kikao hiki kwa sababu ni mtu muhimu sana kuweza kufanikisha mpango wetu, kwanza ni mtoto wa mjini halafu vilevile ishu kama hizi anaziweza………” Akatulia na kuwasha sigara ambayo tayari alishaibana kwenye mdomo wake kisha akaendelea. “…..Unajua hii ishu wewe unaiona nyepesi lakini hatuwezi kufanikisha peke yetu, huyu jamaa ana gari lake ambalo tunaweza kulitumia kufanikisha mpango wetu. Yaani ukishachukua hizo fedha unaingia kwenye gari la cheusi ambalo litakuwa tayari kwa lolote eneo la tukio, kisha tunasepa na kumwachia vumbi huyo Bwege wako.” “Hapo, nimekubali mchizi wangu.” Aliongea Mary huku akiruhusu meno yake meupe yaliyojipanga vema kuonekana. *** Ilikuwa yapata saa 9.15 mchana. Akitembea kwa tahadhali kubwa Alex Taisamo alikuwa Kariakoo mtaa wa Narung’ombe. Kwa umakini zaidi akatembea kuelekea kwenye moja ya ghorofa iliyopo pale. “Habari yako.” Alimsalimia mlinzi aliyeko mapokezi. “Nzuri, karibu.” “Ahsante, nahitaji kufika ofisi za MJ Security.” “Ghorofa ya kwanza upande wa kushoto chumba cha pili kutoka mwisho.” Akapanda ngazi za jengo lile chakavu kiasi kuelekea Mj security. Alishangazwa na uchakavu wa kuta za jengo lile ambao ungeweza kudhibitiwa vema kwa kupakwa rangi ya mafuta au maji. “Ngo,ngo,ngo…..” aligonga. “karibu.” Aliitikiwa huku ikifuata sauti ya kikohozi cha mvutaji mzuri wa tumbaku au sigara. Akafungua mlango na kuketi kwenye kiti huku akimuelekea mzee wa makamo ambaye alimkuta ofisini humo. “Karibu, sijui nikusaidie nini?” Aliongea mzee huyo ambaye alionekana kuwa na madaraka katika kampuni hii ya ulinzi. “Nahitaji kuonana na Meja mstaafu, Silvester Rutakinikwa.” “Ha, ha, ha….. Karibu sana, yaani wewe umelitamka kwa ufasaha sana jina lake. Hapa wengi wanaita Meja Ruta tu au meja kwa wavivu wa kurefusha maneno.” “Ahaa, kumbe ana jina fupi hivyo, inafaa maana halipotezi muda.” Yule mzee akaangua kicheko tena, alionekana wazi kuwa mtu mcheshi ambaye alipenda utani. “Oh, Meja Ruta ingia chumba hicho,lakini kama ni shida ya kikazi hata mimi unaweza kunifikishia.” “Hapana ni ya binafsi.” “Alijibu huku akifungua mlango wa chumba kidogo ambacho kiliandikwa DIRECTOR.” “Karibu kijana.” Alikaribishwa na sauti nzito yenye mikwaruzo wakati anaingia kwenye chumba hicho kidogo. Akapiga saluti kabla ya kukaa. “Karibu, keti tafadhali.” “Ahsante.” Akakaa na kutulia kidogo kabla ya kuanza kuongea. “Bila shaka utakuwa umenisahau Meja.” “Hapana, sina tabia ya kuwasahau watu kama watu ninachosahau huwa ni majina yao. Nakumbuka vema kama mara ya mwisho tulikutana Angola kwenye zoezi la uteguaji mabomu.” Ilikuwa ni wakati wa Alex kupatwa na mshangao jinsi kichwa cha yule mzee kilivyokuwa na kumbukumbu nzuri. “Ona sasa, nimekukumbuka mpaka jina bila shaka ni Taisamo…. Si hivyo tu nafahamu vema kama unatafutwa na millitary police.” Alikuwa kama aliyepigwa na shoti ya umeme baada ya kusikia taarifa hizo kutoka kwa huyo mzee. “Ooh, samahani mkuu kabla sijaongea lolote ningependa kujua umefahamu vipi haya yote.” “Nilikuwa kwenye kitengo ulichopo ndani ya jeshi, napenda ufahamu kuwa ukiwa ndani ya kitengo hicho mara nyingi huwa unaendelea kutumika hata kama umestaafu hasa kwenye maswala ya ushauri. Hivyo leo saa 10.30 Alfajiri nimepokea baadhi ya taarifa zako. Pia saa 3.00 nikapokea taarifa kuwa umekusanya fedha zote ulizopewa kwa ajili ya kazi ni kweli?” Alex alishusha pumzi kisha akaegemea kiti. “kabla hujanieleza shida yako naomba unieleze uliwezaje kuchukua fedha pale benki na kisha kuondoka salama?” “Nitakueleza Meja, lakini kwanza napenda kufahamu kwanini kama umeyafahamu yote hayo hujatekeleza wajibu wako?” “Kijana, hii kazi yako unatakiwa kuwa na akili inayofanya kazi haraka sana. Kwa tukio ulilolifanya leo ulihitajika kutoroka na kutokomea sehemu ambako jicho la kijeshi lingekuwa gumu kukufikia lakini kitendo chako cha kuja kwangu nimekitafsiri haraka sana kuwa unahitaji msaada inaonesha kuna tatizo hapa.” “Sawa ngoja nikujibu swali lako. Benki nilitumia kanuni ya kisaikolojia zaidi, baada ya kuchukua kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwenye akaunti yangu mara nikamuona yule keshia akiongea na simu
Nilikuwa simsikii lakini sura yake ilionesha wazi kuwa mimi ndiye ninayezungumziwa hivyo nilichomoa bastola na kuikamata vema mkononi kwa isahara ya kwamba yeyote atakayejaribu kunizuia nitamlipua, si hivyo tu pia nilimkazia jicho la kiaskari.” “Safi sana sasa niko tayari kusikiliza shida yako.” “Meja, kuna risasi mbili ambazo zinatofautiana zimetolewa katika mwili wa Mheshimiwa Makamu wa Rais, nataka kujua ni bastola za aina gani zimetumika maana sijawahi kuona aina hizi za risasi.” “Sawa nitakusaidia lakini nashangaa kuona unaendelea kufanya kazi ambayo umeshaiacha, kwa lengo gani?” “Ni kweli nimetangaza kuacha kazi lengo kuu likiwa ni kufanya kazi kwa uhuru zaidi kwani kuna hisia za usaliti naanza kuziona sielewi nini kinatokea.” Baada ya kusema hayo akamsimulia Meja mkasa mzima mpaka kufikia hapo. Meja alimkazia macho Alex huku akiwa ameshangazwa na kilichotokea. “Oh God, kuna tatizo.” “nisaidie Meja, mpaka sasa hivi ni wewe tu ndio nimekueleza ukweli wote.” “Ok, lete hizo risasi.” Akatoa kifuko kidogo cha karatasi ambacho kilikuwa katika mfuko wa suruali yake akampatia Meja Rutakinikwa. Akaitazama ile ya kwanza kisha akaitazama ile ya pili. Alex aliyaona wazi macho ya Meja jinsi yalivyotafsiri mshtuko wake. “Mh, Luteni, Luteni, Luteni…… hii sio mission uliyostahili kuifanya peke yako. Hizi risasi ni mbili tofauti lakini ni ishara ya ukubwa wa tatizo.” “Kivipi?” “Usiwe na haraka, acha nikueleze kwa tuo ninachokifahamu juu ya silaha zilizotumika…….” Akakohoa kidogo na kuwasha sigara ambayo ilikuwa kwenye mfuko wa kulia wa shati. Akaanza kuvuta huku akiutazama moshi ulivyokuwa unaelekea angani. Kisha kama aliyezinduka akamgeukia Taisamo. “Kuanzia sasa, unatakiwa kufahamu kuwa una jukumu zito mbele yako na unatakiwa kuifanya hii kazi kwa umakini zaidi kuliko ilivyokuwa hapo kabla, nakuonya usimuamini yeyote mpaka umekamilisha hii kazi. Niko nyuma yako kwa msaada pale utakapohitaji.” Akatulia tena na kuvuta sigara yake kisha akaendelea. “Hii risasi ya kwanza ni ya bastola ya kisasa aina ya bereta92 ambayo imeanza kutengenezwa mwaka 1975 na kampuni ya Fabbrica d’Armi Pietro Beretta ya Italia lakini kwa sasa imeboreshwa sana, ina wastani wa uzito wa gram 950,urefu wa milimita 217, ina uwezo wa kupiga kwa shabaha nzuri zaidi kwa umbali wa mita 50 mpaka 100 ingawa kwa mtumiaji mzuri anaweza kuitumia hata meta 200 na ikaleta madhara, inatumika kwa matumizi ya kijeshi na nchi za Amerika na zile za mashariki ya kati, Kwa hapa Tanzania zilikuja rasmi kwa watu wa usalama wa Taifa, kumbukumbu yangu inaonesha kuwa ziliingia kumi tu hapa nchini, ingawa nimestaafu lakini bado mambo mengi yanayohusiana na silaha nahusishwa ili kutoa ushauri.” Akatulia kidogo na kumkazia macho Alex ambaye alikuwa anasikiliza kwa makini maelezo hayo. “Kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa kuwa muuaji hakuwa zaidi ya umbali wa mita mia na hilo gari lilitumika kama kisingizio, pia huyo muuaji lazima atakuwa ni mtu wa usalama wa Taifa au si Mtanzania kwani Utoaji wa silaha hizi unatofautiana na zile nyingine.” Akashusha pumzi na kuvuta tena sigara yake huku akitafakari kwa makini zaidi. “Sasa hii nyingine ndio balaa kabisa,ni FN57 hii ni bastola hatari, bora na ya kisasa zaidi. Hii imetengenezwa nchini Ubelgiji inatumiwa sana na mashirika ya kijasusi ya magharibi kama CIA la Marekani, MOSAD ya Israel pia FSB ambalo lilikuwa likijulikana kama KGB la Urusi. Hapa Tanzania zililetwa tano tu moja ilikuwa kwa ajili ya Jenerali, nyingine alipewa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa na tatu zilizobaki walipewa walinzi maalum wa Rais.” Akatulia na kumtazama Alex Taisamo ambaye alikuwa anakuna kichwa. “Nafikiri tunahitaji mfumo mpya wa Idara yetu ya kijasusi.” Aliongea Alex baada ya kukaa kimya muda mrefu. “Una maana gani unaposema mfumo mpya wa kijasusi?” “Nakusudia kuwe na shirika au idara itakayojiongoza yenyewe na kuwasimamia wanasiasa, hii ya kwetu naona inaongozwa na kusimamiwa na wanasiasa.” “Unaonekana kuwa na mawazo mazuri Luteni lakini kwanza rudi kwenye kazi yako, tafakari kwa kina nini cha kufanya kwani hali ninayoiona ni nzito na inanitisha sana.” “Ok Meja, tuna mengi ya kujadili lakini nahisi muda hautoshi. Natakiwa kuondoka, naweza kurudi kwako saa na wakati wowote au vinginevyo utatakiwa kushuhudia maiti yangu kwenye Jeneza, kama nitakufa kabla ya kuonana na Jenerali naomba umfikishie kila ambacho sijafanikiwa kukifikisha kwake. “na iwapo yeye ni miongoni mwa wahusika itakuwaje?” “Ah, nashindwa kukujibu Meja, utafanya uchunguzi wako ili uweze kubaini kama anahusika au vinginevyo.” *** Hakufikiria kabla kuwa baada ya kuahidiwa milioni kumi Mary anaweza kuwa na wazo la kutoroka na fedha zake. Akiwa amepigwa na butwaa kwa kitendo cha Mary kukimbia na begi la fedha na kujitoma kwenye gari ambalo ni wazi liliandaliwa kwa ajili ya kazi hiyo akapatwa na mshangao mwingine wa mwaka, alishuhudia gari lile likishambuliwa na watu waliokuwa na sare za polisi wakiwa kwenye defender 110. Mary ambaye alikuwa anamaliza kuingiza mguu wa mwisho alirushwa juu kabla hajaangukia upande wa pili wa barabara. James alishuhudia begi la fedha ambalo lilishikwa na Mary likifunguka na fedha kutawanyika angani kitendo kilicholeta msisimko mkubwa kwa watu wenye shida zao. Licha ya hali ngumu ya kimaisha hakuna aliyekuwa na muda wa kwenda kuokota noti hizo wakati milipuko ya risasi inaendelea. Pale aliposimama aliweza kumuona vizuri dereva wa gari lile jinsi alivyoharibika vibaya kifuani kwa risasi ambazo zilifanya kazi yake vema. Hakuwa na shaka kuwa dereva, Mary na yeyote aliyemo kwenye gari lile amekufa. “Kwanini?” Alijiuliza huku akiongeza utulivu. Dakika kadhaa baadae hali ikawa shwari, Masharubu hakuwepo tena wakati tukio linaendelea. Makabi aliendelea kuwa kama mtazamaji wa filamu akaendelea kuganda pale aliposimama huku akiwaangalia watu ambao walikuwa wanarudi eneo la tukio. Polisi ambao walifanya shambulizi lile nao hawakuwa nyuma. Nusu saa baadae baadhi ya watu walianza kuliacha eneo la tukio, akaamua kuwafuata watu wanne ambao walikuwa wanasimuliana tukio lile. Akajiunga nao huku akisikiliza mjadala ule wa kusisimua. “Ebwana, jamaa anatisha yaani amewatoka palepale!” “Lakini kakosea, we unaingia vipi eneo la tukio na kitambulisho cha kupigia kura?” Aliongeza mwingine. “Kwani amefahamika?” “We hujasikia pale watu wanaulizwa kama wanamfahamu James Makabi?” “Mi nimechelewa, jamaa alibugi sana we unatembea vipi na kitambulisho cha kura kwenye ishu kama ile.” “Dah, lakini kawatoka utamu… yaani kama komando!” Aliendelea kusifia jamaa mwingine. “Lakini Fedha zote zile ni za bandia kwanini?” Aliuliza yule wa kwanza. “Dah, hapo sasa. Inaelekea jamaa ndio ishu zake, tusubiri taarifa ya habari.” “Ishu zipi, zakutengeneza fedha za bandia?” “We hujasikia askari wanasema aliyetoroka ni mtu hatari sana?” Aliamua kujitoa kwenye kundi hilo. Alijihisi kutaka kupoteza fahamu. Bado taswira ya Mary ilimjia akilini. “Nimemsababishia kifo, lakini tamaa yake imemponza pia.” Aliwaza huku akielekea kituo cha daladala. Aliingia kwenye moja ya daladala ambalo hakuangalia linaelekea wapi. *** Kwa mtu wa kawaida lilikuwa ni jambo la kustaajabisha kwa Alex Taisamo kujificha kwenye nyumba ya kulala wageni ambayo haikuwa mbali sana na kambi ya Jeshi. Hakukosea, alijua wazi kuwa kuna msako wa siri ambao unaendelea dhidi yake, yeyote aliyekuwa anamtafuta asingeweza kufikiria kuwa Taisamo anaweza kujificha karibu na kambi ya jeshi.
“Ngo,ngo, ngo….” Mlango uligongwa kwa nguvu kitendo kilichomshtua Alex. “Fungua mwenyewe” Mtu aliyeko nje aliendelea kufoka. “Unataka nini?” Aliuliza Taisamo huku akiwa na wasiwasi. “Fungua bwana, ukituzingua tunavunja mlango.” Taisamo aliingiwa na hofu kwa kujuwa kuwa ficho lake limegundulika.Kijasho chembamba kikaanza kumtoka. “Ikibidi kuua ua.” Alikumbuka maneno ya mmoja wa walimu wake Kapteni Isack Kihengu. Akapapasa bastola yake aina ya SIG P228. “Subiri nafungua.” Kabla hajafungua akachungulia kwenye tundu la ufunguo, akabahatika kuiona sura ya mmoja wa watu walioko nje. Haikuwa sura aliyoitarajia ilikuwa sura ya kawaida ambayo isingeweza kuwa na kile alichokiwaza licha ya kuonesha dalili ya hasira na shari. Akafungua mlango na kushuhudia watu sita wakiingia ndani kwa fujo. “Yuko wapi mke wangu?” Alihoji mmoja kwa hasira, wakati huo huo akamuona muhudumu wa Guest naye akiingia. “E bwana, ndio utaratibu gani huu wa kuingiliana vyumbani?” “Samahani bro, hata mimi wamenilazimisha tu wanasema wamekuja kufumania.” “Maelezo mazuri, lakini nafikiri itakuwa ni bora maelezo hayo utakapoyatoa kwa polisi ambao watakuja hapa muda si mrefu baada ya kupata simu yangu.” Alijitutumua Taisamo huku akionesha hasira. Kidogo wale watu walioingia wakaanza kuingiwa na wasiwasi na kupunguza jazba na kelele zao. “We, una uhakika mkeo kaingia huku?” Aliuliza mtu mwingine ambaye alijifanya kuwa na busara kuliko wenzake. “Sasa naomba wote msubiri na maelezo yenu yatafuata kituoni.” “E bwana, njagu huyo hamuoni hata sura yake?” Aliropoka mtu mmoja na kutoka mbio mle chumbani huku akifuatiwa na wenzake. Hakuna aliyekuwa tayari kati yao kukabiliana na Polisi. Wote wakatimua mbio na kumwacha Muhudumu wa guest ambaye aliitumia fursa hiyo kwa kumuomba radhi Taisamo. Baada ya Muhudumu kuondoka Taisamo akajilaza kitandani huku akishusha pumzi. “Hii si dalili nzuri, kesho narudisha chumba.” Aliwaza huku akitazama saa na kupuuza njaa ambayo ilishaanza kumsumbua. Alianza kuyapitia mawazo ya Meja Rutakinikwa kwa kichwa. “Bereta92, zililetwa kumi kwa idara ya Usalama wa Taifa, kwanini watu wa usalama wa Taifa wamuue Makamu wa Raisi, Je ni mpango wa idara au baadhi ya watu ndani ya Idara?” Alijiuliza huku akitikisa kichwa. Fikra zake akazipeleka kwenye FN57. Aliweza kukumbuka vema maelezo ya Meja mstaafu kuwa hiyo walipewa watu maalumu watano akiwemo aliyemtuma kufanya kazi, au jenerali yuko nyuma ya pazia? Kwanini zitumike bastola za aina mbili tofauti? Au kuna watu tofauti walikuwa na ugomvi na marehemu? Na yule aliyetumia gari alitumwa na nani? Marehemu alikuwa na tatizo gani kwa Usalama wa nchi? Kwanini yote haya yametokea baada ya kutangaza nia ya kugombea Uraisi? Alijiuliza maswali hayo kwa haraka na kujikuta akikosa jibu. Akazirudisha fikra zake kwa jinsi alivyokuwa anamfahamu marehemu. Alikuwa ni mtu muungwana, mchapa kazi na asiye na makundi ndani ya chama. Kubwa zaidi alikuwa kipenzi cha wengi. Inawezekana sababu za kisiasa zimesababisha yote haya. Akaamua kuandika kwenye kidaftari chake, sababu za kisiasa zinaweza kuwa chanzo cha yote haya. “Sasa nahitaji chakula, angalau nimeweza kupiga nusu hatua.” Aliwaza huku akitazama saa yake ambayo ilionesha kuwa ni saa 4.22 usiku. Kesho naanza rasmi kazi yangu.
3 HARUFU YA UKWELI
………. Jambazi mmoja aliyefahamika kwa jina la James Makabi amefanikiwa kutoroka eneo la tukio. Zawadi nono ya dola 2500 za kimarekani itatolewa kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa jambazi hilo Sugu. Kishindo cha mshituko kilimkuta James alipokuwa anasikiliza taarifa hiyo ambayo aliikuta katikati ya taarifa ya habari ya redio ndogo ya mpenzi wake Tamasha. “Dear, utafanya nini sasa?” “Nimechanganyikiwa Tamasha Mpenzi, naomba msaada wako tafadhali.” “Njia ni tatu tu, kuendelea kujificha kwa umakini zaidi, kutoroka na kwenda mbali kabisa na macho ya polisi au kujisalimisha Polisi.” “Polisi?” “Ndiyo Polisi.” “kujificha kwa zawadi nono iliyoahidiwa ni jambo gumu, kutoroka ni ngumu na hatari zaidi kwani kila kona kuna makachero, kidogo hilo la kujisalimisha Polisi lina unafuu lakini polisi wenyewe nao hawaaminiki.” “Fanya kitu kimoja dear.” “Enhe.” “Ongea na waandishi wa habari kuwa umeamua kujisalimisha. Usiwaeleze ukweli wote isipokuwa wafahamishe wazi kuwa unaomba msaada wa wakili ili uweze kueleza chanzo cha yote hayo.” “Wazo zuri, lakini kama wameweza kumuua makamu wa Raisi unafikiri kuna urahisi wowote wa kuondoka eneo la tukio nikiwa salama?” “Una wakati mgumu sana dear, lakini nafikiri ni muhimu kwako ukijisalimisha Polisi.” “Ok, nakubaliana na wewe kwani kadri nitakavyoendelea kujificha, ndivyo ninavyojitia matatizoni zaidi, nitanya hivyo kesho.
*** “Google, Bi Jesca Ole Nunga,” alitamka Taisamo huku akiandika jina alilolitaja kwenye kiboksi cha google kwenye tovuti hiyo kubwa ambayo ni maarufu kwa utafutaji wa vitu na mambo mbalimbali ikijulikana zaidi kama ‘search engine’ akatulia na kusubiri kwa sekunde chache kabla haijamletea vichwa vya habari vingi. MKE WA MAKAMU WA RAISI AZINDUA MRADI WA KINA MAMA, MKE WA……. Alikutana na vichwa vingi akavutiwa na kile kilichosema. HISTORIA YA MAMA OLE NUNGA. Akafungua na kuanza kusoma. Baada ya kumaliza alikuwa amekipata alichohitaji. “Ni mwalimu, shule ya sekondari ya Wazazi Tabata Kimanga.” Aliandika maneno hayo kwenye kikaratasi kidogo kisha akamlipa muhudumu wa mkahawa ule wa Intaneti ‘Internet cafe’ akaondoka. Saa 8.43 alikuwa maeneo ya Kimanga mwisho. Akaamua kuingia kwenye mgahawa kwanza kabla hajaenda shuleni hapo. “Nipatie maziwa na keki tatu.” Aliagiza. Baada ya muda mfupi akaletewa vitu alivyohitaji. Akala kwa utulivu huku akiwa makini kutazama kama kuna mtu anamfuatilia. Alikuwa karibu na wanawake wawili ambao walikuwa wanaongea kwa kunong’ona. “Vipi shosti na leo mama hajafika kazini?” “Mwenzangu, si nimesikia kwa Headmaster kuwa ameacha kazi?” “Ameacha kazi?” “Ndiyo, anasema amechoshwa na watu wanaomfuata mara kwa mara.” “Kwani kuna watu wanamfuata?” “Yaani toka kifo cha mumewe amekuwa akifuatwa sana ana wasiwasi maisha yake yako hatarini.” “Mungu wangu, ina maana anawajua waliomuua mumewe?” “Hapana, kuna wakati alitaka kujua kwa madaktari kile walichogundua kutokana na kifo cha marehemu mumewe, toka hapo amekuwa hana amani kwani anaandamwa mno na watu asiowafahamu na wakati mwingine kupata vitisho.” “We umewahi kumtembelea toka kuzikwa kwa marehemu mumewe?” “Mh, shoga. Yaani sina hamu.” “Kwanini?” “Yaani ile nyumba ina ulinzi mkali tofauti na kipindi cha marehemu.” “Usiniambie, sasa kwanini ulinzi uwe mkali wakati Vice ameshakufa?” “Mh, tuyaache shoga…..” Aliongea dada aliyekuwa anajibu maswali huku akiweka vizuri kitabu chake mkobani. Alex aliwatazama vizuri akabaini kuwa ni walimu. Hakuona sababu ya kusitisha uchunguzi wake ingawa alikuwa amepata mambo mengi zaidi ya alivyotarajia. Akatembea taratibu akiiacha barabara inayoelekea Kisukuru na kufuata ile inayoelekea shule ya sekondari ya wazazi Tabata. “Hatua moja kamili.” Aliwaza huku akiwa katika mlango ulioandikwa Headmaster. Akagonga mlango na kuingia baada ya kukaribishwa. “Habari yako dada.” Nzuri, salama.” Alijibu dada ambaye alikuwa kwenye meza yenye kompyuta akiandika kwa kutumia kicharazio ‘keyboard’ “Salama kabisa.” “Sijui nikusaidie nini?” “Nina shida ya kuonana na mkuu wa shule.” “Amesafiri kikazi.” “Msaidizi wake…..”
“huyo kaacha kazi.” “Aaah, kumbe yule mama kaacha kazi.” Alijifanya kumfahamu. “Yaani, tunasikitika sana maana alikuwa mchapakazi kubwa.” Aliongezea yule dada na kumpa uhakika wa alichokuwa anahitaji. **** Saa 2.30 usiku alifika maeneo ya Oysterbay. Aliifahamu vema nyumba ya marehem Ole Nunga. Haikuwa mbali sana kutoka kituo maarufu cha polisi cha Osterbay. Akapita mbele ya nyumba hiyo na kujionea jinsi askari wenye silaha walivyokuwa wameiweka chini ya uangalizi mkali. “Kwanini?” Alijiuliza wakati akipita kana kwamba hana mpango na nyumba ile. Ilikuwa nyumba kubwa ya ghorofa moja huku ikiwa imezungukwa na uzio mkubwa wa matofali. Aliweza kuiona miti ya aina mbalimbali ambayo ilipandwa kwa ustadi mkubwa. Baada ya kutembea umbali wa mita kama mia nane akafuata kichochoro kinachoelekea kushoto ambacho kinatokea nyuma ya nyumba ya Marehemu Ole. Akafanikiwa kutokea nyuma ya nyumba bila kufikiwa na jicho la yeyote ambalo lingeweza kunusa dhamira yake. Akiwa nyuma ya nyumba kadhaa ambazo zilifanana kidogo na ile ya mheshimiwa, alitembea taratibu huku akihofia sana mbwa ambao kama wangethubutu kubweka basi ingekuwa tatizo kwake. Aliposogea karibu na nyumba ya mheshimiwa alikutana na miti ambayo ilimsaidia kujificha akikwepa taa kali ambazo zilizunguka nyumba nzima kiasi cha kuwezesha kuonekana kwa pini au sindano iliyoanguka usiku wa manane. Hofu ilianza kumtawala pale alipokuwa anafikiria namna ya kupanda ukuta ule, sio kwamba ulikuwa mrefu kiasi cha yeye kushindwa kuingia ndani tatizo lilikuwa ni hofu ya kukutana na walinzi wengine. Akaruka na kukamata sehemu ya juu ya ukuta, mikono ikafanya kazi kama jeki ya gari kwa kuinua sehemu ya mwili iliyobaki, akachungulia ndani na kulakiwa na ukimya. Akauvuta mwili wote na kulala sehemu ya juu ya ukuta ule. Akatulia kwa sekunde chache kisha akaangukia ndani na kufanya kishindo kidogo ambacho kingeweza kumshitua yeyote aliyeko karibu. Kwa mwendo uleule wa kunyata akatembea taratibu huku akienda upande wa mbele wa jengo lile. Hofu ilianza kuchomoza kadri alivyokuwa anazidi kusogea upande wa mbele wa jumba lile. “Kwanini wakati marehemu yuko hai hakukuwa na ulinzi kama huu?” Alijuliza swali ambalo alijikuta likimuongezea hamasa ya kazi. Akiwa kwenye kona ya jengo lile alichomoka mbio na kwenda kusimama kwenye mti mmoja ambao ulikuwa usawa wa ngazi fupi ambazo zilikuwa zinaelekea kwenye mlango mkubwa wa kuingilia ndani. Akatoka kwenye maficho ya mti ule kwa kasi ya mita mia moja hadi kwenye mnazi ambao ulikuwa usawa wa mlango. Aliwasikia walinzi wakiongea kwa sauti za chini. Kizuizi baina yake na hao walinzi kilikuwa ni gari aina ya Toyota Landcruiser ambalo lilikuwa limeegeshwa usawa wa mnazi. Akatulia dakika kadhaa kabla ya kupiga hatua kuelekea mlango wa kuingilia ndani. Akajaribu kufungua, lakini ulikuwa umefungwa kwa funguo. Akachomoa rundo la funguo ambazo zilikuwa mfukoni. Kila alipokuwa anajaribu ufunguo alihakikisha kuwa macho yake ameyaelekeza getini licha ya kuzuiwa na gari. Kijasho chembamba kilikuwa kinamtoka, alihisi kubanwa na pumzi. Mapigo ya moyo wake yalikuwa yanaenda kasi. Hatimaye moja ya funguo zake ikafanikisha zoezi lile. Akafungua mlango na kuingia ndani taratibu huku akihakikisha anarudisha mlango. Baada ya kufanikiwa hatua hiyo akaanza kutembea taratibu kuelekea ngazi zinazoelekea juu. Akatembea kwa kunyata huku viatu vyake vya mpira vikificha kelele za mchakato wa nyayo zake. Alipofika usawa wa chumba kimoja akasikia sauti za watu waliokuwa wanaongea. “Sasa utafanyaje mama.” “Mimi sijui la kufanya mwanangu, wameninyang’anya paspoti wamenilazimisha kuacha kazi na wamenizuia kuongea na mtu yeyote bila ya usimamizi wao.” “Kwani baba aliwahi kukudokeza wasiwasi wake wa kuuwawa?” “Hapana isipokuwa aliwahi kunieleza mzozo wake na baadhi ya viongozi ambao walikuwa hawampendi kutokana na kufuatilia na kutaka kuvujisha siri za ufisadi katika wizara mbalimbali.” “Kwa hiyo waliomuua baba watakuwa mafisadi?” “Bila shaka na kuna mengi ambayo siwezi kukueleza kwani ni hatari kuyafahamu, sasa ona haya maisha gani tunalazimishwa mpaka kufikia saa 3 tuwe tumelala, ndiyo maana nilikuomba ubaki hukohuko Kyela kwani hapa mambo si mazuri si unaona jumba lote hili nimeachwa peke yangu?” “Kwanini hakuna hatua zozote za upelelezi zinazoendelea?” “Sifahamu kama zipo au hazipo, ninachofahamu ni askari ambaye alipewa jukumu hilo, alishambuliwa pale tu alipojaribu kuhojiana na mwandishi wa gazeti la muungwana ambaye alikuwepo eneo la tukio sina uhakika iwapo huyo askari yuko hai au ameshakufa.” Taisamo alihisi hatari iliyopo kwa kuendelea kusimama pale bila ya kuingia ndani. Akakinyonga kitasa cha mlango wa chumba kile taratibu kisha akaingia ndani kama mtu ambaye hana wasiwasi. Akaufunga ule mlango na kuwageukia mama na mwanae ambao walikuwa wamezama kwenye mazungumzo mazito. Alikutanisha macho yake na macho yaliyojaa woga ya mke wa marehemu Ole Nunga. “Samahani mama, sikuwa na namna mzuri ya kuhudhuria kikao chenu zaidi ya hii niliyoitumia.” Alianza kuongea baada ya kuwaona wote wakiwa wanatetemeka kwa woga kisha akaendelea. “Sikufahamu kuwa upo kwenye wakati mgumu kiasi hiki, pole sana.” Kisha akachomoa kitambulisho chake na kumwonesha yule mama ili kumuondoa hofu. Yule mama na msichana wote walikuwa wamekaa kitandani. Bado yule mama alionesha kutomuamini Taisamo. “kwa kifupi, mimi natokea kwenye kitengo maalum cha upelelezi ndani ya jeshi nimekufuatilia kuanzia shuleni kwako Tabata….” Kisha akamueleza yote kuanzia yale maongezi na wale walimu mpaka kule Ofisini. “Kwa hiyo ulitaka nikusaidie nini?” “Mama wewe ni sehemu muhimu sana ya upelelezi wangu. Mambo matatu tu nataka kuyafahamu kutoka kwako. Jambo la kwanza ni maadui wa marehemu kama una wafahamu wa ndani nan je ya chama, jambo la pili ningependa kufahamu sababu ya uadui huo mwisho ningependa kufahamu kama kulikuwa na mabadiliko yoyote ambayo marehemu alikuwa nayo kabla ya kifo chake.” “Mwanangu kabla sijakujibu lolote, kwanza nataka kufahamu umewezaje kuingia humu ndani bila kuzuiwa wakati ulinzi ni mkali?” “Usihofu mama, najua bado una wasiwasi na mimi, nimeingia kwa njia za panya sijapitia huko getini kama unavyofikiri. Najua unajiuliza jinsi nilivyoweza kupita huko ukutani maana ndio njia pekee iliyobaki, napenda ufahamu kuwa mimi si mwanajeshi tu bali ni mwanajeshi maalum.” “Lakini si unajua hatari inayoweza kutokea kwa kuongea na wewe mambo mazito kama haya?”
“Ni kweli na nitajitahidi kukulinda kadiri ya uwezo wangu.” “Utanilinda vipi?” “kukulinda kwangu ni kwa jambo hili kulifanya kuwa la siri, siwezi kumweleza yeyote kama kuna lolote nimelisikia kutoka kwako mpaka nikishamaliza kazi hii kama kutakuwa na ulazima wa kufanya hivyo sasa naomba unijibu mama.”
“kuhusu maadui alikuwa nao wengi ndani ya chama na si nje ya chama, sababu kubwa za uadui ni mambo mawili tu, Jambo la kwanza ni cheo chake kwani kama unavyofahamu kila mtu mwenye uchu wa madaraka huwa anatamani nafasi kama ile, jambo la pili ni misimamo yake ya kupinga ufisadi, nafikiri unafahamu wazi kuwa chama kimepoteza dira kila mmoja anatamani kuwa kupe badala ya kuona aibu? Kuhusu swali lako la tatu ni kweli marehemu alikuwa na mabadiliko makubwa sana kabla ya kifo chake, mara nyingi alikuwa anaweweseka usingizini. Baadhi ya maneno aliyokuwa anaongea ni….. Sitaki lazima nigombee, demokrasia iko wapi….Yapo mengine mengi ambayo pengine yanatokana na kuufikiria sana uchaguzi. Zaidi ya hapo mwanangu hakuna ninachofahamu kwani marehemu alikuwa msiri sana na hakutaka kunishirikisha katika mambo yake mengi ya kisiasa.” Akatulia na kumkazia Macho Taisamo kama anayetaka kuulizwa swali la ziada. “Na huyu….” Huku akimnyooshea kidole yule binti. “Ni binti yangu, mimi na marehemu tumebahatika kupata watoto wawili tu wa kwanza ni huyu Jeska na wa pili ni Zakayo ambaye ameondoka siku chache baada ya mazishi kurudi chuoni Japan.” “Nilikuwa nakusikia jinsi ulivyokuwa unamsimulia binti yako matukio ya kifo cha baba yake ina maana hakuwepo msibani?” “Huyu tulichelewa kumpa taarifa kwani naye alikuwa chuoni Uganda, tulisubiri amalize mitihani yake.” “Pole sana Jesca.” Aliongea huku wakipeana mikono. “Ahsante.” Alijibu huku akitumia mkono wa kushoto kupangusa machozi ambayo yalianza kutiririka kama matone ya mvua kwenye kioo cha gari. “Lakini nina wazo mama, naona hapa kama hapakufai nahisi kama uko hatarini. Unaonaje ukiondoka hapa.” “Mwanangu, nashukuru unaonekana kuwa na mawazo mazuri, hicho ndicho tulichokuwa tunakijadili kabla na mwanangu lakini tatizo tutatokaje hapa ndani? Siruhusiwi kutembea peke yangu pia hata mwanangu naye kazuiwa” “Nitakusaidieni, hakuna njia zaidi ya kutoroka kwani hatujui hawa jamaa wana dhamira gani.” “Utatutoaje huko nje wakati kuna askari?” “Usihofu, kuna ngazi humu ndani?” “Ipo.”
*** JAMBAZI LAJISALIMISHA POLISI Gazeti moja la kila siku lilikuwa miongoni mwa magazeti kadhaa yaliyotoa taarifa ya tukio hilo la aina yake. Halikuwa jambo la kawaida kwa majambazi kujisalimisha toka muheshimiwa Alphonce Kanyanga atolewe wizara ya mambo ya ndani. Ni waziri ambaye alifanya kazi kwa ustadi mkubwa na kufanikisha majambazi kadhaa kujisalimisha wenyewe polisi huku wakikabidhi silaha zao. Toka aachie wizara hiyo mambo yamekuwa yakienda ovyo na kila kitu kuvurugika. Leo kwa mara ya kwanza chini ya waziri ambaye si tishio kwa majambazi anatokea jambazi na kujisalimisha mwenyewe polisi. Gazeti moja likaongezea kwa kusema ANA SIRI NZITO AMBAYO ATAITOA MAHAKAMANI. Habari hii ilikuwa gumzo katika jiji hususani baada ya kutokea kwa mauaji kadhaa ambayo hayaeleweki chanzo chake. Kuuwawa kwa Makamu wa raisi, Mwandishi wa habari, daktari na muuguzi kuliamsha hisia za hofu na udadisi kwa wananchi walio wengi. Kujisalimisha kwa jambazi huyo kulizuwa minong’ono kuwa huenda anafahamu siri za mauaji hayo.
*** Simu iliendelea kuita na kumkera Selemani Mahundi mkuu wa gereza la Ukonga ambaye alikuwa amejilaza kwenye sofa pale sebuleni. Hakujisikia kupokea simu hiyo kutokana na uchovu aliokuwa nao. “We mama Juma, naomba uniletee hiyo simu.” “Unataka ukate, si useme tu niikate hukuhuku?” “Niambie kwanza nani anapiga ndipo ukate.” “Kamishna Mkuu.” “Nini, ilete haraka.” Usingizi wote na uchovu aliokuwa nao ulikimbia kama mtu aliyesikia simba ananguruma nje ya nyumba yake. “Halow afande shikamoo.” “Marahaba Mahundi, nafikiri una taarifa juu ya ujio wa mtuhumiwa muhimu sana kwenye gereza lako.” “Ndiyo mkuu, amewasili kama nusu saa iliyopita tumeshampokea na tumetekeleza majukumu yote kama ulivyohitaji.” “Ok, sasa huyo ni mtu muhimu sana na tumepokea maagizo kutoka wizarani kuwa asihojiwe chochote na yeyote, hakikisha kuwa anakaa sehemu ya peke yake asipate fursa hata ya kuongea na wafungwa au mahabusu wenzake.” “Nimekuelewa mkuu, vipi kuhusu mwanasheria kama atahitaji kuwasiliana nae?” “Hilo pia limezuiwa hiyo ni special order kutoka makao makuu.” “Sawa afande nitatekeleza.” Usingizi wote ulikuwa umetoweka na sasa akaamua kuhamishia macho yake kwenye runinga. Kipindi alichokuwa anaangalia kilikuwa ni cha uchambuzi wa magazeti yanayotoka jioni. “Familia ya marehemu Ole Nunga aliyekuwa makamu wa raisi yatoweka.” Alisikika mtangazaji huyo na kumfanya mkuu huyo wa gereza kupoteza kabisa uchovu uliosalia. Akaamua kukaa vema na kuisikiliza taarifa hiyo.
*** Akiwa ndani ya maficho mapya katika nyumba ya kulala wageni inayojulikana kama kusini guest house iliyoko eneo la Temeke mwisho, ndio kwanza alikuwa anamaliza kula ugali na nyama choma ambavyo aliviagiza kutoka mgahawa ulioko nje. Akashushia na juisi baridi ya ukwaju. Hakujisikia kunywa kilevi chochote katika wakati huo mgumu ambao hakujua nguvu ya kumtafuta ni kubwa kiasi gani. Saa 5.30 simu ya Taisamo ilianza kuita. “Hallow nani mwenzangu.” “Teacher Suzzy hapa, mbona huonekani Taisamo uko wapi?” “Niko safarini nitarudi baada ya wiki mbili.” “kuna wageni wengi sana huwa wanakuja kukuulizia hapa nyumbani.” “Huwa wanajitambulisha.” “Kuna mmoja tu ndiye alijitambulisha, anasema anaitwa Rose.” “Yaani huyo tu ndiye umemkumbuka haraka?” “Kwa sababu ni mwanamke halafu alisema mnafanya kazi ofisi moja, sasa nilikuwa nashangaa mtu mnayefanya naye kazi ofisi moja anashindwaje kujua taarifa za safari yako.” “Suzy, tunaweza kuonana?” “we si uko safarini tutaonana vipi?” “Kesho nitakuja Dar mara moja kwa ajili yako tu.” “kuna nini?” “Nafikiri tutaongea zaidi tutakapoonana.” “Nafikiri kama ni maongezi tu basi tuongee kwenye simu.” “Hapana Suzy, unajua simu inawafaa zaidi watu waoga wasiojiamini.” “Sikuelewi unamaanisha nini?” “kuna jambo nataka kukueleza lakini sitopenda kuliongea kwenye simu kwani nachelea kuingia katika kundi la wanaume waoga.” “Kama jambo lipi?” “Dah, we mwanamke mbona unachimba sana.” “We sema tu, mi nitajua ni mwanaume jasiri ambaye umelazimika kutokana na sababu ambazo haziwezi kuzuilika.” “Nakupenda.” “Mh, halafu Rose!” “Huyo Rose ni mfanyakazi mwenzangu na hata hivyo simfahamu.” “He, Unanishangaza sasa Rose amekuja hapa anaonesha dalili zote za kukupenda we unasema humfahamu unashindwa vipi kumfahamu mfanyakazi mwenzio?’ “Yeye ni mwandishi wa makala za uchumi pale ofisini, na ofisi yetu ni kubwa sana wengine huwa hatufahamiani kama huyo Rose namfahamu kwa kusoma tu makala zake za uchumi.” “Lakini yeye anakufahamu na anakupenda.” “Umejuaje?” “Mimi ni mwanamke naomba uniamini Rose anakupenda.” “Mimi nimekupenda wewe naomba kesho tuonane.” “Niko tayari kuonana na wewe lakini kwa swala la mapenzi nakushauri uwe na Rose.” Baada ya kukata simu Taisamo akazirudisha fikra zake kwa Rose. Ni nani huyu Rose na kwanini bado anamfuatilia? Kwanini Suzy yuko tayari kukutana na mimi wakati anaonesha kutokuwa tayari? Alianza kuingiwa na wasiwasi juu ya usalama wake katika mikono ya Suzy hasa alipofikiria picha alizopigwa na dokta na jinsi zilivyoweza kuingia ndani. Mawazo mengi yaliyokuwa yamesababishwa na matatizo mazito anayokabiliana nayo kwenye kazi yalikatishwa na usingizi mzito uliomchukua ghafla. Usingizi huo ulitawaliwa na ndoto nyingi za kutisha, zikitawaliwa na mauaji na damu ambayo aliishuhudia. Aliziona maiti za nesi Belinda na msichana wake wa kazi zikiwa zinavuja damu mbichi huku akiwa amesimama nyuma yake, ghafla akatokea mwanamke ambaye alijitambulisha kwa jina la Rose na kumfahamisha kuwa amekuja kumsaidia kumpata muuaji, akapeana naye mkono kwa furaha lakini ghafla yule mwanamke akachomoa bastola na kumuelekezea Taisamo. “Lazima nikuue mbwa wewe.” Alifoka yule mwanamke. Akashtuka kutoka usingizini huku jasho likimvuja. Alihema kwa nguvu kutokana na hofu kubwa. “Ina maana Rose ananisaka aniue?” Alijiuliza huku akiwa amekaa kitandani. Mawazo hayo hayakuchukua muda mrefu kwani punde yalikatishwa na mlio wa simu iliyokuwa chini ya mto. “Nani tena.” Alilalamika huku akinyoosha mkono wake kivivu vivu. “Sikiliza Alex, hapa ni makao makuu ya Jeshi la wananchi. Unahitajika ufike hapa sasa hivi kabla jeshi halijaamua kutumia nguvu kukutafuta, hatua uliyofikia ni mbaya zaidi kwani umefanikiwa kuwateka mke wa makamu wa Raisi na binti yake na haifahamiki umewaficha wapi, mbaya zaidi ni kwamba hutafutwi na wapelelezi wa jeshi tu hata wa usalama wa Taifa na wenzetu wa CID pia wanakutafuta ingawa tofauti hapa ni kwamba sisi tunajua tunamtafuta nani lakini wenzetu hawamjui wanayemtafuta.” Akakata simu na kuirudisha pale alipoitoa. Dakika hiyohiyo usingizi wote ulitoweka, maana alipata simu ya mtu ambaye alikuwa ‘sirias’ kuliko alivyomzoea, mtu asiyemfahamu, mtu anayemwendesha kama rimoti Rose ni nani huyu Rose? Aliinuka kitandani na kuvaa nguo zake haraka haraka, baada ya kujiona yuko sawa akatoka na kwenda kujichanganya sehemu ambayo ilikuwa na vinywa ji huku watu wachache wakiwa wamekusanyika hapo. Kulikuwa na runinga moja ambayo macho ya watazamaji wachache yalikuwa yameelekezwa hapo huku wale wachache wengine wakiendelea kunywa bia. “Naona umeshindwa kulala!” Alisikika muhudumu wa nyumba ile ya kulala wageni ambaye alihudumia wateja wa vinywaji pia.
“Aah, kitanda kinachosha, nipatie maji tafadhali yasiwe ya baridi.” Aliendelea kuikodolea macho runinga ile huku kiukweli akiwa haoni kabisa kinachoendelea. Ghafla, kama aliyezinduka kutoka usingizini akayaelekeza macho yake kwenye Runinga huku akiwa na umakini unaotakiwa. Ni taarifa ambazo zilikuwa zinasomwa kwenye ile runinga. “…. Kwa taarifa tulizonazo ni kwamba hadi hivi sasa Familia hiyo ya marehemu Ole Nunga haifahamiki iliko na wala watekaji wake, sambamba na tukio hilo jambazi aliyeamua kujisalimisha bado yuko katika mikono ya dola na atafikishwa mahakamani baada ya kukamilika mahojiano, habari kamili mtaletewa kesho baada ya kupatikana taarifa ya kamanda wa polisi ambaye ataongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari na maelezo.” Ilimaliza sehemu ya taarifa hiyo ambayo ilikuwa inasomwa katika moja. Baada ya taarifa hiyo aliamua kurudi chumbani kwake huku akisahau kuchukua maji yake ambayo hakuyanywa kabisa. Akili yake ilikuwa imechoka kutokana na kuwaza kupita kiasi. Akafunga mlango na kwenda kujitupa kitandani, hakukumbuka hata kuvua nguo.
*** Msichana mrembo alitembea kwa mwendo wa kinyonga kuelekea kwenye moja ya viti vilivyokuwa wazi katika eneo hilo la hoteli. Hakuonekana kuwa na haraka licha ya kuangaza macho yake huku na huko kwa nia ya kumtafuta mwenyeji wake. Alikuwa amevaa gauni refu la rangi ya dhambarau lenye mng’ao lakini lenye mpasuo wa wastani kwa mbele ambao ulifika usawa wa magotini, ile sehemu ulipokomea mpasuo ilikuwa na ua zuri lenye rangi za bluu bahari na zambarau. Akiwa na kimo cha wastani alikuwa na umbo la kuvutia ambalo lilimfanya awe kivutio kwa jicho la kiume ambalo lingetua kwake. Wanaume wachache waliokuwa ndani ya ukumbi huo wa vinywaji katika hoteli ya Rovena walishindwa kujizuia kumtazama binti yule, wengine wakashindwa kuzuia hisia zao kwa kumkazia macho yao kwa namna ambayo ingefanya yeyote aliyekuja na mkewe apigwe kofi la uso au shavu. “Niko hapa malaika.” Sauti ilimshitua. “Ooh, Jirani.” “Karibu ukae teacher Suzy.” “Ahsante.” “Umependeza saaana.” “Ahsante, wewe mbona uko hivyo?” “Nikoje?” Aliuliza Taisamo. “Ni siku chache tumepoteana lakini unaonekana umekuwa mnyonge na pia umepungua kama ulikuwa unaumwa vile, vipi kuna tatizo?” “Agiza kwanza unachohitaji Suzy kisha tutaongea.” “Nahitaji kinywaji chochote ambacho hakina kilevi kama Vitamalt, bavaria chochte kile.” “Kwanini?” “Situmii kilevi cha aina yoyote.” “Ok. Hakijaharibika kitu, chakula?” “Chips kuku.” “Ok.” Wakati wanaendelea kujadiliana muhudumu wa kike ambaye alikuwa nyuma yao alisimama kwa utulivu huku akisubiri wamalize majadiliano yao. Baada ya mjadala huo mfupi wakaagiza vitu walivyohitaji. “Enhe, tumeshaagiza naomba unijibu maswali yangu.” “Nafikiri ni ugumu tu wa maisha.” “Alex Taisamo, kwanini unanifanya kama mtoto mdogo?” “He, nani kakutajia jina langu lote?” “Ndio maana nakuambia usinifanye mtoto mdogo, nimekuuliza makusudi hayo maswali ili kama una tatizo ninaloweza kukusaidia nifanye hivyo, niambie ukweli una tatizo gani?” “Suzy, u mwanamke mwerevu sana nazidi kukupenda lakini nataka kujua kwanini umekuwa na hisia hizo juu yangu?” “Siku ambayo ulikuwa unaniaga pale nyumbani ulikuwa na kila dalili ya mtu aliyechanganywa na jambo, macho yako hayakuwa na utulivu pia ulikuwa na tabasamu bandia. Si hivyo tu toka umeondoka umekuwa unafuatwa na kuuliziwa mara kwa mara na watu wenye kila dalili za ukachero, hivi ninavyokuambia kuna taarifa ambazo nimetonywa na mmoja wa waliokuwa wanakutafuta kuwa umemteka mke na mtoto wa marehemu muheshimiwa Ole Nunga. Ukweli toka hapo nimekuwa nakuogopa lakini kuna kitu kama siamini vizuri hivi…. ndio maana nataka kutoka kwako maelezo ya kina ili niweze kukusaidia kama inawezekana kwani pale ndani tumeshapewa namba za simu ambazo kama utaonekana tunatakiwa kutoa taarifa mara moja.” Akatulia na kumkazia macho Alex Taisamo ambaye alikuwa mtulivu na hakuruhusu mshtuko muda wote aliokuwa anapewa taarifa hiyo. “Kitu gani kinakufanya usiwaamini hao makachero?” “Nasikia hiyo nyumba ya makamu wa raisi ina ulinzi mkali hasa baada ya kifo cha Muheshimiwa, kwa jinsi ninavyokufahamu ingawa ni muda mfupi toka tufahamiane bado siamini kama unaweza kufanya kitendo kama hicho.” “Ok, nimekuelewa Suzan oh sorry suzy” “hakuna shida umepatia tu mi naitwa Suzana lakini Suzy ndo limezoeleka zaidi.” “Vema. Ukweli ni kwamba ninatafutwa, tena sana. Msaada ninaoutaka kutoka kwako ni taarifa za mtu yeyote ambaye atakuja kuniulizia kama……” “Kwa hiyo ulichoniitia hapa si mapenzi ila ni hilo la kutaka kujua nani anakutafuta?” “Sikiliza Suzan, hata angekuwa nani lazima angebadilisha mada hivi unafikiri kutafutwa ni jambo zuri?” “Kwa hiyo hatutajadili tena kuhusu mapenzi yetu?” “Suzan, nashindwa kukuelewa.” “Kivipi?” “Bado hunionei huruma hata kwa hayo matatizo yanayonikabili?” “Nafikiri hatukukutana hapa kuzungumzia hayo matatizo yako, au ndio ulitumia ujanja huu wa kuniita hapa ili ujue kinachoendelea nyumbani na si mapenzi kama ulivyonieleza? Kama ni hivyo basi nieleze kwa kina bila kutafuna maneno chochote kinachokuhusu juu ya sakata hili vinginevyo utanifanya nikufikirie vibaya.” “Suzy, ni wewe kweli?” “Nimekuwaje?” “Sikuelewi, ghafla umekuwa mkali hutaki mjadala uende kidiplomasia.” “ni wewe ndio umeanza kuharibu hiyo unayoita demokrasia, umekuwa mwongo sana na hata kama nitakubali ombi lako la kuwa mpenzi wako sijui itakuwaje…. Kumbuka ulinifahamisha kuwa wewe ni mwandishi wa habari pia ulinieleza kuwa uko wapi sijui safarini lakini ninachokiona hapa ni uongo mkubwa, wewe ni mwanajeshi unafahamika hivyo na kila mmoja pale ndani kwanini ulitaka kuniongopea?” “Mhhhhh.” Alishusha pumzi na kuyaelekeza macho yake juu, ama kwa hakika lilikuwa shambulizi la ghafla sana. “Suzana.” “Abee.” “Naomba kwa leo tuachane, najua unautaka ukweli ambao unaweza kukugharimu.” “Naomba maelezo ya kina tafadhali.” “tuonane baada ya mwezi mmoja.” Alisikika Taisamo huku akiitazama bili yao ambayo ililetwa muda mfupi uliopita.
***
Alifumbua macho yake kabla ya kuyafumba tena kwa haraka kutokana na mwanga mkali ambao ulimpiga moja kwa moja kwenye macho yake. Alihisi kichwa chake kuwa kizito kuliko kawaida. Uwezo wake wa ufahamu ulikuwa mdogo lakini huku ukipata nguvu kadri muda ulivyokuwa unasonga mbele. Sasa fahamu zake zilianza kupata nguvu, alijijua kuwa yeye ni Inspekta, sasa hapo yuko wapi? Lilikuwa ni swali gumu ambalo liliongeza nguvu ya fahamu yake. Alijikuta akianza kuvuta kumbukumbu ya matukio. Alikumbuka jinsi alivyomuaga mwanawe mtoto wa marehemu mama yake mdogo kuwa anaelekea kazini…. Kisha… “Ah, kisha nini?” Alijikuta akishikwa na hasira zaidi kwa kushindwa kubaini kilichoendelea baada ya hapo. Ghafla alijikuta akipatwa na mshtuko baada ya kukumbuka kuwa amepewa jukumu zito la kupeleleza kifo cha makamu wa Rais. “Hivi nimefikia wapiiii…” swali lilipita kichwani mwake na kumfanya aanze kurejewa na kumbukumbu. “John Oscar… aah, ameuwawa halafu nikashambuliwa… no it means I’m…. no niko hai…. Kwa hiyo hapa ni hospitali? Na vipi kuhusu kamishna ambaye alikuwa ananipigia simu? Mh …..” Alijikuta akipatwa na wazo jipya baada ya kumkumbuka Kamishna. Aliinuka na kukaa kitandani huku akianza kuyasanifu mazingira ya chumba kile. Mbele ya kitanda chake kulikuwa na kikabati kidogo chenye magurudumu ambacho hakikuwa na chochote zaidi ya bomba la sindano ambalo lilikuwa kwenye kifungashio chake. Mbele zaidi ya nyuma ya kile kikabati kidogo kulikuwa na kabati kubwa la chuma ambalo lilikuwa na rangi ya kijani mpauko kabati hilo lilikuwa na ‘code number’ ambazo haraka Inspekta alitambua kuwa yupo hospitali ya taifa ya Muhimbili Taasisi ya mifupa MOI. Sasa hakuwa na shaka kuwa yupo hospitali baada ya kipigo cha kushtukiza ambacho alikipata alipoenda kwa John Oscar ambayea alimkuta akiwa ameuwawa. Ni wazi kuwa muuaji hakutegemea ujio wa ghafla wa Inspekta, lakini kwa nini Kamishna alikuwa kama amemchelewesha? “Ooh, umeamka mama. Shikamoo!” Muuguzi ambaye aliingia ndani muda huo alimshitua Inspekta kutoka kwenye kina kirefu cha mawazo. Inspekta alimwangalia yule Muuguzi kwa macho ya mduwao huku akishindwa kujibu salamu yake. “Nakusalimia mama.” “Marahaba, nani kanileta hapa hospitali?” “Umeletwa na askari wenzio.” “Wako wapi kwa sasa?” “Huko nje wako wawili ambao wapo zamu, ikifika asubuhi anakuja mmoja tu ambaye anaondoka jioni.” “Eh, ina maana huu ni usiku?” “Ndiyo mama ni saa nane na robo sasa.” “Mungu wangu ina maana nimelala hapa kwa masaa zaidi ya kumi nambili?” “Pole sana mama lakini hii ni siku ya tatu sasa uko hapa hospitali.” “What?” “Ndivyo ilivyo lakini tunamshukuru Mungu kwani umekuwa salama.” “Mh.” “Kwa sasa inabidi nikuchome sindano mbili kama nilivyoagizwa na daktari.” “Ok, fanya kazi yako binti” Akafungua lile kabati kubwa na kutoa chupa kadhaa za dawa, kisha akamgeukia Inspekta. “Hii moja ni ya usingizi ambayo itakuchukua masaa sita kutoka sasa, sasa sijui nimfahamishe yule mkubwa wenu kwanza au… maana ni usiku mwingi.” “Mkubwa yupi ina maana kuna mtu anafuatilia taarifa zangu?” “Ndiyo, alijitambulisha hapa kuwa ni kamishna nani… sijui nani vileee.. ah nimemsahau kidogo lakini aliniambia kuwa nimfahamishe mara tu utakaporejewa na fahamu.” “Yukoje?” “Ni mrefu mweusi.” “What? Alikupa namba yake ya simu au alikuambia utumie ya ofisini? alikuwa na sare za kazi?” Maswali ya haraka yalimtoka Inspekta. “Namba alinipa tena ni ya simu yake ya kiganjani, hakuvaa sare za kazi alikuwa amevaa suti nyeusi na kofia nyeusi ya duara kama zile wanazovaa waendesha farasi kwenye Tv.” “Sikiliza nesi, usithubutu kumfahamisha kuwa nimezinduka kama inawezekana hata hiyo sindano ya usingizi usinichome.” “Hapana, hii ya usingizi lazima nikuchome kama alivyoagiza daktari.” “Sawa lakini kwanza niandikie hiyo namba ya huyo mtu kabla ya kunichoma sindano sawa?” “Sawa nimekuelewa mama.” Baada ya kuandika akamgeukia Inspekta Tunu. “Haya mama kaa vizuri nikuchome sindano.” “Hapana, hutonichoma sindano, siko tayari kuharakishiwa kifo namna hiyo.” “Ni maelezo ya dokta mama.” “Sikiliza nesi.. njoo nikudokeze kitu sikioni….” Nesi akasogea nae akamnong’oneza.
***
James Makabi alishangazwa na mienendo ya pale gerezani, tofauti na mara ya kwanza ambapo alikuwa mfungwa alishangaa kuona akiwa chini ya uangalizi mkali tena la kushangaza zaidi ni baada ya kugundua kuwa hata baadhi ya askari magereza walikuwa wanamwogopa. Kwake halikuwa jambo la kawaida. Kwa upande mwingine alianza kujilaumu kwa kitendo chake cha kujisalimisha kwenye mikono hiyo ya sheria ambayo kiasi fulani alianza kuitilia mashaka. Kama ni ujambazi mbona kuna watuhumiwa na wafungwa wengi mle gerezani lakini kwa nini hawakupewa ulinzi mkali kama ule? Hofu ya maisha yake kuwa yako hatarini ikazidi kumtawala. Akahisi kuwa njama za Mjomba Masharubu zitakuwa zinaendelea na sasa atakuwa amehamishia huko gerezani. Kama alikuwa na nguvu kubwa ya ushawishi kiasi cha kuweza kutolewa gerezani kwa msamaha wa Raisi basi anao uwezo mkubwa wa kushawishi hata akauwawa hukohuko gerezani. Wazo hilo lilipopita kichwani mwake akajikuta akijiuliza swali la ghafla. Huyu mjomba ni nani hasa? Swali hilo lilianza kumtesa na kumtia mashaka kwani alihisi kuwa Mjomba ni mtu mzito ambaye nyuma yake kuna watu wazito zaidi yake. Lakini kwanini wamemuua makamu wa Raisi? Kama ni uzito naye si alikuwa mzito mwenzao? Akiwa kwenye fikra hizo mara mlango wa ule wa chuma wa chumba alichopo ukafunguliwa. Askari mweusi mkakamavu akamkodolea macho kabla ya kumsukumia bakuli la chuma lililojaa uji. “samahani afande.” Alianza Makabi huku akimkodolea macho askari yule ambaye alionekana kama mwenye haraka. “Naomba unisaidie kitu kimoja tu.” “Nikusaidie nini ongea fasta usije kunisababishia majanga hapa!” “Ahsante afandea angalau wewe umeweza kunisikiliza” “Punguza ngonjera wewe, sema shida yako si unajua wewe ni mtuhumiwa ghali kuliko watuhumiwa wote kuwahi kutokea.” “Mtuhumiqwa ghali?” Lilipita swali kichwani mwake. “Nahitaji kuonana na wakili sijui utanisaidiaje!” “Wakili?” “Ndiyo afande.” Akageuza macho huku na kule kabla hajaendelea kumsaili mtuhumiwa. “Suala lako limefungwa na wakuu kutokana na uzito wa tuhuma zako.” “Tuhuma zipi?” “Mimi sizijui kama hutajali si vibaya ukinidokeza.” Koplo Rashidi Chande alijikuta akiuliza swali ambalo siku zote alijiuliza yeye mwenyewe tu huku akikosa jibu. Ni zipi tuhuma za huyu mtu? Kwanini wakuu walizuia hata kuongea naye? “Afande ni mambo mazito, nakudokeza wewe kama wewe na kwa kuwa ni mtu wa kwanza kunisikiliza ni matumaini yangu kuwa utakuwa msiri na kunisitiri kwa jambo hili ambalo limegubikwa na usiri mkubwa” Akamsimulia kwa ufupi mkasa wake uliomkuta mpaka kufikia pale huku akimalizia na tukio la makabidhiano ya fedha jinsi lilivyogeuka mtego wa panya kwa kuuwawawa watu ambao hawakuwamo. Koplo Rashidi akajikuta akitetemeka na kijasho chembamba kikimtoka, midomo ilimkauka akajikuta akishindwa kuongea. Alimkazia macho Makabi lakini ukweli alikuwa hamuoni kabisa fikra zake zilikuwa kilomita kadhaa nje ya jengo. Semburi Makwanga jina hilo ndilo lililomjia haraka huku moyo wake ukienda mbio. Alimkumbuka rafiki yake huyo ambaye ni mwandishi wa habari, mara nyingi alikuwa akimpatia taarifa mbalimbali za matukio yanayojiri gerezani naye akimpatia kile kinachoitwa hela ya soda. Tabasamu la hofu likatanda usoni pake huku akiondoka eneo lile bila hata kumuaga Makabi. “Kuumbe… mh!” Alijisemea koplo huku akimaliza na mguno hafifu, pesa aliitamani lakini bado hofu ilimtawala kwani alijua wazi kuwa anacheza na jambo ambalo linaweza kuitikisa nchi.. Licha ya hatari ya jambo hilo kwa nchi bado ilikuwa ni taarifa nzuri kwa mwandishi wa habari za uchunguzi kwani ingempaisha na kumjengea jina uraiani licha ya heshima ambayo angeipata kazizini kwa wakuu wake wakazi. Si hivyo tu ni habari ambayo ingelijenga gazeti na kulifanya lipendwe hivyo kuliongezea kipato. Aliinua mkono wake wa kushoto na kuikazia macho saa yake ya mkononi aina ya Seiko5, zilikuwa zimebaki dakika 15 atoke kazini lakini aliona kama yamebaki masaa kumi kutokana na hamu yake ya kukutana na Semburi. “Hii itavunja rekodi, jamaa lazima wanitoe mshiko wa nguvu.” Aliongea kwa sauti ya chini huku akielekea upande wenye kibanda kidogo cha kukabidhiana kazi.
***** Eneo Fulani la jiji la Dar es salaam, Alex Taisamo alitembea kwa kasi huku akitazama huku na huko kuhakikisha iwapo yuko salama. Alilifikia lango kubwa linaloingia kwenye moja ya makampuni makubwa ya uuzaji wa magari. “Habari yako ndugu.” “Nzuri, sijui nikusaidie nini?” “Naomba kufika ofisi ya manunuzi ya magari.” “Ooh, karibu sana tena kuna mzigo umeingia jana tu!” “Ok, Ahsante wacha niwahi maana hii ni saa nane muda wa kufunga unakaribia.” “Hapana mkuu, hapa huwa tunafunga saa kumi na mbili jioni.” “Sawa.” Alijibu huku akiwa ameshapiga hatua kadhaa kutoka eneo lile. Hakupata shida kuingia ofisi aliyohitaji ndani ya jengo lile kubwa ambalo lilizungukwa na ukuta mrefu wa tofali za saruji, kila mlango alioutazama ulikuwa na maandishi mlangoni. KITENGO CHA MAUZO. “Habari za kazi.” Alisalimia huku akivuta kiti ambacho kilielekeana na mkuu wa kitengo cha mauzo ambaye alikuwa ameweka kibao kilichokuwa kinamnadi mbele yake huku kikiwa na jina lake ambalo lilisomeka kwa kifupi Mwita.M.B. “Salama kabisa, karibu sana.” “Ahsante.” “Sijui naweza kukusaidia?” “Bila shaka, nahitaji kupata kumbukumbu ya uuzaji wa magari aina ya Nissan Patrol” “Sidhani kama naweza kukusaidia kwa hilo kwa sababu hizo ni taarifa za kampuni na hatupaswi kuzitoa hovyo.” “Ni vizuri tukitambuana naitwa Luteni Taisamo.” Akachomoa kitambulisho chake na kumkabidhi yule jamaa. “Ndiyo Luteni, sijaona uhusiano wa kazi yako na hivyo vitu unavyovihitaji hivyo nashindwa kushawishika.” “Ni uelewa mdogo wa mambo ya ulinzi na usalama wan chi yetu, unaonaje nikikuhusisha wewe na kifo cha makamu wa Raisi muheshimiwa Nunga maana gari lililotumika ni Nissan Petrol ambalo limenunuliwa katika ofisi yako?” Lilikuwa shambulizi la ghafla kwa mkuu yule wa kitengo cha mauzo abalo lilimfanya ageuke mnyonge ghafla. “Sasa utanihusisha vipi na kitu ambacho kimeuzwa na kimetumiwa na mtu mwingine huko?” “Kukataa kwako kutoa ushirikiano ni moja ya dalili nzuri kabisa ya kuwa unahusika na unafahamu mpango mzima.” “Isiwe tabu mkuu kama jambo lenyewe liko hivyo ngoja nikuangalizie kile unachohitaji.” “Nitashukuru kwa ushirikiano wako.” “Sijui unahitaji kumbukumbu ya mwaka mzima?” “Hapana.” Akainua kichwa juu huku akifumba macho kwa kuvuta kumbukumbu ya kile alichohitaji. “Nahitaji kumbukumbu ya miezi miwili iliyopita.” “Unahisi hiyo gari ilikuwa mpya?” “Ndivyo ilivyo na ingekuwa ni vigumu gari kutembea bila kusajiliwa zaidi ya muda huo bila kuzusha hoja za wazi kwa wananchi.” “Ok, ngoja niiprint maana ninayo humu kwenye kompyuta.” Aliongea huku akijiuma uma midomo. Dakika chache baadae ile taarifa aliyoihitaji ilikuwa mezani, akachukua mashine maalumu ya kubania pini. “Ina maana huna secretary?” “Yuko likizo.” Taisamo akautumia muda ule mfupi kusoma taarifa ile aliyopewa kisha ghafla akamgeukia yule mkuu. “Naomba kujua namba hii ya gari ilinunuliwa na nani?” “Nakala huwa zinabaki kwenye kitabu cha risiti ambacho kinakaa kwa mkaguzi wa ndani wa hesabu za kampuni.” “Nakiomba hicho kitabu, nataka kujua gari lenye namba ya injini hii lilinunuliwa na nani.” “Sawa ngoja nikuangalizie huko kwa mkaguzi.”
****
Saa 7.30 usiku mlango wa chumba kidogo ambacho alifungiwa James Makabi ukafunguliwa, askari magereza wawili wenye sare zenye nembo za sajenti kila mmoja walikuwa mbele yake. “Tufuate.” Aliamrisha mmoja ambaye alikuwa na macho mekundu na sura ya ukatili kuliko mwenzake. Akainuka pale kwenye kirago huku moyo ukimwenda mbio na kuanza kuwafuata. Kilichomfanya awe mwepesi kuwafuata ni mazungumzo aliyoyafanya na koplo Rashidi, akili yake ilimtuma kuwa huenda mwanasheria ambaye aliomba kuonana nae amewasili, lakini kwanini iwe usiku wa manane? Swali hilo kidogo lilimtatiza lakini akaendelea kufuata bila kuuliza. Moyo ulizidi kwenda mbio alipoona wanapita kwenye lango la gereza bila kuulizwa na askari wanne ambao walikuwa zamu. Gari ndogo la kizamani aina ya Toyota Corolla lilikuwa limepaki huku ndani kukiwa na dereva ambaye alikuwa ameegemea usukani bila shaka akiwasubiri. Dereva hakuwa na sare kama wale wengine, alikuwa amevaa shati jeusi la mikono mifupi huku akiwa amechomeka airphone kwenye sikio la upande wa kulia. “Vipi shwari?” “Poa kaka.” Alijibu mmoja huku akimuelekeza James kukaa siti ya katikati. Gari iliondoka taratibu huku kukiwa hakuna mazungumzo yoyote ndani ya gari. Makabi aliitafsiri hali hiyo kuwa ni ya hatari kwake. Kutokana na giza Makabi alishindwa kuelewa ni wapi walikuwa wanaelekea. Dakika kumi na tano baadae alihisi wakielekea eneo ambalo lilikuwa nje ya mji, wakaacha barabara kubwa na kuingia vichochoroni ambako kulikuwa na nyumba mojamoja tena zikiwa mbalimbali. Baada ya kama dakika kumi wakaifikia nyumba moja ambayo ilikuwa imezungushiwa seng’enge, gari ikapiga honi kama mara tatu kisha lango likafunguliwa. Mwanga wa rangi nyekundu ulikuwa unatoka ndani. Bado Makabi alishindwa kutafsiri maana ya tukio lile, akaendelea kuwa kimya akisubiri kitakachojiri. Baadae wakatoka watu wawili wenye miili iliyojengeka vema kimazoezi wakiwa wamevaa fulana zilizopanguliwa makusudi huku zikiacha nje mabega yao, zilikuwa na nembo ya fuvu la kichwa cha mtu kifuani. Wote wawili walikuwa wamenyoa kipara huku mmoja akiwa amefuga ndevu ambazo zilichongoka na kufanana na za mchezaji mmoja ambaye anachezea klabu kongwe ya ligi kuu ya Tanzania, hata kwa sura alifanana na mchezaji huyo huyu alizidi kwa umbo kwani alikuwa katika namna ambayo watu mtaani wangemwita ‘Baunsa’. “Teremka.” Aliamrisha askari wa upande wa kushoto huku akiteremka kumpisha makabi, akarudi kwenye gari na kumwacha Makabi chini ya wale mabaunsa wawili ambao walimbeba kindakindaki kumeleka ndani. Akapelekwa kwenye chumba kimoja ambacho kilikuwa cha mwisho kabisa katika korido ya nyumba ile. Ulipofunguliwa mlango ndipo alipopatwa na mshtuko wa mwaka, hakuamini macho yake kwa kile alichokiona. Mpenzi wake Tamasha alikuwa amefungwa kwenye kiti cha chuma ambacho kilikuwa kimechimbiwa ardhini na kujengewa vizuri kwa zege, alikuwa anaonekana wazi kujeruhiwa kwa vipigo, alipoangalia vizuri kile kiti kilikuwa kimeunganishwa na waya uliotoka kwenye swichi ya umeme. Mdomo wa Tamasha ulikuwa umevimba kwa kipigo ambacho Makabi alishindwa kukielewa kilikuwa kinatokana na kosa lipi, alipomuangalia vizuria akagundua kuwa hata jicho la kulia nalo lilikuwa limevimba na kufanya wekundu. Alihisi hasira na kutaka kufanya makeke lakini alipoangalia upande wake wa kushoto na kuwaona wale Mabaunsa akanywea. Alipoangalia kona nyingine akamuona mwanaume ambaye alikuwa amefungwa kamba kama mpenzi wake. Tofauti na mpenzi wake huyo jamaa alikuwa amefungwa kwa umakini zaidi huku akionekana kupata kipigo kikali zaidi ya kile cha mpenzi wake.
“Hebu kaa hapo. Nawe kama hutatoa ushirikiano yatakukuta kama yaliyowakuta hao Mbwa wenzako.” Alisema huku akimnyooshe kiti ambacho kilikuwa kimeelekea kwenye dirisha kubwa. Akakaa na kulielekea dirisha lile ambalo lilikuwa linaonesha mandhari ya nje. Aliweza kuuona vema uzio wa seng’enge ambao ulifuatiwa na miti na vichaka ambavyo vilileta ugumu kidogo kulifahamu eneo lile. Hakukuwa na dalili ya nyumba karibu, alihisi kuwa zile walizozipita wakiwa kwenye gari ambazo zilikuwa takribani kilometa nne au tano kutoka pale zilikuwa nyumba za mwisho na ile ilikuwa eneo la peke yake kabisa. “Kaa, unashangaa nini?” Ilikuwa ni amri kali iliyofuatiwa na kofi kali la shavu ambalo lilimfanya aone vitu kama nyotanyota hivi. Hakutaka kufanya ubishi kwani alielewa kuwa ubishi wowote ungemsababishia kipigo kikali kama wale aliowakuta, akatulia kama maji ya mtungini akisubiri kuhojiwa. “Tunataka kujua nani na nani wanafahamu tukio lako na Mjomba Masharubu.” “Mpenzi wangu Tamasha ambaye ni huyo hapo kwenye kiti na askari magereza ambaye alikuwa zamu juzi mchana kule magereza.” “Vizuri unaonesha ushirikiano nzuri, ila napenda kukufahamisha kuwa huyo askari anaitwa Koplo Rashidi na kwa sasa ameshatangulia kuzimu kama ulivyomtanguliza jembe letu moyo.” Aliongea jamaa wa mzuzu huku akizunguka zunguka kwa namna ya kutakabari. “Pili nataka kufahamu picha ya mjomba Masharubu ambayo ilikuwa nayo kwenye simu kama bado ipo au uliifuta.” Makabi akatulia kidogo na kukumbuka jinsi alivyomuongopea Masharubu kuwa alimpiga Picha, akatabasamu kimoyomoyo kwani alifahamu wazi kuwa alimkamata pabaya Masharubu huku akitambua wazi kuwa hiyo ilikuwa ni fursa nzuri kwake kuchelewesha kifo au kipigo. “Ile picha bado ipo kwenye simu nyumbani kwangu.” “Usitufanye watoto wadogo, simu ulimwachia huyo mbwa wako na tumeipekua hatujaona picha.” Aliongea baunsa wa ndevu huku kauli yake hiyo ikisindikizwa na teke kali lililomsukuma sakafuni huku akifuatiwa na kiti mgongoni. Akajiinua na kufuta damu kidogo ambayo ilitokana na kuchanika kidogo sehemu ya juu ya mdomo.
***** Saa 10.30 alfajiri mlango wa chumba alicholazwa Inspekta Tunu ulifunguliwa, akaingia muuguzi aliyekuwa anamuhudumia akiwa na mfuko mweusi wa nailoni. Akampatia Inspekta ambaye aliufungua kwa kiherehere na kuchungulia kilichomo, akatabasamu baada ya kugundua kuwa nesi ametekeleza ombi lake ipasavyo. Ndani ya ule mfuko kulikuwa na koti jeupe ambalo huvaa madaktari. Haraka hara akavaa na kutoka nje ya wodi ile huku akiwapita askari waliokuwa wanasinzia pale nje. Baada ya kutoka akatembea kwa haraka huku akipishana na wauguzi wachache ambao walikuwa nje ya wodi zao, hakuna aliyejishugulisha kutaka kumtambua hivo ilikuwa rahisi kwake kutoka nje ya eneo hilo. Hofu yake ilikuwa pale getini kwani alihisi angetambuliwa na mlinzi kuwa sio daktari kutokana na kuwazoea madaktari. Bado alikuwa anahisi maumivu makali ya kichwa lakini hakuona sababu ya kukaa hospitali na kusubiri kitu ambacho alihisi ni kuzidi kuharibika kwa jambo asilolifahamu. Bahati ilikuwa upande wake kwani alipovuka tu getini alidakwa na dereva teksi. “Wapi dada?” “Magomeni usalama.” Alijibu kwa mkato huku akikaa kwenye siti iliyokuwa nyuma ya dereva. Akiwa kwenye gari alivuta fikra na kumbukumbu mbalimbali juu ya matukio yote kuanzia kupigiwa simu na kamishna mpaka kushambuliwa na mtu asiyemfahamu. Haikuwachukua muda mrefu kufika eneo la magomeni usalama. Aliteremka kwenye gari na kumlipa dereva kiasi alichohitaji kisha akatembea kwa kasi kuelekea kituoni. Alikutana na askari kadhaa ambao hawakuweza kumtambua haraka hivyo akakosa haki yake ya kupata heshima ya kiaskari. “He, afande!” Alikuwa koplo Peter Mkwabi ambaye alianza kushtuka baada ya kumuona Inspekta Tunu akiwa kwenye mavazi ya kidaktari. “Nifuate.” Aliongea neno moja tu huku akimuashiria koplo yule kuwa amfuate. Baada ya kukaa kwenye kiti chake alimkazia macho Koplo ambaye kama askari wengine aliowapita pale kaunta nao walionesha mshangao wa wazi lakini wakashindwa kumuuliza bosi wao nini kilichojiri. “Nini kinaendelea juu ya mauaji ya makamu wa Rais, uchunguzi umefikia wapi?” Mkwabi alimwangalia kwa wasiwasi bosi wake huyo ambaye hakutaka hata salamu jambo ambalo si la kawaida. “Afande Kamishna amezuia kufuatilia lolote linalohusiana na kifo cha makamu wa Rais mpaka wewe utakaporuhusiwa kutoka hospitali.” “What? Kwa hiyo tunatakiwa kuanza upya?” “Utaanzia ulipoishia afande.” “Ah, hii ni sawa na kuanza upya, naomba kuwasiliana na Sajenti Kasweyaga.” “Huyo kapewa uhamisho, anahamia wiaya ya Tunduru mkoa wa Ruvuma.” “He, lakini si atakuwa bado hajaondoka.” “Yaani ni usiku wa siku ile ambayo wewe ulishambuliwa akapokea simu kutoka kwa kamishna kuwa anatakiwa kuhamia Tunduru hivyo ajiandae, siku ya pili akapewa kila kilicho chake.” “Unakusudia nini unaposema kila kilicho chake.” “Fedha zote za uhamisho, gari ambalo litasafirisha mizigo yake pia kalipwa pesa za Night ya miezi miwili, yaani jamaa kadondokewa na dhahabu mkononi.” “Acha ujinga wewe hiyo si dhahabu, kuna mambo mazito hapa yanaendelea hii nchi saa……..” Hakumaliza badala yake alijishika kichwa kwa kukata tamaa. “Nitapambana kufa na kupona.” Alisema kwa sauti ndogo yenye kuonesha hasira huku akiinuka kwenye kiti na kumwacha Koplo akiwa amepigwa na butwaa. Huku akiwa na mavazi yaleyale ya kidaktari alitoka ofisini na kuelekea eneo la Magomeni mikumi ambako kulikuwa na teksi nyingi. “Wapi dokta?” Aliuliza dereva huku akimkodolea macho Inspekta ambaye alifikiri ni dokta. “Nipeleke Kawe”
Taisamo alikaa dakika kadhaa akisubiri nakala ya risiti ya manunuzi ya gari ambalo lilisababisha ajali ya makamu wa Raisi. Alikuwa kwenye fikra nzito muda huo alishindwa kuelewa kwa nini ilikuwa ni lazima kwa makamu wa Raisi, yaani mtu mmoja anashambuliwa kutoka pande tatu tofauti? Alikuna kichwa kwa kidole chake cha shahada. Mara mlango ukafunguliwa badala ya yule aliyemtarajia akaingia Msichana mrembo. “Unaitwa na mkurugenzi.” Taisamo akainuka bila kuongea lolote na kumfuata yule dada. Akapandisha ngazi hadi ghorofa ya kwanza wakaifuata korido ndefu hadi ofisi ya mwisho kabisa ambayo ilikuwa imeandikwa mlangoni DIRECTOR. Hakumuona tena yule Afisa mauzo na badala yake alimkuta mzee mnene mwenye nywele nyingi nyeupe. Mzee huyo alikuwa na rangi ya maji ya kunde, uso mpana na pua bapa. Alikuwa amevaa suti ya rangi ya kijivu. Alimtulizia macho yake yule mzee huku akistaajabu ule mzunguko ambao ulikuwa umeanza. “Habari kijana.” Alisalimia yule mzee kwa sauti nene yenye mikwaruzo bila ikionesha kuathirika kwa pombe. “Nzuri, shikamoo mzee.” “Mh, ahsante. Nimelipata ombi lako lakini utaratibu ulioutumia sio utaratibu wetu wa ofisi kwani ilibidi uandike barua kisha ungejibiwa baada ya siku tatu sawa?” alimtazama huku akisubiri jibu la kukubaliana na kauli yake hiyo. “Mzee, kuna mambo mengine ni ya dharura hivyo subira haifai tena.” “hilo sio ombi na kwa kawaida hakuna ninachozungumza kikarudi nyumba.” “Ni kweli lakini nasikitika kukufahamisha kuwa nalazimika kuvunja utaratibu wako, na nitakulazimisha kufuata taratibu zangu kwa nguvu.” “Kijana, naona umekosa adabu ondoka ofisini kwangu.” Wakati anamaliza kauli hiyo tayari alikuwa anatazamana na mdomo wa bastola ambayo ilikuwa imeshaondolewa kitunza usalama. “dakika mbili zinatosa kuchagua kati ya kifo au kutoa risiti ninayoihitaji.” “Sijawahi kuona mtu anayefanya mambo ya kipumbavu kama wewe, unafikiri ni jambo rahisi kiasi hicho wakati kuna kamera maalumu za usalama zinakumulika, na unanichekesha zaidi kwa kutofahamu kuwa umezungukwa na askari wenye silaha nzito.” Kauli hiyo ilimalizika ikifuatiwa na kauli nyingine nzito kutoka nyuma yake. “Weka silaha yako mezani halafu urudi nyuma hatua kadhaa, kabla hatujasambaratisha kichwa chako.” Haikuwa sauti ngeni katika masikio ya Taisamo, alikumbuka moja kwa moja kuwa ni sauti ambayo aliisikia nyumbani kwa dokta Kilonzo. “Umemuua dokta, umemuua nesi na sasa unakuja kunimaliza mimi?” Alihoji Taisamo akiwa amenyanyua mikono juu. “Leo jua linawaka usitegemee kuwa litazimika ghafla kama ulivyozimika umeme nyumbani kwa dokta.” “ni kweli lakini leo ni wewe ndiye utakayezimika.” “Unachekesha sana na hii inathibitisha kuwa kweli mfa maji haachi kutapatapa, yaani unafikiri unaweza kunusurika katika kibano kama hiki?” Taisamo aligeuka taratibu na kukutana na sura kavu za watu wanne wenye bastola. “Bado unaweza kuendelea na jeuri mbele ya wanaume kama hawa?” “Wanaume waoga ambao wanamfuata mtu mmoja tena wote wakiwa na bastola.” “Mzee tunafanyaje sasa?” Aliuliza yule muuaji wa dokta. “Nimepewa agizo kuwa anatakiwa afikishwe kunakohusika na kama hatatoa ushirikiano ndani ya siku mbili……” “Achinjwe?” alidakia muuaji wa dokta. Taisamo alikamatwa kwa nguvu na kuishuhudia sindano ikididimia begani kwake. Dakika chache baadae alihisi kizunguzungu na hatimaye akapoteza fahamu. Hakujua tena kilichoendelea hadi pale alipozinduka na kujikuta kwenye chumba kipana chenye dirisha kubwa la kioo. Hakuwa peke yake kulikuwa na mwanamke ambaye alifungwa kwenye kiti kama alivyofungwa, tofauti na yeye huyu alionekana kujeruhiwa sehemu kadhaa za mwili wake kwa kipigo. Taisamo alikuwa anakiona kifo chake waziwazi, hakuona kama kuna dalili ya kunusurika mbele ya mikono ile ya madhalimu. Kilichokuwa kinamsikitisha ni kuwa mpaka muda ule alikuwa hajafumbua mafumbo kadhaa juu ya mauaji yale, alitaka angalau kwa hisia kujua ni nani anaweza kuhusika na mauaji yale, si hivyo tu kwanini mzunguko ule ni mkubwa na unawahusisha watu kadhaa. Kuna nini kinaendelea?
Mara mlango ukafungulia na kumfanya aondoke kwenye dimbwi la mawazo. Mtu aliyeingia alikuwa na umbo la wastani kiasi ilikuwa ni vigumu kuelezea iwapo alikuwa ni mrefu au mfupi, alikuwa amevaa shati jeupe na tai nyeusi, chini alimalizia kwa suruali nyeusi na viatu vya rangi ya kahawia. “Habari yako bwana Taisamo.” “Nzuri.” Alijibu Taisamo kwa mkato huku akimtolea macho ya shauku yule mtu. “Una nafasi nzuri tu ya kujiokoa kwenye madhila haya nayo ni kutoa ushirikiano kwa kujibu maswali nitakayokuuliza, uko tayari?” Taisamo hakujibu chochote akabaki kumkodolea macho tu yule mtu. “Kwanza nataka kujua umetumwa na nani na mpaka sasa umefikia wapi, pili nataka kujua familia ya marehemu Ole Nunga umeipeleka wapi na nani alikutuma kwenda kuiondoa?” “Ningefurahi sana kama ungeweza kunifahamisaha wewe ni nani na umetumwa na nani ili tuweze kufahamiana maana njia uliyotumia kunialika kwenye huu usaili wako inanitia shaka.” “Sitaki nikulazimishe kuzungumza naomba unijibu maswali yangu.” “Nami sitaki unilazimishe kujibu.” Jibu hilo likafuatiwa na teke kali la kifuani ambalo lilimfanya akohoe mfululizo. “Nimekwambia nataka majibu la sivyo……” “Mutaniua kama mulivyomuua muheshimiwa?” “Nini wewe? John njooni mumshugulikie huyu kiumbe.” Dakika chache baadae zilikuwa ni za kipigo kikali kwa Taisamo, akapoteza fahamu huku shati lake jeupe likiwa limetapakaa damu. Alipozinduka alishangaa kukuta nyongeza ya mtu mwingine huyu akiwa mwanaume naye akiwa kwenye mateso kama yake. Akatulia huku akishangazwa na mambo yale ambayo yalikuwa yanatokea kama ndoto katika maisha yake. “Huyu naye ni nani?” Lilimpitia swali kichwani mwake huku akishuhudia kipigo kikali kikiendelea kwa Yule mgeni. “James Makabi nafikiri ulistahili sana kuitwa Makapi, badala ya makabi…” Alitulia Yule mtu na kumwangalia kwa Dharau James huku Taisamo akiyatazama yale mambo kwa kustaajabu. “Ndiyo lazima niwe makapi si ndio mlivyopanga nimuue muheshimiwe makamu wa…..” Hakumaliza kauli yake kali likamsukuma tena sakafuni safari hii akifikia uso na kuchanika kidogo eneo la kidevuni. “Kama hatutapata majibu ya kuridhisha wewe, na hao mbwa wenzio leo mnatandikwa risasi, hivi ninavyokueleza zimebaki dakika arobaini tu.” Taarifa hiyo ilimfikia Taisamo na kumshtua sana, alijua wazi kuwa jamaa hawana utani na ni lazima watatandikwa risasi lakini alikuwa na shauku kubwa ya kumfahamu Makabi na uhusiano wake na kifo cha makamu wa Raisi. Kufa akiwa hajategua kitendawili kile ilikuwa karaha nyingine kubwa sana kwake.
*******
Wakati Inspekta Tunu anaingia kwenye gari ndipo akashikwa bega, alipogeuka macho yake yakakutana na Mrakibu mwandamizi wa jeshi la Polisi Benard Kagasheki. “Vipi Inspekta mbona umetoroka hospitali?” “Ooh, habari afande.” “Salama, nimetoka hospitali sasa hivi nilikuwa nakuja kuuliza kituoni kwako kama wana taarifa zako baada ya kukukosa.” “Duh, mbona ulikuja mapema sana?” “Ni kweli, nilikuwa nataka kujua hali yako na kama inawezekana pale ulipofikia kwani jukumu anataka kupangiwa mtu mwingine na wewe unahamishwa kutoka makao makuu kwenda mkoa wa Rukwa.” “Eti…….!!!!” Aliduwaa Inspekta Tunu huku akiwa haamini anachokisikia. “Ndivyo jopo la wakuu lilivyopanga” “Yaani napangiwa haya mambo nikiwa mahututi kitandani…… afande hebu nielezeni nini kinaendelea hapa mbona sielewi?” “Si vema kujadili mambo haya huku barabarani kama, utanifuata ofisini kwangu saa mbili na nusu.” Alitamka mrakibu kasha akatembea kwa haraka kuliendea gari ambalo lilikuwa limeegeshwa upande wa pili wa kituo kile cha teksii. Zilipita dakika kadhaa huku Inspkta Tunu akiwa ameganda pale akishangaa jinsi mambo yanavyobadilika katika namna ya kushangaza, kikubwa kilichomshangaza ni kuona kuwa Mrakibu alikuwa akimfuatilia hatua kwa hatua. Angeweza kutuma askari wa cheo cha chini kumfuatilia lakini kitendo cha kuja mwenyewe tena katika namna ile ya kushtusha kilimpa wakati mgumu sana. “Vipi tunaondoka ?” Aliuliza dereva teksi huku akishindwa kujua ni lipi sahihi kati ya kumwita afande au dokta kwani aliyasikiliza maongezi ya Inspekta na mkuu wake mwanzo hadi mwisho. “Hapana, nahitaji kurudi ofisini kwanza.” “Poa.”
**********
“Hawajatoa ushirikiano bosi….” Aliongea kwenye simu mmoja kati ya watu wane ambao walikuwa kwenye chumba alichofungiwa Taisamo. “Kwa hiyo tuwauwe wote au ….” “Sawa.” Alisikika akijibu Yule mtu. Bosi kasema wapigwe risasi wote. Watu watatu wakaondoka na kumwacha mmoja ambaye alikuwa na bunduki aina ya SMG. “Maliza kazi Kiongozi… sisi tuko huku nje.” Aliongea Yule ambaye muda mfupi alikuwa anaonge na simu na kumwacha jamaa akiikoki bunduki kwa furaha kubwa. Taisamo alimtazama jamaa kwa huzuni na kutaka kumbembeleza lakini akasita. “Naanza na huyu mwanamke, umesikia Makabi? Nataka usikie uchungu kama niliyousikia siku uliyomuua mshikaji wangu Moyo.” Alimlenga vizuri usawa wa kichwa huku akitabasamu kwa furaha kubwa kabisa. “Pwaaaaaa……… Kishindo kikubwa kilisikika huku kikifuatiwa na mtawanyiko wa vitu. Taisamo alitoa macho ya hofu huku akijaribu kujitoa kwenye kiti bila mafanikio. Damu zilitapakaa sakafuni, kishindo kilicholeta mshtuko kilimkuta kila mmoja mle ndani, ilikuwa ni patashika.
***** Inspekta Tunu alijiinamia alichanganyikiwa huku akiwa hajui nini alitakiwa kufanya muda huo. Akashikanisha vidole vyake kwa nguvu na kubana meno kwa hasira. Nini kinaendea? Swali lilipita kichwani mwake na kumfanya aingiwe na ghadhabu zaidi. “Hii nchi ina utawala wa sheria kweli au nimazingaombwe tu?” Alivuta saraka lililokuwa pale mezani kisha akachomoa karatasi na peni na kuziweka pale mezani. Alitumia muda wa dakika chache kutafuna kizibo cha peni kabla ya kuanza kuandika .
YAHUSU KUACHA KAZI…………. Ndivyo alivyoanza baada ya kutanguliza anwani zote muhimu ambazo zinatakiwa kwenye barua za kikazi. Hasira zilikuwa zimemtawala na alihisi kuwa yuko sahihi kwa hatua hiyo ambayo alitaka kuichukua. Ilimchukua dakika kumi kukamilisha barua ile. Akaegeme kiti na kujikuta akipitiwa na usingizi kwani bado dawa zilikuwa zinamlewesha. Kelele za askari ambao walikuwa wanaingia kazini ndizo zilizomshutua kutoka usingizini. Akachukua ile barua na kuipitia upya huku akitikisa kichwa kuonesha kuridhika na kile alichoandika. Akatoka mle ofisi huku akipishana na askari kadhaa ambao hawakuficha mshangao kutokana na Inspekta kuja na mavazi ya kidaktari. “He, ina maana kaja mara moja tu kutoka hospitali?” Askari mmoja alimuuliza mwenzake. “Hata mimi sielewi, halafu kwanini kavaa mavazi ya kidaktari?” “Jamani, si bora tungemuuliza?” Mwingine alitoa hoja. “wee, mimi nilikuwa wa kwanza kutaka kumuuliza lakini jinsi sura yake ilivyo inaonesha kuna jambo. Askari ambao walikuwa wanaingia zamu asubuhi ile walikuwa wanaendelea kuulizana maswali ambayo majibu yake alikuwa nayo Inspekta Tunu. Alitembea kwa haraka safari hii akivuka kituo cha magomeni cha usalama na kuelekea Mikumi, alikuwa anayafanya hayo akiwa katika akili ambayo si ya kawaida, alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa. Kamishana, mrakibu… sijui na nani mwingine hawa wote wanahusika. Aliwaza huku akiwa ameshavuka barabara na kuelekea upande wa pili ambako kulikuwa na hospitali ya Magomeni. Ghafla, akakumbuka kitu akajikuta anasita kuendelea na safari. “Yaa, siku mbili kabla ya kuhamia kituo kipya nitakuwa nimepiga hatua kubwa sana.” Aliwaza huku akirudi na kuelekea tena kituo cha teksi cha mikumi. “Yaa, lazima niikamilishe hii kazi haraka iwezekanavyo !” Alijisemea kwa sauti ndogo wakati akiwa karibu kabisa na kituo kile ambacho alifika hapo kabla. “Wapi mama.” Aliuliza dereva teksi. “Nipeleke kawe, lakini kwanza tupitie CRDB nataka kutoa pesa kwenye ATM.” “Usijali mama.” Alijibu huku akijitoma kwenye gari.
********
Taisamo alikuwa anatarajia kuiona risasi ikisambaratisha kichwa cha Tamasha ambaye hakumfahamu jina. Lakini katika hali ambayo hakuitarajia akashtushwa na kishindo cha risasi ambayo ilipasua dirisha lile la kioo.na kumfikia kichwani Yule adui ambaye alikuwa amedhamiria kuwaua. Kisha likafuatia tukio lingine ambalo lilimpa maswali mengi kuliko majibu. Dirishani alipenya msichana mrembo ambaye hakuwa mgeni katika macho ya Taisamo. “Suzan…. Teacher Suzy….” Alibwabwaja kama mtu anayeweweseka. “Hapana… ah no nitambue kama teacher Suzy halafu baadae utanitambua kama Kapteni Rose kutoka makao makuu ya jeshi la wananchi Tanzania. Taisamo aliduwaa na kuacha mdomo wazi. “Kumbe wewe ndiye Rose” “Hatuna muda wa kupoteza Luteni naona umeumia sana, hii inaitwa Rescue mission na ni dakika saba tu natakiwa kukamilisha hii kazi. “Rose, teacher Suzan……. “ Alizidi kubwabwaja lakini Yule mwanamke aliyejitambulisha kama Kapteni Rose hakujishugulisha kumjibu badala yake alikuwa anahangaika kumfungua Tamasha ambaye alikuwa kwenye hali mbaya zaidi. Vishindo vya watu waliokuwa wanakuja kasi havikumshtua kapteni ambaye alionesha kufanya kazi yake bila wasiwasi. Dakika chache baadae zilisikika sauti za kitasa wakati kinafunguliwa na mtu aliyeko nje. Kapteni Rose aliruka dimbwi la damu na kusimama upande wa kulia wa mlango. Watu wawili waliingia ndani kwa kasi huku mmoja akiwa na bastola mkononi. Walikuwa ni wale mapandikizi ya watu ‘mabaunsa’ kama wanavyojulikana mtaani. Ulikuwa ni wakati wa ajabu zaidi kwa Taisamo kwani alishuhudia ile bastola ikielea hewani baada ya kupanguswa kwa teke kali na Rose au Suzy mpangaji mwenzie kama alivyo mfahamu hapo kabla. Haikuishia hapo pale alipofungwa alikuwa akishuhudia staili kali za Goju-ryu hii ni aina ya kareti ya kijapani ambayo inachanganya staili nyepesi na ngumu kwenye makabiliano. Go inamaanisha ngumu huku ikihusisha makabiliano ya moja kwa moja kama urushaji wa mateke na mikono ile Ru ni laini au nyepesi ambayo inahusisha zaidi minyumbuliko na mitembeo rahisi anayoifanya mtu wakati wa pambano. Hivyo goju-ryu inahusisha mbinu zote hizi ikiwa ni pamoja na kuepa,kuzuia na kupangua makonde na mateke. Aliziangalia staili hizi kutoka kwa mwanamke mrembo mwenye cheo cha kapteni ambaye alikuwa akimsumbua mara kadhaa kwa simu kumbe akiishi naye nyumba moja bila kumfahamu. Dakika chache zilizofuata alishuhudia vijana wale wawili wakiwa sakafuni bila fahamu. Ni aina ya upigaji ambao alikuwa hajawahi kuuona kokote. Hili lilimshangaza sana Taisamo na kujikuta akihusudu aina ile ya upigaji.
“Dah, Jeshi halikukosea kukupa cheo hiki Rose.” Alitamka Luteni Taisamo huku akimkazia macho kapteni Rose ambaye alikuwa anamfungua kamba alizofungiwa pale kwenye kiti. Rose hakujibu kitu badala yake aliendelea kufungua alipomaliza akaenda kumfungua Makabi. “Hatuna muda wa kujadili, nimebakiwa na dakika moja tu ya kukamilisha mpango wangu sote tutapitia hapa dirishani, wewe (huku akimuoneshea kidole Makabi ) Kwa kuwa hujaumia sana utamnyanyua huyu mwanamke kisha mimi nitampokea kwa nje. Luteni najua uko vibaya lakini jitahidi tuondoke hili eneo kwa sasa sio eneo zuri. Taisamo huku akichechemea nae alikua akijivuta kuelekea pale dirishani, wote wakapita pale Dirishani salama bila kupata purukushani.
********
Usiku wa manane ndani ya ukumbi uleule. Mkuu aliinua kichwa akawatazama wajumbe waliohudhuria mkutano kwa dakika kadhaa na kwa macho makavu huku akijilamba kingo za midomo yake ambazo zilianza kukauka. Alinyanyua glasi ya maji ambayo ilikuwa pale mezani akajimiminia funda tatu za haraka kabla ya kuyarudisha macho yake kwa wajumbe. Wajumbe walikuwa na shauku kubwa ya kutaka kujua nini kimejiri mpaka kufikia hapo. “Mambo hayajakaa sawa.” Alianza Mkuu na kutulia kwa dakika kadhaa kana kwamba alikuwa amemaliza kongea. Bwana Wahuva Kilale alikuwa miongoni mwa wajumbe wa mkutano huo, naye alikuwa anasubiri kwa shauku kubwa nini ataongea mkuu. “Tumefanya kazi ya ziada ya kumuondoa mtu ambaye angetuletea matatizo lakini tumeharibu sana kwani jahazi sasa linaenda mrama na kama hatutakuwa makini tunaelekea kuanguka kabisa kisiasa” Akatulia na kuwaangalia wajumbe ambao waliganda kwenye viti kama barafu ndani ya jokofu, kila mmoja alikuwa ametoa macho ya hofu kumuelekea mwenyekiti. “Wengi mlikuwa hamfahamu, lakini kwa taarifa ni kwamba kuna watu walijaribu kunusa kuhusu kifo cha makamu wa Raisi lakini tukawadhibiti huku tukitoa uhamisho kwa wengine ili kuvuruga utaratibu wao, kimsingi hatukuwaogopa wao kama wao na wala hakuna mamlaka inayoweza kututikisa zaidi ya habari hizi kufika kwenye vyombo vya habari na masikio ya wananchi.” Akatulia na kuwatazama tena wajumbe huku akitafunatafuna meno yake. Nafikiri nyote mtakuwa mashuhuda jinsi tulivyoweza kuwafunga mdomo waandishi kadhaa wa habari huku wengine tukiwapa warning kwa kuwang’oa kucha na meno, ni zoezi ambalo limetusaidia sana kwani wameacha kusema na wale waliotaka kusema wameogopaUtaratibu huu utatumika kwa yeyote atakayeonekana kutishia maslahi yetu. Lakini bado kuna tatizo inaonekana kuna watu nje system wamelivalia njuga suala letu, tulishafanikiwa kuwaweka mikononi wale ambao walionekana kuwa kikwazo lakini taarifa zilizopo ni kuwa hao watu wametoroka na wameokolewa na mtu au watu wanaodhaniwa kuwa na ujuzi wa hali ya juu. Sasa kinachonishangaza ni kuwa watu wote muhimu tunao hapa nani tena anahusika na sakata hili?”
*********
Taisamo aliendelea kumkazia macho Suzy kwa kustaajabia mambo aliyoyafanya. “Wewe mwanamke ni balaa, yaani siamini kama kuna mrembo mwingine kama wewe ambaye badala ya kukaa mbele ya kioo akihangaikia uso wake kwa kuuremba kwa mainjofesi….. Dah yaani sijui niseme nini.” “Ha ha ha umefanya kazi nzuri Taisamo wewe ni mwanaume wa shoka, tulikuwa tunakufuatilia hatua kwa hatua Jenerali kakusifia sana.” “Ha! Ina maana mlikuwa manafahamu kuwa sihusiki na yale matukio?” “Mwanzo tulikutilia Mashaka lakini kilichokusaidia ni kutoa taarifa kwa Meja ingawa ilikuwa vema taarifa ile ungeipeleka moja kwa moja kwa Jenereli lakini hakijaharibika kitu kwani ulikuwa katika mazingira ambayo yalikufanya ushindwe kujiamini.” “Kwani Meja anahusikaje na kitengo wakati alishastaafu siku nyingi?” “Kitengo ni zaidi ya unavyofikiri, Meja amestaafu katika majukumu ya kawaida lakini bado tuko naye kwenye M.I tena ni mshauri mkuu wa mambo ya silaha.” “Kwa hiyo nanyi mmegundua nini upande wenu?” “Uchu.” “Uchu kivipi?” “Tumegundua kuwa muheshimiwa anaondoka madarakani huku bado akiyapenda madaraka hivyo ili kuendelea kutawala nje ya madaraka ni lazima awaweke watu ambao watakuwa kama rimoti yake huku yeye akitawala nyuma ya mgongo.” “Sasa kama muheshimiwa ndio Muhusika mkuu unafikiri sisi tutawezaje kutatua hili?” “Ziko njia tatu tu, leo wakuu watakaa kuamua ni njia ipi itumike, Kwanza ni kumuua muheshimiwa na kuuvunja mtandao wake ambao unahatarisha amani na uchumi wan chi, pili ni kumlazimisha muheshimiwa kujiuzulu na tatu ni jeshi kuchukua nchi na kudhibiti kila kitu.” “Sawa na wale wawili ambao tulikuwa nao umewafahamu?” “Ndiyo ni Jemsi Makabi na mchumba wake Tamasha, Makabi katueleza kitu kuanzia jinsi alivyolazimishwa kusababisha ile ajali na hatimaye kufanikiwa kunusurika.” “Dah, kwa hiyo ni yeye ndiye kasababisha ile ajali! Mh… ajabu kweli, sasa huyu ni mtuhumiwa au inakuwaje?” “Kutokana na mazingira ya ajali tumekubaliana nae kuwa hakutaka kumuua muheshimiwa kwani iwapo angekuwa na nia hiyo basi lilikuwa jambo rahisi sana kwake kummaliza kwa ajali ile.” “Kwa hiyo mmemrudisha kwake?” “Hapana yeye ni shahidi muhimu sana kwetu na kwa mujibu wa maelezo yake tumebaini kuwa anayehusika ni afisa mwandamizi wa idara ya usalama wa Taifa ambaye anajulikana kama Othmani Geresha huku akitumia jina la bandia la Mjomba Masharubu ambalo amekuwa akilitumia sana kwenye kupanga mikakati yake ya mauaji pia tunasubiri kumweka katika himaya y.” “Hapana ni mtu hatari sana ambaye kwa pamoja tunatakiwa kumtia mikononi mwetu kwa umakini mkubwa kwani vinginevyo itakuwa ni hatari kubwa na kwa kutambua hilo mkuu katuongezea nguvu, Tutaongezewa watu wengine wawili ambao ni Sajenti Jesca Mpangala na Staff sajent Mariam Goza.” “Duh, kwanini nimeletewa wanawake watupu?” “Ha ha ha ha Othmani Geresha ni mtu hatari sana na ana akili na mbinu nyingi lakini udhaifu wake tumegundua uko kwa wanawake.” “Lini tutaanza hiyo kazi maana nina hasira sana na hao jamaa.” “Ni baada ya kupata ripoti kamili kutoka kwa Inspekta Tunu wa jeshi la polisi………” “Ni Inspekta ambaye aliamua kuacha kazi wakati yeye ndiye alikuwa ameshikilia upelelezi wa tukio hili tulipofuatilia tukagundua kuwa kuna tatizo hivyo leo tutapokea maelezo yake kisha tutayaunganisha katika misheni yetu.” “Kwa nini tusianze na Yule mkuu wa kampuni ya uuzaji magari maana anaonekana kuwa mshirika mkubwa wa uovu huu!” “Ni wazo zuri lakini yote hayo ni baada ya kupata taarifa kutoka kwa Inspekta ambaye mpaka sasa yupo kwenye mahojiano maalumu na Jenerali.” “Dah, kwa hiyo hii kazi nitaifanya na warembo watupu.” “Ha ha ha mimi basi tena.” “Wewe ni zaidi ya warembo Suzy ah… no Rose dah halafu sitasahau yaani we unanipigia simu kumbe uko ndani mlemle.” “Ok, sasa wacha nikamsikilize Jenerali anasemaje maana nahisi atakuwa amemaliza kuongea na Inspekta.”
****** Saa 4.30 usiku, Othman Geresha alikuwa amekilaza kichwa chake kwenye kona ya moja ya sofa ghali. Macho yake alikuwa ameyaelekeza kwenye Tv ambayo muda huo alikuwa ameizima. Hakuwa anaona chochote kilichokuwa mle ndani, fikra zake zilikuwa nje kabisa kwa mara ya kwanza alijihisi kuwa kwenye hatari kuliko wakati wowote ule, alihisi kuwa alitakiwa kufanya mauaji kuliko wakati wowote ule ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kunusurika na mikono ya maadui zake. Alijaribu kutafakari namna maficho yale yalivyoweza kubainika na hatimaye kuokolewa kwa Taisamo na wenzake. Akiwa kwenye tafakuri hiyo mara simu yake ya mkononi ikaanza kuita. “Ndiyo mkuu.” “Tuonane hapa namba tatu.” Aliskia sauti kutoka upande wa pili. “Sawa mkuu.” Akakata simu na kuuendea mlango kwa haraka. Aliendesha gari huku akiwa na mawazo mengi sana, hakujua kwanini mambo yameharibika kuliko wakati wowote ule. Ndani ya dakika ishirini na mbili alikuwa katika viunga vya ofisi hiyo nyeti. Ambapo sekunde sitini baadae alikuwa ana kwa ana akikabiliana na mkuu wa idara ya usalama wa Taifa nchini. “Geresha, hatuna muda wa kupoteza kwa sasa kwani tukifanya mchezo sio watu wetu tu watakaoanguka bali hata chama kinaweza kuanguka kuna hatari ya kuingia watu wanaoitwa Wazalendo madarakani, wakishaingia wao watu wengi watapoteza heshima zao, nataka ufahamu mambo ambayo ulikuwa huyafahamu, Kwanza kuna akaunti zetu ziko nje ambazo baadhi ya wapinzani wameanza kunusa nusa huko, haya yote yanahitaji kuzimwa tena wakati mwingine kwa kuwaondoa hata wenzetu ambao tunaona wanaweza kuwa kikwazo pia.” Akatulia kidogo Mzee huyo ambaye alionekana kutokuwa katika hali ya kawaida siku hiyo. “Sijakupa nafasi ya kuongea kwa sababu hata wewe mwenyewe unafahamu kuwa hali ni mbaya na inahitaji kurekebishwa haraka iwezekanavyo, hivyo kuna majina ya watu ambayo tumekuwekea ndani ya bahasha hii, wanatakiwa kuondolewa haraka sana kabla mambo hayajazidi kubadilika na mara hii tunatumia Plan B hatutatumia tena Plan A, hivyo ni kuua bila kuhoji.” “Nimekueewa mkuu nakuhakikishia kuifanya kazi hii kwa umakini zaidi kwani hata mimi nimeona jinsi mambo yalivyoharibika.” Alisikika Makabi huku akichukua ile bahasha yenye majina hayo. Kisha akanyanyuka pale kitini na kuelekea nje moja kwa moja tayari kwa maandalizi ya kazi hiyo aliyopangiwa.
********
Ndani ya nyumba ile ya kisasa ambayo ilikuwa inamilikiwa na Jeshi la wananchi Maafisa wanne wenye vyeo tofauti walikuwa kwenye mjadala mkali jinsi yakuanza kazi yao. “Kwa hiyo tutaanza pale kampuni ya magari, sajenti Jesca utatangulia ofisi ya mkurugenzi halafu sisi tutafuata dakika tano baadae sawa?” Aliuliza kapteni Rose. “Sawa mkuu, lakini natakiwa kufanya nini nikishafika?” “Wewe ni askari tumia mbinu yoyote ya kumchelewesha, tumeweka hizo dakika tano ili kama ataleta watu kukuvamia tuwatie nguvuni kwa pamoja.” “Unafikiri anaweza kufanya kama alivyonifanyia mimi.” Alihoji Taisamo. “Inawezekana pia, lakini tunahakikisha kifaa chake cha mawasiliano kiko hewani ili kama kuna dharura yoyote tuweze kufahamu.” “Hakuna shida.” Alijibu sajenti Jesca kwa kujiamini. “Tunaondoka dakika ishirini kutoka sasa, nafikiri kila mmoja yuko tayari kwa kazi, kama kuna swali au hoja anipatie sasa hivi” Taisamo akakohoa kabla ya kuzungumza. “Naomba nisaidiwe kitu kimoja Kapteni, nataka kujua mmiliki wa gari lenye nambari za usajili TKD 2341.”
“Unaweza kutudokeza anahusika vipi na hili sakata letu.” “Ndiyo, ile siku ambayo aliuwawa dokta, muuaji alitoroka kwa gari lenye namba hizo kwa bahati mbaya sikuwahi kufuatilia zaidi kutokana na muingiliano wa mambo kama ulivyoona.” “ok, hilo tutamwachia Inspekta Tunu atalifanyia kazi kupitia kwa watendaji wenzake.” “Si mlisema ameacha kazi?” “Ni kweli, lakini bado anaweza kuwa msaada mkubwa sana kwetu kupitia kwa watendaji ambao alikuwa nao hapo awali.” “Ok itakuwa vema.”
*********
Sajent wa jeshi la wananchi kutoka kitengo maalum cha MI alikuwa anapandisha taratibu ngazi zinazoelekea kwenye ofisi ya mkuu wa kampuni ile ya uwakala wa magari aina ya NISSAN PATROL, nyuma alifuatiwa na wanajeshi watatu wenye vyeo vya kapteni, Luteni na Staff sajenti. Macho ya kawaida yasingeweza kufahamu kuwa walikuwa safari moja. Akagonga mlango wa osfisi na kisha kuingia ndani. “Karibu Aunt.” Sauti nyororo ya kike ndiyo iliyompokea tofauti na matarajio yake. “Ahsante naweza kuonana na bosi?” “Hapana…ah sina uhakika atakuja muda gani maana si kawida yake mpaka saa nne hii awe hajafika kazini.” “Ok.Nitarudi tena baadae kidogo.” Alimaliza kauli yake hiyo kwa kuubamiza mlango wa ofisi ile. Nje wale maafisa wengine wa jeshi walikuwa wameshafika usawa wa lango la kutokea nje kwani kila mmoja alikuwa amevaa kisikilizio maalum ambacho kilimwezesha kujua kilichokuwa kinajiri ndani kati ya sajenti Jesca na yeyote yule. Baada ya kulifikia gari lao aina ya Landrover 110, Taisamo alimgeukia Rose. “Wapi sasa au kwa Kamishna?” “Hapana, tutafika nyumbani kwa huyu jamaa (huku akinyooshea mkono majengo ya ile kampuni ya magari) kisha tutafika nyumbani kwa kamishna halafu tunamalizana na Geresha ambaye atatuonesha njia jinsi ya kumpata mkuu wa kampeni hii.” “Mpango nzuri.” Hatimaye ilisikika sauti ya Staf sajent Mariam Goza dereva wao ambaye mara nyingi alikuwa anapenda ukimya jambo ambalo lilimshangaza sana Taisamo. “Unakufahamu nyumbani kwake?” Aliuliza Taisamo. “Ndiyo tunazo details zake zote, anaishi Upanga karibu na kituo cha zamani cha polisi, nyumba namba 54K” “Duh, uko makini sana kapteni.” “Lakini si zaidi yako na nahisi hii ni mara ya mission ya mwisho kwangu kuwa juu yako baada ya hapa tutakuwa nafasi sawa au utakuwa zaidi yangu.” Baada ya dakika Arobaini gari lilikuwa katika eneo lililokusudiwa, kama ilivyokuwa mwanzo safari hii pia chambo alikuwa Sajenti Jesca. Alipolifikia lango akabonyeza kitufe cha kengele ambacho kilikuwa upande wa kulia wa lango. Ilimchukua sekunde chache kushuhudia lango likifunguliwa. “habari za kazi” “Nzuri sijui nikusaidie nini?” “naomba kuonana na Mr. Kairuki” “Ulikuwa na ahadi naye?” “Hapana.” “Basi ngoja niongee nae kwanza.” Alisikika yule mlinzi huku akiliacha lango likiwa wazi na kuelekea ndani. Mariam Goza alitumia fursa hiyo kulisogeza gari pale langoni. Kisha Taisamo akawapa ishara wenzake ya kuingia moja kwa moja kule ndani. Dakika mbili zilikuwa zimepita bila yule mlinzi kutoka nje, Taisamo akausukuma mlango na kuingia ndani huku akifuatiwa na maafisa wengine wa jeshi. Yule mlinzi alikuwa ametumbua macho huku mikono ikiwa kiunoni akistaajabia kile alichokuwa anakiona. Maafisa wale wa jeshi walijumuika katika mduwao ule kwa sekunde chache. “Vipi ndugu nini kimetokea hapa.” “Dah, sielewi ndugu zangu mimi ni kama ninyi tu ingawa nimetangulia kuikuta hii hali.” Alijibu Mlinzi huku akiushangaa mwili wabosi yule wa kampuni ya uwakala wa magari ambaye alikuwa amepigwa risasi kifuani na kufanya kidimbwi cha damu pale sakafuni ulipolala mwili ule. “Ni nani alikuwa na marehemu mara ya mwisho.” “Nafikiri ni vema maswali hayo nikiwajibu polisi.” “Sisi ni zaidi ya hao polisi.” Alijibu Kapteni huku akitoa kitambulisho chake na kumkabidhi. “Mlinzi alikitazama kile kitambulisho na kujikuta akitumbua macho kwa mara nyingine kumshangaa dada yule mrembo kupewa cheo kikubwa cha kijeshi. “Nafikiri ni vema ukitujibu maswali yetu.” “Mtu wa mwisho kuja hapa ni rafiki yake mkubwa ambaye sidhani kama anaweza kuwa yeye.” “Unaweza kutuelezea jinsi alivyo huyo mtu?” “Ni mrefu, mweusi, pua yake ni pana na hupendelea sana kuvaa suti nyeusi na kofia ya pama.” “Oh, huyo atakuwa Geresha.” Aliongea kapteni Rose. “Ni kweli kapteni, nafikiri sasa tubadilishe huu mpango, badala ya kuanza na hao wengine ni bora tuanze na huyu Geresha la sivyo atasababisha madhara makubwa sana.
*****
Saa 4.30 usiku, Geresha a.k.a Mjomba Masharubu alikuwa anaondoka nyumbani kwake kwa pikipiki aina ya Boxer. Hakufahamu kuwa alikuwa ameongozana na kikosi maalum cha kijeshi chenye watu wanne. Mwendo wake ulikuwa wa wastani hivyo ilikuwa ni fursa nzuri kwa wawindaji wake kumfuatilia kwa umakini zaidi. Safari yake ilimfikisha kwenye Baa maarufu ya SIMBA KAPAKATWA iliyopo maeneo ya Ilala boma. Kama kawaida yake aliingia hapo akiwa na lengo la kuondoka na mrembo ambaye angemvutia usiku huo. “Jesca nafasi yako hiyo.” “Yap, ngoja nimuwahi.” Alisikika Sajenti huku akiwa nje ya gari. Kwa mwendo wa madaha aliingia mle ndani na kutafuta meza ambayo ilikuwa karibu kabisa na pale alipokaa Geresha. Geresha hakujishugulisha na Jesca badala yake muda mwingi alikuwa anabofyabofya simu yake kana kwamba kuna mtu alikuwa anawasiliana naye jambo ambalo lilimtia mashaka Sajenti Jesca. Kwa sifa alizozisikia kuhusu Othman Geresha hii haikuwa tabia ya kawaida. Kwanza mtu mwenyewe alikuwa anakunywa soda tofauti na matarajio yake kuwa ni mnywaji mzuri wa pombe na huwa hana tabia ya kulewa kijinga. Ghafla akamuona Othman Geresha akiondoka kwa kasi kuelekea upande wa vyooni. Sekunde chache baadae likafuata tukio jingine la aina yake. Taa za mle ndani zilizimika ghafla na kisha ikafuata milipuko ya bastola ambayo ilileta taharuki kubwa na kuwafanya watu waache viti vyao na kuanza kutawanyika huku kila mmoja akipiga kelele anazozijua kutokana na hofu. “Msaada kapteni nimevamiwa….. oooh..aaaaah.” Sauti ya mtu aliyekuwa kwenye matatizo iliwafikia kapteni,Luteni na Staf Sajenti ambao walikuwa wanasubiri wakiwa kwenye gari. Hakukuwa na mashauriano tena kila mmoja alishika vema bastola yake na kukimbia akielekea eneo la tukio. “Kuweni makini si mmesikia hizo bastola zinavyopigwa kiufundi na mpigaji si mmoja tena inaonekana wamedhamiria kuua na si kutisha watu.” Alisikika taisamo kwa sauti iliyojaa ghadhabu. Jesca alikuwa hasikiki tena badala yake zilikuwa ni sauti za watu waliokuwa wanakimbizana tena zikielekea kupungua. Mtafaruku pale ndani ulikuwa mkubwa kiasi kwamba ilikuwa ni vigumu kwa maafisa wale wa jeshi kupenya kirahisi kutokana na uwingi wa watu waliokuwa wanatoka eneo lile. “Anatoroka, mtafuteni sajenti mimi namfuatilia.” Alisikika Taisamo huku akiikimbilia ile pikipiki aina ya boxer ambayo ilikuwa imewashwa tayari kwa kuondoka. Alifanikiwa kwenda hatua kadhaa ndipo bastola ya Luteni ilipofanya kazi na kumpata bega la kushoto kwa nyuma. “Shiiiiiiit……….” Aliropoka Geresha huku akimalizia kwa tusi zito la hifadhini. Akajitupa chini huku bastola ikiwa mkononi. Taisamo alikuwa makini na hakutaka kuruhusu kosa lolote wakati huo. Akamfyatulia risasi nyingine mkono wa kulia na kumfanya adondoshe ile bastola. Ghafla akasikia milipuko mingine ya bastola kutoka mle Baa. Yalikuwa ni majibizano makali baina ya Maafisa wale wawili na watu wanne waliokuwa na silaha. Taisamo hakutaka kupoteza muda medani ya kivita ilimtuma kuwa wakati ule alitakiwa kutoa msaada kwa wenzake. Huku akiwa katika mbio kalindipo kwa mshtuko mkubwa alipogongana na mtu aliyekuwa anakimbia kutoka ndani. Kwa msaada wa taa za jengo la jirani alimtambua! Walikutanisha macho yao huku kila mmoja akihema.
“Tumekutana tena rafiki, umenikumbuka.” “nakukumbuka sana, sasa unasemaje?” “Ulikatisha maswali ambayo nilikuwa namuuliza dokta sasa leo nataka kufahamu huyu Mkuu ni nani na bila shaka jibu unalo wewe.” “Unafikiri ni rahisi kiasi hicho kupata jibu?” “Ni rahisi sana Mr.Majogo, kumbe jeshi linaamini kuwa lina watu mahiri wakati watu wenyewe ni wasaliti tena tumekuamini na kukuweka kitendo muhimu cha MI nawe unatuangusha kiasi hiki? “ Ilikuwa ni sauti ya Rose ambaye alikuwa nyuma ya yule jamaa huku akiwa na bastola mkononi machozi yakiwa yanamtiririka mashavuni mwake, hiyo ilikuwa ni ishara tosha kwa Taisamo kuwa Sajenti Jesca amepoteza maisha. “Dondosha bastola yako chini kabla hatujakulipua.” Sajini mtumishi ‘staff sajent’ Mariam Goza alifoka baada ya kufika eneo lile. “Kumbe unamfahamu huyu?” aliuliza Taisamo. “Huyu ni Elias Majogo ana cheo cha Meja na ni kiongozi wa Unit nyeusi, sasa nashangaa kiongozi anakuwa hivi sijui anaowaongoza watakuwaje!” “Meja tafadhali mtaje mkuu kwa usalama wako.” “Bado si rahisi kapteni siwezi kujibu maswali yako wala ya Luteni, nyote ni wadogo sana kwangu ingawa mmebahatika kuniweka katika himaya yenu.” “Utajibu tu hapa huna ujanja Meja.” “Nikiwa kaburini labda…” alijibu huku akilamba mikono yake. “Anajiua mzuie…..” Alipiga kelele Rose akimwamrisha Taisamo kumzuia Meja lakinini alikuwa amechelewa. “Duh, jamaa alikula kiapo kibaya sana yaani alikuwa na sumu mkononi!” Alistaajabu Staff Sajent Goza. “Vipi hali ya Jesca?” “Jesca ameuwawa na nimeshatoa taarifa anakuja kuchukuliwa, Vipi umemkosa Geresha?” Alimaliza kwa kuuliza. “Geresha nimempiga risasi na kwa jinsi alivyo hawezi kutoroka inabidi naye achukuliwe kwani atakuwa msaada mkubwa sana kwetu.” “ Ok inatakiwa abanwe usiku huuhuu.”
******
Mazishi ya Sajenti Jane yalifanyika kwa heshima zote za kijeshi huku akiwa amepandishwa cheo na kuwa Warrant officer class one. Mazishi yake yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kijeshi huku taarifa ya kifo chake ikiahidiwa kutolewa baada ya wiki mbili. “Enhe sasa nini kinafuata?” “Tunatakiwa kumaliza kazi iliyobaki.” “Tunaanzia wapi?” “Tutaanza na ripoti tuliyoletewa na Inspekta.” “Mbona kama ile ripoti itakuwa inaturudisha kwa watu waliokufa?” “Hapana, bado hatujafahamu chochote kutoka kwa kamishna wa kanda ya Dar es salaam.” “Wazo zuri kwa hiyo tunatakiwa kwenda ofisini kwake?” “nafikiri ni vema ikiwa hivyo.” Wakachukua gari la jeshi ambalo lilikuwa na namba za kiraia, safari hii wakiwa peke yao bila kumshirikisha Goza. “Bado unanipenda Luteni!” Aliuliza Rose huku wakiendelea kukata mitaa kuelekea kwenye jengo la makao makuu ya Polisi kanda ya Dar es salaam.s “Kwanini usingeniuliza swali hilo bila kutaja cheo changu” “Ha ha ha ha vizuri, nafikiri tutaongea zaidi tukikamilisha hii kazi.” “Sawa, tutaongea na nitakuonesha jinsi ninavyokupenda.” “Sasa mbona unaendeleza hii mada.” “Ok, I’m sory dear.” “ha ha ha ha nani Rose au Suzy?” “Teacher Suzy.” Waliendeleza utani wakati wanakaribia majengo ya Polisi makao makuu kanda ya Dar es salaam. “Mimi nitabaki kwenye gari.” “Kwanini tusiende wote.” “hii ni mission yako mimi nilipewa mission ya kuja kukuokoa tu.” “Ok.” Alijibu huku akiubamiza mlango wa mbele na kuanza kutembea kuelekea kule ziliko ofisi.” “Habari yako Dada!” Alimsalimu mmoja wa askari ambao aliwakuta pale kaunta. “Nzuri, nhe eleza shida yako….” Alisikika yule dada kwa sauti iliyojaa dharau. “Nahitaji kuonana na Kamishna.” “Kamishna yupi, hapa makamishna ni wengi.” “Kamishna wa kanda maalum.” “Eh, kwani una shida gani maana mkuu yuko bize sana leo mara aende ikulu mara arudi sasa sio ugomvi na mkeo ndio uende kwa kamishna.” “Ni muhimu nahitaji kumuona!” Mara hii aliongea akiwa ametoa kitambulisho chake. “Ok, pita huku kulia pandisha hizo ngazi floor ya kwanza mlango wa tatu upande wa kushoto, utaona hapo mlangoni kumeandikwa kamishna lakini sina uhakika kama bado yupo ofisini.” Akapita kimlango kidogo cha pale kaunta na kuelekea upande aliolekezwa. “Karibu.” Dada aliyekuwa nyuma ya kompyuta kubwa aina ya Fujitsu siemens alimkaribisha Taisamo. Taisamo alitumia muda mfupi kuisanifu ofisi ile ambao ilikuwa ni ndogo kabla ya kuifikia ofisi kuu ya Kamishna. Alijua moja kwa moja kuwa anaongea na katibu muhtasi wa mkuu huyo. “Ahsante, habari yako.” “Nzuri, sijui nikusaidi nini?” “Nahitaji kuonana na Kamishna.” “leo yuko bize sana na ametoa agizo kuwa hahitaji kuonana na mtu yeyote yule.” “Ok, Vema lakini mimi sio mtu yeyote.” Aliongea Taisamo huku akiwa ameshafungua mlango wa ofisi ya kamishna. Hata hivyo hakukuwa na yeyote ofisini. “Yuko wapi?” “Wewe sio mtu yeyote, unashindwaje kujua aliko?” “Ok, kzi njema.” Aliongea Taisamo huku akimwacha yule mwanamke mwenye cheo cha koplo akiwa amebinua midomo yake kwa hasira. “Vipi?” “Aliuliza kapteni Grace wakati Taisamo akiwasha gari.” “Huyu tumuibukie nyumbani kwake tena usiku.” “Kwanini?” “Nahisi upatikanaji wake siku hizi ni mgumu kidogo.” “Ok, Twenzetu.”
Aliyainua macho yake juu, akatazama jinsi Pangaboi lilivyokuwa linazunguka, upepo wa feni ulimpunguzia adha ya joto na mbu. Aliitazama tena barua ya Mrakibu mwandamizi wa jeshi la polisi ndugu Benard Kagasheki akatikisa kichwa kwa masikitiko. Barua ilikuwa inamtaka kutoa sababu za msingi zilizomfanya aandike barua ya kuacha kazi. “Nitamjibu, lakini nafahamu fika kuwa anajua kwanini naacha kazi, hili jeshi limejaa dhulma, unafiki, usaliti, wizi na ujambazi. Yaani liko kinyume kabisa na yale linayoyapigania.” Aliwaza huku akiwa ameishika mkononi ile bahasha ambayo ilikuwa na muhuri pale juu ambao ulikuwa umeandikwa CONFIDENTIAL. Ghafla kama aliyekumbuka jambo akainuka pale kitandani. Akaangalia saa ya ukutani ilikuwa ni saa 4.10. “Muda unaruhusu.” Alijisemea kwa sauti ndogo huku akijizoazoa pale kitandani. “Kuna kitu nilikuwa sijakamilisha na siwezi kukiachia njiani.” Aliwaza huku akifunga mlango wa chumba chake. “Leo nikuandalie nini mama mkubwa.” Leticia mtoto wa mdogo wake alimuuliza wakati anavuka kizingiti cha nyumba. “Sina uhakika kama nitarudi mapema lakini ningependa sana nipate ugali na samaki.” Alijibu huku akiiacha nyumba ile ambayo aliishi yeye na huyo mtoto wa mdogo wake ambaye. Alitembea hatua kadhaa hadi barabarani ambako alikodi pikipiki iliyomfikisha kariakoo mtaa wa Muheza. “Asante.” Alisikika dereva bodaboda baada ya kupewa pesa yake. Aliiendea nyumba aliyoihitaji kisha akabisha mlango kama mara tatu hivi. “Kariiibu.” Sauti ya kike ilisikika kutoka ndani. Sekunde chache baadae mlango ukafunguliwa na mwanamke wa makamo. “Karibu.” “Asante, habari yako.” “Samahani sijui naweza kumuona mwenye nyumba?” “Hapana baba amesafiri lakini majukumu yote katuachia sisi.” “Wewe ni mwanawe?” “Ndiyo.” :Unaitwa nani?” “Mwamtumu.” Alijibu huku akionesha wasiwasi kwa mbali. “Ok, kuna maswali mawili matatu ambayo ningehitaji majibu kutoka kwako.” “Sawa, karibu ndani.” Inspekta akasimama huku yule dada akifunga mlango. Akaongozana na yule dada hadi kwenye chumba kidogo ambacho kilikuwa na kitanda, viti na vyombo mbalimbali. “Karibu.” “Asante.” Alijibu huku akichomoa kitambulisho chake. Mwamtumu alikiangalia kile kitambulisho kwa haraka. “Sijui utakunywa nini!” “Hapana nashukuru, sihitaji chochote kwa sasa.” “Enhe, bila shaka ni kuhusu John.” “Ndiyo umejuaje?” “Toka ameuwawa John hapa huwa hawaishi watu wanaokuja kuuliza hili na lile kuhusu John. Tena wengine wameacha na namba zao za simu hapa .” “wanataka nini hao walioacha namba za simu?” “Kuna huyu mmoja ambaye amejitambulisha kuwa ni Kamishna yeye ametoa maagizo ya kupelekewa taarifa kama kuna askari yeyote atafika hapa kuulizia lolote juu ya kifo cha John.” “Nawe umekuwa unafanya hivyo?” “Ningekuwa nafanya hivyo iwapo ningeachiwa hela ya vocha.” “Vizuri, kuna kitu chochote cha marehemu ambacho kilikuja kuchukuliwa na ndugu zake au yeyote yule?” “Hapana, waliwahi kuja baadhi ya ndugu zke hapa lakini hawajachukua chochote walisema mpaka familia itakapokaa na kuamua nini kifanyike.” “Sawa, sasa nitaomba kuingia huko chumbani kwa marehemu”
“Hakuna tatizo funguo ziko hapa, na utaongozana nami.” Ilikuwa ni mara ya pili kwa Inspekta kuingia ndani ya chumba hiki ambacho alijikuta akiambulia kipigo kilichomsababishia kulazwa. Alizunguka hapa na pale huku kwa umakini mkubwa akitazama mpangilio wa kila kitu mle ndani. Hakuchelewa kukiona alichohitaji. Ilikuwa ni Laptop ambayo ilivunjwavunjwa. Na kubaki ikiwa kama takataka fulani. Kwa umakini mkubwa Inspekta aliipindua ile Kompyuta pakato. Akatabasamu baada ya kukiona alichokihitaji ingawa hakuwa na uhakika na uzima wake. Hardisk ndogo ilikuwa inaning’inia nyuma ya ile kompyuta. “Mwamtumu!” “Abee!” “Kuna mtu yeyote ulimuona akitoka na kamera humu ndani?” “Hapana, isipokuwa yule anayeitwa sijui kamishna alikuja na watu fulani waliichezea ile kamera kisha kuna kitu walikichomoa humo ndani halafu wakaihifadhi kamera kwenye begi.” “Ok, nashukuru sasa mimi naondoka na hiki (huku akionesha Harddisk) tafadhali naomba usimwambie yeyote kuwa nilikuja hapa kama kuna lolote utanifahamisha namba yangu ni hii hapa” Akampa kikaratasi kidogo ambacho kilikuwa na namba yake. “Mh. Haya “ Alijibu Tunu ambaye kiumri hawakupishana sana na Inspekta. Safari hii hakutokea mlango wa sebuleni badala yake alipitia mlango wa uani. Akatembea taratibu huku akiangaza macho yake huku na huko kuangalia kama anaweza kupata usafiri. Alilazimika kutembea mita mia moja ndipo alipokutana na pikipiki. “Boda boda?” “Ndiyo shangazi, wapi unaenda?” “Nifikishe Kawe.” “Ok. Usijali.”
Alipofika nyumbani kwake haraka haraka akaelekea chumbani kwake, akachuchumaa na kufungua kabati ndogo la kitandani ambalo alikuwa anahifadhi vitu vyake muhimu. Hakuchelewa kukipata alichokihitaji. Ilikuwa ni harddisk ya nje ambayo alikuwa anaitumia kuhifadhia taarifa zake nyeti. Alichokifanya ni kuiondoa ile harddisk ndani ya jumba lake na badala yake akaiweka ile harddisk aliyoichukua nyumbani kwa marehemu John Oscar. Kisha akaiwasha kompyuta yake ya mezani ambayo ilikuwa mle chumbani. Kwa kutumia program ya Ava find akatafuta faili la picha akalipata. John alikuwa anayapanga mafolda yake kwa tarehe na Mwezi, hivyo likawa zoezi rahisi kwa Inspekta. Akawa anafungua picha moja baada ya nyingine nyingi zikiwa ni za lile tukio la kuuwawa kwa makamu wa Raisi. Baada ya kutembeza picha kwa dakika kadhaa ndipo alipoiona picha ambayo ilimshitua. Aliitizama kwa makini na kujikuta akitokwa na jasho kisha hofu ikamtawala. Akainua simu yake na kupiga namba fulani. “Shikamoo mkuu!” Baada ya kujibiwa akaanza kutoa maelezo.
******
Saa 11.23 Gari lililomchukua Kapteni Rose na Luteni Taisamo lilikuwa katika viunga vya nyumba ya Inspekta Tunu. Walipiga honi mara mbili kisha Inspekta Tunu akatoka na kusimama mlangoni. “Karibuni sana.” “asante.” Alijibu Taisamo. “Karibuni ndani.” “Ahsante sana.” Safari hii alijibu kapteni. Wakamfuta hadi chumbani huku wakiwa na hamu kubwa ya kujua alichowaitia. Alikuwa hajaizima ile kompyuta hivyo macho yote yalihamia kwenye kioo hicho. Wote kwa pamoja wakazidisha umakini. Picha hiyo ilikuwa inaonesha gari la makamu wa raisi likiwa limepinduka kwa upande mmoja huku kwa upande mwingine kukiwa na watu wawili siti ya nyuma ya gari ndogo la polisi. Mtu mmoja alikuwa ameshika bastola ambayo alikuwa ameilenga gari ya makamu wa Raisi wakati yule mwingine alikuwa atazama tukio lile. “Dah, huyu si kamishna?” “Ndiye haswa.” Alijibu Inspekta na kuwafanya Taisamo na Rose watazamane. “Ok kazi kwenu, huu ndio ulikuwa msaada wangu kwenu kama nilivyoombwa na Jenerali.”
******** Saa 4.33 nyumba ya kamishna ilikuwa imezungukwa na wanajeshi kumi waliopewa kazi maalum ya kuchunga nyendo za Kamishna kuanzia nyumbani kwane. Wanajeshi wakiwa wamekata tamaa ghafla wakamuona mkuu huyo akiingia lakini safari hii ikiwa ni msafara wa magari matano. Taisamo na Rose walikuwa kwenye kundi hili . “Ah, no… kuna tatizo kapteni.” “Nini tena?” “Msafara huu naona kama Rais naye yumo.” “Kivipi, naliona gari lake binafsi.” “sasa tufanyeje?” “Mfahamishe Jenerali nafikiri kazi itakuwa imeishia hapa.” Rose hakufanya ajizi akapiga simu kwa Jenerali ambaye mara moja alimfahamisha Rose kuwa yuko njiani. “Ndo ninachompendea huyu mzee, muda wote yuko tayari kwa lolote.” “Hawakukosea waliompendekeza kushika nafasi hii.”
*******
Utulivu ulikuwa umetawala nyumbani kwa kamishna, kikao kama hiki kilikuwa kikifanyika hapa kwa mara ya kwanza kabisa. Kama kawaida muheshimiwa Rais au Mkuu kama alivyojulikana kwenye vikao hivi vya siri alikuwa ndiye mwenyekiti wa mkutano huu wa siri. “Ndugu wajumbe, nafikiri hii ni mara yetu ya kwanza kukutana kwenye eneo hili baada ya wenzetu kadhaa kupoteza maisha, tulikuwa na mtandao mzuri ambao tayari umeshaanza kuvurugwa. Lakini napenda mfahamu kuwa huu sio mwisho wetu kwani kuna makosa machache ambayo yalisababisha hali hii ijitokeze, hata hivyo hatua tuliyopiga ni kubwa na ni ya ushindi kwani Muheshimiwa OLE NUNGA alikuwa kikwazo kikubwa cha mipango yetu. Leo tumekutana hapa baada ya siku mbili za majonzi ya vifo vya wapendwa wetu…………………………..” Akatulia kidogo na kumeza funda mbili za maji ya baridi kisha akaendelea. “………………..Leo nina jambo muhimu sana nataka kuwaeleza, safari hii tumeamua kijiti ashike ndugu Tobias Tambo. Huyu amekuwa na ushirikiano nzuri sana nasi na si mtu mropokaji kama mlivyomuona wakati alipokuwa waziri wa mambo ya ndani, naamini ni mtu ambaye atatulinda sisi na familia zetu, ni mtu ambaye baada ya kuambiwa kuhusu nafasi hii ameahidi kuwa atapambana na yeyote atakayejaribu kugusa zile akaunti zetu zilizoko nje ya nchi…(yakasikika makofi) hivyo nawaomba musiwe na wasiwasi bado tutaendelea kuwa na sauti na nchi hii hata kama tutakuwa nje ya madaraka (Yakapigwa makofi mengine safari hii ikiwa ni pamoja na sauti ya minong’ono)….. Nafikiri naondoka madarakani nikiwa nimefanya mambo makubwa sana kwenu mfano ni IGP hapo … ndugu zako watano wako Benki kuu hawa tu wanatosha kusaidia ukoo wenu ukiacha wale wengine ambao wako kwenye mashirika makubwa, Tumeendelea kuhakikisha kuwa tunashika nafasi katika makampuni, mashirika na taasisi muhimu….. Ni kazi kubwa nimeifanya ya kuleta mapinduzi haya ambayo yametufanya tuzishinde sera za Josi Mkulu ambaye alikuwa na mifumo ambayo ilitufanya viongozi tufanane na raia wengine. Tumejaza nafasi zote muhimu kama kuna zilizosalia basi hizo wataambulia wale wengine ambao si wenzetu, nawashukuruni nyote na nitahakikisha kama mwenyekiti wa chama mgombea wetu anashinda.” Alimaliza na kupigiwa makofi. Ghafla, mlango wa sebule ulifunguliwa. Kikosi cha wanajeshi watano kikaibukia pale kikaoni kikiongozwa na Jenerali Nalinga. “Muheshimiwa, tumebahatika kusikia hotuba yako yote na jambo zuri zaidi ni kuwa imerekodiwa. Kwa maslahi ya nchi na usalama wa Taifa nyote mtachukuliwa kambini, ili kuhitimisha jambo hili kistaarabu utatakiwa kufuata maelezo ambayo utapewa na jeshi, vinginevyo ni kukubali jeshi lichukue nchi nawe ushtakiwe na mahakama maalumu ya kijeshi…….” Alitulia Jenerali ambaye hakuwa na masihara. Rais muheshimiwa Herman Makwaya alikuwa anatetemeka huku jasho likimvuja. Wote wakajikuta wakiwa chini ya ulinzi na kuondoka na kikosi kile cha wanajeshi.
****** James Makabi na Tamasha walikuwa wamepumzika katika moja ya baa za maeneo ya kiwalani wakipata kinywaji baada ya kuachiwa huru kutoka chini ya uangalizi wa jeshi. Wakati huo Runinga iliyokuwa imefungwa pale baa ilikuwa inarusha taarifa ya habari. Habari ya kwanza ndiyo ambayo iliwasisimua wengi mle ndani. “Dar es salaam, Muheshimiwa Rais Herman Makwaya amefanya mabadiliko makubwa katika ngazi mbalimbali za uongozi hapa nchini, mabadiliko hayo ameyafanya akiwa amebakiza miezi sita tu ya kuondoka rasmi madarakani, katika mabadiliko hayo amewaachisha kazi wakuu wote wa vyombo vya ulinzi isipokuwa jeshi la wananchi na nafasi zao zitachukuliwa na watu wengine mapema mwezi ujao. Pia amemteua Inspekta Tunu Nzowa kuwa Kamishna wa makosa ya jinai, huku akiwapandisha vyeo Luteni Alex Taisamo na Kapteni Rose Mwingira ambao wote wanafikia ngazi ya Meja. Aidha muheshimiwa ametangaza kuachia nafasi ya uenyekiti wa chama, amesema kuwa kutokana na umri na hali yake ya kiafya anahitaji kupumzika sasa hivyo hatajihusisha tena na siasa katika maisha yaliyobaki…….”
“Mh, Afrika!” Aliguna huku akimshika mkono Tamasha na kuinuka pale alipokaa.
SAA mbili kasorobo, Mustafa baada ya kufika ofisini, kabla ya kuanza kazi haja ilimshika na kuelekea msalani. Baada ya kumaliza kujisaidia alikwenda kwenye sinki la kusafishia mikono ili ajisafishe. Alivua pete ya ndoa na kuiweka juu ya sinki kisha alijimwagia sabuni ya maji mikononi na kuanza kunawa.
Simu iliyokuwa mfukoni ilianza kuita, kwa vile hakuweka mlio ilitetemeka kuonesha ilikuwa inaita. Hakuipokea kwa vile bado alikuwa na sabuni mikononi, hivyo alinawa haraka na kufuta mikono kwa taulo dogo ili apokee simu. Lakini kabla hajaipokea ilikuwa tayari imekatika. Ingawa ilikuwa imekatika lakini aliitoa ili aangalie nani aliyekuwa akimpigia, kabla hajaangalia simu iliita tena, kwa vile ilikuwa mkononi aliangalia na kukuta jina la Shehna. Japokuwa alishtuka kuona jina lile ambalo kwake lilikuwa geni. Aliamini kuzungumza na aliyepiga angemjua kwa vile jina lilikuwa kwenye simu yake. Alibonyeza kitufe cha kupokelea na kusema: “Haloo.” “Haloo Mustafa, asalam aleiykum,” ilikuwa sauti ya lafudhi ya kimwambao. “Waleiykum msalaam,” Mustafa aliitikia huku akiifikiria sauti ile na kutaka kumjua aliyempigia ambaye jina na sauti yake vilikuwa vigeni akilini mwake. “Upo wapi?” sauti ilimuuliza. “Nipo ofisini.” “Nipo ofisini kwako muda tu, lakini mwenyeji wangu sikuoni.” “Nakuja basi.” “Fanya haraka kuna sehemu nawahi, nilipita ofisini kwako mara moja.” Mustafa alitoka haraka kumuwahi mgeni huyo, alimpita sekretari wake bila kumuuliza kitu japokuwa haikuwa utaratibu mzuri kumruhusu mgeni aingie ofisini bila mwenyewe kuwepo. Mara zote sekretari wake alikuwa akimruhusu mtu kuingia pale aliporuhusiwa kufanya hivyo. Lakini kwa kauli ya mgeni kuingia ofisini ilionesha ameruhusiwa bila ridhaa yake. Alipoingia ndani alishtuka alipokuta hakuna mtu ofisini, lakini harufu ya manukato mazuri ilisambaa kila kona. Alitoka haraka ili amuwahi kwa kuamini huenda aliamua kutoka baada ya kuchoka kumsubiri. Lakini aliamini hakutumia muda mrefu msalani. Alikwenda hadi getini kwa mlinzi na kumuulizia. “Eti kuna mgeni ametoka sasa hivi?” “Mgeni! mgeni gani?” mlinzi ilionesha kushtuka. “Mwanamke.” “Bosi, toka uingie wewe hajaingia mtu yeyote.”
“Hapana, labda ulitoka eneo la kazi, mgeni alikuwa ofisini kwangu sasa hivi.” “Bosi hakuna mgeni yeyote zaidi ya dada Sara ambaye alikutangulia kuingia kabla yako.” “Mmh! Hebu ngoja.” Mustafa alirudi hadi ofisini na kumuuliza Sara, sekretari wake akuyekuwa bize na kazi kwenye kompyuta. “Sasa mgeni ametoka?” “Mgeni gani?” Sara naye alionesha kushtuka. “Aliyekuwa ofisini kwangu sasa hivi?” “Bosi, hakuna mgeni yeyote aliyefika hapa, kwanza ilianza lini nimruhusu mgeni aingie ofisini kwako bila ruhusa yako?” “Sasa huyu mgeni kaingiaje na kapitia wapi?” “Bosi mgeni unayemsema umemuona wapi?” “Hebu njoo ofisini.” Sara na Mustafa waliongozana hadi ofisini ambako harufu ya manukato makali ilikuwa bado ikinukia. “Bosi pafyumu nzuri kama hii umeitoa wapi?” Sara alisema huku akinyanyua pua zake kuivuta. “Sara, haya manukato nimeyakuta baada ya kurudi kutoka msalani.” “Muongo!” Sara alishangaa. “Kweli kabisa, yanaonekana ni ya huyo mgeni aliyeingia ofisini kwangu.” “Sasa kapitia wapi?” “Hebu subiri.” Mustafa alisema huku akichukua simu yake juu ya meza, aliangalia namba iliyoingia yenye jina la Shehna na kuipiga. Simu ilionekana kuwa bize inazungumza. “Simu yake inaongea.” “Mmh! Si ulitoka nje, mlinzi anasema kuna mgeni aliingia?” “Hata yeye anasema hajamuona.” “Mmh! Mtu gani tusimuone wote basi atakuwa jini.” “Hapana si jini, nitampigia tena.” Mustafa aliachana na mambo ya mgeni asiyeonekana, alikumbuka amesahau pete yake msalani wakati akimuwahi mgeni. Alikwenda hadi sehemu ya kunawia mkono, alishtuka kukutana tena na harufu ya manukato aliyokutana nayo ofisini kwake. Alipoangalia juu sinki hakuiona pete yake. Alishtuka na kuangalia chini labda imeanguka vilevile hakuiona, aliingia msalani kuitafuta pia huko hakuiona. Akili yake ilimweleza kuwa pete ile aliivua wakati akitaka kunawa mikono. Alitoka hadi kwa Sara kumuulizia. “Sara kuna mtu ameingia msalani wakati nlipoingia ofisini?” “Hakuna.” “Unajua wakati nanawa niliweka pete yangu ya ndoa juu ya sinki, baada ya kuzungumza na simu niliwahi ofisini lakini ajabu nimerudi sijaikuta.” “Mmh! Umeangalia vizuri?” “Nimeangalia, Sara au leo sikuja na pete?” “Umekuja nayo, si unakumbuka nilikutania siku ukiipoteza utamwambia nini mkeo.” “Nakumbuka, sasa imekwenda wapi?” “Mmh! Mbona mauzauza leo.” “Huwezi kuamini ile harufu ya manukato nimekutana nayo tena msalani.” “Wewe!” Sara alishangaa. “Kweli Sara.” “Bosi, hebu tulia kwanza inawezekana leo umeamka na mawazo mengi kutokana na ishu ya wifi. Nilikueleza mkienda Mbagala kila kitu kitakuwa sawa, yule mama kawasaidia wengi. Sema bosi tatizo ulilificha sasa hivi ungekuwa na mtoto.” “Ni kweli, jana niliporudi nimemkuta wifi yako analia.” “Tatizo?” “Lilelile la mtoto, anasema sijui kawasikia watu wakimsema kwa mafumbo kwamba yeye ni tasa.” “Hukumweleza tuliyozungumza jana?” “Nimemweleza lakini anasema amechoka na uongo wa waganga, tangu tuanze kuhangaikia mtoto huu mwaka wa tano sasa.” “Mwaka wa tano?” Sara alishtuka. “Ndiyo, na fedha tulizopoteza tungeweza kujenga nyumba kubwa na gari mbili.” “Bosi yule mama kiboko wapo waliokata tamaa kama yeye lakini walipotumia dawa zake walipata watoto.” “Mbona kuna sehemu tulikwenda na kuelezwa hivyohivyo mpaka waliopata watoto tuliwaona, lakini alipotumia hakupata kitu.” “Hebu nendeni Mbagala tuone.” “Alikubali kwa shingo upande, hivi namsubiri amesema atanipitia saa tano tuelekee huko Mbagala.” “Basi bosi kapumzishe akili labda baadaye utakumbuka ulipoiweka pete.” Mustafa alirudi ofisini kwake na kukaa kitini, alijitazama vidole vyake asiamini kama kweli hakuja na pete. Akiwa bado anavishangaa vidole vyake simu yake iliita, alipoangalia alikutana na jina la Shehna. Aliipokea:
Haloo.” “Haloo Mustafa samahani, niliwahi kutoka kwa vile kuna sehemu nilitakiwa kuwahi.” “Umepitia wapi?” “Jamani Mustafa kuna njia ngapi ya kuingia na kutokea ofisini kwako?” “Moja.” “Basi ndiyo niliyopitia.” “Mbona sekretari wangu hajakuona?” “Nimemkuta yupo bize ila sikutaka kumsumbua kwa vile mlango wako ulikuwa wazi.” “Huyo hajakuona, na mlinzi?” “Sikumkuta inawezekana alikuwa msalani.” “Mmh!” “Mustafa unaguna nini?” “Aah! Basi yaani bado ujio wako umekuwa kitendawili, pete yangu umechukua?” “Mustafaa! Niichukue ili iweje tuna uhusiano?” “Hapana.” “Sasa pete yako niichukue vipi wakati hatuna uhusiano wa kimapenzi?” “Nashangaa.” “Umemuuliza mkeo?” “Nimuulize nini ikiwa nimeondoka nikiwa nimeivaa?” “Mustafa acha ubishi, hebu muulize mkeo.” “Nitamuuliza.” “Muulize sasa hivi kisha nitakupigia,” Shehna alisema na kukata simu. Mustafa hakutaka kuendelea kubisha aliamua kumpigia simu mkewe lakini alijua ni kuchochea matatizo kwa vile alikumbuka aliondoka nyumbani na pete kidoleni. Baada ya simu kupokelewa upande wa pili alimuuliza mkewe; “Samahani mke wangu eti pete nimeiacha nyumbani?” “Ndiyo, nashangaa kuiona kwenye sinki la kunawia mikono msalani.” “Ooh! Afadhali,” Mustafa alishusha pumzi ndefu. “Mbona umeshusha pumzi ndefu?” mkewe alimuuliza. “Yaani nimeitafuta kila kona ofisini nilidhania nimepoteza.” “Una tabia ya kuvua pete?” mkewe alimuuliza. “Ninapotoka msalani sitaki ipate maji.” “Basi pole mume wangu uliisahau, mi namalizia kazi nakuja.” “Hakuna tatizo.” Mustafa alikata simu na kushusha tena pumzi na kuamini kabisa siku ile aliamka akiwa na mawazo mengi. Lakini kitu kingine kilichomshangaza harufu ya manukato aliyoyasikia ambayo hakuwahi kuyasikia maishani mwake. Simu yake iliita, ilikuwa ya Shehna. Aliipokea: “Haloo.” “Vipi, mkeo amesemaje?” “Amesema niliisahau nyumbani.” “Sasa inakuwaje unanishushia lawama?” “Samahani nilichanganyikiwa.” “Sasa kuna kitu muhimu kilinileta asubuhi ya leo ambacho kimekutesa kwa miaka mitano.” “Kitu gani hicho?” Mustafa alishtuka. “Mtoto.” “Umejuaje?” “Mustafa acha kujitoa akili, habari za mkeo kukosa mtoto kwa miaka mingi uliniambia mwenyewe na kuhangaika kwa waganga wa kila aina wa ndani na nje. Uliniambia umepoteza fedha nyingi lakini hakuna manufaa yoyote. Kutokana na kuhangaika sana imefikia hatua ya kukata tamaa japokuwa mnataka kwenda leo Mbagala kujaribu mara ya mwisho uongo kweli?” “Kweli, nilikuambia lini?” “Sasa inamaana ningejuaje bila wewe kuniambia?” “Basi nimechanganyikiwa kiasi cha kusahau kama niliwahi kuzungumza na wewe ishu hiyo.” “Tuachane na hayo, Mustafa nataka nikusaidie mkeo kupata mtoto lakini naomba na wewe unisaidie shida yangu.” “Shida gani?” “Kwanza nataka mkeo apate mtoto mengine yatafuata, ila naomba uniahidi mkeo akipata mtoto na mimi utanisaidia?” “Nakuahidi ukinisaidia mke wangu kupata mtoto unachokitaka kama kimo ndani ya uwezo wangu nitakusaidia pia nitakupa zawadi kubwa sana.” “Basi naomba msiende kwa mganga dawa nitampelekea mimi.” “Nitaamini vipi kama utakayompa ni dawa?” “Utaamini mkeo akishika ujauzito mwezi huu.” “Mmh! Sawa.” Baada ya mazungumzo alikata simu na kutulia akiwaza huku akiamini matatizo ya mkewe kuchelewa kupata mtoto yamemchanganya sana hasa baada ya familia yake kuingilia kati na kumtaka aoe mwanamke mwingine kutokana na sheria ya dini yake. Siku zote hakutaka kuongeza mwanamke mwingine kwa kujua atakuwa hakumtendea haki mkewe pia kufanya vile ni kumnyanyapaa. Kibaya zaidi alijua angemuumiza mkewe kama mwanamke aliyemuoa angepata mtoto ungekuwa ukatili mkubwa kwa sababu wote hawakuwa na tatizo la kiafya zaidi ya kuchelewa tu kupata mtoto. Akiwa katika lindi la mawazo simu yake iliita, alipoangalia alikuwa mkewe, aliipokea: “Haloo mke wangu.” “Mume wangu pole na kazi.” “Asante.” “Eti kuna dada mmoja anaitwa Shehna amenipigia simu na kunieleza matatizo yangu kama niliwahi kumweleza na kunieleza kuwa amezungumza na wewe kuhusu dawa ya matatizo yangu na kuniambia nisiende tena kwa waganga dawa atakayonipa itatoa majibu mwisho wa mwezi huu?” “Hata mimi kaniambia hivyo… hebu subiri kuna mtu anagonga mlango.” “Sawa.” Baada ya dakika tatu mkewe alipiga tena simu ambayo aliipokea. “Ehe, mke wangu.” “Kuna kijana kaleta kichupa kidogo chenye maandishi ya Kiarabu, kasema kapewa na dada mmoja ambaye hakumuona sura kutokana na kuvaa hijabu iliyomziba uso.” “Kwa hiyo tusiende Mbagala?” “Hebu tuangalie na uongo wake.” Mustafa alikubaliana na mkewe wasiende tena kwa mganga, alimpigia simu Shehna kutaka kumshukuru. Lakini simu haikuwa hewani, aliachana naye na kuendelea na kazi zake. *** Kutokana na wingi wa kazi, Mustafa alirudi nyumbani usiku na baada ya chakula walikwenda kuoga na kurudi kitandani. “Mume wangu Shehna alisema tukutane kimwili saa nne kamili ili yai la uzazi lisipotee,” mke wa Mustafa alimweleza mumewe. “Alikupa maelekezo jinsi ya kutumia hii dawa?” “Ooh! Nilisahau kumuuliza.” “Sasa tutafanyaje?” “Namba yake si unayo mpigie.” Mustafa alinyanyuka kitandani na kwenda kuchukua simu, alitafuta jina la Shehna ili ampigie lakini ajabu halikuonekana. “Mbona jina lake silioni kwenye simu?” “Kwani alipokupigia hukusevu namba yake?” “Namba yake ilikuwemo kwenye simu.” Mkewe naye alichukua simu yake kuangalia namba ya Shehna ambayo hakuiona. “Hata kwangu siioni.” “Sasa tutafanyaje?” “Yaani najilaumu kutomuuliza maelekezo ya dawa, sasa hatujui tumywe au tujipake.” “Heri maandishi yaliyoandikwa kwenye chupa yangekuwa ya Kingereza tungeweza kusoma maelekezo lakini Kiarabu siambui hata moja.” “Sasa tutafanyaje na muda unakaribia?” “Hatuna jinsi kwa vile hakutupa maelekezo pia namba yake haipatikani,” Mustafa alinyamaza baada ya simu yake kuita, aliichukua na kuitazama na kujikuta akitamka kwa sauti. “Shehna.” “Amepiga?” mkewe aliuliza huku akinyanyuka kutaka kuona kwenye simu. “Ndiyo.” “Pokea haraka kabla hajakata.” Mustafa alipokea simu. “Haloo Shehna.” “Jamani mbona una pupa hivyo mwanaume wewe.” “Lazima niwe na pupa kutokana na muda kusogea bila kuwa na maelezo ya matumizi ya dawa uliyotupa.” “Ni kweli niligundua nilifanya kosa najua muda umekwenda sana, sasa chukua ndoo ya maji weka maji yaliyomo kwenye hicho kichupa nusu kisha mkaoge kwa vile muda utakuwa umekaribia baada ya kuoga jifuteni maji. Kabla ya tendo, kila mmoja ajipake mafuta hayo sehemu zake za siri ndipo muingiliane baada ya tendo kila mmoja anywe kidogo kisha muonge tena kwa kuweka mafuta yaliyobakia kwenye chupa na kulala.” “Samahani Shehna.” “Bila samahani.” “Tunaweza kuoga na sabuni?” “Hapana, mnaoga hivyo hivyo.” “Sawa nimekuelewa.” “Mlikuwa mnataka mtoto gani?” “Ye yote.” “Mbona moyoni wewe unataka mtoto wa kiume?” “Ni kweli lakini atakayepatikana nitampokea.” “Na mkeo?” “Ye yote,” alisema Mustafa. “Mbona unamsemea.” “Yeyote tu ni mtoto,” mke wa Mustafa alijibu kwa sauti. “Mbona uliweka nadhili mtoto wa kwanza akiwa mwanamke utampa jina la mama yako?” “Ni kweli, lakini atakayekuja nitampokea.” “Sasa mnaweza kukubaliana mnataka mtoto gani atangulie, kama wa kike mtakunywa hayo mafuta kabla ya tendo kama wa kiume, mtakunywa baada ya tendo.” “Tumekuelewa.” “Mna swali?” Shehna aliuliza. “Hatuna.” “Haya usiku mwema.” “Na kwako pia.” Baada ya simu kukatika Mustafa alimgeukia mkewe na kumuuliza. “Nina imani umesikia, unataka tutangulize mtoto gani?” “Wa kike.” “Kwa nini asianze wa kiume?” “Si umesema upo tayari kupokea mtoto yeyote.” “Naomba mke wangu unipe upendeleo kwa huyu wa kwanza.” “Umeshindwa vipi kunipa upendeleo mkeo wa pili awe wa kiume?” Walijikuta wakisahau muda ulikuwa umekwisha hivyo walitakiwa kutekeleza walichoelekezwa. Mpaka wanakubaliana muda walioelekezwa ulikuwa umevuka zaidi ya dakika kumi na tano. “Mke wangu tumevusha muda tulioambiwa tutafanyaje?” “Kwani saa nne imevuka?” “Lakini alisema saa nne juu ya alama.” “Ilikuwa kutufanya tuwe makini zaidi, lakini muda haujapita sana.” Walikwenda kuoga kwa kufuata maelekezo yote, baada ya kuoga walijipaka manukato na kunywa kwa vile walikubaliana kutanguliza mtoto wa kike. Baada ya hapo alikutana kimwili na baada ya tendo walikwenda kuoga na kurudi kitandani kulala. *** Usiku, Mustafa aliota akifanya mapenzi na mwanamke nzuri wa kiarabu ambaye alimweleza anataka kuzaa naye. Siku ya pili aliamka amechoka sana kutokana na kutumika mara mbili kwanza na mkewe pili katika njozi. Alipoamka hakumueleza mkewe alivyoota, alioga na kupata kifungua kinywa na kuwahi kazini. Mustafa akiwa kazini simu yake iliita, ilikuwa ya Shehna, aliipokea haraka. “Haloo Shehna!” “Aah! Mustafa, tanguliza asalamu aleykumu.” “Ooh! Samahani, asalamu aleykumu.” “Waleykumu salamu.” “Haya bibie niambie?” “Nilitaka kukusalimia tu, pia kukueleza jinsi ulivyonifurahisha kwa kutunza siri zako.” “Siri gani?” “Unajua wanaume wengi kila kinachotokea huwaeleza wake zao.” “Mimi kimenitokea nini?” “Unakijua, lakini hukutaka kumwambia mkeo.” “We’ umejuaje?” “Mustafa tuachane na hayo, mbona jana umeniangusha?” Shehna alibadili mada. “Kivipi?” “Niliwaambia mfanye mapenzi saa ngapi?” “Saa nne.” “Ndiyo muda uliofanya?” “Hapana lakini haikuvuka sana.” “Mustafa niliwaeleza saa nne kamili lakini mmevuka muda, kwa nini umepuuza maagizo yangu?” “Samahani kwa hilo.”
Mmh! Sijui…halafu kwa nini hukufurahia uamuzi wa mkeo?” “Nimefurahi ndiyo maana tumekubaliana kutanguliza mtoto wa kike.” “Si kweli Mustafa, moyoni hujafurahia uamuzi wa mkeo kwa kulazimisha kutangulia mtoto wa kike kitu kitakachompa matatizo mtoto atakayezaliwa.” “Kwa nini?” Mustafa alishtuka. “Kuukunja moyo wako wakati wa tendo la ndoa tofauti na siku zote. Mimba iliyoingia umeitia sumu.” “Sumu?” Mustafa alishtuka. “Ndiyo, ili kuiondoa unatakiwa kuukunjua moyo wako bila hivyo mtoto atakuwa na matatizo.” “Nimekuelewa.” “Basi mi nikuache ufanye kazi.” “Nashukuru ila nilikuwa na hamu sana ya kuonana na wewe.” “Usiwe na wasi Mustafa utaniona mpaka utanichoka kwanza tumalize tatizo linalowakosesha raha kwa muda mrefu.” “Asante, nitakusuburi.” Mustafa alikata simu na kujikuta akiwa katika mawazo mengi juu ya mtu anayejiita Shehna. Alijiuliza ni nani mtu anayeyajua maisha yake kiundani pia kujua hata mambo yaliyojificha bila kumwambia. “Huyu mwanamke atakuwa nani…mmh! au…ha…hapana siyo lazima atakuwa mganga tu siyo jini.” Mustafa aliendelea kuwaza juu ya kauli tata za Shehna ambazo hakuelewa nini hatima yake. Alijiuliza alijuaje kama kitendo cha mkewe kulazimisha mtoto wa kike wakati yeye alitaka wa kiume kitu ambacho alimkubalia kwa shingo upande yeye alifanya siri lakini Shehna alitambua na kumtisha kuhusu ujauzito ambao yeye alisema uliingia siku ile usiku. Alijiuliza sumu hiyo ni sumu gani ambayo inaweza kuleta matatizo katika ujauzito ule na moyo wake ataunyoosha vipi. Kuingia kwa sekretari wake kulimkatisha mawazo yake. “Bosi vipi naona upo mbali?” Sara alisema akiwa ameshika faili mkononi. “Kawaida tu.” Sara alimpa kazi aliyomuagiza kuifanya, baada ya kumpa alimuuliza. “Jana nilisahau kukuuliza mlikwenda Mbagala?” “Sara tumetoka hapa saa ngapi?” “Kweli, jana kazi zilitushika, kwa hiyo wifi alienda peke yake?” “Hakwenda ila mwisho wa wiki atakwenda.” Sara alitoka na kumuacha Mustafa akiwaza na kuwazua aliyoelezwa na Shehna. **** Jioni wakati Mustafa anajiandaa kurudi nyumbani alipokea simu toka kwa mkewe. “Haloo mpenzi,” alipokea kwa madaha kama kawaida yake anapopigiwa na mkewe. “Mume wangu yupo wapi?” mkewe alizungumza sauti ya mtu anayeumwa sana. “Mke wangu mbona unaongea hivyo?” sauti ya mkewe ilimshtua. “Na…na…u…mwa.” “Nini?” Mustafa alitaharuki. “Na…na…,” sauti ilinyamaza ghafla na kusikia kishindo upande wa pili. Mustafa alijikuta akitaharuki na kutoka mbio ofisini kuelekea nje kwenye gari lake ili awahi nyumbani kujua mkewe alipatwa na nini. Alimpita sekretari wake aliyekuwa katika maandalizi ya kuzima vyombo vya umeme ili watoke na bosi wake. Alishangaa bosi wake akitoka mbio kuelekea nje bila kumsemesha, Sara aliacha kazi na kumfuata ili ajue kulikoni. Alimuona akielekea kwenye gari lake akiwa kama amechanganyikiwa, alimkimbilia na kumuuliza: “Bosi vipi?” “Sara hebu subiri,” alisema huku akiwasha gari. “Bosi kuna nini mbona mbiombio kwenye gari au kuna kitu cha kutisha kimetokea ofisini?” Sara alizidi kuhoji. “Sara niache kwanza,” Mustafa alisema huku akiwasha gari na kuliondoa kwa kasi kuelekea getini na kumpigia kelele mlinzi afungue. Mlinzi alifungua haraka, Mustafa alilitoa gari kwa kasi kwa kuliingiza barabarani bila kuangalia na kuelekea nyumbani. Mlinzi alimfuata Sara na kumuuliza: “Vipi! Kuna nini?” “Hata najua! Nimemuona akitoka ofisini mbio hata sijui kapatwa na nini?” Sara naye alikuwa amepatwa na mshangao. “Hukumuuliza?” “Majibu yake hayaeleweki! Kila nilipomuuliza majibu anajua mwenyewe, kaacha vitu vyake vyote vya muhimu koti, lap top.” “Mmh! Basi kuna kitu kimempata si bure.” “Nina wasiwasi kuna kitu kimemtokea ofisini.” “Twende tukaangalie.” “Nani aingie ofisini? Toka juzi Bosi simwelewi mambo yake, nina wasiwasi bosi anataka kurukwa na akili,” Sara alisema. “Mmh! Hapana, asingeweza kuendesha gari vile.” Wakati wakijadiliana yaliyomtokea bosi wao, Mustafa alikuwa akiwaza nyumbani na kushindwa kuelewa nini kilimpata mkewe ambaye muda mfupi uliopita alizungumza naye akiwa katika afya njema. Alipofika nyumbani kwake alisimamisha gari lake nje ya nyumba yao na kukimbilia ndani bila kufunga mlango wa gari. Alipoingia ndani alishtuka kumkuta mkewe amelala chini akiwa amepoteza fahamu. Alijaribu kumwita lakini hakuitikia, alimbeba na kutoka naye nje ili amuwahishe hospitali, alimuweka siti ya nyuma ya gari na kufunga mlango. Naye alizunguka upande wa pili na kuingia ndani ya gari. Alipowasha gari liligoma kuwaka, alishangaa. Alipoangalia kwenye geji ya mafuta ilimshtua kuona mafuta yalikwisha. “Shit,” alisema kwa sauti huku akipaga ngumi kwenye gari. Mara simu yake iliitaka, huku akivuja jasho kutokana na tatizo la mkewe. Alijifuta kwa shati jasho lililokuwa likimvuja kama maji kisha aliitazama simu na kuona aliyepiga ni Shehna. “Haloo,” alipokea pumzi zikiwa juu. “Mbona hivyo?” sauti ya Shehna ilionesha kushtuka. “Nina tatizo.” “Tatizo gani tena Mustafa?” “Mke wangu yupo hoi hata sijui anaumwa nini?” “Mmh! Isiwe mimba?” “Mimba?” Mustafa alishtuka. “Eeeh, unashtuka nini?” “Mimba hiyo imeingia lini?” “Jana.” “Acha utani, hakuna mimba inayoweza kuingia mara moja na kuanza kumsumbua mtu.” “Mustafa kila mimba ina uingiaji wake.” “Basi yote nitayajua hospitali.” “Unampeleka hospitali ili iweje?” “Ana hali mbaya sana, kwanza sijui kama mzima.” Kauli ile ilimfanya Shehna aangue kicheko kitu kilichomshtua Mustafa na kuhoji. “Mbona unacheka?” “Nani alikuambia mimba ugonjwa?” “Shehna una uhakika gani kama ni mimba?” “Uhakika ninao, mrudishe mkeo ndani kwa vile haumwi.” “Hapana siwezi kufanya hivyo lazima nimpeleke hospitali.” “Haya fanya unavyotaka, lakini usinitafute wala tusilaumiane,” Shehna alitoa kauli ya kitisho. Kauli ile ilimshtua Mustafa na kumfanya ajiulize Shehna ana maana gani. “Shehna ulikuwa unataka nifanyeje?” ilibidi awe mpole. “Mrudishe kwanza ndani.” “Kisha?” “Mrudishe kwanza.” “Sawa.” Mustafa alimchukua mkewe na kumrudisha ndani akiwa katika hali ileile ya kupoteza fahamu. Baada ya kumlaza kwenye kochi alichukua simu ili kuwasiliana na Shehna. Alipochukua simu alikuta bado ipo hewani aliita. “Haloo Shehna.” “Abee Mustafa.” “Tayari.” “Kile kichupa cha manukato kipo?” “Sijui.” “Kiangalie kama kipo kisha chukua maji kwenye sahani ya bati nyeupe kiweke kisha mpake kichwani. Akiamka mpe anywe na mengine mpake tumboni.
Mustafa alikwenda chumbani na kukikuta kichupa juu ya meza ya kujipodolea. Alikichukua na kwenda kwenye kabati na kuchukua sahani ya bati nyeupe ambayo aliiweka maji na kukiweka kile kichupa na kufanya maji yale kunukia. Alifanya kama alivyoelekezwa kwa kumpa maji kichwani. Ghafla mkewe alifumbua macho. “Husna,” alimwita kwa sauti ya chini. “Abee mume wangu,” aliitika kwa sauti ya chini huku akipepesa macho. “Vipi?” “Safi,” alijibu kwa sauti ya chini huku akikaa kitako. “Unajisikiaje?” “Mmh! Sijambo.” “Kwani ilikuwaje?” “Yaani nilikuwa natoka chumbani ghafla nikaanza kujisikia vibaya..yaani vibaya sana. Nikapata wazo la kukupigia simu, nilijitahidi kukujulisha lakini ghafla kilikuja kiza kizito kilichoendelea sikujua.” Mustafa alimpa maji anywe, lakini mkewe alihoji. “Ya nini?” “We kunywa.” Mkewe alikunywa, yaliyobaki alimpaka tumboni. “Mume wangu mbona sikuelewi?” “Ndiyo tiba yako.” “Kwa nini tusiende hospitali.” “Shehna amekataa.” “Alikuja.” “Ndiyo,” Mustafa alimdanganya mkewe. “Jamani mbona hakukaa ili nimuone, yaani yule dada anaonekana mwema sana. Kwani anasema hali hii inatokana na nini?” “Mimba.” “Mimbaa!” Husna alishtuka. “Ndiyo, anasema imeingia kwa mtindo huo.” “Ndiyo nasikia leo mimba ikiingia mara moja mtu unaona mabadiliko makali.” “Basi mke wangu inaonekana mambo ya jana mimba imeingia.” “Siwezi kuamini mpaka nikapime.” “Duka la dawa lipo jirani kanunue kipimo.” Snura alinyanyuka ili atoke nje, mara simu yake iliita. Alirudi kwenye kochi na kuichukua ilikuwa inatoka kwa Shehna. “Asalam aleykum,” alipokea Husna. “Waleykumu salam,” aliitikia Shehna kwa lafudhi ya mwambao. “Niambie shoga yangu, yaani umeniudhi kweli.” “Kwa nini tena shoga?” “Yaani kumbe jana umekuja hata kusubiri tuonane?” “Nilikuwa na haraka, la muhimu afya mengine majaaliwa tutaonana tu.” “Naona umenipigia simu una lipi shoga yangu?” “Vipi unaendeleaje?” “Mmh! Namshukuru Mungu.” “Mambo ya kawaida, siku zote mimba zina ujaji wake kwa vile ni mara ya kwanza lazima imekusumbua.” “Shoga hii siyo mimba, mimba gani ya siku moja?” “Husna acha ubishi, mimi ndiye najua.” “Kwanza shoga, wewe ni nani mganga au ji..” Husna alikata maneno. “Malizia tu si ulitaka kusema mimi jini siyo?” “Hapana shoga.” “Utanijua tu muda si mrefu kama mimi mtu, jini, mganga au mchawi,” Shehna alisema kwa sauti kali kidogo. “Samahani shoga sikuwa na maana hiyo bali kukujua tu,” Husna alijitetea. “Si nimekueleza utanijua wasiwasi wako nini.” “Kuhusu ujauzito siwezi kuamini japokuwa nina dalili zote za ujauzito huenda ni malaria mi nataka kupima ili nihakikishe.” “Husna naomba suala lako usichanganye na masuala ya kizungu,” Shehna alimpa onyo mke wa Mustafa.
“Sawa nimekuelewa shoga.” “Najua majibu yako yamejaa unafiki sasa ukienda kinyume tusilaumiane.” “Nimekuelewa shoga.” “Nataka hili umweleze na mumeo, sawa?” Shehna alisema kwa sauti kali. “Sawa.” Simu ilikatika na kumfanya Husna arudi kwenye kochi na kukaa, safari ya kwenda duka la dawa baridi ikakatika ghafla. Mustafa alishtuka na kumuuliza mkewe. “Vipi mbona huendi dukani?” “Shehna amekataa.” “Amekataa nini?” “Nisiende kununua kipimo cha mimba wala nisikitumie.” “Amejuaje unataka kwenda kununua?” “Nimemwambia nataka kuhakikisha kama kweli nina ujauzito nakwenda kununua kipimo cha mimba.” “We unasemaje?” “Niseme nini? Mmh! Ipo kazi.” “Kwa hiyo huendi?” “Amesema suala la ujauzito wangu tusichanganye na mambo ya Kizungu.” “Kwa hiyo hata ukiumwa?” “Sijui muulize wewe.” “Mmh! Sawa.” Walikubaliana kutotumia dawa za Kizungu kipindi chote cha ujauzito japokuwa Husna moyoni hakuamini kama alikuwa mjamzito na kutaka kufanya kwa siri ili kupata uhakika. *** Sara baada ya bosi wake kuondoka katika mazingira tata alifunga ofisi na kuchukua vitu vya bosi wake ampelekee nyumbani ikiwa pamoja na kwenda kujua nini kilimsibu. Alikodi gari na kuelekea kwa bosi wake, akiwa njiani ghafla usingizi ulimpitia. Ajabu aliposhtuka alijikuta kitandani kwake akiwa amelala na mizigo ya bosi wake ameishikilia mkononi. Alipopepesa macho alishangaa kuona jua kama la asubuhi. Alinyanyuka kitandani na kushangaa kukuta mlango ukiwa wazi. Aliweka vitu kwenye kochi na kuangalia saa ya mkononi iliyomuonesha ni saa mbili asubuhi. Alishangaa kujiona akiwa nyumbani amelala na vitu alivyokuwa akimpelekea bosi wake. Alijawa na mawazo na kujiuliza alipotoka kazini na kukodi gari alimwambia dereva ampeleke kwa bosi wake au nyumbani kwake? Akakumbuka alimwambia ampeleke kwa bosi na si nyumbani. Alijiuliza kama alikwenda nyumbani kipi kilimsibu mpaka akalala na nguo zake bila kuvua viatu na mkoba wenye ‘laptop’ na koti la bosi wake. Bado alikuwa njia panda kuhusiana na kurudi nyumbani na kulala bila kula wala kufunga mlango. Mara simu iliita ilikuwa ya bosi wake, aliipokea. “Haloo bosi.” “Sara upo wapi?” “Nyumbani.” “Unaumwa?” “Hata siumwi.” “Mbona hujafika kazini?” “Bosi hata sijui niseme nini?” “Basi wahi ofisini huwezi kuamini nina nusu saa nipo nje ofisi imefungwa.” “Mungu wangu, jana nilijisahau na kuondoka na funguo.” “Basi wahi.” Sara alioga haraka na kubadili nguo kisha alikodi bodaboda kuwahi kazini huku akimuhimiza dereva akimbize pikipiki. Alifika ofisini baada ya dakika tano, Sara alimsalimia bosi wake na kufungua ofisi, Mustafa akaingia ndani. Alimkabidhi vitu vyake na kurudi kwenye eneo lake la kazi kumalizia kiporo ndipo amuuliza bosi wake jana ilikuwaje na kumweleza yaliyomtokea. *** Husna mke wa Mustafa akiwa nyumbani peke yake moyo ulimsukasuka juu ya hali aliyonayo ambayo alielezwa ni ujauzito lakini alikatazwa kutumia kipimo cha Kizungu kutambua kama ni mimba. Alijiuliza kama akikitumia nini kitakuwa, alimtuma mtoto dawa katika duka la dawa baridi akamletee kipimo kile. Baada ya kuletewa alikwenda msalani na kujisaidia haja ndogo na kuiweka kwenye kikopo kisafi na kurudi nacho chumbani.
Alikiweka kile kikopo chini na kukichukua kipimo, alikifungua ili akitie kwenye kikopo chenye haja ndogo. Mara simu yake iliita alipoitazama ilikuwa inatoka kwa Shehna. Aliipuuza na kukiweka kile kipimo kwenye haja ndogo ili kuhakikisha kama ana mimba kweli. Kilipogusa tu kwenye haja ndogo, alihisi kama tumbo limechafuka ghafla. Ajabu nyingine haja ndogo iliyokuwemo kwenye kikopo iligeuka damu mbichi iliyotoa harufu kali. Alishtuka akiwa anashangaa hali ile, alizidi kushtuka kusikia hali ya majimaji ukimtoka chini kama ya kuziona siku zake. Alipoangalia alishtuka kuona nguo yote umetota kwa damu. Chini damu ilitengeneza michirizi aliyotapakaa sehemu kubwa kuonesha ametokwa na damu nyingi. Kizunguzungu kilikuwa kikali alijitahidi kunyanyuka kwa kujilazimisha na kufanikiwa kuishika simu yake. Aliitafuta namba ya mume wake kwa shida na kupiga na kupokelewa upande wa pili. “Haloo,” Mustafa alipokea. “Mu..mu..me wangu na..na ..ku..fa,” baada ya kusema vile simu ilimponyoka na yeye akajitupa chini kama mzigo na kupoteza fahamu. Mustafa alishtuka na kujiuliza mke wake amepatwa na nini tena. Hakutaka kutoka kama jana yake kwa kumshtua sekretari wake, alimuaga kwa sauti ya kawaida iliyoficha siri nzito ndani. “Sara nafika nyumbani mara moja.” “Mbona hivyo kuna usalama?” “Kawada tu.” Alitoka hadi kwenye gari lake na kuwasha kuwahi nyumbani huku akijiuliza mkewe amepatwa na nini. Aliendesha gari kwa mwendo wa kasi hadi nyumbani, baada ya kusimamisha gari alikimbilia ndani. Alipoingia ndani alishtuka kukuta damu imetapakaa chumba kizima. Alishtuka kuona kikopo kikiwa na damu na ndani yake kuna kipomo cha mimba. “Mungu wangu mke wangu kafanya nini?” Mustafa alishika mikono kichwani. Alimshika mkewe aliyekuwa amelala sakafuni ambaye alionekana kapoteza fahamu huku akiwa ametokwa damu nyingi. Alijikuta akishindwa afanye nini baada ya kujua mkewe kafanya kosa kwenda kinyume na maelekezo ya Shehna. Alimnyanyua na kumpeleka bafuni ambako alimfanyia usafi na kumrudisha kitandani, lakini wakati huo bado alikuwa amepoteza fahamu. Alibaki njia panda asijue ampeleke hospitali au afanye nini. Akiwa katika taharuki simu yake iliita, alipoangalia ilikuwa inatoka kwa Shehna, aliipokea haraka. “Haloo Shehna.” “Haloo Mustafa, vipi mbona kama una tatizo?” “Ndiyo, mke wangu ana matatizo.” “Matatizo gani tena?” “Yaani hata sijui, anatokwa damu.” “Kwanza upo wapi?” “Nipo nyumbani.” “Ha! Umeondoka sangapi wakati nimeingia nimeliona gari lako.” “Sasa hivi.” “Basi mi nipo ofisini kwako, utawahi kurudi?” “Shehna, yaani matatizo ya mke wangu unayaona madogo?” “Siyo madogo ya kujitakia.” “Sasa unanishauri nini?” “Kuhusu nini?” “Tatizo la mke wangu.” “Ulikuwa unahitaji msaada wangu ipi?” “Wa ushauri wako.” “Mpeleke hospitali.” “Si ulitukataza?” “Lakini mkafanya.” “Siyo mimi ni mke wangu.” “Basi mpeleke hospitali kwa hilo sina msaada wowote kwako lipo nje ya uwezo wangu.” “Haina tatizo kwenda hospitali?” “Mustafa mi siyo mganga, wahi hospitali utampoteza mkeo,” Shehna alisema kwa sauti kali kidogo. “Sawa nimekuelewa.” “Sasa unarudi saa ngapi?” “Sijajua.” “Ukimpeleka hospitali lazima atapata kitanda, nitakusubiri ukichelewa nitaondoka.” “Sawa.” Baada ya kukata simu Mustafa alimchukua mkewe na kumuwahisha hospitali. Alipofika alipokelewa na wauguzi na kukimbizwa wadini na kumuacha Mustafa nje akisuburi. Baada ya vipimo majibu yalionesha ujauzito umetoka. Mganga alimwita ofisini na kumweleza tatizo la mkewe. “Vipimo vinaonesha ujauzito umetoka.” “He! Kweli alikuwa na mimba?” Mustafa alishtuka. “Ndiyo kwani ulikuwa hujui?” “Ha..ha….ndiyo.” “Vipi Bwana Mustafa mbona unababaika?” “Kulikuwa na dalili lakini hatukuwa na uhakika.” “Aah! Bwana Mustafa, unaniangusha siku hizi suala la ujauzito si la kusumbuka kwa vile mkiwa na wasiwasi mnakwenda duka la dawa baridi ambalo nina imani siku hizi lipo kila kona, unanunua kipimo na kupata uhakika.” “Na..na sababu ya kutoka ujauzito?” “Inawezekana alianguka na kulilalia tumbo.” “Duh! Sasa itakuaje?” “Atafanyiwa usafi na kuongezwa damu kutokana na kupoteza damu nyingi kisha tutaangalia hali yake kwa kesho, ikiendelea vizuri tutamruhusu.” “Kwa hiyo naweza kumsubiri?” “Hapana kaendelee na majukumu ya ujenzi wa taifa ila acha namba yako ya simu tutakujulisha hali ya mkeo, yangu utaangalia katika business card yangu,” Daktari alimkabidhi kadi Mustafa. “Nashukuru, lakini tatizo siyo kubwa?” “Siyo kubwa, damu ndiyo iliyopotea nyingi, lakini jioni ya leo atakuwa vizuri.” “Nashukuru dokta.” Mustafa alitoka na kurudi nyumbani kufanya usafi wa damu iliyomtoka mkewe. Lakini alishtuka kukuta nyumba ipo katika hali ya usafi hakuna hata na chembe ya damu sehemu.
Hakutaka kuwaza sana aliwasha gari na kurudi kazini, alipofika alishtuka kukutana na manukato makali ambayo aliamini ni ya Shehna. Alipoingia tu Sara alimwambia. “Bosi hukupishana na mwanamke mwenye hijabu hapo mlangoni?” “Hapana.” “Mmh! Kapitia wapi? Sasa hivi katoka.” “Basi sijamuona.” “Yaani sasa hivi hata dakika haijafika, nina imani hata getini hajafika.” “Amesemaje?” “Anashida na wewe.” “Hakutaja jina lake?” “Amesema ukifika niseme sijui Shena.” “Shena au Shehna.” “Shehna, unajua tena lafudhi ya Kimwambao.” “Duh!” Mustafa alisema huku akigeuka na kukimbilia nje amuwahi mgeni wake. Mpaka anafika getini hakumuona mtu yeyote, alimfuata mlinzi na kumuuliza. “Shabani kuna mgeni amepita hapa?” “Ndiyo.” “Mwanamke au mwanaume?” “Mwanamke aliyevaa hijabu.” “Ameenda wapi?” “Baada ya kutoka nje lilipita gari ambalo lilimchukua.” “Duh! Yaani alipotoka tu gari lilipita?” “Amesimama barabarani kama dakika mbili hivi akisubiri, baada ya muda gari lilisimama na yeye kuondoka.” “Atakuwa ameenda wapi, kwa nini hakunisubiri?” “Kwani bosi hukuonana naye?” “Sikuonana naye.” “Yaani mmepishana, baada ya wewe kuingia na yeye akatoka.” “Mungu wangu sasa nimepishana naye wapi?” Mustafa alijilaumu kwani alikuwa ana hamu ya kumuona Shehna kwa macho baada ya kuvutiwa na sauti yake iliyomfanya aamini ni mwanamke mzuri. “Yupo vipi?” “Kwa kweli umbile kalificha na vazi alilovaa ni mweupe, kwa lafudhi yake anaonekana kama Mpemba vile. Ila yule mwana mke ana umbile la utata. ” “Kwa nini unasema hivyo?” “Toka anaingia na kutoka, upepo ulikuwa ukiisukuma nguo yake na kuonekana ramani ya umbile lake na kuonesha mwanamke mzuri sana. Kwani bosi hujawahi kuonana naye?” “Sijawahi.” “Mbona alivyokuuliza kama mnajuana sana?” “Kwenye simu si kwa kuonana.” “Labda atarudi.” “Mmh! Sidhani.” Mustafa aligeuka na kurudi ofisini, alipofika kwa msaidizi wake Sara alimuuliza. “Vipi bosi umemuona?” “Walaa.” “Anapaa?” “Hapana nimekuta ameisha panda gari na kuondoka.” “Bosi nilipokueleza ungetoka ungemuwahi.” “Labda atarudi.” “Nina imani atarudi amekusuburi sana.” “Sijui atarudi?” “Yaani unatoka tu yeye akaingia kama mmepishana mlangoni, nilimweleza akuwahi akasema atakusubiri. Baada ya kuchoka alitaka kuondoka nilimsihi akusubiri, akakubali. Nilikutafuta kwenye simu lakini haukuwa hewani.” “Mbona simu yangu sijazima?” “Yaani kila nikipiga inakata.” “Labda mawasiliano.” Mustafa alipotaka kuingia ofisini Sara alikumbuka kitu. “Bosi.” “Unasemaje?” “Ha…halafu mbona manukato ya yule mwanamke yanafanana na yale ya siku ile tuliyoyakuta ofisini kwako?” “Hata mimi nayasikia, yupo vipi?” “Kwa kweli sikumuona mwili mzima ila ni mrembo sana mrefu tena anayejijali sana.” “Poa, akirudi nitamuona,” Mustafa alijibu huku akienda ofisini kwake. Alipofika alikaa kwenye kiti na kutulia kwa muda kabla ya kuanza kazi, aliwaza kuhusu hali ya mke wake na yaliyomtokea.
Alishangaa kiburi cha mkewe kukaidi amri ya Shehna kwa kutumia kipimo cha mimba wakati alikatazwa. Alijikuta akimlaumu mkewe kwa ukaidi alioufanya kufikia hatua ya kupoteza ujauzito.
Pia hali aliyoikuta nyumbani kwake ilimtisha sana na kushangazwa kukuta kumesafishwa, hakuna dalili za damu kumwagika. Alijikuta akijiuliza nani aliyefanya usafi ule wakati anaondoka nyumbani hakukuwa na mtu yeyote lakini aliporudi alikuta pamefasafishwa. Wazo lake lilikuwa labda shoga yake alipita kumsalimia na kukuta hali ile na kuamua kufanya usafi. Lakini kilichomshtua ni sehemu yenyewe ya tukio kuwa chumbani kwake na kushangaa kama shoga yake aliingia chumbani na kufanya usafi. Aliamini kama ni shoga yake lazima atapiga simu kuuliza kilichotokea. Mustafa akiwa katikati ya mawazo, Sara aliingia na faili la kazi na kushangaa kumkuta bosi wake amezama kwenye dimbwi la mawazo. “Bosi vipi?” “Poa,” Mustafa alijibu huku akinyanyua uso kumtazama Sara. “Upo sawa?” “Kiasi.” “Mmh! Bosi basi jana hata sielewi kilichonitokea!” “Kitu gani Sara?” Basi bosi baada ya wewe kuondoka, ghafla nilichukua vitu vyak…” Kabla Sara hajaendelea kumhadithia, alinyamaza baada ya kusikia sauti ya mtu mapokezi. Alitoka kwenda kumuangalia, alipofika alishtuka kutomkuta mtu. Lakini ghafla alishangaa kusikia kizunguzungu, alikwenda kwenye kiti chake na kukaa. Baada ya kukaa alisikia usingizi mzito, alipojaribu kujiepesha, usingizi ulimpitia. Sara aliposhtuka alijikuta amelala kwenye kochi nyumbani kwake akiwa na nguo zake za kazini. Alishtuka na kujiuliza kinachomtokea ni kweli au anaota, alikumbuka tukio kama hilo lilimtokea jana yake wakati akimpelekea bosi wake vitu vyake baada ya kutoa mbio na kuviacha ofisini. Baada ya kukodi gari ambalo aliingia na kumweleza dereva ampeleke anapokaa Mustafa na kushangaa kujikuta amelala nyumbani akiwa na vitu vya bosi wake. Alijiuliza ni kitu gani huwa kinamtokea na kujikuta kwenye hali ile ambayo ilianza kumtisha. Kwa vile muda ulikuwa umekwenda baada ya kuangalia saa na kumuonesha ni saa mbili usiku, alikwenda kununua chipsi na soda kisha akapanda kitandani kuitafuta siku ya pili. ***
Mustafa baada ya kutoka kazini, alipitia hospitali kuangalia hali ya mkewe inaendeleaje. Alimkuta hajambo kiasi ila mwili ndiyo haukuwa na nguvu hivyo kuendelea kuwepo hospitali mpaka siku ya pili. Hakutaka kumuulizia ilikuwaje mkewe akakaidi amri ya Shehna na kufanya aliyvotaka. Aliamini sehemu nzuri ya kulizungumza suala hilo ni nyumbani hasa baada ya kuhakikishiwa na daktari kuwa kesho yake angetoka. Hakutaka kumsumbua mkewe, alimuacha apumzike na yeye kurudi nyumbani. Alipita kwenye mgahawa na kuchukua chakula cha kubeba ili akalie nyumbani. Alipofika nyumbani, alioga na kupata chakula kisha alichukua ‘laptop’ yake na kucheza gemu ya magari ili kuutafuta usingizi. Akiwa katikati ya mchezo, alisikia mlango ukigongwa huku akiitwa jina lake, aliacha kucheza gemu na kutoka sebuleni. Alitulia kabla ya kufungua mlango kusikilizia ni nani anayegonga usiku ule. “Nani?” aliuliza kwa sauti ya juu kidogo. “Mimi,” sauti ya kike ilijibu ambayo haikuwa ngeni masikioni mwake lakini hakuikumbuka ni ya nani. “Wewe nani?” “Shehna.” “Ka..ka..ribu,” Mustafa alishtuka na kupata kigugumizi cha ghafla baada ya kusikia jina la Shehna. Alifungua mlango na kulakiwa na harufu nzurii ya manukato, ilikuwa tofauti na aliyoizoea siku zote, ilikuwa nzuri zaidi. Mbele yake alikuwa amesimama mwanamke mzuri sana aliyekuwa amevalia vazi refu la gauni la kumeremeta lililoacha mabega wazi na kufunikwa na mtandio. Chini alivaa viatu virefu, alipoangalia nje hakuona gari lolote lililopaki jirani. Kutokana na viatu vile venye kisigino kirefu, aliamini asingeweza kutembea kwa miguu umbali mrefu. “Karibu ndani.” “Asante,” Shehna alisema huku akiingia ndani na kulinyanyua juu gauni lake lililokuwa linaguza chini. Shehna alikwenda kukaa kwenye kochi na kutulia, Mustafa baada ya kufunga mlango alirudi kukaa kwenye kochi lingine. “Karibu sana,” Mustafa alimkaribisha tena. “Asante za hapa?” “Mmh! Nzuri kiasi,” Mustafa alijibu huku akimuibia Shehna kumtazama kutokana na uzuri wake, kitu alichokigundua Shehna na kusema huku akiondoa mtandio kichwani na kuziacha nywele zake ndefu nyeusi zionekane vizuri. Aliachia tabasamu kama ua la mchana linavyochanya, macho yake makubwa kidogo yaliyopakwa wanja yaliongeza uzuri wake. Yalioneka yameumbwa kwa mahaba tu. “Mustafa usipate shida ya kuhangaika kunitazama, una uhuru wa kunitazama upendavyo wala usiniogope.” “Ha..ha..una..na,” kutokana na kushindwa kujiamini maneno yalipandana. Mustafa kwa mara ya kwanza alimuona mwanamke mzuri katika maisha yake. Hakugundua kasoro yoyote kwa Shehna, kumbukumbu zake zilimkumbusha ndiye mwanamke aliyefanya naye mapenzi katika ndoto. “Mustafa mimi mtu wa kawaida najua uzuri wangu utakubabaisha, nione kama nyama yoyote isiyo na mfupa kwenye kisu kikali.” “Unatu..tumia kinywaji gani?” Mustafa alijikaza na kumuuliza. “Kwa leo sihitaji kitu nataka tuzungumze kitu ili niondoke zangu.” “Kitu gani?” “Mustafa unakumbuka nilikuahidi nini?”
“Vingi, sijui kipi kimoja wapo.” “Kuhusu matatizo yako.” “La kunipatia mtoto.” “Umempata?” “Sijampata.” “Kwa nini?” “Hatukufuata ushauri wako.” “Toka muanze kuhangaika mkeo aliwahi kupata dalili za ujauzito?” “Hapana.” “Kwa hiyo kazi yangu nilimaliza?” “Bado kwa vile sijapata mtoto.” “Utapata vipi na mkeo hataki mtoto?” “Sasa utanisaidiaje?” “Mustafa naomba sasa hivi unisaidie nilichokuomba.” “Kama kitu kimo ndani ya uwezo wangu nitakusaidia.” “Nataka mtoto,” Shehna alisema huku akimtazama kwa macho yake ya huruma yaliyojaa mahaba. “Mtoto!” Mustafa alishtuka. “Ndiyo.” “Mimi nitampata wapi?” “Unawezaje kumpatia mkeo mtoto?” “Kwa kukutana kimwili.” “Basi na mimi namuhitaji kwa njia hiyo.” “Yaani mimi nifanye mapenzi na wewe?” “Ndiyo, kwani kuna ubaya?” “Si unajua mimi ni mume wa mtu?” “Mustafa hujawahi kutembea nje ya ndoa yako?” Swali lile lilimfanya apate kigugumizi kulijibu kwa vile alikuwa na mwanamke aliyempangia chumba na siku nyingine alikwenda kulala kule na kudanganya amekwenda safari ya kikazi. “Mustafa unaiheshimu sana pete ya ndoa kwa vile mkeo ni mkorofi na ana wivu sana, lakini huiheshimu ndoa yako. Au mimi kutaka kuzaa na wewe umeniona malaya?” “Ha…ha…pana Shehna sijakufikiria hivyo.” “Sasa nipe jibu moja, utanipatia mtoto au hunipi?” “Nitakupatia.” “Nimefurahi kusikia hivyo, nakuahidi kukupa zawadi kubwa sana katika maisha yako.” “Nitafurahi sana.” “Mustafa natoka mara moja nitarudi muda si mrefu.” “Kwa hiyo nifunge mlango.” “Usifunge narudi sasa hivi.” *** Mustafa aliota akifanya mapenzi na Shehna huku akiahidiwa kuwa tajiri mkubwa duniani kama atampatia ujauzito. Aliposhtuka usiku alijikuta amelala sehemu ngeni machoni mwake. Ilikuwa sehemu nzuri sana ambayo hakuwahi kufika. Pembeni yake alikuwepo Shehna aliyepitiwa na usingizi. Wote walikuwa wamelala kwenye shuka moja bila ya nguo nyingine, Mustafa alishtuka na kujiuliza ile ni ndoto au kweli. Alijaribu kujifinya ili apate ukweli alihisi maumivu, alijiuliza alikuwa wapi na alifikaje. Ghafla alishikwa na usingizi na alipoamka alijikuta kitandani kwake akiwa amechoka sana. Alionesha alitumika usiku lakini bado alibakia njia panda kama alitumika Shehna alikuwa wapi. Alinyanyuka na kwenda bafuni kuoga, nyumba nzima ilikuwa ikinukia manukato ya Shehna. “Mustafa,” sauti ya Shehna ilimshtua. “Naam.” “Chai tayari,” Shehna aliingia chumbani akiwa amejifunga mtandio bila nguo nyingine na kuufanya mwili wake mantashau uonekane wazi. Alimshika mkono hadi mezani kulipokuwa na kifungua kinywa kitamu kilichomfanya Mustafa amsifie. “Hakika Mungu kakujalia kila kitu.” “Kama nini?” “Mambo ya siri na bayana.” “Asante, nioe basi niwe mke wa pili.” “Itabidi nifanye hivyo.” “Wewee! Mkeo atakufa kwa kihoro ana wivu sana.” “Sasa itakuwaje?” “Shida yangu kwako mtoto tu nakuacha na mama wivu wako.” Baada ya chai waliondoka pamoja kwa Mustafa kupitia hospitali na Shehna kushukia kwenye mataa ya barabarani. “Mustafa nishushie hapa.” Mustafa alimshusha na Shehna alienda zake japo hakujua anakwenda wapi wala anakaa wapi. Alielekea moja kwa moja hospitali kumuona mkewe.
Mustafa akiwa njiani kuelekea hospitali alikuwa mtu mwenye mawazo mengi kutokana na kila kitu kilichomtokea na kujiuliza Shehna ni kiumbe wa aina gani? Japokuwa alikuwa mwanadamu wa kawaida lakini matukio yake yalimchanganya sana na kujikuta akiingia hofu ya kila alichokiona ambacho hakikuwa cha kawaida. Aliushangaa uwezo wa Shehna wa kuelewa vitu vingi vinavyoonekana na vilivyojificha. Alikuwa amefanya siri ambayo hata mkewe na watu wengi hawakuijua kama ana nyumba ndogo. Lakini yeye aliijua bila kumwambia, alijiuliza ni nani kwenye uganga hayupo kwa vile alionekana mwanamke mrembo tena mwenye kujipenda. Tofauti na waganga wengi ambao wengi wao huwa hawajipendi, mavazi yao huwa ya kujiachia wala hawajui mapambo na manukato. “Sasa Shehna ni nani…au jini? Ha…hapana huko nimefika mbali,” Mustafa alijiuliza na kukataa mwenyewe. “Mbona jana niliota nimelala naye sehemu nzuri lakini nilipoamka nilijikuta nipo nyumbani kwangu? Na Shehna alirudi saa ngapi na kwa nini hakuniamsha mpaka niliposhtuka asubuhi na kujikuta nimetumika kutokana na kufanya naye mapenzi ya ndotoni. “Mmh! Shehna mbona anataka kunipa mtihani mzito, anataka nizae naye kwa ahadi ya kumpatia mtoto kupitia kwa mke wangu. Sasa mbona ametaka azae yeye kwanza? Mmh! Kazi ipo.” Alijikuta amefika hospitali bila kupata jibu kitu kinachomtatiza kuhusu Shehna. Aliingia hospitali na kwenda chumba alicholala mkewe, alimkuta akiwa amejiandaa kutoka baada ya kupewa ruhusa mapema. “Yaani mume wangu unajua naumwa unaniacha mpaka saa hizi?” Husna alimuuliza kwa hasira. “Tabia hii imeanza lini, hata salamu unafikia kunilaumu, ningekufa ungefurahi?” Mustafa alijibu kwa hasira. “Ufe na nini?” “Kwa vile hukutaka kujua haina muhimu, unaendeleaje?” Mustafa naye alikuwa mkali kwa mkewe. “Nisamehe mume wangu nilichanganyikiwa baada ya kuchelewa kukuona wivu uliniingia, ulipatwa na nini mume wangu?” “Ilitakiwa tusalimiane tujuliane hali kisha tuzungumze mambo mengine.” “Ni kweli, nisamehe mume wangu nimekosa wivu wakati mwingine ugonjwa.” “Nimekukataza mara ngapi sipendi wivu wa kijinga, kila siku umekuwa ukiniona akili yangu unawaza ujinga.” Mustafa alimjia juu mkewe kwa vile alikuwa amepata nafasi, naye alikuwa amechoka na wivu wa kijinga wa mkewe ambao uligeuka kero kitu kilichosababisha kuanzisha uhusiano na mwanamke ambaye mkewe alimshtumu anatembea naye. Mwanamke huyo ilitokana na kushtumiwa na mkewe kwa hisia bila ukweli. Kwa hasira alifanya kweli kwa kutembea na yule mwanamke ambaye baadaye alimfanya nyumba ndogo na kumuhamisha mtaa ule na kwenda kumpangia sehemu nyingine na kuendeleza mapenzi kwa siri. Siri ile aliijua peke yake hata rafiki yake hakujua kama ana nyumba ndogo, lakini alishangaa Shehna kuijua. “Mume wangu huna dogo, nimekosa nisamehe.” “Sawa, vipi unaendeleaje?” “Namshukuru Mungu sijambo japokuwa mwili hauna nguvu.” “Pole mke wangu, wakati nakuja kuna mwendesha pikipiki alijigonga kwenye gari langu, watu wakajua nimemgonga wakataka kunipiga lakini askari wa barabarani alifika na kuniokoa,” Mustafa alitengeneza uongo ili kumpoza mkewe. “Jamani pole mume wangu!” Husna alisema kwa sauti ya huruma. “Asante.” Mustafa alimchukua mkewe na kurudi naye nyumbani, alipofika alijikuta akitaka kujua kipi kilimfanya akaidi amri ya Shehna. Baada ya kutulia kwa muda alimsemesha mkewe. “Mke wangu.” “Abee, mume wangu.” “Kipi kilichokufanya umuue mtoto wangu?” “Mume wangu kupima ujauzito ni kumuua mtoto?” Husna alishtuka. “Shehna alituambia nini?” “Mume wangu utaamini vipi una ujauzito bila kupima?” Husna alijitetea. “Si alitukataza?” “Ndiyo! Lakini bado nilishindwa kumuamini, mume wangu kwanza Shehna ni nani mbona masharti yake ya ajabuajabu?” “Mke wangu tumehangaika sehemu ngapi tumepewa masharti mangapi tuliyoyatekeleza, yaani hili ndilo umeliona gumu?” “Mi nimechoka kila siku masharti magumu.” “Ha! Mke wangu umeweza kulala makaburini kutafuta mtoto, umeona kazi kutotumia dawa za kizungu ikiwa hali yako ilikuwa nzuri?” “Mume wangu mimi nina wasiwasi huyu mwanamke si mwanadamu!” “Mke wangu shida yetu mtoto au kujua Shehna ni mtu au jini?” “Mi simuelewielewi.” “Mke wangu Shehna si jini ni mwanadamu pia si mganga.” “Ni nani?” “Nimekuambia mtu.” “Kama si jini wala mganga ni nani mbona unataka kutusaidia?” “Yule dada alipatwa na tatizo kama letu kuna siku nilimsikia akizungumza na mtu jinsi alivyohangaika kutafuta mtoto na kufanikiwa kupata. Nilivutiwa na habari zake na kumuomba anisaidie. Aliahidi kunisaidia na ndicho alichotusaidia, sasa mke wangu kipi kilichokutuma kuniulia mwanangu?” Mustafa alimuuliza akiwa amemkazia macho mkewe. “Mume wangu sikujua,” Husna alikuwa mpole. “Sasa tutafanya nini? Lazima Shehna tumemuudhi tutafanyaje, kumbuka mke wangu tumehangaika sehemu ngapi hatukuona dalili za mimba hata siku moja. Lakini dawa ya Shehna siku moja na mimba juu.” “Dah! Sijui itakuwaje ukimuona naomba uniombee msamaha, nipo radhi kufuata masharti yoyote atakayonipa.” “Mmh! Sijui!” “Mume wangu tusitake kujihukumu, najua lazima atapiga simu, naomba umweleze aje nyumbani ili nimuombe msamaha au nimfuate popote.” “Sawa nikimuona au kunipigia simu nitafanya hivyo.” Mustafa alimuaga Husna na kwenda kazini kwa vile alichelewa kutokana na kumfuata mkewe hospitali. *** Mustafa baada ya kufika ofisini, alijawa na mawazo kuhusiana na matukio yote yaliyokuwa yakimtokea. Bado alikuwa njia panda kutokana na Shehna mwanamke mrembo aliyeonesha mapenzi mazito kwake. Lakini mambo yake yalionekana kama yana muujiza yaliyokuwa kila siku yanamstaajabisha. Alijiuliza alimjulia wapi mpaka kumpenda kiasi kile, kutokana na mavazi na vito vyote alivyovaa vilikuwa vya thamani kubwa sana. Ilionesha anatoka katika familia yenye uwezo mkubwa sana. Alipanga akikutana naye amuulize vizuri ajue alimuonea wapi na kipi kilichomfanya ampende na kupelekea kutaka kuzaa naye na si mwanaume mwingine. Sara akiwa bado yupo katika dimbwi la mawazo, sekretari wake aliingia ofisini na kushangaa kumkuta bosi wake amezama kwenye mawazo. Toka aingie ilikuwa ilimeta saa moja bila kugusa kitu zaidi ya kuzama kwenye mawazo. Alimwita na kumfanya ashtuke. “Vipi bosi mbona upo mbali kimawazo?” “Wee acha tu, vipi unasemaje?” alijibu huku akifuta mikono usoni na kujinyoosha kama mtu mwenye usingizi au aliyechoka sana. “Nimekupigia simu ya mezani nashangaa inaita bila kupokelewa, naingia ndani naona upo kwenye dimbwi la mawazo. Unajua bosi siku hizi sikuelewi kabisa inaonekana hapo sawa.” “Nipo sawa, ulikuwa unasemaje?” Mustafa alijibu huku akijiweka sawa kitini na kuiweka sawa Laptop iliyokuwa juu ya meza. “Kuna mgeni wako.” “Duh! Akili yangu haijakaa sawa mwambie arudi baadaye,” alijibu huku akifungua kazi kwenye desktop. “Lakini mgeni unamjua?” “Kwani nani?” “Yule dada mrembo.” “Ooh! Kumbe Shehna mwambie apite.” “Unaona!” Sara alisema huku akitabasamu na kutoka nje. Mustafa alishtuka na kushangaa kumfuata ofisini ikiwa walilala pamoja na kuachana muda mfupi. Akiwa ameinama alishtuliwa na harufu ya manukato na sauti tamu ya Shehna. “Asalamu aleykum Mustafa.” “Waleykum salam Shehna.” Alinyanyua uso na kukutana na Shehna akiwa katika vazi la hijabu iliyomziba mwili mzima. Baada ya kuketi aliiondoa nikabu iliyomziba uso na kufanya aonekane vizuri kisha alitikisa nywele zake nyingi nyeusi na kufanya zichanue kama ua huku tabasamu mwanana akilichanua na kumfanya Mustafa kujiona kama yupo ndotoni. Alitulia na kumtazama Mustafa aliyekuwa ametulia kama mtu aliyekuwa akitazama picha nzuri na kuitikia kama ameitwa. “Abee mpenzi,” Shehna aliitikia bila kuitwa kitu kilichomshtua Mustafa na kumuuliza: “Shehna mbona unaitikia? Sijakuita.” “Mustafa uniite mara ngapi?”Shehna alimtazama Mustafa usomi huku macho yake makubwa kidogo ya kusinzia yaliyopakwa wanja na kufanya azidi kupendeza. Hakika Shehna alikuwa mrembo wa warembo. “Haki ya nani Shehna sijakuita,” Mustafa alijitetea kwa kuamini toka aachane naye hajapiga simu wala kuonana naye. “Huna kitu unachotaka kuniuliza?” Shehna alimuuliza huku amemkazia macho ambayo yalizidisha uzuri wake.
Ninacho lakini nilijua tutaonana jioni.” “Sawa angeniuliza jioni lakini toka ufike una muda gani?” “Zaidi ya saa nzima.” “Umeishafanya kazi gani?” “Bado sijaanza.” “Kwa nini?” “Sina kazi nyingi ningefanya wakati wowote.” “Kwa hiyo Mustafa unataka kunidanganya hata mimi?” “Kwa nini unasema hivyo?” “Mustafa toka uingie kuna vitu vinakutatiza na kujikuta muda mwingi ukijiuliza maswali mengi ambayo unaamini mwenye majibu yake ni mimi, uongo?” “Kweli.” “Haya niulize.” “Kwa nini tusizungumze jioni kwa vile huu ni muda wa kazi!” “Mustafa mi si mjinga kuacha kazi zangu na kuja kukusikiliza, najua leo huwezi kufanya kazi mpaka upatiwe majibu ya maswali yako.” “Umejuaje nataka kukuuliza?” “Mustafa muhimu kwa muda huu kujua nimejuaje au kukujibu maswali yako.” “Samahani Shehna.” “Mustafa kama nisingekuwa mimi usingemruhusu mtu kuingia ndani, uongo kweli?” “Kwa baadaye lazima ningewaruhusu.” “Kwa hiyo niondoke?” “Ha…hapana.” “Unajua kuna kitu kimenifurahisha sana leo ambacho nimepanga kukuzawadia, lakini unataka kuniudhi.” “Shehna samahani kama nitakukosea lakini naamini wewe ni mtu muhimu sana kwangu.” “Ndiyo maana nipo hapa.” “Kuna mengi ya kukuuliza nashindwa nianze na lipi.” “La mkeo.” “Umejuaje?” “Mustafa acha kuwa mgeni wa dunia kushtuka kila kitu, uliza ili ujibiwe si kujua nimejuaje.” Mustafa alizidi kumshangaa Shehna kuyajua yaliyojificha moyoni mwake, alijiuliza yeye ni kiumbe wa aina gani mwenye uwezo wa ajabu kama ule? Hakuwa na jinsi alimueleza aliyoelezwa na mkewe juu ya kumuomba msamaha kwa yote yaliyotokea. “Mustafa nimemsamehe kwa vile nakupenda lakini mkeo ana kiburi, masharti mengi amekuwa akiyavunja matokeo yake mnatumia fedha nyingi na nguvu nyingi bila mafanikio.” “Sasa utanisaidiaje?” “Unataka msaada wangu upi?” “Bado tunataka mtoto.” “Mmechelewa.” “Kivipi?’ “Unakumbuka nilikuambia nini?” “Vitu vingi, kimoja wapo?” “Kuhusu kupata mtoto.” “Si ulisema utanipa mimi kwanza ndipo nikupe wewe.” “Ni kweli, lakini makosa ya mkeo yamefanya mambo yabadilike.” “Kivipi?” “Zoezi la mimi kupata mtoto nimelianza usiku wa leo.” “ Sasa tatizo nini?” “Tatizo hatuwezi kushea watu wawili kupata mtoto kwa vile wewe sasa hivi una mbegu moja baada ya mkeo kuiharibu ya kwanza iliyokuwa yake.” “Mmh! Kwa hiyo unataka kuniambia na wewe mjamzito sasa?” “Hapana.” “Kwa nini hukupata wakati dawa unaijua?” “Mimi ni tofauti na mkeo lazima nilale na wewe mwezi mzima mfululizo, tukiacha hata siku moja tumeharibu dozi na muda huo wote usikutane na mkeo.” “Dah! Itawezekanaje nilale mwezi mzima na mke wangu bila kukutana naye, akinitaka nitafanyaje?” “Wala usihofu hawezi kukugusa mpaka mwezi uishe.” “Mmh! Sawa.” “Nina imani swali moja nimekujibu uliza lingine.” “Nafikiri hili ndilo la muhimu mengine siyo muhimu sana.” “Mustafa yote muhimu, nipo hapa kukufanya uwe huru na kuondoa wasiwasi wote.”
“Mmh! Anyway, hivi Shehna tulionana wapi kabla na kipi kilichokuvutia kwangu kupelekea kutaka kuzaa na mimi na kuwaacha wanaume wengi wasio na wanawake?” Shehna kabla ya kujibu alicheka kidogo kisha alitabasamu huku aibu ya kike ikimtawala na kuanza kuchezea kucha na kupeleka vidole mdomoni. Mustafa alitumia muda ule kuusanifu uzuri wa Shehna na kushangaa aibu iliyompata kutokana na swali lake. “Shehna kama swali langu limekuudhi naomba unisamehe, naweza kubadili swali,” Mustafa alijihami. “Hapana, sivyo hivyo swali lako lazima nilijibu kwa vile nipo hapa kwa ajili ya kuondoa wasiwasi wa moyo wako. Mustafa huwezi kuamini nimekupenda muda mrefu sana hata kabla ya kuwa na Husna. “Mapenzi yangu hayajaanza leo ni muda mrefu nimekuwa nakupenda. Katika maisha yangu nilitamani uwe mume wangu lakini kuna vikwanzo ambavyo vilisababisha nichelewe kukueleza ukweli wa moyo wangu. “Bahati nilipata safari ya ghafla na kuondoka bila kukueleza dhamira yangu ungeweza kunisubiri. Niliporudi nilikuta tayari umeoa lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kutaka hata nipate angalau ukumbusho wa sura yako, ndiyo maana nikataka kuzaa na wewe. “Wakati napanga hivyo, niligundua una maumivu moyoni mwako kutokana na kuchelewa kupata mtoto. Baada ya kufanya uchunguzi, ilionesha umepoteza fedha nyingi kwenda kwa waganga bila mafanikio. Niliamini nikitatua tatizo ambalo limekunyima furaha, utakuwa tayari kunisikiliza na mimi shida yangu. “Ndipo nilipokutafuta kwa njia ya simu na kukupa maelekezo ambayo mwenyewe uliona maajabu lakini kiburi cha mkeo kikaharibu kila kitu. “Kwa vile nilipanga baada ya wewe kupata mtoto ndipo na mimi nipate wangu, basi baada ya mkeo kuvuruga ratiba, itabidi unipe kwanza mimi ujautito ndipo nikupe dawa ya kutafuta mtoto mwingine ambayo mkeo anatakiwa kuwa makini kosa lingine litamfanya awe tasa, hatazaa mpaka anakufa. “Mustafa kama nilivyokueleza mapenzi yangu kwako hayakuanza leo bali muda mrefu, tumeonana sehemu nyingi lakini inaonesha umenisahau. Unakumbuka siku moja tulikutana ukitoka kufanya usaili ambapo ulikuwa mnyonge baada ya kujua amefanya vibaya. “Nilikueleza kuwa pamoja na kufanya vibaya lazima jina lako litachaguliwa kati ya matano na kubakishwa jijini Dar. Najua ulishangaa lakini baada ya muda, ilitokea kama nilivyokueleza. Unakumbuka ulikutana na nani akakueleza habari zile?” Maneno yale yalimfanya Mustafa ashtuke na kurudisha kumbukumbu nyuma miaka nane iliyopita. Siku aliyokwenda kufanya usaili wa kazi ambako walitakiwa watu watano katika watu mia moja waliokuwepo. Katika watu waliofanya vibaya katika usaili ule yeye alikuwa mmoja wapo, katika maswali kumi aliyoulizwa alijibu matatu hata nusu hakufika. Hata waliokuwa wakiwafanyia usaili, walimkatisha tamaa baada ya kumweleza hakuweza kufika nusu tofauti na wenzake zaidi ya sabini waliotangulia. Aliondoka akiwa hana matumaini. Lakini alipotoka nje ya ofisi ili aelekee nyumbani, aliitwa na msichana aliyekuwa amevaa hijabu iliyomziba mwili mzima na kuonekana macho. “Mustafa.” “Naam,” aligeuka kumtazama aliyeonekana anamfahamu, hakuweza kumuona uso zaidi ya macho. “Pole.” “Ya nini?” “Ya kufanya vibaya.’ ‘Umejuaje?” “Mbona umeniangusha kwa nini umeshindwa kujibu maswali yale mepesi?” “Yaani hata sijui.” Yule msichana aliyarudia maswali yale na kumuuliza: “Sasa hapa swali gani gumu?” “Yaani hata mimi nashangaa, basi tena nitajaribu sehemu nyingine.” “Mbona umekata tamaa mapema?” “Kama nimefanya vibaya huku zaidi ya watu sabini wamefanya vizuri huku nafasi tano tu zinatakiwa, kuna nini hapo?” “Usiwe na wasiwasi katika hizo nafasi tano, wewe utakuwemo na ndiye utakayebakia Dar.” “Wewe nani?” “Mustafa shida yako kujua mimi nani au wewe kupata kazi na kuteuliwa kubakia Dar?” “Shida yangu kupata kazi.” “Basi subiri muda ufike.” “Nitajuaje?” “Utapigiwa simu.” “Wataijuaje namba yangu ya simu wakati hawakuchukua kwa vile ni mmoja ya watu waliofanya vibaya.” “Namba yako nitawapa.” “Namba yangu umeipata wapi?” “Mustafa hujawahi kuigawa namba yako?” “Nimegawa basi nitashukuru japokuwa najua hakuna kitu.” “Siku tukikutana utaniambia.”
Mustafa aliagana na yule msichana mwenye lafudhi ya mwambao bila kumuuliza jina. Siku moja akiwa hana hili wala lile alipigiwa simu kujulishwa amefanikiwa kupita katika mchujo wa usaili na yeye ndiye aliyefanya vizuri kuliko wote anatakiwa kubakia Dar es Salaam. Alishtuka sana lakini hakuamini aliona kama watu wanamchezea akili, siku ya pili alikwenda ofisini kujaribu lakini alipotaja jina lake alikabirishwa na kujaza fomu ya kuajiliwa na wiki iliyofuata alianza kazi kwa kupewa ofisi na sekretari pamoja na mshahara mzuri. Lakini Mustafa alisahau kama kuna mtu alimweleza taarifa kuwa atapita kwenye usaili na atabakia jijini Dar japokuwa alikuwa amefanya vibaya sana. Furaha ya kupata kazi ilimfanya asitumie muda kuwaza ilikuwaje mpaka kupita na msichana yule alijuaje. Mustafa alitulia na kuvuta kumbukumbu kisha aliteremsha macho kumuangalia Shehna na kuamini kabisa ndiye yeye. Kwa lafudhi aliyoitumia japokuwa alimuona macho tu aliamini kabisa ndiye msichana aliyemtabilia mambo ya ajabu. “Dah! Kweli.” “Kweli nini?” Shehna alimuuliza akiwa anamtazama usoni. “Nimekumbuka, hivi ulijuaje mi nitapita wakati nilikuwa najua nimefanya vibaya?” “Leo siyo siku yakeikifika nitakueleza, mpaka hapo nina imani baadhi ya vitu umevielewa kama una swali niulize.” “Swali lingine nilitaka kujua wewe unakaa wapi katika familia yenu mpo wangapi, kwa sasa unajishughulisha na nini. Wewe ni mganga au nani?” “Ninapokaa si rahisi kukuelekeza mpaka twende pamoja, katika familia yetu tupo watatu wote wanawake mimi ni mtoto wa mwisho na swali la mwisho mimi si mganga wala mnajimu ila Mungu kanipa uwezo wa kuyajua matatizo ya mwenzangu.” “Kwa nini huwezi kupata ujauzito kwa mara moja kama mke wangu?” “Dawa ya haraka nilikuwa nayo moja ambayo nilimpa mkeo hii inachelewa, kwa vile nami nina hamu ya mtoto sina jinsi lazima nitumie njia ya muda mrefu.” “Kingine unajua sijawahi kulala nje ya nyumbani kwangu nitafanyaje?” “Mustafa nyumba ndogo huwa unalala nayo nyumbani kwako?” “Mmh!” Mustafa aliguna baada ya kujua ameumbuka. “Najua wasiwasi wako kulala nje ya nyumba yako mwezi mzima, nitalala na wewe mwezi huo mzima nyumbani kwako na kitandani kwako.” “He! Na mke wangu atakuwa wapi?” Mustafa alioshtuka. “Atakuwepo ndani.” “Siwezi kufanya mapenzi ndani na mke wangu akiwemo itakuwa kumdhalilisha.” “Mustafa naomba unisikilize, wewe kila siku naomba ukilala usiku wakati mnataka kulala hakikisha wewe unakuchelewa kulala usikubali hata siku moja mkeo akukute kitandani. “Mkeo akiisha lala utaingia bafuni kuoga na kujipaka mafuta nitakayokupa. Isipande kitandani hakikisha mlango wako umeurudisha bila kuufunga au dirisha ili nikija nisipate tabu ya kuingia. “Ukiishapanda kitandani usilale na nguo ya ndani kisha hakikisha mkeo analala ukutani wewe lala katikati ya kitanda mimi nikija nitalala mwanzoni mwa kitanda. Mpake mkeo mafuta kichwani kisha lala.” “Mmh! Nitaweza kweli, mbona unanipa mtihani, kwa nini tusiwe tunakutana hotel na tukimaliza haja zetu, narudi nyumbani kulala?” “Mustafa kutafuta kwangu mtoto natakiwa kupata dozi ya mara tatu kwa usiku mmoja hivyo lazima nilale na wewe.” “Una maanisha dozi ya kivipi.” “Ya saa sita, saa tisa na kumi na moja alfajiri, unaweza kulala nje?” “Shehna mbona unanipa mtihani mgumu.” “Mbona wako niliuweza wa kwenda kubadili matokeo ya usaili ili upite kama ningekamatwa ningekuwa wapi?” Shehna alimuuliza Mustafa akiwa amemkazia macho huku sura ya uzuri iligeuka kama mzee na kumtisha Mustafa.
“Mustafa nimejitolea katika mambo yake mengi ambayo wewe huyajui, yaani kwa hili moja umeshindwa. Unakumbuka ulitaka kufukuzwa kazi mimi ndiye niliyerekebisha mahesabu ili ubakie kazini? Wewe ni mtu gani usiyejiuliza kila kosa lako halionekani?” Shehna alimuuliza huku machozi yakimtoka. Kauli ile ilimshtua sana Mustafa na kuzidi kumshangaa Shehna na kujiuliza ni kiumbe wa aina gani. Alikumbuka baada ya kupata nyumba ndogo alijikuta akitaka kumfurahisha, alijikuta akifanya ubadhilifu wa fedha kazini kwake. Taarifa ilifika ofisi kuu na kufanya mahesabu ya ghafla huku akisimamishwa kazi kupisha wafanye mahesabu. Kitendo kile kilimshtua Mustafa na kujikuta akipandwa na presha na kulazwa hospitali kwa kujua hana kazi na lazima afungwe kwa vile alichota zaidi ya milioni kumi na tano. Siku ile akiwa hospitali majira ya usiku wa manane aliamshwa na daktari binti mrembo wa Kiarabu aliyekuwa amesimama pembeni ya kitanda chake. Alikuwa amevalia mavazi ya kidaktari na miwani myeupe nywele zake zilikuwa ndefu na nyeusi. Alikuwa binti mrembo sana, hakuwahi kumuona mwanamke mzuri kama yule katika maisha yake na kumwita jina lake. “Mustafa.” “Naam.” “Pole sana.” “Asante.” “Tatizo nini?” “Wanadamu wabaya wamenisingizia nimekula fedha ya kampuni wakati sijala hata senti tano.” “Mustafa kuwa mkweli, fedha umekula. Heri ungeijengea familia yako, wazazi wako wanaishi maisha ya kubahatisha kuliko ulichokifanya kumhonga hawara.” Kauli ile ilimshtua Mustafa na kujiuliza yule daktari amejuaje au kuna mtu alimwambia, ilibidi amuulize amejuaje. “We umejuaje?” “Mustafa muhimu si kujua nimejuaje zaidi ya kukusaidia usifukuzwe kazi na kufungwa.” “Utafanyaje?” “Kazi hiyo niachie mimi,” Mustafa alizidi kumshangaa daktari atamsaidia vipi, daktari alitabasamu na kuzitikisa nywele zake ndefu nyeusi zilizoongeza uzuri wake. “Mustafa bai.” Mustafa siku ya pili aliposhtuka alijua ile ilikuwa ni ndoto kwa vile pale hospitali hakukuwa na daktari wa vile. Lakini ajabu siku iliyofuata alielezwa arudi kazini kila kitu kimekutwa kipo sawa hakukuwa na hasara yoyote kwenye fedha ya kampuni. Japokuwa aliona kama ndoto iliyo na ukweli, hakutaka kushughulika nayo zaidi ya kushukuru kuponea tundu la sindano. “Mustafa unakumbuka siku hiyo?” Mustafa baada ya kuvuta kumbukumbu alijikuta akizidi kumshangaa Shehna na kujiuliza ni kiumbe gani aliyekuwa karibu ya matatizo yake muda wote na kujiuliza amekuwa akijuaje na kutokea kumsaidia. Alijiuliza alifanyaje mpaka hesabu zikakutwa zipo sawa wakati alijua tayari hana kazi na jela ilikuwa ikimwita. Shehna baada ya kumuona Mustafa amehama kimawazo, alimuuliza tena swali lake la awali. “Mustafa unakumbuka? Au umesahau maana akili yako ina ubongo wa samaki.” “Nakumbuka.” “Uliiba hela hukuiba?” “Niliiba.” “Unajua kwa nini ulibakia kazini?” “Sijui.” “Hukujiuliza uliporudishwa kazini wakati ukijua umefanya makosa?” “Kwa kweli nilipitiwa kwa hilo.” “Mustafa wewe ni mwanadamu gani usiyejiuliza unakwenda kama mnyama?” “Hata sijui nikuambie nini ili unielewe.” “Inaoneka hata ukipewa kitu hujui kusema asante.” “Shehna ukisema hivyo utanionea, kwa vile mazingira yake yalikuwa kama muujiza au kitu cha ndotoni. Hata wewe baada ya kunifanyia ulitakiwa kujitokeza na kunieleza ili nijue kwa kumshukuru.” “Basi elewa yote hayo niliyafanya kwa ajili yako, kama nilivyokueleza nilipata safari ya ghafla, pia nilitaka kujitokeza muda muafaka kama huu.” “Ulifanyaje?” “Leo siyo siku yake muhimu ni hili langu, kwa nini hili langu dogo hutaki kunisaidia hujiulizi kuna wanaume wangapi lakini nimekupenda wewe?” Shehna alimuuliza huku machozi yakimtoka na kuyafanya macho yake kuwa mekundu na kuongeza uzuri wake kama njiwa manga. “Basi nitajitahidi kufanya unavyotaka japokuwa unanipa mtihani mzito.” “Si mtihani kama unavyoona, hebu jaribu leo utaniambia fanya yote niliyokuelekeza kama mkeo atajua basi mimi navunja mapenzi na wewe.” “Shehna sitaki kukupoteza,” Mustafa alichangwanywa na uzuri wa Shehna. “Basi fanya hivyo.” “Nitafanya kwa ajili nakupenda.” Shehna alifurahi na kwenda kumkumbatia Mustafa na kumpiga mabusu.
“Katika siku uliyonifurahisha leo imezidi siku zote, Mustafa ukizaa na mimi nitakupa zawadi kubwa ambayo hukuwahi kuiota maishani mwako.” “Nitashukuru.” “Kingine ulichonifurahisha kutengeneza uongo kwa mkeo juu yangu, imenifanya nizidi kukupenda.” “Lazima nifanye hivyo wewe ni mtu muhimu sana kwangu.” “Basi acha nikuache uendelee na kazi tutaonana usiku.”
“Hakuna tatizo.” Shehna aliaga na kuondoka na kumuacha Mustafa akiendelea na kazi, baada ya muda Mustafa alitoka kufuata kitu kwenye gari. Alipofika mapokezi alishangaa kukuta rafiki yake kipenzi James akimsubiri. “Ooh! James umefika zamani?” “Kama nusu saa nimeambiwa una mgeni.” “Mbona ametoka muda mrefu.” “Bosi ametoka kapitia wapi?” Sara aliuliza. “Jamani si hapa au ulipitiwa na usingizi?” “Hatujamuona mtu, mgeni mwenyewe labda jini?” Sara alisema jina ambalo siku zote lilikaa mdomoni kwake na kumchefua sana Shehna na kupanga kumkomesha na tabia yake ya kumwita jini. Alipanga usiku kabla ya kwenda kwa Mustafa aanzie kwa Sara ili kumkomesha aachane na kufuatilia mambo yake. “Sara sitaki tena kusikia ukitamka jina hilo, siku hizi umenizoea sana eti eeh? Unasema lolote mdomoni mwako,” Mustafa alimfokea Sara ilikuwa ni mara ya kwanza kukasirika toka aanze naye kazi miaka saba iliyopita. “Samahani sana bosi,” Sara alishtuka huku woga ukimtawala. “Katika siku uliyoniudhi leo umeniudhi sana, una bahati nina mgeni ningekufukuza kazi sasa hivi,” Mustafa alisema kwa hasira mpaka povu likamtoka mdomoni. “Bosi nisamehe, nilisema kwa utani sikujua kama nitakuudhi kiasi hiki,” Sara alijitetea. “Nitamalizana na wewe baadaye ngoja nizungumze kwanza na mgeni wangu.” “Kwani tatizo nini mpaka ukwazike hivyo?” James aliuliza. “James, tuzungumze yetu huyu nitamalizana naye.” James ilibidi anyamaze kwa vile hakujua chanzo cha Mustafa kukasirika vile kilitokana na nini, siku zote alimjua ni mkimya na mpole. Waliingia ofisini huku Mustafa akiwa bado ana hasira, kabla ya kuzungumza aliinama kwa muda kuonesha Sara amemuudhi sana. “Kwani best kipi kimekukwaza hivyo?” “U…u…u na..,” Musfata alinyamaza baada ya simu yake kuita, alipoangalia aliiona inatoka kwa Shehna aliipokea. “Haloo.” “Mustafa.”
“Naam.” “Mbona kama haupo sawa?” “Kwa nini?” “Sauti yako inajieleza.” “Si huyu mshenzi leo atanitambua namfukuza kazi.” “Kwa nini?” “Sikufurahia alivyokuita.” “Ananiitaje?” Shehna alijifanya hajui kitu. “Eti anakufananisha na jini.” “Hapana mpenzi usimfukuze kazi.” “Kwa nini?” “Ameropoka kwa bahati mbaya, sitaki mimi kuwa na wewe tuongeze maadui.” “Kwa hiyo?” “Mpe onyo tu, hawezi kurudia.” “Ana bahati bila wewe ningemfukuza kazi sasa hivi.” “Msamehe kuanzia sasa fungua moyo wako zungumza na mgeni kwa uchangamfu.” “Sawa nitafanya hivyo.” “Naomba ucheke kidogo basi,” Shehna alisema kwa sauti tamu iliyofanya Mustafa acheke. “Haya mpenzi wangu kazi njema.” “Asante nawe siku njema.” Wakati huo Sara alikuwa kwenye hali mbaya kwa kujua siku ile ndiyo ya kufukuzwa, kazi ilimshinda, mapigo ya moyo yalimwenda mbio. Alijiinamia kwenye meza huku mkono mmoja ukiwa kifuani kuzuia mapigo ya moyo yaliyokuwa yakienda kwa kasi. Mustafa baada ya kuzungumza na mgeni wake alitoka kumsindikiza, alishangaa kumkuta Sara akiwa amejiinamia huku akilia kilio cha kwikwi. “Sara una nini?” “Sina kitu, nitafanya nini nawe hutaki kunisamehe?” “Yale yameisha ila siku nyingine kuwa makini na kauli zako kwa wageni wangu hasa Shehna.” “A…a…sante bosi sirudii tena,” Sara alitaka kumshika miguu, lakini Mustafa alimuwahi kumshika na kumnyanyua juu.
Majira ya usiku Mustafa alikumbuka maelekezo aliyopewa na Shehna, alimuacha mkewe atangulie kitandani na yeye kubaki sebuleni akijifanya kuwa bize na lap top yake. Mkewe alimshangaa mumewe siku ile kuwa bize vile wakati alimwambia hawezi kufanya kazi za ofisini akishafika nyumbani. Baada ya kumsubiri mumewe kitandani kwa hamu kubwa, alishangaa kuona haji. Alitoka hadi sebuleni na kumkuta akijifanya yupo bize la Laptop yake. “Mume wangu imeanza lini muda wa kulala uanze kazi?” “Kuna kazi nilitakiwa lazima niifanye baada ya kufika, lakini nilisahau siwezi kulala bila kuifanya ili asubuhi nikifika kazini nifanye kazi nyingine,” Mustafa alitengeneza uongo. “Lakini si ni wewe uliyesema baada ya kazi ni nafasi yangu?” Husna alimuuliza mumewe huku amemkazia macho. “Ni kweli mke wangu, lakini hii imetokea dharura.” “Mmh! Sawa, sasa mimi nina hamu na wewe itakuwaje?” Kauli ile ilimchanganya sana Mustafa na kujiuliza itakuwaje kama mkewe atatangulia kukutana naye kimwili kabla ya Shehna, wakati alielezwa kukutana na mkewe mpaka mwezi upite. Alipata wazo la kumwambia asubiri ili avute muda wa kumfanya mkewe apitiwe na usingizi. “Mke wangu hebu nivumilie kwa muda huu.” “Mmh! Sawa lakini kumbuka nilijiandaa leo kwa ajili yako.” “Najua mke wangu, kuwa na subra namalizia nakuja sasa hivi.” “Basi na mimi nitakaa hapa nikusubiri mpaka akimaliza tutakale,” Husna alisema huku akikaa kwenye kochi. “Mke wangu imeanza lini kulindana kama kibaka na polisi?” “Yaani leo sijijui, natamani tukae pamoja mpaka umalize kufanya kazi zako, kitanda leo nimekiona kichungu bila wewe mume wangu.” “Mmh! Sawa,” Mustafa alikubali kwa shingo upande. Mkewe alijilaza kwenye kochi na kutazama mumewe aliyekuwa akijifanya yupo bize huku kichwa kikimuwanga kutokana mkewe kuonekana kama anajua nini kinatakiwa kufanyika. Muda ulikatika bila mkewe kuonesha dalili za kulala, alijiuliza atafanyaje ili mkewe alale na Shehna aje ndani. Alipoangalia saa ya ukutani ndiyo ulikuwa saa sita kasoro za usiku,alijikuta alikosa raha kabisa. Alijikuta akitamani kulala kwani na yeye kichwa kilianza kuwa kizito kwa usingizi. Wakati akiwaka yale mkewe macho yalikuwa makavu hakuonesha dalili zozote za kulala huku macho yakiwa kwenye Runinga.
Alijifanya kutoka nje kumtazama Shehna kama atakuja ili amuwahi na kumueleza kuwa siku ile hali ilikuwa mbaya wafanye kesho japokuwa alijua atakuwa amemuharibia dozi. Aliamini zoezi alilolitaka Shehna alilikuwa ngumu kutekelezeka hasa kulifanyia nyumbani kwake chumbani kwake na kitandani anapolala na mkewe na mkewe akiwepo kilikuwa kitu kisichowezekana kwa akili ya kawaida. Aliifunga Laptop yake na kunyanyuka huku akijinyoosha kidogo na kumfanya mkewe aseme. “Dah! Afadhali umemaliza yaani leo hata sijielewi jinsi nilivyo na hamu na wewe imekuwa kama siku ya fungate,” Husna alisema huku akijiweka vizuri kwenye kochi ili anyanyuke. “Nakuja,” Mustafa alisema huku akielekea nje. “Usiku wote huu unakwenda nje kufanya nini?” “Mke wangu maswali gani hayo?” Mustafa alisema kwa ukali kidogo. “Mume wangu kukuuliza ni ubaya gani mimi mkeo nina haki ya kukuuliza chochote.” “Nakuja,” Mustafa alisema huku akifungua mlango na kutoka nje na kumuacha mkewe akirudi kujilaza kwenye kochi kumsubiri mumewe. Mustafa siku ile alimshangaa mkewe kuwa vile na kujiuliza labda amejua nini kinaendelea usiku ule. Alitoka nje kwa kuamini lazima kwa muda ule Shehna atakuwa amefika nje. Wakati akiwaza hayo Shehna alikuwa amefika muda mrefu, aliyaona yote yaliyokuwa yakitendeka na jinsi Mustafa alivyokuwa akiteseka kwa jinsi mkewe alivyogoma kwenda kulala na jinsi ya kuyashinda masharti ya kukutana kimwili na mkewe ambaye siku ile alionesha kumtaka sana. Alijifikiria jinsi ya kumsaidia Mustafa kwa kumfanya mkewe alale kwa hiyari yake bila kulazimishwa. Shehna alifurahi baada ya kumuona Mustafa akitoka nje alijua ametoka kumtafuta ili kumpa hali halisi ya ndani. Alimuacha atoke nje kisha alimsogelea Husna mke wa Mustafa na kumpuliza usoni na kukaa pembeni. Husna alijikuta akisikia usingizi mkali bila kujielewa usingizi mzito ulimpitia. Mustafa baada ya kumtafuta Shehna kwa kuzunguka nyumba bila kumuona, alisogea mpaka mbele ya nyumba labda yupo barabarani lakini hakumuona. Baada ya kutomuona alisimama kwa muda kujiuliza atafanyaje ikiwa muda umekwenda na lazima akapande kitandani na ilikuwa lazima ampe mkewe haki yake ya ndoa kwa vile hakuwa na sababu ya kumnyima.
Aliamua kurudi ndani akiwa amejikatia tamaa ya kutimiza masharti ya Shehna, alipofika sebuleni alishangaa kukuta hakuna mtu. Alijua labda amekwenda msalani, alibeba Laptop yake na kuingia chumbani, alishangaa kumkuta mkewe chumbani amelala hajitambui. Alishtuka usingizi wa dakika tano kumkuta mkewe amelala kama mtu aliyelala saa mbili zilizopita wakati anatoka alikuwa macho makavu. Hakuamini, aliona kama anamtania au alifanya vile ili kumtega. Alisogelea kitandani na kumwita mkewe kwa sauti lakini alionesha ana usingizi mwingi hata alivyomgeuza alionesha kweli amelala. Hakuamini zoezi lake kufanikiwa akiwa amekata tamaa kwa vile naye alikuwa na usingizi. Alichukua chupa ya manukato aliyopewa na Shehna, alikwenda bafuni kuoga na kujipaka nanukato yale. Kabla ya kupanda kitandani alihakikisha mlango amerudisha bila kufungwa, kisha alipanda kitandani na chupa yake ya manukato. Kwa vile mkewe alikuwa ameisha lala alimsogeza ukutani na yeye kulala katikati. Alifuata maelekezo ya kutolala na nguo ya ndani, alitoa nguo zote na kupanda kitandani akiwa mtupu. Alichukua mafuta kidogo na kumpaka kichwani mkewe ambaye alikuwa katikati ya usingizi mzito. Naye alijilaza pembeni ya mkewe, haikuchukua muda usingizi ulimpitia. Katikati ya usiku aliamshwa kwa kubembelezwa, alipofumbua macho alimuona Shehna amesimama pembeni ya kitanda akiwa amejifunga mtandio mwepesi ulioonesha mwili wake mzuri uliokuwa hauna kitu ndani. “Shehna,” Mustafa alishtuka na kutaka kuongea kwa sauti. “Shiiii!” Shehna alimkataza asitoe sauti. Aliondoa mtandio aliojifunga na kuutupa pembeni kisha alipanda kitandani na kujilaza pembeni kwa Mustafa ambaye alikuwa akitetemeka huku jasho likimtoka, alijiuliza mkewe akiamka na kumkuta mwaname juu ya kitanda chake atamwambia nini. Hali ile Shehna aliiona. “Mustafa,” alimwita kwa sauti ya chini. “Mmh!” Mustafa alishindwa kutoa sauti. ‘Wasiwasi wako nini?” “Shehna nakupenda lakini unanitia kwenye matatizo.” “Naomba uniamini hakuna kitu chochote kitakachotokea, mkeo hawezi kuamka mpaka kesho asubuhi.” “Umejuaje?”
“Niamini.” “Sawa,” Mustafa alikubali kumridhisha Shehna lakini alitetemeka mpaka utumbo. Shehna alipomuona Mustafa hayupo naye kimawazo alianza kumpapasa na kulifanya joto lisambae mwili mzima na kujikuta akijisahau kama yupo kwenye kitanda chake na mwisho kuzama kwenye penzi zito ambalo hakuwahi kulipata katika maisha yake. Shehna pamoja na kuwa mwanamke mrembo pia mapenzi aliyajua kwa kiwango cha hali ya juu. Kama kawaida, Shehna baada ya kupata dozi yake ya mara tatu, aliondoka na kumwacha Mustafa kwenye usingizi mzito. *** Sara baada ya kuponea tundu la sindano kufukuzwa kazi alijikuta akimchukia Shehna na kumuona ni kiumbe mbaya katika maisha yake. Kabla ya kuja kwake alikuwa akielewana na bosi wake ambaye siku zote alikuwa mpole na mwenye hekima, hakuwahi kumfokea hata siku moja. Lakini toka alipokuja yule mwanamke imekuwa kinyume kabisa. Alijikuta akikumbuka matukio ya kushangaza toka siku ya kwanza alipoitwa ofisini na Bosi wake kuulizia kama kuna mgeni ameingia ofisini. Tokea hapo amejikuta akikutana na matukio ya ajabu ya kupanda teksi na kujikuta nyumbani na lingine la kulala ofisini kitu ambacho siku za nyuma hakikuwahi kumtokea. Na tukio la siku ile la kutaka kufukuzwa kazi bila kosa lilizidi kumfanya amchukie sana. Siku ile aliporudi nyumbani alijikuta mwenye hasira nyingi, kila aliyemuona alijua siku ile hayupo vizuri. Shoga yake wa karibu Happy baada ya kufika nyumbani alimfuata chumbani kumsalimia. Alishangaa kumkuta amekaa kwenye kochi bila kuvua viatu na mkoba wake mkononi huku machozi yakimtoka. “Shoga vipi mbona hivyo?” Sara hakumjibu, alichukua kitambaa na kujifuta machozi, hali ile ilimfanya shoga yake adhanie labda amefiwa.
“Shoga una msiba?” Alitikisa kichwa kukataa. “Sasa nini?” “Naomba kwanza maji,” Sara alisema kwa sauti ya kukwaruza. Shoga yake alikwenda kwenye friji na kuchukua maji kwenye jagi na kumuwekea kwenye glasi. Baada ya kunywa maji kwa mkupuo yaliyopunguza hasira, alishusha pumzi ndefu na kusema. “Shoga kuna tukio moja leo linimeniudhi sana.” “Tukio gani?” Sara alimweleza kilichomtokea na kutaka kufukuzwa kazi pamoja na matukio yote yaliyomtokea. Shoga yake alishtuka sana. “Sara unayosema ni kweli?” “Kweli kabisa, matukio ya yule mwanamke nina wasiwasi nayo, huenda yule ni jini si mwanamke wa kawaida.” “Mmh! Huenda kweli, lakini si nasikia majini wana kwato kwa chini, uliziona?” “Yule ni mwanadamu wa kawaida lakini muonekano wake si wa kawaida hata manukato yake sijawahi kuyasikia sehemu yoyote!” “Mmh! Mungu wangu kama ni jini unafikiri itakuwaje?” “Dawa yake naijua, nakuapia kama ni jini atakimbia mwenyewe kuna vitu nitakwenda navyo kazini.” “Vitu gani?” “Mifupa ya nguruwe au nyama yake, kama ni jini hawezi kuja tena ofisini na nitamwambia bosi kama yule si mtu ni jini.” “Basi fanya hivyo.” “Tena shoga nimejikuta nina hamu ya kiti moto, nakwenda kumchukua ili nimlie nyumbani.” “Unachukua kiasi gani?” “Nusu na ndizi nne nikipiga na bia zangu mbili nalala vizuri.” “Shoga nunua kilo moja maana hata mimi nina hamu nayo sana.” “Poa nitakuchulia na ndizi mbili.” “Hakuna tatizo.” “Yaani kidogo kuzungumza na wewe hasira zimepungua, nakuapia nitamkomesha.” “Kwa kufanya hivyo, utamuweza.” Sara alijitapa huku akivua viatu kisha alibadili nguo na kuelekea bafuni kuoga. Alipanga akitoka kuoga aende kwenye baa ya Macha iliyokuwa ikiuza kitimoto ili akatimize adhima yake ili ajue kama Shehna ni jini au mtu. Alioga harakaharaka, alipotoka kuoga alijifuta maji na kujifunga upande wa khanga moja chini na nyingine alijitanda kwa juu. Alichukua noti ya elfu kumi na kutoka kuelekea kwenye baa hiyo. *** Mustafa aliposhtuka usingizini alijishangaa kujikuta kitandani na mkewe lakini Shehna hakuwepo. Alipoangalia saa ya ukutani ilimuonesha ni saa kumi na moja kasoro alfajiri. Wasiwasi wake ulikuwa labda ameamka na kwenda bafuni kuoga kabla ya kuondoka. Aliamka haraka kitandani huku akimtazama mkewe asiamke muda ule kabla hajajua Shehna yupo wapi. Alikwenda hadi bafuni lakini hakumkuta mtu akatazama msalani pia hakukuwa na mtu. Alikwenda mlangoni na kukuta umerudishiwa, alijua ameshatoka. Kwa vile muda ulikuwa bado alirudi kitandani, alipojilaza usingizi ulimchukua mpaka aliposhtuliwa na mkewe kukiwa kumekucha. Alipofumbua macho kulikuwa kumekucha alinyanyuka kuelekea bafuni kuoga, alipotoka kuoga alikuta mkewe ameshamuandalia kifungua kinywa. Baada ya kufungua kinywa, alimshukuru mkewe kwa kumbusu shavuni na kutaka kuelekea nje lakini mkewe alikumbuka kitu na kumuuliza. “Mume wangu umefikia wapi?” “Kuhusu nini?” “Kuhusu Shehna, bado hujawasiliana naye?” “Alinipigia na kumueleza, alisema kiburi kimejaa na dharau ndicho chanzo cha kuharibikiwa mambo yako ameapa kama utaendelea na tabia zako chafu utakufa bila mtoto.” “Muongo amejuaje mimi nina tabia chafu?” Alimweleza kila alichoelezwa na Shehna kilichosababisha ashindwe kushika ujauzito, Husna alichanganyikiwa siri zake zote kuwa nje na kujikuta akitaka kumjua Shehna ni nani, alijiuliza ni kiumbe gani anayejua mambo yake ya siri kiundani ambayo hakuna mtu mwingine aliyekuwa akiyajua. Akiwa bado yupo katika dimbwi la mawazo, Mustafa alimuuliza. “Lipi la uongo katika niliyokuambia?” “Mmh! Shehna kiboko, kayajuaje haya?” “Si kujua kwa nini anajua mambo yako, la muhimu kujua kwa nini natumia fedha na nguvu wakati mwenzangu huna ushirikiano?” Mustafa alizitoa hasira zake kwa mkewe baada ya kuonesha hakuwa na ushirikiano katika kutafuta mtoto. “La..lakini mume wangu unamuamini vipi Shehna, yule ni mgombanishi tu,” Husna alijitetea. Mara simu ya Mustafa iliita alipoangalia aliiona inatoka kwa Shehna, aliipokea. “Asalam aleykum.” “Waleykum Salamu, mmeamkaje?” “Salama.” “Mbona hujatoka kwenda kazini?” “Si huyu mshe…”
Weee! Mustafa unataka kusema nini, usithubutu tena kumwita mkeo mshenzi, tatizo nini?” sauti ya Shehna ilikuwa kali kidogo iliyomkata kauli. “Si..si..,” aliingiwa na kigugumizi. “Mustafa nakuamini kwa nini unataka kuharibu mambo, tatizo la mkeo umeishalijua ulitakiwa uzungumze naye kwa sauti ya upole kuliko kuzungumza kama mhuni.” “Samahani nilipandwa na jazba.” “Mpe simu mkeo.”
Mustafa alimpa simu mkewe aliyekuwa akitokwa na machozi huku akiamini ndoa yake imekalia kuti kavu baada ya siri zake kuwa nje kutokana na kiburi chake cha kutofuata masharti ya kupata mtoto wakati mumewe alikuwa amepoteza fedha nyingi. Alipokea simu katika sauti ya kilio, huku akiwa na donge moyoni baada ya kujua yule ndiye mbaya wake hata akiachika yule ndiye mchawi wake. “Haloo.” “Haloo, asalam aleiykhum.” “Waleiykhum msaalam.” “Vipi mbona unalia?” “Ha..ha..pana.” “Ni hivi yaliyopita yamepita, kama kweli unataka mtoto acha mambo ya kijinga, kuchanganya dawa za uzazi utakuwa mgumba. Wa kulia ningekuwa mimi kwa vile gharama ya dawa niliyowapa ni kubwa zaidi ya kununua gari la kifahari, lakini mwisho wa yote ukafanya kiburi chako ambacho kuna siku kutakuharibia maisha yako. “Sasa nasema hivi kuanzia leo nitakupa dawa ya kuoga na kujipaka kwa mwezi mzima bila kukutana na mumeo. Baada ya mwezi ruksa kukutana na mumeo, sasa upo tayari nikuletee hiyo dawa?” “Ndi..ndiyo.” “Usiseme kutufurahisha, litoke moyoni lisije la kutokea ukasema sijakuambia, najua moyoni mwako unaniona adui. Lakini napigania ndoa yako la sivyo siku zako zilikuwa zikihesabika… Unazungumza vizuri na familia ya mumeo kama zamani?” “Hapana.” “Unajua kwa nini?” “Sababu ya kuchelewa kupata mtoto.” “Sasa kwa nini unafanya mchezo wa kitoto.” “Hata sijui, labda nimerogwa.” “Hujarogwa na mtu bali kiburi chako, kama utaendelea nacho nyumba utaiacha bado unaipenda. Wa kukutoa ndani ni ndugu wa mumeo, nakuibia siri kuna msichana ametafutwa kuja kukutoa ndani, hivyo sasa kazi kwako kufuata masharti ili ubakie katika nyumba yako au vinginevyo.” “Sasa kwa mwezi huo hawatakuja kunitoa ndani?” Husna aliingiwa na uoga. “Hawawezi, we nisikilize mimi kila kitu kitakwenda vizuri.” “Ninakusikiliza dada yangu.” “Ukifanya hivyo utanifurahisha, nakuahidi kukupa zawadi kubwa sana maishani kwako.” CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Nakuahidi dada yangu kukufurahisha, nitayafanya yote utakayoniambia.” “Utakuwa umefanya jambo zuri, haya mpe simu mumeo.” Husna alichukua siku na kumpa mumewe aliyekuwa bado amesimama koti na mkoba wake vikiwa mkononi. Mustafa aliipokea simu. “Haloo.” “Nina imani kila kitu tumemaliza, sasa sitaki ufikie alipotaka kufikia kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa.” “Nashukuru, kama amekuelewa mi sina tatizo.” “Haya baba wahi kazini.” “Nashukuru.” Mustafa alikata simu na kumgeukia mkewe na kumweleza. “Nina imani mmemalizana naye.” “Ndiyo mume wangu, nisamehe kwa yote.” “Yote yameisha tumefungua ukurasa upya.” “Asante mume wangu.” Walikumbatiana kisha Husna alimpokea mumewe alivyobeba na kumsindikiza mpaka kwenye gari. Kabla ya kuingia walikumbatiana na kubusiana kisha Mustafa aliingia ndani ya gari na kuondoka kuwahi kazini. Alikwenda moja kwa moja mpaka ofisini, alishangaa kuikuta ofisi haijafunguliwa, kwa vile tangu siku Sara alipochelewa ofisini ufunguo mmoja alikuwa akiondoka nao mwenyewe. Alifungua na kuingia ndani ambako alikuta ofisi imejaa vumbi na uchafu kutokana na kutofanyiwa usafi.
Alijiuliza Sara amepatwa na nini mpaka muda ule hajafika ofisini, aliingia ofisini na kuweka vitu vyake kisha alitoa simu na kumpigia, simu iliyopokelewa na mwanamke upande wa pili. “Haloo.” “Haloo, nazungumza na nani?” “Maria.” “Sara yupo wapi?” “Alitoka jana kufuata chakula lakini ajabu mpaka kunakucha hatujamuona.” “Sasa kaenda wapi?” “Hata sisi tunashangaa kibaya hata simu hakuchukua.” “Mmh! Sawa.”
Mustafa alikata simu na kujikuta akichoka na kukaa kwenye kochi lake huku akijawa na mawazo ya kujiuliza Sara atakuwa amekwenda wapi. Akiwa katikati ya mawazo alisikia mlango wa ofisi ukigongwa alijua Sara ndiyo anafika. “Ingia,” alisema kwa sauti. Mlango ulifunguliwa na kutanguliwa na harufu nzuri ya manukato aliyoyazoea ya Shehna, mara aliingia shehna katika vazi la gauni refu la kitambaa cha kitenge na kiremba chake alionekana mwanamke mzuri kuliko siku zilizopita. Mustafa kuzungumza alishindwa alibaki kamtumbulia macho kama siku yake ya kwanza kumuona. “Mustafa kushangaa gani huko kama ndiyo leo siku yako ya kwanza kuniona?” alimuuliza huku akimsogelea alipokuwa amekaa. “Shehna lazima nimsifu Mungu kwa utundu aliofanya kukuumba, Shehna wewe ni mwanamke mzuri wa wazuri, uzuri wako kama nyoka anayejibadili mwili wake, kila siku uzuri wako unaongezeka, wa leo unashinda wa jana pia naamini wa kesho utauzidi wa leo.” “Mmh! Kawaida sema bado hutatuliza macho kwangu unaniangalia kwa wasiwasi, kama ungekuwa hunitazami kwa wasiwasi wala usingenishangaa. Nilichokibadili asubuhi hii ni nguo tu, mimi ni yuleyule wa jana wa leo na kesho vilevile.” “Wewe unaweza kusema hivyo, najuta kuchelewa kukujua mapema.” “Ulinifahamu mapema lakini hukunitilia maanani, nilikuja kwako kila wakati lakini labda uliniona mwanamke malaya.” “Ha..ha..pana, sijakufikiria hivyo!” “Sasa tatizo lako nini?” “Nina wasiwasi wenye fedha zaidi yangu wataninyang’anya.” “Kwani nipo wapi siku zote wasikunyang’anye wakunyanganye leo?” Shehna alimuuliza huku akimuangalia jicho tata lililozidi kumchanganya Mustafa na kutamani heri angekuwa mkewe wa ndoa. Lakini bado aliona maisha ya Shehna asingeyaweza kwani kila alipokutana naye alikuwa na nguo na vito vya thamani ambavyo aliamini hawezi kuvinunua. Shehna aligundua alichokuwa akikiwaza Mustafa baada ya kukaa kimya kwa muda. Alimshtua kwa kumwita jina lake. “Mustafa.” “Naam.” CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Kwa nini unajibebesha mawazo mazito ambayo sivyo unavyonifikiria?” “Umejuaje?’ “Si kujuaje, bali nataka kukuthibitishia maisha yangu na wewe ni tofauti unavyonifikiria, kila kitu juu ya mustakabali wetu niachie mimi.” “Sawa nimekuelewa.” “Na..na mbona ofisi chafu?” “Nashangaa mpaka muda huu msaidizi wangu sijamuona, ha..halafu nasikia toka jana usiku hajarudi.” Kauli ile ilimfanya Shehna acheke kicheko cha umbea kilichomfanya Mustafa ashtuke na kuhoji. “Vipi mbona unacheka kama unajua kinachoendelea.” “Walaa, nimecheka tu.” “Yaani hapa nimechanganyikiwa ngoja nimwite mlinzi ufanye usafi.” “Walaa, kazi hiyo nitaifanya miye.” “Hapana Shehna, acha ataifanya mlinzi.” “Kwani mimi kufanya kuna nini?” “Utajichafua bure wakati watu wa kuifanya kazi hii wapo.” “Basi leo nitaifanya mimi, naomba unipishe mara moja.” “Sawa, basi nipo nje kwa mlinzi.” “Hakuna tatizo.” Mustafa alitoka nje na kumuacha Shehna ofisini, kabla ya kufanya kitu aliangua kicheko cha mfululizo kufurahia alichomfanyia Sara mwanamke aliyemuona asidi aliyetaka kushindana naye. Kisha alijishika kwenye paji la uso na kutulia kwa muda, mara vijakazi na watwana toka ujinini walipiga magoti mbele yake na kumuuliza. “Mwana wa Mfalme wa jini la bahari ya dhahabu una shida gani unayotaka tukufanyie?” “Nataka baada ya muda mfupi ofisi yote uwe safi kuliko siku zote.” “Hewala mwana wa mfalme.” Vijakazi na watwana waliingia katika kazi ya usafi iliyochukua dakika tano kila kitu kilikuwa safi ndani. Kilibadilishwa kila kitu na kuwekwa pazia nzuri la halili na kuifanya ofisi ipendeze mara dufu. Baada ya kufanya usafi walipiga magoti mbele ya Shehna na kusema…. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Mtukufu mwana wa Mfalme wa jini la bahari ya dhahabu tumemaliza kazi, kama kuna kasoro tupo tayari kwa adhabu yoyote kutoka kwako.”
“Hapana nawamini.” “Asante mwana wa mfalme.” Shehna hakuwa na shida ya kukagua kwa kuamini majini walikuwa wakijua usafi kuliko mwanadamu. “Nimefurahi kwa yenu nzuri, mnaweza kuondoka.” Kufumba na kufumbua vijakazi na watwana walitoweka na kumuacha Shehna alifurahia hali nzuri ya kupendeza ya ofisi. Alitoka nje na kumwita Mustafa aliyekuwa akizungumza na mlinzi. Alikwenda ndani na kuishangaa ofisi ilivyopendeza tofauti na siku zote. “Duh! Kazi hii imeifanya peke yako?” “Umemuona nani akinisaidia?” “Hongera sana.” “Asante, ila kama Sara hatatokea na kesho funguo iache mlangoni, nitakuwa nawahi mapema kufanya usafi kabla hujafika mpaka atakaporudi kazini .” “Nitafanya hivyo.” “Mustafa mimi si mkaaji ilikuja kukushukuru wa mapenzi yako matamu, hakika leo nimefaidi usichana wangu kwa kupata penzi lililokamilika. Nakuahidi baada ya kushika ujauzito nitakupatia zawadi kubwa sana.” “Wala usihofu, lakini nina wasiwasi wa kuharibu masharti yako.” “Wala usiwe na wasiwasi, asubuhi umenilaisishia kufanya mambo yetu bila mkeo kukusumbua. La muhimu kufanya yote kama niliyokuelekeza.” “Nitafanya hivyo.” “Basi nikuache uendelee na kazi.” “Nashukuru.” Walikumbatiana kisha Shehna aliondoka na kumuacha Mustafa alimsindiza kwa macho. ***
Wiki nzima ilikatika bila kuonekana kwa Sara huku Shehna akiendelea kufanya usafi kila siku na kuifanya ofisi izidi kupendeza. Kwa hali ile ilifikia hatua ya Mustafa kuomba Sara isirudi tena kutokana na usafi uliokuwa ukifanywa na Shehna uliifanya ofisi yake isifikiwe kwa kila aliyeingia na kutaka kupatiwa mtu mwenye uwezo wa kufanya usafi kama wa ofisini kwake. Wakati wote huo kila siku Shehna alikwenda nyumbani kwa Mustafa na kufanya naye mapenzi kitandani kwake huku mkewe akiwa amepitiwa usingizi. Siku zote alifuata masharti aliyopewa kuyafanya kabla ya kulala. Zoezi kubwa kwake lilikuwa kumpaka mafuta mkewe ambayo humfanya alale mpaka asubuhi bila kugeuka na kuacha wafanye mambo yao bila yeye kujua kinachoendelea. Mustafa alifanya vitu vyake siku zote kwa umakini mkubwa kwa vile mkewe hakuweza kukutana naye tena kimwili baada ya kuelezwa na Shehna ili aweze kupata mtoto huku akiendelea kutumia dawa alizopewa. Hata kulala sehemu ya ukutani hakulazimishwa kwa vile lilikuwa moja ya masharti ya dawa. Siku zote alifanya kama alivyoelekezwa, lakini siku moja alirudi nyumbani akiwa amechoka sana na kusahau kumpaka mafuta mkewe kwa kuamini aliisha mpaka. Usiku kama kawaida Shehna aliingia ndani na kunyanyua Mustafa na kwenda naye bafuni kuoga baada ya kuoga alirudi kitandani na kuanza kuandaana kisha waliingia kwenye tendo. Hatua ya awali iliisha kila mmoja alifurahia penzi la mwenzake kisha walipumzika kwa muda ili kujiandaa kwa hatua nyingine. Shehna kama kawaida alimpa Mustafa maji ya kunywa yaliyomrudishia nguvu na kurudi tena bafuni kuoga na kuingia hatua ya pili. Mapenzi yalipopamba moto Shehna aligugumia kimapenzi kwa kuusifia uwezo wa Mustafa kimapenzi. Kwa vile mke wa Mustafa hakupakwa mafuta ya kumlaza, sauti ya kulalamika kimapenzi ilimshtuka usingizini.
Alipoangalia pembeni yake alimuona mumewe akifanya mapenzi na mwanamke mzuri wa Kiarabu, wote walikuwa katikati ya tendo. Alitulia kwa muda na kujiuliza alichokiona ni kweli au anaota. Alikaa kitako na kupekecha macho yake kama kweli amelala au yupo macho, akili yake ilimweleza hakulala bali yupo macho na anachokiona ni kitu cha kweli wala si cha ndotoni. Alijiuliza yule ni mwanamke gani asiye na woga aliyeingia ndani mwake bila hofu, alijiuliza tabia ile ya mumewe kuingia na mwanamke ndani na kufanya naye mapenzi kitanda wanacholala bila woga, imeanza lini? Wakati akiwaza vile, Shehna alishtuka baada ya akili yake kutambua mke wa Mustafa ameamka na kuangalia kilichokuwa kikiendelea pembeni yake. Alijibadili ghafla na kutoweka kitandani na kumuacha Mustafa akilalamika kwa kumwita jina lake. “Shehna mpenzi unaenda wapi?” Shehna hakujibu, alisogea pembeni ya mke wa Mustafa na kumpuliza usoni, usingizi mzito ulimchukua Husna na kurudi kitandani kulala. Baada ya kulala, Shehna alimuuliza Mustafa aliyekuwa hajui nini kilichokuwa kikiendelea. “Mustafa umefanya nini?” “Kuhusu nini mpenzi?” “Kwa nini hukumpaka mafuta mkeo?” “Nilimpaka.” “Muongo! Tutamwambia nini mkeo ikiwa ameona kila kitu?” “Kwani aliamka?” “Ameamka na ameona kila kitu.” “Mungu wangu!” Mustafa alishika mikono kichwani. “Basi mi naondoka na hutaniona tena katika maisha yako,” Shehna alisema kwa hasira huku akielekea alipoweka nguo zake. “Usifanye hivyo mpenzi, nakuhitaji kuliko kitu chochote, inawezekana uchovu ulisababisha nipitiwe. Naomba unisamehe sana.” “Mustafa nakupenda sana, lakini masharti yangu ya kuendelea kuwa na wewe yatakuwa magumu sana kuliko mwanzo na nina imani utayashindwa.” “Nakuahidi kuyatekeleza yote.” “Kweli?” “Kweli kabisa.” “Unajua nakupenda?” “Tena sana.” “Kesho mkeo lazima atakuuliza kuhusiana na alichokiona usiku huu kwa vile aliendelea na usingizi atataka ukweli kutoka kwako. Wewe kataa kwa vile hana uhakika kwa kile alichokiona kama ni kweli au ndoto.” “Sawa nitafanya hivyo.” “Kwa vile amelala tuendelee na dozi ya mwisho lakini kuanzia kesho tunabadili mfumo.” “Sawa mpenzi nipo radhi kwa lolote.” Walikwenda kuoga na kurudi kumalizia dozi ya mwisho kisha Shehna aliondoka na kumuacha Mustafa usingizini. *** Husna alikuwa wa kwanza kuamka mumewe alikuwa bado amelala, alimuangalia na kujikuta akivuta kumbukumbu ya usiku na kujiuliza alichokiona usiku kilikuwa kweli au ndoto kwa vile toka aolewe na Mustafa, hakuwahi kutokewa na tukio kama lile kwa sababu alimuamini sana mumewe kwa uaminifu wa ndoa yao kwa kipindi chote pamoja na matatizo yote, hakuwahi kumdharau wala kumsaliti. Kwa akili ya kawaida aliamini kabisa aliamka usiku na kukuta mumewe akifanya mapenzi na mwanamke wa kiarabu. Lakini kilichomshtua mbona ameamka asubuhi kutoka usingizini? Kila lililokuja mbele yake lilimchanganya, ili apate jibu la kitendawili chake aliamua kumuamsha mumewe. Baada ya kumtikisa kwa muda huku akimwita kwa jina lake, Mustafa alishtuka usingizini na kumgeukia mkewe. “Vipi?” alimuuliza huku akilazimisha macho kufumbuka. “Mume wangu hebu amka.” “Kuna nini?” “Si uamke,” Husna alisema kwa sauti kali kidogo. Mustafa aliamka na kukaa kitako ili amsikilize mkewe. “Mume wangu,” alianza kwa kumwita. “Naam.” “Kuna kitu kimetokea sijui ni kweli au ndoto.” “Kitu! Kitu gani?” Mustafa alijifanya kushtuka. “Kuna kitu nimekiona usiku, kimenichanganya sana.” “Kitu gani?” Mustafa alimuuliza huku akifikisha macho yake na kupiga miayo ya uchovu wa kulala. Husna alimweleza mumewe kila kitu alichokiona ambacho yeye aliamini haikuwa ndoto. Kwa vile alielezwa na Shehna kilichotokea na nini ajibu, alimwambia mkewe. “Kwa akili ya kawaida kitu hicho kinaweza kufanyika?” “Hata mi nashangaa, lakini nakumbuka niliamka na kukaa kabisa.”
“Baada ya kukaa nini kiliendelea?” “Sikumbuki zaidi ya kushtuka alfajiri na kujikuta nimelala.” “Sasa wasiwasi wako nini?” “Ndipo hapo ninapo changanyikiwa kilikuwa nini.” “Hebu achana na ndoto, hivi kweli nilete mwanamke ndani na kufanya naye mapenzi kitanda tunacholala, imeanza lini?” Mustafa alizidi kujifanya kumshangaa mkewe. “Hata mi namshangaa.” “Hebu achana na ndoto za kijinga.” “Basi samahani mume wangu kama nimekukwaza.” “Walaa, una haki ya kuniuliza chochote.” Wakiwa katikati ya mazungumzo simu ya Mustafa iliita, alipoangalia ilionesha inatokwa kwa Shehna. Aliipokea na kuzungumza naye. “Haloo.” “Haloo, asalam aleykum.” “Waleykum salam.” “Vipi mmeamkaje?” “Mmh! Salama.” “Kweli?” Shehna aliuliza. “Kweli.” “Mbona kama mkeo ana tatizo?” “Sijui ameota nini.” “Ameota nini?” Shehna alijifanya kushtuka. “Sijui ameniona eti mimi nina fa…fa..” “Hebu mpe mwenyewe azungumze, acha kung’ata maneno,” Shehna alimkata kauli Mustafa. Mustafa alimpa simu mkewe aliyekuwa bado amesimama pembeni ya kitanda. Husna aliipokea na kuzungumza. “Asalam aleykum.” “Waleykum salam, eti mpenzi kuna nini?” Shehna alimuuliza kwa sauti ya upole. Husna alimweleza kama alivyomweleza mumewe kilichotokea usiku. Baada ya kumsikia alisema: “Mpenzi hizo ni ndoto ambazo huvunja ndoa nyingi kwa vile mtu huota ukiwa macho na kuweza kuamini ni jambo la kweli. Hizo ni ndoto tu, lakini mumeo akirudi kazini atakupatia dawa ya kujipaka wakati wa kulala haitakutokea tena.” “Nitashukuru kwa kweli ilinishtua sana.” “Pole mpenzi.” “Asante dada yangu, jamani nina hamu ya kukuona tutaonana lini?” ” Utaniona tu usiwe na wasiwasi hata mimi nina hamu na wewe, unasema uliyemuota akifanya mapenzi na mumeo uliiona sura yake?” “Ndiyo.” “Kwa mfano akutokee mbele utamjua?” “Nitamjua nilimuona vizuri sana japo nilikuwa naota.” “Basi mpenzi nikimaliza mizunguko yangu nitakuja utanichoka mwenyewe.” “Walaa labda unichoke wewe.” “Basi mpenzi usiendekeze ndoto.” “Nimekuelewa.” Shehna alimalizia kuzungumza na Husna na kumalizia kuzungumza na Mustafa kisha alikata simu. Mazungumzo yake yalirudisha imani moyoni kwa Husna na kuamini aliyosema Shehna yalikuwa na ukweli mkubwa. Baada ya moyo wake kuamini ile ilikuwa ndoto, alimtayarishia mumewe maji ya kuoga na kifungua kinywa huku moyo wake ukiwa mweupe. Mustafa baada ya kufungua kinywa alimuaga mkewe na kuelekea kazini, kama kawaida alikuta ofisi imesafishwa. Akiwa ofisini Shehna alimtokea kabla hajaanza kazi na kuzungumza naye sakata la usiku. “Mustafa nilitaka kukulaumu lakini umenilahisishia kazi, yale mafuta niliyokupa kumpaka mkeo mpe ajipake mwenyewe. Hakikisha unamkumbusha kujipaka kabla hajalala, itatusaidia kumteka bila kujijua.” “Yaani nashukuru sana sijui bila wewe ingekuwaje?” “Ungekataa tu, lakini lazima angeuliza kwa watu na kutaka kuchimba na kuujua ukweli.” “Unafikiri angeujua ingekuaje?” “Mmh! Tungejua tifanyeje japo ingetusumbua kidogo.” “Nashukuru sana mpenzi umenisaidia.” “Basi nikuache ufanye kazi.” “Nashukuru.” Shehna aliaga na kuondoka na kumuacha Mustafa akijiandaa kuanza kazi ya siku ile.
Msichana mmoja alionekana amelala chini ya mti mkubwa pembeni ya barabara kuu ya kutoka Dodoma kwenda Mpwapwa akiwa amejifunga kipande kichafu cha khanga kwa chini na juu matiti yalikuwa wazi. Miguu ilikuwa pekupeku, ilijaa tope lililokauka na kujaa vumbi. Wasamaria wema waliopita njia ile waliamini yule ni mwendawazimu, lakini ilikuwa ajabu kwa eneo lile hakuna hata mmoja aliyekuwa akimfahamu. Toka watu walipomuona amelala chini ya mti, ilipita zaidi ya saa sita bila kugeuka kitu kilichowatisha na kufikiria labda amefariki. Walimsogelea na kumtikisa, alifumbua macho kuwatazama lakini alikuwa amechoka kwa njaa na uchovu. Walimchukua na kumpeleka kwenye makazi ya watu na kumpatia chakula baada ya kushiba, walimpatia maji ya kuoga na nguo. Alionekana ni mtu mwenye akili zake timamu wala si kichaa kama walivyomfikiria. Baada ya kutulia, walimuuliza maswali kutaka kujua ametoka wapi na amefikaje pale. “Unaitwa nani?” “Sara.” “Umetokea wapi?” “Dar es salaam.” “Umefikaje huku?” “Kwani huku wapi?” aliuliza huku akipepesa macho kuishangaa sehemu ile ambayo ilikuwa ngeni kwake. “Hapa ni Kongwa njia ielekeayo Mpwapwa.” “Kongwa si Dodoma?” Sara alishtuka. “Ndiyo.” “Waongo!” Sara alibisha haku haamini kufika Dodoma kwa kutembea usiku mmoja tena kwa miguu. “Dada kwani sehemu hii unaijua?” “Mmh! Hapana.” “Duh! Uliondoka kwako lini?” “Jana usiku?” “Mmh! Upo sawa kiakili?” mmoja alimshangaa majibu ya Sara. “Na wala sijawahi kuugua ugonjwa wa akili.” “Basi hapa ni Kongwa.” “Mungu wangu, nimefikaje huku?” Sara alishtuka huku macho yakimtoka pima. “Kwani ilikuwaje?” Sara aliwaeleza jinsi alivyopotea baada ya kutoka kwake kuelekea kwenye banda la chipsi kununua chakula cha usiku na kujikuta akipotea njia na kushangaa kujiona yupo katikati ya pori na kutembea bila kufika mpaka alipofika chini ya mti ule alfajiri, akiwa amechoka sana na kuamua kupumzika kwa vile hakujua anapoelekea. “Haiwezekani utoke Dar kwa miguu jana usiku ufike Dodoma alfajiri!” mtu mmoja alipingana na maelezo ya Sara. “Basi hapa ni Kongwa mkoa wa Dodoma ndiyo maana tuna wasiwasi na maelezo yako huenda akili yako haipo sawa.” “Akili yangu iko sawa, kwani leo ni siku gani?” aliuliza baada ya kumuona watu wakipita kuelekea kanisani. “Jumapili.” “Mungu wangu! Haiwezekani nitoke nyumbani Jumatatu mpaka leo Jumapili, haiwezekani nitembee kwa miguu wiki nzima, nimewakosea nini kunitesa hivi,” Sara alilalamika huku akitokwa machozi. “Kina nani?” “Hata najua, Mungu atanilipia.” Sara alianza kulia na kuwafanya wasamaria wema kumbembeleza, baada ya kunyamaza. Aliwaomba msaada wa kumrudisha Dar kwa vile muda ulikuwa umekwenda, walimpa hifadhi ya kulala pale ili siku ya pili alfajiri wampandishe basi mpaka njia panda kisha apande basi kurudi Dar. Usiku kucha hakulala kuwaza yaliyomtokea, kwake hakuamini, aliamini tukio lile ni la ndotoni halina ukweli wowote. Siku ya pili aliamshwa alfajiri na wenyeji wake na kupandishwa mabasi yanayokwenda njia panda ili apande yanayokwenda Dar es Salaam. Baada ya kupanda haisi iliyompeleka njia panda ambapo alipanda basi la Shabib na kutulia kwenye siti, basi likiwa linakwenda aliangalia mapori ya njiani ambayo yalimfahamisha yupo safarini lakini bado hakuamini njia nzima alikuwa akijiuliza nini kilichomfanya afike mkoani Dodoma kwa miguu bila kuchoka wala kudhurika na wanyama wakali. Pamoja na kuamini yumo ndani ya basi, bado hakuamini tukio lililomtokea ni la kweli. Kwake aliamini ile ni ndoto iliyomchanganya na akiamka asubuhi atajikuta yupo kitandani amelala. Basi lilingia Dar majira ya saa sita na nusu mchana, bado Sara hakuamini. Aliteremka kwenye basi baada ya abiria kuanza kuteremka.
Baada ya kuteremka aliangalia pesa yake ya nauli aliyokuwa amefunga kwenye khanga chakavu. Alifungua na kuikuta elfu moja iliyochafuka kwa udongo wa kijijini, chini alikuwa amevaa ndala rangi mbili moja nyekundu na nyingine bluu. Nywele zake zilikuwa timutimu. Sara alionekana kweli mwana kijiji kutokana na jinsi alivyokuwa, muda wote hakujiona kwani kama angejijua alivyo asingeweza hata kutembea kutokana na jinsi anavyojipenda. Hata alipotaka kupanda daladala konda alimuona wa kuja na kumsemesha maneno ya kejeri. Sara hakujali aliingia ndani ya daladala hadi Kinondoni Kanisani anapokaa. Baada ya daladala kusimama aliteremka na kuelekea kwake. Alipokaribia alishangaa kuona mlango wa chumba chake ukiwa wazi. Shoga yake Happy aliyekuwa amekaa nje alikuwa wa kwanza kumuona na kushtuka kufuatia rafiki yake huyo kuwa katika mavazi ya ajabu, gauni lililochanika mabegani khanga iliyopauka na kandambili rangi mbili. “Sara!” Happy alimwita kwa sauti ya juu.
Sauti ile ilikuwa kama kitu kilichomzindua toka usingizini na kujikuta naye akijishangaa. “Shoga ulikuwa wapi? Jamani mbona umevaa nguo za ajabu?” Kauli ile ilimfanya ajichunguze na kujikuta akijishangaa mavazi aliyovaa na kujikuta akiangua kilio huku akisema. “Mungu wangu! Kumbe kweli nilidhani ndoto.” “Kumbe kweli nini jamani?” Happy alitaka kujua. Sara hakusema kitu alikimbilia ndani na kujitupa kitandani na kuanza kulia kilio cha sauti na kuwafanya majirani wakusanyike nje ya chumba chake. Happy ndiye aliyeingia ndani kutaka kujua shoga yake alikumbana na nini, kitu kilichofanya atoweke nyumbani kwa wiki nzima na kurudi akiwa kama mwana kijiji. “Sara umepatwa na nini?” Happy alitaka kujua. “Mmh! Hata simamini nitembee usiku kucha mchana kutwa kwa siku sita bila kupumzika mpaka Dodoma?” “Dodoma?” Happy alishtuka. “Ndiyo dada hata siamini hizi nguo nimepewa na wasamaria wema wa Kongwa walioniokota nikiwa nimelala barabarani.” “Wewee!” Sara alishtuka. “Yaani kama nisingepanda Hiace toka Kongwa kisha basi la Shabiby ningebisha na tiketi yake ni hii,” Sara alimuonesha Happy tiketi ya basi ambayo ilionesha ilikuwa ya siku ile. Baada ya Sara kuisoma akili yake bado haikuamini shoga yake kwenda Dodoma kwa miguu aliona kama mchezo wa kuingiza. “Sara, siku ile si ulisema unakwenda kununua nyama ya nguruwe na ndizi?” “Ndiyo shoga yangu, nimetoka vizuri mpaka karibu kwa Macha Kitimoto. Ghafla nilijishangaa kujikuta katikati ya pori hata sijui ni pori gani.” “Wewee!” Happy alizidi kushtuka. “Yaani niliogopa mpaka haja ndogo ikanitoka, kibaya zaidi nyuma yangu kulikuwa na milio ya ajabu ya kutisha na kunifanya nikimbie kwenda mbele japosikujua ni wapi nilipokuwa nakimbilia. Kila nilivyokuwa nikikimbia ndivyo sauti za kutisha zilivyokuwa zikinisogelea na kunifanya nizidi kukimbia. “Nakumbuka upande wa khanga wa juu ulinidondoka lakini sikuujali zaidi ya kuyaokoa maisha yangu ambayo niliyaona yapo hatarini. Kandambili nilizokuwa nimevaa zilinidondoka na kujikuta nakimbia pekupeku huku nikikatiza kwenye vichaka na kukanyaga miba. “Kutokana na kutokewa na vitu vile vya kutisha ambavyo sikudhania kukutana navyo hata siku moja, nilijua ile ni ndoto tu wala si kweli. Baada ya kukimbia kwa muda mrefu bila kupumzika, nilianza kusikia vichomi kwenye mbavu na kunifanya nishindwe kutembea. “Zile sauti za kutisha zilizidi kunisogelea nikaona kama nitazubaa basi nitakufa. Nilijilazimisha kukimbia huku nimeshika mkono kwenye mbavu. Nilikwenda hivyo kwa kuchechemea mpaka nilipotokea kwenye mti mkubwa. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwa vile nilikuwa nimechoka sana, nilijiegemeza kwenye mti mkubwa pembeni ya barabara, pamoja na alfajiri ile kuwa na baridi kali lakini usingizi ulinichukua. “Mpaka nilipoamshwa na wanakijiji, sikuamini waliponiambia pale ni Kongwa Dodoma na muda ule ni saa nane mchana, kingine kilichonishangaza kuelezwa siku ile ni Jumapili wakati niliondoka nyumbani Jumatatu. “Yani bado siamini kutembea kwa mguu kwa wiki nzima, kibaya zaidi nakumbuka nilitembea usiku mmoja lakini imeonekana nilitembea wiki nzima. Kama nilitembea wiki nzima, mbona sikuuona mchana zaidi ya usiku tu?” Sara alihoji huku machozi ya uchungu yakimtoka. “Dada hiki ni kituko yani lazima uende kanisani ukaombewe, lazima watakuwa ni wachawi tu walikuchukua.” “Na..na..kwe…,” Sara alisita kuzungumza baada ya kumuona nguruwe amekaa kwenye kiti alichokaa Happy, alipiga kelele za uoga. “Mamaa nakufa nguruwe.” “Sara nguruwe yupo wapi?” Happy alimshangaa rafiki yake. “Si..si…,” alituliza macho na kushangaa kumuona aliyekaa mbele yake ni Happy na si nguruwe kama alivyoona.. “Sara upo sawa?” Happy aliamini rafiki yake hayupo sawa. “Ni..ni..hapana..hapana,” Sara alituliza macho yake baada ya kumuona tena nguruwe kwenye kochi hakupiga kelele, alitulia na kufikicha macho ili kupata uhakika kama kweli kilichopo mbele yake ni nguruwe au anaona maruweruwe. Baada ya macho kutulia alimuona tena shoga yake Happy wala si nguruwe. “Happy naomba nipumzike, siko vizuri sijielewi kabisa.” “Sawa dada lakini kwanza nenda ukaoge ili kuufanya mwili upumue.” “Sawa,” Sara alisema huku akivua nguo alizokuja nazo na kuchukua taulo ili aende bafuni. Alichukua sabuni na mswaki kisha alitoka nje na kumuacha shoga yake akimfanya usafi wa chumba. Sara alielekea nje alipofika mlangoni alisita kutoka baada ya kuona nguruwe wamejaa uani. Alizidi kushangaa na kumwita Happy kwa sauti. “Happy njoo.” Happy aliacha kufanya usafi na kusogea mlangoni. ‘Vipi?” “Eti nje unaona nini?” “Kawaida, kwani umeona nini?” “Nguruwe.” “Nguruwe?” Happy alishtuka. “Hebu ngoja,” Sara alisema huku akipekecha macho na kuona wapo wapangaji wenzake na si nguruwe.
“Mmh! Mbona mwaka huu wangu.” “Shoga kuna umuhimu twende kanisani ukaombewe.” “Ngoja nikaoge.” Sara alikwenda hadi bafuni na kuoga kisha alirudi ndani bila hali ile kumtokea tena. Kwa vile alikuwa amechoka sana, alipanda kitandani na usingizi mzito ulimchukua. **** Siku ya pili Sara alidamka mapema na kuoga kisha alitoka kwenda kazini kwa kumuaga shoga yake Happy. Happy alimuuliza alivyolala. “Vipi umelala salama?” “Namshukuru Mungu nimelala salama, wacha niwahi kazini japo sijui bosi wangu kama atanielewa.” “Atakuelewa tu kwani kilichotokea si cha kawaida.” “Mmh! Ngoja niwahi.” “Mi nilikuwa na wazo.” “Wazo gani?” “Nilikuwa na wazo la kwenda kwanza kanisani ukaombewe pepo mchafu.” “Wazo zuri lakini lazima nifike kwanza ofisini nijue hatima yangu ndipo twende huko kanisani.” “Basi ukirudi jioni tutapanga.” “Sawa.” Sara aliagana na shoga yake na kuwahi kazini kama kawaida kwa kuwahi ili afanye usafi kabla bosi wake hajafika.
Mlinzi alimpa ufunguo kama kawaida, alifungua ofisi na kushtuka kuikuta safi imeisha safishwa. Hali ile ilimshtua na kumfanya atoke nje mpaka kwa mlinzi na kumuuliza;
“Eti nani kafanya usafi?” “Wapi?” “Ndani ya ofisi?” “Wewe ndo wa kwanza kuja sijamuona mtu yeyote.” “Kwa…kwa niiii toka nilipoondoka nani alikuwa akifanya usafi?” “Kwani da Sara ulienda wapi?” “John si muhimu kujua, nijibu swali langu.” “Toka uondoke sijawahi kumuona mtu akifanya usafi, nakumbuka siku ambayo wewe hukuja bila taarifa nilitaka kwenda kufanya usafi lakini bosi alinikataza, tokea siku hiyo sijamuona mtu akifanya usafi.” “Ina maana toka niondoke hakuna mtu uliyemuona anafanya usafi?”
“Sijawahi kumuona.” “Mbona ofisi inaonesha imefanyiwa usafi muda si mrefu tena wa hali ya juu?” “Basi majini ndiyo yamefanya usafi,” mlinzi alisema kwa utani. “John na wewe umeligundua hilo?” “Lipi?” “La kuwepo na jini ofisini?” “Mi nimesema tu, hilo jini lifanye usafi kwa ajili gani?” “Kama mimi nilikuwa sifanyi usafi, basi nani amefanya?” “Mmh! Labda bosi.” “Nataka kukuambia hapa kuna mchezo, unamjua yule mwanamke?” “Mwanamke gani?” “Yule mrembo anayekujaga ofisini.” “Ndiyo.” “Yule nina wasiwasi siyo mtu wa kawaida.” “Una maanisha nini?” “Mimi simwelewi huenda ni jini!” “Jini? We acha mambo ya ajabu angekuwa jini tungemuona?” “Nakwambia ipo siku utakubaliana na mimi.” “Kwa hiyo bosi wateja wake wengine ni majini?” “Hebu kwanza nikuulize?” “Uliza.” “Tangu niondoke yule mwanamke kaja mara ngapi?” “Kwa kweli sijamuona.” “Muongo!” “Kweli.” “Basi we subiri kama ni yeye nitakomeshana…na…na,”Sara alinyamaza baada ya kuliona gari la bosi wake likisimama getini. Hakutaka kuongeza neno alichepua mwendo kuwahi ofisini, alijisikia vibaya bosi wake kumkuta eneo lile badala ya ofisini. Lakini alipanga kujitetea alikuwa akimuuliza kitu mlinzi. Mustafa toka akiwa ndani ya gari alishtuka kumuona Sara, baada ya kupaki gari alielekea ofisini na kupokewa na Sara kama ilivyokuwa kawaida na kupeleka vitu ndani. Wakati wa kupokelewa alitaka kukataa lakini hakuona sababu ya kukataa, alimuacha apokee lakini alitaka maelezo ya kina atakapomuuliza ili aendelee na kazi lakini kinyume na hapo alipanga kumfukuza kazi kwani tangu aondoke hakukuwa na pengo lolote. Baada ya kutulia kwa muda Sara aliingia ofisini kwa bosi wake akiwa hajiamini na kufika kusimama mbele ya bosi wake. Mustafa aliacha kusoma gazeti la siku ile na kunyanyua uso wake kumtazama. “Shikamoo,” Sara alimuamkia kwa kupiga magoti. Ilikuwa mara ya kwanza Sara kumuamkia kwa heshima vile jambo ambalo hakuwahi kulifanya siku za nyuma. Mustafa alijikuta akimshangaa Sara kwa kitendo kile, wakati huo Sara alishtuka
kuona aliyekaa mbele yake si bosi bali nguruwe. Alituliza macho ili kupata uhakika. Hakukuwa na mabadiliko zaidi ya kuona nguruwe amesimama kwenye kiti cha bosi wake akichezesha pua. Alikaza macho kuangalia kama alichokiona ni kweli au maruweruwe. Bado hali ilibakia ileile ya kumuona nguruwe mbele yake, alipekecha macho ili kuikataa hali ile kwa kuamini yale yalikuwa maruweruwe kama yaliyomtokea jana yake.
Aliamini yule ni nguruwe kweli wala si bosi wake baada ya kutoka mlio wa nguruwe ambao ulimfanya apige kelele za woga. “Mamaa nakufa!” Alishangaa nguruwe yule kuzungumza kwa sauti ya kibinadamu: “Sasa unaogopa nini wakati ulifunga safari kunitafuta mpaka Dodoma, nimekuja unapiga kelele.” “Ha..hapana..hapana,” Sara alikataa huku akitikisa kichwa. “Mimi muongo hujatoka nyumbani kwako kunifuata unilete ofisini?” “Ha..ha..hapana,” Sara kwa woga haja ndogo ilimtoka bila kujijua. “Saraaaa!” Sauti kali ya Mustafa ilimshtua. Hakuitika alishika mikono masikioni kuzuia sauti ya nguruwe, alishangaa kumuona bosi wake akiwa amesimama mbele yake huku akimshangaa. “Sara nini?” alimuuliza kwa sauti kubwa baada ya kushindwa kumuelewa. “Nakufa bosi,” alisema huku pumzi zikimtoka kama alikuwa akikimbizwa na simba. “Sara kipi kinakuua?” “Mungu wangu nakufa..nakufa mimi,” Sara alisema huku akikaa chini baada ya nguvu kumuishia na kuhema kwa nguvu. Mustafa alizunguka meza na kumsogelea Sara aliyekuwa amekaa chini, alimshika kichwani na kumuuliza kwa sauti ya upole. “Sara una nini?” Sara pumzi zilikuwa zimemjaa na kushindwa kuzungumza, alijiuliza amekumbwa na nini kwa vile kitu kama kile kilikuwa hakijawahi kumtokea. Sara alikuwa akitetemeka na jasho kumtoka kitu kilichozidi kumtia kwenye wakati mgumu Mustafa kwa kuamini angesema angejua tatizo lake. Akiwa katika kizungumkuti asijue nini kimemtokea Sara ambaye aliendelea kuhema huku macho kayatoa pima. Mlango uligongwa na kumfanya ahamishe macho yake kuelekea mlangoni bila kuitikia. Mlango uligongwa tena hakutaka kumkaribisha mtu ndani kutokana na hali ya Sara ilivyokuwa aliamua kusogea mlangoni.
Alikwenda hadi mlangoni na kufungua, alijikuta akikutana uso kwa uso na Shehna. “Ha! Karibu!” “Mbona umeshtuka?” “Sikutegemea kukuona.” “Kwa nini unasema hivyo au kuna muda uliopanga mimi kuja hapa.” “Walaa, karibu.” “Asante.” Sauti ya Shehna ilimshtua Sara ambaye mapigo ya moyo yaliyoanza kupoa, yalianza upya tena kwa kasi kubwa. Alijiuliza nini hatima yake kama kweli ni jini na kama ndiye aliyekuwa akimfanyia mchezo ule nini atamfanya. Alitamani kumuomba msamaha lakini alijiuliza ataanzia wapi ikiwa hana uhakika yale yalikuwa mawazo yake tu. Shehna aliingia ndani ya ofisi na kushtuka kumuona Sara amekaa chini. “Mustafa! Shoga yangu kafanya nini tena?” “Yaani nashangaa ameingia ofisini tu na kuanza kupiga kelele.” ”Kelele! Kipi kimemtisha?” Sara alijikuta njia panda kutokana na maneno ya Shehna yalimshangaza na kuona kama mawazo yake ni tofauti na alivyokuwa akifikiria. “Ha…halafu si ulisema alisafiri amerudi lini?” “Ulinisikia vibaya nilisema haonekani ofisini sikujua amekwenda wapi.” “Sasa nini kimemsibu?” “Hata najua? Namuuliza amegeuka bubu, yaani nachanganyikiwa.” “Sasa kipi kimemsibu jamani shoga yangu?” Shehna alisema huku akimsogelea na kumuinamia Sara. “Eti Sara umepatwa na nini?” Sara bado mdomo ulikuwa mzito kwa vile mapigo ya moyo bado yalikuwa juu. “Mustafa niletee maji ya baridi niwekee kwenye glasi.”
Ofisini walibakia Mustafa na Sara aliyekuwa amesimama. “Kaa,” Mustafa alimwambia Sara. Sara alikaa kwenye kiti, Mustafa aliendelea kusimama. “Sara,” alimwita.” “Abee.” “Una tatizo gani?” Sara ilibidi amueleze mkasa mzima kuanzia siku aliyotoka kwenda kununua nyama ya nguruwe. Lakini alificha kufuata nyama ya nguruwe na kusema alifuata chakula cha usiku na yaliyomtokea na vituko vilivyokuwa vikimtokea toka siku aliyofika nyumbani na ofisini. “Sara mbona unafanya utani.” “Kweli bosi, siwezi kusema uongo.” “Kwa hiyo hata hapa ilitokea?” “Kule ilikuwa tisa kumi hapa mpaka sauti katoa.” “Mmh! Itakuwa nini? Hebu ngoja,” Mustafa alisema huku akielekea mlangoni na kuufungua kisha aliita. “Shehna njoo.” “Vipi mmemalizana?” “Hebu njoo mara moja.” Shehna aliingia ofisini na kusimama pembeni ya Mustafa ili kusikiliza alichoitiwa. “Unasemaje?” Alimweleza yote yaliyomtokea Sara, baada ya kumsikiliza alisema. “Mmh! Pole, lakini maji aliyokunywa yatamsaidia haitamtokea hali ile tena.” “Kwa hiyo aendelee na kazi au akapumzike?” “Mwache akapumzike ili kesho aanze kazi vizuri.” Mustafa alimpa ruhusa Sara akapumzike ili kesho aende kazini, Sara alishukuru na kuondoka na kutaka kutoka lakini alikumbuka alichafua chini kwa haja ndogo baada kumtoka bila kujijua kutokana na hofu ya maruweruwe. Alikwenda msalani kuchukua Mop kwa ajili ya kufanya usafi, alipoingia Shehna alimuwahi na kumwambia. “Shoga kapumzike nitakusaidia mimi.” “Acha tu dada.” “Hapana kapumzike.” Sara alikubaliana kumpa Mop Shehna na kuondoka kuelekea nyumbani, lakini Shehna alimwambia Mustafa. “Mustafa mpeleke Sara, ukirudi utakuta nimemaliza kufanya usafi.” “Sawa.” Mustafa alitoka kumpeleka Sara nyumbani na kumpa nafasi Shehna kufanya usafi. Baada ya kuondoka tu Shehna aliwaita vijakazi wake ambao walianza mara moja kazi ya usafi. Mustafa alimpeleka Sara mpaka nyumbani na kumuacha kisha alirudi nyumbani na kumkuta Shehna kaisha maliza kazi ya usafi. Baada ya kuachwa Sara aliingia chumbani kwake na kujikuta akianguka kilio kutokana na matukio yaliyokuwa yakimuandama kila kukicha. Katikati ya kilio aliisikia tena sauti aliyoisikia wakati alipomuona nguruwe ofisini kwa bosi wake. “Kulia siyo dawa zaidi kuacha kuyafuata mambo yasiyo kuhusu la sivyo utageuka nguruwe kabisa.” Sauti ile ilimfanya anyamaze na kujiuliza kitu gani ambacho amekuwa akikifuatilia zaidi ya kutaka kumjua Shehna ambaye kwa jinsi alivyomuona na upole wake aliamini si jini bali kiumbe cha kawaida tena mwenye upendo tofauti na alivyomfikiria. Hakuamini mwanamke mrembo kukubali kusafisha haja yake ndogo. Lakini alimuhakikishia hali ya kumtisha haitamrudia tena, haikuwa kama alivyomwambia na kusikia sauti ile. Akiwa hajapata jibu simu yake iliita, namba ilikuwa ngeni. Alipokea na kuzungumza. “Haloo.” “Sara umefika salama?” sauti haikuwa ngeni lakini hakuwa na uhakika nayo ilibidi aulize. “Nani?” “Mi shogayo Shehna.” “Aah! Dada nimefika salama.” “Ile hali haijatokea?” “Ndi..ndiyo.” “Mbona kama una wasiwasi?” “Ni kweli kuna sauti naisika kwa mara ya pili lakini siielewi.” “Inasemaje?”
Ofisini walibakia Mustafa na Sara aliyekuwa amesimama. “Kaa,” Mustafa alimwambia Sara. Sara alikaa kwenye kiti, Mustafa aliendelea kusimama. “Sara,” alimwita.” “Abee.” “Una tatizo gani?” Sara ilibidi amueleze mkasa mzima kuanzia siku aliyotoka kwenda kununua nyama ya nguruwe. Lakini alificha kufuata nyama ya nguruwe na kusema alifuata chakula cha usiku na yaliyomtokea na vituko vilivyokuwa vikimtokea toka siku aliyofika nyumbani na ofisini.
“Sara mbona unafanya utani.” “Kweli bosi, siwezi kusema uongo.” “Kwa hiyo hata hapa ilitokea?” “Kule ilikuwa tisa kumi hapa mpaka sauti katoa.” “Mmh! Itakuwa nini? Hebu ngoja,” Mustafa alisema huku akielekea mlangoni na kuufungua kisha aliita. “Shehna njoo.” “Vipi mmemalizana?” “Hebu njoo mara moja.” Shehna aliingia ofisini na kusimama pembeni ya Mustafa ili kusikiliza alichoitiwa. “Unasemaje?” Alimweleza yote yaliyomtokea Sara, baada ya kumsikiliza alisema. “Mmh! Pole, lakini maji aliyokunywa yatamsaidia haitamtokea hali ile tena.” “Kwa hiyo aendelee na kazi au akapumzike?” “Mwache akapumzike ili kesho aanze kazi vizuri.” Mustafa alimpa ruhusa Sara akapumzike ili kesho aende kazini, Sara alishukuru na kuondoka na kutaka kutoka lakini alikumbuka alichafua chini kwa haja ndogo baada kumtoka bila kujijua kutokana na hofu ya maruweruwe. Alikwenda msalani kuchukua Mop kwa ajili ya kufanya usafi, alipoingia Shehna alimuwahi na kumwambia. “Shoga kapumzike nitakusaidia mimi.” “Acha tu dada.” “Hapana kapumzike.” Sara alikubaliana kumpa Mop Shehna na kuondoka kuelekea nyumbani, lakini Shehna alimwambia Mustafa. “Mustafa mpeleke Sara, ukirudi utakuta nimemaliza kufanya usafi.” “Sawa.” Mustafa alitoka kumpeleka Sara nyumbani na kumpa nafasi Shehna kufanya usafi. Baada ya kuondoka tu Shehna aliwaita vijakazi wake ambao walianza mara moja kazi ya usafi. Mustafa alimpeleka Sara mpaka nyumbani na kumuacha kisha alirudi nyumbani na kumkuta Shehna kaisha maliza kazi ya usafi. Baada ya kuachwa Sara aliingia chumbani kwake na kujikuta akianguka kilio kutokana na matukio yaliyokuwa yakimuandama kila kukicha. Katikati ya kilio aliisikia tena sauti aliyoisikia wakati alipomuona nguruwe ofisini kwa bosi wake. “Kulia siyo dawa zaidi kuacha kuyafuata mambo yasiyo kuhusu la sivyo utageuka nguruwe kabisa.” CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Sauti ile ilimfanya anyamaze na kujiuliza kitu gani ambacho amekuwa akikifuatilia zaidi ya kutaka kumjua Shehna ambaye kwa jinsi alivyomuona na upole wake aliamini si jini bali kiumbe cha kawaida tena mwenye upendo tofauti na alivyomfikiria. Hakuamini mwanamke mrembo kukubali kusafisha haja yake ndogo. Lakini alimuhakikishia hali ya kumtisha haitamrudia tena, haikuwa kama alivyomwambia na kusikia sauti ile. Akiwa hajapata jibu simu yake iliita, namba ilikuwa ngeni. Alipokea na kuzungumza. “Haloo.” “Sara umefika salama?” sauti haikuwa ngeni lakini hakuwa na uhakika nayo ilibidi aulize. “Nani?” “Mi shogayo Shehna.” “Aah! Dada nimefika salama.” “Ile hali haijatokea?” “Ndi..ndiyo.” “Mbona kama una wasiwasi?” “Ni kweli kuna sauti naisika kwa mara ya pili lakini siielewi.” “Inasemaje?”
“Inasema niache kufuatilia mambo yasiyonihusu la sivyo nitageuzwa nguruwe kabisa.” “Kwani unafuatilia nini?” Shehna alijifanya kuuliza. Swali lile lilikuwa gumu kwa vile asingeweza kumueleza anamfuatilia yeye, alibidi adanganye kwa kusema: “Dada wee nimfuatilie nani?” “Haiwezekani sauti hiyo kutokea mara ya pili, kama kuna kitu unakifuatilia achana nacho kwa vile kila kitu cha ajabu kikikutokea kina sababu.” “Nimekusikia dada yangu.” “Hebu acha kufuatilia hicho ulichotaka kukifuatilia tuone nini kitatokea.” “Sawa dada.” “Basi mdogo wangu oga kisha kunywa maji ya baridi ulale.” “Nitafanya hivyo dada.” Sara alikwenda kuoga kisha alikunywa maji ya baridi na kujikuta akipitiwa na usingizi mzito. ***
Sara aliamka siku ya pili bila kutokewa na mauzauza yoyote, alikwenda hadi kazini kama kawaida na kukuta ofisi haijafanyiwa usafi. Aliingia katika kazi ya kufanya usafi kama kawaida yake na kusubiri muda wa bosi wake kufika. Baada ya muda Mustafa aliwasilili na kupokewa na Sara. Kama kawaida alichukua vitu vya bosi na kwenda kuviweka ofisini, Mustafa alipoingia ofisini alishangaa kukuta ofisi chafu. Hata hali ya hewa haikuwa kama ile aliyoizoea wakati wa Shehna akifanya usafi. Alitoka hadi kwa Sara na kumuita. “Sara njoo mara moja.” Sara alinyanyuka na kwenda kwa bosi wake kumsikiliza alijua anaitiwa kazi ya siku ile. Alipofika alikutana na swali lililomshtua. “Sara kazi imekushinda?” “Kwa nini bosi?” “Mbona ofisi inanuka kama zizi la ng’ombe.” “Bosi mbona mi sisikii harufu yoyote mbaya?” “Ina maana husikii harufu mbaya ya ofisi?” “Bosi kipi kimeongozeka, nimefagia na kufuta kama siku zote sasa hiyo harufu kama zizi imetoka wapi?” “Sara kazi imekushinda heri usingerudi ofisi yangu ikaendelea kusafishwa na Shehna, unakuwa kama upo bustanini lakini kurudi kwako hakuna ulichokifanya zaidi ya kuongeza uchafu.” “Bosi mbona sikuelewi hiyo harufu kama beberu ipo wapi?” Ghafla ndani ya ofisi ilisikia harufu nzuri ya manukato aliyoizoea, alimwambia Sara aondoke. “Sara kaendelee na kazi.” “Asante bosi.” Sara alitoka na kwenda kuendelea na kazi, wakati akifanya kazi alijikuta mtu mwenye mawazo mengi juu ya tukio la muda mfupi uliopita la bosi wake kumgeuka kuwa hajafanya usafi na kusema ofisi inanuka kama zizi. Kilichomshangaza kingine kilikuwa harufu nzuri ya manukato iliyoingia ghafla ofisini ambayo hakujua yametoka wapi. Hakutaka kusema kitu aliendelea na kazi na kupanga akitoka kazini jioni lazima aende kwa mganga wake ili amuangalizie kinachomtokea ni nini kwa vile haikuwa hali ya kawaida kwa mtukio yote. Wakati akiwaza vile alishtuliwa na sauti ya Shehna. “Shoga za kazi?” CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Ooh! Dada karibu,” alisema huku akionesha kushtuka. Shehna alikuwa amevaa dela zuri lililonakshiwa na nyuzi za hariri, alikuwa amenawiri na kupendeza alionekana mwanamke mrembo zaidi ya siku zote. “Asante.” “Da Shehna hongera umependeza sana.” “Nashukuru.” “Karibu dada a’ngu.”
“Nimekaribia, vipi umeamkaje?” “Namshukuru Mungu leo nimeamka salama.” “Vipi ile hali ilitokea tena?” “Kwa kweli mpaka nakuja kazini nashukuru hali ile wala sauti haijanitokea tena.” “Kama nilivyokueleza, zingatia uliyoambiwa na ile sauti yana sababu, utashangaa mambo yako yatakwenda vizuri.” “Asante dada kwa msaada wako pia nitazingatia ushauri wako.” “Vipi bosi yupo?” “Yupo pita.” “Hapana muulize kwanza.” Sara alinyanyua simu na kumpigia Mustafa aliyemwambia amruhusu aingie. “Dada pita.” “Asante.” Shehna aliingia ndani ya ofisi alikutanisha macho na Mustafa aliyekuwa akiangalia mlangoni. “Wawooo mpenzi.” Mustafa alijikuta akitoka kwenye kiti chake na kwenda kumpokea kwa kumkumbatia kisha alimchumu. “Asante mpenzi,” Shehna alishukuru baada ya kubusiwa kwenye shavu. Waliachana kwa kila mmoja kukaa sehemu yake, Shehna alionekana mwenye furaha usoni mwake tofauti na siku zote. Alimuangalia Mustafa usoni alitaka kusema neno lakini aliishia kutabasamu na kufanya uzuri wake uongezeke. “Vipi mpenzi?” Mustafa alimuuliza huku naye akijenga tabasamu mwanana lililokuwa likimpa uhuru Shehna kuzungumza. “Mmh! Mustafa nashukuru sana.” “Kwa kipi?” ;Kwa vyote, lakini kimoja ndicho nimefurahi sana tena sana sipati kusema.”
“Vipi hivyo na kipi kimekufurahisha sana?” “Nikwambie?” Shehna alimuuliza Mustafa huku akimtazama kwa jicho la aibu. “Niambie mpenzi,” alitoa tabasamu la kumruhusu aseme kilichokuwa moyoni mwake. “Kwanza nashukuru kwa kunipa nafasi moyoni mwako, pili kunivumilia kwa usumbufu wangu, tatu kunipa penzi ambalo sijawahi kupata katika maisha yangu yote na kubwa zaidi nimekuja kukueleza sasa hivi mimi ni mjamzito.” “Wewe!” Mustafa alishtuka. “Kweli kabisa, unakumbuka jana ilikuwa siku ya ngapi mimi kulala kwako?” “Mmh! Hata sikumbuki.” “Muone!” Shehna alisema huku akimshika kidevu Mustafa. “Jana mpenzi ndiyo ilikuwa siku ya mwisho ya kukutana kimwili, mpaka juzi bado sikuona mabadiliko. Nilichanganyikiwa mtoto wa kike, lakini penzi ulilonipa jana lilikuwa tamu ajabu kidogo nife kwa raha kumbe watoto walikuwa wanaingia.” “Kweli?” “Kweli kabisa nami si muda mrefu nitaitwa mama.” “Hongera!” Mustafa alisema huku akizunguka meza na kumkumbatia. “Hongera wewe kunipatia nilichokitafuta kwa muda mrefu.” “Basi tuongere wote.” “Mustafa mpenzi, kuanzia leo hatutaonana mchana kwa vile sipendi kutembea na tumbo.” “Mbona bado sana?” “Siwezi kutembea, familia yetu ikibeba ujauzito husumbuka sana.” “Sawa mpenzi, lakini nyumbani si utakuja?” “Hapana ila nitawatuma watu wakufuate usiku siku mojamoja na alfajiri watakurudisha.” “Hakuna tatizo.” “Ila mpenzi kwa mwezi mzima hatutaonana nakwenda nyumbani mara moja kufanya mambo ya kimila baada ya kupata ujauzito.” “Mmh! Mpenzi nitateseka, nimekuzoea sana.” “Usiwe na wasiwasi nitakuwa nawe karibu muda wote.” “Tutakuwa pamoja kivipi wakati hautakuwepo kwa mwezi mzima?” “Kila siku nitakuwa katika ndoto zako na ukiamka wala hutakuwa na majonzi, usiku utakuwa kama mchana tena upo na mimi.”
“Sawa,” Mustafa hakutaka kubishana na Shehna kwa kuamini kabisa alikuwa akipewa moyo kwa kujua siku zote furaha ya ndotoni ni maumivu ya asubuhi. “Nilitaka kusahau, sasa hivi ruksa kukutana kimwili na mkeo.” “Hata bila ya dawa?” “Yaleyale mafuta mtajipaka sehemu za siri kabla ya kukutana, ila lazima mkutane mara mbili kwa wiki, Jumatatu na Ijumaa.” “Kwa nini tukutane siku hizo?” “Ndizo siku zenye nyota ya mtoto zaidi ya hapo mtakuwa mnatenga maji kwenye kinu.” “Basi tunaweza kukutana siku zote ila Jumatatu na Ijumaa ndiyo muhimu.” “Mustafa hiyo unapanga wewe, hii ni dozi ya kutafuta mtoto mkienda kinyume na hapo mtoto mtamsikia kwa kilio, akilia nyumba ya jirani.” “Nimekuelewa mpenzi.” “Najua sasa hivi huna matatizo ya fedha, kama utakuwa na shida amka usiku, washa udi utaweza kuniona ndotoni na kunieleza matatizo yako, kama ni fedha kabla ya kuondoka washa udi acha ufunguo mnapouacha ili niweze kukuletea hela.” “Shehna hivi wewe ni nani hasa?” “Kivipi?” “Bado nipo njia panda, wewe ni mganga au ji.., hapana sivyo ila naomba uniweke wazi maana mpaka sasa nipo njia panda,” Mustafa alimuuliza huku amemkazia macho. “Mustafa kipi kimekufanya unitilie shaka hivyo mpenzi wangu?” Shehna alimuuliza Mustafa huku machozi yakimtoka, kitu kilichomfanya Mustafa ajutie swali lake. “Basi samahani mpenzi kama swali langu nimekukwaza.” “Mustafa mpenzi kipi nimekufanyia kibaya mpaka unifikirie hivyo au umenichoka mpenzi wangu? Mapenzi yote ninayokupa unayaona bureee?” Shehna aliendelea kulia huku machozi yakimtoka kama maji. Mustafa alijikuta akijilaumu kwa swali lake ambalo liliharibu furaha yake ya siku ile. Alijutia nafsi yake kwa swali la kipumbavu lakini aliendelea kumbembeleza Shehna amsamehe kwa swali lake lile. “Shehna mpenzi nisamehe kwa swali langu la kipuuzi.” “Mustafa mpenzi nikujali vipi? Siku zote nimekuwa nikikujali mbona sijawahi kukuuliza swali kama hilo?
“Au wema wangu wa kujitolea kwako ndiyo umeniponza?” Shehna alilia mpaka akawa mwekundu. Mustafa alichanganyikiwa na kujikuta akitoka kwenye kiti chake na kwenda kupiga magoti mbele ya Shehna na kuanza kulia huku akiomba msamaha kwa kuamini Shehna ni mtu muhimu sana katika maisha yake kutokana na kumsaidia vitu vingi. Kilio cha Mustafa kuomba msamaha kilimshtua Shehna ambaye siku zote hakupenda kumuona Mustafa akitoa machozi mbele yake. Alimshika na kumnyanyua na kutazamana kila mmoja, macho yake yakiwa yamejaa machozi. Machozi ya Shehna yalimfanya aongezeke uzuri maradufu na kuzidi kuutesa moyo wa Mustafa, kumpoteza kiumbe mzuri kama yule. “Mustafa,” Shehna alimwita kwa sauti ya kinanda. “Naam.” “Nisamehe mpenzi,” Shehna alisema huku akimfuta machozi kwa mtandio. “Shehna huna kosa, mwenye makosa ni mimi niliyetoa machozi yako.” “Hapana Mustafa nakupenda sana, nimeumizwa na machozi yako, narudia tena naomba unisamehe.” “Nimekusamehe japo sioni kosa lako, naomba na mimi unisamehe.” “Nimekusamehe mpenzi wangu nami nashukuru kwa kunisamehe.” Walikumbatiana kila mmoja akirudisha furaha yake. Baada ya utulivu wa muda, Shehna alimuomba Mustafa atoke nje mara moja. Alimruhusu hakuchelewa alirudi baada ya dakika mbili akiwa na vinywaji mkononi. Aliviweka juu ya meza na kwenda kwenye friji ndogo na kutoa glasi mbili.
Alimimina kinywaji kile kwenye glasi na kumpa Mustafa. “Karibu mpenzi.” “Asante,” Mustafa alisema huku akikipokea. Alikunywa funda mbili na kumumunya midomo kisha alisema: “Aaah! Mpenzi kinywaji kitamu sana umepata wapi?” “Nilituma mtu nyumbani alete wakati nakuja kukuaga.” “Ni kitamu hakika sijawahi kukinywa toka nitoke tumboni kwa mama yangu.” “Utazidi kuvipata maadamu tuko pamoja utakula vitamu zaidi ya hiki. Hii chupa utakuwa ukichukua glasi moja kila siku. Mpaka narudi nitakuta hujamaliza.” “Shehna wewe ni mtu muhimu sana katika maisha yangu, nitakupenda, nitakutunza na kukuheshimu siku zote za maisha yangu.” “Mustafa mpenzi mimi si mkaaji, nilikuja kukujulisha habari za ujauzito wangu na kukuaga.”
“Sawa mpenzi nimekuelewa nami nitafuata yote uliyonielekeza bila kufanya makosa.” “Nitafurahi, kumbuka nakupenda sana Mustafa.” “Najua.” “Naomba usinisaliti.” “Nakuahidi sitafanya hivyo labda nife.” Walikumbatiana kwa muda kila mtu aliyasikia mapigo ya moyo wa mwenzake kisha waliachiana na kusindikizana nje. Alipofika mapokezi Shehna alimuaga Sara. “Shoga nikukimbieni.” “Jamani, lini utakuja kwangu tuongee?” “Tutapanga.” “Haya shoga sisi tunaendelea na kazi.” “Ila zingatia yote tuliyozungumza ili uishi kwa amani.” “Nitafanya hivyo.” “Haya kwa heri.” “Haya shoga.” Mustafa alitoka na Shehna hadi nje, alishangaa kutoona usafiri wowote nje uliomleta, alijiuliza ataondokaje. “Shehna unatumia usafiri gani?” “Utanisindikiza mpaka njia panda kuna gari la nyumbani litanipitia.” “Sawa.” Waliingia kwenye gari la Mustafa na kumpeleka mpaka sehemu aliyotaka na kumwambia. “Niache hapa kuna gari litanipitia sasa hivi.” “Sawa.” Mustafa alisimamisha pembeni ya barabara kwenye mti wenye kivuli na kumwambia: “Haya mpenzi nenda salama daima nitakukumbuka.” “Jamani Mustafa si mwezi tu.” “Kwa umpendaye siku moja mwaka.” “Najua, hata mimi nilipenda ujauzito huu niulee na wewe, lakini mila lazima nifanye tambiko bila hivyo naweza kupoteza wanangu.” “Haya mama naheshimu kwa vile ni kwa ajili yetu.” Waliagana kwa kukumbatia kwa muda kisha Shehna aliteremka kwenye gari na kwenda kusimama chini ya mti, Mustafa aliondoa gari kurudi ofisini. Siku ile Shehna hakutaka kuondoka kwa mtindo wake wa kutoweka ghafla, alihofia baada ya utata uliojitokeza kwa Mustafa ilibidi afanye vile ili wajue ni kiumbe cha kawaida wala si kama wanavyomdhania. Baada ya kumuona Mustafa ametoweka naye alitoweka ghafla na kurudi chini ya bahari.
*** Sara baada ya kumaliza kazi aliondoka kuelekea kwa mganga wake ili apate ukweli wa kitu kilichomsumbua. Ili kukwepa foleni alichukua bodaboda kuelekea kwa mganga Vingunguti kwa vile walitumia usafiri ule waliweza kukwepa foleni za barabarani na kutumia nusu saa kufika kwa mganga. Kwa vile hakutaka dereva wa bodaboda ajue anakwenda wapi, aliteremka mbali kidogo na nyumba ya mganga ambayo ilikuwa vigumu mtu kujua mpaka aelekezwe. Alitembea hatua kama hamsini na kutokea uani kwa mganga, alikuta wateja zaidi ya nane waliokuwa chini ya mti, wanawake sita pamoja na yeye jumla wakawa saba na mwanaume mmoja alikaa kwenye benchi palipokuwa na nafasi. Kwenye mkeka kulikuwa na wanawake watatu walikuwa wamejionyoosha na kuchukua nafasi kubwa. Baada ya kuketi na kuwasalimia kwa vile alikuwa mzoefu alitoa simu yake kwenye mkoba na kumtumia ujumbe mganga kumjulisha alikuwa nje.
Baada ya muda alitoka kijana mmoja mwenye umri isiozidi miaka 30 akiwa amevaa suruali ya jinsi na tisheti, ukimuangalia harakaharaka utajua brazameni. Hakusema neno lolote, alimwita Sara kwa ishara ya mkono na kumwelekeza apite ndani. Baada ya kuingia alikutana naye nje ya chumba cha uganga. “Karibu.” “Asante, za siku?” “Nzuri, umeadimika sana.” “Mambo mengi ustaadh wangu.” “Karibu ndani, maana nimefanya upendeleo.” “Najua ndiyo maana nikatuma ujumbe, niliogopa kupiga,” Sara alisema huku akiingia ndani ya chumba cha mganga na kuketi kwenye mkeka. “Mmh! Lete habari,” mganga alisema. “Habari nzuri, ile kazi ilikwenda vizuri yule bwana alirudi na alifanya kama ulivyosema, kwa sasa amekwenda nje kikazi, akirudi anakamilisha kila kitu.” “Sasa mbona hukurudi tumalize kazi?” “Ndugu yangu kuna mambo yalinitokea ambayo sijawahi kutokewa toka nizaliwe.” “Mambo gani?”‘
Sara alianza kumueleza mauzauza yaliyokuwa yakimtokea kuanzia kupotea njia mpaka kuona nguruwe na sauti alizokuwa akisikia, pia wasiwasi wake kwa Shehna. Mganga baada ya kumsikiliza alichukua kitabu cha uganga, karatasi na kalamu na kuandika vitu kwenye karatasi nyeupe kisha alifungua kitabu kuangalia alichoandika kilimaanisha nini kutokana na maelezo ya Sara. Baada ya kusoma kwa muda alimuangalia Sara na kumuuliza swali; “Unasema sauti ilisemaje?” “Ilisema nisifuatilie mambo yasiyonihusu la sivyo nitageuzwa nguruwe kabisa.” “Kwa nini unafuatilia?” “Kuna mambo yananitatiza.” “Ndiyo kuna kitu nimekiona hapa, inavyoonekana hakuna tatizo lolote zaidi ya kufuata maelekezo uliyopewa na ile sauti. Hutakiwi kupewa dawa yoyote zaidi ya kuisikiliza ile sauti. Kinyume cha vile mganga yoyote atakayejifanya anajua, moto utamuwakia.” “Kwa nini?” “Hapana hakuna, tatizo unalo wewe kutaka kuingilia visivyo kuhusu achana nayo uwe salama, zaidi ya hapo utajuta kuzaliwa.” “Sasa utanisaidia vipi?” “Msaada ni kuacha kufuatilia visivyokuhusu.” “Una maana ile hali haitatokea tena?” “Ikutokee vipi nawe umeacha kufuata mambo yasiyokuhusu.” “Nitamjuaje anayenifanyia mchezo huo?” “Sara kuwa muelewa, achana na mambo yasiyokuhusu, umjue ili iweje? Zaidi ya hapo sina msaada wowote wa kukusaidia.” “Hakuna kinga yoyote?” “Kinga ya nini?” “Inaweza kunitokea tena.” “Kama utayapuuza yale maneno na kujifanya unajua utageuzwa nguruwe na hakuna wa kukurudisha.” “Mmh! Sawa.” “Una lingine?” “Kwa leo sina ila mwisho wa wiki nitakuja kwa ajili ya mambo yangu.” “Karibu sana.”
Sara aliagana na mganga wake na kutokea mlango mwingine na kutoa nafasi kwa wateja wengine kupata huduma. Alitembea taratibu hadi kwenye kituo cha bodaboda na kukodi mpaka nyumbani kwake. Baada ya kufika kwake alikuwa mtu mwenye mawazo mengi kutokana na majibu ya mganga. Alijiuliza kwa nini mganga alikataa kumsaidia, bado hakukata tamaa. Alipanga kwenda kwa mganga mwingine ili kupata ukweli aliamini kabisa mganga yule wa awali uwezo wake mdogo. Kwa vile ilikuwa bado mapema, alichukua simu yake na kumpigia shoga yake anayeishi Kigogo. Baada ya simu kuita kwa muda, ilipokelewa upande wa pili. “Haloo Sara.” “Eeh! Mwaju za sahizi?” “Nzuri, vipi shoga?” “Eti mzee Gogo yupo?” “Yupo, kwani vipi?’ “Nilikuwa nina shida naye.” “Kwa lini?” “Leo hii.” “Mbona usiku?” “Siwezi kulala mpaka nimuone kuna mambo yananitatiza.” “Mambo gani hayo ambayo lazima uende usiku huu.” Sara alimweleza sababu ya kutaka kuonana na mzee Gogo, baada ya kumsikiliza, alishusha pumzi na kusema: “Mmh! Shoga una haki ya kwenda muda huu kwa mzee Gogo.” “Sasa tunafanyaje?” “Nakusikiliza wewe.”
“Basi kodi Bajaj nipitie nitalipa.” “Nipe dakika ishirini nitakuwa hapo jiandae nikifika tunaondoka.” “Wala sina shida ya kujiandaa utanikuta nje nakusubiri.” Sara hakutaka kuoga alichukua pochi yenye pesa na kutoka kumsubiri shoga yake, baada ya muda Mwajuma alifika na Bajaj ambapo Sara aliingia na kuelekea Tandale kwa mzee Gogo. Kwa vile walipitia njia za nyuma walikwepa foleni na kufanikiwa kufika kwa mzee huyo mapema.
Walikuta watu bado hawajaondoka, walikaa kwenye benchi kusuburi muda wa kuingia ndani. Wakiwa wamekaa kwenye benchi alitoka mzee wa makamo kichwa chote kilikuwa kimejaa mvi aliyekuwa amevaa fulana ya mikanda chini alijifunga kaniki. Kwa vile alikuwa amezoeana na Mwaju alipomuona alishtuka na kumuuliza. “Vipi tena mama, mbona usiku?” “Shida tu mzee wangu.” “Karibu hapa ndiyo kwa mzee Gogo asiyeshindwa na kitu.” “Asante, vipi tutapata upendeleo?” “Nipe dakika kumi nitakuiteni.” Mzee Gogo alikwenda kwenye mti uliokuwa pale uani na kuchukua vitu kisha alirudi ndani kuendelea na kazi. Baada ya muda alitumwa mtu kwenda kuwaita, waliingia ndani na kukaa kwenye mkeka. “Karibuni.” “Asante.” Mzee Gogo alitulia kwa muda akipanga vizuri dawa zake kisha alinyanyua macho na kusema: “Mmh! Mabinti mna tatizo gani?” “Shoga yangu ndiye mwenye tatizo.” “Eti mama una tatizo gani?” alimgeukia Sara. Sara alimueleza mikasa iliyomkuta na jinsi mganga aliyekwenda jioni ile kukataa kumtibu. Baada ya kumsikiliza alichukua kikopo kilichokuwa na unga mweupe ambapo alichota kidogo na kuumwaga mbele yake na kutulia kama anatazama kitu. Alitulia akikaza macho kwenye unga ule kisha alisema: “Ni kweli kabisa ni jini.” “Nani?” “Huyu mpenzi wa bosi wako.” “Mungu wangu una maanisha Shehna?” “Ndiyo.” “Sasa tutafanyaje?” “Wewe unataka tumfanyeje?” “Tumpoteze kabisa.” “Kumpoteza itakuwa vigumu kwa vile tayari amekuwa mpenzi wa bosi wako.” “Na ndiye aliyenitesa vile?” “Ndiyo.”
“Tumfanyeje ili kuvunja penzi na bosi wangu pia asinifuatefuate?” “Kuvunja urafiki ni vigumu kwa vile tayari ana ujauzito wa bosi wako.” “Sasa tutafanya nini?” “Labda kumuua tu.” “Sawa.” Baada ya kusema vile alichukua chupa ndogo na bakuli dogo na kumimina maji yake kisha alizungumza maneno ambayo hawakuyaelewa. Ghafla mganga alinyamaza na kuanza kung’ata maneno mara mtetemeko mkubwa ulitokea ndani ya chumba cha uganga lakini nje hakuna aliyejua nini kinaendelea. Wakiwa wameingiwa na wasiwasi walishtuka kumuona mganga akijishika mikono shingoni kama anamzuia mtu asimkabe na kuliacha bakuli likianguka chini na kumwaga maji. Sara na shoga yake walishtuka kumuona mganga akihangaika kama anapigana na mtu aliyeonekana kumkaba shingoni ambaye hawakumuona. Mara walimuona akianguka kama mzigo huku mikono yake ikiwa bado shingoni na kuanza kurusha miguu na kufanya dawa zilizokuwa pembeni yake kutawanyika ovyo. Walinyanyuka walipokuwa wamekaa kwa woga, mganga aliendelea kurusha miguu kama kuku aliyekatwa kichwa kisha alitulia. Baada ya kutulia waliogopa kumsogelea na kutoka nje kumwita msaidizi wake. Aliingia na kwenda alipokuwa amelala mzee Gogo. Walimkuta macho na ulimi vimemtoka nje akiwa amekufa. Sara na shoga yake waliona msala utawageukia walitoka taratibu bila kuaga na kurudi nyumbani. Njia nzima Sara alijiuliza maswali na kukumbuka maneno ya mganga wa Vingunguti aliyemweleza kuwa mganga yeyote atakayetaka kuingilia kesi ile lazima moto umuwakie. Alipofika kwake aliteremka na kumuacha shoga yake akirudi nyumbani kwake Kigogo.
Alipofika alijikuta akizidi kukosa amani moyoni mwake na kujiuliza nini hatima yake baada ya kukaidi amri ya sauti ya kuacha kufuatilia mambo yasiyo muhusu Kilishomshtua zaidi kujua Shehna ni jini na ndiye aliyekuwa akimfanyia mauzauza yale. Alijiuliza atamtazamaje hasa baada ya kumuasa aache kufuatilia mambo yasiyo muhusu. Alipofika nyumbani hakuwa hata na hamu ya kula, alinunua soda na keti, alikula kisha alioga na kupanda kitandani. Usiku wa manane akiwa amelala alishtushwa na sauti kali ya vicheko mfululizo, alifumbua macho kutazama na kukutana na kiza kizito. Vicheko viliendelea mpaka kikawa kero masikioni mwake, mapigo ya moyo yalimwenda mbio kwa hofu. Alipapasa pembeni ya kitanda na kushika swichi ya kitandani na kuwasha taa. Ilipowaka alishtuka kuona viumbe wa ajabu mbele yake wakiwa wamesimama sambamba na ukuta. Walikuwa watu weusi sana wanne wenye mikia mifupi kama ya mbuzi na pembe ndogo kichwani. Sara alishtuka na kutetemeka kwa hofu huku haja ndogo ikimtoka bila kujijua.
Alijiuliza wale ni kina nani na wamefuata nini, wazo lake lilielekea moja kwa moja kwa wachawi. Akiwa bado hajajua nini kinaendelea aliiona ardhi ikipasuka na kuingia mwanamke aliyekuwa amekaa kwenye kiti cha dhahabu cha kifalme kilichokuwa kimebebwa mabegani na wanaume wengine wanne weusi wenye miili mikubwa na mikia kama wenzao lakini hao walikuwa na pembe moja katikati ya kichwa tofauti na wale wengine waliokuwa na pembe mbili. Wale viumbe wa ajabu waliendelea kukibeba juu kiti kilichokaliwa na mwanamke mrembo mpaka ardhi iliyopasuka kujifunga ndipo walipomtua chini. Sara aliendelea kutetemeka huku akiwa amejikunyata upenuni mwa kitanda akiwa umesogea ukutani kabisa. Yule mwanamke alikuwa amempa mgongo, alipopiga kofi aligeuzwa kumtazama, Sara hakuamini macho yake kumuona aliyekuwa mbele yake ni Shehna rafiki wa bosi wake. Baada ya kutulia alipiga makofi, viumbe vile vya ajabu vilitoweka na kubakia peke yake akiwa bado amekaa kwenye kiti chake cha dhahabu. Baada ya kubaki wawili, Shehna aliteremsha pumzi nzito na kunyanyuka kwenye kiti na kusimama. Alimtazama Sara aliyekuwa bado amejikunja pembeni ya ukuta kwa woga. Alitembea taratibu kukizunguka chumba, alipompa mgongo alishtuka kumuona Shehna ana mkia mkubwa kama wa kangaroo lakini ule ulikuwa umenenepa sana. Alipofika mwisho wa ukuta aligeuka akiwa amegeuka sura yake na kuwa ya kutisha meno yake yaligeuka kama ya ngiri juu ya paji la uso kulikuwa na pembe mbili kama za faru. Macho yake yalikuwa yakiwaka moyo, alicheka kicheko kizito kilichofanya Sara atokwe damu masikioni. Shehna alikuwa kiumbe cha kutisha ambacho Sara hakuwahi kukiona maishani mwake, kwa sauti kali Shehna alisema huku moto ukitoka mdomoni. “Sara umenichimba sana, sasa umenijua haya niambie shida yako?” “Ni..ni ..samehe She..she…” “Sara sitakusameha lazima utajua faida ya kiburi chako, nilikuonya kwa sauti hukusikia nikaja mwenyewe hukunielewa, nina imani ulitaka uone nini kitatokea baada ya wewe kufuatilia mambo yasiyokuhusu. Nimekutisha ninavyojua lakini kichwa chako kimejaa kiburi nami nataka nikuonesha jeuri yangu. “Sitakuua bali nitakupa adhabu ya kipindi chote nitakapokuwa sipo chagua adhabu moja, nikugeuze Nguruwe, Chura, Funza maisha yako yote yawe kwenye kinyesi, bundi au mbwa?”
Sara hakujibu, alijitahidi kumsogelea Shehna ili amuombe msamaha. “Shehna nisamehe shoga yangu.” “Wewe si shoga yangu, mlitaka kuniua na mganga wako bila kosa, nimekukosea nini Sara?” Shehna alirudi katika umbile la kibinaadamu na kuanza kulia machozi ya damu. “Ni sa..samehe sirudii tena.” “Sitaki kusikia sauti yako, umetaka kunijua leo umenijua mimi ni jini, ujini wangu umekuathiri nini katika maisha yako?” “Najua nimekukosea naomba unisamehe sirudii tena.” “Sara sitakusamehe ukichelewa kuchagua adhabu yako nitakugeuza kiumbe cha ajabu kisicho na mfano.”
Sara alijikuta kwenye wakati mgumu wa kuamua ageuzwe kiumbe gani, kabla hajapata jibu Shehna alipiga makofi mara walitokea viumbe wawili vya ajabu vinavyotisha sana tofauti na vyote vilivyotangulia. “Naam binti wa mfalme wa bahari ya dhahabu una shida gani?” “Enyi watwana wenye roho chafu nataka mumtafutia adhabu yoyote kali huyu mwanadamu mnataka nimepa adhabu gani?” “Kwa nini tusimbanike kama mbuzi karibu na jua?” mmoja alipendekeza adhabu. “Hapana adhabu hiyo kali sana, nataka ya kumtesa ili atambue siri aliyoitaka kuijua faida yake ni nini.” “Sisi hatuwezi kuchagua adhabu ndogo binti wa mfalme, tunaomba wewe uchague adhabu yoyote kwake tunajua amekuudhi sana. Adhabu yetu kwake ni kifo tena cha maumivu makali zaidi ya hapo hatuna adhabu.” “Basi mnaweza kunipisha nitoe adhabu yangu.” Baada ya kusema vile viumbe wa ajabu alitoweka na kubakia Shehna katika umbile la kawaida la mwanamke nzuri katika vazi pana kutokana na ujauzito wake na Sara ambaye alikuwa akitetemeka mpaka utumbo. Alimuangalia kwa muda Sara aliyekuwa amejikunyata kwa woga upenuni mwa kitanda kwa sauti ya upole alimwita. “Sara.” “A..a..bee.” “Unaniweka katika wakati mgumu katika maisha yangu wa kukufanya kitu kibaya. Sikupenda kukufanyia chochote kibaya, narudia nimejitahidi kukuelekeza lakini umekuwa na masikio ya kenge mpaka utoke damu. Kwa vile umekataa kuchagua adhabu mimi nitakuchagulia adhabu, nilifikilia nikugeuze nguruwe lakini hiyo kwangu ni adhabu kubwa, nimejifikilia kukugeuza funza maisha yako yake kwenye kinyesi nayo hiyo nimeona ni adhabu kubwa. “Adhabu ndogo kuliko zote nimeonelea nikugeuze uwe mbwa ambaye atakuwa unazurura mitaani na kupigwa nawe na lakini sitaruhusu wakuue. Chakula chako nitakijua mimi utakula mara moja kwa siku. Nina imani utajua thamani ya kiburi chako.” “Nitakuwa mbwa mpaka lini?” Sara alijitahidi kuuliza. “Mpaka nitakapojifungua.” “Shehna shoga yangu hakuna adhabu nyingine zaidi ya hiyo?” “Sara mimi huwa sitoi adhabu bali umewaona watoa adhabu na adhabu zao, kama ningewaachia sijui ungekuwa kwenye hali gani?” “Nipunguzie shoga yangu.” “Sara unanichelewesha muda wangu umekwisha.” Baada ya kusema vile alinyoosha kidole ghafla Sara aligeuka mbwa, kisha Shehna alipiga makofi na viumbe wa ajabu walitokea. Aliwaonesha ishara ya macho huku akipanda kwenye kiti chake. Walikibeba juu ghafla ardhi ilipasuka na wao kuzama ndani yake kisha alijifunga na kuwa kama mwanzo. Sara alibakia juu ya kitanda huku akiamini yeye ni mtu wala siyo mbwa, lakini bado hakuamini kilichotokea ni kweli zaidi ya kuota ndotoni. Siku ya pili aliamka asubuhi kama kawaida na kutoka nje kwenda kuoga ili awahi kazini lakini watoto wa jirani walipiga kelele kumuona mbwa. Kitendo kile kilimfanya Sara arudi ndani lakini alishangaa kusikia. “Amekimbilia ndani kwa ma’ mdogo Sara,” alisema mtoto mmoja. “Kwani Sara yupo wapi?” alimsikia jirani yake mama Saidi akiuliza. “Sara..Sara,” Happy alimwita kwa sauti. Sara aliyekuwa chumbani kwake aliitika kwa sauti. “Abee nimo ndani,” lakini ilitoka sauti ya mbwa kufoka. “Jamani mbwa huyu katokea wapi na Sara kaenda wapi asubuhi yote na kuacha mlango wazi,” jirani mwingine alisikika akisema. “Jamani tufanyeni msaada wa kumtoa huyo mbwa ndani,” mtu mwingine alitoa wazo huku majirani wakizidi kukusanyika. “Na kweli labda kichaa anaweza kutuuma pia hata watoto wetu.” Jirani mmoja alishika fimbo na kuingia chumbani kwa Sara na kushtuka kumuona mbwa juu ya kitanda. Alimtishia kumpiga ili atoke nje lakini Sara alitaka kujitetea kwa kuwaeleza kuwa yeye si mbwa ni mtu kama watu wengine lakini aliishia kumfokea kitu kilichoonesha anataka kumuuma. Ilibidi jirani amtandike fimbo iliyomfanya Sara atoe ukelele wa maumivu na kutoka nje ili kuokoa kipigo kile na kutokomea mitaani. Kila mtaa alipopita watoto walimpiga mawe kitu kilichozidi kumweka kwenye wakati mgumu yeye alijifahamu ni mwanadamu na si mbwa lakini kila kona alipopita aliitwa mbwa. Alitafuta jumba bovu na kuingia humu kujificha japokuwa kulikuwa na kinyesi ambacho kilimnukia harufu mbaya. Lakini aliamini ile ni sehemu salama kwake kuliko kuzurula mitaani na kupugwa mawe na watoto.
Sara alijikuta kwenye wakati mgumu wa kuamua ageuzwe kiumbe gani, kabla hajapata jibu Shehna alipiga makofi wakatokea viumbe wawili wa ajabu wanaotisha sana tofauti na waliotangulia. “Naam binti wa mfalme wa bahari ya dhahabu una shida gani?” “Enyi watwana wenye roho chafu nataka mumtafutie adhabu yoyote kali huyu mwanadamu, mnataka nimpe adhabu gani?” “Kwa nini tusimbanike kama mbuzi karibu na jua?” mmoja alipendekeza adhabu. “Hapana adhabu hiyo kali sana, nataka ya kumtesa ili atambue siri aliyoitaka kuijua faida yake ni nini.” “Sisi hatuwezi kuchagua adhabu ndogo binti wa mfalme, tunaomba wewe uchague adhabu yoyote kwake tunajua amekuudhi sana. Adhabu yetu kwake ni kifo tena cha maumivu makali zaidi ya hapo hatuna adhabu nyingine.” “Basi mnaweza kunipisha nitoe adhabu yangu.” Baada ya kusema vile wale viumbe wa ajabu walitoweka na kubakia Shehna katika umbile la kawaida la mwanamke mrembo katika vazi pana kutokana na ujauzito wake na Sara ambaye alikuwa akitetemeka mpaka utumbo. Alimuangalia kwa muda Sara aliyekuwa amejikunyata kwa woga ubavuni mwa kitanda, kwa sauti ya upole alimwita. “Sara.” “A…a…bee.” “Unaniweka kwenye wakati mgumu katika maisha yangu wa kukufanya kitu kibaya. Sikupenda kukufanyia chochote kibaya, narudia nimejitahidi kukuelekeza lakini umekuwa na masikio ya kenge mpaka utoke damu. Kwa vile umekataa kuchagua adhabu mimi nitakuchagulia adhabu. Nilifikiria nikugeuze nguruwe lakini hiyo kwangu ni adhabu kubwa, nimejifikiria kukugeuza funza wa kwenye kinyesi maisha yako nayo nimeona ni adhabu kubwa. “Adhabu ndogo kuliko zote nimeonelea nikugeuze uwe mbwa ambaye atakuwa unazurura mitaani na kupigwa mawe lakini sitaruhusu wakuue. Chakula chako nitakijua mimi, utakula mara moja kwa siku. Nina imani utajua thamani ya kiburi chako.” “Nitakuwa mbwa mpaka lini?” Sara alijitahidi kuuliza. “Mpaka nitakapojifungua.” “Shehna shoga yangu hakuna adhabu nyingine zaidi ya hiyo?” “Sara mimi huwa sitoi adhabu bali umewaona watoa adhabu na adhabu zao, kama ningewaachia sijui ungekuwa kwenye hali gani?” “Nipunguzie shoga yangu.”. “Sara unanichelewesha muda wangu umekwisha.” Baada ya kusema vile alinyoosha kidole ghafla Sara aligeuka mbwa, kisha Shehna alipiga makofi na viumbe wa ajabu walitokea. Aliwaonesha ishara ya macho huku akipanda kwenye kiti chake. Walikibeba juu ghafla ardhi ilipasuka na wao kuzama ndani yake kisha alijifunga na kuwa kama mwanzo. Sara alibakia juu ya kitanda huku akiamini yeye ni mtu wala siyo mbwa, lakini bado hakuamini kilichotokea ni kweli zaidi ya kuota ndotoni. Siku ya pili aliamka asubuhi kama kawaida na kutoka nje kwenda kuoga ili awahi kazini lakini watoto wa jirani walipiga kelele kumuona mbwa. Kitendo kile kilimfanya Sara arudi ndani lakini alishangaa kusikia. “Amekimbilia ndani kwa ma’ mdogo Sara,” alisema mtoto mmoja. “Kwani Sara yupo wapi?” alimsikia jirani yake mama Saidi akiuliza. “Sara…Sara,” Happy alimwita kwa sauti. Sara aliyekuwa chumbani kwake aliitika kwa sauti. “Abee nimo ndani,” lakini ilitoka sauti ya mbwa kufoka. “Jamani mbwa huyu katokea wapi na Sara kaenda wapi asubuhi yote na kuacha mlango wazi,” jirani mwingine alisikika akisema. “Jamani tufanyeni msaada wa kumtoa huyo mbwa ndani,” mtu mwingine alitoa wazo huku majirani wakizidi kukusanyika. “Kweli labda kichaa anaweza kutuuma pia hata watoto wetu.” Jirani mmoja alishika fimbo na kuingia chumbani kwa Sara na kushtuka kumuona mbwa juu ya kitanda .
Alimtishia kumpiga ili atoke nje lakini Sara alitaka kujitetea kwa kuwaeleza kuwa yeye si mbwa ni mtu kama watu wengine lakini aliishia kumfokea kitu kilichoonesha anataka kumuuma. Ilibidi jirani amtandike fimbo iliyomfanya Sara apige kelele kwa maumivu na kutoka nje ili kujiokoa na kipigo kile na kutokomea mitaani. Kila mtaa alipopita watoto walimpiga mawe kitu kilichozidi kumweka kwenye wakati mgumu, yeye alijifahamu ni mwanadamu na si mbwa lakini kila kona alipopita aliitwa mbwa. Alitafuta jumba bovu na kuingia humo kujificha japokuwa kulikuwa na kinyesi ambacho kilikuwa na harufu mbaya, lakini aliamini ile ni sehemu salama kwake kuliko kuzurura mitaani na kupigwa mawe na watoto. *** Shehna baada kumtia adabu Sara japokuwa moyo wake haukupenda kutoa adhabu yoyote, alirudi nyumbani kwao na kuingia chumbani kwake na kuanza kulia sana, kitu kilichomshtua mama yake Bi Zaldau, mke wa mfalme wa bahari ya dhahabu aliyempenda sana mwanaye Shehna kama mboni ya jicho lake, hakupenda hata siku moja kumuona akiumizwa na kitu. Akiwa amejipumzisha chumbani kwake, alishtuka kuona machozi yamemdondokea kifuani, ile ilimjulisha mwanaye ana tatizo na muda ule alikuwa akilia. Alijiuliza kipenzi chake Shehna kipi kimempata mpaka kulia machozi mengi yaliyomfikia yeye, alikwenda moja kwa moja chumbani kwa mwanaye na kumkuta akiendelea kulia. “Shehna,” alimwita na kumfanya mwanaye ashtuke na kujifuta machozi haraka kisha alimgeukia mama yake. “Shehna mwanangu una tatizo gani mama?” “Hapana mama sina tatizo bali nimemkumbuka mpenzi wangu Mustafa.” “Shehna nilikueleza mapema kuwa kama unamtaka mwanadamu, mtafute asiye na mke ungeweza kuja naye huku.” “Mama, Mustafa nilimpenda muda mrefu sana lakini ninyi ndiye mliyenichelewesha kuonana naye mpaka akaoa mwanamke mwingine.” “Ulikuwa bado hujatimiza umri wa kukutana na mwanaume.” “Hata kama bado, nilitakiwa nionane naye mapema ili asioe mwanamke mwingine anisubiri mimi.” “Hilo kweli tulifanya kosa, lakini mbona linawezekana kurekebishika.” “Utalirekebisha vipi wakati ana mke tayari?” “Si tunampoteza mkewe.” “Hapana mama siwezi kufanya hivyo, kosa la mkewe lipi mpaka apotezwe?” Shehna alimkatalia mama yake kumuua mke wa Mustafa. “Basi tumfanye asiwe na hamu na mumewe.” “Vilevile sioni kosa lake.” “Halafu mbona inaonesha kinachokuliza sicho unachonieleza, ulitoka na Kubash, mlikwenda wapi halafu juzi nilimuona Shush akiwa na damu mikononi, kuna nini ambacho sikijui?” mama Shehna mke wa mfalme wa bahari ya dhahabu Malkia Bi Zaldau alihoji. “Mama ndicho kinachoniliza, kuna msaidizi wa Mustafa ananifuatilia sana, nimejaribu kumtisha lakini hasikii. Jana usiku alikwenda kwa waganga wawili, mmoja alikataa kumtaka kumfanyia kazi yake lakini wa pili alikubali na kutaka kuniua. Wakati nimejilaza, nilianza kupoteza nguvu na kumwita Shush haraka awahi kumzima yule mganga kwani angechelewa ningekufa mimi.” “Sasa umempa adhabu gani?” “Nimemgeuza mbwa.” “Shehna mtu anataka kukuua, unamgeuza mbwa adhabu gani hiyo isiyolingana na dhamira yake mbaya?” mama yake alikasirika. “Mama hata kumgeuza mbwa kwangu nimeona ni adhabu kubwa sana, nilitaka kumuacha lakini imebidi nifanye hivyo.” “Mwanangu huruma gani hiyo ya kujiumiza?” “Mama, kosa lake kwenda kwa mganga bila hivyo wala asingenisumbua, nimemuua mganga kwa vile alitaka kuniua, zaidi ya hapo nisingesumbuka naye.” “Mmh! Sasa kinakuliza nini?” “Sipendi kuingia katika dhambi ya kulazimishwa.” “Basi kama umempa hiyo adhabu inatosha, usilie mwanangu.” “Sawa mama nimekuelewa.” Shehna alijilaza kifuani kwa mama yake kuonesha amekubaliana naye.” *** Mustafa alishtuka, siku ya pili alishtuka kufika kazini na kukuta ofisi bado imefungwa, alifungua na kuingia ndani. Ofisi ilikuwa chafu, hata hali ya hewa ilikuwa mbaya. Alijiuliza Sara atakuwa wapi mpaka muda ule, kitendo cha kuchelewa kazini kilizidi kumfanya amchukie Sara na kupanga akifika lazima amfukuze kazi. Alishindwa kukaa ndani kutokana na hali aliyokuwemo na kutoka nje, alikwenda hadi kwa mlinzi ili akamwambie afanye usafi. Kabla hajafika kwa mlinzi, simu yake iliita. Alipoangalia ilikuwa inatoka kwa mpenzi wake Shehna. Aliipokea na kuzungumza. “Haloo mpenzi.” “Haloo laaziz, vipi mpenzi wangu?” “Safi tu.” ITAENDELEA
“Haloo laaziz, vipi mpenzi wangu?” “Safi tu.” “Mbona kama mnyonge?” “Bwana huyu msichana ananichanganya sana.” “Kafanya nini?” Shehna alijifanya kuuliza. “Hajafika mpaka saa hizi yaani ofisi chafu.” “Basi usikonde mpenzi wangu baada ya dakika mbili watakuja wasichana wangu kuja kufanya usafi uwape nafasi tu.” “Hakuna tabu.”
Baada ya muda kidogo wasichana wawili warembo walibisha hodi kwenye geti, Mustafa alipowatazama alijua ndiyo waliotumwa na mpenzi wake Shehna. “Asalaam aleykum,” wale wasichana waliwasalimia kwa bashasha na sauti tamu. “Waleykum salaam, nina imani ninyi ni wageni wangu?” Mustafa aliuliza. “Swadakta, hatuna muda tuoneshe hiyo kazi.” Mustafa aliongozana nao hadi ofisini, baada ya kuwaonesha mmoja alisema: “Haya tupishe tufanye usafi.” “Hakuna tatizo,” Mustafa alijibu huku akitoka nje na kuwaacha wale wasichana. Baada ya kutoka walipiga makofi, haikuchukua muda waliongezeka wengine ambao walifanya kazi ya usafi kwa muda mfupi. Baada ya usafi wenzao walitoweka na kuwaacha wale wawili. Nao walitoka hadi alipokuwa amekaa Mustafa getini na mlinzi walipokuwa wakizungumza tabia za Sara zilivyobadilika tofauti na zamani. Walipofika walimweleza kwa sauti tamu yenye lafudhi ya kimwambao. “Bwana sisi tunakukimbia tuna imani utafurahia usafi wetu.” “Nina waamini, nashukuru sana.” “Haya si tukukimbie.” “Haya, msalimieni sana Shehna.” “Salamu zimefika.” Wasichana wale walitoka nje ya geti na kutembea kufuata barabara, baada ya kuwa sehemu ambayo walijua Mustafa hawaoni walitoweka ghafla kurudi chini ya bahari. Mustafa alirudi ofisini na kuikuta ofisi inapendeza kila kitu kilikuwa kimesafishwa ndani kulikuwa na hewa na harufu nzuri ya manukato. Alikaa kitini na kuanza kazi huku akiamini kama atamuoa Shehna basi ataishi maisha sawa na peponi. *** Kila usiku Mustafa alifuatwa akiwa ndotoni na kujikuta yupo sehemu nzuri akiwa amelala pembeni ya Shehna aliyekuwa amelala huku tumbo lake likizidi kukua. Lakini alikuwa amevaa gauni jepesi lililoziba tumbo lake. Usiku sana Shehna alizima taa na kuondoa nguo zake na kumruhusu Mustafa alichezee tumbo lake lakini ikiwa gizani. Siku zote Mustafa alifurahi kuwa karibu na mpenzi wake na kutamani siku zote awe karibu yake. Tumbo la Shehna halikuwa likimsisimua lakini hakupata nafasi ya kuliona, siku zote alimbembeleza kuliona Shehna alimwambia avute subira. Mustafa alikubaliana na mpenzi wake. Katika siku alizolala alishangaa tumbo la Shehna kuwa kubwa akilala akiwa hana nguo tofauti na akimkuta amevaa nguo. Ile ilimfanya apange kumvizia wakati amelala ili awashe taa aone sababu ya tumbo lile kuwa kubwa tofauti na matumbo ya kawaida ya wanawake wenye mimba. Wakati huo Sara aliendelea kuteseka na baridi na njaa hakutoka kwenye nyumba ile mbovu mpaka kiza kilipoingia, aliogopa kutoka muda ule kwa kuhofia kupigwa na kuumizwa. Kiza kilipoingia ndipo alipotoka na kurudi nyumbani, lakini alipofika sehemu ya chumba chake ambacho kilikuwa kimefungwa alisikia mtu akisema: “Jamani yule mbwa wa asubuhi amerudi tena.” “Jamani huyu mbwa atakuwa ametumwa tu, tena amesimama kwenye chumba cha Sara.” “Jamani lazima kutakuwa na tatizo, Sara jana si alilala chumbani kwake ajabu asubuhi tukumuona na kukuta mlango upo wazi na mbwa huyu alitoka ndani. Ajabu tulimfukuza asubuhi usiku amerudi,” shoga yake Happy alisema. “Sasa na Sara atakuwa wapi?” “Hapa ndipo tunachanganyikiwa maana hajaaga kama amepata dharura usiku.” Sara yote aliyasikia akiwa bado amesimama kwenye mlango wake, lakini alishindwa kuzungumza kwa kuhofia kubweka na kuwatisha kitu kitakachowafanya wamfukuze kwa kumpiga.
“Hapa ndipo tunachanganyikiwa maana hajaaga kama amepata dharura usiku.” Sara yote aliyasikia akiwa bado amesimama kwenye mlango wake, lakini alishindwa kuzungumza kwa kuhofia kubweka na kuwatisha, jambo ambalo lingewafanya wamfukuze kwa kumpiga. Akiwa bado amesimama mlangoni alisikia akiitwa jirani yake kwa sauti aje amfukuze. “Baba John, yule mbwa wa asubuhi amerudi tena,” mama John alimwita mumewe. Sara alijua majanga bado yanamuandama, alilia kilio cha kimyakimya kwa kuogopa kutoa sauti kuwatisha. Alijiuliza atajitetea vipi ikiwa hawezi kuzungumza sauti ya kibinadamu. Alimuona jirani yake baba John akitoka ndani na kuuliza: “Yupo wapi?” “Yule pale kwenye mlango wa Sara.” “Huyu mbwa anatafuta kufa hapa subiri,” alisema kwa sauti ya hasira aliyoisikia Sara. Baba John alisogea pembeni na kuchukua gongo ili ampige, Sara alishangaa kusikia sauti iliyokuwa ikimtokea bila kumuona anayezungumza ikisema: “Sara ondoka haraka watakuumiza.” Sara hakuchelewa alitimua mbio, alipoondoa mguu tu gongo lilitua kwenye mlango na kutoa sauti, alisikia sauti ya baba John akisema: “Bahati yake lingempata angekufa, ——- kafie mbele kama umetumwa.”
Kilichomuumiza akili kilikuwa ukubwa wa tumbo kila wakizima taa lakini akiwa na nguo zake za kulalila ilikuwa mimba ya kawaida. Alijiuliza kwa nini wakizima taa linakuwa kubwa na kingine kwa nini hataki kumruhusu kulichezea tumbo lile kwenye mwanga! Alipanga siku ile usiku amtegee Shehna amelala awashe taa ili kutaka kujua kwa nini usiku tumbo lake linakuwa kubwa sana. Aliendelea na kazi kama kawaida huku taarifa za Sara zikizidi kumchanganya kutokana na kuelezwa hajulikani halipo wala hakuaga. Mazingira ya kutoweka yalikuwa yakilingana na ya mara ya kwanza kitu kilichomfanya ajiulize Sara ana matatizo gani yanayosababisha kutoweka bila taarifa. Alikumbuka maelezo aliyopewa na Sara siku aliyorudi kazini baada ya kupotea kimiujiza alitoka kwenda kununua chakula cha usiku na kujikuta akiwa katika pori la kutisha na baada ya kutembea bila kujua na kutokea Dodoma. Kingine kilichomshtua kuambiwa kuna mbwa alikutwa chumbani kwa Sara baada ya kumfukuza alirudi tena usiku na kusimama kwenye mlango uleule. Alijiuliza kipi hasa kimempata Sara na ana siri gani ambayo yeye na majirani zake hawaijui. Alipanga akienda kwa Shehna kumueleza tatizo lile labda angeweza kumsaidia. Usiku ulipoingia kama kawaida aliposhtuka usingizini alijikuta yupo pembeni ya mpenzi wake Shehna. Kama kawaida tumbo lilikuwa la kawaida lililokuwa katika nguo nyepesi ya kulalia. Baada ya kuliwazana wote walipitiwa usingizi, Mustafa
hakulala sana alishtuka mapema na kutulia kitandani alilichezea tumbo la Shehna ambalo lilikuwa haliishi hamu kwa vile lilimpa raha ya ajabu kila alipolipapasa. Alitulia kwa muda kusubiri Shehna usingizi umkolee, baada ya muda alimsikia akikoroma. Alijua usingizi umemkolea. Aliteremka kitandani taratibu na kuelekea kwenye kandili ya dhahabu, aliiwasha huku akitetemeka aliipandisha mwanga ili aone vizuri. Baada ya kuwasha taa na kumulika kitandani, alishtuka kuona kiumbe cha ajabu juu ya kitanda. Sura ilikuwa ya mpenzi wake Shehna lakini tumbo lake lilikuwa la ajabu lililokuwa kubwa na pembeni lilikuwa na rangi kama magamba ya nyoka na chini alikuwa na mkia mnene unaoungana na tumbo. Mustafa alishtuka sana na kuanza kutetemeka, kingine kilichomshtua kuona kitanda walichokuwa wamelalia kilikuwa juu ya maji katika ya bahari. Mshtuko uliompata ulimfannya aanguke chini na kupoteza fahamu. Baridi kali lilimuamsha Shehna usingizini, alipofumbua macho alishtuka kukuta amelala juu ya bahari. Haraka alijirudisha katika umbile la kawaida, palepale usiku mwili wake ulirudi kama kawaida na kuwa chumbani kwake lakini kandili ilikuwa ikiwaka. Alijiuliza nani aliyeiwasha taa ile, alishangaa kujikuta peke yake na kujiuliza Mustafa alikuwa wapi! Alipoteremka kitandani alishtuka kumkanyaga mtu, alipoangalia alimuona Mustafa akiwa amelala chini amepoteza fahamu. Alijua tayari siri yake ilikuwa hadharani, alijiuliza atamwambia nini Mustafa amuelewe kuwa yeye ni jini pia alijiuliza akimueleza ukweli atakuwa tayari kuendelea kuwa naye! Shehna alianza kulia kitu kilichomshtua mama yake baada ya kudondokewa na machozi. Malkia Bi Zaldau mke wa mfalme wa bahari ya dhahabu alikwenda katika chumba cha mwanaye. Alipofika alimkuta jasho likimtoka japokuwa kulikuwa na hali ya baridi, alishangaa kumuona Mustafa amelala chini. “Vipi?” Shehna ilibidi amweleze mama yake kilichotokea aliposhtuka usingizini.
*** Siku zilizidi kukatika huku Mustafa akiwa katika hali ya ububu na Sara akiwa katika umbile la mbwa. Mateso makubwa yalikuwa kwa Sara ambaye aliendelea kuishi maisha ya kujificha kukimbia watoto kumpiga mawe na kulala kwenye majumba mabovu. Chini ya bahari, Shehna alipata nafuu haraka sana na kuweza kukaa hata kula mwenyewe baada ya kupoteza fahamu kwa miezi mitatu iliyotishia uhai wake. Kukubali kwa Mustafa kuendelea kuwa katika hali ya ububu na kuyakubali maelekezo ya mganga, ile ilimsaidia sana kuwahi kupata nafuu. Kama mkewe Mustafa angekuwa mbishi lazima angewapoteza mumewe na
Shehna pamoja na watoto waliokuwa tumboni. Baada ya kupata nafuu alitaka kujua Mustafa yupo katika hali gani kwani aliamini hasira za mama yake lazima angemfanya kitu kibaya. Katika vitu vyote alimkataza mama yake kumuua hata kumpa adhabu kali mpenzi wake. “Mama mpenzi wangu yupo katika hali gani?” “Nilimgeuza bubu ili asitoe siri mpaka muongee wenyewe na kukubaliana.” “Nimepona, vipi hali yake kwa sasa?” “Bado sijamtoa ububu lakini niliyaangalia maisha yake ya siku zote, ila amenifurahisha kutotafuta dawa kwa ajili ya kutibu ububu. Kitendo kile kimesaidia wewe kupata nafuu upesi.” “Mustafa ni msikivu sijui kwa nini siku ile hakutaka kunielewa mpaka akawasha taa.” “Wewe ndiye mwenye makosa, ulitakiwa kujitambulisha mapema kwa vile alikuwa akikupenda sana, angekuelewa.” “Mama nilihofia kumueleza mimi jini, angenikimbia.” “Ona sasa alikuwa anatoa siri nje kwa vile alikuwa hakuelewi, kila kitu kingekuwa wazi, ububu na uelewa wake ndiyo nafuu yako, bila hivyo ungekufa, hali ilikuwa mbaya.” ‘Sasa nifanye nini?” “Aletwe leo aambiwe ukweli lazima atakuelewa tu.” “Sawa mama.” Malkia Zaldau mke wa mfalme wa bahari ya dhahabu mama wa Shehna walikubaliana na mwanaye usiku wa siku ile Mustafa apelekwe chini ya bahari. *** Mustafa alishituka usingizini na kujikuta akiwa pembeni ya Shehna ambaye tumbo lake lilikuwa limeongezeka katika umbile la kibinadamu lililokuwa ndani vazi la kulalia. Shehna alikuwa akimtazama huku macho yakiwa yamejaa machozi na kuongeza uzuri wake. “Shehna.” “A..abeee,” aliitikia kwa sauti ya kilio. “Nisamehe mpenzi wangu.” “Huna kosa, nisamehe mimi.” “Kwa kosa gani mpenzi?” “Nimekutia kwenye mateso bila kosa.” “Shehna huna kosa bali mimi ndiye niliyeshindwa kukusikiliza.” “Hapana Mustafa mwenye makosa ni mimi kushindwa kukueleza ukweli mapema.”
*** Siku iliyofuata Sara alishtuka asubuhi na kujikuta kitandani kwake, aliamka na kwenda kuoga. Alipotoka nje, majirani zake walimshangaa na kumuuliza alikuwa wapi. Aliwajibu alikuwa safari ila wangezungumza vizuri jioni akirudi kazini. Alikwenda kazini kama kawaida. Akiwa kazini alijawa na mawazo mengi juu ya maswali ya majirani zake, alijiuliza akirudi atawaeleza alikuwa wapi baada ya kuondoka ghafla. Mawazo yalipokuwa mengi, aliamua kwenda kwa bosi wake kuomba ushauri, baada ya kumsikiliza alimwambia: “We wanyamazie tu.” “Wasumbufu sana watataka kunichimba, nitashindwa kuwajibu.” “Ulikuwa na wazo gani?” “Kuhama pale.” “Hakuna tatizo.” Mara simu iliita Mustafa alipoangalia alikuta ni Shehna, alisema kwa sauti. “Shehna.” “Anasemaje shoga yangu,” Sara alisema kwa tabasamu. Alipokea simu: “Haloo mpenzi.” “Nipe Sara.” Mustafa alimpa simu Sara. “Haloo shoga,” Sara alisema baada ya kuchukua simu. “Ni hivi, ukitoka hapo usirudi nyumbani, umeshahamishwa.” “Nimehamishiwa wapi?” “Masaki, nyumba inatazamana na duka la jumla, nina imani hayo yatakuwa maisha yako mapya.” “Asante shoga, ufunguo?” “Mustafa atakupeleka sehemu yako mpya.” “Asante shoga.” “Haya kwaheri.” Sara alimpa Mustafa simu, baada ya kupokea alipewa maelekezo na Shehna, baada ya kukata simu alimgeukia Sara na kumueleza. “Ukimaliza kazi nitakupeleka.” “Duh! Siamini nikitoka kazini nakwenda Masaki, siamini nami nimekuwa mtu wa matawi ya juu!” Sara alisema akishika kifua. “Hongera, ulitaka kumtibua bure kumbe mambo mazuri yalikuwa yakija.” “Mbona nimekoma.” “Nina imani tatizo lako limekwisha, kaendelee na kazi.” “Sawa bosi,” Sara alirudi kuendelea na kazi. Muda wa kutoka Mustafa alimpeleka Msaki kwenye nyumba aliyoelekezwa na Shehna. Ilikuwa nyumba nzuri iliyokuwa na kila kitu ndani, hakukuwa na kitu chochote kutoka chumbani kwake zaidi ya vitu vyake vyote muhimu. Sara aliendelea kumshukuru Shehna na kuona kumbe jini ni umbile lakini wapo wenye roho nzuri kushinda hata wanadamu. *** Mwezi moja kabla ya kujifungua, Shehna alimweleza Mustafa kuwa muda ule anatakiwa kuwa sehemu maalum ambayo hatakiwi mtu yeyote kuingiza zaidi ya mzazi wake na mkunga tu. Pia alimweleza kuonana naye itakuwa baada ya miaka mitatu. Mustafa alikubaliana naye, hakuwa na kipingamizi.
Alimwambia anywe glasi moja ya maji, mkewe alifanya hivyo, baada ya kunywa hali ilitulia lakini alikuwa amechoka sana, alipanda kitandani kulala. Alipoamka alijishangaa kukuta tumbo limekuwa kama ujauzito wa muda mrefu.Ile hali ilimshtua na kumpigia simu mumewe kumweleza kilichotokea. “Usiogope hiyo ni hali ya kawaida huenda ujauzito huo uliingia muda mrefu, dawa niliyokupa imeufukua hivyo usiwe na wasiwasi. Kama vipi nenda hospitali ukapime hali yako.” “Mume wangu hunipendi, tuliambiwa nini na Shehna?” “Amesema sasa tunaweza kwenda.” “Hapana tafuta ufumbuzi mwingine, sirudii kosa kidogo nife,” Husna aliogopa kurudia kosa. “Usiwe na wasi mke wangu, Shehna ameruhusu, basi subiri nije nikupeleke mwenyewe.” “Kama hivyo sawa.” Mustafa aliacha kazi zake na kurudi nyumbani kumfuata mkewe na kumpeleka hospitali, alipofika nyumbani alishtuka kuona tumbo la mkewe limekuwa kubwa la ujauzito wa muda mrefu. Lakini alificha mshtuko wake kwa kuhofia kumshtua mkewe na kuona kitu cha ajabu kimemtokea. Alimchukua na kumpeleka hospitali ambako katika kufanyiwa vipimo ilionesha ujauzito upo sawa. Daktari alishangaa kukaa nao zaidi ya miezi mitano bila kufika hospitali, alimuonya asifanye vile tena kukaa na ujauzito kwa muda mrefu vile. Baada ya maelekezo waliruhusiwa kurudi nyumbani akiwa amechoka kama ujauzito wote ulipitia hatua zote kufikia hatua ya kumchosha vile. Walikubali na mumewe kukaa na siri ya chanzo cha ujauzito ule, ilikuwa tofauti na ujauzito anaoufahamu. Miezi miwili baadaye ujauzito ulipofikisha miezi saba kwa vipimo vya hospitali na maelezo ya Shehna, Husna alishikwa na uchungu mkali na kukimbizwa hospitali. Kutokana na muda wa ujauzito ule, wengi waliamini ni maumivu ya tumbo tu, lakini kulionekana dalili zote za kujifungua. Baada ya kufikishwa Husna aliendelea kuugungulia huku mkono mmoja umeshika kiuno na mwingine kichwa kutokana na maumivu makali ya uchungu. Wauguzi walimkimbiza wodini wakiwa hawana uhakika kama siku ile ndiyo ilikuwa ya kujifungua. Baada ya kumfikisha walimpandisha kitandani huku Husna akiendelea kulalamika katika dalili zote za kujifungua. Ilibidi wampe huduma ya kujifungua, Husna alianza kusukuma mtoto, ghafla ulitoka moshi uliowafanya wote walewe na kusinzia. Muda huo Shehna alimtuma jini wa kike kumpeleka mtoto wake wa kiume aliyekuwa akifanana na baba yake na kumweka pembeni ya Husna. Baada ya muda wote walishtushwa na kilio cha mtoto. Mtoto alikuwa amesha katwa kitovu kabisa na kusafishwa. Hakuna aliyejua nani kafanya vile, kila mmoja aliamini mwenzake ndiye kafanya. Walimpa hongera mzazi kwa kupata mtoto wa kiume mwenye afya nzuri, hali ya mzazi nayo ilikuwa njema. Alipelekwa wodini kwa huduma zaidi. Baada ya taratibu zote, Husna aliruhusiwa kutoka hospitali na kurudi nyumbani na mwanaye ambaye kila aliyemuona alisema anafanana na baba yake. Mustafa alijua kila kitu na kubaki na siri nzito moyoni huku amani akirudi nyumbani kwake kwa familia kufurahi na kusema mpaka wamtishe ndipo atafute mtoto. Japokuwa yule mtoto alikuwa wa kwake lakini hakuwa wa mkewe bali wa jini Shehna. Siku nazo zilikatika muda nao ulisogea mtoto wa Shehna kurudi kwa mama yake. Miezi mitatu ilipotimu, alitumwa jini kumfuata mtoto, akiwa katika umbile la kibinadamu mwanamke aliyevaa kiheshima. Jini Shaunani alitembea taratibu na kubisha hodi kwenye nyumba ya Mustafa. Wakati huo mke wa Mustafa alimkuta amemaliza kumnyonyesha mtoto, alikwenda kufungua mlango na kumuona mwanamke mzuri aliyekuwa akinukia manukato kama anayotumia mumewe. “Karibu.” “Asante,” mgeni alijibu huku akiingia ndani. Alipofika aliketi na kusema: “Habari za hapa.” “Sultani hajambo?” lilikuwa jina la mtoto ambalo Mustafa aliambiwa ampe mtoto na ndilo lilikuwa jina lake la ujijini. “Hajambo.” “Hebu nimuone.” Husna bila wasi alimkabidhi mtoto jini Shaunani ambaye alikuwa mcheshi sana. Kutokana na ucheshi wake, alimzoea haraka Husna, hakuwa na wasiwasi alimuomba samahani. “Samahani mgeni natoa vyombo vya mtoto.” “Hakuna tatizo.” Husna alirudisha vyombo vya mtoto jikoni na kurudi kumsikiliza mgeni, baada ya kukaa alimkaribisha tena. “Karibu mgeni.” “Asante,” kabla Husna hajaongeza neno simu iliita na kumshangaza kuitia chumbani wakati alikuwa nayo muda mfupi na hakurudi chumbani. “Jamani hii ajabu simu nilikuwa nayo hata sijui niliondoka nayo muda gani kwenda nayo chumbani.” CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Labda umesahau haiwezi kujibeba yenyewe, kasikilize huenda ni shemeji,” jini Shaunani alisema. Husna alinyanyuka na kwenda kupokea simu, kitendo cha kuingia chumbani tu. Jini Shaunani alitoweka na mtoto. Husna alipofika chumbani alishangaa kukuta simu haina ‘missed calls’. Alishangaa wakati alisikia simu ikiita kabisa hata mgeni alisikia. Alitoka sebuleni alishangaa kukuta sebule tupu, hakuna mgeni wala mtoto wake. “Mgeni…mgeni,” aliita kwa sauti. Hakukuwa na jibu alitoka nje labda ametoka vilevile hakukuwa na jibu lolote, alijiuliza atakuwa amekwenda wapi. Alitoka hadi nyumba ya pili labda wamemuona mtu akiwa na mtoto nao walisema hawajamuona. Alimpigia simu mumewe kumueleza kupotea ghafla kwa mwanaye. Taarifa ile haikuwa ngeni kwa Mustafa, alijua mtoto keshachukuliwa na mama yake. Alirudi nyumbani haraka ili kumtuliza mkewe ambaye muda ule alikuwa amepagawa. Alipofika alimkuta amepagawa akilia ovyo mikono kichwani. Husna alipomuona mumewe alimkimbilia na kumkumbatia na kuendeleza kilio. “Mume wangu mwanangu ameibiwa!”
“Haloo laaziz, vipi mpenzi wangu?” “Safi tu.” “Mbona kama mnyonge?” “Bwana huyu msichana ananichanganya sana.” “Kafanya nini?” Shehna alijifanya kuuliza. “Hajafika mpaka saa hizi yaani ofisi chafu.” “Basi usikonde mpenzi wangu baada ya dakika mbili watakuja wasichana wangu kuja kufanya usafi uwape nafasi tu.” “Hakuna tabu.”
Baada ya muda kidogo wasichana wawili warembo walibisha hodi kwenye geti, Mustafa alipowatazama alijua ndiyo waliotumwa na mpenzi wake Shehna. “Asalaam aleykum,” wale wasichana waliwasalimia kwa bashasha na sauti tamu. “Waleykum salaam, nina imani ninyi ni wageni wangu?” Mustafa aliuliza. “Swadakta, hatuna muda tuoneshe hiyo kazi.” Mustafa aliongozana nao hadi ofisini, baada ya kuwaonesha mmoja alisema: “Haya tupishe tufanye usafi.” “Hakuna tatizo,” Mustafa alijibu huku akitoka nje na kuwaacha wale wasichana. Baada ya kutoka walipiga makofi, haikuchukua muda waliongezeka wengine ambao walifanya kazi ya usafi kwa muda mfupi. Baada ya usafi wenzao walitoweka na kuwaacha wale wawili. Nao walitoka hadi alipokuwa amekaa Mustafa getini na mlinzi walipokuwa wakizungumza tabia za Sara zilivyobadilika tofauti na zamani. Walipofika walimweleza kwa sauti tamu yenye lafudhi ya kimwambao. “Bwana sisi tunakukimbia tuna imani utafurahia usafi wetu.” “Nina waamini, nashukuru sana.” “Haya si tukukimbie.” “Haya, msalimieni sana Shehna.” “Salamu zimefika.” Wasichana wale walitoka nje ya geti na kutembea kufuata barabara, baada ya kuwa sehemu ambayo walijua Mustafa hawaoni walitoweka ghafla kurudi chini ya bahari. Mustafa alirudi ofisini na kuikuta ofisi inapendeza kila kitu kilikuwa kimesafishwa ndani kulikuwa na hewa na harufu nzuri ya manukato. Alikaa kitini na kuanza kazi huku akiamini kama atamuoa Shehna basi ataishi maisha sawa na peponi. *** Kila usiku Mustafa alifuatwa akiwa ndotoni na kujikuta yupo sehemu nzuri akiwa amelala pembeni ya Shehna aliyekuwa amelala huku tumbo lake likizidi kukua. Lakini alikuwa amevaa gauni jepesi lililoziba tumbo lake. Usiku sana Shehna alizima taa na kuondoa nguo zake na kumruhusu Mustafa alichezee tumbo lake lakini ikiwa gizani. Siku zote Mustafa alifurahi kuwa karibu na mpenzi wake na kutamani siku zote awe karibu yake. Tumbo la Shehna halikuwa likimsisimua lakini hakupata nafasi ya kuliona, siku zote alimbembeleza kuliona Shehna alimwambia avute subira. Mustafa alikubaliana na mpenzi wake. Katika siku alizolala alishangaa tumbo la Shehna kuwa kubwa akilala akiwa hana nguo tofauti na akimkuta amevaa nguo. Ile ilimfanya apange kumvizia wakati amelala ili awashe taa aone sababu ya CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ tumbo lile kuwa kubwa tofauti na matumbo ya kawaida ya wanawake wenye mimba. Wakati huo Sara aliendelea kuteseka na baridi na njaa hakutoka kwenye nyumba ile mbovu mpaka kiza kilipoingia, aliogopa kutoka muda ule kwa kuhofia kupigwa na kuumizwa. Kiza kilipoingia ndipo alipotoka na kurudi nyumbani, lakini alipofika sehemu ya chumba chake ambacho kilikuwa kimefungwa alisikia mtu akisema: “Jamani yule mbwa wa asubuhi amerudi tena.” “Jamani huyu mbwa atakuwa ametumwa tu, tena amesimama kwenye chumba cha Sara.” “Jamani lazima kutakuwa na tatizo, Sara jana si alilala chumbani kwake ajabu asubuhi tukumuona na kukuta mlango upo wazi na mbwa huyu alitoka ndani. Ajabu tulimfukuza asubuhi usiku amerudi,” shoga yake Happy alisema. “Sasa na Sara atakuwa wapi?” “Hapa ndipo tunachanganyikiwa maana hajaaga kama amepata dharura usiku.” Sara yote aliyasikia akiwa bado amesimama kwenye mlango wake, lakini alishindwa kuzungumza kwa kuhofia kubweka na kuwatisha kitu kitakachowafanya wamfukuze kwa kumpiga.
“Hapa ndipo tunachanganyikiwa maana hajaaga kama amepata dharura usiku.” Sara yote aliyasikia akiwa bado amesimama kwenye mlango wake, lakini alishindwa kuzungumza kwa kuhofia kubweka na kuwatisha, jambo ambalo lingewafanya wamfukuze kwa kumpiga. Akiwa bado amesimama mlangoni alisikia akiitwa jirani yake kwa sauti aje amfukuze. “Baba John, yule mbwa wa asubuhi amerudi tena,” mama John alimwita mumewe. Sara alijua majanga bado yanamuandama, alilia kilio cha kimyakimya kwa kuogopa kutoa sauti kuwatisha. Alijiuliza atajitetea vipi ikiwa hawezi kuzungumza sauti ya kibinadamu. Alimuona jirani yake baba John akitoka ndani na kuuliza: “Yupo wapi?” “Yule pale kwenye mlango wa Sara.” “Huyu mbwa anatafuta kufa hapa subiri,” alisema kwa sauti ya hasira aliyoisikia Sara. Baba John alisogea pembeni na kuchukua gongo ili ampige, Sara alishangaa kusikia sauti iliyokuwa ikimtokea bila kumuona anayezungumza ikisema: “Sara ondoka haraka watakuumiza.” Sara hakuchelewa alitimua mbio, alipoondoa mguu tu gongo lilitua kwenye mlango na kutoa sauti, alisikia sauti ya baba John akisema: “Bahati yake lingempata angekufa, ——- kafie mbele kama umetumwa.”
“Jamani huyu ni mchawi, huyu mbwa si bure, iweje ang’ang’anie hapa tena kwenye chumba kimoja cha Sara?” alisema Happy kwa uchungu. Sara alitimua mbio mpaka nyumba ya jirani na kutweta huku akijiuliza nini hatima ya maisha yale?Alijiuliza atalala wapi usiku ule wenye baridi, kama angekuwa na uwezo wa kibinadamu basi angechukua kamba na kujinyonga. Njaa na kiu vilimshika, asingeweza kula jalalani au maji machafu. Kwake kilichobadilika kilikuwa umbile tu lakini akili ilikuwa ileile ya kibinadamu. Wingu la mvua lilitanda na baridi ilizidi kuwa kali na kumfanya atetemeke, ilionesha mvua kubwa inaweza kuteremka wakati wowote. Aliona sehemu anayoweza kujistiri usiku ule ni mule kwenye jumba bovu lenye harufu kali ya kinyesi. Alijiuliza nini hatima yake hata kama usiku ule utapita na atawezaje kulala na njaa na kesho yake aamke? Hakuwa na jinsi kwani wingu lilikuwa zito, alikimbilia kwenye jumba lile na kuingia ndani ili mvua isimkute. Alisogea kwa ndani na kutafuta sehemu kavu kisha alijilaza chini, moyoni alijuta kutosikiliza maneno ya Shehna. Kiherehere chake kilimponza na kujiuliza hata kama Shehna ni jini, bado hakumuhusu kwa vile Mustafa hakuwa mumewe, wala ndugu yake na ujio wake pale hakumuathiri chochote. Sara alilia sana lakini hakuna aliyesikiliza kilio chake kwa vile kilikuwa cha kujitakia, hakikuwa na pole. Njaa nayo ilizidi kumchonyota kwa vile toka asubuhi hakuwa ameweka kitu chochote tumboni wala kunywa maji. Hakuwa na jinsi, alikubaliana na yaliyokuwa mbele yake na kumuachia Mungu aamue maisha yake. Majira ya saa saba usiku, mwanga mkali ulimpiga machoni, alipoangalia vizuri aliwaona wanawake wawili wazuri waliokuwa wamesimama mbele yake na kumwita jina lake. “Sara.” Alishindwa kuitikia kwa kuhofia kubweka, aliwaangalia tu huku akijiuliza wale ni akina nani na wamejuaje yupo pale. Wale wasichana warembo walimwambia atoke ndani, alinyanyuka na kuwafuata. Alishangaa kuwasogelea bila kushtuka, alipowasogelea walimshika kichwani, ghafla Sara alirudi katika umbile la kibinadamu. “Sara tumetumwa na Shehna tukuletee chakula.” “A..asa..sante,” Sara alishukuru huku akipiga magoti. Alijua baada ya chakula atabakia katika umbile lake la kibinadamu, alitoka nje ya jumba lile na kurudishwa kwenye chumba chake kisha akala chakula kile kitamu na kunywa maji. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Baada ya kula na kushiba alielezwa maneno yaliyomnyong’onyesha na kutamani ardhi ipasuke na kummeza. “Sara, samahani tutakurudisha katika umbile la adhabu kisha tutakurudisha tulipokutoa.” “Jamani nisameheni, sirudii tena, nikirudia nifanyeni vyovyote,” Sara alipiga magoti kuwaomba msamaha. “Sara sisi hatujui sababu ya wewe kugeuzwa mbwa, tumetumwa tukuletee chakula tu, zaidi ya hapo hatuna mamlaka yoyote.” “Na..naomba unikutanishe na Shehna nimweleze haya.” “Sara unatuchelewesha,” walimshika kichwani mara moja Sara akarudi katika umbile la mbwa. Wale wasichana warembo walitoweka ghafla na kumuacha Sara nje ya jumba bovu walipomtoa na kumrudisha. **** Mustafa kila alipokuwa kazini, alikuwa na maswali mengi juu ya tumbo la Shehna kuwa kubwa kama puto lililojazwa hewa lakini lilikuwa laini na kupenda kulishika muda wote hata kumfanya kila siku alale kwa muda mchache.
Kilichomuumiza akili kilikuwa ukubwa wa tumbo kila wakizima taa lakini akiwa na nguo zake za kulalila ilikuwa mimba ya kawaida. Alijiuliza kwa nini wakizima taa linakuwa kubwa na kingine kwa nini hataki kumruhusu kulichezea tumbo lile kwenye mwanga! Alipanga siku ile usiku amtegee Shehna amelala awashe taa ili kutaka kujua kwa nini usiku tumbo lake linakuwa kubwa sana. Aliendelea na kazi kama kawaida huku taarifa za Sara zikizidi kumchanganya kutokana na kuelezwa hajulikani halipo wala hakuaga. Mazingira ya kutoweka yalikuwa yakilingana na ya mara ya kwanza kitu kilichomfanya ajiulize Sara ana matatizo gani yanayosababisha kutoweka bila taarifa. Alikumbuka maelezo aliyopewa na Sara siku aliyorudi kazini baada ya kupotea kimiujiza alitoka kwenda kununua chakula cha usiku na kujikuta akiwa katika pori la kutisha na baada ya kutembea bila kujua na kutokea Dodoma. Kingine kilichomshtua kuambiwa kuna mbwa alikutwa chumbani kwa Sara baada ya kumfukuza alirudi tena usiku na kusimama kwenye mlango uleule. Alijiuliza kipi hasa kimempata Sara na ana siri gani ambayo yeye na majirani zake hawaijui. Alipanga akienda kwa Shehna kumueleza tatizo lile labda angeweza kumsaidia. Usiku ulipoingia kama kawaida aliposhtuka usingizini alijikuta yupo pembeni ya mpenzi wake Shehna. Kama kawaida tumbo lilikuwa la kawaida lililokuwa katika nguo nyepesi ya kulalia. Baada ya kuliwazana wote walipitiwa usingizi, Mustafa
hakulala sana alishtuka mapema na kutulia kitandani alilichezea tumbo la Shehna ambalo lilikuwa haliishi hamu kwa vile lilimpa raha ya ajabu kila alipolipapasa. Alitulia kwa muda kusubiri Shehna usingizi umkolee, baada ya muda alimsikia akikoroma. Alijua usingizi umemkolea. Aliteremka kitandani taratibu na kuelekea kwenye kandili ya dhahabu, aliiwasha huku akitetemeka aliipandisha mwanga ili aone vizuri. Baada ya kuwasha taa na kumulika kitandani, alishtuka kuona kiumbe cha ajabu juu ya kitanda. Sura ilikuwa ya mpenzi wake Shehna lakini tumbo lake lilikuwa la ajabu lililokuwa kubwa na pembeni lilikuwa na rangi kama magamba ya nyoka na chini alikuwa na mkia mnene unaoungana na tumbo. Mustafa alishtuka sana na kuanza kutetemeka, kingine kilichomshtua kuona kitanda walichokuwa wamelalia kilikuwa juu ya maji katika ya bahari. Mshtuko uliompata ulimfannya aanguke chini na kupoteza fahamu. Baridi kali lilimuamsha Shehna usingizini, alipofumbua macho alishtuka kukuta amelala juu ya bahari. Haraka alijirudisha katika umbile la kawaida, palepale usiku mwili wake ulirudi kama kawaida na kuwa chumbani kwake lakini kandili ilikuwa ikiwaka. Alijiuliza nani aliyeiwasha taa ile, alishangaa kujikuta peke yake na kujiuliza Mustafa alikuwa wapi! Alipoteremka kitandani alishtuka kumkanyaga mtu, alipoangalia alimuona Mustafa akiwa amelala chini amepoteza fahamu. Alijua tayari siri yake ilikuwa hadharani, alijiuliza atamwambia nini Mustafa amuelewe kuwa yeye ni jini pia alijiuliza akimueleza ukweli atakuwa tayari kuendelea kuwa naye! Shehna alianza kulia kitu kilichomshtua mama yake baada ya kudondokewa na machozi. Malkia Bi Zaldau mke wa mfalme wa bahari ya dhahabu alikwenda katika chumba cha mwanaye. Alipofika alimkuta jasho likimtoka japokuwa kulikuwa na hali ya baridi, alishangaa kumuona Mustafa amelala chini. “Vipi?” Shehna ilibidi amweleze mama yake kilichotokea aliposhtuka usingizini.
“Shehna nani kawasha taa?” mama yake alishtuka kuiona hali ile. “Sijui mama, labda Mustafa.” “Ina maana hukumueleza taratibu zetu?” “Nilimueleza hata sijui likuwaje mpaka akawasha taa?” “Ina maana alifanya kiburi cha kibinadamu?” Bi Zaldau aliuliza kwa hasira. “Mama yaani sijui nimechanganyikiwa, jinsi ya kumuamsha na kumuuliza, lakini naogopa kumueleza mimi ni jini.” “Hivi vitu vyote unavyomfanyia hajashtuka na kukuona kiumbe wa ajabu.” “Huwa anashtuka lakini akili yake ilionekana ngumu kukubaliana kuwa mimi jini.” “Akijua jini?” “Anaweza kuniacha nami nampenda sana.”
“Basi tumfanye hamnazo.” “Hapana mama sitaki awe hivyo, ana familia inamtegemea unafikiri akiwa hivyo atafanyaje kazi?, Lazima atafukuzwa.” “Kila kitu tutaipa familia yake na wewe kuwaeleza masharti ya kukaa naye, hatakiwi kwenda kwa mganga mpaka ujifungue.” “Mamaa, umesahau mimi sitakiwi kutoka huku kipindi hiki.” “Mmh! Hapo ndipo penye tatizo.” “Au nimrudishe kwao.” “Kumrudisha umechelewa, fanya hivi, mtume jini mmoja akachukue nguo zake kwake kisha tumrudishe ofisini ili akishtuka aamini alikuwa amelala na kuota akiwa ofisini.” “Labda tufanye hivyo.” Walimchukua na kumrudishia fahamu kabla hajajitambua walimpuliza na kumfanya apitiwe na usingizi. Waliwatuma vibaraka kwenda kuchukua nguo za Mustafa nyumbani kwake na kuzipeleka haraka kisha walimvisha na kumpeleka ofisini kwake. Kama kawaida ulifanyika kwanza usafi kisha walimweka kwenye kiti chake na kumuacha amelalia meza na kuondoka. Mlio wa simu ulimshtua Mustafa kwenye usingizi mzito, alijishangaa kulala ofisini kitu ambacho kilikuwa hakijawahi kumtokea hata siku moja. Alipiga miayo na kuangalia saa yake, ilimuonesha ni saa tatu asubuhi. Simu iliyokuwa pembeni yake iliendelea kuita, aliichukua na kukuta inatoka kwa mkewe, alipokea mara moja. “Haloo mke wangu.” “Mpenzi, vipi leo?” “Kivipi mke wangu?” “Imekuwaje leo umeondoka bila kuniaga?” Swali hilo lilimchanganya sana Mustafa na kujiuliza aliwezaje kuondoka bila kumuaga mkewe, kila alivyojiuliza alikosa jibu. Ukimya wa kujiuliza maswali ulimfanya mkewe kumuuliza. “Mume wangu.” “Naam.” “Mbona hunijibu, au ulikuwa na kazi muhimu ofisini?” “Ndiyo,” Mustafa alikubali ili kuepusha maswali asiyoyaelewa kwa wakati ule. “Hata kama hivyo, basi ungenipigia simu kunijulisha maana nimeshtuka kuamka asubuhi bila kukuona kitandani.” “Yaani simu yako ndiyo iliyonishtua na kuachana na kompyuta toka nilipoingia,” alitengeneza uongo unaofanana na kweli japokuwa bado alikuwa hajielewi kwa vile alikuwa hakumbuki kama asubuhi alitokea nyumbani kwake. “Pole mume wangu, lakini upo salama?” “Asante nipo sawa sijui wewe mpenzi wangu niliyeondoka bila kukuaga.” CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Mi sijambo, hujambo imeongezeka baada ya kuishusha presha yangu.” “Pole sana mke wangu.” “Asante, basi nikuache ufanye kazi.” “Asante mke wangu.” Baada ya kukata simu alijikuta mtu mwenye mawazo mengi sana baada ya kujikuta amelala ofisini bila kukumbuka alifika pale muda gani mpaka kumfanya alale ofisini tena kwa muda mrefu. Alinyanyuka kitini na kujinyoosha mwili uliokuwa umechoka sana. Baada ya kujinyoosha na kutengeneza nguo zake vizuri, alitoka nje ili kuzungumza na mlinzi kutaka kujua amefika saa ngapi mpaka kujikuta muda ule amelala. Alikwenda hadi getini, mlinzi alipomuona alimshangaa na kumuuliza kwa sauti ya juu. “Bosi leo umelala ofisini?” “Kwa nini?” “Sijakuona kupita pia macho yamevimba kwa usingizi.” “John, jana nilipotoka hukuniona?” “Nilikuona, ajabu sijakuona kupita kuingia lakini unatokea ndani ya ofisi.” “Una uhakika hujaniona napita kuingia ofisini?” “Sijakuona ndiyo maana nakushangaa.” “Mmh! Ipo kazi.” “Kwani vipi, mbona kama huelewi?” “John hebu njoo ofisini.” Mustafa aliongozana na mlinzi hadi ofisini ili wazungumze vizuri kwani muda ule alikuwa hajielewi. Baada ya kufika ofisini, Mustafa alimweleza mlinzi. “Kaa chini.” John alikaa kwenye kiti kumsikiliza bosi wake, Mustafa baada ya kukaa alitulia kwa muda kuvuta kumbukumbu kwa yote yaliyomtokea na kutaka ushauri kwa mlinzi kwani alianza kuchanganyikiwa baada ya baadhi ya mambo kuyaona kama mauzauza. Muda wote John alikuwa ametulia akimuangalia bosi wake aliyekuwa ameinama. “John,” Mustafa alimwita huku akinyanyua kichwa kumtazama. “Naam.” “Kuna kitu kinanichanganya sana.” “Kitu gani bosi?” “Kuna baadhi ya mambo siyaelewi ni ya ndotoni au kweli?” “Mambo gani?” “Unamjua yule mwanamke mzuri anayekuja hapa?” “Ndiyo.” “Unamuonaje?” “Kivipi?” CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Muda wote John alikuwa ametulia akimuangalia bosi wake aliyekuwa ameinama. “John,” Mustafa alimwita huku akinyanyua kichwa kumtazama. “Naam.” “Kuna kitu kinanichanganya sana.” “Kitu gani bosi?” “Kuna baadhi ya mambo siyaelewi ni ya ndotoni au kweli?” “Mambo gani?” “Unamjua yule mwanamke mzuri anayekuja hapa?” “Ndiyo.” “Unamuonaje?” “Kivipi?”
SASA ENDELEA… “Unamuona yupo kama wanawake wengine?” “Ndiyo, kwani vipi?” “Ushawahi kuona mwanamke mzuri kama yule?” “Mmh! Sijawahi wewe umemtoa wapi, kwa kweli ni mzuri sana tena sana ajabu kila nikimuona mwili unanisisimka na mapigo ya moyo hunienda mbio.” “Unajua kwa nini?” “Hata sijui.” “Mimi nawasiwasi na yule mwanamke ni ji….” Mustafa alinyamaza ghafla baada ya kumuona aliyekaa mbele yake hakuwa mlinzi John bali Shehna akiwa anamtazama uso wake umejaa machozi ya damu. Alishtuka sana mpaka akaanguka chini ya kiti, John aliyekuwa amekaa kwenye kiti alishtuka kumuona Mustafa akishtuka na kuanguka vile. Alimuokota na kumkalisha chini kisha alimnyanyua kumrudisha kwenye kiti, lakini ajabu kila alivyoongea sauti haikutoka. John alishtuka na kujitahidi kumwita Mustafa ambaye alinyanyua mdomo kuzungumza kakini sauti haikutoka. Alimpigia simu mkewe ambaye naye alifika mara moja. Alishtuka kumkuta mumewe kwenye hali. “Vipi ilikuwaje?” alimuuliza mlinzi. “Tulikuwa tukizungumza ghafla nilimuona mwenzangu akishtuka na kuanguka chini. Nilipomuinua kila alipotaka kusema sauti ilipotea.” “Sasa kipi kimempata jamani mume wangu?” Husna aliuliza. “Hata mi nashangaa, kwa kweli siku ya leo simuelewielewi kabisa bosi.” “Inawezekana ni malaria tumuwahishe hospitali.” Mustafa kila alipojaribu kuzungumza sauti haikutoka, alikwishajua makosa yake kwa kutaka kutoa siri ya Shehna ambaye alifahamu kuwa si kiumbe cha kawaida kutokana na matukio yaliyokuwa ya kimtokea japo awali hakutaka kukubaliana na akili yake kuwa Shehna si kiumbe cha kawaida. Aliamini yote yaliyotokea haikuwa ndoto bali kweli baada ya kuupata ukweli wa wasiwasi wake wa tumbo la Shehna. Vyote alivyoviona na kujikuta amelala katika ya bahari aliamini moja kwa moja mpenzi wake si mtu wa kawaida bali jini japokuwa hakuwahi kumuona. Alijiuliza nini hatima yake baada ya kutaka kuitoa siri ya Shehna ambayo hakutaka kiumbe chochote akijue. Aliwasikia aliyopanga jinsi ya kumpeleka hospitali, aliwakatalia kwa kutikisa kichwa na kuomba kurudishwa nyumbani kwa kuwaandikia kwenye kalatasi. “Sasa mume wangu utaponaje?” “Nirudisheni nyumbani,” aliwaandikia kuwasisitiza wasimpeleke hospitali. Lakini alipoulizwa anaumwa nini aliwambia hajui ila wamrudishe nyumbani. Mkewe alikubaliana na mumewe na kumrudisha nyumbani. Mustafa alitegemea kupata simu kutokwa kwa Shehna naye apate nafasi ya kuomba msamaha. Lakini wiki ilikatika bila dalili zozote za simu kutoka kwa Shehna, kazini hakuweza kwenda kwa wiki nzima ilibidi apewe mtu mwingine nafasi ile huku kampuni ikijitolea kumtafutia matibabu. Hospitali zote alizokwenda halikuonekana na tatizo lolote, Mustafa aliogopa kuwaeleza sababu ya yeye kuwa vile kwa kuhofia adhabu zaidi toka kwa Shehna. Baada ya tiba ya hospitali kushindwa, watu walimshauri Husna kuangalia upande wa pili labda mumewe kachezewa. Mustafa pia hakutaka kwenda kwa mganga kwa kuhofia kukatazwa kwa mkewe kwenda kwa mganga na Shehna wakati wa matatizo. Lakini ilibidi akubali kwa vile ndugu zake wasinge muelewa. Ilipelekwa kwa mganga mmoja Vingunguti, alipofika walisubiri kwa muda ndipo walipopata nafasi ya kuonana na mganga. Alikuwa mganga kijana lakini alikuwa mtu aliyejijengea sifa kutokana na kuwasaidia watu matatizo yao. Baada ya kukaa mganga alitaka kujua wateja wake wana tatizo gani. Husna mkewe alimuhadithia mganga toka siku ya kwanza kutokewa na tatizo lile kutokana na maelezo ya mlinzi na hatua walizochukua mpaka siku ile waliyompeleka mbele yake. Baada ya kuwasikiliza alishika mkono wa kulia kwenye paji la uso, baada ya muda akitikisa kichwa kama amesisimka na kuanza kutua mbwewe mfurulizo kisha aliweka mkono sikioni kama anasikiliza simu na kuwa kama anakubaliana alichokisikia kupitia kiganja chake cha mkono na yeye alijibu kwa kusema: “Eeh… ndiyo… ndiyo…ndiyo… sawasawa…sawasawa… hapana…eeh…ndiyo… hapana…sawa..sawa nimekuelewa.” Baada ya kuzungumza vile kwa zaidi ya robo saa alitoa mkono sikioni na kuwatazama wateja wake kwa kutembeza macho kwa kila mmoja huku macho yake yakionekana kumeremeta kama ya simba na kuwatisha wateja wake. Wote walikuwa kimya wakimsikiliza kwa sauti kama mtu anayevuta moshi wa kitu ndani alisema: “Tatizo nimeliona, lakini linaonesha mwenyewe analijua tatizo.” “Kwa hiyo unatusaidia vipi?” “Dawa yake hakuna ila naomba wote mtoke abakie mgonjwa,” mganga aliomba kuachwa peke yake na mgonjwa. “Mmh! Kwa hiyo ndiyo atapona?” Husna aliuliza. “Naomba kwanza mtoke.” Walitoka nje na kumuacha Mustafa na mganga, baada ya kutoka mganga alitulia kwa muda kisha alimwita Mustafa kwa jina lake. “Mustafa.” “Naam,” sauti ilitoka. “Unajua tatizo lako?” “Ndiyo.” “Kwa nini ulifanya vile?” “Nilikuwa na wasiwasi na mpenzi wangu kutokana na mimba yake, ndiyo maana nilikiuka masharti yake ili nione gizani kuna nini.” “Unajua kilichompata msaidizi wako?” “Sijui.” “Ubishi kama wako, sasa hivi ni mbwa.” “Mungu wangu!” Mustafa alishtuka na kushika mdomo. “Baada ya kufanya kosa la kwanza bado umeendelea kufanya kosa lingine la kutaka kutoa siri ambayo ni yako peke yako hatakiwi mtu kujua. Ni kweli mpenzi wako ni jini hilo ulitakiwa kulijua mapema na si kwa kuitoa siri nje.” “Jini?” Mustafa alishtuka. “Unashtuka nini wakati matukio yote yalikuwa si ya kawaida, kwa vile bado ilibakia siri, mpenzi wako kila alipozima taa aligeuka kuwa jini kamili na tumbo lile kubwa ni mimba yake.” “Sasa nitafanyaje?” “Kitendo cha Shehna kuja mbele yako wakati unataka kutoa siri nje, amesababisha maumivu makali ya tumbo sasa hivi yupo hoi. Msaada wako ni kuendelea kuwa hivyohivyo ili ibakie siri mpaka ajifungue, kama atakufa lazima na wewe utakufa kwa vile tayari kuvuli chako kimo ndani ya damu yako ambayo wale wanao walio tumboni katika ujauzito ile. “Hukutakiwa kuuona tumbo akiwa katika umbile la kijini, ungeweza kufa muda uleule, lakini mapenzi ya jini yule ni makubwa sana. Kwa vile bado hukutaka kuelewa ukutaka kutoa siri ile hapo ndipo ulipopewa adhabu ambayo itaisha mpaka ajifungue.” “Lini?” “Baada ya miaka miwili.” “Miaka miwili niwe hivihivi?” Mustafa alishtuka.
Baada ya miezi saba atakapojifungua.” “Mmh! Miezi saba niwe hivihivi?” Mustafa alishuka. “Hiyo ndiyo faida ya kiburi chako na adhabu hiyo ni ndogo kuliko zote ambazo amezitoa mama yake baada ya Shehna kuingilia kati kitendo chako kile kimemuumiza sana mama yake. Bila hivyo ulitaka kugeuzwa hamnazo.” “Mungu wangu, sasa utanisaidia vipi?” “Sina msaada wowote zaidi ya kuitumikia adhabu yako, zaidi ya hapo ukitaka chokochoko utapotea wewe na waliokuzunguka.” “Siwezi kuonana na Shehna nimuombe msamaha?” CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Yupo katika uangalizi mkali baada ya kutoka ujinini bila idhini ya wazazi wake ili kukuzuia usiitoe siri yake na kumsababishia matatizo makubwa sasa hivi hana kauli, hajiwezi kwa lolote.” “Kwa hiyo utakuwaje?” Mustafa alishtuka. “Adhabu yako ni kuitunza siri hii kwa miezi saba, cha kuomba Shehna apone upesi ili uweze kukupunguzia adhabu au kukuondolea ububu.” “Kwa hiyo baada ya mazungumzo narudia katika hali ya ububu?” “Ndiyo usalama wako.” “Itanibidi nikubali sina jinsi,” Mustafa alikubali kwa shingo upande. Baada ya makubaliano aliitwa Husna mke wa Mustafa na mtu aliyemsindikiza ambao waliamini watakuta mabadiliko ya kukuta akizungumza. Lakini ilikuwa tofauti na mawazo yao, Mustafa alikuwa bado yupo katika hali ya ububu. “Umefika wapi?” Husna aliuliza. “Nimejitahidi kadri ya uwezo wangu imeonesha ugonjwa huu utatoka taratibu bila kutumia dawa yoyote.” “Itachukua muda gani?” “Sijajua, ila msirogwe kwenda kwa mganga yeyote eti amponye, dawa atakayompa ndiyo itakayomfanya awe bubu milele.” “Kwa hiyo hata panadol tusimpe akiumwa?” Husna aliuliza. “Dawa zote mpeni, ila si za kutibu ugonjwa huu, msikubali kumpeleka kwenye maombi ya aina yoyote au kwa mganga yeyote. Ukifanya hivyo mtanikumbuka.” “Sawa tunashukuru.” Baada ya kukubaliana na mganga walimchukua mgonjwa wao ambaye ilikuwa vigumu kuamini anaumwa kwani alikuwa kwenye hali ya kawaida na kurudi naye nyumbani.
*** Siku zilizidi kukatika huku Mustafa akiwa katika hali ya ububu na Sara akiwa katika umbile la mbwa. Mateso makubwa yalikuwa kwa Sara ambaye aliendelea kuishi maisha ya kujificha kukimbia watoto kumpiga mawe na kulala kwenye majumba mabovu. Chini ya bahari, Shehna alipata nafuu haraka sana na kuweza kukaa hata kula mwenyewe baada ya kupoteza fahamu kwa miezi mitatu iliyotishia uhai wake. Kukubali kwa Mustafa kuendelea kuwa katika hali ya ububu na kuyakubali maelekezo ya mganga, ile ilimsaidia sana kuwahi kupata nafuu. Kama mkewe Mustafa angekuwa mbishi lazima angewapoteza mumewe na
Shehna pamoja na watoto waliokuwa tumboni. Baada ya kupata nafuu alitaka kujua Mustafa yupo katika hali gani kwani aliamini hasira za mama yake lazima angemfanya kitu kibaya. Katika vitu vyote alimkataza mama yake kumuua hata kumpa adhabu kali mpenzi wake. “Mama mpenzi wangu yupo katika hali gani?” “Nilimgeuza bubu ili asitoe siri mpaka muongee wenyewe na kukubaliana.” “Nimepona, vipi hali yake kwa sasa?” “Bado sijamtoa ububu lakini niliyaangalia maisha yake ya siku zote, ila amenifurahisha kutotafuta dawa kwa ajili ya kutibu ububu. Kitendo kile kimesaidia wewe kupata nafuu upesi.” “Mustafa ni msikivu sijui kwa nini siku ile hakutaka kunielewa mpaka akawasha taa.” “Wewe ndiye mwenye makosa, ulitakiwa kujitambulisha mapema kwa vile alikuwa akikupenda sana, angekuelewa.” “Mama nilihofia kumueleza mimi jini, angenikimbia.” “Ona sasa alikuwa anatoa siri nje kwa vile alikuwa hakuelewi, kila kitu kingekuwa wazi, ububu na uelewa wake ndiyo nafuu yako, bila hivyo ungekufa, hali ilikuwa mbaya.” ‘Sasa nifanye nini?” “Aletwe leo aambiwe ukweli lazima atakuelewa tu.” “Sawa mama.” Malkia Zaldau mke wa mfalme wa bahari ya dhahabu mama wa Shehna walikubaliana na mwanaye usiku wa siku ile Mustafa apelekwe chini ya bahari. *** Mustafa alishituka usingizini na kujikuta akiwa pembeni ya Shehna ambaye tumbo lake lilikuwa limeongezeka katika umbile la kibinadamu lililokuwa ndani vazi la kulalia. Shehna alikuwa akimtazama huku macho yakiwa yamejaa machozi na kuongeza uzuri wake. “Shehna.” “A..abeee,” aliitikia kwa sauti ya kilio. “Nisamehe mpenzi wangu.” “Huna kosa, nisamehe mimi.” “Kwa kosa gani mpenzi?” “Nimekutia kwenye mateso bila kosa.” “Shehna huna kosa bali mimi ndiye niliyeshindwa kukusikiliza.” “Hapana Mustafa mwenye makosa ni mimi kushindwa kukueleza ukweli mapema.”
“Shehna nimekuelewa, najua una wasiwasi lakini ulitakiwa kunieleza mapema, nilikuwa na wasiwasi wewe labda nani lakini akili yangu ilikataa.” “Kwa hiyo umenielewa mimi ni nani?” “Ndiyo.” “Hutaniacha?” “Nilikueleza mapema sitakuacha maishani mwangu wewe ni kiumbe muhimu sana. Najuta kutaka kukupoteza wewe, mimi mwenyewe na watoto wetu watarajiwa.” “Mustafa ukitoka hapa hutaitoa siri hii kwa watu?” “Sitatoa, nimejua makosa yangu sitarudia, Shehna wewe ni kiumbe mwenye huruma sana na mapenzi mazito.” “Kesho utarudi katika hali yako, ukiamka rudi kazini kama kawaida, usihoji kitu chochote ukifika endelea na kazi zako.” “Sawa nimekuelewa.” “Mustafa nitafanya kila kitu ili maisha yako yawe juu baada ya kujifungua nitakubadilishia kazi nataka uwe mmoja wa matajiri duniani.” “Asante mpenzi wangu,” Mustafa alimkumbatia Shehna kwa furaha. “Naomba usiniogope kwa vile ushanijua.” “Siwezi, nakupenda Shehna.” “Baada ya kunipa zawadi ya mtoto baada ya mimi kujifungua mkeo naye atapata mtoto. Nisingempa dawa ya ujauzito mkeo kwa sasa kwa vile nisingeweza kujifungua mpaka ajifungue yeye hivyo ningeteseka kwa uchungu kwa muda mrefu.” “Nimekuelewa mpenzi.” Baada ya mazungumzo ya kimabaha walilala kwa Shehna kuzima taa na kuondoa nguo zote kumuachia Mustafa kulichezea tumbo lililokuwa zimezidi kuwa kubwa. Ilikuwa ni siku ya furaha kwake. Alipanga siku nyingine amuombee Sara msamaha ili atolewe kwenye umbile la kimbwa. ***
Siku ya pili Mustafa aliposhtuka asubuhi alijaribu kumwita mkewe sauti ilitoka. “Mke wangu.” “Ha! Jamani Mungu mkubwa umepona mume wangu?” Husna alikurupuka usingizini baada ya kusikia sauti ya mumewe. “Ndiyo.” “Jamani Mungu mkubwa, siamini kama mume wangu leo ukizungumza sauti inatoka!” “Niandalie maji nioge ili niwahi kazini.” “Unataka kwenda kazini?” “Ndiyo.” “Kwani unajua ulikuwa kwenye hali gani?” “Najua, si sauti ilikuwa haitoki sasa naweza kuwasiliana na wateja kama kawaida.” “Si ungeiangalia hali yako kwa wiki ndipo uende kazini?” “Ni kweli, lakini naamini nimepona.” “Mmh! Haya.” Mkewe Husna alinyanyuka kitandani na kwenda kumwandalia maji mumewe, baada ya kuoga na kupata kifungua kinywa aliondoka kwenda ofisini. Mlinzi alipomuona alishtuka. “Ha! Bosi.” “Vipi John.” “Umepona?” “Ndiyo, nipo ofisini,” Mustafa hakutaka mazungumzo mengi aliingia moja kwa moja ofisini na aliikuta ipo katika hali ya usafi aliouzoea japo hakuwepo kwa muda mrefu. Hakukuwa na mabadiliko yoyote naye hakuhoji kitu kama alivyoelekezwa na mpenzi wake Shehna. Alifanya kazi kama kawaida mpaka jioni na kurudi nyumbani. Husna alizidi kumshangaa mumewe na kutaka kujua tatizo lile lilitokana na nini. Baada ya chakula cha usiku wakiwa kitandani alitumia nafasi ile kumuuliza mumewe kilichomsibu. “Mume wangu pole kwa matatizo, maana asubuhi sikuweza kuzungumza na wewe baada ya kutoka kuwa na haraka ya kuwahi kazini.” “Asante.” “Hivi nini kilichokusibu kupoteza uwezo wa kuzungumza mpaka mganga akasema hutakiwi kutumia dawa yoyote?” “Mke wangu tuacheni na hayo.” “Hapana mume wangu, ni mimi ndiye nilikuwa nateseka kuishi na wewe muda wote ukiwa bubu. Lazima kuna kitu kilichosababisha hali ile, hata mlinzi alishtuka kuona ukibadilika ghafla wakati mlikuwa mkizungumza.” “Naomba uachane na hayo mke wangu kwa vile nimepona.” “Kwa nini?” “Kuwa mwelewa au unataka nirudi katika hali niliyokuwa nayo?” “Hapana.” “Basi tuachane na hayo.” “Nimekuelewa mume wangu.” Mustafa aligeukia upande wa pili na kuvuta shuka, mkewe naye alijisogeza karibu na mumewe na kumkumbatia kuitafuta siku ya pili. *** Kama kawaida Mustafa alishtuka na kujikuta akiwa pembeni ya mpenzi wake, uso wa Shehna ulikuwa na tabasamu pana na kuzidi kuongeza uzuri wake. Alimuangalia sana Mustafa kama anataka kusema kitu na kufanya aulize. “Vipi mpenzi?” “Najua kuna kitu kinakuumiza akili siku nzima.” “Kitu gani?” “Kuhusu Sara.” “Ni kweli, nilipanga kumuombea msamaha, nina imani wote tumekukosea.” “Mustafa wewe hujanikosea lakini Sara kanikosea sana kafikia hatua ya kutaka kuniua!” Shehna alisema kwa sauti ya kilio. “Adhabu aliyopata nina imani hawezi kurudia tena.” “Mustafa nitamleta mbele yako aseme siku akirudia sitampa adhabu bali kumuua, nimefanya hivyo kwa ajili ya mapenzi yangu kwako.” “Nakuahidi kuusemea moyo wake hatarudia tena.” “Sawa.” Shehna alinyanyuka na kutoka nje na kupiga makofi, vijakazi na watwana walifika haraka mbele yake kumsikiliza. “Naam binti wa mfalme wa bahari ya dhahabu unasemaje?” “Kamleteni Sara mbele yangu.” “Sawa binti mfalme.” Alitoweka ghafla na kumuacha Shehna akirudi ndani, kabla hajaweka makalio chini Sara alikuwa mbele yake katika umbile la kimbwa. Mustafa alishtuka kumuona mbwa mbele yao. “Mustafa usishtuke huyu ndiye Sara.” “Ha! Usishangae, sijawahi kuona kiumbe mwenye kiburi kama huyu mwanamke.” Sara yote aliyasikia lakini aliogopa kusema kuomba msamaha kwa kuogopa kubweka na kuwatisha. Machozi yalimtoka na kupiga magoti kuomba msamaha kwani mateso aliyopata asingeyasahau mpaka anakufa. Mustafa machozi ya uchungu yalimtoka kumuonea huruma Sara anavyotaabika. Shehna alimshika Sara kichwani, ghafla alirudi katika umbile la kibinadamu. Hakusubiri maelezo, Sara alijitupa chini ya miguu ya Shehna kuomba msamaha. “Shehna shoga yangu najua jinsi gani nilivyokukosea, nipo chini ya miguu yako haki ya Mungu, sitarudia tena kukufuatilia wala kufuatilia mambo yasiyonihusu. Nimeamini sisi wanadamu ndiyo wabaya, pamoja na mabaya yote niliyokutendea, hukuniacha nilale na njaa wala nile jalalani. Nakuahidi kama utanibakiza na umbile langu la kibinadamu, nitakuwa kiumbe kipya, sitajiingiza tena katika mambo yasiyonihusu.” “Nina imani sasa unanijua, mimi ni nani?” Shehna alimuuliza huku akimtazama kwa jicho kali.
“Shehna.” “Nilipokuja kwako ulinionaje?” Sara alishindwa kujibu alibakia kimya, Shehna alimuuliza tena. “Ulikwenda kwa waganga ili kuchunguza kama mimi ni nani?” “Ji..” hakumalizia, aliogopa kusema. “Malizia tu, kwani nilipokuja kwako nilikuambia mimi ni nani?” “Jini.” “Baada ya kunijua?” “Shehna, nimekukosea naomba unisamehe sitarudia tena, najutia nafsi yangu,” Sara alilia kilio cha majuto. “Mustafa elewaneni na Sara ili likitokea, mimi simo tena,” Shehna alijitoa kwenye kiburi cha Sara. “Sara, ukitoka hapa, ya hapa yaache hapahapa ukiropoka litakalokukuta utalia na nafsi yako.” “Kaka Mustafa sirudii tena, nimejifunza kiburi si maungwana.” “Nina imani mmeelewana leo sitazungumza chochote siku ukinitibua, nitakufanya kiumbe cha ajabu, siwezi kukuua tu ila cha moto utakiona.” “Shehna nakuapia sitathubutu kusema chochote wala kufanya lolote.” “Kesho utaamka asubuhi nyumbani kwako, majirani wakikuona lazima utakutana na maswali mengi, usiwajibu kitu, oga wahi kazini.” “Nimekuelewa shoga yangu.” Shehna alimshika Sara kichwa na kujikuta akipitiwa usingizi mzito, aliwaita wasaizidi wake wamrudishe nyumbani kwake ili asubuhi aamkie kitandani kwake. Baada ya Sara kuondoka, Shehna alimgeukia Mustafa aliyekuwa ametulia akimtazama na kumwambia: “Mustafa, kuanzia leo sitaonekana mchana wala kufika kazini kwako.” “Kwa nini?” “Sina tena uhuru wa awali, najiuliza atakaponiona mchana utanionaje au Sara akiniona ofisini atanionaje?” “Nina imani kila kitu kimeisha, nimesha kuelewa, siwezi kukushangaa.” “Kwako, lakini kwangu itachukuwa muda kujionesha wazi kwako.” “Sasa nikiwa na shida na wewe?” “Utaniona mara moja lakini si kama mwanzo.” “Mmh! Sawa,” Mustafa alikubali kwa shingo upande. “Mustafa naomba ukubaliane na mimi ili twende sawa.” “Nimekubali mpenzi.”
*** Siku iliyofuata Sara alishtuka asubuhi na kujikuta kitandani kwake, aliamka na kwenda kuoga. Alipotoka nje, majirani zake walimshangaa na kumuuliza alikuwa wapi. Aliwajibu alikuwa safari ila wangezungumza vizuri jioni akirudi kazini. Alikwenda kazini kama kawaida. Akiwa kazini alijawa na mawazo mengi juu ya maswali ya majirani zake, alijiuliza akirudi atawaeleza alikuwa wapi baada ya kuondoka ghafla. Mawazo yalipokuwa mengi, aliamua kwenda kwa bosi wake kuomba ushauri, baada ya kumsikiliza alimwambia: “We wanyamazie tu.” “Wasumbufu sana watataka kunichimba, nitashindwa kuwajibu.” “Ulikuwa na wazo gani?” “Kuhama pale.” “Hakuna tatizo.” Mara simu iliita Mustafa alipoangalia alikuta ni Shehna, alisema kwa sauti. “Shehna.” “Anasemaje shoga yangu,” Sara alisema kwa tabasamu. Alipokea simu: “Haloo mpenzi.” “Nipe Sara.” Mustafa alimpa simu Sara. “Haloo shoga,” Sara alisema baada ya kuchukua simu. “Ni hivi, ukitoka hapo usirudi nyumbani, umeshahamishwa.” “Nimehamishiwa wapi?” “Masaki, nyumba inatazamana na duka la jumla, nina imani hayo yatakuwa maisha yako mapya.” “Asante shoga, ufunguo?” “Mustafa atakupeleka sehemu yako mpya.” “Asante shoga.” “Haya kwaheri.” Sara alimpa Mustafa simu, baada ya kupokea alipewa maelekezo na Shehna, baada ya kukata simu alimgeukia Sara na kumueleza. “Ukimaliza kazi nitakupeleka.” “Duh! Siamini nikitoka kazini nakwenda Masaki, siamini nami nimekuwa mtu wa matawi ya juu!” Sara alisema akishika kifua. “Hongera, ulitaka kumtibua bure kumbe mambo mazuri yalikuwa yakija.” “Mbona nimekoma.” “Nina imani tatizo lako limekwisha, kaendelee na kazi.” “Sawa bosi,” Sara alirudi kuendelea na kazi. Muda wa kutoka Mustafa alimpeleka Msaki kwenye nyumba aliyoelekezwa na Shehna. Ilikuwa nyumba nzuri iliyokuwa na kila kitu ndani, hakukuwa na kitu chochote kutoka chumbani kwake zaidi ya vitu vyake vyote muhimu. Sara aliendelea kumshukuru Shehna na kuona kumbe jini ni umbile lakini wapo wenye roho nzuri kushinda hata wanadamu. *** Mwezi moja kabla ya kujifungua, Shehna alimweleza Mustafa kuwa muda ule anatakiwa kuwa sehemu maalum ambayo hatakiwi mtu yeyote kuingiza zaidi ya mzazi wake na mkunga tu. Pia alimweleza kuonana naye itakuwa baada ya miaka mitatu. Mustafa alikubaliana naye, hakuwa na kipingamizi.
Muda ulipofika Shehna alijifungua watoto mapacha watatu wa kike wawili na wa kiume mmoja. Ilikuwa ni furaha ilioje kufanikiwa kupata watoto toka kwa mwanadamu. Wakati wa kujifungua mawasiliano kati ya Mustafa na Shehna yalipotea, siku zote Mustafa alikuwa na hamu ya kuonana na Shehna lakini masharti yalimzuia. Shehna baada ya matukio yote ya kuhatarisha maisha yake alikatazwa na wazazi wake asionekane mchana katika umbile la kibinadamu kwa muda wa miaka mitano nyongeza ya miaka miwili. “Shehna kama mtoto umepata, sasa tulia kama ukiwa na shida na baba wa watoto wako tutamleta hukuhuku akiwa ndotoni baada ya miaka mitatu. Lakini kuonana naye akiwa na akili timamu ni baada ya miaka mitano.” “Kwa hiyo nitarudi lini kama zamani?” “Baada ya miaka kumi na tano ruksa kurudi t-ena katika umbile lako la kawaida na kutembea mchana kila mtu atakuwa amesahau yote yaliyopita hata watoto kumtembelea baba yao.” “Sawa.” Kuanzia siku ile Shehna aliendelea kulea wanaye kwa muda wote huo hakuweza kuwasiliana na Mustafa japokuwa alijua mzazi mwenzie alikuwa katika mawazo mazito ya kumtafuta mpenzi wake. Lakini aliheshimu maelekezo ya wazazi wake kwa kuhofia kwenda kinyume na kukutwa na matatizo. Wakati Shehna akipewa maelezo na mama yake upande wa pili nyumba ya Mustafa ilikuwa inawaka moto baada ya wazazi wa Mustafa kumjia juu mtoto wao kutokana na siku kukatika bila kupatikana mtoto. Pamoja na kuwasihi wawe wavumilivu kwa vile mtoto ni siri ya Mungu hawakukubaliana naye. Walitaka aachane na Husna kwa vile walikuwa wakitaka mjukuu, aliwaeleza mwaka ule ukiisha bila mkewe kushika ujauzito ruksa kuivunja ndoa yao. Wazazi wake walimkubalia na kumweleza mwaka ukikatika bila mtoto watampelekea mke nyumbani kwake.
Mustafa aliondoka kwao kichwa kikimuuma na kujiuliza zawadi aliyotaka kupewa na Shehna ya mkewe kushika ujauzito atapewa lini. Upande mwingine alimlaumu mkewe kwa kitendo chake kukiuka masharti ya Shehna muda ule wangekuwa na mtoto. Kibaya zaidi muda ule alikuwa amepoteza mawasiliano. Alirudi nyumbani akiwa mnyonge sana, hakujua hatima ya ndoa yake kwa kuona mwaka unaweza kukatika kabla mkewe hajashika ujauzito na kufanya wazazi wake kumletea mke mwingine. Usiku wa siku ile alichukuliwa na kupelekwa chini ya bahari, aliposhtuka alijiona yupo pembeni ya Shehna ambaye wakati huo hakuwa na tumbo kubwa. Ile ilimjulisha moja kwa moja tayari Shehna amejifungua. “Pole mpenzi wangu.” “Sijapoa kwa vile ndoa yangu inavunjika wakati wowote.” “Najua ndiyo maana nimekuleta huku kabla muda wake, ilikuwa kazi nzito kuwashawishi wazazi wangu uje huku wakati ni juzi tu nimejifungua. Kwanza napenda kukupa hongera ya kuwa baba wa watoto wangu. “Mungu kajalia nimejifungua mapacha watatu wawili wa kike mmoja wa kiume, wa kike ni wazuri kuliko mama yao na wa kiume ni mzuri kama baba yake. Kwa vile muda wangu wa kutoka huku bado. Niliwaomba wazazi wangu uje tujadiliane ili kuiokoa ndoa yako.” “Nitashukuru.” “Sasa kuna kitu nataka tukifanye iwe siri yetu, kwa sasa itakuwa vigumu kwa mkeo kushika ujauzito mpaka watoto wangu wafikishe mwaka. Kwa muda uliozungumza na wazazi wako lazima utapita na wazazi wako watavunja ndoa, najua na wewe unampenda sana mkeo.” “Ni kweli.” “Ni hivi nitampatia mkeo mimba tupu ambayo itakuwa ya muda mfupi kuliko mimba zote. Muda ukifika atakwenda kujifungua, kitakachotoka tumboni mwake kitakuwa upepo ambao utafanya wakunga wapitiwe na usingizi mfupi pamoja na mkeo. Sauti ya mtoto ndiyo itakayo washtua wakiamka watakuta mtoto pembeni ya mama yake.” “Umesema atakuwa na mimba hewa na tumboni kutatoka hewa mtoto huyo atatoka wapi?” “Mustafa nipo kwa ajili yakuokoa ndoa yako, kati ya wanangu nitamtoa mmoja ambaye wakati wamelala ataletwa na kuachwa hapo ili wakishtuka wajue amejifungua.
Nina imani baada ya hapo kesi itakuwa imeisha kwa wazazi wako kuamini mkeo siyo mgumba.” “Kwa hiyo utamuachia huyo mtoto?” “Hapana nitampa kwa miezi mitatu, kisha nitamchukua. Nahofia akianza kukua atakuwa na tabia za ajabu ambazo zitawachanganya hasa mkeo na majirani. Kwako atakuwa mwoga kwa vile ni baba yake lakini kwa mtu mwingine itakuwa vigumu kumsikiliza.” “Utamchukua vipi?” “Atapotea katika mazingira ya kutatanisha, usishtuke nitakuwa nimemchukua mwenyewe.” “Sisi utatuachaje?” “Najua mkeo ataumia kupotelewa na mwanaye, mbembeleze kwa vile baada ya muda mfupi atashika mimba ya kweli na kuzaa mtoto wa kwenu asiye na masharti.” “Mmh! Sawa.” “Mustafa usihuzunike kwa vile sina jinsi lazima nifanye hivyo ili kuokoa ndoa yako, nitakupa dawa utampa kwenye maji akinywa atakuwa na dalili zote za ujauzito. Najua atashtuka mwambie anywe maji glasi moja kuituliza. Ujauzito huo utakuwa wa miezi mitano safari hii nendeni hospitali ili wazazi wako wajue ujauzito kumbe ni wa muda mrefu, baada ya miezi miwili atajifungua.” “Sawa.” Mustafa aliposhtuka akijikuta amelala kitandani kwake akiwa na dawa mkononi. Aliamka na kutulia kitandani kwa muda akikumbuka yote aliyoelezwa na Shehna, hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali ili kuiokoa ndoa yake. Asubuhi kabla ya kwenda kazini alimpa mkewe dawa aliyopewa usingizini na Shehna, baada ya mkewe kunywa alimuaga na kwenda kazini. Alipofika kazini kabla ya kuanza kazi mkewe alimpigia simu hali yake ni mbaya kama mtu mwenye ujauzito wa muda mrefu.
Alimwambia anywe glasi moja ya maji, mkewe alifanya hivyo, baada ya kunywa hali ilitulia lakini alikuwa amechoka sana, alipanda kitandani kulala. Alipoamka alijishangaa kukuta tumbo limekuwa kama ujauzito wa muda mrefu.Ile hali ilimshtua na kumpigia simu mumewe kumweleza kilichotokea. “Usiogope hiyo ni hali ya kawaida huenda ujauzito huo uliingia muda mrefu, dawa niliyokupa imeufukua hivyo usiwe na wasiwasi. Kama vipi nenda hospitali ukapime hali yako.”
“Mume wangu hunipendi, tuliambiwa nini na Shehna?” “Amesema sasa tunaweza kwenda.” “Hapana tafuta ufumbuzi mwingine, sirudii kosa kidogo nife,” Husna aliogopa kurudia kosa. “Usiwe na wasi mke wangu, Shehna ameruhusu, basi subiri nije nikupeleke mwenyewe.” “Kama hivyo sawa.” Mustafa aliacha kazi zake na kurudi nyumbani kumfuata mkewe na kumpeleka hospitali, alipofika nyumbani alishtuka kuona tumbo la mkewe limekuwa kubwa la ujauzito wa muda mrefu. Lakini alificha mshtuko wake kwa kuhofia kumshtua mkewe na kuona kitu cha ajabu kimemtokea. Alimchukua na kumpeleka hospitali ambako katika kufanyiwa vipimo ilionesha ujauzito upo sawa. Daktari alishangaa kukaa nao zaidi ya miezi mitano bila kufika hospitali, alimuonya asifanye vile tena kukaa na ujauzito kwa muda mrefu vile. Baada ya maelekezo waliruhusiwa kurudi nyumbani akiwa amechoka kama ujauzito wote ulipitia hatua zote kufikia hatua ya kumchosha vile. Walikubali na mumewe kukaa na siri ya chanzo cha ujauzito ule, ilikuwa tofauti na ujauzito anaoufahamu. Miezi miwili baadaye ujauzito ulipofikisha miezi saba kwa vipimo vya hospitali na maelezo ya Shehna, Husna alishikwa na uchungu mkali na kukimbizwa hospitali. Kutokana na muda wa ujauzito ule, wengi waliamini ni maumivu ya tumbo tu, lakini kulionekana dalili zote za kujifungua. Baada ya kufikishwa Husna aliendelea kuugungulia huku mkono mmoja umeshika kiuno na mwingine kichwa kutokana na maumivu makali ya uchungu. Wauguzi walimkimbiza wodini wakiwa hawana uhakika kama siku ile ndiyo ilikuwa ya kujifungua. Baada ya kumfikisha walimpandisha kitandani huku Husna akiendelea kulalamika katika dalili zote za kujifungua. Ilibidi wampe huduma ya kujifungua, Husna alianza kusukuma mtoto, ghafla ulitoka moshi uliowafanya wote walewe na kusinzia. Muda huo Shehna alimtuma jini wa kike kumpeleka mtoto wake wa kiume aliyekuwa akifanana na baba yake na kumweka pembeni ya Husna. Baada ya muda wote walishtushwa na kilio cha mtoto. Mtoto alikuwa amesha katwa kitovu kabisa na kusafishwa.
Hakuna aliyejua nani kafanya vile, kila mmoja aliamini mwenzake ndiye kafanya. Walimpa hongera mzazi kwa kupata mtoto wa kiume mwenye afya nzuri, hali ya mzazi nayo ilikuwa njema. Alipelekwa wodini kwa huduma zaidi. Baada ya taratibu zote, Husna aliruhusiwa kutoka hospitali na kurudi nyumbani na mwanaye ambaye kila aliyemuona alisema anafanana na baba yake. Mustafa alijua kila kitu na kubaki na siri nzito moyoni huku amani akirudi nyumbani kwake kwa familia kufurahi na kusema mpaka wamtishe ndipo atafute mtoto. Japokuwa yule mtoto alikuwa wa kwake lakini hakuwa wa mkewe bali wa jini Shehna. Siku nazo zilikatika muda nao ulisogea mtoto wa Shehna kurudi kwa mama yake. Miezi mitatu ilipotimu, alitumwa jini kumfuata mtoto, akiwa katika umbile la kibinadamu mwanamke aliyevaa kiheshima. Jini Shaunani alitembea taratibu na kubisha hodi kwenye nyumba ya Mustafa. Wakati huo mke wa Mustafa alimkuta amemaliza kumnyonyesha mtoto, alikwenda kufungua mlango na kumuona mwanamke mzuri aliyekuwa akinukia manukato kama anayotumia mumewe. “Karibu.” “Asante,” mgeni alijibu huku akiingia ndani. Alipofika aliketi na kusema: “Habari za hapa.” “Sultani hajambo?” lilikuwa jina la mtoto ambalo Mustafa aliambiwa ampe mtoto na ndilo lilikuwa jina lake la ujijini. “Hajambo.” “Hebu nimuone.” Husna bila wasi alimkabidhi mtoto jini Shaunani ambaye alikuwa mcheshi sana. Kutokana na ucheshi wake, alimzoea haraka Husna, hakuwa na wasiwasi alimuomba samahani. “Samahani mgeni natoa vyombo vya mtoto.” “Hakuna tatizo.” Husna alirudisha vyombo vya mtoto jikoni na kurudi kumsikiliza mgeni, baada ya kukaa alimkaribisha tena. “Karibu mgeni.” “Asante,” kabla Husna hajaongeza neno simu iliita na kumshangaza kuitia chumbani wakati alikuwa nayo muda mfupi na hakurudi chumbani. “Jamani hii ajabu simu nilikuwa nayo hata sijui niliondoka nayo muda gani kwenda nayo chumbani.”
“Labda umesahau haiwezi kujibeba yenyewe, kasikilize huenda ni shemeji,” jini Shaunani alisema. Husna alinyanyuka na kwenda kupokea simu, kitendo cha kuingia chumbani tu. Jini Shaunani alitoweka na mtoto. Husna alipofika chumbani alishangaa kukuta simu haina ‘missed calls’. Alishangaa wakati alisikia simu ikiita kabisa hata mgeni alisikia. Alitoka sebuleni alishangaa kukuta sebule tupu, hakuna mgeni wala mtoto wake. “Mgeni…mgeni,” aliita kwa sauti. Hakukuwa na jibu alitoka nje labda ametoka vilevile hakukuwa na jibu lolote, alijiuliza atakuwa amekwenda wapi. Alitoka hadi nyumba ya pili labda wamemuona mtu akiwa na mtoto nao walisema hawajamuona. Alimpigia simu mumewe kumueleza kupotea ghafla kwa mwanaye. Taarifa ile haikuwa ngeni kwa Mustafa, alijua mtoto keshachukuliwa na mama yake. Alirudi nyumbani haraka ili kumtuliza mkewe ambaye muda ule alikuwa amepagawa. Alipofika alimkuta amepagawa akilia ovyo mikono kichwani. Husna alipomuona mumewe alimkimbilia na kumkumbatia na kuendeleza kilio. “Mume wangu mwanangu ameibiwa!”
Alijitahidi kumbembeleza na kumueleza watamtafuta, walipeleka taarifa polisi na kwenye vyombo vya habari lakini ajabu walipotafuta picha za mtoto hawakuziona. Taarifa ilitawanyika kila kona ambayo siri yake alikuwa akiijua Mustafa. Familia ya mume nayo iliungana na Husna katika tukio lile. Japokuwa mtoto alikuwa amepotea lakini hali ya amani ilikuwepo kwenye ndoa na wazazi kuamini mkwe wao siyo mgumba. Walimpa moyo kuwa awe makini na watu wasiojulikana kutokana na tabia za watu kuiba watoto wachanga. Mustafa alitengeneza uongo kwa kumueleza kuwa Shehna amesema asilie kwa vile mtoto wao atarudi na kumfanya aishi kwa matumaini. Kupotea kwa mtoto kulifanya wazazi wa Mustafa waendelee kumpa moyo Husna kwa kuhofia kumuumiza kwa kumkumbusha maumivu ya kuibiwa mtoto wake. Baada ya miezi saba kukatika, usiku mmoja Mustafa aliota akizungumza na Shehna akimueleza kuwa ni muda muafaka mkewe kushika ujauzito wa kweli. Shehna aliendelea kumueleza mtoto yule atakuwa chini ya ulinzi wa majini mpaka atakapokuwa ndipo atarudishwa chini ya wazazi wake. Lakini wakati huo ndugu zake watakuwa wamekua, wataendelea kumlinda siku zote za uhai wake. Baada ya wiki moja akiwa kazini mkewe alimpigia simu kumweleza mumewe hali aliyohisi, Mustafa alijua dalili zile zilikuwa majibu ya ndoto aliyoota, walipokwenda hospitali vipimo vilionesha ujauzito wa mwezi mmoja. Ujauzito ule ulikuja kawaida wa miezi tisa tofauti na mimba ya ajabu iliyotangulia ya miezi miwili tu mtoto kuzaliwa. Ujauzito ulikwenda vizuri ulipotimiza miezi tisa alijifungua salama mtoto wa kiume, Husna baada ya kujifungua alimlinda sana mwanaye ili asirudie kosa la awali. Mtoto alikuwa katika malezi mazuri, Mustafa na Sara waliendelea na kazi zao huku Sara akiwa na somo kubwa maishani mwake kuwa mwanadamu anaweza kuwa mbaya kuliko jini pia kutofuatilia lisilokuhusu. Hakuamini kama majini wana roho nzuri siku zote aliamini ni viumbe wabaya kumbe wapo wazuri na wabaya kama wanadamu.
Mustafa alisubiri miaka mitatu ili aende kwa Shehna kwa njia ya ndoto kuwaona watoto wake japo wa kiume alimuona. Mtoto wao naye alikuwa vizuri bila kujua akiwa mkubwa atakuwa na tabia gani? Mwisho.
hichi kisa ni cha msichana jini aitwae nargis ni kisa cha ajabu kimenza kiajabu ila utakielewa tu usijali
Nargis baada ya kutoa onyo kali kwa mke wa Sule anaamua kuua ndege wawili kwa jiwe moja. Kabla ya kurudi chini ya mwamba wa baharini anaamua kwanza kuingia mawindoni kumtafutia dada yake nyeti za wanaume waliooa. Akiwa ameanza kukata tamaa anakutana na mzee Samweli, mzee mwenye uchu wa ngono. Nini hatma ya mzee Samweli mbele ya jini Nargis. Kuyajua yote TWENDE USICHOKE…
Mzee Samweli aliwasha gari na kufuata barabara ya Sam Nujoma, baada ya gari kutulia alimgeukia binti aliyeonekana kukamilika kila kiungo. Na pombe alizokunywa zilizidi kumtoa akili na kumuongezea hamu ya ngono akiwa tayari kumpa kiasi chochote cha pesa ili afanye naye ngono garini. “Binti usiku wote huu unatoka wapi?” “Natoka Bagamoyo kwa mjomba nimefika muda huu ndiyo nilikuwa nasubiri gari.” “Ooh pole, umeolewa?” “Bado,” Nargis alimjibu huku akimlegezea macho.
“ Nina imani usiku wa leo tunaweza kuwa pamoja, etii!” “Ikiwezekana.”
Mzee Samweli kutokana na hamu ya ngono kumpanda alijikuta akipaki gari pembeni ili akidhi haja zake, mara nyingi shughuli zake alikuwa akimalizia kwenye gari kwa kulaza kiti kwa nyuma.
“Humu humu?” Nargis aliuliza baada ya mzee Samweli kupaki gari pembeni na kumsogelea.
“Si lazima guest humu humu panatosha mambo ya guest siku nyingine.”
“Mmh, sawa,” Nargis alikubali huku akivua nguo zake na kubakia mtupu tayari kwa tendo la ndoa. Naye mzee Samweli alivua nguo zake kwa uchu baada ya kuliona umbile maridhawa la Nargis, wakati anajiandaa kufanya tendo lile mikono ya Nargis ilibadilika na kuwa na makucha makali. Alimshika sehemu za siri za mzee Samweli na kumng’oa. Mzee Samweli alipiga kelele za maumivu makali, kwa kuwa alikuwa amefunga vioo sauti yake iliishia ndani ya gari. Nargis baada ya kupata alichokitaka aliondoka na kurudi kwao. Dada yake aliyekuwa na hasira kali baada ya kumsaka mdogo wake kwa udi na uvumba kila kona ya dunia bila mafanikio alipomuona alishangaa na kujawa na furaha baada ya mdogo wake akimletea kitu alichokitaka. Alijikuta akitabasamu kwa furaha na kumkumbatia.
Nargis alitumia nafasi ile kumuomba dada yake aachane na wazo baya la kumdhuru mpenzi wake Thabit.
“Mdogo wangu leo umenifurahisha sana, nakuahidi kumlinda mpenzi wako na sitamdhuru tena.”
“Asante dada, ” Nargis alimkumbatia dada yake kwa furaha. “Lakini pamoja na kumuacha chonde chonde usimueleze siri zetu sisi majini, wanadamu nawajua lazima watatuangamiza. Na nikijua umeitoa siri nje ujue sitakuwa na simile nitamfutilia mbali, pia vitu alivyoviona kituo cha Mwenge ibakie siri yake moyoni mwake.” “Nitafanya hivyo dada yangu sitatoa siri yetu, kuhusu kuitoa siri ya Mwenge niliisha mueleza mapema.” “Ukifanya hivyo ruksa kuwa na mpenzi wako, na kama atakuwa msiri hata mimi nitampenda.”
Baada ya kukubaliana na dada yake aliondoka na kwenda kwa Thabit ambaye alimuacha kwa muda mrefu. Aliondoka bila kuaga kuwahi chini ya mwamba bahari, kwa haraka alisahau hata kufuta damu zilizokuwa zimemtapakaa mikononi baada ya kumtoa mzee Samweli sehemu za siri. Alipofika chini ya mwamba wa bahari alimkuta Thabit amelala kwenye kipande cha mwamba akiwa amejikunja kwa baridi. Nargis alimuonea huruma na kujikuta akiingiwa na hofu na kushindwa kuelewa atamwambia kitu gani ambacho kitamtuliza Thabit. Alimsogelea huku akipoteza kujiamini na kumtikisa taratibu, Thabit alishtuka huku mwili ukiwa umekufa ganzi kwa baridi kali la chini ya mwamba wa bahari. Cha kwanza kukiona Thabit kwa Nargis ni damu zilizokuwa mikononi mwake, damu zile zilimshtua sana. “Mpenzi vipi tena umeumia?” “Ha..ha..pana,” Nargis alijibu huku akijiangalia mikono na kujiona ameumbuka kubakia na damu mkononi. “Damu hizo za nini?” “Ni..ni…ni, Thabit achana nazo.” “Au umemuua mtu?” “Thabitiii,” kauli ya Thabit ilimvunja nguvu Nargis na kukosa cha kujitetea. “Nargis kwanza ulikwenda wapi, mbona umekuja kunitesa huku chini ya mwamba wa bahari na baridi kali.” “Nisamehe mpenzi wangu kila nitendalo ni kwa ajili ya kuyalinda maisha yako.” “Ulikwenda wapi?” Thabit alimuuliza huku akizidi kujikunyata kwa ubaridi mkali uliokuwa ukivuma kama mvua inayonyesha. “Nilikwenda kumkataza mke wa Sule asifanye alichokikusudia.” “Alitaka kufanya nini?” “Kwani alikuambia atakupa nini?” “Kitunguu saumu na mfupa wa nguruwe.” “Vitu vile sisi hatupatani navyo, ukiwa navyo mimi na wewe tungekuwa mbali mbali na kama tungekuwa mbali mbali basi dada angeweza kukuua kwa urahisi usingekuwa na kinga tena.” “Kwa hiyo umemkataza?” “Nimemkataza lakini akizidi nitamshikisha adabu.” “Utamuua?” “Siwezi kumuua ila najua nitakachomfanya, sipendi kumuua mtu kwani ni kitu ambacho nakichukia sana.” “Unasema unachukia kuua na hii damu ya nini?” “Thabit lazima niwe muwazi kwako ili uelewe kila nikifanyacho nafanya kwa ajili gani” “Nakusikiliza.”
“Thabit, mimi kuwa na wewe haikuwa vita kati yangu na familia yangu tu, bali hata kwa wanadamu ambao nao walitaka kuhakikisha wanavunja uhusiano wetu. Na vita hii bado endelevu kwa kuamini bado kuna watu wataendelea kutuchimba ambao wote sitawaruhusu kunichezea.
Baada ya kumuonya mke wa Sule ilibidi nimtafutie dada nyeti za mwanaume ambazo huzipenda. Kibaya au kizuri siku ile ilikuwa ngumu kupata, hata mimi nilianza kuchemka na nilipofanikiwa mimi peke yangu nilifurahi sana na nilipompelekea alifurahi nami nilichukua nafasi ile kukuombea msamaha kwa dada, nakuahidi yule mtu ndiye wa mwisho sitaua tena.”
“Alisemaje?” “Amekusamehe na pia kukuongezea ulinzi, ila amekuonya kila ukionacho huku na popote iwe siri yako siku ukiitoa siri hii ujue na mauti yanakufika hata kabla hujamalizia kuitoa siri hiyo.” “Umesema hutaua tena, je dada yako akitaka nyeti za mwanaume tena utafanyaje?” “Nitamueleza nina imani atanielewa, sasa hivi najipanga kuimarisha penzi langu ambalo lilinikosesha raha.” “Basi nirudishe nikalale nasikia baridi.” “Thabit leo nilikuwa na hamu ya kulala na wewe nyumbani, kwa vyovyote tukienda nyumbani na kusikia harufu ya huku watajua tulikuwa wote hivyo watakuwa na wasi wasi tumekuja kufanya nini.” “Kwa hiyo?” “Nitakurudisha kwako ila tafuta chumba kwa siku mbili hizi uhame.” Nargis alimkumbatia Thabit walipaa wote na kujikuta wakitokea mbele ya mlango wa Thabit. Nje ya nyumba alimkuta Sule akiwa amempakata mtoto wake mdogo aliyekuwa akilia. “Vipi mbona mtoto analia?” Thabit aliuliza huku akifungua mlango ili aingie ndani.” “Aah, shemeji yako amekwenda dukani,” Sule alidanganya. Kauli ya Sule ilimfanya Nargis acheke kimoyomoyo kwa kujua mke yupo wapi kwa muda ule.
Thabit na Nargis waliingia ndani na kumuacha Sule akimsubiri mkewe ambaye alijua amekwenda kufuata mavi ya nguruwe na mifupa yake. Muda ule alijikuta katika wakati mgumu kutokana na mwanae kulia mfululizo bila kuchoka akimtaka mama yake. Muda ulikatika bila kuona dalili za mke wake kurudi na seheme yenyewe ilikuwa ya dakika tano. Wakati huo mtoto wake ndiyo alizidisha kulia, Nargis kwa ajili ya kuwatia adabu kwa kitendo walichotaka kufanya na mkewe, alimuaga Thabit kuwa anakwenda msalani na kumuacha amejilaza kitandani.
Alijigeuza kiumbe wa kutisha ambaye Sule hakumuona ila mwanae na kuanza kumtisha mtoto wa Sule ambaye alizidi kupiga kelele za woga kila alipomuona Nargis katika umbile la kutisha. Sule uzalendo ulimshinda na aliamua kumfuata mkewe ili ajue amepatwa na masaibu gani kutokana na muda kuzidi kukatika huku mtoto akizidi kulia tena alikuwa akipiga kelele za kuogopa kitu kutokana na kutishwa na Nargis.
Sule alikwenda hadi kwenye banda la nguruwe lakini hakumuona mkewe, alijiuliza atakuwa amekwenda wapi. Nargis naye aliendelea kumtisha mtoto wa Sule ambaye alikuwa akipiga kelele njia nzima. Kuteseka kwa Sule, Nargis alifurahi sana. Moyoni aliona Thabit ndiye atakaye waokoa kwa vile angeshtuka akimuona anachelewa, baada ya mshike mshike wa zaidi ya nusu saa, Nargis alimuacha Sule na kurudi ndani kwa Thabit. Alipofika alimkuta Thabit amejilaza, alitoa nguo zake na kujilaza pembeni ya Thabit kwa kumkumbatia.
*** Mke wa Sule alijikuta akitembea umbali mrefu bila kujua anakwenda wapi, alijikuta akitembea siku tatu bila kujua na siku zote alizotembea ilikuwa ni usiku. Kwa akili yake aliona ametembea siku moja na usiku mmoja, lakini ilikuwa adhabu aliyopewa na Nargis kama onyo la kutaka kufuatilia mambo yake. Alijikuta akitembea mpaka kuna pambazuka bila kupumzika, alishangaa kufika sehemu ambayo ilikuwa ngeni kwake. Miguu yake ilijaa matope na michubuko mingi kuonesha alikuwa akipita kwenye miba bila kujua. Alionekana nusu mwenzawazimu, kila aliyemuona alimshangaa kwani eneo lile hakukuwa na mwendawazimu kama yule.
Mke wa Sule akiwa mtu aliyekuwa akishangaa mazingira yale ambayo yalikuwa mageni machoni mwake, machoni mwa watu alionekana mtu aliyechakaa, nywele zake zilikuwa timutimu nguo zilikuwa zimechanika mwili ulikuwa umejaa vumbi na chini alikuwa peku huku miguu ikiwa imejaa tope. Alitembea kwa kuchechemea kuwasogelea watu ili kutaka kujua pale ni wapi, alimsogelea kijana mmoja aliyekuwa ameshikilia maembe kwenye mfuko wa Rambo aliyokuwa akiuza kwa wasafiri waliokuwa wakipita na mabasi ya mkoani.
“Samahani sasa.” “Bila samahani,” muuza maembe alimsikiliza huku akimshangaa. “Eti hapa ni wapi?” “Kwani dada unatoka wapi?” “Dar es Salaam.” “Dar es salaam! Huku umefikaje?” “Kwani huku wapi?” “Kabla sijakujibu umetokaje Dar mpaka kufika huku?” “Kaka yangu mbona swali juu ya swali, kwanza nieleze hapa ni wapi?”
“Hapa ni Msamvu.” “He! Msamvu, si ipo Morogoro?” Mke wa Sule alishtuka kusikia amefika Msamvu kwa miguu. “Eeh, kwani vipi?” “Mungu wangu ina maana nimetoka Dar kwa miguu mpaka huku.” “Dada akili yako ipo timamu kweli?” “Ipo timamu wala haina tatizo ila sijui huku nimefikaje?” Wakati wakiulizana maswali watu walikuwa wakijikusanya kumsikiliza mke wa Sule ili kujua kapatwa na masahibu gani kwani alionekana kuchanganyikiwa mikono ilikuwa kichwani asiamini kama kweli ametembea kwa miguu toka Dar hadi Msamvu Morogoro.
Mke wa Sule alijikuta akilia mikono kichwani na kuona muujiza wa ajabu kutembea kwa miguu toka Dar mpaka Msamvu Morogoro bila kuchoka. Watu walizidi kujisogeza na kumuweka kati huku wengine wakitaka kujua ilikuwaje atoke Dar mpaka Morogoro kwa miguu. “Eti dada imekuwaje mpaka umefika huku?” Mtu mmoja kati ya watu waliomzunguka alimuuliza. Kabla ya kujibu alitulia na kukumbuka jinsi alivyokutana na Nargis mpenzi wa Thabit mwanamke aliyethibitisha kweli ni Jini kutokana na jinsi alivyotokea tokea na kubadilika kwa sura toka ya Devi mtunza nguruwe mpaka ya kwake halisi.
Alikumbuka onyo alilopewa na kufuatilia maisha yake, moyoni aliapa kupambana na Nargis mpaka tone la mwisho la damu yake. Akiwa ameinama ameshika kichwa mtu mmoja aliyekuwa amesimama pembeni alisema: “Jamani huyu mwanamke lazima atakuwa na tatizo la ugonjwa wa akili hawezi kutembea toka Dar mpaka huku kwa miguu ni muongo na pia alalolisema halijui.” “Jamani ndugu zangu sina tatizo la ugonjwa wa akili nina akili zangu timamu, na nisemayo ni kweli kabisa.” “Sasa mbona hutuelezi ilikuwaje ukafika huku kwa miguu?” “Kuna mpangaji mwenzetu alitongoza mwanamke ambaye tunaamini ni Jini.”
“Jiniiii?” Wote walishtuka kusikia Jini. “Eeeh, Jini…..,” mke wa Sule alinyamaza ghafla baada ya kumuona Nargis katika kundi la watu waliokuwa wakimsikiliza aliyekuwa akimuangalia kwa hasira na macho kuwaka kama taa.
Mke wa Sule baada ya kupewa adhabu nzito ya kutembea kutoka Dar mpaka Morogoro kwa miguu kwa siku tatu, Nargis anaamua kumpa onyo kali mke wa Sule kwamba kama ataitoa siri ile, basi atamgeuza nguruwe. Mke wa Sule baada ya kubanwa sana na mumewe juu ya wapi alipokuwa siku tatu, anaamua kuusema ukweli. Nini adhabu yake kwa Nargis kama akitoa siri ile? Ili kuyajua yote TUWE PAMOJA TENA… “Mungu wangu unataka kuniambia niliondoka juzi na kutembea kwa siku tatu mpaka Morogoro?” “Morogoro?”Sule naye alishtuka. “Ndio mume wangu, ndiyo maana nimefika Morogoro kwa miguu.” “Morogoro kwa miguu?” “Ndiyo.” “Na Dar umerudije?”
“Hapana mke wangu au una siri yako.” “Siri yangu! Ya nini?” “Inawezekana una mwanaume mwingine kwa hivyo unataka kunizungusha,” Sule alimjia juu mkewe. “Mume wangu umefika huko?”
“Haya nieleze kwa siku tatu ulikuwa wapi?” “Mume wangu unanipa mtihani mzito.” “Hakuna cha mtihani nataka ukweli,” Sule alimjia juu mkewe. Mkewe ili kuilinda ndoa yake ilibidi awe mpole na kukubali kueleza ukweli. “Mume wangu sina jinsi liwalo na liwe.” Wakati huo sauti ya Jini Nargis ilizidi kutanda masikioni kwa mke wa Sule. Alijifanya hasikii sauti ile na kuamua kumueleza ukweli mumewe. “Basi mume wangu juzi baada ya kutoka hapa nilikwenda moja kwa moja kwa Davi kutunza nguruwe lakini njiani nilikutana naye, kuonesha alikuwa akinifuata. Nilimshukuru na kutaka kunipa ule mzigo, Ha! Si ndio mtu yule akageuka.” “Akageuka? Akageuka kivipi?” “Si..si..si..akageuka na….”
Hakumalizia alimshangaa mume wake akipiga kelele za mshtuko. “Mama nakufa,” usoni kwake kulikuwa kukichuruzika damu, kitu kilichomshangaza mke wa Sule. Pembeni yao kulikuwa na paka mmoja aliyekuwa amemrukia usoni na kumparua, na kumsababishia michumbuko na michirizi ya damu usoni. “Vipi mume wangu?”
“Nooo, haiwezekani” “Haiwezekani nini?” “Paka huyu ametoka mdomoni mwako.” “Muongo!” Mkewe alishtuka. “Kweli wakati unazungumza niliona mdomo wako ukiongezeka ukubwa mara paka huyu akatoka mdomoni kwako na kunirukia usoni mwangu na kuniparua.
“Mamaaaa yaani paka huyu katoka tumboni mwangu?” “Yaani ni ajabu na kweli paka ametoka mdomoni mwako.” “Mungu wangu nimekwisha, paka…eeeh muone anazidi kuwa mkubwa kama mbwa,” Mke wa Sule alishtuka kumuona yule paka akitutumka. “Au ndio jini…”
Kabla hajamalizia kumtaja jini, yule paka aliingia mdomoni kwa Sule na kumfanya mkewe apige kelele za woga. “Mama, mume wangu.” Baada ya paka kumuingia kinywani mkia ulibakia unaonekana mdomoni, muda huo Sule alikuwa ameanguka chini na kukauka kama kipande cha mti kilichopigwa na jua kwa muda mrefu. Mkewe alimtikisa mumewe aliyeonekana amekufa na kuangua yowe, wa kwanza kuingia ndani alikuwa Thabit. “Vipi shem kuna nini mbona unalia, kuna usalama?” “Hata nashindwa kuelezea.”
“Mbona yupo hivi.” “Thabit mpenzi njoo mara moja,” sauti ya Nargis ilitoka nje. “Shemu nakuja.” Thabit alitoka nje na kumuacha mke wa Sule amechanganyikiwa, kabla hajajua nini kinaendelea paka alitoka mdomoni kwa Sule na kusimama pembeni na kuzidi kumtia hofu mke wa Sule kwa kumuogopa yule paka aliyekuwa akijikuna kichwani kwa miguu ya nyuma. Akiwa bado anamshangaa yule paka, ghafla alibadilika na kuwa jini Nargis, kwa jicho la hasira lililokuwa likiwaka kama taa na uso ulioweka makunyanzi na kuonekana kama wa mzee. Hakuwa Nargis yule mwanamke mrembo mwenye urembo wa shani usiochosha kuutazama.
Alikuwa kiumbe mwingine kabisa ambaye kila dakika uso wake ulizidi kupoteza uhalisia wake. Mke wa Sule aliingiwa na hofu na kujikuta akitetemeka kama kamwagiwa maji yaliyotoka kwenye maporomoko ya barafu. Meno yaligongana, akawa anajiuliza atamueleza nini Nargis amuelewe. Alitamani kumlamba miguu ili amsamehe lakini bado ilikuwa ngumu kwani alikuwa amemuonya kwa mara mbili na yeye kuonesha ukaidi. Kwa sauti kali kama ya radi iliyoingia masikioni mwake na kusababisha ngoma moja ya sikio kupasuka na kutoa damu alisema; “Ushaniona mimi ni mwanadamu mwenzako siyo wa kuchezewa?” “Ha..ha..hapana..nisamehe,” mke wa Sule aliomba msamaha. “Nyamazaaaa pumbavu mkubwa mshenzi usiyestahili huruma hata kidogo, adhabu yangu ni ile ile kukugeuza nguruwe.” “Nisamehe sirudii tena,” mke wa Sule alizidi kumuomba msamaha Nargis. “Sitakusamehe kamwe kwa ubongo wako uliojaa kiburi.” “Sikuwa na jinsi kwani kama ningekaa kimya mume wangu angeniacha nilijitahidi kumficha lakini sikuwa na jinsi.” “Kwa kuwa kiburi ndiyo sehemu yako ya maisha, nitaanza na mumeo na mtoto kuwageuza nguruwe na ukiendelea na wewe nitakugeuza nguruwe.”
Baada ya kusema hayo alinyoosha kidole kwa Sule na mwanae ambao muda ule ule waligeuka na kuwa nguruwe. Baada ya kuwageuza nguruwe alitoa onyo lingine. “Hili ni onyo la mwisho kama husikii nitajua nikufanye nini.” Baada ya kusema hivyo alifyonya na kutoka nje katika umbile lile lile la mwanadamu. Mke wa Sule hakuamini, mumewe alikuwa chini akiwa amelala katika umbile la nguruwe na mwanae alikuwa kitandani katika umbile la nguruwe. Alimkumbatia mumewe ambaye muda ule alikuwa nguruwe kamili na kuangua kilio kilichomfanya Thabit arudi tena ndani. Alipofika alishangaa kumuona mke wa Sule akiwa amemkumbatia mumewe huku akilia.
“Shemu kulikoni leo?” “Mume wangu kageuzwa nguruwe.” “Nguruwe?” “Ndio shemeji ona hata mwanangu hapo kitandani amekuwa nguruwe.” “Shemu akili zako kweli zipo timamu?” ”Ndiyo shemeji.” “Mbona nguruwe mwenyewe simuoni?”
Kauli ile ilimfanya mke wa Sule kushtuka na kujishangaa kujikuta amemkumbatia mumewe katika umbile la kibinadamu pia mtoto wake kitandani alikuwa katika umbile la kibinadamu. Alijikuta akijishangaa na kumshangaa mumewe aliyeonekana kuchoka, hata aliponyanyuka chini hakuzungumza neno lolote zaidi ya kupanda kitandani na kujilaza. Muda wote Thabit alikuwa amepigwa na butwaa asimuelewe mke wa Sule kuonekana kama mtu anayeugua ugonjwa wa Maralia. “Shemu upo sawa?” “Nipo sawa, mke mwenzangu yupo?” “Yupo.”
“Ooh, basi.” “Ulikuwa unasemaje?” “Aaah, basi tu.” Thabit alitoka na kumuacha mke wa Sule akiwa njia panda na kushindwa kuamini kilichotokea. Aliamini kabisa yote yaliyotokea si kweli bali ni vinii macho. Alipanga kupambana na Jini Nargis bila kuogopa vitisho vyake vya viini macho.
Siku ya pili mke wa Sule hakuamini alidamka alfajiri kuwahi bagamoyo kwa mzee Kigobile, akiwa kituo cha basi cha Buguruni sheli akisubiri daladala ya Mwenge mtu wa pembeni yake alimsalimia. “Za asubuhi dada.” “Kabla ya kujibu aligeuza shingo amuone anayemsalimia ni nani, moyo wake ulipasuka baada ya kumuona ni Nargis. Midomo ilikuwa mizito kujibu na kujikuta akijisaidia haja ndogo bila kujitambua kwa woga. “Dada mbona unanishangaa hivyo au hukupenda nikusalimie?” “Ha..ha..hapana,” alijibu kwa kubabaika. “Mbona unaonekana una wasiwasi?” “Aah, nipo sawa.” Ajabu macho yake aliizoea ile sura iliyokuwa mbele yake kumbe haikuwa ya Nargis bali mwanamke mwingine ambaye hakuwa akifanana hata kidogo na Nargis. Alimshangaa yule dada ambaye naye alimuuliza baada ya kumuona mwenzake kama kachanganyikiwa kwa salamu yake. “Kwani dada salamu yangu imekushtua sana?” “Aah, tuacheni tu.” “Mmh, unakwenda wapi?” “Mwenge.” “Ooh, kumbe tupo pamoja basi.” “Hakuna shinda.” “Una mgonjwa?” “Hata, kwa nini mbona unaniuliza hivyo?” “Uso wako unaonesha kuna kitu kimejificha moyoni mwako.” “Kweli, mama yangu kalazwa Lugaro” “Kumbe tuko sote, nami nina mgonjwa huko.” “Ooh, pole basi tupo pamoja.” “Mwenzangu unaitwa nani maana nimetokea kukuzoea haraka?” “Naitwa Mariamu, na wewe?” ”Nargis.” “Eeh?” Mke wa Sule alishtuka baada ya kusikia jina la mbaya wake. “Kwani vipi?” “Umesema unaitwa nani?” “Nasra.” “Umesema Nargis au Nasra?” “Mariamu unaonekana una mawazo mengi kiasi cha kushindwa kunisikiliza vizuri, naitwa Nasra.” “Nikusikilize vizuri vipi wakati wewe mwenyewe umenitajia jina la Nargis.” “Mariamu kwa ushauri wangu kama kuna mtu mwingine wa kwenda hospitali bora ungerudi nyumbani kupumzika. Maana akili yako leo haiko sawa.” “Walaa, ipo sawa kabisa.” Mke wa Sule alijikuta akiingia wasiwasi wa yule mwanamke aliyekuwa akizungumza naye huenda ni Jini Nargis ambaye alimfuatilia ili ajue anakwenda wapi alfajiri ile. Wakati huo daladala iliyokuwa na watu wachache ilisimama kituoni, yule mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Nasra alikimbilia ndani ya gari na kuwahi siti mbili moja yake na nyingine ya mke wa Sule. Lakini mke wa Sule miguu ilikuwa mizito kuingia kwenye gari lile. Yule mwanamke aliyewahi kwenye gari alimwita ili akae kwenye siti iliyomshikia. “Shoga mbona umeganda kama sanamu, njoo nimekushikia siti.” ITAENDELEA
Wakati huo daladala iliyokuwa na watu wachache ilisimama kituoni, yule mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Nasra alikimbilia ndani ya gari na kuwahi siti mbili moja yake na nyingine ya mke wa Sule. Lakini mke wa Sule miguu ilikuwa mizito kuingia kwenye gari lile. Yule mwanamke aliyewahi kwenye gari alimwita ili akae kwenye siti iliyomshikia. “Shoga mbona umeganda kama sanamu, njoo nimekushikia siti.” “Tangulia shoga kuna mtu namsubiri.”Daladala ile iliondoka na kumuacha mke wa Sule kituoni, baada ya kuondoka alijikuta akijawa na mawazo juu ya yule mwanamke ambaye amekuwa akigeuka kila dakika mara Nargis mara mwanamke mwingine mara jina la Nargis mara Nasra.Japo magari yaliongezeka wazo la kwenda tena Bagamoyo alilifuta kwa siku ile, aliamua kurudi nyumbani kufanya shughuli zingine. Alirudi nyumbani taratibu hadi karibia na kwao, alipofika alishangaa kuwaona Thabit na Nargis wakitoka kuoga.Kwa vile aliwaona yeye kabla hawajamuona, aligeuza kwa kuamini yule mwanamke hakuwa Nargis bali wasi wasi wake. Lakini hakufanya kosa kwa vile asingeweza kuongozana naye Lugaro hospital sehemu ambayo haikuwa kusudio lake.Kwa haraka aligeuka na kurudi kituoni ili awahi safari yake ya Bagamoyo kwa mganga Kigobile. Alipofika kituoni kwa haraka alipanda daladala lililokuwa limejaa na kusimama hadi Mwenge. Alipofika Mwenge aliingia kwenye daladala ya kuelekea Bagamoyo.Alitulia kitini kwa vile siti zilikuwa zimebakia chache gari haikuchelewa, baada ya kuenea abiria kwenye siti iliondoka kituo cha Mwenge na kuelekea Bagamoyo. Moyoni mke wa Sule alimuomba Mungu amfikishe salama na mganga amkute. Safari iliendelea huku akiwa amejituliza kwenye siti yake, gari lilivuka Tegeta huku likishusha abiria wa safari fupi na kupandisha waliokuwa wakienda Bagamoyo. Gari lilipofika Bunju mke wa Sule alishtuka kumuona mtu kama Nargis akitelemka katika gari alilokuwa amepanda na kushangaa mbona hakumuona muda wote mpaka wakati wa kushuka.Bado aliamini ni moyo wa wasi wasi wa kumuhofia Nargis, gari nalo liliendelea na safari yake kwa kushusha na kupandisha watu njiani. Alishangaa wote walitozwa nauri lakini yeye hakuguswa. Alijiuliza ina maana konda amemsahau au vipi.Gari lilisimama kituoni Bagamoyo, watu walitelemka, kwa vile alikuwa amekaa nyuma alikuwa wa mwisho kutelemka. Hakutaka kuondoka bila kulipa alifungua pochi yake alipe nauli.“Umeisha lipiwa dada yangu,” konda alimweleza mke wa Sule.“Na nani?” “Na dada mmoja mrembo mwenye asili ya Kisomali.”“Mmh, dada mmoja alinijuaje?”“Mimi nitajuaje aliniambia na dada huyo hapo nyuma alikuonesha wewe.”“Mungu wangu, dada huyo alipandia wapi?”“Mlikuwa ameongozana kwa wewe kuwahi kuingia na kukaa siti ya nyuma na yeye alikaa ya mbele nyuma ya dereva.”“Mmh, alitelemkia wapi?”“Kwani vipi nakuona umejaa wasiwasi.”“Kaka yangu huu si muda wa maswali zaidi ya kusubiri jibu.” “Dada yule aliteremkia Bunju”“Mungu wangu nimekwisha,” mke wa Sule alisema huku akishika kichwa. “Kwani vipi, mbona sikuelewi.”“Kaka yangu weee tuyaache.”“Kwani kuna ubaya dada yule alipokulipia?”“Hakuna tatizo, alitaja jina lake?”“Sikumuuliza jina lake kwa vile alikuwa na shida naye, ila alikuwa na mkufu mmoja wa Dhahabu wenye kidani kilichoandikwa jina la Nargis.”“Eti nani?” Mke wa Sule alishtuka kusikia jina lile.“Nargis” “Mungu wangu nimekwisha amenifuata mpaka huku.”“Kwani yule dada ana ubaya gani mbona anaonekana mstaarabu kama angekuwa adui yako asingekulipia.”“Mmh, makubwa.”“Kwani vipi dada?”Konda wa daladala alizidi kumshangaa.Mke wa Sule aliona anapoteza muda kwani hata kama angemueleza yule konda asinge msaidia chochote. “Hayana muhimu sana kuyajua,” alisema huku akiondoka kuelekea maeneo ya mganga ambayo yalikuwa nyuma ya uwanja mkongwe wa mpira pale Bagamoyo wa Mwana Kalenge. Alitembea mwendo mdogo mdogo kuelekea kwa mganga huku moyo wake ukiwa mzito kwa kuamini huenda kila kona aliyopita lazima Nargis atakuwa yupo pembeni yake.Baada ya mwendo mfupi mke wa Sule alisimama ili aamue moja kurudi au aendelee na safari yake. Wazo moja lilikuwa arudi Dar japo ameisha fika Bagamoyo, lakini moyo mwingine ulimueleza aende kwa mganga huenda maeneo yale akaogopa kujitokeza. Aliamua bora aende kwa mganga kwani aliamini Nargis alikuwa akimhofia na ndiyo maana alikuta akimtolea vitisho.Alikwenda hadi kwa mganga bila kizuizi chochote na kuingia ndani ya uzio wa nyumba ya mganga, kulikuwa na watu wachache kama kumi. Naye alijisogeza kwenye foleni ya watu baada ya kusalimilia alikaa pembeni na kusubiri zamu yake.Ajabu ilipita zaidi ya saa nzima bila mtu aliyeingia ndani kutoka, ilibidi watu waanze kuzungumza juu ya mgonjwa huyo kuchelewa kutoka kwani alichukua muda mrefu. Baada ya muda pazia ilifunguliwa na mgonjwa aliyeingia kuonana na mganga alitoka. Mke wa Sule hakuamini alichokiona mbele yake, mgonjwa aliyetoka ndani kwa mganga alikuwa Nargis, hakukubaliana na macho yake aliyapikicha ili kuondoa wazo la kufikirika. Kabla hajapata ufahamu wa kitu alichokiona Nargis alimsamilia.“Ha! Mpenzi na wewe huku unafika?”Mke wa Sule mdomo ulikuwa mzito kwa kuamini bado kile alichokiona ni kiini macho. “Basi mimi natangulia tutakutana nyumbani.”Baada ya kusema vile bila kusubiri majibu ya mke wa Sule, Nargis aliondoka.Wakati huo wagonjwa wengine waliendelea kuingia. Japo alikuwa akisogea aliamini siri yake yote ipo nje hata akienda kwa mganga huenda alichokidhamiria kisitimia.Lakini alipiga moyo konde na kujisemea: “Liwalo na liwe.”Ilipofika zamu yake aliingia kwa mganga huku akiwa na mawazo lukuki kichwani juu ya kumueleza mganga kilichompeleka, akikiri adanganye na kuacha kukisema kilichompeleka huko Bagamoyo.Aliingia ndani kwa mganga na kukaribishwa kwenye mkeka.“Karibu mama yangu,” mzee Kigobile alimkaribisha.“Asante babu.”“Karibu uketi mjukuu wangu.” Mke wa Sule aliketi kwenye mkeka na kutulia kumsikiliza mzee Kigobile aliyekuwa akiweka vizuri dawa zake zilizokuwa zimedondoka chini kwenye kapu dogo lililokuwa pembeni yake. “MH! Mjukuu wangu una shida gani?” alimuuliza bila kumtazama.“Babu mimi naitwa Mariamu Musa natokea Dar maeneo ya Buguruni…,” alitulia kidogo na kuendelea kusema.“Babu nina tatizo moja linanisumbua.”“Tatizo gani hilo?”“Mh!” Alijikuta akishindwa aanzie wapi hasa baada ya kumuona Nargis akitoka ndani, alishindwa kuelewa kule kwa mganga alifuata nini. “Vipi mama mbona upo mbali una tatizo gani?” Mzee Kigobile alimshtua katikati ya dimbwi la mawazo.“Eti mzee yule mwanamke alikuja kufanya nini?”“Mwanamke gani? Sina tabia ya kutoa siri za wateja wangu kwa vile kila mtu anayekuja hapa ana matatizo yake ambayo ni siri yake.”“Mh! Basi wacha tu nirudi nina imani huwezi kunisaidia.”“Mbona sikuelewi, huyo mwanamke unayemsema anahusiana vipi na matatizo yako?” “Ndiye aliyenifanya nifunge safari kuja huku.”“Mh! Una matatizo naye?”“Tena makubwa.”“Mwanamke gani huyo?”“Kuna mwanamke mrembo shombe wa Kiarabu.”“Shombe wa Kiarabu?” Mganga alionesha kushtuka.“Ndiyo tena alichelewa sana kutoka.” “Si kweli leo sijahudumia mteja kama huyo.”“Babu una siri gani na huyo mwanamke au babu siku hizi huwezi kutusaidia sisi wateja tusio na uwezo?””Binti mbona sikuelewi, akili yako ipo sawa?” Kauli ile ilimshtua mke wa Sule na kuamini huenda alichokizungumza sicho. Alikumbuka hata Msamvu Morogoro alipofika kwa miguu watu walimuuliza swali hilo hilo. Alituliza akili yake akiamini huenda hofu ndiyo iliyomtawala kufikia hatua ya kuchanganyikiwa na kufikia hatua ambapo kila apitaye mbele yake alimfananisha na Nargis.Baada ya kutulia kwa muda aliamini kabisa yote yanayomtokea ni viinimacho, lakini alikumbuka Morogoro alipotokea na haikuwa kiini macho bali wa ukweli. Hapo alizidi kuwa njiapanda, lakini aliamini akifika kwa mganga ambaye anafahamika kuwa kiboko ya majini basi atakuwa salama zaidi.Alijikuta akiamua kusema ukweli huku akirudia kauli yake ya awali ya liwalo na liwe. Alijitengeneza vizuri na kuanza kumweleza kilichompeleka pale.“Babu,” alianza kwa sauti ya chini kumwita mganga.“Rabeka.”“Nina tatizo.”“Tatizo gani?”“Kuna kitu kinanisumbua na kutishia uhai wangu.”“Kitu gani hicho mama?”“Kuna jini linanisumbua.”“Jini?” “Ee..ee.ee..ha.ha.a.pana,” mke wa Sule alipatwa na kigugumizi cha ghafla baada ya kumuona aliyekuwa akizungumza naye si mzee Kigobile bali jini Nargis. “Eeh, unasema nani anakusumbua?”Mke wa Sule alituliza macho yake kuhakikisha kama alichokuwa anakiona mbele yake kilikuwa au kilikuwa kiinimacho.Aliyekuwa mbele yake hakuwa mganga Kigobile bali Nargis aliyekuwa amevaa kama mganga na kujifunga rubega na kiremba chekundu. Mwili wake alionekana wazi uliokuwa mweupe usio na doa. Mke wa Sule alifikicha macho tena asiamini aliyekuwa mbele yake ni Nargis kweli au amechanganyikiwa. Aliamini kama kweli ni Nargis basi adhabu yake ni kubwa ambazo alishindwa kuifananisha na kitu chochote.“Vipi mbona umepigwa na mshangao wa ghafla?” Sauti ya mganga Kigobile ilimshtua mke wa Sule ambaye alikuwa kama mtu aliyerukwa na ufahamu. Alipoangalia vizuri bado alibakia njia panda asipate jibu la kile alichokiona mbele yake, kilikuwa kweli au ni mauzauza ya dunia. Aliyekuwa mbele yake alikuwa mganga Kigobile na si Nargis. “Binti mbona sikuelewi tulikuwa tunzazungumza vizuri mbona umebadirika ghafla?”“Aaa..aa..babu,” mke wa sule alipatwa na kigagaziko.“Una tatizo gani?” Kabla ya kujibu alijiangalia kwa kujikagua kama ni yeye au mwingine, alipepesa macho kukiangalia chumba cha mganga ambacho hakikubadilika chochote na aliyekuwa mbele yake ni mzee Kigobile. Alivuta pumzi ndefu na kuzishusha alijipa moyo na kujisema kwa sauti ya ndani kuwa liwalo na liwe hata mbele ya sura yake asimame nani atasema shida yake.“Mmhu, binti mbona unaonekana haupo sawa?” “Ni kweli babu kuna mwanaharamu mmoja anataka kunichezea akili yangu, nahitaji msaada wako.”“Msaada upi maana nilipokuuliza ulichokisema ulishtuka na kukuona ukinishangaa kama nimegeuka simba.”“Ni hivi babu nyumba ninayo ishi kuna mpangaji mwenzangu tuna wasiwasi mpenzi aliyenae ni Jini.” “Kwa nini unasema hivyo?””Toka ameanza mahusiano kumekuwa na mambo ya miujiza ambayo si ya kibinadamu,” mke wa Sule alielezea yote aliyokutananayo toka alipoanza kumfuatilia Nargis na onyo alilopewa.” Mzee Kigobile baada ya maelezo yale alitoa simbi kwenye kikopo na kuzitazama kisha alizitupa juu ya msala wake. Aliziangalia kwa kuma huku akisoma moja baada ya nyingine kisha alinyanyua uso wake na kusema.“Binti.”“Abee babu.” “Ni kweli kabisa huyo mwanamke ni Jini, tena jini hilo lipo chini ya miamba bahari, lakini jini huyu ni mwenye huruma sana tofauti na majini mengine ni jini asiyependa kuua. Jini huyu anaitwa Nargis ambaye ana dada yake aitwae Hailati.Jini huyu alitokea kumpenda Thabit na kumlinda na kifo siku ambayo Thabit aliona miujiza pale kituo cha basi cha Mwenge. Aliweza kumshawishi Thabit na kukubali kwenda chini ya bahati kulala bila kujijua. Hata Thabit alikuwa na wasiwasi na mpenzi wake ambaye aliogopa kujitambulisha kwa kuhofia familia yake kumuua Thabit. Jini Nargis alijikuta anaingia katika kazi ya kuua si kwa hiyari yake bali kwa shinikizo la dada yake. Kutokana na matatizo yaliyompata kutokana kutendwa na wanadamu basi wamekuwa maadui zao wakubwa. Nargis amekuwa akikutisha ili uache kumfuatilia lakini umekuwa mbishi, tena kichwa ngumu.”“Sasa mganga maelezo hayo hayanisaidii utanisaidia vipi?” “Nitakupa dawa za kufukiza na kuoga ili kumfanya asikufuate.”“Lakini shida yangu kubwa ni kummaliza kabisa.”“Kwa nini ummalize wakati yeye hakutaka kukumaliza.” “Siwezi kuishi kwa raha kama ataendelea kuwepo.”“Mmh, sawa nitakupa dawa hiyo ambayo inatakiwa ujasiri kaichimbie kwenye mlango wa Thabit akiiruka na mchezo unaishia palepale.” “Ndiyo ninayoitaka.”Mzee Kigobile alimpa mke wa Sule dawa ambayo alielezwa aifanye pindi afikapo nyumbani kwa kuanza kuichoma na kufukuza vitu vibaya majini na wachawi. Baada ya kulipa pesa aliaga na kuondoka, akiwa na furaha moyoni kwani aliamini amepata dawa ya kumkomesha adui yake. Alipofika kituoni alipanda daladala ambayo ilikuwa imebakiza siti chache, alibahatika kupata siti ya mbele alikaa kwenye siti yake kusubiri gari liondoke kituoni. Baada ya daladala kujaa safari ya kurudi Dar iliwadia, alitulia kitini huku akiomba Mungu gari lifike salama ili akamuonesha Nargis kuwa yeye ni nani kama alimtembeza kwa miguu kwa siku tatu basi yeye atampoteza katika ramani ya dunia . Gari lilikwenda huku dereva akitembeza gari kwa kasi kutokana na barabara kuruhusu, mke wa Sule naye alikuwa akiimba taratibu nyimbo ya taarabu iliyokuwa ikiimbwa kwenye gari ile kwa kuifuatiliza. Gari liliondoka Bagamoyo na kuanza kuitafuta Bunju, dereva nae alizidi kukanyaga mafuta, gari lilopokuwa linateremsha mtelemko uliokuwa karibu ya daraja wote waliokuwa mbele walishangaa kuona mti mkubwa uliokuwa katikati ya barabara ambao ilikuwa vigumu kuukwepa na kasi ile. Dereva alijitahidi kwa uwezo wake wote kuukwepa ule mti mkubwa ulikuwa katikati ya barabara na gari kuhama njia na kuangukia chini ya daraja.
Abiria wote walipiga kelele za kuhofia maisha yaoGari liliangukia bondeni na kufanya watu wote wapate majeraha hata hivyo hakuna abiria aliyekufa, wasamaria wema walijitokeza kuwasaidia majeruhi hao. Mke wa Sule aliyekuwa amebanwa sehemu za kifua alibebwa na mtu mmoja aliyemuweka mbali na gari lililokuwa limepinduka.Dereva naye hakuamini baada ya gari kupinduka mti mkubwa aliouona awali hakuuona tena barabarani. Alipomuangalia mtu aliyekuwa akimsaidia mke wa Sule kwa kumnyoosha viungo vilivyokuwa vikimuuma, ghafla alihisi mapigo ya moyo nayanaenda kasi na kupata mshtuko uliosababisha apoteze fahamu. Baada ya kupata ufahamu alijikuta kwenye miamba ambayo hakujua kule ni wapi pia kulikuwa na harufu kali, alisikia kama mawimbi yakipiga kwa nje kuonesha ni karibu na bahari akiwa peke yake amelala juu ya mwamba wenye baridi. Alisimama na kujiuliza yupo maeneo gani na alifikaje huko, kwani alikumbuka kwa mara ya mwisho alikuwa katika majeruhi waliopata ajali ya gari baada ya dereva kuukwepa mti hewa na kulifanya gari kupinduka.Kilichomshtua ni harufu ya mafuta ambayo hupendwa kutumiwa na adui yake Nargis. “Mariamu mwanamke katili,” sauti aliyoizoea iliisikia.Hakujibu bali mapigo ya moyo yalimwenda mbio na kujua siku zake za kuishi duniani zilikuwa zimefika kikomo. Alipogeuka alikutana uso kwa uso na Nargis akiwa katika uso wa tabasamu tofauti na siku zote anapokasirika uso wake hugeuka kama wa mzee. Alihisi tumbo la kuhara likimshika kwa hofu, lakini Nargis aliendelea kutabasamu huku akipiga hatua taratibu kumsogelea.“Mariamu,” alisema huku akipiga makofi ya dharau, mke wa Sule alibakia kimya.“Mariamu nakuita sitaki kiburi, nimekusamehe sana huu ni wakati wa mimi kukuonesha ni nani, nina uwezo gani na nilichokuahidi nitakitimiza.”“Sa…sa…mahani Nargis,” mke wa Sule alipiga magoti mbele ya Nargis. “Niite Jini si Nargis.”“Ha…ha…pana wewe si Jini.”“Mariamu nimefanya kila hila uachane na nyendo zangu imeshindikana, kwa mdomo wako umedhamiria kuniangamiza. Mariamu nimekufanyia nini kibaya ambacho kimekufanya uwe adui yangu?Nimejitokeza kwa kila aina ili ujue kila ukifanyacho mimi nipo jirani yako, lakini inaonesha jinsi gani ulivyo na roho ngumu, Mariamu una masikio ya kenge husikii mpaka utoke damu na sasa muda wako umefika. Sina nia ya kukuua bali kukutesa japo wewe ulidhamiria kuniua, nimeipindua gari makusudi ili niweze kukupata baada ya kuipata dawa ambayo kweli ingeniangamiza. Baada ya kupinduka gari dawa zile zimepotea na kunipa nguvu za kukupata.Ni kweli wewe ni mwanamke jasiri ambaye hakika ulikuwa umefanikiwa kuniangamiza kwani baada ya kufika nyumbani nisingekuweza tena. Na kwa vile dawa ya mlangoni nisingeiona basi nilikuwa naangamia bila kujua.Mariamu hebu leo nielezee nilichokukosea mpaka kufikia hatua ya wewe kunitafuta usiku na mchana ili uniangamize?” Swali lile hakujibu alibakia kama bubu.“Mariamu usiniudhi nitakufanya kitu kibaya ambacho hujafanyiwa toka uzaliwe.” Uso wa Nargis ulibadilika na kuweka makunjanzi.“Kabla sijakujibu nieleze huku wapi na nimefikaje?” Mke wa Sule aliuliza kwa ujasiri huku moyoni akijisemea liwalo na liwe.“Huku ni chini ya mwamba bahari ambako huwafunga majini na wanadamu wenye kiburi, juu yetu kuna bahari kama unavyosikia mawimbi yake.” “Haya nieleze shida yako nini kwangu?”“Sina shida na wewe ila nataka nitimize ahadi niliyokuahidi, nitakugeuza nguruwe na kwenda kukutia kwenye banda la nguruwe la jirani yenu na mwisho wa wiki utakuwa mmoja wa nguruwe watakaochinjwa.”“Eti?” Mke wa sule alishtuka.“Eeh, nilitaka kukutesa kama nilivyokuahidi lakini kila nitakapo kuona moyo wangu utakosa amani, lakini nawe ukipotea katika sura ya dunia itamaliza malumbano yasiyo ya msingi.”“Usinitishe fanya lolote huna uwezo wa kuniua ila Mungu pekee.”“Napenda viumbe wenye kiburi kama wewe.” Baada ya kusema vile Nargis alimnyooshea kidole mke wa Sule na kumuamuru ageuke nguruwe.“Kuanzia sasa maisha yako yatakuwa katika umbile la nguruwe.”Baada ya kusema vile pale pale mke wa Sule aligeuka nguruwe, lakini mke wa Sule kwake hakuona mabadiliko yoyote zaidi ya kujiona yupo kawaida.“Mbona sijabadilika?” Aliuliza kwa kiburi.“Mh! Sogea pale kwenye jiwe linalong’aa kama kioo ujione.”Mke wa Sule aliona utani kwa kuamini Nargis alikuwa akimuogopa na kuamua kumtisha kila kukicha. Aliposogea kwenye jile lile lililokuwa kama kioo alishangaa kuona mbele ya jiwe lile kuna nguruwe. Hakuamini alijaribu kuchezesha mikono nguruwe aliyembele yake alifanya vile, aliinamisha kichwa vile vile nguruwe yule alifanya vile. Kila alichokifanya nguruwe yule alifanya na kumfanya aamini kabisa yule nguruwe ni yeye.Lakini bado hakuamini alijua ni kiini macho tu Nargis cha kuendelea kumtisha ili aachane naye. Akiwa bado anajiangalia asijimalize kama kweli yeye ndiye anayeonekana katika umbile la nguruwe Nargis alisogea karibu yake na kumsemesha.“Najua bado huamini ila mwisho wa wiki utaamini ukiwa mmoja wa nguruwe watakao chinjwa.”“Nargis usinitishe hiki ni kiini macho tu huwezi kunigeuza nguruwe wewe si Mungu,” Licha ya vituko vya Nargis, mke wa Sule hakutetereka. “Nitakuacha huku na usiku nitakufuata na kukupeleka kwenye banda la nguruwe wenzako.”Baada ya kusema vile Nargis aliondoka na kumuacha mke wa Sule chini ya miamba bahari. Hakumfunga kamba alimuacha huru na kumfanya mke wa Sule azunguke kila kona ya miamba ile bila mafanikio.Majira ya usiku Nargis alimchukua mke wa Sule aliyekuwa katika umbile la nguruwe na kwenda kumuweka katika banda la nguruwe kisha aliondoka na kumuacha mule. Kwa mara ya kwanza toka atoke tumboni kwa mama yake mke wa Sule alikumbana na adhabu kali. Ndani ya jumba lile kulikuwa na uchafu na harufu kali ambayo haivumiliki kwa mtu kukaa mule kwa muda mrefu, mwanzo alikuwa akijitahidi kuwakimbia wale nguruwe wasimsogelee kwani alijiamini kabisa yeye ni mwanadamu na wale ni nguruwe.Kwa kuwa alikuwa na muonekano wa nguruwe jike, nguruwe dume walimsumbua sana kumtaka kimapenzi kitu kilichomfanya akimbie bandani lakini hakuweza kutoka nje. Harufu kali ya nguruwe waliokuwa wakimsogelea kwa kuamini ni nguruwe mwenzao ilimkera sana.Siku hiyo alilala na njaa baada kushindwa kula uchafu waliokuwa wakila nguruwe, alitamani kufa kuliko mateso yale na kama Nargis angetokea mbele yake, angempigia magoti na kumuomba amuue au amsamehe. Njaa na kiu ilikuwa kali hakukuwa na maji zaidi ya maji ya tope ambayo nguruwe halisi waliokuwemo bandani walikuwa wakiogelea na kunywa. Alisogea pembeni ya banda na kuanza kulia kilio kilichokuwa kikitoa mlio wa nguruwe. Muda ulivyozidi kwenda ndivyo kiu na njaa kali vilivyokuwa vikimshika, alihisi kizunguzungu huku nguruwe watoto wakimsogelea kutafuta kunyonya. Aliwasukuma kwa miguu na kuwapiga vikumbo vilivyowafanya waanguke chini na kumuacha. Mke wa Sule alimuomba Mungu amuue kuliko adha ile ya kuteseka kukaa na viumbe ambavyo ni haramu na najisi hasa yeye akiwa muislamu. Kiu kilipokuwa kikali alijaribu kunywa maji yenye mchanganyiko na matope lakini alipofikisha pua yake maji yalimshinda kutokana na harufu kali yaliyokuwa yakinuka. Alijuta kumfuatilia Nargis kiumbe ambaye hakuwa na ubaya na yeye zaidi ya kumuonya asimfuatilie nyendo zake.Alijilaumu kwa kushindwa kuwa msikivu na matokeo yake kuishi kama nguruwe tena kwenye banda chafu lisilostahili mwanadamu kuishi. Alijiuliza ataishi vile mpaka lini na kukumbuka kauli ya Nargis ya yeye kuchinjwa mwishoni mwa wiki akichanganywa na nguruwe wengine. ITAENDELEA
Alijilaumu kwa kushindwa kuwa msikivu na matokeo yake kuishi kama nguruwe tena kwenye banda chafu lisilostahili mwanadamu kuishi. Alijiuliza ataishi vile mpaka lini na kukumbuka kauli ya Nargis ya yeye kuchinjwa mwishoni mwa wiki akichanganywa na nguruwe wengine. Kufika hapo alilia huku sauti yake ikiwa kero masikioni mwa watu kutokana na kusikika zaidi kutokana na hali ya hewa ya usiku kuwa imetulia. Ubaridi wa usiku nao uliendelea kumtesa kwa kumpiga bila huruma. Njaa na kiu baada ya kumshika sana na kumfanya aanze kuona kizunguzungu na kiza kinene. Miguu haikuwa na nguvu alijilaza kwenye tope huku baridi likizidi kumuingia mwilini. Kila dakika alimuomba Mungu amchukue kwani mateso yalikuwa makubwa sana maishani mwake. Sehemu chafu inanuka asiyostahili mwanadamu kuwepo, njaa kali na kiu hakuna chakula zaidi ya chakula kichafu cha nguruwe wale. Akiwa amejikatia tamaa alishtuka kujiona ametolewa nje ya banda akiwa katika umbile lake halisi la kibinadamu. Alishangaa na kujiuliza nani aliyemtoa na hali ile ni kweli au ni kiini macho, kabla hajapata jibu alimuona Nargis amesimama mbele yake. Mke wa Sule alichanganyikiwa na kuamini ile ni nafasi pekee ya kuomba msamaha, alipiga magoti mbele ya Nargis. “Nargis najua nimekosa naomba unisamehe.”“Mariamu sicho kilichonileta, nimekuletea chakula na maji kwa kujua huwezi kula chakula na maji yake ya nguruwe.” “Ni kweli Nargis nateseka mwenzio naomba unisamehe sirudii tena,” Mke wa Sule aliomba msamaha akiwa amepiga magoti huku akilia kilio cha majuto. “Mariamu kuwa muelewa, sikufuata ujinga wako bali nimekuletea chakula usife na njaa na utakuwa ukila mara moja kwa siku mpaka siku utakayochinjwa na nyama yako kuliwa na watu,” Nargis alisema kwa sauti isiyo na mzaha hata kidogo. “Nargis najua kiasi gani nimekukosea, nipo chini ya miguu yako sitarudia tena.”“Mariamu wewe si wa kusamehewa na ukizidi kuniudhi nitaongeza mateso ya kuutia madonda mwilini wako na kukufanya utolewe kwenye banda na kukufanya utangetange kwa kupigwa mawe kila atakapo kimbilia na kifo chato kitatokana na kipigo cha wanadamu.” “Usifanye hivyo Nargis, nakuahidi siwezi kurudia na nikirudia nifanye lolote.”“Kama uliweza kutaka kuniangamiza na dawa ulibeba pamoja na kukutisha kila kona bado dhamila yako ya kuniangamiza ilikuwa pale pale. Wewe ni kenge huwezi kusikia mpaka utoke damu masikioni.”“Basi niue kabisa kuliko kunitesa hivi.” “Sina uwezo huo ndio maana kifo chako kitakuwa cha kupigwa na kuzilai kisha utachinjwa.”“Na leo sikuachi mpaka uniue nifanye lolote sikuachi,” mke wa Sule alijitutumua.“Kabla hujanigusa nitakutengeneza kiumbe wa ambabu afadhari nguruwe, kwanza usinipotezee muda wangu kula chakula niondoke zangu.” Mke wa Sule kutokana na njaa aliyokuwa nayo hakuona umuhimu wa kubishana zaidi ya kukishambulia kile chakula kilichokuwa kitamu na maji matamu ambayo hakuwahi kula na kunywa maishani mwake. Baada ya chakula hakujua Nargis amepanga kumfanya nini, baada ya kula alimshukuru Nargis ambaye hakuihitahi shukurani ya kinafiki.“Sina haja ya shukurani zako mwanaume shetani usiye na huruma.”“Hapana Nargis ni mawazi mabaya ya kuamini majini ni viumbe vibaya lakini wewe umeonesha kumbe ni viumbe wapole na wenye huruma. Nimejifunza kupitia kwako nisamehe usinifanye kitu chochote kibaya mateso ya muda mfupi nimetamani kufa lakini sikuwa na uwezo huo. Chonde Nargis usinitese tena inatosha Nargis nateseka kumbuka mimi ni mwanadamu sifai kukaa na wanyama tena wachafu kama nguruwe.” “Nimekuleta huku na maana yangu, wewe si ulikuwa ukitafuta maji na mifupa ya nguruwe ili uniangamize nimeamua nikulete kabisa ukae nao ili uweze kuniteketeza vizuri”“Nisamehe Nargis ni shetani tu kanipitia nipo chini ya miguu yako.”
“Nafikiri umeshiba, rudi katika umbile lako la kinguruwe ili urudi kwa wenzako, naona unanipotezea muda sicho kilichonileta. Nimekusamehe husameheki, nimekutisha hutishiki, bado unaitaka roho yangu bado unaomba nikusamehe. Nargis baada ya kusema vile alinyooshea kidole mke wa Sule ambaye kabla hajasema kitu alibadilika na kuwa nguruwe na kurudishwa kwa nguruwe wenzake. Mke wa Sule alipojaribu kumuomba msamaha lakini alitoa mlio wa nguruwe, hakuwa na jinsi zaidi ya kunyamaza kimya. Sule alichanganyikiwa baada ya mkewe kutoonekana kwa siku tano, wasi wasi wake mkubwa ulikuwa kwa Nargis mpenzi wa Thabit lakini alishindwa kutibitisha kuwa Nargis ndiye chanzo cha matatizo ya mkewe kwa vile hakuwa na ushahidi japo aliamini hivyo.Na aliogopa kumuuliza Thabit kwa kuwa ataulizwa ilianzaanzaje mpaka kufikia hatua ile. Wazo la haraka lilikuwa kwenda kwa mtaalamu wa tiba za asili mwenye uwezo wa kushindana na majini ili kujua mkewe siku tano alikuwa wapi. Kama siku tatu alizopotea alikuwa Morogoro kwa kutembea kwa miguu baada ya kukutana na Nargis. Siku aliyopanga kwenda kwa mganga ilikuwa ndiyo siku baadhi ya nguruwe kuchinjwa kwenye banda alilomo mke wake. Mke wa Sule aliendelea kuteseka kuishi maisha magumu na nguruwe katika banda moja na kula mara moja kwa siku.Siku hiyo ilipofika aliingia mtu bandani na kuhesabu nguruwe wa kwenda kuchinjwa na mke wa Sule alikuwa katika idadi ile. Walipakiwa kwenye gari kupelekwa sehemu ya kuchinjia, mke wa Sule alitamani atoe sauti kuwa yeye si nguruwe lakini kila alipotoa sauti ilitoka ya nguruwe.Sule naye alidamka asubuhi kuwahi kwa mtaalamu ambaye hakuwa mbali alikuwa Mtoni kwa Azizi Ali. Kwa kuwa mganga huwa na watu wengi alipandia gari Buguruni-Chama. Ilikuwa ajabu ya Mungu alipotelemka alijikuta yupo Kisarawe mkoa wa Pwani, hakuamini kwani alipanda daladala iliyopigwa debe Buguruni Mtoni-Mtongani. Ilibidi apande daladala nyingine iliyokuwa ikirudi mjini.Baada ya kupanda daladala alitulia kitini akiwa haamini kama kweli alipanda gari la kuelekea Kisarawe na si Mtoni kwa Azizi Ali. Baada ya muda gari lilirudi mjini ili aelekee Buguruni kwa mganga kuulizia habari za mkewe. Gari lilirudi hadi Buguruni ambako Sule alipanda gari liendalo Mtoni kwa Azizi Ali. Gari lilipoanza kuondoka alipitiwa na usingizi mzito mpaka linafika mwisho wa safari Mtoni Mtongani alikuwa bado amelala. Kutokana na ugumu wa usafiri gari lilipofika abiria waliwahi kuingia na kukaa kwenye siti, hakuna aliyejua kama Sule alitoka na daladala ile Buguruni.Safari ilianza tena kuelekea Buguruni, Sule alishtuliwa na konda kumdai pesa.“Mzee acha kulala nipe nauli.”“Mara ngapi?”“Mzee sijadai nauli kwa mtu yoyote toka abiria waingie.”“Kaka si nimekupa mia tano ukanirudishia mia mbili na hamsini muda mfupi uliopita?”“Mzee wangu sijachukua hata senti ya mtu.”Mara konda alitoa shingo nje kuita abiria baada ya daladala kusimama Vetenari kwa kupaza sauti.“Buguruni mia mbili,” kauli ile ilimshtua Sule na kuhoji.“Konda tunatoka Buguruni au tunarudi Buguruni?”“Mzee tunatoka Mtoni tunakwenda Buguruni.” “Mungu wangu ina maana gari mpaka linafika na kurudi mimi nilikuwa nimepitiwa na usingizi?”“Kwani ulikuwa unakwenda wapi?” abiria mwenzake aliyekuwa pembeni yake alimuuliza.“Mtoni kwa Azizi Ali na nilipandia Buguruni, ajabu usingizi wa ajabu ulinipitia na kujikuta narudi nilipotoka.”“Ooh, pole unaweza kushukia hapa ili upande gari lingine.”Sule alitelemkia Vetenari kwa hasira ya kupotea na gari mara mbili aliamua kutembea kwa miguu kwani aliamini kwa njia ya mkato ya kupitia Mwembe Yanga hawezi kuchelewa. Alitembea kwa mwendo wa kasi kuokoa muda, lakini alijikuta akitembea mwendo mrefu bila kufika. Kitu kilichomfanya achoke sana, kingine kilichomshangaza mazingira aliyokutana nayo yalikuwa mageni kwake. Sule alitembea mpaka ikafikia hatua akawa haoni anapokwenda kiu ya maji ya kunywa na njaa kali vilimshika na kiza kilianza kuingia. Hakuamini kutoka Vetenari kwa miguu hadi Mtoni kwa Azizi Ali kunaweza kuchukua masaa kumi.Alitafuta mti wa mwembe uliokuwa mbele yake na kujipumzisha.Hayo yalikuwa kwa Sule, mkewe naye baada ya kuchanganywa katika kundi la nguruwe wa kuchinjwa, walifikishwa kwenye machinjio na kupangwa foleni kwa kuuawa mmoja mmoja. Mke wa Sule alikuwa wa tatu katika nguruwe kumi waliokuwa wakichinjwa siku ile.Alishuhudia nguruwe wa kwanza akitandikwa nyundo nzito kichwani na kupoteza fahamu kisha alichinjwa, wa pili ilikuwa vile vile alipokea kipigo kizito na kuchinjwa. Ikafuata zamu ya mke wa Sule ambaye haja ndogo na kubwa vilimtoka pamoja na kulia kilio huku akiomba msamaha kuwa yeye si nguruwe bali mwanadamu. Lakini kauli yake hakuna aliyeisikia zaidi ya kutoa mlio wa nguruwe.Alisogezwa kwenye sehemu ya shuruba kwa mtoa ufahamu wa nguruwe, aliinua nyundo nzito juu tayari kuishusha kwenye kichwa cha mke wa sule.Mke wa Sule alifumba macho kusubiri kipigo kile, lakini kabla nyundo haijashushwa mtu aliingia bila hodi na kusema.“Samahani ndugu usimuue huyo nguruwe.”“Kwa sababu gani?” mpiga nguruwe aliuliza.“Nilikuwa namtaka huyo nguruwe.”“Aah, bwana mbona wapo wengi kumbe ni hilo usinipotezee muda.”“Huyu ndiye niliyempenda, na nitamnunua kwa kiasi chochote nimempenda kwa kuwa ni jike, kwani mimi ninaye dume msumbufu nikimpelekea jike litapunguza usumbufu pia ninataka nguruwe wengi.”“Hakuna tatizo.” Mke wa Sule hakuamini kupona katika kifo kile japo aliamini yule atakayemchukua atampeleka katika banda lingine la nguruwe na kumfuga. Kibaya zaidi ni kupandwa na nguruwe dume ili azae watoto ambao yule bwana atatunza kwa ajili ya biashara.Mke wa Sule alisogezwa pembeni na kuchukuliwa nguruwe mwingine ambaye alimuona akichukua kipigo kimoja na kutulia. Moyoni alijisemea “Nilikuwa mimi nakutwa na yale, eeh Mungu niepushe na shari hii na nyingine tena.”Baada ya yule bwana kulipa pesa alitoka sehemu ya machinjio na nguruwe wake, alimpandisha kwenye gari na kuondoka naye.Wakati akiwa ndani ya gari usingizi mzito ulimpitia mke wa Sule, aliposhtuka alijikuta kwenye umbile la kibinadamu, sehemu iliyokuwa ngeni kwake, ghala harufu ya manukato ya Nargis ilisikika nyumba yake.Alipogeuka alimuona akiwa amesimama ameshika mikono yake kwa mbele kwa sauti ya upole alisema.“Mariamu.”“Abee.” “Nina imani baadhi ya viumbe hawajui thamani ya maisha yao na mmoja wapo ni wewe, nilikutoa kwa muda kwenye kifo kile cha kuchinjwa lakini baada ya mazungumzo haya ukinijibu vizuri toka chini ya moyo wako nitakusamehe na kukurudisha kwa mumeo ambaye kutwa nzima hajui anakwenda wapi. La utashindwa nitakurudisha kabla nguruwe wale hawajachinjwa na wewe uwe mmoja wapo. Mariamu kipi kinachokukera mimi kuwa na Thabit?” “Hakuna basi tu upumbavu.”“Upumbavu, roho mbaya?”“Roho mbaya.” “Shida yako nini kwangu?”“Nilikuwa na wasiwasi huenda wewe ni jini.”“Baada ya kujua mimi ni jini?” “Najua majini ni viumbe wabaya hivyo ungeweza kutudhuru.”“Kwa hiyo ukaamua kunidhuru mimi?”“Ni kweli nilitaka kufanya hivyo.” “Kwa hatua hiyo mwanadamu na majini yupi kiumbe mbaya?””Mwanadamu.”“Mbona mimi sijakudhuru?” “Nisamehe Nargis, sirudii tena kumbe ninyi ni viumbe wema sana sikujua.”“Sasa sikiliza hili ni onyo la mwisho, kama hutasikia nitajua cha kukufanya ila sitakuwa na simile wala kuuliza zaidi ya kutenda.” “Nimekuelewa dada yangu sirudii tena tamu ya ukaidi wangu nimeiona kama nisiposikiliza sitakuwa mwanadamu mwenye akili timamu.”“Yangu yameisha rudi nyumbani kwako.” “Asante Nargis” “Mariamu sihitaji asante zako za kinafiki zaidi ya kuyatekeleza yote niliyokwambia.”“Niamini Nargis huyu ni Mariamu mpya msikivu na nyenyekevu.”“Mmh, haya tutaona.” Baada ya kauli ile Nargis alipotena na kumuacha mke wa Sule akishangaa yupo wapi na atarudije nyumbani. Baada ya kutuliza akili alijishangaa kujiona yupo nyuma ya nyumba wanayoishi. Alizunguka na kutokea upande wa mbele, alishangaa kukuta mlango wa chumba chao umefungwa. Kwa vile alijua funguo wanapoweka alifungua mlango na kuingia ndani, kutokana na uchovu alipitiwa usingizi mzito.Sule naye alishtuka usingizini saa saba za usikukutokana na mvua kali ya upepo iliyokuwa ikinyesha, alichanganyikiwa asijue pale alipokuwa ni wapi na wapi akimbilie kutokana na kiza kinene na mvua kali. Yalikuwa mateso mazito kwa Sule ambayo hakuwahi kukumbana nayo katika maisha yake. Kingine kilichokuwa kikimchanya ni kilio cha mtoto mdogo mwenye sauti kama ya mtoto wake aliyeonesha naye ananyeshewa na mvua na kuomba msaada wa baba yake. Sule alijikuta akitapatapa kuifuata sauti ya mtoto yule ambayo hakujua inatokea wapi. Alijikuta akisahau mateso yake na kuanza kuifuatilia sauti ile kwa kuamini akifanya uzembe wowote mtoto wake anaweza kupoteza maisha kwa mvua ile kali iliyoambatana na upepo mkali. Sauti ya mtoto ulizidi kutanda katika ngoma za masikio ya Sule na kumfanya azidi kuifuata ili ajue mwisho wa sauti ile. Alizidi kuifuata ile sauti huku akimuomba Mungu amsaidie amuone mtoto wake akiwa hai. Katika kumbukumbu zake alikumbuka aliamka asubuhi kuwahi kwa mganga ili ajue sababu ya kupotea kwa mke wake. Lakini alijikuta akitokewa na mambo ya ajabu ya kupotea kila alipotaka kwenda kwa mganga kitu ambacho hakikuwahi kumtokea toka azaliwe. Sauti ya mtoto iliendelea kulia huku akiendelea kuifuata na mvua nayo ilizidi kumpiga huku baridi la usiku nalo likimuingia mpaka kwenye mifupa. Ajabu nyingine alijiona akitembea umbali mrefu mpaka aliposhtuka kulikuwa kumepambazuka nakujishangaa kujiona yupo karibia na nyumbani kwake miguu ikiwa amejaa tope kwa kutembea peku kwenye mvua. Ajabu alipofika nyumbani kwake sauti ile ya mtoto wake ilisikika ikitoka ndani kuashilia mwanae ndani analia. Alipofika aliingia ndani kwani mlango ulikuwa umefunguliwa, ndani alimkuta mtoto kitandani peke yake. Mara aliingia mkewe aliyetoka msalani. “Vipi tena mwenzetu mbona hivyo?” Mkewe alimuuliza baada ya kumuona mumewe alivyokuwa hoi nguo ilikuwa imebaki nusu shati suruali nayo kama alivamia msitu wa chui na kumnyambua chini miguu ilikuwa na tope kama alikuwa akilima jaruba. “Mmh, weee acha tu safari yako ya Morogoro leo ilinipata.”Kauli ili ilimshtua mke wa Sule na kuamini aliyefanya vile huenda ni Nargis ili asifike alipokuwa amedhamilia kwenda. “Mmh, kwani leo uliamka kwenda wapi?”“Si unajua mke wangu ulipotea katika mazingira ya kutatanisha, jana alfajiri niliamka ili niende kwa mtaalamu kujua huenda yule mt…” Kabla hajamalizia sentesi yake mkewe alimshika mkono mdomoni kumzuia aseseme na kusema.“Mume wangu komea hapo hapo.” “Kwa nini au una ajenda yako.”“Nakuomba unisikilize mimi nipo chini ya miguu yako, kuanzia leo tufanye kila linalotuhusu sisi wenyewe lisilotuhusu tuachane nalo.” “Mke wangu mbona sikuelewi hata la kupotea kwako pia hata hili na mimi kupotea siwezi kukaa kipya.”“Atiii,” Kopi zito lilitua kwenye shavu la Sule.“Wee mwanamke imeanza lini na leo iwe mara ya pili kunipiga.”“We ni kiumbe gani usiyesikia unajua mimi nilikuwa wapi, ungejua usingethubuti kunyanyua hata unyayo wako kunitafuta.” “Basi inawezekana unanidanganya una mwanaume.”“Mume wangu unaupungufu gani wa ufahamu muda mfupi unasema yapi yamekukuta, kama mbishi fuatilia nyayo za damu utarudi jina.” “Wewe ni mwanamke tu huwezi kunishauri upumbavu, lazima nijue sababu ya wewe kupotea na pili, itakuwaje mji niliozaliwa nipotee sikubali hata kidogo.” “Mume wangu ungejua maisha niliyokuwa naishi usingethubutu kusema hayo, chonde chonde mume wangu yote yaliyopita tuachane nayo.” Mke wa Sule alimpigia magoti mumewe kumuomba mumewe asitake vita na Nargis kwa kuamini kupotea kote kule ni kwa Nargis na hakutaka kumzuru zaidi ya kumtisha.
Lakini Sule bado alionekana mbishi na kutaka kujua mwisho wa yote lazima aende kwa mtaalamu kwa vile mateso aliyoyapata yalimtisha. “Mke wangu kwani tatizo nini?”“Ubishi ndiyo ulionifikisha hapa sina hamu ya kuvifuatilia visivyonihusu, naweza kusema sisi wanadamu ni wabishi pia tuna roho mbaya pengine kuliko viumbe vyote.”“Kwa nini unasema hivyo?”“Bila huruma ya yule niliyetaka kumtenda ningekuwa kiumbe wa ajabu na maisha niliyoishi kwa wiki nzima yasikie si ya kuomba uishi,” mke wa Sule alimsihi mumewe huku akitokwa na machozi.“Basi nielezee ilikuwaje ili nami nijue.” Kabla hajasema kitu alisikia sauti ya Nargis nje, hofu ilimtanda na kutoka nje ili kupata uhakika. Alipotoka nje alimuona Nargis akiwa amesimama nje ya mlango wa Thabit, kwa hofu alimsalimia.‘Za saizi dada?”“Mmh, nzuri tu shemu hajambo?””Hajambo, e.e..ti,” mke wa Sule alipatwa na kigugumizi alipotaka kuuliza kitu. “Ulikuwa unasemaje?”“Mume wangu analazimisha nimueleze nilipokuwa, nimweleze?”“Mweleze tu.”“Ni hayo tu dada.”Mke wa Sule alirudi ndani na kumueleza mume wake yote yaliyomtokea mpaka kufikia siku ile kuwepo pale.“Utani huo mke wangu.” “Kweli kabisa mume wangu, bila huruma yake sijui ningekuwa katika hali gani. Ila nakuomba siri hii usimwambie mtu yeyote zaidi yangu mimi na wewe, la sivyo atakacho tufanya Mungu anajua.”“Mh! Lakini kweli ulichokifanya kilikuwa hakikuhusu, bora tuachane naye pia hapa tuhame.”Wakiwa katikati ya mazungumzo mlango uligongwa, alimruhusu aingie. Alikuwa Thabit.“Ooh, best karibu.”“Asante.”“Shemeji yupo?”“Yupo ulikuwa na shida naye?”“Walaa, nilikuwa namuulizia tu.”“Jamani mi si mkaaji ila nimekuja kuwaaga leo ninahama.”“Una hama, unahamia wapi?”“Nitawajulisha kwa kuwa bado mpo wala msihofu nitawajulisha.”Thabit baada ya kusema hayo aligeuka na kuondoka akiwaacha mtu na mkewe wakitazamana. ****Nargis baada ya kumkomesha mke wa Sule na mumewe aliamua kurudi chini ya bahari na mpenzi wake Sule kupumzika kwani muda mwingi aliutumia kushindana na mke wa Sule. Hata wazazi wake hali ile waliiona ilikuwa ikijionesha katika uso wake uliochoka na kukata tamaa.“Vipi Nargis mbona upo hivyo tumekuruhusu uwe na mwanadamu mbona unaonekana huna raha?” Mama yake alimuuliza.“Hakuna kitu mama nipo sawa.”“Mh! Upo sawa kweli mwanangu?”“Nipo sawa mama.” “Mh! Sawa.”Mama Nargis hakuridhika na majibu ya mtoto wake alimtuma mtoto wake mkubwa wa kike ambaye ni shoga na mdogo wake Nargis ili kumchunguza mtoto wao ana tatizo gani. Hairat dada yake mkubwa Nargis alimfuata mdogo wake ambaye alionekana mtu mwenye mawazo kila alivyofikiria kiburi cha mke wa Sule kilimkosesha raha kwani hakuamini kama kweli vitisho vyote vile ataogopa. Alimkuta akiwa amezama kwenye dimbwi la mawazo juu ya kitimtimu cha wiki mbili cha kumdhibiti mke wa Sule hata kushindwa kulifaidi penzi lake kwa Thabit. Alipofika kutokana na mawazo hakuweza kumuona dada yake mpaka alipomshtua.Alishangaa kumuona mdogo wake akibubujikwa na machozi tena akiwa sehemu ya peke yake kitu kilichouumiza moyo wake.“Nargis mdogo wangu unalia nini?”Nargis alishtuka na kumtazama dada yake huku akijitahidi kufuta machozi yaliyokuwa yakitoka bila kizuizi.“Hapana dada kawaida.”“Nargis kawaida unalia, sijawahi kukuona ukilia haiwezekani wewe ni kipenzi changu tena ni kipenzi cha familia. Tumekuruhusu uolewe na mwanadamu ili kuupa furaha moyo wako lakini imekuwa kinyume.Nargis mdogo wangu najua Thabit kakutenda, hili nililijua mapema ndiyo maana nilikuonya na wazazi nao walikuonya lakini umekuwa kichwa ngumu, matokeo yake kuikosesha furaha nafsi yako.Nakuahidi kumkomesha Thabit kwa mkono wangu wewe najua si mama huruma, sasa niachie hiyo kazi na kwa vile umemleta mwenyewe humu ndani hatoki,” Hailat alisema kwa hasira baada ya kumuona mdogo wake akiteseka kwa ajili ya wanaume wa kibinadamu. ITAENDELEA
Nakuahidi kumkomesha Thabit kwa mkono wangu wewe najua si mama huruma, sasa niachie hiyo kazi na kwa vile umemleta mwenyewe humu ndani hatoki,” Hailat alisema kwa hasira baada ya kumuona mdogo wake akiteseka kwa ajili ya wanaume wa kibinadamu.
“Dada wala Thabit hausiki hata kidogo,” Nargis alimtetea Thabit. “Sasa ni nani ninavyo kufahamu hakuna kiumbe kitakacho kutoa chozi zaidi ya Thabit kwa kuwa mapenzi nayajua, vile vile mapenzi upofu. Ona mwili wako ulivyopungua kwa wiki mbili hebu niambie ukweli ili nikusaidie. Na sasa hivi mimi na wewe tunaingia vitani kuwaua wanaume wote hatuangalii ameoa au hajaoa kila atakayetua anga zetu tunaye.” “Dada Thabit ananipenda na siri hii nimemficha, niliogopa nikimueleza anaweza kuniacha.”
“Siri gani?” Nargis aliamua kumueleza dada yake jinsi mke wa Sule alivyomsumbua na kupania kumtoa dunia. “Mdogo wangu unaona jinsi wanadamu wasivyo na maana, sasa yeye lilikuwa linamuhusu nini heri angekuwa na uhusiano na Thabit. Lakini mdogo wangu njia ni ndogo kubali tummalize Thabit ili tujiepushe na wanadamu uishi maisha ya raha.”
“Dada Thabit ndiye uhai wangu, bila Thabit labda ningechukua uamuzi mzito, kanitamkia toka moyoni mwake ananipenda na hataki kunipoteza.” “Mh! Sawa, lakini kumbuka kuna vita kubwa kuliko hii ya mke wa Sule pale tu maisha ya Thabit yatakapoanza kuwa mazuri lazima familia yake itamtaka aoe.”
“Amesema atakataa.” “Na wakimlazimisha.” “Kila mwanamke atakayemuoa nitamuua.” “Hilo neno, haya ngoja nikamueleze mama yako.” Hailat alimuacha mdogo wake na kupeleka taarifa kwa mama yao mzazi sababu ya Nargis kuwa vile.
HAILAT alimfikishia taarifa mama yake ambaye baada ya kusikia alikaa kimya kwa muda kisha alisema kwa sauti ya upole.
“Hailat mdogo wako ana vita kubwa kuliko aliyopambana nayo, ya mtu mmoja imemtoa kamasi, ataweza ya familia na walimwengu waliomzunguka Thabit?”
“Hilo mama nalijua kwani maisha na tabia za wanadamu nazijua vizuri, mama kupenda kubaya hata mimi kuna wakati nilipinga maelezo yetu kuhusu tabia za wanadamu ambao humgeuka kiumbe mwenzake kama kinyonga.”
“Ni kweli Hailat kwa vile ndiyo ameanza kupenda na ugonjwa wa mapenzi ni mbaya kuliko ugonjwa wowote tuna kazi ya kumuelewesha.”
“Hilo nalijua, Nargis anampenda sana Thabit haoni hasikii kwa ajili ya Thabit.” “Wanadamu ni viumbe wabaya sana kuliko hata nyoka, hebu angalia mateso aliyopata mwanangu kwa ajili ya mtu asiyehusika naye bali tu kiherehere na kufikia hatua ya kutaka kumtoa roho.” “Mama unajua mwanao kaniudhi sana, siku hizi sitapi chakula changu kwa ajili ya kumuacha mdogo wangu afurahie maisha ya mapenzi na kufanya mauaji ya wanaume wenye wake kupungua.
Kitendo alichofanyiwa mama nitahakikisha sasa hivi sichagui yoyote nitakayekutana naye mbele yangu awe ameoa au hajaoa tena sasa hivi nguvu zote kwa wanawake wote nitampotezea mbali.”
“Lakini kabla hujachukua uamuzi huo lazima tukae naye chini tupange naye, naamini vita iliyopo mbele huenda ikatupata hadi sisi.” “Kwa kusema hivyo unafikiri tutafanya nini ili kujikinga na balaa linalotaka kuja mbele yetu?” Hailat alimuuliza mama yake.
“Dawa ni moja, kumuua Thabit.” “Etiii?” Hailat alishtushwa na kauli ya mama yake.
“Najua unashtuka lakini ukweli ndio huo la sivyo kuendelea kwa Nargis kuwa na Thabit kutatuweka katika hali mbaya pengine kupoteza kizazi chetu chote.” “Mamaaa,” Hailat alibakia mdomo wazi.
“Nataka nikuambie kitu, kwa tabia Thabit ni mpole tofauti na wanaume uliokutana nao wewe, tatizo waliomzunguka watataka kuzua chokochoko baada ya Nargis kumtengeneza kimaisha. Hapo itakuwa vita kubwa ambayo moyo unaniuma lazima tutampoteza Nargis na pengine na sisi wote.”
“Mmh, mama hizi habari mbona nzito, kumbuka kumpoteza Thabit huenda nasi tukaingia katika vita nzito na Nargis kwani hawezi kukubali kumpoteza Thabit alinihakikishia kwa mdomo wake bora apotee yeye na sio Thabit.”
“Sikiliza nataka tufanye siri moja ambayo Nargis asijue tujifanye tunampenda sana Thabit lakini akili kwenye kichwa. Siku moja nitakutuma ukamuue kwa mkono wako bila mdogo wako kujua.”
“Mama ni mpango mzuri lakini Nargis lazima atagundua na vita kuhamia ndani.” “Wewe ulikuwa na wazo gani?” “Tumwite Nargis tumuulize mipango yake na Thabit na baadae tumueleze madhara ya yeye kuwa na Thabit na hatima ya maisha yake kama atang’ang’ania kuwa naye.”
Walikubaliana kumwita Nargis ili wamueleze hatima ya maisha yake kama atakuwa na Thabit. Hailat alimfuata mdogo wake ambaye alikuwa chumbani kwake amekaa kitandani na Thabit alikuwa amepitiwa usingizi. Baada ya kufika kwenye sebule alikaa pembeni ya mama yake kusikiliza alichoitiwa.
“Nargis,” mama yake alimwita. “Abee mama.” “Kwa nini unakuwa msiri kwa mambo mazito?” “Mama nilijua nitayamaliza mwenyewe kama yangenishinda ningeomba msaada wenu.”
“Kwa nini ulikuwa unalia?” “Ni hasira mama, wanadamu ni viumbe wabaya sana.” “Si tulikuambia?”
“Ni kweli lakini nitapambana nao mpaka pumzi zangu za mwisho.” “Sasa raha ya mapenzi iko wapi, si heri ungeachana na Thabit ili ufurahie maisha.” “Mama sina raha ya maisha bila Thabit.”
“Mmh! sawa, lakini kumbuka vita inayokuja mbele ni kubwa kuliko uliyoimaliza.” “Hilo nalijua ila nitaondoa huruma hiyo ndiyo dawa ya viumbe wabishi.” “Nargis mwanangu una kazi ya kumzuia Thabit asioe baada ya kumtengenezea maisha.”
“Amenihakikishia haoi mwanamke mwingine zaidi yangu.” “Yeye anaweza kukataa lakini kiumbe chochote kilichokamilika lazima kitatakiwa kuoa ili familia yake ipate watoto wa kuongeza ukoo.”
“Siyo siri siku zote sikuona mwanaume anayewafaa, dawa yenyewe ulimfanyia mwanaume anakuganda kama ruba.” “Mmh sawa, sasa nani?”
“Utaanza wewe mkubwa ambaye umri unazidi kukimbia.” “Mmh, haya lini?” “Kesho.”
Walikubaliana kuanza kampeni ya kumteka Thabit kimapenzi. Nargis aliyekuwa amekaa sebuleni alihisi maumivu makali ya kichwa na kupiga kelele za maumivu zilizomshtua Thabit na kutaka kujua kulikoni.
Nargis aliendelea kupiga kelele huku akijipiga chini, Thabit alimuwahi mkewe na kumshika kabla hajajiumiza zaidi. “Vipi mke wangu? Mbona hivyo?”
“Walimwengu bado hawajachoka kunisakama.” “Kuna nini tena mke wangu au bado mke wa Sule anakufuata?” “Jirani…Jirani mume wangu,” Nargis alisema kwa sauti ya uchungu. “Jirani gani tena?”
“Mama Sakina na wanaye wanapanga kuniangamiza na kukuchukua wewe, sikubali nitaua mtu.” “Mke wangu usifanye hivyo, nitawadhibiti.” “Huwezi mume wangu, huwawezi wanadamu wana mbinu za hatari sana.” “Kama ni hivyo nitakwenda kuwaeleza kuwa sihitaji kuwa na mtu, nina mke wangu.”
“Hawawezi kukuelewa Thabit, ninyi wanadamu ni wabishi na mna roho mbaya sana, kosa langu nini mpaka kila mwanadamu kuitaka roho yangu. Ina maana wanaume wameisha mpaka wakung’ang’anie wewe…. Mmh nimeamini aliyosema mama sasa yanajidhihirisha. Nitajua chakufanya.” Nargis alinyanyuka kusimama wima kisha alishika mkono kwenye paji la uso kabla ya kutoweka alimwambia Thabit. “Samahani mpenzi, nakuja sasa hivi, nafika kwa mama.” Baada ya kusema vile alipotea na kwenda moja kwa moja chini ya bahari, alipofika mama yake alimshangaa kumuona kwenye hali ile.
“Vipi tena mwanangu?” ”Wanadamu mama.” “Wamefanya nini tena?”
“Wanapanga kuninyang’anya Thabit wangu.” “Hili mbona nililijua mapema? Wanadamu kazi yao kusubiri utengeneze kisha wachukue. Ni viumbe wanaopenda kutumia nguvu kuny’ang’anya.”
“Tena mama yao ndiyo kapanga kuwapeleka kwa mganga ili wamtengeneze mume wangu awapende wao na kuninyang’anya.” “Mmh, sasa unafikiri utafanya nini?” “Mama mimi sitakuwa na huruma nao nitawafutilia mbali.”
Mama yake alimwangalia kwa muda mwanaye kisha alimvuta karibu na kumnong’oneza kwa muda kisha alimuuliza mwanaye; “Kufanya hivi unaonaje?”
“Mmh, ngoja nijaribu, lakini..” “Hakuna cha lakini kama watataka kushindana tumia nguvu hizo kwa vile sasa hivi tupo karibu na wewe muda mwingi kuangalia maisha yako kwa vile tunajua vita na wanadamu ni nzito.”
“Sawa mama, acha nimuwahi mume wangu maana nimemuacha yupo katika sintofahamu.” “Haya muwahi mumeo ila dada yako akijua patachimbika.” “Basi mama usimwambie.” “Hakuna tatizo muwahi mumeo.” Nargis aliondoka huku akiwa na uso wa tabasamu tofauti na alivyokuja, alikuwa na siri aliyopewa na mama yake mzazi Malkia Zebeda. *** Siku ya pili mama Sakina aliwaamsha wanaye alfajiri ili kujiandaa kwenda kwa mganga kumfanyia dawa Thabit amuoe mmoja wa wale mabinti zake wawili. Binti mkubwa aliyeitwa Sakina alikuwa wa kwanza kuingia bafuni kuoga, bafuni kulikuwa na kioo kikubwa kilichoonesha mwili wa mtu kwa sehemu kubwa.
Sakina baada ya kuingia bafuni alianza kuoga huku akiutaza mwili wake kwenye kioo, kila dakika aliutazama mwili wake na kuamini anafaa kuwa mke wa Thabit kijana tajiri. Kila dakika alipokuwa akioga alijitazama kwenye kioo na kuusifia mwili wake.
Alipomaliza kuoga alisimama tena kwenye kioo na kujitazama huku akijifuta mwili, alipokuwa akijifuta alimuona Nargis kwenye kioo ikionesha yupo nyuma yake, alishtuka sana. Aligeuka kwa haraka ili amuone lakini ajabu hakuona kitu chochote nyuma yake.
Alikwenda hadi mlangoni na kuuangalia labda mlango upo wazi kuna mtu kaingia na kutoka. Lakini mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani, alipuuza kuiona ile taswira ya Nargis kwenye kioo. Baada ya kuridhika mlango umefungwa na hakuna mtu mwenye uwezo wa kuingia ndani, alirudi na kusimama tena mbele ya kioo kujiangalia.
Wakati akijifuta maji ili atoke baada ya kuitwa na mdogo wake aoge haraka ili nao waoge na kuwahi kwa mganga. Sakina alishtuka tena kuiona tena sura ya Nargis kwenye kioo, alitulia bila kugeuka na kumuona Nargis alikuwa na kitu kama unga mweusi aliokuwa ameshikilia kwa mikono miwili.
Wasiwasi ulianza kumuingia na kuamini nyuma yake hakukuwa na kitu cha ndotoni bali ni kweli kuna mwanamke tena mwanamke wa Thabit waliopanga kumtoa ndani ya nyumba. Hakukubaliana na ile hali baada ya kumuona yule mwanamke kwenye kioo akimsogelea.
Alipogeuka alikutana kweli na Nargis alipiga kelele za woga alizozisikia mama na mdogo wake. Lakini alikuwa amechelewa Nargis aliupuliza unga mweusi uliokuwa mkononi mwake ambao ulimpata Sakina mwilini. Dakika ile ile mwili wa Sakina ulianza kuota manyoya kama ya mbwa, Sakina alishtuka kuuona mwili wake umegeuka kama wa mnyama.
Wakati huo Nargis alikuwa amepotea, hakuamini kama kweli mwili wake umeota manyoya kama mbwa. Ili kuhakikisha, aligeuka kwenye kioo kuangalia kama kweli anachokiona ni kweli au ni njozi za mchana. Alipojiangalia kwenye kioo alijiona amegeuka mbwa mwenye umbile la kibinadamu.
Alishtuka na kupiga tena kelele ambazo kila mmoja tena alizisikia na wakati huo mama na mdogo wake walikimbilia bafuni kuangalia Sakina amepatwa na nini.
“Najua kiasi gani unavyoteseka kwa ajili yangu, yote ni mapenzi ya dhati. Nargis mimi nipo tayari kwenda kuishi na wewe chini ya bahari au popote upendapo ili kuona furaha ya moyo wako inakuwepo kila siku huku tabasamu lako mwanana likirudi usoni kwako kama zamani. Nakupenda Nargis sipendi uumie kwa ajili yangu,” Thabit alisema huku akimnyanyua Nargis alipopiga magoti. “Asante mpenzi.” Nargis alimkumbatia Thabit kwa furaha baada ya kukubali ombi lake, alijiuliza Thabit amekubali mama yake ataupokea vipi uamuzi wake wa kwenda kuishi na mumewe chini ya maji huku akipambana na familia ya Thabit. Baada ya kupigwa na mfagio na viatu Sakina aliamua kutoka nje ya nyumba huku akiwa na majonzi mazito kutokana na hali iliyomkuta, alijisogeza mpaka upenuni wa ukuta na kujikunyata akiwa aamini ile hali ya yeye kugeuka mbwa. Alijikuta akilia kwa uchungu kwa sauti ya juu ambao ilikuwa ya mbwa, sauti yake ilikuwa karaha masikioni mwa watu. Aliamua kulia kimya kimya kwa kuhofia kugeuka karaha kwa mama na mdogo wake waliomuona ni mbwa. Mama na mdogo wake baada ya kumtoa nje yule mbwa bila kufahamu ndiye Sakina, walianza kumtafuta Sakina kila kona, lakini bila mafanikio. Kila kona waliyofika walimwita lakini hawakusikia sauti yake na kuzidi kuchanganyikiwa Sakina atakuwa wapi. Sakina aliwasikia wakimwita na kumpita alipokuwa amejilaza na kuzunguka nyuma ya nyumba huku wakimwita kwa sauti ya juu. Japo aliwasikia lakini alishindwa kuitikia kwani alipoitikia alitoa sauti ya mbwa kitu ambacho kingefanya afukuzwe kabisa eneo la pale. “Sasa atakuwa wapi Mungu wangu,” mama Sakina aliuliza akiwa amejishika mkono mmoja kiunoni. “Mama hata mimi nashangaa.” “Sasa atakuwa amekwenda wapi?” “Mama haya ni maajabu dada Sakina alikuwa akioga muda si mrefu, lakini cha ajabu aonekani, kingine kilichonishtua ni kutoka mbwa bafuni.” “Ile sauti ya dada yako ilitokea wapi?” “Mama, wote si tumesikia akipigia kelele bafuni.” “Sasa atakuwa wapi?” “Hapo ndipo nazidi kuchanganyikiwa.” “Sasa tutafanyaje, na muda unazidi kukatika, nilitaka tuwahi kwa mganga kisha turudi kuendelea na mambo mengine,” “Hii kali haijawahi kutokea dada alikuwa bafuni haonekani mbwa ambaye hakujulikana kapitia wapi tumemkuta bafuni.” “Mimi nafikiri hakuna haja na kupoteza muda tufanye twende kwa mtaalam, kama Sakina alikuwa hataki kwenda siangesema kuliko kutukimbia.” “Mama una uhakika gani kama ametukimbia, kapitia wapi?” “Hii siri unaijua wewe na dada yako, kwanza sioni umuhimu wa kwenda kwa mganga kama mnanichezea akili.” “Mama kilichotokea hata mimi sielewi wala hakuna ujanja wowote.” Wakati wakibishana wingu zito lilitanda na kuteremka mvua nzito, Sakina alijibanza pembezoni mwa nyumba yao kujikinga na mvua ile. Lakini mvua ilikuwa kubwa ya mawe yenye upepo mkali. Sakina alijikuta akilowa lakini alishindwa kuingia ndani kwani aliamini bado wanamwona mbwa. Yalikuwa mateso ambayo kwake hakujua sababu ya yeye kufanywa vile, mvua iliendelea kumpiga pamoja na baridi kali viliendelea. Kila mungurumo alijikunja kwa hofu katika maisha yake aliogopa mlio wa radi ya mvua. ******* Baada ya mvua kukatika alipita mtu mmoja ambaye alikuwa mtaalam wa tiba za asili, macho yake yenye kuona mbali alipomwangalia Sakina mwanzo alimwona ni mbwa wa kawaida. Lakini tafsiri ya macho yake yalimuonesha yule si mbwa wa kawaida bali mwanadamu aliyegeuzwa mbwa. Alijiuliza nani aliyefanya vile, alitoa chumba yake ndogo yenye mavumba meupe na kuyanusa baada ya muda aliiona picha ya Sakina kugeuzwa mbwa ikijirudia. Baada ya kugundua hali ile alicheka mwenyewe kisha alijisongeza mpaka kwenye nyumba yao Sakina na kubisha hodi bila kumfanya lolote yule mbwa. Mdogo wake Sakina alifungua mlango na kumkaribisha ndani mgeni aliyekuwa mgeni machoni mwao. “Karibu.” “Asante,” mgeni aliitikia huku akiingia ndani. “Karibu mgeni,” mama Sakina alimkaribisha mgeni baada ya kuingia ndani. “Asante, najua mlikuwa na safari,” mgeni alisema baada ya kukaa kwenye kochi. “Umejuaje?” CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Na safari yenu mmeikatisha baada ya kupotea mtu mmoja.” “Jamani mbona makubwa umejuaje?” “Kibaya zaidi mmemkana mwenzenu na kumfukuzia nje bila huruma ambapo alinyeshewa na mvua yote.” “Baba mbona hatukuelewi,” mama Sakina alishindwa kumwelewa mgeni. “Ni vigumu kunielewa, kumbukeni safari yenu ndiyo iliyozua tafrani yote ya mwanao kugeuzwa mbwa.” “Mbwa, ina maana yule mbwa tuliyemkuta bafuni ndiye Sakina?” “Ndiye yeye.” “Mungu wangu, nini kilichomgeuzwa mbwa?” “Ji..ji….” Kabla hajaendelea upepo mkali ulivuma mule ndani na kusababisha vitu vyepesi kutupwa nje ya nyumba sauti ya mbwa ilikuwa juu ikionesha kuna kitu kinamtisha. Mtaalam alipotoka alishangaa kutomkuta yule mbwa. Wakati huo upepo mkali ulikuwa ukizidi kujaa ndani na kusababisha vumbi iliyofanya watu wasionane. Yule mgeni alinyoosha mkono na kuyasema maneno katika lugha ya kiarabu akiukemea, baada ya kunyoosha mkono upepo ulitulia, kilichowashtusha wote kilikuwa kumuona jini Nargis mbele yao akiwa ameshika mkono kiunoni kitu kilichowashtua wote waliokuwemo mule ndani.
Nargis, baada ya kupata upinzani mkubwa kutoka kwa mtaalamu yule, aliamini kabisa upinzani alioambiwa na mama na dada yake juu ya ubaya wa wanadamu, yalikuwa yakitimia. Baada ya kumchukua Sakina katika umbile la mbwa na kumficha kwenye pori lililotisha lenye majoka na wanyama wakali.
Sehemu aliyomficha walinzi wake walikuwa nyoka wakubwa waliokuwa wamemweka kati. Wakati huo alikuwa amemrudisha kwenye umbile la kibinadamu. Sakina akiwa katika umbile la kibinadamu, aliingiwa na hofu kutokana na nyoka wakubwa yaliyokuwa karibu yake lakini hakuna hata moja lililokuwa na habari naye.
Nargis wakati akimpeleka kwenye pori lile aliokota kamba ambazo alizitawanya na kisha kumfanyia Sakina kiini macho ambacho aliamini kabisa wale ni nyoka. Lakini kama angekuwa na ujasiri angezipita zile kamba na kukimbia bila kufanywa lolote japo asingefika mbali lazima angeangukia mikononi mwa Nargis.
Nargis baada ya kumuacha Sakina porini sehemu aliyoamini hakuna wa kumuona, aliondoka na kwenda kutafuta msaada kwa mama yake ambaye angesaidia kumpa ushauri kwani aliamini kwake ngoma ni nzito baada kuuona uwezo wa mtaalam ambaye alimtishia maisha.
Nargis alikwenda chini ya maji kuonana na mama yake Malkia Zebeda kumweleza masahibu yaliyomkabili kuhusiana na ndoa yake kwa wanadamu kuiandama kila kukicha. Mama yake alipomuona alijua mtoto wake ana jambo ambalo lilimnyima raha.
Kati ya vitu ambavyo malkia Zebeda vilivyo mkosesha raha ni pamoja na wanaye kuteswa na mapenzi ya wanadamu, ambao walikuwa wakiwapa mateso mazito kwa kulazimisha mahusiano nao. Ilikuwa ni vigumu kwa jini kukubali kuachana na mpenzi wake hasa anapoonja penzi la mwanadamu lenye joto ambalo huwachanganya majini.
Malkia Zebeda mara nyingi huwakanya watoto wake ambao huwa wabishi na mwisho wa siku hupatwa na majuto. Hailat dada yake Nargis naye alikuwa mbishi lakini mwisho wake aliwachukia wanadamu mpaka kuanzisha kampeni ya kula nyeti za wanaume waliooa ambao walimdanganya na siku ya mwisho aliambulia maumivu.
Alimuona Hailat ana afadhali kuliko mdogo wake ambaye aliamini kumficha mwanadamu chini ya maji ni vita kubwa. Aliwaogopa wanadamu ambao viumbe wenye hila mbaya ambayo inaweza kuupoteza ukoo mzima. Aliona tatizo la Nargis ni baya ambalo kwake alitafuta mbinu ya kukabiliana nalo.
Malkia Zebeda alituliza akimtazama mtoto wake ambaye uso wake ulionesha yupo katika kipindi kigumu maishani mwake. Toka alipoanzisha uhusiano na Thabit na kwenda kulala kwa bwana yule, amekuwa mtu mwenye matatizo aliyekosa raha kwa ajili ya kulilinda penzi lake kwa mumewe. Mama yake aliona matukio yote yaliyomtokea mtoto wake kwenye mboni za macho ya mwanaye.
Hakutaka kuyasema, aliyoyaona kwenye macho ya mwanaye, alimwuuliza kama hajui kitu ili apate ukweli wake.
“Mmh, tatizo gani tena?” “Mama nilikuwa na mawili japo moja wakati najiandaa kuleta ujumbe wangu lilitokea ghafla, nilipotaka kupambana nalo maji yalikuwa mazito.”
“Ni kweli yote yamejionesha kwenye macho yako nilitaka useme mwenyewe kwa mdomo wako.” “Mama utanisaidiaje?” “Mwanangu nilikueleza tokea mwanzo kuwa unachoking’ang’ania ni mauti yetu.” “Mama nahitaji msaada siyo malumbano.”
“Msaada wangu ni mmoja tu, kuokoa maisha yetu na ukoo wetu, ni wewe kuachana na Thabit.” “Mama suala la kuachana na Thabit, sahau, la muhimu ni kunieleza moja mtanisaidia kwenye vita hii au hamuwezi.”
“Kwa vile kisu kimegusa mfupa, hatuna jinsi kuingia vitani, uwezo wa huyo mganga ni mdogo sana. Tutaweza kummaliza bila kutusumbua, lakini wavumao baharini mwanangu si papa tu, mtihani unaokuja mbele ambao nauona ni hatari kwa maisha yatu.”
“Mama kama kufa kila kiumbe kitakufa na kila kiumbe hufa kwa ahadi kilichoumbwa nazo mbele ya Mungu, kuongopa kifo ni kijidanganya.”
“Mama kama kufa kila kiumbe kitakufa na kila kiumbe hufa kwa ahadi kilichoumbwa nazo mbele ya Mungu, kuongopa kifo ni kijidanganya.”
“Kwahi upo radhi tufe kwa ajili ya mapenzi yako.”
– “Mama waliokufa wote hawakufa kwa ajili ya mapenzi.” “Sawa nimekuelewa.”
Walikubaliana kumuongezea nguvu Nargis kupambana na mtaalam aliyepewa kazi ya kumrudisha Sakina katika umbile la ubinadamu. Taarifa ile ilimpa nguvu Nargis na kurudiwa na furaha, alimwaga mama yake na kurudi nchi kavu alipomuacha Sakina akilindwa na majoka makubwa ya kiini macho. Kabla ya kwenda kwa Sakina alirudi kwa mumewe Thabit.
Baada ya Nargis kuondoka, malkia Zebeda alifanya kikao cha siri na mwanaye mkubwa ili kumdhibiti Nargis asilete balaa chini ya bahari. Vita aliyoiona mbele yao ilikuwa kubwa sana ambayo lazima itawashinda na kuwasambaratisha. “Abee, mama vipi, nilikuona na mwanao yupo wapi?”
“Kaondoka.” “Hata bila kuniaga au kunisalimia?” ”Si wewe, amekuja hapa jicho limemtoka kama kakabwa shingo.”
“Nini tatizo?” “Si mtu wake wa amri ya Mungu.” “Imekuwaje tena?”
“Niliyomweleza sasa yanamtokea, leo kakutana na mtihani mdogo kachanganyikiwa. Nilikuwa nataka uifanye ile kazi mara moja.” “Ipi hiyo?” “Ya kummaliza Thabit.”
“Mamaaa!!” Hailat alishtuka kwa mara ya pili. “Siyo ombi bali amri bila hiyo maisha yetu yapo mashakani, kibaya zaidi anataka kumleta mumewe chini ya bahari.”
“Ili?” “Waishi huku.” “Mmh, sasa itakuwaje, akijua je?”
“Hawezi kujua kuna kazi yake moja utaifanya ya kummaliza mganga mmoja aliyetaka kushindana na sisi. Tukimaliza ile kazi lazima Nargis atatuamini na hiyo ndiyo nafasi ya kummaliza Thabit bila kujua.” “Mmh sawa, lakini akigundua!”
“Hawezi kugundua lolote.” Walikubalia kufanya mpango wa siri wa kumuua Thabit, kwa kuifanya kazi ya kwanza ya kummaliza mganga anayetaka kumrudisha Sakina katika umbile la kibinadamu toka umbile la mbwa.
“Kwa hiyo baba unatuambiaje?”Mama sakina aliuliza. “Kwa kweli nilivyouliza kuhusu ng’ombe mweupe asiye na doa wamenieleza kuwa mpaka wamtume mtu akamtafute bara. Sasa hatujui atapatikana lini na muda huo mtoto wenu ataendelea kuteseka na hatujui amepanga nini huenda anataka kumuua. Kwa sasa inaonesha kamficha kwenye pori moja bado hajampeleka chini ya bahari kwa kazi ya haraka tutafanikiwa kumrudisha. Tena tuna bahati moja kazi kubwa ni kumrudisha kwani kwa sasa hayupo katika umbile la mbwa.” “Sasa baba, si bado ataendelea kutufuata?” “Hiyo ni kazi ndogo nitawapeni dawa ambayo naamini itawasaidia sana hawezi kuwafuata tena.”
“Na kuhusu kumpata Thabit?” “Kwa vile tumekosa dawa za kumpatia jini ambazo zingembembeleza na kumrudisha Sakina kwa hiyari yake huku tukiliahidi kutomfuata tena. Hatuna jinsi lazima tutumie nguvu, kutokana na uwezo wangu wa kukabiliana na majini sina budi kuingia kazini. Siku zote kuna mambo mawili jema likishindikana basi tumia la shari, kwa hiyo kazi nitaifanyia nyumbani kwa vile hapa sina dawa nyingi, nitakachokifanya nitamrudisha Sakina na kumpa dawa ya kinga kesho nikija nitakuja kamili na dawa ya kummaliza kabisa huyo jini.”
Kauli ile ilimfanya Nargis aliyekuwa na Thabit chumbani kwao ahisi maumivu makali ya kichwa na kuanza kupiga kelele ambazo Thabit alikuwa ameisha zitambua. Nargis alijipiga ukutani mpaka akatoka damu kwa hasira, alishika mkono kwenye paji la uso na kutoweka. Ndani ya nyumba ya mama Sakina upepo mkali ulivuma kama wa mwanzo uliotupa vitu vyepesi nje ya nyumba. Mama Sakina na mwanae waliingia wasiwasi kwa kuamini jini Nargis amerudi.
Vumbi lilikuwa kubwa kwa uchafu wa nje kuingia ndani pamoja na majani yaliyokatika kutokana na hasira za Nargis. Nargis alijipigiza kwenye ukuta wa nyumba mpaka nyumba ikatikisika, yote yale yaliwafanya mama Sakina na mwanae wazidi kuwa na hofu. Mganga alinyoosha mkono kushindana na upepo uliokuwa mkali kwa muda mrefu tofauti na mwanzo. Haikuwa rahisi kuuzuia kitu kilichomshtua mganga na kuamini anakazi kubwa kupambana na jini yule mwenye hasira. Kwa haraka alitoa kichupa chake kidogo na kuvuta dawa ya unga ambayo ilimfanya atoe chafya mfululizo.
Ghafla naye macho yaligeuka rangi na kuwa mekundu huku mishipa ya kichwa ikimsimama hata sauti yake iligeuka na kuwa nzito. Mwili wake nao ulivimba kidogo kwenye mikono mishipa, ilimsimama naye alionekana kama kiumbe cha ajabu. Aliukemea ule upepo uliokuwa umejaza uchafu mwingi ndani toka nje ikiwemo miti makaratasi majani makopo nk. Mpaka upepo unatulia ndani ya nyumba kulikuwa kumegeuka kama dampo la muda mrefu. Mbele yao kulikuwa na Nargis aliyekuwa amesimama akivuja damu kichwani huku machozi yakimtoka.
Baada ya kumnywesha maji ya dawa Sakina alirudiwa na fahamu kwa kujishangaa kuwepo nyumbani. Hali aliyoiona ilimshtua na kuhoji mbona ndani kumejaa uchafu. Walimueleza hali ilivyokuwa, hakusema kitu kila alivyokumbuka alivyokuwa na sehemu aliyokwenda kuwekwa na Nargis alikokuwa analindwa na nyoka wakubwa wasio na mfano, machozi yalimtoka. Mganga baada ya zoezi lile zito aliwaaga na kuwaahidi kurudi kesho yake ambako angefanya zoezi la kinga na kummaliza jini Nargis na wao kumpata Thabit. Aliwaaga na kuwaacha na zoezi zito la kutoa uchafu uliokuwa umejaa ndani.
Nargis alipotoka nyumbani kwa mama Sakina alikwenda moja kwa moja porini alipomficha Sakina, lakini ajabu hakumkuta na aliporudi nyumbani kwao Sakina alimkuta akiwa na ndugu zake wakisomba uchafu kuutoa ndani. Alipojaribu kuisogelea ile nyumba moto mkubwa uliwaka na kumfanya asogee mbali. Kwa hasira alijipiga chini na kutoa kishindo kikubwa nilichowashtua wote. Walipoangalia sehemu iliyotokea kishindo kile, wote walishtuka kumuona Nargis akitoka kwenye vumbi.
Ajabu vumbi lilipotulia alitoweka katika mazingira ya kutatanisha, hali ile iliwatia hofu na kuwafanya wakimbilie ndani na uchafu uliobakia wasiutoe tena. Waliomba Mungu siku ya pili ifike upesi ili mganga arudi na kuifanya kazi aliyowaahidi.
NARGIS baada ya kumkosa Sakina porini alikomficha na kumkuta nyumbani kwao roho ilimuuma na kuamua kumfuatilia lakini alikutana na kizingiti kikubwa kuonesha wamejidhatiti kupambana naye. Aliamini kabisa ngoma ile ni nzito na maisha yake yapo hatarini. Wasiwasi wake mkubwa ulikuwa iwapo taarifa zile atazipeleka kwa mama yake lazima ataelezwa aachane na Thabit, kwake kuachana na Thabit ilikuwa sawa na kuondolewa moyo mwilini mwake. Lakini kwa mambo aliyoyaona kwa mtaalamu yule aliamini kabisa kwake ni maji mazito.
Hakuwa na jinsi zaidi ya kwenda kuomba msaada wa haraka kwa mama yake Malkia Zebeda, kama kawaida mama yake baada ya kufika aliyaona yote, kwenye mboni za macho yake hakukuwa na haja ya kujieleza. Alipofika tu mbele ya mama yake mama yake alimkata kauli.
“Unataka kusema nini, nimekueleza tokea mwanzo wanadamu ni viumbe wabaya sana hushikilia yasiyowahusu ili tu wawaharibie viumbe wengine, wao kwa wao hawapendani itakuwa sisi viumbe tusioonekana. Nimekueleza toka mwanzo kuwa tatizo kubwa ni mumeo lakini unaking’ang’ania kifo, lakini hatuna jinsi, tutahakikisha tunakulinda kwa nguvu zote.
Kuhusu yule mganga dada yako nimemtuma anakwenda kuifanya ile kazi, kama atashindwa basi nitaongeza nguvu mimi, lakini namuamini anaweza kumaliza kazi ile.” “Na wale wabaya wangu?” “Nao pia hawawezi kufanya lolote wasikutie hofu.”
“Mmh, sawa.” “Lakini kumbuka kuna vita nzito mbele yetu inakuja ambayo nina imani hatutaiweza.” “Mama tutapigana nayo mpaka tone la mwisho.”
“Kama unajua hivyo mbona umechemsha.” “Ndiyo maana nikaja kwenu.” “Hivi Nargis hakuna wanaume wa kijijini walio wazuri?” “Wapo.” “Sasa kwa nini unamng’ang’ania mwanadamu ana uzuri gani kumshinda Zahal au Mehoob?” “Mama kila ndege hutua mti aupendao na si kila unachokipenda wewe mimi nakipenda au ninachokipenda mimi wewe utakipenda ndio maana tunatofautiana kwa Thabit. Kwangu Thabit ni mwanaume mwenye mapenzi ya dhati kwangu tena aliyejitoa mhanga kwa maisha yangu.”
“Tunajua Thabit hana tatizo na kama wanadamu wote wangekuwa kama Thabit kwa kweli dunia nzima ingekuwa na amani.”
“Sasa mtu huyo nikimpoteza nitampata wapi tena?” “Kwani hakuna majini walio na upendo kupita huyo mwanadamu?”
“Wanaweza kuwepo, lakini niliapa sitaolewa na jini wala kumpoteza Thabit labda kwa mapenzi ya Mungu na si mkono wa kiumbe chochote.”
“Basi hakuna tatizo tutakulinda.” “Nitashukuru.”
Baada ya kutolewa hofu na mama yake Nargis aliamua kujipumzisha chini ya bahari kusubiri taarifa za dada yake aliyekwenda kwa mganga. Kwa upande wa pili Hailat dada yake Nargis aliendelea kumsubiri mganga aliyekuwa njiani akirudi nyumbani kwake kutengeneza dawa kwa ajili ya kupambana na Nargis.
Hailat akiwa katika umbile la nyoka mkubwa akimsubiri mganga kwa hamu kubwa, mganga alipofika kwake hakuwa na wasiwasi wowote. Nje ya nyumba yake alikuwa na wagonjwa waliokuwa wakisubiri tiba yake. Aliwasalimia na kuingia ndani kwa kufunua pazia ya kitambaa chekundu.
Alishtuka kumuona nyoka mkubwa aliyekuwa amejaa chumbani, alipotaka kurudi nyuma ili akimbie mkia ya yule nyoka wa ajabu ambaye hakuwahi kumuona wala kuhadithiwa maishani mwake ulimzunguka na kumkunja kiunoni na kumrudisha ndani.
Alipotaka kukimbia hakuwez, kichwa cha nyoka yule aliyekuwa na ukubwa wa ajabu kilipungua na kuwa sawa na chatu kilianza kumsogelea taratibu usoni huku nyoka yule akitoa ulimi wake uliokuwa umegawanyika na kuonekana ana ndimi zaidi ya kumi.
Nyoka alipomkaribia mganga alipiga kelele za kutaka kuomba msaada, alipofunua mdomo ili apige kelele nyoka yule aliingia mdomoni na kujivuta taratibu na kuingia mwilini mwa yule mganga. Joto la nyoka lilikuwa kubwa liligandisha damu ya mganga iliyomfanya aage dunia.
Baada ya kumaliza kazi yake alijitoa mwilini kwa mganga na alijirudisha katika umbile la kibinadamu na kuuangalia mwili wa mganga kwa dharau, aliukanyaga kwa miguu huku akiugeuza. Moyoni alijisemea. “Kumbe nilijiandaa kwa nguvu nyingi kumbe mtu mwenyewe hata kiganjani hajai,” aliitemea mate maiti ya mganga kisha akacheka mfululizo kwa sauti ya juu sauti iliyosikika hata kwa wateja waliokuwa wakisubiri huduma za mganga yule.
Kabla ya kuondoka alijikuta akiiwaza kazi nzito ya kumuua Thabit mume wa mdogo wake Nargis. Aliamini kazi ya kumuua Thabit si kubwa tena nyepesi kuliko ya mganga, lakini wasiwasi wake mkubwa Nargis akigundua kuwa yeye ndiye aliyemuua mume wake hali itakuwaje? Alijikuta akijisemea mwenyewe kwa sauti ya chini. “Kazi hii nimemaliza bado ya Thabit,” Hailat alicheka tena mfululizo kisha alishika kwenye paji la uso na kutoweka eneo lile kurudi nyumbani kupeleka taarifa ya kazi aliyoifanya.
Sauti ya Hailat ya kucheka mfululizo iliwashtua wagonjwa ambao waliamua kuingia ndani ya kilinge kutaka kujua sauti ile kali ya kike ilikuwa ya nani. Wao waliamini mpaka muda ule hakukuwa na mtu ndani, lakini kicheko kile kiliwafanya waingie ndani kuona kuna nini. Ndani hakukuwa na mtu zaidi ya mwili wa mganga ukiwa amelala chini mdomo ukiwa wazi, ajabu ya Mungu sehemu zote zilizokuwa wazi katika mwili wa mganga zilitoa funzo kuonesha mtu yule amefariki wiki moja iliyopita. Wote walipata mshtuko kwa mtu kupita dakika tano akiingia ndani tena amewasalimia na kuwaeleza wangoje atengeneze mazingira mazuri ili awapatie tiba.
Lakini ajabu ya karne, dakika tano tu mtu amekufa na kuoza na kutoa funza kila kona ya mwili kama mtu aliyekufa wiki nzima. Kila mmoja alitaharuki kufikia hatua ya watu kuondoka eneo la mganga bila kuaga huku kila mmoja akisema la kwake ilikuwa hali ya kutisha sana.
Hailat dada yake Nargis baada ya kumuua mganga alirudi chini ya maji kurudisha taarifa kwa mama yake kuhusiana na kazi aliyotumwa. Alipofika mama yake kama kawaida alikwishayaona matukio yote kwenye mboni za macho za mwanaye. Kabla hajasema alimkumbatia kwa furaha huku akisema: “Asante sana mwanangu kazi nzuri umefanya.”
Hailat hakusema kitu alitabasamu na kuinama kuonesha kupokea hongera za mama yake, lakini moyoni alikuwa na kazi nzito mbele yake ambayo kila alipoifikiria mapigo ya moyo yalimwenda mbio. Aliamini kabisa kitendo atakachokifanya kwa Thabit na mdogo wake agundue basi ingekuwa vita nzito ambayo mwisho wake ungekuwa mbaya sana.
Alitamani kumueleza mama yake aachane na mpango ule wa hatari lakini aliogopa kama lingetokea tatizo basi yeye angebeba msalaba ule. Alikumbuka katika watu ambao walifanya makosa makubwa alikuwa yeye pale alipokaidi ushauri wa mama yake na mwisho wake ukawa majuto kwake. Wakati Hailat akiwa katika mawazo mazito juu ya kutekeleza amri ya kumuua shemeji yake, mama yake alimwita Nargis aliyekuwa amejilaza baada ya mshike mshike uliomtoa jasho.
“Ooh, asante sana dada, sasa nitaishi kwa amani na mume wangu.” Nargis alimkumbatia dada yake kwa furaha ya ajabu, kitendo cha Nargis kufurahi baada ya kuuawa mganga na kuamini mume wake atakuwa salama kilimuumiza sana Hailat na kujikuta akitokwa machozi ya uchungu ya kufikiria kama mdogo wake atajua aliyemuua ni dada yake nini kingefuata.
Mdogo wake tukio lile aliliona na kushangazwa na kitendo cha dada yake kuangua machozi badala ya kufurahi. “Dada mbona unalia?” Sauti ya mdogo wake ilizidisha uchungu moyoni mwake na kumfanya ajitoe mikononi mwa mdogo wake na kukimbia nje kulia kilio cha kwikwi. Kitendo kile kilizidi kumchanganya Nargis kabla ya kufanya lolote alimuangalia mama yake ambaye hakuonekana kushtushwa na tukio lile, kitu kilichoongeza kumweka njia panda. Baada ya kuona mama yake akiona tukio lile la kawaida, aligeuka ili atoke nje kwenda kumuuliza dada yake nini kimemsibu. Lakini kabla hajanyanyua mguu mama yake alimwita. “Nargis!” “Abee mama.” “Unataka kwenda wapi?” “Mama ina maana alichokifanya dada cha kawaida?” “Sasa cha ajabu nini?” “Mama, mtu mzima kulia kitu cha kawaida?” “Hebu ngoja.” Mama yake alitoka nje na kumuacha Nargis amesimama, Malkia Zebeda alitoka nje na kumkuta mwanaye akiwa ameinama huku akiendelea kulia. Alipofika alimshika mgongoni na kumuuliza.
“Unalia nini?” “Mama umenipa mtihani mzito.” “Wa kawaida ni wasiwasi wako tu.” “Mama unafikiri Nargis akijua kutakuwa na usalama kweli?” “Hawezi kujua, kitendo cha kumuua mganga umemrudishia imani na kutuamini na kujua sasa hivi tupo upande wake. Kama utamuua Thabit lazima tuungane naye katika msiba mzito ili kuondoa wasiwasi upande wetu.” “Mama unajua jinsi gani tunavyompenda Nargis.” “Hilo najua ndiyo maana nafanya mpango huu ili kumuweka salama zaidi.”
“Mama hakuna mpango mwingine zaidi wa huu wa kumuua Thabit?” “Huu ndiyo mpango utakaomuweka salama mdogo wako na sisi pia.” “Mh! Sina jinsi kuufanya lakini ni mpango wa kwanza kuufanya kwa shingo upande.” “Mwanangu siku zote kumponya mgonjwa wa jipu ni kumtumbua na si kumuonea huruma, maumivu ya kutumbuliwa ni mafupi kuliko maumivu ya jipu lenyewe.” “Mh! Sawa.”
“Sasa mdanganye mdogo wako kilio chako kinatokana na maumivu aliyoyapata kupambana na mganga ili ajue kazi aliyoifanya ni kubwa kwa ajili yake nusra utoe roho.” “Sawa mama nitamwambia.” Walikubaliana na kurudi wote ndani.
***** Baada ya kukaa ndani kwa siku nzima bila kutoka nje kwa ajili ya kumhofia jini Nargis, siku ya pili walisubiri bila mafanikio walipatwa na wasiwasi na kujiuliza kulikoni mganga mpaka muda ule hajaonekana. Siku ya pili nayo ilikatika wakiwa ndani na mganga hakuonekana. “Jamani mganga atakuwa wapi mbona hakuonekana kama alivyotuahidi baada ya kutuachia vita nzito na jini.”
“Lakini mama mganga pamoja na kwamba haonekani lakini si alitueleza tunaweza kufanya mambo yetu bila jini kutufanya lolote,” mdogo wake Sakina alisema. “Tena kweli tumekaa ndani bure tulikuwa na uwezo wa kufanya shughuli zetu bila wasiwasi wowote.” mama Sakina alikumbuka kauli ya mganga. “Mnaonaje kesho tuende kwa mganga siamini kama tutapotea kwa vile amesema kuwa yeye ni maarufu sana maeneo yale,” Sakina aliongezea. “Basi kama hivyo uchafu huu ambao tuliuacha kumsubiri mganga tuuondoe usiku huu huu.” Walikubaliana wote kwa pamoja na kuanza kuutoa uchafu uliokuwa umebakia ndani baada ya mkwara wa jini Nargis. Waliutoa uchafu wote na kufanya usafi kisha walilala kusubiri siku ya pili waende kwa mganga. ********** Siku ya pili walidamka mapema kuwahi kwa mganga ili wajue nini kilichomfanya asitokee siku ya pili. Kutokana na ramani waliyopewa hawakupotea walipomuulizia walielekezwa na kwenda moja kwa moja kwa mganga. Ajabu hapakuwa na mtu yeyote maeneo ya mganga, walisogea hadi kwenye nyumba na kupiga hodi. “Jamani wenyeji hodi!”
Lakini hapakuwa na jibu, waliita kiasi cha kukata tamaa, Sakina aliamua kwenda chumba cha mganga akaangalie huenda kuna mtu yumo ndani ambaye angeweza kuwapa maelezo ya mganga. Sakina alifunua pazia na kuingia ndani. Alipotupa macho mbele alikutana na tukio la kutisha lililomfanya apige kelele za woga na kuanguka chini akapoteza fahamu.
Sauti ya mshtuko iliwashtua mama Sakina na mwanaye waliokuwa nje wakisubiri majibu ya Sakina aliyeingia ndani. Pamoja na kupata mshtuko na hofu tele moyoni hawakuwa na jinsi zaidi ya kuingia ndani kuangalia Sakina amekutana na kitu gani cha kumtisha.
Waliingia huku wakitetemeka kwa mwendo wa kunyata, Sada mdogo wake Sakina, ndiye aliyetangulia akifuatiwa na mama yake. Alifunua pazia taratibu na kutanguliza kichwa, macho yake yalitua kwenye mzoga wa mganga uliokuwa ukitoka funza kila kona na sehemu zake zingine zilionekana zimeliwa na funza. Maiti yake ilionesha kama mtu aliyekufa mwezi mmoja uliopita kwani sehemu za macho zilikuwa zimeliwa na funza, lakini ajabu alikuwa hanuki.
Pembeni ya maiti ya mganga alikuwepo Sakina aliyekuwa amelala chali huku funza wakianza kumtambaa kwenye mikono na nguo, walikuwa wakitoka katika maiti ya mganga. Sada alishtuka kama dada yake na kupiga kelele za mshtuko na kuanguka juu ya mwili wa dada yake na kupoteza fahamu.
Mama yao alitaharuki kuona watoto wake waliotangulia kuingia ndani wamepiga kelele za woga na kunyamaza. Alitamani akimbie lakini damu ilikuwa nzito kuliko maji, alipiga moyo konde na kuamua kuingia ndani huku akisema “Liwalo na liwe.”
Alifungua pazia kwa nguvu na kuwa tayari kupambana na lolote lililokuwa mbele yake, mzoga wa mganga ulimshtua na kumtisha sana, lakini alijikaza kike kuhakikisha anakabiliana na lililokuwa mbele yake. Alimlaani shetani kimoyomoyo kisha alimuinamia Sakina aliyekuwa ameanza kutambaliwa na funza na kumnyanyua kumtoa nje kwa shida kutokana na umri wake na uzito wa mwanaye.
Alimshika mikono na kumburuza hadi nje kisha alimrudia mdogo huku akiendelea kumuomba Mungu kimoyomoyo amuepushe na mtihani ule. Alifanikiwa kuwatoa wote nje na kuwapatia huduma ya kwanza kwa kuwamwagia maji yaliyokuwepo kwenye pipa nje ya nyumba ya mganga. Wote walirudiwa na fahamu, baada ya kurudiwa na fahamu hawakutaka waendelee kuwepo eneo lile kwani waliamini ni hatari kwa usalama wao. Alirudi hadi kituoni ambako walipata gari kurudi kwao, njia nzima kila mmoja alikuwa kimya akitafakari kifo cha kutisha cha mganga. Mwili wake kuonekana kama mtu aliyekufa mwezi mmoja uliopita, hawakuamini kifo cha siku moja mtu aoze kiasi kile.
Walipofika nyumbani Sakina na mdogo wake Sada waliangua kilio kutokana na kifo cha mganga pia hali aliyokuwa nayo iliyoufanya mwili uharibike huku baadhi ya sehemu ya mwili kuliwa na wadudu. Mama yao aliingia kazi ya kuwabembeleza wanae ambao hofu iliwajaa baada kuuona mwili wa mganga ulivyoharibika. “Mama lazima atakuwa yule mwanamke jini,” Sakina alitoa wazo baada ya kunyamaza kulia.
“Mmh, kweli inawezekana,” mama aliunga mkono. “Mama kama kweli ni yeye hatuoni maisha yetu yapo hatarini?” Sada alihoji.
“Ni kweli lazima maisha yetu yatakuwa mashakani,” mama yao aliongezea. “Sasa mama tufanye nini kabla mambo hayajaharibika?” Sakina aliuliza. “Ni kumtafuta mganga mwingine la sivyo tutaumia, Jini yule ni hata….”
Kabla hajamalizia upepo ulianza kuingia ndani taratibu na kupeperusha mapazia. Kila dakika upepo uliongezeka huku milio wa kuvuma kwake ukisikika. Hali ya wasi wasi ilitanda na kuamini mbaya wao amefika, Sakina na Sada wote kwa woga walijisogeza kwa mama yao na kumkumbatia kwa nguvu.
“Jamani wanangu tumuombe Mungu, lakini kama atatokea mimi sina ubavu wa kumzuia.” “Yaani mama najuta kujiingiza katika vita isiyonihusu,” Sakina alisema huku akizidi kumshikilia kwa nguvu. “Mama tukipona tuachane naye,” Sada naye alisema.
Wakiwa wanajadili vile upepo ule ulipungua taratibu kisha ulitulia kabisa, baada ya upepo kutulia kilisika kicheko kama mtu amechekea mbali na sauti yake kusafirishwa na upepo. Baada kicheko kunyamaza hali ya utulivu wa awali ulijirudia.
Kwa vile muda ulikuwa bado hawakutaka kupoteza muda, mama yao aliwaeleza waende kwa mganga mwingine aliyekuwa Kigamboni. Baada ya kukubaliana hata bila kuoga wala kubadili nguo, waliondoka kwenda kwa mganga Kigamboni.
CHINI YA BAHARI Baada ya mpango wa kumziba macho Nargis kufanikiwa wa kumwua mganga, malkia Zebeda alimwita tena mwanaye mkubwa wa kike, Hailat, dada yake Nargis.
“Hailat.” “Abee mama.” “Nafikiri sasa wakati muafaka umefika wa kummaliza shemeji yako.”
“Ni kweli mama, lakini kwa nini moyo unaniuma kila nikifikiria kufanya kitendo hicho?” “Mwanangu umefanya mauaji mangapi hili likushtue.” “Mama si kunishtua bali uzito wa tukio lenyewe.”
“Nikueleze mara ngapi kumtibu mgonjwa wa jipu ni kumtumbua na si kumuonea huruma. Litumbue jipu ili tuishi kwa amani, ningeweza kufanya hivyo mimi lakini Nargis akigundua kutakuwa hakuna wa kumtuliza.” “Mama kwa hiyo msalaba unanibebesha mimi?” “Kama itatokea, nitajua jinsi gani ya kumaliza tatizo hilo.” “Mmh, sawa lakini kuna kitu kizito kinakuja mbele ambacho huenda kikasambaratisha familia.” “Ni wasi wasi wako, kamwe hawezi kujua nani aliyemuua mume wake.” “Mama una uhakika na ukisemacho?”
“Na siku hiyo atashinda huku, mpaka unamaliza kazi na kurudi nyumbani ndipo nitamruhusu. Kutokana na kuwa na vita na jirani yake lazima atawajua ni wale, nasi tutampa nguvu kuwafutilia mbali. Nakuhakikishia siku hiyo na mimi mama yenu nitashiriki nikumbuke enzi zangu.”
Mama Sakina na wanae walipofika feri walipanda pantoni kuelekea Kigamboni, baada ya watu kujaa pantoni ilianza kutembea taratibu kuelekea upande wa pili wa bahari. Pantoni ilipofika katikati ya maji, ghafla upepo mkali ulizuka baharini na kuifanya pantoni kuyumba.
Ilikuwa hali ya kutisha kwa kila mtu kulilia roho yake, upepo ambao haukuwahi kutokea baharini, uliendelea kuvuma kwa nguvu na kuifanya pantoni kuchota maji na baadhi ya watu kuangukia kwenye maji. Mmoja wa watu walioangukia kwenye maji alikuwa Sakina.
Taarifa za pantoni kutaka kupinduka zilifika katika jeshi la majini ambalo lilichukua meli ya uokoaji na kuwahi eneo la tukio kuokoa watu walioangukia majini. Walifanikiwa kuwaokoa wote kasoro Sakina peke yake ndiye hakuonekana.
Lilikuwa pigo jingine kwa mama Sakina na kuamini ule haukuwa upepo wa kawaida ila wa jini Nargis. Jeshi la uokoaji wa baharini lilifanya msako kwa kutumia vifaa vya kisasa kumtafuta Sakina akiwa hai au amekufa. Lakini kila kona chini ya maji hawakuona kitu.
Baada ya kumkosa ikabakia kitendawili kwa watu waliokuwa wamefika salama Kigamboni. Kila mmoja aliamini siku ile ndiyo ilikuwa siku yao ya mwisho kutokana na ukubwa wa upepo ulioyumbisha pantoni ambayo ilionekana kuzama.
Mama Sakina na mwanae Sada wote waliangua kilio kumlilia Sakina aliyepotelea ndani ya maji. Waokoaji walisema wamekata tamaa kwani wametumia vifaa vya kisasa kumtafuta Sakina bila mafanikio na kutoa taarifa kwa mtu yeyote atakayeuona mwili wake atoe taarifa.
Baada ya watu wote kuondoka walibakia mama Sakina na mwanaye Sada kujipanga wafanye nini baada ya Sakina kupotelea majini. “Mama kwa nini tusiachane na yule jini?” “Mmh kweli, lakini kwa vile sisi tumebakia salama hatuwezi kurudi nyuma lazima twende kwa mganga tukajue dada yako yupo wapi.”
“Mamaaa, lakini tunakuwa wabishi kama kenge mpaka tutoke damu masikioni!” “Sada kwa vile wewe ni mtoto hii imeishakuwa vita hatuna budi kupambana nayo.” “Mama utawezaje kushindana na kiumbe asiyeonekana?” “Ni kweli, lakini viumbe hawa ukiwaogopa sana wanaweza kukufanya wanavyotaka.”
“Mamaaa, kwa nini tusirudi?” “Hapana maji tumeishayavulia nguo hatuna budi kuyaoga, na bila ya hivyo hatuwezi kumrudisha dada yako.” “Unataka kuniambia dada Sakina hajafa?” “Inawezekana kama kachukuliwa na jini, lakini kama kwa amri ya Mungu lazima atakuwa amekufa, lakini kupotea kwake nina imani hajafa.” “Mamaaa mbona kila siku dada Sakina?” “Unataka safari ijayo uchukuliwe wewe?” “Aku, jini nitazungumza nalo nini?” “Kwani dada yako alizungumza nalo nini?” “Mama vitu hivyo si vya kuomb….”
Sada alinyamaza ghafla na kukishangaa kitu ambacho mama yake alipokiangalia hakukiona. Mama Sakina alikitazama kitu kilichomfanya Sada anyamaze lakini hakukiona ilibidi amuulize mwanaye ambaye alikuwa bado amekitumbulia macho kitu kisichoonekana.
“Wee Sada,” alimshtua. “E…eh…eeh,” Sada alishtuka kama mtu aliyekuwa amepigwa na bumbuwazi. “Umeona nini mbona umenyamaza ghafla?” “Mmh,” aliguna bila kusema kitu. “Vipi kuna nini mbona unanitisha?” “Ina maana wewe mama huoni?” “Nini?” “Yule mwanamke jini.”
“Mwanamke jini! Yuko wapi?” ”Mama si amepita mbele yetu na wewe nimekuona ukimtazama na kupotelea kwa watu.” “Hapana sijamuona huenda umemfananisha.” “Hapana mama mwenyewe namjua vizuri.” “Kwani aliku….”
Mama Sakina naye alinyamaza ghafla na kukaza macho kuangalia mbele, safari hii ilikuwa kazi ya Sada kumshangaa mama yake anaangalia nini. Kila alivyoangalia mbele hakuona kitu lakini mama yake aliendelea kuangalia mbele kwa makini. Ilibidi Sada amshtue mama yake. “Mama vipi tena.” “Nimemuona.”
“Nani?” “Mwanamke jini.” “Yupo wapi?” “Sada ina maana humuoni yule anaondoka karibia na lile gari linalokuja.” “Mama mbona mimi sioni kitu.” “Huo utani si yule,” alimuonesha kwa kidole.
“Mamaa, sioni kitu chochote.” “Aah, basi tuachane naye.” “Mama turudi nyumbani, asije akatuua kama mganga.” “Acha woga kifo kimeumbwa, siwezi kurudi nyuma mpaka nijue hatima ya mwanangu.” Mama Sakina aligoma kurudi lakini moyoni alijawa na wasi wasi kwa vile jini Nargis alielekea mbele njia ya kuelekea kwa mganga. Lakini alipiga moyo konde na kuamua kwenda kwa mganga.
******* Nargis baada ya kuipepesua pantoni kwa upepo mkali alifanikiwa kumnyakua Sakina kwenye kundi la watu na kwenda naye moja kwa moja kwenye gareza la chini ya miamba-maji. Nargis alionekana mwenye hasira kuliko siku zote, baada ya kumfikisha chini ya gereza alimfunga kamba na kuanza kumtandika kwa hasira. Sakina alipigwa mpaka akapoteza fahamu ndipo alipomuacha akamrudisha katika hali yake ya kawaida na kuanza kumhoji kwa nini amekuwa mbishi kutaka kufuatilia maisha yake.
Sakina akiwa anavuja damu kila kona ya mwili, alifungwa kwenye mwamba kama anasurubiwa msalabani. Nargis alimsogelea Sakina aliyekuwa ameinamisha kichwa akiendelea kulia huku damu zikimtoka puani na mdomoni, alimshika chini ya kidevu na kuunyanyua uso wake.
“Wee shetani wa kike nimekukoseeni nini mpaka kuamua kunifanya hivi?” “Naomba unisamehe,” Sakina aliomba kwa sauti ya kichovu kutokana na kipigo alichopata na mwili wake kumuuma kila kona.
“Ninyi siyo watu wa kusameheni, nimekugeuza mbwa ili kukutisha lakini amekuja mtu na kuwatia kiburi, nafikiri mmeona nguvu zangu jinsi nilivyomfanya. Sikuwa na nia ya kukufanya hivi ila umenilazimisha. Kuanzia leo nitakugeuza nguruwe na kukuacha huku milele, sitaki kukuua kwa vile huna uwezo wa kuniua zaidi ya kutegemea msaada wa kiumbe kingine.
Nakuhakikishia kukuletea mama na mdogo wako katika umbile nitakalokugeuza wewe, nina imani viumbe wapumbavu maisha yenu yanafaa huku.” “Tusamehe dada Nargis.”
“Undugu wa jini na binadamu ulianza lini, wanadamu kwa wanadamu hamwelewani, itakuwa sisi majini. Mimi si dada yako, mimi ni jini adui yako,” Nargis alisema kwa hasira. “Hapana dada Nargis, ni mama ndiye aliyenilazimisha kuyafanya haya, naomba unisamehe.” “Ninyi wanadamu hamsikii upo kama kenge mpaka mtoke damu masikioni.”
“Najua tumekukosea, tupo chini ya miguu yako.” “Unajua mama yako kwa sasa anafanya nini?” “Hata sijui.”
“Mlikuwa mnakwenda wapi?” Swali lile lilikuwa zito kwa Sakina kwa kuamini Nargis alikuwa anajua walikuwa wanakwenda wapi, alibakia kimya bila kujibu swali. Nargis alimtazama kwa jicho kali lililomfanya aangalie pembeni kwa woga na aibu.
“Nijibu la sivyo nitakufanya kitu kibaya kuliko nilichokufanya.” “Kwa mganga.”
“Kufanya nini?” “Kukuzuia nimpate Thabit.” “Wanaume wote wamekwenda wapi mpaka mumng’ang’anie mume wangu?”
“Hatukujua kama ameoa.” “Mganga alipowaeleza kuwa mimi ni mke wa mtu mlifanya nini?” “Kwa hilo tunaomba utusamehe“ “Hujanijibu niwasamehe kwa lipi?”
“La kutaka kukuachanisha na Thabit.” “Na mimi kunifanya nini?” “Dada Nargis tumekosa dada yangu, ni roho mbaya lakini tutajifunza kutokana na makosa.” “Hujanijibu, na mama yako sasa anakwenda wapi?” “Siwezi kujua dada Nargis.” “Ngoja nikuoneshe jinsi mlivyodhamiria vibaya juu yangu kisha mnaomba msamaha.”
Nargis alinyoosha mkono mbele sehemu ya mwamba, ilikuwa kama sinema, mbele yake aliwaona mama yake na mdogo wake wakielekea kwa mganga. “Umewaona?” “Nimewaona.”
“Pamoja na kuwatisha mama yako amekuwa mbishi, sasa nitamgeuza kiumbe cha ajabu.” Baada ya kusema vile alichota maji ya bahari kwa mkono na kuyanyunyizia kwa mama Sakina, ambaye alianza kujikuna mwili mzima kama aliyemwagiwa upupu huku akilia. Sakina alimshuhudia mama yake akivua nguo na kubakia mtupu kwa ajili ya kujikuna, ghafla alimwona mama yake mwili wote ukitoka mapele makubwa.
Sakima alimsikia mama yake alivyokuwa akilia huku akiendelea kujikuna akiwa mtupu baada ya kuzitupa nguo zote. Mdogo wake Sada alionekana akijitahidi kumvalisha nguo mama yake lakini alishindwa kutokana na jinsi mama yake alivyokuwa akijitupa chini.
Sakina roho ilimuuma na kutamani kumuombea mama yake msamaha, lakini bado hakujua hatima yake mbele ya Nargis aliyekuwa na hasira za ajabu.
*** Wakati Nargis akiendeleza mateso mazito kwa mama Sakina na familia yake, ndani ya kasri ya Malkia Zebeda chini ya bahari, mpango ulipangwa na kupangika juu ya kifo cha Thabit mume wa Nargis. Malkia Zebeda alimwita mwanaye mkubwa Hailat kumweleza cha kufanya siku ile. “Nafikiri leo ndiyo siku mwafaka wa kutekeleza nililokutuma.”
”Kazi ile ni ya muda mfupi mpaka arudi atakuta mzoga wa mtu.” “Mama hatujui yupo wapi, huoni huo ni mtego tunaojiingiza wenyewe, kwa nini tusimtafute ili tujue kumndanganya na mimi nifanye kazi uliyonituma.”
“Hesabu zangu zinaonesha kifo cha Thabit ndani ya saa moja lijalo zaidi ya hapo hatutamweza tena.” “Sasa mam..”
“Hailat si muda wa mazungumzo sasa bado dakika hamsini inanionesha Thabit yupo nyumba sasa hivi.” Hailat alikubali shingo upande kwenda kumuua Thabit shemeji yake mume wa mdogo wake Nargis.
Wakati mpango ule ukiwa umepamba moto, Sada mdogo wake Sakina aliyechanganyikiwa na hali ya mama yake aliyepagawa ghafla na kuanza kupiga kelele kuwa anawashwa mwili mzima kiasi cha kuvua nguo mbele za watu bila aibu.
Wapita njia walijua yule mama ni mwendawazimu kutokana na kupiga kelele huku akijikuna na kuvua nguo zote. Sada alijitahidi kumvisha nguo lakini kila nguo ilipomgusa mwilini ilikuwa kama ina miba na kuziogopa kugusa mwilini mwake. Kila alivyojikuna uchungu uliongezeka, ghafla mwili ulianza kutoka mapele makubwa kila kona huku mengine yakitoa usaha na kumfanya atoe harufu iliyowafanya watu wamkimbie na kubakia peke yake na mwanae ambaye alivumilia harufu mbaya iliyokuwa ikitoka mwilini kwa mama yake.
“Mungu wangu nakufa nawashwa mimi, oooh nakufa jamani nisaidieni,” mama Sakina aliomba msaada kwa wapita njia lakini hakuna aliye shughulika naye. “Mama si uvae nguo,” Sada alimmbembeleza mama yake.
“Siyo kwamba sitaki kuvaa nguo, kila ikigusa mwili wangu inakuwa kama ina miba, naumbuka mwanangu,” mama Sakina aliona dunia nzima ikimkimbia na kumwacha peke yake. “Mama nilikwambia unaona sasa.” “Mwanangu najuta, najuta kukubishia.”
“Sasa tutafanyaje, hii hali inatisha.” “Sina jinsi mauti yananisubiri tu mwanangu, naumia jamani.” Kilio cha majuto kilisikika chini ya maji kwa Sakina kushuhudia mateso ya mama yake na kilio cha kukata tamaa. Alitamani kumpigia magoti kumuomba msamaha Nargis ili amsamehe mama yake na mateso yale mazito. Lakini bado aliamini makosa aliyofanya ni mazito na bado aliendelea kushindana naye.
Nargis aliyekuwa amesimama ameshika mkono mmoja kiunoni, alimgeukia Sakina aliyekuwa akibubujikwa machozi ya uchungu wa mateso mazito ya mama yake. Alijikuta akisahau hata mateso yake na akili yote kuhamia kwa mama yake aliyekuwa akiteseka na kuadhirika kwa watu kumuona kama mwendawazimu. “Umemuona mama yako?” “Nimemuona,” Sakina alijibu kwa sauti ya kilio.
“Unajua wanadamu ni viumbe wanafiki sana, siku zote hujificha nyuma ya machozi kwa kisingizio cha kuonewa kumbe dhamira yenu ilikuwa mbaya sana ya kuniua ili mumpate Thabit. Siamini nilichokifanya kinalingana na kosa mlilofanya.
Nimekuwa nikiingia kwenye matatizo na wanadamu kila kukicha, hata leo hii nimuokote mwendawazimu na kumponya kisha awe mume wangu, mpo mtakaojitokeza na kumtaka huku mkitumia kila hila kuniondoa dunia.
Sijamkosea mtu maisha yangu yananihusu mwenyewe na nilipoamua kumpenda Thabit nilijua hana mtu ndiyo maana nilimchagua lakini leo hii mmetokea watu mnaojifanya mnajua kupenda.
Thabit kwani amezuka kama uyoga usio na mbegu, si alikuwepo sasa vipi leo aonekane mbele ya macho ya wanadamu. Nataka kukuuliza swali nakuomba unijibu bila hivyo adhabu ya mama yako itakugeukia wewe.” “Uliza tu dada yangu, nitakujibu bila kukudanganya.” “Jini na mwanadamu nani mbaya?”
“Kwa kweli katika maisha yangu najua majini ni viumbe wabaya ambao hutumika kutoa roho za watu.” “Na mwanadamu anayemuua mwenzake ni jini?” “Hapana.”
“Wewe umetoa mimba mbili na kutoa roho za viumbe visivyo na hatia na wewe ni jini?” “Hapana.” “Sasa kwa nini mmuone jini ndiye muuaji?” Sakina alikosa jibu na kuangalia chini kwa aibu, Nargis aliendelea kumuuliza maswali. “Na wanaoua Maalbino ni majini?” “Hapana.” “Kila kitu hapana, mbona hamuogopani ninyi wanadamu, viumbe wenye hila na roho mbaya. Na hata hao majini wanaoua watu hutumwa na ninyi wenyewe wanadamu, ndiyo maana angamizo kubwa katika karne zilizopita ni kwa wanadamu na si majini. Nafikiri mnaona jinsi gani wanadamu mlivyo wabaya kuliko majini mbele ya Mungu.
Nimekuwa kiumbe mwenye huruma lakini huruma hiyo imenifanya nikose amani moyoni mwangu. Nilimuua mganga kwa sababu alikuwa akijua udhaifu wetu, tulimuwahi kabla hajafanya lolote. Lakini kiumbe anayemtegemea mtu huyo huwa hatusumbui sana, humtisha na akizidi humgeuza kiumbe wa ajabu. Hili litakuwa onyo la mwisho mkirudia tena nitafumba macho na kuutoa uhai wa kila kiumbe kitakacho taka kuingilia maisha yangu.
Wakati Nargis akitaka kutoa msamaha kwa Sakina na mama yake dada yake Hailat alikuwa akiandaa kwenda kummaliza Thabit aliyekuwa nyumbani peke yake na vijakazi ambao walikuwa majini. Aliondoka hadi kwenye nyumba anayoishi mdogo wake na mumewe.
Akiwa katika umbile la ndege, kwa vile kulikuwa na vijakazi majini wasio na uwezo mkubwa wa nguvu za kijini, alipofika aliitia nyumba ile kiza kizito na kufanikiwa kuwafungia chumba kimoja vijakazi wote kwa nguvu za kijini ambazo ziliwafanya washindwe kutoka.
Baada ya kufanikiwa kuwafungia chumbani majini vijakazi, alirudi hadi sebuleni alipokuwa amekaa Thabit akisikiliza nyimbo zenye mahadhi ya kiarabu ambazo Nargis alikuwa akizipenda sana. Hailat alimpima Thabit na kumuona mwepesi sana.
Lakini kabla ya kumvaa alijikuta akimuonea huruma shemeji yake huku akifikiria Nargis atapokea vipi kifo cha mumewe. Bila kutarajia machozi yalianza kumtoka kwa kumuonea huruma shemeji yake.
Muda aliopewa na mama yake ulikuwa unazidi kuyoyoma zilikuwa zimebakia dakika ishirini, hakuwa na jinsi aliamua kumvaa Thabit, huku akisema liwalo na liwe.
Hailat alimfuata Thabit aliyekuwa amejilaza kwenye kiti cha uvivu huku akibembelezwa na nyimbo laini za mahadhi ya Kiarabu. Upepo ulioingia ndani ulimshtua Thabit na kujua ule ni ujio wa majini ambao mara nyingi aliutumia Nargis kuingia ndani.
Lakini ujio ule alikwishauacha na kuingia ndani katika hali ya utulivu ya mwanamke mwenye heshima kwa mumewe. Nargis pamoja na kuwa jini alikuwa na mapenzi mazito kwa mumewe kwa kumfanyia yote anayotakiwa kuyafanya mwanamke aliyeolewa kwa mume wake, vitu vilivyomteka Thabit kufikia hatua ya kutoona mwanamke yoyote duniani kama Nargis.
Hakuna kiumbe yoyote angeweza kumbadilisha Thabit imani yake kwa majini viumbe wapole wenye upendo kuliko wanadamu ambao kutenda mabaya ni sehemu ya maisha yao. Thabit aliamini mkewe Nargis alikuwa anarudi, lakini upepo ulizidi kiasi cha kumtisha.
Aliponyanyua macho juu alishangaa kuona joka kubwa likiingia dirishani na kumfuata alipokuwa amekaa. Thabit alishtuka alipotaka kupiga kelele joka lile lilimuingia mdomoni kwake, kwa vile alikuwa na nguvu ndogo za kijini alizoambukizwa na Nargis.
Yule nyoka alipoingia kichwa na shingo alimshika ili asiingie wote, ikaanza vita nzito ambayo ilifanya vitu vyote ndani vipasukepasuke kutokana na Hailat kulazimisha kuingia ndani na Thabit alimshikilia asiingie ndani. Kila alipolazimisha alikuwa akimtoa upande mmoja kwenda mwingine na kumpigiza popote atakapoangukia na kusababisha vitu vyote ndani kuvunjikavunjika. Thabit aliamini maisha yake yalikuwa mikononi mwake huku akiomba mkewe atokee. Muda ulizidi kukatika huku vita ikiwa kubwa. Wakati vita ikiendelea Nargis chini ya bahari hali ilimbadika ghafla na kujua kuna hatari iliyokuwa ikiendelea, lakini hakujua ipo wapi. Kwa haraka aliwachukua mdogo wake Sakina na mama yao aliyekuwa amerudiwa na akili na kuwaficha kwenye gereza la chini ya bahari ili aende akaangalie hatari inatoka wapi.
Baada ya kumuacha mama Sakina na watoto wake chini ya mwamba bahari, alitoka moja kwa moja hadi kwao na kumkuta mama yake ambaye alishtuka kumuona Nargis. “Mama kuna usalama?” “Upo, kwani vipi?”
Nargis hakusema kitu aligeuka na kutoka kasi kuwahi nyumbani kwake mama yake alijaribu kumwita, hakuitikia waka kugeuka alikimbilia nyumbani kwake. Mama yake alipoangalia muda zilikuwa zimepita dakika tano za ziada kwa muda aliompa mwanaye kumtoa roho Thabit.
Alicheka kwa kuamini Hailat kishamaliza kazi kwa hiyo haraka ya mwanaye ilikuwa ya bure, kwani angekuta mzoga wa mtu. Hailat baada ya kuhangaika kuingia ndani na kushindwa alianza kukosa pumzi ndani ya Thabit hapo alianza kutapatapa kuokoa maisha yake, alifanikiwa kumpigiza sehemu Thabit akalegea na kumuachia. Muda ulikuwa umezidi dakika moja.
Alikuwa akitweta akiwa na majeraha ya kujipigiza na mwili ulikosa nguvu kwa ajili ya kukosa pumzi kwa muda mrefu. Akiwa bado anajikongoja pembeni mwa mwili wa Thabit, kwa mbali alisikia kishindo cha mdogo wake kikija kwa kasi. Aliuacha mwili wa Thabit uliokuwa umelala chini ukitokwa na damu kila kona na kutimua mbio.
Nargis aliingia ndani mwake kwa kasi, jicho lake lilitua kwenye mwili wa mumewe aliyekuwa amelala chini huku akitokwa damu kila kona ya mwili. Alipoangalia ndani ya nyumba vitu vyote vilikuwa vimevunjikavunjika kuonesha kulikuwa na mapigano mazito. Aliuinamia mwili wa mumewe ambaye alikuwa nusu mfu kwa jinsi alivyokuwa.
Nargis alilia sana kumkuta mumewe nusu mfu huku akiwa hajui hatima ya kipenzi mumewe, mwanaume anayempenda kuliko kitu chochote duniani.
Alipoangalia mdomoni alionekana ameumizwa sana, macho yake yalimuonesha shambulio lile halikuwa la kibinadamu wala ushirikina wa miti shamba ila nguvu za kijini. Mdomo wa Thabit ulikuwa umeishaanza kuoza na kutoa funza, Nargis kwa haraka alimkojolea Thabit mdomoni na kumpaka mkojo sehemu zote za majereha ili kuua sumu ya kijini ambayo ingeuozesha mwili wake.
Baada ya kumsafisha Thabit ambaye alikuwa nusu mfu, alimlaza kitandani na kuwatoa wajakazi wake waliokuwa wamefungiwa chumba kimoja. Kabla ya kuondoka aliapa kwenye mwili wa Thabit ambao haukuwa na dalili za kurudiwa fahamu.
“Naapa kupambana na yoyote hata akiwa mama yangu mzazi kama Thabit atakufa nami nitakufa kwa ajili ya kumpigania. Thabit mume wangu natoka nitapata jibu la tatizo lako.”
Alimpiga busu shavuni na kuondoka kuelekea nyumbani kwao kupata ukweli wa tatizo la mumewe. Akiwa njiani kwenda kwao alijawa na mawazo juu ya tukio lile la kutaka kuutoa uhai wa mumewe, aliamini vita yake kubwa ilikuwa kwa wanadamu kumbe hata baadhi ya majini. Kilichomuumiza roho ni aliyetumwa alipania kumuua mumewe, alitembea kwa mwendo wa kasi huku akilia.
******* Hailat baada ya kufanikiwa kutoroka kumkwepa mdogo wake, alirudi nyumbani akiwa hoi kutokana na kujipigiza sehemu mbalimbali akilazimisha kuingia mwilini kwa Thabit. Mwili ulijaa majeraha na kumfanya atembee kwa shida. Mama yake alipomuona alishtuka , lakini alitumbukia nyongo baada kuyaona matukio yote kwenye mboni za jicho la mwanaye. “Vipi imekuwaje tena?” alimuuliza macho yakiwa yamemtoka pima. “Mama hata siamini, yule mtu si bure bila kujitahidi kujiokoa angeweza kuniua; alinishika vibaya nikawa mbele siendi nyuma sirudi kila nilivyompigiza alining’ang’ania. Mama ilikuwa aibu nilikuwa nafia tumboni kwa Thabit, mpaka ananiachia nilifanya kazi.
Mpaka analegea muda umekwisha hata nguvu za kufanya lolote sikuwanazo na muda huo mwanao alikuwa anakuja, sijui angenikuta bado nipo mdomoni kwa mumewe kutokana na jinsi nilivyochoka angeniuliza pale pale. Sasa sijui atajua ni mimi, mama kazi kwako la sivyo mpasuko unaokuja sijui nani atauzima, ila akichelewa kidogo atakuwa mumewe kaoza mwili.”
“Namsikia anakuja tena kwa kishindo, fanya hivi; nenda chumbani kwangu ili asijue upo wapi.” Kabla hajanyanyua mguu Nargis alitua mbele yao kama jini la kutumwa akiwa amebadilika mwili na kuwa mweusi kwa hasira.
Wote walishtuka kumuona Nargis amesimama mbele yao, alikuwa amebadilika na kuwa mweusi kama kisiki cha mpingo kwa hasira. Aliwatazama wote huku dada yake akiangalia pembeni kwa aibu. Mama yake hali ile aliiona na hali ya hatari ilikuwa imeisha jitangaza mbele yao.
“Hailat nenda ndani,” Malkia Zebeda alimwambia mwanaye. Kabla hajapiga hatua kuelekea chumbani kwa mama yake Nargis aliruka na kusimama mbele ya dada yake. “Nataka mnieleze majeraha haya ameyapata wapi?” “Utajua tu, mwache akapumzike,” mama yao malkia Zebeda aliingilia kati kunusuru hasira za mwanaye mdogo.
“Mama… mmetimiza mliyotaka kutimiza mmemuua mume wangu kwa nini?” “Nani kamuua?” “Ninyi, tena mmeumbuka majeraha ya dada bado mabichi.” Hailat moyoni alijuta kutimiza agizo la mama yake kwa kuamini duniani hakuna siri ya zaidi ya mtu mmoja. Aliamini mdogo wake kama atamkamata hataweza kushindana naye kwa vile alikuwa ameumia sana na kuchoka.
“Nakuuliza kwa nini umemuua mume wangu?” Alimuuliza kwa sauti ya juu yenye ukali wa radi. Hailat hakuwa na jibu zaidi ya kumuangalia mama yake amtetee. Mama yao aliona kila dakika Nargis alipanda juu na dada yake alizidi kunywea, kabla hajasema kitu. Nargis alimvaa dada yake ambaye alikuwa ameathiriwa na majeraha na kuchoka kutokana na kukosa hewa kipindi kirefu mdomoni kwa Thabit.
Akiwa na nguvu za ajabu alimpigiza mfululizo dada yake kwenye kuta za chini ya bahari kuzidi kumtia majeraha mwilini. Hakuwa na uwezo wa kujitetea, mama yao naye alizidiwa nguvu. Nargis alimbana dada yake chini kwa kumshika kwenye koromea, alipania kumuua kama alivyotaka kumuua Thabit.
Japo aliamini Thabit bado hajafa lakini alikuwa na matumaini madogo ya kuendelea kuishi kutokana na sumu ya kijini kumwingia mwilini. Mama yake kuona hali imekuwa mbaya aliwaita walinzi wa chini ya bahari majini Kashi yenye ngozi nyeusi kama lami, yenye nguvu za ajabu za kuweza kupasua miamba. Walipofika walimuondoa Nargis juu ya dada yake huku vidole vikiwa vimeanza kupenya kwenye shingo vikutanie upande wa pili.
Walimtoa kwa nguvu na kumuweka pembeni. Vidole vya Nargis vilianza kupata damu iliyoanza kutoka katika shingo ya dada yake, kama wangechelewa kidogo angemuuliza pale pale. Nargis hakukubali aliendeleza vita na majini Kashi ambayo hayakuwa na ruhusa ya kumpiga zaidi ya kumkamata.
Kutokana na nguvu za hasira alizokuwa nazo Nargis ilikuwa vita kubwa ya kumtuliza. Aliweza kuwaua majini Kashi matatu. Hapo yaliona yanafanya utani kwani kumkata hivi hivi wasingeweza. Moja lilimpiga kofi zito lililomfanya apoteze fahamu. Mama yake aliamuru achukuliwe apelekwe kwenye jela chini ya miamba bahari, walipofika kule chini waliwakuta wanadamu ambao hawakujua wamefikaje kule. Taarifa zilipomfikia malkia Zubeda aliyekuwa na hasira kwa kitendo cha mwanae kukosa adabu kwa ajili ya penzi la mwanadamu.
Aliwaamuru watu waliokutwa kule chini ya miamba bahari wafikishwe mbele yake, Mama Sakina na wanae walifika mbele ya malkia Zebeda. Kabla ya kujieleza aliona mambo yote kwenye mboni za macho yao, baada kutambua kilichosababisha kuwa kule aliwaruhusu kurudi duniani na kuwaahidi kuwasaidia Sakina aolewe na Thabit.
Alitumwa kijakazi mmoja kwenda nyumbani kwa Thabit kumpelekea dawa ya kumpaka, alipofika alikuta Thabit amelala kitandani nusu mfu. Alimpaka dawa ile na nyingine alimnywesha, baada ya muda Thabit alirudi katika hali yake ya kawaida.
Malkia Zebeda alipanga kifungo cha mwanae kiwe miaka kumi chini ya bahari kwa utovu wa nidhamu, lakini adhabu ilipunguzwa miaka mitano huku akimuahidi kama atarudia basi atamfunga milele huku akiwa kipofu.
Nargis aliumia chini ya miamba bahari huku akipanga siku akitoka atakacho kifanya hakitasahaulika na mauti yake yatakuwa siku ileile. Aliapa kuiteketeza familia nzima ya mama Sakina. Kilichomuuma zaidi kilikuwa ndoa ya Thabit na Sakina mwanamke aliyemsumbua na kumsamehe kwa makubaliano ya kutomfuatilia mume wake.
Kila alilolifikiria roho ilimuuma, lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali yote hakuwa na uwezo wa kutoka kwenye kifungo muda wote alikuwa chini ya majini meusi Kashi. Nargis hakuamini kuona Thabit anaoa wakati walikubaliana hataoa mwanamke mwingine zaidi yake.
Lakini maumivu yote yaliyeyuka moyoni na kuapa siku atakayotoka kifungoni ndiyo siku ambayo itakuwa safari yake ya kuzimu. Aliamini katika maisha yake Thabit ndiye mwanaume sahihi kwake ambaye alimpigania mpaka hatua ya mwisho.
Thabit baada ya kuhakikishiwa Nargis hatamuona tena, alimuoa Sakina kwa msaada wa jini Zebeda Malkia wa bahari ambaye alikuwa chaguo la wote. Lakini kila usiku alimuota Nargis aliyekuwa kwenye mateso mazito chini ya miamba bahari kwa ajili yake. Hali ile ilimkosesha raha kufikia hatua ya kutaka kuachana na mkewe amfuate Nargis lakini hakujua atafikaje chini ya bahari.
Siku zilikatika huku Thabit akiwa na mkewe Sakina na utajiri alioachiwa na Nargis ukizidi kushamiri. Siku moja usiku ulizuka moto ambao hawakujua umetoka wapi, Thabit na mkewe walichokumbuka ni shuka waliojifunika. Moto ule uliteketeza nyumba yote hakuna kilichopatikana.
Siku ya pili Sakina alirudi kwao na huo ukawa mwanzo wa maisha ya taabu ya Thabit ambaye kila alichokifanya kilikuwa kibaya. Nguo za kuvaa na kula yake ilikuwa matatizo. Alitamani kujiua lakini kifo kilimkimbia, alimkumbuka mkewe Nargis na kuamini kumuoa Sakina ndiyo chanzo cha yote.
Hakuwa na jinsi zaidi ya kuamua kila siku kushinda na kulala pembeni ya bahari kumsubiri Nargis. Thabit alikuwa mwenda wazimu kamili asiye kumbuka kuoga wala kuchagua chakula. Maisha yake yote duniani aliamua kuyamalizia baharini.
Wapo waliomuona mwendawazimu lakini yeye alikuwa na akili timamu, aliapa hatatoka baharini mpaka Nargis amalize kifungo chake.Huu ni mwisho wa simulizi yetu, najua unataka kujua baada ya kifungo cha Nargis baada ya miaka 50 kizazi cha nargis kinakuja duniani kwa mtoto wa nargis aitwae balkees kuja dunian na mambo yalianzia hapa sasa endelea taratibu ili achukue simu ampigie baba yake amfuate eneo lile ambalo lilikuwa limemuweka katika hali ya hatari. Aliponyanyua uso achukue simu iliyokuwa kwenye kwenye dash board, alishtushwa na mwanga mkali kama jua la saa saba mchana. Aliangalia katikati ya bahari palipokuwa kunatoka mwanga ule. Alituliza macho baada ya kumuona mwanamke aliyekuwa amevaa gauni jeupe lilikuwa liking’aa kutokana na mapambo yake.
Hali ile ilimfanya asahau yalitomtokea muda mfupi na kutuliza macho kumuangalia yule mwanamke aliyekuwa akitembea juu ya maji huku nyuma akisindikizwa na wasichana walikuwa wamebeba vikapu vidogo vilivyokuwa na maua ambayo walimwagia kila hatua ilivyopigwa huku wakiimba nyimbo nzuri.
Suzana alijikuta akipata ujasiri wa ajabu kwa kufungua dirisha kidogo ili aweze kusikia watu wale walikuwa wakiimba kitu gani. Zilikuwa sauti nzuri kama za kaswida zilizoibwa kwa lugha ya kiarabu. Nyimbo zile zilimvutia na kujikuta akiwa na hamu ya kuwaona watu wale waliokuwa wakitembea juu ya maji huku kwa mstari mbele akitangulia yule mwanamke ambaye usoni kwake kulikuwa kunawaka kama taa na kushindwa kuiona sura yake vizuri.
Suzana alijikuta akisahau kama wale watu walikuwa wakitembea juu ya maji zaidi ya kushangazwa na sherehe ile ambayo toka azaliwe hajawahi kuona sherehe ya aina ile ya mtu mmoja kutangulia mbele wengine kumfuata nyuma huku wakimuwagia maua na kumwimbia nyimbo nzuri.
Baada ya muda watu wote walikaa mstari mmoja, kisha yule mwanamke aliyekuwa amepeneza kuliko wote alipita katikati yao na kupigiwa vilegele huku akitupiwa maua. Manukato ya maua yalisambaa mpaka ndani ya gari la Suzana alilokuwa amefungua kioo kidogo kusikia nyimbo alizokuwa anaimbiwa yule mwanamke ambaye alionekana kama bibi harusi lakini muda wote hakumuona bwana harusi wala mwanaume kwenye kundi lile.
Yule mwanamke alipita kwenye mstari mpaka mwisho alitembea peke yake bila kufuatwa na mtu kisha aligeuka na kuwapungia mkono wenzake ambao nao walimpungia huku wakimrushia maua. Baada ya kutembea kidogo Suzana alimshuhudia yule mwanamke alikunja gauni lake usawa na kifua na kushangaa kumuona akitembea ndani ya maji yaliyokuwa yamemfika tumboni.
Suzana alijikuta akishtuka na kujiuliza yupo ndotoni au anaona kweli, kilichomshangaza ni umbali aliotoka yule mwanamke akitembea juu ya maji. Lakini cha kushangaza alipokaribia ufukweni alionekana yupo ndani ya maji yaliyomfikia tumboni.
Aliendelea kumtazama amuone anakwenda wapi, yule mwanamke baada ya kutoka ndani ya maji alitembea juu ya mchanga kulifuata lile gari. Kila hatua ilivyokuwa akipiga ilizidi kumtisha Suzana, alijikuta akimshangaa kutaka kuijua sura yake. Alituliza macho yake kwenye uso wa yule mwanamke aliyekuwa akiisogelea gari huku manukato makali yakizidi kujaa ndani ya gari.
Kilichomshangaza zaidi ni sura ya yule mwanamke alikuwa akifanana naye kwa kila kitu umbile na sura. Suzana alishtuka na kufunga kioo haraka ili mtu yule ambaye yeye alimuona wa muujiza asiingie kwenye gari. Yule mwanamke alisogea kwenye gari na kuligusa, ajabu baada ya kuligusa lile gari alitoweka ghafla.
Suzana akiwa anatetemeka alijaribu kuwasha gari kwa mara nyingine, ajabu ya Mungu gari liliwaka aliondoka eneo lile kwa mwendo wa kasi. Alipofika nyumbani kulikuwa kumekucha, alikwenda kuoga haraka ili awahi kanisani kwani muda ulikuwa umekwenda.
Baada ya kuoga alirudi ndani, lakini alishtushwa na harufu ya manukato ambayo aliyasikia muda mfupi darajani gari lake lilipozima na kuenea hadi ndani ya gari lake. Hakutaka kulifikiria sana lile kwa muda ulikuwa umekwenda, alikwenda kwenye kabati kubadili nguo ili awahi kanisani.
Baada ya kumaliza kubadili nguo alijikuta akiingiwa na uvivu na kwenda kukaa kwenye kitanda haikupita muda. Usingizi mzito ulimshika na kulala bila kujielewa, aliposhtuka usingizini alishtuka kuiona familia yake yote imesimama mbele yake. Alijiuliza kuna nini, alipojiangalia alijiona alikuwa amevaa nguo za kuendea kanisani.
“Suzana upo sawa?” Mama yake alimuuliza. “Mbona unaniuliza hivyo? Halafu mbona kama wote mlikuwa mnalia kuna nini mbona mnanitisha?
Nini kimemtokea Suzana mpaka familia yake ikusanyike mbele yake huku wakitokwa na machozi.
Simulizi : Chaguo Langu Ni Wewe Sehemu Ya Pili (2)
Siku hiyo alifika mapema tofauti na waatoto wengine,kwa vile kulikuwa na watoto wachache waliokuwa wakianza kucheza michezo yao uwanjani hapo Jongo aliona heri ajitafutie sehemu aketi na kumsubili rafiki yake Shamsa.Muda wote Jongo alipokuwa amefika hapo akiwa amekaa pale chini ya mwembe yake yakivuta hisia huku na huko labda atamuona rafikiye lakini haikuwa hivyo Shamsa hakuonekana. Licha ya watoto wengi kuanza kujazana katikati ya uwanja huo mkubwa lakini hakuonekana mpaka baadae Jongo akiwa amejiinamia huku akiwa mwenye masikitiko kutokumuona yule rafiki aliyemchangamsha siku iliyopita. Jongo akiwa amejawa na udhuni juu ya kutokumuona rafikiye aliyemtegemea kukutana nae tena siku hiyo.Ghafla alistuka aliposikia kitu kikimtambaa shingoni mwake haraka alijipangusa kwa kutumia mkono wake,wakati akijiweka sawa alihisi tena kama kuna mtu nyuma yake,haraka Jongo alizungusha fimbo yake na kuelekeza kule alipohisi kitu kikimfuata.Alirejesha tena fimbo yake,zikapita kama dakika moja alisikia tena kitu kikimtambaa shingoni mwake haraka Jongo aliruka huku akigeukia kwa nyuma na kuipeleka fimbo yake safari hii akiwa wima amesimama. “Aisee! muoga sana wewe?” “Alla! Kumbe ni wewe shamsa?”Jongo alihamaki baada ya kusikia sauti ya shamsa “Yes, ni mimi Shamsa Samir “Shamsa alimjibu huku akiangua kicheko kilichomuacha hio Jongo “Kwanini unanitisha sasa?”Jongo aliuliza kwa hamaki “Nilitaka nijue kitu kutoka kwako” Shamsa alijibu huku akicheka “Kitu gani Shamsa”Jongo alimmtupia swali linguine “Kama una hisia….na sasa nimefahamu hilo” “Na sasa umefahamu lipi kwa utafiti wako?” “Kweli unazo hisia tena nzito sana yaani kabla sijakugusa umeshajua kama kuna mtu aliyekuwa akikufuata?” ”Ndio hivyo lazima nifahamu ilo kama wewe unavyomuona mtu wa karibu yako aliyekuwa mwema na mmbaya nami nAweza kulifahamu hilo”Jongo alimjibu “Aisee! upo vema sana “ “Yaani hata wewe ukae mbali yangu lakini nikisikia sauti yako tu nishakufahamu kama ni wewe”Jongo alimwambia “Ni vema ukiwa hivyo ili kupambana na maadui pindi wanapotaka kukudhuru” CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Siku hiyo Shamsa alipokuwa akija uwanjani hapo aliwakuta mwenzake wameshafika na kuendelea kucheza michezo yao wale wenye kamba waliruka, wenye mpira walicheza ili mladi kujiridhisha roho zao kama tabia za watoto zilivyo. Kwamba mbali alimuona Jongo ameshafika na kuketi pale chini ya mwembe,kama kawaida aliwapa mpira watoto wengine naye alikwenda kule alipokuwa amekaa Jongo.Alipofika hapo hakutaka kuwa na haraka,alijifikilia na kuamua kumtega Jongo,Hakutaka kukaa karibu na Jongo ila alitaka kumstua.Shamsa alipofika hapo alizunguka huku akinyata mpaka nyuma ya mwembe huo ambapo Jongo alikuwa ameegemea,haraka Shamsa akaokota jani la mwembe huo lililokuwa limedondoka jirani yake na kulishika mwanzo wa jani hilo na kulipeleka nyuma ya shingo ya Jongo.Kwa vile Shamsa alitumia ncha ya jani hilo kulipitisha shingoni mwake, Jongo alistuka ghafla na kujipangusa kisha akatulia.Shamsa alipoona Jongo akiendelea na mambo mengine alimlipitisha tena jani hilo safari hii kwa nguvu kidogo kisha alikimbia haraka mpande wa pili ndio Jongo alipoona kitu kisicho cha kawaida hakanyanyuka na kugeuka nyuma haraka huku fimbo yake mkononi ikipapasa huku na huko.Haraka Shamsa alianza kucheka na kujitokeza mbele yake,Jongo alinywea baada ya kusikia sauti ya Shamsa,hakuwa na budi akaamua kuketi tena chini ya mwembe huo huku akiwa amefedheheka kinamna.Siku hiyo waliongea mambo mengi wakafahamiana na kutambua kuwa ni wenyeji wa mikoa tofauti huku Shamsa akiwa ni mzigua kutoka Tanga huku Jongo akijitambulisha kuwa ni mzaliwa Morogoro kabila lake likiwa mluguru.Shamsa alimwambia Jongo siku hiyo alionekana kufika mapema tofauti na siku zote alizokuwa akiwai kufika.Jongo hakumjibu upesi kutokana na kujisia aibu Fulani hivi,ila Shamsa alijua yote hayo kwa sababu yake yeye ndio maana alionekana Jongo kuchangamka tofauti na siku zote. “Unaoneka siku hizi mwenye furaha ya wazi sijui kwanini”Shamsa alimuuliza baada ya kumuona Jongo akiwa kimya akitabasamu “Kwa sababu yako, Shamsa wewe ni rafiki mwema kwangu”Jongo alimwambia “Nashukuru kama kwa ajiri yangu kukufurahisha” “Shukurani zije kwako rafiki mwema”Jongo alimwambia “Nami nazipeleka kwa mungu muumba ashukuliwe” “Aminii” “Hivi uliniambia unasoma shule gani vile?”Shamsa alimuuliza “Majengo….ni hapo tu jilani na mnala wa voda “Hivi unasomaje hapo nawe uoni kwani kuna walemavu?”Shamsa aliuliza maana hakuwa akijua kama shule hiyo walemavu wapo pia “Kuna mwalimu wetu anaitwa Uweso yeye uja kila siku kutufundisha sisi walemavu wa uwoni” “Aisee! Kumbe shule hiyo ina walemavu? “Ndio Shamsa ila tupo wawili tu mimi na mwenzangu, tunatumia mashine za brela kusomea”Jongo alimfafanulia “Hongera sana, unasoma darasa la ngapi” “Darasa la tano sasa sijui wewe unasoma darasa la ngapi? “Mwaka huu naingi darasa la nne katika shule hiyo hiyo ya majengo” “Karibu sana rafiki mwema Shamsa”Jongo alimkaribisha “Nashukuru sana rafiki yangu….tupo pamoja” Shamsa na Jongo waliongea mambo mengi wakiwa wamekaa peke yao mwembeni hapo, wakasahau michezo iliyowaleta pale ,siku hiyo ilikuwa kwa mazungumzo tu sijui walipanga hama hawakutarajia.Shamsa alisahau kabisa kucheza na wenzake hata hivyo hawakuwa na mda nae wao waliendelea kucheza na kuruka ruka kama kawaida yao hawakumjali Shamsa wala Jongo.Muda uliwadia saa kumi na mbili iligonga kwa adhana kusikika msikiti wa jilani na uwanja huo kuwa taarifu wakazi wa maeneo hayo wajongee masjid kumsujudia mtume.Watoto waliopo pale uwanjani wana kawaida yao,adhana ikisikika wanajua moja kwa moja muda umefika kurejea majumbani mwao na ndivyo ilivyotokea watoto walianza kutawanyika na kurejea majumbani mwao.Shamsa na Jongo nao waliagana huku Shamsa akimshika mkono Jongo na kumuongoza njia kisha walipofika mbele kutokea njia nyingine iliyompeleka Shamsa nyumbani kwao waliagana hapo na Jongo aliongoza njia inayoelekea nyumbani kwao huku akiwa mtu mwenye furaha isiyoelezeka. ********** “Shkamoo baba”Shamsa alimsabahi baba yake baada ya kufika nyumbani “Marhabaha…ujambo binti yangu?” “Sijambo baba”Shamsa alijibu huku akikaa kwenye sofa karibu na baba yake “Wewee….ala! Nenda kakoge kwanza, angalia miguu yako ilivyokuchafuka”Mama yake alimsema “Jamani mama naenda, ila nilikuwa namsalimia baba kwanza”Shamsa alisema huku akinyanyuka “Jamani nini kwani mwenyewe ujioni miguu ilivyo umechafuka vilivyo” “Sawa…..mama lakini hata sio michafu”Shamsa aliongea wakati akielekea mlango wa kutokea uwani mwa nyumba hiyo. “Na ujisugue vizuri maana wewe”Mama yake alimwambia huku akimsindikiza na macho yake.
Shamsa alioga na kujisafisha vizuri bafuni mle kisha alitoka na kuingia ndani ya chumba chake.Baada ya dakika tano Shamsa alitoka akiwa amevalia upande wa kanga na blauzi ya mikono mirefu. Akiwa ameketi sofani pale alipokuwa amekaa kwa mara ya kwanza alimsogelea baba yake na kuanza kuzungumza nae kile kilichokuwa moyoni mwake.Maana baba kwa mtoto ni tablet iliyoshindiliwa na msumali mirefu yenye king’ang’anizi.Wakati Shamsa akitaka kuzungumza na baba yake,mama yake alikuwa makini akimsikiliza na kumshangaa kitu gani alichokuwa akitaka kumwambia na kumzonga baba yake usiku huo.Wakati Shamsa akianza kuongea kwa mkato mkato lakini mama yake alielewa kitu ambacho mtoto wake alitaka kuzungumza.Bi.Ramla alimtupia jicho kali sana mtoto wake alihisi utoto ndio uliokuwa ukimsumbua mpaka kufikia kumwambia baba yake juu ya huko anapokwenda kucheza.Kwanza mama yake alijua maongezi ya mtoto wake yatahusu juu ya masomo na shule aendayo,lakini haikuwa hivyo yeye alithamini sana mchezo kuliko masomo.Licha ya uzembe wake juu ya masomo lakini alikuwa na uelewa mkubwa sana kwenye masomo yake,alikuwa akishika nafasi ya pili darasani.Ndio maana wazazi wake walikuwa wakimuacha acheze anavyotaka lakini darasani hawakutaka ashuke kimasomo zaidi ya kupanda mpaka siku nyingine alifikia nafasi ya kwanza darasani……CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kipindi hicho Shamsa alizungumza na Baba yake alimuuitikia tu huku akizungusha kichwa lakini hakuwa na uelewa anachozungumza mtoto wake, aliona alichokuwa akizungumza kilikuwa hakina maana yoyote kwake.Shamsa alimwambia ya kwamba “Baba nimeenda kucheza na kupata mchumba, anampenda hadi mama” mwanamke au mwanaume huyo rafiki yako?” Bwana Samir alimuuliza mtoto wake, Mwanaume baba tena anatembelea fimbo” Shamsa alisema. “ Bwana Samir akapiga moyo konde na kupotezea kwa kauli ya mtoto wake,hakutaka kumuuliza chochote mkewe akaona Shamsa alikuwa bado mtoto sana mwenye umri wa miaka kumi alafu leo apate mchumba huko wanapocheza ni maajabu haya.Aliendelea na kazi zake huku akiendelea kumuitikia mtoto wake kwa kuzungusha kichwa.Alipoona Shamsa amemzunguka sana huku akiwa afanyi kazi zake kwa amani akaamua kunyanyuka na kuingia zake ndani huku akimuacha mke na mtoto wake wakimshangaa.Bi.Ramla alimwangalia mtoto wake kwa jicho la unaona sasa, Shamsa alishangaa sana pale alipomuona mama yake akimwangalia,bila kupepesa mara moja akajua kauli aliyoitoa itakuwa imemtatiza sana baba yake na alimwangalia mama yake na kumsogelea karibu kisha akamwambia. “Mama Rafiki mwenyewe wa kiume ambaye ni mlemavu wa uoni anayeitwa Jongo, pia naye ni mwenyeji wa mkoa huu sasa anasoma katika shule ambayo kesho mimi nakwenda kuanza”Shamsa alimwambia mama yake baada ya kumuona akiwa amefura “Lakini mwanangu kwanini ukuniambia tangu mwanzo mpaka uje kusema mbele ya baba yako? “Hapana mama naona yote ni kheri juzi tu ndio nimejuana nae ni rafiki tu wakawaida” “Sawa sasa ni rafiki ulivyosema ni mchumba,ujui kama umemuuzi baba yako?” “Hapana mama nimetania tu niwasikie wazazi wangu mtasema nini”’ “Umefanya makosa sasa unaona mpaka baba yako amekasilika” “Sio mchumba wangu kweli mama natania”Shamsa alijitetea “Sasa tutafanya nini ili baba yako harudi kwenye hari ya kawaida” “Mwambie anisamehe mama sina mchumba mie”Shamsa alimwambia mama yake “Usirudie tena kulopoka lopoka tu”mama yake alimkanya “Sawa mama nimekuelewa”Shamsa alishukuru na kuelekea chumbani mwake huku mama yake akinyanyuka na kuingia chumbani. ************ Angali Shamsa akiendelea kuwaza,usiku ulizidi kukoma mbu nao waliendelea kumtafuna kwa furaha.Angani kulikuwa baridi na upepo uliojaa ulikuwa ukivuma.Alizidi kujikunyata kwenye kitanda maridhawa akijikinga dhidi ya upepo wa baridi uliokuwa ukimiminika kimyakimya.Macho yake hayakuweza kuona mbali na pale alipokuwa amejistiri kutokana na kiza kushida uoni wa mboni zake.Hakujua siku iliyofuata atakwenda na nani shuleni hapo,alitamani usiku ukuche kuwai kuamka na kwenda shuleni ili kukutana na rafiki yake Jongo.Shamsa aliwaza mambo mengi kutokana na kuelewa jinsi ya kufika shuleni hapo alijua moja kwa maoja shule atakayokwenda kusoma ndiyo atakayokuwa anafundisha mama yake.Usiku ulikuwa umekwenda Shamsa akiwa bado kitandani mawazo mengi kichwa na usingizi ukamchukua akalala fofofo mpaka asubuhi.Shamsa aliamshwa na mama yake akaamka na kujiandaa kwa ajili ya kuwai shuleni.Ilipofikia saa mbili asubuhi yeye na mama yake wakatoka nyumbani na kulekea shuleni,muda wote Shamsa alikuwa mtu mwenye furaha moja kwa moja mawazo yake yalienda na kuzama juu ya kijana Jongo alimfikiria sana Jongo na sasa akajua lazima anakwenda kuonana na Jongo shuleni hapo.
Baada ya mwendo wa nusu saa walifika waliona mbele yao kukiwa na kibao cha msingi kilichoandikwa Manispaa ya Nyegenzi Shule ya msingi Nyakabungo mkoani mwanza.Shamsa alijua sasa shule anayotakiwa kusoma ndio hiyo na sasa anakwenda kuanza.Bi.Ramla alikwenda moja kwa moja mpaka ofisi ya mwalimu mkuu akiwa na Shamsa pembeni yake,alipoingia tu mle ndani Bi.Ramla alianza kumsalimia mwalimu mkuu ambaye ni mwanamama wa makamo na kisha kumpatia kitambulisho pamoja na makalatasi ambacho yanadhibitisha anatakiwa kufundisha katika shule hiyo.Pia Ramla alitoa kalatasi kadhaa toka ndani ya mkoba wake na kumkabidhi Mkuu huyo,akazipitia kisha akainuka na kumtaka Bi.Ramla amfuate.Waliongozana mpaka sehemu ya chumba kimoja kilicho kati ya jengo hilo mwanamke huyo alifungua mlango kwa funguo aliyokuja nayo tokea kule ofisini.Mlango ukafunguka nao wakazama ndani,muda wote Bi.Ramla alikuwa amemshikilia mwanae aliyeonekana kuwa na shauku kubwa ya kutaka kuingia darasani. “Mama Ramla…mtoto jina lake nani?”Mama huyo alimgutusha Ramla macho yake yakiwa juu ya meza kubwa uliyokuwepo ofisini humo. “Anaitwa Shamsa Samir Nassoro”Bi.Ramla alijibu “Anasoma darasa la ngapi”Aliendelea kumuuliza mwanamke huyo huku akiangalia kalatasi yenye maelezo kwa hiyo “Darasa la nne” Bi.Ramla alijibu “Fomu pamoja na maelezo yake nimeyaona na kuyapitia sasa mimi na wewe tunaelekea ofisi ya waalimu kisha nitampeleka Shamsa darasani” “Haina tatizo nashukuru sana”Bi.Ramla alimwambia “Usijali tupo pamoja na karibu sana” Bi.Ramla aliongea na mwalimu huyo kisha akampeleka upande wa pili wa jingo hilo ambapo ndipo ilipokuwa ofisi ya waalimu wote, Bi.Ramla akatambulishwa na mwanae akapelekwa darasani ambapo alishangaa pale alipowakuta watoto wengi ndio wale aliokuwa akicheza nao pamoja kule uwanjani Laah! Alishangaa na furaha angali mdomoni,ila hakumuona rafiki yake wa ubani Jongo.Shamsa aliudhunika sana moyoni mwake ila alijiapiza na kujipa moyo na kusubili mpaka muda wa kurejea nyumbani utakapowadia aende kumuuliza hapo ndipo atakapolipata jibu kama anasomea shuleni hapo au nyingine. *******CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Shamsa na Jongo waliwahi kufika sana kuliko watoto wenzao waliokuwa wanacheza katika uwanja huo.Wao walikua wanacheza kwa furaha na kuongea huku wakigongana mikono ikawa ni desturi ya wawili hao kupenda kuongea peke yao uwanjani hapo.Siku zilikatika kwa mazoea yao kushamili,furaha na buraha ilitawala na kuchanua kwenye nyuso zao,walishikana na kuzunguka pamoja kama makinda wawili. Siku moja Shamsa alifika lakini Jongo hakufika alijipa subira na kusubili kwa muda lakini Jongo hakutokea siku hiyo Shamsa alikuwa mpole kila wakati wenzake walimwambia wacheze pamoja lakini yeye akujali nafuu yake ilikuwa Jongo.Hakuweza kula wala kulala sababu ya Jongo, hakusoma wala kuandika kisa hakumtia machoni Jongo looh! Shamsa siku mbili tu alikuwa amepungua mwili wake sababu ya Jongo.Wenzake walijitahidi kumchangamsha ili kuondokana na mawazo ya Jongo lakini ilishindikana Shamsa akaona maneno mengi kwa wenzake akaamua kuondoka uwanjani hapo na kurejea nyumbani.
Siku iliyofuata Shamsa alikwenda shuleni kama kawaidi aliingia kila darasa kumtafuta Jongo lakini hakumuona aliambulia patupu ata alipojaribu kuwauliza wanafunzi wa darasa hilo aliambiwa kuwa Jongo anasoma katika shule hiyo ila yafikia siku mbili Jongo hakuonekana shuleni na wengine hawakupajua nyumbani kwao.Muda wa kurejea nyumbani uliwadia,wanafunzi wote walirejea majumbani mwao,Shamsa aliangaza huku na uko labda atamuona lakini wapi mawazo yalimdanganya.Muda wa kucheza ulipowadia Shamsa alifika mategemeo yake yakiwa kuonana na Jongo sasa yaliyeyuka pia siku hiyo Jongo hakutokea tena upweke ulimtawala alikaa peke yake chini ya mwembe huo akimfikiria Jongo.Shamsa hakutumia muda mwingi kukaa maeneo hayo aliondoka na kurudi nyumbani kwao,Bwana Samir na mkewe walimuona mtoto wao akiwa kwenye hali hiyo waliamua kumuuliza kulikoni mtoto kuwa katika hali hiyo, Shamsa hakusema kitu chochote wala akujibu alipitiliza mpaka chumbani kwake na kujitupa kitandani.Bi. Ramla hakujua kitu gani kimempata mtoto wake,alimfuata mpaka ndani na alipomuuliza kama anaumwa,alijibu hakuwa mgonjwa na mama yake alizidi kumdadisi ili kujua kitu gani kimempata mwishowe Shamsa akamdanganya mama yake kuwa amepigana na rafiki yake aliyekuwa wakigombea mpira.Bi.Ramla alicheka kisha akamtaka mwanae kuwa na amani,Shamsa hakumwambia ukweli juu ya hali aliyokuwa nayo kumkosa kijana Jongo.
Siku nyingine tena Shamsa alikwenda kucheza ila hakumwona Jongo akamua kuwauliza wenzake kama kuna anayepajua nyumbani anapokaa Jongo.Watoto wengi waliokuwepo uwanjani hapo walimshangaa baada ya kumsikia msichana kama Shamsa akimuulizia kijana Kipofu.Yalikuwa ni maajabu kwao kwani kutokuwepo Jongo kwa siku tatu uwanjani hapo watoto wale waliona nafuu kwao,hawakupenda kabisa uwepo wa Jongo uwanjani hapo walimuona binadamu aliye na kasoro.Kijana mmoja aliyekuwa akikaa karibu na nyumbani kwa kina Jongo akamuelekeza ilipo nyumba ya mama Jongo,kwa uwelewa wake haraka alitambua njia ya kumfikisha katika nyumba aliyoelekezwa ndipo nyumbani kwa kina Jongo.Shamsa hakutaka kuchelewa aliongoza njia na kuifuata barabara na kisha kukata kulia,kama alivyokuwa ameelezwa.Njia nzima Shamsa alimuwaza Jongo,hakujua huko anapokwenda kama atafanikiwa kumuona au atakuwa amedanganywa nyumba na vijana wale wasiompenda Jongo,aliwaza yote hayo kichwani mwake. Kwavile hapakuwa mbali na pale uwanjani, dakika sita tu alifika mbele ya nyumba aliyokuwa imepakwa rangi ya kahawia, Moja kwa moja Shamsa alitambua nyumba hiyo ndio alipoelezwa ndipo anaipokaa Jongo.Alisogea mpaka karibu na mlango wa kuingilia ndani ya nyumba hiyo, yenye baraza ndogo, akiwa pale kibarazani ili kubisha hodi, kabla mkono wake uliokuwa amekunja vidole vyake ili kutaka kugonga. Ghafla mlango huo ukafunguliwa na kukutana uso kwa uso na Mama wa makamo akiwa anatoka ndani, Shamsa hakumjua ni nani aliyekuwa mlangoni, akiwa akitetemeka moyo wake ukienda kasi akamsalimia. “Shkamoo…..mama”Shamsa alisalimia “Marhabaha ujambo mtoto mzuri”Mama Jongo alimjibu “Jongo yupo?”Shamsa aliuliza “Mmmh! Hee yupo, vipi kwani?”
Shamsa hakumjibu alichofanya yeye ni kumhulizia Jongo kama amemkuta au kama anakaa nyumbani hapo, Mama yule alishangaa kwani ahikuwai kutokea hata siku moja awe mtoto au mkubwa kuja kumulizia mwanae. Mama Jongo akamjibu “Ndio yupo ila anaumwa” Shamsa alifurahi kusikia majibu hayo kutoka kinywa mwa mama huyo,aliongea tena haraka “Samahani mama naweza kumuona” Mama Jongo akamkaribisha ndani na macho yake yakimwangalia mtoto huyo’’Shamsa alipita ukumbini moja kwa moja mpaka sebuleni alimuona Jongo amelala kwenye kochi moja la watu wawili lililokuwepo pale sebuleni.Alienda moja kwa moja huku macho yake makali yakitua pale alipolala Jongo,Shamsa kwa huruma alijua Jongo anaumwa sana alimkalibia na kisha akamuhita “Jongo…!” japo alikuwa anaumwa lakini Jongo hakuweza kuisahau sauti ya Shamsa haraka aliitika kwa kumwita jina “Shamsa…!”Shamsa aliitika “Yes Jongo” Jongo alihoji “Umewezaje kufika nyumbani?”Shamsa alimjibu nimeona kimya nikaamua kukuulizia kwenu ndio maana nipo hapa’’Shamsa alifurahi sana muda wote ule mama Jongo alikuwa pembeni anawaangalia wawilia hao wakiongea kwa furaha…..
Muda wote Shamsa na Jongo walikuwa sebuleni wakiongea hili na lile,baadae mama Jongo alimtaka anyanyuke ili anywe uji.Jongo aliposikia sauti ya mama yake alimuitikia na kumtaka mama yake amtambulishe kwa rafiki yake.Kweli muda si muda Jongo akaanza kumtambulisha Mama yake kwa Shamsa wote walifurahi kwa pamoja wakapeana mikono kwa bashasha na Shamsa alimsaidia Jongo kunyanyuka na kukaa vizuri kwenye kochi ili anywe uji.Mama Jongo alikuja na kikombe cha uji alipotaka kumnywesha Jongo ,Shamsa aliomba apewe yeye kikombe cha uji na kumnywesha Jongo,Mama Jongo alimwangalia na kisha akamuuliza kama ataweza kumnywesha mtoto mwenzake.Shamsa alimuhakikishia ataweza ndio Shamsa alichukua kikombe kutoka mikononi mwa Mama Jongo na kumnywesha Jongo.Jongo alikunywa uji kwa amani akijua aliyekuwa akinywesha alikuwa Shamsa mpaka alipomaliza alirudisha Kikombe kwa Mama Jongo na kuendelea kucheza nae kuongea nae mpaka muda wa yeye kurudi nyumbani aliaga na kumuahidi Jongo atakuja tena kesho yake. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Kesho yake alifika alikwenda shuleni kama kawaida walikutana huko huko, kila wakati na muda wa mapumziko Shamsa ahisikiapo kengere ukimbilia darasa anaposoma Jongo na Mariamu ambao wote ni walemavu. Shamsa akiingiapo darasani humo umkuta Mariamu na Jongo wakiwa wamesogeleana wakisoma pamoja anakeleka sana,ikafikia kipindi akawa anamchukia Miriamu,Jongo alielewa kutokea kwa hali hiyo lakini hakuwa na jinsi.Kila siku Shamsa hakuchoka kuwa karibu na Jongo wakawa wanaongea na kucheza mpaka Siku alipopata nafuu Jongo walifika uwanjani kwa watoto wenzao wanapokuwa wakicheza kila siku.Walikuwa pamoja mpaka walipomaliza shule, Jongo alichaguliwa kusoma Shule ya watoto walemavu sababu ya ulemavu wake wa huoni na Shamsa alisoma kwingine tofauti na Jongo.Waliendelea na masomo huku wakiwasiliana na kukutana kwa ajiri ya masomo yao kila siku mpaka wakafikia kidato cha pili na kuufanya mtihani wao kwa mafanikio makubwa na kufanikiwa kuingia kidato cha tatu.Shamsa alikuwa msichana aliyepevuka kiakili na kimwili hata Jongo nae alikuwa mvulana sharobalo mwenye umbo matata linaloweza kumchanganya mwanamke yoyote atakaye bahatika kumtiha machoni mwake.Kutokana na ukaribu uliozoeleka kutoka kwa wawili hao hali ilikuwa tete kwa Shamsa juu ya Jongo,alikuwa amezimika kimahaba,alimpenda sana Jongo toka ndani ya moyo wake,kila siku zilinavyozidi kwenda ndivyo Shamsa alivyozidi kumpenda Jongo ila hakudhubutu kuufungua mdomo wake na kumwambia kwani hisia zake alizionesha wazi juu ya kijana Jongo mwenye ulemavu wa macho. “Hee! Jamani hee msibomoe nyumba zetu bora mtulipe kwanza”ilikuwa sauti ya mama Jongo “Kulipwa mtalipwa ila mnapewa utaratibu jinsi ya kukabiliana na bomoa bomoa itakayoanza hivi karibuni”Mwenye kitu aliwaambia wananchi hao waliokuwa ofisini hapo “Siliza mwenye kiti…sisi wengine hatuna nyumba za kukaa zaidi ya hapo unapopaona sasa unafikiri mkitoa hapo mtatupeleka wapi na kutulipa hamtaki” “Kweli kabisa wananchi tunaonewa sana ardhi ni zetu wenyewe alafu serikali inaingilia kati na kututaka tuondoke sasa tutakwenda wapi? Mwengine alidakia “Mie siondoki mpaka niwaone waje kubomoa” “Kweli kabisa jirani heti tupo barabarani…watu wenyewe hawaitengenezi hiyo barabara yenyewe miaka yote ipo vile vile wanatuonea tu hawa”
Wananchi walilalamika serikali kuwataka wazibomoe nyumba zao zilizokuwa kandokando ya barabara kwani barabara hiyo ilitakiwa kupanuliwa na kuongezwa ukubwa.Mama yake Jongo naye alikuwepo, akililia haki yake ya kulipwa ndipo aondoke ndani ya nyumba hiyo.Hakuwa peke yake walikuwa watu wengi sana nyumba zao zilikuwa zimepigwa herufi ya X kwa sababu ya kuwa zimejengwa barabarani. Aiku hiyo waliambiwa kitakapokuja kijiko cha kubomoa wasilalamike kwa ajiri ya kazi hiyo.Siku zilizidi kwenda Mama Jongo aliendelea kufuatilia pesa yake na akafikia muda maalumu wakalipwa pesa zao ili waondoke ndani ya nyumba hiyo.Mama Jongo alikuwa na wakati mgumu sana hakujua ataenda wapi kwa wakati huo alikaa na kufikiria aliamua kutafuta kiwanja au kununua kabisa nyumba maeneo ya nyumbani kwao alipotokea Morogoro.Baada ya siku mbili tatu aliwaulizia ndugu zake wanaoka Morogoro kufanikiwa kupata nyumba kubwa kwa kiasi cha milioni kumi na mbili. Hakutaka kupoteza muda alipopata taarifa ya kwamba amefanikiwa kupata nyumba hivyo alihama kimakazi na kuamia mkoani morogoro akiwa na mtoto wake Jongo.Huo ndio ulikuwa Mwisho wa kuonana kwa wawili hao, Shamsa na Jongo wenyewe walikutana kabla ya kuagana na kuhaidiana kukutana tena kama mungu akijaalia.Shamsa alilia sana kila wakati alimfikilia sana Jongo alijilaumu kwa nini hakumwambia dhamira yake kwani alimpenda sana Jongo na sasa ameondoka huku atakuwa na kwa wasichana wengine. ******** Siku ya siku iliwadia ya Mama Jongo kuondoka, ndugu na majirani walisaidiana kupakia vyombo kwenye gari.Ilikuwa siku ya majonzi makubwa kwa Shamsa na Jongo, hakuna aliyejua ukweli kilichowaliza watoto wao.Shamsa alimlilia Jongo alijua huo ndio ulikuwa mwisho wao kuonana, watu wengi waliwabembeleza na kuwatuliza lakini Shamsa wala hakuwasikiliza alimsihi Jongo hasiondoke.Wakati yote hayo yakiendelea Mama yake Shamsa alizipata taarifa kutoka kwa majira zake wakimtaka aende kumwangalia mtoto wake jinsi anavyo mlilia Jongo.Mama yake alishangaa haraka alitoka na kuelekea huko alipoelekezwa ndipo mwanae alipokuwa.Bi.Ramla alienda huku kichwani mwake akiwa na mawazo kibao kuhusu yale aliyoambiwa na majirani kuhusu mtoto wake Shamsa,alipofika hapo alishangaa akiwa mbele ya nyumba moja kati ya nyumba zilizopo katikati ya mtaa wao. “Shamsa ….mwanangu vipi tena?” Bi.Ramla alibwabwaja huku akimfuata mwanae kule aliko “Mama Jongo…mama anaondoka”Shamsa alianza kulia upya “Hee! Mwanangu nyamaza basi nasi tutaondoka mbona unalia kama mtoto” “Jongo mama ananiacha”Shamsa alilia kama mtoto “Sasa Binti yangu unacholilia ni kitu cha ajabu sana…embu nyamaza jamani” “Namtaka Jongo Mama ni rafiki yangu wa muda mrefu sana”Shamsa alibwabwaja huku akiendelea kulia “Basi nyamaza twende nyumbani sasa”Mama Shamsa alimshika mkono mwanae na kuanza kumvuta kuelekea nyumbani.
*********** Baada ya Jongo Mama yake kuondoka Shamsa aliendelea kuishi nyumbani kwao na wazazi wake huku akiwa hana raha kama zamani, mama yake alijua hali hiyo kutokana na kuondoka kwa kijana Jongo hila hakuwa na la kufanya juu ya uwamuzi wa mzazi wa Jongo kuondika.Kila siku alilia na kuomboleza juu ya kijana Jongo, hakujua atampata wapi tena kijana anayempanda kana huyo.Arusha ni kubwa hakujua ataanza vipi kusafiri mpaka mkoa huo kumtafuta Jongo ila alijiapia lazima siku moja waonane tena na Jongo.Siku zilizidi kwenda Shamsa alizidi kupungua kimwili huku kiakili akiwa hajakaa sawa.Kila wakati aliweuka na kumkumbuka Jongo kwani alimpenda sana kuliko kitu chochote….. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Siku zinavyozidi kwenda ndivyo hali ya Shamsa alivyozidi kuwa mbaya,Bi.Ramla alishangaa sana ila zaidi baba yake Bwana Samir ndio kabisa maana hakujua kitu gani kilichokuwa kimemsibu mtoto wake mpaka kupatwa na hali ya kukonda na kudhoofika.Kila siku Bwana Samir alikuwa akiketi chini na kumuuliza mtoto wake kitu gani kilichokuwa kikimsababishia kuwa katika hali hiyo,Shamsa hakuweza kumjibu baba yake kwani kila wakati kilio tu, ndio ilikuwa kazi yake pekee.Siku moja Uzalendo ulimshinda Bi.Ramla alipoona hali ya mtoto wake inavyozidi kuwa mbaya alihamua kumueleza ukweli wa jambo mume wake kuhusu Binti yao Shamsa.Bwana Samir alimsikiliza mkewe kwa umakini kisha Samir hakutaka kumuona mtoto wake akipotea katika masomo yake kwani tayari ilifikia wiki nzima bila Shamsa kutokea shuleni kama ilivyo kawaida yake sababu ya uchovu aliokuwa nao juu ya mawazo.
Siku iliyoata Bwana Samir alirudi nyumbani akiwa ameongozana na Mama mmoja wa makamu, Mama huyo alikuwa mnene kidogo mwenye sura pana na macho yake yalikuwa makubwa kama goroli. Muda wote mama huyo alionekana akitabasamu, usoni wake uliwaka kutokana na tabasamu hilo meno yake meupe yote yalionekana.Siku hiyo Bwana Samir alimletea mtoto wake mwana saikolojia baada ya kuafikiana na mkewe nini cha kufanya juu ya hali hiyo.Ndipo walipoamua kumtafuta mwana Saikolojia kuzungumza na mtoto wao ili kumjenga na mtengeneza kiakili na kimwili.Siku hiyo walipofika Bwana Samir na mgeni huyo waliingia moja kwa moja mpaka chumbani kwa Shamsa na kumkuta akiwa amelala usingizi,bila kuchelewa Bwana Samir alimuhamsha na kutaka kuzungumza nae.Shamsa aliamka na kukaa kitandani huku macho yake yakiwa yamekodolea mama huyo aliyekuwa amevaa miwani usoni mwake huku lile tabasamu lake mwanana alilichanua sawia.
“Shamsa binti yangu…nimekuletea Anti hapa anataka kuzungumza nawe” “Sawa baba sijui anataka nini? Shamsa alimtupia swali baba yake “Anataka kukuweka vizuri kisaikolojia binti yangu” “Yes! Shamsa ujambo mdogo wangu?”Dada huyo alimsalimu “Sijambo shkamoo!”Alimsalimia “Marahaba unaendeleaje?”Mama huyo aliuliza “Mmmh….kwani uliambiwa naumwa?” “Hapana sio kwamba unaumwa…” “Kumbe kinachokusumbua nini? Baba yake aliwai kumuuliza “Lakini baba mimi siumwi kitu” “Sasa kwa nini unadhoofika namna hiyo wewe, kitu gani kinachokusumbua sema basi?” “Bwana Samir nimeshakijua kinachomsumbua mtoto wako hivyo niachie mimi nifanye kazi yangu atakuwa anasumbuliwa na saikolojia huyu” “Haa! Baba anataka kunifanya nini? Shamsa alihamaki baada ya kusikia maneno hayo “Usijali binti hakuna kitu kibaya juu yako zaidi ya kuzungumza nawe tu ndio dawa yake” Muda wote Shamsa akiongea na baba yake pamoja na yule mwanasaikolojia Bi.Ramla alikuwa akiwasikiliza kwa umakini huku akitikisa kichwa chake kwa masikitiko makubwa juu ya hali aliyokuwa nayo mtoto wake. Alimuona Bwana Samir akitoka ndani ya chumba hicho na kumuacha Shamsa akiwa na Mama huyo aliyejulikana kwa jina la Janeth. Wakati Bi.Janeth akianza kuzungumza na Shamsa Bwana Samir na mkewe walikuwa chumbani kwao wakizungumza kuhusu hatima ya mtoto wao.Hawakutaka kukaa mahali hapo kutokana na kumchanganya mtoto wao juu ya yale anayoambiwa.Hivyo waliamua kumuacha ndani humo akiwa na mwanasaikolojia huyo.Wakiwa ndani ya chumba hicho wanawake wawili ambao ni Bi.Janeth na Shamsa wakizungumza juu ya hali aliyokuwa nayo na kwa vile Bwana Samir alikuwa amemueleza kila kitu mama huyo juu ya kile kinachomsibu mtoto wake.
Shamsa alikuwa kimya akimwangalia na kumsikiliza yale Bi Janeth aliyokuwa akimwambia kuhusiana na urafiki wake kwa Jongo. Upendo ni neno la kiswahili linalojumlisha idadi kadhaa ya hisia, kuanzia mahaba, pendo hata upendo wa Kimungu.Ni kwamba kitenzi “kupenda” kinaweza kurejea aina za hisia, hali na mitazamo tofautitofauti, kuanzia ridhaa ya jumla ya kitu unachokipenda mfano utamwambia mama yako “napenda chakula hiki”, hapo utakuwa umeshapata hisia juu ya chakula hicho.Mvuto mkali kati ya binadamu ni mapenzi kwa mfano utamsikia mama yako akisema “Nampenda mume wangu”. Umuhimu wa matumizi na maana, pamoja na utata wa hisia zinazohusika, hufanya kuwe na ugumu katika ufafanuzi, hata kulingana na hali nyingine za kihisia uliyonayo juu ya kijana huyo. Ukifikiria unaweza kugundua mapenzi kwa kawaida yanarejea hisia za ndani zisizoelezeka, tena za kudumu kwa mtu mwingine. Hata hivyo, maelezo haya pia yanashirikisha hisia tofauti, kutoka kuwa na urafiki wa kimahaba hadi ukaribu wa kihisia kwa mwanaume kupelekea kutokea kitendo cha mapenzi.Ndio maana wazazi wako wanapenda kuwa karibu nawe ili usiingie katika mkumbo huo, kwani kiingia huko utaaribikiwa zaidi ya hapo ulipofikia.Kuna mapenzi ya aina mbalimbali husimamia mafungamano kati ya akili zako na moyo, kutokana na umuhimu wake mkuu katika saikolojia, ni mojawapo ya maudhui yanayopatikana sana katika kupenda.
Ingawa desturi au chanzo cha mapenzi ni suala ambalo hujadiliwa mara kwa mara, sura tofauti ya neno hili zinaweza kuwekwa wazi kwa kuamua nini si mapenzi.Kama njia ya kawaida ya kuonyesha hisia chanya ni aina kubwa ya kupenda kupitiliza, mapenzi kwa kawaida hugonganishwa na mazoea kupita kiasi.Kama pendo ambalo linaegemea zaidi kwenye uhusiano wa kirafiki kuliko wa kingono, mapenzi kwa kawaida hugonganishwa na tamaa na kama uhusiano kati ya watu, unaohusisha mahaba, pia urafiki wa ukaribu zaidi, ingawa neno mapenzi linaweza kutumika pia kwa urafiki wa karibu katika njia fulani fulani lakini usiwe wa kupitiliza.Wakati yanapojadiliwa kidhahania, mapenzi kwa kawaida yanarejelea pendo kati ya watu, hisia alizonazo mtu kuhusu mtu mwingine. Mapenzi mara nyingi yanahusisha kutunza au kujiainisha na mtu au kitu, ikiwa ni pamoja na nafsi ya mtu.Aidha, katika tofauti za kiutamaduni katika kuelewa mapenzi, mawazo kuhusu upendo pia yamebadilika sana kadiri ya wakati.
Baadhi ya wanahistoria wanahusisha dhana za kisasa za mapenzi ya kimahaba na Ulaya wakati au baada ya Karne za Kati, ingawa kuwepo kwa mahusiano ya kimahaba kabla ya wakati huo kunaonyeshwa na ushairi wa kimapenzi wa kale na sio ya sasa utaaribika binti. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Kutokana na utata wa dhahania ya mapenzi, mjadala juu ya mapenzi kwa kawaida hupunguzwa hadi maneno yaliyopitwa na wakati, na kuna mithali kadhaa kuhusu mapenzi, mojawapo ikiwa ile ya watoto wadogo. Pendo hushinda mambo yote ambapo mhusika anakuwa hawezi kufanya kitu zaidi ya kuwa na msongo wa mawazo kama ulivyo wewe, hivyo basi unatakiwa uhachane na mawazo hayo uende shule ukasome na sio kumuwaza mtu ambaye ujui alipotokea.Mapenzi kati ya watu wawili ni hisia za nguvu kuliko kumpenda mwingine kwa jumla. Mapenzi yasiyotuzwa ni hisia za mapenzi ambazo haziwezi kulipwa au kurudishwa. Mapenzi kama haya yanaweza kuwepo kati ya wanafamilia yako tu na sio kwa marafiki. Pia kuna matatizo kadhaa ya kisaikolojia yanayohusiana na mapenzi.Katika historia ya mtu na dini ndizo taaluma ambazo zimeelekeza sana suala la mapenzi. Mapenzi yamegawanyika katika sehemu tatu zinazolingana ambazo ni tamaa, mvuto na pendo. Tamaa huwafunua watu kwa wengine, mvuto wa kimahaba huwahamasisha watu kuzingatia nishati yao kwa kuhusiana kingono na pendo linahusisha kustahimili mwenzako au mtoto kwa muda wa kutosha.
Tamaa ni hamu ya mwanzo ya ngono ambayo inahusisha kutolewa kwa wingi kwa kemikali. Athari hizi huwa hazikai zaidi ya wiki chache au miezi michache.Utafiti uliofanywa hivi karibuni na wanasayansi umeonyesha kuwa kadiri watu wanavyoendelea kupendana, ubongo huwa unatoa aina fulani za kemikali, ikiwa ni pamoja na ‘pheromones’, ‘dopamine’, ‘norepinephrine’, ambayo hufanya kazi sawa, kuchochea kiini cha furaha kwenye ubongo na kusababisha ongezeko la mapigo ya moyo, kupoteza hamu ya kula na kulala, hisia kali za msisimko juu ya mtu huyo. Utafiti umeonyesha kwamba hatua hii kwa jumla hudumu kuanzia mwaka mmoja na nusu hadi miaka mitatu. Nakubunia nadharia ya miraba mitatu ya mapenzi Bi.Janeth akaendelea na akasema mapenzi yana vipengele vitatu tofauti ambavyo ni urafiki, kujitoa, na uchu. Urafiki ni aina ambayo watu wawili huambiana siri na mambo kadhaa kuhusu maisha yao binafsi. Kuwajibika, kwa upande mwingine, ni matumaini kuwa uhusiano huo ni wa kudumu. Aina ya mwisho na inayopatikana sana ni mvuto wa kingono au uchu. Mapenzi ya uchu ni kama yanavyoonyeshwa katika kupumbazwa kimapenzi pamoja na mapenzi ya kimahaba. Aina zote za mapenzi hutazamwa kama mchanganyiko tofauti wa vipengele hivi vitatu.Shamsa alikuwa amenyamaza tuli akimsikiliza kwa umakini mkubwa sana Mwanasaikolojia huyo.Alikuwa amkimueleza hali aliyokuwa nayo kuhusu kijana Jongo, kuondoka kwake kumekuwa na madhara makubwa sana katika familia yake, kwani kipindi hicho alitakiwa ajitahidi kusoma ili aweze kufaulu mitihani yake.
Baada ya kuzungumza Bi.Janeth aliaga na kuondo huku Bwana Samir akiwa mtu mwenye furaha baada ya kumuona mtoto wake akiwa mwenye tabasamu mwanana lililochanua kwa huba.Bi.Ramla alifurahi zaidi pale alipoingia chumba cha mtoto wake na kumkuta Shamsa akiwa mwenye tabasamu pana usoni mwake huku mikononi mwake akiwa ameshikilia kitabu kilichoandikwa “Mahusiano katika maisha yangu”Bi.Ramla alikiangalia kitabu hicho mara mbili mbili kisha akamfuata mahali pale alipokuwa amekaa mtoto wake.Hakujali kumsingikiza mgeni aliyekuja kumpa ushauri mtoto wake badala yake Bwana Samir ndio aliyemsindikiza mgeni huyo. “Vipi Mwanangu…umemuonaje mwalimu?” Bi.Ramla aliuliza kwa mbwembwe “Sawa tu mama …nimemuelewa na amenishauri vizuri sana”Shamsa alijibu kwa furaha “Hongera mwanangu kama umemuelewa unatakiwa ufuate ushauri wake sasa mama”Bi.Ramla alisema “Rakini mama ndio basi tena kuonana na Jongo, kwanini nisionane nae hata siku moja tu?” “Lakini mwanangu si umemsikia mshauri alivyosema…hutakiwi kuwaza sana na kulazimisha kitu wakati mungu hajakupangia”Bi.Ramla alisema ‘Sawa mama nimekuelewa nitafuata ushauri wenu nyote” “Vizuri mwanangu unatakiwa usome sasa hachana na vitu visivyokuwa na msingi kwako” ‘Sawa nimekuelewa mama”
Baada ya mazungumzo kwa mzazi na mwanaye yalikuwa ya furaha hata pale Bwana Samir naye aliingia chumba humo na kuendelea na mazungumzo yao.Bwana Samir na mkewe walimsihi mtoto wao kuwa na amani siku zote na kurejea shuleni ili kuweza kufanya mtihani wake wa kidato cha nne.Shamsa hakuwa na kinyongo aliweza kuwasikiliza kwa umakini mkubwa wazazi wake kwa vile ushauri wa Bi.Janeth kumuingia akilini hakuwa na namna alikubaliana na wazazi wake kisha kwa pamoja wakakumbatiana na mtoto wao. *********** Ulikuwa mwaka wa pili sasa tangia Jongo na mama yake wahame mji wa Mwanza.Shamsa akiwa kidato cha nne hakiwa hajui chochote kinachoendelea juu ya kijana Jongo,hakuwa na mawasiliano nae wala kuzisikia habari zake.Muda wote alipenda kuwa pamoja na marafiki zake.Hakika hakupenda kuwa karibu na wanaume kwani alijua madhara yake juu ya kuwa na ukaribu nao kwani alifundwa na Bi.Janeth kutokuwa karibu na wanaume hao kimazoea.Siku zilikimbia kama mwewe angani mwaka wa pili ukafikia Shamsa kuingia kidato cha nne.Alisoma kama kawaida mpaka ikafikia kipindi cha kufanya mtihani wa kidato cha nne, alifanya mtihani wake na kuushinda vyema kwa harama za juu .Shamsa akafaulu kuingia kidato cha tano katika shule ya sekondari Mwika iliyopo mkoani Moshi. Aliendelea na masomo ya sekondari huku akiwa msichana mrembo mwenye shepu ya kumpagawisha mwanaume yoyote aliyetokea mbele ya macho yake.Shamsa alikuwa mtoto pekee katika familia ya bwana Samir na mkewe Bi.Ramla.Shamsa alikuwa mwenye sura nzuri macho makubwa ya kuregea hakika alikuwa mzuri wa kuvutia.Kipindi cha kuanza masomo,Shamsa aliondoka Mwanza na kuelekea mkoani Moshi.Aliondoka akiwa mtu mwenye mawazo sana hakujua jinsi gani atakaa mbali na wazazi wake,Zaidi kilichokuwa moyoni mwake ni kuonana na kijana Jongo aliyeondoka miaka miwili iliyopita.Alianza masomo yake Mjini Moshi lakini muda wote alionekana mtu mwenye mawazo hata waalimu pamoja na wanafunzi wenzake walijua ila hawakuwa na namna ya kumhoji kuhusiana na tatizo hilo. Shamsa aliendelea na masomo yake kwa muda wote wa miaka miwili na kukaa bila kurudi Mwanza kwani Mama yake hakutaka mtotowake arejee nyumbani angali bado akiwa hajamaliza masomo yake .Hivyo kipindi chote hicho alisoma bila kurejea.Hata kipindi cha likizo hakuruhusiwa kurudi mwanza badala yake alikwenda kwa dada yake aliyekuwa akiishi dare s salaam.Kidato cha tano akamaliza akaingia kidato cha sita kwa furaha huku akijua muda wa kumaliza masomo unawadia ili kurejea nyumbani kwa wazazi wake… CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Wakati huo Shamsa akikalibia kumaliza kidato cha sita alikuwa akisumbuliwa sana wanaume mbalimbali hasa wanafunzi wenzake walimtaka kimapenzi.Katika kidato cha sita kulikuwa na kijana mmoja mtanashati anayeitwa Rashid,Kijana huyu hakutaka kuvumilia, hakuwa radhi kuuonamoyo wake ukiteseka na wakati mtu ambaye angempa pumziko alikuwepo katika dunia hii.Hakutakiwa kusubiri, aliogopa kuchoka na hivyo akapanga siku ya kumfuata Shamsa kwa ajili ya kumwambia ukweli jinsi moyo wake ulivyojisikia.Alijipanga sana muda wa kutoka darasani, akaanza kujivuta kwa ajili ya kuzungumza na Shamsa.Hakuwa nafasi, wakati yeye akitaka kumsogelea msichana huyo mrembo na kumwambia ukweli, tayari wanaume mbalimbali waliwai kumfuata Shamsa na kumtaka kimapenzi.
Moyo wake uliumia mno,hakuamini kama ingeshindikana kabisa kuzungumza naye.Hakavumilia,akasubiri siku nyingine amfuate na kumwambia shida yake.Rashidi alikuwa mtoto wa bilionea mkubwa ambaye alitokea kumpenda msichana Shamsa.Utajiri mkubwa aliokuwa nao baba yake ulionyesha dhahiri kwamba hakuwa na hadhi kubwa kwa msichana Shamsa.Hakutaka kujali hilo,alipomfuata Shamsa utajiri wake aliuweka pembeni alitanguliza mapenzi kwani aliamini kwamba pesa zisingeweza kununua mapenzi,hata kama angekuwa na pesa kiasi gani angeishia kununua ngono na si upendo. “Kumbe kwa staili hii sitaweza kuongea naye,ngoja nitafute namba yake ya simu”aliwaza.Hilo ndilo alilolifanya,kaitafuta namba ya msichana huyo.Kuipata haikuwa kazi kubwa,watu wengi walikuwa nayo,alipoipata tu,akatafuta siku na kumpigia simu kwa lengo la kuonana naye. “Wewe nani?”Aliuliza Shamsa baada ya kupokea simu “Rashidi!” “Okay! Nikusaidie nini Chidi?”Aliuliza Shamsa “Kuzungumza na wewe” “Kuhusu?” “Stori tu za kawaida” “Samahani! Sina muda kaka yangu!” “Shamsah! “Naomba unielewe! Sina muda!” Alisema Shamsa kisha akakata simu
Hakukoma, hata siku iliyofuata aliendelea kumsumbua na kumtumia meseji nyingi mno.Hayo ndio yalikuwa maisha yake na baada ya wiki mbili, ili kuepusha usumbufu Shamsa akakubaliana na Rashidi na kuonana naye. “Tuonane wapi?”Aliuliza Shamsa “Bwalo la shule basi” “Hapana sihitaji kuonekana kwa mtu yoyote yule, labda twende nje ya shule” “Sawa Sema wewe basi, au kama vipi tuonane darasani siku ya jumapili” “Sawa”
Siku ya jumapili ndani ya darasa, walikuwa wamekaa meza ya nyuma kabisa na pale walipo walikuwa wamezama ndani ya maongezi.Rashid alimwambia shida yake Shamsa hakuwa tayari kumuelewa kwani mawazo yake yote kwa wakati huo yalikuwa kwa Jongo, ambaye hakujua mahali alipokuwa kwa wakati huo. Shamsa alijiapia lazima amtafute Jongo popote alipo na kumuweka mikononi mwake.Wakati Rashid akiendelea kumueleza shida yake,wala Shamsa hakuwa na habari naye,mapenzi yote ndani ya moyo wake yalikuwa juu ya kijana Jongo,hakika chaguo lake lilikuwa ni Jongo hakuwa mwengine.Ikafikia kipindi Shamsa akachoka kumsikiliza Rashid kwa maneno aliyokuwa akiambiwa na kijana huyo aliona kama mkuki uliochoma moyoni mwake.Lakini Rashid hakuchoka kumbembeleza na kumpa ahadi nzuri,hata hivyo Shamsa hakutaka kuendelea kumsikiliza hivyo alinyanyuka kitini kisha akakusanya vitabu vyake na kuondoka.Rashidi alijalibu kumzuia Shamsa asiondoke lakini alichelewa tayari msichana huyo alikuwa ameshaondoka ndani ya darasa hilo na kurejea hosteli. ******* Kijana Jongo wakati akiahamia mkoani morogoro na mama yake hakika ilikuwa majonzi makubwa kwake baada yam kutengana na rafiki yake wa kipekee Shamsa.Hakujua kama hapo alipofikia atapata rafiki atakayempenda kama Shamsa.Mama yake alikuwa na wakati mgumu sana kumbembeleza mtoto wake juu ya kuondoka Mwanza na kumuacha yule ampendaye.Baada ya siku mbili tatu Jongo alipelekwa shule ya sekondari Kigurunyembe kuendelea na masomo yake akiwa kidato cha tatu.Jongo aliendelea na masomo yake akiwa mremavu wa macho,wataalamu mbalimbali waliendelea kufika shuleni hapo ili kuendelea kumfundisha Jongo.Wakati Jongo akifundishwa peke yake alijiona mnyonge,mkiwa mwenye simanzi juu ya uhuru wa kucheza na watoto wenzake.Hapo ndipo mawazo yalipojirudia juu ya msichana yule dada aliyekuwa akicheza nae pamoja mjini mwanza,alijipa moyo na kujisemea lazima amtafute popote pale Shamsa ili awe karibu naye. Jongo alisoma na kuhitimu kidato cha nne huku akiwa kijana mtanashati mwenye kuvutia, kipindi chote hicho Jongo kutengana na Shamsa hakuna hata mmoja kati yao aliyewai kumpigia simu mwenzake.Ingawa walikuwa hawana simu kipindi wakiwa sekondari hivyo baadae Jongo alipewa simu na mama yake ili aweze kuwasiliana na watu wake wa karibu.Hata hivyo licha ya Jongo kuwa na simu lakini mawasiliano yake kwa Shamsa yalishindikana kwani hakujua jinsi gani ataipata namba ya Shamsa kwa wakati huo.Hata hivyo hakukata tamaa alizidi kumuweka moyoni msichana huyo mrembo.Alijifikiria kuandika barua hili aweze kuituma kwa anuwani ya shuleni kwao lakini alipokumbuka ya kwamba kwa kipindi hicho tayari Shamsa ameshamaliza masomo yake ya kidato cha nne sasa atakuwa ameamia shule nyingine kuendelea na masomo. Kipindi hicho Jongo alikuwa yupo tu nyumbani baada ya kumaliza kidato cha nne hakuweza tena kuendelea na masomo yake kwa kidato kinachofuata.Alijisikia vibaya sana kukaa tu nyumbani, alipenda kusomo ila kwa alama alizopata hakuchaguliwa kuendelea kidato cha tano.Jongo alijipa moyo kwani hakutaka kukaa tu nyumbani alimuomba mama yake ampeleke hata kusomea ufundi mama yake alikubali ila alimwambia ya kwamba asubiri mpaka pale atakapopata pesa ndipo atampeleka kusomea humakenika.Jongo alifurahi na kumwambia mama yake sawa yeye yupo tayari kwa lolote ili mladi apate angalau ufundi utakao muwezesha kujikimu kimaisha hapo baadae.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Baada ya siku mbili tatu hadithi ikawa hile hile mama upate pesa unipeleke nikapate elimu iweze kutukombua kiuchumi.Jongo alimlilia mama yake kila simu alimbembeleza lakini mama yake hakuwa na pesa hivyo alimuomba kuvumilia mpaka pale atakapopata pesa atampa na kwenda kusoma kile anachokitaka.Jongo hakuwa na jinsi aliamua kunyamaza ili kujua hatma ya maisha yake kila kitu alimuachia mama yake maana hakuwa na msaada wa mtu mwingine zaidi ya mama yake pekee. ********
Simulizi : Chaguo Langu Ni Wewe Sehemu Ya Tatu (3) Wakati Shamsa akiendelea na masomo yake muda mwingi aliutumia kumfikiria sana Jongo alijua umbali uliopo kutoka moshi shuleni anaposoma na mkoani morogoro walipoamia kina Jongo hakukuwa na umbali wa kutisha,hivyo alijipa ujasili lazima ipo siku atakutana na Jongo.Shamsa alinedelea na masomo mpaka mwaka wa mwisho kufanya mtihani kidato cha sita ukawadia akaushinda vyema kuendelea na chuo kikuu cha mlimani kilichopo jijini dare s Salaam.Shamsa alilia kwa furaha pale alipotangazwa kuchaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Dar es Salaam alijua sasa nafasi ya kuonana na Jongo ndio hiyo imewadia.Moro na Dar sio mbali lazima nitafika kuonana na Jongo” Alijisemea Shamsa huku akiwa ahamini kama kweli anakwenda kujiunga na chuo kikuu mlimani.
Baada ya utaratibu kufanyika na Shamsa kujiunga na Chuo kikuu, aliweza kuanza masomo yake huku akiwa mgeni kwa wanafunzi wenzake ambao alikutana nao Chuoni, Ilimchukua muda mrefu kidogo hadi kuzoea mazingira ya Chuo na kuzoeana na wanafunzi wenzake lakini alijitahidi japokuwa kulikuwa na changamoto mbali mbali za Vyuoni ikiwemo ukosefu wa mahitaji na fedha za kujikimu. Lakini hakushindwa mara moja akaweza kuzoea mazingira ya Chuo na kuzoeana na wanafunzi wenzake kitu ambacho kilimrahisishia masomo yake kwa kuweza kujumuika na wenzake wakijisomea.Shamsa alipendekeza kusomea masomo ya Uchumi, alisoma masomo hayo kwa muda wa miaka mitatu (3) ambapo aliweza kusonga mbele na hatimaye kuhitimu Shahada ya Uchumi.Bi.Ramla alikuwa na furaha kutwa nzima alionekana akicheka na kufurahi hata kama jambo lenyewe sio la kuchekesha lakini yeye alicheka.Furaha ya Bi.Ramla ilisababishwa na kutokuwa pamoja kwa mtoto wake kuwa na mawazo yaliyokuwa yanambana sasa yamekwisha na zaidi amefurahi kumuona binti yake akimaliza chuo bila matatizo….
Baada ya Shamsa kumaliza chuo kikuu pale mlimani siku ya kurejea majumbani mwao iliwadia, Shamsa alikusanya kilicho chake na kuagana na marafiki zake akaelekea nyumbani Mwanza kwa wazazi wake.Bi.Ramla alipomuona mtoto wake hakuamini alimkimbilia kwa furaha na kumkumbatia hata Bwana Samir aliporejea nyumbani alifurahi alipomuona mtoto wake akiwa na afya tele.Bwana Samir na mkewe Ramla waliamua kumfanyia sherehe mtoto wao, Shamsa alifurahi sana kumuona wazazi wake wakimpenda na kumjali.Siku ya tatu mbele tangia siku ile aliyorudi Alhamisi.Siku ya jumamosi sherehe kubwa ilifanyika nyumbani kwa bwana Samir kumpongeza mtoto wao kumaliza chuo,tafrija hiyo fupi yenye manjonjo kibao ilitawaliwa na matukio ya ajabu ajabu.
Kwanza kabisa Shamsa hakuwa na amani kwa sherehe hiyo,kwani kukosekana kwa Jongo kulimfanya kukosa furaha kila wakati alikaa na kumfikiri sana Jongo.Usoni mwake alionekana kuwa na furaha lakini moyoni haikuwa hivyo alimuwaza sana Jongo mpaka mwenyewe alijishangaa.Kipindi sherehe ikiendelea huku mziki mkubwa ukiwaburudisha wageni waalikwa Shamsa aliyekuwa amekaa kando ya mama yake,alishangaa alipomuona kijana mmoja akija na kumsabahi.Kila wakati kijana huyo alimwangalia Shamsa huku akikwepesha macho yake.Muda wa kukalibia kuisha kwa sherehe kijana huyo alikuja na kumtaka Shamsa amfuate sehemu kuna ujumbe anahitaji kumwambia. Shamsa hakusita alinyanyuka na kumuaga mama yake na kumfuate kijana yule. Baada ya kusogea gizani alishangaa mkaka huyo akimkumbatia kwa nguvu, Looh! Shamsa alistuka akaingiwa na woga, alipomuuliza kwanini anafanya hivyo, jamaa huyo akamwambia amevutiwa nae tangia siku aliporudi nyumbani hapo. “Mmh we mkaka mie bado mwanafunzi naomba uniachie, mie sitaki matatizo”Shamsa alilalamika “Wala sio matatizo, mimi nakupenda sana naomba uwe mpenzi wangu nakuahidi kukupenda milele nitakupa chochote unachotaka” “Aka mie sitaki bhana, kwanza unijui sikujui sasa utanipendaje?”Shamsa alikataa “Kama hutaki basi nipe japo kimoja tu moyo wangu uridhike” “Tafadhali naomba uniachie nitapiga kelele sasa hivi” “Hapana Shamsa sina nia mbaya nawe”
Aliposema hivyo Shamsa akajua anaachiwa kumbe kijana huyo alizidi kumbana kwa nguvu,Shamsa alijitahidi kujitoa huku akisema sitaki lakini hakuitikia,Shamsa alitamani mama yake atokee labda atamuhachia.Kosa alilofanya ni kugeuka upande mwengine na alijua atajitoa kumbe alijidanganya tayari kijana huyo alishika maziwa ya Shamsa na kuanza kuyachezea.Taratibu Shamsa alihanza kusikia hali hisiyo ya kawaida kwake,mwili ulimsisimka,akajikuta akisahau kila kitu na kuanza kumpa ushirikiano wa hali ya juu “huyu mkaka atakuwa na dawa haiwezekani” Shamsa alijisemea kimoyo moyo huku akizidi kumpapasa kifua chake.
“We kaka jamani aah! Oppss! ass! mama wee ayiii apoo apo!” Shamsa alianza kutoa miguno baada ya huyu mkaka kupeleka vidole shimoni, njoo ukae hapa yule jamaa akamwambia Shamsa huku akiwa amemshika mkono.Kifua cha msichana huyo kilmchanganya,mawazo yake yalikuwa mbali kabisa, akamvuta Shamsa mpsks chini ya bustani ya mauwa na kumlaza chini kisha kumshika huku na kule.Haraka Shamsa aliishika mkono wake uliokuwa dhamini kidole safari ya kwenda shimoni na kuukandamiza ili kidole kichezee nanilii vizuri huku akizidi kulalamika.Laakini yule kaka hakukoma alizidi kupeleka mkono wake na kuzama shimoni.Yule jamaa alivyomuona Shamsa anazidi kulalamika alizidisha utundu safari hii akamfuata usoni na akampa ulimi naye Shamsa hakuwa na pingamizi zaidi ya kuupokea kwa mikono miwili.Kwani tangia Shamsa azaliwe hakuwai kuyajua mapenzi alikuwa anasikia tu mapenzi matamu lakini utamu wake hakuwai kuuonja zaidi ya kusikia tu kwa marafiki zake.Siku hiyo kweli raha utamu aliusikia kila kona ya mwili wake. Muda huo wazazi wake wakiwa hawajui kinachoendelea Shamsa na jamaa huyo walizidi kubadilishana juise asilia huku kidole kikizidi kuheza na hisia za msichana huyo.
Ilikuwa ni taabu kubwa sana kwa Shamsa kila alipojaribu kumuangalia vizuri kujana huyo alishindwa kumtadhimini jinsi fujo alizokuwa akiamfanyia na jinsi alivyokuwa muonekano wake ulikuwa tofauti na mawazo yake.Kijana huyo alionekana kuwa kijana mrefu mwembamba wastani mwenye macho makubwa,Shamsa hakuwa na jinsi kila alichokuwa akikifanya kijana huyo alijisikia huru alijiachia vile alivyojisikia.Jamaa alimparamia kisha kumvua nguo yake ya chini.Sasa kitendo cha kuvuliwa nguo yake ya ndani kulimtia uwoga zaidi Shamsa akaanza kupiga kelele.muda mwingi alikuwa akijitahidi kumtoa mwanaume huyo kifuani mwake lakini hakutoka,aling’ang’ania kama ruba.Kwa kasi ya ajabu akaanza kumvua nguo yake ya ndani na hivyo jamaa akaanza kumuingilia.Shamsa akaanza kulia kwa maumivu makali chini ya kitovu, sauti yake haikutoka kwa kuwa alizibwa mdomo na mziki ukiendelea kupiga.Alilia mno aliangaika kujitoa mikononi mwa mwanaume huyo lakini akashindwa kabisa.
Damu zikaanza kumtoka chini ya kitovu, alisikia maumivu makali mno zaidi ya kitu chochote kile, jamaa hakujali machozi ya Shamsa wala hakufikilia kiasi gani msichana huyo akiumia.Alichokuwa akikijali ni kupiga pushapu,kwenda juu na kurudi chini.Raha za kijana huyo asiyemjua jina lake wa sura yake zilimkolea Shamsa na kupelekea kujisahau kabisa kama alikuwa katika sherehe tena yake mwenyewe.Wakati kijana huyo akiendelea na nia yake ya kutaka kutimiza kile alichokuwa akikifanya, ghafla akapita mtu pale walipokuwa wamesimama.Haraka yule kijana alimuhachia Shamsa na kumtoa maungoni mwake,Shamsa alishangaaa kwa kitendo hicho huku akiwa mwenye hofu alijizoa zoa pale chini haraka na kusimama.Alipogeuka nyuma na kumuona baba yake akija huku akiwa ameongozana na watu wawili.Shamsa nguvu zilimwishia miguu ilimtetemeka na mapigo ya moyo wake yakimdunda.Wakat Shamsa akimshuhudia baba yake akitembea kwa hatua kumbwa aligeuza shingo yake ili kumuona kijana huyo hatachukua hatua gani kwani alishajua ya kwamba tayari wamefumwa.Muda wote kijana alikuwa akihema kama jibwa koko alipata wazo la kukimbia na kupotelea gizani na ndivyo alivyofanya,haraka alitokomea gizani na kumuacha Shamsa mahali hapo akijizoazoa…….
“Vipi binti yangu mbona muda wote upo huku…kitu gani kimekutokea?”Bwana Samir aliuliza baada ya kufika pale “Hapana Baba najisikia vibaya najisikia kupatwa na tumbo la kuharisha”Shamsa alimjibu baba yake “Pole binti yangu…mbona ujasema hujui kama kuna wahuni”Baba yake alimfokea “Najua baba lakini sikuwa na nguvu ya kutembea kwa wakati huo” “Haya… haraka twende “Bwana Samir alizidi kumkoromea mtoto wake “Sawa baba “Shamsa alimjibu baba yake na kuongoza njia kuelekea kule walipo wageni waalikwa. Bi.Ramla alishangaa alipomuona mtoto wake akiwa kama mtu asiyejitambua,mara moja alijua kuna kitu kitakuwa kimempata mtoto wake,maana hakuwa na furaha kama alivyokuwa mara kwanza.Bi.Ramla hakukubali alimsogelea mumewe na kumuuliza kulikoni mpaka mtoto kuwa katika hali hiyo,Bwana Samir alimjibu vile ilivyokuwa lakini Bi.Ramla aliona haitoshi akamsogelea mtoto na kumwangalia kuanzia juu mpaka chini,wakati Bi.Ramla akimwangali Shamsa hakuwa na habari ya macho ya mzaziwe nae mawazo yake yote yalikuwa juu ya kijana huyo.Aliwaza jinsi kijana huyo alivyomfuata na kumtaka waongee kumbe alikuwa na lake jambo loo! Alijuta kumfuata na bahati yake ndio ingekuwa kwenda kunyonyolewa na manyoya yote yangemtoka.Shamsa aliwaza kimoyo na kumshukuru baba yaje kuja maeneo hayo kumuokoa kama sivyo angekiona cha moto siku hiyo.
Shamsa mwanangu”Mama yake alimshika begani baada ya kumuona hakiwa hana hili wala lile “Yes mama”Shamsa alimuitikia mama yake kwa wasiwasi “Kitu gani kimekutokea mwanangu?” “Hapana mama mbona nipo sawa” “Hapana Shamsa binti yangu wewe ni mkubwa sasa embu nitoe hofu mama yako?”Mama yake alisema ‘Najua mama…..hata kama mimi nimekuwa lakini haipaswi kufanyiwa kitu kama hicho “Kitu gani tena mwangu?”Bi.Ramla aliuliza kwa jazba “Lakini sioni sanbabu ya kukueleza we hacha tu mama”Shamsa alimwambia mama yake “Mimi ndio mama yake….usiponiambia mimi nani mwengine utamwambia na kutatua matatizo yako?”Bi.Ramla alimsihi binti yake “Sawa mama nimekuelewa na nitakueleza kwa sasa naomba nikapumzike” “Haa, Shamsa mwanangu sherehe bado hatujamaliza jamani”Mama yae alilalamika Licha ya Bi.Ramla kumsihi mtoto wake hasiondoke wasubili shughuli imalizike lakini Shamsa hakumsikiliza mama yake alinyanyuka na kuondoka kuchani kwake huku akiwaacha ndugu na jamaa wakibaki wakimshangaa.Hakuna aliyekuwa akifahamu juu ya hali aliyokuwa nayo Shamsa zaidi ya yule jamaa aliyekuwa akimfanyia kitendo hicho uchochoroni.Zilipita dakika kadhaa Shamsa hakutokea wala kusogea zaidi ya kugaragara kitandani huku mama yake akiwa pembeni akimbembeleza ili wakamalize shughuli lakini katu hakukubali kutoka tena ndani.Muda wote alikuwa mawazoni alimuwaza na kumfikilia kijana yule sasa alimchukia na kumuona ibilisi hasiyekuwa na mbele wala nyumba alitaka kumualibia ndotozake,alimchukia na kumrahani kwa kitendo alichokuwa akitaka kumfanyia.hapo hapo mawazo yalihama na kuanza kumfikiria kijana Jongo hakujua kwa namna gani pale mwanza kuna vijana wanaomtafuta na kumtaka kimapenzi.Lakini haku hakutaka kumsaliti mpenzi wake aliyempenda toka moyoni mwake,hakuna mwengine aliyekuwa tayari kuwa naye zaidi ya chaguo lake, ingawa hakufahamu halipo lakini alimpenda siku zote. Siku zilipita na kusogea huku Shamsa akiendelea kuishi nyumbani kwa wazazi wake, kuna kipindi wakati Shamsa aakiwa pamoja na Jongo alimuuliza anampenda hama laa, lakini Shamsa hakuwa na jibu dhabiti mbele yake.Kwa kipindi hicho hakuweza kumwambia chochote kwa kuwa lilikuwa swali ambalo hakulitegemea kuulizwa kwa wakati huo.Hata ukaribu wao kirafiki ulijengwa kwa heshima kama kaka na dada, kutokana na yote hayo lakini Shamsa alimpenda sana kijana Jongo. Basi kama kupenda Shamsa alipenda hasa,kila alipokuwa akimfikilia Jongo uchu mlimjaa na kumtesa kumkumba hali yake kipindi cha nyuma ikaanza kurudi,kutwa nzima wazo tele kichwani mwake anashinda na kulala huku kichwa kikimzunguka.Bi.Ramla na mumewe Samir walimuona mtoto wao katika hali hiyo hila hawakuwa na namna ya kumsaidia kwani hawakujua ugonjwa uliokuwa ukimsumbua.Muda mwingi mama yake alishinda nae karibu akimwangalia na kusikitika juu ya hali aliyokuwa nayo binti yake amesoma amemaliza na sasa amerudiwa na hali hii kweli mwanangu atakuwa anasumbuliwa na nini jamani,hee mungu amekukosea nini binti yangu,kama ni dhambi wengi wanakosea kama ni mateso kwanini umtese binti yangu pekee.Hakika nakuomba umsamehe kiumbe chako hiki,umpe afya na fanaka wewe ndio kimbilio lake.Bi.Ramla aliomba na kusugua meno akimlilia mwanae,ikafikia kipindi Bi.Ramla akahisi majirani watakuwa wamemtupia jini mtoto wake kutokana na kile allichokuwa amekisikia chini kwa chini ya kuwa watu wa mwanza ni wabaya sana tena watakuwa wamemchezea mchezo mchafu mtoto wake kwa sababu ya mafanikio aliyoyapata katika masomo yake. Bi.Ramla akaanza kuingiwa na mashaka juu ya maneno hayo yaliyokuwa yakiongelewa chini kwa chini bila yeye kutambua.Kutokana na maneno hayo kumuingia akilini mwake na kumchoma Bi.Ramla alimgusia mumewe na kumueleza kile ambacho majilani wake walikuwa wakikizungumza juu ya mtoto wao Shamsa kuwa na Jini lililokuwa likimsumbua mpaka kumpelekea kupoteza nguvu kama alivyokuwa. “Mume wangu kila siku nasikia habari za kuumwa kwa mtoto wetu” “Habari za kuumwa kivipi yaani?”Bwana Samir alishangaa na kumuuliza ilivyokuwa “Majirani kutwa wanaongelea juu ya hali aliyokuwa nayo shamsa ya kwamba ametupiwa jinni” “Hapana mke wangu sisi ni wacha mungu kwa nini unaamini maneno hayo, Shamsa atakuwa anasumbuliwa na masuala yake yale ya kipindi kile” “Hee! ina maana bado tu anasumbuliwa na huba” “Ndio huba inamsumbua…Unakumbuka kipindi kile alivyokuja yule mama mwanasaikolojia?” “Nakumbuka mume wangu lakini mbona kipindi hicho mpaka sasa imepita karibia miaka mingapi na alikuwa amesharudi kwenye hali yake ya kawaida jamani” Bi.Ramla alilalama “Sasa wewe utajuaje kama Shamsa amelogwa wewe?”Bwana Samir alimtupia swali mkewe “Ukisikia lisemwalo basi lipo na kama halipo basi linakuja hilo tafadhali tusipuuze bwana mtoto mwenye mmoja tu huyu tukimpoteza tutapata wapi mwengine”Bi. Ramla alifoka “Sawa mie ndio nakwambia hivyo mwanao anasumbuliwa na mapenzi huyo ugonjwa usiokuwa na dawa ila dawa anaijua mwenyewe huyo muulize” Bwana Samir alisema kwa ukali huku akiwa mwenye dhihaka Bi.Ramla hakutaka kumsikiliza mumewe alichofanya yeye kwa wakati huo alimuacha mumewe pale sebuleni na kumfuata mtoto wake chumbani.Kilichokuwa kinampa mashaka Bi.Ramla kumuona mtoto wake akiwa amedhoofika mwili wake,tabasamu alikuwepo usoni mwake akafikiria kitu gani kinachomsumbua Shamsa kama mapenzi hakuona sababu ya kumfanya mwanae kuwa katika hali hiyo.Shamsa hakuwa mtokaaji nyumbani,wala hakuwa mtu wa kujichanganya na wasichana wenzake ukimuona Shamsa yupo nje ujue ametolewa na mama yake kwa ajili ya kupata hewa tu na muda mchache baadae umrudisha ndani kiukweli Shamsa amekuwa mgonjwa wa mapenzi.Baada ya kuingia chumbani humo alimkuta mtoto wake kama kawaida akiwa amelala kitandani akigalagala hana hili wala lile. “Shamsa mwanangu?” “Abee! Mama” “Una nini binti yangu kitu gani kinachokusumbua?” “Hakuna kinachonisumbua mama” “Naomba uniambie ukweli, Shamsa wewe ndio binti yangu wa kipekee unanipa wakati mgumu sana mama yake”Bi.Ramla alimwambia kwa upoleCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Najua mama lakini sioni kama kuna sababu ya kukuambia ingawa unafahamu hilo”Shamsa alimwambia mama yake huku machozi yakimtoka “Kitu gani mwanangu mbona mimi sielewi kinachokusumbua au umerogwa mama” “Ndio mama hata mie nahisi nimelogwa na si mwengine aliyeniloga zaidi ya Jongo” “Hee, unasemaje we mtoto…hati Jongo ndio kakuloga kivipi?”Bi.Ramla maswali yalimtoka mfululizo “Ndio mama ninamaanisha Jongo ameuteka moyo wangu nahitaji kuonana nae na si vinginevyo” “Hee! we Shamsa mwanangu una akili timamu kweli au ndio umelogwa kweli mama?’ “Sina uhakika na hilo mama kiukweli nampenda sana Jongo ndio chaguo langu mama nakuomba umtafute popote alipo Jongo” “Ina maana akipatikana Jongo ndio itakuwa mwisho wa matatizo yako?” “Bilashaka mama nitakuwa sawa ndio maana nikasema Jongo ndio aliyeniloga” ‘Sawa nitalifanyia kazi hilo…lakini mwanangu mtu mwenyewe si unamjua jinsi alivyo ni mlemavu yule macho hana mwanangu” “Najua mama hivyo Jongo nimempenda jinsi alivyo na si vinginevyo’ “Basi haina tatizo mwanangu utapona kabisa mama”Ramla alimpoza mwanae
Bwana na Bi. Ramla walikuwa wakijadili juu ya hali aliyokuwa nayo mtoto wao, Bi.Ramla alimueleza kila kitu mumewe kile alichozungumza na mtoto wake, Bwana Samir hakushituka wala kugwaya zaidi alimwambia mkewe juu ya kumuhamisha Shamsa kuelekea kuishi Dar na mwanza kwani kipindi akiwa shuleni hawakuwai kusikia habari za kuumwa kwa mtoto wao zaidi ya arejeapo mwanza ndio ikatokea kama ilivyotoke. Ina maana matatizo yote yapo jijini mwanza na sio huko alipotoka basi haina budi tumpeleke Dar es Salaam.Wazazi walikubaliana kumpekea Shamsa Dar es salaam kwenye nyumba ambayo alikuwa akiishi shangazi yake Shamsa ambaye ni dada wa Bwana Samir.Dada huyo aliachiwa nyumba hiyo na kaka yake baada ya kuhamia jijini Mwanza.Hivyo Bwana Samir na mkewe waliafikiana kumpeleka Shamsa jijini Dar es Salaam kukaa kwa Shangazi yake anayeitwa Maimuna mwenye watoto wawili mapacha.Walijua kumuamisha jijini Dar es salaam mtoto wao ingekuwa nafuu kumuwaza na kumfikiria Jongo ambaye hawakujua alikuwa wapi kwa wakati huo……
Moyo hauhimili mshawasha wa mfululizo.Hasa mshawasha wenyewe ukitokana na mtu unayempenda au tamaa ya utajiri.Moyo wa Shamsa ulikuwa na mapenzi makubwa juu ya kijana Jongo alimpenda kama pumzi ya maisha yake mwenyewe.Aliposikia maneno yake kipindi cha nyuma akisema haikuwezekana katika maisha yake kukataa haja iliyotakiwa na wazazi wake. Alikubali kusafiri pamoja na kwenda kuishi mjini alikopenda.Siku ya safari iliwadia huku Shamsa akiwa tayari wima akimsubilia Baba yake kumpeleka standi ya mabasi na kumpandisha garini kwa ajili ya kufika mapema jijini Dar es salaam.Baada ya robo saa Bwana Samir alikuwa tayari ameketi akisubili gari daladala kuondoka pembeni yake akiwa Binti yake Shamsa.Kitu ambacho Bwana Samir hakukitarajia ni furaha aliyokuwa nayo Binti yake, maana alishangaa kwani tangu Shamsa arejee nyumbani akitokea chuoni hakuwai kumuona akicheka na kufurahi kama siku hiyo.Alipomuuliza kitu gani kilichomfurahisha Shamsa alimjibu baba yake ya kwamba kilichomfahisha ni safari ya kwenda alimueleza zaidi furaha aliyokuwa nayo juu ya mji huo kwanza aliupenda na pili alifurahi kwa mara nyingine tena kukutana na marafiki zake waliotendana kwa muda mrefu.Bwana Samir alimwangalia mwanae na kuachia tabasamu kitu ambacho hakuwa akikipenda bwana huyo ni kutengana na mtoto wake,alipenda muda wote Shamsa awe karibu yake lakini hiyo haikuwezekana binti yake alikuwa kwenye wakati mgumu kutokana na kuathirika na huba.
Baada ya mwendo uliochukua takribani saa nzima, wakawasili standi ya mabasi.Shangwe na vifijo vilisikika kutoka kwa makondakta na wapiga debe kadhaa waliokuwa nje ya lango la kituo cha mabasi cha Mwanza.Kutokana na wingi wa mabasi na yote yakiwania kuwai muda na safari kwa wakati ili wajaze abilia zao.Bwana Samir alimsaidia binti yake mizigo na kuipakia ndani ya gari la RahaLeo linaelekea Dar es Salaam.Shamsa alipanda ndani ya gari na Safari ya kuelekea jijini Dar ikaanza,Kabla gari alijaanza kutoka stand hapo Bwana Samir alikuwa amekumbatiana na Binti yake waliagana kwa majonzi makubwa kuliko hata mama yake aliyemuacha nyumbani kwa wakati huo.Gari iliacha ardhi ya mwanza na kuelekea jijini Dar es Salaam.Njia nzima Shamsa alionekana kuwa na mawazo tele kichwani mwake aliwaza na kumfikiria kijana Jongo,hakujua kama huko aendako atamkuta hama hatomkuta lakini akajipa moyo lazima ataonana nae kama sio Dar basi popote pale atakwenda kumtafuta. Gari ilikuwa mwendo kasi ilipanda mabonde na kuyashusha.Hali ya hewa ilikuwa baridi kwani Shamsa alikaa kiti cha dirishani, hivyo baridi lilikuwa likimpiga kisawa sawa alipoona baridi likizidi akianza kutetemeka akaamua kufungua mkoba wake na kuchukua upande wa kitenge chake na kujifunika ili kupunguza baridi.Gari lilizidi kuchanja mbuga na kusonga mbele, masaa mengi yalipita akiwa bado ndani ya gari, kutwa nzima walishinda alikula na kulala akiwa bado wasafiri.Saa Sita usiku gari iliingia jijini Dar es salaam.Upande wa kushoto wa mlango wa kuingilia Shamsa alimuona Shangazi yake akiwa nje ya mlango wa kuingilia.Shamsa alimuona alishindwa kuvumilia alijitokeza kutoka dirisha na kumuhita shangazi yake.Shangazi Zuwena alikuwa amekuja kumpokea baada ya kufahamishwa kwa siku hiyo ndio binti huyo atafika,haraka Shangazi Zuwena alimpungia mkono Shamsa na hapo akaingia moja kwa moja mpaka pale gari hiyo iliposimama. “Waoooh! Anti yangu jamani” Zuwena alisema kwa furaha huku wakikumbatiana “Jamani Shangazi…….” “Habari za huko mwanangu?” “Salama Shangazi…shkamoo” “Marhabaha mwanangu hawajambo huko?”Zuwena alimuuliza kwa furaha “Hawajambo Shangazi” “Vipi masomo mwanangu?” “Salama kabisha namshukur mungu nimemaliza salama shangazi” “Karibu sana mwanagu” “Ahsante Shangazi” Shamsa ana Shangazi yake waliingia ndani ya tax ya kukodi kisha na safari ya kuelekea Ilala boma ikaanza.Njia nzima Shamsa alikuwa mwenye furaha mpaka Shangazi yake alishangaa maana jinsi alivyoambiwa sivyo alivyomuona alivyo.Laah! Shamsa furaha yote ilitoka wapi huko kwao alionekana kuwa mtu mwenye mawazo mengi, yaliyopelekea kuwa mgonjwa wa kulala nyumbani na kuamka bila kufanya jambo lolote.Wazazi wake wameamua kumleta kwake ili kuondokana na mawazo hayo sasa anaonekana kweli mawazo yamemtoka hakuelewa kitu gani kinachosababisha kuwa mwenye tabasamu muda wote.Tangia kufika ubungo ambapo bado hata hakufika nyumbani kwa shangazi yake anafurahia njiani,kuna kitu gani hapa au kuna bwana aliyeiteka akili yake,alifikiri yote hayo Shangazi yake bila kumuuliza kitu akasubiri afikapo nyumbani amuulize mwanae maswali yaliyo chumbani mwake bila kukosa majibu. Baada ya mwendo mrefu walifika nyumbani walipokelewa na mlinzi wa nyumba hiyo ambaye kabla Bwana Samir ajaondoka alimuomba kuendelea na kazi kama kawaida hata kama nyumba hiyo atapangisha au kukaa mtu mwingine mlinzi atabaki kuwa yeye.Bwana Samir alipenda kumuacha mlinzi huyo kutokana na maisha yake kipindi kirefu alikaa na kuishi ndani ya nyumba hiyo mchana na usiku hakuwa na pa kwenda zaidi ya kulindwa nyumba hiyo.Hakuwa na mke wala mtoto ila kila mwishoni mwa mwaka Bwana Samir upendelea kumpa likizo ya mwezi mzima kwa ajili ya kwenda nyumbani kwao kuwasalimu wazazi wake pamoja na familia yake kwa ujumla.Mwana huyo anayeitwa Samwel alipenda kuwa karibu na familia ya Sami rata kipindi Shamsa alipokuwa amezaliwa mlinzi huyo alionekana kuwa kijana ila kwa siku hiyo ambayo Shamsa alirejea kutoka Mwanza alimuona kama babu.Lakini kiukweli hakuwa na uzee wa kutisha japo alishaanza kuchaka lakini haikuwa sana. “Oooh! Jamani Shamsa umekuwa hivyo binti”Mliza alishangaa baada ya kumuona Shamsa akiingia usiku huo “Yes! Anko habari za hapa?” Shamsa alimsabahi bwana Samwel “Salama kabisa za siku na miaka tele…jamani umekuwa mkubwa hivyo”Samwel alishangaa kipindi Bwana Samir alipoondoka na mtoto wao alikuwa ndio kwanza darasa la pili sasa leo anakuja akiwa binti mkubwa aisee! Alishangaa “Shkamoo Anko Samwel” Shamsa alimpa heshima yake “Marhaba Shamsa karibu tena dare s Salaam” “Ahsante Anko nimeshakaribu na nimeshafika” Shamsa alimjibu
Bwana Samwel alibeba mizigo ya Shamsa huku akiwa na furaha,Shangazi Zuwena naye alimsaidiana na Shamsa kubeba mabegi yaliyobakia na kuingiza ndani.Baada ya Shamsa kuoga na kubadilisha nguo Shangazi yake alimuandalia chakula huku wakiendelea kuongea maongezi ya hapa na pale kuhusu habari za jijini Mwanza.Wakati Shamsa na Shangazi Zuwena wakiendelea na maongezi Shangazi akajikuta akianza kumwambia Shamsa juu ya habari zake za kuwa mgonjwa.Shamsa alishangaa kusikia habari za kuumwa kwake ziliwezaje kufika mpaka kwa Shangazi yake,mawazo yakamjia ya kwamba mama na baba yake watakuwa wamemwambia Shangazi kwa kile kilichokuwa kinamtatiza.Wakati Shangazi Zuwena akimwambia maneno hayo Shamsa alikuwa makini akimsikiliza kila neno alilokuwa akiambiwa lilijengeka kichwani mwake.Lakini Shamsa wala hakufungua mdomo wake alikaa tu kimya akimsikiliza Shangazi zuwena alivyokuwa akibwabwaja.Ikafikia kipindi Shamsa akashinda kuvumilia kile alichokuwa amekisikia kutoka kinywani mwa Shangazi kilimchanganya,Shamsa aliamua kumjibu kile ambacho kilimkeleketa moyoni mwake. “Hivi Shamsa mwanangu kitu gani kilichokuwa kunakutatiza?” Shandazi alimuuliza “Ni ugonjwa wa kawaida tu Shangazi kwani mwili ulikuwa umechoka tu “Mmh…haiwezekani Shamsa mwili uchoke ndio ukufanye wewe kuwa kwenye hali hiyo mboa ni maajabu hayo?” “Lakini Shangazi mbona nipo sawa nimeweza kusafiri salama bila matatizo njiani”Shamsa alijitetea “Sawa wazazi wako wameniambia kila kitu kuhusu kulichokufanya kuumwa” “Najua kama wamekwambia lakini hilo lisikuchanganye Shangazi mimi mzima kama unavyoniona” “Najua mapenzi ndio yaliyokufanya kuwa kwenye hali hiyo na mapenzi hayo hayo sasa yamekurudisha kwenye hali yako ya kawaida” “Kwanini unasema hivyo Shangazi wala mimi sina mpenzi” “Sawa na huyo kijana Jongo uliyekuwa ukimtaja kila wakati je umekutana nae au yopo Dar es Salam ndio maana ulipofika hapa furaha yako ilionekana wazi” “Hapana Shangazi yangu, Jongo sijui halipo ila nina imani nikiwa hapa Dar nitamtafuta na kuonana nae” “Ndio maana nauliza tena je huyo Jongo yupo jijini hapa?” “Hapana Shangazi Jongo hayupo hapa…kipindi cha nyuma aliniambia wanaamia morogoro nadhani hapo ndipo alipo” “Sawa basi tuishie hapa kwa leo naomba upumzike” Bi.Zuwena alisema huku akiwa mtu mwenye mawazo,licha ya ukalimu wake mama huyo hakuwa tayari kumuona binti wa kaka yake akipata matatizo ya kimapenzi huku akiwa ampendaye ajulikan alipo.Muda wote huo Shamsa alikuwa slikuwa akimwangalia tu Shangazi yake hakujua jinsi gani maneno yake yalivyokuwa yakimchanganya Shangazi huyo,hivyo ndivyo ilivyokuwa Shangazi alimnyanyua Shamsa toka kitani hapo na kumuongoza kuelekea chumbani kwake kule alipokuwa akilala zamani wakati akiwa binti mdogo na leo ndipo alipotakiwa kulala kwani chumba hicho kilitengwa kwa ajili ya mtoto wao huyo.Shangazi zuwena alikuwa amekisafisha vizuri chumba hicho na kumtandikia samani kwa vitambaa nadhifu,Shamsa alipoingia tu ndani ya chumba hicho alishangaa alipokuta midoli ya kuchezea watoto alipojalibu kuiangalia vizuri aliikumbuka kuwa midoli hiyo ilikuwa yake kipindi cha nyuma mama yake arejeapo Kazini upendelea kumnunulia na kumletea.Leo hii yafikia miaka kumi na moja iliyopita midoli hile mpaka leo ilikuwepo alijiuliza bila kupata jibu kamili alichoamua yeye alijitupa kitandani na kulala huku akiwa ameikubatia midoli hiyo mikubwa.
********* Jongo alikuwa mtu mwenye mawazo lukiki juu ya umaskini aliokuwa nao mama yake,aliwaza na kuwazua juu ya hali aliyokuwa nayo,hakujua mwisho wa maisha yake utakuwaje.Kipindi furani Jongo umuwaza sana msichana Shamsa hakujua kwa wakati huo Shamsa alikuwa wapi na halikuwa kwenye hali gani.Alifikiria kipindi anaondoka alimuacha Shamsa kwenye majonzi makubwa sana leo hii hakujua huko alipomuacha kama Shamsa bado yupo Mwanza au yupo wapi.Kipindi hicho Jongo alikuwa tu nyumbani akimsubili mama yake apate chochote juu ya m lo waliotarajia kuupata,ilitokea siku wakala wakashiba walimshukuru mungu lakini kuna siku nyingine ushinda bila kulala yote walimshukuru mungu kwa kuwapa uhai.Siku moja Jongo akiwa mtu mwenye mawazo juu ya hali aliyokuwa nayo alishangaa alipowasikia watu ila hakujua idadi ya watu hao mpaka pale alipokuja kuambiwa ya kwamba watu hao walikuwa wasamalia wema waliotokea jijini dar es Salaam kuja kumsaidia.Jongo hakuamini kile alichokisikia alimsogerea mama yake aliyekuwa amekaa karibu yake na kumsika mkono mama yake naye akimsika mwanae hapo mama huyo alianza kulia huku akimwangalia mwanae akiwa ahamini kile alichokisikia.Mwanangu leo anasaidiwa kipindi kirefu wameangaika na kuangaika wakitafuta msaada,leo hii mungu amekisikia kilio chake na sasa mfute machozi mungu wangu.Mama huyo aliomba kwa sauti huku akiwa amemshikiria mwanae mikono,Mama Jongo alilia huku akiwa hakui kitu gani anacholilia hama ni furaha au hudhuni juu ya mtoto wake kupata msaada. “Mama nyamaza basi tuwape habari juu ya ujio wetu hapa”Mwanamke mmoja wa makamo alisema “Sawa mama nawasiliza”Mama Jongo aliwajibu huku akifuta machozi kwa ncha ya kanga yake “Mimi naitwa Jeska na mwenzangu hapa anaitwa Mwamvita na huyo hapa ni Jonh” “Karibuni sana” Jongo aliwakalibisha “Tumekuja hapa kwa ajili yako Jongo” “Kwa ajili yangu…kivipi yaani mnatokea wapi?” Jongo alianza kuwahoji “Sisi ni wafanyakazi toka shirika la Good neigbour usaidia watoto walio kwenye mazingira magumu” “Nashukuru kuwafahamu karibu sana” “Tunashukuru pia, tumekuja hapa kwa ajili ya kukupa taarifa ya kwamba umechguliwa na shirika letu kukusomesha ufundi wowote ili uweze kujikimu kimaisha hapo baadae je upo tayari?” “Nipo tayari tena nawashukuru sana kwa moyo wa kujitolea” “Usijali kijana sisi tupo kwa ajiri ya kusaidia jamii hivyo basi kilio chako tumekisikia na sasa tupo tayari kukusaidia” “Sawa nashukuru sana”
Watu hao wanawake wawili na mwanamume mmoja walikuwa mbele ya nyumba ya mama Jongo wakiongea na kumpa ahadi kijana aliyekuwa amekwisha kata tamaa kipindi kirefu.Ilikuwa kama ndoto kwa Jongo kusikia maneno ya kusaidiawa,kwenda kusoma kwake siku zote ilikuwa ndoto isiyokuwa na mwisho wake.Hakika alisikitika sana alipomfikiria mama yake kubaki nyumbani pekee akitafuta cha maana ili kujikimu kimaisha.Kati ya wageni hao yule mwanamume aliyekuwa mrefu mwembamba alikuwa ni mtu makini sana wala hakuwa akicheka muda wote tangu alipofika pale alikuwa mtu wa kununa tu wala hakuufungua mdomo wake na kutoa kauli sasa aliongea.Mwanaume huyo wa makamu alikuwa amechomekea vizuri shati lake alikuwa akimwambia Jongo kile ambacho alipaswa kukifahamu kuhusu Good neibour inahusiana na nini.Kutokana na uwelewa wake mkubwa kuliko umri wake mara moja Jongo alielewa na kufahamu kile ambacho alipaswa kufanyiwa kwa wakati huo.Kusaidiwa na kupata msaada ilikuwa ni jambo jema kabisa kuliko kitu kingine,alichoambiwa Jongo na mama yake kutoka kwa washirika hao ya kwamba Jongo alitakiwa kwenda kusomea kitu chochote ambacho alikipenda na kile ambacho kinaendana na mazingira yake sababu ya ulemavu wa uwoni (kipofu).
Jongo alikuwa na wakati mgumu kuchagua kile ambacho alitaka kusomea alipenda sana kuwafundi makenika au fundi umeme lakini hakuelewa jinsi gani ataweza kufanya kazi yake kwa umakini yote sababu ya upofu ndio aliyokuwa kikwazo kikubwa kutoka kwake.Lakini Jongo hakukata tamaa ndani ya mawazo yake halijipa moyo pale alipokuwa akimwangalia mwanaume huyo akiwa na kidaftari kidogo na kalamu yake ikiwa imeegemeza ndani ya daftari akiandika.Hapo Jongo akapata hamasa sasa akafunua mdomo wake na kusema kile alichodhamilia kukisema “Napenda kuwa mwalimu,niwafundishe watoto wenye ulemavu kama mimi ili waweze kupata elimu na kuona ya kwamba walemavu nao wanaweza”Jongo alimaliza kusema maneno hayo huku akiwa ameinama chini machozi yakimlengalenga,haraka mama yake alimkumbatia mtoto wake kwa majonzi makubwa. Bwana yule mrefu aliyekuwa akiandika maelezo juu ya kalatasi yake alimwambia Jongo na mama yake ya kwamba Jongo anatakiwa kuelekea jijini Dar es Salamu kwa ajili ya kwenda kutafutiwa na hatimaye kuanza chuo cha uwalimu ambacho atalipiwa na shirika hilo la Goodneighbour.Jongo alivyosikia maneno hayo Laa! Hakuamini kile alichokisikia alirukaruka kama mtoto mdogo kwa manjonjo aliwakumbatia wageni hao nao wakafurahi na kukumbatiana kwa furaha. Siku iliyofuata asubuhi na mapema Jongo alikuwa tayari ameshajiandaa akiwasubili wageni wale waliokuja jana nyumbani kwao kumfuata.Wageni hao walikuwa tayari wameshawasiliana na wenzao na kujenga mazungumzo juu ya kumchukua kama walivyoagizwa na mkuu wao kutoka Goodneighbour kama wanavyojulikana.Jongo na mama yake walikuwa katika mazungumzo,mama yake alimwambia kile ambacho kilikuwa moyoni mwake.Jongo hakuwa na la kusema zaidi aliishia kulia na kumungonya maneno kama aliyeshikwa na kugugumizi.Lakini ukweli ulibaki kuwa Jongo anaondoka kuelekea jijini dar es Salaam.
Kwa mbali walionekana wageni wale waliokuja Jana nyumbani hapo sasa walikuwa wamewasili wakiwa hawana mafurushi mengi kama jana yake.Walipofika hapo walimchukua Jongo na kumuacha mama yake akiwa kwenye majonzi makubwa lakini moyo alimshukuru mungu wake kwa kile alichomtendea mtoto wake.Jongo aliongozana na wageni hao na kupakiwa kwenye gari na safari ya kuelekea jijini Dar es Salaam iliponza.Muda mwingi Jongo alikuwa mtu mwenye mawazo hakujua kitu gani kilisababisha mpaka kuwa katika hali hiyo alimuwaza sana mama yake kwani yeye ndio aliyekuwa ndugu pekee kwake.Hakuwa tayari kumuacha mama yake lakini kwa msaada alioupata wala hakuona tabu ndio alifurahia kupita maelezo hakika kitu moyo wake ulipenda sana kusoma.Baada ya kufika dare s Salaam taratibu zilifanyika wahusika walishauriana na maamuzi yakafanyika Jongo akapelekwa chuo cha ualimu West Dar es Salaam Teachers Collage.Aliandikishwa na kuanza masomo yake huku akiwa amepangiwa hosteli kwa muda maalumu. Jongo alianza masomo yake katika chuo cha uwalimu West kilichopo manispaa ya Ilala,Jongo alikuwa mtu mwenye mashaka makubwa kabla ajaanza chuo lakini muda ulivyokuwa ukizidi kwenda ndivyo naye alivyozidi kuyazoea mazingira chuoni hapo.Alikuwa akipenda sana kufuatilia masomo kile alichokuwa akifundishwa yalimuingia pima ndani ya ubongo wake, hata pale masomo yalipokuwa yanamtatiza ambapo hakuelewa umfuata mwalimu wake na kumuomba amuelekeze kwa mara nyingine tena.Waalimu walikuwa na mazoea nae wala hawakuwa na kinyongo juu ya yake hata wanafunzi wenzake alielewana nao vizuri bila matatizo yoyote.Siku zilipita miezi nayo ikasogea sasa yafikia miezi mitano sasa tangia Jongo kuanza masomo chuoni hapo.Siku moja Jongo akiwa anajisomea darasani kwa mbali alisikia sauti kutoka nje ya darasa,sauti hiyo ilimchanganya na kumpa wakati mgumu alijalibu kuisikiliza kwa makini sana sauti hiyo lakini akubahati kuikumbuka vizuri sauti hiyo ilikuwa ameisikia wapi na je mwenye hiyo sauti yenyewe ni nani.Alijifikiria mara mbili mbili mwishowe tena baadae sana mtu huyo ameshaondoka ndipo alipoikumbuka sauti hiyo ilikuwa ya msichana mmoja mrembo kwa kipindi kirefu sana hakupata kuisikia sauti hiyo lakini kwa uwelewa wake macho hakuona lakini kwa hisia na masikio yake alijua na kutambua kila kitu kilicho mbele yake. Laah! Alipata kiwewe. Shamsa Samir yule msichana waliyekuwa wakiishi pamoja Mwanza, yule msichana aliyekuwa akimpenda siku zote akimsumbua na kumlilia ili hasiondoke na mama yeke,leo hii anaisikia sauti yake imetokea wapi,au miujinza au ndotoni hapana Jongo hakutaka kukubali haraka alinyanyuka kwenye kiti chake akaishika fimbo yake na kuanza kuongoza njia kuufuata mlango.Lakini kabla hajafanya dhamira yake mlangoni alisikia sauti ya mwalimu akiingia ndani ya darasa hilo ikabdi Jongo kurejea kwenye kiti chake akakaa.Wakati mwalimu akifundisha Jongo akili yote ilikuwa juu ya sauti aliyoisikia hakutaka kukubali kama kweli Shamsa yule msichana ampendaye dhati na kipindi kirefu sana wamepotezana baada ya kuondoka jijini Mwanza na kuamia Morogoro na mama yake.Lakini yawezekana akawa yeye Shamsa ndiye aliyekuwa amefika pale kwa ajiri ya kutembelea au kuna kitu ambacho amekifuata au inawezekana akawa naye anasoma chuoni hapo. Muda wote aliona kama vile yupo ndotoni akujua Shamsa aliwezaje kufika shuleni pale.
******** Wakati shamsa akiendelea kuishinyumbani kwa Shangazi yake alionekana kuwa ni mtu mwenye mawazo sana kuhusu habari ambazo alimwambia Shangazi yake juu ya alichokuwa kinamsumbua.Shamsa aliona wazazi wake watakuwa wametendea kosa kutangaza kwa kila mtu kile ambacho kilikuwa kinamsumbua.Mwenyewe hakujua kama shangazi yake alikuwa mgonjwa angali angejua kama Shangazi yake alifahamu juu ya ugonjwa wange angefika huku akijifanya bado mgonjwa.Kule kulipomfanya kuwa na furaha ndipo kulipeleka mpaka Shangazi yake kumuuliza kile alichokuwa akiumwa huko nyumbani kwao Mwanza.Siku iliyofuata Shamsa aliamka saa sita mchana kutokana na uchuvo wa safari alichelewa kuamka,Shangazi Zuwena alimka mapema na kutengeneza kifungua kimya akanywa na kutoka kuelekea kwenye biashara zake huku akimuacha Shamsa akiwa bado amelala.Wakati Shangazi akitoka na kuondoka mlinzi alimuona hivyo alijua moja kwa moja Shamsa alikuwa bado yupo ndani amelala,wakati huo walikuwa wamebaki watu wawili tu ndani ya nyumba hiyo ambao ni Mlinzi na Shamsa aliyekuwa chumbani kwake amejifungia.Tofauti na siku zote Mlinzi alikuwa na shauku ya kutaka kujua Shamsa kama ameamka au bado amelala,taratibu alinyata mlinzi na kufungua geti akimchungulia Shangazi zuwena alipoelekea.Alipolidhika ya kwamba Shangazi huyo ametoka kwa safari hisiyokuwa ndefu sana kwani hakumuaga zaidi ya kumwambia anatokana.
Haraka mlinzi alifunga geti kwa komeo na kuingia ndani kwa nia ya kutaka kuonana na Shamsa.Kwani mlinzi huyo tangia usiku uliopita alipomuona mtoto wa bosi wake amekuwa msichana mrembo alivutiwa nae, alimpenda na kumtamani hakuelewa kwa kiasi gani alivyotokea kumpenda msichana huyo mdogo.Kila alipokuwa akipiga hatua kuelekea ndani ya nyumba hiyo mapigo ya moyo wake ndivyo yalivyozidi kuongezeka,aliufikia mlango na kushika kitasa akafungua na kuingia ndani alipitiliza mpaka sebuleni.Alipofika sebuleni alikaa sofani huku akipiga piga kirungu chake mkononi macho yake yakiwa juu ya mlango wa chumba cha msichana huyo.Alikikagua chumba hicho kuanzia juu mpaka chini,akaangaza huku na kule akitafuta namna ya kukikalibia na hatimaye kuingia ndani ya chumba hicho.Maji yalizidi unga anganyanyuka na kukifuata chumba hicho na kushika kitasa,mlango mkafunguka akazama ndani huku akinyata bila kugundulika wala kumshtua aliyelala ndani ya chumba hicho.Mlinzi alisogea mpaka kilipo kitanda cha msichana huyo bila kujitambua wala kujielewa mlinzi aliona kama yupo dunia nyingine jinsi alivyokuwa akisisimka.Mwili mzima jasho lilimtoka huku naniliu yake ikiwa imesimama dede pale alipomuona Shamsa akiwa amelala kifudi fudi huku shepu ya msichana huyo mweupe upande wa nyuma akiwa amefungashia vilimchanganya kupita maelezo. Hee! bwana hee nikwambie!!! …
Kweli Shamsa alikuwa amefungashia tena tako kubwa lilikuwa nyumba chini ya mgongo wake, alikuwa mweupe kama shombe shombe huku sura yake ikiwa pana iliyochongoka vizuri na midomo ya kuvutia.Kiukweli mtu aliyekuwa akipita mbele ya msichana hacha kuchanganyikiwa kwao wengi walishindwa uvumilivu walimfuata kabisa na kumtongoza lakini Shamsa aliwatolea nje huku akijua anaye mtu mmoja ambaye moyo wake ulimchagua. Ilipita kama dakika kumi mlinzi huyo akiwa bado anamwangalia kuanzia juu mpaka chini ya miguu yake, hakuamini kama kweli msichana aliyekuwa mbele yake ndiye aliyekuwa yule mtoto aliyekuwa akimbeba na kumbembeleza kipindi cha nyumba kama kweli watoto wa kike hawachelewi kukua alijisemea moyoni mwake.Hakutaka kusubiri akatoa mkoto wake na kuanza kumpapasa Shamsa ambaye alikuwa mbali na usingizi wala hakuelewa kama kuna mtu aliyekuwa akimsumbua kwa wakati huo.Wakati mlinzi alipokuwa alifanya yake ghafla Shamsa alishtuka na kuamka uwiii! Shamsa alizubaa dakika nzima akimwangalia mlinzi akijibalaguza mahali hapo, haraka Shamsa hakutaka kusubili alipiga ukemi mkubwa ulimfanya mlinzi huyo kuogopa looh! Ulitaka kunibaka wewe baba vipi?”Shamsa aliongea baada ya kumuona mlinzi akitimua mbio kuufuata mlango na kutoka nje. Shamsa alijikagua vizuri na kujikuta yupo safi taratibu alitoka na kumfuata mlinzi. “Hivi wewe unaitaka kazi yako hama?” “Hapana mwanangu nisamehe nilikuja tu kukuamsha kumbe ulikuwa umelala”
Kabla Shamsa hakumaliza kuzungumza kile alichokuwa anamwambia mlinzi huyo roho ilimdunda macho yalimtoka Kama mjusi aliyebanwa na mlango pale aliposikia mtu akigonga geti kwa jazba.Ooo! Mlinzi aliruka juu huku rungu lake likidondokea kule mwili ukimtetemeka tofauti na mwanzo alijua hakuwa mwengine zaidi ya Shangazi Zuwena, haraka Shamsa aliondoka na kuingia ndani huku akiwa mtu aliyekeleka.Mlinzi alikuwa na mashaka makubwajuu ya Shangazi zuwena hakujua jinsi gani atakavyomkolomea kama atakuwa amesikia maongezi yaliyokuwa wakionge na Shamsah.Mlinzi hakujali sana alisogelea geti na kufungua mlango kisha Shangazi Zuweni alimpiga jicho kali sana mpaka mlimzi akaogopa,hakujua amepatwa na nini mawazo yake yote Shangazi amesikia kile kilichotokea.Bila kutarajia alimuona Shangazi akimsogelea na kumuuliza kulikoni mpaka akachelewa kumfungulia mlango,lakini mlinzi aliishia kumuangalia kisha akatikisa kichwa kwa masikitiko huku akisogeza pembeni na kumjibu ya kwamba alikuwa ndani ndio maana alichelewa kufuangua.
Shangazi Zuwena alikuwa amefura kwa hasira alimwangalia mlimzi huyo mara mbili mbili kisha alimtazama kwa ghadhabu na fedheha akimtaka usiludie tena tabia hiyo,mlinzi alimkubalia huku akimnyooshea mkono na kumuomba msamaha.Shangazi huyo wala hakusema kitu zaidi aliongoza njia na kuingia ndani.Shangazi alipitiliza moja kwa mpaka ndani alishangaa alipomkuta Shamsa akiwa mtu mwenye mawazo,alimsogelea na kumuuliza kilichomsibu. “Kitu gani kimekusibu binti yangu?”Shangazi zuwena aliuliza kwa mashaka “Hakuna kitu Shangazi”Shamsa alijibu kwa unyonge “Niambie Shangazi….au ndio yale matatizo yako?”Shangazi alimhuliza “Hapana Shangazi nimeota tu ndoto mbaya Shangazi” “Oooh! Pole sana mwanangu”Shangazi alimpa pole Shamsa “Ahsante Shangazi …soon nitakuwa sawa” “Sawa mwanangu basi mimi ngoja nikaandae kifungua kinywa”Shangazi alisema “Sawa Shangazi”
Katu Shamsa akutaka kumwambia ukweli wa kile kilichotokea Shangazi yake alifikiria kumuona Shamsa kwenye hali hiyo alifikiri kuwa ni yale matatizo aliyoambiwa na Baba Samir pamoja na mkewe juu ya hali aliyokuwa nayo mtoto wao.Shamsa alifurahi alipomuona Shangazi yake alivyomuelewa na kama angekuwa mama yake basi lazima angetakiwa kuongea kile kilichomsibu lakini kwa shangazi huyo haikuwa hivyo.Hata hivyo ndivyo Shamsa alivyopenda hakutaka kumsumbua Shangazi yake wala hakuona haja ya kumuelezea kile ambacho kilimtokea juu ya mlinzi hiyo aliyekuwa kama ndugu kwake.Akayamezea moyoni mwake yakabaki na kuyafutika kifuani mwake kwa mashaka mazito huku akimuacha mlinzi naye akijiuliza juu ya hali hiyo huku akijiapia hatoweza kwenda tena kumsumbua msichana huyo ambaye ni mtoto wa bosi wake kwani aliipenda sana kazi yake hivyo hakuwa tayari kupoteza kazi kwa ajiri ya mapenzi.Siku zilipita na miezi kadhaa imekatika huku Shamsa na mlinzi wakibaki kuwa kama mtu na mzazi wake kwani Shamsa alimtahadharisha kwa mashaka na kazi yake juu ya kumfuatilia tena anaweza kumshitakia baba yake huko alipo na kupelekea kufukuzwa kazi kwa mzee huyo ni kitu ambacho kilikuwa kigumu kwake.
Siku zilipita na hatimaye miezi ikafikia mlinzi amesahau kabisa kile kilichotokea kati yake na Shamsa, kwani hakuna aliyejua juu ya kilichotokea kati ya wawili hao pekee.Siku moja Shamsa alikwenda kutembelea vyuo vya Uwalimu mbalimbali ambavyo vilikuwa wakisoma marafiki zake aliosoma nao jijini Mwanza na Dar.Siku hiyo Shamsa alianzia chuo cha Uwalimu Amazon kisha ilipofika saa sita akaelekea chuo cha West kilichopo Jirani na nyumbani kwao Ilala.Alipofika hapo Shamsa alifurahi alipokutana na wanafunzi wengi aliosoma nao shule ya msingi Ilala Boma,wengi wao walikuwa wasichana kama yeye wengine walimpongeza na kumshukuru kwa kufika shuleni hapo kuwatembelea.Shamsa akuwa na mashaka zaidi alikumbatiana na wenzake kwa kukutana shuleni hapa na kuwapa somo juu ya elimu aliyokuwa nayo kisha kwa pamoja na marafiki zake wakiwa na baadhi ya waalimu wa chuo hicho walimtembeza kujionea mazingira ya chuo hicho.Shamsa alifurahi sana alitembelea kila sehemu iliyozunguka mandhali ya shule hiyo ilivutia alitamani siku nzima ashinde shuleni hapo.Baada ya muda kwenda na kiza kuanza kuingia Shamsa aliagana na marafiki zake kisha safari ya kurudi nyumbani ilipoanza……….
Kipindi cha miezi miwili mbele Shamsa alikuwa amefanikiwa kupata kazi jijini Dar es Salaam maeneo ya Posta.Alifanya kazi ndani ya shirika la usafirishaji,kwa kipindi kifupi cha muda wa miaka miwili Shamsa alikuwa mtu mwenye mafanikio makubwa kwa sana aliweza kuwatunza wazazi wake pia licha ya kuwa akiishi ndani ya nyumba ya wazee wake lakini pembeni alikuwa na nyumba yake hakutaka kukaa peke yake aliamua kupangisha wapangaji waliokuwa wakimlipa kodi kama kawaida.Pia alifungua biashara zake binafsi ili kuweza kuendesha maisha ya kila siku.Jambo lake la kuolewa halikuwa ngeni kwa wazazi wake ila hakuwaambia atakae muoa nani kwani bado alikuwa anamtafuta Jongo. Siku zote Shamsa alikuwa ana lake moyoni,alifanya kazi kwa bidii matarajio yake kupata pesa na kujimiliki vizuri kwa hilo liliwezekana kwa asilimia zote.Alifanya kazi kwa moyo wa kijituma na kupata mafanikio mazuri yaliyopelekea kuheshimiwa kila sehemu na aliyokatiza aliitwa malkia wa nguvu.
Mnamo tarehe mbili mwezi wa saba mwaka 1999 .Siku ambayo Mzee Samir na mkewe Bi.Ramla walikuwa wamerejea jijini Dar es Salaam baada ya Bwana Samir kumaliza mkataba wake wa miaka kumi na mbili ndani ya jiji la Mwanza.Kipindi chote hicho Bwana Samir na mkewe walifahamu juu ya maisha anayoishi mtoto wao baada ya kupata kazi,hakuna kilichohalibika zaidi ya Shamsa kuwataka wazazi wake waende kuishi pamoja ndani ya nyumba yake na nyumba yao waendelee kumuachia Shangazi kuishi hapo.Bwana Samir alifurahi na mkewe wakaenda kuishi kwenye nyumba ya mtoto wao Kigamboni.Bi.Ramla alikuwa na kazi moja ya kumshawishi mtoto wake kuolewa ili aweze kuzaa watoto naye apate wajukuu.Shamsa hakuwa tayari kufuata ushauri wa mama yake kwani alikuwa na lake rohoni juu ya Jongo,alimpenda na kumdhamini kama barafu wa moyo wake.Alijipangia mwenyewe lazima ipo siku atakutana na Jongo kisha watafunga ndoa. Siku moja Shamsa wakati anatoka kazini akamkuta mama yake yupo Nyumbani tena sebuleni akiwa na Mvulana pamoja pamoja na Msichana ,Shamsa alimsalimia mama yake pamoja na wale wageni aliokuwa nao sebuleni hapo kisha kuwakalibisha.Shamsa akiwa sofani aliwachangamkia na aliongea nao kidogo,hapohapo mama yake alichukua nafasi na kuwatambulisha kwa Shamsa wageni hao kuwa yule mvulana mrefu mweupe kidogo anaitwa Abdul na yule Msichana anaitwa Aisha ila hakumwambia lengo la kuja na wale wageni.Baada ya maongezi machache na utambulisho Shamsa aliomba awaache sababu yeye ametoka kazini muda huo hivyo anaenda kukoga.Shamsa aliingia chumbani kwake na kubadilisha nguo kisha alielekea maliwatoni kuoga.Shamsa alipomaliza kuoga alitafuta nguo yake nadhifu na kuishusha mwilini mwake. Muda mfupi alitoka na alipofika sebuleni aliwakuta vile vile wale wageni wakiongea kwa siri kubwa na mama yake.
Simulizi : Chaguo Langu Ni Wewe Sehemu Ya Nne (4) Bi.Ramla pamoja na wageni wake walikuwa wakiongea maneno ya chini kwa chini, Shamsa alipitiliza mpaka mlangoni na kumuaga mama yake anakwenda Saluni kutengeneza nywele zake kutokana na ugeni huo Mama yake akamwambia kuwa akirudi atamkuta anamsubili kwa hamu kubwa sana kwani ana mazungumzo ya maana juu yak. Shamsa alimwambia Mama yake atochelewa kurudi kwani anakwenda kuosha tu nywele na sio kusuka kama ilivyo siku nyingine. Kipindi chote hicho ambaye ni Aisha na Abdul pamoja na Bi.Ramla walikuwa kwenye maongezi ambapo Mama Shamsa alimtaka yule Abdul afanye awezalo aweze kumuoa mwanae kwani amemchagua yeye awe mume wa mwanae.Abdul alimwambia Bi.Ramla kuwa asiwe na mashaka kwa hilo atalitimiza kwa muda mfupi tu ujao. “Shaka ondoa nitahakikisha kila kitu kinakwenda sawa na Shamsa atakuwa mke wangu”Abdul alisema huku akijiamini “Nimefurahi sana kusikia hivyo mwanangu nitakuwa nawe kwa kila jambo” “Usijali Bi.Ramla Shamsa atafurahi mwenyewe maana kila kitu kitakwenda sawa nitajitahidi Ili kumpa furaha mtoto wako na si vinginevyo”Abdul aliongeza “Itapendeza maana hata yeye atafurahi mwanangu kupata mume kama wewe ili kuondokana na mawazo ya huyo kipofu wake” “Ndio maana nimekwambia tulia tu niachie mwenyewe mambo haya yatakwenda sawa”
“Hakika nakuamini Abdul wewe upo makini sana kwa jambo hili” “Usijali mama pia waweza kuniambia kama mwahitaji kitu chochote nimfanyie huyo kijana?” “Hapana mwanangu kwa wakati huu naomba umchote kwanza Shamsa hapo baadae tutaona kama akikataa basi tutajua jinsi ya kumfanya Jongo” “Sawa ila uwe makini sana kile ambacho unahitaji kukifanya, kumpatia pesa mtu na kufanya ukatili wa namna hii inatakiwa akili ya nyongeza” “Najua ninachokifanya ni kumlinda binti yangu juu ya kijana huyo kipofu, sijui kitu gani alichokipenda juu ya kipofu huyu, sijui nifanye nini ili aweze kuachana na mwanangu”Bi.Ramla alilalama “Lakini yawezekana Shamsa atakuwa na upendo kupita maelezo juu ya kijana huyo ujue moyo ukipenda vingine uwezi kuelewa” “Hata kama amempenda lakini mimi mama yake sijampenda kijana huyo awe na mwanangu,pia nakupa pesa yangu ili uweze kufanya kile nilichokwambia” “Sawa Bi.mkubwa nimekuelewa sana nitafanya kile nilichokuahidi kwamba nitakuwa naye siku zote za maisha yangu pesa yako tu mama”Abdul alisema huku akiwa mtu mwenye hali ya ulevi Baada ya masaa machache Bi.Ramla akiwa na wageni wake ambao Shamsa hakuwa akiwafahamu kwa wakati huo.Waliongea mambo mengi ambayo Shamsa hakujua kile kinachozungumzwa na kuja nyumbani hapo kwa wageni hao wakiwa na mama yake.Baada ya muda kwenda Shamsa akarudi na kuwakuta Mama yake na wageni hao wapo vile vile kama alivyowaacha Shamsa alipitiliza na kuingia chumbani kwake huku akiwa na mawazo tele kichwani,hakujua hatma yake juu ya kumpata Jongo alimtafuta kila sehemu lakini ilishindikana alijaribu kutembea morogoro nzima kumtafuta Jongo pia hakufanikiwa kumpata hivyo ndivyo ilivyokuwa na mawazo tele kichwani yamemuandama.Shamsa akiwa juu ya kitanda chake chumbani amejipumzisha muda huo alitega masikio yake aliposikia sauti za wageni hao wakiagana na mama yake kisha wakaondoka.Siku hiyo Shamsa aliboleka sana pale alipomuwaza mama yake kusudio lake nini hasa kuja na wageni nyumbani kwake kisha kumtambulisha kwa majina yao tu na sio kama kufahamishwa kiundani kama ndugu au majirani. Shamsa alipohakikisha wabeni hao wameonda kwa kuchungulia dirisha kwake na kuangalia getini aliwaona wageni hao wakitokomea nje na mama yake alifunga geti na kurudi tena ndani. Shamsa naye alituka mpaka sebuleni na kumkuta mama yake akiwa amekaa macho yangali kwenye runinga alimwangalia mama yake kwa mashaka makubwa hakujua kitu gani kilikuwa kimetokea mpaka akaongozana na watu kama hao.Siku hiyo mama Shamsa alikuwa kwenye mawazo sana juu ya kumuondoa Jongo mikononi mwa mtoto wake, alijiapia lazima atamtafuta Jongo kwa udi na uvumba ili kumuangamiza kibasa hasikuwepo machoni mwake. “Mama, kitu gani ambacho kinakutatiza naona kama una wawazo sana? Shamsa alimuuliza mama yake baada ya kukaa kitini “Hapana binti yangu, nipo kawaida sana mwanangu”Bi.Ramla alimjibu “Nilitaka kukujuza ya kwamba Naomba uniambie kile ulichotaka kuniambia, maana ulisema una mazungumzo nami”Shamsa alimwambia “Sawa, nilichotaka kukuambia ya kwamba Baba yako ameamua ya kwamba tuondoke hapa nyumbani kwako na kurudi katika nyumba yetu kutokana na Shangazi yako kuondoka nyumbani hapo na kuamia katika nyumba yake hivyo nasi tunatakiwa kuilinda nyumba yetu mwanangu” “Sawa mama haina tatizo kama mmeamua hivyo basi sina pingamizi kwenu”Shamsa alimjibu mama yake “Kuanzia sasa hatuonekana hapa isipokuwa siku moja moja tutakuja kukusalimu mwanangu wala usijali” Bi.Ramla alimpoza mwanae “Lakini mama sijajua kuhusu wito wa wageni uliokuja nao ndio kina nani?” “Shamsa mwanangu si nimekutambisha kwao mara hiyo umesahau mama?”Bi.Ramla nae alimtupia swali mwanae “Sio kwamba nimewasahau la hasha sijawai kuwaona wala kuwasikia hapo kabla” “Sawa yule msichana anayeitwa Aisha ni mwalimu mwenzangu yule ni mgeni shuleni hivyo amekuja kuniulizia kuhusu ratiba ya kesho kazini”Bi.Ramla alijitetea “Okay sawa je, yule mwanaume?”Shamsa alimtupia swali lingine mamaye “Yule mwanaume ni rafiki wa yule mwalimu niliyekueleza mwanangu usiwe na mashaka sana juu ya ugeni huo wana nia nzuri nawe, amekuulizia sana maana wanapenda kuwa rafiki yao” “Hee! Mama Urafiki wa aina gani huo?”Shamsa alihamaki “Urafiki wa kawaida tu mwanangu wala sio kwa nia mbaya”Mama yake alimjibu “Sawa, tuachane na hayo nakupa funguo ya akiba mama kama siku nyingine unakuja upite tu ndani moja kwa moja maana mara nyingi naweza kuwa sipo nyumbani” Mama yake alifurahi na kumshuku mwanae.
Siku moja Shamsa alijipangia ratiba ya kurudi mapema kazini ili apate muda wa kwenda kutembea kwa marafiki zake pamoja na kuonganisha nyumbani kwao Ilala kwani ndipo yalipokuwa makazi mapya kwa Jongo. Lakini jambo hilo hakulifahamu kumtafuta hata siku hiyo alikuwa kama alivyokuwa kawaida yake alipotoka alielekea moja kwa moja hadi nyumbani kwa baba yake lakini Ilala nzima alizunguka hakumuona japo alisikia kuna mtu akiitwa sana kwa jina hilo ila hakuwa na uhakika kama anayeongelewa alikuwa Jongo yule anayemtafuta.Shamsa alikuwa kawaweka watu wa kumsaidia kumtafuta Jongo pia alipojaribu kufanya mawasiliano nao hakupata jibu la kulizisha kwani Jongo hakuonekana sehemu popote pale. Je, alikuwa wapi, kama ndani ya chuo jina lake lilikuwepo ndani ya orodha ya wahitimu wa chuo hicho sasa amekwenda wapi na Je, shule ipi aliyopangiwa kufundisha baada ya kumaliza elimu yake? ………
Mawazo yote yalikuwa yamemzunguka Shamsa juu ya mtu ampendaye Jongo alikuwa amemuacha kwenye wakati mgumu kwanini hakumwambia mapema kile ambacho kilikuwa kikimtatiza.Siku hiyo baada ya Shamsa kumkosa Jongo alirudi nyumbani akiwa amechoka sana kutokana na kazi ndefu.Alipofika mlangoni Laah! Alishangaa na kukuta mlango upo wazi hakushituka alijua ni mama yake hata alipoingia sebuleni alikuta mkoba kwenye meza iliyopo sebuleni hapo, ulimfanya aondoe shaka kabisa Shamsa alijitupa sofani ili kujipumzisha kwenye kochi.Ghafla akiwa hana hili wala lile macho yakiwa juu ya dali alisikia sauti ya kiume ikimsalimia alistuka na kunyanyuka sofani haraka na kusimama wima na kugeuka mzima mzima hakutaka kuitikia wala kusema neno.Alikuwa mwanamume wa mashaka machoni mwake alijionyesha alimkumbuka fika yule mwanaume ndiye yule aliyewakuta nyumbani hapo akiwa na mama yake pamoja na yule msichana.Abdul alipomwambia kuwa yeye ametumwa na mama yake kuja kumliwaza, Shamsa alimwangalia kwa jicho kali na kushangaa ndipo alipohoji.
“Umefikaje ndani ya nyumba yangu wewe?” “Mama yako ndio aliyenikabizi funguo ili nije kukusaidia kazi za hapa nyumbani pamoja na kuwa na wewe siku ya leo” “Hee! wewe una maana gani sasa mpaka unadhubutu kuingia ndani kwangu?’Shamsa alimuuliza kwa hasira “Nimeamua kufanya hivyo kwa sababu yako nakupenda ndio maana nimekuja kuwa nawe siku ya leo”Abdul alionge kwa kujiamini “Yaani wewe heti uwe nami inawezekana kweli?” Shamsa alimjibu kwa dharau “Inawezekana Shamsa niamini nakupenda na nina uwezo wa kukutimidhia kwa kila kitu” “Hapana sihitaji mwanaume wa aina yoyote” “Nakuomba sana Shamsa wewe ndio chaguo langu…..Nakupenda mama”Abudul alilalama “Hee! we vipi utanipendaje wakati hatujuani hata”Shamsa alisema “Nipo chini ya miguu yako Shamsa” “Nimesema sitaki naomba utoke ndani ya nyumba yangu”Shamsa alisema kwa ukali “Kwa hilo Shamsa umefika mbali” “Iwe mbali au karibu nishasema ondoka ndani ya nyumba hii”Shamsa aliongeza kwa ukali “Sawa kuondoka nitaondoka lakini sio kwa kunifukuza kama hivyo”Abdul alilalamika “Utaondoka muda gani sasa?”Shamsa aliuliza kwa mashaka “Muda si mrefu nitatoka ila nataka nikwambie kiu” “Sema nakusikiliza” “Si nimekwambia nakupenda”
Muda wote Shamsa aliona vituko kutoka kwa kijana huyo hakutaka kuongea zaidi alimwambia anaenda chumbani kwake kupumzika muda mfupi ujao anataka kutoka kwenda kwenye biashara zake binafsi.Abdul alikubali huku akimwangalia Shamsa kwa jicho la tamanio na kumuambia ya kwamba anampenda na kumdhamini sana yupo tayari kwa kila jambo ili kuhakikisha anakuwa mikononi mwake.Kisha Jongo alimwambia ameshamchagulia nguo za kuvaa ambazo alimnunulia kama zawadi kwa upendo wake zipo ndani ya mfuko,Abdul alipomaliza kusema maneno hayo alichukua mfuko uliokuwepo hapo mezani na kumkabidhi. Shamsa aliupokea kwa mashaka makubwa akaufungua palepale na kuangalia kilicho ndani ya mfuko huo kama kweli ni nguo.Shamsa alitabasamu na kumwangali Abdul ambaye alikuwa na sura yenye bashasha, akaondoka na kuingia chumbani kwake.Alipoingia tu chumbani aliziangalia na kujalibu nguo hizo, alipoona zimemkaa sawa na kumpendeza aliziweka vizuri kitandani kisha alienda kuoga na baada ya muda alirudi. Hata pale alipotaka kuvaa nguo nyingine alishindwa moyo ulimsuta alijiona mkosaji kuupokea mzigo huo na kuuweka tu ndani ,akaamua kuvaa alizonunuliwa na Abdul ili kumfurahisha , baada ya kuvaa alitoka hadi sebuleni ili kumuonyesha Abdul zawadi aliyomnunulia ilikuwa imempendeza kweli Abdul alishangaa alipomuona Shamsa akiwa amebadilika na kuwa msichana mrembo wa huba.Shamsa alimshukuru Abdul kwa zawadi hiyo kisha aliongoza njia maana hakutaka kuzungumza sana na kijana huyo alimuaga kuwa anatoka kwa safari zake akimtaka naye atoke ili aweze kufunga mlango wa nyumba yake.Abdul hakutaka kutoka,badala yake aliendelea kukaa mahali hapo na kumwambia kabisa Shamsa kile alichokusudia kuwepo hapo nyumbani kwa siku hiyo, Shamsa hakuwa tayari alitoka na kumwacha Abdul ambaye mama yake alimtambulisha kama Rafiki wa mwalimu mwenzake Laah! Shamsa haikumuingia akilini kabisa, akawaza Abdul mwenyewe alisema ni mfanya kazi ambaye atamsaidia kazi za pale nyumbani.Kumbe hakuwa ni mwalimu bali ni kijana wa mitaani hakaona ni majanga sasa yamemkumba. Muda wa saa moja jioni Shamsa akiwa anarejea nyumbani kwake alikuta mlango upo wazi safari hii wala hakushituka kama mara ya kwana alishajua ya kwamba kijana huyo alikuwapo na wala hakuwa na dalili ya kuondoka siku hiyo.Wakati Shamsa akiingia ndani huku akitafakari juu ya kijana huyo kuvamia nyumba yake yote sababu ya mama yake Bi.Ramla,hakuwa na namna.Baada ya Shamsa kuketi sofani huku mawazo tele kichwani yametawala,Alikuja kustuliwa na Abdul akimwambia ya kwamba yeye alikuwa ameshapika na sasa chakula kipo mezani tayari ameivisha.Laah! salale Shamsa alishangaa akasimama wima na kumkatalia,Abdul akukubali kushindwa mwanaume kama yeye kubembeleza na kushawishi aliweza na ndivyo alivyofanya alimsogelea Shamsa pale aliposimama na kumwambia “Unajua jinsi gani nilivyoumia kutoka nje na kutafuta masoko ili nikuandalie chakula mpenzi wangu lakini mwenzangu utaki kula,sasa wataka nani ale mpenzi,nakuomba ule ata vijiko viwili tu vinatosha mpenzi nami nitapata furaha na buraha ndani ya moyo wangu”.Shamsa alimsikiliza kwa makini sana alimshangaa pale alipoingiwa na moyo wa huruma na kumuangalia Abdul kwa anavyolalamika akiwa chini ya miguu yake,Shamsa akaamua kula chakula hicho kilichopikwa na mkono wa mwanaume hasiyemjua.
Shamsa alikula chakula kwa mbwembwe huku aibu ikiwa imemkaba moyoni mwake. Na alipomaliza kula chakula hicho akamsifia Abdul kwa uwezo wake wa kupika chakula kitamu kama kile,alimshukuru kwa chakula kizuri Abdul alifurahi na kumtaka asiwe na shaka kwa hilo. Muda wote Shamsa na Abdul walikuwa kwenye maongezi ya hapa na pale huku wawili hao wakionekana kuwa na furaha ndani ya mioyo yao.Waliongea mpaka saa tatu ya usiku ndipo kijana Abdul alipoaga na kuondoka huku akimtaka Shamsa hasiwe na wasiwasi juu ya kile anachokifanya. Shamsa hakuwa na papala alimwangalia tu Abdul akimuaga kwa ukalimu wa hali ya juu.Walipoachana kwa Abdul kuondoka Shamsa alikuwa na maswali mengi yasiokuwa na majibu kuhusu mwanaume huyo ambaye alikuwa mgeni machoni mwake.Shamsa ni kama kawaida yake mawazo yake yalihama mara moja na kumfikiria kijana Jongo kile ambacho alikihisi moyoni mwake kumpenda sana kijana huyo kuliko kitu chochote.Asubuhi kulipokucha aliingia kwenye vituo vya watu wenye ulemavu ili kuweza kuhoji kama kuna uwezekano wa mtu kumfahamu Kijana Jongo au kubahatika kumuona, siku hiyo ilikuwa haina matumaini tena kwa Shamsa kwa jinsi alivyompenda Jongo kwani alirudi nyumbani bila mafanikio.
Siku zilizidi kwenda wiki siku zikapita bila Jongo kuonekana wala Abdul kuonekana akija nyumbani kwake,Shamsa mawazo yalimuendea kombo alijihisi kuumwa kila wakati lakini wala hakukubaliana na hali hiyo ya kushidwa.Alikaa chini na kujiuliza kile kinachomsumbua na hakujua hatma ya kijana ampendaye Jongo wala hakujua atampata wapi Jongo.Siku hiyo Shamsa alirudi mapema nyumbani alipofika alikuta tena mlango wa nyumba yake upo wazi, Shamsa alishtuka aliingia mpaka ndani na kuelekea hadi jikoni hakumuona mtu.Alitafuta huku na kule kila chumba akimwita mama yake lakini hakuna aliyemuhitikia basi aliingia chumbani kwake na kujitupa kitandani.Shamsa alikuwa ametingwa na mawazo mengi sana juu ya hali aliyokuwa nayo,alisikitika na kujutia huku akimlaumu mama yake juu ya hali aliyomuachia juu ya mwanaume anayemsumbua nyumbani kwake.Alijifikilia jinsi gani atamdhibiti Abdul ili asiweze kuinga tena nyumbani kwake bila ruhusa sababu ya funguo aliyokuwa nayo.Shamsa alikusanya mawazo yake na kupata jibu ya kwamba lazima abadili funguo ili aweze kumdhibiti kujana huyo hasiyemfahamu zaidi ya kuletwa na mama yake…..
Muda mfupi baadae Shamsa akiwa amejilaza kitandani ndani ya chumba chake alisikia Sauti ya mtu akikohoa katika bafu analolitumia ndani ya chumba hicho kwake.Alistuka na kukaa kitandani huku macho yake yakiwa kwenye mlango wa choo kilichomo ndani ya chumba hicho. Moyo ulimuenda mbio Shamsa sasa akiwa hajui hafanye nini kwa wakati huo, mawazo yakamjia akaamua kusubili ili kumuona mtu atakayetoka ndani ya choo hicho.Hakiwa hajui nani atakayetoka, alikaa ndani ya chumba chake huku akitetemeka hasira zimemkaba akitamani kuvamia chooni na kumtoa mtu huyo.Muda huo huo bila kupepesa Shamsa macho yamemtoka pima kuyaelekeza mlangoni mwa choo hicho, pale alipoona mlango wa msalani ukifunguliwa.Laaah! mdomo alihacha wazi, hakuamini macho yake pale alipomuona Abdul akitoka maliwatoni akiwa amevalia bukta tu, ulikuwa mtihani mkubwa sana kwa Shamsa, kwani Abdul alikuwa hedsome boy hasa, alivyoumbika kwa umbo lake matata lililojengeka kwa mazoezi Shamsa alijikuta akikaa chini macho ymeganda maungoni mwa Abdul. Alijikuta akimtamani sana na kile kifua chate kipana ilikuwa mtihani kwa Shamsa, mwanamke yoyote angetokea kumkuta kwenye hali kama hiyo basi lazima angeshawishika kwa uzuri wa Abdul.Muda huo huo Abdul nae alifahamu hali aliyokuwa nayo Yaani wewe umeamua kunifanyia Shamsa, hivyo alitumia nafasi hiyo kumsogelea mahali alipokuwepo Shamsa.Alipoona hivyo Shamsa aliamua kuangalia na kusogea upande mwingine huku akimtaka Abdu asimsogelee badala yake avae nguo zake.
“Yaani wewe umeamua kunifanyia kitendo kama hicho?”Shamsa alimuuliza angali macho pembeni “Ndio Shamsa sababu nakupenda sana nipo kwa ajili yako”Abdul alijibu kwa kujiamini “Hapana wewe utawezaje kunisaidia Mimi…sihitaji msaada wa aina yoyote” “Hapana sina msaada wowote kwako zaidi ya mapenzi nakupenda sana” Abdul alilalamika “Ndio nimekwambia sihitaji msaada wa aina yoyote kutoka kwako naomba uondoke nyumbani kwangu”Shamsa alisema kwa hisia “Sawa nitaondoka lakini sidhani kama kuna mtu akayetokea kukupenda kama mimi”Abdul alilalamika “Kama hayupo basi yupo njia anakuja wala sitakubali kuwa nawe” “Please Shamsa niangalie mara mbilimbili unifikilie maana nakupenda sana sipo tayari kukukosa”
Shamsa alinyanyuka na kutaka kuondoka ,kabla hata hajapiga hatua mbili mbele Abdul alimuwai na kumshika mkono,Shamsa aliruka kutaka kujiondoa mikononi mwa afla wakajikuta Abdul lakini ilishindikana kwani alikuwa ameshikilia vilivyo na kumdhibiti maungoni mwake.Kukulu kakala zilianza Shamsa akimtaka Abdul amuachie lakini Abdul aliendelea kumshikilia kinguvu.Ghafla wanajikuta wakidondoka kitandani kwa pamoja wakagalagala na kulifanya shuka kujikunja, Shamsa aliogopa sasa akakusanya nguvu zake zote kutaka kujiondoka kitandani hapo alishindwa kumbe Abdul alikuwa amemshika vizuri kiunoni looh! Shamsa aligwayana hakuweza kutoka hakatulia.Abdul akaona nafasi ndio hiyo kutaka kufanya kile alichodhamilia kukifanya, taratibu Shamsa akaanza kuingiwa na joto la huba baada ya kumgusa Abdul kifuani mwake kumbuka alikuwa na bukta tu wala hakuwa na nguo nyingine.Shamsa aliweweseka kutaka kutoka maungoni mwa Abdul lakini mwenzake alimng’ang’ania kisawa sawa wala hakuona haja ya kumuachia. “Lakini kitu gani inanifanyia wewe mwanaume”Shamsa alibwata huku akijaribu kujiondoa mikononi mwa Abdu “Unajifanya uelewi kinachotokea basi utaelewa tu”Abdul alisema huku pumzi zikimuishia “Nakuomba uniache tu ukijalibu kunibaka utanikosea sana “ “Hapana Shamsa ataka uwe na amani sababu nakupenda wewe”Abdul alimjibu “Niachie basi tuzungumeze, sasa unavyonibana hivi unafikiri nitawezaje kuongea” “Sawa basi kaa nakuacha mpenzi wangu”Abdul akamuachia Shamsa
Shamsa haraka alinyanyuka toka kitandani na kujiweka vizuri kisha alisimama wima kando ya kitanda hicho,hakika alimuhacha njia ya panda Abdul hakutegemea kama Shamsa ataweza kumchomoka kiaina namna hiyo.Sasa aliwezaje kumkosa tena mwanamke kama huyo,Abdul hakuwa na jinsi alimwangalia kwa jicho la matamanio makubwa,alimpenda na kumtamani sana ila hakuwa na jinsi tena kwani mali alihiacha mwenyewe.Shamsa alipitiliza moja kwa moja mpaka sebuleni na kukaa sofani huku akitetemeka.Muda huo huo Abdul nae alivaa nguo zake na kumfuata Shamsa sebuleni.Abdul alifika sebule akiwa na aibu moyoni mwake uso kaukinja huku akitazama chini wala hakuwa na haja ya kuangali kile kilichopo sebuleni hapo zaidi ya sakafuni. Shamsa alipomuona Abdul akikaa naye sofani Shamsa hakusema neno zaidi alimtakaAbdul aondeke na hakuwa tayari kumuona akiendelea kuwepo nyumbani hapo.Abdul hakuongea neno zaidi alivaa viatu vyake kisha akaondoka, baada ya Abdul kutoka muda huo huo Shamsa aliuwai mlango na kuufunga kwa ndani akarudi sofani huku akitweta.
Siku inayofuata hakutoka kabisa nyumbani kwake hata Abdul alipofika, alimkuta Shamsa yupo sebuleni aligonga mlango na alipofunguliwa Abdul aliingia moja kwa moja mpaka sebuleni.Baada ya kusalimiana Shamsa alimwangali kijana huyo huku akiwa na mashaka alimuuliza kile alichomleta tena ndani ya nyumba hiyo,Abdul alimjibu ya kwamba ametumwa na mama yake kuja kusuluisha kwa yale yaliyotokeaa.Shamsa akuendelea kuongea zaidi alijiuliza kama mama yake aliyajua vipi yale yaliyotokea jana,alishikwa na mshangao zaidi pale alipomuona mama yake akija nyumbani kwake bila ya taarifa ina maana walikuwa msafara mmoja Abdul na mama yake. Shamsa alijiuliza bila kupata jibu mwishowe alisikia mlango ukigongwa na mama yake akaingia ndani huku akiwa na tabasamu mdomoni mwake.Shamsa alinyanyuka na kumkaribisha mama yake kisha wakakumbatiana, Abdul aliwaangalia mama na mwana walivyokuwa wakikumbatiana kwa huba. Bi.Ramla alikaa sofani huku akiwa na mashaka kuhusu kile alichoambiwa na Abdul, hakujua kama Shamsa alikuwa ampendi Abdul zaidi moyoni mwake alimpenda kijana Jongo. “ Habari za huku mama “Shamsa alimsalimia mama yake “Salama tu mwangu niambie maendeleo yake”Bi.Ramla alimjibbu “Salama tu,naona leo umewai maana nilikuwa na safari ya huko huko”Shamsa alimjuza mama yake “Hivyo ulikuwa unataka kuja nyumbani, mbona ujaniambia” “Ndio maana nikakuambia umeniwai, hata hivyo karibu…Vipi Baba nae anaendeleaje?” “Baba yako ajambo mwanangu anakusalimia”Bi.Ramla alimjibu “Nashukuru….lakini mama bora umekuja nataka kujua huyu kijana ni nani?” “Si nilikuambia Rafiki wa yule mwalimu mwenzangu….vipi kwani kunanini? “Sio kweli mama naomba uniambie ukweli mama” “Hahaha….Shamsa bwana matendo yote anayokufanyia bado hujajua huyu ni nani? “Matendo yake ni dhahiri kwamba mwanaume huyu umenitafutia wewe ili aje kunioa mimi kwangu haiwezekani mama”Shamsa alisema “Ha! Shamsa binti yangu mpe nafasi mwenzako” “Hee! Mama jamani unannikuwadia kwa huyu mtu nisiyemjua” “Hapana mwanangu, naona siku zote hupo ndani ya nyumba hii peke yako ndio nikaamua nikutafutie mwenzi wa maisha mwanagu “Bi.Ramla alisema bila woga “Hapana mama mimi ndio mwenye maamuzi siwezi kukubaliana na hilo mama”Shamsa alimwambia mama yake huku machozi yanamtoka.
Shamsa kwa hasira alitoka sebuleni na kuingia chumbani kwake huku akimuacha mama yake akiwa pamoja na yule kijana Abdul.Baada ya muda Shamsa alitoka chumbani kwake, uwii! Alishangaa akajishika kiuno looh! Alichokiona kilimuwaza mdomo wazi,alistuka alipomkuta mama yake akiwa amejiacha kihasara kwenye sofa moja alilokuwa amekaa pamoja na yule kijana anayedai kuwa ni rafiki wa mfanyakazi mwenzake.Shamsa alishikilia mdomo wake kwa kitendo alichokiona kwa mama yake mzazi akiwa anadendeka na Abdul,haijamuingia akilini hata lakini mama yake na kijana huyo walishtuka haraka na kukaa vizuri walijua hakuwaona kumbe mwenzao tayari alishayaona waliyokuwa wakifanya.Shamsa aliduwaa kwa sekunde kadhaa bila kusema neno Shamsaalipitiliza mpaka mlango na kuwaaga kuwa natoka kuelekea kwa rafiki yake aliyepo Tandika, mama yake alimuitikia kisha akatoka. Matembezi yake Shamsa alikuwa mwenye mawazo kila hatua anayopiga ndivyo alivyokuwa akizidi kuwaza na kuwazua mpaka akahisi kichwa kikimuuma na kamasi zikimtoka.Alikwenda moja kwa moja mpaka standi kisha akapanda gari la tandika na kufika nyumbani kwa rafiki yake anayeitwa Rose……
Siku hiyo Shamsa alikuwa hana furaha kutokana na hali hiyo hata rafiki yake Rose alitambua tofauti aliyokuwa nayo Shoga ake,Akaamua kumuuliza kilichomsibu lakini Shamsa wala hakuwa na namna ya kumjibu shaga yake huyo kwa kile alichikioni kule nyumbani kwake alipomua mama yake na yule kijana Abdul wakifanya yao.Alimezea moyo wakazungua kile kilichomleta ya kwamba Shamsa alimuulizia rafiki yake Rose amefikia wapi juu ya kumuona kijana Jongo,Rose hakuwa na namna alijibu rafikiye pale alipokuwa amefikiajuu ya kumpata Jongo.Alimwambia kwamba alimwambia kwamba alimfuatilia Jongo baada ya kusiikia ndani ya chuo cha Uwalimu West Ilala.Alipoenda kule aliambiwa jinsi anapoishi jinsi alivyofika jijini Dar na kwa kipindi hicho Jongo alikuwa ameshaajiliwa jijini kwenye shule moja ya watoto walemavu inayoiwa Uhuru mchanganyiko iliyopo Buguruni.Shamsa alivyosikia hivyo alishangaa moyoni alijawa na furaha japo hakumuona hila kufahamu kwake alipo ndio faraja pekee aliyokuwa nayo.Baada ya maongezi hayo Shamsa na rafikiye walishinda pamoja huku wakiongea maongezi ya hapa na pale kisha ilipohitimu saa kumi ya jioni Shamsa alimuaga Rose kisha safari ya kurejea nyumbani ilipoanza.
Ilikuwa jioni kwenye foleni kubwa Shamsa alimuona kijana mmoja Kipofu na fimbo yake mkononi, anatoka kwenye Super Market moja maeneo ya Buguruni Malapa huku akitembea kuelekea pembeni mwa barabara. Shamsa alipata mshituka bahada ya kuhisi kitu kati ya yule kipofu aliyemuona nje ya gari alilokuwepo, akiwa anaendelea kumwangalia yule kijana aliyekuwa akipiga hatua huku akifuatisha fimbo aliyokuwa mkononi mwake.Shamsaalianza kuvuta hisia akamtazama viruri yule kaka pale nnje, kama anamfananisha na mtu aliyewahi kumuon. Kabla Shamsa hajafaya lolote, alianza kufungua dirisha ili amwangalie vizuri ghafla ikaja Bajaji mpaka aliposimama yule kipofu, wakati kijana huyo akipanda Bajaji kuna mdada alitoka dukani anakimbilia sehemu iliposimama Bajaji huku akiita Kaka Jongo” yule kijana kipofu aliitikia na dada huyo alipofika pale alimpa mfuko alioshika. Shamsa aliona yote hayo akiwa ndani ya gari ila alishtuka, alipomuona live yule kijana aliyepewa mfuko Haa! Alishangaa mdomo ukiwa wazi alipomuona Kipofu huyo akipanda Bajaji kisha dereva aliondoa kwa mwendo wa kawaida. Shamsa haraka alimuomba konda kumpisha mlangoni, konda akagoma kwa vile alikuwa katikati ya barabara tena kwenye foleni hivyo asubiri kituoni,lakini Shamsa aligoma alimbembeleza vya kutoka huku akimuomba dereva kumruhusu konda wake kwani kuna jambo la muhimu ameliona lakini watu wote walikuwa kimya wengine wenye busara zao wakimtaka asubili kituo kipo jirani atatushwa Shamsa aligwaya na kutulia kusubili foleni.Akiwa amesimama mlangoni macho yake yaliiona ile bajaji iliyompakia Jongo ikaondoka.
Baada ya kukataliwa kushushwa hapo dari ilifanikiwa kusogea konda akamshusha Shamsa kituoni kisha aliongoza moja kwa moja kwenda kule ilipoelekea hile Bajaji.Shamsa alipata kiwewe alipomuona Jongo ameshapita akiwa ndani ya Bajaji hiyo. Shamsa alivuruga akili yake hakujua la kufanya kwani alikuwa tayari ameshamkosa Jongo, wala hakukata tamaa haraka mawazo yalimjia alimfuata yule mdada aliyetoka dukani na kumletea mfuko kijana yule kipofu.Alipoingia tu ndani kumuuliza yule dada kama kijana aliyetoka mle kununua vitu na kumkimbilia kumpelekea mfuko wake jina lake anaitwa Jongo? Alipojibiwa ndiyo hakuridhika na kuamua kuuliza tena kwa mara ya pili jibu lilikuwa lilelile kwamba ndiyo huyo anayeitwa Jongo. Shamsa alirudi mpaka pale stand ya daladala aliona achukue pikipiki ili kuifuatilia ile Bajaji iliyombeba Jongo, alipofika hapo alielekea zinapopaki pikipiki na kuongea dereva kisha kuanza kuifuata Bajaji ilipoelekea kwa mwendo kasi.Alifuata kwa kuhisia barabara lakini hakufanikiwa kuiona, muda wote huo dereva bodaboda alimshangaa, hata alipomuliza kitu gani kimetokea lakini Shamsa alikuwa anahema wala hakuwa na muda wa kujibu .Hivyo dereva huyo alibaki na maswali kibao maana hakujibiwa kitu, baada ya kufuatilia na kuikosa bajaji huyo aliamua kumuomba dereva ampeleke nyumbani. Siku hiyo Shamsa alirudi nyumbani akiwa amechoka sana, alipofika aligonga mlango maana alijua ya kwamba amewaacha Bi.Ramla na Abdul, kweli mlango ulifunguliwa alitoka mama yake akiwa amevaa kanga moja akiwa amejifunga juu ya kifua chake na nyingine ameizungushia kiunoni.Shamsa alishangaa zaidi kumuona mama yake akiwa katika vazi hilo alihamaki hakujua kwa nini siku hiyo mama yake alikuwa kwenye hali hiyo hakuelewa.Kitu alichokifanya Shamsa baada ya kuingia ndani alijitupa sofani macho yake yakiwa juu ya kufua cha mama yake kuanzia juu mpaka chini,Bi.Ramla wala hakujali alipitiliza moja kwa moja mpaka ndani ya chumba alichokuwa akilala na mume wake kabla ajaondoka nyumbani kwa mwanae.Shamsa alikuwa na mashaka makubwa hakujua mama yake siku hiyo alipatwa na nini mpaka kuwa katika hali hiyo alimwangalia jinsi alivyokuwa akitembea kwani aligundua kitu kisicho cha kawaida pale alipomuona mama yakke nywele zikiwa zigizaga huku makalio yake yakitikisika na kuonyesha kama ndani ya makalio hayo kukuwa na nguo ya ndani aliyovaa zaidi ya kujitupia kanga hizo.Shamsa alizidi kumakinika pale sebuleni alipoviona viatu vya Abdul vikiwa pembeni vimeifadhiwa, nguvu zilimuishia hakujua kama mwanamume huyo alikuwa sehemu gani,haraka alijipa nguvu alinyanyuka na kuelekea jikoni alimtafuta lakini hakumkuta, alirudi tena chumba kingine mpaka msalani kote alimtafuta lakini hakukuwa na uwepo wa kijana huyo.
Sio kama Shamsa hakuwa akimpenda Abdul la hasha alipata mashaka juu ya uwepo wa Mama yake na kijana huyo ndani ya chumba alichoingia mama yake.Ni chumba ambacho kilikuwa ndicho alizokuwa akiweka ubavu wake na mumewe mahali hapo, sasa Shamsa akakihesabia chumba hicho ni cha heshima kwa baba na mama yake.Alifikiri kwamba baba yake amekuja na labda yupo ndani na mama yake lakini mawazo hayo Shamsa aliyapinga wala hakuona kama yalikuwa sahihi kuwa akilini mwake.Alifikiria kwa jinsi gani mama yake amebadilika kiasi hicho,hakutaka kupoteza muda aliongoza chumbani kwake huku akiwa na mawazo juu ya mahali alipo kijana Abdul.Shamsa akiwa nyumbani kwake alikuwa mtu mwenye mawaza ghafla akiwa chumbani mwake alisikia sauti ya ajabu ikitokea ndani ya nyumba yake,alistuka alitoka kitandani na kutoka mpaka sebuleni akasikiliza vizuri na kughundua kwa sauti hiyo inapotokea.Shamsa moyo ulianza kumuendea mbio baada ya kukifikia chumba walichokuwa wanalala wazazi wake hapo kabla hawajaondoka.Akasikia sauti na biguno ya mahaba , shamsa alizidi kuchanganyikiwa hakuamini kile alichokua anakisikia alisogelea karibu kabisa na mlango wa chumba hicho kisha ajivutz mpaka ukutani na kushikilia mlango huo akachungulia ndani kuptia tundu la funguo. Looh! Shamsa alipagawa hakuamini kama funguo ilikuwa imeziba kuona cha ndani kinachoendelea, hakukubali hali hiyo alichungulia tena na tena akagongana na kutu cha kushangaza hakuamini macho yake aliona kila kitu kilichokuwa kimetokea ndani ya chumba hicho. Zaidi alishangaaakaona kizunguzungu kwa jambo lile aliloliona kupitia utundu wa funguo pembeni yake, maana funguo ilikuwa ikining’inia kwa ndani.Mda huo alisikia mama yake akibishana na Abdul chumbani wakiwa peke yao Shamsa hakuamini,aliona kama yupo ndokani lakini kiukweli ndio ilikuwa kweli pale alipojichunguza kuwa hakuwa akiota bali ilikuwa kweli.Shamsa hakutaka kuangalia kinacoendelea maana alikuwa ameshawaona wakivyokuwa wakibishana namna ya kutoka ndani ya chumba hicho kama kufanya walikuwa wameshayafanya tayari sasa walisubili kutoka naye Shamsa ndio akarudi….
Wakati wote huo Bi.Ramla akibishana na Abdul jinsi ya kutoka ndani ya chumba walichokuwepo, Shamsa yeye alikuwepo tu sebuleni amejituliza macho yake yakiwa ameyaelekeza kuangalia chumba walichokuwa. Hakika ilikuwa fedhaha kubwa Shamsa kumuona mama yake kulala chumba kimoja na kijana huyo, moja kwa moja mawazo yalimjia juu ya usariti uliotawala yaani hakuelewa kwa jinsi gani alikuwa kwenye hali hiyo.Mama yake alimueleza juu ya kijana huyo juu ya kuwa ni rafiki ya maana kwamba mpenzi wa yule mama mwenzake lakini leo hii anakuja kila kukicha nyumbani kwake na kujifanya anampenda. Ametumwa na Bi.Ramla kumsaidia kazi kumbe ni muongo kabisa akamtongoza lakini Shamsa alimkatalia ndipo leo anakuja kuwafuma wakiwa chumbani na mama yake Loo! Laana iliyoje kwa mama mtu mzima kutembea na kijana mdogo Shamsa alichoka.
Wa kwanza kutoka alikuwa alikuwa Abdul kisha nyuma yake alitokea Bi.Ramla wote wakiwa wamevaa nguo zao kama ya kwamba walikuwa tu wametulia ndani ya chumba hicho kumbe Shamsa alikuwa ameshajua kinachoendelea kati yao.Cha kushangaza Abdul alipitiliza mpaka mlangoni kisha alivaa viatu vyake na kutoka bila kuaga,Bi.Ramla alijipindapinda na kukaa sofani huku macho yake yakimwangalia kwa kuibia mwanae.Shamsa hakutaka kuzungumza kitu alimwangalia mama yake anaye naye alikuwa akimwangalia wakajikuta wakigonganisha macho yao na Bi.Ramla akatazama pembeni kwa aibu.Shamsa alipoona hivyo hakutaka kumuuliza kitu mama yake badala yake alinyanyuka na kuingia chumbani kwake,lakini Bi.Ramla alijisikia vibaya kwa aibu aliyokuwa nayo alimuita mwanae lakini Shamsa hakuwa na muda naye alipitiliza na kuzama chumbani kwake.
Siku iliyofuata Shamsa alienda kazini alifanya kazi zake kama kawaida lakini hakukaa sana na kuamua kuomba ruhusa kwa madai ya kwamba anajisikia kuumwa kichwa hivyo aliomba kwenda hospitali.Shamsa alipotoka hakwenda hspitali kama alivyodai badala yake alikwenda kwenye ile supermarket ya jana yake alipomuona kijana aliyemfananisha kama ndio Jongo. Alipofika aliingia ndani na kumkuta yule dada wa jana aliyekuwa akimuhita, Shamsa alipofika ndani ya duka hilo kwa bahati nzuri alimkuta dada huyo mrefu mwembamba kwa adabu akamsalimia. Shamsa hakutaka kupoteza muda akaanza kujieleza na kumtaka dada huyo ambaye alikuja kujitambulisha kuwa anaitwa Mwanahamisi, Shamsa alimtaka amsaidie jinsi ya kumpata Jongo. Haikuwa kazi ngumu kwa Mwanahamisi kumjibu Shamsa kile anachokijua juu ya kijana huyo mwenye ulemavu wa macho.Mwanahamisi alimueleza Shamsa ya kwamba kuna msichana mmoja anayeitwa Zainabu ambaye yeye ni rafiki yake mkubwa hivyo kupitia rafiki yake huyo ambaye ni dada wa Jongo atafanikiwa kuonana naye. Mwanahamisi aliendelea kumjuza ya kwamba mara nyingi Jongo upendelea kufika hapo akiwa pamoja na dada yake ambaye ni Zainabu. Jongo pamoja na dada yake huyo wanaishi pamoja maeneo ya Tabata ila yeye hakupajua tabata sehemu gani hivyo alimtaka amsubiri kwani Zainabu anaweza kufika siku hiyo. Shamsa alimshukuru Mwanhamisi kisha walipeana namba za simu kisha Shamsa hakutaka kuondoka alikuwa tayari kukaa hapo hili kumsubili muda huo ambao Zainabu alitarajiwa kufika.
Jioni ilipofika Shamsa akiwa hapo hapo amejiinamia akiangalia saa yake kama imefika muda ambao alitakiwa kuonana na dada wa Jongo. Alikaa macho yake yakiwa kwenye saa kubwa iliyopo ndani ya duka hilo jicho la pili lilikuwa likiangaza kwenye llango kuu la kuingilia ndani ya duka hilo.Kila mteja aliyekuwa akiingia Shamsa alimtupia jicho akijua ya kwamba ndio mtu aliyekusudia kuonana nae lakini haikuwa hivyo, alikaa na kusubili mpaka akachoka na kukata tamaa.Shamsa akiwa mtu mwenye mawazo sana juu ya kijana Jongo mara ghafla alistushwa na Mwanahamisi akimwita jina lake, Shamsa alimshangaa pale dada huyo aliponyoosha kidole kikimuelekezea msichana mmoja akitembea kule walipoketi.Moja kwa moja Shamsa amawazo yalamtoka sasa alimwangalia kwa makini msichana huyo mrembo, ilikuwa kama saa kumi na moja jioni Dada huyo aliingi huku Mwanahamisi akimkaribisha kwa bashasha tele usoni mwake, huku akimwita jina la Zainabu.Yule msichana mrembo Zainabu alifika na kuanza kusalimiana na Mwanahamisi kisha akamsalimi Shamsa bila kuchelewa Zainabu akaanza kutafuta vitu anavyovitaka kutoka ndani ya duka hilo. “Samahani anti?” Shamsa alimwambia baada ya kumfuata Zainabu kule alipokuwa “Bila samahani dada!”Zainabu alimjibu “Naomba unisaidie kitu kimoja dada” “Nimabie dada kama kikiwa ndani ya uwezo wangu nitakusaidia”Zainabu alimjibu “Nadhani unaitwa Zainabu wewe ni dada ake na Jongo?” Shamsa aliuliza “Yes! Jongo ni mdogo wangu” “Sawa naomba unisaidie nionane naye tafadhali”Shamsa aliomba “Unataka kuonana na Jongo kuna tatizo?” Zainabu aliuliza “Hapana…mimi ni rafiki yake ninayeitwa Shamsa, tulisoma wote jiji Mwanza”Shamsa alijibu“Oooh! Wewe ndiye msichana Shamsa?” Zainabu aliuliza kwa wahika huku akiwa mwenye tabasamu usoni mwake “Ndio mimi dada, naomba kuonana na Jongo namtafuta sana”Shamsa alisema “Hata Jongo pia anakutafuta sana mdogo wangu, kila siku simulizi yake Shamsa naona leo akikuona itakuwa furaha sana kwake” “Hanishindi mimi hapa nilipo natamani angekuwa mbele ya macho yangu, nampenda sana Jongo” Shamsa alitoa hisia zake “Usijali tutayazungumza cha zaidi Jongo yupo salama tunaishi pamoja nyumbani hivyo nisubili nikimaliza tu kukusanya vitu basi tutakwenda pamoja”Zainabu alimwambia Maneno ya Zainabu yalikuwa yenye barafu ndani ya moyo wa Shamsa, alijawa na furaha kusikia habari za Jongo alitamani dada huyo amalize upesi ili kuwai kumuona Jongo.Shamsa alijipa moyo na kumsubili Zainabu mpaka pale alipomaliza, wakaanga na dada mwenye duka hilo na safari ya kuelekea nyumbani kwa kina Jongo ilianza.Njia nzima Shamsa alikuwa mtu mwenye mawazo, hakuamini kama kweli siku hiyo ndiyo siku ambayo anakwenda kukutana kwa mara nyingine na Jongo. Hawakukawia kufika tabata kutokaa na siku hiyo kutokuwa na foleni, mtu wa kwanza kuingia ndani alikuwa Zainabu, Shamsa alifuatia nyuma huku akiwa na mashaka kukutana Jongo siku hiyo kulipa kiwewe..
Zainabu alipofungua mlango tu, Shamsa hakuamini macho yake yalikutana na Jongo aliyeketi kwenye kochi lililokuwa sebuleni, Shamsa alishindwa kujizuia alikimbia moja kwa moja na hadi karibu alipoketi Jongo na hapo hapo akajikuta machozi yakimtoka. Kwa bashasha aliyokuwa nayo akamuhita kwa hamaki “Jongo!” alishtuka kwa vile hakujua kama dada yake amekuja na mgeni, Jongo kwa mshangao akakulupuka na kuuliza “nani tena wewe?, kabla Shamsa hajajibu Mama Jongo alitokea naye kwa mshangao akalopoka na kumuhita “Shamsa!” wakati wote huo Zainabu alikuwa anawaangalia hasijue la kufanya, akamuona Shamsa akinyanyuka na kwenda alipokuwa Mama Jongo amesimama kwa hamaki. Shamsa kama swala alimrukia Mama Jongo kwa pamoja wakakumbatiana.Kila mmoja alionekana kuwa na furaha huku Jongo akiwa kwenye mshangao hakuamini wala hakutarajia kama Shamsa angekuja kukutana nae tena. Alijiuliza kichwa mwake iweje Shamsa apajue pale nyumbani? Na kama ameulizia je, amejuaje kama yupo jijini dar, alikumbuka siku moja miaka miwili iliyopita akiwa chuoni alisikia sauti ya Shamsa lakini hakubahatika kumuona. Jongo alinyanyuka na kusimama akionekana mtu mwenye mawazo na kumuuliza mama yake. “Mama huyu ndie Shamsa ninayemfahamu mimi?” “Ndiyo Jongo mwanangu huyu unayemsikia ndio Shamsa uliyekuwa ukimuulizia kila siku”
“Hapana mama mbona kama unanidanganya, naomba Shamsa usogee karibu yangu”
Shamsa alisogea karibu na Jongo huku machozi yakimtoka, alipofika karibu na Jongo alimshika mkono na Jongo naye akafanya hivyo na kuanza kumpapasa Shamsa Pajini mwa uso wake Shamsa yalizidi kumtoka pale Jongo alipomshika juu ya jicho lake na kukutana na kipele kikubwa cheusi kinachojulikana kama kidoti. Hapo ndipo Jongo alipolidhika kama kweli aliyekuwa mbele ya macho yake alikuwa Shamsa. Bila kutarajia Jongo machozi yalimtoka, si kwa hudhuni yalikuwa machozi ya furaha, Shamsa japo alikuwa akilia pia ila hakutaka kumuona Jongo akitokwa na machozi alichukua kitambaa chake na kuanza kumfuta machozi. Jongo alimwambia Shamsa ya kwamba “nimekutafuta kwa muda mrefu bila ya mafanikio mpaka nikakata tamaa ya kukutana tena nawe” Shamsa kusikia maneno hayo alisikitika na kumkumbatia tena Jongo. Muda wote walikuwa wamekaa chini wametulia wawili hao na kuanza kuongea, ambapo kila mmoja alimwambia mwenzie jitihada alizozifanya kumtafuta mwenzie.Siku hiyo ilikuwa ya furaha kwao kwani kutokana na mambo yote yaliyokuwa yakifanyika nyumbani kwake wala hakuwa na haja ya kurudi mapema, Shamsa alichelewa kutoka nyumbani kwa kina Jongo.Aliondoka usiku sana na aliporudi nyumbani alimkuta Mama yake anapika, Shamsa hakuhoji kitu badala yake alimsalimia mama yake na kuingia chumbani. kwa shingo upande Bi.Ramla alimwita mwanae ili wazungumeze,Shamsa hakusita alimkubalia mama yake na kueleke sebuleni. “Shamsa binti yangu naomba usinifikirie vibaya mama” Bi.Ramla alisema baada ya kuketi sofani “Sawa mama lakini naomba uiambie ukweli kuhusu huyo Abdul ni nani?” “Abdul ni kijana wangu uwa ananisaidia mambo mengi sana hivyo naomba usinifikirie vibaya mwanangu” Bi.Ramla alijitetea
“Lakini mama si ulinitambulisha ya kwamba Abdul ni rafiki wa yule dada, kumbe ulikuwa unanidanganya”Shamsa alisema “Hapana Shamsa siwezi kukudanganya” Bi. Ramla alisema kwa hofu “Nimeshajua kama Abdul ni Baba yangu mdogo hee! Wala sio kama ulivyokuwa ukidai” “Sio kweli kama natembea na huyo mvulana ni mdogo kwangu angalia, niwezaje kutembea nae wakati baba yako yupo jamani”Bi.Ramla alijitetea “Unayosema wewe ndio unadanganya mama nimeyaona kwa macho yangu unayoyafanya mama” “Haa! We mtoto umeyaona wapi kutuona tukitoka chumbani ndio tushafanya, hapana usifike huko binti yangu”
“Hapana sitaweza kunyamaza lazima nimwambie baba” “Shamsa huyu Abdul anakupenda wewe anataka akuoe mwangu” “Hati anioe wakati ameshalala na wewe mama lakini mbona sikuelewi kabisa jamani”Shamsa alimwambia mama yake yale aliyoyaona wakiyafanya na hivyo kupelekea Mama huyo kujisikia vibaya kupita maelezo. Yote hayo Shamsa hakujali hivyo alimtaka mama yake kuwa na amani lakini si kuendelea tena kuwa na Abdul ahachane naye kabisa la sivyo atamueleza baba yake yake.Bi.Ramla alimsihi mwanae asifanye hivyo ili kuondokana na matatizo yatakayoweza kutokea.Shamsa alimkubalia mama yake kisha alimwambia habari juu ya kumuona Jongo, b. Ramla alijifanya kufurahi lakini kumbu moyoni alikuwa na kinyongo na Jongo hakumpenda mwanae kuwa na mwanaume huyo kipofu.
Siku hiyo muda wa kulala Shamsa alikuwa mwepesi sana tofauti na siku zote,alichukua simu yake na kumpigia Jongo.Haraka Jongo alipokea simu hiyo na kuiweka masikioni mwake kisha wakaanza kuzungumza mambo mbalimbali,Jongo alifurahi sana kumsikia Shamsa akizungumza ahadi walizokuwa nazo juu ya mahusiano yao. Walimaliza kuzungumza kisha kila mmoja akimtakia mwenzake awe na usiku mwema na Shamsa akahaidi siku inayofuata atakwenda tena nyumbani kwa mama Jongo. Asubihi kulipokucha kama kawaida Shamsa alijiandaa kisha alitoka mpaka sebuleni ili kumsalimu mama yake, alipofika sebuleni alikuwa tayari ameshajiandaa kwa ajili ya kutoka kwenda kwa Jongo.Shamsa hakutaka kumuaga mama yake kama anakwenda kwa Jongo badala yake alimuaga anakwenda Kazini, Shamsa alianzaf safari hadi Tabata nyumbani anapoishi Jongo.Alipofika aliwasalimia kisha hakukaa sana alimuomba mama Jongo amchukue Jongo ili waende kutembea, Mama Jongo hakuwa na pingamizi alikubali Shamsa na Jongo waende wanapotaka kwenda.
Siku hiyo Shamsa alikuwa na furaha sana walitoka huku Shamsa akiwa na Bajaji iliowapeleka mpaka Msasani Beach Club. Walikunywa wakala na kusaza huku wakiongea mambo mengi juu ya maisha yake Jongo baada ya kuachana nae jijini mwanza, kisha Jongo naye alimueleza ya kwamba alipoamishwa shule ya sekonda alikaa sana nyumbani ndipo baadae walitokea wasamalia kumsaidia kumleta jijini Dar. Jongo aliendelea kumueleza baada ya kusaidiwa akajiunga na chuo cha uwalimu pale Ilala walimlipia ada pamoja na mambo mengine kisha kufanikiwa kuhitimu ndani ya miaka mitatu akawa mwalimu kamili aliyetunukiwa Diploma.Sasa ameajiliwa kufundisha shule ya msingi uhuru mchanganyiko, Jongo alisimulia zaidi ya kwamba pale anapoishi ni kwa dada yake Zainabu alimuomba waishi pamoja mpaka pale atakapomaliza kuijenda nyumba yake huko mpiji magoe……
Shamsa alimpa hongera yake na kufikia hapo alipofikia ni juhudi za muumba wa mbingu na ardhi kwa uwezo wake, kwani ndio aliyefanikisha kukutana kwao, Shamsa na Jongo walishinda pamoja mpaka jioni. Shamsa alipoona muda umekwenda na walitakiwa kurejea nyumbani walitoka na kutaka kupanda bajaji yao waliokuwa wamekodi kwenda na kurudi. Ilikuwa majira ya saa kumi na mbili kuelekea saa moja jioni kiza nacho kikianza kuingia, Jongo alimuomba Shamsa akubali ili amvalishe pete ya uchumba ili aweze kutambulishana kwa wazazi. Shamsa hakuamini alimuuliza Jongo alipoipata Pete hiyo, Jongo alimuomba kwamba Shamsa akubali kuvalishwa Shamsa alikubali kisha aliomba aelezwe aliinunua wapi na kwa muda gani maana usiku wa jana walikuwa wote na asubuhi pia alifika nyumbani kumchukua sasa kama kwenda alikwenda saa ngapi kuinunua? Jongo alimueleza ya kwamba Pete hiyo alimuagiza dada yake siku nyingi sana kabla hawajaonana kwani alimueleza dada yake juu ya msichana Shamsa ndipo alipokubali kuinunua pete hivo na kuiweka ndani mpaka pale watakapokutana na kumvisha na kweli yametokea sasa pete ilitakiwa ivishwe sehemu yake.Hakika ilikuwa furaha sana kwao, kiukweli Shamsa alimpenda sana Jongo kwani yeye ndio alikuwa chaguo la moyo wake.
Muda wote huo Jongo akiongea Shamsa alikuwa akilia kwa furaha, taratibu alinyoosha mkono wake na kuachia kiganja chake, Jongo naye alishika pete hiyo na kuivisha kidoleni mwa Shamsa kisha wote kwa pamoja wakakumbatiana kwa furaha.Wala hawakutaka tena kuendelea kukaa mahali hapo walipanda bajaji iliyokuwa ikiwasubili muda wote wakaongoza njia kurudi nyumbani kwa mama Jongo Tabata.Walifika nyumbani kwa Mama Jongo, walimkuta mama huyo akiwasubili kwa hamu kubwa, baada ya kufika na kuketi sofani Jongo alimueleza Mama yake kuhusu mahamuzi yaliyofikia. Mama Jongo hakuwa na pingamizi lolote juu ya maamuzi yao kwani Mama huyo anajua walipotoka mpaka walipofikia pia alifurahi mno mwanae kumuoa mtu ampendaye.Siku hiyo Shamsa na Jongo walipanga siku ya kwenda nyumbani kwa wazazi wake Shamsa, hawakutaka kuchelewa, walipanga siku inayofuata ndio watafanya taratibu za kufika nyumbani hapo kujitambulisha.Siku hiyo Shmsa aliongea mambo mengi sana huku wakiwa na furaha ya hali ya juu kwa kila mmoja wapo, alimueleza Jongo na mama yake kuwa kesho yake ndio walitakiwa kwenda kujitambulisha nyumbani kwao. Jongo na mama yake walikubali japo waliona harakalakini hawakuwa namna.Shamsa aliongea kwa muda kisha akaaga na kuondoka nyumbani kwake huku akiwa mtu mwenye mawazo, alimuwaza sana Jongo kila wakati alijiangalia kidoleni na kuishikashika pete yaani akionekana ahamini kile kilichotokea. Haikuchukua muda Shamsa alifika nyumbani kwake huku akiwa mtu mwenye furaha alitamani Jongo awepo jirani yake wayafurahie maisha. Baada ya kufika nyumbani hapo alipitiliza moja kwa moja mpaka sebuleni, aliangaza huku na kule lakini nyumba ilikuwa kimya kabisa, hata alipokwenda chumbani mwa mama yake pia hakukuwa na mtu moja kwa moja akajua ya kwamba mama yake tayari alikuwa ameshaondoka.
Kutokana na furaha aliyokuwa nayo siku hiyo Shamsa hakutaka kusubili alichukua simu na kuwasiliana na wazazi wake, wazo la kwanza alimpigia mama yake na kumuuliza kama ameondoka nyumbani hapo. Bi.Ramla alimuitikia mwanae kwa sasa yupo nyumbani kwake akiwa na mume wake Samir, Shamsa alimueleza mama yake kuwa siku inayofuata atamleta mchumba atakayemuoa, wazazi waliitikia kwa furaha ila ilikuwa furaha zaidi kwa mama mtu akijua ataletewa amtakaye yeye yaani Abdul. Kesho yake muda aliowaambia wazazi wake kama atafika Shamsa uliwadia mama na baba yake walisubili kwa hamu ili wamuone mkwe wao, Mara walisikia mlango ukigongwa na walimtaka anayegonga apite. Kama mawazo yao yalivyokuwa walimuona Shamsa akiingia huku akimsaidia Jongo kuingia sebuleni na kuketi nae kwenye kochi, wakati wao wanaingia ndani ulikuwa na mshangao kwa wazazi kwani hawakujua yule ndiye mkwe wao mtarajiwa mwenyewe? Bi.Ramla hakuwa na namna alisubili utambulisho kutoka kwa mtoto wake. Kisha wazazi waliwakalibisha na kuwasalimia pia walimchangamkia mtoto wao na wageni aliokuja nao kisha ukimya ulitawala mpaka Shamsa alipoamua kumtambulisha Jongo kwa wazazi kama Mume mtarajiwa. Mama yake Shamsa alishtuka akamuliza mwanae “huyu ndiye mwanaume unayetaka akuoe?” mama Shamsa akiwa katika mshangao Shamsa alijibu na akiwaeleza kuwa alimchagua muda mrefu, ndiye mwanaume atakayemfaa na pia wanapendana sana. Baba yake Shamsa Bwana Samir aliingilia kati na kumpongeza binti yake“Hongera sana Mwanangu usiwe na wasiwasi najua kwa kiasi gani umeteseka juu ya kijana huyu” kwa kumpoza mwanae kwa sababu anajua vizuri mkewe kuwa hakulizika na yule mwanamume mlemavu wa macho.
Bwana Samir alimfuata Jongo na kumkalibisha kwa mikono miwili na kumtaka ajisikie yupo nyumbani, Kwa kitendo cha bwana Samir kumpa faraja Shamsa ilikuwa furaha kwa Jongo kwani alijua jinsi alivyo mlemavu, ingekuwa vigumu kukubalika na wazazi wa Shamsa kwa sababu ya ulemavu wake. Shamsa na Jongo walifarijika na kuongea kwa muda mrefu huku wakionesha furaha waliyokuwa nayo juu ya mapenzi yao.Bwana Samir alifurahi ila Bi.Ramla alionyesha chuki ya wazi kwa mwanamume huyo Kipofu, Jongo alifahamu ilo kwa hisia kuhisi mama huyo kukaa kimya.Hata alipojalibu kuhoji kilichotokea mpaka mama kukaa kimya Shamsa hakuwa na muda wa kumjibu alimtaka Jongo kuwa na hamani, kwani asingejisikia vizuri kwa tabia aliyoinesha mama yake.Baada ya maongezi ya hapa na pale Bwana Samir alimuuliza Shamsa wangependa harusi ifanyike lini, Shamsa alitaka ifanyike mwezi unaofuata haraka iwezekanavyo. Mama na baba yake walishtuka kusikia kauli ya mtoto wao kuona akitaka harusi ifanyike haraka namna hiyo, Shamsa hakuwa na jibu la maana alichoamua yeye ndio ifanyike mwezi ujao. Shamsa aling’ang’ania ndivyo alivyoamua mwenyewe shughuli ifanyike kama kawaida, walipomaliza mazungumzo yao Shamsa na Jongo waliaga na kutaka kuondoka, Jongo anyanyuka na kumfuata Baba Shamsa vizuri alipewa mkono na kuagana kisha alimfuata Bi.Ramla kutaka kumuaga Mama huyo hakuitikia kitu wala mkono hakuupokea. Jongo hakujali hivyo aligeuka na kuanza kutoka nje ya nyumba huyo na kuondoka.
Shamsa na Jongo walipokuwa wanatoka na kuondoka Bi. Ramla aliachia sonyao kali lililomfanya mumewe Samir kumwangalia jicho kali kwa fedheha.Jongo alikosa kuelewa kwa nini Mama Shamsa hakuwa na furaha na hivyo hakujua kama harusi itafanyika hama haitofanyika ila hakuonyesha dalili ya kushtuka au kushangaa kwa jambo hilo.Waliondoka wakiwa ndani ya Bajaji waliyoikodi, wakati wakiwa njiani wakirejea nyumbani Jongo alimuambia Shamsa kuwa harusi haitaki kufanyika haraka inahitaji subira.Shamsa alishtuka kusikia vile kutoka kinywani kwa Jongo Shamsa alimuuliza “kwani wewe mwenzangu utaki kunioa mimi” Jongo alimjibu “sina maana hiyo ila tunahitaji muda hili mambo yaende sawa” Shamsa alishindwa kuelewa na kutaka kuelezwa kwa kirefu alikuwa na maana gani. Sauti ya Shamsa ilimfanya Jongo kujua kam amekasilika kusikia vile maana ni kweli Shamsa amekasilika kwani ni muda mrefu alikuwa anasubiri jambo hilo litokee kwa wawili hao.Ilibidi Jongo amueleze alivyokuwa akihisi na kuwa na mashaka juu ya mama yake Shamsa. “Shamsa naona mama yako ajalizika na mimi kukuoa wewe kwa hiyo tunahitaji muda wa kumshawishi mama yako ili akubaliane nasi na kutupa Baraka”
“Hapana Jongo wewe ndio changuo langu kumbuka niliyekupenda ni mimi” Shamsa alijibu maneno hayo kwani yalikuwa yamemuingia akilini mwake na kumfanya apunguze makali, sababu yeye alijionea mwenyewe jinsi mama yake alivyomchukia Jongo ikabidi Shamsa amuulize, “Sasa unafikiri tutafanyaje kama tusipochukua maamuzi mapema” “Sijui cha kufanya kwa sasa maana naona mama yako hayupo tayari kutuona pamoja”“Hapana haiwezekani kututenganisha tena, basi naomba kuanzia sasa tuishi pamoja nyumbani kwangu” Shamsa alisema kwa kujiamini
Simulizi : Chaguo Langu Ni Wewe Sehemu Ya Tano (5)
Halikuwa wazo baya wala gumu kwa Jongo kwani alikubali mara moja, Shamsa hakuwa na kinyongo alimpeleka Jongo nyumbani kwao kisha wakaagana watakutana siku inayofuata na yeye kurudi nyumbani kwake. Shamsa alipofika nyumbani kwake alimkuta Abdul, Shamsa alishangaa sana hakujua afanye nini kwa wakati huo hata alipomsalimia, hakuitika badala yake alipokea lawama kutoka kwa Abdul. Shamsa alimshangaa Abdul akiwa ana hasira akidai amemsaliti kwa kutembea na mwanaume kipofu wakati wameshakubaliana waanze kuwa marafiki kisha ndio uchumba utafuata.Shamsa alimsikiliza kisha akamwambia pole yake kwa kupoteza muda kwani kipindi chote alikuwa na mpenzi aliyekuwa akimtafuta kwa muda mrefu sasa amempata.Abdul alikuja juu ghafla na kupinga maamuzi ya Shamsa, Shamsa alipomuona Abdul yupo kwenye hali hiyo nae hasira zikamjaa akamtaka ampe funguo yake ya nyumba, kwani mwenyewe ameshampata mchumba wake wa siku nyingi na kesho anakuja kuhamia nyumbani hapo kuishi pamoja. Abdul hakuwa na namna alitoa funguo kwenye mfuko wake wa shati lake na kumtupia Shamsa bila kuonyesha dalili yeyote kama alikuwa nazo zaidi ya moja kisha aliondoka kwa hasira. Shamsa alimsindikiza kwa macho hadi mlangoni na kupotelea gizani…..
Siku iliyofuata asubuhi na mapema Shamsa alienda kumchukua Jongo nyumbani kwao alipofika alikaa mpaka mchana wakiongea mambo mabalimbali na mama Jongo. Ilipohitimu saa kumi za jioni Shamsa na Jongo waliagana na Mama Jongo kisha kuanza safari ya kurudi Nyumbani kwa Shamsa. Siku hiyo Jongo na Shamsa walikua ndani ya nyumba ya Shamsa, walikuwa watu wenye furaha hata walipotembelewa na ndugu na jamaa waliona sahihi kuwa wawili hao waliishi na furaha kupita kiasi ni mama yake Shamsa tu ndiye aliyekuwa hana furaha na mahusiano ya mwanae hata siku moja hakumpenda Jongo.
Siku moja Bi.Ramla na kijana Abdul aliyekataliwa na Shamsa walipanga kuonana sehemu ili wayajenge juu ya harusi inayotaka kufanyika kati ya Shamsa na Jongo. Walipokutana Mama Shamsa hakuwa na amani hata kidogo alianza kumwambia kile kilichokuwa kinamtatiza
“Hata mimi mama sipo tayari kumkosa na kumpoteza Shamsa kirahisi namna hii, nampenda sana binti yako ila ujui tu”
“Sawa ndio maana nimekuhita hapa ili tujue cha kufanya” alisema Bi.Ramla
“Ikiwezekana kumuua Jongo basi itakuwa vizuri” Abdul alitoa wazo
“Hapo sasa umenena kijana wangu ndio maana napenda vijana wakakamavu kama wewe, ila tu kama huyu kijago akishauawa najua Shamsa hatokubali kuolewa na wewe kwa sababu ameshajua mahusiano kati yangu na wewe” Bi.Ramla alimwambia
“Hee! Unasemaje? Shamsa amejuaje, umemwambia au?” Abdul aliuliza maswali mfululizo
“Sikumwambia ila ametuona tulichokuwa tunafanya tukiwa chumbani”
“Mmmh! Lakini aitakuwa tatizo nitafanya kila njia niwe nae” Abdul alisema kwa kujiamini “Sasa tuzungumze kilichotuleta ni kwamba Shamsa atasafiri hivi karibuni kikazi hivyo itakuwa nafuu kumteka Jongo au nitampigia simu usiku kumwambia kwamba naumwa lazima atatoka na kumuacha Jongo peke yake hapo itakuwa vizuri zaidi” Bi.Ramla alisema walikubaliana na kuagana na kupanga kuonana siku nyingine. Siku ya jumamosi majira ya saa saba usiku Shamsa na Jongo wakiwa wamelala hawana hili wala lile, ghafla simu ya Shamsa ikaita walistuka haraka Shamsa aliichukua na kuangalia mpigaji alikuwa mama yake akapokea na kuiweka sikioni. Simu upande wa pili ilisikika mama yake akidai na kulalamika kwamba amezidiwa ghafla na anataka msaada wa kupelekwa hospitali, Shamsa alitoka usiku hakuona haja ya kumsumbua. Hakutaka kumuamsha Jongo sababu alilala fofofo pia Mama yake alimsihi asisumbuke kumwamsha Jongo sababu ya hali yake ya kutokuona wasije kumsumbua.Shamsa alimwacha Jongo akiwa kwenye usingizi, Shamsa alipotoka nje na kuingia kwenye gari ambalo lilikuwa linamsubili baada ya kumpigia dereva amfuate na kuondoka, huku nyuma Abdul aliingia ndani na kufungua mlango mdogo wa geti ambao alikuwa ameuchongesha. Abdu alikuwa na msichana yule ambaye Bi. Ramla alimtambulisha mwanae kuwa ni mwalimu mwenzake. Waliingia mpaka sebuleni na kusimama nje ya mlango wa chumba cha kulala cha Shamsa kisha na kuanza kushauriana jinsi ya kumbeba Jongo wakamuue na wamtupe polini, wakakubaliana, waliingia ndani. Abdul alichukua kichpa kidogo kisha akamimina dawa kwenye kitambaa kilichokuwa mikononi mwake kisha akamfunika nacho juu ya pua ya Jongo kisha akambeba Jongo mpaka nje kisha walikuta gari ikiwasubili wakampakia Jongo na wapo wakaingia kisha wakaondoka mpaka polini walianza kumpiga na kumwagia maji. Jongo alishtuka fahamu zikamrudia na kujikuta yupo sehemu tofauti na alipokuwa mara kwanza kitandani sasa alipapasa chini akahisi majani na watu wawili wamemzunguka wakiwa wameshikilia mapanga na visu wakivinoa. Jongo alihisi kitu cha ajabu kikimgusa mgongoni mwake moja kwa moja alifahamu lilikuwa panga limemgusa mgongoni mwake, alijalibu kupiga kelele lakini Abdul alimzuia na kumwambia akijalibu kufanya hivyo basi mara moja atakitoa kichwa chake. Aisee Jongo alichoka akanyama huku machale yakimcheza kuhusu watu hao, waliendelea kumuuliza maswali ambapo Jongo hakuweza kuwajibu zaidi alisisitiza kuhachiwa, lakini wao waliendelea kumpiga mpaka Jongo akapoteza fahamu na kuanguka chini kama mzigo.Hawakutaka kupoteza muda Abdul na yule msichana walimchukua na kumtupa kichakani ndani ya poli hilo, kisha walikimbia kwa woga wakijua kuwa Jongo tayari ameshakufa. Akiwa ndani ya tax Shamsa alikuwa mtu mwenye mashaka usiku huo, hakujua mama yake amepatwa na tatizo gani, alijiuliza mara mbilimbili ila hakupata jibu. Shamsa aliwasili nyumbani kwa mama yake, alimuomba dereva wa tax amsubili ili akamuangalie mama yake yupo kwenye hali gani kama ikiwezekana wampeleke hozpitali, dereva alikubali na Shamsa mara moja akagonga geti kubwa na mlinzi alimfungulia. Shamsa hakumsalimia mlinzi wala kumuuliza kitu akazama ndani, mlinzi alimshangaa kitu gani kilichokuwa kimetokea kwa usiku huo, alitoka akiwa na mashaka makubwa na kuifuata ile gari iliyopaki nje. Huku Shamsa aliingia mpaka ndani akakuta taa imezimwa akaiwasha kisha akapitiliza mpaka chumbani mwa mama yake huku akiita Mama….Mamaaa, Maama…Shamsa aliita bila kuitikiwa alifufungua mlango wa chumba cha mama yake na kuingia ndani na kuwasha taa, alipoingia tu macho yake yalitua juu ya kitanda alicholala mama yake. Shamsa alimsogerea mpaka karibu kabisa na kitanda hicho kisha akaanza kumuamsha mama yake laikini kila akimuamsha Bi.Ramla alikuwa kimya, alimtingisha tena lakini wapi Bi.Ramla alikuwa kimya kitandani hakukohoa wala kutikisika alilala chali huku povu likimtoka mdomoni. Shamsa alichanganyikiwa kumuona mama yake akiwa kwenye hali hiyo alitoka mpaka nje na kumkuta mlinzi hayopo alihita kwa sauti kubwa akiomba msaada.Mlinzi pamoja na yule dereva wa tax aliyokuja nayo pale nje waligutushwa na sauti hiyo, kwa pamoja walikimbilia ndani ya nyumba hiyo na kumkuta Shamsa akiangaiki huku na kule kumwamsha mama yake. Mlinzi alipoona hivyo walisaidiana na dereva na kumnyanyua Bi.Ramla na kumtoa nje na kumpeleka mpaka kwenye gari wakamuingiza ndani.Shamsa akaingia siti ya nyuma akiwa amemkumbatia mama yake, huku dereva haraka alipanda ndani ya gari na safari ya kuelekea hospitali ilipoanza.Muda wote Shamsa alikuwa akimlilia mama yake huku kijasho chembamba kikimtoka hakutaka kumuona mama yake akipoteza maisha kwa wakati huo, njia nzima alimuomba mama yake jinsi gani awasaidie ili wafike hospitali salama na mama yake atibiwe na kupata nafuu.
Gari ilikuwa mwendo kasi ilipita mitaa na maeneo mbalimbali na hatimaye waliwasili hospitali ya Amana, Dereva alipiga honi geti likafunguliwa na Gari ikapita mpaka ndani na kuegeshwa Bi.Ramla akafumbua macho yake na kumtazama mwanae ambaye alikuwa akilia hasijue la kufanya. Ghafla Shamsa alishtuka alipomuona mama yake akinyanyuka na kukaa kitako, Dereva nae sasa alikuwa wima akiwa tayari kumnyanyua mgonjwa kumuingiza mapokezi ile anafungua mlango tu aliachia mdomo wazi akimshangaa Bi.Ramla alivyokuwa kama mzimu nywele zote timtimu. Looh! Shamsa hakutaka kuamini mara wahudumu nao walikuwa wanafikika kuwasaidia kumbemba mgonjwa. “Habari, mgonjwa mwenyewe yuko wapi tafafali” mhudumu mmoja alisema kati ya wezake watatu “Huyu hapa…” Shamsa alisema bila kupepesa na kumnyooshea kidole mama yake “Oooh! Kumbe anaweza kutembea haina haja ya kitanda, basi njoo mama tukusaidie twende kwa daktari” Muuguzi huyo alisema “Njoo nikushike mkono twende Bi.Mkubwa” Mwingine nae aliongeza Bi.Ramla alitoka mwenywe ndani ya gari na kuongozana huku wauguzi wawili wakiwa wamemshika huku na huku na kumsaidia kumpeleka mpaka kwa daktari. Daktari alipomuona alishangaa alijua labda mama huyo hana akili timamu maana Bi.Ramla alikuwa akicheka tu hovyo, Shamsa alijieleza jinsi ilivyokuwa maana Bi.Ramla kila alipouliza kitu gani kinachomsibu yeye alijibu wala hakuwa mgonjwa hivyo aliomba tu wamrudishe nyumba lakini Shamsa alisisitiza mama yake kuwa mgonjwa alitakiwa kupata matibabu.Daktari na manesi walishauriana jinsi ya kufanya maana Bi.Ramla aligoma kupatiwa kipimo chochote na kusisitiza hakuwa mgonjwa kama alivyokuwa bali usingizi tu ulimchukua na kumfanya kuwa vile alivyokuwa, Shamsa hakuwa na namna alikubali mama yake apewe dawa na kurejea naye nyumbani na ndivyo ilikuwa Bi.Ramla aliandikiwa dawa za marelia wakidhamilia ya kwamba itakuwa imempanda kichwa hivyo walimuandikia kuanza dozi.Shamsa na Dereva wa tax aliyokuja nayo walikuwa wamechoka haswa, Bi.Ramla alikuwa amewachanganya yaani ametoka nyumbani mgonjwa kufika hospitali mgonjwa anasema kwamba haumwi kumbe ilikuwaje, alidanganya au alifanya kusudi ? Baada ya nusu saa Jongo alilejewa na fahamu zake ndipo taratibu kumbukumbu zilianza kumrudia mpaka akawa sawa, alikumbuka kuwa alikuwa ametekwa na watu asio wafahamu. Hapo hapo akaanza kuogopa akijua kuwa wale watu bado wapo mahali hapo, Jongo akaanza kusema “jamani nioneeni huruma mimi sina kosa lolote lile mnaniua bure” aliongea maneno mengi huku akibwabwaja lakini hakuna aliyemjibu.Alipoona kimya hakuna dalili ya kuwa na mtu maeneo hayo alianza kuinuka na kukimbia hovyo huku mikono yake ameielekeza mbele kumsaidia kujikinga na kitu kibaya.Jongo hakujua sehemu aendako alifuata tu kijia cha nyasi na hatimaye baada ya hatua mbili tatu alikutana na barabara kubwa ya waendao kwa miguu, kwa hatua za haraka aliifuata barabara hiyo kubwa. Jongo alikuwa akitembea kwa pupa kama mtu aliyekimbizwa hofu ilimjaa tele moyoni mwake aliwaza na kumuomba mungu wake amsitiri na kumfikisha salama nyumbani.Jongo alitembea kwa kila hatua na kipande chake cha mtu kilichokuwa mkononi mwake akikitanguliza mbele, akafikia kwenye nyumba mmoja ya nyasi ndefu aliichunguza kwa pale nje ile nyumba kisha akaketi akimuomba mungu wake atende miujinza kama kuna mtu ndani ya nyumba atokee kumsaidia.
Ghafla Jongo akiwa nje ya nyumba hiyo alitokea Mzee mmoja mwenye ndevu nyingi, Mzee huyo akashangaa kumuona mtu nje ya nyumba yake, alisogea hili kumuangalia vizuri mtu huyo. Alishangaa alipomuona kijana kipofu akiwa amegeemea kiwambaza cha nje ya nyumba yake, Mzee huyo aliyeitwa Kilapo alijongea mkapa mlangoni mwa nyumba yake na kumsalimia Jongo. Jongo alishituka kusikia sauti ya mtu akimsabahi haraka aliitikia kwa mashaka na hofu moyoni mwake akahamkia, Mzee Kilapo aliitikia na kumkaribisha huku akimuangalia na kuingia ndani kwake kisha akatoka. Mzee Kilapo alimwangalia Jongo kwa mara nyingine tena kisha akamuuliza alipotokea.
“Yaani historia ndefu sana mzee wangu nakuomba unisaidie maji ya kunywa kwanza”Jongo alisema
“Sawa wala usijali kijana wangu” Mzee Kilapo alisema na kuingia ndani kisha akatoka na maji kumpati Jongo akapokea
“Kijana wangu naona kama una majeraha sijui umepatwa na maswahibu gani, niambie kilichokusibu” Mzee Kilapo alisema baada ya kumchunguza Jongo
“Mzee nilikuwa nimetekwa na vijana nisiowafahamu, walikuja nyumbani usiku wakanichukua bila kujijua, nilipokuja kuzinduka nikajikuta polini nimezungukwa na jamaa mmoja akiwa na mwanamke. Walinipiga na kunitesa mpaka nikapoteza tena fahamu, baadae nilipokuja kuzinduka sikusikia sauti zao wala sikujua walipokuwa ndio nikajikuta Napata nguvu na kutembea mpaka nikafikia hapa”Jongo alimwambia
“Aisee! pole Sana kijana nikupatie huduma kwanza kisha mengine yatafuata”
“Hapana mzee wala nisikupe taabu nahitaji mawasiliano kama inawezekana nifike kwanza nyumba au nimjulishe mama naona atakuwa ananitafuta muda huu”
“Kwa hilo usijali nitakupeleka mjini kwa baiskeli yangu kisha utapiga simu na kupanda gari kurejea nyumbani lakini kwanza subili utapate hata kifungua kinywa”
“Sawa Babu nashukuru sana kwa msaada wako”
Mzee Kilapo aliingia ndani kisha akachemsha maji, yalipopata moyo aliyatoa na kuanza kumkanda Jongo sehemu alizoumia, baadae alibadika chai na ilipoiva walikunywa pamoja na Jongo.Mzee huyo alimkilimu Jongo alimpa kila aina ya huduma kisha na dawa akampatia na kumataka apumzike ili yeye aende kuijaza upepo baiskeli yake kwa jirani.Baada ya nusu saa Mzee huyo alirejea na kumtaka Jongo ajiandae kwa ajili ya safari ya kumuongoza mjini, walianza safari kwa amani, Mzee Kilapo aliwa dereva na Jongo akikaa nyumba kwenye kiti cha abilia akisikilizia baiskeli ikiyoyoma. Walipanda mabonde na kuyashusha milima, hatimaye wakawasili mjini wakiwa na amani, Mzee Kilapo alimuongoza Jongo kwenye kibanda cha kupigia simu, kisha Jongo alitaja namba za mama yake na simu upande wa pili ikahita.Jongo alimueleza mama yake jinsi ilivyokuwa na jinsi pale alipofika alimuomba mama yake ajiandae kumlipia nauli kwani yeye anapanda tax itakayomfikasha nyumbani.Mama yake alikmkubalia mwanae huku akiwa na mashaka makubwa juu ya hali aliyokuwa nayo mtoto wake. Baada ya kumaliza kuongea simuni Jongo alimgeukia Mzee Kilapo na kumwambia ampeleke zilipo tax, Mzee huyo alishangaa atawezaje kupanda tax kwa umbali uliokuwepo kuanzia Kibaha mpaka dar ni nauli nyingi lakini Jongo hakujali wala hakutaka kupanda gari ya kawaida kwa kuofia usalama wake hivyo mzee Kilapo alimuelewa akampeleka zilipo tax. Jongo waliongea na dereva wa tax walielewana atampeleka kutoka kibaha mpaka Dar kwa shilingi 30,000. Jongo alikubali kisha aliagana na Mzee Kilapo kisha safari ya kurejea jijini ilipoanza.Walitumia masaa mawili kufika jijini Dar,Jongo alimueleza kabisa mahali anapoishi mama yake dereva akamfikisha mpaka Ilala Boma kisha dereva alisimamisha gari mbele ya nyumba yao.
“Hallow Jongo” Shamsa alitamka
“Hallow Shamsa kwema mke wangu?”
“Kwema kiasi Jongo..Mbona kimya sana upo wapi?”
“Nipo kwa mama nilipata matatizo makubwa sana” Jongo alisema
“Najua ukufahamu nilipotekwa na kupelekwa msituni kuteswa” Jongo alimwambia
“Umetekwa na nani Jongo mbona unanichanganya mpenzi?” Shamsa alilalama
Shamsa hakutaka kusubili haalijilaumu kukaa kimya muda wote bila kujua kama Jongo anaendeleaje nyumbani alipomuacha peke yake, alijilaumu kwanini alimuacha Jongo peke yake, alipata wapi ujasili wa kutoka huku akimuacha Jongo amelala hakujua kama mtu aliyemuacha alihitaji msaada kwa namna gani. Yote hayo alijiwazia huku akiwa makini kumuangalia mama yake, Bi.Ramla alikuwa tuli ametulia kwani aliyasikia maongezi yote yaliyokuwa yakisimuliwa kati ya mwanae na Jongo, hivyo yeye akuongea kitu alichukizwa na kitendo cha Jongo kuwa hai tena, hili akulionyesha usoni mwake bali lilikuwa likimtibua ndani ya moyo wake aliwalaumu sana Abdul na mwenzake kumuacha kijana huyo kipofu akiwa mzima.Haraka Shamsa alinyanyuka kwa hasira na kutoka mpaka nje kisha akaanza safari ya kuelekea nyumbani kwa mama Jongo…….
Baada ya mwendo wa boda boda Shamsa aliwasili nyumbani kwa Mama Jongo akiwa na mashaka makubwa, alipoingia tu ndani alimkuta Jongo na mama yake sebuleni, Shamsa alishangazwa na hali aliyomkuta nayo Jongo.Mama Jongo alipomuona Shamsa alihamaki na kumkalibisha kwa shingo upande, baada ya Shamsa kuwasalimia na kutaka kujua kitu gani kilikuwa kimemtokea mpenzi wake huyo, Mama Jongo alimwangalia kwa jicho kali kama kwamba Shamsa alijua kila kitu kilichomsibu kumbe hakuwa akijua chochote kinachoendelea.
“Mama Mbona Jongo yupo hivi…. sana kwema mama?” Shamsa aliuliza kwa mshangao
“Unauliza nini wewe…..ulichofanya unadhani kizuri kwa mwanangu?” Mama Jongo alijibu kwa dharau
“Hapana Mama ulikuwa ni usiku sana na niliona nikimuamsha nitamsumbua Jongo kwani nilitoka kumpeleka mama yangu hospitali, maana alinipigia simu usiku wa manane kichwa kikimsumbua nikaamua kuondoka na kumuacha Jongo chumbani” Shamsa alimjibu
“Unamwona mwanangu mlemavu si ndio, unamfanyia vitu vya makusudi utamuachaje peke yake nyumbani, alafu unanidanganya eti umempeleka mama yako hospitali wakati ulikwenda kwa wanaume wako” Mama Jongo alibwata
“Hapana Mama nakuambia ukweli muulize hata Bi.Ramla atakuambia kilichomsibu” Shamsa alishtuka kuona mama mkwe wake yupo kwenye khari hile
“Wewe na mama yako lenu moja ulimtaka mwanangu ili kumtesa kisha umuue”Mama Jongo alisema
“Jongo sielewi kwa nini wewe na mama mnanishutumu kwani nimefanya kosa kutoka bila kukuaga, sikutaka kukusumbua mpenzi” Shamsa alimlalamikia Jongo
“Bora ungekaa huko huko bila mimi kujua lakini ndani ya nyumba yako wanakuja watu kunichukua wanipeleke kuniua nimekukosea nini Shamsa” Jongo alilalama
“Sijakuelewa una maana gani Jongo kusema hivyo?” Shamsa alimtupia swali
“Sababu ya mapungufu yangu sioni hili wala lile, dhamani kwako imeshuka ndio uniingizie watu ndani sababu ni nyumbani kwako Shamsa, waje kuniua bora usingenipeleka nyumbani kwako, Ndio Kama tabia zako za ushenzi namna mimi nawe basi tena tuachane sitaki kuteska” Jongo alisema huku akilia
Maneno ya Jongo yalimshtua Shamsa kwa kweli akilini mwake akujua nini kimetokea, alijitahidi kumweleza kuwa alienda kumpeleka mama yake hospitali, hivyo hakuwepo ndani usiku huo yeye akitekwa lakini Jongo hakumwelewa.Jongo alinyanyuka ghafla na kutaka kuingia chumbani lakini mama yake alimuwai na kumzuia, akamshika mkono akimtaka arudi kitini wayamalize. Badala ya Jongo kukubali lakini alikataa alijivuta ili kuunasua mkono wake toka mikononi mwa mama yake lakini ilishindikana Jongo alijikuta akiponyoka mikononi mwa mama yake na kuteleza akadondoka chini kama mzigo na kuzimia.Shamsa alipata kiwewe kumuona Jongo pale chini ametulia na mama Jongo nae liweweseka hasijue la kufanya, kwa pamoja walishauriana kumbeba Jongo na kumpeleka hospitali.Baada ya kufika hospitali Jongo alipatiwa matibabu haraka na hatimaye kuamka, dokta alimwita Shamsa na mama Jongo kuwataalifu ya kwamba Jongo alipata mshtuko pia kwa vipimo zaidi inaonyesha ana presha na ndio imesababisha yeye kuanguka na kuzimia kwa mshtuko aliopata.Ilikuwa taarifa njema kwa Shamsa na mama Jongo kwani kila mmoja alinyoosha mikono juu na kumshukuru mungu baada ya kumnusulu na matatizo mengine Jongo. Baada ya kutoka chumbani kwa dokta Shamsa alimtaka mama yake Jongo waongee pembeni na Shamsa akatoka na kuwaacha wawili hao wakizungumza.
Baada ya muda mama Jongo alitoka, Shamsa alimuliza mama Jongo alichoambiwa na Daktari kisha nae akamwelezea jinsi Jongo alivyopata mshtuko na sasa ameandikiwa dawa za kutumia akiwa nyumbani. Shamsa alifurahi na kumkumbatia mama Jongo huku akimuomba msamaha na kumueleza hatoweza tena kwenda sehemu bila kumuaga Selemani wala baya kama lile kujitokeza tena. Jongo akiwa kwenye chumba cha kulazwa mgonjwa mama yake aliingia akiwa na Shamsa pembeni, Jongo alipogundua mama yake ndiye aliyeingia alifurahi Sana na kuonyesha furaha wazi wazi wala hakuja kama Shamsa alikuwepo pia. Alishambiwa na dokta kama hakuna tatizo na tayari alihusiwa kurea nyumbani. Wakati Wakiwa kwenye maongezi ya furaha mama yake aliingizia swala la Shamsa pale pale kuhusu kuuguliwa na mama yake Jongo hakuelewa mama yake kwa nini alianzisha mazungumzo hayo Jongo alibadilika mara moja na kuacha kumuangalia mama yake. “Mwanangu najua unampenda Shamsa au naongopa?” Mama Jongo alianzisha mazungumzo kisha akaedelea
“Mwanangu mahusiano si kitu cha kuchezewa ni lazima upitie mambo mengi na usimlaumu Shamsa kwa mambo yaliyotokea, inawezekana yeye hakufahamu kitendo ulichofanyiwa kwani huna ushaidi kamili mwanangu?”
“Mama inauma mi sijui nani aliyenifanyia kitindo hiki jamani au mama wewe unajua?”
“Hapana mwanangu hamna mzazi anayemtakia mabaya mwanae, unatakiwa kukumbuka wapi ulipotoka na Shamsa pia ufikilie jitihada za Shamsa kahakikisha upo kwenye furaha na la mwisho ufikilie sasa upo kwenye wakati gani na unamuhitaji Shamsa ili kuishi pamoja kama mke na mume” Mama yake alisema……
Maneno ya mama yake yalianza kumuingia akilini Jongo pia aliona anahitaji kuwa karibu na Shamsa kwani ndio mapenzi yake yalipo na ndiye chaguo la moyo wake. Jongo alikuwa mtu mwenye mawazo alifikilia jinsi gani alipopata shida kumtafuta Shamsa, akajikuta kweli toka moyoni akimpenda Shamsa pia hakutaka kumuumiza. Alijisemea moyoni inanibidi nisamehe tu kwa yaliyotokea Jongo na mama yake walikumbatiana kwa furaha tena, Mama Jongo alimtaka Shamsa asogee karibu yao ili azungumze na mwenzake. Jongo alishangaa kumbe wakati akiongea na mama yake kila kitu Shamsa alikisikia ina maana alikaa kimya huku mama yake alijua kama Shamsa alikuwepo chumbani humo ila hakumwambia. Shamsa alikuwa na woga kwani hakujua ahanzie wapi kuhusu kosa linalomkabili, Shamsa alianza kwa kumsalimia Jongo na Jongo alitikia kwa furaha na buraha kama kawaida kisha Shamsa aliendelea kumuuliza hali yake Jongo kisha akamuomba msamaha kwa kile kilichomtokea kwani yeye hakuwepo ndio maana yote hayo yakatokea.Jongo akafurahi kusikia Shamsa akitubu na kuomba msamaha naye kwa moyo mkunjufu akamsamehe.Shamsa alifurahi kuona ya kwamba Jongo amekubali kumsamehe na kuelewa kile kilichotokea kama Shamsa hakuwepo wakati akitekwa. Kwa furaha na upendo Shamsa na Jongo wakakumbatiana huku Shamsa na kumuahidi haitokuja kutokea tena akatekwa au kufanyiwa kitu kibaya.
******* Wakati Shamsa akiondoka bila kumwambia mama yake alijua kila kitu alichokuwa akiongea na simu juu ya hali aliyokuwa nayo kijana Jongo.Bi.Ramla hakutaka kusubili maana rohoni alijutia kwanini alimkabidhi Jongo mikononi mwa Abdul aliyekuwa akimuamini kumbe ilikuwa kazi bule wala hakukikamilisha kile kilichokuwa kinahitajika kufanyika.Bi.Ramla alinyanyuka na kuingia ndani akachukua simu yake na kumpigia Abdul na kumueleza kile alichokuwa amekisikia kutoka kwa Shamsa. Abdul hakuamini aliamua kumupigia mwenzake na kumueleza kile alichoambiwa naye alishangaa kwani wao walijua tayari Jongo ameshakufa, walilaumiana kwanini hawakuwa tayari kumpima Jongo kwa kile kilichokuwa wamekifanya kilikuwa kitu cha uzembe wa hali ya juu.Wakapanga kukutana ili wajue kwa namna gani watamtafuta tena Jongo ili kufanikisha kile walichodhamilia.
Baada ya Bi.Ramla kuzungumza na Abdul na kupanga kwa namna gani watakuwa pamoja kufanya mahamuzi, Bi. Ramla alishangaa akawaza na kuwazua kwa jinsi gani atamdhibiti Jongo kuwa na mwanae. Kiukweli akupenda kumuona Shamsa akiwa pamoja na Jongo hivi alihakikisha atafanya kila njia ili kumualibia Jongo kuwa pamoja na Shamsa.Siku hiyo ilikuwa mbaya kwake japo alijifanay mgonjwa kumbe hakuwa mgonjwa ila yote sababu ya kutaka kumuua na kumpoteza Jongo.Lakini hata hivyo Bi.Ramla anatembea na Abdul je atafanikisha vipi kwa kijana huyo Abdul kuwa na mapenzi kwa mwanae wakati yeye pia anatembea nae, hivyo itakuwaje sasa haya tungoje tuone itakavyokuwa mimi na wewe tunasubili.
******* Siku moja Shamsa alikuwa nyumbani kwake baada ya wao kumalizana na Jongo kuruhusiwa hospitali, siku hiyo Shamsa hakwenda kazini alikuwa mapumziko ametulia sebuleni akiongea na Jongo story za hapa na pale. Shamsa alikuwa mwingi wa furaha mara wakiwa wanaendelea na maongezi yao simu ya Shamsha akaiangalia simu hiyo kwa makini maana hakujua namba ya mpiga ilitokea tu bila jina hivyo alipatwa na mashaka juu ya hali hiyo. Alipiga moyo konde na kuipokea simu hiyo, wala hakuamini masikio yake kile alichokisikia kuwa kwa siku hiyo ya mapumziko akihitajika kazini, kila alipojalibu kumuuliza mpigaji wa simu hiyo ni nani lakini mtu huyo wala hakumjibu badala yake simu ikakatwa na kutokuwa hewani tena. Shamsa hakutaka kuchelewa wala kuipuuza simu hiyo Shamsa alimwambia Jongo kuwa anatoka mara moja na kwenda ofisini. Kwa vile Jongo alikuwa ameyasikia maongezi ya Shamsa kweny simu akammpa ruhusa Shamsa ya kwenda, kabla ya kwenda Shamsa alimpigia simu Zainabu dada yake Jongo aje nyumbani kwake ili kukaa na Jongo.Zainabu alikubali na kudai kwamba atachelewa kidogo kufika Shamsa alimuelewa, alipokata simu ya Zainabu simu ya Bi.Ramla ikaingia Shamsa alipokea na simu upande wa pili ikasikika.
“Vipi Mwanangu upo nyumbani, maana mimi nipo njiani nakuja kwako”
“Hapana mama muda huu najiandaa nataka kutoka ila ni vizuri kama ukija utamkuta Jongo” Shamsa alisema
“Kwani wewe unakwenda wapi muda huu”Bi.Ramla alijifanya kuuliza kimtego
“Nakwenda ofisini muda huu mama maana nimepigiwa simu muda si mrefu hapa kuna dharura mama”
“Sawa mwanangu hakuna tatizo mwanangu itakuwa vizuri mimi nitafika hapo muda si mrefu”
Wakati Shamsa akiongea na mama yake Jongo alikuwa makini akimsikiliza mpenzi wake anachozungumza na mama yake, hata pale alipoambiwa juu ya Bi.Ramla kuja nyumbani hapo Jongo hakusishtuka wala kuteteleka juu ya mama huyo.
******* Mama Shamsa alipomaliza kuongea na mwanae huku moyoni akiwa na furaha ya kweli kabisa kwa kile alichopanga kummaliza kijana huyo kipofu. Akatafuta sehemu yenye majina na kumpigia simu Abdul kumueleza kwa kile kilichofanyika ya kwamba Jongo atakuwa peke yake nyumbani kwani ndio nafasi pekee waitumie kumuua kabis.Abdul alimueleza kila kitu na kuelezana jinsi walivyopanga na kukubalia nafasi hiyo waitumie vizuri bila kugundulika kwa mtu yoyote. Baada ya muda Bi.Ramla alikuwa mbele ya duka la dawa na kununua sumu aina ya dawa za unga utumika kuuwa wadudu kama panya mende na kunguni, akuna aliyegundua dawa hizo amezinunua kwa madhumuni gani hivyo wala hakuonyesha dalili yoyote maana hakuwa na muda na mtu. Alipotoka dukani akachukua tax na kuelekea nyumbani kwa Shamsa, alipofika alikuta Shamsa ndio anatoka akiwa kwenye bajaji, akamuambia dereva tax asimamishe gari pembeni kidogo na nyumba hiyo bila kuuliza kitu, wakiwa kando kando ya barabara Bi.Ramla na dereva walimuona Shamsa akiwa ndani ya bajaji na dereva wa bajaji hiyo alikata kona na kuifuata barabara kuu kuelekea mjini…. Bi.Ramla hakutaka kusubili hivyo yeye alishuka na kuingia ndani, alipofika sebuleni alimkuta Jongo amekaa kitini peke yake, Jongo alihisi kuna mtu akiingia alipohita jina la ndugu yake hakuitikia badala yake alisikia sauti ya mama yake Shamsa, akidai kuwa yeye ndiye aliyeingia pia alipigiwa simu na Shamsa kuwa aje amuangalie mpaka pale dada yake Zainabu atakapofika.Bi.Ramla alipotaja jina la Zainabu basi Jongo aliondoa wasi wasi moyo wake ukapoa na kuamini kile alichokisikia, akamsalimi Bi.Ramla kisha alitulia lakini Bi.Ramla alimuhitikia kwa kejeli bila Jongo kuona mama huyo alivyommwangalia kwa dharau.Wakati Bi.Ramla akiendelea kuzungumza na kumzugazuga Jongo mlango ulifunguliwa na Abdul akaingia ndani huku akiwa mwenye mashaka, macho juu ameyatoka akimtazama Bi.Ramla kwa tahadhari.Bi.Ramla akaamua kuvunja ukimya akamtambulisha Abdul kwa Jongo lakini Jongo machale yakamcheza akashtukia kitu lakini hakutaka kujionyesha akatulia.
“Ah asante mi nishatosheka tayari” Jongo alijibu kwa hamaki
“Jamani nimekuja kukuona nisikufanyie chochote kwa nini lakini baba, hata juice?” Bi.Ramla alisema
“Asante ila usijisikie vibaya sana mama ningehitaji Juice ya maembe ipo kwenye friji” Jongo alisema huku akitabasamu
“Ah usijali subiri nikakuchukulie, nakuletea sasa hivi usijali”Bi.Ramla alisema huku akinyanyuka sofani
Bi.Ramla alikwenda kuchua juice aliyoambiwa na Jongo, alifungua friji kisha akatoa jagi lenye juice ya embe iliyosangwa na kuimimina kwenye glasi moja wapo iliyokuwa juu ya meza kubwa sebuleni hapo. Alipomaliza kuimimina juice hiyo aliweka ile sumu kwenye juice hiyo iliyokuwa kwenye glasi kisha akairudisha ya kwenye jagi frijini na kumpelekeaJongo.Jongo aliipokea glasi hiyo na kuanza kuifakamia juice yote bila kubakisha, Bi.Ramla alifurahi sana kumuona Jongo ameinywa Juice hiyo bia kugundua. Muda si mrefu wakiwa sebuleni hapo ilisikika sauti kutoka kwa Jongo akilalamika tumbo likimuuma, hapo Bi.Ramla na Abdul walikuwa kimya wakimuangalia Jongo alivyoshikilia tumbo lake, wao walishaona sumu tayari ishaanza kufanya kazi yake. Abdul alinyanyuka na kuanza kuondoka Bi.Ramla naye taratibu alinyanyuka na kuondoka wakamuacha Jongo peke yake akilia kwa uchungu, Jongo alipiga kelele akitaka msaada. Kwa vile alijua kuwa ndani ya nyumba hiyo walikuwa wawili yaani yeye na Bi. Ramla aliona amuombe mkwewe huyo amsaidie akaanza kumuhita Bi.Ramla aliyekuwepo, kwa muda huo wala hakuitikiwa, Jongo alirudia kuhita tena na tena lakini sauti yake haikuwa na mafanikio kwake.
Bi.Ramla na Abdul waliongozana huku wakikazana kuwai kutoka ndani ya nyumba hiyo lakini mungu si adhumani wakati wanatoka walikutana nje na dada yake Jongo ambaye ni Zainabu aliyekuwa amepigiwa simu na kudai atachelewa kufika na kweli amechelewa.Japo Abdul na Bi.Ramla walimuona dada huyo hawakumtilia maanani na kumdharau hatoweza kuwatambua, Zainabu aliwaangalia kwa makini kwani alipatwa na mashaka juu ya watu hao ndani ya nyumba hiyo, hivyo alihisi kitu kutokea haraka akaingia ndani bila kuwaangalia watu hao walipoelekea. Alipofungua tu mlango alisikia makelele kutoka kwa mtu akiugulia maumivu, alipoisikiliza vizuri sauti hiyo mara moja akaitambua kuwa ya ndugu yake Jongo.
Haraka alikimbilia sebuleni ndipo aliposhtuka zaidi alipomuona Jogo akiwa peke yake sakafuni akigalagala huku mapovu yakimtoka mdomoni naye mikono akishikilia tumbo lake. Zainabu alichanganyikiwa alienda karibu na pale alipolala Jongo na kuanza kumnyanyua huku akimuliza nini kilichokuwa kinamsumbua. Jongo alimwambia Zainabu huku kama alikunywa juice anayohisi kuwa na sumu huku akilalamika kwa maumivu, kusikia hivyo Zaina haraka alifungua friji na kwa bahati nzuri aliyakuta maziwa haraka alirudi bila kulifunga friji na kuanza kunywesha Jongo maziwa hayo. Jongo alikunywa kwa pupa ili kuokoa maisha yake baada ya dakika mbili Jongo alianza kutapika pale sebuleni, Zaainabu kuona hivyo haraka alichukua simu na kumpigia Shamsa. Kwa muda huo Shamsa alikuwa hapatikani hivyo dada hiyo alibonyeza namba kadhaa na siku ya upande wa pili ikasikika kutoka kwa mama yake Jongo. Baada ya kama dakika tano Jongo akiwa hana hili wala lile amelegea na kuishiwa nduvu pale sakafuni, Zainabu alisikia mlio wa gari nje ya nyumba hiyo mara moja akajua ya kwamba Mama yao alikuwa amefika kuwasaidia.
Punde mama Jongo na kijana wa makamu wakaingia ndani ya nyumba hiyo na kumkuta Zainabu akimlilia kaka yake kwa uchungu, wao walimchukua Jongo na kumpeleka hospitali, huku nyumbani walimuacha Zainabu peke yake ikiwa Mama Jongo na kijana huyo msamalia mwwema wakimpeleka Jongo hospitali. Ndipo Zainabu alipoamua kumpigia simu Shamsa ambaye sasa simu ilikuwa inapatikana, baada ya Shamsa kusikia kile alichoambiwa na Zainabu haraka hakutaka kubaki kazini aliacha kazi ofisini na kukimbilia hospitali Amana alipoelezwa……..
Njia nzima alikuwa mwenye mawazo hakuelewa kitu gani kimempa mpenzi wake, Shamsa alimuomba dereva wa bajaji kuongeza mwendo ili kuwai.Baada ya nusu saa waliwasili hospitalini hapo, Shamsa alishuka na kuingia mapokezi kisha kuulizia hali ya mpenzi wake muuguzi wa zamu alimuelekeza kwa madaktari kabla hajafika chumba cha daktari alimuona Zaina akiwa na mama yake wameketi wakisubili kuingia chumba cha daktari. Shamsa hakutaka kusubili aliwafuata na kuwamuliza nini hasa kilichokuwa kimemtokea mpenzi wake, Zainabu alimwambia jinsi alivyomkuta Jongo na kuomba msaada kisha wasamalia wema walimsaidia kumpeleka hospitali. “Kwani madaktari wamewaambiaje, nini kimedhuru mwilini mwake? Shamsa aliuliza maswali mfululizo, Zainabu alimwangalia kwa udhuni kisha akamwambia kuwa Jongo amekunywa sumu na hawakujua sumu hiyo amepewa na mtu hama amekunywa mwenyewe.
Zainabu alimueleza Shamsa jinsi alipokutana watu hao ambao walikuwa wametokea nyumbani kwake akiwa mwanamke mtu mzima na kijana wa kiume, Shamsa alishangaa aliposikia maneno hayo, aliwaza na kuwazua juu ya watu hao maana Zainabu hakuwajuwa watu hao kina nani hata Bi.Ramla hakuwai kumuona zaidi ya siku hiyo na hakujua kama ndio mama yake Shamsa. Kinachomumiza Shamsa kichwa kuwa Jongo kapata wapi sumu wakati nyumbani kwake hawana sumu ya aina yoyote ile, Shamsa kichwa kilimgonga sana alifikilia na kukumbuka tukio lililotokea na lile lililowai kumtokea mpenzi wake huyo, akapata jibu kama kuna mtu atakuwa anamfuatilia na kutaka kumuua mpenzi wake Jongo hivyo akaona kabisa watu hao walioingia ndani ya nyumba yake ndio waliompa Jongo sumu hiyo.
Shamsa alikuwa amefura kwa hasira hasijue la kufanya kwa wakati huo alimgeukia Zainabu na kumtaka amjulishe jinsi watu hao walivyo na huyo Mvulana aliyeingia alikuwaje. Zainabu alimfafanulia jinsi watu hao walivyo na mama huyo mtu mzima jinsi muonekano wake ulivyo, Kwa umakini mkubwa alivuta kumbukumbu na kuona taswira ya mama yake ikimjia kichwani mwake.Shamsa jinsi alivyoelezwa hakupata shida kumtambua Bi.Ramla na Abdul, alichokifanya Shamsa baada ya kuujua ukweli wenye ushahidi tosha aliondoka bila kuaga na kuelekea kituo cha polisi buguruni na kuandikisha jalada kwa maelezo yote aliyoyatoa kama alivyoambiwa na Zainabu pamoja na kuonganisha yale ya utekaji. Baada ya Shamsa kujieleza na kufunga mashtaka aliongozana na Askari watatu wakiwa ndani ya difenda na safari ya kuelekea nyumbani kwa mama yake ilipoanza.Shamsa hakuwa na huruma hata kidogo kwani kwa kitendo alichomfanyia mpenzi wake kilionyesha Mama yake kuwa na dharau kwake kumpenda kijana huyo kipofu. Baada ya mwendo wa robo saa kutoka kituoni Buguruni mpaka Ilala boma hawakuchukua muda sana walifika nyumbani hapo na kuwakuta Bi.Ramla na Abdul wakiwa sebuleni wanakunywa na kufurahi huku wamefungulia muziki kwa sauti ya juu sana. Shamsa alikuwa wa kwanza kuingia ndani huku maaskari wawili wakimfuata kwa nyuma, Bi.Ramla alipomuona mwanae alimkaribisha kwa furaha, Shamsa alimuangalia kwa dharau kisha akamuuliza mama yake “mama anafanya nini, mbona umebadilika sana mama yangu mpaka unafikia kutaka kumuua Jongo kijana wa watu” Bi.Ramla hakujibu badala yake alimuona Abdul akinyanyuka na kuanza kumfuata, kabla ajamfikia mlango ulifunguliwa na Askari wawili waliingia ndani. Kwa uwoga aliokuwa nao kwa polisi hao wenye siraha mikononi mwao Abdul alirudi nyuma na kuanza kukimbia kipitia mlango wa uwani, Lakini hakufanikiwa kufika mbali kwani tayari Askari hao walikuwa wamejipanga na kitakachotokea hivyo walimkamata Abdul pamoja na Bi.Ramla na kuwafunga pingu huku wakianza kumpa kipigo Abdul……
Walipakiwa ndani ya difenda na safari ya kuelekea kituoni ilipoanza, njia nzima Bi.Ramla alikuwa akilia tu na kumtaka mwanae amsamehe, lakini Shamsa hakutaka kuzungumza kitu kwani alijisikia kumchukia mama yake kwa kitendo alichomfanyia Jongo alistahiri adhabu. Hata walipofika kituoni kipigo sasa kikaanza upya wakiwataka waseme ukweli nani aliyekuwa amehusika na tukio hilo la kumpa sumu kijana Jongo.Abdul alipoona maumivu yanamzidi kuongezeka kutokana na kipigo hicho aliamua kujisalimisha na kuamua kusema vitendo vyote kwa mabaya waliyomtendea Jongo yeye pamoja na Bi.Ramla. Shamsa alishangaa kuona mama yake ndio mhusika mkuu wa maovu yale, hakuwa na la kusema aliwaacha polisi wafanye kazi yao kisha aliwasiliana na baba yake juu ya jambo hilo na kumueleza kila kitu kuhusu mama yake na Abdul.Bwana Samir kipindi chote hicho alikuwa mjini Mwanza akifanya kazi kwa muda, hivyo hakuwa akifahamu kitu gani kilichokuwa kinaendelea juu ya mama yake na Shamsa, ndio maana alivyoelezwa alishangaa kusikia mkewe yupo kituo cha polisi kwa kosa la kukusudia kuua .Bwana Samir alimtaka mtoto wake kuwa mvumilivu ili siku inayofuata atafika dar kulishughulikia jambo hilo.
Shamsa alirejea hospitali na kumkuta mama yake Jongo pamoja na Zainabu wakiwa wamekaa kwenye mabenchi ya hospitalini hapo, Shamsa aliwasogelea na kuwauliza habari za muda huo, wakamjibu ya kuwa ni nzuri kwani wamefanikiwa kumuona Jongo akiwa anaendelea vizuri ingawa fahamu bado hazijarejea sawasawa. Mama Jongo alimuangalia Shamsa kwa umakini kisha akamuuliza nini kimetokea huku alikotoka, Shamsa alikosa la kujibu maana donge lilikuwa limemkaba kooni alipotaka kuzungumza alishindwa na kuanza kulia, Zainabu alianza kumbeleza Shamsa na baadae aliponyamaza aliwaeleza ukweli kile kilichotoka.
Wakati wakiwa kwenye maongezi walimuona daktari akija maeneo yale waliokuwa wamekaa, alipofika hapo alimtaka Shamsa kwenda wodini kwani mgonjwa anamuhitaji kuzungumza nae kabla ya mtu mwingine kuingia. Shamsa aliposikia anaitwa aliacha mdomo wazi na kumkimbilia daktari na kumuliza nini kimetokea, Daktari alimwondoa wasi wasi Shamsa kwa kumwambia kuwa mpenzi wake Jongo anaendelea vizuri, hivyo alimtaka amfuate ofisini kwa maelezo zaidi ili aweze kwenda kumuona Jongo wodini. Shamsa aliongozana na Mama Jongo mpaka kwa daktari, walipoketi vitini Daktari aliwaeleza ya kwamba wamefanya kila liwezekanalo kuokoa maisha ya Jongo, lakini wamekumbana na changamoto nyingi mpaka kupelekea kukata tamaa kutokana na mgonjwa kuchelewa kurejewa na fahamu zake. Hivyo mungu amewapigania hatimaye wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuokoa maisha ya kijana huyo.Shamsa na Mama Jongo walikumbatiana kwa furaha walimgeukia Daktari na kumshukuru sana, Shamsa alimuhaidi kumpatia zawadi Daktari huyo lakini daktari alimwambia ni wajibu wao kufanya kazi kama inavyotakiwa ila cha msingi amshukuru mungu tu.
Shamsa na Mama Jongo walitoka mpakaa nje na kumkuta Zainabu akiwasubili, waliongozana mpaka wodiani alipolazwa Jongo, walipoingia tu wakasikia Jongo akihita jina la Shamsa. Haraka Shamsa alihitika na kukimbilia kitandani pale lipokuwepo kijana huyo amelala huku dripu ya maji ikiingia mwilini mwake.Shamsa alimbusu shavuni Jongo na kumpa pole mpenzi wake kisha Jongo akamueleza kuwa mama yake Bi.Ramla alivyokuwa mbaya kwa kwenda nyumbani kisha kumpatia Juice aliyokuwa ameweka sumu ili kuua.Shamsa macho yalimtoka na kumtaka Jongo amsamehe kwa kumuamini mama yake kumbe hakuwa mtu mzuri kwake, Jongo alimsamehe na kumwambia kuwa kosa ni la mama yake hivyo kama msamaha angetakiwa kuomba mama yake na sio yeye hivyo anyamaze kulia.Shamsa alinyaza kulia huku akijiapiza ya kwamba atoweza kuja kumsamehe mama yake kwa kitendo alichokifanya.
Siku iliyofuata Shamsa akiwa nyumbani alisikia mlango ukigongwa, alipokwenda kufungua alikutana na Baba yake Bwana Samir akiwasili kutoka Mwanza, Shamsa alifurahi kumuona baba yake alimpokea mizigo yake na kumkaribisha. Shamsa alipoingiza mizigo ya baba yake ndani kisha akarejea na kuchukua maji kisha kumpatia baba yake kama alivyohitaji.Bwana Samir alipokea kisha alipiga funda moja kinywa kisha akaishusha na kuiweka glas mezani. Muda wote Shamsa alikuwa akimwangalia baba yake asijue la kufanya kwani aliona itakuwa aibu kama akimueleza uchafu aliokuwa akiufanya mke wake.
“Haya niambie binti yangu kitu gani hasa kilichomfanya mama yako kuwekwa ndani” Bwana Samir alimuuliza mtoto wake baada ya kusalimiana
“Yaani baba we acha tu…Mama Amebadilika sana siku hizi” Shamsa alisema huku akikaa vizuri sofani
“Amebadilika kivipi, ameiba au?” Bwana Samir aliuliza kwa mshangao
“Sio hivyo ni hivi unakumbuka siku ile nilipokuja hapa kumtambulisha Jongo?”
“Yes, nakumbuka sana jinsi alivyokuwa akionyesha kuchukizwa na uwamuzi wako”
“Ni kweli mama alichukia na mpaka nisemavyo nahisi bado anachukia na ndio sababu kuu iliyompeleka polisi”
“Sasa Baba niambie maana sijui kisa kamili zaidi ya kuonganisha” “Bi.Ramla alikuwa na kijana anayeitwa Abdul sijui kama unamfahau, huyo kijana ndiye aliyekuwa akimpa jeuri ya kujifanya anajua kila kitu”
“Abdul ndio nani huyo kijana, anatokea wapi?
“Simjui anapotokea wapi ila alikuwa mtu wake mama kwa muda mrefu tu”
“Alikuwa mtu wake kivipi yaani mbona unanichanganya” Bwana Samir aliuliza kwa hamaniko
“Siku moja niliwakuta wamelala chumbani humu kwenye chumba chenu kile hivyo sikuwa na namna kukueleza baba yangu juu ya hali iliyotokea, cha kushangaza huyo kijana anataka anioe mimi nilipokataa kuachana na Jongo ndipo visa na matukio kila kukicha wakimfanyia kijana wa watu”
“Hee! ina maana mama yako alikuwa ananisaliti si ndio, alafu wewe unajua umeshindwa kuniambia kwa kipindi chote hicho?” Bwana Samir alifura kwa hasira
“Hapana mzee wangu nilikuwa sina uhakika na jambo hilo hivyo nilikuwa nachunguza ndipo nilipobahini kuwa ni kweli” Shamsa alijitetea
“Sasa wapo kituo gani?” Bwana Samir aliuliza kwa hasira
“Wapo kituo cha polisi Buguruni” Shamsa alisema
Kutokana na hasira za kitendo hicho alichofanya Bi.Ramla Bwana Samir alikuwa hashikiki mpaka Shamsa akaanza kumuogopa baba yake kwa siku mzee huyo hakuwa na masihara, hivyo Shamsa alimuacha kama alivyokuwa ila moyoni alijirahumu kwa kumuambia jambo hilo sasa hajui kitakachotokea katika familia yao. Shamsaalimnyenyekea baba yake na kumfuata kisha kumpigia magoti mbele ya miguu yake na kumtaka amsamehe Mama yake kwa kitendo alichokifanya kwani anaamini atajirekebisha.Bwana Samir akamuambia mtoto wake yeye hayupo tayari kumsamehe mwanamke huyo mwenye roho mbaya kiasi hicho, kwani alifanya unyama na ukatili kwa Jongo hivyo wamuache kwanza apate adabu kula adhabu kwa hiyo wawaachie polisi ili wakubaliane na Serikali watachoamua na sheria ifuate mkondo wake. Shamsa alimkubalia baba yake ila waliagana siku inayofuata asubuhi na mapema kwenda polisi kufuatilia inavyoendelea…..
Baada ya siku mbili kupita Jongo aliruhusiwa kutoka hospitali na kurudi nyumbani kwa mama yake, Shamsa akawa kila siku uenda kushinda nyumbani kwa mama Jongo ili kuwa karibu na mpenzi wake huyo mpaka pale hali yake itakapotengemaa. Siku moja wakati Shamsa akiwepo, pia Jongo na Zainabu wamekaa nyumbani hapo, walikuwa wakiongea maongezi ya hapa na pale, Ghafla bila kutarajia Jongo akimtaka Shamsa aifuatilie kesi kuhusu mama mkwe yaani Bi.Ramla. Shamsa alihachia tabasamu pana usoni mwake kisha akamwambia Jongo ya kuwa Baba Bwana Samir ndiye anayeifuatilia kesi hiyo hivyo yeye haijui kinachoendelea, Jongo alifika mbali zaidi akisema kwamba Kesi ya Bi.Ramla angependa ifutwe kwa sababu alishamsamehe siku nyingi sana. Yalikuwa maongezi ambayo yaliwaacha watu wote mdomo wazi, baada ya muda mfupi baadae walikuja wageni akiwepo Bwana Samir na rafiki yake kumwangalia Jongo.Hapo sebuleni sasa watu waliongezeka walikuwepo baba yake Shamsa, rafiki yake Mzee Mashaka, Mama yake Jongo na dada yake Jongo Zainabu, wakati wanasalimiana Jongo alionekana kuwa mnyonge alimtaka Bwana Samir amueleze jinsi gani kesi ya mkewe inavyoendelea. Bwana Samir alimueleza ya kwamba sababu ya kukosa ushahidi wa kutosha hivyo kila siku Kesi inasimamishwa sababu haijakamilika, hivyo alingoja ushahidi ili wasomewe mashtaka na kuukumiwa. Jongo hakulidhika na majibu hayo hata walipotaka ahachane na jambo hilo lakini Jongo aling’ang’ania wafanye iwezekanavyo, ili Bi.Ramla atoke.
Shamsa na baba yake walifuatilia jambo hilo kwa kiasi kikubwa huku Jongo akimtumia mjomba wake wasaidiane kufanikisha kumtoa na kuifuta kabisa kesi hiyo inayomkabili mama Shamsa. Baaba ya wiki moja mbele walifanikiwa baada ya kulipia na kumtolea dhamana ya shilingi milioni kumi na mbili, na baada ya siku kadhaa Mama Shamsa alitoka mahabusu na kurejea nyumbani. Tofauti na siku zote Bi.Ramla muda mwingi alikuwa mtu mwenye mawazo hakujua kama kijana yule Abdul atawezaje kutoka maana kumuacha kwake mahabusu ilionekana kwamba kesi zote za mama Shamsa alizibeba kijana huyo na ndio ilikuwa mwisho wake lazima haukumiwe kwa kosa kama hilo. Baada ya siku ya pili kupita tangia atoke mahabusu Bi.Ramla aliomba apelekwe nyumbani anapoishi Jongo ili aende kumuomba msamaha mkwe wakemtarajiwa, Shamsa na Baba yake walikubali na siku iliyofuata wakampeleka Bi.Ramla nyumbani kwa mama Jongo.Mama Shamsa alipofika nyumbani kwa Mama Jongo alimkuta Jongo na mama yake wameketi sebuleni, Mama Shamsa aliwasalimia kisha alimfata Jongo na kumpigia magoti kisha kuanza kuomba msamaha.
Jongo kwa huruma na unyenyekevu alimshika mkono mama Shamsa na kumnyanyua na kumuambia “nilishakusamehe tangia zamani mama, kuwa na amani kabisa” Bi.Ramla alishindwa kujizuia machozi yakamtoka kujutia kitendo alichokifanya kwa pamoja walisimama kisha wakakumbatatiana kwa furaha na Shamsa kumkumbatia mama yake na kumuambia“Kwa pamoja tumekusamehe Mama sahau yaliyopita tugange yajayo” Kwa hudhuni Bi.Ramla alilia machozi ya furaha akamfuata mumewe Samir naye akanyanyuka sofani wakakumbatiana na Shamsa naye akamfuata Jongo akamkumbatia kwa nguvu huku akimbusu sehemu kadhaa katika paji lake la uso huku akimuambia Jongo “ Chaguo langu ni wewe!” Wote wakafurahai na makofi yakasikika wote wakiwaangalia Jongo na Shamsa walivyogandana. Hapo ndio ukawa mwanzo wa maisha ya furaha na amani kwa Shamsa na Jongo kwani baada ya miezi miwili harusi ikafanyika kwa furaha na kwa muda mchache Shamsa alipata ujauzito na kujifungua watoto mapacha wawili wa kike na kiume aliwapa majina ya Amina na Amani wote wakiwa wazima wenye afya bora na hapo ndio ukawa mwisho wa ubaya wa mama Shamsa. MWISHO
“Nimekosa magoli zaidi ya 9000 katika maisha yangu, nimepoteza mechi zaidi ya 300 katika maisha yangu, niliaminiwa mara 26 kuwa nitaipa timu yangu ushindi lakini nikashindwa. Nilishindwa tena na tena na tena katika maisha yangu NDIO MAANA NIKAFANIKIWA- Michael Jordan, mchezaji wa zamani wa mpira wa kikapu.”
HALI haikuwa shwari katika kota za polisi maeneo ya Mabatini jijini Mwanza, shida ya maji ilisababisha baadhi ya maaskari kwenda kazini pasi na kuiloweka miili yao panapo maji. Umeme nao uliwalazimu wengi wao kuzipiga saluti huku nguo zao zikiwa hazijanyooshwa. Hii haikuwa shida sana kwa kundi kubwa.
Majira ya saa tatu kasorobo gari la maji liliwasili, lilikuwa ni agizo la serikali baada ya vilio kuwa vingi kutoka kwa wafanyakazi hawa watiifu. Akina mama wakatoka nje na kuikimbilia ile gari na kujikuta wameunda foleni ya kutisha huku kila mmoja akimuhimiza mwenzake asiruhusu mtu kuingia mbele yake kwani kila mmoja ana haraka na anayahitaji sana hayo maji. Kama ilivyo ada, panapo shida ustaarabu husafiri kwenda mbali. Akinamama watu wazima walikuwa wakipigana vikumbo haswa, huyu anamsukuma mwenzake aliyesukumwa naye anasukuma. Ilikuwa ni vita ya kimyakimya. Mwanamke mmoja mkimya alikuwa anatokwa jasho kutokana na kusimama muda mrefu katika ile foleni. Alikuwa akiitumia kanga yake kujipangusa lile jasho huku moyoni akilaumu sana kampuni inayohusika na usambazaji maji jijini humo kutokana na kushindwa kurekebisha tatioz hili lililoendelea kudumu hadi kwa siku kumi. Wakati anapanga foleni mbele yake walimtangulia watu wasiopungua thelethini, lakini sasa walibaki takribani saba. Akapata ahueni na tumaini jipya likazaliwa katika moyo wake wa subira. Macho yake yakiwa yanatazama mbele muda wote mara akagutushwa na mguso wa kusisitizwa katika bega lake. Akageuka… “Naomba unijazie hizi ndoo mbili foleni yako ikifika.” Sauti kavu ya kike ikamweleza, akashindwa kuelewa kuwa lilikuwa ombi ama amri. “Mama, nenda ukapange foleni tafadhali.” Akajibu kwa mkato kisha akapiga hatua mbele baada ya foleni kusogea. “Kwani ukinijazia utapungukiwa nini, watu wengine wana roho mbaya kama nini… ndoo mbili tu!” Mama mtaka kutekewa maji akabwatuka. “Kha! we shangazi vipi, we mwenzetu ushakoga unanukia pafyumu hapa, sie twanuka jasho halafu unataka urahisi tu. Ebwaneee kapange foleni huko…” Sasa mwanadada akajibu jeuri. “Na nitachota kabla yako, malaya mgeni wewe…” Akabwatuka huku akiondoka zake kama aendaye kupanga foleni. Yule binti akatamani kuendeleza shari lakini mmoja kati ya wanawake waliosikia mtafaruku huu akamwonya kuachana na ile shari. Akatii! Baada ya dakika mbili anamwona yule mama akiongoza njia kuelekea katika bomba….. Macho yakamtoka pima asiamini kuwa ni kweli yule mama mnukia manukato anachota kabla yake, hasira zikajijenga katika moyo na kichwa chake. Kweli akateka ndoo mbili. Akajitwika moja kichwani na nyingine ikaning’inia katika mkono wake wa kuume. Kisha kusudi kabisa akajipitisha mbele ya hasimu wake ambaye alikuwa akisota bado katika foleni. “Kinyamkera utangoja mpaka miguu izame tumboni…” Neno chafu likamtoka yule mama. Uvumilivu ukampiga chenga mwanadada akachomoka katika foleni akamvamia yule mama, ndoo ikamtoka kichwani na ile ya mkononi ikatua chini. Ukafuata ugomvi mkubwa kati ya mama mtu mzima na mwanadada. Mwanadada alikuwa hodari akamrarua vyema yule mama mtu mzima huku akimpa zawadi ya kapu la matusi. “Wewe Janeth wewe…. mke wa Inspekta huyo. Mungu wangu eeh! umefanya nini sasa… ungevumilia Janeth. Tumeshamzoea huyu hapa kota mbona sisi… ndo tabia zake.” Janeth akabaki kuduwaa, yaani kuwa mke wa inspekta ndo awe na tabia kama hizo. Janeth hakuwa akielewa sawa juu ya hivyo vyeo, kwake ikawa kama ndoto tu. Baada ya saa moja kupita askari wawili wakafika kota za polisi mabatini wakamkamata Janeth ambaye alikuwa akiishi peke yake kwa wakati huo baada ya kaka yake ambaye ni askari kusafiri na mkewe kwenda kijijini. Akawekwa rumande kwa siku nne! Ilikuwa ni mara yake ya kwanza, hivyo aliteseka mwili na akili. Alitoka akiwa amekonda mno. Akapewa onyo kali juu ya kosa lake la kumshambulia mke wa Inspekta.
_____
KILA aliyekuwa nje alimwona Janeth alivyokuwa anapepesuka, kijana mmoja akawahi kumpokea tofauti na wengine waliobaki kusikitika bila kutoa msaada. Akamfikisha hadi ndani, akatoka nje na kumletea maji ya kuoga, kisha akamkaribisha chai. Baada ya huduma hizi Janeth akachangamka kidogo. Wakazungumza mawili matatu kisha kijana akajitambulisha wakati anataka kuaga. “Naitwa Martin, Konstebo Martin Nguzu” “Lipi jina lako, Konstebo ama Martin. Maana umeanza Martin ukasita kisha ukaanza na Konstebo….” Janeth akahoji. Martin akatokwa na tabasamu hafifu kisha akamfafanulia Janeth kuwa Konstebo sio jina bali ni cheo katika jeshi la polisi. Hakumweleza kuwa ni cheo cha chini kupindukia…
______
JIJINI Dar es salaam hali ya hewa ilikuwa tulivu lakini joto halikutoroka liliendelea kuweka kambi jijini humo. Joto hili halikuyaathiri maji ya bahari ya hindi, hivyo watu walijazana katika fukwe mbalimbali kwa ajili ya kupambana na joto hili linalokera. Katika ufukwe maarufu wa Koko mamia walikuwa wamejitosa katika maji wakijaribu kuzisahau shida zao kwa kuogelea. Kijana mmoja alikuwa pembezoni akitazama watu wanavyoshindana kuyakata mkaji kwa mbwembwe. Alifurahia kutazama zaidi kuliko na yeye kujumuika katika maji yale. Si kwamba alikuwa hajui kuogelea la! Maamuzi tu… Na vile alikuwa mgeni jijini Dar hakutaka kuleta ujuaji aje aibiwe nguo zake aishie kudhalilika kwa kutembea nusu uchi na nguo za kuogelea barabarani. Wakati anaendelea kutazama waogeleaji hakuacha kuangaza fahari nyingine ya macho. Mabinti warembo wa Dar es salaam! Alikiri kuwa hayakuwa maneno matupu, ni kweli ni warembo mno. Urembo ambao unaweza kusababisha mwanaume kukiuka viapo vyake…. Katika kutazama vivutio hivi likapita kundi la watu watatu. Mwanaume mmoja na wanawake wawili….. Akaisikia sauti ambayo haikuwa ngeni sana katika masikio yake. Akasimama wima na kuanza kufuatilia kundi lile ili aweze kuona ni nani anayezungumza sauti ile. Akaongeza mwendo na kulifikia lile kundi. Kishya akapiga moyo konde na kuwasemesha…. Wakasimama! “Samahani…. kuna sauti naifananisha kati yenu.” Akarusha kete yake. Wakacheka! “Ehee! sauti yako dada, si ngeni kabisa katika masikio yangu. Sijui kama tumewahi kuonana…” “He! kaka, wenzako wanafananisha sura wewe unafananisha sauti, utajuaje labda uliisikia kwenye Televisheni ama huduma kwa wateja…” Akajibu kwa nyodo kiasi. “Au ndo yaleyale anayoyasema mama yenu… mnafanana misauti hiyo hatari…” “Eti kaka labda ulimsikia Zubeda ukadhani ndo mimi…” akajazia dada yule mrefu na aliyeumbika vyema hasa hasa miguu yake. “Mimi naitwa Nguzu, Martin Nguzu. Sijui kama umewahi kulisikia jina hili.” Akajaribu kujitambulisha huenda atakumbukwa. “Samahani kaka, sijawahi kusikia hilo jina hakika.” Alijibu kiupole. “Labda umewahi kukaa Mwanza. Huku Shamaliwa, Igoma ama Nyegezi…” Alizidi kutafuta uthibitisho. “Mh! kaka huyo mtu unamdai ama maana si kwa kulazimisha huko. Huu ni msako haswa…” Dada wa pembeni akachombeza. “Hebu ngoja, kwanini tuandikie mate….” Dada aliyefananishwa akasema kisha akachukua simu yake akabofya na kuweka sikioni. “Eh! Da Zuu kuna mtu kakufananisha huku….” Aliongea huku anacheka. “Anaitwa Zungu sijui nani…” “Naitwa Nguzu…” alirekebisha upesi Martin. “Anaitwa Nguzu, hebu ongea naye bwana. Maana alivyotuganda looh!” Akampasia simu Martin Nguzu. “Habari, naitwa Martin, Konstebo Martin Nguzu…” Akafanya utambulisho kama alivyowahi kufanya jijini Mwanza kwa mwanadada aitwaye Janeth lakini huyu wa sasa ni Zubeda. Maongezi yalichukua takribani dakika moja kabla simu haijarejea mikononi mwa dada aliyefananishwa. “Ndiye..” akashusha pumzi martin huku akitabasamu. “Kumbe ni askari looh! ningeshangaa mlugaluga tu aje kuhangaika na watu asiowajua.” Hatimaye yule mwanaume akazungumza. Mwanaume aliyekuwa pamoja na mabinti hao. “Amesema nikupatie nambari yangu umtumie sasa hivi anipigie.” tabasamu halikujipa likizo katika midomo yake pindi alipokuwa akiyatamka hayo. Ikawa hivyo. namba ikatumwa lakini hakupigiwa simu… Usiku wa saa nne simu yake ikaita… Alikuwa ni Janeth ambaye kwa sasa anajulikana kwa jina la Zubeda. Ni miaka mitatu ilikuwa imepita tangu waonane mara moja tu jijini Mwanza. Wamekutana tena jijini Dar es salaam!
Maisha ya Martin yalikuwa tulivu bila ubaya na mtu. Huenda yangedumu katika utulivu huu kwa miaka mingine mingi, lakini kukutana na Janeth aitwaye Zubeda kwa sasa ikawa ni safari nyingine ya kutisha!
“Nimejifunza katika maisha yangu kuwa walimwengu watasahau vyote ulivyosema, pia watasahau vyote ulivyofanya lakini kamwe hawatasahau ULIVYOWAFANYA WAJISIKIE aidha vibaya ama vizuri….”
Honi ya gari ilisikika mlinzi akafungua kizingiti kidogo kilichopo getini akaisoma nambari na kutambua kuwa ilikuwa nambari ya bosi wake. Upesi akalifungua geti vyema gari ikaingia ndani. Tofauti na siku zote, siku hii gari lilipita hadi nyuma ya nyumba. Mlinzi hakufuatilia kwa sababu tayari alimuona bosi wake kupitia kioo cha mbele. Gari lilizimwa kisha akashuka mwanadada ambaye hakuhitaji kukuonyesha mali zake nyingi ili uweze kumweka katika kundi la wanadada wapambanaji wa mjini ambao wamefanikiwa kuzikusanya noti na kuizoea harufu yake. Alikuwa amevalia sketi fupi iliyoruhusu mapaja yake kuonekana japo kwa kuibiaibia, mkononi alishikilia simu mbili ambazo kwa bei ya harakaharaka unajenga nyumba kijijini kwenu kwa kutumia tofali za kuchoma na kuezeka kwa bati zenye hali nzuri na zinabaki senti kadhaa za kununulia jenereta dogo litakalofanya nyumba yako iwe kivutio kwa watoto mpaka wazazi wa hicho kijiji unachoishi nyakati za usiku. Kwa mwendo wa madaha akaufungua mlango wa nyuma, akashuka kijana ambaye hawakuwa wakiendana hata kidogo. Huyu alikuwa mrefu wa haja mweusi na ambaye alionekana kuwa mwingi wa mazoezi kwa jinsi umbile la kifua chake lilivyogawanyika. “Nguzu, hapa nd’o ninapojilaza walau siku ziende…” Alizungumza mwanadada ambaye Nguzu alipaswa kumtambua kama Zubeda na kusahau kabisa kama aliwahi kulijua jina la Janeth maishani mwake. Nguzu alikuwa amejiandaa kisaikolojia kuanzia awali kuwa yule Janeth wa Mwanza aliyeswekwa rumande kwa sababu ya kumzongazonga mke wa inspekta atakuwa amebadilika mno. Lakini hakudhani kuwa angeweza kuwa anaishi katika nyumba nzuri kiasi kile, kuendesha gari zuri namna ile. Umbo lake nalo lilikuwa limenoga, hakuwa yule kimbaumbau wa Mwanza mabatini. Mate ya matamanio yakamruka Nguzu. Akatamani gari, akatamani nyumba na maisha mazuri kwa ujumla. Lakini angeyapata kwa wepesi gani ilihali alikuwa amegotea katika cheo cha ukonstebo katika jeshi la polisi na hapo alikuwa na majukumu lukuki yaliyojua kuutafuna vyema mshahara wake mdogo kila ulipokuwa unaingia. Alipoingiza mguu wake sebuleni akazidi kughafirika, maisha ya Zubeda yalikuwa yanamkera si kwa sababu ni mabaya la! alikuwa na maisha mazuri kupindukia. Akajaribu kuanza kujifananisha naye walau kidogo, Zubeda anamiliki luninga bapa yeye anamiliki ile modeli ya zamani yenye kisogo mfanowe mlima kilele cha mlima Kilimanjaro. Nguzu akasonya na kupuuzia uwiano aliotaka kuuweka. “Huenda ameolewa na kibopa hapa mjini! Acha matamanio Nguzu!” alijionya Nguzu na hapo akamuuliza Zubeda juu ya masuala ya mahusiano. Upesi Zubeda akajibu kuwa hajaolewa na hatarajii kuolewa hivi karibuni. Matamanio ya Nguzu yakarejea upya!. “Njoo uione nyumba yangu Martin, Konstebo Martin Nguzu!” Zubeda akaiga namna Nguzu alivyokuwa akijitambulisha. Nguzu akatokwa na cheko la haja! Wakapita huku na kule hadi wakakifikia chumba cha Zubeda. Hapa ndipo Nguzu akahisi kuwa Zubeda ni mwongo tu hakuwa akiishi peke yake, na hii ni baada ya kuiona sare ya jeshi la polisi katika chumba kile. “Hivi wanawake wataacha lini uongo wao jamani! kwani akiniambia kama ameolewa mimi nitapoteza fahamu ama?” Alijiuliza huku hamu ya kukisaili chumba ikimwisha. “Zubeda una uhakika haujaolewa?” Kwa ghadhabu kiasi fulani akahoji. “Eeh! sijaolewa vipi unataka kunitolea mahari.” akajibu na kutupa utani juu yake. “Na hizo sare..” Akahoji huku akikodoa macho ya kumsuta Zubeda. “Ooh! sijakueleza kumbe, unapaswa kunipigia saluti Konstebo Martin Nguzu, mimi ni koplo Zubeda Msangi.” alijibu kiuchangamfu sana. Nguzu akabaki mdomo wazi, moyo ukaingiwa uchungu asiamini kuwa yule binti ambaye miaka kadhaa nyuma hakuwa akijua hata nini maana ya Konstebo leo hii ni Koplo. Cheo kimoja juu yake. “Nadhani mwakani naweza kuwa ssajenti kama Mungu akipenda!” Alimalizia Zubeda. Mungu akipenda?? akajiuliza Nguzu, ina maana Mungu haoni kuwa mimi ninahitaji zaidi kuliko huyu mwanamke au? akajiuliza katika nafsi yake na asipate majibu mjarabu. Zubeda akatoa picha mbalimbali na kumwonyesha Nguzu, siku akiwa anaapa na picha kadhaa akiwa mafunzoni. Nguzu akapwaya! Kumbe kweli!! Akagutuka Akapigia mstari kuwa hana hadhi yoyote mbele ya Zubeda. Kikubwa alichomzidi ni kwamba yeye alikuwa mwanaume na Zubeda mwanamke, lakini hata akijitoa ufahamu kuhusu hilo bado Zubeda naye angejitapa kuwa yeye ni mwanamke na Nguzu hajawahi wala hatakuja kuwa mwanamke. Nimepatikana leo! Alikiri Nguzu huku kijasho chembamba kikiulowanisha mgongo wake. Bahati iliyoje kiyoyozi kilikuwa kinapepea, la sivyo kile kijasho cha usoni kile kinachoibuka ghafla mtu akiwa katika taharuki kingemuumbua Nguzu.
Zubeda alijitahidi kadri alivyoweza kumfanya Nguzu ajisikie yu huru lakini haikuwa heri katika moyo wa Nguzu. Lakini jitihada za Zubeda kuujenga ukaribu baina yake na Nguzu hatimaye ile safari yao ambayo ilianzia jijini Mwanza ikafikia palipotarajiwa. Ilikuwa ni siku nyingine ya kukutana kwao, walianza kwa kukumbushiana juu ya lile sakata la shida ya maji kota za polisi jijini Mwanza wakaunganisha na sekeseke la Zubeda kukabana na mke wa Inspekta. Wakafikia lile tukio la Nguzu kujitolea kumsaidia Zubeda kuanzia maji ya kuoga na baadaye chai. Sasa Zubeda akamtaka Nguzu amtengenezee tena chai, Nguzu akafanya zaidi ya chai akampikia Zubeda ugali wa dona, nyama na mboga za majani. Pishi likamnogea Zubeda akajikuta anataka tena na tena…… Mwishowe mapishi yakawa mapishi. Uhusiano wa kimapenzi ukaibuka. Lakini ulikuwa uhusiano wa kisasa uliotawaliwa na lugha za kisiasa. Uliojaa masharti lukuki. “Martin, sina la kukuficha safari yangu hadi hapa nilipo imetawaliwa na mikato mingi. Hadi sasa ninajihusisha kimapenzi na mume wa mtu, sio kwamba ninampenda kwa dhati ila nitakosa adabu nikisema kuwa simuheshimu. Ninamuheshimu sana moyo wangu unanishuhudia katika hili. Ujue niliwapuuzia vijana vijana hawa ama niwaite watoto, wao wanachoweza kukufanyia kwa ustadi mkubwa ni kukuburudisha mwili tu lakini kwenye masuala ya maisha wanakudumaza. Halafu wanabana sana yaani, ikitokea amekulipia kodi basi anataka kila siku aje kuifaidi kodi yake chumbani… looh!” Martin Nguzu akajikuta anatokwa na kicheko kwa jinsi Zubeda alivyokuwa analalamika. Ni kweli lakini haikuwa masihara! “N’do hivyo Martin yaani inafikia hatua unajuta, na vile damu inachemka anaweza akakuvunja mgongo. Nikaona hapana siwezi, nikajiweka kwa kile kibabu kina pesa na kuja hapa ni mara moja moja….. Jiulize Martin, kibabu kimenitafutia cheti cha fomfoo kwa jina hili la Zubeda, kimepambana nimeenda jeshini, kimepambana sijapitia msoto jeshini na hatimaye nimepata kazi. Kwanini nikidharau….. nakuapia kwa mizimu yote Martin, katu sijawahi kujihusisha na mapenzi na mwanaume mwingine tangu nianze kuwa na Inspekta. Wewe unakuwa wa kwanza tafadhali nakuomba sana usije ukaniharibia, usijekuwa kama vijana wenzako wanaopenda ngono kama walitangaziwa kuwa ukifanya sana unaongeza umri wa kuishi…..” Akamalizia kwa utani kisha akampiga busu baridi kabisa Konstebo Nguzu katika papi za midomo yake. Konstebo akajiona yu daraja moja na inspekta ama ikibidi hata mkuu wa majeshi. Busu pekee! Mahusiano yakaanza. Hawakuliona giza lililokuwa linawanyemelea. Wakapumbazwa na mwanga wa mwishomwisho wa mshumaa!. Mbaya zaidi Nguzu hakutaka japo kulijua jina la inspekta ambaye anammiliki Zubeda. Penzi likanoga Nguzu akambatiza Zubeda jina maridadi la kimahaba. Jina linalotamkika kwa sauti tulivu ya kiume na kuleta hamasa panapo faragha. Akamuita Zuu!
_____ MUHARIRI wa gazeti la SIRI KALI alikuwa akiiendesha gari yake kwa mwendo wa kasi isiyohatarisha maisha yake ili awahi nyumbani. Kuna kitu alihitaji sana kupata uhakika kama kinaenda sawa na anavyodhania. Ilikuwa kawaieda yake kutopenda kuwa mtu wa kuacha mambo juu juu kama ilivyokawaida ya wengine. Tangu akiwa shuleni alitambulika kwa waalimu wote kutokana na usumbufu wake, alikuwa hakubali kitu kimpite asikielewe kisha akae kimya tu. Aliwasumbua sana waalimu kiasi kwamba ada yake ilikuwa inakwenda kihalali kabisa. Tabia yake hii ikaendelea hata katika utu uzima wake akiwa kazini, aliifanya kazi yake kiustadi pasi na kubahatisha na pale alipohisi kuna utata aliwahi kutafuta uhakika kwa wanaojua zaidi yake. Kutokana na gazeti alilokuwa anafanyia kazi kujihusisha sana na masuala ya siasa muhariri huyu alijiundia urafiki na na vitabu vya siasa ya afrika na dunia kwa ujumla lakini hakuwa mbali na masuala yahusuyo jeshi la polisi ambalo aligundua kuwa lipo jirani sana na siasa kuliko majeshi ya nchi za bara la ulaya ama Amerika. Utendaji kazi wake wa kiwango cha juu ukamsababisha apewe jina ambalo hakuwahi kulisikia waziwazi zaidi ya tetesi pekee. Wafanyakazi wenzake wakamuita Juma kimbelembele badala ya jina lake la kuzaliwa Juma Kiwele. Hakujali maisha yakaendelea.
Alipofika nyumbani akabadili nguo zake na kisha bila kupumzika akamuaga mkewe akaondoa hadi mtaa wa tatu, akaimalizia safari yake kwa mzee wa kale ambaye alikuwa na rundo la magazeti ya miaka ya nyuma. Kuna kitu aliwahi kukiona akahitaji kukiona tena kiuhakika. Mzee akamwachia ukumbi, akafukunyua kwa juhudi bila papara hatimaye akalipata gazeti la mwaka 1982. Kuna waraka ulikuwa umechapishwa. “Kwa macho yangu nilitazama mwanangu wa kwanza akiuwawa mbele ya macho yangu, niheri angefyatuliwa risasi moja na kupoteza uhai. Alinyanyasika kabla ya kupoteza uhai, walimkata sikio lake ili akiri kuwa tumehifadhi bunduki ndani ya nyumba yetu, walimvunja magoti yake ili akiri kuwa sisi si raia wa Tanzania. Roho iliniuma sana haswa nilipokumbuka zile harakati za kugombea uhuru angali nikiwa kijana mbichi sana, nilipigana kufa na kupona kwa ajiri ya nchi yangu leo hii mwanangu anavunjwa miguu ili akiri kisichokuwa na ukweli. Sikuwa na la kufanya, akapoteza maisha wakatangaza kuwa alijaribu kutoroka akatandikwa risasi akapoteza damu nyingi kabla ya kugeuka maiti. Haikutosha hii, wakamwendea mke wangu kipenzi, bahati nzuri kwake hakupitia mateso bali alipoteza maisha baada ya kugundua kuwa mwanaye angali mfu! Sikuwahi kuwa na bunduki lakini sasa ninayo, sikuwahi kuwa na roho mbaya lakini niliyonayo ninakaribiana na ibilisi, ninapoandika waraka huu bila kujalisha kuwa utachapishwa ama la nitakayoyafanya naomba nisilaumiwe na ninajua kuwa ipo siku nitakufa. Mkibahatika kuyaona maitiyangu na myape adhabu kwa kushindwa kuwa na moyo wa kusamehe! Wakati mnayaadhibu maiti yangu mjiulize kila mmoja kwa nafsi yake. Je? ungelikuwa wewe ungelistahimili uliyoyashuhudia?? Walidhani mimi ni mfu kwa mabaya waliyoutenda mwili wangu, lakini Mungu akawa upande wangu nikabaki hai…
Florian Ngengekuzenza Nguzu, 1982.”
Waraka ule wa aina yake ukakomea pale, na baada ya hapo ukimya ukatanda mpaka miaka mitatu baadaye ambapo liliibuka kundi lililotikisa nchi, ujambazi ukakithiri utekaji na mambo yote ya kutishia amani. Waraka ule ukiwa umesahaulika mmoja kati ya watekaji anakamatwa anabanwa na kusema kuwa kiongozi wake anaitwa Nguzu Ngengekuzenza lakini katu hajawahi kumtia machoni. Msako unapita lakini hakuna walichoambulia. Hakuna aliyetambua ni wapi mzee yule alikuwa amejificha…. Mtindo wa matukio aliokuwa akiutumia Ngengekuzenza ambaye alisadikika kuwa mkuu wa oparesheni hiyo isiyokuwa na jina ulikuwa mtindo wa akili nyingi kuliko nguvu. Wakilinda huku analipua kule, wakiachia hapa anaingia mzima mzima. Lakini hakuna aliyewahi kumtia machoni. Mnamo mwaka 1988, Ngengekuzenza anakutwa amepoteza maisha mtaroni bila kuwa na jeraha wala ujumbe wowote. Maswali mengi yakabaki bila majibu. Wengine wakisema hili hawa wanalipinga bila kuwa na hoja za msingi.
Muhariri akamaliza kupitia alichotaka kupitia kisha akapitia majina yote ya askari waliokuwa wamehamishiwa katika vituo mbalimbali jijini Dar es salaam. Konstebo Martin Nguzu! Jina hili likamkuna sana Juma, akawa anatamani sana kuonana na askari huyu amuulize mawili matatu iwapo ana uhusiano wowote na mzee yule wa miaka ya themanini aliyetikisa nchi na kisha kukutwa amepoteza maisha bila jeraha lolote. “Nitamtafuta taratibu tu..” alijisemea wakati akiyaweka sawa magazeti yale mengi ili aweze kuaga na kuondoka. “Kama ni yeye nitaandika makala ambayo itanipa Tunzo ya mwandishi bora. Kupata Tunzo na ujana huu mbona ni fahari sana. Nitawakomesha ofisini watanitungia jina jipya kwa soni itakayowakumba” Alijisemea huku akiwa wima na tabasamu pana usoni. “Babu kuna gazeti moja ninatoka nalo.” “Ukumbuke tu kurudisha na kulitunza vyema mjukuu wangu Juma.” Babu akamsihi. Juma akaaga na kutoweka. Hakuelekea nyumbani badala yake alifuata uelekea tofauti ili ausogelee mwanga kuhusiana na martin Nguzu. Alisahau kuwa mwanga haumwepushi mtu kupotea njia, mamia kwa mamia hupotea njia mchana kweupe na jua likuwa linaimulika dunia.
“Siku mbili za msingi katika maisha yako ni SIKU YAKO YA KUZALIWA na ile siku utakayogundua NI KWANINI UMEZALIWA….”
KUPENDWA RAHA, tena raha hii huja pale unapoyaona waziwazi mazingira ya penzi lenu kudumu sana. Mapenzi mengi yanayohusisha watu wengi wasiokuwa na uwezo mzuri kifedha huvunjika mapema kwa sababu ya kutowajibika. Sasa penzi la Konstebo Nguzu lingevunjikaje? Zuu haombi kuongezewa salio kwenye simu, halalamiki kununuliwa simu mpya, ukiona anaomba kulipiwa kodi basi huo ujumbe ameutuma bahati mbaya huenda alikuwa anamaanisha ni yeye anataka kumlipia Nguzu kodi ya pango, haombi kununuliwa nguo badala yake analalamika kuwa kabati limejaa mno hana pa kuweka nguo nyingine. Sasa penzi linavunjikaje hapo, labda wachokane tu! Nguzu hakuwa na mpango wa kuchoka penzi hili. Penzi lililomfanya anawiri na kujisahau kabisa kuwa yeye ni Konstebo, kuna kipindi aliwahi kujiona kuwa yungali Mkuu wa majeshi yote ya ardhi na anga nchini Tanzania. Mapenzi bwana!
Ikiwa imepita miezi takribani minne tangu gundi ya huba iwaunganishe wawili hawa huku lile pepo la wizi wakilihalalisha na kuwa halali. Konstebo Nguzu alikuwa eneo lake la kazi majira ya asubuhi. Ilikuwa yapata saa mbili na dakika chache asubuhi katika kituo cha polisi Magomeni usalama, mgahawa ulikuwa umesheheni tayari wateja ambao asilimia kubwa walikuwa ni askari wa kituo kile. Nguzu akiwa mmoja kati yao Si kwamba raia wema hawakuruhusiwa kutumia mgahawa ule lakini kama ilivyo ada ya Tanzania, raia wanawaogopa askari wao na askari wanapenda kuogopwa. Watachangamanaje? Mama muuza alikuwa amejikita katika kuwahudumiwa supu na chai askari waliokuwa wakiwania, kila mmoja akitaka kuhudumiwa wa kwanza ili aingie katika majukumu yanayomuhusu. Vyeo hadi kwenye chakula cha kulipia? Nguzu alinung’unika katika nafsi yake baada ya kuambiwa ampishe askari mwenzake ahudumiwe kwanza kwa sababu tu alikuwa amemzidi cheo. Akatii! Kanuni muhimu kabisa katika jeshi, akawa ameifuata.
Kitendo cha kukatishwa zamu yake kikamfanya anune, kisha akaghairi kunywa supu akaagiza soda baridi akaketi na kuanza kunywa. Hata kabla soda haijafika robo, akatakiwa kumpisha kiti mkubwa wake mwingine aketi. Sasa ladha ya soda ikabadilika ghafla na kuwa chungu mithiri ya pombe inavyokuwa kwa mnywaji wa siku ya kwanza. Akiwa ameegemea ukuta alijitazama begani hakuwa na nyota hata moja mwenzake alikuwa ameanza kuchafuka begani. “Konstebo!” Sauti ikamtoa katika lindi la mawazo. Akageuka huku na kule kutazama ikiwa ni yeye anaitwa ama kuna konstebo mwingine jirani na yeye. Hakuwepo! “Konstebo!” akaitwa tena kwa cheo chake, cheo cha chini kabisa katika jeshi la polisi. Akaitikia wito, akamwona yule bwana mwenye cheo cha Inspekta akimwonyeshea ishara kuwa kiti kipo wazi aketi. Akaruka upesi akatua katika kiti. Kitendo cha kupewa kiti na Inspekta kikarejesha ladha ya soda ile na ubaridi ukapenya vyema kooni. Akiwa katika utulivu wa hali ya juu bila kuingilia mazungumzo aliyoyakuta alibaki kuinywa soda yake kwa hatua ndogo ndogo. Lakini alikuwa anatetemeka, na hapa akagundua kuwa kuketi na watu wanaomzidi vyeo lilikuwa jambo lililomuathiri kupindukia. Masiko yake yalikuwa wazi kusikiliza mazungumzo ya wawili aliowakuta pale. Ilikuwa ni kuhusu kesi fulani iliyoonekana kuwasumbua vichwa, alitamani kuchangia hoja kidogo lakini akakumbuka kuwa wenzake walisahau ni lini mara ya mwisho kuwa katika cheo chake cha chini. Akaufunga mdomo. Lakini kichwani alikuwa anazungumza akijaribu kuwashauri wawili hawa ni kitu gani wanapaswa kufanya kuhusiana na kesi iliyokuwa mikononi mwao. “Hawa watu nyota zao zote ni bure kabisa, sasa wao wanaona suluhisho ni kumkamata mke wa mshtakiwa. Je kama huyu bwana alimwoa huyu mwanamke ili kumfurahisha mama yake tu.. atajali nini? Mi binafsi sioni kama ni suluhuhisho….” akatokwa na tabasamu jepesi. Inspekta akaliona. “Vipi Konstebo mbona unatabasamu, ni utamu wa haya mazungumzo ama…” “Hapana afande, ni utamu wa hii soda, sijatumia siku nyingi sana…” Akajibu kwa utulivu wa hali ya juu. “Unaitwa nani Konstebo…” “Konstebo Nguzu, Martin Nguzu afande!” “Unaitwa nani..” akauliza tena, Konstebo Nguzu akajitambulisha tena kwa ukakamavu.
“Sawa Konstebo Nguzu. Unaweza kutupisha kidogo sasa!” Inspekta alimwamuru, Konstebo Nguzu akajiondokea huku kichwani akiona ni jambo la fahari sana kujihusisha kimapenzi na Koplo Zubeda. Kwani kwa kufanya hivyo anayapooza maumivu yake yote ya kuamrishwa hovyo kila mara. Amri alizoamini kuwa ni dharau!
Akiwa yu katika fukuto la ghadhabu, simu yake ya mkononi ikaitwa. Akalitazama jina na kupokea upesi. Walau alikuwa amepigiwa na Koplo Zubeda, mwanamke aliyekuwa anamfariji na kumpa raha, hali iliyomfanya kuzisahau shida zake. Wakazungumza kwa dakika kadhaa kujuliana hali kisha wakaagana huku wakipeana ahadai kedekede. Kisha wakaingia kazinui, kila mmoja katika kituo chake. Nguzu Magomeni na Koplo Zuu Chang’ombe polisi Temeke.
_______
SIMU YA JUMA (Kimbelembele) ilimweka, bado alikuwa kitandani maana hiyo ilikuwa ni siku yake ya mapumziko. Koplo Mtani, jina lilisomeka. Akapokea upesi. “Amakweli ukiwa unakitafuta kitu kwa dhati sana unaweza usikipate ila huwa kinajileta wakati umekata tamaa tayari.” Alianzisha maongezi bila kusalimia. “KUnani tena afande.” “Leo nimekutana na Nguzu wako. Tena tumeketi meza moja asubuhi kweupe pee! Kumbe ni ka konstebo, kapole halafu kakijana tu. ” Alijibu kwa bashasha Koplo Mtani. Juma akaketi kitako, na kuuliza maswali mfululizo. Koplo akayajibu yote kiufasaha na kumweleza kuwa siku inayofuata afike kituoni amwonyeshe mtu wake. Damu ya muhariri wa gazeri la Siri Kali ikachemka, ubinafsi alioanza nao ukaendelea kumtawala hakumwambia mtu ni mpango gani anao dhidi ya Konstebo Martin Nguzu. Kwanini amshirikishe mtu angali aliamini kuwa anenda kuandika makala pekee?? Amakweli maarifa mengi, mbele kiza! Maarifa ya muhariri Juma Kihwele (Kimbelembele) hayakumfanya ang’amue kuwa si kila mtembezi hujua uelekeo. Akatamani siku iliyotajwa ifike upesi. Masaa akayaona hayasogei, hayawi hayawi mwezi ukaondoka zake baada ya kumaliza utawala wake wa muda, jua likatoka katika usingizi wake na kuisalimia dunia. Akaianza siku na kauli dogoshi ya Koplo Mtani, ‘Ni ka konstebo , kapole halafu kakijana tu’.
“Ukihisi unaweza kufanya jambo fulani, sawa UPO SAHIHI. Ukihisi hauwezi kufanya jambo fulani, sawa UPO SAHIHI pia. Maamuzi ya KUWEZA ama KUTOWEZA yapo katika himaya yako……”
KIMBELEMBELE kilimfanya Juma Kihwele akose usingizi kabisa, alijigeuza huku mara ageuke kule. Alijisemesha kwa sauti ya chini na kucheka mwenyewe. Mzigo wa kimbelembele kile ulikuwa mzito sana na dhahiri ulionekana kumwelemea. Akaamini kabisa bila kukigawa kidogo kile kimbelembele basi huenda pasingekucha. Akamuita mkewe chumbani. “Dear, nimeshindwa kulala mwenzako” “Ushaanza! hapo unataka kuniambia matukio yenu ya kisiasa huko. Mi siyawezi.” Alijibu mkewe huku akiketi. “Bora ingekuwa habari za siasa, ya leo kubwa kuliko. Jamani mapenzi haya..” akasita akajikohoza kisha akaendelea. “Unamfahamu Koplo Zubeda Msangi.” “Eeh! namfahamu si huyu mama wa hapo mtaa wa pili. Uliyeniambia wakati ule kuwa ni nyumba ndogo ya Inspekta nani vile.” “Eewala! Inspekta Kobo.” Akahitimisha kwa madoido muhariri Juma Kihwele wa gazeti la SIRI KALI. “Kafanya nini tena maana we nawe na kazi yako. Kuna habari kaandikwa ama…” Akahoji kwa utulivu akionekana kuwa bado hajavutiwa na simulizi hiyo ya mumewe. “Bora angekuwa ameandikwa… Sikia ipo hivi, nilikuwa namfuatilia kijana mmoja hivi ni askari. Kuna vitu kadhaa nahitaji kujua kuhusu yeye. Huwezi amini katika kumfuatilia nikamwona anakuja hadi nyumbani kwa Koplo. Kama kawaida yangu nikitaka kujua jambo sichoki, nikaendelea kusubiri hadi walipotoka. Kwa kifupi Koplo Zubeda Msangi anajihusisha kimapenzi na hako kakijana kapole Konstebo Martin Nguzu ambaye nahitaji kufahamu mambo kadhaa kuhusu yeye.” Akamaliza na kumtazama mkewe. Bado hakuonekana kuvutika! “Ubaya ni kwamba huyo sijui Konstebo sijui Inspekta wote siwajui vizuri. Nd’o nashindwa kuelewa unashindwa kulala kwa nini haswa. Kisa Zubeda anajihusisha na mtu mwingine amakiasa nini. Nifafanulie basi….”
“Mke wangu, katika kazi yetu ya uandishi kuna mambo mengi. Kuna baadhi ya fursa huja zenyewe machoni, hapa unabaki kupima mzani nani anakupa pesa nyingi. Je? ni bosi wako ofisini ama ni huyo muhusika wa hii habari…” “Kwa hiyo unataka kuigeuza biashara hiyo habari? Na wewe ulipolala na yule dada wa mapokezi nani aligeuza biashara lile tukio lako ama wewe tu nd’o wayaona mabaya ya wenzako….. nilijua umeniitia mambo ya maana kweli mume wangu. Huo muda ningekuwa nimemfundisha Mariam kuhesabu moja hadi kumi na ameelewa kabisa. Yani we sijui upoje tu…” Akasimama na kutoka nje akiuacha mlango wazi.
Juma akabaki kimya kabisa, mkewe alikuwa amemgusa pabaya mno. Hakutaka kuikumbuka kabisa siku aliyofumaniwa na mkewe juu ya suala hilo la kujihusisha kimapenzi na msichana wa ofisini kwao. Ni kweli haikuandikwa popote, lakini hii haikuwa sababu nzito ya yeye kuachana na hili aliloligundua.
Ukimya huu haukumaanisha kuwa Juma aliamua kuachana na jambo hili. Akaona mtu sahihi wa kumshirikisha ni Koplo Mtani ambaye alimfahamu fika kuwa alikuwa ni mojawapo kati ya askari wasiokuwa waadilifu, rushwa ilikuwa rafiki yake wa karibu mno. Kuisubiri asubuhi aliona ni kosa la jinai. Akanyanyua simu na kumpigia kisha akamshirikisha hatua kwa hatua huku akiweka sharti la kutomtaja Inspekta anayejihusisha kimapenzi na Zubeda…
Licha ya kuwa mahiri sana katika kazi yake, lakini aliwapuuza wakongwe waliotangulia mbele ya haki waliponena kuwa hakuna siri ya watu wawili. Juma Kimbelembele alikuwa ameisambaza na ipo kwa watu wawili naye akiwa wa tatu. Kumshirikisha jambo lile Koplo Mtani kukampa ahueni, akajigeuza mara kadhaa akasinzia huku akiwaza kuigeuza habari hii mtaji. Aliamini fika kuwa hatakosa milioni kadhaa kibindoni ikiwa atazipanga karata zake vyema.
Wakati yeye anasinzia salama akiwa amejipunguzia uzito kiasi fulani katika mawazo yake. Upande mwingine nd’o kwanza palikuwa panakucha.
_____
MAPENZI RAHA, nilikuelezeni awali. Lakini huwa raha iso’ kifani wakutanapo wawili wanaopendana kwa dhati. Halafu wasipishane sana umri na mitazamo katika uwanja huo wa mahusiano ya kimapenzi. Muunganiko kati ya Konstebo Nguzu pamoja na Koplo Zuu ulikuwa wa aina yake, waswahili wanasema upele ulikuwa umepata wakunaji.
Siku hii hakuingia kazini mapema, aliwasiliana na mwenzake aliyekuwa na askari mwenzake aweze kumwakilisha katika majukumu yake hadi majira ya saa sita mchana. Ikawa hivyo! Nguzu akaamkia nyumbani kwa Zuu, wawili hawa walioshibana wakaanzia kupata kifungua kinywa kilichoandaliwa na Zuu mwenyewe. Walikula kisha wakalishana huku wakisifiana mambo kadha wa kadha. Baada ya kula wakashushia maji ya matunda. Kilichofuata ni Zuu kumshika mkono na kumkongoja chumbani Konstebo Nguzu, haikuwa mara yao ya kwanza kuingia katika chumba hiki. Awali Nguzu alikuwa akiogopa sana kufumaniwa lakini mazoea yakajenga kibanda cha kudumu katika mwili wake, kisha kwa sifa mazoea yakajibadili jina yakawa tabia. Chumbani wakagida mvinyo wa bei ghali, kisha wakakubaliana waende kuogeshana bafuni. Simu ya Nguzu ikaita ikawakatili uhondo wao. “Jamali ananipigia, ngoja nimsikilize.” Alimweleza Zuu kabla hajapokea ile simu. Zuu akaelewa. Baada ya kuongea kwa sekunde chache akakata simu, taharuki kiasi ikamvaa usoni. “Nahitajika kituoni muda huu, mkuu wa kituo ananihitaji ni amri.” alizungumza konstebo Nguzu huku akiwa amemkazia macho ya matamanio koplo Zubeda Msangi (Zuu). Uzuri Zuu naye alikuwa ni askari alijua vyema maana ya amri. Kwa unyonge akakubali matokeo. Akamuaga Nguzu kwa kumbusu katika papi za midomo yake. Machozi yakamtoka Zuu na asijue ni kwa nini yanamtoka wakati Nguzu akimuaga. Wakakubaliana kuonana jioni ya siku hiyo wamalizie walichopanga kufanya asubuhi hiyo. Wakabusiana tena kwa mara ya pili. Nguzu akatoweka, uzuri alikuwa amebeba sare zake za kazi na alikuwa amezivaa tayari. Akachukua usafiri wa pikipiki moja kwa moja kuelekea kituoni.
_____
UKIMWONA mtu mzima yu katika kilio pasi na sababu za msingi basi ana matatizo ya ziada katika akili zake, ama la ana tabia ya kulialia tangu utoto wake. Lakini ukimwona mwanaume aliyekabiliana na majambazi kwa kutumia silaha, akawasambaratimba licha ya kupigwa risasi kadhaa zilizouvunja mguu wake. Ukimkuta huyu analia peke yake, kaa mbali kidogo kwanza uumize kichwa, si kilio cha kawaida asilani. Inspekta Kobo alikuwa analia kama mtoto mdogo ofisini kwake. Alikuwa na miaka arobaini na nane, heshima ya kuwa inspekta pekee haikutosha kuthamini mchango wake katika jeshi la polisi. Wakati wa ujana wake alitambulika kwa jina la Vandame kwa jinsi alivyokuwa akiyapenda mapambano, kwake tukio la ujambazi likitokea nd’o alikuwa anafurahi kwenda kukabiliana nao. Tena alipenda sana wakiwa na silaha. Na hapo alikuwa na cheo cha chini bado, juhudi zake zikampandisha juu na hatimaye anazeeka akiwa Inspekta. Haikutosha lakini walau.
Mlango wake uligongwa, akajifuta machozi upesi na kisha akamkaribisha aliyehitaji kuingia. Mlango ukafunguliwa akausikia mshindo wa ukakamavu kisha ikafuata saluti. Akaipokea kinyonge sana! “Konstebo Martin, Martin Nguzu afande nimeitikia wito wako afande!” Kikakamavu mgeni akajitambulisha. “Keti” akamsihi. Nguzu akajitua katika kiti kilichokuwa jirani yake. “Una umri gani konstebo?” “Miaka ishirini na saba afande!” “Ninaitwa Mathew Koboko, ama inspekta Kobo. Naamini hatujawahi kuonana, zaidi ya yote mimi sijawahi kukuona.” akatulia akamtazama Nguzu. Nguzu akatikisa kichwa kukubali. “Nina miaka arobaini na nane sasa, umri umenitupa mkono, siko imara sana nilivunjika mguu nikiwa nalitumikia jeshi, mkono wangu wa kuume pia unatetemeka mara kwa mara kwa sababu ya kutumia sana bunduki, mgongo wangu sio mzima sana nikiketisana naumia, nikitembea sana naumia. Akili yangu pekee nd’o ipo salama. Salama kwa asilimia zote” Akatulia na kumtazama Nguzu usoni. Kisha akamwomba radhi kabla hajapenga kamasi nyepesi zilizokuwa zikimwandama. “Umeoa Nguzu?” “Sijaona afande!” “Mimi nimeoa mtoto wangu wa kwanza unamzidi miaka michache lakini ana mwili mkubwa zaidi yako.” Akatulia na kulazimisha tabasamu kisha akaendelea tena. “Nimekuita hapa ili nizungumze na wewe. Mimi kama Kobo na wewe kama Nguzu tena ni sawa na kijana wangu, lakini hapa tuzungumze kama wanaume wastaarabu walioketi baa kabla pombe hazijachanganya vichwa vyao. Najua wewe umekunywa pombe lakini sidhani kama umepitisha kiasi…” “Nipo timamu afande!” “Lakini umekunywa kidogo sivyo.” “Hapana afande!” Akakanusha Nguzu. Inspekta Kobo akasimama taratibu, akayaendea maboksi kadhaa yaliyokuwa pale ofisini, akapekua boksi moja na kutoa chupa akaiweka mbele ya Nguzu. “Nimekusamehe kwa kunidanganya kwa mara ya kwanza, usinidanganye tena kwa sababu hivi vyuma katika mguu wangu havinizuii kuurusha ukakufikia.” akaiacha ile chupa na kurejea katika kiti chake. “Haukuishia kunywa pombe pekee, Martin Nguzu umejipulizia marashi niliyoyanunua jijini Paris Ufaransa. Kwa kifupi umetoka nyumbani kwangu bwana mdogo. Nyumba inayonipa mimi faraja….” Akasita na kumwacha Nguzu apagawe kwanza. Hakika alipagawa, hakuamini kuwa siku yaikeinaanza hivyo. Akatambua kuwa yupo ana kwa ana na mume mwenzake. “Nilikwambia nimeoa Nguzu, lakini nipo salama zaidi nikiwa na Zubeda. Simtumii kwa sababu ya pote nilipomtoa, najua hajakwambia kiundani ni wapi nimemtoa… hawezi kukueleza kuwa nilimkutaanajiuza nikamnunua na hapo nikawa nimeyanunua maisha yake jumlajumla. Alikuwa amefyatuka akili zake na alikuwa amekata tamaa, nilitumia muda na uwekezaji mkubwa sana kumkomboa kutoka janga lile. Narudia tena ninaye mke ninayempenda hata kama yeye hanipendi, lakini kwa Zubeda ni sehemu ninayokuwa salama zaidi. Siwezi kukulaumu eti umeniingilia katika anga zangu, kama ningekulaumu hata usingeiona sura yangu bali ni mimi ningeiona sura yako baada ya wewe kukatwa kichwa na vijana wangu. Nimeona niwe mstaarabu kidogo, maana na huu uzee nikiwa mkaidi haina maana ya kuwa mzee sasa. Nguzu, imetosha kuingia nyumbani kwangu, niache basi nisije kufa na magonjwa ya moyo wakati risasi hazikuweza kuniua. Ujue nimelia sana leo hadi nimejishangaa, nimetambua wazi kuwa ninampenda sana Zubeda. Nawe ninakuomba uwe balozi wangu wa kweli, mtafute Zubeda mwambie mzee Kobo anampenda sana na sijawahi kumuwazia mabaya hata siku moja. Msihi haswa kuwa asinirudishe katikaujana wangu kwa namna yoyote ile. Unaweza kuondoka Konstebo Nguzu Martin Nguzu….” Alimaliza Inspekta Kobo kinyonge. Nguzu akasimama akiwa anatetemeka sana, jasho likimtoka. “Nenda nyumbani ukapumzike ukitoka humu ndani, nimekupatia mimi ruhusa hii Nguzu.” Nguzu akasimama huku akihema juu juu akapiga saluti na kutoweka pale ndani. Inspekta akamsindikiza kwa macho hadi alipotoweka.
______
Simu yake ilimgutusha kutoka katika dimbwi la mawazo. Ilikuwa ni namba ya Zubeda. Akatambua kuwa tayari mambo yamezidi kuharibika. Akapokea huku akiwa anatetemeka sana, moyoni mwake akitamani hii iwe ndoto ya mchana. “Laazizi! ukwapi?” Sauti tulivu kabisa ikahoji. “Nyumbani vipi kwani?” “Kuna tatizo Nguzu… tena linaweza kuwa tatizo kubwa sana tukilipuuzia.” “Ni kuhusu inspekta?” Nguzu akauliza. “Si bora kingekuwa kile kibabu ninakiweza kile. Kuna mtu anaitwa Juma Kihwele sijui unamfahamu?” “Hapana jina hilo ni geni kwangu Zuu. Kuna nini? na ni nani huyu?” “Amenipigia simu anasema yeye ni muhariri na anahitaji tuonane kwa mazungumzo juu ya mimi kujihusisha kimapenzi na Inspekta halafu na sasa nipo na wewe. Sijui ameyatoa wapi haya maneno, Nguzu atatuharibia huyu wakati ambao sio muafaka hata kidogo. Nimekupigia maana hili linatuhusu mimi na wewe, nataka tumuwahi.” Aakaweka kituo. Nguzu akapagawa, wakati anawaza kuwa ni jambo juu ya inspekta linakuja jingine khusu mwandishi. “Nakusikiliza wewe, tunamuwahi vipi sasa?” akauliza kinyonge mno. “Njoo nyumbani usiku tupange, kama saa tatu hivi.” “Hapana Zuu sitaweza kuja hapo usiku wa leo. Huoni kama tutazidi kulikuza tatizo… kwanini tusikutane sehemu ambayo sio hapo kwako?” “Sawa panga wewe halafu utanifahamisha basi…” Akamaliza na kukata simu. Nguzu akahisi kuugua, kama sio homa basi ni Malaria kali kupindukia. Utamu utamu sasa ukageuka uchungu! Hata kabla hajamweleza Zubeda yaliyojiri katika ofisi ya Inspekta Kobo yanatokea haya mengine ghafla! Akapanga kukabiliana na hili jambo kabla halijakomaa, akasimama imara akapiga saluti na kujiapiza kuwa hatalala tena na kulialia kama mtoto badala yake atapambana kiume. Hakujua kuwa wakati yeye akiamua kusimama,kuna ambao walikuwa wakikimbia mbio kali kwa nia ya kumzamisha katika shimo lenye kiza kinene.
“WAKATI mzuri zaidi wa kufanya mabadiliko katika maisha yako ulikuwa ni miaka kumi iliyopita….. WAKATI mwingine mzuri zaidi ni SASA! Usije ukathubutu kusema kuwa umechelewa kufanya mabadiliko katika maisha yako……fanya SASA”
ALIJARIBU kujiaminisha kuwa huenda amesikia vibaya, akazidi kujikunja kitandani ili asinzie vizuri. Lakini mlango ulipiga kelele tena, kuna mtu alikuwa anaugonga. Akiwa na mawenge ya usingizi aliufikia mlango na kuufungua bila kuuliza ni nani alikuwa anahitaji kuingia. Hakuwa katika fahamu zake taslimu. “Nani?” aliuliza baada ya kuwa ameufungua mlango na kukutana na kiza kinene. Badala ya kujibiwa akasukumwa ndani, kisha tochi kali ikayamulika macho yake akashindwa kutambua kunani mbele yake. Akajaribu kutokwa na pigo la ‘Karate’ aliyojifunza akiwa kambini lakini akaishia kupiga ukuta na kutokwa na ukelele wa maumivu. Mwanga ule ukapotea na kisha taa ya chumbani kwake ikawashwa. Akayapikicha macho yake na hatimaye aliweza kuona ni nani alikuwa mgeni wake asiyetoa taarifa. Mkojo ukatoka mbio katika kibofu usiangalie kuwa pale si maliwatoni ama msalani. Ulipofika karibu na mlango wa kutokea ukamstahi. Haukutoka! “Nguzu, mbona unawahi sana kulala.” Ilikuwa sauti tulivu kabisa ya Inspekta Kobo ndani ya nyumba anayoishi Konstebo Nguzu. Konstebo Nguzu aliishiwa hamu zote, akabaki katika hali isiyoeleweka. Inspekta Kobo akaketi. Nguzu akajilazimisha akapiga saluti. “Nguzu, ni masaa mangapi yamepita tangu tuzungumze?” aliuliza kwa utulivu uleule. Kabla Nguzu hajajibu yeye aliendelea. “Umenogewa na mali yangu ama? Yaani kweli nimekuita kwa upole na ustaarabu wa hali ya juu kiasi kile lakini kumbe usiku huu umepanga tena kukutanana Zubeda! Mbona unanifanyia hivyo konstebo….” Alizungumza kwa kulalamika Inspekta. Nguzu kimya! “Naomba unitazame machoni wakati unajibu swali hili.” Akasita kisha akaendelea baada ya NGuzu kumtazama. “Unampenda Zubeda kwa dhati ya moyo ama unampenda kwa sababu ni yule mwanamke ambaye hawezi kukulilia shida badala yake wewe nd’o waweza kumlilia shida?” Swali zito likamponyoka inspekta Kobo. Nguzu akabaki kimya tena huku akionekana wazi kuzidiwa na uzito wa swali lile na pia alikuwa hajaizoea hali ya inspekta kuwa ndani ya nyumba yake. “Martine Nguzu kwa kumbukumbu zako unafahamu inachukua muda gani kupanda kutoka cheo kimoja kwenda kingine katika jeshi la polisi?”
“Miaka mitatu..” Sasa alijibu huku amani ikiwa imetoweka. “Unajua kuwa yaweza kukugharimu miaka walau kumi na nane kufikia cheo changu…. lakini mimi sikutumia miaka kumi na nane kuwa inspekta, nilifanya makubwa sana… nilikuwa nina roho mbaya mno na nilikuwa nikiikamata bunduki nakuwa shetani kamili.” akaupitisha mkono wake na kuichomoa bastola yake kutoka mahali alipokuwa ameihifadhi. Sasa Martin Nguzu aliweza kuzungumza hata ambayo hajaulizwa. Mara aseme Zubeda ndiye alimlaghai mara aseme hatarudia tena…
“Sina maana mbaya kuiweka bastola hii katika mkono wangu, ninajaribu kukueleza na unielewe vyema. Ningekuwa nimekuvamia hapa kwako kwa sababu unahusika na uuzaji wa madawa ya kulevya ama ujambazi, muda huu mguu wako mmoja ungekuwa unasubiri muda tu ukakatwe. Lakini sipo hapa kupambana na wewe Nguzu nipo hapa kukusihi tu, kama inawezekana naomba uniachie Zubeda wangu, nasisitiza ninajaribu kukusihi tu na wala sio kukulazimisha. Niachie huyu binti, amepitia mengi magumu nimejaribu kuitafuta furaha yake walau kidogo tu, nimewaumizawengi kwa kutumia bunduki sitaki kuumiza tena kwa kutumia moyo.” akasita na kumwomba Martin maji ya kunywa, bahati nzuri hayakuwa mbali. “Konstebo mfano mimi najitoa katika maisha ya Zubeda nakuachia wewe, je? utaweza kumjazia mafuta ya gari lake? utaweza kumnunulia nguo za gharama kiasi kile, utaweza kumbadilishia samani za ndani ya nyumba yake? utaweza kuwalipa wafanyakazi wake? Utaweza Nguzu?. Kama jibu ni hapana basi nikikuachia Zubeda kuna watu watakuja kukusaidia majukumu nawe utajikuta unaumia moyo huku ukilia kama mtoto. Kwanini nikuache uyapitie hayo sasa…. kwanini nikuone upo katika njia mbovu nisikueleze ukweli. Nguzu kama Zubeda anakueleza ukweli, atakuwa amekueleza kuwa ninaenda kwake mara ngapi na ninashiriki naye tendo mara ngapi….. nadhani huwa anahisi mimi nimezeeka, ila sijazeeka Nguzu nipo imara mno tatizo ni moja tu, sio ngono iliyoniweka pale….. sio ngono Nguzu” Akashindwa kuendelea kuzungumza, chozi la mtu mzima likaiangukia sakafu ya Nguzu. Huruma kali ikamshika Nguzu, akataka kusema neno lakini Inspekta akamzuia na hapo akaaga na kuondoka zake bila kuhitaji hitimisho. Huu ulikuwa mtihani mkubwa sana kwa Nguzu, akaitazama saa yake tayari ilikuwa saa nne kasoro dakika chache usiku.
_____
JUMA KIHWELE alikuwa nje akipunga upepo huku akingojea kwa hamu simu kutoka kwa Koplo Zubeda ili waweze kumaliza zoezi lao. Alikuwa nje kwa maksudi makubwa, hakutaka mkewe ajue kuwa ameendelea na ule mpango wa kuitumia ile habari ya Zuu kujihusisha na wanaume wawili kujiingizia kipato jambo ambalo mkewe hakuwa ameliunga mkono kabisa. Kila mara alitazama simu yake kama kuna ujumbe wowote kutoka kwa Zuu, lakini hadi majira ya saa tatu usiku bado hali ilikuwa ya ukimya. Moyo wa subira ukaanza kuingiwa uchovu akafikiria kumpigia simu na kumchimba mkwara kuwa iwapo hatafanikisha kuonana kwao basi asimlaumu pakikucha. Akiwa katika kusubiri kule akaliona gari likipaki eneo fulani jirani na upeowa macho yake kisha akashuka mtu ambaye anamfahamu vyema. Kimbelembele kikachukua nafasi yake. Akataka kuhakikisha kuwa anamfahamu vipi mtu yule. Inspekta! akastaajabu. “Jamani si inspekta Kobo huyu.” akajiseme huku akisubiri kuona anaenda uelekeo gani, alipopita naye akafuata nyuma. Moyoni alijua wazi kuwa Zuu atakuwa amemweleza kila kitu inspekta, ile mipango yake ya kuvuna chochote kitu akaiona inapoteza uelekeo. Macho yake yaliyolizoea giza yakamwona inspekta akienda moja kwa moja nyumbani kwa Martin Nguzu. “Wanaenda kukubaliana nini hawa viumbe eeh!” alijiuliza hukiu akitamani kujisogeza hadi jirani na ile nyumba aweze kuvuna mawili matatu. Lakini alihofia kufumaniwa kisha kudhalilishwa.
Akarejea ndani ya nyumba yake, alipofika nakuiona kamera yake akapata wazo jipya. “Hawa wawili wanajihusisha na mwanamke mmoja, kwa namna yoyote ile kuna namna fulani ya kutoelewana itajitokeza. Na kama wakipigana basi nitanasa picha nyingine muhimu kwa ajiri ya gazetini.” Wazo hili jipya likamfanya atoke nje na kamera yake akaenda hadi chini ya mti akaketi huku akiiona vyema nyumba ya Nguzu. Kiupepo chenye ubaridi wa wastani kikaungana na mawazo tele ya Juma Kihwele na kuunda usingizi. Jumaakajikutaamesinzia akiwa eneo lile. Alikuja kushtuka baada ya kusikia makelele… akakurupuka akidhani kuna wizi umetokea mahali. Macho yake yakakutana na moshi ukifuka katika nyumba ya Nguzu. Nyumba ilikuwa inatetekea katika namna ya kutisha sana. Moshi mweusi tii uliichafua anga. Mungu wangu! akahamaki Juma, kisha akaiweka sawa kamera yake na kwenda kupiga picha kadhaa jinsi tukio lilivyokuwa likiendelea. Moyo wake ulikuwa unadunda sana. aliulaumu usingizi uliompitia chini ya mti na kusababisha asiweze kuona tukio lilitokea katika mazingira ya namna gani. Akatimua mbio mpaka pale lilipokuwa limeegeshwa gari alilokuja nalo Inspekta. Hapakuwa na kitu. “Inspekta amemchomea ndani Nguzu?” alijiuliza Juma huku akiwa na kimuhemuhe kipya kuliko kile cha awali cha kugundua kuwa wawili hawa wanajihusishakimapenzi na mwanamke mmoja. Magari ya zimamoto hayakufika usiku ule… nyumba ikateketea yote na kusalia majivu.
Juma alirejea nyumbani kwake akiwa hayuko sawa kabisa, alimfikiria mkewe na kutaka kumshirikisha juu ya kitu kilichokuwa kimetokea lakini alikumbuka majibu yake wakati anataka kufuatilia mkasa ule yalivyokuwa. Akasita kumshirikisha, hili la sasa lilikuwa zito mno na lingeweza kumtia hatiani angefanya kuliropoka. “Kwa hiyo kulikuwa na watu ndani?” Mkewe alimuuliza juu ya hiyo nyumba iliyoungua, kwani tayari alikuwa amesikia kwa majirani na alijua wazi mumewe hawezi kupitwa na habari ile. “Yaani hapa sina moja wala mbili.” alijibu kwa ufupi. Na hakutaka kuzungumzia tena jambo lile akaingia bafuni kuoga kisha akalala.
Kitu cha kwanza asubuhi ni kujua kama habari ile tayari imepata mwanga. Naam! Ikatangazwa kuwa nyumba imeungua kwa chanzo ambacho bado hakijajulikana na inasadikika kuwa askari mmoja amepoteza maisha akiwa ndani ya nyumba hiyo. Nambari ya askari yule ikatajwa na kisha jina likatambuliwa baadaye. Konstebo Nguzu alikuwa katikati ya moto ule na alikuwa ameangamia.
_____
Taarifa hii ya habari ikasikilizwa na masikio ya Koplo Zubeda Msangi aliyekuwa anaendesha gari lake kuelekea nyumbani kwa Nguzu ambaye alikuwa hapatikani katika simu ilihali walipanga kuonana usiku ule. Zubeda akiwa amevimba kwa hasira alikuwa anaenda kumlaumu waziwazi Nguzu kuwa si mtu anayejali hata chembe. Kulisikia jina lake likitajwa kuwa hayupo duniani tena, Zubeda akajikuta akikanyaga pedeli ya kuongezea mwendo wa gari badala ya kupunguza mwendo na mara akajikuta akikwepa kitu asichokijua gari ikatumbukia mtaroni, Zubeda ambaye hakuufunga mkanda wake akajibamiza katika kioo na kupoteza fahamu palepale huku damu nyingi ikimtiririka.
Kwa sababu ilikuwa asubuhi, askari waliokuwa barabarani waliwahi sana kumtambua koplo Zubeda ambaye alikuwa ndani ya sare zake za kazi. Simu za upepo zikapigwa upesi kutoa taarifa ile.
“ANZIA hapo ulipo, TUMIA hicho ulichonacho, FANYA kile unachoweza….”
KILIANZA kitanda kumsaliti, kila mtindo aliojaribu kukilalia ukagoma kumburudisha. Akastaajabu kitanda chake mwenyewe lakini amtii. Akasimama wima na kukitazama kwa sekunde kadhaa jinsi kilivyokosa nidhamu. Akaondoka bila kukiaga na kuelekea sebuleni,huko akajibwaga katika kochi kubwa lililokuwa sebuleni, hili likampokea vyema na ule mbonyeo ukamfurahisha. Heri yako bado unanitii! akajisemea, huku akiukunja mguu wake na kujaribu kuvuta taswira ya kitu kilichomfanya ashtuke usiku wa manane na kuanza kubabaika. Moshi mnene! hiki nd’o kitu kilichokuwa kikitishia afya ya akili yake kwa wakati ule. Akainyanyua simu yake na kujaribu kupiga katika nambari alizokuwa amepiga awali na hazikuwa zikipatikana. “Ni kweli Sule anavuta bangi tena sana tu, lakini sidhani kama bangi yake inaweza kumfanya akafanya upuuzi mkubwa namna hii…” Akajisemea huku akiketi. Alipoketi na kuwa kimya kwa muda kidogo akakumbwa na kitu ambacho kilimfanya ashindwe kuketi bali kusimama wima kabisa. Kuna vitu viwili vilikivamia kichwa chake, ulikuwa ni mfano wa picha ambazo zilikuwa gizani na sasa akabaini kuwa aliziona lakini pasi na uhakika. Picha ya kwanza ilikuwa ni mtu chini ya mti. Ni nani yule? akajiuliza huku akijilazimisha kuing’arisha picha ile katika kumbukumbu zake. Haikung’aa! Picha ya pili ni ya mwanaume akizungumza, na haikuwa ngeni sauti ile katika masikio yake. Haikuwa sauti aliyokuwa akiishikia mara kwa mara kama ilivyo sauti ya mkewe ambaye ni daktari. Hii ilikuwa sauti ambayo aliwahi kuisikia asijue mwaka wala tarehe, hakukaribia kukumbuka hata mahali alipowahi kuisikia. Ila aliwahi kuisikia. Baada ya miaka mingi ya mapambano na kisha kuamua kutulia tuli baada ya kuvunjika mguu wake, akabaki katika mapambano ya kalamu na karatasi huku akiwa yu katika chumba tulivu chenye urafiki wa dhati na kiyoyozi. Kwa jicho lake pevu kabisa Inspekta Kobo akajiona anaungiza mguu wake mbovu katika mapambano mapya. Licha ya mkewe kuwa daktari inspekta alipendasana kumshirikisha masuala yake pindi yanapomwendea kombo. Na hili lilikuwa limemnyima usingizi, akabofya simu yake na kumpigia mwenza wake, simu ikaita lakini haikupokelewa. “Yupo chumba cha upasuaji huyu…” alijisea na hakujaribu tena kupiga. Akafikiria kumpigia mpenzi wake wa siri, koplo Zubeda, akajiuliza mara mbilimbili kisha akaikumbuka ile kauli mbiu ya ‘ukivuka mipaka basi siri mweleze mkeo unayempenda kwa dhati lakini kamwe usitapike siri zako mbele ya hawara. HAWARA hana dhamana… Inspekta akakiri kuwa anampenda sana Zubeda lakini tahadhari lilikuwa jambo la muhimu sana. Akarejea katika kochi akaketi. “Nguzu atakuwa amekufa ama? na kama hajafa itakuwaje upande wangu…” alijiuliza Inspekta asipate wa kumjibu. Watoto wake walikuwa wanaelea katika dimbwi la usingizi mzito. Mawazo juu ya mawazo hatimaye usingizi ukamwonea imani, ukamsomba na kumuunganisha katika dimbwi walilokuwqa wakisafiri watoto wake kwa wakati ule. Dimbwi la usingizi…..
Asubuhi akaamka akijisikia ahueni na akijaribu kujisahaulisha kuhusu kiza kilichojiri usiku uliopita. Akiwa anafanya jitihada za kuyafuta haya akaipokea taarifa juu ya kuchomwa kwa nyumba aliyokuwa akiishi konstebo Nguzu, kilichosalimika ni nguo zake zilizokuwa zimeanikwa katika kamba iliyokuwa mbali kidogo na nyumba. Si kichwa wala fuvu lake kilichosalia katika moto ule wa kutisha. Inspekta akazishusha pumzi zake, akaanza kutembea huku na kule katika himaya ya nyumba yake. Akaunda mfano wa mzazi mdogo katika kichwa chake, akahisi uhai wa Nguzu ungeweza kuwa hatari sana kwake. Hatari kwa sababu alikuwa na ubaya naye nafsi ya Kobo ikakiri kuwa ilikuwa imechefukwa haswa kutokana na uwepo wa Nguzu. Kwa hatua hii ya kuzimika moja kwa moja akahisi kuwa itakuwa ni nafuu kubwa kama mtu aliyeingiliwa na mchanga jichoni akifanikiwa kuutoa na kisha jicho lake kubaki huru. Lakini uhai huohuoungeweza kumweka matatani kwa sababu Nguzu angehojiwa juu ya nani amehusika katika moto ule, angwataja watu ambao ana ubaya nao, kwa nini asilitaje jina la inspekta Kobo kama jina la muhimu zaidi!! Ni heri amezimika. Alihitimisha Inspekta Kobo. Akahamia upande wa pili wa mzani, Nguzu amekufa vipi? Je? ninahusika? akajiuliza, kisha akachukua simu na kupiga tena nambari aliyokuwa akihangaika nayo usiku uliopita. Haikuwa inapatikana… Hapo akarukia sehemu ya pili, ni nani alikuwa chini ya mti, na ni sauti ya nani aliisikia upande mwingine… Haya yalikuwa maswali magumu zaidi. Maswali yaliyosababisha aamue kuwa upande wa yeyote yule ambaye amefurahia kifo cha Konstebo Nguzu. Akaufunga ukurasa wa mawazo mazito juu ya ni nini atafanya ili Zubeda atulie na kuachana na Nguzu. Sasa aliwaza ni kitu gani amfanyie asije akazama kwa mwanaume mwingine kama ilivyokuwa kwa Nguzu. Akaamua kumfanyia ugeni wa ghafla utakaotawaliwa na upya mkubwa sana kutoka kwake… Akiwa mwenye kubwa tabasamu aliingia maliwatoni kujisafi mwili wake. Kisha akalivamia jokofu na kutoa maji ya matunda. Akaigida kwa fujo glasi ya kwanza mpaka ikamalizika. Kisha glasi ya pili akainywa taratibu huku akiwa anaipanga ratiba yake kwa siku hiyo. Simu yake ya mkononi ikatoa mlio kumaanisha kuwa kuna ujumbe mpya umeingia. Akaifungua upesi kwa sababu simu ilikuwa kiganjani kwake. “Bosi, shemeji kapata ajali yuko Temeke hospitali. Amekula mzinga na Suzuki yake” Ujumbe ule wa maandishi ukawa kama ulioambatana na umeme mkali kuzidi kipimo, ukautekenya mkono wa inspekta glasi ikamtoka mkononi, kisha akaanguka chini kama mzigo baada ya miguu kuelemewa. Mpasuko wa glasi na kishindo cha mwili mzito wa inspekta vikawashtua watoto waliokuwa wameamka tayari. Balaa jingine likaibuka. Walipiga mayowe huku wakiiitana kwa kusisitiza kuwa baba yao angali katika tatizo kubwa. Inspekta Kobo alijaribu kusimama ili alete amani kwa watoto wake lakini akabaini kuwa hawezi kusimama, ule mguu wake ulioungwa kwa vyuma ulikuwa umeyumba. Tusi pekee katika lugha ya kiitaliano alilolifahamu likamponyoka huku akiipigapiga sakafu. Kelele zilivyozidi akatoa onyo, akawafokea watoto wake huku akijinadi zaidi ya mara mbili kuwa yeye ni mwanajeshi kamili wasihamanike. Maneno ya shujaa huyu yakatuliza munkari, akafikishwa hospitali katika hali ya utulivu kabisa bila papara za kuwafanya majirani watambue kuwa inspekta Kobo amekumbwa na balaa.
_______
MAJIRA YA saa nne usiku kiwiliwili cha kiume kikiwa katika koti kubwa lililoungana na kofia yake kilikuwa kikikatiza katika wodi ya wanawake kwa mwendo wa haraka huku kichwa chake kila mara kikinyanyuka juu kutazama uelekeo wa mbele na kisha kuinama tena. Safari ile iliyojaa umakini iliishia katika chumba kilichojitenga mbali na wodi za wanawake. Watu wawili walimpokea kimyakimya na kumwingiza chumbani, akamwona mgonjwa wake. “Nakupenda sana Zubeda.” Lilikuwa neno la kwanza kumnong’oneza yule mgonjwa kisha akainama na kumbusu. Zubeda akajaribu kutabasamu kidogo. Inspekta Kobo alizungumza machache na Zubeda kisha akamweleza kuwa siku inayofuata atakuwa na muda mrefu zaidi wa kuzungumza mengi. Akaaga na kuondoka!
Alitumia usafiri wa pikipiki, upesi akarejea nyumbani kwani kwa ratiba ya mkewe ilivyokuwa siku hiyo alipaswa kuwa nyumbani majira ya saa tano usiku. Inspekta aliwasili baada ya dakika chache tangu saa tano ilipotimia. Hofu ilimtawala kidogo kwa sababu ya maswali ambayo angepokea kutoka kwa mkewe lakini pia angelaumiwa sana kwa kuanza mizunguko mapema kiasi hicho badala ya kupumzika. Hakumkuta mkewe nyumbani, akaanza kujilaumu sana kwa kuhofia ujio wa mkewe, huenda angeweza kuendelea kuzungumza na Zubeda kwa muda mrefu zaidi.
Wakati akiwaza haya, Daktari Kobo ambaye ni mkewe alikuwa katika chumba cha mgonjwa akijaribu kuzungumza naye kwa lugha ya upole kabisa, ni kawaida ya madaktari kuitumia lugha inayoleta tumaini kwa mgonjwa. Tofauti na ulivyokuwa utaratibu wa siku zote aliouzoea mgonjwa yule alistaajabu kuona mlango wa chumba kile alicholazwa unafungwa kwa ndani na yule daktari mwanamke. Kisha mwanamama yule akakisogelea kitanda na kumjulia hali. Mapigo ya moyo ya yule mgonjwa yakaanza kwenda mbio kupita kawaida. “Bila shaka sina haja ya kujitambulisha…. na hakika sijaja kwa ubaya humu ndani. Unaitwa Zubeda na unajihusisha kimapenzi na mume wangu wa ndoa Inspekta Kobo.” Akaweka kituo kisha akamwinamia mgonjwa yule. “Nimekusudia kuzungumza na wewe kwanza kwa sababu wewe ni mwanamke mwenzangu, unafahamu nini kuhusu kifo cha Konstebo Nguzu?” Swali lile lilikuwa kama upinde wenye moto mkali mbele yake. Likamchoma haswa Zubeda. “Sijui lolote.” alijibu kwa ufupi mno. “Zubeda, narudia tena, sipo hapa kwa sababu ya wivu wa kimapenzi, nina umri wa miaka thelathini na tisa sasa, nimeishi na inspekta kwa zaidi ya miaka kumi na nane. Nilikuwa ninao wivu zamani sio sasa…. ninawapenda sana watoto wangu sitaki wakose huduma zababa yao na huenda katika hili ni msaada pia kwako.Kuna taarifa ambayo haijazagaa kuwa wewe na inspekta mmeshirikiana kuichoma nyumba ya Nguzu huku yeye akiwa ndani na kusababisha mauti yake. Hili nd’o lililonileta hapa….. ungekuwa ni wivu wa mapenzi ningeagiza wakuchome sindano moja tu na siku inayofuata ungehamishiwa mochwari tayari kwa maziko, na mwili wako unmgeoza licha ya kupigwa na ubaridi wa mochwari. Sina nia mbaya… naomba unipe ushirikiano. Wewe na inspekta mpo matatani. Kumbuka kuwa IGP hapatani na inspekta Kobo sana, atawanyoosha katika hili. Niambie kama mmehusika ili tuweke kando masuala ya mapenzi kisha tuketi pamoja na kuitafuta suluhu kabla vithibitisho havijatapakaa.” Maneno ya dokta Kobo yalikuwa mazito mno, Zubeda hakuamini kile alichokisikia, hakuwahi kuzungumza na inspekta Kobo hata siku moja juu ya mpango huu wa kinyama kiasi hicho. “Ukiachana na hiyo njama, sijawahi hata siku moja kuzungumza na inspekta juu ya konstebo Nguzu.” “Sema hayati…” Dokta alimrekebisha. Marekebisho haya yakamuumiza Zubeda katika moyo wake, alikuwa amemzoea mno Martin Nguzu. Sasa anaambiwa amepoteza maisha. “Inspekta Kobo nd’o mtu wa mwisho kuingia nyumbani kwa marehemu kabla moto haujaimeza nyumba ile. Hivi unadhani wakuijumlisha na tatizo la wewe kuwa na wapenzi wawili kwa waikati mmoja kuna mtu atahitaji ushahidi wa ziada. Zubeda utapotea vibaya mno, mimi sijui sana sheria lakini kama nikichaguliwa kutoa hukumu katika hili basi nikiwapeleka gerezani miaka michache kabisa ni thelathini thelathini. Wauaji wakubwa nyinyi..” Jazba ikataka kuchukua nafasi akatulia kwa muda kujizuia na hali ile. “Shangazi, sijui lolote kuhusu huu mpango unaousema, sijawahi kuzungumza na Inspekta juu ya lolote kuhusu Nguzu. Hii ni kweli ya moyo wangu…” “Sawa kama haujui. Mimi naondoka…” alizungumza doktahuku akiyanyanyua mabega yake juu. Akauendea mlango na kutoweka…..
_______
LILIANZA kuwa saa moja, kisha likafuata la pili yalipofika matatu subira ikafikia kikomo. Inspekta Kobo akachukua simu yake na kujaribu kumpigia mkewe amuulize nini kinajiri hadi hajafika nyumbani hadi muda huo. Simu iliita kidogo kisha ikakatwa. Alipojaribu tena haikuwa ikipatikana. Akajaribu kupiga ofisini wakaelezea kuwa Dokta Kobo alitoka kazini tangu saa mbili usiku, wakastaajabu kupokea simu usiku wote huo wa kuuliziwa kwake. Inspekta Kobo ambaye tayari alijiona ni mtu ambaye ameandamwa na majanga ya ghafla akaingiwa mchecheto, haikuwa kawaida kwa mkewe hata kidogo kuchelewa nyumbani. Akafikiria kuwapigia rafiki zake wachache aliowafahamu lakini mshale wa saa ulimfanya aone haya. Saa nane usiku kumuulizia mke! Hapana…. Akaendelea kungoja huku pepo la wivu likianza kumchokonoa, akajiuliza ikiwa yeye ameweza kuwa na mwanamke nje inashindikana vipi kwa mkewe? Swali hili likamghadhabisha na kujiona hatendewi haki hata kidogo ikiwa ni kweli mkewe amediriki kufanya hayo. Usingizi ulimsomba majira ya saa kumi na moja kasoro dakika chache. Akagutuka saa moja na nusu asubuhi na bado mkewe alikuwa hajarejea nyumbani wala simu yake ya mkononi haikuwa ikipatikana. Hofu ikatanda maradufu…..
LILIANZA kuwa saa moja, kisha likafuata la pili yalipofika matatu subira ikafikia kikomo. Inspekta Kobo akachukua simu yake na kujaribu kumpigia mkewe amuulize nini kinajiri hadi hajafika nyumbani hadi muda huo. Simu iliita kidogo kisha ikakatwa. Alipojaribu tena haikuwa ikipatikana. Akajaribu kupiga ofisini wakaelezea kuwa Dokta Kobo alitoka kazini tangu saa mbili usiku, wakastaajabu kupokea simu usiku wote huo wa kuuliziwa kwake. Inspekta Kobo ambaye tayari alijiona ni mtu ambaye ameandamwa na majanga ya ghafla akaingiwa mchecheto, haikuwa kawaida kwa mkewe hata kidogo kuchelewa nyumbani. Akafikiria kuwapigia rafiki zake wachache aliowafahamu lakini mshale wa saa ulimfanya aone haya. Saa nane usiku kumuulizia mke! Hapana…. Akaendelea kungoja huku pepo la wivu likianza kumchokonoa, akajiuliza ikiwa yeye ameweza kuwa na mwanamke nje inashindikana vipi kwa mkewe? Swali hili likamghadhabisha na kujiona hatendewi haki hata kidogo ikiwa ni kweli mkewe amediriki kufanya hayo. Usingizi ulimsomba majira ya saa kumi na moja kasoro dakika chache. Akagutuka saa moja na nusu asubuhi na bado mkewe alikuwa hajarejea nyumbani wala simu yake ya mkononi haikuwa ikipatikana. Hofu ikatanda maradufu…..
Asubuhi akapokea ujumbe mfupi kutoka kwa mkewe. “Nipo salama mume wangu, nipo kwa mama mdogo. Kuna jambo limenichanganya naomba uniache kidogo natafuta suluhisho. Watazame watoto…” Inspekta akaufuta ujumbe ule. Alimjua vyema mkewe, haikuwa mara ya kwanza kuwa katika hali hiyo na kuamua kuwa mbali na mumewe. “Nimemkwaza nini huyu?” alijiuliza lakini akipata ahueni kuwa mkewe yupo salama. _____
Mwanaume mweusi sana mwingi wa misuli katika mikono yake alikuwa amejitwika mfano wa gunia katika bega lake, mwili wake ulitokwa jasho lililoufanya ung’are kana kwamba ametoka kuogelea katika dimbwi la mafuta ya kula. Alijitutumua na gunia lile huku akitweta. Lilionekana kumzidia, lakini hakuwa tayari kukubaliana na hali ile moja kwa moja. Macho yake makali mithiri ya nyoka yalikuwa makini kutazama huku na kule ikiwa kuna kitu kibaya aweze kujihadhari. Zaidi alililinda lile gunia kuliko alivyowaza kujilinda yeye mwenyewe. Alipoufikia mlima aliliweka chini lile gunia akapumzika kidogo kisha akajitwika tena na kuendelea na safari ile ambayo mwisho wake haukuwa bayana ikiwa ni wa matumaini ama la. Kilima kikamalizika akaanza kupita katika vichaka vya hapa na pale, mwisho akaufikia mto na kuanza kuogelea. Gunia likiwa juu kabisa, japo lililowana lakini haikuwa kwa kiasi kikubwa sana. Mkondo wa maji ulikuwa una nguvu sana lakini bwana yule mwenye misuli mingi alifanikiwa kuwa imara zaidi akapenya na kutokea upande wa pili. Huko akapokelewa gunia lile huku akipongezwa na wenzake wawili waliosaidiana lile gunia. Hawa nao walikuwa imara sana mmoja akiwa mfupi na mwingine mrefu. Wote weusi miili yao, wakaendelea na safari ya gunia lile kuelekea pahali lilipohitajika kufikishwa. “Hivi mali itakuwa salama kweli?” Mmoja akahoji wakati wa pumziko fupi la kubeba gunia lile. Swali lile likazua ukimya wa muda, wakalitazama gunia kwa pamoja. Kisha wakaangaliana kana kwamba waliambiana sekunde za kulitazama na sekunde za kutazamana. Ukafuata mguno kwa pamoja tena. “Unahisi jamaa atakuwa amefanya madhara yoyote?” aliyeulizwa swali naye akauliza swali kabla hajajibu alichoulizwa. “Au tufungue kidogo?” Swali tena kutoka kwa muulizwa. Swali hili likawafanya tena walitazame lile gunia kwa muda, halafu bila kukubaliana wala kupingana wakalibeba lile gunia safari ikaendelea. Hawakulifungua! Ilikuwa safari ya masaa kadhaa hadi walipolitua gunia mahali lilipostahili. Wakatulia wakilitazama kwa takribani dakika moja kisha wakainama na kulifungua gunia lile. Waliacha wazi kisha wakatoweka. Zikapita dakika kadhaa akaingia bwana aliyebeba bakora mkononi mwake, akalifikia lile gunia bila kusema neno lolote akaanza kuishusha bakora yake mara kadhaa guniani. Gunia lilikuwa limetulia tuli bado. Akazidisha juhudi kuliadhibu gunia lile na chochote kilichokuwa ndani yake huku akizungumza maneno mengi ya kulifokea na mengine ya kusihi. Jasho lilikuwa limemlowesha mwili mzima na alikuwa anatetemeka sana. Baada ya bakora ya kwanza kuonekana haitoi adhabu ipasavyo akabadilisha bakora, akachukua ndefu zaidi. Akaizungusha kwa ghadhabu zote akaitua katika gunia. Gunia likatikisika! Mchapaji akatulia tuli asiamini kile alichokuwa anakiona, akaanza kupiga mayowe akiwaita wenzake kutokea katika giza. Kelele zile zikawa tishio kwa mali iliyokuwa katika gunia lile.
“KONSTEBO ALIYECHOMEWA NDANI YA NYUMBA, Mengi yamejificha!” “MAPENZI CHANZO CHA KONSTEBO KUUWAWA” “KONSTEBO NGUZU. SI KIFO CHA KAWAIDA”
Vichwa vya habari vya magazeti matatu vilisomeka katika namna ya kutatanisha, ni nani ajihusihe na kifo cha konstebo iwe amekufa kifo cha kawaida ama ameuwawa? Wachache sana, hata makonstebo wenzake wasingejihusisha. Lakini vichwa hivi vya habari viliwashtua watu watatu kutoka pande tofauti lakini wawili kati yao walizungumza lugha moja huku muhusika wa tatu akiwa katika sintofahamu.. wawili wale walizungumza lugha ya biashara… Wa kwanza kupagawa alikuwa ni Juma Kimbelembele muhariri wa gazeti la SIRI KALI, alichanganyikiwa kabisa kwa sababu ni yeye pekee aliyejiona ana umiliki wa habari kuhusu kifo cha Konstebo Nguzu kwa kuchomewa ndani huku akikihusisha na masuala ya mapenzi. Penzi kati ya Konstebo na Inspekta Kobo. Ajabu sasa anatazama gazeti linaizungumzia habari kwa kuhusisha yaleyale aliyoyaita siri. Mbaya zaidi siri hii alikuwa ameiuza tayari na pesa ilikuwa ikitembea katika miradi yake mingine.
Upande wa pili, Dokta. Kobo mke wa Inspekta alikuwa anaelekea kurukwa na akili, kwa ajiri ya mume wake na familia kwa ujumla alikuwa ametokwa na pesa nyingi sana kwa ajili ya kumziba mdomo Juma ili asiandike habari zozote juu ya mume wake hasahasa skendo la kuwa kimapenzi na Koplo Zubeda. Hata siku tatu hazijapita anaziona habari zile. “Nimetapeliwa au?” alijiuliza akiwa katika chumba cha hoteli aliyojihifadhi mpaka pale ghadhabu zake juu ya mumewe zitakapomalizika. Alihofia kulala kitanda kimoja na mume wake ambaye amemsaliti, aliogopa sana shetani mpenda kifo asije kumwingia kichwani na kumsababisha amdunge mume wake sindano ya sumu. Aliijua hasira yake hasahasa ambapo mumewe angejaribu kumwongopea zaidi. Licha ya kujifaragua wakati yupo hospitali kwa Zubeda kuwa hana mapenzi ya dhati sana kwa mumewe, aliongopa na moyo wake ulilijua fika hilo. Daktari huyu hakuwa na mahali pengine pa kuzilaza hisia zake zaidi ya kifuani kwa Inspekta Kobo. Sasa angali anapambana mumewe asijafuliwe jina lake, tayari mambo yamekuwa kinyume. Akanyanyua simu yake na kumpigia yule muhariri Juma aliyemfuata na kumshirikisha juu ya habari ile na kumtaka wafanye biashara. Simu haikupokelewa. Akatuma ujumbe mfupi ulioambatana na kitisho kikubwa.
Mmoja asiyekuwa na moja wala mbili alikuwa ni Inspekta Kobo. Habari hii ilimfanya akayatafuta magazeti yale mara moja, akaziendea kurasa zilizoelezea kwa kina juu ya habari ile. Akashusha pumzi kidogo baada ya kukuta jina lake halijawekwa wazi lakini mwandishi wa makala ile alionyesha kujua kila kitu ni vile hakuamua kutajha katika makala hii ili aje kuuza magazeti mengine wakati mwingine atakapoamua kulianika jina la muhusika waziwazi. Inspekta akakumbuka kile kiwiliwili chini ya mti. Akaamini kuwa ni kiwiliwili kile kilimuona wakati anaingia na kutoka. Yule mwandishi alijuaje nitaenda kwa Nguzu eeh! alijiuliza Inspekta huku ikimjia pia ile sauti aliyoisikia usiku ule. Sauti ambayo si ngeni lakini alikuwa ameisahau tayari. “Lakini sijamuua Nguzu mimi. Mungu wewe ni shahidi. Niliitafuta amani tu….. nilipanga kumuua lakini nilighairi wanishushudia mwenyezi Mungu.” Alizungumza peke yake Inspekta huku moyo wake ukiona haya kwa sababu ni mwaka mzima na miezi ilipita bila kuingia katika nyumba za ibada. Akarejea katika magazeti yale na kusoma majina ya waandishi wa habari zile. Akabaini kuwa zile habari zilifichwa jina la mwandishi wakaishia kufanya mazoea yao ya kuandika kuwa imeandikwa na MWANDISHI WETU. “Attaccati a sto cazzo” Akabwatuka lile tusi pekee la kiitaliano analolifahamu huku akiyatupa yale magazeti mezani. “Who the hell is mwandishi wetu?! eeh! kwani sisi hatujui aliyeandika habari hiyo ni mwandishi wenu you bastard!” Alilalama peke yake huku sasa akiwa wima. Akajaribu kuwafikiria wafanyakazi wa magazetini ambao ni wasumbufu. Ambao siku hazipiti hawajapiga simu jeshi la polisi kuuliza maswali kadha wa kadha. Akainyanyua simu yake na kupiga katika kitengo cha mawasiliano jeshi la polisi. “Komredi, umekuwepo kwenye shifti tangu jana?” akaulizia. “Nimekaa siku ya tano leo, mwenzangu anaumwa. Vipi afande…” “Naulizia kama kuna simu yoyote kutoka gazeti la SIRIKALI…” “Lile gazeti la Juma Kihwele..” akauliza kimasihara. wakacheka kidogo kwa sababu walimjua vyema. “Yule bwabna sijui atakuwa anaumwa. Leo siku ya sita au saba hakuna simu kutoka kwake.” Inspekta akashukuru na kukata simu. “Huyu mjinga kuna kitu anajua, hawezi kukaa kimya siku zote hizi.” alijisemea huku akichukua kalamu yake na karatasi kisha akaainisha mambo kadhaa. MOJA, Juma Kihwele anaijua hii habari lakini ameogopa kuiandika kwa jina lake….. PILI, haijui hii habari lakini alivyo na kimbelembele anaifuatilia kwa kina akiandika awalipue wahusika.
Yote mawili yalimaanisha kuwa Juma ni mtu muhimu sana katika hili jambo. Inspekta akaingia chumbani kwake, akaitoa bastola yake mafichoni na kuitazama kwa muda kisha akasema nayo. “Let’s go to work boy! (Twend’zetu kazini)” Simu yake ya mkononi ikaita wakati akiipachika bastola yake pahali alipozoea kuipachika. Ilikuwa ni simu kutoka kwa mkewe….. Mapigo ya moyo yakaenda mbio sana.
Inspekta akashukuru na kukata simu. “Huyu mjinga kuna kitu anajua, hawezi kukaa kimya siku zote hizi.” alijisemea huku akichukua kalamu yake na karatasi kisha akaainisha mambo kadhaa. MOJA, Juma Kihwele anaijua hii habari lakini ameogopa kuiandika kwa jina lake….. PILI, haijui hii habari lakini alivyo na kimbelembele anaifuatilia kwa kina akiandika awalipue wahusika.
Yote mawili yalimaanisha kuwa Juma ni mtu muhimu sana katika hili jambo. Inspekta akaingia chumbani kwake, akaitoa bastola yake mafichoni na kuitazama kwa muda kisha akasema nayo. “Let’s go to work boy! (Twend’zetu kazini)” Simu yake ya mkononi ikaita wakati akiipachika bastola yake pahali alipozoea kuipachika. Ilikuwa ni simu kutoka kwa mkewe….. Mapigo ya moyo yakaenda mbio sana. Akaipokea ile simu huku akiwa anatetemeka mikono yake katika namna iliyomtishia amani. Alipoiweka simu sikioni kimya kikatanda kutoka upande wa pili. “Mama! Mama! Mke wangu… ongea basi mama.” alizungumza kwa upole wa hali ya juu. Badala ya kujibiwa akaanza kusikia pumzi zikipishana kwa kasi sana na hapo akaanza kukisikia kilio. Dokta Kobo alikuwa analia. Suala la mkewe kuangua kilio ikawa kama msumari wenye ncha kali unasukumwa katika paja lake angali ana fahamu zote. Maumivu! “Mama Melinda! una nini mke wangu nieleze… au niambie basi upo wapi nije sasa hivi.” Alisihi Inspekta Kobo lakini simu ikakatwa bila kusikia neno lolote. Akapagawa.
______
SHAMALIWA, Mwanza.
Umati wa watu haukuwa mkubwa sana. Walikuwa ni wanafamilia walioridhia ile taarifa ya kifo cha ndugu yao. Mama mzazi wa Nguzu hakuisha kulia na kulalamika kuwa alimkanya mwanaye asijiunge na jeshi lakini hapohapo akikiri kuwa ugumu wa maisha ulikuwa chanzo cha yote hayo. Waliojaribu kumbembeleza walikuwa wamefikia kikomo na sasa walimwacha alie kuzimia na kisha kuzinduka peke yake. Kuzika majivu! Mama yake alikataa kata kata, alidai kuwa hakuyaaga majivu katika kituo cha basi bali alimuaga mwanaye tena kwa kumkumbatia, leo hii akubali kuyazika majivu asiyoyajua? Hapana… akasimama kidete na wanafamilia wakamuunga mkono, hawakufanya maziko hayo. Ambaye aliamini Martin Nguzu amefariki sawa, ambaye hakuamini sawa. Mama Martin hakuwa katika upande wa walioamini. Na kila alipojaribu kuamini, lilikuja wazo jingine kuwa yawezekana mwanaye amefanyiwa ubaya tu. Sio kifo cha kawaida. Ndivyo walivyo akinamama. Ule uchungu wa mwana unasababisha haya.
Siku ya tano ikiwa inayoyoma na jambo hililikiwa limepunguza makali mioyoni mwa wengine kasoro mama mtu. Majira ya usiku ule uliingia ugeni ambao hakuna aliyeutilia maanani, maana kwa kipindi hicho watu walikuwa wanakaa nje, ndugu na jamaa wanacheza mchezo wa karata mpaka usiku wa manane na wengine kulala nje kabisa. Huyu bwana alikuwa mkimya kabisa na koti lake kubwa la kuzuia baridi, alijitikisa kwa sababu za msingi tu na hakugeuka huku wala kule, alikuwa amejiinamia. Kadri muda ulivyozidi kwenda na watu walizidi kupungua, wengi walienda kulala. Huu nd’o muda ambao yule bwana alijitikisa tena kwa kiasi kikubwa. Alisimama! Akapiga hatua kadhaa bila mtu yeyote kumtilia mashaka, akasogea pembezoni akaichomoa pakti ya sigara na kutoa moja, akaiwasha na kuuvuta moshi wake ndani ya kifua chake na kwa umaridadi kabisa akaupuliza angani kisha akautazama unavyotokomea angani. Akafanya vile takribani mara tatu, kisha akaizima. Akapiga hatua nyingine tena akaufikia mti kisha akaanza kuyatazama mazingira ya pale kwa uchache akahisi ni wakati muafaka wa kufanya kusudio lake na hakuona jambo lolote la kumzuia. Akapiga hatua huku mkono wake ukiwa katika mifuko yake, akajipitisha jirani kabisa na kundi la akina mama wawili waliokuwa wamejilaza. Akamwona muhusika wake. “Ndiye!” akajisemea. Kisha kwa kitendo cha upesi sana akainama, akamziba mdomo na kisha akaichomoa silaha yake na kwa lugha ya vitendo akazungumza naye. “Ukileta vurugu nitakuchinja.” Huku akiwa amemdhibiti vyema kabisa akamnyanyua wakaondoka kutoka katika eneo lile. Alipomfikisha pembeni kiasi akampiga teke kali miguuni, kisha akatua naye chini. “Mzee Majenga anaishi wapi?” lilikuwa swali kavu kabisa kutoka katika sura ngumu. Mama akabaki kuhangaika asijue ni nini hiki kinatokea angali ana kovu la msiba wa mwanaye wanatokea watu kumuuliza juu ya mzee Majenga. “Alihamia Shinyanga.” alijibu kwa ufupi. “Nitakuua sina masihara. Alihamia lini na awali alikuwa ana anishi wapi? nani ndugu zake?” Alijaza maswali mazito. “Kama mwanangu mmemchoma moto, ukinichinja hautakuwa umefanya dhambi mpya. Nipeleke kwa mwanangu, sina jibu jingine….” Alijibu kikaidi. Huku nafsi yake ikiwa radhi kabisa yule bwana amuue ili aondokane na huu uchungu wa kuishi bila mwanaye. Mkono wenye nguvu ukashusha ngumi katika bega la yule mama kisha kiganja kikawahi kuziba mdomo. Maumivu yakanyimwa kilio. Yule mama akabaki kuhema juu juu huku akiwa ameyakodoa macho yake. “Sasa utanijibu vizuri kabisa sivyo. Mzee Ma…” hakuweza kumalizia akahisi kuna mguso fulani kwa mbali katika bega lake. Akageuka bila hofu yoyote, akakutana na giza likiwa ndani ya giza. Lakini hili halikuwa giza ambalo linaweza kutembea. Ngumi kali ikatokea katika lile giza la maajabu, ngumi moja ikatua katika koo la yule bwana. Akajaribu kukohoa akawa ameikohoa roho yake. Umauti ukamfika. “Mama!” giza lile likaita. Mama aliyekuwa anahema juu juu huku akiwa anafanya dua maalumu kwa ajili ya kuiaga dunia akarejea katika fahamu zake. Haikujalisha giza lile lilikuwa totoro kiasi gani, mama alitambua ubini wake ipasavyo. “Martin!” akaita. “Nipo hai mama.” akajibiwa. Mama akaamka akaketi kitako asiamini kuwa alikuwa anapokea miujiza katika uzee wake.
Ubaya wa wanawake siku zote ni pale akili zao zikitulia. Mwanzo alikuwa ametulia tuli akizungumza na lile giza, lakini baada ya akili kukaa sawa akaanza kupiga mayowe. Mkono ukawahi kumziba mdomo. “Mama, huyu alikuwa anataka nini kwako.” “Simjui.” “Mama, sijauliza kama unamjua. Alikuwa anataka nini?” “Muulize labda wewe atakueleza vizuri.” “Hakuna mzoga uliowahi kuzungumza katika dunai hii mama. Nieleze..” “Amemuulizia mzee Majenga…. yule mzee alikuwa rafiki sana na babu yako. Wewe humjui…” alitoa maelezo yale. Majenga! Jina lile likapiga katika kichwa chake kwa kujirudiarudia, ni jina hili lilimjia punde tu baada ya kurejewa na fahamu asijue nani aliliingiza katika kichwa chake. “Uliponaje mwanangu, nyumba iliteketea yote ile. Tuliona kwenye Televisheni..” mama alimuuliza. “Mama usimwambie mtu yeyote kama umeonana na mimi, mimi nipo hai na ninaamini nina kazi kubwa ya kufanya kabla sijasimama hadharani na kuutangazia uma kuwa ninaishi.” Alisihi Nguzu. Kisha akamkumbatia mama yake na kumbusu shavuni. Upesi mama akaipapasa shingo ya nguzu katika giza lilelile. Na hapo akatokwa na tabasamu pana lililosindikizwa na machozi ya furaha. Aliyekuwa mbvele yake alikuwa yuleyule mtoto aliyetoka katika tumbo lake. Martin Nguzu! Ameponaje? hilo halikuwa swali lililomuhangaisha…… Bora uzima. Walizungumza kwa dakika kadhaa kuhusu Majenga kisha wakaagana.
Akiwa anafanana na giza kwa jinsi alivyovaa alitembea kwa tahadhari kubwa huku akiamini wapo wengine wanaweza kuvaa kama yeye na kufanana na giza, akapiga hatua na kutoweka eneo lile. Begani akiwa na mzoga wake…
_______ LILIANZA tumbo la kuhara, kila akiingia chooni linapoa anarejea chumbani. Linaanza tena anakimbilia chooni, linapoa. Alikuwa amechanganyikiwa mno. Hali hii ikamkumbusha kuwa angali akiwa mwanafunzi alikuwa anaugua haswa akisikia kuwa kuna bakora kwa ajiri ya wachelewaji ama ambao hawajafanya vyema kazi waliyoachiwa. Hivyo alikuwa mstari wa mbele kabisa kufanya kazi zote ipasavyo, kuheshimu sheria na kanuni za shule. Na hata ilipotokea migomo hakutaka kushiriki, wenzake wakambeza na kumweka katika kundi la wanafunzi waitwao ‘MBWA WAOGA’ shuleni. Alikuwa tayari kuitwa majina yale lakini alitambua kuwa anaitii sheria vyema. Akaishi hivyo na akakua hivyo. Akiwa katika utu uzima wake ana familia na yupo kazini, anajaribu kuisahau asili yake anaitaka pesa nyingi kwa njia zisizokuwa halali. Jaribio lake la kwanza linakuwa kuuza habari aliyoinasa mahali. Kabla mchezo haujanoga anajikuta matatani. Akatamani nyakati zirudi nyuma kidogo tu asijihusishe na hili jambo asilani. Lakini ni saa pekee inaweza kurudi nyuma na si wakati. Juma Kihwele alikuwa amekamatika. Akafikiria mtu wa karibu yake wa kuweza kumshirikisha hilo jambo, hasahasa ujumbe kutoka kwa Dokta. Kobo uliomfanya kupata tumbo la kuhara ghafla. Mkewe, hapa asingethubutu kugusa hata kidogo kwa sababu tayari alikuwa amemwonya kuachana na masuala ya kufuatilia habari zisizomuhusu. Akafikilia kukimbilia msikitini walau amweleze kiongozi wake wa dini. Huku napo akaona pagumu kuingilika, maana huku ni mambo kunyooshwa tu hakuna kona kona. Kila sehemu aliyoiwaza akaona haiingiiliki. Mwisho akajiwekea maamuzi ambayo aliyapa jina la ‘NANI ATAMFUNGA PAKA KENGELE’ Katika maamuzi haya yeye alikuwa panya. Akawavika vyeo vya U-paka Inspekta na mkewe. Kisha akamchagua inspekta Kobo kwa kujipa imani kuwa yule ni mwanaume mwenzake hivyo watazungumza na yatamalizika tu. Akaingia bafuni akausafisha mwili wake, akavalia nadhifu kisha akaamua kujihukumu. Akachukua simu yake na kuipekua nambari za Inspekta Kobo. Akajihisi kutetemeka wakati anapiga simu ile. Kitetemeshi kikaisha alipogundua kuwa simu ile haipatikani. Akachukua maamuzi ya kumpigia Koplo Mtani yule aliyemsababisha akajiingiza katika mchezo huu asioujua. Lakini maamuzi yake yakayeyuka baada ya kujiona kuwa atakuwa anawaingiza watu wengi katika hili jambo aliloliita kuwa ni maongezi ya kiume dhidi ya Inspekta Kobo. Kwa sababu alipajua ofisini kwake akaamua kwenda kimyakimya wakayamalize. Akatoka na kuingia katika gari yake, akaitazama tasbihi iliyokuwa inaning’inia katika kioo cha ndani cha gari lake. Kisha akawasha gari na kuondoka zake. Baada ya dakika moja, gari jingine dogo likatoweka na kumfungia tela. Hakujua kuwa wakati anawaza kumfunga paka kengele na wengine waliwaza hivyohivyo juu yake. Kwa wakati mmoja Juma ‘kimbelembele’ alikuwa panya na hapohapo paka. Kiumbe wa ajabu kupindukia!
Aliiendesha gari yake kwa utulivu huku kila mara akijilaumu nafsi yake kwa tamaa za ajabu ajabu. “Tazama nimejenga nyumba nzuri kabisa, hata kama sijahamia bado lakini nina uhakika wa kuhamia siku yoyote, nina gari na nimekaribia kumnunulia mkewangu la kwake, nina amani ya nafsi, mtoto wangu anaishi vizuri kabisa, anasoma shule nzuri. Hiki nini kiliniingilia kichwani nikapatwa na tamaa mimi lakini, eeh! Ninaheshimika ofisini, bosi ananipandishia mshahara kila leo. Ni kipi nilitaka tena Juma mimi. Yaani shuleni waliponiita kimbelembele nilichukia na kuwaona hawanipendi, sasa najionea mwenyewe. Ona sasa naanza kuhangaika na kimbelembele changu, mtu mwenyewe Inspekta unakuta ana hasira zake huko anipige mabuti, mi kupigana sijui, jeshi lenyewe sijapitia….. Hivi Juma nilikuwaje mimi eeh!” alilalamika kwa sauti ya chini, malalamiko yaliyopelekea machozi kuanza kumbubujika. Akashindwa kuona mbele vizuri, akaamua kuegesha gari lake kando. Akajifuta machozi. Akaitazama simu yake na kugundua kuwa ilikuwa inaita pasi na kutoa mlio. Akakumbuka aliiweka simu yake iwe katika hali ile. Akaishika kwa utulivu na kutazama. Ni mkewe alikuwa amempigia. Akampigia kuuliza kulikoni. “Mume wangu naomba urudi nyumbani muda huu, sasa hivi mume wangu… atawaua watoto huyu. Njoo mume wangu…” Alizungumza huku amepagawa mno mke wa Juma. Simu ikakatwa bila kusubiri majibu kutoka upande wa pili. Lile tumbo la kuhara lililosumbua kuanzia akiwa nyumbani likayasikia mazungumzo haya, kwa kirehere cha hali ya juu likatamani kusikia zaidi. Likatoa wawakilishi palepale akiwa ameketi katika kiti chake cha gari…. Hali ya hewa ikachafuka…
“YAKIMBIZE maisha ama la acha maisha YAKUKIMBIZE. Uchaguzi ni wako siku zote…”
ALIBAKI katika mzubao kama mwanaume aliyemwona mwanadada mwenye mvuto akijongea kwenda upande wake akajilaghai katika kichwa chake kuwa amekutana na bahati ya mtende akajiandaa kumpokea, kisha mrembo yule anatokwa na neno la ghafla. “Kaka umesahau kufunga zipu yako..” Mzubao huo ulimkumba Juma Kihwele, alipotoka katika mzubao akahamia katika mlowano katika suruali yake. Chozi likamtoka alipotambua kuwa haikuwa ndoto bali alikuwa kama anavyojiona. Mbele na nyuma palikuwa pameshirikiana kumfedhehesha. Ubahili akauweka kando, kabla harufu ile haijawafikia wasiohusika Juma Kihwele akapandisha vioo vya gari lake kisha akawasha kiyoyozi. Alitambua wazi kuwa kiyoyozi hakitakuwa na msaada mkubwa lakini walau linatimia lile neno la ‘Mchuma janga hula na wa kwao’ kwanini yeye ale na wasiomuhusu? Acha ale na kiyoyozi…. Akaigeuza gari kwa kasi akiwa ametaharuki. Akawa amebadilisha uelekeo na kuelekea alipokuwa ametoka. Jambo lile likawa na maana nyingine kwa waliomtazama… ______________________ KITENDO kile cha kubadilisha uelekeo kikawashtua wale waliokuwa katika gari iliyokuwa ikimfuatilia toka alivyoliacha geti la nyumbani kwake. Dereva akabweka na kuwashtua wenzake, wote hawakuamini walipoiona gari ile ikiondoka kwa mwendo mkali. Kila mmoja akabaki kumlaumu mwenzake kwa kuukosa umakini. Lawama zisingekuwa na msaada wowote dereva akapambana naye kutafuta njia ya kugeuza gari ili afukuzane na lindo lao walilolivizia kuanzia linatoka nyumbani Sasa lindo limewatoroka ghafla. Wakabaki kujiuliza ni wapi ambapo waliteleza hadi yule bwana akawaona…. Swali hili likawafanya waanze kuamini kuwa bwana Juma ana watu wengi nyuma yake ambao wanamsaidia katika suala la ulinzi. Hapa wakaongeza umakini na ile hali ya kumchukulia Juma kama mwandishi asiyekuwa na tahadhari katika maisha yake ikatoweka. Hawakujua kuwa Juma Kihwele alikuwa amevurugwa vibaya mno, na hata ule mwendo kasi wa ghafla ulikuja ghafla kama ulivyoonekana na hakujua kama alikuwa anafuatiliwa. JUMA aliwasili nyumbani, bila kujali kuwa alikuwa amechafua nguo yake alishuka upesi na kuingia ndani ya nyumba yake huku akiwa amenyoosha mikono yake juu kama namna ya kujisalimisha ili wavamizi wakijitokeza kwa nia ya kushambulia basi awe amejitetea tayari kuwa hana madhara yoyote kwao. Huenda wataingiwa na huruma juu yake. Hicho nd’o kitu pekee alichoweza kufanya kwa wakati ule. Alilivuka geti lake huku akijilaumu kwa ubahili wake uliokithiri wa kushindwa kumlipa mlinzi ili awe analinda masaa ishirini na nne badala yake akaona usiku nd’o wakati pekee wenye hatari akaamua kulipia masaa kumi na mawili. “Mlinzi mwenyewe analinda na rungu?” Alitoa kauli ya kupuuzia majuto yake. Alitembea hatua kwa hatua hadi akaufikia mlango wa kuingilia ndani ya nyumba yake akabaini kuwa ulikuwa umefungwa kwa nje. Bila shaka mvamizi yupo nje. Huku akiwa anatetemeka akaufungua ule mlango, akaikuta familia yake yote ikiwa inatazama ukutani. Mama mwana pamoja na shemeji yake aliyekuwa pale kwa ajili ya likizo. “Jamani…. kuna nini mke wangu?” Akamuuliza, mkewe akageuka huku akiwa anatetemeka na asiamini kuwa aliyesema naye alikuwa ni mumewe. Akaanza kuangua kilio huku yote anayoyasema yasisikike vyema kiasi cha Juma kuanza kumkaripia kuwa anapaswa kuzungumza kwa utulivu ili wajue ni kitu gani kinaendelea. “Ni nani alivamia hapa na kukueleza upige simu.” “Simjui, sijawahi kumwona hata siku moja.” “Anafananaje? na ni kitu gani anataka kwangu…” Mkewe akamsogelea Juma na kumkumbatia, hakuwa na sababu nyingine ya kumkumbatia bali kumsihi waende chumbani. “Hapana… tuzungumze hili jambo kwanza tuelewe muafaka!” alipinga vikali. Mke akamsogelea tena na safari hii akamueleza ukweli kuwa alikuwa ananuka, anapaswa kwenda kusafisha mwili wake kwanza. Akili ya Juma ikaingiwa na mchecheto, akatembea kinyonge kabisa kuelekea chumbani. ___________________
NJE ya nyumba ya Juma wale waliokuwa wakimfungia tela walikuwa wamewasili tayari na waliegesha gari lao mbali na nyumba yake. Walikuwa watatu na walitembea kama wasiofahamiana katika suala hili. Kila mmoja alijiweka katika shughuli zake, ilimradi iwe ngumu kujulikana kuwa kuna jambo wanafuatilia. Umakini wa sasa ulikuwa umezidi wa awali ambapo walimchukulia Juma kirahisi sana. Sasa walikuwa makini kana kwamba wanapambana na adui mwenye hatari sana zaidi yao. Silaha zao ziliwekwa tayari tayari. Jicho moja pevu lilikuwa katika kona ngumu kufikika, lilikuwa limewapokea kuanzia walipowasili awali, wakamfungia tela Juma akiwashuhudia. Kisha akatengeneza vamizi la kumrejesha Juma nyumbani bila maafa yoyote, ili aendelee kuwasoma watu wanaomfuatilia Juma. Akaivamia nyumba na kutoa kitisho kikali. Zoezi likafanikiwa Juma amerejea na wao wamerejea. Ni akina nani hawa? na wanataka nini kwa Juma? haya yalikuwa maswali ambayo yalihitaji kupatiwa majibu upesi sana kabla naye hajajua ni kitu gani anaweza kufanya katika mchakato huu. Aliitoa taarifa hii ya mashaka yake juu ya watu anaowaona eneo hilo, taarifa ikapokelewa huku akisisitizwa kuwa makini zaidi. Masaa yalizidi kwenda bila kuona juhudi za watu wale kuingia ndani ya nyumba ya Juma, walibaki kurandaranda huku na kule bila kujua kuwa wanafuatiliwa. Kwa kuwatazama jinsi walivyokuwa wanatembea na kufanya mawasiliano alihisi yawezekana ni askari waliopo kazini, ama waliopoteza kazi zao, na kama si maaskari basi yawezekana waliwahi kupata mafunzo ya kijeshi kwa sababu maalumu. Akajinyoosha kidogo mwili wake na kujipima ikiwa anaweza kukabiliana na vijana wale. Wakati anajinyoosha akabaki kujicheka kuwa anauhangaisha mwili wake wa nini wakati ana kijana wake wa kazi ambaye kamwe hazeeki. bastola kiunoni! Majira ya saa tatu usiku akapiga hatua na kujichanganya barabarani, na hapohapo akageuka muigizaji, akazuga kuwa amelewa na anayumbayumba. Lengo lake likiwa kumfikia mmoja kati ya wale vijana. Akafanikiwa kupita jirani na kijana mmoja, akajikuta akicheka ndani ya moyo wake alipotambua kuwa hata kijana yule naye alikuwa katika fani ya maigizo na alikuwa yu katika kitengo cha kuigiza kuwa ni kijana anayetumia madawa ya kulevya na sasa ametulia tuli baada ya kujidunga. Safi! akajisemea kisha akamchokoza. Akamsema maneno yanayoudhi huku akiendelea kujiweka katika hali ileile ya ulevi. Yule bwana hakujibu kitu badala yake aliendelea kuwa mtulivu. Wakati wote huu alipokuwa anamfanyia bughudha katika sikio lake alikuwa na kifaa kidogo kilichokuwa kinatumika kwa ajiri ya mawasiliano. Yule bwana aliyekuwa amejiweka kama mtumiaji wa madawa ya kulevya hatimaye alinyanyua kichwa chake na kumtazama huyu mlevi kwa chati jinsi alivyokuwa anahangaika kumchokoza. “Naomba uondoke hapa.” alizungumza maneno machache kisha akainama. Mlevi akaanza kucheka huku akidiriki kumzongazonga yule bwana, alifanya vile kwa sababu alijiamini kuwa yule bwana hana ubavu walau wa kuingiza hata ngumi moja katika mwili wake iwapo watakusudia kutupiana makonde na hata akifanikiwa kutupa konde halitamletea athari. “Naomba uniache uondoke hapa wewe mlevi.” alisisitiza. Lakini yule mlevi bado aliendelea kuwa pale. Mara atukane hivi mara aimbe vile. Bwana aliyeketi akazidiwa na kero zile, akasimama wima na kumrushia ngumi kali yule mlevi, mlevi akaikwepa bila kujibu pigo. Kukwepwa kule kukamfanya awe makini zaidi na yule mlevi. Macho yakamkagua haraharaka huku wakitazamana kama majogoo. Akajaribu kurusha teke, mlevi akakwepa. Wakati yule mlevi anakwepa teke lile, yule bwana aliyekuwa akikabiliana naye akaona kitu kilichomtisha. Aliiona bastola. Na hapohapo akazungumza maneno yaliyomchanganya yule bwana mlevi wa kuigiza. “Angusha mbuyu kuna nyoka.” Maneno yale yakasafiri upesi katika akili ya yule mlevi wa kuigiza, akajaribu kuyafanyia kazi upesi lakini hakuweza kupata maamuzi sahihi. Jicho likamtazama mlevi yule kutokea mbali kabisa katika kifaa maalumu, mlango wa chuma ukafunguliwa kisha mwanga ukatoka bila mlio wowote, mwanga ukasafiri kwa kasi kubwa na kisha ukaweka makazi ya muda katika kifua cha yule mlevi wa kuigiza. Akatokwa na yowe kidogo kisha akaanza kujitupa huku na kule. Maneno aliyoongea hayakuwa nyoofu akaamua kunyamaza huku damu ikimtiririka. Yule bwana aliyekuwa ameweka kambi chini ya mti ule akampekua na kutoa bunduki katika kiuno chake. “Zahoro! huyu mjinga alikuwa na bunduki, huyu hakuwa mlevi aisee. Katumwa huyu hakutakiwa kuuwawa…… dah!” alizungumza kwa kutumia kifaa kilichokuwa sikioni. Maneno yale aliyozungumza yakapita moja kwa moja kwenda mahali ambapo hawakutaka yafike. Na hawakujua kama yanavuka mipaka hiyo. Yule bwana marehemu alikuwa akiwasiliana na mtu mwingine kabla hajauwawa. Hivyo alisikia yote hadi mwisho. ____ INSPEKTA KOBO akachanganyikiwa upya, hii ni baada ya kuyasikia maneno yaliyozungumzwa katika kifaa kilichokuwa sikioni mwa kijana wake aliyemtuma kufuatilia mienendo ya Juma Kihwele. Alisikia sauti yake wakati akitapatapa na mwisho akaisikia ile sauti ya mtu aliyekuwanaye. “Ni akina nani hawa?” alijiuliza huku aking’ata vidole vyake baada ya kukiri kuwa kuna watu hatari katika sakata hili ambalo kwa namna yoyote ile linaelekea kumwangukia na kumzika kabisa. Kijana wake alikuwa ameuwawa! “Angusha mbuyu kuna nyoka…” Hii sauti ikawa inajirudia katika kichwa chake. Ni kama aliwahi kusikia mahali… “Yeees!” akarusha ngumi hewani, alikuwa amekumbuka kuwa sauti ile aliisikia usiku ule alipokwenda kwa Nguzu kwa ajili ya kumsihi aachane na Zubeda wake na alipoondoka nyumba ile ikachomwa moto na kuaminika kuwa imeondoka na uhai wa Nguzu. “Huyu ni nani lakini? na kwanini wamchomee kijana wa watu ndani eeh!” akawaza na kuwazua kisha akaamua kutoka nje. Akaingia katika gari yake na kunyoosha moja kwa moja hadi hospitali aliyokuwa amelazwa Zubeda. Akaingia moja kwa moja katika kile chumba kile ambacho alikuwa amekiwekea walinzi wa siri hasahasa baada ya mkewe kuingia mle ndani na kumuhoji Zubeda mambo mazito. “Zubeda kila kitu kimeharibika na mambo yanazidi kuharibika, huu sio wakati wa kuzungumzia kilichotokea hapo katikati, huenda hicho kina unafuu. Naomba usikilize hii sauti kwa umakini na unieleze kama umewahi kuisikia… naomba usinifiche hata kama umeisikia katika mazingira ambayo haupendi mimi niyafahamu.” Akamwinamia na kumwekea kifaa sikioni kisha akakiwasha kile kifaa, Zubeda akaisikia sauti ya yule mwanaume ikizungumza yote iliyozungumza. Koplo Zubeda akatikisa kichwa kuwa hakuna anachokielewa. Inspekta Kobo akashusha pumzi zake kwa juhudi zote, mambo yalikuwa yanazidi kuwa magumu. “Vipi kuhusu Zahoro? unalifahamu hili jina?” “Nawafahamu Zahoro kadhaa, ila sina ukaribu nao.” “Kuna mjinga anaitwa Zahooro nahisi amemuua kijana wangu.” alizungumza kwa uchungu Inspekta huku akitazama juu. Na alipoushusha uso wake alizungumza na Zubeda. “Hautaendelea kulalia hiki kitanda, kuna watu wanaisaka roho yako wakati huu. Hakuna ninayemuamini kukulinda, nataka nikulinde mimi mwenyewe.” Inspekta akanong’ona kwa hisia kali huku akiwa anamtazama Zubeda moja kwa moja machoni. Kabla Zubeda hajasema lolote Inspekta akaendelea, “Mke wangu ana hasira sana najua, lakini si sababu ya mimi kukuacha wewe katika hali isiyokuwa salama. Yameniumiza mengi katika hii dunia ya mapambano, nitajitonesha upya nikishuhudia maiti yako” “Mlinde zaidi mkeo…” Zubeda akaingilia kati katika hilo. “Yupo katika ulinzi wa hali ya juu.” Alijibu Inspekta na hakutaka maongezi yaendelee, akatoweka kwa ajili ya kufanya hatua zote za kumwondoa Zubeda katika hospitali ile. Zoezi likafanikiwa. _________________
KUKUTWA ametupwa mtaroni? Tena akiwa hana jeraha bali alama moja tu katika shingo lake… Pigo la aina gani hii? Nani alitoa pigo hilo barabara! Haya yalikuwa maswali mfululizo yaliyopita katika kichwa cha kiongozi wa oparesheni isiyokuwa na jina rasmi. Hii ni baada ya kupokea taarifa kutoka jijini Mwanza kuwa kijana wake anayemuamini kupindukia alikuwa ameuwawa kwa kupigwa pigo moja kali kabisa shingoni. Tabasamu hafifu lilimdondoka wakati anajaribu kufikiria upya juu ya jambo hili. Akanyanyua mkonga wa simu yake, akataka kupiga mahali akaghairi na kubaki akielea katika mzani wa maamuzi. Akaushusha ule mkonga na kunyanyua simu yake ya mkononi. Akabofya nambari zilizokuwa zimetoka kumpatia taarifa kutoka jijini Mwanza. “Kwa hiyo umesema hakuna sehemu nyingine aliyojeruhiwa? Je ujumbe wowote kwa ajili yetu?” akatulia na kusikilizia upande wa pili ukijibu. Baada ya majibu akazungumza kwa ukali kidogo. “Ongea na Cheyo, aamrishe askari wake wazunguke kila kona hapo Shamaliwa wakamate vibaka wote wanaorandaranda kijinga jinga mitaani. Wawabane watasema kama waliona hilo tukio. Mwambie asiache mtu hata mmoja.” Waliendelea kuzungumza kwa sekunde kadhaa kisha simu ikakatwa. Jijini Mwanza baada ya masaa mawili eneo la Shamaliwa nje kidogo ya jiji hapakuwa mahali salama hata kidogo, ukizurura unakamatwa, ukikaa unakamatwa ukicheka unakamatwa ukilia unakamatwa. Hadi waliokutwa wanakata majani ya ng’ombe nao walikamatwa. Kamata kamata ile ikazua jambo juu ya jambo _______________
KONSTEBO MARTIN NGUZU alikuwa anajaribu kuutafuta usingizi katika kitanda ambacho kilitawaliwa na kunguni waliokuwa na maksudi mabaya, taa ikiwashwa wanatoweka na ikizimwa wanaingia uwanjani kuinyonya damu ya Nguzu. Mchezo huu wa kunguni wale ukawa kikwazo kikubwa kabisa kwake. Lakini hakuwa na yeyote wa kumlaumu kwa sababu alikusudia kujihifadhi katika nyumba ile ambayo lingetokea lolote lile angeweza kupiga ngumi moja pamoja na teke kisha dirisha likahama pahali pake na kuacha njia. Bughudha hii ikamnyanyua mpaka nje, akazurura huku na kule pasi na uelekeo maalumu. Katika kuzurura huku akaona haitakuwa jambo la heri kuzurura huku kichwa chake kingali wazi. Akafanya tathmini ya muda mfupi huku akijishangaa namna ambavyo yu hai, lakini zaidi zilikuwa ni hisia mpya zinazokisumbua kichwa chake. Majina mapya na mtazamo mpya katika fikra zake, jina Majenga lilikuwa la kwanza kabisa kujenga naye urafiki. Sanjari na jina hili kuna ndoto ambazo zimekuwa zikimfuata bila kukoma, mara amuote mama yake mzazi na alipoifuata ndoto ile na kurejea jijini Mwanza anamkuta mama yake akiwa mikononi mwa mtu mbaya. Anatokwa na pigo moja, pigo lililomwangusha yule bwana moja kwa moja. Kuhusu lile pigo akajiuliza upya, ni lini amekuwa na uwezo wa kuangusha mtu kwa ngumi moja pekee? Jibu lilikuwa rahisi sana kuwa hakuwahi kuwa na uwezo huo hapo kabla. Utata mwingine uliomsumbua ni kuhusu magazeti yaliyoandika kuhusu kifo chake. Kifo gani? Alijiuliza, lakini swali hili halikumshtua hata kidogo. Kufa si jambo dogo ujue? alijisemea huku akiendelea kuzurura. Hata tukio la kukuta pesa katika nguo aliyoianua katika kamba usiku ule baada ya kujinasua katika kifusi katika nyumba iliyokuwa imeanguka bado kilimtatanisha. “Nani wa kusahau pesa katika nguo ndani ya jiji la Dar es salaam!!” alijisemea na kujikuta akitokwa na tabasamu kubwa sana kulikumbuka jiji lile na vituko vyake. “Mzee Majenga kuna kitu anapaswa kunieleza, sidhani kama nipo kawaida.” aliweka hitimisho lile. Wakati anarejea katika chumba chake akaanza kumuwaza tena mama yake mzazi. Nini kinatokea? alijiuliza huku hofu ikianza kumwingia. Hakutaka kupuuzia hii hisia iliyomjia ghafla, akajiahidi kuwa siku inayofuata atalazimika kurejea jijini Mwanza. Akarejea katika kile chumba chenye kunguni wapenda sifa. Akajilaza na kusinzia. Alfajiri ilimkuta barabarani, akadandia gari na kurejea jijini Mwanza. Ilikuwa kama hisia zake zilivyomuelekeza, alipoingia jijini Mwanza hata kabla hajajikita katika upelelezi wa chinichini akatambua juu ya kamakakamata ya wakazi wa Shamaliwa nje kidogo ya jiji la Mwanza. Akajipeleka Shamaliwa kuhakikisha tu! Mama yake alikuwa mojawapo kati ya watu waliokuwa mikononi mwa polisi. Cheko la hasira likamponyoka, akatembea hadi katika kituo cha mabasi akajiweka katika basi ndogo iliyokuwa inafanya safari zake kuelekea Nyegezi. Akatulia katika nafasi iliyokuwa wazi. Mkononi akiwa na pesa kamili kwa malipo ya nauli ya kutoka Shamaliwa hadi Mabatini. Alishuka mbali kidogo na kutembea kwa miguu taratibu hadi zilizopokuwa nyumba za polisi. Nyumba zilezile alizoishi pale miaka kadhaa nyuma. Nyumba zile zikaikamata akili yake, akaukumbuka ule ugomvi kati ya Janeth ambaye baadaye alibadili jina na kuitwa Zubeda jinsi alivyokwidana na mke wa inspekta na mwisho kujikuta akitupwa rumande kwa siku kadhaa. Kumbukumbu zaidi za kumwandalia binti yule kifungua kinywa zikamfanya ayakumbuke mapenzi yao motomoto baada ya kukutana jijini Dar es salaam huku Zubeda akiwa ni Koplo na yeye akisalia katika nafasi yake ya ukonstebo. Tabasamu liliunda kibanda katika uso wa Martin, akatembea upesiupesi hadi katika nyumba mojawapo akaitazama kwa sekunde kadhaa, kisha akapita kwa kasi akaelekea nyumba nyingine, hii nayo akaitazama upesi upesi. Akafanya vivyo hivyo katika nyumba nane. Baada ya kuridhika kuwa alikuwa makini kabisa kwa kila hatua aliyopita katika makazi yale pasi na mtu kumshtukia akaamua kuzua balaa alilopanga kulizua. Lilikuwa balaa haswa! MARTIN Nguzu hakuwa mgeni eneo lile la kota za polisi Mabatini, hivyo hata sasa hakutembea eneo lile kama mgeni. Udhaifu wa ulinzi aliufahamu vyema na uwepo wa kiwanja cha mpira katika maeneo yale ya kota yalisababisha iwe ngumu sana kwa mtu kupatwa na hisia zozote za kutisha juu ya ugeni wa hapo kota. Nguzu alilifikia upesi eneo alilohitaji kufikia kisha akatazama kama kuna mabadiliko. Hapakuwa na mabadiliko ya aina yoyote ile, akatabasamu na kujiwekea alama za ushindi waziwazi. Majira ya usiku wa saa mbili akarejea eneo lile kwa ajili ya kutekeleza agano lake la kuhakikisha kuwa mama yake anakuwa huru kwa namna yoyote ile. Wakati huo alikuwa ameanza kupata majibu kuwa mtihani uliopo mbele yake haukuwa mdogo hata nukta. Mfumo wa umeme eneo la kota ya polisi Mabatini ulikuwa mbovu kupindukia, nyaya za umeme zilipita chini kwa chini katika namna iliyotia kero kutazama. Wazazi wenye watoto nd’o walijitahidi kupigia kelele hili suala lakini majibu yalikuwa yaleayale ya siku zote. “Kilio chenu kimesikilizwa!” Hiki kilio kikaenda miaka nenda rudi huku kikigeuka kuwa kichekesho na si kilio tena. Hakuna jema lililoboreshwa. Kama nyumba zenyewe zinatia kichefuchefu vipi kuhusu huo umeme?? Nguzu aliikuta hii hali katika safari yake ya kutoka kuzimu na kurejea tena duniani na sasa yupo katika ile ardhi aliyozaliwa miaka mingi iliyopita. Zile kota za polisi alizoziona angali akiwa anasoma, sasa hazitamaniki zinazidi kukera kuzitazama. Anarejea katika anga zile kwa sababu maalumu. Anatazama pande zote na kuzichimua kwa umakini zile waya. Akautazama uelekeo na kuchagua dakika ya kufanya balaa alilopanga kulifanya. Akazihesabu dakika akachuchumaa kisha akaziachanisha nyaya kadhaa. Giza likaingia katika eneo lile ghafla. Sauti za manung’uniko zikasikika huku na kule. Manung’uniko yale hayakudumu kabla Nguzu hajazua taharuki kubwa. Akazigusanisha zile waya na hapo mlipuko mkubwa ukasikika eneo la chooni. Akatimua mbio na kwenda upande mwingine na huko akagusanisha nyaya ukatokea mlipuko wa kushtukiza eneo ambalo zamani lilikuwa likitumika kama bwalo la chakula. Sasa hali ikawa mbaya, wapo waliotoka nusu uchi ndani ya nyumba zao, wengine wakabeba vigoda badala ya watoto. Hali ilikuwa tete! Nguzu naye akachanganyikana katika ile taharuki na kujifanyaamepotea njia, akaingia katika nyumba mojawapo ambayo watu walikuwa wametoka kwa hofu.Akaikwapua simu na kuondoka nayo, upesiupesi akaitumia simu ile ya upepo kutoa taarifa ya kutisha kwa maneno machache mno. “NINGEWEZA KULIPUA HIZI KOTA NA KUUA KILA KIUMBE HUMU NDANI. SIJASHINDWA ILA NI SALAMU TU. WAACHWE HURU WOTE WALIOKAMATWA BILA MAKOSA. OVA!” Hakujitambulisha jina akaiacha simu ile ikizungumza peke yake huku akiuliza yeye ni nani.
Kama salamu za kivita hii ilikuwa imetangazwa katika namna ya kutisha kutoka kwa adui.
Ule upande uliofanya ukatili huu wa kuwakamata watu wasiokuwa na hatia ukaanza kutetemeka huku kila mmoja akijutia maamuzi haya ya ajabu. Na hapo likaongezeka swali jipya juu ya adui mpya aliyejiamini kiasi kile cha kupitiliza akavamia kota za polisi na kuchafua hali ya hewa. Wakati wanaukosa usingizi, Martin Nguzu alikuwa amelala katika nyumba ya kulipia yenye hadhi ya kawaida. Uzuri wale ndugu zake wa Shinyanga hawakumtembelea usiku huu. Hapakuwa na Kunguni! ______
GARI iliingia kwa mwendo wa kawaida na kulikaribia geti la nyumba aliyokuwa akiishia Juma Kihwele. Namna gari ilivyoingia haikutisha hata kidogo, lakini namna alivyoshuka aliyekuwa ndani ya gari ndiyo iliyovuta umakini wa watu waliopendezwa na kujua yasiyowahusu. Ni wachache tu yaliwahusu. Alishuka mwanamama na kuubamiza mlango, kisha kwa mwendo wa harakaharaka alitembea kulielekea geti kuu la kuingilia ndani. Mlangoni akamkuta mlinzi, kwa mbali wakaonekana kuzozana. Mlinzi anamzuia asiingie naye analazimisha kuingia. Mlinzi akazidiwa nguvu, yule mama akaingia mbiombio ndani ya ile nyumba. Akaufikia mlango na hapo akakutana na mwenye nyumba. Ujio ule wa ghafla ukampagawisha Juma Kihwele. Lakini hakupata nafasi ya kujiandaa kabla yule mama hajamvamia na kumkwida shati lake. “Nipatie pesa zangu Kihwele, muda huu nazihitaji.” Alikoroma yule mama aliyekuwa na misuli imara. Juma Kihwele huku akitweta akajaribu kumtuliza yule mama, lakini ilikuwa kazi bure kabisa. Mama alizidi kufoka kwa sauti ya juu sana. Hatimaye mke wa Juma akatoka akiwa amembeba mtoto wake. Kulikuta sakata lile akamtua mtoto wake na kuingia katika tukio lile moja kwa moja. Wivu wa mapenzi! Hicho ndo cha kwanza kilichovamia kichwa cha mke wa Juma! Mke mwenza… Hili nalo likamvamia na kumsulubu, ni kitu ambacho hakutaka kitokee japokuwa dini ilikuwa inaruhusu kabisa. Lakini ingekuwa kwa amri yake angezuia hili jambo kwa mume wake pekee, kwa wengine angeliacha kama lilivyo. “Huyu ni nani Juma?” Aliuliza kwa shari kiasi. Juma akashindwa kujibu. “Wewe ni nani mama, na nini kinatokea hapa?” Akamgeukia yule mwanamke mpenda shari. “Naitwa Dokta Kobo, ninamdai mumeo. Naomba anipatie pesa zangu nijiondokee hapa.” Alijibu kwa kirefu. Juma Kihwele akafanya kosa kubwa kupinga kuwa hadaiwi kitu chochote na yule mwanamke. Dokta Kobo hasira zikamjaa, akamkwida vyema zaidi Juma. Na hapa sasa ukazuka ugomvi, mlinzi akasogea eneo la tukio kwa ajili ya kumsaidia bosi wake. Kuona kuwa wanaompinga wamekuwa wengi, Dokta Kobo akaingiza mkono katika pochi yake kubwa kiasi. Akarudi nyuma na hapo akatoa bunduki. Wacha wee! Wivu ukasahaulika, ubabe wa mlinzi nao ukaenda likizo huku rungu lake likimtoka mkononi, Juma akakaza mwendo wakamfuatia wenzake wakitimua mbio. Huyu akiita mama yule anaita Mungu wangu na mwingine haongei. Mbio! Dokta Kobo akamtazama vyema Juma Kimbelembele anavyokimbia kwa uoga huku akipiga mayowe, ndani ya sekunde chache akayahesabu maovu yote kutoka kwa bwana huyu na hapo akaufikia uamuzi wa kumuhukumu. Akaielekeza silaha yake kule alipokuwa Juma Kimbelembele, kisha akaanguka chini na kutua kwa kutumia goti moja, akamweka Juma katika shabaha. Vilevile kama alivyowahi kufundishwa na mume wake ambaye ni ana cheo cha inspekta katika jeshi la polisi. “Kafie mbele mwanaharamu mkubwa wewe…” Likamtoka neno lile na kisha akakifikia kitufe cha kufyatulia. Mlio mkubwa ukasikika!
_______
GIZA lilikuwa limetanda wakati fahamu zikirejea kinyonge katika mwili wa dokta Kobo. Alijihisi maumivu kwa mbali lakini alipojipapasa hakuwa na jeraha. Akatulia kwa muda kisha akakumbuka kwa juhudi zote ni wapi alitoka hadi kulifikia giza lile. Kama kawaida yake hakuwa mwenye papara, hili ni moja kati ya jambo lililopelekea inspekta Kobo kumtolea mahari upesi na kumuoa moja kwa moja. Akazikusanya fikra zote na tabasamu hafifu likamtoka. “Nimetekwa!” alijisemea huku akijiandaa kukabiliana na huo ukweli. Akaukumbuka mlio mkali wa risasi uliopelekea ashindwe kukivuta kitufe cha kufyatulia na kumwondoa duniani Juma Kihwele. Kwa maksudi akaanza kukohoa ili wenyeji wake waweze kujisogeza karibu yake. Kimya! akabaki kuusikia mwangwi wa kikohozi chake mwenyewe. Akakohoa tena, bado hali ilikuwa ileile. Akasitisha zoezi lile akasimama na kuanza kupapasa gizani akijaribu kutafuta mwanga wa kutoka katika eneo lile ikiwa ni kweli hajatekwa. Aliendelea kupapasa bila kukutana na kitu chochote kile. Akajipapasa na kukuta amepungukiwa bunduki pamoja na mkoba wake. Akatambua wazi kuwa alikuwa amepekuliwa. Hakuwa na hofu kubwa. Hiyo ilikuwa ni asili yake. Katika kazi yake ya udaktari alishuhudia wagonjwa wengi wakipoteza maisha, wengine mikononi mwake wengine katika mikono ya madaktari wengine. Hivyo hakuwa akikihofia sana kifo. Alijua ipo siku atakufa… Na sasa alijiona katika mdomo wa kifo. Aliendelea kutembea zaidi akipapasa huku na kule. “Ni akina nani hawa? na wanataka nini?” Alijiuliza huku akiendeleza bidii katika kupapasa. “Mamaaaaaa!” kelele kubwa zilisikika ghafla mbele yake na hapo akasikia vishindo vikiambaa kwa kasi. Mungu wee! nini hiki? alijiuliza huku kwa mara ya kwanza akianza kupatwa na wasiwasi moyoni. Akatulia tuli katika giza lile akisubiri kitakachojiri. Hakuna aliyesogea, akasikia gari likiwashwa na kisha akauona mwanga kwa mara ya kwanza. Mwanga ulipenya katika mboni ya macho yake katika namna ya kumsumbua. “Tulia hapohapo mwanga mkubwa wewe!” sauti ikamuamrisha. Akatulia tuli huku akikumbuka nidhamu ya kunyoosha mikono yake juu. Hatua zilizizidi kusogea hadi alipokuwa. “Toa hicho kitambaa” Akaamrishwa. Akaanza kujitazama. “Toa kitambaa usoni!!” sauti ikaamrisha tena. Ni hapa ambapo akili ya daktari Kobo ilifanya kazi. Wakati wote aliokuwa akipapasa katika kiza kinene alikuwa na kitambaa usoni. Ajabu!
Akajipapasa na kukifungua kile kitambaa. Ndio palikuwa na giza lakini sio kiza totoro kama alichokuwa akitembea kwa kupapasa. Taa za gari zilikuwa zinammulika, akaendelea kunyanyua mikono yake juu hadi alipofika mwanaume mmoja akiwa na mkuki na rungu. “Wewe ni nani usiku huu hapa na umefika vipi hapa. Tiketi yako ipo wapi? na kwanini haujatoka ndani hadi wakati huu…” Maswali debe yalitiririka. “Sijui kitu chochote jamani.” alijibu kwa shida, koo lake lilikuwa limekauka. “Unajua hapa ni wapi?” “Sijui lolote, sijui hata nilipotoka mpaka kufika hapa.” aliendelea kusisitiza. Taa zikazimwa! sasa aliweza kuwaona watu wawili zaidi, wote wanawake na kwa mbali akauona ufukwe. Alikuwa jirani kabisa na bahari. Kuhusu ni kitu gani kimetokea hakujua pa kuanzia lakini bado alihisi kuwa hajapaa hadi kufika katika ufukwe ule asioufahamu. “Nipo wapi hapa jamani?” aliuliza ili apate mwanga. Kabla jibu halijatoka, vikasikika vishindo na miale ikaanza kuonekana kuanzia mbali. Wote wakageuka nyuma kutazama kinachojiri. “Kuna hatari hapa ndugu zangu. Ikiwa vyema tuondoke hapa” Yule bwana aliyefanania na mlinzi alitoa shauri. Na hapo wale wanawake wawili wakaingia garini, kisha akafuata mlinzi na katukatu wakagoma kumbeba Dokta Kobo hata alipowasihi zaidi kuwa huenda alikuwa ametekwa. Gari ikaanza kuondoka taratibu ikipambana na ule mchanga mwingi wa ufukoni mwa bahari. Tulivu haikudumu, risasi zikaanza kufyatuliwa kuelekea lilipokuwa gari. Dokta Kobo, akakimbia kwa kasi sana kuelkea yalipokuwa maji. Shukrani za dhati zilikuwa kwa tabia yake ya kupenda kufanya mazoezi ya viungo kila siku. Aliyafikia maji na kujirusha upesi ndani yake. Risasi ziliendelea kurindima huku gari lile ambalo sasa tairi moja lilikuwa limepasuliwa tayari likipambana kujinasua kutoka katika eneo lile. Akiwa ndani ya maji dokta Kobo aliliona balaa jingine likimnyemelea, aliiona mbwa yenye afya ikijongea kule alipokuwa yeye huku ikibweka sana. Mbwa ilizama majini, sasa haikuwa ikibwrka tena lakini ilikuwa na usongo wa hali ya juu. “Come on lazy dog!!” alijisemea huku akijaribu kufanya hichoalichopanga kufanya. Akaendelea kuyakata maji huku kila mara akikumbuka kuiita ile mbwa. Alijua hawezi kuendelea kuogelea tu bila kupambana. Na alichokipanga wakati wake ukafika. Mbwa ikamrukia na kumrarua na makucha yake. Dokta Kobo akaukumbuka utoto wake akaujumlisha na ujana wake jinsi alivyokuwa fundi katika kukata maji. Wakati akiwa mwanafunzi wa shule ya msingi alikuwa akiwazidi hadi wanafunzi wa kiume katika kukata maji. Sasa yu katika maji kwa sababu maalumu sio mashindano ya kawaida ya mshindi kutunukiwa cheti, katika hili mshindi angetunukiwa uhai. Dokta Kobo anayeyajua maji akavuta pumzi na kutoa nje mara kadhaa kisha akajigeuza na kumweka mbwa chini yake kisha wote wakazama. Kilichofuata yalikuwa mashindano ya nani awezaye kuzitunza pumzi zake kwa muda mrefu awapo ndani ya maji. Ni mbwa ama ni dokta Kobo. Mbwa alisahau kuwa alikuja pale kwa lengo la kushambulia, sasa alikuwa anahaha huku akinywa maji mfululizo bila mpangilio. Dokta Kobo alikuwa makini katika kuzitunza pumzi zake na wakati huo alimdhibiti yule mbwa asiweze kupanda juu kuvuta hewa. Sekunde zake za uvumilivu zilipofikia ukomo. Akaiunganisha mikono yake miwili katika shingo ya yule mbwa kisha akairuhusu ile mbwa ifurukute. Ikafurukuta na kumleta juu, akavuta pumzi za kutosha. Mbwa asiye na akili kama za Dokta Kobo akabaki kuhema hovyo. Dokta Kobo akazama tena ndani ya maji, na hii ikawa safari ya mwisho. Alipoibuka alikuwa hai peke yake, mbwa iligeuka mzoga wa ajabu unaoelea ndani ya maji kwa mara ya mwisho. Dokta Kobo katika kichwa chake mpambano wa uhai ulikuwa haujamalizika nd’o kwanza ulikuwa unaanza. Aliwaza na kuwazua akaukumbuka ule usemi wa wanamtaa usemao mume/mke si ndugu yako. Akajaribu kuuhalalisha usemi ule katika hili linaloendelea. “Ina maana Kobo mume wangu amemuua Nguzu na sasa anataka kuniua mimi kwa sababu nimejua ama?” alijiuliza huku akiendelea kuyakata maji kwa makini kabisa kujiweka mbali na hatari. Akayakumbuka mema yote waliyoyapitia katika ujana wao, na sasa katika utu uzima huu yasahaulike?? Alijiuliza na kuingiwa na ukakasi mkubwa sana katika kuupata usahihi. Zubeda! Jina hili likamshambulia ghafla, akahisi wawili hawa lao ni moja. Wamekolezana kimahaba wamemuua Nguzu na sasa hawataki usumbufu wowote ule wanataka uhuru wameamua kumtokomeza. “Koboko mume wangu? Hapana…. hawezi kunifanyia hivi mimi.” Alijiuliza na kujipatia jibu japokuwa hakutaka jibu lile limuathiri na kuwa jibu la uhakika. Baada ya kukatab maji kwa juhudi zote na kuamini kuwa yu mbali na ile shari. Alienda hadi ufukweni akajinyoosha na kuvuta pumzi za kutosha. Hakujua ilikuwa ni saa ngapi na mbaya zaidi hakujua maadui wake walikuwa upande gani kwa wakati ule. Subira! ndo kitu pekee kilichohitajika kwa wakati ule pale alipokuwa. Akaendelea kutulia mtaalamu yule wa magonjwa ya moyo. Dakika takribani arobaini zilitimu bila purukushani yoyote, lakini hapakuwa tulivu zaidi. Miale ikaanza kuonekana, akiwa ametuliapalepale akajigeuza upande wake wa kushoto na kuona kundi la watu wakirandaranda huku wakimulika maeneo mbalimbali. Daktari Kobo akajipima nguvu katika mwili wake, asingeweza kukimbia walau mita mia mbili bila kuanguka. Maji yalikuwa yamemdhaifisha sana. Mapigo yake ya moyo yakaongeza kasi na kujiona kuwa ule ulikuwa mwisho wa ujanja wake katika hili tukio. Akayafumba macho yake na kutazama angani. Akajilazimisha kutabasamu lakini haikuwezekana. Hofu ya kifo ilikuwa jirani yake.
Simulizi : Konstebo Nguzu Sehemu Ya Tatu (3) Miale ikaanza kuonekana, akiwa ametuliapalepale akajigeuza upande wake wa kushoto na kuona kundi la watu wakirandaranda huku wakimulika maeneo mbalimbali. Daktari Kobo akajipima nguvu katika mwili wake, asingeweza kukimbia walau mita mia mbili bila kuanguka. Maji yalikuwa yamemdhaifisha sana. Mapigo yake ya moyo yakaongeza kasi na kujiona kuwa ule ulikuwa mwisho wa ujanja wake katika hili tukio. Akayafumba macho yake na kutazama angani. Akajilazimisha kutabasamu lakini haikuwezekana. Hofu ya kifo ilikuwa jirani yake. _______
UMATI mkubwa wa watu ulikuwa unasukumana kutazama tukio lile la kustaajabisha. Huyu alisema hivi yule naye akapinga na kusema vile. Baadaye majira ya saa nne asubuhi umati ulitawanyishwa baada ya askari kufika eneo lile na kuwasihi wasogee mbali. Wakiwa wametangulizana na wataalamu wa afya, polisi waliwaacha wataalamu wale wawapatie majibu ikiwa mwili uliolala pale chini ulikuwa hai ama tayari kwa kuzikwa. Ule ubishani uliokuwa kwa raia juu ya mwili ule ukahamia kwa maaskari watatu, na wao wakaanza kubishana chini chini juu ya mwili ule. Askari mmoja alisimamia upande mmoja na wawili wakiunganisha nguvu kutetea hoja yao. “Yupo hai lakini moyo wake unapiga kwa tabu sana.” Mtaalamu wa afya alitoa majibu, askari wakafuata taratibu zote na kuuingiza mwili katika gari ya wagonjwa huku wakikumbuka kupiga picha eneo lote ambalo waliukuta mwili ule. Waliondoka pale na kuucha ubishani ukiendelea, na wale askari nao waliendelea kubishana lakini hii ya sasa ilikuwa katika namna ya utani tu. Gari likaingia barabarani huku likipiga ving’ora. Kutoka Kariakoo sokoni hadi Muhimbili sio kitambo kirefu sana hasahasa kwa gari hili ambalo linapishwa njia na magari mengine. Hivyo hata msafara huu haukuchukua kitambo kirefu kuifikia hospitali. Mwili ukashushwa huku ukipokelewa na wauguzi. Askari wakiwa bado na wawakilishi wao katika hili. Hapa sasa hapakuwa na kufananisha tena, ulikuwa ni mwili ulioibeba sura iliyokuwa ikifahamika vyema katika hospitali ile ya taifa. Sura ya dokta Kobo! Jina ambalo umaarufu wake sasa ulikuwa umezidi tangu apotee kazini pasi na taarifa yoyote ile, kupotea huku kukakifanya kitengo kinachohusika na masuala ya moyo kupwaya sana. Dokta Kobo alikuwa mtaalamu sana, lakini ucheshi wake na moyo wa upendo vilimfanya kuacha pengo alipokosekana. Sasa anarejea akiwa katika machela, hana fahamu na hajulikani kama atapona. Wauguzi na madaktari walilia huku wakimwombea dua aweze kupona.
Kutokea hospitali ya Muhimbili, simu ikapigwa kwa mume wa dokta Kobo yaani Inspekta Kobo.
SIMU hii ilifika katika wakati mbaya sana. Inspekta Kobo alikuwa amechanganyikiwa mno. Walinzi wa siri aliowaweka kumwangalia mkewe na nyendo zake walikuwa wamemueleza kuwa dokta alikuwa ameshindia siku nzima ndani ya chumba cha hoteli aliyofikia, walipojaribu kupeleleza chumba kile wanatanabai kuwa dokta Kobo alipitia mlango wa dharula kutoweka ndani ya chumba kile hivyo hawakujua ni wapi ameelekea. Jitihada za kumsaka zikagonga mwamba. Asubuhi akiwa bado hajajua nini hatma ya mke wake kipenzi anapokea ujumbe wa kitisho. “MKEO AMETAPIKA KILA KITU.” Ujumbe huu ulimaanisha kuwa mkewe amesema kila kitu. Kuhusu hili hakushtuka sana kwa sababu alikuwa akimuamini sana mkewe jinsi alivyokuwa jasiri pengine kuwazidi wanaume wengi tu. Hofu yake ilikuwa usalama wa mkewe ambaye kufikia hapo alijua kuwa alikuwa ametekwa tayari. Mawazo yake yalizunguka huku na kule na kumlazimisha kuwa watu hao wamemuua mke wake. “Kama mmemuua mke wangu, mtaijua gharama halisi ya mguu wangu uliopotea kwa sababu ya kupambana…” Akamalizia na tusi lake la kiitaliano. Lakini kwa mara ya kwanza akajikuta akilitoa tusi hilo kinyonge sana. Inspekta Kobo akagundua kuwa alikuwa yu na uoga wa ajabu mno, uoga ambao hajawahi kuwa nao hapo kabla. Ni hapa alipokiri kuwa yumkini damu nzito kuliko maji lakini penzi ni zito kuliko vyote, maji na damu ukivichanganya pamoja. Inspekta akakiri kuwa katika mapambano ya zamani hakuwa muoga kwa sababu aliingia katika mapigano huku katikati ya uwanja wa mapambano pakiwa hakuna ndugu yake wala mtu anayempenda, hivyo hata akifa mtu kwake haikuwa tatizo. Sasa anawatukana watu walioshika hatamu ya maisha ya mkewe kipenzi. Inspekta akatubu kimyakimya. Wakati anakiri kuwa anawaogopa watekaji, simu yake ikaita. Nambari ilikuwa ngeni, akajua wazi kuwa huyo atakuwa ni mtekaji na sasa anataka kutoa masharti ili mkewe apatikane huku akiwa hai ama akaidi na kupokea kichwa cha mkewe kikiwa kimelowa damu mbichi na ujumbe wa kukera ‘tengeneza supu unywe kama kweli ulikuwa unampenda’ Inspekta akaipokea simu ile kwa upole kabisa. “Inspekta Kobo!” sauti kutoka upande wa pili ikamuita. Akaitikia ‘rabeka’ “Samahani kwa usumbufu mkuu, lakini mimi ni daktari hapa Muhimbili. Sijui kama una taarifa zozote kuhusu mke wako. Daktari Anna Kobo.” Sijakuelewa taarifa kuhusu nini?” aliuliza kwa upole vilevile huku akiketi chini. “Yupo hospitali hapa, naona amepatwa na hitilafu kidogo ila kila kitu kipo sawa. Itafaa ukifika huku.” Taarifa iliishia pale. Inspekta alitamani kuuliza maswali mengi lakini hakuna hata moja lililotoka hadi simu inakatika. Jasho lilikuwa limeulowanisha mgongo, uso, kwapa na kifua. Inspekta alikuwa ameoga jasho huku amekaa tu bila kukimbia. Jasho lile likamfadhaisha mno, aakaanza kujipepea na gazeti lililokuwa mbele yake. Bado halin hii ilimbughudhi, akajikaza kikakamavu na kusimama akaukaza mwili wake kisha akajikumbusha kanuni za kijasiri za jeshini. Alipomaliza akabiga saluti, kisha akajiwekea kiapo kuwa hatatumia tena muda mwingi kutetemeka, kutokwa jasho na kunung’unika badala yake atautumia muda mwingi kutafuta majibu ya maswali yanayokielemea kichwa chake. Akaipapasa bastola yake na kisha akasemanayo. Kana kwamba inamsikia. “Unaonaje kama nikizitoa hizi risasi kwenye chemba kisha ziwe eneo husika tayari tayari kwa kupasua kichwa cha mtu atakayethubutu kunishambulia. Maana si unajua hawa wapinzani wangu wananijua nami siwajui….. sema nawe unazingua ungekuwa na macho tungesaidiana. MI naangalia kulia we kushoto….” Alizungumza huku akiziweka risasi katika njia yake. Watoto waliozoea kutazama picha za mapigano wanasema ‘akaukoji mjegeja wake’. Safari ya kuelekea hospitali kupokea taarifa mbaya kabisa kuwa mkewe alikuwa hai lakini alikuwa amezikosa fahamu zake. Kwa lugha ya kigeni ‘alikuwa katika coma’. Ni heri angekuwa amepoteza fahamu, dokta Kobo hakuwa kabisa na fahamu zake. Na haikujulikana zitarejea lini. Inspekta alichoka! Alijikaza chozi lisimtoke, hakuweza. Yalibubujika kama mtoto mdogo. Akatoweka hospitali na kwenda kumalizia kilio chake katika kitanda alicholala Zubeda kule kwenye eneo la siri aliloamua kumuhifadhi. Kwa wakati huo hakujali jambo jingine zaidi ya watu wake wa karibu wanaoingia matatani kwa sababu yake. Hasira zake akazihamishia kwa Juma Kihwele.
Kumbukumbu za jina lile zikasababisha sharubu zake kusisimka. Akaendelea kuhisi kuwa huyu bwana ndiye aliyeandika zile habari, na kama aliziandika basi kuna mawili. Anasakwa na waliompa tenda hiyo chafu ili wammalize asije kutoa siri, ama la yupo mikononi mwa watu wabaya tayari kwa kuuwawa.
“Zuu, hivi bi mkubwa hakukueleza ni nani aliyempa maneno yale mazito?” Inspekta alimuuliza koplo Zubeda kwa upole kabisa. “Hapana hakutaja jina lolote wala hakuelekea kufanya hivyo. Alikuwa anajua anachokifanya wakati anazungumza na mimi.” Alijibu kwa kirefu huku akiwa ameketi. Hali yake kiafya ilikuwa inaridhisha. “Vipi kuna kitu kipya unahisi?” Zubeda akajazia swali. Kimya kikatanda kabla inspekta hajaelezea hisia zake juu ya mwandishi wa habari aitwaye Juma Kihwele. Ili kuusadikisha ukweli akazimwaga hadharani sifa za kimbelembele alizonazo muhariri huyo. Sifa zile zikamfanya Zubeda amuunge mkono inspekta katika hisia zake zile. “Nilimsikia daktari akizungumzia juu ya risasi kushambulia nyumba ya Kihwele, usiku uliopita nadhani.” “Risasi? nani na nani walikuwa wanarusha?” Swali la kipuuzi likamponyoka. Akawa mnyonge alipogundua kuwa ameuliza kipuuzi. Hakurekebisha! Akatwaa simu yake na kupiga kwa rafiki yake wa kitengo cha mawasiliano. Akamuuliza nini kimejiri. Taarifa zikatoka kuwa inasadikika kuwa familia ya Juma Kihwele yaani mke na mtoto pamoja na ndugu mmoja ilikuwa imepotea. Nguo zilizotapakaa damu zimeonekana na hazijulikani kama ni majeraha ama zinamaanisha vibaya kwa wahanga. Hadi wakati huo hakuna anayehusishwa na tukio hilo moja kwa moja.
Taarifa ile iliyakaanga maini ya inspekta Kobo, uzuri sauti ilikuwa yasikika vyema hivyo hata Zubeda alisikia kila kitu. “Zuu mpenzi wangu, huu mkasa utanizeesha upya. Nilijidanganya mkasa huu utanichangamsha na kuwa kijana….. ajabu nazeeka tena kwa kasi mno. Sijui kuwaza vizuri, sijui kujikaza, yaani nimekuwa kama fala hivi aliyevuta sigara bwege halafu hana uhakika wa chakula cha mchana wala usiku. Badala ya kulia kiume nalia kama mwanamke. Looh! mkasa huu unanibadili hadi jinsia mimi inspekta Kobo.” Alilalama kwa uchungu mno huku akijitahidi chozi lisimdondoke. Zubeda akafanya kosa kumbembeleza, Inspekta akaanza kulia kama mtoto. “Wameanza na wewe wamekusababishia ajali, wamemzimisha mke wangu huko, na bado wanaendelea kuniumiza kichwa…..aah! Si wanikamate na waseme nini wanataka eeh! Kwani mimi ni mwanadamu wa kwanza kumsaliti mke wangu eeh! Mimi ni wa kwanza nauliza, mbona wameniandama hivi mimi lakini.” Kwa kilio hiki Zubeda alikiri kuwa inspekta alikuwa amekamatwa pabaya.
Wakati kilio hiki kikiendelea simu yake ya mkononi ikatoa mwanga. “Angalia ni nani anapiga, kama ni namba mpya naomba usipokee. Sitaki kufia humu ndani, waniache nikafie ndani ya nyumba yangu.” Alizungumza kwa hisia za malalamiko. “Anapiga Komredi Kitengo.” Zubeda akamtajia jina linaloonekana pale. Inspekta akaipokea simu huku akiilazimisha sauti yake iwe ya kawaida tena. “Halafu komredi, si uliniambia kuwa unapenda sana samaki aina ya Sato na Sangara wa Mwanza?” Mpigaji aliuliza lile swali. Inspekta mdomo ukamfunguka asiamini aliyepiga simu ile alikusudia kumsumbua kwa swali la kizembe namna ile. Zubeda yeye alijikuta anatabasamu. “Mbona kimya komredi ama pweza wa jiji washakuvuruga hutaki tena sato.” aliendelea. “Komredi… najisikia usingizi mkuu. Niache nilale…” alijitahidi sana kulinda heshima iliyopo kati yao. “Hivi Sato hata Shinyanga wapo au ni Mwanza tu?” Mpiga simu hakujali zile busara. Inspekta akatamani kulitoa lile tusi lake la akiba lililo katika lugha ya kiitaliano lakini huyu mpiga simu licha ya kuwa na utani waliheshimiana sana. Akabaki kujichekesha tu.. “Haya jiandae kwenda kula sato, hakikisha unaniletea walau mapande matatu yaliyokaushwa na mimi nijue utamu wa sato wa Mwanza.” “Una maana gani komredi?” Akauliza inspekta. “Ndani ya siku mbili hadi tatu mtapelekwa Shinyanga nyie mnaojifanya mnajua sana kutumia bunduki na kulenga shabaha. Kuna kazi inawaita huko, nimekuibia siri tu ili usije ukasema sikukuagiza mapema sato.” Alizungumza kwa utulivu kwa kuamini taarifa ile itakuwa njema kwa inspekta Kobo ambaye alikuwa mpenzi wa mapambano enzi zake. “Komredi lakini mimi nimezeeka tayari na nimevunjika mguu mnajua… mbona..” Akataka kuendelea kulaumu akasita kwa kugundua kuwa analalamika sehemu isiyokuwa sahihi hata chembe. “Sio wewe pekee kuna wenzako pia wamestaafu lakini umaridadi wao katika mapambano unawarudisha kazini.” Mazungumzo yalimalizika na kumwacha inspekta akiwa katika mtihani mwingine mzito. Mkewe yu katika ‘coma’ hawara yake anajiuguza bado na sasa anatakiwa kwenda Shinyanga kwa oparesheni maalumu. Oparesheni asiyoijua. Na alimtambua vyema mkuu wake akisema amesema. Ukimjibu kuwa una mgonjwa anakuomba vyeti vyako ulivyofuzu mafunzo ya udaktari hadi ubaki kumtibu mgonjwa, ukisema unaumwa anakuambatanishia daktari katika msafara wa kwenda katika tukio. Kwa kifupi hapakuwa na sababu ya kukwepa majukumu akiyatoa. Na kingine kibaya ni uhasama uliokuwepo baina yake na kiongozi wake wa juu. IGP! Uhasama usiokuwa na historia maalumu. Ila uliendelea kuwepo. Njia pekee ya kukwepa majukumu kiutoka kwa IGP ilikuwa ni kujiua. Alikuwa hakwepeki! Inspekta Kobo alichoka sana. Ndani ya masaa machache akausikia waziwazi udhaifu uliouchota mwili wake. Alipoupeleka mguu wake ofisini akakumbana na barua aliyoitarajia. Wito!
GIZA lilikuwa ndani ya giza kwa mara nyingine, Konstebo Martin Nguzu alikuwa amempokea mama yake ambaye alikuwa mmoja kati ya wahanga wa ile kamatakamata iliyofanywa kwa masilahi ya watu wachache waliokuwa wamekerwa baada ya mwenzao mmoja kuuwawa kifedhuli. Ghafla bin vuu mambo yakabadilika, kota zikatishiwa kuchomwa. Wakagwaya na kuwaachia huru wale waliokuwa wamekamatwa katika namna ya uonevu. Ni giza hilihili sasa lipo ndani ya giza tena, ana kwa ana na mama yake mzazi. Martin Nguzu alimpa pole mama yake huku akiwa na haraka sana ya kujua ni wapi hasa anapoweza kumpata Majenga waweze kuzungumza na kutambua ama kujitambua upya yeye ni nani na kwa nini haya yote yanatokea. Hasira zake bado zilikuwa dhidi ya inspekta Kobo aliyeamini kuwa alimchomea ndani ya nyumba kisa mapenzi. Alipona vipi na nini kinaendelea katika maisha yake haya nd’o makuu aliyojiuliza. Kuhusu kutafutwa kwa Majenga na watu asiowajua kukapunguza ile hisi yake kuwa chanzo cha kiila kitu ni mapenzi. Akabaini kuwa lipo la nyongeza. Mama Martin ambaye hakuwa ameimarika sana kiafya safari hii alionyesha ushirikiano wa hali ya juu, usiku uleule alimpeleka Martin hadi nyumba aliyowahi kuishi mzee Majenga ambapo baadaye alipangisha na kuondoka zake kuelekea Shinyanga. “Ila Shinyanga sijamuona kabisa…” Nguzu alizungumza wakati wanaelekea katika nyumba ile. “Bado haujabadilika mwanangu, yaani Shinyanga kubwa vile wewe umtafute mtu usiyemjua na ukampata kabisa. Labda muujiza ama maigizo.” Mama alimkata juu kwa juu Nguzu, haikuwa mara ya kwanza hali ile. Tangu utoto wake. Mtoto hakui kwa mama! Walipewa ushirikiano mkubwa sana walipowasili eneo lile, uzuri mtoto wa mzee Majenga alikuwa anaishi katika chumba kimojawapo, na alikuwa pale kama msimamizi wa nyumba ile. “Kumpata kwa leo itakuwa ngumu sana, maana leo watu wametoa kodi. Na yule akipata kodi anamalizia katika ulevi wake.” Mtu aliyekuwa anawapa maelekezo alisema kwa masikitiko. “Unaweza kujua baa ambazo hupenda kuzitembelea?” Nguzu aliuliza kwa udadisi. “Bora angekuwa anaenda baa, huyu anaingia vilabuni, ana usemi wake unaosema kwamba mia mbili ya baa ni elfu kumi ya kilabuni” Martin akajikuta anatokwa na tabasamu hafifu kwa kusikia haya. Ghafla wakamwona yule mwenyeji akiwafanyia ishara ya kusikiliza kwa makini zaidi, wakasikia sauti ya mtu akiimba. “Ni yeye… looh! leo amewahi kurudi hivi?” alishangaa na kuwashawishi Nguzu na mama yake washangae pia. “Halafu….. halafu….. mama huyu kamfanana…. aahm! eeeh!” akaanza kujiuma uma. Alikuwa amemtazama Nguzu vizuri. “Ninafanana naye sana alikuwa binamu yangu….” Nguzu akaiwahi hii kesi na kuisawazisha. Mtarajiwa akawasili akiwa anaendelea kuimba nyimbo zake, nyimbo zilizomburudisha yeye pekee. Hakuwa peke yake….. Alikuwa na chupa kadhaa za pombe. “Mnataka kuhama…. mnahama hama na hamjalipa kodi yangu.” Alizungumza huku akiwa hana hata uwezo wa kuona mbele vizuri, sembuse kung’amua kuwa kuna mtu anataka kuhama. Akasogea kwa kunesanesa bila kuvunja chupa hata moja akawafikia. “Shkamoo mama….. eeeh! mama nawe umehadimika kweli.” Alisalimia baada ya kumtambua mama Martin. Salamu ilijibiwa, yule mwenyeji akajitoa katika mkutano huu akawaacha watatu hawa wakizungumza. Walijitahidi hivyohivyo kuelewana japokuwa ilikuwa ngumu kwani yule mlevi kila mara alikuwa anasahau alichozungumza dakika kumi nyuma. Mlevi huyu hakujua ni kiasi gani alikuwa faida kwa Martin Nguzu
ASKARI aliyetegemewa na kuaminiwa zaidi alikuwa makini na silaha yake, alikuwa amejinyoosha chini na kunyanyuka kidogo sana usawa wa kifua na kuendelea. Bunduki yake kubwa ilikuwa imelazwa vyema katika muinuko huku akiona kila kitu kilichokuwa kikikatiza mbele yake. Alitulia katika lindo lile kwa dakika nyingi akingoja walilotarajia litokee waimalize vyema siku yao. Kilikuwa ni kikosi cha watu saba tu cha siri kilichokuwa kikitambua nini kinaendelea katika giza hili. Majira ya saa nane usiku mchakacho ulisikika kutoka katika kichaka kimojawapo, mlengaji akatulia tuli bila kufanya shambulizi. Alihitaji kupata uhakika wa kile alichokuwa anakwenda kukishambulia. Barua kutoka kwa IGP ilielezea kuwa jambazi aliyekuwa anasakwa miaka mingi alikuwa mjini Shinyanga na huko alitarajia kuanzisha kampeni ya kuvamia na kuiba katika taasisi mbalimbali za kifedha. Huu ukawa wakati wa askari kujitafutia nyongeza ya nyota kwa kumtia mikononi jangili huyo aliyekuwa anasifika kwa hatari yake na roho mbaya. Simu ya upepo ilikuwa imeshikiliwa na askari mwingine, kazi yake ilikuwa moja tu kumweleza mlengaji nini cha kufanya ikiwa patakuwa na mabadiliko. Mlengaji hakupaswa kutikisika ama kujihusisha na mawasiliano mengine kwa sababu angeweza kuipoteza shabaha yake. Mchakacho ule ukaongezeka tena, mlengaji akaendelea kutulia. Na hapo redio ya upepo ikakoroma ikitoa taarifa kutoka upande wa pili. “ANGUSHA MBUYU KUNA NYOKA! ANGUSHA HUO MBUYU…” Sauti ile ikamfikia mlengaji, akaanza kutetemeka mikono nyake. Ile sauti haikuwa ngeni na lile neno hakuwa akilisikia kwa mara ya kwanza. Ni siku kadhaa nyuma alilisikia katika simu ya upepo kutoka kwa kijana wake wa kazi aliyeuwawa kwa kupigwa risasi. Mikono ikazidi kutetemeka, sauti ile nayo ikazidi kusisitiza neno lilelile. ‘angusha mbuyu’ Mapigo ya moyo yakaongezeka kasi yake. Adui akajitokeza kutoka katika kichaka, mlengaji akatakiwa kufyatua na kumwangusha adui. “Afande Kobo, fyatua!!” mshika simu alimwamrisha Kobo aliyekuwa aanatetemeka na silaha yake. Inspekta Kobo akaachia risasi ya kwanza, ikaenda malikiti. Haikumkaribia adui badala yake ilimpa taarifa kuwa kuna hatari inawazunguka. Kobo akamuona adui akirudi mbio kichakani, na baada ya sekunde chache hakutoka peke yake, lilikuwa jopo la maana lenye silaha za maangamizi. Mpambano ukaanza. Kobo akajaribu kutupa risasi nyingine, akakosa! Ile kauli ya angusha mbuyu ilikuwa ikimsumbua kichwa chake. Anayeitoa sauti ile ni nani? na kwanini alimuua kijana wake? na ni kipi kinamfanya amfuatilie Juma Kihwele kama yeye alivyokuwa anamfuatilia. Mlolongo huu wa maswali ukazidi kumpoteza, kwa mara ya kwanza katika maisha yake anafyatua risasi tatu na hakuna hata moja iliyomlenga muhusika. Kitimtimu kikaanza. Askari saba ambao umri umewatupa mkono dhidi ya jopo la vijana majangili kumi na watano. Risasi ziliruka hewani kwa fujo, huyu anarusha yule anajibu. Inspekta Kobo alikuwa kama mpira wa kona, anakimbia huku na kule angali silaha anayo, badala ya kumkabili adui yeye anajiuliza ni nani mwenye ile sauti inayosema ‘angusha mbuyu’ Wasiwasi mara mbili, kwanza dhidi ya hao vijana majangili na pili juu ya adui ambaye wapo naye katika mpango huu kamambe. Nguzu akatamani kumuuliza askari mwenzake ambaye alikuwa anashikilia simu, amuulize yule ni naji alitoa ile amri. Lakini, licha ya kuamini kuwa ule wakati haukuwa wa kuuliza maswali bali kila mmoja kuutetea uhai wake. Hata nafasi hiyo pia hakuipata kabla ya kukiona kichwa cha yule askari kikisambaratishwa vibaya mno na risasi iliyotoka inapotokea. Madonge mazito ya damu yakamrukia wakati akijirusha pembeni zaidi asijekukumbwa na balaa la kusambaratishwa. Inspekta Kobo alikuwa anahema juu juu huku akiomba dua Mungu amtunze asife usikun huo. Taswira ya mkewe ambaye yu katika kuzimia ilimvamia. Akahisi kuwa kifo chake kitasababisha mkewe akirejewa na fahamu zake naye apoteze maisha kwa mshtuko wa kupoteza mume. Sasa hofu ya kifo ilimtawala waziwazi…… Akaiweka sawa silaha yake na kujipa maneno ya ujasiri kupindukia ambayo yangeweza kumrejeshea ari yake ya upambanaji. Aliiweka vyema silaha mkononi, ikawa inateleza. Kwa mara ya kwanza bunduki yake ikawa inamsaliti. Akairudisha katika bega lake na kujipapasa kiunoni, akaichukua ile bastola yake anayoiamini kupindukia akaiweka sawa mkononi, hii yenyewe ilimuheshimu ikakaa sawa. “Serenaserena afande Kobo…. Kobo…” Sauti ikamuita kutokea gizani. Ilianza na utambulisho wao wa siri waliokuwa wamepeana. Inspekta Kobo akabonyea chini kisha akatoka ‘mkuku’ hadi alipoisikia sauti ile. Alimkuta mwenzake akiwa katika dimbwi la damu akiogelea bila kupenda. Hali yake ilikuwa mbaya sana, na alionekana muda si mrefu ataikimbia dunia kuelekea popote anapoamini kwa imani yake. “Kimbia, hatari…. viumbe hawa hatari. Tunateketea wote….” Alizungumza kwa sauti ya chini sana. Akaweka kituo na kuhema kwa nguvu zote. “Hakikisha unaishi ili kuwa shuhuda…. viumbe hatari sana wana siri zote. Usimuamini mtu jiamini wewe mwenyewe kuanzia sasa….. kuna wasaliti kati yetu.” alizidi kusihi. “Na… naku.. nakuf… nakufa afande.” Alizungumza huku akizidi kukauka koo lake na sauti kufifia. Ikawa kama alivyojitabiria!
Inspekta akazidisha umakini, akabaki na maswali lukuki, ni kwanini bwana yule anamweleza kuhusu wasaliti ndani yao, kwanini amemchagua yeye na amemuamini vipi kuwa yeye sio msaliti? Mwenzao huyu!! alijisemea huku akiondoka kutoka eneo lile. Sasa kila upande ulikuwa umetulia, ilikuwa ni vita ya kuviziana baina ya pande hizi mbili. Inspekta hakutaka kumuamini mtu yeyote zaidi. Alitilia maanani uhai wake pekee. Akakimbia hadi alipolifikia shimo asilojua matumizi yake, akatumbukia na kutulia ndani yake. Alikuwa macho kabisa kisije kumdhuru chochote kitu. Aliendeleakutulia hadi palipokucha akauona mwanga. Lakini mwanga huu ulikuwa ukingojewa na watu wengi. Ile Inspekta anatoa kichwa chake nje akakutana na sauti kali zikimkaripia asithubutu kufanya jambo lolote lile atue silaha zake chini na kisha kunyanyua mikono yake juu. Alijitahidi kujitambulisha lakini hakuna ambaye alimsikiliza. Akatii, kwa umakini wa hali ya juu askari wenye sare wakamkaribia na kumtia pingu mikononi na miguuni. Ajabu! Alistaajabu ni kipi kimejiri hadi kujikuta katika balaa kubwa kiasi kile tena ghafla. Alionywa asithubutu kusema jambo lolote lile. Akaingizwa katika gari lenye ulinzi mkali kupindukia. Hawakutaka kulala tena Shinyanga. Amri ikatolewa kuwa iwe isiwe lazima inspekta Kobo afikishwe jijini Dar es salaam, na hiyo ilikuwa ni amri na sio ombi. Inspekta Kobo hakuamini, vijana walio chini yake ki-cheo walikuwa wanamlinda huku wakimkaripia mara kwa mara. Alifedheheka ila hakuwa na la kufanya. Huu ukawa mwanzo wa safari mbaya na ya kutisha. Wakati anaiacha ardhi ya Shinyanga, katika ardhi hiyohiyo harakati mpya ilianza kusukwa.
FLORIAN NGENGEKUZENZA NGUZU.
USHINDANI wa nani kwao matajiri nilishindwa mapema sana, kila walichokuwanacho sisi tuliishia kukiona tu. Hatukuwanacho wala hatukukaribia kukipata. Miaka ya elfu tisa mia na arobaini (1940), ni wale watoto ambao baba zao walikuwa wakijipendeza kwa wakoloni pekee ndo wangeweza kuwa na maisha yenye unafuu. Katika hapa sikuwa mshindani wake. Tulipata nafasi mara chache sana kucheza michezo ya kitoto, hatukuwa tukishindana sana. Miaka ikazidi kwenda hatimaye ikafika wakati wa kwenda shule, huku napo hapakuwa na ule ushindani wowote. Alisoma katika shule ambazo walivaa viatu na sare nzuri angali sisi miguu yetu iliunda urafiki wa kinafiki na miba pamoja na matope. Kitu pekee tulichopata katika maisha yetu duni ni aibu za wazazi wetu pindi waliponyanyaswa na mkoloni. Kisha baada ya hapo wanatusimulia simulizi za mashujaa wao ambao na wao walikuwa wakikiri kuwaogopa hawa watu wenye ngozi nyeupe. Simulizi hizo zilinijenga barabara, katika akili yangu. Nikajikuta ni kijana ambaye uzalendo ulikuwa katika moyo wangu. Baba yangu mzazi ambaye alipigana vita ya Majimaji huko Songea alikuwa akiniongezea ujasiri, ni kweli alikuwa akinyanyaswa na wazungu na aliwaogopa kweli lakini alikuwa akinieleza kuwa katika vita ile kwa mkono wake wa kuume akiwa na rungu kubwa aliwauawa wazungu watano. Kwake ulikuwa ni ushindi mkubwa sana kumtandika mkoloni na bunduki yake mkononi. Ni kweli watanganyika wengi walipoteza maisha lakini hii ilikuwa alama kubwa sana kuwa waliutaka uhuru kwa namna yoyote. Baba alinieleza kuwa baba yake ambaye ni babu yangu alipoteza maisha kwa kunyongwa, na ni yeye ndiye alikuwa mmiliki wa jina la Nguzu ambalo maana yake ni NGUVU. Jina Florian nilipewa na hawa ngozi nyeupe waliojifanya miungu katika ardhi yetu, silipendi jina hilo. Naitwa Ngengekuzenza Nguzu. Yaani ‘Aliyerithi Nguvu’. Baba yangu alinipatia jina lile kwa sababu aliniamini sana, nami nikajikuta najiamini mno. Maisha magumu hayakuiathiri akili yangu, sijui mnaitaje kwa kizazi chenu hiki cha Tanzania, lakini wakati wa Tanganyika tulisema akili zinachaji, akili zangu zilikuwa zinachaji mno. Nilifanikiwa kulimaliza darasa la nne la mkoloni. Wakoloni bwana licha ya unyanyasaji wao lakini walikuwa makini sana, wakiona mtu ana akili sana wanamuwahi ili baadaye aje kuwa upande wao na aseme mazuri tu juu yao. Mkoloni akupatie elimu utaanzaje kumsema kwa mabaya angali tayari unaweza kusema’yes no’ kwa sababu yake!! Hata mimi waliniwahi na hapa ndipo nilikutana na Joseph Kazeze. Na upinzani ukaanza rasmi. Wakatupeleka shule ya upili ambayo kwa sasa mnaiita Tabora boys lakini wakati ule iliitwa Tabora Central school. Ilikuwa shule ya vipaji maalumu haswa. Wanafunzi wengi walikuwa ni watoto wa machifu, ni baadaye sana walianza kuchukua wanafunzi wa kawaida. Kwa wakati ule nadhani ni mimi na wengine wachache sana tuliokuwa tunasoma pale lakini si watoto wa machifu. Mitihani ya hapa ilikuwa ni kutoka vyuo vya uingereza. Hawakutufundisha kuhusu yetu bali walitaka tuyajue yao. Hata hayo yao bado nilipata alama za juu. Urafiki kati yangu na Joseph Kazeze ukaanza kuyeyuka, hakutaka kupitwa alama na mtoto wa kimasikini kama mimi. Tulipoenda jeshini mwisho wa kidato cha tatu kama ilivyokuwa ada nilikuwa bora zaidi yake katika kila kitu. Hakupenda kabisa, ila mimi sikujua kama ni kwa kiasi kikubwa vile. Tukarejea tena kumalizia kidato. Katika uchaguzi nikateuliwa kuwania uongozi, Joseph naye akawania. NIkamwangusha na kuwa kiongozi wake! Wakati ananipa mkono wa hongera ndipo niliiona chuki katika macho yake. Nikapuuzia. Nikasema ikiwa wote tunatoka Mwanza, ya nini kuchukiana sasa. Nikadhani yale yataisha… Kutingwa na uongozi nikasahau kabisa kuketi na Joseph tuzungumze. Chuki ikakomaa! Baadaye yakaibuka mapenzi, nadhani hapa ndipo chuki ilibalehe na kuota mapembe! Joseph alimpenda binti ambaye alikuwa akinipenda mimi. Kuzidiwa huku kete Joseph akaleta ubabe na kunivimbishia kifua. Mara ya kwanza nilimwacha, ya pili akanifuata tena akinitaka ugomvi, nikamweleza bayana kuwa sisi ni ndugu wa mji mmoja asiwe vile. Akanipuuzia na siku hii akanisukuma nikaanguka. Nilipoinuka nilimfundisha kuhesabu moja mpaka kumi kwa lugha ya kirusi. Somo lilikuwa gumu na kila mara alianguka chini, kila akijaribu kunyanyuka namtandika ngumi ya uso. Akapasuka juu ya jicho lake, nami nikawa napiga palepale. Siku hii nikatambua kuwa majina yana maana yake. Ngengekuzenza Nguzu (Aliyerithi Nguvu) Nilikuwa nimerithi haswa. Ugomvi huu ulitikisa shule. Ajabu yake ilikuja katika maamuzi, tulipigana na mgomvi alikuwa Jose lakini katika adhabu nikachukuliwa mimi. Tabora Central School ilikuwa shule ya kijeshi wakati wetu, hata sare zetu zilikuwa za kijeshijeshi, tulivalia kombati za kaki kama wanazovaa wanamgambo, kila kitu kiliendeshwa kikakamavu, hapakuwa na adhabu za viboko. Nilivyoadhibiwa nikikusimulia unaweza ukahisi huyu bwana kachanganyikiwa na sasa ananidanganya. Niliingizwa katika chumba chenye giza nene na hapo nikaanza kulazimishwa kwenda mbele, kadri ninavyokwenda mbele ninazidi kuinama chini kutokana na muundo wa kile chumba, hatimaye paji la uso likayakaribia magoti. Chumba kikabanwa nikawa siwezi kusogea mbele wala kurudi nyuma. Niliumia mno, nikaamini kuwa sasa ninakufa. Waliniacha kwa masaa mengi sikumbuki hata. Waliponitoa nilikuwa nyang’anyang’a. Wakanipelekaq msituni, huko sasa niliadhibiwa na wazungu. Walimwachia mbwa wao anikimbize na nilipewa ruhusa ya kukimbia kumzidi. Nilivyochoka vile ningeweza vipi, si waliutaka uhai wangu tu wapuuzi wale. Basi kama ni mchezo basi mbwa alipata wa kucheza naye, nakimbia hatua kadhaa naanguka mbwa anafika na kuning’ata wanamfukuza. Wananiambia nisimame tena ninakimbia wanamwamuru mbwa anikimbize, ananifikia na kuniangusha ananing’ata. Niliteseka mno! Baada ya hapo nikapokea viboko kumi na viwili vya mkoloni. Nilinyooka.
Joseph hakuadhibiwa nilipotoka kule kwenye adhabu nyinginyingi za kutisha nikaelezwa kuwa nimefukuzwa shule na wakati huohuo aliyechukua nafasi yangu katika uongozi ni Joseph Kazeze. Nililia! Nililia sana. Nikapakiwa katika gari moshi, elimu yangu ikaishia pale nikarejea kuwa mtumwa. Nilipambana hivyohivyo hadi siku ile mwalimu Julius Kambarage Nyerere alivyokabidhiwa nchi huru. Walau hali ikaanza kuwa ya heri, sikutamani kusoma tena. Tayari nilikuwa nina familia ya mtoto mmoja niliyempa nikiwa Mwanza baada ya kufukuzwa shuleni. Sikupata mtoto huyu na yule mwanamke aliyetuletea uhasama baina yangu na Jose. Nilizaa na maskini mwenzangu tukalea kimaskini hivyohivyo. Niliamua kuanzisha familia kwa sababu sikuwa na familia tena, baba yangu alifariki na mama vilevile. Halikuwa jambo la ajabu kwa wakati ile kupoteza familia yako. Nikamsahau Joseph Kazeze katika kichwa changu. Niliamini yote yaliyotokea Tabora Central School ni mambo ya ujana tu. Nilikuja kulisikia jina hili katika siasa. Eti Joseph Kazeze ni mjumbe sijui wa kamati gani katika chama tawala. Hii ilikuwa mnamo mwaka 1977. Niliamua nisijihusishe na habari zozote kuhusu Jose kwa sababu kwa kufanya hivyo nilikuwa nakumbuka chanzo cha mimi kuishia kati katika masomo yangu na sasa sina thamani yoyote katika jamii. Miaka mitatu baadaye yule mwanaharamu akaanza kunizongazonga tena. Alinibomolea nyumba yangu. Japokuwa hakuja yeye moja kwa moja lakini nilijua kupitia waliokuja, akanibambikiza kesi kadhaa bahati nzuri ilikuwa upande wangu nikawa natoka salama. Huwezi kuamini, akavuka mipaka baada ya kuona kila analofanya si kitu kwangu. Hivi unaweza ukaamini Jose Kazeze akaamua kumposa upya mke wangu! Andika kila ninachokueleza usiache walau neno moja, yote yana maana sana. Nd’o hivyo bwana Joseph akamlaghai mke wangu ajuavyo yeye, alikuwa na gari lake aina ya Land Rover ya chama tawala basi aliitumia hii kuishika akili ya mke wangu. Yule mwanamke naye alikuwa mjinga kweli, ujue nilishamweleza kinagaubaga kuhusu uhuni wa Jose lakini akashawishika akaniacha eti. Hivi kama sio kuumizana nafsi ni nini hiki, kweli Joseph ambaye alikuwa ana pesa tayari anaamua kuniingilia anga zangu, tena bora ingekuwa kwa mwanamke ambaye ni kigoli, mwanamke huyu alikuwa amecharazwa bakora za mkoloni haswa hatamaniki, alikuwa amechanjwa mwili mzima chanjo za kinga ambazo ziliaminiwa na makabila mbalimbali. Haya yote akajifanya hayaoni…. akaamua kuniadhibu. Alifanikiwa! Nilimwambia mwanangu juu ya alichonifanyia mama yake. Nilimweleza huku ninalia. Akatangaza kumchukia milele! Basi rafiki yangu akabaki kuwa huyo mwanangu wa pekee, niliyemuita jina Salama. Mama Salama akahamia katika maisha ya Joseph Kazeze.Iliniuma mno, huyu bwana katumia cheo chake kulipiza kisasi angali mimi sikufanya lolote enzi zile Tabora kwa kumkomesha. Sasa mwanamke nikamuachia, sifa zote nikamuachia lakini yule bwana kumbe hajaridhika. Hapo sasa zile jazba za enzi za shule zikarejea nikajisema kuwa nchi hii ni huru kabisa, tena sio uhuru wa bendera. Hakuna utumwa tena labda ukusudie mwenyewe. Ajabu anajitokeza mjinga mmoja mwenye ngozi kama yangu ananirudisha utumwani. Siku ya tukio sikumuaga Salama!
“Naomba kwa leo tuishie hapo mzee wangu Majenga….. sitaki kusikia kilichotokea. Nakuomba sana alfajiri tutaendelea na mkasa huu. Nimefurahi sana kukukuta ukiwa hai mzee. Na badi nashangaa uliweza vipi kutunza karatasi hizi kila ulipoenda na kutarajia siko moja utamsomea mtu” Martin Nguzu lizungumza kwa hisia kali, sauti yake ilikuwa baridi mno. Alikuwa ameguswa mno na maandishi yale. “Niliwahi kumsomea mama yako, sijui hata kama alinisikiliza kwa makini maana alikuwa analia kila akisikia lolote kuhusu hayati Ngengekuzenza Nguzu ambaye ni baba yake mzazi.” Alijibu Majenga kwa utulivu. Na hapo akaitoa miwani yake usoni. Akajifuta machozi. “Babu yako alikuwa mtu wa aina yake sana. Namuona hai ndani ya macho yako…” Akaongezea huku akimshika begani Martin Nguzu. Nguzu akamsaidia kuinuka, akamkokota mpaka ndani akamsaidia kukiandaa kitanda chake akamwacha akilala. Naye akaenda katika chumba kingine akalala.
Wakati Martin Nguzu na mzee Majenga wanakubaliana kulala ili siku inayofuata waendelee kusoma maandishi yale ambayo Nguzu aliamini kuwa si haba yatampa mwanga kidogo juu ya matukio yote yanayotokea. Upande mwingine palikuwa panapambazuka. Inspekta Kobo akiwa na pingu miguuni na mikononi mwake alikuwa katika mahojiano mazito sana. Mdomo wake ulikuwa umeanguka na na kubaki wazi kutokana na kipigo kikali alichopokea, midomo hii iliyokosa ushirikiano ilisababisha udenda ulioambatana na damu umwagike katika namna ya kusikitisha sana. Mguu wake uliokuwa umeunganishwa kwa vyuma ulikuwa umepigwa na sasa baadhi ya vyuma vilikuwa vinachungulia nje. Damu nzito iliyoganda katika chuma kile ilisaidia kuficha ukweli wa mambo. Inspekta hakuwa na uwezo wa kutembea na hakulazimishwa kutembea badala yake aliburuzwa hadi akafika mahali alipohitajika. Macho yake mekundu yalikuwa makubwa sana, na yalikuwa yakiviringika huku na kule katika namna ya kuomba huruma ya yeyote yule mwenye mamlaka ya juu yake.
Hakutokea japo mmoja wa kumtetea. Maelezo aliyokuwa ameyatoa waliosikiliza hayakuwakuna kabisa na hivyo wakaona suluhu ni kumbana vyema kwa kumuumiza ili aweze kutapika siri zote alizomeza. “Inspekta Kobo, hili ni agizo la mwisho kabisa la kukubembeleza wewe kusema ukweli wote ili ubaki kuwa salama ama la tutatumia nguvu. Na hatushindwi!” Sauti ya kusihi iliyojaa madaraka iliunguruma. Inspekta akastaajabu, hawa mabwana tayari walikuwa wameitengua taya yake, wakaupoteza njia mguu wake na sasa yungali mahututi katika bahari ya maumivu, sasa anaelezwa kuwa asiposema ukweli watatumia nguvu. Nguvu! alistaajabu… Nguvu gani zaidi ama watamkaliza katika kiti chenye shoti ya umeme, au watampiga risasi? Hizi nd’o nguvu ambazo walikuwa hawajatumia. “Mkuu nilichokiandika katika maelezo yangu ni hicho hicho sijaongopa hata nikishtuliwa usiku wa manane siwezi kupindisha ukweli huo.” Alijibu kwa shida sana. “Kama uliweza kupindisha shabaha yako maksudi na kumwacha hai jambazi mkorofi ambaye tumehangaika miaka nenda miaka rudi kumsaka unashindwa vipi kuupindisha ukweli?” Alihoji kisha akasimama wima na kuendelea kuzungumza. “Kobo, katika maisha yako ya kulenga shabaha umeangusha mibuyu mingapi iliyoleta ukorofi?” “Mingi sana afande.” alijibu kwa sauti ya chini. “Umetunukiwa shani ngapi kutokana na kulenga kwako shabaha?” “Tano afande.” “Unaikumbuka shabaha yako ngumu kupita zote?” “Ahh! mmh! ndio afande, ni ile ya kutoka ghorofa moja kwenda nyingine.” aliendelea kujibu upesiupesi. Bila kujua nini hatma ya maswali yale. “Unaukumbuka umbali kimakadirio?” “Mita mia tano….” alijibu kwa utulivu. Na safari hii sauti ilikuwa chini zaidi kwa sababu aliijua nia ya maswali yale. “Yaani nusu kilometa sivyo? Na haukuwa katika utulivu wowote, na uliweza kuipata ile shabaha bila kukosa. Na ilikuwa ni usiku….. halafu leo hii unapiga risasi tatu maksudi unamkosa adui anayetikisa taifa. Kobo! Kwa kitendo chako hicho cha kumuacha adui wa taifa unadhani watanzania wapo radhi kukusamehe? Mimi kama mtanzania siwezi kukusamehe… nastaajabu wanakuchelewesha nini kukutia kitanzi bazazi wewe…. uliyechagua kumlinda mwanaharamu mwenzako!” Sasa alikuwa amewaka yule bwana aliyekuwa anamuhoji Inspekta Kobo. Na alikuwa anatetemeka mno. Inspekta alikuwa amekamatwa pabaya. “Ok! unalipwa shilingi ngapi kila anapofanya uhalifu wake…. tuzungumze kama wanaume na haya mambo yaishe. Maana Tanzania mambo ya kitanzi tulishayafuta, na hata ukifungwa maisha huyo mwanaharamu atakuja kukutoa tu utakuwa huru. Haya nieleze tu, unapewa kiasi gani kulisaliti jeshi la polisi katika oparesheni kabambe namna ile.” Swali likatupwa. Inspekta Kobo akafadhaika mno, kwa sababu hakuwa kama walivyodhania. Alipojaribu kupinga, hasira za yule bwana zikamuangukia. Akapokea teke kali katika shingo yake, akarushwa na kutua pembeni akabaki kukoroma huku damu ikimtoka puani. Akatamani kuelezea ukweli wa kila jambo lakini hakuona kama ataeleweka maana katika maandishi yake hakuandika kuhusu mashaka yake juu ya ile sauti inayotamka ‘ANGUSHA MBUYU’. Hakuandika kuhusiana na kifo cha utata cha Martin Nguzu na hakugusia hata kidogo juu ya mahusiano baina yake na koplo Zubeda. Angeanza kuelezea hayo angeonekana ni muongo mara mia zaidi ya alivyochukuliwa awali. Inspekta akaamua kubaki kimya. “Inspekta Kobo hivi unajua kuwa hii kesi yako inaweza kuhesabiwa kama kesi ya uhaini na itakuweka pabaya wewe na familia yako, ama unajitazama wewe na masilahi yako pekee hauitazamani familia yako. Haumtazami mkeo ambaye hadi sasa hajui kinachoendelea ulimwenguni, hujali kuhusu watoto wako unajitazama wewe pekee. Sasa mimi nimekusihi sana imetosha naandika ripoti tusilaumiane katika hili.” Alizungumza kwa sauti tulivu kabisa huku akiwa anamtazama Inspekta Kobo. Maneno yale juu ya familia yake yalimvuruga Kobo aliyejitambua wazi kuwa hana kosa lolote lile, lakini la kufanya nd’o hakuwa nalo. Akarejeshwa katika chumba alichokuwa anafungiwa mle akiwa peke yake. Tofauti na siku nyingine ambapo chumba hiki kilikuwa kinazimwa mwanga wa taa na kubaki katika giza siku hii kilikuwa kina mwanga na zaidi kiliongezeka kiti. Nanyongwa!! Hisia zikakipiga kichwa cha inspekta Kobo, tumbo likaanza kuunguruma kwa hofu ya kuupoteza uhai wake. Akaingizwa pale chumbani. Kimya kikatanda kwa dakika zisizopungua tatu. Kisha zikasikika hatua zikijongea katika kile chumba. Mlango ukafunguliwa na askari wawili, kisha kwa mwendo wa taratibu akaingia Inspekta jenerali wa polisi (IGP). Mwili wa inspekta Kobo ukaingiwa na ubaridi mkali sana, akaunyanyua uso wake na kumtazama bwana yule nadhifu kabisa aliyekuwa katika mavazi yake ya kazi. “Funga mlango!” akawaamuru wale askari. Wakatii! kisha wakaondoka na kuliacha eneo lile likiwa na watu wawili pekee. Mwili wa Kobo ulikuwa umesulubika sana, lakini kwa kumtazama bwana huyu mwili ukajiona kuwa inayokuja nd’o suluba taslimu. Kobo alitambua kuwa IGP aliisubiri hii nafasi kwa hamu sana ili aweze kumnyoosha na sasa alikuwa ameipata. Iwe isiwe atamwadabisha. “K” IGP akaita kwa upole. Inspekta akamtazama kisha akaitika kwa shida sana. “Pole sana rafiki yangu. Pole!” IGP aliketi vyema. Unafiki! Kobo akajisemea. “Kabla sijazungumza mengi na wewe ninapenda kukueleza kuwa ninakupenda sana rafiki yangu, huwezi kuamini haya lakini elewa kuwa nimejaribu zaidi ya mara tano kuonana na wewe lakini nimeshindwa kwa sababu sikuwa tayari kukuona katika hali hii. Umeteseka sana K” alizungumza kwa hisia IGP. Hali hii ilimtisha Kobo, akajiuliza anachokisikia ni sahihi ama kuna namna ya ulaghai. Yaani huyu bwana ajisikie vibaya kwa yeye kuwa katika wakati ule mgumu. Haiwezekani. Inspekta Kobo akakumbuka vitisho vyote alivyowahi kupewa na IGP wakati huo akiwa hajapewa dhamana hii ya juu katika jeshi la polisi. “K, yale yote yalikwisha kwa upande wangu. Nimetafiti sana na nikagundua kuwa wewe haukuwa chanzo cha mke wangu kuwa mlemavu. Niliumia sana awali na kujikuta nikikuchukia lakini nimeikubali hiyo hali na nipo hapa kwa ajili ya kukusaidia tu! Tafadhali sema nami” “Niliyoyasema ni hayohayo.” Akajibu kwa ukaidi Kobo, bado alikuwa na hisia za chuki dhidi ya IGP bado hakuamini kuwa wao ni marafiki tena. “K, sikiliza ndugu yangu. Ukaidi hautasaidia kitu chochote kwa wakati huu. Laiti kama ningekuwa juu ya sheria ningeamuru uachiwe huru na ubaki kujuta na nafsi yako ikiwa ni kweli umefanya yote hayo ama la. Lakini kwa hili mimi sina ninalazimika kuiheshimu sheria ya nchi, sio kuivunja kisa ninakuonea huruma. K, tafadhali nieleze ni nini kilitokea….” IGP alizungumza kiukarimu kabisa. Inspekta Kobo akaamua kurusha karata yake ya kwanza. Akaelezea kwa ufupi sakata la Nguzu, hakulitaja jina la mwanamke ambaye alikuwa anahusika. Akaitaja ile sauti ambayo aliisikia usiku wa tukio la Nguzu kuchomewa ndani na kisha akaitaja tena sauti ileile ilisikika siku ambayo alikuwa ameishika bunduki yake tayari kwa kufanya shambulizi. “Nikapagawa sana kugundua kuwa licha ya kwamba nimelenga shabaha kwa ajili ya kummaliza adui ila ndani yetu pia kuna adui. Tena adui asiyekuwa na huruma aliyeiteketeza kwa moto nyumba ya askari mwenzetu pasi na huruma kabisa. Nilitetemeka sana, hata lile agizo alilonipa la kuushusha mbuyu lilinikwaza badala ya kunihamasisha. Hakika nilikuwa natetemeka…”Alimalizia. Palepale IGP akamsogelea na kumnong’oneza jambo kwa kusihi. “Usiyaseme maneno haya popote pale. Umeniamini mimi imetosha sana na ninakuahidi italeta manufaa. Nimeupata mwanga.” IGP akatulia kidogo kisha akarusha suala jipya kabisa ambalo lilikuwa jipya kwa inspekta Kobo. “Umesema juu ya Nguzu kuchomewa ndani ya nyumba yake, unadai ulienda kuzungumza naye usiku ule. Sawa kabisa…. na je Majenga unamfahamu vipi?” “Ma nani?” “Majenga” Aklajibu IGP huku akimtazama kwa ukaribu kabisa inspekta Kobo. “Sijawahi kulisikia jina hili katika maisha yangu.” “K, mbona hutaki kuamini kuwa ningali upande wako? nieleze nijue ni wapi nakusaidia rafiki yangu. Ujue kuna watu watatu wameuwawa huko Shinyanga na huu mlolongo wote unakuangukia wewe. Ndugu zao wamechachamaa si kidogo, huyo Majenga ni nani Kobo! Tell me…” alianza kupandwa na ghadhabu IGP. “Simjui na sijawahi kulisikia jina hilo Gervas, mbona unanilazimisha kutema maneno ambayo akili yangu haijawahi kuyameza. Simjui huyo Majenga for God’s sake!!” Aling’aka inspekta Kobo huku akimtaja IGP kwa jina lake. IGP akaanza kufura kwa hasira, akajitahidi kujiweka katika hali ya kawaida. Akauliza tena na tena bila majibu kubadilika. Inspekta Kobo akasimamia analoliamini! IGP akamtazama kwa sekunde kadhaa, akatoa kitambaa chake mfukoni na kujipangusa matone ya jasho na mwisho akamtupia Kobo neno la mwisho. “Pambazuko hili litakuwa baya sana kwako na sitakuwa na namna ya kukusaidia. Nimejaribu sana Kobo nawe umeona. Umekataa kumtaja Majenga na unamjua waziwazi….” Akasubiri kidogo, Kobo akamtazama kisha akalazimisha tabasamu na kisha akazungumza. “Nimekuwa na mapambazuko mabaya sana tangu mke wangu apate janga lile, nimekuwa na mapambazuko mengine mabaya tangu vijana wako, vijana niliowafundisha ukakamavu jeshini walipougawana mwili wangu na kufanya kwa vitendo yale niliyowafundisha, mapambazuko mabaya hayataanza leo ama kesho yalianza tangu uliponituhumu kuwa nimeshiriki kumfanya mkeo awe mlemavu wa miguu angali nilijaribu kadri ya uwezo kuokoa maisha yake, niliokoa maisha yako pia Gervas kwa kukusukuma ili usipigwe risasi, nikawa na mapambazuko mabaya ulipozisahau fadhila zangu, ni pambazuko gani baya zaidi unaloniahidi sasa… eeh! pambazuko gani unalolisema, pambazuko la kupoteza uhai? Kuteswa? Kufungwa gerezani maisha yangu yote? Hakuna pambazuko la ajabu hata moja kati ya hayo, ni wewe utayaishi mapambazuko ya ajabu siku utakapoujua ukweli angali nimenyamaza katika kile kimya cha milele, Attaccati a sto cazzo.” akaweka kituo huku akimalizia kwa kutokwa na lile tusi lake murua katika lugha ya kiitaliano. IGP akabaki kuganda, midomo ikimchezacheza asijue ni maamuzi gani ayachukue. Akatoweka pale na kwenda nyuma ya mlango. Akajibanza pale na machozi yakaijua njia yake, yakayalowanisha mashavu, kamasi nyepesi zikatoka kuchungulia nini kinaendelea katika uso wa IGP. IGP alikuwa analia kiume!
_____
Majira ya saa sita usiku aligutuka kutoka usingizi huku jasho likimtoka sana. Majenga! jina hili likakivamia kichwa chake, akaketi kitako na kuanza kukumbuka juu ya maneno yale aliyokuwa akiyasoma yule mzee. Akatamani asubuhi ifike upesi aweze kuendelea kusikiliza ni kipi ambacho kitakuwa na faida kubwa sana kwake. Akamaizi kuwa licha ya kushtuka vile na kuandamwa na jina hilo lakini pia alikuwa pia amebanwa na haja ndogo. Na choo kilikuwa mita nyingi kutoka chumba alichokuwa amelala. Akapatwa na uvivu sana huku akijilaumu kwa kukataa kunywa maji mengi baada ya chakula cha ili asije kupata shida kama hizi usiku na sasa amezipata shida zilezile. Akajivuta taratibu kuelekea choo kilipokuwa. Nje palikuwa kimya sana, walisikika wale viumbe wanaopenda kulala mchana kisha usiku wanazurura kusumbua viumbe wengine. Popo! Umbali wa choo ulimtatiza sana, akajiona mpuuzi sana giza lote lile kuna vichaka vya hapa na pale ni kwanini ahangaike na choo. Akakiendea kichaka kidogo alichokiona karibu yake. Akakidhi haja yake lakini hakuweza kugeuka kabla ya kusikia sauti ikimuamuru asimame. Akasimama tuli! “Kwanini unakojoa vichakani we tahira?” sauti ikakaripia. Martin Nguzu akastaajabu, tangu afike pale Shinyanga sauti karibia zote zilikuwa zinaambatana vyema kabisa na lafudhi ya kisukuma, iweje hii sauti inakuwa na miporomoko ya pwani ama Zanzibar? Hakujibu kitu! “Nakuuliza weye mwanaharamu…” “Nisamehe tafadhali…” Hatimaye akazungumza. “Mzee Majenga analala chumba kipi hapa? na ni nani ako….” Swali likatupwa. “Analala nyumba kubwa!” “Geuka utupeleke upesi..” Nguzu akageuka na kukutana na mambo aliyoyazoea. Mitutu ya bunduki. Walioibebwa waliishika kizembe sana. Ni vile hawakujua kuwa ile hatari inayodhaniwa kuzikwa katika tanuru la moto, iliishia kung’arishwa na kuwa dhahabu yenye thamani kali huku ikiwa na makali ya kisu kipya. Walisimama wanaume wawili, mmoja akiwa na bastola mkononi mwake. Huyu aliielekeza kwa Nguzu. Nguzu akajitia kutetemeka huku akiwasihi wasimuue. Kutetemeka kule kukawazidishia uzembe. Mmoja aliyebaki akasikika akizungumza kwenye simu kuwataarifu wenzake kuwa wamefika eneo la tukio na muda si mrefu watauchukua mzigo wao. Walitembea hatua kumi kuelekea ilipokuwa nyumba ya mzee Majenga na familia yake. Nguzu alizihesabu zile hatua vyema huku macho yake yakiwa makini sana kutazama kitu. Hatimaye akakifikia, kilikuwa ni kigogo kilichokuwa njiani. Akakikanyaga na kujikwaa maksudi. Akaanguka chini huku akitokwa na yowe la hofu. “Inuka hanithi wewe…” Kauli hii aliisubiri Nguzu kwa hamu, mkono wake ulikuwa tayari na jiwe, akatumia sekunde chache kubaini kuwa mshika bastola yule hakuwa anakaribia kufyatua, kidole chake kilikuwa mbali kabisa na kifyatulio. Safi sana! akajisemea na hapo akajitutumua ainuke. Alipoinuka akaliachia lile jiwe likampata bwana mwenye lafudhi ya kipemba usoni, kapiga yowe huku bunduki ikimtoka. Yule mwenzake akajiweka sawa kufanya shambulizi kwa kutumia bunduki. Nguzu akajirusha huku goti lake likitangulia mbele hadi katika kifuani kwa adui. Akambwaga chini. Nguzu akaitwaa ile bunduki. “Acha ujinga dogo, vita sio kama kunywa urojo unakunywa hata kama ni kibogoyo. Vita inahitaji watu majasiri.” Alimwonya alipomuona akitafuta bastola. Yule bwana akatulia asiamini kuwa kibao kimewageukia wao. Mwenzake alikuwa amekodoa macho. “Mwambie jamaa aje moja kwa moja eneo la tukio, ukiongeza neno nakuua muda huu, na usipoongeza nitakuua baadaye.” Nguzu akaamrisha. Simu ikapigwa jamaa akazungumza aliyopaswa kuzungumza. Kisha simu ikakatwa. “Nilikueleza ukiongeza neno nakufanyaje?” “Unaniua!” “Na usipoongeza?” “Utaniua baadaye. Nisamehe tafadhali sisi tunatumwa tu” alijibu huku akitetemeka. Nguzu akamgeukia yule mpemba. “Shehe! mwenzako kaongeza neno tayari, anasema nimsamehe na sikusema hivyo.” Hakusubiri jibu, akaigeuza bunduki, hakutaka kupoteza risasi akaizamisha bunduki katika kifua cha yule bwana singe ikaingia nzima nzima. Akagalagala kuusaka uhai wake. Mpemba akakurupuka akairukia bastola. Lakini hakuweza kufyatua kabla Nguzu naye hajamrukia na kumkanyaga mkono. “Swahiba, nakukumbusha tena huu sio urojo kila mtu anakunywa.” akamtia ngumi kali katika paji la uso wake. Ilikuwa ni vita ya kistarabu sana, mtu akianguka chini waliolala wanajua ni maembe yanaanguka, wanajigeuza upande wa pili na kuendelea kuota ndoto zao. Hawakujua kuwa roho zilikuwa zinatoka na uwanja ule ulikuwa umegeuka kuwa wa kivita. Nguzu akambana maswali yule mpemba, akajibu kuwa huyo anayekuja ndiye kiongozi wao, wenyewe hawajui kiundani juu ya tukio lile. “Kwa maana hiyo unamaanisha wewe hauna umuhimu wowote kwangu sivyo.” “Walah! naapa mie wanionea bure tu sina nijualo.” Jibu lile likawa la mwisho. Kama hauna maana unabaki na Nguzu kufanya nini. Akaunganishwa katika safari ya mwenzake aliyekuwa ametulia tayari. Nguzu akaweka windo lake kumngojea huyo aliyeitwa mjua mengi. Windo hili likazua safari mpya ya Konstebo Martin Nguzu kurejea jijini Dar es salaam. Jiji ambalo linaamini kuwa yu kwa muumba akijibu tuhuma zinazomkabili. Huku wengine wakiamini bado anahangaika na adhabu ya kaburi.
ILIKUWA safari iliyojaa katika kichwa chake ghafla baada ya vita ile ya usiku iliyoondoka na uhai wa watu watatu ambapo mmoja kati yao alikuwa ni kiongozi wao kwa mujibu wa maelezo yao. Martin Nguzu ambaye sasa hakuwa akiushangaa uwezo wake wa kukabiliana na maadui alikuwa amewaangusha wengine watatu huku akifanikiwa kuwapokonya bunduki tatu pamoja na risasi za kutosha kabisa Hakutaka kulala baada ya kuhakikisha ameitelekeza ile miili mbali na ngome ya mzee Majenga. Alimwamsha mzee Majenga na kumweleza kwa ufupi juu ya kilichotokea. Tofauti na matarajio yake kuwa taarifa ile itamtisha sana Majenga, hii ilikuwa kinyume. Mzee Majenga akatokwa na kicheko kidogo kisha akampigapiga kifuani Martin Nguzu na kumwita kwa jina la babu yake. “Ngengekuzenza Nguzu umezaliwa upya…” Kauli ile ilimtoka na kumwacha Martin Nguzu katika pumbazo asielewe ni kitu gani bwana yule alimaanisha. “Mimi nimezeeka kijana wangu, niliisubiri sana hii vita kwa muda mrefu lakini imekuja nikiwa mzee tayari. Nenda ukapambane hii ni vita yako na inakuhusu. Nakuachia haya maandishi niliyoyaandika bila kuongeza wala kupunguza neno kutoka katika kinywa cha hayati babu yako anayeishi sasa katika nafsi yako. Hakikisha unayamaliza yote kabla haujaivaa hiyo vita…… mimi nitakuwa salama kabisa na tutakutana nikiwa hai, na hata nikifariki ni kwa sababu ya uzee tu…” Aliongea kwa ujasiri mkuu. Kisha akachechemea hadi ndani na kuchukua makaratasi yaliyoandikwa kwa kalamu akamkabidhi Martin. “Nilikuwa napenda sana kuandika na babu yako alikuwa anapenda sana kunisimulia, nadhani ni maneno hayo kwa ufupi yatakupa jawabu nilikutana vipi na babu yako.” Majenga alitoa kauli ile na Martin akaipokea lakini alikuwa na swali la ziada. “Niliokoka vipi katika ule moto jijini Dar es salaam?” “Mzee wako asingeweza kukuacha uangamie. Wazee wa zamani hawakuwa wa kawaida, akinuia jambo linakuwa kama lilivyo, nadhani ni kutokana na kutenda dhambi chache nd’o maana Mungu alikuwa akiwasikiliza.” Alifafanua na kuzidi kumvuruga Martin. Akagundua mvurugano ule, akaongezea “Kasome haya yote kabla hujaamua wapi pa kuanzia” Maongezi yakaishia hapo. MAANDISHI YA NGENGEKUZENZA. Ubaya ni kwamba wakati wa ukoloni, sisi watu wa rangi nyeusi hatukuishia tu kunyanyaswa na ngozi nyeupe katika uhai wetu, hata ulipokuja ustaarabu wa kuhifadhi maiti zetu sisi tuliwekwa katika kundi la mbwa koko aliyefia jaani baada ya kukabwa na mfupa aliodhani ni mnofu. Ukipata bahati sana unafukiwa, ila ni waafrika wachache waliokuwa na bahati, wengi tulitunukiwa nuksi. Ukiwa na nuksi unaachwa hapohapo ulipofia ama unasogezwa kidogo porini, ukawe chakula kwa wanyama wenye tabia ya uvivu katika suala la kuwinda na ndege wanaoona sifa kudonoa donoa. Hata babu yangu alikuwa na nuksi vilevile baada ya kufariki alitupwa, akaipata bahati akiwa maiti tayari waafrika kadhaa wakamfukia. Baada ya kuupata uhuru wetu nikawa naitembelea ile sehemu niliyoaminishwa kuwa babu yangu alifukiwa pale, pakawekwa alama nami nikawa naenda kumsalimia na kuzungumza naye bila kujali ananisikia ama la! Sasa yule mwanahizaya baada ya kuona haitoshi kumchukua kiharamia mke wangu na kuniacha katika jitimai, akaona hata! hii haitoshi huyu bwege bado anapata raha. Akaanza kuniandama kivingine, najua aliwatuma mashushu wake waliokiamini na kukiabudu chama chao kuliko Mungu wa mbinguni na miungu ya porini. Hawa wakamfikishia habari kuwa ninayo furaha nyingine, furaha ya kuzungumza na babu yangu makaburini. Ikapita ajenda katika siku nisiyoijua na baadaye ikawa ni amri bila kutahadhalishwa. Eneo lile lilipaswa kupandwa miti, mara lilitakiwa kupita barabara. Sikuelewa hata kidogo, na hakuna aliyesubiri nielewe. Kwani Ngengekuzenza nani mpaka aelewe? Lile nililoamini kuwa ni kaburi likavunjwa na huyu mkoloni mshenzi mwenye rangi kama yangu huku akiiga miondoko ya wazungu na afro yake kichwani akiipaka kalikiti na kuwa laini kama nywele za mkoloni. Lugha yake pia ilifanana na yao. Poor Joseph Kazeze! Kama ni kunipiga, hapa alinipiga na mjeledi wa chuma nikaangukia pua huku mikono yangu ikishika makaa ya moto. Huyu mjinga aliniweza hakika! Uchungu wangu ule nikamshirikisha mwanangu Salama nikamweleza kuwa Jose anataka kuvuka mipaka ambayo ameivuka tayari, yaani sielewi anachotaka. Salama alinisihi niachane naye, nikaona hajui uchungu ninaoupitia kwa kupokonywa mke na kisha hapohapo nikapokonywa furaha yangu. Babu yangu! “Salama, nikiachana naye akagundua nina furaha kuwa na wewe atakuchukua na wewe pia….” nilimwambia Salama. Wazo hili likamkuna na kuiona hatari ya waziwazi. “Sasa utamfanya nini?” “Yule ni mjinga tu kwangu, nataka nimfanyie yale mambo ambayo wajanja huwafanyia wajinga wanaodhani pesa nd’o ujanja.” nilimweleza huku nikiona wazi kuwa hanielewi. “Unataka upigane naye?” aliniuliza. “Nikipigana naye wote tutakuwa levo ileile ya ujinga, nataka nimpige ili tuunde daraja kati ya nani mjinga na nani mjanja.” “Lakini baba, huyu ana pesa na cheo atakusumbua sana. Yaani nina uhakika hautafikia hata nusu ya azma yako.” “Kwanini unasema una uhakika.” nilimuuliza salama. “Si kila kitu kipo wazi, ana pesa na vyeo na zaidi ana kundi kubwa la watu linalomzunguka.” “Nd’o maana unasema ni hakika?” “Ndio baba” “Sikiliza mwanangu Salama na uliweke hili milele katika maisha yako, hapa duniani kuna kitu kimoja tu nd’o cha uhakika vingine vyote si vya uhakika. KIFO pekee ndo jambo la uhakika, kila mtu atakufa hii haina mjadala. Ujiue, unyweshwe sumu, ugongwe na gari ama hata ukilala usiamke. Vyote vina maana moja tu ya uhakika…. asije akakudanganya mtu kuwa jambo hili ni uhakika… anakulaghai na wewe unayemsikiliza na kumkubalia unakuwa upande wa mjinga. Sipendi uwe mjinga siku moja….” Nilimsomea mambo yale. Yakamuingia na kumpa ujasiri naye akanibariki katika uamuzi wangu na hiyo ilikuwa ni mnamo mwaka elfu tisa mia themanini na tatu ama nne kama sijasahau. Sijui itakuwaje miaka ya huko mbele lakini enzi zetu hizi hapakuwa na ulinzi wa kutosha kwa viongozi, ulinzi huo tuliusikia tu na kuuona walipokuja viongozi kutoa nje, Mwalimu Julius Nyerere alihamasisha sera za kuishi kijamaa, nasi tukaamua kuishi kama ndugu. Hapakuwa na wa kumpinga kirahisi mwalimu. Ukitaka kumpinga sisi tunakwambia nenda ukapambane kuileta Tanganyika huru ndipo ujilinganishe na mtaalamu huyu. Hivyo tuliishi kijamaa sana, halikuwa jambo la ajabu kukutana na mwalimu Nyerere barabarani na kusalimiana naye kwa kushikana mikono. Sasa vipi kuhusu mjinga huyu anayeitwa Joseph Kazeze? Sidhani kama kwa miaka yenu huko mbeleni itakuwa hivi. Nahisi hata balozi naye atatafuta ulinzi… Nilikueleza awali kuwa tangu nilipokuwa mtoto nilikuwa nina uwezo mkubwa sana darasani, hata akili yangu haikuwa ndogo katika kufikiri. Nikaamua kuitumia akili yangu kumwonyesha yule bwana nini maana ya mwanaume kutoa machozi. Kwakweli nilimkosesha amani! Kwanza nilifurahia kile kitendo cha mwalimu Nyerere kutowafukuza wazungu baada ya kutupatia uhuru, hivyo upatikanaji wa silaha hadi miaka ya themanini bado ulikuwa ni mwepesi sana, unaweza kuipata bunduki hata kwa kubadilishana na gunia la mahindi pekee. Zilikuwa zimezagaa. Nami nikajipatia bunduki yangu, uzuri nilipitia jeshini hivyo sikuhitaji kufundishwa lolote. Nikamuaga mwanangu kuwa naanzisha mapambano rasmi. Sikuwahi kuua ila nilijeruhi sana. Nilianza na baba yake mzazi, akiwa katika mizunguko yake. Nikamteka na kumpiga kipigo cha mbwa mwizi, akavunjika mkono. Sikumtumia salamu Jose Kazeze kama ni mimi ili aendelee kuhadaika. Akafuata mdogo wake, huyu nilimfungia safari hadi Morogoro, nikamkamata na kumfunza adabu asiweze hata kuiona sura yangu. Jose Kazeze kitu alichosahau ni kwamba sisi tulikuwa marafiki na nilimfahamu vyema yeye na familia yake. Niliendelea kumpa presha bwana yule kwa kufikia hatua ya kuvamia kwake nikarusha risasi zikavunja vioo vya nyumba aliyokuwa akiishi lakini sikumdhuru mtu na sikutaka kumdhuru. Uwezo wangu katika kupanga matukio ulianza kunishangaza hata mimi, kila nikilala na kuamka nawaza pigo jingine. Jose akaanza kukonda! Mara akaachana na yule mwanamke aliyenipokonya. Nami sikurudiana naye mjinga yule aliyekosa hata nukta ya akili. Nilikuwa nina hasira kali. Baadaye baba yake alifariki, kwa magonjwa mengine sijui kama na kile kipigo kilichangia. Sikujali! Siku mbili baada ya kuzikwa nikaenda makaburini, huku nikaweka bomu nililolipata kwa bei nzuri tu. Likafanya mlipuko uliotikisa nchi. Hakuna kilichobaki zaidi ya jeneza kusambaratika huku na kule. Hili lilikuwa pigo kubwa zaidi, wanandugu wakalundikana nyumbani kwa Jose Kazeze kujadiliana nini kinaendelea. Nikavamia na huko na kurusha bomu jingine katika choo kilichokuwa mbali kidogo na nyumba na hii ni baada ya kuhakikisha hapakuwa na mtu ndani yake. Mparangano uliojitokeza nilijikuta nacheka mwenyewe. Amakweli mtenda akitendwa…. Jose akazidi kuzorota kiafya. Ni hapa ndipo nikaamua kumweleza bayana ili kama ni kufa kwa mshtuko afe tu, who cares? Hakufa! Ila alipagawa vibaya mno, na hapo ndipo ikaanzishwa oparesheni ya Ngengekuzenza Nguzu anasakwa auwawe. Kisa ni jambazi, yakaundwa matukio ya kushangaza kunihusu mimi na hapo nikaanza kusakwa rasmi. Nilijua kuwa hali ni mbaya, nikaraejea kwa mwanangu… usiku wa mwisho kumwona mwanangu. Akanieleza kuwa yu mjamzito, nikamweleza kuhusu kinachoandikwa na magazeti ya serikali huku nikimweleza kuwa moyo wangu u radhi kuwa nimemuweza yule bwana. Zaidi ya hayo nikamsihi kuwa iwapo atazaa mtoto wa kiume basi amwite Nguzu! Tulikumbatiana huku sote tukishindwa kuyazuia machozi. Nikaondoka na kuja kwako Majenga unihifadhi nikusimulie ya kuandika kama ulivyohitaji wewe kijana wangu. Na nimejitahidi sana kukusimulia. Maandishi yale yaliacha nafasi kubwa kisha ikafuata aya ambayo mwandishi wake alikuwa ni Majenga.
Mnamo mwaka 1988 mwezi wa kumi na moja mzee Ngengekuzenza mwenye msongo wa mawazo kwa kuishi maisha ya mashaka kila kukicha aliniaga kuwa anakwenda msalani, ilikuwa majira ya usiku. Hakurejea mapema nikalazimika kutoka pamoja na mbwa kwenda kumtafuta. Nilimtafuta sana hadi pambazuko likanikuta nikiwa namtafuta, mbwa asiyechoka ndiye alinihimiza kumsaka mzee wangu nimpendaye. Hatimaye nikaufikia mti ambao alikuwa amejitia kitanzi. Nasikitika kuwa sikuwahi kukiri kuwa ninamfahamu mzee yule kwa sababu za kiusalama, alikuwa anasakwa sana na jeshi la polisi kama jambazi sugu. Niliporejea ndani nikakutana na karatasi katika kitanda alichokuwa akilalia. Haikuwa na maneno mengi sana aliniandikia kama nilivyokuwa nimefanya tayari. “Umenihifadhi kwa moyo wote wa upendo, wewe ni kijana wangu nikupendaye. Ninaomba uendelee kunitunzia maneno yangu….. utawapatia wajukuu zangu ili wajifunze kuwa babu yao hakuwahi kuwa mtu dhaifu hata kama nilionewa, babu yao sikuwahi kuwa jambazi hata kama watayaona maandishi hayo, pia kwa imani yangu kuu naamini kuwa sijafa kirahisi rahisi. Mizimu ya mababu zangu waliouwawa kifedhuli utumwani imeniambia kuwa najipumzisha ila ipo siku nitazaliwa na nitazaliwa katika damu yangu mwenyewe. Ninapumzika Majenga ila nikizaliwa tena usishangae. Naamini mizimu hii kulikoni dini walizotuletea wakoloni, dini zilizotuongopea kuwa Mungu ni mzungu, zikaenda mbali na kusema kuwa Mungu anaishi katika majengo yao waliyoyajenga. Dini za kishenzi zilizonipatia jina la kishenzi, Frolian na kunipokonya jina la kishujaa kutoka kwa babu yangu. Dini zilizotulaghai kuwa kila asemacho yule mzee mweupe anayesimama mbele yetu basi ni sawa, anatuona tunateseka na anasema tumwachie Mungu, nasi tukijaribu kupambana anasema tena sisi ni watu wabaya sana na hatufai kuwekwa kundi la wanadamu. Dini zao hazijaniambia kuwa siku moja nitarejea, lakini wazee wangu ambao tuliwalilia njaa wakatusikia katika miti, tuliwaomba kila kitu na walikuwa wakweli. Wazee hawahawa wamesema nami, acha nipumzike ila ipo siku nitarejea na sitakuwa wa kujificha tena. Kwaheri mjukuu wangu!” Kisha akwakeka hitimisho Majenga kwa wino mzito. “MNAMO MWAKA 1988 BABU YETU Ngengekuzenza aliaga dunia na ni mwaka huohuo mwanaye Salama alipata kujifungua… yule mtoto akaitwa NGUZU” _________________
NGUZU alibaini kuwa alikuwa anatetemeka baada ya kuimaliza sentensi ile ya mwisho. Akaituliza akili yake na kutaka kumaizi ni kitu gani kimempa majibu katika maandishi yake. Kwanza, aliamini katika mizimu na kimyakimya akakiri kuwa mzimu wa babu yake ungali ndani yake. Pili, Jose kazeze yawezekana aliweka kisasi cha kudumu, baada ya familia yake kunyanyaswa akaisambaza ile chuki kwa wajukuu na vitukuu kama wapo. Hivyo yawezekana mmoja kati ya kitukuu ama mjukuu alikuwa akilishambulia jina la Nguzu popote atakapokutana nalo hivyo naye alikuwa ameshambuliwa. Mambo haya mawili yakamwacha katika sintyofahamu nyingine mpya. Akajaribu kulitaja jina la Inspekta Kobo…… akatazama kisa chake hadi kuja kumchomea ndani ya nyumba yake. Hili akaliweka katika mabano, yawezekana kuna watu wengine walihusika katika hili jambo. Akayakumbuka maneno ya yule kiongozi wa waliotumwa kumkamata Majenga. Akakumbuka kuwa yule bwana ndiye aliyemueleza juu ya Inspekta Kobo kuwa yungali rumande akituhumiwa kwa kesi mbaya kabisa inayoweza kumtokomeza uraiani, lakini alimtajia jina la kiongozi wao mkuu ambaye hata wao hawakuwahi kumwona hapo kabla. Zumbe! Nguzu akafuatilia katika mitandao mbalimbali kutazama huyu mtu ni nani katika serikali ili ajue je? ana uhusiano na ukoo wa Kazeze? na kama hana uhusiano ni kitu gani anataka? Kichwa kikamuuma alipojikuta anayo orodha kubwa sana katika kichwa chake. Na kadri basi lilivyoikaribia ardhi ya jijini Dar es salaam,mara moyo wa Nguzu ukapiga kwa nguvu sana. Kuna kitu alikuwa amekisahau kwa muda mrefu. Koplo Zubeda! Mungu wangu! Akahamanika kutokana na hali ile ambayo ilimtokea naye asijue ni kwanini imekuwa hivyo ghafla wakati analikaribia jiji na si wakati yupo mbali?
MAJIRA YA saa saba usiku Martin Nguzu alikuwa akirandaranda katika kona mbalimbali za jiji la Dar es salaam kusaka hoteli ambayo angeweza kulala kama si kupumzika mpaka patakapokucha na kuutaza uelekeo ambao anapaswa kuanza nao. Hakuwa na mashaka yoyote ya kuufichaficha uso wake, habari zake zilikuwa zimesambaa lakini si picha yake. Wasambaze picha yake kwa cheo chake cha u-konstebo kwani hawana mambo mengine ya kuandika. Alifanikiwa kupata hoteli ya bei ya wastani, akafanya malipo na kujiandikisha kwa jina batili. Akakabidhiwa chumba. Alipoingia na kuufunga mlango akaiwasha taa, akakiona kioo kikubwa jirani na mlango. Akajitazama jinsi alivyokuwa, kimaumbile alijiona yungali vilevile lakini ndani ya mwili wake alijihisi yupo ngangali sana tofauti na awali. Bila kutarajia akajikuta akimuwaza tena Zubeda. Akiwa palepale mkabala na kioo alifikiria ule ukaribu wao jinsi ulivyokuwa ukimpa raha ya kipekee, raha iliyomfanya ajikute akimwonea wivu inspekta ambaye alisemekana kummiliki Zubeda, kuna kipindi alikuwa akitamani hata kumdhuru yule inspekta ambaye ndiye kikwazo pekee kilichokuwa kati yake na penzi la uhuru baina yake na Zubeda. Nguzu alikuwa akitamani kumtambulisha Zubeda kwa marafiki zake kama shemeji yao, ukiachana na kuufurahisha moyo wake na pia kuuweka wazi udhibiti wake dhidi ya Zubeda, Sifa pia kilikuwa ni kigezo cha kutamani uhuru ule. Nani ambaye angeacha kumsifia kuwa anamiliki ‘mtoto mkali’ Zubeda alikuwa mzuri, urembo wake haukufichika hata alipojitundika katika gwanda zake za kazini. Askari wengi walikiri kuwa binti huyu alikuwa wa aina yake, na hii ni sifa waliyoitoa huku akiwa katika gwanda zake. Nguzu alikuwa amepata fursa ya kuziondoa zile gwanda kisha akamvesha kanga moja nyepesi mwanadada huyu na kisha kuambatana naye maliwatoni. Macho yake mawili yenye nguvu yakifanikiwa kutazamana ana kwa ana na mzigo wa matiti ambayo yalikuwa yamevuka kidogo ule muda maarufu wa ‘saa sita’ lakini hayakuwa mbali sana kufananishwa na muda huo hasahasa yakipewa msaada mdogo wa sidiria. Macho ya Zubeda yangeuamuru mwili wa mwanaume yeyote atakayemtilia maanani kujikuta ukisisimka na donge la hamu kumshika. Macho yake makali angali akiwa kazini yalikuwa yanatepeta wakiwa wawili na Nguzu na kumfanya Nguzu ashangazwe na hali hii. “Huyu mtu aliupata vipi ukoplo wa polisi? Kwa macho haya tepevu?” Haya ni baadhi ya maswali aliyojiuliza kabla hajachoshwa na mikono laini ya Zubeda. Mikono ambayo hakuamini hata kama inao uwezo wa kuzishika pingu na kumlazimisha mtuhumiwa azivae. Ajabu Zubeda alisifika kwa kuwahenyesha watuhumiwa. Kuhenyesha watuhumiwa?? Ilishangaza! Lakini Nguzu naye akajikuta anahenya kupambana na msisimko uliokuwa ukimkumba kila mara mikono ile ilipomgusa. Na hapo akakiri kuwa hata yeye ni mtuhumiwa pia na alikuwa anahenyeshwa wawapo chumbani wawili. Kweli Zubeda ni kiboko! Kumbukumbu hizi zikajirejesha nyuma kwa kasi ya ajabu, Nguzu akakumbuka jinsi alivyokutana na Zubeda jijini Mwanza. Akaukumbuka utambulisho wake wa kijivuni dhidi ya Zubeda ambaye hakuwa na cheo chochote wakati ule na hata jeshini alikuwa hapajui. “Naitwa Martin, Konstebo Martin Nguzu!” Tabasamu likamponyoka na kujikuta akipiga saluti ya kihuni. Akakiendea kitanda na kujirusha hapo kwa fujo zote. Kitanda kikahimili kishindo! Na hapo kikaanza kuufyonza ule uchovu wote na kuugeuza kuwa raha ya kipekee. Usingizi ukampitia…..
_____
MAHAKAMA kuu ya Tanzania ilikuwa imesheheni haswa, maaskari walikuwa wanafanya kazi ya ziada kuwazuia watu waliozidi kumiminika pale mahakamani. Punde ikasikika amri ya kumaanisha kuwa jaji na baraza zima la wazee lilikuwa linaingia pale mahakamani. Kimya kikuu kikatanda ikiwa ni ishara ya kuheshimu mahakama. Akiwa na pingu miguuni na mikononi kisha pingu hizo za miguu na mikono zikaunganishwa na mnyororo mgumu aliongozwa hadi katika kizimba. Alipofikishwa kizimbani akafunguliwa zile pingu, akaingia akiwa huru kizimba kikafungwa. Macho yake yaliyozama ndani na kuzidi kuonekana kuwa ni makubwa yaligeuka huku na kule, safari hii hakuwa na uoga tena alikuwa ameikubali hali halisi. Macho yake yakatua katika kiti alichokuwa ameketi mama yake aliyepooza upande mmoja. Licha ya kwamba alikuwa amelia sana hadi machozi kumkauka aliweza kuhisi machozi ya moyoni yakimlowanisha. Wakagonganisha macho yao, akamwona mama yake akizungumza maneno yasiyoweza kusikika hata kidogo huku machozi yakimtoka kwa wingi. Aliamini kuwa mama yake alikuwa akimwombea kwa Mungu ili kesi ile ipate muujiza wa yeye kushinda. Uchungu uliomshika alitamani angepewa walau nafasi moja tu ya upendeleo naweze kuzungumza na mama yake, amkumbatie na kumfariji. Jicho lile likaendelea kubarizi pale ndani ili aweze kuwaona watu wengine ambao huenda anawajua. “Marafiki hawana maana!” Alijisemea baada ya kuhakikisha kuwa hakuna rafiki yake hata mmoja aliyefika mahakamani hapo. “Kwa hiyo wameogopa kuwa nitawachoma ama?” alijiuliza. Hakupata muda wa kujiuliza zaidi wakati jicho lake likitua katika kiti kingine upande wa kushoto. Macho yakagongana tena na huyu mkaaji wa kiti hicho. Zubeda! Walitazamana kwa sekunde kadhaa kabla Martin Nguzu hajakwepesha macho yake. Hakutaka kumwangalia binti huyu aliyekonda sana na kuonekana wazi alikuwa akitawaliwa na uchungu mkubwa. Alipomaliza kuzungusha macho yake akamwona jaji akitoa ruhusa ya mwendesha mashtaka kumuuliza maswali mshtakiwa. Maswali yalikuwa magumu sana, akayajibu kadri alivyoweza. Mengi alikuwa ameyasahau kabisa. Miaka sita mahabusu bila kesi kusikilizwa, angekumbuka nini sasa.
Wakati wote huu alikuwa akishangaa kumwona wakili kwa ajili ya kumtetea. “Lakini nilimkataza mama kuhangaika kuweka wakili.” Martin Nguzu alijiuliza huku akitikisa kichwa chake kama namna ya kusikitika. Akakiri kuwa katika ulimwengu huu mzazi ni mzazi lakini mama ni bora zaidi kuliko baba. Mama anaumia sana akimwona mwanaye katika wakati mgumu wakati baba huhesabu ugumu ule kama changamoto na kusema ‘kijana wangu amekua na atatatua changamoto hizo’ mama huinama chini na kusema ‘mtoto wangu anateseka’ Ni hii tofauti aliikiri katika kesi yake hii. Mama mzazi aliyepooza mwili alikuwa mahakamani kushuhudia kile kiumbe alichokileta duniani baada ya suluba ya miezi tisa, kisha kuhangaika katika malezi. Hakujali kupooza kwake, hakujali kuwa yawezekana mwanaye akahukumiwa kifungo cha maisha gerezani ama kunyongwa kabisa kwa jinsi kesi ilivyokuwa. Alichokifuata pale ni kumwona mwanaye kwa jicho lake mwenyewe. Kama alivyomuona wakati amemzaa, alihitaji kumwona tena katika ugumu huu, ugumu wa kukondeana kwa sababu ya mateso na lishe duni, ugumu wa kuwaza kufia jela. Mama alibaki kuwa shuhuda wa mwisho! Ni nani kama mama kwani? Wakili alisimama na kutema vifungu vya sheria ili kumnusuru Martin Nguzu kutoka katika janga lile. Alionekana kuijua vyema sheria lakini upande wa mashtaka ulionekana kuwa imara zaidi, sura nyingi zilitawaliwa na hasira kali. Hasira hii iliboreshwa zaidi na mavazi yao, walifanania na kundi la mafia ambalo limemshukia mwenzao baada ya kuwasaliti na sasa wanataka kumpa adhabu ya kumzika huku akiwa hai akaupiganie uhai wake akiwa chini ya ardhi. Nguzu akamgeukia jaji ambaye alionekana mwingi wa chuki kuliko haki. Jaji alipounyanyua uso wake Nguzu akajikuta anagundua kitu kipya kabisa. Ile sura ya jaji haikuwa njgeni machoni mwake hata kidogo. Hofu ikamjaa ya kutotendewa haki juu ya kesi ile ambayo alitambua wazi kuwa ni vile tu amekosa mashahidi lakini haikuwa ikimuhusu kabisa na alitakiwa kuwa mtu huru. Jaji yule akaanza kusoma vipengele kimoja baada ya kingine kwa utulivu sana. Ni kama aliyeelekea kutoa hukumu, hii ilimshangaza sana Martin. Hukumu inatoka vipi kirejereja hivi bila kesi ile kupewa muda wa baraza la wazee kuipitia na kutoa mitazamo yao. Jaji alisoma taratibu huku kila mahali akijaribu kumbana Nguzu. Na hatimaye kauli ikamtoka. “UTANYONGWA MPAKA UFE” Mungu wangu! Nguzu akamwona mama yake mzazi akitua chini kama mzigo, watu wakakimbilia alipokuwa ili kumwokoa. Palepale akawaona askari wanne wenye ghadhabu wakisogea katika kile kizimba na pingu kwa ajiri ya kumchukua na kumpeleka katika mahabusu ya mahakama kabla hawajampeleka gereza la Ukonga. Gereza pekee ambalo washtakiwa waliohukumiwa kunyongwa mpaka wafe huhifadhiwa huko mpaka siku ya hukumu yao. Kuwaona watu wale kukamchanganya Nguzu, na jaji alikuwa amefunga mjadala tayari. Nguzu akaona haiwezekani, akawahi kujirusha akaidaka silaha ya askari mmoja na mara moja akaielekeza alipokuwa yule jaji. Jaji akakodoa macho yake alipojikuta anatazama ana kwa ana na bunduki iliyoshikwa na mtu asiyekuwa na masihara hata chembe. Akafyatua risasi kiufundi lakini yule jaji akawahi kujificha chini ya meza. Na hapohapo Nguzu akaisikia sauti ya kike ikimpigia kelele kumtahadhalisha. Ilikuwa sauti ya Zubeda! Akageuka na kukuta amechelewa tayari, bunduki nyingine ilikuwa inaelekea kufyatuliwa ili yeye adhurike. Ilielekezwa kifuani pake. Akajikuta anapiga mayowe ya hofu huku akikiziba kifua chake kwa mikono yake. Bunduki ikacheua. “Mamaaaa nakufaaa!” alipiga kelele kubwa sana na hapo akajikuta akibiringita kama chaguo lake la mwisho. Akashangaa kujikuta anaelea hewani. Akaanza kutapatapa akirusha miguu huku na kule. Hatimaye akasimama wima tena. Hakuwa mahakamani! alikuwa amesimama katika kitanda huku akiwa amejifumbata mikono yake katika kifua chake. Ndoto! Jasho lilikuwa linamwagika vibaya mno, bado moyo ulikuwa unapiga kama unaotaka kutoka nje ya kifua chake. Alikuja kutulia baada ya dakika kumi na hapo ndipo akakiri kuwa ile ilikuwa ni ndoto lakini ndoto ya ajabu sana. “Yule jaji yule! Yule jaji ni nani!? Jaji, jaji….” Nguzu alibaki kusema kama ambaye anajaribu kulazimisha kung’amua vitu kutoka katika ile ndoto ya ajabu ambayo hakutaka kuamini eti ilikuwa ndoto ya kawaida. Alihisi yule ni babu yake anasema naye. Hofu ikatanda alipokumbuka kuwa alihukumiwa kunyongwa katika ndoto yake. Hofu ya kifo ikamjaa, akaanza kuhofia uwepo wake katika jiji la Dar es salaam. Jiji ambalo ipo ile mahakama ya ndotoni na pia lile gereza wanalohifadhiwa wafungwa wa adhabu ya kunyongwa mpaka kufa. Hiki nini? alijiuliza. Bado hofu iliishi naye, akamkumbuka mama yake alivyokuwa akimlilia na hata alivyoanguka baada ya hukumu ile kutolewa. Hofu ya kifo ikiwa haijaisha ikapanda hofu nyingine. Hofu ya kumpoteza mama yake mzazi pindi atakaposhuhudia matatizo yakimpata. Nguzu akakiri kuwa huu mpambano ulikuwa maji ya shingo kwake naye alikuwa hajui kuogelea vyema. Akaamini kuwa alikuwa anahitaji watu watakaosimama pamoja naye. Kwa mara nyingine tena jina Zubeda likakiandama kichwa chake. “Kwanini Zubeda?” alijikuta katika swali hili. Hisia mbili zikaanza kupambana, mojawapo ilikuwa hisia za mapenzi. Nguzu akakiri kuwa alikuwa akihangaishwa na jina Zubeda kwa sababu tu aliwahi kumpa burudani ambayo ilikatishwa ghafla bila kufika ukingoni. Pili alihisi kuwa anahitaji kupata msaidizi na msaidizi wa kweli katika vita hii ni koplo Zubeda. Kujua hisia ipi ni ya kweli nd’o ukawa mtihani mzito. “Ngoswe penzi kitovu cha uzembe” Usingizi ulimkuta Nguzu akiwa katika uchambuzi hafifu wa kitabu hiki maarufu , alianza kwa kumpa kongole mwandishi Edwin Semzaba kwa kuandika kitabu hiki, kisha akahamia kwa Ngoswe na Mazoea na hadi anasinzia alikuwa amefikia mahali ambapo Mazoea ameanza kuzoeana na Ngoswe! Hii ni baada ya Ngoswe kumuhadaa kuwa atamtorosha waende wote mjini…… Alisinzia akiwa anatabasamu, bila shaka ni vile visa vya Ngoswe vilimpa tabasamu.
ASUBUHI ilimkuta konstebo Martin Nguzu katika ofisi ya gazeti mojawapo kati ya yale yaliyoandika habari ya kifo chake na kisha kusemekana aliyeandika ni ‘mwandishi wetu. Kama ilivyomkera inspekta Kobo na kujikuta akiponyokwa na matusi ya kiitaliano, kwa Nguzu ilikuwa vilevile lakini hakuwahi hata siku moja kuota ndoto za kiitaliano. Yeye aliponyokwa na matusi mfululizo ya kisukuma. Lakini hakuishia kutukana tu, aliamua kupiga hatua na aliamini hatua hii inaweza kuwa ya muhimu zaidi kumfikisha katika hatua nyingine. Akalisoma gazeti lile na kuyapata mawasiliano ya muhariri mkuu wa gazeti hilo. “Huyu jamaa lazima anawajua waandishi wake wote, wenye majina na wasiokuwa na majina wanaojiita ‘mwandishi wetu’. Atawataja ama atakula maumivu yao…” Alizungumza konstebo wakati akizungusha macho yake huku na kule kabla hajazama ndani ya ile ofisi. Awali alipanga kwanza kumjua sura huyu bwana na kisha ajiweke katika lindo zuri aweze kuijua gari yake. Baada ya kujua hayo angeachana naye na kisha kumpangia siku ya shambulizi. Alijua kuwa amezisahau taarifa zile tayari, na hata hao akina’mwandishi wetu’ walikuwa wanaendelea na maisha yao mengine. Mambo yakaenda tofauti, Nguzu akiwa amejivesha miwani ya jua katika uso wake huku akiziachia nywele zake wazi kwa maksudi kabisa. Hazikufanania na nywele za askari, hasahasa wa cheo cha konstebo. Nguzu alikuwa katika hali ya utofauti. Alianzia mapokezi na kuulizia ni wapi atampa muhariri, katibu muhtasi akauliza ikiwa ana shida binafsi ama ya kiofisi. Maswali yao yaleyale kila siku! Nguzu alijisemea kabla hajajibu, “Shida ya kiofisi dada.” “Ok! nyoosha moja kwa moja hadi katika ile korido kisha pinda kushoto utaiona ofisi, keti katika foleni subiri huduma.” Nguzu akainama chini kidogo huku akijishika kifua chake kama ishara ya kushukuru. Akatoweka! Alimkuta bwana mmoja mwenye mvi akiwa anangoja kuingia, akaketi pembeni yake. Bwana mwenye mvi akaanzisha soga kuhusu siasa mara ahamie katika mpira wa miguu, huku ndipo alizidi kumpoteza Nguzu. Ushirikiano wake pekee ukawa ‘ndio’ ama kujichekesha. Hatimaye mzee akaingia na kutoka baada ya muda mfupi. Bila shaka muhariri hakuwa tayari kusikiliza soga nyingi kutoka kwa yule bwana. Ikawa zamu ya Nguzu. Hofu ikamwingia hakutambua kama yupo sahihi katika hatua ile ama ameitupa karata yake vibaya. Akaufungua mlango na kuingia ndani huku akitambua kuwa yeyote yule anaweza kustaajabu kuhusu ile miwani lakini alifurahi kwa sababu ni watanzania wachache sana anaweza kukuona haupo sawa katika jambo fulani naye akawa kimya asikwambie badala yake anamweleza rafiki yake kisha wanacheka! Hee! Watanzania?! Tusaidiane kujishangaa. Kweli! hakuna aliyemuuliza. “Karibu!” Sauti nyembamba lakini ya kiume ilimkaribisha huku mikono ikimwonyesha mahali pa kuketi. Martin akaketi. “Naitwa Sebastian! natokea Temeke Dar es salaam.” Alianza kujitambulisha. Muhariri hakuonyesha kujali juu ya lile jina, Nguzu akaendelea. Sasa akayafungua magazeti kadhaa aliyokuwa ameyashika mkononi akayatua mezani. “Nakusikiliza bro..” Sauti ile iliyotawaliwa na kiburi cha kuwa muhariri ilizungumza. “Nilikuwa nataka kuuliza…” “Ulikuwa unataka ama nd’o unataka kuuliza mkuu?!” Muhariri akamuwahi Nguzu. Nguzu akafadhaika na kuamua kutuliza akili yake, tayari alishagundua kuwa alikuwa anakosa kujiamini. Akajipa sekunde kadhaa akaingia tena kushambulia. “Nauliza, hizi habari ambazo anaandika mwandishi wetu, ni nani anaziandika na kwa nini asijitambulishe kwa majina yake.” Akaweka kituo. “Samahani umeuliza ama umetoa lalamiko!” Muhariri mwenye nyodo akazungumza, sasa aliachana na kazi alizokuwa anafanya akamtazama Nguzu huku akiyabetua mabega yake. “Nimeuliza.” “Ni utaratibu wa kiofisi. Ukihitaji ubadilishwe utapaswa kuandika barua na kuiweka kuleee kwenye sanduku la maoni. Sijui kuna la ziada lililokutoa Temeke bwana…. bwana…” Akalisahau jina lake na kulipuuzia. Konstebo Martin Nguzu akanywea na kujiona anazidiwa karata hivihivi mchana kweupe. Akapaniki! Akasimama wima, akawa anayetafuta neno la kuzungumza linakikataa kinywa linarudi kichwani. Akaona haifai kuendelea kusimama hivyohivyo. “Huyu aliyeandika hii habari ni nani?” Akafoka. Bado alikuwa wima. Muhariri hakuligusa lile gazeti badala yake akainyoosha shingo yake na kuona nini anaonyeshwa. Akakutanisha macho yake na habari juu ya kifo cha Nguzu na kuhusishwa sababu za kimapenzi na mengineyo. Akajikuta anarudi nyuma kwa kasi, uso wake ukiitangaza wasiwasi yake. Akaishika simu na kutaka kubofya nambari kadhaa, palepale Nguzu akauwahi ule mkono na kuugandamiza. Kisha ili kuimarisha usalama akachomoa kisu kikubwa kutoka katika ficho lake. “Huwa ninaua bila taarifa maalumu, sipendelei ufe hivyo. Jibu swali langu.” Hakuonekana kuonyesha mzaha. Muhariri akalitambua hilo. “Sijaandika mimi.” “Mwandishi wetu ni nani?” “Mwandishi wetu… sim… simj..” Ngumi kali ikatua katika shingo ya muhariri. Ilikuwa ngumi maalumu kwa ajili ya kumzuia yule mwanadamu anayependa kuongea kwa sauti ya juu, kumpunguza uwezo wa kupiga kelele na kujikuta akinong’ona. Nguzu alimwacha akihangaika pale akauendea mlango na kuufunga! “Simu yako ya mkononi…” Alisema kisha akautega mkono wake. Muhariri akaikabidhi huku akilia kwa sauti yake ile nyembamba ambayo ngumi kali ilizidisha ule wembamba na kujikuta akigumia kama mtoto wa kike. Nguzu aliipekua ile simu upesi upesi katika sehemu za jumbe mbalimbali, hakupata ujumbe wa kumvutia. “Unapendelea kufia ofisini ama nyumbani kwako?” “Si… aahm! nisamehe si… nitasema lolote utakalo.” “Unanijua mimi?” “Sikujui.” “Ni nani huyu mwandishi wetu na anapatikana wapi?” “Niliandika mimi… lakini hata mimi nilipewa.” “Nisikilize we fala…. ndoto yangu moja ambayo nahitaji kuitimiza ni siku moja nimuue mtu akiwa ofisini nimkatekate nimtie kwenye mfuko wa rambo, kisha nitoke na ule mfuko niingie nao katika daladala niutelekeze huko. Vyombo vya habari vishindwe kuelewa vitaandika nini kuhusu kifo hicho…… Nina hasira ya kutimiza ndoto zangu. Nakupa nafasi ya mwisho kujieleza ukitetereka natimiza ndoto yangu. Nakuhakikishia kuwa sitaacha walau tone la damu humu ndani kwa ajili ya wapelelezi.” Nguzu alizungumza huku akiwa amemkazia macho muhariri. Kijasho kikamwagika… Akatapika kila alichokuwa anakijua katika ile habari iliyoandikwa na ‘mwandishi wetu’. _____
JAMBO la kwanza lililokituliza kichwa cha Martin Nguzu ni juu ya inspekta Kobo. Nguzu alistaajabu asimini hata kidogo kuwa aliachoelezwa kipo kama kilivyo. Licha ya kukiri kuwa yule muhariri alikuwa ‘chamtoto’ sana na asingeweza kuficha lolote kwa kitisho alichompatia lakini bado hakutaka kumpatiliza na kumwamini kwa asilimia zote. Nguzu alitoka pale moja kwa moja akisimamia wazo lake kuwa kwa namna yoyote ile ni lazima afike nyumbani kwa Koplo Zubeda, aliamini kuwa ni huku ambapo angeweza kuupata mwanga zaidi katika hatua zake. Alikiri kuwa kuonekana kwake mbele ya Zubeda kutazua kizaazaa cha aina yake ambacho kinaweza kusababisha majirani wakajazana kutaka kujua nini kinatokea. Nguzu akajipa tahadhari kubwa sana kuwa ni lazima umakini utangulie mbele kuliko kiherehere cha kutaka kukutana na Zubeda ambaye kichwani anaamini Nguzu ameuwawa. Ili kuondoa macho mengi kumfuatilia juu ya alichokuwa anahitaji kufanya Nguzu akaamua kufanya uvamizi wake mchana kweupe. Alilipenda giza lakini alijua linavutia wengi sana…. Akauchagua mchana kwenda nyumbani kwa Zubeda. Akajiapiza kuwa Zubeda akionyesha dalili zozote za kuwa upande usiokuwa wake basi hatasita kumshukia kama mwewe anavyomshukia kifaranga na kumwacha mamaye akipiga kelele asiweze kutoa msaada. Majira ya saa nane mchana alikuwa analitazama geti la kuingilia nyumbani kwa Zubeda. Hali ya ukimya ilitawala sana, akategea mpaka alipowaona wanaume wawili wakipita kuelekea njia ile naye akaunga tela ili asionekane kama anajihusisha kwa lolote na nyumba ile. Akapita na kuangaza huku akiulazimisha ule ukimya umwingie akilini na kumpatia jawabu la ni kitu gani kinaendelea. Kimya kilimtatanisha! Si kwamba hapajawahi kuwa kimya ama huwa ni sehemu yenye kelele za kutisha, ila ni mwili uligoma kuupokea ukimya ule katika namna ya kawaida. Alilipita geti lile kwa mara ya kwanza huku akifanikiwa kujifunza kuhusu mazingira yale upesiupesi, mara ya pili aliporudi alilifikia geti na kubisha hodi. Mlinzi akajitokeza na kufungua. Hakusema kitu akabaki kumsikiliza Nguzu mwenye miwani nyeusi. “Ni mgeni wa Zubeda! Koplo Zubeda..” Nguzu akajitambulisha huku akigundua kuwa huyu mlinzi ni mpya sio yule wa awali. Akasaili eneo lililomzunguka yule mlinzi na kugundua kuwa hata silaha imebadilika. Sub Machine gun! Akaduwaa, kunani mpaka Zubeda aamue kuajiri mlinzi ambaye ana utaalamu wa kutumia silaha hii tena mchana kweupe. “Sub machine gun!” akajikuta anajisemea kichwani kwake, kana kwamba ni mashairi ya wimbo anaotaka kuukariri. “Wewe ni nani?” Mlinzi akauliza. Polisi! Machale yakamcheza Nguzu kwa jinsi mtu yule alivyouliza lile swali, hakuwa mlinzi wa kawaida huyu alikuwa polisi. “Naitwa Sebastian Madeko. Ni jirani…” alijitambulisha. “Nisubiri hapa!” mlinzi alimwamrisha kisha akapiga hatua kwenda katika mlango wa nyumba ya Zubeda. Nguzu akamwacha hadi alipoufikia mlango akawa makini kumtazama atazungumza na nani….. Alishatambua kuwa hali haikuwa shwari, ni aidha Zubeda alikuwa matatani ama la alikuwa analeta matata. Mlinzi akarejea baada ya dakika mbili. “Twende!” akamwambia huku akimkazia macho. Nguzu hakutaka kuionyesha hofu yake badala yake alijiandaa kwa mapambano. Mlinzi akalifunga geti vyema kabisa kabla ya kumwongoza Nguzu kuelekea katika mlango wa kuingilia nyumba ya Zubeda. Wakaufikia mlango, Nguzu hakuendelea kuwa kondoo. Katika mlango ule wa kioo, aliweza kumsoma yule mlinzi, kuna shambulizi alijiandaa kumkumba nalo kabla hawajaingia ndani ama kuishia palepale. Nguzu akawa sekunde moja mbele, akatokwa na teke maarufu kwa jina la ‘Shukrani ya punda’. Lilikuwa teke la nyuma! Mlinzi ambaye hakutarajia pigo lile akapepesuka mpaka chini, alimanusura bunduki yake imuue yeye mwenyewe kwa kumchoma kooni. Macho yakamtoka pima! Nguzu akawahi kukitoa kisu chake na kujitoa mpaka pale chini kisha akadidimiza katika mkono wa mlinzi. Akatokwa na yowe kubwa kwa muda mfupi, Nguzu akachomoa ile ngumi yake ya kupunguza sauti. Ikamwingia yule bwana na palepale akaiondoa miwani yake. “Naitwa Martin, Konstebo Martin Nguzu. Sikijui kifo bado, ukifanya mfano wa kunidanganya utakijua kifo kabla yangu.” Alifoka Nguzu huku midomo yake ikitetemeka. Mlinzi hakuamini alichokuwa anakiona, alijiona akiwa anatazamana na mzimu wa Nguzu ambaye anasadikika kuwa ni mfu. “Ni nani amekuagiza kulinda eneo hili na ni nani yupo ndani ya nyumba hii zaidi yako?” Mlinzi akajifanya hajasikia. Nguzu akatokwa na ngumi kali hii ikatua katika sikio la kuume la mlinzi. Hakuweza kutokwa na yowe kubwa, damu ikaanza kumtoka. Nguzu akatokwa na tabasamu wakati akimuuliza kuwa ni kipi chepesi kusikia swali ama ngumi? Mlinzi yule ngangari akaanza kutokwa na kamasi. Bwege alikuwa amepatikana! “Nipo mwenyewe…. nipo mwenyewe usiniue.” “Amekuagiza nani?” “Inspekta…. Inspekta Kobo.” Alijibu kwa utulivu. Nguzu akaishiwa hamu! hakutarajia jibu lile. Huu ukawa ni mkanganyiko mpya kutoka katika majibu ya muhariri na huyu bwana mlinzi. ____
Akamtazama kwa jicho lililotangaza chuki ya waziwazi kabla hajamtundika swali jingine katika namna ya kisharishari. “Muonekano wake upoje huyo bwana wa kuitwa Kobo. Huku akikumbuka kuwa akijifanya hajasikia swali lile basi kifuatacho ni kubamizwa ngumi na kuulizwa swali la kukera safari hii aliwahi kujibu. Akauelezea wajihi wa inspekta Kobo. Nywele ndefu nyeupe zinazojaribu kuuficha uwalaza wake, ndevu fupi zenye uwiano sawia na nywele zake katika rangi. Umri wake ukichezea miaka sitini hadi sitini na nane. Konstebo Nguzu akachoka upya! Huyu hakuwa inspekta Kobo aliyekuwa akimfahamu yeye. Lakini kilichomjaza nguvu upya ni ule utambulisho ulikaribiana na ule ambao alielezwa na muhariri wa gazeti baada ya kumbana vizuri. Konstebo akiwa anajiandaa kumuuliza tena yule bwana swali jingine, akafanya kosa kuitazama anga kama anayefikiria aulize kwa namna gani nyingine ili apate mwanga mkali anaouhitaji katika giza lile nene. Yule muhanga alitokwa na teke kali likatua vyema katikati ya mapaja ya Nguzu, teke lile likamfanya Nguzu ainame. Naam! adui alihitaji hivyo. Uso ukawa jirani naye, akatokwa na teke kali sana lililoongezewa uzito na kiatu kigumu alichokuwa amevaa. Uzito huu ukatua barabara katika uso wa Nguzu. Ilikuwa mchana ghafla ukawa usiku kwa Nguzu pekee. Pigo lile lilimsukuma mpaka mlangoni. Akaingia na ule mlango, kiuno kikapokea maumivu stahiki. Konstebo Nguzu akajaribu kurejea katika mapambano lakini giza lilikuwa linamuharibia, hakumwona adui yake. Sanjari na hilo alikuwa akipambana kuilamba damu iliyokuwa inamtoka puani. Adui alikuwa amechachamaa. Alijaribu kutapatapa lakini adui hakumwachia nafasi, ni kama alimaanisha kutaka kuondoka na roho ya Nguzu na hakuhitaji kumuuliza swali lolote lile. Nguzu alibaki kuikumbatia sakafu wakati mateke yasiyokuja kimpangilio yakimwandama. Pumzi zikaanza kumsaliti, na hapa akajaribu kwa mara ya mwisho kuusaka uhai wake ambao yule bwana alitaka kumpokonya angali hajamaliza shughuli yake. Akaituliza akili katika maumivu. Kitu ambacho wanadamu wachache sana wanaweza. Kasumba ya mwanadamu akisikia mlio wa risasi anaanza kukimbia asijue kama anaikimbia ama anaikimbilia risasi. Nguzu akautafuta uelekeo wa yale mateke makali yaliyomaanisha kuua. Akaupata uelekeo wa mpigaji, na jinsia livyokuwa anapiga hovyo akatambua bayana kuwa anatumia zaidi hasira na hapohapo anapoteza muhimili wa umakini. Teke lilipomwingia akajitutumua na kusimama wima, na kujirusha kulekule katika uelekeo wa adui yake. Karata sahihi! Akamsomba yule bwana na kutua naye chini. Majogoo mawili yaliyochoka haswa yalikuwa yamelaliana. Na heri tele ziwe kwa kwa jogoo lililomlalia mwenzake. Martin Nguzu alikuwa juu. Hakuweza kurusha ngumi, kuchimba mikwara wala lolote lililoonyesha umwamba. Wote walikuwa wanahema juu juu. Martin akapambana na kufanikiwa kuyafumbua macho yake. Likafumbuka jicho moja kwa shida sana. Akamwona adui yake akiwa mdomo wazi, anahema juu juu! Akaiona shingo ikiwa wazi. Akajitutumua akaifikia na kuikaba, anayekabwa akaanza kurusha mikono kuzuia kitendo kile. Hakika walikuwa wamechoka! Vishindo vilisikika kwa mbali, Nguzu akahisi hatari kubwa inakuja mbele yake….. Uwezo wa kupambana kwa wakati ule hakuwanao, kama huyu aliyechoka anashindwa hata kummalizia vipi hao wanaokuja huku wakiwa na nguvu mpya. Akajigeuza na kutua chini kisha ukaanza mpambano mpya wa kila mmoja kujaribu kusimama. Nguzu akajaribu akaanguka, mwenzake naye yakamkuta yaleyale. Nguzu akakerwa na hali hii ya kujikuta mnyonge angali oparesheni ikiwa mwanzo kabisa. Hali ikazidi kuwa mbaya alipomwona yule mlinzi akifanikiwa kusimama wima, akayafuatilia macho yake yakiwa yanaangaza huku na kule hatimaye kwa pamoja wakajikuta wakiitazama bastola iliyokuwa imetulia sakafuni ikisubiri yeyote ajuaye kuitumia na aitumie. Nguzu alitamani nguvu zimjae na akimbilie kule kuiwahi lakini hakuwa na nguvu za kutosha na alikuwa katika maumivu bado. Kifo kikanukia katika namna ya kukera. Yule mlinzi akaanza kujivuta kwa kasi kuifuata bastola ile, Nguzu akaanza kujiona yu mjinga kukisubiri kifo chake bila dalili zozote za kupambana. Akapitiwa na fikra za harakaharaka juu ya hayati babu yake, aliyemrithisha jina hilo lenye maana kubwa. Nguzu ‘chikichia’ hapa hapafai tena! alijionya huku akiangaza lilipo kimbilio. Hakuliona kimbilio kabla hajamwona yule mlinzi akigeuka huku akiwa na bastola mkononi. Akafyatua hovyo kwa mara ya kwanza, bastola isiyokuwa katika kiwambo cha kuzuia sauti ikatoa mlio mkubwa. Mlio huu ukamuhamasisha Nguzu kujitutumua na kukimbia. Alikimbia ndani ya ile nyumba huku akiamini kuwa ataukuta wazi ule mlango aliokuwa anaufahamu ili aweze kutokea upande mwingine. Hofu ya kifo ilizidi kujenganaye urafiki, alijitutumua akaufikia mlango. Mungu wangu!! ulikuwa umefungwa kwa kutumia mnyororo. Hakuwahi kuiona hali kama hii hapo kabla. Huku nyuma akawa anamsikia yule mlinzi akitoa matusi yote huku kila mara akimaanisha kuwa iwe isiwe lazima amuue. Nakufa! Hatimaye Nguzu akakiri, lakini hakubaki kibwegebwege afe bila kupambana. Akausukuma mlango wa chumba cha Zubeda ambacho enzi zile alikuwa akiingia huku amebebwa mgongoni na koplo yule mwenye asili ya Tanga lakini akiishi zaidi Mwanza. Sasa aliingia katika chumba hiki huku akiwa anasota, jicho moja likiwa linaona kwa tabu huku lile jingine likiwa limefumba kabisa. Hamadi! mlango ulikuwa umezuiwa na kitu kwa ndani. Hofu ya kichwa chake kusambaratishwa na risasi ikamfanya Nguzu ajitupe mzima mzima na kufanikiwa kukisogeza kizingiti. Akajikuta ndani ya chumba. Sauti ya yule mlinzi nayo ikazidi kutapatapa ikitishia kuua. Chumba kilimkaribisha Nguzu katika hali ya utulivu, utulivu ule ulimtisha zaidi, akajaribu kufikiri ni wapi atajificha ili kumkwepa mshika bunduki. Uvunguni! hili lilikuwa wazo la kizembe lakini walau naye aliwaza. Akaanza kujitutumua aingie uvunguni, akaanza kujivuta kwa kutumia tumbo. Hakuzama sana kabla hajabamizwa ghafla na kitu kigumu katika paji la uso wake. Ile anajaribu kujiweka sawa akatandikwa teke kali usoni, akajikuta yungali nje ya ule uvungu huku akiwa nusu hai nusu mfu. Alikuwa amepiga magoti damu zikimvuja. Hazikupita sekunde nyingi kiumbe akauona mdomo wa bunduki ukitangulia kutoka katika ule uvungu. Nipokee baba nakufa mimi Nguzu! alijifanyia dua upesiupesi. Na hapo mlango ukasukumwa akamsikia yule mlinzi akiendelea kuropoka. Nguzu akatambua kuwa nyuma yake palikuwa na mtutu na pia mbele yake alijionea waziwazi. Swali likabaki juu ya nani atakayekuwa wa kwanza kufyatua ili auondoe uhai wake. Yule wa uvunguni akawa wa kwanza kufyatua. Risasi ikapenya jirani kabisa na sikio la Nguzu, ikafanya mlio kama wa nyuki mwenye hasira. Kisha kishindo kikafuatia, Nguzu akatua chini akiangukia tumbo. Kichwa chake kikawa jirani kabisa na ule mdomo wa bunduki iliyotokea uvunguni. Na hapo akaviringika na kutoa uvunguni mshambuliaji yule aliyemkosa Nguzu maksudi na kumlipua aliyekuwa nyuma yake. “Nilijua kuwa umekufa duniani, lakini si katika moyo wangu. Nikaamini tutakutana mbele ya haki, sijui kama ni mahali sahihi tulipokutana Martin, konstebo Martin Nguzu.” Sauti imara ya kike ilizungumza. Nguzu hakuhitaji macho yake katika hili, masikio pekee yalitosha kutambua kila kitu. Hatimaye kinywa kizito kikajitutumua na kuzungumza. “Koplo Zuu!” “Nihakikishie kuwa sitakiwi kukulipua kwa sababu u mmoja kati yao…” “Si..sijui kitu hapa. Usilipue koplo.” Alisihi Nguzu. Zubeda akamdaka na kumsimamisha. Nguzu akakosa muhimili akataka kuanguka, Zubeda akatega mgongo wake kama alivyokuwa akiutega zama zao za furaha. Nguzu akatua juu yake. Zubeda akaanza kupiga hatua kutafuta uelekeo, Nguzu akiwa anakoroma. Hali yake ilikuwa mbaya sana. Zubeda naye alikuwa anajitutumua, mguu wake mmoja ulikuwa haujaimarika.. Zubeda akiwa ndiye anayetegemewa alijaribu kufikiria juu ya uwepo wao pale ndani. Hapo kabla alikuwa amefanikiwa kuua na kisha kumpokonya bunduki mtu aliyewekwa kwa ajiri ya kumlinda asiweze kuleta bughudha yoyote. Walimpatiliza kwa sababu ya miguu yake kuwa na mushkeli. Dharau zao zikawafanya wapunguze ulinzi na kumwacha mbabe mmoja. Yakamtokea puani! Wakati Zubeda akiendelea kufikiria ni nini kilitokea hadi akabadilishiwa ulinzi ghafla, kutokea ule ulinzi aliowekewa na inspekta Kobo hadi ulinzi huu wa ajabuajabu. Akalishuhudia geti likifunguliwa na gari ikaingia huku askari watano waliovalia sare wakitangulia mbele. Balaa! Akajaribu kumshirikisha Nguzu aliyekuwa bado hoi. Nguzu hakuwa na la kuchangia. Askari yule imara ndani kwa ndani na legelege kwa umbo la nje alitoweka mpaka chooni. Huku aliweza kuona kila kitu kilivyokuwa kinaendelea nje. Alimtua Nguzu na kumsihi anywe maji yanayotoka katika bomba ili aweze walau kupata nguvu kiasi. Wakati huo akiendelea kuilazimisha akili yake ifanye kazi kwa kasi zaidi kuhusu tukio linalokuja mbele yao, alifahamu fika kuwa hakuna namna ya kuwa salama angali mle ndani kuna maiti mbili. Kwa namna yoyote yeye na Nguzu watayamalizia maisha yao gerezani. Maji yalikuwa msaada mkubwa sana kwa Martin Nguzu. Hayakumfanya kuwa imara sana lakini walau macho yake yaliweza kuona na aliweza kupumua vyema kwa sababu aliweza kuyaondoa mabonge ya damu yaliyounda uzio mbele ya pua zake na kumsababisha apumue kwa mdomo badala ya kutumia pua. “Martin, Martin!” Zubeda aliita kwa kunong’ona. Konstebo Martin akaupokea wito ule kwa kutulia akimsikiliza. “Askari wote wanatuzingira.” alimweleza kana kwamba Nguzu alikuwa anafahamu tayari juu ya uwepo wa ugeni ule.. “Akina nani? wako wapi?” Zubeda hakumjibu badala yake alimsaidia kunyanyuka na kisha akamwelekeza kila alichokuwa akikiona kwa nje. Walichoka! __________________
BAADA ya kukataa kata kata kubadili maelezo yake, amri ilitolewa ya kwenda kupekua nyumba ya inspekta Kobo ili iweze kubainika kama anayo mawasiliano yoyote aliyowahi kufanya na kikosi cha majambazi kilichoinyanyasa Shinyanga kwa wakati ule huku askari kadhaa wakiangushwa na kupoteza maisha. Msako wa kwanza haukuzaa matunda yoyote waliyoyatarajia. Walikata tamaa huku wakianza kuamini yawezekana kuwa inspekta Kobo aidha hajuani na lile kundi ama la ni mafia aliyefuzu mafunzo yote stahiki. Yaani hata umkate mguu akisema sijui ni sijui. Anameza maneno yake na kuingia nayo kaburini… Wakiwa wanakaribia kuondoka, askari mmoja akafika na kitu kipya. Akamtupia swali Kobo. “Hii nyumba unayoishi ni mali ya nani?” “Binafsi.” Alijibu kwa sauti iliyokata tamaa. “Umeijenga mwaka gani na umeanza kuishi humu lini?” “Huu ni mwaka wa kumi sasa naishi humu.” Jibu lile likamfanya askari yule afanye tabasamu hafifu kabla hajamtundika pagumu bila yeye kujua. “Umejenga nyumba nyingine tofauti na hii?” “Hapana!” “Mtu akifika hapa kukutafuta na asikupate je? ni wapi zaidi anaweza kukupata?” “Kazini kwangu.” Jibu la sasa likayafanya meno ya yule askari yaonekane kwa sababu ya kicheko kidogo. Na hapo akayabwaga makaratasi kadhaa mbele ya maaskari wenzake na Kobo akayashuhudia. Alikuwa ni mnyonge lakini haya yalimtia unyonge zaidi. Mikataba! Mikataba baina yake na mmiliki wa nyumba aliyokuwa akiishi hawara yake. Koplo Zubeda! Alitamani ardhi ifunguke atumbukie humo, alijiona waziwazi kuwa alikuwa anaelekea pabaya. Kwanza alidanganya kuwa hana makazi mengine zaidi ya hayo, pili mikataba yote aliiandikisha kwa majina yake na si ya Zubeda. Mkataba wa mwisho aliuandikisha miezi miwili tu iliyopita. Anakwepa vipi rungu la sheria? Watamuhesabu kama mnyang’anyi ambaye analo eneo la siri kwa ajiri ya kufanyia shughuli zake haramu. Inspekta Kobo akaumia zaidi kwa sababu alikuwa anakwenda kumweka Koplo Zubeda na maaskari aliowaweka kumlinda matatani. Wote hawa watahesabika kuwa ni chama kimoja cha kimafia na wataminywa kama alivyominywa yeye hadi kufikia hapo alipo. Akaunganisha meno yake kwa uchungu mkubwa. “Tunaenda moja kwa moja hadi katika nyumba hii. Ukithubutu kutudanganya utajutia uongo wako” Akachimbwa mkwara, akamtazama yule bwana kwa jicho kali, akajilaumu sana kwa sababu alikuwa na pingu, vinginevyo angefanya shambulizi kwake. Hakupendelea masuala ya kuchimbwa mkwara! Inspekta Kobo akawaelekeza nyumba ile inapopatikana, na hata asingewaelekeza bado kuna namba ya nyumba iliorodheshwa katika ile mikataba. Bila kusahau kiherehere cha mmiliki wa nyumba ile kuweka nambari yake sahihi kabisa ya simu ya mkononi na ile ya ofisi. Wakatoweka kuelekea nyumbani kwa Zubeda!
ZUBEDA hakuamini macho yake pindi alipomshuhudia inspekta Kobo akishushwa garini huku akiwa hajiwezi walau kutembea, nguo yake kwa mbali kabisa ilionekana kumpwaya, na ilikuwa imefubaa huku mabakamabaka yaliyoashiria kugandiana kwa damu yalionekana. Donge la uchungu likamkaba kooni, akajikuta yungali katika mfadhaiko mkubwa sana. Hakujua ni kwanini Kobo yu katika hali ile lakini kichwani aliitabiri kuwa haikuwa ya heri hata kidogo. “Martin…… Inspekta Kobo…” Alimwita kutoka pale alipokuwa ameinama bafuni. Martin akajikuta akisimama wima na hapo akawa amejitonesha mbavu zilizokuwa katika maumivu makali. Hakujikunja tena, akanyoosha shingo akakiona kile ambacho Zubeda alikuwa anakiona. Mpango huu ulikuwa maridhawa kabisa. “Hatuchomoki!” Zubeda alijikuta akitokwa na kauli ile ya kukata tamaa. Kauli ile haikuelea sana hewani kabla mlipuko mkubwa haujasikika na palepale askari wawili walio katika sare wakaanguka chini. Mmoja aliyekuwa amemshika Kobo ili aweze kutembea alimwachia na Kobo akatua chini mzimamzima. Akatulia! Hapoikazuka vita mpya, Nguzu na Zubeda wakashindwa kuelewa hii vita inahusisha pande ngapi. Wakati wanaamini kuwa ni pande mbili pekee sasa wanashangaa kuwa wao hawahusishwi na wakati huohuo vita inaendelea. Milio ya risasi za kuviziana ikaendelea huku askari wakipokea amri kalikali kutoka kwa kiongozi wao. Mambo yalikuwa magumu haswa! Asakari walikuwa wamepagawa, ni kama walikuwa hawajatarajia upinzani wa aina ile kutoka katika nyumba ile aliyokuwa akiishi Zubeda. _______ HAKUWA katika mavazi yake yaliyowatisha wengi pindi walipomuona, hakuwa katika kiti chake cha kuzunguka huku akipokea taarifa zilizopaswa kumfikia yeye na kisha kutoa maamuzi. Hakuwa katika nafasi yake ya kuwasiliana na raisi wa jamuhuri wa muungano. Alikuwa katika fulana yake pamoja na bukta laini, na alikuwa chumbani kwake. Vyeo vyote aliamua kuviweka kando. Alichoingia nacho pale chumbani ni thamani ya urafiki. Hakuwa na roho mbaya, na hilo alilitambua vyema bali alikuwa ni mtu anayesimamia haki na usawa. Ukimwona ana roho mbaya kwa sababu tu amekushinda kwa kuusema ukweli basi alikuwa tayari kuonekana hivyo. Aliijua mipaka yake vyema, hakuwa shabiki wa mateso wala vifo vya hovyohovyo. Alikuwa na weledi wa kutosha na hii haikuwashangaza wenzake baada ya kusikia jina lake likitajwa kuwa atakuwa mkuu wa majeshi ya polisi. Hata yeye hakushangaa, maana hakupewa cheo kile kwa bahati mbaya. Alistahili! Sasa alikuwa hayafikirii yote haya, alikuwa akimfikiria Kobo, ambaye alitokea kuwa rafiki yake sana mpaka mtafaruku ulivyokuja kuwaweka mbali kidogo kisha madaraka yakahakikisha wapo mbali kabisa. Kwa kufumba ama kufumbua macho IGP hakuacha kuiona sura ya Kobo ikiitaka huruma yake, akayakumbuka maneno ya Kobo juu ya mkewe ambaye yu katika kuzimia. “Nampenda sana mke wangu, ninapaswa kumuomba msamaha. Kama haitafaa mimi kubaki huru nakusihi rafiki yangu na mkuu wangu nifanyie upendeleo nisining’inie katika kitanzi kabla mke wangu hajazinduka.” Maneno haya yalimuumiza mno, akajaribu kuelekeza macho huku na kule ili asahau kuhusu Kobo lakini akajikuta akilitazama tukio la Kobo kujitoa muhanga na kumsukuma kando ili asipatwe na risasi iliyomkusudia. Akajikaza hisia zisimwendeshe lakini chozi likamsaliti. Akajikuta analia! Akayakumbuka maneno makali ya Kobo juu yake alipomwambia kuhusu pambazuko baya kupindukia. “Jitazame yawezekana pambazuko hili likakuandama wewe pindi utakapogundua kuwa sikuwa nyuma ya maovu haya.” IGP akasimama na kujifuta machozi pamoja na jasho lililoanza kumtoka. Akachukua simu yake na kumpigia msaidizi wake, ambaye pia alikuwa ni rafikii yake nje ya madaraka hayo. Akajaribu kumweleza kwa kifupi, akaeleweka na hatimaye wakachukua maamuzi ya kutuma watu watatu wa ziada katika tukio hili kutazama jinsi linavyokwenda. Walikuwa ni vijana wanaoaminika sana kiuwezo katika mapambano na pia katika umakini. Walau IGP aliweza kulala vyema baada ya kufanya hatua za mwisho kabisa za kutambua ikiwa Kobo anastahili jela ama la? Majira ya saa kumi jioni alishtuliwa na simu yake ya mkononi. Ni nambari aliyompatia msaidizi wake ili lolote litakalotokea waweze kupeana taarifa. Akaipokea upesi ile simu. “KIjana mmoja ameuwawa na mwingine amejeruhiwa begani.” Taarifa ile ilimtisha mno IGP. Alitambua kuwa jambo hili lina uzito lakini hakukadiria uzito ule kufikia huku kwa vijana ngangari kama wale kutetemeshwa. Akamsihi aongeze vijana na amri iwe moja tu, warejee na majibu. “Kiongozi kuna kitu kingine cha ziada.” Alisema kisha akamwacha IGP apumue kidogo. “Ile sauti uliyoniambia imesikika tena. ‘SHUSHA MBUYU KUNA NYOKA…” “Ni sauti ya nani?” Aliuliza kwa utulivu wa hali ya juu. “Aliyeisikia ni marehemu tayari. Lakini ni mmoja kati ya timu uliyoipa dhamana ya kwenda kuikagua nyumba ya Kobo.” “Na ni nani anayeshambulia ikiwa sio hao wapekuzi?” “Kuna safu nyingine kutoka katika kona za nyumba waliyoenda kuipekua. Kuna vita ya pande zaidi ya mbili mkuu.” “Ongeza vijana, fanya wanane. Wahakikishe wanaleta majibu.” “Sawa. Afande…” Alijibu na kukata simu. Hali ilikuwa mbaya tayari. _____ INSPEKTA KOBO alianguka mwili wote lakini hakuzimika macho yake. Alitulia kama aliyekwishapoteza uhai tayari. Aliendelea kutazama mashambulizi yalivyokuwa ya kutisha, kuna jambo alikuwa akilisoma. Wapinzani waliokuwa wamejificha katika kuta na dari walikuwa wakifanya mashambulizi ya akili sana huku hawa waliomsindikiza kukagua nyumba walikuwa wengi lakini bure kabisa. Walikuwa ni watu wanaotii sheria tu, wakiambiwa waachie risasi wanamimimina hovyo bila kumaanisha kudhuru! Akiwa palepale alizungusha macho yake huku na kule, na mara akatua katika madirisha ya nyumba ile. Akaona kama kivuli kikivuka upesi kwa kuinama chini. Kivuli kile alikuwa amekizoea sana, kama kisingekuwa chenyewe basi kingekuwa ni pacha ya kile alichokizoea. Zubeda! Inspekta akatokwa na jina lile huku akiwa bado amenasa pale chini, kulia kwake pakiwa na mwili wa askari aliyetokwa na uhai tayari. Kwa umakini wa hali ya juu akajisogeza mita kadhaa taratibu hadi akawa jirani kabisa na yule askari. Muda wote macho yake yaliwatazama wale washambuliaji waliojificha. Alishagundua tayari kuwa washambuliaji walikuwa wanaye mdunguaji wao na alijua vyema kazi ya kudungua maana alikuwa hakosi kila akishambulia. Faida kuu kwa Kobo ni kwamba huo ulikuwa moja kati ya mchezo wake uliompandisha cheo upesi na mchezo huohuo ulikuwa umemuingiza matatani. Shabaha! Kobo akainyakua silaha ya askari mfu pale chini. Akatabasamu baada ya kuitambua kuwa ni silaha aipendayo. Akatulia tena kama mfu huku akiangalia ni wapi anapoweza kuanza kushambulia. Alitambuwa wazi kuwa hawezi kushambulia kwa muda mrefu kabla nguvu hazijamwisha na pia kuchabangwa risasi na kupoteza maisha hivyo alihitaji akifanya shambulizi liwe kubwa na lenye maana kubwa. Akiwa bado katika kuliandaa shambulizi aliisikia simu ya upepo jirani na lile gari waliloingia nalo pale ikiunguruma maneno kadhaa ya kusihi. Hakuwa na uhakika kama msikilizaji wa ile simu aliamua tu asiijibu ama simu ilikuwa haina msikilizaji. “Shusha mbuyu kuna nyoka. Shusha sasa hivi ova!” Sauti ile ilitokea nyuma ya gari ambalo lilikuwa limeharibika vibaya kutokana na milipuko ya risasi. Mapigo ya moyo yakaongeza kasi, umakini ukatoweka akataka kukurupuka lakini alipokumbuka kuhusu ‘sniper’ aliyejificha mahali fulani aliendelea kutulia. Punde baada ya amri ile kutoka mita kadhaa hadi kuufikia ukuta mrefu kiasi ulioizunguka nyumba ile akasikia kishindo kikali, na kisha kikasikika kilio. Kuna mwanaume alikuwa amemezeshwa risasi tayari. Alikisia Huyu ni nani? alijiuliza kisha akajigeuza na kuilalia ile bunduki na kuendelea kubaki kana kwamba hana uhai. Alikuwa na uhakika wote kuwa alichokisikia katika simu ni sauti ileile iliyomkosesha shabaha na utulivu mjini Shinyanga na kisha kumletea majanga. Lakini safari hii ilisikika katika simu ya upepo. Hakufahamu fika ni nani mzungumzaji na alikuwa upande upi. Na punde baada ya kauli ile shambulizi likafanyika. Ni nani huyu? likabaki kuwa swali zito kwa Kobo. Tukio la Kobo kuichukua bunduki hadi kuilalia lilikuwa likifuatiliwa vyema na mdomo wa bunduki iliyokuwa tayari kukohoa risasi. Kobo hakujua, aliamini kuwa umakini wake ulikuwa wa kiwango cha juu zaidi. Baada ya shambulizi lile akazisikia hatua zikisogea kwa kujiamini kuja mahali alipokuwa. Akazivuta pumzi zake kisha akaanza kuzitoa nje taratibu kabisa. Akakisikia kiatu kigumu kikimkanyaga mguuni. “Huyu tayari… hamna kitu humu.” bwana aliyekuwa anamkanyaga akatoa jibu lile. “Chapa risasi kabisa kujihakikishia, hakawii kuwa hai akatuharibia.” Iliamrisha sauti nyingine kwa ukali iliyotawaliwa na madaraka. Kobo akaanza kuweweseka pale chini, alijilazimisha kuendelea kutulia kana kwamba ni mfu lakini kitendo cha kusikia kuwa anapaswa kuchapawa risasi ili kuhakikisha juu ya uzima ama kifo chake, hii ilikuwa ni sahihihi mbaya kabisa. Kobo hakumsikia yule aliyeamriwa akijibu kitu chochote, alishindwa kuelewa nini maana ya kimya kile. Hakutaka kucheza bahati nasibu ya ‘nitakufa ama wataniacha’ Akaamua kutumia nguvu zake za mwisho na njia pekee iliyosalia katika kujitetea. Akageuka upesi mtutu wa bunduki katika mikono yake tayari kwa kufyatua. Lakini hakuwa na mwendokasi wake wa zamani, Kobo huyu alikuwa mgonjwa, mzito, asiyeweza kuona vyema. Hakuwa Kobo anayetisha tena. Inspekta Kobo alikuwa amechelewa tayari……
“Nayaweza yote kwa Imani na jitihada”
Kama alivyoona ndivyo ilivyotokea, yule bwana akafyatua risasi. Kobo hakutarajia kama angepata nafasi ya kusikia risasi ile ikivuma pembezoni mwa sikio lake. Lakini hivyo ndivyo ilivyokuwa. Shabaha iliyumba malikiti. Kobo akapata muda wa kufumbua ili atazame kama ataweza kubiringita tena ili akwepe kwa mara nyingine tena. Akayahimiza macho yake kutazama…. Macho yakakutana na kitu cha kutisha, haikuwa risasi ya kawaida… hii ya sasa asingeweza kuikwepa asilani. Ilikuwa pana sana, hata kama angebiringita kwa kasi kuu bado asingeweza kujinasua. Inspekta Kobo akasalimu amri kwa kuitanguliza mikono yake kukabiliana na kitu kile kikubwa. Kilipomkaribia zaidi akayafumba macho yake. Kikatua juu yake, upepo ukakata! Kobo akarejea katika ulimwengu wa waliopoteza fahamu wasijue namna ya kuzitafuta.
__________
MIILI miwili ilikuwa imebebana bila kukusudia, yote isiyojiweza na bila budi kujibweteka mwili mmoja juu ya mwingine. Miili hii ilitazamwa kutokea mbali na vikundi viwili visivyokuwa na majina rasmi ya kuvitambulisha. Kukosa majina hakukumaanisha ule uwepo ni batili. “Unahisi bado anapumua yule?” Sauti dadisi ya Zubeda ilimuuliza Nguzu. “Uhakika pekee ninaoweza kuuthibitisha ni kwamba yule bazazi nimemfyatua barabara katika chembe ya moyo wake…” Alijibu huku akiwa bado na umakini wa hali ya juu.
Kundi la pili lilikuwa katika mfadhaiko, wakati likiamini kuwa limeunyakua ushindi na kilichosalia ni kuvikwa taji mara shambulizi linatoka wasipopajua na kumsambaratisha mwenzao aliyekuwa anangojewa waweze kuondoka eneo lile. Makundi yote mawili yalibaki katika tahadhari hakuna aliyekuwa tayari kwenda kuwatenganisha wawili wale waliolaliana. Mmoja akiwa ni mwili na mwenza wake akiwa ni mwili na roho pamoja na fahamu zilizokwenda likizo isiyokuwa na muda maalumu.
“Martin…. bila kujalisha kama mzee Kobo atainuka ama la, bila kujali kama tutabaki hai ama la. Naomba unisamehe mimi kwa yote yaliyotokea” Sauti tulivu ya Zubeda ilipenya katika masikio ya Martin Nguzu. Hakuitoa silaha yake katika lindo lake katika watu wale wawili waliolaliana mmoja akiwa ni Inspekta Kobo. “Unavyozungumzia kuwa hai ama la kana kwamba ni pipi ambayo unaweza ukaamua kuimung’unga ama la na isikupunguzie lolote. Uhai unayo thamani kubwa sana usiuongelee kijuu juu hivyo” Akamjibu kwa kumnanga. Koplo Zubeda akabaki kimya huku hatia ikimsulubu na kujiona yu mkosaji mkubwa sana. Hakukumbuka kujiuliza ni lipi basi kosa lake?
KUTOKEA upande wa pili, tumaini la ghafla katika pori la mfadhaiko liliibuka, aliyeshuhudia akawasihi na wenzake nao waone. “Oya…yupo hai aisee… namuona anatikisika” Alisema na kuwavuta wenzake kutazama kwa makini, kweli mwenzao alikuwa anajitikisa. Ile hulka ya wanadamu waonapo jambo wasilolitarajia hujikuta wakiisahau misingi yao yote na kujikuta katika mkumbo wa liwalo na liwe, haikuwa upande huu badala yake ilikuwa upande wa pili. Zubeda anayesukumwa na hatia ya kupendwa kwa dhati kisha kuja kumsaliti Inspekta Kobo na hatimaye kumweka katika kitanzi kile ilikuwa inamponza. Konstebo Nguzu naye alihitaji sana kujua ni nini hatma ya Kobo pamoja na makundi yanayoshambulia yana nia gani. Hakuamini hata kidogo kuwa yawezekana kabisa kuwa eti chanzo ni yeye tu hadi haya yote yanatokea. Kama ni yeye kwanini wahukumiwe hata wasiokuwa watu wa ukoo wake? Wakati akiwaza na kuwazua akaikumbuka sura tulivu ya Kobo iliyojaa hekima na busara siku aliyomuita na kumsihi aachane na Zubeda wake! Huruma kuu ikamvamia. Hali hizi ziliwafanya wasisimke walipoona ile miili pale chini ikijitikisa. Nguzu akamuhakikishia Zubeda kuwa aliyejitikisa ni Kobo si yule hayawani aliyejaribu kumfyatua. Zubeda hakuamini upesi, Nguzu akajitoa muhanga kwenda kumwokoa Kobo, huku nyuma shughuli ya kulinda usalama wake akaiacha mikononi mwa Zubeda. “Kiumbe yeyote atakayejaribu kunidhuru, fyatua usifikirie mara mbilimbili. Ule muda utakaotumia kufikiri nd’o muda ambao macho yako yatakishuhudia kifo changu. Hiki cha sasa kitakuwa kifo taslimu.” Nguzu alimweleza Zubeda. Kisha akamkumbatia kwa nguvu sana, akamtazama machoni na kuzungumza kwa sauti tulivu. “Naitwa Martin Ngengekuzenza Nguzu. Jina langu lina maana kubwa kulikoni uhai wangu… kwa lolote lile nikianguka naomba nifukiwe kwa jina hilo.” Akamaliza na kumbusu Zubeda katika papi za midomo yake. Akaondoka akimwacha Zubeda akipambana machozi yasiyazibe macho yake. Alihisi lile ni busu na kumbatizi la mwisho kutoka kwa kijana yule machachari. Umakini ukarejea baada ya Konstebo Nguzu kuingia ukumbi wa vita, Zubeda askari mkakamavu akaishikilia vyema silaha yake, akavuta pumzi na kushusha akajiandaa kukabili kwa lolote kama alivyoelekezwa. Umbali wa kutoka mlangoni hadi ulipokuwa mwili wa Kobo haukuwa mita nyingi sana, lakini ilikuwa ni zaidi ya kilometa kadhaa kwa Nguzu kutokana na kutokuwa na uhakika ni wapi anaweza kuwepo adui awezaye kuitoa roho yake mara moja. Akapiga hatua huku uoga ukishamiri katika moyo wake, alijitia ujasiri kwa maneno aliyoelezwa na mzee Majenga kuwa hatakufa kwa sababu mzimu wa babu yake unaishi naye mpaka atakapoitimiza azma yake. Hatua takribani kama tano kabla hajaufikia ule mzoga juu ya mwili. Kilio kikubwa kikasikika kutokea katika dirisha ambalo alibaki Zubeda kama mlinzi wake wakati akielekea kumkomboa Kobo. Upesi Nguzu akaiweka vyema silaha yake lakini hakujua ni wapi afyatue kabla hajaisikia sauti kali nyuma yake ikimwamuru kutulia kama alivyo. Nguzu alikuwa mikononi mwa watu wabaya! Nini kimejiri kwa Zubeda?? alibaki akijiuliza wakati huu ambapo alimuhitaji sana mwanamama yule ili kuweza kumkomboa. Kimya! hapakuwa na shambulizi lolote la kumkomboa. “Taratibu kabisa angusha silaha yako chini, bila kuinama walau sentimita moja” Sauti ikachimba mkwara zaidi. Nguzu hakusubiri onyo la pili akaiachia bastola yake itue chini naye abaki na Mungu pekee kama mlinzi wake wa haja. “Wananiua wapuuzi!” alijisemea “Sogea mbele kwa hatua za taratibu kabisa. Bila shaka sina haja ya kukumbusha kuwa ukifanya upuuzi wowote ule hautakumbuka chanzo cha kifo chako….” sauti ile tulivu inayojiamini iloiendelea kumwongoza Nguzu. Nguzu akatii! Alikuwa kama hayawani ama zuzu asiyejua ‘a’ wala ‘ba’. Kifo pekee nd’o kitu ambacho aliwaza kwa wakati huo. “Shusha mbuyu mwamba….” Sauti tofauti na ile iliyokuwa inamwongoza ilizungumza kwa kukaripia na kuonyesha uharaka. Mbuyu? Nguzu akajiuliza asijue ni kitu gani kimemaanishwa katika kauli ile tata. Hakuwa tayari kuuwawa namna ile bila kuimaliza kazi yake, lakini pia hakuwa walau na akili ya ziada ya kujiokoa. Utajiokoa vipi ungali jirani na mdomo wa bunduki usiokuwa na huruma ukifunguliwa? “Mpigie tajiri…” Sauti iliyokuwa ya kwanza kumtetemesha Nguzu ilizungumza. Baada ya sekunde chache, mazungumzo yalisikika upande uliosikika zaidi ulikuwa upande wa kwanza huku aliyepigiwa simu akisikika kwa mbali sana. Simu haikukatwa iliachwa hewani na hapo Nguzu akarushiwa swali. “Unaitwa nani? na upo hapa kwa shughuli gani?” Nguzu akafikiria kuhusu kuongopa kuhusu jina lake, lakini akachagua kucheza karata nyingine. “Naitwa Martin, nipo hapa kwa ….” “Martin nani?” Swali lilitupwa, hadi sasa alikuwa hajaziona nyuso za maadui zake. “Martin Nguzu!” Akamalizia. “Acha upuuzi, hatuna muda wa kupoteza,” alijibu kwa hasira kisha akarejea katika simu yake, “Tajiri… huyu mjinga anasema anaitwa Martin Nguzu. Hana faida kwetu…” “Naitwa Martin, Konstebo Martin Nguzu. Sijawahi kufa lakini nakijua kifo. Jaribuni kuniua mara ya pili huenda nikakijua kifo” Nguzu akapigilia hofu na utata mwingine. Alikuwa ameupata ujasiri wa hali ya juu sana. Wale mabwana wawili hawakuelewa ni kipi anachojiamini angali hana silaha na wakiamua ni sekunde moja tu wanammaliza. Mazungumzo katika simu yakaendelea huku akibaini sasa kuwa mpiga simu alimuhitaji akiwa hai. Lakini hilo si pekee lililomjengea ujasiri. Kuna jambo la ziada ambalo lilihesabika kwa sekunde kadhaa kabla halijabadilika na kuwa kindumbwendumbwe! Ilikuwa ghafla sana, Nguzu akaruka upande wa kushoto bila wale watu kumtarajia kama atafanya hivyo. Palepale milipuko miwili ya risasi ikasikika. Mayowe ya hofu na maumivu yakasikika.
“Usithubutu walau kujitikisa, maana nitafyatua jicho lako badala ya bega!” Sauti iliyoongea kwa tabu kabisa ilitoa maelekezo. Bwana aliyekuwa anazungumza na simu akabaki kutulia tuli asiamini kilichokuwa kinatokea. Inspekta Kobo kutoka katika usingizi wa kifo alikuwa amechota medali zake za ushujaa palepale chini. Nguzu pekee ndiye aliyeutambua uhai wake, na aliamua kumuamini walipozungumza kwa ishara za macho. Ishara ambazo ni wao pekee wangeweza kuelewana kwa sababu wamepitia mafunzo ya kijeshi. Nguzu akajitokeza na kuiwahi ile silaha ambayo ilimponyoka yule aliyesambaratishwa na Kobo kwa shabaha moja iliyojikita katika kifua chake moja kwa moja.
“Nahitaji ujibu swali uliloniuliza hapo kabla. Ni nini unafanya hapa na unafanya kwa manufaa ya nani? Niko tofauti kidogo na wewe… sichimbi mkwara huwa natenda. Ukichelewa kunijibu nakuvunja miguu…..” Nguzu akiwa anatazama na bwana yule aliyepagawa alizungumza. Yule bwana akapagawa asiamini anaonana ana kwa ana na Kontebo Martin Nguzu ambaye wanaamini kuwa walimteketeza ndani ya nyumba. Hakuwa na budi kujieleza vyema kabisa. Nguzu akashtuka jina la muhusika wa haya lilipotajwa. Lilikuwa jina refu lakini ubini wa ‘KAZEZE’ ukamwacha katika namna ya kupigwa butwaa. Jina ambalo lipo katika kitabu cha babu yake, mzee Florian Ngengekuzenza Nguzu, jina lililosheheni chuki, visasi na unyanyasaji. Jina hili linasikika tena katika maisha yake. “Ina maana Joseph Kazeze alikiacha kisasi chake kirithiwe na watoto wake ama?” Nguzu alijikuta akiuliza kwa sauti, lakini asipate mtu sahihi wa kumjibu. “Zu…Zubeda yupo wapi” Inspekta Kobo akiwa ameketi chini aliuliza kwa sauti ya chini sana, bila shaka alikuwa katika maumivu bado. Swali lile likamshtua sana Nguzu, alikuwa amesahau kabisa kuwa kuna mlipuko ulikuwa umesikika kabla hajadhibitiwa na mabwana wale waliodai kuwa walikuwa wameagizwa na mkuu wa majeshi mstaafu, Jeremiah Stamford Kazeze. Kukosa kule utulivu kukaondoka na umakini wake. Yule mtumwa akamvamia Nguzu upesi na teke kali ambalo liliiondoa silaha yake mkononi. Akarusha teke la pili ambalo lilielekea kupasua fuvu la kichwa cha Nguzu. Nguzu akawahi kuinama. Wakati anajiandaa kumkabili akajikuta akikabiliana na madonge ya damu. Kobo alikuwa amejipima tena umakini wake kama upo sawa. “Usingemuua Inspekta…” “Angekuua wewe…. amepitia mafunzo ambayo wewe hujawahi hata kuyaona kwenye luninga…. hata hivyo sijamuua labda aamue kufa mwenyewe tu…” Hatimaye Inspekta alisimama kwa tabu, wakati huo Nguzu alikuwa ametangulia kwenda kuitambua hali ya afya ya Zubeda ambaye bila shaka alishambuliwa. Hakika alikuwa amepoteza fahamu, risasi ilikuwa imemkwangua begani na kumtupa ukutani. Halikuwa jeraha kubwa sana, hata alivyoshtuliwa kwa kumwagiwa maji ilikuwa rahisi kwake kusimama na kutambua kila kilichokuwa kinaendelea. Kigiza kilikuwa kinaanza kuingia wakati watatu hawa wakiwa wamepata fursa ya kuwa mbali na ile nyumba na walikuwa wameweza kujadili kwa ufupi sana juu ya kisa hiki. Hakuna aliyegusia suala la mapenzi ya kuchangia, walitazama zaidi uhai na amani yao. Inspekta akashauri wafanye mchakato wa kuwasiliana na IGP waweze kuupata msaada wa upesi sana dhidi ya Kazeze IGP mstaafu waliyeamini fika kuwa yupo nyuma ya yote haya. Wakati wao wanafikiria namna ya kuwasiliana na IGP…. ni wakati huohuo IGP mstaafu Kazeze alikuwa yu njiani kuelekea nyumbani kwa IGP.
JOTORIDI lilikuwa la wastani lakini hiyo ilikuwa kwa wale wenye amani pekee. Mashaka ya mwandishi wa habari, Juma Kihwele ‘kimbelembele’ yalisababisha mwili wake utokwe jasho mara zote zlizokuwa akifikiria ni mbinu gani za ziada atazitumia kuweza kuipata tena amani yake na uhuru. Hapo kabla shuleni alikuwa nguli wa kusaliti wenzake linapokuja suala la mgomo. Hakuwa mtu anayeweza kupigana, kila penye shari yeye alijiweka kando na alikuwa shahidi wa kwanza ulipohitajika ushahidi wa nani ameanzisha ugomvi. Hali hii ilifanya walimu wampende lakini alichukiwa na wanafunzi. Mbaya zaidi darasani alikuwa anaongoza, chukia usichukie nd’o ilibaki hivyo. Baadhi ya wanafunzi ambao walijikuta matatani kutokana na ushahidi wa Juma Kihwele waliishia kumwekea viapo ambavyo kwa macho ya kibinadamu ilionekana wazi kuwa ni maneno ya mkosaji. Walimweleza kuwa ipo siku atajutia uoga wake, kiherehere chake na hapohapo akili zake za darasani hazitamwokoa. Aliishia kucheka na kuendelea kuhsika namba za juu darasani. Baada ya miaka mingi kupita Juma amejichanganya na kujiingiza katika ‘dili’ alilolichukulia kuwa ni pesa nyepesi, sasa yu mikononi mwa watu ambao ili uone jino lake moja ni pale tu atakapokuwaanapiga mwayo. Kinyume na hapo zilikuwa ni ndita na lugha za ukali kila mara. Juma Kihwele analazimishwa aelezee ana ubini gani na Martin Nguzu ambaye aliendelea kutambulika kama hayati Konstebo Martin Nguzu. Juma alikuwa ametema kila alichokuwa anakitambua lakini bado hakuonekana kama amesema lolote, hakuwa amepigwa sana, vibao kadhaa na mateke yasiyodhamiria kuvunja lakini kipigo hicho kwa Juma alijihisi anapaswa kuorodheshwa katika kitabu cha rekodi za dunia kama mwanadamu aliyewahi kupigwa kupita wote duniani na bado anapumua. Juma hakujua maana halisi ya kipigo. Maelezo ya Juma Kihwele yakalileta mezani jina la Inspekta Kobo na Koplo Zubeda. Juma akamtaja Zubeda kuwa anajihusisha kimapenzi na Inspekta Kobo na hapohapo alikuwa anajihusisha na Konstebo Nguzu. Jibu hili likaongeza umakini kwa waliotumwa kumuhoji, majibu yakatumwa na kufika sehemu husika. IGP Mstaafu Jeremia Kazeze akayatazama majina yale kama maadui zake, yeyote aliye karibu na Nguzu kwake alikuwa ni adui asiyefaa kuishi. Sumu aliyomezeshwa na babu yake na kisha baba yake ilikuwa imekolea na ilikuwa muda wa kuitema. lakini urithi si kwa magonjwa tu, hata nidhamu ya akili unaweza ukarithi. Hayati Florian Ngengekuzenza Nguzu wakati anamsimulia Majenga kwa ajili ya kuandika kumbukumbu ya kizazi chake alimuhesabu Joseph kazeze (babu wa Jeremiah) kama mshamba anayetumia cheo chake kijinga. Ngengekuzenza alijihesabu kama mshindi kwa vita vyote dhidi ya Joseph Kazeze, na kweli alimtandika ipasavyo kwa mbinu chache tu ambazo kwa Joseph Kazeze zilikuwa ngeni na zilizosheheni suluba kubwa. Sasa wawili hawa walikuwa wamepumzika tayari katika nyumba zao za milele. Ngengekuzenza Nguzu akijitoa uhai kwa kujinyonga huku Joseph Kazeze akikamilisha safari yake kwa shinikizo la damu. Shinikizo lililosababishwa na mapigo kutoka kwa Ngengekuzenza Nguzu. Chuki haikuishi katika moyo wa Konstebo Martin Nguzu na hakujua hapo kabla kuwa kuna vita mbayo haikuwahi kukamilika, lakini Jeremiah Kazeze yeye alibaki na chuki kuu. Akafuata misingi aliyorithishwa ikiwa pamoja na mbinu za ‘kikuda’za kukabiliana na adui zake. Akavishwa cheo cha IGP na kukitumia kusulubu wowote aliodhani ni maadui. Akamaliza muda wake huku akiwa hajakutana na jina Nguzu. Akiwa hana cheo jina lile linamjia ghafla mezani kwake. Vita mpya inaanza, vita mbayo haikuonekana kama inatisha. Jeremia Kazeze anatuliza akili yake na kufikiria ni kifo gani kitamfaa zaidi Konstebo Martin Nguzu, kifo ambacho kitakuwa ni kisasi sahihi kwa yale yaliyomtokea babu yake miaka ya nyuma. Hatimaye anamchagulia adhabu ya kuchomwa moto dunia kisha akakutane na mwingine katika safari yake nje ya dunia. Mpango mdogo unasukwa kwa akili ileile ndogo, Nguzu anachomewa ndani ya nyumba yake. Wakati wa utafiti wa kuzifuatilia nyendo za konstebo Nguzu. Wanapata jambo jipya, mahusiano kati ya Nguzu, Zubeda na Inspekta Kobo. Jeremiah anachekelea na kuamua kumuuzia kesi ile Inspekta Kobo. Oparesheni inafanyika na jalada linakaribia kufungwa. Mwishoni mwa mchezo anatokea Juma Kimbelembele akijaribu kuandika makala juu ya yaliyotokea. Anakuwa amenunua kesi pasi na kujua kuwa ni kesi kubwa. Upande wa Jeremia Kazeze ukaamini fika kuwa yule bwana kuna uwezekano anafahamu ni wao wanahusika katika kuiteketeza nyumba ya Nguzu. Upesi akaamuru kundi jingine linalomtii limfuatilie kwa ukaribu kila hatua ambayo atakuwa anapita. Ni katika kufuatilia huku yanazuka mengine makubwa. Sasa Juma Kimbelembele yu katika mikono yao.
Anatamani walau kupambana lakini uwezo huo hana. Amelia kama mtoto lakini haijatosha kulainisha sauti za watu wale wanaozungumza kama wauguzi wa wodi ya vichaa walioshindikana. Kila mara wanafoka!
Ilikuwa siku nyingine tena katika mazingira yaleyale, lakini sura ngeni ilimjia. Ilikuwa ni ngeni kwa pale ndani na sura hii ilimpa tumaini jipya kwa sababu alikuwa akiifahamu vyema. Alikuwa ni mkuu wa jeshi la polisi mstaafu. Jeremia Kazeze. Juma Kihwele akajihesabia kuwa amekutana hatimaye na mtu ambaye atamuelewa na kumwokoa. Hakujua kuwa amekutana na anayewatuma wale aliowaona kama mashetani yanayoishi. “Haujambo?” Jeremiah aliuliza kifedhuli. “Sija… shkamoo… sijambo..” alijiumauma katika kujibu. “Martin Nguzu alikufa ama hakufa? na kama hakufa nataka kujua ni nani aliyehusika katika kumwokoa…” Sauti kavu ya Jeremia ilihoji. “Sijui lolote muheshimi…” kabla hajamaliza kumjaza cheo alipokea kofi kali katika shingo yake. Yowe la hofu likamponyoka. “Nahitaji jibu tofauti na sijui.” “Muheshimiwa mi naapa haki ya…” Hata hii kauli pia haikumalizika kabla hajapokea kofi jingine, hili la sasa liliuchana mdomo wake. “Umeona biblia ama msaafu humu ndani? Sihitaji viapo nahitaji majibu…” Juma Kimbelembele sasa alikuwa amepatikana. Alijaribu kutuliza akili yake na kuchagua jibu la kutoa lakini alihofia kuwa linaweza lisiwe na ushawishi.. Lakini ni heri kuzungumza kuliko kuwa kimya dhidi ya mtu yule aliyekuwa mbele yake. “Nyumba iliungua mkuu, sikumuona akitoka hai. Alikufa na wanahabari waliandika…” “Wanahabari ni akina nani hadi unawataja kama utetezi wa hayo unayosema?” “ Kimya! hakuwa na la kujibu. “Una uhakika alikufa?” “Nyumba iliteketea…” alijibu kinyonge lakini unyonge wake haukumzuia Jeremia kumbutua tena, safari hii kwa kutumia mguu wake. Juma akajikaza hakupiga kelele kubwa licha ya kuumia. Jeremia Kazeze akatoa picha kadhaa akamtupia Juma Kihwele akawa anatazama nazo. “Unafahamu hicho ni nini?” “Ndio mkuu, nyumba ya hayati Nguzu baada ya kuteketea” “Ooh! Kila mtu anajua nyumba iliteketea, sijafunga safari kutoka huko mbali kuja kupata uthibitisho kuwa nyumba iliungua….. najua kusoma na ninaona pia… nahitaji kujua wewe na Nguzu ni washirika katika ngazi ipi?” “Wallah! naapa sina ushirika wowote na marehemu…” “Unavyosema marehemu kama vile uliuzika mwili wake… sikiliza wewe mtoto. Kama unayaficha unayojua kuhusu Nguzu, hautajificha kuizika miili ya wapendwa wako. Kwa mkeo nitajitahidi ubaki uso pekee ili usije kugoma kuuzika mwili ukisema sio mkeo, ila hutapata hamu ya kukiuona kiwiliwili chake, na ukijitia shujaa kukiona utakuwa unakiota ndotoni kila siku na itakuwa ndoto ya kutisha…” Akaweka kituo na kutoka nje. Juma alipojaribu kuzungumza akaishia kujikaza asijikojolee zaidi wakati tayari keshajimwagia kojo muda mrefu tu.
JEREMIA KAZEZE mwenye akili kiwango cha babu yake aliona njia pekee ni kuwahi kwa IGP kwa ajili ya kujisafisha na kuyaweka sawa mazingira ikiwa tu jambo lolote litaharibika zaidi. Aliziona dalili za kuangushwa kama alivyoangushwa babu yake zikimnyemelea…. Ilikuwa yapata majira ya saa mbili usiku. Haukuwa utaratibu wa Kazeze kumtembelea mara kwa mara IGP, ni yeye aliyependa kutembelewa kwa sababu ya kumzidi kiumri na urithi wa tabia ya kupenda sifa za kijinga alioupata kwa babu yake. Siku hii ilikuwa tofauti zaidi, tena saa mbili usiku. Mbaya zaidi hakupiga simu kutoa taarifa. Alipokelewa bila mashaka, taarifa za walinzi zikapitishwa ndani na ruhusa ikatolewa. Kazeze akaingia kuonana na IGP.
Tofauti na nyakati nyingine walizowahi kuonana, hii ilikuwa tofauti sana. Kila mmoja alikuwa katika ulimwengu wake. Licha ya kujilazimisha kuonenekana kuwa wapo sawa ila nafsini hali ilikuwa wazi. Mgeni alianza kuelezea juu ya ujio wake usiku ule, akaanza kuulizia hatma ya Inspekta Kobo na sakata la kujihusisha na majambazi sugu mkoani Shinyanga. IGP akamweleza juu juu kuwa hadi wakati huo Kobo alikuwa amekataa kukiri kuwa aliikosa shabaha ile maksudi na anaapa kuwa hajihusishi na kundi lile. “Nawe umeamini?” Aliuliza kwa mshangao.. IGP akaduwazwa na swali lile, japokuwa haikuwa mara ya kwanza kukerwa na maswali ya yule aliyemtangulia. Kwanini ananichimba huyu?! Alijiuliza kisha akatabasamu na kujibu, “vijana wangu wanaendelea kumuhoji. Watanipatia majibu ninawaamini sana…” “Na unafahamu lolote kuhusu mauaji ya askari wetu mtiifu, konstebo Nguzu aliyechomewa ndani ya nyumba?” “Naam! na nilifika eneo la tukio, vipi kuna jipya?” “Inspekta Kobo anahusika kumteketeza, inasemekana Nguzu anajua kuhusu Inspekta Kobo kujihusisha na kundi lile, na alikuwa anakaribia kuvujisha siri..” “Unasema Nguzu anajua kama yupo hai mkuu….” “Aam! Nguzu alikuwa anajua…” Akarekebisha huku akijaribu kujichekesha. “Upo ushahidi wowote wa kumweka hatiani Kobo?” “Kuna mwandishi wa habari alishuhudia kila kitu, kuanzia muda wa kuwasili hadi muda wa tukio?” “Aisee! aliarifiwa na nani hadi kuweza kuzijua nyendo za askari makini kama Kobo!” Alijibu IGP. Kitendo cga Kobo kuitwa askari makini kikamkwaza Jeremia Kazeze. “Unamuita makini na kwa maksudi kabisa ameacha kumsambaratisha jambazi sugu, jana watu nane wameuwawa huko Shinyanga, wawili kati ya hao ni askari wetu na pasi na shaka muhusika ni huyohuyo aliyeachwa apumue na Kobo. Leo hii unaendelea kumvesha nishani ya umakini? Are you damn serious brother?” Alilalama. “Nimvishe jina gani ambalo litakuridhisha na kuyanyoosha mazungumzo yetu?” IGP akahoji, Jeremia akatambua kuwa kile ni kijembe. hakujibu. “Anyway, nina taarifa njema sana zinaweza kusaidia katika kuboresha hizo tuhuma” IGP akazungumza kisha akaiacha kauli ile hewani ili imuingie vyema bwana Jeremia. Jeremia akahoji kwa kimuhemuhe. “Ni taarifa gani mkuu…” “Nimepigiwa simu na mtu anayedai kuwa yeye ni konstebo Martin Nguzu. Na tayari nimeagiza vijana wangu wafuatilie alipo na kumtia nguvuni, bila shaka atatusaidia sana katika kukamilisha upelelezi… tukimuunganisha na huyo mwanahabari wako, sioni Kobo anachomokea wapi….” Alimalizia huku akiwa anamtazama kwa macho ya kuibia Askari mwenzake. Moyo wa Jeremia ulipiga kwa nguvu sana, hakuamini kile alichokuwa anakisikia, alijiona kile kikombe anachomwandalia Kobo kikigeukia upande wake ndani yake kikiwa na uji wa mto ambao anapaswa kuunywa bila kupooza. Mbaya zaidi kile kikombe kilikuwa cha bati. Akatamani kutoa kauli yoyote lakini kauli yenyewe ikagoma kuunganika. Koo lilikuwa limekauka. “Nisaidie maji ya kunywa!” Jeremia akamwomba IGP. IGP akatabasamu kisha akaitazama meza, Jeremia alikua ana kikombe cha maji mbele yake. Ajabu alikuwa hakioni! “Kwani Nguzu yupo hai au?” Akatokwa na swali la kizembe. “Kitu pekee ninachofahamu ni kwamba nyumba yake iliteketezwa, kuhusu uhai nitakuongopea,Vipi kwani?” IGP akazidi kuzungumza kwa utulivu kabisa na hapohapo akiifurahia hali ya kupagawa ya Jeremia Kazeze. “Kwani Nguzu yupo hai au?” Akatokwa na swali la kizembe. “Kitu pekee ninachofahamu ni kwamba nyumba yake iliteketezwa, kuhusu uhai nitakuongopea,Vipi kwani?” IGP akazidi kuzungumza kwa utulivu kabisa na hapohapo akiifurahia hali ya kupagawa ya Jeremia Kazeze. Na hapo IGP akashuhudia tembe za jasho zikiumuka katika mgongo wa pua ya Jeremia. Uoga! Anaogopa nini sasa? Ina maana jamaa ana ‘kamisheni’ katika kutekeleza mauaji ya Nguzu? Kwanini mtu aliyewahi kuwa na cheo cha juu kama huyu ahusike katika mpango mdogo kama ule. Haya yalipita katika kichwa cha IGP kwa kasi kubwa. Kwa upande wa IGP mstaafu Jeremia Kazeze alikuwa anajaribu kuutuliza muhimili wake wa kufikiri, alijiona yu katika kupagawa tayari na alihisi IGP ameanza kumgundua kuwa anapagawa. Akajivika ukakamavu huku akijizuia asitazamane ana kwa ana na IGP kwani aliogopa kupepesda macho yake. “Nadhani sasa mimi niende” Jeremia alizungtumza kwa kuridhika. “Mkuu, kwa hiyo huyu Nguzu tunamfanyaje ikiwa kweli anapatikana angali hai wakati sote tunajua amepoteza maisha?” IGP akamtundika swali lililojaa maswali ndani yake. “Nani? Nguzu…aah!” Jeremia akatetereka. Kichwani mwake akajiona yu katika kumi na nane za IGP na sasa alikuwa anajaribu kucheza naye atakavyo na ikiwa ataghafirika na kumkwatua basi uamuzi ulikuwa ni ‘penati. “Akikamatwa inabidi hapo sheria tu ichukue mkondo wake… no way out! Lazima Nguzu aadabishwe. Period!” Jeremia akajikaza kishupavu akajibu kama mtu aliyeshtuliwa toka usingizini akaulizwa moja jumlisha moja akajibu nne kwa sauti ya juu, akiamini yu sahihi IGP akaponyokwa na tabasamu jepesi kabla hajamdhihirishia Jeremia kuwa mojawapo kati ya watu wanaoitwa mabwege basi yeye kama si kiongozi wao basi ni msaidizi. “Sheria ya kumshtaki kwa kuchomewa nyumba ama tutamuadabisha katika ‘engo’ ipi afande” IGP akatupa bomu jingine dogo lenye mlipuko mkali. Jeremia akajiona jinsi anavyodhihirisha kuwa yungali fala katika ubora wake. Na kupitia maswali yale ni namna ya kuitwa fala bila tusi hilo kutajwa. Ilimuuma! Hakutaka kuendelea kulithibitisha hilo mbele ya bwana yule ambaye alikuwa mdogo kwake kimri. “Kwa hiyo unataka akikamatwa aachwe tu bila hata kusaidia upelelezi?” Akauliza kwa ghadhabu. “Hapana mkuu, yule kukamatwa muhimu tena muhimu sana….” IGP akajibu kichangamfu kisha akamalizia, “Ishu hapa ni tunamshtaki kwa lipi? Kudanganya uma kuwa amekufa kumbe hajafa? kujichomea ndani ya nyumba au tunamshtaki kwa kuwa hai?” Jeremia akagundua anachezewa ngoma iitwayo shere. Ngoma wanayochezewa wajinga bila kujua wanadhihakiwa. Akaaga na kuondoka kwa mara nyingine.
______
SAFARI ya kulifikia gari lake ilikuwa ndefu sana, Jeremiah alijiona katika akili yake anatembea kama kitoto kinachojifunza kutembea, kikijiona kinao uwezo wa kumkimbia mama yake, angali mama anapunguza mwendo maksudi ili kichukue ushindi kitoto kile. Miguu yake ilikuwa kama inayopambana kutangulia kupiga hatua, wa kulia unataka utangulie na wa kushoto unahitaji nafasi hiyo. Ikafikia hatua akili yake ikawqa haiwazi kitu kingine zaidi ya kuwaza namna ya kuiamuru miguu yake ipeane heshima stahiki japo kwa dakika hizo chache tu za kulifikia gari lake. Miguu ikatii! Akalifikia gari. Walinzi wakamkabidhi silaha yake ambayo waliichukua kabla hajaingia ndani kwenda kuonana na IGP, akaziona saluti alizopigiwa zikiwa ni kama ishara inayochukiwa na vijana wengi wafanyiwapo. Macho yake hayakuona saluti ya heshima bali aliwaona vijana kadhaa wakiwa wanamzomea na kumwonyeshea ishara ya kidole cha katikatika katika mpangilio wa vidole kiganjani. Hasira zikazidi kumchemka, akapanda garini. Akatoweka huku akikiri kuwqa katika maisha yake yote, hii ilikuwa mara yake ya kwanza kujikuta amewekwa mtu kati na siweze kujing’atua. Aliendesha kwa mwendo wa wastani, hakuelekea nyumbani kwake na hakujali kuhusu hilo na hakufikiria walau kumpa taarifa mkewe. Alizoea kumwendesha kama alivyokuwa na tabia ya kuendesha askari waliokuwa chini yake wakati wa cheo chake. Kitu kama mwiba mdogo kikaichoma akili yake wakati akiendelea kuendesha gari, akawakumbuka haohao askari wenye vyeo vya chini walivyo na hatari wakipewa amri. Akajiona jinsi watakavyomfunga pingu huku mara kwa mara wakimfokea badala ya kumwelekeza nini cha kufanya. Wakati huo akiitwa mtuhumiwa. Na baadaye akaziona kero za kulishwa chakula kibovu, kuhesabiwa kwa kupigwa bila sababu pamoja na kulala sehemu moja na chawa kunguni na kadhalika pindi atakapokuwa mahabusu rasmi. Mapigo yake ya moyo yakapiga kwa nguvu zaidi, hakutaka haya yamtokee. Lakini katika yote haya hakusita kutabasamu na kisha kutoa sauti ya chini. “Ukoo wa Nguzu ni kiboko!” Pongezi hizi zikamkera na kujikuta akipiga honi bila sababu zozote za msingi. Safari yake ikaishia nyumbani kwa Veto! Kiongozi wa kikundi cha vijana waliokuwa wakimtii, wakati na baada ya utawala wake. Muunganiko huu ni pamoja na wale waliopewa vyema hovyohovyo bila kuwa na sifa, ama ambao watoto wao waliingizwa jeshini kwa kauli moja tu ya aliyekuwa IGP. Jeremia Kazeze! Wangemlipa nini zaidi ya kuwa vibaraka, wenzetu waliwaita ‘puppets’. Hakumpigia simu Veto hapo kabla, tabia ya ujivuni ilimtawala na kujiona kuwa anaweza kwenda kwa IGP bila kupiga simu, ya nini kumpigia simu Veto ambaye nd’o kwanza anapambana aweze kuupata u’inspekta? Hakupiga! Alifika bila kujali kuwa ule ni usiku sana, akagonga hodi mara kadhaa, hatimaye akaufungua mlango mkewe ambaye bila shaka alikuwa amelala sebuleni kwa kupitiwa na usingizi ama akimngoja mwenzi wake. “Shkamoo shem!” Mwanadada yule alitoa salamu. “Vipi yupo huyu?” Jeremia akaipuuza ile salamu akahoji yaliyomleta. “Hajarudi hadi muda huu lakini niliwasiliana naye akanieleza kuwa iwe isiwe atakuja nyumbani shem” alijibu kwa nidhamu, bila shaka alikuwa akijua nguvu ya mtu aliyekuwa mbele yake. “Alisema atakuja saa ngapi na wakati anakupigia alikuwa ameanza kuja ama?” “Hakusema lolote shemeji… ila alini…” “Sawa.. nitampigia simu.” Akamkatisha. “Labda ujaribu wewe, maana nimejaribu sana hapatikani, hadi nimeanza kupata mawazo. vipi kwani mbona sielewi.” “Ambacho huelewi ni kipi na ni wewe umeongea naye kwenye simu?” Akang’aka. Mke wa Veto akawa mpole!
Wakabaki kutazamana kama kuku, kuku mmoja akiwa amechoka mwingine akiwa muoga sana. Ukimya uliotanda kati yao ukasababisha chochote chenye kutoa sauti kiweze kusikika. Jeremia akasikia mchakacho ndani ya nyumba. “Upo na nani ndani?” Alihoji kama anayesuta “Niko.. mwe.. aah! nipo na binamu yangu..” “Binamu yako yupi?” Akahoji tena sasa akiwa amemkazia macho makali. tayari alihisi kudanganywa. Na hapo ikasikika sauti ya kike yenye kila dalili za kuongea kwa shida ya kukabiliwa na usingizi mkali sana. “Nani kwani… eeh!” Kabla sauti ile haijamalizika, Jeremia Kazeze ambaye alikuwa amerithi tabia ya kukurupuka kutoka kwa babu yake alimsukuma mke wa Veto na kuingia naye ndani kwa fujo. Bila kutarajia akaitoa bastola yake asijue ni kwa nini alikuwa ameamua kufanya vile. Wazo la kuwa yule mwanamke anamwongopea na Veto alikuwa yu ndani lilimfikisha hapo, akaamini kuwa Veto amenunuliwa tayari na upande mwingine. Hivyo ilikuwa ni vita tayari. Vita dhidi ya kijana wake mtiifu. Giza lilikuwa limekikabili chumba, alivyoingia Jeremia mara ghafla taa ikawashwa, akababaika na kutamani angekuwa na macho memngi aweze kuona kila upande. Mbele yake alikuwa Veto aliye hoi kabisa, kushoto alikuwa anatazamana na Inspekta Kobo ambaye alikuwa anaonyesha hali ya uchovu sana lakini anayetabasamu. Wakati anajifikiria ni kipi anapaswa kusema akayaona macho makali ya Veto yakimulika kumaanisha kuna kitu nyuma yake, upesi akageuka na silaha yake. Na pale akakutana na teke kali lililopiga silaha yake ikatua chini, kisha mpiga teke yule akafanya ujuzi wa ziada akazunguka na mguu uleule kisha akambamiza Jeremia katika kichwa chake. Jeremia kazeze aliyesahau masuala ya mazoezi na kuruhusu mwili wake kuwa legevu wenye manyama uzembe alikuwa amepatikana. Lakini alijaribu naye kurusha ngumi ya hovyo, ikamkosa aliyekusudia, akayumba na kuliacha tumbo lake lililochomoza kitambi kama walivyo askari wengi wa Tanzania. Tumbo lile likapokea tiba mbadala ya kuzuia kitambi. Mateke mawili ya upesiupesi yakadunda katika tumbo lile. Jeremia akatapika maji aliyokunywa nyumbani kwa IGP. Kinywa kile kikawa kimefanya kosa la jinai kutema maji katika zulia lililokuwa na thamani ya juu, mpigaji akatokwa na ngumi nyoofu lakini ya kushtukiza ikakibamiza kile kinywa, kikaacha kutema maji kikatapika damu nzito. Jeremia Kazeze akaanguka chini na kutulia magoti. “Naitwa Martin, konstebo Martin Nguzu! Sikijui cheo kingine zaidi ya ukonstebo nilionao” Utambulisho ukatoka hatimaye. Huku anayejitambulisha akiwa amekunja ngumi za mikono yote miwili na mwili wake ukitetemeka sana. Jeremia akaamini hiyo ilikuwa siku yake ya kushuhudia muujiza, anazungumza na maiti. “Sikurithi cheo chochote kutoka kwa babu yangu nisiyermjua kwa sura wala sauti, nilirithi hiki unachokiona mbele yako mheshimiwa, sikurithi kupigiwa saluti wala kupiga saluti kinyonge. Sikurithi roho ya kuua bila sababu na sikurithi udhaifu wa kufa kizembe. Ninaishi katika misingi ya Florian Ngengekuzenza Nguzu, unaishi katika misingi ya Joseph Kazeze. Babu yangu alishinda, aliniachia huu ushindi na katu hautakuja kupotea kirahisi, mliweza kuuteketeza mwili wangu lakini sio rahisi kuupoteza mzimu wa babu yangu. Unapambana na mzimu, kama upo tayari unaweza kusimama tena ujaribu kuurushia ngumi mzimu!” Alifoka kwa ghadhabu zote Martin Nguzu. Jeremia Kazeze akabeua damu. Angesema nini zaidi ya kuendelea kutema tu damu.
Baada ya Nguzu kumaliza aliyotaka kusema, akasimama Inspekta Kobo. Pamoja na udhaifu wake uleule, hakuna aliyetarajia kuwa angeweza kuwa imara tena mpaka ambapo angepata tiba ya kutosha. Naye akambana Jeremia Kazeze kadri alivyoweza, na hapo akataja alipo muandishi Juma Kihwele na familia yake, akalazimishwa kupiga simu na watu wale waachiwe huru mara moja. Jeremia hakuamini hata kidogo kuwa alikuwa anachezeshwa ngoma ya namna ile na vijana wale. Hakuwa na la kufanya akatii. Maelezo ya ziada yakatolewa, simu ikapigwa kwa IGP kuhusu ujio wa Juma Kihwele katika himaya yake. IGP wakati anapigiwa simu ile alikuwa tayari katika sare zake na alijisikia faraja kwenda kuimaliza vita ile angali ana nyota tele katika bega lake.
Vita ilikuwa inaelekea ukingoni kabisa, Konstebo Martin Nguzu akaingia katika chumba kimojawapo na kumkuta Koplo Zubeda akiwa katika usingizi mzito. Akamwinamia na kuzungumza naye maneno kadhaa ambayo aliamini fika kuwa hataweza kuyasikia. Kisha akambusu katika paji lake la uso. Akaliendea dirisha kubwa la kioo, akaruka na kutoweka akipishana na gari kadhaa za polisi zikiwa zinalikaribia eneo lile.
Wazo la kwanza lililomuondoa ni Zubeda. Asingeweza kuendelkea kuwa naye katika mahusiano mwanamke ambaye ni usingizi wa inspekta Kobo, pia asingekuwa na amani kumwona binti yule katika mahusiano mengine hata kama ataachana na Inspektra. Pili ni upindishaji wa sheria katika ardhi aliyokuwa ameikanyaga, masuala ya kubebana kwa sababu ya kujulikana aliyafahamu wazi kabisa. Akakihesabu cheo nchake cha ukonstebo, cheo cha Zubeda ukoplo na Inspekta Kobo. Akajaribu kufananisha na kile cha Jeremiah aliyewahi kuwa mkuu wa majershi ya polisi IGP. Akaamini fika kuwa lolote linaweza kutokea, aidha kuzimishwa hapohapo na kisha taarifa kubadilishwa kuwa waliuwawa wakikabiliana na polisi, ama la kubadilishiwa kesi kabisa na kuonekana walimteka Jeremia na kumtesa kesi ambayo katu isingeweza kuwaacha bila hatia. Miaka thelathini ingewahusu pamoja na mateso makali.
Konstebo Martin Nguzu, akayaweka mapenzi kando, akautazama usalama wake. Kubwa zaidi alikiri kuwa hakuwa yeye yule konstebo mnyonge, huyu alikuwa imara na alikuwa na kazi kubwa zaidi za kufanya kuliko kuendelea kuwapigia saluti watu kama Jeremia Kazeze. Konstebo Martin Nguzu akazidi kukata mitaa jijini Dar es salaam, hatimaye akaipata nyumba ya kulala wageni. Akamtazama muhudumu aliyekuwa ana mawenge ya usingizi. Akaulizia bei ya chumba akatajiwa, akalipia na kushangaa anapewa funguo bila kusajili jina lake. “Hee! unaniruhusu tu naingia kama unanijua vile.” “Ah! bro we kalale bwana…” “Hapana lazima niandikishe la si hivyo nilale bure.” akatilia mkazo. Huku akiwa amekereka yule binti wa mapokezi akampatia daftari huku akihangaika kuipata kalamu. Hatimaye Nguzu akaishika vyema kalamu, akautazama mstari wa kuandika jina, akatokwa na tabasamu la ushindi kisha akaandika kwa herufi kubwa kiasi cha kuingilia hadi mstari wa chini. “KONSTEBO MARTIN NGUZU” Hakujaza sehemu nyingine zilizosalia. Akamkabidhi daftari akiwa amelifunika na kuamini fika kuwa kwa jinsi alivyoelemewa na usingizi hataweza kusoma, na hata akisoma ataambulia patupu. Alivyokifikia chumba, akaitoa bunduki yake. Akatoa risasi na kisha akauvamia ukuta na kuandika kwa kukwangua rangi. Huku akiifurahia hali hii, alijiona hana namna nyingine ya kufanya sherehe zaidi ya hii. Akauchubua vyema hadi ukasomea alivyotaka. “NAITWA MARTIN, KONSTEBO MARTIN NGUZU” Akapiga saluti na kisha akalala vyema. Alfajiri akatoweka. Akaelekea popote watu wanapoelekea lakini mwisho wake akiutambua yeye mwenyewe.
Simulizi : Wanawake Ni Wauaji ?! Sehemu Ya Kwanza (1)
“Kwanza kabisa napenda kumshukuru mungu kwa kunipa pumzi na afya njema hadi leo hii niko hai japo niko tofauti sana na awali hadi wasionijua wakiniona hii leo wanadhani nilizaliwa hivi… La hasha! Ila leo nitawaambia ukweli wa yote yaliyonisibu na yanayowasibu wanaume wengi kila siku ktk dunia hii ya leo. Nakumbuka babu aliwahi kunambia na kunisihi niwe makini sana na wanaake pindi nitapokuwa mkubwa na alinifundisha niwasome na niwaelewe wanaake ni watu wa aina gani, lakini sikuwahi kuamini maneno yake hadi yalipokuja kunisibu haya na ndipo nilipokumbuka na kuelewa maneno ya babu.
Aaaaagh! Wanawake ni mama zetu na ni pambo la dunia na ndio maana mungu aliwaumba ili watufariji na watulee lakini ukweli bado unabaki kuwa wanawake ni watu hatari sana kwetu wanaume. Hebu tukumbuke hata kwenye hadithi za watu wa kale kwenye vitabu vya dini tukianzia mwanzo kabisa wa dunia enzi za Adam na Hawa/Eva. Adam alitii kila kitu ktk mamlaka aliyopewa na mungu lakini mwishoe anakuja kumkosea mungu kwa kutenda dhambi aliyoponzwa na mkewe Hawa baada ya kushawishiwa na Shetani, Eeeh, amini usiamini shetani ni vigumu sana kumuingia mwanaume hivyo anamtumia mwanamke kama alivyomtumia Hawa kwenda kumlubuni mwanaume kama alivyolubuniwa Adam na kujikuta mwanaume anaumia kwaajili ya upendo na kumuamini sana mwanamke pasi na kuelewa kiundani udhaifu mkubwa wa mwanake mwenyewe.
Tuachane na Adam, tukumbuke Samsoni mtu mwenye nguvu sana aliyewapa tabu sana Wafilisti enzi hizo lakini mwishoe anakuja kukamatwa na kupata mateso makali baada ya kulubuniwa na Delila aliyetumiwa na Wafirist kubaini siri za nguvu za Samsoni. Eee, Samsoni nae akaponzwa kwaajili ya mwanamke na si yeye wala Adam tu tukumbuke hata mtu wa kwanza kufa alikuwa ni mwanaume na sababu ya kifo chake kilitokana na Mwanamke!! EE ni wanaume wengi mno wameponzeka kwaajili ya wanaake na mmoja wao ni mimi na ndio maana leo hii nasema WANAAKE NI WAUAJI. Najua wengi mtanielewa vibaya hususani wanaake lakini naomba msizime t.v zenu ili mnielewe vizuri kwanini hasa nimekazania kusema Wanaake ni Wauaji…. Hii ni asili iliyoanza toka kwa mwanamke wa kwanza kabisa kuumbwa na bado ipo na itakuwepo na itawaumiza wanaume wengi sana wasiokuwa makini na ndio maana hata mungu hakuwahi kushusha nabii wa Kike. Wanaake ni wadhaifu wasiokubali udhaifu wao na ndio maana nawaita Wauaji..
Achilia mbali vitabu vya dini tukija kwenye maisha yetu ya kila siku lini ulishawahi kusikia Mwanaume katupa katoto kachanga? Naamini kama mimba wangekuwa wanabeba wanaume usingesikia neno Kutoa Mimba. Hivi ushawahi kujiuliza mwanamke ana moyo wa namna gani?!! au Unadanganywa na maumbile yake na sauti raini unajisahau na unaacha kuwa makini nae? hivi hujui kwamba Simba Dume ana muungurumo mkubwa sana lakini Jike ndie jasiri wa kuua..? huo ni mfano tu lakini nataka unielewe na uwe makini kwanini nasema WANAAKE NI WAUAJI…””””” ” Ilikuwa ni sauti kutoka kwenye luninga kutoka kwa bwana mmoja mlemavu wa macho na miguu akiongea ktk kipindi cha YA WALIMWENGU LIVE kilichokuwa kinarushwa kupitia kituo cha BEKATV kila siku za Jumaapili asubuhi na marudio yake Jumaamosi jioni.
Nilikaa kwenye sofa huku nikiwa nimeshikilia kikombe cha chai, kwa umakini mkubwa macho na masikio niliyaelekezea kwenye TV huku nikichukua rimoti na kuzidisha sauti kwa lengo la kumsikia yakinifu yule bwana kwani mada yake ilinistua na kunigusa sana hali iliyochochea niwe na shauku kubwa ya kusikiliza hiyo story yake ili nielewe vizuri kwanini anasema wanaake wote ni wauaji….!!!??
Nilitulia na kujikuta nashindwa hata kupeleka chai mdomoni na kubaki nimeshikilia kikombe nikimsikiliza kwa makini pindi yule bwana alipokuwa anazungumza ambapo aliendelea kwa kusema….
“Nakumbuka miaka kumi iliyopita nilikuwa na maisha mazuri kabisa nay a furaha mimi na mke wangu kipenzi baada ya kufunga ndoa, ki ukweli nilimpenda sana mke wangu nae alionesha mapenzi hasa na kunisahaulisha maumivu niliyopata kutoka kwa mke wangu wa kwanza tuliyeachana muda mfupi tuu baada ya kukaa kwenye ndoa kwa miaka mitatu na kuanza visa vilivyosababisha nimuache aishi maisha aliyotaka yeye na ndipo baada ya miezi kadhaa nilipompata huyu mwanamke wangu mwengine aliyeonesha kuwa na vigezo vyote nilivyohitaji na mwaka mmoja tu katika mahisiano yetu tuliamua kufunga ndoa kabisa. Kiukweli mke wangu nilijivunia uzuri aliokuwa nao upole wake na tabia ya kupenda ibada na mara nyingi alinibadilisha kwa maneno matamu na kunisihi niache kunywa pombe na kweli ilifika kipindi niliacha pombe na taratiibu nilipunguza kabisa kuvuta sigara kutoka pakiti moja kwa siku hadi ikafika mahali siku nzima nikavuta sigara mbili tu, hali iliyofanya hadi walionijua kunishangaa na kumsifu sana mke wangu na ndipo name nilizidisha moyo wa kumpenda na kumpa uhuru wa kila kitu kwani nilimuamini mno…”
Alinyamaza Yule bwana kasha aliendelea…….
“Kila nilichofanya nilihakikisha lazima mke wangu ajue na nilisikiliza sana na kufata ushauli wake kuliko mtu mwengine akisema nisifanye kitu frani name nilitii akisema nifanye name nilitii hiyo yote nilifanya nikiamini namjenga na kumuonesha kiasi gani namthimini bila kujua kua kuna ugonjwa m baya nilikuwa naufuga.. Awali sikuona tofauti yoyote wala kuhisi kama kuna kitu nakosea zaidi nilianza kusikia minong’ono kutoka kwa majirani na baadhi ya ndugu zangu kuwa napelekeshwa na nimetawaliwa na mwanamke, kiukweli nilichukizwa na habari zile na kugombana na baadhi ya ndugu zangu waliomsema vibaya mke wangu nikiamini fika wanataka watugombanishe na wananionea wivu kwa kupata mke wa namna ile kwani maisha yetu yalizidi kunyooka siku hadi siku. Aaaaaagh.. kuna muda huwa nahisi kama ndoto vilee kwani sikujua kabisa kumbe kuna bomu nalitengeneza mwenyewe ambapo baadae litapolipuka litaniletea madhala makubwa na kama si kuniua basi litanipa ulemavu wa kudumu kama ilivyotokea baadae…. Aaaagh, mke wangu!!!…”
Alivyozidi kuongea Yule bwana ndivyo nami nilivyozidi kutulia kumsikiliza kwa makini huku nikibofya bofya rimoti kuongeza sauti mara kwa mara utafikiri nina ubovu wa masikio. Nilimuangalia kwa jicho la shauku ya kujua yaliyomsibu kwani alitia huruma pia alionesha kuna mazito yalimkumba hadi kusababishiwa ulemavu ule. Lakini kabla sijafaidi vizuri hadithi ya Yule bwana ghafra umeme ulikatika na kila kitu kuzimika.
“Aaaagh, kum*m*ake Tanesco bwana kama maboya!!!” Nilinyanyuka kwa hasira na kuzima Switch ya TV na kuwasha switch ya taa ili umeme utaporudi tuu taa inijulishe mapema.
Wakati huo ile chai ilikuwa ya baridi kabisaa na sikuambulia kunywa hata chembe ndipo nilipoenda kuimwaga na kurudisha kikombe na muda huo nilikumbuka kuwa nimeacha simu ndani kwenye chaji na isitoshe tulikuwa na miadi ya kukutana na mchumbaangu Mariam au Mamu kama nilivyozoea kumwitaga. Nilikuta simu ikiwa na missed call tisa msg nne na nilipofungua zote zilikuwa toka kwa mamu. Nilizisoma zile msg ambapo mojawapo iliandikwa hivi…
MBONA HUPOKEI SIMU WALA HUJIBU MSG ZANGU? KAMA UPO NA MALAYA WAKO SI UNAMBIE TU NISIJE..!!
“hahaa Wanaake bwana..” Nilijisemea moyoni na kuingia sehemu ya ujumbe kui reply ile msg lakini kabla sijabonyeza Send mlango uligongwa na nilipoenda kufungua alikuwa ni Mamu kipenzi change ambapo nilifurahi kumuona nilimkumbatia na kum busu japo alionesha wazi kuwa kanuna kisha aliingia na kunipita bila kusema chochote na kwenda kukaa Sebureni. Nilibaini kuwa amenuna kutokana na kutopokea simu yake na nilijua sasa nina wajibu wa kum bembeleza nimuweke sawa . “Unakunywa nini bebi..”
“Sitaki kunywa chochote niache..”
Jiubu lake lilizidi kunihakikishia kuwa nina kibarua ka kubembeleza mtu mzima sasa lakini kabla sijafanya hayo yote mara taa ya sebureni iliwaka na ndipo nilipokumbuka kuwasha TV kwanza niendelee na kile kipindi huku moyoni nikiwa na shauku na mamu nae amsikie Yule bwana juu ya story yake na kuwatuhumu kuwa Wanaake wote ni Wauaji.
Mada ya Yule bwana hasa kauli yake ya kuwa wanaake wote ni wauaji ilimchukiza sana Mamu na kuamua kuzima TV kwa hasira.
“Aaag! Wee vipi?” “Vipi nini!!?” “Si uache tuangalie sasa unazimia nini..!!” “Hivi Hussein kwa akili zako timamu unaona hiki kitu anachokizungumza huyu mpuuzi ni sahihi!!” “Kitu gani..” “Kusema wanaake ni wauaji..” “..Mh! hapo kumjaji moja kwa moja itakuwa ngumu, sasa nitamjaji vipi wakati hata story yenyewe sijaisikia!! anaweza kuwa sahihi au si sahihi inategemea na point zake mwenyewe.” ..”Hivi nyinyi wanaume mpoje!!!”
Aliwaka Mamu kwa sauti ya juu na kusimama huku akinitazama kwa hasira kutokana na majibu yangu.
“Hivi mnatuchukuliaje sisi wanaake eeh!!?” “Kivipi baby.. mbona tunawakiana sasa.” “Sio Nawakaa.. ila nakwambia ukweli acha kuwa na mitazamo ya kijinga au ndio kashakulisha ujinga huyo mpuuzi mwenzio…! Kwa hiyo na mimi muuaji si ndio, au unanionaje!!” “Hapana baby sijamaanisha hivyo..” “kumbe unanionaje..” “Unaweza kuwa muuaji au si muuaji inategemea tuu..” “Aahaa.. kwa hiyo hadi mamaako aliyekuzaa Muuaji, dada zako wauaji, shangazi zakoo si ndio..!” “Sasa mamu hayo matusi..” “Matusi nini.. si Wanaake ni Wauaji!!! We vipi.. Hebu nipishe huko nisije nikakuua buree..”
Alichukua mkoba wake pale kwenye sofa kwa hasira Mamu alielekea mlango wa kutokea ulipo na kutoka huku akiubamiza kwa nguvu ule mlango. “Aaagh!! Sasa huo mlango umekukosea nini..”
Nilibaki nimetahayuri pale kwenye kiti huku nikiwa nimechanganyikiwa kwa jinsi Mamu alivyonibadilikia huku nikijilaumu upande mwengine kwa kusababisha mpenzi wangu kuwa na hasira mara tatu zaidi alivyoingia.
Niliuendea mlango na kuokota funguo zilizodoka pindi ulipobamizwa na Mamu kasha nilirudi na kujitupa kwenye sofa huku akili yangu ikiwa haipo sawa niliiwasha tena TV safari hii nikiwa sina mzuka kabisa wa kuangalia kile kipindi ambacho ndio kilikuwa kinaishia lakini kuna maneno ya mwishoni ya Yule bwana yalipenya vizuri masikioni mwangu na kukistua kichwa change kidogo pindi aliposema…..
“Najua wanaake wengi wataobahatika kunisikiliza na kunitazama watanichukia na kuona nimewadhalilisha na kuwatusi. Na mimi sitoshangaa wala kuogopa hilo kwa sababu najua kuwa wanaake tayari wana ulemavu wa asili ambao mungu aliwaumba nao kwa dhumuni la kuwa wasaidizi na wafariji kwa wanaume tu. Mwanaume hajaumbwa kwaajili ya mwanamke ila mwanamke aliumbwa kwaajili ya mwanaume na ndio maana tunaambiwa kuwa mwanamke ametoka ubavuni kwa mwanaume. Lakini udhaifu wao ndio unafanya tuone mpaka leo hii wanaake wakitaka kushindana na wanaume nah ii kutokana na kuwa mwanamke ni rafiki mkubwa wa shetani anayetumiwa ktk kuiharibu dunia na hata baadhi ya wasomi wa dini wanatwambia wanaake wengi sana wataingia motoni.
Mungu ameweka mifano mingi sana ya wazi kuwakumbusha wanaake kuwa mwanaume ni kiongozi na anapaswa kunyenyekewa na mwanamke japo kwa akili mbovu za wanaake wengi wanaona kufanya hivyo ni ujinga kwani hata wao wanaweza kufanya wanayofanya wanaake.. ha ha haa yaani hata mifano ya wanyama hawaioni!! Wazee waliosema Wanaake mwalimu wao kipofu walikuwa na maana kubwa sana ambayo sasa wengi hawaizingatii.
Cha mwisho nakukumbusha wewe mwanaume unayenitazama hususani wewe uliegombana na Mkeo au mpenzi wako hivi punde chanzo kikiwa hiki kipindi na hii mada yangu… Nataka ujue kwamba uko katika wakati mgumu sana na huyo mwanamke.. tena nakusihi uwe makini nae sana.. Ukipuuza siku moja yanaweza kukukuta kama yaliyonikuta mimi hata kama hautakuwa na ulemavu wa viungo kama mimi. Kuweni makini na wanaake wanaume wenzangu..”
Nilishtuka kwa maneno yale na kuhisi kama naambiwa mimi moja kwa moja.
Muda mfupi baada ya kile kipindi kuisha nikiwa nimeketi huku kichwa changu kikiwa na mawazo kibao nikijiuliza mwenyewe nishike yapi niache yapi huku nikikumbuka na kauli za Mchumbaangu kipenzi. Nikiwa nimeduwaa nikifikiria jinsi ya kusorve tatizo langu ili nimueke sawa mamu mara msg iliingia kwenye simu yangu, Nilipoichukua kuifungua alikuwa ni Mariam.
Msg ilisomeka hivi… “”” Hussen nashukuru sana kwa matusi yako ya kuwa eti mi ni muuaji haina shida ila kama ulikuwa hunitaki na ulikuwa unatafutia sababu ungenambia mapema tuu kuliko kupoteza muda wangu.. Nashukuru sana nakutakia Maisha Mema..”””
Sio siri msg ya Mamu ilinichanganya sana kwani sikutaraji kabisa kama kile kipindi kinaweza kusababisha yote yale, Niliisoma mara mbili mbili ile msg na kuamua kumpigia mpenzi wangu Mamu lakini simu yake iliita bila kupokelewa. Sikuchoka niliendelea kupiga lakini bado haikupokelewa na mara nyengine ilikatwa na mwishoe nikawa nasikia sauti ya huduma kwa wateja wakinambia kuwa namba ninayopiga inatumika.
Niliachana na simu na kuingia bafuni kuoga niliporejea chumbani nikatupia pamba kama kawaida yangu. Eeeh.. kupendeza ilikuwa kawaida kwangu kutokana na jinsi nilivyojua kupangilia mavazi hadi watu wengi kitaani wakawa wananita bitozi, si unajua tena uswahilini kila chocho unayokata ukiwa umejitupia sana watu macho kodooo.
Nilirejea sebureni baada ya kujiridhisha kwa nguo nilizovaa siku hiyo na kabla sijatoka nilipiga tena simu ya Mamu lakini jibu lilikuwa lile lile kwamba namba ninayopiga ipo bize.
Sikuwa na jinsi ilibidi nitoke na kuchukua bodaboda kuelekea kwa kina Mariam nikiwa na nia na madhumuni ya kwenda kuomba msamaha ili mapenzi yetu yaendelee kwani nilimpenda sana na nilijua kama nisingeenda muda huo basi ingebidi nisubiri hadi wiki ijayo kwani nisingepata nafasi kutokana na kuwa kazini muda mwingi na kuchelewa kurejea.
Baada ya mwendo wa dakika kumi tulifika maeneo ya kina mam na kumlipa ujira wake yule dogo aliyenileta nami moja kwa moja nikaanza kuongoza njia ya kwa kina Mamu huku nikiwazia jinsi ya kuanza.
“Karibu baba.” Nilikaribishwa na mamaake niliyemkuta akiwa nje amekaa kwenye kolido ya nyumba yao akiwa anasukwa na mwanae mwengine wa kike mdogoake Mamu. “Asante mama shkamoo” “Marahaba baba za huko” “Safi tu mama sijui nyinyi” “Sisi ka unavyotuona tunamshukuru mungu enhee mbona hivyo baba kwema!” “hehee.. Kwema tu mama” Nilijibalaguza kwa kujichekesha baada ya kuhisi huenda mama Mamu kashastukia mchezo nikiwazia kwa kurudi Mariam mapema vile na ujio wangu pia lakini nilikuja kushangaa baada ya mama Mamu kuniuliza swali ambalo nilikuta nashindwa kulielewa na kuuliza tena badala ya kujibu mithili ya mtu mwenye matatizo ya masikio.
“Unasemaje mama!!?” “Nimekuuliza mwenzio yuko wapi..? maana alituaga anakuja huko kwako muda mrefu tu aliondoka hapa sasa umenishangaza nawewe umekuja muda huu ukiwa pekeako, ndio maana nimekuuliza kwema?”
Nilijikuta nashusha pumzi kwanza mara baada ya kusikia na kubaini kuwa Mamu hajafika kwao tangia muda ule alipoondoka kwangu.
“Vipi baba mbona huongei..! unatutisha wenzako” Ilikuwa ni sauti iliyonizindua kwenye dimbwi la mawazo ya ghafra nilipokuwa nafikiria alipoenda Mamu muda wote ule hajafika kwao. Niliogopa kimtindo kwa kuhisi kama kitampata kitu kibaya huko basi namimi nitahusika kwa kiasi kikubwa pia nilivyoelewa kuwa Mamu atakuwa kachanganyikiwa sana na anaweza kujifanyia hata kitu kibaya mwenyewe kutokana na kujua kiasi gani ananipenda na mara nyingi hakutaka nimuudhi kabisa.
“Hah, ni hivi mama kweli Mamu alikuja lakini hakukaa sana akadai kuwa kuna vitu amesahau so, nimsubiri kuwa anarudi nyumbani kuchukua hivyo vitu na atakuja tena, sasa nimekaa na nilipoona anachelewa sana ndipo nikaamua kuja huku kwa lengo la kumfata yeye. Sasa ulivyoniuliza ndio mana nimeshangaa ina maana hujamuona huku kurudi..!” “Hee!! We babaa eeh ina maana awe karudi afu mi nikudanganye! Mwanangu hajarudi na si mzurulaji hebu usitufiche baba nambie umemuacha wapi mwenzio au nini kimetokea huko kwenu..?” “Hakuna chochote mama” “sasa mbona hueleweki eleweki simu unayo kwanini hukumpigia kujua alipo hadi unakuja kumuulizia” “Okeeey, samahani mama nimekumbuka alinambia kabla ya kuja huku kuna sehemu kwa shogaake angepitia kule mwenge. Tena ngoja nimfate huko kabisa nahisi hajatoka” Ilinibidi kudanganya na kuongea maneno ya matumaini hasa mala baada ya kumuona yule mama akizidi kubadilika.
Kiukweli nilitambua fika kuwa Mariam anapendwa sana na mamaake muda mrefu tuu na ukizingatia yule mama alikuwa na watoto wawili tu wote wa kike na babayao alifariki muda mrefu sana hivyo hata jinsi alivyowalea wanae walikuwa si watu wa kutokatoka ovyo wala kuzurula hivyo kitendo cha kusikia mwanae hayupo kwangu kilianza kumpa presha kidogo nami nikatumia akili ya ziada kumpunguza na kumkwepa kwa kujidai naenda Mwenge kwa huyo shogaake Mamu.
“Baba naomba utavyorejea uje na mwanangu tafadhali, kwanza kisheria na kidini bado hujakabidhiwa. Asilale hukoo” Aliongea yule mama kipindi hiko nilikuwa nimesimama na kuaga kisha niliondoka kuelekea stendi ya daladala nikiwa na mawazo tele mara mbili na niliyokuja nayo.
* * * * *
Safari yangu ilinipeleka mpaka pande za fukwe za coco na lengo halikuwa kuogelea wala kufanya mazoezi bali ni kupunguza angalau robo mawazo yaliyoandama kichwani mwangu siku hiyo na kufikiria ni heri tusingekutana tu siku hiyo na Mamu kwani mipango yote ya kufurahi pamoja wikiendi ile iliyeyuka ghafra kama machoci ya samaki kwenye maji.
Niliwazia nitamwambia nini yule mama endapo Mariam asingeonekana siku hiyo kabisa. Niliwaza pia ina maana Mamu anaweza akajifanyia tukio hata la kunywa sumu kwa kajiugomvi kale tuu! Na kama akifanya hivyo nini kitanikuta baadae..! si ndio itakuwa basi tena.
Niliwaza mambo mengi sana na kuchukua tena simu kupiga nmba ya Mamu lakini bado jibu likawa lilelile ndipo nilipogundua sasa Mamu atakuwa kanireject. Nilijisonyea moyoni na kuemtumia msg nikimsihi na kumuomba popote alipo basi arudi nyumbani haraka wanamtafuta. Japo nilituma zaidi ya meseji tano lakini hakuna hata moja iliyojibiwa.
Nikiwa bado nimekaa juu ya jiwe moja nikining’iniza miguu huku nikiirusharusha na kuangalia watu mbalimbali waliofurika week end ile wakiogelea na kufurahia maisha. Nikiwa nimeangaza huku na kule moyo wangu uliripuka ghafra nilipomuona bint mmoja akiwa kavaa kipensi chepesi kifupi kilichom bana bara bara huku akiacha sehemu kubwa za mwili wake nje ambapo kifuani alijisitiri na kisidiria kidogo cha kamba kutokana na udogo wa matiti yake. Kilichonistua zaidi si umbo lake tuu na mavazi yake bali nilipouona uso wake vizuri akiwa kashikwa kiuno na baunsa mmoja ambae kushoto kwake alishika pila kubwa la kuogelea. Hakuwa mwengine yule bint bali kipenzi changu Mariam akiwa na yule njemba wakielekea majini huku wakionesha nyuso za furaha. Nilijikuta mwili unatetemeka kwa hasira na midomo kunicheza cheza huku macho yakiwa hayaamini kile kilichokuwa kinaonekana.
“Shiiiiiitttttt!!!!!!…?!~!!”
Niliruka pale juu ya jiwe na kujikuta nakanyaga maji licha ya kuwa nilivaa raba na suruali yangu ya jeans lakini sikujali wala kufikilia hilo nilitembea haraka kule alipokuwa kipenzi changu Mamu na yule boya na kabla hawajafika kwenye kina cha kuogelea niliwakuta na kulianziasha palepale.
“Mamu hapa unafanya nini na huyu ni nani..!?” “Hii we kaka vipi.. Eti baby unamjua huyu!!?” Alijibu kwa taharuki Mariam huku akimuangalia yule baunsa na kujisogeza jirani zaidi na kujifanya hanijui kabisaaa. Moyo ulinichoma na kujikuta naongea huku midomo ikinicheza cheza kwa hasira na kutoamini kama yule ndie Mamu ninayemjua mimi au kivuli chake. “Mamu !!? hivi umepatwa na nini lakini..!” “Hivi baby unamuelewa huyu..” Aliongea Mamu kauli iliyonichoma zaidi ya msumali uliopigiliwa katikati ya kidonda na kubaki natazamana na yule baunsa huku nae akionesha kunishangaa na kukereka “Oyaa mwana, usitupotezee muda katika starehe zetu hebu jikatae haraka kabla cjakufanya kitu mbaya sasa hivi, tena usinihamshie wazimu oooohoooo Tokaa Bwegeee..” Aliongea yule baunsa na kunisukuma lakini nami sikukubali japo sikuwa baunsa wala kuwahi kucheza mchezo wa ngumi nilijikuta namsukuma na mimi. “afu nawewe kum* tu usinizingue hizo nyama tu hata kwenye sambusa za kichina zipo. Hunitishi wala nini.” Nilibwatuka baada ya kumpush yule njemba lakini hamadi!! Nilistukia napigwa ngumi kali ya meno iliyonipeleka moja kwa moja chini na niliponyanyuka ili nikabiliane nae alinibamiza na lile pila usoni hadi nikaona cheche za moto mbele yangu na nafsi yangu kutamani watu waje kutugombezea lakini tofauti na ubaya wa watu wa Dar ndio kwanza walikusanyana na kuzunguka eneo lile kutazama video ya bure huku kipenzi changu Mamu ndio kwanza hakuonesha kujali chochote.
‘’’’PWAATCHAAA’’’’
Kelele za maji zilisikika pindi nilipodondoshwa kwa mara ya pili na kuloana mwili mzima na mengine kuniingia puani na mdomoni. Kilichonisikitisha zaidi ulinzi eneo la fukwe naweza kusema kama haukuwepo kabisa kwa raia zaidi askari wachache walikuwepo eneo la nyuma za fukwe wakilinda magari yaliyopack huku wengine wakiwa maeneo yale ya ndani ya kumbi na kujisahau kama raia wa nje hasa akina sisi wa hali ya chini pia tunahitaji kulindwa hasa linapotokea kasheshe la uonevu kama lililonikumba mda ule.
Nilipiga hesabu za harakaharaka na kuona kama nitazembea zaidi naweza kufa kwani Yule baunsa alinichachamalia hasa baada ya kuona watu wanamshangilia. Nilinyanyuka kwa mbwembwe huku nikijifanya nami namtafuta nimpachinge zangu ndipo ghafra kwa kwa kasi ya kope niliinama sambamba na kutoa ukelele wa hatari na kumrushia maji usoni Yule baunsa na alipozubaa tu sekunde zilezile nilipenya kwenye ukuta wa watu na kukimbia eneo lile huku watu wakizomea huku wengine wakicheka hali ya kuwa mwenzao nilizidiwa bila hata kunionea huruma na kwa mbali kipindi nakimbia nilisikia kicheko cha sauti ya juu toka kwa mpenzi wangu Mamu huku nae akinizomea pia. Daaah!! ktk siku nilizowahi kujisikia vibaya na kupatwa aibu kubwa na sitoweza kuzisahau na hii pia ni mojawapo, kwani nilijisikia vibaya sana na sikumbuki vizuri speed niliyotoka nayo kama yule baunsa alinifukuzia ama laa, lakini nilichokuja kukumbuka vizuri zaidi ni pale nikiwa ndani ya daladala mara baada ya kustuliwa na sauti ya dada mmoja.
“Wee kaka vipi! Simama vizuri unaniroweshaa…!!” Sauti hii ilinifanya nijibane zaidi mlangoni aliposimama konda Huku abiria wengi wakinishangaa kwa jinsi nilivyoonekana kwani siku hiyo jua lilikuwa kali sana nami nililowa chapachapa tena nikiwa nimepiga pamba za nguvu na raba kali.
Ilinibidi nishuke tu kituo cha mbele kwa aibu na kuanza kupiga hatua mdogo mdogo na njia nzima kila niliyepishana nae aligeuka kunishangaa si mkubwa wala mtoto yaani niligeuka bonge la kituko cha siku kila nilipopita. Nilizama geto na kubadili zile nguo na nilipojitazama kwenye kioo ndipo nilipobaini kuwa nilikuwa na uvimbe (nundu) kwenye paji la uso pia mdomo wangu wa chini ulipasuka kidogo na kulikuwa na vidamu vimegandia sehemu ya kidevu. Nilijisonyea mwenyewe na kumlaani Mariam kwa alichonifanyia huku nikimshukuru Mwenyezi mungu kwa kuniokoa kwenye mikono ya baunsa yule na muda uleule nilikumbuka kuifuta kabisa namba yake kwani nafsi yangu tayari iliingia kinyongo na sikutamani kuja kuonana nae kamwe..!! Lakini nilipotazama mifukoni kutafuta simu nayo sikuiona hata wallet yangu nayo haikuwepo ndipo nilipobaini kuwa nilividondosha navyo kwenye hekaheka ile na kukumbuka kuwa hata kwenye daladala nauli sikulipa wala konda hakunidai hata nilivyoshuka kule njiani. Nilishusha pumzi na kumshukuru tena mungu na kuwazia hata nitaponunua simu sitokuja kuleinew line wala sitomtafuta tena Mariamu kivyovyote.
* * * * *
Ilipita wiki nzima nikiwa mnyonge sana kuanzia kazini mpaka mitaani sikuwa na shauku hata ya kutaka kujua maendeleo ya mamu niliamua kujieka bussy na mambo mengine huku upande wa pili moyoni nilikubaliana na maneno ya yule bwana kuwa inawezekana kuwa kweli wanaake ni wauaji. Niliwazia endapo yule baunsa angenizimisha ama kuniua yote ingekuwa kwa sababu ya Mamu… pia niliwaza kuwa ina maana mamu alidhamilia muda mwingi kufanya vile ama alifanya kama kulipa kisasi kwa maneno yangu? Lakini ikawaje iwe mapema vile tena siku ileile. Nilichoka na kuendelea kumlaani licha ya kuwa ukweli nilimpenda sana.
Miezi ilipita na hatimae ilikatika miezi nane nikiwa sijawahi kuwa na mahusiano mengine yoyote wala kukutana kimwili na mwanamke yeyote. Na katika siku hizo tulipata safari kikazi mkoani Arusha na ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kufika Arusha. Jiji la Arusha lilikuwa tofauti sana na Dar kuanzia hali ya hewa hadi tabia za watu, sio siri ktk kipindi kifupi nilijikuta nalipenda sana jiji lile. Nakumbuka siku moja usiku nikiwa nimelala niliota ndoto kuna sehemu tumeenda kufanya kazi muda wa mapumziko mchana tulizunguka eneo moja ambapo nilikutana na msichana mrembo sana na katika maongezi nilipomuuliza jina alinambia kuwa anaitwa Zai. Nilishtuka usingizini na kufikilia sana ile ndoto na siku mbili baadae nilishangazwa na taarifa kuwa inatakiwa tufike eneo ambalo nililiota na tulipofanya kazi ilipofika mida ya chakula na mapumziko ya mchana nilishangaa tulikuwa tunazunguka maeneo yenye mandhali ileile kama niliyoiota na kilichokuja kunishangaza zaidi na zaidi nikiwa na mshikaji wangu tunatembea tulipishana na msichana mrembo sana na tuliangaliana huku sura yake ikiwa haina tofauti kabisa na yule niliyemuota na chaajabu zaidi nilijikuta namwita jina lile nililoliota kwa mara tatu mfululizo hadi rafiki angu niliekuwa nae alinishangaa
“Zaiii, Zaaii.. Zainaab..”
“Oya unamjua au unaropoka tu..” Aliniuliza rafiki angu pindi nae alipogeuka na kuona yule binti kasimama nami bila kusita nikaamua kumfuata. “mambo Zai..” Nilimsalimia. “Poa, ila mi mbona sikukumbuki na sidhani kama tuliwahi kuonana!!?” “ni kweli unaweza kuwa sahihi kwa upande mwengine miili yetu haijawahi kuonana ila nafsi zetu ziliwahi..” “kivipi mbona sikuelewi.” “Utanielewa tu, kama hautajali chukua namba zangu hizi tuwasiliane zaidi” Niliongea na kumkabidhi kikadi changu cha mawasiliano huku nae akikipokea kwa mshangao akiwa haelewi tulikutana vipi nami sikungoja maswali zaidi niliondoka na kumkimbilia rafiki yangu ambae alibaki ameduwaa muda wote niliposimama na yule mrembo.
“mwanangu mbona sikusomi!!” “hahahaaa hamnaaa utanisomaa tuu.” “heee! Hayaa, sema mtoto mkali kishenzi, umemjuaje, ?” “nitakwambia tuu usiogopee” Nilimzuga mshkaji japo bado alionesha hajaridhika na majibu yangu lakini kwa upande wangu kichwani nilijiuliza sana imekuaje nimeota ndoto na imetokea vilevile..!! Nilihisi ujinga kama nitamwambia mshkaji eti nimemuota yule dem nilijiua asingeniamini kabisa kwani ni nadra sana mtu kumuota mtu asiyemjua akamtajia mpaka jina harafu siku si nyingi wakakutana tena kiukweli na ikawa vilevile.
Tulirudi kuendelea na kazi na chaajabu siku zilipita sikupigiwa simu na Zai wala kupata sms yake na kwakuwa sikuchukua namba yake iliniwia vigumu kumtafuta na hata tulipotembelea tena yale maeneo sikuwahi kumuona hadi muda wa kuwepo Arusha ulipoisha na safari ya kurejea Dar ilijili na kukusanya vitu vyetu na kurudi rasmi jijini DSM.
* * * * * * *
Ilipita miezi minne sawa na mwaka mmoja tangu niachane na Mariam na nilikuwa nimehama kabisa lile eneo nililokuwa nakaa awali na nilipanga sehemu nyengine mbali kabisa pembezoni mwa jiji. Siku hiyo nilipotoka kuoga baada ya kurudi kazini nilikuta simu ikimalizia kuita na nilipocheki namba ilikuwa ngeni na kulikuwa na missed calls nne . Nikiwa bado nina taulo niliamua kuipiga ile namba huku nikiwa nimesimama najiangalia kwenye kioo cha dressing table na haikuchukua muda kuita sana upande wa pili mara ilipokelewa na sauti raini ya kumtoa nyoka pangoni ilisikika. ‘’’Hallow, samahani naitwa Zai nipo hapa Arusha uliwahi nipa hii namba siku moja japo ni muda kidogo ulipita nilikuwa na matatizo nilisahau kukupigia.. nadhani naongea na mtu sahihi..” Sio siri nywele zote zilinisisimka kusikia sauti ya mrembo ambae niliwahi kumuota na kukutana nae nilipokuwa Arusha kikazi na nilishakata tamaa ya kuonana nae tena lakini ikawa ajabu leo kanitafuta baada ya kimya kingi kupita. Kwa kutoamini kwangu nilijikuta namjibu harakaharaka. “kweli kabisa ni mimi Hussein hapa upo wapi Zai..” “Mi niko Arusha na leo asubuhi nilipokiwa napangapanga nguo zangu kwaajili ya safari kesho ndio nikaikuta namba hii kwenye begi langu moja niliihifadhi na nilishasahau lakini nilipoiona tu ndo nikakukumbuka hivyo nimeona vyema nikuage pia unikumbushe umenijuaje au kama unaweza tuonane leo maana umenitia shauku sana ya kujua umenijuaje” “Oooooh, unasafiri kesho.. wapi sasa” “naenda Dar” “Dar!!! Haha mungu mkubwa mi mwenyewe niko Dar kule nilikuwa kikazi tu”
Nilimjuza Zai na tukaongea mengi sana juu ya safari yake ambapo alinambia kuwa ndio mara yake ya kwanza kuja jijini DsM na safari yake ni kwaajili ya masomo ya elimu ya juu na angefikia kwa shangazi yake huko Kinondoni japo alinilazimisha nimwambie tulionana wapi lakini nilimzuga kuwa tutapoonana nitamkumbusha. Na kweli baada ya Zai kufika jijini na ilipofika wiki moja siku ya jumapili ilibidi nizuke pande za Kino kuonana nae kwani alidai asingeweza kutoka hivyo angenisubiri stend tuongee kwa dakika japo tano, nami sikuremba nilijisongesha pande zile nilipofika stend na kweli nilipompigia alikuja. Moyoni nilifurahi japo kichwani sikuamini kama yule mrembo wa ndoto leo niko nae kwa mara ya pili na bila mbwembwe nyingi nilijikuta namwambia ukweli kuwa hatukuwahi kuonana lakini niliposema nafsi zetu ziliwahi kuonana nilimaanisha kuwa niliwahi kumuota na akanitajia mpaka jina. “hahahahahaaa usinichekeshe bwanaa hebu nambie kweli” Alicheka na kwa mara ya kwanza nilimshuhudia vizuri kiasi gani alivyokuwa mrembo hadi nashindwa kuelezea. “kweli Zai na ndivyo ilivyokuwa ila mi nahitaji tuwe karibu zaidi ya hapa” “kivipi..” “namaanisha tuwe na mahusiano ya ndani kabisa na endapo utakuwa radhi niko tayari kukuoa hata kesho Zai kwani naamini wewe ni mwanamke niliyeelekezwa na mungu moja kwa moja kwenye maono” Niliongea kwa herufi kubwa lakini maneno yangu safari hii hayakumfurahisha Zai na kujikuta ananiaga huku akinambia kuwa anachelewa kwao pia akinisisitiza kama ndio haja na nia ya kumtafuta kumbe ilikuwa na lengo lile basi nisahau kabisa haitakuja tokea. Nilijaribu kumzuia ili anisikilize zaidi lakini Zai hakusimama na aliondoka nami ikabidi nigeuze huku nikijilaumu upande wa pili kwa kuwahi kumwambia vile kabla hata sijamueka karibu zaidi.
* * * * * Baada ya wiki mbili ikiwa kila siku nilimtumia msg asubuhi Umeamkaje mchana Umeshindaje na ile ya usiku mwema lakini hata moja haikuwa kujibiwa na Zai zaidi ya ujumbe uliorudi kuwa msg imepokelewa. Sikuchoka nilimtumia msg mbalimbali za vituko na vichekesho bila kuacha zile za kuomba msamaha tena nikimsihi kama kumwambia kwangu vile ndio ilikuwa kosa basi anisamehe sitonyanyua tena mdomo wangu juu ya mada ile ila tu asinikasilikie.. lakini pia hakujibu.
Baada ya muda nilianza kukata tamaa lakini nakumbuka siku moja ijumaa majira ya usiku nilipokea msg iliyotoka kwa Zai ambayo aliandika kuwa anahitaji kuonana na mimi kwa mara nyengine lakini safari hii alihitaji aje ninapoishi. Sikuamini nilipoisoma nami kwa haraka nilimuelekeza na kumuahidi kuwa asubuhi angenikuta stend japo nilijua kuwa kesho yake pia nilihitajika kazini lakini nilijikuta naua kazi na baada ya kumaliza kuchart na Zai nilituma msg ya msiba kazini na kuwambia kuwa nisingefika kesho nitasafiri kwenda msibani Mwanza.
Kesho yake kama ndoto majira ya saa tatu asubuhi Zai alinipigia kuwa yuko njiani nami nilifika stend mapema na kweli mtoto alishuka huku akiwa kavaa gauni lefu na mtandio tulisalimiana na kumuomba tufike tukaongelee nyubani japo awali alidengua lakini mwishoe alikubali na taratibu tulianza kuifata njia ya getto huku moyoni nikiwa siamini kabisa na swali pekee lililoniumiza kwa muda huo ni kwamba ndio nimekubaliwa ombi langu au kuna lengine tena …! Lakini kuna muda nilijiuliza kaswali kengine ka uzushi kuwa hivi huyu bint Zainabu ni binaadam wa kawaida au isije kuwa ni jini linanifanyia mchezo..!! Nilimuangalia pindi tunaingia ghetto na kukaa kimagutumagutu sebureni mara baada ya kumuhudumia kinywaji alichohitaji na kufungua maongezi lakini ajabu nilishangazwa zaidi na kile alichokuwa anaongea Zai siku hiyo na kubaki na bumbuwazi zito sana na kutoamini nisikiacho Daaah!!… Unajua alisemaje..?
Zai alinsema hivi.. “Kiukweli kwanza naomba nisamehe kwa kutopokea simu yako wala kujibu msg zako, lakini nilikuwa nafikilia sana swala lako kwani sijawahi kuwa na mwanaume japo nakutana na majaribu ya kutongozwa mara kwa mara na huku Dar nilichofata ni masomo tu na ndivyo nilivyoapa ila sijui inakuaje nakufikiliaga na leo nimeamua kuja ili nikuhakikishie kuwa nimekubali lakini kwa masharti matatu..”
Aliongea na kunyamaza nami nikatumia nafasi ile kumeza mate na kukaa vizuri.
“sharti la kwanza naomba tusikutane kimwili mpaka utaponioa…” Aliongea huku akinikazia macho nami nikatikisa kichwa juu chini juu kwa ishara ya kukubali na kumruhusu aendelee hilo sharti lengine. “Lapili nipe mda nisome usinipigie simu ovyo hadi nikutafute mimi na kila mwezi tuonane mara moja tu tena maongezi yetu yasichukue zaidi ya nusu saa” Aliniangalia huku mi nikiwa tuli namsikiliza akaendelea. “Na la mwisho uniapie kuwa hutokutana kimwili na mwanamke yeyote hadi utaponioa..” Alimalizia Zai huku akinikazia macho nami nikayatafakari harakaharaka yale masharti na kwajinsi nilivyotokea kumpenda sana Zai nilijikuta nakubali haraka huku nikijinadi… “Ondoa shaka kabisa mke wangu mtarajiwa niko tayari kufata masharti yote hayo na nakuapia sitokuja kuvunja hata moja niamini..” Alinyanyuka Zai na kunikumbatia lakini chaajabu nilipomtazama machoni nilishangaa kuona anatokwa machozi. “Vipi mbona unalia tena” “hamna ni mapenzi tu.. Nakupenda sana Zungu” Nilishangaa Zai aliponiita jina la Zungu kwani lilikuwa ni jina langu la utani enzi niko shule ya msingi sasa sikujua kalijuaje wala sikumbuki kama niliwahi mtajia mtu jina hilo na mbona ni miaka mingi mno hata kazini hakukuwa na mtu aliyenijua kwa jina hilo hata mwenyewe nilishalisahau.. Nilitaka kumuuliza lakini nilijikuta napotezea na kusahau hadi pale aliponiaga na kumsindikiza awahi kwao huku moyoni mwangu nikiwa na furaha iliyopitiliza.
Na huo ndio ulikuwa mwanzo wa ukurasa wa kitabu changu kipya chenye kava zuuuurii la mapenzi ya dhati lililonakshiwa kila aina ya mvuto na kumpendeza yeyote akionacho kitabu hiko na kutamani kukisoma bila kujua kuwa ndani yake kuna kurasa zenye maandishi mazuuuuuri mno ila yana Misamiati migumu sana yenye tafsiri mbaya sana sana sana na za kuumiza. Daaah!! laiti ningejua nisingeendelea kusoma misamiati hii na kuipuuza bila kujua maana yake. Na Laiti ningefunua kwanza nyuma ya kitabu kujua tafsiri yake nadhani kitabu changu ningekisoma kwa tahadhali na umakini mkubwa ama nisingekinunua kabisaaa lakini Mwe!! Tafsiri niliyoikuta kwenye kurasa ya mwisho imekuwa matokeo tu ya haya niyaonayo baada ya dhalau yangu ya kutosoma hata dibaji na kukimbilia kusoma nisiyoelewa maana kiundani nikifurahia kwa kukodolea macho picha za michoro mizuri kwenye zile kurasa bila kujua siri na maana yake na nilipomaliza kufunua kurasa ya mwisho kulipofafanuliwa maana nikawa nishachelewa sanaaaaa Daaah!! Aaaaaaaaagh… amini usiamini baabaaa aaaaaaaa WANAAKE NI WAUAJI.
*<>* *<>* *<>*
Naam, mpenzi msomaji hiyo ilikuwa ni hadithi ndefu iliyojaa maumivu iliyokuwa inasimuliwa na bwana mmoja wa umli zaidi ya miaka hamsini aliyeitwa Hussein akionekana amekaa pembezoni mwa fukwe nzuri ya Sun rise huku pembeni yake alionekana ameketi kijana mmoja wa umli usiozidi miaka ishirini na saba akiwa anamsikiliza kwa umakini mkubwa, huku wote wakiwa wamevalia suti kali sana. Lakini alipofikia pale Hussein alinyamaza na uso wake ulibaki ukiwa unatililikwa na machozi na Ghafra kilisikika kilio cha kwikwi kutoka kwa bwana yule (Hussein) na ndipo sasa kazi ikawa kwa yule kijana waliokuwa sambamba pale fukwe kuanza kum bembeleza na kumtuliza.
Ilikuwa ni siku ya furaha kwa familia ya mzee Mwinchande kufatia kuhitimu elimu ya juu kwa kijana wao mpendwa mtoto wao pekee Shaaban. Baada ya sherehe za kumpongeza kuisha siku hiyo Shaaban alikaa na mzee wake kwa niaba ya mazungumzo juu ya hatua itayofata kuhusu elimu aliyoipata huko Nairobi Kenya alipokaa zaidi ya miaka mitatu kimasomo.
“Mwanangu nimefurahi umefauru vizuri na umerejea salama lakini sikufurahishwa na kile ulichoenda kujifunza na laiti ningejua mapema sikufichi nisingegharamia pesa zote zile sababu najua ulichojifunza hakitokusaidia hapa nchini kwetu labda ungekuwa ulaya.” “kwanini baba ila mi ndio nilitokea kupenda tena sijui kwanini nilipenda ghafra hivyo kwani hata kabla sijajiunga na chuo sikuwazia kama ningeenda kusomea saikology na maisha ya viumbe”
Aliongea na kujitetea Shaaban lakini msimamo na alichokuwa anaongea mzee Mwinchande kilibaki palepale na alimuhakikishia kama atang’ang’ana na elimu hiyo basi asubirie kuendelea kukaa nyumbani na kutafuta kazi.
Na kweli baada ya kikao kile siku zilienda Shaaban alizunguka huku na kule kutafuta kazi juu ya kile alichokisomea lakini ikawa vilevile kama alivyoambiwa na babaake na hatimae mwaka ukakatika bila kufanikiwa lakini hakukata tama aliamua kurudi chuo kuendelea zaidi lakini miaka miwili baadae aliporudi bado hali ikawa vilevile hakuna kazi hata alipofungua ofisi yake kibongobongo bado ilikuwa bure tu. Ugomvi mkubwa uliokuwepo kwa babaake ukawa palepale kuwa Elimu ya Saikology na mahusiano ya maisha ya viumbe hususan kibongobongo na Afrika mashariki pia ilionekana haina umuhimu sana japo watu wengi walionekana kuwa na matatizo hayo bila wao wenyewe kujijua.
Na kweli safari hii Shaaban baada ya kuona kuwa hakukuwa na dalili yoyote ya faida ya alichosomea hatimae sasa aliamua kumuomba msamaha babaake na kumtaka amsaidie ushauli pia cha kufanya kwani kiukweli alichokisomea ni kikubwa na muhimu lakini hakina faida upande wa kipato imekuwa kama kazi ya kujitolea tu na kwa kipindi hiko chote aliweza kuwasaidia watu mbalimbali mashuleni na kwenye semina lakini bado hakukuwa na chamaana alichokivuna zaidi ya kupigiwa makofi ya hapa na pale, kula misosi ya semina na kuendelea kuishi nyumbani tu akitegemea wazazi huku na umli nao unasogea.
“Sikia mwanangu mi nilikuwa nakuangalia kwanza nilijua tu ungerudi kwenye mawazo yangu .. sasa usijali elimu unayo vyeti unavyo nataka ulithi kazi yangu wiki ijayo nitakupeleka makao makuu, kwani mwezi ujao ndio usaili unaanza .. usijali naamini pia huko utapata nafasi ya kuitumia kazi yako kwani kuna mengi sana kwa wafungwa” Aliongea mzee Mwinchande na safari hii Shaaban hakuwa na pingamizi japo awali hakutaka kabisa kuja kuwa askali magereza kazi aliyoifanya babaake kwa miaka 35 na kipindi hiko Alishastaafu.
Siku zilienda na kweli shaaban alijiunga na jeshi la magereza na kwenda mafunzoni miezi sita baadae akawa askali magereza na kutokana na juhudi na elimu yake haikuchukua muda mrefu mbele alijikuta anapandishwa vyeo na hatimae kuwa Kamishna kwa miaka minne tu. Mwaka mmoja baadae akiwa kamishna alihamishwa na kupelekwa kwenye gereza moja lililohusisha wafungwa wa makosa mazito mazito mara baada ya mkuu wa gereza lile kuugua na kufa ghafra na huko ndipo alipokutana na story ya mfungwa aliyekuwa pale kwa zaidi ya miaka ishirini na tano akijizolea umaaarufu jera kwa jina la Babu bubu alilotungwa na wafungwa wenzake kutokana na kuwapo gerezani kwa muda mwingi na kituko kikubwa alichokuwanacho ni kutopenda kuzungumza wala kujichanganya na wenzake na muda mwingi anapotulia hutumia kuandika maneno ya ajabu ajabu na hata kwenye kuta za jera alitumia mawe kusugua na kuandika japo alishaadhibiwa sana na kuteswa juu ya swala hilo lakini hakukoma kwa miaka yote ile yalikuwa ni mazoea yake na aliharibu kuta nyingi kwa michoro yake na maneno ya ajabu kama mtu aliyechanganyikiwa na alihukumiwa pale kifungo cha maisha kilichotokana na kesi iliyomkabili ya mauaji mara baada ya kuwakatakata viungo familia yake mwenyewe kwa imani iliyosadikika kuwa ya kishirikina, na ni kwa dhumuni la kujipatia utajiri kwa njia ya mkato, na hata hivyo kutokana na serekali kutoamini nguvu za giza na kutolidhika na ushahidi huo pekee ndipo ulipofanyika ushahidi wa kisayansi kwa kufanyiwa vipimo huenda alirukwa na akili lakini alipochunguzwa na kufanyiwa vipimo zaidi vya kitaalamu bado majibu yalionesha kwamba hakuwa na tatizo lolote la akili hivyo alifanya yote kimakusudi na ndipo hukumu ilipotoka na haikuruhusiwa rufaa yoyote kwa mfungwa yule.
Kilichomshangaza zaidi Kamishna Shaaban ni baada ya kufatilia michoro ya huyo mfungwa kwa umakini kabisa ambae kiumli alikuwa kama babaake na alipoichunguza zaidi kwa uyakinifu aligundua kuna maneno ndani yake yaliyosomeka ‘’’WANAAKE NI WAUAJI’’’ Na huu ndio ukawa mwanzo wa Kamishna Shaaban kumtafiti na kumchunguza huyo mfungwa akianzia historia ya mafaili yake hadi kuhukumiwa na kuletwa pale huku moyoni Shaaban akiapa lazima atafute jinsi ya kuongea na huyo mtu kwani maneno yake yalionesha yana siri nzito na maana kubwa kwenye maisha yake.
Kazi ilikuwa ni nzito kuyatafuta mafaili yale ya zamani yakiwa yametengwa sehemu maalum na kwa kuwa Shaaban alikuwa ni Kamishna na mkuu wa gereza lile kwa muda mara baada ya mkuu wa gereza wa awali kufariki ghafra naye kuletwa pale kukaimu tu mpaka jeshi litapomchagua mkuu mpya rasmi, hivyo alitumia wadhfa aliokuwa nao kuwaagiza askali walioshughulika na utunzaji wa kumbukumbu na mafairi ya wafungwa na kuwaagiza watafute faili la Hussein Muhondogwa aliyefungwa pale kwa zaidi ya miaka 25 na watapolipata wamletee mara moja.
Na kweli baada ya siku kadhaa faili lilipatikana na maelezo yalionesha kuwa mtuhumiwa yule aliyejulikana kwa jina la Hussein alihukumiwa pale kwa kosa la kuwaua kwa kuwakatakata viungo mkewe na mwanae ambae alikuwa mtoto mdogo wa kiume wa umli wa miezi isiyozidi sita ikiwa ni familia yake aliyokuwa anaishi nayo na imeonekana kuwa mtuhumiwa alidhamiria kufanya hilo tukio kwa imani ya kishirikina kuwa angekuwa tajiri baadae na ndio sababu kabla ya tukio alipanga nao safari ya mbali huko kijijini ili kufanikisha zoezi hilo kirahisi na katika hali ya kupoteza ushahidi ilibidi akubali kupigwa na watu alioshilikiana nao na kujitia kuzimia kwa kuidanganya serikali kuwa walivamiwa. Hukumu yake ilionesha kuwa alifungwa kifungo cha maisha sambamba na kazi ngumu.
Baada ya kusoma yote yale Kamishna Shaaban kwa kutumia uwezo wake binafsi na uzoefu aliokuwa nao ndipo alipoanza kazi ya kumfatilia Hussein au babu bubu kwa njia ya kuwaagiza baadhi ya askali wa chini waliokuwa wanawasimamia zaidi wafungwa. “Hakikisha Coplo unampiga picha kwa kila akifanyacho na uwe unanirekodia nyendo zake zote huko site, sawa..” “Sawa mkuu” Yalikuwa ni moja ya maagizo kutoka kwa Kamishna Shaaban kwenda kwa coplo mmoja kati ya askali waliowasimamia kina Hussein huko walipokuwa wanaendaga kuvunja mawe (kokoto) . Kama kawaida yake Hussein alipokuwa huko hakutaka story na yeyote zaidi ya kufanya kazi kwa nguvu sana licha ya umli wake kuwa ni mtu mzima lakini bado mwili wake ulikuwa na nguvu huku uso wake muda wote ukionesha ni mtu mwenye mawazo mengi sana na ikawa kawaida saa nyengine atabasam na kujichekea mwenyewe tena kwa sauti kubwa na anapofanya hivyo ndipo anapoongeaga maneno yake ya ajabu ajabu na mwishoe alisema Wanaake Ni Wauajiiii..
Wafungwa wenzake walishamzoea na walichukulia kawaida kwani hata walipojaribu kumuuliza kwa kuongea nae alikuwa ni zaidi ya bubu na hakutaka kabisa kuzungumzia hilo kwani alijijua maisha yake ndio yameishia pale. Lakini zile rekodi na picha zilipomfikia Kamishna Shaaban toka kwa vijana wake mbalimbali aliowapandikiza kumfatilia mfungwa yule zilizidi kumpa picha ktk halmashauli yake ya kichwa hususani ktk kitengo cha utafiti na akaona kuna umuhimu mkubwa wa kuongea na huyo mfungwa ndipo siku moja majira ya saa mbili usiku waliingia maaskali kumi kule ktk vyumba vya wafungwa na kumchukua Hussein mkuku mkuku huku wakiwa wamemfunika kitambaa usoni na kumpiga pingu huku Hussein akiwa hajui kwanini imekuwa hivyo na wapi wanampeleka ndipo alijaribu kuwafanyia fujo na kujikuta anapigwa kitako cha bundukio kichogoni mwake na kupoteza fahamu. Anakuja kustuka Hussein baada ya kumwagiwa maji usoni na kujikuta amekalishwa kwenye kiti na mbele yake alikaa mtu ambae hakumfahamu ikizingatiwa hakuvaa sare zozote.
Alikuwa ni Kamishna Shebby na baada ya kukutana na Hussein pale aliwaamuru vijana wamfungue pingu kwanza japo awali kidogo wale askali walisita kutokana na kumjua Hussein ni mtu hatari kutokana na mwili mkubwa alioutengeneza huko huko jera kwa kufanya kazi ngumu mfululizo na alionekana mfungwa wa ajabu kadri siku zilivyozidi kwenda mbele hakuwahi kuwa na rafiki jera wala mazoea na mtu hivyo waliona si salama kumuacha aongee na muheshimiwa wao akiwa hajadhibitiwa walau mikono lakini cha ajabu Kamishna Shebby aling’ang’ania na kusisitiza wampe uhuru wamfungue na wampeleke akaoge kwanza. Baada ya hapo huku askali wakiwa wanamshangaa pia kamishna wao hasa pale alipokaa nae meza kuu ya chakula mtuhumiwa yule na kuamuru kula pamoja hali iliyomshangaza hata Hussein mwenyewe kwani hakukumbuka mara yake ya mwisho ilikuwa lini kula chakula kizuri kama kile na hakuwahi kukiona toka amehukumiwa pale.
Baadae kwa uzoefu mkubwa na waajabu aliokuwa nao kwenye kuisoma saikology ya mtu Kamishna Shaaban alianza kumchombwezachombweza kwa maneno Hussein na kumuonesha heshima kubwa hasa kwa kumtunuku jina la ‘baba’ ambalo Hussein ktk maisha yake hadi kipindi hiko akiwa na miaka hamsini na kitu hajawahi kuitwa baba. Alisikia faraja kidogo moyoni Hussein licha ya kuificha machoni lakini alistaajabishwa zaidi na tabia na ukalimu aliyoonyeshwa na kijana yule ambae bado alikuwa mgeni machoni mwake kutokana na kuwafahamu watu wengi pale Gerezani.
Kamishna Shaaban nae hakuwa na papala zaidi aliamua kumtembeza tembeza eneo lile la mjengo ambapo Hussein licha ya kuwepo pale kwa muda mrefu lakini hakuwahi kufika maeneo yale na hakupaelewa vizuri japo alijua ilikuwa ni ndani ya maeneo ya gereza lile. Tena huku wakiwa wawili tu baada ya kuwasihi walinzi wasimzongezonge pindi anapokuwa na mfungwa yule Kamishna Shaaban au Shebby aliongea mada tofauti tofauti akimsimulia mfungwa yule ambae muda mwingi alikuwa ni mtu wa kukaa kimya tu na baadae aliwaruhusu askali kumrudisha tena walipomtoa. Siku hiyo Hussein hakulala zaidi ya kufikilia juu ya yule kijana na muda wote huo hakujua kama yule ndie Kamishna mpya aliyeletwa pale.
Hali ile iliendelea sasa ikawa mazoea kila inapofika week end jioni bila ghasia wala kufichwa Hussein aliongozana na askari waliokuwa wanakuja kumchukua na kwenda kukutana na Kamishna Shebby na kujumuika kwa chakula pamoja na kuangalia tv na kubadilishana mawazo ya hapa na pale japo kwa upande wa Hussein hakupenda kabisa kuongea kutokana na kuamini hana zaidi alichokibakisha duniani zaidi ya kungojea siku yake ya kufia gerezani tu, lakini maneno ya Shebby na hali aliyokuwa anamuonesha kila siku za wiki heshima na unyenyekevu aliokuwa anamfanyia ndipo taratiiibu zilianza kubadilisha imani na hisia za Hussein na kuanza kuona maisha ni kawaida tu na kupunguza vituko vyake japo mara nyingi alikuwa mkali na kutopenda kuulizwa swali juu ya kile alichokuwa anaropokaga na kuandika kuwa Wanaake ni Wauaji.
Lakini pia Kamishna Shaaban (shebby) hakuchoka na alitumia mbinu mbalimbali m badala na ndipo siku hiyo alimtoa eneo tofauti kabisa Hussein tena kwa siri iliyojulikana na askali wachache wakubwa baada ya kuagiza ziletwe suti mbili kali na moja wapo alivalishwa Hussein huku nae akivaa yake na hata magari yalipotoka Askali wengi hadi wa getini hawakujua kama kuna mfungwa mmoja anatoka na kamishna zaidi walidhani ni kiongozi mwengine tu wa jeshi. Na ndipo msafara wa gari mbili ambapo moja ikiwa na walinzi maalum waliovaa kiraia pia kwa dhumuni la kumpa ulinzi kamishna anapokuwa nje pia ya gereza na ndipo Kamishna Shaaban alipomuamuru dereva wake kuwa aongoze msafara ule kuelekea maeneo ya viwanja vya Sun rise beach.
Walipofika Sunrise beach na kutokana na mazingira yale yalimfanya Hussein akumbuke mambo mengi hasa mara baada ya kuliona jua la nje na wanawake mbali mbali wakiogelea huku wakikumbatiana na waume zao wakifurahia maisha. Mboni za Hussein zilistaajabishwa na jiji jinsi lilivyokuwa kubwa huku kila kitu kikiwa katika mitindo tofauti kidogo aliyoiacha kabla ya kwenda jera na aliona wanawake wengi sana pande zile kuliko wanaume na hilo alilibaini mara baada ya kila mwanaume aliyemtazama kuona alizungukwa na mwanamke zaidi ya mmoja. aliwatazama sana wale wanawake na ghafra aliangua kicheko cha ajabu sana “ha ha ha ha aaa HAHAHAHAAAAA ..” Alicheka Hussein kwa sauti ya juu na kumfanya Shebby amuulize kulikoni, lakini alichojibu Hussein Babu bubu kilimshtua hadi muhudumu wa kike aliekuwa kakaa meza ya jirani ukiachilia mbali wale walinzi wengine.
“Wanawakeeee… wanawakeeee .. wanawaaaake wazuuuri sana mwananguu ukiwatazama kwa nje tu, ila kwa ndani ni wabaya sanaaaa tena saaanaaaa na ni WAUAJI wakubwaaaa.. ha ha ha hahaaa..” Aliongea kwa mara ya kwanza na kuendelea kucheka Hussein na ndipo Kamishna shebby alipobonyeza kitufe cha record ktk simu yake kwani alijua sasa ule wakati alioutafuta na kuusubiri kwa muda mrefu sasa umetimu, hivyo alimuuliza na kumpekecha kujua kulikoni zaidi kilichokuwa nyuma ya pazia kwa bwana yule? na kweli taratiiiibu ndipo Hussein alijikuta kwa mara ya kwanza akianza kufunguka na kusimulia historia yake na chanzo cha yeye kuja kufikia vile. Na alianzia kukumbuka na kusimulia kwa kuanzia siku ile aliyokuwa anaangalia kile kipindi cha ya walimwengu kutoka BECKER TV na hadithi yake ndio ilianzia pale.
Baada ya kusimulia yote yale hadi alipofikia pale alipojuana na Zai msichana mrembo aliyemuota na kukutana nae hadi alipomshangaza kwa kumtaja kwa jina lake la utani la utotoni na jinsi mapenzi yao yalivyochanua ghafra na kupendana kuliko kifani licha ya kupewa masharti magumu matatu. Lakini alipofikia hapo ndipo Hussein alipoanza kulia sana na Kamishna Shaaban kuanza kumfariji na kumsihi kwa maneno matamu kuwa asihofie sana aendelee kumsimulia tu ili aielewe kauli yake ya kuamini kuwa Wanaake Ni Wauaji.
*<>* *<>* *<>* <EnDeLeA> _______ Kum bembeleza mtu mzima ilikuwa si kazi ndogo pia muda nao ulienda sana na kutokana baadhi ya watu kuanza kutega masikio kujua kulikoni hasa walipoona kuna mtumzima mmoja alietinga suti kali ya heshima anatokwa machozi hivyo kama unavyojua ukimuona mtu mzima analia mbele za watu ujue kuna jambo na kwa kukwepa kujaza watu ndipo Kamishna Shebby sambamba na vijana wake waliamua kuondoka haraka na kurejea gerezani na baadae baada ya kurudishwa kwenye chumba cha siri na kuvalishwa nguo zake za gerezani aliamuru Hussein ahamishwe toka sero za awali na kupelekwa sero za v.i.p ambako walifungwa watu wenye pesa na viongozi wakubwa.
Ndipo siku nyengine ilikuwa saa sita za usiku Babu bubu (Hussein) alichukuliwa kama kawaida na kupelekwa kwenye chumba kimoja kikubwa kilichokuwa na masofa mazuri huku kamera mbalimbali zilitegwa na kamishna Shebby pasi na kujua yeyote kwenye chumba kile ndani ya makao ya Kamishna gerezani pale ndipo Hussein alijikuta akiendelea kuhadithia ile story ambayo aliapa awali kuwa ingebaki kuwa siri moyoni mwake.
Kiukweli japo masharti aliyonipa Zai yalikuwa magumu sana lakini kutokana na upendo wa ajabu niliokuwa nao nilijikuta navumilia na kusubiri na taratibu miezi ikasonga na nikaanza kuisoma tabia nzuri na ya kipekee aliyokuwa nayo Zai. Kwanza alipenda dini alikuwa muislam safi sana pili alikuwa ana akili za kipekee mno na zaidi ya yote alijiheshimu tofauti na wasichana wengi niliowajua.
Siku zilisonga na hatimae mwaka mmoja ulikatika na siku hiyo Zai alinipigia simu tena kuwa anakuja getto nami nikafanya usafi harakaharaka na alipofika siku hiyo nilishangaa jinsi alivyokuja huku akiwa na begi kubwa la nguo na zaidi ni mada aliyokuja nayo nikajikuta nabaki mdomo wazi pale aliposema.
“Hussein amini mimi ni wako na sasa nimekuwa wako rasmi. Najua huna kipato kikubwa lakini una uwezo wa kunioa hata kesho, ukweli mi huku sikuja kusoma wala sina ndugu zaidi nilikuja kufanya kazi za ndani tu kwa mama mmoja wa kichaga aliyekuja kuniomba kwetu ila samahani nilikudanganya awali na kukupa masharti yote yale kwa lengo la kukujua vizuri ili uniimanishe kama umenipenda kweli au umenitamani na wanaume wote walionitongoza na kuning’ang’ania niliwakubalia wote na kuwapa masharti hayo matatu na woote walijitahidi kuvumilia lakini walishindwa baadae na hakuna hata aliyefika miezi sita lakini wewe umekuwa wa ajabu kwangu na naamini ndie mume bora kwangu… naomba unipokee kwani kule nimeondoka rasmi kutokana na manyanyaso na tabia za pale nyumbani.”
Nilibaki namuangalia Zai kile alichokuwa anakisema huku nikifikilia kichwani mwangu nimkubalie harakaharaka vile au kuna uongo anauendeleza tu kwani baadhi ya mambo ya Zai yalinistaajabisha kidogo hasa kuniamini na kunambia mi ni waajabu ilihali tulikuwa hatukai wote lakini kiukmweli toka niachane na Mamu sikuwahi kufanya ngono hadi dakika ile. Na ukichochea upendo niliokuwa nao na uzuri wa Zai nilijikuta namkubalia na kupanga nae safari siku tatu zijazo twende huko kijijini kwao Arusha.
Ulipotimu usiku kwa mara ya kwanza baada ya Zai kusali alipanda kitandani na kulala pamoja na mimi huku akiwa kava gagulo na kiblauz alinibusu na kunambia kuwa nisitamani wala ntusifanye ngono hadi siku tutayofunga ndoa na kuninong’oneza kuwa yeye ni bikra pia. Moyoni sikuamini hata kidogo alichosema Zai kwani alikuwa mrembo mno si rahisi kudumu na bikra hadi umli ule… niliona kuwa sasa nadanganywa na ktk umli wangu wote ule nilikuwa sijawahi kukutana na mwanamke bikra.
Usiku huo usingizi haukuja kabisa kila mara nilimuangalia Zai alivyolala umbo lake zuri lilivyojichora namba nane nilijikuta paipu yake inasimama na nyege za mwaka zikisisimua mwili wangu baada ya taswira za pepo chafu kutawala hisia zangu nilijikuta najisogeza karibu kabisa na Zai na kuanza kumpapasa kiuno na taratibu nilianza kupeleka mkono ndani ya gagulo lake na kukutana na kufuri lake lililoficha sehemu zake za utamu na kujikuta mate yakinijaa mdomoni kama fisi mwenye njaa aliyekutana na mzoga mbele yake.
Niliendelea kumpapasa taratibu nikiwa makini kabisa ili nisimstue usingizini na hatimae mkono wangu hususani vidole vyangu vile vya kati viliweza kupenya katika pachupachu ya chupi na kukutana na kajoto ka ajabu kutokea kwenye mashine ambayo sikuamini kama kweli ni mpya kabisa na haijawahi kutumiwa hapo kabla. Katika hali nisiyoitarajia nililazimisha kwa ustadi mkubwa kupenyeza kidole changu kile ambacho ukimnyooshea mtu lazima mgombane, Sikuamini pindi nilipoona kila dariri kuwa ni kweli ile mashine ilikuwa mpya na nilipolazimisha kupenyeza kidole kwa kuvisukuma vile vijinyama vilivyoziba njia Zai aliruka na kushtuka kwa sauti ya juu name kuutoa mkono haraka na kujigeuzia pembeni kwa speed ya hali ya juu.
“Hussein baby kwanini unataka kunifanyia hivyo?… tuseme huniamini nilivyokwambia!!? Mimi ni bikra kweli sijawahi kuguswa na mwanamme yeyote na niwewe pekee niliyekuamini na nahitaji uwe mume wangu wa ndoa ndio itakuwa raha siku utayonifungulia njia hii ya starehe ya wapendanao… baby najua una hisia lakini naomba vumilia tuu honey” Maneno ya Zai yaliweza kumrusha ibilisi aliyenishika ghafra na kujikuta Napata moyo na nguvu na kumkumbatia huku nikimuomba samahani na kumuahidi sitamgusa tena mpaka tutapooana. “So sorry baby.. sitorudia tena ni shetani tu alinipitia nikataka kukujaribu ili nihakikishe but sitorudia tena mpaka siku tutapohalalisha ..”
Niliongea maneno haya kwa busara ya hali ya juu nae Zai bila kinyongo aliniitika kwa kichwa na kunibusu kisha tukalala na sikumgusa tena hadi kulipokucha na mishe mishe ziliendelea hususani kwenda kukata tiketi kwajili ya safari huko kwao na siku mbili baadae niliaga tena kazizni ambapo nilipewa likizo ya wiki moja kwaajili ya kumaliza msiba niliodanganya awali na kutumia fulsa hiyo kusafiri na Zai mpaka jijini Arusha ambapo tulipanda tena gari lililotupeleka vijiji vya ndani ndani kabisa.
Tulipokelewa vizuri pia bibiake Zai alikuwa mcheshi mno baada ya kufika alituandalia chakula cha asili na katika jambo ambalo sikulitarajia ni mara baada ya Yule bibi kuelewa kila kitu kuhusu mimi na Zai na hata kabla sijajitambulisha Yule bibi alinitajia kila kitu na kunambia bintie hakumficha chochote awali kuhusu mimi na tayari wajomba zake waliujua ujio wetu na wiki hiyo hiyo watatufungisha ndoa ili tuwe mke na mume rasmi.
Sikuwa na kiasi kikubwa cha pesa lakini nilishangaa kusikia mahali tutalipana wenyewe zaidi nilitakiwa kutoa elfu hamsini tu kwaajili ya mila zao. Nilishangaa sana kumpata mke haraka vile tena kwa bei chee namna ile sikuamini kabisa na baada ya ndoa usiku wake tulitengewa chumba maalum kwaajili ya kulala na ndio ikawa mwanzo sasa wa kujilia lile tunda ambapo purukushani ilikuwa kubwa sana kwani zai alibana miguu na kuogopa sana nami nilikuwa jasiri wa kumkamata na kumdhibiti hatimae niliweza kumsongomeka msumari japo haukuingia wote na kwa shida sana Zai alipiga kelele mno za maumivu na chaa ajabu alipopiga zile kelele nilisikia sauti ya vigeregere nje ndipo nilipogundua kuwa kulikuwa na watu walikuwa wanatusikilizia.
Tulikaa siku saba kabla hatujarudi Dar ambapo tulifungashiwa zawadi kibao kwaajili ya kwenda nazo na nilipokuwa njiani niliwasiliana na ndugu zangu baadhi ambao walikuwa wananisubiri kwa hamu kubwa huku wengi wakiwa wamenilalamikia kwa kitendo cha kwenda kuoa pasi na kuwataarifu mapema. Safari yetu ilifikia kwa Mjomba kakaake na marehem mama kwakuwa sikuwa na wazazi kipindi hiko na tuliwakuta baadhi ya ndugu na kutupokea vizuri tu na kuanza kuwatambulisha mke wangu lakini chaajabu kipindi nawatambulisha nilipofika kwa baba mkubwa ambae alikuwa ni mganga wa kienyeji aliposhikana mikono na Yule bint alimuangalia sana hadi Zai alionesha kusikia aibu na jicho la ba mkubwa kidogo lilinishangaza hata mimi. Nilipomuangalia zaidi mke wangu alikuwa kainamisha kichwa chini huku baba akiwa bado kamkazia macho na kugeuza shingo kisha kunitazama kwa mshangao hali iliyoanza kidogo kunipa wasiwasi.
Lakini nilijibaraguza na kukenua meno kwa kucheka kidogo huku nikijiiminisha kuwa hali aliyoonesha baba huenda ilikuwa ya masihara na kautani kidogo nikiamini alishangaa kuona nimewezaje kung’oa kifaa kama kile. Nakumbuka baada ya pongezi na zawadi mbalimbali ambapo napo kulikuwa na sherehe ndogo kwa niaba yangu, usiku uliingia tukalala lakini asubuhi na mapema nilipoamka na kutoka nje nilikutana na Ba mkubwa ndipo aliponiita na kunivutia pembeni. “Pole sana kwa safari mwanangu” “asante baba.. vipi kwema” “kwema, ila naomba nikuulize swali” “lipi baba” “hivi huyu bint kabla hujenda kuoa ulishawahi kuishi nae japo mwezi mmoja au miwili?” Swali la ba mkubwa kidogo lilinibabaisha kujibu na kujikuta nauliza swali badala ya kujibu
“kwani vipi baba..” “hapana .. nimekuuliza tu mwanangu maana hukutwambia mapema kama unaishi na mtu baada ya yule Mariam aliyekuwa anakuja kwako mara kwa mara pia hukutwambia kama mliachana na umepata mchumba mwengine, lakini pia mwanangu kwanini hukumjulisha ndugu yeyote kama ungekuwa na safari ya kwenda kuoa..? tena mkoa wa mbali kabisa eeh..! hii imenitisha kidogo. ni afadhali ungeoa mtu wa nyumbani mwanangu sidhani kama huyu bint ni chaguo lako sahihi kabisa.” Maneno ya baba yalininyima raha kidogo kwa kuona kama wananisimanga zaidi ili hali nilishaomba radhi hapo kabla na kauli yake ya kuwa afadhali ningeoa mtu wa nyumbani kidogo ilinichefua kwa kuona sasa wanataka kuanza kumnyanyapaa mke wangu nimpendae mapema ile. Uso wangu kidogo ulibadilika sambamba na sauti pindi nilipomjibu tena ba mkubwa na kumwambia “daah! Kiukweli ndio maana niliwaomba msamaha mapema tu baba kuwa nilipitiwa, lakini mimi ni mtu mzima na jua zuri na baya hivyo mkae mkijua namtambua vizuri sana mke wangu na sikukurupuka kumuoa ni chaguo langu sahihi kabisa.” “Basi vizuri Mwanangu kama unamtambua vizuri, ila kumbuka Mpotea njia mara nyingi si Muulizaji”
Aliongea ba mkubwa na kuingia ndani na kuniacha nimesimama pale nje nikitafakari kidogo maneno yake na methali zake za mafumbo huku nikifikilia picha ya jana yake alivyoonana na mke wangu Zai na jinsi alivyomuangalia, nilijikuta najisonyea mwenyewe na kumpumbaza ba mkubwa moyoni kuwa kumbe bado ana akili za kizamani kabisa na mila potofu za kuchaguliana mke.
Nilipuuzia huku nikijichekesha kupotezea hasira iliyoanza kuubadilisha uso wangu na kurudisha tabasamu bandia ili mtu mwengine asinigundue asubuhi ile japo moyoni nilichefuka kidogo kisha nikaamua kurudi chumbani na baada ya sherehe kuisha siku hiyohiyo niliaga kwa ajili ya kuondoka japo awali mjomba tulikubaliana kuwa tungekaa siku tatu lakini nilieka visingizio kaza wa kaza hasa kuhusu kazini mpaka wakanielewa japo moyoni sababu kubwa ya kutaka kuondoka mapema ile ni baada ya kutibuliwa na ba mkubwa.
Na ndipo tulisindikizwa mpaka kule nilipokuwa naishi na baadhi ya ndugu waliotoka kijijini kwa kina Zai ili kupafahamu tulipoishi na waligeuza asubuhi hiyo na kutuacha wenyewe pale ndani na baadhi ya ndugu wa palepale mjini. Baada ya nasaha mbalimbali hatimae kila mtu akaondoka na maisha mapya kabisa baina yangu na Zai yakaanza rasmi na yalinoga siku hadi siku. Siku zote nilimshukuru mungu kwa kupata mke bora na mwema kama yule lakini ujinga mkubwa niliofanya ni kupuuzia swali na maneno ya Ba mkubwa yaani Laiti ningeyatilia maanani japo kidogo maneno ya ba mkubwa nadhani yasingenikuta yoote haya baadae… loh!! Kweli muda mwengine wanaume ujasiri wetu unatuponzaga kwani katika miaka miwili tu ya ndoa yetu ilitosha kabisa kuamini na kukumbuka maneno pia ya yule mlemavu wa kile kipindi kilichorushwa na kituo cha Becker TV nilichoangalia miaka mitano iliyopita hadi kupelekea kugombana na mchumbaangu wa awali kwa sababu tu ya ile mada na kauli ya msimuliaji kuwa Wanaake ni Wauaji.
Ni ngumu kunielewa harakaharaka lakini usijali utanielewa tu. Ukweli mke wangu alikuwa mtu wa kufatilia ibada sana, alinisihi na kuniasa mara nyingi huku akinionya kwa upole mara kwa mara na kunisomea hadithi mbalimbali kuhusu watu waliomuasi mungu karne hizo na adhabu walizozipata. Taratiibu nilijikuta nami nikianza kufatilia ibada na ndipo maendeleo yetu yalizidi kuwa mazuri na tulinunua kiwanja huko kigamboni na kuanza kujenga huku mke wangu akiwa msimamizi mkuu. Mwaka mmoja baadae ikiwa ni miaka mitatu baada ya ndoa yetu nakumbuka siku hiyo majira ya jioni nikiwa ndani ya daladala nikitokea kazini kama kawaida nikiwa nimesimama na kutokana na wingi wa watu waliokuwa wanahitaji huduma ya usafiri jioni ile wakitokea makazini na mashuleni tulijikuta tukiwa tumebanana mno ndani ya daladala ile.
Nakumbuka vizuri tukiwa kwenye foleni kuna mtu alienisalimia akiwa amesimama nyuma yangu na niliitikia pasi na kugeuka kumtazama japo sauti yake sikuifahamu lakini alionesha kunifahamu zaidi kutokana na kunisalimia kwa kunitaja na jina, aliongea nami kwa sauti ya chini na kunambia ana ujumbe wangu. Nilishindwa kumuelewa hali iliyonifanya nijalibu kujigeuza sasa nitazamane nae lakini kutokana na m banano wa watu nilishindwa kufanya hivyo hadi nilipoona napenyezewa bahasha ndogo kwa juu nami nikaipokea japo sikuelewa ni barua ya nini na inatoka wapi lakini nilijipa imani watu watapopungua mbele nitaongea nae huyo mtu ili anieleweshe zaidi na kilichomo ndani ya bahasha ile japo nilielewa kuwa ni barua lakini sikujua inatoka wapi na ni kwa dhumuni gani.
Gari ilisogea na kweli kituo cha mbele watu wengi walipungua ndipo nikapata nafasi ya kugeuka na kumtafuta yule aliyeniongelesha na kunikabidhi barua lakini cha ajabu kila niliyemtupia macho kuhisi ndie alibaki nae kunikodolea na kunishangaa tu na kujieka bussy na mambo yake, Nilihisi na kujilidhisha huenda akawa kashuka pale kituoni gari iliposimama lakini nilijiuliza kwanini hata hajaniambia kama anashuka? Niliachana nae na kuendelea na yangu huku nikiwa na shauku ya kufika haraka nyumbani niweze kusoma kile kilichoandikwa ndani ya ile barua.
Nilifika nyumbani na kupokelewa vizuri na kipenzi changu kama kawaida na kumnyanyua mwanangu kipenzi ambae alikuwa anakaa chini kipindi hiko kwani tayari mungu alitubariki mtoto mmoja wa kiume na niliipenda na kuijali sana familia yangu. Mara baada ya mke wangu kipenzi kuniekea maji bafuni na nilipomaliza kuoga nilitoka kuja sebureni kwa ajili ya kupata msosi lakini niliikumbuka ile barua na kurudi chumbani na kuichukua kwa shauku ya kuisoma kujua dhumuni lake ndipo nilipotulia sebureni nikiwa nasubiri msosi kipindi hiko mke wangu alikuwa busy jikoni ananipakulia ndipo nikaanza kuisoma barua ile ambayo nje haikuwa na anuani yoyote lakini kadri nilivyozidi kuisoma ndivyo mapigo yangu ya moyo yalivyozidi kuongezeka. aaaagh! Kamishna babaaaa….. Naikumbuka vizuri ile barua iliandikwa hivi.,………………..
…………………………………………………………………………………………….. NDUGU, POLE NA MAJUKUMU NA HONGERA KWA KUISHI NA MWANAMKE MZURI NA KUJIMILIKISHA MTOTO. NISINGEPENDA KUONGEA ZAIDI ILA NIA NA MADHUMUNI YA KUKUANDIKIA HII BARUA NI KUKUONYA NA KUKUTAHADHARISHA JUU YA MKE WANGU UNAYEISHI NAE. SIKUWA HAPA JIJINI KWA MUDA MREFU KIDOGO LAKINI NIMEPATA HABARI ZOTE JUU YA JANJA YAKO ULIYOTUMIA HADI KUITEKA NA KUILAGHAI FAMILIA YANGU. SASA KWA USALAMA WAKO NAKUPA SIKU SABA TU. ANZA KUHESABU KUANZIA KESHO UMRUDISHE HUYO MWANAMKE KWAO ARUSHA NA HUO NDIO UTAKUWA USALAMA WAKO. ZAIDI YA HAPO UTAJITAFUTIA MATATIZO MAKUBWA YATAYOKUFANYA UJUTE MILELE NAMI NISINGEPENDA YAKUKUTE MAJUTO. AHSANTE. WAKO….. MR. X
………………………………………………………………………………………………
Nilishindwa kuielewa ile barua licha ya kuirudia kuisoma zaidi ya mara tatu na mke wangu alinishangaa pindi aliponitengea chakula na kubaki nimeduwaa tu na barua ile huku uso wangu nao ulishaanza kubadilika ghafra hali iliyomfanya anisogelee na kuniuliza kwa upole nami sikumjibu zaidi ya kumpa ile barua ambapo aliisoma nae alianza kushangaa na kuonesha wazi hakuielewa kabisa hasa aliponiuliza kuwa ile barua ya nani? Nilimjibu nimepewa mimi ni yangu na inanihusu mimi na yeye. Aliniuliza tena imetoka wapi, hapo ndipo niliposhindwa kuwa na maelezo ya kutosha zaidi ya kuitaka ile barua na kuisoma tena lakini sikuambua chochote zaidi ya mke wangu kuniapia na kunisihi kuwa ule ni ujinga wenye uongo wa kutupwa wala haumlengi yeye inawezekana muhusika amekosea. Nilikubaliana na mke wangu lakini pia nilijiuliza mbona amepataja Arusha? ilihali kweli mke wangu nimemuolea huko? Na atasemaje yule ni mke wake wakati nimemuoa takribani miaka mitatu? Na kwa maelezo ya ile barua niligundua kuwa mwandishi alimaanisha kuwa nilimchukua yule mwanamke akiwa ana mtoto mdogo… hahahaha hapo nilijikuta nikicheka mwenyewe moyoni kwani mke wangu nilimuoa akiwa m bichi kabisaaaa na bikra yake na alikuwa hajawahi kuguswa wala kujihusisha tendo na mtu yeyote zaidi yangu hadi anapata ujauzito na kurudi kwao kwa miezi minne ya mwisho walipomuhitaji akaugulie huko na baadae alijifungua salama mtoto wa kiume na niliwaacha mpaka mtoto alipotimiza miezi miwili ndipo nilipowafata kuwachukua na kuendelea na maisha. Niliamini wazi hiyo barua imekosewa tena si kidogo na nilitamani sana kumuona yule aliyenipa ile barua.
Lakini swali lililonishangaza tena mbona yule mtu alinitaja kwa jina langu kabisa akionesha kunifahamu kabla ya kunipa ile barua? Hapo nilikosa jibu kamili lakini niliamua kupotezea na siku zilienda ambapo zilipita siku nne tangu nipate ile barua ndipo siku nyengine tena nikiwa kwenye daradara safari hii nilipata siti sikuwa nimesimama kama siku ile na wala watu hawakuwa wengi sana kutokana na kuwahi kutoka kazini siku hiyo ndipo nikiwa ndani ya ile daradara mara simu yangu iliita na nilipoitoa mfukoni kuangalia aliyekuwa ananipigia ilionesha ilikuwa namba ngeni machoni mwangu ndipo nikaipokea kujua nani aliyekuwa ananipigia lakini nilipopokea tu kabla sijasema ‘hallow’ nilianza kuisikia sauti ya aliyenipigia ikinikumbusha kuwa zimebaki siku tatu na kuniasa nisije kupuuza nilichoambiwa kwenye ile barua kisha simu ilikatwa.
“HALOOW!! NANI WEWE??” Nilipayuka kwa sauti ya juu hadi nikawastua abilia wenzangu na kunishangaa ambapo nilionesha kuchanganyikiwa kwa hasira na ndipo nilipojaribu kuipiga ile namba lakini cha ajabu haikupatikana kabisa hata niliporudia zaidi ya mara tano ndipo nilipoamua kutuma msg lakini nayo haikuleta majibu kama imefika.
Nikiwa nimepagawa ndani ya daradara nikitafakari cha kufanya mara simu iliita tena kwa mara nyengine na nilipoiangalia namba nayo ilikuwa ngeni lakini ilikuwa tofauti na ile niliyopigiwa muda mfupi na mtu nisiyemfahamu. Nilishusha pumzi na kuipokea kwa sauti ya upole lakini nilijikuta nastaajabu nilipoisikia sauti ya aliyenipigia ilikuwa tofauti na ya yule wa mwanzo lakini mada ilikuwa ileile hasa aliponambia. “Usipanick ndugu yangu na kuwastua watu kwenye daladala ila nakupenda sana ndio maana nakusihi na kukukumbusha kuwa zimebaki siku tatu na hujatekeleza maagizo ya kwenye barua nakusihi tafadhali fanya hima sasa kwa usalama wako’’’ Nilibaki nimeganda safari hii pasi na kujibu chochote hadi simu ilipokatika nilibaki nimeduwaa huku kichwa kikijawa mawazo lukuki nikihisi sasa kuna uwezekano wa kile nilichodhalau kikawa na ukweli ndani yake lakini ni ukweli upi huo kama sio udanganyifu na kutaka kuporwa mke wangu kinguvu? Niliangaza kona zote ndani ya gari ile nikihisi waliokuwa wananifanyia kale kamchezo huenda niko nao ndani ya gari ile lakini sikuambulia chochote zaidi ya watu nao kunishangaa tu kwa kuchanganyikiwa kwangu. Nilijisikia aibu sana kwa mara nyengine nikikumbuka aibu iliyonipata kipinde kile baada ya kupigwa na baunsa niliyemfumania na mchumbaangu Mariam.
Gari ilifikia kituoni na taratiiiibu nilishuka na kuelekea nyumbani ambapo siku hiyo mke wangu alinigundua kuwa siko sawa tangia aliponipokea nje na kuingia ndani ambapo nilijibwaga kitandani bila kuzungumza chochote. Haikuwa kawaida yangu kurudi bila kumkumbatia mke wangu na kumnyanyua mwanangu kwa furaha huku nikimchekesha chekesha na kucheza nae na ndipo kwa mshtuko mke wangu aliniuliza kulikoni lakini nilizuga kwa kudanganya kuwa naumwa na alipohoji kuhusu kwenda hospitali nilidanganya kuwa nishakunywa dawa za maralia kazini na ningependa kupumzika muda huo. Nililala kitandani huku mke wangu akiwa pembeni akinifariji sambamba na mwanangu aliekuwa akinichezea chezea mikono. Moyo uliniuma sana na kumlaani shetani aliyekuwa ananiandama kutaka kuisambaratisha familia yangu.
Nilifikilia kupiga simu polisi na kutoa taarifa zile lakini kabla sijafanya hivyo nilinijia wazo la kumtafuta babaangu mkubwa ambae alikuwa mganga wa kienyeji na moyo ulinisukuma kumtafuta yeye moja kwa moja pasi na mtu mwengine kutokana na lile tukio lililojili miaka mitatu iliyopita na maneno yake ya mafumbo aliyoniambia nilihisi huenda kuna kitu ambacho alikijua mapema kuhusu mke wangu.
Safari hii sikutaka kumwambia ukweli moja kwa moja mke wangu juu ya kilichonikuta tena nikihofia kumtisha pia nilijipa mda wa kutafakari kitu cha busara cha kufanya na akili bado ilinituma moja kwa moja niwasiliane na ba mkubwa tu nimuhadithie kila kitu huenda yeye akawa na msaada mzuri wa kiushauli na cha kufanya. Takriban siku mbili nilishindwa kwenda kazini na nilipopata nafasi ya kuwa pekeangu baada ya mke wangu kuniaga kuwa anaenda bombani kuchota maji ndipo nilimpigia simu ba mkubwa na kumuelekeza yaliyojili ambapo hakuonesha kushangaa sana wala kustushwa na habari zile ila alinionya nisithubutu kutoa taarifa polisi wala kwa mtu yeyote kwanza kabla sijaonana nae na aliniomba na kunisihi sana nifanye hima niende kwake haraka ikiwezekana kesho au jioni ya siku hiyo ambapo kwa mujibu wa ile barua ndio ilikuwa siku ya saba. Nami sikutaka kuremba japo nilijua safari ya kwa bamkubwa ilikuwa mbali kando kando ya mkoa wa pwani mpakani mwa dare s salaam lakini niliona niondoke na familia yangu jioni ile ile kwa kuhofia tusije kuvamiwa usiku bure na watu wa huyo Mr.X kwani namba yangu tu ya simu waliijua sembuse nilipokuwa naishi?
Mke wangu aliporudi kuchota maji nilimsihi ajiandae kwa safari haraka ambapo nae alishangaa mno lakini hakupinga hivyo tulijiandaa pamoja na lisaa limoja baadae tayari tulikuwa tupo safarini kuelekea kwa ba mkubwa. Moyo wangu kidogo ulianza kupata amani na kupata shauku ya kuonana na ba mkubwa kwani alisaidia na kuaminika na watu wengi mno hivyo niliamini kama tatizo letu kuna nguvu za giza ndani yake basi litakuwa limeisha kabisa kwani ba mkubwa nae alikuwa ni nooooowmaa ktk maswala ya kwechekweche na tunguli.
Saa tatu kasoro usiku tulishuka eneo husika na kuchepuka kukifata kibarabara chembamba kilichoelekea huko alipopatikana ba mkubwa ambapo kulikuwa na umbali wa kilometa kama mbili kukifikia hiko kijiji. Kwa kuwa ulikuwa usiku na giza lilishaingia huku kukiwa na kijimbaramwezi kwa mbali ilibidi tutumie tochi kumulikia na njia nzima kulikuwa kimya sana.
Nakumbuka baada ya mwendo kidogo tukiwa tumebakiza kama kilometa moja na nusu kufika mke wangu aliniomba ajisaidie haja ndogo kwani alibanwa mno na asingeweza kuendelea mbele nami nilimuonya ajisaidie palepale njiani asiingie polini kwani kuna wadudu wengi kwenye majani na ndipo nilipompokea mtoto na kusimama kumsubiria.
Nikiwa nimesimama mke wangu anajisaidia ghafra nilisikia chakala chakala na nilipogeuka nilishangaa kumuona mtu aliyevaa kininja akininyang’anya mtoto kwa nguvu na kabla sijafanya lolote kujitetea mara kwa nyuma nilipigwa na kitu kizito bila kumuona aliyenipiga na kujikuta naanguka chini huku kwa mbali nilisikia ukulele wa mke wangu kipenzi Zai akisema.
Sitoweza kuisahau kamwe kauli ile ya Mke wangu Zai.. Zai wangu kipenziii msichana wa ndoto yangu niliyeamini nimeoneshwa na Mungu lakini leo hii anatoa kauli iliyoniaminisha na kuniumiza moyo wangu kupelekea kupoteza fahamu pindi nilipoanguka baada ya kugundua kuwa kumbe mchezo wooooooootee nae alihusika na aliujua vizuuuuri. looh! Ama kweli adui wako mkubwa ni mtu wako wa karibu na Udhaniae ndie sie ila sie ndie. Nilijihisi nakaribia kufa huku nikijiuliza kumbe Zai aliishiii kwa kuniigiziaa?!! aaaaaghh!!!!!… Ni vigumu sana kuaminilll! lakini Chunga sana baaabaa Kamishnaaa usiombe kabisa yakukute kama yaliyonikutaaaa. Siku hiyo ndio kwa mala ya kwanza niliikubali thabiti ile kauli kuwa Wanaake ni Wauaji, nami nakazia kabisa leo hadi siku ya kufa kwangu nitasema kuwa WANAAKE NI WAUAJIIIIII.
*<>* *<>* *<>*
Kilifuata tena kilio cha sauti ya juu na kwikwi kutoka kwa Hussein na kazi ikabaki kwa Kamishna Shaaban Mwinchande kum bembeleza na kumtuliza ili apate kuelewa na kubaini kilichoendelea ktk hadithi yake baada ya kurudiwa na fahamu. Safari hii sasa hata Kamishna Shaaban mwenyewe alijikuta nae machozi yakim bubujika kwa jinsi alivyokuwa anasikiliza kisa kile cha Hussein na zaidi alipomtazama uso wake wa kiutuuzima uliokuwa unatiririkwa machozi kama mtoto kadri alipokuwa anasimulia na alionesha dhahili kuwa ana ghadhabu kubwa juu ya wanaake kwani ktk hadithi yake ile hadi muda huo ilibeba maumivu tu na mateso yote ameyapata sababu ya mwanamke aliyempenda na pia kwa uzoefu wake wa kusoma saikology za watu Kamishna shebby alizidi kumuamini na kubaini kuwa kweli mfungwa yule alionewa na hakuwahi fanya ubaya wowote. Lakini maswali bado yalibaki kichwani mwa Kamishna Shebby na alitaka kujua zaidi ilikuaje hadi kukawa na uthibitisho wa maiti hizo mbili ya mkewe na mtoto? na iweje huyo Zai mke wa Hussein afahamiane na hao watu na kueka mbinu kisha wamgeuke pia na wamuue sambamba na mtoto? ilikuwaje kuwaje hapo… na huyo Mr. X ni nani kwa mujibu wa barua ya kutatanisha aliyoipata Hussein. Japo alikuwa mtaalamu sana Shaaban na alijaliwa ubongo mwepesi ktk kufikiri na kufumbua jambo lakini kwa maswali yale yaliyosumbuka kichwa chake muda ule juu ya hadithi ya Hussein hakuweza kupata majibu ya haraka zaidi ya kumsihi mfungwa wake (Hussein) ajikaze ili aendelee kumsimulia kilichotokea baada ya kurudiwa na fahamu mpaka kukamatwa na kuhukumiwa.
Siku hiyo Hussein japo maumivu yalikuwa mazito mno moyoni mwake kwa kukumbuka mapito yaliyoinyamazisha ndoto zake na kujikuta anazeekea jera akisubiri kifo tu lakini alijitahidi na alipania kuwa aweke kila kitu wazi kwa kijana yule ambae awali hakutambua kama ndio kamishna lakini sasa alijua na hakuwa na jinsi zaidi ya kumuelezea kila kitu hasa baada ya kugundua ni askali kiongozi mwenye moyo wa kipekee sana. Huku akifuta mafua baada ya kimya cha zaidi ya dakika arobaini Hussein aliendelea kusimulia ilivyokuwa mara baada ya kupigwa na kitu kile kichwani hali iliyompelekea kuanguka na kupoteza fahamu.
Simulizi : Wanawake Ni Wauaji ?! Sehemu Ya Pili (2)
Nilistuka mara baada ya kuhisi hali ya ubaridi na unyevunyevu na nilipotaka kuamka nilijihisi kichwa kuwa kizito sana lakini nilijitahidi na kukaa kitako pale njiani huku nikitazama huku na huko kuangalia kama kuna watu wanakuja niombe msaada ama sivyo nikusanye nguvu nipige mayowe raia waje wanisaidie japo nilijua kuwa pale nilipo kuna zaidi ya kilometa moja kufika kwenye makazi ya watu ambako ndiko pia alipatikana babaangu mkubwa yule mganga wa kienyeji na ndio nia ya safari ile tulikuwa tunaelekea kwake. Sikujua ilinichukua muda gani mpaka niliporejewa na fahamu kwani nilijikuta niko mwenyewe pale chini.
Lakini niliponyanyua mkono wangu na kutokana na mbalamwezi kuchomoza muda ule nilishangaa kuona umetapakaa damu halkadhalika na mkono mwengine. Nilijikagua haraka haraka kuona wapi nimeumia lakini bado sikuhisi jeraha lolote mwilini mwangu zaidi ya jeraha dogo kichwani ambalo lilikuwa halivuji damu kivile. Lakini pia nilipoangalia chini vizuri nilishangaa kuliona panga usawa ule nilipolala likiwa limeloa damu pia kulionekana michilizi ya damu kuelekea kwenye kichaka kimoja eneo lile. Nilijikuta nikilishika lile panga kwa mshangao na kuligeuza geuza kuhakikisha kama ni kweli au macho yangu yalikuwa bado yana mawenge,! lakini nilipofanya vile akili iliniaminisha kuwa kile nikionacho ni kweli wala si mawenge na hapo ndipo nilipogutuka na kulitupa haraka chini lile panga na kujikuta nimepata nguvu za kusimama na kuanza kunyata kwa umakini kufatilia ile michilizi ya damu kujua nini kilichopo pale kwenye kichaka. Lakini kabla sijakifikia kile kichaka mara nilianza kusikia kelele kelele za watu wengi waliokuwa wanakuja kwa mwendo wa kasi wakitokea ile njia iliyoelekea kijijini na punde tu nilipogeuka niliona mianga ya tochi ikinimulika huku kwa mbali nikisikia baadhi ya maneno waliyokuwa wanaongea wale watu. “Mwanaharamu mwenyewe si ndio yuuleeee..” “Enheeeee yule yule si unaona midamu ilee..” “Aliyeua auaweeee hebu tupisheni sie mbona hamtembei tutamkosaaa..”
Zilikuwa ni moja ya kauli nilizozisikia toka kwa wale watu huku wengine wakianza kukimbia kuja pale niliposimama nami nikabaki nimeganda kwanza nikiwashangaa na nilipokaza macho kutazama vizuri niliwaona wengine wakiwa wamebeba silaha za jadi na macho yao wote wakinilenga mimi hasa baada ya kunionaa. “Uuuuuaaaa Huyooooo..” “PIGA UUAAA..” Ukelele huu ambao uliambatana na kurushwa kwa mkuki ambao kwa bahati nzuri ulinikosa na ndipo akili ikanicheza na kunionya endapo nitachelewa sekunde kadhaa watu wale wataponikaribia zaidi wataniua kwani walionesha wazi walikuwa hawaji kwa wema wala huruma hata chembe juu yangu. Nilijikuta naruka na kuanza kutimua mbio huku upepo mkali ukinipitia ghafra karibu na kichwa baada ya kurushwa kwa rungu moja kubwa ambalo niliamini lingenipata huenda ningezima pale pale kama sio kufa kabisa.
Nilikimbia kwa speed ya kunusuru maisha yangu huku nikifata kile kibarabara kilichoelekea barabara kuu kule tulipotoka na nyuma yangu bado niliandamwa na watu wale wenye hasira kali ambao sikuwa na uhakika wa moja kwa moja kuwa ni wanakijiji au ni miongoni mwa wale walionivamia awali!? Lakini kabla sijafika mbali mbele yangu kulisikika mlio wa gari sambamba na mwanga mkali wa taa zilizonizuia kuona vizuri na kujikuta naingia porini lakini mara ile gari ilisimama ghafraa na nilisikia vishindo vya watu wakiruka na kunizunguka huku ukelele wa mlio wa risasi ukisikika kuwatuliza wananchi waliokuwa wanakuja ndipo nilipotulia hasa baada ya kusikia kauli zao na kugundua kuwa walikuwa ni polisi. “tulia hivyo hivyo usikimbie zaidi mikono juu sisi ni maafsa wa polisi..” Ilikuwa ni sauti ya mmoja wa watu walioruka kwenye gari akinisihi na kunisogerea pale niliposimama huku nami nikitii na kuona sasa afadhali msaada umepatikana. Ajabu aliponifikia cha kwanza nilipigwa pingu na kugongwa mabega na kitako cha bunduki hali iliyonistaajabisha na kunikosesha kabisa nguvu.
“Wananchi tunaomba mtulie, mshatoa taarifa kwetu hampaswi tena kuchukua sheria mkononi. kwa pamoja naomba mtusaidie kuona eneo lenyewe la tukio hasa ni lipi na jee mtuhumiwa husika ndie huyu mliyekuwa mnamfukuzaa?”
Sauti hizi zilizidi kunishangaza na kunishtua kwani mpaka muda huo sikujua nini hasa nilichofanya yaaani badala ya kupewa msaada ndio kwanza nataka kuuawa? Nilikamatwa suruali na kuanza kutembezwa mpela mpela na wale askali wakiwafata wananchi ambao nao waliongozwa na mtu mmoja kuelekea kule niliposhambuliwa hususani eneo lile la kichaka ambako sikubahatika kuona kilichopo na ndipo mara baada ya askali kufika pale huku wakiwa na matochi makubwa yenye mwanga mkali tulishuhudia maiti mbili ya mama na mtoto mdogo zikiwa zimekatwa katwa vibaya. Nilijihisi kuchanganyikiwa hasa baada ya kuona nguo za kale katoto ndio zilezile alizovaa mwanangu siku hiyo. Nilipiga kelele kwa kumlilia zaidi mwanangu nikiamini nae wamemuua sambamba na mke wangu lakini chaajabu ndio kwanza nilizidi kuchezea vitasa na maneno makali kutoka kwa wale mapolisi huku wengine wakinipiga picha.
“Afande Jacobo sogeza gari pia afande Dula weka hilo panga vizuri hapo mbele hakikisha mtu yeyote asilishike direct bila groves pia inabidi turisachi hili liuaji vizuri tuone kama kutakuwa na ushahidi zaidi.. hakikisheni kila tukio linapigwa picha” Aliongea afande mmoja alioonekana mkubwa wao, wakati huo wote mi nilikuwa nalia sana huku wananchi wakinitazama kwa hasira mno.
Ajabu kilichonistua zaidi na kufanya nipoteze fahamu kwa mara nyengine ni mara baada ya kuanza kusachiwa kabla ya kupandishwa kwenye difenda. Ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni kwani kwenye mifuko yangu ya mbele ya suruali nilikutwa na kipande cha kiganja cha mkono wa mtoto kikiwa kimezungushiwa hirizi. Aaaaaghhh!!!!!!!!! sikuaminiiii hata chembe nikionacho na mara ndipo nilipojihisi kizunguzungu cha ghafra na network zangu zilizima palepale.
Nilirejewa na fahamu mara baada ya kustuliwa kwa kumwagiwa maji mengi ambapo nilikuwa nimelala kifudi fudi ndani ya bodi la difenda iliyokuwa imesimama na nilipoinua kichwa niligundua nilikuwa peke yangu lakini nilipogeuka sasa kutazama vizuri ndipo nilipoona gari nyingi za polisi zikiwa zimepaki huku askali wengi sambamba na waandishi wa habari walikuwa wamesimama wakinipiga picha nikiwa kwenye ile Difenda hadi walipopanda askali wengine na kunishusha mkuku mkuku huku wakinisukuma na kuniongoza kwenye jengo moja ambalo niliponyanyua uso niliona maandishi makubwa yaliyosomeka KITUO KIKUU CHA POLISI KINONDONI
Nilijua sasa kumbe hatukua kule polini bali tupo mjini na ni katika kituo kikubwa cha polisi ambacho awali nilizoea tu kukisikia na kukiona kwa mbali huku sikuwahi kuwaza hata siku moja kama nami ningekuja kuingia eneo lile kama mtuhumiwa tena kwa kesi mbaya mno. Sikujua tulichukua mda gani kutoka kule porini kutokana na kupoteza kwangu fahamu na mpaka muda ule akili zangu hazikukaa sawa kabisa na kila kilichokuwa kinaendelea niliona kama ndoto ama sinema tu na si kitu halisi japo ukweli ulibaki kuwa haikuwa ndoto wala sinema. Nakumbuka baada ya kuvuliwa mkanda na viatu nilisongomekwa katika selo moja huku nyuma yangu nikiandamwa na virungu mfululizo hasa pale nilipotaka kusimama kuongea chochote lakini nafasi hiyo sikuipata. Niliingia ndani ambapo kulikuwa na mahabusu wengine wakinishangaa kwa jinsi nilivyokuwa, nilijituliza na kukaa kitako kwenye kona ya kuta ya selo ile na kujikuta naanza kulia kwa uchungu mkubwa hasa nilipokumbuka maiti zile ambazo nilikuwa na uhakika kuwa ni za familia yangu hususani nilimlilia sana mwanangu kipenzi kwa kuuawa bila kosa lolote.
“Oyaaa M baba mbona unaleta uduanzi sasa… hebu tukaushie usituchulie hapaa tutakunjenga ooohooo..”
Ilikuwa ni sauti ya kiteja iliyondamana na kofi lililonikuta kichogoni na kunistua kwenye dimbwi la huzuni na mawazo na kunifanya nipunguze mdadi wa kulia kwa sauti na kubaki machozi yanaendelea kububujika yenyewe huku nikiomba kupambazuke haraka. Asikwambie mtu selo pabaya sana hakuna hata chembe ya raha, harufu mbaya ya kinyesi tulichokuwa tunalala nacho kikiwa kwenye ndoo mpaka asubuhi ndio mtu anaenda kumwaga, hakukuwa na vigodolo wala shuka ya kujifunika na siku watu wakiwa wengi unakosa hata sehemu ya kukaa na kubaki umesimama daaah!! ni afadhali walau maisha ya huku jera japo nayo si mazuri. Nakumbuka baadae asubuhi yake nilichukuliwa na kuingizwa katika chumba maalum cha mahojiano na mateso na huko nilikutana na askali watatu mmoja wao alikuwa mrefu mtu wa milaba minne ambae ndie alienikalisha kwenye kiti cha chuma na kuanza kunihoji huku wengine wakiandika na kurecord.
“Taja lijina rako upesi..” Alianza kuniuliza kwa ukali kidogo yule afande baunsa. “Naitwa Hussein afande.. hus..sein..” Nilijibu huku nikiwa na hofu. “Taja vizuri bwana Lihuseni nani?” “Hus..sein.. Bakari..kaka.” “Nani likaka lako wewe?! sina dogo likatiri na Riuaji kama wewe Ebo!.. haya sema kwanini uliua familia yako?” “Familia yangu!! hapana.. afande sijaua yeyote mbona..!!” “KELELE.. Tuna ushahidi wa kutosha na tumekukamata eneo la tukio. Unataka kudanganya chombo cha dora wakati vielelezo vyote tunavyo?..! lichawi likubwa wewe ngoja nikupe chai kwanza..” Aliongea kwa hasira yule afande huku wenzake nao wakinikandamiza zaidi kwa tuhuma za ukatili ambao sikuwahi hata kuuwaza kama kuna binaadam anaweza kufanya vile kwa familia yake mwenyewe aliyoipenda. Nilifungwa barabara kwa kuinamishwa nikiwa nimekaa kwenye kiti kile cha chuma kilichokuwa na mfano wa kisturi (hakina uegemeo) huku viwiko vya mikono yangu vikiwa sambamba na magoti yangu na kubananizwa pamoja hali iliyofanya nibaki nusu nimekaa nusu nimeinama na ndipo mateso makali yalipoanza sambamba na mijeredi.
Niliumia sana na kulia mpaka sauti ikaanza kunikauka kutokana na mateso yale makali asubuhi ile. Niliwaambia na kuwaapia kadri nijuavyo kuwa sijahusika na tukio lolote baya zaidi ya kwamba mimi na familia yangu ndio tulivamiwa lakini maneno yangu ndio ilikuwa kama chachu ya kufanya mateso yaongezeke zaidi. Nilitamani hata kifo kije muda ule lakini nacho kilikuwa mbali na mimi. Oooh! sikuamini kama Hussein mimi ambae sikuwa na rekodi hata ya kushtakiwa kwa mjumbe tu ktk makuzi yangu wala kuwahi japo kumtishia mtu na kiwembe achilia mbali kumkata, lakini leo hii nateswa vikali kwa kosa la kuwakatakata na kuwaua vibaya mwanamke na mtoto mdogo? tena eti ni familia yangu? yaani mke wangu na mwanangu mwenyewe!!? aaaaaghhhhh!!!!! kwa mara nyengine nilizimia tena katikati ya mateso yale makali.
Nilizinduka baada ya siku mbili na kujikuta nipo hospitali nikiwa nimetundikiwa madripu huku mkono mwengine ukiwa umefungwa pingu sambamba na kona ya kitanda nilicholalia na pembeni yangu bado kulikuwa na ulinzi mkali. Sikuwa na cha kuongea zaidi ya kububujikwa machozi tu huku moyo wangu ukiniambia kuwa ndio nishaangamia tena sitoweza kubadilisha ukweli labda utokee muujiza. Baada ya kupata ahueni nilichukuliwa tena mkuku mkuku na askali kisha nikapandishwa kwenye difenda na ndipo mlio wa toori toori (king’ora) ulisikika na safari ilianza kutokea pale hospitali mpaka tulipofika kwenye jengo moja ambalo nililijua vizuri tu kwa nnje kwani ilikuwa ndio njia yangu kubwa ya kupita pindi niendapo na nirudipo kazini, aaaah! ama kweli usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Leo hii hussein mimi naletwa sehemu hii!!? tena kwa staili hii..? Nilijiuliza pindi niliposhushwa na kuzungukwa na askali wenye bunduki na kuanza kuelekea kwenye jengo lile huku eneo zima kukionekana watu wengi hasa waandishi wa habari. nakumbuka nilinyanyua kichwa kwa mara nyengine na kuyasoma vizuri maandishi yale makubwa yaliyokuwa kwenye lango kuu la lile jengo yaliyosomeka MAHAKAMA KUU YA TAIFA. Nilishusha pumzi na kichwani niliisikia sauti ikinambia ‘Umeangamia Hussein’
Sikuwa na chaguo zaidi ya kutii kila nilichoelekezwa mule ndani ambapo zamu yangu ilipofika niliongozwa na askali wawili na kufikishwa kizimbani kusikiliza kesi inayonikabiri. Niliangaza huku na kule ndani ya mahakama ile huku kila niliyemtazama alinitazama kwa jicho baya tu na hali iliyoniashiria kuwa nina kesi nzito sana na mbaya mno, nilibaki nimeinamisha kichwa na masikio yangu kuyaelekeza kwa hakimu pale juu japo akili zangu tayari zilishanambia kuwa Nimekwisha. Hakimu yule ambae alikuwa ni mwanamke alianza kusoma kesi yangu kama ifuatavyo…..
…………. ” Ndugu Hussein Bakari, Unashtakiwa na jamhuli kwa kesi inayohusu mauaji ya kikatili na ya kinyama kama ifuatavyo;……. Mnamo tarehe kumi mwezi wa pili mwaka huu majira ya saa tatu usiku makao makuu ya jeshi la polisi kitengo cha mawasiliano ya dharula ilipokea simu kutoka kwa msamalia mwema iliyotoa taarifa kuhusu mauaji ya kinyama yaliyokuwa yanaendelea pembezoni mwa jiji maeneo ya Kibamba karibu na kijiji cha Hakipo. Taarifa ilidai zaidi kuwa huyo kijana (msamalia mwema) akiwa anatoka kijijini kwa mbali aliona mwanaume akiwa na panga mkononi wakibishana na mkewe huku wakinyang’anyana mtoto mdogo ambapo alimsikia mwanamke akimlalamikia mumewe kuwa waachane na ushauli wa mganga wasimuue mtoto wao ni heri wafe masikini, lakini mwanaume alikuwa m bishi na kumtishia mkewe kuwa kama ataendelea kubisha basi atawaua wote na ndipo hapo msamalia yule alishuhudia mwanaume yule akimrushia mapanga mfululizo mkewe na kuanza kumkatakata na kwa kuwa yule msamalia hakuonwa na yule muuaji na alishindwa kusaidia chochote kuzuia mauaji yasiendelee ndipo alipokimbilia kijijini kutoa taarifa kwa wanakijiji wenzake baada ya kupiga simu polisi na hapo ndipo vijana wa polisi walipotoka haraka kuelekea eneo husika ambako walimkuta mtuhumiwa bwana Hussein Bakari akikimbizwa na raia wenye hasira kali huku akiwa katapakaa damu mwili mzima.
Kwa uzoefu na mbinu za kiusalama, polisi waliweza kuwashawishi wananchi watulie baada ya kumkamata mtuhumiwa na kisha kupelekwa eneo husika ambako ilikutwa miili ya marehemu ikiwa imekatwa katwa vibaya sana na walilikuta panga lililogandiwa damu lililoaminika kuwa lilitumiwa kwa mauaji na kama hiyo haitoshi pia walipomsachi mtuhumiwa walimkuta na kiganja cha mkono wa mtoto kikiwa kimezungushwa kwenye kitambaa chekundu kilichofungwa kwa hirizi ikisadikika kuwa mtuhumiwa Hussein alifanya mauaji hayo kwa imani ya kishirikina. Mwisho wa kunukuu .. ” …………..
Nilinyanyua macho na kumtazama yule mama hakimu kipindi ananisomea kesi yangu huku mwili wote ukiwa umekufa ganzi nilijikuta napiga kelele kwa sauti ya juu sana ambayo sikuwahi kuitoa toka kuzaliwa kwangu “HAPANAAAAAAA…. HUO NI UONGOOOOOOO”
Hakimu aligonga nyundo baada ya kuanza minong’ono kutoka kwa mawakili na watu waliokuwepo pale mahakamani kutokana na kitendo changu cha kupiga kelele huku nikiambiwa kuwa ni kosa kisheria kwa mujibu wa katiba sikupaswa kuongea mpaka niruhusiwe na baada ya hapo ndipo mahakama ikabaki tena kimya na hakimu aliendelea kwa kusema kuwa sitakiwi kujibu chochote siku hiyo ilikuwa ni kusomewa shtaka tu ila kesi itakuja kusikilizwa rasmi baada ya miezi miwili na dhamana juu yangu ilifungwa kutokana na aina ya kesi iliyonikabiri hivyo ikalazimika nifikishwe segerea kusubiri tarehe nyengine ya kesi. Sikuamini hadi muda naingizwa kwenye karandinga na safari ya Segedansi (segerea) ilianza huku nikiwa nimepoteza kabisa matumaini ya kuishi na kumuomba mungu akilete kifo upesi kije kinichukue lakini bado kifo kilikuwa mbali nami. Nilijikuta naongea na mungu mithili ya binaadam mwenzangu ninayemuona huku nikimlaumu kwanini hanitendei haki au muujiza wa kuniokoa kwenye matatizo yale mazito yaliyonikumbuka ilihali anajua fika kwamba sijatenda kosa lolote?
Pia nilimlaumu sana mke wangu ambae hadi muda huo imani ya kuwa nae amefariki sikukubaliana nayo kwani maiti ya yule mwanamke haikufanana na alivyokuwa mke wangu ila niliamini kuwa nimechezewa mchezo mchafu na watu walioshilikiana na mke wangu mwenyewe na kuniulia mwanangu aaaaaah!! nini kilimsibu mama watoto wangu hadi akawa tayari kuacha mwanae anauawa na yeye kuondoka na mwanaume mwengine akiniachia majanga mwanaume niliyempenda na kumthamini siku zote? Ina maana Zai alikuwa msaliti..!? aagh.. lakini mbona sikuwahi kuona walau chembe ya tabia yake mbaya? Daah niliishia kujiuliza maswali ambayo yalizidi tuu kuniongezea maumivu na sikuwa na chaguo zaidi ya kukubali kuwa sasa mimi ni mtuhumiwa wa kosa la mauaji na hapa segerea ndio makazi yangu mapya mpaka pale nitapohukumiwa.
Nikiwa nimeshaanza kutumikia maisha ya kukosa uhuru ndani ya segerea nikisubiri hukumu yangu, Kumbe upande wa nje kona zote za jiji na mikoa ya jirani kesi yangu nayo ilikuwa moja ya gumzo midomoni kwa watu. Vyombo vya habari hususani magazeti ya udaku yaliandika na kuchapisha picha mbalimbali zilizohusu tukio langu la mauaji ya kinyama tena kwa familia yangu kwa sababu tu ya kutaka utajiri. Kila aliyenifahamu alishangazwa na kustushwa sana na habari zile na kutokana na mazingira niliyokutwa na vithibitisho vya uhakika vilivyoolozeshwa kwa mujibu wa habari vilifanya hata walionijua kuamini habari zile na kunilaani kuwa kumbe upole na ustaarabu niliokuwa nawaonyesha ulibeba siri nzito moyoni mwangu tena za kishirikina….!!
Ilinichoma sana na haya niliyapata toka kwa rafiki yangu kipenzi aliyejitolea kuja kuniona segerea mara baada ya ndugu na marafiki wengine kunisusa na kutotamani kuniona huku wengine wakihofia kujitokeza na kuthibitisha kuwa wananijua huenda ikawaponza kukamatwa na wao kuisaidia polisi juu ya ukatili wangu. Niliangalia baadhi ya vichwa vya habari vya magazeti aliyokuja nayo rafiki yangu yule japo niliishia kuyaona kwa mbali kupitia kidirisha kidogo cha nondo kilichokuwa katikati ya ukuta uliotutenganisha huku nikiwa bado chini ya ulinzi na uangalizi mkubwa tofauti na watuhumiwa na wafungwa wengine waliokuwa pale segerea kwa muda ule. Sikujua ni kwa sababu tuu ya uzito wa kesi yangu ama ndio taratibu za pale kwa mtuhumiwa mpya au laah.
Rafiki yangu hakunificha kitu kuhusu kazini na maagizo ya bosi kuwa nishafutwa kazi wala nisitegemee msaada wowote wa kiofisi. Daah!! yaani kwa jinsi nilivyoitumikia kwa moyo mmoja ile ofisi na kujituma kwangu kote tena kwa uaminifu wa hali ya juu sikuamini kama leo hii wameshindwa hata kuja kuniona na kunisikiliza ili walau waniekee hata wakili wa kunitetea juu ya tuhuma zile lakini loh! wao pia wamekuwa mstari wa mbele kwa kunitenga. Niliishia kutokwa machozi tu kila habari niliyokuwa naipata kutoka kwa rafiki yangu yule wa kweli na pekee aliyekuwa na moyo wa kumfariji mtuhumiwa wa kesi mbaya ya kutisha kama yangu lakini hakusita kuniamini nilichomuelekeza na kunipa moyo kuwa nisichoke kumuomba mungu kwani hakuna linalomshinda na haki yangu itasimama tu nisihofu.
Muda mfupi baadae askali walikuja kuniondoa baada ya muda kuisha na kuwapisha watu wengine ktk kidirisha kile na nilimshuhudia rafikiangu akinitazama kwa jicho la kunisikitikia na kukata tamaa hadi nae machozi yalianza kumdondoka. Nilirudi ndani ya jengo lile la kujichanganya na mahabusu wenzangu lakini haukupita muda mrefu tena niliitwa na askali wawili walinichukua kwenda kuongea na mtu mwengine ambae sikujua ni nani harafu tayari muda wa kuongea na watuhumiwa ulishakwisha. Niliongozwa na kuelekea tena pale kwenye kidirisha na niliponyanyua macho kuchungulia ni nani mwengine aliyekuja kuniona nilijikuta napata faraja na kuangusha kilio cha matumaini baada ya kumuona mtu yule na kugundua ni baba mkubwa. Nilielewa wazi ni ba mkubwa pekee ndie aliujua ukweli juu ya tatizo langu na ni yeye tu ndie nilimpigia simu kumuelezea matatizo yote na vitisho vilivyokuwa vinaniandama hadi ukweli juu ya safari yetu aliujua kwani tulikuwa tunaelekea kwake.
“Usilie mwanangu Hussein, huu ndio ukubwa baba huwezi kujiita mkubwa bila kukupitia mitihani mwanangu na unapopata mtihani inabidi utulize akili ujue jinsi ya kukabiliana nao usijiferishe kabla hujajaribu kuufanya mtihani wako hata kama utauona mgumu kiasi gani. Lakini kumbuka kauli yangu miaka ile nilikuonya kwa kukwambia kuwa ‘Mpotea njia mara nyingi si muulizaji’ laiti ungeifanyia kazi kauli yangu ile tu nadhani ungeniuliza mapema na pengine haya yote yasingekufika leo hii. Lakini sikulaumu sana kwa kupotea kwako kwa kuwa bado niko hai nitahakikisha nakutetea kadri niwezavyo kuhakikisha haki inatendeka kwani najua wazi huna kosa mwanangu, wewe si muuaji, wamekupakazia tuu na hata mkeo nina imani kabisa yuko hai. Usilie wala usihuzunike amini mungu yu nawe na ataweza kukuokoa kama utamuamini kwani kumbuka tatizo lako si kubwa mbele ya matatizo makubwa yaliyowahi kuwakuta watu na mungu akawaokoa. Usijali baba tuko pamoja nami nishajiandikisha kama shahidi wako siku ya kesi nitakupigania. “
Maneno ya Ba mkubwa yalinitia nguvu sana na faraja lakini hayakuzuia machozi yaliyokuwa yananidondoka yaache. Nilishangaa pia kuona hisia zangu zimelingana kabisa na maneno ya ba mkubwa kuwa Zai si yule mwanamke aliyeuawa siku ile na kubaini kuwa kumbe ba mkubwa alikuwa na siri nyingi kuhusu mke wangu Zai..! ina maana alimjua hapo kabla ama vipi? na jee sasa hivi yuko wapi? hapo nilikosa jibu kabisa pia nilitamani kumuuliza Ba mkubwa kuhusu huyo Mr. X kama anaweza kuwa anamtambua lakini muda wa kuendelea kuongea haukuturuhusu mara baada ya askali kumtoa ba mkubwa kule nje nami kurudishwa ndani kabisa ya gereza.
Siku zilienda hatimae ilipita miezi miwili nikiwa segerea na ilifika tarehe ya kesi yangu ambapo siku hiyo asubuhi na mapema niliingizwa kwenye karandika sambamba na watuhumiwa wengine wenye kesi tofauti tofauti na safari kuelekea mahakamani ilianza tukiwa chini ya ulinzi mkali.
Tulifika kwenye viwanja vya mahakama kuu na kutelemshwa ambapo siku hiyo niliushuhudia umati mkubwa ulifurika huku wengi wao wakinyoosheana vidole kuelekezea kwangu ndipo nilipobaini kuwa ni kweli kesi yangu ilikuwa ni moja ya habari iliyotikisa. Zamu yangu ilipofika nilifikishwa kizimbani na siku hiyo sikuwa nalia kama ilivyokuwa siku ile ya kwanza. Nilimudu kutazamana na watu waliokuwepo mule ndani ya mahakama japo wengi wao walinitazama kwa jicho baya lakini niliwapuuza na kuwasikitikia kwa kutojua walitendao.
Macho yangu niliyaelekeza kila pembe ya mahakama kwa umakini mkubwa nikimtafuta ba mkubwa na kweli nilimuona nae alikuwa ananitazama na kunipa kwa kuinamisha kichwa kuwa yupo pamoja nami na nilitegemea pia ushahidi wake pekee kuwa ndio utetezi mkubwa kwangu. Niliendelea kuangalia kona nyengine kwa makini kujua kama kuna mwengine ninayemfahamu kaja kusikiliza kesi yangu na kipindi hiko hakimu alikuwa ndio anaanza kuisoma tena ile kesi nami ktk kupepesa pepesa macho huku na kule nilimuona rafiki yangu kipenzi yule aliyenitembelea segerea na tulipokutanisha macho alitabasam kwa kunionesha ishara kuwa yuko pamoja nami. Nilijisikia faraja kwa namna furani na kumshukuru mungu kwa kuwajua rafiki na ndugu wa kweli kwangu kwani ni vigumu kumtambua rafiki wa kweli au ndugu wa kweli kama hujapatwa matatizo makubwa.
Siku hiyo ndio nilizidi kuielewa na kuimbuka misemo mingi ya wahenga ambapo awali nilichukulia kama burudani tu kwa watoto lakini baada ya majanga nikakubali kuwa Akufaae kwa dhiki ndie rafiki pia umdhaniae sie ndie, kwani sikuamini kama mjombaangu aliyetoka tumbo moja na mamaangu angeweza kunisariti na kutofika ilihali nilimthamini na kumsaidia sana huku nikimpuuza ba mkubwa kuwa ana mila za kizamani lakini leo hii niliyempuuza ndie kaja kunifariji jera na mahakamani yupo ila yule niliyemtegemea awali hata salamu zake za kunifariji sikuzipata. Ina maana ameamini mimi …
Hussein bubu aliendelea kumshangaa yule kijana pindi alipokuwa anabisha kutaja jina lake na kung’ang’ana na kusema kuwa wanawake ni wauaji mpaka yule kamanda alipopewa agizo na mkuu msaidizi wa gereza kuwa amuache ndipo alipoachwa na kujumuishwa na wafungwa wenzake kisha kupewa sare zao kabla hawajachanganywa na wenzao ndani ya lile gereza.
Muda wote cj4 alikuwa kimya na mara nyingi alionekana mtu wa mawazo sana hata walipokuwa wanatolewa na kupelekwa kwenye kazi za kuvunja kokoto ambapo Hussein bubu yeye alikuwa kwenye kitengo cha kusambaza maji ya kunywa kwa wafungwa wenzake. Hali ya mfungwa yule mpya kutopenda kuzungumza na kufanya kazi kwa nguvu huku akionesha ni mtu mwenye mawazo mengi ilianza kumvutia Hussein bubu na kujikuta anaweka ukaribu nae kwa siku tano tu baada ya kuja kwake na Hussein alijifariji moyoni kuwa yule ni mtu pekee anayeweza kukaa nae kwani alihisi yaliyomkuta ni makubwa kama yaliyomkuta yeye. Lakini kichwani kwa Cj4 alikuwa na nia moja tu ya kutimiza agizo alilopewa na Mkuu wa majeshi lililotoka kwa Amiri jeshi Mkuu mh Rais wa jamhuri a Muungano wa Tanzania. Ukaribu alioutengeneza kwa mbinu maalum na kumteka Hussein bubu pasi na kutarajia ilikuwa moja ya hatua kubwa aliyoidhamiria Cj4 na taratibu Hussein alianza kufunguka kumpekua Cj4 ili kujua kulikoni kilichompata japo awali Cj4 alionesha ugumu wa kutopenda ukaribu na Hussein lakini baada ya wiki moja aliamua kuwa mpole na kipindi cha mapumziko ama chakula walikaa pamoja na taratibu Cj4 alianza kumsimulia Hussein mkasa wake wa uongo lakini uliomhuzunisha sana Hussein na kujikuta nae anamsimulia mkasa wake mpaka yuko pale na ndipo walipotengeneza urafiki.
“Laiti kungekuwa na askali muelewa na mwenye roho nzuri nadhani angesikia kilio changu na kunisaidia lakini daaah!! nawachukia sana hawa askali wetu wooote wapuuzi na makatili watupu” alilalama siku moja Cj4 alipokuwa anapata chakula cha jioni sambamba na Hussein bubu. “Dah! pole mwanangu lakini kumbuka si askali wote wabaya.” alitetea Hussein bubu “Hapana mzee we kufungwa kote huku na kuteseka kwa kesi usiyoitenda hadi unafikia huko mbona hajatokea hata askali mmoja kujipendekeza walau kiuongo kwa kukuonea huruma ama kukusaidia kivyovyote?? hawa wanyama tuu usiwaamini babu” alizidi kukazia Cj4 lakini alifanya haya yote kwa makusudi ili kumtia katika kumi na nane zake Hussein pasi na kutambua na kuanza kufunguka ajenda kuu aliyoifata na siku hiyo ilikuwa ni siku ya kumi na mbili tangu afungwe pale na siku tano tangu wawe marafiki.
“Sikia nikwambie mwanangu, mi mwenyewe awali niliamini hivyo na nilikaa kimya zaidi ya miaka ishirini lakini baadae alitokea askali ambae sikuwahi kuwaza hapo awali kama anaweza kuwepo askali mwenye roho ya imani tena mkubwa kama huyo bwana ambae alinihurumia na kufanya kila jitihada za kunisaidia na kuutafuta ukweli wa kesi yangu japo ni ya miaka mingi sana. aaah! usihofu mwanangu wewe kesi yako bado changa sana usijikatie tamaa hivyo naamini kama yule kijana asingepatwa matatizo na angekuwepo nadhani toka siku ile ya kwanza unaingizwa hapa angeshakwita kutaka kujua kilichokusibu na ungestaajabu mwenyewe.”
“Mh! siamini mzee kama kuna mtu kama huyo… yaani atake kukusaidia juu ya kesi yakoi ya miaka mingi? angeanzia wapi??” “Aaagh! baba inabidi uamini tu kwani hiki nikuambiacho si ndoto” “Mh! basi huenda atakuwa alikuongopea tuu kwa kuwa wewe upo ndani usingejua chochote.” “Naamini asilimia zote hakuwahi kuniongopea kwani hata matatizo yaliyosababisha asiwepo hapa leo hii naamini ni kwasababu yangu asilimia tisini.” aliropoka Hussein na kutupa plate ya chakula na kusogea pembeni huku machozi yakianza kumtoka baada ya kujitonesha kidonda chake makusudi na kuanza kumkumbuka Kamishna Shebby ambae mpaka muda huo hakujua anaendeleaje japo alijua kuwa alinusurika kule kwenye shambulizi Mkuyuni. Ukaribu wa Dokta Asha na Kamishna Shebby ulianza kuwavuta katika hisia moja mioyoni mwao japo kila mmoja alibaki akimuonea soni mwenzake hasa Kamishna Shebby. Hata mzee Mwinchande na mkewe walibaini kitu hiko na walitamani mtoto wao amuoe yule Dokta hasa walivyoona jinsi alivyokuwa anamuhudumia kwa upendo na ilikuwa kawaida halali hadi muda Shebby amelala na kabla Shebby hajaamka ye anakuwa tayari yuko macho. Yaani kwa jinsi Dokta Asha alivyojituma kumuhudumia Shebby hadi mzee Mwinchande akaona kile kiasi anachomlipa hakitoshi japo ilikuwa ni zaidi ya milioni kumi kwa wiki.
* * * Siku moja ambapo ilikuwa siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Kamishna Shebby huku wakialikwa watu wachache sana katika hoteli maaalum waliyoikodi kwa niaba ya tafrija ile. Shebby akiwa bado kumbukumbu zake hazijakaa sawa aliongozwa na Dokta Asha katika kila steji wakati tafrija ilipokuwa inaendelea hadi wakati wa zoezi la kukata keki japo aliweza kusimama bila kutegemea gongo na kutembea mwenyewe lakini bado balance ya mwili ilikuwa haijakaa sawa na ndio sababu Dk, Asha hakuwa mbali nae. Ki ukweli dk Asha na Kamishna Shaaban walipendezana sana na hata wahudumu wa hoteli walijua kuwa ni wapenzi lakini haikuwa hivyo na kabla Shebby hajamlisha yeyote keki mc alimuomba azungumze chochote kuhusu siku yake ile ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake na ndipo taratibu baada ya kukamata kinasa sauti na kuangalia huku na huko Kamishna Shebby alianza kuzungumza na kila mtu alitulia akimtazama na kumsikiliza kwa umakini.
“Kwa kweli kikubwa namshukuru sana Mungu kwa kunifikisha umli huu japo bado naumia moyoni mwangu kwa kushindwa kukumbuka yaliyonikuta hadi muda huu pia napenda nichukue nafasi hii kumshukuru sana tabibu wangu aliyejitoa kwa hali na mali kuhakikisha nakuwa mzima na kutembea kama zamani ila ningependa pia nimwambie kitu kilicho moyoni mwangu na kila mtu nataka asikie ili nimuaminishe pia nimuhakikishie kuwa hiki ninachoongea kinatoka kweli moyoni mwangu na si vinginevyo…” alipofika hapa kamishna Shebby alinyamaza kidogo na kumtazama dk Asha aliyeonesha nae kuwa na shauku kubwa ya kusikia hiko kitu ndipo Shebby alipoendelea “Dokta Asha.. Dokta Asha Nakupenda sana na naomba ukubali niwe wako ili tuunganike na kuwa mke na mume siku za usoni tuzidi kutengeneza ukaribu na kuzalisha familia bora pamoja. Naomba unikubali Asha na kama utanikataa naomba uthibitishe mbele ya wote wanaonisikia sasa hivi humu ndani. Kwanini niutese moyo wangu kwa kuficha ukweli halisi uliomo? Nakupenda sana dokta Asha nikubali tafadhali..” Maneno ya Shebby yalimstua kila mtu aliekuwa ukumbini na kufanya watu wote wamgeukie Dokta Asha ambae alijikuta anainamia chini kwa aibu na mshangao kwa kutoamini kama kweli mgonjwa wake ambae hata yeye mwenyewe alishaanza kuwa na hisia nae za uhitaji wa kuwa karibu zaidi lakini hakufikiri wala kuzani kama Shebby angefikia hatua ile ya kutamka maneno yale hadhalani vile.
mzee Mwinchande alitabasamu sambamba na mkewe mara baada ya kumsikia mtoto wao wa pekee akisema yale maneno na kuanza kumpigia makofi kwa ujasiri aliouonesha na kuwafanya na watu wengine taratibu kuanza kumpigia makofi Kamishna Shaaban na hapo ndipo mc alipochombweza kidogo kwa maneno ya bashasha na kupiga wimbo mmoja wa kizungu ulioimbwa na westlife ujulikanao kama Queen of my Heart na hapo ndipo Dokta Asha alipoinuka huku uso wake ukibubujikwa na machozi mepesi ya furaha na kwenda kumkumbatia Kamishna Shebby kwa kuashilia kuwa alikubali kwa moyo mmoja ombi la kamishna Shebby. Na hivyo ndivyo mapenzi baina ya kamishna Shebby na Dokta Asha yalivyoanza rasmi.
* * * * * *
Cj4 alimsogelea Hussein bubu na kumshika bega “Pole sana mzee wangu lakini kwanini unaamini kuwa matatizo yaliyompata yamesababishwa na wewe” aliuliza kwa upole Cj4 na kumfanya Hussein akiuvunja tena mwiko wake aliojiwekea na kuanza kumuhadithia kwa ufupi kilichotokea baina yake na Kamishna Shebby kwa kuamini kuwa yule aliyekuwa anaongea nae ni mfungwa mwenzake aliyeponzwa na mwanamke na kubambikiwa kesi ya kuhuzunisha kama yeye bila kujua sivyo alivyofikiri bali alikuwa anatoboa siri kwa Komandoo aliyeletwa pale kwa kazi hiyo maalum ya kutafuta kilichomsibu kamishna Shebby hadi aende kwenye mission ya siri iliyopelekea vifo vya askali wenzake na kusababisha kupoteza kwake kumbukumbu. “Kwa hiyo daah! kumbe kuna mtu anajiita mr.X ndie aliyekuwa anamuumiza kichwa huyo Kamishna?” “We acha tu mwanangu ila nakuomba habari hii usije kuongea na mtu mwengine yeyote kwani sipendi kabisa matatizo mengine yatokee. Sina imani na huyo Mr.X huenda akawa jini ila namuomba Mungu siku moja nije kumuua mimi mwenyewe kwa mikono yangu.” alisisitiza Hussein bubu na muda huo huo firimbi ilipulizwa na muda ulikuwa umeisha wa kupumzika hivyo walinyanyuka na kuendelea na kazi.
Lakini baada ya siku tatu baadae Hussein bubu anastushwa na taarifa za kutoweka kimaajabu kwa mfungwa ambae ndie yule rafiki yake walietokea kuzoeana ghafra. Hakuzielewa haraka tetesi zile ambazo zilizuka kwa wafungwa wengine ambao walikuwa wamefungwa ukanda mmoja na yule kijana swahiba wa Hussein kutokana na yeye kuwa upande mengine ambao alihamishiwa kipindi cha nyuma kwa msaada wa Kamishna Shebby. “Kh!! sasa katorokatoroka vipi? au alikuwa jini yule?? “ lilikuwa ni moja ya swali lililomuumiza kichwa Hussein baada ya kuthibitisha kuwa yule kijana hayupo tena ndani ya gereza na kuna timu ya maaskali iliyotumwa kufanya msako juu yake.
* * * * * *
Ndani ya kijiji cha mkuyuni stendi kuu iliyokuwa mkabala na soko alionekana kijana mmoja aliyevaa nguo chakavu akishuka kwenye roli lililotokea mjini na kuja pale mkuyuni kwa ajili ya kupakia ndizi. Akiwa kabeba fuko lake la rambo na mkononi kashika pingili ya mua aliokuwa anaumenya taratibu kwa mdomo huku akipiga hatua mdogo mdogo kutokea kule kwenye lile roli mara baada ya kuwashukuru wahusika waliokaa mbele akionesha dhahili alibebwa kwa msaada tu, ndipo yule kijana alianza kuchanja mbuga na kuelekea mabondeni akiifata njia moja iliyoelekea ndani kidogo ya maeneo ya soko huku watu wengi aliokuwa anapishana nao walionesha kumshangaa japo hakujua walimshangaa kwa jinsi alivyo au kutokana na ugeni wake pale Mkuyuni.
“Samahani babu shikamoo” alisalimia yule kijana alipomkuta babu mmoja akiwa kabeba jembe akielekea njia ile aliyokuwa anaenda yeye. “Asante mzukulu, kugenda kwani?” aliuliza yule mzee ambae ilionesha kiswahili chake hakikuwa kizuri zaidi aliongeama kwa lugha ya kirugulu ambayo haikumpa tabu sana yule kijana. “natafuta sehemu mzee nitayoweza kupata chumba cha bei nafuu sana niweze kujisitiri” “Ng’andaaa mh! tuke huku kwani we mgeni mzukulu?” “Ndio babu” “Tapata tuke hakuna ng’anda zimema” aliongea yule babu na kuongozana na yule kijana hatimae wakafika kwenye kijiji kimoja ambapo kulikuwa na nyumba ambayo ilikuwa kama imetelekezwa kutokana na matukio yaliyowahi kutokea mtaa ule na alionekana mama mmoja aliyerukwa akili (chizi fresh) akiwa pekee anayeishi pale. “Ahano ng’anda hii mzukulu tuke kwa mjumbe ukamlongele akusaidile utawasa tu mzukulu”
alionesha ile nyumba yule mzee kisha kwenda nae sambamba kwa mjumbe ambae hakuwa mbali na eneo lile na ndie alikuwa kama mmiliki wa haki ya nyumba ile na walipofika mzee alisalimiana na mjumbe kisha kumkabidhi mgeni wake huku akimsisitiza amsaidie. “sawa kijana karibu, Enhee umetoka wapi, unaitwa nani, na ipi hasa shida yako” “Mzee mi naitwa Ndonga ni mgeni kabisa nimetokea Kilosa nilipoenda kumtafuta kakangu ambae sikufanikiwa kumpata baada ya kutoka kwetu Kigoma na kumtafuta kwa muda mrefu hadi nikakosa muelekeo pale kilosa ndipo nilipoelekezwa kuwa alihamia hapa mkuyuni sasa naomba unisaidie sehemu ya kulala hata kwa kulipia pesa kidogo kwani uwezo wa kulipia guest sina na ndio nimeelekezwa hapa na yule mzee tafadhali sana mjumbe naomba msaada wako nihifadhi mtoto wako”
aliongea kwa lugha ya upole na unyenyekevu yule kijana na kumfanya mjumbe amtazame huku akifikiria jinsi ya kumsaidia. “Mh! kijana wanguuuu kiukweli hapa mkuyuni nyumba ni gharama japo unapaona kijijini ila kuna nyumba moja ambayo inaweza kuwa rahisi kuipata kwa kuwa ilikuwa ya marehemu babaangu kabla hajamuuzia mganga furani ambae nae alishafariki, lakini sasa pale kuna matatizo kidogo yalitokea na watu wote waliikimbia ile nyumba kasoro mama mmoja ambae kidogo akili zake hazipo sawa ndio yupo pale. sasa sidhani kama patakufaa ama wewe ulionaje?” “Mh! mzee wangu yani mi siwezi kubagua sehemu ilimradi nihifadhi ubavu wangu kwa visiku hivi nikiendelea kumtafuta ndugu yangu” “Sawa sasa itabidi nikuandikishe kisha nikupeleke sehemu yenyewe hapo mbele tu ila naomba uwe muangalifu usije kuthubutu kumghubudhi yule mama japo akili zake hazipo vizuri” “ondoa shaka kabisa mjumbeee Aaagh! Mungu akubariki sana baba kwa msaada wako” alishukuru huku akipiga magoti yule kijana na kutoa noti ya shilingi elfu tano iliyochakaa sana kutokana na fundo alilolifunga sehemu za pensi lake alilofunga kwa mkwiji wa kamba ya mti.
Baada ya kuafikiana na mjumbe alipelekwa kwenye ile nyumba iliyokuwa imepooza na kwa nje walimuona yule mama ambae aliwaangalia tu bila kusema kitu na baada ya mjumbe kumuonesha chumba cha kutumia huku akimwambia kuwa kama atakaa wiki moja pasi na kuonana na huyo nduguye itabidi ampeleke kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa ili atambuliwe na ikiwezekana aandikishwe kama mkazi wa eneo lile ili kila mtu aelewe ujio wake. Baada ya hapo Mjumbe alitoka mule ndani na kumuacha yule kijana akikung’uta mavumbi kwenye kile chumba kilichokuwa na mkeka na kigoda cha miguu mitatu tu. “Shabbashh Nice Step creat another good Chance” alijisemea mwenyewe yule kijana na kugonganisha mikono yake huku akiwa na furaha mno moyoni mpaka usoni. Hakuwa mwengine yule kijana bali ni Komandoo Jumanne ama Cj4.
* * * * * *
Baada ya siku kadhaa kupita tangu kufanyike ile tafrija ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwa Kamishan Shaaban na kuanza rasmi mahusiano ya kiuchumba baina yake na Dokta Asha, siku hiyo walionekana wakiwa wawili maeneo ya fukwe huku dereva ambae alikuwa ni mlinzi pia aliyetumwa na jeshi la polisi kwa niaba ya kuchunga usalama wa Kamishna Shebby alikaa sehemu moja ya juu akiwaangalia wapendanao Shebby & Asha wanavyokokotana na kurushiana maji maeneo ya fukwe huku wakiwa na nyuso za furaha.
“Nakupenda sana Asha” “Hata mimi Shebby tena nilikupenda toka siku ya kwanza nilipokuona” “Haa acha utani Ashaa” “Kweliii” “sasa kwanini hukunambia mapema hadi nimekuanza mimi” “aaah! si nlikuwa naogopaa!” “tehtehteheee huyoo”
Basi ilikuwa full upendo maeneo ya fukwe pindi walipokuwa wanataniana na kuchombwezana baina ya Kamishna Shebby na Dokta Asha. Hata jioni yake waliporudi nyumbani kwenye jengo kubwa la kifahari la mzee Mwinchande bado waliendelea na utani wa hapa na pale mpaka wanaingia kulala ambapo ulikuwa ni usiku wa tatu toka waanze kulala pamoja lakini walilala kindugu ndugu kwanza kutokana na maelezo ya Dk Asha kuwa inahitajika Shebby kujiponesha zaidi na atapokuwa sawa aende kujitambulisha kwao pindi ataporudi na wakioana ndipo watapata uhuru wa kucheza sebene pamoja muda wote hasa nyakati za giza.
Lakini muda mwingi Kamishna Shebby anapokuwa amesinzia Dk Asha hutumia wakati huo kumuangalia vizuri Shebby na kumpekua sehemu za kichwa huku akimuonea sana huruma hadi muda mwengine machozi yalimtoka bila kujitambua Asha lakini hakuwa na chochote cha kumwambia Shebby zaidi ya kunyamaza na kumsikitikia. * * * * * *
Asubuhi na mapema ndani ya Kijiji cha Mkuyuni kwenye nyumba ile ile ya mzee Mnyungunyungu ambayo shabaha na mipango ya Cj4 ilienda barabara na kutua sehemu husika kabisa na hesabu zake alizopiga awali ili kubaini kilichowakumba askali na kilichoikumba ile familia zaidi akitafuta ukweli wa huyo mr X.
Alijinyoosha pale ndani na kutoka nje asubuhi na mapema na kuelekea kule kwenye choo ambapo njia yake ilionesha kuwa na majani majani yaliyoashilia kuwa kile choo alichokuwa anaenda yeye hakikutumiwa muda mrefu kidogo. Alitembea taratibu huku akipiga hesabu nyingi kichwani kutokana na maelezo aliyokuwa nayo juu ya tukio la mtu wa mwisho wa familia ile ambae inasemekana alikutwa amejinyonga ama amenyongwa pindi alipoenda chooni. Kwa kutumia akili za kijeshi na mbinu hadimu alizokuwa nazo Cj4 alisimama ndani ya kile choo na kuangalia juu ambapo kulikuwa na matawi makubwa ya miti yaliyokatisha na kuvuka kile kipaa cha choo ambacho kilikuwa hakijaezekwa na alitumia dakika tano kutazama vizuri kule juu na kuanza kurudi nyuma huku akivuta taswira na kutengeneza picha kichwani mwake ambapo alianza kuona yule mtu alipoingia pale chooni na aliangalia kwa juu na kuona kamba iliyotengenezwa mtindo wa kitanzi kikubwa ikishushwa taratibu na kumvaa pindi aliposimama na kabla hajafurukuta kitanzi kikapandishwa na kumkaba shingoni.
Alizunguka kwa nyuma ya choo Cj4 harakaharaka huku ile taswira ikiwa bado kichwani mwake na kuangalia upande wa juu na kuona kuwa alilala mtu shupavu na makini aliyevaa nguo maalum na vifaa vya kininja akiwa anaivuta ile kamba kwa kuizungusha kwenye skurul aliyoifunga kwenye tawi ambayo ndio ilishikilia ile kamba maalum aliyomshushia na kumkaba yule bwana aliyekuwa chooni na kupanda juu taratibu huku akiwa anapapatika na kushindwa kutoa sauti kwa jinsi alivyokabwana na pindi alipofikishwa juu kabisa ya lile tawi alikuwa tayari ashakufa na alichofanya yule ninja aliyekuwa anamuona kwa taswira tu kuwa alichomoa skurul baada ya kuivinga kamba yenyewe kisha kumuacha yule mtu akiwa ananing’inia pasi na kumgusa mithili ya mtu aliyejinyonga mwenyewe.
Alizunguka tena Cj4 na kuendelea kuiona taswira kuwa yule Ninja alishuka na alipofika chini akaondoka kabisa eneo lile. Ndipo akaanza kufata hatua alizohisi moja kwa moja alipita yule muuaji. Wakati huo Cj4 alikuwa makini mno na akiwa anaendelea kutokomea kabla hajafika mbali alistuka baada ya kusikia mtu akipiga chafya na alipogeuka kumtazama alimuona kwenye kichaka kilichokuwa jirani na ule mti mkubwa na ilionesha wazi yule mtu alikuwa anamtazama kwa muda mrefu tu hasa kwa jinsi nae alivyostuka baada ya kutazamana uso kwa uso na Cj4
“Afadhali mzee nadhani wewe utanisaidia” aliongea Cj4 na kupiga hatua kumfata yule mtu ambae alikuwa ameshika Mundu (panga la kienyeji) na kifuko kilichokuwa na maembe ambapo alijibainisha pale pembezoni mwa mti mara baada ya kujua kuwa kaonekana pindi alipokuwa anamshangaa yule kijana. “Mh! mbona sikufahamu baba?” aliuliza kwa hofu kidogo yule babu ambae alimtazama vizuri Cj4 na kupatwa woga nae wa ghafra hasa alivyomtazama sehemu za kifua na mikono huku uso wake ukionesha ni mtu wa tofauti sana kwa jinsi alivyokuwa bussy muda uliopita kabla hajamstua kwa kupiga chafya. “Mi mgeni hapa mzee wangu nimeingia jana tu na nimesaidiwa na mjumbe kulala hapa lakini alinambia kuwa wenyewe waliikimbia hii nyumba na watu wengi wanaiogopa sasa ndipo nami nilipokuja chooni kujisaidia moyo umeniripuka na kujikuta nakuwa na woga sana ndio maana nilikuwa naondoka nikajisaidie kule porini.” “Hee! baba basi mi naenda shamba we kajisaidie tu huko hata wanakijiji wengine mbona wanajisaidiaga porini.” aliongea yule mzee na kuanza kuondoka huku moyoni mwake akiwa na hofu bado “ “Samahani lakini babu naomba nisikilize kama utakuwa na uwezo wa kunisaidia” alisisitiza Cj4 na kumshika mkono yule babu aliyekuwa ameanza kuondoka eneo lile. “Mwe!! haya nokutegeleza” alijibu mtindo wa sitaki nataka yule babu na kusimama tena “Ni hivi babu hebu njuu kwa huku kwanza nataka tuongee kitu muhimu na nitakupa pesa nyingi ili unifichie siri hii babu, ukweli mimi ni Polisi na nimetumwa hapa kupeleleza juu ya kilichotokea hapa juu ya mtu aliyenyongwa siku za nyuma, na nimekuja kuondoa uoga uliotawala eneo hili” aliongea safari hii kwa sauti ya chini Cj4 na kumfanya yule mzee atulie na kusikiliza kwa umakini huku moyo wake ukifurahi ghafra kwa kujua kumbe yule ni mwanausalama.
Ndipo yule mzee alianza kumfata taratibu kwa kunogewa na story aliyokuwa anahadithiwa na Cj4 huku wakiingia kwa msituni kidogo kukwepa watu wasiwaone pia yule mzee alimuongoza Cj4 hadi maeneo yale yalipowahi kutokea mauaji ya Askali miezi kadhaa iliyopita baada ya kuulizwa kama anapafahamu. “Mh! baba nakuahidi ambe hajatuona mtu tukiongea,! na eneo hili watu wengi wanaogopa kufika hadi sasa hivi, basi hatojua mtu yeyote habari zako baba Niamini.” aliongea yule babu pindi walipofika eneo lililoshona majani mengi na miti mikubwa. “Ni kweli mzee, lakini tatizo hata Askali aliyekuja kupeleleza awali alifanya ujinga kwa kumuamini mzee kama wewe na mwishoe akamsaliti na kusababisha Mauaji kwa askali wengine.” Alinena kwa sauti tofauti iliyokuwa serious zaidi Cj4 na kumfanya yule mzee astuke hadi akaangusha kile kifuko chake cha maembe na na kabla hajageuka alistukia kashakamatwa kichwa kwa mikono shupavu ya Cj4 na kuanza kubinywa hadi sehemu za taya zikaanza kupishana na hakuwa na uwezo walau wa kutoa sauti ama kupiga kelele. “Kawaambie huko uendako kuwa Umekumbana na mstari Mwekundu wa CJ4” Mara Cj4 aliponena maneno hayo tu palepale alipindua kwa nguvu kichwa cha yule babu na kuivunja shingo yake kisha kumuachia na kudondoka kwenye manyasi ambapo alianza kupapatika pale chini kwa zaidi ya dakika kumi mpaka akatulia na kuaga dunia rasmi.
“Kama na wewe uliekwa na mr.X ufanye uchunguzi wa watu wataokuja kuchunguza hapa basi ajue kuwa mbinu zake zimezeeka” aliongea Cj4 na kuchukua ile mundu ya yule babu na hapo aliuvinga mkono wake mmoja kwa kile kifuko kilichokuwa na maembe baada ya kumwagika pale chini kisha akatumia mkono ule wenye mfuko wa naironi kukamata sikio la yule babu na kuanza kukata ngozi yote upande wa sikio la kulia sambamba na sikio lenyewe kisha alimgeuza na kufanya vile vile upande wa sikio la lengine na kumuacha. (“sasa na waje tu wakupime pindi watapojua”) aliwaza moyoni Cj4 huku akiifuta futa damu ile mundu kwenye manyasi na kuzishika vizuri zile ngozi zenye vipande vya masikio na kuanza kupiga hatua kadhaa kuelekea kule alipotoka na alipokaribia kwenye ule mti wa awali alisimama na kuchimba kishimo cha futi moja na kuzizika zile ngozi kisha akafukia na kuweka weka nyasi juu yake ambapo ilikuwa vigumu sana mtu kubaini kama sehemu ile imechimbwa. Alifanya hayo yote ili hata kama wataigundua ile maiti mapema na kuja wachunguzi kupima watachojua ni kuwa amevunjwa shingo tu, lakini hawatapata alama zozote za muhusika aliyemvunja hususani zile za mikono. Baada ya kuhakikisha mambo safi huku akiwa makini asionekane na mtu yeyote alinyanyuka na kuelekea hadi pale kwenye kile choo kwa uangalifu na kuitumbukiza ile Mundu chooni lakini alipotoka chooni tu na kufunua kile kigunia kilichofungwa kama mlango alikutana uso kwa uso na mtu akiwa kasimama pale pale mlango wa choo.
* * * * * *
)(‘nashukuru nimemchunguza ananipenda na kuniamini kweli, usiwe na wasi tena tuko pamoja’)( yalikuwa ni maneno ya ujumbe mfupi wa kwenye simu aliyokuwa anasoma Kamishna Shebby pindi alipostuka usingizini baada ya alert ya simu ya dk Asha iliyokuwa kitandani kuita na alipogeuka na kumtazama Asha alikuwa bado yupo kwenye usingizi mzito japo ilikuwa tayari ni alfajiri ya saa kumi na moja. Aliichukua simu na kukuta ulikuwa ni ujumbe uliorudishwa baada ya kushindwa kufika kwa mlengwa na kubaki hewani kwa zaidi ya masaa 24 na alipoamua kuufungua kuona alichokuwa ameandika mchumba wake ndipo alipokutana na hayo maneno ambayo hakujua ni nani aliyekuwa ametumiwa na Asha ujumbe huo kutokana na namba husika kutoseviwa jina. alianza kuipekua simu ya asha na kuangalia charting za meseji za nyuma lakini hakukuta ujumbe wowote zaidi ya ule ambao ulirudishwa na mtandao husika baada ya kushindwa kumfikia mlengwa. Muda huo huo Asha nae alizinduka na kumshangaa Kamishna Shebby akiwa bussy na simu yake lakini alibaki anamtazama bila kumstua wala kusema lolote na kugeukia tena upande wa pili na kuendelea kulala. “ukimaliza baby naomba nimtumie message mama” aliongea kwa sauti ya kivivu Asha na kumfanya Shebby atabasamu baada ya kujua kumbe Asha alishamuona muda mrefu kuwa anapekua simu yake na ndipo Shebby alipoacha upekuzi zaidi baada ya kuona jinsi Dk Asha alivyokuwa hana wasi hata kidogo kwa kuchezea simu yake na kuamini kuwa hakuna tatizo lolote japo awali alichanganywa kidogo na ile message. “Eeh! baby harafu kuna message yako imerudishwa” aliongea Shebby huku akimkumbatia kwa nyuma Asha pale alipolala ubavu na kumpitishia simu yake ambapo Asha alipokea na kuitazama message yenyewe. “Aaaagh! mamaa naee.. mh! mme wangu na wewe hupitwi?” “kivipi tena honey” “sasa hii message ulivyoisoma umeelewa nini?” “hahahaa Asha my love, message umeandika wewe mimi nitaielewaje wakati sijui hata uliyemtumia nani na mlianzia wapi.” “hehehee Hiloo, oteaa sasa..” “Mh! nimeshindwa kuotea baby hebu nijuze..!” “heheheee acha wivu bwana huyu mama” “MAMA!!” “Hee! sasa unastuka nini huyu mamaangu na niliongea nae jana na kumpa habari za mahusiano yetu na ndipo aliponiuliza kuwa nina hakika unanipenda kweli? lakini nilimuahidi nitamjibu ndipo baadae nilimtumia hii massege, sasa ajabu ipi..!! sema kabla sijakuvunja mguu tehtehteheee” aliongea huku akiongezea utani Asha na kugeuka upande ule aliolala Shebby na kutazamana usoni na mwishoe wote waliangua kicheko hasa baada ya Asha kuzungusha zungusha macho yake na Kujitunisha mashavu kama mtu aliyetumbukiza kitu kikubwa zaidi ya uwezo wa mdomo wake. “ha ha hahaa Dokta mzimaaa kumbe muda mwengine kama kitotoooo hahahahaaaa” “tokaaa hapaaa hiloo mbona we Polisi zimaaa lakini umeshindwa kuluka mto kitandani umekuwa ovyo hata umeshindwa kuramba asali iliyotelekezwa na nyuki kwa kuhofia guu kuoza aahahahahaaaaa” “Asha ashaa Ashaa Ashaaaa!!!! Ngoja sasa” aliongea kamishna Shebby baada ya utani wa Asha kumgusa kidogo na kuanza kumchezea chezea maungo yake raini yaliyofichwa na nguo nyepesi alizovaa usiku. “ha ha ahaa bwanaaaaniniiiiiii..Niacheee basiiii” aliongea kwa sauti ya kudeka Asha kipindi hiko Shebby alikuwa serious zaidi baada ya Achumani kichwa wazi kuanza kufurukuta na kututumsha bukta aliyovaa akitaka kutoka akasalimiane na mwajuma mficha asali.
Mchezo wao wa kutekenyana na kubimbilishana kitandani ulidumu kwa zaidi ya dakika arobaini kabla ya wote kujikuta wakiwa kama walivyozaliwa na kuanza kurambana rambana taratibu kama vitoto vya mbwa mwitu huku Achumani kichwa wazi wa shebby akizidi kudondosha mate ya uchu wa kuiramba asali ya mwajuma iliyofichwa katikati ya pachupachu ya mapaja ya Dokta Asha na kumfanya Kamishna asahau kama mguu wake mmoja ulikuwa na jeraha pia mifupa bado haikuungana vizuri na hata lile swala kuhusu message aliyoisoma na kumchanganya alfajiri ile alilisahau kabisaaa kuliulizia tena kujua ile namba ilikuwa ya nani? Zaidi mawazo na akili yote ya Kamishna Shebby ilihamishwa na mautamu yaliyokuwa mbele yake kutoka kwenye mwili laini wenye joto la huba wa Dokta Asha. Kilichofuata ni miguno ya kimahaba na purukushani za hapa na pale kipindi Kamishna Shebby na Dokta Asha wakivunja amri ya sita mule ndani na kuishi kwenye sayari ya ajabu kwa takribani nusu saa kabla ya kila mmoja kuridhika na kubaki hoi huku wakiwa wamekumbatiana na kuangaliana machoni kama majogoo yaliyotoshana nguvu. “Aaagh! siamini Asha kumbe bado mtoto kabisa?” aliongea Shebby na kumpelekea Asha mdomo na kuanza kunyonyana ndimi huku wakifonzana mate kwa hisia kali. “Nakupenda sana Shebby kumbe na wewe fundi kiasi hiki Mhh! kama Simbaa!!” aliongea kwa sauti ya kudeka Asha na kumlalia kifuani Kamishna Shebby.
* * * * * (MKUYUNI) ……………
Alistuka kidogo na kushusha pumzi Cj4 baada ya kumtazama machoni yule mtu na kugundua kumbe alikuwa yule mama mtoto wa marehemu Mnyungunyungu aliyerukwa akili na alipomkazia macho ndipo yule mama alipojichekesha na kuanza kujifunua nguo huku akikimbia na kucheka kwa sauti ya juu. (“Mh! huyu naeeee ok nitajua cha kufanya”) aliwaza moyoni Cj4 wakati akielekea kwenye ile nyhumba na kuingia chumbani kwake kuendelea kurekodi kile alichokuwa anakitafiti.
Mpaka dakika hiyo Cj4 aliweza kujua sababu zilizompeleka Kamishna Shebby pale mkuyuni na alielewa kuwa yule mfungwa Hussein bubu hakuwa na makosa yoyote ila alijua kuwa mchezo ule unachezwa na huyo mtu anayejiita Mr X ambae alikiri moyoni mwake Cj4 kuwa huyo mr X ni mtu anaetumia akili nyingi sana kuliko nguvu na ana wafuasi wengi. Lakini alitafakari sana mule ndani na kuona jinsi ya kumpata mr X kirahisi ni sawa na hakuna kwani atakuwa anamtafuta mtu kwenye mzunguko asioujua kwani huwezi kumshinda mtu mwenye akili kwa kumtafuta ilihali humjui ila yeye anakujua kama unamtafuta na alibaini kuwa jinsi ya kumtafuta mr X ni kumtafuta pasi na yeye kujua kama anatafutwa na njia aliyoiona ni sahihi ni kumuingiza mr X kwenye mzunguko wa mission yake ili aweze kumtambua pasi na yeye kutambulika. (“Yap thats is a Solution”) alijisemea kimoyo moyo Cj4 na kunyanyuka haraka kuanza kujipachika mwilini vitu vichache muhimu na pale pale alichomoa simu na kupiga kwa mkuu wa Majeshi na kumuelekeza jibu alilolipata kwa siku moja tu baada ya kutua Mkuyuni na Mkuu wa Majeshi aliporidhika alimuamuru kuwa afanye hima arudi makao makuu na yeye ataongea na Muheshimiwa Rais ili wafanye vile alivyopendekeza. Na ndipo baada ya hapo kwa kutumia mbinu za Kikomandoo Cj4 aliweza kutoweka Mkuyuni baada ya kuwasili na kukaa masaa 24 pekee.
-(IKULU~DSM)- …………………..
Kikao cha siri kwa dharula kilikuwa kinaendelea ambapo alionekana Mh Rais sambamba na wazili wa ulinzi na mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama bila kumsahau Kamanda mkuu wa jeshi la polisi huku pembeni yake akionekana Jaji mkuu wa taifa. Mada iliyokuwa inaendelea ni juu ya swala zima lililojiri miezi ya karibuni kule Mkuyuni juu ya shambulio la polisi na kutojulikana sababu na muhusika wa shambulio hilo huku wakiongozwa mjadala ule na ripoti maalum kutoka kwa Komandoo waliyempandikiza kufanya utafiti na kugundua kuwa chanzo cha Kamishna wao kuliingiza jeshi kwenye misukosuko ni kutaka kuujua ukweli wa kesi ya zaidi ya miaka ishirini ya mfungwa mmoja aliyekuwa kwenye gereza lake ili apate kuifufua na kumsaidia baada ya kugundua kuwa alihukumiwa kimakosa na kiuonezi. Ripoti ya Cj4 ilikiri kuwa ni kweli huyo mfungwa ambae aliitwa Hussein alihukumiwa kimakosa lakini si kimakusudi bali kutokana na mchezo mchafu wa akili nyingi uliokuwa unachezwa na mtu asiyejulikana jina lake halisi wala makazi na wadhfa wake zaidi ya kutumia kivuli cha jina la MR.X
Na iliongezea kuwa mr.X bado yupo na ana mtandao mkubwa na ni vigumu sana kum baini kwa kutuma wapelelezi bali ripoti ilishauri cha kufanya ni kumuingiza Mr X kwenye mtego utaofanya atume wapelelezi na majasusi wake na hapo ndio itakuwa rahisi kumpeleleza na kupambana nae. Na njia ya kumuingiza mr X kwenye huo mtego ni kumtoa gerezani na kumuacha huru kwa kupitia kipengele cha msamaha wa rais mfungwa Hussein na wafanye jingo itayowawezesha watu wengi wasikie na hiyo itakuwa njia ya mr X kutuma watu wakamuue Hussein ili asiongee mengi zaidi aliyoyajua na hapo ndipo wao watapata nafasi ya kuunasa mtandao wa mr X na mr X mwenyewe kwani watapandikiza ulinzi yakinifu kwa Hussein popote atapokuwa.
“Jaji unasemaje, unakubaliana na hiyo ripoti ya kijana wetu?” aliuliza muheshimiwa Rais mara baada ya wakuu wote wa jeshi kukubaliana na ripoti ile kasoro Jaji ambae bado alikuwa anafikiria kitu.
“Mh! muheshimiwa ripoti sio mbaya sana ila nilikuwa na wazo japo najua hata nikipingana nayo itakuwa ishapita kutokana na uchache wangu na wingi wenu lakini napenda kupendekeza wazo langu kuwa kwanza tunalazimika kuonana na wastaafu wa kipindi hiko na kuwahoji kwa pamoja hasa wakuu wa usalama kwani naamini kwa akili za huyo mr.X lazima atakuwa alikuwa mmoja wa wakuu wa usalama nchini na si mtu wa kawaida na pengine alipendwa sana na wananchi na alikuwa na sifa hapa nchini ambayo hataki ipotee wala ichafuliwe. kwa hiyo napendekeza wapatikane watu kama wazili wa ulinzi mstaafu wa kipindi hiko, mkuu wa majeshi kwa bahati mbaya hatunae ila yule wa polisi uzuri bado yu hai yupo huko Morogoro.” aliongea Jaji kauli iliyomfanya mh Rais kutikisa kichwa kwa ishara ya kukubali.
“Enheee harafu huyu kamanda wa pilisi namkumbuka vizuri miaka ile si mzee Cyplian kama sikosei… na isitoshe tulikuwa nae katika shughuli ya kuwaaga marehemu siku ile na alinambia kuwa kumbe yule mkuu wa kituo Mkuyuni aliyeuawa alikuwa mwanae.” alidakia kamanda mkuu wa jeshi la polisi “Basi vizuri Jaji itabidi tufanye hivyo pia ila kwa njia ya kijeshi na usalama zaidi tutayafanya hayo yote kwa pamoja aachiwe huyo mfungwa na kipindi hikpo hiko wastaafu muhimu tutakuwa nao faragha na itakuwa rais zaidi kubaini kama mmoja wao akawa ndie Mr X” aliongezea mkuu wa Majeshi na baada ya makubaliano hayo kikao kilifungwa.
* * * * * *
Saa zilikatika, siku zilisonga na baada ya wiki kadhaa tena mbele hatimae Kamishna Shebby alipona vizuri mguu wake na kuweza kutembea kwa ufasaha huku mapenzi baina yake na dk Asha yakipamba moto siku hadi siku hali iliyowafurahisha na kuwachochea wazazi wa Shebby kutaka kuona mtoto wao akimuoa kabisa yule daktari wa kipekee. Hata moyoni mwake dk Asha alizidi kumpenda Kamishna Shebby na kuwa radhi kuolewa nae.
Siku moja majira ya usiku sana ikiwa ndio ilikuwa siku ya mwisho kwa dk Asha kuwepo pale kwenye jumba la mzee Mwinchande baada ya kumaliza shughuli ya kumtibu kijana wake na ilipaswa arejee kwao ili kama taratibu za ndoa zianze kufanywa na ataporejea awe Mke rasmi wa Kamishna Shebby, ndipo usiku huo baada ya Shebby kupitiwa na usingizi Dokta Asha alinyata na kuchomoa pakiti ya sindano kwenye moja ya mabegi yake ya dawa na kuchukua kichupa kimoja kilichokuwa na dawa maalum ya ganzi na usingizi ndani yake na kuichoma kwa kuiingiza ndani ya bomba la sindano kabla ya kumchoma taratibu Shebby ambae alikuwa kalala fofofo na baada ya dakika kadhaa ndipo alipochukua kifaa maalum mithili ya bastora ambapo ndani yake kulikuwa na bomba la sindano kubwa na nyuma sehemu ya kushikia kulikuwa na waya wa umeme ambao aliupeleka mpaka kwenye socket na kuichomeka kisha kuiwasha na kumsogelea kitandani Shebby. “am so sorry baby kwa kufanya haya bila ya ridhaa yako but it’s all about Love”
aliongea mwenyewe Dk Asha na kum busu kwenye paji la uso Shebby ambae tayari alikuwa ndani ya nusu kaputi na ndipo taratibu alikamata lile bomba lililo katika muundo wa bastora na kumpekua Shebby sehemu za kichwani pale alipokuwa anapenda sana kumshika na kupatazama kwa muda mwingi huku akionesha kumuhurumia muda mwengine hadi akawa analia na taratibu aliuelekeza mdomo wa lile bomba na kubonyeza kitufe furani mithili ya kile cha kuruhusu risasi itoke huku akiutuliza kwa umakini mkono wake kwa kuundamiza ule mdomo wa bomba huku akizungusha kijidude kilichokuwa pale ulipoanzia waya ulioelekea kwenye umeme na ndipo mara kwa ndani ya bomba kulianzakuonekana damu zikiingia baada ya kusikika mlio wa ‘prruchuu’ ndani ya bomba na kuonekana kijisindano kidogo ndani yake kilichotoka kichwani mwa Shebby.
Alichukua pamba na kuibandika pale kichwani mwa Shebby haraka haraka na kuchukua sprit maalum na kuimwagia pindi tu alipotoa lile bomba mfano wa bunduki ili kukata vijidamu vilivyoanza kutoka kupitia kijitobo chembamba kilichosababishwa na ile sindano kubwa iliyotoka ndani yake na kufonza damu sambamba na kile kijisindano kilichotoka kichwani mwa Shebby.
“Ohh! my God, pole sana honey hope now mambo yataanza kurudi nakuwa sawa polepole. Najua hautajua nami sitomwambia mtu honey.” aliendelea kujisemea Dk Asha mithili ya kuwa alikuwa anaongea na Shebby ilihali Shebby hakuweza kusikia wala kuhisi chochote. Asha alikuwa mtaalam sana kwani aliweza kupakausha na kupashona na vijiuzi maalum vyenye rangi kama ngozi ya binaadam kabla ya kukibandika chengine kwa matilio maalum yaliyoweza kuziba kabisa na kuwa vigumu sana mtu kubaini kama sehemu ile ya kichwa cha Shebby kulikuwa na jeraha lolote.
Baada ya hapo alisafisha vizuri na kukitoa kile kisindano kilichotoka kichwani mwa Shebby kilichokuwa ndani ya bomba na kukitazama kwa umakini kabla ya kukihifadhi kwenye matereo yake na baada ya kuhakikisha kila kitu kipo sawa alimchumu Kamishna Shebby kisha na yeye kulala.
Asubuhi kulipambazuka na kamishna Shebby aliamka kama ilivyoada na kumkuta dk Asha akiwa anajiandaa andaa kuonesha kuwa aliamka muda mwingi “so baby mi mkataba wangu ndio hivyo tena, sasa kama kupona kwako ndo na mapenzi yameisha tutajua pindi nitapokuwa kwetu” aliongea na kufanya utani kidogo dk Asha kipindi hiko Shebby alibaki kalala chali pale kitandani akiwa kaegama kwenye mito akimuangalia Asha huku moyo wake ukitamani asiondoke. Lakini hakukuwa na jinsi ukweli ulibaki kuwa mkataba wa Asha kuendelea kuwapo pale ulikuwa umeisha na ni zaidi ya milioni miamoja sabini ziliingizwa kwenye account yake kwa muda ule mfupi alioutumia kukaa pale kwa mzee Mwinchande na kumuhudumia Kamishna Shebby. Lilikuwa ni jambo la furaha sana kwa familia nzima mara baada ya Shebby kujiandaa na kutoka sambamba na dk Asha pale kwenye sebule yao kubwa ambapo kulikuwa kumekatwa upande kwa niaba ya vikao vya dharula na kuungana na familia nzima iliyokuwa tayari eneo lile kwa dhumuni la kufanya tafrija fupi ya kumuaga dk Asha na kumshukuru kwa yote aliyofanikisha kuhakikisha Kamishna Shebby anarudi kwenye hali ya kawaida.
Tafrija iliongozwa na mzee Mwinchande mwenyewe kwa kutoa maneno ya hekima na nasaha kwa Asha huku akimsisitiza aendelee kuwa na moyo ule wa kipekee na asije kubadilika pindi watapotuma watu kwaajili ya kujitambulisha huko kwao kwani walihitaji kuunganisha undugu na ukaribu kabisa kwa njia ya kuolewa na mtoto wao Kamishna Shebby. “Nashukuru sana baba nami sitoweza kubadilika kwani ukweli nampenda sana Shebby” aliongea kwa sauti laini Asha na kuwafanya wote watabasamu na baada ya tafrija kuisha gari maalum aina ya Lange ambayo ilikuwa ni mali ya Dk Asha iliondoka sambamba na escot kutoka kwa kamishna Shebby mpaka maeneo ya jilani kabisa na alipokuwa anaishi Asha ambapo alidai kuwa anaishi na mamaake na isingekuwa vyema Shebby kufika moja kwa moja japo ilijulikana kuwa alikuwa ni mgonjwa wake. Na hapo ndipo walipoachana Shebby na Asha japo mawasiliano yaliendelea kuwapo huku mawazo yao yakilenga siku ziende haraka ili waoane na kuwa pamoja.
* * * * * Kwa mara nyengine Cj4 anaonekana akiwa kavaa mavazi ya kipolisi yenye cheo cha Inspector huku akiwa anaendeesha gari aina ya Land cruiser nyeupe ya kipolisi speed kali kwenye barabara ya vumbi na safari yake ilimpeleka hadi mbele ya kituo kikuu cha polisi Mkuyuni ambapo baada ya kushuka alipigiwa saloot na askali aliowazidi cheo mahala pale na moja kwa moja alienda kukutana na mkuu mpya wa kituo na baada ya kusalimiana alijitambulisha. “Naitwa Inspector Sudy kama ulivyoipata taarifa ya ujio wangu nimekuja kwa nia ya kukutana na baba wa marehemu mkuu wa kituo aliyekutangulia kwa ajili ya kwenda nae makao makuu Dar.” aliongea kwa ukakamavu Cj4 japo ukweli hakuwa askali polisi bali ulikuwa ni mpango wa siri tu uliofanywa na viongozi wakubwa ili iwe rahisi kufanikisha zoezi la kwenda na mzee Cyplian kwa mahojiano maalum ya siri ili wapate kumvumbua huyo Mr.X “Sawa Inspector basi utaongozana na vijana wachache wataokupeleka mahala anapoishi mzee Cyplian” alijibu mkuu wa kituo na baada ya hapo amri ilitolewa na ndipo Difender moja iliyowabeba askali watatu iliongoza njia na kufuatiwa na gari ya Cj4 moaka kule ambako alikuwa anaishi baba wa marehemu Ocs John ambae ni mzee Cyplian
Baada ya mwendo wa dakika ishirini waliingia mbele ya nyumba moja ya kifahari licha ya kuwa ilikuwa kijijini mbali na barabara kuu lakini ilitosha kumjuza mpita njia wa eneo lile kuwa mtu aliyejenga pale si mtu wa kipato cha chini.
Mara baada ya gari kusimama na walinzi ambao pia walikuwa ni askali wa jeshi la polisi walifungua geti na kuukaribisha ule ugeni ulioongozwa na inspector fake Cj4 mpaka ndani ya sebule kubwa baada ya kukaribishwa na kuruhusiwa na mzee Cyplian kwa njia ya simu ya upepo pindi askali alipomjuza juu ya ugeni ule na muda mfupi Cj4 alipokuwa ameketi sebuleni mzee Cyplian alianza kushusha ngazi taratibu huku akiwa amevalia suti nadhifu na mkononi mwake akiwa na bluefcase ndogo na kufika pale sebureni. “Karibu sana kijana, nina taarifa zote za ujio wako na nilikuwa nakusubiri wewe hahahaa karibu sana mwanangu.” aliongea mzee Cyplian na kupeana mikono na Cj4.
Hakukuwa na muda wa Kupoteza zaidi ya Cj4 kuongozana na mzee Cyplian mara baada ya kuagana na familia nzima aliyoikuta pale akiwemo mama mzazi wa marehemu Ocs John na baada ya kutoa pole kwa mara nyengine aliaga na safari ilianza huku akiescotiwa na ile Difender mpaka morogoro mjini ambapo Difender ilirudi Mkuyuni nae kunyoosha tairi kuwahi Dar es Salaam huku kichwani mwake akipiga hesabu juu ya maswali ya kumuuliza yule mzee kabla hawajafika sehemu husika.
* * * * * *
Akiwa amekaa sebuleni akifatilia taarifa ya habari ikiwa ndio wiki yake ya mwisho kuendelea kuwapo nyumbani baada ya kupona vizuri, kamishna Shebby alistushwa na habari iliyokuwa inatangazwa muda huo juu ya wafungwa walioachiwa huru kwa msamaha wa rais huku kivutio kikubwa kikiwa kwa mfungwa mmoja ambae kesi yake ilitikisa miaka mingi naye si mwengine bali ni Hussein Bakari a.k.a babu bubu jina la utani alilopachikwa akiwa huko gerezani. Macho yalimtoka Shebby baada ya kukumbuka kitu na kujikuta anaropoka kwa sauti ya juu na kumuita babaake aje pale sebureni aone.
“Baabaaa babaaa njoo , Nimekumbukaaa.. Aaagh!! nimekumbukaaa Nimekumbukaaa babaaa” aliongea kwa furaha Shebby na kuwafanya wazazi wake warudi huku wakiwa na taharuki kwa shangwe na maneno ya mtoto wao. “Vipi mwanangu?” “Nimekumbuka baba, kumbukumbu zangu sasa zimerudi aaahhh!” “Allahu akbaaru Allaaaah akbaaaaar” alishukuru na kufurahi mzee Mwinchande huku wakikumbatiana na mkewe baada ya kijana wao kuthibitisha kuwa kumbukumbu zake zimerejea sawia. “Kipi kimekukumbusha mwanangu?” aliuliza kwa furaha na kutoamini mzee Mwinchande “Taarifa ya habari, ngoja nimpigie Asha nimwambie nae Mungu amenisaidia nimekumbuka kila kitu sasa sina wasiwasi tena pindi nitapokutana na Kamanda kwa mahojiano aaaaah!!! masikiiini rafiki angu Kimarooo…” aliongea Shebby lakini mwishoe alijikuta anaanza kulia mara baada ya kumbukumbu zake kumrudisha Mkuyuni na kuliona tukio zima lililojili miezi kadhaa nyuma na zaidi alimkumbuka rafiki ake kipenzi Kimaro na kuanza kulia kwa uchungu sana. “pole babaa polee ndio uanaume na misukosuko ya kazi zetu hizo pole baba”
alimfariji mwanae mzee Mwinchande huku akimkumbatia wakati huo mamaake alibaki anawatazama huku machozi nae yakimtoka “Babaa!! inatisha sanaaa, babaaa inaniumaa sanaa lazima nilipe KISASI” aliongea kwa hisia zenye uchungu sana Shebby lakini babaake alimtuliza na kumsihi asije kuthubutu kufanya hivyo “chonde chonde mwanangu mi mwenyewe ni askali mzoefu sana nakusihi na kukuomba sana kwa usalama wako futa kabisa hayo mawazo” “kivipi baba?” “Kwa sababu ni hatari ya maisha yako hebu fikiria unataka kulipa kisasi je unamjua huyo unaetaka kumlipizia?” “Nitamtafuta mpaka nimjue sitokubali ni heri nife nikiwa namtafuta hata nitapokutana na wenzangu huko mbinguni watanipokea vizuri kuliko kukaa kimya na kufa bila kufanya kitu wakati mimi ndie niliyewaponza wengine”
alisisitiza Shebby huku akiwa amekasirika mno baada ya kumbukumbu zake kuendelea kumiminika kichwani mwake mithili ya bomba la maji lililokuwa limefungwa muda mrefu na sasa limefunguliwa koki. “Hee! Shebby mwanangu kumbuka hata ufanyeje huwezi badilisha ukweli kuwa rafiki zako wamekufa na mtu uliyekuwa unamtetea kaachiwa huru sasa iweje bado unang’ang’ania kumtafuta mtu usiyemjua hata jina?” “Namjua babaa..”
“Unamjua!!!” “Hee, Nitatumia jina hilohilo analolitangaza mwenyewe na Kifo chake lazima nikishuhudie mbele ya macho yangu.” “Hee basi tulia baba unasema unamjua jina? ndio nani sasa?” aliuliza mamaake wakati huo babaake alikuwa kataharuki na haamini jinsi mwanae alivyobadilika ghafra namna ile. “Mama, Baba nawapenda na nawaheshimu sana naomba mnisamehe kwa kubishana nanyi ila niacheni nipambane na huyu mtu anayejiita Mr x.” “MR X!!!?” “Ehh! Mshenzi mwenyewe anaitwa Mr X” aliongea Shebby kwa hasira na kuelekea chumbani kwake moja kwa moja huku akijiapiza kulipa kisasi na kumlaani mr X akiwaacha wazazi wake wakiwa wanatazamana wasijue la kufanya au la kumwambia kijana wao.
* * * * * *
“Pole sana mzee wangu kwa kumpoteza shujaa akiwa bado na umli mdogo vile” alivunja ukimya Cj4 mara tu walipoanza kukaribia mkoa wa Pwani na kuzifufua hasira za maumivu zilizokuwa kifuani mwa Kamanda mkuu wa Jeshi la polisi mstaafu mzee Cyplia. “Aaagh! yaani mwanangu unavyosema hivyo unazidi kunitonesha kidonda cha mwanangu John! aaagh! mungu ampumzishe kwa amani.” “Daah! binafsi mzee wangu nimeamua kujikita katika upelelezi wa kujua kilichotokea kwani inasemekana chanzo kabisa ni mfungwa aliyekuwa gereza alilosimamia Kamishna wetu yule mtoto wa kamanda wako msaidizi enzi zenu “ “Aaagh! ndio mtoto wa Mwinchande!” “eeh, sasa kumbe alikuwa katika mpango wa kumsaidia yule mfungwa baada ya kujua story yake na ukweli halisi wa kesi ulikuwa kule morogoro lakini alipoenda kufanya tafiti na kusaidiana na askali wa kule ndo yakatokea ya kutokea” “Mh! sasaa kidooogo naanza kupata mwangaza” aliongea mzee Cyplian na kumfanya Cj4 azidi kutuliza umakini kwani tayari moyoni mwake alishaanza kumuhisi huenda yule mzee akawa ndie Mr X lakini aliamua kuongea vile ili kumpoteza na kujifanya hajamstukia kitu ili iwe rahisi kumteka kimazungumzo “Mwangaza gani tena mzee wangu”
“Kwa yaliyotokea ila naamini hadithi ya huyo mfungwa ndio funguo ya kumjua muhusika aliyewafanyia unyama wanangu.,,,,” kauli ya mzee Cyplian ilibeep ubongo wa Cj4 wakati huo tayari walikuwa wanaingia Chalinze lakini mara ghafra kabla mzee Cyplian hajaendelea wala Cj4 hajauliza chochote ghafra walishangaa kuona basi lililokuwa linatokea njia ya Tanga likipitiliza na kuingia mkuku mkuku barabara kuu huku likiwa limewasha taa na kupiga honi mfurulizo kuashilia kuwa aidha dereva limemshinda au limekata breki na kutokana na speed aliyokuwa anakuja nayo Cj4 alijikuta anashindwa kusimama na kuhamia barabara ya pili ili apate kulikwepa lakini bahati haikuwa yake baada ya kukutana na kiuno cha tela la roli lililofunga breki za ghafra kwa kuogopa kulivaa basi lililokosa muelekeo na kusababisha tela kugeuka kuelekea usawa wa gari la kina Cj4 huku kikisikika kishindo kikubwa sambamba na milio ya breki iliyosababisha cheche kuwaka barabarani na kelele za hofu toka kwa wafanya biashara na watu mbalimbali zilizosikika Chalinze nzima.
Hakuna aliyeelewa jinsi gani ile gari ndogo Landcruiser nyeupe iliyokuwa inaendeeshwa na Cj4 ilivyofika fika kule kwenye tawa za umeme tena ikiwa imechakazwa mno sehemu za mbele, na baada ya watu kukimbilia hususani wale wahuni na vibaka mpaka pale ilipokwamia ile gari walimshuhudia mzee mmoja kwa ndani akiwa kabanwa ipasavyo kwenye kiti na bashboard huku ule upande wa dereva kukiwa patupu na ndipo vijana wale wa kihuni walipong’ang’a kuuchomoa mlango mmoja uliojikunja ili wapate kuingia na kuitoa blufkes waliyoiona kwa ndani wakiamini lazima kutakuwa na hela tu.
Lakini kabla hawajafanya hivyo walistushwa na sauti ya mtu akiwaamuru waondoke haraka ikitokea nyuma yao na walipogeuka kutazama walimshuhudia askali mmoja ambae mavazi yake ya juu yalichafuka kwa damu iliyokuwa inaendelea kuvuja kutokea kichwani na ndipo wale wahuni wote walipotimua mbio. Hakuwa mwengine bali ni Cj4 dereva wa ile gari nyeupe iliyokwamia pale kwenye matawa ya umeme akiwa na jeraha lililokuwa linavujisha damu nyingi huku ikiwa haieleweki alitokajetokaje kutokana na kubondeka vibaya hasa ule upande aliokaa yeye. Alimuangalia mzee Cyplian na moyo kumuuma zaidi mara baada ya kugundua kuwa alishafariki pale eneo la tukio na hapo hapo kwa speed bila kujali damu zilizokuwa zinamvuja Cj4 alianza kukimbia kuelekea barabara kuu ambapo jumla ya magari sita yalipata ajali iliyosababishwa na lile basi lililopoteza muelekeo ambalo lilianguka na kuseleleka upande wa pili hadi kwenye vibanda vya mama lishe na kusababisha maafa makubwa mara baada ya derva kulazimisha kukata kona licha ya mwendo kasi lililokuwa nao. Kitu cha kwanza kufanya Cj4 akiwa kama mtu aliyechanganyikiwa alisimama na kulitazama eneo lile la ajali na kuanza kupiga hesabu alizozijua yeye wakati huo maaskali ndio walikuwa wanawasili eneo lile licha ya kwamba kituo hakikuwa mbali na mahala palipotokea ajali. (”Hii ni ajali ya Kutengeneza kabisaaa,”)
aliwaza Cj4 na kukimbilia kwenye ile basi na kuvunja kioo cha mbele kwa kupiga teke kali na alibahatika kumchomoa dereva ambae licha ya kwamba hali yake ilikuwa sio nzuri lakini alijitahidi kuzungumza “Jitahidi kuongea mimi ni askali nimekushika, nambie mara ya mwisho mlisimama wapi kwa ufasaha kabisa” alionga Cj4 kumuuliza yule dereva ambae alitoa maelekezo kwa shida huku akimwambia kuwa gari iliferi breki baada ya kuhisi waya maalum uliopita kwenye propela ulioshikilia vipira vilivoenda kukamata ringi za taili za mbele kuwa ulikatika ghafra na hakujua chanzo. maneno yale ya yule dereva yalizidi kumuaminisha Cj4 kuwa ile ajali ilitengenezwa tu sio bure lakini kama imetengenezwa wamefanyafanya vipi hao watu? hapo akakosa jibu ndipo alipotaka kumuuliza tena yule dereva mara askali wengine walifika eneo lile na kuanza kuwatoa majeruhi wa kwenye basi wakishilikiana na wananchi huku naye Cj4 akipigiwa saloot na askali aliowapita cheo na wakimsihi wampeleke nae akatibiwe kwani alikuwa kaumia sana kichwani licha ya kuwa yeye mwenye alijiona yuko sawa
Na wakati akiwa kasimama akiangalia pilika pilika zilizokuwa zinaendelea za uokozi na wapiga picha eneo lile mara macho yake yaligongana mara mbili na macho ya binti mmoja aliyevalia kiislamu usoni mwake akifichwa na nikabu nyeusi akiyaacha macho tu huku akitembea kwa madaha bila wasi kuelekea sehemu aliyopaki gari yake ndogo lakini kila alivyokuwa anapita alipogeuka macho aliyaelekezea kule kwa Cj4 na kwa ile Landcruide iliyobondeka kwenye Tawa za umeme na hapo hapo aret ya hatari iligonga kichwani na Cj4 na kuhisi yule mwanamke ndie aliyesababisha ile ajali na kuanza kupata ufumbuzi basi huenda mzee Cyplian hakuwa mr.X kama alivyomuhisi awali ila alitia shaka kuwa huenda mzee Cyplian kuna vitu alivijua kuhusu mr X na ndio maana mr X amewatuma vijana wake kufanya ujanja wowote ili mradi wahakikishe mzee Cyplian hatoboi ukweli wala siri yoyote kuhusu mrX. Lakini akiwa na maswali lukuki Cj4 kila alipomtazama yule bint moyo ulimtuma amzuie tu kwani macho ya yule binti yalionesha wazi kuna kitu anataka ahakikishe kule ilipodondokea ile gari na ndipo alipowaponyoka polisi wenzake na kukimbilia upande wa pili ilipokuwa ile gari ya yule bint ambayo ndio ilikuwa inaondoka taratibu eneo lile lakini kwa bahati mbaya zaidi Cj4 alianza kujisikia kizunguzungu kabla hajafika na kujikuta anadondoka katikati ya barabara ambayo ilikuwa inazungushiwa utepe wa kuzuia magari yasipite upande ule na macho yake yaliishia kuitazama kwa mbali ile gari pindi alipokuwa anadondoka na kupoteza fahamu.
* * * * * *
Akiwa amekaa huku mawazo na hasira juu ya yaliyopita hususani mr X na vifo vya rafiki zake huku akiwazia kukutana na Hussein bubu, ndipo Shebby alistushwa na sauti ya babaake pindi alipokuwa anaongea kwa njia ya simu kwa mshtuko mkubwa na kumfanya atoke na kukimbilia sebuleni aliposimama mzee Mwinchande akiendelea kuongea na simu. “Vipi baba nini kimetokea?” aliuliza kwa taharuki Shebby baada ya kuuona uso wa babaake ukionesha kushangazwa na kustushwa na alichokuwa anakisikia “ajali mwanangu” “Ajali? nani tena!” “Mkuu mstaafu wa jeshi la polisi Kamanda Cyplian anasadikika amepata ajali mbaya wakati akiwa njiani kuja Dar” “Kha!! ilikuwaje sasa, si yule babaake marehemu ocs wa Mkuyuni?”
“haswaaa, yaani aaagh! namkumbuka vizuri alikuwa mkubwa wangu na mtu wa karibu kipindi hiko daah!” “Daah! shit, amepona?” “Bado hatujapata hakika” Baada ya Shebby kuzipata habari zile muda ule ule alichukua simu yake na kumpigia kamanda wa mawasiliano ya idala ya dharula na alipouliza walithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na tayari kuna timu ya vijana ilikuwa njiani kuelekea huko.
Aliingia ndani Shebby na kujiandaa kwa kuvaa gwanda zake hali iliyowashangaza wazazi wake na kumuuliza kulikoni lakini alichojibu kiliwashangaza wote. “Baba najua ni ajali tu imetokea lakini kuonana na mzee Cyplian ni jambo la muhimu sana kwangu ktk njia za kumjua mr X” alijibu Shebby na kutoka mkuku na kuchukua gari aina ya Jeep na moja kwa moja aliondoka kwa speed maeneo ya kwao mara baada ya mlinzi kufungua geti huku akiwa hataki kusikia chochote toka kwa babaake ala mamaake.
Mwendo aliokuwa anatembea Shebby nimeshindwa hata kuuelezea mara baada ya kupita maeneo ya Kibaha na kutembea upande ambao ulikuwa haumruhusu lakini alifosi hivyohivyo huku akipiga honi mfurulizo lakini ghfra alipokuwa anapandisha kilima cha kuingia Mlandizi almanusura nae apate ajali baada ya kukosana na gari ndogo aina ya toyota creaster uso kwa uso na kusababisha wote wayumbe na yule dereva mweney wa toyota bado kidogo atumbukie mtaroni lakini nae alikuwa mtaalam sana na alifanikiwa kuidhibiti gari na kutulia tena barabarani na kuangalia nyuma kwa kutumia site mirror ambapo aliishuhudia ile Jeep nayo ikiendelea kuambaambaa pembeni ya barabara na kukaa sawa huku speed ikiwa pale pale. Chaajabu alitabasamu yule dereva badala ya kuchukia na kuendelea kupiga gea na hakuwa mwengine bali ni yule yule binti aliyejiziba uso kwa nikabu ambae Cj4 alimtilia shaka kule Chalinze.
Upande wa Shebby alikuwa nusu mzima nusu kichaa kwani alipoituliza tu gari mwendo ukawa uleule tena utadhani ndio kaambiwa aongeze vile huku akizipita gari kibao zilizokuwa zinaenda polepole kutokana na foreni nae kuweza kupita barabara ya pili akisaidiwa na sare alizovaa hakuweza kusimamishwa na askali yeyote mpaka alipoukaribia msafara uliokuwa unaelekea eneo lilelile la ajali na kufika nao pamoja.
“Wapi mzee Cyplian? wapi mzee Cyplian?!” aliuliza Shebby mara tu ya kusimamisha gari ambalo wengi walilikwepa kwa jinsi lilivyokuwa linakuja kasi na polisi wa pale wote walishindwa cha kufanya mara baada ya kumuona dereva wake akiwa kawazidi cheo wote waliokuwapo pale. “Wapi mzee Cyplian” aliuliza tena Kamishna Shebby safari hii akimfata Seneor Inspector ambae ndie alikuwa mkubwa wa pale kipindi shughuli za uokoaji zikiendelea.
“mkuu ndio sasa ivi ambulance iliyobeba mwili wake imetoka.” “Whaat! ina maana amefariki?” “Ndio mkuu ila ambulance ile ndio yupo inspector aliyekuwa anamuendeesha nae hali yake si mbaya sana ila amepoteza fahamu” aliongezea yule s.inspector huku akiionesha kwa kidole ambulance iliyokuwa inatoka na palepale Kamishna Shebby aliingia kwenye gari na kuifatilia ile ambulance mpaka hospital ya Tumbi na pindi ilipopaki alishangaa kuona yule mgonjwa ambae ndie Inspector aliyekuwa anamuendeesha mzee Cyplian akishuka mwenyewe huku akiwa na bandeji kubwa kichwani akiwakataa polisi na madaktari waliomleta pale kuingia hospitali na kuichomoa ile sindano ya dripu aliyowekewa kwenye gari na kuanza kuondoka huku akiwa kama mtu aliyechanganyikiwa lakini anajiamini mno. Hapo ndipo Shebby aliposhuka na kumfata yule inspector ambae ndie Cj4 huku akiwazuia askali wote waliokuwa wanajaribu kumzuia na kumuingiza hospital na kutokana na ukubwa wa Shebby wote walitii na hapo kwa mara ya kwanza Shebby alionana uso kwa uso na Cj4 huku akiwa hamjui ni nani hasa nae Cj4 alitabasam kuonana na Shebby huku akiwa anajua kila kitu ni nani hasa nyuma ya pazia.
“Nakufahamu wewe ni Kamishna Shebby nilisimama kwenye nafasi yako kuendeleza ulichokiacha, tuwahi haraka Dar kabla hajatoweka.” aliongea Cj4 na kuingia kwenye Jeep huku Shebby akiwa ametumbua macho akiwa haelewi nini anamaanisha yule inspector na imekuaje aongee kwa kujiamini vile ilihali yeye ni mkubwa kuliko yule inspector. “Twende Kamishna tuiwahi crester iliyombeba muuaji.” Alipoongea maneno haya sasa Shebby alielewa kitu haraka na kuwahi kwenye gari na kuigeuza kwa fujo huku askali na madaktari wote wakishangaa kile kilichokuwa kinaendelea.
Ilikuwa ni ajabu na kweli ndani ya vichwa vya watu kwa kila aliyeiona ile gari jinsi ilivyogeuzwa na kuondoka eneo lile kwa speed ya hatari mithili ya gari ya mashindano huku Cj4 akiufurahia ule mwendo ambao kwake yeye Kamishna Shebby aliona kama vile gari ilikuwa haitembei kabisa. “Inspector! Umesema ni Creaster nyeupe?” aliuliza Shebby huku akiwa makini na barabara ambapo aliwasha taa zote full mbali na kuwa haukuwa usiku. “Yap yap nyoosha mguu nyooshaa” alijibu Cj4 kwa msititizo na kikatawala kimya baina yao zilibaki kusikika tairi za gari zikilalamika honi mfurulizo na muhemo wa injini tu.
Lakini walipofika maeneo ya Kibamba pale njia panda ya kijiji cha Hakipo walishangaa kuuona moshi mzito umetanda pia waliuona umati wa watu kwa mbali na askali wa usalama barabarani sambamba na gari ya zima moto huku askali moto wakiwa bussy kuzima moto uliokuwa unawaka na kusababisha hali ya hewa pale kuwa na ukungu uliosababishwa na Moshi. Walisimama na kushuka mkuku mkuku eneo lile na kuwahi kushuhudia kilichotokea wakiwa na wasiwasi isije kuwa ni yuleyule mtu aliyekisiwa na Cj4, na kweli baada ya kushuka na kusogea kuangalia kilichokuwa kinawaka walishangaa kukuta ni gari ndogo na walipoichunguza vizuri ilikuwa ni ileile Toyota Creaster aliyokosa kosa kugongana nayo Shebby na ndio ile aliyopanda yule mwanamke aliyemtilia mashaka Cj4 “Vipi afande ilikuwaje?” aliuliza Kamishna Shebby kwa mmoja wa askali barabarani (trafic)aliyekuwapo maeneo yale baada ya kupokea heshima yake “Ni ajabu kidogo mkuu, tulipigiwa simu na raia wema kwamba kuna moto umezuka kutoka kwenye hiyo gari na umekutwa mwili wa mwanamke mmoja ambae inasadikika alikuwa dereva wa hiyo gari akiwa kaungua vibaya mno.” alijibu yule afande na kumfanya Shebby akune kichwa na kushusha pumzi lakini Cj4 alicheka na kumvutia pembeni Kamishna Shebby.
Vitendo vya Cj4 kutomtetemekea wala kueka nidhamu ya uoga kwa Shebby ilizidi kumshangaza Shebby na kujiuliza huyu ni askali gani mwenye cheo kidogo kuliko yeye lakini haoneshi kuogopa wala kumnyenyekea mkubwa wake na kufikia hadi hatua ya kumshika mkono na kumvutia pembeni? lakini alijikuta anashindwa kumkatalia wala kumuuliza na kukubali kusogea nae pembeni. “Vipi inspector?” aliuliza Shebby kwa taharuki mara baada ya kuvutiwa pembeni na Cj4 wakati yeye alikuwa bado anahoji kilichotokea. “Tushamkosa, kashatuzidi akili” “Kivipi?” “Huyu mwanamke muuaji” “Muuaji, lakini mbona na yeye amekufa! hapa lazima kutakuwa na mtu aliyemuua” aliongea Shebby kauli iliyopingwa na Cj4 “Hapana Kamishna, huyu mwanamke ni special Killer na anajua kupoteza ushahidi. nina imani yule aliyeungua si yeye” aliongea Cj4 na kumfanya Shebby abaki na taharuki akishangaa maneno ya Cj4, na kuanza kuhisi huenda huyu si askali wa kawaida
“Sikia Shebby, washa chombo twenzetu turudi taratibu eneo la tukio ukaniache hapa hakuna kitachoweza kutusaidia ila maswali yote unayojiuliza nitakujibu tukiwa njiani” aliongea Cj4 na kumfanya Sheby awe mpole na kuingia kwenye Jeep na kuanza kuendeesha kuelekea walipotoka huku akiwa anajiuliza mara mbili mbili kuhusu inspector wake ambae licha ya kuwa ameumia sehemu za kichwa na hata ile bandage aliyofungwa kwenye ambulance ilianza tena kuvujisha damu lakini hakuonekana kujali. “Enhee, kwanini Inspector unalazimisha turudi tena eneo la tukio?” “Kule ndipo tutapata uelekeo wa sababu za ajali na alipotokea muuaji aliyetuzidi akili.” “Kivipi sasa katuzidi akili?” “Si umeona katengeneza kifo fake!!” “Kifo fake? kwa hiyo unataka kusema yule aliyeungua si muhusika?”
“Ndio maana yake ni kamchezo kadogo sana, nahisi kumbukumbu zako zimerudi unakumbuka nini kuhusu Mkuyuni?” alijibu Cj4 na kumuunganishia swali Kamishna Shebby lililofanya amtazame na kuamua kumjibu kiunagaubaga “Mkuyuni nakumbuka vifo tu” “Nina mashaka na muuaji wa Mkuyuni anaweza kuwa yuleyule mwanamke aliyesababisha ajali” aliongea Cj4 maneno yaliyomfanya Kamishna Shebby kufunga breki za ghafra za gari na kupaki pembeni huku akimuangalia kwa mshangao Inspector wake. “Unasema??” aliuliza Shebby mithili ya mtu aliekuwa na matatizo ya masikio mara baada ya kusimamisha gari. “Nina wasiwasi na yule mwanamke aliyesababisha ajali ndie aliyewashambulia Mkuyuni.” “Khaaa! wewe ni Inspector kweliiiii ama umevaa sare tu?” aliuliza Shebby akionesha kuanza kuwa na wasiwasi na Cj4 kutokana na maneno yake kugusa mulemule “Hapana mimi ni Inspector kwa sasa… Naitwa Inspector Sudy kama ilivyoandikwa” alijibu Cj4 na kumshangaza sana Shebby “Sawa Inspetor hata mimi naanza kukubaliana na wewe kuwa ule mwanamke ndie aliyetushambulia Mkuyuni” aliongea Shebby na kumfanya Cj4 amuangalie kwa umakini na ndipo Shebby alipozidi kufunguka “Nilimshuhudia muuaji wa Mkuyuni kabla hajanipiga risasi ya mguu, alikuwa ni Ninja wa kike ila kwa bahati mbaya nilimjua kwa sauti tu na muonekano lakini sikubahatika kuona walau macho yake yalivyo kutokana na miwani aliyovaa” “So, unadhani kwanini alikuacha? wakati wenzako wote aliwaua?” aliuliza Cj4 “Mh! kwakweli hata mimi sikudhani kama angeniacha ila nakumbuka alichosema kuwa eti nina bahati na kunipa agizo toka kwa mr X kwamba nisije kuthubutu kumtafuta tena mr X kwa usalama wangu. Lakini pia kuna kauli alinambia ambayo ilinichanganya sana hadi sasa”
“Ipi hiyo?” “Alinambia iwapo nataka kupambana na Mr X basi inatakiwa nianze kufanya mazoezi ya kusimama juani na kupambana na kivuli changu mpaka nikikamate” “Aaaahaa sasa naanza kupata taswira” aliongea Cj4 huku akifikiria kitu na kumshangaza zaidi Kamishna Shebby. “Taswira gani tena Inspector!” “Juu ya mr X” “kivipi?” “Nina wasiwasi mr X ni mtu aliye katika mzunguko wa maisha yako ya kila siku.” “Mhh! mbona sikuelewi unamaanisha nini?” “Namaanisha mr X ni mtu anayekujua vizuri na inawezekana nawe ukawa unamjua pia, na anapatikana katika sehemu kuu tatu” “Mbona sikuelewi wee Inspector? ni sehemu gani hizo?!” “Usipanic Shebby, nina wasiwasi mkubwa kuwa mr X ni mtu anayepatikana katika mzunguko wa maisha yako ya kila siku yaani kazini, serikalini ama nyumbani.” “Nyumbani?” “Yap, huenda akawa na ukaribu hata na babaako mzazi, au huenda akawa moja ya wakuu wako wa kazi ama kiongozi mkubwa serikalini aidha mstaafu ama bado yupo madarakani” maneno ya Cj4 yalizidi kumchanganya kabisa Shebby na kabla hajauliza tena lolote ndipo Cj4 alianza kufungua vifungo vya shati ya sare ya kipolisi aliyovaa na kuisogeza pembeni vest yake na kumuonesha eneo la kifua Shebby ambae macho yalimtoka baada ya kuona mchoro wa bawa na alama za Komandoo wa Jeshi.
“Usistuke nimeingia kwenye hii kazi kwa msaada wa kupoteza kwako fahamu, mimi si polisi ila kama unataka kazi hii ifanikiwe na tumgundue huyu mshenzi mdogo inatakiwa asijue mtu yeyote kama kumbukumbu zako zimerudi” aliongea tena Cj4 huku akifunga vifungo vya shati yake na wakati huo wote Shebby bado alikuwa katumbua macho akiwa haamini kuwa kumbe yule aliyekuwa anazunguka na kuzungumza nae muda wote ni Komandoo wa heshi!! “Zingatia Kamishna kwa usalama wako na urahisi wa kazi hii. take care twenzetu tukapate mchoro eneo la tukio lakini kumbuka hii tunajua mimi na wewe” aliongea tena Cj4 na ndipo Kamishna Shebby alipoanza kuondoa gari huku akiitika kwa kichwa akiwa bado haamini kilichokuwa kinaendelea hadi serekali wampandikize Komandoo katika kazi ile.
* * *
Baada ya Kamishna Shebby na Cj4 kufika tena Chalinze eneo la tukio na kufanya utafiti wa siri walioujua wao kabla ya Cj4 kukubali kujishusha na kuingizwa tena kwenye ambulance ambayo ilitokea ikulu pasi na mtu yeyote kujua na madaktari waliokuwa mule karibu wote walikuwa ni wanajeshi lakini walifanya hayo kwa agizo la mkuu wa majeshi kuwa wao ndio waondoke na yule dereva wa marehemu mzee Cyplian kwa lengo la kuwazubaisha hadi polisi wengine wasijue nini kinaendelea kwani isingekuwa vyema Cj4 kutibiwa na raia ama polisi wa kawaida.
Baada ya Kamishna Shebby kuondoka eneo la tukio huku akiwasiliana na baadhi ya wakubwa zake akijifanya bado kumbukumbu zake hazijarudi kama alivyoagizwa na Cj4 alifika nyumbani huku kichwa kikiwa kinamuwaka moto akiyakumbuka maneno ya Cj4 na kuona kweli mr X anatumia akili nyingi sana na inawezekana kabisa yupo katika mzunguko wa maisha yake ya kila siku. (‘Mh! sasa itakuwa nani? au mh Wazili? mhh sidhani.. au Kamanda mkuu anatuzunguka? Mh! !!’) aliwaza Shebby usiku pindi alipokuwa ndani lakini mara akiwa katika mawazo mazito alipokea ujumbe wa sms kutoka kwa Dk Asha ambae alikuwa mchumbaake akimlaumu kwa kupata riport kuwa alielekea eneo la ajali iliyotokea mchana huo mbali ya kuwa bado likizo yake ilikuwa haijaisha. Alitabasamu na kuendelea kuchart na baby wake Asha japo ukweli moyoni alikuwa na mawazo mengine kabisa.
* * * * *
Siku kadhaa zilisonga huku ukweli wa chanzo cha ajali ya Chalinze ukibaki kuwa wa kubahatisha na hata kile kikao cha siri alichopanga mh Rais kifanyike kiliahilishwa kwanza na kuupisha msiba uliozuka ghafra wa Kamanda mkuu mstaafu wa jeshi la polisi mzee Cyplian na kuzidi kuwachanganya wakubwa wa serikali washindwe kuthibitisha moja kwa moja juu ya ajali ile ilikuwa imetengenezwa ama laah. Hii hata mkuu wa Majeshi ilianza kumpa wasiwasi mara baada ya kupokea ripoti toka kwa Komandoo waliyemchomeka na kumwambia kuwa ajali ile ilisababishwa na watu wa mr X so, ni lazima kwenye kikao cha siri walichofanya kutakuwa na spy anayevujisha siri kwa mr X ama mr X mwenyewe anaweza kuwamo kwenye vikao vyao. Na ripoti hii ilifikishwa kwa mh Rais tu na kukubaliana na ushauli wa mkuu wa majeshi kuwa haina haja ya kutangaza tena ile ripoti wala kueka tena kikao huku akimuahidi kuwa kijana wake shupavu ataifanya hiyo kazi na mr X atakuja kuletwa mbele ya macho yake siku moja.
Kamishna Shebby alirudi rasmi kazini huku akiigiza bado kumbukumbu zake hazijarudi na kuwashangaza tena wazazi wake ambao awali walikuwa na uhakika kuwa mtoto wao kumbukumbu zimerudi. Hali hii ilimliza sana mamaake Shebby na kumuombea kila siku alipokuwa anasali akiwa haelewi inakuaje mtoto wao mara kumbukumbu zirudi mara zipotee tena? Hata mzee Mwinchande hii ilimshangaza sana lakini ukweli ulibaki katika moyo wa Shebby na Cj4 huku wakiendeleza mission yao ya siri ya kumnasa mr.X pasi na mtu yeyote kujua.
* * * *
Ilikuwa ndio siku rasmi ya kutoka kwenye makazi ambayo hakutegemea kama angetoka tena mara baada ya msamaha wake kutangazwa na kupitishwa wiki chache zilizopita na Mh Rais wa Tanzania. Geti kubwa lile la mwisho lilifunguliwa kwa mitambo ya umeme na oparator aliyekuwa kwenye moja ya jengo la usalama wa gereza lile na mwanga wa nje ukaanza kummulika Hussein babu bubu huku akiwa haamini kama kweli leo hii anakuwa huru kwa mara nyengine japo alikuwa hajui wapi aelekee kwani wenzake wote waliotangazwa kuachiwa walipokelewa na ndugu jamaa na marafiki kadha wa kadha waliokusanyana nje ya geti la gereza kuwasubiri isipokuwa yeye tu. Akiwa kava nguo mpya alizonunuliwa na serikali huku mkononi kabeba kijibegi kidogo chenye nguo za kubadilisha na shuka ikiwa ndio vitu pekee alivyoambulia kama msaada kutoka serikalini juu ya maisha yake mapya anayoenda kuyaanza huko uraiani.
Alimshukuru mungu na kuanza kupiga hatua mdogo mdogo akiifata barabara ndogo ya lami iliyoenda kukutana na barabara kubwa katika njia panda ambapo kulikuwa na stendi ya daladala japo hakujua hata akifika hapo stendi atapanda gari ya wapi ama atafikia wapi na mfukoni alikuwa na kiasi cha shilingi elfu tano aliyorudishiwa ikiwa ni pesa aliyokutwa nayo kipindi anakamatwa miaka iliyopita ambayo kwa kipindi hiko ilikuwa haina thamani kabisa ya kumsaidia mtu walau siku tatu. Lakini akiwa anaendelea kupiga hatua huku kichwa akiwa kakiinamisha chini akienda huku anatafakari mara alisikia muungurumo wa gari ikitokea nyuma yake upande ule wa gereza na kuchapukia pembeni kwa kuipisha lakini alishangaa ile gari ikisimama karibu yake na kushushwa kioo na mara sauti ya mtu ambae alikuwa dereva wa ile gari ilisikika akimwita na aliposogea kuchungulia hakuamini kuona ni Kamishna Shaaban na ndipo alipoingia garini akiwa haamini kama amekutana tena na kijana aliyetokea kumuhusudu kupita binaadam yeyote tangia aanze maisha ya jera. “Kamishna baba!! aah, siamini mwanangu kumbe umerudi” aliongea huku chozi la furaha likimdondoka Hussein babu kwa kutoamini kabisa hasa mara baada ya Shebby kuvua miwani meusi aliyovaa na kofia.
“Nimerudi baba nakaribia wiki sasa, hongera sana kwa kupata uhuru hatimae unarejea uraiani” alijibu Shebby kwa furaha ya kukutana tena na Hussein “Ahsante mwanangu leo hii nimekumbuka sana maneno yako pindi nilipokuwa natoka rasmi pale getini daah! mwanangu pole sana kwa matatizo.. Naomba unisamehe sana” aliongea Hussein huku akiendelea kufuta machozi yaliyokuwa yanatililika mashavuni mwake ghafa kila alivyokuwa anamuangalia Kamishna Shebby “Hapana baba, hupaswi kuniomba msamaha kwani ile ilikuwa ni moja ya kazi. Usijali babaangu kwakuwa leo hii upo huru hata moyo wangu umefurahi sana najua kazi niliyobakiza ni moja tu” “Kazi gani tena baba” “Nataka kumjua huyo mr X nilipe kisasi” “Haa! sasa kisasi cha nini tena mwanangu wakati mi nishakuwa huru! isitoshe naomba swala hilo niachie kwani mi mwenyewe nataka nilipe kisasi kwa mr.X nishasali sana miaka yote nikiwa jera kumuomba Mungu anitendee muujiza siku moja nitoke jera na nikamuue mr X kwa mikono yangu na mpaka sasa naona Mungu kashaanza kunijibu dua zangu. Futa mawazo ya mr X mwanangu sitaki nikuponze tena hii ni kazi yangu sasa ni zamu yangu” aliongea Hussein babu kwa hisia kali na safari hii machozi yaliacha kumtoka huku akimuangalia kwa umakini Shebby ambae sasa alianza kuiondoa gari taratibu na kuelekea kule alipokuwa anaelekea Hussein na alipoifikia ile barabara kuu alikunja upande unaoenda kutokea Kongowe. “hahaha, hapana baba si rahisi kama unavyofikiria lakini pia sifanyi kwa sababu ya wewe tu bali nafanya kwa sababu ya rafiki zangu wote waliokufa”
alijibu Shebby huku akizidi kuongeza mwendo wa gari “Mwanangu nakuomba chondechonde mi sina ubora wowote niliobakisha wala thamani hapa duniani hivyo hata kama kumuua kwa kumpiga nisipoweza, niko tayari hata nijilipue tufe wote lakini si wewe kurudi tena kwenye matatizo baba nakuomba” alisisitiza Hussein lakini Shebby hakuonesha kujali sana zaidi ya kuongeza mwendo mpaka walipoipita Kongowe na kuanza kuufata muelekeo wa mbagara na walipofika Mbagala Zakiem aliingiza gari kwenye parking ya hoteli moja mpya ya kisasa iliyokuwa pale Zakiem na kumuomba Hussein waongozane kuingia kwenye ile hoteli na kumshangaza sana Hussein mara baada ya kushuhudia Kamishna Shebby akimlipia chumba na bili ya chakula cha wiki nzima pale hotelini. “Usijali baba utakaa hapa kwa wiki moja kipindi nikikutafutia makazi rasmi ya kuishi usiwe na wasiwasi simu hii utatumia kwa mawasiliano endapo kutatokea tatizo, line yake imeunganishwa na kifurushi cha wiki na ina namba mbili tu zilizoseviwa na zote ni za kwangu.. Kuwa na amani baba”
Ni maneno ya Shebby pindi walipoingia kwenye chumba cha hoteli kilichokuwa ghorofa ya pili ambapo Hussein alibaki kataharuki tu akiwa haamini moyo wa yule kamishna na vile anavyojitolea kiasi kile kumsaidia ilihali hawana undugu wowote. “Mi nahitajika kuwahi tena gerezani baba, ila hii Elfu hamsini itakusaidia kwa matumizi madogo madogo na ya dharula” “Asante babaaa.. aaaah Asante sana mwanangu Mungu akuzidishieeee eeeh!! Akulinde na kila shari jamaniiii Asante babaaa” alishukuru hadi akapiga magoti Hussein lakini Shebby alimuinua na kumsihi asijali kabisa kisha aliagana nae na kutoka hadi ilipopaki gari yake. [“Hallow, yah Cj4 kazi kwako sasa tayari nishafanikisha yupo chumba namba 90 ghorofa ya pili”] yalikuwa ni maneno ya Shebby kwa njia ya simu akiongea na Cj4 mara baada ya kuingia ndani ya gari yake na kuanza kugeuza kuondoka maeneo yale. Ulikuwa ni mchezo wa akili nyingi waliokuwa wanaufanya Kamishna Shebby na Cj4 na muungano wao hakukuwa na mtu mwengine yeyote aliyekuwa anaujua, na kumbe Cj4 alikuwa na jukumu la kuchunga usalama wa Hussein babu na kumfatilia pale kwenye ile hoteli ama ikitokea ametoka ama kama kuna mtu yeyote atayekuja kuufatilia uwepo wake pale basi atashughulika nae. Naam na huo ulikuwa ni ulinzi na usalama mkubwa uliomzunguka Hussein pasi na yeye mwenyewe kujua hadi atapojulikana mr X ni nani.
Simulizi : Wanawake Ni Wauaji ?! Sehemu Ya Tatu (3)
[[“Mwanangu vipi kuhusu yule binti naona siku zinaenda na wewe uko bussy sana wala huoneshi kujali kama awali, ooohoo angalia wasije kuwahi wenzako!”] [“Daah, baba bwana… Mbona siku bado ila nitajitahidi basi wiki hii nimtafute mshenga tuandike barua ipelekwe au unasemaje baba”] [[“Akaah mimi sio muoaji shauri yako mwanangu ila kumbuka alivyokusaidia yule binti..!” [“Nakumbuka baba”] [[“Basi ufanye hima kama utashindwa kumtafuta huyo mshenga basi itabidi uje huku tukutafutie”]] [“sawa baba”] Yalikuwa ni maongezi kwa njia ya simu baina ya Kamishna Shebby pindi alipokuwa ndani ya ofisi yake pale gerezani akizungumza na babaake ambae ni mzee Mwinchande aliyekuwa nyumbani muda huo na kumkumbushia swala la kumuoa Dk Asha. Ukweli jambo la mr X ndilo lililomchanganya sana Shebby na kusahau jambo la ndoa kwa wakati huo huku akiumia kila alipokumbuka vifo vya askali wenzake na kuzidi kupata motisha ya kumtafuta mr X.
Kesho yake majira ya asubuhi na mapema Kamishna Shebby mara baada ya kufanya mawasiliano ya siri na Cj4 kama ilivyokuwa kawaida na taratibu yao waliyojiekea na kupeana riport zote muhimu walizozibaini katika mikakati yao ya siri juu ya mr X, ndipo Shebby alipomuelekeza Cj4 kuwa ataelekea huko hotelini kukutana tena na Hussein akitaka ampe kazi itayofanya awe anatoka mara baada ya kusikia kuwa tokea siku alipomuacha hajatoka kwenda popote kutembea wala hakukuonekana dariri za mtu yeyote kutaka habari zake wala wale maspy wa mr X. Na kweli majira ya saa nne asubuhi Shebby aliwasili pale hotelini na kukutana na Hussein bubu. “Karibu baba karibu sana” alikaribisha Hussein akiwa mwenye furaha pindi alipofungua mlango na kumkuta aliyemgongea kuwa ni Kamishna Shebby “Ahsante sana baba” alijibu Shebby na kuingia ndani. “sasa baba ilikuwa nije kesho lakini nimekuja leo kwa sababu frani zitazofanya nikuongezee muda wa kuendelea kuwepo hapa lakini nilikuwa naomba unisaidie jambo moja” “Usijali baba, usijali kabisa nakusikiliza na kabla hujasema naamini niko tayari kama litakuwa ndani ya uwezo wangu” alijibu na kukaa vizuri Hussein huku akimuangalia na kumsikiliza Kamishna Shebby kwa umakini mkubwa. “Sawa mzee wangu, ni hivi… Kipindi nilipokuwa nauguza jeraha la mguu nilitokea kupendana na binti ambae ndie alikuwa daktari wangu alienisaidia kwa kiasi kikubwa sana hadi nikafikia hatua hii ya kuwa kama awali…”
“Ndio baba endelea” “Sasaa, nilimuahidi kuwa nitafanya mpango wa kujitambulisha kwao ili tufanye taratibu za kufunga ndoa na kuwa mke na mume…. sasa Shida yangu baba nakuomba wewe uwe mshenga wangu unisaidie kuandika barua ya posa nikupeleke hadi nyumbani kwao na wewe ndie utayeingia na kunitambulisha sambamba na barua.” “Mh! mwanangu lakini mbali na kukutibu tu umechunguza tabia yake kiumakini?” “Kwa hilo baba sina shaka” “Haya mwanangu mimi kwako sina pingamizi kwa hilo, fanya tuiandike hiyo barua na hata leo hii ukitaka unipeleke niko tayari kwa hilo kwa moyo mmoja ila nasaha zangu kwako ziko palepale usiwaamini wanawake wala usiwachukie kumbuka kuwa Wanawake ni Wauaji” aliongea Hussein na kumfanya Shebby atabasamu na ndipo alipotoka na kurejea tena akiwa na bahasha sambamba na karatasi na kwa msaada wa Hussein wakaanza kuiandika barua.
* * * * * *
“Mamaaa, mamaa, mama kaa tayari tayari leo usitoke kwenda popote” “Kivipi Asha mwanangu mbona ratiba zako sizielewi!” “mama bwana, ni hivi… yule mchumba niliekwambia barua yake inakuja leo” “Hee, ni wewe kweliii Asha au mwengineee” “Ni mimi mama mbona huamini!?” “Mh! unajua toka uliponambia siku ile nilichukulia mzaha kwa itikadi zako za kutojichanganya na watu, sasa sijui imekuwaje kuwaje hadi ulikubali kuacha shughuli zako na kumtibu mgonjwa yule tena ukidiliki kukaa kwao kwa zaidi ya miezi miwili na kama haitoshi unarudi na kuniambia ndio mchumbaako? au mlikuwa mnafahamiana muda mrefuu!!!” “hahaha hapana mama ni mapenzi tu, basi si unajua wewe ndie mama na wewe ndie baba. Ikija barua ijibu malizana nao bhaasi ahhaha” “Hahahaaa haayaa mwanangu nimekuelewa” Yalikuwa ni mazungumzo ya dk Asha akiwa na mamaake ndani ya nyumba moja ya kifahari ambayo walikuwa wanaishi wao wawili tu yaani mama na mwana. Haikujulikana kama yule mama alikuwa na watoto wengine ama laah, lakini mara nyingi pale alikuwa anaishi na Asha ambae yeye alikuwa mtu wa kutoka mno na alihakikisha mamaake anakuwa ni mwenye furaha siku zote.
Baada ya masaa matano kupita yule mama akiwa amekaa sebuleni mara alarm ya mlango iligongwa na alipoinuka kufungua alikutana na mlinzi wao wa getini akiwa kasimama mlangoni. “Samahani mama, kuna mzee furani anahitaji kuonana na nyinyi vipi nimruhusu apite?” “Mruhusu tu” “Sawa Asante mama” alijibu mlinzi na kukimbilia tena getini na kumruhusu kuingia ndani ya jengo huyo mzee aliyemzungumzia ambae alikuwa ni Hussein bubu mara baada ya kuoneshwa nyumba husika na Shebby ambae alikuwa kasimamisha gari mita hamsini na eneo lilipokuwa geti la kuingilia kwa kina Asha. “Habari mama” “Salama karibu” alijibu yule mama ambae alikuwa na mwili wa wastani mara baada ya kusalimiwa na Hussein na kumruhusu akae.
Hussein hakuchelewa kujielezea kilichomleta pale na yule mama hakuonesha kupinga wala kuwa na maswali mengi zaidi ya kukubali na kuipokea ile barua “Ahsante sana mama kwa ukarimu wako, vipi lakini mzee bado hajarudi kazini.?” “haha Hapana usijali mzee kwa bahati mbaya hatunae siku nyingi” “Oooh pole sana mama” alijibu Hussein na kunyanyuka akijiandaa kuaga mara baada ya kupewa tarehe ya kuja kuchukua barua ya majibu lakini kabla hajaaga alikumbuka kitu frani “samahani mama hivi unaitwa nani.?” “Ahaa mi naitwa Zena Hamisi Kidongo” alijibu huku akiwa katabasamu yule mama lakini ikawa tofauti kidogo kwa Hussein mara baada ya kulisikia lile jina. “ZENA HAMIS KIDONGO!!?” “Eeeh kwani vipi baba mbona umeonesha kulishangaa kidogo jina langu baya sana nini?” “Hapana mama, hilo jina sio geni sana labda nikuulize unamfahamu Mariam Hamis Kidongo” “MARIAM? Haah!! huyo ni Marehemu dadaangu kabisa we umemjuaje na alifariki miaka mingi sasa”
alistaajabu yule mama na kumuangalia kwa makini Hussein ambae alijikuta anakaa chini kabisa akiwa kapigwa na bumbuwazi zito usoni mwake na machozi kuanza kumtoka akiikumbuka barua ya mariam iliyomuelekeza kuhusu ugonjwa wake na habari juu ya mtoto wake wa kike ambae alikuwa anaitwa Asha na kuanza kuamini kuwa huyu aliyekuja kumchumbia huenda akawa ni mwanae kabisa kwani hata jina alilotajiwa na Shebby pindi walipokuwa wanaandika barua ni Asha Hussein “Zenaa.. Oooh! Mi naitwa Hussein.. aaagh ndioooo Hussein Bakari… Hussein yule wa dadaako Mariam” aliongea huku machozi yakimtoka Hussein kama mtoto “Haa! Ina maana wewe ni Shemeji Hussein tuliyesikia umefungwa maisha sijui Kunyongwaa aaagh Ashaaaaaaaa ni mtoto wako aliekuachia dada!!aaaaaaaa Munguuuuu” alistaajabu yule mama na kuangusha kilio kilichomstua Asha mara baada ya kusikia anaitwa na kuanza kushuka haraka juu alipokuwa na kufika sebureni ambapo hakuamini alichokuwa anakiona na hakujua kisa na mkasa mpaka mamaake na yule mzee ambae alijua ni mshenga kugalagala chini wote wakiwa wanalia kwa uchungu mithili ya familia moja iliyopokea taarifa ya kifo cha ghafra kwa mtu waliyempenda na kumtegemea.
“Mamaa .. maaamaa!!! Vipi nini kimetokea tena?” alifika haraka pale sebureni Asha huku akiuliza kwa mshangao na kumuinua mamaake ambae hakuwahi kumuona akiwa analia kwa uchungu kiasi kile tangia apate fahamu zake mara baada ya kurudi kutoka India alipokuwa amepelekwa akiwa bado mdogo na wafadhili walioishi nae kwa zaidi ya miaka kumi kabla ya kufariki kwao nae na alipofuzu masomo yake ya udaktari hakutaka kuendelea kubaki nje zaidi ya kurejea nyumbani Tanzania ambapo alipokelewa na mamaake yule ambae alimuonesha mapenzi kama mtoto wake wa kumzaa mbali na ukweli kuwa mamaake mzazi hakuwa yeye.
“Mamaa mamaaa hebu nyamazeni basi mnambie nini kimetokea! Eti we mzee umeleta habari gani tena iliyomkosesha furaha mamaangu?” aliuliza kwa hasira Asha na kumuangalia Hussein bubu ambae yeye aliacha kulia kwa sauti na kukaa kitako akimtazama Asha akiwa haamini kama hii leo anakutana na mwanae ambae hakuwahi hata kum beba akiwa mtu mzima tena mrembo na asilimia kubwa alifanana na mamaake ambae alikuwa mwanamke wa kwanza kumpenda kwa dhati Hussein mbali ya kuwa alikuja kumtenda vibaya. “Asha, hapana mwananguuuu…. Usiongeeee kwa sauti hiyooooo… aaaaaaah Najua itakuwa ngumu kuelewa harakaharakaaa mamaaa .. ila huyo mzee unayemuona mbele yakooo ndiee….ndieeeee…. ndie babaako Mzaziiiiii….hiiiii” aliongea kwa kujikaza kisabuni yule mama mbali ya kuwa alikuwa na uchungu mzito moyoni mara baada ya kujitonesha kidonda cha kumkumbuka marehemu dadaake. “Whaat!! Mamaaa!!?..”
alitaharuki Asha na kugeuka kumtazama Hussein kwa mshangao wa hali ya juu na kumtazama tena mamaake ambae sasa nae alikaa kitako na kuanza kujifuta machozi kwa kanga huku akimuangalia mwanae Asha ambae alikuwa bado kataharuki. “Asha mwanangu, huyo ni babaako.. Huyo ndie Hussein babaako ambae tulikuficha ukweli miaka yote ila leo nitahadithia kila kitu na yoote ambayo huenda hata Shemeji Hussein hukuyajua… naomba Asha unisikilize kwa umakini sana mwangu.” aliongea kwa uchungu Zena huku akijifuta tena machozi ambayo yalikuwa hayakomi kumtoka na kumfanya Asha aungane nao na kukaa kabisa pale chini huku upande wake wa kushoto alionekana Hussein na kulia kwake alionekana mamaake ambae ni Zena. “Asha… Asha kwanza naomba utambue mimi si mamaako mzazi, nimeumia sana leo na naikumbuka sana barua ya dada aliyoniachia sambamba na maneno yake ambayo yote yalisafiri na maji mara baada ya mafuriko siku chache baada ya kifo chake kabla hawajaja wale wafadhili kukuchukua kwa msaada ulipokuwa darasa la nne baada ya kupita miaka sita ya maisha magumu na maajabu yako shuleni. Mwanangu japo ilionekana sahihi kukuacha uende kulelewa na watu wengine tena ukiwa na umli wa miaka kumi tu na japo faida yake nimeiona na naiona mapaka sasa unanilea lakini ukweli nimeenda kinyume kabisa na maagizo aliyoniachia dadaa ambae ni mamaako. aaagh! Hussein unisamehe sikuwahi kumleta Asha wala kumwambia ukweli ambao dada alinisisitiza pindi atapokua nimwambie… Eee Mungu nisamehe lakini sidhani kama nimechelewa, naahidi sasa nitawaambia ukweli wote nilioujua kuhusu Asha Dada na Hussein.” sauti ya mkwaluzo iliyoonesha dhahili imebeba maumivu mazito kutoka moyoni ilisikika ikitoka midomoni mwa Zena na kumfanya hata Dk Asha aanze kulengwa na machozi huku Hussein bubu yeye ndio kabisa alibaki kaganda kama sanamu akili na masikio yote aliyaelekeza kwa Zena japo macho muda wote yaliganda kwa Asha. Alimeza funda la mate Zena huku akirekebsha sauti yake kwa kukohoa kidogo kwa kujikaza kiume na kuanza kusimulia kisa chote kilichokuwa nyuma ya pazia juu ya maisha ya Mariam na Asha.
* * * * * (MIAKA 23 ILIYOPITA) <<<<====>>>> ………………Simulizi Ya Zena……………….. ^^^ Sintoisahau ile siku dada aliponipigia simu akiwa anaongea kwa shida sana akinisihi niende haraka kwake kwa sauti ambayo ilinitisha na kunipa wasiwasi hali iliyonipelekea niache shughuli zote nilizokuwa nafanya nyumbani na kukimbilia kituo cha daladala pasi na kumuaga yeyote wala kumsubiri mama ambae alikuwa ameenda kwenye shughuli ya harusi ya mtoto wa rafikiake mwananyamala, nilisimama kituoni na muda mfupi ilitokea daladala iliyokuwa inaelekea kule nilipokuwa naenda ambako ndipo alipopanga dada Mariamu na mara baada ya daladala ile kusimama kituoni nilipanda na baada ya mwendo wa dakika kadhaa gari ilifika kwenye kituo nilichokuwa nashuka na kushuka huku nikitembea mwendo wa haraka haraka kumuwahi dada ambae nilikuwa najua kuwa anaumwa lakini sikuwahi kuwaza kama ugonjwa aliokuwa anatuambia ungeweza kumzidia na kumfikisha katika hali mbaya kiasi kile kama nilivyotafsiri kupitia sauti yake niliyoisikia simuni muda mfupi.
Sikuamini pindi nilipoingia ndani moja kwa moja na kumkuta mtoto wa dada ambae ni Asha kipindi hiko akiwa na miaka minne tu akiwa analia pale chini huku akimtingisha mamaake aliekuwa amelala huku nzi wengi wakiwa wamemjalia sehemu ya koo na mdomo ameuacha wazi ulimi kiwa umemtoka mithili ya mtu aliyekuwa amebanwa na kitu shingoni.
‘Daaadaa!!….daadaaaa..!’ Niliita kwa uchungu na kumsogelea pale chini huku machozi yakinitoka nikiwa sielewi nini kimempata dadaangu kufikia katika hali ile ya kushindwa hata kuitika na kubaki akinitazama tu huku macho yake yakitokwa machozi mfululizo na kunijengea imani ni kiasi gani alikuwa anapata maumivu makubwa sana ya ugonjwa ambao hadi dakika huo nilikuwa sijaujua hadi pale nilipojitutumua kumuinua kwa lengo la kumrudisha kitandani kabla sijafanya taratibu za kuita gari ya kumuwahisha hospitali na hapo ndipo niliposhangaa kuona uchafu uliokuwa unatoka chini kidogo ya shingo ya dada karibu na eneo la bega tena ajabu ulikuwa unatokota kadri alivyokuwa anataka kujaribu kusema kitu ama kumeza mate na kunifanya nitaharuki na kugundua sababu za nzi wengi kumzonga dada Mariamu. ‘Aaaaaaaah..daadaangu nini tena kimekupata?!!’ Nilijikuta najisemea mwenyewe huku machozi yakinitoka kila nilipokuwa namuangalia na Asha alivyokuwa analia tena huku akiwa kashika bakuli ya plastiki mkononi akitingisha miguu ya mamaake bila kujali uwepo wangu.
“maamaaa tata ujiiii… mama ujiiiii..” Sauti na maneno ya Asha yalizidi kuniliza na kubaini kuwa zaidi kilichokuwa kinamliza Asha ni njaa na ilionesha wazi hakukupikwa chochote siku hiyo toka asubuhi na masikini ya Mungu mtoto mdogo kama Asha ambae bado akili yake ilikuwa haijakomaa, hakuwa anajua nini kimempata mamaake hadi wamekaa na njaa muda wote na hakuwa na chochote cha kufanya kwa umli wake zaidi ya kumtingisha kwa kumuamsha mamaake apike basi huo uji ambao niligundua ndio kilikuwa chakula kikubwa alichokizoea yule mtoto. Sikuwa na cha kufanya zaidi ya kutoka kuomba msaada kwa majirani mara baada ya milango mengine miwili ya ile nyumba iliyokuwa na vyumba vitatu tu alipopanga dada kuonekana makufuri yakining’inia na kuashiria wahusika hawakuwepo na kwa bahati mbaya hata wale majirani niliowafata ambao asilimia kubwa niliwakuta wanawake baada ya waume zao kuwa kwenye mishughuliko hawakuweza kabisa kunipa msaada. Hali hii ilinishangaza mno kwanini wale majirani wamekuwa na roho mbaya kiasi kile kwani kila niliyemfata kumuomba tena huku nikiwa nalia kama mtoto alionesha kunihurumia na nia ya kunisaidia lakini nilipomuelekeza nyumba yenyewe basi hubadilika na kuzuka sababu nyengine tofauti huku wengine wakidiriki kunicheka kabisa na kunitajia kiasi kikubwa cha pesa kama nitakuwa nataka msaada wao.
Nilihumia na sikujua sababu za msingi kwanini waltu wa pale walimchukia sana dadaangu na kushindwa kunisaidia walau kumbeba kumfikisha barabarani stendi ya Taxi kwani kiukweli eneo lile alipokuwa anaishi dada hakukuwa na njia ya kuruhusu gari lolote kufika hata bajaji. Sikuwa na jinsi nilijikaza tena kiume na kupiga moyo konde nilikimbia kama mwizi ama kichaa moja kwa moja hadi pale stendi na kuwaita vijana wawili ambao nilipatana nao kiasi furani cha pesa na kukubaliana nami kwenda kum beba huyo mgonjwa kumleta kwenye Taxi ambayo nayo niliongea na dereva wake aliekubali kutusubiri.
Nilitangulia ndani na kumfunika dada vizuri hususani sehemu za juu kuuficha uchafu uliokuwa unavuja na kutoa harufu kali kwa kitenge changu ambacho nilijifunga kiunoni na kujikuta nabaki na skin tight ndefu ambayo awali nilikuwa siwezi kutembea mtaani nikiwa nimevaa yenyewe tu pasi na kujifunga walau kanga ama kitenge lakini siku hiyo nilijikuta najisahau kabisa kwa kuchanganyikiwa na laiti kama nisingekuwa na walau hiyo skin tight basi hata uchi kabisa ningetembea pasi na kujijua wala kujihisi.
Lakini kila nilipokuwa namuangalia dada alinionesha machoni kuwa kuna jambo anataka kunambia lakini anashindwa na nilipomtazama kwa makini alinipa ishara kwa kuangalia kwenye dressing table yake na kuniangalia mimi, alifanya vile kama mara tatu ndipo nilipoenda kuangalia hapo kwenye dressing table kuna nini na nilipekuwa kuangalia ndipo nilipoiona bahasha kubwa ya barua ikiwa imeandikwa jina langu kwa nje na ndipo nilipomuangalia dada ambae aliniashilia kwa macho kuwa ndio hiko kitu alichomaanisha lakini kwangu sikuona umuhimu wa kukaa chini kuanza kusoma barua wakati dadaangu amelala anateswa na maumivu makali..!! Nilichofanya niliitumbukiza kwenye handbag yangu ile barua na kuwaruhusu wale vijana waingie ambapo walipoingia niligundua mshtuko wao na adha ya harufu ya ajabu waliyokutana nayo mule ndani ambayo mimi sikuihisi nilipoingia hadi pale nilipojionea kidonda cha dada kilichokuwa kinavuja uchafu na hata hivyo sikukerwa hata chembe kwa ile harufu zaidi ya kuniongezea simanzi. “Dada, mzima huyu?” “Aaagh! Fanu maswali gani hayo? we kamata huko tum bebe tumpeleke…. unauliza mzima!! sasa toka lini mtu aliyekufa akawa anatoa ukoromo?”
maneno ya kijana wa mwanzo yalinichoma sana japo sikuweza kujibu chochote lakini niliumia sana kuona dadaangu kipenzi akifananishwa na maiti angali yu hai kwa kigezo cha ile harufu..!? Aaaaah!! ama kweli wanaadamu tunakufuru kubwa. Afadhali kauli ya yule mwenzake aliyemjibu kidogo ilinifurahisha japo sikuipenda pia kwani dadaangu alikuwa hakoromi bali alikuwa anaugulia maumivu makali aliyokuwa anayapata lakini kile kidonda ndicho kilichokuwa kinaifanya sauti yake kusikika kama mkoromo kutokana na kutokota kwake kadri alivyokuwa anachezesha koromeo. Nilimnyanyua na kum beba Asha ambae bado alikuwa kashikilia bakuli lake akilia na kutoka nae nikiwa nyuma ya wale vijana waliom beba dadaangu Mariam na sikukumbuka hata kufunga mlango zaidi nilikuwa makini na kumshika Asha ubavuni nilipom beba kutokana na kulia kwake na nilipandwa na hasira zaidi mara baada ya kupita hatua chache kwa majirani wale ambao walininyima msaada awali na kuwakuta wameeka vigenge vya umbea kwenye baraza zao huku macho yao yakiwa kwetu na tolipofika karibu walinyamaza na kuishia kutututazama na tulipopita ndipo waliangua kicheko kikubwa kwa pamoja. ”’HEEHEEEEEE KAPIMEEEEEEEE”’
Nilitamani nirudi nikachambane nao lakini nilishindwa na kubaki nimefura hasira iliyochanganyika na maumivu mpaka tulipofika pale stendi ambapo kila aliyetuona hakuacha kutushangaa wakati dada alipokuwa aningizwa kwenye ile Taxi nami nikamnunulia soda na Keki mbili Asha mara baada ya kumalizana na wale vijana, na hapo kidogo kelele za kilio cha mwanangu Asha zilipungua pindi tulipoingia kwenye ile Taxi na kumueka mbele huku mimi nikikaa nyuma na kumpakatia dada ambae sauti aliyokuwa anaitoa iliyo mithili ya ukoromo ilizidi kuongezeka na kuniumiza zaidi kwa kugundua kuwa maumivu yanazidi mwilini mwa dadaangu kipenzi.
Nilimuamuru dereva kutuwahisha mwananyamala hospitali na kumpigia simu mama muda uleule gari ilipoanza kutoka na kumuelekeza hali ya dada huku nikimficha juu ya kidonda cha ajabu kilichokuwa shingoni kwa dada kwa kujua kuwa mamaangu anakuwaga na uoga unaoambatana na presha ya kushuka hasa anapomuona mwanae anaumwa sana ama kazidiwa hivyo hata ile kauli yangu kuwa nampeleka hospitali ilitosha kumstua kule aliko na mara baada ya taxi yetu kufika hospitali mwananyamala niliwakuta tayari mama na baadhi ya rafiki zake waliokuwa kwenye shughuli wakiwa na nyuso za huzuni getini huku mamaangu akiwa peku kabisa licha ya kuwa alitoka nyumbani akiwa amependeza na zaidi alivaa viatu ambavyo alinunuliwa na dada Mariam.
Ilibidi nishushe kioo na kuwapungia kuwaelekeza kuwa Taxi wanayoitazama inayoingia sasa ndiyo niliyomo na kweli walianza kuifatilia hadi iliposimama ndani ya ile hospitali na ndipo mama alipoingia kumchungulia dada pindi nilipomuacha na kwenda kuwaita manesi ambao walikuja haraka na kitanda cha matairi kwa nia ya kuja kum beba dada. Moyo uliniuma sana nilipotoka na kumkuta mama akiwa analia huku ameshikwa na wale shoga zake na manesi wa mwananyamala sitoweza kuwasahauuu….. aaaaaagh nakumbuka jinsi walivyokuwa wanampakia dada kwenye kitanda kile mithili ya mzigo mbali na kelele za ukoromo wa maumivu na kusababisha kile kitenge nilichomtanda kwa kuziba eneo lile la jeraha kufunuka na kudondoka na hapo kila mtu aliyekuwa jirani alistaajabu kushuhudia ule uchafu ambao hata mimi nilishangaa kuona umezidi mara dufu huku lile tundu likiwa si dogo kama nilivyoona awali bali liliongezeka na ilitaka moyo sana kulitazama. ””Aaaaaaaaaaaaaaaaaaagh, Mariaaaaamu Mwananguuuuuuuuu”” Sintoisahau kauli hii ya mama angu.. mamaetu kipenzi aaagh, Sikujua kabisa kama ile siku niliyomuambia ‘mama umependeza sana leo umekuwa kijana kabisa’ asubuhi yake pindi aliponiaga anakwenda kwenye shughuli ya harusi ya rafiki ake wa miaka mingi Mwananyamala kama itakuwa ndio siku yetu ya mwisho kucheka pamoja….!
Aaaaah sikuwaza wala kuhisi kama ipo siku mamaangu atanitoka ghafra namna ile tena mbele ya macho yangu na watu wengi kiasi kilee aaaah, masikini Zena mimiii nitalia na nani na tulizaliwa wawili tu na dadaangu ambae ndio nae alitoa ukoromo wa sauti ya juu uliotokea kwenye lile tundu na kurusha uchafu mwingi sambamba na damu mithili ya bomba mara baada ya kitenge kilichokuwa kinaburuza na kukanyagwa na nesi kudondoka na mama kupiga ule ukelele uliopelekea kuanguka chini. aaaaaaaaaah kwanini hamkunambia ndugu zangu kama mmepanga kuondoka pamoja kwenye ulimwengu wa mauti na kunifanyia suprize iliyoutesa moyo wanguuu na kuniachia upweke wa milele!!??…… aaaaaaaaaaah Nilijikuta nami nawasindikiza mama na dada kwa kupoteza fahamu pindi nilipokuwa nashuhududia vifo vyao ambapo mama alitapatapa na kukata roho pale chini muda mfupi baada ya kudondoka huku dada Mariam nae alimalizikia muda mfupi baada ya kutoa ule mkoromo mkubwa mithili ya firimbi uliorusha mafunda ya uchafu na damu. Sintosahau maneno ya yule daktari alipokuwa ananipa maelezo ya uthibitisho wa vifo vya ndugu zangu siku moja baadae pindi nilipopata fahamu na kuruhusiwa wodini. Alinambia kuwa kifo cha mamaangu kilisababishwa na presha iliyoshuka ghafra kupita kiwango vilevile dadaangu Mariam kifo chake kilisababishwa na kansa hatari ya koo. Sintosahau kabisa hata mara baada ya ndugu na majirani kuungana nami hospitali na kuchukua maiti kurudisha misiba ile ya kihistoria moyoni mwangu mpaka nyumbani na baada ya taratibu za mazishi kukamilika hatimae mama na dada wote walizikwa siku moja na makaburi yao yalifatana. aaaah! Mungu awaeke mahali pema. Siku moja kupita baada ya mazishi ilibidi nitoke na vijana wa kiume wachache sambamba na mzee wetu wa mtaa tuliokuwa tunaishi tuliyezoea kumwita babu japo hakuwa na undugu wa damu na sisi lakini alikuwa jirani mwema na alisifika kuwa mzee mwenye busara sana. Safari yetu ilikuwa ni kule alipokuwa anaishi dada Mariam kwa niaba ya kukusanya vitu vyote lakini hatukuamini baada yakufika na kukutana na habari za uvamizi na wizi uliotokea siku moja iliyopita ambapo vitu vyote muhimu vya dada viliibiwa na chumba kubaki cheupe mithili ya mtu aliyehama. Japo ilituuma lakini tulipiga moyo konde na kushukuru tu, kwani iwapo tumempoteza mtu kabisa sembuse hivo vitu? tuliwaaga wale wenyeji tuliowakuta kwenye vile vyumba viwili ambavyo siku ile nilipokuja kumchukua dada vilikuwa na makufuri tu.
Yule mzee alinisaidia kuongea na wale majirani visilani mara baada ya kumuhadithia mkasa ulipoanzia ambapo kwa busara zake aliweza kuambua sababu kuwa kumbe dada Mariam alikuwa ni mtu wa kujiona ona sana kipindi anaishi pale na mashoga zake watatu waliopanga pamoja huku mmoja wao akiwa si mwanamke bali ni shoga kabisa tena mbaya zaidi waliitumia ile nyumba kama dangulo la kuingiza wanaume hali iliyokuwa inawakera sana majirani kwa vile kujiona kwao, kutoshiriki kwenye misiba ya wenzao na matatizo mengine huku wakiwa ni watu wenye nyodo nyingi na ndio sababu kuu za kuwachukia wote na kuwatenga. Hapo kidogo nilielewa lakini bado sikulidhika na yale waliyonionesha lakini niliamua yote kuyapuuza na kurudi nyumbani sambamba na yule mzee na wale vijana.
ulipita mwezi mmoja baada ya kumaliza matanga ndugu wote walitawanyika na kuniacha nikiwa na mwanangu Asha mtoto wa marehemu dada bila msaada wowote wa kimalezi zaidi ya kuniachia maneno ya pole na maisha mema na huo ndio ukawa mwanzo wa maisha mapya ya misukosuko na mazoea baina yangu na Asha.
Lakini kabla hazijaanza tabu na misukosuko ambayo sikutaraji kama yatatukuta mimi na mwanangu yule niliumizwa na kulizwa na kitu kimoja ambacho nilikikumbuka mwenyewe baada ya kusahau kwa muda mrefu….. Kitu chenyewe ni barua, barua ambayo ilionesha wazi kwa nje ilinihusu mimi, barua ambayo sikujua imebeba nini hasa ndani yake, barua ya mwisho ambayo muandishi wake nilijua kama hatoniandikia tena barua nyengine milele, ila kwa barua ile niliweza kuihisi sauti yake akiongea pindi nilipokuwa nasoma hati ya maandishi yake, barua toka kwa marehemu dada Mariam ambayo licha ya kupotea kwake kutokana na janga kubwa la mafuriko ya mwaka lililokuja kutokea wiki chache baada ya kuisoma lakini maneno yake yaliendelea kuishi akilini mwangu kila nilipomkumbuka yeye ama nilipomuangalia Asha. Barua yenyewe ilikuwa hivi…………….
^……………………………………………………………………….^ Mdogo angu Zena, naandika barua hii nikiwa na maumivu makali sana sehemu za shingo na kifua hususani kooni na hivi sasa uvimbe ambao awali ulikuwa kwa ndani lakini sasa umezidi kutokeza nje ya shingo, najua muda wowote unaweza kupasuka na kuimaliza safari yangu ya hapa duniani kuianza safari mpya kwenye ulimwengu wa ahadi kwa kila mja aliyeumbwa. Uvimbe huu si wa jipu la kawaida bali ni ugonjwa ambao nimeuficha kwa zaidi ya miaka miwili kutokana na aibu na kutopenda niwatie majonzi mapema lakini kwa kuwa sasa naona ule wakati wa kuumbuka umefika nimeamua kukuweka wazi ukae ukijua kinachoniua ni nini.. Hiki kinachonitafuna Zena ni Kansa.
Kansa ambayo imesababishwa na wadudu wabaya waliotoka kwenye mbegu za mwanaume nisiyemjua ambae kumbe alikuwa na ugonjwa m baya sehemu zake za kutungia mbegu nami bila kujua nilijikuta nazipokea mdomoni kwa kumnyonya uume wake mpaka anafika kilele kinywani mwangu nikijua nampagawisha ili nimchune vizuri kumbe nilikuwa naeka lehani maisha yangu mara baada ya bakteria hatari ambao sijawahi kuota kama wapo walipoingia na kueka makazi pembeni ya koo langu kutokana na ukweli huwezi kutema chote kile kichofika kwenye ulimi na hiyo ndio ikawa mwanzo wa tatizo ambalo nilikuja kugundulika tayari nimechelewa.
Ni aibu lakini nimeamua kutubu kwa kukuandika ukweli huu mdogo angu Zena nakusihi kama nawe una tabia ya kunyonya tupu za wanaume kwa kuamini ndio unamkoleza nakusisitiza acha haraka tabia hiyo na hili uje kumfunza hadi mtoto ninayemkabidhi kwako baada ya kifo changu. Narudia Zena kumbuka kinachoniua dadaako na simjui ni mwanaume yupi aliyeniachia hawa bakteria walioshindika kutokana na kuwafanyia mchezo huu karibu kila mwanaume niliekutana nae kimwili kasoro mwanaume wangu wa kwanza na yule wa pili ambae ndie baba halali wa mtoto huyu nae ni shemeji ako niliyemuacha kimakosa mimi mwenyewe baada ya kumsaliti sana ambae ni Hussein.
Zena nakukumbusha pia hata utapoolewa ukiwa na mumeo usikubali kumuacha awe anakunyonya tupu yako mpaka unafika kishindo kwani kuna hatari kubwa ya magonjwa ya ajabu kupitia sehemu za siri si kwa mwanaume wala mwanamke ambayo mengi hayajaibuka ila leo hii mimi nimekuwa mfano wa mavuno ya tabia hizi chafu ambazo asilimia kubwa ya vijana si wa kike si wa kiume wanafanya haya kila siku ilihali sehemu husika zipo. Basi waambie wataokusikia habari za kifo changu labda utasaidia kuwaokoa baadhi yao japo najua wengi watakupuuza na hata wataokaidi basi waache waendelee ila wajue yanaweza kuwakuta kama yaliyonikuta mimi kwani hizi ni zama za mwisho wasiige mafunzo ya kishetani yanayosambazwa kwenye mikanda ya ngono. Kifo kinauma sana hasa kifo cha dhihaka kama hiki… Dawa pekee ya haraka niliyoambiwa na daktari ni kukata sehemu inayoshambuliwa lakini sasa mimi nashambuliwa koo maana yake hata nikikatwa haitakuwa tiba.
Huo ndio ukweli Zena najua mwanangu hatolelewa na babaake wala hajawahi walau kushikwa mkono na babaake ambae wote tunajua maisha yake anayamalizia gerezani. Basi nakuomba pindi utapokuwa unamlea Asha mlee katika maadili tofauti sana Zena mdogo wangu na uwe unampeleka walau mara moja kwa mwaka gerezani akamuone babaake kwani taarifa za uwepo wake naamini anazo. Kumbuka Zena kumbuka mpeleke Asha madrasa akajifunze elimu ya dini. Naamini kifua chake kitapojaa imani na jina la mungu litapokaa kinywani naamini atafauru majaribu mengi ya kishetani na kamwe hatokuwa mwanamke muuaji kama walivyo wanawake wengi wa leo nikiwemo mimi na wewe kwa kitendo chako cha kutoa mimba zaidi ya mara mbili tulipokuwa shule. Nakusihi nawe utubu mdogo wangu na uzingatie usije kumpa mtu mwengine amlee Asha naogopa asije kuharibika na kuwa mwanamke muuaji akaja umiza wanaume kama mimi nilivyomuumiza babaake.
Kwa heli Mdogo angu, mimi natangulia…. Mungu akipenda tutaonana kwenye ulimwengu wa mauti pindi nawe utapokuja mwaka wowote.
^……………………………………………………….^
Barua ya dada ilifufua msiba upya moyoni mwangu huku nikilia kwa uchungu sana kwani hata mimi nilikuwa na tabia hiyo ya kunyonya tupu za wanaume lakini daaaah! kumbe harufu na uchafu ule ambao ulikuwa unatokota shingoni mwa dada ni kansa ya koo?!! Tena chanzo chake ni mchezo ambao hata mimi nilikuwa ni mmoja wa wachezaji wake…!! aaagh nilipogundua na kukumbuka mateso ya dada hadi pale alipotoa mkoromo mkubwa tena sauti ikitokea kwenye tundu lililokuwa linarusha uchafu wa usaha na damu hadi kufa kwake…. Nami kuanzia muda huo niliapa kamwe sitoruhusu mwanaume aninyonye utupu wala mimi kumnyonya utupu na kuahidi kuutumia mdomo wangu kwa kula, kunywa na kuramba vile vilivyohalalishwa tu.
Lakini mwezi mmoja baadae lilitokea janga la mvua iliyosababisha mto uliopita jilani na pale tunapoishi kufurika na maji kupasua kwenye makazi ya watu ikiwemo nyumba yetu majira ya usiku ambapo nilichobahatika ni kujiokoa mimi na mwanangu Asha niliyeachiwa na dada na hapo ndipo tulipogeuka wahanga wa mafuriko tulioishi katika kambi maalum uwanja wa taifa baada ya kupoteza makazi kwa zaidi ya miezi miaka miwili. Serekali yetu imejaa hila na rushwa kwakweli japo machoni na midomoni haiko hivyo kwani baada ya kupewa ile kambi kipindi cha janga lile na kutusaidia miezi michache ya awali, ndipo walipotutelekeza kabisa na hapo nami nikakata shauli baada ya kumpata bwana ambae alitukaribisha kwake kabla ya kumuhama baada ya manyanyaso na kumuonesha chuki za wazi mwanangu Asha ndipo nilipopanga maeneo ya uwanja wa fisi na kujiajili kwa kuutumia mwili wangu. aaaag Moyo unaniuma sana kwa nilichofanya kwani nilimpeleka Asha kwenye shule ya watoto walio kwenye mazingira magumu sana na yatima na kumuacha kwa muda huko mwanangu Asha si kwa lengo kuwa simpendi bali kwa kumueka mbali na mazingira yale ambayo nilijua yatamuharibu kisaikolojia pindi atapokuwa anaona mamaake kila siku nalala na wanaume tofauti tofauti.
Siku zilikwenda huku kipato changu kikiongezeka na kuwa namtembelea mara kwa mara mwanangu Asha ambae alikuwa anazidi kunipenda siku hadi siku na pia nilizidisha mapenzi kwake hasa baada ya kipaji chake cha elimu kuonekana kwa wafadhili wa kihindi miaka minne tu tokea aishi pale na alipata bahati ya kupendwa na wale watu ambapo zilifanyika taratibu za kuondoka nae kwenda kumsomesha huko japo awali nilitaka kukataa lakini kwa ushauri wa watu na walimu wake sambamba na kalatasi za serikalini na kuhakikishiwa kuwa mwanangu hawezi kupotea na hii ni kwa faida yetu wote pindi atapofanikiwa huko kwani hata mimi nilishindwa kumlea hadi nikampeleka pale ndipo akiwa na miaka kumi tu niliweza kuvunja vunja zaidi yoote niliyoagizwa na dada Mariam juu ya Asha na hiyo ndio safari ya mafanikio yaliyokuja kuibuka na kufaidi matunda ya mwanangu Asha na kwa bahati mbaya dawa nilizokuwa natumia nisipate mimba ziliniletea madhala pale nilipohitaji mtoto nilishindwa kabisa kubeba mimba na nilipochunguzwa nilihakikishiwa haitawezekana kubeba mimba na ndio sababu hadi leo sina mtoto yeyote zaidi ya mwanangu Asha ambae siku zote aliamini mimi ndie mamaake mzazi.
<<<===>>> ……………………….. * * *
Kipindi Zena akimalizia simulizi yake iliyowafanya Hussein bubu na dk Asha kubaki wanadosha machozi kwa uchungu mkubwa huku wakiwa wameshabadilisha kila aina ya mikao wakimtazama Zena bila kujua kumbe mlango ulikuwa unagongwa muda mrefu sana na walichostushwa ni baada ya kufunguliwa na kusikia viatu vya mtu akiingia pale sebureni na walipogeuka wote walimshuhudia Kamishna Shebby akiwa amesimama baada ya kuingia tena akiwa amestaajabu kupita kiasi kwa kile alichokuwa anakiona watu wamekaa chini wameyaacha makochi na zaidi wote walikuwa wanalia.
“Vipi Asha?! samahani mama kwa kuingia pasi na ruhusa.. vipi mzee wangu mbona sielewi kwema??” aliongea kwa taharuki Kamishna Shebby na kusogea pale walipokaa kina Hussein baada ya mama mdogo wa Asha kumruhusu kwa ishara nae akae tu sofani huku nao wakijizoazoa kuketi vizuri kwenye masofa wakiwa bado na nyuso za huzuni. “Vipi mzee wangu, umenitisha sana baada ya kuchelewa Asha.. Mama nini kimetokea hapa?” aliuliza Shebby huku akiwatazama machoni ndipo Hussein alipoanza kumsimulia kisa kizima na kumfanya Kamishna Shebby abaki ameduwaa.
“Kha!! Ina maana Asha ni mwanao!!! yaani kumbe wewe niliyekutuma ni baba Mkwe!? Eee Mungu mbona siamini..” “Amini hivyo baba, mimi ni mama mdogo tu wa Asha na huyu ndie babaake kweli kabisa wala sio utani hata mimi siamini kama leo hii tumekutana” aliongea Zena kwa majonzi “BABA” Kwa mara ya kwanza Hussein masikioni mwake aliisikia sauti ya mtoto wa kike akimwita baba tena mtoto ambae hakuwahi kuilea hata mimba yake, walijikuta wananyanyuka kwa pamoja Asha na Hussein na kukumbatiana kwa nguvu huku wote wakilia lakini kilio cha sasa kilikuwa ni cha furaha. “sikuwahi kufikiria hiki kitu jamani babaangu pole sana kwa yaliyokukutaa” “Aaaah! mwanangu usinipe pole mamaaa nisamehe sana mimi nilichelewa kujua uwepo wako aaa” Ilikuwa ni furaha ya baba na mwana kujuana huku Zena na Shebby wakiwa wamekaa wakiwaangalia na kumshukuru Mungu kabla nao hawajasimama na kuungana nao pamoja kuwafariji.
Baada ya kuliwazana na kila mtu kurejea katika hali ya kawaida huku furaha ya aina yake ikiwa kwenye moyo wa kila mmoja ndipo Asha aliposimama na kumshukuru sana Kamishna Shebby kwa ukalimu aliomuonesha babaake huku akimuomba babaake (Hussein) kuanzia siku hiyo afanye makazi yake pale kwenye ile nyumba wakti pia akimtafutia makazi mengine mazuri ya kuishi lakini ajabu Hussein alikataa na kumwambia Asha maneno ambayo hakuyatarajia. “Asha mwanangu nakupenda sana na nimefurahi mno kukujua, lakini wewe ni mwanamke na sasa upo mbioni kuolewa na mwanangu wa hiyari ambae nataraji atakuwa mkwe wangu mwema siku zote, kwa sasa furahia kuwepo pale mpaka mtapooana ndipo kwa amri ya Mkwe wangu ndipo nitatoka na kukaa sehemu nyengine mtayojadili kwa pamoja nikae lakini si kwa amri wala matakwa yako binafsi.” Maneno mazito ya Hussein yalitosha kuutafsiri moyo wa Asha kiasi gani babaake alikuwa na mapenzi mazito na mchumbaake hivyo alikubaliana na mawazo ya babaake ila alimuomba Kamishna Shebby amruhusu basi alipie yeye gharama za pale hoteli na kwa mapenzi ili mradi mpenzi wake alidhike Shebby alikubali.
Baada ya hayo kumalidhika ndipo Hussein alipomuomba Asha alete kalamu na karatasi kwa niaba ya kuijibu ile barua tena mbele ya Shebby mwenyewe ambae awali alitaka awapishe nje ili wajadiliane vizuri lakini Hussein alimzuia na Zena alikuwa radhi Hussein amalize kila kitu. “Nimekuja kama mshenga na sasa naichana bahasha na kuijibu barua kama baba, Asha mwanangu taja mahali yako ya Ndoa.” “Mh! baba si utaje wewe tu” “Hapana wewe ndie unayeolewa” “sawa basi mi…. mi Elfu kumi tu inatosha” “Safi sana mwanangu”
alijibu Hussein na kuendelea kuandika na alipomaliza alimkabidhi Shebby palepale. “Mwanangu tuachane na mambo yote barua hii ifike nyumbani ukitaka kuoa hata kesho njoo nitatoa mimi hiyo elfu kumi ya Asha japo ni katika pesa zako ulizonipa, hakuna gharama nyengine zaidi ya hiyo elfu kumi huku kwetu” alisisitiza Hussein na kumshangaza mno Shebby lakini ukweli ndio ukawa hivyo na lilikuwa jambo geni kabisa kwa mila na desturi za kibantu barua kujibiwa mbele ya muhusika wa kiume na kumkabidhi yeye moja kwa moja.
Baada ya hapo ndipo Hussein na Shebby walipoondoka huku wakiwaacha Zena na Asha wakiwa nusu wameamini nusu hawajaamini kwa kilichotokea siku hiyo.
* * * * * * MKESHA WA MAWAZO
^^^^^^^^ HUSSEIN BUBU ______________ Usiku wa siku hiyo ulikuwa mgumu kwa Hussein kupata usingizi kwani muda wote mawazo yalimpeleka mbali sana huku akiwa haamini kama leo yuko huru na kumbe yule daktari bingwa Asha aliyesaidia kumtibu mtu aliyemsaidia yeye kwa moyo ni mwanae na kwa uwezo wa Mungu alifanya kazi ya kumsaidia jeraha baya alilopata Shebby mpaka amepona kabisa na kujikuta wanakuwa wachumba? Alijikuta anageuza msikiti chumba cha ile hotel mala baada ya kujiazinia mwenyewe na kuanza kusali usiku kucha ambapo kila alipopumzika aliomba dua na kumshukuru Mungu na kuendelea kusali.
(“Aaaaaah! kweli Mungu wewe ni Mkubwa sana na mwenye sifa za kipekee, Nakuomba kama ulivyonitendea muujiza wa kutoka jela na ukafanya kunikutanisha na mwanangu ambae nilijua habari zake nikiwa jela na kukata tamaa ya kumuona tena, basi baba nakuomba kama ulivyofanya hayo yote basi iwe hivyo na kwa Mr X niweze kumjua na kulipa kisasi kwa mikono yangu”) Na hiyo ndio ilikuwa dua kubwa ya Hussein bubu katika nafsi yake kila alipopumzika na kumshukuru Mungu na alisali huku mawazo yake hayo ambayo alikuwa nayo toka jela yakijirudiarudia akilini mwake
^^^^^^^^^^^ KAMISHNA SHAABAN ___________ Si Hussein tu, mambo yalikuwa hivyo pia kwa Kamishna Shebby ambae nae alikosa lepe la usingizi kwa kufikiria mengi sana huku akivuta picha siku ya kwanza anakutana na Hussein bubu. (“Daaah! Mungu kweli wa ajabu na ameeka siri nzito sana katika maisha ya kila kiumbe yalivyo mbele kutokana na mzunguko anaomuonesha kabla daa…. Yaani kumbe muda wote natoa msaada kwa mtu ambae imeandikwa ndie baba mkwe wangu!!! “) aliendelea kuwaza Shebby (“Nina sababu zote za kumtafuta mshenzi mr.X na kulipa kisasi bado niko sahihi kwa hili”) aligeuka Shebby pale kitandani na kuchukua simu iliyokuwa pembeni ya mto na kumtumia txt Cj4 akimjuza kila kitu kilichotokea kule walipopeleka posa ambacho awali hajamjuza. )(‘So huyo mkeo mtarajiwa Hussein kumbe ni babaake?’)( iliingia sms ya Cj4
na Shebby kumjibu ndipo sms ya Cj4 ilipoingia nyengine )(‘Kuwa makini sana na mchumbaako hupaswi nae kumwambia habari zozote za mipango yetu’)( ))(‘Sawa lakini kwanini unasema hivyo’)(( )(‘Kumbuka upo kwenye mchezo na mr X sasa usikubali uchezeshe na mr X kwenye huu mchezo ila wewe ndie umchezeshe mr X ktk huu mchezo na hapo tutamshinda.. Kumbuka kama Hussein bubu tumemumtoa kama chambo harafu mwanae kumbe ni mchumbaako nina shaka hili mr.X analijua na isije kuwa na huyo mchumbaako akawa anachezeshwa na mr X kwenye huu mchezo pasi na yeye kujijua’)( SmS ya Cj4 ilimfanya Shebby ashushe pumzi na kuirudia mara mbilimbili huku moyoni akikili kuwa kuna upana mkubwa sana wa kimbinu na fikra baina yake na Cj4
DOKTA ASHA ______________
Kwa upande wa Dokta Asha yeye ilikuwa tofauti kidogo, naweza kusema yeye ndie alikuwa na mawazo mazito pengine kuliko wote. Alijikuta anagalagala kitandani akigeuka huku na kule kuulazimisha usingizi ambao ulimuhama kabisa kutokana na mawazo mengi yaliyoibuka kichwani mwake mara baada ya kuujua ukweli na kuonana na babaake. Muda wote maswali mazito yasiyo na majibu kamili yalizidi kuandama kichwa cha Asha na kumnyima amani ya kusinzia usiku kucha. (“Hivi kwanini lakini imekuwa hivi? aagh! Kwanini sasa? Aaaaaaaaaa!!? Kumbe Mungu Yupo? leo ndio Nimeamini lakini Kwanini?!!”)
alijiuliza maswali haya Asha mara nyingi kupita kawaida huku akijipigapiga kichwa chake na kadri alivyokuwa anajiuliza ndivyo hasira zilivyozidi kumshika na kuvimbisha kifua chake na hapo ndipo alipoamua kunyanyuka kwa style ya aina yake nusu sarakasi kwa jinsi alivyoizungusha miguu na kujibetua kiwiliwili akitegemea kichwa kabla ya kujirusha na kutua nje ya kitanda tena akiwa kasimama mbele ya dressing table yake ndogo anayotumia kujiremba na hapo ndipo alipoisukuma kuisogeza pembeni na ukutani pale kulipozibwa na dressing table kulionekana picha yake mwenyewe lakini ajabu alipoiondoa ile picha kulionekana batani kama za simu ambazo alitumia kuingiza namba alizozijua mwenyewe na hapo hapo kwa ajabu pale aliposimama kulipokuwa na dressing table kulipoanza kudidimia kwenda chini taratibu akishuka kama lifti na hatimae Asha alibukia kwenye chumba kimoja kidogo sana kilichokuwa na Kompyuta screen touch maalum za kisasa zikiwa kwenye kila upande wa kuta za kile chumba pamoja na kiti kimoja sambamba na mashine special za kuscan huku taa za rangirangi zikiwa zinawaka muda wote na Kompyuta zote zilikuwa on.
Alikaa harakaharaka huku akili zake zikiwa na mawazo mazito ndipo alipoandika ujumbe uliosomeka. ‘NATAKA NIKUONE’ na kusimama akihema huku akizunguka zunguka kusubiri jibu lakini mara jibu lililokuja alipolifungua liliustua zaidi moyo wake ambalo liliandamana na picha ya babaake aliyemjua siku hiyo tu tena ujumbe ulisema ‘KWANZA MALIZA KAZI YA KUIONDOA ROHO YA HUYU’
“Whaat..!!?” alitaharuki Asha na kushindwa kujua aujibu vipi ule ujumbe na akiwa anatafakari mara ujumbe mwengine uliingia na alipousoma ulimpa maelekezo husika sambamba na kumuonesha picha ya hoteli ambayo alifikia Hussein na kona zote za ulinzi wa ile hoteli. (‘I can’t do this’) aliwaza Asha na kufungua ripoti za nyuma alizokuwa anatumiwa sambamba na picha juu ya watu ambao mission zake alizimaliza na kiasi cha pesa alichokuwa anatumiwa. Moyo ulimuuma na kujutia kwanini amekubali kushawishika na kazi za mtu ambae hakuwahi kumuona hata siku moja katika maisha yake? Kulikuwa na siri nzito sana moyoni mwa dk Asha juu ya safari ya maisha yake nchini India ambayo hakukuwa na yeyote anayeijua zaidi yake yeye mwenyewe.
………………. (^((^((^(((^^”Aaaagh!! Kweli nyie WANAWAKE NI WAUAJI hatari sana tena msiorudi nyuma WALA KUFIKIRIA hasa pale mnapopewa nafasi ama amri huitumia vizuri ili mzidi kuimanishwa na muonekane bora kuliko wanaume. Ila KUMBUKA kuwa wewe si wa kwanza kutumiwa na mr.X na laiti UNGEMJUA YAKINIFU huyo anaekutuma kesho anaweza kukuua hata wewe endapo atasikia upo kwenye mazingira hatarishi na maisha ya siri yake….. hahahahaaaa tatizo WANAWAKE HAMFIKIRII hah haha Ila nami nakwambia hii uliyoipata leo ni bahati kubwa sana ni bora tu uitumie lakini nakuahidi ukiniacha hai lazima nije kukutafuta na utalipa Damu zote zilizovuja leo. Naapa sitokuja kukuacha hai kama leo utaniacha hai na umwambie mr.X asijidanganye MWISHO WAKE UPO na atakufa kifo kibaya na cha mateso aaghhh..” ^^)))^)))^))^))^) ……………..
Ilimjia kichwani sauti hii ambayo aliiongea Kamishan Shebby kumwambia yule Ninja wa kike kule Mkuyuni pindi alipobong’onyolewa mguu, hii inamaanisha kumbe dk Asha ndie yule ninja aliyetumwa Mkuyuni na ni kibaraka wa mr X lakini kilichomuuma leo ni kuujua ukweli juu yake harafu kutomjua Mr X “WHO FUC** ARE YOU..!!!?” alipiga kelele za hasira Asha na kupiga teke kile kiti kilichokuwa mbele yake na kukipaisha hadi kwenye screen moja ya computa na kuivunja palepale.
Hayo ni maajabu machache sana kati ya mengi aliyokuwa nayo Dokta Asha. Mzuri wa sura na umbo lakini nyuma ya pazia ni hatari sana ana nguvu na trick za kila aina za kimafia. Ukweli yeye ni Muuaji wa Kimataifa wa siri anayetumiwa na Mr X muda mrefu na kashawaua wengi sana nyuma ya pazia waliojaribu kumpekenyua Mr.X kwaajili ya kumchafua.
Yeye ndie yule Ninja wa Mkuyuni na mr X ndie aliyesababisha kumueka jilani na Kamishna Shebby mara baada ya kumuarifu atautumia mtandao wake kumshawishi babaake Shaaban ambe ni mzee Mwinchande pasi na kujua chochote akubali kumwita yeye ambae kwa nje dunia ilimjua kama daktari awe tabibu namba moja na Mr X huyohuyo ndie aliyemtupa ajenge mahusiano na Kamishna Shebby ili aolewe nae na iwe rahisi kumdhibiti na kujua mbinu zote zitazopangwa juu yake kwani Shebby ndie alionekana mwenye kihelehele cha kumjua sana mr X. Lakini mbali na hayo yoooooote Ukweli ni Kwamba Dk Asha hakuwahi kuongea ana kwa ana na Mr X wala kumuona. Na ndio kitu kikubwa kilichokuwa kinamuumiza sasa… lakini kwanini miaka yote anafanya kazi na kuwasiliana na mtu asiyemjua ? kaanza anza nae vipi na wapi hadi imefikia kuamini na kumtumikia hali ya kuwa hamjui ? Imekuaje awe na sifa ya udaktari bingwa lakini kumbe pia ana sifa ya uuaji? Hakika maisha ya Asha yalibeba maswali mengi sana ambayo kama hujayasoma na kuyajua maisha yake nyuma ya pazia yalivyokuwa basi hutoweza kuwa na majibu yake.
”I hate You Mr X…. I’ll Find You….. and I’ll Kill You” aliongea kwa hasira kwenye mike moja maalum iliyoconnectiwa na mitambo yake iliyokuwa mule ndani Asha na kuituma moja kwa moja kwa Mr X na hapo ndipo alipoanza kuvunja vunja computa na kuharibu kile chumba chake cha siri huku akilia kwa uchungu lakini mara majibu yalirudi kwenye kompyuta moja ambayo alikuwa bado hajaivunja na alipoyafungua alistaajabu baada ya kusikia sauti ya Mr X ambayo mara nyingi huwa inaeditiwa juu kwa juu pindi inapotumwa na kila siku hua inabadilika badilika na safari hii ilikuwa nzito na ilianza kwa kicheko kikubwa sana kumuonesha Asha Mr X jinsi gani anajiamini na amemdharau sana licha ya kwamba alikuwa Ninja mmoja hatari mno asiyejulikana. ‘ ”’hahahahahahaaaa Asha wewe ni mtoto mdogo sana ambae huna mbinu hata robo ya kunitambua zaidi ukijieka wazi utakuwa ndio Umejiangamiza mwenyewe hahahahaaa, Ukitaka kupambana na mimi na wewe itakubidi ufanye zoezi kama nililokuagiza umwambie Shebby afanye hahaha, tulia kwenye mchezo wetu Asha nakupa siku saba tu kama nilivyompa babaako Hussein miaka ile na uanze kuhesabu kuanzia Kesho.
Kumbuka wewe ni nyota wa mchezo wangu wa Vipofu. wewe ni Kipofu wangu mzuri kati ya vipofu wangu wengi wanaocheza mchezo huu wa pamoja unaonieka salama mpaka sasa na kunifurahisha kila ninapoutazamaa hahahaaaa Asha Hussein pole sana, ni bora ungejiengua mapema kipindi kile nakusajili katika Mchezo wangu. Umekaa na kukua katika mchezo huu na umekomaa nao Asha utawezaje kutoka? hahahahaaa kama ulikuwa Huujui Mchezo niliokuweka ucheze basi unaitwa Mchezo Wa Vipofu uliounza pindi tu ulipoingia kwa mara ya kwanza ndani ya ndege iliyokufikisha India ukiwa na wafadhili wako niliowaua miezi michache baadae hahahahahahahaaaaaaaa My Name is Mr X huwezi kucheza na mimi kwani nilishakupofua miaka mingi huna macho Asha. hahahahahahahaaaa”””’ Ilimalizikia ile sauti kwa kicheko kilichomfanya Asha abadilike zaidi na kubinuka sambasoti mara alipoikwanyuma kwenye umeme ile computa na kuibamiza chini kwa hasira na hapo ndipo alipojibinua tena na kufungua sehemu moja kulipokuwa na kijimlango chengine na ndipo mbele yake alitazamana na mavazi yake ya kazi sambamba na silaha zote. “We tumia macho yako mimi natumia hisia zangu…Lazima Tuone Kati ya mimi Kipofu na wewe Mwenye Macho nani Atashinda Mchezo” aliongea maneno haya Asha na kuanza kuvaa mavazi yake ya kazi kwaajili ya kuianza kazi ya kupambana na Mr X kutoka kwenye Mchezo wa Vipofu.
*<>*<>*<>*<>*<>* ^ ^ ^ – MIAKA 17 NYUMA – ——————————- MCHEZO WA VIPOFU ( ASHA HUSSEIN ) ___ _______________
Akiwa haamini kama kweli ni yeye leo hii yupo kwenye ndege ile kubwa ambayo ilikuwa inachana mawingu angani huku pembeni yake amekaa na bwana mmoja raia wa India akiwa na mkewe mwenye asili ya Kizungu, aliendelea kugeuka geuka na kuwatazama watu wale aliowajua kama mr & mrs Rajesh ambao hawakuisha kumuonesha tabasamu mtoto yule wa makamo waliyemjua kwa jina la Asha Hussein.
Safari ilikuwa ni nzuri na salama kwao na muda wote Asha aliwaza maisha aliyomuacha mamaake na kujiapiza kamwe hatoenda kuichezea bahati ile iliyomuangukia miguuni mwake pindi atapoanza masomo yake nchini India kama ilivyokuwa nia na madhumuni ya wale watu ambao walikuwa ni wafadhili waliojitolea kwenda kumsomesha kwao hasa kutokana na uwezo wa ajabu wa akili waliougundua kuwa nao yule mtoto pindi walipokuwa na ziala ya kuwatembelea na kuwasaidia watoto wasomao kwenye shule ambazo zilitokana na mfuko wao walio-share na serikali ya Tanzania zilizowajumuisha Yatima na watoto waishio kwenye mazingira magumu ili wapate elimu.
Akili za Asha na uwezo wa kufauru alama za juu hususani masomo ya sayansi ndio kilikuwa kivutio kikubwa kwa wale wafadhili kufata taratibu na kumchukua kwa niaba ya kwenda kumuendeleza kwao ambapo waliamini ndipo kuna elimu bora zaidi itayoweza kumuinua kipaji chake hususani katika sekta ya utabibu kwa vile alivyofauru sana Biology na maneno yake mwenyewe alipoulizwa anataka kuwa nani mara zote Asha alijibu kuwa Doctor.
Ndege waliyounganisha kutokea SA iliwasili ktk jiji la Mumbai baada ya safari ndefu ambapo wasafiri walianza kushuka na kwa mara ya kwanza mboni za Asha ziliweza kuitazama Mumbai na kukanyaga ardhi ya India akiwa na miaka kumi tu, huku akiwa anashangaa ukubwa wa ule uwanja na ndege kubwa nyingi ambazo zilikuwa tofauti na zile alizoziona Dar se salaam Tanzania. Walitembea taratibu huku akigeuka geuka nyuma kuangalia ule uwanja Asha alikutanisha tena macho na baba mmoja muafrika aliyemuonesha tabasam na kumkumbuka kuwa walionana toka uwanja wa ndege Tanzania na alimpatia zawadi ya kimdoli cha bata pindi alipokuwa ndani ya ndege kabla haijaruka DsM na hapo Asha nae alitabasam na kumpungia yule mtu.
Walifika nje ya uwanja na kuingia kwenye gari moja ya kisasa aina ya Hummer milango sita iliyokuwa inawasubiri wenyeji wake ambapo kwa Asha alikuwa anajionea maajabu tu lakini ndio ulikuwa ukweli bibi na bwana Rajeesh walikuwa watu wenye pesa sana. Lakini walipoanza kuondoka yule bwana muafrika nae aliingia kwenye taxi na kumuamuru dereva aifatilie ile Hummer taratibu ila achunge asiwe anaikaribia sana.
Na kweli aliweza kuifatilia ile Hummer hadi ilipofika eneo husika na kusimama nje ya geti moja kubwa na kwa upande wa yule bwana wa kiafrika aliyekuwa kwenye Taxi alimuamuru dereva apitilize kwenye ile njia asisimame. hadi baada ya mwendo mfupi alimuamuru aingie kwenye Hoteli moja iliyokuwa jirani na kule walipoiacha ile Hummer na baada ya yule bwana kumlipa ujila wake yule dereva taxi aliondoka na kumuacha mteja wake akiingia kwenye jengo la lile hoteli hadi sehemu ya mapokezi.
Kulikuwa na siri nzito yule bwana iliyomfanya afike india na muda mwingi katika kila stage anayopiga kuna mtu alikuwa anachart nae na kumpa maelekezo kunachoendelea. )(‘ Weldone, kazi nzuri Tyga andaa mbinu ya kuwa nae ndani ya mwezi mmoja’)( Ulikuwa ni ujumbe mfupi kutoka kwenye simu ya yule bwana aliyeitwa Tyga pindi alipokuwa ndani ya chumba cha hoteli ile mara baada ya kumaliza taratibu zote za malipo. )(‘Woryout Boss’)( alijibu kwa kifupi na kuendelea kukichunguza kile chumba pande zote na baada ya kulidhishwa nacho alitupia kibegi chake kidogo alichokuwa nacho kitandani sambamba na Kapelo aliyovaa kisha akavua nguo zote na kubaki na bukta ndogo na hapo alianza kujinyoosha kwa kufanya mazoezi ya ajabu ya kujipinda pinda na kila kiungo kilijigosha hadi alipokuwa anajipinda kukawa kimya bila kugosheka kiungo ndipo aliporidhika na kuingia bafuni kuoga.
Aliporudi alikuta simu yake ikiwa imeingia ujumbe wa picha na video uliomfanya atabasam na mara alipoufungua alianza kushuhudia garden huku camera ikionesha kuchukuliwa bila utulivu lakini haikumzuia kuona mazingira machache hadi sehemu za ndani za nyumba moja ya kifahari huku akisikia sauti za watu waliokuwa wanaongea na mtoto aliyebeba ile kamera mpaka pale alipokiona chumba alichokuwa anakaribishwa yule mtoto na mara aliona kitanda kipindi hiko sasa kamera ilitulizwa na hapo ndipo alipomuona mtoto Asha akikaa pale kitandani baada ya kuelekezwa mazingira ya chumba chake na bafu. (“Good baby, soon Asante kwa ushilikiano wako”) aliongea yule jamaa na kuzitazama picha muhimu zilizotumwa na kuyasoma mazingira ya nyumba ya bwana Rajeesh na chumba cha Asha.
Wakati hayo yakiendelea kwa bwana Tyga upande wa Asha baada ya kuoneshwa mazingira na mrs Rajeesh muda wote yeye alikuwa na ule mdori aliozawadiwa na yule baba wa kiafrika ambae hakuwa anamjua pia hakuwa anajua ule mdori ni nini hasa. Hata Rajesh na mkewe walichukulia ile kama zawadi na walijua ule ni mdori kama ilivyo midori mengine bila kujua mdori wa Asha uliotengenezwa kwa mfano wa bata ni mdori maalum uliokuwa na uwezo wa kutuma mawasiliano ya sauti na picha huku ukirekodi kwa video kamera maalum zilizotengenezwa kama macho ya ule mdori huku kwenye upande wa mdomo wa mdori kwa ndani kulikuwa na memori maalum iliyounganishwa na kinasa sauti huku wire mwengine uliokuwa upo ndani ya ule mdori ukiwa na kadi special inayoconnect vyote na kutuma signa kwa wahusika wa ule mdori.
Mara nyingi Asha alipenda kucheza na mdori wake kutokana na kukosekana mtoto saizi yake wa kuongea nae kwenye nyumba ya Rajesh kipindi akingojea nafasi ya kupelekwa shule kama alivyoahidiwa na hali ile ilimfanya azunguke nae karibu kila kona ya nyumba na kuwasaidia watu wamiliki wa mdori kuzidi kuchukua picha muhimu za jengo ile kupitia mdori ule wa bata.
Baada ya wiki mbili Asha alipewa habari za kupata shule na aliambiwa angejiunga nayo siku tatu zijazo. Habari ile ilimfurahisha sana na siku ya siku ilipofika mr. Rajesh pamoja na mkewe waliingia kwenye gari sambamba na Asha kumpeleka kwenye hiyo shule maalum ambayo huko watu walikuwa wanasomea lengo tu. Yaani kama unataka kuwa daktari wa mifupa basi utasome udaktari wa mifupa kama unataka kuwa daktari wa moyo halkadhalika utasomea ndoto yako hiyo basi ilimradi lazima baada ya miaka kumi utakuwa professional kabisa.
Lakini siku hiyo walipokuwa njiani kuelekea kwenye hiyo shule ambayo ilijitenga kidogo na jiji la Mumbai na hata njia ya kufika kwake ilikuwa lazima ukatishe kwenye msitu mmoja wa serikali ambao ulikuwa kimya sana ndipo unaibukia kwenye milima ilipokuwa hiyo shule ambapo kulikuwa na majengo mengi makubwa na hostel za wanafunzi. Nia na madhumuni ya chuo kile kuwa mbali na jiji ni kuwapa wanafunzi muda wa kusoma na kutuliza akili zao na hata Rajesh alipendezewa na shule ile na kuamini itamfanya Asha asome na kutimiza malengo yake. Katika hali ambayo hawakuidhania wala kuitarajia bwana Rajesh alipokuwa anakaribia kumaliza kile kieneo chanye msitu mara mbele yake kwenye kona alilikuta roli likiwa limeharibika tena limeziba bara bara lakini punde tu aliposimama walitokea vijana watatu wakiwa wamejifunga vitambaa usoni na kuanza kulishambulia gari la mr Rajesh na kuharibu haribu matairi yote na kuyatia pancha.
“Msiniue jamani msituue semeni mnataka sh ngapi niwape tafadhalini” aliongea Rajesh baada ya wale vijana kuacha kurindimisha risasi na kuwaamuru wote waliokuwa ndani ya gari ile watoke nje. kwa Asha ilikuwa ni kilio na mikojo kuanza kumtoka kwa hofu na kujilaumu kwanini amekubali kuja kwenye nchi ambayo kumbe haina amani hata kidogo, alikuwa hakuwahi kusikia milio ya risasi ikipigwa live hapo kabla zaidi ya kuangalia kwenye picha za kivita.
Lakini Mbali ya Rajesh kujitahidi kujitetea na kuitetea familia yake haikutosha kuwatia moyo wa huruma wale watu ambao walionesha walikuwa hawahitaji pesa za Rajesh zaidi walianza kummiminia risasi tano za kifua palepale na kumpeleka Rajesh chini mbele ya macho ya mkewe na Asha. “Nehiiiiiiiiii” alipiga kelele mke wa Rajeshi na kumlalia mumewe aliyeanguka chini muda mfupi huku damu nyingi zikiruka na kutapakaa eneo lile lakini nae alipigwa risasi ya kichwa na hapo ndipo alibaki Asha akilia huku akiwa kafumba macho kwani alijua tu lazima na yeye auliwe na wale watu na hakuweza kujitetea vyovyote kwani hakuweza kuzungumza kihindi wala kiingereza chake kilikuwa cha kitoto sana kile cha kutajisha lakini Rajesh ilikuwa rahisi kuongea nae kutokana nae kujua kiswahili japo rafudhi yake haikuwa nzuri.
Lakini akiwa kachuchumaa amefumba macho Asha akilia kwa uchungu huku mwili ukiwa umekufa ganzi ndipo mara alisikia muungulumo mwengine wa gari ikija kasi na kufunga breki karibu na gari yao iliyoshambuliwa na hapo ndipo aliposikia milio ya risasi ikirindima mfurulizo na vioo vya gari vikipasuka kwa zaidi ya dakika tatu na kumfanya azidi kutetemeka kwa hofu na kujikojolea zaidi huku akiwa hajui nini kinaendelea. Lakini baada ya ukimya alisikia sauti za viatu na hatua za mtu akimsogelea na hapo alijua sasa ndio mwisho wake hivyo alisali kwa na kutulia akijiandaa kuisikia risasi ikipenya mwilini mwake lakini ajabu haikuwa hivyo alishangaa kuhisi akishikwa bega na huyo mtu baada ya kumsogelea zaidi. “Inuka binti Usiogope” aliisikia hii sauti iliyomfanya ageuze shingo kumuangalia muhusika ambapo hakuamini hata kidogo mara baada ya kuiona sura ambayo haikuwa ngeni machoni mwake.
~ SIKU MOJA KABLA ~ ______________
[“Ndio bosi ni Holt Mandu Academy, sawa kabisa nimeielewa na leo ndio nakutana na vijana niliopanga nao issue na ili waone tofauti nawalipa asilimi 60 kabisa katika makubaliano…. sawa bosi hilo halina shida kabisa andika kabisa The Game is Over”] alionekana Tyga akiongea kwa simu akiwa chumbani mwake kule hotelini na baada ya hapo alitoka nje na kukodi taxi kama kawaida mpaka maeneo ya kusini mwa jiji la Mumbai aliposshuka na kuingia kwenye bar moja huku muda mwingi alionekana kuwa bussy na simu.
Alifika na kukutana na jamaa mmoja baada ya kusalimiana alimpa ishara amfate na hapo ndipo walipoelekea usawa wa kauta na kufungua kilango kilichotokea kwenye kiukumbi kidogo kirefu kilichokuwa kinawaka taa zenye mwanga hafifu huku kikiwa na milango mingi pande zote. Baada ya mwendo kidogo ndipo yule mwenyeji wake aliyekuwa na asili ya ki Asia alipofungua moja ya mlango uliowakutanisha kwenye ukumbe mwengine ambao kulionekana watu wakijidunga wengine wakifanya mapenzi bila kujali huku moshi wa marujuana ukiendelea kufuka kwenye vinywa vya wale watu. waliachana nao na kufika mbele ya mlango mmoja ambao juu yake Tyga aligundua kumetegwa kamera kimtindo. Baada ya mwenyeji wake kubonyeza alarm sauti ilisikika kutokea kwenye kitasa kilichokuwa na spika ikiwaruhusu waingie na huko walikutana na Bonge la mtu (mnene sana) aliyekuwa kakaa kwenye kiti cha kuzunguka huku mwili wake ukiwa umepigwa machata ya michoro ya ajabu ajabu. “Umeleta Advance?” aliuliza yule bonge pindi Tyga alipotoa bahasha ya khaki iliyovimba ambayo ndani yake kulikuwa na noti za dollar mia mia karibu vibunda kumi na kila kibunda kimoja kilikuwa na noti mia. “Safi sana hahahaaa. umefanya nikupe vijana wangu wa daraja A hahaha Zanjili, Jackson, Vijay, nyinyi ndio mtafanya kazi tuliyotoka kuijadili na huyu jamaa kesho” aliongea yule kibonge mara baada ya kuchana bahasha na kuzihesabu zile pesa. Baada ya kila kitu kuwa sawa Tyga alikabidhiwa funguo za gari ambayo ndio alitakiwa atokee nayo eneo la tukio na kisha alipewa bastora mbili ndogo zilizojazwa risasi za bandia.
“Mchezo ni mwepesi sana na utachukua dakika kumi tu, wewe itakubidi uwe makini kuifatilia gari yao pindi itapokuwa inatoka mpaka kukaribia ile kona subiri kama dakika tano then unatokeza mkuku na kumuhadaa binti unayemuhitaji kwa kuwapiga risasi za kifua vijana wangu wataojifanya wamekufa ili kumtoa hofu bint ndipo utadondosha bahasha yetu yenye hele zilizobaki na utokomee eneo lile then mchezo uliobaki watajua vijana wangu jinsi ya kuumalizia.” alitoa maelekezo ya mwisho yule kibonge na kupeana tano na Tyga aliyeikubali moja kwa moja ile mbinu na kuondoka.
Na hivyo ndivyo ilivyokuwa kesho yake kumbe kuanzia muda mr Rajesh akiwa na mkewe na Asha wakitoka tayari Tyga alikaa sehemu husika na mara gari ya mr Rajesh ilipoanza kutoka aliifata nyumanyuma hadi yote yaliyoenda kutokea pale na yeye ndie aliyekuja kumuhadaa Asha kama muokozi wake baada ya kuwapiga risasi za uongo wale watu waliojiziba nyuso na kuangusha bahasha iliyokuwa na salio pale chini kisha kumfata Asha aliyekuwa ameinama chini ya gari ya mr Rajesh ambae alishafariki na mkewe kisha akamshika bega Asha ambae alipogeuka Tyga alimuonesha tabasamu kama alivyomfanyia siku ile aliyomzawadia mdori wa bata na siku waliposhuka uwanja wa ndege wa Mumbai na muda huo ilikuwa mara ya tatu wanatazamana uso kwa uso na mtoto Asha.
* * * * * *
“Usiogope bint ni salama sasa” aliongea tena Tyga kwa lugha ya Kiswahili ambayo alijua ndio anaielewa kiufasaha sana mtoto Asha na kumuinua pale chini na kumkumbatia. Hakuwa na jinsi Asha zaidi ya kumkumbatia yule baba (Tyga) aliyegeuka kuwa mkombozi wa maisha yake muda ule huku akifarijika pia kusaidiwa na mtu aliyemuona tangia uwanja wa ndege nchini kwao (Tanzania) na aliamini moyoni mwake kuwa Mungu ameamua kumuonesha muujiza ambao hakuwahi kuuota wala kusimuliwa hata siku moja kama upo.
Yaani anawapoteza wenyeji wake waliojitolea kumchukua tangia huko kwao katika mazingira ambayo hata kama asingeuwa na wale watu bado aliamini angekufa kwa kuuawa hata na wanyama wakali katika msitu ule kwa kukosa muelekeo wapi aende vipi aombe msaada nani angemuelewa ikiwa hajui kihindi hata kidogo? tena mbaya zaidi alisikia sifa za ubaguzi za watu weusi tokea yupo shule..! Lakini leo hii anasaidiwa na mtu wa kwao kabisa baada ya kumfariji tena kwa maneno ya lugha ya Kiswahili.
“Pole sana mtoto usiogope haya twende haraka tuondoke hapa kabla hawajaja wengine” aliongea Tyga na kumshika mkono Asha ambae awali alisita na kugeuka kutazama walipolala wafadhili wake mr&mrs Rajesh “Tuwachukue babaaa na mamaa” “Hatutaweza binti wameshakufa hao” ndivyo alivyojibiwa na Tyga ambae alimshika mkono nae Asha alimfata hadi kwenye gari aliyokuja nayo Tyga na kuingia ndani yake ambapo gari ilichekechwa na kugeuzwa kiufundi palepale na kuanza kurudi ilipotoka huku Asha akiwa hajui wanapoenda lakini hakuacha kuchungulia nyuma kupitia kioo cha ndani cha ile gari akiwa haamini kama kweli maisha ya watu wenye hela zao aliotokea kuwapenda na kuwazoea wiki chache tu alizokaa nao kama ndio kweli yameishia pale msituni.
Hakuna aliyejua kilichoendelea baina yao baada ya kufika maeneo ya mbali na eneo la msitu huku Asha akiwa hana la kufanya zaidi ya kumsikiliza yule aliyeamini ni muokozi wake chochote atachomwambia. “Unaitwa nani binti?” “Asha” “Ooh! Asha nani?” “Asha Hussein” “Sawa mimi unaweza kunita Uncle Tyga” “Anko Taiga!!” “Eeh, Uncle Tyga ni mfanyabiashara wa Tanzania ninaezunguka hapa India na kwengineko, nilikuona kwenye ndege si ndio wewe?” “Eeh, Uncle Tyga” “Basi usiwe na wasiwasi sawa eeh” “Sawa lakini naomba nisaidie unirudishe kwetu” “Hilo halina tatizo Asha kwani huku uliokuja nao wale kina nani?” “Wafadhili walinichukua ili wanisomeshe na ndio walikuwa wananipeleka shule” “Oooh! pole sana kumbe unapenda kusoma?” “Ndio” “sasa kama anatokea mfadhili mwengine akachukua nafasi ya wale waliokufa ili akusomeshe huku, utakuwa tayari tena kurudi nyumba?” “Hapana kama nitapatiwa shule napenda sana nisome” “Basi vizuri” Ndivyo walivyoanza kuzoeana baina ya Tyga na Asha kipindi hiko gari ilikuwa katika High Way speed kali na kuanza kuliacha jiji la Mumbai huku Tyga akimsemesha semesha Asha ambae mwishoe alipitiwa na usingizi na baada ya gari kutembea kwa zaidi ya masaa manane tena kwa speed ya nguvu hatimae waliingia katika jiji la Delhi ikiwa tayari majira ya usiku. aliamshwa Asha na kumfata mwenyeji wake mara walipofika kwenye nyumba moja ya kizamani ambayo ilionesha ilikuwa haikaliwi na mtu kwa muda mrefu hasa mara baada ya kuingia ndani na kukuta mazingira yalivyo.
“Karibu Asha utakuwa unakaa hapa kwa muda na habari njema ni kwamba nimelifikiria sana swala lako na nimezungumza kwa ujumbe wa simu na bosi wangu ninayefanya biashara zake kuwa yuko tayari kushika nafasi za wale wafadhili na atakusomesha hadi pale unapohitaji mwenyewe na kukuhudumia kwa kila kitu” habari hizi ziliukonga moyo wa Asha na kujikuta anasahau matatizo yalliyotokea muda mfupi na kumpigia magoti Tyga kwa kumshukuru. “Hapana usinishukuru sana mimi. Utamshukuru vizuri bosi wangu siku ya kumuona” “sawa Uncle Tyga, kwa hiyo nitasoma?” “Utasoma Asha” “Lini Uncle” “Kesho jioni nitakupeleka kwenye hiyo shule ni nzuri na ni salama zaidi ya ile waliyokuwa wanakupeleka wale, si umeona mwenyewe njiani kulikuwa na majambaza..?” “Ndio Uncle” “Basi usijali Asha, si umesema unataka kuwa daktari” “eeh” “Basi huko utakuwa zaidi ya daktari na hii ni kwa mujibu wa bosi wangu ambae kumbuka ndie msaada mkuu kwako” alisisitiza Tyga na kumpatia Asha mfuko uliojaa nyama za kuku wa kukaangwa sambamba na mikate ya maziwa huku mfuko mwengine ukiwa na Juice kubwa ya matunda.
Na huo ndio ukawa mwanzo wa kufahamiana kwa Asha na Tyga ambae mpaka muda huo hakumuambia Asha jina halisi la huyo bosi wake ambae Asha nae alimjengea moyo wa upendo na ukarimu kabla hata hajamuona huyo bosi na aliamini kuwa ndie mkombozi wake wa elemu ambayo alidhani kashaikosa pindi aliposhuhudia wafadhili wake wakiuawa.
* * * * *
Siku mbili baadae Tyga akiwa sambamba na Asha ndani ya gari majira ya jioni walifika eneo moja lenye mitimiti mingi baada ya mwendo mrefu na kufika kwenye geti moja lililoandikwa kwa lugha ya kijapani na kuingia mara baada ya kufunguliwa na walinzi walioonekana eneo lile. Asha hakujua kama pale anapoletwa ndio shule kwenye hadi baada ya kuambiwa na Tyga ashuke kwani wamefika shule. Mazingira hakuyaelewa kwani hayajakaa kishuleshule na hakukuonesha dariri ya watu kufika mara kwa mara eneo lile kutokana na kupooza kwake. Lakini ukweli ukabaki kuwa pale ndio shule penyewe alipoahidiwa na bosi wa Tyga kuwa atasomeshwa bure mpaka atimize ndoto zake.
Hali ya mazingira awali yalimuia ugumu sana kutokana na uchache wa wanafunzi ambao asilimia kubwa walikuwa wanawake lakini siku hadi siku alianza kuyazoea na kuyapenda masomo ambayo walikuwa wanafundishwa pale shuleni na walikuwa wanalala pale pale huku zile siku za mwisho wa wiki alikuja Tyga na kumtembelea huku akimletea zawadi mbalimbali kutoka kwa bosi wake ambae sasa na Asha alimtambua kwa jina la mr X. “Msalimie sana mr X uncle mwambie nampenda sana nashukuru kwa msaada wake” yalikuwa ni maneno ya Asha siku moja mara baada ya kuletewa zawadi nyingi na Tyga huku akimwambia zimetoka kwa bosi wake ambae ni mr X na Asha alizidi kumpenda na kumuhusudu mr X kupita maelezo kwa kuamini ndie mfadhili wake na mtoa msaada kwa yote yale yanayofanikishwa na Tyga bila kujua kumbe yupo katika mchezo wa vipofu alioingizwa na mr X na kupofuka pasi na kujitambua Asha.
Ile shule mbali na kuwa na walimu wachache waliokuwa wanadeal na swala la mifupa ya binaadamu tu lakini ilikuwa na mazoezi mengi kila siku ya viungo na walimu wakubwa wa mazoezi walikuwa wajapan na huu ndio ukawa mwanzo wa Asha kujifunza ushupavu pasi na yeye kujua huku akiendelea na masomo ya mifupa ya binaadamu bila kusahau practical kibao walizifanya pale shule na baada ya miaka miwili ugeni wote ulimtoka Asha na akawa mzuri sana kwenye mazoezi ya viungo na kutokana na kuwa bado msichana aliweza kuwa mwepesi zaidi hali iliyomfurahisha sana Tyga aliyekuwa anaenda pale mara kwa mara.
Baada ya miaka mitano Asha alimaliza mafunzo pale na wakati huo tayari alikuwa na umri wa miaka kumi na tano ndipo alipohamishwa na kupelekwa kusini kabisa mwa India na Tyga na huko ndipo mchezo mzima ulipoanza mara baada ya kukutanishwa na mzee mmoja Ninja wa Kijapani ambae alijiekea makazi kusini mwa India na haikujulikana alifahamiana vipi na mr X zaidi ya maelekezo tu aliyopewa Tyga kuwa ampeleke Asha huko.
“Kwanini nalazimika kufanya hivi Uncle Tyga?” “Kwa sababu ya usalama wako wa baadae Asha na msaada kwa bosi” “Usalama kivipi Uncle na msaada gani tena kwa bosi?” “Dunia sasa kuna watu wabaya sana Asha, si unakumbuka kilichotokea kwa mfadhili wako wa kwanza bwana Rajesh?” “Ndio” “sasa pale kama ungekuwa na taaluma nyengine zaidi ya kulia ungeweza kumsaidia na kumuokoa na ndivyo ilivyo kwa mfadhili wako huyu hadi ameamua kujificha kwa kuogopa watu wabaya wanaomfatilia kila siku wakitaka wamjue na wamuue” “kwanini sasa Uncle?” “kwa sababu watu wabaya sana na wana wivu hasa kwa watu wema wanaosaidia wengine.”
“Daaah!! kama ni hivyo Uncle nami niko tayari kabisa kulipa fadhila na kumlinda bosi mr X kwa watu wote wabaya sitokubali nae wamuue kama Rajeesh” “sasa itakubidi uvumilie na ukubali haya mafunzo na huyu babu tutakuwa pamoja siku zote, shika simu hii ongea na mama” aliongea tena Tyga na kumtolea Asha simu na kumshangaza mno baada ya Tyga kuipiga na kuzungumza na mama mdogo wa Asha aliye Tanzania. Hili ndio jambo kubwa ambalo Asha hakuwahi kujiuliza Tyga alianza vipi mawasiliano na mamaake lakini ni kwamba Tyga miaka yote alikuwa na mawasiliano na mama Asha na kumliwaza juu ya maendeleo ya mwanae japo kwa upande wa mama mdogo wa Asha alikuwa anajua anaongea na walewale wafadhili ambao walimchukua mwanae kwenda kumsomesha India. (MIAKA 10 BAADAE) …………
Ilikuwa ni ndani ya uwanja wa Ndege wa Mumbai walionekana wasafiri wakipanda ndani ya ndege ile kubwa iliyokuwa inafanya safari zake moja kwa moja mpaka bara la Afrika ktk nchi yaTunisia. Ndani yake alionekana msichana mrembo sana Asha akiwa kakua sasa tofauti na alivyoingia kwa mara ya kwanza kwenye ule uwanja miaka kumi na tano iliyopita. Safari hii hakuwa na mtu mwengine yeyote katika safari yake, hata yule mtu aliyewahi kumpa mdori miaka ile na kuja kugeuka ndugu yake wa pekee mara baada ya kumuokoa katika shambulizi lililopoteza nafsi za watu waliomfadhili na kumfikisha katika ile nchi, pia nae hakuwa nae kwenye ile ndege safari hii.
Akiwa anaendelea kujisomea kitabu huku akiwa haamini kama leo hii amekuwa Daktari Special wa mifupa na mishipa ya binaadam tena akiwa na vyeti vya uthibitisho kutoka kwenye chuo kikubwa sana India ambacho kiukweli hakuwahi kabisa kusomea hiko chuo japo ni kweli alikuwa na ujuzi mkubwa wa kutibu mifupa iliyovunjika na kuifanyia uparation kuiunga samba na mifumo ya mishipa yote ya mwili wa binaadam. Hakujua mbinu gani zilitumika katika kumsaidia kupata kile cheti kilichoonesha alidumu kwenye kile chuo tangia angali na miaka kumi lakini alikumbuka maneno ya Tyga pindi alipokuwa anamuaga na kumpa jukumu la kuhakikisha usalama wa bosi wake Mr.X unakuwa mikononi mwake.
{{”'”Asha, kumbuka wewe ni Lady Ninja uliyevaa kivuli cha Dokta kwaajili ya ulinzi wa siri na usalama wa bosi wetu Mr X ambae kuna maadui ndani ya ngazi ya serikali wanamuinda kutokana na kuwafichua watu wabaya na kuwasaidia kwake wanyonge. Nakukabidhi nafasi yangu niliyodumu kwa muda wa miaka ishirini sasa nikiwa kama mlinzi wa siri wa Mr X. Sidhani kama tutaonana tenahuku ninapoenda ila nategemea utafanya vyema na kulipa fadhila kwa bosi mr.X … Namba yako ya siri ni 9121 ktk code maalum utayokuwa unawasiliana nae mkuu””}} {“sawa Uncle Tyga, vipi nitaonana nae sasa maana natamani kumuona pia nimshukuru mbele yake.”} {{“Utamuona lakini kwanza inabidi umuoneshe kivitendo mission yoyote atayokupa ambayo itahatilisha maisha yake hakikisha unaimaliza haraka kabla haijawa tatizo, naamini ukiweza mission tatu atakuamini zaidi na utakutana nae ana kwa ana. Kuna kiasi kikubwa cha pesa ushawekewa kwenye account yako. Mama tayari anaishi kwenye nyumba maalum aliyoijenga mkuu kwa kupitia jina lako ila hii siri ya huku ibaki kwenye kifua chako, kumbuka kile kiapo unatakiwa kila mtu akujue wewe ni Daktari bingwa wa mifupa lakini usikubali kuajiliwa popote. Safari njema My Lady Ninja””}}
Aliyakumbuka maneno haya aliyokuwa amezungumza na Tyga mara ya mwisho pindi alipofuzu mafunzo ya udunguaji wa Kininja na kupewa jalibio la kustukiza mara baada ya siku moja kutelekezwa kimakusudi na Tyga na kumuacha katika balaa kwenye kundi la wahuni zaidi ya 25 lakini aliweza kuwadhibiti na kuwavunja vunja wote lakini mwishoni alipotaka kuondoka eneo lile ambalo lilikuwa nyuma ya bustani moja kulipokuwa na Bar na kambi ya siri ya kuuza madawa ndipo ghafra alitokea Ninja ambae alisumbuana nae sana kupambana nae ili kuokoa maisha yake mbali na kwamba yeye Asha hakuwa na nguo zake za kininja wala silaha na alishatoka kupambana na watu zaidi ya ishirini lakini aliweza kula sahani moja na yule Ninja hadi baada ya nusu saa alipoanza kuzidiwa mbinu Asha ndipo yule Ninja alimuacha Asha baada ya kuona ameanza kumzidi huku nae akiwa kakiona cha mtema kuni kutoka kwa yule binti na hapo alikubali na kumsogelea kisha alijifunua uso na kumshangaza Asha baada ya kugundua kuwa alikuwa anapambana na Uncle Tyga. Ndipo Tyga alipomwambia maneno hayo ya kuagana nae kisha alipotea kwa kutumia uchawi wa Kininja mbele yake. Alitabasamu Asha wakati akikumbuka yale kipindi hiko ndege ilikuwa tayari iko angani ikikata mawimbi na kuzidi kuliacha bara la Asia.
* * * * * *
Na kweli Asha mbali na kupokelewa kwa shangwe pindi alipounganisha ndege kutoka Tunisia mpaka Jijini Dar, Tanzania alipomkuta mamaake ambae ni Zena akiwa na wapambe kadhaa waliokwenda kumpa sapoti hususani sifa aliyorudi nayo ilimfurahisha sana wazili wa Afya wa Tanzania kwa kuona wataalam wanazidi kuongezeka nchini, lakini kitendo cha Asha kukataa ajira yoyote nchini na kutangaza kuwa atajiajili mwenyewe yaani awe anakodiwa kwa kazi maalum itayowashinda madaktari wa pale hususani maswala ya mifupa na mshipa basi atakuwa radhi kusaidia lakini si kuajiriwa kabisa na kuwa mfanya kazi wa kila siku.
Kauli hii kila mtu aliielewa anavyojua yeye lakini hakuna aliyejua nini kinaendelea nyuma ya pazia ya maisha ya Asha na kwa kutumia kode maalum aliyokuwa anawasiliana na mr X aliweza kupata maelekezo yote muhimu na siri ya nyumba ile hususani chumba chake ambacho kumbe kilikuwa na sehemu maalum iliyotengenezwa kwa mfumo wa lifti na chini yake ndipo kulikuwa na chumba cha mawasiliano na maelekezo juu yake nini afanye kuhusu usalama wa bosi wake ambae alimpenda na kumuhusudu kama muokozi wake mbali ya kuwa hajawahi kumuona katika miaka yote toka afahamu uwepo wake.
* * * * * *
Ikiwa ni miezi mitatu imepita tangia arejee nyumbani Tanzania huku akiendelea na mawasiliano ya siri na bosi wake ambae siku zote hakuwahi kufikiria sana wala kuhoji sababu za kujificha kwake ama kutopenda kuzungumza nae ana kwa ana. Kila akikumbuka wema aliofanyiwa na Uncle Tyga kule india hadi alivyomuokoa na kumsomesha hata kumuunganisha na kuaminiwa na bosi wao kuchukua nafasi yake ndivyo alivyozidi kumpenda mr.X na mara zote usiku aliingia kwenye chumba chake cha siri na kuwasiliana nae na ndipo siku hiyo alipokutana na ujumbe wa picha ya kijana askali magereza pamoja na maelezo kiurefu yaliyosema…..
^^^ ^^Huyo ni Shaaban Mwinchande, Kamishna wa polisi na mkuu wa gereza la Nyato lile la wafungwa wenye makosa makubwa nchini. Babaake ni adui wangu mkubwa na sasa anamtumia mwanae ili aweze kujua nilipo kwaajili ya kuniangamiza^^ ^^Picha hii ya chini huyu ni mzee mganga wa muda mrefu anaitwa Mnyungunyungu, aliwahi kuwa rafiki angu miaka ya nyuma lakini baadae akawa msariti kwa tamaa na kujiunga na mzee Mwinchande babaake huyo Kamishna Shebby anayetaka kunijua kwa udi na uvumba na kuniua^^ ^^Sasa My Lady Ninja location ya tukio ni Mkuyuni Morogoro huko utakutana na mzee huyu unayemuona hapa chini… Anaitwa Aly77 namba zake ni hizo yeyey ndie anayechunga usalama wangu pale na ndie alietuma taarifa za huyo kijana aliyeenda kunitafuta kwa mzee Mnyungunyungu ambae ni kweli kuna baadhi ya taarifa zangu muhimu ila Aly77 ameshamdhibiti mzee Mnyungunyungu na huyo Kamishna kaondoka huko, lakini najua lazima atarudi tena kutaka habari zangu toka kwa mtoto wa mzee Mnyungunyungu ambae ni huyu umuonae sasa kwenye picha, yeye ndie mganga wa pale anayejua fununu zangu na ni hatari kwa maisha yangu kama atabaki hai na kuzitoa siri kwa maadui zangu. ^^ Kazi kwako Lady Ninja okoa maisha yangu.^^
^^^ Baada ya kuupata ujumbe ule na kuzirusha zile picha kwenye Memory yake, Asha aliandaa mavazi yake ya kazi na kuyaweka kwenye begi dogo kisha usiku uleule aliandika ujumbe mfupi na kuuacha mezani akimuarifu mamaake pindi atapoamka kuwa amepata dharura kisha alitoka na kuingia kwenye gari yake ndogo ya kifahari taratibu safari ya Morogoro Mkuyuni ilianza.
Kwa kutumia code alizopewa aliweza kuwasiliana na huyo mzee aliyeitwa Aly77 ambae ndie aliyemuekea sumu maalum iliyokuwa inamtafuna mganga Mnyungunyungu taratibu hadi kufikia kuwa hoi bin taaban. Miaka yote alijichomeka pale kijijini yule mzee ambae alionekana mcha Mungu kutokana na tabia yake ya kupenda kuswali na kuvaa kanzu na kibaraghashia kumbe nyuma ya pazia hakuwa hivyo alikuwa anafanya kazi ya mtu ambae alikuwa anamsaidia kipato na kuiwezesha familia yake pia mzee Aly77 ndie alikuwa baba mzazi wa Tyga na alijitolea kufanya kila kitu kwa mr X mara baada ya kusaidiwa miaka iliyopita pindi mwanae alipopata ugonjwa m baya uliotakiwa asafirishwe India nae kwa kukosa uwezo alijikuta anapita huku na huko kuomba msaada ndipo alipokutana na msaada wa mr X kupitia mwana mama Mrembo ambae alisafiri na Tyga hadi India pamoja na babaake na huko waliishi mwaka mzima mara baada ya oparation na siku zote yule mama aliwasisitiza kuwa msaada ule walipatiwa na Mr X na hiko kikawa chanzo cha yule mzee kumuhusudu mr X hasa baada ya kuambiwa kuwa mwanae ambae ni Tyga atasaidiwa zaidi na mr X kusomeshwa nchini Japan hadi atimize malengo yake nae mzee Aly alipewa kisa kizima kama alivyopewa Asha na Tyga juu ya kujificha mr X lakini yote hayo mzee Aly hakujali wala hakuwa na haraka ya kumjua huyo mr X zaidi ya kuwasiliana nae kwa simu zenye code maalum, na kupewa maelekezo muhimu huku kila mwisho wa wiki pesa iliingizwa kwenye account yake.
Na safari hii waliunganishwa sambamba mzee Aly77 na Dokta Asha katika mission ile ya kuisambaratisha familia ya Mzee Mnyungunyungu ili Kamishna Shebby na wenzake wasije kujua siri zozote kuhusu Mr. X Na hivi ndivyo mchezo ulivyokuwa unachezwa katika location ya Mkuyuni ambao Mr X ndie alikuwa mtengenezaji na mtazamaji na aliishia kufurahi na kujisifu kwa vile ambavyo mambo yalianza kutokea Mkuyuni kwenye mchezo ambao wachezaji wake walitumia akili na mbinu nyingi lakini kwake yeye aliuita Mchezo wa Vipofu.
Haikuwa shida kwa Asha baada ya kuwasili usiku wa manane Mkuyuni na kukutana kwa siri na mzee Aly77 ambae alimpa maelekezo yote muhimu na zaidi kuhusu simu fake waliyopiga na kumuhadaa mganga yule mtoto wa Mnyungunyungu kwa kudhani kuwa anaongea na mteja wao wa siku nyingi juu ya kukutana kesho kwa niaba ya dawa ambazo sharti lake lazima aamke asubuhi sana akaziandae na kutokana na hali ya mazingira ya pale kijijini watu kuchelewa sana kuamka huo utakuwa wasaa mwepesi kwa Lady Ninja kufanya kazi yake ya kummaliza kwani endapo kina Shebby wakirudi na kuongea na yule bwana basi ajue fika tayari siri ya maisha ya tajiri wao mr X yatakuwa hatarini sana kwani waliamini pia Shebby anafanya kazi ile kwa shinikizo la babaake bwana Mwinchande ambae kwa maelekezo waliyopewa na mr X ni kuwa Mwinchande ni adui ake anayemtafuta miaka mingi ili amuue baada ya kumfichua ubaya wake kipindi akiwa polisi mkubwa na hivyo ameeka kisasi ambacho kinapitia mgongoni mwa mwanae anaejua kuwa mr X ni mtu m baya kutokana na hadithi za uongo alizopandikizwa na babaake (Mzee Mwinchande).
Kazi ilikuwa kama kumsukuma mlevi kwenda kilabuni ama kumfungulia mlango wa choo aliyebanwa na tumbo la kuhara, yaani namaanisha kazi ilikuwa nyepesi mno kwa Lady Ninja kumuondoa duniani mtoto wa mzee Mnyungunyungu pindi tu alipoingia kibandani mwake bila kujua kwa juu kuna LadyNinja anamuinda na pindi alipokua wanainama yule bwana ili akae hapo hapo Lady Ninja Asha alijiachia kiwiliwili na kunining’inia mithili ya popo huku mikono yake kwa speed ya hatari ilifanikisha kupora panga dogo aliloshika yule mganga na kumkata eneo la koromeo huku mkono mwengine akimzuia kwa kumnusisha unga wa dawa frani zilizomfanya yule mganga ashindwe kupiga kelele na kubaki anatapatapa kwa krusha miguu akiwa amekaa amezuiwa kichwa na Lady Ninja huku ameshikishwa kipanga kilichonasia shingoni mwake wakati koromeo lililokatwa liliendelea kurusha damu mithili ya bomba la maji. Ndipo hapo aliporidhia yule muuaji na kumuachia kichwa baada ya kuona damu zimepunguza kasi ya kuluka hapo nae alijikunja tena Lady Ninja na kujiachia chini ambapo alitumia dawa maalum za uchawi wa Kininja kisha akatoweka kimaajabu eneo lile.
Alisikilizia kwenye maficho yake ya siri kwa siku mbili huku akipewa taarifa na mzee Aly77 kuhusu kinachoendelea baadae na hapo akapata habari za kuja tena kwa Kamishna Shebby na kuziwasilisha kwa code maalum ya mr X kupitia simu yake iliyofungwa chipu ambayo haisomi kwenye mtandao mwengine wowote wa kawaida. )(‘Sikia My Lady Ninja, hao watu wamenizidia ubaya sasa nami ni mtu mwenye huruma sana lakini muda mwengine sina jinsi kwa kuwa ni maadui na wamenianza, sasa hakikisha unaua wote wataojifanya kimbelembele, tena usije kumuacha mjukuu wa Mnyungunyungu huyo kijana ndie mrithi wa kila kitu hapo.. ili kuwazuia kabisa hao askali hakikisha na huyo humuachi hai pia Askali wote watakaotaka kukuzuia ua mara moja kasoro Kamishna wao Shebby yeye mpe onyo na umwambie kama anataka kupambana na mimi basi akafanye mazoezi ya kusimama juani na kukamata kivuli chake’)( Ndivyo ujumbe wa mr X ulivyosomeka na hapo ndipo Lady Ninja alipoweka mtego wake wa pili palepale msibani juu ya mti mkubwa kwa zaidi ya masaa 12 bila kusinzia wala kupepesa jicho akiwa kabanisha juu ya tawi moja lililokuwa usawa wa kile choo akiamini lazima yule mjukuu wa Mnyungunyungu aliyepewa amri ya kumuua iwe isiwe atakuja tu pale chooni kujisaidia. * * * * * *
Na kweli Kipindi kina Kamishan Shebby na st,sirjent Kimaro wanaondoka muda mfupi baada ya shughuli ya mazishi kumalizika ndipo yule kijana akiwa na ndoo yake mkononi aliingia bafuni kwa lengo la kujisaidia haja Kubwa na hapohapo kwa mtindo wa ajabu na aina yake Lady Ninja aliweza kukirusha kitanzi maalum cha waya ambao aliuunganisha kwenye mashine ndogo aliyoifunga juu ya tawi la pili alipokuwapo na kweli kile kitanzi kilifika usawa wa shingo ya yule kijana na kabla hajapiga kelele kwa mstuko Lady Ninja aliwahi kutight kitanzi kwa kutumia ile machine na kuanza kuzidi kuzungusha skurul iliyokuwa ikiukusanya ule waya kwenye mviringo wake wa ile machine.
Na hivyo ndivyo alivyokuwa ananyongwa yule kijana na Lady Ninja Asha aliyekuwa kalala juu ya tawi la ule mti na kumpandisha juu yule kijana kupitia wire uliotight barabara shingoni mwake na pindi alipofika usawa alioutaka Lady Ninja alichomoa kamba nyengine ya Katani na kuifunga juu ya tawi baada ya kutengeneza kitanzi kisha akampachika shingoni yule kijana ambae tayari alishakuwa marehemu na kuulegeza tena ule waya wake kwa kutumia ileile mashine yake maalum na baada ya hapo alimvua kitanzi cha waya na kumuacha akining’inia kwa kitanzi cha kamba ya katani.
)((“Nimemaliza kazi Bosi”))( aliwasiliana na mr X, Lady Ninja Asha pindi aliposhuka kwa style ya kipekee pale juu ya mti pasi na kuonekana na kuingia kule maporini kwenye makutano yake ya siri na mzee Aly77. ))(“Weldone My Lady Ninja, Ushawekewa Mil, 200 kwenye account yako, lakini Umebakiza mtu mmoja ambae hana budi nae auawe”)(( )((“Nani bosi”))( ))(“Mzee Aly77”)(( )((“Aliy77!!? si mwenzetu huyu?”))( ))(“Kuna kitu bado hujaelewa Lady Ninja, ila ni muhimu ufanye hivyo kwa sababu ya usalama zaidi na uhai wa siri yako kama Dokta Asha huna budi kummaliza huyo babu kwani anaweza kustukiwa na hana mbinu wala si mwepesi kupambana kama wewe kutokana na hali yake pia hutakiwi kuwa na share kwa kazi hii kuanzia sasa kila kitu utaongoza mwenyewe Lady Ninja”)(( )((“Sawa bosi, nasubiri signal yake ya kukutana nami nimalize mchezo”))( ))(“All the Best My Lady”)((
Na hayo ndio majibu aliyoyapata Lady Ninja Asha kutoka kwa Mr X mara baada ya kumjuza kilichokuwa kinaendelea na ndipo aliposubiri signal ya kukutana na mzee Aly77 ili atimize agizo la bosi wake ambae ni Mr X.
Na kweli baada ya muda mzee Aly77 alimtumia signal maalum Lady Ninja na kukutana pale kwenye kimsitu huku mzee Aly77 akiwa anahema mno kuonesha ni mtu aliyekuwa anakimbia kwa hofu pia. “9121, Toweka eneo hili mara moja kuna msako unaendelea, yule Kamishna Shebby amekuja na polisi wengi sana uuuphh daah! Toweka haraka hapa si salama sasa mi nataka nirudi wasije kunitafuta harafu wakakosa kuniona uuuppph” aliongea huku akitweta mzee Aly77 lakini katika hali ambayo hakuitarajia palepale Lady Ninja Asha alichomoa kisu na kumkita kifuani kwa Nguvu. “AAAAAAAAAAGHH..” Alitoa ukelele wa maumivu mzee Aly77 na kuanguka chini na muda uleule Lady Ninja alisikia sauti za miguu ya watu wakikimbilia eneo lile nae bila kupoteza muda aliruka beki mfurulizo kurudi nyuma mpaka usawa wa miti mingi mikubwa ambapo alidanda danda kwa speed ya Ajabu na kuibukia juu ya mti mmoja ambao aliamini isingekuwa rahisi kuonekana. Hapo aliwashuhudia askali wengi wakiongozwa na Kamishna Shebby wakija mkuku eneo lile alipotoka ambapo alimuacha mzee Aly77 akiugulia maumivu pale chini akiwa bado hajakata roho.
Lady Ninja alifungua zipu ya mfuko uliojengewa na sambamba na mavazi yake na kutoa kifaa kimoja kimoja ambpo alipomaliza kuviunganisha ilionekana bunduki kubwa ya udunguaji ikiwa kamili. Na hapo ndipo alipojieka sawa na kuanza kumlenga mzee Aly77 mara alipoona amepakatwa na Kamishna Shebby akilazimishwa kusema kitu. Alisogeza lenzi na kumjaza vizuri kabisa sehemu za kichwa mzee Aly77 na papo hapo alifatua risasi iliyofumua kichwa cha mzee Aly77 mbele ya kamishna Shebby kabla hajatoboa siri yoyote.
Kitim tim ndio kilianzia pale Kamishna Shebby alipotoa ukelele na kuwaamuru vijana wake wakae makini watafute alipo mdunguaji, lakini bila presha wala papara Lady Ninja Asha aliendelea kumtungua askali mmoja mmoja na kuzidi kumchanganya Shebby hasa pale alipomshuhudia rafiki ake kipenzi st,sajent Kimaro akipoteza maisha na kuingia kwa kiza kilichowafanya washindwe kuona vizuri, lakini kwa Lady Ninja mambo yalikuwa mepesi kwani alivaa miwani maalum ya kuonea usiku. )(“Amebaki mwenyewe Shebby bosi”)( alichart kimtindo pale juu ya mti na mr X ((“Huyo mvunje mguu tu inatosha ili asikufate lakini hakikisha unampa Onyo nililokwambia”))( Msg ilirudi na kipindi hiko Shebby alikuwa anahangaika akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa kwa hasira akimtukana muuaji huku akimlaumu kwa kuua watu wasio na hatia na kumlazimisha kama kweli anajiamini basi asijifiche bali ajitokeze wapambane. Kipindi akiyasema hayo Shebby na kutupa bastora yake alikuwa maeneo ya mti uleule aliokuwa Lady Ninja Asha ambae aliamua sasa kushuka kwa kutumia kamba maalum aliyoinasisha kwenye lile tawi huku akitoa kicheko cha dhalau. Na hiyo ndio ilikuwa mara ya kwanza Kamishna Shebby kukutana na Lady Ninja Asha kabla hajageuka kuwa Dokta wake na hatimae kuwa mke mtarajiwa.
Baada ya mabishano ya Shebby na Lady Ninja hadi kufikia kumpiga risasi ya mguu na kuchomoa bastora ndogo iliyokuwa na risasi maalum yenye kisindano kidogo ambacho mtu akichomwa nacho kikagusa karibu na fuvu la kichwa basi kinapoteza kumbukumbu zote muhimu ambazo muhusika alikuwa anazifikiria na kumpoteza. Alifanya hayo yote kwa niaba ya usalama wa mr X. Aliamini mr X ni mtu mwema anayewindwa na wabaya siku zote. Hakujua kama amepofuliwa na kile anachojua ama kuona kuhusu mr X sivyo hivyo kabisa. alimpiga risasi ya ile sindano kichwani Shebby ambae alipoteza fahamu palepale.
* * * * * *
Baada ya Lady Ninja kumaliza na kuzima kabisa tukio lililotaka kuvumbua siri na ukweli wa bosi wake ambao hata yeye aliyeulinda hakuujua wala hakuwahi kumfikiria sivyo bosi wake ambae mbali na kutoonana nae lakini alimuheshimu siku zote na kufata matakwa ya kile alichoamrishwa nae kutokana na vile alivyosaidiwa na kujengwa kiimani juu yake tangia anaokolewa kwenye msuko suko kule India bila kujua kuwa yote ilikuwa mipango.
Baada ya kurudi kama kawaida yake siku hiyo hiyo aliingia kwenye kile chumba chake cha siri na kukuta ujumbewa Mr.X kuwa akae tayari muda wowote atapigiwa simu kwa niaba ya kwenda kumtibu Kamishna Shaaban kupitia mbinu ambayo hakufafanuliwa zaidi ya kuambiwa kuwa Mzee Mwinchande ameshatekwa kiakili na kuaminishwa yeye tu (Asha) ndie atayeweza kumtibu vizuri mwanae kutokana na kuchanganyikiwa kwake baada ya kupata taarifa ya tukio. ))(“Kumbuka Lady Ninja, kinachokupeleka pale sio kumtibu tu, bali ni kujieka karibu na ile familia kama alivyowahi kujieka Aly77 kwenye familia ya Mnyungunyungu. nawe jichomeke na umtibu kwa umakini sana pia fanya kila mbinu hadi aanze kukupenda na ukifanikiwa kumteka kimapenzi utakuwa umemaliza kazi kwani utaelewa kila kitu kama kutakuwa na ubaya unasukwa juu yangu naamini utanisaidia mapema”)(( Ndivyo alivyoagizwa na Mr X mara baada ya kuwasiliana nae kwenye kile chumba chake cha siri kisha alitoka na kweli alipigiwa simu na mtu asiyemfahamu akihema na kumuomba afanye msaada wa moyo wake ili kuweza kumsaidia mtoto wake ambae ameshambuliwa huko Mkuyuni.
Taarifa zile alizipokea kwa masikitiko makubwa Lady Ninja ambae sasa alijivisha kivuli na kuwa Dokta Asha kisha akamuaga mamaake na kwenda kukutana na mgonjwa yule ambae babaake alimtangazia kumlipa dau nono ili tu ahakikishe mwanae anarudi na kuwa kama zamani.
Na kweli Dokta Asha alikuwa mtaalam sana wa maswala yale na alikuwa na cheti cha kimataifa. Alimtibu Kamishna Shebby kwa moyo wa kivuli cha Dokta Asha lakini akiwa anatega makucha kama Lady Ninja jasusi wa mr X. Siku zilienda na alizidi kumuonesha mapenzi mgonjwa wake na kumyeyekea mno hali iliyofanya afauru kuanza kumteka akili yeye Shebby mpaka wazazi wake wakatokea kumpenda Asha na kuombea aolewe na mtoto wao bila kujua kiundani Asha ni nani.
Kama walivyosema wahenga ‘Mapenzi hayajalibiwi’ na ndivyo ilivyokuwa kwa Asha mara baada ya kuzidi kuwa karibu na Kamishna Shebby ndivyo alivyojikuta anazidi kumpenda kweli na moyo wa huruma kuanza kumjia kila alipomuona akilalama kupoteza kwake kumbukumbu na mara nyingi alitamani amsaidie kwani alijua yote yanayomsibu lakini alipokumbuka kiapo alichoapa mbele ya Tyga kuhusu kutii na kufatwa matakwa ya mr X, ilimlazimu aache kama ilivyo japo kuna muda alikuwa anaumia kweli juu ya Shebby na kupelekea hadi machozi kumtoka. Na ndipo usiku mmoja ambao ndio ulikuwa wa mwisho kuwepo pale kwa mzee Mwinchande alipokata shauli na kuamua kumtibu Shebby akiwa kwenye usingizi mzito baada ya kumchoma sindano maalum ya usingizi na kufanikisha zoezi la kumtoa kisindano kilichokuwa kichwani mwake kilichomfanya asiwe na kumbukumbu vizuri.
Lakini usiku huo huo aliporudi katika makazi yake ndipo alipokutana na ujumbe mwengine kutoka kwa Mr X ukimlazimu afanye haraka kuzuia ujio wa mtu mmoja ambae alisahauliwa kuwa ni adui mkubwa wa mr X ambae anakuja jijini na askali mmoja shupavu kwa niaba ya kumchunguza wapi alipo Mr X. ))(“Fanya Mbinu unayojua wewe Lady Ninja kuhakikisha huyo mzee hafikishwi jijini akiwa hai”)(( alituma agizo mr X sambamba na docoment zenye maelekezo zaidi kuhusu huyo mzee ambae alikuwa na urafiki na mzee Mwinchande ambae nae ni adui wa mr X kwa mujibu wa maelezo aliyokuwa anampa Asha. )((“Worry out I’ll do my Best”))( alijibu ujumbe ule Asha na kuchomoka kama kawaida yake usiku huku akiacha ujumbe mezani swala ambalo mamaake aliyekuwa anaishi nae alishalizoea japo hajawahi kuhisi vibaya mwanae anaendaga wapi na kufanya nini zaidi alimuombea arudi salama na kukubali pale alipokuwa anajibiwa kifupi tu na Asha pindi alipomuuliza mara nyingi alisema ‘nimepigiwa simu ya dharula, nimeona haina haja ya kukusumbua usiku’ Na kutokana mwanae alikuwa special kwa utabibu wa mifupa wala hakuhoji zaidi yule mama ambae ni Zena.
Signal maalum za satelite zilitumwa na kuonesha kidoti cha gari iliyokuwa imem beba mzee Cyplian kupitia saa aliyovaa Asha pindi akiwa kwenye gari yake ndogo aina ya Toyota Crester nyeupe akielekea Morogoro na alipokaribia Chalinze signal ilionesha gari husika inakaribia maeneo yale na kwa mwendo inayotembea ingetumia dakika ishirini tu kufika pale na hapo ndipo alipoisogeza gari yake maeneo ya Shelly na kushuka kisha akaelekea ile njia ya Tanga huku akiwa makini na kupiga hesabu ya mbinu ambayo alipanga kuitumia na kwa hesabu zake haraka haraka ziligota pindi alipoiona basi moja iliyokuwa inatokea Tanga na kusimama pale juu maeneo ya Polisi Chalinze na ndipo alipoisogelea na kujichanganya na vijana waliokuwa wanauza matunda kisha kimakusudi alidondosha pochi yake na kumfanya ainame kuiokota ndipo alipobonyeza pete yake maalum ya mionzi mikali na kuirengesha usawa wa ringi ya taili za mbele kulipoingia waya za breki na kuzikata pasi na mtu yeyote kujua na wakati huo pia alipoangalia saa yake signal ilimuonesha ile gari iliyom beba mzee Cyplian imebakiza dakika tano tu kupita pale Chalinze. (“Camoon, go, go, go”) aliwazia na kujisemea moyoni Lady Ninja ambae safari hii alivaa mavazi ya kiislam hususani kwa wale washika dini na wenye itikadi kali kwani alivaa hadi nikabu usoni mwake. Na kweli mara ile gari ilianza kuondoka kwa mbembe sekunde zile zile na ile gari aliyokuwamo mzee Cyplian ndio ilikuwa inafika eno lile na kilichofuta pale ni kishindo na honi nyingi mara baada ya dereva wa basi kushindwa kulicontrol basi lake kwa kukosa breki na kukata kona huku akiyagonga magari mengine na kulikosakosa lile alilokuwamo mzee Cyplian. Kipindi hayo yote yakitokea Lady Ninja alikuwa makini sana tena kama sie yeye vile aliwashuhudia hadi polisi wakifika maeneo yale kudumisha usalama na ndipo nae alipoanza kusogea upande wa chini huku akijiapia hawezi kuondoka hadi ahakikishe mzee Cyplian amepoteza maisha pale na ndipo alipokuwa anaangalia kule ilipotokomea gari iliyombeba muhusika aliona aliona dariri zote za kufauru mission yake hasa pale alipomuona kijana ambae aliamini ndie dereva wa mzee Cyplian akiwa anavuja damu huku kachanganyikiwa akili. Alikutana nae macho kwa macho na alishangaa kuona macho ya yule askali dereva akiwa anamtazama kwa kumshuku mno na hapo alinyanyuka kumfata kule alipokuwa anaenda, nae Lady Ninja alijiandaa kumlipua kwa mionzi iliyokuwa kwenye pete yake lakini kama bahati yule askali ambae alikuwa ni Cj4 alidondoka na kupoteza fahamu kipindi hiko Lady Ninja aliingia kwenye gari yake na signal ilikuja toka kwa mr X kuwa mission yake imeenda vizuri na ndipo hapo aliwasha gari yake taratibu na kuanza kuondoka huku akimuwazia yule askali ni mtu mwenye mbinu kiasi gani hadi alimtilia shaka kuhusika na ajali ile ambayo ingekuwa vigumu sana kwa mtu wa kawaida kusema eti imetengenezwa. Na hapo ndipo alipokuwa njiani alipokosana kugongana na Jeep ambayo alipoiona tu alitabasam kwani aliijua vizuri kuwa ni ya mumewe mtarajiwa ambae ni Kamishna Shebby na alifanikisha kutoka maeneo yale na alipofika mbele kutokana na fikra juu ya askali yule aliyezimia kule aliona ni vyema apoteze ushahidi kabisa mara baada ya kusimamisha gari maeneo ya kibaha ambapo alimpa lifti bint mmoja na walipofika Kibamba aliipaki gari njia panda ya kijiji cha Hakipo. “Samahani dada, naomba ukae hapa huku ukikanyaga kanyaga breki nataka kucheki huku nyuma kama taa inawaka maana hiyo display sielewi imekuaje sasa.” Aliongea Asha na kumfanya yule binti mpenda lifti kukaa kwenye kiti cha usukani bila kujua ni trick ya yule mtu nae alianza kufanya kama alivyoagizwa lakini Asha alipozungukia nyuma tua aliwasha mionzi yake hatari iliyomulika lile gari kwa dakika moja na papo hapo ilianza kuwaka moto huku akiwa amelock milango yote alianza kuondoka taratibu eneo lile na kumuacha bint wa watu akiteketea garini.
“NOOOOO” Alizidi kupiga kelele Asha mara baada ya kutoka kwenye mawazo mazito na kukumbuka mission ile ya mwisho aliyomfanyia mr. X kupelekea kuua watu wengi wasio na makosa kwa ajili ya manufaa ya mtu mmoja aliyemgeuza kuwa kipofu kiakili na mawazo juu yake pasi na kujitambua na leo hii alitaka akamuue mtu ambae anajua fika alikuwa ni babaake mzazi.
Aliumia sana Asha mara baada ya kukumbuka yote yale yaliyopita na kujikuta akilia kwa uchungu mno na kuijutia nafsi yake. “Nilikuamini sana Mr X, siku zote nilijua wewe ndie mtu muhimu kwangu na umejitolea kufanikisha maisha yangu kuwa bora kumbe ulikuwa na vitu unavitaka toka kwangu na ulijua fika mimi ni nani na kwanini unanitumia. aaah!! Umenifanya kipofu wako kwa muda mrefu sana.. Nadiriki kusema wewe ni zaidi ya SHETANI. Ndio wewe ni Shetani Mr X shetani mkubwaaa na lazima Ufe kikatiri…” Alinung’unika Asha huku akigugumia kwa maumivu na kuhisi kama nafsi zote za watu alizozikatisha uhai zimesimama mbele yake zikimshutumu na kumzomea.
Ukweli hakupanga mwenyewe kuwa na mahusiano na Shebby japo baada ya tendo lile la kikubwa walilofanya siku moja ndio lilichochea kasi zaidi na ashki ya kumpenda kweli Shebby. “Nimeua weeeengi wasio na hatia kwa ajili ya Shetani mmoja!!? hapana sikubali kwa hili hata kidogo lazima Nilipe vifo vya watu wote japo nilivitenda mwenyewe kwa mikono yangu lakini nina sababu zote za msingi. LAZIMAAAAAA..” Alizidi kupayuka mwenyewe Asha kwa hasira huku akizidi kupiga mateke vitu vilivyokaa jilani yake na kuchomoa connector zote zilizofungwa chumbani kwake zilizokuwa zinamuwezesha kuwasiliana na Mr. X baada ya Connector zote kuzima signal zenyewe automatic mara baada tu ya mr X kutuma ujumbe ule wa sauti akimcheka kwa nguvu na ndipo alizima kabisa mitambo yote iliyokuwa inamuunganisha na Asha.
Lengo la Mr. X ni kusambaratisha kila aliyekuwa na kisasi nae na hapo alitumia akili nyingi kutengeneza mchezo ule wa vipofu ambao wachezaji walimuhusudu bila kujua wanaomuhusudu ndie adui yao waliyepaswa wapambane nae na kwa kuwa walikuwa hawalioni hilo ndio maana mchezo wake akauita wa vipofu. Alifikiria mateso mazito aliyokumbana nayo babaake. Alikumbuka vifo vya wafadhili wake na kugundua kuwa yote ilikuwa ni trick ya kuingizwa ktk mchezo na Mr X akimtumia Tyga ambae pia aliamini kuwa amehadaika na mchezo wa Vipofu aliokuwa anaucheza mr X lakini kitu kimoja hakujua kabisa Asha kama yule mzee Aly77 aliyemuua kule Mkuyuni ni baba mzazi wa Tyga.
Alivalia mavazi yake ya kazi Usiku ule ule alikaa tayari kwa ajili ya kuianza kazi ya kumsaka Mr X na alijua wapi aanzie japo hakujua wapi amalizie. “I Must Find You Mr. X” Alijiapiza Asha baada ya kuyatinga mavazi yake ya Kininja na silaha zake zote muhimu usiku huo huo aliharibu kila kitu kilichokuwa kinamuunganisha na mr X mule ndani kisha akafanya uchawi wake wa Kininja na mara ulitokea moshi wa ajabu mule ndani akatoweka na kuibukia nje ya nyumba yao ambapo style aliyotembea nayo sasa hivi ilikuwa tofauti kabisa na awali kwani alienda mwendo wa haraka mno na sehemu zengine aliweza kudanda kwenye mistimu na kupita juu ya nyaya sa umeme pasi na kuonekana.
Asikwambie mtu hakuna Ninja aliyekamilika asiyekuwa na mazingaombwe na ndivyo ilivyokuwa kwa Lady Ninja Asha ambae alifundishwa mambo mengi na mzee wa Kijapani ambae alikuwa ni Full Ninja Master na aliyatii mafunzo na kuyafata kwa moyo wote huku uvumilivu akiuweka mbele na hiyo ndio ikawa sifa ya uwezo wa ajabu aliokuwa nao leo hii. Aliamua sasa kujitolea maisha yake kupambana na mtu asiyefahamika anayetumia akili nyingi huku akiwa na wafuasi wasiofahamika. Alijua ni hatari lakini alijiamini pia hakuifikiria kabisa ndoa yake iliyo mbeleni yeye na Kamishna Shebby wala hakuona umuhimu wake kwa wakati huo zaidi ya umuhimu wa kukatisha uhai kwa mtu aliyeamini ni Shetani aliyepindukia Mr X.
Safari yake ya wizi wizi usiku ule huku jiji likiwa limepoa kabisa ilimpeleka hadi maeneo ya mbagara na mbele yake aliliona jengo kubwa la hoteli ambayo alipangiwa babaake pale. (“Lazima nifanye mbinu nimuhamishe hapa baba kabla huyu Chizi hajatuma kinyago wake mwengine aliyempofua kuja kumaliza azma yake”) Aliwaza Lady Ninja Asha na kutoa tena ile dawa yake ya unga maalum ambayo akiishika kwa style maalum aliyofundishwa na kutamka maneno ya Mzimu wa Kininja aliyoyajua mwenyewe, basi hupotea na kuacha moshi mdogo eneo lile na hutokea mahala ambako alikukusudia akilini kabla hajafumba macho na kusema yale maneno. Na ndivyo ilivyokuwa ambapo Asha alinuia na kuieka akilini picha ya nyuma ya hoteli ile ili iwe rahisi kuingia kimya kimya lengo kuu likiwa ni kumuhamisha babaake pale hotelini na kumpeleka sehemu nyengine ambayo aliamini inaweza kuwa salama ili amuondoe kwenye Rada ya Mr X.
* * * * * *
Kwa upande wa Cj4 yeye alikuwa ndani ya nyumba moja iliyokuwa jilani na ile hoteli alipokuwa amepangiwa Hussein babu bubu huku muda wote alikuwa makini mno na kila kitu kilichokuwa kinaendelea hotelini pale mara baada ya kutega kamera maalum ya kijeshi kwenye usawa wa dirisha lake na kuchukua upande wa V ya hoteli ile kwa mbele, pia kamera nyengine aliitega kwenye chumba cha guest iliyokuwa upande wa nyuma ya hoteli ile na kwa jinsi alivyoitega ilikuwa ngumu mno mtu kuona ama kujua na kwa kutumia kamera hizo mbili aliweza kurekodi kila kilichokuwa kinaingia na kutoka kwenye ile hoteli kwa kutumia compyuta yake aliyoiconect na zile kamera.
Usiku huo kama kawaida alikuwa anawascan watu aliokuwa anawatilia shaka na kuchukua picha zao pasi na wao kujua kila aliyekuwa anaingia au kutoka mule hotelini na kwa kutumia compyuta yake maalum aliyoiconect na zile kamera. Vilevile kitu kilichozidi kuzipa upekee zile kamera za Cj4 ni setting zake za moja kwa moja pindi inapommulika mtu yeyote mwenye silaha ama silaha yoyote ilikuwa inatuma Alarm kwenye compyuta yake na kumpiga picha muhusika na kutuma moja kwa moja kwa mtaalam Cj4.
(“Mh! kila kitu kipo sawa, mbona huu mchezo Mr X hauvagai au kashaustukia…!! Camoon Mr X”) aliwaza Cj4 pindi alipokuwa anacheki cheki jengo la hoteli hususani usawa wa ghorofa kilipokuwa chumba cha Hussein ambako napo kulifungwa kamera kwa siri na Kamishna Shebby ambayo ilikuwa inaonesha kinachoendelea mule ndani na kutuma moja kwa moja kwa Cj4 na kwenye simu ya Kamishna Shebby. Yote hayo walifanya kwaajili ya usalama wa Hussein bubu na kumtega Mr X kwa kumtumia Hussein bubu kama chambo pale hotelini kwani walijua kuwa shabaha iliyobaki kwa Mr X ni kwa Hussein bubu tu na akifanikiwa kumuua na huyo atakuwa kamaliza kila kitu na kamwe hakutakuwa na sababu ya kumtaja wala kumzungumzia tena. Lakini yote yale yalikuwa yanaendelea pasi hata na Hussein mwenyewe kujua japo na yeye alikuwa na kiu na shauku ya kumuua Mr X na kila siku alikuwa anasali ili utokee muujiza amuue kwa mkono wake Mr X.
Lakini Cj4 akiwa amejipumzisha baada ya kuangalia kona zote kuwa ni salama mara Alarm ilibeep ktk kompyuta yake kumuashiria kuna hatari katika zone moja ya eneo alilotegesha kamera na hapo ndipo kwa speed alifungua kuangalia na alimshuhudia mtu aliyevaa mavazi ya Kininja akiingia kinyemera kwenye nyuma ya jengo la hoteli kulipokuwa na bustani kubwa na tayari alishaua walinzi wawili pasi na eneo la mbele ya Hoteli kujua chochote. “Karibu kwenye Mchezo wee Mbuzi” aliongea kwa Hasira Cj4 na kuchukua Kisu chake kikubwa kilichokuwa na dira kwenye mpini wake sambamba na wire maalum wa silva kwa niaba ya kwenda kuoneshana kazi na yule Ninja aliyeamini ametumwa na Mr X na alienda pale kwa niaba ya kumaliza kazi aliyotumwa na Mr X nayo ni kummaliza Hussein babu bubu.
Ndipo muda ule ambo Cj4 anatoka na kuanza kupita Kikomando akichanganya na Uninja ndani yake alishangaa alipokuwa anakaribia kwenye ile bustani kukukuta kuna timbwili limeibuka lililomshangaza mno na lililomfanya kwanza ajibanze sehemu kulishuhudia mwisho wake utakuaje. Naam lilikuwa ni Timbwili la Maninja wawili tena wote wakiwa wamevaa mavazi meusi yanayofanana sana. Hali hii ilimchanganya Cj4 na kuamua kubanza pale kwenye moja mti uliokuwa kwenye ile bustani huku akiwa haelewi wapi ametokea Ninja mwengine wakati awali alimuona mmoja na je yule Ninja mwengine ni nani na kwanini wanapigana pale? Pia kati ya wale Maninja wawili yupi Ninja mwema na yupi Ninja m baya?
Alijiuliza maswali haya Cj4 ambayo hakujua majibu yake na alijua ni ngumu kujua majibu yake hadi atapozidiwa Ninja mmoja ndipo ataangalia yule mwengine atachukua maamuzi gani akimmaliza mwenzake, kama atachukua maamuzi ya kupanda kwenye hoteli kwa nia ya kwenda kummaliza Hussein bubu basi atadeal na huyo kwani ni mbaya lakini kama atachukua hatua ya kuondoka basi huyo atakuwa Ninja ambae hana chuki na mtu yeyote bali huenda kaja kutoa msaada kwa Hussein bubu ama alikuwa na kisasi na yule Ninja mwengine ambacho kaja kumlipizia. Lakini pia alijiuliza Cj4 kama kuna Ninja kati ya wale anapigana kwa niaba ya kumtetea Hussein ni Ninja gani huyo? maana mission ya usalama wa Hussein ipo katika mikono yake na mikono ya Kamishna Shebby sasa huyo Ninja ametokea wapi? ama hakika Cj4 alipata mtihani wa maamuzi kipindi akiangalia ule mpambanu lakini pia aliamini katika moja ya mawazo yake basi kuna wazo sahihi kabisa kuhusu wale maninja waliokuwa wanaendeleza kasheshe pale bustanini.
Mapigano makali ya wale maninja huku mmoja akiwa mwepesi sana kuruka na kukwepa vidubwana alivyokuwa anarusha mwengine ambavyo vilikuwa vikimkosa vinazunguka na kurudi kwenye mikono ya mrushaji wake na katika harakati zile mara Ninja yule aliyekuwa anaruka mno alipokitwa na kile kidubwana kimoja maeneo ya tumbo mara baada ya Ninja mwenzangu kumzidi ujanja mdogo katika urushaji na kumsababishia akwepe tofauti na kuingia kwenye kumi na nane za Ninja mrusha vidubwasha. Hapo sasa Cj4 kuna kitu alianza kukigundua baada ya yule Ninja aliyechomwa kile kidubwasha mithili ya msumeno wa round kuanza kuzidiwa kutokana na maumivu na kumpa nafasi ya kushambuliwa zaidi na Ninja mwenzake mpaka ikafikia sasaameanguka chini hana ujanja huku mkono mmoja ameshikilia pale tumboni mwake ndipo yule Ninja alipoanza kumsogelea na kumsimamia mbele yake huku akimwambia maneno ambayo Hussein yalimsaidia kuwatofautisha wale Maninja na kumjua m baya ni yupi mwema ni yupi. Na wakati yule Ninja akimtambia kwa maneno makali mwenzake aliyekuwa katika hali mbaya tena akimtambia zaidi kwa kuamua kuvua maski ile ya Kininja inayoficha uso na kumuwezesha Cj4 kumuona sehemu za Kisogo na kugundua yule ni Ninja dume tena alionekana kichwa chake kikiwa na mchanganyiko wa nywele nyeupe na nyeusi kuonesha kuwa yule ni Ninja mwenye umli mkubwa yaani sio kijana japo alionekana bado strong na mwenye mbinu kwa vile alivyomuona akipambana. Hapo sasa Cj4 alimshuhudia yule Ninja mzee akichomoa lile panga lake kubwa la Kininja kwa niaba ya kummaliza Ninja yule aliyezidiwa kwa kuchomwa na kidubwasha ambae tayari Cj4 aligundua kuwa ndie Ninja mwema na hapo aliona itakuwa uzembe mkubwa kuacha Ninja yule mwema auawe mbele ya macho yake wakati ana uwezo wa kutoa msaada na aliamini anaweza kumdhibiti yule Ninja mzee baada ya kumsoma toka awali alipokuwa anapambana na Ninja mwenzake na alizigundua mbinu alizomshindia Ninja mwenzake ambae aliamini pia ingekuwa si mbinu zile za ujanja ujanja basi hata yule aliyejeruhiwa angeweza kumdhibi. Alichungulia Cj4 na kupiga mahesabu ya haraka pindi yule Ninja aliponyanyua panga kwa dhumuni sasa la kummaliza mwenzake bila huruma ambae alikuwa na dariri zote za kukata tamaa na kusubiria kifo na hapo ndipo Cj4 alipoinunua ile kesi kwa style ya kipekee na ajabu.
Simulizi : Wanawake Ni Wauaji ?! Sehemu Ya Nne (4)
Baada ya Asha kufanya mazingaombwe yake na kuyayuka then kuibukia pale bustanini, alistaajabu kuona maiti mbili za walinzi na alipocheki kwa mbele alimuona Ninja kama yeye akisota mpelampela kuelekea usawa wa chumba kile cha Hussein bubu kwenye ghorofa la ile hoteli. Alijua sasa tayari kumekucha, na kama ilivyokuwa kwenye mawazo yake kuwa mr X lazima kuna kipofu wake atamtumia kuja kufanya ile kazi baada ya yeye kuikataa na kujua kuwa amejua hadi kufikia kumzimia mitambo ya mawasiliano kati yao alijua sasa na yeye ni miongoni mwa adui wa mr X na yule Ninja katumwa kuja kufanya ile kazi akimaliza lazima atumwe kwake pia hivyo akaona ule ndio wasaa na kwakuwa amewahi lazima kapambane nae.
Aliruka beki kavu mfurulizo Lady Ninja Asha na kumzuia kwa mbele yule Ninja ambae nae alikuwa hajategemea ujio wake lakini alijua kuwa yule kaja kumzuia kufanya kazi muhimu aliyotumwa na hapo ndipo kasheshe likaanza. “Wee ni Muasi, Lazima Ufe leo hapa hapa ni bora umejileta” aliongea yule Ninja lakini Lady Ninja hajajibu chochote zaidi alianza kumshambulia kwa mateke ya angani mfurulizo hadi akaanza kumrudisha nyuma japo nae yule Ninja hakuwa wa mchezo.
Pambano lilikuwa kali sana na ikafika sasa Asha alikaribia kummudu yule Ninja lakini mara yule Ninja akabadili mapigo na kuanza kutumia ‘Invisible Knifes’. Ni visu special vidogo sana vya duara vyenye meno makubwa sita ambavyo hurushwa kwa uchawi wa kininja na kama huujui uchawi huo hata kidogo kamwe huwezi kukikwepa hata kimoja lakini uzuri japo Asha yeye hakuwa na vile visu lakini alikumbuka mafunzo aliyopata kwa yule babu wa kijapani kule India na maelekezo ya maneno ya kichawi anayopasa kutamka pindi anaporushiwa ‘Invisible Knife’ na Ninja yeyote na jinsi ya kuvikwepa. Na ndivyo alivyofanya Asha kwa wepesi wa ajabu aliweza kuvikwepa kwepa vile visu kwa kubinuka binuka huku nae akijaribu kupeleka mashambulizi lakini kwa bahati mbaya kisu kimoja kilimpata mara baada ya yule Ninja kumzidi ujanja na kumuhadaa kwa kumtishia kisha akamtokea upande wa pili na kuvirusha vitatu kwa mpigo na hapo ndipo Lady Ninja Asha alishindwa kuvikwepa vyote.
“Hhahahahahahaha” kilisikika kicheko cha yule Ninja na kuendelea na pambano huku Lady Ninja akiwa na maumivu makali sehemu za chini ya tumbo kutokana na kunasiwa na kile kisu lakini alijitahidi kupambana ili kumzuia yule Ninja asiende kumuua babaake. Alizidi kuelemewa Asha na yule Ninja kibaraka wa mr X hasa kutokana na kutoneshwa palepale na yule Ninja na kuzidi kukisukumia ndani ya nyama zake za tumbo kile kisu kidogo kilichonasia na hatimae Lady Ninja alikosa kabisa nguvu na kuanguka chini. “Hahahahahaaa 9121 Lady Ninja, sikuwahi kutegemea kama utakuja kuwa msariti kiasi hiki.” Alicheka kwa dharau yule Ninja na kuongea kwa uchungu huku akimsogelea taratibu Asha pale alipoanguka. “Wewe ni kipofu uliye kwenye Mchezo wa Mr X hujui ukweli wowote, kama unaniua tafadhali Niue mimi tu lakini si babaangu, tafadhali huyo uliyetumwa kumuua ni babaangu tafadhali sana badala yake niue mimi” aliongea huku akisota sota kurudi nyuma Lady Ninja Asha hakuwa na ujanja wowote, maumivu yalimzidia hakuweza kupambana tena, alikuwa tayari kufa yeye lakini si babaake aliyemjua siku moja tu kabla ya matatizo yote yale.
“Aaaahaaa, vizuri sana kumbe ni babaako hahahahaha yaani hata kama isingekuwa amri ya mr X lakini kwa vile nimejua babaako basi lazima ningemuua tu, na Nitamuua ila kwanza naanza na wewe” alijibu yule Ninja mara baada ya kusikia kumbe Hussein bubu aliyetumwa akamuue ni baba wa Lady Ninja. “Lakini mbona unataka kufanya unyama kwa mzazi wangu ambae hana hata muda toka arudi Uraiani? mbona huna huruma wewe…! hebu fanya ingekuwa mzazi wako wewe ungejisikiaje?” “Ahaaaaa Umeongea vizuri sana Lady Ninja, wewe ni mtoto mdogo kwenye vita vya wanaume lazima utoe mikojo… Umeongea vizuri sana, labda nataka ukumbuke vile ulivyoasi na kumuua babaangu. Ulitegemea na wewe babaako atabaki mzima? Laiti ningejua kama mtoto ninayempa msaada siku zile ndie atayekuja kumuua babaangu basi ningekuua palepale India ulipomwaga mikojo ya hofu” aliongea safari hii yule Ninja akiwa kasimama jirani kabisa na Asha ambae alisota mpaka kwenye ukuta wa jengo na hakuwa na pa kuendelea zaidi.
Muda wote Asha alipigwa na butwaa mara baada ya yule Ninja kuongea maneno yale, hakufahamu ni babaake gani aliyemuua ila kauli ya kusaidiwa India ndio iliyomstua zaidi na zaidiiii…. ni pale yule Ninja alipoamua kuvua mask yake iliyokuwa inaficha uso na kumfanya Asha azidi kutaharuki japo yeye hakuvua ya kwake. “AAAH!! UNCLE TYGA..!?” “Ndio Mimi Mtoto wa Mzee ALY77” Aliongea Ninja Tyga huku akichomoa kisu kikubwa cha kininja kwaajili ya kummaliza kabisa Asha ambae aliamua kufumba macho baada ya mwili wote kufa ganzi na kukumbuka kuwa ni kweli alimuua mzee Aly77 lakini ilikuwa ni agizo toka kwa Mr X na hakuwahi kujua kama ni babaake na Tyga ambae aliagana nae miaka michache iliyopita kule India. Lakini ghafraaaaaaaaaaa alishangaa Asha kusikia ukelele wa maumivu kutoka kwa Uncle Tyga uliomfanya afumbue macho na hakuamini alichokuwa anakiona mbele yake juu ya ujio wa kidume ambae alikuwa hajavaa Kininja wala nguo za sare ya aina yoyote iliyomtambulisha yeye ni nani, huku chini alimuona Uncle Tyga akiwa ananyanyuka kwa hasira na usoni damu zikimvuja hali iliyomfanya Asha ashangae zaidi asijue kapigwapigwa vipi sekunde zile chache na yule mtu ambae alisimama mbele yake na alipomuangalia kwa umakini kwa jinsi alivyosimama tu… Aliamini huyu ni zaidi ya Ninja. Na huyo si mwengine bali ni Cj4.
Na kweli kile alichokifikiria Lady Ninja Asha na ndivyo ilivyokuwa kwani mbali na mbinu, uzoefu na ujanja aliokuwa nao Tyga katika maswala ya upiganaji na uninja lakini kwa Cj4 alionekana bado kabisa hajaiva kutokana na mapigo aliyokuwa anapelekewa hata yeye mwenyewe Tyga alishangaa. “Nani wewe unaingilia ugomvi usiokuhusu!!?” alilalama Tyga mara baada ya kuanguka kwa mara ya pili na kutema mate yaliyochanganyika na damu nyingi sambamba na meno mawili ya mbele mara baada ya kupokea nakozi za ajabu kutoka kwa Cj4 aliyakuwa anamchanganyia mapigo matatu kwa wakati mmoja. “NANI WEWE!!!?” Aliuliza tena kwa kufoka Tyga huku akijizoazoa tena pale chini damu zikizidi kumvuja baada ya swali la awali kutojibiwa kwa mdomo zaidi ya kupelekewa mateke mfurulizo ya angani ambayo alifanikiwa kuyapanch yote lakini alistaajabu pindi yule mtu ambae hakumjua alipotua chini tu ghafra alimfatua mguu kwa kumchalaza na wire furani uliomvinga na kumchota mtama Tyga na kudondoka kama gunia la viazi. Alisimama na kujikaza kiume Tyga huku akirudia rudia kuuliza lile swali ambalo Cj4 hakunyanyua mdomo kumjibu zaidi alimjibu kwa mkong’oto wa hali ya juu uliopelekea sasa Tyga kuona nyota nyota.
Wakati mwanaume Cj4 akiendelea kumfunza adabu Tyga kwa kumuonesha vita vya kiume ndipo Lady Ninja Asha alipotumia ule uchawi wake wa Kininja na kufanikiwa kuondoka eneo lile na kutokea upande wa pili ambapo alitembea hivyo hivyo japo alikuwa na maumivu makali sehemu zile alizoumizwa na Tyga hususani pale tumboni kulipokuwa na kile kisu cha kininja. Huku nyuma bado Tyga alizidi kudhibitiwa na Cj4 na hatimae alizimishwa kwa kupigwa kata ya shingo iliyopelekea kuteguka ule mshipa uliopitia nyuma ya sikio na kupoteza fahamu. “The Game is start, Mr X you are the Next…” aliongea Cj4 huku akiwa kamkanyaga kifua Tyga pale chini alipopoteza faham na kuchomoa kijiantena kilichokuwa katika saa yake kubwa ya mkononi ambayo pia ilikuwa kama simu na hapo ndipo alipotuma location za mawasiliano kwa Kamishna Shebby na signal ilipofika tu alipiga simu muda ule ule bila kuchelewa kutokana na yeye kule alipokuwa alikuwa kwenye usingizi wa mawenge kutokana na mawazo ya ndoa yake na Asha pia vile alivyojua kuwa Hussein bubu ni baba mkwe wake. [“Muangalie usoni atakuwa ni mwanamke tu, Nakuja sasa hivi”] aliongea Shebby kwa njia ya simu mara baada ya kupata signal maalum ya Cj4 na kupewa taarifa kwa ufupi kilichojili.
Na kweli baada ya pale CJ4 alimnyanyua Tyga ambae alikuwa kapoteza fahamu na kutimka nae kwa umakini eneo lile hadi mahala ambapo aliamini pametulia wakati huo signal iliyokuwa inampa mwelekeo Kamishna Shebbyikiwa on. Nusu saa baadae Shebby alifika pale na gari ndogo akiwa mwenyewe walimpakia Tyga na kuondoka nae kuelekea maeneo ya Kongowe njia iliyoelekea gerezani kwa Shebby na huko walipanga kumuingiza kwenye gofu la nyumba moja ya zamani iliyokuwa haishi mtu yeyote ili wamfungie mule kwaajili ya kumuhoji juu ya Mr X. “Kumbe walikuwa wawili?” aliuliza Shebby pindi wakiwa njiani “Yah! walikuwa wawili ila mmoja nimemuacha aende” alijibu Cj4 “Kwanini sasa?” “Kwa sababu alikuwa mwema” “Mwema?! Kivipi wakati nae ni Ninja” “Kwa sababu ni Ninja wa kike” “Cj4 umefanya kosa huyo wa kike ndie nilikuwa namtaka haswaaaaa nina imani ndie aliyetushambulia Mkuyuni” Alilalalma Shebby baada ya kusikia kumbe walikuwa wawili lakini Cj4 amemzalau wa kike na kumuacha aende.
Aliumia Shebby kwani hasira zake kuu ni kumjua yule Ninja wa kike ili amuue kwa mkono wake kama alivyomuahidi siku ile endapo atamuacha hai. Lakini kwa Cj4 alishagundua kitu kutokana na kusikia maongezi ya yule Ninja na kuhisi kwa asilimia tisini kuwa mchumba wa Shebby waliyeenda na Hussein bubu kukutana nae ndie yule Ninja aliyemsaidia pale lakini hakutaka kumwambia haraka Kamishna Shebby kwa kuwa alijua kuwa yule Lady Ninja alitumiwa kimakosa na Mr X kwa kuwa alikuwa katika mlolongo wa watu waliotakiwa kupotezwa na Mr X.
* * * * * *
Alirudi Asha na kufanikiwa kuibuka chumbani kwake pasi na mtu yeyote kujua. Alijiangalia kwenye kioo cha chumbani kwake mara baada ya kuvua mask yake ya Kininja na kuchukua sindano aliyoichoma dawa ya kuzuia maumivu na kujidunga eneo lile la tumboni. Na bada ya nusu saa maumivu yalikata kwa nguvu ya ile dawa hapo ndipo alipochojoa mavazi yake ya kininja na kubaki na nguo ya ndani kisha alichukua visu maalum vya oparation vilivyokuwa chumbni kwake mule na kujituliza mbele ya kioo na kuanza kujichana huku akijibinya kwa nguvu kuondoa kile kisu kwenye nyama zake za tumbo. Kitendo alichokuwa anakifanya Asha kilikuwa si cha kitoto kwani ilihitajika ujasiri wa hali ya juu sana kufanya kama alivyokuwa anafanya Asha tena huku akijiangalia kwenye kioo mpaka akafanikiwa kutoa kile kibisu cha kininja kilichonasia kwenye nyama za tumbo lake.
Baada ya hapo Lady Ninja Asha alianza kujishona taratibu sehemu ile ya jeraha kwa umakini mkubwa mpaka akafanikiwa kumaliza kabisa na kubaki na alama ya mshono eneo lile la chini kidogo ya tumbo. Ndani mwa Dk, Asha ilikuwa nusu ya hospitali kwani kila kitu muhimu kilikuwepo na aliandaa haya yote kwa kujua kuwa katika kazi zake siku moja inaweza kumpata balaa na kujisaidia mwenyewe na ndivyo ilivyokuwa siku hiyo. Alijifunga bandage yenye dawa maalum eneo lile la mshono na kuizungushia kiunoni ambapo ilibana vizuri kisha alisafisha eneo lote lililokuwa na dam dam na kujilaza chali kitandani akiwaza nini hatma yake ya baadae na huyo Mr. X
(“Hivi yule aliyenisaidia ni nani hasa? Na kwanini alikuja eneo lile Mh! Inaonekana ni mtu hatari sana tena sana lakini kwanini alikuwepo pale? Au anajua kinachoendelea pale ? Natamani ningemjua nimuulize lakini sidhani kama anaweza kuwa salama kwangu”) Aliendelea kuwaza Asha akiwa pale kitandani wakati huo tayari ilikuwa inaingia alfajiri na maumivu ya mshono yakaanza upya na kumuongezea zaidi mawazo kwani alijua kabisa vile visu vinakuwaga na sumu ndani yake pindi vikiingia kwenye nyama ya binaadam. Japo aliweza kukitoa lakini aliamini tayari mwilini mwake ana sumu ya Invisible knife na itakuaje endapo atajulikana kuwa na jeraha atadanganyaje? au hiyo ndoa kama itapangwa haraka ataolewaje…? Alifikiria Asha na kujiuliza maswali haya yaliyomfanya chozi limtoke kwa mara nyengine. Hakujisikitikia yeye kama atakufa mapema kwa sumu iliyo mwilini mwake bali alisikitika endapo atakufa kabla ya kumuua Mr X.
“Twambie nani Mr X na wapi alipo?” lilikuwa ni swali toka kwa Kamishna Shebby akimuuliza mateka wao yule ambae ni Tyga. “Sijui unazungumzia nini” alijibu Tyga kwa kujiamini mbali na kuwa uso wote ulikuwa umechakaa hata hakuweza kuona vizuri kutokana na uvimbe na damu zilizokuwa bado zinamvuja. “Narudia twambie wapi Mr X alipo na ni NANI??” “Nimeshasema sijui unamaanisha nini wala sijawahi sikia hiko kitu” bado aliendelea kutia ngumu Tyga wakati huo Cj4 alikuwa anasikia kile alichokuwa anajibu Tyga lakini alimuacha Shebby aendele kumuhoji huku upande wake binafsi alikuwa na mtu mmoja akimuhabarisha kinachoendelea nae si mwengine ni mkuu wa majeshi tu.
“Nani Mr X??????” “SI-JU-I” Mabishano yaliendelea ambapo safari hii Cj4 aliamua kutoka kule nje alipokuwa na kurudi speed hadi kwa Tyga bila kumuuliza kitu chochote alichomoa kisu chake cha kikomandoo na alipomfikia Tyga tu alikamata sikio na kulikata lote palepale mbele ya Kamishna Shebby aliyekuwa anatumia maneno mengi kumuhoji Tyga. “Aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaghhhhhhhhhhh” Alipiga yowe la maumivu Tyga mara baada ya Cj4 kumpangusa sikio na kulieka mbele yake pasi na huruma. “Sasa Muulize tena kama atakuwa hasikii vizuri au haelewi nakuja baada ya dakika kumi kumalizia la upande wapili” Aliongea Cj4 na kunyanyuka tena kwenye sehemu ile waliyoiandaa mapema kipindi wanasuka mchezo wao wa kumnasa Mr X hivyo ndani ya lile gofu haikumaanisha tu waliingia kwa dharula ama walibahatisha. bali walikuwa walipaandaa mapema kwa kujua lazima Mr X atatuma mtu wake wa kummaliza Hussein bubu.
Kitendo cha Cj4 kumkata kwanza sikio Tyga bila kutumia muda wa kubembeleza kumsemesha wala kumuuliza kidogo kilimstaajabisha Shebby ambae yeye hasira zake muda wote zilikuwa kwa Ninja wa kike ambae Cj4 alimuacha aende. Maumivu yalikuwa makali sana kwa Tyga lakini bado msimamo wa kumficha Mr X ulikuwa palepale hali iliyomtia hasira zaidi na Shebby aliyeamua kumzibua sehemu za sikio zilezile zilizokuwa zinarusha damu na kupelekea Tyga kupoteza fahamu. “Huyu atasema kweli?” aliuliza Shebby kwa kuhisi kuwa yule mateka wao anaonesha yuko tayari kabisa kufa kuliko kusema ukweli kuhusu mr X “Kwa kuwa ana mdomo atasema tu kile anachokijua kweli, ukimshindwa utanambia nije nimsemeshe” alijibu kwa kujiamini Cj4 na kuingia tena mmule ndani alipozimia Tyga. Lakini alipokuwa anamsogelea kumkaribia pale chini alisikia mlio wa kitu mithili ya alarm ya saa ya kimulimuli ikibeep kwenye mavazi ya Tyga ambapo alimpekua harakaharaka ndipo alipostuka baada ya kugundua kumbe kwenye lebo ya nyuma ndani ya kola ya gwanda ile ya kininja aliyovaa Tyga kulikuwa na maneno madogo ambayo kumbe yalishonewa na wire wenye signal maalum za bomu la kuendeeshwa na rimoti… Yaani lile vazi zima la Kininja lilitengenezwa kwa nyuzi maalum za baruti nyeusi ikiwa na maana combat aliyovaa Tyga lilikuwa ni bomu. Hii ilimstua na kumshangaza Cj4 kwa kuhisi kuwa hata yule Ninja mwenyewe hakuwa anajua kama amevaa bomu muda wote na sasa namba zake zimeingizwa kwenye systim na rimoti imewashwa na ishaanza kuhesabu japo pale haikuwaonesha itahesabu kwa dakika ngapi. “Tokaaaa Shebby Rukia nje harakaa Tokaaaaa” alikimbia Speed kutoka nje Cj4 na kumkamata Kamishna Shebby kuruka nae kwa nje ya ile nyumba pindi alipokuwa anashangaa Cj4 alipokuwa anampigia kelele za kutaka arukie nje wakimbie eneo la kile kibanda.
Waliangukia mita kumi na lile gofu huku Shebby akiwa bado haelewi, Cj4 alimshika tena mkono na kuanza kukimbia nae pamoja kuelekea mbali zaidi na lile gofu. “CJ….Vi…..” alitaka kuongea kitu Shebby lakini kabla hajamalizia alistushwa na kishindo cha mlipuko kutokea nyuma yao na alipogeuka hakuamini kuona gofu lile alilokuwemo mateka wao likisambaratika kwa moto.
“Shiit Cj4 ina maana umeamua kumlipua!!?” aliuliza kwa mshangao Kamishna Shebby pindi alipokuwa anashuhudia ule mlipuko uliowasha moto ghafra kule kwenye gofu walilomfunga mateka wao Tyga. “Huu sio muda wa kuuliza Kamishna bado tupo kwenye mchezo wa Mr X japo na sisi tumeanzisha mchezo wetu ndani yake tuondoke hapa haraka.” aliongea Cj4 na kukimbilia kule ilipo gari yao sambamba na Shebby na kujitoma ndani yake ambapo safari hii dereva alikuwa Cj4 mwenyewe. “Lakini kwa nini umemlipua?” “Mimi sie niliyemlipua ila ni Mr X mwenyewe” “Mr X?? Kamlipua lipuaje sasa” “Kwa kutumia akili za siku nyingi kabla hajatafuta wachezaji nyota wa kuucheza mchezo wake” majibu ya Cj4 si kwamba yalikuwa yanamsaidia Shebby kutatua maswali aliyokuwa nayo, bali ndio kwanza yalikuwa yanampa maswali mapya ambayo yalikuwa yanamuonesha mwanga jinsi ya kutafuta majibu pasi na kuuliza tena. “So what is Next..?” aliuliza Shebby japo alihisi wanaenda kwa Hussein bubu ila alitaka kujua kama itawalazimu wamuhamishe ama waendelee kumtega palepale lakini jibu la Cj4 lilizidi kuonesha tofauti baina ya KOMANDOO wa JESHI na KAMISHNA wa POLISI. “Next mimi nitadili na Hussein wewe pitiliza alfajiri hii hii kwa mchumbaako na umuhamishe pale anapoishi haraka kwa usalama zaidi”
“Mchumbaangu? Ina maana dokta Asha?” “Ndio hivyo, all the best Kamishna” Alijibu maneno haya Cj4 wakati huo tayari gari ilifika pale Mbagara karibu na ile hoteli kulipoonekana kun mkusanyiko wa watu na maaskali polisi hususani sehemu ile ya nyuma kwenye bustani. Alishuka Cj4 na kumuachia usukani Shebby ambae alikuwa bado anayatafutia ufumbuzi majibu ya maswali ya Cj4 huku akipiga gia kuelekea kwa mchumbaake kwa kufata kauli ya mtu aliyeamini kwa moyo mmoja kuwa amemzidi mbinu na akili ya vita.
Lakini ukweli ni kua Cj4 alibaini mchezo uliotegwa na Mr X kwa wale Maninja wake hasa alipowaona wanapambana usiku wake sare zao zilishabihiana karibu kila kitu na kubaini kuwa matereo ndio yaleyale na system ndio ile ile hivyo kuna uwezekano mkubwa na yule Ninja mwengine akalipuliwa na mavazi yake ambayo aliamini wazi kuwa hajui kama ni bomu. Na kwa kuwa alihisi kwa asilimia kubwa kuwa yule Ninja ni mchumbaake Shebby aliyevaa kivuli cha Dokta Asha na yote hayo aliyabaini kupitia maongezi yao wenyewe pindi walipokuwa wanapambana bustanini. Hivyo aliamini kama asipoenda mtu kumtoa kule basi maisha yake nayo yatakuwa hatarini.
* * * *
Aliamka asubuhi ile Asha na kujichoma tena sindano ya kuua maumivu kabla hajatoka kuelekea chini akiwa na maana ya kufanya mazoezi ya kutembea kwa kupandisha ngazi na kutroti kidogo ili kukipa shurba kidonda chake kibichi kisijivute na kumfanya astukiwe na watu kama alikuwa na jeraha mwilini mwake. Alivaa full tracksuit na kwa jinsi alivyokuwa anatembea kwenye ngazi mara baada ya kutoka chumbani kwake ilikuwa ni vigumu mno kumtambua kama ana jeraha la mshono mwilini mwake. Mazoezi ya kupanda na kushuka ngazi yaliendelea wakati huo bado mamaake alikuwa hajaamka na kutoka chumbani kwake.
Akiwa anafanya yale mazoezi mepesi ya kupanda na kushuka vingazi mulemule ndani bado mawazo yalikuwa mengi sana kichwani mwake Asha hususani kuhusu kifo cha Mr X. Hakuwahi kumuona alivyo wala kujua wapi alipo hata historia yake alikuwa haijui zaidi alichojua kipindi cha nyuma kuwa mr X ni mtu mwenye kutetea haki za watu na kuwasaidia na kuwafichua wabaya na ndio sababu ya kuwa na maadui waliokuwa wanataka afe ili akosekane mtu wa kuwafichua na kusaidia wengine. Awali aliamini hayo lakini sasa ameujua ukweli kuwa wote waliokuwa wanamtafuta mr X kwaajili ya kumuua walikuwa sahihi kabisa. Lakini ugumu unakuja ni kugundua picha halisi ya mr X na jina lake halisi ama hata wadhfa aliowahi kuwa nao kwani ingesaidia kumgundua na kumpata kiurahisi. “Mwisho wako unakuja… Mwisho wako ndio huu, Mwisho wako unakuja , Mwisho wako ndio huu” aliongea haya maneno Asha kwa hisia huku akiwa kama anaimba pale alipokuwa anapandisha ngazi na kushuka.
Lakini mara akiwa bado anapandisha na kushuka pale kwenye ngazi ndipo aliposikia mlio wa kitu cha alarm ukitokea chumbani kwake kama vile alivyokuwa anasikia Cj4 na kumfanya Asha asijue Alarm ile ni ya nini kwa kuwa yeye hajawahi kuset alarm yenye mlio kama ule. Alianza kupandisha taratibu kurejea chumbani kwake kuangalia hiyo alarm ilikuwa ya nini, lakini akiwa anapandisha kabla hajaufikia mlango wa chumbani mwake alijikuta moyo unamuenda mbio na kusita kuingia kwanza na kusimama mlangoni kusikilizia akiwa anajishauli inapotokea hiyo alarm na kupata hisia ni pale kitandni alipozivua nguo zake za Kininja usiku aliporudi na hapo kidogo alijipa moyo kuwa hakuna kitu kibaya na ndipo alipotaka kufungua mlango lakini Hamaaaaaadiiiii…….!!! Alirushwa yeye na Mlango baada ya mlipuko wa ajabu kutokea ghafra mule chumbani na kumstua hadi mamaake aliekuwa analala chumba cha chini. ”Aaaaaaaaaaaaaaaaaghhhhhh”
“Ashaaaa!!! Ashaaaa Ashaaa Mwananguuuu Jamaaaaniii msaadaaa… Motoooo Moootoooo” alipagawa Zena huku akimbuluza Asha kwa nje kumtoa pale alipodondokea na kwa bahati nzuri alidondokea kwenye Sofa huku ule mlango uliofatuka kwa mlipuko na kurushwa sambamba nae ukiwa umedondokea sakafuni na hapo ndipo moto ulianza kukamata zuria pale chini taratibu. “Jamani msaaadaaaaaa aaaaaah” alipiga yowe Zena lakini kumbe mlinzi pale getini alishatimua mbio muda mrefu mara baada ya kishindo kizito kilichosikika upande ule wa juu ya nyumba chumbani kwa Asha sambamba na fungu la moto lililofumuka angani mithili ya wingu na kushuhudia hadi vigae vilivyokuwa upande ule vikifumuka kwa mlipuko ambao uliwatisha hadi majirani na wapita njia waliokuwa karibu na eneo lile.
Akiwa anahangaika mwenyewe Zena kumvuta Asha huku akiogopa hali ya usalama mule ndani mara baada ya moshi kuanza kutanda hususani na ule moto ulioshika zuria kuzidisha kasi yake ya uwakaji, alizidi kuchanganyikiwa Zena na kulia kama mtoto mdogo hasa kila alivyomtazama Asha alikuwa kalegea mwili mzima hasemi wala hatazami. “Ashaaaa mwaanaaanguuuu Ashaaaaa amkaa mamaaaa” hakuweza kum beba kutokana na umli na nguvu chache alizokuwa nazo Zena lakini hakuweza kumuacha pia alijitahidi kumnyanyua sehemu za juu na kumbuluza vivyo hivyo kuelekea mlango wa kutokea nje mara baada ya kuona msaada umeenda kombo. Lakini mara ghafra mlango ulifunguliwa kwa nguvu na mwanaume aliingia huku akiwa kachanganyikiwa mno haamini kile alichokuwa anakiona. “Ashaaaaaa ASHA Wanguuu” alitoa ukelele wa maumivu na mshangao Kamishna Shebby mara baada ya kuingia na kumkuta Zena akimkokota Asha aliyekuwa katika hali mbaya huku sehemu zake za chini ya tumbo kukionekana damu kumvuja kwa wingi. “Mama Tangulia haraka nje kabisa Usishike hilo geti la mlangoni niachie mimi” alinena Shebby na kutoa tahadhari ile huku akimnyanyua Asha mara baada ya kuona cheche zikizidi kwenye socket za umeme mule ndani na ule moto wa kwenye zuria ulianza kudaka masofa na mapazia makubwa yaliyokuwa Dirishani pale Sebuleni.
Alinyanyuka huku akiwa kam beba Asha Kamishana Shebby na kutoka nae haraka haraka na kuelekea alipopaki gari kule nje na kumkuta Zena akiwa kasimama huku ameeka mikono kichwani. “Mama ingia kwenye gari twende mamaaa” aliongea Shebby kwa sauti ya kazi zaidi kutokana na uchungu aliokuwa nao na kumfanya Zena afungue mlango wa nyuma na kutangulia kukaa pindi Shebby alipomuingiza Asha na kumlaza huku mapajani mwa Zena, ndipo baada ya kuufunga mlango Shebby alizunguka upande wake haraka na kuingia ndani ya gari kuondoka eneo lile ambalo tayari moto ulianza kuwa mkubwa kule kwenye ile nyumba na watu walianza kuzongea huku wengine wakipiga simu sehemu za usalama wa zimamoto kitu ambacho Zena na Shebby hawakukikumbuka wala kujali zaid walichanganyikiwa na hali aliyokuwa nayo Dokta Asha. (“Mr X MR X lazima nikuue lazima nikuue na Ninja wako malaya wako unayemtumia lazima nae Nimuueee Lazimaaa damu ya mchumbaangu ilipwe hata kama atabaki hai..”) aliwaza moyoni Shebby huku akiendeesha gari speed kuwahi hospitali kuokoa maisha ya mchumbaake kipenzi, mkewe mtarajiwa, thamani ya moyo wake hasa alipokuwa anakumbuka alivyotibiwa mguu wake, mwanamke aliyeamini ndie mke bora wa kumuoa kutokana na sura yake ya bashasha, upole na upendo wa dhati aliomuonesha kipindi anamtibu. Nae si mwengine ni Dokta Asha ambae mpaka muda huo Shebby hakujua kuwa yule ndie Ninja wa kike aliyekuwa anatumiwa na Mr X.
* * * *
Kelele za watu pamoja na ving’ora vya polisi vilivyokuwa vinasikika upande wa chini ya jengo la Hoteli ile ndio zilizomsababisha Hussein bubu aamke alfajiri ile na kuelekea usawa wa dirisha la chumba chake kile alichopangiwa na Shebby kwenye ile hoteli. Alishangaa sana mara baada ya kuona umati wa watu wengi sambamba na polisi wakiwa eneo la bustani kubwa iliyokuwa nyuma ya ile hoteli usawa wa vyumba vile vya upande aliokuwepo. (He!! Nini tena kimetokea?”) alijiuliza mwenyewe kimoyo moyo baada ya kuona kuna ambulance iliyokuwa inapakia miili ya watu wawili iliyokutwa imeuawa mahala pale pa bustani alfajiri ile hali iliyomstua zaidi Hussein na kuamua kuvaa nguo zake harakaharaka ili apate kwenda kule chini akajionee mwenyewe kilichokuwa kinaendelea.
“Nini kimetokea hapa?” alimuuliza swali bwana mmoja baada ya kushuka chini na kupenya penya kwenye jopo la watu mpaka alipofika nyuma ya yule bwana aliyekuwa amesimama sehemu za mbelembele kulipozungushiwa warning tape za police kutoruhusu mtu yeyote kusogea eneo lile la tukio zaidi ya wana usalama waliokuwa wanafanya kazi yao ya upelelezi na utafiti wa kina kujua kilichowasibu wale maiti waliokutwa pale. “Kuna walinzi wameuawa hapa” alijibu yule bwana “Walinzi…!!” alitaharuki Hussein “Eee, bwana walinzi wamevamiwa na watu wasiojulikana na kuchomwa na vitu vya ncha kali shingoni kila mmoja” “Kwani walikuwa wangapi?” “wawili” “na walinzi wengine je?” “Wengine walikuwa upande wa mbele kule naona hawajasikia wenzao wlipokuwa wanauawa” “Duh! kwa hiyo hao majambazi wamefanikiwa na kuiba?” “Dah! ndugu yangu hata mimi mwenyewe mpita njia tu sio msemaji wa hoteli wala polisi we sikiliza tu fatilia utajua kila kitu” Alijibu yule bwana mara baada ya kuona maswali ya Hussein yanazidi kuwa mengi.
Aliangalia huku na huko Hussein huku akiwa na maswali ya wale watu waliovamiwa upande ule wa nyuma ambao ulinzi ulikuwa mchache kutokana na kutoonekana kuna thamani kubwa ya kuchukua zaidi eneo lile lilikuwa kama la kupumzika wageni tu, tofauti na eneo la mbele ambapo pia kulikuwa na parking kubwa ya magari na ndio kulikuwa na mashine za ATM na milango ya kuingilia mule hotelini. (“sasa hawa majambazi gani wamevamia na kuua watu upande huu huku kukionekana hakuna madhara menggine yoyote upande wa mbele? Mh! itakuwa visasi tu hivi sio bure”) aliwaza Hussein huku anaangaza macho huku na huko na mara alipogeuka kwaajili ya kuondoka pale kuna mtu alimuona upande wa pili aliyemstusha kidogo macho yake. (“Haa!..!>>!) alipigwa bumbuwazi huku akiwa haamini kama mtu anayemtazama pale ndie au sie na kuanza kusogea haraka ili avuke barabara eneo lile la upande wa pili kumuwahi kabla hajaondo kwani ni mtu ambae alikuwa anamkumbuka vizuri sana na alipomuona moyo wake ulistuka na kubadilisha mapigo kwani hakuwahi kufikiria kama atamuona tena mtu yule ambae sasa alikuwa mita chache tu mbele ya macho yake.
Alikuwa ni Cj4 nae alishamuona Hussein muda mwingi tu japo alijifanya kutomuona na katika hali ya kumzuga na kumpoteza maboya alisubiria roli moja ambalo lilikuwa linapita pale barabarani pindi lilipowaziba tu baina yao alizunguka haraka na kuingia kwenye ile nyumba ya wageni ambayo ndio alikuwa amefikia na kupandisha juu chumbani kwake mpaka dirishani na kuanza kumuangalia Husein ambae sasa alionekana kutamtafuta.
(“Mh!! kaendea wapi sasa yule kijana!!?”) alijiuliza Hussein kipindi akitafuta na kutomuona Cj4 ambae alichokuwa anakumbuka yeye ni kwamba alikuwa mfungwa mwenzake kule gerezani ambae nae alikuwa na mkasa kama wake na hata alipoingia gerezani kwa mara ya kwanza alikuwa na maneno kama yale yale aliyoyaamini yeye kuwa Wanawake ni Wauaji lakini kilichokuja kumshangaza baada ya kuzoena nae alikuja kutoweka kwa kutoroka jera na jitihada zilifanywa za kumtafuta lakini hadi anatoka gerezani alikuwa hajapatikana wala hata dariri za kuonekana kwake. (“Mh! mbona maajabu haya, au mzimu!!) alijisemea moyoni Hussein mara baada ya kuona hakuna hata dariri ya uelekeo wa yule mtu aliyekuwa amekusudia kumfata pale na kuamua kugeuza kurudi tena kule hotelini.
Lakini wakati wote huo Cj4 alikuwa anamtazama Hussein na kumfanya atabasam kw vile Hussein alivyoonekana kuhaha kwa kumtafuta yeye bila kujua ameelekea wapi wala kutambua kama yuko nae pale kila siku.
* * * *
Kwa speed ya hatari yenye umakini wa ajabu Kamishna Shebby aliweza kuiingiza gari mpaka hospitali kuu ya Jeshi la polisi Kilwa road na pindi gari iliposimama walikuja watu wa machera haraka haraka kutokana pia na kuitambua gari ile ilikuwa ya nani na aliposhuka tu ndio kabisa huduma za kumtoa Asha garini zilifanywa haraka sana na kwa umakini mkubwa.
Alionekana kudata Kamishna Shebby huku akiwa anazunguka zunguka wodini pindi Asha alipoingizwa chumba cha upasuaji bada ya kutolewa taarifa kuwa alirushwa na mlipuko hivyo madaktari walihisi huenda pia kuna vyuma au vibati vimeingia mwilini mwake hususani sehemu ya tumbo kulipooneaka kuvuja damu kwa wingi. (“Ama zako ama zangu.. ama zako Ama zangu..”) alirudia rudia Shebby maneno haya huku akiimaliza korido na kurudi mwanzo akifika mwisho anarudi tena mwanzo huku kichwa kakiinamisha wakati huo Zena alikaa kwenye viti vya kusubiri wagonjwa akilia kwa uchungu. Baada ya nusu saa alitoka Dokta mmoja kwenye chumba cha upasuaji.
“Vipi Dokta?!” aliuliza Shebby kwa mshtuko huku akiwa na shauku ya kujua kilichoendelea kwenye kile chumba cha upasuaji. “Usijali mkuu, maendeleo ni mazuri tu inaonesha zaidi alipata mshtuko wa moyo uliosababisha presha kuwa chini sana lakini hana majeraha makubwa wala mwilini mwake hakuna kipande chochote cha chuma au chenye ncha kali, kwa sasa wanarekebisha mshono aliokuwa nao ambao ndio ulifumka na kumsababishia damu nyingi kuvuja” majibu ya yule Dokta yalishusha presha aliyokuwa nayo awali Shebby kwa kiasi kikubwa na ndipo alipomfata na mama (Zena) kumuelezea lile na kumtoa wasiwasi kisha alimuachia kiasi cha ths laki moja kwa niaba ya dharula yoyote itayojitokeza pale nae aliahidi kurudi baada ya muda mfupi ujao. Alitoka na kuingia kwenye gari huku mawazo yake kichwani yakiwa kwenda kukutana na Cj4 ambae alizidi kumuona mchawi wa mbinu kwa kugundua vitu ambavyo yeye hakuvifikiria.
Lakini akiwa njiani alikumbuka vizuri maelezo ya yule daktari pindi alipotoka chumba cha upasuaji na alipoyafikiria vizuri maneno yake kuna kitu kimoja kilianza kumchanganya na kutoelewa. (“Mshonooo, mshonooo. Mh!! mbona sikumbuki kama Asha aliwahi kuwa na mshono. mshonooo!!.. mshono gani tena huo?!!”) aliwaza Shebby na kujiuliza mwenyewe pindi alipokuwa njiani baada ya kukumbuka vizuri maelezo ya yule daktari.
* * * *
“Huwezi amini Cj yaani kabla hata sijafika kwenye ile nyumba kwa macho yangu nilishuhudia mlipuko upande wa juu na nilipoingia sikuamini hali niliyomkuta nae Asha .. Daaah!! Mr X naamini nitapomuua nitapata thawabu Dah!” aliongea Shebby mara walipokutana kwa siri na Cj4. “Kwa hiyo mchumbaako vipi?” “Mungu amesaidia nimemuacha hospitali kwa matibabu zaidi ila kuna kitu sijakielewa” “Kipi hiko?” “Nimeambiwa jeraha lililokuwa linavuja damu tumboni kwa Asha ni la mshono..” aliongea Shebby kauli ambayo Cj4 aliichekecha harakaharaka na kupata uhakika sasa kua mtoto wa Hussein ambae ni mke wa Kamishna Shebby ndie yule Ninja aliyemsaidia usiku baada ya kuchomwa na kisu cha kininja tumboni hivyo alijua mshono unaozungumziwa pale laima atakuwa amejishona mwenyewe usiku uliopita na kutokana n msukosuko wa bomu umefumka. “Sasa neno Mshono limekuchanganya nini? mbona mi naona kawaida.” alijibu Cj4 kwa kumzunguka Shebby kwani hakutaka kabisa agundue mapema mchumbaake ni nani.
“Sikia Cj, sijawahi kumuona na mshono Asha wala hajawahi kunambia hiko kitu.” “hahahaha, tatizo Shebby unapanik mapema, nataka ukumbuke kuwa mshono unamaanisha sehemu ambayo iliwahi kufumka ikazibwa upya. sasa unajuaje kama kipindi cha nyuma mchumbaako aliwahi kufumka sehemu hizo?” “Mh! sasa ndio uachie na kuvuja damu?” “Inawezekana kishindo kilikuwa kikubwa.. Ila mi nataka nikushauri kuwa fanya jitihada mapema tu umuoe Asha” “Mh! Cj mi naona kwanza tumalize hili la mr X” “Hapana, unajua mr X anatumia akili na mambo yake mengi aliyaeka kwenye mipango kabla hayajatokea. sasa ili akuchanganye anataka kudili kwanza na watu uwapendao. Ndio maana nakwambia muoe kwanza Asha mueke jilani harafu hapo sasa hata mr X mwenyewe utakuwa umeshamzunguka” Ushauli wa Cj4 hakuutarajia kabisa Kamishna Shebby lakini hakutaka kuupinga kwani moyo wake tayari ulikuwa unamuamini sana Cj4 na kumkubali hivyo aliongea na wazazi wake ambao walikubali lifanyike hilo jambo haraka hususani mzee Mwinchande limpongeza mno mwanae kwa maamuzi aliyofikia lakini kwa kile kilichotokea kwa Asha Shebby alizificha taarifa zile nyumbani kwao kwa kuogopa kuwatisha pia kwa kuzingatia ushauri wa awali aliopewa na Cj4 na hata Hussein babu bubu hakuambiwa kilichompata mwanae zaidi ya kuja kusikia habari za nyumba kuwaka moto huku akidanganywa ni kwa shoti ya umeme kipindi ambacho wakazi wote (Zena na Asha) hawakuwepo pale nyumbani.
* * * * *
Siku ileile masaa machache baada ya Shebby kuondoka Asha alirejewa na fahamu wakati huo tayari madaktari walikuwa wamemaliza kumshona vizuri sehemu ile ya chini ya tumbo kulipoachia. Kutokana na kupungukiwa damu ililazimika kuongezewa chupa nne za damu na usiku huo alilala pale wodini huku upande wa Shebby alihaha na kufanikiwa kuwakodia nyumba nyengine nzuri maeneo ya jilani na ile hoteli aliyopngiwa Hussein kwa kujua kuwa pale amewaeka kwenye usalama kwa uwepo wa rada za Cj4.
Baada ya kila kitu kuwa sawa upande wa Cj4 siku hiyo asubuhi na mapema alitoka kinyemela pale alipokuwa anaishi pasi na kumuarifu Shebby na alielekea kule hospitali akiwa amevaa sare zake za kipolisi zilizomtambulisha kama Inspecta na kufanikiwa kuingia wodini kumuona mgonjwa ambae siku hiyo ndio ilikuwa siku yake ya kuruhusiwa. Hakukuwa na vizuizi wala maswali mengi pindi alipotaka kukutana na yule mgonjwa, ila kukaibuka mstuko na taharuki kubwa kutoka kwa yule mgonjwa ambae ni Asha pindi alipokutanisha macho na Cj4 ambae nae alistuka kidogo baada ya yale macho kuyakumbuka vizuri siku ile ya ajali ya kule chalinze ambayo ilipelekea kupoteza kwa maisha mtu muhimu aliyetakiwa kuhojiwa juu ya upelelezi wa kum baini Mr X.
Asha alijitahidi kuificha hali ile ya mstuko wake machoni lakini Cj4 alimgundua vizuri sana na kwake yeye hakuonesha mstuko wowote machoni zaidi ya kumsogelea na kumpa pole kabla hajaanza kumuuliza maswali ambayo Asha alibaki kama bubu asijue aanzie wapi kuyajibu. “Hebu nambie unajua nini zaidi kuhusu mr X, wala usinifiche ila nataka unijuze mr X alikupa neno gani la mwisho pindi ulipoasi?” Aliuliza Cj4 kwa sauti ya chini sana lakini iliyosikika vizuri masikioni mwa Asha na kubaki anababaika aanzie wapi na hapo ndipo Cj4 alipomuachia kikaratasi cha namba za mawasiliano kisha akatoka taratibu na kumuacha Asha ametumbua macho kwa taharuki. (“Khaa! huyu si ndio yule Afande wa Chalinze? kajuaje kama niko hapa? kajuaje mambo yangu na Mr X?”) alijiuliza maswali haya Asha ambayo alijua fika kuwa hakuna mtu wa kumfata moja kwa moja akampa majibu yale bila yeye mwenyewe kuyatafutia ufumbuzi kupitia yule yule mtu.
Baada ya masaa mawili Kamishna Shebby nae alifika pale hospitali na kufanya utaratibu wa kuwatoa na kuwapeleka kwenye makazi mapya aliyowatafutia. “Mama kwa sasa mtakuwa hapa kipindi tunafanya taratibu za kumaliza hili suala la ndoa, nataka Mungu akitujaalia tulifanye hata wiki ijayo” “Wiki ijayo?” “Eeh mama” “Atakuwa kashapona vizuri kweli!?” aliuliza kwa mshangao yule mama kutokana na kuona mambo yamekaa jilani sana tofauti na alivyodhani baada ya Asha kupatwa matatizo “Kwa hilo usijali mama, kama yeye alivyoniuguza na tukakaa wote hadi kuwa wachumba basi nami nitamuuguza tukiwa wote kama mtu na mkewe, naamini Mungu ndie anayetupangia tukutane aktika vipindi vigumu vya mataaizo kama hivi” aliongea Shebby maneno ambayo Zena aliyaelewa na kukubali “Lakini naomba mjitahidi baba asijue kama ana mshono mwanae mtamchanganya” aliwakumbushia nao walikubali jambo lile na Hussein bubu hakuambua kujua ukweli juu ya kilichompata Asha zaidi ya kujua makazi mapya na kuingojea hiyo siku ya kumuoza mwanae kwa udi na uvumba.
Kwa upande wa Asha ilikuwa ngumu sana kwa kumtazama tu ukagundua kuwa ana jeraha mwilini mwake kwa jins vile alivyokuwa anajichangamsha na kujiweka lakini kuna kitu kimoja kilimuumiza akili zake na kuufanya usiku ule wa kwanza kwenye yale makazi mapya kuwa mgumu sana upande wake na si kwa sababu ya kufikiria juu ya ndoa bali ni kwa sababu ya ule ujio wa askali ambae anakumbuka alionana nae siku ile aliposababisha ajali iliyopelekea kifo cha mzee Cypilian. Alishangaa kila alipomuangalia Shebby hakuonesha dariri zozote za kumstukia zaidi alipowahi kumuuliza juu ya mshono kule hospitali nae alijibu aliwahi kweli kufanyiwa upasuaji mdogo wa kidole tumbo (appendex) wiki za karibuni na alifanya siri ili asimtie hofu mamaake na uongo huo Shebby aliuamini kabisa. Usiku huo Asha hakuwa na jinsi ilibidi amtafute hewani yule askali na kweli alipopiga tu zile namba Cj4 alipokea na baada ya kujua anayeongea nae alimuuliza swali lile lile na Asha hakuwa na jinsi ilibidi aongee yote anayoyajua na kumpa lile neno la mwisho aliloambiwa na mr X ambalo lilikuwa sawa kabisa kama alilowahi kuambiwa amwambie Shebby.
* * * *
Mipango ya ndoa ya Kamishna Shebby na Dokta Asha ilizidi kushika kasi kwenye vichwa vya wanafamilia ambapo kwa upande wa mzee Mwinchande na mkewe ilikuwa ni zaidi ya furaha na walifanya utaratibu na kuongea na sheikh mkuu wa jiji la Dar ndie aje kuwa mfungishaji Ndoa hiyo ambayo Mwinchande alipania kuifanya iwe ya kipekee sana japo mipango yake ilikuwa ni ya muda mfupi.
Na hatimae baada ya maandalizi yote kukaa katika mstari (kuwa sawa) Kamishna Shebby alikutana tena kwa siri na Cj4 siku moja kabla ya ndoa kwa maongezi maalum. “Sikia Shebby, kesho ni siku kubwa sana na muhimu katika kujua muelekeo wa Mr X” aliongea Cj4 “Kivipi kiongozi” “Kumbuka neno la mwisho la mr X uliloambiwa na yule Ninja.” “Yap nakumbuka lile fumbo” “sasa kwa kuwa kesho kutakuwa na wageni wengi kwenu wanaokutambua nina wasiwasi kutakuwa na ugeni wa Mr X pia kwa kuwa anakutambua. Na hii ndio inanifanya na mimi kuja kwenye hiyo sherehe lakini hakuna atayejua kama nimekuja zaidi yako lakini pia nawe hutoniona kama nimekuja lakini nitakuja.” alichanganya maneno Cj4 na kumfanya Shebby akubali lakini asijue maana halisi ya maneno yale zaidi alipata picha kuwa kuna uwezekano kweli mr X akahudhulia hiyo sherehe au akatuma mtu wake kwaajili ya kuwamaliza katika hiyo sherehe ya harusi iliyotarajiwa kufanyika kesho yake.
“Kitu chengine Shebby umepangaje kuhusu Hussein akitoka hapo hotelini?” aliuliza Cj4 “Nimepanga nikamnunulie nyumba sehemu salama.” alijibu Kamishna Shebby kauli iliyopingwa na Cj4 “Hapana Shebby, hakuna nyumba iliyo salama kwa Hussein kabla ya kifo cha Mr X” “sasa Unanishauri vipi kiongozi” “Inabidi ukae na wazazi wako uwaombe waishi na Hussein pale kwenu kidogo hiyo itakuwa salama kwake” “Kwa hiyo unananambia Hussein akaishi nyumbani ndo itakuwa salama?” “Ndio hivyo nionavyo” “Sio kama nitasogeza maadui wanaomuinda nyumbani?” “Hapana Shebby, hiyo ndio njia ya msingi” “sawa kiongozi” Kamishna Shebby alikubali tena swala la pili lililotolewa na Cj4 na kuagana huku wakitakiana kila la kheri hiyo kesho yake ambapo Cj4 atakuja kwa ngazi maalum ya kuwachunguza wageni wataofika ili apate kumtambua Mr X.
* * * * *
Wageni na viongozi mbalimbali waliendelea kumiminika katika ukumbi maalum uliokodiwa kwa niaba ya sherehe za kuwapongeza bwana Shaaban Mwinchande na bibi Asha Hussein kwa muungano wao wa kimwili na kuwa kitu kimoja kama ilivyo katika maandiko yaani mke na mume.
Ilikuwa ni majira ya saa kumi jioni mara baada ya ndoa iliyofungwa majira ya saa nne asubuhi katika Msikiti mkubwa kabisa jijini chini ya Sheikh mkuu. Ilikuwa ni furaha sana kwa kila mtu hususani Hussein yeye muda wote alikuwa na leso akifuta machozi kwa kutoamini kama leo amefanikiwa kumuoza mwanae kwa mtu ambae alitokea kuwa chachu ya yeye kutolewa jera. Ilikuwa ni furaha kwenye sherehe ambayo kweli ilikuwa ya kipekee na wageni walikuwa wengi sana kuanzia viongozi wastaafu waliokuwa na urafiki mkubwa na mzee Mwinchande miaka hiyo pamoja na viongozi wa usalama hususani jeshi la polisi na magereza. Bila kusahau wageni wengine tu waalikwa ambao wao hawakuwa na wadhifa wowote nchini.
Akiwa amekaa upande maalum kulipotegwa kwa wazazi wa kiumeni na wale wa kikeni Hussein muda mwingi alikuwa na furaha lakini kila anapogonganisha macho na mamaake Kamishna Shaaban alijikuta anapata mshtuko muda mwengine ambao hakujua unatokea wapi lakini alikuwa anaupotezea. Kuna wakati hasa ule wa kula keki na kupiga picha ndio kabisa Hussein alizidi kuushangaa moyo wake kuongeza mapigo kila anapoangaliana na yule mama hasa wakati walipokaa pamoja na mzee Mwinchande, Zena na yule mama Shaaban alijikuta kama anatamani kumuuliza kitu lakini hakujua ni kitu gani na kuishia kujichekesha tu.
kulikuwa na wapiga picha waalikwa tofauti tofauti kwenye ule ukumbi na mmoja wapo kati ya wale wapiga picha alikuwapo Cj4 ambae ilikuwa ni vigumu sana kutambulika kwa mtu yeyote aliyekuwa anamjua hapo kabla kwa ule muonekano alioingia nao pale. Hata Shebby alipokaa na mkewe jukwaa kuu kusikiliza nasaha za hapa na pale kutoka kwa wazazi na watu wengine, macho yake muda mwingi yalikuwa yanaangaza huku na huko ndani ya ukumbi kwa lengo la kumuona Cj4 lakini hakufanikiwa kumgundua japo alikuwa jilani nae muda wote kwani wapiga picha walikaa mbelembele ya eneo la tukio ili kuweza kuchukua na kupiga picha vizuri.
Muonekano wa Cj4 siku hiyo alikuwa na Mustachi mkubwa tu sambamba na miwani ambayo kwa nje ni kama ya macho lakini haikuwa hivyo na hata mustach aliokuwanao ulikuwa wa bandia. Alichokuwa anafanya kwa kutumia ile kamera Cj4 ni kurekodi video huku akiwachukua karibu wageni waalikwa hususani wale wastaafu wote nia na madhumuni pindi atapoondoka akirudie kuikagua kwa umakini ile video apate kumjua mr X kwani aliamini kivyovyote mr X lazima angekuja mwenyewe sehemu ile ya ukumbi na iwapo atakuja basi amani itatawala lakini iwapo mr X asipokuja aliamini kuna tukio lolote lingeweza kutokea hivyo muda wote alikuwa makini kwa hayo yote mawili Cj4.
Kwa jinsi mambo yalivyoenda vizuri pale ukumbini hakukuwa na aliyegundua wala kuhisi kama yule bibi harusi ana jeraha la mshono tumboni na hiyo ilibaki siri ya watu wachache tu japo wengi walisikia tukio la kuungua kwa nyumba ya Dokta Asha.
* * * * *
Sherehe ziliisha majira ya usiku sana na kutokana na sababu maalum fungate la Shebby na Asha lilipangwa kufanyika palepale kwenye Jumba kubwa la kifahari la mzee Mwinchande. Nyumba ile nyengine aliyokodi Shebby ililipiwa na kukabidhiwa Zena kuwa nyumba yake huku kwa upande wa Hussein bubu alijumuika pamoja na wazazi wa Kamishna Shebby kwaajili ya makazi ya muda pale kwenye jumba la Mwinchande kipindi ambacho Kamishna Shebby atapokuwa anamtafutia makazi rasmi ya kudumu.
Alfajiri na mapema ndani ya jengo la mzee Mwinchande kwa mara ya kwanza Hussein bubu alijiona kweli yuko huru mara baada ya kulala katika chumba kikubwa chenye mandhali ambayo hajawahi hata siku moja kulala tokea kuzaliwa kwake mpaka pale alipofikia. Usiku huo alimshukuru sana Mungu kwa yote yaliyoendelea na aliendelea kumuomba kama ilivyokuwa kawaida yake kuwa amsaidie aweze kumtendea muujiza alipe kisasi kwa kumuua Mr X kwa mikono yake. Japo kwa akili ya kawaida ilikuwa ni kazi ngumu na ni kitu kama cha kufikirika tu kutokana na wengi waliokuwa mashupavu na uwezo wa vita kushindwa walau kumjua mr X sembuse Hussein ambae kashaanza kujiishia umri umemtupa mkono harafu aweze kumuua? Lakini kwa Mungu Hussein aliamini hakuna linaloshindikana aliamini kabisa imani thabiti na kumuomba kila siku japo alijua kuua ni dhambi lakini kwa dhambi ya kumuua Mr X aliiomba na kuikubali kwa moyo mmoja kuliko kumuacha hai.
“Aslaam alaykum” alisalimia mzee Hussein asubuhi ile pindi alipotoka na kumkuta Mzee Mwinchande upande wa sebuleni ambapo alikaa kwenye mswala akisoma qur’aan baada ya kusali sala ya alfajiri. “Waaleikum salaam warahma tullah wabarakatul” alijibu kiurefu kabisa Mzee Mwinchande kwa rafudhi maridhawa ya kiarabu kuonesha jinsi gani dini imelala kwenye ubongo wa Mzee Mwinchande. Moyoni Hussein alijisikia faraja sana kukutana na familia ya wacha Mungu kama ile na akiwa maeketi kwenye moja ya sofa akimtazama babaake Kamishna Shebby akisoma qur aan kwa utulivu kabisa na kumliwaza Hussein japo alikuwa hajui tafsiri yake na alipata imani ya kumuelewa vizuri Kamishna Shebby kwanini kawa mtu tofauti mwenye roho nzuri, kumbe kwa sababu amelelewa na watu wenye imani na kuishika dini. Akiwa ametabasamu pale sebuleni mara alimuona kwa mara nyengine mamaake Shebby ambae rich ya kwamba nae umli kidogo ulisogea lakini pindi anapokutanisha nae macho moyo wake unastuka sana na hadi muda mwingi alipuuzia na hakujua kwanini lakini safari hii asubuhi mara tu aliposikia sauti ikimsalimia na kuinua kichwa chake kuitikia huku akimtazama akili yake ilimletea picha iliyomfanya apigwe na bumbuwazi hadi yule mama alishangaa. Alitamani kumuuliza kitu palepale lakini ulimi wake ulikuwa mzito na kubaki kimya lakini akilini tayari ilikuja picha ya mwanamke aliyewahi kumpenda miaka mingi. Picha ya mwanamke aliyemuamini kupita kiasi. Picha ya mwanamke aliyeweka doa katika historia ya maisha yake mpaka kufikia pale alipo. Picha ya mwanamke huyo iliyomjia akilini haikuwa picha ya mwanamke yeyote mwengine bali ni picha ya Zainabu. Mwanamke aliyeuteka moyo wa Hussein na kumuonesha mapenzi ya dhati yaliyomfanya awali Hussein ajione yeye ndie mwanaume bora kuliko wote lakini mwisho wa siku mwanamke huyo ndie aliyekuja kutoa kauli iliyomfanya Hussein miaka yote abaki na imani kuwa wanawake ni wauaji. Alimtazama mama Shebby mke wa mzee Mwinchande na kwenye macho yake aliweza kuiona taswiera ya Zai wake aliyesingiziwa alimuua mwenyewe sambamba na mtoto wao wa kiume ambae aliushuhudia mwili wake ukiwa umekatwa kichwa na viganja ambavyo vilikutwa mifukoni mwake. Lakini hata hivyo aliamua kulipotezea lile wazo kichwani na kumuomba Mungu kimoyo moyo amuondolee akili ya kumuwaza sana Zai kwani kuna muda aliamini kabisa Zai amekufa lakini kuna muda pia hakuamini na alihisi kuwa Zai hajafa ila waliyemuulia pale ni mtoto wake kipenzi aliyekuwa na miezi mmne tu. Lakini japo alijitahidi kupotezea bado kuna vitu akiviona kwa yule mama ambae yeye hakuonesha kumjua Hussein hapo kabla hata kidogo, vilimfanya amkumbuke sana Zai mke wake na kitu kikubwa kwanza ni uvaaji wa Kiremba. Jinsi ambavyo alikuwa akimtazama mama Shebby ule ufungaji wake kiremba cha kitenge ulimfanya pia amkumbuke sana Zai ambae nae alipenda sana kufunga kiremba tena kwa mtindo wa kipekee ambao wengi walikuwa hawafungi vile na ajabu mtindo ule wa mkewe Zai kwa mara nyengine aliukuta kwa mama Shaaban. Kitu cha pili kusoma (kuimba) qaswida hasa nyakati za asubuhi. Hili nalo aliligundua kwa mama Shebby siku hiyo asubuhi alipoonana nae tena na kumshangaa kupita kiasi alikuwa anatembea huku akiimba qaswida jambo ambalo hata mkewe Zai ndio alikuwa analipenda sana. Lakini mbali na sababu hizo pia kulikuwa na sababu nyengine akizifikiria zinamkatalia kuwa mama Shebby si Zai na moja ya sababu hizo ni umri wa Shebby ambae uliandikwa kwenye daftari maalum siku wanafungishwa ndoa kuwa Asha alikuwa na miaka 29 anakaribia 30 jambo ambalo lilikuwa sahihi kabisa kwani alipokuwa anapelekwa jera baada ya kuhukumiwa barua ya mchumbaake wa zamani Mariam ilionesha kuwa tayari Asha ana miaka mitatu na yeye amekaa miaka 26 gerezani. Lakini kwa upande wa Kamishna Shebby yeye umri wake ulionesha ni miaka 28 jambo ambalo lilikuwa tofauti kabisa kwani miaka hiyo 28 ndio kwanza alionana na Zai Arusha na hakuwa na mtoto wala hata alivyokutana nae mwaka uliofuata baada ya kushinda mitihani aliyopewa na Zai alimkuta ni bikra yaani yeye ndie alikuwa mwanaume wake wa kwanza kwa hiyo aliamini wazi kuwa Zai hakuwahi kuwa na mtoto mwenye umri mkubwa kama Shebby kwani mtoto wao kipenzi wa pekee aliyezaa na Zai alichojua aliuawa miaka 26 iliyopita. Kwa kigezo cha umri wa Shebby kilimuondoa kabisa kwenye mashaka ya kumfananisha mamaake Shebby na aliyewahi kuwa mkewe ambae bado hakuwa na uhakika kama alikufa au mzima bi Zainab.
* * * * *
Usiku baada ya sherehe zile kuisha na watu wote kutawanyika alionekana Cj4 ambae alikuja na pikipiki moja iliyomtambulisha kama mpiga picha kutoka ofisi ya wazili wa mambo ya ndani na hata kitambulisho alichokuwa amevaa kilionesha hivyo na kila aliyemuona aliamini hivyo kutokana na kumtambua muhusika wa kile kitambulisho na muonekano wa Cj4 hakuna aliyemtilia hofu hadi wakati anaondoka pale ukumbini.
Safari yake ilimpeleka hadi sehemu moja pembeni ya barabara kulipokuwa na daraja na kusimamisha pikipiki ile nyuma ya gari moja ndogo iliyokuwa imeegeshwa pembeni na kushuka lakini aliachana na ile gari yeye alienda moja kwa moja hadi chini ya barabara uvunguni mwa lile daraja ambalo lilikuwa limekauka maji, na alipotoa simu yake ya mkononi kumulika mule uvunguni alionekana mtu mmoja ambae alifanana nae sana jinsi alivyojiweka, akiwa kafungwa kamba mikono na miguu huku mdomoni kazibwa na plasta kubwa. “Good mr, kazi imeisha kama nilivyokuahidi siwezi kukudhuru kwa kuwa mimi si mtu m baya ila ukitaka kuujua ubaya wa mtu upoje uende ukatoe siri kuwa aliyekwenda kwenye ile sherehe ya harusi hukuwa wewe.” aliongea Cj4 na kumtoa plasta ile iliyokuwa mdomoni mwa yule jamaa aliyekuwa na kitambi kiasi sambamba na mustachi mkubwa. Alibakia anahema tu yule bwanakipindi Cj4 akimfungua zile kamba na alipomaliza alimrudishia kitambulisho chake sambamba na funguo ya pikipiki kisha akatoa memory iliyokuwa ndani ya ile kamera na kumkabidhi kamera tupu. “Zingatia ndugu niliyokwambia” aliongea Cj4 na kutoka mule darajani huku yule bwana akiwa amesimama haamini hadi pale aliposikia gari ikiwashwa na kuondoka ndipo nae alipotoka mbio kule na kuwasha pikipiki yake na kuondoka.
Baada ya kufika ndani ya chumba chake alichokodi kwenye ile guest Cj4 alianza kubadilisha muonekano wake kwa kuondoa ule mustach wa bandia na kuanza kubambua mfuko wa plastik maalum uliobanwa tumboni mwake na kumuonesha kama aliyekuwa na kitambi cha wastani pindi alipovaa shati ile kubwa sambamba na kikoi.
Mara baada ya kumaliza kupambua vitu vya bandia mwilini mwake ndipo alipotumbukiza ile memory kwenye compyuta yake na kufungua mafaili ya video alizoshoot kwenye ile sherehe ya harusi ya Shebby ndipo kwa umakini mkubwa Cj4 alianza kufatilia matukio na nyuso za watu aliokuwa anawachukua ili kuhakikisha na kubaini kwa mbinu zake za kikomando kati ya wale wageni waliohudhulia pale nani alikuwa Mr X.
Alitulia kwa umakini mkubwa Cj4 kutazama yale matukio yaliyokuwa yanaendelea kipindi cha shughuli ile lakini kadri alivyokuwa anaangalia bado hakuona tofauti kwa mtu yeyote wala kupata taswira nani kati ya wale watu waliokuwepo kwenye ile shughuli ni Mr X? Aliangalia hadi mwisho bila kumuhisi mtu yeyote aliyeoneka kuwa na utofauti furani ambao ungemsaidia kumtambua mr X na ndipo alipoamua kuianzisha upya safari hii akipunguza speed ya utembeaji wa picha na kueka ule wa taratibu na kiminato (slow motion) Aliangalia tena kwa umakini mno wakati huo kila hatua aliyoichukua na mwishoe aliimaliza tena hadi mwisho bila kupata picha wala taswira ya kumjua huyo mgeni aliyeamini kuwa lazima atakuwepo kwa kuwa kauli za mr.X zenye mafumbo mazito kwake Cj4 aliweza kuyatatua kiasi yale mafumbo na kujua lazima Mr X atakuwa kwenye mzunguko wa maisha ya Kamishna Shebby iwe katika ngazi ya jeshi la polisi ama kwa marafiki wakuu wa babaake mzazi mzee Mwinchande kutokana nae alikuwa ni moja ya askali wakubwa enzi hizo hivyo alikuwa na mtandao wa karibu na watu wengi ambamo Cj4 aliamini lazima miongoni mwao atakuwa ndie Mr X.
Lakini safari hii alipofika mwisho kuna kitu kimoja alikiona akagundua hakipo sawa. Hapo ndipo alipoanza kurudisha nyuma na kueka slow motion zaidi vile vipande vya Hussein bubu na kuna kitu akaanza kukibaini na kukitilia shaka. Ni vile Hussein muda mwingi alionekana alikuwa anamuangalia sana mamaake Kamishna Shebby tena kwa kumuiba iba. Alikaa vizuri Cj4 na kumzoom Hussein sehemu za macho yake na kugundua kuwa kuna kitu alikuwa anakifikiria ama anakifananisha kwa jinsi alivyokuwa anamtazama mamaake Kamishna Shebby. (“Mh! hapa hapa ndipo pa kuanzia.”) alijiambia akilini Cj4 na kumsogeza kwa karibu mamaake Kamishna Shebby sehemu za uso na kumplay katika slow motion kumchunguza vile alivyokuwa anamuangalia Hussein na hapo napo kuna kitu alikisoma kuwa mama Shebby hakuweza kabisa kumuangalia Hussein hata kwa sekunde kumi, na mara alipogonganisha macho na Hussein aliyakwepesha kiujanja na kugundua sehemu alipoyaelekeza ni upande aliokaa mumewe ambae ni babaake Kamishna Shebby. “Mh!” Aliguna Cj4 na sasa alianza kumzoom babaake kamishna Shebby ambae ni mzee Mwinchande lakini kila alivyoitafuta tofauti yoyote kutoka kwa mzee Mwinchande kwa kile alichokiona kwa Hussein na mama Shebby hakuweza kuona chochote kutoka kwa Mwinchande. Alimueka katika slow motion ile ya chini kabisa lakini muda wote aligundua kuwa mzee Mwinchande alikuwa na furaha na muda mwingi alionekana yuko bussy na kile kilichokuwa kinaendelea ukumbini hususani kuwatzama bibi na bwana harusi.
Alirudia tena Cj4 kwa upande wa Hussein na mama Shebby walivyokuwa wanapelekeana macho na hapo aliikumbuka vizuri story ya Hussein juu ya maisha yake yaliyopita mpaka anaingia jera na kuanza kupata hisia inawezekana Hussein akawa anamfananisha mama Shebby na mkewe ambae ilisemekana alimuua. “Hapa hapa kuna alama ya Mr X.” alijisemea mwenyewe Cj4 lakini kila alipotaka kumshuku babaake Shebby alijikuta moyo unakuwa mzito kukubali japo akili ilianza kumpeleka huko. (“Inawezekanaje huyu akawa ndie mke wa Hussein? Mh! ila pia inawezekana na kama ndio nina mashaka na babaake Shebby akawa ndie Mr X. ilaaaaa…. Agh! Nina wasiwasi na hapa hapa”) aliwaza na kujisemea moyoni Cj4 na kujilaza kitandani wakati huo tayari ilikuwa alfajiri. “Mzee Mwinchande upo katika mstari wangu wa mashaka. Hii sasa itakuwa mission yangu peke yangu.” alitamka maneno haya Cj4 na kueka nia sasa mtu atayedili nae katika kumchunguza ni baba wa Kamishna Shebby ambae ni mzee Mwinchande, na hili alipanga kulifanya bila kumwambia hata Kamishna Shebby ambae ndie aliyekuwa anashirikiana nae katika mission zao za siri juu ya kumtafuta na kumnasa Mr X.
* * * * *
“Ibada ni jambo jema sana mzee mwenzangu.” “Kweli kabisa.” “Mwenye kufanya ibada hujieka jilani na Mungu na kujilinda na Sheitwaan” “Naam.” “Mimi na mke wangu kama unavyotuona, sisi ni waislam safi kabisa na kila siku tunafanya ibada na ndio sababu nyumbani kwetu kuna amani na ndoa yetu imedumu miaka mingi.” “Daah! kweli kaka hongereni sana.” “Ahsante lakini hata wewe si mzee kama unaamua.” “Kuamua kivipi kaka.” “Amua uoe ili upate utulivu si unajua ng’ombe hazeeki maini?” “KUOA!? hahahaa hapana kaka mimi maisha yangu nitayamalizia hivi tu.” alijibu Hussein bubu huku kipindi akizungumza na Mzee Mwinchande pale sebuleni majira ya mchana.
Mzee Mwinchande alikuwa anamuelezea Hussein habari nyingi nzuri na jambo kubwa alikuwa anamsisitiza juu ya imani yake kwa Mungu. Maneno ya mzee Mwinchande yalizidi kumfanya Hussein amsome kuwa ni mtu mmoja mzuri sana na moyo wake ulifanana na wa Kamishna Shebby kwa vile alivyoonekana mwenye kujali na kuthamini wengine. “Hivi unajua vizuri kusali?” aliuliza mzee Mwinchande “Mh! hapana kiukweli nimesahau dua nyingi sana za kusoma wakati unasali” alijibu Hussein bubu. “Basi mi nataka kuanzia leo uwe unajiunga nami tusali pamoja hususani alifajiri na usiku ndio mida mizuri sana kusali na kuomba” aliongea mzee Mwinchande huku akipekua chini ya screen kubwa iliyokuwa ukutani pale sebuleni ambapo kwa chini kulijengewa kama kikabali maalum cha kuhifadhia vitabu na hapo alitoa kitabu kimoja kilichoandikwa SALA NA MAFUNZO YAKE, kisha alimkabidhi Hussein. “Hiki kitabu kitakusaidia sana katika kujua kusali sala zote za kiislam.” “Asante sana kaka, daah! Nashukuru kwa kweli kwa kuonesha kunijali.” alijibu kiunyenyekevu Hussein wakati huo mke wa mzee Mwinchande alikuwa anashuka ngazi akitokea sehemu za juu ya nyumba yao na kama kawaida yake Hussein alipokutanisha tena macho na mama Shebby moyo ulimripuka tena na safari hii kuna kitu chengine alikiona ambacho kiliustua zaidi mtima wake.
Alibaki amemkodolea macho mama Shebby ambapo kikubwa alichokuwa anshangaa Hussein ambacho alikigundua ni alama ya baka la mstari mweusi juu ya paji lake la uso eneo lilipoanzia nywele kuota. Alama hii safari hii aliiona vizuri baada ya ushungi aliojifunika mke wa mzee Mwinchande (mama Shebby) kufunuka bahati mbaya na alikuwa hajavaa kiremba kama ilivyokuwa kawaida, na hata chanzo cha kuvaaga kiremba Zai ilikuwa ni kwasababu ya kuficha baka la mstari pale juu ya paji la uso ndio maana ufungaji wake Kiremba ulikuwa wa kipekee sana, sasa imekuaje na mama Shebby nae awe na mitindo ya kufunga kiremba kama Zai harafu kumbe na yeye ana baka la mstari mweusi?
(“Mh! hapana sasa nina wasiwasi”) alijisemea moyoni Hussein na kumuaga kwanza mzee Mwinchande akizuga kwenda chooni lakini ukweli hakuwa na haja yoyote zaidi alienda kukaa kufikiria kile alichokuwa amekiona pale nyumbani kwa mkwewe Kamishna Shebby. (“Inakuaje kuaje mama Shebby afanane vitu vingi na mke wangu Zai? au ni kweli yeye huyu! Eee Mungu naomba unisaidie nipande ufumbuzi wa uhakika wa hili suala”) aliwaza na kuomba kimoyo moyo Hussein pindi alipokuwa chooni akilifikiria sana lile jambo na alijaribu kukumbuka mambo mengi aliyokuwa anayapenda mkewe Zai kipindi hiko ili iwe rahisi kuzidi kuyapima na kuyafuatilia kwa mama Shebby kama kuna uwezekeno wa kufananisha mambo mengine zaidi. (“Mh! lazima nifanye hivi nione, ina maana kama kweli huyu ni yuleyule Zai mke wangu basi naamini babaake Shebby ndie adui angu Mr X mwenyewe. Mh!! lakini sasa mbona babaake Shebby haoneshi hata chembe kama ana moyo m baya? hafanani hata kidogo na vitendo vya mwana izaya Mr X.”) aliendelea kufikiria Hussein na hatimae alitoka kule chooni na kurudi sebuleni alipokuwa Mzee Mwinchande na kuendelea na maongezi yao. “Basi inshaallah mzee mwenzangu, wewe tulia kisome kwa umakini sana hiko kitabu tuwe tunajumuika wote hapa kuswali suna za usiku na faradhi ya alfajiri” “Nashukuru kaka, usihofu.”
* * * *
Siku zilienda huku fukuto likizidi kufukuta kifuani na kichwani mwa Hussein juu ya kumtilia mashaka siku baada ya siku mama Shebby ambapo safari hii kila ile tabia sugu aliyokuwa anaikumbuka kuwa Zai alikuwa nayo alibaini kuwa hata mamaake Shebby alikuwa nayo na hii ikazidi kumpa uhakika wa asilimia nyingi kuwa akitafutacho ndicho akionacho. Lakini uzito wa kuamini hilo unakuja pale kila jinsi alivyomtazama mzee Mwinchande alkuwa hafanani kabisa kuwa ni mtu mwenye moyo wa kikatiri na roho mbaya kama alivyo mr X kwani kama kweli mamaake Shebby ni Zai basi bila shaka babaake Shebby ni Mr X na hata akiwa siye bado Zai atajua wapi alipo kwa kuwa katika maneno ya mwisho ya mke wake Zai kabla hajapoteza fahamu baada ya kupigwa na kitu kizito siku ile walipovamiwa na Ninja wa mr X pindi walipokuwa wanaelekea kwa baba mkubwa ambae alikuwa mganga mzee Mnyungunyungu. Lakini bado swali lengine lilikuja kichwani mwa Hussein bubu kama basi yule atakuwa Zai harafu yule mzee Mwinchande asiwe Mr X hivi usalama wao ungekaakaa vipi miaka yote hadi wanafikia pale wakati yeye tu aliponzwa kwa kuishi na Zai tena alikuwa mkewe kabisaa lakini bado Mr X alimfanyia matukio makubwa na wote waliokuwa na habari walau za tetesi kuhusu mr X waliuawa. Sasa inakuaje kwa mtu anayejua kila kitu kuhusu mr X akaachwa hai hadi muda ule wakati mr X mwenyewe bado yu mzima?
Maswali yalikuwa mengi sana kwa Hussein babu bubu na kila alipoamka na kuwa anasalishwa na mzee Mwinchande yeye mawazo yake yalihama kabisa akiwa haamini kile akifikiriacho na mara akawa anaamini lakini bado akawa anaomba Mungu azidi kumpa uyakinifu zaidi katika lile swala na kila siku alitamani kumuuliza mama Shebby jina lake harisi ni nani lakini alishindwa wala hakujua aanzie wapi. Baada ya siku saba fungate la kinyumbani nyumbani la Dokta Asha na Kamishna Shebby liliisha na kufanikiwa kuondoka na mkewe kuishi kwele yale makazi aliyoandaliwa na serikali kule karibu na gereza ambapo kulikuwa na nyumba za kisasa zilizojengwa na serikali kwa niaba ya makamishna wote nchini. Na ulipotimu ule usiku ambao Shebby aliondoka Hussein bubu alipatwa na ndoto ya maajabu sana……..
””””’ (^^”Tumuue tu mke wangu.^^”) ((“^^ Hapana mume wangu kwa adhabu ya awali imetosha mbonaa!?^^”)) (^^”Hapana mke wangu atatusumbua huyu tusipofanya haraka.”^^) ((“^^Mh ! sidhani kwani wewe unatakaje^^”) (^^”Vizuri, chukua dawa hii ujitahidi ifike kwenye chakula atachokula au maji atayokunywa hapo ataanza kumung/unyuka taratibu na hatochukua miezi mitatu atakufa”^^) ((“^^Haya ila moyo unaniuma daah!^^^”)) (^^”Usiumie Zai mke wangu”^^) ””””” “Hee!” alikurupuka Hussein mara baada ya kumuota mama Shebby na mzee Mwinchande wakijadili suala la kumuua. Alikaa kitandani huku akihema na kuifikiria ndoto ile na pale pale lilimjia wazo atoke anyate kuelekea juu chumbani kwa mzee Mwinchande na Zai lakini hakujua aende kufanya nini ila alijikuta moyo unamsukuma atoke aende huko. Aliangalia saa ilikuwa ni saa saba za usiku ndipo alipoanza kufungua mlango na kunyata taratibu kuelekea kule juu kulipokuwa na chumba cha mzee Mwinchande na mkewe. Katika hali ya ajabu na mshangao mkubwa Hussein pindi alipokaribia tu kumbe muda huo mzee Mwinchande na mkewe walikuwa hawajalala wala hawakuwa chumbani zaidi walukuwa kwenye korido moja ya kisasa pale juu iliyotengenezwa kwa niaba ya kupumzika na kula kipupwe cha upepo wa bahari. Kilichomstua zaidi Hussein si kutolala kwao bali ni maneno waliyokuwa wanaongea.
“Unaona Zai mke wangu, hii picha ya video ni siku ilee, hapa nahisi ndio alikugundua na kujifanya anaenda chooni kujisaidia kumbe kufikiria tu kwa kile alichoanza kukihisi. Nilikwambia mapema mke wangu, sasa acha kwanza nimpofue ili iwe rahisi kumpoteza jumla” aliisikia vizuri kauli hii ya mzee Mwinchande iliyomfanya agande kwa mshtuko wa hasira na maumivu ya ajabu baada ya kujua ukweli sasa kumbe yule ni kweli Zainab mkewe na mzee Mwinchande ni Mr X. Alianza kunyata taratibu Hussein bubu huku mapigo yake ya moyo yakienda kasi kupita kawaida akiwa haamini kabisa kama kweli leo hii amemtambua adui yake kwa mtindo ambao hakuwahi kuufikiria hata siku moja wala kuuota. Alifanikiwa kufika mwisho wa ngazi taratibu na kuendelea kunyata kwa umakini mkubwa na kilichomsaidia zaidi alikuwa pekupeku ambapo mara alipofanikiwa kuukuta mlango wake na kuingia ndani tu aliufunga taratibu na ndipo alipofanikiwa hata kushusha pumzi ambayo alikuwa kaibana muda wote alivyokuwa ananyata kurudi mara tu aliposikia sauti ya mzee Mwinchande na mama Shebby ambae sasa aligundua kuwa ni Zainab yule yule mke wake wakijadili juu ya kumuua.
“Uuuuuphhhhhhhhh” Alihema kwa nguvu Hussein huku akiwa kaegemea ukuta wa pale chumbani pindi alipoufunga mlango na kujikuta akisota kwa mgongo taratibu mpaka akakaa kitako pale chini huku mikono kiwa ameiweka kichwani. (“Heeee! Mungu kumbe muda wote niko katika chaka la Simba mla watu aliyevaa ngozi ya kondoo? hapana aaa uuupphhhh”) aliongea moyoni Hussein huku machozi yakimtoka akiwa anasugua sugua mikono kwa nguvu pale chini lakini mara aligundua kitu kilichomfanya ainuke haraka na kuzima taa kisha kujilaza kitandani moja kwa moja na kujifunika mwili wote. (“Huyu ni mshenzi mwenye mbinu nyingi sana, kama aliweza kunitegea kamera chooni nadhani hata humu chumbani kamera haikosi, sasa hapa inabidi niwe makini kabla hajawahi kunistukia kama nimemstukia ili niweze kumuua kiurahisi. Lakini nitamuua ua vipi mshenzi huyu? Aaaah.. Kivyovyote lazima nimuue. Naamini Mungu aliyeniotesha haya na kunnikutanisha nae ndie atayeniongoza na kunionyesha njia rahisi ya kummaliza huyu mshenzi loh! Kumbe mr X ni babaake kijana aliyenisaidia kutoka jera? au isije kuwa ndie Mwinshehe wangu?”) aliwaza Hussein na kufika mbali zaidi mara alipotia shaka isije kuwa na Kamishna Shebby akawa ndie Mwinshehe, jina la mtoto wake alieuawa akiwa na miezi minne tu.
(“Zainabu…Zainabu…Zainabuu Mke wangu kumbe hukufa? aaaagh! Wanawake ni Wauaji kweli aaaaagh, au kwa sababu uliniona masikini Zai, si ungenambia tu nikuache uende salama nami nibaki salama…!!! Aaaaagh! Eeeeh Mungu kwaniniii Kwaniniiiiiiiii??!!!”) aliendelea kusema na moyo wake Hussein huku machozi yakimtoka mfurulizo na moyo kumuenda mbio kupita kawaida. Mwili wote wa Hussein bubu ulibadilisha homon ghafra na kuanza kutetemeka kwa hasira mithili ya mgonjwa wa homa aliyemwagiwa maji ya baridi.
(“Aaaagh! Zaiiii…Zaiii… Zaii!!!!? siaminiiiii aaaaaaaaaaaagh. Wanawake ni Wauaji….. Wanawake ni Wauaji….. wanawakeeeee!?”) (……………………..) (…………………..) (……) (…”Zai ulijua kumbe ile barua ni ya nani lakini ulikanusha Zai? aaagh! Ulinipa moyo nipuuze kumbe kila kitu ulijua… aaagh! umemgeuka mumeo kwa ajili ya tamaaa kwa mtu baradhuli na katili kama huyu? Eti Mr X. aaaaagh! Samson alimuamini Delila kuwa mwanamke anayempenda bila kujua kumbe Delila anatumiwa kumchunguza na maadui zake. Yaliyokuja mkuta Samson mwanaume yeyote kweli yanaweza kumkutaaa. Zai!!!? Lazima nawe ufe”) Uchungu na mawazo aliyokuwa nayo Hussein uliendelea hadi pale alipostuliwa baada ya mlango kugongwa. “Nani?” aliuliza Hussein kwa sauti iliyojaa mikwaruzo. “Swalaaa swalaaa.. Salaaa. swala ni bora kuliko usingizi” aliisikia sauti ya Mzee Mwinchande akimuamsha waende wakasali na kugundua kuwa tayari ilitimu alfajiri. (“Kum**aako lazima Nikuue Mshenzi wewe.”) aliongea moyoni kwa hasira na kushuka pale kitandani hussein na kuwasha taa ili ajiandae kwaajili ya kuungana na adui yake katika kumuomba Mungu (kusali) pamoja.
* * * * *
“Mme wangu, mme wangu Nakupenda sana” “Hata mimi nakupenda sana mke wangu Asha” “Lakini sidhani kama nastahili upendo huo” “Kwanini usistahili sasa! Unastahili kabisa na una haki nikupende zaidi ya hapa” “Kweli?!” “Kweli kabisa mke wangu. Kwanini unaniuliza hilo?” “Kwa sababu nina wasiwasi.” “Wasiwasi!!? wasiwasi gani tena mke wangu.. Ondoa wasi kabisa Asha siwezi kuja kukutenda kwa mwanamke yeyote yule. Kwako mimi nimefika kabisa kama ni meli imetia nanga.” “Najua ni rahisi kusema hivyo kwa sasa, lakini sidhani kama kila siku utasema hivyo. Naamini kuna siku utanichukia kupita kiasi na nina wasiwasi utaniua.” “WHAT!!?”
Alistuka Kamishna Shebby baada ya kusikia kauli ile ya Asha pindi walipokuwa wanazungumza alfajiri ile wakiwa kitandani. “Asha baby, mbona leo umeamka ukiwa na maneno makali sana?” “Kwasababu ya maumivu baby” “Maumivu? yapi tena” “Ya mshono tuu” Alizuga Asha pindi alipotaka kumwambia ukweli Kamishna Shebby juu ya yote ambayo hakuyajua kuhusu yeye lakini alijikuta anaamua kumkwepa baada ya moyo wake kuwa mzito ghafra na kushindwa jua aanzie wapi. “Pole sana baby, sasa maumivu yako ya mshono ndio yasababishe nikuchukie? niache kumchukia mshenzi mr……….” alisita Shebby baada ya kutaka kuropoka juu ya mr X na kukumbuka kauli na ushauri wa Cj4 kuwa asimzungumzie wala kumtaja Mr.X hata kwa mkewe ama wazazi wake bila kujua huyo anayemficha anajua mengi zaidi ya anavyomuona. “Unasema umchukie Mr..!!? mr. ndio nani?” aliuliza kimakusudi Asha na kuzidi kumpoteza kisaikology Shebby aliyeamua kutunga uongo wa palepale ambao Asha alijifanya kuukubali.
Maisha yao mule ndani kila mmoja alikuwa na siri ambayo mwengine haijui na mtu aliyekuwa anawaunganisha kwenye hiyo siri kila mmoja hajui kama mwenzake huyo mtu anamjua ama anawasiliana nae, na wote kwa pamoja walimuamini sana huyo mtu na kumsikiliza kutokana na mioyo yao kukiri kuwa huyo mtu amewazidi kila kitu kuanzia mbinu hadi uwezo wa kupambana kimwili.
Na hakuwa mwengine huyo mtu bali ni Komandoo aliyeaminiwa kati ya makomando kutoka Jwtz naye ni Komando Jumanne au Cj4. ambae sasa nae aliwaingiza kwenye mchezo Shebby na Asha baada ya kugundua siri ambazo aliona ili apate majibu inabidi acheze mwenyewe mchezo kama alioutengeneza Mr X ule wa vipofu lakini tofauti yeye aliwaweka vipofu rafiki zake, watu asio na visasi nao na kwa sababu maalum zenye faida kwao wote
Siku hiyo tofauti na siku zote Kamishna Shebby alitoka alfajiri sana majira ya saa kumi na moja kasoro na baada ya Kamishna Shebby kutoka tu ndipo Asha alipoamka haraka na kuchukua simu yake na kupiga tena ile namba ya siri aliyopewa na Cj4 kule hospitali kwa shauku akiwa anataka ushauri kwa Cj4 nini afanye juu ya ukweli anaouficha kwa mumewe juu yake na mr X. [“Hallow kaka Inspekta”] aliongea Asha mara baada ya simu kupokelewa upande wa pili. [[“Lady Ninja, leta ripoti ulichopata.”]] ilisikika sauti upande wa pili na kumfanya Asha ashushe kwanza pumzi baada ya kuona yule mtu ambae yeye alikuwa anadhani ni Inspekta kuwa anajua mengi sana kuhusu yeye hasa baada ya kusikia anamwita Lady Ninja. [“Naomba unisaidie ushauri kwani natamani kumwambia ukweli mume wangu lakini nahisi huu ukweli unaweza kuwa ndio mwisho wa upendo baina yetu isitoshe nami nampenda kweli sasa. msaada tafadhali huu uongo unaniumiza nafsi”].
[[“Hupaswi kuwa na haraka kumwambia sasa, unachotakiwa uwe unakwenda mara kwa mara kule kwa wakwe zako naamini sasa Mr X rada yake haipo kwenu kwanza ipo kwa babaako.”]] aliongea Cj4 na kumpa maelekezo yale Asha ambae aliyakubari kwa moyo mmoja na baada ya kukata simu alianza kutafakari yale maneno ya Cj4 kuwa kwanini Mr X sasa hana habari na wao bali ataendelea kwanza kudeal na Hussein ambae ni babaake aliyekuwa kule kwenye Jumba kubwa la mzee Mwinchande? (“Mr X sawa anadeal na babaangu, lakini kwanini Inspector ananambia niende mara kwa mara?! Mh!! nina wasiwasi na haya maneno kitaalam kama anamaanisha mr X hayuko mbali na pale..!”) aliwaza Asha baada ya kukata simu.
Wakati huo nae Shebby alikuwa njiani akienda huko huko kwa Cj4 kama kawaida toka amefariki Kimaro na kupona kwake mguu hakutaka kabisa kuendeeshwa hata alipobembelezwa na serikali kutokana na heshima aliyokuwa ametunukiwa lakini alikataa katakata na alifanya hivi kutokana na mission zake za siri sambamba na Cj4. Shebby akiwa kwenye gari yake mawazo yote alifikiria sana mazungumzo ya mkewe na aliona kama kulikuwa na kitu cha zaidi alichotaka kusema yule mwanamke lakini alighairisha ghafra na kuzuga story nyengine na kumbe Shebby hata alivyokuwa anamuitikia haikumaanisha alikuwa hajastukia kama kuna kitu Asha alikuwa ameficha lakini alichofikiria kwa nini anaficha? Lakini kwa kuwa alikua na mtu wanaesaidiana kwenye mission yao ya kumnasa mr X na kwa sababu ya kuamini huyo mtu ana uwezo mpana sana wa mbinu na fikra aliamua kwanza kukutana nae alfajiri amuelezee na kile alichokuwa anakihisi yeye ili wapate ufumbuzi zaidi wa mambo.
Ulikuwa ni ujanja wa Cj4 alioutengeneza kwa Shebby na Asha na sasa ilikuwa ni yeye tu anawacontrol wote wawili pasi na kujitambua wenyewe. Asha ametoka kuongea nae na mara alipokata simu hazikupita dakika ishirini na Shebby nae aliingia.
* * * *
“Asalamu alykum bwana, swala muda ndio huu Mwenyezi Mungu anatuamuru tuamke tumuombe nae atatujibu…” aliongea mzee Mwinchande mara baada ya Hussein kufungua mlango na kutoka. “hahaaa Kweli kabisa daah!” alijibu Hussein kwa kujichekesha machoni lakini moyoni alikuwa na hasira kupita kifani juu ya mzee Mwinchande baada ya kumgundua kuwa ndie alikuwa mr.X mwenyewe. Lakini kilichomsaidia Hussein ni vile jinsi alivyoweza kuyaficha ya moyoni na kuvaa uhalisia wa kitu tofauti kabisa na hii kwa kuwa alijua mtu hatari mr X yupo mbele yake kwa hiyo itakuwa hatari zaidi kama akiwahi kugundua yaliyo moyoni mwake.
Walisimama sehemu ile ya kusalia na mzee Mwinchande alisimama mbele yake akiwa ndie Imam (kiongozi wa sala) huku Hussein bubu akisimama nyuma ya mzee Mwinchande akiwa maamuma (muongozwaji wa sala) na hapo ndipo Mwinchande alipofungua sala. “Allaaaaaaaahu Akbaaar.” (Mwenyezi Mungu ni Mkubwa) alitamka mzee Mwinchande na Hussein aliongoza vile japo moyo ulimuuma na kujikuta machozi yanaanza kumdondoka tena kipindi Mwinchande akisoma pale mbele kuiongoza sala yao. (“Yaaani nakubali kabisa kusalishwa na adui yangu? Yani eti nimuombe Mungu pamoja na adui yangu tena yeye ndie awe ananiongoza kumuomba Mungu? hapana… Hapanaaa”)
aliongea mwenyewe Hussein moyoni mwake huku akimuangalia mzee Mwinchande kwa hasira pale mbele akijaribu kutafakari nini amfanye ili aweze kutimiza azma yake na nafasi aliyoiomba zaidi ya miaka ishirini? Nafasi ambayo aliona ndio ile leo hii iko mbele yake na mr X adui yake aliyesubiri muujiza wa kumjua utokee kwa miaka mingi na sasa imekuwa hivyo yuko mbele yake na amempa kisogo. (“Inawezekana bahati hii nisiipate tena akaja kuniwahi huyu mshenzi.”) alifikkiria tena Hussein huku akigeuka geuka kutazama maeneo yale yalivyokaa kaa akiwa kama mwenye kutafuta kitu wakati sala ilipokuwa inaendelea na alijua kwa upande wake lile jambo la kugeuka geuka tayari lilikuwa lishamuharibia sala lakini aliona yuko sahihi kwani hawezi akasalishwa na shetani harafu hiyo sla ifike kwa Mungu.
Aliamini kabisa mr X ni shetani wala hapaswi kabisa kuishi na aliamini kuwa asingeweza kuendelea kuvumilia kwa siku tatu zaidi bila kustukiwa na mr X kilichokuwa moyoni mwake. Na katika kugeuka geuka kwake hatimae alibahatika kukiona alichokuwa anaaangaza angaza macho kukitafuta na hakikuwa chengine bali ni kipande cha chuma kilichokuwa kinatumiwa kwaajili ya kupasulia nazi na alikiona jana yake usiku pindi yule mfanyakazi wa ndani alipokisahau kukirudisha sehemu husika mara baada ya kukitumia kipindi akiangalia filam kwa sebuleni na kukisahau juu ya sink dogo karibu na mlango wa jikoni nyuma kidogo na eneo walilokuwa wanasali.
(“Shabbashhhhhh, najua hii yote ni Mungu amemfanya yule bint kukisahau na kunikumbusha mimi nikitumie kama silaha ya kummaliza adui wa watu aliyesimama mbele yangu”) aliongea Hussein wakati huo walikuwa wamesimama tena baada ya lakaa (sujuda) ya kwanza ambapo mzee Mwinchande akiwa hana habari aliendelea kusoma kwa madaha kabisa taratibu bila kujua wala kuhisi nini kinaendelea nyuma yake ambapo Hussein bubu alikuwa ananyata taratibu sana kinyume nyume hadi kulipokuwapo kile chuma na kukikamata kwa nguvu na kuanza kunyata tena kumsogelea mzee Mwinchande huku mapigo yake ya moyo yakizidi kasi kadri alivyozidi kupiga hatua hadi alipofika mita chache kabisa na kujiandaa kwa nguvu zote kumshambulia adui yake. (“Leo ndio Historia inaandikwa.”) aliongea kimoyo moyo na kujihesabia mwenyewe Hussein lakini mara ghafra alistuka kusikia sauti ya miguu ya mtu akishuka ngazi kwa haraka kutoka juu kuja kule sebureni tena akiwa anakimbia.
“Mume wanguuu Mume wanguuuuuu Babaaaaa……” alikuwa ni Zainab mamaake Kamishna Shebby akikimbia kuwahi kule chini mara baada ya kuona kinachotaka kutokea kupitia kwenye screen yao maalum iliyokuwa chumbani inayoonesha maeneo ya nyumba ile kupitia kamera ndogo zilizotegwa kila kona kwaajili ya usalama na kurekodi kila kinachoendelea mule ndani.
Lakini pindi anatoa ule ukelele kumpa tahadhari mzee mwinchande ambae alikuwa anajiandaa kusujudu ndipo Hussein bubu alipowahi kwa kumtandika vyuma vya kichwa mfurulizo na kwa nguvu zote. “KUFAAA KUFAA KUAFAA” Alipiga kelele Hussein kipindi anamshambulia mzee Mwinchande kwa nguvu zote mpaka walipodondoka pale chini ambapo kwa sekunde zisizozidi arobaini tayari damu nyingi zilikuwa zinamvuja mzee Mwinchande aliyekuwa anapapatika sebule nzima huku Hussein bubu akiwa kamng’ang’ania bado anampelekea dozi ya kutosha kwa kumpiga kwa nguvu na kile chuma hali iliyosababisha sasa damu kuwa inamrukia Hussein na mbaya zaidi alianza kupasua hadi fuvu la kichwa. “Hoooooooooooooooooooooooooooooooooo…” alipiga kelele na kuanguka pale mwisho wa ngazi Zainab huku akiwa haamini kile alichokuwa anakiona kikitokea mbele ya macho yake. “Uuughhhhrrrrr..Ughhhrrrrrr..” alikoroma koroma kwa nguvu Mwinchande kila Hussein alivyokuwa anamporomeshea kipigo cha kihistoria. “Kufaaaaaaa Mshenzi weweee kufaaaaaaaa, Kufaaaaaaa” alikuwa nusu kapagawa Hussein na alizidi kupata nguvu pindi alipokuwa anatoa dozi kwa mzee Mwinchande ambae sasa alionesha wazi tayari alikuwa anamalizikia roho huku akiwa amepasuka vibaya sehemu za kichwani na paji la uso damu zikiwa zimetapakaa sehemu ile ya kusalia hadi maeneo ya jikoni katika kikirikakara zilizokuwa zinaendelea.
Kelele za Zainab na Hussein ziliweza kumuamsha dada wa kazi aliekuwa chumba cha chini karibu na jiko ambapo alipotoka hakuamini kile kilichokuwa kinaendelea mara baada ya kumshuhudia Hussein bubu akiwa anamshambulia kwa nguvu zote mzee Mwinchande pale chini huku kwa mbele maeneo ya ngazi zilizoelekea vyumba vya juu alionekana mamaake Kamishna Shebby akiwa ameanguka huku kaishiwa nguvu akilia bila kutoa sauti. Ubaya wa nyumba ile ilivyotengenezwa ni kuwa na vioo vya tinted pia madirisha yalikuwa hayafunguliwi kutokana na AC iliyokuwa inawashwa masaa 24 na kama ukitaka upepo halisia unapandisha sehemu za juu kabisa, na kwa sababu hiyo hata walinzi waliokuwa nje hawakujua chochote kilichokuwa kinaendelea ndani. [“Hlloooo, halloooooo, halooo kakaa shebiiii babaaa hukuuu aaaah muwahi babaaaaanakufaaaa… “] aliongea huku nae akilia yule msichana wa kazi mara baada ya kukimbilia tena ndani mwake na kuamua kumpigia Kamishna Shebby kumpa taarifa ili awahi kuja kutoa msaada kwa kile kilichokuwa kinaendelea pale. “HAHAHAHAHAHAHAHAAAAA” alicheka kwa nguvu Hussein mara baada ya kuona Mzee Mwinchande katulia na kaacha kupapatika. “hahahahahahahahahahaaaaa” Alicheka tena huku safari hii akimpiga piga kwa nguvu sehemu za mdomo na kuanza kumvunja meno bila kujali hata zile damu zilizokuwa zinamrukia huku akiwa na Furaha ambayo toka anaingia Jera hajawahi kufurahi kwa nguvu Hussein kama siku hiyo. “ASANTE BABA MUNGU” Aliinua kichwa juu na kushukuru Hussein bubu kwa kuona ile ndoto yake na maombi kuwa aje kumuua Mr.X kwa mikono yake muda ule ilikuwa imetimia na hatimae kweli Mzee Mwinchande ambae ndie alikuwa Original MR.X aliuawa kwa mikono ya Hussein babu bubu baada ya usumbufu wa zaidi ya miaka 28. Baada ya Hussein Kuhakikisha hakuna Jipya tena kwa Mr X aliinua uso wake na kumtazama mama Shebby pale chini ambae alikuwa amekosa nguvu kabisa hakuweza hata kunyanyuka zaidi ya kuwa anasota kuelekea juu ya ngazi zile kwa hofu huku akilia mara baada ya kumuona Hussein amenyanyuka kwa hasira na macho yote alikuwa kayaelekeza kwake.
Simulizi : Wanawake Ni Wauaji ?! Sehemu Ya Tano (5)
“Leo kuna kitu kimoja tu, kilinichanganya kuhusu mke wangu.” alionekana Kamishna Shebby akiongea na Cj4 kwenye sehemu yao maalum waliyokuwa wanakutana kwa mazungumzo pasi na mtu yeyote kuona. “Kitu gani hiko?” aliuliza Cj4 “Kwenye mazungumzo yake nikiwa kama askali mzoefu sasa niligundua kuna kitu ananificha kinachonihusu kabisa” “Mh! hebu nipe nukuu yake.” “Alianza maongezi akiwa makini na kunimaanishia kuwa niamini kama ananipenda, lakini alivyoendelea alinambia kuwa ila anaona hastahiri mimi kumpenda vile na nilipomuuliza sababu akanambia ana wasiwasi kwa vile ninavyompenda kuwa sitompenda hivyo siku zote. Nilipomuuliza kwanini ana wasiwasi huo ndipo akanambia kuwa anahisi kuna siku nitakuja kumchukia sana na hata kumuua…. Dah! hapa ndipo nilipochoka na kuhisi lazima kuna kitu tu. Hawezi kuanzisha mada yenye maneno makali kama yale yaani mimi Nimuue mke wangu mwenyewe?” aliongea Shebby wakati huo Cj4 alikuwa anmsikiliza kwa umakini mkubwa.
“kwa hiyo hukumuuliza kwanini amefika mbali hivyo?” “Nilimuuliza kiongozi.” “Akasemaje” “aagh! jibu lake nililiitikia tu lakini halikuwa na ukweli wowote nilijua tu ni Zuga” “sawa aliemaje?” aliuliza Cj4 lakini wakati Shebby anataka kujibu mara simu yake ambayo ilikuwa na line ile ya nyumbani tu ndipo ilipoita na kuipokea ambapo sauti ya upande wa pili ilimfanya abadilike ghafra uso. “Vipi Shebby?” “Kumekucha Mkuu Mr X ameamua kuivamia nyumba yetu alfajiri hii kule kwa mzee.” aliongea Shebby ndipo mkuku alikimbilia kwenye gari pamoja na Cj4 ili kuwahi nyumbani kwao ambako ilionesha wazi kuna matatizo mazito.
“Nani huyo kapiga simu?” aliuliza kwa sauti nCj4 wakati huo Shebby aligeuza gari kwa fujo na kugonga mti upande wa nyuma kabla hajatia gea ya mbele na kukanyaga mafuta kwa fujo bila kujali kishindo cha nyuma alipogonga kumetokea madhala kiasi gani. “Nani kakupigia Shebby?” aliuliza tena Cj4 huku akibamiza dashboard kwa kofi kali baada ya kuona Shebby yupo kimya huku akili yake ikiwa mbali sana. “Ni mfanya kazi… Ni dada wa kazi kiongozi… aaagh! anaongea huku analia na nilisikia sauti za vitu vikiongwa gongwa…” aliongea kwa pupa Shebby wakati huo barabara waliyokuwa wanapita mbele yake kulikuwa na kijiforeni kilichomfanya ahamie bara bara ya pili huku akivipana vile vizuizi vidogo vya barabara na kusababisha gari iruke ruke na kutaka kudondoka pasi nae kujali kuwa anaingia upande usiomruhusu ambao haukuwa na magari mengi na wala hakupunguza mwendo Shebby aliendelea kukanyaga mafuta huku akizikwepa kwepa gari zilizokuwa zinakuja mbele yake.
Kelele za honi zilisikika kwa fujo kama zile kelele za mavuvuzela katiaka kombe la dunia kule south pindi Shebby alipokuwa anakosana kosana kugongana na gari nyengine zilizokuwa zinakuja mbele yake na hiyo yote ilikuwa kutaka kuwahi nyumbani kuzuia matatizo yaliyokuwa yanatokea muda ule akihofia mr X asiwadhuru watu wote wa familia yake hususani baba na mamaake pamoja na mkwewe ambae ni Hussein bubu. “Cj4 ushauri wako safari hii umeniponza. Aaaagh! umeona kumuacha Hussein bubu nyumbani matatizo yanatokea na kuwaumiza watu wasiohusika kabisaaaaa aaah! ona tunawaponza watu wengi zaidi? Ni bora tungemueka sehemu ya kumlinda wakati tukimsaka Mr X.” alilalama Kamishna Shebby huku machozi yakimtoka wakati kichwa chake kilipotengeneza mazingira ya nyumbani na kuona jinsi wazazi wake wanavyoumizwa na watu wa Mr X. Wakati Kamishna Shebby akilalama Cj4 yeye alikaa kimya na kuvuta picha na kuona lazima Hussein ndie aliyeanzisha kasheshe huko baada ya kugundua kitu kuhusu Mr X, na si wala kwamba kuna mtu zaidi kavamia ile nyumba na kusababisha mauaji.
Gari iliiingia mkuku na kugonga geti hadi walinzi walistuka mno na hapo Kamishna Shebby alipiga teke mlango mdogo wa geti baada ya kushuka kwenye gari huku akiwa ameikamatia bastora ndogo mkononi na kustaajabu kukuta walinzi wakiwa wamejificha kwaajili ya kupambana na uvamizi waliotaraji kutokea na wao kushangaa kuona ni Kamishna Shebby. Tofauti ya Shebby kwa upande wa Cj4 yeye hakuingilia pale getini zaidi alizunguka eneo la nyuma ya ukuta na kurudi nyuma kutafuta speed ya kukimbia kidogo kabla hajaruka beki kavu tatu zilizompeleka moja kwa moja hadi ndani ya fance sehemu kulipokuwa na bustani ya kupumzika na bwawa kubwa la kuogolea na ajabu zaidi Cj4 alijipanga kwa vita akiwa mikono mitupu.
* * * * “Zaaainaab.. Zaiiiiinaaaab.. Zainaaaaaabuuuu leo na wewe lazima ulipe damu ya mwanangu.” aliongea Hussein bubu huku akipiga hatua kumsogelea mama Shebby kwa hasira pale chini alipokuwa anasote huku akilia kwa uchungu. “Hapaanaaaa, hapaaanaa .. aaah! Haaapaana Mume wanguu.” alijitahidi kutoa sauti mama Shebby japo hakufanikiwa kuitoa kwa nguvu kama vile alivyoilazimisha ila ilitosha kusikiwa na Hussein. “Mume wako? Mume wakoo!! hahahaha Mume wako unaemlilia huyu Shetani mtoa roho za watu? hahahaa nakusafirisha sasa hivi umfate huko aliko ila kwanza nataka unijibu swali moja Zai… KWANINI ULINIGEUKA NA KUSABABISHA KIFO CHA MWANANGU NA KUNIHARIBIA MAISHA YANGU YOTE???” Aliuliza Hussein kwa hasira iliyokuwa inamfanya hadi atetemeke mwili mzima pindi alipokuwa amemfikia mama Shebby ambae ni kweli kabisa ndie Zai wake yule yule. “Hapana Hussein, hapana sikujua kabisa kama yangekuja kutokea mazito kiasi hiki wala sikuweza kuyafanya yasiendelee kutokea aaahggggg nimejiponzajeeee mieeeee.” aliongea kwa uchungu Zai na kuendelea wakati huo Hussein alikuwa anazidi kutetema kwa hasira akingojea jibu la Zai kabla hajaanza na yeye kumponda ponda kichwa chake kwa kile chuma kilichotapakaa damu.
“Hussein, unastahiri kabisaaaaa kufanya haya Mume wanguuu…….” “STOOOOOP. Nihadithie kwanini na wala usinite Mume wangu. Utafanya nikuue kabla hata sijasikiliza jibu lako.” alimkatisha kwa hasira na kumpelekea Kofi moja kali lililomfanya Zai kupasuka lipsi ya mdomo baada ya kujing’ata kwa kupigiza kichwa pale kwenye ngazi. “sawaaaa… sawaaa .. sawa..aaaghhhhh, wala sikumwambia Mr X akuue, wala sikupanga mwanangu azushiwe kuuliwa nawe pamoja na mimi mwenyewe, wala sikuyajua hayo yoteee Hussein. Naomba uniaminiiiii… Ila tatizo wewe hukuwa Mume wangu wa Kwanza kunioa na kunilipia mahali japo ulikuwa mwanaume wa kwanza kuniingiza katika ulimwengu wa mapenzi. Sikuona jinsi gani ya kukwambia ukweli hadi unielewe na kuniruhusu nikaishi kwa mume wangu. Hussein najua leoo upo sahihi na mimi ndie niliekuwa nastahiki kulipa nafsi za hao wote.. Lakini unadhani ningefanyajeee? huyo Mr X ndie mume wangu kabisa wa kwanza aliyejulikana hadi na wazazi wangu….. wewe umemjua bibi tu Hussein lakini mimi nilikujua muda mrefu kabla hatujahamia Arusha.
Na ahadi yako ya utotoni hasa vile ulivyonambia kama utani naona leo inakuwa kweli aaaaaaaah!! Nataka ujue kabla hujaniua kuwa mimi ni KINOGE rafiki ako wa utotoni ZUNGU.” aliongea kwa uchungu zaidi Zai na kumshangaza tena Hussein baada ya kutajiwa kwa mara ya pili jina la Zungu na kukumbuka siku aliyokubaliwa kuwa na mahusiano na Zai alimwita jina hilo lakini alijikuta anachoka zaidi na kushangaa baada ya kujua kitu ambacho hakuwahi kukijua kumbe Zai ni Kinoge msichana waliyependana mno toka watoto na mara ya mwisho walipoteana wakiwa darasa la tatu. “Haaa, KINOGE??!!” Alitahayuri akiwa bado na hasira Hussein na ndipo kichwani mwake ilipokuja taswira na picha ile ya Kinoge pindi walipokuwa watoto.
………………………… ZUNGU => Kinoge Ona huyu ndio mtoto wetu, huyu ndio mimi hapo na huyu wewe harafu huyu aliyelala hapa adui nimekufuma nae anataka kuninyang’anya nimempiga nimemuua sasa nakupiga na wewe hapo hahaha nakuacha unalia harafu nam beba mwanangu tunaondoka hukoooo. KINOGE => hahaha Zungu bwana, sasa kama wewe baba na mimi mama unafikiri adui atatoka wapi? tutakuwa tunapendana kama baba angu na mama angu si eti eeh? ZUNGU => haya ila mi nitampenda sana mwanangu kama baba alivyokuwa ananambia kuwa mimi ndie ndugu yake na sio mamaangu kwani ana ndugu zake. Na wewe utakuwa na ndugu zako na mimi ndugu yangu mwananguuu. KINOGE => Jamani Zungu, utakuwa unanipiga? ZUNGU => Akuuu, ila nikikukuta na adui nitampiga hadi afe na wewe nitakupiga kibao kimoja tu.. ^^^^^^ (<<<>>>) ^^^^ (<<<>>>) …………………
Yalikuwa ni mawazo ya Hussein bubu pindi alipokumbuka mara ya mwisho kuongea na Kinoge siku hiyo majira ya jioni walipokuwa wanacheza mchezo wa kibaba baba huku akiwa ametengeneza watu wa kufinyanga kwa udongo na Kinoge alikuwa anapikapika kwenye vifuu. Maneno ambayo aliwahi kuyaongea kitoto toto katika michezo ya watoto leo hii yamekuwa na ushabihiano mkubwa sana na kilichokuwa kinatokea japo hakuwahi kuwaza, kuhisi wala kujua kama Zai ndie rafiki ake wa utotoni yule aliyekuwa akimwita mchumbaake kabla ya wazazi wake kuhama na hakujua walihamia wapi na hata alipokua mkubwa ilifika wakati Hussein alisahau kabisa habari za Kinoge.
Lakini mbali na hayo yote bado msimamo wa Hussein ulibaki palepale, alishadhamiria kumuua na Zai na alikuwa anasubiri jibu moja tu lenye sababu za msingi kwani yote yale aliyokuwa anazungumza Zai ilikuwa kama anazunguka tu. “Uwee Kinogeee uwe Zaaiii nataka kujua kwanini ulifanya yote yale na kuwa tayari kuimwaga damu ya mwanangu kinyama namna ile hata kichwa chake nisikionee?? Wee ni mwanamke wa aina gani!!??? Lazima leo Ufe na hii si kwa niaba yangu tuu, bali ni kwa niaba na damu ya mwanangu mliyeniekea viganja vyake mfukoni ili mkanifunge vizuri Wanyama Mbwa wakubwa nyiee… Hii ni kwaajili ya damu ya mwangu Mwin she heeeeeee….” aliongea kwa uchungu Hussein na kukikamatia vizuri kile chuma huku akiwa kanyoosha mikono yake juu kwa niaba ya kuanza kumshushia kisago mama Shebby au Zainabu au kwa jina la utoto Kinoge. Lakini akiwa kakamata kile chuma akinyanyua mikono kabla hajakishusha kichwani mwa Zai, ndipo alipopiga ukelele wa kukanusha kile alichokisema na kukiamini Hussein. “HAPANAAAA, SIJAWAHI KUUA DAMU YANGU.” Kauli hii ilimfanya kwanza Hussein asite na kumuuliza Zai. “Unamaana Gani? Nini kilitokea juu ya Mwanangu?!!” “Hakuna kibaya chochote kilichompata mwanetu Mwinshehe… Mwanao mzimaaaa na ni rafiki ako mkubwa tuuu…” “NINI? Unamaanisha nani? Kamishna??” “hiiiiihiiii Nisameeeeheeee .. Ni kweliiiii Kamishna Shebby ndie mtoto wetu yuleyule Mwinshehe hiiiiigggr … Eeee Munguuuu wanguuuuuuu” Aliongea mama Shebby na kumzidisha machungu na taharuki Hussein aliebaki katumbua macho huku akiwa haamini kile anachokisikia masikioni mwake. “NINI???!” “Ndio hivyoooo aaah!! kweli mimi ni mkosaaaaji lakini Shaaban ndie mwnetu yule yule Mwinshehe na hata ile alama bado anayo pale nyuma ya shingo karibu na bega japooo aaaagh haaataa Mwin-chaaande umemuuua bila kutambuaa ukweli huuuuuuu” kilio cha mama Shebby sambamba na maneno yake kilizidi kumkasilisha Hussein bubu ambae alizidi kutetemeka kwa hasira kuhu machozi yakimtoka na kuchirizika mashavuni huku yakisukuma damu iliyomgandia Hussein ambayo ilimrukia pindi alipokuwa anamuua mzee Mwinchande Mr. X. “Ina maaaaanaaa Zaii.. aaah UmeniekaaUchiiii umenitukanisha vya Kutoshaaaa!!!!! HaaH! siamini mimiii Zainab?? Kinoge?? Mwanamke wa ndoto zangu leo acha maneno yangu yatimieeee” aliongea kwa uchungu sana Hussein huku akizidi kunyanyua juu kile chuma na kukaza mikono. “Wanawake ni Wauaji… Aaaagh! Wanawake ni Wauaji nyinyiii… Ona kwa sababu yako watu wangapi wamekufa Zai..Ona ulivyonitukanishaaa… Onaa sasaa wanangu mwenyewe nimewaoza mwenyeweeeeee!!! haaaaaaaa… siwezi kumlaumu Asha wala Shebby iiiiiihhh Umenitukanajeeee!!? Kinogeee Hustahiri kabisa kubaki hai.. Hustahiri kabisa kuishi Zaiiii hata ninavyokuua leo sipaswi kuhukumiwa kwa hilo kwani hukumu yangu ya kukuua ilishapitishwa na kuitumikia miaka mingi sanaaaaaaa Zai kuishi sasa HUSTAHIRIIII” Aliongea kwa hasira sana Hussein na sasa alikuwa anataka kushusha kile chuma kichwani mwa Zai ambae alijua sasa mwisho wake umewadia na hakuwa na ujanja wa kumkimbia Hussein bubu pale zaidi ya kufumba macho kusubiri kusikia chuma kikitua kichwani mwake na kusambaratisha fahamu zake zote kabla ya kuiacha dunia na kwenda kwenye makazi ambayo hajui yakoje. Lakini kabla Hussein bubu hajashusha kile chuma kichwani kwa aliekuwa mkewe miaka hiyo bi Zainab ndpo ghafraaaaaaaaaaa mvunjiko wa kioo cha dirisha ulisikika sambamba na mtu aliyevaa mavazi ya polisi magereza mwenye cheo kikubwa alieonekana akiingia kwa mtindo wa kuruka huku mikononi akiwa kakamata mguu wa kuku (bastora ndogo) kishupavu kabisa na pindi alipoangukia tu mule ndani sekunde ileile kwa mbali alipomuona Hussein bubu akiwa anataka kumuua mamaake mzazi huku kushoto kwake akiuona mwili wa babaake mzazi ukiwa umepasuliwa vibaya sehemu za kichwa, nae palepale akiwa kakunja goti mguu mmoja alipiga kelele za uchungu huku akimfatulia risasi yule mtu aliemsimamia mamaake akitaka kumshushia vyuma vya kichwa na alimtambua kabisa kuwa yule ni nani ila aliamini kuwa amechanganyikiwa. “HUSSEEEEENIIII BUUBUUUUU” Alipiga ukelele Kamishna Shebby huku akiachia risasi mfurulizo kumuelekezea Hussein lakini sekunde ile ile kwa style ya ajabu kabisa alistukia kiatu kikubwa aina ya buti kikitua mikononi mwake Kamishna Shebby na kumshuhudia mwanaume wa shoka Cj4 akitokea upande ule wa juu kwenye ngazi na si kwa kushuka ngazi bali ni kwa kuruka nje ya ngazi na kutua pale alipokuwa anadondoka Hussein bubu na kumdaka kimaajabu na kubimbilika nae hadi maeneo ya mlango wa jikoni ambapo Cj4 aliingia na Hussein bubu na kujibanza nae nyuma ya Friza la kuekea nyama jikoni. “aaaaaghrrr Na-kuuu-ku-mbuu-uu-k-kk-kaa raf–f-fiki–ang-gu” aliongea kwa shida Hussein bubu mara macho yake yalipokutana na macho ya Cj4 aliekuwa kampakata nyuma ya lile friza lililokuwa karibu na mlango wa kuingilia jikoni. “Polee rafiki angu mimi nipo hapa. Utapona tu” “We-ni-As–ss-sskari?” “Kweli rafiki angu mimi naitwa Cj4 ni askali niliyetumwa na serikali kwaajili ya kujua ukweli wako uliomfanya Shebby ashambuliwe kule Mkuyuni ila sasa kila kitu kipo sawa rafikiangu jikazee” aliongea harakaharaka Cj4 huku akimuangalia kwa huruma Hussein bubu ambae damu zilianza kumvuja mdomoni na hata nyengine kuchuruzika kwenye mikono ya Cj4 na kugundua kuwa kuna risasi zilimpata Hussein mgongoni na kujilaumu Cj4 moyoni kuwa alichelewa kumuokoa Hussein.
“Cj4 kama umeungana na huyo Muuaji wa familia yangu tambua na wewe ni adui yangu sasaaaaa.. Aaaaaaggggggghh” aliongea kwa hasira Shebby pindi alipoinuka na kuiokota bastora yake pale ilipodondokea na kuanza kuelekea kule jikoni alibimbilikia Cj4 na Hussein bubu. “Mwananguuuuuu Shebbyyyyy usimuuue Husseeeeein ni babaaakoooo” alipiga ukelele Zai ambae ni mamaake Kamishna Shebby ili kumzuia mwanae kutoendelea kufanya kile alichokifanya muda mfupi uliopita baada ya kufatua risasi mfurulizo zilizomfanya abaki kainama huku akiziba masikio na macho kwa uoga. “Shebiii mwananguuuuu nisikilizeeeee” alizidi kupiga kelele Zai lakini Shebby hakujali wala kusikia maneno ya mamaake kwa hasira alizokuwa nazo kwa kuhisi pia huenda na mamaake alikuwa kachanganyikiwa kwani anawezaje kumtetea mtu aliyekuwa anataka kumuua muda si mrefu? na tayari kamuua hadi mumewe? aliona wazi mamaake kachanganyikiwa na alikuwa tayari kupambana na Cj4 ambae alionekana kumtetea Hussein bubu. (“Huyu sasa anazidi upuuzi, acha kwanza nimfunze kuwa wanaume wanapokuwa kazini hutanguliza umakini mbele na si upendo.”) ilikuwa ni sauti ndani ya moyo wa Cj4 huku akimtoa mapajani mwake Hussein bubu pindi aliposikia vishindo vya hatua za minyato vya Shebby vikiwa vimekaribia pale mlango wa jikoni.
“Shebby mwanangu mimi Sijachanganyikiwaaaa wala huyooo unaetaaka kumuua hajaachanganyikiwaaaa… Nataka Ujue mimi ndie Zainab mke wa Hussein na wewe ndie mtoto wake aliyesingiziwaa kamuuaa na huyooo unayejuaa babaako ndie MR X..” kauli hii ya mama Shebby aliyokuwa anaiongea kwa sauti ya uchungu sana na maumivu ndiyo iliyomfanya Shebby asiamame ghfra na kujikuta hadi ile bastora iliyokuwa mkononi mwake ikimdondoka chini kwa mshtuko mkubwa na kugeuka kumtazama mamaake aliekuwa anasota kumfata pale aliposimama mlango wa kuingilia jikoni. “Mwananguuu Shebby, Hussein ndie babaako kweli kabisaaa. Ni kweli kabisaaa kweli sisi wanawakeee ni wauajiii aaaaaaaaaghhhh Nisamehe mwananguuuu” aliongea huku akilia Zai akiwa amekamata miguu ya Shebby aliejikuta anashindwa kuongea lolote zaidi ya kuchezesha midomo tu kwa mtetemo ambao ulikuwa haukujulikana kama ni hasira au maumivu.
Maneno yale pia yalisikiwa vizuri sana na Cj4 na hata Hussein mwenyewe aliekuwa anahangaika na roho yake huku kila alivyojitahidi kuongea ndivyo damu zilipozidi kumvuja mdomoni na kubaki anaongea na Cj4 kwa kumtazama tu na alifanya hivyo hata pale Cj4 alipotaka kumlaza chini kwa kujiandaa kumuadhibu Shebby, Hussein bubu alimtazama kwa jicho lile la kumzuia asifanye hivyo. “MAMAA !!! Ina maana….” alitaka kusema kitu Shebby na kujikuta akishindwa ndipo alipokimbilia ndani mule jikoni kumuangalia Hussein bubu na kumkuta akiwa kashikiliwa na Cj4. “Amini hivyo Shebby ukweli huyu ndie babaako.” alikazia Cj4 pindi Shebby alipoingia ghafra na hapo Hussein alijikuta kama anapata nguvu tena mara baada ya macho yake kukutana na uso wa Shebby na kumuashiria asogee pale na ainame. Kwa mwendo wa ‘sielewi’ na taharuki nyingi alisogea Shebby na ajabu alipoinama tu Hussein aliweza kumuinamisha zaidi na kumuingiza mkono begani mwake kupitia ile kora ya shati ya Shebby na hapo mkono wa Hussein ulikutana na uhisio wa alama kama ile ya lengelenge mtu kaungua ama viuvimbe vyeusi vinavyowatoka watu (sunzua) kikiwa kwa urefu kuelekea maeneo ya begani. Shebby alistuka na kutaka kuutoa mkono wa Hussein lakini Cj4 alimzuia aache na baada ya Hussein kuridhika aliutoa ule mkono huku akiwa katabasamu hali iliyowashangaza na hata mamaake Shebby nae aliingia kule jikoni kwa mtindo ule ule wa kusota mithili ya mlemavu huku akiwa bado analia huku akimsisitizia Shebby kuwa yule ndie babaake. “ww-wa-ww-waa-aa-n-..” alibabaika kusema Hussein na kujikaza kumwambia Shebby na Cj4 pale kwa mara nyengine na wote wakiwa wametaharuki Hussein bubu akarudia tena. “uwwwan-aa-ang-uu Wa-na-wa-ke ni- Wa—u-aj-i.” na hiyo ndio ilikuwa kauli ya mwisho ya Hussein bubu na kuaga rasmi dunia akiwa mikononi mwa Cj4 huku pembeni yake alikaa mwanae ambae ni Shebby na kwa mbele mlangoni alionekana Zainab mamaake Shebby. “BAABAAA” Aliita kwa nguvu Shebby na kujipiga piga kichwa kwa majuto kwani alijua fika risasi zilizofatuliwa kwa mikono yake mwenyewe Shebby ndio zilizosababisha umauti wa mtu ambae alikuwa hajui kwanini moyo ulimsukuma mno kumsaidia na leo hii anajua akiwa amemuua kwa mkono wake akijua anamtetea mtusahihi kumbe sivyo. Lakini toka hivyo Shebby alisimama na kutoamini kama yule ni babaake na yule ndie Mr X na wazo hili lilipomjia alikumbuka kauli ya yule marehemu Mnyungunyungu kuwa mr X ana alama usoni nahapo alijikuta anaingiwa roho mbaya nusu chizi Shebby alirudi pale ilipokuwa maiti ya mtu aliyeamini siku zote ni babaake na kuanza kumpekua usoni ambapo alikuwa na mdevu nyingi na katika hali ambayo hakuitaraji ni kweli aligundua alama ya X iliyokuwa usawa wa chini ya kidevu karibu na koromeo na hapo ndipo alipoanza kuamini sasa kuwa kweli yule mtu aliyedhani babaake alikuwa ndie mr X na jina X lilitokana na ile alama yake ambayo huwezi kuiona kwa kumtazama tu, lakini alijiuliza kwanini yamekuwa yote yale? ndipo hapo kwa uchungu mno Shebby alianza kulia huku akimuuliza swali mamaake kwanini imetokea yote hayo. “Maaaaaa Why? kwanini mama yamekuwa yote hayaa? aaaaghh” Maumivu aliyokuwa nayo Shebby hayapaswi hata kusimuliwa kwa jinsi alivyokuwa anaumia huku akifikiria kwanza kamuoa dadaake, pili kamuua babaake wa kweli, tatu ni kwanini mamaake aliishi na siri iliyokuwa inapoteza roho za watu kila siku??? “Mwanangu Shebby ni kweli sistahiri kabisa kuishiii aaaaah! leo nimejifunza wakati tayari ni too late, ila naamini mwanangu mimi ndio chanzo cha yote hayaa… Eee Mungu naomba unipe tu hukumu inayostahiki juu yangu ….. Shabaan mwanangu vyovyote utachoamua unisamehe ama usinisamehe lakini ukweli mimi ndie chanzoooo aaaaaaaah! Ama Kweli sisi Wanwake ni Wauaji.”
CHANZO
( MIAKA 50 NYUMA ) …………………………… ……………
Ilionekana familia moja ya bwana na bibi Juma wakiwa katika kupanga panga vitu vyao husasi mabegi na kadhalika huku vijana wengine watatu walionekana kubeba viti, mbao za kitanda sambamba na magodoro wakipeleka nje na kupakia kwenye gari moja aina ya Canter iliyopaki karibu kabisa na ile nyumba ikionesha dhahiri bwana na bibi Juma walikuwa wanahama sehemu ile na kuhamia sehemu nyengine kwenye makazi mapya.
Wakati heka heka za kuhama zikiwa zinaendelea, upande wa pili kulipokuwa na nyumba inayotazamana na ile ambayo walikuwa wanaishi bwana na bibi Juma alionekana kijana mdogo wa kiume mwenye umri usiopungua miaka 12 akiwa amekaa mlangoni ameshika tama huku akiwa na huzuni kubwa wakati anaishuhudia familia ile ikihama pale mtaani kwao. Moyo ulimuuma sana yule mtoto ambae alikuwa maarufu pale mtaani kwa watoto wenzie kwa jina la Zungu japo jina lake halisi halikuwa hilo. Kilichokuwa kinamuumiza zaidi si kuhama kwa bwana na bibi Juma bali ni kuondoka pamoja na mtoto wao mdogo wa kike aliyekuwa na umri wa miaka 8 ambae alikuwa ni rafiki ake mkubwa sana shule na mtaani walicheza wote na mara nyingi walipenda kujiita baba na mama. “Kinoge mbona humuagi rafiki ako Zungu si unamuona alivyopooza” aliongea bwana Juma kumuambia mwanae yule wa kike ambae nae alionesha kutoipenda kabisa ile safari na alijisikia moyo kumuuma hata kumuaga kwa mdomo rafiki ake zaidi ya kumuangalia kwa jicho huruma na kumnyooshea mkono wa kwaheri pindi alipokuwa anapandishwa ndani ya gari ile mara baada ya kila kitu kumalizika kupakiwa. (“wewe ndie rafiki niliekuzoea, leo hii unaondoka na kuniacha mwenyewe. Najua huko utapata rafiki mwengine utayecheza nae kama mimi kibaba baba lakini jua kama nikimuona nitamuua kwa kua atakuwa tayari adui yangu.”) aliwaza maneno mazito sana yule mtoto Zungu pindi alipoishuhudia gari ile ikiondoka eneo lile la mtaani kwao na kumuachia msiba mzito wa upweke moyoni mwake.
“Hussein mwanangu, usiwe mnyonge hivyo. Ndugu yako nipo hapa si nishakwambia…? mimi ndio ndugu yako babaa” ilikuwa ni sauti ya mwanaume mtu mzima iliyosikika nyuma ya mlango alipokaa mtoto Zungu ambae jina lake halisi alikuwa anaitwa Hussein. Sauti ile ilimfanya Hussein ageuke huku machozi yaliyojazana machoni muda mrefu alipokuwa anawaangalia kina Kinoge wakihama bila kupepesa macho, yalianza sasa kutiririka mashavuni mwake na kumtazama kwa uchungu yule mtu aliyemsemesha. “baba, babaa unajua inauma sana. sasa wewe umewezaje kukaa mwenyewe na kuvumilia bila kulia pindi mama alipoondoka?” aliuliza mtoto Hussein na kumfanya yule mtu ambae alikuwa ni babaake mzazi amnyanyue pale na kumkumbatia kwa nguvu huku akimsihi atulize kwanza moyo kwa kumshikashika kichwa akizichezea nyele zake ndogo za kipilipili huku mkono mwengine akimpigapiga mgongoni. “Mwanangu Hussein, mbona ni rahisi sana baba…! ni rahisi mwanangu twende ndani nikakuhadithie” aliongea babaake Hussein na kumchukua mwanae mpaka chumbani kuwapisha wapangaji wengine waendelee na shughuli zao mida ile pale ukumbini waliposimama jilani na mlango wa kutokea.
“Mwanangu mamaako amekuacha ungali una miaka mitano lakini japo nilimkumbuka ila haikuwa sababu ya kunifanya niwe mnyonge na kukosa kabisa furaha. Unajua kwanini?” alianzisha maongezi babaake Hussein pindi walipokua wamekaa kitandani pale chumbani kwao. “hapana baba, sijui” “Kwa sababu wewe ulikuwepo, unajua kwanini uwepo wako ulikuwa sababu ya mimi kukosa huzuni na kuwa na furaha mbali ya kuwa mamaako hakuwepo tena?” “Hapana baba sijui.” “Kwa sababu wewe ndie ndugu yangu na yule alikuwa mke wangu na ndio maana ameolewa tena na mwanaume mwengine na hata huko anaweza kuondoka tena na kuolewa pengine.” “aaah, sasa baba na mimi mama sio ndugu yangu?” “Hapana mwanangu, wewe ni zaidi ya ndugu yako kwa sababu wewe ni mwanae na yeye ni mamaako unapaswa kumuheshimu na kumtembelea mara kwa mara.” “sawa baba, kwa hiyo Kinoge sipaswi kumlilia kwa kua sio ndogo yangu na huko aendako anaweza kupata rafiki kama mimi na wakihama tena atamuacha na kwenda kupata rafiki mwengine ikawa hivyohivyo eeeh..” “Ni kweli kabisa mwanangu, hutakiwi kumuweka sana moyoni mwanamke mwengine zaidi ya mamaako mzazi ambae hawezi kuondoka na kukuacha moja kwa moja hata uwe uweje, ila hawa wengine mwanangu usiwaamini kabisa na kuwaeka sana moyoni kwani wataweza kukusababishia maumivu na mateso makubwa pindi watapogeuka na kwenda kwengine.” “sawa baba” “Ndio hivyo mwanangu hupaswi kuumia mimi nipo na hata kama nisipokuwepo amini wa kukusaidia kweli ni mwanaume mwenzako japo wanawake ndio wanaoonekana kuwa na mioyo mepesi ya kusaidia lakini bado msaada wa ukweli upo kwa mwanaume baba. haya nyamaza wewe ni mmwanaume shika hela hii kanunue chapati uje tunywe chai” “Asante baba nimeelewa, nami nakuahidi sitoumia tena kwa sababu ya Kinoge” aliongea Hussein na kufuta machozi baada ya kuchukua pesa kwenda kununua hivyo vitafunwa huku akimuacha na tabasamu zito babaake.
* * * * *
Safari yao iliwachukua masaa mengi garini siku hiyo tokea asubuhi ile walipoliacha jiji la Dar na kuingia jijini Arusha majira ya saa moja usiku ambapo safari bado iliendelea mpaka kwenye vijiji vya mbali na Arusha mjini na huko ndiko kulikokuwa na makazi mapya ambayo walihamia familia ya bwana na bibi Juma pamoja na mtoto wao kipenzi aliyeitwa Kinoge. “haaa! mamaa ndio tumefika hapaa!!?” aliuliza kwa mshtuko Kinoge pindi alipoyaangalia mazingira waliyofikia kwa nje ambapo muda huo wale vijana waliopakia vitu kule jijini walikuwa wanavishusha wakipewa maelekezo pa kuviingiza na bibi mmoja ambae ndie alikuwa mwenyeji wao aliyewapokea. “Kinoge kwani wee unapaonaje si pazuri tuu.. tena huku kuna maembe na machungwa kibaoo unayopenda furaaaahi basii.” mama alijaribu kumliwaza mwanae ambae sasa alikuwa tayari kakunja uso kutokana na kuchukizwa na mazingira yale ya kijijini. Aliangalia kwanza hakukuwa na umeme, hakukuwa na barabara nzuri, nyumba zilikuwa zipo mbalimbali hali iliyomuumiza Kinoge na kuona ni afadhali wangemuacha jijini Dar na rafiki ake Zungu asingekuwa mpweke kuliko kuletwa pale ambapo aliamini hata marafiki wa kucheza nao kama Zungu hawakuwepo. “iiihhhhhhyyaaaaaaaaaa.. sipaaatakiii mimiiii… Nirudiisheeeni kwa Zunguuuuu” alianza kulia kwa sauti Kinoge na mamaake kujitahidi kumnyamazisha wakati huo babaake alikuwa anasombelea vitu na kuvipanga kwenye ile nyumba pamoja na wale vijana.
Baada ya shuguli zote za uhamiaji kukamilika na ile gari waliyokuja nayo kuanza safari kuelekea mjini na hatimae sasa Kinoge aliamini kuwa kweli wamefika na hasa pale alipokuja babaake na kumwambia. “Mwanangu Kinoge, maisha ni mlima leo unapanda kesho unashuka harafu maisha ni popote usiangalie mazingira kwanza ukayakimbia unafikiri hata kule mjini kulikuwa vile? kule napo kulikuwa kama huku.. Watu wakahamia na kupasafisha wakaishi na kupatengeneza hadi leo umepaona vile. Basi hata huku napo kutakuwa kama vile endapo tutakaa na kupatengeneza. Haya twende ndani ukasalimiane na bibi eeeh” Maneno ya babaake ndio yaliyompa nguvu Kinoge na kupiga moyo konde kuwa tayari kuanza maisha mapya.
Bwana Juma ambae ni baba mzazi wa Kinoge yeye alikuwa ni mwalimu wa shule ya msingi na wakati huo alikuwa amepata uhamisho wa huko Arusha ambapo aliuomba yeye mwenyewe ili apate nafasi ya kurudi nyumbani kwa mamaake ambae alikuwa mzee na alihitaji uangalizi wake na kwa kuwa miaka mingi aliipoteza Dar mpaka anazaliwa Kinoge na kufikia umri ule alikuwa hajawahi kufika pale kijijini lakini sasa hawakuwa na budi wote kwa pamoja walihamishia makazi kijijini kabisa. Na huo ndio ukawa mwanzo wa Kinoge kupotezana na Zungu.
Maisha ya pale kijijini yalikuwa magumu sana kwa Kinoge na si ugumu wa kula au kuvaa bali ni ugumu wa kuchangamka na marafiki. Hakukuwa na watoto wengi kama ilivyokuwa Dar na mambo yao yaliendeeshwa kimira sana tofauti na Dar walivyokuwa wanaishi kizungu na kujiachia sana. Na hata alipoamishwa shuleni bado mambo yalikuwa magumu na alikosa kabisa marafiki wazuri walioendana na rafiki ake aliyemuacha Dar ambae alikuwa amemzoea kwa jina la Zungu.
Upweke uliendelea kwa Kinoge miezi mitatu zaidi kabla ya siku moja ambapo alishuhudia ugeni wa watu kadhaa nyumbani kwao walioeka kikao na wazazi wake kwa muda mrefu huku yeye akiwa amekaa nje na mtoto wa kiume aliyekuja na wale wazee ambae yeye alionekana mkubwa kuliko Kinoge na kuliko hata rafiki ake wa Dar Zungu. “Eti wewe unaitwa nani?” Kinoge alimuuliza rafiki ake yule mpya waliekuwa wanacheza wote pale nje. “Naitwa Mwin-Chaa-nde umeona mjina wangu huoo!!!? wewe jee?” alijibu yule mtoto na kumuuliza tena Kinoge swali “Mi naitwa Kinoge.” “KINOGE!!!?” “Eeeh” “hahahahahahaaaaaaaaaaaa” “sasa mbona unanicheka?!” “Una jina la Kishaaaambaa Duh!.. Kinoge??!” alicheka sana na kustaajabu yule mtoto wa kiume aliyejitambulisha jina la Mwinchande na kulicheka jina la Kinoge kabla wazazi wake hawajatoka mara baada ya kumaliza kikao mule ndani na kuagana nae huku Kinoge akiwa amekasirika kwa kuchekwa na Mwinchande juu ya jina lake.
Na huo ndio ukawa mwanzo wa Kinoge kukutana na Mwinchande ambae nae alihamishiwa shule ile aliyokuwa amepelekwa lakini tofauti Mwinchande alikuwa darasa la sita huku Kinoge ambae awali alikuwa anaingia darasa la tatu ila alianzishwa tena la pili kutokana na kuwaishwa sana shule. Mazoea yao yaliyoambatana na utani ndio ikawa sababu Kinoge kutaka kubadilishiwa jina na wazazi wake ambao awali walijua ni mambo ya utoto lakini walipoona mtoto wao anang’ang’ana sana na kukosa furaha na amani shuleni na mtaani ndipo alipofika la tatu walifanya masahisho ya jina Shuleni na kumwita jina la Zainab. Jina ambalo lilitolewa na bibiake, mama wa babaake waliekuwa wanaishi nae pale kijijini.
Kuanzia siku hiyo Kinoge alifurahi sana na kulitangaza kila sehemu jina lake jipya huku akiwa hataki kabisa mtu amwite jina la Kinoge. Safari hii alimtambia rafiki ake yule ambae hakujua wanakoishi lakini ilikuwa kawaida kila baada ya siku mbili wazazi wake walikuwa wanakuja kukutana na wazazi wa Zai kuzungumza na katika hali ya kushangaza siku hiyo Zai alishangaa kuona wazazi wa rafiki ake wakija kwao huku mikononi wakiwa wameshika kamba zilizokuwa zinawavuta Ng’ombe wawili wakubwa na kuwaingiza katika zizi moja la miba lililokuwa awali kwaajili ya mbuzina kuwachanganya wale ng’ombe. Awali ya yote Zai alikuwa hajui nini Kinaendelea kwani mifugo ilizidi kuletwa taratibu na hatimae baada ya mwaka mmoja lilijengwa zizi kubwa lililokuwa na Ng’ombe sita sambamba na mbuzi wanane wote wakiwa wameletwa na wale wazazi wa yule rafiki ake wanaetaniana taniana aliyeitwa Mwinchande ambae mwaka huo ndio alikuwa yupo darasa la saba huku Zai akiwa darasa la tatu.
Kumbe nyuma ya pazia kilichokuwa kinaendelea na ambacho kimeongelewa na wazazi wa pande zile mbili ni juu ya kuwaunganisha watoto wao ili watapokuwa wakubwa waishi pamoja. Na hivyo wazazi wa Mwinchande walikuwa wanalipia kabisa mahali ya mtoto wa bwana Juma ambae ni Zai ili awe mke halali wa mtoto wao wa kiume ambae ni Mwinchande. Habari ile ambayo kumbe hata Mwinchande alikuwa anaijua na pindi alipokuwa anamwita Zai mke wangu nae Zai akimwita Mwinchande mume wangu akihisi ni utani tu bila kujua kuwa tayari kuna ukweli ndani yake hadi siku moja alipoitwa na wazazi wake na kumwambia kuwa anapaswa awaheshimu sana wale watu aliokuwa anawaona wanakuja na Ng’ombe pale nyumbani kwani wamelipia gharama za yeye kuja kuishi na Mwinchande baadae pindi atapomaliza masomo yake. Ilikuwa ni kawaida kimila kipindi hiko kuwaoza watoto wangali wadogo japo serikali ilipiga marufuku suala hilo na kuwapa adhbu kali kisheria wale waliobainika kuwaoza mabint zao wangali watoto lakini pia ilikuwa ngumu kuwagundua kama ilivyokuwa kwa Zai na Mwinchande ambao wazazi wao waliwahimiza kuhusu shule.
Baada ya shughuli za kimila kukamilika kipindi hiko Mwinchande alimaliza darasa la saba na Zai ndio alikuwa anaendea darasa la Nne waliunganishwa kwa kufungishwa ndoa ya siri nyakati za usiku na kuanzia siku hiyo kila mmoja alipewa nasaha na kuonywa na wazee kuwa asije kuthubutu kumtaka mtu mwengine wa kuishi nae hapo baadae kwani tayari wao ni mke na mume na watapokuwa wakubwa hawataoana tena bali wataishi pamoja na kuanzia siku hiyo jukumu la huduma za Zai lilisimamiwa na wazazi wa Mwinchande.
* * * * *
Mikosi ilianza kumkumba Hussein miezi michache baada ya kumpoteza kwa kuhama rafiki ake kipenzi aliyekuwa akitaniana nae kama mkewe na hatimae babaake kipenzi ambae ndie aliamini rafiki wa ukweli nae alifariki dunia.
lilikuwa ni zaidi ya pigo kwa mtoto Hussein japo ndugu wengi walitaka kumchukua lakini hatimae aliondoka na mamaake ambae nae haikupita miezi mitatu alifariki ghafra na kuzidi kuongeza pengo la uyatima moyoni mwa Hussein na hapo ndipo alipochukuliwa kulelewa na mjombaake kaka wa mamaake lakini bado hakuwa tena na furaha kwa kuwapoteza wazazi wake mfurulizo namna ile pia aliumizwa mno na maneno ya watu yaliyokuwa yanasemwa mitaani kuwa wale wazazi wake wote walikuwa na virus vya Ukimwi na ndio ilikuwa chanzo cha kuachana kwao miaka mitano iliyopita. Aliumia sana Hussein kwa kuwa tayari alikuwa darasa la nne na mambo ya Ukimwi walishaanza kufundishwa tokea darasa la tatu na alijua kuwa ni ugonjwa m baya na wa aibu mtu kukutwa nao kwa hiyo wanaohadithia wazazi wake walikuwa na ugonjwa huo aliwachukia sana na kuwaona ni watu wabaya upande wake.
Maisha na kwa Mjomba hayakuwa ya kudumu sana baada ya kuchukuliwa na babaake mkubwa aliyekuwa mganga wa kienyeji lakini huko nako alikaa muda mchache kabla shangazi yake kumchukua baaaaasi ilimradi Hussein alikua kwa kulelewa kama mpira wa kona mpaka ile siku alipowashangaza watu kwa kusema anataka aishi mwenyewe kwenye nyumba ya kupanga.
Maisha yalienda ilimradi siku zinaenda na Hussein alisoma kwa Shida mpaka anamaliza darasa la saba hapo ndipo alipoanza kuhangaika mitaani kufanya kazi mbalimbali ili mradi mkono uende kinywani na hakuchoka kujituma. Muda wote alipenda kujichanganya na watafutaji wenzake huku akiwa na ndoto siku moja maisha ataweza kuyamudu nae kujenga nyumba kutimiza mawazo ya babaake ambae mpaka anafariki hakuweza kuwa na nyumba japo alitamani kufanya hivyo.
Wahenga walisema ‘Mungu hamtupi Mja wake’ na ndivyo ilivyokuwa kwa Hussein miaka sita baada ya kuhitimu darasa la saba alibahatika kupata kazi kwenye kampuni moja ambayo iliweza kumlipa pesa zilizomuwezesha kuyamudu sasa maisha yake na kuheshimiwa hata na baadhi ya ndugu zake kwa juhudi alizozionesha na hapo sasa alianza kuyafurahia maisha.
Kipindi hiko alikuwa ana umri wa miaka 21 na hapo ndipo alipoanzisha mahusiano na msichana mrembo aliyeitwa Mariam huku akiwa kasahau mambo mengi ya utoto akiwemo yule rafiki ake wa utotoni aliyeitwa Kinoge. Mapenzi yake na Mariam yalikuwa mazuri mwanzoni lakini baadae kidudumtu kiliingia mara baada ya mwaka mmoja wa mahusiano yao pindi alipokuwa anaangalia kipindi cha YA WALIMWENGU kupitia Becker TV ambapo kulikuwa na mada ambayo msimuliaji alilaani kuwa Wanawake ni Wauaji. Mada hiyo ndio iliyompotezea muda Hussein na kusahau juu ya ahadi ya kukutana na mpenzi wake yule ambae tayari karibu robo tatu ya ndugu zake walishamjua. Ugomvi wao wa ghafra uliosababishwa na kile kipindi mara baada ya Mariam kufika pale kwa mchumbaake na kukuta muda mwingi akiwa bussy na tv kuliko yeye na zaidi alichefuliwa na kile kipindi hali iliyomfanya Mariam aondoke kwa hasira na katika kumtafuta kwake Hussein kwa mara ya kwanza ndipo alipoyaelewa maneno ya kile kipindi mara baada ya kuchezea kichapo cha aibu ndani ya fukwe za coco pindi alipomfumania Mariam akiwa na mwanaume mwengine na hapo ndipo alipoapa kutopenda tena, lakini mapenzi yana nguvu sana na hii ilidhihiri mwaka mmoja baadae baada ya maisha ya kibachela walipopata safari ya kikazi Arusha huko ndipo alipokutana na msichana ambae awali alitokea kumuota kabla hawajaonana kweli akiwa na rafiki ake. Msichana huyo ndie Zai kama alivyoota lakini hakuwahi kufikiria kama Zai yule ndie Kinoge rafiki ake wa utotoni.
* * * * *
Kwa upande wa maisha ya Zai mara baada ya kuozeshwa kimila akiwa bado mtoto maneno ya wazee na wazazi wake yalimjengea hofu ya kuja kukiuka kuwa hajaolewa au kuwa na mwanaume mwengine. Na kwa hali ile ilibidi ampende zaidi Mwinchande na hasa mara baada ya wazazi wake kufariki kwa ajali mbaya ya gari iliyotokea Arusha mjini na hatimae Zai alibaki yatima pindi akiwa darasa la sita wakati huo Mwinchande alikuwa kidato cha tatu akisomea Arusha mjini na ilikuwa kila mwisho wa wiki alirudi kijijini na kuleta zawadi mbalimbali kwa mkewe ambae nae sasa alikuwa anaelewa nini maana na aliamini kuwa Mwinchande ndie mumewe na hana uwezo wa kupinga hilo. Alisahau kabisa habari za Hussein ama Zungu kama alivyopenda kumwita mwenyewe na aliridhia ndani ya moyo wake pindi atapomaliza masomo kuishi na Mwinchande kama ilivyo mipango kwani alikuwa tayari ni mumewe. Lakini kipindi cha kiangazi watu wakiwa katika kuandaa mashamba bahati mbaya lilitokea janga la moto pale kijijini. Moto ulioacha misiba ya kihistoria na huzuni kubwa kwa wanakijiji mara baada ya nyumba nyingi kuungua na mifugo ikiwemo nyumba ya kina Mwinchande ambapo msiba mzito ulitokea mara baada ya wazazi kushindwa kujinusuru na kuteketea huku Mwinchande pekee ndie akisalimika halikadhalika kwa kina Zai napo bibi pamoja na mjukuu wote walifanikiwa kutoka salama japo nyumba yao na zizi vyote viliungua.
Ulikuwa ni zaidi ya msiba kilio kila kona serikali na manispaa ya jiji la Arusha waliwasaidia wahanga wa moto na kuwatengea eneo kulekule kijijini. Kwa upande wa Mwinchande alikuja Shangazi yake aliekuwa anaishi jijini Dar na kujitolea kuondoka nae kumuendeleza kielimu Huko japo shangazi alijua kuwa tayari mwanae ana mke aliyeozeshwa kimila lakini alipuuzia na kuona ni mila potofu na ndio sababu ya kumuacha Zai aendelee kusoma pale kijijini na hata siku Mwinchande anaondka na Shangazi ake mara baada ya kumaliza misiba bibi alimpa moyo mjukuu wake Zai kwa kumwambia asiwe na wasiwasi mumewe anaenda kutengeneza maisha yao na atarudi kumchukua.
Lakini mambo yalizidi kwenda kombo baada ya miaka kuzidi kupita toka kuondoka kwa Mwinchande na shangazi yake huku maisha pale kijijini yakizidi kuwa magumu mpaka pale alipomaliza darasa la saba na kujikuta akikaa zaidi ya miaka miwili mbele bila kuuona uso wa mumewe hadi siku moja alipokuwa katika mizunguko Arusha kipindi hiko alikuwa na umri wa miaka 17 alistuka pindi alipoitwa jina na mtu asiyemfahamu japo kwa mbali sura yake haikuwa ngeni ila alificha. Hakujua mwnzo kama yule ndie Zungu wake kipindi cha utoto na Zungu hakujua kuwa yule ndie Kinoge wake wa utoto na kwa bahati mbaya hayo majina yalikuwa yashakufa kwao wote. Zungu alifahamika zaidi kwa jina la Hussein ambalo Kinoge alikuwa hajalizoea na Kinoge pia alifahamika kwa jina la Zainab ambalo Zungu hakuwahi kulisikia kabisaaaaa.
Baada ya kukutana na yule kijana ambae hakutaka kumwambia jina lake alilijua vipi wakati hawajawahi onana Zai aliondoka huku akiwa na namba ya simu ya yule kijana ambae alimsihi na kumwambia atapompigia ndipo atamwambia amelijuaje jina lake. Na kutokana akilini mwa Zai kuhisi kama kuna taswira ilikuwa inamjia juu ya yule kijana hakusita sana kuichukua ile namba huku akiwa nae anaumiza kichwa pindi alipoondoka kufikiria wapi aliwahi kumuona yule mtu. Lakini kwa bahati mbaya alipofika nyumbani alisahau kabisa ile namba mara alipoiweka kwenye begi na yote ilichochewa na mawazo mengine aliyokuwa nayo juu ya mumewe Mwinchande kwani licha ya uzuri aliobarikiwa Zai lakini bado aliweza kujidhibiti na kujitunza kwa wanaume mbalimbali akikwepa vishawishi akiamini yeye ni mke wa mtu lakini huyo mumewe amekuwa mpotevua na miaka ikawa inazidi kupogoma.
* * * * *
Walionekana vijana wapya wa polisi wakiwa wanapangiwa maeneo baada ya kuhitimu mafunzo ya pili ya jeshi la polisi na kuajiliwa kuwa askali rasmi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. Kila mtu alifurahi pindi majina yalipokuwa yanatajwa na mahala husika ambapo miongoni mwa majina ya wale askari wapya lilisikika jina la Mwinchande na mahala alipopangiwa ambapo ilikuwa ni mkoa wa Pwani Kibaha. Alikuwa ndie yeye Mwinchande mume wa Zai mara baada ya kusoma mpaka kidato cha sita na kwenda kujiunga na jeshi la polisi baada ya kufanyiwa mpango na shangazi yake.
Nyota ilikuwa upande wake Mwinchande toka ajiunge na jeshi la polisi kwani baada ya mwaka mmoja zilitokea nafasi adhimu ya vijana watano waliohitajika kwenda israil kuchukua mafunzo mapya yaliyokuwa yanatolewa jinsi ya kupambana na waharifu wanaotumia akili nyingi tofauti na zile mbinu zilizokuwa zinatumiwa na nchi nyingi za kiafrika hususani Tanzania walichofundishwa ni jinsi ya kumdhibiti na kupambana na muharifu kwa utumia nguvu zaidi na silaha inapobidi. Nafasi ilikuwa imetolewa kila nchi askari watano na kwa bahati nchi ya Tanzania miongoni mwa askari wengi walioomba hiyo nafasi, mwisho wa siku majina matano yalivyotoka na jina la Mwinchande lilikuwa miongoni mwa Askari wanaohitajika kwenda huko Israel ambapo kozi nzima ilikuwa ni ya miaka miwili.
Na huo ndio ukawa mwanzo wa Mwinchande kuvuka mipaka ya nchi na kuzidi kutanua milango yake ya kufikiri na kujengeka fikra pana huku moyoni mwake akimkumbuka mke aliyeozeshwa na wazazi wake na mara zote Mwinchande aliamini yule ndie mkewe na hatoolewa na mwengine kwa kuwa wao hawakuachana. Na kwa jinsi alivyokuwa anamchukulia Zai moyoni na kumpenda aliamini atamkuta tu hata kama atakaa zaidi ya miaka mitano huko Israel na hii ilimpa moyo kutokana kabla hajaondoka alimpa maagizo rafiki ake aliyekuwa mganga wa kienyeji ambae alifahamiana nae mara baada ya kuugua ghafra kipindi akiwa mgeni pale pwani na kuonekana matatizo yaliyomkumba yalikuwa ni ya kienyeji baada ya watu washirikina kumjaribu na hapo ndipo alipopewa msaada na mkuu wake wa kituo ambae alikuwa ni Inspector Cyplian kwa kumpeleka kwa mtaalam wa mitishamba na ramli aliyesifika ambae alikuwa anapatikana katika kijiji cha Hakipo kilichokuwa maeneo ya Kibamba pembezoni kabisa mwa jiji la Dar. Hapo ndipo urafiki wa Mwinchande na Mganga yule ambae alifahamika kwa jina maarufu la Mnyungunyungu ulianza baada ya kuwa anamtembelea mara kwa mara na hata zilipotokea zile nafasi alimlilia Mnyungunyungu aangalie uwezekano wa kulifanya jina lake ling’ae na liwe miongoni mwa majina yatayochaguliwa kwenda kwenye hiyo kozi. Na kweli jina lake lilipotoka Mwinchande alizidi kuamini kuwa Mnyungunyungu kweli ni kiboko na ndio kikawa chanzo kabla hajaondoka alimuhadithia kila kitu kuhusu mkewe aliyeozeshwa angali shule na alimuomba Mnyungunyungu afanye dawa ambayo itamuwezesha pindi atapoonana na yule mkewe asije kubadilika yaani ampende vilevile kama zamani hata kama kuna mwanaume atakuwa kashaingilia kati kipindi yeye hayupo. Na hili ndilo lililomuaminisha Mwinchande ambapo pia alimuomba shangazi yake kama atapata muda aende akamchukue mkewe kule kijijini japo alijua kwa Shangazi yake kufanya vile itakuwa ngumu kutokana yeye hakuipenda kabisa ile mila iliyotumiwa. Na baada ya wiki kadhaa toka uteuzi ule ufanyike hatimae ndipo Mwinchande alipoungana na wenzake kwa safari hiyo ya nchini Israel kwaajili ya hayo mafunzo maalum.
* * * * *
Siku zilikatika kwa upande wa Zai maisha ya kusubiri yalizidi kumchosha lakini bibi ndie alikuwa mstari wa mbele kumsihi na kumpa moyo kuwa mumewe atarudi tu kwani ile ni mira na haivunjiki kamwe. “Bibi mi sidhani kama kweli Mwinchande atarudi kunichukua wakati huko mjini nasikia kuna wanawake wengi wazuri kama nini..” “Hapana mjukuu wangu Zainab Mwinchande ni wako, yule ni mume wako.. Atarudi tu kukufata wee subiri mjukuu wangu, kikubwa ni kuzidi kujisitiri na kusali kila siku.. Usiache kabisa kusali na kumuomba Mungu yeye ndie mjuzi.” alisisitiza sana bibi Zai mara Zai alipokuwa anahoji juu ya suala lile la kurejea tena kwa Mwinchande.
Lakini baada ya muda tena ndipo ilipokuja barua pale kijijini iliyotokea jijini Dar ikimtaka Zainab afanye safari ya kwenda huko ambapo anaishi mumewe. Na barua iliandikwa na shangazi wa Mwinchande mara baada ya kuona Mwinchande akimuulizia sana juu ya kumfata huyo mkewe ambae yeye hakumpenda kabisa wala kumuhitaji kwani alihisi kile kilichofanyika ni dhulma tu kuwachagulia watoto wanaume/wanawake wa kuishi nao. Lakini aliona kwa kuwa Mwinchande mwenyewe king’ang’anizi, aliamua kutuma tu hiyo barua kama ataweza huyo bint aende kama atashindwa basi na ndani ya barua pia kulikuwa na namba yake ya simu.
Moyo wa furaha ulimripuka sana Zai baada ya kupata ile barua na kufanya mawasiliano na shangazi mtu. Nahapo sasa ilibaki kazi ya kufuafua na kujiandaa kwenda Dar es salaam jiji ambalo aliondoka akiwa bado mtoto na toka miaka hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kurejea tena jijini. Lakini wakati akipekuapekua ndipo alipokiona kile kikaratasi chenye namba za simu za yule kijana aliyewahi kutana nae siku moja na hapo ndipo alipokumbuka kumpigia akiwa na shauku ya kujua alimjuaje? kwani upande wake alishindwa kabisa kumkumbuka vizuri. Mara baada ya simu kupokelewa na Zai kujitambulisha alimuuliza tena lile swali huku akimuomba amwambie walipoona na hadi kumfahamu kwani hawatoweza kukutana tena kutokana na safari yake ya jijini Dar. Lakini alishangaa baada ya yule kijana nae kumwambia kua yuko huko huko Dar na pindi atapofika basi wataonana na atamwambia alimjuaje.
Alisafiri salama usalimini toka Arusha hadi katika jiji la Raha na Karaha na alipofika ubungo alipokelewa na Shangazi yake Mwinchande na kufika nae Kinondoni ambapo ndipo walipokuwa wanaishi. Wiki moja baadae Zai alifanya mawasiliano na kukutana na Hussein maeneo ya stendi Mkwajuni baada ya kumuacha shangazi yake akiwa amelala mchana ule lakini alipofika kuongea na Hussein nia na madhumuni kujua alimjuaje juaje alishangazwa na majibu ya Hussein eti kuwa alimuota ndotoni. Akilini mwake Zai alihisi hawa ndio wale wanaume aliowasikia wapenda ngono na kumtaka kila msichana mzuri na hivyo alimkataa kabisa palepale na kumsisitizia kuwa yeye kilichomleta Dar ni masomo na si vinginevyo, jambo ambalo moyoni mwake alijua si kweli lakini hakuona umuhimu kumwambia vile kutokana na jinsi yeye mwenyewe alivyo.
Aliporudi ndipo kwa mara ya kwanza alianza kuigundua roho mbaya aliyokuwa nayo Shangazi ake Mwinchande mara baada ya kumkuta ameamka. “Hee! yaani wewe huna hata mwezi tayari ushavijua hadi vichochoro vya kukuniwa?… Wewe ni bint wa aina gani unafanywa hadi mchana huu tena ugenini..? haya utanambia ulipokuwa wapi na umalaya wako usije kuniulia mwanangu..” alibwata shangazi na kuanza kumpiga Zai na ufagio uliokuwa pale ukumbini kama mtoto mdogo.
Maisha yalienda kwa mtindo huo pale nyumbani na kipindi hiko chote hakuwahi kupata nafasi ya kuzungumza na mumewe ambae ni Mwinchande aliyekuwa huko Israel ktk mafunzo maalum na hadi unakatika mwezi tayari Zai maisha ya pale kwa Shangazi yalimkifu mno na hadi kufikia kukubali moyoni mwake kuachana na Mwinchande ili apate mwanaume mwengine ambae kidogo kwao kunaweza kuwa na amani kuliko maisha ya pale kwa shangazi vile anavyofanyiwa mara kwa mara na kupewa maneno ya kashfa na kejeli asijue wapi zinapotokea huku akiambiwa kuwa asije akamuua Mwinchande kutokana na tabia yake ya umalaya ambao hakuujua kabisa na ukweli hakuwahi kukutana kimwili na mwanaume yeyote tokea kuzaliwa kwake. Hali ile ilimfanya siku moja amkumbuke Hussein na kutamani kumfahamu zaidi. Lakini aliwaogopa sana wanaume Zai hali hiyo ilimfanya kabla hajampigia Hussein simu alipiga kijijini kwao Arusha kwa Ustaadh mmoja aliyekuwa na utaalam mkubwa wa kusaidia watu kupitia Marohani (Majini) na ndie huyo aliyemfundisha yeye Qur’an. Mara alipompigia simu simu na kuongea nae kwa kujiiba siku moja majira ya usiku ndipo alipomuelezea juu ya kijana aliyekutana nae toka Arusha na kwa mara ya pili Dar ambae alimwambia kuwa eti jina lake aliliota, hivyo alikuwa anataka Ustaadh kupitia marohani yake wajaribu kumtazama huyo kijana kama ni mwanaume mzuri au ni wale wahuni wenye tamaa na ndipo hapo Ustadh yule alipofanya mambo yake baada ya kutaka jina la huyo kijana na vile alivyo ndipo baada ya dakika kadhaa Ustadh alianza kuzungumza lakini safari hii kwa sauti tofauti na ya awali na Zainab aligundua kuwa sasa anayezungumza nae ni Jini. [[“Zainab, huyo Kijana ni mwanaume mzuri sana kwako kuliko huyo unayeamini mumeo kwa sasa. Japo nae anakupenda…! lakini si mume bora kwako kama huyo Hussein. Pia labda tukwambie kitu huyo Hussein ndie mumeo ambae Allah amekuandikia uwe nae na kupata familia na ukumbuke mwenye kumiliki Ndoto nini Mwenyezi Mungu pekee… Amemuonesha Hussein wewe ni nani sasa baada ya kutojua kuwa ulibadilishwa jina.. Yaani ina maana kama hujui yule Hussein ndie yule yule rafiki ako wa utotoni uliyemjua kwa jina la Zungu. Na inaonesha wazi Mungu ndie anayewakutanisha nyinyi ili muungane muwe kitu kimoja na amini kabisa kulingana na nyota zenu zilizong’aa pamoja tangia wadogo kuwa matatimiza ndoto zenu kama mkiwa pamoja. Hussein ana ndoto ya kujenga nyumba na kama akikuoa hautopita muda mrefu atajenga kweli na wewe una ndoto ya maisha ya furaha na watoto wawili wa kwanza awe wa kiume na wa pili wa kike, na kama utaolewa na Hussein kwa mapenzi yake Mungu utapata ila kama haitakuwa hivyo basi niyi nyote hamtotimiza ndoto zenu pia utengano wenu wowote ule unaweza kuleta madhara ama dholuba kubwa, tena Dholuba kubwa sana litaloponza hata nafsi za watu wasio na hatia….. Kumbuka haya Zainabu jua kama hutokuwa muwazi na kumwambia Hussein kuwa uliwahi kuolewa kimira basi jua utakuwa bado unatengeneza dhoruba kubwa zaidi kwa jinsi nyota za huyu mumeo zinavyoonyesha. Muombe sana Mungu Zai usiufiche ukweli ingali bado mapema. waaadhaa Salaaam..”]] Ndivyo alivyomaliza yule Jini aliyeongea na Zainab kupitia Ustadh na maneno yake yalimfanya Zainab apigwe bumbuwazi baada ya kusikia kuwa kumbe yule kijana ndie yule Zungu wake wa utoto. Alijikuta anatabasam na kumshukuru Mungu kumkutanisha tena na Zungu japo alijua kuwa Zungu hamkumbuki na hakutaka amkumbushe kwani alijua angesababisha maswali kuwa mengi mwisho wa siku akayajua mabo ambayo hakutaka ayajue. Na hapo ndipo alipompigia simu Hussein na kumuomba amuelekeze anapoishi ili aweze kwenda mwenyewe wakaongee kirefu zaidi juu ya kile alichokizungumza awali.
* * * * *
(“Wanaume ni watu waongo kweli, yani Mwinchande kumuamini kote leo hii ameondoka ameniacha nimekuja kukaa na shangazi na hata muda wa kuongea na mimi hana?! sasa hat huyu lazima nimpe masharti kabambe nisiamini moja kwa moja kwa sababu eti nimeambiwa na kiumbe mwenye uwezo wa kuona zaidi yangu.. Lazima nimpe mtihani”) Yalikuwa ni mawazo akilini mwa Zai siku aliyokuwa anaenda kukutana na Hussein na kweli baada ya mazungumzo yao alimpa masharti magumu sana matatu ambayo yote Hussein alikubaliana nayo na kumshangaza sana Zai aliyejikuta furaha inamzidi na kumkumbatia Hussein huku akijisahau na kumwita jina la Zungu ambalo lilistua masikio ya Hussein lakini mwishoe alipuuzia tu japo kuna muda alitamani kumuuliza amelijuaje lile jina lakini kutokana na kuwehuka ghafra kwa vile alivyokubaliwa huku akiwa kaekwa kwenye mabano ya mtihani ambao kwa upande wake aliamini lazima ataufauru kwani aliweza kukaa mwaka mzima kabla hajaonana na Zai baada ya kuachana na mchumbaake wa awali Mariam ambae kumbe alikuwa na mimba changa siku wanaachana na hakulijua hilo hadi kipindi hiko anakubaliana kuwa wapenzi na Zai tayari upande wa pili Mariam alishajifungua katoto ka kike.
Lakini baada ya miezi kadhaa Mwinchande alirejea Tanzania kwa dharula maalum mara baada ya wenzao wawili kufariki katika mazoezi maalum ambayo hayakuekwa wazi huku yeye Mwinchande akibaki na alama ya kuchomwa na kitu cha ncha kali maeneo ya shavu ambayo alama ile iliyojichora herufi ya X haikuekwa wazi nini hasa kilichopelekea zaidi ya yeye mwenyewe kukiri kuwa aliumia kwenye hayo mafunzo na wenzake wawili wote walikufa kwa bahati mbaya kwenye hayohayo mafunzo. Na mara baada ya Mwinchande kurudi na kumkuta mkewe wa mila alifurahi mno japo hakupata muda wa kukaa nae na kuzungumza mipango kutokana na kupewa wiki moja tu na Taifa ili watapomaliza kuistili miili ya wenzao basi na wao warejee wakamalizie hiyo kozi ambayo ilijumuisha askali kutoka nchi mbalimbali. Lakini kuna jambo ambalo Mwinchande aliliona la muhimu sana lililomfanya siku mbili kabla ya safari ya kurudi Israel aliomba ruhusa ya uongo ya masaa sita ambayo aliyatumia kurudi nyumbani na kumchukua mkewe hadi kwa rafiki ake yule mganga aliyeitwa Mnyungunyungu nia na madhumuni ikiwa ni kumuonesha live huyo mkewe aliyewahi kumuongelea japo Zai hakuelewa kitu na nia ya pili ilikuwa ni yeye mwenyewe kufanyiwa dawa itayomuwezesha kufuzu vizuri kwenye hayo mafunzo na hapo ndipo Manyungunyungu alipomfanyia kitu maalum na kuipitisha dawa aliyoiita ‘Kauzibe’ kuwa itamfanya awe mtu asiyeonekana iwe kwenye vita au matatizo yatayomfanya atafutwe na kadhalika na alimwambia pia ile dawa ua ‘kauzibe ‘ itaweza kudumu mwilini mwake kwa miaka thelathini, jambo ambalo Mwinchande alilifurahia mno. na kumpa zawadi kubwa ya fedha taslimu Manyungunyungu kabla ya kuondoka na mkewe na kumrudisha nyumbani nae kurudi kambini kureport na baada ya siku mbili walirudi tena Israel
Siku zilienda haraka na baada ya kuondoka Mwinchande kama kawaida huku mateso na manyanyaso yalirudi na kuzidi kwa Zai pale alipoishi na yule Shangazi, ikafika muda Zai akiwa anaongea na yule Ustaadh kwa njia ya simu alikuwa hadi analia jambo lililomfanya Ustaadh aende kumshawishi bibiake Zai kuwa akubaliane nae wamruhusu mjukuu wake kuondoka tu pale na kuja na huyo mwanaume aitwae Hussein ambae Ustaadh alimuhakikishia yule bibi kuwa huyo ni mwanaume bora kuliko wanavyofikiria. Na kutokana na kuheshimika sana kwa yule Ustaadh pale kijijini ndipo bibiake Zai alipokubali bint ake ampeleke huyo mwanaume kule kijijini wamuozeshe tu akaishi maisha ya amani na upendo kuliko pale alipokuwa anateseka na kunyanyaswa bila sababu ya msingi. Na hayo yote yalitimia baada ya mwaka ambapo Zai aliamua kumfanyia Suprise Hussein na kuamua kuubatilisha ule uongo wake wa awali pindi aliposema kuwa alikuja Dar kwaajili ya masomo na badala ya kumwambia ukweli kama alivyopewa yale maagizo na yule jini wa Ustaadh. alijikuta Zai akiuvua uongo ule wa shule na kujivisha uongo mwengine kuwa alikuja kwaajili ya kazi zandani na yote yale alifanya vile kwaakili zake kuwa Hussein ndio atamuelewa na kumpokea kuliko angesema kuwa aliolewa basi asingeaminiwa na angeachwa kwenye mataa. Kumbe hakujua kabisa Zainab kama uongo wake alioendelea kuufuga kwa maslahi ya muda ule… ulikuwa unatengeneza hasara kubwa ya baadae.
Baada ya Zai kuhamia kwa Hussein na kumhakikishia kuwa yeye alikuwa bado bikra hasa mara baada ya Hussein kutaka kulazimisha wafanye mapenzi usiku, safari ya kwenda kijijini kwao ilipangwa ndani ya wiki hiyo ambapo katika hali ya kupagawa na penzi la msichana mrembo Zai, Hussein alijikuta anakubali na kupanga safari hiyo bila kuwasiliana na ndugu zake na mwishoe waliondoka wawili tu mpaka kule kijijini Arusha ambapo Ustadh yule yule ndie alihusika kuwafungisha Ndoa hiyo iliyomshangaza hata Hussein mwenyewe baada ya kutajiwa mahali ndogo sana kiasi aliona kama ndoto kumuoa msichana mrembo na mwenye tabia za kipekee kama Zai kwa pesa ile. Lakini ukweli ulibaki vile Hussein alimuoa Zai kabla ya kufanyiwa sherehe ndogo ya kimila usiku wake na kulala pamoja kwa mara ya kwanza aliweza kumuingiza katika ulimwengu wa kiutu uzima Zai mara baada ya kumtoa bikra kulekule shamba na kumbe kulikuwa na mabibi maalum wa mila waliokuwa wanasikilizia kujua mjukuu wao wa kike alijitunza kiasi gani lakini waliposikia ukelele walijua hapo ndio penyewe na kuangusha kicheko kilichowajulisha ndani Zai na Hussein kuwa kuna watu walikuwa wnawachungulia.
Hawakukaa sana pale kijijini baada ya ndoa ya ghafra iliyohudhuliwa na watu wachache mno, ndipo Hussein alipomchukua mkewe kurejea jijini Dar na kuwataarifu habari zile ndugu zake kwa njia ya simu ambao wengi walimlaumu kwa kuoa pasi na kuwaarifu mapema na ndipo mjombaake Hussein alipomuandalia tafrija fupi ya kumpongeza ambayo alimwambia atapofika tu afikie pale kumtambulisha mkewe kwani na ndugu wengine watakuwepo pamoja. Na ndivyo ilivyokuwa baada ya Hussein na Zai kuwasili jijini Dar walifikia kwa mjomba ambapo baadhi ya ndugu wa Hussein walikuwepo kumpongeza na kuwatakia kila la kheri katika maisha yao mapya wanayoenda kuyaanza. Lakini katika utambulisho mmoja wa ndugu wa karibu kabisa wa Hussein upande wa babaake ambae alikuwa ni mkubwa kuzaliwa aliyejishughulisha na mambo ya tiba asilia au uganga alimshangaa mno mara baada ya kumuona bibi harusi na kubaki na maswali mengi kichwani mwake asijue aanzie wapi kuongea na mwanae juu ya mkewe ambae alionesha kuwa anampenda kupita kiasi. Hakuwa mwengine huyo ndugu bali ni Mnyungunyungu ambae hata Zai alipoiona sura ya mganga Mnyungunyungu alistuka moyoni mwake lakini alijitahidi kuficha ili watu wasigundue chochote juu yake zaidi ya yule mganga Mnyungunyungu kuzidi kumuangalia kwa taharuki. Hali ile Hussein hakuipenda na hata kesho yake Mnyungunyungu alipojaribu kumpa maneno ya kumfanya amuulize kulikoni juu ya mkewe lakini Hussein ndio kwanza alimkingia kifua mkewe na hakutaka kusikia chochote kibaya kikihisiwa wala kusemwa juu ya mkewe kwani kitendo tu cha kumkuta Zai bikra akiwa na umri ule tena mwenye uzuri wa ajabu kuanzia sura mpaka umbo na bado kaweza kujilinda na vishawishi kutoka kwa wanaume mbalimbali..!? Hakika bikra ya Zainab ilikuwa silaha tosha ya uaminifu kwa Hussein asitake kusikia maneno eti Zai alishawahi kuwa na mwanaume tena ingekuwa kichekesho kabisa kwake kama angesikia eti huyo uliyemuoa ameshaolewa muda mrefu. Halkadhalika yote na yote Hussein na Zainab waliweza kuanza maisha yao mapya kama mke na mume rasmi.
Siku zilienda baada ya Hussein na Zainab kufunga ndoa na kama alivyotabiri yule jini aliyeongea nae Zai kupitia Ustadh wake kuwa pindi atapoolewa na Hussein basi ndoto zao zitatimia pamoja kutokana na nyota zao zinavyosoma, na ndivyo ilivyokuwa kwani baada ya mwaka mmoja tu waliweza kupata pesa iliyowawezesha kuknunua kiwanja huko Kigamboni. Upendo wao ulikuwa unazidi kuimalika siku baada ya siku kila wanavyoonana yaani walipendeza mno. Kwa kiasi kikubwa Zai aliweza kuifanya tabia ya Hussein izidi kuwa nzuri na kuwashangaza hadi rafiki zake hasa alipoanza kusali. Hali hii iliongeza amani na furaha wala hakuna aliyewaza kati yao kama ipo siku watakuja kunyoosheana walau vidole lakini kumbe bado ile siri aliyokuwa anaifuga Zai ilikuwa inazidi kulimong’onyoa shina la mti wa wapendanao pasi na yeyote kujua wala kuhisi.
Baada ya mwaka mmoja ndipo shughuli za usimamizi wa ujenzi zilianza huku Zai akiwa ndie msimamizi mkuu kutokana na Hussein kubanwa na mambo ya kazi na kutaka kumuonesha mkewe jinsi gani anamuamini. Lakini siku baada ya siku kadri nyumba kule ilivyozidi kusogea na kuanza kufika usawa wa madirisha, siku moja Zai majira ya jioni alipokuwa yupo kwenye Pantoni amesimama alistushwa na sauti ya mtu mmoja akimwita kwa jina lake kutokea kwenye gari moja kubwa ya Maofisa wa polisi na alipogeuza macho kumtazama aliyemwita hakuamini kabisa pindi alipomuona askari aliyevaa sare yenye vyeo vingi huku akiwa na wenzake wawili kwenye ile gari na hakuwa mwengine yule polisi bali ni Mwinchande. Moyo ulimripuka sana Zai pindi alipomuona Mwinchande na hofu pia ilianza kutanda kwenye ubongo wake na kushindwa kujua jinsi ya kumtoka toka hasa alipomuona akifungua mlango wa ile gari na kushuka kumfata pale aliposimama. “Kweli Mungu muacheni aitwe Mungu aaaaah! ni zaidi ya miezi mitatu toka nimerejea nakutafuta wewe tu mke wangu kila kona hadi Arusha sikuoni… Dah! lakini leo hatimae Mungu kanionesha. Najivunia sana mke wangu Zainab, habari za siku..?” aliongea kwa furaha Mwinchande mara baada ya kufika pale aliposimama Zai amba alitamani ayeyuke kwa jinsi moyo ulivyokuwa unamuenda mbio akishindwa atunge uongo gani ili iwe rahisi na salama kwake kumuepuka Mwinchande kwani tayari pia yeye ni mke wa Hussein tena wameoana kila mmoja akiwa na akili timamu mbele ya Sheikh tofauti na wao waliozesha ozeshwa tu kiila na walikuwa wote hawajui kitu kuhusu Ndoa, hasa Zai kwani ndie alikuwa mdogo sana. Lakini alishindwa kujua aongee neno gani la kueleweka mbele ya Mwinchande muda ule? na huo ndio ulikuwa mtihani kichwani mwake kipindi hiko Pantoni ilikuwa inaegesha upande wa Posta.
“Zai mbona unaonekana kujifikiria mke wangu! twende basi tutaongea vizuri.” aling’ang’aniza Mwinchande mara baada ya kuona Zai amejibu ile salamu kinyonge na alipoombwa waingie kwenye gari alionekana kusita huku akifikiria kitu. Alichowazia zaidi ni vipi akubali aondoke na Mwinchande wakati tayari kuna Hussein anamsubiri nyumbani? Aliamua kutunga uongo ili amuepuke Mwinchande siku hiyo lakini bado uongo wa Zai haukuwa na nguvu mbele ya Mwinchande. “Nakuomba mume wangu nakuomba sana, mimi ni wako na Mungu ametukutanisha tena ila hebu angalia ni ghafra sana tumekutana ni muhimu uniache kwanza niende kwa huyu mama, harafu nikishaaga na kuweka mambo sawa basi Kesho tutakutana mume wanguuu” alizidi kuomba Zai na safari hii kidogo Mwinchande alilegeza uzi. “sawa basi kwa kuwa kesho jioni tutakuwa na safari inabidi unitafute mapema asubuhi nitakuelekeza wapi nilipo tuweke mipangon ya maisha yetu sawa mke wangu.” aliongea Mwinchande na kumkabidhi namba za simu Zai sambamba na Elfu hamsini za nauli ya daladala hiyo kesho na hapo ndipo alipofaulu Zai kumkwepa Mwinchande siku hiyo lakini alijua kuwa kesho ana kibalua chengine kigumu jinsi ya kuondoka hiyo asubuhi kukutana na Mwinchande. Moyo wake ulijikuta unakuwa na hofu kila anapomfikiria Mwinchande kuliko Hussein na ikumbukwe hiyo yote ni kwa sababu ya dawa aliyotengenezewa Mwinchande juu yake Zainab.
Na kweli siku ya pili yake aliwasiliana na Mwinchande kwa siri na kukutana nae maeneo ya hoteli ya Kilimanjaro. Kabla hajatoka Zai alifanya utundu wa kuchanganya ndimu (…) kuji(……..) kwenye(………..) mwishoe alifanikiwa kujitengenezea bikra ya uongo ili iwe silaha yake kwa mumewe Mwinchande kwani alijua lazima watapokutana atataka ahakikishe kama kweli hajamsariti na kulingana na mila za kwao mwanamke aliyekuwa si bikra hafai kuolewa na ndio kigezo cha wazee wengi kuwaoza mabint zao mapema ili wasije watia aibu hapo baadae.
Na kweli alichokifikiria Zai ndicho kilichotokea kwani pindi tu Mwinchande alipokuwa na Zai chumbani alianza kumdadisi. “Mke wangu wewe ni mzuri sana tena sana, hivi hujashawishika kweli?!!” aliuliza Mwinchande huku akimshika sehemu za paja Zai aliyekuwa anajifanya bado mtoto. “Aiii, Jamaani ina maana huniamini? Mi bado nipo kama ulivyoaniacha mume wangu nimejilinda sana kukusubiri.” alijibu kwa kudeka Zai na kuzidi kumpa matamanio Mwinchande. “Kweli?!” “Kweli mume wangu.” “Basi acha nihakikishe kabla sijasafiri leo.” aliongea Mwinchande huku akizidi kumpapasa Zai “aaagh, jamaaani mi naogopaaa.” alizidi kudanganya Zai na kumfanya Mwinchande aanze kutumia nguvu ambapo ukweli walisumbuana sana huku Zai akibana miguu na kurusha mateke lakini kutokana na mbinu alizokuwa nazo Mwinchande ukijumlisha na hamu ya tunda, mwishowe alifauru kumsongomeka dungio lake alilolijaza mate ya kutosha ili iwe rahisi kumuingilia na ndipo Zai alipopiga kelele ndani ya kile chumba kama amekanyaga mwiba kwenye kidonda cha unyayoni na kumfanya Mwinchande achomoe taratibu gunguso lake ambalo lilibahatika kuingia kidogo na kutokana na hamu iliyochochewa na usumbufu alioupata alijikuta Mwinchande akifika kilele palepale alipoanza kulirudisha nyuma kwaajili ya kulichomoa “Ooooooooghh Shiit..” Aliugulia kwa mautamu Mwinchande pindi alipokuwa anajitua mzigo wa nye* na alipoitoa kabisa aliamini kwa kuona kweli damu zimetapakaa kwenye dunguaji lake na kufurahia moyoni kwa kuweza kumtoa katika utoto mkewe yeye mwenyewe hali iliyomfanya aamini kweli Zai ni mwanamke wa kipekee.
Kazi ilibaki kum bembeleza Zai aliyekuwa analalamika kuhisi maumivu makali sehemu zake huku akilaani mapenzi kumbe yanaumiza vile na kuzidi kuziteka hisia za Mwinchande kuamini kuwa kweli Zai alikuwa mtoto sana. Ilibidi Mwinchande amuachie kiasi kikubwa cha pesa Zai na kumtaka afanye mpango wa kurudi Arusha ili akamchukue rasmi kwa utaratibu na baraka za bibi waweze kuwa pamoja. Nae Zai alikubali kabisa na akilini aliona mchezo aliouanzisha anaweza kuumaliza bila tatizo japo aliuanzisha bila kujua ataumalizaje.
* * * * * Siku zilienda kwa mara ya kwanza Zai aliweza kumsariti mumewe Hussein bila kuwaza kama itafika siku atamfanyia hivyo Hussein. Na siku ambayo Zai anakutana na Mwinchande pale hotelini alikuwa tayari ana Mimba changa ya wiki tatu hali iliyomfanya baada ya kupita wiki ambapo ndio alikuwa anaingia mwezini alishangaa kuona amepitiliza na kuamua kwenda kupima kimya kimya kwanza akiwa na kigezo kikubwa cha kutoka nyumbani ni kwenda kuangalia ujenzi kigamboni. Alipima na kugundulika kuwa na mimba ya Mwezi mmoja na alipopiga mahesabu aligundua kwa asilimia zote mia mimba ni ya mumewe Hussein lakini aliwaza itakuwaje Mwinchande atapokuja kugundua kuwa yeye ni mjamzito? Na je atawezaje kuishi na wanaume wawili kwa wakati mmoja? (“Aaagh! Mungu atanisaidia siwezi kutoa hii Mimba, Mwinchande hatoweza kugundua kitu namvutia pumzi wiki tatu namwambia ninavyojisikia na Hussein ananiamini sana nitamuomba ruhusa ya kwenda kijijini nikafanyiwe dawa ili Mimba ikue salama na nitatumia muda huo kukutana na Mwinchande ili aniamini zaidi tutafika kwa bibi… aaagh, nitampanga tu bibi atanielewa… Nikishampelekea sukari na mkate hatokuwa na neno na uzee ule. Mchezo mdogo tu mwishoe nitajua yupi bora nimfate. mh! ila wananishanganya.. lakini acha nitumie akili za ziada za kuzaliwa naamini kila kiru kitakuwa sawa.”) Aliwaza na kujiambia akilini mwake Zainab mara baada ya kujigundua ni mja mzito.
Mbali ya kuwa mcha Mungu wa kusali, mwenye kupenda kujisitiri, mkwepa vishawishi, mpole, mtaratibu, ana roho nzuri, mkalimu…. lakini bado alisahau kuwa yeye ni mwanamke na Mungu amemuumba kuwa mtu wa pili Duniani baada ya mwanaume. Alijisahau kuwa upeo wake wa kufikiri na utendaji hasa juu ya maswala yajayo umewekewa ukumbi finyu tofauti na mwanaume. Alisahau kuwa mwanamke ubongo wake hucharge taratibu sana kuliko mwanaume hasa katika maamuzi ya haraka na magumu. Laiti angejua maamuzi aliyokuwa anayafanya siku ile aliyokutana na Mwinchande yangekuja kuleta balaa kubwa baadae, basi angekubali alaumiwe mwenyewe tu siku ile na aachwe na Mwinchande kwa maneno ya kashfa ambayo yangemuumiza kwa siku kadhaa lakini baadae maisha yangeendelea na kila kitu kingebaki hadithi. Lakini aliogopa lawama Zai. Aliogopa kuonekana mwanamke aliyekosa uvumilivu na kumsariti mtu ambae tayari alikuwa mumewe, pia aliona kama ataenda kinyume na Mwinchande anaweza kuwa ameenda kinyume na matakwa ya wazazi wake. Lakini alisahau kujiuliza, mbona alishamsariti Mwinchande na kuolewa na Hussein? na mbona sasa amemsariti na Hussein? japo alijiona yuko sawa kwa upeo wake lakini Zainab hakuwa sawa kabisa na kadri siku zilivyozidi kwenda mbele alijikuta anazidi kutengeneza bomu hatari zaidi ya Nyuklia asilojua hata jinsi ya kulitegua.
* * * *
Akiwa safarini Mwinchande ambae alikuwa anamuendeesha Kamanda mkuu mpya wa Jeshi la polisi nchini ambae pia aliwahi kuwa mkuu wake wa kituo alichoanzia kazi pale Kibaha mkoa wa Pwani aliyeitwa Cyprian Ng’umbilwa. Tabia za Cyprian kupenda sana wanawake zilikuwa zinamkera sana Mwinchande lakini alishindwa jinsi ya kufanya na hata hiyo safari waliyokuwa wanasafiri siku hiyo majira ya jioni wakienda jijini Arusha haikuwa kwa niaba ya kazi ama ziara yoyote zaidi alikuwa anampeleka kwa kimada wake tuu. Na hiyo ilikuwa ni safari ya tatu ya kuunganisha juu kwa juu mara baada ya kutokea Mwanza, Shinyanga kulipokuwa na kikao maalum cha makamanda wa polisi na sasa badala ya kurudi Dar Cyplian aliamuru msafara wote utangulie na yeye kuondoka na Kiraia na Mwinchande ambae alikuwa anaaminiwa sana kutokana na uwezo alioupata huko Israel na alipewa jukumu la kumuendeesha Kamanda mkuu wa jeshi na kufundisha makamanda mbinu maalum za nadharia alizozipata huko Israel japo yeye alikuwa zaidi kwa kujua na vitendo. Mawazo yake zaidi Mwinchande yalikuwa kwa Zai ambae siku hiyo mapema alimpigia simu kumjuza kuwa yeye ni mjamzito na alinasa hiyo mimba siku ileile ya kwanza walipokutana vilevile keshokutwa yake alikuwa anarudi rasmi Arusha. Mwinchande alifurahi awali akijua wakiunganisha Dar mapema angemuwahi mkewe lakini kitendo cha mkuu wake kilimfanya aendeeeshe gari huku akiwa na hasira sana moyoni mwake lakini ilikuwa ngumu mno kubaini usoni mwake.
Baada ya siku mbili za utumwa jijini Arusha siku hiyo ambayo Mwinchande mapema aliwasiliana na mkewe aliyemuelekeza kuwa yuko safarini na hiyo siku ndipo ilipotakiwa sasa kurejea na Kamanda Cyplian jijini Dar lakini Mwinchande aliweza kufanya ujanja ujanja hadi wakachelewa na Zai alipofika stand na kumpigia simu Mwinchande aliyeenda na gari akiwa na bosi wake wakati wakiwa tayari kuondoka na hapo ndipo macho ya Cyprian yalipoiona sura nzuri ya Zainab na kujikuta anaapa nafsini mwake kumpata pasi na kujua ni mke wa Mwinchande.
“Yule mwanamke uliyesimama nae pale ni nani?” aliuliza Cyprian baada ya Mwinchande kurudi garini. “Aliwahi kuwa mwanafunzi mwenzangu.” “Basi vizuri naomba ufanye chini juu nimpate, hakika nitaoa kabisa hahaaaa” aliongea huku akicheka Cyprian bila kujua anatonesha kidonda kisichoguswa na hapo ndipo kukaanza tatizo mara baada ya Cyprian kuamua kushuka mwenyewe kumfata Zai kuongea nae ambae alikuwa amesimama akingojea gari ya kwenda kijijini kwao ifike mara baada ya kuongea na Mwinchande. (“Huyu mkuu ananitaka ubaya sasa… Anatafuta kifo”) aliongea moyoni kwa hasira Mwinchande pindi alipokuwa anamuangalia Cyprian akimsemesha Zai na baada ya muda alishangaa kuona Zai ameamua kuchukua taxi kuondoka baada ya kuona ushawishi wa Cyprian unazidi. “sasa Mwinchande yule bint inaonekana amekuzoea sana wewe na mimi hafahamu kama ni mtu mkubwa hivyo hakikisha tukifika Dar unafanya utaratibu wa gharama yoyote nimpate.” “sawa mkuu.” alijibu Mwinchande na kuwasha gari kuondoka eneo lile huku moyoni akijiapiza endapo kama mkuu wake akiekea mkazo suala lile anaweza hata kumuua. Alishindwa kumwambia kuwa yule mkewe kwa kuwa hakukuwahi kuwa statement yoyote toka anapokelewa kuwa ana mke na yule alikuwa ndie mkuu wake toka anakuwa polisi hivyo alimjua vizuri japo hakuijua siri yake na Zai.
Baada ya siku kadhaa kupita Mwinchande alipoona usumbufu unazidi kwa bosi wake siku hiyo aliamua kumchana ukweli bila kujali ukuu wake wala nini. “Sikia kiongozi, ujue nimekuvumilia sana lakini naona bado unakazania sasa nataka ujue yule mwanamke nina mipango nae tayari.” aliwaka Mwinchande hadi Cyprian alishangaa na hapo walijikuta wanatengeneza bifu la kijinga na Cyprian alikosa ujanja jinsi ya kumuadhibu Mwinchande zaidi alimtafutia safari kimakusudi kupitia wazili wa mambo ya ndani na kulichomeka jina la Mwinchande awe miongoni mwa maafsa wataoenda kwenye kozi nyengine ya ngazi ya juu ya kipolisi nchini India, lakini nia na madhumuni ya Cyprian ni kumkomoa Mwinchande wakose wote akisahau kuwa upande mwengine anamtengenezea nafasi ya kuheshimika zaidi.
* * * * *
Kwa upande wa Hussein hakuona kazi wala ajizi kumuacha mkewe aliyempenda na kumuamini vilivyo kuwa aende Arusha kwao kwa safari ya mwezi mmoja kutengenezewa dawa juu ya mimba aliyokuwa nayo kwa kuhofia mambo ya wanga na wachawi.
Hakuwahi kuwaza wala kufikiria kama kuna mchezo wowote unachezwa nyuma ya pazia na hata Zai alipofika kijijini alimlewesha maneno bibiiake na kwa bahati mbaya yule Ustaadh alikuta amefariki ambae alifikiria kuongea nae ampe msaada wa kusolve tatizo lake alilolianzisha na hivyo baada ya kumkosa tena Ostaadh wake yule hakutaka tena mtu mwengine ajue suala lake nakutokana na bibi kuwa mzee sana alikosa amri kwa kile alichokuwa anamwambia mjukuu wake hasa kutokana na bibi kuanza kupoteza kumbukumbu kutokana na kuzeeka sana.
Baada ya mwezi ndipo Zai kweli alirudi kuishi na mume wake kipindi hiko Mwinchande walipata tena safari ya India ambapo jina lake lilichomekwa na Cypian kwaajili ya kumkomesha tu asifanikiwe kumpata yule bint bila kujua kuwa tayari alikuwa me wa Mwinchande kimila.
Miezi ilisonga na hatimae kwa mara nyengine Hussein alisafiri na Zai mpaka kijijini kwao na kumuacha kipindi akiwa na mimba ya miezi sita nae kurudi katika mihangaiko yake ya kujiandaa kwani alijua anakwenda kuwa baba siku si nyingi. Lakini baada ya miezi tisa kutimu hadi Zai anajifungua kule kijijini Mwinchande ndie aliyekuwa wa kwanza kufika mara baada ya kutoroka mara moja India na kurudi Arusha ambako alikaa kijijinisiku mbili kwa shauku ya kumuona tu mtoto aliyeamini ni wake na yeye alikuwa mwanaume wa kwanza kumbeba mtoto yule huku akiwa na furaha mno. “haaaaaa… babaangu amezaliwa.Babaangu amezaliwaa huyu ni Shaaban.. huyu ni Shaaban” alizunguka na kufurahi Mwinchande huku akiwa amekibeba katoto kale kachanga na kumpa jina la Shaaban.
Hila iliyofanyika ni kwamba Hussein alicheleweshwa kupewa habari za kujifungua Zai kwa kuhofia asije kugongana na Mwinchande ukawa mtihani kwake. Hakufikiria kuwa hata yale yaliyofanyika bado kuna mtihani na mdudu m baya aliyekuwa anazidi kumfuga. Hata hivyo Hussein alishindwa kusafiri kutokana na kuyumba kiuchumi na kuamua kuwangojea ubungo baada ya miezi miwili tokea Zai ajifungue na kweli hatimae Zai alirejea akiwa na mtoto wake wa kiume na kumfurahisha sana Hussein pindi alipomuona mwanae na kumkumbatia huku akifurahi. Zainabu alijisikia fahari kuwatengenezea furaha wanaume wawili kwa wakati mmoja huku moyoni akijiona amecheza kama pele. “Oooooooh! babaangu huyoooo aaaah.. Huyu Mwinshehe kabisaaa aaammm.. Mwanangu Mwinshehee.” alifurahi sana Hussein na kuingia ndani ya Taxi pamoja na mkewe ambae alikuwa ana siri kubwa sana juu ya mtoto yule ambae tayari ana baba wawili kwa wakati mmoja. Tena kila mwanaume akijinasibu na kumfurahia mtoto yule akimpa jina la babaake kwa heshima kubwa. Kwa pamoja Mwinchande na Hussein wote walimuamini sana Zainabu kutokana na kumuona ni mwanamke wa kipekee sana kitabia na uzuri hivyo walimuamini wote kupita kiasi bila kujua kinachoendelea kichwani mwake na kusahau kuwa Zainabu hata aweje ila bado ni Mwanamke na mwalimu mkuu wake ni Kipofu.
Matatizo yalianza baada ya Mwinchande kurudi tena nchini ambapo kutokana na kufuzu kwake kwa alama za juu jeshi la polisi lilimtunuku vyeo zaidi na heshima yake kuongezeka mpaka kuwa kamanda mkuu msaidizi wa polisi nchini. Lakini muda mfupi baada ya uteuzi na kupata heshima kubwa katika jeshi la polisi Mwinchande shauku yake ilihamia kwenda Arusha kumchukua mkewe Zainabu na mwanawe Shaaban. Na hapo ndipo kisanga kilipoanza kubumbuluka mara baada ya kutofanikiwa kumkuta mkewe kijijini na bibi kukosa maneno yenye kueleweka hali iliyomfanya Mwinchande machale kumcheza na kuanza kufanya utafiti kwa watu wa kijijini waliomjua Zai.
Waswahili wanasema kuwa ‘mtu atakunyima chakula si neno’ na ndivyo ilivyokuwa mara baada ya Mwinchande kufanya utafiti wa siku mbili tu na kupata tetesi kuhusu Hussein japo hakujua kama alimuoa ila wambea walimwambia kuwa walimuona huyo mwanaume pale kwa bibi na wakatoa tetesi kuhusu jijini walipokuwa wanaishi hali iliyozidi kumpa mwanga na kumrahisishia Mwinchande jinsi ya kumnasa huyo mwanaume ambae aliona kuwa ni m baya wake kupita maeleazo, haiwezekani amtoroshe mkewe na mtoto. Na ndipo baada ya kurudi Dar aliongea na vijana wake wa polisi waliobobea kwenye upelelezi na kuwakabidhi picha za mkewe Zai wamtafute kimya kimya maeneo yale ya jiji aliyopata maelekezo kule kijijini na ndipo zoezi la kumsaka Zai na kumpeleleza kwa siri lilifanikiwa na kuanza kumpeleleza mwanaume aliekuwa anaishi nae na kupata habari zake zote muhimu na hapo ndipo Mwinchande aliamua kumuandikia barua la onyo Hussein tena aliamua atumie mbinu ya jina litalomuweka kwenye mabano ili kama atakiuka aweze kumfanyia unyambisi bila shida. Na katika kulifikiria jina ambalo litakuwa maalum kwake siku hiyo akiwa chumbani kwake usiku akijiangalia kwenye kioo ndipo lilipomjia wazo mara baada ya kuiona ile alama ya X chini kidogo ya shavu lake na kuona jina kivuli litalofaa kwake ni MR X. Ila kabla hajafanya hayo yote alimtafuta Zai ambae alikuwa na line ya siri aliyoitumia kuwasiliana na Mwinchande kwa njia ya sams lakini Hussein hakuwahi kugundua uwepo wa hiyo line. (“Haiwezekani kabisaaa..! Dah! Yaani Zai asinisariti muda wote huo aje anisariti leo hii? tena akiwa na mtoto mdogo? hapa kuna mchezo tu na huenda huyo jamaa akawa mchawi na kama hii ripoti a vijana kudai kuwa ana udugu na Mnyungunyungu basi hii itakuwa dawa tu si bure”) Aliwaza sana Mwinchande na kuanza kuandika mwseji nzito kwenda kwa Zainab. Baada ya Zai kupata ujumbe toka kwa Mwinchande wa kumuonya kuhusu usariti wake, aliamua kujitetea na kudai hata yeye hajui ilivyokuwa kuwa na hapo alizidi kumtia hasira Mwinchande aliyeamini kuwa hiyo njia iliyotumiwa si kosa la Zai bali ni uchawi wa Hussein na madawa. Na hapo ndipo barua ya onyo ilipotumwa kwa Hussein na kupewa siku saba ahakikishe amemrudisha yule mwanamke kijijini kwao Arusha.
Ni ujanja na akili nyingi uliotumiwa na askali mpelelezi mmoja kumkabidhi Hussein ile barua ambayo ilipofika kwa Zai tu, alikanusha mdomoni na kujifanya hajui kitu lakini moyoni alijua kila kitu kuwa ile barua ilimuhusu yeye na mtu aliyejitambulisha kuwa Mr X ni mumewe wa kimila anayeitwa Mwinchande. Kwa upeo wake Zai alijitahidi kujiiba na kuwasiliana na Mwinchande akimsihi asilipe ubaya wowote kwa yule mwanaume aliyemlaghai kichawi na kumtorosha wala wasifikie habari ya kumpiga na kumuua. Suala lile la Zai awali Mwinchande aliligomea kwani alichohitaji yeye Hussein auawe kabisa.. Lakini kutokana na ombi la hisia kali tena za kiuungu na dini alilokuwa analiwasilisha Zai mara kwa mara ndipo lilimkubalisha Mwinchande na kumwambia Zai kuwa hatomuua tena Hussein kwa mikono yake.
* * * *
“Inspector wewe utaongoza hawa macoplo kwenda kuchukua zile maiti za ajali ambazo bado hawajatokea ndugu wa kuzichukua, kuna ya mama na mtoto aliyekatika kichwa mfanye haraka sasa.” ilikuwa ni mipango nyeti ya Mwinchande katika mtego alioudhamiria mara baada ya kupokea sms kutoka kwa Zai kuwa wanaelekea kule kwa baba yao mkubwa Manyungunyungu na wakati huo Mwinchande alikuwa katika hospitali ya Tumbi kulipoletwa maiti nyingi zilizotokana na ajali mbaya ya basi maeneo yale ya kibaha. Alichokifanya Mwinchande harakaharaka na kutokana kuwa na makazi pia pale Kibaha aliondoka yeye na rafiki ake mmoja aliyempata kwa kumpa msaada wa matibabu ya mwanae na katika kuishi alipenda kumfundisha uninja na ndie aliyempa siri kidogo kuhusu yeye japo zilikuwa za uongo lakini rafikiake yule alimuamini mno hasa kwa msaada aliouonesha kwake kwa kumsaidia mwanae ambae alijua angekufa hivyo hata na yeye kumsaidia kwenye ile kazi aliona ni haki kabisa. Hakuwa mwengine bali ni Ally ambae Mwinchande alipenda kumwita seven seven kutokana na kujuana nae siku ya tarehe 7 mwezi wa 7 hivyo akwa anamwita jina la Ally77. Na hapo ndipo walipochukua mavazi yao ya kazi (Kininja) ambayo waliyaweka kwa pembeni ya gari muda wanatoka na kuwahi Kibamba walipoiacha gari na kutembea kwa miguu karibu na ile jia panda walipochepuka na kuyavaa sasa mavazi ya Kininja na kupita njia za msitu mpaka sehemu moja waliyoona panafaa kutimiza lengo. “tega upande ule mi natega upande huu, vijana wangu wanakuja taratibu na maiti. Nishampanga mke wangu akifika eneo hili atachutama kukojoa na hapo mimi nitatoka kumnyang’anya mtoto huyu mpuuzi kwani lazima amshike yeye na wewe utatoka nyuma yake na hilo gongo hakikisha unampiga maeneo yale niliyokuelekeza.” alitoa agizo Mwinchande na kueka mipango sawa.
Na ndivyo ilivyokuja kuwa mpaka Hussein anakuja kukamatwa na kusingiziwa kesi ya mauaji baada ya kuzimia pale chini punde alipopigwa na Ally77 ndipo muda zile maiti zilifikishwa na nguo alizovaa Shaaban alivalishwa yule maiti mtoto na kusogezwa pale kichakani huku mpelelezi mmoja akiwa maeneo karibu ya kijiji akingoja amri ya kwenda kuwaibua wananchi wenye hasira kali. Zai alilia sana kwani alijua Hussein angeachwa tu pale na kuamka kujikuta pekeake lakini hakujua kama kuna mpango mwengine wa Mwinchande juu ya kumuua Hussein japo si kwa mkono wake lakini aliamini kisheria lazima atanyongwa.
Na hatimae Hussein alianza maisha ya jela na Mwinchande pamoja na Zai walianza maisha yao mapya katika jumba kubwa la kifahari ambalo ndani yake kulikuwa na chumba maalum kilichotengenezwa kwaajili ya mawasiliano maalum aliyokuwa nayasuka Mwinchande ili siku moja nchi isije kugundua kile alichokifanya na aliapa kuilinda siri yake mpaka mwisho wa maisha yake na kutokana na mbinu nyingi alizozipata Israel na India aliiendeleaza mission zake na kukichimba kizazi cha Hussein hasa mara baada ya kumuona bint mmoja aliyekuwa na mtoto wa kike akilia kule mahakamani na kudai kuwa yule mtoto ni wa Hussein na alikuwa na barua yake ambayo askali aliyeipokea aliitwa na Mwinchande mwenyewe ambapo aliifungua na kuisoma ile barua ndipo aliporuhusu ipelekwe huko gerezani kwa muhusika nae akaanza kufanya mipango ya kumueka katika anga zake mtoto wa Hussein aliyeitwa Asha.
Na hiko ndio kilikuwa CHANZO cha Mwinchande kugeuka kuwa mtu m baya na muuaji kwa kila anayeona anahatarisha siri zake.
“Mwananguuuuuuuu Shaaaabaani mimi ndie mkosaaaajiii iiiiiih Najuutaa leeeeooooo aaaaaaaaaaaaaagh iiiiiiiiiiiiiih Ona sasaa watuu niliowapeendaaa, watuu waliojitahidi kunionesha kila aina ya upendoooo, waliniaminiiii lakini leo nimewauaaaaa…. aaaaaah!! Mwanangu Shebby wewee si muuuajii wala babaako Hussein si muuajii hata Mr X piaaaaa. kwaani yoooote hayaa chanzo ni mimiii japo sijamuuaa mtuu kwa mkono wanguuuuuu… Lakini mimi ndie muuajii…Ooooooooooh eeeeeeeeeeeeh” aliendelea kulia kwa uchungu sana Zainab mara alipokuwa anawasimulia chanzo cha matatizo Kamishna Shaaban na Cj4 aliyekuwa ameipakata maiti ya Hussein bubu huku wote machozi yakiwatoka baada ya kujua chanzo kizima. “Maamaa, maamaa, mama ina maana Asha ni dadaangu? Mama!!! umeacha nimuoe dadaangu?!! aaaaagh.” aliumia zaidi Shaaban na alijua kuwa Asha hajui chochote kinachoendelea pale lakini kumbe Asha alishatumiwa ujumbe mfupi na Cj4 kumtaka kufika pale kwa kina Shebby haraka kutoa msaada kwani uvamizi umetokea. Cj4 alifanya vile makusudi tu ili awaoneshe uwezo wa Asha ulivyo na kweli mara ghaaaaaaaaafraaaaa wakiwa wametahayuri wote ndipo walipomshuhudia mtu akiingia kwa style ya salakasi za ajabu kupitia dirisha lile alilovunja Shebby pindi akiingia na mara baada ya kuingia yule mtu na kutua mbele yao wote walishangaa kumuona ni mwanamke aliyezuia uso kwa nikabu nyeusi huku akiwa kavaa track suit juu na chini mikononi akiwa na visu vidogo zaidi ya vinane alivyovishika kimaajabu kwenye pachu pachu ya vidole vya mkono na kumfanya Shebby atake kuiwahi bastora yake lakini Cj4 alimkata ngwala punde tu alipotaka kuinuka na kumwambia. “Huwezi ua tena kwa wasio na hatia mbele ya Cj4. Yule ni dadaako mke wako adui wa adui yako na yeye ndie Lady Ninja Asha.” maneno yale yalimfanya Shebby ataharuki zaidi hasa pale Asha alipodondosha vile visu chini na kupiga magoti akilia kwa uchungu kwa kubainika na kuona kile kilichokuwa mbele yake huku akifungua nikabu yake na kwa mara ya kwanza akawa dhahiri shahiri mbele yao kwa kuwahakikishia asemacho Cj4 na hapo hata Shebby alijikuta anapoteza fahamu kwa taharuki.
<<<< MIAKA 15 BAADAE >>>> ^^^^^^^^^^^^ * * * ^^
Ni katika makaburi ya Makanya Dar es Salaam wanaonekana watu wawili wakiwa wote wamevaa nguo nyeusi mmoja akiwa ni mtu mzima na mwengine mtoto wa miaka isiyozidi 14 wakiwa wamepiga magoti mbele ya makaburi yaliyojengewa kwa mtindo wa kufanana baada ya kuyasafishia na walionekana walifika pale kwa muda mrefu sana na kulikuwa na hadithi ndefu aliyokuwa anaisimulia yule Mkubwa kwa yule mtoto huku akimuonesha onesha makaburi yale.
“Hadithi hii imeniuma sana baba Cj4 aaah!! Mungu wasamehe ndugu zangu wote, kwa hiyo nini kilitokea sasa baada ya baba kujua kumbe mama alikuwa Ninja mara aliporudiwa fahamu?” aliuliza yule mtoto. “Baada ya babaako Kamishna Shebby kuzinduka ilikuwa tayari kashachelewa mara baada ya bibi ako kuzidiwa ghafra kwa presha iliyomshuka pindi alipogundua kumbe mumewe babu yako Mr X alikuwa amemtumia mamaako zaidi ya alivyojua yeye, kwani bibiako alijua kama mumewe anamtumia Asha lakini si kwa mauaji bali ni kumueka tu karibu ili amfiche kama yeye ni mtu m baya dhidi ya babaake ambae ndie babu yako mzazi Hussein. Ilibidi sasa mamaako amuwahi kakaake ambae pia ni babaako pale chini pindi alipozinduka lakini nae alichelewa hata mimi pia nilichelewa kumuwahi kutokana na kumuweka chini babu yako Hussein aliyekuwa kashakufa na kumuwahi bibi yako Zai kwa kumpa msaada bila kujua nyuma yangu Shebby amezinduka na kwa kuchanganyikiwa kwa kile akionacho alishindwa kujizuia na kuiokota tena bastora yake na hapo nilisikia tu mlio wa risasi sambamba na kelele za mamaako Asha na nilipogeuka hakuwa Asha aliyepigwa risasi bali ni Shebby mwenyewe alijipasua kichwa na kusambaratika ubongo palepale..” alipofika hapa kidogo alisita na kwa mara ya kwanza Cj4 chozi lilimdondoka hadhalani toka afuzu mafunzo ya Ukomando Cuba zaidi ya miaka 20 iliyopita. “Mwanangu Hussein, sikumbuki lini ilikuwa mara ya mwisho kutoa chozi kwani hata kipindi yale yote yanatokea sikudondosha chozi. Zaidi nilisimama kiume kukabiliana nayo kwani ilibidi nimuache bibiako Zainab niliyeona wazi kuwa yupo katika hatua za kumalizikia baada ya presha kushuka sana na kushuhudia mwanae akijimaliza na hapo ilibidi niluke kishujaa kumuwahi mamaako Asha ambae nae alikuwa anataka ajimalize kwa bastora ile ile aliyojimalizia babaako. Jinsi nilivyoruka sikuwahi kufundishwa wala kudhani kama nina uwezo wa kuluka vile, lakini ndivyo ilivyokuwa niliweza kumuwahi mamaako na kumuokoa mbele ya kifo alichokuwa anajitengenezea mwenyewe na nilichokifanya niliubetua mshipa wake mdogo wa fahamu uliokuwa nyuma ya sikio na kumzimisha. Hapo ndipo nilipoweza kuwasiliana na mkuu wangu wa majeshi na kumpa taarifa zote kabla sijaondoka eneo lile huku nikiwa nimem beba mamaako ambae sikujua kumbe tayari tumboni ulikuwapo wewe.” Story ya Cj4 ilimuuma sana yule mtoto lakini alionesha alikuwa jasiri sana na mwenye moyo wa uvumilivu kwani alikuwa anatokwa machozi lakini aliweza kusikiliza kwa umakini na kuuliza maswali muhimu. “Kwa hiyo baba Cj ilikuwaje sasa ulipoondoka na mama hasa pale fahamu zilipomrudia?” “Mwanangu Hussein, mamaako kwanza alichelewa sana kupata fahamu hadi nilianza kuhofu lakini alipopata fahamu nilikuwa nae kwenye kambi maalum ya kijeshi ambapo ndipo nilipoelekea mara baada ya kutoka pale kwenye ile nyumba. Niliongea nae na kumpanga kwa maneno ya kishujaa na mbinu maalum ambazo utakutana nazo pindi utapokuwa kama mimi hapo baadae, nikikutazama naona wazi utakuwa zaidi ya mimi. Basi mamaako japo ilikuwa ngumu kuelewa lakini tuliweza kumdhibiti ndani ya kambi ile iliyokuwa haijulikani kabisa na watu wengi hadi kwa wanajeshi wengi wenye vyeo vya chini. Japo alikuwa ni wa kuzimia mara kwa mara lakini hatimae aliweza kutulia taratibu kadri siku zilivyozidi kwenda hadi tulipomgundua kuwa alikuwa na mima baada ya kumfanyia vipimo vya utrasound pindi tulipoona tumbo linazidi kuwa kubwa na kugundua uwepo wako. Sikuweza kuhudhulia mazishi ya babaako, bibiako, babu ako na babu ako mlezi wa babaako Mr X ambao wote walizikwa kwa pamoja hapa kama unavyoona makaburi yao yalivyofatana kwa sababu ya kuwa karibu na mamaako na kumliwaza japo niliweza kuyashuhudia baadae kupitia rekodi kamili ya ule mkanda tulioutazama tena sote jana usiku. Serikali ndio waliolizima suala lile baada ya taarifa za ripoti yangu kamili kufika kwa muheshiwa Rais.” “sawa baba, sasa mama nae alikufa kufa vipi?” “Mamaako kilichomuua ni sumu iliyokuwa mwilini mwake iliyokuwa ikimtafuna muda mrefu. Sumu hiyo ilitokana na kile kisu cha kininja alichochomwa na Tyga siku ile usiku… Kwa hiyo siku aliyokuwa anajifungua ndio siku aliyofariki pindi alipokuwa anakupush kwa nguvu kumbe alikuwa anajimalizia baada ya sumu kushambulia sana maeneo ya uti wa mgongo na mbavu. Mamaako alikufa kishujaa kwa kuwa aliweza kuvumilia hadi akafanikisha kumzaa Shujaa mpya ambae ni wewe mwanangu Hussein niliyeamua kukupa jina hili la babu yako ambae pia alikufa mikononi mwangu lakini kupitia wewe nikaona kama amezaliwa tena mikononi mwangu. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa Hussein wewe ulikuwa chini ya usimamizi wangu wala hukuwa na ndugu yeyote zaidi yangu…. Simama sasa nataka nikuulize nami maswali yangu.” aliongea Cj4 na kusimama sambamba na mtoto Hussein ambae ndie alikuwa mtoto halali wa Marehemu Dokta Asha au Lady Ninja na Marehemu Kamishna Shebby.
“Ulivyoelewa historia yako asili yake na matatizo yote chanzo ni nini?” “MWANAMKE” alijibu Hussein bila hata kusita. “Vizuri na je, ulivyosoma historia ya ushujaa wa Samson dhidi ya Wafiristi hadi siri zake zikabainika na kukamatwa kupata mateso makali hadi alipoomba nguvu kumrudia na kufa pamoja na mamia ya watu je nae kilichomponza hasa chanzo ni nini?” “MWANAMKE” alijibu tena Hussein. “Vizuri sana, na vipi kuhusu asili ya dhambi ya baba etu Adam kusariti ahadi aliyopewa na mungu na kushawishika kula lile tunda, kihistoria ulivyosoma shetani alimtumia nani kumshawishi kiurahisi Adam.” “MWANAMKE” “Ni kweli mwanangu Hussein na hivi unajua kwanini Wanawake ni wengi kuliko Wanaume?” “hapana baba Cj4, sijui.” “Basi ni kwasababu mtu wa kwanza kufa alikuwa ni mwanaume na alikuwa mtoto wa Adam aliyepigana na ndugu yake sababu ikiwa ni mwanamke. na hapo ndipo uwiano wa namba ulipozidi. Kwa hiyo kwa uelewa wa kawaida kabisa umeona kumbe hata mtu wa kwanza kufa chanzo ilikuwa nini?” “MWANAMKE baba Mh!!” “Huo ndio ukweli ambao alikuwa anamaanisha babu yako wala si uchizi.. hivi unajua chanzo cha mimi kukuhadithia hadithi ya maisha ya asili ulipotokea chanzo ni nini?” “Ndio baba chanzo ni Halima mtoto wa baba Kanali Suma mara baada ya kusababisha nimepigana na kumuumiza Amos mtoto wa Luten Frenk.” alijibu kwa upole Hussein. “sawa kwa hiyo Halima ni nani?” “ni mwanamke baba” “kwa hiyo chanzo cha kukuhadithia ukweli huu na kukuonesha video ya mazishi mpaka sasa tupo hapa chanzo ni…..?” “MWANAMKE” “Ndio, sasa umejifunza nini hapa.” “Naapa baba Cj4 mbele za Mungu, mbele ya makabuli haya ya ndugu zangu kuwa nitakuwa makini makini sana na Wanawake kamwe sintokuwa mzembe wa kuwaaamini kwa asilimia zote kwa kuwa Wanamke wana ulemavu wa upeo na udhaifu wa asili.” aliapa kwa nguvu na sauti ya kumaanisha Hussein. “sawa unadhani kwanini umeapa hivyo? hivi kiapo chako uko sahihi kweli?” “Naamini baba Cj4 nipo sahihi, na ili nikuaminishe nipo sahihi kusema kuwa ‘wanawake wana ulemavu wa upeo na udhaifu wa asili’ nataka nikuulize swali.” “Uliza tu mwanangu.” “Je ni dini gani kati ya ukristo na uislam pamoja na matawi yake inasema Mungu alituma manabii na mitume wanawake kwaajili ya kuwaogoza na kuwaokoa watu?” “Mh!! HAKUNA mwanangu wala sijawahi kusikia.” “unadhani Mungu ana upendeleo kwa wanaume?” “Hapana, ila ninachojua Mungu alimuumba mwanamke kwa sababu ya kumtuliza na kumliwaza mwanaume.” “kwa hiyo hapo baba ndipo kwenye ‘ulemavu na dhaifu wa asili ya mwanamke’ japo wenyewe hawataki na naamini mwanamke asiyekubali kuwa dhaifu mbele ya mwanaume naamini ni muuaji na mwanamke asiyekubali kuwa ana ulemavu wa upeo basi atajiamulia vitu kama bibi Zai na faida yake ataiona mwishoni na atakuwa muuaji tu.” aliongea kwa uchungu Hussein na Cj4 alishangaa kuona maneno ya Hussein mtoto yanashabiana na nukuu za marehemu Hussein mkubwa na kuamua amkumbatie kwa nguvu pindi alipoona anazidi kuongea huku akilia na kumsihi sasa inatosha waondoke. “Basi mwanangu basi mwanangu tuondoke sasa ila zingatia haya na ufanye utafiti na uwaokoe wanaume wengi wasiojua hili pamoja na kuwaelimisha wanawake wakubali udhaifu wao ili matatizo zaidi yasiendelee kutokea na kabla hujaongea nao wala kuwasimulia waulize kwanza je, WANAWAKE NI WAUAJI..!? sikiliza na uhesabu majibu yao kisha uwasimulie story hii na ikiwezekana uiandike kabisa na uitolee Kitabu ili wengi wakipate na mara utapomaliza kuwasimulia/kuandika waulize tena kwa mshangao swali lilelile la mwanzo kuwa WANAWAKE NI WAUAJI..!? uone tena majibu yao.”
Simulizi : 666 Nyayo Za Kuzimu Sehemu Ya Kwanza (1)
Upepo ulivuma mno,miti na majani ilionekana kuinama kutokana na kushndwa kupambana na pepo
ile kali,giza lilikua kali sana kwa kuwa mwezi ulikua umefunikwa gubigubi na wingu zito jeusi
lisiloonyesha hata
kama mvua itanyesha.utulivu wa hali ya juu ulitawala,hakuna kilichosikika zaidi ya milio ya kiuoga
ya mbwa na vijidudu vidogo vidogo vya usiku,kila kibatari kilichowashwa ilhali na moto ilizimika
kutokana na kutokua
stahimilivu na hali iliyokuwepo,hakukuwa na mtu yeyote alieonekana yu nje akifanya jambo
lolote,na ni kutokana na hali ya ajabu ya ghafla iliyotawala katika lile eneo.Kwa mbaali angani
ilionekana nyota ndogo
ikichomoza,ghafla sauti ya kuamuru ilisikika kutoka kwenye kijumba cha msonge ikisema..
“sukuma,jitahidi Vero sukuma!…enhee..tena…tena!!..ewaaah!…umepata mtoto wa kiume Vero!” sauti ya mama Marinda mkunga wa jadi Maarufu kijijini iliskika..iliyoambatana na tendo na
kumsaidia bibie
Veronica kupata mtoto wake wa kwanza kabisa,upepo ulitulia ghafla,hali iliyomfanya Mama Utopi
kupumzika na zoezi la kukikinga kibatari kisizimwe na upepo ili shughuli ile ya Ukunga iliyokua
inafanyika ipate kuisha
salmini,alikiweka kile kibatari chini na kusogea karibu zaidi ili apate kumshuhudia mtoto aliyeingzwa
ulimwenguni..
“mbona hata halii?”
akauliza mama Utopi kwa shauku kubwa ya kufahamu, “mie mwenyewe sijui,kwani miaka yangu yote ishirini ya ukunga sijawah kukutana na hili jambo mtoto kutolia ingali anaonyesha yu mzima kwa kuchezesha mikono na miguu yake….. Na isitoshe…ni wa baridi mno! Zaidi hata ya maji ya asubuhi ya mtoni!”
alisema kwa msisitizo mama Marinda huku akimtolea macho mama Utopi aliesimama,Vero
Mama marinda wakiwa wanajibizana.Mama marinda aliemshkilia mtoto alianza kuingiwa na
hofu,alimtazama yule mtoto kwa macho yakinifu hakupata jibu,alionekana ni mtulivu
mno,hakuonyesha dalili ya kucheka wala
kulia,Mama Marinda akaanza kuhisi mapigo yake ya moyo yanaenda mbio,jasho lililojaa uoga
taratiibu lilishuka…
Mama Marinda alianza kuhisi mapigo ya moyo yanaenda mbio kuliko kawaida,mikono yake
iliyomshka mtoto ilianza kutetemeka,alitoa macho kwa mshangao na ghafla aliropoka.. “mama Utopi embu mchukue huyu mtoto,haraka!!” naye mama Utopi bila kujivunga aliinama na kumtwaa mtoto akiwa na kiulizo kichwani.. “kwani vipi jamani?” aliuliza Vero baada ya kuiona ile hali linayoendelea pale, Mama Marinda alikua kimya akionekana kubanwa na mawazo hali iliyompa nafasi mama Utopi
kunena.. “mwanao ni wa tofauti Vero?” “kivipi?” “kwanza halii,pili ni wa baridi mno!” “mmmh…haitokua ni kwasababu ya hali ya hewa?” “sidhani,mana hata hali yenyewe imebadilika tu baada ya wewe kusikia uchungu,na sasa hivi
umeshajifungua huoni kama hali imetulia?” alisema Mama Utopi huku akimtazama Vero alieonekana anafikiria jambo kutokana na kauli
aliyoambiwa,aliona Vero anapata shida kuongea na ni kutokana na kutoka kujifungua na hali ilikua
inaonyesha dhahiri ya kwamba kachoka,hakutaka muongelesha tena na alimsihi apumzike kwa
muda,mama Utopi alimtazama vizuri mtoto aliyembeba huku mikono yake ikistahimili baridi
lililoonekana kuanza kumzidia,allivua khanga yake na kubakia na gauni tu lililochoka la rangi
nyekundu lenye maua maua kisha ile khanga akamfunikia tena mtoto ili kujikinga na mikono yake
vilevile na kumkinga mtoto na hali ya hewa.Mama Utopi,mmama mwembamba mwenye uweupe wa
mbali na kichwani akiwa kasuka vibutu vibutu vilivyoonekana kufumuka fumuka alimgeuzia shingo
mama Marinda,alimuona bado butwaa ya mawazo imemshika…na yupo tu pale kifikra,alimstua.. “we mama Marinda!” “Abee!…” kwa kukurupuka aliitika, “vipi wewe?” “mmmh…embu njoo nje tuongee kidogo” alijibu Mama Marinda huku akitoka nje ya ile nyumba ya msonge akifuatiwa na Mama Utopi baada
ya kumkabidh Vero mwanae, walisogea kidogo mbali na ile nyumba hali iliyoashiria ya kwamba maongezi yao ni ya siri. Mama Marinda aliangalia kushoto na kulia kama kuna mtu,akatengenezea khanga yake rangi kijani na manjano yenye nyota nyekundu,akakuna kichwa chake kilicho na mvi zilizotosha
kujionyesha kisha kwa msisitizo akasema.. “hivi unayakumbuka maneno ya yule mganga?”…
“unayakumbuka maneno ya mganga?” “maneno yapi tena?” “si yale ya kizazi cha nyoka… Hukumbuki?” alizidi kusisitiza mama Marinda, “aahaaa!..nishakumbuka,enhe?” “sasa wewe huoni kama inahusiana na haya?” “yapi?” “nawe!..he! Si haya ya huyu mtoto!… Hukumbuki mganga alituambia kwamba,kwanza siku akizaliwa hali ya hewa itabadilika na kua ya
kutisha naa…..” “ndioo!..pia nakumbuka alituambia kwamba nyota ndogo itachomoza!” (haraka wakanyanyua nyuso zao na kutazama angani) “haa!…si unaiona!” kwa tahamaki alisema mama Marinda huku akinyooshea kidole nyota ile, “ndio mama Marinda,naiona!” alijibu kwa mshangao mama Utopi, “sasa tunafanyaje?” sura yenye wasi wasi ya mama Marinda ilitamka, “mmh…mi nadhani hapa si pa kukaa tena,mana yule mtoto ni hatari sana!…si unakumbuka alituambia
kwamba akifungua macho yake wote wasio na imani thabiti juu yake watapata majanga..!!” “ndio!…tuondoke haraka iwezekanavyo tumuache atajijua yeye na mumewe!!” aling’aka mama Marinda,walishikana mikono na kuanza kukimbia haraka wakipita katikati ya msitu
mzito ilipo njia nyembamba ya kuelekea kwao,milio ya mbwa na wadudu ilizidi kuwatisha na
kuwafanya waangalie nyuma kila mara kwa hofu,mama Marinda alianza kuchoka kukimbia,uzee na
mwili wake ulikua ni kikwazo tosha kwake kuendelea na safari,ilibidi wapumzike
kidogo…..wakusanye nguvu kisha wamalizie safari yao iliyobakia kidogo kuikamilisha,walilaumu
nafsi zao kwa tamaa ya pesa ya mzee Ndolanga mume wa Vero iliyowafanya waingie kwenye
matatizo yote hayo,kwani kama wangelijua wasingejisumbua na kujihusisha na ile shughuli,katikati
ya mapumziko yao mafupi walisikia sauti na vishindo vya watu vinakuja,haraka walijificha,punde si
punde walishuhudia wazee watatu waliojifunika gubi gubi wanaotumia msaada wa fimbo
kutembea,wakiwa wanajongea bila uoga huku wakionekana kufurahia jambo… Ghafla wale wazee walisimama,mmoja wao akasema.. “nasikia harufu ya binadamu hapa..” huku akipepesa pepesa macho yake mekundu, mwingine akadakia.. “naisikia hata mimi pia!..” macho ya wakina Mama Marinda yalitoka na mioyo ilipiga mbio mithili ya mkizi
baharini,walishikana kwa uoga,waliwaona wale wazee wakiwa wanarudi kuelekea upande wao huku
wakiwa wanatazama tazama wakitafuta kitu! * * * * “mama Marinda tukimbie!..” alinong’oneza mama Utopi, “mie siwezi tena,miguu inaniuma!” “jitahidi jamani,huoni wanazidi kuja!.. Na wanasikia harufu yetu!!” alizidi kusisitiza mama Utopi huku wakiwa bado wamejificha na wale wazee wapo hatua kumi tu toka
walipo… “tupige tu ukunga watu waje watusaidie” “usiku wote mzito huu nani atajitoa nje ya nyumba yake?… Twende mam a Marinda…twendeee!!” alimshka mkono na kuanza kukimbia,alikua mbele ya mwenzake na aliutumia mkono wa kushoto
kumkokotea… Wale wazee hawakuonekana wakikimbia,walisimama tuli huku macho yao yakiwa yanawatizama
wakina mama Marinda wanaokimbia,hawakufika umbali mrefu,mkono wa mama Marinda
ulimponyoka mama Utopi,kama gunia la ulezi alidondoka chini!!. “mama Marinda…amka twendee!..amkaa!!… “siwezi!…siwezi!!..miguu yangu imefungwa na majani mama Utopi!..siwezi kuitoa!!… Mama Utopi nisaidieee navutwaa!” mama Utopi alijitahidi kumpa mkono mama Marinda lakini hakufanikiwa,Mama Marinda alivutwa
haraka kwa kasi ya ajabu,sauti yake ya kuomba msaada ilizidi kupotelea msituni,na haikuskika kabisa.Mama Utopi hakua na cha kufanya,aligeuka na kuanza kukimbia kwa kasi
zaidi….machozi yakimtoka na moyo ukidunda kwa nguvu kutokana na uoga na hofu nzito
iliyomshika,aliona umbali wa kufika nyumbani umeongezeka,na kila akijitahidi kuongeza kasi ilikua
kama ni kazi bure,mapafu yalimbana…na alihisi kama hapati pumzi,ilimbidi asimame kidogo apate
kuhema,hakua na amani kabisa,alikua anatizama kila pande kuthibitisha usalama wake,machozi
yalizidi kumtoka alipofikiria mwenzake aliekua nae muda si mrefu hayupo tena,ilikua ni kama
mchezo wa kuigiza alipomshuhudia mwenzie akivutwa na majani na kupotelea kabisa,alitupia macho
upande wa kulia,aliona mwanga wa taa umbali wa kama hatua ishirini na tano toka alipo,akili yake
ilimuambia kwamba pale ni kwa mama kadogo,haraka bila kupoteza muda aliamza kukimbia
akielekea upande huo. Alifungua kwa pupa geti la makuti la ile nyumba,aliingia ndani na kuanza kupepesa pepesa macho
aone wapi atapata msaada,ghafla alisikia sauti kali iliyompasua wake moyo.. “wow! Wow!..wow!” alistuka mno kuona mbwa watatu wakimfuata,alianza kurudi nyuma kwa tahadhari huku
akiwaangalia mbwa wanaomsogelea,kwa nguvu aliropoka kuomba msaada.. “mama Kadogoo!!..mama Kadogoo!” sauti hiyo ilimstua mama Kadogo aliekua ndani amelala na mumewe,na zaidi aliogopeshwa na sauti
kali za mbwa zilizofika vizuri masikioni mwake,alimuamsha haraka mumewe,ilikua kidogo kazi nzito
kwani alikua ametekwa vilivyo na usingizh mzito,ila kwa bugudha za kutosha alizozifanya
zilifanikisha kuondoa mang’amung’amu ya mumewe, “nini mama Kadogo?” “nimesikia sauti nje ya mwanamke inaniita..na huskii mbwa wanavyobweka kwa nguvu??” aliuliza mama Kadogo, bila kuchelewa baba Kadogo alichukua panga lake chini ya kitanda kisha akatoka nje kwa
kasi,alipofika nje alishuhudia mbwa wake wakiwa wanamparua parua mmama ambaye alikua bado
hajamfahamu ni nani,aliwaamrisha mbwa wake waache lile tendo na haraka walitii amri,alimsogelea
yule mtu na kugundua ya kwamba ni mama Utopi,aliloa damu kutokana na majeraha makubwa
aliyosabishiwa na wale wanyama,alikua anagugumia kwa maumivu na huku akitetemeka.
“mama Marinda tukimbie!..” alinong’oneza mama Utopi, “mie siwezi tena,miguu inaniuma!” “jitahidi jamani,huoni wanazidi kuja!.. Na wanasikia harufu yetu!!”
alizidi kusisitiza mama Utopi huku wakiwa bado wamejificha na wale wazee wapo hatua kumi tu toka
walipo… “tupige tu ukunga watu waje watusaidie” “usiku wote mzito huu nani atajitoa nje ya nyumba yake?… Twende mama Marinda…twendeee!!”
alimshka mkono na kuanza kukimbia,alikua mbele ya mwenzake na aliutumia mkono wa kushoto
kumkokotea… Wale wazee hawakuonekana wakikimbia,walisimama tuli huku macho yao yakiwa yanawatizama
wakina mama Marinda wanaokimbia,hawakufika umbali mrefu,mkono wa mama Marinda
ulimponyoka mama Utopi,kama gunia la ulezi alidondoka chini!!. “mama Marinda…amka twendee!..amkaa!!… “siwezi!…siwezi!!..miguu yangu imefungwa na majani mama Utopi!..siwezi kuitoa!!… Mama Utopi nisaidieee navutwaa!”
mama Utopi alijitahidi kumpa mkono mama Marinda lakini hakufanikiwa,Mama Marinda alivutwa
haraka kwa kasi ya ajabu,sauti yake ya kuomba msaada ilizidi kupotelea msituni,na mwishowe
haikuskika kabisa.Mama Utopi hakua na cha kufanya,aligeuka
na kuanza kukimbia kwa kasi zaidi….machozi yakimtoka na moyo ukidunda kwa nguvu kutokana na
uoga na hofu nzito iliyomshika,aliona umbali wa kufika nyumbani umeongezeka,na kila akijitahidi
kuongeza kasi ilikua kama ni kazi bure,mapafu yalimbana…na alihisi kama hapati pumzi,ilimbidi
asimame kidogo apate kuhema,hakua na amani kabisa,alikua anatizama pande kuthibitisha usalama wake,machozi yalizidi kumtoka alipofikiria mwenzake aliekua nae muda
si mrefu hayupo tena,ilikua ni kama mchezo wa kuigiza alipomshuhudia mwenzie akivutwa na majani
na kupotelea kabisa,alitupia macho upande wa kulia,aliona mwanga wa taa umbali wa kama hatua
ishirini na tano toka alipo,akili yake ilimuambia kwamba pale ni kwa mama kadogo,haraka bila
kupoteza muda aliamza kukimbia akielekea upande huo.
Alifungua kwa pupa geti la makuti la ile nyumba,aliingia ndani na kuanza kupepesa pepesa macho
aone wapi atapata msaada,ghafla alisikia sauti kali iliyompasua wake moyo.. “wow! Wow!..wow!” alistuka mno kuona mbwa watatu wakimfuata,alianza kurudi nyuma kwa tahadhari huku
akiwaangalia mbwa wanaomsogelea,kwa nguvu aliropoka kuomba msaada.. “mama Kadogoo!!..mama Kadogoo!”
sauti hiyo ilimstua mama Kadogo aliekua ndani amelala na mumewe,na zaidi aliogopeshwa na sauti
kali za mbwa zilizofika vizuri masikioni mwake,alimuamsha haraka mumewe,ilikua kidogo kazi nzito
kwani alikua ametekwa vilivyo na usingizh mzito,ila kwa bugudha za kutosha alizozifanya
zilifanikisha kuondoa mang’amung’amu ya mumewe, “nini mama Kadogo?” “nimesikia sauti nje ya mwanamke inaniita..na huskii mbwa wanavyobweka kwa nguvu??” aliuliza mama Kadogo,
bila kuchelewa baba Kadogo alichukua panga lake chini ya kitanda kisha akatoka nje kwa
kasi,alipofika nje alishuhudia mbwa wake wakiwa wanamparua parua mmama ambaye alikua bado
hajamfahamu ni nani,aliwaamrisha mbwa wake waache lile tendo na haraka walitii amri,alimsogelea
yule mtu na kugundua ya kwamba ni mama Utopi,aliloa damu kutokana na majeraha makubwa
aliyosabishiwa na wale wanyama,alikua anagugumia kwa maumivu na huku akitetemeka.
“mnasema nini??” “sisi ni mamajusi wa kishetani!..na tumekuja kumlaki mfalme wetu!!..” “m..m..mfa..mfalme…yu..yu..yupi!” aliuliza Vero huku akitetemeka, “mfalme Chernobog,Mungu mweusi!”
Vero macho yalizidi kumtoka,hofu ilichochea ndani yake,alimuangalia yule mtoto aliembeba
akamuona anatabasamu!…aliporudisha macho juu,aliona wale wazee watatu tayari washaingia,alisk ia moyo umepasuka ghafla….hakuvuta tena pumzi,mwishowe akapoteza fahamu.Neno
CHERNOBOG lina asili ya urusi,ni
mchanganyiko wa majina mawili,cherno ikimaanisha ‘nyeusi’ na bog imaanishayo ‘mungu’,kwahiyo
kwa pamoja huza neno ‘mungu mweusi’ kama anavyoitwa mtoto yule na wale wazee.
Mtoto alichukuliwa kutoka kwenye mikono ya Vero aliepoteza fahamu,kila mzee alimbusu kwenye
paji la uso na kuongea maneno fulani yaliyozid kulitunza tabasamu la yule mtoto. Ghafla alifungua macho yake,hayakua ya binadamu wa kawaida na hata alipopanua mdomo
wake,hakua na ulimi wa binadamu
wa kawaida,vyote vilikua ni viungo vya nyoka,tabasamu lenye afya lilichomoza kwenye kila sura ya
wale wazee,kwa pamoja wakasema.. “baruch haba chernobog.. Ooh baruch haba”
lugha ya kiebrania(Hebrew) ikimaanisha ‘karibu mungu mweusi,ooh karibu!’ ..Vero bado fahamu hazikumrudia,hivyo hakupata kushuhudia kilichokua kinajiri,alijiona yu ndani ya
giza nene akipepesa macho huku na kule kuutafuta mwanga,akiwa katika harakati hizo mara ghafla
alihisi mkono umemgusa begani,haraka aligeuza yake shingo kwa hofu kuangalia ni nani,hakuona
na mekundu wakicheza na kuimba huku wakimrusha rusha yule mtoto juu juu!!..
Baada ya dakika tano lile zoezi lilikoma,sauti ya mzee mmoja aliyekua ameshikilia fimbo yenye
alama ya msalaba ikasema..
“wana wa utawala wa kiza huu ni wakati wetu!!” “amen!” wakaitikia wale wengine huku wakiinamisha vichwa vyao, “na tupo hapa kumlaki mfalme atakaetuöngoza mpaka pale tutakapoikamata dunia!!” “ameen!” “na kuanzia leo jua halitochomoza,na ni ishara ya kutokua na mipaka kwenye maamuzi!” “Ameen!” “ila sadaka ya mtu mmoja haitoshi kabisa kumpokea mfalme wetu,hivyo basi inahtajika nyingine ya
ziada!!..” “ameen!” “na nendeni mashariki na magharibi,kaskazini na kusini..MKAITWAE!!!!….”
Wale watu walitawanyika huku na huko kwenda kutafuta sadaka kwa ajili ya mapokezi ya mungu
wao CHERNOBOG yani ‘mungu mweusi’,macho yao mekundu,miili yao ya kijivu iliyofunikwa na
mavazi meupe na mekundu ilizidi kuchanja mbuga pande zote nane za dunia kwa ajili ya kuifanisha
tafrija yao.
Baba Kadogo alizidi kutembea kuelekea mbele,alibakisha umbali usio mrefu sana kukamili sha safari yake aliyodhamiria,ghafla panga lilimponyoka,akainama akaliokota akaendelea na
safari,baada ya hatua mbili tatu panga likamponyoka tena!
Moyo ukaguma,akapata wasiwasi kuhusu ile hali,ila hakujali sana,aliinamisha tena mgongo wake
akaliokota,mara ghafla akahisi upepo umempita kwa haraka! Mwili wake wote ukasisimka!
Ujasiri wake ukaanza kupata mashaka,moyo wake nao taratibu ukaanza kuchanganyia mbio,alihisi
tena muda mrefu panga likamponyoka kwa mara ya tatu!
Milio ya hatari ikaanza kuita kichwani mwake,nafsi yake ikamtonya ya kwamba hayuko salama,bila
kuuliza mara mbilimbili wala kupoteza muda wa ziada aliinama na kuliokota ganga kisha akaanza
kukimbia!!
Hakuruhusu miguu yake isimame wala kupunguza kasi,alikimbia kadiri ya uwezo wake huku akihema
juu juu kwa pupa kuitafuta oksjeni,tahamaki alisikia vishindo kwa nyuma vinakuja kwa kasi! …Baba Kadogo alieanza kuloa uoga na kujuta kwanini hakusikia ile kauli ya mkewe alizidi kuongeza
Kabla ya kujikusanya na kuinuka,tayari alishazungukwa na watu watatu waliopendezeshwa na
mavazi meupe na mekundu!! Sauti kali ya maumivu ya baba Kadogo iliskika kwa nguvu kutoka msituni “aaaaaahhh!!!!!!” kisha tena kukawa kimya, idadi ikawa ni watu wawili waliokwenda kwa ajili ya sadaka tayari! * * * * * * * *
mama kadogo alihisi moyo wake umelipuka ghafla! Alikosa amani,moja kwa moja alihisi kuna jambo baya limechukua nafasi,alitoka kwenye dirisha
alipokua anachungulia na kumsubiria mumewe,kiuchovu na kimawazo akaelekea kwenye kiti alipo
mama Utopi ambaye bado fahamu hazikumrudia,alikaa kihuzuni huku akishika tama,
hivi?….eh mungu saidia!” “koh!-koh!” ghafla kikohozi cha mama Utopi kikaskika! Haraka mama Kadogo aligeuza yake shingo na kumtazama, “mama Utopi!” “ab..bee!” “vipi mama unajiskiaje?”
“……mmm,mikono inaniuma na miguu pia..inavuta sana!” alisema mama Utopi huku sura yake ikiakisi maumivu aliyokua nayo, “usihofu mama,itapoa tu kwani dawa iliyoekwa kwenye hizo bandeji ni kiboko..” “ahsanteni jamani…ahsanteni sana”
alisema mama Utopi huku akikunja kunja sura kutokana na miale ya maumivu kumpitia, “haina shida mama,ila samahani sana kwa wale mbwa wetu waliokujeruhi..” “wala usihofu mwanangu..” “hivi mama ilikuaje kwani?” “mh…mama Kadogo,tumekwisha!!” “tumekwisha? Kivipi yani…sijaelewa!”
“kile kizazi cha nyoka alichotuambia mzee Otongo yule mganga..kimewadia!!” “eh? Umekionea wapi??” “mtoto va Vero!..mtoto wa Vero ndie yule…. (kabla hajamalizia alikatishwa na hodi toka mlangoni) “ngo! Ngo! Ngo!” “nanii?”
aliuliza mama Kadogo huku macho yakiwatoka kwa uoga, “mimi Baba Kadogo!” sauti toka nje iliskika,
mama kadogo alifikiria kidogo,kisha akataka kuinuka ila mama Utopi alimzuia haraka! Kisha akamuuliza, “una uhakika huyo ni Baba Kadogo??” swali lililomstua mama kadogo na kumfanya aanze kutia shaka, * * * * * * * “mh..lakini ni sauti yake hiyo ninayoisikia?” “haijalishi mama Kadogo…inabidi uwe makini,embu nenda kachungulie pale dirishani kuhakiki” “nenda basi wewe” “ah..ah si mume wako? Nenda wewe!” walisakiziana kwa uoga, “lakini mama utopi…mi…mi..naogopa! Au tumuamshe Kadogo aje atusaidie?” “atusaidie nini? Kwani tunajifungua hapa?… Jiamini mtoto wa kike,tupo wawili humu we nenda tu,mie ningeenda sema miguu inanivuta kweli!” alitamka mama Utopi kwa ujasiri huku akifichama hisia zake za uoga, mama Kadogo alinyanyuka na taratibu alianza kujongea kuelekea kwenye dirisha,alitizama tizama
nyuma kila mara kumuangalia mama Utopi ambaye alikua anampa ishara za kujiamini na kuzidi
kusogea,aliunyanyua mguu wake wa kulia kumalizia umbali uliobakia wa kulifikia dirisha,ghafla
alishtushwa na hodi ya mara ya pili iliyotoa sauti kali na kuutikisa mlango! “ngo!! Ngo!! Ngo!! Ngo!!” aliyatoa macho na haraka aliyageuzia kwa mama Utopi alieonesha kwamba naye kashtushwa! Alishindwa kuizuia miguu yake,alikimbia haraka kurudi alipotoka kuungana na mwenzie alieonekana
naye kujawa na uoga uliomeza ule ujasiri wake wa kuigiza, “umesikia hiyo??…mh,sasa hivi nenda wewe!” “mimi?…kwa we ulifika?!” “mie sijafika ndio ila nilikaribia karibia!” “sasa kwani sie tulikubaliana kukaribia karibia ama kufika pale dirishani?” aliuliza mama Utopi kwa sauti ya chini, “ngo!!! Ngo!!! Ngo!!! Mama kadogo fungua!!!” sauti tena ya kuamuru iliskika toka nje ikiambatana na mlio wa nguvu wa mlango,kwa mara hii haikua tena ya Baba kadogo iliyokua mwanzoni,ilikua ni sauti nzito ya kutisha! “mama Utopi hiyo si sauti ya mume wangu!!” kwa mshangao uliojaa uoga alibwatuka mama Kadogo, haraka waliinuka wakakimbilia chumbani na kuacha sebule tupu,waliingia chumba cha kwanza
kabisa kilichokua karibu yao ambacho ni chumba cha Kadogo mtoto wa pekee wa mama Kadogo,hali
ya kuingia kwa kukurupushana ilimfanya Kadogo astuke toka kwe usingizi,alipigwa na butwaa na
kile kitendo cha kuona mama yake anajaribu kuingia chini ya uvungu wa kitanda chake,na
alipogeuza shingo upande wa kushoto alishuhudia mama wa rafiki yake kipenzi mama Utopi akiwa
anafanya jitihada za kuchungulia dirishani, “mama kuna nini?” aliuliza kadogo,hakuna aliyejibu swali lake kila mtu alionekana yu bize kufanya kile kilichoonekana
kumleta lile eneo,mama Kadogo baada ya kushindwa kuingia uvunguni alikua amesimama akipepesa
pepesa macho yake kushoto kulia juu na chini kuona ni wapi ambapo anaweza kujishkiza na kusahau
kabisa ya kwamba mwanae bado anamuangalia kimshangao na anasubiri jibu la swali lake
alilouliza,wakati hilo zoezi linachukua nafasi sauti ya mama Utopi aliekua anachungulia dirishani
ilipata kuskika, “mama kadogo,mbwa wako wote wamekufa!!” “wamekufa? Nani kawaua?” “sasa mie ntajuaje na wote tupo ndani? Alafu nilivyochungulia upande wa mlangoni sijaona mtu!” “we! Ujaona mtu?..sasa ile sauti iliyokua inabisha hodi ni ya nani?” “hapo sasa!!..au kazunguka kwa nyuma?” “mh mungu wangu!..mie hata sielewi,yani hapa haja zote zimenibana!” “mie naona bora ya wewe,mwenzio hapa miguu inatetemeka na moyo unanienda mbio kweli!” “mama kwani kuna nini??” Kadogo alilirudia swali kwa msisitizo baada ya kuona maongezi yaliyokua pale hayaelewi, Mama kadogo alitazamana na mama Utopi kwa muda kidogo,kisha akajibu “lala tu baba wala usiogope..” “mama silali mpaka uniambie kuna nini mbona mnaonekana mnaogopa?” “haina shida mwanangu,hakuna chochote baba eenh…wala usiogope we lala tu” “kweli Kadogo wala usihofu hakuna kitu” alidakia mama Utopi huku akililazimisha tabasamu kumjazisha Kadogo ujinga, mama Kadogo alisita kumwambia ukweli mwanae kwa hofu kua unaweza kulirudisha tatizo ambalo
huwa linamsumbua la mshtuko wa moyo,hivyo alijitahidi kuuzika ukweli kwa uso wa bandia na
maelezo yasiyo sahihi ili aepushe jambo lingine kutokea, wakiwa katika maongezi mafupi ya kuubadilisha ukweli katika macho na masikio ya Kadogo,ghafla
walishtushwa na sauti toka nje zilizokua zinaimba! “nao ni utawala wa giiiiza! Nao ni utawala wa kiiiiza! Wasio amini kuwaumiza! Na watakaoungama kuwahimiza! Sita! Sita! Sita! (sauti nyingine ikidakia) kwenye paji la uso! Sita! Sita! Sita! Kwa Sita! Sita! Sita! Tunawasilisha! Sita! Sita! Sita! Tunawakilisha!!” kisha sauti ikatulia kwa muda kidogo,sauti nyingine ya mtu mmoja ikaskika.. “kama wataka jiunga na ulimwengu, kama wataka kuishi tangu na tangu, toka nje upewe alama ya maisha! Toka nje na yote yatakwisha! Ila ukibaki humo ndani utakua ni wa sadaka!!”
Mama Utopi baada ya kusikia hayo alidondoka chini kama mzigo,akapoteza fahamu! Kazi ilibakia kwa mama Kadogo ambaye tayari aliishalowesha khanga yake kwa mkojo,masikini mwanae nae alikua anachungulia dirishani akiyatoa macho yake kwa kutoamini,watu waliokua pale nje na mavazi yao meupe na mekundu walioonekana hawana muda wa kupoteza,wapo serious na wanasubiri ujio wao,aligeuza macho yake kwa mama yake akauliza, “mama hawa wakina nani?” hakujibiwa kama alivyotarajia,mama yake alikua amezubaa na mdomo ulikua mzito kuufungua,macho yalikua yamemtoka na kichwani alikua anajaribu kujiuliza kwamba yupo ndotoni ama ni kweli? Alishtuliwa na sauti ya mwanae Kadogo iliyouliza tena kwa mara ya pili ikiambatana na tendo la kumsukuma sukuma ili kumrudisha kwenye fahamu, “mama hawa watu ni wakina nani?” “njoo…njoo! Sogea haraka!!!” alielekeza mama Kadogo,alimvuta mwanae baada ya kumkaribia kisha akamueka mgongoni,kabla ya kujitoa ndani ya chumba alimuangalia mama Utopi aliyezirai,kwa uchungu akasema “inanibidi nifanye hivi,samahani sana” kisha haraka alitoka ndani ya nyumba kwa kupitia mlango wa nyuma, alikimbia sana kadiri ya uwezo unavyomruhusu kutokana na mzigo wa mtoto aliokua nao mgongoni,alikatiza mashambani kama hana akili nzuri,alikimbia na alikimbia maskini kuokoa maisha yake na ya mwanae mwenye umri wa miaka saba tu,kila alipokimbia bado aliona haitoshi hivyo alizidi kuendeleza zoezi,baada ya muda wa dakika arobaini na tano alichoka na alikua anahema kama mbwa,alimshusha mwanae na wakaanza kutembea haraka haraka wakielekea mbele wasikokufahamu kutokana na giza kali lililotawala machoni mwao, “mama tunaelekea wapi?” “sijui,ila twende tu” “mama mi naogopa…ni giza sana!” “nisikie mwanangu,hatuna la kufanya zaidi ya hili tulifanyalo sasa kama tungependa kuishi zaidi,tusogee tu mbele kwa mbele tutajua cha kufanya hukohuko” “mama…kwani yupo wapi baba?” “sijui yupo wapi!” “hatujamuacha nyumbani?” “hayupo nyumbani,aliondoka na hajarudi mpaka sasa hivi” alijibu kiuchungu mama Kadogo, “he! Mama ile nini?” “wapi??” kiuoga haraka aliuliza, “kile kinachowaka!” “mh nadhani ule ni moto,ila…ni nani atakua kauwasha?” aliuliza mama Kadogo huku wakiwa wamesimama na mwanae kibutwaa, baada ya muda kidogo walimuona mzee mmoja akitokea na kuni alizozishika mkononi kisha akazirushia kwenye ule moto,kumbukumbu za mama Kadogo zilimwambia kwamba yule ni mzee Otongo mganga wa jadi wa pale kijijini kwao na ndie yule aliyekua anawaonya juu ya ujio wa kizazi cha nyoka ambacho sasa hivi ndicho kinachoanza utawala,bila kupoteza muda alimshika mwanae mkono na kuanza kumswaga kuelekea lile eneo, “mzee!..” aliita mama Kadogo na kumfanya mzee Otongo ataharuki kwa kutokutegemea, “we nani?” “mie mama kadogo!” “mama Kadogo? Umefikaje huku?” “mzee tumekimbia nyumbani,lile jeshi la 666 lilituvamia!” “yote mmeyataka nyie!!!” “mzeee!” “hakuna cha mzee,yote mmesababisha nyie wenyewe!…ni mara ngapi nilikua nawaambia kwamba Vero auwawe?” “mzee sasa mimi ningewezaje?” “unataka kuniambia kwamba kijiji chote cha Igesambo kingeshindwa kufanya hilo jambo? Mume wako ni shujaa,na anajulikana kijiji kizima,kwanini hakufanya hivyo kuokoa maisha yetu??” “lakini mzee wangu sidhani kama huu ni muda wa kuzozana na kulumbana,inabidi tutafute suluhisho la haya..” “suluhisho gani unavyodhani? Kwanza una uhakika hata wa kuiona baadae hapo ulipo??!” alifoka mzee Otongo huku mate yakirukaruka toka mdomoni, “kwahiyo mzee Otongo tusubirie tufe tu hivihivi?” “sina matumaini tena,mke wangu wameshambeba,watoto wangu pia watatu washachukuliwa,na Kilembo yule msaidizi wangu tayari ashapigwa chapa kwenye paji lake la uso,amekua mfuasi wao!” “kwahiyo mzee wangu hakuna cha kufanya kabisa?” aliuliza tena mama Kadogo kwa sura ya udadisi, “sijui yani,sijui! Tegemeo letu lipo tu sehemu moja mama Kadogo,sehemu moja tu!” “sehemu ipi hiyo tena mzee Otongo??..” aliuliza, Mzee Otongo alionekana anafikiria jambo,kisha alifungua kinywa chake kwa mjazo akasema “kila saa naangalia angani,kila mara nanyanyua nyuso yangu kuielekeza juu kutizama na kuchunguza kama kuna tumaini lolote litakalochipukia,tumaini letu ni kuchomoza kwa nyota nyingine angani,nyota itakayoamsha matumaini yetu yaliyokufa,nyota itakayozima uoga wetu na kuangaza amani yetu..” ghafla sauti ya kitu kilicho kwenye mwendo iligota kwenye masikio yao,walitoa macho kwa uoga,mapigo ya moyo yakaanza kuchochea kasi hasa ya Mtoto Kadogo mwenye matatizo ya moyo,walitizamana kwa macho ya viulizo na midomo iliyogoma kufunguka,joto likatotesha nguo zao,haraka wakainuka na kukimbia kwenda kujificha! Kadogo alikua anahema juu juu na kwa nguvu hali iliyomfanya mzee Otongo amzibe mdomo,ubavu wa mzee yule uliegemeana na wa mama Kadogo aliyekua anatetemeka hivyo mtetemo wote ule uliokua unampitia mama Kadogo alikua anausikia,walitoa macho na kufumba kabisa midomo yao ili wasiskike,huku wakishuhudia watu wale walio idadi ya watu watano wakiwa wanapepesa macho yao kutafuta watu kwa ajili ya sadaka zaidi,mzee Otongo alinong’oneza.. “mama Kadogo tuondoke hapa si salama” “mh tukiondoka si watatuskia?” “hapo walipo wananusa harufu yetu na ndo mana unaona wamekazania hili eneo” “kwahiyo?” “tuondoke taratibu kabla hawajatugumia” alizidi kutia msisitizo mzee Otongo, baada ya muda si mrefu walinyanyuka taratibu toka kwenye kibanda kilichokongoroka walipokua wamejificha,walianza kunyata kama watu wanaohesabiwa hatua,pole pole huku macho ya tahadhari yakiwa yanawatizama wale watu mara kwa mara,mioyo yao ilikua inadunda kwa kasi hasa Kadogo ambaye ana matatizo,alitoka jasho mno ikiwa ni moja ya viashiria ya kuanza kuzidiwa,damu ilikua inazunguka kwa kasi mwilini na mama yake aliligundua hilo,alianza kuhisi mkono wa mwanae alioushika unapoteza nguvu na hakua na jinsi zaidi ya kumnyanyua na kumweka mgongoni,waliendeleza zoezi la kunyata kunyata na kunyata mpaka pale mzee Otongo alipotoa ishara, “tukimbie mama Kadogo!” na mbio zikaanza kama za farasi,mzee Otongo alitangulia sana mbele na kumuacha mama Kadogo nyuma hali iliyomfanya aamue kumsaidia mama Kadogo mtoto anaeonekana kumchosha ili wakimbie zaidi,mkono wa mama Kadogo ulishikwa na mzee Otongo kinguvu hasa ili usiponyoke,walijitahidi sana kukimbia huku wakipambana na hali ile ya baridi la usiku na visiki na mawe mbalimbali yaliyoonekana kuwaumiza miguu yao,hawakujali hilo ila walilenga tu kusogea mbele na kuokoa roho zao.Mgongo wa mzee Otongo ulionekana kuhimili mzigo wa mtoto Kadogo ila mama Kadogo ambaye alitoka kukimbia kabla ya kukutana na mzee Otongo alionekana hana nguvu tena ya kuendelea na zoezi lile,alisimama huku akishika kiuno,akasema.. “mzee….uuh!…uuh..siwezi tena!…nimechoka!” “mama Kadogo jitahidi,hatujawaacha mbali sana wanaweza wakatufikia!” “mzee Otongo….uuuh..uuh!..nimechoka sana aisee..!” huku akiinama, “mama Kadogo!!” “abee…mzee Otongo” kiuchovu aliitika “embu angalia ile!!” “nini tena??” mama Kadogo aliuliza, “ile angani! Ni nyota nyingine ama macho yangu!!?” haraka mama Kadogo aliyarusha macho yake angani kutizama alichoelekezwa, “ndio!! …eh!..ndiooo jamani! Ni nyota nyingine mzee Otongo…ni nyota nyingine!!!” “ha! Mama Kadogo kuna mmama ana uchungu wa kujifungua sasa hivi tunavyoongea!! Na ndie atazaa mtoto atakaetuokoa,mama Kadogo tumaini li hai!..huree!!” “sasa huyo mmama yupo wapi??” “kijiji cha pili toka ilipo Igesambo,na inabidi tumuwah kabla huyo mama hajadhuriwa na Jeshi la 666 kwani wakiiona tu ile nyota watamtafuta kwa udi na uvumba ili wamtokomeze!!…haraka inuka mama Kadogo,haraka tumuwahi mtoto anekuja!” haraka mama Kadogo alieanza kupata nyuso yenye mwanga wa matumaini aliinuka na wakaanza kutembea harakaharaka kwa dhumuni la kukusanya nguvu ya kukimbia hapo mbele,kushoto kulia kushoto kulia miguu yao ilipiga maksai wakitafuta kijiji cha pili toka kilipo Igesambo,kijiji cha Utowele,kijiji cha wavuvi na wakulima kama imaanishavyo jina lake,kukifikia kijiji cha Utowele inabidi wavuke mto mkubwa Inguvai,wapite safu ya milima Iramba kisha ndipo watakapokanyaga ardhi ile ya mwanga,ardhi ya tabasamu,ardhi ya mapinduzi na ardhi ya ukombozi,baada ya safari yao kutimiza nusu saa walianza kusikia maporomoko ya maji yaliyowajulisha ya kwamba wapo karibu na mto,mto Inguvai usiopungukiwa na maji misimu yote ya mwaka kutokana na kutokea kwenye safu ya milima Iramba ipokeayo mvua za kutosha zipendeshazo msitu kwa umbijani, ilihitaji uangalifu mkubwa sana kuvuka mto ule hasa muda ule wa usiku,maji yake yana nguvu mno na yanatosha kabisa kumpeleka mtu mzima hata mnyama yeyote endapo akitumbukizwa. Walivyowasili kwenye kingo za ule mto mzee Otongo alimshusha chini kadogo,kisha aligeuza sura yake na kumtazama mama Kadogo akisema “inatubidi tusali mama Kadogo,mungu awe nasi na atushike mkono,atuongoze kuuvuka mto huu,na pia atuongoze tuivuke milima ile…na hata kama mmoja asipofanikiwa isiwe mwisho wa mapambano.umenisikia mama kadogo?”
“Inatubidi tusali mama Kadogo,mungu awe nasi na atushike mkono,atuongoze kuuvuka huu mto,na pia milima ile….na hata mmoja wetu asipofanikiwa isiwe mwisho wa mapambano yetu.umenisikia mama Kadogo?” sura yenye msisitizo isiyotania ya mzee Otongo iliyatamka yale maneno.
“sawa mzee Otongo,inatubidi tupigane mpaka tone la mwisho la damu yetu,inabidi tufe tukijaribu” alieleza mama Kadogo huku chozi likimlengalenga. Aliyatupia macho ya huruma kwa mwanae,akachuchumaa akambusu kwenye paji la uso kisha aliinuka na kusema “sasa tunaweza kuvuka..” akamueka mwanae mgongoni,akaanza kusogelea maji ya mtoni taratibu huku akitanguliwa na mzee Otongo. Mto Inguvai hauna daraja la kumuwezesha mtu kuvuka kwa urahisi,ni utashi wa mtu tu ndio unaotakiwa ili aweze kurukia mawe yaliyokuwepo pale kwa ajili ya kuikuta ng’ambo,ilimuwia vigumu sana mama Kadogo kurukia yale mawe kwani ukiachana na lile
giza la ule muda bado alikua na mtoto mgongoni,walisogea hatua mbili tatu huku moyo wa kila mtu ukidunda kwa uoga na tumbo la kila mtu likisokota kwa uoga pia,mawe waliyokua wanayakanyaga yalikua yameshika utelezi hivyo ilihitaji uangalifu mkubwa na bado miguu yao iliyo peku ilikua inapitiwapitiwa na maji kitu kilichoashiria ya kwamba maji ni mengi kiasi cha kukaribia
kufunika yale mawe yatumiwayo kama kivushio,hakukua na muda wa kutosha wa kuangalia nyuma,kila mtu aliyatoa macho kwa kiasi kikubwa ili yapambane hata kidogo na lile giza lililopo ili apaone pa kuutuliza mguu wake,walizidi kusogea na mwendo wao wa kinyonga na ilibakia kama mawe matano tu ili waweze kupita kile kizuizi,ghafla sauti kubwa ya mlio wa pembe la ng’ombe iliskika!!
Haraka kwa uoga mama Kadogo aligeuka nyuma kabla sauti ya mzee Otongo kufika masikioni mwake ya kwamba hatakiwi kugeuka!!
Mguu wake wa kulia ulio mbele uliteleza na kumfanya aifungue mikono yake kwa ajili ya tahadhari ya anapodondokea na kumuacha Kadogo aliekua kambeba mgongoni akidondoka kwa urahisi!!!
Mikono yake miwili ilishikilia mawe kwa nguvu na kumfanya abakie salama kwa kutopelekwa na maji ila mwanae Kadogo ambaye kamwili kake hakakutosha uzito kushindana na ile nguvu ya yale maji alibebwa kama kikaratasi akimuacha mamaye akilia kwa uchungu bila msaada wowote!!
Mzee Otongo ilimbidi arudi nyuma kitaratibu,alishika mikono ya mama Kadogo iliyoanza kuzidiwa nguvu na kuanza kumvuta kwa lengo la kumuondoa kwenye yale maji yenye kasi kubwa!!
“mama Kadogo jitaahiiidiiiiiiii!!!!..” “mzee Otongo niache tu nife! Mwanangu jamani!!!!!” “mama Kadogo hatuna muda wa kupotezaaa!!!!.. Tafadhali jitahidi utoke kwenye hayo maji nguvu inaniishiaaa!!!!!” “mwanangu Kadogo jamaniii!!!” “mama Kadogooo!!!…tafadhali nadhani unakumbuka nilivyokuambia kabla hatujavuka..tafadhali jitahidi utoke,tafadhali nguvu zinaniiiishaa!!!” kwa nguvu aliropoka huku akikunja sura! * * * * upande wa pili wa shilingi jeshi la 666 lilikusanyika,ile mbiu ya pembe la ng’ombe iliyopigwa ilikua ni ishara ya kwamba wanaitwa,walisimama kwa utulivu na usikivu,na tahamaki ndani ya jeshi hilo mama Utopi alikuwepo!!..na si tu huyo hata mama
Marinda na Vero!!…walishapigwa chapa,hivyo walishakua chini ya utawala wa Chernobog!! Mzee mmoja asie mfupi wala mrefu yani saizi ya kati alisimama mbele yao,mkononi alishika fimbo yenye alama ya nyota nyekundu na kimavazi alinawirishwa kwa rangi nyeusi na nyeupe,macho mekundu na lips zake pana ziliönyesha ana kabiliwa na jambo,bugudha na hasira zilionekana kumteka!!
Kabla ya kufungua mdomo na kunena jeshi la 666 liliinamisha vichwa na kudhihirisha ya kwamba alie mbele ni mkubwa wao, “ni nyota ndio iliyotuita! Ni kwasababu ya nyota tupo hapa!! Nyota nyingine imechomoza angani,nyota itishiayo nyota ya CHERÖBOG!!!..nyota imaanishayo ya kwamba kuna mtoto anazaliwa,nyota imaanishayo hatari kwa utawala wa giza,nyota itakayoamsha tena Jua lililopotea,nyota itishiayo makazi ya KUZIMU duniani!!!
Hakikisheni huyo mtoto haponi! HAKIKISHENI MNAMTOKOMEZA KABLA JUA HALIJACHOZA TENA!!! HAKIKISHENI
MNAMMALIZA HARAKA IWEZEKANAVYO!!!” “Ameen!!”
Walikimbia kwa kasi ya ajabu,hasira na dhamira ya kweli ikitawala vichwa vyao,kila mmoja kwenye paji lake la uso alikua na alama ya 666 ikiashiria na kuthibitisha ya kwamba anamilikiwa na utawala wa giza,utawala wa wapinga mwanga,utawala wa nyama na damu,utawala wa mungu mweusi,utawala wa CHERNOBOG,macho yao mekundu na pua inusayo harufu ya binadamu,miili yao ya baridi na yenye rangi ya kijivu bila kusahau masikio yao yaliyosimama yalikua ni sare zao mbali na nguo zao nyekundu na nyeupe,walitumwa wakamuangamize mtoto aliezaliwa,walitumwa wakamtokomeze haraka iwezekanavyo kabla ya jua kuchomoza kwani ni hatarishi kwa utawala wao na ni hatarishi kwa malengo yao,baada ya muda wa dakika arobaini na tano walishawasili kwenye kingo za mto Inguvai!!! Je wakina mama Kadogo wako wapi? Kwa mbaali juu ya safu ya milima Iramba mzee Otongo na mama Kadogo walionekana wakizidi kukwea,walizidi kupanda milima kwa lengo la kwenda upande wa pili kumuwahi mtoto aliezaliwa kabla ya kuchukuliwa au kuwahiwa na jeshi la 666,miili yao ilikua imechoka kutokana na zoezi lile gumu lakini hawakujiruhusu wapumzike kwani walifahamu ya kwamba jeshi la 666 li njiani na tayari watakua na taarifa juu ya uzao ule,wote walikua wanahema kama mbwa hasa mama Kadogo ambaye bado uchungu wa kupotelewa na mwanae ulikua umemtawala moyoni,alishindwa kuzuia machozi yasimtoke lakini pia hakutaka aruhusu miguu yake isimame,alimuita mzee Otongo alie mbele yake kisha akampa mkono wake wa kulia,akasema “nahisi kichomi!” ..mzee Otongo akamvuta na kumkumbatia kwa nguvu kisha akamnong’oneza.. “imebakia umbali wa kama nusu saa kufika kijiji cha Utowele,imebakia huo umbali tu ili tulikute tumaini letu,imebakia tu umbali huo kwa ajili ya maisha yetu.hapa nilipo nina kiu na miguu inanivuta mno,lakini unanihitaji ili tuendelee,na mimi pia nakuhitaji ili niendelee,tafadhali jitahidi tukamilishe tulichokianzisha” yale maneno yalimpa motisha kubwa mama Kadogo,alishusha pumzi ndefu kisha wakaanza tena kutembea kuelekea mbele kwa mbele. Wafuasi wa jeshi la 666 bila kujiuliza mara mbilimbili walijitosa ndani ya mto Inguvai,mto wenye maji yenye kasi na nguvu ya hatari,lakini cha kushangaza walipiga mbizi mithili ya samaki na hakuna hata mmoja wao alieonekana kuzidiwa!!..hata mama Utopi mama Marinda na Vero waliopigwa chapa tayari walionekana kumudu yale maji!! Mikono yao ilikua na nguvu ya ajabu na pia nyuso zao zilionekana kupambwa na alama ya moto ya tarakimu 666! Baada ya kufika upande wa pili wa mto,pua zao zilianza kuvuta harufu ya binadamu na haraka bila kupoteza muda walianza kuifatilia kwa mwendo wa kasi,huku macho yao yalioakisi mwezi yakionekana kung’ara mithili ya paka!! Umbali waliopo wao ulikua ni kama kilomita moja kamili tokea walipo wakina mama Kadogo,ila kwa ile kasi waliyokua nayo ilikua ni hatarishi na hivyo uwezekano wa kuwafikia ulikua ni mkubwa ukizingatia matatizo ya vichomi na miguu inavyowapa mtihani mama Kadogo na mzee Otongo. Jeshi lile la 666 halikua na utofauti wowote na wanyama,hawakua na huruma hata kidogo kutokana na mioyo yao kubadilishwa na kua ya kishetani,maumbo yao pia hayakua ya binadamu wa kawaida,kuanzia kwenye vidole na kucha mpaka kwenye unywele,walikua na nguvu mno na ni kutokana na giza lililopo na ndio mana walipopewa maagizo waliambiwa wayatekeleze kabla ya jua kuchomoza kwani ndio utakua ukomo wa nguvu zao za ajabu! Walizidi kujongea kwa kasi bila kuonyesha dalili yoyote ya kuchoka huku wakiwa wamepangana kimstari!…mara ghafla mwenzao alie mbele alisimama kisha akageuza shingo na kuwaambia wenzake “nimeona watu kule juu!!!”
Mungu wangu wale walikua wakina mama Kadogo!! Jeshi la 666 liliongeza kasi huku macho yao yakieka msisitizo kwa wale watu kwa mbali waliowaona,mzee Otongo alihisi watu wanakuja kwani alisikia vishindo vikubwa na sauti za watu ambao hazikuleta maana masikioni mwake,aligeuka na kumshika
mkono mama Kadogo na kuanza kukimbia nae kwa kasi!!. “mama Kadogo kimbia wanakuja!!!” kwa tahamaki alitamka huku akimvuta mama Kadogo alietia kidogo uvivu,mzee Otongo alijitahidi kumburuta mama Kadogo alieonekana kama mzigo kwa nguvu zake zote na hakutaka kabisa kumuachia,mama Kadogo hakutamka neno lolote kitu
kilichoonyesha ya kwamba alishakata tamaa hata ya kuishi!!..hata kasi yake ya kukimbia ilikua ni ile ya kukosa matumaini kabisa! Jeshi! Jeshi! Jeshi la 666 lilizidi kuwakaribia wakina mama Kadogo na huku mbele yao akionekana mama Utopi ndie aongozae msafara!
Kanzu yake aliyovalishwa yenye rangi nyeupe nusu na nyekundu haikutosha kumzuia kukimbia kwa kasi mithili ya simba alieona swala,aliruka viunzi na visiki,aliruka mashimo na vizingiti lengo kichwani likiwa moja tu,la kumuangamiza mtoto aliezaliwa na kuua wote wale waonekanao vikwazo kwao, kimbia! Kimbia! Kimbia!
Alizidi kusema mzee Otongo kwa sauti iliyokaribia na kulia huku bado aliekua anamvuta akiwa kimya na mzito kama furushi la dhambi!
Hayawi hayawi yakawa! Mama Kadogo alipigwa na gongo mgongoni na kudondoka kama mzigo chini!! Alilia kilio cha maumivu kilichokwangua hadi sakafu ya moyo wa mzee Otongo aliegeuka na kushuhudia jeshi! Jeshi! Jeshi la 666 likiwa tayari karibu nae lishawadia, alipigwa kofi moja kali lililomrusha mbali mithili ya mtu aliepigwa na shoti ya umeme!
Hata kabla ya kufungua macho yake alisikia mgongo wake ukiita kwa mlio wa nguvu uliosababishwa na kupigwa na gongo! Aaaaaaahhh!! Alilia mzee Otongo kwa uchungu wa maumivu ambao haukusaidia hata kidogo kumuokoa na kipigo alichokua anakipokea toka kwa jeshi! Jeshi! Jeshi la 666,alipigwa kipigo cha mbwa mwizi! Alipigwa kila eneo na alichanwa chanwa mgongoni na makucha ya wale watu walio na mioyo ya wanyama! Hakuwahi kuhisi maumivu kama yale toka azaliwe na mama yake Lenaka miaka arobaini na mbili iliyopita ndani ya kijiji cha Igesambo! Macho yake yalianza kupoteza muelekeo na yakaanza kuelekea juu kisha yakafumba kabisa!
Upande wa nyuma hatua kama tano mama Kadogo alikua bado anashushiwa kipigo na wanawake wenzake wakina mama Marinda,Vero na mama Utopi waliokua wanyama tayari chini ya CHERNOBOG!! Hawakua na fikra za huruma hata kidogo! Hawakua na mioyo ya kibinadamu! Hawakumjua tena mama Kadogo na akili yao haikua tena ya binadamu hivyo walitumia kila zana ikiwemo mikono yao iliyo na kucha mithili ya simba kumjaza alama za kutosha mmama yule alieonekana yu kimya!!
Kabla ya wao kuridhika na lile zoezi ghafla jua lilianza kuchomoza,anga likaanza kuwa la kahawia na giza likaanza kupotea!! Walipigwa na butwaa na kuwehuka huku wakitoa sauti za ajabu na wakikimbia huku na huko bila mpangilio kurudi kule walipotokea,walichanganyikiwa baada ya kuona ile hali na zile chapa zao zilizo juu ya mapaji yao ya uso zilianza kufuka moshi uliodhihirisha ya kwamba wanaungua!!! Hae hae lile eneo lilikua! Lakini bado mama Kadogo na mzee Otongo walikua kimya huku miili yao ikivuja damu!!
Kabla ya wao kuridhika na lile zoezi ghafla jua lilianza kuchomoza,anga likaanza kua la kahawia na giza likaanza kupotea!! Walipigwa na butwaa na kuwehuka huku wakitoa sauti za kupayuka na wakikimbia huku na huko bila mpangilio kurudi kule walipotokea,walichanganyikiwa baada ya kuona ile hali na zile chapa zao zilizo juu ya mapaji yao ya uso zilianza kufuka moshi uliodhihirisha ya kwamba wanaungua! Hae hae lile eneo lilikua! Lakini bado mzee Otongo na mama Kadogo walikua kimya huku miili yao ikivuja damu! Kuchomoza kwa jua kulithibitisha kushindwa kwa CHERNOBOG (Mungu mweusi),lengo la kumuangamiza mtoto aliezaliwa ilibidi lifanyike haraka na kwa ufanisi mkubwa kabla ya jua kuchomoza kwani nguvu zake zina mipaka,zina mipaka? Ndio zina mipaka,wakati wa usiku huwa ni kali na za kutisha zaidi na ndio mana walitaka watekeleze ule mpango kabla ya jua kuchomoza ili kuhakikisha ya kwamba jua halitokutana tena na uso wa dunia,hivyo utawala utakua wao daima na milele! Masaa yalizidi kusonga huku miili ya mzee Otongo na mama Kadogo ikianza kuzongwa zongwa na Inzi waliofuata majeraha makubwa waliosababishiwa na jeshi! Jeshi! Jeshi la 666,saa nne asubuhi isiyotambulika madakika yake watu watatu waliokua katika shughuli za uwindaji toka kijiji cha jirani Utowele waliiona miili ile miwili iliyolala kama mizoga,walishtushwa na lile jambo! Na moja kwa moja walidhani ya kwamba watakua wamedhuriwa na wanyama wakali wa msituni kwani safu ya milima Iramba ina wanyama wakali kama chui na simba ambao ni mara chache kuonekana mida ya asubuhi na mchana,mapigo ya moyo ya mzee Otongo yalisikika kwa mbali sana! Vile vile na ya mama Kadogo kitu kilichoashiria ya kwamba hawana muda mrefu maisha yao yatarudi yalipotokea,yani mavumbini. Wale watu watatu,mmoja akiwa ni mzee wa makamo na wengine wawili wakiwa vijana,waliibeba ile miili na kuelekea kijijini kwao,ilibidi wasitishe lile zoezi la uwindaji kwa sababu za kibinadamu,je watapona? Hilo lilikua ni swali lililokita kichwani mwa wale watu walioonyesha roho za utu. Baada ya mwendo wa robo saa waliingia kijiji cha Utowele,kijiji walichokua wanakitafuta wakina mama Kadogo kabla ya kukumbwa na la kuwakumba,kijiji chenye wakulima na wafugaji kwa kiasi kikubwa,kila mtu alishangazwa na ile hali! Na pia walibumbazwa na lile tendo! Hawa mbona wametuletea mizoga? Hilo ndilo swali lililokuja kichwani kwa kila alieshuhudia lile tukio,haraka taarifa zilienea! Kila mtu alieona alimtaarifu na mwenzie,mwisho wa siku kijiji kizima! We baba Madhifa mbona umetuletea mizoga kijijini kwetu??? Maswali yalirushiwa kwao,kila walipotaka kujibu walikumbana na lingine! Na hali ilikua mbaya zaidi baada ya kusema kuwa wameiokota msituni,wanakijiji walicharuka! Waliwataka wakina baba Madhifa na wanae wawili wairudishe ile miili kwani wanaweza wakaleta laana kwenye kijiji chao,hakuna alietaka kuwasikiliza kwa maelezo zaidi na ukizingatia wakina baba Madhifa ni jamii ndogo ya wawindaji kwenye kijiji cha Utowele kilichojazwa kwa kiasi kikubwa na wafugaji na wavuvi. Tokaaa!!! Peleka mizoga yako huko!!!!! Hatutaki maiti tusizozijua kijijini kwetuuu!!..we una okota okota tu!! Maneno ya kebehi na kashfa yalirushwa kwao yaliyochanganyikana na dharau kutokana na hadhi yao ndogo ndani ya kijiji cha Utowele,waligeuka na kuanza kurudi msituni walipotokea baada ya kuona zoezi lao lilioambatana na utu limepingwa vikali na wanakijiji wenzao,ghafla kabla ya kutokomea,sauti ilisikika toka kwa mmoja wa wanakijiji aliyeonekana ni mkubwa kiumri akitokezea toka kwenye mlango wa nyumba ndogo ya udongo iliyojaa moshi ndani kutokana na shughuli ya upikaji dawa aliyokua anaifanya, “suubiiiiiirrrriiiinii!!” huku akiambatanisha na zoezi la kupunga mkono! “waleteni hao watu!!” “sio watu,ni miili ile! Wamekufa!” sauti ya mmoja wa wanakijiji iliskika ikipinga, “nyamaza!! Nani kakuambia wamekufa??” aliuliza yule mzee na kufanya kidogo ukimya utawale huku macho ya wanakijiji yakionesha kujawa na hofu, baada ya muda mfupi baba Madhifa alikua ashafika kwenye eneo la tukio na wanae wawili waliowabeba wakina mzee Otongo na mama Kadogo,waliiweka ile miili chini kama walivyoelekezwa,yule mzee akaanza kuikagua!
Ilichukua kama dakika kumi yule mzee akiitizama na kuipekua ile miili huku wanakijiji wakiwa wamemzingira,aliinua macho yake na kutoa amri ya ile miili kuingizwa ndani,wale vijana wa baba Madhifa walitekeleza hilo jambo haraka,waliingiza ile miili ya
mzee Otongo na mama Kadogo ndani ya kale kajumba kadogo cha udongo cha yule mzee alieonekana kuheshimiwa na kusikilizwa na wanakijiji,bila ya kujivunga yule mzee nae aliingia ndani na kuwaacha nje wanakijiji waliokua na shauku kubwa ya kutaka jua kinachoendelea,baadhi yao walianza onekana wakijiondoa kwenye lile eneo taratibu na kwenda kuendelea na
shughuli zao zingine huku bado midomo yao ikiteta lile tukio lililoonekana kuchota hisia zao kwa kiasi kikubwa,wakati hayo yote yanachukua nafasi kuna baadhi ya wanakijiji walikua hawana habari kabisa kuhusu lile tukio!!…labda kutokana na kubanwa na
hali husika,umbali wa nyumba kumi na tano toka pale pa yule mzee kulikua na nyumba moja tulivu ya udongo iliyopakwa chokaa iliyofanya ionekane ni ya kipekee kidogo tofauti na nyumba zingine,madirisha yake makubwa yapitishayo hewa na sauti bado
hayakutosha kuwajuza watu walio ndani juu ya kinachoendelea kwa nje,nyuso zao zilijawa na tabasamu na huku wakionekana
kutowaza kabisa yanayojiri ulimwengu mwingine, “enhe..sasa nimpe jina gani?” lilikua swali alilouliza mdada mmoja aliemshika mtoto akijulikana kama Julina huku akitabasamu “mmh mie mwenyewe sijui,we si ndo mama bwana! Mie kazi yangu ya ukunga nshaimaliza” alijibu mama Halima,mmama mwenye rangi ya maji ya kunde,mkunga maarufu kijijini aliebakia baada ya kifo cha mama Ramla miaka miwili iliyopita, “au tumsubirie baba yake?” “utakavyoona wewe ni sahihi…”
“ujue nini mama,mimi ni kama mwanao,sina utofauti na mwanao Halima,sijui hata nikushukuru vipi kwa kweli,namsubiria tu mume wangu arudi ndipo tutakapojua cha kufanya” “wala usihofu mwanangu,ujue hii kazi ya ukunga ni kama karama kwangu,si ajira!! Kwahiyo naifanya kwa ajili tu ya kuwasaidia
wanizungukao kwani baada ya mwanangu Halima kufariki,kila mtoto nizalishae ni kama mtoto wangu”
“pole sana mama,kifo cha Halima kiliniachia pia pengo kubwa,kama unavyojua,alikua ni rafiki yangu mkubwa! Yeye ndo kwa kiasi kikubwa alinishawishi niole na Kitanzi” “tuachane na hayo mwanangu nisije nikatonesha donda lililoanza kupona,ila mumeo Kitanzi yupo wapi saa hizi?” “mmmh…hata sifahamu kwa kweli,aliahidi kuwa atakuwepo hapa usiku wa jana,lakini mpaka saa hizi sijamtia kwenye zangu mboni”
nyuso zao zilificha matabasamu yalionawiri hapo kabla,mawazo yakaonekana kuwashika hatamu,Julina alianza kupata hofu,mama Halima akaligundua hilo.. “sikiliza mwanangu,ujue sisi binadamu tunapanga na mungu pia anapanga,hivyo huwezi jua,tuombe tu uzima!” “mmh kweli mama..”
kidogo maongezi yaliingiliwa na kilio cha mtoto,mtoto alieonekana hana muda mrefu ulimwenguni,haraka Julina alitoa titi lake la kushoto na kumyamazisha nalo,uso wa Mama Halima ulionekana unaficha jambo,na hata macho yake yalikua yanasadifu ya kwamba ana kitu ndani ya mtima chamsumbua.. “mama vipi??..mbona hivyo tena!” “mmh,kuna kitu kinanitatiza kusema kweli,jana usiku wakati tupo katija zile shughuli za kufungulishana nilisikia kelele!!” “kelele??…si kelele zangu hizo ama?” “hapana!…mara ya kwanza ilikua ni kelele ya kike,na mara ya pili ilikua ya kiume!!!” “wee!..mie mbona sikuzisikia??” “usingeweza kuzisikia,uchungu uliokua nao usingekuruhusu ufanye hilo..” “mama una uhakika na hilo jambo??”
aliuliza Julina kwa umakini huku akimtikisatikisa mwanae kitaratibu, “asilimia zote!…na ubaya ni kwamba kila ninapotulizana,zile sauti hunirudia masikioni!!!!!” kwa msisitizo alinena Mama Halima huku akiyatoa macho,hofu ikaanza kumrudi Julina tena!!…huyo atakua sio mume wangu kweli?? Alijiuliza moyoni,kabla hajapata majibu,hodi ikaskika!
Ilimbidi mama Halima ainuke na kwenda kuchungulia dirishani kabla ya kufungua,he!! Alishuhudi mabibi wawili wageni machoni wakiwa mlangoni!!..aligeuza shingo yake na kumtizama Julina kwa tahadhari, “unawajua hawa watu?” aliuliza, “wakina nani?” “njoo uwaone!”
alielekeza kwa sauti ya chini iliyokamatwa na kauoga, Julina aliwatazama wale mabibi kupitia pale dirishani kisha akamjibu mama Halima kwa kunong’oneza, “mmh mh,siwajui!!!”
Cha kushangaza walivyorudisha tena nyuso zao dirishani kutizama nje…hawakuona kitu!!!!..Pah!!!..tik-tak!!! Tik-tak!!! Tik-tak!!! Tik-tak!!..mioyo yao ilianza kwenda kasi ya ajabu!!! Bumbuwazi lilikamata midomo yao bara-bara! Macho yaliwatoka mithili ya kwamba wamemshuhudia shetani akionja pepo!!!..walitupiana macho ya uogo wakiulizana wameenda wapi??? Swali lililopasua hisia zao mithili ya shoka kali lililotoka kiwandani kwenye gogo bua lililochoka! Mungu wangu..watafanyaje sasa?? Hilo lilikua ni swali la pili rejea lililokita vichwani mwao kama hitimisho!!! Hapakukalika tena!!..nyumba ilizidi kuwa ndogo kwao! * + * + * koh-koh! Sauti ya kikohozi cha maumivu kiligona sikioni mwa mzee Patili,aligeuka haraka na kuangalia kilipotokea akagundua ya kwamba chatoka kwa mzee Otongo aliekua amelala chini chali,alitabasamu kwa mbali,jitihada za dawa yake aliyompaka zilionekana kuvuta kheri,hakutaka kupumbazwa na hilo jambo,aligeuka na kuendelea na shughuli yake ya kumpaka dawa mama Kadogo taratibu akimalizia miguuni baada ya mikononi na usoni akijitahidi kuyaziba majeraha na dawa ile ya unga yenye rangi ya kahawia,mchanganyiko wa miti mbalimbali iliyosagwa. Chumba kilitawaliwa na moshi kwa kiasi kikubwa,lakini hilo halikuonekana kumkwaza mzee Patili,kwani tangu na tangu,enzi na enzi amekua katika yale mazingira ambayo hasa huchangiwa na shughuli zake za upikaji dawa,mvi ziligoma kabisa kuja kichwani japokua umri uliruhusu hilo,uso wake ulio na makunyanzi ndio uliothibitisha ya kwamba kala chumvi,mzee Patili alikua ni zahanati tosha pale kijijini,akiheshimika na kusikilizwa kama marehemu baba yake aliemrithisha hizo kazi.Baada ya kumaliza ile shughuli ya upakaji dawa,alishusha pumzi ndefu kisha akajituliza kwenye kigoda chake chenye ufa kwa mbali uliodhihirisha ya kwamba ni cha muda mrefu,haraka akili yake ilimtumbukiza kwenye lindi la mawazo,lindi la mawazo mazito juu ya ndoto aliyoota usiku wa kuamkia hiyo alfajiri,ndoto ile ilionekana kumkosesha amani na hata raha vilevile na kila alipotaka kuitafutia ufumbuzi hakupata kitu!!! Alitizama juu ya dari kimawazo huku kichwa kikiegemea mkono akijaribu kuitumikisha akili yake iliyojaa uzoefu wa maisha kumpa majibu, ghafla!!!! “mzee patili funguaaa!!!” sauti za kile zilisikika toka nje, “niniii???..nyie wakina nani!!!” kwa tahamaki aliuliza, “Julina na mama Halima!!!..tafadhali tufungulie haraka!!” alijibiwa,alijinyanyua toka kwenye kile kigoda haraka na kuelekea mlangoni,akaufungua mlango na haraka kwa papara waliingizana wakina mama Halima!! “nyie vipi???” aliuliza mzee Patili,hakujibiwa,akauliza kwa mara ya pili kwa sauti ya msisitizo! “nyie kuna nini?? We mama Halima vipi na huyu Mzazi tena!!!” huku wakihema kwa pupa wakajibu, “kuna wabibi wawili!!” “wamefanya nini?” “wa..wa..walikua wanagonga..mm..mlang..mlango..” “halafu haraka wakapotea!!!” Julina akamalizia sentensi huku akiwa kamkumbatia mwanae na mikono itetemekayo!, “wakapotea!!! Wakaelekea wapi??” “hatujuuii!!!!” julina alidakia, “he! Mzee Patili hawa waliolala hapa chini wakina nani???” aliuliza mama Halima baada ya kuiona ile miili ya mama Kadogo na mzee Otongo pale chini,Julina pia mwenye damu iliyotawaliwa na uoga nae alistuka baada ya kuona hilo,akatahamaki “mungu wangu!!!! Mzee Patili hawa wakina tena???” “msijali kuhusu hao watu,waliletwa hapa na baba Madhifa,waliokotwa toka porini,embu punguzeni uoga na presha enh…tulieni embu,tulieni kisha mnielezee kilichojiri” aliwatuliza mzee Patili. Mzunguko wa damu wa Julina uliongeza kasi kutokana na uoga! Alikua anahema kwa kasi,mama Halima vilevile! Mzee Patili ilimbidi anyamaze huku akiwashuhudia wale wakina mama kwa jicho la kutafakuri hali ile iliyowatokea,moshi uliokuwemo mule ndani ulianza kumuathiri mtoto,akaanza kupaliwa na kikohozi hali iliyomfanya mzee Patili kumshauri atoke nje,kiuoga alijibu “nani?? Mie!! Ah-ah sitoki nje! Wale wabibi watanifata!!!” mzee Patili aliamua kumaliza zogo,alimnyakua mtoto toka kwenye mikono ya mama yake Julina kisha akatoka nae nje,hali ya kushangaza Julina nae kwa uoga akatoka nje!!!!
ITAENDELEA
Simulizi : 666 Nyayo Za Kuzimu Sehemu Ya Tatu (3)
“vipi tena si ulisema hutoki nje??” aliuliza mzee Patili,
“eh! Yani mie nibaki peke yangu ndani??..wale mabibi si watanifuata!!” akajibu Julina huku macho ya uoga yakipendezesha uso wake mwembamba mweusi.Punde si punde mama Halima nae alitoka nje na kujumuika na Julina na mzee Patili aliembebelea mtoto,walianza kuteta kuhusu wale mabibi na pia bila kusahau ndoto ya mzee Patili iliyowashangaza na kuwaogopesha wakina Julina kwa kiasi kikubwa! “mito ilikua miekundu,haikuskika tena sauti za ndege,milio ya shida na malalamiko ndio iliyotawala,harufu ya kifo na umauti ndio iliyoshika hatamu,miti ilipendezeshwa na miili iliyoning’inia kwa kunyongwa,na mioyo ya binadamu ilikua ni ya wanyama,tena wanyama haswa!!!”
alizidi kudadavua mzee Patili ile ndoto huku macho ya wakina Julina yakiwa yanakaribia kutoka kwa mshangao!! Akaendelea, “kila mmoja niliemuona alikua na chapa ya namba mwilini mwake!” “chapa!!..ipi tena??” Julina aliuliza kwa mjazo wa kutaka kujua,kwa masikitiko alijibu mzee Patili “chapa yenye namba tatu,sita zilizorudiwa mara tatu,yani 666!!!..cha kutofautisha tu kilikua ni wapi hiyo chapa
ilipokuwepo,wengine kwenye mapaji ya uso,wengine mikononi,wengine mapajani na kadhalika! Maisha hayakua kama yalivyo,maisha hayakua kama tunavyoyajua,kila mtu muoga na maisha yake alikubali kubandikwa chapa itakayomuwezesha kuendelea kuishi,na wale wenye misimamo yao,walinyongwa kama kuku!!!”
maneno hayo yalizidi kuteketeza amani ndani ya mioyo ya wakina Julina na pia kuzidi kupalilia roho ya uoga iliyochipukia kwa kasi!!….taswira ya kile kilichokua kinaelezewa na mzee Patili ilikua imejengeka ndani ya vichwa vyao hivyo kuipa mwanya hisia za uoga kukumbatia mioyo yao iliyokua inaenda mbio!! Udadavuaji wa ndoto ulizidi kutolewa na mzee Patili,lakini kabla ya kumalizika alikuja mama Tito kwa kasi huku akiwa kashikilia
kichwa na anapiga ukunga,ilikua haiitaji vipimo kujua ya kwamba alikua kwenye matatizo!! “uuuuwwwiiiiiiii!!!!….Maamaaa weee!!! Mungu wangu eeeenhh!!!…jamaniiiiii!!!!” “mama Tito vipi tenaa???” aliuliza mzee Patili kwa hamaki huku wakina Julina wakiwa wameishiwa pozi kwa mshangao!! “mume wangu jamaniii!!!!…mume wangu..mungu wee!! Mume wangu Jamanii!!!!!” “sasa mume wako kafanya nini???” “nimemkuta mume wangu kanyongwa kule shambani,jamani baba Tito wanguuuuuwwii!! Mume wangu mie ntaishijeee!!!” sauti kali ya kilio ya mama Tito iligonga kwenye masikio ya wanakijiji,haraka lile eneo lilifurika watu,habari za kunyongwa Baba Tito zilihamsha taharuki,msururu wa watu ulianza safari na kuelekea eneo la tukio wakiwemo mzee Patili na wakina Julina ambao hawakutaka kabisa kubaki pale kijijini.
Sauti za vilio vya wanawake ilipata kusikika vizuri,tahamaki ilimshika kila mtu,kuona mwili wa baba Tito ukiwa unaning’inia kwenye mti ule wa muembe halikua tendo la kawaida kabisa machoni mwao! Hisia za uoga zilitawala na baadhi yao wenye roho ndogo walizirai akiwemo Julina!!
Nani amefanya haya?? Na amefanya kwa madhumuni gani?? Kila alieshuhudia lile jambo alijiuliza na kuwauliza wenzake pia,sauti ya kilio cha mama Tito iliyokua inazidi kupotelea kutokana na kukaukiwa sauti ilizidi kuchimbua na kumwagilia huzuni iliyodamiri lile eneo,na pia tukio la kumpepea Julina aliezimia liliendeleza hofu mioyoni.
Mwili wa Baba Tito ulishushwa na kufunguliwa toka kwenye kile kitanzi,na taratibu ulibebwa kupelekwa kijijini kwa ajili ya shughuli za mazishi huku bado maswali mengi yakizaliwa ndani ya vichwa vya watu waliokua pale juu ya kipi hasa kinachoendelea. Wakati safari ya kurudi kijijini ikiwa inaendelea ghafla mjadala mzito ulianzishwa,mjadala uliokua unaongelea juu ya ujio wa Mzee Otongo na mama Kadogo kama sababu kubwa iliyopelekea ile hali,yani ujio wao ndio umeleta laana pale kijijini na ndio mana mambo ya ajabu yameanza kuchukua nafasi!!
Asilimia kubwa ya watu walionekana kuafiki hilo jambo isipokua Mzee Patili aliesimama kidete kukanusha hilo kwa nguvu zote na kutetea tendo lake la kuwapokea wale watu kwamba lilikua sahihi. Mama Halima hakua na la kuchangia kwani hakushuhudia hayo mambo na pia Julina hakupata hiyo fursa kwani alikua bado hajazinduka,mtoto wake alikua amebebwa na mzee Patili na mwili wake ulikua mgongoni mwa Mama Halima! Je itakuaje? Na ni nani anahusika na hayo mauaji? Wakina mze Otongo watakua salama mbele ya wanakijiji? Kwa mbali sauti za vilio zilifika kwenye masikio ya mzee Otongo,mwili wake bado ulikua unavuta kwa maumivu japokua fursa ya kuishi bado ilikuwepo mikononi mwake,tumbo lilikua linamuuma kwa sana ilihali na kichwa kutokana na dhoruba kali aliyokumbana nayo ya Jeshi! Jeshi! Jeshi la 666! Alitaka kujiinua,mungu wangu!! Alisikia mpasuko wa maumivu umepita mgongoni pahh!!…ka sauti ka kulalamika kakaitika..aaaahh!!! Kilichoashiria ya kwamba maumivu yamegota penyewe,aliurudisha mwili wake chini na kugeuza shingo kutizama pembeni alipomuona mama Kadogo ambaye bado fahamu hazikurudi kwenye makao yake,alipandisha na kushusha macho yake juu ya mwili wa mama Kadogo na kushuhudia jinsi gani majeraha yalivyoshika utawala,kila pande ya mwili wake ilikua na jeraha na hata alivyojiangalia mwilini mwake aligundua hilo,macho yake yakaanza kubarizi lile eneo alilokua,kuanzia juu chini na pembezoni,umbali wa hatua tano toka alipokua kulikua na jiko litumialo kuni,na sufuria ilikua juu ya mafiga.kilichomo ndani ya sufuria kilionekana kuchemka kwani sauti ya kutokota kupita kiasi na mvuke mkubwa kutoka kwenye sufuria zilithibitisha hilo,mzee Otongo alitambua hicho kitu lakini mwili wake usingeweza kumruhusu kusogea kutokana na mzigo wa maumivu aliokua nao,sauti za watu zilizidi kufika masikioni mwake na mwishowe alisikia mlango unafunguliwa,alikua ni mzee Patili,macho yao yaligongana na kidogo kamshangao kiliwapitia,taswira ya mzee Patili haikua ngeni machoni mwa mzee Otongo ila haikua hivyo kwa mwenzie ambae ilikua vigumu kumtambua kutokana na kile kipigo kumchakaza sura yake kwa kiasi kikubwa,hawakuongea kitu,mzee Patili alifunga mlango na mkono wake mmoja uliokua haujamshikilia mtoto na kufanya sauti za wanakijiji zilizokua bado zinaruruma kwa nje juu ya ujio wa wageni pale kijijini zififie kidogo, “vipi unaendeleaje??” mzee Patili aliuliza, “…mmm..kichwa kinanigonga mno,mgongo nao,vilevile tumbo!!!…issshh!!” alilalamika mzee Otongo, “usihofu,mpaka jioni utakua ushapata unafuu kwani hiyo dawa niliyokupaka ni nzuri sana kwa majeraha na kutuliza maumivu..” “ahsante sana!..eti,kwani hapa ni wapi??” aliuliza mzee Otongo ili kupata uhakika wa pale alipo baada ya nafsi yake kumtonya kwamba ni utowele, “upo kijiji cha Utowele kwa sasa,kwani nyie mlikua mnatokea wapi na mnaelekea wapi??” “tulikua tunatokea Igesambo,na safari yetu ilikua ni kuja hapa Utowele..” “mmmh…kufanya nini??” aliongezea swali lingine,mzee Otongo alijivutavuta huku akipambana na maumivu na mwishowe akakaa,kisha akajibu kwa tabu.. “lengo letu lilikua ni kumuwahi mtoto aliezaliwa..” kauli hiyo ilimshtua mzee Patili! Hakuna mtoto aliezaliwa kijijini zaidi ya yule aliembeba,mtoto wa Julina!!!” kwa hamu ya kujua akaongeza swali lingine.. “mtoto aliezaliwa?? Wa nini hasa??” “huyo mtoto ndie uhai wetu,ndie tumani letu na utawala wa giza ulilijua hilo na ndio mana walitujeruhi,kutudhoofisha na kufanikisha lengo lao la kumuwahi,na hata huku kuchomoza kwa jua ni ishara ya uzao wake….ila yu hatarini na inabidi alindwe kwa nguvu zote kwani jeshi! Jeshi! Jeshi la 666! Wanamsaka kwa hali na mali wamtokomeze!!” maneno yale yalipenya mpaka kwenye mishipa ya damu ya mzee Patili na hapo ndipo alipoanza kupata mwanga juu ya ndoto aliyoiota,lakini kuna kitu aligundua! Haraka akauliza “wewe ni Otongo??” “naam…ndie mimi!..bila shaka wewe ni Patili!” “haswaa mie ndie!” kile kitu kilimshangaza sana mzee Patili,ni muda mrefu umepita toka walipokua pamoja kutokana na uhusiano wao wa kikazi wa kiganga na hakutegemea kama wangekutana katika ile hali!! Ila bado mawazo yalizidi kumsonga kichwani!!! * * * * nje ya kijumba cha mzee Patili bado wanakijiji walionekana kuteta hasa juu ya kifo cha baba Tito ambaye mwili wake ulikua ushahifadhiwa ndani kwake,kutokana na ugumu wa kujua kinachoendelea kila mwanakijiji alitupia hisia zake juu ya wale wageni waliofika ya kwamba kwa njia moja au nyingine wanahusika,nani unadhani?? Ni hawa hawa tu!! Mbona hayajawahi kutokea tangu na tangu?? Hii ni laana!!! Hawa watu wametuletea laana!! Tutakwisha jamani!!! Wanakijiji walipayuka,ngebe za wanakijiji zilizopamba moto juu ya kukemea na kulaani tendo la ujio wa wale wageni bado hazikubadilisha kitu!!! ALINYONGWA MWINGINE MTU MWINGINE!!! NA TENA ALIKUA NI MAMA TITO!!!…PEMBENI YA MAITI YA MUMEWE!!! nani anafanya haya mauaji? Kwanini anaua?? Amedhamiria nini?? Nini hatma ya wakina Mama Kadogo mbele ya kiza cha jamii??
Mama weee!!!..mama Tito kanyongwa jamaaanii!!! Mungu eeee!! Tunakwisha uuuwii!!! Ndivyo alivyosikika mama Kurwa alietoka kwenye nyumba ya mama Tito kwa lengo la kumpa pole kwa kifo cha mumewe,huku akikimbia mikono kichwani mithili ya mtu aliechanganyikiwa machozi na uoga ilionekana kuitawala sura yake!! Hakuna alieamini hizo habari mpaka walipoenda kushuhudia na kukuta jambo lile ni kweli limejiri!! Macho yao yalishudia Mama Tito akiwa kaning’inizwa na kamba nyekundu kama ile iliyomnyonga mumewe muda si mrefu,ulimi ulikua nje na damu ilionekana kutoka puani na masikioni!!!! Mchanganyiko wa hasira na uoga ulitawala mioyoni mwa wanakijiji,kifo kwa mara ya pili mfululizo!! Hata masaa hayajapita,tena mume na mke!!!..ni nani anaeyafanya haya?? Jamani hii si bure…ni laana inatuua!!!…ni nani aliewaleta wale watu lakini?? Ni
baba Madhifa!!…haraka wanakijiji wasiopungua idadi ya watu thelathini,wake kwa waume,watu wazima kwa watoto kwa jazba kubwa walianza kuelekea kwa baba Madhifa!!…chuki iliyokuwepo kati ya jamii ya wakulima na wavuvi juu ya wawindaji ilizidi kushamiri kwa kiasi kikubwa,baba Madhifa sasa ndie alieokana kama chanzo,kitendo chake cha kuwaokoa wakina mzee Otongo ilikua ni hukumu tosha! Mawe na dhana zingine kama mapanga mikononi mwa wanakijiji zilikua ni kipimo tosha cha kuonyesha kinachoenda kujiri,hakukua na amani tena!!
Masikini baba Madhifa,hakua na hili wala lile,kuzaliwa kwake kwenye jamii ndogo ya wawindaji ndio kosa lake kubwa,hakuna wa kuwatetea mbele ya wanakijiji wengine,hakuna wa kuwasikiliza!! Walipowasili kwenye uwanja wa nyumba yake haraka shughuli za ubomoaji na uharibifu zilianza!! Mawe yalirushwa kama risasi kwenye nyumba ile ya udongo bila hata kuangalia na kuuliza kama mna watu ndani,sauti za kejeli matusi na kebehi zilisindikiza
bara-bara shughuli hiyo na hatimaye waliamua waichome kabisa waridhishe roho zao zilizokua za kinyama baada ya kushuhudia mauaji ya wenzao wawili,je hilo ni suluhisho?? Hawakufikiria hicho!! Baba Madhifa na wanae hawakuwepo,walirudi msituni kuendelea na shughuli zao na hata Mama Madhifa vilevile alikua kisimani akichota maji,Mungu alikua upande wao kwani kama wangelikuwepo ni dhahiri wangelikua mishikaki!! Lile zoezi halikuishia pale tu kwa baba Madhifa,liliendelezwa kwenye nyumba zingine zote za jamii ya wavuvi zilizokuwepo karibu na kuwafanya wabakie mithili ya vifaranga waliokimbiwa na mama,hawakuweza kufanya kitu,hawakua na uwezo huo,ila waliumia sana rohoni! Kwanini wao?? Au ni kwasababu wao hawahesabiki ndani ya kile kijiji?? Walikua kama yatima,walishindwa kuyazuia machozi.
Sasa wamebaki wakina mzee Otongo,je kipi kitawakuta?? Wale wanakiji baada ya kuridhika na walichokifanya hawakutaka kupoteza muda,miili ya Baba Tito na mkewe ilizikwa na kuhitimisha zoezi la kumuacha Tito yatima kamili,majonzi na simanzi zilitawala lile eneo bila kusahau na hisia za uoga, Julina na Mama Halima ni miongoni mwa watu waliokuwepo eneo la tukio japokua hawakuhusika kurusha hata jiwe moja kwenye nyumba ya baba Madhifa,chozi lilitiririka kwenye kila jicho la mmojawao ila hasa mama Halima,moyo wake ulikua umebeba siri
nzito juu ya vile vifo,siri ambayo hakuna hata mmojawao anayoijua isipokua yeye,ni yeye pekee aliekua anafahamu ya kwamba mama Tito hakuuwawa bali alijiua kwani alimshuhudia mama Tito kwa macho yake akiichukua ile kamba iliyomnyonga mumewe kule shambani na ndio hiyo aliyoitumia kujimalizia na yeye pia,aliogopa kusema!! Na chozi lilizidi kumshuka haswa!!! * * * * * Mama Madhifa baada ya kuweka ndoo yake ya maji kichwani taratibu alianza kujivuta kuelekea nyumbani kwake,macho yake aliyoyatupia mbele ya safari yalimruhusu aone moshi mzito ukitokea kijijini,alipata mashaka,maswali yalikuja kichwani juu ya nini hasa kinachojiri huko kijijini,masikini hakufahamu ya kwamba nyumba yake na za wenzake ndo zinateketea.
Aliongeza kasi kidogo inayoendana na umri wake wa miaka hamsini na tatu ili aweze kuwahi ila ghafla alikabwa na mtu tokea nyuma!!! Puuh ndoo ilidondoka na maji yakamwagika!!! Aliangaika kutetea uhai wake lakini hakufanikiwa!!..mara haraka akavishwa kitanzi chekundu tayari kwa KUNYONGWA!!!
Alikabwa kwa nguvu mno akashindwa kupumua kabisa,macho na ulimi vilitoka nje!! Aliburuzwa kama zigo la maganda ya viazi na ile kamba shingoni mpaka ulipo mti mmoja mkubwa wa mkaratusi,akaning’inizwa mithili ya nyama buchani,maisha yake yakakomea hapo,kikatili mno aliuwawa,hakupata hata fursa ya kujua yaliyotokea kule kijijini,hakupata hata fursa ya kumuona mumewe tokea muda wa asubuhi,hata mwanae wa mwisho ampendae,Madhifa.
Hakuna alieshuhudia chochote,hakuna jicho lililoona lolote hivyo bado ilikua ni siri juu ya nani anaeua na kwanini anaua vilevile,kwanini anatumia kamba nyekundu?? Pia lilikua ni swali ambalo bado wanakijiji walikua hawajalipa nafasi vichwani mwao,hali ilizidi kuwa tete na ya kuogofya…ndani ya masaa yasiozidi matano tayari watu watatu walikua washaenda na maji kwa kifo kinachofanana!!
Baba Madhifa na wanae wawili walikua washawasili kijijini,hali ya kuona moshi mzito toka kijijini iliwafanya waache shughuli zao za uwindaji na kwenda kujua kinachojiri,walipofika kijijini hawakuona watu kama inavyokuwaga ni dhahiri walikua wameenda sehemu fulani ambayo wao hawakuifahamu,haraka walielekea ilipo nyumba yao,hawakuamini macho yao,hawakuamini walichokiona,nyumba yao ilikua tayari gofu na nyumba zingine za wenzao nazo ndio zilikua zinamalizikia kwa moto,haraka waliwafuata wenzao waliokua wamejikusanya kihuzuni hatua kama kumi toka walipo kwa dhumuni la kuuliza ili kujua hasa kilichotokea,kiunyonge waliwajibu ya kwamba wanakijiji ndio wamefanya hayo,baba Madhifa alipata hofu kubwa moyoni!! Mke
wangu yu kwapi?? Aliuliza haraka kwa taharuki akajibiwa ya kwamba alienda kisimani,bila ya kuchelewa aliwaagiza wanae wawili ambao walikua ni wa kiume;Madhifa na Khadhifa kwenda kumjulia hali mamayo huko kisimani,haraka walikimbia
kuelekea huko! Masikini hawakujua ya kwamba mama yao tayari alishaning’inizwa ni ndege tu wa mizoga ndio wanaofaidi,walikimbia kwa kasi na nguvu zao zote huku mioyoni mwao wakiwa wanasali mama yao awe salama,Madhifa alishindwa kuzuia machozi na hofu kubwa ilishika wake moyo,alimpenda sana mama yake.
Baada ya mwendo wa robo saa walikuta ndoo chini waliyoitambua ya kwamba ni ya kwao lakini hawakumuona mama yao!! Ilibidi waanze kufuatilia alama zilizoashiria ya kwamba mtu aliburuzwa toka eneo lile zilizowapeleka mpaka karibu na eneo ambapo mama yao alinyongwa,ndege wa mizoga walisaidia kuhitimisha zoezi.
“Khadhifa!!!..yule anaening’inia pale mtini ni nani???…sio mama yule!!!” sauti iliyotepeta uoga ya Madhifa iliuliza, “He!! Mbona kama ni yeye!!!!”
alijibu Khadhifa,haraka walisogea na kugundua ya kwamba walichobashiri ni kweli,alikua ni mama yao! Damu zilitawala dela lake kwa kiasi kikubwa kutokana na kunyofolewanyofolewa na ndege wa mizoga,macho yake yaliokua nje yalikua yashanyofolewa na hata ulimi pia,sura yake ilikua ngumu kutambulika!!!
Haraka Khadhifa ambae ndie mkubwa alifukuza wale ndege na kupanda juu ya mti kwa ujasiri na kufungua ile kamba kuruhusu mwili wa mamaye kushushwa chini,walimshusha na kumbeba kisha safari ya kuelekea walipotoka ambapo baba yao anawasubiri ilianza,hawakua na mama wala nyumba tena,uchungu usioelezeka ulitawala mioyo yao,moja kwa moja walifahamu
ya kwamba waliochoma nyumba yao ndio wanaohusika na kile kifo,yani wanakijiji!! Chuki kubwa ilipandikizwa mioyoni,roho ya kisasi ilikamata hasa vichwa vyao,hawakutaka kukubali lile jambo liende vile vile tu,hawakukubali roho ya mama yao iende peke yake yani bure kabisa kwa ule unyama aliofanyiwa,hisia za kuwa wawindaji wa watu badala ya wanyama zilizuka!!
Baada ya muda kidogo waliwasili kwenye uwanja wa nyumbani kwao sura zao zikiakisi vya kutosha mioyo yao ilivyo na uchungu,walihisi kama wamekabwa rohoni tena hisia hizo zilizidi hasa baada ya kumuona baba yao,walishindwa kupata jibu juu ya nini watamueleza kwani walimuonea huruma,lakini ghafla walianza kulia kama watoto,kilio ambacho walijitahidi kukizuia tokea muda mrefu,kilio ambacho kilimfanya baba yao ashtuke,kilio kilichofanya baba yao aanguke kwa presha kama kiroba!! * * * * * * * upande wa pili wanakijiji waliokua kwenye mazishi ya baba na mama Tito walimaliza shughuli zao,walijiondoa toka kwenye lile eneo la makaburi huku bado habari za uoga juu ya ile hali zikitapakaa,bado hofu iliwashika na walishasahau kabisa dhambi waliyotoka kuitenda ya kuchoma nyumba za watu wanaowahisi wao ni chanzo,walikua kimakundi makundi lakini ghafla mama Halima alimvuta pembeni Julina na kumwambia kwa kumnong’oneza kiumbea..
“mama Tito hakuuwawa!!” “unasema??” “ndio hivyo kama ulivyonisikia..!” “we umejuaje??” “nilimshuhudia kwa macho yangu akiichukua ile kamba iliyomnyonga mumewe,na ndio hiyo kajinyongea!” “weeeh!!” “we si ulizimia,ungeyaonea wapi?? Ila!!..uufunge huo mdomo wako,tena uufunge hasa!” “ntaweza kweli??” alidakia Julina.
“kwanini usiweze??…ushaanza!!” kwa ukali kidogo mama Halima alitamka, “sawa mama nitajitahidi kadri ya uwezo wangu” Julina alimtia moyo,waliendelea na safari yao ya kuelekea majumbani taratibu huku wakiwa washaachwa nyuma na wenzao,stori ndogo ndogo zilitawala maongezi yao hasa juu ya tendo lile la uchomaji moto wa nyumba zakina Madhifa kitu walichoonekana kupinga kupinga kabisa japokua walikua hawana uwezo wa kuongea mbele ya umati wa wanakijiji,wangeonekana wasaliti.taratibu walitembea bila hofu walishasahau
kidogo mambo ya vifo kutokana na kupumbazwa na vijistori vidogo vidogo vya hapa na pale,ila ghafla Julina alisimama kisha akasema.. “mama Halima,nina hofu” “nini tena Julina mwanangu? Mwanao si yupo kwa mzee Patili..” alisema mama Halima huku akirudi nyuma kumfuata, “sio juu ya mtoto wangu Mama,ni juu ya mume wangu Kitanzi!…ni muda sasa hajarudi,sijui nae atakua ashanyongwa??”
“mh-mh,usiseme hivyo bwana kwanza embu twende nyumbani ukapumzike mana tokea usiku ulipojifungua upo kwenye heka heka tu hata mtoto wako atakua anakuhitaji mno kwa sasa,tafadhali twende!” kidiplomasia mama Halima alipooza jambo lililotaka kuzuka,alimshika mkono Julina na kumvuta waende.
Nyuma ya mama Halima na Julina alionekana mtu anakuja kwa kasi! Pande la mtu,pande la mbaba! Mweusi tii kwa rangi na kichwani alikua hana nywele kabisa,yani upara!!
Mikono yake miwili mikubwa iliyoshiba ilikua imeshikilia kamba nyekundu,macho yake makubwa mekundu yalisadifu hamu kubwa iliyo moyoni mwake,masikio yake yalizoea makelele ya kuomba msamaha ya watu mbalimbali na hata pia mikono yake ilizoea kunyofoa roho za watu,alikua ni mnyongaji!!!
Ghafla mama Halima alihisi kitu akageuka nyuma haraka,hakuona kitu!! Wasiwasi ulimteka moyo,akamwambia Julina “nahisi kuna kitu!” huku akigeuka geuka nyuma, “nini tena hiko??” Julina mama uoga haraka aliuliza, “bado sijafahamu! Ila tuongeze mwendo Julina,twende!!”
haraka mbio zikaanza,maumivu bado yalikua na Julina kwani si muda mrefu toka atoke kujifungua lakini uoga wake ulimsaidia mno kumkimbiza,tayari moyo wake ulishawasha jenereta,ulikua mbio mno kuliko hata wa yule aliehisi kitu,yani mama Halima!! Joto lilipanda mwilini mwake,kajasho kauoga kalimteremka! Mungu wangu nisaidie!! Alijiambia moyoni.
Baada ya muda kidogo waliwafikia wenzao wakaungana nao,walishusha pumzi ndefu ya kutoamini kama wamefanikiwa huku mioyo yao ikianza kutulia taratibu,walijuta kwanini walibaki. Lile jitu lilitokomea,halikuonekana tena,halikujulikana lilielekea wapi!! Lilichokipanga hakikufanikiwa,wakina
mama Halima waliponea chupuchupu watiwe kitanzini kama isingelikua hisia zao zilizowastua,hivyo nani anafuata?? Hiko kilikua ni kitendawili. Upande wa pili wa shilingi nyumbani kwa mzee Patili maongezi madogo madogo yalichukua nafasi,fahamu
zilishamrudia mama Kadogo japokua majeraha bado mwilini yalimsumbua na pia vilevile kichwa kilikua kinamuuma,dawa alizopewa na yule mzee sio siri zilimsaidia vilevile mzee Otongo.
Maongezi yao yaliokua yanaendelea yalishindwa kufikia hitimisho kwani kila walipojadili kuhusu vilivyotokea huko nyuma bado hawakupata jibu kwamba vimeishia wapi,ni ngumu kuamini kama lile jeshi limewaacha tu
vilevile,walipata kidogo mashaka,walikua hawafahamu ya kuwa kuna mauaji yanaendelea kijijini,walikua hawajui kabisa juu ya hilo,walikua hawafahamu ya kwamba sasa jeshi la 666 limekuja kivingine!! Muda ulianza kuruhusu jua lizame,taratibu giza likaanza kuingia,wanakijiji kutokea kwenye mazishi walianza
kuitia miguu yao ndani ya kijiji,mila zao na desturi haziruhusu kulaza maiti,hivyo mtu akifariki mapema tu anazikwa akapumzike kwa amani,kila mwanakijiji alielekea kwenye nyumba yake,tito aliekua yatima yeye alichukuliwa na mama Kurwa,mmama mmoja muongeaji sana mwembamba ambaye ni jirani yao,mama
Halima na Julina moja kwa moja walielekea kwenye nyumba ya mzee Patili,kumpasha habari na kumchukua mtoto waliemuacha hapo kwa muda.Habari zile ziliwashtua sana! Mauaji ya watu wawili ndani ya kijiji kwa kunyongwa kilionekana kuamsha hisia ya kwamba ujio wa jeshi la 666 umewadia! Mama Kadogo na mzee Otongo pia walihisi vivyo hivyo!
Upande wa pili mzee patili na wakina mama Kadogo walijisikia vibaya juu ya taarifa ya kuchomwa kwa nyumba za wakina baba Madhifa na walijiona wakosefu mbele zao.
Ngo! Ngo! Ngo! Hodi iliita,mzee patili aliinuka na kwenda kufungua,alikua ni Khadhifa! Alikuja kumuita mzee patili akawasaidie kwani baba yao yupo kwenye hali mbaya!! Mzee Patili alishangazwa na zile habari na hasa alishangazwa zaidi baada ya kuambiwa hicho kitu kilijiri baada ya kuleta mwili wa mama yao waliokuta umenyongwa maeneo ya kisimani,haraka mzee Patili alichukua madawa fulani kisha mbio zikaanza kuelekea eneo la tukio!
Kutokana na kaumbali kalichopo walichelewa,walipokaribia walisikia sauti ya kilio waliyoitambua ni ya Madhifa! Hofu zikajazwa mioyoni mwao! Nini tena hiki jamani?? Walijiuliza huku wakiongeza kasi!!
kutokana na kaumbali kalichopo walichelewa,walipokaribia walisikia sauti ya kilio waliyoitambua ni ya Madhifa! Hofu zikajazwa mioyoni mwao! Nini tena hiki jamani? Walijiuliza huku wakiongeza kasi! Haraka waliingia ndani,mzee Patili bila kuchelewa alichukua madawa yake aliyoyabeba na kuanza shughuli ya kumpakaa dawa baba Madhifa alielazwa chini na kidogo alimmezesha kwa kumfungua kinywa,ilikua ni dawa ya kumrudisha kwenye fahamu,aliwaambia hivyo wakina Madhifa waliokua na hofu kubwa ya kumpoteza baba yao kama walivyompoteza mama yao,uzoefu wa mzee Patili kwenye yale matukio ulifanya jambo lisiwe gumu kihivyo,baada ya kupaka ile dawa aliwahitaji watulie ifanye kazi na baada ya muda kidogo itaonyesha matunda,aliutumia huo muda kwena kuangalia maiti ya mama Madhifa iliyokua imefunikwa gubigubi,ilimtetemesha mno na kumuogopesha,maiti ilikua haitamaniki na yenye kutisha kutokana na majeraha makubwa iliyonayo,shingoni kulikua na alama ya kamba iliyoashiria ya kwamba ilimkaba vilivyo,aliifunika kisha akayarushia macho yake kwa wakina Madhifa,hawakua na amani hata kidogo,roho ya chuki na kisasi ilichipukia mioyoni mwao,hofu ya kumpoteza baba yao na uchungu wa kumpoteza mama yao uliwafanya machozi yatiririke yakisindikizwa na kwikwi za kilio,aliwaonea huruma sana na kichwani akajiuliza leo hawa watoto watalala wapi?? Akatikisa kichwa kwa masikitiko kisha akaangalia anga lililokua kiza kuashiria giza lishaingia. Baada ya muda usiopungua robo saa baba Madhifa alianza kupiga chafya! Alirudi duniani!! Wakina Madhifa hawakuamini lile tukio,ilikua ni kama miujiza mbele ya macho yao!! Haraka walimkimbilia baba yao kwa kutaka kumjulia hali,tabasamu zilizoambatana na machozi zilionekana kwenye nyuso zao,walimkumbatia baba yao kwa nguvu huku wakilia! Walitia huzuni,mzee Patili nae chozi lilimshuka taratibu,lile jambo lilimgusa wake moyo. Hakukua na muda tena wa kupoteza,walifahamu hakuna msaada wowote wangeupata toka kwa wanakijiji na ukizingatia hawakuhuitaji hata kidogo,waliungana na wanakijiji wenzao na mzee Patili wakauzika mwili wa mama yao,hisia za kwamba alinyöngwa na wanakijiji zilifutwa baada ya mzee Patili kuwapa tahariri ya kua yale mauaji hayahusiki na mwanakijiji yoyote bali ni kwamba yanafanywa na jeshi la 666 lililowadhuru wale watu waliowaokoa japokua kwa kiasi kimoja yameleta mkanganyiko,hisia za uoga ziliwatetemesha na ukizingatia kwa ule usiku iliwabidi walale nje baada ya nyumba zao kuchomwa. * * * * pembeni ya nyumba ya mama Kurwa upande wa kushoto kulikua kuna mti mkubwa wa muembe ambao ukitoka huo nyumba ya mzee Yosso ndio ilikua inafuata,hali ya giza iliyokuwepo ilifanya mti ule kutoonekana vizuri na kutisha kidogo,pembeni yake alikua ameegemea mwanaume mmoja alieshikilia kamba mkononi akipiga mahesabu kichwani,ni lile jibaba pande la mtu lililowakosakosa wakina mama Halima,ni yule mnyongaji!!! Mungu wangu! Sasa lilikua ndani ya kijiji tena karibu na nyumba ya mama Kurwa na mzee Yosso au baba Matata,lilikua linafanya nini pale?? Hilo halikufahamika ila taratibu lilianza kujongea na kuusogelea mlango wa mzee Yosso au baba Matata,lilipokaribia liligonga mlango….ngo! Ngo! Ngo! Hodiiii! Kwa sauti ambayo haikuendana hata kidogo na mwili wake! Ilikua ni sauti ya kike tena ya mama Kurwa ambaye ni jirani!!… Karibuu! Alijibiwa tokea ndani,kwa kua halikua na lengo la kuingia ndani lilibakia pale nje likisubiri mlango ufunguliwe,mama Matata aliekua na mumewe ilihali na mwanae wakila ilimbidi ainuke taratibu na kuelekea mlangoni kumfungulia aliegonga,ni kosa kubwa alilitenda hakujua kama alipeleka nafsi yake kifoni!! Alipokwa kama pochi! Lile jibaba leusi kama giza lililokuwepo lilimbeba mama Matata na kuanza kupotelea nae maporini!! Makelele ya mama matata ya kuomba msaada yalisikika vizuri kutokana na utulivu wa mawimbi usiku hivyo kupelekea wanakijiji kushtushwa kwa kiasi kikubwa bila kusahau mumewe ambaye ndie aliekuwa wa kwanza kutoka nje kwa hamaki! Hakumuona mkewe! Alianza kukimbia kufuatilia sauti aisikiayo huku akiita jina la mkewe kwa nguvu! Ile sauti haikuskika tena! Ilitokomea na lile jibaba,ilitokomea porini!! Baba Matata hakuona kitu,mkewe akawa tayari ashakwenda!! Alieka mikono kichwani huku akilia kama mtoto,hakua na la kufanya aligeuza na kuanza kurudi kijijini kichwani mawazo yakimsonga na moyoni hofu ikimtinga!! Akili yake yote ikawa sasa ni kwa mama Kurwa kwani sauti ya yule aliekua anagonga ilikua ni yake,alikimbia,alipofika kijijini alikuta watu wameshajazana,sauti ya mama Matata iliwatoa majumbani mwao hasa ukizingatia hofu zao zilishawashwa tokea mapema siku ile,minong’ono ilitawala,baada ya kumuona baba Matata,walimfuata na kumuuliza kilichojiri,hakujibu kitu,alimfuata mama Kurwa huku akitoa macho,akauliza kwa ukali! “mke wangu yuko wapi???” huku akimnyooshea kidole! Mama kurwa alibanwa na kigugumizi,hakua na la kujibu! Ghafla mmama mmoja akaropoka.. “jamani kuna mtu pale kwenye mti ananing’iniaa!!!” alimnyookea moja kwa moja mama kurwa huku akitoa macho,kwa ukali akauliza! “mke wangu yuko wapi??” mama Kurwa alikosa cha kujibu,kigugumizi kilimbana,ghafla mmama mmoja aliropoka! “jamani kuna mtu ananing’inia pale mti!!!” Baba Matata aliachana na mama Kurwa na kukimbilia kwenye huo mti kushuhudia alichosikia,hakuamini macho yake kwa alichokiona! Alikua ni mkewe!! Alivishwa joho jekundu kitanzi kikimning’iniza! Damu zikiwa zinamtoka puani na masikioni! Aliishiwa nguvu za miguu akakaa chini na kuanza kulia!! Matata nae aliposhuhudia mwili wa mamaye unaning’inia katika ile hali kilio kilizidi kuchukua nafasi!! Baba na mwana wakawa wanalia kilio kilichoshindwa kutofautisha mkubwa na mdogo.Mwili wa mama Matata ulishushwa na kitanzi kikafunguliwa,wanakijiji walitawaliwa na hofu mara mbili ya ile iliyokuwepo mwanzoni,kushuhudia watu kunyongwa kwa siku mara tatu kama dozi haikua kitu cha kawaida,haikua kitu cha mzaha kabisa,ni kitu cha kuogopesha mno!! Kila mwanakijiji aliruhusu chozi la hofu na uchungu litoke huku wakiwa wanajiuliza mioyoni kwamba ni nani anaefuata sasa baada ya wale,miili ilikua inatetemeka na msamiati ‘hamu ya kulala’ haikua kabisa kwenye kitabu chao cha ile siku,nani alale kwa ile hali?? Hata mtu kukaa peke yake ilikua ni mtihani!!! Wakati baba Matata na mwanae wakiendeleza kilio baadhi ya wanaume waliokuwepo pale walijivuta pembeni na kuanza kuteta jambo, “sasa jamani ndio hivyo kama tunavyoona,tunazidi kutokomea! Sasa tunafanyaje sisi kama wanaume??” alieleza mzee Rama,baba wa watoto saba akaae nyuma ya nyumba ya mama Kurwa,alikua ni kiongozi mkubwa wa kuwashawishi wanakijiji wakachome nyumba za wakina Madhifa, “mh kusema ukweli hata mie naogopa hapa nilipo,ujue hiki kinatisha!” “ah-ah! Kila mtu anafahamu kuhusiana na hilo,sisi kama wanaume tumejivuta pembeni ili tuangalie ni jinsi gani tutakavyolikabili,hatuwezi tukakaa tu hivi,tutakwisha!” Mzee Rama alimdadavulia Tambwe alieonekana kutia mushkeli, “kusema ukweli hili jambo si la mchezo hata nukta,mimi nadhani ya kwamba si binadamu wa kawaida anaefanya haya!…Nilisikia kwa masikio yangu sauti ya mama Matata ikielekea msituni lakini cha kushangaza tumemkuta kaning’inizwa kwenye ule mti!!” mwalimu Baraka alichangia huku akiunyooshea kidole ule muembe, “hata mie nahisi hivyo,hiki kitu kitatuwia vigumu sana,kumdhibiti mtu asiye wa kawaida yataka moyo ukizingatia hatujui hata yupoje!” mzee Rama alisema,Lutiko aliekua kimya nae akachangia baada ya mzee Rama “mi nadhani mtu mkubwa ataetusaidia ni mzee Patili,yeye ana ujuzi na haya mambo!” “ni kweli! Hilo wazo zuri,nadhani mnaelewa ya kwamba nyumba ya mzee Patili ipo mbali na za kwetu na hata yaliyojiri hapa bado hayafahamu,sasa inabidi tumjuze!” wazo hilo lilionekana kuungwa mkono na wale waume,kazi ikawa ni nani atakaejitolea kwenda kumpa taarifa mzee Patili,kila mtu alikua anahofia kwenda kule kwa kale kaumbali mwenyewe ilikua ni kama kujitoa sadaka,hakuna alietaka,kila aliechaguliwa aliuliza kwanini mimi?? Hivyo ikawa ngumu kufikia hitimisho. Wakati hayo yanachukua nafasi Matata aliufata mwili wa mama yake na kuanza kuuangalia kwa kutoamini huku machozi yakimtoka,alijiuliza juu ya ile nguo aliyovishwa mama yake hakupata jibu,kuna kitu aligundua kwenye ile nguo haraka akaita Babaaa!! Sauti iliyowastua na kuwateka hisia wanakijiji wengine,baba Matata bila kuchelewa alifika eneo aliloitwa na mwanae akauliza “nini mwanangu??” huku macho yakiwa mekundu kama nyanya kwa kulia, “kuna kitu kimeandikwa kwenye hii nguo aliyovalishwa mama!!” “nini tena hiko??” aliuliza Baba Matata,kutokana na kutojua kusoma aliamuru mwanae amsomee,matata akasoma kisha akasema.. “imeandikwa BADO KIDOGO!!!” * * * * * Baada ya shughuli ya mazishi kuchukua nafasi ilimbidi mzee Patili afunge safari ya kurudi kwake,aliwaaga wakina Madhifa waliokua wanatayarisha tayarisha kwa ajili ya usiku ule,walimshukuru kwa msaada na pia vilevile aliwahaidi atakuja kesho kuwasaidia shughuli za ujenzi,walifurahi kusikia hilo ila bado nyuso zao zilishindwa kujifungua kwa furaha,mioyo yao bado ilikua na huzuni. Ilikua ni tendo la ajabu kwa mzee Patili kuondoka na kuelekea nyumbani mwenyewe kwa ule muda ukizingatia vitu vya kutisha vilivyochukua nafasi kijijini,alikua na hofu lakini hakutaka iwe sababu ya yeye kubaki,aliamini kama siku imewadia hawezi likwepa hilo,mikono aliweka nyuma na kwa kasi kidogo alikua anatembea akipita miti na vichaka huku sauti za wadudu wa usiku zikigota masikioni mwake na kumfanya ageuke geuke mara kwa mara,baada ya muda kidogo alikaribia na kwake,macho yake aliyoyarusha mbele yalimruhusu aione nyumba yake ya udongo vizuri,ghafla alisimama!! Macho yake yalimshuhudia pande la mtu likiwa linasogelea mlango wake na mkononi akiwa na kamba,hofu ikagota moyoni,mtu yule alikua mgeni machoni mwake na alihisi vibaya juu yake,akasogea karibu huku akinyatanyata aweze kumuona vizuri,mara lile jitu likagonga hodi Na mtindo ule ule alioutumia kwa mama Matata!! akasogea karibu huku akinyata aweze kumuona vizuri,mara lile jitu likagonga hodi kwa mtindo ule ule alioutumia kwa Mama Matata! Nini hiki? Alijiuliza mzee Patili,kutokana na uoga wa watu waliokuwepo mule ndani tendo la kufungua mlango lilichukua muda,mama Kadogo na mzee Otongo hawakuweza kufungua
kutokana na miili yao yenye majeraha na maumivu kutowaruhusu,mama Halima na Julina walio wazima walikua na hofu hivyo kufanya lile zoezi lichukue muda kutendeka,lakini lile jibaba lililokuwepo mlangoni lilihisi kitu,lilipepesa macho yake huku likinusanusa na kugundua jambo,lilisikia harufu ya binadamu hivyo likafahamu ya kuwa haliko peke yake pale nje,haraka lilitoweka! Mzee Patili alijitahidi kufikicha zake mboni
lakini hakuona kitu! Alishangazwa mno na lile jambo,haraka alikimbia mpaka mlango ulipo na kuanza kubisha hodi huku akitamka kwamba yeye ni mzee Patili! Maswali na hofu yalijazana vichwani mwa waliokua ndani,mara ya kwanza walipoisikia hodi iliambatana na sauti ya kike ila sasa hivi wanaisikia sauti ya kiume tena ni ya mzee Patili! Walisita kufungua.
Tendo la busara lililofanywa na mama Halima la kuchungulia dirishani ndilo lililowashawishi kumfungulia mzee Patili baada ya kugundua ndie,aliingia ndani na kuwaeleza yote aliyoyashuhudia tokea alipotoka mpaka alipomuona lile jitu mlangoni,walishtuka sana na vilevile walishukuru hawakuifungulia hodi ile kwani ingekua
ni hadithi nyingine sasa hivi,mzee Patili alizidi kulielezea lile aliloliona.. “yule mtu alikua ameshikilia kamba nyekundu! Na hasa zinafanana na zile zilizotumika kuwanyongea wakina baba Tito! Hicho kitu kilinishangaza sana!” “mungu wangu! Jamani tuhame hiki kijiji tutakwisha!” kiuoga alinena Julina akiwa anamnyonyesha mwanae, mama Kadogo akasema, “sidhani kama hilo ni suluhisho,kila tutakapoenda watatufata mpaka pale watakapohakikisha ya kwamba lengo lao limefanikiwa!” kauli ile iliwashtua mama Halima na Julina waliokua hawajui kiendeleacho,haraka wote wakauliza “lengo! Lengo gani hilo??” mama Kadogo akazidi kunyumbua,
“haya mambo yote yajiriyo ndani ya kijiji chenu yalitokea vilevile kijijini kwetu Igesambo,watu wetu wengi wa karibu wameuwawa na wengine wamejiunga kwenye jeshi la 666 lililo na itikadi moja tu ya kuusambaza utawala wa Ibilisi wao alieingizwa duniani,ilibidi tukimbie kuokoa maisha yetu kwasababu hatukutaka abadani kuungana na mashetani wale,lakini kuonyesha ya kwamba mungu yu upande wetu,alizaliwa mwana mwingine! Mwana ambaye ndie tumaini letu na vilevile anaweza akawa kifo chetu!”
“nani huyo??” Julina aliuliza kwa papara huku akimtizamatizama mwanae, mama Kadogo akaendelea, “huyo mtoto ndie hasa lengo la hawa watutafutao na watuuwao,namaanisha jeshi la 666 kwani ni hatari kwao na huyo mtoto ndie hasa yatubidi tumlinde kwa hali zote kwani ndie tumaini na mwanga wetu,tukimruhusu afe,tumeruhusu utawala wa kiza!” mzee Otongo nae akadakia
“mtoto huyo ana alama kwenye paja lake la kushoto kwa chini,alama ya nyota!” mama Halima na Julina walishtushwa na ile kauli! Kwani mtoto yule alikua na hiyo alama! Macho ya Julina yakatoka kwa uoga! Huku akitetemeka akasema “haiwezekani!! Ah-ah! Haiwezekani jamani,haiwezekani!!! Mtoto wangu! Hapana!” * * * *
Bado wanakijiji walikua wamekusanyana mbele ya nyumba ya mama Kurwa na baba Matata,hakuna hata mmoja alieonekana na dalili wala hamu ya kurudi kwenye viota vyao na kulala,hali ilikua tete mno mioyoni mwao! Mada kubwa iliyokua inaongelewa ni juu ya ule ujumbe uliokutwa kwenye lile joho alilovishwa mama Matata baada ya kunyongwa uliosomeka BADO KIDOGO!! Hawakuelewa ulikua unamaanisha nini? Kila mtu alisema yake juu ya hilo.
Kutokana na hofu kulowanisha nafsi zao waliamua kukaa pale pale mpaka usiku utakapokwisha na kuiona adhuhuri,hawakua na lingine la kufanya zaidi ya hilo waliloona ya kwamba ni salama kwa maisha yao.Baba Matata na mwanae walikuwepo sebuleni,huzuni iliwafanya wakose cha kusema na kuwa kimya,ilikua ni
ngumu bado kuamini ya kwamba mtu waliekua nae muda si mrefu ni marehemu sasa hivi! Baba matata aliona mzigo wa majukumu waongezeka,Matata mwenye miaka tisa bado alikua anahitaji malezi ya mama yake na ukizingatia yeye si mkaaji nyumbani,kichwa kilivuruga. Ghafla upepo mkali ulipiga lile eneo!! Upepo usio wa kawaida kabisa!! Vibatari vilivyokua vinatoa mwanga vyote vilizima na kufanya giza totoro kushika hatamu!! Wakina mama walipiga makelele ya uoga na kila mtu hofu iliita ndani yake! Miili ilitetemeka kwa uoga,mioyo ilizizima kwa hofu!!
Mchakato wa kuwasha vibatari ulipofanikiwa watu wawili hawakuonekana!! Hawakujulikana walielekea wapi…hawakujulikana walibebwa na nani!! Mtoto mmoja wa mzee Rama na mmama mmoja wa makamo walishabebwa!!! Mungu wangu! Sauti zao zilisikika zikiishilia kama ilivyokua kwa mama Matata!! Matumbo yalichemka,jasho liliteremka!! Wengine walizirai kwa uoga,na wengine walitamani kujimaliza!!!!
Matumbo yalichemka,jasho liliteremka!! Wengine walizirai kwa uoga,na wengine walitamani kujimaliza!! Vilio vya wamama na watoto vilimeza ukimya wote wa usiku,ile sehemu haikukalika kabisa! Wake waliwakimbilia waume zao ilihali na watoto vilevile!
Mzee Rama na mkewe waliumia sana kumpoteza wao mwana,japokua walikua saba lakini hawakuhitaji kumpoteza hata mmoja wao machoni pao,machozi vilio na mafua ya uoga na uchungu vilitawala,kila mtu akawa anatizamatizama nyuma kwa hofu ya usalama wake binafsi.
Wakati taharuki bado imeshika nafasi,miili ya watu waliobebwa koroboi zilipozima ilionekana tena ikining’inia kwenye ule ule mti wa muembe aliotundikwa mama Matata!! Mavazi yao waliyokua wamevaa hayakuonekana wala kujulikana yalielekea wapi,walikua wamevishwa majoho mekundu kama alilovishwa mama Matata na yote yakiwa na ujumbe ule ule uliosomeka BADO KIDOGO!! Masikio yao na midomo ilikua inavuja damu na huku macho na ulimi vikiwa vimetoka nje!! Walitisha sana,hasa wakionekana wakibembea na kamba zao nyekundu shingoni! Idadi ya waliokufa na kamba kwa ile siku ikawa ni tano tayari.je mchezo
utaendelea vilevile?? Na sasa ni yupi alie kwenye zamu?? Maswali hayo yalijaza vichwa vya wanakijiji. Ilibidi kifanyike kitu sasa,kukaa tu pale kwa kutegemea ni salama ilikua si sahihi,mzee Rama na mwalimu Baraka walijitolea kwenda kwa mzee Patili kwa lengo la kumpa taarifa ili awasaidie kwa lolote kunusuru maisha yao yaliyo mikononi,waliwaaga wanakijiji huku wakiwaomba wawaombee wafike salama kwani safari
iliyombele yao ni ya kutisha,hofu ilikuwemo mioyoni mwao lakini hakuna jinsi jambo lile ilibidi litendeke,mke wa mzee Rama na wanae sita waliobaki walikua hawana matumaini kama baba yao atarudi,walimuangalia kwa huzuni huku wakimpungia mkono wa kheri,mwalimu Baraka nae alikua anajilaumu nafsini kwanini alikubali kuja kufundisha kijiji kile,ndio serikali ilimpangia lakini aliona alifanya kosa kuja lile eneo,ni bora angekataa hata kama ingehatarisha kibarua chake,mambo yanayojiri yataka moyo.
Safari ilianza,taratibu mwalimu Baraka na mzee Rama wenye baraka za usalama kutoka kwa wanakijiji walikua wanajongea,hofu waliyonayo mioyoni iliwafanya washindwe kujizuia kugeukageuka nyuma na mioyo kwenda mbio,lakini nyuso zao zilificha hayo,kila mmoja alikua anataka kudhihirisha kwa mzenzie kwamba haogopi.
Wakiwa kwenye mwendo mwalimu Baraka aliitoa simu yake iliyofeli mtandao tokea majuzi kwa lengo la kujua wakti,alishtushwa sana na alichokiona,muda uliokua unaonyeshwa na simu yake haukumwingia kabisa akilini! Ni muda mrefu umepita tangu giza liingie lakini bado saa ilikua inasema ni saa MOJA NA NUSU
USIKU!! lile jambo lilimfanya mwalimu Baraka ahisi saa yake imepoteza majira lakini bado alipata maswali kichwani kwamba hii tabia ya kupoteza majira imeanza lini kwani alikua ameiseti saa yake hivyo hata likitokea jambo lolote bado majira huwa palepale,alipata hofu lakini hakutaka kumshirikisha mzee Rama,alinyamaza na safari ikaendelea,lakini ukweli ni kwamba muda ulikua hausogei,yani ulisimama palepale! * * * Julina baada ya kupewa somo zito na wenzake,aliituliza hofu yake,akatambua thamani ya mwanae na hakuwahi tarajia kwamba angekua mtu wa kumzaa mtoto ambaye angehitajika kwa ule muda,alijivunia hilo.Mzee Otongo hakutaka kumficha Julina,bayana alimjuza ya kuwa asipoteze muda kumsubiria mumewe kwani ni dhahiri atakua ameuwawa na Jeshi la 666 tangu yeye ni baba wa kiumbe hatarishi kwao,hii habari
ilimsikitisha sana Julina japokua nae alikua na hisia hizo hizo japo hakua na uhakika,chozi lilimdondoka,alimpenda sana mumewe Kitanzi na hata ndoa yao haikufikisha hata miaka miwili,bado alikua na hamu nae na ukizingatia hajamuona mtoto ambaye mkewe alimleta ulimwenguni,ilitia huruma.
Kila mtu alie mule ndani aliuona usiku ni mrefu,walitamani kuona mwanga wa jua ukipendezesha tena macho yao,waliona usiku ni hatari kwao hivyo mioyo yao ilishikwa na tamaa kubwa ya kuona tena miale ya jua itakayoamsha matumaini yao,sauti za wadudu ziendeleazo huko nje zilizidi kuwaogopesha,hasa Julina. Ngo! Ngo! Ngo! Sauti toka mlangoni iliwasili masikioni na kuwashtua kidogo,kama kawaida mama Halima alikimbilia dirishani na kuchungulia ni wakina nani,kisha akawatonya wenzie “ni wakina Madhifa!” “wafungulie!” mzee Patili akasema,
wakina Madhifa waliingia ndani kwa haraka huku wakihema kwa nguvu hali iliyowatisha na macho yao yalikua yanamimina machozi,kwikwi ikiwabana na kuwazuia kusema walilodhamiria,ilibidi mzee Patili awatulize kwanza ili waweze shusha presha na kusema kilichowaleta,baada ya kutulia wakasema “Mama Linda na mumewe wamenyongwa!!”
kauli hiyo iliwafanya wakina mzee Patili mioyo ipasuke kwa mshangazo na kuanza kwenda kasi!!! Ilikua ni kama tamthilia kwenye masikio ya mzee patili aliewaona hao watu muda si mrefu,wakiwa kwenye taharuki na butwaa wakasikia hodi tena!! Ya Mara hii ilikua ni ya wakina mzee Rama na mwenzie mwalimu Baraka! Je itakuaje? Nao pia wakasema kilichowaleta,watu watatu ambao ni mama matata,mtoto wa mzee Rama na mmama mmoja wa makamo wamenyongwa katika mazingira ya kutatanisha na aliewanyonga hajulikani,kwa ujumla taarifa za vifo zilizomfikia mzee Patili zilikua tano!! Alishangazwa na hiyo
idadi,na si tu yeye hata wakina mzee Otongo na wakina Julina!! Hofu ziliwashika mpaka kwenye ukucha,puh! Julina akadondoka na kupoteza fahamu!! Mtoto aliekua amembeba aliwahiwa
haraka na mama Halima na ilikua rahisi kwake kwa kua walikaa karibu,shughuli za kumpepea kumrudisha kwenye fahamu zikaanza haraka!! Mzee Rama na mwalimu Baraka wakapata kibarua cha muda cha kupepea huku wakina Madhifa wakiwa tu pembeni wakishuhudia hayo,uadui bado uliwatenganisha.
Baada ya kamuda kadogo Julina alirudi kwenye fahamu zake. Uhasama uliokuwepo baina ya makundi mawili yaliyokuwepo pale ulionekana dhahiri,wakina Madhifa walijitenga kabisa na wakina mzee Rama kwani ndio wanahousika na uchomaji wa
nyumba zao,vilevile mzee Rama hakujumuika nao kwa kudhani ku yote yajiriyo chanzo ni wao na alikua anawatizama wakina mzee Otongo kwa jicho baya kutokana na imani yao kua wale wageni pia huchangia kutokea kwa hali husika,mwalimu Baraka yeye hakua upande wowote kwani yeye si mwenyeji pale kijijini,mzee Patili aligundua huo mkanganyiko,kazi ya kuwatuliza wale watu wenye imani tofauti ziendeshazo mioyo yao ilibidi ifanyike,aliamini ya kua umoja utakaokuwepo
baina yao ndio utakaokua silaha kubwa ya kujilinda na kukabiliana na linalowasibu,elimu hasa juu ya kinachoendelea ilihitajika kwenye vichwa vyao na vya wanakijiji wote ili iwe kama chachu ya mabadiliko na mwanzo wa mapambano,alitumia busara,aliwauliza wakina mzee Otongo kama
wanaweza jongea wakajibu watajitahidi,akawapa ujumbe wakina Madhifa ya kwamba wakawaite wenzao yani jamii ya wawindaji na wakutane kwa mama Kurwa,walitii walichoambiwa,wakatokomea kwenda kuwasilisha,kisha akawaambia wakina Julina na wakina
mzee Otongo wainuke na safari ianze ya kuelekea huko walipotokea wakina mwalimu Baraka,yani kwa mama Kurwa ambapo ndipo wanakijiji walipokusanyika,akachukua vibuyu vyake viwili kisha safari taratibu ikaanza wakiwemo watu nane;mama Kadogo na mzee Otongo
waliokua wanachechemea,Julina na mama Halima aliembeba mtoto,mzee Patili mwalimu Baraka na mzee Rama.Japokua walikua wengi lakini bado kale kamchezo ka kuangaliangalia nyuma hakakukoma,kila kaupepo kalipopiga miili yao iliiteka misimko ya kioga hasa Julina
alieng’ang’ania awe katikati ya watu,ni sauti za miguu yao tu ndio ilyosikika walipokua wanapita,kote kulikua kimya ukiondoa vikelele vidogodogo vya vijidudu vya usiku,muda huo wote waliokua njiani mzee mzee Patili alikua anafanya kazi ya kuvitikisa vile vibuyu vilivyomkononi,haikujulikana kazi yake ni nini na hakuna mtu aliemuuliza,walimuacha afanye mambo yake kwa uhuru.
Hatimaye walifika walipokua wanaelekea,watu waliokua wamejikunyata kwa kukosa matumaini waliamka na kumlaki mzee Patili,aliwapa mwanga wa kufanikiwa,akikua mwema kwao kwa ule muda,walisahau kabisa walichokifanya huko nyuma,ila ujio wa wakina mama Kadogo na mzee Otongo uliwashtua wanakijiji,moja kwa moja minong’ono ikaanza kururuma….mzee Patili hakuvumilia hilo,aliufungua mdomo wake kwa ukali akasema
“acheni upumbavu wenu usio na msingi!! Huo ujinga ndio upelekeao hali kua mbaya zaidi na hautupi unafuu wowote! Nani asiemjua huyu mzee Otongo?? Si nawauliza nyie! Ni mara ngapi alikua anakuja hapa kijijini na kuwasaidia matatizo mbalimbali?? Iweje leo unaufungua mdomo wako na kumnyooshea kidole,mshausahau wema wote alioutenda kwenu? Mbona mnakua na vichwa vya panzi na mioyo y kutu!”
wanakijiji wote walitulia na kusikiliza kwa makini na roho zao zilianza kuwasuta,mzee Zptili akaendelea kunena…”umoja wetu ndio unaohitajika,kugawanyika kwetu ndiko kunapoipa mwanya kushindwa kwetu,nawaambia kama tusipokua pamoja,shingo zote zilizokuwepo hapa zitaonja kamba nyekundu kama waliopita!! Tutanyongwa kama kuku!!”
alizidi kusisitiza kwa sura ya mkazo,muda si muda wakina Madhifa wakaingizana,ukimya bado ukawa umetawala,masikio na macho yao alipewa mzee Patili aliesimama mbele.Baada ya mzee Patili kurudufisha imani za waliokua wanamsikiliza,aliwakaribisha wakina mzee Otongo na mama Kadogo kwa lengo la kutoa somo juu ya hali iliyojiri,waliwadadavulia na kuwanyumbulia wanakijiji kwa undani tangu walipotokea na nini kimewaleta hasa. waliwadadavulia na kuwanyumbulia wanakijiji kwa undani tangu walipotokea na nini kimewaleta hasa.Maneno na maelezo yaliyotolewa na wakina mzee Otongo yalionekana kuwatisha zaidi wanakijiji,habari za jeshi la 666 zilikua ni za kuogofya na zenye kutaka ujasiri kuzisikia,hakukua
na jinsi ilibidi waambiane ili wapate pa kuanzia,elimu hasa iliyokua inatolewa juu ya kiendeleacho ndicho kilikua cha kwanza kisha hayo mengine yachukue nafasi,zoezi lilifanikiwa na kumalizika salama huku likianzisha ukurasa mpya wa maisha yao ambao walikua hawajautambua,nia na
nguvu yote ya wanakijiji ilielekezwa juu ya kumlinda yule mtoto aliezaliwa na mengine pia kama watakavyoelekezwa kufanya na viongozi wao waliowateua ambao ni Mzee Patili,mama Kadogo na mzee Otongo,hakukuwa na ubishani tena wala minong’ono isiyo na msingi,sasa kila tendo lililochukua nafasi lilikua ni maelekezo dhabiti toka kwa viongozi wao,hakuna alietia dosari.
Mzee Patili aliwataka wanakijiji wajipange mistari miwili ya kijinsia,bila kuchelewa wakajipanga,alivichukua vibuyu vyake na kimoja akamkabidhi mama Kadogo kisha akampa maelezo madogo tu yaliyofanikisha kumjuza kiendeleacho,zoezi la kuwapaka wanakijiji dawa
usoni na mikononi kwa lengo kuu la kudhoofisha nguvu za adui wao lilichukua nafasi,mzee Patili akiwa anapakaa mstari wa wanaume na wavulana huku mama Kadogo akiwa anashughulika kwenye mstari wa wanawake na wasichana,idadi ya wanakijiji iliyokuwepo haikuendana na kiasi
cha dawa husika hivyo ilipelea,watu kama ishirini hawakua wamepakwa dawa kitu kilichompa maswali mzee Patili juu ya nini hasa cha kufanya,baada ya kufikiria kidogo aliwachagua wanaume wawili (mrisho na tabwe) kisha akawaagiza waende nyumbani kwake kwa lengo la
kuchukua dawa ili apate malizia waliobaki,ujasiri waliopewa na dawa walizopakwa ziliwafanya wasijifikirie mara mbilimbili,haraka walijiondoa lile eneo na kueleke walipotumwa. Wakati hayo yote yanachukua nafasi lile jibaba linyongaji lilikua likishuhudia,kwa mbali lilijificha
kwenye mapori ila macho yake mekundu makubwa yalimfanya aone vizuri kilichokua kinafanyika,hakua peke yake kwa sasa hivi kama ilivyokua,pembezoni yake alikuwepo mwanamke mmoja mwenye macho ya paka na ulimi mwekundu!!! Alijivika kaniki nyeusi na
kiremba chekundu kilichositiri mapembe yake vizuri,ngozi yake ilikua na rangi ya kijivu na masikio yake yalikua marefu ilihali na kucha za mkononi,sasa walikua wawili kwa idadi,jeshi la 666 liliongeza mashambulizi!!! Wanakijiji watahimili hili??
Lile pande la mtu jeusi na yule mwanamke mithili ya paka walitabasamu na kuruhusu meno yao ya kutisha kuonekana,walipeana ishara,wakashika njia na kuelekea kule wale wanaume walipotumwa,yani kwa mzee Patili kwa lengo la kuzuia zoezi la uletaji dawa,lile Pande la mtu mkononi lilishikilia kamba nyekundu kama ilivyokawaida yake na yule mdada mithili ya paka akiwa na kisu kirefu!!!
Matamanio yao ya kuua bila kuchelewa na kufanikisha lengo lao yaliwafanya wajione wanachelewa kwa kutembea,hivyo walianza kukimbia huku macho wakiwa wameyatupia mbele!! * * * * * * * mrisho na mwenzake walishafika eneo husika,walikua ndani ya kijumba cha mzee Patili wakifanya jitihada za kusaka dawa waliyotumwa,uwepo wa dawa nyingi mule ndani ulifanya zoezi liwe gumu kwani kila dawa waliyoipata walipoinusa waligundua sio yenyewe,ilichukua kama
muda wa dakika saba mpaka walipoitia mkononi iliyolengwa,waliangaliana kwa tabasamu kisha wakaelekea mlangoni,Mrisho aliunyoosha mkono wake na kuuvuta mlango,mlango ukagoma kufunguka!! Alizidi kutumia nguvu zaidi lakini bado matokeo yakawa yaleyale,mlango uligoma
kabisa kufunguka!!! Ikabidi amuachie Tabwe nae ajaribu lile zoezi,hakuna aliefanikiwa,bado hawakuweza kuufungua,hofu ilianza kuchochewa mioyoni mwao,wakaangaliana kwa uoga huku kajasho kakitirika,Tabwe huku akitetemeka akasema..
Tabwe alionekana kukubaliana na hilo wazo lililoonekana ni pekee kwa ukombozi wao,bila kuchelewa harakati za uvunjifu zikaanza kikamilifu kwa kutumia mateke,hawakua na habari ya kuwa lile jibaba linyongaji na yule mdada mithili ya paka walikua kwa nje wakiwasubiri kwa hamu zote ili kuongeza idadi ya waliokwenda na maji na kusafisha njia ya kufanikisha lengo lao,puh!! Mlango ukatupwa kule na nguvu ya teke zito la wakina Mrisho!! wakatoka nje,he!!! hawakuamini walichokiona!! Kitendo cha kugonganisha macho na yule mdada mithili ya paka
lilikua ni kosa kubwa!!! Walinyong’onyea na kupoteza nguvu,wakadondoka chini kama mizigo tii!!! Lile Jibaba likasogea karibu yao huku likitengenezea vitanzi tayari kwa ajili ya
kuwanyonga,macho ya yule mdada yalishalainisha zoezi kwa kudhoofisha ile dawa waliyopakwa hivyo kuruhusu zoezi la unyongaji kuchukua nafasi kama kawaida!!!!
Lile jitu baada ya kuwafunga vitanzi wakina Mrisho alianza kuwaburuza kama nyama!! Halikujali kitu chochote juu yao na wala sura yake haikuonyesha hata chembe ya kulifikiria hilo.Walipowadia kwenye mti mmoja wa mkuyu,waliwatundika wale watu,wakaungana na shingo zingine zilizoonja kamba nyekundu, utofauti wao na wale waliotangulia ni kwamba wao walinyongwa bila mioyo yao iliyochukuliwa na yule mdada mithili ya Paka aliekua na mahitaji nayo,walibaki na mashimo tu yaliyokua yanamimina damu!!! Ile Mioyo iliingizwa kinywani mwa yule dada na moja kwa moja ilianza kutafunwa mithili ya keki huku lile jibaba likishuhudia,baada ya kumaliza lile tendo ghafla walibadilika na kuchukua sura za waliowauwa!! Lile jibaba liligeuka na kua Tabwe huku yule mdada akiichukua sura ya Mrisho!! Taratibu huku wakiwa wameshikilia mifuko isiyojulikana ilitokea wapi walianza safari ya kuelekea kule wanakijiji walipo!! Hapakukalika tena!! Hatari ilizidi kuchukua nafasi!! * * * * * * * Baada ya muda mrefu kupita bila ujio wa wakina Mrisho mzee Patili na wanakijiji wengine walianza kupata hofu,akili zao zilianza kuruhusu mawazo mabaya kupenya na mioyo yao ilianza kupokea taarifa za simanzi,wanakijiji waliokua hawajapakwa dawa walikua na hofu mara mbili kwani wao walijiona si salama ulikilinganisha na wenzao,walitamani wakina Mrisho waje haraka ili nao miili ipate kunawiriwa na dawa ambayo waliiamini kwa asilimia zote itakua kinga madhubuti kwao dhidi ya hali endelevu,walisali mioyoni,waliomba sana mungu wao apate kutanakabali sala zao. Muda si muda Mrisho na Tabwe feki waliingia,wanakijiji waliokwisha kata tamaa walilipuka kwa furaha na kuwalaki kwa upendo ulioonyesha matumani,masikini ya mungu hawakufahamu kwamba wale siyo,mzee Patili aliupokea mfuko aliopewa na haraka akawaambia wale waliokua bado hawajapakwa wajipange mstari,wakapanga,akaanza kuwapakaa kama ilivyokua mwanzoni ila sasa hivi alihusika kwenye kuwapaka wote yani wanaume na wanawake wakiwa wamepanga mstari mmoja tu,kutoka na dawa waliyopakwa wanakijiji wengine Tabwe na Mrisho walishindwa kustahimili,walisogea pembeni mbali na wanakijiji wengine,kujitenga kwao kulimpa kidogo maswali mwalimu Baraka alieamua kuwafuata kwa lengo la kuwapongeza kwa ujasiri wao,alipowakaribia aliwapa mkono wa kheri uliopokelewa na Mrisho ambaye ni yule mdada mwenye roho ya paka,kha!! Alishtuka mno mwalimu Baraka!! Mkono wa Mrisho ulikua wa baridi mno mithili ya barafu,hali hiyo ilimpelekea autoe mkono wake haraka na kuuliza… “we Mrisho mbona mkono wako wa baridi hivi???” “kawaida tu,si unajua tulikua tunakimbia ili tuwahi!!” alijibu Mrisho,mwalimu Baraka hakuridhika na lile jibu hivyo akauliza tena “sasa kama mlikua mnakimbia mbona mlichelewa??” swali hilo lilifanya kidogo Mrisho akwame,alimuangalia mwenzie Tabwe aliewahi akajibu, “tatizo kule kwa yule mzee ndo’ kulituchelewesha,madawa yaliku mengi mno!!” “ah-ahaa! Ila poa haina tatizo,hongereni bwana kwa ujasiri wenu mliouonyesha! Bella alikua ana wasiwasi kweli..teh! Teh!” mwalimu Baraka alimtania Tabwe kuhusu mchumba wake Bella,cha ajabu uso wa Tabwe ulimdhihirishia mwalimu Baraka ya kua halikua hajui kiongeleachwo, “Bella?? Ndio nani??” aliuliza Tabwe swali lililozidi kumshangaza mwalimu Baraka!! Moyo wa mwalimu ulisita,alipata hofu,hakutaka kukaa tena pale,taratibu aliaga na akajiondoa lile huku maswali kichwani yakizidi kupapaliwa na kuchipukia. Lile jibaba lilimuangalia mwenzie alie ndani ya sura ya Mrisho kisha akamuuliza.. “unadhani atakua amegundua chochote??” “sidhani,ila kama ukiniuliza ni moyo wa nani ninaoutaka kwa sasa,dhahiri nitakujibu ni wake!” “ile dawa waliyopakwa nayo itaanza kufanya kazi muda gani? Mbona kama inachelewa??” “tuliza munkari,ipe kama nusu saa,utaona majibu yake nadhani unafahamu huwa sibahatishi” alijigamba bimdada, “nafahamu hilo,ila ile dawa waliyoipakaa ni kali mno! Nadhani uliona jinsi tulivyokua tunapata shida alipokuwepo yule mbaba” “ni kweli,ila siwezi kuondoka mpaka nione ikifanya kazi!” “sawa.” maongezi yakakomea hapo. Hayawi hayawi yakawa!! Dawa waliopakwa watu wa awamu ya pili ilianza kufanya kazi bara-bara!! Miili yao ilianza kuwasha hatari!! Na kila walipojikuna ngozi ilitoka na kuruhusu damu iruke kama bomba!! Makelele ya kuomba msaada yaliteka ile sehemu!! Muwasho wa ajabu usiovumilika uliwafanya wawe machizi kwa kuranda huku na kule wakipiga makelele kwa nguvu!!!! Mzee Patili alishikwa na butwaa!! Wanakijiji walitawaliwa na taharuki!! Walipotizama wakina Mrisho wako wapi,HAWAKUWAONA!! Mungu wangu!! Wale waliokua wanawashwa wakaanza kukauka na kuwa magofu meupe kama chumvi!! Wale waliokua wanawashwa wakaanza kukauka na kua magofu meupe kama chumvi!!! Kilio kilichobeba uchungu na uoga kilipata kutoka vizuri toka kwenye midomo ya wakina mama na watoto,vilevile mioyo ya wakinababa ilikita kwa nguvu na macho yao yalitoka kwa kutoamini,ulikua ni kama mchezo wa kuigiza,sehemu ile yote ilitawaliwa na magofu ishirini na mawili yote yakitokana na ile dawa ya awamu ya pili! Wanakijiji walipungua kwa kiasi kikubwa,watoto wengi walipoteza wazazi,wanawake wengi walipoteza waume zao,na hata vile watu wengi walipoteza watu wao wa karibu,simanzi iliyoje!!! Mzee Patili alichanganyikiwa kabisa,hakujua cha kufanya japokua mzee Otongo alikua anajitahidi mno kumtuliza,alijiona yeye ndie muuaji na hata baadhi ya wanakijiji walianza kufikiria hivyo,walifikiria ya kwamba vile vifo ni dhahiri vimesababishwa na mzee Patili ilihali wengi wao bado walikua kwenye tahamaki ya njia panda hasa baada ya wale walioleta dawa kupotea kiajabu machoni mwao!! Mama Kadogo aliutumia ule mwanya kuita rai na kuteka hamsha za wanakijiji,kwa kujiamini alisimama mbele yao na kusema “Jamani..jamani!! Naomba tusikilizane! (ukimya ukatawala lakini bado vikwikwi na vimafua vya vilio vilikua vinachukua nafasi)….katika vita hii tunayopambana nayo kufa kwa mtu au watu isiwe kitu cha kutushangaza,mtu yeyote kwa muda wowote anaweza akafa kwenye mapambano haya hilo inabidi liwe kichwani,naomba tusiruhusu roho za simanzi ziweke kiza kwenye njia yetu bali roho ya ushupavu na ya kusonga mbele,ni hakika tumezidiwa akili na hili jeshi la 666 katika huu mchezo,waliutumia ipasavyo ule mwanya tuliowapa wa kuwatuma wale vijana,nadhani hilo halina maswali…tumeona kwa macho yetu walivyopotea kiajabu na kuudhihirishia uma ya kwamba wao sio wale tuliowategemea!” haraka Mwalimu Baraka alidakia “hakika mama,hakika!! Wale hawakua wakina Mrisho kama tulivyodhani,mie mwenyewe naweza nikasema hivyo kwa ushahidi wangu mdogo nilioushuhudia,walikua ni watu wa baridi mno! Na hata baadhi ya maswali niliyowauliza walishindwa kabisa kujibu,kusema ukweli nilipata hofu lakini sikuwa na uhakika asilimia mia hivyo nikaamua nijitoe lile eneo kimyakimya!” maneno hayo ya mwalimu Baraka yaliamsha minong’ono miongoni mwa watu,mama Kadogo aliwatuliza na kisha akaendelea kunena.. “ni matumaini yangu dawa tulizopaka zina msaada kwetu,bado ninaamini hivyo japokua hili tukio la wakina Mrisho linaweza kuwatia mashaka mioyoni,hapo ndipo tunapoweza kurudia kauli yangu ya mwanzoni ya kwamba walituzidi akili,nahisi kuna kitu walichokifanya hawa jeshi ambacho bado hatujakifumbua….” (kabla hajamalizia mzee Rama kwa jazba alidakia) “sasa tufanye nini?? Hamuoni ya kwamba tunaendelea tu kufa!! Au nyie bado hamjatosheka???” kauli ya mzee Rama ilizua tena minong’ono na malumbano,baadhi ya wanakijiji walionekana kumuunga mkono na baadhi yao walionekana kumpinga,makundi mawili yakazaliwa miongoni mwao!! Ni dhahiri imani zao haba zilianza kuwachonyota,mzee Patili taratibu alisimama na kuelekea pale alipo mama Kadogo kisha akawaomba utulivu kwa muda ili apate kunena,wale waliokua bado na imani nae walifunga midomo yao na kumpa masikio lakini wale ambao imani zao zilitiwa doa hawakujali hilo,waliendelea kururuma tu,mzee Patili akatoa tamko.. “kama imani yako haiko nami tena,sitofanya jitihada zozote kuiinua maana umeamua hivyo,kama nilikua nanyi tokea ujana nikiwahudumia na bado imani zenu zina madoa kuhusu mimi,hakuna chochote ninachoweza fanya kwenu kwa sasa.Ninaelekea upande wa kulia nilipotokea,kama bado una imani nami waweza nifuata,kama huna imani nami waweza kubaki..” sura ya mzee Patili ilionekana si yenye furaha,alikua anawaza jambo na dhahiri alionekana ameumia,alishika njia ya kuelekea nyumbani kwake na kundi la watu huku nyuma lilimfuata akiwemo Julina mwenye mtoto aliebeba matumaini yao,bila hata kuonyesha aibu usoni mzee Rama nae na wenzake walioonyesha kutia shaka juu ya mzee Patili nao walikuwemo ndani ya msafara wakiivuta miguu yao kumfuata,hawakufanya hivyo kwa kupenda bali iliwabidi kwani mtoto ambaye ndie ngao ya matumaini alikua upande ule hivyo hawakua na jinsi,mzee Rama bado alikua na gubu jeusi lililokua linamkereketa,hakupendezewa kabisa na ile hali ya uongozi wa mzee patili,wivu ulimkua unamsumbua kwa kiasi kikubwa,alitaka yeye ndie awe anasikilizwa na yeye ndie awe anatoa amri,wivu ulimshika mishipa yake ya damu,akili yake ilimtuma amuibe yule mtoto wa Julina,alifahamu fika ya kua akimmiliki yule mtoto jamii nzima itamsikiliza yeye kwani ndie atakaekua ameshikilia matumaini yote ya wanakijiji,atafanyaje sasa?? Alijiuliza kichwani mwake,baada ya kupata jibu haraka alimvuta mwenzie pembeni na kumwambia.. “unataka kufa na wewe,ama??” swali hilo lilimshangaza alieulizwa,kiuoga nae akajibu.. “hapana!!” “sasa nisikilize nitakayokuambia…”
“unataka kufa na wewe ama??” swali hilo lilimshangaza alieulizwa,kiuoga nae akajibu “hapana!” “sasa nisikilize nitakayokuambia..” “enhe..” “najua wewe ni mwenzangu na ninakuamini hautoniangusha,hivi we unadhani haya yote yanayojiri ni sababu ya nani??” “mh…kusema ukweli mie sijui!” “we unahisi ni nani??” “mmmh….labda ni hawa wageni au….” “ah-ah! Hawa wageni waliruhusiwa na nani??” “…….mzee Patili!” “unavyodhani ni nani sasa hivi anatuua??” “si lile jeshi la 666 walilotuambia!!” “..kwani wale ndio waliowapakaa nyie dawa??” “hapana! Ni mzee Patili!”
“majibu yote yapo wazi kama unavyoona,huyu mzee ndio kikwazo kwetu,na hivi ninavyokuambia ni kwamba lengo lake si kukabili jeshi la 666 kama anavyotudanganya bali anataka amtumie yule mtoto kwa malengo yake binafsi,yani kujinyanyua na kufanikisha hamu yake ya uongozi!! Hivyo basi ili atudhoofishe na asafishe njia yake anatupunguza idadi kama unavyoona…!!”
haikuishia hapo tu,kukaa kwake nyuma ya ule msafara alikutumia kama ngazi ya kuigeuza mioyo ya wanakijiji,alipenyeza uongo kwa walio karibu na kufanikiwa kuiteka mioyo yao yenye imani haba,na alitamani zaidi.
Baada ya muda msafara wa wanakijiji uliwasili kwa mzee Patili,walishangazwa na hali waliyoikuta ikiwemo mzee Patili mwenyewe,mlango haukuwepo sehemu yake na mwanga wa mwezi uliokuwepo uliruhusu kuonekana unga fulani wa manjano chini mzee Patili aliougundua kwamba ni dawa ile aliyoiagiza,alama za miburuzo zilizokuwepo chini ziliwatia mashaka hivyo
wakasogeza koroboi na kuanza kuzifuatilia mpaka pale zilipowafikisha kwenye miili ya wakina Mrisho iliyokua imetundikwa! Macho yaliwatoka kwa kushuhudia zile maiti zilizokua zinaning’inia na mashimo vifuani,machozi na simanzi havikuzuilika kuwa miongoni mwao,miili ile ilishushwa na kumpa ruhusa mzee Patili kuikagua kisha akatoa neno.. “watu waliotumwa ni wazi walivamiwa! Nadhani mazingira husika yanaeleza hivyo,dawa niliyoiagiza tumekuta imemwagika,mlango umevunjwa,vilevile wamenyongwa! Hiki ni kielelezo tosha ya kua dawa iliyoletwa kule haikua sahihi..” alivuta pumzi kidogo kisha akaendelea
“miili ya wakina Mrisho japokua imenyongwa kama ile mingine lakini kuna utofauti juu yao,utofauti huu unatudhihirishia ya kwamba kuna kiumbe kingine ambacho ni hatari kwetu kimeongezeka,na ndio hasa kinachohusika na hii mioyo iliyobebwa! Inatubidi tuongeze kinga yetu!”
mzee Patili akanyamaza kidogo,ila taratibu mzee Otongo alimkaribia na kuanza kumnong’oneza kitu hali iliyohamsha vimaongezi vya chinichini hasa kutoka kwa mzee Rama aliekua anapigilia misumari maelezo yake ya uongo aliyoyaingiza ndani ya vichwa vya watu huku akihakikisha mzee Patili hagundui hilo.
Baada ya mzee Patili na Otongo kujadili waligundua cha kufanya japokua ilikua vigumu kuwaeleza watu,kazi ngumu ilibidi ifanyike na pia ilihitaji watu jasiri watakaojitolea kuifanikisha,baada ya kujiulizauliza sana mzee Patili aliamua apasue jipu, “tunahitaji dawa kwa ajili ya kuongeza kinga yetu madhubuti,kama nilivyowaambia hapo kabla ya kwamba ni lazima kinga yetu iendane na mazingira husika,sijamaanisha ya kuwa tuliyonayo haifai,hapana,ila inabidi tuiongeze nguvu…” alishindwa kuendelea,mzee Otongo ikabidi aendeleze alipoishia.. “tunahitaji Mdigidigi!!” “Mdigidigi!!!” wanakijiji walihamaki,
“ndio Mdigidigi!!…na kama tunavyojua haipatikani hapa karibu…….” “ndio! Ni mpaka mtoni!!” “haswaa!..Mpaka mtoni!…inabidi tuwe na ule mti ili tuweze tengeneza dawa,tatizo ni kwamba tutaipataje?” Otongo aliuliza, mama Kurwa akatoa maoni yake “inabidi watu wafuate kama ni hivyo!!”
kauli hiyo ilizua mjadala mzito,hakuna mtu alieonekana yu tayari kufanya hicho kitu kwani waliona ni kama kujiingiza kwenye mdomo wa kifo wenyewe,kila mtu alitaka kuilinda roho yake.
Katika hali ya kushangaza mzee Patili alinyamazisha watu na kuwataarifu ya kwamba ataenda yeye mwenyewe,taarifa hiyo badala ya kunyamazisha mjadala iliuzua zaidi,uamuzi wa mzee Patili kwenda kutafuta ule mti ilipokelewa na mawazo tofauti,asilimia nyingi ya watu walionekana kutoafikiana nalo huku wengine wakiliunga mkono….wakati taharuki bado ikichukua nafasi sauti ya mzee Rama tokea nyuma kabisa ilipata kusikika ikisema.. “mimi nitaenda huko mtoni!…mimi nimejitolea kwenda!! Nitumeni!”
hakuna mtu alietegemea kuisikia hiyo kauli tena toka kwenye kinywa cha mzee Rama,miguno na maswali ya chinichini ilizuka lakini hivyo vyote havikubadilisha uamuzi wake,alijisogeza mbele kabisa ya umati huku akimtizama mzee Patili,kisha akarudia kauli yake.. “nitume mimi!!” “nitume mimi!” mzee Rama alirudia kauli yake huku akimtamzama mzee Patili machoni,macho yao yaliyokua yanatazamana yalihakisi hali ya shari,tabasamu alilokua nalo mzee Rama halikua la wema,lilificha uadui mkubwa wa wivu ndani yake na pia malengo makubwa ya kimapinduzi.
Mzee Patili aliwageukia wanakijiji huku akiwa na sura ya kufikiri akasema… “ameamua kujitolea,siwezi nikamzuia,maombi yetu yawe nae aweze fanikisha kile tulichodhamiria.” baada ya kusema hayo maneno aliingia ndani na kuchukua fimbo fulani akamkabidhi mzee Rama kwenye mkono wa kuume kisha akamshika bega na kumpa maelekezo madogo juu ya ile fimbo,jinsi gani atakavyoitumia kumlinda,pia akamtakia safari njema.Mzee
Rama baada ya hayo maelekezo alimuaga mkewe na wanae huku akiwahaidi ya kwamba atarudi,akamfuata kijana mmoja aitwae Sadiki ambae ndie wa kwanza kumrubuni juu ya mzee Patili kisha akamuambia waende pamoja,alikubali na safari ikaanza. Mzee Rama aliamini ya kwamba ile ni moja ya fursa adimu aliyokua anaitafuta kwa muda mrefu,japokua ni ya hatari lakini hakujali hilo,aliweka maisha yake rehani,eidha afe au afanikiwe kumpindua mzee Patili.
Safari ilitawaliwa na ukimya wa hali ya juu kutokana na kila mmoja wao kutoruhusu mdomo wake ufunguke,mwanga mwanana wa mwezi uliokuwepo uliwafanya waone wakanyagapo hivyo kutokua na hitaji la koroboi,mioyo yao ilikua inasema na mungu wao lakini ilikua ni zaidi ya hivyo kwa mzee Rama aliekua anasema na akili yake hasa juu ya nini atakachofanya afanikishe lengo. Huku safari ikiendelea wingu zito taratibu lilianza kufunika mwezi uliokua unatoa nuru,giza totoro likaanza kuingia na kuwapa wakati mgumu wakina mzee Rama kwa kutoona walipokua wanaelekea! Sadiki aliekua ameshikwa na uoga maradufu alivunja ukimya
“..sasa mzee tutaendaje na hili giza??…si bora turudi tu!” mzee Rama alitulia kwa muda bila kujibu,kisha kwa sauti ya msisitizo akasema… “hatuwezi kurudi hilo sahau kabisa,tumeamua kujitolea na hii ndio maana ya kujitolea,wingu lipitalo lisikufanye ukageuza wako moyo,baada ya muda hali itarudi mahali pake”
baada ya mzee Rama kutoa hilo jibu ukimya ukarudi tena,hakuna alieongea zaidi,miguu yao ilizidi kusogea mbele taratibu kwa kukisia njia huku wakiyatoa macho yao ili yapambane na hali ile ya kiza iliyotawala,bado sadiki alikua na kinyongo moyoni lakini lile jibu alilopewa lilimfunga mdomo wake,hakua na jinsi,ilimbidi afuate kile atakachoelekezwa na ilikua ni robo saa sasa tangu waanze safari,walishakiacha kijiji chao kwa umbali wa kutosha japokua umbali wa maana bado ulikua mbele yao,walipiga konde.
Wingu jeusi taratibu lilianza kuacha mwezi uchomoze hivyo kuruhusu mwanga urejee na kuamsha matumamini ya wakina mzee Rama,waliongeza kasi sasa baada ya uhakika wa njia huku bado vinywa vyao vikiwa vimefungwa na macho yakitizama wanapoelekea,ghafla walisikia sauti za watu tokea nyuma zikiwaita!!! Mioyo yao ililipuka kwa uoga puh!! Kusikia majina katika hali kama ile ni kitu kilichowashangaza mno!! Mzunguko wa damu ukaanza kwenda kama mbio za marathoni! Shingo zao zilizowageuza nyuma hazikuwashuhudisha chochote,hawakuona kitu ila walisikia sauti!!..Miili ilitetemeka!!
“kimbiaaa Sadiikii!!” kauli hiyo ya mzee Rama ilikua kama kipenga kilichoruhusu mbio zianze,kila mmoja alikimbia kadiri ya uwezo wake huku akitizamatizama nyuma kuangalia kama wanafuatwa,umri wa mzee Rama ulikua ni kikwazo kikubwa kwani ulimfanya asiweze kukimbia kwa kasi kama Sadiki aliekua mbele yake,kila alipojitahidi kuvuta makasia ya mbio alihisi miguu inauma japokua alijitahidi kujizuia asisimame,mioyo yao ilikua inagonga kwa nguvu mno na jasho lilianza kutotesha nguo zao huku wakihema kama mbwa!! Fikra za kujutia uamuzi alioufanya zilianza kumtawala Sadiki mloe,atafanya nini sasa katikati ya ile safari?? Hakua na jinsi zaidi ya kuifungua miguu yake iokoe maisha yake.
Upepo mkali wa baridi ulimpita ghafla mzee Rama na kumfanya mwili mzima uite kwa msisimko wa ajabu!! Cha kustaajabisha ule upepo ulipomfikia Sadiki ulimbeba na kutokomea nae maporini!! Sauti yake nzito ya kuomba msaada ilifika vema kwenye masikio ya mzee Rama aliekua hana cha kufanya zaidi ya kutoa macho kwa kutoamini anachokiona,kama mchezo wa kuigiza Sadiki alipotelea kabisa..sauti yake nayo pia ikatokomea huko!!!
Mzigo wa hofu lawama na majuto ukatuama ndani ya moyo wa mzee Rama,alisimama huku mikono ikiwa kichwani,macho yakimtoka na jasho likimchuruza,alijiuliza mara mbilimbili kwanini ule upepo haukumbeba yeye akakosa jibu kabisa,hakujua ya kwamba ile fimbo iliyomkononi ndio iliyomuokoa,mkojo taratibu ulianza kutiririka katikati ya mapaja yake na kufanya nguo aliyoivaa iloe chepechepe,haraka wazo la kutaka kurudi kijijini likamjia kichwani,kwa macho ya uoga alitizama alipotokea na kuona kiza kimetawala,alipotizama na anapoelekea aliona hali ileile!! Harufu ya kifo ikaanza kugonga puani kwake,makelele ya umauti yakaanza kuita masikioni mwake!!
Harufu ya umauti ilianza kugonga puani,makelele ya kifo yalianza kugonga masikioni!! Alitembea kama hatua tano kurudi nyuma alipotokea akahisi moyo wake unamsuta,alikumbatia kile kifimbo alichokua nacho kisha akageuka tena na kuendelea na safari kama kawaida,tumbo likichemka na mwili ukitetemeka huku nguo ikiwa imelowa ndembendembe. Nyuma ya mzee Rama hatua kama ishirini walikuwepo watu wawili wanasogea taratibu huku macho ya mmoja wao yakiwa yanang’aa mithili ya paka,mungu wangu!! Walikua ni wale mapatna wauaji,lile jibaba na yule mdada mwenye roho ya paka! Walionekana wanajadiliana jambo fulani lililoonekana kuwateka hisia,baada ya muda kidogo walinyamaza na kuendeleza zoezi lao la kumfuata mzee Rama taratibu bila
mwenyewe kusikia,masikini mzee Rama aliekua mwenyewe alikua hana hili wala lile,alikua hatambui ya kwamba bado anafuatwa na wale watu waliowaita,alikua hatambui ya kwamba nae anaundiwa mipango kabambe ya kumalizwa. Dakika kama kumi na tano tu zilibakia ili mzee Rama aweze kuufikia mto Inguvai,miti ya midigidigi aliyotumwa ilikua inapatikana tu kwenye kingo za mto huo na si pengine popote,masikio yake yalianza kusikia sauti za maporomoko ya maji na sauti hiyo ilizidi kufika masikioni
mwake kila alipozidi kujongea,alishukuru mungu anakaribia lakini kichwa kilikua bado kizito kuchambua ya kwamba atafanikiwa kurudi kijijini au la! Hicho kitendawili alishindwa kabisa kukitegua.
Penye nia pana njia wahenga hawakukosea hata chembe kusema hivyo,nia ya mzee Rama kufanikisha lengo lake ilianza kuchomoza pale alipofanikiwa kuupata mdigidigi alioagizwa,hakutaka kuvunga muda,haraka alinyofoa matawi kadhaa,alipoona yanatosha hakuondoka kama ilivyotakiwa afanye,alianza shughuli za kutafuta mti mwingine aina ya Mtiriri tena kwa juhudi kubwa! Na hata alivyoupata aliunyofoa matawi
mengi ukilinganisha na aliyoyatoa kwenye mti wa mdigidigi,si kwa sababu miti ile ya mitiriri ni mifupi na rahisi kupatikana,hapana! Alikua ana malengo binafsi,matumaini yake ya kishenzi yalilala kwenye ule mti ambao ni sumu kubwa na mti hatari zaidi,alikua na lengo gani nao?? Je malengo yake ni kuua wanakijiji?? Hayo yote yalikua moyoni mwake binafsi,safari iliyotawaliwa na hofu ya kurudi alipotokea ikaanza rasmi taratibu huku kichwani kwake akijenga picha ya kufanikiwa.
Mzeee Ramaaaaaaa!!!! Sauti ya kike yenye nguvu ilisikika toka nyuma ikimuita! Mama yangu!! Mzee Rama alichanganyikiwa kabisa! Mara ya kwanza alipoisikia ile sauti Sadiki alibebwa,je sasa hivi kuna mwingine zaidi yake?? Hapana! Alikua ni yeye tu! Hakua na mkojo tena wa kutoka,moyo wake ulianza kudunda kwa pupa na miguu yake ya kizee ilianza kuchanganyia mbio!! Mkono wa kulia akishikilia fimbo na
matawi aliyoyakunjakunja ya mdigidigi na huku wa kushoto akibebelea majani ya mtiriri,magoti yake ya kizee yalianza kumvuta kwa maumivu,alijitahidi mno asisimame ili auokoe uhai wake lakini mwisho alishindwa,maumivu yalizidi mno na hata pumzi haikua nae tena!! Alisimama akihema kwa pupa huku sura yake ikitawaliwa vilivyo na uoga,alikodoa kutizama nyuma hakuona kitu kama kawaida!! Nafsi yake
ikamtonya kifo kimewadia,alipogeuza macho yake mbele aelekeapo uso kwa uso alikutana na yule mdada!!! Mzee Rama alifanya kosa kubwa kumtizama machoni kwani ndipo nguvu kubwa ya lile jini ilipo,alipoteza nguvu kabisa na kudondoka chini kama zigo..Fimbo kule!!
Lile jini lilimsogelea mzee Rama aliedondoka,macho yake mithili ya paka yaking’aa kama mwezi,masikio yake marefu yakichezacheza na ngozi yake ya kijivu ikitoa jasho,kiremba chekundu kilichokuwepo kichwani kilificha mapembe yake na kupunguza kidogo ubaya wake wa kutisha.Alipiga makofi mawili kwa mtindo wa mkono wa kushoto kuufuata wa kulia,ghafla mwili wa mzee Rama uliokua chini ukainuka
kimaajabu huku uso wake ukionyesha ya kua hajui kinachoendelea,yani hana fahamu,lile jini likapiga tena makofi ila ya sasa hivi yalikua ya haraka na pia kiganja cha kulia kilifuata cha kushoto,ghafla akapotelea na kua kama upepo! Kisha kwa madaha likamvaa mzee Rama!! Macho yaliyokua yamefumba yakafunguka! Mwili uliokua umelegea na kunyong’onyea ukapata nguvu ya ajabu!! Majani ya mtiriri na matawi ya mdigidigi yaliyotawanyika chini yakaokotwa na kutiwa mkononi kisha tabasamu mwanana lililoakisi furaha ya yule jini alie ndani likajaza uso wa mzee Rama,taratibu kwa maringo yote likaanza kujongea kukitafuta kijiji cha Utowele alipo adui wao mkubwa waitajie kumtokomeza,ili kuifanya safari yake iwe ya kuvutia na kufurahisha alikua anaimba njia nzima huku akiuchezesha mwili ule wa kizee,lile jibaba linyongaji nalo ghafla likatokea na kumpa kampani mwenzie. Je wanakijiji watapona?? Au ndio watapukutika kama mwanzoni?? Awamu hii mzee Patili ataeleweka?? Na vipi kuhusu mzee Rama na malengo binafsi??
Safari ilikua kabambe mno,walicheza na kuimba bila woga wowote kwani walishafahamu ya kwamba muda si mrefu watakamilisha kile walichoagizwa,kazi ilikua kwa wanakijiji waliokua wanasubiria dawa ingali wanaletewa kifo!! ‘ya nini uepuke chumvi ingali jirani ni bahari?’ huo msemo ni dhahiri ulikua unaendana na tukio halisi kwani wanakijiji walionekana wakisumbuka kweli kukwepa kifo bila kufahamu kwamba kilikua pembeni (jirani).Zilibakia dakika chache tu kuingiza miguu kwenye kijiji cha Utowele,lile jibaba linyongaji lilipotelea kusikoju likana na kumuacha yule bimdada aliekua ndani ya mwili wa mzee Rama aendelee na safari,mkono wake wa kushoto alioshikilia baadhi ya majani ya mtiriri sumu aliusogeza karibu na macho
yake,alichezesha kope zake kwa muda tu na ghafla yale majani yalibadilika na kua ya mdigidigi!! Kwa madaha aliyachanganya na yale ya mdigidigi halisi yaliyokuwepo mkono wa kuume,kama kawaida tabasamu likachomoza usoni mwake na kwa maringo akamalizia kaumbali kalikobaki.
Wanakijiji waliokua wamejikunyata kwa hofu na ukimya ukiwa miongoni mwao walilipuka kwa furaha baada ya kumuona mzee Rama,ilikua ngumu mno kuamini macho yao hasa familia yake!! Kusema ukweli ni asilimia ndogo iliyokuwepo mioyoni mwao iliyokua ikishuhudia kufanikiwa kwake,walimlaki kwa furaha huku wakimbeba na kumrusharusha mithili ya mtoto! Nyimbo za
kishujaa zikipamba tukio na wakisahau kabisa kuuliza yu wapi alieenda nae(sadiki).Mzee Patili,mama kadogo na mzee Otongo walikuwepo ndani wakifanya shughuli ya upakaji dawa,walitoka nje baada ya kusikia makelele ya wanakijiji,ilikua ngumu pia kwao kuamini macho yao pale yalipomshuhudia mzee Rama aliekua anarushwa na wanakijiji,muda mfupi tu baada ya wakina mzee Patili kutoka ndani wanakijiji walimshusha mzee Rama ili apate fursa ya kuwasilisha kile alichoagizwa,mzee Rama nae
hakufanya ajizi,taratibu alianza kujongea huku akishikilia yale majani akielekea walipo wakina mzee Patili,mzee Patili aligundua jambo la tofauti haraka akauliza.. “sadiki yupo wapi??” “ameuwawa!!” kifupi alijibu jini lile lililojivika mwili wa mzee Rama na kuwashtua wanakijiji,bado mzee Patili alitia wasi,akauliza tena “fimbo niliyokukabidhi ipo wapi??”
lile jini lilijing’atang’ata kutoa maelezo yaliyonyooka hali iliyoanza kumpa mashaka mzee Patili na hata pia wakina mama Kadogo,mzee Patili hakutaka kuuliza swali lingine,alimshukuru mzee Rama kwa niaba ya wanakijiji na kumtakia baraka toka kwa mungu kisha aliingia na yale majani ndani na kumuacha mzee Rama akiwa amesimama pale nje karibia na mlango.
Udhaifu mkubwa wa yule jini kwenye mioyo ya binadamu ulianza kujionyesha,harufu ya binadamu iliyokua inagusa pua yake ilianza kumpa hamu kubwa na kuruhusu mate kuchuruza!! Mama Kadogo aliekua pembeni hofu ilianza kumteka akamshtua mzee Otongo ashuhudie lile jambo,si mate tu! Hata macho yake yalianza kubadilika badilika!! Kutokana na kuwapa mgongo
wanakijiji hakuna alieshuhudia hayo zaidi ya mzee Otongo na mama Kadogo,tamaa ya kula mioyo ilizidi kumtawala kichwa kumpelekesha na kumsahaulisha kusubiria malengo yake yatimie,taratibu lilianza kusogeza miguu yake na kuelekea ndani alipo mzee Patili!!! Mama Kadogo alishindwa kunyamazia hilo akapayuka kwa nguvu.. “mzee Patili huyo anaaakujaaaa!!!!”
huku akinyooshea kidole na macho yakimtoka,sauti ile kali ya tahadhari iliwastua mno wanakijiji ilihali na mtu lengwa ambae ni mzee Patili,haraka mzee Patili aliuvuta mkono wake uliokuwepo ndani ya mfuko fulani mweusi na kumrushia unga wa kahawia lile jini usoni!! Sauti kali mno ya kulalamika mithili ya paka ilisikika toka kwenye kinywa cha yule jini!! Alijibamiza huku na huko na
kuhangaika mno huku akifikicha fikicha macho yake yaliyopokea ile dawa!!! Ilikua ni kama ndoto kwa wanakijiji waliokua wanashuhudia lile jambo kwa macho na mioyo ya hofu,walishuhudia mwili wa mzee Rama ukipotea na kuwa wa lile jini halisi!! Kiremba chake kinachoficha mapembe yake kiliruka huko na kuruhusu pembe zake mbili mithili ya mbuzi na chapa yake ya 666
kuonekana!!! Liliangaika mno huku likilia kila aina ya mlio,macho yake yaliyoingia dawa yalianza kufuka moshi ulioashiria ya kwamba nguvu yake inateketea na taratibu lilidondoka chini na kutulizana!!! Wanakijiji wakiwa bado wameshikwa na mshangao na wasijue la kufanya walisikia sauti nzito isiyoeleweka ilalalamikayo inasogelea lile eneo!!!…..loh!! Walipogeuza macho yao kushoto walimuona lile jibaba linyongaji likija kwa kasi ya ajabu na
kamba yake mkononi!!! Macho yakimtoka na sura ikiakisi ghadhabu kubwa aliyokua nayo!! Kabla hata halijafanya chochote kwa nakijiji walioanza kukimbia huku na kule kuokoa maisha yao jua lilianza kuchomoza!!! Mwili wake mkubwa mithili ya tembo ulianza kufuka moshi kama sigara kali!!! Nalo likaanza kutapatapa kama samaki nchi kavu! * * lile jibaba nalo likaanza kutapatapa kama samaki nchi kavu!! Macho ya wanakijiji waliokua wemejificha hayakuamini yalichokishuhudia,lile Jibaba ilikua kama mtoto kwa jinsi lilivyokua linajibaraguza na kurukaruka huku na kule kwa mitindo yote,ni dhahiri miale ya jua lililochomoza ilimuunguza kupita kiasi na alishindwa kabisa kuvumilia hilo,alitia huruma mno kwa jinsi alivyokua
akilalamika,waweza sahau mabaya yote aliyoyatenda kwa jinsi alivyokua anateseka,hatimaye mwili wake ulikua majivu kabisa na wa yule mdada pia,hakuna kilichobaki juu yao na huo ndio ukawa mwisho wao,chereko nderemo na vifijo zilitawala. Je wanakijiji wataishi kwa amani sasa?? Ni swali lililohitaji ufumbuzi mzito. * * * * * * (Dar es salaam,Msasani) mchungaji Josiah alikua amejipumzisha juu ya kitanda chake sita kwa sita akiitawanya miguu na mikono kwenye pande zote nne za kitanda,ni dhahiri huduma ya kiroho aliyoifanya jana usiku ilimchosha mno kwani japokua jua lilikua lishachomoza mwili wake bado ulionekana kutamani kitanda ambacho hakikushushiwa hata neti ya kumzuia na mbu,alijigeuza kivivu na kuendelea kuvuta makasia ya usingizi mpaka pale aliposhtushwa na mlio mkali wa simu yake ya kichina yenye muito wa nyimbo fulani ya injili ya muimbaji
maarufu nchini,macho yake yaliyotawaliwa na mang’amung’amu ya usingizi yalifunguka kwa mbali kuangalia ni nani anaepiga,alishtushwa kuona ni Askofu Emmanuel haraka aliiweka simu sikioni.. “shalom Askofu!” “shalom Josiah…vipi unaendeleaje?” “safi tu namshukuru mungu aisee..” “ni kweli mungu aliejuu ashukuriwe,sasa Josiah…” “naam Mtumishi!” “embu fika hapa kanisani mara moja kuna kitu cha muhimu inabidi tujadiliane” “haina shida mtumishi wa mungu,nitakuwepo hapo muda si mrefu!” “sawa,bwana mungu awe nawe..” “amina,awe nawe pia mtumishi..”
maongezi yakakata,mchungaji Josiah aliekua amechoka kama mbwa kutokana na shughuli pevu aliyofanya jana aliamka kwa kujivutavuta na kuelekea bafuni kupata maji,hakuweza kabisa kumbishia Askofu hivyo hakua na jinsi zaidi ya kutekeleza kile alichoambiwa na mkubwa wake ukizingatia yeye bado ni mchungaji mwanafunzi kwani si muda mrefu tangu aanze rasmi shughuli zile
za uchungaji.Ilichukua kama dakika thelathini na tano kwa mchungaji Josiah kumaliza kabisa zoezi la kujiandaa,alipanda daladala chapchap na kufika kanisani haraka tu kutokana na ukaribu uliokuwepo,alipoingia tu kanisani macho yake yaliweza kumuona
Askofu Emmanuel akiteta jambo na mtu fulani alievalia suti nyeusi,kabla hata ya yeye kufika walishamaliza maongezi yao na yule mtu akapanda gari na kuondoka,Askofu Emmanuel alimkaribisha mchungaji Josiah na moja kwa moja walielekea ofisini walipowakuta watu kama kumi wenye vialama vyeupe shingoni vilivyoashiria ya kwamba ni wachungaji,baada ya salamu za hapa na
pale majadiliano yalianza baada ya kufunguliwa na sala nzito toka kwa Askofu,kikao kile hasa kilikua kinahusu usambazwaji na uenezaji wa neno la bwana kama ilivyoagizwa,kilikua ni mahususi kwa ajili ya kujadili mikakati itakayowezesha injili kufika mahali ambapo hapajafikika,kanisa lilihitaji kufungua matawi yake zaidi ili iweze kuwafikia watu wengi zaidi waliohitaji huduma za kiroho
sehemu mbalimbali za nchi hasa vijijini,baada ya masaa mawili kikao kilikwisha kwa kumteua mchungaji Josiah asimamie shughuli ya kwenda kusambaza injili mkoani mbeya na kutia msingi wa kanisa,hakuamini kilichotokea kwani aliona ile ni kazi kubwa ambayo hakustahili apewe,haikua na jinsi,Askofu Emmanuel alimuamini na ukizingatia mchungaji mzoefu Isaya alikuwepo mkoani Arusha
kiroho,ilipangwa siku ya kufunga safari na idadi ya watu watakaokuwepo kisha mchungaji Josiah alirudi nyumbani kwake kwa ajili ya kuendelea na mapumziko.
Alipojirusha kitandani usingizi haukuja kama alivyotegemea,moja kwa moja akili yake ilianza kupitia kile alichoambiwa na kidogo kupata mawazo,ila katikati ya yale mawazo taratibu tabasamu lilichomoza usoni mwake na kuupendezesha uso wake mrefu wenye dimpoz,hakuna mwingine alieleta hilo tabasamu zaidi ya Rachel Mwakatwila mwanakwaya mahiri pale kanisani aliyewekwa kwenye
orodha ya wale waendao kutoa huduma,moyo ulilifurahia hilo,fursa adimu aliyokua anaisaka imekuja mikonomi mwake,nini nataka zaidi?? Kazi ni kwangu!! Alijiambia mchungaji Josiah. * * Jumatano alfajiri na mapema mchungaji Josiah,Rachel na watumishi wengine wawili walianza safari ya kuelekea mkoani mbeya kwa kutumia bus,kitendo cha mchungaji Josiah kupewa fursa ya kukata tiketi ilitumika vema kwani aliutumia ule mwanya kukata tiketi iliyomueka karibu na Rachel kitulizo chake cha moyo,safari nzima ilitawaliwa na vijistori vya hapa na pale na vicheko vya haja,Josiah alisahau kabisa cheo chake cha uchungaji mbele ya Rachel,stori zilinoga,ila mwishowe Rachel alibebwa na uchovu wa safari akamlalia mchungaji Josiah begani.
kila mara Josiah alipomtizama Rachel alielalia begani kwake alijihisi amani,alitamani alalie na kwenye moyo wake vilevile,hakujua cha kufanya ili aweze muingiza Rachel kwenye system ukizingatia cheo chake cha uchungaji,kuhisiwa vibaya mbele ya jamii na kunyooshewa kidole vilimtia hofu pia hisia za kukataliwa zilizidi kumtisha,alisema tu na moyo wake mkavu unaoumia.
Mwendo wa kasi wa bus ulifanya baadhi ya abiria walipuke kwa maneno wakimshutumu na kumsema dereva,makelele na malalamiko yao yalimuamsha mchungaji Josiah toka kwenye usingizi mzito wa mawazo juu ya Rachel aliokua nao,hakuchangia chochote kwani hakuna alichoshuhudia ila aliona watumishi wenzake wawili David na Rio wakijibizana na baadhi ya abiria juu ya mwendokasi wa gari,alipomtizama Rachel alikua bado amelala hivyo nae hakujua lolote linalojiri.
Baada ya muda kidogo bus lilipaki kwa ajili ya kuruhusu abiria wapate cha kutia tumboni,mchungaji Josiah alimuamsha Rachel aliekua bado amelala kisha wakaenda kupata msosi na kurudi ndani ya gari,muda si mrefu gari nalo lilijiondoa lile eneo na kuendelea na safari ya kuelekea jijini mbeya,shibe na uchovu vilimlemea mchungaji Josiah na sasa ikawa ni zamu yake
kulala,usingizi mzito uliombeba ulimpeleka mpaka kwenye ardhi ya ndoto ya ajabu isiyopata kusemeka,alijiona yupo kwenye giza zito nene na hajui pa kuelekea,miguu yake iliyokanyaga chini ilihisi baridi kali na kufanya mwili wake uitike kwa mtetemeko,moshi mzito ulimzunguka na kumfanya akohoe huku akihangaika kuitafuta pumzi kwa hali na mali ilhali moyo na akili yake vikishika kasi ya uoga,alikohoa na kukohoa,alikohoa mno mpaka kifua kikaanza kuita kwa maumivu!! Alikohoa mpaka
macho yakaanza kububujika machozi na kuhisi kichomi!! bado kikohozi hakikukoma hata kidogo,aliendelea kukohoa tena zaidi na zaidi mwishowe akaanza kukohoa damu!!! Mapigo ya moyo yalienda sawa na mbio za farasi wa mashindano,mzunguko wa kasi wa damu ulifanya baridi alilokua nalo lipotelee,joto liingie na kuruhusu vijasho kuchuruza mpaka sehemu za siri,kila alipojitahidi kuzuia kile kikohozi ule moshi ulizidi ongezeka na kumpalia hivyo kutompa machaguzi,mishipa ya uso ilimsimama
na koo nalo likaanza kuuma!! Koh!-koh!-koh!-koh!-koh! Bado alizidi kukohoa!!….mchungaji Josiah alianza kushindwa kumudu mwili wake,mkojo ulianza kumchuruza na kufanya nguo yake ya ndani kuwa tepetepe,bado kikohozi hakikukoma wala kupungua kasi!! alitia huruma na imani mno kwa jinsi alivyokua anahangaika,alishindwa kabisa kusimama kwani miguu ilikwisha nguvu hivyo akapiga magoti na kuendelea na lile zoezi la kukohoa tena sasa akihisi mkono umemkaba shingo!!! alizidi kutoa damu na
kutapatapa mpaka pale alipoisikia sauti nzito isiyojulikana imetokea wapi ikimwambia RUDI ULIPOTOKA!!!! kisha kufuatiwa na kicheko kikali cha kishetani!! Ha!-ha!-ha!-ha!-ha!-ha!-ha! Baada ya hayo maneno mchungaji Josiah alishtuka toka kwenye usingizi huo mzito kwa pupa na kuwastua abiria wengine waliokuwepo karibu ikiwemo Rachel alie jirani.Rachel kwa tahamaki alimuuliza mchungaji… “vipi mtumishi,kuna nini???”
mchungaji Josiah alishindwa kujibu,alionekana akihema kwa pupa huku akipepesapepesa macho kushoto na kulia kuhakikisha mazingira aliyopo,baada ya kutulia kidogo ndipo alipoanza kumuhadithia Rachel kile alichokiona kwenye ndoto,Rachel alishtushwa pia na zile habari na kumtaka mchungaji Josiah wasali ili mungu atie mkono katika safari yao,walishindwa kuwashirikisha watumishi wenzao kwani walikua usingizini,wakiwa katikati ya sala walisikia sauti kali za abiria kisha ukafuata
mlio mkali Puh!!!! presha kali iliwasukumiza mpaka mbele na kujigonga kwa nguvu!! gari liligonga!!….muda si muda gari nalo likaanza kubiringita kwa nguvu!!! Vilio vya maumivu na uoga vilitawala ndani ya gari!! Baada ya dakika kama tano gari lilitulia huku bado vilio vya baadhi ya abiria vikiskika kwa nguvu vikiomba msaada,wengi wao walikua kimya huku miili yao ikivuja damu,wengine walionekana wakilia huku wakigusa sehemu waliyodhurika au kujeruhiwa,watoto wadogo wawili wenye miaka si
juu ya mitano walionekana wakiwa wamelaliwa na gari hivyo sehemu kubwa ya miili yao ikawa imesagika,haikuhiaji utaalamu wowote,walikua wamekufa,hamaki mmama mmoja mjamzito alionekana tumbo limepasuka!! Ilitia huruma na ilisisimua kwa kutisha!! Damu iliyomwagika ilifanya nyasi zote zilizokuwepo kuwa nyekundu,lile eneo lilikua kama machinjioni!! Huku akijikokota taratibu kutokana na maumivu mazito aliyokua anapata mchungaji Josiah alipata kuita kwa taabu..”Reeecho!!” hakuna aliyeitika,nae muda si muda alipoteza fahamu!!
“Reeecho!!” hakuna alieitika,nae muda si muda akapoteza fahamu!! Watu waliokaribu walianza kusogelea eneo la tukio huku wakitoa macho kwa kutoamini,wengi wao walishika vichwa na sura zao zilionekana zenye huzuni na masikitiko makubwa,dhahiri lile tukio liliteka hisia zao mno kwani macho yao hayakuwahi kushuhudia ajali mbaya kama ile.Shughuli za uokoaji zilichukua Nafasi,wakazi wa yale maeneo walionekana kujitolea mno kutoa miili ya watu iliyokwama ndani ya gari ambayo mingi ilipoteza uhai na kuharibika vibaya,ilikua ngumu kuitambua kwa urahisi kutokana na kuchakazwa na ajali,palinuka damu lile eneo na pia vilio vya baadhi ya walionusurika kufa na washuhudiaji vilevile vilitawala,ilikua ni zaidi ya msiba.
Ilichukua kama dakika hamsini na tano kwa ambulance ya hospitali kuu ya Iringa kufika eneo la tukio,udogo wa ambulance hiyo ulifanya zoezi liwe gumu hivyo wengi wao waliozidiwa walipoteza maisha ukizingatia na umbali uliokuwepo mpaka hospitalini,zoezi lile lilidumu mpaka saa mbili ya usiku ambapo ndipo taarifa ziliposambaa na kwenye vyombo vya habari juu ya ajali hiyo mbaya
kuwahi kutokea,ilimshangaza kila alieshuhudia na pia kila alieisikia,hofu kubwa ilitanda mioyoni mwa watu waliohisi eidha ndugu jamaa na marafiki walipanda lile gari kwani taarifa zilionesha kuwa ni idadi ndogo ya watu iliyopona ukilinganisha na ya waliobakia majeruhi,miongoni mwa hao watu alikua ni Askofu Emmanuel aliezipata hizo habari kwenye breaking news ya Redio moja maarufu,alichanganyikiwa mno kwani alijua fika watumishi wake walipanda lile gari,aliwajulisha wenzie na mkakati wa kuelekea
hospitali kuu ya Iringa ulipangwa ufanyike haraka iwezekanavyo kesho yake asubuhi kwa kutumia gari la Dayosisi. Mochwari ya hospitali kuu ya Iringa ilijaa hivyo baadhi ya maiti zilifunikwa tu na kuachwa mawodini,ilikua siku bize sana kwa wauguzi wachache waliokuwepo pale,hata pia madaktari wengine ambao hawakua na zamu na walio likizo waliitwa kazini wasaidie jahazi,bado walikua wachache mno kukidhi matakwa yote.
Mchungaji Josiah bado fahamu hazikumrudia,kichwa chake kilizungukwa na bandeji nzito iliyoshiba nyeupe huku sindano ya dripu ikipenyeza dawa mwilini mwake,uso wake ulionekana umejaa kutokana na kuvujia damu hata mikono yake vilevile ilivishwa P.O.P,alikua ndani ya wodi ya wanaume sanjari na David isipokua tu Rio alieaga dunia kutokana na kupasuka fuvu la kichwa,upande wa wodi ya wanawake bibie Rachel alikua hana hali nzuri pia,mashine ya kupumulia ilijaza uso wake kutokana na mfumo wa upumuaji kushindwa kufanya kazi baada ya uvunjikaji wa mbavu,vilevile mguu wake wa kushoto ulivunjika,alitia huruma.
Wakati mchungaji Josiah akiwa bado hajarudi katika hali yake ya ufahamu alipata kuota tena kwa mara ya pili,sasa hivi alijiona amekaa na Rachel pembeni wakiteta jambo,matabasamu yaliyopendezesha nyuso zao ziliashiria ya kwamba walichokua wanaongelea kiliwakonga nyoyo,kila mtu alifurahi na dhahiri stori zilikua zinasonga vema.Ghafla Josiah alihisi ameshikwa begani na
mtu tokea nyuma,alipogeuza shingo yake kutizama ni nani aliefanya hivyo hakuona kitu na hata uso wa Rachel ulionyesha hauna habari na lile tendo,aliamua kupotezea na stori kama kawaida zikaendelea,kale kamchezo bado hakakukoma! alihisi tena mkono umemgusa begani kwa mara ya pili na alipogeuka hakuona kitu tena!! alianza kupata hofu,alipomtonya Rachel juu ya hilo alipuuzia
na kumwambia ni stress tu hizo hivyo kufanya mchungaji Josiah atulie tena ila kwa imani ndogo na hofu ya kuonekana muoga mbele ya mwanamke,baada ya dakika mbili tatu ule mchezo uliendelea!!….mchungaji Josiah alihisi mkono umemgusa tena begani,alipogeuka haraka kuangalia hakushuhudia chochote!!…akili yake ikamtonya kwamba pale si pa salama,alimuambia tena Rachel juu ya hilo na sasa wakalichukulia jambo serious,waliinuka na kuanza kujiondoa lile eneo,wakiwa njiani walihisi watu
wanaongea na kucheka nyuma yao ila kila walipotizama hawakuona chochote!!..tendo hilo lilizidi kujirudia na kuwatia uoga maradufu,mbio zilianza huku wakiwa wameshikana mikono! Kila mara waligeuka geuka nyuma kutizama kama wanafuatwa,japokua hawakuona kitu ila bado sauti za watu zilifika masikioni mwao!! kitendo hicho cha kutizama tizama nyuma mara kwa mara kulifanya Rachel ajikwae na kumpa Josiah kazi ya kumdaka,cha kushangaza Rachel alipounyanyua uso wake
ulionekana si wa Rachel yule ajulikanae,macho yalikua makubwa na meno yalitokeza nje kama mamba!!! Uso wake wa maji ya kunde ulikua mweusi kama mkaa na masikio yake yakawa marefu kama punda!!! Mungu wangu! mchungaji Josiah aliyatoa macho kwa kushangaa,bila kujiuliza mara mbili mbili alianza kukimbia kwa kasi toka pale Rachel alipo,katika hali isiyo ya kawaida Rachel aliebadilika sura alikua anamkimbilia Josiah huku akilalamika kwanini anamkimbia kwa sauti yake ileile halisi!! Ghafla mchungaji Josiah alizinduka toka ndotoni huku akipiga makelele makubwa na kustua watu waliopo mule wodini!!! *
ilibidi muuguzi aje haraka kumjulia hali,Josiah alionekana akigugumia kutokana na maumivu makali aliyokumbana nayo,kichwa chake kilichofungwa bandeji kililemewa na maumivu vilevile mkono uliofungwa P.O.P ulimvuta bila kusahau uti wa mgongo,alitulia kitandani kama alivyoelekezwa na muuguzi ya kwamba anahitaji mapumziko,ila
kabla ya muuguzi kuondoka Josiah aliomba jambo fulani lililodhihirisha ya kwamba fahamu zimerudi mahala pake,huku akivumilia maumivu aliyokua anayapata alimwambia yule muuguzi akamuangalizie mwenzie ambae ni
Rachel huku akiambatanisha na maelezo ya mtindo wake wa nywele alionao na nguo aliyovaa,bila kinyongo yule muuguzi alilipokea lile ombi,alimtaka Josiaha apumzike wakati yeye akienda kulitekeleza hilo,roho ya Josiah sasa ikawa imetulia huku ikisubiria taarifa kwa hamu kubwa isiyoelezeka. * * Mwanga uliochipukia baada ya wale viumbe wauwaji kufa iliwawezesha wanakijiji kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo ujenzi,nyumba za wakina Madhifa zilijengwa kwa ushirikiano mkubwa wa wanakijiji,nyumba ya mzee Patili vilevile.Ilikua ni saa tatu ya usiku hivyo mwanga ulishamezwa na giza,kila mwanakijiji alikuwemo ndani ya kiota
chake akiendelea na shughuli mbalimbali hivyo kufanya huko nje kua kimya! hakuna kilichoendelea huko nje zaidi ya upepo wa taratibu kutikisa matawi ya miti na kutengeneza sauti fulani,milio ya bundi nayo ilipamba tukio. Julina alikua ndani kwake akimnyonyesha mwanae wa pekee aliebeba tumaini la watu huku akimchezeachezea
mashavu na kumfanya mtoto atoe tabasamu la kupendeza,furaha ya mtoto ni furaha ya mama hilo lilionekana kwani kila mwanae alipotabasamu nae alishindwa kulizuia la kwake,alisahau kabisa upweke aliokua nao kwa kutokuwepo mume wake,kila alipotizama sura ya mwanae mwenye afya alipata amani na furaha moyoni kwani ndicho kitu pekee alichokua nacho kwa sasa,furaha yake iliingia dosari pale tu masikio yake yalipoisikia hodi
tokea mlangoni,asili yake ya uoga ilimfanya achungulie dirishani kuhakiki ni nani,alipogundua ni mama Halima alimfungulia mlango hasa ukizingatia ujenzi uliofanyika mchana ulifanya nyumba yake iwe katikati ya nyumba za wanakijiji hivyo hofu kuwa adimu kwake,vijistori vya hapa na pale viliendelea kati ya Julina na mama yake wa hiari
mama Halima,baada ya muda kidogo Julina alimkabidhi mama Halima mtoto wake ili aweze mpakulia japo chakula atie sunna,ilikua ni kosa kubwa!! Mama Halima hakua mama Halima aliedhaniwa,mama Halima halisi alikua yu nyumbani kwake akipika chakula,baada tu ya mama Halima yule feki kupewa yule mtoto alijiinua taratibu
huku akizuga kumbembelezabembeleza na kumuimbia nyimbo za kikabila mtoto alieonekana kumkataa kabisa kwa kulia kwa sauti kubwa huku akirusharusha mikono,hali ile ilimshangaza kidogo Julina kwani mwanae hana tabia hiyo ukizingatia huwa anatulia tuli akibebwa na mama Halima,hakulichukulia kwa uzito hilo jambo hivyo
aliendelea kupakua wali kwa ajili ya mama Halima,alipomgeuzia mgongo tu yule mama Halima feki aliutumia ule mwanya kuufungua mlango taratibu huku akinyata na kutoka nje na mtoto!!! Julina alihisi sauti ya mtoto wake anaelia imefifia hivyo aligeuza haraka shingo yake kutizama,moyo wake ulikita puh!!! Hakumuona mwanae na masikio yake yalizidi kusikia sauti ya mwanae inazidi kufifia!! haraka alitoka nje huku akipiga makelele ya nguvu
yaliowashtua wanakijiji!! makelele yake na ya mwanae aliekua anakimbizwa na yule mmama yalitosha kabisa kuwatoa wanakijiji nje ya nyumba zao, haraka habari zilisambaa na haraka wanaume walianza kumkimbiza yule mama aliekua amemshikilia mtoto huku akiwa na sura ya mama Halima!! mikono yao ilishika silaha mbalimbali za
jadi tayari kwa ajili ya kupambana kumuokoa mtoto alie tegemeo kwao!! wanakijiji waliobakia walishikwa na simanzi kubwa,walimshirikisha mungu wao kwenye sala awasaidie lolote baya lisije likajiri kwani ni dhahiri walifahamu ya kua endapo yule mtoto akipotea basi hawana budi,watakua chini ya utawala wa CHERNOBOG,yani mungu mweusi! Nini kitakachojiri? Jasho jembamba la hofu lilitirika! * Baada ya mchungaji Josiah kurudishiwa majibu kwamba Rachel yu hai moyo wake ulijawa na furaha,alimuona pia David pembeni yake hivyo hofu yake ikawa ni kwa Rio ambae hakumtia machoni,saa nne usiku juu ya alama ikawadia.
Wodi ilikua kimya mno,macho ya mchungaji Josiah hayakua na usingizi hata kidogo kutokana na kulala mno ndani ya basi hivyo yalikua tu yakipepesapepesa vitanda mbalimbali vilivyopo,baada ya muda kidogo Josiah alitekwa na mawazo mazito,mawazo hasa juu ya ndotoa alizoziota ile siku,alitafakari sana lakini hakupata jibu la ndoto hata
moja hivyo akakosa amani.Huku bado akili yake ikiwa inabarizi ndani ya kisiwa cha mawazo alihisi mlango wa wodi unafunguliwa! Ukimya uliokuwepo ulifanya sauti ya mlango kufika vizuri masikioni mwake,haraka alirushia macho kwenye ule mlango!! Baada ya mlango ule kufunguliwa hakuna mtu aliyeingia,ulikua unaenda tu mbele na kurudi nyuma ukisindikizwa na sauti za malalamiko,moyo wa mchungaji Josiah ulitokota kama maji mafigani na alipotizama ni nani mwingine anashuhudia hakuona mtu! Wote walikua wamelala na wengine walikua washakufa,alimeza mate,sala fupi ya kuwa salama ilifuata kimoyonimoyoni.Kila alipojitahidi kupotezea lile swala alishindwa! Aliuona usiku ni mrefu,kuinuka na kwenda kuangalia pia alishindwa kutokana na majeraha aliyonayo hivyo alibakia tu na gubu moyoni.Ule mchezo wa mlango kufunga na kufunguka wenyewe ghafla
ulisimama,mchungaji Josiah akakazia macho kuangalia kunani,hakuna kitu kilichoendelea ila kwa mbali sauti ya nyimbo ilianza kusikika,nyimbo isiyoeleweka inanena lugha gani! Wala nyimbo isiyoeleweka ina maanisha nini! Mara ya kwanza mchungaji Josiah alidhani masikio yake yanamdanganya ila alivyozidi kuisikia ile sauti ndipo alipoamini ya kwamba asikiacho ni sahihi,haikutosha hiyo tu…sauti ya kugonga gonga ilisikika toka juu ya paa!! nini hiki?? Mchungaji Josiah alijiuliza,sauti ya nyimbo za ajabu na za kugongwa paa zilizidi kumchanganya na kumuogopesha,imani yake ilianza kuterereka.Baada ya muda kidogo zile sauti
zilikoma,hazikusikika tena hivyo kuruhusu ukimya utawale na mchungaji Josiah kupumua,kuisha kwa kioja kile ulikua ni mwanzo wa kingine,sauti za miguu ikitembetembea ndani ya wodi ilianza kufika vema katika masikio ya Josiah,mungu wangu!!…mwili ulianza kusisimka na moyo ukaanza kudunda kama kitenesi pale alipohisi ile sauti ya miguu itembeayo inakaribia kwake!!…mchungaji Josiah alijifunika na shuka gubigubi kwa uoga asione kitakachoendelea huku joto na hofu vikimmimina jasho vya kutosha,mkono ulimgusa mgongoni na sauti ya kike ikaskika.. “kaka! nini shida??” * * * Jitihada za wanakijiji kumkimbiza yule mmama zilianza kuzaa matunda,ni hatua chache tu zilisalia ili wafanikishe lengo la kumkamata aliemuiba mtoto,yule mmama baada ya kuona anazidi kukaribiwa na wale wanaume alianza kuhofia usalama wake hivyo alimrusha mtoto huko!! wanaume wanne waliokua wanamkimbiza walisitisha lile zoezi na kwenda haraka kumtizama mtoto na kumuachia upenyo yule mmama wa kupotelea maporini,walimuinua yule mtoto na kuanza safari ya kurudi kijijini kwao,kitendo cha kumuokoa yule mtoto kilikua ni cha faraja mno kwao na hata wanakijiji walilifurahia hilo kwa kiasi kikubwa! matumaini yao yaliyopotea
yalirudi mahala pake na hapo ndipo mtoto alipopewa jina,akaitwa RENZO ikimaanisha TUMAINI kwa kilugha chao. Baada ya furaha ya muda juu ya lile jambo wanakijiji walirudi tena majumbani mwao,ulinzi wa yule mtoto haikua tu inamhusu Julina bali kila mwanakijiji hivyo walihamasishana juu ya hìlo,vikoroboi vilizimwa na vitanda vikalaliwa. Upande wa pili wa kijiji cha Igesambo ambapo ndipo yaliyopokua makao ya jeshi la 666 mambo hayakua mambo!..kushindwa kwa jaribio la kwanza la muda usiosogea na la pili la kumuiba mtoto kulifanya kusilalike wala kusilike,ni dhahiri viongozi wao
walichukizwa mno na lile jambo na ilibidi mipango mizito iundwe,kikao kizito kiliitishwa,wazee watano waliovaa majoho mekundu na meupe walikusanyika na baada ya muda kidogo alikuja mwingine alievalia joho jeusi tii! sura yake ilikua nyeusi na macho yake yalikua meupe,wale wengine watano walisimama na kumuinamishia kichwa yule alieingia na kudhihirisha ya kwamba ni mkubwa kwao,baada ya kufanya hivyo wale wazee wote ikiwemo na yule mkubwa wao waliinama na kusujudu huku wakitaja jina la mungu wao CHERNOBOG,kisha kikao kizito kilichukua nafasi..
“ni kwanini hasa tunashindwa???” aliuliza yule mzee aliekua ameketi kwenye kiti kikubwa akizungukwa na wengine watano,kwa jina Abbadon. “majaribio yetu hayakua na nguvu Oh shalom Abbadon,hivyo yaliweza kupanguliwa kiurahisi na wale binadamu” alijibu mzee wa kwanza kabisa toka kwenye mkono wa kushoto wa yule mkuu wao, “mnashindwaje na binadamu?? mnashindwaje na damu na nyama?? mnataka niambia kwamba wamewazidi akili??” aliuliza tena Abbadon,mzee wa pili tokea mkono wake wa kulia akajibu..
“hatukufanya udadisi wa kutosha ili tuweze fahamu wapi ni nguvu yao na wapi ni udhaifu wao hicho ndicho kilipelekea hasa kushindwa kwetu..” “kipi hasa ni nguvu yao??” “kuna mzee aitwae Patili alie kijijini kwao,ni kikwazo kikubwa kwetu kutokana na kuwa na utaalamu utupao mushkeli!!” “kwahiyo mmeamua kufanya nini sasa??” Abbadon kwa msisitizo aliuliza,mzee mmoja aliekua kimya tokea kikao kianze alinyanyuka taratibu na kusema.. “Oh Shalom Abbadon,mimi kama Alvah mratibu mipango ningependa kuchukua fursa hii kuomba radhi kwa kushindwa kufanikisha majaribio yangu ila ningependa nipewe nafasi ya mwisho na endapo nisipofanikisha lengo nitawajibika” hiyo kauli ilionekana kuwastua wazee wengine na kumpenya Abbadon moyoni,akaendelea “naomba nipewe jaribio la mwisho,jaribio litakalobeba imani yangu kwako Shalom Abbadon na kwa mungu wangu CHERNOBOG..!!!”
Palikua kimya vya kutosha,kila mtu alie kwenye kile kikao alimpa masikio ya uelewa Alvah mratibu wa mipango kama alivyoapishwa mapema tu baada ya uzao wa mungu mweusi CHERNOBOG,huku akijiamini na akiyanyoosha maelezo yake ya msingi juu ya jaribio lingine lifuatalo baada ya yale mengine kugonga mwamba,jaribio lililozito na jeusi,jaribio lililobeba ushindi na
kushindwa,jaribio litakalotabiri yatakayojiri,jaribio lililoshika nyadhifa yake na mwanzo au ukomo wa Mungu wake,ilikua hatari mno na ni dhahiri vita ilitangazwa.Macho ya Alvah yaliakisi mno kile alichokinena,yalikua makali na ya msisitizo vilevile yaliendana na uzito wa lile jaribio alinenalo,huku akinyoosha kidole alipata sema
“kafara ya watu ishirini yahitajika upesi! tuliyoipata leo jioni ilikua ni thelathini tena kwa mkupuo baada ya kupindua basi liendalo jijini mbeya,idadi iliyopelea ni ishirini ili niweze fanikisha lengo,ili niweze fanya jaribio zito litakalotusafishia njia kufikia mafanikio yetu hakika!!”
Abbadon alipata yasikia hayo yote na kumpenya,alimuamini Alvah vya kutosha kwani ni mchapakazi na dhahiri alikua anastahili kile cheo alichokua nacho,japokua alishindwa kwenye majaribio ya mwanzoni bado imani ilikua upande wake,hakukua na mtu aliyeonyesha kutilia shaka alichokinena hivyo kufanya hitimisho lipatikane kwa urahisi na kikao kufungwa ili kuruhusu shughuli za upatikanaji wa kafara za kuongeza nguvu jaribio zifanyike,waliinama na kusujudu kama mwanzoni wakiongozwa na Abbadon huku wakitamka baadhi ya maneno kwa sauti nzito ya kutisha “Oooh…Shalom CHERNOBOG!..eeeehh!…Shalom CHERNOBOG! Ukapate kutwaa!!” kisha kikao kikafungwa kwa kunyunyuzia damu ya mbuzi aliechinjwa muda huohuo. * * Sauti aliyoisikia mchungaji Josiah akiwa ndani ya shuka alilojitwika ilimstua zaidi kwani ilikua inafanana na ile ya muuguzi aliemjulia hali muda si mrefu,hakujibu chochote,mdomo ulikua mzito na alikua anatetemeka mno,moyo uliokua unaenda kasi mithili ya maporomoko ya mto Owen ulikua unaomba mkono wa mungu utanakabali huku akizidi kujikunja kama kifaranga cha kuku kilicholoana na kuachwa na mamae, “kaka vipi kwani???”
sauti tena ileile ya kike ilisikika huku ikiambatana na zoezi la kumgusagusa Josiah alieloa uoga ndembendembe.Bado Josiah hakujibu lolote hali iliyompa mashaka yule muuguzi aliekua anamsubiria atoe kauli, “jamani we kaka kuna nini??”
muuguzi wa watu alievalia nguo ya rangi ya karoti aliuliza tena kiupole,bado Josiah hakujibu chochote ila aliruhusu macho yake yapenye na kuchungulia kupitia shuka lile jepesi na kuhakikisha aongeae,alimuona muuguzi yule mweupe saiz ya katikati akiwa na sare zake zilezile alizokua nazo muda ule,hofu kidogo ikapungua akalishusha shuka lile lililokua limemfunika mpaka kichwani na kumuangalia muuguzi yule kwa macho ya aibu,huku akitabasamu akasema
“za saa hizi dada??” “safi tu kaka,vipi kwani mbona ulikua katika ile hali???” “ah! Kawaida tu dada,ni maumivu tu yalikua yananisumbua kusema ukweli” “maumivu???” “ndio!” “ehh!! wapi panakusumbua kaka yangu??”
“huu mkono mlionifunga hii P.O.P unaniuma sana,kichwa nacho kinanipasua!” “pole sana,usihofu lakini utazidi kupata nafuu kadiri unavyozidi kusonga mbele,cha umuhimu upumzike vya kutosha na usiwe unajikunjakunja kama ulivyofanya kwani utajisababishia maumivu zaidi na hiyo sindano ya dripu yaweza kuchomoka!” “sawa dada,haina shida!!….naa vipi kuhusu yule dada niliyekuagizia mchana,anaendeleaje??” “usihofu yupo sawa tu,sasa hivi anapumzika..”
mchungaji Josiah alitamani yale maongezi yasiishe kwani alijihisi ana amani zaidi kutokana na ule uwepo wa yule mdada,ila yule muuguzi ilibidi aondoke ili akawajulie hali na wengine hivyo alimuaga mchungaji Josiah na kujiondoa lile eneo. * Sauti kali za mbwa na bundi zilipamba usiku ule wa saa saba,mwezi ulikua unang’aa mno kutokana na kutokuwepo kwa mawingu angani na pembeni yake kulikua na nyota mbili zing’aazo,nyota ya upande wa kushoto ilikua inang’aa kupita nyingine hivyo kuashiria ya kwamba kuna litakalojiri,upepo wa baridi nao ulipuliza taratibu na kufanya miti na majani viiname,haikua ya kawaida,nyota ile
ing’aayo zaidi ilizidi kung’aa na kufanya mwanga wake kuwa mkali mithili ya mwezi,hakuna aliyeligundua hilo kutokana na watu kuwa vitandani kwa muda huo na hata baadhi yao waliokua macho sehemu mbalimbali kama kwenye kumbi za starehe na kwenye magari ya masafa marefu hawakulitambua hilo,ulikua ni wakati wa jeshi la 666 kutawala!!!! ile hali yote iliyokuwepo ilikua ni
kionyeshi ya kua usiku ule ulikua ni wa kafara,watu walikua wanatafutwa kwa ajili ya kafara ya kuongezea nguvu jaribio la kumtokomeza RENZO,mtoto pekee alieye kikwazo kwao kuushika ulimwengu,idadi ya watu kama ishirini na tano ikiwa imevalia majoho yenye rangi nyeupe na nyekundu na huku nyuso zao zikiwa na chapa ya 666 walishika njia kuelekea mahospitali yalipo,walianza na hospitali kuu ya Iringa!! Mchungaji Josiah na wenzake waliopo huko watapona??
(mwanga wa giza)
walianza na hospitali kuu ya Iringa!! Hatari ilioje?? Waliingizana taratibu huku wakinyata,kila kilichonenwa na kiongozi wao aliyekua ni mama Marinda ndicho kilichotekelezwa,macho yao yaliyoakisi mwanga wa mwezi yaliwafanya waonekane mithili ya paka! Masikio yao marefu na mjazo wa tarakimu 666 kwenye mapaji ya uso ilizidi kuwafanya waonekane wanyama ukiachilia
mbali na miili yao yenye rangi ya kijivu.Geti la hospitali lililo kuu kuu hata halikuguswa hivyo hamna kelele iliyozalishwa.Miguu yao iliyo peku ilikanyaga chini kiustaarabu huku macho yao yakiangaza angaza huku na kule kiusalama zaidi.Mikono yao yenye kiu ya kutekeleza walichoagizwa ilianza kufanya kazi kwa mlinzi mzee waliemkuta fofofo kwa usingizi.Walimnyonga kama kuku bila
kumpa fursa hata ya kusema lolote,akajazilishia idadi.Macho yao yakaelekezwa kwenye wodi ya wanaume alipo mchungaji Josiah,taratibu wakaanza kujongea huku wakipangana mstari,mbele akiwa mama Marinda kiongozi,walikua wanatisha mno na vilevile walikua wananuka kifo! Hilo ndio jeshi la 666.Mkono wa mama Marinda wenye michirizi ya mishipa na kucha ndefu ulishika kitasa na kufungua taratibu kisha akachungulia,baada ya kurudisha kichwa chake alitoa amri iliyotekelezwa bila ya maswali,waliingia watu watatu,wanaume wawili na mwanamke mmoja wakanyooka mpaka kwenye kitanda cha kwanza
kabisa,walipogundua ya kwamba alielala pale ashafariki waliachana nae na kujongea kwenye cha pili,wakamkuta aliepale mzima ila usingizi mzito umembeba,haraka wakatawanyika na kukizunguka kile kitanda kutokana na idadi yao,wakafumba macho na vinywa vyao vikaanza kutetema maneno fulani ya lugha ya ajabu yenye maana ya kutanakabali kafara yao,mara ghafla yule mtu aliekua amelala pale akatapatapa kama anaenyongwa na baada ya muda kidogo akatulia tuli kumaanisha ashakufa! Mtindo ukawa ni
uleule,wakasogea kwenye kitanda kinachofuatia.Wakati hayo yote yanachukua nafasi mchungaji Josiah alikua hana habari,alikua akikoroma kutokana na usingizi mzito uliombeba na kitanda chake kilikua ni cha sita tokea walipo wale wauaji wa kafara. Macho yakafumbwa tena na sala ya kuitanakabali kafari ikafanyika,mwingine wa kitanda kinachofuata nae akaenda na maji,wale
watu watatu wauaji wakasogelea kitanda kingine kifuatacho wakakuta aliepale kafariki hivyo wakakiruka na kwenda kingine,idadi ya vitanda vilivyobaki ili mchungaji Josiah akutwe vikawa ni vinne tu.Kama kawaida mchezo ukaendelea,mgonjwa aliyekuwepo pale nae akarusharusha miguu kisha akaenda na maji kwa ajili ya kafara.Idadi ya waliouwawa ikawa ni wanne akiwemo mlinzi
aliefungua dimba.Bado haikuwatosha,walisogelea tena kitanda kifuatacho alipo mzee mmoja asumbuliwaye na figo,kitambi chake kilikua kama kichuguu kwani alijifunika na shuka gubigubi akilala chali.Hawakutaka kupoteza muda,kama kawaida waliyafunga macho yao wote na kutetema maneno fulani kwa lengo la kuitanakabali kafara yao,yule mzee akarusharusha miguu yake kuitetea roho yake lakini mwishowe akatulia tuli na mapigo ya moyo yakazizima.Wakasogelea kitanda kingine!!! * * Ndani ya kanisa la Under the God Fontain sala nzito ilikua inaendelea ikiongozwa na askofu Emmanuel Mgaya,wachungaji watano pia walikuwepo kwenye mkesha ule wa dharura ulio maalum kwa ajili ya kumuomba mungu awaweke mikononi watumishi wake waliokumbwa na ajali wakiwa njiani kwenda kumtumikia.Kila aliyekua pale alisema na mungu kwa njia na uwezo wake.Sauti zao pekee ndizo zilizosikika kwa ule muda wa usiku totoro,wakiomba kwa nguvu huku sura na matendo yao vikiakisi ni kwa jinsi gani lile jambo lilivyo serious kwao na jinsi gani linavyowagusa.Miili yao iliyokua ikipata joto kutokana na sala hiyo nzito ilikua inapoozwa taratibu na feni aina ya SOLCE hivyo basi kuwafanya wazidi kudumu kwenye maombezi. * * * Wale watu watatu wauaji waliwadia rasmi kwenye kitanda cha mchungaji Josiah,walikizunguka kama kawaida na bila kupoteza muda walifunga macho yao na kuanza kutetema maneno kama walivyofanya kwenye vitanda vilivyopita.Baada ya muda wakafungua macho yao kutizama majibu,Josiah bado alikua anahema,waliangaliana kwa mshangao kisha wakarudia tena lile tendo kwa uhakiki zaidi.Walipofungua tena macho yao wakamkuta mtu bado mzima,walishangaa sana juu ya hilo huku wakijiuliza ni wapi wamekosea,wakiwa wamepigwa bumbuwazi walisikia sauti ya makofi tokea kule mlangoni iliyowaashiria ya kwamba wanaitwa,wakageuza na kuanza kukimbia kuelekea langoni na kisha kupotelea kabisa.Josiah alishtushwa na sauti na sauti za watu zilizokua zinaishia,alipotizama huku na kule hakuona kitu,muda si mrefu yule muuguzi akaingia mule ndani akiwa na sura iliyojaa uoga.
Simulizi : Msafara Wa Mamba Sehemu Ya Kwanza (1) Siku zote kwenye msafara wa mamba huwa haukosi kenge na mijusi. Msichana Herena bila kutegemea amejikuta akisafiri kwenye msafara wa mamba yeye akiwa kama kenge. Lakini yote ni kutokana na siri nzito ya mama yake ambayo imekuwa majuto kwake, lazima amlaumu mama yake kwa nini hakumueleza ukweli. Ni ukweli gani huo fuatana na mtunzi kwenye mkasa huu wa kusisimua. **** Ni kweli toka nizaliwe nilikuwa simjui baba yangu lakini hiyo haikunipunguzia kitu chochote kwenye maisha yangu. Mama yangu alinilea maisha mazuri kwa kunipa chochote kinachokihitaji, ikiwemo elimu ambayo ni bora katika ulimwengu wa leo wa sayansi na tekinorojia. Nilisomeshwa shule za gharama tokea kindagate mpaka elimu ya sekondari. Mama yangu alikuwa na mapenzi ya kweli kwangu kwa kunilea kama mboni ya jicho lake. Lakini pamoja na kulelewa malezi ya kudekezwa , sikuielewa tabia ya mama yangu kuwa na mabwana tofauti tena wenye pesa. Kila mwanaume niliyemuona nilitambulishwa kama mjomba, mwanzoni sijui ilikuwa akili ya utoto nilijua kweli wale ni wajomba. Lakini baada ya kukua na kupata akili pamoja na mama kuniona bado mtoto nisiyejua chochote. Nilitambua kuwa wale si wajomba bali wanaume wa mama. Hapo moyo ulinishtuka na kumuona mama yangu kama anajichimbia kaburi kwa mikono yake.Yaani kila kukicha mama yangu alibadili wanaume kama nguo, ni kweli Mungu alimjalia umbile na sura ya mvuto. Lakini matumizi yake aliyatumia vibaya ya kuudharirisha utu wake. Pamoja na kutofurahia tabia za mama yangu lakini sikuwa na uwezo wa kumwambia asifanye vile. Kwanza ningeanzia wapi pili ningemuelezaje? Angeniuliza nina uhakika gani na yale niyasemayo ningemjibu nini. Maisha yaliendelea huku na mimi nikiendelea na masomo yangu, wakati huo nilikuwa kidato cha pili. Kutokana na uwezo wangu wa akili nilifanya vizuri mtihani wa kidato cha pili na kufanikiwa kuingia kidato cha tatu. Siku nilipopata matokeo nilirudi nyumbani nikiwa na furaha tele moyoni ya kuweza kuingia kidato cha tatu. Nilipofika nyumbani sebuleni nilimkuta mama akiongea na mzee mmoja ambaye kama sikukosea macho yangu alikuwa mkurugenzi ya moja ya benki jijini. Nilipoingia nilikwenda moja kwa moja hadi kwa mama na kumkumbatia huku nikipiga kelele za furaha “Yoyooo mama nimepitaaa.” “Usiniambieee!” mama alijibu huku akinikumbatika kwa nguvu. “Kweli mama, tena pamoja na rafiki yangu Fatuma.” “Oooh hongereni sana.” “Asante mama,” nilijibu huku machozi ya furaha yakinitoka. “Sasa mwanangu nitakutayarishia zawadi yoyote uitakayo.” “Ooh, asante mama nashukuru, mama unakumbuka ulisema utaninunulia simu ya laki tano?” “Kama nilivyo kwambia ahadi zangu zipo palepale.” “Vipi huyu ni binti yako?” aliuliza yule mgeni. “Ndio…tena wa pekee.” “Mmh! Basi na mimi naongezea zawadi.” “Anko zawadi gani?” niliuliza kwa shauku. “Kwanza nitakulipia kidato cha tatu mpaka cha nne, kisha nitakutafutia shule ya hadhi ya juu ambayo utasoma kidato cha tano na sita kisha kitakutafutia chuo nje ya nchi.” “Usiniambie Anko,” nilijikuta nimemkumbatia Anko kwa furaha bila kujijua. “Usiwe na wasi jione mtu mwenye bahati, leo hii nitakufungulia akaunti kwenye benki yangu, sawa binti?” “Mjomba Mungu akuzidishie.” “Asante.” Kama kawaida yangu nilikwenda chumbani kwangu ambako kulikuwa na kila kitu. Kutokana na tabia za mama hakupenda nitumie sebule zaidi ya kuniwekea vitu muhimu chumbani kwangu. Kama tivii na redio kubwa pamoja na kompyuta. Siku zote nikimaliza kuongea na mama huenda chumbani kwangu na kukutana naye kipindi cha chakula, mara nyingi mama alipenda tule pamoja. Nilikwenda chumbani kwangu na kuendelea na programu zangu za mazoezi ya kompyuta. Nikiwa chumbani kwangu mama alinifuata kunieleza kuwa mjomba wa benki anataka kuniaga. Nilikwenda hadi sebuleni na kumkuta mjomba akijiandaa kuondoka, aliponiona alinisogelea na kunishika kichwani huku akichezea nywele zangu fupi: “Herena kesho njoo ofisini ukitoka shule ili upigwe picha na kukufungulia akaunti yako.” “Sawa Anko, lakini kesho siendi shule mpaka shule itakapofunguliwa kwa ajili ya kujiunga na kudato cha tatu.” “Ooh, vizuri basi kesho njoo na mama yako ili nimpe pesa za malipo ya miaka miwili na wewe ufungue akaunti yako kabisa.” “Asante Anko Mungu akuzidishie,” sikuamini yote aliyokuwa akiyasema niliona kama ndoto. Mjomba huyu alikuwa tofauti na wote ambao walikuja pale nyumbani wengi walinipa pesa si suala la maendeleo yangu. **** Siku ya pili mimi na mama tulikwenda hadi pale kwenye ile benki, tulipokelewa kama waheshimiwa fulani. Mkurugenzi mwenyewe ndiye aliyesimamia kufungua akaunti yangu japo kulikuwa na watu wengi. Baada ya kufungua akanti Anko ambaye nilijua ni mpenzi wa mama yangu alimpa mama pesa ambayo sikujua idadi yake. Tulipotoka pale benki tulikwenda moja kwa moja hadi shule ambapo mama alilipa karo ya shule ya miaka miwili nikishuhudia kwa macho yangu. Baada ya pale tulirudi nyumbani nikiwa na furaha tele na kuwa na uhakika wa maisha yangu kwa kupata elimu mpaka mwisho wa pumzi yangu. Malengo yangu yalikuwa ni kusoma kwa bidii ili nifike mbali kielimu na kuweza kupata kazi ambayo ingenifanya nisiwe mwanamke tegemezi. Moyoni nilijiapiza kamwe sitaifanya kazi chafu kama ya mama ya kutouthamini mwili wake na utu wake. Japo hakuwa na mume lakini alitakiwa atafute bwana mmoja ambaye ndiye atakaye kuwa mume wangu na kujijengea heshima mbele ya jamii. Kwa hali ile niliuapia moyo wangu nitasoma kwa bidii zote na kwa nguvu zangu zote. Nakumbuka siku moja niliporudi nyuimbani kutoka twesheni, sebuleni nilimkuta mama na mwanaume mwingine. Sio siri kwa mara ya kwanza nilichukizwa na kitendo kile cha kukosa heshima na kushindwa kujiheshimu. Ilikuwa ni wiki tu nimepata ufadhiri wa kusomeshwa mpaka mwisho wa maisha yangu. Nilijiuliza kama atatokea Anko wa benki na kuikuta hali ile kungekuwa na usalama kweli au hatima yangu itakuwa nini kama sio kukatishwa kwa huduma muhimu ambazo ndizo ufunguo wa maisha yangu. Kuliko kutegemea kitega uchumi cha mwili. Kwa kweli nilikasikilika sana na kujikuta nikisimama mbele ya mama na yule mgeni kama jini la kutumwa na kuuliza: “Mama huyu nani?” “Aaah huyu Anko Mody,” alijibu huku akinilazimisha nikubaliane na upuuzi wake. “Anafanya nini hapa?” “Herena ni maswali gani, unafikili bila kuwa karibu na watu hawa maisha yetu yatakuwa magumu.” “Mama Mungu akupe mara ngapi, huyu bwana atakusaidia nini?” “Herena hebu toka mbele yangu umefikia hatua ya kunikosea adabu mbele ya wageni au kwa vile nakupenda sana?” “Noooo mama nasema hivi naomba mgeni aondoke sitaki kumuona,” niligeuka mkali kama pilipili. “Herenaaaa! Hebu ondoka mbele yangu sitaki kukuona nitakubadilikia sasa hivi,” mama alinitisha, pamoja na vitisho vya mama sikuwa tayari kuendelea kuuona uchafu ule. Nilijua yule atakuwa wa mfano. Niligeuka na kuelekea jikoni ili nije nimuonyeshe mama mimi ni nani?
Nilikwenda hadi jikoni na kutafuta kisu lakini nilipata kisu kidogo, nilipekua pekua lakini sikufanikiwa kupata kisu kikubwa. Nilipoangalia pembeni nilikutana na sufulia aliyokuwa imejaa maji machafu ya vyombo tulivyolia usiku. Kwa bahati mbaya siku ile mfanyakazi alikuwa anaumwa na vyombo vilinisubiri mimi. Nilibeba lile sufulia la shombo ya vyakula tulivyokula jana yake usiku. Nilitoka nalo hadi sebuleni na kumkuta mama akiendelea kuongea na mgeni wake bila wasiwasi wowote. Bila kuwashitua nilikwenda hadi pale na kumwagia mgeni shombo la uvundo wa samaki na mchanganyiko wa vyakula. Alijaribu kuyakwepa lakini alichelewa shati lote lilijaa ukoko, nilifoka kwa sauti: “Nasema toka la sivyo yatakukuta makubwa,” nilisema yale huku nikielekea jikoni kutafuta chochote cha kumpigia na zaidi ningemuitia kelele za wizi. Nilikwenda hadi jikoni huku nikilia kwa uchungu na kupitia kisu cha mkate na kutoka nacho. Mama aliponiona alipiga kelele akimwambia yule mgeni akimbie. Baada ya mgeni kukimbia nilikitupa kisu chini na kuanza kulia. Mama alinibembeleza huku akiniomba msamaha: “Basi mwanangu nimekosa.” “Mama haya ni maisha gani?” “Basi mwanangu, lakini hawa ndio wanaoendesha maisha yetu ya kila siku.” “Hapana…hapana si kweli, hivi mama mngekuwa na mjomba sijui ba’ mdogo mmoja kama yule wa benki ungekuwa amepungukiwa nini?” “Ni kweli, lakini yule ni mume wa mtu wakati wowote anaweza kukata mawasiliano tutaishi vipi. Kama unavyojua mama yako sina mume sina kazi lakini mwanangu unaishi maisha mazuri pengine kuliko watoto wengi wenye wazazi wawili.” “Yote unayosema sikatai, lakini ulitakiwa kuwa na mwanaume mmoja ambaye atakuwa kama mumeo. Sio kila mwanaume wako mama kwa mtindo huu kuna kupona kweli?” “Mwanangu hiyo ni mipango ya Mungu.” “Mipango ya Mungu pamoja na kujilinda.” “Basi nimekusikia mwanangu nitafanya hivyo.” Kuanzia siku ile pale nyumbani mwanaume mmoja aliyeruhusiwa alikuwa Anko wa benki tu.Wote niliowakuta niliwatoa kama siwajui, huku nikiwaeleza baba amerudi. Waliponihoji alikuwa wapi niliwajibu hiyo siyo juu yao. Lakini toka niliwapiga marufuku wale wanaume, mama naye akawa tena si wa kushinda nyumbani kama zamani. Kila niliporudi nilikuwa simkuti, ilifikia hatua ya kupita hata siku mbili bila kuonana. Kuna kipindi Anko wa benki alipokuja nymbani hakumkuta na simu alipompigia ilikuwa haipatikani. Kweli mzowea punda farasi kupanda hawezi, ilionyesha mama yangu jinsi gani alivyopenda kuwa na wanaume wengi na kuamua kuwafuata baada ya kuwapiga marufuku kuwaona pale nyumbani zaidi ya Anko wa benki. Siku moja nilipokwenda kumtembelea Anko wa benki, siku ile sikumkuta kwenye hali yake niliyoizoea. Alionekana kama mgonjwa kitu kilichonifanya nihoji kulikoni. “Anko vipi unaumwa?” “Herena mama yako ana matatizo gani?” “Kwa nini Anko?” “Yaani nimeisha mfumania na wanaume tofauti zaidi ya watano na kumsamehe, lakini sasa imetosha mimi na yeye tumeisha vunja mkataba,” kauli ile iliushtua moyo wangu na kujikuta nikipiga ukelele wa mshtuko. “Toba! Mbona mkosi huu,” nilisema yale huku nikishika mikono kifuani kwa mshtuko. “Lakini Herena pamoja na kuvunja ukataba na mama yako, bado nitaendelea kukuhudumia kama nilivyo kuahidi. Nimesikia juhudi zako za kumkanya mama yako, hiyo imenipelekea kutositisha huduma zangu kwako. Nitakufanyia kama nilivyokuahidi ila mimi na mama yako inatosha. Herena mimi mtu mkubwa siwezi kuchangia wanuka jasho.” “Ooh! Mungu mkubwa, asante Anko,” nilimshukuru nusra nimalambe miguu. Niliporudi nyumbani nilimkuta mama yupo kwenye hali ya kawaida kama hakuna kitu kilichotokea. Ilionyesha kiasi gani mama yangu jinsi moyo wake ulivyo na sugu, hakubabaika na kitu wala kuonyesha mabadiliko yoyote. Baada ya shughuli za kutwa nzima na chakula cha usiku, nilikaa na mama na kumuuliza juu ya Anko wa benki. “Mama vipi Anko wa benki?” “Kuhusu nini?” “Eti mmekorofishana?” “Tatizo nini? Huli…huvai….husomi?” “Hapana mama.” “Alinikuta na amenicha, kuondoka kwake sipungukiwi na kitu amenikuta nifurahia maisha na nitaendelea kuyafurahia maisha.” Mmh maneno ya mama yalinifanya niwee mpole kwa kuwa hakuonyesha kubabaika na tukio lililotokea japo kwa upande wangu liliutikisa moyo wangu. Nilimuaga mama na kwenda kulala huku nikilaani kiburi cha shetani cha kumpotosha mama yangu. ****** Siku zilikatika na mama aliendelea na tabia zake za kuuza mwili wake bila kuangalia madhara yake siku za usoni. Anko wa benki na yeye aliendelea kuhudumia bila kinyongo huku akinipa pesa za matumizi ambazo kwa upande wa mama zilikuwa zimekata eti kwa sababu ya kuwatimua wanaume zake. Mama akaanza kuumwa kidogo kidogo, kila tulipokwenda hospitali tulitibu na kupata nafuu. Kuna kipindi hushikika na kulala kitandani na kushindwa kutoka nje. Maradhi yale mama yangu yalimfanya ayumbe kidogo. Lakini mama alikuwa na pesa kidogo benki ilimsaidia kutupunguzia ukali wa maisha. Pesa nyingi alizitumia kwa waganga wa kienyeji kwa kusema amerogwa. Pesa benki zilipoisha, ilibidi na mimi nizichukue nilizoingiziwa na Anko wa benki. Kwa kweli pesa zilikuwa nyingi kidogo, ambazo zilitusaidia kupunguza makali ya maisha ikiwa pamoja na kumsaidia kulipia malipo ya waganga pamoja na dawa alizoagizwa kununua. Alipopata unafuu kidogo alitoka kama kawaida yake. Lakini kila alipokuwa akitoka alirudi asubuhi akiwa hoi na kunisababishia nisiende shule ili kumuhudumia. Kutokana na hali ya mama kumzidia kila akienda kulala nje, nilimshauri ajipumzishe ili kuangalia hali yake. Nilishukuru Mungu mama yangu alinisikiliza na kuamua kutulia nyumbani. Mabwana walipomfuata niliwafukuza kama wizi, japo mama aliniomba niwaache waingie ndani. Kusikuwa tayari kukubali uchafu ule kutokana na wao kusababisha mama na mjomba wa benki kuachana. Kila nilipomkumbuka mjomba wa benki roho iliniuma sana. Lakini ningefanya nini kwa vile ni mtoto mdogo kila nitakacho mweleza atakiona cha kitoto. Kwa kweli pamoja ya ugumu wa maisha sikuwa tayari kukubali kuwaona wanaume wa mama ndani kwetu. Mama alinikubalia kwa shingo upande, nami sikulegeza uzi wa kuhakikisha hali ya mama yangu inaimalika. Namshukuru Mungu kipindi kile nilikuwa likizo muda mwingi nilikuwa karibu ya mama. Faraja nyingine niliyoipata ni kutokana na kukuta akiba yangu Anko wa benki ameniongezea. Nilikuwa sina budi kumfuata kazini kwake kumshukuru. Aliponiona alifurahi sana kwa kwenda kumtembelea, aliniuliza hali ya mama. “Herena vipi mama yako yupo?” “Yupo, lakini alikuwa akiumwa” “Oooh mpe pole, anaendeleaje?” “Sasa hajambo kidogo.” “Na tabia zake?” Mmmh lilikuwa swali gumu, lakini nilijilazimisha kujibu.
“Kidogo ametulia.” “Una uhakika gani?” “Siku hizi muda wote yupo nyumbani.” “Labda sababu ya ugongwa.” “Hapana sasa amebadilika,” nilimtetea mama ili Anko alirudishe moyo kwa mama. “Unajua nini Herena?” “Hata Anko?” “Yaani mama yako amenichanganya sana, nilikuwa nina mipango mizuri sana kwenu, hasa wewe.” Kauli ile iliuumiza moyo wangu na kujikuta nikimlaumu mama kwa tamaa zake za muda mfupi, nilijikuta nikijibu kwa sauti ya unyonge. “Ndiyo hivyo tena sina jinsi, akili za mtu haziazimwi.” “Lakini Herena kuna kitu nimekuandalia kizuri sana.” “Kipi hicho Anko?” nilijikuta nikiuliza kwa shauku kujua nini ameniandalia. “Taratibu Herena, utakijua siku si nyingi.” “Sawa Anko nakisubiri kwa hamu kubwa.” Niliagana na Anko wa benki na kunipa pesa za matumizi laki mbili. Yaani sikuamini ukarimu wa Anko, nilitamani kama angekuwa baba yangu mzazi. Nilijikuta nikitembea barabara nzima huku nikilia na kutamani kumjua baba yangu. Nilifika nyumbani macho yamenivimba kwa kulia njia nzima, hata dereva wa teksi alinishangaa na kutaka kujua kulikoni. Lakini nilimdanganya mama yangu ni mgonjwa na nilikuwa natoka kwa baba. Nilipoingia ndani mama alishtuka kuniona nikiwa kwenye hali ile, alinikimbia na kunihoji kutaka kujua kulikoni?. Nilijikuta nikijitupa chini na kuendeleza kilio, kilicho mchanganya mama. “Herena mwanangu umekuwaje?” sikumjibu niliendelea kulia huku nikigaagaa chini. “Vipi umeibiwa?” “Heri ningeibiwa.” “Sasa umekubwa na maswahibu gani?” “Mama baba yangu ni nani?” nilimuuliza bila sauti ya kilio ilikuwa sauti kavu inayohitaji jibu sahihi. “Herena nini?” mama aliniuliza kama hakunisikia vizuri. “Mama namtaka baba yangu.” “We mwana yameanza lini?” “Leo.” “Kwani tatizo nini?” “Tatizo ni kwamba namtaka baba yangu, kila mmoja ana baba na mama heri baba yangu ningejua amekufa ningejua moja” “Herena mbona mwanangu unanipa kazi nzito.” “Mama kunieleza baba yangu ni fulani hiyo ni kazi nzito?” “Mmh! Mwanangu sijui nianzie wapi?” “Mamaa uanzie wapi kivipi au sio mtoto wako uliniokota?” “Mwanangu wapi unakoelekea huku?” “Kuna ugumu gani kunieleza baba yako fulani, kama huwezi ni wazi mimi si mwanao.” “Herena naomba suala la baba yako uliache kama lilivyo.” “Hapana mama kuna umuhimu kumtafuta baba na mama yangu wa kweli.” “Herena mwangu kwa haki ya Mungu mimi ni mama yako mzazi.” Mama alijiapiza miungu yote. “Kama wewe ni mama yangu baba yangu ni nani?” Mama kabla ya kujibu aliinama kwa muda, mara nilimuona akidondokwa na machozi. Japo sikupenda kumuona mama yangu hata siku moja akitokwa na machozi kwa ajili yangu. Lakini kwa suala lililokuwa mbele yangu sikuwa na huruma kwa mama zaidi ya kuelezwa ukweli. Nilimuacha mama alie na akimaliza anieleze ukweli juu ya mzazi wangu wa kiume yupo wapi. Mama alitulia kwa muda huku akiendelea kububujikwa na machozi. Baada ya kulia kwa muda alinyamaza na kuvuta kamasi nyepesi. Kisha aliniangalia kwa jicho lililokuwa jekundu na kuanza kuvimba, sio siri nilimuonea huruma mama yangu hasa kutokana na hali aliyokuwa nayo. Baada ya kuniangalia aliniita jina langu “Herena.” “Abee mama.” “Mwanangu kwa nini leo umeniuliza neno hili?” “Mama hivi kuulizia juu ya baba yangu kuna ubaya? Roho uniuma kila niwaonapo wenzangu na baba zao. Vilevile naamini kama baba yangu angekuwepo aibu hii isingetokea.” “Herena mwanangu kwa ukweli wa moyo wangu baba yako simjui.” Kauli ya mama ilikuwa ya kuchekesha lakini kwangu ni kama kuupasua moyo bila ganzi “Eti nini?” nilimuuliza nikiwa nimemsimamia mbele kama jini la kutumwa. “Ni kweli kabisa mwanangu baba yako simjui.” “Mama yangu mbona unanichekesha, baba yangu humjui mimba yangu ilijitunga?” “Herena mwanangu japo sikutaka ulijue hili ambalo linaweza kuupokonya moyo wako furaha ya kila siku. Ndio maana nilikubali niadhirike mwanangu, lakini nihakikishe unaishi maisha yenye furaha na kutopungukiwa na kitu,” mama alimeza mate kisha aliendelea. “Herena mwanangu maisha niliyoishi mama yako sikupenda hata siku moja mwanangu uyajue, lakini sina jinsi zaidi ya kukueleza ukweli. Herena mimi mama yako nimefikia kufanya kazi hii baada ya kuikimbia elimu na kuyakimbilia maisha. “Ukweli mama yako nimeacha shule nikiwa darasa la sita, baada ya kudanganywa na mwanaume mmoja aliyenitoroshea mjini. Mwanzo nilijua mama yako nimepata, kutokana na kuishi maisha mazuri tofauti na ya kijijini. Mwanangu kumbe bwana yangu alikuwa ni jambazi. Siku moja nikiwa ndani nimekaa kwenye tivii, niliona picha ya jambazi lililouawa. Picha iliposogezwa karibu, mwanangu nilichanganyikiwa. Kibaya zaidi pale sikuwa nawajua ndugu zake, sikutaka kujitokeza. “ Bwana yangu alizikwa na jiji, nami eneo lile sikuweza tena kukaa kwa kuhofia macho ya watu. Vilevile nilijua lazima wana usalama watataka kujua siri zaidi ya mume wangu. Nilihama usiku usiku na kuhamia sehemu ya mbali ambako nilikuwa sijulikani. “Huku niliyaanza maisha nikiwa peke yangu, japo ilikuwa peke yangu sikuona tatizo lolote kutokana na hawara yangu kuniachia pesa nyingi. Kwa kweli sikupungukiwa na kitu na kujiona nitaishi maisha yoyote niyatakayo . Niliyaishi maisha ya kuitanua na kwenda kumbi zote za starehe wakati nikiwa na baba yako huyo.” “Ina maana ndiye baba yangu?” nilimuuliza mama “Hapana kwa vile nilishea naye mwili ni baba yako.” “Nimekuelewa, endelea.” “Basi mwanangu kama ujuavyo mali bila daftali huisha bila habari na bandu bandu humaliza gogo. Pesa ziliisha taratibu bila kujua kuja kushtukia pesa zimekwisha na mimi ndio hivyo sikuwa na mradi hapo ndipo mama yako nilipoingia kwenye kazi ya kutumia mradi wa mwili wangu. “Aliyenifundisha ni shoga yangu ambaye tulikuwa majirani mwanangu japo kazi ilikuwa ya kunidhalilisha lakini ilikuwa inalipa na kunipunguzia ukali wa maisha. Kutokana na kutembea na wanaume wengi nilijikuta nashika ujauzito na aliyenipa sikumtambua. “Hiyo ndiyo iliyokuwa mimba yako, kwa kweli mpaka leo baba yako simjui mimba yako niliipata kwenye ukahaba. Mimba yako kidogo initoe roho baada ya kujaribu kuitoa bila mafanikio. Ukweli Mungu hakupenda nikuue bila sababu, baada ya kushindikana nilikubali kuilea na kufanikiwa kujifungua salama. Kutokana matatizo niliyokumbana nayo niliamua kukitoa kizazi.” Kufika hapo mama aliinama na kububunikwa na machozi kisha alijifuta na kuendelea kunipa simulizi nzito. Roho iliniuma sana kwa kujua mimba yangu imepatikana kwenye biashara ya mwili hivyo kushindwa kumjua baba yangu. “Basi mwanangu, baada ya kujijua sina kizazi nilihamishia mapenzi yangu yote kwako. Nilihamishia nguvu zangu zote kwako kuhakikisha unapata maisha mazuri elimu bora ili usijeishi maisha niliyoishi mama yako.” Mama alitulia kama anawaza kitu kisha aliendelea kunipa simulizi ambazo kwa upande wangu zilikuwa sawa na kuupasua moyo wangu bila ganzi. Sijui maumivu yake yako vipi ukiyapimia, nilishindwa kulia kutokana na kumuonea huruma mama yangu kwa simulizi yake ambayo hakupenda niijue.
ILIPOISHIA: Mama alitulia kama anawaza kitu kisha aliendelea kunipa simulizi ambazo kwa upande wangu zilikuwa sawa na kuupasua moyo wangu bila ganzi. Sijui maumivu yake yako vipi ukiyapimia, nilishindwa kulia kutokana na kumuonea huruma mama yangu kwa simulizi yake ambayo hakupenda niijue. SASA ENDELEA… Mashavu ya mama yalibeba michirizi ya machozi na macho yake yalikuwa yamevimba na kuwa mekundu kwa kulia kilio cha kwikwi kilichoambatana na simulizi. “Mwanangu sikupenda hata siku moja uijue historia hii najua lazima itaujeruhi moyo wako na kukufanya upoteze mwelekeo wa maisha yako. Sitajisikia furaha pale nitakaposikia amevunjika moyo wako aliouonyesha katika masomo… Mwanangu Herena japo sipendi kuongea habari hizi mbele yako, mama yako nilibweteka na uzuri wangu na kujiona nina rasilimali ya kuweza kunisaidia katika maisha yangu. Mwanangu uzuri umeniponza mama yako.” Kufikia hapo mama alianza kulia na kushindwa kuelewa uzuri umemponza kivipi. Nilitulia tuli huku roho ikiniuma na machozi yalishindwa kujizuia yalitoka bila kupenda, nilimuonea huruma mama yangu. Baada ya kufuta machozi na kamasi nyembamba aliendelea kunisimulia. “Mwanangu uzuri nilionao mama yako nilifuatwa na wanaume kama malkia wa nyuki. Mama yako nilishindwa kuchagua nimkubali yupi kila mmoja alimzidi mwenzie dau. Kwa kweli kila aliyekuja nilimpokea niliweka masirahi mbele. “Muda mfupi mama yako niliweza kuishi maisha nusu ya peponi, huku nikikutunza kama mboni ya jicho langu. Ajabu nyingine mwanangu nilijikuta nimekumbwa na ugonjwa wa ngono wa kutoridhika na mwanaume mmoja. “Mwanangu unashangaa kuachana na Anko wako wa benki, mbona hata mshipa wa fahamu haunigongi. Nimeachana waziri mkubwa serikalini nini nilichokikosa na ndiye aliyenijengea nyumba hii na kuninunulia vitu vyote na benki aliniwekea pesa lukuki. “Tena..” mama alisita kidogo kuendelea kuzungumza na kujifikiria jambo na kuamua kuendelea kunisimulia “Mwanangu japo maneno mengine hupaswi kuyasikia lakini hakuna jinsi kwa vile sipendi kosa nililolifanya unalirudia. Yaani mwanangu vitu vingine mbona aibu yaani sijui nimerogwa ugonjwa gani wa kupenda ngono kupindukia… Anko wako wa Serikalini alinifumania na muuza mchicha.. mmh we acha yaani muuza mchicha mwenyewe pesa nilikuwa nampa mimi,” Mmmh yaani sijui niseme nini nilimuangalia mama yangu na maneno yake kwa kumshusha na kumpandisha bila kupata jibu. Nilijua hakuna ugonjwa bali ni kujiendekeza na matokeo yake kuwa wazoea. “Basi mwanangu kama nilivyo kwambia mama yako nilikuwa kama malkia wa nyuki nilipo achana na Muheshimiwa yule nilipata muarabu mmoja ambaye sikukaa naye sana kutokana na tabia zake chafu ambazo hizo hupaswi kuzijua ila elewa tulishindwana tabia. “ Kwa kweli sikuyumba hata siku moja na maisha yaliendelea kuwa mazuri. Nina imani hata siku moja hukuteteleka katika maisha yako, hata uliponiuliza kuhusu baba yako na kukukanya uliziba mdomo wako. “ Lakini ajabu tabia yako iliyobadilika ghafla tena yenye msimamo ilinichanganya sana. Pamoja na kukutisha hukuonekana kutetereka na msimamo wako ulikuwa pale pale kuhusu kuwafukuza wanaume zangu. Niliweza kusalimu amri na nyumba yangu kwa kweli imerudisha heshima. “Niliamua kufanya mambo yangu nje ya hapa, lakini kwa bahati mbaya nimeandamwa na maradhi. Kwa kweli nilishindwa kutulia nyumbani kutokana mradi wangu wa mwili nisingeweza kutulia nyumbani. Kutokana na sehemu kubwa ya mahitaji yangu kupatikana kwa njia ya kuutoa mwili wangu. “ Sina budi kukushukuru kwa kuweza kunizuia kutoka nje ili kuokoa hali yangu. Kwa kweli nilikuwa siamini hata siku moja kama akili za mtoto zinaweza kumsaidia mtu mzima. Kweli usidharau usicho kijua, ila leo umekuja na mapya ya kutaka kujua kumjua baba yako sina budi kukueleza ukweli. “Naomba unisamehe mwanangu, hiyo ndiyo kweli ila nakuomba mwanangu habari hizi zisikukatishe tamaa”. Mama alinipigia magoti, kwa kweli roho iliniuma na kumuonea huruma mama yangu. Nilimshika mabegani na kumnyanyua, tulikumbatiana kila mmoja alilia na kumlowesha mwenzake machozi. Mama alikuwa wa kwanza kunyamaza na kuninyamazisha mimi, nilinyamaza na kumuomba mama japo maji yameisha mwagika abadilike tabia. Mama alikubali kubadilika ili kuilinda afya yake na kumuomba aende kwa Anko wa benki kumuomba msamaha. Lakini mama alikataa alisema katu hawezi kurudiana na mtu aliyeachana naye. Sikuwa na uwezo wa kumlazimisha, nilimuomba mama tuanzishe mradi ili tuepukane na maisha tegemezi hata kama mjomba atakapositisha huduma zake. Tuliyaanza maisha mapya ambayo japo hatukuwa juu kiuwezo, lakini mama alibadilika kwa kiasi kikubwa. Kwa kweli hata mimi moyo ulitulia japo sikumjua baba yangu na jinsi mimba yangu ilivyopatikana, sikutaka habari zile zinikatishe tamaa. Niliamua kusoma kwa bidii ili kujikwamua na hali iliyokuwa ikija mbele yetu. Anko wa benki aliendelea kunihudumia kama mtoto wake, na hali ya mama iliendelea kuimalika siku hadi siku. Ajabu mama alinenepa na kunawili, wakati huo mama alikuwa amefungua palepale nyumbani duka la kuuza vocha na kupigisha simu pamoja na kuuza mawigi na vitu vya kike. Kidogo ilisaidia kupata pesa ndogo ndogo za matumizi, pesa zote nilizoingiziwa na Anko wa benki niliongezea kwenye duka na kuongezea vipodozi. Lilionekana duka lililoshiba na kuweza kutupatia kipato chenye kutuwezesha kuweka angalau pesa kidogo kwa wiki. Kweli mzowea punda farasi hamuwezi, mama baada ya kupendeza akaanza kubadilika na kurudia tabia yake ya awali ya ukahaba. Kila nilivyo mkanya alikuja juu na kusema yeye anajua zaidi yangu kwa vile ameona jua kabla yangu. Mama alibadilika kwa kiasi kikubwa na kurudi nyumbani amelewa, tabia zile zilinichanganya kwa kiasi kikubwa na kusababisha hata kuyumba kimasomo. Mama hakutaka kabisa kunisikiliza na mara nyingi alikuwa mkali kwa kutotaka kunisikiliza. Siku moja nilikwenda ofisini kwa Anko wa benki, kwa kweli hakunipokea kama ilivyo kawaida. Nilishangaa na kumuuliza kulikoni, aliyonieleza yaliniacha mdomo wazi kwa kusema: Kuwa amekutana na mama yangu kwenye pati akiwa na mkewe yaani mke wa Anko. Mama alikuwa na mwanaume wake, alipomuona alianza kumtukana na kusema pesa zake ndizo zinazo nitia mimi kiburi cha kukosa heshima. Kwa hiyo alimuomba aache mara moja kumihudumia. Mjomba alisema alipata aibu mbele ya mkewe na kusababisha ugomvi mkubwa na mkewe. Kwa hiyo ameamua kusitisha huduma kwangu mara moja. Kauli ile ililivuruga tumbo langu na kunifanya nisikie tumbo la kuhara. Nilimbembeleza mjomba, lakini hakuwa tayari kunisaidia na kuniuliza swali: “Herena.” “Abee Anko,” niliitikia huku nikilia. “Mimi mzazi wako?” “Hapana.” “Nina imani una baba yako, lakini nimeamua kubeba jukumu la kukulea kutokana na tabia zako na juhudi zako kimasomo. Na nilikuwa sikujui bila mama yako na mama yako ndiye aliyenipiga marufuku sasa mimi nifanyeje?” “Hapana Anko naomba unisaidie nitakimbilia wapi?” nilipiga magoti mbele yake. “Herena itakuwa vigumu kama aliweza kunieleza vile mbele ya mke wangu nikirudia si atanifuata nyumbani au hata kusema nimekubaka na kunishushia heshima yangu..Mfuate baba yako.” “Anko, sina baba.” “Mimba mama yako amejibebesha?” “Nilipatikana kwa njia ya kukutana na wanaume tofauti na kushindwa kumjua baba yangu,” ilibidi nijivue nguo mbele ya Anko labda ningepata msamaha, lakini haikusaidia kitu. “Ooh, pole sana ndio hivyo sina jinsi siyo mimi ni mama yako nina imani huenda amekuandalia maisha mazuri ndio maana amekuambia amewahi kuona jua hivyo muachie. Hata ulipofikia hujui pesa alipata vipi, tena sasa hivi analipa. Amerudi kwenye hali yake ya zamani. Utapata baba mpya au yatari ameisha mpata.” Maneno ya Anko niliona sasa yanaelekea kunisimanga, sikutaka kuongeza neno niligeuka na kuondoka. Sikuwa na haja ya kulia japo moyo uliniuma, nilijikaza mtoto wa kike na kurudi hadi nyumbani. Nilipoingia ndani nilimkuta mama na mwanaume wa kizungu walikuwa wakinywa pombe kali, aliponiona alinyanyuka ili anikumbatie. “Wawooo..my Babiiii.” Aliponisogelea ili anikumbatie nilimsukuma na kuanguka chini, sikutaka kumuangalia nilikimbilia chumbani kwangu huku nikilia.
Mama alinifuata na kuniuliza nalia nini, nilimweleza upuuzi wake wote alioufanya kwa mjomba. “Najua amekujaza maneno ya uongo, lakini nataka nikupe habari njema mwanangu.” “Habari gani?” nilimuuliza mama huku nikimtazama macho yaliyojaa machozi. “Umemuona yule mgeni?” “Ndiyo mama.” “Basi yule ni rafiki yangu wa siku nyingi alikuwa amekwenda kwao Ulaya lakini amerudi na kunitafuta na kuniulizia maendeleo yako. Nilimweleza uchungu wako katika elimu, ameahidi kukusomesha mpaka Ulaya.” “Mama huyu ndiye mwanaume wako wa mwisho au bado una tamaa za mwili?” japo swali lilionesha kukosa adabu lakini ilikuwa lazima nimuulize. “Kwa nini unaniuliza hivyo?” “Anaweza kuwa na nia njema lakini akamtibua kama Anko wa benki.” “Mwanangu nimechoka kukutia jaka moyo, sasa hivi natulia ili mwanangu nawe upumzike.” “Mmh! Sawa.” “Basi njoo umsamilie Anko wako.” Nilifuta machozi na kutoka hadi sebuleni alipokuwa amekaa Anko mzungu akinywa pombe kali. Alionekana mtu mwenye maono ya mbali kwa jinsi alivyoniuliza na ahadi alizotoa. “Anko nitashukuru sana.” “Ni bidii yako tu nikuhakikishia kuyabadili maisha yako ili ije umsaidie mama yako, mama yako kanipa sifa zako hivyo itakuwa kazi nyepesi kukufikisha unapotaka na zaidi.” “Nitashukuru sana Anko.” “Jione mwenye bahati katika maisha yako, na kesho tunaanza mipango ya paspoti ili ukimaliza elimu ya sekondari ukasomee chuo Ulaya nchi utakayoichagua na chuo unachokitaka.” Kwa kweli ilikuwa surprise kubwa kwangu baada ya Anko wa benki kujitoa kunisaidia kwa ajili ya maneno ya mama. Kilichoniumiza moyo ilikuwa tabia ya mama ya kutoridhika na mwanaume mmoja. Niliapa kupambana ili kuibadili tabia yake japo tabia ya mtu ni kama ngozi kuibadili ni kazi kubwa. Anko mzungu siku ile alilala pale nyumbani huku akiniahidi kumaliza matatizo yaliyokuwa yakitutatiza. Mama alipewa pesa nyingi mbele yangu kwa ajili ya masomo yangu na kumshukuru Mungu kumrudisha mwokozi. Siku ya pili ilikuwa wiki endi hivyo sikwenda shule, baada ya kufungua kinywa, mama na Anko mzungu walikwenda mjini na kuniacha nyumbani peke yangu nikicheza gemu kwenye laptop ya Anko. Majira ya mchana Anko mzungu alirudi peke yake nilipomuuliza mama yupo wapi alisema alienda kushughulikia masuala yangu ya paspoti yangu. Baada ya kupumzika alikwenda kwenye friji na kutoa pombe kali na kusogea karibu yangu kwenye kochi na kuanza kunywa. “ Herena unatumia pombe?” “Hapana Anko.” “Hata kidogo.” “Ndiyo Anko.” “Jaribu kidogo.” “Hapana Anko sipendi pombe na nimeapa kutokunywa katika maisha yangu.” “Mmh! Sawa, basi kachukue juisi kwenye friji ili kila mtu awe na kinywaji.” Sikutaka kubishana na Anko nilikwenda kwenye friji na kuchukua juisi na kuiweka kwenye glasi na kurudi kuendelea kucheza game. Nakumbuka kuna kipindi nilikwenda msalani niliporudi niliendelea kucheza game huku nikinywa juisi yangu. Lakini ghafla macho yalianza kupoteza nguvu kama mlevi na Anko alinibeba kunipeleka ndani, baada ya hapo kilichoendelea sikujua. Nilishtuka usingizini na kujikuta kitandani kwangu, nilijinyanyua kitandani huku kichwa kikiwa kizito, nilipojiangalia nilishtuka kujiona nimeingiliwa kimwili uonesha nimebakwa. Sikuamini hali ile linyanyuka kitandani mwili wote nikihisi maumivu makali. Nilitoka hadi sebuleni na kuwakuta mama na hawara yake wakiwa wamekumbatiana katika mapenzi mazito. Nilisimama na kuwaangalia kwa muda na kushindwa kuelewa aliyenibaka alikuwa ni yule mzungu au nani. Nilisimama niliwaangalia huku machozi yakinitoka kwa uchungu, wa kwanza kuniona alikuwa ni hawara ya mama, alinyanyuka na kunifuata nilipokuwa nimesimama na kunivutia kifuani kwake na kuniuliza kwa sauti ya chini. “Vipi Helena una tatizo gani?” Sikumjibu nilijitoa mikononi mwake na kurudi nyuma, alipotaka kunisogelea nilimsukuma. Mama alishtuliwa na hali ile na kutaka kujua kwa nini nimekuwa kwenye hali ile. Alinifuata nilipokuwa nimesimama na kutaka kujua kwa nini nipo kwenye hali ile. “Helana mwanangu mbona kila siku huishi vituko, haya tena una nini?” “Mama uliyoyataka yamekuwa,” nilimjibu mama huku nikilia. Mama alishtuka na kutaka kunishika, lakini niligeuka na kuelekea chumbani kwangu. Mama alinifuata nyuma hadi chumbani kwangu, nilipofika nilijitupa kitandani na kuanza kulia. Mama alinisogelea ili kujua nina tatizo gani?. Nilimuelezea mama hali niliyojikuta nayo muda mfupi baada ya kuamka, nilimuonyesha mama hali nilijikutanayo baada ya kuamka, mama hakuamini na kutaka kipi kilichonifanya nilale wakati aliniacha nikijisomea. Sikumficha nilimweleza jinsi ba mdogo alivyonishawishi kunywa pombe lakini nilikataa na kunywa juisi na baadaye kupoteza kumbukumbu na kujikuta nimelala na nilipozinduka ndipo nilipokuta nimeingiliwa kimwili. Baada ya maelezo yale na kuona mwenyewe kwa macho yake nilimuona mama akiinama kisha alikuna kichwa na kuniuliza. “Helena mwanangu unataka kuniambia baada ya kuondoka Anko wako alirudi peke yake?” “Ndiyo mama, hata mimi nilishangaa lakini sikuwa nalakuhoji.” “Mmh! Sawa, basi leo atanitambua na uzungu wake, pesa zake zisiwe kigezo cha kunibakia mwanangu.” Mama aliyekuwa amekunywa kidogo nilimuona pombe zikimtoka na kujifunga kanga kama anakwenda kucheza mdundiko. Alitoka kama Faru, nami nilimfuata nyuma ili nione mama anataka kufanya nini. Mama alikwenda hadi alipokuwepo yule mzungu aliyekuwa akiendelea kunywa pombe taratibu. Mama alipofika alimsimamia mbele yule mzungu huku ameshikilia chupa ya pombe kali mkononi. “Mr Hans amemfanyaje mwanangu?” “Ooh taratibu, kwani vipi” alijibu yule mzungu huku akinyanyuka kitini kumfuata mama. “Mr Hans sihitaji kusogelewa ila nataka jibu umemfanyaje mwanangu?” Mama alikuwa mkali na nywele zilimsimama kwa hasira. Yule mzungu alionesha kutoshtuka na kauli ya mama aliendelea kumsogelea pamoja na kupigwa stop ya kumfuata. Nilishtushwa na mlio wa chupa kupasuka kwenye kichwa cha mzungu, alikuwa mama aliyempiga chupa iliyompasua vibaya, mzungu alipiga kelele za maumivu. “Unaniua mama Herena.” “Kufa shetani mkubwa wee,” mama kwa hasira alichukua chupa nyingine ya pombe iliyokuwa juu ya meza ili amuyongeze mzungu aliyekuwa ameanguika chini, lakini nilimuwahi ili asimuumize zaidi. “Mama basi utamuua.” “Wacha afe mshenzi hawezi kunichezea mimi na mwanangu, kwanza kwa kipi hasa?” Mama alikuwa amepandisha hasira.
“Kufa shetani mkubwa wee,” mama kwa hasira alichukua chupa nyingine ya pombe iliyokuwa juu ya meza ili amuyongeze mzungu aliyekuwa ameanguika chini, lakini nilimuwahi ili asimuumize zaidi. “Mama basi utamuua.” “Wacha afe mshenzi hawezi kunichezea mimi na mwanangu, kwanza kwa kipi hasa?” Mama alikuwa amepandisha hasira. “Mama tupige simu polisi,” nilimshauri. “Tena kweli na lazima afie gerezani.” Mama alipiga simu polisi baada ya muda polisi walifika na kumchukua yule mzungu na kumfungulia kosa la kubaka. ****** Baada ya kuvunja mahusiano na mzungu, mama aliamua kuachana na wanaume na kuendelea na biashara zetu. Pamoja na kutokuwa na mtu wa kutufadhiri hali ya kimaisha haikuwa mbaya, vilevile nilimshukuru Mungu mama yangu kutulia na kuachana na wanaume. Maisha yalikuwa mazuri tuliweza kufurahia maisha bila kuwa tegemezi, nami niliendelea kusoma bila tatizo lolote, mama aliyatamani yale maisha tungeishi tokea awali. Kwa kweli mama yangu alipendeza na kurudisha heshima iliyopotea. Mwaka mmoja baadaye mama alianza kusumbuliwa na maradhi yasiyoeleweka, Mara leo kichwa kesho miguu kukosa hamu ya kula, ile hali nilimshauri mama twende hospitali. Lakini mama alikataa kwa kusema. “Herena mwanangu wanadamu siwema, lazima wameniroga kutokana na maisha yetu kuonesha maendeleo.” “Sawa mama, lakini twende hospitali kwanza.” “Hapana twende kwa mganga, nina mganga wangu mmoja lazima atanieleza ukweli.” Basi sikuwa na jinsi nilikubaliana na mama kwenda kwa mtaalamu wa miti shamba. Tulipokwenda mama alipewa dawa nyingi za kunywa na kuoga, japo hali ya mama ilikuwa na unafuu kidogo lakini haikumuwezesha kufanya kazi zaidi ya kushinda ndani. Matibabu ya mama yalikula pesa nyingi, tulijikuta tukiyumba kiuwezo na kufikia hatua ya duka kufilisika na mimi pesa zote benki kukatika. Utafikili labda ulisubiri pesa zituishie ndipo ugonjwa wa mama uzidi. Nilichanganyikiwa mtoto wa kike hali ya mama ilikuwa mbaya na pesa zilikuwa zimetuishia. Nilijiuliza niende wapi kuomba msaada, wazo lilikuja niende kwa mjomba wa benki nikamuelezee hali halisi ili anisaidie. Siku ya pili nilikwenda hadi benki kwa mjomba, aliponiona alinikarisha kwa heshima zote, kitu kilichonipa moyo wa kusaidiwa. “Herena za siku mbona umepotea sana?” Ajabu badala ya kumjibu nilianza kububujikwa na machozi kitu kilichomshtua mjomba na kuhoji. “Herena vipi mbona unanidondoshea machozi?” Sikumjibu upesi niliendelea kuinama nikiendelea kudondosha machozi, Anko aliponiona simjibu na kuendelea kudondosha machozi alinyanyuka kwenye kiti chake na kuzunguka kunifuata nilipokuwa nimekaa. “Herena kuna nini tena mbona unanitisha?” Aliniuliza huku akinikanda mabegani. “Hali ya mama ni mbaya sana.” “Ooh pole sana, anasumbuliwa na nini?” Aliondoa mkono mabegani na kuzichezea nywele zangu chache. “Hata sijui kila siku hali yake inazidi kubadilika.” “Mm’hu kumbe ndilo hilo, vipi hospitali mmekwenda?” “Hataki anang’ang’ania kwa waganga wa kienyeji.” “Sasa alikuwa unahitaji nini kwangu?” “Msaada Anko.” “Msaada upi huo?” “Wa pesa.” “Mmh, Herena najua unaelewa ugumu wa maisha kwa sasa,” alizungumza huku akizunguka meza na kurudi kwenye kiti chake. “Ndiyo” nilijibu kwa kifupi. “Unataka kuniambia nitamsaidia kivipi ikiwa hata familia yangu ina matatizo nayo inanitegemea mimi?” “Anko kiasi chochote kila sio lazima kiwe kikubwa.” “Herenaaa, dunia hii ya leo pesa haitoki bure nina imani we mkubwa sasa una miaka mingapi?” “Anko miaka yangu ya nini?” “Herena hebu nijibu sihitaji swali.” ” 19.” “Mmh, umekuwa mtu mzima una uwezo wa kumsaidia mama yako.” “Kumsaidia kivipi na kazi sina.” “Upo tayari kumsaidia mama yako?” “Sijakuelewa kivipi?” Nilishindwa kumwelewa Anko. “Ukipata kazi nyepesi yenye malipo makubwa.” “Nipo tayari kama nikiipata,” alijibu bila kujua kazi hiyo. “Ok, njoo leo saa mbili usiku pale ABC Hotel.” “Aah, Anko kama kazi ya hotel nitapata muda gani wa kusoma?” “Herena mbona unakuwa si muelewa, nani amekwambia kazi ya hotelini.” “Sawa Anko nitakuja.” Nilinyanyuka ili niondoke nilipogeuka ili niondoke Anko aliniita. “Herena.” “Abee Anko,” niliitika huku nikigeuka kumwangalia. Bila kusema kitu aliinama na kuvuta droo na kutoa pesa. “Herena hizi zitakusaidia kwa matumizi ya leo na nauli, usikose sawa?” “Sawa Anko Mungu akuzidishie,” nilimshukuru Anko huku nikizipokea pesa ambazo sikuzihesabu. “Atuzidishie sote.” Baada ya kuzipokea niligeuka na kuondoka huku moyoni nikimshukuru Anko kwa kuonesha utu japo maneno ya mama kuonekana kumchefua. Nilijikuta nikiionea wivu familia yake kwa kuwa na mzazi wenye ubinaadamu. Nilipofika nje ya ofisi nilizihesabu zile pesa nilizopewa, sikuamini macho yangu pale nilipokuta laki mbili taslimu. Nilibadili wazo la kupanda daladala na kukodi bajaj, kwanza nilipitia sokoni na kununua mahitaji muhimu ambayo nyumbani hayakuwepo pamoja na dawa za mama zilizokuwa zimekwisha. Mahitahi yangu yote nilitumia elfu sitini. Nilirudi nyumbani na kumweleza mama jinsi Anko alivyonisaidia na jinsi alivyodhamilia kunisaidia zaidi kwa ajili ya kazi ya muda mfupi na kupata pesa kidogo za kuweza kumsaidia. Nilimuona mama yangu akilia na kujuta kuachana na Anko na maneno machafu aliyomtolea. “Herena mwanangu nikipata nguvu kidogo nitakwenda kumuomba msamaha.” “Ndicho kilichobaki, kwa jinsi ninavyomjua lazima atakusamehe.” Baada ya shughuli za siku nzima, nilifanya kazi zangu harakaharaka ili kuwahi miadi na Anko ABC saa mbili usiku. Majira ya saa moja baada ya kumuogesha mama na kumpatia chakula cha usiku nilimuaga mama ili nimuwahi Anko asije kukasirika. Nilikodi bodaboda hadi ABC Hotel njia nzima nilikuwa najifikilia ni kazi gani hiyo mpaka tukutane hotelini. Lakini wazo lingine liliniambia huenda ni kunikutanisha na wakubwa wenzake ambao watanipa kazi kama mtoto wake, nilifuata maelekezo kama alivyonielezea. Nilipokelewa na muhudumu na kunielekeza sehemu ya kumsubiri Anko. Aliniuliza natumia kinywaji gani, nilimjibu soda japo nilikuwa na hamu ya bia ya baridi. Nikiwa pembeni ya ukumbi nikinywa soda yangu taratibu, nilishtushwa na mkono alionigusa begani nilipogeuka nilikutana na Anko.
ILIPOISHIA: Nilipokelewa na muhudumu na kunielekeza sehemu ya kumsubiri Anko. Aliniuliza natumia kinywaji gani, nilimjibu soda japo nilikuwa na hamu ya bia ya baridi. Nikiwa pembeni ya ukumbi nikinywa soda yangu taratibu, nilishtushwa na mkono alionigusa begani nilipogeuka nilikutana na Anko. “Aaah kumbe Anko, karibu.” “Asante, Helena umenifurahisha sana kwa kwenda na wakati nina imani hata hiyo kazi utaifanya vizuri na kupata malipo manono.” “Nitashukuru Anko maana hali ni mbaya sana.” Anko alivuta kiti na kukaa karibu yangu, huku akinichanulia tabasamu aliniuliza. “Vipi mama yako anaendeleaje?” “Aaah kidogo hajambo japo bado.” “Nina imani mambo yatakuwa mazuri baada ya leo.” “Hata mimi ndilo ninalo liomba kila siku.” Anko aliagiza pombe kali na kuanza kunywa taratibu na mimi nilikunywa soda yangu taratibu huku nikiwa na shauku kujua ni kazi gani hiyo nyepesi yenye malipo manono. “Herena mbona unakunywa soda? hujawahi kunywa pombe?” “Mara moja moja sana.” “Ooh, usiniogope kunywa hii au unataka bia?” “Kilimanjaro ya baridi.” Nililetewa kilimanjaro ya baridi na kunywa taratibu huku nikisubiri kuelekezwa hiyo kazi. Nilijikuta nakata bia ya tatu bila kusikia lolote, mara ililetwa nyama choma ambayo tuliishambulia wote. Muda wote sikuwa na wasiwasi wowote kutokana nilivyokuwa na Anko. Nilijikuta nikichanganya vinywaji vikali na baridi, mwisho kilichoendelea sikujua. Niliposhtuka nilijikuta kitandani nimelala na pembeni yangu kulikuwa na mwanaume amelala. Nilipojichunguza vizuri nilijikuta sina nguo yoyote zaidi ya shuka niliyojifunika. Nilijikuta nikipandwa na gadhabu na kujiuliza ina maana kazi nyepesi aliyonitafutia Anko ni ukahaba. Nilipeleka mkono sehemu za siri na kujikuta nimeingiliwa. Roho iliniuma sikuamini kama kweli Anko ndiye aliyenipeleka kwenye kazi ile au aliniacha na mtu kunichukua kama msamalia mwema na kunigeuza kitoweo. Mtu aliyekuwa amelala pembeni yangu ambaye alionekana eneo la kifua lililokuwa limesheheni manyoya, alikuwa bado kwenye usingizi mzito tena akikoloma. Nilijikuta napata wazo na kuchukua kitu chocho kilichokuwemo mule ndani nimpige nacho kwa kitendo cha kuniingilia bila idhini yangu. Nilijinyanyua kitandani huku nikiwa na hasira kwa kitendo nilichotendewa na mtu ambaye alikuwa kwenye usingizi mzito. Nilisimama na kuivuta ile shuka ili nifuate nguo zangu, sikuamini kukuta yule mwanaume aliyekuwa uchi wa mnyama ni Anko. Nilijikuta nguvu zikiniisha na kuhisi kizunguzungu na kuanguka chini kilichoendelea sikujua. Nilipozinduka nilijikuta nikiwa nimelazwa kitandani nikiwa na nguo zangu. Niliposhtuka nilimuona daktari akiwa amesimama pembeni yangu. Nilijiuliza pale nimefikaje na kwa nini nipo kitandani ikionesha ni mgonjwa. Anko alikuwa amesimama pembeni akifuta jasho kwenye paji la uso, nilitulia tuli nikiwaangalia wote waliokuwemo mule chumbani. Taratibu kumbukumbu zilinirudia na kujikuta nikianza kulia na kutaka kunyanyuka kitandani huku nikisema kwa uchungu “Ankoooo.. kwanini Anko?” Kabla ya kunijibu nilimuona akimpa ishara yule daktari atoke nje ya chumba naye alifanya hivyo. Chumbani tulibakia wawili tu, nilinyanyuka na kutaka kusimama lakini alinishika kifuani na kunirudisha kitandani. “Herena hebu tulia.” “Hapana Anko kwa nini umenifanya hivi au kwa ajili ya umasikini wangu?” “Hapana Herena nina malengo mazuri sana kwako.” “Anko..Anko..ya.a.ani huwezi kunisaidia hadi unitumie, ni unyama gani huu?” nilijikuta nikilia kwa uchungu na kukumbuka maisha ya tabu ya mama yangu ndiyo yaliyopelekea niwe kwenye hali ile.” “Usifikilie hivyo mimi siwezi kukutumia ila nataka uwe mke wangu mdogo.” “Anko ni uchafu gani huo yaani utembee na mama yangu halafu utembee na mimi? Hata siku moja.” “Sikiliza Herena usiwe mjinga mimi sina uhusiano wowote na wewe lakini nimekuwa nikikusaidia kwa kiasi kikubwa. Nina imani nikikuoa kabisa matatizo ya mama yako tutayatatua kwa kiasi kikubwa. Kama kutokea imeisha tokea, hivi mimi ni kiumbe gani nitakaye fanya kazi isiyo na malipo.” “Anko Mungu angekulipia.” “Herena unanichekesha, ni nani aliyekweenda kwa Mungu akarudi akasema amelipwa malipo kwa matendo yake mema. Siku malipo ya duniani ubakia duniani na ndio maana tunafanya kazi na kupata mshahara na hatusubuiri malipo ya kwa Mungu si tungekufa njaa. “Sikiliza mipango yangu kwako ni ya muda mrefu toka mama yako alipokata mahusiano na mimi. Herena kilichotokea nina imani hutakijutia ila jione kiumbe mwenye bahati, hebu fikilia leo nakupa laki tano siku ya mwanzo wa mahusiano yetu nina imani huu ni ukurasa mpya wa ukombozi wa maisha yenu..Kamata hizi.” Alinipa burungutu la pesa na kunikabidhi mkononi, nilisita kuzipokea lakini alining’ang’aniza. Nilijua yameisha tokea na hali ya mama ni mbaya na pa kukimbilia sina niliamua kuzipokea. Baada ya kuzipokea nilifuta machozi kwa kwenda bafuni kunawa uso, niliporudi nilimkuta Anko akinisubiri na kuniambia. “Herena nina imani jioni tutakutana hapa hapa, nina mpango wa kumpeleka hospitali mama yako kwa ghalama yoyote.” Nilijikuta nikijilamu kwa kumchukia Anko ambaye hakunipunguza kitu chochote hata nikiendelea naye bado nitabakia Herena yule yule. Vilevile tatizo la ukata na matibabu ya mama yatapata ufumbuzi. Nilimkubalia Anko kukutana naye jioni, tuliagana na kunipa elfu 50 za nauli ya kuja jioni. Jumla ya pesa alizonipa siku ile zilikuwa laki nane, yaani asubuhi ya jana laki mbili na nusu na usiku laki tano na nusu. Nilirudi nyumbani na kumkuta mama akiwa amelala, sikutaka kumwamsha kwa vile nilikuwa nimeisha kula, nuilikwenda bafuni kuoga na kupanda kitandani. Asubuhi nilikutana na mama ambaye alitaka kujua hatma ya safari yangu. Nilimdanganya mama kuwa mambo si mabaya ila nimetakiwa kurudi jioni ya siku ile. Nilimficha mama kuwa nimepata pesa, nilijua lazima atakuwa na wasiwasi na kutaka kujua pesa zote zile kwa kazi gani, nilizificha ndani kwa ajili ya kututatulia matatizo yetu. *** Kuanzia siku ile nikawa nyumba ndogo ya Anko nikiwa nimemrithi mama yangu mzazi. Lakini ilikuwa siri kubwa ambayo mama hakuijua, na matibabu ya mama yalikuwa mazuri yaliyorudisha hali ya mama upya. Kwa kweli maisha yalikuwa mazuri na Anko kukubali kutusaidia kwa kisingizio ananiona kama mwanaye wa kuzaa. Sikuwa na sababu ya kuacha kunihudumia kiumbe nisiye na hatia, mmh kumbe tulikuwa tunamla mama kisogo. Shule niliendelea kama kawaida, sikuwa tena yule Herena msichana mbishi mwenye msimamo mkali kwa walimu wapenda ngono. Siku za nyuma nilikuwa nipo tayari kuadhibiwa na walimu niliowakataa kimapenzi. Lakini baada ya kujua faida ya mwili wangu wa kunisaidia kwenye matatizo, sikuwa tena mbishi, mwalimu alipotaka kuniadhibu bila kosa nilimuuliza tatizo nini, jibu aliniambia kwani sijui, basi nilimwambia anione kwa wakati wake. Herena nilijikuta nikipoteza mwelekeo kwa kuwa mama huruma kwa kugawa mapenzi ovyo bila kuhofia hatari iliyopo mbele yangu. ******** Siku zilivyozidi kwenda nilijikuta hata hamu ya masomo inapotea na muda mwingi nilifikilia mapenzi hasa penzi la Anko. Nlijikuta nikiacha shule kwa sababu ya ugomvi wa kila siku na wanafunzi wenzangu juu ya kuchangia mabwana yaani walimu. Kingine ni ile hali ya kuutoa mwili wangu bure kwa walimu na pindi nikataapo huambulia adhabu kali. Ajabu ilikuwa tofauti na awali nilipomueleza Anko juu ya uamuzi wangu wa kuacha shule, aliupokea kwa mikono miwili. Hakuonyesha kunijutia kwa uamuzi wangu mgumu, alinieleza kitu ambacho kwa kweli siku ile nilikufurahia sana kumbe…Anko alinieleza kuwa “Herena kusoma kote ni kwa ajili ya kupata pesa kama una mtu mwenye pesa kusoma kuna maana gani? Unakosa nini Helena muda si mrefu nitakamilisha jumba lako la kifahari pamoja na usafiri wa nguvu. “ Wewe sasa hivi hutakiwi kuumiza akili yako bali kuituliza na kula raha ya maisha, au hujui wanaume tumeumbwa kuwatafutia wanawake. Herena maisha mazuri yanakusogelea kwani hujui kusoma?” “Najua.” nilimjibu huku nikimtazama usoni, wakati huo nilikuwa nimemlalia mapajani tukiwa juu ya kitanda ndani ya nyumba ya wageni. “Kingereza unaongea kwa ufasaha sasa tatizo nini?” “Hakuna mpenzi.” “Hapo ndipo ninapokupendea, unajua mama yako angekuwa kama wewe sasa hivi ningekuwa nimemjengea ghorofa lakini kwa vile ameichezea bahati nafasi hiyo ni yako. Kula raha mtoto wa kike umri bado unaruhusu.” Yalikuwa maneno yaliyonivimbisha kichwa na kujiona mimi ndiye mimi, ni mwanamke niliye bahatika kuliko wanawake wote. Baada ya kuacha shule kwa kweli sikuwa Herena yule uliyenizoea, muda mwingi niliutumia kujipodoa na kuvaa nguo za gharama. Pamoja na kufanya upuuzi ule sikumuacha mbali mama yangu nilimpa kipa umbele katika kumshughulikia matibabu yake. Kwa kweli pesa haishindwi na kitu. Mama alijenga afya yake kwa mara nyingine, kwa kweli mama alinishukuru kwa kuyaokoa maisha yake. Uamuzi wa kuacha shule nilipomweleza mama kwanza alikuja juu, lakini nilimueleza sababu za muhimu moja walimu kunitaka kwa nguvu kimapenzi na Anko kuamua nipumzike huku akinitafutia shule nyingine. Nilitengeneza uongo ambao mama aliukubali. Kuanzia hapo hakuna aliyeulizia maisha yangu zaidi ya kila kukicha kuongeza huduma nyumbani. Siku moja mama aliniambia kitu ambacho kilinishtua. “Mwanangu Herena siwezi kukuzuia kwenye matamanio ya mwili ni wazi kuna mtu ana mahusiano na wewe. Ninacho ogopa ni Anko wako kujua huenda akapunguza au kukata kabisa huduma zake. “Hivyo basi sipendi tumuudhi kwa mara nyingine samahani ilizidi hugeuka kero. Pia mwanangu kama kweli huyo mwenzako anakupenda basi usikubali akugeuze gunia la mazoezi. Mlete hapa atambulike kisha muwe mke na mume naogopa mwanangu anaweza kukupa ujauzito na kukukimbia. “Nitajisikia vibaya siku moja ukija kuishi maisha kama yangu, haya sio maisha ni maisha yasiothaminika katika jamii yetu. Pia mwanangu sipendi siku moja uingie kwenye msafara wa Mamba wakati wewe ni mjusi hata ukenge hujafikia.” “Una maana gani mama?” “Mwanangu ugonjwa wa ukimwi ni mbaya ukikupata yataka ujasiri la sivyo unaweza kuyakatisha maisha yako kwa kuhofia aibu. Hivyo mwanangu chukua taadhari kabla ya hatari, nife unizike sio ufe uniache.” Mmh! Maneno ya mama yalikuwa mengi pia angejua huyo anayemzungumzia ni Anko sijui angesemaje. Ni kweli nilikuwa nimefanya makosa kutembea na mwanaume ambaye tayari ameisha tembea na mama yangu ambaye alikuwa sawa na baba yangu. Lakini siku zote makosa ndiyo huzaa kosa, sikuwa na njia nyingine ya kunusuru uhai wa mama uliokuwa ukichungulia kaburi zaidi ya kujirahisi kwa Anko. Nilifanya siri kama tulivyo kubaliana na Anko kwa kuogopa domo la mama pale atakapojua tumeoga bwawa moja. Hali ya mama ilitengamaa na kujikuta akirudi kilingeni kama kawaida, kwa kweli sikumchunguza ana fanya nini zaidi ya muda mwingi kujishughulisha na mambo yangu. Siku zilivyozidi kwenda ndivyo na mimi nilivyoondoa woga na kutembea na Anko popote alipotaka kwenda. Safari zake nyingi za nje nilikwenda naye kama mkewe, huwezi kuamini nilinenepa na kupendeza hata mimi nililitambua hilo. Niliweza kuondoka na Anko na kwenda naye mikoani zaidi ya miezi miwili na kutumbua maisha. Kilichonifurahisha ni hali ya mama kuongezeka kuimalika na kuweza kufanya kazi zake kama zamani. Mama naye baada ya kupata kurudi kwenye hali yake ya kawaida alirudia kazi yake ya ukahaba. Pamoja na kujua athari zake lakini moyo ulinisuta zaidi ya kumuacha afanye atakavyo. Ahadi ya Anko ilianza kukamilika pale aliponipeleka kwenye Site kunionesha ujenzi wa nyumba yangu. Nilijikuta nikimshukuru Anko kwa kuonesha ananijali sikujutia uamuzi wangu wa kuchangia mwanaume mmoja na mama. Tokea hapo sikusikia ya mnadi swala msikitini au mgonga kengele kanisani. Siri siku zote ya mtu mmoja akizidi wa pili si siri tena. Hilo sikuhofia kwa kujua hata mama aliipata nafasi kama ile na alijimwaga bila woga. Naikumbuka siku moja ambayo itakuwa vigumu kunitoka akilini na ndio mwanzo wa kuelewa nini nilichokuwa nikikifanya na kunipelekea kuandika walaka huu.
Nina imani kila anaye soma asichukulie kama haditi tamu au kisa cha kusikitisha bali ni somo tosha maishani. Tatizo langu sipendi mtu mwingine limkute nitajisikia vibaya na kuona ujumbe wangu hukuwafikia walengwa. Elimu si darasani tu, la hasha elimu ni chochote kikutokeacho mbele yako chenye mafunzo kwa kuona au kusikia. Ilikuwa siku ambayo iliniingiza dunia nyingine ambayo sikuitegemea kuuingia hata siku moja japo ndipo nilipokuwa nikielekea. Ilikuwa ni siku ya jumamosi majira ya saa tatu usiku nakumbuka nilikuwa na wiki sijarudi nyumbani baada ya kuwekwa kwenye hoteli ya kifahari na Anko. Niliwasiliana na mama kwa njia ya simu na kunipa moyo kuwa hali yake ni mzima wa afya nje hofu kubwa ilikuwa kwangu. Nilimtoa hofu kuwa yangu hali ilikuwa salama salimini, hakutaka kujua nipo wapi zaidi ya kuniombea dua niendelee kuwa salama. Siku hiyo baada ya kukaa upande wa baa na kunywa pombe ambazo nilimuona kama Anko zimemzidia. Nilimnyanyua ili nimrudishe chumbani. Kwa kweli nilipata shida kumnyanyua na kuweza kumtembeza kwa shida, tulikwenda kwa shida sana huku tukiyumba kama gari umetatika senta bolti. Nilimtoa kwenye baa na kumpeleka kwenye vyumba vya kulala. Kutokana uzito nilimfikisha kwa shida hadi mlangoni na kuanza kufungua mlango kwa funguo. Nilimzuia kwa mguu ili asiende chini na kujitahidi kufungua mlango. Sauti ambaye haikuwa ngeni masikioni yangu lakini akili yangu haikukubali kama ni yenyewe iliniita nyuma yangu: “Helena ni wewe?” Niligeuka akili yangu asiamini ni kweli ile sauti ni ya mama yangu mzazi, haikuwa tofauti na mapokeo yangu kuwa ni kweli ni mama yangu mzazi mama Herana. Nilishindwa kumjibu haraka nilikuwa kama mwanga aliyeshikwa akiwanga mchana kweupe. “Huyu nani?” aliniuliza ikionesha haamini macho yake. “Anko.” “Imeanza lini? Helena mwanangu siamini nimekubali duniani hakuna kitu cha bure.” Mama alionekana amepagawa nina imani hakupenda nichangie mume mmoja na yeye. Wakati huo Anko alikuwa bado amelala chini sakafuni. “Herena mwanangu kwa nini usiulize kabla ya kuingia kwenye msafara huu, mmh, kweli msafara wa Mamba haukosi kenge na mijusi. Siamini na sitaamini mpaka naingia kaburini kama mwanangu umeingia kwenye msafara wa Mamba usiokuhusu. “Wasiwasi wangu umekuwa kweli, Herena kwa nini lakini umeingia kwenye msafara wa mamba?” “Kwani mama tatizo nini, huyu si baba yangu mzazi pia mliisha achana na mwisho nilifanya hivi kuokoa maisha yako,” nilimjibu mama huku nikijikaza kutokana na hali aliyoonesha mama yangu aliyekuwa akizungumza huku machozi yakimtoka. “Herena huwezi kuniokoa huku akijiangamiza, nilikueleza mara ya mwisho kuwa sipendi uishi maisha yangu. Kwa nini mwanangu umechukua kila kitu kwangu, kwa nini hukutaka kuendelea na tabia yako ya awali ya msimamo leo hii umeingia kwenye msafara wa mamba. “ Oooh! Mwanangu yaani leo nimesikia uchungu kama siku iliyokuleta duniani, uchungu huu ni wasiwasi kukupoteza duniani.” Maneno ya mama niliyaona kama uchuro, nilimweleza sehemu ile si muhimu muhimu ya kuyazungumza kwa kina ni nyumbani. Mama hata yule bwana aliyekuwa naye alimuacha na kuondoka huku akilia. Mwanaume aliyeongozana naye alibakia njia panda asijue nini kinaendelea. Nami nilitumia nafasi ile kumwingiza ndani Anko aliyekuwa hajitambui kwa pombe. ****
Siku ya pili niliporudi nyumbani nilimkuta mama macho yamemuiva na kuvimba kuonesha amelia kwa muda mrefu. Hali ile ilinitisha na kujiuliza kuna kingine kilichomliza mama yangu au ni kilekile cha kunikuta na Anko. Niliamini kikubwa kilichomuumiza ni kuchangia mwanaume mmoja na mwanaye. Lakini kwa upande wangu sikuona kosa kwa vile Anko hakuwa baba yangu wa kunizaa pia alikuwa ameachana na mama. Kingine nilichokiamini kuwa nipo sawa kilitokana na msaada mkubwa wa Anko uliosababisha hali ya mama kurudi katika hali yake ya kawaida. “Mama kuna nini?” nilimuuliza mama. “Ina maana hujui?” “La kunikuta na Anko?” “Mwanangu kwa nini unajiua ukiwa bado maisha hujayajua.” “Kivipi mama?” “Umeingia kwenye msafara ya mamba bila kujijua wakati wewe ni mjusi.” “Kivipi?” “Leo mwanaume ni muuaji asikuue kama mimi mama yako.” “Lakini mama Anko ndiye aliyeshikilia maisha yetu baada ya wewe kuugua.” “Kivipi?” mama alitaka kujua. Ilibidi nimweleze sababu ya kuwa na Anko na sababu kubwa alikuwa yeye baada ya kumtukana mbele ya mkewe na kuamua kukata misaada. “Mama kuwa na Anko sikupenda bali ilibidi nikubali ili kuokoa maisha yako bila hivyo ningekupoteza. Pia Anko amekuwa na malengo makubwa kwangu kwa vile hakutaka kunichezea ameninunulia gari na sasa hivi na muda si mrefu nitaingia katika jumba la kifahari.” “Mmh!” mama hakuwa na la kusema aliinama wakati huo nilikuwa nimemsogelea kwa vile kitendo cha kutoa machozi kiliniumiza sana. “Mama najua kiasi gani nimekukosea adabu ya kutembea na mwanaume uliyewahi kuwa naye ambaye sawa na baba yangu. Lakini mama sikuwa na jinsi kuuvua utu wangu kwa ajili ya maisha yako mama yangu. Mama wewe ni kila kitu kwangu kama nitakupoteza nitakuwa mgeni wa nani. “Hivyo basi mama naomba unisamehe nipo chini ya miguu yako, sikuwa na nia mbaya zaidi ya kutafuta njia ya kukomboa hali yetu ya maisha kibaya zaidi hali yako mama ilikuwa mbaya sana ya kutishia amani ya moyo wangu.” “Herena mwanangu nakujua vizuri jinsi ulivyokuwa na msimamo, najua Mr Joel ametumia mwanya huo kunichanganya na mwanangu. Kwa vile mna malengo siwezi kuingilia. Vipi mkikutana mnatumia mpira?” “Mpira kivipi?” “Kondomu.” “Ndiyo mama si unajua siwezi kumuamini mpaka tupime kwa vile anataka mtoto,” nilimdanganya mama kwa kujua lazima angenilaumu sana kama ningemwambia ukweli. “Kama hivyo afadhali,” mama alishusha pumzi ndefu kitu kilichonishtua na kuuliza. “Mbona hivyo mama?” “A’aa kawaida, ila usikubali kufanya naye mapenzi mpaka mwenye mkapime.” “Sawa mama.” Maneno yangu kidogo yalimfanya mama arudi kwenye hali yake ya kawaida, japokuwa jioni ya siku ile nilitakiwa kukutana na Anko nimuomba radhi ili niwe karibu na mama. Siku ya pili mama aliamka katika hali nzuri kitu kilichonipa nafasi ya kuweza kutoka. Mchana Anko alinipigia simu kuwa ana safari ya nje ya mkoa hivyo alinitaka mapema kwa ajili ya mipango ya safari. Nilimuaga mama ambaye muda huo alionesha hana kinyongo tena.
Maneno yangu kidogo yalimfanya mama arudi kwenye hali yake ya kawaida, japokuwa jioni ya siku ile nilitakiwa kukutana na Anko nimuomba radhi ili niwe karibu na mama. Siku ya pili mama aliamka katika hali nzuri kitu kilichonipa nafasi ya kuweza kutoka. Mchana Anko alinipigia simu kuwa ana safari ya nje ya mkoa hivyo alinitaka mapema kwa ajili ya mipango ya safari. Nilimuaga mama ambaye muda huo alionesha hana kinyongo tena. “Herena mwanangu naomba kabla hamjaondoka mkapime afya zenu kwanza.” “Sawa mama.” Niliagana na mama na kwenda sehemu Anko aliyosema anikute, wakati namsubiri nilikuwa na mawazo mengi juu mama kung’ang’ania kupima na kushusha pumzi ndefu baada ya kumwambia natumia kinga. Nilijikuta nikipata wazo la kijinga la kutafuta cheti cha kununua ili kumpelekea mama aondoe wasiwasi kwa Anko. Baada ya ziara ya kikazi tulitotumia siku nne nje ya mkoa, nilibahatika kununua vyeti viwili vyenye majibu mazuri kuwa wote tupo sawa. Niliporudi nilimpa mama, baada ya kuvipokea mama alivisoma na kusema kwa mshtuko. “Unataka kuniambia Anko wako naye yupo salama?” “Ndiyo mama, mbona umeshtuka?” “Walaa! Kawaida tu,” kauli ya mama ilinitisha na kutaka kujua mbona hakufurahia zaidi ya kuyashangaa majibu ya Anko. “Mama mbona sikuelewi?” “Nipo sawa, kwani hospitali aameambiwa nini?” “Wametupongeza na kutuomba turudi baada ya miezi mitatu ili kupata uhakika wa majibu.” “Kama hivyo hakuna tatizo.” Siku zilizidi kukatika huku nikiendelea kula raha na mzee mzima, nakumbuka siku moja tukiwa hotelini na Anko, mkewe alilengeshwa na wapambe aje afumanie. Siku hiyo nilitamani ardhi ipasuke inimeze kwa kujua mkewe anaweza hata kuniua. Lakini ilikuwa tofauti baada ya mkewe kuingia ndani aliangua kilio huku akimlaumu mumewe. Maneno aliyoyasema yalikuwa kama msumeno ulioupasua moyo wangu bila ganzi. “Mume wangu hii tabia ya kuendelea kuua wasichana bila kosa utaisha lini, hebu mwangalie huyo binti alivyo mdogo sana na mwanao wa mwisho. Hivi wanao wakifanyiwa hivi utafurahi? We binti mlipokutana mmetumia kondomu?” Nilikataa kwa kichwa kwani uoga ulikuwa umenitawala. “Si kweli hiyo kondomu ipo wapi? Ona sasa, umeniumiza mimi mkeo hukuridhika sasa unaisambaza tu, binti inawezekana hunijui mimi ndiye mkewe mzee Joel. Mume wangu ni muathirika anayesambaza virusi kwa kuwahonga wasichana wadogo na kufa nya nao ngono zembe. Ukitoka hapa kapime ili ujue hali yako lakini muongope mwanaume kama ukoma” Kauli ilinishtua na kunifanya ninyanyuke kitandani na kupitia nguo zangu zingine nilimalizia kuvaa kwenye korido. Nilipofika nje nilikodi gari hadi nyumbani, bahatu nzuri nilimkuta mama. Nilipomuona niliangua kilio kama nimefiwa. Mama alinishangaa na kutaka kujua kulikoni kuwa katika hali ile. “Vipi tena kulikoni?” “Kumbe kweli Anko muathirika.” “Una maana gani kusema hivyo?” “Mkewe kanihakikishia kuna nini hapo.” “Kakuhakikishia nini?” “Kuwa Anko ni muathirika.” “Sasa wewe unamuamini nani mkewe na vipimo?” “Mama nilikudanganya kuwa nimepima kumbe uongo.” “Eti!?” “Kweli mama nilinunua cheti ili kukudanganya?” “Mungu wangu, Helena mwanangu kwa nini ulifanya hivyo?” “Mama ni akili za kitoto.” “Sasa una uhakika gani kama umeathirika?” “Sikutumia kinga mara nyingi nilipokutana naye.” “Lakini bado huwezi kujua kama umeathirika bila kupima.” “Hapana mama, nasikia kawaambukiza wengi.” “Si nilikuambia ukapindisha maneno, lakini bado usijihukumu, unatakiwa kwenda kupima ili kujua ukweli.” Nilikubaliana na mama kwenda kupima muda ule ule, baada ya kuoga na kubadili nguo. Tuliongozana wote hadi kutuo cha ushauri nasaha ili kujua afya yangu, tulivyo fika kituo cha ushauri na kupima virusi vya ukimwi. Katika kuchukua namba ya kuingia nilikutana na shoga yangu niliyekuwa nasoma naye shule moja. Aliponiona alishtuka na kuniuliza. “Helena kulikoni huku?” “Hidaya mambo ya kucheki afya si unajua tumecheza sana rafu.” “Ni kweli, hata mimi ndicho kilichonileta, una taarifa?” “Zipi hizo?” “Za mwalimu Zakayo,” mimi kiroho pa! “Taarifa zipi?” “Helena upo wapi wewe?” ”Hidaya sikuwemo muda mwingi jijini.” “Kwa taarifa yako, mwalimu Zakayo amejinyonga baada ya kugundulika ameathirika.” “Mungu wangu tumekwisha.” “Kweli tumekwisha, wanafunzi kibao na walimu waliotembea naye wote wameumia na mimi nimeona nije nipate ukweli sijui wewe shoga yangu.” Mmh, kweli nilikuwa katikati ya balaa nyuma mwalimu mbele Anko, sikuamini kama ningetoka salama. Wazo la haraka lilikuwa kama nikikutwa nimeathirika ninywe sumu ili kuikimbia aibu ya kuvishwa nepi. Kwa vile Hidaya alikuwa ameisha chukua kadi, nami nilikwenda kuchukua kadi kusubiri zamu yangu kuitwa kwenye vipimo. Baada ya kuchukua kadi nilirudi kusubiri kuitwa, Hidaya alitangulia kuitwa baada ya muda alitoka. Zamu yangu nami ilifika niliitwa na kuingia ndani. Nilipokelewa na dada mmoja mpole ambaye alivyo hukufanya mtu uondoe wasiwasi wa moyo. “Karibu mdogo wangu.” “Asante.” “Mm’hu,” alionesha kuuliza nini kilichinipeleka pale. “Kama hivyo dada nimekuja kujua afya yangu.” “Ooh, vizuri kipi kilichokushawishi kupima.” “Nafikili kuunga mkono kauli mbiu ya Muheshimuwa Rais Tanzania bila ukimwi inawezekana.” “Vizuri sana, je ukijikuta umeathirika utafanyaje?” “Sina la kufanya kwa vile nimeisha athirika kinachotakiwa ni kufuata masharti yanayotakiwa ili niishi muda mrefu.” “Vizuri, na ukijikuta upo salama?” “Vile vile sitakubali kufanya ngono zembe huku nikimuhimiza mwenzangu naye kupima afya yake ili tufanya ngono salama.” “Vizuri sana binti kwa uelewa wako, sasa hivi utaelekea chumba cha kutolea damu.” Nilinyanyuka hadi chumba cha kutolea damu kisha nilirudi nje kusubiri vipimo. Baada ya muda Hidaya alitangulia kuchukua majibu yake, muda kidogo alitoka akionesha kuchanganyikiwa hata kujigonga mlangoni wakati wa kutoka. Niliamini hata mimi nilikuwa nimekwisha, mapigo ya moyo yalinienda kwa kasi, nilimuomba Mungu aniepushe na balaa lile lililokuwa mbele yangu. Jasho lilinitoka kwa hofu la majibu, mama aliliona lile na kunipoza “Najua upo katika wakati mgumu, lakini kila kitu kipo katika mpango wa Mungu zuri au baya yatakiwa tulipokee ili tukabiliane nalo. Jibu baya lisikutishe tupo pamoja kuambikizwa si kufa,” mama alinitia moyo.
ILIPOISHIA: Niliamini hata mimi nilikuwa nimekwisha, mapigo ya moyo yalinienda kwa kasi, nilimuomba Mungu aniepushe na balaa lile lililokuwa mbele yangu. Jasho lilinitoka kwa hofu la majibu, mama aliliona lile na kunipoza. “Najua upo katika wakati mgumu, lakini kila kitu kipo katika mpango wa Mungu zuri au baya yatakiwa tulipokee ili tukabiliane nalo. Jibu baya lisikutishe tupo pamoja kuambikizwa si kufa,” mama alinitia moyo. SASA ENDELEA…
Wakati huo jina langu liliitwa ndani kuchukua majibu, nilitulia kwa dakika moja bila kutikisikia kisha nilionyanyuka juu. Mama alinivutia kwake na kunikumbatia kisha alioniruhusu nikapokee majibu. Moyoni nilishindwa nimlaumu nani japo Anko alijijua na kunifanyia kitu kama kile. Niliingia hadi chumba cha ushauri, nilipofika nilikaa kwenye kiti kusubiri majibu, palipita utulivu huku mshauri akipitia majibu yangu nami nilitulia tuli huku mapigo ya moyo yakienda mbio. Baada ya kulitulia zaidi ya dakika nzima bila maelezo yoyote mtoa nasaha aliniita jina langu “Helena” “Abee,” niliitikia kwa mkato. “Umejiandaa vipi kupokea majibu?” “Mpaka naamua kuja kupima nilijiandaa vilivyo na kuwa tayari kwa jibu lolote litakalo tokea mbele yangu kwa vile sina wa kumlaumu.” “Una uhakika gani kama mwenzako ameathirika?” “Hilo halina mjadala mkewe ndiye aliyesema.” “Mmh! Si kweli, uhakika ni kupima kujua afya yake.” “Sawa lakini naomba jibu langu.” “Kwa hiyo majibu nikupe sasa hivi au nikupe kwa siri?” “Dada yangu kuna siri gani wewe lipasue hilo jipu nivune nilichopanda.” “Bado majibu yako yanaonyesha…,” aliposita kidogo nilihisi mwili kupandwa na joto la ajabu na kunifanya nitokwe na jasho jingi, nilimsikia akirudia. “Majibu yako yanaonyesha damu yako ni safi,” alinieleza huku akitabasamu. Mmh! Kauli ile niliisikia lakini sikuamini niliona kama nipo ndotoni nilijikuta nikimuuliza “Etiii! Unasema?” “Ni kweli majibu yako ni safi ndiyo maana ulitakiwa umpime mwenzio ili ujue afya yake.” “Lakini dada kuna umuhimu gani wa kumpima mtu wakati mimi afya yangu ni nzuri lazima na mwenzangu atakuwa na afya nzuri. Ni wazi watu walipandikiza maneno ili tuachane.” “Hapana mdogo wangu bado si kumuamini kwa vile wewe umejikuta salama. Huwezi jua labda ni mgonjwa la muhimu ni kwenda naye kupima ili upate uhakika.” “Mmh! Sawa lakini hapa yeye alinihakikishia afya yake ni salama na kuwa tayari kwenda kupima wakati wowote.” “Itakuwa vizuri kabla ya kukutana naye kimwili mkapime ili mjue afya yake, vilevile hiyo haitoshi mtatakiwa kutumia kinga hadi miezi mitatu mtakaporudi kuhakikisha afya zenu wakati huo kila mmoja awe muaminifu kwa mwenzake.” “Sawa dada nashukuru yaani huwezi kuamini jinsi nilivyo furahi.” “Naomba furaha yako ikamilike kwa mwenzio naye kupima ili muishi kwa uhakika kufuta ule uvumi wa mwenzio kuwa na matatizo katika afya yake.” “Sawa nitafuata kila ulilo nieleza na kulifanyia kazi.” Nilikumbatiana na mshauri na kutoka nje nilimkuta mama akinisubiri kama kawaida yake aliniwahi kunikumbatia. Sikuacha kutokwa na machozi ambayo yalikuwa ya furaha kwa mara nyingine kukutwa nipo safi. “Vipi mwanangu majibu yanasemaje?” “Mama majibu yangu ni mazuri nipo salama.” “Ooh! Mungu mkubwa inatosha sasa,” kauli ya mama ilinitisha kidogo. “Inatosha nini mama?” “Kuanzia leo nisikuone ya yule mwanaume nasema inatosha nimechoka kila siku kupatwa na ugonjwa wa moyo Mungu anakupenda lakini bado mapenzi yake unayapiga teke.” “Mama huwezi kumhukumu Anko bila kuwa na ushahidi wa kutosha. Nina uhakika kama mimi nipo salama na yeye yupo salama.” “Herena mwanangu naomba uwe muelewa kwa nini unakuwa mbishi?” “Mama hata wewe ulinieleza kuwa usimhukumu mtu kwa macho bali kuwa kuijua afya yake tena kwa kupima.” “Ni kweli nakuomba kama unataka kuendelea na Anko wako basi tuondoke wote mguu kwa mguu kuja kupima ili nipate uhakika nami nijue ugonjwa sikuupata kwake na maneno ya mkewe ni ya uongo.” “Sawa mama ili kupata ukweli nitampigia simu ili tuje pamoja leo hii kupata ukweli na kung’oa mzizi wa fitina.” Baada ya kukubaliana na mama nilimpigia simu Anko aje pale kituo cha kupimia afya na kutoa ushauri kwa wagonjwa pamoja na vijana. Simu upande wa pili ilipokewa. “Halo mpenzi unasemaje?” “Ni hivi kutokana na kauli ya mkeo kuwa wewe ni muathirika naomba uje ili twende tukapime kwenye kituo cha afya kilichopo karibu na benki ya NMB.” “Herena mimi ni mtu mwenye hadi siwezi kwenda kwenye vituo vya uchochoroni.” “Kwa hiyo?” nilimuuliza. “Njoo ofisini unipitie twende kwenye hospitali moja yenye hadhi yangu tukapime japo niliisha kueleza mimi ni salama ili kukuhakikishia njoo twende ili kuondoa ule wasiwasi wako.” “Hakuna tatizo nakuja sasa hivi” “Okay nakusubiri” Nilikata simu na kumgeukia mama ambaye aliniwahi kwa swali “Vipi amekubali.” “Ndiyo lakini amesema twende kwenye hospitali kubwa yenye vifaa vya kisasa.” “Hakuna tatizo, lini?” “Sasa hivi.” “Basi tusipoteze muda tuongozane pamoja.” Tuliingia kwenye gari na kuelekea kazini kwa Anko, tulipofika nilimjulisha nimeisha fika namsubili nje. Alinieleza anatoka baada ya dakika chache, baada ya dakika kama tano Anko alitoka na kuja hadi kwenye gari langu. Nilimuona akishtuka kidogo baada ya kumuona mama. “Vipi upo na mama?” “Ndiyo ingia garini twende.” “Hapana tutatumia gari langu, lako utaliacha hapo nitamtuma mtu alipeleke kwako kwani baada ya kutoka hospitali nitawarudisha moja kwa moja nyumbani kwenu.” Tuliteremka wote na kuingia kwenye gari la Anko ambalo aliendesha mpaka moja ya hospital kubwa jijini. Kabla ya kuteremka alituomba tumsubili na yeye kuingia ndani ya hospitali. Alirudi baada ya robo saa kisha alituomba tuteremke na kuongozana naye hadi ndani ya hospitali.
Tulikwenda moja kwa moja hadi kwenye chumba cha daktari mkuu, aligonga mlango na kukaribishwa. Tuliingia wote hadi ndani na kupokelewa na mwanaume mmoja mtanashati aliyependeza kwenye vazi lake la udaktari. Alipotuona alitukaribisha huku akimchangamkia Anko kuonyesha wanafahamiana. “Ooh, Mr Joel za siku?” “Nzuri doctor Ambe” walikumbatiana kisha alitugeukia na sisi. “Ooh, karibuni sana.” “Asante” tulijibu kwa pamoja, baada ya kutukaribisha alimgeukia Anko “Mhu mzee una tatizo gani?” “Bwana kwanza kabla ya yote ningependa kukutambulisha nilioongozana nao. Huyu hapo ni mchumba wangu na anayefuata ni mama mkwe.” “Ooh! Karibuni sana shemeji karibu sana..Mama karibu sana.” “Asante” tulijibu kwa pamoja. “M’hu mna tatizo gani?” “Mimi na mchumba wangu tumekuja kupima afya zetu ili kujua tupo sehemu gani.” “Mmh, vizuri ni jambo zuri sana na la ujasiri, lakini naomba niwaulize swali.” “Uliza tu dakta,” Anko alimruhusu. “Ni nini kilichowapelekea kuja kupima afya zenu?” “Ni hali ya kawaida kwa watu walio makini kujua afya zao ili waishi kwa matumaini.” “Urafiki wenu una miaka mingapi?” “Miwili sasa.” “Mr Joel mbona mmekaa muda mrefu sana mpaka kuchukua jukumu la kupima au mliisha pima kabla?” “Kila mmoja ameisha pima kivyake zaidi ya mara mbili na kila mmoja alikuwa na majibu mazuri.” “Mnataka kuniambia nini kilicho wapelekea leo wote mje mpime kwa pamoja?” “Ni kutoana shaka kwetu sote si unajua siku hizi kuna vyeti vya kununua, unafikili mwenzio mzima kumbe unakuchimbia kaburi.” Maneno ya Anko yalinitoa hofu moyoni mwangu kutokana na kuonyesha jinsi gani anavyo jiamini na afya yake. “Mnataka kuniambia kipindi chote mlitumia kinga katika kukutana kimwili?” “Mmh mara chache na kwa vile tuna mpango wa kuoana na kupata watoto tumeamua kujua hali zetu kabisa.” “Je, kama kuna mmoja atakutwa ameathirika hapo mtachukua uamuzi gani?” “Kwani bado nitaendelea kuwa naye kutokana na mapenzi yangu ya kweli kwake kwa kutumia kinga wakati wa tendo vilevile kuwa karibu yake ili usijione mpweke na kumhimiza yote tutakayo elezwa na washauri,” Anko majibu yake yalinipa moyo kuonyesha jinsi gani alivyo na utu moyoni. “Na wewe?” alinigeukia mimi “Hata mimi nitakuwa naye karibu kama alivyojibu Anko.” “Shemu nikikuangalia bado msichana mdogo una mtoto?” “Hata.” “Nina imani unatamani kuwa na mtoto kama ilivyo dhamira ya kiumbe chochote kupata mtoto ili kujenga familia. Swali kama imetokea mwenzako ameathirika nawe kuendelea kuwa naye kwa kukutana kwa kutumia kinga, vipi kuhusu suala la mtoto?” ” Ni vigumu kulisema kwa sasa lakini kama itatokea tutajua vinsi gani ya kulitatua kupitia wataalamu kama nyinyi.” “Na kwako mzee?” alimtupia swali Anko. “Kwangu bado haitakuwa vibaya kwa vile tayari nina watoto.” “Kwa mfano usingekuwa nao?” “Kwa kweli naungana na mwenzangu kwa kutulia na kupanga kwa kuwashirikisha wataalamu kama nyinyi nina imani ufumbuzi lazima utapatikana.” “Japo nina maswali mengi sitapenda kuwapotezeeni muda kutokana na mambo ya msingi kuyajibu. Sasa mpo tayari kuchukua vipimo?” “Ndiyo,” tulijibu kwa pamoja. Baada ya kujibu daktari alichukua kitabu cha kalatasi za vipimo na kutuandika majina kila mmoja na kutuelekeza chumba cha kuchukulia vipimo (Maabara). Tuliongozana na kumuacha mama ofisini kwa mganga mkuu na sisi kuelekea chumba kuchukua vipimo. Tulipofika tulikuwakuta wauguzi ambao walichukua vipimo vyetu na kutoka chumba cha vipimo na kurudi ofisini kwa daktari kusubiri majibu ya vipimo vyetu ambavyo kwa upande wangu nilikuwa na uhakikia wa asilimia mia nipo safi wasiwasi wangu kwa Anko. Tulipotoka nje ya chumba ili tuelekee ofisini nilisikia jina langu likiitwa kwa nyuma. “Herena.” Sikuiitikia moja kwa moja kutokana na majina ya watu kunafanana, nilijua naweza kuitikia kumbe kuna mtu mwingine anaitwa. Niligeuka ili kupata ukweli kujua ni nani anaye niita. Nilipokutana na shoga yangu ambaye tulipotezana tokea darasa la saba. “Ha! Maimuna ni wewe?” “Ni mimi Herena, mmh, umekuwa mama mzima.” Shoga yangu alikuwa amevalia mavazi uuguzi wa hospitali ile, tulikumbatiana kwa furaha. “Mm’ hu shoga za siku?” “Mungu anajalia.” “Vipi mbona hapa una matatizo gani?” “Haa! Shoga si unajua tunaunga mkono kampeni ya Rais kuwa Tanzania bila ukimwi inawezakana.” “Kwa hiyo unataka kuniambia umekuja kupima?” “Ndiyo maana yake?” “Mbona unaonyesha furaha majibu tayari nini?” “Bado ila lazima ujipe moyo.” “Na yule iliyefuatana naye ndiye baba yako nini?” “Yule ndiye usingizi wangu.” “Utani huo yaani mzee Joel ni mpenzi wako?” “Kwani vipi mbona umeshtuka?” “Mmh hata, lakini si ana mkewe yule?” “Sasa ndugu yangu ukitaka kuyajua yote hayo utakufa na njaa si wajinga waliosema tutabanana hapahapa kama yeye kamuoa na mimi nyumba ndogo.” “Mmh hata mambo yako yanaonekana.” “Kwanini unasema hivyo?” “Si unaona sisi tuona tegemea mshahara tuna tofauti kubwa na ninyi mtoto shavu shavu. Kwahiyo umekuja kupima na mzee?” “Shoga siku hizi majibu ya upande mmoja yana ualakini, hivyo tumekuja wote ili tujue nani anachoma nyumba.” “Mmh vizuri, sasa shoga ukitaka kutoka unipitie ili tuelekezane pa kupatana baada ya kazi.” “Hilo halina taabu, huwezi kuamini Mai jinsi nilivyofurahi lazima ufike ninapoishi mpenzi.” Niliagana na Maimuna na kwenda moja kwa moja hadi ofisini kwa daktari. Nilimkuta mama na Anko wakinisubiri, baada ya kuketi daktari alinyanyuka na kutoka nje ya ofisi na kutuacha peke yetu wakati huo kulikuwa kumeletwa vinywaji kwa ajili yetu. Baada ya dakika kama saba daktari alirejea na kuketi sehemu yake na kuendelea kunywa juisi iliyokuwa nusu glasi. Baada ya dakika tano majibu ya vipimo yaliletwa. Japo sikuwa na wasiwasi sana lakini mapigo ya moyo yalienda mbio kiasi. Nilipomuangalia Anko yeye alionyesha hana wasiwasi, alikuwa ni mtu mwenye tabasamu muda wote huku akiendelea kunywa kinywaji chake. Daktari baada ya kupitia kalatasi zote za majibu yetu alipumua kidogo kabla ya kunyanyua macho na kututazama wote kisha alisema: “Jamani majibu yetu ni haya sasa mnataka nimpe kila mmoja au niyatoe mbele yenu?” “Hapa hakuna siri ndiyo maana tumekuja pamoja,” nilijibu kwa niaba ya wote. “Majibu yapo kama hivi nitaanzia kwa mama, wewe majibu yako yanaonyesha damu yako ni..” aliposita moyo ulinipasuka na kujua nimekwisha labda vipimo nilivyopima asubuhi ni vya uongo.
“Damu yako inaonyesha ni safi..” sikusubiri maneno mengine nilijikuta nimemvamia mama na kuanguka naye chini kwa furaha, baada ya kunyanyuka na kukaa kitini huku nikifuta machozi kwa kitambaa. Daktari aliendelea kutusomea majibu. “Inaonyesha jinsi gani moyo wako ulivyo na furaha, sasa ningependa nitoe majibu ya upande wa pili ili baadaye tuweze kuzungumza kwa urefu nini cha kufanya baada ya majibu yote.” Alitulia akisoma majibu ya Anko na kutufanya wote kuwa kimya kumsikliza Anko ana majibu gani? “Majini ya Mr Joel yanaonyesha damu yako ni..” alitulia kidogo na kuendelea “Damu yako ni safi.” Ha! sikujua jinsi nilivyomrukia Anko kwa furaha kwa kukutwa na yeye damu yake ni safi. Nilijikuta nikijawa na furaha kuondoa ule utata wa mama juu ya kujua Anko ni muathirika. Anko yeye alicheka wala hakuonyesha kushangazwa na majibu yale ile ilionyesha jinsi gani alivyokuwa na uhakika tofauti na mimi. Baada ya kupata majibu tulikumbatiana wote kwa furaha na kutoka ofisini ili kurudi nyumbani. Kabla ya kuondoka nilikumbuka kumuaga shoga yangu Maimuna, nilikwenda hadi kwa Mai kumuaga kuwa narudi nyumbani na kutaka kupeana maelekezo ya kupatana. Mai iliponiona kabla ya kuingia ofisini mwao alitoka na kunifuata nje. Cha kwanza kabla ya yote aliniuliza: “Vipi majibu yenu?” “Mungu ametusaidia wote mambo yamekwenda vizuri.” “Hata Mr Joel?” “Ndiyo kwani vipi?” “Aaah ni kitu cha kujivunia maana nimeshuhudia zaidi ya watu wanne waliofika kupima na wapenzi wao kukutwa mmoja ameathirika kwa upande wako imekuwa jambo la heri hongera sana mpenzi,” Mai alinikumbatia kisha aliniuliza: “M’hu shoga hebu nipe maelekezo ya kukupata.” Nilimpa namba yangu ya simu na kumwelekeza ninapoishi. “Usiniambie yaani una nyumba na gari?” “Mbona hayo madogo kuna duka kubwa la nguo nitalifungua wakati wowote katikati ya jiji.” “Mmh, hongera sana, nikuache umuwahi shemu ila jioni nitafika kwako nina mazungumzo muhimu sana si una kaa na shemu?” “Hapana nakaa na mama yeye huja na kuondoka na hivi karibuni tulikuwa tumetengana baada ya wafitini kumzulia mpenzi wangu ameathirika.” “Kina nani hao?” “Si mama yangu mzazi na mke wa Joel mama Jose waliompakazia ni wivu tu nashangaa hata mama yangu kunionea wivu lakini leo limemshuka.” Niliagana na Mai na kuwawahi mama na Anko ambao walikuwa wameisha ingia kwenye gari. Anko aliponiona aliniuliza: “Vipi mbona umechelewa?” “Nilipitia msalani mara moja,” nilimdanganya sikupenda ajue nimechelewa kwa sababu gani. “Tuliingia kwenye gari na kuturudisha nyumbani huku akipanga siku ya pili kufanya sherehe ya kunivisha pete ya uchumba. Kabla ya kuondoka alinijulisha kuwa siku ya kesho yake tungekwenda kufungua duka langu kubwa la nguo Kariakoo. Mmh! Niliona jinsi gani Mungu alivyo niwashia taa ya mafanikio japo mama yangu alionekana kutofurahishwa na mafanikio yale. ****** Ajabu baada ya kutoka hospitali mama alionekana kutokuwa na furaha kitu kilichonitia wasiwasi, nilijiuliza mama yangu alipenda Anko akutwe na ugonjwa kwa nini asifurahie mwanaye nipo na mwanaume ambaye yupo salama. Majira ya saa moja za usiku simu yangu iliita nilipoangalia ilikuwa ya Maimuna, niliipokea na kuzungumza. “Haloo shosti lete habari.” “Herena nimefika nipo karibu na kwako lakini barabara imenichanganya.” “Okay nakuja mara moja kukuchukua upo wapi?” “Nipo njia panda.” Nilitoka nje na kwenda hadi njia panda na kumkuta Mai ambaye nilimchukua na kwenda naye hadi nyumbani. Nilimtambulisha kwa mama ambaye alimfurahia. “Ooh, karibu mwanangu.” “Asante mama.” “M’hu shoga karibu sana,” nilimkarisha huku nikienda kwenye jokofu kumletea kinywaji. Baada ya kumletea kinywaji nilikaa pembeni yake nikiwa na shauku la kumsikiliza shoga yangu niliyepotezana naye kipindi kirefu. “Lete stori mmh, ni muda mrefu,” niliyaanzisha mazungumzo. “Ni kweli Herena vipi hukuendelea nilijua sasa upo chuo kikuu?” “Mmh, we acha mambo yaliingiliana na kunifanya niyaache njiani.” “Kwa sasa unajishughulisha na nini?” “Kwa kweli sina kufanya zaidi ya kulelewa na shemeji yako na kila ukionacho hapa ni yeye.” “Hongera.” “Asante vipi wewe umeisha olewa?” “Bado ila shemeji yako ni yule daktari wa hospitali ninayofanya kazi tupo mbioni kukamilisha.” “Nina imani kila jema Mungu atalipa wepesi.” “Nitashukuru…Samahani Herena ..si.si.jui,” Mai kidogo aliingiwa na kigugumizi kitu kilichonifanya niwe na wasiwasi na swali lake. “Vipi Mai mbona hivyo?” “Sijui nitakacho zungumza hakitakuchukiza kwani Herena wewe ni rafiki yangu wa siku nyingi na shuleni ulikuwa mtu wangu wa karibu nakumbuka mara nyingi ulikuwa mstari wa mbele kutuasa wasichana tujiepushe na ngono.” “Ni kweli kabisa.” “Amini usiamini maneno yako ndiyo yaliyonifikisha hapa nilipo, napenda kutoa shukurani zangu asante sana.” “Nashukuru kuwa ni mmoja wa viumbe vinavyokumbuka fadhira nami nashukuru kwa hilo.” “Herena siku zote nilikuamini wewe kama kioo changu popote nilipokwenda, hivyo basi nilitegemea kukuta upo kwenye taasisi ya ushauri nasaha kwa ajili ya kuwasaidia wasichana ambao wamekuwa wakipotea siku hadi siku kwa kugeuzwa asusa kwa wanaume wakwale. “Wanaume wamekuwa wakieneza magojwa kwa wasichana wadogo ambao wengi wao umaskini ndiyo unaowaponza. Herena umaskini ni ugonjwa mbaya sana kuliko hata ukimwi. Umaskini unaua umaskini unapumbaza umasikini unafilisi umaskini unapoteza utu wa mtu umaskini unakunyima maamuzi na kukubali kila kitu ili tu mkono uende kinywani.” Mai alizungumza mpaka machozi yakamtoka na sauti yake kubadilika kuwa na majonzi, baada ya kutulia kidogo aliendelea kuzungumza: “Herena wenye pesa wamekuwa wakituua kwa kutumia uwezo wao wa kipesa na umaskini wetu uliotutambaa mpaka kwenye mboni ya macho.” Nilijikuta nikishindwa kumwelewa Mai maneno yote yale alikuwa na maana gani ilibidi nimuulize: “Shoga mbona leo umekuja na mada hiyo una maana gani?” “Herena wewe ni shoga yangu sipendi nikuone ukiangamia nikikuona.” Kauli ile ilinishtua na kunifanya nikae vizuri kwenye kochi kutaka kujua niangamie kwa sababu gani. “Mai una maanisha nini?” “Hivi wewe na Joel mmejuana muda gani?” “Mbona unaniuliza hivyo?” “Herena jibu swali sio kuuliza swali juu ya swali.” “Muda mrefu.” “Unamjua vizuri?”
ILIPOISHIA: Kauli ile ilinishtua na kunifanya nikae vizuri kwenye kochi kutaka kujua niangamie kwa sababu gani. “Mai una maanisha nini?” “Hivi wewe na Joel mmejuana muda gani?” “Mbona unaniuliza hivyo?” “Herena jibu swali sio kuuliza swali juu ya swali.” “Muda mrefu.” “Unamjua vizuri?” SASA ENDELEA…
“Kivipi?” “Maisha yake kwa ujumla.” “Ndiyo,” nilimjibu kwa mkato. “Si kweli humjui vizuri Mr Joel,” Mai alinikatalia bila kumwelewa. Maneno ya Mai yalizidi kuniweka njia panda na kushindwa kumwelewa alikuwa akimaanisha nini. “Mai mbona kama sikuelewi?” “Ni vigumu kunielewa ila utanielewa muda si mrefu.” “Ehe una maana gani?” “Herena mimi namfahamu vizuri Mr Joel kwani ile ndiyo hospital yake na siri zake naweza kusema nazijua mimi kati ya wafanyakazi wote.” “Unataka kuniambia ulikuwa mwanamke wake?” niliona Mai alitaka kunirusha roho. “Sivyo ufikiliavyo, unajua Mr Joel ni rafiki mkubwa wa mchumba wangu hivyo ana siri zake nyingi ambazo aliniambia kama mchumba wake pale Mr Joel alipokuwa akija na wasichana kupima afya zao.” “Sasa Mai umekuja kunirusha roho ili niachane na mpenzi wangu, Mai unajua japo ni rafiki yangu naweza kukubadilikia sasa hivi naomba uzungumze mengine yaliyokuleta kuhusu mpenzi wangu hakuna cha kututenganisha. “Walianza ooh ameathirika yote ili kunitilia mchanga chakula changu. Lakini leo umewaumbua watu , hilo halijaisha nawe unakuja na yako kujuana imekuwa nongwa au nawe ni mmoja wa wake wenzangu?” “Herena kila unalofikiria sivyo la muhimu ni kuwa msikivu, mimi simtamani Mr Joel ila kilicho nileta hapa ni umuhimu wa ukaribu wangu na wewe. Sipo tayari kukuona ukiangamia nikikuona wakati bado una nafasi ya kuokoka.” “Mai kuwa muwazi ulikuwa ukitaka kusema nini juu ya Mr Joel?” “Japo hili ni siri kati mume wangu na Mr Joel lakini kisu kimegusa mfupa. Herena ndio maana mwanzo nilisema wenye pesa wanatumaliza, kubali usikubali Mr Joel ni muuaji mkubwa.” Kauli ile ilifanya nihisi kama kuna kitu kimechoma katikati ya moyo wangu. “Mungu wangu Mai una maana gani kumwita mpenzi wangu muuaji mkubwa?” “Herena ndugu yangu yule mzee ni hatari anatumia pesa zake kueneza virusi vya ukimwi kwa wasichana na mwanamke yoyote mzuri. Ni wasichana wengi amewaumiza ambao ninaowafahamu ni zaidi ya wane.” “Mai ni maneno gani hayo ya uongo unayoyaleta nilikuona tokea mwanzo ukimtolea macho mpenzi wangu tangu nilipokutambulisha. Kwa hiyo naomba utoke taratibu kabla sijakasirika,” nilimbadilikia. “Herena hebu punguza munkali ninacho kizungumza ni kwa faida yako leo na kesho tusije nyoosheana vidole au kulaumiana kwa kujua jambo na kukaa kimya.” “Nimesema tokaaa…kama hutaki nitakumwagia maji ya moto unajifanya rafiki kumbe mnafiki…tokaaa.” Nilijikuta nimepandisha jazba na kumfukuza Maimuna kwa sauti ya juu kitu kilichomfanya mama atoke chumbani baada ya kutuacha tuzungumze. Alipotoka alinikuta nikimnyanyua Mai kwa nguvu ili nimtoe nje japo Mai aling’ang’ania kama shetani wa kutumwa. “Herena vipi tena mbona hivyo?” “Mama huyu ni mmoja wa maadui zangu.” “Maadui zako kwani tatizo nini? Hebu muache kwanza.” “Kila kukicha maadui wanaongezeka juu ya penzi langu na Anko wananiona nafaidi naye huyu kaja na mapya. Mama leo mwenyewe umeamini kuwa Anko afya yake ni salama yeye analeta umbea kuwa Anko ni mmuaji kamuua nani kama alikataliwa si yeye.” “Hebu punguza jazba eti mwanangu tatizo nini?” mama alimuuliza Mai. “Mama sikiliza mimi na Herena ni marafiki wa muda mrefu sana sema tulipoteana. Kwa kweli leo nilipomuona nilifurahi sana ila furaha yangu ilitumbukia nyongo baada ya kujua rafiki ya shoga yangu ni yule muuaji mkubwa.” “Una maana gani kusema ni muuaji?” mama alimuuliza. “Mama Mr Joel ni muathirika wa kipindi kirefu zaidi ya miaka saba sasa ila amekuwa akitumia madawa ya kuongeza nguvu. Hata mkewe mama Jose ni muathirika ila mkewe amekuwa akifuata ushauri wa daktari. Ila mumewe amekuwa kiwembe kwa kuusambaza ugonjwa kwa wasichana wadogo hasa wanafunzi na wanawake wazuri. “Kwa vile hammjui vizuri ule sasa hivi si mwili wake alikuwa ana mwili mkubwa sana ila kutofuata ushauri kila kukicha akija hospital anapungua uzito.” Yalikuwa maneno mapya yaliyonifanya nirudi hadi kwenye kochi na kukaa nikifikilia kauli ya Maimuna ilikuwa na ukweli gani. “Kwa nini unasema hivyo wakati leo tu tumetoka kupima na kukutwa wote wapo sawa?” Mama alimuuliza. “Ni kweli majibu yameonyesha sawa ila ukweli unabakia palepale kuwa Herena yupo sawa ila Mr Joel ameathirika.” “Mbona hapo sikuelewi mwanangu aathirike kivipi majibu yameonyesha yupo sawa?” mama alishangaa. “Mama ile ni siri nzito ambayo ameibeba mchumba wangu na baadhi ya madaktari wa ile hospitali ambao hupewa pesa kupindisha ukweli.” “Unasema?” Nilijikuta nimeropoka na kukaa kitako. “Ukweli ndio huo kila siku anapobanwa na wasichana kupima hawezi kupima sehemu nyingine zaidi ya hospital yetu. Kama mnaona mimi muongo mwambie mwende hospitali nyingine kama atakubali.” Tulijikuta tukitazamana na mama kila mmoja alikosa jibu Mai aliendelea kuzungumza: “Kwa kweli nimekuwa nikiumia kitendo cha Mr Joel kuwadanganya wasichana. Lakini leo kisu kimegusa mfupa sikuwa radhi kukuona ndugu yangu mtu niliyemuona kama taa yangu ukiumia nakuona lakini ukweli ndio huo.” “Mmh! Kweli naamini maneno yako mwanangu lazima nami niseme ukweli mimi mama yako nimeathirika na mtu aliyeniambukiza nilijua ni yeye lakini mwanangu alikuwa mbishi nina imani ukweli umeujua.” Nilikuwa kama nipo ndotoni nisipate jibu juu ya kuathirika kwa Anko iweje aathirike mimi niwe mzima. Japo niliamini kwa upande mmoja lakini kwa upande wa pili bado moyo ulikuwa mzito. Kwa ushahidi Maimuna alitotolea vyeti vya Anko vilivyoonyesha ameathirika na jinsi maendeleo yake ya chembe za CD4 mwili. Baada ya wote kuvitazama nilijikuta nikitokwa na machozi na kunyanyuka hadi kwa Mai na kumpigia magoti kumuomba msamaha. ****************** Siku ya pili nilikwenda hadi kwenye kituo cha kupima na kutoa ushauri juu ya ugonjwa wa ukimwi. Baada ya kufika nilikutana na mshauri ambaye sikuwa mgeni kwake. Aliponiona alinikaribisha pamoja na kunikumbuka lakini jina langu hakulikumbuka. “Karibu mdogo wangu.” “Asante dada yangu.” “Kama sikosei ni jana tu ulikuwa hapa?” “Ni kweli dada yangu.” “Mm’hu ulikuwa na tatizo gani?” “Nilikuwa na swali moja juu ya maambukizi ya ukimwi.” “Uliza tu.” “Hivi kuna uwezekano mtu mwenye ukimwi kutembea na mtu asiye na ukimwi na asipate?” .
“Ndiyo.” “Kwa nini?” “Inategemeana na damu ambayo uliyonayo ambayo hairuhusu virusi kuingia mwilini.” “Mmh! Ina maana mtu kama huyo kama ni mwanamke anaweza kuwa na mwanaume mwenye virusi na kuweza kuzaa nae?” “Si vizuri kiafya hasa unapomgundua mwenzio ameathirika ni muhimu kutumia kinga muda wote.” “Kwa nini wakati siwezi kuupata huo ukimwi?” “Sikiliza mdogo wangu mwenzio anapokuwa ameathirika na wewe kuwa salama unatakiwa kuishi naye kwa taadhari kubwa hasa katika jambo la kukutana kimwili. Huwezi kujua nguvu ya chembe zako hai zinaweza kukosa nguvu kama kila siku utazipiganisha na maradhi. “Hivyo inaweza kuwa rahisi hata magonjwa mengine kukuingia na kukusababishia mwili wako kukosa kinga na kukufanya ufe kwa urahisi.” “Na mwenye ukimwi wa muda mrefu huweza kupoteza nguvu kwa muda gani?” “Inategemea usikivu wake kwa kufuatilia ushauri wa wataalamu, kama atakuwa mfuatiliaji wa masharti ataishi kwa muda mrefu huku afya yake ikiwa nzuri. Lakini akienda kinyume na hapo lazima mwili wake utapoteza nguvu na kufa haraka au kuandamwa na maradhi ambayo yatamtesa mpaka kifo chake.” “Mbona kuna mtu ambaye anaonekana ni muathirika wa muda mrefu lakini bado anaendelea kuishi na hali yake nzuri japo afuatilii matibabu?” “Si kweli kama hafuatilii masharti lazima kuna mabadiliko mwilini mwake na atakapopatwa na ugonjwa wowote ni rahisi kufa. Pia wapo wanaofanya mtindo wa kubadili damu kwa wenye pesa lakini huwa hawajui kila wanapokwenda kinyume na mashriti huuchosha mwili na siku moja hufa kama mdhaha na afya zao. “Wengi huwa hawajui mwili unapopoteza kinga hutakiwa kufuata masharti ili kuuweka salama muda wote. Usifikili kubadili damu au kula madawa makali na kwenda kinyume na masharti yake mwili huchoka na kufika kipindi hushindwa kufanya kazi na mtu kufa ghafla.” “Kwa hiyo unataka kuniambia hata mtu mwenye afya asiyefuata masharti hukumu yake ni hiyo?” “Ni kweli kabisa.” “Sasa dada yangu nilikuwa na tatizo moja lililonirudisha kwako leo, ni hivi nina rafiki wa kiume mtu mzima ambaye ana mke. Lakini kila kona wanasema kuwa ni muathirika, lakini jana tulipopima alionekana yupo salama.” “Sasa tatizo nini?” “Bado kuna watu wamenihakikishia kuwa ni muathirika kwa ushahidi wa vyeti, sasa utanisaidia vipi?” “Mimi nakushauri usisikilize maneno ya watu kwa vile mmepima mmeonekana wote mpo salama, subiri miezi mitatu mkapime tena ili kujua ukweli wa mambo.” “Kuna mtu amesema kuwa Anko ananunua vyeti hapo kuna ukweli gani?” “Mmh! Hapo pagumu kidogo..sasa ni hivi kwa vile vipimo vya hapa naviamini mwite aje hapa ili tuchukue vipimo vyetu kwa mara nyingine ukweli utajulikana tu.” “Sidhani kama atakuja vituo hivi vidogo haviamini.” ‘Tatizo si udogo wa kituo, cha muhimu ni mitambo ya kisasa yenye kuona vizuri bila ubabaishaji.” “Mmh ngoja nimjaribu.” “Sikiliza mdogo wangu nipe hiyo simu nitampigia mimi kumwita kuwa wewe nimekuokota hapo nje akiwa ameanguka akifika tutalazimisha akibisha mweleze ukweli. Kama kweli yupo salama atakubali.” Nilimpa simu yule dada ambaye alimpigia simu ambayo Anko aliipokea na kuahidi angefika muda si mrefu. Haikuchukua muda Anko alifika na kunikuta nimekaa mbele ya meza ya mshauri, alipofika mshauri alimkaribisha. “Karibu mzee wangu.” “Asante” alikaa kitini huku akinishangaa. “Vipi dear kuna tatizo gani?” “Mmh! Afadhari umekuja, dada huyu ndiye bwana yangu naomba utupime wote,” nilisema huku nikimkazia macho. “Tupime nini tena?” aliuliza kwa mshtuko. “Afya zetu.” “Herena sasa utakuwa mchezo si jana tu tumepima sasa vipimo vya leo vya nini, labda miezi mitatu ingekuwa imefika.” “Sikiliza Sweet siku zote ili kupata ukweli wa kitu lazima upime sehemu zaidi ya tatu ili tuwe na uhakika wa afya zetu.” “Siku zote vituo vidogo kama hivi vipimo vyake si vya kweli unaweza kukajikuta upo salama kumbe umeathirika au ujikute umeathirika kumbe upo salama.” “Kwani tatizo nini kama bado huamini vipimo vya jana ruksa twende tukarudie sasa hivi.” “Sawa lakini tuanzie hapa.” “Hapa siwezi kupima kituo hiki ni chini ya hadhi yangu.” “Wanakuja hapa hata mawaziri wenye nyadhifa serikalini itakuwa wewe, nasema hivi hapa tunapima tena,” nilisisitiza baada ya kuona kama anataka kukwepa. “Siwezi kama ndicho ulichoniitia sina muda wa kuwepo hapa tutaonana baadaye.” “Mr Joel kwa taarifa yako nakujua vizuri kuwa vyeti vyote unanunua, umemuua mama yangu na mimi unataka kuniua siyo,” mtoto wa kike yalinitoka. “Ni maneno gani hayo Herena mimi nimemuuaje mama yako?” “Unajua vizuri sasa kama hutaki kupima siwezi kukulazimisha, ninacho kuomba kuanzia leo mimi na wewe inatosha bado nayahitaji maisha.” “Lakini kwa nini umefikia huko ni jambo la kuelewana.” “Na kuelewana ni kukubali kupima tena mimi mbona najitolea iweje wewe ukatae.” “Siviamini vipimo vya hapa.” “Aaaha kumbe unavikubali vile vya kule ambavyo umewahonga madaktari ili upate kutuua vizuri.” “Hivi Herena na maneno yako machafu nikipima na kukutwa salama utaniambia nini?” Anko alizungumza huku akitetemeka. “Nikuambie nini zaidi ya kuongeza upendo kwako.” “Basi nipo tayari kupima,” Anko alisema kwa jazba. “Hilo ndilo lililobakia mengine hayakuwa na muhimu,” nilimwambia huku mshauri akiangalia marumbano yetu. Anko alikaa huku jasho likimtoka, mshauri alimtuliza kwa kumuuliza “Mr nani vile?” “Joel,” Anko alijibu kwa mkato. “Samahani Mr Joel japo kupima ni hiyari ya mtu lakini suala la kujua hali za wanamahsiano si vizuri mmoja kupima na mwenzake kutopima bado mtakuwa hamjatatua tatizo. La muhimu ni wote kujua afya zenu ili mjue muishi vipi katika kutimiza malengo yenu. “ Kutokana na maelezo ya mwenzio kusikiliza habari za pembeni kuwa wewe ni muathirika japo mwanzo aliziba macho lakini imefikia kikomo sasa kwa hiyo una unafasi nyingine ya kudhigilisha ukweli.” “Lakini daktari si jana tu tumepima wote na kukutwa tupo salama sasa nashangaa tatizo nini?” “Sikiliza mzee Joel kuna taarifa ambazo nina imani leo zitapata ukweli kuwa wewe una urafiki na madaktari wa hospital unayotibiwa hivyo kukufichia siri zako kwa kutoa majibu ya uongo.” “Nani kasema habari hizi za uuaji?” Anko macho yalimtoka pima.
“Si wakati wa kutafuta mchawi vipimo ndivyo vitakavyo waonyesha wachawi wenu.” “Haya tupime.” Mshauri baada ya kuandika majina yetu tulikwenda chumba cha kupimia vipimo kisha tulirudi kwenye kiti tusubiri majibu ambayo yalichukua robo saa. Baada ya majibu kufika mbele ya meza nilishangaa kumuona Anko akijipekua kama amepoteza kitu. Alitoa pochi yake na kutoa noti ya elfu kumi na kunipa “Herena niletee vocha ya simu mara moja.” “Mwache tu nitamtuma mtu afuate,” mshauri aliingilia kati mzungumzo. “Hapana, kwenye pesa huwa simuamini mtu, wacha tu my daring afuate.” Sikutaka mabishano nilinyanyuka na kutoka nje ya kituo kwani maduka hayakuwa mbali. Nilinunua haraka na kurudi ndani, nilishangaa mjomba alinyamaza ghafla baada ya kuniona na kuniuliza. “Vipi umepata?” “Ndiyo.” “Vizuri, samahani mpenzi nilisahau kukuagiza ya elfu 20 naomba umenilee nyingine.” “Dear hebu kwanza tusikilize majibu mara moja nyingine tutanunua tukitoka.” “Mwache tu kwanza si unajua kuna wateja wengine tumewagandisha kwa kipindi kirefu kwa ajili ya kuwapa upendeleo kutokana na uzito wa tatizo lenu.” “Okay daktari lakini iwe hivyohivyo.” Nilijiuliza iwe hivyo hivyo nini, sikutaka kuhoji nilikaa kitini kusikiliza majibu yetu. Baada ya utulivu wa dakika moja mshauri alituita majina yetu. “Herena.” “Abee.” “Mzee Joel.” “Naam.” “Majibu yenu majibu yake kama ifuatavyo ila kwa yoyote ambaye hatakubaliana na majibu haya bado ana nafasi ya kwenda mbele zaidi kupata ukweli. Lakini kipimo chetu ni cha uhakika na kutoa majibu ya kweli yasiyo na utata hata kidogo,” mshauri alitulia kumeza mate na kupitisha jicho lake kwa kila mmoja kisha alisema: “Ila kabla sijatoa majibu nini malengo yenu?” “Ni kuwa mke wa pili wa mzee Joel,” nilijibu. “Kwa mfano mzee joel ameathirika na wewe mzima utayapokeaje majibu yako?” “Nitayapokea kama yalivyo lakini sitaendelea na mwenzangu kwa vile hakuwa mkweli kwangu,” nilijibu. “Hapana Herena hapo utakuwa hujamtendelea haki mwenzako, ina maana wewe ukikutwa unao na yeye hana utachukua uamuzi gani?” “Nitamsikiliza mwenyewe ana semaje, uamuzi wowote atakaoutoa itakuwa sawa kwa upande wangu.” “Eti mzee Joel vipi ukikutwa wewe upo sawa na mwenzako ameathirika utachukua hatua gani?” “Kwa upande wangu kwa vile nina mapenzi ya dhati kwa mwenzangu sitamtenga nitakuwa naye bega kwa bega hadi mwisho wa maisha yake kwa muda wote kuwa karibu yake ili kumtoa mawazo potofu kuwa mwenye virusi hana rafiki au rafiki wa mwenye virusi ni mwenye virusi.” “Asante sana mzee Joel kuonyesha ukomavu kwenye janga hili ambalo wengi huwatelekeza wenzi wao. Je, kama wote umejikuta mpo salama mtafanyaje? Nitaanza ni Herena.” “Mmh mimi nitamshukuru Mungu kwa kunilinda pili nitazidisha mapenzi yangu kwa mwenzangu na tatu nitaendelea kuwa muaminifu kwake.” “Vizuri Herena, na mzee wangu?” “Mimi nitamshukuru Mungu na kuendelea kuwa muaminifu na mwenye mapenzi ya vitendo yenye kutoka chini ya uvungu wa moyo wangu na kumtimizia vyote nilivyo muahidi.” “Nashukuru kuwasikieni ni watu mnaoonyesha mapenzi ya kweli kwa kila mtu kwa mwenzake. Mwisho vipi kama wote mjikute mmeathirika mtachukua uamuzi gani?” swali lile kidogo lilinitisha kwa kuonyesha ukweli fulani, lakini nilijikaza ili kupata ukweli. “Mm’hu Herena naona kama upo mbali kidogo?” aliniuliza baada ya kuhama kimawazo. “Aaah, nipo sawa,” nilijibu huku nikijiweka sawa kitini. “Ehe, utachukua uamuzi gani?” “Kwa vile mimi nipo chini ya mtu nitamsikiliza mwenzangu ana semaje.” “Sawa, lakini nataka maoni yako mwenyewe.” “Nitaendelea kuwa karibu na mwanzangu na kuwa mshauri mwema katika kuafuata yote tulishauriwa na daktari na kufuata kila nilichoelezwa kulinda afya zetu.” “Mmh vizuri sana Herena na mzee wangu?” “Mimi kama mimi naamini ukimwi si kifo bali ni ugonjwa unaotakiwa kufuata masharti yake ambayo humfanya mtu aishi maisha marefu bila tatizo, hivyo basi nami nitakuwa bega kwa bega na mwenzangu kuhakikisha hatuendi nje ya masharti ya kuishi kwa usalama.” “Nashukuru kwa uelewa wenu mkubwa ambao utanisaidia kuyasema majibu yangu bila hofu,” alitulia kwa kuzichukua kalatasi za majibu juu ya meza na kuzipitia kwa mara ya mwisho kisha alituuliza swali: “Mmesema mahusiano yenu yana muda gani?” “Mmh ni mwaka wa tatu sasa,” nilijibu kwa niaba ya wote. “Na katika mahusiano yenu huwa mnatumia kinga au bila kinga?” “Hutumia siku moja moja hasa kipindi cha hatari ya mimba zaidi ya hapo huwa hatutumii.” “Mmh….sawa,” alivuta pumzi kwa ndani na kuzitoa kisha alisema kwa sauti ya chini iliyosikika. ” Majibu yenu yanaonyesha kama ifuatavyo nitaanza na Herena, majibu yako yanaonyesha damu yako ni salama.” Nilipiga magoti kwa mara nyingine na kunyanyua mikono juu kwa kusema: “Asante Mungu.” Baada ya kushukuru nilirudi kitini kusikiliza majibu ya Anko yalikuwa yakisemaje, lakini niliamini yote yaliyokuja juu ya Anko ni uongo ili kututenganishe. Nilitulia tuli kusikiliza majibu ya Anko: “Majibu ya pili ya Mr Joel yanaonyesha damu yake ni cha…” Hakumalizia Anko alimkata kauli. “Muongo mkubwa ndio maana nilikataa kupima vipimo vya uchochoroni.” Nilimshika Anko na kumkalisha kitini huku nikimuomba awe mtulivu. “Mpenzi tatizo nini hebu tumsikilize kwanza nawe utazungumza nakuomba uwe mpole.” “Hapana Herena huyu binti anataka kunivunjia heshima yangu tu,” Anko alisema huku jasho zikumtoka kwa wingi kwenye paji la uso.
Baada ya kutulia huku akitweta nilimruhusu mshauri aendelee “Kwanza kabla ya kumalizia kutoa majibu kuna kitu nataka nikiweke wazi. Mr Joel kwa tabia yako utaendelea kuueneza ukimwi kwa kutumia pesa zako kuwahonga washauri na madaktari wasiojua thamini ya maisha ya watu. “Hivi hiyo laki tano yako inalingana na uhai wa Herena? Kama kweli ulikuwa ukimpenda Helena kwa nini usimwambie ukweli kuwa wewe ni muathirika ili mjue mjikinge vipi kuliko kuueneza bila woga. “ Ni kweli nina shida na hela lakini si kwa mtindo huu, nimejitolea kufanya kazi hii kwa ajili ya kuokoa maisha wa watu na si kuangamiza maisha ya watu. Kwa nini unaonekana ni mwelewa lakini si kwa vitendo zaidi ya kuzungumza mdomoni lakini moyoni una dhamira mbaya. “Mr Joel kuwa na virusi vya ukimwi si aibu siku hizi watu wameelimika. Kujitangaza ni kujikinga na kujiingiza kwenye vishawishi vya kufanya ngono na watu wasio kujua. Hivi ni wangapi katika dunia hii wenye mawazo wa kiuuaji kwa kuusambaza ukimwi kwa watu wasio na hatia. “Si kwa wanaume hata wanawake wengi wamekuwa na tabia hiyo wanapojijua wameathirika na wana pesa hutumia pesa zao kufanya mapenzi na vijana wadogo kwa kuwapa pesa nyingi na kufanya nao mapenzi bila kinga. Huo si ujanja bali kuliangamiza taifa ambalo nguvu kazi yake ni vijana. “ Hivyo nakuombeni kama tulivyo zungumza awali, bado mna nafasi ya kuendelea kuwa pamoja kwa kutumia kinga na kupunguza kukutana kila wakati ili kuupa mwili nafasi ya kujenga uwezo wa kujilinda. “Namalizia kwa kutoa ushauri kwa wote waliojitolea kuokoa maisha ya watu juu ya janga lolote si ukimwi tu. Wajitoe kwa ajili ya kuokoa si kuangamiza, pesa utakayopewa ili upindeshe ukweli hujui ni bomu ambalo hata wewe linaweza kukulipukia. “Hivyo basi tuwe wakweli na wawazi kwa yoyote atakayetaka kuangamiza wenzake kwa ajili ya pesa zake ili wafe wengi. Ni nani aliyekuambia ukimwi ni kifo, ukimwi ni ugonjwa kama ugonjwa wowote unaweza kufa na ugonjwa mwingine tofauti na ukimwi na mwenye ukimwi akaendelea kuwepo. “Ndugu zangu kama majibu yanavyo onyesha mmoja yupo safi na mmoja ameathirika. Ni wazi Mr Joel uliisha pata ushauri juu ya ukimwi mara ya kwanza ulipokutwa nao. Nakuomba ufuate ushauri wa washauri ili uishi muda mrefu. “Mwisho nakuombeni muondoke salama na kuendelea kuwa karibu na mwenzako katika kupeana moyo na kufarijiana.” “Siwezi kuendelea kuwa na muuaji mzoefu kumbe umenituma vocha ili uniue….Asante dada yangu Tanzania tukiwa na moyo kama wako ile kauli mbiu ya Rais Tanzania bila ukimwi unawezekana. “Lakini kwa walio tanguliza masrahi yao binafsi ambayo hayainufaishi nchi kauli hiyo itakuwa sawa na kumpigia mbuzi gitaa,” nilijikuta nikizungumza kwa uchungu baada ya kugundua Anko kila siku alikuwa akinizunguka na kuitafuta roho yangu kama Zilairi mtoa roho. “Nooo sivyo hivyo dada huyu bwana hafai lazima nimfungulie kesi kwa kosa la mauaji.” “Hapana usifanye hivyo watu hawa ni kuwaelimisha tu.” “Hivi ni wangapi amewaambukiza akiwemo mama yangu mzazi hakulidhika aliitaka na roho yangu.” “Herena ni shetani lakini bado nakupenda na nina mipango mingi juu yako,” Anko alinipigia magoti mbele yangu kuniomba msamaha. “Mipango mingi ya kuniondoa duniani kwa kuwahonga wote wanajihusisha na upimaji wa maambukizi ya ukimwi.” “Samahani mzee Joel pesa yako hii hapa,” yule mshauri alitoa laki tano na kumpa Anko lakini niliziwahi na kuzichukua kisha nilimrudishia yule mshauri. “Asante yako kwa kuokoa maisha yangu.” “Hapana, nashukuru,” mshauri alizikataa. “Si kweli ulichokifanya ni ujasiri wa ajabu hii hela nakupa mimi naomba upokee.” Alipokea zile hela kisha nilimuaga na kuondoka huku Anko akinifuata kwa nyuma. Nilipofika kwenye gari langu niliingia ndani na kung’oa nanga japo aliniita na kulikimbilia gari langu. Nilikwenda hadi nyumbani ambako nilimkuta mama na kumweleza hali halisi juu ya hali ya Anko na ujanja aliousema Mai juu ya kuhonga watoa majibu. “Nina imani ukweli umeupata sasa unasemaje?” “Siwezi kumtenga ila nitakuwa naye karibu kama sehemu ya familia si mpenzi na nina mpango wa kutafuta mchumba wa kweli ili anioe.” “Nina amani sasa utaamini kinywa cha mkubwa kinanuka lakini maneno yake hayanuki.” “Ni kweli mzazi wangu hili limekuwa kusudio la Mungu ili liwe fundisho kwa wengine.” “Nina imani ukijiunga na kikundi cha kutoa ushauri utakuwa mwalimu mwema.” “Mmh nitaweza?” “Kwani hao wameweza vipi ushinde wewe unayejua ABC ya maambukizi ya ukimwi.” “Nitajaribu.” Tukiwa katikati ya mazungumzo tulishangaa kumuona Anko amesimama mbele yetu kama mwanga aliyekamatwa mchana. Nilijikuta nikipandwa na hasira na kunyanyuka kitini na kumfukuza. “Nakuomba utoke muuaji mkubwa.” “Hapana Herena hebu msikilize anataka kusema nini,” mama aliingilia kati. “Hapana mama siwezi kumsikiliza kwa lolote muuaji.” “Herena nasema rudi nyuma na ukae chini, hata kama ungeambukizwa nisinge mlaumu, ni wewe uliyeanza kununua vyeti kuficha ukweli leo ndio umejua athari zake,” kauli ya mama ilinifanya niwe mpole ghafla na kumuacha Anko aseme kilicho mleta: “Ndiyo baba unasemaje?” mama alimuuliza kwa sauti ya chini. “Leo nimekuja kuomba msamaha kwako na kwa Herena kwa kitendo nilichokitenda ambacho si cha kibinadamu. Naweza kusema umejua nimeathirika baada ya mke wangu kupima wakati wa ujauzito. “Na wakati huo nimeisha achana na wewe, lakini kwa Herena nilimpenda niliogopa kumwambia ukweli kutokana na kumpenda sana. Ninachokuombeni mnisamehe nami nitalipa fidia pia kuanzisha kitengo cha ushauri nasaha juu ya ukimwi ikiwa pamoja kukupeleka kusoma zaidi.” Hatukuwa na muda wa kumtafuta mchawi kwa kila mmoja wetu alikuwa na makosa. Hivyo tulikubaliana kwa pamoja kushirikiana kuanzisha NGOS kwa ajili ya kutoa matangazo juu ya kujikinga na maambukizi ya ukimwi. **** Baada ya muda nilikwenda kusomea mambo ya ushauri nikiwa kama mkurugenzi wa shirika la NI KWELI, likiwa na maana Ni kweli ukimwi upo tuache ubishi. Baada ya kumaliza tuliaji watu wengi, tulianza na mashule hasa kwa kutoa elimu kwa walimu kwa tabia zao chafu za kutembea na wanafunzi. Kisha tulimalizia kwa wanafunzi kwa kuelewa nini kilicho wapeleka pale shuleni ni elimu na si mapenzi. Pia shirika letu liliandaa kongamano kubwa la vituo vyote vya ushauri nasaha na kupima virusi kwa kuwa wakweli ili kuokoa nafsi za watu. Nilitumia matukio yangu kama somo kwa wote ili tuwe wakweli na wawazi kwa kuweka masrahi ya taifa mbele kuliko kuwema maslahi binafsi. Shirika letu kwa muda mfupi liliweka kupata misaada mingi kutoka kwa wahisani na kuweza kupanuka na kuzunguka Tanzania nzima kwa kutoa elimu ya ukimwi kwa mafanikio makubwa. Mfano wangu ndio nilioutumia kwa kutoa elimu ya kweli. Tuligawa vipeperushi na vitabu bure mashuleni juu ya umuhimu wa elimu na kujilinda na ukimwi. Anko na mkewe walikuwa walezi ambao waliongeza nguvu kwenye kampuni yetu. Namalizia kwa kusema Ukimwi upo na unaua, kila mmoja asimpime mwenzie kwa macho bali mkapime wote ili kujua afya zenu. Vile vile usichukulia kipimo cha mwenzako kujua afya yako bali kupewa mwenyewe. Pia kwa wote ulijitolea kuokoa maisha ya Watanzania ili tuendane ya kauli mbinu ya mkuu wa nchi Tanzania bila ukimwi inawezekana. Kama kutanguliza maslahi ya taifa mbele na si masilahi binafsi itawezeakana. Mwisho ni maofisini na mashuleni tusipo kuwa makini ukimwi utatumaliza hasa wanaopenda rushwa ngono ambao ndio hatari mkubwa katika kueneza virusi vya ukimwi. Namazia kwa kufuata yote tuliyozungumza tokea mwanzo wa mkasa huu Tanzania bila Ukimwi inawezekana.
JIJI la Dar es Salaam linatingishika, wezi sugu wanaingiza noti bandia, watu wanaibiwa. Baadhi wanauza majumba, magari na viwanja. Wafanyabiashara hatari wa dawa za kulevya nao wanacharuka, wanatangaza hali ya hatari kwa atakayeonesha kuwaingilia. Patashika linatokea, Dar es Salaam inakumbwa na misukosuko na mauaji ya kutisha.
“Kama unayathamini maisha yako jiweke pembeni”. Amri inatolewa, “Vinginevyo yatakupata makubwa”. Onyo linatolewa kila pembe ya jiji. Polisi wanagwaya, mauaji ya kutisha yanatokea, tishio linakuwa kubwa zaidi. Rais anapaza sauti, “Lazima hali hiyo ikomeshwe vinginevyo, hatuwezi kuvumilia…”.
Mashujaa kadhaa wanajitokeza kuikabiri hali hiyo. Maiti zao ziokotwa kando ya bahari. Teacher anatua uwanja wa ndege wa Dar es Salaam na kukabiliwa na mtihani mkubwa, gari lake linashambuliwa, anaponea chupuchupu. Lakini anaapa kuikabibiri hali hiyo ngumu. SASA ENDELEA.
NDEGE ndogo ya kukodi ya Kampuni ya ndege za Coastal ilishuka taratibu kwenye uwanja wa ndege wa mjini Musoma, baada ya kuwa angani kwa takribani dakika ishirini na tano hivi ikitoka katika Jiji la Mwanza. Mara baada ya ndege hii kutua kwenye uwanja huu, ulioko karibu kabisa na ukingo wa Ziwa Victoria, eneo maarufu la Makoko, nilikuwa miongoni mwa abiria watatu tuliosafiri kwa ndege hii kutoka Mwanza ambako tulibadilishiwa ndege.
Hii ilitokana na uwanja wa ndege wa Musoma kutokuwa na uwezo wa kupokea ndege kubwa kwa sasa. Baada ya ndege hii kutua, nilitwaa mfuko wangu mdogo uliosheheni vifaa vyangu muhimu vya safari, taratibu nikavuta hatua kutoka ndani ya ndege hii nikiwa tayari kuelekea nje.
Sikuwa na sababu ya kwenda haraka kutokana na hali ya ndege hii kuwa ndogo, hivyo nilisubiri wenzangu watoke kwanza ndipo nami niweze kutoka. Baada ya kukanyaga ardhi ya mji wa Musoma nilitembea taratibu, mkoba wangu begani, nilipita mapokezi na sehemu ya mapumziko ya wageni mashuhuri, nikaelekea kwenye maegesho ya magari ya kukodi nje ya uzio wa uwanja.
Hali ya hewa ya mji wa Musoma ilikuwa ya kuvutia sana, wingu zito lilitanda angani, kuashiria dalili ya mvua. Hali kama hii pia tuliikuta tuliposhuka kwenye uwanja wa Mwanza ambako tulikuta mvua ya kutosha. Kiasi fulani nilivutiwa na hali hii ya ubadiridi hususan kutokana na joto kali nililoliacha Jijini Dar es Salaam.
“Haraka, nipeleke Mkendo tafadhali”, nilimwambia dereva teksi, baada tu ya kuingia na kuketi ndani ya gari yake iliyokuwa imeegeshwa karibu na sehemu niliyotoke.
“Sawa mzee”, alisema dereva huyo huku akiwasha gari na kufunga mkanda, nami nikafanya hivyo. Wakati anaanza kuondoka aliuliza, “Mkendo ipi?”, alihoji dereva huyo huku akiondoa gari taratibu kutoka kwenye maegesho ya uwanja wa ndege.
“Mkendo… Nadhani utaniacha baada ya njia panda ya mtaa wa Iringo”, nilimwambia.
“Nadhani dakika tano”, alisema huku akiingia kwenye barabara kuu ya Majita, akaongeza mwendo tukaelekea katikati ya mji. Baada ya kuzipita ofisi za Shirika la Umeme Tanzania Tanesco, nilivunja ukimya uliodumu kwa dakika kadhaa.
“Vipi hali ya samaki katika mji huu, wanapatikana?”, nilimuuliza, taratibu akageuza shingo kunitazama, kiasi fulani alionekana kushangazwa na swali langu.
“Samaki!… alihoji kwa mshangao.
“Ndio… Mbona kama imekushituawa sana, wanapatikana?”.
“Samaki bwana ni wengi sana. tatizo ni bei. Samaki kama Sato wanauzwa kwa bei mbaya sana, viwanda vimeleta shida, minofu ya samaki katika mji huu ni lulu, inasafirishwwa nje ya nchi, wakazi wa hapa tunaachiwa mifupa”, alisema kwa utani huku akinitazama usoni akicheka.
“Mifupa ya samaki?”, nilimuuliza. Niliwahi kusikia kuwa idadi kubwa ya samaki wanaovuliwa Ziwa Victoria wanapelekwa viwandani na kusafirishwa nje ya nchi, wenyeji wanaambulia mfupa mkubwa wa katikati na kichwa. Maelezo yake yalinifanya nihamasike kuuliza maswali mengine zaidi.
“Hiyo mifupa unayodai kuwa ndiyo inauzwa kwa wananchi, inafaa kuwa chakula?”.
“Samahani kaka, wewe ni mgeni katika mji huu?”, alihoji kijana huyu ambaye umri wake haukutofautiana sana na wangu.
“Mgeni mwenyeji, ni mzaliwa halisi wa mkoa huu, nimeishi sana mjini hapa, enzi zetu tulipokuwa wadogo samaki walikuwa wengi sana, sato, sangara, nembe ilikuwa usiseme, ukishuka Mwigonero samaki wa kumwaga, nasikia siku hizi hawapatikani ndiyo nashangaa”, nilimwambia wakati anaingia kwenye mzunguko wa barabara za Nyerere na kuacha ile ya Sokoni.
“Basi labda nikudokeze, mapanki ni sehemu ya samaki waliotolewa minofu kwa ustadi mkubwa na kubaki kichwa na mfupa mkubwa wa katikati, mabaki ambayo huuzwa tema kwa watu wa kipato cha chini, hii inatokana na bei ya samaki kuwa juu sana. Ndiyo hali halisi ndugu yangu, samaki tunawasikia kwenye bomba tu huko viwandani”, alifafanua kijana huyu.
“Aisee, sasa nimekupata. Kumbe ndivyo ilivyo…”, nilinyamaza kidogo nikitafakari kisha nikamuuliza. “Kwanini serikali isiingilie kati, kuwasaidia wananchi wapate maisha bora, nina maana kuwa yatengwe maeneo ya wavuvi wa samaki kwa ajili ya wananchi wenye kipato cha chini, viwanda navyo vinunue kwa bei ya juu kidogo ili kuweka usawa”.
“Nchi hii kaka, wananchi hawana maamuzi, tumewapa wenzetu dhamana wanaitumia kujinufaisha wao na matumbo yao, tatizo pia liko kwetu wabongo, tunajua kulalamika tu lakini hatuna maamzi ya kukataa jambo”, alisema, baadaa ya kunyamaza kwa sekunde kadhaa, akageuka kunitazama. Labda hii serikali mpya italeta maisha bora”.
“Labda, tusubiri tuone, maana watendaji ni walewale walioshindwa”, nilimwambia akacheka.
Baada ya kupita kwenye mzunguko wa Barabara ya Nyerere, tukauacha mtaa wa Sokoni, tukaingia kwenye Barabara ya Nyerere, baada ya kituo cha mafuta cha GAPCO karibu na ilipokuwa karakana ya mabasi ya United. Sambamba na uwanja wa shule ya msingi Mkendo, tukaingia kushoto ulipo mtaa mdogo wa Rutiginga, moja mitaa yenye historia kubwa mjini Musoma. Inasemekana mtaa huu ndiyo wa kwanza kuwa na kinadada wanaouza miili yako. Baada ya kuuacha mtaa huu wa Rutiginga, moja kwa moja tukatokea barabara kuu ya Mkendo.
“Nimelazimika kupita njia hii kukwepa msongamano wa magari eneo la standi ya mabasi, muda huu kunakuwa na foleni kidogo”, alisema wakati akisubiri kuingia mtaa wa Mkendo.
“Usijali, mitaa hii naifahamu vizuri pengine zaidi kuliko wewe, hata tungepita barabara ya Uhuru bado ilikuwa sawa tu”, nilimwambia akatabasamu wakati akisimama mbele ya studio ya Issa Mkate, nilitoa kiasi cha pesa nikampatia akashukru na kuondoka.
Nilikuwa nimewasili mkoani hapa kwa likizo fupi ya upendeleo, niliyopewa na Mkuu wangu wa kazi, Kanali Benny Emilly, ambaye ndiye Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi. Lakini kabla ya kuondoka Dar es Salaam nilipanga ratiba fupi ya kuonana na watu kadhaa. akiwemo rafiki yangu kipenzi Luteni Kanali Charles Matumbi anayeishi mtaa huu wa Mkendo.
Kwa mjibu wa ratiba yangu mjini Musoma sikuwa tayari kuonana na mtu zaidi na Luteni Kanali Matumbi, nikihofia kuharibu ratiba yangu, kwani nilipanga pia kufika kijijini kwetu Nyamuswa, Wilayani Bunda ambako nilipanga kukutana na mama yangu mzazi niliyempenda sana. Baba yangu niliyempenda sana alikwisha tangulia mbele ya haki. Nimekuwa nikijiuliza maswali maswali mengi kwa nini Baba yetu tuliyempenda alikataa kula chakula hata akadhoofu na kupoteza maisha. Hii ni siri ya Mungu aliyetuumba na kutufanya tuishi kwa muda katika ulimwengu.
Likizo hii fupi ilitolewa na Mkuu wangu wa kazi Kanali Emilly kwa upendeleo, baada ya ofisi yake kupokea hati ya utambulisho wa kimataifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kutambua mchango wa utendaji kazi wangu nikiwa mlinzi wa amani wa umoja huo. Baada ya kushiriki kazi za ulinzi wa amani katika mipaka mbalimbali ya ndani na nje ya Tanzania. Kazi niliyofanya kwa uaminifu mkubwa, nikiwa mkuu wa operesheni za kijeshi kwenye baadhi ya mipaka.
Kwa takriban miaka miwili nilihudhuria kozi na masomo mbalimbali ndani na nje ya nchi yetu na kutunukiwa vyeti na shahada mbalimbali, katika ngazi za Ukamanda, Utawala na Ukufunzi katika Shule na Vyuo vya Kijeshi vya ndani na nje ya nchi. Uangalizi wa Amani katika kituo cha SADC Regional Peacekeeping Training Centre, kilichopo Harare Zimbabwe, ambako nilirudi kufundisha kozi fupi za ‘UNITED NATIONAL MILITARY OBSERVARS’ na ‘UNITED NATIONAL STAFF OFFICES’ kwa nyakati tofauti.
Nikiwa nimeshiriki kazi za uangalizi wa amani katika mpaka kati ya Ethiopia na Eritrea, kwa miezi saba nilifanya kazi hiyo nikipewa dhamana ya mkuu wa operesheni, nikishirikiana na baadhi ya maofisa kutoka katika nchi za Marekani, Norway, Poland, Romania, Kenya, Zambia, Nigeria, India, China na Ukraine. Waliofanya kazi chini yangu kwa nyakati tofauti.
Kutokana na utendaji wangu kama mlinzi wa amani ‘Observer’ wa UN kwenye mpaka wa Ethiopia na Eritrea, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alinitunuku Medali ya amani, ambayo ilimfanya Kanali Emilly afurahishwe sana. Kutokana na utashi wake ameweza kuiongoza Idara hii nyeti kwa ufanisi mkubwa, kutokana na umri wake kufikia wakati wa kustaafu, serikali iliona kuwa bado anaweza kuhimili mikikimikiki ya kazi aliyoizoea wakamuongezea mkataba wa miaka miwili.
Kutokana na uwezo na msimamo wake huo Kanali Emiily amekuwa akishiriki katika kazi za hatari, ambazo zimemjengea heshima. wakati serikali inaangalia nani atakuwa mrithi wa Kanali Emilly, ilimuongezea mkataba wa miaka hiyo miwili, kitendo ambacho kiliungwa mkono na kila mpenda amani duniani.
Baada ya kumaliza kazi na kupewa medali hiyo kama ilivyo kwa wahitimu wengine kutoka mataifa mbali mbali duniani, nilirejea Dar es Salaam nikiwa na matumaini ya kupata hati ya heshima ambayo ni zawadi kwa jeshi na serikali ya Tanzania.
Kama kawaida hati hiyo ilitumwa kwa Jeshi la Tanzania na kupokelewa na Kanali Emilly, ikinielezea kuwa, nimehitimu vizuri na kupata alama B, alama ambayo ni ya juu kutolewa na Chuo hicho, kilichoko kaskazini mwa Jiji la Moscow, nchini Urusi.
Kanali Emilly alifurahishwa sana mimi kupata alama hiyo ya juu, aliniita ofisini kwake na kunikebehi kwa maneno ya utani kiasi kwamba nami niliamini kuwa ndoto zangu zilikuwa ndoto za Kimweri.
Kanali Emilly alitania, “Yawezekana mambo yalikuwa mazito Teacher, sikutarajia, kijana shupavu kama wewe kuchemka, pole sana mwanangu”, alisema Kanali Emilly mimi nikimwangalia usoni kwa makini.
“Yawezekana mambo yalikuwa magumu, sikutarajia kupata matokeo ya kushangaza kama unavyosema, nilijipanga vizuri, kama imetokea hivyo sina jinsi”, nakumbuka jinsi nilivyomwambia Kanali Emilly akacheka. Umejisikiaje kufanya vibaya, Teacher?”, alihoji tena.
“Nimejisikia vibaya sana, sidhani kama yupo anayependa kufanya vibaya”, nilimwambia.
“Taarifa yako itatoka ubaoni mchana leo, ni taarifa mbaya sana, sina njia nyingine lazima itoke kama ilivyo kawaida”, aliniambia huku akionesha tabasamu, lililonishangaza.
“Naomba isiwekwe kwenye ubao”, nilijaribu kumshawishi akakataa.
“Hapana, unataka niharibu kazi ili nikufurahishe wewe, sikukutuma kufanya madudu”, Kanali Emilly alisema kwa hasira sura yake ilibadilika, nilitoka ndani ya ofisi yake nikitafakari aibu itakayonipata baada ya taarifa hiyo kutolewa.
Nilijiuliza nini nimefanya wakati wa kozi sikupata jibu, nilitembea huku moyo wangu ukisononeka, nikaelekea Kantini, ambako nilikunywa chai na chapati moja tena kwa shida, kisha nikaelekea ofisini kwangu.
Tofauti na jinsi nilivyotarajia, kidogo nipoteze maisha kwa furaha, ubao wa matangazo ulisomeka kuwa nilifaulu vizuri na kupata alama B, alama ambayo ukiipata katika chuo hicho, unatunukiwa cheti cha heshima na Rais wa nchi yako kwa niaba ya Mkuu wa Chuo.
Nilimtafakari Kanali Emilly sikupata jibu, niliporejea mazungumzo yetu ya awali kuwa nimemfedhehesha, nikabaini kuwa Mzee huyu alikuwa akinitania kama ilivyokuwa kawaida yake.
Sikupoteza muda, nilimpigia simu kumfahamisha nilivyofaulu kwa kupata alama B, ambayo tuliipata maofisa wawili, mimi kutoka Tanzania na Meja Charles Katasi wa Jeshi la Uganda.
Kanali Emilly aliniita ofisini kwake na kunifahamisha kuwa, yaliyotokea ni sababu ya furaha aliyokuwa nayo baada ya kupokea hati hiyo. “Unatakiwa Ikulu saa nne ya asubuhi kesho, faili lako limepelekwa kwa Rais, atakubabidhi hati hiyo yeye mwenyewe, maofisa wa ngazi za juu wa Jeshi watakuwepo, inafurahisha sana Teacher”, Kanali Benny alisema huku nikijisikia mwenye furaha ya ajabu kuonana na Rais kesho.
Nilivaa vizuri, nikajipanga pamoja na familia yangu, baada ya kujiweka sawa tulielekea Ikulu, Kanali Emilly na viongozi wengine wa ngazi za juu wa Jeshi walifika kushuhudia tukio hili la aina yake.
Baada ya Rais kunikabidhi hati yangu ya heshima alisema maneno machache, akitoa maagizo kwa maofisa na makamanda wangu kuhakikisha wanathamini mchango wangu na kuongeza vijana na kuwahamasisha kufuata nyayo zangu.
Kutokana na heshima hiyo, nilipewa nafasi ya kutoa neno la shukrani, baada ya kusema niliitwa kupiga picha za kumbukumbu na Rais, maofisa wa Jeshi, familia yangu, wakiwepo watoto wangu wapendwa, Masey, Changasi na Warioba ambaye alibebwa na Rais.
“Karibu Teacher”, mawazo yangu yaliingiliwa na sauti nzito ya Luteni Kanali Matumbi.
“Asante Kamanda”, niliitika huku tukashikana mikono, tukakumbatiana kwa furaha.
“Ni Afande Matumbi?”, nilimuuliza kwa utani na bashasha.
“Hakika ni mimi, wewe ni Teacher?”, yeye pia aliuliza.
“Mwili huu unakula nini Kamanda?”, nilimtania.
“Samaki na viazi”, alijibu kwa utani.
Luteni Kanali Matumbi alinipokea mkoba wangu, kisha mkono wake wa kushoto akaushika mkono wangu wa kuume, tukatembea kuelekea ndani.
“Umenikumbusha mambo ya zamani Teacher, bahati mbaya sana historia hazijirudii, ingekuwa hivyo tungefanya maandalizi ya kutosha kuzirudia historia”, alisema tukacheka.
“Kweli kabisa, unakumbuka opereseni ya kula chakula cha wanafunzi wenzetu kule chuoni Nachingwea”, nilimkumbusha.
“Operesheni ipi hiyo Teacher, maana tumefanya mambo mengi?”, aliuliza wakati tunaingia kwenye sebule ya nyumba yake.
“Wakati wa mafunzo ya awali kule Fam seven teen Nachingwea, tulianzisha operesheni ya kula chakula cha wenzetu, unamkumbuka yule Bahati kutoka Kigoma?”, nilimuuliza.
“Unamkumbuka bwana, alikuwa kijana mchafu sana, alipenda kuiba mchele stoo wakati wa fatiki na kujipikia vichochoroni”, nilimkubusha.
“Bahati… namfahamu sana, alikuwa Kombania C, una kumbukumbu sana Teacher, njaa bwana ni baraa, sikujuwa operesheni ile iliendeshwa na nani?”, alisema akitabasamu.
“Niliifanya mimi”, nilimwambia tukacheka tena. “Maana Bahati alivunja rekodi kwa kukimbia na kofia ya chuma la moto lililokuwa na ubwabwa.
“Ni kweli alitoka Kigoma”.
“Huwezi kuamini, tulijiandaa kama kawaida yetu, baada ya kuwazingira na kuwaachia upenyo ili aweze kukimbia, huku tukiwa tumefunga makaratasi meupe miguuno na upande wa kulia wa mkono mfano wa Military Polisi, tulimkurupusha bwana…”, nilisema huku Meja Matumbi akishika tumbo kwa kucheka. “Lakini ilikuwa kama abiria chunga mzigo wako, akakimbia na mzigo, tukaambulia patupu”.
“Eheee, alikuwa makini sana katika masuala ya misiso”. Siwezi kumsahau, tulipomkurupusha tu, kitendo cha haraka, tena bila kuchelewa, alibeba kofia ya chuma, tena likiwa la moto…, aisee alimudu kukimbia nalo”, nilimwambia huku tukicheka sana.
Baada ya kucheka sana, huku tukikumbushana mambo yaliyotokea wakati tukiwa chuoni, chakula na vinywaji vililetwa tukaanza kula huku tukiulizana hili na lile.
“Teacher”, Luteni Kanali Matumbi aliniita.
“Ndio Kamanda”.
“Kulikuwa na uvumi kuwa Rais wa Sudani Omari al Bashir anatafutwa ili akamatwe na kufikishwa kwenye Mahakama ya kimatafa ya uhalifu wa kivita, kujibu tuhuma za mauaji, uvumi huo uliishia wapi, naamini wewe kiasi fulani unafahamu kinachoendelea”.
Nilivuta pumuzi nikazishusha, nilitafakari kuhusu swali la Meja Matumbi, nikaamini kuwa hata yeye mizozo na migogoro katika nchi za kiafrika inamsumbua sana akilini.
“Ni kweli, mwaka jana mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC, ilitoa hati ya kukamatwa kwa kiongozi huyo wa Sudani, niliwahi kumwambia hata Kanali Emilly kuwa ni vigumu mno kwa kiongozi wa nchi kama Bashir kukamatwa na kufikishwa kwenye mahakama hiyo wakati bado anaongoza nchi, ni vigumu sana”.
“Hakika ni vigumu Teacher, lakiniiii…, wakidhamiria kabisa kabisa wanaweza kufanikiwa”.
“Wampate wapi, ni vigumu sana Bashir kukamatwa”, nilisisitiza.
“Kuna ugumu gani, kwani huyu Bashir hafanyi ziara nje ya Sudani… Wanamvizia akitoka tu, wanamtiwa mikononi, sidhani kama inashindikana”, alishauri Luteni Kanali Matumbi.
“Wewe unaona rahisi, nikwambie sasa, huyu Mzee pamoja na kuwepo hati ya mahakama ya uhalifu wa kivita, amefanya safari zaidi ya kumi nje ya nchi yake, tena bila woga, ni vigumu mno”, nilimwambia akabaki amekodoa macho.
Nilichukuwa glasi ya maji nikanywa kidogo, nilimwangalia kama ana la kusema, nilipoona ananiangalia bila kusema kitu nikatambua kuwa jambo hili limemgusa mno, maana ni mmoja wa maofisa wapenda amani wenye msimamo usioyumbishwa.
“Mbona umenyamaza Mkuu, kama vile umegushwa mno na jambo hili”.
“Teacher, kama ungeweza kujua moyo wangu ulivyo, hakika ungeelewa nini natafakari, viongozi wa aina ya Bashir ndiyo wanaochangia machafuko barani Afrika, mtu mmoja anasababisha mauaji ya mamilioni ya watu, haipendezi Teacher”, alisema kwa uchungu.
“Ni kweli, lakini utafanyaje, migogoro imekuwa migogoro, watu wanauana kama wanyama, hii yote inatokana na udhaifu wetu, angalia mfano mtu kama Jonas Savimbi, aliumiza watu wengi nchini Angola, amewaachia watu vilema vya maisha, ICC haikuwa na ubavu, iliishia kusema na kulaani tu, mpaka alipouawa. Kwanini walishindwa kumtia mikononi?”, nilimwambia.
“Wewe unadhani nini kifanyike kukomesha mauaji ya waafrika, maana kwa takwimu za haraka nchi zaidi ya 30 zinakabiliwa na migogoro mikubwa, inayotishia amani ya dunia, na kati ya nchi hizo zaidi ya ishirini ziko barani Afrika”, alihoji.
“Cha kufanya ni kumuomba Mungu, kwa sababu kila siku mataifa makubwa yanatengeneza silaha, na silaha hizi hazitengenezwi kwa ajili ya wanyama, zinatengenezwa kwa ajili yetu, ili uweze kuwa na nguvu kijeshi, lazima uwe na silaha za kisasa, kila taifa linatamba dhidi ya taifa lingine, unadhani amani itapatikana?”, nilimuuliza akakuna kichwa.
“Azimio la Umoja wa mataifa la kupiga marufuku mapinduzi ya kijeshi duniani linatekelezwa kweli?”, alihoji.
“Hata kama linatekelezwa, mbona halina meno, toka azimio hilo lipitishwe na Umoja wa Mataifa ni nchi ngapi zimepinduliwa na kuongozwa kijeshi, tumeshuhudia baadhi ya nchi Umoja wa Mataifa ukiingilia kati, na sehemu zingine wakisita kufanya hivyo eti ni kuingilia mambo yao ya ndani”.
“Kweli Teacher, ni nyingi”, Luteni Kanali Matumbi alisema kwa sauti ya upole.
“Aisee, tutafute siku nyingine tutaongea zaidi, muda wangu wa kuwepo hapa Musoma umekwisha, labda tuonane Jumamosi wakati narudi Dar es Salaam, nitajitahidi kuwahi ili tuongee zaidi”, nilimuomba Luteni Kanali Matumbi baada ya kuona muda unayoyoma.
“Nilitegemea utalala Musoma, nimekufanyia maandalizi ya kila aina, hebu lala Musoma leo nikutembeze kidogo uone mji”, alishauri nikatingisha kichwa kutokubaliana naye.
“Usijali, lazima niondoke leo, nina shauku kubwa ya kumuona mama yangu mzazi, wajuwa tena Afande, baba na mama ni mungu wa dunia, pamoja na kwamba baba alikwisha tangulia mbele ya haki, tafadhali tuonane siku nyingine”, nilisema nikisimama kutoka sehemu niliyoketi, maana nilikuwa nimekula na kunywa vizuri.
“Ok, sina jinsi Teacher, nilitegemea kuvuna uhondo zaidi kutoka kwako, basi bwana, ngoja nikutowe”, akabeba mkoba wangu tukaelekea nje.
“Usisahau kupita hapa hiyo Jumamosi, nitafanya maandalizi ili usafiri Jumapili”, aliongeza, huku nikitingisha kichwa kukubaliana na mawazo yake, japokuwa haitawezekana kurudi hapa kutokana na ratiba yangu niliyojiwekea. Baada ya kuagana na Luteni Kanali Matumbi nilitafuta usafiri wangu binafsi nikaelekea Nyamuswa.
Jijini Dar es Salaam, kilifanyika kikao cha siri katika nyumba moja ya mfanyabiashara maarufu wa dawa za kulevya. Mfanyabiashara huyu alifahamika kila pembe la Jiji, akiitwa Mzungu Carlos Dimera, Umbo lake lilitosha kabisa kuogopwa na wapinzani wake. Asili ya mzungu huyu ilikuwa ni Corombia. Kutokana na uwezo wake wa kushawishi, Carlos aliweka matawi kadhaa katika nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini. Ndiye aliyeitisha kikao hiki kwa siri kubwa
Kutokana na uwezo wake wa fedha na ushawishi aliokuwa nao kwa baadhi ya viongozi wa serikali kadhaa za Afrika, Carlos Dimera aliweza kuanzisha vikosi kadhaa vya uhalifu ndani ya nchi kadhaa, mojawapo ya vikosi hivyo ni usafirishaji wa shehena kubwa ya dawa za kulevya, kikosi cha wizi kutumia noti bandia na kikosi maalumu cha mauaji dhidi ya watu aliowaita vihelehele. Vihelehele ni wale walioonekana kuingia mambo yake.
Kikao hiki ambacho yeye Carlso Dimera aliwa Mwenyekiti wake, kiliwakutanisha watu wachache, akiwemo mwanamke mmoja tu, Mwana mama huyu aliitwa Hawa Msimbazi, ambaye kutokana na uwezo wake wa kupanga mambo yakawa, wenzake walimfananisha na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani, Condoliza Rice. Hawa alifananishwa kwa mambo mengi na Mmarekani huyo mwenye asili ya Afrika. Tofauti yao ni kwamba yule alikuwa mtendaji katika Serikali ya Marekani, huyu alikuwa mfanyabiashara wa dawa haramu za kulevya Tanzania.
“Mambo yote yamekamilika kwa asilimia tisini na tisa, vijana wamejipanga vizuri kufanikisha kazi hii, kama itakwenda salama kama tulivyojipanga, nawahakikishia kila mmoja atachagua nchi gani atapenda kuishi pamoja na familia yake”, alisema Hamis Nombo, mmoja wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya ambaye kiutendaji ni mtaalam wa mipango katika kikosi.
“Sijui hata niahidi nini, jambo hili si gumu kama mnavyodhania, mambo yote yamefanyika, kama alivyosema Nombo hii ni nafasi yenu kuamua wapi mtapenda kuishi, baada ya kazi hii kumalizika kila mmoja ataihama nchi hii akatumbue raha huko atakapopenda kwenda”, alirudia Dimera.
“Bosi, hakuna sababu ya kuumiza vichwa, vijana wamejipanga vizuri, bahati nzuri ni kwamba muda mfupi uliopita wana spoti wetu wametuletea taarifa kuwa serikali imewatuma vijana wawili kutoka Jeshi la ulinzi kuangalia mambo fulani fulani, watoa taarifa wetu wanasema, vijana hao wametumwa kwa siri, baada ya kuona polisi wanasuasua”, alisema Hawa.
“Safi sana, aliyekuita Condoliza Rice hakukosea, kazi unazofanya ni kielelezo kuwa jambo hili litafanikiwa, cha msingi sasa, watume vujana wako waonane na askari hao, ili wapewe ahadi zao kabisa, lakini pia wasiwaendee mikono mitupu, nadhani pia waingizwe kwenye orodha ya malipo yetu na wafahamishwe”, alishauri Carlos Dimera.
“Jambo hilo limefanyika hata kabla sijasema katika kikao hiki. Mambo ameleta taarifa. Amesema askari hao ni miongoni mwa Makomandoo mahili sana, wana uwezo mkubwa mno, tayari tumeingia nao mkataba. Wako upande wetu sasa”, alisema Hawa Carlos akitabasamu.
“Ni jambo zuri sana Hawa, lazima muelewe kuwa kufanya ishu na watu hatari kama hao lazima tuwe tumejiandaa vizuri pia, tuwe makini nao isije ikawa tunamalizana nao halafu wanaanza kutusumbua”, anashauri Nombo.
“Kweli, lakini niwaambie jambo moja, hebu tumalize kazi kwanza, mengineyo yatakuja baadaye”, Dimera alishauri.
Baada ya ukimya wa sekunde kadhaa, kila mmoja akitafakari hili na lile, Carlos aligonga meza, akatoa angalizo, “Cha msingi tuwe makini na kila hatua tunayopita na kutoka, ahadi yangu kwenu ni malipo mazuri mara dufu, jiandaeni kuishi vizuri.
“Lakini pia tusimsahau Teacher, maana waswahili wanasema usipoziba ufa utajenga ukuta”, alikumbusha Aloyce Jackina, aliyekuwa kimya kwa muda mrefu.
“Hana chochote huyu Teacher, jambo hili likiisha tukafanikiwa kuvuka vikwazo, Teacher atakuwa na nafasi gani?”, alihoji Dimera.
“Ni tahadhali tu natoa bosi”, aliongeza Jackina.
“Umefanya vizuri, ili tuongeze nguvu na umakini”, alisema Hawa.
“Kwa maana hiyo tunaachana baada ya kikao hiki, nawatakia mafanikio mema, tufahamishane kila hatua tutakayokuwa, cha msingi ni kutunza midomo yetu. Tukionana kila mmoja awe na jibu la nchi gani atakwenda kuweka makazi yake ya kudumu” alisema akisimama.
Baada ya kikao hicho, Carlos Dimera alikuwa na kikosi kingine chumba cha pili, watu wawili nadhifu sana walikuwa wakimsubiri. Watu hawa walikuwa wamemaliza kazi waliyotumwa na sasa walikuja kupata maelezo ya kazi nyingine.
“Nimesikia kilio mitaani, watu wanalia, tamaa zao zimewafanya walie, kazi yenu ni nzuri sana, nimefarijika, rafiki yangu mmoja kutoka polisi kituo cha kati amenidokeza kuwa kesi zilizofunguliwa hapo ni waliobiwa kwa mpango wetu, wakati hao bado wanalia na kusaga meno wapo wengine wenye tamaa ya kupata utajiri wa haraka. Wewe Oliver Mapunda hakikisha unaingia Chuo Kikuu Mlimani. Maprofesa pamoja na elimu yao katika dunia, ni wepesi kuingia katika kipindi, wakiingia usifanye makosa”, aliagiza Carlos Dimera. “Naam, nimekusoma bosi”, anadakia Oliver Mapunda aliyekuwa kimya akiwa amefunga mikono yake kifuani.
“Kuna wastaafu waliolipwa mapesa yao baada ya kustaafu, wakati bado wanatafakari nini wazifanyie pesa hizo, sisi tunazitaka. Wewe Masta Bolendile, kazi yako ni hiyo, lakini usiishie hapo, tafuta mahusiano ya karibu na watendaji wa mashirika ya umma, hawa wana mapesa mengi, lakini ni wagumu kuzitoa, tukijipanga vizuri tutazichukua”.
“Naam bosi”, anasema Bolendile.
“Dakika chache zilizopita nimetoka kuzungumza na wenzenu upande wa pili, nimesema baada ya kazi ngumu na nzito iliyo mbele yao, kila mmoja apendekeze nchi gani atapenda kuweka makazi yake ya kudumu, kazi yao ni nzito, kazi ya hatari zaidi ya hii yenu”.
“Kazi zote zina hatari bosi”, Bolendile aliingilia mazungumzo.
“Sawa, lakini hii kazi yenu tunatumia sayansi na teknolojia zaidi, hata ukikamatwa na polisi haina uzito sana. Lakini ‘nga’, umekutwa na unga, lazima yatoke mawe ya uhakika. Naamini kila mmoja amepata mgawo wake sawa. Mtaniletea taarifa za kazi hii baadae. Kila mbinu itumike Teacher auawe, iwe kwa risasi, kisu au hata akitumiwa msichana ammalize kwa sumu, Kwaherini”. Akafunga kikao na kuondoka.
Nyamuswa kama ilivyo kwa miji mingine midogo, iliyoko Bunda, mkoani Mara, ulikuwa umechangamka kwa kiasi, wananchi kutoka sehemu mbalimbali zinazouzunguja mji huu walipishana huku na huku wakifanya mahitaji. Ilikuwa Jumapili ya mwisho wa mwezi. Siku ambayo kila inapowadia wenyewe huiita SIKU YA MTERA NYAMUSWA.
Nilikuwa nimewasili kijijini hapa dakika chache zilizopita, lakini barabara iendayo nyumbani kwa wazazi wangu ilikuwa imefungwa na wafanyabiashara waliokuwa wakiuza bidhaa mbalimbali. Kama ilivyo kawaida yangu, niliutwaa mkoba wangu nikaunjika begani, kisha nikamruhusu dereva aliyenileta aondoke, kwani hakukuwa na njia ya kupita.
Haikupita sekunde mkoba wangu ulipokelewa na Taabu dadangu kipenzi, sikumuona jinsi alivyotokea, alionekana mwenye furaha kupita kiasi, labda alifutahi kuniona tena baada ya kuwa mbali nae kwa muda.
“Pole na safari”, alisema Taabu.
“Mungu amesaidia, habari ya nyumbani?” nilimuuliza wakati tunapita kwenye kundi la watu kuelekea nyumbani.
“Mama pia nilimuona”. alisema akaangaza macho kumtafuta.
“Mwache, mwache asafishe macho. Atanikuta nyumbani”. nilisema huku tukitembea na baadhi ya watu wakitusindikiza kwa macho.
Dakika kadhaa mama naye alifika, hakufanya ajizi moja kwa moja alikuja na kunikumbatia. “Pole na safari mwanangu”, Akaanza kulia, “Ulizoea kutukuta na baba yako, sasa hayupo tena”, alisema mama huku machozi yakianza kumtoka. “Ametuachia ukiwa”, alilala.
Machozi ya mama yalinifanya niwe kimya kwa sekunde kadhaa nikitafakari hili na lile, “Nyamaza mama, kilichotokea ni kazi ya Mungu, baba yatu ametutangulia tu, siku moja tutamuona. Siku zote baba alikuwa akisema hatapenda tumtangulie sisi, alitaka atangulie yeye, kwa kuwa siku yake ilifika, mapenzi ya Mungu yalitimizwa, alihitajika kutoka miongoni mwetu”, nilisema huku nikimuacha mama na kuliendea kaburi la baba kwa ajili yakufanya maombi mafupi.
Baada ya kumuombea mama, tulianza kuzungumza habari nyingine, mama alitaka kujua habari ya safari zangu nje ya nchi, nilimweleza kifupi kuhusu mafanikio ya safari hizo kwa nchi yetu na jinsi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alivyonizawadia tuzo maalum nilipokuwa katika kazi ya ulinzi wa amani. Alionyesha kufurahishwa sana na maelezo yangu, japokuwa hakujua nini heshima ya tuzo hiyo.
Kwa vile nilikuwa nimetoa taarifa mapema niko njiani, mama na dada waliniandalia chakula nikipendacho, ugali na samaki aina ya ningu na nembe. Nimetokea kupenda aina hii ya samaki, ambao hupatikana sana Ziwa Victoria.
Ilipofika saa tisa mchana, nilipita mitaa kadhaa nikiangalia mji, nilivutiwa na maendeleo yaliyokuwa yakifanywa na baadhi ya vijana. Watu walikuwa wengi, na sehemu za starehe kama baa na hoteli zilikuwa zimejaa watu huku wengine wakicheza pool, karata na bao la solo. Nililazimika kumtembelea shemeji yangu mpendwa Mama Feka, ambaye kwa muda mrefu alikuwa na shauku ya kuniona.
“Ah, karibu sana molamu”, alisema Mama Feka akinikumbatia.
“Nafasi ya upendeleo molamu, nina muda mchache sana wa kuwa hapa Nyamuswa, nimehofia jambo moja, nimeogopa usijesikia nilikuwepo na sikukutafuta, sidhani kama ungenielewa?”, nilimuuliza. “Nisingekuelewa kabisa, habari ya Dar… Nadhani umeingia leo”.
“Yes, nimeingia leo na ratiba yangu imebana mno, lakini nitajitahidi kuwepo hapa kwa siku mbili tatu hivi”, nilimwambia.
“Naamini utakuwa umekula, twende maduka saba nikupe japo bia mbili molamu”, alisema. Kabla sijasema kitu haraka aliingia ndani. Hakuchukua hata dakika moja akatoka ameshika kitenge mkononi. “Haya togende molamu”, akatangulia, nikamfuata, tukaelekea hapo maduka saba.
Sehemu hii ilikuwa imechangamka kiasi, vijana ninaowafahamu na nisiowafahamu walikuwa hapa wakiangusha moja moto moja baridi, nilipungiana mikono na vijana hao waliokuwa wakibisha kuhusu mchezo wa mpira, Ligi Kuu ya Tanzania Bara, kati ya Yanga na Simba. Mmoja wa vijana hawa alionekana mwenye jazba sana. “Mwamuzi alichangia kuharibu radha ya mchezo, huwezi kutoa kadi nyekundu dakika za mwanzo kama vile”, alisema kijana huyo kwa ghadhabu.
“Ulitaka aachwe aendelee kufanya makosa uwanjani?”, alihoji kijana mwingine ambaye pia alisimama kuonyesha msisitizo.
“Molamu, huwezi kuamini baada ya mchezo wa Yanga na Simba, ngumi zilipigwa hapa, wengine wakilalamikia kadi nyekundu iliyotolewa na mwamuzi, wengine walidai eti mwamuzi alikuwa sahihi kutoa kadi hiyo, yaani ni vurugu tupu”, alisema Mama Feka nikimwangalia kwa makini.
“Molamu, wewe ni shabiki wa timu gani?”, nilimuuliza.
“Aaah molamu… Mabingwa watetezi Yanga Afrika, nikuletee kadi yangu ya uanachama, usije kusema mimi ni shabiki kishoka”.
“Umesema, nimekuelewa molamu”, nikasimamam kuelekea mahali vijana hao walikuwa wakibishana bila mpangilio.
“Mimi nilijua kabisa kuwa mwanamke hawezi kuchezesha mchezo kama ule”, alirukia kijana mwingine.
“Sikilizeni”, niliwahadhalisha.
“Tumsikilize mzee, naamini alikuwa uwanjani, sisi tunabishana kwa kuona mchezo katika luninga”, alisema Adul Light, mmoja wa vijana hao.
“Kwani luninga ina tofauti gani na kuwa uwanjani, si kila kitu kinaonyeshwa laivu”, alidakia kijana mwingine.
“Ndio maana nikaomba mnisikilize… Lazima mtambue kuwa mchezo wa soka unaendeshwa kwa kanuni na sheria za mchezo, mnaweza kumlaumu mwamuzi wa mchezo huo kuwa alimtoa mchezaji wa Simba kwa kadi nyekundu, lakini ukweli ni kwamba mwamuzi hakutoa kadi nyekundu…”
“Unaona sasa. Inaonekana hukufika hata uwanjani, maana hujui kama mwamuzi alitoa kadi nyekundu, eti jamani mwamuzi hakutoa kadi nyekundu?” alihoji kijana huyo akionyesha kuwa na jazba.
“Ungenisikiliza kwanza”, nilimsihi kijana huyo.” akakubaliana nami. Haraka nikamuomba mtoa huduma awapatie vinywaji. “Kama nilivyotangulia kusema, mchezo wa soka unaendeshwa kwa kanuni na taratibu. Dakika chache baada ya mchezo huo kuanza, mwamuzi alitoa kadi ya njano, kimsingi mchezaji alipaswa kujihami, asifanye makosa. Lakini kabla hata dakika kumi hazijapita akafanya kosa lililostahili kadi ya njano, akapewa yelow card ya pili. Kanuni za soka zinasema, mchezaji akizawadiwa kadi mbili za njano, atapewa kadi nyekundu ili aende nje. Ndiyo maana nikasema hakupewa kadi nyekundu, ila kadi mbili za njano zilimfanya mwamuzi kutoa kadi nyekundu. Si matakwa yake, ni kanuni za mchezo”, nilifafanua.
Vinywaji vikaletwa tukaanza kunywa,
“Hali hii iliwahi kuwakuta hata Yanga, wachezaji wake wawili walitolewa uwanjani kwa nyekundu, na hii si kwa Yanga na Simba tu, tumeshudia hata ligi za Ulaya”, anabaisha Abdul.
“Yes, kadi nyekundu ni sehemu ya mchezo, ndiyo maana mwamuzi anakuwa nazo mfukoni. Lakini pia yafaa mfahamu kuwa mwamuzi anapowajibika pale uwanjani, kuna mamlaka zingine juu yake, kama atakuwa amekwenda kinyume na kanuni anaadhibiwa”, niliwadokeza, wakaonekana kunielewa.
Mara ujumbe mfupi ukaingia kwenye simu yangu, Ujumbe ulisema. “UMEZUKA MOTO NA KUUNGUZA JENGO LA OFISI ZETU ZILIZOKO MTAA WA AZIKIWE, VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA HUSUSAN KIKOSI CHA ZIMA MOTO NA UOKOAJI KINAENDELEA NA KAZI YA KUZIMA MOTO HUO, UNATAKIWA KUREJEA HARAKA KWA AJILI YA TAtHIMINI”, Col. Ben. Kwanza nilicheka, mapigo ya moyo wangu yakaongezeka.
“Molamu, nimepata ujumbe wa kushtua kidogo, natakiwa kurejea haraka Dar, es Salaam, hivi tunavyozungumza, moto umezuka ghafla unateketeza jengo la ofisi zetu mtaa wa Azikiwe, kwa hiyo nalazimika kuondoka sasa hivi”, nilisema wote wakaonekana kushangazwa. Aaah molamu, sina bahati na wewe, jitahidi kuvumilia uondoke kesho mapema”.
“Muda huu utapata usafiri gani kaka?” alihoji Abdul Light.
“Kama nitaweza kufika Mwanza mapema, saa tatu usiku kuna ndege, bahati nzuri rubani wa ndege hii ni mtu wangu wa karibu, nitamjurisha aniwekee nafasi, nilipenda kuwa nanyi, lakini hali ndiyo kama mlivyoona”, nikasimama na kuwaaga kwa mara nyingine nikaondoka.
Ilikuwa saa mbili na dakika arobaini hivi usiku, nilipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Jijini Mwanza, niliwahi kufika uwanjani hapa kama ambavyo inatakiwa abiria wasichelewe kufika kwa ajili ya ukaguzi. Baadhi ya abiria walikuwa wakilalamikia kuachwa na ndege ya saa tisa kwa sababu tu walichelewa kufika uwanjani hapo kwa wakati.
“Nitawashitaki mahakamani, haiwezekani nilipe nauli mara mbili, huu ni wizi”, alisema kijana mmoja aliyekuwa karibu yangu, “Tena niliwahi nusu saa kabla, lakini wakanigomea”, alisisitiza kijana huyo.
“Hata mimi nimewahi nusu saa kabla lakini nikazuiwa kuingia ndani, sasa natakiwa kulipa tenai inashangaza”, alisema mama mmoja kwa jazba. “Haiwezekani, haiwezekani…” aliongeza.
Akili yangu ilikuwa juu ya kuungua kwa jengo la ofisi zetu Dar es Salaam. Lakini nilishangazwa vipi vyombo vya habari kama Televishen na redio havikuwa vimeripoti habari ya tukio hilo kubwa. Labda lilikuwa agizo kutokana na unyeti wa ofisi hizi, Nilijiuliza mambo mengi, baada ya kutafakari kwa kina nikijiuliza hili na lile, wazo likanijia. Nikapiga simu kwa Peter Twite, Dar es Salaam.
“Sikiliza Peter, kwanza habari ya saa hizi… Una taarifa zozote kuhusu ofisi zetu Dar es Salaam?. Niko Mwanza” nilimuuliza baada ya salaam.
“Habari si nzuri Mkuu, moto umezuka ghafla na kuteketeza kabisa ofisi zetu, ninavyoongea niko sehemu ya tukio na kazi ya kuzima moto inaendelea, Kanali Emilly anakusubiri kwa shauku kubwa”, alisema Peter Twite nikashangaa.
“Ananisubiri… kwanini anisubiri kwa shauku… Nitasaidia nini mimi wakati tayari maji yamekwisha kumwagika?”, nilimuuliza akacheka.
“Ukubwa dawa, labda ana jambo lingine la ziada, linapotokea tatizo kubwa kama hili, kila mtu huwa na mtazamo wake, utamsikia ukifika Dar”.
Abiria walikuwa wengi. Ili niweze kusafiri usiku huu, nilikuwa nimewasiliana mapema na rubani wa bdege hii, Mapambano Mussa, kumfahamisha kuhusu umuhimu wa safari yangu, akanihakikishia kuwa nitasafiri na ndege ya saa tatu na nusu.
Mawazo yangu yalikuwa juu ya tukio la kuungua kwa ofisi zetu Dar es Salaam. Sasa akili yangu ilikuwa imeamini baada ya Peter Twite naye kunithibitishia hivyo. Nilipita sehemu ya ukaguzi, baadhi ya abiria walikuwa wakilalamikia gharama kubwa ya kulipia ndoo zenye samaki. Papo hapo pia kulikuwa na malipo ya karatasi laini ya kuzuia harufu. Niliumizwa gharama hizi zilizobuniwa na watu kwa ajili ya kuwaongezea mzigo abiria.
Chumba cha abiria kilikuwa kimejaa, waliobahatika kukaa walikaa na waliokuwa na bahati mbaya kama mimi tulisimama. Ndege ndogo zilikuwa zikiruka na kutua, bila shaka zilikuwa za kukodi. Mara nikamuona abiria mmoja anasimama na kukiacha kiti chake, nilinyata taratibu nikaketi.
“Samahani kaka, usikae pana mwenyewe hapa”, alisemama mama mmoja.
“Pana mwenyewe!”, nilimuuliza kwa mshangao. “Mama, sehemu kama hizi huwa hazina mwenyewe, hizi ni sehemu za huduma, kila mmoja ana haki ya kuketi, mbaya ni kumuondoa mtu kwenye kiti alichowahi kuketi, lakini kama amesimama mwenyewe na mimi nikakaa kuna tatizo”, nilijaribu kufafanua.
“Lakini kama mwenzio amewahi tayari ana haki ya kuwa sehemu yake”. alisema.
“Si kusudio langu kulumbana na wewe, hebu angalia tiketi yako”, akaifungua ili kuangalia, “Angalia namba yako utakayoketi”, akafanya hivyo, baada ya kuangalia kwa sekunde kadhaa akageuka kuniangalia. “Namba iliyoandikwa kwenye tiketi hii ndiyo abiria mwingine hawezi kuingilia, hata mahakamani utakwenda kifua mbele”, nilisema huku nikisimama kumpisha asijeniona mkorofi.
“Keti tu kaka, wajamaa hawabanani, sote ni abiria, tusikosane kwa sababu ya kiti”, alisema mama huyu, nikatabasamu.
“Usijali mamangu, samahani kwa maneno yangu ya utani, usiyachukulie kama ndivyo nilivyo, ni katika kutania tu, tunaposafiri katika chombo kimoja, tumekuwa ndugu katika safari, nikianguka hapa nyote mtaacha kazi zenu kunisaidia, vivyo hivyo na wewe, ukianguka hapa nitakuwa wa kwanza kukusaidia”.
“Shetani apishie mbali, tena ashindwe kabisa kwa jina la yesu”, alidakia mama huyu, mimi nikacheka na baadhi ya abiria pia wakacheka. Foker 27, ndege ya abiria ya shirika la ndege Tanzania iliruka kutoka uwanja wa ndege wa Mwanza saa tatu na dakika arobaini usiku, tayari kwa safari ya kuelekea Dar es Salaam. Abiria wote ndani ya ndege tulikaa kimya tukisubiri hatma yetu. Maana kutoka Mwanza. Ukanda wa Ziwa ViCtoria hadi Dar es Salaam ilipo Bahari ya Hindi ni mwendo wa saa moja na nusu hivi.
“Wewe ni mwenyeji kidogo Dar es Salaam?” Mzee mmoja wa makamo aliniuliza baada ya ndege kuruka na kukaa sawa.
Kwa sababu ambazo sizijui nikamjibu, “Hapana. Leo itakuwa mara yangu ya pili kuingia Dar es Salaam. Una tatizo mzee wangu?”, nilimuuliza.
“Nimeitwa kwenye kikao cha wafanyabiashara. Kikao kimepangwa kufanyika kesho saa tatu asubuhi, eneo la Sinza. Hii ni mara yangu ya kwanza kuingia katika jiji hili”, alisema mzee huyu.
“Kikao kuhusu nini?” nilihoji.
“Ni mambo ya biashara tu. Kuna watu wanatoka nje kwa ajili ya mazungumzo, tumekuwa tukiwasiliana nao kwa njia simu na email, sasa kesho tunakutana rasmi”, alifafanua.
“Vizuri, siku hizi dunia imekuwa kijiji, kila aina ya mawasiliano, usafiri na mambo mengine huwezi kupotea, hata mimi tukishuka nachukua taksi kuelekea Kigamboni waliko ndugu zangu. Wewe unahusika na biashara gani?”.
“Biashara ya nyumba za kulaza wageni Mwanza na Shinyanga, pia nasafirisha abiria kati ya Mwanza na Bariadi, mkoani Simiyu. Kwetu kabisa ni Simiyu”.
“Oh hongera sana, nilikuwa na ndoto ya kuwa mfanyabiashara mkubwa kama wewe lakini ndoto yangu haikutimia, nikaishia kuwa Mwalimu wa shule ya msingi huko Bunda, mkoani Mara”, niliongopa.
“Ualimu si kazi mbaya, sasa hivi waalimu ndiyo wanaangaliwa na serikali kama kioo. Rais wetu hataki mchezo, naamini baada ya mwaka mmoja waliokuwa wanachukia kazi ya ualimu sasa wataitafuta wasiipate”, alisema mzee huyu, pamoja na matamshi yake kuwa ya kiswahili chenye rafudhi ya Kisukuma, nikaanza kuelewa kuwa ni mzungumzaji mzuri.
“Nimefurahi sana kusikia maneno hayo, zamani kazi ya walimu ilikuwa nzuri sana, sijui kilipita nini walimu wakaonekana si lolote, binafsi namshukru sana Rais wetu, kama hali itaendelea hivi heshima yetu itarudi. Nitakupa namba yangu ya simu, pia utanipa namba ya simu yako ili tutafutane kesho baada ya wewe kumaliza kikao”, nilimwambia akaonekana kufurahishwa na maneno yangu.
“Umefuata nini Dar es Salaam?”, alihoji.
“Mdogo wangu ni askari polisi, yuko kituo cha kati”. Baada ya kupeana namba za simu mazungumzo yakaendelea. Tuliongea mambo mengi kuhusu biashara hizi na zile. Nilianza kumpenda mzee huyu, alionekana muungwana sana, labda ndiyo siri ya mafanikio yake.
“Nitakutafuta kesho tukimaliza kikao, nitakuelekeza mahali nilipo, utakuja tutaongea mawili matatu”, alisema wakati ndege inashuka taratibu kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere, Dar es Salaam.
“Naitwa Julius, Mungu akitujaalia tukionana tena tutafahamiana zaidi, nitakuita Bunda siku moja, japokuwa si rahisi masikini kama mimi mwalimu kumuita tajiri kama wewe na ukaja kunitembelea, kama unavyojua masikini kwenda kwa tajiri mara kwa mara ni sawa, lakini tajiri kwenda kwa masikini, akafuate nini?”, nilimwambia.
“Hiyo inategemea na aina ya mtu. Sikiliza Mwalimu Julius, kwanza mimi naitwa Paul Mwifa, nina hoteli Mwanza inaitwa New Rehema, nyingine iko Shinyanga kwa jina hilo na Baria pia. Lakini sina majigambo, uliza wanaonifahamu, nitakukaribisha siku moja utaamini maneno yangu”, alisema huku tukianza kutoka ndani ya ndege hii.
Nilichukua mkoba wangu mdogo nikauvaa, kwa kuwa nilikuwa karibu na mlango wa kutokea wa nyuma nilimuaga mzee Mwifa nikatoka taratibu kuelekea nje. Nilipita sehemu ambayo abiria husubiri mizigo, kwa vile sikuwa na mzigo wa kusubiri nikapita moja kwa moja kuelekea nje. Watu wengi walifika uwanjani hapo kusubiri wageni, baadhi walibeba mabango yenye majina ya watu. Nilipita kimya kimya nikisumbuliwa na baadhi ya madereva taksi, hatmaye nikavutiwa na maelezo ya dereva mmoja nikaingia kwenye gari lake tukaondoka kuelekea mjini.
Wakati dereva wa gari hii anaanza kuondoka uwanja wa ndege, kupitia kwenye kioo cha kushoto, niliweza kuwaona vijana wawili wakikimbia na kuingia kwenye gari iliyokuwa imeegeshwa karibu na sehemu ya malipo ya gharama za uwanja.
“Jitahidi nina haraka kidogo”, nilimwambia dereva akaongeza mwendo. Tulipofika kwenye kizuizi cha kukagua tiketi za malipo, gari hiyo ilisimama nyuma yetu, dereva wangu aliingiza kadi ya malipo, kizuizi kikafungua kuashiria kuwa tumeruhusiwa kupita. Gari hilo pia likafuata taratibu kama tulivyofanya nalo likapita. Ilikuwa BMW nyeusi, ndani kulikuwa na vijana wawili, ambao hata hivyo sikuweza kuwaona vizuri. Haraka nilifungua mkoba wangu nikatoa lens yangu ndogo ambayo hunisaidia kuona vitu vya mbali. Kulikuwa na vijana wanne, kila mmoja alionekana kuwa majukumu yake kama wenyewe walivyokuwa wamepangiana. “Ingia kituo cha mafuta”, nilimwambia dereva wa gari hii akanishangaa.
“Gari yangu ina mafuta ya kutosha, sisi huwa tunajaza full kwa ajili ya kuepuka usumbufu kwa abiria wetu, ni agizo la uwanja, kwa hilo usihofu”, alisema.
“Nataka kuingia Super Market kidogo”, nilidanganya.
“Hapa wanafunga saa nne usiku, sasa ni saa tano na nusu, labda tujaribu Super Market ya Uchumi”, alishauri kijana huyu aliyekuwa akiendesha Toyota Carina muundo wa TI.
Mbele yetu nikaliona gari lingine aina ile ile ya BMW, rangi ya blue, nilipovuta lens yangu kulikuwa na vijana wawili nao wakiwa tayari kutimiza kazi waliyotumwa. Nilijilaumu kwa kutokuweka tahadhari, lakini kwa vile nilikuwa nimegundua hali hii mapema nikajiweka tayari kwa lolote ambalo lingetokea.
Mara ujumbe mfupi ukaingia kwenye simu yangu, ‘KUWA MAKINI BOSI, NYOKA MWENYE SUMU KALI ANATEMBEA KARIBU NA MIGUU YAKO, AKIKUNG’ATA UMEKWISHA’. Wakati tunavuka kwenye taa za kuongoza magari za uwanja wa ndege. Gari lililokuwa mbele yangu lilipungua mwendo ili kuruhusu gari letu lianze kupita kwenye taa hizi.
Ghafla nilisikia kelele za risasi, wakati huo nilikuwa tayari nimejitupa nje na kuliacha gari likiseleleka kuelekea mtaroni. Mara lilitokea Lori lililobeba takataka na kuigonga BMW iliyopunguza mwendo ili kuturuhusu sisi tupite, Vijana wawili waliovalia mavazi yaliyoficha nyuso zao waliruka kutoka kwenye lori na kurusha risasi kuyashambulia magari hayo.
Ilikuwa asubuhi ya misukosuko, vurugu na jitimai, wakazi wa Jiji la Dar es Salaam walikimbia bila mpangilio. Kila mmoja akijaribu kuitetea roho yake, wakati askari kutoka Kikosi Maalum cha Polisi wa Kutuliza Ghasia walipokuwa wakitekeleza moja ya majuku yao ya kuzuia fujo katikati ya Jiji. Wakitumia magari yao ya kazi aina ya Landrover Defender TDI za jeshi la polisi Tanzania, zikiwa na rangi ya blue, bunduki maalum za kurushia mabomu ya moshi zikiwa mikononi mwao. Askari hawa walipita mitaani kifua mbele, wakirusha mabomu ya machozi huku na huku ili kutimiza wajibu wao huo.
Magari haya yaligawanyika katika pande mbili mengine yalielekea upande wa Mnazi Mmoja. Mengine yakaelekea upande wa Ilala, ili kuwakabili vyema wananchi hawa waliodaiwa kukaidi agizo la serikali lililowakataza kufanyabiashara katikati ya jiji. Askari hawa waliendelea kurusha mabomu kila mahali palipoonekana kuwa na mkusanyiko wa watu kuanzia wawili. Hali hii ilionekana sawa na mchezo wa kuigiza. Sikufurahishwa na kitendo hiki cha askari kurusha mabomu bila mpangilio, wananchi sasa walikimbia huku na huku mfano wa Pundamilia waishio kwenye mbuga za wanyama za Serengeti, wanapofukuzwa na mnyama mwenye njaa kali Simba. Hata hivyo kulikuwa na ukaidi wa wazi kutoka kwa raia hawa, ambao walionekana wazi kukaidi amri hii iliyotolewa na polisi kupitia chombo maalum cha kukuza sauti. “Amri ya Jeshi la Polisi, mnatakiwa kutawanyika haraka, vinginevyo tutatumia nguvu kuwatawanya”, sauti ilisikika kutoka katika chombo hicho maalum. Wakati huo mimi nilikuwa nimesimama kwenye ukuta wa Shule ya Msingi Uhuru, karibu na makutano ya Barabara ya Uhuru na Msimbazi, nikifuatilia kwa karibu kasheshe hilo, ambalo kwa kiasi fulani lilibadili sura nzuri ya Jiji la Dar es Salaam, hali ya utulivu ikatoweka na hofu ikachukua sehemu yake. Kumbukumbu za mauaji yaliyosababisha kuwa na wakimbizi wengi katika nchi za Congo, Rwanda na Burundi ikanirudia kichwani. “Hali hii ikiachwa iendelee hivi kama ilivyo sasa, itatuletea matatizo siku za usoni”, nilijisemea moyoni. Nilikumbuka somo la usalama wa ndani, nilifundishwa somo hili na Luteni John John, wakati huo nikiwa mwanafunzi huko Monduli, mkoani Arusha, kuwa askari wanapashwa kufuata taratibu zilizowekwa wakati wa kukabiliana na hali kama hii, kukaidi amri halali. Kila mahali ambapo askari hao waliona kuna mkusanyiko wa watu, walisogea na kurusha kombora, hali ilikuwa mbaya, karibu kila upande kilio kikubwa kilikuwa ni kuwashwa macho, kutokana na moshi huo kuwaingia machoni. Ili hali hii isikupate lazima ufumbe macho, jambo ambalo ni vigumu kukwepa. Mimi pia nilikumbwa na kadhia hii, baada ya bomu lililorushwa kuanguka na kulipuka karibu kabisa na mahali nilipokuwa nimesimama. Kutokana na uzoefu wangu katika majanga kama haya, nilifanikiwa kutoka eneo hilo haraka bila kupatwa na madhara makubwa. Kila kikubwa cha watu ilikuwa ni kuwashwa macho, wengine walikimbilia maji ili kusafisha nyuso zao, lakini wakabaki kutetea kile walichoona kinafaa. Kiasi nilibaini kuwa askari hawa hawakuwa makini katika kutekeleza majukumu yao, nilibaini kuwa iwapo wananchi hawa wakipata silaha zenye ubora kama walizonazo wao huenda wangesalimu amri kutokana na mpangilio wao kuwa mbovu, “Mmmh mfano hali hii ingetokea katika nchi za wenzetu na askari hawa wakafanya mchezo kama hivi, itakuwaje?” nilijiuliza. “Mabomu haya yanayorushwa hovyo, hivi askari hawa hawaoni kuwa wanaitia hasara serikali”, alisema mama mmoja wa makamo alisimama karibu yangu akiyahaha kuyasafisha macho yake. “Hakuna hasara mama, mabomu haya yamenunuliwa na serikali kwa kazi hii, lakini hayakupaswa kutumika sasa, sioni sababu ya tembo kupigana na sungura, polisi wanatumia nguvu kubwa kupambana na adui ambaye hana silaha yoyote ya hatari, nikisema silaha nina maana hata wembe sidhani kama wamebeba hawa”, nilisema. “Kwanini wasitumie silaha kama hizi kukomesha matukio ya ujambazi yaliyokithiri nchini, au kuwakamata maharamia wanaosumbua wanachi katika maeneo ya mipaka na sehemu ya bahari, ambako kila siku tunasikia meli zinatekwa”, alishauri mama huyu. “Kuhusu suala la ujamnazi ni kweli silaha hizi zingesaidia sana mama, lakini hili na kukabiliana na maharamia wanaoteka meli hapa, polisi hawahusiki, hilo ni jukumu la wanajeshi, majukumu ya polisi ni kukabiliana na raia wakorofi, kama hawa waliogoma kutia amri ya serikali”, nilimwambia mama huyu akaonekana kutabasamu. “Nimejifunza kitu kutoka kwako kijana wangu, kumbe mipakani ni jukumu la wanajeshi? Nimeelewa sasa mwanangu”, aliongeza mama huyu aliyekuwa na rafidhi ya mkoa wa Mtwara. Pamoja na rafidhi yake kuwa ya kimakonde, alionekana mama mwenye busara nyingi, baada ya kumtafakari nikabaini kuwa huenda ni mmoja wa viongozi wa taasisi za wanawake ama mjasiriamali. “Kuwasumbua wananchi kwa kuwapiga mabomu kama hivi wewe kwa mtazamo wako unaona sawa?”, aliniuliza. “Si sawa kabisa, lakini pia lazima uangalia chanzo nini? Serikali imetenga bajeti ya kuagiza silaha kama hizi, kwa ajili ya kazi kama hii, lakini busara ilihitajika kwanza, sijui kama wamefuata njia hizo, pengine inatafutwa sababu ili kupunguza masalia ya silaha hizo”, nilimwambia akanikazia macho halafu akacheka. “Kuwachokoza wananchi ili uwarushie mabomu?, hilo umejaribu kuweka chumvi, sijui, labda kwenye Serikali za Kidikteta”, alisema tukacheka huku nikimuaga baada ya hali ya vurugu kutulia kidogo. Gari langu dogo aina ya VW Golf, lenye muundo wa polisi ambalo wengi hawalijui, nililiegesha ndani ya uzio wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, nilifanya hivyo kuepuka hali hii, ambayo baadhi ya watu huitumia kuwaibia wengine kwa mgongo wa watu wenye msimamo mkali. Kilichonifikisha katika eneo hili ni kamba maalum niliyokuwa nikihitaji kuinunua, kamba hii ilikuwa na maana kubwa katika kazi zangu za hatari. Nilikuja kuinunua kamba hii baada ya kutokea shambulizi la kushitukiza wakati niliposhuka Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere. Sikujua walionishambulia walikusudia nini. Lakini pia taarifa ya kuteketea kwa jengo la ofisi zetu iliyotolewa na Kanali Emilly, ambayo si kweli iliniongezea tahadhari. Nilijikuta nikitafakari hili na lile, nikiwaza na kuwazua, nilibaini kuwa kuna tukio la hatari limetokea hivyo, Kanali Emilly alinihitaji haraka ofisi kwake, akalazimika kugeuza lugha, kuwa ofisi zetu tunateketea kwa moto. Hata nilipofuatilia tukio hilo kwenye vyombo vya habari, taarifa hiyo haikuwepo. Hata nilipoongea na Peter Twite, ilionekana hakuna tukio la kuungua jengo la ofisi zetu barabara ya Azikiwe. Baada ya kupata kitendea kazi kilichonileta eneo hili. Yaani, kamba nyembamba lakini madhubuti kwa ajili ya mambo yangu, nilijiondoa taratibu, nikatembea kwa tahadhari kubwa kuelekea lilipo gari langu, kila mtu karibu yangu alionekana kuwa adui yangu, waswahili wanasema uking’atwa na nyota, ukiguswa na ujani unashtuka, ndiyo hali niliyokuwa nayo, nililikagua gari hilo vizuri, baada ya kujiridhisha nikaingia na kuliodoka taratibu kuelekea Posta, ofisini kwa Kanali Emilly.
Niliendesha gari taratibu kuelekea kwenye ofisi zetu zilizoko Barabara ya Azikiwe. Kichwa changu kilishika hili na lile, nilijiuliza maswali mengi ambayo hata hivyo nilikosa maelezo yake. Nilijilaumu kwa kutozima simu yangu ya mkononi nilipokuwa kijijini kwetu Nyamuswa, ningefanya hivyo, pengine sasa ningekuwa nafaidi samaki, kuku wa kienyeji na maziwa ya mtindi.
Kutoka Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, nilipokuwa nimeegesha gari, nilipita kwenye Barabara za Shauri Moyo na Uhuru nikaibukia kwenye taa za kuongoza magari za Karume, ambapo nilisimama kusubiri ruhusa ya taa hizi. Nilipoingia kwenye Barabara ya Rashid Kawawa, niliongeza mwendo kidogo ili kuwafanya madereva wa magari ya nyuma yangu yasipate usumbufu. Nilipolipita eneo la Msimbazi Centre, niliiacha barabara hii nikaingia kulia halafu kulia tena nikaupita Uwanja wa mpira wa Kaunda, unaomilikiwa na Klabu ya Yanga ya Dar es Salaam.
Shambulizi la usiku uwanja wa ndege liliniongezea hofu na umakini katika kufanya maamuzi, nilijiweka tayari kwa lolote, kila mtu alionekana kuwa adui yangu, nilijiuliza maswali mengi, ningekuwa wapi muda huu iwapo shambulizi lile lingefanikiwa, sikujua sababu za watu hao kufanya shambulizi hilo lililolenga kuniondolea maisha, moyo wangu haukuwa na amani tena, nililitilia shaka kila gari lililoonekana kuwa nyuma au mbele yangu.
Ilikuwa vigumu sana kwa mtu asiye na uwezo wa ziada kama wangu kulibaini gari ninaloendesha, nililazimika kutumia gari hii Toyota Brevis ya rafiki yangu Tigani, ili kukwepa shambulizi lingine, japokuwa dunia ya sasa ya sayansi na teknolojia hakuna jambo la siri, lolote laweza kutokea.
Shambulizi hilo lilinithibitishia kuwa watu hawa hawana mchezo na wamejipanga vizuri katika mipango yao ya kazi, nilimtafuta Luteni Fred Libaba kwenye simu yake, baada ya kumpata nilimuuliza mahali alipo akanijulisha kuwa yuko Wizara ya Mambo ya Nje kwa kazi maalum nikamtaka asirudi ofisini mpaka nitakapomjulisha ili baadaye tuonane juu kwa juu nje ya ofisi. **********************
Wakati huo, kikao cha dharura kilifanyika nyumbani kwa mzungu Carlos Dimera. Kikosi maalumu cha matapeli wa kisasa kabisa kikiongozwa na mzungu huyu kilikutana kwa siri kujadili hatua za kuchukua baada ya shambulizi la kumuua Teacher kutofanikiwa.
“Nani aliongoza mpango wa mashambulizi ya usiku kule uwanja wa ndege?” akiwa amechukizwa sana Carlos Dimera aliuliza baada ya wajumbe wote muhimu kufika kwenye kikao hiki.
Tofauti na kikao cha awali kilichofanyika juzi, ambapo Carlos alifanya mazungumza na washiriki pande mbili, kila upande aliupangia majukumu yake, safari hii aliwakutanisha wote, kilikuwa kikao cha pamoja, kikiwahusisha wataalam wa wizi madini feki, watakatishaji wa noti bandia na wasafirishaji wa dawa za kulevya.
“Bosi Carlos… Vijana walijipanga vizuri mno, tulikuwa na asilimia zaidi ya mia kumaliza kazi hii, kwa hili tusitafute mchawi, lazima ufahamu katika mawindo, kuna kuwindwa pia, ndicho kilichotokea usiku. Lakini tukuhakikishie kuwa kutenda kosa siyo kosa, kosa ni kulirudia hilo kosa, leo itakuwa mwisho wa maisha ya Teacher, popote atakapoonekana amekwisha”, alisema Nombo. “Sitaki kusikiliza hadithi za Abunuasi hapa, natoa nafasi ya mwisho, kama Nombo alivyosema kazi hii iishe leo mapema ili tupate uhuru wa kufanya mambo yetu, tukionana kesho tusizungumzie habari ya Teacher tena, nimetenga kiasi cha pesa kwa ajili ya sherehe kubwa, mkimaliza kazi hii vizuri tukutane tupongezane kwa kazi nzuri”, Carlos Dimeta alieleza.
“Pamoja na kikao hiki cha dharura, Nyati, Simba na Chui wako katika mawindo, tunawasiliana kila baada ya dakika tano au kumi, kama unavyowajua vijana hawa bosi, jua la kesho Teacher hawezi kuliona kabisa, hasa nikimfikiria Nyati alivyo Teacher amekwisha”, alieleza Jackina.
Baada ya mpango huu kuwekwa sawa, mjadala mwingine ulianza, walibuni mbinu nyingi za kuchukua pesa kwa wafanyabiashara matajiri na baadhi ya wastaafu walioorodheshwa bila kusababisha madhara. Mbinu hii ilipangwa na Carlos mwenyewe, mzungu huyu alikuwa na mbinu nyingi na kuwafanya washiriki wa mtandao huu kutegemea zaidi mawazo yake.
Pamoja na kumiliki pesa nyingi, ambazo walifanikiwa kuziiba kwenye mabenki kadhaa ya Dar es Salaam. Pia waliweza kusafiri ndani na nje ya nchi wakitumia hati bandia na mbinu hizi na zile kujipatia pesa.
Carlos Dimera alikuwa karibu na baadhi ya viongozi wa serikali. Nchini Tanzania, alikuja nchini kwa mgongo wa mwekezaji aliyekuja kujenga kiwanda cha kutengeneza tembe maalumu za kope za urembo wa akina dada. Kutokana na ukarimu wake alifahamiana na kila mtu. Machoni mzungu huyu alionekana kama rafiki wa kila mtu, lakini moyoni alikuwa adui mkubwa wa maendeleo ya taifa.
Kumbukumbu zilionyesha kuwa mzungu Carlos Dimera alikuwa amefukuzwa kutoka katika baadhi nchi za Afrika ambako alibainika kufadhili vikundi vya wahalifu. Nchi ya mwisho kutimuliwa ilikuwa Rwanda, ambako aliishi kwa zaidi ya miaka mitatu, akitokea Kampala, nchini Uganda baada ya kutiliwa shaka. Alipoingia Dar es Salaam Tanzania hakuwa mgeni katika nchi ya Afrika Mashariki, kwani alimudu kuongea kwa ufasaha lugha ya kiswahili hivyo haraka aliweza kuunda mtandao wake na kuanza kazi rasmi.
Maofisa kadhaa wa idara za serikali, waliokuwa na dhamana ya kusimamia pesa za umma waliibiwa kwa mbinu hizi na zile, baadhi waliona aibu kuripoti taarifa hizo polisi wakihofia kufukuzwa kazi wengine wakijipeleka polisi wenyewe wakidanganya wamevamiwa na majambazi.
Baada ya kuingia Jijini Dar es Salaam, haraka Carlos aliweza kujenga hekalu au jumba kubwa la kisasa kando ya bahari na kuiomba serikali imruhusu kuweka walinzi wake binafsi, baada ya kupata kibali, aliweka ulinzi mkali kuzunguka jumba hili, akiwatumia askari wa kukodi kutoka kitengo maalum cha ujasusi cha Havana, nchini Cuba.
Vinywaji na vyakula vya aina mbalimbali vililetwa, wajumbe walikula, wakanywa na kusaza, wakiifurahia faida ya kazi yao, kila mmoja alionekana mwenye furaha kupita kiasi, wakimuomba mungu awasaidie kufanikisha jukumu lililokuwa mbele yao.
Pamoja na wajumbe hawa, Carlos Dimera, alikuwa na vijana wengine watatu ambao huonekana kwa nadra sana. hawa waliokuwa wamehitimu vizuri mafunzo ya ujasusi sehemu mbalimbali duniani, vijana hawa pia aliwatumia kwa nadra sana, hususan pale Simba, Chui na Nyati wanapokuwa wameshindwa kutimiza moja ya majukumu yao. Simba, Chui na Nyati walikuwa mfano wa mbwa mwitu, kazi yao kubwa ilikuwa kuteka au kuua watu pale wanapoagizwa kufanya vile.
Kufukuzwa kwa Carlos katika baadhi ya nchi hizo haikumfanya kuvunja mitandao yake huko, kazi ziliendelea kama kawaida kwani ndiye aliyeanzisha utapeli wa noti za bandia, pia ndiye muasisi wa kutegesha vyura, mijusi na wadudu kwenye baadhi ya ofisi za serikali na hivyo kuwafanya watumishi wa ofisi hizo, Mawaziri, Makatibu Wakuu wa Wizara na Wakurugenzi kuzikimbia ofisi zao wakiamini kurogwa na wakati huo huo vijana wa Carlos Dimera wanageuka kuwa waganga hodari wa tiba na kufanikiwa kujipatia mapesa mengi kutoka kwa vigogo hao. “Bosi, nakuhakikishia vijana wako tayari kwa kazi, tumefanya mengi kupitia ubunifu wa kichwa chako, ili tusonge mbele lazima mtu afe, mtu huyo anajiita Kapteni Teacher, kama alipona katika shambulizi la jana, leo hawezi kuchomoka, vijana wameapa”, alisema Hawa kwa kujiamini.
Mwana mama huyu alikuwa katili na kipenzi cha Carlos Dimera, alikuwa na sifa kadhaa za kumfanya awe kipenzi cha mzungu huyu, moja ya sifa hizo ni ukatili pia alikuwa na uwezo wa kubadili jambo, akalisimamia kwa nguvu zake zote hata likawa sheria au kanuni.
“Sikilizeni, nimepata ujumbe wa maandishi kutoka kwa wanaspoti wetu, kama mtakumbuka wiki iliyopita tuliweza kuchukua kiasi kikubwa cha pesa kwa watu wawili, mmoja ni Waziri mstaafu huko Mikocheni, mwingine ni mfanyabiashara wa Sinza”. Carlos Dimera aliwaeleza.
“Naam bosi, kilikuwa kibarua kigumu mno, lakini tuliweza kufanikiwa, kuna nini bosi?” alihoji Jackina aliyekuwa kiongozi wa operesheni hiyo.
“Wahusika wametoa taarifa polisi. Lakini sina tatizo na jeshi la polisi, hawa ni watu wetu wanachukua mshahara hapa, mbaya ni kwamba malalamiko yamepelekwa idara ya usalama inayosimamiwa na wanajeshi, Hawa amesema tuna watu wetu huko lakini haitoshi, wanajeshi ni kigeugeu. Jaribio la jana lilikusudia kumuua Teacher na kutoa onyo, baada ya jaribio hilo kushindwa naamini adui yetu atajipanga vizuri zaidi, akionekana popote ua kwanza”, alisema Carlos Dimera.
Baada ya kutafakari kwa sekunde kadhaa, Jakina akasimama, “Taarifa kutoka kwa wana mtandao wetu ni kwamba idara hii inawategemea sana maofisa wake wawili. Huyu Kapteni Teacher na mwingine anaitwa Fred, huyu ni afisa wa cheo cha Luteni.
“Safi sana Jackina, ndiyo sababu nakuamini sana, naamini kazi yako itafanyika vizuri, ukitoka hapa pita kwa mhasibu akuongezee nguvu, ikiwezekana Teacher na huyu Fred wasilione jua la kesho. Lakini jitahidi kuwahadharisha vijana wako wasiende kichwa kichwa kwa watu kama hawa”, Carlos Dimera alishauri.
“Kuhusu hilo ondoa shaka bosi, hivi tunavyoongea vijana wako nyuma yake, tumewahadharisha wasiwe na papara, kazi hizi hazitaki papara, subiri wakati ufike, utasikia”, alisema Jackina kwa kujiamini.
“Naamini kuwa wote mmeinjoy vizuri, haya ndiyo maisha, nani kati yenu atapenda kurudi kijijini, aanze maisha ya kijijini, unaamka alfajiri na jembe mkononi, mazao baada ya miezi sita, unavuna, bado kuna usumbufu kibao, ikiwemo kukopwa mazao na usilipwe kwa wakati au hata usilipwe kabisa”, alihoji Nombo.
Baada ya kupanga mipango ikapangika, kikao kilivunjwa, huku Carlos akisisitiza kupewa taarifa ya kifo cha Teacher mapema iwezekanavyo.
Ofisi zetu ziko ghorofa ya juu katika jengo la Benjamin Wiliam Mkapa. Baada ya kuegesha gari kwenye maegesho ya Hotel JB Belmont, nilikwea ngazi mbili tatu nikaitafuta lifti iliyonipeleka juu kabisa. Shambulizi la usiku lilinifanya niliweka ulinzi wa kutosha kuzunguka eneo la ofisi zetu.
Kazi yangu ya kwanza niliyofanya usiku baada ya kutuliza akili yangu ni kuwasiliana na Sajenti Julius Nyawaminza, huyu ni Komandoo aliyebobea, akilitumikia jeshi katika vikosi vya Zanzibar. Nilimwagiza kufika haraka Dar es Salaam, kwa vile Unguja ni karibu alifika Jijini asubuhi na kujiweka kwenye pointi niliyompangia awe.
Kwa kuwa vijana wetu wa Dar es Salaam wanafahamika kwa kiasi fulani, nilipanga kuwatumia kwa kazi zingine, hivyo niliwasiliana pia na Luteni, Claud Mwita kutoka vikosi vya Komandoo mkoani Morogoro, ambaye pia aliweza kufika kwa wakati, akafanya kile alichoelekezwa kufanya.
Nilichelewa kwa dakika kadhaa kufika ofisini kwa Kanali Emilly kama ambavyo tulikuwa tumeafikiana, kuchelewa kwangu kulitokana na mipango ya hapa na pale, maana mtu akikuanza utani lazima ujiandae kutaniana naye, lakini pia akikuanza uchokozi muonyeshe kuwa amepita njia mbaya.
Mapokezi nilipokelewa na Linnah David, Katibu Muhtasi wa Kanali Emilly, “Ulikuwa wapi Teacher? Mzee anakusubiri kwa shauku kubwa, amesema ukitia pua tu, usisimame, moja kwa moja ingia ofisini kwake”, Linnah alitania.
“Vipi hali yako Linnah, sikukuacha ofisini, nilisikia wewe pia umepata likizo kulikoni? Au ndiyo umeitwa haraka kama mimi?”, nilimuuliza akatabasamu.
“Nitakwambia ukitoka kwa bosi”, alisema Linnah huku akinihimiza kuingia ndani ya ofisi ya Kanali Emilly.
Mapigo ya moyo wangu yalianza kunienda mbio, sikujua kilichotokea hata nikaitwa haraka kiasi hiki, taratibu niligonga mlango wa ofisi ya bosi, baada ya kusubiri kwa sekunde kadhaa nilitasua kitasa cha mlango na kuingia ndani. Kanali Emilly aliponiona haraka alisimama na kunielekeza sehemu ya kuketi. Nilishangazwa na hatua hii, kunielekeza mahali pa kukaa karibu kabisa na yeye tofauti kabisa na kawaida yake.
Kanali Emilly alikuwa mzee wa makamo, lakini mwenye busara na nguvu nyingi, hakuwa mwepesi wa kushindwa jambo. Baada ya kupeana mikono na mimi kuketi mahali aliponielekeza, aliinua simu yake ya mezani akamwagiza Linnah atuletee vinywaji. Kabla ya kukata simu, Kanali Emilly alimtaka Linnah kuongeza vinywaji kwa ajili ya wageni wanaokuja. Mimi nikabaki kimya.
“Karibu sana Teacher, pole kwa kukatisha likizo yako fupi, nimekuita kwa sababu kuna tatizo limetusibu, tutakuwa na wageni hapa ofisini muda si mrefu, wanakuja kuongea na sisi, tutawasikiliza, tutashauriana nini cha kufanya”, alisema Kanali Emilly, aliinua tena simu yake ya mezani akaongea na watu ambao mimi sikuwajua, akawajulisha kuwa mimi nimefika hivyo waje ofisini kwake. “Kuna tatizo gani bosi, maana sielewi kinachoendelea?” nilimuuliza Kanali Emilly.
“Kuna tatizo kidogo limetoke. Nikaitwa haraka nyumba kubwa, kutakiwa kurudi kwako haraka ni agizo la Rais. Wakati tunawasubiri hawa ndugu zetu, nitakudokeza kidogo kilichotokea”, alifungua droo ya meza yake, akatoa bahasha kubwa iliyojaa mapesa, pia akatoa kiboksi kilichojaa makaratasi yaliyoandaliwa kama pesa, akanipatia.
“Hizi ni pesa zangu?”, nilimuuliza Kanali Emilly akache
“Ziangalie kwanza Teacher, halafu nitakueleza sababu”.
Zilikuwa pesa nyingi zinazotumika katika mataifa mbalimbali duniani. Zilikuwepo noti za shilingi elfu kumi za kitanzania, nilizipitia noti hizi moja baada ya nyingine, sikuona tofauti. Niliendelea kuziangalia noti hizi kwa umakini mkubwa, zilikuwepo noti za Saandaang Piso zinazotumika Jamhuri ya watu wa Philipines, Diez ya Uruguay, Paundi ya Misri, Birr ya Ethiopia, Yen ya Japan na Won ya Korea Kusini.
Niliendelea kuzipitia pesa hizi kwa umakini sana, Kanali Emilly alikaa kimya akiniangalia, sikufahamu lengo la mzee huyu kunipatia pesa hizi niziangalie tu. Niliendelea na zoezi la kuzikagua noti hizi, Rupiah ya Indonesia, Rupee ya Pakistan, Rand ya South Afrika, Afghan ya Afghanistan, Rouble ya Belerus na Peso ya Cuba.
Kulikuwa na idadi kubwa ya noti, ni vizuri nikutajie aina zote za noti zilizoko mbele yetu ili uweze kunielewa vizuri, kabla mzee hajasema jambo.
Aina nyingine ya pesa sikuwahi kuziona kabisa, kama Rouble ya Russia, Litu ya Luthuania, shilingi ya Kenya, Franc ya Afrika ya Kati, Real ya Brazil, Drams ya Armenia, Lira ya Uturuki, Krone ya Denmark na Riyal ya Saudi Arabia. Zingine ni Paund ya Sudan, Lei ya Romani, Dong ya Vietnam, Dollah ya New Zealand, Peso ya Argentina, Dinar ya Libya, Hryvmy ya Ukraine, Sum ya Uzbekistan, Kwacha ya Zambia, Franc ya Kongo, Franc ya Chad, Dinar ya Algeria, Rouble ya India, Franc ya Cameroun, Mark ya Ujeruman na Dollar ya Marekani.
Baada ya kuzipitia pesa hizi, nikazirejesha mikononi mwa Kanali Emilly, ambaye alizijaza kwenye bahasha kubwa, akaniangalia kwa sekunde mbili tatu, alipoona nimekaa kimya nikimwangalia akatoa bahasha nyingine iliyojazwa makaratasi yaliyokatwa kwa mpangilio mzuri mfano wa pesa. Karatasi hizi zilifungwa kwa mafungu sawa na noti, zikitofautiana kwa ukubwa wa aina ya pesa husika.
Niliendelea kuumiza kichwa changu, nilijiuliza sababu ya Kanali Emilly kuleta pesa hizi mbele yangu, kilichoanza kunizindua ni haya makaratasi yaliyokatwa mfano wa pesa, mawazo yangu hayakunipeleka mbali, nikahisi kuwa huenda karatasi hizi zimekamatwa kwa matapeli waliotapakaa kila kono ya miji ya Afrika Mashariki na duniani, wakiwaibia watu kila siku.
“Naam kamanda wangu, nifahamishe sasa. Kuna habari gani mkuu?”, nilimuuliza baada ya kumaliza kazi ya kuzipitia karatasi alizokuwa amenipatia. “Hizi noti na karatasi nahisi zimekamatwa kwa matapeli”, niliongeza.
“Afadhali tungekuwa tumewakamata, Teacher hili ni tukio linalotia huruma sana, huwezi kuamini nikikueleza kile kilichofanyika, watu wameuza majumba, magari na wengine wamefirisika kabisa kutokana na pesa na karatasi hizi ulizoziona”, Kanali Emilly alieleza.
“Ehee?”, nilihoji huku nikikiweka tayari kumsikiliza. Mara simu ikaita, akainua mkonga wa simu na kuiweka katika sikio lake la kushoto, baada ya muda alisema, “Waruhusu wapite tafadhali”, akaweka simu chini.
“Teacher, kabla sijakueleza hali halisi ya tukio hili, bahati nzuri wahusika wamefika, utawasikiliza kwa makini, wataeleza kilichowasibu, sidhani kama tutashindwa kuwasaidia katika hili”, alisema Kanali Emilly.
“Itategemea na kazi yenyewe bosi, kama ujuavyo hii ni dunia, hata uwe mjuzi wa kuogelea kiasi gani, iko siku maji yatakuzidi ujanja, unaweza kuingia mpaka kimo fulani ukashindwa kuendelea, lolote laweza kutokea”, nilimwambia. Sikuona vizuri kumsimulia kuhusu tukio la usiku, hivyo nilimezea.
Mlango wa ofisi uligongwa, Linnah akaingia akifuatiwa na watu wawili waliotakata vizuri, ukiwaangalia huhitaji kuuliza, moja kwa moja niliamini kuwa watu hawa ni vigogo kutoka serikalini ama matajiri wenye mapesa yao.
Sajenti Julius Nyawaminza aliwasili bandarini, Dar es Salaam kwa Meli ya Kilimanjaro II majira ya saa moja na dakika ishirini asubuhi akitokea Visiwani Zanzibar. Baada ya kuwasili Dar es Salaam, kutoka bandarini, Nyawaminza alitembea kwa miguu yake hadi eneo la Posta mpya kama alivyokuwa ameelekezwa. Kijana huyu alikuwa na shauku ya kufanya kazi aliyokuja kuifanya Dar es Salaam, alifikiria mambo mengi aliyozungumza na Teacher usiku, akajiona mwenye bahati kipindi hiki kuitwa kufanya kazi katika mazingira aliyokuwa akiyasubiri kwa siku nyingi. Baada ya kuhitimu kozi mbalimbali za kijeshi ndani na nje ya nchi, Sajenti Julius Nyawaminza alipangiwa kazi katika vikosi vya Zanzibar. Akiwa Visiwani Zanzibar, alifanya mazoezi yake ya kawaida kila siku akisubiri hali mbaya itokee. Yeyote angemuona barabarani kwa bahati mbaya asingeamini kuwa kijana huyu ni moto wa kuotea mbali, kama huamini mtafute umchokoze ili uamini haya niyasemayo.. Begani, Nyawaminza alining’iniza mkoba wake mdogo wenye vifaa vyake kadhaa vya kazi. Alipofika eneo la Posta mpya alinunua gazeti la michezo, akaketi kwenye mojawapo wa vibanda vya abiria wanaosubiri usafiri vilivyoko mbele ya jengo la Benjamini Wiliam Mkapa na Benki ya CRDB. Luteni Claud Mwita, kutoka mkoani Morogoro, naye pia alikuwa amewasili katika eneo hilo, yeye alitumia usafiri wa bodaboda kutoka Ubungo, alifanya hivyo kutokana na hali ya barabara za Dar es Salaam asubuhi kuwa na msongamano wa magari mengi, hususan wakati wa kuelekea katikati ya Jiji. Kama alivyofanya Sajenti Julius Nyawaminza, Claud Mwita alitafuta gazeti ya michezo, baada ya kupitia vichwa vya habari vya gazeti hili, akatafuta uelekeo akaweka makazi yake ya muda akisubiri taarifa kutoka kwa Teacher. Pamoja na kusoma magazeti, vijana hawa walifika hapa kwa kazi maalum, kuangalia aina ya watu wanaofika eneo hilo na muda wa kukaa kusubiri usafiri wa daladala ama taksi zilizoegeshwa katika eneo hilo. Kila mmoja kwa wakati wake alituma ujumbe mfupi wa maneno kumfahamisha Teacher kuwa tayari amefika na yuko kwenye pointi ya kazi. Nao Simba, Nyati na Chui kama wanavyofahamika, walifika eneo hilo mapema zaidi, hawa waligawana njia za kuingia na kutoka katika jengo hilo, Simba akiulinda mlango mkuu wa mbele unaoangalia kituo cha daladala, Nyati akajiweka upande wa kuingia na kutoka magari, Chui akaimalisha ulinzi kwenye mlango mdogo unaotokea sehemu ya maduka kama unatokea barabara ya Jamhuri. Teacher aliingia ofisini kwa Kanali Emilly na kuonyeshwa karatasi zilizoandaliwa mfano wa noti, lakini zilikuwa bandia. “Karibuni”, Kanali Beny Emilly alisimama kuwakaribisha wageni hawa. Kwa sheria za kijeshi ilinilazimu mimi pia kusimama ili kumuunga mkono bosi wangu. Baada ya wageni hawa kushikana mikono na mzee huyu, wakanishika mkono. “Karibuni, karibuni sana, mnaweza kuketi”, Kanali Emilly alirudia kusema huku akiwaonyesha sehemu za kuketi. “Shukrani sana”, walisema wageni hawa kwa pamoja huku wakiketi taratibu kwenye viti vilivyokuwa mbele yangu. Kutokana na uzoefu wangu wa kazi nikabaini kuwa wageni hawa walikuwa na tatizo zito linalosumbua nafsi zao. “Karibuni tena ndugu zangu, karibuni sana hapa ofisini kwangu, huyu kijana ndiye Teacher ambaye niliwafahamisha amesafiri, nikaona ni vizuri tumsubiri awepo ili tuzungumze wote kuona namna ya kusaidia jambo hili”, Kanali Emilly alisema akiwaangalia wageni hawa. Halafu akanigeukia, “Teacher, hawa ni wageni wetu, nimefarijika kukuona umerejea wakati muafaka kabisa, dunia ya sasa hakuna siri, jana niliitwa Ikulu kwa mheshimiwa Rais, nimeulizwa maswali mengi ambayo nimekosa majibu, nikaamini kuwa ukirudi tutajadiliana na majibu yatapatikana, ndivyo ninavyoamini”, alisema huku nikimwangalia kwa makini. Aliinua simu yake ya mezani akampigia Katibu Mahsusi wake Linnah, akamwambia atuletee vinywaji juisi, soda, maji na sambusa. Haikupita hata dakika tano, vinywaji vililetwa, tukaanza kunywa huku kila mmoja akiliweka tayari koo lake kwa mazungumzo. “Mko tayari kwa mazungumzo yaliyowaleta, ni muda muafaka sasa kuzungumza?”, Kanali Emilly aliwauliza watu hawa. “Naam, tunaweza kuanza mazungumzo yetu”, alisema mmoja wa watu hawa huku akimwangalia mwenzake usoni, mfano wa mtu anayeomba ridhaa ama kibali kwa ajili ya kuanza kutoa maelezo. “Itapendeza kama mtaeleza kuanzia mwanzo ili tuwe pamoja na Teacher katika mazungumzo haya”, Kanali Emilly aliwaeleza watu hawa, halafu akanigeukia mimi”, “Teacher jana nilikutana na watu hawa, walinisimulia kwa undani kuhusu jambo hili lakini itapendeza zaidi wakirudia mbele yako ili upate picha kamili” aliniambia. “Kijana au Teacher kama mzee wetu anavyokuita. Naamini utaelewa vizuri nikianza kwa kujitambulisha, sisi ni nani tunatoka wapi na tumefika hapa kwa sababu gani?”. “Naam”, nilijibu kwa mkato. “Asante. Mimi binafsi naitwa Enock Nyanda, mkaazi wa Msasani ni mfanyabiashara maarufu hapa Jijini Dar es salaam”, alisema huku akiniangalia, nikamuonyesha ishara aendelee. “Huyu mwenzangu anaitwa mzee Sadik Tagazi, makazi yake pia ni Msasani, ni mfanyabiashara wa siku nyingi… Kijana wangu, naamini nitaeleweka vizuri kwako nikisema wazi kuwa tamaa ya kupata mali nyingi imeniponza mimi, imemponza hata huyu mzee mwenzangu, tumeingizwa mjini, nimeibiwa kiasi kikubwa cha pesa, huyu mzee mwenzangu pia amefanyiwa hivyo hivyo, tumeumizwa”, alisema huku machozi yakianza kumtoka, jambo ambalo kwa kiasi fulani liliushitua sana moyo wangu. “Ehee, ilikuwaje mpaka mkaibiwa kiasi kikubwa cha pesa kama ulivyosema”, nilihoji huku akili yangu ikibadilika, maana tukio hili ni moja ya matukio ya kawaida ambayo huwatokea watu kila siku, mawazo yangu yakarejea shambulizi la usiku, nikajiuliza ni wizi huu wa pesa uliosababisha nishambuliwe na kuponea chupuchupu. “Labda, niseme wazi kuwa watu hawa wametumika teknolojia ya kisasa sana, naamini kwa teknolojia hii hata nani angeibiwa, mimi ni mtu makini sana, lakini huwezi amini nimeibiwa kirahisi mno”, anaeleza mzee Sadik ambaye kwa muda mrefu alikuwa kimya. “Ni teknolojia ipi hiyo, mbona mnazunguka tu hamsemi wazi?”, niliwauliza. “Nimewapa nafasi ya kuzungumza, ndiyo maana nikasema uwanja ni wenu, tusipoteze muda, cha msingi elezeni nini kilitokea mpaka mkaibiwa, jambo hili ni kweli linaweza kumpata kila mtu, lakini mengine ni uzembe wa mtu”, alisema Kanali Emilly kwa hasira. “Si kusudi letu kupoteza muda, tunataka kueleza jambo hili kwa kinagaubaga zaidi ili muone jinsi ya kutusaidia pia kuwanusuru ndugu wengine wanaokusudiwa kuibiwa kama sisi, nashauri mwenzangu aanze maana yeye ana taarifa nzuri na muhimu zaidi”, alisema mzee Enock. “Leo ni tarehe ngapi”, alihoji mzee Sadik. “Leo… Jumatatu ya Machi 21, unataka kusema nini?”, Kanali Emilly alieleza na kuhoji. “Ehee ni jambo zito lakini nitafanyaje, Machi 13, mwaka huu watu wawili nadhifu sana walifika ofisini kwangu… Nitaeleza kwa kifupi, utaniuliza maswali itakapobidi”, alisema mzee Sadik. “Baada ya watu hawa kufika ofisini kwangu, tulianzia mbali sana, niliamini ni watu safi, tena waungwana sana, wakajitambulisha kuwa wanafanya kazi katika ubalozi mmoja nchini Tanzania, baada ya kujitambulisha walitoa karatasi fulani kuwa hizo ni dola za Kimarekani ambazo hazijasafishwa”, alinyamaza kidogo ili kumeza mate. Linnah aliingia ofisini kwa Kanali Emilly akiwa amebeba faili kubwa, aliliweka sehemu ya mafaili yanayoingia halafu akaniangalia na kufinya jicho lake, nikatabasamu akatoka. “Ehee, leta habari, baada ya kuonyeshwa karatasi hizo ambazo walidai ni dola wewe kama wewe uliamini kuwa ni dola?”, nilimuuliza. Alionekana kupagawa, kiasi fulani alionekana mwenye aibu kiasi. “Teacher, ukweli ni kwamba hawa jamaa zetu wameibiwa lakini inashangaza jinsi wanavyoona abu kueleza ukweli kuhusu tukio hili, kwa uzoefu wangu, baada ya kukutana nao na kuzungumza nao jana, nimeamini kuwa hawapendi jambo hili litoke nje, yaani kwenye vyombo vya habari, hilo tumelizingatia, sasa watueleze kwa undani jambo hili lilivyotokea”, Kanali Emilly alieleza. “Kama ulivyosema, itakuwa fedheha iwapo tukio hili litarushwa kwenye vyombo vya habari, vinginevyo hakuna tunachoficha, ndio maana nikasema tumeibiwa, wezi wametumia teknolojia ya kisasa kabisa, hata hivyo mimi na mwenzangu tunakiri kuwa tamaa ya kupata utajiri zaidi imetuponza. Kama ambavyo nilivyotangulia kusema, watu hawa walijitambulisha kuwa wanatoka ubalozi wa Marekani na walifika kwangu wakidai kuwa wanatafuta mtu mwaminifu ili wamkabidhi hizo dola azisimamie wakati wa kusafishwa, na kwamba mtu waliyemuona ni mimi”, alisema mzee Sadik. “Uliwauliza, walikufahamu vipi?”, nilimuuliza. “Naam, niliwauliza wamenifahamu vipi, pia niliwauliza wanajuaje kuwa mimi ni mwaminifu katika masuala ya pesa, mmoja wao alisema amepata kusikia sifa zangu na ndiye aliyependekeza waje kwangu, mara moka nikayaamini maneno yake”, alisema mzee Sadik. Nikajiweka vizuri kwenye kiti ili niweze kusikia habari hii, maana kwa kiasi fulani ilianza kuusisimua mwili wangu, “Baada ya hapo nini kiliendelea?”. “Baada ya kuongea mambo kadhaa na watu hawa, nikiuliza maswali nao wakijibu, hatmaye walinidokeza kuwa baada ya tukio la wizi wa dola milioni mbili za Kimarekeni, lililotokea Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, usafirishaji wa dola, paundi na pesa zingine zinazoingizwa nchini Tanzania ulibadilishwa, sasa zinaingia kama karatasi halafu zinasafishwa kwa dawa maalumu ili zianze kutumika kama dola”, alinyamaza kidogo ili kupisha swali, alipoona nimekaa kimya akaendelea. “Nilihoji pia, ili kujuwa kama ni tukio hilo la wizi tu lililopelekea pesa zote zinazoingizwa nchini Tanzania kuchafuliwa, pia nilitaka kujuwa hali hiyo ni kwa Tanzania peke yake, watu hao ambao walikuwa wakiongea taratibu kwa kujiamini sana, walisema uhalifu umeongezeka sana duniani hivyo mamlaka za fedha zimeona hiyo ndiyo njia salama zaidi ya kusafirisha pesa”, alieleza. Aisee ni stori tamu sana, endelea nakusikiliza”, nilisema huku Kanali Emilly akitabasamu. “Baada ya majadiliano ya muda mrefu, maofisa hawa waliodai kuwa wanatoka Ubalozi, walitoa mfano wa karatasi kadhaa zikiwa na rangi nyeusi, wakadai kuwa hizo ni dola orijino ambazo huletwa nchini na baadaye kusafishwa kwa dawa maalumu ambayo walisema pamoja na kupatikana kwake kuwa vigumu, wao wanajua mahali pa kuipata na kazi hiyo ikafanyika vizuri. Una swali?”, aliuliza huku akiniangalia usoni, macho yetu yalipokutana, alionekana wazi kuwa mwenye aibu. “Teacher, karatasi anazoeleza mzee Sadik nimekuonyesha kabla hatujaanza mazungumzo”, alisema Kanali Emilly nikatikisa kichwa kukubaliana naye. “Sasa ilikuwaje ukaamini kuwa hizi karatasi ni dola?”, nilimuuliza baada ya kusimama, nikazichukua zile karatasi alizonionyesha Kanali Emilly, nikamuonyesha, maana maelezo haya yaliniingia vizuri, nikasahau kama nilikuwa likizo. “Lo, sijui shetani gani aliniingia, mwanzo sikuwaanini kabisa, nilipanga kupiga simu kuwajulisha polisi kuhusu watu hawa ili wakamatwe, lakini baadaye nilishawishika kuwaomba vitambulisho vyao, hakika vilikuwa vitambulisho vya ubalozi wa Marekani, nikaanza kuyaamini maneno yao, nikaingia kwenye mtego baada ya mmoja wa maofisa hawa kutoa dawa na kusafisha karatasi kadhaa ambazo ziligeuka kuwa dola halali kwa matumizi. Hakika nilianza kusadiki, baada ya kudai kuwa dawa waliyonayo ni kidogo haiwezi kusafisha zaidi ya karatasi ishirini”, alinyamaza kidogo akachukua glasi yake ya juisi akanywa kiasi huku midomo yake ikimcheza mfano wa mtu aliyekutana na baridi kali. “Teacher, nakuhakikishia kuwa, kazi ya kusafisha karatasi hizo na kuwa dola ilifanyika mbele ya macho yangu, nilifuatilia tukio hilo kwa umakini wa hali ya juu. Karatasi kumi ziliingizwa kwenye dawa nikiona, baada ya sekunde kadhaa zikatolewa zikiwa tayari zimebadilika na kuwa dola mia mia za Kimarekani, wakati huo boksi kadhaa zilikuwa kando zikiwa zimesheheni karatasi hizo, hakika nikauona utajiri mkubwa mbele yangu, nikajua sasa nimeukata”, alisema mzee Sadik, alinyamaza kupisha kama kuna mtu mwenye swali, alipoona kimya akaeleza. Baada ya karatasi hizo kusafishwa na kila moja ilikuwa dola mia za Kimarekani kuonekana, walinikabidhi, halafu wakaanza kusafisha karatasi ambazo walidai ni paundi za Uingereza ambazo pia zilipotakata zilikuwa paundi mia kila moja. Wakadai dawa hiyo imeisha nguvu, wanatafuta watu wa kusaidia ili karatasi hizo zisafishwe na kuwa dola. Wakanipatia dola zilizosafishwa ili niende sehemu ya kubadilishia pesa kuthibitishe kama ni dola halali, nikafanya hivyo, hakika zilikuwa dola halali kabisa, nikajiona mwenye bahati kuonana na watu hawa”. “Aisee, kweli hapo hakuna ujanja, lazima utaibiwa tu”, nilimwambia akacheka kidogo huku akisisitiza kuwa huo ni wizi ambao si rahisi mtu kukwepa, labda uwe fukara. Na jamaa hawa hawamfuati mtu asiye na kitu. “Tamaa ya kupata pesa nyingi imeniponza”, alisema akitoa kitambaa cha jasho mfukoni akafuta machozi yaliyokuwa yakimtoka. “Karatasi walizokuja nazo ofisini kwako na kudai kuwa ni dola ambazo hazijasafishwa, waliziacha kwako?”. niliuliza.
“Yes, waliziacha karatasi hizo kwangu huku wakisisitiza kuwa nisitoe taarifa hii kwa mtu yeyote, wakadai kuwa wangerudi kesho yake mapema kuangalia kama nimebadili dola, ili tuangalie uwezekano wa kupata pesa za kununua dawa kwa ajili ya kusafisha karatasi zilizobaki, ambazo walidai iwapo zitasafishwa zote ni zaidi ya shilingi bilioni tano za Tanzania, nilifurahi sana”, alisema mzee huyu. “Kama ndivyo, mbona wewe umefaidika”, nilimwambia. “Hapana, nimeumia sana Teacher, waliporudi mara ya pili walinieleza kuwa karatasi hizo zina thamani kubwa sana, ni mapesa ya kigeni yanayosubiri kusafishwa, kwa hiyo waliniomba mimi kama mwenyeji wao niwatafutie mtu mwenye pesa ili tununue dawa na kusafisha karatasi hizo, ambazo wao walidai kuwa waliziiba ubalozini”, anabainisha. “Ndipo wewe ulipotoa pesa?”, nilimuuliza. “Hapana, kwa vile walinieleza kuwa dawa ya kusafisha karatasi hizi inauzwa kwa bei mbaya, nilimfuata mzee mwenzangu, Enock Nyanda, baada ya kumshawishi alikubali tushirikiane kutoa pesa ili dawa ipatikane, ndipo kazi ya kutafuta dawa ilipoanza”. “Hapo ndiyo patamu sasa, ehee?”, niliteka masikio. Baada ya utaratibu wa pesa kupatikana, maofiosa hawa kutoka ubalozi walituambia kuwa, sehemu ambayo tunaweza kupata dawa ni kwenye maabara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Walishauri kuwasiliana na Profesa waliyedai kuwa anahusika na maabara ya chuo, baada ya kuwasiliana naye kwa simu yake ya mkononi, alitupangia muda ya kwenda kumuona”, alitulia kidogo, akaonesha hasira iliyokuwa katika nafsi yake, halafu akacheka. “”Watu hawa walijipanga vizuri”, nilijisemea. “Hakika, kwa mchezo huu walijipanga vizuri kuhakikisha wanafanikiwa”, alirukia Kanali Emilly. “Inaonyesha hivyo. Maana siku iliyofuata tulifika eneo la chuo kikuu, tukakutana na Profesa mmoja anaitwa Davis Magajimbo, kwa vile alikuwa ametuelekeza sehemu ya kumuona, Baada ya kumfahamisha kuwa tunahitaji dawa ya kusafisha dola, alitueleza kuwa dawa hiyo inauzwa bei mbaya na ili kuipata lazima zipatikane shilingi milioni mia moja za kitanzania”, alisema, baada ya kutafakari kidogo akaendelea. Kutokana na thamani ya dola na wingi wa karatasi zilizokuwa zimeandaliwa kwa ajili ya kusafishwa, tulikubali kutoa kiasi hicho cha pesa kwa Profesa, ambaye alitukabidhi dawa huku akidai kuwa dawa hii ni nyingi sana, akashauri kama ikibaki tutaitumia wakati mwingine. Haraka tuliwasiliana na maofisa wa ubalozi kuwajulisha kuwa dawa imepatikana, nao hawakuchelewa kufika”. “Walipofika ikawaje?”, niliuliza. “Kufika kwa maofisa hawa kulitupa faraja, walishauri dawa hiyo ihifadhiwe vizuri kwenye jokofu, ili kazi ya kusafisha dola kwa vile ni nzito ifanyike kesho yake mapema alfajiri, kwa madai kuwa kuna kazi nyingine wanaifanya wakati huo ili kesho yake wasiwe na ratiba nyingine”, alisema mzee Enock ambaye alikuwa kimya kwa muda mrefu. “Ah, jambo hili lilipangwa kwa ustadi wa hali ya juu, tulihifadhi dawa hii vizuri kama watu hawa walivyoagiza, siku ya pili walifika mapema alfajiri kama walivyoahidi, walinihimiza nitoe dawa ili kazi ya kusafisha dola ianze”, alipofika hapo machozi yakaanza kumwagika “Usilie tafadhali, hii ni hali halisi ya dunia, unaweza kulala masikini ukaamka tajiri, ama ukalala tajiri ukaamka masikini, yote ni mipango ya Mungu”, niliwaambia ili kuwatia moyo
“Teacher, sasa tunawasaidiaje wazee hawa?”, lilikuwa swali kutoka kwa Kanali Emilly. Kutokana na swali hili, nilitembea hatua tatu kutoka nilipokuwa nimesimama, halafu nikarejea tena kwenye kiti nilichokuwa nimeketi awali.
“Inategemea…”, nilijibu kwa mkato,
Baada ya kutafakari kwa muda, huku tukiangaliana kama mabubu, nililazimika kumweleza Kanali Emilly kuhusu mkakati wangu wa kazi zilizokuwa mbele yangu.
“Afande…, kabla sikaingia kazini rasmi, naomba utambue kuwa kujiingiza katika jambo hili, ni sawa na kuanzisha vita, nasema hivi kwa sababu watu waliofanya uhalifu huu wana mtandao mkubwa mno. Hawa ndio wahusika wakubwa wa dawa za kulevya, ndio wahusika wa uhalifu wa kila aina. Swali langu ni kwamba, uko tayari kwa mapambano na watu hawa?”, nilimuuliza.
“Potelea mbali, lolote liwe, dunia itatukumbuka kwa hili, tukilimaliza salama tutashukru, tukiishia njiani naamini wapo watakaokuja kuliendeleza”, Kanali Emilly alisema huku akisimama kuonyesha msisitizo. “Niko tayari kabisa”.
Nililazimika kumweleza Kanali Emilly, kuhusu shambulizi la jana usiku uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, akaonekana kushangazwa, nami nikatumia nafasi hiyo kumweleza jinsi nilivyojipanga kukabiliana na watu hawa, maana walikuwa wamenianza.
“Afande, kutokana na umuhimu wa jambo hili, nimelazimika kuwaita vijana wetu wawili, Luteni Claud Mwita kutoka Morogoro na Sajenti Julius Nyawaminza kutoka Zanzibar, hawa ni makomandoo wenye uwezo mzuri, bahati nzuri wako karibu na eneo hili. Hapa ofisini nimeamua kuwatumia Luteni Fred Libaba na Sajenti Peter Twite tu, nina sababu za kufanya hivyo”, nilidokeza.
“Sababu gani hiyo Teacher, wakati idara yetu hapa inao vijana wenye uwezo mzuri tu, wangeweza kukusaidia kwa karibu zaidi, jambo hili linahitaji ushirikiano wenu”, alishauri.
“Afande, nimelazimika kufanya hivi kwa sababu, sielewi ilibainika vipi kuwa nimesafiri, ilifahamika vipi kuwa niko kwenye ndege nikirejea Dar es salaam, na sijui nini kilisababisha hata watu hawa wakanishambulia baada ya kutoka kwenye ndege, hilo linanitia shaka”, nilimwambia. “Hawa vijana tutawashirikisha kwa kazi nyingine, kuhusu hii watuache kwanza. Kama utapenda operesheni hii iwe na mafanikio utaniwia radhi kwa hilo”.
“Umesomeka, hakuna ubishi katika hilo. Kuna la ziada?”.
“Hapana”, nilimwambia, baada ya ukimya wa sekunde kadhaa nilimwambia kuhusu ujio wa shemeji yangu Mama Feka. “Afande, kama ulivyosikia nikiongea na simu, shemeji yangu tunayeshibana sana yuko njiani kuja Dar es Salaam, pamoja na kwamba anakuja kwenye mahafari ya chuo kikuu, kwa vyovyote vile atapenda kufikia kwangu, kama unavyojua familia yangu nimeihamisha kabisa ili sasa vita vianze, itakuwa vita ya kufa au kupona”, nilisema kwa hasira.
“Sasa kuhusu huyu shemeji yako utafanyaje, maana nyumbani kwako sasa si sehemu salama kama ulivyosema?”, alihoji Kanali Emilly.
“Nafikiria kumshirikisha katika vita hivi, maana ujio wake unaweza kuwa faida au hasara, lolote laweza kutokea”, nilimwambia Kanali Emilly akaonekana kunishangaa.
“Kwanini umeamua kufanya hivyo Teacher?. Huyu shemeji yako ataweza kumudu hali ngumu ya vita ambavyo hatujui nani adui na rafiki?”.
Nilitumia dakika mbili tatu kumweleza Kanali Emilly, kuhusu uhodari wa Mama Feka. Nilimweleza jinsi mama huyu alivyo na msimamo imara katika kutekeleza majukumu yake, nilieleza historia yake fupi, kuwa kabla ya kujiunga na chuo kikuu huria cha Tanzania, alifanya kazi kama mwalimu wa michezo katika shule kadhaa, lakini kabla ya hapo alikuwa ameshiriki mafunzo mbalimbali ya kijeshi kwa mjibu wa sheria.
“Kuhusu hilo nakuachia utaamua mwenyewe. sasa umepanga kumtumiaje huyo shemeji yako, au ni siri yako?”.
“Hapana, ndiyo maana nikakushirikisha kuhusu jambo hili. Afande, Mama Feka ni mwanamke mrembo sana, ni mwanamke ambaye anaweza kumshawishi mwanaume yeyote akaingia katika himaya yake. Labda nikudokeze jambo moja”.
“Itakuwa vizuri”.
“Hapa Dar es Salaam, kuna mtandao wa uhalifu ukiongozwa na mzungu mmoja aitwae Carlos Dimera, kama unavyojua taratibu na sheria za nchi yetu huwezi kumkamata mtu bila kuwa na ushahidi wa kutosha. Taarifa nilizonazo ni kwamba huyu Carlos anapenda sana wanawake warembo, kwa Mama Feka ataingia, akiingia amekwisha”, nilifafanua. “Ni mpango mzuri Teacher, tufanye kila iwezekanavyo watu hawa wakamatwe na ushahidi, hii itasaidia kuwafikisha mahakamani, nikutakie kazi njema, tuwasiliane kila hatua utakayofikia, ukihitaji msaada wa aina yoyote usisite kunijulisha, kuanzia sasa ofisi hii itaacha mambo mengine yote ili tushughulikie jambo hili”, Kanali Emilly alisema.
“Nikutakie kazi njema, tuombe mungu ndiye mwenye dhamana ya uhai wetu, lolote likitokea itakuwa kwa mapenzi yake, lakini pia tuko tayari kufa kutetea wengi”, nilisema huku tukisimama. Tukashikana mikono.
Muda ulikuwa umeyoyoma sana, nilitoka ofisini kwa Kanali Emilly, huku mawazo mengi yakiwa yamenizonga juu ya jambo hili, nilijiuliza kuhusu mbinu walizotumia watu hawa, kiasi fulani nilijikuta nikicheka mwenyewe na kuwasifu kwa jinsi walivyoweza kufanikisha mpango wao wa wizi na kuwaacha wazee hao kwenye mataa. Nilifungua mlango nikatokea mapokezi. Linnah aliponiona akasimama.
“Pole sana bosi wangu, naona kikao kilikuwa kirefu kupita maelezo”, alisema, mama huyu askari mwenye cheo cha Staff Sajenti, lakini aliheshimiwa sana kutokana na utendaji kazi wake uliotukuka.
“Ndiyo mambo ya kazi. Sikiliza Linnah, naomba nisaidie kazi moja muhimu sana, niitie Sajenti Peter Twite aje ofisini kwangu haraka, ikiwezekana aingie kwa siri. mtu zaidi yako asijue”, niliagiza halafu nikaingia ofisini kwangu.
Nilipanga kumtumia Peter kufanya kazi maalumu, kazi ya kimafia, ambayo ingetusaidia kumaliza jambo hili haraka. Baada ya muda mfupi Peter aliingia ofisini kwangu.
“Jambo Afande?” alinisalimia.
“Jambo. Habari ya toka usiku wa jana, Peter ujumbe wako ulinisaidia sana, maana sikujua lolote litatokea, sijui ingekuwaje?”, nilimuuliza.
Peter akatumia muda huo kueleza mambo yalivyokuwa uwanja wa ndege, akaeleza jinsi alifika uwanja wa Julius Nyerere kwa ajili ya kunipokea, uwanja wa ndege alikutana na watu ambao aliwatilia shaka, kutokana na uzoefu wake wa kazi baada ya kuwawafanyia utafiti alibaini kuwa walikuwa katika mpango wa kumsubiri mtu.
“Ilikuwa vigumu saba kuwabaini, baada ya kutulia na kusoma mazingira ya uwanja wa ndege, nilibaini magari mawili aina ya BMW, moja likiwa limeegeshwa karibu kabisa na sehemu ya kutokea abiria na lingine liliegeshwa sehemu ya kutokea magari. Ulipoanza kutoka wewe watu wawili walilikimbilia gari la mbele, ambalo lilianza kuondoka, lingine likasuri gari ulilopanda liondoke ndipo wao walifuate gari hilo kwa nyuma. Haraka nikakutumia ujumbe wa tahadhari”.
“Ama kweli ulifanya kazi ya ziada, sikuwa na mashaka kabisa, bila wewe pengine siku ya leo ingekuwa ya maombolezo kwangu, asante Peter”, nilimshika mkono.
“Usijali mkuu, haya ni matunda yako, kumbuka wewe ndiye uliyenifundisha haya, ulinifundisha jinsi ya kunusa harufu mfano wa mbwa, Nikushukuru kwa kunifikisha hapa”, alisema Pete.
“Tuachene na hilo, sasa nataka ufanye kazi moja ya muhimu sana, nimemwambia Mzee Emilly kuwa mapambano yameanza, ni mapambano makali ambayo yafaa tuyapigane sasa, hakuna jinsi, kazi yako tafuta vijana watano, wawe raia wa kawaida tu, lakini waendesha bodaboda jijini, ingia nao mkataba, lakini wapatie pamit na alama ili wasisumbuliwe na migambo. Pikipiki zao waziegeshe kwenye barabara kubwa tano za jiji. Yaani Morogoro road, Ali Hassan Mwinyi, Nyerere road, Kilwa road na Bibi Titi Mohamed, ukimaliza hilo tuwasiliane nitakuelekeza kazi nyingine”, niliagiza.
“Nitalifanya hilo haraka sana bosi”, alisema Peter.
“Ok, usikose kunijulisha, kumbuka kuwafahamisha kuhusu matumizi ya pikipiki hizo, maana tumepanga kuwatumia wao katika kazi fulani, isifike wakati wakatushangaa, kazi kwako”.
Niliwasiliana na Luteni Claud Mwita kumuuliza kama uwepo wake eneo hilo umebaini nini akanidokeza kuwa watu ni wengi, pamoja na kufanikiwa kufahamiana na Sajenti Julius Nyawaminza, wameimalisha ulinzi katika eneo hilo.
Simba, Nyati na Chui, wao walikuwa eneo hilo wakitembea hatua kadhaa kwenda upande mwingine na kurejea kwenye pointi huku silaha zao ndogo, zikiwa tayari zimeondolewa usalama. Risasi zikiwa chemba tayari kwa lolote.
Baada ya kupanga mipango yangu, niliyoofanya kimya kimya, nilifungua mkoba wangu mdogo, nikatoa kamba niliyoinunua Kariakoo. Ilikaribia kuwa saa moja ya usiku, giza lilianza kuifukuza nuru, niliwasiliana na wenzangu. Claud Mwita, Julius Nyawaminza na Fred Libaba nikawaomba tuonane kwenye Mghahawa wa YWCA uliopo hapo Posta Mpya kwa ajili ya chakula cha jioni.
Pamoja na kwamba Mghahawa huu uko karibu kabisa na kituo cha Daladala cha Posta Mpya, wengi hawakupajua, lakini pia niliwahadharisha wenzangu kuwa makini. Nilishauri kila mmoja achukua chakula na atumie meza tofauti, baada ya hapo tutakuwa na mazungumzo yetu binafsi nje ya eneo hilo. Taratibu nilifungua mlango wa ofisi yangu nikachungulia kwa nje, nilitafuta sehemu ya siri nikazificha funguo za gari, halafu nikawasiliana na David, mmoja wa vijana wanaofanya kazi karibu yangu, nikamfahamisha mahali nilikohifadhi funguo hizo ili azichukue na kuipeleka gari kwa aliyeniazima, rafiki yangu Edgar.
Hapakuwa na dalili yoyote ya kuwa na mtu, hata Linnah alikuwa ametoka na kufunga ofisi yake, nilitoka haraka na kuivamia lifti iliyonishusha ghorofa ya kwanza. Nilitembea haraka hadi kwenye maegesho ya magari, sikutaka kupoteza muda, nilichungulia upande wa pili lilipo jengo la ofisi za benki ya CRDB. Baada ya kujiridhisha kuwa hakukuwa na mlinzi eneo hilo wakati huo, nikairejesha kamba yangu kwenye mkoba, baada ya kujiridhisha kuwa hakuna kikwazo cha kunisumbua.
Niliangalia nyuma na upande wangu wa kulia na kushoto, sikumuona mtu, lakini kwa vile jengo hili linalindwa kwa kamera maalumu za usalama, nililazimika kufanya jambo moja ili kamera hizo zisinione. Nilisogea kwenye kivuli, nyuma ya magari kadhaa yaliyoegeshwa hapa, nikatumia nafasi hiyo kujirusha chini, upande wa jengo la CRDB. Haikuwa shida kwangu kuruka sehemu kama hiyo.
Lango la kutokea bado lilikuwa wazi na kwa vile kuna ofisi zingine juu ya ghorofa hili, nilitoka na kuwapita walinzi na baadhi ya askari polisi waliokuwa kwenye kibanda chao cha ulinzi. Nielekea shell ya Gapco, nikakavuka barabara na kuingia YWCA, Wenzangu wote walikuwa wamefika na tayari walikuwa wamepata chakula.
Tulisalimiana na kupeana ishara, kwa vile Mghahawa huu ni wa kujihudumia mwenyewe, na njaa ilikuwa karibu iniue nilielekea kwenye dirisha la huduma, nikaagiza chakula, ambacho nilikula haraka haraka, ili kwenda sawa na wenzangu, ambao kila mmoja alikuwa na hamsini zake.
Wakati huo Carlos Dimera alikuwa akiwasiliana na wakala wa kusafirisha mizigo kutoka Bogota, nchini Corombia, wakala akimjulisha kuwa baada ya masaa ishirini na nne mzigo huo ambao ni dawa za kulevya, utakuwa umewasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
“Tunahitaji maelezo kutoka kwenu, hivi tunavyoongea hapa shehena ya dawa za kulevya imetua salama katika uwanja wa ndege Addis Ababa, nchini Ethiopia. Tumelazimika kupitishia mzigo nchini Ethiopia badala ya Ouagadougou, nchini Burkina Faso kama ilivyokuwa awali kwa sababu za usalama, taratibu zote za mzigo kuondoka Ethiopia kesho zimekamilika, kazi kwenu, vipi hali ya usalama huko?”, Carlos Dimera aliulizwa.
“Dar es Salaam, Tanzania hali si mbaya sana, japokuwa kuna mawingu na mvua za hapa na pale, lakini haziwezi kutuzuia kuendelea na majukumu yetu. Kuna wingu moja limetanda angani kuashiria mvua, lakini wataalamu wa hali ya hewa hapa Tanzania wanasema wingu hilo halina madhara, waganga wako kazini kuhakikisha wingu hilo halidondoshi hata tone moja la maji, kuhusu hali ya uwanja wa ndege wa Dar es Salaam ni nzuri sana, tunausubiri”, alieleza Carlos Dimera kwa simu ya mkononi.
“Oke, lakini kuweni makini sana katika jambo hili, nasikia serikali ya Tanzania sasa hailali?.”
“Kuhusu hilo ondoa shaka kaka, niko na mtandao unaoeleweka, mtandao wa vijana wa mjini ambao nimewafundisha mbinu za kila aina, hata hili wingu lililotanda angani mwisho wake wa kutanda na kuleta hofu ni leo, wingu hili halitakuwepo tena”, alisisitiza Carlos.
Baada ya Carlos Dimera kumaliza kuongea na simu hiyo, aliingiwa na hofu kidogo, alisimama akatembea hatua mbili, halafu akajiuliza maswali kadhaa, akainua simu yake ya mkononi na kuongea na Nombo.
“Uko wapi Mr. Nombo?”, alihoji Carlos Dimera.
“Niko katikati ya mji bosi, nimelazimika kuja huku kuongeza nguvu kwa vijana, kazi hii lazima iishe leo bosi, kuna habari mpya?”, Nombo alihoji.
“Hakuna habari mpya, isipokuwa wakala wa kusafirisha mizigo anauliza, hatua gani tumefikia, mzigo umewasili salama Addis Ababa, Ethiopia, yamebaki masaa ishirini na nne tu mzigo uwasili Dar es Salaam, na wingu bado limetanda angani, unadhani kuna uwezekano wa kuliondoa?”, Carlos Dimera aliuliza.
“Tulia bosi, tumuombe Mungu atasaidia, maana uwezekano ni mkubwa mno, kwa vile hujafika kwenye uwanja wa mapambano, ungeshuhudia adui alivyowekwa kati, hakika jengo lote la Benjamin Mkapa liko chini ya usalama wetu, kila anayetoka na kuingia anaonekana, kuhusu hilo usijali, leo ndiyo mwisho wa wingu hili, labda utokee muujiza gani”.
“Niwatakie kazi njema, jitahidini bwana jambo hili liishe mapema leo, vinginevyo nitume kikosi kazi?, hawa jamaa zetu wapo tu wanasubiri kazi kama hizi, mkishindwa semeni”, aliuliza Carlos.
“Hakuna sababu, mapambano ya mchana yangeleta shida kidogo, maana watu walikuwa wengi eneo hili, lakini sasa hali iko shwari, hili giza litatusaidia pia. Kunywa, kula ukiamini kuwa kazi hii imekwisha”, Nombo alieleza, Carlos akapata faraja na matumaini.
Baada ya sisi wote kupata chakula cha jioni kwenye Mghahawa huu wa YWCA, tulitoka mmoja baada ya mwingine kama tulivyoingia, lakini tukiwa nimewapa ishara ya kukutana sehemu nyingine ambayo tutafanya mazungumzo na kupanga mipango yetu kwa siri.
Kabla ya kutoka ndani, niliwasiliana na Mama Feka, ili kujua wapi amefika, akanifahamisha kuwa amefika salama Jijini Dar es Salaam. Nilimfahamisha kuwa nitamtafuta kesho, hivyo atafute hoteli itakayomfaa apumzike kwani alikuwa amesafiri kwa muda mrefu.
Wakati tunatoka ndani ya Mghahawa huu wa YWCA, nilisikia kelele za risasi, zilizosikika kutoka upande wa pili, zikafuatiwa na harufu ya baruti. Kwa sisi wazoefu wa mambo ya silaha, mara moja nikahisi jambo. Watu walikimbia kuelekea upande tuliokuwa, ghafla kwa muda mfupi hali ya usalama ilikuwa imetoweka katika eneo la Posta Mpya.
Tuliangaliana na wenzangu, moyo wangu ukaingiwa na hofu, nikahisi jambo la hatari limemtokea David. Tulianza kusogea taratibu eneo la tukio. Nilifungua mkoba wangu nikatoa moja ya kofia zangu za kuficha sura, nikaivaa ili kuficha sehemu ya uso wangu.
“Tukimbie, majambazi yamevamia na kuua watu, mwenyezi mola tusaidie”, mama mmoja wa makamo alisikika huku akikimbia kuyanusuru maisha yake./ “Sijawahi kuona unyama kama huu, binadamu kumuua binadamu mwenzao tena mbele ya watu utadhani wanaua mnyama”, alieleza mzee mmoja aliyekuwa amelala kwenye mfereji wa barabara ya Azikiwe.
Toyota Carina TI, ambayo David alikuwa akiendesha kutoka kwenye maegesho ya magari ghorofa ya kwanza, ishambuliwa na kuteketezwa vibaya kwa kombora ambalo halikujulikana, David aliuawa katika shambulizi hilo. Waliofanya shambulizi hilo hawakufanya makosa. Nilisikitishwa sana, lakini kwa kiasi fulani nilijiona mwenye bahati, maana kazi yangu sasa ingekuwa rahisi au ngumu zaidi.
Polisi hawakuchelewa kufika eneo la tukio, waandishi wa habari pia waliwasili na kamera zao, mimi na wenzangu Claud Mwita, Julius NYawamizna na Fred Libaba tuliangalia tukio hilo kwa dakika kadhaa tukiwa mbali kiasi, halafu tukapeana ishara ya kuondoka eneo hilo. Hata kama ungekuwa mtaalamu wa hisia kiasi gani hakika usingeweza kubaini ishara zetu, labda uwe mmoja kati yetu.
Kutokana na uzito wa tukio hilo, niliwasiliana na Peter Twite, nikamfahamisha klichotokea, nikamwelekeza mambo ya matatu ya kufanya, afike haraka eneo la tukio na kutoa taarifa kwa Kanali Emilly, ahakikishe majina ya marehemu hayaripotiwi kwenye vyombo vya habari, ofisi anayotoka marehemu iwe siri na mwili wake uhifadhiwe mahali salama mpaka tutakapomaliza kazi.
Baada ya kutoa agizo hilo kwa Twite, tulikubaliana kuonana kwenye Mghahawa wa Chief Pride, uliopo mtaa mdogo wa Chaga, katikati kabisa na barabara za Jamhuri, upande wa kushoto na Libya, upande wa kulia. Tulipanda ngazi hadi ghorofa ya kwanza, hapakuwa na wateja zaidi ya meza na viti. Wakati tunapanda ngazi, muhudumu alitufuata kwa nyuma, tulipoketi akawa tayari kutusikiliza. Tuliagiza vinywaji kila mmoja alichoona kinamfaa.
“Nadhani hapa patatufaa kwa mazungumzo, au mnasemaje bosi?”, Fred alihoji baada ya muhudumu wa Mghahawa huu kuondoka.
“Pamoja na kwamba sijaelewa lolote kuhusu kilicho mbele yetu, lakini kwa utulivu huu, nashauri tuifanye sehemu hii iwe kwa ajili ya kukutana tukiwa na dharura. Naamini kazi tuliyoitwa kuifanya itakuwa ngumu, lakini tutashinda”, alieleza Claud.
“Sikilizeni, naamini mpaka sasa adui zetu wanasherehekea ushindi wakidhani nimekufa, David ameuawa kinyama, wamemuua wakidhani ni mimi, sasa kabla jua la kesho halizachomoza, yatupasa kufanya kazi ya ziada, kujua wauaji wanapatikana wapi, wanafanya nini? Sababu zilizowasukuma kutushambulia, tukilijua hilo, kazi yetu itakuwa rahisi, tofauti na hapo tutakuwa tunajisumbua kutwanga maji ndani ya kinu”, niliwaeleza.
Vinywaji vililetwa mezani, tukaanza kunywa huku kila mmoja akieleza mpango kazi wake. Baada ya kila mmoja kutoa mchango wake huku Fred akijaribu kuweka kumbukumbu ya maandishi, nikakumbuka kuhusu, Carlos Dimera.
“Wakati mwingine linapotokea tukio la kushitua kwa aina hii, akili yangu hulazimika kufanya kazi ya ziada. Fred…, unaweza kumfahamu mzungu mmoja anaitwa, Carlos Dimera?”.
“Yaa. Ndiyo, Carlos Dimera namjua, huyu jamaa ndiye tajiri mwenye kile kiwanda cha kutengeneza tembe za malaria, Huyu jamaa anatajwa kuwa mtu safi na mwaminifu kwa serikali, pia anatajwa kuwa mstari wa mbele katika kusaidia jamii, ana nini?”, Fred alihoji.
“Yatupasa kumchunguza haraka iwezekanavyo. Nimewahi kusikia minong’ono kuhusu yeye, lakini nisimchumie dhambi, nataka kujua anaishi wapi, anapendelea mambo gani?”, nilimuuliza Fred.
“Huyu Carlos, anaishi Mikocheni A, ukiziacha taa za usalama barabarani za Morocco, barabara ya kwanza kabisa ingia kulia, nimewahi kuonyeshwa na rafiki yangu mmoja Inspekta wa polisi. Anasema walikwenda kupokea msaada wa Pikipiki kumi za kuwasaidia polisi kufanya doria, ndipo nilipobaini kuwa ni mtu safi. Ni matajiri wachache sana wenye moyo wa kusaidia suala la usalama wa raia”, alifafanua Fred.
“Siyo sababu, yafaa achunguzwe, na kazi hii lazima tuifanye usiku huu, huyu jamaa kwa nyakati fulani, binafsi nilijaribu kufuatilia nyendo zake, sikupata mambo makubwa sana, lakini nilipata mashaka kidogo, sasa nitamfuatilia kwa undani zaidi ili nijiridhishe”, nilisema.
“Inspekta Judith, aliyenionyesha nyumbani kwake alinidokeza kuwa wakati anawakabidhi Pikipiki hizo, Carlos mwenyewe aliwaeleza polisi kuwa binafsi anachukia sana vitendo vya uhalifu, akaahidi kutoa magari mawili maalumu kusaidia doria, ndiyo maana najiuliza”, Fred alieleza.
“Siyo sababu, wahalifu wana mbinu nyingi, hujaona wachawi walivyo wakarimu, anakufanyia vitendo vya ushirikiana huku akikuonyesha wema. Hata ukielezwa kuwa huyu ndiye mchawi wako huwezi kuamini, kutoa msaada haitoshi kukufanya uwe mwaminifu”, Nyawaminza alieleza.
“Hakika”, Claud alisapoti.
“Ndugu zangu, Claud na Julius, kwanza poleni kwa safari, niwaombe radhi kwa safari ya kushitukiza, nimelazimika kuwaita ili tusaidiane kupigana vita iliyoko mbele yetu”, nilitumia nafasi hiyo kuwaeleza kila jambo, kuanzia wazee walioibiwa kwa mtindo wa noti bandia na jinsi dawa za kulevya zinavyoingizwa nchini na kuchangia kuharibu maisha ya ambani ni nguvu kazi ya taifa na kizazi cha sasa.
“Tuko pamoja”. “Kuanzia sasa, mtaziacha kazi zenu zote, mtayaacha majukumu yenu yote, tukabiliane na jambo hili, si kazi rahisi kama tunavyodhani, kuwakabiri watu hawa ni sawa na kuwa mkononi na tiketi ya kwenda ahera, kwa vile tuliapa kuilinda Jamhuri yetu, hatuna budi kuifanya kazi hii”, niliwaambia huku wote wakiniangalia kwa macho makavu.
“Hakuna shaka kuhusu hilo Kamanda”, alieleza Claud, Julius akatikisa kichwa kuunga mkono.
Nikatumia nafasi hiyo pia kuwaeleza wenzangu kuhusu ujio wa shemeji yangu Mama Feka, nikawaeleza nilivyopanga kumtumia mwana mama huyu.
“Ataweza?”, alihoji Nyawaminza huku akicheka.
“Naamini ataweza, Mama Feka ni mmoja kati ya wanamke jasiri sana”, niliwahakikishia, halafu nikamgeukia Fred, “Sikiliza Fred, hawa jamaa watafutie mahali pa kulala leo, kuanzia kesho hatutakuwa na muda wa kulala, lakini iwe maeneo ya Sinza, Kinondoni au hata Kijitonyama, mimi nitakwenda nyumbani kwangu wakati huu, kuna vifaa vyangu vya kazi nitachukua halafu nitamtafuta Carlos, hata wewe pumzika maana kesho utakuwa na kazi nyingi zaidi”.
“Asante”, Fred alishukuru.
“Angalizo, jambo hili bado ni siri, pale ofisini hakuna anayejua mpango huu zaidi ya Mzee Emilly, Twite na wewe Fred, hatuna sababu ya mtu mwingine kujua, ndiyo sababu ya kuwaita hawa jamaa, Claud na Nyawaminza. Of rekodi”, nilionya.
“Nimekusoma”, alieleza Fred.
“Fred, wakati unakwenda kulala, hakikisha unapata ratiba ya huyu Carlos, ujuwe ni mtu wa aina gani, anapenda nini, ana msimamo gani, nani rafiki zake wa karibu na hiki kiwanda chake kinakidhi haja? tumia akili zaidi kuliko nguvu”.
Wakati huo kulikuwa na sherehe kubwa nyumbani kwa Carlos Dimera, vinywaji vya kila aina vilikuwa mezani, nyama za kila aina zilitafunwa, muziki laini ukipenya katika masikio ya watu hawa, kila mmoja akiyatafakari maisha baada ya kazi nzito.
“Umefanya kazi nzuri sana Nombo, kuanzia sasa mshahara wako unaongezwa mara mbili zaidi, lakini hata, Simba, Nyati na Chui pia posho zenu zimeongezwa, mmefanya kazi nzuri sana. Kumfuatilia adui kuanzia usiku wa jana, leo asubuhi, mpaka jioni mnamaliza kazi ni jambo kubwa mmefanya. Kuondoka kwa mbwa huyo ni ushindi kwetu”, Carlos Dimera alieleza.
“Wakati mwingine lazima ujifanye kama mwendawazimu ili kazi yako iwe nzuri. Nguvu ya Nombo kwenye uwanja wa mapambano imesaidia sana, milango yote ya kuingia na kutoka ilikuwa chini yetu, tulisubiri mpaka mwisho, alipotoka tu akakutana na kifo, wakati ndugu zake wakiomboleza sisi tunakula raha”, Nyati alieleza.
“Sasa ni wakati wa kula na kunywa, kazi yenu imenifurahisha sana, sina budi kuwaambia nawapenda sana, shehena kubwa ya dawa za kulevya yenye utajiri, itaingia Dar es Salaam, kesho alasiri, taratibu zote za kupokea mzigo huo zimefanyika, kunyweni lakini msilewe”, Carlos alishauri. Wakaendelea kunywa huku wengine wakicheza muziki.
Wakaendelea kula, kunywa na kucheza muziki
Ilikaribia kuwa saa sita na nusu za usiku, niliposhuka kwenye taksi iliyonitoa katikati ya mji, nilipenya uchochoroni, nikapita nyuma ya Kanisa la KKKT, lililopo Kijitonyama, nikaambaa na ukuta wa kanisa hili nikaibukia kwenye barabara ya vumbi inayoelekea nyumbani kwangu. Nilitembea haraka haraka, nilipoufikia mti ulio karibu na nyumba yangu nikasimama na kuufanya kuwa ngao yangu.
Eneo hili lilikuwa kimya kabisa, ni nyumba yangu pekee iliyokuwa katika hali ya giza. Hii ilitokana na familia yangu kutokuwepo. Baada ya kujiridhisha kuwa hali ilikuwa shwari, nilinyata mfano wa paka, nilipoufikia ukuta wa nyumba, nilitoa funguo za mlango wa siri ulioko nyuma ya ya nyumba, nikaufungua taratibu, nikaurejesha kama ulivyokuwa, nikasubiri kwa sekunde kadhaa halafu nikasogea na kuingia.
Kwa vile hali ya usalama haikuwa nzuri, familia yangu niliihamishia sehemu nyingine, nilitumia nafasi hiyo kukagua usalama wa eneo la nyumba yangu, nilipohakikisha kuwa hakuna dalili zozote za hatari, nikauendea mlango wa nyumba, nikaufungua kwa tahadhari nkajitosa ndani.
Ndani ya Nyumba hii kulikuwa kumepekuliwa sana, kabati ya nguo iliyoko chumbani kwangu ilikuwa imepekuliwa na baadhi ya nguo na vitu vyangu vingine kuachwa bila kuvirejesha mahali pake. Nadhani waliamua kuviacha hivi baada ya kujiridhisha kuwa waliniua katika shambulizi la Posta kwa hiyo waliamini kuwa siko tena duniani. Lakini walikosea jambo moja. Hakuhakikisha nani alikuwa akiendesha gari lile walilolishambulia.
Kiasi fulani nilicheka mwenyewe, maana nilijua sasa kazi imeanza, niliyakumbuka maneno ya Rais wa kwanza wa Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, alipokuwa akitangaza vita dhidi ya majeshi dhalimu ya Ndul Iddi Amin Dada wa Uganda. Kilichonisisimua zaidi ni pale Mwalimu aliposema, ‘RAFIKI ZETU WALIOKUWA WANASEMA MWALIMU ACHA, SASA WAKAE PEMBENI, WATUPISHE, MAANA HATUTAWASIKILIZA TENA, ILI SASA UBISHI UISHE’. Maneno haya ya Mwalimu Nyerere yaliniongezea hamasa, nililiendea kabati langu maalumu lenye dhana zangu muhimu za kazi, kabati hili lilikuwa sehemu ya siri, nikalifungua kabati hilo lililoko ukutani, nikatoa fulana mbili maalumu zisizopenya risasi (bletproof), nikazihifadhi vizuri kwenye mkoba wangu, halafu nikatoa bastola mbili aina ya M9 zisizotoa sauti, zote zikiwa zimejazwa risasi kumi na mbili kila moja kwenye magazini zake, nikazifutika kwenye mapaja yangu, moja kulia na nyingine kushoto. Nikatoa magazini zingine nne zenye risasi za ziada, mkasi wa kukata vyuma na kisu kidogo nikaviweka kwenye mkoba wangu.
Kichwa changu kilijawa na mambo mengi, nilijiuliza hili na lile, nikishika hili na lile. Niliwakumbuka wenzangu, Luteni Claud Mwita, Fred Libaba na Julius Nyawaminza, moyo wangu ukajawa na matumaini ya ushindi. Maana kila mmoja alikuwa na hamasa ya kuingia kwenye uwanja wa mapambano.
Baada ya kutoa vifaa hivyo, nilirudi hatua moja nyuma, nikasimama nikitafakari nini kingine kitanisaidia zaidi katika mapambano na watu hawa, nikaikumbuka ngazi yangu ambayo mimi huitumia kupanda au kushuka kwenye majengo makubwa. Pamoja na kwamba nilikuwa na kamba maalumu niliyoinunua Kariakoo kwa ajili ya kazi hiyo, nikalazimika pia kuichukua ngazi. Usidhani ni mzigo mkubwa, ilikuwa ngazi ya kisasa kabisa, unaweza kuiweka hata kwenye mkoba wako na mtu asijuwe ulichobeba.
Sasa nilikuwa tayari kwa mapambano na watu hawa, nilipiga magoti chini nikamuomba mungu wangu, nikawaomba bibi na babu zangu ili wanisaidie. Nikayakumbuka maneno mazuri ya waswahili, ‘AKUANZAE MMALIZE’ nikaapa kufa au kupona. Ama zangu ama zao.
Baada ya kupiga maombi, nilitoka ndani ya nyumba yangu na kuacha kila kitu kama nilivyokikuta, Hasira na woga vyote vilikuwa ndani ya nafsi yangu, nikajiuliza iwapo nitaishia njiani katika vita hivi nani atakuja kuviendeleza. Imani ikanijia kuwa iko siku atapatikana kijana mkeleketwa wa atakayewasha moto na kuendeleza mapambano hadi kieleweke.
Saa yangu ya mkononi ilinieleza kuwa ni saa nane kasoro dakika chache usiku, nilipenya kwenye uchochoro nikatokea Chuo cha Ustawi wa Jamii, eneo hili lilikuwa na wasichana kadhaa wanaouza miili yao, waliponiona walinigombea, lakini mimi sikuwajali, niliwapita kimya kimya nikatafuta taksi iliyonishusha karbu na taa za usalama barabarani za Morocco.
Muda huu magari yalikuwa machache barabarani, baada ya kushuka kwenye taksi iliyonileta, nilitembea haraka kurudi nyuma, kama Fred alivyokuwa amenielekeza, nilianza kuhesabu nyumba moja baada ya nyingine, nikiitafuta nyumba ya Carlos Dimera, hatmaye nikaiona.
Eneo hili lilikuwa limezungukwa na miti mingi, kwa vile nilikuwa nimevaa nguo nyeusi, nililipita geti kuu la kuingilia ndani. Nilifanya hivi ili kuona kama kulikuwa na mtu yeyote eneo hilo. Baada ya kujiridhisha nilirudi nikinyata taratibu na kwa tahadhari kubwa, nikauparamia mti uliokuwa karibu na ukuta, nikatulia juu kwa sekunde kadhaa, nikiangalia ndani ya ngome hii. Nilipoona hali ni shwari niliifungua ngazi yangu, nikaifunga juu, halafu nikashuka taratibu kwa hadhari, hatimaye nikajitosa ndani.
Mwanga mkali wa taa ulilifanya eneo hili kuwa la usalama wa kutosha, muziki laini ulisikika ndani ya jengo lililokuwa mbele yangu. Nililala kifudifudi, nikakuloo hadi nyuma ya dirisha lililokuwa na kelele ya muziki, nikautumia mti mkubwa uliokuwa eneo hili kujikinga ili nisionekane.
Chumba hiki kilikuwa kimejaa watu, Carlos Dimera alikuwa ameketi juu ya kiti kikubwa, huku wasichana wawili warembo wakifanya kazi ya kumpepea asipate jasho, vijana kadhaa walikuwa wakicheza muziki, huku wengine wakipata vinywaji.
“Jamani, makamanda wangu, mmeinjoi hamjainjoi?” Carlos aliwauliza vijana wake.
“Tumeinjoi sana bosi, tumekunywa, tumekula, tunacheza muziki”, walisema.
“Kama nilivyosema, mzigo unaingia usiku, sasa sitaki mlewe, tuna jukumu kubwa mbele yetu, Teacher amekufa sawa, lakini hatujui nani atafanya nini, au siyo jamani?”, Carlos Dimera alieleza.
“Hakika, lakini nikutoe hofu bosi, kifo cha Teacher kitasababisha wengine waogope kabisa, ni mtu mwendawazimu ambaye ameona kilichompata mwenzake, halafu aingie kichwa kichwa, itawachukua muda”, Nombo alidakia.
“Ndiyo, lakini mnajua wanaweza kujiuliza kwanini Teacher ameshambuliwa na kuuawa kinyama namna ile?”, Carlos Dimera aliuliza.
“Maswali lazima yawepo, nakuhakikishia mzigo utaingia na kusambazwa kwa amani kama ilivyokuwa, huyu mshenzi alikuwa kikwazo kikubwa kwetu, kifo chake ni faraja kubwa katika familia yetu”, Hawa Msimbazi alieleza.
Nilikaa kimya nikiwasiliza washenzi hawa, nilijiuliza kwanini hawakuweka ulinzi wa aina yoyote katika eneo hili, lakini nikabaini kuwa hofu ya kuvamiwa na mimi ilikuwa imewatoka baada ya kubaini kuwa niliuawa katika shambulizi lile.
“Kanali Emilly ameagiza lazima wwatu hawa akamatwe wakiwa na ushahidi, vinginevyo tutakuwa tumefanya kazi ya bure”, nilijisemea mwenyewe, maana bila hivyo walikuwa katika himaya yangu, ningewaita wenzangu tukawatia mikononi, lakini tutakuwa tumefanya kazi ya bure. “Wakala anasubiri taarifa kutoka kwangu ili mzigo uondoke Addis Ababa, Ethiopia. Hatutaki kufanya makosa, shehena iliyopo stoo ni ndogo, mzigo unaotarajiwa kuingia ni mkubwa kiasi cha matumizi ya miezi sita, kazi kwenu, kuingia kwa mzigo huu kutawafanya wote kuuaga umasikini”, aliwaeleza Dimera.
“Bosi, tumejipanga vizuri mno, waswahili wanasema kila anayetaka cha uvunguni sharti ainame, maana yangu ni kwamba, kila atakayeonekana kuingilia anga zetu, mauti yatamkuta, Teacher ni mfano wa kuigwa na wenzake”, Jakna alifafanua.
“Basi, maneno yenu yamenitia nguvu, Jakna, unajua utaratibu wa kupokea mzigo, panga halafu utanijulisha, nitawasiliana na wakala ili kuwajulisha hali halisi ya Dar es Salaam. Kama ilivyo kawaida yetu, Hawa Msimbazi, utasimamia taratibu za kupokea mzigo. Sitaki mpango wetu huu uferi”, alisisitiza.
Walizungumza na kujadili mambo mengi huku nikiwasikiliza, nilimshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kufika hapa na kusikia upuuzi wao, ilionekana kuwa hofu yao ilikwisha kabisa baada ya kufanya shambulizi lililomuua kijana wetu David.
Dakika kumi zilikuwa zimenitosha kabisa, baada ya kudaka baadhi ya maneno ambayo niliamini yatanisaidia katika kazi yangu, nilijitoa taratibu, nikapita sehemu ile ile ya awali, nikatoa ngazi yangu na kuondoka eneo hili salama usalimini. Nikiamini kuwa habari hizi zitamshangaza sana Fred.
Baadhi ya maofisa walikuwa wameugeuza uwanja wa ndege kuwa njia ya kupitisha dawa za kulevya. Raymond Keneko, alikuwa Afisa Mwandamizi Kitengo cha Ukaguzi wa mizigo. Kiutendaji ukimuona utaamini kuwa ni mtu makini, mwenye msimamo wa kati, asiyeyumbishwa katika kazi zake. Lakini alikuwa mmoja wa watu hatari, dhaifu waliopenda kupokea zawadi kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa, bila kujua kuwa zawadi hizo ni kishawishi. Ndiyo kwanza Kenoko alikuwa amefikisha umri wa miaka arobaini na saba. Akiwa mmoja wa watumishi wachache wa uwanja wa ndege waliokuwa wakipokea pesa nyingi kutoka kwa mzungu Carlos Dimera, kila wakati mzigo wa dawa za kulevya unapokuwa njiani kuletwa Jijini Dar es Salaam. Asubuhi hii wakati Kenoko akipata kifungua kinywa nyumbani kwake, alipokea ujumbe kutoka Hawa Msimbazi, ukimjulisha kuwa malighafi za kiwanda cha kutengeneza vidonge vya malaria zilizokuwa zimekwama nchini Ethiopia baada ya kukosa usafiri sasa tayari kuletwa Tanzania. Kutokana na uzito wa ujumbe huo, Raymond Kenoko alilazimika kuacha kila kitu mezani, akafanya maandalizi yake na kuondoka haraka kuelekea kazini. Mkewe na watoto waliyajua vizuri majukumu yake, hivyo hawakushangazwa na kitendo cha kuacha chakula mezani. Alipofika ofisini, aliwapanga vizuri watu wake, aliweka kila jambo katika mstari, akipita kila idara inayohusika na ukaguzi wa mizigo akiweka mambo sawa. Baada ya kila jambo kuwa limefanikiwa, aliwasiliana na Hawa Msimbazi. “Nakujulisha kuwa kazi yangu imekwisha, kazi imebaki kwenu dadangu, njia zote za kuingia na kutoka ziko wazi. Mwambie Carlos asihofu, kila idara imejulishwa kuhusu kuingia kwa mzigo huo, bahati nzuri ni kwamba wakuu wa idara zote wamepewa amri kuushughulikia mzigo wenu haraka, wanasubiri mgao wao”, Raymond Kenoko alimjulisha Hawa Msimbazi. “Umesomeka kakangu, Carols mwenyewe amesema malipo yako yataongezwa, kazi unazofanya kwa upande wetu zinastahili nyongeza, mimi kama mwakilishi wake, naahidi kuongeza posho zaidi”, alisema na kukakata simu. Kisha aliwasiliana na Carlos Dimera. “Habari ya asubuhi bosi?”, Hawa alimsalimia Carlos. “Niko salama, una habari gani nzuri?”, alihoji Carlos Dimera. “Habari nzuri ni kwamba Uwanja wa ndege kumeeleweka. Taratibu zimekwenda vizuri, Mr. Raymond anasema kwa upande wao hakuna shaka, kazi imebaki kwetu, tena amenihakikishia kuwa idara zote zinazohusika kupokea mizigo zimejulishwa kuhusu kuingia kwa mzigo huo, hali ni shwari”. “Nimekupata Condeliza Rise, maana hauna tofauti kabisa na mwana mama wenye jina hilo, kazi alizofanya akiwa Waziri wa Mambo ya Nje Marekani, zilitosha kumfanya awe kivutio kwa wanawake wenzake duniani. Ngoja niwasiliane na wakala ili mzigo usafirishwe kwa ndege ya usiku leo. “Fanya hivyo bosi, kilichonisisimua zaidi ni kwamba, huyu Raymond ambaye ndiye Afisa mkaguzi, anasema njia ziko wazi”. “Asante Hawa, wapange watu wako vizuri mkaupokee mzigo huo, sitaki kusikia jambo baya limewakuta”, Carlos alibainisha. “Tuko tayari kwa mapokezi na kwa lolote, napata faraja kwamba, Raymond amesema hali ni nzuri kuliko wakati wote, hususan baada ya Waziri aliyekuwa akiwafuatilia na kuweka kamera za CCTV uwanjani hapo kuhamishiwa wizara nyingine, hii imetuongezea nguvu na matumaini”, Hawa alisema. “Oke, niwatakie kazi njema na mapokezi mema, lakini tuwasiliane, kila hatua mtakayokuwa mnijulishe, lolote laweza kutokea”, Carlos alieleza wasiwasi wake. “Ni kweli bosi. Tutakujulisha”, aliongeza Hawa Msimbazi. Baada ya Carlos kuongea na Hawa. Alifanya mawasiliano ya mwisho na wakala. “Habari ya asubuhi kaka?”, Carlos Dimera alisalimia. “Huko Tanzania ni asubuhi, Addis Ababa ni mchana, tunakula chakula, leta taarifa?”. “Ndio maana nikakupigia. Najulisha kuwa hali ya Dar es Salaam ni shwari kabisa, vijana wako tayari kupokea mzigo, kulikuwa na mvua za rasharasha na mawingu ya hapa na pale, lakini sasa yamedhibitiwa, itakuwa vizuri mzigo ukiingia Dar es Salaam leo usiku. Hali ni nzuri”, Carlos Dimera alieleza. “Mzigo uko tayari, kilichokuwa kikisubiliwa ni taarifa za awali kutoka kwenu, hata hivyo Mamlaka za usalama nchini hapa Ethiopia zilianza kuhoji kuwepo kwa mzigo huu, lakinimaofisa wetu makao makuu Bogota, Colombia waliwasiliana na mamlaka za hapa na kuzijulisha kuwa mzigo huu unaopita, naamini utaingia leo Dar es Salaam”, alieleza wakala. “Asante na samahani kwa kuchelewa kutoa taarifa za awali, hii imetokana na hali ya usalama nchini Tanzania kuwa si ya kuaminika wakati huu, kiasi fulani mambo hayaeleweki. Serikali ya sasa haitabiriki, kwa kuwa mipango imekaa vizuri sasa tuko tayari kupokea mzigo, ambao utawafanya vijana wengi wa nchi hii kupoteza mwelekeo baada wakivuta dawa hizi za kulevya”, Carlos alieleza na kukata simu.
Ndio kwanza nilikuwa nimeamka kutoka usingizini, kuchelewa kwangu kuamka si kwamba mimi ni mtu mvivu, la hasha, hali hii ilitokana na mimi kuchelewa kulala usiku kutokana na kazi nilizofanya. Kama wewe ni binadamu mwenye huruma, utaona ni jinsi gani mimi nilistahiri kulala mpaka muda huu. Ilinilazimu kulala KB Hoteli iliyoko Mabibo ili asubuhi niweze kuonana na shemeji yangu Mama Feka, ambaye pia alifikia katika hoteli hii. Kilichonitoa usingizini ni kelele ya mwito wa simu iliyopigwa na Peter TWite, Vinginevyo ningeendelea kuuchapa usingizi, nilijivuta taratibu na kupokea simu. “Jambo Mkuu”, sauti ya Peter ilipenya masikioni mwangu. “Oh Peter, Jambo. Habari ya asubuhi”. “Habari nzuri mkuu, nakujulisha kazi uliyonituma, vijana wako kwenye pointi kama ulivyoshauri, kuwatambua kila mmoja amevaa fulana na kofia nyeusi za NSSF. Ili kuepusha usumbufu, nimewajulisha wavae kofia ziangalie nyuma, maana anaweza kutokea mtu mwingine amevaa vile ikawa shida”, Peter alieleza. “Asante Peter, kama nilivyokufahamisha, usishughulike na jambo lolote mpaka nitakapokujulisha, usizime simu, usiwe mbali na eneo lako, kuna kazi moja itabidi uifanye majira ya saa tisa alasiri hivi. Usiniangushe”, nilisisitiza. “Siwezi, siwezi kabisa kukuangusha mkuu. Utakapokuwa tayari kunituma kazi yoyote utanifahamisha, nafahamu wakati tuliomo bosi, niamini tafadhali”. “Usijali Peter, wewe endelea mpaka nitakapokujulisha vinginevyo”. “Tuko pamoja”. Niliwasiliana na Luteni Fred Libaba nikamjulisha mahali nilipokuwa, niliagiza awachukue Luteni Claud Mwita na Sajenti Julius Nyawamiza, awalete KB Hoteli chumba namba kumi, floo ya pili. Nikamjulisha kuwa wakifika wanipigie simu. Ningia maliwatoni, nikafanya usafi wa mwili wangu, nilikoga, nikanyoa ndevu na kujiweka vizuri, halafu nikashuka chini kwa ajili ya kifungua kinywa. Sebastian alikuwa mmoja wa rafiki zangu, kazi yake ilikuwa dereva taksi, alifanya kazi zake sehemu mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam. Kijana huyu ndiye aliyenileta hapa usiku, nikamfahamisha pia anifuate saa mbili asubuhi na tayari alikuwa amefika kunichua. “Umelala saa ngapi Seba?”, nilimuuliza. “Hizi kazi zetu hatuna muda wa kulala, dereva taksi halali kaka, unaposubiri wateja, ndiyo nafasi ya kulala hiyo”, alieleza Sebastian. “Nitakuwa na wageni, nahitaji kutumia gari yako kwa shughuli zangu binafsi. itakuwa siku ya leo na kesho, nitakulipa”, nilimwambia. “Hakuna shaka kaka, funguo za gari hizi hapa, ukimaliza mambo yako utanijulisha, iwe siku mbili, wiki au mwezi”.
Baada ya kupata kifungua kinywa, nilisimama, wakati najiandaa kurejea chumbani kwangu, Fred, Claud na Nyawaminza waliingia. “We Fred, ina maana mlikuwa karibu sana?”, nilimuuliza. “Hata sisi tumelala Mabibo, niliwaambia wenzangu, Teacher asipolala Sinza, basi atalala Mabibo, utabiri wangu umekuwa sahihi”, alieleza Fred. Tulipanda ngazi tukaingia chumba namba kumi, “Karibuni, baada ya kutoka nyumbani kwa Carlos usiku, niliona vyema kulala hapa. shemeji yangu Mama Feka yuko chumba namba nane, kwa kuwa tumekutana wote hapa, ngoja nimwite aje mbele yenu, itakuwa vizuri mkimfahamu”, niliwaeleza wote wakatingisha vichwa kukubaliana nami. Nilisimama kwa sekunde kadhaa nje ya mlango wa chumba namba nane, nilijiuliza maswali kadhaa, ambayo majibu yake yalielekea kunishinda. Nilijiuliza kuhusu kazi ninayotaka kumtuma mwana mama huyu, ni sahihi au namuingia katika matatizo. Hata hivyo nilipiga moyo kinde, nikagonga mlango, akaniruhusu kuingia. Mama Feka alikuwa amevaa kaptula na fulana, zilizomfanya apendeze sana. Jasho jingi lilikuwa likimtoka mwilini kwa sababu ya mazoezi, aliponiona akasitisha mazoezi na kunisalimia, “Sema shem wangu, umelala salama?”. “Niko salama kabisa shem, ama kweli wewe ndiye Cnthia Rothrock wa ukweli, nimelala hapa chumba namba kumi, niko na wenzangu, wanahitaji kukuona, ukimaliza mazoezi yako, njoo room namba kumi tuzungumze kidogo”, nilimwambia. “Dakika moja”, alisema Mama Feka nikatoka nje na kumwacha akijiandae. Maana vitu vingine vya shemeji sina ruhusa ya kuviona.
“Tumsubiri kidogo, anakuja, alikuwa katika mambo ya kujiweka sawa kiafya”, niliwajulisha wenzangu, waliokuwa kimya, wakainua vichwa vyao juu kuonyesha ishara kuwa wamenielewa.
Wakati tunamsubiri Mama Feka, niliona ni vyema nitumie nafasi hii kuwaeleza habari ya usiku. “Fred, niliwahi kukwambia siku zote usiamini maneno ya mtu, wakati tunamsubiri Mama Feka, labda nitumie nafasi hii kukujulisha kuwa Carlos Dimera si binadamu wa kawaida, ni aina ya mnyama tena hatari zaidi ya chui”, akanitolea macho na kunishangaa.
“Ehee, imekuwaje bosi, maana kiasi fulani umenishitua?”, alihoji Fred kwa shauku kubwa.
“Sikiliza Fred, huyu mzungu rafiki yako, au sijui ni nani kwako, anamiliki kikosi kikubwa cha uhalifu hapa jijini, sasa nakwambia tukifanya mchezo tumekwisha, take care”, nilimwambia.
“Si rafiki yangu kabisa, kumbuka nilikwambia habari za huyu mzungu nilielezwa na rafiki yangu mmoja wa polisi, binafsi sijawahi hata kukutanishwa nae”, alijitetea.
“Basi elewa hivyo, mimi nilimtilia shaka mapema kabisa, ndiyo maana nimejiridhisha baada ya kufika nyumbani kwake usiku. Huyu mzungu ndiye chanzo cha mambo yote ya uhalifu hapa jijini, sasa nasema ama zake ama zangu, amejiandaa vizuri sana, lakini sisi pia tuko vizuri, au vipi jamani?”, niliwauliza wenzangu huku wote wakiniunga mkono.
“Sasa ajiandae kukutana na mkono wa sheria, watu kama hawa siku zao ni arobaini, mwisho wake umetimia, kama ulivyosema, ama zake ama zetu, naamini tutashinda”, Julius Nyawaminza alieleza kwa hasira.
Niliwaeleza kila jambo, jinsi nilivyoingia nyumbani kwa Carlos Dimera, hali ya ulinzi ilivyokuwa na mipango yao ya uhalifu waliyokuwa wakipanga. “Walikuwa katika sherehe, eti wakisherehekea kifo changu, cha ajabu hawakuweka ulinzi wa aina kabisa, wameamini nimekufa, siku wakiniona watatamani ardhi ipasuke”.
“Kama ndivyo kwanini tusiwakamate mapema ili kuokoa muda?”, Claud alihoji na kuongeza, “Maana kila kitu kiko wazi, sasa sijui tunasubiri nini mkuu?”.
“Ni kweli kabisa Claud, kama inawezekana wakamatwe wakati ni huu sasa”, Nyawaminza alirukia kuunga mkono maneno ya Claud.
“Hapana, tusikurupuke kufanya jambo ambalo halina tija kwa taifa. Sikilizeni, ingekuwa kazi ni kuwakamata tu, ningewaita hata usiku tukawamata kama kuku, lakini tutakuwa tumefanya kazi ya bure, lazima muelewe kuwa nchi yetu inatawaliwa kwa mjibu wa sheria, huwezi kumtia mtu hatiani bila kuwa na ushahidi. Fred… unadhani inawezekana, haya sawa, tutamfikisha mahakamani kwa kosa lipi?”, niliwauliza.
“Hakika bosi, itakuwa vigumu kumkamata mtu bila ushahidi, nashauri tufanye kila njia wakamatwe na ushahidi”, alishauri Fred, wote tukamuunga mkono.
“Leo tutafanya kazi moja ndogo, lakini yenye faida kubwa kwetu. Fred jiandae tutakwenda kumkamata mtu mmoja anaitwa Raymond Kenoko, huyu jamaa ni Afisa wa Uwanja wa ndege, Claud na Nyawaminza nitawaelekeza cha kufanya, halafu…”, kabla sijaendelea mlango uligongwa, Mama Feka akaingia.
“Habarini za asubuhi”, Mama Feka alisalimia.
“Oh, nzuri, nzuri”, tulimwitikia kwa pamoja. suluali ya blue na fulana ya njano, alizovaa zilimfanya apendeze sana, aliingia na kusimama mfano wa mtu anayesubiri kupandishwa kizimbani.
“Pole na safari shem wangu, pole kwa kukukatisha usingizi wako, pole kwa kila nililokukosesha kulifanya asubuhi ya siku ya leo”, nilimuomba radhi.
“Usijali shem”, Mama Feka alisema kwa mkato huku akitabasamu.
“Jamani, huyu mwana mama ni shemeji yangu kabisa, ametoka Nyamuswa kwa ajili ya kushiriki mahafari ya chuo kikuu huria, lakini kabla hajafika huko chuoni nikamuomba aonane na sisi kwa ajili ya mambo fulani fulani ambayo tutamuomba atusaidie”, niliwaeleza wenzangu wakatingisha vichwa.
“Kazi gani tena shem? Mbona unanitisha jamani”. “Usiogope molamu, labda nieleze moja kwa moja utanielewa”. Nilitumia nafasi hiyo kuwatambulisha wenzangu kwake ili awafahamu, halafu niliendelea. “Hapa jijini limeibuka kundi moja hatari la wafanyabiashara wa dawa za kulevya, hawa jamaa ndiyo wanauzia watu madini feki kama umewahi kusikia, wanateka watu na kuwapora mali zao mchana na usiku, wanaibia watu kwa mtindo wa noti au dolla bandia, mji umechafuka kwa ajili yao, sasa sisi hatukubaliani nao”, nilimwambia.
“Umenikumbusha mbali, mwanangu aliwahi kuibiwa kwa mtindo wa madini feki, wakachukua ada yote ya shule, hao watu ni wauaji kabisa”, alieleza Mama Feka.
“Pole, sasa kinara wao yuko hapa ni mzungu, huyu mzungu ndiye anafadhili mambo haya, lakini kumkamata imekuwa ngumu kidogo”, nilieleza.
“Kuna ugumu gani shem?, mtu kama huyo si anakamatwa tu jamani, mwanangu alilia sana siku hiyo, alikuja na chupa akidai ameuziwa madini, iliniuma sana jamani, kwa hiyo ulitaka nieleze ilivyokuwa?”, aliuliza.
“Hapana shem, kuna jambo moja la msingi sana ambalo tumelijadili na wenzangu kwa muda mrefu, baada ya kutafajari kwa kina, tukaishia kukuchagua wewe utusaidie kufuatilia mambo fulani, ambayo yatatuwezesha kumtia hatia mtu huyo”, nilimwambia akacheka.
“Ehe, mnataka mimi nifanye nini?”, alihoji.
“Tunataka tukutume ujiingize upande wake iwe rahisi kwetu kumkamata na ushahidi, unasemaje shem?”, nilimuuliza.
“Heeee, shem hivi inawezekana mtu akajipeleka mwenyewe jehanam, si hatari hiyo, kwanza mimi nimekuja Dar kwa kazi nyingine, aaah itakuwa ngumu, hivi nitaanzaje kujiingiza huko?”, alilalama Mama Feka huku akisimama.
Nilishika kichwa, nikainamisha uso wangu chini, nilianza kutafakari hili na lile nikitafuta majibu lakini nikakosa. Wenzangu, Claud Mwita, Julius Nyawaminza na Fred Libaba nao walikuwa kimya wakiniangalia.
“Keti tafadhali shem”. Nilitumia nafasi hiyo kumweleza mambo mengi yanayoweza kumfanya binadamu akaonekana shujaa kwa watu, nilimuomba arejee alipokuwa ameketi. Nikasimama, nilitembea kutoka kona moja ya chumba hiki kwenda upande mwingine.
“Samahani shem, si kusudio langu kukuingiza kwenye moto, kukutuma ujiingize upande ule si kwamba tutakuacha tu, tutakuwekea ulinzi wa hali ya juu, tutakufuatilia wakati wote, kuhusu usalama wako ondoa shaka”, nilieleza.
“Sawa, lakini nitaanzaje kujiingiza upande wao, kwanza wataniamini vipi?”.
“Tunataka kujaribu kitu kimoja, tumepata taarifa kuwa huyu mzungu Carlos Dimera, anapenda sana wasichana wazuri, kila anapowaona hupagawa, ndiyo maana nikasema kwako itakuwa rahisi atanasa, na akinasa hatutakuacha tu, tutakufuatilia kila hatua utakayokuwa”, nilimwambia.
“Mmmm, sasa naanza kukuelewa, unataka nitumie mbinu zangu huyo mzungu Carlos anipende au sivyo?”.
“Ndivyo tunavyotaka”, Nyawaminza aliyekuwa kimya kwa muda mrefu akitafakari aliongeza.
“Majaribu haya, sina jinsi, niko tayari kuwasaidia sasa natakiwa kufanya nini?”.
“Tutakuwezesha kwa pesa na mavazi. Tumepata ratiba kuwa huyu mzungu kila siku lazima afike Msasani Shopaz Plaza kwa ajili ya kununua vitu vidogovidogo vya kula, halafu huenda Seaclif Hoteli, akitoka hapo, hujirusha kwenye muziki, California Dreema. Shem, hakikisha wewe pia unapatikana maeneo hayo, akikuona tu atakushobokea, lakini uwe mwangalifu sana”, nilimuasa.
“Kazi hiyo niachie mimi, nawahakikishia huyu mzungu kwangu atanasa, chezea Cnthia wewe, niko tayari kuanza kazi hiyo”, alisema Mama Feka hofu ikiwa imemtoka. Niliwasiliana na Peter Twite kumjulisha hatua tuliyokuwa, nilitumia nafasi hiyo kumwelekeza ratiba ya kazi atakapokuwa na Mama Feka. Tulimpangia kazi ya kumpeleka sehemu alizopangiwa, yaani Shopaz Plaza, Seaclif Hoteli na California Dreema.
Wakati vyombo vya ulinzi na usalama nchini vikifuatilia kwa makini na karibu matukio ya kutisha ya uhalifu yaliyokuwa yakiendelea Jijini Dar es Salaam. Watu kadhaa walifika vituo vya polisi kutoa maelezo ya jinsi walivyo tapeliwa.
Mfanyabiashara John Roman, afika Kituo Kikuu cha Polisi, Sokoine Drive, baada ya kuibiwa kwa njia ya mtandao, Shaaban Ismail, baada ya kubaini kuwa ameibiwa, alifika haraka kituo cha polisi Oysterbay, ambapo maofisa wa polisi walichukua maelezo yak.
John Roman ni mmiliki wa klabu ya ‘Toroka Uje’ ambaye aliibiwa pesa nyingi kwa njia ya mtandao. Alifika polisi akionyesha namba za simu za nje zilizotumika kuwasiliana nae na kumfanya atume pesa nyingi, akiwaomba polisi watumie uwezo kuzifuatilia namba hizo.
Akihojiwa na polisi wa zamu waliokuwa kituoni hapo, John Roman alieleza kuwa, awali alipokea ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika ADB, ukimweleza kuwa ameteuliwa kuwa mrithi wa Hayati John Bryson wa Uingereza, aliyekuwa na akaunti katika benki hiyo, lakini alifariki dunia na kuacha pesa nyingi..
Maelezo ya John Roman yalimshawishi Afisa wa Polisi kumhamishia chumba maalumu cha mahojiano, afisa huyo alifanya hivyo baada ya kuvutiwa na taarifa hiyo. Alipoingia ndani ya chumba hicho, askari huyo alimtaka bwana John Roman kulielezea vizuri kuhusu tukio hilo.
“Nimekuleta katika chumba hiki ili tuweze kuzungumza kwa uwazi zaidi, tukio hili ni moja ya matukio ya uhalifu yanayotokea karibu kila siku, naomba uanze kueleza toka mwanzo wa tukio hili mpaka sasa, usifiche kitu na usione aibu. Eleza mpaka ulivyofika hapa”, Inspekta Judicate alieleza, akijiweka sawa kuandika maelezo yake.
“Ni hadithi ndefu Afande, lakini nitahitahidi kueleza kama ilivyo, naamini polisi mba mbinu zetu ambazo zitasaidia kuwakamata watu hawa. Maana kichwa changu hakifanyi kazi vizuri, nimevurugwa”, John Roman alieleza.
“Usijali, maji yakimwagika hayazoleki, lakini maelezo yako yataisaidia polisi katika upelelezi wa tukio hili, cha msingi usifiche jambo”, Inspekta Judicate alimhakikishia.
“Asante sana Afande, nakumbuka siku tatu zilizopita nilipokea ujumbe kupitia email yangu, ukiuliza kama mimi ndiye John Roman raia wa Tanzania Bara, nilipojibu ndiyo, nilipokea ujumbe mwingine ukiniuliza nahusika na biashara gani, nilipojibu kuwa namiliki klabu. Hawakutuma ujumbe tena, isipokuwa walinipigia simu wakitumia namba za nje ya nchi”, alinyamaza kidogo ili kumeza mate, baada ya kutafakari aliendelea.
“Afande, watu hawa ni wajuzi wa hali ya juu, aliyenipigia simu alijitambulisha kwa majina ya Roggers Peter, akidai kuwa ndiye Mtendaji Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, ambayo Makao Makuu yake ni Ouagadougou nchini Bukinafaso, Afisa huyu alinieleza kuwa benki imenichagua mimi kuwa mrithi wa mali za marehemu John Bryson, raia wa Uingereza aliyekuwa na pesa nyingi katika benki hiyo, nilipohoji inakuwaje niteuliwe kuwa mrithi wa mali za mtu nisiyemjua, Afisa huyo alinieleza kuwa huo ni mpango wa siri wa benki na kwamba watanitumia nyaraka mbalimbali za marehemu John Bryson, ikiwa pamoja na hati ya kifo ili nizitumie kupokea pesa hizo kama urithi alioniachia. Lakini akaniasa kuwa mwaminifu, akidai kuwa kuna dola milioni sita za kimarekani ambazo zitaletwa Tanzania kwa jina langu, nitazipokea uwanja wa ndege, halafu tutagawana”, alieleza.
Inspekta Judicate aliyekuwa akiandika maelezo hayo kwa haraka na kwa umakini, aliuliza “Kumbe Makao Makuu ya Benki hii yako Bukinafaso?”
“Hata mimi ndiyo nafahamu hivyo, maana sikuwa na uhakika”.
“Oke. Kwa jinsi inavyoelekea ni kweli watu hawa ni wajuzi katika kutenda uhalifu, ehee, ikatokea nini sasa?”.
“Nilishawishika kwenda kwenye mtandao, kama unavyojua dunia sasa ni kijiji, sikuchelewa nikaandika neno Mtendaji Mkuu wa ADB, likatokea jina la Roggers Peter, nikaanza kuyaamini maneno ya mtu huyo, baada ya muda nikapokea taarifa na nyaraka mbalimbali za marehemu John Bryson, ikiwa pamoja na hati ya kifo, ikieleza kuwa alifia nchini Uingereza na kuzikwa huko”, alinyamaza kidogo kupisha kama kuna swali.
“Hizo nyaraka ulizipokea kwa njia gani?”, Inspekta Judicate alihoji.
“Documenti zote za tukio hili zilitumwa kwa njia ya mtandao, na kweli zilikuwa zinaendana na tukio lenyewe, ilifika wakati nikaanza kuwaamini, mimi ni mtu makini sana lakini sijui nilipatwa na jinamizi gani?”, alieleza John Roman huku akitoa nyaraka hizo na kuzikabidhi kwa Inspekta Judicate.
Inspekta Judicate alizipitia documenti hizo moja baada ya nyingine, akiziangalia kwa makini, halafu akaziweka kando.
“Ehee, nini kikatokea sasa, maana unanieleza hadithi ambayo hakika ni tamu masikioni mwangu, endelea?”. “Jana asubuhi, nilijulishwa kuwa benki imewatuma maofisa wake wawaili, Mohamed Mussa na Seif Mtigino kusafirisha pesa hizo hadi Dar es Salaam, nilitakiwa kufika uwanja wa ndege saa sita mchana kwa ajili ya kupokea pesa hizo. Kwa kuwa pesa zina mambo mengi, nilimuomba Afisa wa Jeshi la Ulinzi, Kapteni Masey anisimamie kupokea pesa hizo, lakini alinikatalia, akidai kuwa huo ulikuwa utapeli, kiasi fulani nilimlaumu, lakini sasa nimeamini kuwa alikuwa na nia njema”, alieleza John Roman.
“Afisa huyo wa Jeshi hakukueleza chochote zaidi ya kusema uache ni utapeli, kama wewe mwenyewe ulivyosema hapa?”.
“Afisa huyo yeye alikataa tu, akidai kuwa hao ni matapeli na kwamba hawezi kupoteza muda wake kunipeleka kwa matapeli eti nikatapeliwe, lakini pia alinisihi niachane na mpango huo, lakini sikumwelewa, ndiyo nazinduka usingizini sasa baada ya kuwa tayari nimeibiwa, tena nakumbuka alinieleza kuwa Benki ya Maendeleo ya Afrika ni kwa ajili ya maendeleo ya nchi za Afrika tu, haiwasiliani na mtu mmoja mmoja, pia alieleza kushangazwa na mtindo wa kusafirisha pesa hizo kuja Tanzania, ningemsikiliza hakika nisingekutwa na jambo hili”, alieleza machozi yakimtoka.
Inspekta Judicate alikuna kichwa cheke, huku kalamu yake ikiwa mdomoni kwa mshangao, alimwangalia John Romani kwa macho makali. “Kumbe ulipewa darasa la kutosha na bado ukaendeleza ujinga wako, aisee wewe ni kichwa maji kweli, lazima ufahamu kuwa maofisa wa Jeshi wana mbinu nyingi, kama alivyokushauri ungemsikiliza, au ungetoa taarifa kituo chochote cha polisi”.
“Ni kweli, hata mimi najiuliza sasa, sijui niliingiwa na tamaa au shetani gani, maana wakati wote mimi ni mtu makini sana”, alieleza John Roman.
“Wewe si mtu makini, ungekuwa makini usingekaidi ushauri wa Afisa wa Jeshi”, Inspekta Judicate alieleza kwa sauti ya kukatisha tamaa. Alimwangalia John Roman kwa macho yake makali, macho ya mwanamke Afisa wa polisi, aliyewiva katika utendaji kazi wake.
“Ni kweli Afande, unajua linapotokea jambo kama hili ndiyo mtu unajifunza, kwa kuwa limetokea sina jinsi kujifunza”. alieleza John Roman kwa unyenyekevu.
“Ehee, kwa hiyo hizo dola ndiyo zikaletwa Dar es Salaam au ilitokea nini tena?”, alihoji Inspekta Judicate kwa shauku.
“Ilipofika saa tano jana, nilipokea simu nyingine kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kwa majina ya Mohamed Mussa, akadai kuwa yeye Afisa kutoka ADB, akanijulisha kuwa ndege iliyokuwa ikitoka Bukinafaso kuelekea Dar es Salaam, Nchini Tanzania imepata hitlafu ikiwa angani na kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Entebe, Nchini Uganda, hivyo, akashauri nitume haraka dola elfu ishirini za Marekani ili waweze kuondoka Entebe kuja Dar es Salaam, wakidai kuwa visa zao zikiisha kabla ya kufika Dar es Salaam, itabidi warudi tena Bukinafaso, jambo ambalo wao binafsi hawapendi litokee”.
“Ukatuma pesa hizo?”.
“Mdiyo, ikanilazimu kuwatumia hizo pesa”.
“Kwa nini hukuwaambia watumie pesa walizokuwa wakisafirisha kuleta Dar es Salaam. Maana kama ni pesa walikuwa nazo tena nyingi. Dola milioni sita ni pesa nyingi, ni zaidi ya shilingi bilioni kumi za Tanzania, inakuwaje utume pesa?”, Inspekta Judicate alihoji.
“Niliwashauri watumie pesa hizo walizokuwa wakisafirisha, lakini wakadai kuwa taratibu za Benki haziruhusu pesa hizo kufunguliwa mpaka zifike sehemu husika, nikawaeleza kuwa mimi ni mlengwa wa pesa hizo, naruhusu zitumike, lakini hawakunielewa, wakadai kuwa zikifunguliwa itakuwa vigumu kupokelewa na wakala wa Dar es Salaam, atakayethibitisha kama pesa hizo zimefika salama Tanzania, ikanilazimu kutuma kiasi hicho haraka iwezekanavyo”, alieleza.
“Mama yangu, baada ya kutuma pesa hizo ikatokea nini?”, Inspekta Judicate alihoji.
“Baada ya kutuma pesa hizo. Simu zao hazikupatikana, kuanzia ya aliyejiita Mtendaji Mkuu wa ADB, pamoja na maofisa wote waliohusika kunipigia simu, lakini pia nilipotoa taarifa kwa mamlaka zingine ili kuzuia pesa hizo zisichukuliwe, nilikuwa nimechelewa, hali halisi ndiyo hivyo Afande”, alieleza John Roman.
“Mmmm, iko kazi, maana inawezekana watu hawa wako hapa hapa Dar es Salaam, naamini pia wanakufahamu, ndiyo maana wakaweza kupata hata namba zako za simu na majina yako, ok, ngoja tujaribu jinsi ya kukusaidia, pia taarifa hii tutaipeleka kwa wenzatu wa usalama ili nao waifanyie kazi”, Inspekta Judicate alieleza huku akisimama.
“Nitashukru”, John Roman nae alisema huku akimshika mkono wa wakaagana.
Wakati huo, Mama Feka alikuwa amewasili kwenye maegesho ya magari ya Msasani Shopaz Plaza, alifika eneo hili mapema kwa ajili ya kazi moja, kumshawishi Carlos Dimera ampende. Alikuwa ameketi ndani ya gari aina ya Ford Pick Up yenye rangi ya kijani, ambayo vioo vyake vilikuwa vyeusi, hivyo si rahisi kuonekana kwa mtu anayepita nje.
Aliketi kwenye viti vya nyuma vya gari hii Doble Cabine, huku wakiteta mawili matatu na Peter Twite, aliyemleta hapa. “Cha msingi uwe makini sana na watu hawa, naamini Teacher hawezi kumtuma mtu asiyemwamini, amekuamini ndiyo maana amekutuma katika kazi hii”, Peter Twite alimwambia Mama Feka.
“Nitajitahidi sana, naamini siwezi kuwaangusha, sijui kitokee nini, lakini nitajitahidi kupambana, najiamini”, Mama Feka alimwambia Peter. Alichukua picha ya Carlos Dimera iliyokuwa kwenye mkoba wake, akaingalia kwa mara ya mwisho, halafu akairejesha mahali ilipokuwa.
“Baadaye”, Mama Feka aliaga.
“Kila la heri, usiogope, maana kila utakapokuwa tutakuwepo pia”, Peter alieleza, Mama Feka akashuka kwenye gari na kuingia upande wa Supermaket hii kubwa iliyoko Barabara ya Kawe, Dar es Salaam.
Dakika kadhaa baadaye, Carlos Dimera aliwasili eneo hilo, akifuatana na mpambe wake, Jackna, walipoukaribia mlango wa kuingilia ndani, Jackna alikimbia na kuufungua mlango huo, ili Dimera aweze kupita. kama ilivyo kawaida yao, Walipoingia ndani haraka Jackna, alianza kusukuma tololi, akiwa nyuma ya bosi wake, ambaye wakati huo alikuwa akichagua vitu kadhaa anavyopenda kununua katika Supermaket hii. Mama Feka aliyekuwa upande huo, akitafuta jinsi ya kuwasiliana na watu hawa, alibeba kikapu mkononi, akasogea mpaka kwenye pembe ya mwisho ya Supermaket, mapigo ya moyo yakamwenda mbio, akajiuliza mawili matatu, akapata jibu. Haraka akazunguka upande wa pili, alipofika sehemu ya makutano, hakuchelewa, akamgonga Jackina kama bahati mbaya, vifaa vyake zikamwagika chini.
“Vipi wewe kaka unatembea kama kipofu?”, Mama Feka alihoji.
Jackina alihamaki, haraka akainua mkono wake juu ili aushushe katika mashavu ya Mama Feka, lakini Carlos Dimera alikuwa mwepesi akaudaka mkono wa Jackina na kumzuia.
“Jackina, acha bwana, usipende kuwapiga watoto wazuri kama huyu, Mungu aliwaumba ili waupendezeshe ulimwengu”, Carlos Dimera alisema huku akitembea taratibu kuelekea kwa Mama Feka. “Pole sana, usijali kwa lililotokea”, hakafu akamgeukia Jackina, “Haraka okota vitu vyake, nitamlipia bili”. Jackina aliinama na kuokota vitu vilivyokuwa vimemwagika na kuvirejesha katika kikapu.
“Utaongeza nini malkia ili nikulipie bili?”, Carlso Dimera alimuuliza Mama Feka aliyekuwa amesimama akiwaangalia kwa hasira.
Alichukua kikapu chake, akatembea hatua mbili, halafua akawageukia na kusema, “Sikiliza kaka, mimi sibabaiki na rangi yako, kwetu si masikini kama unavyodhani, sina shida ya kulipiwa bili, tunajiweza ndiyo maana nikaja hapa, kaa na pesa zako, lakini pia mwambie huyu bwege wako avae miwani ili siku nyingine aweze kuona”.
“Shika adabu yako we malaya”, Jackina alifoka.
“Malaya ni wewe unayetembea kama kipofu”,
“Nyamaza Jackina, mbona hunielewi, usipende kugombana na wasichana”, Carlos alimtuliza Jackina huku Mama Feka akiondoka. “Ni msichana mzuri sana”, aliongeza Carlos.
“Lakini, anaonekana kuwa hana adabu bosi”.
Kama ilivyo kawaida yake, Carlos Dimera, aliwasili katika Hoteli ya Seaclif, ambako hukutana na wageni kutoka nje ya nchi, ambao hufika nchini kwa ajili ya biashara haramu ya dawa za kulevya. Mara hii alifika hapa ili kuonana na mtu maarufu sana duniani, mtu ambaye vyombo vya habari vya dunia humtaja karibu kila siku.
Hakuwa mwingine, huyu ni Emilio, mtoto wa Pablo Escoba, aliyekuwa mwanasiasa, mbabe wa dawa za kulevya, raia wa Colombia ambaye historia inaonyesha hakuwa na mfano. Kijana huyu Emilio, alikuwa amewasili nchini kwa ajili ya kuonana na Carlos Dimera. Alimtambua Carlos kama mtu wa karibu, kutokana na historia zao.
Mtoto huyu wa mbabe wa dawa za kulevya, ambaye baba yake alitoka katika familia ya mwalimu na mkulima, aliambatana na msichana mrembo, Serina Wilson.
Jakna hakuruhusiwa kusikiliza mazungumzo ya Carlos na mgeni wake Emilio, hivyo aliketi katika meza nyingine karibu akisubiri. Wakati wote Carlos alikuwa hafanyi kosa, alijua kufanya kosa moja kunaweza kumgharimu. Aliwatumia hawa kupokea na kusambaza dawa, lakini mambo yake ya ndani, hakupenda kuwashirikisha kabisa.
“Karibu sana, hii ndiyo Tanzania”, Carlos alimwambia Emilio, wakasimama na kushikana mikono.
“Asante sana Carlos, vipi hali ya biashara hapa?”, Emilio alihoji.
“Tuko vizuri”, Carlos alijibu kwa mkato.
“Si kweli Carlos, nimelazimika kuja hapa, ili tuzungumze kwa kirefu kidogo, nini tatizo, haiwezekani mzigo ukwame Adis Ababa kwa muda mrefu kiasi hicho, halafu unasema uko vizuri?”, Emilio aliuliza.
“Kuhusu hilo tumelimaliza, ni kweli kulikuwa na tatizo kidogo kwa wenzetu wa uwanja wa ndege, lakini jambo hilo limekwisha, kila kitu kimekaa vizuri, mzigo unaweza kuwasili Dar es Salaam leo, kuhusu hilo, ondoa shaka, tumelimaliza”.
“Nini kilikwamisha huo mzigo kuingia hapa, kama ni pesa mnazo za kutosha, mnaweza kumnunua mtu yeyote, au unasemaje Carlos?”.
“Hilo halina ubishi, ilitokea tatizo ngazi za juu, huko serikalini, mtu mmoja alipewa cheo akajiona tayari amekuwa Mungu, akahamia uwanja wa ndege, baadhi ya watu wamekamatwa, lakini si wa upande wetu, hata hivyo pesa imefanya kazi yake, mtu huyo ameondolewa, mzigo unaingia leo, mamlaka zote zina taarifa kuhusu mzigo huo kuingia”, Carlos alieleza.
“Nilitaka kujua hivyo, haiwezekani nchi ndogo kama Tanzania kuwe na usumbufu wakati wa kuingiza mzigo, wakati nchi kubwa kama Marekani, China, Japan na South Afrika mzigo unaingia haraka na bila shaka. Nimekuelewa Carlos, nitaondoka leo, hakikisha biashara yetu inashamili na kupata watumiaji wengi zaidi, huo ndio msimamo wetu”, alieleza Emilio huku akisimama kwa ajili ya kuaga na kuelekea kwenye helikopita iliyomleta eneo hili.
“Hatutalala, amini hivyo”, alidokeza Carlos huku wakipeana mikono ya kwaheri, akaaga na kuondoka, akiacha maswali mengi kwa Carlos. .
Baada ya Emilio kuondoka, Carlos alimwita Jakina.
“Tukiendelea kucheza ngoma za sindiba, tunaweza kupoteza kazi, unamfahami huyu jamaa?”, Carlos alimuuliza Jakina.
“Hapana”, Jakina alieleza.
“Huyu ni Mkurugenzi wa Shirika la Tuwezeshe, anatoka Marekani, alipenda kuonana na mimi kwa ajili ya mambo fulani, tukimaliza kazi hii salama, nitamuomba twende wote, yaani mimi na wewe tuishi Marekani, ukaishi huko Jakina”, Carlos alidanganya. “Hakuna kitakachoharibika bosi, tumejipanga vizuri mno, naamini mzigo utaingia usiku huu, Hawa amefanya kila jambo, hakuna wa kuzuia”, Jakina alijinasibu.
Wakati huo, Mama Feka alikuwa ameketi upande wa pili kwenye kona akiwaangalia. Alipoona sasa ni wakati mwafaka, alitoka na kujipitisha mbele yao. Mama Feka alipita mbele ya meza waliyoketi Carlos na jakina, kama hajawaona vile akatafuta meza akaketi.
“Bosi, umemuona yule dada mshenzi wa Supermarket?”, Jakina alimuuliza Carlos.
“Na wewe husahau, kama alikukela msamehe, nenda mwambie aje aketi na sisi hapa”, Carlos aliagiza.
“Achana na huyo mshenzi, atatupotezea muda wetu, mbona wasichana wapo wengi tu bosi”, Jakina alieleza msimamo wake.
“Hapana, nimesema nenda mwambie aje hapa”.
“Mkorofi yule bosi”.
“Jakina, elewa kuwa si ombi, nasema nenda mwambie aje aketi na sisi hapa, ni wakati wa kumuomba msamaha kwa yaliyopita”, Carlos alieleza huku Jakina akisimama,
Huku mapigo yake ya moyo yakimwenda kasi, Jakina alitembea hadi mahali alipoketi Mama Feka. Aliona njia pekee ni utani, hivyo alimtokea kwa nyuma na kumshika bega.
“Helo, hujambo mrembo”, alisema Jakina huku Mama Feka akigeuka. Macho yao yalipokutana, Mama Feka akaonyesha mshangao wa uongo.
“Haaa, wewe ndiye yule kipofu wa Supermarket?”, Mama Feka alihoji.
“Anaomba uhamie kwenye meza yake, tupate chakula pamoja”.
“Tupate chakula pamoja, nikikuita kipofu unachukia, hapa unaona nakula, halafu unasema tukapate chakula pamoja na bosi wako, mbona siwaelewi?”.
“Tunaweza kuhama na chakula chako, tafadhali niruhusu nikubebee chakula”, Jakina aliomba.
“Hapana, mwambie bosi wake sina muda huo”, Mama Feka alieleza.
“Sawa, lakini unapoteza bahati yako”, Jakina alimwambia.
“Acha ipotee”, Mama Feka alieleza kwa kujiamini.
Jakina alirejea kwenye meza ya Carlso.
“Yule msichana ni jeuri sana, anasema hana muda wa kuonana na wewe, nimemwambia anapoteza bahati amesema acha ipotee, anajiamini sana, yawezekana ni mtoto wa kigogo”, Jakina alieleza.
“Achana naye, iko siku atanasa”, Carlos alieleza, baada ya kupata vinywaji na chakula, Carlos na mpambe wake Jakina waliondoka. ****************
Niliendesha gari kwa mwendo wa kasi ili tuwahi kufika. Wakati huo nilikuwa nikiendesha gari aina ya Isuzu Troupe steshen wogan yenye rangi ya kijani, Fred alikaa kimya akiniangalia, bila shaka aliuhofia mwendo wangu. Tulipofika kwenye taa za kuongoza magari zilizoko katikati ya Barabara za Mandela na Uhuru, eneo la Buguruni, nilisimama ili kusubiri ruhusa ya taa hizi.
Kila mmoja alikaa kimya akitafakari nini hatma ya jukumu lililokuwa mbele yetu, magari yalipoanza kuondoka, niliongeza mafuta nikayapita baadhi ya magari yaliyokuwa mbele, tulipofika kwenye taa za Tazara, zinazoruhusu magari yanayotumia Barabara za Nyerere na Mandela, tulisimama tena hadi zilipoturuhusu kuendelea na safari.
Dereva wa gari lililokuwa mbele yetu alinionysha ishara ya taa, nikalipita gari hili kwa mwendo wa kasi, nadhani dereva huyu alitambua haraka tuliyokuwa nayo, akaamua atupishe. Ni madereva wachache sana barabarani wenye uelewa kama huyu, nilipiga honi ya asanye, nikaongeza mwendo. “Uko vizuri”, nilimwambia Fred aliyekuwa kimya.
“Niko sawa”, alisema huku akiniangalia.
“Lolote laweza kutokea, lazima tukubaliane na hali hiyo”, nilimwambia Fred.
“Najua hivyo bosi, lolote laweza kutupata, lakini naamini kuwa tutashinda, wewe ukisimamia jambo sidhani kama linashindwa”, alinipamba.
“Ni kweli, lakini kila jambo na wakati wake”, nilisema wakati nikiingia kwenye maegesho ya magari ya Uwanja wa Ndege. Nilitafuta mahali pazuri nikaegesha gari.
“Fred… Hapa tumekuja kufanya kazi moja tu, kumkamata Afisa Ukaguzi, tukifanikiwa kumkamata huyu, kazi yetu itakuwa rahisi, vinginevyo itategemea kudra za Mwenyezi Mungu”.
“Atakamatwa tu”, Fred alisema kwa kujiamini.
“Sikiliza Fred, ingia ndani omba kuonana na Mr. Raymond Kenoko, ndiye Afisa Ukaguzi mwandamizi. Utakapomuona, mwambie kuna mgeni wake ndani ya gari, akifika hapa tumemaliza kazi”, nilimwambia Fred. Aliniangalia kwa sekunde kadhaa halafu akavuta shati na kutoa bastola yake ndogo, akaigagua.
“Iweke hapo kwenye droo ya gari, hapa si mahali pake”, niliagiza, akafungua droo ya gari akahifadhi silaha yake, akafungua mlango wa garu na kutoka taratibu kama ilivyo kawaida yake.
Kwa wasiomfahamu Fred, ni mmoja wa vijana watanashati, mtaratibu, hata vitendo vyake huvifanya taratibu, ukimuona ghafla unaweza kudhani ni mtu zoba, lakini ukihitaji undani wake, unaweza kuingia kwenye mto wenye mamba ili asikutie mikononi mwake.
Wakati nikimsubiri Fred, niliwasiliana na Kanali Emilly, kumuomba ajiweke tayari kuonana nasi wakati wowote kuanzia sasa. Niliwasiliana pia na Claud Mwita na Julius Nyawamiza kuwatahadharisha na hali ya sasa pia kuwaandaa kwa kazi.
Nikiwa ndani ya gari niliweza kuona kila mtu aliyekuwa karibu yangu, nikisaidiwa na aina ya vioo ya gari hii, kwani mtu akiwa ndani haonekani kabisa, lakini unaweza kumuona mtu wa nje kwa ufasaha zaidi. Mara Fred alifungua mlango akaingia.
“Huyu jamaa ametoka hapa dakika ishirini zilizopita, wanasema amekwenda kupata chakula pale Transt Motel, tumsubiri hapa au unasemaje bosi?”, Fred alihoji.
“Hapana, hapana twende haraka”, nilisema huku nikitoa shilingi elfu moja ili Fred akalipie ushuru wa maegeshi ya uwanja.
Haraka nikaliweka gari barabarani, nilipoona taa za Barabara ya Nyerere zitatuchelewesha kupita, niliamua kuliingiza gari huku madereva wa magari mengine wakitupigia honi, nikapenya na kuliegesha gari mbele ya Transt Motel, karibu kabisa na Reli ya kati.
Nilitoa picha ndogo ya Raymond Kenoko nikaiangalia kwa mara nyingine, haikuwa rahisi kumfahamu moja kwa moja hivyo ilitulazimu kutumia akili zaidi. Mara nikawaona watu wawili wakitoka ndani ya Transt Motel, walifanana urefu na maumbo yao, akili yangu ikacheza.
“Atakuwa mmoja kati ya hawa. Shuka muite kwa jina, atakayeitika ndiye”, nilimwambia Fred akafungua mlango na kuita, “Habari ya kazi Mr. Ray?”.
“Nzuri kaka, habari yako”, Raymond alisema huku akisogea ili kumshika Fred mkono, mwenzake alitembea hatua chache akasimama kumsubiri. Bahati nzuri alivaa kitambulisho chake shingoni, kikiwa na jina la RH Kenoko.
“Samahani kwa usumbufu, naitwa Jabir Idrisa, nimefika ofisini kwako nikaelezwa kuwa umetoka kwa ajili ya chakula, nikaona nikufuate, kwa ufupi ni kwamba nina mzigo umekwama, lakini nimeelezwa kuwa nikikuona waweza kunisaidia, sasa tunafanyaje kaka?”, Fred alidanganya.
“Nani kakutuma uje kwangu?” Alihoji kwa sauti nzito.
“Carlos”, Fred alidanganya.
“Ahaa, sawa sawa, ni mzigo tofauti na unaoingia leo?”, alihoji.
“Ndiyo, ni aina nyingine, labda tuingie ndani ya gari ili tuelekezane vizuri, uangalie uwezekano”.
“Hakuna shaka”, Raymond Kenono alisema huku akimuelekeza mwenzake atangulie ofisini. Fred alifungua mlango wa gari wakaingia.
“Mnanipeleka wapi jamani?”, Raymond Kenoko alihoji, wakati naingiza gari kwenye Barabara ya Nyerere kuelekea mjini, baada ya kuiacha barabara inayoingia Uwanja wa ndege.
“Uwe mpole kaka, sehemu ambayo utaweza kujibu maswali yetu vizuri”, nilimwambia kwa sauti ya ukali kidogo. Nilifungua droo ya gari nikatoa kitambulisho changu, nikamuonyesha.
“Nimekosa nini jamani?”, alihoji kwa sauti ya kukata tamaa huku mikono yake ikitetemeka.
“Sikiliza kaka, sisi ni watu wema kabisa, watumishi wenzio katika serikali, huna budi kutulia na usijaribu kufanya lolote ambalo linaweza kuyahatarisha maisha yako”, Fred alimwambia.
“Nimekuelewa kaka, sasa napaswa kufanya nini? kama kuna tatizo linahitaji ufafanuzi tuzungumze tu, dunia ya sasa hakuna siri, mnilinde jamani”, Raymond Kenoko alieleza.
“Sikiliza Mzee Ray, tunakuhitaji kwa mazungumzo ya dakika ishirini hivi, halafu tutakuacha utarudi kazini kwako, cha msingi ni ushirikiano, wewe unajua kwa nini tumekukamata, naamini hivyo”, nilimwambia. “Hapana, hakika sijui lolote”, alisisitiza.
“Sawa, kama hujui tutakusaidia kujua, cha msingi ni wewe kuwa na ushirikiano”, Fred alisema.
Tulipofika kwenye makutano ya barabara za Nyerere na ile inayokwenda Vingunguti, tuliiacha barabara ya Nyerere, nikachepuka na kuingiza gari kwenye barabara ndogo ya dharura, inayopita kushoto, pembeni mwa barabara hii ya Nyerere, nikaliongeza gari mwendo.
“Mtanisaidiaje?”, alihoji.
“Kuhusu nini?”, Fred alimuuliza.
“Kuhusu kusaidiana ili tumalize jambo hili lisifike mbali, maana ukipuuzia upole, kitakuwa kidonda”, alibainisha.
“Ni kweli, lakini ni jambo gani wakati wewe umesema hujui kwa nini tumekukamata?”, nilimwambia.
“Kwa vyovyote vile kutakuwa na sababu, haiwezekani maofisa kama nyie mnikamate tu bila sababu, lazima ipo sababu ndiyo maana nikasema tuzungumze kirafiki, tusiharibiane kazi. Tusaidiane”, alijitetea.
Mara simu yangu ya kiganjani ikaita, Kanali Benny Emilly alitaka kujua tumefikia wapi, maana kabla hatujatoka uwanja wa ndege kuelekea Transt Motel nilimjulisha wapi atusubiri, nilimweleza kila kitu akatuelekeza mahali alipo.
Tulipofika kwenye ofisi za kiwanda cha sigara cha Master Mind, kilichoko kando ya barabara hii, geti la kuingia liliachwa wazi, hivyo niliingiza gari moja kwa moja. Kama unavyojua sheria inaturuhusu kutumia ofisi yoyote ya umma na binafsi mahali popote, wakati wowote kwa ajili ya usalama wa nchi. Kanali Emilly alikuwa amefika mapema sehemu hii na kuandaa ofisi ya muda, kwa ajili ya kazi hii.
Meja Iddi Satara, mmoja wa wasaidizi wa karibu wa Kanali Emiily alinionyesha ishara nikalisogeza gari mahali alipokuwa, wakati haya yanafanyika Raymond Kenoko alibaki ameduwaa asijue la kufanya.
“Mtanisaidiaje?”, alijitetea kwa mara nyingine.
“Amini tutakusaidia, twende kwanza uongee na mkubwa, cha msingi uwe mkweli, vinginevyo utaozea jela, haki ya Mungu”, nilimwambia wakati tunatoka ndani ya gari, tukaelekea kwenye ofisi ya Kanali Emilly ya muda.
Kanali Emilly aliketi mbele ya meza kubwa iliyozungukwa na viti kadhaa vya wageni, ilikuwa ofisi ya kuvutia sana, Meja Satara alimuonyesha Raymond sehemu ya kuketi, bila ajizi akaketi.
“Karibu bwana Raymond Kenoko, Afisa Mkaguzi Mwandamizi wa Uwanja wa ndege. Naitwa Kanali Benny Emilly, kwa ufupi mimi ndiye nimewatuma vijana wangu wakukamate, ili ufike mbele yangu ujibu maswali mawili matatu, halafu tunakuachia, kikubwa hapa ni ushirikiano, tusaidie tukusaidie, bila shaka umenielewa?”, Kanali Emilly alimwambia.
“Ndiyo baba, niko tayari kujibu maswali yako na kutoa ushirikiano unaotakiwa”, alijibu kwa hofu.
“Una muda gani sasa toka umepata ajira serikalini?”, Kanali Emilly alimuuliza.
“Miaka kama ishirini na sita hivi”, alijibu.
“Miaka kama ishirini na sita, unaonyesha kuwa huna hakika”, Kanali Emilly alihoji.
“Ni miaka ishirini na sita, hakika ni ishirini na sita sasa”, alisisitiza.
“Umeoa?”.
“Ndiyo baba, nimeoa”.
“Una watoto?”.
“Yes, nina watoto watatu”.
“Wazazi wako hai?”.
“Hapana, wote ni marehemu”.
“Una nyumba ndogo, namanisha mke mwingine?”.
“Unamfahamu mwana mama mmoja anaitwa Hawa Msimbazi?”, Kanali Emilly alimuuliza Raymond.
“Hapana, simjui”.
“Humjui, na huyu mzungu anayeitwa Carlos?”, swali hili lilimchanganya kidogo, akaweweseka.
“Simjui pia”, alisema huku akitingisha kichwa chake kukataa kwa msisitizo.
“Unamjua”, nilirukia.
“Siwezi kusema kitu ambacho sikijui, haki ya Mungu simjui Hawa wala Carlos”, alisisitiza kwa mara nyingine.
Kanali Emilly alisimama, alitoka mahali alipokuwa ameketi akatembea hadi kwenye mgongo wa Raymond. Mzee huyu alikuwa na huruma kwa kila kiumbe kilichotengenezwa na Mungu, lakini pia alikuwa katili kwa viumbe vilivyokuwa hatari kwa maisha ya viumbe wengine. Alipenda kucheka sana, lakini pia alikuwa mwenye hasira sana.
“Unadhani sisi ni wapumbavu, unadhani hatuna kazi zingine za kufanya mpaka tukulete hapa, nilitegemea utakuwa muungwana, utajibu maswali yangu vizuri kama tulivyoanza, kumbe naongea na mpumbavu. Sikiliza, naomba ujibu swali langu. Unamfahamu Carlos Dimera”, Kanali Emilly alihoji kwa sauti ya kutisha.
Raymond aliinamisha uso wake chini, akabaki kimya. Kanali Emilly aliendelea kusimama nyuma yake, akisubiri jibu.
“Sikiliza, wewe ni raia wa Tanzania, tena mtumishi wa umma, Carlos ni mzungu, ametoka mbali sana, mpaka anafika hapa nchini, taarifa zake zote tunazo, mpaka anawasiliana na wewe kuhusu mzigo uliokwama Adis Ababa, Ethiopia tunajua, nashangaa kwanini unaficha jambo ambalo liko wazi kabisa”, nilimwambia.
“Mr Raymond, unakumbuka kabla hatujapanda gari uliniuliza swali gani, ulisema ni huu mzigo unaoingia leo au mzigo mwingine, sasa unaficha nini inaeleweka hivyo”, Fred alimwambia.
“Raymond, unataka usaidiwe au uishie jela?”, Kanali Emilly alimuuliza.
“Naomba nisaidiwe”, alisema huku machozi mengi yakimtoka.
“Tutakusaidiaje wakati hutaki kufunguka, jaribu kusema ukweli ili tuangalie jinsi ya kukusaidia”, Meja Satara alieleza.
“Kabla sijasema chochote naomba mnihakikishie usalama wangu, huyu Carlos ni mtu hatari sana, anaweza kuniangamiza”, Raymond alieleza.
“Kuhusu hilo ondoa shaka, tutakulinda kwa gharama yoyote”, Fred alimwambia.
“Na vipi kuhusu familia yangu?” alihoji.
“Kuhusu familia yako, wako chini ya uangalizi wa jeshi la polisi kabla hata hatujakukamata, hivi tunavyoongea hapa mkeo na watoto wako mikononi mwa polisi, lakini kwa ajili ya usalama wao tu”, nilimwambia akaonekana kushangaa.
Baada ya maelezo hayo, Raymond alieleza kila kitu kuhusu Carlos, alieleza jinsi alivyotambulishwa kwake na Denis, Afisa Ukaguzi mstaafu, ambaye sasa ni marehemu, alieleza jinsi alivyofahamiana na Hawa Msimbazi na mengine mengi, pia alieleza mbinu wanazotumia kuingiza dawa za kulevya nchini, na mkakati wa kuua yeyote anayeonekana kuingilia biashara yao.
“Asante, kazi yako imekwisha, Meja Satara, hakikisha huyu jamaa anapelekwa mahabusu ya siri mpaka nitakapojulisha vinginevyo”, Kanali Emilly aliagiza.
“Hakuna tatizo mkuu”, Meja Satara alieleza huku akijiandaa kuondoka na Raymond.
“Mlisema mtanisaidia, imekuwaje?”.
“Tulisema tutakusaidia baada ya kazi hii kwisha salama”, nilimwambia. Kiasi fulani nilifurahi kumkamata mtu huyu, maelezo yake yalitufanya tupate mwanga. Niliwapigia simu Claud na Nyawaminza kuwafahamisha kilichotokea wakaeleza furaha yao.
Wakati huo Mama Feka alikuwa kwenye foleni ya kununua tiketi ya kuingia California Dreema. Alivaa vizuri kiasi cha kumfanya mwanaume yeyote kuingiwa na tamaa, baada ya kupata tiketi yake alipenya mlango na kujitosa ndani ya ukumbi huu.
Muziki laini ulikuwa ukipenya masikioni mwa wapenzi wa starehe, kila mmoja alionekana akicheza na mpenzi wake, huku wengine wakiwa wameketi kwenye meza za pembeni wakiupiga mtindi.
Kama ilivyo kawaida yake, Mama Feka alipita akatafuta sehemu nzuri ambayo anaweza kuonekana kwa urahisi, alifanya hivi baada ya kuwa amemuona Carlos Dimera na wapambe wake wakiwa wameizunguka meza iliyojazwa vinywaji vya kila aina.
Ili aweze kuonekana, Mama Feka alianza kulicheza rhumba, alicheza vizuri huku akigeuka kila upande, kijana mmoja aliyekuwa karibu yake alivutiwa na mwana mama huyu, hivyo akajisogeza na kumuomba wacheze. Lakini hilo lingemfanya auhalibu mtego wake, alichofanya Mama Feka ni kumkwepa kijana huyo, akaendelea kucheza peke yake, kijana huyo kwa aibu akajiondoa eneo hilo.
Jakina alifanikiwa kumuona Mama Feka, hakufanya ajizi, haraka alizifikisha habari kwa Carlos, ambaye alikuwa ameketi kwenye meza ya vinywaji na akina dada kadhaa.
“Bosi, unamuona yule mbabe wa Supermarket?”, Jakina alimwambia Carlos Dimera.
“Yuko wapi?” Dimera alihamaki.
“Yule anacheza peke yake pale”.
“Oh, nimemuona, sasa sikiliza, tafuta mbinu ya kuwafanya hawa malaya wengine wasinisogelee, asije akaniona mhuni. Kwa vile wewe na yeye damu zenu zimetofautiana, acha niende mimi mwenyewe, nimuombe tucheze kidogo”, Carlos alimwambia Jakina huku akielekea mahali alipokuwa Mama Feka.
“Helo, habari yako?” Carlos alisalimia baada ya kumshika bega. Haraka Mama Feka aligeuka na macho yao kukutana.
“He, na wewe unakuja huku?” Mama Feka alihoji.
“Mimi ni mtu wa starehe, lazima nifike sehemu kama hizi, nimekuja kukuomba tucheze kidogo”, Carlos aliomba.
“Unataka ucheze na mimi wakati mlitaka kunipiga kule Supermakrt?”.
“Ilikuwa bahati mbaya, waswahili mnasema wanaogombana ndiyo wanaopatana, pole kwa yaliyotokea, msamehe kijana wangu hakuwa na nia mbaya”, Carlos alieleza.
“Sawa, nimekuelewa, karibu tucheze”, Mama Feka alifurahi kupata nafasi hiyo, wakaanza kucheza huku wameshikana.
“Unaitwa nani?” Carlos alihoji.
“Sweety”.
“Oh, jina zuri sana, unafanyakazi gani Sweety?”.
“Niko nyumbani tu, nimemaliza shule, ndiyo natafuta kazi”.
“Umesomea nini?”
“Mambo ya Maabara”, Mama Feka alidanganya.
Oh, very god, umepata kazi, mimi namiliki kiwanda kikubwa cha madawa”.
“Asante, na wewe unaitwa nani?”.
“Carlos, au ukipenda unaweza kuniita Carlos Dimera”.
“Wewe ni Mtaliano?”.
“No, hapana, si kila mzungu Mtaliano. Mimi ni raia wa Colombia”, Carlos alifafanua.
“Unafanya kazi gani?”.
“Yaani mimi nifanye kazi, mimi ni mfanyabiashara, business men”.
“Unafanya biashara gani?”.
“Ohoo, sasa hapa umekuja kustarehe au kunihoji”.
“Hapana, nilitaka tufahamiane tu”.
“Utanifahamu tu, si bado tuko pamoja”.
“Sawa”, wakaendelea kucheza.
Mama Feka akamshukru Mungu kwa kazi aliyoifanya kwa muda mfupi, aliyakumbuka maneno ya Teacher kuwa Carlos ni mtu hatari, lazima awe makini, akaupiga moyo wake konde na kujiweka tayari kwa lolote, akimtanguliza Mungu katika jukumu hilo zito, lililoko mbele yake. Boing 787, mali ya Shirika la Ndege la Uholanzi, iliwasili na kutuwa taratibu kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius K. Nyerere, Jijini Dar es Salaam, majira ya saa nne na dakika arobaini na tano usiku. Baada ya abiria wa Dar es Salaam kutoka ndani ya ndege hii. Kazi ya kutoa mizigo ilichukuwa masaa kadhaa, hatmaye kila abiria alitoka na mzigo wake, baada ya kutimiza masharti.
Mimi na wenzangu, Claud Mwita, Julius Nyawaminza na Fred Libaba, tulikuwa tumewasili uwanjani hapa masaa mawili kabla ya ndege hii kushuka katika ardhi ya Tanzania, wakati huo tukitumia magari manne tofauti. pia tukiwa tumejiwekea usalama wa kutosha. Tulijipanga vizuri kwa lolote. Ili kufanikisha kazi iliyokuwa mbele yetu, Claud na Nyawaminza, walitumia gari ndogo aina ya Toyota IST rangi ya Blue yenye vioo vyeusi ambavyo mtu hawezi kuona ndani.
Nje kabisa ya uwanja, liliegeshwa gari lingine lililochaa aina ya Suzuki Escudo, vijana wawili waliovalia mavazi machakavu, Tumain Changasi na China Kilinda, walionekana wakihaha kurekebisha sehemu ya gari hii, Ukweli ni kwamba vijana hawa walikuwa hapo kwa kazi maalumu,
Claud aliyekuwa akiendesha gari IST, aliliingiza gari upande wa pili kwenye maegesho ya taksi. Kama ilivyo kawaida baadhi ya madereva taksi wanaoegesha magari yao eneo hili walilifuata gari hilo ili kumfahamisha dereva kuwa sehemu hiyo magari ya watu wa kawaida tofauti na taksi hayaruhusiwi.
Vijana wawili wawili ambao ni madereva taksi haraka walilifikia gari hili na kugonga kioo upande wa dereva, Taratibu Claud alishuka kioo hicho na kuacha ufa kidogo ili aweze kuwasikiliza.
“Ondoa gari, eneo hili ni kwa ajili ya taksi tu”, alisema mmoja wa vijana hawa aliyeonekana kuwa na jazba, Clauud alimwangalia kwa sekunde kadhaa halafu akauliza..
“Kwenu, ondoa gari ndiyo salamu?”.
“Salamu ya nini, nimesema ondoa gari lako, hii ni sehemu ya taksi tu, vinginevyo gari lako litafungwa minyororo na faini yake ni elfu hamsini, mimi nakusaidia usipigwe faini wewe unaleta jeuri, ukitaka salamu tii sheria kwanza”, kijana huyo aliongeza kwa jazba.
Ok, kama unaona fahari, enedelea kupaza sauti yako”, alisema huku akipandisha kioo cha mlango cha upande wake na kuwaacha vijana hao wakiendelea kusuburi. Walisimama kwa dakika kadhaa halafu wakaondoka huku wakilalama.
Kabla ya kufika eneo hili, nilikuwa nimewaelekeza wenzangu kila kitu. Fred akiwa peke yake alitumia gari ndogo aina ya Toyota Starlet, rangi nyekundu iliyochoka kidogo, aliliegesha gari hilo karibu na sehemu ya kutokea abiria, bahati nzuri Fred hakupatwa na misukosuko ya kuulizwa maswali kama wenzake.
Mimi nikitumia gari ndogo pia, Toyota Corolla, ambalo pia mtu akiwa ndani huwezi kumuona kutokana na vioo vyake kuwa vyeusi, nililiegesha gari kwenye barabara ndogo inayotoka kituo cha mafuta cha PUMA. Karibu yangu kuliwekwa bango linalokataza magari kuegeshwa mahali hapo, nikalipuuza/
Niliwakumbuka vijana wetu wa bodaboda ambao Peter Twite aliwaweka sehemu mbalimbali kwa kazi maalumu, nikajuwa huu ndiyo muda wao itakapobidi.
Tulikuwa tumejipanga vizuri. Hatukufanya kosa hata kidogo, tukiwasiliana kila baada ya dakika chache, hatmaye, Fred alinidokeza kwa njia ya simu kuwa mambo yamewiva. Nikajuwa kazi imeanza, nilichukua bastola yangu iliyokuwa kwenye droo ya gari nikaiondoa usalama.
Mara nikaliona gari wanalotumia Claud na Nyawaminza linapita taratibu mbele yangu, mapigo ya moyo ya moyo wangu yakanienda kasi. Baada ya muda mfupi, Mitsubishi Pajero lenye rangi nyekundu ambalo dereva wake aliwasha taa, kuashiria hatari lilipita likikifuatwa kwa nyuma na gari kubwa Lori aina ile ile ya Mitsubishi, dereva wa gari hilo alijaribu kuyapita magari yote yaliyokuwa mbele yake, akaliingiza kwenye Barabara kuu ya Julius Nyerere kwa ajili ya kuelekea mjini huku gari lingine likiwafuata kwa nyuma.
“Kumekucha”, nilimwambia Claud kwa njia ya simu ya mkononi, “Endesha kwa mwendo wa kasi kidogo, yapite magari ya adui, angalia msifanye chochote, nitalianzishea mimi”, nilimwambia wakati naingiza gari langu kwenye barabara ya Nyerere. Magari yoteyalipokipita kituo cha mafuta cha OILCom, karibu na stendi ya daladala ya Kipawa, mimi nilikuwa karibu yao zaidi. Haraka niliwasha taa za mbele, nikaanza kulichezesha gari langu, nikimbana dereva wa gari la mbele kumtaka aegeshe gari hilo kando ya barabara, vivyo hivyo, Fred alifanya kwa gari kubwa lililobeba mzigo, magari yote matatu yalichepuka kutoka barabara kubwa na kuegeshwa kando.
Hawa Msimbazi aliyekuwa katika mawani meusi, akionekana kama haelewi chochote, alishusha kioo upande wa pili wa dereva, “Nini unatuvamia kama sisi wahalifu?”, aliuliza,macho yake yalipokutana na yangu akaanza kugwaya.
“Habari ya kwako, samahani kwa usumbufu, bila shaka unajuwa kwa nini tumewasimamisha hapa?”, nilimuuliza.
“Hapana, sijui kwanini tusimamishwe, mzigo wetu ni malighafi za kiwanda kwa ajili ya kutengeneza tembe za kutibu malaria. Tunaziingiza nchini baada ya kufuata taratibu zote za serikali”, Hawa Msimbazi alieleza huku akishuka kutoka ndani ya gari hilo.
“Una hakika?”, nilimuuliza baada ya Fred kusongea karibu. Claud na Nyawamiza wao walibaki ndani ya gari wakiangalia usalama wetu.
“Hakika kabisa, taratibu zote za kuingiza mzigo huu zimefanyika, upekuzi umefanyika, hatujaingiza mzigo tofauti na matakwa ya serikali”, alisisitiza.
“Si kweli, fungua tuhakikishe”, niliagiza.
“Wewe ni mtaalam wa kugundua aina ya poda zinazoingizwa nchini na kupelekwa viwandani?, haifunguliwi mpaka ifike sehemu husika, hii ni malighafi hatari, unaweza kunusa sumu ukafa, tukaulizwa kwanini tuliruhusu”.
“Nimesema fungua tuhakikishe”, nilimwambia kwa sauti ya ukali kidigo, baada ya kujiuliza akarudi ndani ya gari na kujaribu kupiga simu, lakini nilikuwa mwepesi kuchukuwa simu hiyo. Nilitoa kisu changu kidogo kilichokuwa mfukoni nikazikata kamba.
Kulikuwa na shehena kubwa ya dawa za kulevya, aina tofauti tofauti, nilimwangalia mwanamama huyu kwa hasira, wakati huo alikuwa akiniangalia kwa macho ya hasira pia, akitweta nikaliona gari la akina Tumaini linasogea kwa ajili ya kuimalisha ulinzi,
“Unamfahamu, mtu mmoja anaitwa Raymond Kenoko?”, nilimuuliza.
“Raymond Kenoko?, Mmmm, simjui”, alijbu baada ya kutafakari.
“Humjui mtu aliyefanikisha mpango wenu wa kuingiza dawa za kulevya hapa nchini?. Mtu aliyewatengenezea mazingira ya kutoa huu mzigo”.
“Nimesema simjui, hivyo usilazimishe kujibu swali ambalo sijui”.
“Sawa, mtakutana mahakamani, huu ni ushahidi wa kutosha kabisa kuwatia hatiani, haya ni madawa ya kulevya aina ya heroin”, nilimwambia.
“Kama ni madawa ya kulevya mimi siyajui, usinihusishe na mzigo huo, si wangu”. Hawa Msimbazi alieleza msimamo wake.
Tuliwachukuwa watu hawa na kuwahifadhi sehemu ambayo pesa haiwezi kutumika, nilijione mwenye bahati kufanikisha nusu ya zoezi hili, Hawa Msimbazi na wenzake walikuwa kimya wakitafakari kilichotokea. Shehena kubwa ya dawa za kulevya iliyokuwa iingizwe nchini imekamatwa na kufuta ndoto zao za kupata utajiri.
Gari moja ambayo hata sisi hatukuitilia shaka, ilisimama hatua kadhaa, kutoka mahali tulipokuwa, watu wanne walitoka ndani ya gari hiyo na kutuangalia kwa hasira, Fred alipojaribu kuwafuata walirudi ndani ya gari na kuondoka kwa mwendo wa kasi, wakiacha vumbi. Hata hivyo Claud alijaribu kulifuata gari hilo, likapotelea eneo la Vingunguti.
*************************
Carlos Dimera ndiyo kwanza alikuwa amerejea kutoka kwenye starehe, habari za kukamatwa kwa Hawa Msimbazi na vijana wake wengine zilionekana kumshitua sana, Jakina Nombo na wengine walikuwa wameduwaa wasijue cha kufanya.
“Kwanza niwafahamishe, huyu ni mchumba wangu, anaitwa Sweety”, Carlos alisema huku akiwaangalia vijana wake, halafu akamgeukia Sweety, “Mpenzi, hawa ni wafanyakazi wangu, jione uko huru, usihofu kuwa na sisi, kilichotokea tutakirekebisha, ni ajali katika kazi”, alieleza Carlos.
“Asante, nakushukuru sana baby kwa kunitambulisha, habari zenu?”, Mama Feka alisalimia.
“Habari nzuri, mbaya yote ni habari”, Nombo alisema.
“Oke, sasa nataka kujuwa, ilikuwaje mkaleta taarifa za uongo, kuwa Teacher ameuawa, Nombo wewe ndiye ulileta taarifa hiyo, ilikuwaje kuleta taarifa ambazo huna hakika nazo?”, Carlos alihoji kwa sauti ya kutetemesha.
“Bosi Carlos, huu si wakati wa kulaumiana, waswahili walisema maji yakimwagika hayazoleki, cha msingi ni kuangalia nini kifanyike kuwaokowa wenzatu, halafu mambo mengine yatafuata”, Jakina alieleza.
“Ndiyo, lakini ni vyema kujuwa, ukisema tuangalie mbele, bila kukumbuka nyuma, hatuwezi kufanikiwa, taarifa iliyopo ni kwamba Teacher aliuawa wakati wa shambulizi, gari yake iliteketezwa vibaya kwa mjibu wa Nombo. Leo ameharibu mipango yetu, mtu mmoja Teacher ambaye siamini kabisa kama ana mbinu za kutushinda”, Carlos alieleza kwa hasira.
“Hakika ninaposikia habari hii, nashindwa kuamini bosi, tulimfuatilia Teacher kuanzia mwanzo mpaka anaingia Benjamin Mkapa, gari aliyoingia nayo ni ile ile iliyopigwa kombora, mtu mmoja alikufa katika shambulizi hilo, siami”, Simba alibainisha.
“Yule ni mpelelezi wa siku nyingi, huenda aligundua kitu akampa mtu mwingine kuendesha gari hilo, kama yuko hai basi ni mjuzi wa hali ya juu, mbinu za ziada zinahitajika”, Nyati aliongeza.
Mama Feka alikaa kimya akiwasikiliza kwa makini, kiasi fulani aliogopa maneno ya watu hawa, alimuonea huruma Teacher, akajiona mwenye bahati kufanikiwa kuingia ndani ya ngome hiyo, lakini pia akijiuliza, iwapo atabainika itakuwaje.
Waliongea mambo mengi, wakipanga hili na lile, hatimaye wakaweka azimio kuwa mzigo mwingine wa dawa za kulevya ulikuwa stoo uhamishwe haraka iwezekanavyo, kupisha upekuzi wa polisi baada ya hapo utarejeshwa na kuingizwa sokoni.
“Walichofanya ni kupunguza kasi tu, lakini hii itatuongezea kasi zaidi, mtu mjinga, mtu asiyependa kuishi maisha ya kifahari, wenzake wanakula kuku na bata, yeye anakosa usingizi kwa ajili ya kuziba mianya ya wengine”, Carlos alilalama. “Binadamu hatulingani bosi”, Nombo alisema.
“Wakati huu msilale, fanyeni kazi usiku huu mpaka alfajiri tupate taarifa za Hawa na wenzake wamewekwa kituo gani cha polisi, shilingi ngapi inahitajika kumaliza jambo hilo, mzigo uhamishwe, kazi zingine zote zisimame mpaka hapo nitakapowajulisha vinginevyo.
“Ametuchokoza, ajiandae kulia”, Jakina alieleza huku akisimama.
Ni wakati wa kuwashirikisha wageni, wamesafiri kutoka huko kuja hapa nchini kwa kazi moja, kufanikisha jambo hili”, aliagiza Carlos.
Watu wote walikaa kimya ndani ya chumba cha mkutano. Carlos Dimera alionyesha dhahiri hali ya woga na hasira, akivuta sigara kubwa iliyosokotwa kwa karatasi ngumu, alitembea kutoka kona moja ya chumba hiki kwenda kona nyingine huku akitafakari kwa kina kilichokuwa kimetokea. Alijitahidi kuvuta sigara hiyo mpangilio na kupuliza moshi mwingi hewani. Hali iliyowafanya wafuasi wake wapatwe na hofu.
Mama Feka au Sweety, kama alivyojitambulisha kwa Carlos, alikuwa mmoja wa watu waliokuwa ndani ya chumba hiki cha mkutano wa siri, akishiriki kama mjumbe wa kawaida. Lengo la Carlos ilikuwa kumshirikisha mama huyu katika biashara ya dawa za kulevya.
Mzungu huyu aliutambua urembo wa Mama Feka, awali alikuwa ameteta na Jakina, kuwa unapokuwa na msichana mrembo kama huyu kwenye biashara yako asilimia tisini mambo yatakuwa shwari. Hata aliposhiriki kikao hiki wajumbe walilitambua kusudi la Carlos, wakampokea Mama Feka kwa mikono miwili.
Mfano wa mtu aliyeshikwa na kigugumizi, Carlos alivunja ukimya uliokuwepo kwa kusema. …”Imenishangaza mno, watu makini, watu mnaojitambua, kuyachezea maisha yenu mbele ya Simba mwenye njaa, sielewi nini kimewalevya mpaka mnazidiwa maarifa na wajinga?. Haiwezekani, Hawa na Tony wakamatwe kama kuku, halafu, shehena yote ipotee. Lakini cha ajabu na kusikitisha zaidi, wenzetu hawa wamefika mahakamani. Mmmmm, imenifedhehesha sana Nauliza kila baada ya dakika kuhusu hatima ya jambo hili, wakubwa wanataka kujua nini mkakati wetu au tumejipangaje kumaliza tatizo hili, pesa si tatizo, mtu mmoja, mtu mmoja mpuuzi hawezi kufanya tuonekane wapuuzi”, alitembea tena kutoka upande mmoja wa chumba hiki kwenda upande mwingine huku wajumbe wakimwangalia.
“Inachosema ni hakika bosi, lakini usitishwe na ukimya huu, ukadhani labda tumeridhishwa na jambo hili, niseme wazi kuwa adui anaishi kwa mbinu, ambazo hakika siku zake za kuishi sasa zinahesabiwa, hivi tunavyoongea, vijana wetu wako katika msako mkali kujua mjinga huyu yuko wapi. Naamini msako huu utafanikiwa haraka iwezekanavyo, kwani tunatumia vifaa vya kisasa”, Nombo alieleza.
Haraka Jakina akasimama, tofautu na mwenzake aliyeongea ameketi. “Kama ulivyosikia bosi, mahakama ilikuwa itoe hukumu ya kesi hii leo, lakini kutokana na jitihada kubwa zilizofanywa, hukumu imeahilishwa mpaka kesho ili tuweze kujipange. Nakuhakikishia Hawa na Tony kesho wakati kama huu watakuwa huru, mwanasheria wetu pia ni mtu makini sana, cha msingi tuwe wavumilivu, tumalize tatizo hili ndipo tujiulize wapi tulijikwaa”, Jakina alieleza.
“Maneno mazuri sana, lakini hayana ufumbuzi wa jambo hili, kila mmoja anaongea kwa mtazamo, kama tunaweza kuwatoa Hawa na Tony kwenye mikono ya sheria, swali langu ni je, huu mzigo utapatikana au utapotea?. Tunapojadili jambo nyeti kama hili, lazima tuangalie uwezekano huo pia”, alihoji.
“Swali zuri bosi. Mara tu baada ya Hawa na Tony kukamatwa, haraka tuliwasiliana na watu wetu katika vitego mbalimbali vya usalama wanaopokea mshahara kutoka kwetu, kuwajulisha kilichotokea, hakika ushirikiano wao ni mkubwa mno. Kama unavyojua msimamo wa serikali sasa, unapofikishwa mbele ya mahakama na ushahidi, moja kwa moja unakumbwa na kifungo, lakini maofisa hao ndiyo waliofanikisha mahakama kusogeza hukumu ya kesi hii mbele ili tuweze kujipanga”, alisema Nombo.
“Baby naomba uketi”, Mama Feka alimwambia Carlos kwa sauti ya mahaba. Sauti ya Mama Feka, ilimfanya Carlos, atabasamu kidogo.
“Asante Sweety wangu, usijali mpenzi, mambo yanapokwenda ndivyo sivyo, lazima tuketi na kutafakari njia sahihi, usiogope Sweety mpenzi, uwe na amani nitaketi”, Carlos alisema, halafu akaendelea. …”Jamani, tupunguze maneno, tupunguze porojo, jukumu lililo mbele yetu ni zito mno, yatupasa kujipanga vyema, Hawa na Tony ni watu kutoka miongoni mwetu. Nasema kwa gharama yoyote lazima watakuwa huru kutoka katika mikono ya sheria. Nataka kuona jambo hill linafanyika haraka iwezekanavyo, hebu jiulize mfano ungekuwa wewe ingekuwaje?”, Carlos alihoji baada ya kutoa agizo.
Lakini Carlos na kikosi chake walikuwa wamekosea jambo moja. Hawakujua kama, Mama Feka alikuwa hapo kwa kazi maalumu, alitumia simu yake ya kiganjani kwa usiri wa hali ya juu kurekodi mazungumzo hayo na kuyatuma wakati huo huo moja kwa moja kwenye simu ya Teacher. Carlos Dimera na wafuasi wake waliendelea kujadiliana hili na lile, waliongea mambo mengi, wakipanga hili na lile, hatimaye wakafikia mwafaka.
“Nitalala usingizi mnono iwapo nitasikkia Teacher amekufa, sasa naagiza, kwa gharama yoyote ya pesa, atafutwe ikiwezekana auwawe haraka kabla ya hukumu kesho, uwepo wake unaweza kuharibu mipango yetu”, Carlos alisisitiza, huku kila mmoja akipewa jukumu lake.
Hata hivyo, Carlos Dimera aliamua kutumia uzoefu wake wa siku nyingi katika kazi hizi za hatari, aliwatuma kwa siri, vijana wawili Gabriel na George, bila kuwashirikisha wenzake. Hawa walikuwa wakiishi nchini Tanzania kwa siri, wakisubiri matukio kama haya. Vijana hawa wenye uzoefu mkubwa wa mambo ya ujasusi walipewa jukumu la kumtafuta Teacher.
Carlos, aliwaamini sana vijana hawa, waliokuwa wakifanya mazoezi wakati wote, aliujuwa vizuri muziki wao, Ni vijana ambao wakitumwa kukileta kichwa cha mtu yeyote, wanaweza, kutokana na imani yake kwao, aliwaagiza kumleta Teacher mbele yake akiwa hao ili athibitishe kuwa ndiye, halafu amuue yeye mwenyewe. Hili alilifanya kwa siri kubwa, bila hata Sweety kujuwa. Mara nyingi majasusi hutumia mbinu tofauti katika kufanikisha mambo yao, Gabriel na George waliishi nchini kwa siri, hakuna mtu aliyefahamu uwepo wa majasusi hawa. Hata Jakina aliyekuwa karibu zaidi na Carlos hakuwajuwa vijana hawa.
Gabriel na George walikuwa majasusi waliohitimu mafunzo ya juu ya ujasusi katika vyuo mbalimbali duniani, walilingana kwa kimo na umri, walionekana kama mapacha, lakini ukweli ni kwamba kila mmoja alikuwa na sifa zake,
George akiwa amezaliwa katika mji wa Kano, nchini Nigeria, huku Gabriel akiwa raia wa Afrika Kusini. Vijana hawa walikutana katika chuo kimoja nchini Cuba, ambako walishabihiana kwa kila kitu, hata walipohitimu mafunzo yao ya ujausi walipangwa pamoja, baada ya kununuliwa na wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya kwa ajili ya kulinda maslahi yao.
*************************
Wakati huo huo, mkutano mwingine wa siri, ulifanyika katika Hoteli ya King Air katikati ya Jiji la Bogota, nchini Colombia, ambapo Wafanyabiashara wakubwa, matajiri wa dawa za kulevya walikutana kwa siri kama ilivyo kawaida yao.
Watu hawa walikutana kujadili mafanikio ya biashara yao pamoja na shehena yao kubwa ya dawa za kulevya kukamatwa Jijini Dar es Salaam, Tanzania na watu wao kufikishwa mahakamani.
Emilio, mfanyabiashara kigogo, aliyefika Dar es Salaam, kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kuingiza dawa hizo, ambazo awali zilikwamba Ethiopia, alitakiwa kuwaeleza wakubwa hawa kwa nini shehena hiyo ikamatwe baada tu ya kuingia Tanzania.
“Inawezekana hatukuwa makini wakati wa kusafirisha shehena hii? Tanzania kama Tanzania ndiyo njia yetu ya kusafirisha dawa za kulevya kwenda katika nchi nyingine za ukanda wa mashariki. Leo tujiulize, nini kimetokea mpaka shehena hii hii kubwa ikamatwe?”, Mfanyabiashara tajiri, ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa mtandao huu, Enock Jonson, alihoji.
“Ni wakati wa Emilio kutoa maelezo, ndiye mtu wetu pekee aliyesafiri hadi Dar es Salaam, lengo la safari ilikuwa kuweka mambo sawa, sasa kama hali ya usalama nchini humo ilikuwa hairuhusu, ilikuwaje wewe ukaruhusu shehena hiyo kuingizwa bila kuwa na uhakika wa hali ya usalama nchini Tanzania”, Stephan Bad ambaye kiutendaji ndiye msimamizi mkuu wa biashara ya dawa za kulevya alihoji.
Emilio alikohoa kuweka koo lake sawa, alipaswa kueleza ukweli. Tabia ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya kumuua mwenzao haikuwa tatizo. “Naomba kueleza kuwa wakati naingia Dar es Salaam juzi, njia zote zilikuwa vizuri na wazi kabisa, tukumbuke kuwa nilikwenda Dar es Salaam, baada ya shehena hiyo kukwama, Adis Ababa, Ethiopia, Carlos alikuwa amenieleza kuwa hali haikuwa nzuri wakati huo, lakini baada ya kuweka mambo sawa, hali ikawa shwari, sasa si wakati wa kulaumiana, vijana wanajaribu kila njia kuweka mambo sawa. Tusubiri”.
“Wakati mwingine tuwe makini na jambo hili, tusikurupuke kutoa maamuzi”, Stephan Bad alieleza. “Hakika, lakini nimesikia kuwa nchini Tanzania sasa njia nyingi zimefungwa, serikali ya nchi hiyo imekuwa macho zaidi, lakini watu wetu Dar es Salaam wamefikishwa mahakamani leo, Carlos amenihakikishia kuwa watatoka kesho,
Hakimu wa kesi hiyo ni mtu wa upande wetu, inasemekana alishinikizwa atoe huku leo, lakini pesa imefanya kazi yake, ametumia vifungu vya sheria kuweka mambo sawa, jambo hili litakwisha kesho”, Emilio alidokeza.
“Punda afe mzigo ufike, nchini Tanzania hatuna mkataba na mtu zaidi ya Carlos Dimera, hao wengine ni vibaraka tu, lazima mtambue kuwa tuna nguvu kubwa Dar es Salaam, hao waliokamatwa tuwaache wafungwe, ili iwe rahisi kuupata huo mzigo, nakuhakikishia wakifungwa hawa itakuwa na nafasi nzuri kwetu kuupata mzigo huo”, Stephan Bad alieleza msimamo wake.
“Itakuwa ngumu zaidi, Carlos amenihakikishia uwezekano wa kuwatoa upo, hakuna sababu ya kuwatosa”, Emilio alishauri.
“Hapana, wakati mwingine tumia akili yako ya ziada, fahamu kuwa watu hawa wakifungwa, serikali itatangaza kuteketeza shehena ya dawa hizo, lakini kabla hazijateketezwa zinarejeshwa kwetu, wahusika wanateketeza maboksi na makuti ya mnazi chini ya ulinzi mkali, hatimaye mzigo unaingia sokoni, ndivyo tunavyofanya”, Stephen Bad alieleza.
“Ushauri mzuri, Carlos aelezwe kuhusu jambo hili, japokuwa siamini kama anaweza kukubaliana nasi”, Emilio alidokeza.
“Hili ni agizo, asikubali yeye nani? Nakuhakikishia Emilio, kama tuna nia njema ya kuupata mzigo huo, hatuna budi kuwatosa Hawa na Tony, waliokamatwa, lakini ukijaribu mbinu nyingine tumeumia”, Stephan Bad alisisitiza.
“Hofu yangu ni kwamba tunaweza kukosa mama na mwana”, Emilio alidokeza.
“No. Usihofu kabisa, nakuhakikishia hii ndiyo njia salama ya kupata mzigo huo, unakumbuka kilichotokea Msumbuji na Congo? sasa una shaka gani?”, Enock Jonson alihoji.
Baada ya majadiliano ya muda mrefu, hatimaye kikao kiliafiki kuwa, Hawa na Tony watoshwe. Carlos Dimera alipewa taarifa ya siri kuhusu mwafaka huo, akautafakari msimamo huo. Lakini hakuwa tayari kuutekeleza
Hali ya utulivu katika Jiji la Dar es Salaam, kiasi fulani ilikuwa imetoweka, Gabriel na George waliokuwa wamehitimu vizuri mafunzo ya ujasusi, katika nchi mbalimbali duniani, waliingia katika mitaa ya Jiji la Dar es Salaam kwa kazi moja tu, kumsaka Teacher. Majasusi hawa wakiendesha magari mawili tofauti, mmoja akiendesha Toyota Brevis yenye rangi ya Blue, mwingine alikuwa ndani ya Toyota Verosa yenye rangi ya Zambarau. Carlos Dimera aliuamini sana utendaji kazi wa vijana hawa, akasubiri kuona nini matokeo. Mfano wa panya wa Suwa, wenye uwezo mkubwa wa kunusa na kutegua mabomu ardhini, majasusi hawa Gabriel na George, walianza kunusa harufu. Wakitumia mtambo maalumu wa kunasa mawasiliano, hatmaye walifanikiwa kuingilia mawasiliano ya Teacher, mara tu baada ya kuipata namba yake ya kiganjani. Mtambo huo maalumu uliweza kuonyesha mnara unaotumika kwa mawasiliano ya Teacher, baada ya kufanikiwa kuupata mnara huo, kazi ya majasusi hawa, ilikuwa kufuatilia uelekeo wa mahali mnara huo ulipo.
Carlos Dimera, alikuwa amewaeleza majasusi hawa kila kitu kuhusu Teacher, aliwaeleza jinsi Teacher alivyo mwepesi na mjanja wa kubaini mambo. Dimera alimwelezea Teacher kuwa ni mtu mwenye hisia kali katika tasnia hiyo. Hivyo aliwayaka walijiweka vizuri mara mia zaidi kwa ajili ya mapambano. iwapo hali hiyo itatokea.
Hatmaye mtambo ukawafikisha Kinyerezi, kila wanapotafuta uelekeo, mtambo nao unaonyesha mshale wa mawasiliano ya simu husika. kila waliposogea mlio fulani ulisikika ndani ya mtambo huo, kuashiria uelekeo ulikuwa sahihi. Hatmaye wakaifikia Hotel Bella, iliyoko Kinyerezi, nje kabisa ya Jiji la Dar es Salaam, eneo ambalo dakika chache zilizopita Teacher alikuwa amewasiliana na watu kadhaa. Majasusi hawa waliamini kuwa Teacher atakuwa amekia hotelini hapo kwa vile katika eneo hilo, hakukuwa na Hotel nyingine. wakajiweka sawa, wakapanga kuivamia.
Ukweli ni kwamba, baada ya Teacher kufanikiwa kuwaburuta mahakamani, Hawa na Tony, alikubaliana na wenzake Fred, Claud na Nyawaminza, kila mmoja apumzishe akili sehemu aliyoona inamfaa, wakisubiri mahakama kutoa hukumu dhidi ya watuhumiwa wa dawa za kulevya, Hawa na Tony. Akatafuta sehemu nzuri ya kupumzisha akili, sehemu ambayo si rahisi adui kuifikia, akajihifadhi Hotel Bella, kwa ajili ya usiku mmoja wa leo, akiisubiri kesho.
Kwa vile Hoteli Bella iko karibu na mitambo ya umeme wa ges ya SONGAS, baada ya majasusi hawa kufanya utafiti kuhusu eneo hilo, waliingia Hotelini hapo mmoja baada ya mwingine, wakikodi vyumba vya kulala, huku wakijisajili katika kitabu cha wageni kwa majina tofauti. George akijiita Mhandisi Hezdori Stephan, kutoka Zimbabwe nae Gabriel, alijiita Mhandisi David John kutoka Comoro.
Wakati Gabriel anajisajili, alitumia nafasi hiyo kukagua majina ya wageni mmoja baada ya mwingine, kilichomshangaza hakukuwa na jina linaloelekea kuwa la Teacher. Hata hivyo, aliamini kuwa Teacher ni mjuzi katika tasnia hiyo, akaziamini hisia zake.
Kutokana na uzoefu katika mambo ya uchunguzi, Teacher hakupenda kusajili jina lake kwenye kitabu cha wageni, badala yake akajisajili kwa majina ya Mrs Martina Fundi, mhasibu kutoka mkoani Mtwara. Lakini kabla ya kuandika katika kitabu cha wageni alimjulisha mhusika wa Hoteli hiyo kuwa atakuja mgeni mwenye majina hayo, akalipa pesa za chumba halafu akaendelea na mipango yake mingine.
Kulikuwa na idadi kubwa ya wageni katika Hotel hii, wengi walikuwa wahandisi kutoka sehemu mbalimbali ya Tanzania, ambao walifika Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya uzinduzi wa bomba la ges lililojengwa na Serikali kutoka Mtwara hadi Kinyerezi, Dar es Salaam.
Majasusi hawa, George na Gabriel walikuwa tayari wameipata taarifa hii ya uzinduzi wa bomba la ges kutoka Mtwara, wakajiita wahandisi.
********************************
Ilikaribia kuwa saa mbili kamili za usiku, niliingia bafuni, nikaoga haraka haraka, baada ya kuvaa suluali na fulana iliyokuwa kwenye mkoba wangu, nilitoka na kuelekea sehemu ya bar kwa ajili ya kusikiliza taarifa ya habari ya usiku pamoja na kupata bia mbili za kutafutia usingizi. Si kwamba chumbani kwangu hakukuwa na televishen, la hasha, nilikwenda sehemu ya bar kwa ajili ya kunywa kidogo.
Muziki wa taratibu ulisikika, sauti za magwiji wa muziki nchini, akina Tx Moshi Wiliam, Joseph Maina, Kamanda Mzee Muhidini Gulumo wa OTTU Jazz zilisikia, kiasi fulani nilitokea kuipenda bendi hii, ninapozisikia sauti za watu hawa, huwa nafarijika na kusahau machungu.
Watu wachache walikuwa wameketi kwenye meza wakipata moja moto, moja baridi, baadhi walikuwa wakijadili kuhusu hali ya maisha ya sasa, mimi nilipita karibu yao, nikatafuta meza ya pembeni nikaketi. Mimi hupenda kukaa meza za pembeni, kwa sababu ambazo nitakudokeza ukinitafuta, ukinielewa sawa, usiponielewa shauri yako.
“Karibu kaka, nikusaidie kinywaji gani?” mhudumu wa hoteli hii aliniuliza baada tu ya kuketi.
“Hapana, hapana kaka, tunauza, labda nimekosea kiswahili, maana yangu unaagiza kinywaji gani, ulipe pesa nikuletee?” msichana huyu alijitetea.
“Nitapata Wisky aina ya Tekla, zinazotengenezwa kwa mkonge?”.
“Bila shaka zipo, ila bei yake imechangamka kidogo”, alibainisha.
“Bei siyo tatizo, hebu niletee hilo Tekla chupa ndogo, usisahau maji ya kunywa, weka barafu nyingi kwenye glasi”, niliagiza.
“Usijali kaka”, akaondoka.
Watu waliokuwa ndani ya bar hii walikaa kimya wakifuatilia taarifa ya habari ya saa mbili. Habari kubwa ni utumbuaji majipu unaofanywa na Serikali. Watu walianza kuchoshwa na habari hii ambayo imekuwa ya kawaida kwenye vyombo vya habari.
Wakati najaribu kutafakari hili na hili na kazi zangu za kesho, mara kijana mmoja alisimama mbele ya meza yangu.
“Habari kaka?” alisema kijana huyu huku akivuta kiti kwa ajili ya kuketi.
“Salama”, nilimjibu kwa mkato, vinywaji vyangu vililetwa, nikaanza kunywa huku nikimtafakari mtu huyu kimya kimya, sikuwa na sababu za kumzuia kuketi, baada ya kushikana nae mikono, akaketi.
“Samahani, naitwa Mhandisi David John kutoka Comoro, nimekuja kama kwa ajili ya kushuhudia uzinduzi wa bomba la gesi, ama kweli huu ni uwekezaji mkubwa katika eneo hili”, alieleza kijana huyu. “Inawezekana”, nilisema kwa mkato
Nilijaribu kumtafakari tena kijana huyu, lakini sikuwa na jawabu la haraka, kutokana na uzoefu wa kazi hii kwa muda niliamini kijana huyu hakuwa mtu wa kawaida, mkono wake pekee ulinidhihirishia hivyo. Nilikunywa taratibu huku nikiwa katika hali ya hofu.
“Samahani kaka, kuna umbali gani kutoka Dar es Salaam hadi Mtwara?”, alihoji kijana huyu.
“Sina hakika”, nilimjibu kwa mkato.
“Inaweza kuwa kilomita mia sita hivi, au zaidi?” aliuliza kwa mara nyingine.
“Nimesema sijui”, niliongea kwa sauti ya kutisha kidogo ili asiendelee kuuliza.
“Nasikia Tanzania kuna bomba la mafuta lililounganishwa na Zambia, hivi ni kweli?” aliendelea kuuliza.
Niliinua glasi, nikanywa wisky yote iliyokuwa ndani ya glasi, “Mimi si Mhandisi. Lakini Wewe umejinadi kuwa ni Mhandisi, kwanini usijue kuhusu hilo bomba la mafuta kutoka Tanzania kwenda Zambia?” akacheka.
Mara nikasikia miguu yangu inaguswa na kitu, nilishituka, lakini nilikuwa nimechelewa. Nilipigwa shoti na kitu ambacho sikukijuwa, miguu na mikono yangu iliishiwa nguvu taratibu nikapoteza fahamu.
Nilizinduka na kujikuta ndani ya chumba kidogo chenye joto kali na giza nene, mikono na miguu yangu ilikuwa imefungwa madhubuti kwa kamba ngumu. Upande wa mikono yangu ulifungiwa kwenye nondo za dirisha, huku miguu ikifungwa upande mwingine kwa lengo la kunizuia kabisa nisiweze kugeuka. Hakika nilikuwa kwenye kitanzi cha mauti.
Kichwa changu kilikuwa katika maumivu makali, nadhani yalisababishwa na aina ya vifaa walivyotumia adui zangu wakati wakiniteka nyara. Nilijaribu kuinua kichwa juu kuangalia jinsi nilivyofungwa sikuweza, nikapoteza matumaini ya kuishi tena katika dunia hii.
Akili yangu ilifanya kazi haraka, nilijiuliza jinsi nilivyofika ndani ya chumba hiki. Baada ya kutafakari kwa kina, nikakumbuka kuwa wakati napata kinywaji pale Bella Hotel, eneo la Kinyerezi, alikuja mtu mmoja akaketi karibu yangu, nakumbuka wakati tunaongea na mtu huyu niliguswa na kitu katika miguuni yangu, nikapoteza fahamu. “Nani hasa wamenileta katia chumba hiki. Kwanini hawakuniua kama kusudi lao lilikuwa hivyo”, nilijiuliza.
Kutokana na giza nene lilolokifunika chumba hiki, sikujua eneo nililokuwa, hata kama kungekuwa na mwanga bado ilikuwa vigumu kujuwa. Milijilaumu kuwaacha wenzangu, Julius Nyawaminza, Claud Mwita na Fred Libaba, nilijiuliza jinsi watakavyopata shida kunitafuta bila mafanikio. Lakini pia niliona vizuri wao kuendelea pale nilipofikia. Nilijiuliza hili na lile, nikakosa majibu ya haraka, nikaishia kukubali matokeo.
Niliwakumbuka watoto wangu wapendwa, Warioba, Changasi na Masey, ambao walikuwa bado wadogo sana wakihitaji msaada wangu, niliwahurumia jinsi watakavyolia baada ya kusikia kifo changu. nijaribu kukumbuka tena niko wapi nikakosa jibu la haraka. Nilimkumbuka mama yangu mzazi, Nyamadoho, nilijiuliza jinsi atakavyolia baada ya kupata taarifa za kuuawa kwangu.
Joto kali ndani ya chumba hiki, lilizifanya nguo zangu za mwilini kulowa maji ya jasho, nilijaribu kwa mara nyingine kupima kiwango cha kamba nilizofungwa upande wa mikono na miguu, zilifungwa kwa uhakika.
Nilisikia watu wakitembea nje ya chumba hiki, halafu mlango ukafunguliwa, mimi nikafumba macho na kurejea katika hali yangu ya awali, ya mtu aliyezimia. Watu wawili waliingia ndani, mmoja aliwasha taa, mwingine akasogeza sikio karibu yangu.
“Bado hajaamka huyu. Nadhani, bado masaa machache atakuwa amezinduka, daktari alisema pigo alilopata litamchukua masaa matatu hadi manne, kwa vile mtu mwenyewe anafanya sana mazoezi”, mmoja wa watu hawa alieleza.
“Mimi sikuona sababu ya kumuacha hai mpaka sasa, watu wa aina hii ni hatari sana, kwa vile bosi ametaka kumuua kwa mikono yake, basi tusubiri azinduke”, alisema mtu wa pili.
“Namsikilitikia sana, maana atakufa kifo kibaya mno, Carlos alivyo na hasira na mtu huyu, anaweza hata kumla nyama”, alisema mmoja wa watu hawa, huku mapigo ya moyo wangu yakinienda kasi.
Halafu wakaingia watu wengine zaidi ya sita, akiwemo mzungu Carlos Dimera. Mmoja wa watu hawa alikuja moja kwa moja karibu yangu na kunimwagia maji mengi kichwani, mengine yaliingia katika masikio, nikajidai kushituka na kujaribu kuvuta kamba ili nisimame.
“Tulia wewe masikini mjinga, umerukaruka hatimaye umeingia kwenye anga zangu. Teacher… ulifanikiwa kututia hasara, umevuruga mipango yetu, lakini waswahili walisema siku za mwizi ni arobaini, leo arobaini yako imetimia. Niliahidi kuwa siku moja nitakuchinja kwa mikono yangu, siku hiyo imefika”, Carlos alisema huku akicheka.
“Ni kweli… kama ulivyosema, siku za mwizi ni arobaini, lakini mimi si mwizi, hata wewe arobaini yako itafika, heri yangu mimi ambaye arobaini imenikuta nikitetea watuwanyonge, jiulize arobaini yako itakuwaje?” nilimwambia
“Kwa taarifa yako nguvu yetu ni kubwa, mtu mwenye pesa hafungwi kaka, ndiyo maana nikasema leo ndiyo mwisho wa maisha yako, wenzako wengi walijaribu wakashindwa, nilijiuliza wewe utaweza? Sasa utauawa baada ya mahakama kutoa hukumu ambayo itawashangaza wengi, Hawa na Tony hawana hatia, pamoja na hilo, madawa uliyokama uwanja wa ndege yatarejeshwa mikononi mwetu…, oh pole sana Teacher kwa kupoteza muda wako”, Carlos alieleza kwa kebehi.
“Sidhani kama hakimu atakuwa mpuuzi kiasi hicho, mpaka akubali kuharibu kazi yake, hata kama nitakufa leo, sijui kifo gani? Lakini siogopi, maana kifo ni kifo tu, hata wewe siku yako itafika, sijui utajibu nini mbele za mungu”, nilimwambia, akasogea karibu yangu na kunipiga kibao kwa hasira.
“Sina muda wa kubisha na mtu mjinga, wengine tunatafuta maisha mazuri, wewe unatafuta kifo, jiandae kufa, kibaya zaidi ni kwamba hata ndugu zako hawataiona maiti yako”, alitamba.
“Hewezi kujisifu kwa kumpiga maiti, ungekuwa mwanaume ungenitafuta wewe ili nikuonyeshe kazi, bila shaka habari yangu umewahi kuisikia ndiyo maana ukakodi majasusi kutoka nje ambao siku chache zijazo watakuwa mikononi mwa serikali, kuniua mimi usidhani utakuwa umemaliza tatizo, serikali ipo tu”, nilisisitiza.
“Hilo unasema wewe, wenzako katika serikali wanapenda kuishi katika maisha mazuri ndiyo maana nikasema hukumu itakayotolewa leo kuhusu Hawa na Tony, itakushangaza hata wewe na wengine wasiojitambua”.
“Mimi najitambua, ndiyo maana nikasema haiwezekani, labda kwa mtu mjinga kama wewe ndiye utaamini hivyo”, nilisema kwa hasira huku nikisikia maumivu makali katika mwili wangu.
“Simba na Nyati, mchapeni huyu mpuuzi”, Carlos aliagiza, wakaanza kunitandika ngumi za tumboni, walinipiga jinsi walivyoweza, nilisikia maumivu makali, lakini kwa vile nilijua hii ndiyo siku yangu ya mwisho, sikujali.
“Nyie vibaraka, mnaotumwa kuwahujumu wenzenu, shauri yenu, siku yenu itafika, mtalia na kusaga meno”, nilisema huku nikipiga kelele.
Baada ya kunipiga sana, mmoja alizima taa, wakatoka ndani ya chumba hiki wakafunga mlango na kuniacha nikiwa nimefungwa madhubuti ndani ya chumba hiki, niliomba mizimu ya kwetu inisaidie, nilimuomba marehemu bibi yangu Matobela, aliyenilea toka nikiwa mchanga. Nilikumbuka jinsi bibi alivyonitokea siku niliyopata ajali katika maeneo ya Gairo, nikitoka Dodoma kurejea Dar es Salaam usiku, bibi akiwa ndani ya mavazi meupe na alinisimamia nikafika salama. Hivyo nilimtegemea leo pia.
Maumivu makali katika mwili wangu nusura nipoteze tena fahamu. Nilimkumbuka Kanali Benny Emilly, Mkuu wa kitengo cha upelelezi, nilijiuliza jinsi atakavyohaha kunitafuta, jinsi atakavyoumizwa na taarifa za kuuawa kwangu, nilijilaumu kwa makosa ya uzembe niliyofanya hata nikakamatwa kama kuku.
Wakati nikiendelea kutafakari, mara nikahisi nyayo za mtu zikiukaribia mlango, sekunde chache baadae taratibu mlango wa chumba hiki ulifunguliwa, mtu mmoja aliingia kwa mwendo wa kunyata. Kutokana na hali ya giza ndani ya chumba hiki, niliangalia kwa makini, alipowasha taa mimi nikafumba macho.
“Teacher, Teacher, Teacher amka”, sauti nyepesi ya Mama Feka ilisikika katika masikio yangu.
“Naam”, niliitika.
“Nilidhani umezimia tena?”, alihoji huku akitoa kisu kidogo kwenye matiti yake na kuzikata kamba zilizofungwa kwenye mwili wangu. “Naomba unisikilize, kuna ulinzi mkali sana huku nje, ukitoka muda huu hutaweza, cha msingi endelea kuwa humu ndani, Carlos anasuburi mahakama imalize kutoa hukumu halafu aje kukuchinja, usihofu, wewe jiweke sawa ili wakija uwe vizuri”, alieleza Mama Feka.
“Lo, Mama Feka, ni wewe kweli Molamu au malaika kashuka kutoka mbinguni, hakika umekuja kuniokoa wakati ambao sikutegemea kabisa, amini siwezi kufa tena, nitajitetea kwa nguvu zangu zote, jinsi ulivyoingia nilidhani Ninja”, nilitania.
“Kama ulivyonielekeza”.
“Tuko wapi hapa?, nilimuuliza.
“Utapajua baadaye, si wajuwa Dar es Salaam mimi mgeni”, akazima taa.
“Umejuwaje niko ndani ya chumba hiki?”.
“Tutaongea baadae Teacher, wako kwenye kikao cha mwisho, wanasubiri taarifa ili Carlos aongee na wewe tena, halafu akuchinje, ndiyo nikatoka kama nakwenda kujisaidia, muda huu si wa kuongea, nikichelewa watanitafakari”, alieleza Mama Feka na kutoweka.
“Kila la heri”, nilimwambia huku nikisimama kuweka viungo vyangu vya mwili vizuri, nilitumia nafasi hiyo kufanya mazoezi ya viungo, niliruka na kupiga push up kadhaa, baada ya kuuandaa mwili wangu kwa kazi, niliuvuta mlango taratibu ili nitoke, kumbe Mama Feka alipotoka aliufunga kwa nje. Ikanibidi kusubiri kitakachotokea. Vifaa vyangu kadhaa vya kazi, ambavyo mimi huvificha sehemu mbalimbali ya mavazi yangu, vilikuwa vimechukuliwa isipokuwa kamba ndogo sana, ambayo niliifungia kiunoni kwangu, kwa muda mfupi nikabaini kuwa watu walioniteka walikuwa wajuzi wa hali ya juu katika tasnia hii. Lakini niliamini kuwa nilikuwa mjuzi zaidi yao. Nilijiuliza kama walikuwa wajuzi wa mambo kwanini wasije wao binafsi kama wao, waliujuwa muziki wangu ndiyo maana walijiandaa, wangekiona cha moto.
Mara nikazisikia nyayo za watu zikiusogelea mlango, haraka nilitumia nafasi hiyo kutoa balbu juu, nikasimama karibu na sehemu ya kuwashia taa. Mlango ulifunguliwa, mtu wa kwanza aliingia akaelekea sehemu ya kuawashia taa, alipobonyeza kitufe ili taa iwake, giza liliendelea kutawala.
“Balbu imeungua”, alisema.
“Haiwezekani, imeungua saa ngapi? Labda kuna sababu”, alihoji mwingine wakati nae akiingia ndani.
Kutokana na hasira niliyokuwa nayo, niliruka na kumpiga mmoja karate ya shingo, nikamsindikiza za teke la kifua akaenda chini, wakati mwenzake akijiuliza nini kimetokea, nilimdaka na kumgeuza mbele nyuma, huku nimembana vizuri kwenye koromero, akashindwa kutoa sauti. Niliwaua haraka sana, halafu nikawaburuza kuwatoa pale mlangoni.
Walikuwa wamevaa mavazi yaliyofanana, suluali nyeusi, makoti ya rangi ya blue na kofia nyekundu, nilichukua mavazi ya mmoja wao aliyekuwa na umbo kama langu nikavaa, niliwapekuwa, kila mmoja alikuwa na silaha kubwa aina ya AK 47, niliitwaa silaha moja na nyingine nikachomoa magazini, nikiwa na matumaini tele. Mimi nikiwa na aina hii ya silaha hata uniletee Kombania nzima ya jeshi, hawaniwezi.
Nilitoa magazini, nikahakiki idadi ya risasi zilizokuwa ndani, kila magazini moja, zote zilikuwa na ujazo sawa, yaani risasi. Bahati nzuri ni kwamba bunduki hii ilikuwa zimekatwa kwenye mtutu wa mbele ili risasi zinapotoka zisitoe sauti.
“Jamal, Jamal…, fanyeni haraka”, sauti kutoka nje ilisikika.
“Njoo uone”, nilisema kwa sauti ya kubana. Akasukuma mlango na kujitosa ndani, alivaa kama wenzake, huyu alikuwa na bunduki aina ya SMG ikiwa begani.
“Unasemaje?” nilimuuliza kwa sauti ya kutisha, aliposikia sauti yangu, akaamini kuwa mimi siyo Jamal, akakurupuka ili atoe bunduki begani, lakini alikuwa amechelewa, nilimpiga risasi ya kifua, akaanguka chini. Nilimvua bunduki yake nikatoa magazini, sasa nilikuwa na risasi za kutosha, kukabiliana na adui wa aina yoyote. Nikajidhatiti na kutoka ndani ya chumba hiki.
Nilijiuliza wapi watu hawa wamepata aina hii ya silaha za kivita, silaha ambazo haziruhusiwi kwa watu binafsi, nilitafuta sehemu nzuri, nikajibanza kisubiri kitakachotokea. Sikuwa na saa lakini ilikaribia kuwa saa nane, tisa au kumi za alfajiri, kutokana na utabiri wangu.
Ukuta mkubwa uliopambwa kwa nyaya za umeme juu uliizunguka ngome hii, nilisikia kelele za mashine zikifanya kazi huku na huko, ilionekana sehemu hii ilikuwa ya viwanda, nilitoa kamba yangu niliyojifungia kiunoni nikaikata kidogo, nilitumia kipande hicho kufunga magazini mbili za risasi pamoja, moja ikiangalia chini na nyingine juu, nilifanya hivyo ili magazini moja itakapoishiwa risasi iwe rahisi kwangu kuchomoa na kupachika nyingine haraka.
Pamoja na kuvaa mavazi kama wao, lakini nilitembea kwa kunyata, maana sikujua wanazotumia mawasiliano gani kwenye ngome hii, taratibu nilitafuta mlango mkubwa wa kutokea, nilipouona, nikafanya kazi nyingine ndogo, kutafuta sehemu waya za umeme zinazolinda ukuta huu zilikotokea, hii pia nilifanikiwa.
Kwenye langu kuu kulikuwa na askari wasiopungua sita, wote wakiwa na silaha aina ile ile AK 47, hawa walikuwa wakitembea huku na huku kuangalia usalama wa eneo hilo.
Mara nikawaona watu wawili wakitoka kuelekea kwenye mahabusu yangu, chumba ambacho nilikuwa nimefungiwa, walivaa sawa na mimi, koti la blue, suluali na kofia nyekundu. Niliwafuata taratibu, nilipowakaribia, niliachia risasi kadhaa zikawapata, mmoja alikufa pale pale, mwingine akapiga kelele za kuomba msaada kutokana na maumivu aliyopata. Kumbe nilikuwa nimechokoza mzinga wa nyuki.
Risasi zilipigwa mfululizo pale nilipokuwa, bahati nzuri nilikuwa nimelala kifudifudi, nilisubiri wasogee, halafu nikaachia tena risasi kadhaa zikawapata. Kumbe walikuwa wengi, wengine wakitoka ndani, hivyo ilinipasa kutumia hesabu zaidi.
Nilipanda juu ya ukuta uliokuwa mbele yangu, niliweza kuwaona vizuri, niliachia tena risasi nikaua kadhaa, nikaruka na kukimbilia upande mwingine, nikiacha eneo hilo likichakazwa kwa risasi. Nilikuwa nimejibanza eneo lingine, walipoona kimya wakasogea, nikatumia nafasi hiyo kuwafyatulia risasi, nikaua askari wao kadhaa na kuhama haraka sehemu niliyokuwa. Wakaichakaza tena sehemu hiyo kwa risasi.
Kelele za askari zilisikika kutoka kila pembe ya ngome hii, wakisema, “piga risasi huyo, ua kabisa”, lakini mimi nilikuwa na kusudi moja tu, kumsaka Dimera, aliyenipiga kibao wakati nimefungwa kamba. Mara nikamuona Dimera, Mama Feka na vijana wawili wakiingia ndani ya gari, lango kubwa likafunguliwa na gari hilo kutokomea nje.
Ilikuwa nafasi nzuri kwangu kumshambulia Dimera, hata kumuua kwa risasi, lakini niliogopa kitu kimoja, ningeweza kuhatarisha maisha ya Mama Feka. Wakafanikiwa kutoweka huku nikirusha risasi bila mpangilio, askari waliokuwa mlangoni walikimbia nami nikapata upenyo na kutoka.
Nilipotoka nje, sikuyaamini macho yangu, kumbe mahabusu yangu ilikuwa ndani ya kiwanda cha Blanket, kilichoko Keko. Nilijiuliza imekuwaje watu hawa watumia sehemu hii, kutokana na muda, niliahidi kulifuatilia baadaye. Nikaondoka
Baada ya mimi kuachana na wenzangu usiku ule, kila mmoja alitafuta uelekeo wake, Luteni Claud Mwita alipanga Elegant Lodge iliyoko kando ya barabara kuu inayotoka Majumba Sita kwenda Segerea. Julius Nyawaminza hakuona sababu ya kwenda mbali, akajihifadhi FQ Hoteli iliyoko hatua chache kutoka Elegant, katika barabara hiyo hiyo ya Segerea. Fred Libaba yeye aliingia Kilimani Lodge akaweka makazi yake ya muda,
Baada ya kufanikiwa kuwatoroka watu hawa, nilitembea kwa tahadhali kubwa, giza lilikuwa bado limetanda kwa nje. Kutoka kiwanda cha Blanket Keko, niliambaa na barabara ya Chang’ombe hadi, hapo nilikodi Bodaboda iliyonipeleka Segerea. Ilikuwa saa kumi na moja kasoro dakika kidogo za alfajiri, nilipobisha hodi kwenye mlango wa chumba cha Luteni Claud Mwita, Elegant Lodge kama tulivyokuwa tumeelekezana awali. Niligonga haraka haraka kwenye mbao za mlango huu mara tatu, halafu nikasubiri kidogo. Giza lilikuwa bado limetanda kwa nje, taa zenye mwanga hafifu zilileta nuru sehemu ya kupita kuingia ndani ya jumba hii la kisasa. Baada ya kugonga nilisubiri kwa muda, Wakati najiandaa kugonga tena, ghafla nilisikia shingo yangu ikiwa baridi, chuma kizito kilinigusa vizuri shingoni, nikatulia na kujiandaa kugeuka kwa mzaha.
Kwanza nilidhani ni utani wa Claud. Wakati najaribu kugeuka nyuma yangu ili nifanye mzaha, sauti nzito ilisikika. Haikuwa sauti ya Claud kama nilivyoizoea. “Tulia kaka, inua mikono yako juu, halafu ugeuke taratibu upande wangu. Onyo, usithubutu wala kujaribu kufanya ujanja wa aina yoyote, maana jaribio lako lolote litakusababishia hasara”.
Utabiri wangu haukuwa umebashiri vizuri kama nilivyoanza nikidhani ni Claud, matumaini yangu ya kutoka salama kwenye mahabusu ya awali yalitoweka. Jasho jembamba lilinitililika. Nilitii amri hiyo na kuweka mikono yangu juu kama nilivyoagizwa kufanya, niligeuka nyuma, macho yangu yalikutana na macho makali yanayong’ara mfano wa jini. Mtu mrefu mnene aliyeshiba vizuri, Bastola yake ikiwa mikononi mbele yangu, alikotoke sikujua.
“Pole sana Teacher, labda nisema leo una bahati mbaya mno, siku ya kufa kwako imefika, hata utende miujiza ya aina gani leo ni siku ya hukumu yako, ni kweli umefanikiwa kutoroka mikononi mwa Carlos Dimera, lakini umeishia mikononi mwangu, Naitwa Ninja Mweusi asiyeshindwa”, alisema mtu huyu aliyefunika uso wake kwa kofia nyeusi na kuruhusu macho yake tu kuona.
Nilimwangalia mtu huyu kwa tahadhari kubwa. Akili yangu ilianza kufanya kazi haraka, nilijiuliza ilikuwaje mtu huyu afike eneo hili la siri, ambalo hata Kanali Emilly hakuweza kulijua. Baada ya kujiuliza na kutafakari, nikabaini kuwa inawezekana mtindo waliotumia kuniteka usiku kule Hotel Bella Vista waliutumia kuwatafuta wenzangu.
“Nimekukosea nini mpaka unitangazie kifo, kwani wewe ni Mungu?” nilimuuliza.
“Usiniulize maswali magumu ya kipuuzi, kwa taarifa yako sikuja hapa kujibu mwaswali, wewe na mpuuzi mwenzio uliyempangishia chumba hiki mmefanikiwa kwa kiasi fulani kurudisha jitihada zetu nyuma, lakini baada ya vifo vyenu, naamini tutaanza kwenda mbele”, alisema mtu huyu kwa sauti ya kutisha na kukatisha tamaa.
“Mwenzangu ni nani?” nilimuuliza tena.
“Bila shaka nimekwambia naitwa Ninja Mweusi. Lakini utanifahamu vizuri baada ya kifo chako, malaika watakuletea sura yangu utanifahamu. Haya, haraka geuka nyuma”, alisema tena kwa sauti ya kutisha, haraka nilitii amri hii nikageuka nyuma.
“Sikiliza, hivyo hivyo ulivyoweka mikono yako juu, tembea kuelekea upande wako wa kushoto, baada tu ya kushuka ngazi utaelekea tena kushoto, mbele kidogo kuna ngazi fupi, baada ya hizo ngazi utaelekea tena kushoto, fungua mlango utakaokuwa mbele yako, utakapotoka nje utaona gari ndogo BMW yenye rangi ya blue, utafungua mlango wa nyuma upande wa dereva itangia ndani, bila shaka utafurahi kuonana na mwenzio”, alisema mtu huyu mimi nikaanza kutembea kufuata maelekezo yake.
Kama nilivyoelekezwa, nilitembea hadi kwenye gari hili, lililokuwa nje. Pamoja na kuingia kwa tahadhali kubwa katika eneo hili, nilijilaumu sana mimi kukamatwa kama kuku. Nilifungua mlango wa nyuma ya dereva, nikaingia ndani. Taa ndani ya gari hili iliwashwa. Claud alikuwa amefungwa mikono kwa nyuma, jasho jingi lilimtoka mwilini, nadhani kwa sababu ya mateso na kipigp alichopata kutoka kwa watu hawa baada ya kumteka. Nilipoingia ndani ya gari hili, haraka mtu mmoja aliifunga mikono yangu kwa kamba ngumu, nikavishwa soksi kichwani ili nisiweze kuoma, mtu mmoja ambaye sikumuona vizuri aliingia na kukaa juu yangu.
“Mnatupeleka wapi? Kama kutuua hata hapa inawezekana”, niliwauliza kwa shauku.
“Sehemu ambayo ni nzuri nyinyi kujibu maswali yetu na baada ya hapo vifo vyenu vinafuata, ni kosa la jinai maiti zenu kuonekana baada ya kuuawa”, alisema mmoja wa watu hawa.
“Mnadhani sisi tutawajibu nini zaidi ya kusubiri vifo vyetu?”, niliwauliza huku dereva akiondoa gari eneo hili.
“Tunakujua kabisa kuwa wewe una kichwa na roho ngumu kama ya paka, lakini leo umekutana na watu wenye vichwa na roho mbaya sana. Tunaweza kuongea na wewe kirafiki, lakini pia tukiona huelewi maana ya urafiki, tutakufanya uongee kwa lazima. Uwezo huo tunao”, alisema mtu huyu.
“Unaweza kumfanya marehemu aseme?”.
“Ikibidi atasema”.
Nilijaribu kutuliza akili yangu ili niweze kuisikia sauti ya mtu huyu vizuri. Alijitahidi sana kuongea kiswahili, lakini hakikuwa kiswahili cha mtanzania halisi. Matamshi ya mtu huyu anaweza kuwa raia wa Congo ama Uganda.
Baada ya mwendo wa dakika kadhaa, gari lilisimama, dereva alipiga honi, tukasikia lango la chuma linafunguliwa. Sauti kutoka ndani ya gari ikahoji. “Bosi yupo?”.
“Bosi ameingia muda si mrefu, anawasubiri”, sauti kutoka nje ya gari ilisikika.
“Tumewaleta hawa washenzi wengine wawili. Idadi yao sasa imefika watatu, huyo mmoja naamini tutamtia mikononi leo”, alisema mmoja wa watu hawa kwa kujiamini. Mapigo ya moyo wangu yalibadilika, akili yangu ilihama, nikaamini kuwa mwisho wetu umefika, nikajiuliza mwenzetu mwingine kati ya Julius Nyawaminza Fred Libaba, nani atakuwa ametekwa kama sisi.
Lango lilifunguliwa, gari likaingia ndani, baada ya mwendo wa sekunde kadhaa lilisimama tena, milango ikafunguliwa watu hawa wakatoka nje. Sisi tulikuwa tumefungwa vitambaa machoni hivyo hatukuweza kuonana kinachoendelea, wala kujua tulikuwa wapi.
“Imekuwaje?” nilimuuliza Claud baada ya watu hawa wote kutoka ndani ya gari na kutuacha peke yetu. “Hata mimi sijui, nasikia maumivu makali sana kifuani, watu hawa ni wajuzi katika mambo ya ujasusi, inawezekana leo ikawa mwisho wa maisha yetu”, Claud alisema kwa sauti ya kukata tamaa.
“Katika maisha, usiogope lolote Claud, kila lililopangwa na Mungu litatimia, acha watuue, wataua wangapi?. Sisi ni binaadamu wa kupita kama ilivyo wao, tukifa leo tutakuwa tumekufa kwa jambo jema, watatokea wengine wataendeleza hapa tulipofikia, mimi naamini hivyo”, nilimwambia.
“Lakini tutakuwa tumeacha pengo kubwa sana, vifo vyetu nadhani vitarudisha nyuma kasi ya mapambano, siogopi kufa ila naumia kuona jitihada zetu zinaishia njiani”, Claud alilalama.
“Siku zote Mungu husikia kilio cha wengi, sisi tunapigana kuokoa wengi, hata tukifa leo, siku moja majina yetu yatasikika miongoni mwa mashujaa… Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema askari shujaa ni yule anayefia vitani, akirudi nyumbani, anarudi na ushindi, tusikate tamaa, nafasi ya kuishi bado ipo, japo ni finyu sana”, nilimwambia.
“Asante kwa kunitia moyo bosi”, Claud alisema kwa sauti ya kujiamini. “Nikiwa na wewe siogopi”. Milango ya gari hili ilifunguliwa tukatolewa ndani kama kuku. Baada ya kushushwa tulisukumwa kupelekwa sehemu isiyojulikana. Eneo hili lilikuwa kimya kabisa, kwa vile tulikuwa tumefunikwa nyuso zetu kwa kofia nyeusi hatukuweza kujua mahali tulipokuwa.
Kofia nyeusi tulizovalishwa wakati tunaletwa hapa ziliondolewa vichwani mwetu, tulijikuta mbele ya Carlos Dimera, alikuwa ameketi kwenye kiti kikubwa akivuta sigara kubwa iliyosokotwa kwa karatasi ngumu. Sekunde chache baadaye Julius Nyawaminza aliunganishwa nasi, alikuwa amechoka sana, nilipomwangalia niliamini kuwa alikuwa katika mateso makali.
“Ulijitia mjanja, ukanikimbia. Lakini waswahili wanasema ndege mjanja hunasa kwenye tundu bovu, kuku hata awe mjanja kiasi gani anategwa kwa mahindi na punje za ulezi tu, nikusifu kwa kuweza kutoroka sehemu ambayo si rahisi mtu kutoroka, hongera sana”, Carlos Dimera alisema huku akiniangalia kwa hasira.
Mama Feka aliketi upande wa kushoto karibu kabisa na Carlos, aliniangalia kwa macho ya wizi halafu akasimama na kuelekea upande wangu. Alivaa mavazi yaliyompendeza sana, suluali nyeusi, fulana ya kijani, raba miguuni na kofia nyeusi. Hakika alionekana kuvutia zaidi.
“Wewe ni binadamu wa aina gani?. Usiku wa kuamkia leo nusura uniue kwa risasi, isingekuwa mipango ya Mungu labda sasa ningekuwa maiti, sasa kabla ya kifo changu, utaanza kufa wewe”, Mama Feka alisema huku akitembea kuelekea kwangu. Alinitandika kibao, nikaona nyita.
“Teacher, kabla hamjaingizwa kwenye chumba cha mateso kama huyu mwenzio alivyofanyiwa, nikuulize swali moja rahisi sana, ukijibu nitawaruhusu muondoke”, Carlos alisema.
“Niliulize”, nilimjibu kwa sauti ya kutojali.
“Yupo mwenzenu mmoja anaitwa Fred, yuko wapi kijana huyu?” Lilikuwa swali kutoka kwa Carlos.
“Simjui”, nilijibu kwa mkato.
“Humjui Fred Libaba?” alihoji.
“Nimesema simjui”, nilijibu kwa msisitizo.
“Kama humjui Fred, basi ina maana hata hawa uliosimama nao hapa mbele yangu… Huwajui?”.
“Hakika siwajui, nimeshangazwa kuunganishwa na watu ambao sijawahi hata kuwaona katika historia ya maisha yangu”, nilisema.
“Usinitie hasira, mpumbavu mkubwa, tafadhali usinifanye nikavua hili gamba la ustaarabu nilililovaa leo, kama utapenda kuliona jua la saa nne leo, jibu maswali yangu”, Carlos alieleza.
“Nitajibu maswali ambayo nayafahamu, lakini usinilazimishe kujibu maswali ambayo binafsi siyajui”.
“Mpumbavu mkubwa, mlipowakamatwa vijana wangu, Hawa na Ton eneo la Kipawa wakiingiza dawa za kulevya, mkawapeleka haraka mahakamani, mliona fahari sana kufanya vile?”.
“Unapomkamata mhalifu wa aina ile lazima ufarijike, mimi kama mimi nilijisikia vizuri, pamoja na kwamba wewe ilikukera, lakini wengi walifurahi sana kukamatwa kwa dawa za kulevya ambazo ni hatari kwa matumizi ya watu”.
“Ahaa, una hakika ni hatari kwa matumizi ya watu. Wewe na hao wengi unaosema mmenufaika nini baada ya watu wangu kukamatwa?”.
“Tumenufaika sana, kuzuia uchafu kuwafikia vijana wetu ni faida kubwa”, nilijibu swali hili kwa kujiamini, maana nilijua nitakufa.
“Mussa hebu mtie adabu huyu paka”, Carlos aliagiza. Kijana mmoja aliyeshiba vizuri alisimama na kunijia, aliponifikia alinipiga ngumi kadhaa nzito tumboni. Aliendelea kunipiga kwa hasira. Sikuweza kumfanya kitu kwani mikono yangu ilikuwa nimefungwa kwa kamba. Nilisikia maumivu makali tumboni, nikavumilia.
Ilikaribia kuwa saa mbili za asubuhi ya Jumatano, siku ambayo ilikuwa rasmi kwa ajili ya mahakama kutoa hukumu dhidi ya watuhumiwa wa dawa za kulevya. Viongozi kadhaa wa Chama na Serikali walifika mahakamani hapa ili kusikiliza hatma ya kesi hii.
Vijana wa Polisi kutoka kikosi maalumu cha kutuliza ghasia walipita huku na huku kuimalisha ulinzi katika eneo hili. Huku magari kadhaa ya Jeshi la Magereza yakiwa na askari wengi kutoka kikosi maalumu wakisubiri. Wafanyabiashara wa dawa za kulevya nao walituma vijana wao kadhaa, ambao walifika mahakamani hapa kusubiri hatma ya Hawa Msimbazi na Tony Sime.
Carlos Dimera, alikuwa amepinga wazo la vigogo wa ngazi za juu katika kundi hilo, waliokutana katika jiji la Bogota, nchini Colombia na kuafikiana kuwatosa watuhumiwa hawa kwa ajili ya kulinda maslahi yao. Dimera alipinga vikali wazo hilo kwani aliwaamini sana vijana hawa. Inasemekana kabla hawajajiunga naye aliwanywesha maji yaliyochanganywa na damu yake. Katika kikao cha dharura kilichofanyika usiku, Dimera na vijana wake walipanga mikakati ya kila aina ili kuwaokoa Hawa na Tony, kutoka katika mikono ya sheria. Hii ilikuwa siku ya tatu kwa watuhumiwa hawa kuwa mikononi mwa vyombo vya sheria, wakisubiri na kuamini nguvu ya pesa itawaweka huru.
Kutoroka kwa Teacher usiku ule kuliwaumiza sana. waliamini kuwa mipango yao haitafanikiwa. Faraja iliwajia baada ya Teacher kutekwa tena alfajiri, wakaamini kuwa mipango yao itakuwa swa.
Mahakama ilifulika watu, kila mmoja akiwaza hili na lile. Ilikuwa imeahilishwa jana kutokana na hoja mbalimbali zilizowasilishwa mahakamani hapo, kufuatia malumbano ya kisheria na leo ilikuwa siku rasmi ya kutoa hukumu. baada ya taratibu zote za kimahakama, kama kawaida, askari maalum alipaza sauti kuashiria kuingia kwa mheshimiwa Hakimu, watu wote alisimama.
Kanali Benny Emilly, ambaye ndiye Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi, alikuwa mmoja wa watu waliofika hapa, Mzee huyu alikuja kusikiliza hukumu ya kesi hii akiwa na baadhi ya wasaidizi wake kadhaa. Kabla ya kufika mahakamani hapa alifanya kila njia kuwasiliana na Teacher, hakubahatika kupata mawasiliano yake. Baada ya Hakimu kuingia na kuketi katika kiti chake, alichukua baadhi ya mafaili yaliyokuwa mezani hapo na kuyapitia moja baada ya jingine, baadhi aliyaweka kando, hatmaye akabakiwa na faili moja mkononi.
“Kutokana na umuhimu wa kesi ya uhujumu uchumi iliyo mbele yangu, nimelazimika kuahilisha kesi zingine zote zilizokuwa zitajwe leo, wahusika katika kesi hizo wafike chumba cha kumbukumbu kwa ajili ya maelekezo zaidi ikiwa pamoja na kupangiwa tarehe nyingine ya kesi, nitasikiliza kesi ya kuhujumu uchumi inayowahusu Hawa Msimbazi nana Tony Sime, bila shaka wapo?”, Hakimu alihoji baada ya kueleza.
“Naam mheshimiwa, wateja wangu wako mbele yako”, alieleza Kyaruzi, ambaye ni mwanasheria upande wa utetezi. akaandika maelezo, baada ya kujiweka sawa, akasema.
“Mwendesha mashitaka”. “Mheshimiwa Hakimu, kesi iliyoko mbele yako ni Kesi namba 208 ya mwaka huu, kama ilivyosomwa hapo awali, washitakiwa Hawa Msimbazi na Tony Sime, wanashitakiwa kwa pamoja kuwa mnamo tarehe 15 ya mwezi huu, huko Uwanja wa Ndega wa Dar es Salaam, walikamatwa na askari wakijaribu kuingiza dawa za kulevya aina ya heroine, ambalo ni kosa la kuhujumu uchumi”, akageuka.
“Mheshimiwa, baada ya watuhumiwa hawa kukamatwa kwanza walikaidi amri halali waliyopewa na askari, wakidai kuwa mzigo wao si dawa za kulevya isipokuwa ni malighafi kwa ajili ya kiwanda chao cha kutengeneza tembe za kutibu malaria. Ili kujiridhisha, malighafi hizo zilipelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali. Ripoti ya Mkemia Mkuu wa Serikali imethibitisha kuwa mzigo uliokamatwa ukiingizwa nchini ni dawa hatari za kulevya aina ya heroin ambazo zimepigwa marufuku na Serikali ya Tanzania kuingizwa hapa hapa nchini”.
Haraka mwanasheria wa utetezi akasimama na kugonga meza, “Mheshimiwa Hakimu, suala la dawa za kulevya si jambo la kufanyia mchezo, kama wateja wangu walivyoieleza mahakama yako tukufu jana kuwa hawahusiki kabisa na dawa za kulevya, inashangaza sana mwendesha mashitaka wa Serikali kung’ang’ania kuwa ripoti ya mkemia mkuu wa Serikali imethibitisha wateja wangu walibeba dawa za kulevya jambo ambalo si kweli”.
Mwendesha mashitaka wa Serikali akasimama tena. “Kama si dawa za kulevya… naomba uieleze mahakama, wewe unadhani watuhumiwa hawa waliingiza nini hapa nchini?. Mheshimiwa kama ishu ni kuagiza mizgo kwanini wasitumie cargo kusafirisha mizigo yao?”.
“Mheshimiwa Hakimu, maelezo ya wateja wangu yako wazi kabisa, wameieleza mahakama yako tukufu kuwa mzigo wao ni maalum kwa ajili ya kutengeneza tembe za kutibu malaria. Tena wakasisitiza kuwa kama mzigo huo ni dawa za kulevya si wao, inawezekana wamefanyiwa njama za kibishara mambo haya yapo. Mheshimiwa, kinachoshangaza ni kwamba mzigo uliokamatwa umepelekwa kwa mkemia mkuu wa Serikali bila wateja wangu kuhusishwa hii haikubaliki. Inawezekana wakafanyiwa hujuma, ndivyo inavyoonekana. Mheshimiwa, mahakama ni chombo cha haki, kisitumike kuwaonea wateja wangu”, mwanasheria wa utetezi alieleza.
“Mheshimiwa, kama nilivyoileza mahakama yako tukufu jana. Narudia, haiwezekani watu hawa wasafiri kutoka hapa nchini, waende nje ya nchi, watumie pesa nyingi kwa ajili ya kufuata malighafi za kutengeneza tembe za malaria. Mheshimiwa, mzigo uliokamatwa ni mali ya washitakiwa hawa. naamini hata wewe unasafiri nje ya nchi, lakini huwezi kuchukua mzigo usioujuwa, hawa ni wafanyabiashara wazoefu wa bishara chafu, wakiachiwa wanaweza kuligharimu taifa”, aliketi baada ya kusisitiza.
“Mheshimiwa, inawezekana kabisa mwendesha mashitaka wa Serikali ana sababu zake binafsi kwa wateja wangu, jambo hili lisichukuliwe kijuujuu, taratibu ziko wazi mheshimiwa, tusitumike vibaya kwa sababu mkemia mkuu wa Serikali, mwendesha mashitaka wa Serikali ndiyo iwe njia ya kuwaumiza wateja wangu, haitawezekana mheshimiwa, kwanza walipaswa kuitwa ili washuhudie vipimo husika, lakini hili limefanyika bila wateja wangu kuhusishwa”, mwanasheria wa utetezi alilalama kwa mara nyingine.
Hakimu aligonga meza, ukimya ukatawala kwa dakika kadhaa. “Hukumu. Nimesikiliza hoja za pande zote mbili kwa makini na kupitia maelezo ya pande zote kwa umakini mkubwa. Hivi niwaulize, inawezekanaje mtu ubebe mzigo usioujuwa kutoka huko nje, ukibadili ndege hii na hii hadi unaingia nchini, mzigo huo huo ukaubeba kwenye magari kuelekea nyumbani bila kujua umebeba nini?”, Hakimu alihoji. “Kama umefanyiwa njama au watu wanataka kuharibu biashara yako ama sifa yako, inawezekana kabisa mheshimiwa, wengi wamekutwa na kashfa za aina hii, naiomba mahakama yako tukufu iwatendee haki wateja wangu”, mwanasheria wa utetezi alirudia kusihi.
Dakika kadhaa zilipita kukiwa kimya, hakimu akiichezea kalamu yake kwa meno, …”Usinifundishe kazi. Naam, Mwendesha mashitaka wa Serikali ameieleza mahakama hii kuwa mnamo tarehe 15 mwezi huu, watuhumiwa wawili, Hawa Msimbazi na Tony Sime, mlikamatwa huko Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, mkiwa na mzigo ambao ripoti ya mkemia mkuu wa Serikali imethibitisha kuwa ni dawa za kulevya aina ya heroin. Jambo hili ni zito, bila shaka unajuwa kuwa dunia nzima imepiga marufuku matumizi ya dawa hizi, sijui hata mmewezaje kutoka huko nchi za mbali, mkavuka ukaguzi pale Uwanja wa ndege, hatmaye mkaingia nchini na kutiwa mbaroni na vijana waaminifu katika taifa hili”, Hakimu alieleza huku wengine wakitazamana.
“Mmmh wamekwenda na maji hawa”, kijana mmoja aliyekuwa mahakamani hapo alimnong’oneza mwenzake.
“Mwanasheria wa utetezi anasema inawezekana wateja wake walibeba mzigo wasioujuwa, lakini wamekiri kuwa walisafiri kwa ajili ya kuingiza malighafi za kutengeneza tembe za malaria, walipoulizwa na mwendesha mashitaka inawezekanaje watu watumie gharama kubwa kusafiri nje ya nchi ili kuingia mzigo wa gharama ndogo ambao haukidhi matumizi, hawakutoa jibu. Walipoulizwa tena kwanini wasitumie njia ya cargo kusafirisha mizigo yao hawakutoa majibu. Hii inaonyesha kabisa watuhumiwa hawa walikusudia kuingiza dawa za kulevya hapa nchini”, Hakimu alieleza.
“Baada ya kusikiliza kesi hii na kupitia vingu mbalimbali vya sheria, nimethibitisha bila kutia shaka kuwa watuhumiwa hawa wana kesi ya kujibu. Kabla sijatoa hukumu, mnaweza kujitetea.
“Mheshimiwa Hakimu, tunaomba huruma yako, kwa upande wangu nina jukumu la kuwalea wazazi wangu ambao ni wazee sana, nina watoto wadogo wanahitaji msaada wangu mheshimiwa, wakinikosa wataathirika sana, naomba huruma unifikirie kwa hilo mheshimiwa, pia nasumbuliwa na tatizo la kifua”, Hawa Msimbazi alijitetea.
“Tunaomba msaada wako mheshimiwa, kimsingi hili ni kosa la kwanza, tunaomba mahakama yako itupunguzie adhabu”, Tony Sime alieleza huku hakimu akiandika maelezo yao kwa makini.
“Kuwa na wazazi wazee, watoto wanakutegemea haikupi tiketi ya kukufanya utende makosa, mbona wewe hukuwaonea huruma watoto wa wenzio, dawa za kulevya ni hatari kubwa. Naam ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye mawazo na tabia kama yenu, nawahukumu kwenda jela kila mmoja miaka kumi na mitano”, wote wakaanguka chini wakati hakimu akitoka mahakamani.
Taarifa za kufungwa jela kwa watuhumiwa wawili wa dawa za kulevya, Hawa Msimbazi na mwenzake Tony Sime, zilisambaa haraka kwenye mitandao ya kijamii. Blog ziliripoti habari hii kwa mbwembwe, waandishi wa mitandao wakipishana kwa vichwa cha habari na maelezo yaliyosisimua wengi.
Blog ya MPIGANAJI iliandika. Breaking News, halafu mwandishi akaweka maneno haya. WAFANYABIASHARA WA DAWA ZA KULEVYA WAKIONA CHA MOTO, WATUPWA JELA MIAKA. 15. Blog ya KAMANDA WA MATUKIO iliruka na kichwa cha habari, DAWA ZA KULEVYA ZAWAPELEKA JELA MIAKA 15, MICHUZI wakaandika, MAHAKAMA YATOA ADHABU NDOGO KWA WAUZA DAWA ZA KULEVYA. Redio zikatangaza habari hii, waliosikia walishangilia.
Shamla shamla ziliendelea mitaani. ulikuwa ushindi mkubwa kwa Serikali. Lakini ghafla habari hii ikagauka msiba. Masaa kadhaa baada ya hukumu, taarifa zikaenea kuwa Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo na kutoa hukumu amepigwa risasi na kuuawa ofisini kwake. Hofu ikatawala. Wakati viongozi wakitafakari kuhusu tukio hili. Habari nyingine inasambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa, askari kadhaa wameuawa na wengine kujeruhiwa vibaya baada ya kutokea mapigano makali wakati wakisindikiza wafungwa.
Taarifa hii ilieleza kuwa wafungwa wawili waliotuhumiwa kuingiza dawa za kulevya nchini, Hawa Msimbazi na Tony Sime, waliokuwa wakipelekwa katika gereza moja Jijini Dar es Salaam wametoroshwa wakiwa wakiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi. Wananchi wakapatwa na masikitiko, Mzee mmoja wa makamo aliposikia taarifa hizi kwenye vyombo vya habari alitoa machozi. Habari zinamfikia Kanali Beny Emilly, anashindwa kuyaamini masikio yake, anasimama sekunde kadhaa mbele ya kiti chake, hofu inamwingia, anajaribu kwa mara nyingine kuinua simu yake ya kiganjani kuwasiliana na Teacher. Bahati mbaya simu hiyo haipatikani anaelekea kuchanganyikiwa, furaha yake inageuka kalaha, machozi yanamlengalenga.
“Nini hii?”, Kanali Emilly anajiuliza wakati akielekea nje ya ofisi yake.
Taarifa hii inawafikia wakubwa wa nchi, vikao vya dharura vinakaa. “Nini kumetokea”, anahoji mkuu wa nchi. “Hili haliwezekani katika nchi hii”, anasisitiza bila kupata majibu. Wasaidizi wake wanajaribu kueleza msimamo.
Simu zinapigwa huku na huko bila mafanikio, “Nani hasa wameshiriki katika tukio hili”, Kanali Emilly anajiuliza kwa mara nyingine.
*************************************
Nilijaribu bila mafanikio kutambua wapi tulipofichwa. Tulikuwa tumesimamishwa mbele ya watu hawa huku mikono na miguu yetu ikiwa imefungwa barabara kwa kamba ngumu. Pamoja na mazoezi makali ninayofanya karibu kila siku, lakini hapa niliyasikia maumivu kutokana na staili iliyotumika kutufunga hizi kamba. Ukweli hata uwe na mazoezi kiasi gani kwa mtindo huu lazima utasikia maumivu.
Wote watatu tulifungwa kwa mtindo mmoja, yaani miguu yetu ikiwa imefungwa kamba, mikono nayo ikiwa imefungwa vizuri kwa nyuma halafu kamba hizo zimevutwa na kufungwa sehemu ya juu. Kwa maana hiyo mikono yetu ilivutwa nyuma ikaangalia juu na kutusababishia maumivu makali sana.
Kelele za mashine na baadhi ya watu zilisikika, hali hii ilinifanya nikabaini kuwa eneo hili lilikuwa la viwanda. Niliwaza na kujiuliza mambo mengi, nilimuomba mungu angalao awanusuru wenzangu Julius Nyawaminza na Claud Mwita ili mimi nichukue nafasi yao.
Nilijilaumu kwa kuweka tahadhali ndogo wakati naingia pale hotelini, hata hivyo sikupaswa kulaumu sana maana tayari nilikuwa katika mikono ya mauti. Hasira na chuki kwa watu hawa zilinijia, nikatamani kufanya miujiza lakini sikuweza tena.
Mlango ulifunguliwa mtu mmoja mnene ambaye sikuwahi kumuona katika historia ya maisha yangu akaingia ndani, alikuwa mtu makamo, mwenye umri kati ya miaka hamsini na sitini, alivaa mavazi yaliyomkaa vizuri na miwani ya jua, mtemba ukiwa kinywani mwake. Alionekana mtu mwenye busara kiasi, lakini kwa uzoefu wangu nikabaini mtu ni mmoja wa watu washenzi pengine zaidi ya Carlos Dimera.
“Karibu Mzee Mtemba”, sauti nzito ya Jackina ilisikika, Mzee huyo alipita taratibu akituangalia kwa tabasam na bashasha, baada ya kushikana mikono na Carlos akaketi.
“Nimekuita ushuhudie vifo vya mbwa hawa. Mzee Mtemba bila shaka unatambua jinsi mtandao wetu ulivyotikiswa, chanzo ni hawa washenzi wanaoamini biashara ya dawa ya kulevya itakomeshwa, ni ndoto ya mchana”. Akainua macho. “Poleni sana, ujinga wenu umewakosti, mimi ni mtu mwenye huruma sana lakini kwenu sintakuwa na huruma kamwe”, Carlos akasisitiza.
“Wewe ndiye unaona hivyo Carlos, lakini pia tambua kuwa mjinga wa leo ndiye mwelevu wa kesho, kufa ni jambo la kawaida katika maisha ya mwanadamu, sisi hatuogopi kufa, naamini siku moja utakufa pia, adhabu yako mbele za Mungu itakuliza milele”, nilimwambia.
“Mwangalie mpumbavu huyu, wakati wewe unakufa leo mimi nataendelea kula maisha, nitatanua kwa raha zangu, pole sana Teacher, wewe ni miongoni mwa watu waliochelewa sana katika maisha. Hebu mtieni adabu mbwa huyu”, Carlos aliagiza. Vijana wawili wakanijia tena na kuanza kunitwanga.
Wakati wote huo Mama Feka alikuwa akichezea simu yake ya kiganjani, sikujua alichokuwa akifanya nadhani alikuwa akiwasiliana na watu wake fulani. Vijana hawa walinivamia na kunipiga ngumi kadhaa tumboni na kunisabanishia maumivu makali zaidi.
“Utalipa, iko siku utalipa”, nilieleza wakati nakaribia kupoteza fahamu.
“Teacher, kama nilivyokwambia hapo awali mtandao wetu ni mkubwa mno, umesambaa dunia nzima, mijini na vijijini, tunao viongozi wakubwa katika Serikali. Huyu Mzee wa Mtemba ndiye Mkuu wa Operesheni ya wizi wa kutumia noti bandia, ambazo nafikiri ulionyeshwa na bosi wako, wengi wameuza majumba yao kupitia mzee huyu”, Carlos alidokeza, sasa nikaelewa sababu za mtu huyu kufika mbele yetu maana niliwahi kumsikia lakini kwa jina la Benny.
Mzee Mtemba akasimama. “Asanteni sana vijana wangu, kama ulivyoelezwa, mimi ndiye kigogo wa opereshani ya noti bandia. Lakini kabla sijaongea nanyi, binafsi nichukue nafasi hii kutoa hongera kwa kazi yenu nzuri, mmejaribu kututia matumbo joto. Mimi ni mfuatiliaji wa siasa za nchi hii, miaka zaidi ya kumi niliyoishi humu, nimegundua kuwa nchi hii haina mwenyewe, ndiyo maana tumeweza kuishi hata bila kufuata taratibu za uhamiaji, nawasikitikia sana vijana hawa ambao umri wenu bado mdogo sana, lakini mtakufa leo, mimi ni mtu wa imani na huruma sana, sipendi kuona mtu akiuawa, lakini nyie mmekitafuta kifo wenyewe, ndiyo maana nimekuja mnijuwe pia nishuhudie vifo vyenu”, alieleza mtu huyu halafu akaketi. “Mzee Mtemba, binafsi nimekuwa nikieleza habari hizi kwa mifano ili adui zangu watambue mimi ni mtu wa aina gani, lakini vijana hawa hawakunisikia eti kwa sababu tu wamekunywa maji ya bendera. Kikosi ninachokiongoza kina nguvu kubwa kushinda dola ya nchi hii, Hawa na Tony wako huru, hebu ingieni ndani”, Carlos Dimera alieleza. Mlango ukafunguliwa Hawa na Tony tuliowakamata na dawa za kulevya na kisha kuwafikisha mahakamani wakaingia wakiwa na nyuso za hasira.
“Asante sana bosi. Tuko huru sasa”, alieleza Hawa huku akionyesha hasira alizokuwa nazo kwangu. “Ulijisikia jasiri kwa kutukamata, lakini ujasiri wako leo umekwisha”, aliongeza.
“Ni kweli, lakini amini utakamatwa tena”, nilimwambia kwa mkato.
“Mpaka itokee. Naamini kifo chako kitawaogopesha wengi, hata mashujaa waliokuwa wakijipanga kujiingiza katika suala hili watakaposikia mwili wako umeokotwa kando ya bahari, mmmh watarudi nyuma”, Hawa aliongeza.
“Hii ni kuwaonyesheni kuwa hatushindwi kitu, kama mzee Mtemba alivyosema, leo ndiyo mwisho wenu kuishi duniani, tulitaka mhakikishe kuwa Hawa na Tony hawafungwi jela, sasa ni wakati mzuri kwenu kupeleka habari hii huko kuzimu, poleni sana”, carlos aliongea kwa kujiamini.
“Tuko tayari kwa lolote, lakini mtambue kuwa hakuna mwenye nguvu zaidi ya dola, sisi tutakufa leo, lakini wapo ambao wataendeleza hapa tulipofika, wengine wamezaliwa tayari, wengine wako katika matumbo ya mama zao”, niliwaambia kwa sauti ya kutetemesha na hasira.
“Yawezekana wewe una mapungufu katika kichwa chako, mtu gani wewe usiyeogopa kifo, mbona wengine wamenyamaza”, alisema Carlos.
“Kunyamaza kwao si kwamba wanakuogopa kufa, wamekudharau sana, nikwambie ukweli, kabla hamjatoka hapa leo mtakuwa mmekamatwa wote, hii ni nchi ya watanzania, hata hawa vibaraka wako pia ni watanzania lakini wasarti wa nchi iko siku yao”, niliwaambia.
“Ombeni Mungu wenu azipokee roho zenu kwa mara ya mwisho, sihitaji kuumizwa kichwa cha…. Carlos alikatishwa na kelele za vishindo na risasi zikasikika kutoka nje. Risasi zikaendelea kulindima, wote tukaingiwa na hofu, ghafla umeme ndani ya chumba hiki ukazimika, kukawa giza.
Baada ya ukimya wa sekunde kadhaa hivi kupita, risasi zikarindima tena huku nafsi zetu zikiwa zimejawa na hofu kubwa. Ghafla taa ndani ya chumba hiki ziliwashwa, vijana wawili nadhifu sana waliingia ndani ya chumba hiki kwa kasi ya ajabu, silaha zao zikiwa mikononi wakazikata kamba zilizofungwa kwenye miguu na mikono yetu kwa visu vikali. Ukweli ni kwamba Vijana hawa sikuwahi kuwajua kabisa.
“Poleni sana bosi, tutaongea baadaye”, alisema mmoja wa vijana hawa baada ya kuzikata kamba tulizofungwa kwa kisu chake imara.
“Usijali”, niliwaambia huku zikinyoosha viungo vya mikono yangu. Risasi zikasikika tena nje, mmoja wa vijana hawa akatufahamisha kuwa tusihofu ilikuwa kazi ya Peter Twite, ambaye alikuwa nje ya chumba hiki kuimarisha ulinzi wetu.
Bahati mbaya ni kwamba, hakuna hata mtu mmoja aliyekamatwa katika vurumai hiyo, Carlos Dimera, Mzee wa Mtemba na vijana wao kadhaa walifanikiwa kutoroka salama kutoka katika eneo hilo. Kazi nzuri iliyofanywa na Mama Feka ilikuwa imenusuru maisha yetu.
Ilikaribia kuwa saa tano za mchana, Wakati wote sikujuwa tulikuwa sehemu gani, baada ya kutoka ndani ya chumba hiki, nilishangazwa kuona kumbe tulikuwa kwenye ofisi za karakana ya Tazara, kando ya barabara ya Nyerere. “Mmmh inakuwaje”, nilijiuliza kwa sauti baada ya kumuona Peter Twite akinijia.
“Pole sana mkuu, tuondoke haraka eneo hili, watu wengi sana wameuawa hapa, tuondoke kabla polisi hawajafika, wanaweza kutuleta nongwa, tukacheelewa”, alisema huku akinishika mkono kunisabahi.
“Ni kweli kabisa Petet, hii inaweza kutuchelewesha pia”, nilimwambia, sisi tukaingia ndani ya gari alilokuwa akiendesha Twite, tukaondoka kuelekea sehemu za Vingunguti. “Wapi Fred?” Niliuliza.
“Fred, tuliwasiliana saa tatu hivi, akaniuliza kama nimesikia taarifa za mauaji ya Hakimu aliyehukumu kesi ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya, nikamwambia nimesikia, akaniuliza kuhusu kutoroka kwa watuhumiwa hao mikononi mwa polisi, nikamjulisha kuwa taarifa hizo ni kweli, mwisho akanifahamisha anawatafuta lakini hawapati, baada ya hapo sijamsikia tena na simu yake haipatikani”, alieleza Twite wakati anavuka kwenye njia ya reli ya Vingunguti.
“Twende Green Pub, nadhani patafaa kwa mazungumzo kidogo wakati tukifikiri na kutafakari tuwafanye nini watu hawa”, nilisema, wakati Peter Twite akizungusha usukani wa gari tukaingia Barabara ya Nyerere na kuelekea eneo la Vingunguti.
“Watu hawa wamejipanga vizuri kutenda uhalifu”, Nyawaminza alisema baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu.
“Inaonyesha hivyo. Lakini tuwe makini sasa, maana jana tu nimekamatwa mara mbili, naamini wanatumia mawasiliano ya mitandao kujua mahali tulipo, sasa tusiamini mtu yeyote”, niliwaasa.
“Hakika. Mimi bado najiuliza ilikuwaje wakaingia kwenye ofisi za umma pale karakana na kuzitumi kama sehemu zao, ingekuwa siku za mapumziko kama sikukuu ama Jumamosi, Jumapili nisingehofu, lakini leo siku ya kazi?” alihoji Twite.
“Tutajua baadae. Hawa ni wahalifu wakubwa, wanachofanya ni kuvamia na kuua wahusika, wanatumia eneo hilo kwa muda halafu wanasepa. Wengine hutumia maeneo hayo nyakati za usiku, lakini hawa wako vizuri mpaka wakati huu mchana kweupe?” nilisema wakati Twite amesimama kwenye taa za kuongoza magari za Jeti.
Tulikuwa na magari matatu, ambayo hayakufauatana kwa karibu kutokana na hali ya usalama. Peter alichepuka tukaingia kwenye barabara mbovu ya vumbi, baada ya kuvuka kizuizi cha reli ya kati, akaingia kulia kama tunarudi katikati ya Jiji. Tukazipitka ofisi za Kiwanda cha BECO, Nilikuwa makini kuangalia kila gari lililokuwa mbele au nyuma yetu, hatmaye tukaingia Green Pub. “Ipo njia ya mkato hapa, lakini nilipita Jeti kwa sababu za usalama”, Twite alidokeza.
“Nilikusoma, ndiyo maana nikawa kimya”, nilijibu wakati tukitafuta sehemu nzuri ya kuketi. Bahati nzuri mwenye sehemu hii rafiki yangu Kinyami Mwitazi ananifahamu, alipotuona alituelekeza sehemu nzuri tukaketi. Bada ya kila mmoja kuagiza kinywaji chake, tukagawanyika, wale vijana wakatafuta sehemu yao mbali kidogo tofauti na sisi.
“Peter, najiuliza sijui hata nikushukru kwa maneno gani. Maana sijui hata ilikuwaje ukajuwa kuwa tumefungiwa pale Karakana?” nilianzisha mazungumzo.
“Ni hadithi ndefu, lakini tumshukru sana Mama Feka, nadhani atafika hapa muda si mrefu. Bosi ulicheza sana kumuingia dada huyu katika kazi hii, bila yeye sijui ingekuwaje?” Peter alidokeza.
Mara Pikipiki kubwa aina ya Honda XL CC 250 ikasimama upande wa pili wa Reli, juu ya pikipiki hiyo kulikuwa na vijana wawili nadhifu, mmoja wa kiume na mwingine mwanamke wote wakiwa wamevalia miwani ya tinted usoni. Msichana mrembo sana alishuka, baada ya kuangalia huku na kule akatembea kuelekea mahali tulipoketi.
“Unamfahamu huyo?” Peter aliniuliza.
“Bila shaka ni Mama Feka, ama kweli ametakata”, nilisema. Yule kijana aliyemleta aliinua mikono, akatupungia halafu akaondoka.
“Na huyo?”.
“Huyo ni kjana wetu, miongoni wale ulioagiza wakae kwenye pointi wakiwa na Pikipiki, vijana hawa hawajalala toka tuanze kazi hii, kama tukiimaliza salama, tusiwasahau, utazani wamewahi kufanya kazi hizi”, Peter alishauri.
“Ni kweli kabisa Peter”.
Baada ya kutushika mikono, Mama Feka alivuta kiti karibu yangu akaketi. “Poleni sana Teacher, nasikia usingizi sana lakini usijali, karibu tutashinda vita nitapata wasaa mzuri wa kulala”, alieleza.
Akaanza kutueleza habari zote, toka nilipokamatwa kule Hoteli Bela Vista Kinyerezi, alivyoniwezesha kutoroka pale kiwanda cha Blanket Keko, kutekwa kwa Julius Nyawaminza, Claud Mwita na hatimaye mimi.
“Shemeji yangu Teacher, kazi hii ni ngumu, lakini nakiri kuwa baada ya wewe kuniingiza katika jambo hili imesaidia kujua mambo mengi, sasa nazijua sababu za watu kuniita Cthia Rothrock, nimewiva sana, angalieni saa zenu”, alisema wote tukainamisha vichwa kuziangalia saa zetu, ilikaribia kuwa saa saba mchana.
“Inakaribia saa saba mchana. Binafsi nimsifu na kumpongeza sana Peter, baada ya kutambua kuwa simu zenu zimeingizwa kwenye mtandao wa mawasiliano na kila mlichofanya pale pale kilionekana, sikuona sababu ya kuwasiliana na simu zenu, nilitengeneza laini yangu ya siri, ambayo nimeitumia kwa ajili ya kuwasiliana na Peter tu. Na kweli imesidia kuokoa maisha yenu, nilichanganyikiwa sana nilipomuona Mzee wa Mitemba, yule Mzee akiitwa maeneo kama yale, mmmh usitehgemee kutoka salama, tumshukru sana Mungu”, alisema.
“Ilikuwaje wakatoroka wakati tulikuwa tumeizingira ofisi ile?, tena ajabu ni kwamba tumeua watu ambao hawahusiki kabisa”, Peter alihoji.
“Pale ndani ya ofisi ile, chini kuna milango miwili ya siri, ukibonyeza kitufe inafunguka unazama na kuna njia ya kutokea sehemu nyingine kabisa, tumepita huko”, alieleza Mama Feka.
“Hawajakushtukia?”, niliuliza.
“Wee, siyo rahisi, unajuwa wakati nawasiliana na Peter, kidogo Carlos anishtukie, lakini nilikuwa nimefanya ujanja fulani, nilifungua sehemu ya game, nikawa nacheza huku natuma ujumbe, kwa kuwa simu yangu niliitoa sauti, basi ilikuwa kazi rahisi kujibu kila swali Peter aliloniuliza”.
Baada ya ukimya wa sekunde kadhaa, akaanza kutueleza tena habari za kutisha na kusikitisha sana, “Watu wengi sana wamepotea, nimeona mambo mengi ya kutisha sana, namshukru Teacher alinijenga kisaokolojia kabla sijaingia huko. wale watu ni hatari sana. Naomba mnisikilize kwa makini sana”, tukajiweka tayari kumsikia huku nywele zikinisiimka kichwani, sikuamini kama Mama Feka angetusaidia kiasi hiki. Kimya kimya nilituma ujumbe wa maandishi kwa Kanali Benny Emilly ili naye afike sehemu hii maana tulikuwa tunajiandaa kuingia vitani.
“Mkishindwa kuwakamata leo, itakuwa ndiyo salama yao, hawatakamatwa tena, wamepanga kutokomea leo, hivi tunavyongea hapa kuna meli ndogo iko ufukweni mwa Bahari, itaondoka nadhani itakuwa saa kumi Alasiri, wana kikosi kizuri sana, wanao vijana mahiri katika mapigano, ili kazi yetu iwe rahisi lazima tujipange sawasawa”, alishauri.
“Tumekusikia”, nilimwambia, halafu nikawageukia wenzangu, “bila shaka wote tumemsikia Mama Feka?”.
“Naam”, walijibu huku tukiendelea na vinywaji. Mara simu yangu iliita nikapokea. Ilikuwa simu kutoka kwa Kanali Emilly.
“Angalia upande wako wa kuume ulipoketi, kuna Pick Up single cabine rangi ya kijani, ina kiturubai nyuma, njoo ingia tuzungumze”.
“Nakuja bosi”, nilisema huku nikisimama. “Jamani, ngoja nimsikilize kigogo, nendeleeni nakuja”, nikawaacha na kuelekea kwenye gari lililokuwa limeegeshwa mbali na eneo tulipoketi. Nilipokaribia dereva wa gari hilo alishuka na kunielekeza niingie upande wake.
“Jambo Mkuu”, nilimsalimia Kanali Emilly baada ya kuongia ndani ya gari hii.
“Jambo, habari ya kupotea Teacher?. Mpaka nikapatwa na hofu kubwa. Ulipatwa na nini Kapteni?” Nikaanza kumweleza kilichonitokea hata nikatekwa na kutoroka kule Kiwanda cha Blanketi. Nikaeleza jinsi tulivyoponea chupchup kuuawa kwenye ofisi za Karakana ya Tazara, maelezo haya kiasi fulani yalionekana kumuumiza rohoni.
“Poleni sana vijana wangu. Siku zote Mungu humsaidia asiye na hatia, yule anayeonewa. Teacher mwanangu, mpaka sasa adui anaelekea kuchanganyikiwa, cha msingi tusilegeza kamba, au unasemaje?”
“Hakika”.
“Mmekwama wapi?”.
Nikaanza kumweleza kuhusu mpango ulio mbele, “Hatujakwama Mkuu, tunachofanya sasa ni kujadili plani B, kuvamia eneo fulani ufukweni mwa Bahari. Taarifa zilizopo ni kwamba wamepanga kutoroka leo jioni wakitumia Meli ndogo ambayo tayari imejazwa shehena ya dawa za kulevya kwa ajili ya kuelekea Mombasa. Na sisi hatutawapa nafasi hiyo, Leo ndiyo mwisho ama wao ama sisi”, nilisema.
“Amina”, Kanali Emilly alisema kwa ishala huku akiangalia juu.
“Samahani, Afande nakuomba shuka kwenye gari twende uongee na vijana, uwape hamasa, vita si lelemama, habari kutoka kwenye vyanzo vyetu ni kwamba adui ana nguvu na vifaa vya kisasa kama silaha na mitambo”, nilimwambia akahamasika, akafungua mlango tukashuka kuelekea kwa wapiganaji. Wote wakasimama, machozi ya furaha yakamtoka.
Mchana huu sehemu nyingi za starehe zilikuwa zimefungwa, hii ni kutokana na agizo la Serikali kuwataka watu wafanye kazi kwanza na kustarehe baadaye, kutokana na hali hii tulipata wasaa mzuri wa kukaa hapa Green Pub kumsikiliza Kanali huyu wa Jeshi, ambaye ndiye Mkurugenzi wa Upelelezi, Benny Emilly. Alikuwa Mzee wa makamo na nywele zake zilikuwa zimebadilika rangi kuwa nyeupe kabisa. Baada ya kufuta machozi ya uchungu yaliyomtoka akiwa mbele yetu, alivuta kiti kilichokuwa karibu akaketi. Tukasogeza viti ili kumsikia atasema nini.
“Wapiganaji wangu shupavu, nyie ndiyo hazina ya nchi yetu, sisi wazee tumechoka, tunaelekea ukingoni, jukumu lenu sasa ni kulinda heshima ya nchi yenu. Mimi sina kawaida ya kutoa machozi mbele ya watoto, lakini leo yamenitoka. Mnajua kwanini yametoka. Nimefurahi sana kuwaona katika hali hii ya umoja, bila umoja hakuna ushindi. Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema Umoja ni nguvu, Mzee Kenyatta naye akasema Harambee, maana ni lilelile. Watanzania wanasubiri ushindi kutoka kwenu. Kabla ya kuja mbele yenu nimeongea na Teacher pale ndani ya gari, amenieleza misukosuko na hatari zilizowakuta, nafurahi kusikia mko salama na hakuna aliyekata tamaa. Ndiyo maana nikatoa machozi baada ya kuwaona mkiwa salama. Teacher amenijulisha pia kuwa leo ni siku ya kufa ama kupona kati yetu na vibaraka wa taifa letu. Pia amenifahamisha kuhusu mama huyu jasiri, ambaye kwa kiasi kikubwa amesaidia kuoko maisha yetu. Asante sana mama”, Kanali Emilly alieleza huku akimshika mkono.
“Hakika, bila Mama Feka pengine taarifa za habari za ndani na nje ya nchi wakati huu zingekuwa zinasimulia habari nyingine kabisa”, Julius Nyawaminza alieleza.
“True. Unachosema ni kweli kabisa”, Claud alirukia.
“Mimi sikutegemea kama mama huyu ataimudu kazi niliyomuomba atusaidie, lakini nilitokwa na hofu aliponidokeza kuwa alipitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa Operesheni Ushindi. Kweli anastahiri kuitwa mshindi”, nilieleza.
“Anastahiri kabisa”, alieleza Kanali Emilly, halafu akaendelea kwa msisitizo. “WAPIGANAJI. Naomba mnisikilize kwa makini sana. Teacher, Julius, Claud, Peter, Mama Feka kama ambavyo Teacher anakuita na Fred ambaye simuoni hapa, Teacher unazo taarifa zozote kuhusu Fred?.” aliuliza kabla ya kuendelea.
“Naam, tunawasiliana, hatuwezi kuwa hapa wote kama wajinga, amenijulisha kuwa yuko pamoja nasi hapahapa karibu kabisa anaangalia usalama wetu, tuko salama bosi”, nilimwambia.
“Oh, vizuri sana. Hii ni mesheni ya aina yake, tujitahidi kwa njia yoyote wahalifu hawa wakamatwe na ushahidi, tusifanye makosa kabisa, sheria za nchi hii zinataka mtu akutwe na ushahidi, ili tushinde vita hii lazima adui akamatwe na kielelezo, yaani hayo madawa ya kulevya yapatikane, vingine tutakuwa tumefanya kazi bure, tutawafikisha mahakamani bila kielelezo?”, Kanali Emilly alihoji baada ya kushauri.
“Tutajitahidi kufanya hivyo. Lakini Afande, kazi kubwa imefanywa na mama huyu shemeji yangu, leo tunaingia vitani wakati yeye hana kumbukumbu za aina yoyote katika kumsaidia endapo itatokea bahati mbaya. Mkuu vita si lelemama, lolote laweza kumpata na muda huu hakuna nafasi tena. Naomba Mama Feka aingizwe katika kumbukumbu zako”, nilimshauri Kanali Emilly akatingisha kichwa kukubaliana na mawazo yangu.
“Hilo halina tatizo kabisa Teacher, kama ulivyotangulia kusema vita si lelemama, tuombe Mungu awasaidie kwa mapenzi yake naamini mtarudi salama, nitafurahi sana kuwaona. Viongozi wote wa serikali wako pamoja nanyi, niwahakikishie tuko pamoja nanyi, niwatakie kila la heri wote”. “Amina”, tulijibu kwa pamoja.
“Naomba muwe makini na waangalifu sana, Mama Feka?” Kanali Emilly aliita.
“Naam baba”.
“Nimeambiwa wewe ndiye unalifahamu vizuri eneo walilopanga kwa ajili ya kutoroka, saidia tafadhali, msiwape nafasi hata kidogo. Kwa vile muda unakwenda sana sasa niwaache mjipange. Mheshimiwa Rais ameahidi kutoa zawadi nono kwenu”.
“Ni kweli baba, mimi si mwenyeji sana katika Jiji hili, hata hivyo nitajitahidi kuwapeleka. Bahati nzuri ni kwamba huyu mzungu Carlos ananiamini sana, niko kwenye orodha ya wanaosafiri. Naweza hata kuwachelewesha ili tufanikiwe”, alisema.
“Tutajitahidi huku tukimuomba Mungu”, nilisema kwa niaba ya wenzangu wote. Kanali Emilly akasimama baada ya kutushika mikono, akaondoka.
Nilitumia nafasi hiyo kuwajenga vijana wangu kisaikolojia. Baada ya kujiweka vizuri tukajigawa katika makundi mawili tofauti, Peter kama ilivyo ada alianza kuondoka na Mama Feka, akawachukua na vijana wetu kutoka Lugalo, wakaondoka kuelekea eneo la Kunduchi Beach. Mimi Claud Mwita na Julius Nyawaminza tukampitia Fred, tukaanza tukaelekea Barabara ya Ali Hassan Mwinyi.
Baada ya kufanikiwa kuuruka mtego wa kukamatwa na vijana shupavu wa Peter Twite pale karakana ya Reli ya Tazara, Carlos Dimera na kundi lake walikimbia na kufanya harakati za kuihama Dar es Salaam. Wakijua mambo sasa yametibuka.
Haraka, Carlos aliwasiliana na Emilio Pablo, kiongozi wa vikundi vya wasambazaji wa dawa za kulevya duniani, bila kupepesa maneno Carlos alimfahamisha kigogo huyo kuwa hali ya hewa ya Dar es Salaam, imegeuka. Akaeleza jinsi walivyopata ushindani kutoka kwa vijana ambao mpaka sasa hawajafahamika.
“Huo ni uzembe wako Carlos, sharti letu unapomkamata adui yako hana budi kuishi hata kwa sekunde moja, maneno gani umefanya. Ok, sasa unahitaji msaada gani zaidi?”, Emilio alihoji.
“Kama nilivyojulisha awali, vijana walifanikiwa kuiba shehena yote ya dawa iliyokuwa imekamatwa na kupelekwa kwa mkemia, mzigo uko salama na sasa tuko katika maandalizi ya kuondoka Dar es Salaam leo mchana kwa boti kubwa sana ambayo tayari iko ufukweni mwa bahari ikisubiri safari.
“Safi, niwapongeze hao vijana kwa kufanikiwa kuufikisha mzigo ndani ya boti salama, lakini unawapeleka wapi, huo ni mzigo kwetu, una hakika mzigo uko salama?’.
“Naam bosi, hilo halina shaka, mzigo uko salama kabisa. kuhusu hao maisha yao yatakoma baada ya kuondoka, Tunaondoka Dar es Salaam mchana tukabiliwa na changamoto moja, Tunaelekea wapi baada ya Dar es Salaam?”. Carlos alihoji. Baada ya kuelezana hili na lile, alikata simu.
Madawa mbali mbali ya kulevya, vifaa kadhaa vya kutengeneza noti bandia, silaha na dhana nyingine zilihamishwa na kuhifadhiwa ndani ya boti kubwa iendayo kasi sana. Boti hii iliyoandaliwa kwa ajili ya safari, kuelekea mahali kusikojulikana. Carlos mwenyewe alipanga kwenda ama Stontown ya Unguja, Visiwani Zanzibar ama Malindi ya Mombasa, nchini Kenya. Lakini pia alijiuliza Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, itakuwaje.
Hakuwa tayari kuwaacha vijana wake, lakini agizo la Pablo Emilio ni lazima wateketee, alionekana kuwathamini, kuanzia wasambaza dawa za kulevya na kundi la watakatishaji wa noti bandia. Ukweli ni kwamba aliagizwa na wakubwa kuwatosa katikati ya bahari na kutokomea kabisa.
“Tumefanya makosa makubwa kuruhusu hali hii. Kutoroka kwa Teacher na wenzake ni changammoto kubwa kwetu, niseme kuwa kazi kubwa iko mbele yetu, nani kati yetu amewahi kumuona nyati aliyejeruhiwa?” Carlos alihoji.
“Ni hatari, nyati anapojeruhiwa haangalii Simba wala Chui, usicheze kabisa na Nyati aliyejeruhiwa, anatwanga kila kilicho mbele yake, miti, mawe”, Jakina alieleza.
“Sasa hiyo ndiyo changamoto iliyo mbele yetu. Nyati aliyejeruhiwa ni hatari zaidi ya Chui, ndiyo maana nimeamua tuhame Dar es Salaam kwa muda, upepo mbaya ukipita tutarudi, sawa jamani”, Carlos alieleza.
“Sawa bosi, kama tunaihama Dar es Salaam, tunakwenda wapi?” Hawa Msimbazi alihoji.
“Tunakwenda kuanzisha makazi mapya na maisha mapya kwa muda. Kuhama sehemu moja kwenda sehemu nyingine ni jambo la kawaida. Ndiyo maana nikasema tunaanzisha makazi mapya na maisha mapya, nawaahidi kuishi maisha mazuri zaidi huko. Kama nilivyosema huu ni upepo, ukipita tutarejea”, Carlos alieleza.
“Tuko pamoja nawe bosi Carlos, kila neno lako kwetu ni sheria. hiki ni kikosi chenye nguvu kubwa zaidi ya vikosi vya jeshi. Hata majeshi ya Marekani huhamisha kambi, kama ni silaha tunazo za kisasa na kila aina”. alisema Jakina kwa kujiamini.
Carlos akainua simu yake ya mkononi. “Hallo Sweety wangu, uko wapi baby?. Wakati wa safari umewadia”, Carlos aliuliza.
“Oh baby, bado niko saloon baby wangu, natengeneza nywele, si umesema tunaihama Dar es Salaam leo?. Nipendeze kwanza”, Sweety alijibu kwa sauti ya nyepesi ya mahaba.
“Tumebakiwa na nusu saa tu kuihama Dar es Salaam, mwambie huyo msusi aongeze bidii, usiniangushe Sweety wangu”. Carlos aliagiza.
“Nimemwambia ajitahidi baby”.
“Uko pande zipi?”
“Maeneo ya Riverside saloon ya rafiki yangu”.
“Ok, sasa nisikilize Sweety wangu, ukimaliza tafuta taksi, mwambie dereva akulete Kunduchi Beach Hoteli, ukifika hapo nijulishe nitakupa maelekezo, usiingie ndani ya hoteli”.
“Asante baby, nitajitahidi kuwahi”.
“Ok”, akamaliza.
*************************
Ilikuwa saa nane na dakika ishirini hivi nilipoegesha gari kwenye maegesho ya kituo cha mafuta cha GAPCO kando ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi huku tukiangalia barabara iendayo nyumbani kwa Carlos Dimera, Peter na Mama Feka walikuwa wametudokeza kuwa Carlos alikuwa akifanya maandalizi mwisho kwa ajili ya kutoroka. Tulisubiri waanze safari hapo saa nane na nusu kama tulivyoelezwa. Gari la Carlos aina ya BMW nyeusi lilikuwa nje kabisa ya geti na kutufanya tuamini kuwa yupo.
Magari kwenye barabara hii yalikuwa mengi kiasi. Kwenye kituo cha Mafuta cha GAPCO, niliegesha gari sehemu ambayo tuliweza kuona vizuri mwanzo na mwisho mwa barabara hii.
Ilipofika saa sane na nusu kamili, lango la nyumba hiyo lifunguliwa, gari moja ndogo rangi nyekundu Pick Up aina ya Isuzu Deep ilitoka ndani taratibu na kuegeshwa mbele ya gari lililokuwa nje. Jakina alikuwa wa kwanza kutoka ndani akiwa amevalia suti nyeusi. Roho yangu ilianza kuingiwa na hofu, nikajua mapambano na vibaraka hawa yameanza. Dakika chache zikapita, Carlos naye akiwa amevalia suti ya aina kama ile alitoka, wote wawili waliingia ndani ya gari iliyokuwa nje. Jakina aliingia upande wa dereva. Carlos akakaa kwenye viti vya nyuma.
Niliinua simu yangu ya mkononi kuwasiliana na Kanali Emilly, “Kamanda, ndiyo tunaelekea kwenye uwanja wa mapambano, uwe tayari tukikuhitaji ufike kwa wakati, ukituona tena ujuwe tumerudi na ushindi, usipotuone basi, ujuwe makubwa yametupata”.
“”Nimeacha kazi zote kwa ajili ya jambo hili, Teacher kama nilivyosema tulipokutana, Mungu yuko upande wetu, unajua kwa nini?. Kwa sababu tunapigania haki ya wengi”. Kanali Emilly alieleza, kabla hajaendelea nikakata simu.
Magari haya mawili yaliondoka taratibu, gari la mbele lilipokuwa hatua chache kabla ya kufika kwenye barabara kubwa ya Ali Hassan Mwinyi lilisimama na kulifanya gari la nyuma pia kusimama. Vijana wawili walioshiba sawa sawa walishuka juu ya miti wakaingia ndani ya gari la mbele safari ikaanza.
Watu waliokuwa eneo hilo walishangazwa na tukio hilo, lakini sisi tulijua hiyo ni mojawapo ya kazi za majasusi. Tulisubiri mpaka wafike kwenye makutano ya Ali Hassan Mwinyi ama Old Bagamoyo na Kawawa, tukaanza kuwafuata kwa nyuma. Unapowafuata watu wa aina hii lazima ujipange sawasawa, vinginevyo itakula kwako. Tuliwafuata kwa siri, walipofika kwenye taa za usalama barabarani za Morocco walichepuka na kuingia barabara iendayo Kawe.
Mchana huu magari yalikuwa mengi kwenye barabara hii, kiasi kwamba haikuwa rahisi mtu kubaini kama anafuatwa. Baada ya mwendo wa kilomita nne ama tano hivi wakaufikia mzunguko unaogawa barabara zinachepuka moja kwenda Kawe na ile ya Mbezi Beach, gari lao lilipunguza mwendo sana, nadhani walifanya hivi kwa kusudi maalum. Walipovuka kwenye mzunguko huu mbele kidogo walisimama. Mtu mmoja aliibuka akitokea kwenye uchochoro, akazungumza na Carlos. Mimi niliwapita kama siwajui nikasimama mbele ya mtu anayeuza mamatunda kwenye baiskeli. Dakika chache baadaye magari hayo yalitupita tukasubiri kidogo halafu tukaanza kuyafuatana tena. Tuliendelea kuwafuata kwa makini hadi walipofika kwenye mzunguko mwingine unaogawa barabara tatu, iendayo White Sends Hoteli na Africana. Magari bado yalikuwa mengi kwenye barabara hii, wakati huo mimi nilikuwa nikiendesha gari ndogo aina ya Golf VW Combi iliyoonekana kuchoka kidogo, waliiacha barabara ya kulia inayokwenda White Sends hoteli, wakaifuata inayokwenda Afrikana.
Tuliendelea kuyafuata magari haya kwa umakini wa hali ya juu sana, walipofika njia panda ya Africana waliingia kulia, wakaendelea na barabara ya Tegeta. Tuliendelea kuwafuata hivyo hivyo. Walipofika kwenye makutano ya barabara iendayo Kunduchi, Salasala na Tegeta, eneo la Mtongani, walipunguza mwendo halafu yakachepuka na kuingia tena barabara ya kulia, nami pia nikaingia kwenye barabara hiyo. Baada ya mwendo wa dakika chache, dereva wa gari la mbele alionyesha ishala ya taa kuwa wanaingia kulia.
“Sasa nimeelewa, wanakwenda Kunduchi Beach hawa. hakuna sababu ya kuwafuata tena”, niliwajulisha wenzangu ambao waliokuwa kimya wakijitafakari. Halafu nikawasiliana na Twite. “Mko wapi Peter na vipi hali ya usalama huko?”.
“Mipango inakwenda vizuri bosi, kama tulivyokujulisha Carlos amepiga simu kwa mara nyingine akimwambia Mama Feka ajitahidi kuwahi ili safari yao ianze, sisi tuko sehemu tunasubiri mjipange kwanza, halafu Mama Feka anachukua taksi kama alivyoelekezwa na Carlos, bahati nzuri ni kwamba eneo hilo nalifahamu kiasi, ukiiacha Kunduchi Beach Hoteli, mbele kidogo kuna wafanyabiashara wa samaki wengi sana”, Twite alinijulisha.
“Mwambie Mama Feka avae ile fulana ya bletprof niliyompa, wakati wowote kazi inaanza, mwambie karibu tunaingia kwenye hatari kubwa zaidi, kuna magari mawili yanaelekea hapo, sisi sasa tunasubiri taarifa kutoka kwako”.
“Taarifa kama nilivyokudokeza kuwa eneo hilo kuna wavuvi, vijana wetu Wilson na Edger tayari wako huko kama wachuuzi wa samaki, wanasema ulinzi ni mkali sana kila gari ama mtu anayeelekea huko anachunguzwa, bahati nzuri leo wageni wengi wanaokwenda Kunduchi Beach Hoteli, Wilson anasema mnaweza kuegesha gari kwenye maegesho ya hoteli halafu mkajua cha kufanya.”
“Umesomeka Peter,” nilisema halafu nikawageukia wenzangu, “Jamani, Peter anasema Wilson na Edger wako kwenye pointi. Vijana hawa wanasema ulinzi ni mkali sana eneo hilo, Sisi tutaingia Kunduchi Beach Hoteli, halafu tutatafuta njia zandani kwa ndani, hata ikibidi kuvunja milango na madirisha vita si mchezo”, niliwajulisha wenzangu.
“Iwe isiwe, leo lazima kieleweke, Teacher tusiwape nafasi tena watu hawa ama zao ama zetu”, Claud alisema.
“Nina usongo na watu hawa, walivyotutesa pale Karakana ya Tazara, ole wao waingie kwenye anga zetu”, Nyawaminza nae alisema.
“Sikilizeni, tunakwenda kuuza roho zetu, lolote laweza kutokea, lazima tujipange sawasawa kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri. Fred utabaki sehemu hii kama akiba yetu, ukiona kimya utajua cha kufanya, pia wasiliana na Kanali Emilly, mwambie asogee eneo hili. Nyingi wengine twendeni kwenye uwanja wa vita”, niliagiza.
“Tuko pamoja”, Fred alisema.
Baada ya kujipanga vizuri, tulikubaliana na wenzangu kuwa tuliache gari letu kwenye maegesho ya magari ya Chuo cha Maofisa wa jeshi pale Kunduchi, tulikubaliana nianze kuondoka, ili wao wafuate. nilitafuta taksi iliyoniacha Kubnduchi Hoteli. Mkoba wangu mdogo uliosheheni vifaa vyangu muhimu vya kazi ukiwa begani nilitembea taratibu nikitafuta sehemu ya vyoo vya upande wa mashariki, nilipovipata niliingia na kujimwagia maji kiasi, halafu nikafumua sehemu ndogo ya juu ya paa nikapanda na kuangalia eneo lote la bahari.
Hali ya eneo hili ilikuwa tulivu kabisa, kwa mbali ndani ya bahari kulikuwa na meli kubwa na ndogo zimeegeshwa katikati ya bahari, bila shaka zinazosubiri kushusha mizigo bandarini, baada ya kujuiridhisha kuwa hali ni salama nilipenya kwenye tundu hili na kushuka upande wa pili kwa tahadhali kubwa. Claud na Nyawaminza nao wakitumia njia hiyo, wote watatu tukafanikiwa kuruka kiunzi hiki salama.
Ndani ya dakika kumi, tayari tulikuwa tumelizunguka eneo lote la bahari. Boti iendayo kasi ilikuwa imeegeshwa ufukweni ikisubiri kuondoka, ilikuwa boti kubwa ya injini mbili, yele magari na mengine kadhaa yalikuwa yameegeshwa kwa mbali kidogo na boti, “Mwambie Mama Feka anaweza kuja sasa”, nilimwambia Peter.
“Kuko salama?”.
“Ndiyo maana nikasema anaweza kuja”, nilimwambia.
“Nafikiri wote tumeona ulinzi ulivyo. Kitu ninachotaka ni kufanya mashambulizi kimya kwanza mpaka tutakapolazimika kuwashambuliwa walioko ndani ya boti. Walinzi sita wanaonekana upande huu. Mimi nitapita kushoto, Nyinyi mtashambulia upande wa kulia. Nawatakia heri”. Tulipeana mikono kimya kimya kwani hatukujua nini kitatokea. Mimi nilikuwa wa kwanza kujitokeza kwenye kimsitu nikabana kama hatua tatu hivi kulikuwa na mlinzi anavuta sigara, mikononi ameshika bunduki kubwa aina ya AKA 47 huku akiangalia kwenye magari. Sikuona sababu ya kutoa silaha, nilimsogelea kimya kimya nikitembelea tumbo. Nilipokuwa karibu kabisa niliibukia na kuziba midomo, akataka kupiga kelele lakini mimi nilikuwa mwepesi zaidi nikazima kelele zake kwa kumnyonga.
Tulikuwa tumekwenda haraka sana, Claud alinyoosha mkono wake wa kulia na kunionyesha ishala kuwa hali ilikuwa shwari. wao walipita wakajibanza kwenye mapango ya mawe ya bahari, mimi nikaendelea kutumia miti kuwasogelea tukiona kila kinachotendeka.
Mlinzi mwingine alikuwa hatua kumi hivi lakini hakujua nini kimetokea. Kwa vile nilikuwa nimevaa mavazi ya mtu niliyemuua mwanzo alifikiri mimi ni mwenzao hivyo nilimfuata nikiangalia chini kama mmoja wao mpaka nilipomfikia.
“Vipi kuna wasiwasi wote?”, nilimwuliza.
Aliinua kichwa.
“Hakuna…..”
Kabla hajamaliza nilimkata karate ya katikati ya kichwa akafa palepale. Nilimwegemeza vizuri kwenye mti nikamwacha kama mtu aliyekaa hai. Claud na Nyawaminza nao walikuwa wamekwenda kasi wakiwa wameua walinzi kadhaa.
Tulikuwa tumefanikiwa kuizingira boti hii kutoka kila upande. Mara nikamuona Mama Feka anawasili katika eneo hili, akitembea taratibu kuelekea kwenye boti. Kama ilivyo kawaida Jakina alitoka ndani ya boti ili kumpokea.
Karibu yangu niliweza kuaona walinzi wawili wakilanda huku na huku, nikaanza kuwanyatia. Kabla sijawafikia nilisikia mlio wa risasi upande wa akina Nyawaminza. Nikajua mambo yametibuka. Nami nikainua bunduki AK 47 niliyoichukua kwao na kuanza kuwateketeza walinzi waliokuwa karibu yangu. Kwa kuwa vita vilikuwa vimeanza rasmi nilikimbia nikirusha risasi bila mpangilio.
Hali ya hewa katika eneo hili ilikuwa imechafuka, kumbe kulikuwa na askari wengi ufukweni, sijui hata walitokea wapi tukaanza kupambana, milio ya risasi iliendelea kusikika. Hali hii ilimfanya Mama Feka akimbie kurudi upande wa magari.
Tuliendelea kupambana na watu hawa kishujaa. Mara nikaona askari wawili wakianguka kutoka juu ya miti, bunduki zao zikiwa mikononi. Kumbe walikusudia kunirushia risasi, wakati wanajiandaa kufanya hivyo Claud, alikwisha kuwaona hivyo akawaua kabla hawajanimaliza.
Nilisikia injini za boti zikiwashwa, nikajuwa wanataka kuondoka, nikamfanyia ishara Claud akaiona na yeye akanifanyia ishara ya kuonyesha kuwa Nyawaminza alikuwa chini ya maji anajaribu kuingia ndani boti. Kuona hivyo nilimfanyia ishara kuwa na mimi nakwenda ndani ya boti hivyo atuchunge wote. Tulikuwa tumeuwa idadi kubwa ya askari waliokuwa wamebaki ni wachache tu.
Niliruka chini huku nikiachia risasi ovyo nikafika kwenye boti. Nilikajitupa kwenye mlango na kujiviringisha mpaka ndani, kama umeme nikarukia na kumpiga risasi nahodha wa boti hii aliyekwa kwenye injini akaanguka ndani ya maji. Huko nje nilisikia bado Claud anaendelea kumimina risasi ili kuwazuia walioko ndani wasitoke nje.
Nilipoinuka niliona kama wamebaki kumi tu ndani; wengine wote tulikuwa tumewateketeza. Nilimwona Nyawaminza nae anaviringisha na kuingia ndani. Wale watu walimwona na kabla hawajapiga risasi niliwahi wawili, wengine wote wakarudi kujificha nyuma.
Nyawaminza aliruka mpaka nilipokuwa.
“Asante bosi umeniponya”,
“Usinishukru ndio sababu tuko wote. Kwanza kazi uliyoifanya wewe na Claud sikuitegemea. Kazi imekuwa rahis kabisa”.
“Kuna watu kama wangapi humu ndani?”.
“Hawazidi kumi, na wote wako upande huu wamejificha. Nafikiri wanamlinda Carlos Dimera”.
Huko nje kulikuwa kimya; Tukajua Claud anasubiri sasa kashi kashi kutoka kwetu.
“Sikiliza Nyawaminza, lazima tuwafanyie ujanja ili tuwapunguze. Mimi nitasimama juu ili niwadanganye. Walivyo wajinga watainuka ili wanipige risasi. Mimi nikiita jina kaa tayari na silaha yako kisha anza kumimina risasi. Mimi nitaruka kitambo, hivyo utawapata kama mchezo. usiogope”. Niliinuka kama umeme nikawaona wote mara moja.
Nikaita
“Carlos Dimera?”.
Hapo hapo kama umeme nikaruka nyuma ya upande mwingine. Walinzi wanne wainuka ili kunitupia risasi huku wakiwa wamejitokeza hadi vifua. Nyawaminza aliwamiminia risasi na kuwashindilia wote risasi katikati ya vifua vyao wakafa pale pale. Nilimwonyesha ya vidole kuwa wamebaki watatu, kwani nilipokuwa nimeruka niliona wako saba.
“Teacher, nilisikia sauti ya Carlos anaita.
“Unasemaje?”, nilimwuliza.
“Naomba tuzungumze”.
“Kuhusu nini tena Carlos, lazima ujuwe kuwa Tanzania haiko tayari kuchezewa, biashara ya dawa za kulevya peleka huko kwenu kusiko na maadili mema katika jamii, watu wanavaa nguo fupi, wanaume wanaoana, hizo imani zibaki kwenu”, nilimwambia.
“Tafadhali tuzungumze?”, aliomba kwa mara nyingine.
“Umechelewa sana Carlos, maana umeigharimu nchi hii, hivyo tutakupeleka mbele ya vyombo vya sheria ndivyo vitakavyo kuhukumu, umeua ndugu zetu wengi, umesababisha vijana wetu kujiingiza katika matumizi ya dawa haramu za kulevya, hufai kuonewa huruma”.
“Huwezi kunichukua hapa nikiwa hai”.
Kumbe wakati huu tunajibishana Mzee wa Mtemba naye na askari wao mwingine nao walikuwa wamejivuta karibu kabisa na mimi. Ghafla nikahisi kuna kitu karibu nami.
“Teacher”, Nyawaminza aliita ambaye pia alikuwa amewaona.
Kusikia tu hivyo, niliruka pale nilipokuwa na wakati huo nikawaona Mzee wa Mtemba na yule kijana mwingine karibu kabisa na mimi wameinua bastola tayari kufyatua. Nilijiviringisha hewani namna ambayo hata wao walishangaa risasi zao zote zikanikosa, wakati ule ule nikaachia za kwangu nikawapata wote nao wakaanguka chini.
Carlos aliinuka akasimama juu, akachukua bastola akataka kujipiga risasi. Bunduki tatu zililia kwa wakati mmoja na kuupiga mkono wake. Kumbe Claud nae alikuwa amefika mlangoni na kuona kitendo alichotaka kukifanya akakizuia. Nyawaminza nae aliona akazuia wakati na mimi niliona nikazuia asijipige risasi.
“Bado tunakutaka ukiwa hai ili ukajibu maswali ya watanzania”, nilimwambia huku bado anashangaa jinsi risasi tatu zikitoka pande tofauti zilivyoweza kupiga kiganja chake tu.
Mara tunasikia kelele za milio ya magari ya polisi.
“Kanali Emilly yuko njiani”, niliwaambia wenzangu ambao sasa tulikuwa tumemzunguka Carlos.
Baada ya mapigano makali yaliyodumu kwa saa kadhaa, tukibishana kwa risasi na watu hawa, hatmaye tulifanikiwa kuiteka boti hii, Carlos Dimera, Hawa Msimbazi, Jakina, Mzee wa Mtemba na baadhi ya masalia ya askari wao walijisalimisha mbele yetu.
Mama Feka alikuja na kunikumbatia, “Hongera sana Teacher, kazi yenu mliyonituma nimeimaliza”, alisema huku akinibusu na kujiegemeza kwenye kifua changu, nikambusu pia. carlos Dimera na wenzake wakabaki wameduwaa.
“Mnamfahamu malkia huyu, anaitwa Sweety, bila huyu kazi ya kuwakamata ingekuwa ngumu, asante sana Mama Feka”, nilisema.
Kanali Emilly alifika akiwa na baadhi ya viongozi wa ngazi za juu Serikalini, Mawaziri wa Ulinzi na Mambo ya Ndani, pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara hizo. Kanali Emilly alitushika mikono na kutuangalia sehemu mbali mbali za miili yetu kama tumepatwa na majeraha. Tulikuwa salama kabisa.
“Wakuu, boti hiyo imebeba vifaa vyote vya hujuma, kuanzia dawa za kulevya, vifaa vilivyotumika kutengeneza noti bandia na baadhi ya silaha za vita ambazo hatujui ziliingiaje hapa nchini”, nilieleza kwa uchungu. Baada ya taratibu zote kufanyika, askari kutoka idara zote tuliwaacha wazee waendelee na mambo yao sisi tukaondoka kishujaa.
Chau cafe Amata Ga Imba aliendelea kunywa kahawa yake polepole kana kwamba hana shughuli nyingine ya kufanya kwa siku hiyo, kichwani akiwa na mawazo mengi sana akipanga na kupangua juu ya maisha yake ya sasa na baadae, alipotahamaki hata kashata alizokuwa akila zilikwisha moyoni akajiuliza kama aliagiza kashata au ameshazila zimekwisha! Hilo nalo likawa jambo jingine ambalo lilikosa jibu kabisa. “Chausiku!!” aliita kwa nguvu kana kwamba aliyekuwa anamuita alikuwa umbali wa kilomita kadhaa lakini kumbe wote walikuwa hapo jirani tu. Watu walishtuka kwa sauti hiyo hata wengine walidiriki kumtupia maneno yasiyostahili “Samahani waheshimiwa!” aliomba msamaha. “Samahani nini mjinga wewe!” mmoja alitamka kwa hasira “Wengine tuna BP utatuuwa bure sura ka Sokwe!” mwingine aliongeza Amata aliumia sana moyoni kwa tukio lile, akainamia mezani, akatikisa kichwa kisha akasimama kwa hasira na kuelekea eneo la kunawia mikono, akajitazama kwenye kioo, akatabasamu, kisha akageuka na kurudi alipoketi kwanza. Kabla hajaketi alisikia sauti nyuma yake, “Umejiona ee? Ka sokwe, tena wa Gombe!” mmoja alimkejeli, wengine wakaangua kicheko cha dharau na kupiga miluzi. Hasira za dharula zikamrudia Amata, akageuka na kuelekea upande ambao sauti ile imesikika “Nani aliyesema vile?” aliuliza kwa kung’aka, wakacheka tena “Ukimuona utamfanya nini? Fala wewe mtoto wa porini!!” mwingine alisema na wengine wakaangua kicheko. Amata alipiga hatua mbili mbele na kumkunja shati yule aliyesema maneno hayo akamuinua kwa nguvu akamrusha chini, huyo akaanguka chini mzimamzima kama gunia, jamaa akanyanyuka kwa hasira na kumvamia Amata, Amata akamdaka na kupiga vichwa vitatu vya nguvu akamsukuma kidogo na kumrushia makonde kama mvua, kijana yule alichanganyikiwa hata hakuweza kujibu mashambulizi alianguka chini mara ya pili. “Ameua! Ameua! Ameua!” kelele za watu zilijaza mgahawa ule mara watu wakajaa wanataka kumshika Amata. Yule kijana bado alikuwa chini hajitambui kwa kipondo cha ghafla alichokipata. Amata aliruka kutoka aliposimama akatua juu ya meza na kutaka kutoroka kwa kupitia dirishani, watu walimgombania kwa kumshika shatia wengine suruali, masikini Amata shati lake lilichanika vibaya akabaki na fulana ya ndani na kuwaachia shati wananchi wenye hasira, aliruka kupitia dirisha la mgahawa huo na kudondokea kwenye lundo la mawe kwa kutanguliza mkono, alihisi maumivu makali ya mkono lakini alipogeuka aliona watu wale wanakuja pale alipo, akanyanyuka na kutimua mbio “Huyo huyo! Kamata muuaji huyo!!” kelele za wananchi wale zilikuwa kama kichocheo kwa kijana Amata kuongeza spidi. Mara kwa mbele aligongana na pande la mtu na kuangushwa mbali, alinyanyuka na kuanza kukimbia tena, watu walitoka majumbani na kumuunganishia kama kawaida ya wananchi. Mbio ziliendelea na wananchi nao hawakuchoka, alitokea kwenye wigo wa nyumba la! Hapakuwa na njia aliruka na kupanda ukuta kisha akatokea upande wapili na kupanda tena alitua chini kwa miguu yake mikakamavu na kutimua mbio lakini la haula! Alipokuwa akijaribu kuvuka kichaka kidogo katika eneo hilo alijikwaa vibaya na kuanguka chini, mchezo umekwisha. Watu wakamkamata na kuanza kumpiga hata kumuumiza vibaya, Mungu si Athumani polisi waliwahi kumuokoa kutoka kwenye mikono ya watu wenye hasira. “Tuachie huyo tummalize! Muuaji huyo!” watu walipiga kelele na wengine bado walidiriki kurusha hata mawe ambayo baadhi yaliwapata askari wale. Askari mmoja akafyatua risasi hewani na watu wale wakatawanyika kwa woga wakikimbia uku na huku wengine wakianguka na kukanyagana vibaya. Amata alichukuliwa mpaka kituo kidogo cha polisi akiwa hatamaniki kwa jinsi alivyolowa damu hata fulana yake aliyobaki nayo baada ya kuwaachia shati watu wale haikujulikana kama ni nyeupe au nyekundu, juu ya jicho lake la kushoto jeraha kubwa lilikuwa bado linavuja damu, mkono wake umevimba, kucha ya kidole gumba cha mguu wa kushoto haikujulikana hata imeng’okea wapi. Askari wale walimpiga Tanganyika jeki bila huruma wala kujali kuwa mwenzao ameumia namna ile wallimkokota tena na makofi juu mpaka kituo kidogo cha polisi na kumlundika selo.
Ndani ya chumba kidogo cha selo katika kituo cha polisi cha kijiji wahalifu walijazana mpaka hewa haikutosha kabisa, walichoka na hata wengine kukosa nguvu, kupoteza fahamu kwa kukosa hewa ya kutosha. Amata aliingia kwenye selo hiyo katika hali ile aliyokuwanayo, akakaribishwa na joto na harufu mbaya haja kubwa na ndogo zilizochanganyika, mwanga hafifu uliopita katika kadirisha kadogo kenye ukubwa wa mlango wa banda la njiwa ndio pekee kalikokuwa kanatoa faraja kwa binadamu hawa waliokuwa na makazi ya muda ndani ya chumba hiki, wote walikuwa na sura za kutisha ambazo bila kuuliza utajua kuwa sasa nimeingia kuzimu Ucku huo ulikuwa mrefu sana kwa Amata, mawazo mengi yalitawala kichwa chake, maumivu makali yaliusumbua mwili wake, alijituliza kimya kwenye moja ya kona za kijichumba hiko huku akisikia kichefuchefu kama mama mjamzito kila mara alitamani kutema mate lakini atatemea wapi watu wamejazana hata wengine wamekaa kwa kupakatana mh! Mawazo yaliendelea kumsonga hata usingizi mwepesi uliokatishwakatishwa kwa nyimbo za kuchukiza za mbu masikioni mwake ulikuja na kuondoka, aliwaza jinsi anavyoishi kwa shida hana baba hana mama, kula yake ya wasiwasi aliona jamii yote haimtaki, dunia imemchukia, ulimwengu unampa adhabu, “Kwa nini mimi?” alijiuliza uliza moyoni mara kwa mara hata alipokuwa kwenye kibanda chake huko shambani kwao ambako alipitisha maisha yake ya ujana tangu wazazi wake walipofariki yeye akiwa na umri wa miaka kumi na tano, mama yake alikufa kwa kuliwa na simba na baba yake alikufa akiwa anamuokoa mama yake dhidi ya simba hao wenye njaa na uchu wa nyama ya binadamu. Kila aliporudiwa na picha hii alilia sana na kujiona kuwa yeye ni binadamu mwenye mkosi, akuwahi kuwa na kaka wala dada isipokuwa ndugu tu ambao pia hawakuwa na msaada nae kabisa. “Amata!!!” aligutushwa na sauti kali ya askari iliyotokea kwenye kadirisha ka mlango wa selo hiyo. “Afande!” aliitikia kwa uchovu na kujaribu kujiinua kutoa alipokuwepo lakini alijikuta anapata kizunguzungu na kuwaangukia wenzake waliokuwa hapo. Alifika mlangoni pale kwa shida mbele yake alimuona msichana mrembo sana kasimama, mrefu wa wastani maji ya kunde, alivalia vizuri suruali yake ya kitambaa nyeusi na blauzi yake nyeupe huku shingoni kafunga skafu yenye mchanganyiko wa rangi, nywele zake fupi zilizokatwa kiumahili na vinyozi wanaojua kazi yao, kiatu chake kirefu kilimfanya aonekane kuwa ni mrembo anayetunzwa na pedeshee fulani. Dada yule alijivuta taratibu mpaka kwenye dirisha lile. Amata alipokea pumzi safi iliyonukia na kuvutia kutoka kwa mrembo huyo, hakuamini anachokiona ni malaika au binadamu, aliduwaa, akapigwa na bumbuwazi, mikono yake ikiwa imeshika nondo mbili zenye kutu alijikuta anaishiwa nguvu. Mrembo yule alishika nondo zile kwa kubana mikono ya Amata akaiangalia sura ya Amata iliyochoka na kukaukiwa na damu.. “Saringo! Naitwa Saringo” alimwambia Amata kwa sauti ya chini “Hunijui, ila utanijua punde tu” aliendelea “Haujaua ila umeumiza vibaya, sasa unastahili zawadi kwa kazi uliyoifanya bila kujua, na zawadi hiyo utaipata ukimaliza kazi yako” Saringo alishusha pumzi na kumwangalia Amata usoni na kumuona jinsi alivyochanganyikiwa, akaendelea kumwambia mashairi yake yasiyoeleweka kwa mtu mwenye akili timamu, sasa kwa kukunja sura akamwambia Amata “ Lazima ufungwe, uishie jela!” akageuka nakuondoka zake. Amata akazidi kulowa jasho, maswali yasiyo na majibu yalimzunguka tena ‘nilijua malaika mwema kaja kuniokoa kumbe malaika mbaya wa mauti kanitembelea’ alijiwazia na kuanza kulia. Amata hakupata jibu mwanamke yule ni nani, na anataka nini, utata. Asubuhi ile kalandinga liliwachukua mpaka mahakama ya kijiji, jalada la Amata lilikuwa la tatu kuitwa, taratibu akiwa na pingu mikononi aliingizwa katika chumba cha hakimu na kusomewa mashitaka ya kudhuru mwili, alijikuta hana cha kukana isipokuwa kukubali, kesi ikahairishwa mpaka baada ya siku kumi na nne. Walipokuwa wanarudi kwenye kalandinga alimuona binti yuleyule akiwa amesimama katika kundi la watu waliokuja mahakamani hapo, muonekano wake ulikuwa tofauti na wote pale kwani ndiye aliyevaa nadhifu kuliko wote ‘huyu ni nani?’ Amata alijiuliza hakupata jibu, moyoni alimlaani kuliko anavyomlaani shetani walipogongana macho Amata alitema mate chini na kumuonesha kidole cha kati. Mara alijikuta anatandikwa kofi la kisogoni au vijana huita‘mbata’ “Panda juu unatuchelewesha!” sauti kali ya askari ilisikika. Amata na wengine wakapanda na lori lile kuondoka kwa kasi.
************
“Una mpenzi mzuri sana, mtoto kaumbika kama Malaika, he he he mbona wewe na yeye hamuendani kabisa au wewe ni mchunga ng’ombe wao!” mmoja wa mahabusu alimuuliza Amata kwa sauti mbaya ya kukwaruza isitoshe inatisha. Amata aligeuka na kumwangalia akatabasamu kwa sura iliyochoka “Simjui hata anatoka wapi” alimjibu “Kwangu ni kama shetani tu yule, anataka kuniua, kunifunga, hilo ndilo limemleta hapa” aliendelea kumueleza yule mahabusu. “Kwa nini aje kukuona asubuhi yote ile? Au kuna uhusiano wowote na kesi yako?” aliendelea kudadisi mahabusu yule, “Sijui chochote! Mbona maswali mengi umempenda? Mfwate basi, mi nshakwambia smjui! Yule ni shetani tu” Amata alijibu kwa hasira kidogo na mahabusu yule hakuendelea na maswali yake.
Kesi ilitajwa tena baada ya siku kumi na nne, Amata na wenzake wakiwa na pingu mikononi waliingizwa katika chumba maalumu cha mahabusu mahakamani hapo, Amata alisimama karibu na mlango, mara ghafla alipata mshtuko mkubwa, hakuamini alichokiona nje ya jingo hilo, akakaza macho kutazama kwa makini akayafikicha kidogo aone labda alikuwa ndotoni lakini hapana alichokiona ni sahihi na macho hayakumdanganya. Hakutaka kupoteza hata sekunde katika lile alilokuwa analiona lakini bahati mbaya hakuweza kusikia kinachozungumzwa. ‘Yule sio Chausiku?’ alijiuliza moyoni lakini pia hakutaka kuyaamini macho yake.
Chausiki Binti Saidi, msichana mfupi mwenye afya njema kibonge, mmiliki wa mgahawa unaojulikana kwa jina la Chau Café, msichana huyu ambaye amekuwa pamoja na Amata, wamesoma shule moja ya msingi kijijini hapo na kucheza michezo mingi ya utoto pamoja, yeye alifanikiwa kufika japo darasa la saba wakati Amata alifukuzwa shule akiwa darasa la tano kwa kisa cha kumpiga mawe mwalimu wake wa darasa. Maisha yalimwendea kombo Amata lakini Chausiku ndiye alikuwa akimfadhili japo kwa hela ya sigara au kikombe cha Kahawa, watu walikuwa wakimbeza sana Chausiku kwa jinsi alivyoonesha upendo kwa Amata hii ikapelekea Chausiku kutokuwa karibu sana na kijana huyu ambaye japo alikuwa mchafu, mkorofi lakini moyo wake ulituama kwake kama maji yatuliavyo mtungini yasipoguswa. Vijana wengi walipenda kwenda mgahawani kwake japo tu roho zao zisuhuzike kwa kumuona binti huyu, wapo waliomdanganya kwa pesa na vitu mbalimbali lakini msimamo wake thabiti haukumfanya ayumbishwe na vitu vyote hivyo bali aliuacha moyo wake utue kama kipepeo atuavyo katika ua alilolichagua. Chausiku aliumizwa sana na kisa kilichomkuta Amata, alijua kuwa Amata kwa hali aliyonayo asingeweza kupata msaada wowote wa kisheria au utetezi katika kesi yake, alijitahidi kufanya kila awezalo ili tu amsaidie Amata katika hili.
Jalada la Amata liliitwa, polisi walimtoa katika chumba kile akiwa chini ya ulinzi na kupelekwa katika chumba cha mahakama, akiwa anapita katika kikorido kidogo cha jengo hilo alisikia sauti nyembamba tamu ikipenya masikioni mwake, ilikuwa si ya mwingine bali Chausiku ambaye alikuwa akilia kwa machozi mazito “Mnyezi Mungu akusaidie” ni maneno aliyomwambia, Amata aligeuka kwa kuiba, alifarijika kuona kumbe wapo katika binadamu awa hawa wanaompenda, kidogo alijisikia mtu kati ya watu. Kesi ya Amata ilikwisha alihukumiwa kifungo cha miaka miwili na miezi sita jela. Waliondolewa mahakamani na Amata alianza kutumikia kifungo chake huko gereza la kilimo Sogera, gereza lenye kazi ngumu, kulima, kupanda, kuvuna, muda wote mkiwa katika matope, maji machafu, mnakula chakula huku mnanyeshewa na mvua, mateso!.
Sogera ni gereza kubwa sana lililoko nje kabisa ya mji wa Mgosola, lilijengwa zamani na wajerumani wakoloni juu ya mlima. Limezungukwa na ukuta usiopungua mita ishirini kwenda juu na chini ya ukuta huo kumepandwa mikonge kuzunguka gereza zima, katika kona zote na katikati ya pande zote kuna vibanda vipatavyo nane juu kabisa vyenye walinzi wawiliwawili kila kimoja wakiwa na silaha kali, juu ya ukuta kumezungushwa waya maalumu ambao una umeme kwa masaa ishirini na nne, doria haziishi nadani ya gereza hili lenye kila aina ya sifa. Amata alifungwa ndani ya gereza hilo, hakuwahi kufikiri hata siku moja kama angefika mahali pale daima alisikia hadithi tu watu wakisimulia na kusifia sifa mbaya za jingo hilo, aliona kuwa sasa ndio amefika mwisho wa maisha yake, jehanum ya duniani, alikata tama ya kuona tena kijiji chake alichokipenda, watu aliyowapenda, michezo aliyoipenda, shamba lake aliloachiwa na wazazi wake, kila kitu kwake aliona kimefika mwisho na kama kuna kitu alichokichukia tangu muda huo ni Saringo msichana mrembo aliyemhakikishia kufungwa na kuozea jela. ‘Shetani huyu! Shetani mkubwa! Aombe nisitoke ila nifie humu, laiti nikitoka namkatakata vipande na nyama nawapa mbwa wale, naapa’ Amata alijiwazia kwa hasira na uchungu. Akiwa bado ameketi kwenye kigodoro kidogo alisikia sauti ya king’ora hakujua kinahashiria nini alipochungulia katika kadirisha ka mlango aliona wafungwa wote wanakimbilia kwenye uwanja mkubwa, mara mlango wake ukafunguliwa “haya mfungwa kwenda kwa wenzio haraka!!” sauti ya askari ilimfanya atoke mbio, alifika na kukaa katika mstari paamoja na wengine. Akasimama askari mmoja katikati akiwa na kipaaza sauti “leo ni sherehe!!!!” alitangaza “tunakaribisha wageni na pia tunapunguza wengine” aliongeza, uwanja ulikuwa kimya sana alisikika yeye peke yake “wale wote waliofika hapa peponi leo waje mstari wa mbele haraka!” alitoa amri Amata na wenzake saba walisogea mbele wakiwa bado na pingu mikononi, wakasimama mbele, hapo waliweza kuona kila kitu kwa vizuri zaidi. “kwanza napenda kukukaribisheni hapa Sogera, sehemu takatifu ambayo huna budi kuacha ujinga wako!” aliendelea kusema “Mnaowaona hapa wote ni watoto wazuri wenye roho nzuri wasiopenda ujinga!” alisema huku akitafuna big G yake, askari huyu mrefu mpana mwenye tambo la kiaskari hasa aliongea maneno haya bila kuonesha tabasamu wala kutikisika, akiwa na bastola yake kiunoni na sare yake ya magereza iliyomkaa vizuri alionekana si wa kuchezea. “Nyie was*nge! Mliokuja hapa wiki hii, hii ngome ya mjerumani, ukitaka kuishi vizuri fuata amri kumi za hapa ndani, ukiambiwa inama, inama, usilete ubishi kwani waliopo hapa ni binadamu kama wewe wana mahitaji”alisema askari yule. Amata aliposikia maneno hayo alisisimka na mwili ulikufa ganzi, askari yule aliendelea… “Usije kujaribu kutoroka, zawadi ya kutoroka ni kama hii mtayoiona sasa!!!” akageuka nyuma akapaza sauti “Afande, lete hao!” mara wafungwa wanne waliletwa wakiwa wamefungwa kamba mikononi wakiburuzwa kama magunia, walijaribu kukukuruka lakini haikusaidia. Pale aliposimama askari yule palikua na jukwaa kubwa lenye kitu kama goli la mpira, lakini juu yake kulikuwa na kitu tofauti, ubao mnene mkubwa wenye tundu la nusu duara lakini katika tundu lile kulikuwa na kitu kilichokamilisha duala lile kiling’aa sana kana kwamba kuna chuma katikati, stailess steel, na upande wa chini wa goli hilo kulikuwa na ubao mwingine kama ule lakini huu kwenye tundu lake haukuwa na kile kitu kama chuma. Mfungwa mmoja aliburuzwa mpaka pale na kufungwa kwa kamba katika goli lile akielezewa chini shingo yake ikiwa imepachikwa kwenye ile nusu duara mwili ukiwa upande wa pili na kichwa upande mwingine, mara kibao kile cha juu kilifyatuka na kuteremka kwa kasi, akiwa bado kapigwa na bumbuazi Amata alihisi kitu kama jiwe la duara kikimgonga miguuni na kuhisi maumivu, alipoangalia chini ni kitu gani hakuamini macho yake, kichwa cha mtu kinachovuja damu mbichi kikiwa kimekatwa kutoka kwa mfungwa yule aliyefungwa pale golini, Amata alichanganyikiwa hajawahi maishani mwake kuona kichwa kisicho na kiwiliwili, akaanza kukimbia.
***************
“Kamata huyo!” amri ilitolewa, askari wawili walianza kumkimbiza, alipigwa ngwala lakini kwa umahiri mkubwa Amata aliruka samasoti na kutua kwa miguu miwili kabla hajakaa sawa alistukia kamba iliyorushwa kwa ustadi ikimfunga shingoni, akageuka na kurusha ngumi iliyompata askari yule sawia shavuni, kabla hajakaa sawa alipigwa teke moja la kifua na kuyumba akaangukia katika mtaro wa maji machafu akatoka kwa haraka alipata pigo lingine maridadi lililompoteza kabisa akaanguka tena, askari wale wakamfunga kamba na kumburuza mpaka uwanjani naye akawekwa pamoja na wale wanaosubiri kunyongwa, akafunikwa nguo nyeusi kichwani asiweze kuona chochote. “He he he safi sana kijana! Umediriki kufanya kosa ambalo leo litagharimu maisha yako!” askari yule aliyekuwa na kipaza sauti alimwambia amata “Mleteni mbele!” akasogezwa mbele ya lile jukwaa la kunyongea “Mtoeni kitambaa!” akatolewa kitambaa “Mfungueni pingu!” akafunguliwa pingu na kubaki huru. Askari yule akasema “umeonesha ujeuri, umempiga askari wangu, sasa utashughulikiwa ili ujue kuwa hapa ni mahali pa pekee” alimsogelea Amata na kumwangalia usoni “kwanza umechoka! Mwili na roho! Nani aliyekuleta huku? Leo utajutia ulichowafanyia wananchi huko uraiani!” alisema yule askari huku amemkazia macho Amata, Amata alimwangalia askari huyu mwenye macho mabaya, mekundu na alikuwa kila akiongea mdomoni mwake kulitoka harufu ya tumbaku na gongo. Askari yule alimzunguka Amata kama mara tatu hivi. “Cockroach! Fanculo! Caputana!” alimtukana Amata kwa lugha ambayo hakuielewa. Amata aliona kuwa sasa mwisho wake umefika. “Aje mwanaume amshughulikie huyu!” aliita askari yule. Mara akajitokeza pande la mtu, lenye mwili mkubwa, kifua kipana, sura yake ilionesha kila dalili ya kutokuwa na huruma na mtu, lilimsogelea Amata pale alipo, Amata akarudi nyuma kidogo, lile jitu likamsogelea zaidi, Amata alishikwa na hofu ya kifo alipogeuka nyuma akakuta watu tayari wamefanya duara kubwa hamna pa kupenya, alihisi pigo moja la mgongo lililompeleka chini alipojigeuza kuangalia juu aliliona lile jitu likinyanyua mguu kumkanyaga akajiviringisha upande wa pili na jitu lile likakanyaga chini kwa nguvu kishindo ambacho kilitimua vumbi, amata kwa kutumia nguvu zote alirusha teke lililompata nyuma ya magoti jitu lile likajikuta limepiga magoti, Amata alijinyanyua haraka. Kelele za wafungwa za kumshangilia Amata zilimpa nguvu akiwa bado anawaangalia wanaomshangilia alipigwa roba maridadi ambayo ilimkosesha pumzi, Amata alikukuruka aliporusha mguu wake kwa nguvu kwa nyuma alilipiga hilo jitu kwenye maeneo nyeti, jitu likamuachia Amata na kujishika maeneo,Amata akaanguka chini akanyayuka haraka na kwa kasi ya ajabu aliruka kitu kama tik tak akalipiga usoni kwa migu miwili, nguvu ile ilimfanya jitu asimame wima bila kujua lakufanya, Amata kijana aliyejaliwa wepesi na kusaidiwa na michezo ya sarakasi aliyokuwa akicheza shuleni aliruka hewani na kumpiga mateke ya kifua, jitu lile lilidaka miguu ya Amata kwa ustadi lakini Amata alijikunja kama samaki na kumpiga kichwa usawa wa pua na kumvunja mfupa wa pua, Amata alianguka chini baada ya kuachiwa na lile jitu ambalo wakati huo lilikuwa linavuja damu puani likiwa limeshika pua, Amata alisogea na kurusha makonde mfululizo yaliyokwenda sawia tumboni ambapo jitu lile liliachia uso na kujishika tumboni na Amata alibadili mashambulizi kupeleka usoni, alitumia mtindo huo kama dakika mbili mpaka jitu lile likawa hoi kabisa. Kelele za wafungwa zikazidi kuufunika uwanja wote askari wakaja kumkamata Amata na kumtoa asije akaleta madhara zaidi. Masikini Amata, hakujua kuwa aliyempiga ndiye mbabe wa gereza hilo, hakuna na haijawahi kutokea mtu akamshinda, wafungwa walimshangilia Amata na tangu hapo akawa na marafiki wengi na kuogopwa na wafungwa wengine.
**************
Maisha yaliendelea gerezani miezi sita ikapita, kazi, mateso, uonevu ndio ilikuwa sera ya maisha yao na Amata akazoea hali hii, kila kukicha hawaishi kupigana na kuumizana kunyang’anyana vyakula na kutaka kuwageuza wenzao, japo Amata hakupenda hali hiyo.
Ilikuwa asubuhi tulivu sana jumapili fulani, watu wengi walikuja kuwatembelea ndugu zao. Amata alikaa kwenye gogo lililopo ndani ya gereza hilo akitafakari hili na lile akimkumbuka huyu na yule. Mara alihisi gogo lile kutikisika alipogeuka alimuona mfungwa mwingine amekaa jirani naye, Amata akamtazama jamaa yule kwa makini sura yake haikuwa ngeni sana lakini hakukumbuka amemuona wapi, alimtazama tena na tena. “Rafiki!” mfungwa yule alimuita Amata kwa sauti ya chini, Amata akaigeuka tena kumwangalia vizuri usoni, Amata akaingiwa na hofu kidogo maana mfungwa huyu hajawahi kukutana naye sura yake ya kawaida tu lakini alipotabasamu aligundua kuwa hakuwa na meno, Amata alisogea pembeni kidogo akamuuliza “wewe ni nani, mbona sijawahi kukuona?” “Umenisahau?! Wewe ni Amata Ga Imba siyo?” Amata alishtuka kuona hata jina lake analijua. “Ndiyo! Mimi ni Amata Ga Imba mwana wa Nkhunulaindo! Nikusaidie nini?” Amata alijibu na kuuliza kishari kwa maana ndiyo hali aliyoizoea sasa. “Mimi naitwa Golam wa Golam!” alijitambulisha kwa Amata, kasha akatoa lile tabasamu lake ambalo lilimfurahisha Amata hata alitamani kucheka, kwa sababu kweli alifanana na Golam ambaye amata aliwahi kumuona katika filam huko kijijini kwao. “Safari imewadia!” Golam alimnong’oneza Amata “Safari, safari gani?” Aliuliza kwa mshangao lakini kwa sauti ya chini “Mimi na wewe tuna safari ya mbali na ngumu sana, safari hii itatugharimu mengi sana lakini mwisho wake tutaishi kama wafalme he he he! Nilikuwa nakungoja, na sasa umefika. Wewe ni Mate ya Simba, kila mnyama atakukimbia, mapori yote yatakuinamia na kukuheshimu, funga mkanda Amata, safari imewadia” Golam aliongea kwa utulivu mkubwa. Amata hakuelewa anachoambiwa wala anachokisikia, aliduwaa tu akitazama upande wapili jinsi pilikapilika za wafungwa na askari zilivyoendelea “Unat…” alitaka kumuuliza Golam lakini alipogeuka hakumuona, Golam alishaondoka pale kitambo na Amata hakuweza kujua ameenda wapi! Amata aliona kama katokewa na shetani la kiume, ‘safari, safari gani, kwenda wapi? Lini? Mh!’ hakuweza kupata jibu juu ya maswali hayo, alinyanyuka pale alipoketi na kuvuta hatua chache kuelekea lango kuu la gereza, alichokiona hakukiamini, ‘Saringo!’ alishaangaa, mara aliitwa kuonana na mgeni wake, alikataa kwenda akamwambia afande kuwa hana mgeni, afande akamsisitizia kwa kuwa alishapewa pesa kidogo na Saringo ili afanye makeke, kwa kuwa wafungwa wa aina ya Amata hawakutakiwa kuonana na ndugu ovyo. Alikwenda lakini moyoni mwake hakutaka maishani kuonana na kiumbe huyu mwenye uzuri uliofunika unyama wake. “Unataka nini tena? Nimeshafungwa! Unataka kuniambia kuwa nitanyongwa, sivyo?” Amata alimwambia Saringo. “Amata! Nimekuja kukuomba msamaha, maneno yale sikutegemea kama yatakuwa kweli, wewe hunijui wala mimi sikujui ila nilitumwa kwako na aliyenituma anakuhitaji sasa!” Saringo aliongea kwa uchungu akimwangalia Amata machoni mwake. Kisha akaingiza mkono kwenye pochi yake akatoa kikaratasi cha rangi ya purple kimekunjwakunjwa akatazama huku na huku akamkabidhi Amata, Amata akakipokea akakificha kwenye nguo ya ndani. Saringo akatoa tabasamu la nguvu kwa Amata, kisha akageuka na kuondoka zake, Amata alibaki anamwangalia akifarijika kuona jinsi mtoto huyu alivyojaaliwa hata upande wa nyuma ‘mashaallah’ alijisemea moyoni, mara alijikuta vurugu kubwa inatokea ndani ya suruali yake ya orange akagundua kuwa macho yamemponza, akarudi ndani. Jumapili hiyo ilikuwa ni siku ya burudani na michezo huwa mara moja kwa miezi mitatu, Amata akaketi kwenye nyasi akiangalia wafungwa wenzake wakisakata kabumbu, kila alipoangalia huku na huku hakumuona Golam, alishindwa kujua kama Golam alikuwa mzuka au mfungwa mwenzake, mara akaanza kucheka mwenyewe alipokumbuka tabasamu la Golam. Aliondoka eneo hilo na kusogea pembeni huku akimuangalia kila anayekutana naye labda atamuona lakini hakufanikiwa, aliendelea kuvuta hatua taratibu akiwa bado na mawazo lukuki na maswali yasiyo na majibu.
Golam wa Golam, mfungwa asiyependa kuongea sana na anayependa kufanya kazi muda wote, alikuwa amepangwa kufanya kazi jikoni kama mpishi na kwa miaka miwili sasa. Golam alifungwa katika gereza la Sogera yapata miaka saba sasa kwa kosa la mauaji, alikuwa hapo akisubiri hukumu yake ya kunyongwa kwa kosa hilo. Alipokuwa gerezani humo hakupenda kujichanganya na wafungwa wengine hakuwa na rafiki na daima alionekana mtu mwenye kupanga kitu fulani, kwa kipindi cha miaka saba hii hata ndugu zake walishajua kuwa amenyongwa, hawakuja kumtazama wala kumtaka hali. Alipata kufahamu njia zote za gereza hilo na ratiba zote za askari za ulinzi wa gereza hilo. Aliwahi kuwa na rafiki mmoja tu ambaye yeye alishanyongwa pale tu alipojaribu kutoroka kwenye ngome hii isiyopenyeka. Akiwa bize na kazi ya kuandaa chakula cha jioni cha siku hiyo Golam alionekana mtulivu sana hata alikuwa anafanya kazi dakika chache na chache anapumzika lakini akizama katika fikra zingine.
Amata alirudi kwenye kichumba chake na kujilaza kwenye kigodoro chake kidogo, baridi ilikuwa kali sana siku hiyo, akiwa amejilaza hapo alipitiwa na usingizi. ‘Watu warefu walikuja wakamkamata Amata, wakambeba juu juu, watu hao Amata hakuweza kuwaona miguu yao wala sura zao, walimpitisha kwenye bonde kubwa lenye manyoka makubwa mengine yana vichwa viwili, manyoka yale yalijaribu kumrukia lakini kutokana na urefu wa hao viumbe waliombeba hawakuweza kumfikia kabisa. Mara walifika eneo kubwa la wazi, pale aliona viumbe wenye vichwa vibaya na vipembe vilivyojinyonga kama vya kondoo, katikati yao kulikuwa na chungu kikubwa kinachotoa mvuke wa ajabu. Mara wale viumbe waliombeba walianza kuwa wafupi mpaka kufikia urefu wa wale wengine, walimpomshusha, Amata ndio aligundua kuwa wale viumbe wana miguu kama ya kuku na mikia pia walikuwa na jicho moja, wakamnyanyua ili kumtumbukiza ndani ya chungu, kumbe hawa viumbe wanakula watu baada tu ya kuwachemsha, Amata alipiga kelele za ajabu….’
***************
Mara alikurupuka kutoka usingizini kumbe alipitiwa na ndoto ya ajabu na mbaya. Jasho lilimvuja kama kamwagikiwa na maji, akitweta kama mtu aliyekimbia mbio fupi za mita mia moja. Alipotulia na kurudi katika hali ya kawaida huku akijiuliza maana ya ndoto hiyo aliona kipande cha karatasi chakavu chini ya mlango, alijinyanyua taratibu na kuokota kikaratasi kile, akakifungua kwa woga, kikaratasi kile kilikuwa kichafu lakini kwa taabu aliweza ona kilichoandikwa kwa muandiko ambao herufi zake ziko mbalimbali, alijaribu kuziangalia vizuri lakini ilimuia ngumu kuelewa ni nini kimeandikwa, alikiweka pembeni, alipoangalia nje kupitia kidirisha kidogo aliona bado ni usiku kwani ni mbala mwezi na nyota ndizo zilizong’aza nje, na mizunguko ya askari walio zamu kwa muda huo. Aliketi tena juu ya kigodolo chake akakunjua tena kijikaratasi kile, alipokigeuza kwa nyuma aliona mchoro wa ajabu, hakuweza kuuelewa mchoro huo, kitu chenye umbo la mraba, ndani yake kuna duara kubwa ambalo lililochorwa X, katikati ya x ile pamewekwa namba tano na mshale uliongalia juu, kabla ya kuishia mshale ule kamstari kengine kalikatisha na kufanya kitu kama mchoro wa dira katika kamstari kale kuliwekwa herufi A upande wa kulia na kuliandikwa lugha isiyoeleweka, Amata aliangalia mchoro ule akaona hamna anachokielewa akakunja kile kikaratasi tena akakiweka chini ya tandiko akajilaza. Kulipopambazuka siku hiyo Amata aligubikwa na mawazo mengi alikuwa mpole sana kama mtu anayeumwa, siku hiyo alitakiwa kwenda na wafungwa wenzake kukata miti kwa ajili ya kuongeza idadi ya kuni kwa matumizi ya gereza. Wakiwa msituni na kazi imepamba moto, waliendelea na kuimba nyimbo mbalimbali za kuhamasishana huku wengine wakipakia magogo lorini, askari mmoja bwana mdogo alisogea karibu na Amata “Mfungwa! Chagua wengine watatu tukashushe mzigo wengine endelea…” alimwambia Amata. Wafungwa wanne wakapanda pamoja na Amata, akiwa amekaa juu kabisa ya lori lile pamoja na askari wawili wenye SMG wakiwa makini na kazi yao, lori lile aina ya Leyland lilikwenda kwa mwendo wa pole likiwa linapanda mlima mkubwa sana. Lilipofika juu ya mlima kabla alijaanza kuteremkia upande wa pili, Amata aligutushwa na mfungwa mwingine “Amata! Cheki nyuma ile yako bondeni ilivo…” alimwambia. Amata akaangalia kwa makini akaweza kuliona gereza ambalo wenyewe huliita nyumba, akaangalia vizuri, lilikuwa linaonekana bondeni hivyo aliweza kuliona vizuri sana. Mara akaona kitu cha ajabu kidogo aliweza kuiona vizuri picha ya gereza lile… aliliona katika mraba na alipokaza macho aliona kwa ndani kuna kama kitu cha duara kilichozunguka, Amata alishangaa sana akaingiza mkono kwenye nguo yake ya ndani akatoa kile kikaratasi mara akakumbuka kuwa alipo hapafai kufanya hivyo “Mfungwa! Telemka huko kaa chini na wenzio!” aling’aka kwa hasira akimnyooshea kiboko chake. Amata alishuka na kujichanganya na wengine. Safari ilitimu wakashuka na kuanza kutelemsha kuni kupeleka jikoni, alipoingia jikoni alimuona Golam kwa mbali akiwa ametingwa na kazi. Golam nae akamuona Amata, akatoa lile tabasamu lake, Amata akamsogelea Golam “Umeona mzigo wako?” Golan alimuuliza Amata kwa sauti ya chini huku wakipanga kuni “Mzigo gani?” Amata akauliza “Karatasi ndogo” Golam akajibu “Ndio! Ni nini kile? Sijaelewa” Amata alimuuliza “Mimi sijui! Nimepewa nikuletee” alijibu Golam “Oooh nani alikupa?” Akauliza Amata “Amesema utamkuta, muonane” Golam alimueleza “Nitamkuta wapi? Nani?” Amata alizidi kuchanganyikiwa kabla hajauliza aliitwa na askari na wakaondoka.
Mvua kubwa ilinyesha jioni ile radi kali zenye ngurumo za ajabu zilendelea. Amata na wenzake walikuwa bado wapo kazini, sasa walikuwa wakirekebisha mitaro ya maji machafu , viatu walivyovaa vilikuwa vimelowa alkadhalika nguo zao zilikuwa chapachapa huku baridi kali ikiwapiga walifanya kazi chini ya uangalizi mkali tena wakati kama huu walifungwa minyororo miguuni. Baada ya kazi hiyo ilipigwa filimbi na wote walitakiwa kusimama katikati ya uwanja ule. Amata akiwa katikati kabisa ambapo nyuma yao kidogo kulikuwa ni sehemu ya kunyongea, mara akasikia sauti ya kitu kama jiwe liliodondokea batini upande wa kushoto akageuka upande ule, kulikuwa na kibanda kidogo kilichotumika kama choo kwa ajili ya askari, akufuatilia sana akageuka kuangalia mbele lakini kuna kitu kilimrudisha macho upande ule, katika mlango wa choo kile kulikuwa na mchoro wa pembetatu iliyojazwa rangi na katikati kulikuwa na duara ambalo halikupakwa rangi, mchoro ule ulimvutia Amata akakumbuka katika kile kijikaratasi upande wa nyuma kuna ule mchoro hapo akagundua lazima kuna siri ndani yake kwa nini michoro hii ifanane, hapo akavuta taswira akakumbuka jinsi alivyoona gereza lile kwa juu wakiwa juu ya mlima akaoanisha hivi vitu vitatu akagundua kuna siri ndani yake ‘labda Golam anafahamu siri hii’ alifikiria moyoni. Mvua kubwa iliendelea kunyesha “Kutokana na hali ilivyo hatuwezi kuendelea na kazi” aliwaambia askari mmoja, kisha akaendelea “mtapanga foleni mtachukua chakula na kwenda kupumzika, hatakiwi mtu kuonekana nje!” Wakiwa katika foleni ya chakula, Amata alikazia macho sana upande ule, alikuwa bado anatafiti kichwani mwake ni kwa nini michoro ile ilifanana na ile ya kwenye kijikaratsi kile kinachoonekana kuchakaa sana pia ni kipande tu je kingine chake kikowapi, alikosa jibu.
**************
Usiku ule tafrija ya maafande iliendelea, pombe za kufa mtu zilikuwa huko, Amata alikuwa ni mmoja wanaosaidia katika tafrija hiyo, lakini akili yake yote ilikuwa ni kuingia ndani ya choo kile aone tu kuna nini, kwa mbali alimuona Golam nae yuko bize kuhudumia katika meza ya wakubwa, brassband iliendelea kupiga mziki wa taratibu. Amata alijaribu kuangalia ulinzi uliopo muda huo aliona hakuna mabadiliko kabisa lakini alijaribu kutafuta nafasi japo aonane na Golam. Alipokuwa stoo akipanga vinywaji kwenye chano mara Golam aliingia moja kwa moja akamfuata Amata “Tutafute muda tukajisaidie!” alimnong’oneza Amata. Amata akapokea kwa mshangao kauli hiyo lakini baadae akaona kuwa lazima Golam anafahamu chochote juu ya choo kile. “Wakianza kuchangamka tu tuonane ili tujue tunaingiaje pale chooni, maana kwa nyuma kuna mlinzi na juu kabisa yupo mwingine na taa kubwa inamulika ule mlango” Golam aliendelea kumdokezea Amata. Akili ya amata ilianza kufanya kazi kwa kasi na shauku ya kuingia pale ilimjaa, lakini aliwaza ‘vipi wasipokuta chochote mle ndani na wakasthukiwa na askari, itakuwaje’ alikumbuka yule jamaa jinsi alivyonyongwa akaingiwa na woga. Lakini alijipa moyo na kuamua kutoa dozi ya pombe ili hawa jamaa wachangamke mapema. Punde si punde, sherehe ilichangamka, watu waliimba na kucheza, Golam akazunguka upande wa Amata akampigia mbinja, Amata alipogeuka akamuona Golam, Golam akampa ishara ya mkono kuwa azunguke upande wa pili wa jengo hilo, alipofika upande huo alikuta miili miwili ya askari ikiwa chini, Golam akamwambia Amata avae uniform ya mmoja wao, akafanya hivyo japo nguo ile haikumkaa sawia lakini alionekana kama mmoja wa maafande, Golam naye akatwaa za yule mwingine halafu wakawavalisha nguo zile za ufungwa, amata hakujivunga akabeba SMG na magazine mbili za akiba akamuoneshea alama ya dole gumba “Naingia vitani!” Amata alinong’ona kwa Golam. Golam aliondokea upande wa pili na Amata upande mwingine, kazi ikaanza. Hadi kufika katika choo kile kutoka walipo akina Amata ni kama mita mia nne hivi na katikati hapo kuna mataa makubwa yanayoangaza hata akipita panya taa zile huzungushwa kufuatilia kinapoelekea kitu hiko, jinsi walinzi walivyo makini. Amata akajiweka tayari na kwa mwendo wa taratibu akiwa amejifunika koti lile la magereza, alivyojipapasa mfukoni alikuta kuna sigara alipoitoa aligundua kuwa ni msokoto wa bangi, Amata akatabasamu kwa sababu ana muda mrefu sana bila kupata hiyo kitu. Aliendelea kupita na kiambaza cha ukuta chini ya vibanda vya walinzi, alipofika upande ule ambako ndiko choo kile kilipo alitulia kidogo kwenye kona moja kwa kuwa aliona mtu akija upande ule aliokuwepo. Amata alisimama kikakamavu akiwa kampa mgongo mara alihisi kashikwa begani alipogeuka taratibu aligundua kuwa alikuwa Golam “Shhhhhh!!!” Golam alimuashiria Amata kutulia kisha akampita na kumpa ishara ya kumfuata, Amata alimfuata kwa nyuma wakazunguka nyuma ya jengo ambalo hutumika kama stoo ya kuni wakalipita na kuendelea mbele kisha Golam akasimama juu ya kitu kama tanki kubwa liliochimbiwa ardhini, akatoa katochi kadogo kama peni ambako alikakuta ndani yan nguo zile akamulika juu ya mfuniko wa tanki lile, kulikuwa na matenki kama matano. Amata hakuelewa Golam anaangalia nini juu ya matank hayo, tank la tatu akamwita Amata kisha akampa ishara ya mkono kumuonesha kwamba ‘ni hapa’, Amata na Golam wakasaidiana kufungua mfuniko hule na walipofanikiwa Golam aliingia wa kwanza na Amata akafuatia kisha wakafunga mfuniko ule kwa ndani.
********
Ndani ya shimo lile kulikuwa na giza nene sana hata huwezi kuona kitu kilicho mita moja mbele yako, Amata alijaribu kukanyaga taratibu na Golam akafuatia, Golam akatoa katochi kake mfukoni na kuangaza kidogo, ni mwanga hafifu sana uliotoka katika tochi ile haikuweza kuangaza mbali, taratibu Amata alimfuata Golam alikoelekea kwa mwendo wa kunyata, ukimya uliokuwa ndani ya shimo lile ulitisha, kawa mwendo ule ule wakiangaziwa na mwanga hafifu, Amata aliogopa sana kutokana na giza lile alitamani kumwambia kitu Golam lakini alishindwa pia aliona labda akifanya hivyo ataaribu utaratibu asioujua, mara ghafla wakasikia kelele kama za mbawa za njiwa arukae kabla Amata hajajiweka tayari Popo mkubwa alipita usoni kwake na mbawa zake zikampiga usoni, Amata alitoa mguno wa sikitiko lakini hakuthubutu kupiga kelele alivumilia tu, bado waliendelea kupiga hatua ndogondogo. Baada ya kutembea kwa mwendo huo kama dakika kumi na tano hivi Golam akasimama ghafla kisha akamzuia Amata kwa mkono wake walisimama katika ukimya wa hali ya juu kama sekunde hamsini hivi. Amata alitamani kumuuliza kitu Golam lakini bado alishindwa ila alihisi kitu fulani kumkaba kooni kutaka kusema lakini aliona sio wakati muafaka japo alipenda kujua hata ni wapi wanaelekea.Walitembea taratibu mwendo kama wa lisaa limoja, masikio ya Amata yalikuwa kama yanataka kuziba kwa ukimya ule ambao hajawahi kuuhisi katika maisha yake, mara akaanza kusikia sauti kama za njiwa dume na jike wakiwa katika harakati za mapenzi na punde tu zikapotea akaanza kusikia sauti za mbu wengi sana wakitaka kuingia masikioni lakini alipopunga mkono wake upande wa sikio hakuhisi kugusa chochote akasikia kama wanamfuata kwa nyuma akageuka hakuona kitu huku akivuta hatua ndogondogo mara akahisi kugonga kitu alipotazama mbele alijikuta amegonga ukuta… hakuna njia… Golam haonekani! Matatizo. Amata alipapasa ukuta ule akaona ulikuwa wa mawe makubwa ambayo si ya kujengwa na binadamu bali ni mwamba mkubwa, mkono wa mtu ukamshika begani Amata akashtuka na kupiga ukelele wa nguvu alipogeuka alimuona Golam, “Usipige kelele !!” Golam akamsisitiza Amata “Utawaamsha mapema!” Aliongeza Amata hakuelewa alichoambiwa na Golam ‘nani wataamka mapema?’ alijiuliza bila jibu Mbele kidogo walikuta kuna milango milango ipatayo kama nane hivi, Golam akasimama akatoa kipande cha karatasi kutoka kwenye nguo yake ya ndani akakimulika kwa mwanga hafifu wa kale katochi ambako tayari betri zake zilishaanza kupoteza nguvu. Golam akawa kama anahesabu kitu fulani katika ile milango kisha akampa ishara ya kumfuata Amata akafanya hivyo, walipita kwenye moja ya hiyo milango huko wakatembea kwa mwendo wa haraka kidogo, Amata aliendelea kusikia sauti za vitu mbalimbali mara watu wanacheka mara wanalia, kwake ilikuwa ni uoga mtupu. Mbele kidogo baada ya mwendo wa kama saa moja ingine Amata alianza kusikia kelele za maji mengi kama mto upitao, akamtazama Golam ambaye alikuwa amesimama kimya kama gogo, akamsogelea akamuona Golam kafumba macho katulia sana hakumshtua akasubiri aone nini kinafuata. “Maji !” Golam alinong’ona na Amata akasikia mnong’ono huo “Sasa tufanyeje?…” Amata naye alijibu kwa swali kwa kunong’ona “Lazima tuvuke, tufuate huu mto… mto Solondo” Golam alimjibu Amata “Mto Solando!?” Amata alishangaa na kumuuliza Golam “Ndiyo. Huu ni mto wa Solondo, lazima tuvuke kwa kuogelea kuna watu wanatusubiri nje, ila tahadhali mto huu una Mamba na maajabu mengi uwe makini, unajua kuogelea?” Golam akamwambia Amata “Najua kidogo sijawahi kuogelea kwenye maji mengi kama haya, hakika nitakufa.” Amata alijibu kwa kuhuzunika “Acha ujinga Amata! Ukisema utakufa, utakufa kweli” Golam alimwambia Amata kwa ukali kidogo na kumtupia swali “haya unajua haya maji yanaelekea upande gani?” Amata kwa uoga akajibu “Sijui mbona hata maji yenyewe siyaoni nasikia mvumo tu” “Ukipiga hatua mbili utatumbukia mtoni. Niambie haya maji yanaelekea upande gani? Tunatakiwa kuelekea upande yanakotoka siyo yanakokwenda…” Golam aliendelea kumuambia Amata.
Golam akachuchumaa na Amata akafanya vivyo hivyo, “Papasa kwa mkono polepole mpaka ufike ukingo wa mto kisha tumbukiza japo kidole uone maji yanaelekea wapi!” Golam alimwambia Amata. Amata akafanya hivyo akapapasa na mara akahisi kafika mwisho wa kanjia kale na kelele za maji ziliongezeka, akaingiwa na woga mkuu, moyo wake ulikuwa unadunda kwa kasi na kijasho kumtiririka. Akayagusa yale maji yalikuwa ya moto kama yako jikoni akahisi mkono wake unavutwa upande wa kulia, akajaribu kuutoa alihisi kama kitu kimemshika mkono kinamvuta majini, nguvu zikamuishia akapiga kelele “Golaaaaaaaammmmmmmmm!!!” Kishindo kikubwa kikasikika cha kitu kutumbukia majini, Golam akapiga hatua mbili mbele akaita “Amataaaaaa!!!” Alipoona kimya akajirusha majini akapiga mbizi maridadi, ndani yamaji yale palikuwa na mimea iliyotambaa akamuona Amata amenasa kwenye mimea hiyo akaogelea na kuanza kumsaidia akitoa kisu chake kidogo na kuanza kukata mimea ile, kila alipokata ilitoa kitu kama damu, alipofanikiwa kumtoa Amata wakaanza kuogelea kinyume na maji haikuwa kazi ndogo. Amata hakuwa mzuri kuogelea kama Golam kila mara Golam alijikuta kamuacha Amata nyuma, Golama akamshika Amata huku upande mmoja kashika kwenye ncha ya jiwe akamvuta Amata kwa nguvu zote na kumuweka mbele yake, wakaendelea kuogelea sasa Amata akiwa mbele na Golam nyuma. Amata akiwa mbele aliendelea kuogelea kwa shida kwa kuwa maji yalikuwa yanasukuma nyuma, Golam alijitahidi kumlinda Amata asije kubebwa na maji. Baada ya kuogelea kama masaa mawili hivi Amata alianza kuona maji yale yanang’aa kwa mwanga wa nje, alikuwa amechoka hata kujisogeza haikuwa rahisi, Golama alimvuta Amata na taratibu walijikuta wanafika nje ya lile pango kubwa lakini bado kasi ya maji haikuwa ndogo, Amata akahisi kitu kimemshika mguu akahangaika kujinasua akashindwa, Golam akajitahidi kumvuta lakini haikuwa rahisi wote walikuwa wamechoka sana, Amata akaponyoka kutoka katika mikono ya Golam, akahisi kuvutwa tena majini mara hii ni kwa nguvu zaidi, alihisi kama mikono ya watu imemshika miguu, alikunywa maji akajaribu kujizuia lakini ikashindikana alilegea na kukosa nguvu kabisa. Golam aliibuka nje ya mto, akarushiwa kamba na kuishika barabara akavutiwa nje “Amata yuko wapi?” aliulizwa, akajibu kwa ishara tu kuoneshea kuwa yuko ndani ya maji. Jiwe kubwa lililosukumwa na maji lilimgonga Amata kwenye paji la uso akachanika ngozi ya usoni damu zikaanza kumvuja kwa nguvu, mara akajikuta ameibuka nje na kunaswa kwenye miti midogo iliyo jirani na hapo, Golam akamuona Amata, wakafanya juu chini na kumnasua na kumleta nchi kavu. Wakakoka moto mkubwa ili kuwapa joto Golam na Amata, wakamsaidia Amata kutapika maji yale na kuzuia damu iliyokuwa inatoka katika jeraha lake. Amata akapoteza fahamu.
************
Msitu wa Solondo ni msitu mkubwa wenye miti mingi na wanyama wakali, ndani yake wanaishi watu wa jamii mbalimbali wenye mila tofauti za kizamani. Watu wengi waliuogopa msitu huo kutokana na kile kilichosemwa kuwa kuna miujiza mingi, uchawi na hatari za kila aina pia waliamini kuwa majini na mashetani hutokea katika msitu huo. Msitu huo ambao wakoloni wa kijerumani na kiingereza walihifadhi mali nyingi sana uliachwa katika hali hiyo hakuna hata aliyediriki kuingia baada ya kusikia kuwa wapo waliojaribu kwenda huko hawakurudi wengine waliliwa nyama na kupotelea huko. Kwa hiyo kila mtu aliogopa hata kuzungumzia. Matambiko na ibada za kijadi zilifanyika katika msitu huo, katikati ya msitu huo kulikuwa na jiwe kubwa sana jeusi ambalo kwa kuliona tu linatisha na inasemekana lilikuwa linaongea, hapo ndipo walipotolea sadaka ya damu jamii walioishi ndani ya msitu huo. Katika jiwe hilo kulikuwa na pango kubwa ambalo ndani yake kulikuwa na mapango madogomadogo mengi, jamii iliyokuwa inaishi katika msitu huo ambayo iliitwa ‘Gorino’ , gorino kwa lugha yao ilimaanisha ‘mla watu’ walikuwa wanawakamata watu wanaoingia ndani ya msitu huo na kuwaficha katika pango hilo ambalo wao waliamini lilikuwa ndio nyumba ya Mungu wao na kila walipotaka kutoa sadaka walichukuwa mmoja wa watu hao na kutoa sadaka ya damu, waliwakata vichwa na kuwatoa kafara, nyama iliyobaki ililiwa na vichwa vilining’inizwa kama mapambo ya eneo hilo hii ilikuwa ni sherehe kubwa sana ngoma zilipigwa na walicheza, hakuruhusiwa mwanamke kusogea hapo kwani waliamini mwanamke atamkasirisha mungu wao. Lakini eneo hili ambalo wakoloni walilitumia kama hifadhi ya mali zao lilikuwa ni lasiri sana kiasi kwamba hata wakazi wa huko na pembezoni hawakujua ukweli huo, madini mbalimbali yaliyohifadhiwa pangoni humo miaka ya elfu moja mia nane hamna aliyeyagusa kwa kutokujua, Msitu huo ulibaki katka hali niyo watu weupe wengi walijaribu kuingia kwa kuwa walijua ni nini kipo huko lakini nao waliishia uko huko.
**************
Amata alirudiwa na fahamu, akiwa pale chini bado alitazama juu na kuona watu watatu kati yao alimtambua Golam ambaye alichuchumaa jirani yake pembeni yake kulikuwa na mwanaume mwingine mwenye asili ya kizungu ambaye hakumjua alimuona mwanamke mwingine naye alikuwa na asili ya kizungu, Amata alizidi kuchanganyikiwa kwani hakuwajua hao wote ni akina nani, ghafla alipata mshtuko ambao ulimfanya anyanyuke ghafla na kushikwa na mshangao kwa kumuona huyu aliyesimama mbele yake sio mwingine ni Saringo. Huyu alimtambua bila kificho kwani kati ya wote huyo ndiye aliyemfahamu kwanza, Amata aliwatazama wote mmoja baada ya mwingine ila alimkazia macho sana Saringo ambaye bado alikuwa hamuelewi uhusiano wake na matukio yote haya. “Amata, kaa chini tuongee kidogo…” Saringo alimuomba Amata. Amata akaketi na wengine wote wakafanya hivyo. Wakiwa wamezunguka moto uliokuwa unawaka hapo alfajiri hiyo ili kuidhibiti baridi kali iliyowanyanyasa, kando yao miti mirefu na mikubwa iliwazunguka, mto mkubwa wa maji mengi yaendayo kasi ulipita eneo hilo, kelele za ndege wakubwa zilisikika. “Hawa unaowaona ni rafiki zangu, huyu anaitwa Bw. Stephan Van Leuwen kutoka Poland na huyu ni rafiki yake kutoka German anaitwa Bi. Hellen Schurman wote ni wakufunzi katika chuo kikuu cha Heidernburg huko Ujerumani, ni wataalamu wa mambo ya kale. Huyu mwengine unamfahamu Golam, huyu ni binamu yangu mtoto wa mjomba wangu, na mimi naitwa Saringo mjukuu wa mzee Koloto.” Saringo alitoa utambulisho huo, kisha akageukia upande wa pili “Huyu anaitwa Amata!” alimtambulisha kwa kifupi “Amata Ga Imba, au mate ya Simba” Golan aliongezea na wote wakatabasamu Amata bado alimkazia macho binti huyu anayeitwa Saringo ambaye alionekana mkakamavu akiwa ndani ya jinsi iliyomkaa vizuri na fulana yake nyekundu ambayo kwa nje aliifunika na kishati cha buluu angavu ambacho hakufunga vifungo ila alifunga fundo kwa chini, buti kubwa nzuri ya kijeshi aliyoitupia mguuni mwake haikuwa ya kawaida. Amata bado alikuwa hajaelewa vizuri kinachondelea hapo alipomtazama yule mzungu ambaye kichwani mwake alivaa kofia kubwa kama ile ya Marlboro akiwa anavuta kiko yake, mgongoni akiwa na begi la kijeshi na mkononi akiwa na bunduki aina ya ‘rifle’, na rafiki yake wa kike mwenye macho makali daima litafuna jojo akiwa kavaa jinsi ya kaki na shati zito pia la kaki, alionekana mtaratibu na mpole kiunoni mwake alikuwa na bastola mbili kushoto na kulia. Amata aliogopa sana kwakuwa kwanza alizoea kuwaona wazungu makanisani tu na wakiwa wamevaa makanzu, alizoea kuona bunduki za kuwindia tu kama gobole ambalo hata yeye aliachiwa na marehemu baba yake. Alikuwa na mawazo mengi yaliyokuwa yakipita kichwani mwake.
“Tuko hapa kwa nia moja tu, tunakwenda ndani ya msitu wa Solondo, sisi watano na wewe tuliona unatufaa, mimi ndiye nilikutafuta kwa gharama kubwa” Saringo alimuambia Amata. Amata akaendelea kumsikiliza kwa makini, Saringo akaendelea “Nilikuja kijijini kwenu kumsalimia shoga yangu Chausiku ambaye unamfahamu sana, nikiwa pale ule ugomvi uliokuhusisha wewe niliuoana na nilivutiwa kwa jinsi ulivyompa mkong’oto yule bwege. Nikafuatilia mwisho wake kuona, nilipojua kuwa umekamatwa na uko polisi nikaja kukutembelea nilikuja tu kukutia hasira na si kingine lakini nilipanga wewe ufungwe nikiwa na lengo moja kuwa kule gerezani utakutana na binamu yangu Golam na kweli ikawa hivyo, Golam nilimpa kazi muda mrefu ya kutafuta mfungwa mkakamavu, mpiganaji, asiyeogopa kitu na ulivyofungwa wewe nikamwambia Golam akuchunguze, siku chache tu akanipa taarifa nzuri ya kuwa ulimpiga hata mtu ambaye wao wote wanamuogopa, ndio hapo tukasuka mpango wa kukutorosha wewe na Golam, na mpango huo tuliusuka mimi na hawa wazungu kwa kuwa sisi tulikuwa na ramani ya gereza lile, njia zote za siri ambazo wenyewe wakoloni walizitumia kuwakimbia maadui pindi wanapovamiwa.” Saringo akakohoa kidogo na kuendelea “Baba wa babu yangu alifanya kazi kama askari wa mkoloni na kituo chake kilikuwa hapo gerezani, wakati huo ikiwa ngome ya mjerumani kabla ya kuchukuliwa na waingereza, yeye ndiye aliiba hii ramani, yeye pamoja na wenzake ndio walikuwa wanaenda Solondo kuhifadhi vitu vingi vya wajerumani, alimpa babu yangu siri hii miaka mingi sana mpaka kwa baba yangu, baba yangu alinipa siri hii na kabla ya kufa kwake alifuatwa na watu wengi sana waliodhani kuwa yeye alikuwa anajua zaidi na amefika huko katika pango la msitu wa Solondo. Kabla hajafa alinipa mkoba wake mchafumchafu nilipoufungua ndani ndio niliona makaratasi ya kizamani na maandishi ya ajabu ajabu siyaelewi, nilihifadhi karatasi zile vizuri, na nilipokwenda masomoni Ulaya ndipo nilikutana na hawa rafiki zangu katika darasa moja, nilipojua vizuri kijerumani ndio nilipojua maana na siri nzito iliyomo katika makabrasha yale, ndio hapo tulipopanga kikosi kazi kuukabili msitu huu wa Solondo hadi tuone mwisho, tukaona wewe pia unafaa kuwepo katika kikosi kazi hiki”.
Amata alibaki ameduwaa ‘Msitu wa Solondo!’ alijiwazia aliona kama yuko katika ndoto labda ataamka lakini haikuwa hivyo. “Saringo!” Amata aliita na kuweka pozi kabla hajaendelea kuongea “unaujua msitu wa Solondo au umeusoma tu kama ulivyosema?” “Sijawahi kuingia msituni ila sasa tumeamua kwenda” Saringo alimueleza Amata “Msitu wa Solondo sio wa kuuchezea, tutakufa sote hakika, kuna mashetani na viumbe vya ajabu, kwa nini tuyakatishe maisha yetu tukiwa bado vijana? Kuna nini kule cha maana? Acheni upumbavu wenu. Golam ndio hii safari uliyotaka twende?” Amata alimuuliza Golam. “Amata! Hii ndiyo safari, usiogope zile ni hadithi tu, wazee hawakupenda twende huko lakini ni msitu tu wa kawaida. Ujue kila kona sasa unatafutwa mfungwa uliyetoroka utajificha wapi? Twende Solondo” Golam alijibu na kutoa tabasamu lake la kuvutia ambalo daima humfanya Amata kucheka. “Hao wazungu wanaweza kutembea kwa miguu? Maana ni safari ya siku kama saba hadi tufike.” Amata aliuliza kwa wasiwasi “Wataweza ndio maana wamekuja.” Saringo alijibu. Amata akatikisa kichwa kuashiria kuwa ameridhika, akanyayuka akaingia kwenye vichaka vya karibu akatokomea huko. Saringo, Golam na wenzao walibaki kumsubiri bila mafanikio.
**********
Walibaki kujadiliana tu nini cha kufanya kwa kuwa hawakujua Amata kaenda wapi na kwa nini. Wakiwa katika butwao hilo mara walisikia kelele za mnyama mwenye hasira kutoka porini wakiwa bado hawapo vizuri mnyama aina ya Ngiri alikatiza kati kati yao kwa kasi ya ajabu alimpiga, Bw Stephan alipigwa kikumbo na kudondoka vibaya kwenye mawe bunduki ikianguka upande mwingine, wengine walikimbia kila mtu upande wake wakiwa wamechanganyana hawaelewi kilichotokea. Bw Stephan aliumia sehemu ya mkono alikuwa akivuja damu. Amata akasimama mbele yao “nauliza tena! Nyinyi mnaweza kuingia Msitu wa Solondo? Huyo ni ngiri tu mmekimbiana hivyo wengine na bunduki zenu mmeshindwa kujipanga kumshambulia, sijui kama tutarudi mi nina wasiwasi.” Amata aliwaeleza huku akitweta. “Amata acha ujinga!” Saringo aling’aka “Sio ujinga mimi nilienda porini kumkurupusha huyo mnyama ili niwapime uwezo wa kukabiliana na hatari za ghafla, maana huko msituni kuna wanyama wakali, na isitoshe kuna mashetani ambayo hata uyaoni kwa macho we utahisi unatandikwa bakora tu! Sasa itakuwaje?” Amata aliwauliza kwa ukali “Haya na tuanze safari mengine tutayaona uko huko!” Saringo aliwaambia wengine.
Safari ya kuingia Msitu wa Solondo ikaanza, Golam akiwa na jisu kubwa kiunoni mwake aliongoza msafara akifuatiwa na Bw. Stephan na bunduki yake kubwa, Saringo akiwa na begi lake la kijeshi mgongoni alionesha kutembea mwendo wa kikakamavu haswa, Bi.Hellen mkimya asiye na maneno mengi aliendelea kuchapa mwendo na bastola zake kiunoni alionekana amejiandaa haswa katika safari ile ngumu. Walipita katikati ya msitu ni ndege na wadudu ndio waliokuwa wanawasindikiza, Amata akiwa na uta wake mgongoni alikuwa wa mwisho katika msafara huo ambao ulikuwa ukiongozwa na Golam hakukuwa na anayeongea kwa wakati wote huo, walikuwa wakifuata kanjia kadogo kanakoelekea milimani, ilionekana kuwa Golam alikuwa mzoefu wa eneo hilo kwa kiasi fulani ukiacha Saringo ambaye aliku na karatasi kubwa tu la khaki ambalo ndani yake kulikuwa na michoro mingi ya ajabu na isiyoeleweka. Amata akiwa hana wasiwasi nyuma ya wote alivuta hatua uku akiwa na mgagi wake mdomoni, baada ya mwendo mrefu wa kama masaa matatu hivi walifika mtoni ambako ilibidi wavuke kwenda ng’ambo ya upande wa pili, maji ya mto yalikuwa yanakwenda kwa mwendo wa wastani, maji haya yaliyochanganyika na udongo yalikuwa na rangi kama chai ya maziwa. Wote walisimama kando ya mto huo wakiyaangalia maji kwa makini “Inabidi tuvuke!” Saringo aliwambia wenzake. Wote wakatazamana na kuanza kujiandaa kwa kuvuka hakuna aliyejua kina cha mto huo wala hatari yoyote iliyopo hapo, hakuna aliyeonekana kuogopa bali kila mtu alionesha ujasiri, Amata alionekana kasimama tu kana kwamba hakuwa mmoja wao katika hilo. “Kuna kamba? Inabidi mmoja aogelee mpaka ng’ambo akafunge hiyo kamba kwenye mti ili wengine iwe rahisi kuvuka” Amata alitoa rai. Na kila mmoja kukubaliana na wazo hilo. Stephan akatoa kamba ndefu ya kutosha Golam akajitolea kuivusha kamba hiyo. Akaichukua na kujifunga kiunoni tayari kwa kuvuka, aliyaangalia yale maji kwanza kisha akachukua podo na uta wake na kuuweka mgongoni tayari kwa kuvuka “Naomba mnilinde” Amata aliwaambia wenzake na kujitoma ndani ya maji aliogelea kwa ustadi sana kukatisha mto huo, maji yalikuwa magumu kwake katika kuvuka. Alikotoka wote walikuwa kimya kumuangalia Amata jinsi anavyoyakata maji japo si kwa ustadi sana wakiwa bado katika kumwangalia mara walimuona Amata akizama kabla hawajajiweka vizuri waliona mkia wa mamba mkubwa ukitokeza juu ya maji “Mamba!!!” Golam alipiga ukelele. Amata alibanwa mguu na mamba alijitahidi kujinasua lakini mamba yule alimzamisha tena, aliipomuibua mara ya pili alichomoa mshale mmoja kutoka katika podo lake na kumchoma mamba yule jichoni, Mamba alimuachia Amata na akajigeuza chali Amata kwa ustadi mkubwa alimchoma tena eneo la kifua mamba yule kisha akajaribu kuogelea kwa kujihami, mamba yule akajinyayua juu Bwana Stephan kwa ustadi mkubwa alimlenga na kumpiga risasi mbili eneo la tumbo mamba yule alijibwaga majini… mfu!. Bw Stephan akashusha bunduki yake na kushusha pumzi ndefu, Amata alifika ng’ambo na kuifunga kamba ile mtini kisa kuwapa ishara wengine kuvuka, mmoja baada ya mwingine walivuka na hatimaye wote walifanikiwa kuvuka. Bi Helen aliuangalia mguu wa Amata lakini haukupata majeraha makubwa alipohakikisha kuwa anaweza kusonga mbele basi safari ikaendelea. Giza lilianza kuunyemelea msitu “Hapa tunaweza kulala” Amata alilisisitiza wakakoka moto na kupumzika. Kila mtu akiwa amejilaza kwa mang’amung’amu. Saringo alilala jirani kabisa na Amata, Hellen akiwa jirani na Stephan, Golam alikuwa mbali kidogo kakaa kaegemea mti peke yake. Usiku mnene ulifika msitu wote ulitulia, moto uliendelea kuwaka polepole, Golam alinyanyukla pale alipo na kuja kwa wenzake “Amata!” akamuamsha Amata kwa upole Amata akaamka, Golam akamuonesha ishara ya mkono kuangalia upande wa pili, Amata aliona wasichana wawili kwenye kamfereji wakiwa kama walivyozaliwa, weupe, warembo wana nywele ndefu. Wakiwa wanatazamana macho na wasichana wale, mara wale wasichana wakaanza kuwaita kwa ishara ya mkono, Golam alichanganyikiwa akiwa kasimama wima mwili wake ukionekana wenye hitaji baada ya kukaa gerezani miaka sita bila kuona hata utupu wa mwanamke alivutiwa na wasichana wale hata kusahau kila kitu na kutamani kwenda. Amata aliwaangalia kwa makini, akili ikamrudia ghafla ‘msituni hapa wasichana hawa wametokea wapi?’. “Golaaammmm” Amata aliita kwa nguvu, ukelele uliowaamsha wengine, Golam aliendelea kuelekea kwa wale wasichana huku akianza kuvua nguo zake, Golam aliwafikia wale wasichana nao wakamdaka na kuanza kufanya mapenzi, kelele za mahaba zilisikika kwa nguvu hata zikageuka kuwa kelele za kutisha za wanyama wa ajabu lakini pale walipokuwepo hapakuonekana mtu tena.
**************
Amata alibaki kaweka mikono yake kichwani huku akitokwa na machozi, Saringo Alishindwa kujizuia kulia kwa sauti na uchungu Hellen alimsaidia kumnyamazisha na kumpa moyo, Stephan alibakia akiangalia kwa mbali japo mkononi mwake alikuwa na bunduki yake kubwa lakini haikuweza kufanya chochote kwani pale walikutana na ulimwengu mwingine. Upepo ulivuma taratibu usiku ule na moto uliendelea kuwaka taratibu, wakiwa wameuzunguka moto huo kila mmoja akiwa kimya akipanga na kupangua yaliyo kichwani mwake “Msitu umemmeza…” Amata alisema kwa sauti ya upole “One down, four to go!” Hellen aliongeza huku akirushia vijiti katika moto. Milio ya bundi na wanyama watawalao usiku vilisikika kutoka ndani kabisa ya msitu huo “Masikini Golam!” alisikitika Saringo, Amata akamsogeza karibu na kumbana ubavuni kwake akimpa maneno ya faraja. Hellen aliinuwa mkono wake wa kushoto na kusoma saa yake iliyokuwa bado inajizungusha kuonesha wakati unavyokwenda, ilitimu saa kumi na nusu alfajiri, akavuta begi lake na kutoa kijiguduluia kidogo na kutengeneza kahawa ambayo wote walikunywa na kuchangamka upya. Alfajiri hiyo ilikuwa tulivu, kibaridi kilipuliza kwa upole, wote wanne walianza safari ya Solondo kwa siku ya pili, “Sasa tuwe makini zaidi maana tunazidi kuingia ndani ya msitu wa Solondo na tunakabiliwa na mauzauza mengi” Amata aliwasisitizia wenzake huku wakiendelea kukatisha pori lile nene, walikokuwa wakienda wote hawakujui isipokua tu kadiri ya maelekezo ya mchoro wa kale ambao mara nyingi Stephan na Saringo waliusoma uliwaelekeza upande Fulani na sasa uliwaekeza kuutafuta mbuyu mkubwa ambao upo huko ndani ya msitu na kwamba kutoka mbuyu huo ndio hasa atapata maelekezo sahihi ya wapi waelekee. Waliendelea mbele huku wakitumia panga kukata manyasi marefu yaliyofanya njia hiyo kuwa ngumu kupita. Amata aliyekuwa mbele alitumia ujuzi wake wote kukata manyasi hayo ambayo kana kwamba yaliwasihi wasiendelee na safari yao ngumu. Wakiwa katika mwendo wa tabu sana dhidi ya nyasi ndefu na vichaka vya kutisha, miba mikali iliyowachoma na kuwakwangua kila upande wa miili yao lakini hawakukata tama hata kidogo, mara wakasikia mvumo kama wa wadudu wengi warukao, Amata alipoinua macho kutazama juu aliona mzinga mkubwa wa nyuki na wengi wakirandaranda huku na huko, Amata akawapa ishara wenzake kuonesha wawe watulivu dhidi ya nyuki hao wenye hasira. Helen alionekana kuchoka sana akiwa kamuegemea Stephan begani huku wakiendelea na safari yao “Tupumzike kidogo” Stephan aliomba kwa kutumia Kiswahili chake cha kubabaisha, jua lilikuwa ni kali mno wakaketi chini ya mti mkubwa na kupumzika wakinywa maji na mikate waliyobeba. “Amata, inaonekana safari za msituni unazijua sana eee!?” Saringo alimuuliza Amata “Nilipokuwa na marehemu baba yangu tulikuwa tukienda kuwinda mara nyingi na yeye ndiye alinifundisha lugha na tabia ya msitu” Amata akajibu huku akiendelea kula mabungo aliyoyachuma porini. “Lugha na tabia ya msitu! Ni vitu gani hivyo?” Saringo aliuliza kwa mshangao, akasogea karibu na Amata kana kwamba alitaka kujua vizuri juu ya maneno hayo. “Msitu huongea Saringo, na una tabia pia kama wewe ulivyo!” Amata alijibu “msitu una mambo mengi sana, hatari kubwa zipo, vyakula vingi vinapatikana na pia wanyama wa kuliwa na kula binadamu wapo” akamtazama Saringo aliyeonekena kuvutiwa na habari hiyo “pia msitu hukwambia juu ya hatari ijayo na ya namna gani, baba yangu alinifundisha haya yote kwa kuwa yeye kalelewa msituni robo tatu ya maisha yake” Amata alimalizia kusema. “Ina maana wewe umeshawahi kuja huku Solondo?” Hellen alimtupia swali Amata “Hapana, ni mara yangu ya kwanza kuja ndani kabisa ya msitu huu, na baba yangu aliniambia nisije kujaribu kuingia maana msitu huu unaaminiwa unakula watu, sikuwahi kuelewa kauli ile lakini sasa nimeijua maana yake!” Amata alimjibu Hellen “Kwa vipi umeijua hiyo kauli?” Stephan alidakia “Golam! Golam amemezwa na msitu” alijibu na kutikisa kichwa kuoneshwa masikitiko yake, kisha akaendelea “tunakokwenda hatukujui lakini hatari kubwa iko mbele yetu, kwa kuwa tumeamua tuendelee, ila tusishangae tutakapopoteana huko mbele” Amata alimalizia kauli yake na kumtolea tabasamu Hellen akageuka upande wa pili kwa kuwa daima hakupenda kumwangalia Amata usoni maana tangu alipomuaona mara ya kwanza kule mtoni mara baada ya kutoroka gerezani alijikuta moyo wake ukimpenda ghafla kijana huyu, fukara asiye na dira ya maisha lakini mzuri wa uso na siha ya kiuanaume zaidi ya hapo kwa ujasiri mkubwa alionao wa kupambana na hatari na kujitolea mhanga, hilo ni swala ambalo Hellen lilizidi kuongeza mapenzi kwa Amata tatizo tu ni kuwa pale alikuwa na mchumba wake Stephan hivyo hakuthubutu kabisa kuonesha hali hiyo, na mara nyingi Saringo alipokuwa jirani na Amata, Hellen alisumbuka sana moyoni. Stephan aliinuka pale alipoketi na kuchukua kimkoba chake kidogo ambacho ndani yake kulikuwa na kibuyu kidogo akaenda karibu na kijito kidogo umbali wa kutupa jiwe, kijito kile kilichosongwa na mitete mingi kilikuwa na maji machache yakitembea kwa taratibu sana. Alipofika pale alichota maji na kujaza kibuyu chake, kisha akaanza kutoa nguo zake ili apate kujimwagia maji. Amata akiwa kwenye maongezi na Saringo na hellen mara Amata akanyamaza ghafla na kutaza kwenye mitete ile akamuonesha ishara saringo ya kumuomba uta wake, amata aliupokea na kujiweka vyema “Nini Amata?” Hellen alimuuliza “Chatu! Nyoka mkubwa anayeweza kumeza mtu” Amata alijibu. Hellen akajificha nyuma ya Amata, Saringo alikuwa akiangalia kwa makini lakini hakuweza kuona cha kufanya alisubiri kuona nini Amata anataka kufanya, kwa upole Amata aliweka mshale sawia katika uta wake na kuvuta kwa nguvu zake zote, mikono yake iliyojaa misuli ya nguvu ilituna na kuonesha kiasi gani nguvu alizotumia kuvuta uta huo, huku akiongea lugha isiyoeleweka akiwa ameuma meno bado hakuachia pigo lake, kilichoonekana ni jinsi tu alivyoutembeza uta huo taratibu sana kutoka upande mmoja kwenda mwingine. Kutoka ndani ya mitete ile nyoka mkubwa alifyatuka kwa spidi ya ajabu kuelekea alipo mtoni alipo Stephan, Amata aliachia uta wake na mchale uliondoka kwa spidi kali kukikabili kichwa cha nyoka yule, hamad!! “Stephannnnnnn!!!!!” Hellen alipiga kelele ya nguvu na Stephan alipogeuka alishuhudia joka kubwa refu lililofungua domo lake likimuelekea, mara alishuhudi kitu kikipita kwa kasi kati yake na joka lile, ulikuwa mshale wa Amata aliopigwa kwa ustadi lakini kutokana na ukelele wa Hellen Joka lile liligeukia upande ulikotoka ukelele hivyo kufanya shabaha ya Amata kuwa ya bure. Joka lile lilijivuta na kuburizika chini likijikunjakunja kuelekea walipo akina Amata, Amata alijinyanyua na kujirusha upande wa pili akimvuta Saringo wakati huo Helleni alijiinua na kujikuta amechelewa, alipigwa ngwala maridadi sana na joka lile na kupaishwa juu, kabla hajafika chini joka lili lilimdaka kwa ustadi mkubwa na kujiviringwa mwilini mwake, likiwa linadondoka kwa kwa kasi, Amata alikuwa tayari kesha vuta uta wake na kuuwachia, shabaha ya ajabu! Mshale ule ulipenya sawasawa karibu kabisa na kichwa cha joka lile, kutokana na maumivu yale joka lile likamuachia Hellen na kudondoka chini Hellen nae akadondoka juu yake, Joka lile likajivuta tena kumkimbiza Amata, amata hakukimbia mbali bali aliuzunguka mti ule waliokuwa wamekaa huku akiweka vizuri mshale wake wa tatu alijikwaa na kuanguka vibaya, joka lile likamtia mkononi likamviriga vizuri, bahati nzuri mkono mmoja wa Amata ulikuwa nje ya mvirigo ule “Amataaaaa….” Saringo aliita,
Saringo aliita na kumrushia kisu ambacho Amata alikidaka kwa ustadi mkubwa na bila kuchelewa alididimiza kisu kile kwenye sehemu ya mwili wa joka hilo, joka likajiinua juu likiwa bado halijamuachia Amata, Amata alisikia mlio mkali na alichokishuhudia ni damu iliyoruka kwa matone makubwa makubwa, joka lile halikuwa na kichwa tena, likaanguka kwa mshindo mkuu, ilikuwa ni risasi kutoka AK 47 iliyopigwa kwa ustadi wa hali ya juu na Stephan na kukitawanya kichwa cha joka lile na kukichanachana vibaya. “Nice shot!!” Hellen alimsifu Stephan, wakakumbatiana na kubusiana kama ishara ya kupongezana. Saringo alimfuata Amata pale alipolala na kumsaidia kujitoa katika joka lile, haikuwa kazi rahisi kuukunjua mwili wa joka lile kubwa ambao kwa wakati huo ulikuwa bado umejiviriga katika mwili wa Amata. Helen na Stephan nao waliungana na Saringo katika kazi hiyo, mara wakafanikiwa na kumnasua Amata ambae uso wake ulikuwa umechafuka kwa damu ya joka lile, wakamlaza vizuri na kumuosha uso wake. Mikono laini ya Saringo ilipita usoni mwa Amata, Amata akajittikisa kidogo na kuushika mkono wa Saringo “Nini Amata?” saringo alimuuliza “Mkono wako laini umenisisimua mwili…” Saringo akatabasamu aliposikia maneno hayo ya Amata “Usianze Amata!” Saringo akasisitiza. Amata aliketi na kutazama vizuri huku na huku, akaokota uta na podo lake akaweka mgongoni… safari inaendelea! Msitu ulizidi kuwa mnene mbele yao, lakini Stephan aliyekuwa na ramani ya wapi wanakokwenda alisisitiza kuelekea upande huo hata kama haukuwa na njia, walisonga mbele, panda milima, shuka, vuka mto pasua vichaka, mvua, jua vyote vilikuwa juu yao, chakula kikubwa kilikuwa ni matunda ya porini ambayo kwao walijitosheleza na kujipatia vitamini za kutosha sio mpaka akuandikie daktari. Jioni hiyo ya siku ya tatu mvua ilikuwa kubwa sana, radi zisizo na huruma zilipasua anga lote na kulifanyia michoro ya kutisha, hapakuwa na pa kujikinga wala kujificha, wote walitota miili hata nguo zao kugandamana na miili yao, walitetemeka kwa baridi kali ya msituni hata miguu ilishindwa kutoa ushirikiano na mwili mara nyingi ilikataa kusonga mbele, hakukua na lakufanya isipokuwa ni kujivuta hivyo hivyo, walitamani jua liwake haikuwa hivyo, walipanda wakoke moto lakini kila kitu kililowana, safari ilizidi kuwa ngumu kwani msitu wote ulifunikwa na ukungu mzito hata mwanga wa tochi haukufua dafu. Amata alisimama na kugeuka nyuma akawaonea huruma wenzake maana walikuwa wakitetemeka kupita maelezo. Saringo alimuendea Amata na kumkumbatia kwa nguvu huku akitetemeka, vivyo hivyo kwa Hellen na Stephan, walivuta hatua fupifupi japo kwa shida kujitafutia mahali pa kupumzika. “Tukae humu mpenzi!” Amata alishtuka kidogo kusikia kauli hiyo toka kwa Saringo, alibaki kujiulizauliza maana hajawahi kuitwa mpenzi katika maisha yake. Amata alitazama na kuona pango pembezoni mwa mti kabla hajaamua cha kufanya Stephan na Hellen wakawa tayari wamejitoma ndani ya pango hilo lenye kiza, “Amata twende!” Saringo alisema huku akimvuta mkono kuelekea pangoni, Amata alimvuta Saringo kwa nguvu na kumkumbatia kifuani mwake, akamkazia macho Saringo alimtazama Amata usoni kwa hasira lakini hakuwa na la kusema alizungusha mikono yake mgongoni kwa Amata na kuikutanisha kisha kuegemeza kichwa chake kifuani mwa Amata. Amata alitulia kimya kwa muda akiangalia lile pango waliloingia akina Stephan “Saringo! Unafikiri hilo ni pango? Isije kuwa mtego tu” Amata alimuuliza Saringo “Wenzetu wameingia wewe hutaki, Amata una nini twende!” Saringo alisisitiza “Saringo! Mbona hatumsikii Stephan au Hellen hata kutuita!? Nina wasiwasi hili si pango la kawaida!” Amata aliposema maneno hayo Saringo akashtuka na kugundua kuwa ni kweli hawa viumbe wawili wangeshawaita lakini kimya yapata dakika kumi sasa, Saringo akamuachia Amata, akaokota kipande cha mti kilicho jirani hapo akakirushia ndani ya pango lile lakini hakusikia chochote hata mdondoko wa kipande cha mti, Saringo akajishika mdomo na kuanza kutoa machozi. “Saringo! Hapa ni msituni, usilie, tulia, jikaze kama mwanamke. Kilichobaki hapa ni kutafuta cha kufanya kwa kuwa sasa tumebaki wawili wenzetu tayari msitu umewameza” Amata alimbembeleza Saringo “Hatuna silaha za kutosha itakuwaje kupambana na maadui?” Saringo alimuuliza Amata. Amata akatazama podo na uta wake akajikuta kabakiwa na takribani mishale kumi na tano podoni, akatikisa kichwa akaingiza mkono kwa ndani ya suruali yake kama anayetaka kutoa dhakari ili ajisaidie, Saringo akasogea pembeni kidogo kwa hofu maana hakujua Amata anataka kufanya nini, alipotoa mkono ukatoka na bastola moja. Saringo alishangaa “Umeipata wapi?” Saringo alimuuliza Amata “Alinipa Hellen nimuhifadhie” alimjibu Saringo na kumtupia swali “unajua kuitumia?” “Ndio!” Saringo akajibu huku akiichukua mikononi mwa Amata na kuigeuzageuza kisha akatikisa kichwa kuashiria amekubali, akajaribu kama analenga kitu, Amata akampatia kibox kimoja cha risasi, Saringo akakipokea na kukihifadhi vizuri… Stephan na Hellen waliingia kwenye kitu kama pango lakini halikuwa pango la kawaida bali ni kama shimo lakini halikuenda chini isipokuwa lilikuwa na mteremko mkali sana, hawakuweza hata kufanya lolote bali waliporomoka ndani kwa kasi ya ajabu na huku kulikuwa na giza nene kuliko giza lenyewe, waliendelea kuseleleka hakuna aliyepiga kelele kwani kati yao kila mmoja alikuwa akitahamaki. Baada ya kama dakika tano za mseleleko ule Hellen alijigonga kwenye kitu kama ukuta au jiwe na kupoteza fahamu, Stephan hakujua afanye nini maana giza ni nene, huku akiwa anavuja damu mkononi mwake kwa kuwa alichunika vibaya sehemu ya nyuma ya mkono wake, alitoa kiberiti na kuwasha angalau apate mwanga kidogo, lakini mwanga ule bado haukufua dafu kwa giza lile. Stephan aliegeme kitu kama ukuta lakini alihisi ulikuwa rafu sana alijaribu kuvuta hisia na kutega sikio lake kwa makini labda atasikia chochote ama watu kuongea au chochote, lakini hakusikia kitu, taratibu macho yalianza kupambana na giza lile na kuanza kuona japo kidogo, akiwa bado katika kutambua kilichopo ndipo aliposikia kwa mbali mtweto wa mtu anayehitaji msaada, mara moja akagundua kuwa bila shaka ni Hellen lakini hakujua upande upi hasa yupo akajaribu kuita kwa upole, lakini bado aliendelea kuusikia ule mtweto ambao kwa sasa ulikuwa wa taratibu lakini ulisikika kutokana na ukimya wa mle shimoni, alijaribu kupanda taratibu haikuwa rahisi kwa kuwa hapakuwa na pakujishikia ila tu alisaidiwa na vipande vya mawe vilivyochomoza huku na huku, mara akamfikia Hellen ambaye alikuwa amenasa kwenye jiwe fulani kumbe hakuwa mbali na pale alipoangukia Stephan, alijaribu kumnasua pale aliponasa na lile jiwe likang’oka kumbe lilishikwa tu kwa udongo, wakaporomoka nalo mpaka pale chini. Stephan alitoa mguno wa uchungu na kishindo kile kilimrudishia fahamu Hellen, Hellen aliangalia huku na huku na kumgeukia Stephan “Tuko wapi Stephan? Amata na Saringo wako wapi?” hellen aliuliza huku akionesha kuweweseka. Stephan alimtuliza akiwa hajui nini cha kufanya zaidi kwa wakati ule alitazama uku na huku na akagundua kuwa lile shimo lilikuwa linaendelea lakini sasa si kwa kwenda chini bali tambarare ambapo unaweza kutembea ukiwa wima, bila kupoteza muda alisimama na kumuinua Hellen, akiwa bado na bunduki yake mgongoni walianza kutembea taratibu ndani ya shimo lile wakiwa hawajui wapi wanakoelekea,Hellen alikuwa anamfuata tu akijua labda Stephan anajua chochote, waliendelea kwenda nusu wakitembea na nusu wakikimbia ili mradi wafike wanakokwenda. Hellen alianza kushikwa na woga aliushika mkono wa Stephan kwa nguvu zote akiwa anatweta kwa nguvu, mara Stephan akasimama akainama na kushika magoti yake huku akitingisha kichwa kwa masikitiko “…tumekwisha! Hellen, sijui hata tuendako”. Alichukua bunduki yake nakufanya kama analenga kitu lakini hakuna alicholenga akafyatua bunduki yake na ukelele wa bunduki hile ulijirudia mara nyingi kabla hakujakua kimya tena, haja yake asikie tu kama kuna mlio mwingine utakaosikika zaidi ya huo wa bunduki hiyo. Taratibu waliendelea kutembea na kutembea mwisho walichoka na njaa iliwashika wakaketi chini na kila mmoja alipitiwa na usingizi kwa muda wake. Safari ilikuwa ngumu kwa Amata na Saringo, chakula chao kikiwa ni matunda ya mwituni na maji ya mtoni, waliendelea kwenda wakiwa hawajui hasa ni upande upi ambao wanatakiwa kuelekea. “Nahisi tunapotea !” Saringo alisimama na kusema huku kajishika kiuno “Tufanyeje sasa! Tuendelee mbele labda tutajua la kufanya” Amata akamjibu huku akimsika mkono akimaanisha safari iendelee. Saringo ambaye wakati huo alioneka uso wote kusawajika kwa uchovu alijivuta kwa hatua za taratibu na kufuata kule alikoongozwa na Amata. “Twende mpaka tupate mahali pazuri pa kupumzika maana jioni nayo imeshakaribia” Amata alimueleza Saringo huku wakiendelea na safari hiyo isiyo na mwisho bali yenye hatari na misukosuko mingi. Baada ya kutembea kwa muda walifika eneo moja ambalo liko wazi sana kama kiwanja cha mpira lakini ilikuwa ni katikati ya msitu, katika eneo hilo kulikuwa na nyasi nzuri za kijani fupifupi lakini katikati kulikuwa na mbuyu mkubwa sana mnene ambao juu yake ulionesha wazi kuwa kulikuwa na mibuyu iliyoning’inia, Amata alisimama kabla ya kuingia katika uwanda ule akatafakari mawili matatu, akamgeukia Saringo “Umeona! Umeona mbuyu ule?” alimuuliza Saringo ambaye kwa wakati huo alikuwa kamuegemea Amata begani kwa upande wa mgongo. “Huu ni uwanja au kitu gani?” Saringo naye alitupa swali kwa Amata, “Hapana huu si uwanja hapa lazima kuna kitu, Stephan alitueleza kuhusu mbuyu siyo ule?” Amata alimuuliza Saringo, kwa hamaki kubwa saringo aliutazama mbuyu ule, kikapita kimya cha dharula. Akatikisa kichwa kwa ishara kuwa amekubaliana na Amata “Yeah utakuwa ndio wenyewe! Alisema upo katikati ya uwanja, ndiyo nimekumbuka, ndiyo utakuwa ni huu” saringo aliongea kwa upole sana katika hali ya kushangaa. “Mbuyu wa Shetani!!!” Amata aliongezea kwa upole uleule “Unasemeje Amata? Mbuyu wa Shetani?!” Saringo alimwangalia Amata usoni na kumtupia swali lile. “Ndiyo Saringo, ule ni mbuyu wa Shetani! Unaitwa Mbuyu Kolo… mbuyu wa maajabu, babu yangu alinisimulia mengi sana juu ya mbuyu huu” Amata alimueleza Saringo huku akiwekaweka manyasi vizuri kwa kukaa chini. “Saringo!” Amata aliita taratibu na saringo alimgeukia “Bee, Amata unasemaje?” huku akikaa katikati ya miguu ya Amata na kumlalia kimgongo kifuani. “Ni nini mnakitafuta huku porini? Na akina Stephan?” Amata alimuuliza Saringo. “Ni stori ndefu sana Amata, ndefu mno” Saringo akashusha pumzi ndefu na kumeza mate kwa shida kutokana na ukavu wa midomo yake. “Niambie tu, maana hapa tutalala ili kesho tujue cha kufanya, ila lazima tulale juu ya mti kuepuka wanyama wakali wenye uchu na nyama tamu yenye chumvi ya Binadamu” Amata alimueleza hayo saringo huku mikono yake akimzungushia saringo kwa mbele kwa kuipitisha chini ya makwapa yake, alifikiri atapata upinzani kwa kitendo hicho lakini la, Saringo aliivuta na kuikutanisha juu ya kifua chake kisha akainamisha kichwa kwa nyuma na kumuangalia Amata kwa juu “nakupenda Amata!” alimwambia huku akitabasamu, Amata akapotezea kimtindomtindo. “Amata! Tukimaliza safari yetu tutakuwa matajiri sana, tunakwenda Solondo kuchukua sanduku kubwa na ndani ya sanduku hilo kuna mali nyingi sana, dhahabu, almasi, yaspi, lulu za aina mbalimbali, mawe ya thamani tofauti” Saringo alimwambia Amata, Amata alimkazia macho saringo “Nani aliyekwambia Saringo?! Solondo ni msitu wa kifo, msitu unaokuwa hai na kumeza kila aingiyae…” Amata alieleza lakini saringo alimkatisha
“Hapana amata, hizo ni hadithi za kale, si za kuamini, wazee wetu walitusimulia ili tuogope kabisa kuingia ndani ya msitu huu lakini ukweli ni kuwa ndani ya msitu huu wajerumani wamehifadhi vitu vingi sana na babu wa baba yangu alikuwa askari wao amekuja sana huku kuleta vitu walivyokuwa wakivichimba huku na huko katika nchi yetu! Watu wengi waliuawa na wajerumani ndio na hawakurudi tena vijijini mwao ndio maana hizo hadithi zenu zikawepo” saringo aliongea kwa jazba “…hadithi zenu !!! hadithi zenu!!!” Amata alijiwazia moyoni akijaribu kulinganisha asemayo Saringo. Amata akashusha pumzi akibaki na maswali mengi kichwani akatoa pera akaanza kutafuna huku akichezesha kichwa chake kama mtu anayefuatisha muziki fulani. Wakiwa katika hali ya ukimya sana kila mtu alizama katika mawazo yake ambayo hakuna mwingine aliyeyajua “Dunia imekuharibu umesahau mila na desturi za nyumbani” aliropoka Amata kumwambia Saringo, Saringo alihamaki kwa kauli ya Amata na kumtazama usoni sasa sio kwa sura ile legevu bali yenye jazba na uchungu “Unasemaje Amata?!.. wewe unaendekeza ujinga na upumbavu wa kijijini! Hujui hata dunia upande wa pili inaendeleaje, lazima maisha yabadilike, mimi naishi mjini naelewa lakini wewe umezaliwa na kukulia huku porini utajua nini, fuata nnayokwambia” saringo alifoka. “ Huwezi kuniamrisha kufuata unayonambia wewe ni mwanamke tu, kama mimi nimekulia huku mshamba wa kizamani kwa nini mlinitafuta katika safari yenu hii isiyo na miguu wala kichwa, na usomi wenu na maendeleo mliyonayo mngefika wapi? Stephan yuko wapi , hellen yuko wapi? Mbona wamepotea bila kujua, na we bado zamu yako. Lazima udumishe mila na desturi, asili itabaki kuwa asili tu!” Amata alifoka pia. “Asili itabaki kuwa asili tu” Maneno haya yalimchoma sana Saringo na yalimrudia mara kwa mara. Saringo akanyanyuka na kusogea pembeni, akaketi na kuikunja miguu yake kuelekea kidevuni huku akiwa kaizungushia mikono yake aliinama na kulia kwa vikwifukwifu. Giza liliufunika msitu taratibu, sauti za ndege na mbweha zilisikika huku na huko, macho ya Amata yalikuwa yanapambana na usingizi uliokuwa unayasumbua huku wadudu nao wakifurahia kuona kiumbe hiko katika makazi yao, hakuona njia nyingine zaidi ya kutafuna matunda yake aliyoyahifadhi vyema katika mkoba suruali yake ile ya kimagereza, huku akitumia nguvu nyingi kujaribu kuangaza angaza kuona kama kuna hatari yoyote inayowakabili, alimwangalia Saringo na kugundua kuwa tayari alikuwa amelala ‘wanawake bwana!’ alijisemea moyoni huku akitikisa kichwa chake kuonesha kukata tamaa. “We mbona unalala kibwege hivyo? Unafikiri uko kwenu hapa!” alimuamsha Saringo kwa kumtikisa na kumwambia maneno hayo, saringo alinyanyua kichwa na kumtazama Amata kwa sura yenye mikunjo ya usingizi na uchovu. Amata alitabasamu na kukumbuka maneno aliyoambiwa na baba yake ‘ukitaka kuchagua mchumba mtazame anapoamka’ hapo alihakikisha baada ya kuona sura ya Saringo alipotoka katika kipande hicho cha usingizi, akarudi alipokaa na kusimama kwa muda kisha alimfuata Saringo, kibaridi kilichukua nafasi yake msituni hapo na wakiwa wamejikunyata kila mmoja kamshika mwenzie ili kupata kajoto wakapitiwa na usingizi uliowachukua kwenda ulimwengu wa mbali.
Saringo alibebwa juujuu na watu wa ajabu wenye mguu mmoja huku wakiimba nyimbo zisizoeleweka, wakizunguka naye katika mduara mkubwa ambao katikati yake kulikuwa na moto mkubwa sana, ngoma zilirindima, wengine walioketi pembeni walionekana kunywa kitu kama pombe kwenye kata kubwakubwa huku wakifurahia na kucheka kwa sauti za ajabu, Amata aliketi palepale akiangalia huku akitetemeka kwa woga wa ajabu, kijasho kilimtoka kila alipotaka kupiga kelele za kuomba msaada alijikuta sauti haimtoki na wale viumbe walimcheka sana, akajaribu kujitikisa hakutikisika kabisa kumbe alikuwa amefungwa katika mti mkubwa uliopo katika uwanja ule ambao ngoma hiyo ya ajabu ilipigwa na kuchezwa na hawa viumbe wa ajabu. Bado wale wengine waliendelea kucheza huku wamembeba Saringo juu kwa juu wakipokezana kwa furaha, mara wakamshusha na kumlaza katika jiwe kubwa lilichongwa kama ngalawa lakini halikuwa na shimo katikati, akiwa kama alivyozaliwa juu ya lile jiwe hakuweza hata kutikisika, Amata aliangalia kwa makini akitaka kujua wanataka kumfanya nini lakini kila alipojitikisa hakutikisika na kila alipofanya hivyo alisikia sauti za ajabu zikimcheka sana aliogopa na kutulia tuli kama maji ya mtungini. Ilikuwa ni sherehe ya ajabu ambayo Amata hakupata kuiona tangu azaliwe katika dunia hii, akiwa katika hali ya kutaharuki hakupenda kuona kinachoendelea, alifumba macho yake kwa nguvu zote lakini bado akili na moyo wake vilitaka kuangalia kinachoendelea, aliyafumbua macho yake na alichokiona kilimchanganya kwa kuwa hakuelewa ni nini na kwa nini,wanawake saba waliokuwa uchi wa mnyama wakiwa wanatokea ndani ya kitu kama pango ambalo liko chini ya mti mkubwa kichwani walijitwika vitu kama vyungu wakiwa wanatembea kwa mwendo wa kurukaruka kwa kuwa walikuwa na mguu mmoja kila mmoja, waliimba nyimbo zisizoeleweka na wale wanaume waliombeba Saringo juu juu na kumlaza pale katika jiwe waliendelea kucheza ngoma ile isiyoeleweka, Amata alikuwa na woga mkuu akitetemeka mwili wote. Wanawake wale walilizunguka lile jiwe na kutua vyungu vilivyokuwa kichwani mwao, mmoja wao aliyeonekana kama ndiye kiongozi wao alitwaa chungu kimoja na kukinyanyua juu kama anayefanya sala fulani, kisha akakishusha akakiweka pembeni ya miguu ya Saringo akaingiza mikono yake na kuchota kitu kama mafuta ya kupikia na kuanza kumpaka Saringo akianzia miguuni kisha na wenzake nao wakafanya hivyo, sasa walimpaka mwili mzima huku wakiongea lugha ya ajabu ambayo Amata alijaribu kuisikiliza lakini hakuilewa ‘hawa viumbe gani?!’ Amata alijiuliza bila majibu, aliendelea kutazama kwa woga. Wanawake wale walipomaliza kazi hiyo walinyanyuka na kurudi kule walikotoka na kumuacha Saringo akiwa kalala pale aking’aa kwa mafuta yale pindi akiangazwa na mwanga wa moto ule akiwa kimya kabisa, Amata hakujua kama saringo alikuwa mzima au la maana misukosuko yote yeye alikuwa kalala kama mfu hakujitikisa wala hakufanya lolote. Mara wale wanaume wakaanza tena ngoma yao sasa kwa uchangamfu zaidi huku wakipiga makelele ya ajabu na kurukaruka, ndipo Amata akagundua kuwa ule mguu mmoja walionao kila mmoja wao huku chini ulikuwa na kanyagio kama la kuku, mara upepo mkali ukaanza kuvuma na wao wakiwa bado wanacheza ngoma yao sasa wakionesha munkari zaidi, mara kutoka katika mti ule ambao waliingia wale wanawake joka kubwa lilibuka kwa kasi ya ajabu, “Ssss……” Amata alijaribu kumuita Saringo lakini sauti haikuweza kutoka hata kidogo, joka lile lilijikunjua kwa kuzunguka likiwa hewani sasa likiwa linaelekea pale alipolazwa Saringo, na liliposikia sauti hafifu ya Amata likageuka huku aliko na kutema mate kwa kasi kumtemea Amata,
******************************
..mara Amata akazinduka kutoka usingizini, alikuwa akihema kama mtu aliyekuwa akikimbizwa, “Saringo, Saringo!” Aliita huku akiweweseka. Alipotulia alijikuta kaloa mwili mzima na pembeni yake kuna kitu kama kata kubwa liliotelekezwa na ndani yake kulikuwa na maji kidogo, ndipo alipogundua kuwa kamwagiwa maji nandiyo ylaiyomfanya akurupuke kutoka katika usingizi wake, lakini nani alimwagia maji hakumjua wala hakumuona, wala Saringo hakumuona eneo lile, nalipoangalia vizuri aligundua kuwa hakuwa pale ambapo alipitiwa na usingizi, hapa ni mahali pengine kabisa ambapo hakupajua kabisa, aliangaza macho huku na kule lakini hakuona dalili ya mtu wala mnyama, palikuwa patupu miti ikiwa imezunguka kwa mbali na katikati palikuwa wazi ni nyasi fupifupi tu zilijaa katika eneo lile. Alijinyanyua kutoka pale alipokaa na kusimama wima, alivuta ukimya kidogo kuona kama kuna kitachotokea awe mtu au mnyama lakini hali libaki kuwa ileile ‘hapa ni wapi?’ Amata alijiuliza lakini hali ilikuwa ni ile ile, mara nyuma yake akasikia sauti ikimwita kwa kunong’ona ikirudiarudia jina lake, amata alitulia na kimya huku akiwa hajui cha kufanya, moyo ulimdunda kwa kasi akageuka taratibu kuona ni nani aliyemuita, Amata alitahamaki, hakuamini macho yake alichokiona. Bibi kizee aliyechoka, ngozi yake imekauka kwa kukosa vitamini, macho mekundu ya kutisha, nywele zote nyeupe na unaweza kuzihesabu, miguu yenye vidole visivyo na kucha, Amata alimwangalia kwa umakini ajuza yule lakini moyoni akijawa na hofu, ‘hakika ajuza huyu angekuwa kwenye mikoa ya upande fulani wa nchi asingekuwepo hii leo hasa kwa macho yake’ mawazo haya yalipita haraka kichwani mwa Amata. Ajuza yule hakuwa hata anatikisika alisimama vilevile huku akisaidiwa kwa mkongojo ule alioushika, alimkazia macho Amata, kwa wakati huo Amata hakujua la kufanya, akimbie? Hapana, Amsalimie? Hakuna jibu, sasa afanyeje hakika ulikuwa mtihani mkubwa sana kwake, “Amata…” bibi yule aliita tena kwa sauti ya kukwaruza na mbaya huku akimwangalia Amata, Amata alimwangalia kwa umakini na kuanza kurudi nyuma taratibu “Usiogope Amata, sogea hapa!” yule bibi alimsihi Amata huku akimuonesha ishara ya kumuita kwa mkono, Amata kwa woga alimsogelea bibi yule na alipomkaribia kabisa mwili wake ulisisimka sana na damu yake kwenda mbio, yule bibi akanyanyua mkono wake na kumpiga Amata kofi utosini, Amata aliona giza nene kisha hakuelewa chochote kinachoendelea.
Saringo aliendelea kutaabika na kuhangaika hakujua ni wapi alipo ila tu aligundua kuwa yuko ndani ya kitu kikubwa cha mviringo, giza kila upande, joto na hewa nzito alikuwa akipambana navyo wakati huo, akijaribu kunyanyuka alishindwa kabisa maana alijigonga kwa juu alijaribu kupiga kelele lakini ilikuwa kazi bure hakuna aliyemsikia huko nje kama alikuwepo. Mara kwa mbali alisikia sauti za watu wakiongea alitega sikio kwa utulivu mkubwa ili angalau asikie wanachokiongea lakini haikuwa hivyo kwani lugha waliyoitumia hakuweza kuielewa hata kidogo ‘Gwelino’ alijiwazia na mara hofu kuu ilimjaa kijasho chembamba kikaanza kumwagika kwani alijua habari za viumbe hawa ambao wanaishi katikati ya msitu huu wa Solondo na hupendelea kula moyo, utumbo, maini na mapafu ya binadamu. Saringo aliona kuwa sasa aliyokuwa akisikia juu ya Msitu wa Solondo yametimia, alijilaumu sana kwa nini na kwa vipi alijikuta akijihusisha na safari hii ngumu na mbaya, alifumba macho yake na kukumbuka maneno ya babu yake aliyokuwa akimsimulia alipokuwa mtoto juu ya safari ya Solondo, alijilaumu sana nafsi yake na roho yake yenye uroho wa utajiri ‘nani aliniambia huku kuna utajiri?alinidanganya! hapana, ni babu alinihakikishia kuwa wamezika mali nyingi huku,ah no! Alinidanganya?’ Saringo alijiuliza na kujijibu, alijilaumu na kujipa moyo, mawazo yake yakamrudisha nyuma sana na kumkumbuka babu yake Mzee Mapendo siku walipokaa wakiota moto naye akamsimulia mengi ya wakati wa ukoloni na utawala wao ambapo hapo ndipo alimsimulia juu hazina iliyofichwa na wajerumani huko Solondo..
Miaka 20 iliyopita… kijijini kwa akina Saringo
Mzee Mapendo aliketi karibu kabisa na moto kwa kuwa yeye aliona baridi wakati wenzake walikuwa wakiona joto kali, pembeni alikuwa na kiko yake na kikombe cha maziwa, wajukuu walikuwa wamemzunguka kama unavyojua babu akaapo. Mzee huyu aliyekula chumvi nyingi alikuwa na maneno mengi ingawaje sasa hakuwa na jino hata moja kinywani mwake, alikuwa ahishiwi simulizi kwa wajukuu zake. Alipenda kujivuna kuwa yeye ni askari imara wa mkoloni aliyeogopwa na kila mtu. “Babu!” saringo aliita kwa sauti kijukuu, wakati huo akiwa na miaka nane darasa la kwanza. “Enhe niambie babu yangu!!!!!” Mzee mapendo alimuitikia kwa bashasha “Babu vidole vyako vya miguumbona sio vitano? Viko vitatu tu!” saringo alirusha swali la uchokozi kwa babuye “A aaa sasa mchumba umeanza udadisi wako! Nikwambie mara ngapi? Hivi vidole vilikatika hukoooo porini huko tukiwa kazini zamani za mkoloni” alijibu kwa kirefu. “Mmmm babu, kazini ndio ukatike vidole!” “Eeeee mama, tulikuwa tunapambana na maadui, mimi nimekwenda vita ya kwanza ya dunia na ya pili ya dunia, mimi askari mtiifu” aliongeza jibu na kuedelea “tulikuwa tunatembea mwendo mrefu kutoka kule kilima cha Saroge kwa mguu wakati huo hakuna mutuka hiz, tumetembea safari ndefu sana tunapanda milima na kushuka mabonde mpaka kuleeee mlima wa Vegani, unaujua mlima Vegani wewe?” alimtupia swali Saringo “Mlima Vegani? Mi siujui babu” saringo alijibu “Aaaaaah kweli huwezi kuujua wewe bado mdogo! Sasa kaa chini hapa nikusimulie!” Mzee Mapendo alimwambia Saringo. Saringo akakaa chini akimtazama babu yake kwa makini huku akifuta makamasi mara kwa mara kwa mikono yake na kufanya sehemu ya kati ya mdomo na pua yake kung’aa kwa makamasi yaliyokauka. Mzee Mapendo akaanza simulizi yake “Tulipokuwa vijana sisi tulikuwa askari wa mkoloni, tulikuwa tunakaa hukoooo Saroge ndiyo ilikuwa kambi ya Mjerumani miaka hiyoooo, sisi tukiwa askari wakakamavu kabisa, tumefuga masharubu yetu tukisimama pale kwenye gwaride aaaaaa mjukuu yaani upepo ukipuliza utasikia kama mtu anapiga mbinja, hiyo ilikuwa ni moja ya sare yetu. Siku moja tukiwa kambini pale king’ola kililia tukatoka ndani wote tukapanga mstari, tukatangaziwa kuwa kuna mgeni amekuja kutoka ujeremani huyu Bwana alikuwa anaitwa aaa nimemsahau kidogo oooh Karl Peter, huyu Bwana alikuwa mrefu na mwenye tambo la kikakamavu haswa alikagua kikosi chetu na aliporidhika tulichaguliwa askari hodari kama kumi hivi na mimi babu yako nilikuwepo. Dhumuni ilikuwa ni kusafiri kwenda huko mlima Vegani alisema kuna mizigo ya kuchukua kupeleka sehemu nyingine. Tulianza safari asubuhi sana kupitia katikati ya pori kubwa, njiani wote tulikuwa kimya sana kila mtu akitafakari juu ya safari ile. Tulifika Vegani baada ya siku mbili, pale mlimani tulikuta watu wengi sana nilishangaa kuona mashimo makubwa makubwa na watu wakiingia na kutoka wamebeba maudongo mengi, sikuelewa ni nini kinaendelea. Pale tukapokelewa na wajeremani wengine wakatupeleka sehemu kupumzika kidogo, tukala halafu ndio tukaambiwa tunatakiwa kusindikiza msafara wa mizigo kwenda Solondo. Asubuhi yake tukaenda katika lichumba limoja kulikuwa na masanduku ya chuma mengi tu ndani yamejaa mavitu mazurimazuri, sisi hata hatukujua ni vitu gani basi tulikuwa na wapagazi wakabeba pale yale masanduku tukaanza safari ya kwenda huko Solondo” Mzee mapendo akakohoa kidogo, kisha akaendelea “safari ile ilikuwa ndefu na ya hatari sana mjukuu wangu, tulipanda milima mikali na kuvuka mito mikubwa yenye mamba wakubwa, tulikutana na nyoka wakubwa wengine wana vichwa viwili tulipambana nao hivo hivo ndio kisa cha vidole vingine kupotea uko huko.” “Sa mlikuwa mnaenda api?” saringo aliuliza “Aah mjukuu wangu, mbali huko kwenye msitu kulikuwa na jiwe kubwa sana chini lina pango kubwa na shimo la ajabu humo ndio tukatengeneza eneo zuri tukachonga ngazi za kupandia na kushuka, tukatengeneza vyumba vingi sana tukahifadhi hayo mamizigo yao, kule wakaweka mamilango makubwa ya chuma na makufuli makubwa funguo wakabeba, mimi mjukuu nikaona hii itakuwa ni mali sana kwa nini wafunge hivi!!!? Tukaongozwa kutoka nje ya hilo pango… mjukuu wangu we hapo walianza kutugawanya makundi makundi kurudi lakini walipanga kutuua sote ili tusije kurudi kule pangoni, muda fulani niliona wanachukua karatasi fulani na kulisoma wakiongea kikwao na kuweka alama fulanifulani kwenye ile karatasi na miti iliyo eneo hilo na mawe walituelekeza kuchonga alama fulani fulani, kisha tukapanda mlima mmoja mkubwa na kusimika chuma kikubwa kimoja kimesimama na kingine kimekatisha katikati yake, ule ndiyo uchawi wao mjukuu, wakatuambia atakayekuja huku atakufa hatorudi tena duniani, tuliogopa sana lakini mimi nikajua huu ni ujanja tu. Mjukuu! wale watu ni makatili bwana!! sisi tulikuwa wanne na wao wawili, tukafika mtoni wakamwambia mmoja wetu avuke kwanza kumbe wanajua kuna mamba alipoingia tu mtoni wale mamba wakamkamata wakamla, halafu wenyewe wanacheka huku wanavuta kiko zao mdomoni, mimi! Mjukuu! nilikasirika sana sikujua nifanye nini, wakatuambia tupite njia nyingine, tukaendelea na safari ile huku kila mmoja wetu akiwa na mawazo mengi”
Mzee Mapendo akaendelea kuchochea kuni zake katika ule moto huku akiendelea kumsimulia habari ile mjukuu wake, Saringo, kisha akaendelea… “Safari ile mjukuu ilikuwa mbaya sana tulipita kwenye nyika kubwa, tukikutana na wanyama wakubwa sana, sasa tulifika sehemu moja kulikuwa na kama kijiji hivi, hapo palikuwa na watu wanaishi lakini watu hawa walikuwa wa ajabu sana, walipotuona walianza kufurahia na kutuzunguka wakitaka kutukamata, walikuwa wanatisha kwa sura, nywele ndefu, wamevaa ngozi, mbaya zaidi walikuwa wanakula watu. Mara tukajikuta katikati ya watu hawa, yule askari mmoja wa kijerumani alianza kuwashambulia kwa risasi kwa kutumia lile bunduki lake kubwa, walipoanza kuona wenzao wanaanguka ndipo walipopata hasira na kutushambulia kwa nguvu, walimkamata mmoja wetu na kumkata kichwa kisha niliona wengine wakinywa damu ile mbichi. Mimi nilifanikiwa kutoroka na mjerumani mmoja tukawaacha wenzetu kule, kwa kweli sijui hata nini kiliwapata. Tulipofika porini yule mjerumani akawa na hali mbaya maana alijeruhiwa sana hakuweza kutembea na kuongea kwake kukawa kwa shida sana alikuwa akitokjwa na damu nyingi mdomoni na sehemu za kisogo chake, hakuchukua muda alikufa, nikabaki peke yangu msituni niliogopa sana, nilipoangalia tulipotoka niliona tu moshi umetanda huko, mjukuu! Hivi vidole vimekatika katika kujaribu kujiokoa na hao wagwelino, hakuna nilichofanya niliamua tu kujaribu bahati yangu, nikachukua yale makaratasi yule mjerumani alikuwa nayo katika mkoba wake na lile libunduki lake, nikatembea msituni usiku na mchana, mwisho nilifika kijijini baada ya siku kadhaa, ule mkoba mpaka leo ninao nimeuning’iniza pale ukutani chumbani kwa bibi yako, ukiwa mkubwa uuchukue ule utakuwa na mambo mengi sana sawa mjukuu ah! ah! ah!, mi ndiyo babu yako shujaa…” alimaliza kwa kucheka huku akimpigapiga Saringo mgongoni. Alipomaliza kusema hayo alikuta kumbe tayari mjukuu wake Saringo ameshapitiwa na usingizi zamani sana na kwake hadithi hiyo ya kishujaa ilikuwa inajirudia kama ndoto mbaya na ya kutisha.
*********************************
Amata alijikuta hana lakufanya baada ya kujikuta kafungwa kamba miguu yake na kuning’inizwa kwenye kitu kama goli la mpira naye yupo kichwa chini miguu juu, kichwa kilimuuma sana hata alikiona kizito, mara kwa mara alijikuta akiona giza na vitu vyeupe vyeupe viking’aa sana vikimzunguka huku na huko. Alipogeuka kwa tabu huku na huko hakuona mtu yeyote isipokuwa mandege makubwa tu yakizunguka na kutua mahali fulani, Amata aliyatambua haraka haya mandege ambayo uyaonapo ujue kuwa kuna mzoga eneo hilo, fahamu zilimrudi polepole Amata na kukikumbuka kile kizee ‘kigagula’ hakuna jirani wa kumuomba msaada, hakuna kiumbe cha kuelewa lugha yake, aliona sasa hapa hana ujanja tena alipenda afe kabla hawa jamaa hawajamfikia akiogopa kupambana na mateso makali bila yeye kujitetea. Inzi na wadudu warukao kwa jinsi zake walikuwa wakimsumbua usoni kutokana na makamasi yaliyokuwa yanamvuja na hakuweza kuyapangusa kwa kuwa mikono yake ilikuwa imefungwa kwa nyuma, alijaribu kuitikisatikisa kuona labda kamba ile inaweza kuwa imelegea lakini haikuwa hivyo. Mara ghafla aliona mti mkubwa uliopo hapo jirani ukitikisika matawi yake na alipoangalia aligundua kuwa ni nyani mmoja mkubwa yuko hapo juu, alijaribu kutoa ishara kwa kichwa labda nyani yule angeelewa kitu lakini haikuwa hivyo hata kidogo. Kwa mbali sauti za viumbe hai zilisikika na kuongezeka zikiwa zinakaribia eneo lile, mara akamuona yule nyani akikimbia tena juu zaidi ya mti na kupiga mruzi mmoja mkali, kumbe alikuwa na wenzake eneo lile wote wakapanda miti haraka na kukaa kimya juu kana kwamba hakuna kiumbe hapo juu. Msafara mkubwa wa watu uliingia pale, watu wakutisha wanaoonekena ni makatili kwelikweli wakiwa wamejichora marangi meupe wamejichanja chale nyingi, kiunoni wamevaa tu kangozi ka kuwahifadhi maeneo yao. Mbele yao wakiongozwa na mmoja wao mwenye tambo kubwa kwelikweli akiwa amebeba lijiti lenye ncha kali linaloonekana kabisa kuwa limelowa damu, nyuma yake walifuata watu kama kumi hivi wanne wakiwa wamebeba kitu kama nyama kinachoning’inia kati ya miti miwili, wakafika pale kwenye kale kauwanja, wakasimama na kushusha ule mzigo, yule kiongozi wao aliongea lugha fulani ya ajabu ambayo Amata hakuielewa, mara wenzake waliitikia kwa kelele huku wakionyoosha juu majiti waliyoyabeba ambayo yalkikuwa na ncha kali na yamelowa kwa damu. Wawili kati yao walitoa ule mzigo, la haula !!! Amata hakuamini alichokiona mwili wa binadamu ambao umetota kwa damu kiasi kwamba hauwezi kuuelewa ni umekumbwa na masaibu gani, Amata alihisi mwili kusisimka na kuchoka kwa wakati mmoja, alitulia palepale akiangalia nini kinaendelea, wakafunga kamba ule mwili kama alivyofungwa Amata na kuja kuning’iniza kwa jinsi ile ile, Amata alijituliza na kufumba macho yake huku akipumua kwa mbali ili wasijue kama ni mzima, walipomaliza kazi hiyo, yule kiongozi wao akasogea kwa Amata na kumwangalia kwa makini sana akachukua kisu kikubwa na kikali akakamkamata Amata upande wa kushoto wa bega lake kisha akacheka kwa sauti ya ajabu na wenzake wakacheka kwa sauti hizo. Amata aliingiwa na hofu ‘mama moyo wangu alihuzunika moyoni lakini alijua basi hakuna kitachosalimika. Yule jamaa akainua bisu lake juu akashusha kwa kasi kuelekea kifua cha Amata, bila kutegemea Amata alimuona lile jitu likiganda na kuanguka kama mzigo, wenzake wakashangaa na kuangalia huku na huku na wasione mtu yeyote, walibaki kujiuliza imekuwaje kwa mwenzao, kiongozi wao, walianza kupiga makelele wakikimbia huku na huku, Amata akajua sasa amekwisha hata yeye hakuelewa kilichotokea alijigeuza kwa tabu kuangalia pale alipoanguka yule mtu, kwa macho hafifu aligundua kuwa mgongoni kwa lile jitu kunakitu kama mwiba wa mchongoma umemchoma, kwa haraka Amata aligundua kuwa hiyo ni silaha hata ri ya ‘Amazonia’ alipata faraja kuwa huwenda kuna binadamu pale aliyefanya kazi ile, kwa hiyo tumaini la maisha lilimjia tena, lakini hakuona dalili yamtu isipokuwa viumbe vile vyenye hasira vikiruka huku na huko wengine wakiwa porini kutafuta chochote, mara wakarudi na aina fulani ya majani wakayapondaponda huku wakiongea lugha ile isiyoeleweka kicha wakamkamulia maji ya majani yale mdomoni yule kiongozi wao baada ya muda kidogo akapiga chafya kama tani mfulululizo akaamka. Amata lijua hapa kazi hii labda huyualiyefungwa hapo kaifanya lakini alipomwangalia aliona ni kama mwili usio na uhai, matone ya damu yakiwa yanadondoka taratibu kutoka mwili wa mtu yule. Amata alijaribu kuangalia kwa machale mwili ule lkini hakuweza kugundua ni wa nani japo alihisi ni wa mmoja wao. Lile jitu likaamka tena sasa likiwa na hasira na kukunja sura yake mbaya sasa halikuwa na huruma hata kidogo, lilichukua lile jiti lake kubwa kuendelea na alichodhamiria. Akiwa kainua tena jisu lake na huku kwa nyuma Amata kabanwa na mti wenye kipago na mtu mwingine ili kuhakikisha lengo lao linatimia. Kabla hajashusha jisu lile mwili wa Amata ulianguka chini, kamba iliyofungwa miguuni mwake ilikatwa kwa ustadi mkubwa sana, Amata alisikia mvumo wa kasi ya kitu kichokata kamba ile, mara moja aligundua kuwa ulikuwa mshale uliorushwa kwa uta wenye nguvu, na aina hii ya mishale ni mishale iliyotengenezwa sana na marehemu baba yake, Amata aliduwaa pale chini hakuelewa nini kinatokea kabla hajapata akili sawasawa alishuhudia mshale mvumo wa mshale mwingine ukielekea upande wake alijigeuza kifudifudi na mshale ule ulipita katikati ya fundo lililofunga mikono yake na kuchoma chini ardhini, sasa kamba ile ilikuwa imefunguka, Amata alisikia mbinja ya ajabu akajiinua haraka aliposimama akapata kizunguzungu cha ghafla kilichomrudisha chini lakini hiyo ilikuwa ni bahati kwake kwani lile jitu lilifurusha jisu lake lililolenga shingo ya Amata lakini shabaha ikakosa malengo, jitu lile lilimfuata Amata pale chini Amata kwa haraka akauchomoa ule mshale pale ardhini na kuurusha kwa mrusho hafifu lakini mshale ule ulitua jichoni kwa lile jitu, damu zikachuruzika kwa kasi, Amata alijiviringa upande wapili na kulifikia lile jisu alilinyakua na kupiga goti moja na kushindilia lile bisu mgongoni kwa lile jitu, lile jitu likatoa mkoromo wa kutisha na kukata roho. Hali haikuwa shwari eneo lile, wale wengine wakaanza kupiga kelele za ajabu na kuanza kumshambulia Amata kwa mapigo ya kifo, kutokana na uchovu aliyonao Amata aliona hapa hata kukimbia hawezi alijitahidi kufanya hiki na kile, mmoja wao alichumpa mbele ya Amata na kumkaba koo kwa mikono yake yenye nguvu na mikavu inayokwaruza, lakini mara Amata alishuhudia mshale mwingine ukizama shingoni kwa huyu mtu na kuanguka chini kama mzigo, waliobaki walipoona hayo wakaanza kutawanyika wakipiga kelele za sasa zilikuwa tofauti na za mwanzo mara kutoka mbali aliona kundi lingine likija upande ule, Amata alishindwa afanye nini, akauendea ule mwili ulioning’inia pale kuutazama vizuri. Wale viumbe waliosalia waliendelea kutandikwa na mishale isiyojulikana wapi inatokea na nani anaerusha. Amata alipigwa na butwaa alipougeuza mwili ule kwa nyuma…
*************************************
‘Kingusu’
“Ah!” alishangaa na kufikicha macho yake kama mtu ambaye haamini ni nini alichokiona. Aligundua tu ni mwili wa binadamu wa kizungu kwa kuwa aliona baadhi ya nywele ndefu ambazo zilisalia kichwani mwa mwili ule, sura yake haikujulikana vizuri kwa jinsi ilivyogandamana na damu nyingi, Amata alijaribu kwa haraka labda angeona angalau jinsia ya mwili huu iliajue kuwa ni Hellen au Stephan, lakini kilichomshangaza mwili ule haukuwa na alama yoyote ya jinsia. Watu wale walizidi kusogea wakiwa na hari ya kufanya mashambulizi kwa adui zao, wale wenzao wote waliokuja na yule kiongozi wao walikuwa wamelala kimya juu ya ardhi bila uhai baada ya kupigwa kwa mishale isiyojulikana wapi inatoka, Amata alisikia mlio wa mbinja uliopigwa kutokea kichakani, alijua maana ya mbinja ile kwani ni baba yake alikuwa akiipiga kumuashiria kuwa hapo kuna hatari utoke haraka, Amata alishangaa maana hakujua ni nani aliyeyafanya haya yote. Alihisi kitu kikimshika bega alipogeuka alikutana uso kwa uso na nyani mkubwa mwenye kichwa cheupe, walitazamana kama sekunde kumi hivi, nyani yule alimshika mkono Amata na kumvutia msituni, Amata alimwangalia nyani yule kwa makini kule msituni ‘Kingusu’ Amata alijisemea moyoni, lakini alishangaa nyani huyu amepata wapi ujasiri au amejuaje kuwa yeye yuko huku msituni! Kwa maana nyani huyu alimuona, Amata alikaa chini ndani ya kichaka kile nyani yule alimletea baadhi ya matunda, Amata alikula na kisha nyani yule akampa ishara ya kuwa amfuate, Amata alinyanyuka na kumfuata nyani yule huku kichwani mwake akijaribu kukumbuka juu yakiumbe hiki cha ajabu..
Miaka 25 iliyopita Kijijini kwa akina Amata.
Mzee Nkhunulaindo, baba wa Amata alikuwa ni mzee anayeogopwa sana kijijini hapo, alipenda sana utani na watu lakini hakupenda mchezo kabisa katika kazi zake, alikuwa na shamba kubwa sana lililolimwa mahindi, mpunga na mboga za ina nyingi, familia yake ya watu watatu yaani yeye mkewe na mtoto wao Amata hawakuwahi kupatwa na janga la njaa hata mara moja. Mzee huyu mashuhuri na hodari hakuna asiyemjua kwa umahiri wake wa kupiga mishale, hii ilipelekea kila mtu kuogopa hata kuingia shambani kwake kwa kuwa alihofia kudunguliwa kwa mshale wa mzee Nkhunulaindo. Baada ya kifo cha mkewe Bi. Vituko, mzee Nkhunulaindo alibaki akiishi na mtoto wake huyo mmoja katika nyumba yao iliyopo shambani mwao, kila siku asubuhi alimfundisha kujiandalia chai na kabla hajaenda shuleni, na aliporudi nyumbani mchana alichukua muda mwingi sana kumfundisha mambo mbalimbali ya maisha, hata Amata alipofukuzwa shule kwa kosa la kumpiga mawe mwalimu wake, Mzee Nkhunulaindo hakuona haja ya kwenda kuomba msamaha kwa mwalimu huyo kwani hakupenda hata siku moja aonekane yuko chini ya mwingine kwa kuwa tu yeye anatokea ukoo wa kichifu. Siku moja Amata alipotoka shule alikuja na kumwambia baba yake kuwa anahitajika shuleni, bila kusita kesho yake wote waliongozana na kukutana na mwalimu wa shule hiyo “Mzee nimekuita kukupa taarifa kuwa mtoto wako amempiga mawe mwalimu wake na kumuumiza, hivyo tumemfukuza shule kuanzia leo hii” mwalimu alimueleza baba wa Amata. Baba wa Amata limwangalia tu mwalimu hakuna alichomwambia, baada ya muda kidogo akajibu “Nimekusikia mwalimu, asante” akamshika mkono mtoto wake na kuanza kuondoka. “Jamani, sasa ndio husemi lolote, Mzee! Si tuyazungumze” mwalimu alimueleza baba wa Amata. “Tuzungumze nini, we umeniambia mmemfukuza shule, sasa! Ungenambia unataka umfukuze shule sawa, lakini ushamfukuza. Mbona mimi baba yake sijasoma na nakulisheni nyote hapa kijijini? Twende mwanangu.” Aliondoka na mwanae na kurudi nyumbani. Mwalimu alibaki akishangaa na hakujua la kufanya. Siku hiyo mzee Nkhunulando, alirudi nyumbani kwa kuchelewa sana akiwa amekunywa pombe nyingi “Mwanangu Amata, usijali, kama wamekufukuza shule wewe utajifunza elimu dunia, elimu isiyo na gharama ila juhudi zako tu katika kutafuta maisha…” alisema hayo kwa sauti ya kilevi huku akijitupa kwenye kiti chake cha ‘mkao wa nyani’ “Watu hatujasoma na tunaishi bwana, na wewe mwanangu utaishi, mimi baba yako nina shamba kubwa na lina kila kitu hakuna mwingine hapa kijijini ananizidi kwa ardhi. Mi chifu bwana nikuombe msamaha… we nani, wajerumani wenyewe sikuwaomba msamaha itakuwa wewe mwalimu! Ha ha ha ha… sisi tunalindwa na mizimu ya kwetu, hapa mtu achezei hapa, na wewe Amata nitakukabidhi kwa mizimu ya kwetu ikulinde na ikuongoze siku zote za maisha yako mpaka utakapoenda kuungana nao…” aliendelea kuongea na mwisho kupitiwa na usingizi pale pale kitini. Siku iliyofuata walikuwa pamoja shambani, Mzee Nkhunulaindo alikuwa akimfundisha mwanawe maana ya mbija mbalimbali, jinsi ya kukabili hatari za porini na kuweza kusikiliza sauti mbalimbali za msituni ilikujua huyu mnyama gani au mdudu gani, alimfundisha jinsi ya kukwepa hatari na kufikiri kabla ya kuamua. “Amata!” Nkhunulando aliita “twende msituni, chukua uta na podo twende” alimuambia Amata, Amata alifanya hivyo na wakaenda msituni, pamoja nao walichukua mbuzi mmoja mweupe na kwenda naye. Njiani waliongea mambo mengi sana, Amata alipata maelekezo mengi sana juu ya kutambua hatari za misitu, na hapo ndipo alipoanza kumsimulia habari za msitu wa Solondo na maajabu yake, Amata alisikiliza kwa makini na kuuliza maswali mengi sana juu ya msitu huo. Amata aliendelea kumfuata baba yake ndani ya msitu ule ulio karibu na shamba lao, baba yake Amata alikuwa daima anapenda kuongozana na mtoto wake huyu, mtoto pekee aliyempata katika maisha yake, alimfundisha mambo mengi sana ya maisha ya kijijini na porini, kila asubuhi alikuwa akimfundisha kupiga mishale kulenga vitu mbalimbali, mzee huyu alifurahi sana kumuona mwanawe akijitahidi kuuvuta uta wake kwa kutumia nguvu nyingi kwa kuwa bado alikuwa na umri mdogo. “Amata mwanangu, wewe unatakiwa kuwa jasiri kama mimi baba yako!” Baba yake alimueleza Amata huku akimpa tunda aina ya bungo alilomchumia msituni humo. Safari ikaishia kwenye jiwe moja jeusi lililofichwa na mimea iliyotambaa karibu jiwe zima, katikati ya jiwe lile kulikuwa na kitu kama tundu hivi, Mzee Nkhunulando akasimama kimya kama dakika tano hivi, kisha akaanza kuongea kwa sauti. “Wazee, nimekuja, leo nimewaletea mjukuu wenu mumtambue mumuone mumjue, maana yeye ndiye atakayebaki katika himaya yetu… mumlinde na mumuongoze katika maisha yake yote..” aliongea mengi sana na kuimba baadhi ya nyimbo huku akilizungunguka jiwe lile. Mara upepo mkali ukaanza kuvuma miti yote ikiyumba kwa upepo kana kwamba inataka kukatika lakini haikuwa hivyo, ndege waliokuwa juu ya miti hiyo waliruka na kupiga kelele kwa lugha zao. Amata aliogopa sana akamshika baba yake kwa nguvu “Usiogope mwanangu, mizimu yetu inaafikiana na lile nililowaomba, usiogope hapa ni mahali salama tu” Nkhunulaindo alimueleza mwanawe Amata. Mara juu ya mti mmoja akashuka nyani mkubwa mweusi mwenye kichwa cheupe akasimama mbele yao, “Inamisha kichwa Amata” Nkhunulaindo alimwambia mwanae, wote wakainamisha vichwa kwa muda walipoinua vichwa hawakumuona nyani nyule. “Haya chinja mbuzi huyo” Amata alipata amri kutoka kwa baba yake, akamkamata mbuzi yule vizuri na kumchinja, damu yake wakaimwagia kwenye jiwe lile mara tatu. Upepo mkali ukavuma tena, sasa na radi ikasikika. Baada ya hapo walirudi nyumbani, ilikuwa tayari imetimu jioni. “Baba, yule nyani alitoka wapi?” Amata alimuuliza baba yake “Ule ni mzimu mwanangu, lakini huwa unatokea kwa mfano wa nyani, anaitwa ‘Kingusu’daima ukimuona usimkimbie, ujue hapo ana jambo la kukuepusha au kukulinda”
*****************************
Stephan hakuelewa kinachoendelea pale alipojikuta katikati ya kundi la viumbe wa ajabu, alishikwa na woga na kutaka kukimbia lakini hakaona hiyo si mbinu nzuri kwa wakati huo, alipogeuka huku na huku aliona kuwa viumbe wale wa kutisha walikuwa wengi sana wakubwa kwa wadogo wakiwa wamemzunguka wanamwangalia kwa macho yao yakutisha. Stephan alivumilia lakini hakika roho yake ilikuwa tayari kutoka naye alijitahidi kuitoa ili awe mfu lakini hakuweza. ‘Majini?’ alijiwazia, ‘hapana Mashetani!’ alijikosoa tena mwenyewe, akikumbuka hadithi za zamani alizosoma huko kwao juu ya majini, mazimwi na Mashetani ila hapo hakujua haya yapo kundi gani, kila mara mwili wake ulimsisimka kwani yalikuwa yakikoroma tu na ndiyo hiyo ilikuwa lugha yao, alipogeuka huku na huku hakumuona Hellen, woga ulimjaa sana ‘watakuwa washamla hawa!’ alijiwazia moyoni, mara nyingi alijikuta akijiwazia moyoni mawazo ambayo hayakuwa na msaada wowote, katika mawazo hayo aliiona ile nyumba yake nzuri aliyoijenga kando ya mto lakini sasa aliona kuwa hatokuja kuingia tena, aliwakumbuka wazazi wake wale wazee ambao sasa wanaishi kwenye kituo cha kulelea wazee akaona kuwa nao watakufa bila kumuona kijana wao, aliwakumbuka wadogo zake ambao baadhi yao walimshauri asiende huko bara la giza lakini hakuwasikiliza sasa aliwaona kuwa walikuwa ni watu wa pekee sana, machozi yalimtiririka hasa alipomkumbuka Hellen, binti aliyempenda sana maishani mwake ijapokuwa alikuwa ni binamu yake. Stephen hakujua nini cha kufanya isipokuwa ni kusubiri hatima yake tu kwa viumbe hawa. Akiwa kajiinamia pale chini alipokuwa amekaa, mara akasikia vishindo vikubwa sana kutokea upande wa pili wa pale alipokaa aliponyanyua kichwa kuangalia ni nini kinatokea alishangaa kuona viumbe wale wakimgombania mwenzao kana kwamba walikuwa wakigombea nyama, Amata alishuhudia jinsi walivyomtafuna mwenzao bila huruma kabisa, Stephen akafumba macho ili asishuhudie unyama huo kabisa, alijiuliza kwa nini walimfanyia vile mwenzao hakupata jibu kamili kwa kuwa hakuelewa ile lugha yao ya mikoromo waliyoitoa vinywani mwao, alibaki kuwaangalia, alijikuta akijipapasa huku na huku lakini hakuona anachokitafuta. Mara akajikuta akili ikimrudia na kujiona pale alipo yuko peke yake, alipoyaangalia tena ya madudu akaona yako bize na kula nyama ya mwenzao huku yakikoroma sana na kutimua vumbi, vishindo vyao viliifanya ardhi yote pale kutetemeka kwa nguvu, Amata akapata wazo la kutoroka wakati huo wale viumbe wakiwa na shughuli ile lakini moyo mwingine ulimkataza kabisa kufanya jambo hilo. Aliangalia tena vizuri eneo lile alilopo, akajiuliza hata akitoroka atatorokea upande gani hakupata jibu, mara alijiwazia kuwa labda Hellen hayupo mbali na pale hivyo atamuacha. Mawazo yalimsumbua kichwa chake hata hakujua lipi akubaliane nalo na lipi aachane nalo. Mara ujasiri wa ajabu ukamjia ‘potelea mbali kwanza nafsi yangu mengine baadae…’ alijiwazia na kuanza kujiburuza taratibu kwa kutumia matako akirudi nyuma nyuma huku akiwaangalia viumbe wale wasije kumgundua, moyo ukiwa unamuenda mbio akijiwazia itakuwaje watakapomuona lakini aliendelea kujikokota kinyumenyume, “Aaaaaaaaaaaaaa help!!!!!!! ” Stephen alipiga ukelele uliofanya viumbe wale kushtuka na kuanza kumfuata huku wakikoroma kama kawaida yao. Baada ya kujisogeza kama mita kumi na tano hivi na kujikuta mikono yake ikitumbukia kwenye kitu kama shimo kwa kuwa alikuwa akisota kinyumenyume huku amekaa katika kichaka kile hakuona hatari yoyote nyuma yake, mikono yake ilitangulia na kufuatiwa na kichwa, mwili na miguu vikimalizikia. Lilikuwa ni korongo refu sana ambalo chini yake kulikuwa na mto mkubwa, Stephen alijiona akianguka kwa kasi na lakini kabla hajafika chini alijikuta akidakwa na mkono mkubwa wenye nguvu na kurudishwa juu kwa kasi ileile, alijikuta uso kwa uso na kiumbe hiki cha ajabu kilichoonesha hasira kwa kitendo chake kile cha kutaka kutoroka, Stephene alijawa na woga akajua kuwa sasa lazima atafunwe mzima mzima, kiumbe kile kilifungua domo lake baya lenye meno marefu na kutoa mkoromo mkali uliomfanya Stephene atetemeke kwa hofu na kutokwa na mkojo bila kujijua, akiwa bado kashikwa na kiumbe kile Stephen alitulia kimya kabisa akisali kwa ukimya sala yake ya mwisho pembeni aliviona vile viumbe vingine vyote vikiwa na sura ya hasira. Yule kiumbe alimtupa chini Stephen, wakati akianguka chini kitu fulani kilimtoka kutoka katika begi lake na kuruka kwa nje mmoja wa wale viumbe akakidaka kabla akijafika chini, ilikuwa ni camera ndogo ya dijitali ambayo muda wote ilikuwa mkobani mwake lakini kutokana na misukosuko yote hii alishasahau hata kama alikuwa na kitu kile mkobani, aliwaangalia wale viumbe wakiigeuzageuza ile camera. Stephen alisikia kishindo nyuma yake na alipogeuka alikuta kiumbe kingine kimeanguka chini, aligeuka haraka kuangalia upande ule wa mwanzo, akaona wale wengine walikuwa bado wanashikashika ile camera, mara akasikia kishindo kingine tena upande mwingine alipoangalia kiumbe kingine kimeanguka, Stephen alipigwa na bumbuwazi hakujua ni nini kinachoendelea mahali pale, moyoni akaanza kujipa moyo labda Hellen yuko eneo lile ndiye anayefanya kazi hiyo, lakini pia aligeuza tena mawazo yake akaona labda Amata kwa kuwa yeye ndio mpiga mishale hodari, akiwa katika kujiuliza yote hayo mara akaona mwanga wa flash ya camera ile ukifyatuka na yule kiumbe aliyeshika ile camera akaanguka kwa kishindo na camera ile ikimtoka mikononi na kuangukia miguuni mwa Stephen ambaye wakati huo alikuwa amekaa akiugulia maumivu ya mgongo. Aliiokota camera ile na kuishika mikononi mwake akiwa na woga mkubwa akaiweka jichoni kama anataka kufotoa picha, wale viumbe walio mbele yake wakatawanyika kwa woga, Stephen akatikisa kichwa kwa ishara kwamba amegundua kuwa mwanga wa flash unawaathiri ndio maana walikuwa wakianguka kila anayemulikwa moja kwa moja na mwanga huo. Stephen akajua sasa hii ndiyo njia ya kutorokea, lakini alijiuliza mwanga huu unawaathiri kiasi gani hakupata jibu!! Alijinyanyua kutoka pale alipo na kuanza kukimbia taratibu, viumbe wale wakaanza kumfuata akasimama na kugeuka akapiga flash moja kiumbe wa mbele akaaunguka na kuangukia mti, kutokana na kishindo kile mti ule ulikatika vipande vipande, Stephen aliendelea kukimbia na mara akaona upepo mkali ukimzunguka na kumnyanyua juu, Stephen hakujielewa kwani alizungushwa kwa kasi ya ajabu akiwa kachanganyika na majani na takataka nyingi, upepo ule ulimchukua kwa muda, akiwa juu aliweza kuona viumbe wale kwa uzuri kabisa, lakini mara aliona viumbe wale wakianza kurefuka kumfuata alipo, kiumbe mmoja alinyosha mkono na kumdaka kumshusha chini, Stephen alifikishwa chini kwa nguvu kiasi kwamba alitoa ukelele wa nguvu, viumbe wale wakaanza kumgombania, Stephan alijaribu kujitikisa kwa nguvu zake zote huku akipiga makelele ya woga, mara akaanguka chini na wale viumbe wote wakarudi nyuma, Stephene alibaki kaduwaa pale chini akiwaangalia viumbe wale wenye uchu wa nyama ya binadamu lakini hakuelewa kwanini viumbe hawa wamemuachia ghafla namna ile na wala hakuwaona kama wana dalili ya kumfuata tena isipokuwa ni mikoromo yao tu iliyozidi kuwa ya kutisha. Viumbe wale walirudi nyuma na kuanza kutawanyika kutoka eneo lile, Stephen akiwa pale chini hakuelewa sababu ya wale viumbe kukimbia ovyo alihisi kabisa kuna hatari eneo lile, lakini alijiuliza je kama hiyo hatari viumbe hawa wanaiogopa kwake itakuwaje! Alikosa jibu aliendelea kuwa pale chini na mara akaona nuru ya jua ikianza kufifia na kiza kikianza kufunika eneo lote lile, jua lilipatwa na mwezi mchana ule, Stephen alipogeuka huku na huku akajikuta yuko peke yake kabisa “God is great!” alijisemea kimoyomoyo kuonesha shukrani yake kwa aliyemuumba, alijinyanyua taratibu kutoka pale huku akichechemea alikimbia kidogokidogo kueleke machakani na kutokomea asikokujua. Safari ilimuia ngumu Stephen, hakujua wapi anaelekea, kiu, njaa, uchovu vyote vilikuwa pamoja naye, alikimbia kwa nguvu zake zote lakini nguvu zilimuishia na kuanguka chini, alijaribu kutambaa haikusaidia, koo lilimkauka kiasi kwamba hata sauti haikuweza kutoka kwa wakati huo, alilala chini katika vichaka kwa utulivu bila kujitikisa akijua kuwa sasa hakuuawa na wale viumbe lakini kiu na njaa ndiyo vitavyomuangamiza, alijigeuza na kulala chali macho yake yakiangalia anga ambalo sasa halikuwa la buluu bali lililofifia kutokana na tukio lile la kupatwa kwa jua. Usingizi mzito ulimpitia kiasi hata hakujitambua, aliamka katika dunia nyingine kabisa ambayo ilimkutanisha na wenzake wote waliopoteana katika msitu ule ‘Msitu wa Solondo’ katika ndoto yake akaona rafiki zake wengi aliyowaacha huko Heidenburg University, aliwaona wanafunzi wake, mara aliyaona makaburi na majitu ya kutisha yakimsongasonga huku na huko, kiza kinene kiliyashinda macho angavu ya Stephen, maswali aliyojiuliza yalibaki bila jibu, nuru ikapotea, nguvu zikamuishia, pumzi zikamtoka kwa taabu, Stephen akalala usingizi mzito.
Saringo akashtushwa na kitu kilichomgusa mgongoni kitu kama tone la maji baridi sana, akafumbua macho taratibu kuangalia nini kilichomgusa,mwanga mkali ukamfikia machoni alipotazama juu akagundua kuwa kumbe alikuwa ndani ya kitu kama chungu kikubwa ambacho kifunikwapo giza lake huwezi kuona hata umbali wa sentimeta mbili, alijishauri kutoka mle ndani lakini aliogopa kwa kuwa hakujua nini atakachokikuta huko nje,alitega sikio lake kwa umakini asikie chochote kitakachosemwa na waliopo huko nje lakini hakuna alichosikia isipokuwa mvumo tu wa upepo mkali ambao hata hakujua unatoka wapi na unaelekea wapi, hofu ilimtoka kidogo na kuchukua uamuzi ‘natoka liwalo na liwe’ alijisemea moyoni ‘ah! Lakini vipi nikikutana na haya majitu huko nje si yatanifanyia mbaya!?’ nafsi nyingine ilimuuliza moyoni ‘ah! Kama kufa ndo nshakufa ngoja nitoke mengine ntajua ukohuko’ alijipa moyo tena kisha kwa nguvu zote alijinyanyua na kujitokeza juu ya ule mdomo wa kile chungu, alichokikuta huko nje hakutegemea kwanza vumbi kali lilimfikia machoni na kumfanya apate shida kwa macho yake kupambana na vumbi lile alijitahidi kufungua jicho mojamoja lakini ilikuwa ngumu, upepo mkali wenye vumbi na matakataka ulifunikiza eneo lote alilopo hata asiweze ona vizuri, bila kusita alipanda kwenye kile chungu na kujirushia nje, akiwa amelala kifudifudi alijinyanyua shingo yake na kuangalia kilichopo japo kwa taabu alisikia kelele na vitu kama nyimbo zilizokuwa zikisikika upande wa pili wa msitu huo, Saringo taratibu alianza kutambaa kwa staili ya nyoka kuelekea kule alikosikia nyimbo zile alihisi kuwa akisimama atembee wangemuona kwa urahisi. Akiwa kachafuka na vumbi lile aliendelea kujisongeza kwa taabu lakini hakuona dalili zozote za kiumbe eneo lile, alipofika ndani ya vichaka alijinyanyua na kukaa kitako akiegemea mti mmojawapo, kelele zile zilisikika kwa nyuma katika umbali mfupi tu, zingine zikishangilia na zingine zikilia, Saringo alijawa na hofu pale tu alipoona mbele yake kiumbe kifupi kikimtazama kwa umakini, alishikwa na hofu kuu alianza kutetemeka na mapigo ya moyo kumuenda mbio, kiumbe kile kilitoa mngurumo wa ajabu huku kikinyanyua sura yake kuangalia juu kama kikiita wengine, domo lake kubwa liliachama na ulimi wake mweusi kujitokeza nje, Saringo alinyanyuka na kuanza kutimua mbio lakini kabla hajafika mbali alijikuta akitumbukia kwenye korongo refu na kufikia kwenye tope zito ambalo hata kujigeuza ilikuwa tabu, tope lenye kunata, alijigeuza huku na huku lakini alihisi uzito sana, alipoangalia alikotoka aliona viumbe kama vile alipovihesabu vilikuwa yapata vitano hivi, pembeni aliona mzizi mkubwa na mrefu ulioning’inia kutoka mti mkubwa uliopo juu ya korongo lile, Saringo alikumbuka mafunzo aliyoyapata alipokuwa katika mafunzo ya jeshi la kujenga taifa, aliushika mzizi ule na kwa taabu sana alianza kupanda kutoka mle ndani ya tope lile zito, alijivuta kuelekea juu taratibu aliweza kufanikiwa huku viumbe wale wakiwa wamesimama palepale Saringo hakuogopa aliendelea kukwea kwa ujasiri mkubwa mpaka kufika juu katika shina la mti ule alijaribu kutazama huku na huku hakuona tena viumbe wale, alijinyanyua na kuanza kufuata kule alikosikia kelele zile, baada ya kutembea mwendo kama wa dakika kumi na tano hivi alijikuta katokea kwenye eneo lile alikokuwa akisikia kelele zile, Saringo alishika midomo yake kwa kutoamini alichokiona pale. alijinyanyua na kuanza kufuata kule alikosikia kelele zile, baada ya kutembea mwendo kama wa dakika kumi na tano hivi alijikuta katokea kwenye eneo lile alikokuwa akisikia kelele zile, Saringo alishika midomo yake kwa kutoamini alichokiona pale, watu wengi sana waliujaza uwanja ule wake kwa waume wakicheza ngoma za ajabu kabisa katika mduara mkubwa, pembeni yao kwa juu kulikuwa na kitu kama jukwaa hivi hapo aliketi mtu mmoja aliyeonekana kama ndio kiongozi wao, mkononi alishika fimbo kubwa na juu ya fimbo hiyo kulikuwa na fuvu la binadamu lilionekana kama la mtoto mdogo hivi, pembeni yake alizungukwa na wanawake wengi waliokuwa nusu uchi kwa kuacha vifua na sehemu kubwa ya miguu yao ikiwa wazi, ilionekana ni sherehe kubwa sana watu hawa wa kutisha walikula na kunywa wakicheza ngoma yao hiyo kwa kila aina ya mtindo wakiwa wamejipamba kwa michoro ya ajabu ajabu katika miili yao, katikati ya mduara huo kulikuwa na watu walioonekana wamefungwa kamba kwa hesabu ya haraka haraka Saringo alipata kuwa wapo kama kumi natano ‘ha! Ina maana huku kuna viumbe kama sisi!’ Saringo alijiuliza lakini jibu hakupata kwa kuwa aliona wengine wakiwa wamefungwa kamba na kuwekwa pale katikati. Saringo alitulia pembeni ya mti ule ili ajue ni nini kitaendelea eneo lile maana sherehe hii haikuleta maana kwake hata kidogo. Aliendelea kujibanza palepale mwili wake ukiendelea kushambuliwa na mbung’o wenye njaa ambao sasa walipata kitoweo bila jasho, uchovu ulimkabili hata kusababisha mwili wake kudhoofu kwa hilo, hakujua hatima yake, hakujua wenzake wako wapi au wamepatwa na nini, hali hii ilimfanya msichana huyu mrembo mwenye maringo na mikogo ya aina aina awe kama kichaa asiye na msaada ukiongeza na matope ambayo sasa hata yeye alishasahau kama yamemganda mwilini mwake alibaki tu kujiinamia kwenye kichaka kile kidogo, machozi yalimlengalenga na macho yake kulowa alimlilia nani hakujua, Saringo alituli palepale kama mtu aliyegongewa kwa misumari hakuthubutu kujitikisa kwa kuwa alihofu kuwa kwa kufanya hivyo angewafanya watu wale wajue kuwa yupo pale. Saringo aligutushwa pale ngoma ilipoongeza kasi na watu kuongeza nguvu za kucheza, mara yule mtu aliye kama kiongozi alinyanyuka na kupiga kelele akinyanyua juu fimbo yake, watu wawili walitokea nyuma ya kiti chake kile wakiwa wamemshika mtu mwingine wakitumia nguvu kumleta pale mbele ya kile kiti, mtu yule alionekena kuwa mkaidi na kutumia nguvu kujinasua lakini watu wale wenye nguvu na tambo kubwa walimdhibiti na kumfikisha pale mbele ya yule kiongozi, kiongozi yule alipiga tena kelele na wale waliokuwa wakicheza ngoma walishangilia kwa kwa kelele za ajabu kisha wakasimama na kugeukia upande ule ambao yupo yule kiongozi wao. Wale watu walifunga yule mateka wao kwenye kisiki cha mti kilichowekwa mahali pale na mmoja wao akachukua mti wenye kipago kama cha manati na kuipachika shingo ya yule mateka kiasi kwamba hawezi kupata pumzi, yule kiongozi alipiga tena ukelele na wale watu wote wakashangilia kwa kelele zile zile, yule kiongozi akachukua jiti kubwa lenye ncha kali na kulididimiza kifuani mwa yule mateka alipolichomoa lilitoka na moyo wa binadamu, damu ziliruka kwa kasi na watu wote wakaanza kushangilia kwa nguvu, ngoma ikaanza upya na kucheza kukaanza tena, yule kiongozi akarudi kwenye kiti chake cha enzi akiwa na ule moyo mkononi huku akionesha kufurahia kile alichofanya. Saringo alisisimka mwili wote na kupata ganzi akaanza kulia kwa vikwifukwifu akiwaomboleza wenzi wake wote na kujijutia nafsi yake maana alijua sasa maiti yake haitaonekena hata na rafiki zake bali italiwa na wanyama na ndege wa Msitu wa Solondo. Giza lilipoanza ingia moto mkubwa uliwashwa mahali pale na sherehe ile iliendelea kwa muda kisha ikasimama, yule kiongozi akaongea maneno machache ambayo Saringo hakuyaelewa maana yake ni nini kwa kuwa walitumia lugha isiyoeleweka. Baada ya maneno yale machache wale watu walishangilia tena kwa sauti kubwa na mara wakawanyanyua wale waliokuwa wamefungwa pale chini na kuwaongoza kuelekea mahali fulani, Saringo aliendelea kuangalia msafara ule ukiingia msituni ‘lazima nione mwisho wake’ alijisemea nakuanza kuufuata msafara ule kwa kupitia pembeni ili tu wasije kumuona. Msafara ule ulipita katikati ya misitu minene Saringo hakujua hata ni wapi wanakoelekea yeye aliendelea kufuata tu kwa kuwa aliamini kuwa labda kati ya wale ambao wamefungwa inawezekana kuna wenzake alijipa moyo nakuendelea kuufuata kwa pembeni huku akimuomba Mungu wake amlinde japokuwa hata kanisa au msikiti hakuujua. Saringo aliona mara nyingi mtu mmoja ambaye alichoka sana katika mateka wale, mara mara kwa mara alikuwa akishindwa kuendelea na safari ile lakini wao hawakujali bali walimburuza na kumyanyua kwa nguvu ili aendelee na safari ile, saringo alishikwa na huruma ya kike lakini hakuthubutu hata kuthubutu kufanya lolote maana alijua hapa akionekana tu itakuwa zamu yake kutolewa moyo kama waliotangulia, alizidi kuufuata msafara ule bila kuchoka huku akichuma kila akionacho porini humo na kula ilimradi tu hakikuwa kichungu wala hakikuwa sumu. . Kiu na njaa vilisumbua koo na tumbo lake akiwa anahemea juju kwa uchovu na kibaridi cha usiku ule kikiendelea kumpa nguvu kidogo Saringo hakuchoka, mwili wote ukiwa umegandamana na matope hata alisahau hili nia na lengo yake ilikuwa tu ni kuona mwisho wa msafara ule uliokuwa umekusanya mateka wale. Mwanga wa mienge iliyowashwa na watu wale ilangaza vema ndani ya msitu ule ‘kama akina Amata hawako kati ya mateka wale sasa wako wapi? Watawezaje kufika katika pango lile tunalolikusudia hali mchoro wa njia yote anao Stephan!’ wazo hilo lilimjia daima na ha po akagundua kuwa si ajabu yuko peke yake ndani ya msitu huu, alijaribu kufikiria uwezekano wa hawa wenzake kuwa pamoja lakini hakuna muunganiko wa matukio ambayo yangewafanya wakutane ‘Stephen na Hellen walipotea pangoni nikabaki mimi na Amata, ah! Amata yupo wapi?’ alijiuliza mwenyewe huku akiendelea na safari asiyoijua ni wapi inaelekea. Akiwa katikati ya msitu ule saringo alichoka sana akainama na mikono yake kushika magotini, alihisi kama mkono wa mtu ukimuinua kichwa chake alipoinuka hakuona mtu yeyote mahali pale, hofu ilimjaa akarudi nyuma kidogo na kugeuka uku na huko lakini hakuona mtu zaidi ya miti ya msitu ule iliyozunguka mahali pale, mara akasikia sauti ya kuning’ona ikimwita “Saringo, Saringo!!!” Saringo aliangaza uku na huko hakuona mtu mbele yake kulikuwa na mbuyu mkubwa sana aliangalia juu ya mti ule hakuna kitu, mauzauza! Alianza kuondoka polepole mara akajikwaa kwenye kitu kama kamba na kuanguka kifudifudi akasikia vicheko vya kike vikimcheka kwa kujirudiarudia, Saringo aliogopa sana moyo ukaanza kwenda mbio akajishika kifuani japo kuhakikisha kuwa moyo huo hautatoka nje! Vicheko vile vilitulia na hali ilikuwa ya utulivu kama mwanzo ni miti tu iliyokuwa ikitikiswa na upepo ndiyo iliyotawala giza hilo, mbala mwezi ilianza kung’aza eneo hilo, Saringo alisimama kimya akijua sasa msafara ule utakuwa umempotea hata asijue wapi ulipo. Akiwa katika kutafakari hayo yote alisikia sauti za watu wakiongea mara mtoto akilia mara vicheko sauti hizi zilikuwa zikitoke pande mbalimbali mara aligeuka nyuma hakuona mtoto alitazama kushoto na kulia hakuona watu, Saringo alizidi kuingiwa na hofu akaanza kutimua mbio kama kichaa, akipita vichakani, alihisi kama mtu anakimbiza nyuma yake lakini hakumuona, alizidi kukimbia huku akitweta kwa nguvu bado alisikia vishindo vya mtu vikimfukuza nyuma yake, akasimama na kugeuka nyuma ‘liwalo na liwe’ alijiambia, lakini hakuona mtu na vishindo vile havikusikika tena, alihisi kuchanganyikiwa zaidi, alipoanza kutembea alihisi kama mtu yuko pembeni yake naye akitembea, saringo akasonya mara akasikia misonyo zaidi ya kumi kutoka pande tofauti, akaanza kukimbia tena sasa kwa kasi zaidi, nyuma yake alisikia vishindo sasa sio vya mtu mmoja bali ni wengi wakimfukuza, saringo alikimbia kwa kasi yake yote huku moyoni akiomba Mungu amsaiidie katika hili, akiwa katika mbio hizo alijikwaa na kuanguka vibaya pale alipoangukia kulikua na mzoga wa mnyama wa skunyingi sana ambao kwa wakati huo ulibaki mifupa tu, alihisi kama mtu akimshika shingoni kumyanyua, Saringo akaokota moja ya ile mifupa na kugeuka kwa kasi tayari kwa shambulizi, vumbi kubwa lilitimka mbele yake kama upepo wa kisulisuli miti na manyasi ya eneo hilo iliyumbayumba bila muelekeo, mara kukawa kimya kumetulia kabisa, Saringo akainua mkono wake kuangalia ule mfupa ‘waoh!!!!’ alishangaa, aligundua kuwa inawezekana viumbe hivi visivyoonekana vinaoghopa aina hii ya mifupa, akachukua na kuupachika kwenye pindo la suruali yake na mwingine akaushika mkononi, akaanza kujaribu kuutafuta ule msafara kama angeuona tena!
**********************************
Miaka saba ilopita Heidelberg University-Ujerumani
Chuo kikuu cha Heidelbeg, (Heidelberg University, Ruperto Carola) ni chuo kikuu cha tafiti kilichopo katika jiji la Heidelbeg, Baden-Württemberg, Ujerumani. Kilianzishwa mnamo mwaka 1386, ni chuo kikongwe sana huko Ujerumani na ni chuo cha tatu kujengwa katika Utawala wa Warumi. Heidelberg kimekuwa chuo kinachotoa elimu mchanganyiko tangu mwaka 1899. Leo hii katika chuo hiki kuna vitivo kumi na mbili na kinatoa shahada, shahada ya uzamili na shahada ya juu. Katika chuo hiki ndipo Bw Stephen Van Leuwen alipokuta na Bi Hellen Schurman wakiwa wakufunzi katika kitivo hii ya mambo ya kale, hawakuzoeana kirahisi kama unavyofikiria wewe sasa hivi bali walifanya kazi chuoni hapo takribani miaka mitano. Siku moja Stephen alipata safari ya kikazi kwenda Chuo kikuu cha Humboltd nacho cha uko huko Ujerumani kuona mabaki ya mjusi mkubwa (dinosauria) yaliyokuwa yamepelekwa huko Ujerumani yakitokea katika moja ya makoloni yao lililojulikana kama Deutche Ost Africa (Tanzania bara ya sasa), katika ziara hiyo ya kikazi ndipo alipopata nafasi ya kuongea na Bi Hellen kwa mara ya kwanza, wakiwa katika kubadilishana mawazo ndipo walipogundua kuwa huko katika bara la giza kuna mambo mengi ambayo wao kama watafiti wa mambo ya kale iliwapasa kuyafahamu. “Ningependa siku moja kufanya safari ya uchunguzi huko Africa” Hellen alimueleza Stephen “Inawezekana kwa kuwa pia kuna historia kubwa sana ya Mjerumani, kwa nini usiitafiti? Twaweza kufanya hilo na kuandika kitabu ambacho kitasaidia kufundishia na pia kuongeza elimu yetu!” Stephen alikazia “Lakini tutafanya tafiti juu ya nini?” Hellen aliuliza “Inabidi tukae tuangalie pamoja, kwa kuwa kuna mambo mengi sana ya kufanyia utafiti” Stephan alijibu huku akiwa katika harakati za kuwasha sigara yake ili avute. “Samahani sipendelei sigara!” Hellen alimwambia Stephan “Oh! Sorry Miss!!!” Stephan aliomba radhi na kuzima sigara ile Mazungumzo yao yalikuwa marefu sana, waliongea mengi sana juu ya mambo kale na historia mbalimbali, lililotokana na mazungumzo hayo lilikuwa ni kufunga safari ya kitafiti huko Africa, lakini wasiwasi wao ulikuwa ni nini cha kufanyia utafiti na wapi pa kwenda. Walirudi tena Heidelberg kuendelea na kazi, mara kwa mara kila mmoja alikuwa ana hamu ya kuonana na mwenzake ili tu kubadilishana mawazo katika hili, Hellen alidhamiria toka ndani ya moyo wake kufanya tafiti mojawapo katika Africa lakini aliogopeshwa na habari nyingi za huko Africa, mara alikata tamaa na mara alijipa matumaini hasa alipokumbuka safari yake aliyoifanya miaka kadhaa nyuma akiwa mwanafunzi katika misitu ya Amazonia aliamini duniani hakuna msitu unaoweza kuufikia huo kwa kila hali. Kwa upande wa Stephan alitokea kumpenda sana Hellen hasa kwa umbo lake zuri la kike waswahili wangeliita namba nane, mwanadada huyu mfupi, mcheshi anayeonekana ni mjuzi wa mambo aligonga mhuri wa penzi katika moyo wa Stephan, kijana jasiri kutoka Poland aliyelelewa na baba yake ambaye alikuwa mwanajeshi aliyepigana vita ya I ya dunia, hakuwa muongeaji sana lakini pia hakuwa mtu wa kukubali kila kitu alichoambiwa, alipenda kusoma na kuchunguza mambo mbalimbali hasa ya kutatanisha, kwa muda huu alivutiwa na wazo la Hellen la kufanya utafiti huko Africa lakini bado hakujua ni nini wangeenda kufanya huko, tangu siku hiyo alianza kusoma vitabu mbalimbali vinavyohusu Africa ili labda angeona chochote cha kufanyia utafiti, haikuwa rahisi sana kwani katika maktaba ya chuo hicho kulikuwa na vitabu zaidi ya elu kumi vyote vikizungumzia mambo kale hasa ya Africa, vitabu hivyo vilimpatia habari za kutisha sana juu ya Africa lakini alijipa moyo hasa alipokumbuka safari yake akiwa mwanafunzi huko Misri katika mapyramid aliamini hakuna sehemu yoyote duniani ambayo ni ngumu kuishi zaidi ya huko ambako ni jangwa na vumbu muda wote. Stephan, kijana jasiri kutoka Poland aliyelelewa na baba yake ambaye alikuwa mwanajeshi aliyepigana vita ya I ya dunia, hakuwa muongeaji sana lakini pia hakuwa mtu wa kukubali kila kitu alichoambiwa, alipenda kusoma na kuchunguza mambo mbalimbali hasa ya kutatanisha, kwa muda huu alivutiwa na wazo la Hellen la kufanya utafiti huko Africa lakini bado hakujua ni nini wangeenda kufanya huko, tangu siku hiyo alianza kusoma vitabu mbalimbali vinavyohusu Africa ili labda angeona chochote cha kufanyia utafiti, haikuwa rahisi sana kwani katika maktaba ya chuo hicho kulikuwa na vitabu zaidi ya elu kumi vyote vikizungumzia mambo kale hasa ya Africa, vitabu hivyo vilimpatia habari za kutisha sana juu ya Africa lakini alijipa moyo hasa alipokumbuka safari yake akiwa mwanafunzi huko Misri katika mapyramid aliamini hakuna sehemu yoyote duniani ambayo ni ngumu kuishi zaidi ya huko ambako ni jangwa na vumbu muda wote. Siku moja akiwa ndani ya maktaba akipitia vitabu mbalimbali, Stephen alimuona msichana mrembo, mrefu wa wastani mwenye mwendo wa madaha, Stephen alijikuta akishindwa kuendelea kusoma kitabu kile na badala yake macho na mawazo yote yalimuelekea msichana yule mweusi mwenye nywele fupi aliyekuwa akiingia maktaba mle kwa ajili ya kujisomea kama ilivyo ada, alimtazama mpaka alipokaa, maadam alikuwa ndani ya maktaba ile basi alijua kwa vyovyote ni mwanafunzi wa chuo hicho alivutiwa hasa na rangi yake iliyotunzwa vizuri. ‘A girl from dark continent!’ alijiwazia moyoni, ilikuwa ni mara yake ya kwanza kumuona mtu mweusi hakuamini anachokiona bali alijiuliza tu jinsi alivyosikia habari za bara hilo la giza na kumbe kuna viumbe vizuri kama hivi vinaishi, haikumuingia akilini hata kidogo. Alinyanyuka alipoketi na kutoka maktabani kwa kuwa alipoangalia saa yake alijikuta kuwa anatakiwa katika kipindi, alichukua baiskeli yake na kuelekea alikotakiwa. Hamu ya Stephan ya kufanya utafiti katika bara lile la giza ilizidi kuchukua nafasi katika moyo wake na hasa alipomuona msichana huyu mweusi, mrembo mwenye kila aina ya mvuto. Alimtafuta tena Hellen na kumueleza juu ya azma hiyo na juu ya yule msichana mweusi, “Labda anaweza kufahamu mambo mengi kuhusu Africa!” Hellen alimueleza Stephan kwa shauku. Walikubaliana kumtafuta ili wajue mengi juu ya alikotoka na hapo ndipo waanze kuandika kile kitabu chao cha utafiti.
Siku tatu baadae… Ruperto Carola Cafe
Hellen na Stephan walionekana wenye furaha sana hasa kwa wazo lao lile walilolipata maana walijua wazi kuwa pindi tu watapokamilisha zoezi hili watakuwa juu sana kitaaluma, kiu yao ya kitafiti hasa juu ya mambo ya kale ilikuwa kubwa sana, lakini bado hawakujua hasa ni nini wanachotaka kukifanya sasa, ni kitu cha hatari kiasi gani wanachokifikiria, Hellen alijiuliza tu kama itakuwa safari kama ile ya Amazonia iliyomchuku wiki tatu kuikamilisha akiishi na wa-Indios na wa-Amazonia ambako alikutana na hatari ndogondogo tu, Stephan aliichukulia labda itakuwa safari kama ile ambayo aliifanya huko Hamunatra katika jangwa la Misri ndani ya mapyramid yaliyosadikiwa kuzikwa watawala wa nchi hiyo nyakati za kale kabisa, wote wawili walijiona ni mashujaa sana kwa safari zao za utafiti walizozifanya katika maisha yao. Stephan alishusha taratibu kikombe chake cha kahawa na kukiweka katika kijimeza kidogo ndani ya mgahawa huo huku akiendelea na maongezi ya hapa na pale na Bi Hellen. Binti mweusi alikuwa amekaa katika kimoja cha viti vitatu vilivyozunguka meza hiyo akiwa na makaratasi machache mkononi mwake. “Naitwa Saringo!” alijitambulisha kwa Hellen na Stephen, hili lilitukia mara baada ya hawa wawili kujitambulisha kwake. Mazungumzo machache yalipita kati yao hasa ya kufahamiana na kujuana zaidi, Stephen na Hellen walivutiwa na uchangamfu wa Saringo, Saringo aliwaambia mambo mengi sana juu ya Africa hasa eneo ambalo yeye anatoka,Deutche Ost Africa, Stephen na Hellen walivutiwa sana na habari za huko na walipenda kujua kama ni kweli au ni za kutunga tu za mababu wa kale. Saringo aliwasimulia mengi sana hasa aliyosimuliwa na babu yake mzee Koloto, baada ya mazungumzo hayo saringo aliwagusia juu ya stori ya babu yake alipokuwa askari wa wajerumani na alivyokuwa akiongoza misafara ya wapagazi kuingia misituni na kuficha vitu visivyojulikana huko kisha kuuawa, “No! Kwa nini waliwaua? Lazima kuna kitu” Hellen aliuliza kwa mshtuko “Labda hawakutaka warudi tena huko, kuhofia kuchukua mali zao” Stephen alijibu “ndiyo, ndiyo, hakika kabisa babu alinambia waliwaua ili wasiweze kurudi, lakini yeye alinusurika na kufanikiwa kubaki hai” Saringo aliwaeleza na kutoa zile karatasi chache zenye michoro ya ajabu na maandishi ya kijerumani. Kwa Stephan haikuwa kitu kigeni michoro ile kwani aliitumia sana alipokwenda huko Hamunatra, kwa haraka haraka aliweza kuisoma na kutambua kilichofichwa katika michoro ile. Stephen alitikisa kichwa kuashiria amegundua kitu, akanyanyua kikombe chake cha kahawa na kunywa kidogo. “Vipi? Stephen!” Hellen aliuliza kwa shauku ya kutaka kujua. Stephen alitikisa tena kichwa na kugeuza geuza mdomo wake, mara alionekana kukunja uso, mara kutabasamu, akaiweka ile karatasi chakavumezani, na kunyanyua kichwa kumwangalia Saringo. “Bingo!” Stephen alitamka neno hilo na kuamka alipokaa akazungukazunguka huku akiwa amefungamanisha mikono yake kwa nyuma kisha akarudi akaketi tena, “Saringo! Unajua Msitu wa Solondo?” Stephen alimrushia swali Saringo, Saringo akaitikia kwa kutikisa kichwa, Stephen akaendelea “unajua Gereza Saroge?” Saringo akaitikia tena kwa kutikisa kichwa, “good! We have to face a big adventure!”. Stephen akachukua zile karatasi na kuzikunja vizuri kisha akampatia Saringo “tunza, urithi ulioachiwa na babu yako” Saringo alizipokea na kuziweka mkobani. “Kama tunaamua kufanya utafiti huu, basi na tujiandae vema sisi watatu ila lazima tupate nguvu ya watu wa ziada kuukabili msitu wa Solondo.” Stephen aliwaeleza akijua kwamba washaelewa kila kitu, “Stephen!” Hellen aliita “ tueleze kwanza kuna nini ulichokiona kisha ndiyo tuone pamoja cha kufanya” Hellen alimueleza Stephan. “Ok! Kadiri ya mchoro huu wakoloni wa kijerumani walipokuwa wanaitawala Deutch Ost Africa walipata vitu vingi sana ikiwemo mali za aina mbalimbali, kwa hiyo walichokifanya ni kuzificha ili vizazi na vizazi vyao vija kuchukua na kuupata utajiri huu mnono, Babu yake Saringo aliifadhi kitu kikubwa asichokijua, huu ni urithi usiopimika kwa mjukuu wake.” Stephen alimaliza maneno yake na kuwafumbua macho wadada hawa wawili ambao walibaki kutazamana bila kujua wanachotazamania ni nini! Walizungumza masuala machache na kukubaliana kuanza shughuli hii ya utafiti wa wapi zilipo mali hizo, na jalada la utafiti huu wakaliita ‘Msitu wa Solondo’. Saringo alizama kwenye mawazo mazito sana na daima alijaribu kuunganisha habari hii aliyoisikia kwa Stephan na ile aliyoelezwa na babu yake mzee Koloto miaka mingi nyuma, alijaribu kufikiria kama kuingia ndani ya msitu ule ni wazo linalowezekana au la, kwa maana alishasikia mengi juu ya msitu ule, hakuwahi kufikiri kwenda huko hata siku moja lakini sasa mawazo makubwa mawili yanagongana kichwani kwake moja likimtaka aende na lingine likimzuia na kumuonesha hatari zote zinazomkabili, alifikiria juu ya mali hiyo aliyoisema Stephen ambayo mpaka hapo hakuna alojua ni mali gani iliyofichwa, Saringo alibaki hajui la kufanya. Hellen kwa upande wake aliona wazo la kwenda huko ni zuri lakini alifikiria adha za porini akilinganisha na zile alizopata akiwa huko Amazon, hakujua aamue nini, alifikiri kuwa endapo watafanikiwa kufika mwisho wa safari yao salama atakuwa ni milionea wa kutupwa mara alijiuliza itakuwaje endapo asirudi huko akaona kuwa maiti yake haitaonekana hata kwa ndugu zake, alikata tamaa na kuona kuwa hilo ni wazo hasi kabisa kwa wakati huo. Stephen alikuwa na mambo mengi kichwani, alijua kama akifanikisha safari hiyo si tu atakuwa kitaaluma lakini pia ataukwaa utajiri usokifani kutokana na mali hizo zilizowekwa porini, alifurahi sana kwa ugunduzi huo hata siku hiyo maisha yake yalibadilika na kuanza kuishi kama kibopa mmoja hivi, wanafunzi wake walimshangaa sana alipoingia katika kipindi akiwa na furaha ya ajabu sana, alifundisha kiasi kwamba muda wa kipindi chake ulikuwa hautoshi, kila saa aliangalia saa yake ile aliyoipenda sana. Saringo aliona sasa ndoto zake zimetimia baada ya kujua kuwa amepata watu ambao wameweza kugundua siri ile ambayo yeye hakuijua kirahisi, aliamua kwenda kusoma katika chuo hicho ili naye apate kujua na kwa bahati mbaya au nzuri anakutana na watu ambao wanafahamu na wameshafanya tafiti kama hizo. Saringo aliiona hiyo ni bahati kubwa sana kwake na aliona kile alichokisubiri kwa miaka mingi kitendawili ambacho hakukijua tatuzo lake sasa kimefika mwisho. Alishusha pumzi kwa nguvu na kujinyoosha pale juu ya kitanda chake huku akitafakari hili na lile ‘nani wa kutupeleka msituni? alijiuliza lakini hakupata jibu, alikumbuka tu mahitaji aliyoambiwa na Stephen ‘mtu anayejua misitu, mwenye nguvu na mkakamavu, nani! Cjui’ alijiuliza na kujijibu kwa namna isiyosawa, Saringo alikuwa kama aliyechanganyikiwa katika kichwa chake, hakujua anachofikiri wala anachokiwaza. Kila alipoamua kuingia ndani ya msitu ule akili yake ilimtoa na kumuuliza maswali yasiyo na ukomo, alimkumbuka mjomba wake Golam ambaye mara tatu alijaribu kuingia katika msitu huo wenye maajabu na kukutana na vitu ambavyo havielezeki na hata mara ya mwisho aalikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa, bangi, gongo vurugu nyingi za mtaani ilikuwa ndiyo kawaida yake. Lakini hakuna kitu kilichomsumbua sana saringo kama jinsi gani ya kupata sehemu ya pili ya ramani ile maana ile ilkuwa ni nusu na nusu nyingine je ilikuwa wapi, hilo lilikuwa swali ambalo halikupata jibu hata kidogo ‘hata kama tukienda msituni tutafikaje kwenye maficho haya, hatuna sehemu ya pili ya mchoro huu, babu alinambia kipande kingine kilibaki kwa yule askari wa kundi la pili, mh! Yuko wapi? Alikufa, mzima au alikitupia wapi au kukificha wapi kipande kile, utata!!!’ Saringo alikosa jibu hata usingizi ulimchukua.
********************************
Kutoka juu ya kilima kile Hellen alianguka baada ya kuteleza vibaya alipokuwa katikati ya msafara ule wa wale watu katili wasio na chembe ya huruma, alining’inia kwa kamba ile iliyofungwa kiunoni mwake, akiwa amechoka na uso wake umesawajika vibaya kwa matope, damu zilizoganda zilimfumba macho, njaa ya siku kadhaa haikupata tiba yake, Hellen alibaki akining’inia kwenye korongo lile huku watesi wale wakimvuta kurudi juu, msafara ulisimama kwa muda. Hellen alifikishwa juu na kujumuishwa na wengine na msafara ule uliendelea, ‘Gwerino’ watu wanaokula nyama za watu daima walikuwa wakifanya matambiko katika mawe na mapango makubwa yaliyopo katikati ya msitu wa Solondo. Siku ya matambiko ilikuwa imefika na katika siku hii hutoa damu za watu na kumwaga kwenye mawe yale ambayo wao waliamini Miungu yao ndimo inamoishi, siku hiyo hawakula kabisa nyama za watu kwa kuwa zote walizipeleka Mzimuni. Msafara ulizidi kuingia ndani kabisa ya msitu ule watu wapatao kama kumi na tano walifungwa kamba viunoni na shingoni wakikokotwa huku wakipigwa sana. Hellen kati ya msafara ule alikuwa amechoka sana hata alitamani afe na asifike anakopelekwa, wenzake aliowakuta wamefungwa hakuwajua hata mmoja wao hakujuwa hata wametokea wapi, hakuelewa lugha inayoongelewa na hawa Gwerino, kibaya zaidi alichokishuhudia ni jinsi wanavyoua watu na kula nyama zao wengine wakinywa damu mbichi, Hellen aliona kuwa hii sio dunia aliyoijua kweli hili ni bara la giza, mara kadhaa amepoteza fahamu na alipozinduka alijiuliza kwa nini alikuja kwenye safari mbaya kama hii. Msafara uliendelea, watu walikuwa ni wengi sana wenye mienge mikononi, magongo makubwa, mavazi yao yakutisha yaliyotengenezwa kama ngozi wengine walivaa vidani ambavyo vilikuwa ni mifupa ya vidole vya watu. Kila Hellen alipoona haya alihisi akili yake kuchanganyika na ubongo, Hellen alichoka kabisa hakuweza kuendelea na safari ile alianguka tena na sasa hali ilikuwa mbaya zaidi hakuweza kusogea hata kidogo. Msafara ulisimama na yule kiongozi alishuka kutoka kwenye kiti kile cha enzi kilichobebwa na wanaume wapatao nane hivi walioshiba kwelikweli. “Kusisi libiko?” yule kiongozi aliwauliza waongoza msafara kwa sauti ya kutisha yenye kukwaruza akimaanisha ‘kumetokea nini’ huku akiwa anajongea taratibu na fimbo yake ambayo juu imepambwa na fuvu la binadamu. “Libiko sinzota, kucholo londigo!” alijibiwa na kiongozi wa msafara akimaanisha ‘hapa kuna kafara moja imechoka haiwezi kufika’ yule kiongozi akatikisa kichwa kuashiria ameelewa alichoambiwa “Kucholo? Losa fo, libeso kolilo, a la to” aliongea kwa kufoka huku akizungukazunguka akimaanisha‘imechoka, basi na tuitoe sasa ili miungu ifurahi’ alimaliza na kuigonga chini fimbo yake kwa nguvu na kupaaza sauti huku mkono wake mmoja ukiwa juu “I lee se?” na msafara wote ukajibu “seeee!!!!” akimaanisha ‘ni sawa?’ msafara ukajibu ‘sawa’ . wale waliokuwa wakilinda mateka wale wakamfungua kamba Hellen na kumnyanyua wakasonga nae mbele kidogo, maana katika utaratibu wao kama kafara haiwezi kufika mzimuni basi mnaweza kutolea popote na damu yake ndiyo mtayoipeleka mzimuni pamoja na moyo. Walifanya mduara na wote walianza kugonga fimbo zao chini wakirudiarudia neno lile “Se, se, se, se”. Hellen alifungwa mikono kwa nyuma na kupigishwa magoti kisha mtu mmoja lisimama nyuma yake na kumuwekea mti wenye mfano wa kipago cha manati mgongoni na kamba moja iliyomzunguka shingoni ikavutwa nyuma mgongo wa Hellen ukapinda na kifua chake kutangulizwa mbele tayari kwa kazi hiyo. Yule kiongozi alizunguka kwa mbele na kukabidhiwa ule mti uliochongwa maalumu kwa kazi hiyo akaunyanyua juu na yule kiongozi alizunguka kwa mbele na kukabidhiwa ule mti uliochongwa maalumu kwa kazi hiyo akaunyanyua juu na alipotaka kuushusha kukipasua kifua cha Hellen alisita ghafla, akashusha mti ule taratibu, watu wote walinyamaza kimya kabisa wakiwa hawajui nini kinachoendelea “Ifime, letose seleke, ke la londigo?, bease keloya londigo” kiongozi yule aling’aka kwa hasira akimaanisha ‘laana, hii sio kafara ni mwanamke huyu?, ivueni nguo hii kafara’ watumishi wa kiongozi yule mara moja walimfungua kamba Hellen na kumvua blauzi yake iliyochakaa kwa uchafu wa aina tofauti, kiongozi yule akamwangalia Hellen na kumeza funda kubwa la mate alipoona chuchu zile nyekundu zilivyosimama kama mishale ya saa sita “seleke!” alitamka neno hilo huku akijipiga mkono wake wa kulia kifuani mara kadhaa akimaanisha ‘laana’, katika utaratibu wao ilikuwa kafara lazima awe binadamu wa kiume na si wa kike, muda wote walipomkamata Hellen hawakujua kama ni mwanamke kwa jinsi alivyovaa suruali ile ya jeans, kilichomshtua kiongozi yule ni jinsi alivyoona vitu vilivyotuna kifuani mwa Hellen ndipo alipofikiri kuwa huyu ni mwanamke na walipomvua blauzi ile waligundua kuwa ni kweli. Wote walijipiga kifuani kwa mkono wa kuume wakirudia neno lile ‘seleke’. Hellen aliondolewa kwenye kundi lile la mateka wengine, akiwa bado amechoka sana alitembea kwa tabu, yule kiongozi alimwita mmoja wa majemadari wake na kumnong’oneza kitu kisha alitoa ishara msafara ule uendelee. Hellen aliingizwa kwenye kitu kama pango na kuwekwa pale huku akiwa amefungwa kamba za miti ili asitoroke. Msafara uliendelea usiku ule na mateka wale sasa walikuwa wamebaki kumi na nne. Akiwa mle pangoni, Hellen hakuwa na lolote la kufanya alitulia tu akisubiri mwisho wake ufike, hakujua ni kwa nini alifungwa pale, macho yake yaliendelea kupambana na giza nene lililotawala msitu ule, mbu na mbung’o walifurajhia kupata damu wasiyoitarajia, hakika ilikuwa ni sherehe kwao usiku ule. Hellen alishuhudia mwanga ule wa mienge ya watesi wake ukitokomea msituni, alitafakari sana lakini hakupata njia ya kumtoa mahali pale, alibaki tu amejikalia huku machozi yakimtoka. Katika msitu ule ni mivumo ya miti na upepo tu iliyosikika na milio ya ndege wasiyopendwa na binadamu, bundi. Akiwa katika kutokujielewa Hellen alihisi vichaka vikitikisika aliogopa sana akaanza macho kuangalia ni kitu gani kilichokuwa hapo, hakuweza kufanya lolote kwa kuwa alikuwa amefungwa kwa kamba mikono na miguu yake, alibaki kuangalia tu kitachotokea, mara aliona kama mtu akitokea vichakani mle akinyata kuelekea pango lile, Hellen alitulia akiangalia nyendo zote za kiumbe kile, mtu yule alizidi kunyata kana kwamba kuna watu ambao hakupenda wamuone alisogea mpaka karibu kabisa na mlango wa pango lile, akiwa anamulikwa kwa mbalamwezi hafifu iliyotoke nyuma yake Hellen hakuweza kuona hata sura ya mtu huyu, alijua tu kwa vyovyote atakuwa ni mmoja wa atesi wake ambaye labda amerudi kuja kujifaidia teka lile baada ya kujua kuwa alikuwa ni mwanamke. Hellen alijibanza kwenye kiambaza cha pango lile akiwa kimya kabisa bila hata kujitikisa alisubiri tu kuona mtu huyo atafanya nini kwake.
************************************************
Amata alipumzika vya kutosha katika kichaka kile ambacho alihifadhiwa na yule nyani, alinyanyuka na kujinyoosha viungo na kujikuta yuko fiti kwani yule nyani alimletea chakula pamoja na mizizi mbalimbali ili kumrudishia nguvu ambazo zilipotea kwa mateso yale, Amata aligeuka huku na kule lakini hakumuona Kingusu eneo lile, Amata alitoka ndani ya kichaka kile na kuangaza huku na huko akanyanyua mkono wake na kubana vizuri midomo yake kisha akapiga mbinja kali ya kumuita Kingusu, alisubiri kidogo lakini hakuona dalili ya Kingusu kuwa mahali pale, alipogeuka kurudi alipokaa alikuta uta wake na podo viko pale akavichukua na kuvibeba tayari kwa safari lakini aende wapi? Hata yeye hakujua. Alipiga hatua mbili tatu akasimama tena hakujua bado ni nini anachotakiwa kufanya, baridi kali ilikuwa ikimpa taabu lakini alijitahidi kuivumilia japo mara kwa mara alikuwa akitetemeka. Akiwa katika kutafakari hili na lile kwa mbali aliona kitu kama moshi kikitokea katikati ya msitu ule, Amata aliangalia kwa makini sana moshi ule na akagundua kuwa kule lazima kuna watu, lakini alibaki kujiuliza maswali mengi ni watu wa namna gani hao, au ni vie viumbe vya ajabu ndivyo viishivyo huko lakini hakupata jibu. Aliendelea kuuangalia moshi ule na akaamua kuelekea uko huko ili akaone kulikoni ‘liwalo na liwe’ alipiga moyo konde na kuanza safari huku moyoni akiwakumbuka wenzake wote ambao mpaka muda huo hakujua wapi walipo japo mmoja wao tu, alijiona sasa kabaki peke yake na kilichobaki ni kufanya juu chini kutoka ndani ya msitu ule na kurudi kijijini kwa kuwa hakujua hata aelekee wapi na upande gani, akili yote ilikuwa ni kurudi alikotoka lakini sasa hakujua hata ni wapi alipo. Alitembea kwa hadhari kubwa sana ndani ya msitu huo kuelekea kule alikoona moshi ule alidhamilia kukabiliana na hatari iwayo yote atakayokutana nayo, mara kwa mara alitembea na kuangalia nyuma maana alihisi kama kuna watu wanaomfuata lakini alipuuzia tu kwa kuwa yeye alifahamu mambo mengi sana juu ya misitu. Amata alipita vichakani na alipopata nafasi mara alikimbia na mara alitembea, alipoendelea mbele mara ghafla alijikuta akitokea kwenye ukingo kama wa shimo kubwa alisimama na kuangaza macho huku na huku hakuona mwisho wa bonde lile, bonge kubwa lililofunikwa na miti mikubwa iliyoshonana kwa namna ya ajabu, Amata alipigwa na bumbuwazi hakujua afanyeje kuendelea na safari yake alipoangalia kule kulikokuwa kukitokea moshi ule aliona bado unaendelea kufuka lakini mahali bado pakali mbali, alipoangalia bonde lile lilikuwa ni kubwa na la ajabu hakuwahi kuona kitu kama hicho, Amata aliamua kushuka bondeni kule kwa kutumia mizizi ya miti mikubwa iliyokuwa ikining’inia aliweka uta na podo lake vizuri na kuanza kuteremka taratibu, kila mara aliangalia aendako na atokako lakini aliona hafiki chini, mara ghafla mzizi ule ukakosa nguvu na kukatika Amata alipiga ukelele na kuanguka kwa kasi kuelekea bondeni alijipiga kwenya baadhi ya miti na kupata michubuko kadhaa mwilini aliendelea kupiga ukelele lakini hakukuwa na mtu eneo hilo isipokuwa ndege wa mwituni, kasi ya kuporomoka chini iliongezeka kila nukta Amata alijua sasa hata akifika chini asingepona, alijikuta anadondokea kwenye kitu kama nyavu kubwa, hakuamini alichokiona uoto uliyojishonashona kama wavu ulimdaka Amata naye alikuwa salama, aligeuka kuangali chini akaona sasa si mbali sana kumbe angeweza hata kuteremka tu kwa kujirusha tu. Alijirusha mpaka chini na kutua kwenye lundo la majani makavu akatulia dakika kadhaa lakini hakuona chochote, aliendelea kutembea kwa hadhari kubwa sana na taratibu kuelekea kule alikoona moshi ule, katika kutembea kule alisikia sauti ya mandege makubwa yakilialia Amata alijua popote penye ndege wale lazima kuna mzoga, alisimama na kusikiliza kwa muda huku akijaribu na kuvuta harufu kuona kama kuna harufu ya kitu chochote kilichooza, haikuwa hivyo. Amata alichomoa moja ya mshale wake katika podo na kuupachika vizuri utani kauvuta kwa mvuto wa wastani kisha taratibu alinyata kuelekea walikojaa ndege wale alipokaribia eneo lile alitulia kimya kuangalia vizuri hakuelewa anachokiona kama ni mzoga wa mtu au mnayama, Amata aliingiwa na woga kidogo aliushusha uta wake uliokuwa tayari kwa kujeruhi na kuushika kwa mkono mmoja alipoangalia kwa makini eneo lile hakukuwa na mzoga wowote Amata alisogea na kushuhudia tu madonge ya damu nzito nzito yametapakaa eneo lile alipigwa na bumbuazi hakuelewa aliyepata masaibu haya ni binadamu au mnyama aliiangalia damu ile kwa makini sana ilionekena tukio hilo halikutokea muda mrefu, Amata alitazama huku na huku na kuona michirizi mingine ya damu imeelekea porini aliifuata kwa hadhari kubwa huku uta wake ukiwa umeshikwa tayari kwa kutoa pigo, akiangalia nyuma na mbele kwa haraka haraka aliendelea kufuata damu zile, mbele kidogo alikuta damu zile zimepotea, alisimama na kuangalia huku akijigeuza taratibu pande zote nne za dunia, akiwa pale chini alihisi kama tone la maji limemdondokea, Amata akanyanyua kichwa chake kuona kulikoni, hakuamini macho yake, mwili wa mwanadamu uliyoraluliwa vibaya ulikuwa kwenye moja ya matawi ya mti ule ukining’inia, Amata aliuangalia mwili ule ukiwa pale juu, machozi ya uchungu yalimdondoka nguvu zikamuisha na hasira ikaanza kuchukua nafasi yake, alitamani amuone aliyefanya unyama ule kama ni mnyama au ni kiumbe wa aina gani, Amata alikwea mti ule na kuuteremsha mwili ule mpaka chini akaulaza na kuangalia vizuri ‘Stephan!’ alijisemea moyoni huku akilia aliugeuzageuza, akaweka mkono wake shingoni mwa mwili ule labda angehisi joto lakini mwili ulishatawaliwa na baridi, alijaribu kugusa kifuani kuona kama kuna dalili ya uhai ah wapi! Amata alijishika kichwa na kukosa la kufanya ‘mwanaume chini!’ alijisemea mwenyewe huku akibubujikwa na machozi mwili wa Stephan ukiwa umelala bila uhai, aikuwa na majeraha ambayo yalionesha kwa vyovyote kuwa ameuawa na mnyama mkali. Amata alibaki amekaa kimya karibu kabisa na mwili ule, akiwa na maswali mengi kichwani mwake akijiuliza na kujijibu ‘vipi wale wanawake wawili, bado wako hai au nao wamekufa?’ Amata akauchukua mwili ule na kufanya shimo la kumtosha Stephan ambaye kwa sasa alishakuwa marehemu, akamsitili kwa heshima iliyomfaa, akafanya tuta mahali pale na kuweka kitu kama msalaba, akasimama mbele ya kaburi lile na kutoa saluti ya heshima “kwa heri kamanda, Hellen na ndugu zako hawatakuona tena” Amata akachukua uta wake na kuanza kuondoka, mara akasita na kugeuka nyuma alikumbuka karatasi zile ambazo Stephen daima alikuwa anazisoma ili kupata uelekeo sahihi alitazama eneo lile hakuweza kuziona, taratibu aliamua kurudi kule michirizi ya damu ilipotokea, Mungu si Athumani alizikuta japo zilipeperuka kwa upepo ila hazikwenda mbali sana pamoja nazo aliokota na ile camera ndogo vyote akavitia kwenye mfuko wake wa suruali ile ya jela na kuendelea na safari yake, poli kwa poli Amata alitokea kwenye uwanda mkubwa ulioonekana kama umetandikwa zuria la kijani aliangalia kwa makini akaokota kipande cha mti na kukirushia lol! Kumbe kuna maji, akaendelea kuambaaambaa na ukingo wa bwawa hilo lakini lengo lake yeye ilikuwa ni kuvuka na kuelekea upande wa pili lakini atavukaje ndiyo lilikuwa tatizo, aliendelea kufuata ukingo ule mpaka alipokuta sehemu nyembamba ambayo aliona hapa angeweza kuvuka kwa urahisi, alipokuwa akijiandaa mara akaona maji yale yakitikisika, akaangalia kwa makini hakuona kitu, Amata akarudi nyuma kidogo mbali na mto ule ili kuona nini kilichopo ndani yake, alikaza macho kutazama magugumaji yale yaliyotuama vizuri juu ya maji ambapo kama huna subira basi unaweza kutumbukia ukijua ni ardhi kavu. Wazo likamjia Amata akaingia porini na aliporudi alikuwa na digidigi mkononi akamrusha majini, La haula! Mamba wakubwa walijinyanyua kugombania nyama ile ambayo hata kwa vipi isingewatosha wote, Amata akapigwa na butwaa baada ya kuona jinsi alivyogundua siri hiyo, akakaa chini akiwa hajui la kufanya lakini kichwani mwake akiwa anafikiri jinsi gani angeweza vuka kwenda upande wa pili ambako lengo lake ni kufika kule kunakofuka moshi akiamini kabisa lazima kuna binadamu wanaoishi huko ila mara kwa mara alijiuliza itakuwaje kama watakuwa ni Gorino alijua kuwa huo utakuwa ndiyo mwisho wake jinsi watakavyomtafuna Wazo likamjia, akaingia tena msituni na kufanya mawindo kidogo, akapata mnyama mkubwa kidogo, akamkatakata vipande vya kutosa kisha akasogea pale kwenye yale maji, Amata akamwaga nyama zile kwa ustadi mkubwa na mamba wale walipokuwa wakigombania yeye alitumia mwanya huo kupita juu ya migongo yao kwa kasi na kufanikiwa kufika upande wa pili, alianguka kwenye majani kisha akaangalia kazi aliyoifanya ilivyokuwa na mafanikio, mamba waliendelea kugombania nyama wakati Amata alishafanikiwa lengo lake, aliamka na kujikung’uta majani yaliyoshikana na nguo yake na kuendelea na safari kuelekea kule alikouona moshi ule, sasa Amata alijikuta kwenye msitu wa upande wa pili, msitu wa kutisha wenye mawe mengi na makubwa, yeye hakujali japo huku uoto mwingi ulikuwa wa miba, alihisi kupambana na hatari nyingi kuliko alikotoka lakini alijipa moyo na kuendelea kutembea msituni mle japo kwa taabu sana.
Msafara wa wagorino ulitokomea katikati ya msitu, na kulipopambazuka ulikuwa umefika mahali hasa palipokusudiwa, katika utaratibu wao walitakiwa kutoa kafara usiku wa saba baada ya jua kupatwa na mwezi. Tukio hilo liliwafanya wao waamini kuwa Mungu wao amekasirika hivyo inampasa kuombwa msamaha kwa kumwaga damu na kula nyama, daima walimtoa yoyote kati yao ikiwa hawajapata binadamu wa kumtoa kafala kutoka jamii nyingine. Safari hii waliamini kuwa Mungu wao ‘Kolilo’ atafurahi kwa kupata damu nyingi hivyo kuwaondolea laana ‘seleke’ kwa kuwa walikamata msafara wa waarabu waliokuwa wakipita huko Solondo katika pilikapilika za kutafuna hazina ile ya kale, tamaa mbaya. Gorino waliwateka wote na kuwatesa sana, waliwaua na kugawana nyama kwa ajili ya kitoweo, baada ya kuona kitendo kile cha jua kupatwa na mwezi walijua Kolilo amechukia hivyo inabidi atolewe sadaka ya msamaha, ndipo walipoazimia waliobaki wote wapelekwe mzimuni na watolewe kafara safi. Katika pilikapilika za kulinda himaya yao ndipo walipomkuta Hellen kando ya mto akiwa amekaa na hajui la kufanya. Hellen alipowaona akajua sasa amepata msaada kumbe kaingia mikononi mwa Gorino ‘wala watu’. Binadamu hawa wa ajabu walifurahia kupata windo bila jasho, Hellen aliongea lugha zote lakini wenzake wakabaki kucheka maana hawakuelewa, walianza kumtomasatomasa wakitaka kugawana minofu ya kiumbe huyu aliyenona sana na wengi wao walivutiwa na nyama ya makalio na mapaja kwa kuwa yalijaa hasa, lakini kabla hawajafikia azma yao ya kumcharangacharanga alitokea mwenzao ambaye aliwaamuru windo lile lipelekwe kwa kiongozi wao kwanza halafu yeye aamue ni nini cha kufanya. Walimfunga kamba Hellen na kuenda nae katika ngome yao, moja kwa moja walimfikisha kwa kiongozi wao aliyejulikana kama ‘Kelume’ kwa cheo chake, yeye akaamua kua Hellen achanganywe na wale waarabu wengine ili asubiri zamu yake ya kuliwa nyama, mpaka hapo hakuna aliyegundua kuwa huyu ni mwanamke. Hellen hakujua la kufanya zaidi ya kupata mshtuko alipoona matukio yanayoendelea pale, mauaji ya kinyama huku ngoma ya ajabu ikichezwa na wanawake kwa wanaume ambao kwa ujumla ni kama walikuwa uchi kwani walijifunika tu sehemu za siri. Ngoma hii ilimkera sana Hellen kwa jinsi ilivyochezwa, kwake aliona watu hawa hawana hata chembe ya adabu lakini wenzake kwao ilikuwa ni burudani na maisha ya kawaida, kwani mara kadhaa alishuhudia wakifanya ngono bila kujali na wenzao wakishangilia, mara waliletewa nyama kwenye vyungu vikubwa tu na kula wakifurahi, nyama ya watu. Hellen alizimia alipoona jinsi Kelume anavyoua mmoja wa mateka na kumtoa moyo kisha kushangilia sana na kuilamba damu iliyouzunguka moyo huo, wengine wakinya damu katika bakuli. Hellen alihisi kufika dunia ya ajabu, alizidiwa na harufu mbaya ya damu, ubongo wake ulichafuka kwa kuona matukio yote yale, alizimia mara kwa mara. Hata alipofungiwa katika lile pango kwake ilikuwa ni shida tu maana alijua wazi kuwa wakimaliza kazi yao huko watarudi kwake, alitamani afe lakini haikuwezekana, akimbie lakini alifungwa kamba, hakuna msaada.
“Lito, seki londigo Kolilo isom” amri ilitoka kwa kelume akimaanisha ‘simama, kafara ya kolilo imefika’ msafara ulisimama alfajiri ile katika jiwe kubwa jeusi lililochongoka juu kama kichuguu cha mchwa, hapa ndipo walipotolea kafara yao, nje yake kulikuwa na mawe mengine mengi mengi yaliyojipanga katika mtindo tofauti. Msafara uliweka kambi kusubiri giza liingie ili kalamu ya kafara itolewe, kwa kuwa kafara yao hutolewa tu wakati wa mbalamwezi na si vinginevyo. Mateka wale walichukuliwa na kuwekwa kwenye pango maalumu ndani ya jiwe lile ili kusubiri wakati, huku nje gorino wakiendelea na ibada zao kwa Kolilo. Ndani ya jiwe lile kubwa lililoko juu ya mlima mmojawapo kati ya mingi katika msitu wa Solondo mlikuwano na shimo kubwa na ndani ya shimo hilo kulikuwa na mashimo mengimengi yenye giza la kutisha, mara nyingi nyakati za usiku huonekana vitu vya ajabu katika eneo hili vinavyosadikiwa ni mashetani. Gorino wao wanaamini kuwa hapo ndipo Kolilo anapoishi kwa hiyo huja kutoa sadaka ya damu na nyama ya moyo katika jiwe hilo.
Amata alijikuta mbele ya gofu, alitazama gofu lile kuona kama kuna dalili zozote za kiumbe kuishi lakini hakuona, polepole alisogelea banda lile liliojengwa kwa mawe na miti, lilikuwa kimya kabisa, kabla hajalifikia kabisa alilizunguka kuona labda kuna chochote au yeyote, lakini jambo la ajabu lilitokea kila alipozunguka alijikuta bado yupo upande uleule, akastaajabu na kushindwa la kufanya akabaki amesimama akiiangalia nyumba ile hali mshale wake tayari upo utani kwa shambulizi. Kutoka nyuma yake akasikia kitu kama ndege kikipipiga mbawa na ghafla juu ya banda lile akatua Bundi mkubwa ambaye Amata hakuwahi kuona maishani. Akavuta uta wake na alipouachia mshale ule uliondoka kwa kasi kumuelekea Bundi yule lakini alishokishuhudia ni mshale kudakwa na Bundi yule vizuri na kwa ustadi mkubwa kwa kutumia mdomo, Amata akabaki mdomo wazi na kushusha uta wake chini taratibu. Bundi yule akatuwa chini na mara upepo wakisulisuli ukavuma vumbi likatimka na majani kupepea kila mahali, alipofumbua macho alikuta ajuza kasimama mbele yake, bibi wa umri mkubwa, Amata alimkumbuka bibi yule “usiogope Amata” ajuza akamsihi Amata kisha akaendelea “umeingia kwenye Himaya yangu, na nilijua utafika tu”. Amata alimkazia macho bibi yule kisha akamuuliza “wewe ni nani?” bibi yule alitoa cheko la kutisha lililomfanya Amata kurudi nyuma hatua chache, cheko lile likatulia na bibi yule sasa alikuwa na macho mekundu sana “mimi si binadamu kama wewe” bibi akamwambia Amata “huku binadamu kama wewe hawawezi kuishi wala kufika wengi hufa na sisi huwala nyama” kisha akaendelea “nimekuona muda mrefu sana na nilikuwa nakufuatilia, sisi tunawaogopa sana ninyi binadamu, lakini tumewazidi maarifa” aliendelea kuongea bibi yule kwa sauti yake ya kutisha. “Unatafuta nini huku Solondo?” bibi akamuuliza Amata “nimewasindikiza rafiki zangu, wamekuja kufanya utafiti wa hazina ya kale, inasemekana ipo huku” Amata alijibu kwa kitetemeshi. Cheko baya lilimtoka bibi yule Amata akaingiwa na woga mkuu “wapo wapi rafiki zako?” bibi akauliza “sijui tumepoteana wote msituni ila mmoja amekufa nimemzika porini” Amata alijibu kwa sauti ya shida, kofi zito lilitua kwenye shavu la Amata na kumpeleka chini. “Umeniuzi sana mimi na wenzangu, kwa nini umeondoa nyama yetu ambayo sisi tulikuwa tukiikausha? Halafu ukaifunga tusiweze kuichukua?” bibi yule sasa aliongea kwa hasira na kumsogelea Amata, Amata alirudi nyuma kwa woga. Hapo ndipo Amata alipogundua kuwa kifo cha Stephen kilitokana na huyu bibi, hasira ilitawala roho ya Amata alitamani kulipiza kisasi lakini alijua hapo hatofua dafu alibaki katulia tu na kumeza mate ya hasira. Bibi yule alinyoosha mikono yake juu na alipoishusha Amata alihisi kama kuna watu wametua kutoka juu lakini hakuwaona kwa macho “fumba macho!” bibi yule alimwambia Amata na Amata akafanya hivyo. Amata alihisi kaupepo mwanana kisha kwa mbali akasikia sauti ikimwambia “fumbua macho” na alipofumbua aliona wasichana wazuri ajabu mbele yake, uzuri wao hajawahi ona maishani mwake Amata alistaajabu na kujiuliza kama wale walikuwa ni binadamu kweli au la, alifikicha macho yake na kutazama tena, bibi yule akamshika mkono Amata na kumpeleka ndani ya banda lile, Amata alisikia sauti za watu waliozama katika mahaba zikizidi kuongezeka, sauti za watu walio katika raha ya ajabu, sauti zile zikaanza kumletea kumbukumbu fulani Amata, akavuta hisia kali “Golaaaaaaammmmm!”
Amata alipiga ukelele baada ya kumuona swahiba wake Golam katika dimbwi la mahaba na wasichana wale akataka kwenda katika chumba kile lakini alizuiwa na bibi yule “huwezi fika walipo” bibi kizee alimwueleza Amata. “Nyie binadamu mnatusumbua sana, kuna mambo mengi tunataka kwenu hasa hisia na akili” bibi kizee alimueleza Amata huku akimuongoza kusikojulikana na nyuma yao kulifuatiwa na mabinti wale warembo wenye nywele zinazoning’inia mpaka chini ya viuno vyao. Walifika eneo tulivu sana lililojaa kila aina ya ufahari, Amata alikaribishwa kuketi katika jiwe moja kati ya mengi yaliyokuwa hapo. Na mabinti wale waliowafuata waliwazunguka na kuketi chini, Amata aliwatolea macho mabinti wale muda wote “Amata!” bibi kizee aliita “jambo mnalolifanya ni jambo la hatari sana, sisi wenyewe na maarifa yetu yote ya nguvu ya chini hatuwezi jaribu, tumeshashindwa muda mrefu” bibi kizee aliendelea kumueleza Amata naye alisikiliza kwa makini “Gorino ni viumbe hatari, si binadamu wale hata sisi wametuzidi uwezo” bibi kizee aliendelea kumuasa Amata, Amata alimsikiliza huku akipepesa macho yake huku na kule. “Tamaa yenu binadamu ndiyo inawafikisha pabaya, kwa nini hamridhiki?” bibi aliendelea kuongea na Amata ambaye kwa wakati huo akili yake haikuwa hapo hata kidogo. “Bibi, naomba unisaidie, bila shaka wewe unajua wenzangu wote walipo” Amata alimkatisha bibi kizee. Cheko la ajabu lilimtoka bibi yule “Kijana nitakusaidia lakini kwa sharti moja, na wewe unisaidie” bibi alijibu na kutoa la moyoni “sema bibi, nipo tayari kukusaidia” Amata alidakia na kujibu, “mimi nataka roho hai ya Kelume” bibi alitoa ombi lake “Kelume! Ni nani huyo?” Amata kwa mshangao aliuliza “ha ha ha ha ha! Kelume ni kiongozi wa Gorino, nataka roho yake hai” Bibi kizee alimjibu Amata, Amata alifikiri sana juu ya ombi lile na alipoinua kichwa chake kumtazama bibi yule alikutana uso kwa uso na Bundi mkubwa aliyesimama juu ya kipande cha mti kilichopo mbele hapo, Amata alimtazama bundi yule mara bundi yule aliruka na kutokomea mbali. Amata alinyanyuka pale alipoketi alipoangalia huku na huko aligundua kuwa yuko mahali tofauti na alipokuwa mwanzo, alitulia kidogo na kuvuta akili. Alivuta hatua chache mbele yake na kupanda juu ya jiwe kubwa lililopo hapo, na alipofika juu alijilaza kifudifudi na kuangalia kwa makini pande zote, kwa mbali aliona kitu kama mlima na chini yake aliona kama kusanyiko kubwa la watu, Amata hakuelewa vizuri kama ni watu au ni nini, aliteremka kutoka katika jiwe lile na kusonga mbele kupitia katika vichaka vyenye miiba na mawe ilimradi tu afike mahali ambapo angeona kwa uzuri zaidi. Aliteremka bonde kubwa kwa taabu sana na alipofika chini aliendelea kwenda kwa umakini zaidi kuelekea upande ule alipowaona wale watu, jua lilianza kuchwea na kagiza mororo kalianza kuufukuza mwanga hafifu ulioujaza msitu huo, Amata alijibanza katika jiwe mojawapo na kutulia akisubiri giza litawale ili ajue nini cha kufanya.
**************************************
Hellen alitulia kimya akifuatilia nyendo za mtu huyo ambaye alikuwa akiingia pangoni mle kwa kunyata, akiwa bado na kamba miokononi na miguuni alijiegemeza katika ukuta wa pango lile. Yule mtu aliendelea kusogea alipo Hellen, akanyoosha mkono wake na kumshika mguu Hellen, Hellen hakuleta tabu yoyote alitulia tu kuona nini kinaendelea, yule mtu alimburuza Hellen hadi nje ya pango, ‘Gorino’ Hellen alishangaa na kuingiwa na woga, sasa alijaribu kujinasua lakini hakuweza kwa kuwa alikuwa amefungwa kamba mikono na miguu, mtu yule alitoa tabasamu baya ambalo Hellen alitema mate, kwa kitendo hiko alistukia kofi moja kali lililomrusha upande wa pili, Hellen alilia kwa uchungu. Huku akijigalagaza kama mtoto. Lile pande la mtu likamjia tena Hellen lilimwangalia kwa sura yake ya kutisha iliyopakwa vitu vya ajabu na kuchanjwa chale nyingi, harufu yake ilimfanya Hellen kuhisi kichefuchefu, Hellen aliliangalia lile jitu ambalo lilionekana lina uchu wa kitu fulani toka kwa hellen, likaanza kuongea lugha isiyojulikana, Hellen hakuelewa chochote kinachosemwa aliendelea kulitazama lilipokuwa linamfuata pale alipo, Hellen alijaribu kujisogeza lakini hakuweza. Lile jitu likamkamata Hellen kwa mkono wake wenye nguvu na kumuinua kutoka pale alipokuwa amekaa, likamwangalia na kuanza kumshikashika makalio na mapaja huku mkono mmoja likiwa limemshika bega Hellen, Hellen alihisi maumivu makali sana begani mwake na hakupenda hata kidogo jitu lile lilivyokuwa linamshikashika namna ile lakini hakuweza kujinasua, lile jitu likaanza kumshika kiunoni taratibu likapitiisha mkono wake kifuani na kuanza kuyaminya matiti, Hellen hakuvumilia hata kidogo alijivuta nyuma kidogo na kuachia kichwa kilichompata kwenye mwamba wa pua, damu nyingi zikaanza kuvuja kwenye pua ya jitu lile, hasira zikatawala, lile jitu likachukua mti uliochongwa mbele ambao walitumia sana katika kutoa mioyo ya binadamu, liliunyanyua na kumshambualia Hellen, Hellen alinyayua mikono yake kujikinga uso, mti ule ulipita karibu na uso wa Hellen, Hellen aligeuka upande wa pili na kushudia mikono yake ikiwa huru kumbe mti ule ulikata zile kamba, kazi! Hellen akiwa chini alijifungua kamba za miguu kwa haraka na kusimama kulikabili jitu lile ambalo lilikuwa bado linajaribu kufuta damu zile. Lile jitu lilipotahamaki lilimuona Hellen akianza kukimbia, lilitoa kamba kiunoni na kuirusha miguuni kwa Hellen, Hellen aliruka samasoti moja na lipotua aligeuka nyuma kuliangalia jitu lile lililokuwa likimfuata kwa kasi, Hellen aliruka teke maridadi lililotua shavuni kwa jitu lile lakini halikuonekana kutetereka hata kidogo, Hellen alipotua chini alipiga goti moja na kujizungusha kwa kasi na kumpa ngwara maridadi lakini jitu lile halikuanguka. Hellen alijinyanyua na kurudi nyuma hatua chache kupanga mashambulizi upya kabla hajajiweka sa alijikuta akipata gumi moja la shavu lililompeleka chini, alijibiringisha na kunyanyuka haraka hakujali maumivu wala damu zilizomtoka mdomoni, alipata gumi linigine nalo likampeleka chini sasa hakuweza kunyanyuka mara moja alitambaa kama mtoto kuelekea kule kulikoangukia ule mti wa yule gorino, jitu lile lilipoona mbinu ya Hellen likamfuata Hellen kwa kasi lakini alichelewa Hellen alichukua ule mti na kujigeuza haraka na kuwa chali, jitu lile lilijirusha kuchukua ule mti lakini badala ya kuuchukua lilijikuta likitua kwenye ncha ya jiti lile ambalo lilididimia katikati ya kifua chake, lilitoa macho mpaka likakata roho, Hellen alilisukuma kwa miguu yake na kulitupa pembeni. Hellen alinyanyuka na kuliangalia lile jitu likiwa najiti lake kifuani ‘kumbe na mi naweza’ alijisemea moyoni, ndipo alipogundua kuwa jino moja lilitoka mdomoni mwake na mawili yamelegea, alitema mate yaliyochanganyika na damu, aliendelea kutema lakini aliona damu ile haiishi aliondoka taratibu eneo lile na kuingia ndani zaidi ya msitu ule, hakuwa hata na hamu ya kutaka kujua nini kimejiri katika msafara ule. Alikimbia taratibu huku akipambana na nyasi ndefu miti yenye miba na mawe yaliyomfanya mara nyingi kupunguza mwendo wake huo. Hellen alijikuta amechoka lakini hakukata tamaa huku akiwa anasali kimoyomoyo aliendelea kukimbia na kuomba akutane na mmoja wao lakini haikuwa hivyo aliendelea kukimbia na kuomba asikutane na wanyama au viumbe wabaya. Giza lilianza kuitawala nuru, Hellen akawa amechoka sana akaanza kutembea taratibu na kwa kuwa alikuwa anaogopa giza aliona njia pekee ni kujificha sehemu au kupanda juu ya mti. Akiwa katika usingizi alisikia mlio wa ngoma kwa mbali kidogo, moyo ulimlipuka na kwenda mbiyo maana aliitambua ngoma hiyo ‘Gorino’alijiwazia akijua kuwa kumbe hawakwenda mbali na walipomuacha, ndiyo maana hata yule mmoja alifanikiwa kurudi kirahisi. Hellen alijitahidi kupanda kwa shida kwenye mti mmojawapo angalau ajiepushe na wanyama wapitao huko chini, na alipokuwa juu ndipo alipogundua kuwa mti ule ulikuwa umebeba mtango uliotambaa vizuri na matango makubwamakubwa yakining’inia “Thanks God!” Hellen alijikuta akiongea kwa sauti na kuanza kuyashambulia matango yale kwa fujo, aliporidhika akapitiwa na usingizi akiwa amekumbatia tawi la mti huo.
Alipozinduka ulikuwa usiku mzito sana aliona kwa mbali moto ukiwaka na ngoma zikirindima, Hellen aliangalia na kupata shauku ya kwenda japo alijua ni Gorino waliopo huko kwa kuwa alishauzoea mdundo wa ngoma ile, alipiga moyo konde akashuka kwa uangalifu wa hali ya juu, aliweka miguu chini taratibu na kutazama huku na kule alipoona usalama upo alianza kutembea taratibu kulikabili bonde kubwa ambalo chini huko ndiko alikoona moto ule ‘itakuwaje wakinikamata’ alijiuliza bila kupata jibu, lakini hakusita alisonga mbele kwa kujiamini lakini kila muda aligeuka nyuma kutazama kama kuna yeyote anayemfuata, mara moja akiwa katika kugeuka nyuma alijikuta akitereza na kuporomoka katika bonde refu, alijipiga katika miti na mawe kadhaa yaliyopo katika poromoko hilo.
******************************
Saringo alinyata kwa ustadi sana akihakikisha hakuna anayeona hata unyasi ukitikisika, punde si punde alitokea kwenye jiwe kubwa sana jeusi ambalo juu yake limebeba mawe mengine yaliyokaa katika mitindo tofauti. Saringo hakuwa na woga hata kidogo akiamini kabisa kuwa kama kufa ni kufa tu, aliendelea kunyata kulizunguka jiwe lile ambalo lilichukua eneo kubwa sana, huku akisikia midundo ya ngoma na nyimbo asizozielewa alijaribu kutafuta sehemu ambayo angeweza kuona ni nini kinaendelea, akiwa katika kuzunguka alichuchumaa nyuma ya jiwe moja ambalo lilikuwa na tundu katikati na kupitia hapo aliweza kuona ngoma ile japo kwa taabu kidogo. Ghafla alihisi mkono wa mtu ukimshika bega, taratibu Saringo aligeuka kwa woga kwa kuwa alikuwa hajui ni nani aliyemshika bega, moyo ulimlipuka na kwenda mbio baada ya kuona gorino wawili wamesimama nyuma yake, alijinyanyuka pale alipokuwa amechuchumaa na kuegemea jiwe akitazamana na wale gorino walioonekana kuwa na hasira kali.
Giza liliivamia nchi, sherehe ya kafara ya Gorino ilianza kwa kuwasha moto katia mienge mingi waliokuwa nayo, ngoma na nyimbo zilirindima katika msitu ule, huku na huku katika mawe yale walionekana kuzunguka na kumwaga vitu fulani fulani. Saringo alitulia kimya kabisa katika moja ya jiwe alilohifadhiwa lakini aliweza kuona kila kinachoendelea mahali pale. Mbele ya jiwe hilo aliweza kuona kitu kama shimo kubwa linaloelekea chini na giza nene lilitawala ndani humo, Saringo alijiuliza kama hapo ndiyo mahali pale alipoelezwa na babu yake au bado alikuwa hajafika, lakini hakuwa na la kufanya kwa kuwa mpaka muda huo hakujua ni nani kafa au yuko hai katika kundi lao zaidi ya Golam aliyepotea msituni.
Mbala mwezi ilianza kung’aa na sherehe ya kafara ilizidi kunoga, Saringo hakuwahi kuona ngoma kama hiyo ya ajabu katika maisha yake, lakini jinsi ilivyochezwa ilimvutia sana na hata wakati mwingine alicheka japo hakutoa sauti. Mara watu wawili wakaja hadi pale alipo na kumfungua kisha kutoka nae moja kwa moja katikati ya ngoma ile, Saringo alijaribu kujinasua lakini mikono ya gorino ilikuwa na nguvu za ajabu Saringo hakuweza hata kutikisika alipiga kelele lakini hazikusaidia, alijikuta katikati ya gorino waliomzunguka huku na huku, Saringo hakuwa na ujanja, hakuwa na lakufanya alibaki kutazamana na Kerume aliyevimba kwa hasira maana katika utaratibu wa mwanamke hakuruhusiwa kuwepo eneo la kafara. “Beliiiigo!!!” Kerume alitoa ukelele na ngoma ile ilinyamaza kimya kikuu kikatawala “ Losa, losa, losa ilo seleke” akimaanisha “hii hii hii ni laana” kwa hasira alizokuwa nazo Kerume hakuweza kujizuia alimsogelea saringo na kumpiga makofi kadhaa ya nguvu yaliyompeleka chini, wafuasi wa Kerume walimnyanyua na kumsimamisha wima, Saringo alikuwa akitweta kwa uchungu na hasira lakini hakuwa na cha kufanya. Kerume aliangalia huku na huku na kumyang’anya mfuasi wake mmoja mti aliokuwa akiutumia katika ngoma ile na bila kuchelewa aliunyanyua na kuuteremsha kwa pigo lisilo huruma kifuani mwa Saringo, Saringo alipiga ukelele wa uchungu pale jiti lile lilipotua mwilini mwake, akapiga magoti na kudondoka chini kifudifudi damu zikimmwagika. Kerume alinyoosha mikono yake juu na kutoa ishara fulani. Mwili wa Saringo uliondolewa katika eneo lile na ngoma ile ilianza upya. Ngoma ilipokolea mmoja wa mateka alitolewa pangoni akiwa na kamba shingoni akivutwa kama mbuzi na kupandishwa juu ya jiwe mojawapo lililo katikati ya kiwanja kile na kulazwa chali, Kerume alishuka kutoka alipokaa na mti wake maalumu kwa kazi hiyo, aliunyanyua na kushusha pigo moja kifuani mwa mtu yule alipouchomoa mti ule ulitoka na moyo, yowe la uchungu lilisikika na mtu yule uhai ukamtoka, wengine walitega midomo yao kunywa damu iliyokuwa inaruka kwa kasi kutoka katika mwili ule. Ngoma ilizidi kuchanganya, gorino wengine walionekana wakitoka katika pango lile na mtu mwingine ambaye alikuwa ni mbishi sana na hakutaka kabisa kwenda, kipigo alichopewa hakikuwa cha kawaida mpaka alipopoteza nguvu walimbeba na kumrusha katika pango lingine kubwa zaidi. Joka kubwa lilimdaka kabla hajafika chini na kumviringa kisha kupotea nae pangoni. Kelele za Gorino zilisikika kwa nguvu zaidi wakishangilia kwa kuwa kafara yao ilipokelewa.
Damu nyingi ziliendelea kumtoka Saringo pale alipotupwa na Gorino ambao walikuwa wakijiandaa kumchuna ngozi ili wapate nyama kama walivyoagizwa, kwa kuwa wao hawakujuwa kama mtu yule amekufa au la, waliendelea kuchuna kamba na kunoa vitu kama visu walivyotaka kutumia kwa kazi hiyo. Walimchukuwa Saringo na kuanza kumfunga kamba mikononi ili wamning’inize tayari kuchuna ngozi ile, walipotaka kumnyanyua ndipo mmoja alisukumwa na mkono wa Saringo kwa nguvu hafifu sana akajua kumbe hajafa “soliti igola!” alimwambia mwenzake akimaanisa mbona hajafa. Alichukua jiti lake na kutaka kumdidimiza Saringo moyoni lakini kabla hajatimiza azma yake alianguka chini na kurusharusha miguu na mikono huku na huku uhai ukimtoka. Mwenzake aliangalia huku na huku hakuona mtu Mwenzake aliangalia huku na huku hakuona mtu alipomwangalia mwenzake alikuta mshale umemdidimia katika koromeo na macho yamemtoka pima, alitazama huku na huku hakuona mtu tena aliweka mikono yake mdomoni akitaka kupiga mbinja akachelewa kichwa chake kilitawanywa na ubongo wote ukamwagika hakuweza hata kufurukuta alirushwa na kuangukia upande wa pili, mwingine alikuwa mbali kidogo akiandaa hiki na kile akashtushwa na kishindo kile akarudi na njiani akakuta kiwiliwili cha mwenzake, alitazama vizuri na kujigeuzageuza, akanyanyuka na kuelekea kule walikokuwa wakitaka kumchuna Saringo, alipofika alikuta mwili usio na uhai wa mwenzake nao umelala pale lakini hakuona ile nyama yao, alionekana wazi kuchanganyikiwa hakujua afanye nini, katika kuzubaa huko kamba ilimnasa shingoni na kumnyanyua juu alirusharusha miguu lakini taratibu sana roho iliacha mwili, mwili wa marehemu yule ulianguka chini na kutulia kimya.
Hellen aliipachika bastola yake kiunoni, akisaidiana na Amata waliubeba mwili wa Saringo aliyeonekana bado anapumua kwa mbali, Hellen alijitahidi kumpa tiba angalau kuokoa damu iliyobaki na kufunga jeraha lile kwa kutumia blauzi yake, Hellen aliamua kubaki na kanguo kepesi ka ndani tu baada ya kuichana blauzi yake ili kumsitiri Saringo, Amata alileta maji na kumnywesha Saringo ambaye alionekana kupoteza nguvu nyingi sana hasa kwa kutokwa na damu, kimvua chembamba kilinyesha usiku ule na hii ilikuwa ni ahuweni kubwa kwa Saringo, Hellen aligundua kuwa pigo lile la Kerume kwa saringo halikutua sawasawa moyoni kwake sipokuwa lilipiga chini kidogo na kuvunja mbavu karibu mbili tatu za juu za upande wa kushoto. Amata aliingia porini nakuja na aina fulani ya majani ambayo aliitafuna na kuweka katika jeraha lile na kufunga vizuri. Walipohakikisha Saringo yupo salama wakaanza kupanga mikakati jinsi ya kuvamia eneo lile, kundi lile la Gorino liliwatisha sana kila walipojiangalia silaha walizo nazo zisingeweza kufanya chochote. Hellen aliifungua ile karatasi aliyopewa na Amata akaangalia vizuri mchoro ule na maandishi yote yaliyoandikwa mle akagundua kuwa pale katika lile jiwe ndiyo kuna pango la hazina. “Tupite nyuma ya jiwe, ili tuwatokee kwa nyuma” Hellen alimuambia Amata kwa kiswahili cha kubabaisha, Amata aliangalia vizuri eneo lile ambalo kwa wakati huo halikuwa umbali wa kutisha waliweza kuona kila kitu kinachoendelea, walimuacha Saringo pale baada ya kumuhifadhi vizuri na wao kuteremka bondeni kisha kwa mwendo wa kunyata walilizunguka eneo lile na kutokea kwa nyuma kama walivyopanga. Walitafuta eneo zuri ambalo wangejificha lakini pia wangeweza kuona vizuri ili kujua nini wafanye, Amata na Hellen walijificha vizuri katika kichaka kidogo lakini si mbali na eneo lile huku wakiwa makini kuona kama kuna chochote cha kuwasumbua, alilivua podo lake na kuhesabu mishale ilobaki, si haba ilikuwa kama ishirini na tano na alipotazama kundi lile alikuta kuna Gorino zaidi ya mia moja Amata alichanganyikiwa akamtazama Hellen ambaye wakati huo naye alikuwa akihesabu risasi alizonazo baada ya kupewa kikasha kile na Amata si haba zilikuwa kama mia na ishirini akamnyoshea alama ya dole gumba Amata naye akajibu kwa mtindo uo huo. “Subiri hapa mi nasogea mbele nione wanafanya nini!” Amata alimueleza Hellen “Wapo kwenye kafara hata mimi nilikuwa kwenye msafara huo, wanaua watu, kuna watu kama kumi na tano hivi” Hellen alimueleza Amata. Amata alijivuta taratibu mpaka karibu na jiwe kubwa lakini hamad! Alijikuta amekutana na Gorino aliyeko katika ulinzi wa eneo hilo, Amata alimtazama na kabla Gorino yule hajakaa vizuri alijikuta akipaa hewani kwa ngwala safi aliyopigwa na Amata, alitua kama mzigo na alipofika chini bisu kubwa la Amata lilidimia kifuani mwa Gorino yule na kupoteza uhai. Amata alitazama huku na huku kuhakikisha usalama kisha akaendelea kusogea upande wa pili kulizunguka jiwe lile, kabla hajakata kona alimuona Gorino mwingine aliyekuwa kasimama akitazama upande mwingine Amata alifikiri atumie mbinu gani kumuondoa lakini alikosa kwa kuwa hakuwa tayari kutumia uta wake kwani alibakiwa na mishale michache, alifikiri kama atumie mikono kumkabili lakini akaona inaweza kuwa mbinu mbaya endapo atazidiwa nguvu, aliokota jiwe la kutosha na kulirusha kwa nguvu zote na kumpiga kisogoni, Gorino yule aliyumba na alipokaa sawa aligeuka nyuma uso uso kwa uso na Amata, Gorino alirusha jiti lake kwa Amata lakini Amata aliepa kwa ustadi na shabaha kukosa uelekeo, Amata alidakwa koo hata akajikuta anakosa nguvu alijikusanya na kupiga kifuti kimoja kati maeneo nyeti ya Gorino yule, kutokana na maumivu yale alimuachia Amata ambaye alichukua nafasi hiyo kumtandika mateke mawili ya usoni yaliyomfanya anyanyuke kisha Amata akajirusha mzimamzima na kutua kwa miguu miwili kifuani mwa Gorino yule ambaye aliyumba tena na kujipigiza kwenye jiwe, damu zilimtoka kwa wingi kisogoni akajibwaga chini na uhai ukaambaa zake, maiti! Amata alipanda polepole juu ya jiwe lile lakini kwa kuwa alikuwa haoni anakoelekea kumbe mmoja wa Gorino alikuwa kule juu, Hellen alimuona vizuri sana Gorino yule lakini alifikiria afanyeje kama angetumia bastola yake basi ile kelele ingewashtua wengine, moyoni aliteseka lakini hakujua afanye nini alibaki kutazama tu kitachotokea. Amata alishika vizuri jiwe la juu ili ajivute lakini mara akahisi kitu kimemkanyaga, hakusita aliendelea kujivuta na hapo alijikuta ameshikwa mikono yake na yote miwili na Gorino yule na kuvutiwa juu ya jiwe lile, Amata alijinyanyua na lipo simama wima alimpiga kichwa Gorino yule na kumsindikiza kwa makonde mfululizo, Gorino alipepesuka lakini Amata alimdaka na kumgeuzia upande wa pili ambapo alimponyoka na kuanguka kutoka juu ya jiwe lile kabla hajafika chini joka kubwa lilichomoza kutoka pangoni na kudaka juu kwa juu na kuteremka nae chini mpaka pangoni Amata alibaki na bumbuwazi.
***************************************
Kule chini ngoma ya Gorino iliendelea na kafara ziliendelea kutolewa, tayari watu karibu watano walikwishauawa kinyama na eneo lote lilikuwa likinuka damu lakini kwa Gorino hiyo ilikuwa ni sherehe kubwa sana waliimba na kucheza wala hawakujua kama kuna wenzao waliokwishapoteza maisha kati usiku huo. Kerume akiwa juu ya jiwe lililochongwa kama kiti na wafuasi wake aliendelea kusherehekea karamu ile ya damu zalondigo, huku akitafuna nyama mbichi. Alitolewa mtu mwingine tayari kwa kafara akapandishwa juu ya jiwe lile la kutolea kafara ambapo wakishamkata kichwa lazima kidondokee pangoni na damu yake kutiririka kuelekea uko huko ambako wao waliamini kuwa Kolilo ndimo anamoishi. Alikuwa ni kijana wa makamu aliyekuwa akileta upinzani wa hali ya juu ili asipelekwe katika jiwe lile, Gorino walimshika vizuri na kumburuza kumpeleka jiweni walimpandisha na kumfunga panapotakiwa tayari kwa kutoa kafara ya damu. Hellen kutoka mbali aliweza kuona kila kinachoendelea na alipoona huyo kijana akamkumbuka kwa kuwa alifungwa jirani yake wakiwa kama mateka kule msituni, alilia kwa uchungu, akachukua bastola yake akaiweka sawa ‘liwalo na liwe’ akajisemea moyoni akaanza kuitafuta shabaha lakini hakujua nani hasa anayemlenga Kerume au wafuasi wake ‘atakayenyanyua mkono wake tu ninaye’ alijisemea huku akiuma meno aliweka bastola yake na domo la revolver lilikuwa tayari tayari kutekeleza litakachoamriwa na mkono wa Hellen. Gorino walipiga kelele kama ishara ya kutekeleza agizo la Kerume, Gorino mmuaji ambaye mwili wake wote ulichafuka damu ya binadamu alinyayua juu lile jiti lake tayari kwa kazi, kabla hajashusha alipaishwa juu na kujibwaga kama mzigo jeraha kubwa lililokuwa kifuani mwake lilimfanya ashindwe kuyashinda mauti, bastola ya Hellen ilifuata maagizo sawasawa. Amata akiwa juu ya lile jiwe alishtushwa na mlio ule na moja kwa moja alijuwa kuwa Hellen keshafyatua risasi na kuwachokoza Gorino. Hali ya eneo lile ilivurugika gorino walitawanyika eneo lote kutafuta adui wao wakiwa na munkari wa kuua yeyote watakeyemuona. Amata alitegemea kwa hali ile wote wangeweza kumuacha Kerume ili amtoe uhai kama alivyokubaliana na Bibi kizee lakini haikuwa hivyo gorino karibu ishirini walimzunguka Kerume wakirukaruka huku na huko ingekuwa wamasai tungesema wamepandisha mori. Gorino walizunguka wakiwa hawajui ni nani wananemtafuta sherehe imevurugika, Amata alijikuta akinaswa kwa kamba mguuni ambayo ilimuangusha kutoka juu ya jiwe lile mpaka chini na uta wake ukimtoka mkononi Gorino ailiyemvuta kwa kamba ile alinyanyua jiti lake ili kumchoma lakini haikuwa hivyo wakati kageuka kuangalia juu alijikuta kichwa chake kikifumuliwa kwa risasi kutoka kwa Hellen, Hellen alihama haraka kutoka katika kichaka kile na kukimbilia nyuma ya mbuyu mkubwa uliopo mahali hapo, sasa kwake ilikuwa ni kama kulipa kisasi kwa yote ambayo walimfanyia akiwa mateka, hakutaka hata kidogo kumpoteza Amata katika macho yake, alibaki bado anamwangalia pale alipoangukia, akiwa anajizoa zoa Gorino mmoja alikuwa akimjia kwa kasi akifuatiwa na wengine nyuma yake huku wakipiga kelele yule wa mbele hakufika kwani nae alipaishwa juu na kifua chake kilifumuliwa vibaya na risasi nyingine ya Hellen, Amata kwa haraka alinyanyuka na kuokota uta wake lakini kabla hajajiweka sawa alipata pigo moja la mgongoni alihisi kupigwa na kitu ka jiwe aligeuka kwa kasi na kuchomoa jisu lake pigo moja la shingo liliruhusu jisu lile kupenya Amata akalichomoa wakati huo akimsindikiza na teke kali la nyuma gorino wa pili ambaye alipepesuka bila uelekeo na kuangukia kando. Kerume alipagawa na kuchuka uta wake wenye nguvu ya ajabu aliweka mchale wake na kuuvuta shabaha kuelekea kwa Amata aliuachia na kasi uliotoka nayo haikuwa rahisi binadamu wa kawaida kuuepa…
********************************************
KIUMBE cha ajabu kilimtokea Saringo katika maficho yake, Saringo ambaye wakati huo hali yake ilizidi kuwa mbaya kwa kupoteza damu nyingi alikuwa ametulia kimya hana la kufanya na alikuwa akiangalia tu nini kitatokea. Alitamani sana kwenda kuwasaidia wenzake kwa kuwa aliona jinsi walivyobanwa na Gorino katika mapambano yale lakini alishindwa kabisa. Alijikaza lakini alikuwa anaogopa mno jinsi kiumbe kile kilivyoonekana, kilisimama mbele ya Saringo na kumwangalia kisha kikamsogelea na kunyoosha mkono wake kuelekea jeraha la Saringo. Kiumbe kile kilikuwa na vidole virefu na kadiri ya umbali vilikuwa vikirefuka kuelekea kwa saringo na alimpogusa jeraha Saringo alihisi ganzi mwili mzima na kuzirai. Bibi kizee alikuwa akipita eneo la mapambanao kwa umbo la Bundi lakini alishindwa kabisa kutoa msaada wowote ka Amata na Hellen, hakuwa mbali kwa kuwa kile alichokubaliana na Amata kilikuwa bado hakijatimia. Katika eneo lile ilikuwa vigumu kwake kujigeuza na kuwa katika umbo lingine kutokana na uchawi wa hali ya juu ambao Gorino waliuweka eneo lote la tambiko, hivyo ilikuwa ni vigumu kwa viumbe vingine kutawala eneo lile au hata kupita ilikuwa ni vigumu kwao. Na katika pambano la Gorino kumuondoa bibi kizee na wasichana wake eneo lile ilikuwa kazi ngumu kwa kuwa kila mmoja alikuwa na zindiko lake mahali pale, lakini Kerume kwa kutumia uta wake wa kichawi aliweza kuwashinda bi kizee na wasichana wake ambao hata wao miaka mingi nyuma walikuwa wakifanya matambiko yao hao, na humo ndani ya pango walihifadhi vitu vyao vingi ambavyo Kerume alipowashinda alifunga kwa kuzindika na nguvu zake za kichawi hivyo bi kizee na wasicana wake wakawa kama watumwa wa Gorino. Bibi kizee alimuomba Amata Roho ya Kerume akimuahidi kumpatia kila atakachopata. Saringo alikimbia taratibu kuelekea eneo la mapambano alimuona Hellen alipokuwa akipambana na Gorino wale kwa kutumia bastola yake ambayo ilikuwa karibu na kwisha risasi. Amata akiwa na uta wake mkononi sasa lengo lake lilikuwa ni kumtafuta Kerume lakini katika pango aliloingia kulikuwa na walinzi watano baada ya mmoja kuuawa, akiwa katika mwendo wa kuchechemea alijaribu kukwepa vishale vya Gorino ambavyo vingi vilimwandama yeye. Hellen hakuamini kumuona Saringo eneo lile, Saringo aliingia katikati na mkononi akiwa na kitu kama mfupa ambao aliutumia kama silaha kwa kuwapigia Gorino wale lakini alichoshangaa ni kuwa kila aliyempiga nao hakuweza kupona, aliendelea kupambana na Gorino waliosalia eneo lile kwani wengine wlitawanyika hawakuonekena ila walijificha kwa kuwa hawakujua la kufanya. Kingusu aliwaandama walinzi wa Kerume kwa kupiga mishale kwa ustadi mpaka walipoukiambia mlango wa pango aliloingia Kerume, Amata alipotaka kuingia alihisi kitu kumpiga kichwani akarudi nyuma na kuangalia juu mmoja wa Gorino alimpiga Amata kwa kutumia kitu kama nazi, Amata alipanda juu ya jiwe na kumrushia kisu kilichompata sawia kifuani. “Amataaaaaaaaa!!!!!” sauti kali ya Saringo ilimfanya Amata ageuke nyuma kitendo hicho ndicho kikamfanya apone kutoka katika msahale uliopigwa kutoka pangoni, mshale wa Kerume mshale wa kichawi usiokwepeka na binadamu, Amata alipepesuka na kuanguka chini, alimuona Kerume akitoka Pangoni na kuja nje, Amata alijiinua haraka na kusimama kidete uso kwa uso na Kerume. Kerume alimvamia Amata kwa nguvu Amata akaepa upande na kumpiga ngwala lakini Kerume aliruka na kusimama sawia, akageuka na kumpiga Amata na kikoto cha mfupa Amata aliyumba na kuanguka karibu na mlango wa pango, Kerume alimfuata akiwa na hasira lakini kabla hajamfikia Amata, Kingusu alifyatua mshale uliopita mbele ya uso wake pale alipoukwepa, Kerume aligeuka na kutazama juu ya mti akamuona nyani mkubwa “Beselo sito!” akimaanisha ‘huu ni mwisho’ akachukua mchanga na kuupulizia kule alipo nyani yule punde si punde nyuki walijaa eneo hilo na kuanza kuuma kila aliyekuwepo. Hellen na Saringo walilala chini lakini haikusaidia, nyuki walimzingira Hellen aliyekuw akijaribu kukimbia kutafuta pa kujificha, Hellen aliumwa na nyuki wnegi waliompelekea kukosa nguvu na kuanguka chini, Saringo hakuwa na la kufanya juu ya nyuki wale wakali. Amata alipata muda wa kunyanyuka na kuegemea jiwe, Kerume alinyanyua jiti lake na kumchoma Amata kifuani lakini Amata alibonyea chini na jiti lile likapiga kenye jiwe, Amata alipita katikati ya miguu ya Kerume na kutokea nyuma yake aliruka teke la kusukuma na kutua mgongoni mwa Kerume ambaye aliyumba kwenda mbele na kabla hajageuka mshale wa Amata ulikuwa njiani alipogeuka tu uso kwa uso na mshale ule lakini Kerume aliudaka kwa mdomo wake akaugeuza na kuurusha kwa mdomo na mshale ule ulichomoka kwa kasi ya ajabu, Amata alishindwa afanyeje lakini kabla hajaamua jambo mshale ule ulikosa nguvu na Amata akaudaka kwa mikono yake. Kerume kwa kutumia kikoto chake cha mfupa alimpiga Amata mapigo ya kifo lakini Amata alikwepa yote kwa ustadi huku akirudi nyuma mwisho Kerume alirusha kikoto kile Amata alikwepa, Hellen alikuwa anajaribu kunyanyua uso wake ndipo alipohisi maumivu makali katika paji la uso, kikoto cha mfupa kilichorushwa na Kerume kilitua usoni kwa Hellen, Hellen aliona giza kuu likiyavamia macho yake, kutoka pale alipodondoka wakati akishambuliwa na nyuki alijilaza tena. Amata alipigwa kichwa na Kerume, alijitoa kwenye mikono ya Kerume na kurusha ngumi mfululizo ambazo zilimpata Kerume lakini hakutetereka hata kidogo. Amata alijifanya kukimbia kuelekea kwa Saringo na Kerume alimfuata, Saringo alimrushia Amata ule mfupa na Amata alipoudaka tu aligeuka na kumtandika Kerume kichwani, Kerume aliyumba na kabla hajatulia Amata alimpiga tena kichwani pigo ambalo lilimpeleka chini Kerume hakiwa hajiwezi, akiwa anatambaa kujisogeza na Amata alikuwa akitembea kumwangalia, akamkanyaga kichwani na kukishindilia kichwa kile katika mawe. Upepo mkali ukaanza kuvuma miti yote ikawa ikiyumba kwa kasi ya ajabu, vumbi lilitimka eneo lote. Amata aliona mwanga wa ajabu uliong’aza eneo lote, mwanga wa rangirangi za kumetameta, Amata akanyanyua uso wake kuangalia mbele na juu ya jiwe lile alimuona Saringo kasimama akiwa na upanga mkononi, upanga uliokuwa ukitoa mianga ya ajabu na mkono wake wa pili ameshika kichwa cha chui. “Saringo!” Amata aliita huku akiondoa mguu wake pale alipomkandamiza Kerume. “Mimi sio Saringo” alisema mwanamke yule huku akishuka mpaka pale chini alipolala Kerume, sasa akiwa uso kwa uso na Amata. Akampa Amata kile kichwa cha chui kisha akanyanyua upanga wake juu kwa mikono miwili. Kelele zilisikika msituni za watu wakilia na kuomboleza, upepo nao aulizidi kuvuma eneo lote, Saringo bandia akashusha upanga na kukata Shingo ya Kerume, kichwa chake kiliachana na kiwiliwili lakini cha kushangaza kiwiliwili kile hakikutoa hata tone la damu. Saringo bandia akakitupa kichwa cha Kerume katika moto uliokuwa ukiwaka eneo lile kisha akachukua kichwa cha chui kutoka kwa Amata na kukisemea maneno fulani ambayo Amata hakuyaelewa na kukipachika kile kichwa cha chui katika kiwiliwili cha Kerume na muda huo huo Kerume akageuka Chui mkubwa wa kutisha, Saringo bandia aliongea maneno fulani na Chui yule akakimbilia msituni. Amata alibaki mdomo wazi huku akionekana na sura ya woga, akageuka nyuma na kumuona Hellen akiwa kalala chini akamfuata na kumtazama alionekana kama hana uhai, aliyageuza macho yake na kuona tayari ni mfu. Amata alidondosha chozi, mara akasikia kama kundi la watu likija mahali pale alipogeuka aliona kundi la Gorino likiwa limesimama nyuma yake. “Usiogope Amata” yule Saringo bandia alisema “Hao wote ni mateka wangu, hawana nguvu tena kwa kuwa Kerume zindiko la kichwa cha chui amerudi alikotoka” aliendelea “Hapo unapowaona hawajaja wenyewe wamekamatwa na kuletwa. Tumerudi kwenye himaya yetu ya Msitu wa Solondo, katika pango la Mtukufu Baghoza hakuna aliye juu yetu ila wote wako chini yetu, na sasa ni zamu yetu kutoa kafara kwa Baghoza” Saringo bandia aliongea na Amata wakati Amata akiwa bado kamshika Hellen ambaye tayari mwili wake ulikuwa wa baridi kabisa. “Amata, umefanya kazi tuliyokuwa tumeishindwa kwa karne na karne, unastahili zawadi kubwa kuliko unavyofikiria.” Saringo bandia alimwambia Amata “U nani wewe? Mbona unafanana na Saringo?” Amata aliuliza “Mimi ni Baghoza, kinara wa roho zisizoonekana. Unisamehe Amata, nilimkuta Saringo anakata roho nikauchukua mwili wake lakini hapa tunavyoongea ameshakufa” Saringo bandia aliinamisha kichwa kuonesha masikitiko “Baghoza!” Amata alitamka na kupiga magoti mbele ya Saringo bandia, akaendelea “Kuliko kunipa zawadi yoyote, naomba nirudishie uhai wa watu wangu” “Ha ha ha ha ha haaaaaa, Baghoza hata kama ndiye mleta mauti na mtoa uhai, siwezi kukutimizia hilo kwa sababu moja” akatulia kidogo kisha akaendelea “Solondo si eneo la kuishi ninyi binadamu, kama sisi hatuji kwenu na sisi hatupendi mje kwetu. Mnafata nini huku?” Saringo bandia aliendelea kumwambia Amata “Wewe hukutaka kuja huku, hata hujui huku kuna nini, ila hawa wenzako wana tamaa ya mali na utajiri hata ijapokuwa wanajifanya wanafanya utafiti, sisi tuna uwezo wa kuona fikra zenu. Amata kumbuka tamaa mbele mauti nyuma, kwa tamaa yao wote wamekufa na hawataamka tena. Ila wewe kwanza umetusaidia kurejesha himaya yetu hatuna budi kukupa zawadi, na ukishaondoka hapa sisi tutaendelea na ibada yetu ya kafara” Saringo bandia alisema hayo huku akiwa na upanga wake mkononi. Aliunyoosha upanga wake na ukaanza tena kutoa ile miale ya mwanga iliyoangaza eneo lote pale katika jiwe, mara upepo ukaanza tena kama mwanzo sasa ulikuwa wa kuzunguka na ukakusanya vumbi kubwa kisha katikati ya upepo ule Amata aliona kama mtu kasimama na ulipotulia alimuona bibi kizee kasimama pale na hakumuona tena yule Saringo bandia. Yule bibi kizee akamsogelea Amata, akainua mkono wake na kutoa pete iliyokuwa iking’aa sana iliyowekwa jiwe la yaspi safi na kwa ndani ilikuwa na madini kutoka sayari ya Uranus. Amata akaipokea na kuigeuzageuza ilikuwa ikitoa rangi nyinginyingi. “Vaa katika kidole cha kati mkono wa kushoto” bibi kizee alitoa maelekezo. Amata akavaa na alipomaliza aliona mji mkubwa sana mbele yake majengo marefu marefu na wanawake wazuri warembo wa kuvutia wenye nywele ndefu, hakika mji ule ulikuwa ni wa kipekee, cha ajabu aliona wanawake tu na ailipogeuka nyuma yeke alijikuta kazungukwa na wadada wengi sana, Amata alistaajabu aliyoyaona hapo, akanyanyua mkono wake na kuitoa pete ile kidoleni, akajikuta yupo palepale msituni na mbele yake bibi kizee akimwangalia, aligeuka nyuma na kuona hakuna wale wasichana isipokuwa Gorino walioletwa pale.
“Vaa katika kidole cha shahada mkono wa kushoto” bibi kizee alimwambia Amata. Amata akavaa pete ile katika kidole cha shahada, mbele yake aliona moto mkubwa ukiwaka katika shimo, cheche kubwa za moto zilikuwa zikiruka na kurudi shimoni, alisikia vilio vya watu wakilia kwa maumivu makali na kusaga meno, Amata aliangalia vizuri na kuona watu wengi wasio na idadi. Amata akatoa machozi akalia kwa vikwifukwifu kwa kuwa aliwaona Hellen, saringo, Stephan na Golam wote wakiwa katika mateso hayo. Aliivua pete ile na kuishika mkononi. Alijikuta tena na bibi kizee. “Bibi kwanini rafiki zangu wapo huku?” Amata aliuliza “Watu wote wenye tamaa ya mali huishia huko, huwezi kuingia Solondo ukafika kwenye jiwe hili kama una tamaa ya mali. Hizi mali ni zetu, kila penye madini na sisi tupo na tunayalinda sana. Hawa Gorino walitufukuza hapa na kuchukua wao, wakamuweka huyo nyoka wao wa ajabu, huyo hakuwa nyoka wa kawaida, mshale wa Kingusu ndiyo umemmaliza huyo Nyoka.” Bibi kizee alimueleza Amata na kisha akanyanyua kichwa chake kuangalia angani akaendelea kusema “ Mwezi umekuwa mpevu, huu ni muda wetu. Amata naomba tuagane, pete hiyo utaivaa kila utapoitaji kuonana na sisi, utaivaa kidole cha kati kisha utaigonga kwa kwenzi mara tatu utafunguliwa mlango, ukigonga mara nne utaomba chochote tutakupa. Tahadhali, usiigonge mara moja wala usiigonge mara mbili.” Bibi kizee alimuasa Amata “Sasa pita katikati ya hilo pango kubwa, huko chini utakuta mambo mengi sana usiogope utakutana na viumbe wa ajabu usiogope, teremka chini mpaka ngazi ya kwanza kutoka ya saba utakuta milango imejipanga nenda mlango wa kwanza kutoka wa tano fungua uingie pale utakuta vitu vingi sana chagua kadiri ya uwezo wako uende zako” bibi alimaliza kuongea “Bibi, nitajuaje njia ya kwenda kwetu? Hata nilivyokuja sijui” Amata aliuliza tena “Amata muda umeisha tunataka tuanze kazi yetu, nenda sasa ingia haraka kimbia, imetosha, tena usigeuke nyuma kabisa” sauti ya bibi ilianza kuwa ya kutisha yenye mwangwi wa ajabu. Amata aliiuacha mwili wa Hellen na kuingia pangoni kwa kasi, nyuma yake alisikia radi kali na ngurumo za ajabu. ??? GIZA nene lilitanda kila kona ya pango lile, Amata hakuweza hata kuona wapi anaelekea, alivuta hatua fupifupi kwa kuwa alihisi kama akiteremka ngazi, nyuma yake alisikia tu kama vitu vikianguka na watu wakipumua kwa nguvu alitamani kugeuka lakini alikumbuka maneno ya Baghoza, alijikaza na kusonga mbele, alizidi kuteremka chini zaidi huku akipapasa kwa kuwa hakuweza kuona hata umbali wa urefu wa mkono wake. Woga ulimtawala, nguvu zilimpungua alihisi akikosa hewa ya kutosha, akiwa bado anaendelea kuteremka alihisi amekanyaga kitu, akarudisha mguu kisha akakanyaga tena akuhisi kile kitu, akaendelea kuteremka ndipo alipohisi mguu wake ukishikwa na kitu kama mikono akaanza kusikia sauti kama ya siafu wengi waliokuwa wakitembea, Amata alifikiri kurudi nyuma lakini alikumbuka maneno ya Baghoza, moyo wake ulikosa la kuamua akanyanyua mguu kwa nguvu lakini bado hakuweza ndipo alipoinama kushika kilichopo mguuni alijikuta akipigwa kofi la utosini lililompelekea kudondoka katika ngazi zile na kuviringika kuelekea chini zaidi. Alisikia sauti za vicheko zikimsindikiza na alipofika chini kabisa utulivu ulirejea kama mwamnzo, sasa hakuweza kusikia vya nje wala vya ndani. Amata alinyanyuka na kuketi, kila mara mwili ulimsisimka lakini hakuweza kuona chochote katika pango lile. Alipokumbuka maelekezo aliyopewa na bibi kizee Amata alihisi kupata ganzi kani hakukumbuka kuhesabu ngazi alizoshuka hivyo hakuweza kujua yuko ngazi ya ngapi, alijishika kichwa na kujilaumu nafsi yake kisha akasimama na kuendelea kushuka lakini hakukuta ngazi za kushuka bali ukuta ulimkinga hakuweza kusonga mbele, aliposhika kushoto na kulia kote aliona vivyo hivyo, hakuwa na budi zaidi ya kurudi nyuma ili aweze kuhesabu ngazi zile. Lakini akiwa katika kutafakari afanyeje maana aliambiwa asithubutu kugeuka nyuma, aliikumbua pete yake aliyopewa na bibi kizee aliunyanyua mkono wake na kuigonga kwa kutumia kwenzi mara nne pete ile ikabadilika na kuwa ya buluu, “ninaomba msaada nimepote pangoni na kuna giza sana” Amata alimaliza kusema kisha kutulia kama sanamu. Upepo mwanana ukaanza kuvuma katika pango lile mara Amata aliiona mienge iliyotundikwa pembeni ya ukuta ule ikiwaka mmoja baada ya mwingine, baada ya muda mfupi pango lile lilikuwa linang’aa, Amata alichomoa moja ya mienge ile na kuanza kupanda ngazi zile kwa kurudi nyuma bila kugeuka. Aliendelea taratibu mpaka alipofika mahali alipoelekezwa, pale akakuta kuna lango kubwa bila kuchelewa na mwenge wake mkononi akaingia na kuvuta hatua chache alihisi kuna viumbe vikipita mbele na nyuma yake vikiwa katika shughuli mbalimbali lakini hakuweza kuviona kwa macho. Pango lilijawa na nyzi nene za buibui kila kona zikiashiria kuwa humo ndani ni muda mrefu hakujaingiwa na mtu. Katika kutazama uku na huku akaona milango kadha wa kadha imejipanga na kuwekwa makufuli makubwa. Alihesabu milango ile lakini ilikuwa ngumu sana kwa kuwa aliona kama inamzunguka, alikata tamaa mara akakumbuka maelekezo ya bi kizee akaaza kuhesabu tena sasa akaupata mlango aliyouhitaji, mlango mkubwa wenye kufuli nene akajaribu kutoa yale mabuibui na kuufikia. Mlango ule ulikuwa na picha ya kichwa cha nyoka mkubwa sana, Amata aliusogelea na akaona kichwa kile kinapata uhai na kufungua mdomo wake tayari kutema mate, Amata aliogopa na kurudi nyuma, alipojaribu kusogea tena ikawa vilevile. Amata akanyanyua mkono wake akaigonga pete yake mara nne “fungua” akatamka neno hilo. Mara aliona kufuli lile likifunguka kana kwamba kuna mtu aliyefungua na mlango ukajisogeza kwa ndani, Amata akajitoma ndani, chumba kilikuwa ni kitupu pembeni kabisa kulikuwa na jeneza lililochongwa michongo ya ajabu ajabu. Amata alisimama na kuliangalia jeneza lile lililojaa vumbi akalishika kufungua, alipoondoa mfuniko wake alipigwa na bumbuwazi, kulikuwa na ngazi zikishuka kuingia shimoni, Amata aliingia na kufuata ngazi zile kuteremka chini kabisa ya shimo lile, ndani ya shimo lile mlikuwa na giza nene, Amata alishuka taratibu akisaidiwe na ule mwenge alioushika mkononi mwake alipokaribia chini alianza kuona vitu viking’aa kutokana na ule mwanga wa mwenge alioushika. Amata alitabasamu alipoona vitu vile vilivyojawa vumbi na buibui kufanya makao yake, sahani, vikombe, vitu mbalimbali vya thamani vilivyotengenezwa kwa madini ya dhahabu, almasi, vito vya madini mbalimbali kama yaspi, quartz, marmar. Amata alibakia kaduwaa hajui wapi shike wap aache, alipouona mkufu alimkumbuka rafiki yake Chausiku ‘huu utamfaa’ alijiwazia. Alizunguka huku na huku na hakujua afanye nini. Alibaki kufikiria hatima ya maisha yake na mawazo yake yalisafiri dunia nyingine akimkumbuka Chausiku binti Saidi ambaye ni muda mrefu hakumuona.
HATIMA Amata akiwa juu ya jiwe kubwa alikuwa na furaha sana alipomuona mtoto wake akicheza na mama yake Chausiku binti Saidi, alitabasamu alipowaona wakikimbizana pale katika nyasi za kijani sana zilizojawa kila aina ya rutuba. Moyo wake uliridhika na ulijawa na furaha alipotazama nyumba yake nzuri kijijini pale, mashamba makubwa aliyokuwa akimiliki, sasa hakuwa mkulima wa jembe la mkono bali alikuwa akimiliki trekta kubwa, mifugo iliyokuwa hapo ilizidi kupendezesha eneo kubwa lililomilikiwa na kijana Amata. Amata alikuwa akiangalia picha alizotengeneza kutoka katika kamera ile ndogo aliyoichukua kwa Stephan, picha za kutisha, picha za Solondo. Aliteremka kutoka katika jiwe lile na kuungana na familia yake katika mchezo ule mzuri, walicheza na kufurahi pamoja Amata, Chausiku na mtoto wao. Hakika Chau alikuwa ana haki ya kuwa na furaha kwani alikataa wanaume wengi sana ili kumsubiri Amata atoke gerezani hakujua hata kidogo masaibu yote yaliyomkuta katika safari yake ya hatari. Alijawa na furaha tu alipomuona kijana huyu yupo pale kijijini lakini sasa akiwa mtu tofauti sana, alimkumbatia kwa furaha zote na baada ya muda mfupi wawili hawa walifunga ndoa na kuishi pamoja na kujenga familia yenye furaha. Na hapa msemo wa wazee ulitimia… ‘Ridhiki ya Mbwa iko miguuni mwake’
SI KILA CHOZI LIDONDOKALO, hudondoka kwa huruma au maumivu, mengine nyuma yake yamebeba siri nzito. Siku zote siraha ya mnafiki huwa machozi, unaweza kuona anakuonea huruma kumbe kikulacho kinguoni mwako, anakutafuna taratibu ukishtuka amekumaliza. Deusi aliamini wote waliomlilia siku ya hukumu yake hasa mkewe na rafiki yake kipenzi walikuwa na uchungu wa kweli, lakini kumbe ilikuwa siri nyuma ya machozi. Ukitaka kujua yote naomba twende pamoja katika hadithi hii tamu. TWENDE SASA….
Gari aina ya Toyota Land cruser GX lilionekana likitembea taratibu mbele ya lango kuu la gereza la Segerea. Askari magereza wa zamu alilifuatilia lile gari huku moyoni akiamini kazi anayofanya na mshahara anaopata kununua gari lile ingebaki ndoto ya mchana. Aliliona gari lile likisimama na kutulia kwa muda bila kufunguliwa mlango, kutokana na uzuri wake aliendelea kulitazama kwa matanio huku akijisemea moyoni’ Wenye fedha wanafaidi.” Baada ya dakika kumi mlango wa gari ulifunguliwa na kuteremka mwanamke mmoja aliyeonekana mjamzito, maisha yake mazuri, akiwa na kitoto kidogo cha kike cha miaka mitatu. Baada ya kutoka nje ya gari, yule mama alichuchumaa kuzungumza na kile kitoto. Baada ya muda yule mwanamke aliingia kwenye gari na kuondoka akimuacha mtoto amesimama peke yake. Alikuwa na boksi la biskuti ameshikilia sambamba na bahasha iliyofungwa kwa uzi mkononi. Kitendo kile kiliacha maswali mengi kwa askari , mbona kitoto kidogo kimeachwa pale. Wazo la haraka lilimjia huenda amekwenda sehemu mara moja atarudi kumchukua mwanaye. Lakini muda uliendelea kukatika bila kuonekana, na kitoto kile kiliendelea kusimama palepale kilipoachwa bila kujitikisa. Wakati huo wingu zito lilitanda na mvua ilianza kunyesha kitoto kile kikiwa pale pale huku kikiangua kilio cha kutaka msaada. Askari magereza alitoka kwenye lindo lake na kukifuata ili kukiondoa kwenye mvua. Alikibeba mpaka kwenye kibanda chake na kukiketisha kwenye benchi, ilibidi aingie kazi ya ziada kukimbembeleza kutokana na kumlilia mama yake. Jicho la askari lilitua kwenye bahasha aliyofungiwa mkononi yenye maandishi makubwa, MKUU WA GEREZA. Alishtuka na kujawa na mawazo mengi juu ya barua ile, alijiuliza kwa nini haikupelekwa moja kwa moja kwa mhusika au kulikuwa na ajenda gani kuachiwa mtoto mdogo barua ya mkuu wa gereza. Wasiwasi wake mkubwa alifikiria labda yule ni mtoto wa pembeni wa mkuu wa gereza hivyo aliletwa pale ili kumsusia. Hakutaka kumpeleka moja kwa moja kwa mkuu wa gereza, kuhofia kuleta mtafaruku ndani ya ndoa yake. Alimuita askari mwenzake aliyekuwa akipita. “John hebu njoo.” “Okote umeamua kuingia lindo na mwanao?” “Kaka wee acha, kuna gari moja la kifahari limesimama mbele ya lango kuu na kumuacha mtoto huyu.” “Halafu waliomuacha walikueleza nini?” “ Lilisimama kule, nilijua labda wamemwacha watamrudia, lakini mpaka mvua inateremka sikuona gari wala mtu. Ilibidi nikamchukue na kumuhifadhi hapa, kilichonichanganya na kutaka msaada wako ni barua aliyokuwa amefungwa mkononi , imeandikwa mkuu wa gereza.” “Eti?” “Imeandikwa mkuu wa gereza,” Okote alirudia kusema. “Sasa mkuu wa gereza na mtoto huyu wanahusiana nini?” “Kuna kitu kimenitisha.” “Kipi hicho?” “Huenda mkuu alimpa mimba mwanamke, leo ameamua kumletea mtoto hapa.” “Mmh! Inawezekana, kwani si yupo ofisini kwake?” “Sijui, nilikuwa naomba msaada niangalizie kama yupo tumpeleke mtoto na barua” “Gari lake sijaliona kupita atakuwa yupo.” “Basi naomba unipelekee na kumpa maelezo haya.” Alikubali kumpeleka, alimbeba na kuelekea naye kwenye ofisi ya mkuu wa gereza, mlango ulikuwa umefungwa, mlinzi wake alimuuliza. “Vipi John mbona na mtoto ofisini?” “Nina shida na mkuu.” “Shida gani?” “Sefu, shida ya mkuu nikueleze wewe?” “Ok, ingia.” John aliingia hadi mapokezi, sekretari naye alishtuka kumuona John amembeba mtoto. “John, vipi mtoto anaumwa mbona hivyo?” “Hapana nina shida na mkuu.” “Sasa hivi amesema hataki kuonana na mtu ana kazi nyingi.” “Najua lakini kuna mzigo wake.” “Huyo mtoto?” “Ndiyo na barua,” alimkabidhi barua ambayo aliisoma na kukutana na jina la Mkuu wa gereza. “Umemtoa wapi?” “Kuna mwanamke kamtelekeza hapo nje na kuondoka.” “Mmh, isiwe nyumba ndogo?” Suzy alisema kwa sauti ya chini. “Hata mimi ndiyo wasiwasi wangu.” “Hebu ngoja nimpigie simu nimsikie anasemaje, unajua John hii kashfa.” “Tena inabidi tusijichanganye tutakimbia kazi.” Suzy alimpigia bosi wake simu. “Halo Afande kuna ugeni wako mzito.” “Nani?” “Kuna mtoto katelekezwa nje ya gereza mkononi ana barua yako.” “Barua yangu! Inasemaje?’ ”Hatujaisoma afande ila kuna jina la mkuu wa gereza.” “Mmh! Hebu mlete ofisini haraka.” John alimbeba mtoto na kuingia naye ofisi kwa mkuu wake, baada ya kupiga saruti alimtua mtoto . Mkuu wa gereza alimuangalia yule mtoto lakini hakugundua kitu chochote katika uso wa mtoto. “Nipe hiyo barua,” John alimkabidhi na kusubiri maelekezo. Mkuu wa Gereza Mzee Sikamtu aliifungua ile barua na kuisoma kwa muda kisha alishusha pumzi na kusema: “John.” “Naam afande.” “Nenda gerezani kaniletee mfungwa Deusi Ndonga njoo naye mara moja,” alisema huku akiweka barua juu ya meza. Baada ya maelekezo John alipiga saruti na kugeuka kisha aliondoka kwa mwendo wa ukakamavu. ******** Ndani ya gereza Deusi Ndonga alikuwa amejiegemeza kwenye ukuta huku maumivu ya moyo wake yalikuwa makubwa zaidi ya yale ya kufungwa gerezani miaka saba. Lakini kitendo cha usaliti wa mkewe Mwaka mmoja toka aingie gerezani kwa kosa la kukamatwa na dawa za kulevya ambazo aliamini kabisa ule ulikuwa mtego alitegewa na bosi wake. Kila dakika aliiona kama njozi ya mchana isiyo na ukweli wa kumuona mkewe akiwa mjamzito, mimba ambayo haikuwa yake. Akiwa katikati ya mawazo jina lake liliitwa. Alinyanyuka na kusogea mlangoni. “Deus unaitwa na mkuu wa gereza.” Deusi alitoka chumba cha gereza na kufuatana askari aliyetumwa na mkuu wa gereza. Akiwa nyuma yake, alijawa na mawazo na kujiuliza mkuu wa gereza anamuitia nini. Na kwa nini amuite ofisini kwake. Alipofika nje ya ofisi John alimweleza Deusi asubiri na yeye kuingia ofisini kwa mkuu wa gereza. Baada ya muda alitoka na kumweleza aingie, alipoingia moyo wake ulishtuka kumuona mtoto pale ofisini. Lakini hakutaka kuhoji kitu kwa vile
aliitikia wito si kuuliza swali. “Deusi,” mkuu wa gereza alimuita baada ya kuketi kwenye kiti. “Naam mkuu.” ”Unamfahamu huyu?” alimuuliza huku akinyoosha mkono kwa mtoto mdogo aliyekuwa ameketi kwenye kochi. “Ndiyo mkuu.” “Unamfahamu vipi?” “Ni mwanangu,” Deusi alijibu kwa utulivu. “Shika barua hii usome,” aliipokea na kuanza kusoma taratibu. Alitembeza macho taratibu kusoma herufi moja baada ya nyingine, kila alichosoma kilikuwa sawa na kuupasua moyo wake kwa kisu butu bila ganzi. Mkuu wa gereza alimfuatilia Deusi alipokuwa akisoma barua huku akishuhudia michirizi ya machozi ikiteremka kwenye mashavu yake. Mishipa ya kichwa ilimsimama na macho kuzidi kuwa mekundu ikifuatiwa na kamasi nyepesi, baada ya kuimaliza kuisoma barua alimwangalia mwanaye aliyekuwa amekaa kwenye kochi akishangaa picha ya mkuu wa nchi iliyokuwa ofisini huku akiendelea kutafuna biskuti zake. Baada ya kumwangalia mwanaye aliyemuonea huruma huku moyo wake ukiongezeka maumivu mara dufu. Katika maisha yake kitendo cha yeye kufungwa gerezani hakikumuumiza moyo wake kwa kuamini ile ni mitihani ya maisha, mwanadamu anatakiwa kupambana nayo. Lakini pigo zito la kwanza lilikuwa kumuona mkewe akiwa na ujauzito usio wake, akiwa bado katika maumivu ya mkewe kukosa uaminifu mwaka mmoja baada ya kifungo chake. Pigo zito zaidi ya bomu la kilo 1000 lililousambalatisha moyo wake lilikuwa kwenye ile barua. Barua ilikuwa imeandikwa hivi: Dear zilipendwa, mume wangu wa zamani, najua kidonda cha kuona mwanaume mwenzako kunijaza tumbo bado hakijapona, lakini sina jinsi, siku zote punda unaweza kumlazimisha kumpeleka mtoni, lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji. Hii ilikuwa sawa na tamaa ya wazazi wangu kunilazimisha niolewe na wewe, mwanaume asiye chaguo langu. Walijua kabisa chaguo la moyo wangu ni Kinape. Kuolewa nawe ilikuwa sawa na punda kumlazimisha kuingia mtoni lakini ilikuwa vigumu kuendelea kuwa na wewe kwa vile si chaguo langu. Baada ya kufungwa kwako ilikuwa ni nafasi yetu ya kujinafasi kufanya mapenzi kwa uhuru mkubwa. Kwa muda mrefu tulikuwa tukifanya kwa wizi, najua itakuuma sana na kuupasua moyo wako kwa kisu butu bila ganzi. Lakini ukweli unabaki palepale nilikuwa sikupendi na sitakupenda milele. Kama Kinape angekuja mapema hata huu uchafu wako usingeingia tumboni mwangu, nilipanga kukinyongea mbali. Lakini moyo wa huruma ulinijia wa kuidhuru damu yangu ilinishika. Nimeamua kukuletea mtoto wako ili ukae naye gerezani. Siwezi kumtunza mtoto wa mwanaume nisiye mpenda, siwezi kuchanganya mtoto wa njiwa na bundi. Mimi kuolewa na Kinape sawa na mshare umerudi porini haukupotea, sasa hivi mimi ni mke mtarajiwawa Kinape. Nakutakia maisha marefu yenye furaha na mwanao gerezani. Ni mimi dear zilipendwa Kilole. Mkuu wa gereza alimshuhudia Deusi akiwa naye kimwili lakini kiakili alikuwa mbali sana, alimuita. “Deusi…Deusi.” “Haiwezekani… haiwezekani, kwa nini lakini, kwa nini mke wangu unanitendea unyama kama huu. Nimekukosea nini? Kwa nini unamtesa mtoto asiye na hatia, kwa nini unanisaliti na rafiki yangu. Eee Mungu kosa langu nini, haya huyu mtoto mdogo nitamweka wapi, anajua nimefungwa anakuja kuniterekezea mtoto. ” Deusi alishindwa kujizuia aliangua kilio cha sauti ya chini. “Deusi pole,” Afande John alimtuliza. “John,” Mkuu wa gereza alimuita. “Naam afande.” “Nipe nafasi nizungumze machache na Deusi.” Baada ya John kutoka, alitulia kwa muda akimwangalia Deusi aliyekuwa akitoa kamasi kwa mkono na kufuta kwenye shati lake. Alinyanyuka na kwenda kwenye friji ndogo ya ofisini na kutoa chupa kubwa ya maji yaliyokuwa nusu na kummiminia kwenye glasi kisha alimpa Deusi. “Pole sana Deusi, naomba unywe maji haya kwanza.” Deusi aliipokea glasi na kuyanywa maji yote kwa mkupuo kisha aliiweka glasi juu ya meza. “Deusi.” “Naam mkuu.” “Kwanza pole sana.” “Sijapoa mkuu.” “Kuna siri gani kati yako na mkeo?”
“Kwa kweli sijui hata kitu kimoja, ni mwezi wa pili sasa, mke wangu ameujeruhi moyo wangu kwa kukosa uaminifu wa kubeba ujauzito usio kuwa wangu.” “Mkeo ulimuoa kwa mapenzi yake au kwa kulazimishwa?” “Kwa kweli mke wangu nilichaguliwa na wazazi wangu nilipokwenda kijijini kuwatembelea. Mwanzo wa ndoa yetu alionesha mapenzi ya dhati kumbe nilikuwa nafuga nyoka, amekua sasa amenimeza. ” “Na Kinape ni nani?” “Kinape alikuwa zaidi ya rafiki, tumesoma na kucheza pamoja kabla ya mimi kuendelea na masomo mpaka kupata kazi katika kitengo cha kuzuia dawa za kulevya.” “Na alifikaje kwako?” “Ni historia ndefu” ****** Miaka minane iliyopita Deusi King’ole baada ya kuanza kazi kama mkuu wa kitengo cha kuzuia madawa ya kulevya. Miaka mitatu katika kazi yake alipata likizo iliyomfanya aende kijijini kwa wazazi wake. Katika watu wa karibu baada ya wazazi wake, walikuwa wazazi wa Kinape ambaye toka wakiwa shule ya msingi waliitwa pacha kutokana na ukaribu wao. Deus baada ya kufika kijijini na kupokewa na ndugu na jamaa ambao walimshangaa kumuona amerudi katika gari la kifahari, wengi walizoea kuliona gari kama lile kwa mbunge wao tu, alipokwenda kujijini kuwatembelea wapiga kura wake. Ilikuwa ni furaha hasa kwa wazazi wake ambao waliamini kazi ya kumsomesha mtoto wao ilikuwa imezaa matunda. Kitu kikubwa alichowaahidi wazazi wake kuhakikisha anayabadili maisha ya familia yake ikiwa pamoja na kuwajengea nyumba ya kisasa na kuwachimbia kisima cha maji. Baada ya kutulia alitaka kujua habari za rafiki yake Kinape. “Jamani Kinape yupo?” “Mmh! Nina siku sijamtia machoni,” mama Deusi alijibu. “Nasikia sijui alikwenda mjini kutafuta kazi,” mdogo wake alisema. “Sasa wewe mjini huko hukumuona?” Mzee King’ole aliuliza. “Baba mji ni mkubwa, mnaweza kukaa miaka kumi bila kuonana na mtu pengine mnakaa kitongoji kimoja.” “Labda siku hizi, siku za nyuma watu tulikuwa tunajuana hata wageni walipoingia tuliwatambua.” “Ni wakati huo baba, sasa hivi mji umepanuka.” “Basi atakuwa hukohuko mjini.” “Na yeye atarudi na gari?” Mdogo wake aliuliza. “Siwezi kujua,” Deus alijibu kwa mkato. “Lakini mzee Solomoni na mkewe si wapo?” Deus aliuliza. “Wapo, waende wapi,” mzee King’ole alijibu. “Basi ngoja nikawaone kabla ya kujipumzisha.” “Haya baba,” mama Deus alijibu. Deus alinyanyuka ili aelekee kwa mzee Solomoni. “Kaka twende wote,” mdogo wake wa kike aliyekuwa anasoma kidato cha kwanza aliomba kuongozana na kaka yake. “Hakuna tatizo,” alijibu huku akimshika mkono. Walikwenda hadi kwa mzee Solomoni, alimkuta mama Kinape akisuka ukiri. “Hodi hapa.” “Karibu,” alijibu huku akiacha kusuka na kumtazama mgeni aliyekuwa amesimama mbele yake. “Shikamoo mama.” “Marahaba, karibu.” “Asante.” “Ndiyo baba,” ilionesha mama Kinape kamsahau Deus. “Mama unamjua huyu?” Salome mdogo wa Deus alimuuliza mama Kinape. “Hata,” alijibu huku akijitahidi kumkazia macho. “Si kaka Deusi huyu.” “Deusi wa mjini?” “Ndiyo.” “Jamani, mwanangu mwenyewe nimemsahau, karibu baba tusameheane, macho ya uzee haya.” “Kawaida, mama za hapa?” “Hebu ngoja kwanza, Salome kamletee kiti kaka yako.” Salome alikwenda ndani na kurudi na kiti cha kukunja, alikiweka pembeni ya mama Kinape. “Wee, Salome kiweke mbele nimuone vizuri,” Salome alifanya kama alivyo agizwa. Baada ya kukaa alianza kuzungumza: “Ndiyo, mama za siku?” “Mmh! Hivyo hivyo tu baba, kila kukicha afadhari ya jana.” “Ni kweli sasa hivi nasikia hata mvua zimegoma.” “Kama unavyoona.” “Baba yupo wapi?” “Ametoka kidogo, ila achelewi, unavyomtaja pengine yupo njiani anarudi.” “Na ndugu yangu?” “Kinape?” “Eeeh.” “Mmh! Kakimbilia mjini.” “Kufanya nini?” “Mwanangu kwani wewe mjini unafanya nini?” “Mimi nafanya kazi serikalini kutokana na elimu yangu.” “Kwa kweli hatujui mjini anafanya kazi gani.” “Anakaa wapi ili nikifika nimtafute?” “Hatujajua ila yeye kasema atalala popote hata sokoni.” “Mmh! Haya.” “Vipi umeoa?” “Bado.” “Unasubiri nini?” “Nilikuwa najipanga.” “Deus wazazi wenu lini tutacheza na wajukuu?” “Nina imani sasa hivi nitafuta machozi yenu.” “Fanya hivyo, usiwe kama mwenzako kila siku kesi za watoto wa watu.” “Sasa mama, wacha nikapumzike ndiyo nimefika nahitaji kupumzika.” “Hakuna tatizo, tuachie basi hata fedha ya unga.” Deus aliingiza mkono mfukoni na kutoa noti moja ya shilingi elfu kumi na kumkabidhi. Kabla hajaipokea alitokea mzee Solomoni na kusema: “Mheshimiwa nami usinisahau.” “Aah, baba.” Deus alisema huku akimgeukia mzee Solomoni, Mzee Solomoni alishtuka kumuona Deus. “Ha! Ni wewe Deus?” “Ni mimi baba.” “Umefika lini?” “Leo.” “Na lile gari la mbunge lililopaki kwenu?” “Si gari la mbunge ni gari langu mwenyewe.” “Ha! Ina maama na wewe siku hizi mbunge?” “Hapana kuwa na gari kama lile halimaanishi mbunge, mtu yoyote anaweza kumiliki.” “Kwa hiyo ni la kwako?” “Ndiyo baba.” “Hata hali yako inajionesha.” “Kidogo kidogo.” “Una habari gani?” Mzee Solomoni alisema huku akimtazama kwa makini Deus. “Nilikuja kuwajulia hali mara moja, ila nimesikitika kumkosa rafiki yangu kipenzi Kinape.” “Yule rafiki yako mpumbavu, tena hana akili, amekimbia kilimo, ona jinsi tulivyochoka wazazi wake yeye anakimbilia mjini. Kibaya anapokwenda hana ndugu wala sehemu ya kufikia,” mzee Solomoni alisema kwa hasira. “Lakini baba si kulalamika, ni kumuombea ili milango ya riziki ifunguke na kupata shughuli yoyote ya kumpatia kipato.” “Kweli kabisa usemayo, kila siku baba yenu analalamika hajui kama ni laana kwa mtoto,” mama Kinape aliunga mkono. “Wazazi wangu nakuahidini kitu kimoja, kwa vile mmesema yupo mjini nitamtafuta kila kona ili kuhakikisha nampata.” “Litakuwa jambo la zuri.” Deus aliagana na wazazi wa Kinape ili arudi nyumbani, mzee Solomoni alikumbusha. “Mwanangu na mimi mbona umenisahau?” Deus aliingiza mkono mfukoni na kutoa noti nyingine ya elfu kumi na kumkabidhi. “Asante sana mwanangu Mungu akizidishie.” “Asante wazazi wangu, atuzidishie wote.” Deusi aliwaaga na kurudi nyumbani, njiani wakati wa kurudi walikutana na binti mmoja aliyekuwa amebeba chupa ya mafuta ya kula. “Shikamoo,” yule binti alimsabahi Deus. “Marahaba.” “Salome, mambo?” “Poa, umemuona kaka yangu anayeishi mjini?” “Kumbe ndiye huyu, shikamoo.” “Jamani Kilole, mbona unataka kumchosha kaka yangu, shikamoo mara ngapi?” “Jamani ya kwanza ya kutomjua, ya pili ya kumfahamu, kuna ubaya?” “Hakuna ubaya, marahaba,” Deus aliitikia huku akitabasamu. “Karibu kwetu kaka.” “Asante.” “Haya nawahi nyumbani, Salome baadaye.” “Haya.” Waliagana na Kilole kila mmoja aliendelea na safari yake, wakiwa wanarudi nyumbani Deus alijikuta akivutiwa na mchangamfu wa Kilole. “Salome, Kilome mtoto wa nani?” “Wa mzee Sikwera.” “Mmh! Mbona huyu msichana simfahamu?” “Kwani ulikuwa unapenda kutembea kijijini, mbona alikuwepo.” “Kumbe, rafiki yako?” “Kiasi, vipi umemependa?” “Basi tu kanivutia kwa uchangafu wake.” “Hata mimi nampenda.” “Ameolewa?” “Mtu yupo kwao, atakuwa ameolewa vipi?” “Kwa hiyo hajaolewa?” “Hajaolewa.” “Kama hajaolewa atakuwa na rafiki wa kiume?” “Kaka swali hilo gumu.” Salome alificha siri ya Kilole kutokana na siku za nyuma kuwa na urafiki wa kimapenzi na Kinape rafiki kipenzi cha kaka yake. Kwa vile Kinape alikuwa na miezi sita toka aende mjini. Hakukuwa na haja ya kumzibia riziki kama kweli kaka yake anampenda.
“Basi tuachane na hayo,” Deus alibadili mada. “Vipi umempenda, kama umempenda nitafurahi siku moja akiwa wifi yangu.” “Ni haraka sana, kila kitu kizuri kinataka subira.” Kutokana na mazungumzo kupamba moto walijikuta wakifika kwao bila kujua, Deus hakutaka tena mazungumzo aliingia chumbani kwake na kujilaza. Kabla ya kulala mawazo yote yalikuwa kwa Kilole. Aliamini kabisa kama hana mtu basi nafasi ile aitumie vyema mpaka anarudi mjini awe amepata jibu la uhakika. wake kuhamishwa na wazazi wake kwa ajili ya tofauti ya dini. Deus alikuwa na Alikumbuka moyoni mwake kuna chumba hakina mpangaji baada ya mpangaji mpenzi wake anayefanya kazi katika shirika la vifaa vya Electonic kama Series Officer. Uhusiano wao ulianza taratibu, mpaka ulipofikia hatua ya kutambulishwa Deus kwa wazazi wa mpenzi wake Halima. Tatizo lilikuwa dini Halima muislamu na Deus mkiristo, wazazi wa Halima hawakuwa na pingamizi kama Deus atabadili dini kumfuata Halima. Deus hakuwa tayari wazazi wake walisema kama ni hivyo hakuna ndoa. Deus alibembeleza wafunge ndoa ya serikali, pia hiyo waliikataa. Hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali kubwaga manyanga kutokana na kushindwa masharti. Miezi sita ilikatika huku ukaribu wake na Halima ukipungua na mwisho kabisa ulivunjika. Wazo la kutafuta mpenzi mwingine aliliweka kando na kujikita katika kuyatengeneza maisha yake na ya wazazi wake kijijini. Baada ya kukaa kwa muda alijikuta turufu yake ya upendo anaitupa kwa Kilole, baada ya kuwaza sana usingizi ulimpitia. ********** Alishtuka jioni, baada ya kuoga na kupata chakula alikaa na mama yake, katika mazungumzo alimgusia mama yake msichana aliyekutana naye wakati akitoka kwa mzee Solomoni. “Mama wakati narudi toka kwa mzee Solomoni, nimekutana na msichana mtoto wa m.. mmm..ze..ee.ee, eti Salome yule msichana tuliyekutana naye ni mtoto wa mzee nani?” Alimuuliza mdogo wake aliyekuwa amekaa mbali kidogo. “Mmh! Kaka bado unaye, kweli kakugusa.” “Salome hebu tuambie mtoto wa nani?” Mama yao alikuja juu. “Mama si Kilole?” “Kilole huyu mtoto wa mzee Sikwera?” “Ndiye huyo huyo.” “Eeh, amefanya nini?” Mama Deus alishusha sauti na kuzungumza kwa sauti ya chini na mwanaye. “Unamuonaje?” “Kivipi?” “Hata sijui, nimempenda alivyo pia ni mchangafu akiwa ndani nyumba haizubai.” “Kwa hiyo unataka awe mkeo?” “Mama mbona kila kitu kinajieleza.” “Kwa kweli ni mmoja wa wasichana wenye heshima hapa kijijini, mengine siwezi kujua lakini ametulia.” “Mmh! Sawa.” “Vipi? Tufanye mpango?” “Kwa sasa ni maandalizi kama atakuwa tayari, basi tujipange kwa harusi baada ya miezi mitatu tufunge ndoa, vipi kuhusu elimu?” “Mi sijui labda umuulize Salome.” “Eti Salome, shoga amesoma mpaka darasa la ngapi?” “Kidato cha nne.” “Kinatosha ataendelezwa kwa vile elimu haina mwisho.” “Basi kazi hii nitaifanya na baba yako leo usiku tutakwenda kwa wazazi wa Kilole.” ******** Usiku ulipoingia wazazi wa Deus walikwenda kwa wazazi wa Kilole kupeleka ujumbe wa Deus. Walipokelewa vizuri, bila kupoteza muda waliwaeleza kilichowapeleka. “Utani huo mzee mwenzangu, Deus aache wanawake wote mjini aje atafute kijijini?” Baba Kilole alisema baada ya kusikia ombi la mzee mwenzake. “Najua utasema hivyo, kila kitu ni uamuzi wa mtu.” “Wala hatujamshinikiza, sijui kamuona leo,” mama Deus aliongezea. “Jamani kampenda au kamtamani?” “Mzee mwenzangu mpaka kuja hapa tumelijadili jambo hili kwa kina.” “Mmh! Haya, umesikia mke wangu?” Baba Kilole alimuuliza mkewe. “Mimi nafikiri hili ni jambo jema, sifikiri tunatakiwa kuhoji sana,” mama Kilole alijibu. “Mke wangu kuuliza si vibaya japo sisi wenyewe tunajua.” “Ni kweli, lakini mpaka kufunga safari basi hawakuja kufanya utani.” “Wazee wenzetu tumekusikieni tupeni muda tuzungumze naye, majibu mtayapata kesho.” “Hakuna tatizo, jambo lolote zuri linahitaji subira.” “Na kama akikubali harusi mnatazamia iwe lini?” “Amesema baada ya jibu zuri kuna miezi mitatu ya maandalizi.” “Kama ni hivyo itatusaidia nasi kujipanga.” Waliagana na kurudi nyumbani, Deus alikuwa na shauku ya kujua wazazi wake wamerudi na jibu gani. Lakini baba yake alimtuliza kwa kumweleza ujumbe umefika jibu watalipata kesho yake. ******* Baada ya kuondoka wazazi wa Deus, mama Kilole alimwita mwanaye aliyekuwa ndio kwanza ametoka kuoga. “Kilole mwanangu.” “Abee mama.” “Unajijua wewe sasa hivi umeisha vunja ungo?” “Najua mama.” “Unajua huu ni mwaka wa ngapi?” “Mmh! Wa tano sasa.” “Kwa hiyo nina imani upo tayari kwa ndoa.” “Mmh! Nitaweza?” “Kilole kila siku ulikuwa unatoroka usiku kwenda kulala kwa Kinape, bado unajiona mtoto?” “Nani anataka kunioa? Kinape! Vipi amerudi?” Kilole aliuliza kwa mshtuko. “Siyo Kinape.” “Nani?” “Mtoto wa mzee King’ole.” “Yupi?” “Deus” “Yule anayekaa mjini?” “Huyo huyo, nasikia mlionana leo.” “Mmh!” Kilole aliguna. “Mbona unaguna?” ”Lakini mama si unajua kila kitu.” “Kuhusu Kinape?” “Ndiyo.” “Wee mtoto hebu acha ujinga, Kinape atakusaidia nini?” “Mama, siwezi kuvunja ahadi yangu na Kinape, ameniahidi anakwenda mjini kutafuta maisha na akirudi anakuja kunichukua.” “Mwanangu haya si ya kuyasema kwa baba yako, ile ilikuwa siri yetu. Baba yako akijua atatuua.” “Mama mimi siwezi kuolewa na mume nisiyempenda.” “Haya maneno yaishie hapa, chonde mwanangu usiangushe, nakuomba ukubali.” “Mama kama nitaolewa nitakuwa sikuolewa kwa hiyari yangu.” “Najua mwanangu, ila nakuomba unifichie aibu hii.” “Mama Kinape nitamueleza nini? Kumbuka nilimuahidi, kuendelea kumsubiri mpaka atakapo rudi na ahadi ni deni.” “Mwanangu, sivyo vyote vinavyo ahidiwa hutimia, kumbuka Deus ni mtu mwenye uwezo mkubwa kimaisha, huoni itatusaidia hata sisi wazazi wako? Hebu ona Mariamu mumewe ana uwezo mdogo, lakini wazazi wake wanaishi maisha mazuri. Deusi amejenga nasikia mshahara wake mkubwa ana gari zaidi ya matatu tofauti na hili alilokuja nalo kama la mbunge, tena ni mtu tunayemfahamu.” “Mama nakubali kwa shingo upande, bado nampenda Kinape,” Kilole alisema huku akibubujikwa na machozi. “Najua mwanangu, lakini inaonesha Deus naye mtu mzuri, si unaona familia yetu, hebu tutoe kwenye dimbwi la umaskini nafasi hii asije pata mwingine tukaijutia.” mama yake alisema huku akiwa amemkumbatia na kumpigapiga mgongoni taratibu. “Sawa mama, sina jinsi lazima nikubali.” “Asante mwanangu.” Mama Kilole aliagana na mwanaye aliyeingia chumbani kwake kulala, alishukuru Mungu mwanaye kukubali kuolewa na Deus. Alipoingia ndani alikutana na mumewe akimsubiri. “Vipi imekuwaje?” “Hakuna tatizo.” “Amekubali?” “Ndiyo.” “Lakini kuna kitu nina wasiwasi nacho,” kauli ile ilimshtua mama Kilole. “Kitu gani?” “Kuhusu uhusiano wa Kilole na Kinape.” “Uhusiano upi?” Mama Kilole alijifanya hajui kitu. ”Wewe ndiye ulitakiwa kunifafanulia na sio kuniuliza.” “Mume wangu, ungeweka wazi ili nielewe unalenga nini.” “Ukaribu waliokuwa nao.” “Ni wa kawaida, Kinape si alikuwa kama mtoto wa familia.” “Mbona nilisikia wana uhusiano wa kimapenzi, sio tumuoze aje atutie aibu.” “Kwa kweli hilo mwenzangu nilikuwa silijui, mbona hukunieleza mapema ili nilifanyie kazi.” “Nikueleze nini wakati siku zote siri za watoto wa kike wanajua mama zao.” “Mume wangu kumbukeni mmekuwa mkitutia lawama wazazi wa kike, kuna mzazi anayetaka mtoto wake wa kike aharibike?” “Mbona mama yako ndiye aliyekuwa akinipa wepesi wa kuzungumza na wewe?” “Kwa vile alijua una nia nzuri, lakini kama ungetaka kunichezea na kuniacha asingekubali.” “Tuachane na hayo, kwa hiyo amekubali?” “Amekubali.” “Na una uhakika bado msichana?” “Mume wangu hilo swali siwezi kulijibu labda umuulize mwenyewe.” “Si swali la baba kumuuliza mtoto wa kike bali mama yake.” “Basi nitamuuliza, kama hana itakuwaje?” “Tujiandae na aibu au kupimwa kukutwa na wadudu.” “Mungu apishe mbali.” “Basi tulale ili kesho tuwape jibu lao.” Lakini upande wa pili wa Kilole alikosa usingizi kuwaza usaliti wake kwa Kinape mwanaume aliyemuingiza katika katika dunia ya wapendanao. Katika maisha yake aliamini Kinape ndiye mwanaume pekee katika moyo, alijiuliza atamwambia nini akimkuta ameolewa. Akiwa amejilaza chali kalalia mikono kwa nyuma, alijikuta kwenye mtihani mzito wa kuingia katika maisha ya ndoa ya mwanaume asiyekuwepo moyoni mwake. Lakini alikumbuka shoga yake Mariamu mtoto za mzee Sadiki jinsi alivyo ibadili familia yake kimaisha baada ya kuolewa na mwanaume mwenye uwezo aliyekuwa akiishi mjini. Aliufananisha uwezo wa mume wa Mariamu haukuwa mkubwa kama wa Deusi mtoto wa mzee King’ole. Deus alikuwa akimzidi mara mia mume wa Mariamu. Mume wa mariamu pamoja na kuwa amejenga nyumba hakuwa na gari, Deus alikuwa na jumba la kifahari na magari ya kutembelea zaidi ya matatu. Japo moyoni bado alikuwa amemjaza Kinape alijikuta akijisemea moyoni: “Liwalo na liwe.” Alivuta shuka na kujilaza, lakini bado usingizi ulimkimbia na kujikuta akikumbuka ahadi aliyopeana na Kinape. “Kinape nakupenda sana, nakuomba usiniache kumbuka wewe ndiye unayeijua thamani ya usichana wangu, wewe ndiye uliyenionjesha tamu ya dunia. Nakupenda kulicho kitu chochote chini ya jua.” Kilole alikumbuka siku aliyomlilia Kinape baada ya kuzijua raha za dunia. “Kilole naheshimu zawadi uliyonipa, nakuhakikishia wewe pekee ndiye utakaye kuwa mke wangu. Nakuomba usinisaliti.” “Sitakusaliti, nakupenda sana Kinape.” Kilole alipoyakumbuka yale alijikuta akitokwa na machozi kwa kuamini kilichopo mbele yake ni maamuzi mazito kama kumeza mfupa. ******** Siku ya pili familia ya mzee Sikwera ilirudisha majibu kukubali Kilole kuolewa na Deus, taarifa ilipoifikia familia ya mzee King’ole walimfikishia Deus ambaye moyo wake ulijaa furaha baada ya ombi lake la kumuoa Kilole kufanikiwa. Alipata muda wa kuonana na mchumba wake kabla ya kuelekea mjini. Iliandaliwa siku maalumu ambayo ilikuwa kufahamiana na kukubaliana kuunganisha ukoo mbili. Sherehe ndogo ilifanyika nyumbani kwa mzee Sikwera baba yake Kilole. Deus na Kilole waliwekwa sehemu maalumu kwa ajili ya kufahamia kwa karibu. Wakiwa kimya kila mtu akitafakari lake Deus alikuwa wa kwanza kuvunja ukimya. “Kilole,” Deus alianza kwa kumuita jina lake. “Abee,” alijibu huku ameangalia chini. “Naomba unitazame basi.” “Sema tu ninakusikia,” Kilole alijibu huku akiwa ametawaliwa na aibu. Deus alitumia nafasi ile kumchunguza Kilole kwa karibu na kugundua vitu vingi sana, haiba na umbile lililojengeka kike hasa. Moyoni aliona muda aliopanga wa miezi mitatu ni mrefu sana. Mvuto wa Kilole ulikuwa mkubwa baada ya kumsogelea kwa karibu. “Asante sana.” “Asante ya nini?” “Ya kukubali ombi langu.” “Mmh,” Kilole aliguna tu. “Kilole nakuahidi kukupenda kwa moyo wangu wote.” “Asante, nami pia nitakuwa mke mwema.” “Pia nakuahidi kukuendeleza kimasomo.” “Nitashukuru kwa vile kiu yangu ya kutafuta elimu haijaisha.” “Nitakuacha kwa muda kwa vile nawahi kazini, ila kila kitu nimewaachia wazazi. Baada ya miezi mitatu tutakuwa mke na mume.” “Hakuna tatizo nitakusubiri.” “Nashukuru kusikia hivyo.” Baada ya mazungumzo na sherehe iliyochukua saa sita familia mbili ziliagana, Deus aliamini kila kitu duniani hupangwa na Mungu, hakuamini kama kijijini kutakuwa na wanawake wazuri kushinda mjini. Aliapa kumlinda Kilole kwa nguvu zake zote. Upande wa pili Kilole bado mzimu wa Kinape ulimsumbua, ulijikuta akilaumu muda mrefu uliopangwa wa harusi. Wasiwasi wake mkubwa ulikuwa kwa Kinape kutokea kijijini kabla ya ndoa ya kuharibu kila kitu. Moyoni aliomba kila alichokijua ili Kinape asionekane kabla ya ndoa yake ili akikutana naye apate cha kudanganya. BAADA YA MIEZI MITATU
Muda ulipotimu Deus alirudi mjini huku akiacha maandalizi ya harusi yake yakianza taratibu ikiwemo kuwekwa ndani kwa ajili ya mafunzo kabla ya ndoa. Deus baada ya kufika mjini aliendelea na shuhuli zake huku watu wake wa karibu akiwapa majukumu ya kufanikisha harusi yake. Muda ulipotimu Deus alimuoa rasmi Kilole na kuwa mke wake wa kufa na kuzikana. Ndoa yao ilijaa kila aina ya furaha huku Kilole ajilaumu kwa uamuzi wake wa kutaka kuikataa ndoa yake na Deus kwa ajili ya Kinape. Maisha aliyoishi kwa Deus hakuyawaza kuishi siku moja. Kwake aliamini maisha yale ni ya ndotoni kumbe yapo kweli.
KINAPE MJINI
Kinape naye baada ya kuingia mjini akiwa na shauku ya kupata maisha mazuri, lakini haikuwa kama alivyodhani. Maisha yalikuwa magumu sana kiasi cha kujiuliza maisha mazuri watu wanayapata vipi. Alijikuta akifanya kazi ngumu mshahara mdogo uliomtosha kula siku moja tu na siku ya pili alipoamka alianza upya. Alijikuta akiingia katika makundi ya wahuni ili aweze kuihimili kasi ya ugumu wa maisha kwa kulala nje ya soko kuu. Kila siku asubuhi walipo amka na kugombea kushusha mazao yaliyoingia sokoni, wazo la kuendelea kuishi mjini aliliona alifai kutokana na mateso ya kukamatwa na askari kila kukicha. Siku aliyopanga kesho yake arudi kijijini ndiyo usiku uliyokuwa mbaya kwake baada ya msako wa wazurulaji kukamatwa na kufunguliwa mashitaka. Kinape alikosa dhamana na kujikuta akihukumiwa miezi mitatu jela. Maisha aliyoishi gerezani yalimfanya kuuchukia mji. Siku alipotoka hakuwa na hamu ya kukaa mjini alirudi moja kwa moja kijijini kwao, hakutaka kuingia mchana kuhofia kuonekana na watu jinsi alivyo konda na mwili kuwa na upele na ukurutu. Aliingia kwao usiku hakuna aliyemuona. Alipofika wazazi wake walishtuka kumuona mtoto wao amedhoofu mwili. Walitaka kujua nini kimemsibu aliwaeleza: “Wazazi wangu nimekoma, kweli kiburi si maungwana jiji limeninyoosha.” Aliwaeleza yote yaliyomsibu mpaka kuingia gerezani. Wazazi wake hawakuwa na neno zaidi ya kumpokea. “Pole mwenetu hayo ndiyo maisha, tumshukuru Mungu umerudi salama, basi tusaidiane kwenye kilimo.” Kinape baada ya kurudi nyumbani kwao hakutaka kuonekana na mtu, aliishi maisha ya kujificha mpaka atakapopona upele na ukurutu. Hakuwa na hamu tena ya kusikia neno mjini, aliapa kwenda mjini kwa kazi maalumu na si kwenda kubahatisha. Kutokana na hali yake ya kukonda na ukurutu hakutaka kuonana hata na mpenzi Kilole. Alipanga hali yake itakapo imalika afya yake ndipo angeweza kujitokeza hadharani, pamoja na kuwa ndani taarifa za kuolewa kwa Kilole zilimshtua sana. Ili kupata ukweli alimuuliza mdogo wake wa kike. “Eti Eliza Kilole ameolewa kweli?” “Ndiyo kaka.” “Nasikia na rafiki yangu Deus.” “Ndiyo kaka.” “Siamini mpaka niende kwa mama Kilole anieleze ukweli, itakuwaje amuoze Kilolo akiujua ni mchumba wangu.” Kinape alijikuta akitoka ndani japo hali yake ilikuwa haijatengemaa vizuri na kwenda moja kwa moja nyumbani kwao Kilelo kupata ukweli wa kuolewa mpenzi wake ambaye ndiye aliyepanga kuwa mkewe. Njiani alijawa na mawazo juu ya usaliti wa Kilole aliyemuhakikisha kumsubiri mpaka atakaporudi. Alipofika nyumbani kwao Kilole alimkuta mama Kilole akianika mpunga, alipomuona alishtuka kwa mambo mawili. Kwanza kumuona Kinape aliyepotea miezi zaidi ya saba iliyopita, pili hali yake iliyodhoofika. Badala ya kumkaribisha alimshangaa. “Shikamoo mama,” Kinape alianza kumsalimia baada ya kugundua mama Kilole alikuwa akimshangaa. “Kinape!” Badala ya kuitikia alizidi kumshangaa. “Naam mama.” “Ni wewe?” “Ndiyo mama.” “Ulikuwa unaumwa?” “Hapana.” “Nini kimekusibu mwanangu?” “Ni habari ndefu mama.” “Hebu karibu ndani,” aliacha kazi zake na kumkaribisha ndani. Baada ya kuingia ndani alimkaribisha kwenye kigoda. “Karibu.” “Asante mama.” “Haya niambie nini kimekufanya uwe hivi wakati unasema ulikuwa huumwi?” Kinape alimueleza yote yaliyomkuta na kumfanya aishie gerezani badala ya kupata kazi. “Ooh, pole sana mwanangu.” “Asante mama.” “Inaonekana ulipoondoka hukuaga, baba yako kila siku alikuwa akilalamika, safari kubwa kama hizo unatakiwa kupata baraka za wazazi.” “Mama tuachane na hayo, kuna kitu kimoja muhimu ndicho kilichonileta hapa.” “Kipi hicho?” “Kuhusu Kilole.” “Kilole kafanya nini?” “Nasikia ameolewa?” “Ndiyo.” “Nani aliyetoa idhini ya kuolewa?” “Kwa nini unaliza swali kama hilo?” “Mama si unafahamu Kilole ni mchumba wangu?” “Najua.” “Sasa kwa nini mmemuoza kwa Deus?” “Uchumba wako na Kilole tulikuwa tunajua sisi lakini baba yake alikuwa hajui lolote, na penzi lenu lilikuwa la wizi halikuwa wazi.” “Hata hivyo lakini si mnajua mimi na mwanao tulikuwa na marengo gani katika maisha yetu?” “Nimekueleza idhini ya kuolewa kaitoa baba yake siyo mimi.” “Kwa nini hukumwambia amechumbiwa?” “Ningeanzia wapi wakati hatukujua upo wapi, ulikuja kutuaga kuwa unasafiri?” “Sikufanya hivyo, kutokana na dharula iliyojitokeza kwa hilo naomba mnisamehe.” “Sasa kama hivyo hatujui ulikuwa wapi tungeweza vipi kukusubiri mtu tusiyejua upo wapi na utarudi lini. Kuolewa ni bahati tusingeipoteza bahati ile ambayo msichana yoyote kijijini asingekubali kuipoteza” “Sawa, lakini kumbukeni wewe na mwanao mmenifanyia ukatiri mkubwa.” “Utatulaumu bure makosa umeyafanya mwenyewe.” Kinape aliaga na kuondoka huku moyo ukiwa na majonzi ya kuolewa mpenzi wake Kilole mwanamke ambaye aliamini ndiye aliyemuonesha raha ya mapenzi. Lakini hakuwa na jinsi kwa kujua siku zote mwenye kisu kikali ndiye hula nyama. MIAKA MIWILI BAADAYE Maisha mjini yaliendelea vizuri kwa Kilole kuzidi kupendeza baada ya kupata mtoto wa kike kwenye ndoa yake. Kijijini kwao nako hakukusahau kwa kupeleka misaada ikiwemo kubadili paa la nyasi na kuweka bati. Mabadiliko yale yalifanya mama Kilole aamini kama mwanaye angeolewa na Kinape angempoteza. Maisha ya Kinape aliyajua mwenyewe kazi yake kubwa kijijini ilikuwa kulima shamba la wazazi wake na mashamba ya watu na kulipwa fedha kidogo. Ugumu wa maisha ulimfanya akate tamaa ya maisha na kuamua kuwa mvuta bangi na mlevi wa pombe za kienyeji. Matumizi yale yalimchakaza na kuoneka amechoka kama alirudishwa gerezani, wazazi wake walisikitika kwa hatua aliyofikia. Hata jina lake alilibadili na kujiita Marehemu mtalajiwa kwa vile aliamini kuwa maisha mazuri ni sawa na ngamia kupita katika tundu la sindano yeye ni wa kusubiri kufa. Kama ilivyokuwa kawaida ya Deus kila baada ya miezi sita alikwenda kijijini kuwatembelea wazazi wake, taarifa za kuwepo rafiki yake Kinape zilimfikia. Baada ya kufika kijijini alikwenda moja kwa moja nyumbani kwao na Kinape ili aonane naye, alipofika alimkuta mama Kinape aliyempokea kwa furaha na bashasha. “Karibu mwanangu.” “Asante mama, za hapa?” “Nzuri kiasi.” “Shikamoo.” “Marabaha.” “Unasema kiasi kivipi?” “Ukimuona Kinape utamtambua?” “Kivipi?” “Kinape anajiita Marehemu mtalajiwa.” “Kwa nini?” ”Amekwisha kata tamaa ya maisha.” “Kwa nini?” “Maisha ya kijijini yamekuwa magumu kwake hata huko mjini alikokutegemea anapaogopa kama kuzimu.” “Yupo wapi?” “Akitoka asubuhi kurudi jioni.” “Mmh, sasa sijajua hiyo jioni itakuwa saa ngapi? Maana nategemea kuondoka saa kumi na mbili jioni.” “Baba wala usisumbuke kumsubiri, hiyo jioni bahati lakini muda wake kabisa ni saa mbili usiku akiwa amelewa.” “Sasa mama, nataka kufufua matumaini yaliyopotea ya Kinape.” “Yapi tena hayo baba?” “Nitamchukua, nina imani kwa muda mfupi atakuwa tegemeo la familia.” “Tutashukuru, kwani tumekwisha kata tamaa na kumuachia Mungu.” “Basi mama mwambie jumapili nitamfuata au kama nitakuwa na kazi nyingi nitamtuma mtu amfuate.” “Sijui baba nikushukuru vipi.” “Wala hakuna cha kunishukuru, Kinape ni ndugu yangu wa damu siwezi kukubali kumuona akiadhirika wakati ndugu yake nina uwezo wa kumsaidia.” “Nitashukuru baba,” mama Kinape alisema huku akitaka kupigia magoti, Deus alimuwahi asifanye vile. Waliagana huku akimsisitiza asisahau kumweleza Kinape siku hiyo asitoke, jioni ilipofika Deus alirudi mjini bila kuonana na rafiki yake kipenzi. **** Kinape aliporudi alikuta salamu kwa mama yake. “Kinape, Deus alikuja.” “Shida yake nini?” “Swali gani hilo mwanangu, Deus si rafiki yako?” “Deus si rafiki yangu ni adui yangu namba moja.” “Kwa nini unasema hivyo?” “Atamuoaje Kilole akijua ni mchumba wangu.” “Kinape, maisha yako yanakushinda ungeweza vipi kukaa na mwanamke?” “Hii haikuwa juu yenu.” “Basi kwa taarifa yako huyo adui yako ndiye anayetaka kuyabadili maisha yako kwa kukurudisha mjini.” “Kufanya nini?” “Deus ni mtu mkubwa sana, siku hizi ana gari kama la mbunge, kweli duniani hakuna mtu mwembamba. Deus kanenepa huyo na kitambi juu, kaacha maagizo kuwa jumapili atakufuata uende mjini.” “Ni umaskini ndiyo utakaonifanya niende kwake, lakini niliapa sitamsamehe mpaka nakufa.” “Lakini unamlaumu bure, nina imani alikuwa hajui, kama angejua sidhani angekubali kumuoa Kilole.” “Kwa nini hakuuliza kabla ya kuoa?” “Ni wazi alifichwa.” “Kama ni hivyo familia ya kina Kilole kimenitendea unyama.” “Kwa hiyo mwanangu nakuomba usiipoteze nafasi hii, nina imani ndoto zako huenda zikatimia.” “Sawa mama nitajiandaa na safari.” “Basi acha kunywa mipombe yako ili kidogo mwili upendeze kwa siku mbili” “Nitafanya hivyo mama.” ******* Siku ya jumapili Kinape alijiandaa na safari ya kwenda mjini kwa ajili ya safari. Saa nne asubuhi gari aina ya Toyota land cruser Vx ilisimama mbele ya nyumba ya mzee Solomoni baba yake Kinape. Kinape alikuwa wa kwanza kutoka nje ili aonane na rafiki yake kipenzi Deusi. Baada ya mlango kufunguliwa, kwanza kuteremka alikuwa Salome mdogo wake Deus, alipomuona tu alipaza sauti: “Kaka Kinape mwenyewe huyo hapo,” alisema huku akigeuza shingo kumuangalia mtu aliyefuatana naye. Alikuwa kijana mmoja mtanashati alisogea hadi alipokuwa amesimama Kinape. “Habari ndugu?” “Nzuri tu, karibu.” “Nina imani wewe ndiye Kinape?” “Hujakosea ndiyo mimi.” ”Vipi wazazi wamo ndani?” “Yupo mama, baba ametoka kidogo.” “Naomba nionane naye.” “Karibu kwenye kigoda nimwite,” Kinape alimkaribisha mgeni kwenye kigoda kisha aliingia ndani kumwita mama yake. Baada ya muda mama Kinape alitoka alipomuona mgeni alimkaribisha. “Karibu baba.” “Asante, shikamoo mama. “ “Marahaba, karibu.” “Asante, mama mimi si mkaaji nimetumwa hapa na brother Deus nimfuate Kinape.” “Hakuna tatizo baba, ndugu yenu mwenyewe huyo hapo.” “Nashukuru nilipofika tu Salome kanionesha, kwa hiyo nilikuwa naomba ruhusa niwahi kuondoka.” “Hakuna tatizo hata yeye mwenyewe amekwisha jiandaa” “Basi tunaweza kwenda.” Kabla ya kuondoka mama Kinape alimwita ndani mwanaye na kumpa maneno ya mwisho. “Kinape mwanangu najua wazi ulikuwa na urafiki wa karibu na Kilole, nakuomba chondechonde achana naye, fuata kilichokupeleka. Kumbuka kosa lako moja linaweza kuwa majuto ya milele. Muogope Kilole kama ukoma muone ni shemeji yako.” “Sawa mama nimekuelewa.” Kinape na Dereva aliyetumwaamfuate aliongozana hadi kwenye gari na kuondoka pamoja. ****** Dereva aliyemfuata Kinape alimjulisha Deus kuwa wamekaribia nyumbani, Deus alimjulisha tayari yupo nyumbani kwa ajili ya kumsubiri mgeni. Sauti ya gari ilimfanya Deus asogee mlangoni kusubiri kumpokea rafiki yake kipenzi waliopotezana muda mrefu. Gari liliposimama dereva alimfungulia mlango Kinape ambaye aliteremka kwenye gari, Deus alipomuona akipaza sauti huku akitoka mbio kwenda kumpokea rafiki yake kwa kumwita jina alilolizoea. “Keiii Piii.” “Dewuuuu.” Wote walikutana na kukumbatiana kwa furaha. “Ooh, karibu sana rafiki yangu.” “Asante nimekaribia” Walishikana mikono na kuiingia ndani pamoja, wakati wanaingia Kilole alikuwa anatoka kwenye friji kuchukua juisi ya mtoto. Macho yake yalipatwa na mshtuko baada ya kumuona Kinape ndani ya nyumba yake mwanaume aliyemkimbia na hakutaka hata siku moja aonane naye na kujibu maswali ambayo aliaminbi kwake ni magumu. Kinape hakushtuka sana kwa vile alijua Kilole yupo wapi na ni mke wa mtu, Kilole glasi ya juisi ilimponyoka na kuanguka chini. “Mke wangu vipi mbona hivyo?” “Ha..ha..pana.” “Kinape, karibu sana hapa ndipo ninapoishi.” “Asante kupafahamu.” “Nina imani nilikueleza tutakuwa na ugeni, naomba basi apatiwe huduma zote muhimu kisha aoneshwe chumba chake,” Deusi alimwambia mkewe. “Ha..ha..kuna ta..ta..tizo.” Kilole alisahau kuokota glasi iliyoangukia juu ya zuria, aligeuka na kuelekea chumba cha mgeni kuangalia kama matayarisho ya mwisho kabla ya kumkaribisha chumba mgeni. Alijikuta akikosa raha kwa kitendo cha mumewe kumwingiza ndani ya nyumba yake mwanaume ambaye lazima atataka majibu ya usaliti wa ahadi yao. Alijikuta akimlaumu mumewe kwa kitendo cha kutomjulisha ni mgeni gani anayekuja. Kwa upande wa Kinape alibakia na siri moyoni hakutaka kumueleza rafiki yake uhusiano wake na Kilole. Pia alikumbuka wosia wa mama yake juu ya kuwa karibu na mke wa mtu japo alikuwa mpenzi wake. ******* Baada ya Kinape kuoga na kubadili nguo Deus alimtambulisha rasmi rafiki yake kwa mkewe Kilole. “Mke wangu, huyu ni rafiki yangu kipenzi Kinape nina imani si mgeni kwako.” “Ni kweli, lakini sikuwa na mazoea naye,” Kilole alimjibu mumewe akiwa ameangalia chini. “Kinape huyu ndiye mke wangu Kilole ambaye ni shemeji yako.” “Nashukuru kumfahamu shemeji.” “Mke wangu, Kinape atakuwepo hapa kwa muda mpaka nitakapomtafutia kazi na yeye kuanza maisha yake.” “Hakuna tatizo, karibu shemeji,” Kilole alimkaribisha Kinape kwa sauti ya chini. Baada ya utambulisho ule, Deus na Kinape walizungumza mengi wakikumbushia mambo ya miaka mingi. Deus alikuwa na furaha tofauti na Kinape aliyejifikiria atatazamana vipi na Kilole mwanamke aliyemsaliti. Usiku ulipoingia waliagana kuonana kesho asubuhi. Chumbani aliyelala usingizi uzuri alikuwa Deus peke yake lakini Kinape na Kilole kila mmoja aliwaza lake. Kilole aliamini kabisa kuolewa na Deus kumeweza kuyabadili maisha yake, alijiuliza kama Kinape ameletwa na mumewe ili amsaidie, angeweza vipi kumtimizia mahitaji yake muhimu. Aliamini Kinape pamoja na kuahidiana kuoana angempotezea muda tu na si kumtengenezea maisha yake. Alijikuta akiondoa hofu moyoni na kuwa tayari kukabiliana na maswali atakayo ulizwa na Kinape. Naye Kinape alijikuta akiumia kwa usaliti wa mpenzi wake wa kuolewa na mtu mwingine. Kilichomuuma sana kilikuwa kuolewa na mtu wa karibu na kibaya zaidi kukaa nyumba moja huku wote wakilishwa na mtu mmoja. Siku ya pili Deus baada ya kujiandaa kwenda kazini alimfuata rafiki yake Kinape chumbani kwake kumuaga. “Best mimi nawahi kazini tutaonana jioni.” “Hakuna tatizo.” “Kila kitu nimemuachia maagizo shemeji yako, nakuomba uwe huru au siyo Keiiii Piii,” Deus alikumbushia enzi zao. ‘Hakuna tatizo Dewuuuu.” Walicheka pamoja na kuagana Deus alitoka chumbani kwa Kinape na kumpitia mkewe aliyembusu kisha walisindikizana hadi kwenye gari. “Bai Bebi.” “Bai honey safari njema, kazi njema.” “Asante mke wangu.” Deus aliondoka na kumwacha mkewe akimsindikiza kwa macho mpaka alipopotea ndipo alipogeuka kurudi ndani. Alirudi taratibu huku akiwa na mawazo mengi juu ya kuwepo Kinape pale, hakutaka hata siku moja katika maisha yake baada ya kuolewa na mtu mwingine kwa kuvunja ahadi yao asikae karibu na Kinape.
Kilole hata alipokwenda kijijini baada ya ndoa hakutaka kuonana na Kinape, aliingia kimya kimya mpaka anaondoka Kinape hakujua. Alijiuliza akimtaka mumewe amuondoe Kinape na kumtafutia sehemu nyingine atamuelewa. Jambo lingine alilojifikiria lilikuwa kama hilo litashindikana basi atatafuta mbinu nyingine kuhakikisha anauvunja urafiki wa Deus na Kinape. Baada ya kuingia ndani alifanya usafi wote muhimu, akiwa jikoni akiandaa kifungua kinywa, Kinape aliamka na kwenda hadi sebuleni. Sebule ilikuwa tupu ila runinga ilikuwa wazi, alikaa kwenye sofa viti ambavyo toka azaliwe hakuwahi kukalia. Taratibu alitembeza macho kuangalia uzuri wa nyumba ambayo ilikuwa na kila kitu, akiwa bado anashangaa alisikia sauti ya vyombo. Aliamini Kilole anaosha vyombo, alinyanyuka na kuelekea jikoni. Alimkuta akikaanga mayai huku amempa mgongo, alimsogelea taratibu bila kumshtua alipomkaribia alimsalimia. “Za asubuhi shemeji,” sauti ile ilimshtua sana Kilole na kumfanya ashike mkono kifuani. “Kilole usishtuke maji yamekwisha mwagika jione huru,” Kinape alimtoa hofu. “Sio hivyo Kinape ni wazazi si mimi,” Kilole alijitetea. “Najua, ndiyo maana nikasema jisikie huru, tupo sehemu ya watu tusije kosa mwana na maji ya moto.” “Nisamehe Kinape bado nakupenda nipo hapa kwa shinikizo, lakini mimi nilikuwa radhi kukusubiri mpaka atakaporudi,” Kilole alijikuta akiomba msamaha huku akibubujikwa machozi ya aibu. “Si kweli Kilole, kwa nini hukuwaeleza ukweli, ina maana mama yako hajui uhusiano wetu. Au ndiyo sababu ya pesa?” “Mama alikuwa anajua lakini alimuogopa baba ambaye hakuujua uhusiano wetu.” “Kilole muongo, baba yake alitufuma mara ngapi asijue?” “Kama alikuona alijua ni mzowezi si muoaji.” “Si kweli kwa nini hukumwambia kuwa mimi ndiye mumeo mtarajiwa au kwa vile sina kitu. Kumbuka Kilole mateso yote niliyoyapata mjini ni kwa ajili yako, nimefungwa kwa ajili yako kutafuta maisha mazuri ili tuje tuishi maisha mazuri. Lakini mwisho wa siku umeamua kunisaliti.” “Niamini Kinape si mimi ni wazazi wangu.” “Kwa nini hukukataa?” “Nilik…,” Kilole alinyamaza baada ya kusikia sauti ya gari, kweli alikuwa mumewe amerudi mara moja. Aliingia ndani haraka na kukutana na Kinape anatoka jikoni, alishtuka kumuona Kinape akitokwa na machozi. Hakumuuliza kitu alikwenda moja kwa moja jikoni, alishtuka kumkuta mkewe anafuta machozi alishtuka sana na kuhoji. “Vipi mbona mnalia, kuna usalama?” Kilole alishtushwa na swali la mume wake na kujilaumu kusahau kufuta machozi. “Mke wangu kuna nini mbona wote mnalia?” Kilole alikosa jibu la kumjibu mumewe alibakia ameinama huku akijiuliza mumewe kama atajua kuwa alikuwa na mahusiano na Kinape ndoa yake itakuwa hatiani. Alitamani kuomba radhi na kumweleza ukweli juu ya uhusiano wake na Kinape na kumhakikishia hawezi tena kuwa na uhusiano naye. Deus bado alikuwa yupo kwenye kizungumkuti asijue nini kimetokea muda mfupi baada ya kuondoka kwenda kazini na kumuacha Kinape amelala na mkewe akirudi ndani. Lakini amerudi na kukuta mabadiliko na mkewe kushindwa kumjibu. “Mke wangu kuna habari za msiba?” “Hapana.” “Sasa kuna nini?” Kilole aliendelea kukosa jibu kwa mumewe, Deus alimwacha mkewe jikoni na kumfuata Kinape aliyekuwa amesimama sebuleni akifuatilia jibu la Kilole ambalo alijua linaweza kuharibu ndoto yake kwa mara ya pili. “Kinape.” “Naam.” “Kuna nini mbona mnaniacha njia panda kuna kitu gani kimetokea muda mfupi baada ya kuondoka?” “Ni jambo la kijijini.” “Jambo gani lililowatoeni machozi?” “Ni kweli, sikutegemea shemeji kuniuliza swali kama lile.” “Swali gani?” Kilole mapigo ya moyo yalimwenda mbio miguu ilianza kumwisha nguvu kwa kuamini kosa moja la Kinape litayagharimu maisha yake yote. Alitamani kumuomba Kinape asiseme ukweli ambao ungemgharimu maisha yake. Alipotaka kumuomba Kinape anyamaze ili akayazungumze na mumewe ndani mdomo ulikuwa mizito alibakia akimuomba Mungu amuepushe na balaa lile. “Shemeji aliniulizia habari za rafiki yake kijijini.” “Sasa habari za rafiki yake na machozi yenu yanahusiana vipi?” Swali lile lilizidi kumuweka katika hali mbaya Kilole kwa kujiuliza yeye alimuuliza swali gani kuhusu rafiki yake lililosababisha watokwe na machozi. “Aliniulizia shoga yake aliyesoma naye ambaye alikuwa rafiki yangu wa kike, mwezi jana tumemzika baada ya kufa kwa uzazi. Kwa kweli kwangu ilikuwa sawa na kutonesha kidonda kilichoanza kupona, nilipomweleza habari zile shemeji alianza kulia kitu kilichonikumbusha maumivu ya moyo ya kumpoteza kipenzi changu aliyekufa na kiumbe changu tumboni.” “Ooh! Poleni sana, sikujua rafiki yangu kama ulipata msiba mzito kiasi hicho, Mungu atakulipia hiyo yote ni mitihani ya maisha.” Deus alimvutia kifuani rafiki yake na kumpigapiga taratibu huku akiendelea kumfariji. “Pole sana rafiki yangu Mungu atakulipia mara mbili.” “Asante.” Alimwacha Kinape na kwenda kumkumbatia mkewe aliyekuwa bado akitokwa na machozi ya hofu. “Pole mke wangu kwa kuondokewa na rafiki yako kipenzi.” “Asante mume wangu.” “Nakuombeni msahau yaliyopita kwani kuendelea kuumia ni kuingilia kazi ya Mungu na kuona kama mmeonewa lakini kumbe hiyo ni njia yetu sote tatizo kutangulia.” “Tumekuelewa, kwangu ulikuwa mshtuko ambao sikuutegemea,” Kilole alijikuta akipata nguvu za kuongeza uongo baada ya Kinape kumuokoa kwenye swali lililokuwa kama kaa la moto mdomoni mwake. “Basi jamani mimi si mkaaji nimerudia flash disic yangu niliisahau juu ya droo ya kitanda.” Deus alielekea chumbani na kumuacha mkewe akiwa bado amesimama, Kilole naye aliamua kumfuata mumewe chumbani. Alipofika alimkumbatia kwa nyuma na kusema kwa sauti ya chini. “Samahani sweet.” “Samahani ya nini tena mpenzi?” “Kwa hali uliyonikuta nayo, sikupenda upatwe na mshtuko kama ule.” “Aah, kumbe hilo mbona la kawaida, si ujajua nakupenda kiasi gani, sipendi kukuona kwenye matatizo, heri niteseke mimi si wewe kipenzi changu.” “Najua, ndiyo maana nikakuomba samahani mpenzi wangu, hata mimi sitaki nikuone unaumia kwa ajili yangu.” “Nashukuru kwa kulifahamu hilo.” “Basi mpenzi nisikucheleweshe, mke mwema ni yule anayemhimiza mumewe katika kazi zake na si yule anayemuacha akiharibikiwa.” “Asante sana mke wangu, lazima nimshukuru Mungu kunipa mke mwema.” Baada ya kuchukua Flash disc Deus alimuaga tena mkewe na kuwahi ofisini. ******** Baada ya kuondoka Kilole alishindwa amshukuru vipi Kinape kwa kumuokoa kwa mumewe kwa kuamini kama angejibu yeye lazima angejichanganya. Wakiwa wanapata kifungua kinywa, Kilole alimshukuru Kinape. “Kinape sikuwezi wewe kiboko sikutegemea ungejibu vile.” “Hiyo mbona kazi ndogo hata kama angenifumania natoka chumbani kwako bado ningeweza kujitetea na yeye angekubali kwa kukiamini nitakacho mweleza.” “Basi nilikuwa na wasiwasi na kujua talaka ipo usoni mwangu.” “Kama nilivyokueleza maji yameisha mwagika hayawezi kuzoleka.” “Usiseme hivyo Kinape, sipendi uumie kiasi hicho.” “Nimeishaumia kinachotakiwa kutuliza maumivu.” “Nitakusaidia kuhakikisha maisha yako yanakuwa mazuri.” “Sawa, lakini naomba tuishi kama mtu na shemeji yake tuondoe mazoea ya karibu yatakayo muondoa wasiwasi mumeo.” “Nashukuru Kinape kuwa muelewa, nakuhakikishia kuyasahau mateso yote ya kijijini na kuyaanza maisha mapya.” MWAKA MMOJA BAADAYE Maisha ya Kinape yalibadilika kutokana na kazi aliyokuwa akifanya, hata hali ya mwili ilikuwa ya mvuto kutokana na maisha aliyokuwa akiishi. Kilole alijikuta akivutiwa na Kinape kila alipopita au alipokuwa amekaa alimwangalia sana. Tofauti ya Deus na Kinape ilikuwa katika mavazi, Deus siku zote alivaa nguo za heshima muda wote tofauti na Kinape alivaa nguo zinazokwenda na wakati kama jeans tisheti na raba za bei mbaya kutokana na pesa aliyokuwa akipata. Kinape alijipenda kwa kujipulizia manukato ya bei mbaya kifuani alikuwa na mkufu mkubwa wa dhahabu. Kila mwanamke alitaka awe wake, lakini alichagua msichana mmoja ambaye aliamini ndiye anayefaa kuwa mkewe baada ya kila kitu kwenda vizuri. Hakuisahau familia yake kitu ambacho siku zote alisisitizwa na rafiki yake ahakikishe kipato anachokipata aikumbuke familia yake kijijini pamoja na kufanya marekebisha ya makazi ya wazazi wake. Kinape alikuwa makini sana katika maisha yake hakutaka mchezo kabisa. Mvuto wake machoni kwa wanawake ulikuwa mateso mazito kwa Kilole na kujikuta akimuona Kinape kama mwanaume pekee mwenye mvuto na uwezo wa kitandani tofauti na Deus, ambaye hakuwa mtundu sana kitandani zaidi ya upendo wa dhati. Kilole alijiuliza atawezaje kumsogeza karibu Kinape ambaye tayari ameisha jitangaza kuwa ana rafiki wa kike ambaye wakati wowote atatambulishwa kwao. Kila alipokuwa Kinape peke yake alitamani kuzungumza naye ili kumweleza jinsi gani anavyoteseka juu yake. Japo hakutaka kuachana na mumewe lakini shida yake wawe karibu ili kukumbushia mapenzi yao ya zamani ambayo aliamini hakuna mwanaume mwingine wenye kumpa raha kama Kinape.
Wakati huo Deus mambo yake yalizidi kuwa mazuri kutokana na kuingiza kipato kikubwa kutokana na takrima ya kazi yake. Aliweza kumpa siri nyingi rafiki yake kipenzi jinsi anavyoweza kupata pesa nyingi nje ya kipato chake cha kawaida. Deus alijikuta akimuamini sana Kinape kwa kumweleza mambo mengi kuhusu uwezo wake wa kipesa na madaraka yake kazini. “Kinape nipo kwenye kitengo cha hatari sana ukiwa mnoko huchelewi kufa, hivyo inabidi uume na kupuliza. Kitengo cha kudhibiti madawa ya kulevya ni kitengo hatari sana vigogo ndiyo wahusika wakuu kama utakamata mizigo yao huchelewi kuhamishwa au kutengenezewa zengwe litakalo kulaza pabaya hata kukumaliza kabisa.” “Kwa hiyo vigogo hawakamatwi?” Kinape alimuuliza Deus. “Utaanzia wapi, nyuma yako kuna wakubwa wanakula kupitia mgongo huo huo, sasa wewe jitie kiherehere.” “Kwa hiyo matumizi ya dawa ya kulevya kwisha ni vigumu?” “Ni vigumu lazima tuseme ukweli.” “Sasa kitengo hicho kazi yake nini?” “Kudhibiti dawa za kulevya.” “Lakini mbona wengine mnawakamata?” “Hao ukiona hivyo hawana mikono ya wakubwa.” “Kwa hiyo unapata posho nene toka
kwa hao vigogo?” “Kweli rafiki yangu, nisingeweza kuwa vitu hivi kwa muda mfupi.” “Alafu unafahamika sana na watu wazito, huwezi kuamini siku ile uliponituma niende kwenye kampuni ile nilipokelewa kama mfalme. Nje niliacha watu wakisota kuomba kazi hata jioni baada ya kazi nilipewa gari la kunirudisha nyumbani, wote pale wanajua Paroko ni ndugu yangu wa damu.” “Hao ndio watu tunaokula nao mjini, waswahili wanasema sema na watu uvae viatu.” ******* Wakati Deus akiuweka wazi uwezo wake wa pesa na njia zinazoingilia, Kilole alikuwa katika wakati mgumu kuhakikisha Kinape kabla ya kuhama mule ndani basi awe ameisha mrudisha katika himaya yake. Siku moja Deus alisafiri kikazi na kuwaacha ndani ya nyumba mkewe, Kinape na mfanyakazi wa ndani. Kilole aliamini ile ni nafasi pekee ya kumsogeza Kinape karibu, Lakini siku hiyo jioni ilikuwa chungu kwa Kilole baada ya Kinape kuja na mpenzi wake nyumbani kumtambulisha. Roho ilimuuma kwa kuamini Kinape amefanya vile ili kumlingishia yeye, alipofika na rafiki yake wa kike Kinape alimtambulisha kwa Kilole. “Shemu huyu ndiye ubavu wangu kama nilivyowataarifu, nilipanga leo awakute wote, lakini kwa vile Swahibu amesafiri nimeonelea si vibaya hata wewe kuwa muwakilishi hata siku akija asionekane mgeni.” “Karibu sana mgeni,” alimkaribisha kinafiki lakini moyoni alikuwa na donge zito. “Asante nimekaribia,” mgeni alijibu huku akijilaza kwenye kifua cha Kinape kama katumwa. “Shemu usione Kinape natakata sababu ya mtoto huyu, kwao wamemlea akalelewa, sifa ziende kwa wazazi wake.” “Mmmh! Kama hivyo hongera.” Siku ile walishinda pale na jioni alimsindikiza nyumbani kwao, aliporudi alimkuta Kilole hayupo katika hali ya kawaida kitu kilichomshtua Kinape. “Vipi shemu mbona upo hivyo, maana naona ghafla umekosa raha au unamkumbuka mzee mbona ni leo tu?” “Kwanza Kinape jina hilo unaloniita silipendi sema hujui tu.” “Jina gani?” “La shemeji.” “Aah, sasa wewe ni nani kama siyo shemeji yangu.” “Niite mpenzi au jina langu.” “Eti?” Kinape alishtuka. “Umesikia sana napenda uniite mpenzi mahawala hawaachani.” “Lakini kwangu wanaachana.” “Kinape kumbuka bado nakupenda.” “Hata mimi nakupenda,” Kinape alimjibu Kilole. “Sasa kwa nini unanionesha mwanamke wako mbele yangu?” “Jamani kuna ubaya gani nami kuwa na wangu mbona mimi sijakuzuia kunionesha kuwa ni mke wa Deus?” “Kinape sikia, kama nilivyokueleza kuwa mimi nilikubali kuolewa kwa shinikizo, lakini nakuhakikishia bado nakupenda na upendo wangu hautakufa milele.” “Sawa, sikatai lakini sasa hivi nitaendelea kukuheshimu kama shemeji yangu na si mpenzi wangu.” “Hilo najua endelea kuniheshimu kama shemeji yako, lakini Deus akiwa mbali utabaki kuwa mpenzi wangu. Nitahakikisha kutokana na uwezo wa mume wangu kukuwezesha kipesa kisha nitaachana naye ili tuishi pamoja.” “Kilole hilo halitawezekana hata siku moja,” Kinape alimjibu huku akimkazia macho. “Litawezekana, kwa vile wewe ndiye mwanaume aliye moyoni mwangu, hakuna mwingine zaidi yako.” “Kilole siwezi kumtendea unyama rafiki yangu kwa ajili ya tamaa zako za mwili, pia siwezi kukorofishana na rafiki yangu kwa ajili yako, sitaki nionekane mwizi wa fadhira kukosa nuksani kwa ajili ya starehe za muda.” “Kama hutaki tumfanye hivyo basi tufanye penzi la siri.” “Kilole hakuna siri katika mapenzi.” “Lipo kama wenyewe tukiitunza siri hiyo.” “Haitawezekana, Kilole mshukuru Mungu kwa kukupa mume wenye uwezo pia mwenye mapenzi ya dhati na wewe. Kwa nini unataka kuichezea shilingi kwenye tundu la choo?” “Kumbuka wewe ndiye uliyenionjesha tamu ya dunia.” “Ni kweli, lakini kisicho riziki hakiliki, haukuwa riziki yangu ndiyo maana ameolewa na mwingine.” “Kama ulijua hivyo mbona ulinilaumu?” “Nilikulaumu kwa haki kwa vile ulivunja ahadi yetu, lakini uliponieleza umeozwa kwa shinikizo la wazazi wako nilikuelewa.” “Kinape nimekubali, basi naomba kwa leo tu ili nipoze machungu ya moyo wangu, usiponipa nitateseka na nitakuwa radhi kuachika na kurudi nyumbani.” “Kilole kwa nini hukusema mapema mpaka umesikia nina mwanamke ndiyo yazuke haya?” “Nilikuwa natafuta nafasi ili nikueleze, kumtambulisha mpenzio ilikuwa kama kuniwahi kuzieleza hisia zangu.” “Nimekuelewa, lakini nakuomba chonde heshimu ndoa yako, kumbuka bomu unalotaka kulitega litatusambaratisha na kijiji tutashindwa kurudi.” “Kinape nakuhakikishia hata Deus akijua hawezi kufanya lolote kwa vile nina siri zake nyingi chafu.” “Lakini kipi unachokikosa kwa mumeo?” “Mapenzi yako, ilinionjesha sasa hivi siyapati.” “Kilole bora lawama kuliko fedheha, nakuhakikishia siwezi kushea mapenzi na rafiki yangu na ukizidi kunilazimisha nitahama hapa. Kuanzia leo nione kama mbingu na ardhi,” Kinape alisema kwa kujiamini bila mzaha. “Wapii? Kinape nakuhakikishia lazima utakuwa mpenzi wangu.” “Labda kwa nguvu za giza.” “Walaa, situmii mizizi wala hirizi wenye hila ni wanawake bwana.” “Tutaona, na sasa naomba unione kama kituo cha polisi kwa muuza unga, Kilole nimeteseka sana kutafuta maisha, mwanga unaonekana unataka kunipeleka wapi, nitawaeleza nini wazazi wangu.” “Wee, maliza yote lakini mwisho wa siku utabakia kuwa mpenzi wangu, kumbuka wewe ndiye uliyenirubuni na kupoteza sifa za usichana wangu, leo hii eti nikuone kama kituo cha polisi na mvuta bangi. Kwa taarifa yako mimi nakuona kama jalala na siku zote ndilo kimbilio la mimi nzi.” “Haya tutaona.” “Si upo, ipo siku utakubaliana na mimi ninachokisema, haiwezekani nitunze mimi wengine wafaidi utamu. Kumbuka Kinape nimekuwa na wewe katika mazingira magumu na uliniahidi ipo siku nitafaidi raha. Leo hii umepata unanikataa.” “Sijakukataa, sasa hivi wewe ni mke wa mtu kuwa muelewa.” “Kwa hili siwezi kukuelewa mpaka naingia kaburini nakuapia ukinikataa nitajiua.” “Umefika mbali, lakini mbona una maisha mazuri mumeo anakuhudumia kila kitu kwa nini unataka kulipiga teke fuko la pesa.” “Kama unataka suruhu tufanye penzi la siri, nakuhakikishia kumheshimu mume wangu wala sitamdharau.” “Kilole najua hutanielewa nakuomba umkemee shetani wa uzinzi.” “Kinape uniniambia hivyo? Leo hii unajua kukutamani ni kuwa na shetani wa uzinzi kama ungejua hivyo usingenihalibia usichana wangu kumbuka nilikueleza mpaka utakaponioa au zawadi kwa mwanaume yeyote atakayenioa. Lakini ulinidanganya kuwa utanioa mbona hukunioa?” Kilole alizugumza huku akilia kwa hasira. “Kilole naomba unisikilize tena unisikilize kwa makini, kabla ya kuja mama yangu alilijua hili na kunieleza nisiwe na wewe karibu hivi akisikia nimefukuzwa na Deus kwa sababu yako nitakuwa mgeni wa nani. Kumbuka sasa hivi wazazi wangu wanaishi maisha ya raha kwa ajili ya Deus huoni kujiingiza katika mapenzi na wewe itakuwa sawa kukata tawi nililokalia?” “Kinape usiwe mwingi wa nahau, Deus hajui lolote kuhusu uhusiano wetu kwa hiyo itatupa nafasi ya kufanya mambo yetu kwa siri bila kujua.” “Kilole narudia tena sitafanya na wala sitegemei kufanya tuheshimiane na kuanzia leo humu ndani nahama nitakuja akiwepo Deus tu.” “Na akikuuliza kwa nini umehama utamjibu nini?” “Nitajua nitakacho mjibu lakini hakitahusiana na wewe.” “Kinape naomba uje unizike, ukiondoka jiandae kusikia msiba wangu.” “Kwa hilo sitakutenga nitahudhuria mazishi yako.” “Yaani upo tayari nife unaniona?” “Kwa hili nipo radhi ufe, nina imani hata bila kuwa na mimi bado utaendelea kufurahia maisha. Kusema utajiua kwa ajili yangu ni uongo mkubwa, kama ungekuwa na mapenzi na mimi usingeolewa.” “Nikueleze mara ngapi nililazimishwa lakini mapenzi yangu yote kwako.” “Nimekuelewa, basi endelea na mumeo.” “Upo tayari nife?” “Kwa hili nipo tayari, sipo tayari kujigeuza nyoka mdogo nimekuwa nammeza mfugaji kwa ajili ya tamaa zako za mwili.” “Kinape nimekuelewa, ila nakuomba kitu kimoja endelea kuniita shemeji na mimi nitakuheshimu kama rafiki ya mume wangu. Nakuahidi sitakutamkia tena maneno ya mapenzi. Nakuomba unisamehe kwa yote yaliyojitokeza, nina imani ukiondoka lazima siri itavuja naweza kukosa Bara na Pwani. “Kinape nisamehe sana, ni mapenzi mazito kwako, lakini nakuhakikishia nitarudia tena nisamehe sana,” Kilole alisema kwa sauti iliyoambatana na kilio. “Nimekusamehe Kilole, tuiheshimu safina hii tunayosafiri pamoja, lolote baya tukilitenda itakuwa sawa na kuitoboa kwenye kina kirefu tutazama wote.” “Nimekuelewa Kinape, nakuomba unisamehe sana.” “Nimekusamehe, asante kwa kunielewa.” Walikubaliana kuendelea na taratibu zilizokuwepo za kuheshimiana kama mtu na shemeji yake na si wapenzi. Kilole baada ya kugonga mwamba alikuwa na mpango mzito moyoni mwake wa kikakikisha anampata Kinape bila mwenyewe kujua. Wakiwa katikati ya mazungumzo simu ya Kinape iliita, alipoangalia aliona ni ya mpenzi wake. “Haloo sweet.” “Haloo darling.” “Niambie mpenzi wangu.” “Vipi upo tayari?” “Ooh, sorry nilikuwa na mazungumzo na shemeji kidogo yamechukua muda ngoja nijimwagie maji.” “Fanya haraka nakuja sasa hivi.” Baada ya kusema vile alielekea chumbani kwake kubadili nguo akaoge ili atoke na mpenzi wake. Usiku wa siku ile walipanga kwenda kwenye kumbi za starehe, Kinape toka awe na mpenzi wake mpya amekuwa akionjeshwa raha za duniani ambazo hakuwahi kuziota. Alipokuwa akielekea chumbani kwake, Kilole alimsindikiza kwa macho huku moyoni akisema “nitakomesha jeuri yake.” Akiwa bado yupo katika hali ya uvivu kutokana na maneno ya Kinape yaliyomkata maini. Alishtushwa na sauti ya Happy mpenzi wa Kinape akiwa katika vazi la kutokea jioni. “Aah, dada kumbe upo sebuleni, ina maana husikii hodi yangu?” “Aah! Kumbe ni wewe nilikuwa mbali kimawazo.” “Dada, shemeji kuondoka asubuhi tu umekuwa hivyo, je, akimaliza wiki?” “Wee acha mdogo wangu, nawe utaolewa utayaona.” “Ahaa! Umeishafika?” Kinape alisema akiwa anatoka bafuni. “Niliona unachelewa nikaamua nikufuate, si unajua mtu chake.” “Na kweli mdogo wangu,” Kilole alijibu huku roho ikimuuma. “Hongera umependeza,” Kinape alimsifia Happy. “Nawe nataka upendeze kama mimi, vaa nguo nilizokununulia.” “Hakuna tatizo dear nipe nusu dakika.” “Aah, wapi nakuja huko huko.” Waliongozana wote hadi chumbani huku Happy akiwa amemkumbatia Kinape. Kilole alijua Kinape amefanya vile kumuumiza roho, lakini aliapa kumshikisha adabu huku akipanga mpango kabambe wa kusambaratisha penzi lile. Baada ya muda walitoka wakiwa wameongozana katika mtembeo wa mapenzi mazito. Kilole aliwasindikiza kwa macho huku roho ikizidi kumuuma jinsi walivyopendana. Alijua maisha yale hakuna sehemu ya kuyapata zaidi ya kuwa na Kinape. Toka aolewe na Deus hakuwahi kwenda sehemu za starehe zaidi ya kwenda kwenye dhifa ya kiserikali. Lakini mashoga zake walimweleza raha wanazozipata wanapokwenda kwenye kumbi za starehe hata kwenye vikundi vya taarabu. Moyoni alijisemea: Leo mjanja lakini ipo siku utanijua mimi na yeye nani zaidi.” Kilole akiwa na mpango mzito moyoni mwake ambao aliujua yeye na Mungu wake, ili kuufanikisha alionesha ukaribu na mpenzi wa Kinape kitu kilichomziba macho Kinape kwa kuamini Kilole amekubaliana na alichomueleza ***** Maisha yaliendelea kama kawaida kwa Kilole naye kumtembea mchumba wa Kinape kuonesha ukaribu. Hali ile iliongeza mapenzi kwa Kinape kuona hali ipo shwari bila kujua kuna bomu zito limepangwa dhidi yake ya kulisambaratisha penzi lake. Wakati huo Kinape alikuwa katika hatua za mwisho kumpeleka happy kijijini kutambulishwa kwa wazazi wake. Kilole alipanga kutekeleza mpango kabla ya Kinape hajampeleka Happy kijijini, aliamini kama atachelewa itakuwa vigumu kuutekeleza mpango wake. Matumaini ya kutekeleza mpango wake yalikuwa makubwa baada ya kupewa na taarifa na mumewe ana safari ya kikazi nje ya nchi kwa siku tano. Siku ilipofika ya mumewe kusafiri ilikuwa tofauti na siku zote, Kilole alionesha kumhitaji mumewe kuliko kipindi chochote kilichopita. “Mke wangu siku tano si nyingi,” Deus alimtuliza mkewe aliyekuwa akilia. “Kwako si nyingi lakini kwangu naona kama miaka mitano,” Kilole alidondosha machozi ya uongo. “Najua basi nitajitahidi safari nyingine tusafiri pamoja.” “Itakuwa afadhari.” “Kinape kuwa karibu na shemeji yako hata ukiwa mbali na nyumbani mpigie simu ili asipate upweke.” Deus alimweleza rafiki yake. “Deus si mpo kwenye Facebook twitter instagram usiku tumieni kuliwazana ili usijione mpo mbali mbali,” Kinape alitoa wazo ili ajiweke mbali na Kilole. “Na kweli mke wangu, kila baada ya kazi nitakuwa pamoja na wewe katika kuchati.” “Lakini si sawa na wewe kuwa pembeni ya ubavu wangu,” Kilole alilia wivu wa uongo. “Basi mke wangu niombee niende salama nirudi salama, si unajua kazi zetu.” “Na ukirudi utimize ahadi ya kuninunulia gari langu,” Kilole alisema kwa sauti ya kideka. “Kila kitu kipo tayari, subiri nikufanyie Surprise.” “Waawoo mpenzi wangu.” Kinape alijikuta akifurahi furaha ya kweli baada ya kuona ndoto yake ya siku moja kuendesha gari lake mwenyewe inatimia. Alimkumbatia mumewe na kumtakia safari njema. “Dear usafiri salama na urudi salama, ukiwa mbali kumbuka umeniacha kama kinda la ndege linalomsubiri mama yake aliyekwenda kutafuta chakula.” “Hilo nalijua, nataka mpenzi wangu na mwanangu muishi maisha nusu ya peponi.” “Asante mume wangu. ” Kilole aliagana na mumewe na kurudi nyumbani na Kinape katika gari moja, wakiwa njiani Kinape alimchokoza. “Ona ulitaka kupoteza bahati yako bure, haya ndiyo mapenzi unayotakiwa kuyapigania.” “Kinape yale yalikwishapita achana nayo. ” Walirudi wote mpaka nyumbani, walipofika Kinape hakukaa aliaga na kwenda kuonana na mpenzi wake kitu ambacho Kilole hakupenda kukisikia. ***** Kilole akiwa peke yake aliamini mpango alioupanga Kinape hawezi kuruka, alichukua simu yake na mkononi na kutafuta jina la mtu, kisha alipiga na kuiweka sikioni kusikiliza. Baada ya kuita kwa muda ilipokelewa upande wa pili. “Haloo Sisiter.” “Haloo Jimmy.” “Ndiyo Sister lete stori, naona leo umenikumbuka.” “Mambo mengi mtu wangu, upo pande zipi?” “Ndiyo nafika kijiweni, ulikuwa unasemaje? Najua wito wako lazima nidake vumba nene.” “Unaweza kuja nyumbani mara moja?” “Hakuna tatizo.” “Basi njoo mara moja.” “Okay, nakuja.” Kilole alikata simu na kutabasamu mwenyewe huku akijisemea moyoni: “Kinape hana ujanja japo mjini aliwahi lakini mimi ndiye mwisho wa matatizo lazima arudi mikononi mwangu na uchumba wake ubakie hadithi.” Kengele ya mlangoni ilimuondoa kwenye mawazo na kumfanya ananyuke kwenda kufungua. “Ooh! Jimmy, karibu.” “Asante Sister.” Baada ya Jimmy kuingia alikaa kwenye kochi la watu watatu, Kilole alikaa kwenye kochi la mtu mmoja. Kwa vile Jimmy alikuwa mbali na Kilole, alimuomba asogee kochi la karibu. “Jimmy, njoo ukae kwenye kochi hili.” Jimmy alinyanyuka na kwenda kukaa karibu yake, Jimmy alionekana mtu mwenye wasiwasi sana. “Jimmy mbona hivyo?” “Mmh! Jinsi tulivyokaa mumeo akitokea inaweza kuwa msala.” “Kwani hajui kama wewe mpiga picha?” “Anajua, lakini naona kama tumekaa karibu sana.” “Wasiwasi wako kwanza mume wangu kasafiri.” “Na mdogo wake?” “Ametoka na hawezi kurudi sasa hivi.” “Haya sister nipe dili basi.” “Kuna kazi nitakupa uifanye, ukiifanya vizuri nitakupa pesa nzuri sana ambayo hukuwahi kuipata toka ulipoanza kazi ya kupiga picha.” “Kazi gani hiyo dada?” “Ya kupiga picha.” “ Mmh! Ni kazi ipi, mbona kama naona kama si ya kawaida?” “Ni kweli, hii itakuwa siri yako na malipo yatakuwa mazuri.” “Kazi hiyo itakuwa lini?” “Ikiwezekana leo hii.” “Poa basi ikiwa tayari nishtue.” “Jimmy, naomba usifanye kazi yoyote kuanzia sasa hivi, nitakulipa pesa ya usumbufu na kazi ikikamilika nitakupa fedha nzuri sana.” “Hakuna tatizo sister, nakuamini dada yangu wa ukweli.” “Nisubiri,” Kilole alinyanyuka na kwenda chumbani, baada ya muda alirudi na elfu 50 na kumpa Jimmy. “Hii ya usumbufu, ya kazi bado.” “Asante Sister.” Jimmy alipokea na kutoka akimwacha Kilole akifurahia mpango wake, alichukua simu yake na kumpigia Kinape. Baada ya simu kuita kwa muda Kinape upande wa pili aliipokea. “Haloo Shemu.” “Kinape upo wapi?” “Nipo na mke mwenzio hapa.” “Waawoo! Nimeipenda hiyo,” . “Kweli?” Kinape alimuuliza. “Kweli, inafurahisha, mmeonesha jinsi gani mnavyo pendana.” “Ndiyo shemeji yangu, una lipi tena?” “Nimesahau kukujulisha kuwa leo ni siku yangu ya kuzaliwa.” “Wawooo, mbona hukuniambia mapema nikuandalie zawadi?” “Nilipitiwa lakini jioni kutakuwa na sherehe fupi ya kifamilia.” “Hakuna tatizo nitakutafutia zawadi nzuriii shemeji yangu.” “Nitashukuru, uje na Happy.” “Hakuna tatizo.” Baada ya kuzungumza na Kinape, alimpigia simu mtengeneza keki ili amuandalie keki ya birthday, ambaye aliwahi kumtengenezea mwanaye alipotimiza mwaka mmoja. “Sakina ninaweza kupata keki ya birthday?” “Lini shoga?” “Leo hii jioni.” “Jamani! Mbona haraka, ya nani?” “Yangu mwenyewe.” “Jamani shoga! Mbona hukunialika?” “Kwani mimi? Shemeji yako ndiye kasema akirudi jioni akute keki, mwenyewe nilikwisha sahau kama leo siku yangu ya kuzaliwa,” Kilole aliunda uongo unaofanana na kweli. “Kwa hiyo jina lako ni lilelile?” “Lipi hilo?” “La Kilole?” “Hilohilo mpenzi.” “Basi hakuna tatizo nipe saa mbili kila kitu kitakuwa tayari.” “Nitashukuru.” Baada ya kuachana na mtengeneza keki, alikumbuka kitu muhimu kilichotakiwa kiwepo pale ili kufanikisha mpango wake. Alimpigia simu mpiga picha, simu iliita kwa muda kisha ilipokelewa upande wa pili. “Oya, sister mambo tayari?” “No, kuna kitu nataka kukutuma kabla ya kazi yetu.” “Kitu gani hicho?” “Eti kete ya unga shilingi ngapi?” “Unga upi?” “Kokeni, sijui heloin.” “Una maanisha madawa ya kulevya?” “Ndiyo.” “Mmh! Ya nini?” “Jimmy, utajua baadaye.” “Sijajua bei yake, lakini sidhani kama inazidi elfu tano kwa kete.” “Basi njoo uchukue fedha ukaninunulie kete mbili.” “Sister unajidunga nini?” “Jimmy, kazi itakushinda.” “Basi Sister nakuja.” Baada ya muda mfupi alifika na kupewa elfu ishirini akanunue kete mbili za unga. Alitoka na kumwacha Kilole akiendelea na maandalizi ya mipango yake ambayo ilikuwa siri yake na Mungu wake. Alimtuma mlinzi kununua vinywaji ambavyo alivijaza kwenye friza, kila kitu kilikwenda kama kilivyopangwa. Kilole baada ya kuridhika na mipango yake kwenda vizuri alijiandaa kuisubiri keki ili akamilishe zoezi lake. Baada ya saa mbili kama alivyoahidia alijulishwa kuwa keki tayari, kwa vile hakutaka kutoka alimuomba mpelekewe. Sakina alimletea keki baada ya nusu saa, wakati huo mpiga picha alikuwa amefika na kumpa kete mbili za unga. “Asante Jimmy, kwa kazi hii nitakupa posho elfu kumi, ila kuna kazi nyingine unatakiwa kuifanya.” “Ipi hiyo?” “Nitakupa namba hii nikikubip ipige, akipokea mwambie anatakiwa kwao haraka sana kuna matatizo.” “Sawa.” “Hakikisha unakaa mkao wa kazi usicheze mbali nakutegemea wewe ndiye steling wa picha.” “Hakuna tatizo sister.” “Jimmy ukiifanya kazi kwa ufanisi nitakupa laki mbili.” “Utani huo sister!” “Sina utani kwa jambo nitakalo kuahidi.” “Sawa, wacha nikuache uendelee na mambo mengine.” Jimmy aliondoka na kumuacha Kilole akitengeneza nyumba kwa ajili ya sherehe ya kutengeneza ya birhtday yake. Sebule aliipamba na kupambika ikawa katika muonekana wa kupendeza.
ILIPOISHIA: “Jimmy ukiifanya kazi kwa ufanisi nitakupa laki mbili.” “Utani huo sister!” “Sina utani kwa jambo nitakalo kuahidi.” “Sawa, wacha nikuache uendelee na mambo mengine.” Jimmy aliondoka na kumuacha Kilole akitengeneza nyumba kwa ajili ya sherehe ya kutengeneza ya birhtday yake. Sebule aliipamba na kupambika ikawa katika muonekana wa kupendeza. SASA ENDELEA.. ******* Majira ya saa mbili usiku kila kitu kilikuwa kimepangwa sehemu yake, Kinape na mpenzi wake nao walikuwepo kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa Kilole. Ilikuwa sherehe iliyozuka kama uyoga, ule ulikuwa mpango wake maalumu wa kuhakikisha nasambalatisha penzi la Kinape na Happy pia kumrudisha mikononi mwake. Kabla ya sherehe kuanza simu ya Happy mchumba wa Kinape iliita, aliipokea na kuzunguza. “Haloo.. eeh .. Nipo kwa Kinape… Kuna sherehe ya kuzaliwa shemeji yake…Eeeh!… Nini? Acha utani.. Mungu wangu nakuja…Aah.. lazima nije?” “Vipi?” Kinape na Kilole waliuliza kwa pamoja baada ya kumuona Happy akitokwa na machozi huku ameshikilia mikono kichwani. “Mama,” alijibu kwa mkato. “Mama kafanya nini?” “Kavamiwa na majambazi walitaka kumpora gari.” “Wamemjeruhi?” “Wanasema hawajamjeruhi, wanaomba niendelee na sherehe lakini lazima nikamuone mama kisha nitarudi.” “Kinape mpeleke mwenzako,” Kilole alijifanya mwema. “Hapana dada ninyi endeleeni tu, nitarudi muda si mrefu, inaonekana tatizo siyo kubwa, nitakwenda peke yangu.” Happy aliwatoa wasi. “Hapana mpenzi lazima nikupeleke,” Kinape alisema. “Lakini kama umesema mama hana tatizo basi wacha nianze sherehe na Kinape ukirudi tutaungana pamoja,” Kilole alitumia nafasi ile kumbakiza Kinape. “Kweli kabisa dada, nisiharibu utaratibu wa sherehe kwa vile ilikuwa ndiyo inaanza.” “Ila shampeni utaifungua ukirudi.” “Hakuna tatizo.” Kinape alimsindikiza Happy mpaka nje, baada ya kuingia kwenye gari na kuondoka alirudi ndani kuendelea na sherehe ya mtego aliyoandaliwa yeye bila kujijua. Wakati Kinape akitoka nje kumsindikiza mpenzi wake, Kilole alitumia nafasi ile kumuwekea dawa ya kulevya kwenye juisi. Kinape aliporudi alikaa kwenye kochi na kuchukua glasi ya juisi na kunywa kidogo huku akimtupia swali Kilole kuvuta muda labda Happy atawahi kurudi. Kilole alifurahia moyoni na kuona mpango wake umekuwa rahisi tofauti na alivyopanga wa kumtumia Jimmy kumtoa Happy kwa simu ya uongo ili kitendo kifanyike kwa haraka. Lakini simu kutoka kwao kidogo imfanye apige yowe la furaha. “Shemu, Deus anajua kama leo ni tarehe yako ya kuzaliwa?” “Anajua na muda si mrefu nitakufanyieni bonge la surprise na mchumba wako.” “La nini tena, mbona umenirusha roho.” “Utaliona muda si mrefu.” “Nigusie kidogo.” “Ukijua haitakushtua, nataka uamini nakupenda shemeji yangu.” “Mmh! Haya.” Kinape alisema huku akichukua glasi ya juisi na kupiga funda zingine tatu na kurudisha glasi chini. Mara alianza kuhisi kichwa kizito, alijitahidi kushindana na hali iliyomtokea kila macho yalizidi kufumba. Kilole alifurahi kuona kila kitu kinakwenda kama kilivyopangwa. Taratibu Kinape alijilaza kwenye kochi, kwa hatua ile Kilole aliona tayari mpango wa awali umekamilika. Alikumbuka mlango upo wazi alikwenda kuufunga, kisha alimpigia simu Jimmy. “Haloo Jimmy.” “Vipi Sister, nipige ile simu?” “Hapana, njoo nyumbani haraka.” “Nipe dakika sifuri.” Alipokata simu mlango uligongwa, alijua Jimmy amefika, alitoka hadi mlangoni na kufungua. Alishtuka kumuona Happy mbele yake, alipotaka kuingia ndani alimshika kifuani na kumrudisha nyuma. “Vipi dada!” Happy aliuliza kwa mshangao. “Kinape kakufuata.” “Kanifuata vipi wakati nimemwambia narudi?” “Amesema huenda mama yako kapata matatizo makubwa.” “Jamani! Sasa kapitia wapi mbona sikumuona?” “Kwa kweli sijui kitu, nimembembeleza akusubiri kakataa.” “Kwa nini asinipigie simu?” “Mmh! Siwezi kujua.” Happy aliamua kumpigia simu Kinape mbele yake, baada ya muda simu iliita ndani. “Mbona simu yake inaita ndani?” “Aliisahau kutokana na papara zake.” “Sasa nikimfuata si nitapotezana naye, bora nimsubiri ndani.” “Happy, kutokana na king’ang’anizi cha mpenzi wako nimeamua kuahisha sherehe mpaka jumamosi.” “Hata hivyo siwezi kusumbuka kumfuata, wacha tu nimsubiri,” Happy alisema huku akitaka kuingia ndani. “Happy kuwa muelewa, Kinape baada ya kuondoka nimemweleza nimeamua kuahirisha sherehe na yeye alisema hatarudi mpaka kesho. Sasa ukimsubiri itakuwaje?” “Mmh! Wacha nimuwahi,” Happy alisema huku akigeuka na kuondoka. Kilole hakuingia ndani mpaka aliposikia sauti ya gari la Happy likiondoka, wakati huo Jimmy alikuwa amefika. “Ooh! Jimmy karibu ndani.” “Asante,” Jimmy alijibu huku akiingia ndani. Alipofika sebuleni alishangaa kukuta kuna kitu kama sherehe, mbele kulikuwa na keki kubwa iliyoandikwa Happy Birthday Kilole na pembeni yake kulikuwa na chupa kubwa ya shampeni. Sehemu nyingine kulikiwa na vinywaji ndani ya glasi. Alipoangalia kwenye kochi alimuona Kinape ameutwanga usingizi. “Vipi Sister naona ulikuwa na sherehe ya kuzaliwa kwako?” “Ndiyo, lakini sicho nilichokuitia.” Jibu lilimfanya Jimmy asiulize kitu zaidi ya kusubiri alichoitiwa. “Ndiyo sister lete maneno?” “Kazi niliyokuitia sasa imekamilika nataka ufuate maagizo yangu, malipo yako nilikuambia kiasi gani?” “Laki mbili.” “Nitakuongezea hamsini, itakuwa laki mbili na nusu.” “Hakuna tatizo,” Jimmy alikubali bila kujua ni kazi gani. Baada ya kuhakikisha mlango ameufunga vizuri alimuomba Jimmy amsaidie kumuingiza ndani Kinape. Walisaidizana kumwingiza chumbani, Kilole alimpeleka katika chumba chao cha kulala kisha walimlaza kitandani. Baada ya kumlaza walitoka mpaka sebuleni kupanga mipango yao. “Sasa sikiliza kazi niliyokuitia ni hii.” “Kazi gani?” “Nataka unipige picha kwenye tukio lote nitakalokuwa nalifanya kisha utaenda kunisafishia na kuniletea picha zote, sawa?” “Picha za tukio gani?” “Nitakalo lifanya muda mfupi usilishangae nina sababu zangu ila nakuomba unifichie siri hii.” “Hakuna tatizo.” “Basi subiri.” Kilole alisema huku alielekea chumbani kwake, Jimmy alibaki akijiuliza anataka kupewa kazi gani. Baada ya muda Kilole alirudi akiwa katika vazi la kanga moja iliyoonesha hakuwa na nguo nyingine ndani. “Jimmy,” alimwita kwa sauti ya chini. “Na..na..aam,” Jimmy alionekana kuchanganyikiwa na umbile la Kilole lililokuwa la utata kwa mwanaume shababi. “Jimiiii, utaiweza kazi kweli?” “Kwa nini?” “Umeona negative umechanganyikiwa ukiona picha si utashindwa hata kuifanya hiyo kazi.” “Niwaweza tu wala usihofu.” “Umeisha andaa kamera yako?” “Ndiyo.” “Basi njoo chumbani.” Jimmy kabla ya kwenda chumbani alifikiria ameitwa na Kilole kufanya naye mapenzi kwa kisingizio cha kupiga picha. Japo alijua mke wa mtu sumu lakini kwa mwanamke aliyeumbwa akaumbika kama Kilole ilikuwa sawa na nzi kufia juu ya kidonda. Uchu wa ngono ulimjaa na kujiona kama mbwa anayejipeleka mwenyewe kwa chatu, alitembea huku mwili wake ukiongezeka joto la matanio. Alipoingia chumbani alishangaa kumuona Kinape amelala kitandani hajitambui akiwa mtupu. Hali ile ilimshtua na kujiuliza kulikoni kuwa vile. Kilole alikwisha msoma Jimmy, ilikumtoa hofu alimwambia: “Jimmy utakachokiona humu ndani kiache kama ulivyokiona, nikisikia chochote tutaonana wabaya, Kabla ya mimi kulikimbia jiji nitaanza na wewe. ” Kilole alitoa onyo kali kwa Jimmy. “Siwezi kufanya hivyo.” “Sawa, sasa naomba upige picha kila tendo nitalofanya na Kinape.” “Tendo gani?” “Usiulize andaa kamera yako,” Kilole alikuwa mkali kidogo. Jimmy hakuongeza swali zaidi ya kufuata maelekezo, muda wote bado alikuwa gizani kutokana na hali iliyokuwemo mule chumbani kwa Kinape kulazwa chali kitandani akiwa mtupu na sehemu zake za siri zilikuwa zimenyanyuka. Kabla hajapata jibu Kilole aliitoa kanga iliyostiri mwili wake na yeye kubakia mtupu. “Jimmy,” alimwita huku akipanda kitandani. “Aah…Eeeh…Na..naa..m.” “Naona umepagawa, sasa kila hatua piga picha, sawa?” “Sawa,” Jimmy alijibu macho yamemtoka pima. Jimmy alimshangaa Kilole mambo ya aibu aliyokuwa akiyafanya mbele yake bila haya, alifanya mapenzi na Kinape aliyekuwa hajitambui kwa kumkalia juu yake. Ajabu Jimmy alijisahau kazi aliyopewa ya kupiga picha na kujikuta akipandwa na mzuka wa ngono. Alimshangaa Kilole mke wa mtu kufanya mpenzi na shemeji yake ambaye alionekana amelewa kupita kiasi. Aliona heri kama amezidiwa angemweleza yeye kuliko kufanya mapenzi na mtu asiyejitambua. Kilole alipofumbua macho alimshangaa Jimmy aliyekuwa amesahau kazi aliyomtuma. “Jimmiiiii,” sauti kali ya Kilole ilimshtua Jimmy aliyekuwa akiangalia Blue print live bila chenga. “Jimmy, umeisha piga picha?” “Samahani Sister,” Jimmy alibabaika. “Samahani nini Jimmy, kazi imekushinda?” “Ha..ha..pana,” Jimmy alibabaika hata kamera alikuwa ameweka chini ili afaidi vizuri mambo ya wakubwa. Aliiokota na kujiandaa kupiga picha huku akitetemeka. ”Naomba upige picha kila hatua sawa?” “Sawa.” Kilole alianza zoezi upya la kijidhalilisha mbele ya Jimmy, naye alipiga picha kila hatua. Baada ya zoezi lake kukamilika, alimuomba Jimmy amuoneshe picha zote. Alichagua zinazofaa na zingine kuzifuta kisha alimuomba Jimmy atoke akamsubiri sebuleni. Jimmy alitoka akiwa katika hali mbaya baada ya kuzidiwa na ashki, kuna kipindi aliwaza hata ambake Kilole. Lakini alikumbuka alikuwa kazini na kazi ile ya hatari aliahidiwa pesa nyingi, alikaa sebuleni kumsubiri Kilole ambaye alikuja baada ya robo saa akionesha ametoka kuoga na kuvalia nguo ya kulalia. “Jimmy, mzigo wako huu hapa, hizi ni laki na nusu, hamsini za kusafishia na laki moja adivansi ukileta picha zangu nakumalizia laki na nusu. Ila kuna zawadi yako kubwa kama utakuwa msiri, kuna kazi nyingine ya milioni moja.” “Wacha!” “Wewe tu kuonesha uaminifu.” “Basi dada kesho saa nne nakuletea mzigo wako, andaa fedha yangu tu.” “Hakuna tatizo, tutaonana kesho, lakini chonde chonde siri hii asijue mtu yeyote.” “Nakuhakikishia siri hii itabakia kwa watu wawili mimi na wewe tu.” “Haya, usiku mwema.”
Kilole aliagana na Jimmy na kurudi ndani, alipofika kitandani alivua nguo zote na kujilaza pembeni ya Kinape. Alfajiri kilevi kilipomwisha Kinape alishtuka usingizini, akili yake alijua aliyelala pembeni yake ni mpenzi wake Happy, lakini alipoangalia vizuri aligundua ni Kilole, alishtuka na kunyanyuka kitandani. Alishangaa kujikuta amelala kitanda kimoja na shemeji yake na kwa hali waliyokuwa kuwa nayo, aliamini lazima walifanya mapenzi. Alijiuliza ilikuwaje mpaka akawa kwenye kitanda cha rafiki yake wakiwa watupu na mkewe. Alinyanyuka haraka kitandani na kupitia nguo zake bila kuzivaa na kukimbilia chumbani kwake. Alipokuwa akipapatika kama kuku aliyekatwa kichwa na kuachiwa, Kilole alikuwa akimuangalia kwa chati huku akichekea moyoni huku akisema: “Kiko wapi, mimi na wewe nani mjanja.” Hakujisumbua aliendelea kulala huku akichelelea moyoni, wakati huo Kinape baada ya kuingia chumbani kwake na kukaa kitandani mikono aliweka kichwani na kujiuliza kilichotokea ni kweli. Ili kupata ukweli alizishika sehemu zake za siri na kukutana na majimaji kumuonesha kabisa katumika. Kila alivyorudisha mawazo yake ilikuwaje mpaka akalala katika kitanda cha rafiki yake kipenzi Deus na mkewe, jibu lilikuwa mbali. Alikumbuka siku ya jana yake kwenye sherehe baada ya kuondoka Happy alibakia na shemeji yake Kilole wakipiga stori huku wakivuta muda kumsubiri Happy ili wafungue sherehe rasmi. Wazo lake la haraka lilikuwa huenda ule ulikuwa mpango wa Kilole kama alivyomuahidi atahakikisha anamrudisha mikononi mwake. Kinape alijiapia kuwa kamwe pamoja na kufanya ujanja ule hawezi kuendelea kuwa mpenzi wake zaidi ya kuhama nyumba. Wakati anatoka kuoga aliona simu yake juu ya kochi, aliichukua na kukuta imezimwa, alielekea nayo chumbani kwake. Alipoingia aliiwasha, haikupita muda ziliingia meseji zaidi ya kumi zote zikuwa za Happy akimlalamikia kwa kitendo alichomfanyia cha kumzimia simu. Wakati akiendelea kusoma ujumbe wa Happy simu yake iliita, alikuwa Happy, alijiuliza atamwambia nini ili amuelewe. Lakini alijikaza kiume na kuipokea kwa kuamini hawezi kukosa cha kumueleza. “Haloo Kinape umenifanya nini?” “Happy mbona huniulizi nimepatwa na nini unaanza kunilaumu.” “Kinape, nilikuambia narudi, lakini nilipofika nyumbani nikakuta hali ya mama ipo sawa, nimerudi nikasikia umenifuata na kusema utarudi kesho. Nilipopiga simu yako kumbe uliiacha ndani kwa kuchanganyikiwa. Kinape, tulikuwa na mpango gani wa kulala pamoja na kusababisha sherehe ya shemeji yako kuvurugika?” Maneno yale yalimpa picha na kujua atamjibu nini ili kumfanya asiendelee kuumia. “Mpenzi nilipokuwa nakuja kwenu, nilipata na ajali na kupelekwa polisi hata simu niliisahau nyumbani.” “Sasa mbona baadaye nilipokutafuta ilikuwa imezimwa?” “Nilikuta haina chaji.” “Kwani ulirudi saa ngapi?” ”Saa nane usiku.” “Ooh, pole upo wapi sasa?” “Nyumbani.” “Nakuja sasa hivi?” “Usije nisubiri kwenu.” “Hapana mpenzi usisumbuke nakusubiri nitakufuata hapo hapo.” “Sipo nyumbani, ndiyo maana nimekueleza nisubiri.” “Kinape si umeniambia upo nyumbani sasa hivi! Mbona sikuelewi?” “Nimetoka nyumbani sasa hivi kuelekea polisi, hivyo namalizana nao nipitie kwenu.” “Mmh! Sawa.” “Usisikitike dia, sawa.” “Sawa dia, nimeumia sana kusikia umelala polisi kwa ajili yangu.” “Hawakukupiga?” “Hawakunipiga nipo sawa dia.” “Ooh! Afadhari nakusubiri, una usafiri au nikufuate na gari?” “Hapana, kuna teksi nilikodi,” Kinape alijitahidi kumzuia mpenzi wake. “Hakuna tatizo mpenzi wangu, angalia usije ukapata ajali tena.” “Unafikiri niligonga walaa, alijigonga mwenyewe mwendesha boda boda wala hakuumia polisi hawana dogo.” “Mbona unaongea hivyo si upo polisi?” “Nipo mbali nao.” “Basi kuwa makini nakupenda sana Kinape, mmmmmmwa.” “Mmmwa,” Kinape naye alijibu na kukata simu. Mara mlango uligongwa, alikuwa Kilole, bila kuitikia alinyanyuka na kwenda mlangoni, alipofungua alikutana naye uso kwa uso. “Za asubuhi shemeji?” Kilole alimsabahi Kinape aliyekuwa akimshangaa. “Nzuri.” “Shemeji chai tayari.” “Asante, nimeshiba.” “Imeanza lini na leo iwe ya pili, kama ulijua hunywi chai kwa nini hukuja kunieleza mapema. Si umenipita jikoni unakwenda bafuni kuoga.” “Sikukuona.” “Basi lazima chai uinywe ndipo uende huko kwa mwanamke wako unayejifanya unampenda kuliko wanawake wote.” “Shemu yote yamefikaje huko, tunazungumzia chai Happy kaingiaje?” Kinape alimuuliza Kilole huku akitengeneza shati lake. “Kama hutaki yote hayo, njoo unywe chai tena kuna kitu nataka unieleze kwa kituo kiniingie. Wewe si ulinikataa iweje univizie usiku?” Kilole alizungumza sauti ya kuonesha hakutendewa haki. “Mimi?” Kinape alishtuka kusikia vile. “Kwani hapa nazungumza na jiwe?” “Mmh! Bado sielewi nini kilitokea jana,” Kinape alisema akiwa ameangalia chini kwa aibu. “Ndiyo maana nikasema kunywa chai tuzungumze.” “Happy ananisubiri.” “Happy wa muhimu kuliko tukio ulilonifanyia jana usiku, ulishindwa kuniambia nikakukubalia kwa hiyari yangu, ukanivizia nimelala huo si ubakaji? Nilijua bado unanipenda ndiyo maana nilikueleza nikupe penzi la siri kwa vile bado naheshimu penzi lako ukakataa. “Lakini asubuhi nashtuka nakuona unakimbia, kweli Kinape wewe wa kunifanyia hivyo?” Kilole alimuuliza kwa msisitizo. “Kilole hili suala linatakiwa tulifanyie kazi si la kukurupuka kulaumiana.” “Sijakulaumu ila nimekuuliza ulishindwa vipi kunieleza una hamu na mimi, siwezi kukunyima, kwa vile wewe ndiye uliyenionesha raha na tamu ya dunia. Hili kwangu si tatizo lakini na mimi nina ombi langu nakuomba nani unitekelezee ili tuwe sawa.” “Mmh! Hata sielewi, basi niache niende kwa Happy ili nikirudi tupange vizuri.” “Kinape umenionjesha naomba unimalizie kabisa.” “Sawa nimekubali, nikirudi nitatimiza haja zako.” “Kinape kuna tatizo gani ukinipa muda huu ili ukitoka usiwe na wasiwasi wa kufikiria nyumbani?” “Mmh! Sawa.” Kauli ile ilimfanya Kilole amsukumie Kinape nyuma na kumuangushia kitandani kwake. Kama kipanga aliyeona kifaranga cha kuku alimsaula nguo zote na yeye kutoa zake chache zilizovaa. Kinape alijikuta akiwa kama mbwa kwa chatu, moyoni alijiapiza atatafuta kila njia ahame pale ili kujiweka mbali naye. Upande wa Kilole aliamini mpango wake umekwenda vizuri tofauti na alivyofikiria na kuapa kumfanyia mambo makubwa Kinape. Baada ya kuondoka chumbani Kinape alibakia ameinama mikono kichwani alijiuliza maswali yasiyo na majibu, ilikuwaje akawa katika kitanda cha Deus, alichokumbuka kuamka asubuhi na kujikuta amelala na Kilole bila nguo bila kujua alifikaje pale. Aliwaza labda ulikuwa mpango wa Kilole aliomuahidi hapo awali, lakini shutuma alizozitoa zilizidi kumchanganya kuonesha amemlazimisha kufanya naye mapenzi bila ridhaa yake. Kitendo kilicho onekana kuwa ni sawa na kubaka. Japo hakupenda kufanya mapenzi tena na Kilole lakini kwa upande mwingine alimshukuru kwa uamuzi wake wa kutomshitaki polisi. Aliamini kama angempeleka basi angeweza kuozea gerezani, kwani ushahidi wote ulikuwepo wa kuonesha amebakwa. Simu yake iliita zaidi ya mara sita na kukatika, aliisikia lakini akili yake ilikuwa mbali sana. Alikumbuka alikuwa na mpango wa kuonana na Happy nyumbani kwao, alinyanyuka na kwenda bafuni kuoga. Baada ya kumnaliza kuoga na kubadili nguo, alipoangalia simu yake alikuta aliyepiga ni Happy zaidi ya mara sita. Hakutaka kumpigia alijua yote atamalizia huko huko akifika, alitoka kuelekea nyumbani kwao Happy. Wakati anatoka sebule haikuwa na mtu alitoka haraka kumuwahi Happy, alipofika mlango wa kutokea nje aliitwa nyuma na Kilole. “Kinape.” “Naam,” aliitika huku akisimama. “Safari ya wapi?” “Si nimekueleza nakwenda kwa Happy.” “Nataka nikuambie kitu kimoja, sipendi kusikia jina la mwanamke wako, kila nikisikia linanitia kichefuchefu.” “Lakini si mchumba wangu?” “Mmh! Sasa hii chai anywe nani?” “Nilimuahidi nitakwenda kwao muda uliopita nikizidi kuchelewa atajisikia vibaya.” “Kinape unachekesha, nisijisikie vibaya mimi niliyekutaka ukanikataa ukaishia kunibaka.” “Yaani sijui hata ilikuwaje hiyo jana!” “Iweje na wewe umeamua kunibaka.” Kauli ile ilimmaliza nguvu Kinape na kubakia amesimama kimya kama amenaswa na sumaku. “Kinape siwezi kukulazimisha mapenzi kwa vile upo na mchumba wako, lakini sipendi dharau.” “Lakini si nimekueleza hali iliyopo?” “Kinape huyo Happy angekujulia wapi kama mimi ningemgomea mume wangu wee kuja mjini?” Kilole alimuuliza huku ameshika kiuno. “Lakini mbona yamekuwa hayo….,” Kinape alinyamaza kimya baada ya mlango kugongwa. Kilole aliamini muda ule Jimmy alikuwa akileta picha, alipofika mlangoni alikutana na Happy. Japo moyoni alichukia lakini alitengeneza tabasamu la uongo.” “Ooh! Happy karibu.” “Asante dada,” Happy alisema huku akimtaza Kinape aliyekuwa amesimama karibu na mlango. “Kinape unanifanya nini, nimekukosea nini mpaka uamue kunitesa hivi?” Happy alisema kwa sauti ya kilio. “Happy mbona umekuwa mtu wa kulaumu bila kuuliza?” “Niulize nini hapa ndiyo polisi?” “Hilo swali gani?” “Kinape ni wazi hunipendi najipendekeza kwako,” Happy alilalamika huku machozi yakimtoka. “Happy unaniamini, huniamini?” “Nikuamini vipi mtu muongo.” Wakati huo Jimmy mpiga picha alikuwa akiingia, ili kupoteza ushahidi Kilole alimueleza Kinape: “Shemu naomba ukazungumzie nje mambo yenu nina mgeni.” “Sawa,” Kinape aliitikia huku akimshika mkono Happy aliyekuwa ameiva na kuwa mwekundu kwa hasira. “Hebu ngoja,” Happy alijitoa mkononi mwa Kinape. “Happy hebu msikilize mwenzako,” Kilole aliingilia kati baada ya kuona Happy akitafuta msaada kwake. “Sikiliza dada, Kinape ananinyanyasa sana.” “Mdogo wangu ngoja nizungumze na mgeni, tutalimaliza nina imani kabisa Kinape anakupenda sana.” Kinape na Happy walitoka nje na kuwaacha Kilole na Jimmy.
Usiku baada ya kutoka kumpiga picha za aibu Kilole, Jimmy alikuwa mtu mwenye mawazo mengi sana. Toka aanze kazi ile hakuwahi kukutana na tukio zito kama lile. Tokio kubwa lilikuwa kuwapiga picha za utupu wake za watu au mastaa wa kike. Lakini la kushuhudia mtu akifanya mapenzi lilikuwa ndilo tukio lake la kwanza lililompa wakati mgumu sana. Alitamani bora Kilole angempa penzi yeye kuliko kufanya mapenzi na mtu aliyekuwa sawa na maiti asiyejielewa. Alijikuta akipata maswali yasiyo na majibu juu ya kitendo cha Kilole kufanya mapenzi na mtu anayemfahamu ni shemeji yake. Alijiuliza kufanya tukio lile huku akipiga picha alikuwa na maana gani, alijikuta akiingiwa na tamaa ya mapenzi kwa kuamini kupitia picha zile lazima na yeye ataweza kumtia mikononi. Wazo lingine lilikuwa kutengeneza pesa zaidi kupitia picha zilezile. Baada ya kuwaza sana akiwa amejilaza kitandani alijikuta akitabasamu baada ya kugundua picha zile zitakuwa sawa jiwe moja kuua ndege wawili. Hakuamini kabisa mwanamke yule pamoja na kumtisha anaweza kumfanyia lolote baya. Kabla ya kulala alirudia kuangalia picha moja moja ili aone zipi zimetoka vizuri na zipi zimeharibika, alijikuta akiwa amepiga picha chache zenye ubora. Kutokana kupatwa na kigagaziko kilichomfanya aifanye kazi katika wakati mgumu. Picha zingine alipiga ukuta badala ya watu, zingine aliwapiga mgongo au kupiga sehemu isiyohusika. Zote ambazo zilikuwa hazifai alizifuta na kubakiza chache ambazo zilikuwa zinafaa. Baada ya kuwaza sana alipitiwa na usingizi mpaka siku ya pili, asubuhi alipoamka baada ya kuoga alikwenda studio kusafisha picha zake. Kama kawaida picha zake za magumashi zilikuwa zinawahishwa kusafishwa kabla hawajaanza kazi yoyote. “Beka kama kawaida piga mara mbili.” “Za nani mwana?” “Kaka aina haja ya kujua, nifanyie kazi haraka.” Beka alimsafishia Jimmy picha mara mbili na kumpatia, alizichukua na kurudi zake nyumbani kwanza kabla ya kuzipeleka kwa mwenyewe. Alipofika alipitia picha moja baada ya nyingine, alichukua za kwake na kuziweka kwenye kabati na zilizobaki alimpelekea Kilole. ******* Jimmy alipofika kwa Kilole alishtuka kumkuta Kinape nusra atimue mbio kwa mshtuko, lakini alificha hofu yake na kuingia ndani. Baada ya Kinape na mpenzi wake kutoka nje walibakia wawili ndani. “Karibu ukae,” Kilole alimkaribisha Jimmy baada ya kuonesha wasiwasi, alijua baada ya kumuona Kinape. “Asante,” alijibu huku akikaa, kutokana na wasiwasi walijikuta akikaa chini. “Jimmy mbona unanitia aibu kazi utaiweza kweli?” “Samahani, unajua nimeshtuka sana.” “Hajui lolote, wasiwasi wako tu.” “Mmh! Nilishtuka sikutegemea kumkuta.” “Tuachane na hayo mzigo wangu upo wapi?” Kilole aliuliza. Jimmy alimpa bahasha ya picha, baada ya kuipokea aliichukua na kwenda nayo chumbani. Hakutaka kuzipitia alichukua kiasi cha fedha alizobakia kwenye deni lao, alipofika sebuleni alipa fedha yake na kumwambia: “Nina imani kila kitu kimekwenda vizuri?” “Nashukuru.” “Jimmy kama kuna kitu chochote nitakueleza.” “Hakuna tatizo.” “Naomba siri hii usimwambie yeyote ikivuja nitajua ni wewe, kwa hiyo usinilaumu kwa lolote litakalokukuta.” “Kwangu shaka ondoa, hakuna kitu kama hicho.” “Nakuhakikishia baada ya muda tegemea zawadi kubwa.“ “Nitashukuru sister.” “Basi baadaye.” Jimmy aliagana na Kilole na kuondoka zake, baada ya kuondoka Kilole alitoka nje na kuwakuta Kinape na Happy wakiwa katika mazungumzo ya kawaida. “Vipi jamani?” “Yamekwisha,” alisema Kinape. “Basi niwaache mimi nipo ndani.” “Hakuna tatizo.” Kilole alirudi ndani na kuingia chumbani kuangalia picha alizoletewa na Jimmy. Baada ya kufungua bahasha alichukua alitoa picha zote na kuzimwaga kitandani na kuanza kupitia picha moja baada ya nyingine. Zilikuwa picha za aibu ambazo hazikuonesha uhalisia wa watu wawili waliokuwa wanafanya mapenzi kwa ushirikiano. Picha zile zingekuwa kwa upande wa pili kwa ajili ya kumdhalilisha zingekuwa nzuri sana. Lakini kama mtego wa kuonesha wanafanya mapenzi alikuwa amefeli. Alijiuliza kama Kinape angegoma kufanya naye mapenzi, picha zile zisingeweza kumshtua kwani ilionesha wazi hakukuwa na ushirikiano wowote wa Kinape kwake. Moyoni alishukuru mkwala wake uliweza kumlainisha lakini kama angetegemea picha zile zisingemsaidia. Alijikuta akipandwa na hasira na kuamua kuzichana zote kisha aliziweka kwenye chombo na kuzichoma moto. Baada ya kuzichoma moto aliamini pamoja na kumtega na kuweza kufanya naye mapenzi bado hawezi kumdhibiti Kinape kwa vile ana uwezo wa kukataa na asimfanye lolote. Wazo lingine lililomjia ni kufanya naye tena mapenzi huku Jimmy akipiga picha wote wakiwa na akili timamu. Aliamini kwa mpango ule ataweza kumdhibiti Kinape pia hata kuweza kuvunja penzi lake na Happy ambalo kila kukicha lilimnyima raha. Alijikuta akijilaumu kwa kupanga mpango mbovu, lakini kwa upande mwingine ulisaidia kuweza kumvuta karibu Kinape mpenzi wake wa zamani. Alitoka nje na kuwakuta Kinape na Happy sebuleni wakizungumza, walipomuona waliacha kuzungumza na kumwangalia. Uso wa Kilole ulionesha kuna kitu kimemsibu. Kinape alijua ni kutokana na Happy kuwa pale. “Dada vipi, bado unamkumbuka shemeji?” “Aah, wapi mbona nimeishazoea.” “Shemu vipi?” Kinape aliuliza. “Nikuone mara moja.” “Hakuna tatizo,” Kinape alijibu huku akinyanyuka. Kilole na Kinape walisogea pembeni, Kinape alijua lazima atagombezwa kuhusu Happy. “Kinape, kwanza samahani kwa kukukatisha kazungumzo na mpenzio.” “Bila samahani.” “Nina ombi moja, leo naomba tulale pamoja, kesho endelea na mpenzi wako.” “Hakuna tatizo.” “Basi endeleeni ma mazungumzo yenu.” Kinape alishangazwa na ustaarabu alioonesha Kilole, lakini moyoni alipanga Deus akirudi lazima aondoke. ****** Kilole alifurahia kukubaliwa ombi lake bila masharti yoyote, alimpigia simu Jimmy kumjulisha kazi nyingine ya usiku ule. “Jimmy.” “Ooh! Sister lete mpya.” ”Ile kazi haikuwa nzuri nataka leo tuirudie.” “Kwa malipo yaleyale?” “Hapana, nitakupa laki na nusu.” “Poa, nije saa ngapi?” “Saa mbili usiku, ila ukifika usiingine ndani nipigie simu, ooh! Nimekumbuka hebu njoo mara moja,” Kilole alikumbuka kazi ile ilitakiwa ifanyiwe maandalizi ili isije kwenda kinyume kutokana na muda wa kurudi mumewe kuwa umekaribia. Wakati huo Kinape na Happy walikuwa wameondoka na kuahidi kurudi jioni. Baada ya muda Jimmy alifika, alimzungusha kwa nyuma sehemu ya dirishani ili kuandaa maandalizi ya kupiga picha za ndani. Baada ya kuandaa eneo vizuri waliagana na kukubaliana kukutana muda huo. Majira ya saa mbili usiku Kinape alikuwa nyumbani, baada ya chakula cha usiku walikwenda chumbani kulala. Kama kawaida Jimmy alikuwa amekwishafika eneo la tukio. Baada ya kupewa taarifa ya kuacha kwa mchezo mchafu, alisogea dirishani na kuchungulia ndani. Ili kupata uhakika kama Jimmy amefika alinyanyuka na kwenda dirishani kama anataka kusogeza pazia, alipoangalia nje alimuona. Alilidhika na kurudi kitandani kuendelea na zoezi lake. Naye Jimmy kama alivyoelekezwa alipiga picha kutokana na jinsi Kilole alivyokuwa akifanya bila Kinape kujua. Japo alikuwa kwenye wakati mgumu huku akijawa na mawazo mtu na shemeji yake kufanya mapenzi. Hakutaka kujua sana, lakini katika siku iliyokuwa ngumu kwake ilikuwa ile. Mpaka wanamaliza Jimmy alikuwa hoi na kujichafua kutokana na kwenda na muvu ya mchezo. Baada ya kumaliza mpango wake Kilole alimtanguliza Kinape bafuni na yeye kutoka nje kuonana na Jimmy. “Vipi umefanikiwa?” Kilole alimuuliza Jimmy baada ya kumuona. “Ndiyo.” “Hebu nione.” Jimmy alimuonesha picha alizopiga katika hatua zote, zilikuwa picha nzuri sana ambazo aliamini kama Jimmy akiziona hawezi kuruka. “Jimmy kazi nzuri.” “Lakini umenipa mateso makubwa.” “Pole nitakuongezea elfu hamsini kwa hiyo itakuwa lakini mbili. Shika laki mbili zingine kesho.” “Hakuna tatizo, kuna lingine?” “Hakuna.” “Basi kesho.” Waliagana kwa Kilole kurudi ndani huku moyo wake ukiwa na furaha, alijikuta akiingia chumbani huku akitabasamu. “Vipi mbona una furaha?” Kinape alimuuliza. “Leo umekumbusha mbali sana.” “Umekumbuka nini?” “Penzi letu lilivyokuwa tamu adhimu, hakika leo nitalala usingizi mtamu.” “Lakini kumbuka kitendo hiki ni sawa na kukata tawi tulilo kalia.” “Hii ni siri yetu.” “Hakuna siri katika mapenzi.” “Basi kwetu itakuwa siri.” “Nimefanya tu lakini si kwa moyo wangu.” “Kinape mbona unataka kutia mchanga kwenye chakula kitamu, kwa vile tumeamua kula nguruwe basi tumchague aliyenona.” “Kumbuka mwenyewe muda si mrefu atakuwa hapa.” “Tutakuwa kama hatujuani, ila siku tukipata nafasi kama kawaida.” Waliendelea kula raha zao mpaka siku ya pili, huku moyoni Kilole akiapa akifanikiwa kuzipata picha zile lazima Kinape arudi mikononi mwake na kuvunja uchumba wake Happy. ***** Jimmy baada ya kufika kwake alijikuta akizidi kuwa na maswali mazito juu ya kitendo cha Kilole na Kinape kumhujumu Deus. Lakini bado alikuwa wazo lake la kuhakikisha kupitia picha zake anampata kimapenzi. Aliamini kama angekuwa na kamera ya kuchukua video basi angepata mkanda ambao angeweza kuuza kwa fedha nyingi siku za mbele. Pia aliona kupitia picha zile angepata faida mara mbili, hakuwa na haja ya kuzichambua kwa vile alizipiga katika ustadi mkubwa. Aliweka kamera yake kwenye kabati na kutoka nje kwenda kutafuta mwanamke wa kulala naye kwani alikuwa kwenye hali ngumu. Jimmy aliposhtuka siku ya pili alijikuta peke yake kitandani, mwanamke aliyelala naye hakuwepo. Hakujishughulisha naye baada ya kuoga aliwahi kusafisha picha, alimkuta Beka na kumweleza amsafishie mara mbili kama kawaida. Baada ya kusafishiwa alizichukua na kuzipeleka nyumbani, alipofika alishangaa kukuta sehemu alipoweka picha alizompiga Kilole mara ya kwanza hazipo. Kilichomshangaza ufunguo wa chumba chake alikuwanao mwenyewe. Alijikuta akishtuka na kujiuliza nani aliyechukua. Alikumbuka changudoa aliyelala naye na kuondoka akiwa amelala ndiye aliyechukua zile picha, alijiuliza amezichukua ili iweje. Wasiwasi wake mkubwa ulikuwa kama zikivunja lazima Kilole atamuona hana manaa hata kumfanyia kitu kibaya. Alipanga usiku akamtafute ili amrudishie picha zake, alichukua picha alizosafisha na kumpelekea Kilole.
Kama alivyoelekezwa akitaka kupeleka picha alitakiwa amjulishe kwa simu ili azifuate mwenyewe kuliko kuingia ndani, kuondoa wasiwasi kwa Kinape. Jimmy alipofika alimpiga simu Kilole aliyekuwa amekaa sebuleni na Kinape wakitazama runinga. Kilole baada ya kuona namba ya Jimmy aliikata simu na kuelekea chumbani bila Kinape kujua kinachoendelea. Alipofika chumbani alimpigia na kumuuliza: “Vipi Jimmy?” “Nimekwishafika.” “Poa nakuja.” Kilole alichukua upande wa kanga na kujitanda ili akirudi asionekane amebeba kitu, alipofika sebuleni Kinape alimuuliza: “Vipi shemu?” “Natoka kidogo.” “Wapi tena?” “Nafika dukani.” “Vipi utachelewa? Maana Happy kanipigia simu nimfuate ili nimpeleke hospitali hajisikii vizuri.” “Sichelewi nisubiri, nafika dukani mara moja.” “Hakuna tatizo.” Kilole alitoka nje na kwenda alipokuwa Jimmy, alipofika Jimmy alijitoa sehemu alipokuwa amesimama. “Vipi tayari?” “Tayari.” “Poa.” Kilole alichukua bahasha na kumpa fedha iliyobakia huku akiendelea kumsisitiza: “Jimmy nimekuamini kukupa kazi ya hatari, kama ukivujisha ishu hii ujue sitaona hatari kunyongwa kwa ajili yako. Nimekupa malipo mazuri ili kuhakikisha ufanyi uzembe wowote, au kuna kitu kimekwenda kinyume na mpango wetu?” “Hapana.” Jimmy alijibu akiwa na wasiwasi wa picha zilizopotea katika mazingira ya kutatanisha. Akiwa katikati ya mawazo Kilole alimshtua: “Vipi mbona kama kauli yangu imekushtua?” “Ha..ha..pana,” Jimmy alibabaika. “Jimmy usiwe umefanya makosa tusije tukalaumiana, japo unaniona mwanamke kwenye hili nitakuwa zaidi ya mwanaume,” Kilole alizidi kusisitiza. “Kilole mbona unanitisha kama uliona siwezi au huniamini kwa nini ulinipa kazi hii?” “Si kwamba nakutisha maelezo yangu naona kama yamekubadili muonekano wako.” “Wasiwasi wako tu, lakini nipo makini kuliko unavyofikiria.” “Mmh! Sawa lakini zingatia hilo picha zote kwenye kamera umefuta?” “Ndiyo.” “Hebu nipe kamera nione.” Jimmy alimpa kamera na kuangalia picha zilizokuwa zimebaki kwenye kamera hakuona picha ya tukio hata moja. “Jimmy nakuamini najua huwezi kuniangusha.” “Usihofu.” Waliagana ili kumpumbaza Kinape alikwenda hadi dukani na kununua vitu vya kutafuna na kurudi navyo ndani. Alipofika sebuleni alimtupia bazoka Kinape na kumweleza: “Unaweza kwenda lakini usichelewe.” “Hakuna tatizo.” Kinape alijibu huku akinyanyuka kujiandaa kwenda kwa mpenzi wake Happy bila kujua Kilole alimtoa kijanja ili apate nafasi ya kuangalia picha zake na kujipanga kumrudisha Kinape mikononi kwake na kuvunja penzi lao. Baada ya kuingia chumbani hakujiamini alijifungia kwa ndani na kuanza kupitia picha moja baada ya nyingine. Zilikuwa picha alizozitalajia zenye kuonesha penzi la ushirikiano, picha zile zilimfanya atabasamu na kujikuta akiruka juu na kujitupa kitandani kuonesha alichokitaka ndicho kilichofanyika. Alijisemea kwa sauti ya chini: “Kinape kwisha habari yake.” Aliziweka picha vizuri na kiendelea na shughuli zake moyoni akiwa na furaha tele. **** Baada ya kumaliza semina ya kikazi Deus alirudi nyumbani Tanzania, uwanja wa ndege alipokewa na mkewe Kilole na mwanaye mpenzi Gift. Pia alikuwepo rafiki yake kipenzi Kinape na mpenzi wake Happy. Baada ya kufika Kilole alijitupa kifuani kwa mume wake kuonesha kweli alikuwa amekosa mahaba yake. “Jamani mume wangu baba Gift, karibu sana nyumbani, yaani siamini macho yangu,” alijiliza machozi ya uongo. “Mke wangu mbona hata wiki haikufika?” “Basi hunipendi mume wangu, yaani nilivyoteseka unasema hivyo.” “Basi mke wangu, mengine tutakwenda kuzungumzia nyumbani.” Jinsi alivyokuwa akideka kwa mumewe Kinape alichekea moyoni na kuona jinsi mwanamke alivyo nyoka kwa kumdanganya mumewe anampenda kumbe anamla kisogo. “Mmh! Kinape za siku mbili tatu?” “Nzuri tu best, za huko?” “Eeh bwana nzuri tu, nimefurahi kuwakuta wote wazima, hii imenipa faraja kuwa wewe si rafiki bali ni ndugu wa damu kwa kuweza kuitunza familia yangu kipindi chote nilipokuwa mbali nayo.” “Ni wajibu wangu kuilinda familia yako,” Kinape alisema huku moyoni ukiumia kwa kitendo cha kutembea na Kilole. “Shemu vipi?” Alimgeukia Happy mpenzi wa Kinape. “Safi, pole na safari shemu.” “Asante, nina imani baada ya kurudi nitafanya kila niwezavyo kuhakikisha mnafunga ndoa.” “Nitashukuru shemeji maana ndugu yako amekuwa mzito.” “Best, umekwisha kwenda kumtambulisha shemu nyumbani?” Deus alimuuliza Kinape. “Nilisubiri urudi baada ya kufika nina imani ni muda muafaka sasa kwenda kumtambulisha mpenzi wangu nyumbani.” Kauli ile ilikuwa kichefuchefu moyoni mwa Kilole na kujisemea kimoyomoyo: “Tutaona mimi na huyu mjinga mwenzenu nani zaidi.” Moyoni aliapa kulivunja penzi la Kinape na Happy kwa msaada wa zile picha. ******** Baada ya Deus kurudi, kutokana na makubaliano kati ya Kinape na Kilole heshima ilirudi na kuitana mtu na shemeji yake. Pamoja na makubaliano hayo Kilole alitamani siku moja moja amtoroke mumewe na kwenda chumba cha Kinape kupata penzi la hamu. Lakini mara zote Kinape alikuwa makini hasa usiku alijifungia kwa ndani na kuwasha muziki kama Kilole atamfuata atasingizia hakusikia. Ilikuwa kama alivyowaza usiku mmoja Kilole alimuacha mumewe amelala na kwenda kwa Kinape. Lakini kikwazo kilikuwa mlango uliofungwa kwa ndani, alipojaribu kugonga kwa taratibu sauti ya mlango ilimezwa na sauti ya muziki uliokuwa ukilia chumbani. Kilole alikasirika na kujikuta akipandwa na hasira akiwa tayari kutumia turufu ya picha chafu ili kumtisha Kinape na kukubaliana na masharti yake. “Kinape mbona jana ulifunga mlango kwa ndani?” Kilole alimuuliza kwa sauti ya chini baada ya kukutana kwenye korido la msalani. “Lini ulikuta mlango upo wazi na ulikuwa na shida gani?” “Hujui au ndiyo ushanichezea kisha uniache?” “Lakini hii si sehemu ya mazungumzo haya, tulizungumza nini mumeo akirudi?” ”Kuzungumza nini, mbona ulifunga mlango?” “Jamani, si chumbani kwangu?” “Ilianza lini ina maana unaogopa kuibiwa.” “Ni utaratibu wangu wa siku zote.” ”Kwa nini uliwasha muziki?” “Sasa hayo ni maswali gani?” “Najua ulifanya vile ili nikigonga usinisikie.” “Lakini lawama za nini, ulinieleza utakuja nikakufanyia hivyo?” “Basi baadaye..” Kilole alisema baada ya kusikia akiitwa na mumewe. Baada ya kuondoka Kilole kuitikia wito wa mumewe, Kinape alibakia amesimama na kuona aliyoyakataa ndiyo yameanza na siku zote penzi kikohozi huwa halina siri. Aliamini njia ya kujiepusha na tatizo lile ni kuhama kisha kufanya mpango wa haraka kukaa na Happy. Alipanga siku ile ile azungumze na Deus kwenda kujitambulisha nyumbani kwao Happy ili siku inayofuata naye ampeleke kijijini kumtambulisha kwa wazazi wake kabla ya kupanga mipango ya ndoa. Aliamua jambo lile kulifanya kwa siri kuepuka vikwazo vya Kilole. Baada ya kufungua kinywa Kinape na Deus walitoka pamoja, njiani alimweleza dhamira yake ya kwenda kujitambulisha kwa kina Happy siku ile. “Mbona haraka sana?” Deus alimuuliza. “Nilipanga leo niende ila nilisahau kukujulisha, nataka kesho niende na Happy kijijini, isingekuwa vizuri kuanzia kwetu kabla ya mimi kujulikana kwao.” “Hakuna tatizo, ni saa ngapi?” “Saa mbili usiku.” “Hakuna tatizo tutakwenda.” Waliagana kila mmoja aliendelea na shughuli zake, Kinape ilibidi asubuhi ile ile ampigie simu Happy kumjulisha kuwa usiku wana ugeni wa kujitambulisha. Japo ilimshtua kuona imekuwa ghafla, lakini ilikuwa habari njema aliyoisubiri kwa hamu kama tone la maji katika kiu kali. Nafasi ile hakutaka kuipoteza kwa kufanya maandalizi ya kupokea ugeni wa mchumba wake. Maandalizi yalikwenda vizuri na kumsubiri ugeni wa usiku huku Happy akiona ndoto yake ya kuolewa na Kinape imeanza kuwa kweli. ***** Deus kama kawaida yake alikuwa hawezi kufanya jambo lililo kuwa nje na ratiba zake za kila siku bila ya kumtaarifu mkewe. Kwa vile walikubaliana na Kinape wakutanie mjini na kwenda moja kwa moja nyumbani kwa mchumba wake. Aliamua kumjulisha mkewe baada ya kumaliza kazi zake majira ya saa moja na nusu usiku. Ujumbe ule ulimshtua Kilole kitu kilichomshangaza mumewe. “Mbona umeshtuka hivyo?” Deus alimuuliza mkewe. “Nimeshtuka kwa vile jambo hilo mmelifanya kwa siri.” “Kuna siri gani kama nimekupigia simu kukujulisha?” “Mbona hamkuniambia toka asubuhi.” “Hili suala nimeambiwa asubuhi njiani na Kinape wakati nakwenda kazini.” “Mmh! Sawa, nawatakia utambulisho mwema.” “Hayo ndiyo maneno, na kesho wanakwenda kijijini kwa utambulisho wa upande wa pili.” “Atiii?” “Mbona umeshtuka tena?” “Sasa mbona mambo mnafanya mambo kienyeji,” Kilole alikuja juu kwa hasira za kweli huku wivu ikimpanda. “Mke wangu kwani tatizo nini, haya si maandalizi ya awali, mipango ya harusi ikianza wewe utakuwa na majukumu makubwa kuliko unavyodhani.” “Mmh! Haya, basi endeleeni na maandalizi mema.” Baada ya kukata simu Kilole alijikuta moyo ukimuuma kwa kusikia habari zile, Alijiapiza kupitia picha zile lazima atahakikisha Kinape hamuoi Happy, alijikuta akipoteza furaha ya siku nzima na kujuta kupokea simu ya mumewe. Baada ya kukata simu alikwenda chumbani na kurudia kuziangalia picha upya huku akiamini picha zile ndiyo suruhu ya kuangaika kwa Kinape. Alizirudisha kwenye bahasha na kuzificha sehemu yake. Utambulisho wa Kinape ulikwenda vizuri huku familia ya Happy akionesha furaha ya mtoto wao kupata mume. Happy akiwa ndiye mtoto wa kwanza kuchumbiwa, baba yake mzazi aliwaahidi nyumba na gari kama zawadi kwa mtoto wake wa kwanza. Kinape naye aliwaahidi kumpeleka mchumba wake nyumbani kwao siku ya kesho yake. Walipewa baraka zote za familia za wazazi wa Happy kwenda kutambulishwa kijijini kwao.
***** Kilole alijikuta akikosa raha na kumfanya atangetange sebuleni kama kuku anayetaka kutaga, akitoka upande mmoja kwenda mwingine, nyumba aliiona chungu. Moyoni aliendelea kujiapiza juu ya kuhakikisha Kinape hamuoi Happy. Alijikuta amesahau hata kupika chakula cha usiku kwa ajili ya kumfikiria Kinape. Honi ya gari ya mume wake ilimfanya akimbilie ndani na kujilaza kitandani kusingizia anaumwa ili asiulizwe chakula cha usiku. Mume wake aliingia ndani alimkuta amejifunika shuka gubigubi. “Vipi mke wangu?” “Sijisikii vizuri.” “Hali hii imeanza saa ngapi?” “Wakati najiandaa kupika.” “Basi amka twende hospitali.” “Nimemeza dawa kidogo kichwa kimeanza kutulia.” “Kwa maana hiyo hujapika?” “Nipike saa ngapi mume wangu, ungeniona nilivyokuwa ungenikimbiza hospitali.”
“Lakini si umekunywa dawa ya kutuliza kwa nini tusiende hospitali?” “Mume wangu huwezi kuamini kuja kwako kama umenipa dawa, sasa hivi sijambo kabisa.” “Mmh! Basi kama ni hivyo, jiandae baadaye twende tukachukue take a way.” Baada ya kutengeneza uongo wake na kufanikiwa bado moyo wake bado uliendelea ulimuuma kila alipomuwaza Kinape na kibaya zaidi habari za kujitambulisha kwao na Happy alimueleza mbele ya mumewe. “Samahani shemeji.” “Samahani ya nini?” “Sikukueleza mapema kuwa naitakwenda kujitambulisha nyumbani kwao na Happy, pia kesho nakwenda kijijini kumtambulisha mwenzangu.” “Mmh! Safari njema,” (moyoni alijisemea tutaona si muda mrefu jeuri yako itakwisha) *** Siku ya pili Kilole alikuwa na wakati mgumu kufikisha ujumbe kwa Kinape ili kuzuia asiweze kwenda kijijini kumtambulisha mchumba wake. Lakini juhudi zake zilikuwa bure, baada ya kuondoka na katika gari moja na mumewe. Roho ilimuuma sana kwa hila za Kinape za kumkwepa kwa kuondoka na mumewe kwenye gari moja. Alijifikiria kupiga simu kumzuia Kinape na kumweleza ukweli juu ya picha zile, lakini alisita kwa kuhofia mabadiliko yoyote yatakayo tokea kwa Kinape lazima mumewe angemtilia wasiwasi na pengine siri kutoka nje kabla ya kutimiza lengo lake. Aliamua kumsubiri akirudi na kuingia anga zake ndipo amlipue. Kinape bila kujua kuna mpango kabambe wa kuvunja mipango yake ya kumuoa Happy. Utambulisho ulikwenda vizuri, familia ya Kinape kumpokea kwa bashasha mchumba wa mtoto wake huku wakimuahidi kumpa ushirikiano mkubwa kufanikisha ndoa ya mtoto wao. Baada ya utambulisho walirudi mjini kujipanga kwa ajili ya maandalizi ya harusi ambayo Deus alimuahidi Kinape kuyasimamia kwa asilimia mia. Kinape aliutumia muda mwingi kumkwepa Kilole kwa kurudi muda ambao atakuwa amewasiliana na Deus kama yupo nyumbani. Hata walipokutana kwa bahati mbaya hakutaka kuzungumza kwa muda mrefu kwa kisingizio cha Deus yupo. Moyoni Kilole alijiapiza hata kumfuata Kinape ofisini na kumweleza uchafu ule kwa kuugeuza upande wa pili kana kwamba Kinape ndiye aliyefanya mchezo ule. Alipanga kufanya vile kabla mipango ya harusi haijaanza, lakini aliamua kuonesha kama halikumuuma baada ya kutumia nguvu bila mafanikio. Siku moja akiwa anaendelea na kazi zake alishangaa kumuona Kinape akirudi mchana ghafla huku akionekana ana wasiwasi mwingi. “Vipi Kinape mbona leo mchana?” “Kuna vitu nilisahau kuondoka navyo asubuhi, hivyo nimerudi kuvichukua,” alisema huku akielekea chumbani kwake. Kilole alimsindikiza kwa macho huku akijiuliza aitumieje nafasi adimu kama ile, wazo la haraka lilimjia aanza kujiliza ili kuonesha kuna kitu kimempata na Kinape akiuliza basi afumue mzinga wa nyuki. Kinape wakati anatoka alishangaa kumkuta Kilole akilia kilio cha kwikwi. “Shemu vipi?” Alimuuliza huku akimsogelea. “Siamini kama unaweza kunifanya uliyonifanyia, sawa hunitaki kwa nini unataka kunivunjia ndoa yangu?” “Kilole mbona sikuelewi!” Kinape alishangaa kusikia habari zile. “Kinape nimekufanya nini?” “Subiri usiondoke uone unyama ulionifanyia, nikiachika utapata faida gani?” Kilole alisema kwa sauti ya kilio. “Mbona sikuelewi nimekufanyia nini?” Kinape alizidi kushangaa. “Nimekuambia subiri halafu uniambie kama ulichokifanya ni haki.” “Fanya haraka nimeomba ruhusu mara moja nifuate kalatasi hizi.” Kilole alikwenda chumbani na kuchukua picha chafu walizopiga wakifanya mapenzi na kumpelekea Kinape aliyekuwa amesimama wima akimsubiri huku akionesha wasiwasi. Alipofika alimpa baadhi ya picha na zingine kuziacha ndani, Kinape alipokea bahasha ya picha na kuanza kutoa picha moja, alishtuka kuziona picha zilizoonesha wakifanya mapenzi na Kilole. “Ha! Hizi nini?” Kinape alishtuka huku akiendelea kuchambua picha. “Nikuulize wewe, kwa nini umeamua kunidhalilisha kiasi hiki, kumbe ulikuwa na lako jambo, hebu fikiria picha hizi zimfikie mume wangu mimi nitakuwa mgeni wa nani?” Kilole aliangua kilio cha uongo na kuzidi kumchanganya Kinape. “Wewe hizi picha umezitoa wapi?” Kinape aliuliza huku jasho la hofu likimtoka. “Kuna mtu kazileta anasema kaziiba kwa jamaa mmoja ambaye amekula naye njama ili kunidhalilisha,” Kilole alisisitiza kama kweli. “Nioneshe huyo aliyeleta picha hizi aeleze kazitoa kwa nani na huyo mwenye picha aseme kama mimi ndiye nilifanya mpango huu. Haki ya nani, leo ndiyo naziona hizi picha, sijui lolote maskini wa Mungu,” Kinape alizidi kujitetea. “Kinape umebadilika baada ya kunivua nguo, shukurani yako kunidhalilisha, kwa taarifa yako najua kabisa nipo uchi pengine si mmoja aliyeziona kuna wengi. Pia wasiwasi wangu huenda zingine zimebaki na hizi ni baadhi ya hizo picha. “Kwa maana hiyo bora nimweleze ukweli mume wangu na kumuonesha hizi picha nijue moja, anisamehe kwa kumuomba msamaha au aamue atakacho amua kwa vile siwezi kumlilia mtu. Inawezekana kabisa ulifanya makusudi ili niachike baada ya kuona nilikusaliti.” “Kilole sijui nikueleza kitu gani ili unielewe, haki ya nani sijui lolote kuhusiana na hizi picha, pia nakuomba usimuoneshe mumeo wala kumueleza tulivyo hujumu ndoa yake, ni hatari si unajua jamaa ana bastora anaweza kuniua.” “Naweza nisimwambie na kukaa kimya, kumbuka nimetoa laki tano ili nipewe hizi picha, kama zipo zingine wanashindwa nini kumuuzia mume wangu. Akijua uchafu wetu sura zetu tutaziweka wapi?” “Yaani nichechanganyikiwa hata sijui nikwambie nini.” “Kinape hii ni hatari.” “Kweli ni hatari tena kubwa, hivi Deus anavyoniamini nitamwambia nini akiona hizi picha?” “Ndiyo maana nikaona bora nijisalimishe kwa mume wangu sina jinsi, kama picha hizi zikimfikia tumekwisha.” “Mmh! Yaani hata sijui nani kafanya mchazo mchafu kama huu?” “Unajua kila kitu lakini unanizunguka, kwani Kinape hapa jiji wapo wangapi?” “Siwezi kujua labda wapo wengi.” “Ina maana hiyo Kinape pia ni ndugu yake Deus.” “Mmh! Yaani aliyeleta kasema hivyo?” “Tena inasemekana umempa laki tatu, ndio maana kataka laki tano ili anipe picha.” “Yaani, nimechanganyikiwa hata nguvu zimeniisha,” Kinape alisema huku akiketi kwenye kochi baada ya nguvu kumwisha ghafla. “Kinape nilikuwa na maamuzi mawili?” ”Yapi hayo?” “Moja la kujisalimisha kwa mume wangu, la pili kumuwahi Deus kabla picha hazijamfikia.” “Utamuwahi vipi?” ”Ikiwezekana hata kumuua huoni hili likifika kwa wazazi litakuwa baya zaidi.” “Mmh! Tumefika mbali sana huo si mpango mzuri.” Kinape alipinga mpango ule. “Basi kama hatuwezi tumwambie.” “Bado huo si uamuzi sahihi.” “Sasa tufanye nini?” “Tutafute njia nyingine zaidi ya hii.” “Mimi nina siri za mume wangu kama tutazifikisha Takuru lazima atafungwa.” “Sasa wewe utabaki na nani?” “Na wewe.” ”Na Happy?” “Kwa ulichokifanya heri niwe na wewe kwa vile siwezi tena kurudi kijijini.” “Hapana, basi tutafute njia nyingine.” ”Hiyo nyingine nipe wewe.” “Sina.” “Basi wacha ninywe sumu ili ufurahi siwezi kuona nahukumiwa kwa kosa la kwako. ” Kilole alimtishia Kinape. “Usinywe sumu bado tunaweza kujipanga kuhakikisha tunamdhibiti.” “Nakupa siku moja kuhakikisha unapata ufumbuzi bila hivyo nitakacho amua tusilaumiane.” “Lakini naomba usimwambie kwanza Deus,” Kinape alijikuta akichanganyikiwa baada ya kukosa jibu la tatizo lililokuwa mbele yake. “Ni wewe wa kunifanya nisimwambie, nataka kabla habari hizi hazimfikia tuwe tumekwishajua tumefanya nini.” “Nimekuelewa, yaani hata kazini sirudi nguvu zimeniisha,” Kinape alichanganyikiwa. “Kinape wewe mwanaume unatakiwa kuonesha unaweza kukabiliana na chochote kinachotokea mbele yako. Mbona mimi niliyetendewa sijachanganyikiwa zaidi ya kupanga mikakati ya kujiokoa na janga hili.” “Najua huwezi kunielewa sijui lolote kuhusiana na hizi picha, kwa kweli zimenichanganya sana.” “Kwa kusema hivyo ina maana nimezipiga mimi?” “Hapana sina maana hivyo, ila nimechanganyikiwa sijui hata nani aliyefanya mchezo mchafu kama huu.” “Ndiyo tunatakiwa tutafute njia ya kujiepusha, kumbuka hili ni bomu likipasuka hakuna atakayepona.” “Basi inawezekana alipoondoka aliweka mpelelezi ili atufuatilie.” “Atufuatilie kwani anajua chochote kuhusiana na penzi letu la zamani?” “Inawezekana kuna mtu anayetujua alipotuona tupo pamoja alimweleza na kuamua kufanya upalelezi.” “Aweke asiweke lazima tutumie njia ya kumdhibiti kabla hajafanya lolote.” “Sasa tutamdhibiti vipi?” “Kwa nini tusimuwekee sumu afe,” Kilole alisema bila wasiwasi. “Kilole mbona mpango huo ni mbaya!” “Unafikiri tukimchelewesha akigundua lazima atatuua kwa risasi.” “Tukimuua tutakosa fadhira hata Mungu atatulaani, tutafute njia nyingine ya kumdhibiti, ngoja nitoke nikirudi nitakupa jibu ila nakuomba chonde usimueleze Deus chochote kuhusiana na habari hii.” “Siwezi hata mimi natamani kuishi maisha marefu.” Baada ya kukubaliana Kinape aliondoka na kumwacha Kilole akifurahia mpango wake umekwenda kama alivyopanga. Aliamini jioni akirudi cha kwanza kitakuwa kuvunja uchumba wake na Happy kisha mengine yangefuata ya kumdhibiti Deus ili abaki na Kinape.
Deus akiwa ofisini kwake akipitia ripoti ya uchunguzi wa wauzaji sugu wa madawa ya kulevya, simu toka kwa sekretari wake iliita. Alipokea mkono mmoja, mwingine ukiwa bado umeshikilia kwenye kalatasi ya ripoti. “Haloo, ofisi ya kuzuia madaya ya kulevya hapa, nazungumza na nani?” “Msamalia mwema.” “Ndiyo Msamalia mwema, nikusaidie nini?” “Mkuu, ndege ya shirika la Swiss air, inayoingia saa kumi na moja jijini Dar kuna dada mmoja mwenye umbile la kati maji ya kunde nywele za kipilipili, amevalia gauni fupi jekundu chini viatu virefu na kwapani atabeba mkoba wa rangi sawa na nguo zake. ”Pia anaweza kuwa miwani ya rangi hiyo hiyo kama atakuwa ameivaa kama ataivua basi chukueni vigezo nilivyo waeleza. Dada huyu ana dawa za kulevya mkamateni na kumpekua.” “Samahani unazungumza toka wapi?” “Si muhimu kujua zaidi ya kufuatilia taarifa niliyokupa, asante.” “Haloo…haloo…” Deus alichelewa simu ilikuwa imekatwa. Alinyanyuka na kutoka hadi kwa sekretari kuulizia simu inatoka wapi. “Haloo Happy, simu inatoka wapi?” “Namba zinaonesha inatoka Itary.” “Asante,” Deus alijibu na kurudi ofisini kwake. Alijikuta akijiuliza aliyetuma taarifa na kujiita msamalia mwema alichokisema kina ukweli au ndiyo kutaka kuwasumbua. Lakini hakutaka kuipuuza taarifa ile, aliwaita vijana wake na kuwapa habari zile na kuwaeleza wafuatilie ndege ile kama kweli yupo huyo mwanamke basi akamatwe na kupekuliwa. Kwa vile ilikuwa imebakia saa moja kabla ya ndege kuingia, aliwahimiza vijana wake kufika eneo husika kabla ndege haijafika. Baada ya kuwapa majukumu vijana wake aliendelea kupitia ripoti ya wauza dawa za kulevya sugu. ***** Majira ya saa kumi ndege ya shirika la ndege la Swiss air iliwasiri uwanja wa ndege wa mwalimu JK Nyerere. Vijana wa Deus alikuwa katika kona yao kama kawaida. Baada ya ndege kusimama na mlango kufunguliwa waliteremka abiria mmoja mmoja waliokuwa katika mistari. Dada mmoja maji ya kunde mwenye nywele fupi gauni jekundu fupi lililoishia juu kidogo ya magoti na viatu virefu alikuwa mmoja ya abiria katika ile ndege. Baada ya kutoka kwenye mlango wa ndege hakuteremka haraka aliangalia mandhali ya Tanzania kisha alivaa miwani yake nyekundu na kuteremka taratibu kwenye ngazi za ndege na kuelekea kwenye ukaguzi. Vijana wa Deus hawakupata shida ya kumuona yule binti aliyeonekana mrembo tena bado mbichi. Walitegemea kusikia chochote kutoka sehemu aliyopitia, lakini alipita salama. Hawakuwa na haraka ya kumkamata walisubiri kuona yupo na nani pia mizigo yake. Baada ya kutoka chumba cha usafiri alielekea kwenye gari aina ya Ranger Rover ‘Vogue’ ya rangi nyeusi iliyokuwa umepaki pembeni. Alipokaribia mlango ulifunguliwa, kabla hajaingia kikosi cha kuzuia dawa za kulevya kilifika na kujitambulisha kisha walimweka chini ya ulinzi msichana yule ambaye hakuonesha wasiwasi. “Jamani vipi?” aliuliza huku akitoa miwani usoni. “Sisi ni askari wa kikosi cha kuzuia dawa za kulevya, tuna wasiwasi na wewe.” “Mna wasiwasi gani?” “Tunaomba ufike kituoni kwa ajili ya upekuzi.” “Mbona mnanishangaza, ina maana wakaguzi wa kiwanjani hawafai?” Aliuliza kwa kuwashangaa askari wale. “Samahani tunaomba ufuate maelekezo yetu.” Wakati huo gari lao lilisimama pembeni yao na kumuomba aingine ndani ya gari. Kabla ya kuondoka yule msichana aliwaomba vitu vyake vitangulie nyumbani. “Jamani vitu vyangu si hivi ngoja nivifungue hapahapa ili muone nimeweka wapi hayo madawa ya kulevya,” Alisema yule msichana huku akifungua pochi yake na kuvimwaga vyote vilivyokuwa ndani ya pochi kisha alitaka kufungua brif case ili vitu vilivyomo ndani avimwage chini waone kuna nini. Lakini walimkataza asifanye vile kwa vile kuna sehemu zake. “Dada kwani tatizo lako nini, wewe twende ofisini, sisi tumetumwa tukukamate mengine anajua mkuu wetu, ingekuwa hatukutumwa wala tusingekusumbua,” askari mmoja alisema. “Lakini kumbukeni nimechoka natakiwa kupumzika.” “Tunajua, lakini sisi tumetumwa, hatuwezi kurudi mikono mitupu wakati mtu tuliyetumwa tumemuona.” “Nani anayenifahamu na kuwatuma mje mnikamate, kumbukeni nitashitaki kwa kunidhalilisha,” binti yule alitishia. “Hatujakudhalilisha kwa vile hakuna mtu anayejua kinachoendelea hapa, zaidi ya wewe kumwaga vitu vyako bila kukuambia.” “Basi turudini chumba cha ukaguzi uwanja wa ndege ili mnikague, ili niwahi nyumbani kuna mtu nimeahidiana kukutana naye.” “Dada kuwa mwelewa, si wewe umevaa gauni jekundu?” Askari mmoja alimuuliza akisoma karatasi bila kumtazama. “Ndiyo.” “Pochi yako nyekundu?” “Ndiyo.” “Miwani nyekundu?” “Ndiyo,” “Na viatu vyako virefu?” “Ndiyo.” “Nywele zako za kipilipili?” “Ndiyo.” “Rangi maji ya kunde?” “Ndiyo.” “Sasa dada haya tumeyajulia wapi sisi?” “Hata mimi nashangaa sijui nani anataka kunichafua?” “Ungekuwa na tofauti na hii iliyoandikwa kwenye karatasi tusinge kugusa lakini kila kilichoandikwa kwenye karatasi unacho kwa asilimia mia,” walimweleza huku akimpa karatasi iliyokuwa na maelezo yote. Askari walikuwa na uhakika kwa pale hakukuwa na ushahidi wowote kuwa yule dada kaingia na dawa za kulevya. Hata kama ilikuwa biashara yake siku ile walikuwa wamechemsha. “Mmh! Sina jinsi twendeni lakini mnanipotezea muda bure,” alijitetea yule msichana aliyeonekana kujiamini katika mazungumzo yake. Kama isingekuwa amri toka kwa mkubwa, waliona hakuna haja ya kumpoteza muda wake bure wangemuachia. Lakini vigezo vyote walivyoelezwa na mkuu wao Mr Deus ndivyo alivyokuwa navyo kwa asilimia mia. Hivyo hawakuwa na budi kumpeleka kwa mkuu wao. Walimuingiza kwenye gari na kumpeleka makao makuu kwa ajili ya upekuzi. Kabla ya kuondoka aliomba mkoba wake ambao hauna kitu utangulie nyumbani. “Sasa kaka zangu kwa vile mkoba wangu hauna kitu naomba basi utangulie nyumbani.” “Dada yetu haturuhusiwi kupoteza ushahidi wowote uliokuja nao, vyote vinatakiwa ili kukamilisha ushahidi.” “Hakuna tatizo,” alijibu kwa kujiamini kitu kilichowafanya askari waamini hana kosa. “Sasa Teddy itabidi nikufuate?” Dereva wa Ranger Rover alimuuliza mgeni wake. “Noo Danny, tangulia nyumbani nitakuja sasa hivi kwa vile nakwenda kukamilisha walichotumwa na mkuu wao. Lakini kwa upande wangu sina tatizo lolote.” Maneno ya kujiamini ya msichana yule yalikuwa na nguvu kubwa ya askari kumuachia lakini kwa vile walikuwa wakitimiza agizo la mkubwa wao hawakuwa na budi kumpeleka. Walimuingiza kwenye gari na kumpeleka makao makuu kwa ajili ya kutimiza wajibu wa kazi. Walipofika walimpitisha chumba cha upekezi na kufanya upekuzi wote wa awali ambao haukuonesha dawa za kulevya. Taarifa alipelekewa mkuu wao Mr Deus. “Mkuu hana kitu chochote.” “Mmempekuwa vizuri?” “Ndiyo mkuu.” “Mmetumia vifaa vya kisasa?” “Vyote mkuu.” “Mmempa chakula kigumu?” “Kila kitu ujuacho tumekifanya lakini hatukumkuta na dawa.” “Sasa aliyenipigia simu alikuwa na maana gani?” “Kwani taarifa zimetoka wapi?” “Kwa msamalia mwema mmoja toka Itaria.” “Ni kweli dada huyu anatoka Itaria.” “Ina maana alikuwa anatudanganya?” “Mkuu, huenda kweli anashughulika na biashara hii, lakini huenda njia aliyotumia si ile ambayo mtu aliyetutumia taarifa anaijua.” “Inawezekana.” “Lakini mmemuonaje?” “Kwa kweli haoneshi wasiwasi zaidi ya kulalamikia muda wake.” “Sasa fanyeni hivi mfuatilie mpaka atakapofikia fanyeni dolia usiku kucha ili tupate kujua kama kasingiziwa au ndiyo kazi yake.” “Tutafanya hivyo mkuu.” “Basi kamwachieni aende.” Kabla kijana wake hajaondoka alikumbuka kitu kimoja na kumwita. “John hebu rudi kwanza.” “Ndiyo mkuu.” “Hebu mleteni hapa kabla ya kuwachia kuna maswali mawili matatu nataka kumuuliza.” “Hakuna tatizo mkuu.” John alitoka baada ya muda alirudi na yule msichana aliyekuwa mrembo kwenye macho ya mwanaume. “Shikamoo,” yule msichana alimsalimia Mr Deus. “Marahaba, hujambo?” ”Sijambo mkuu.” “Karibu ukae,” alimwambia huku akimuonesha sehemu ya kukaa. “Asante,” Alijibu huku akikaa kwenye kiti. Baada ya ukimya mfupi Mr Deus alituliza macho kwa binti yule ambaye alikuwa ameinama chini. “Unaitwa nani?” “Thereza Mayunga.” “Ni Mtanzania?” “Ni Mtanzania mwenye uraia wa Itaria.” “Naomba Paspoti yako.” Teddy alifungua mkoba wake na kutoa paspoti na kumkabidhi Mr Deus, aliipokea na kuisoma kwa muda kisha alimrudishia. “Okay, Wazazi wako wapo wapi?” “Kwa kweli siwajui, ila niliambiwa niliibiwa nikiwa na umri wa miaka mitano na mwanamke mmoja aliyekuwa akikaa Itaria ambaye alinifanya mwanaye mpaka alipokaribia kufa ndipo aliponieleza kuwa wazazi wangu wapo Tanzania ila hakujua wapo wapi. Pamoja na kuniiba bado jina langu na la baba yangu hakulibadilisha.” “Una shughulika na nini?” “Ni mfanya biashara wa vitu mchanganyiko.” “Hapa Dar unafikia wapi na kwa nani?” “Nafikia Masaki kwa ndugu wa marehemu mume wangu.” “Mumeo alikuwa Mtanzania?” “Ndiyo.” “Okay, unaweza kwe…” Mr Deus kauli yake ilikatwa na mlio wa simu ulioingia kwenye simu yake. “Samahani,” alisema huku akipokea simu. “Bila samahani,” alijibu Teddy. Mr Deus alipokea simu na kuzungumza kwa sauti ya chini. “Eeh.” “Mkuu simu ile ya Italia.” “Okay, nipe nizungumze naye.” “Haloo.” “Haloo mkuu.” “Ndiyo.” “Mmemuona?” “Hebu subiri kidogo,” Mr Deus alisema huku akimuomba yule msichana amsubiri nje mara moja. “Hakuna tatizo,” alijibu yule binti huku akinyanyuka na kutoka nje. Baada ya kutoka Mr Deus alirudi hewani. “Ehe! Msamalia mwema.” “Nauliza mmemuona?” “Ndiyo.” ”Mmepata hayo madawa?” “Hatujayapata.” “Nilijua hamuwezi kupata kitu.” “Sasa kama ulijua hatupati kitu kwa nini umetusumbua?”Mr Deusi aliuliza kwa sauti hya ukali kidogo. “Siyo kuwasumbua, niligundua nilifanya kosa katika maelezo ya kuyapata hayo madawa, ndiyo maana nimepiga tena simu haraka.” “Kwa hiyo tutakuwa basi tumechemsha.” “Bado hamjachemsha.” “Tusaidie jinsi ya kuyapata.” “Mkoba wake mwekundu anao?” “Ndiyo.”
“Basi huo ndio wenye dawa hizo.” “Mbona tumempekua hatujaona kitu?” “Huyo dada ni muuzaji wa kimataifa wa dawa za kulevya, hata siku moja hamuwezi kumkamata kirahisi.” “Tusaidie basi tujue ameficha wapi?” “Huo mkoba wake umeshonwa maalumu kwa ajili ya kuvusha dawa za kulevya, una karatasi za lailoni ambazo haziwezi kuruhusu vipimo vyenu kuona ndani kuna kitu gani. Juu kuna manyoya hufanya mkoba huo mtu yeyote asiutilie wasiwasi. Kwa mtindo huo, umemfanya mwanamke huyu aendeleze biashara yake haramu ya dawa za kulevya bila kushikwa.” “Kwa hiyo una maanisha mkoba alishonwa na dawa zake kabisa?” “Ndiyo maana nikasema huyo dada ni muuzaji wa kimataifa, huzunguka sehemu zote bila kukamatwa na kumfanya aweze kujikusanyia fedha nyingi kila kukicha.” “Una uhakika na unachokisema?” “Kwa nini nimewapa picha jinsi alivyo na mmempata bila tatizo, kuna kitu nilichowaeleza akakataa?” “Mpaka sasa upo sahihi.” “Basi pasueni mkoba wake mtanipa jibu, asante.” Baada ya kusema vile alikata simu. Baada ya simu kukatwa, Deus alitumia dakika tano kutafakari maneno ya mtu aliyejiita msamalia mwema ili kutoa uamuzi ambayo kama utakwenda kinyume unaweza kumuhalibia sifa. Aliamuru yule mwanamke aingie, aliitwa na kuingia ndani na kukaa kwenye kiti. “Samahani,” alianza Mr Deus kumtaka radhi Teddy. “Bila samahani mkuu.” “Naomba uniambie ukweli kuhusu sehemu ulipoficha dawa za kulevya.” “Nimeeleza kila kitu, sasa mnataka nini? Sijui lolote juu ya dawa za kulevya nashangaa kunihusisha na biashara hatari kama hizo.” “Naomba nifanye upekuzi kwenye mkoba wako.” “Huu hapa angalia,” Teddy alisema huku akiuweka mkoba wake juu ya meza. “Kabla sijaupasua naomba uniambie ukweli juu ya kuficha dawa za kulevya.” “Mkoba si huo hapo fanyeni muwezavyo utajua ukweli kuwa sihusiki japo kuwa watu wananipaka matope,” Teddy alisema kwa kujiamini. Mr Deus aliagiza kisu ili aupasue mkoba mbele yake, Kabla hajaupasua Teddy alimtaadhalisha. “Kumbuka mkoba huu nimeununua pesa nyingi robo ya bajeti ya wizara moja kubwa katika serikali yako.” “Hiyo siyo juu yako.” “Sema unataka shilingi ngapi ili usiharibu mkoba?” “Sihitaji fedha yoyote zaidi ya kuupasua mkoba huu.” “Haya fanya uwezavyo lakini mwisho wa siku utaumbuka.” Mr Deus hakumsikiliza alichukua kisu na kuanza kuupasua mkoba ili kupata uhakika kwa yale aliyoelekezwa na msamalia mwema. Alipoanza kuupasua mkoba Teddy aliomba asitishe zoezi. “Samahani mkuu.” “Bila samahani,” Deus alijibu akiwa amesitisha zoezi la kuupasua mkoba. “Naomba tuzungumze.” “Tutazungumza nikimaliza, fedha ya robo bajeti ya wizara hata mimi naweza kuilipa peke yangu wala usiwe na wasiwasi,” Mr Deus alijibu huku akinyanyua kisu kukididimiza kwenye mkoba. “Naomba unisikilize kaka yangu,” Teddy alikuwa mpole ghafla. “Juu ya nini?” “Kuhusu huo mkoba.” “Una nini?” “Samahani kaka yangu naomba unisilize mdogo wako.” Mr Deus aliacha kuuchana mkoba na kumgeukia Teddy aliyekuwa akitokwa na jasho japo ofisi ya Mr Deus ilikuwa na kiyoyozi kikali. “Mhu! Unasemaje?” “Najua nimepatikana, lakini naomba msaada wako?” “Umepatikana kivipi na unaomba msaada upi?” “ Kila ulichoelezwa ni kweli?” “Na nani?” “Simjui, lakini inaonekana ananijua vizuri, sasa nifae kwa mvua nitakufaa kwa jua.” “Sijakuelewa,” Mr Deus alimshangaa Teddy. “Ni kweli mfuko huu una dawa na kwa sasa nipo chini ya ulinzi na ukinifisha mahakamani nitafia gerezani, umri wangu bado mdogo. Nakuomba uniokoe kwa hili nipo radhi kukupa kiasi chochote ukitakacho hata ukiacha kazi unaweza kula miaka hamsini bila tatizo.” “Lakini unajua dawa za kulevya ni haramu?” “Najua, na ndiyo maana nipo chini ya ulinzi.” “Sasa nikiwasikiliza wote tutamkamata nani?” “Yaweza usione umuhimu wangu kwako leo, lakini kwangu mimi wewe ni mtu muhimu kama malaika mtoa roho aliyeahilisha kuchukua roho mama mzazi muda mfupi baada ya kujifungua.” “Kwa ubinaadamu ni kweli nilitakiwa kukusaidia, lakini kwa vile ni dhamana niliyopewa na taifa sina budi kuwa na uso wa mbuzi.” “Si kwamba nakulazimisha au nakufundisha kazi, hata hao wakubwa zako waliokutuma wanapokea mrungula. Amini usiamini kuna viongozi katika serikali yako hata viongozi wa dini mwenye heshima katika taifa hili wanaifanya biashara hii. Unaweza kunikamata na nikafungwa, lakini bado utakuwa umechota kikombe cha maji kwenye bahari hutapunguza kitu. “Nina imani msaada wako leo unaweza kukusaidia siku za mbele, mbegu ya wema siku zote haiozi. Naomba unisaidie kwa leo nina imani nitakapotoka huwezi kujilaumu kwa msaada wako. Sema kiasi chochote ukitakacho hata kikipita fedha za mzigo huu nipo tayari kukupa tena muda huu.” Kauli ile ilimfanya Deus alitulie kwa muda huku akiona sura ya yule binti ilivyoonesha kuomba msaada wake. Kila alilolizungumza alililona lina uzito kwake. Taratibu moyo ulilainika na kuona kuna umuhimu wa kumsikiliza yule msichana. “Unajua binti unanipa wakati mgumu,” Deus alisema kwa sauti ya chini. “Kivipi kaka yangu?” “Unajua vijana wangu wakiona nakuachia wakati mimi ndiye kiongozi wao watanielewaje?” “Sikiliza mkuu hakuna hata mmoja anayejua huku ndani kipi kinaendelea, wengi wanajua ni mazungumzo ya kawaida.” “Mmh! Sasa kwa kesi nzito kama hii unanipa kiasi gani?” “Chochote ukitakacho utakachokiona kinalingana na kosa hili.” “Kwa vile wewe ndiye uliyetangaza biashara kusema ili nione kama kinalingana na kosa lenyewe.” “Lakini huu mzigo si utaniachia?” “Itategemea na kiasi cha mzigo utakaotangaza.” “Milioni 50.” “Hailingani na kosa lako, kumbuka hapa nauza kazi naweza hata kufungwa maisha ikigundulika.” “75.” “Okay, nisikuumize sana nipe hizohizo.” “Na mzigo wangu?” “Utaondoka nao, nitapataje mzigo wangu?” “Kama una kijana wako nimuagize aende sasa hivi akachukue mzigo mimi nikiwa hapa akipata utaniruhusu niondoke.” “Itakuwaje?” “Nampigia simu mtu ukisikia kisha unanipa mtu wako nimuelekeze akachukue.” “Okay, fanya hivyo.” Teddy alichukua simu yake iliyokuwa mezani na kubofya namba kisha alisema: “Haloo Tonny.” “Eeh, Teddy.” “Andaa milioni 75 kuna mtu atakuja muda si mrefu.” “Hakuna tatizo, nitamtambuaje?” “Nitakujulisha.” Teddy alikata simu na kumgeukia Mr Deus aliyekuwa akishangazwa na uwezo wa kifedha aliokuwa nao binti yule. Alikubaliana na kauli ya mtu aliyejiita msamalia mwema kuwa binti yule ni mfanya biashara mzoefu pia mwenye utajiri mkubwa. “Basi mjulishe huyu mtu wako ili nimwelekeze akachukue mzigo.” “Hakuna tatizo ngoja nimpigie ili nikupe umuelekeze,” Deus alisema huku akichukua simu na kumpigia rafiki yake Kinape afuatilie dili lile. “Haloo Kinape upo wapi?” “Ndiyo natoka kazini.” “Hebu zungumza na dada huyu akuelekeze sehemu akakupe mzigo wangu.” “Hakuna tatizo,” Deus alimpa simu Teddy ambaye alimuelekeza sehemu ya kukutana ampe mzigo huo. Baada ya maelekezo Teddy alimgeukia Deus na kumuuliza. “Nina imani utaamini kwamba mimi si mtu wa kubabaisha.” “Mpaka tutakapo maliza kazi.” Mr Deus alinyanyua simu na kumwita secretary wake, baada ya muda alifika na kukakamaa kikakamavu mbele ya mkuu wake. “Abee bosi.” “Mletee mgeni kinywaji.” “Sawa mkuu.” Aligeuka na kuondoka, baada ya muda alirudi na sahani iliyokuwa juisi ya paketi na glasi mbili. Aliweka juu ya meza na kuwawekea wote kisha aliwakaribisha. “Karibuni Juisi dada.” “Asante,” alijibu Teddy huku akichukua glasi ya juisi moyo wake ukiwa umeanza kutulia. “Lete stori,” Deus alivunja ukimya. “Ninalo kaka yangu, nakuahidi si leo si kesho msaada wako hutaujutia.” “Kwa nini mnakaa na fedha nyingi kiasi hicho ndani?” “Kaka yangu kazi yenyewe bila ya kuwa na fedha za haraka unaozea gerezani.” Wakati wa mazungumzo simu iliingia toka kwa secretary, alipokea na kuzugumza. “Simu ya Italia mkuu.” “Niachie.” “Haloo.” “Ndiyo msamalia mwema?” “Vipi mzigo umeuona?” “Kazi umeisha tupa tuachie tuifanye,” Deus alijibu kwa jeuri kidogo. “Mkuu sina maana ya kukufundisha kazi bali kufanikisha kukamatwa kwa huyo malaya.” “Asante kazi inakwenda vizuri.” “Mmeziona?” “Hiyo si kazi yako.” “Sawa mkubwa mara hii nimekuwa adui?” “Siyo adui tunashukuru kwa msaada wako mambo mengine ni siri ya ndani hatakiwi mtu mwingine kujua.” “Nakutakia kazi njema.” “Na wewe pia.” Baada ya kukata simu Teddy aliyekuwa akifuatilia mazungumzo yale alijua mbaya wake bado alikuwa akimuandama kwa kufuatilia mpango wake. “Samahani mkuu.” “Bila samahani.” “Naomba nimjue huyo mtu.” “Hapana ni siri ya jeshi.” “Kaka yangu nipo radhi kukuipa pesa ile mara mbili ili nimjue tu.” “Ukimjua?” “Basi tu nitakaa naye mbali.” “Kwa kweli amekataa kutaja jina lake zaidi ya kujiita msamalia mwema.” “Anatokea wapi?” “Italia.” “Asante kwa msaada wako.” Mara simu iliita, Teddy aliipokea na kusema: “Eeh! Tayari hebu mpe simu nizungumze naye,” Baada ya kupewa alizungumza: “Eeh! Umefika?” “Ndiyo.” “Hebu zungumza na mkuu hapa,” alimpa simu azungumze na Kinape. “Eeh! Kinape umefika?” “Ndiyo.” “Ni yeye,” Deus alimgeukia na kumwambia Teddy. “Nipe simu.” Baada ya kumpa alimwambia mtu wa upande wa pili. “Tonny mpe mzigo mpe ulinzi mpaka atakapozifikisha salama.” “Hakuna tatizo.” Teddy alikata simu na kumgeukia Mr Deus na kumuuliza: “Utazipeleka wapi?” “Nyumbani.” “Naomba uzipeleke benki ni nyingi sana sitaki upoteze nguvu zako bure,” Teddy alimshauri Deusi. “Sawa nitafanya hivyo.” “Deus alipigia Kinape simu na kumweleza azipeleke benki katika akaunti ya Kinape yeye angezichukua baadaye. Tonny alimsindikiza Kinape mpaka benki ambapo aliweka fedha yote aliyopewa kwenye akaunti yake. Baada ya kuweka alimpigia simu Deus kumjulisha. “Mkubwa kazi imekwenda vizuri.” “Amekupa zote?” “Ndiyo.” “Shilingi ngapi?” “Milioni 75.” “Ooh, vizuri umeshaziweka benki?” “Ndiyo natoka sasa hivi.” “Basi tutaonana baadaye nyumbani.” “Hakuna tatizo mkuu?” Deus baada ya kupata uhakika kwa Kinape alimgeukia Teddy aliyekuwa akiendelea kunywa juisi taratibu bila wasi kama hakuna kitu cha hatari kilikuwa mbele yake. “Teddy,” alimwita. “Abee.” “Nafikiri kila kitu kimekwenda vizuri.” “Hakuna tatizo, naheshimu sana kazi yako pia muda wako.” “Asante lakini kumbuka umeniweka katika wakati mgumu sana.” “Kawaida tu kaka yangu, nakuapia ulichokifanya leo hutakijutia maishani kwako, huenda leo usione umuhimu wake lakini ipo siku utayakumbuka maneno yangu.”
“Basi wacha nikutoe ili ukapumzike na safari.” “Na kweli muda huu ningekuwa nimelala, hata chakula ningekula jioni baada ya kuamka.” “Pole sana ni harakati za maisha.” “Tunaweza kwenda,” Deus alisema huku akinyanyuka na kuweka vitu vyake sawa kwenye meza. Teddy alinyanyuka na kuchukua mkoba wake wenye dawa za kulevya na kuuweka begani kisha alitangulia kutoka, alipofika kwenye korido la kutokea nje alisimama kumsubiri Deus kuogopa maswali kwa baadhi ya watu ambao angekutana nao njiani. Baada ya kuweka ofisi yake sawa Deus alitoka na kumpitia Teddy kwa kumshika mkono, kwa mtu angewaona kwa mara ya kwanza angeamini wale ni marafiki wanaojuana muda mrefu. Lakini kumbe muda mfupi walikuwa chui na paka. Walikwenda kwenye gari na kuondoka kumrudisha sehemu aliyofikia, lakini Teddy aliomba aachwe sehemu ambako ataingia kwenye gari litakalomfuata na kwenda kwake. Wakiwa njiani Teddy alianzisha mazungumzo. “Nashukuru kwa ukarimu wako.” “Japo unanishukuru, lakini kumbuka nimenilazimisha nimeisaliti nchi yangu kwa damana waliyonipa ya kulinda nchi yangu.” “Huenda leo huijui faida yake lakini narudia kukuapia msaada wako hautakwenda bure, ila nilikuwa na wazo moja.” “Wazo gani?” “Najua kazi hii umepewa na taifa lakini kuna maisha badala ya kazi.” “Hayo najua, ulikuwa na maana gani?” “Hivi ukistaafu utalipwa kiasi gani?” “Kiasi cha kawaida.” “Nina imani hakitaweza kuyaendesha maisha yako?” “Ni kweli kabisa.” “Sasa unaona unafanya kazi ya mamilioni lakini mwisho wa siku unakufa maskini.” “Ni kweli, lakini kazi yetu inalenga kujitolea na si kujitajirisha.” “Wewe unasema hivyo wakati wakubwa zako wanaokutisha usichukue rushwa, wao ndiyo wanaongoza kuwa na utajiri wa kutisha.” “Sasa wewe ulikuwa unanishauri nini?” “Nataka kupitia kazi yako uweze kufaidika ili mwisho wa siku ulie kivulini.” “Kwa hiyo unanishauri nile rushwa.” “Kula rushwa siwezi kukushauri nina imani hii si rushwa ya kwanza inawezekana umeisha kula nyingi, inaonesha kabisa unakula za kawaida mimi nilitaka tufanye biashara kwa muda mwaka mmoja uwe trionea.” “Kazi hii ukiifanyia tamaa huchelewi kushtukiwa na mwisho wa siku unapigwa chini au unategewa mtego na ukinasa unafia gerezani.” “Biashara hiyo nataka tufanye sisi wawili.” “Kumbuka biashara hii mwisho wake mbaya kwa mfano ungekutana na mtu aliyekunywa maji ya bendera ya taifa si ungepotelea gerezani?” “Kabla ya kupotelea gerezani yeye kabla ya jioni jina lake lingebakia historia midomoni mwa watu.” “Una maana ungemuua?” “Siku zote kazi na dawa.” “Nani angemuua wakati wewe umo ndani?” “Mtandao ni mkubwa, miongoni mwenu kuna mtu angemuua.” “Kwa nini mnamuua?” “Kifo chake ni kupoteza ushahidi ili wakubwa wako wapate nafasi ya kunitoa kwa urahisi.” “Kama kuna wakubwa wanaweza kukutoa kwa njia hiyo, kwa nini hukuitumia kuliko kutoa fedha nyingi kiasi hicho?” “Hii ni biashara kati yako na mimi hivyo lazima tukubaliane tukishindani lazima nitumie ya upande wa pili ambayo huwa sipendi kuitumia kwa kuamini kila mwanadamu ni muelewa wote tunatafuta kwa njia ya halali na haramu.” “Kwa nini usiokoe fedha nyingi kuliko kutoa bila sababu.” “Njia ya pili ina faida na hasara zake, faida ni kutoka salama lakini hasara zake kwanza kutoa uhai wa mtu ambao kwa kupitia uwezo wangu wa kifedha huwa sipendi kuutumia. “Pili mara nyingi unaweza kutoka salama lakini mzigo wako ukapotea mikononi mwa dola, mara nyingi ukikamatwa kwanza taarifa zako zinafika katika vyombo vya habari hata kama ukitoka unakuwa umechafuka. Na mzigo nao unakuwa katika stoo kabla ya kuteketezwa hivyo inakuwa vigumu kuupata. Kama nitatumia njia ya kutoa fedha nyingi lakini ukiuza unarudisha faida japo kidogo.” “Inaonesha una fedha nyingi, kwa nini usiachane na kazi hatari kama hii?” “Hakuna mwanadamu anayetosheka fedha kila kukicha matajiri wanabuni miradi kuongeza kipato.” “Lakini si kwa kazi kama hii.” “Basi kwa taarifa yako kuwa watu wana fedha kufuru kwa kazi hii, kutokana na uwezo wao wamekuwa wakiwatuliza wenye viherehere. Hebu tuachana na hayo naomba tufanye kazi niliyokueleza awali, kwa muda mfupi nimeamini wewe ni mtu muhimu sana kwangu.” “Kazi gani?” “Kwa vile upo kwenye kitengo hiki naomba utumie cheo chako kufanikisha biashara hii. Nakuahidi kila safari yangu ikivuka salama una milioni 250.” “Una sema?” Deus aliuliza kama hakusikia. “Nitakapopita salama, nikifika nyumbani nakukabidhi milioni 250 hata kabla sijafanya biashara.” “Kwa mwezi utakuja mara ngapi?” “Itategemea mara moja au mara moja kwa miezi miwili.” “Naomba unipe muda wa kufikiria jambo hili.” “Kama ningekuwa mimi wala nisingesubiri kwani kijua ndicho hiki, ila napenda kukuonya kitu kimoja.” “Kitu gani?” “Kama utakubali kuufanya mpango huu ambao nakuhakikishia kwa mwezi kupitia mtandao wangu utatengeneza bilioni moja.” “Bilioni moja?” “Ndiyo, watu wanne wakiingia kwa mwezi mmoja utakuwa na kiasi gani?” “Nimekuelewa na nini ulichotaka kunionya?” “Nakuomba chonde chonde mpango hatari kama huu usimshirikishe mkeo.” “Kwa nini?” “Wanawake nawajua mvizuri si waficha siri kwenye wakati mgumu, kosa lolote litalotokea kwenye ndoa anaweza kutumia kukuangamiza.” Kauli ile ilimshtua Deus kwani mipango yote ya awali aliyofanya, mkewe ndiye aliyekuwa msiri wake. Lakini alikuwa mstari wa mbele kumshauri mambo ya kimaendeleo hata baadhi ya fedha za rushwa aliziweka kwenye akaunti ya mkewe. “Deus najua kabisa ulimshirikisha mkeo mambo yako ya nyuma, lakini kwa hili naomba iwe siri yako. Watu wengi wanaocheza michezo michafu kama hii huwaua hata wake zao pale wanapoona wamegundua kazi zao za hatari zinazoweza kuwapotezea maisha. Lakini sikushauri umuue mkeo, ila nakuomba ili uweze kuwa tirionea kwa muda mfupi kwani mtando una watu zaidi ya kumi mwezi mmoja wote wakipitia katika mikono yako salama utajikuta ukitengeneza bilioni mbili na nusu kwa mwezi, unataka Mungu akupe nini?” “Nimekuelewa nina imani ukiwa tayari nijulishe, tutaifanya kazi.” “Nashukuru kuwa muelewa, huwezi kuamini wewe ni mtu wa kwanza kumueleza mpango huu wa hatari. Naomba usinigeuke unaweza kunishangaa pamoja na umbile langu dogo lakini nitakachokufanya hutasahau maisha yako yote.” “Ondoa wasiwasi kazi itafanyika.” “Niteremshe hapa watu wangu wamenifuata, mambo mengine tumia namba yangu hii ya simu ambayo ni watu muhimu tu wanayoijua. ” Deus alimteremsha Teddy ambaye aliingia kwenye gari lenye tinted na kutoweka kwa mwendo wa kasi na kumwacha Deus akilisindikiza kwa macho huku akiuona utajiri mbele yake. Baada ya Teddy mwanamke hatari katika kuuza dawa za kulevya kuondoka, Deus alijikuta akipoteza ujasiri wa kulitumikia taifa na kujikuta akiota ndoto ya utajiri kwa kujiingiza kwenye biashara ya madawa ya kulevya. Aliamua kurudi ofisini kumalizia kazi zake ili jioni akakutane na Kinape akiamini kabisa rafiki yake hawezi kumweleza mtu yeyote siri ile kama livyomkataza. ******* Wakati akiwaza yale rafiki yake Kinape alikuwa na furaha ya ajabu moyoni mwake, alipofika nyumbani Kilole alitaka kujua furaha yake inatokana na nini. “Vipi mwenzangu leo mbona una furaha umeongezwa mshahara nini?” “Sasa hivi mimi ni milionea.” “Una maana gani kusema hivyo?” Kilole alihoji. Alimpa picha yote ilivyokwenda, Kilole baada ya kusikiliza taarifa ile alimweleza kitu Kinape. “Mungu mkubwa.” “Una maana gani kusema hivyo?” “Sasa mpango wetu utakamilika.” “Una maana gani?” “Sasa hivi ni wakati muzuri wa kumpotezea mbali Deus.” “Tusifanye hivyo.” “Shauri yako akigundua atakumaliza wewe.” “Kwa hiyo unanishauri nini?” “Kwa vile benki kuna milioni 75 zinatutosha kwangu nina milioni 24 huoni milioni 99 zitatusaidia kufanya mambo mazuri baada ya kumuua tutauza majumba yake mawili na magari kisha tutafungua mradi wowote wa kutuendeleza kimaisha na kuuhama mji huu.” “Hapana tusimuue.” “Lazima Deus afe, ikiwezekana kazi ifanyike leo usiku.” “Hapana tusifanye pupa tunaweza kuozea gerezani au hata kunyongwa kama ikigundulika sisi ndiye tuliyehusika na kifo chake.” “Sasa tufanye nini?” “Hebu nipe muda.” “Muda gani Kinape, mchicha umeisha kolea nazi fedha za kutosha tunazo tunasubiri nini?” “Japo lolote zuri halihitaji haraka,” Kinape alimtuliza Kilole aliyekuwa na pupa. “Mpaka lini?” “Nipe siku mbili.” “Na ziwe siku hizo mbili, ukizidisha utakuta mzoga wa mtu ndani.” “Unataka kujiua?” “Nani afe, nitamnyongelea mbali Deus.” “Punguza pupa kila kitu kitakwenda vizuri.” “Lazima nikueleze ukweli Kinape hakuna mwanaume chini ya jua ninaye mpenda kama wewe.” “Hilo nalijua lakini yote uliyataka wewe.” “Lakini kukubali kwangu kuolewa na Deus huoni faida leo hii akaunti yako kuna milioni 75 hukuwahi kuota kuingiza fedha kama hizi.” “Mmh! Na kweli.” *** Deus baada ya kazi alirudi nyumbani na kupokewa kwa furaha na mkewe huku Kilole akionesha mapenzi mazito kwa mumewe ili kumfumba macho kabla kumtendea unyama. Baada ya chakula cha usiku Deus alimtoa nje rafiki yake ili ampe taarifa za utajiri wa ajabu unaokuja mbele yake. “Unataka kuniambia kwa mwezi utakuwa unaingiza milioni 1000?” “Ndio maana yake, nataka baada ya muda nipabadilishe kijijini kwetu pawe kama peponi.” “Mmh! Mshiko mzito kauli ya yule dada kwa miaka mitano dunia utaishika mkononi.” “Yaani naona kama ndoto.” “Ungekuwa mnoko ungeishia na virushwa vya milioni kumi.” “Basi naomba siri hii isimpe mtu mwingine, nimekupa wewe mtu wa karibu hata mke wangu sitamwambia ni siri ya hatari sana.” “Hii ni siri nzito siwezi kumwambia mtu.” “Hujui dhamira yangu kwako, katika kila fedha itakayo ingia asilimia kumi nitachukua wewe.” “Unataka kuniambia katika milioni 1000 zangu ngapi?” “Milioni 100.” “Wachaaa, usinitie uchizi kwa furaha.” “Lazima nikujali nataka nawe kijiji upabadilishe wajue kweli watoto wao tumekuja kutafuta maisha.” “Kweli nimeamini wewe ni zaidi ya ndugu.” “Nathamini urafiki wetu tumetoka mbali kumbuka ndoto zetu tulipanga kufanya nini?” Baada ya mazungumzo walirudi ndani, Kilole hakuwa na haraka ya kujua walichokuwa wakizungumza kwa kuamini yote angeyajua kupitia kwa Kinape. Usiku nao ulikuwa wa raha kwa Kilole kuendelea kuonesha kumjali mumewe kwa kumpa penzi tamu ambalo lilimpagawisha Deus na kujikuta akimuahidi mkewe gari la milioni 20. Kilole alijisemea moyoni kuwa asali ile aliyomlambisha ni chambo cha kumuingiza kwenye mtego wamlipue hakuwa na mapenzi tena na mumewe na kumuona shetani wa roho yake aliyetamani afe wakati wowote ili afaidi penzi tamu la Kinape. ITAENDELEA
ILIPOISHIA: Kilole alijisemea moyoni kuwa asali ile aliyomlambisha ni chambo cha kumuingiza kwenye mtego wamlipue hakuwa na mapenzi tena na mumewe na kumuona shetani wa roho yake aliyetamani afe wakati wowote ili afaidi penzi tamu la Kinape. SASA ENDELEA… *** Siku ya pili Kinape alichelewa kutoka kwenda kazini kutokana na ishara aliyooneshwa na Kilole kuwa asiondoke ili wazungumze. Deusi aliondoka peke yake kuwahi kazini huku akijiona alichelewa kupata dili kubwa kama zile. Alipofika ofisini aliwasiliana moja kwa moja na Teddy mwanamke muuza unga. “Haloo Teddy.” “Ooh! Brother za asubuhi?” “Nzuri.” “Nina imani una habari njema asubuhi hii?” “Ni kweli, mimi nipo tayari kuifanya ile kazi.” “Ooh! Vizuri sana, tena una bahati washirika wangu wote wapo hapa.” “Kwa hiyo?” “Basi jioni tukutane ili tuzungumze jinsi ya kufanya.” “Hakuna tatizo.” “Nakutakia kazi njema kaka yangu.” Deus baada ya kukata simu alitabasamu kidogo kabla ya kuanza kazi. Wakati yeye anapanga mipango ya utajiri, nyumbani kwake pia kulikuwa na mipango ya kummaliza. Kinape baada ya kujiandaa kwenda kazini kabla ya kutoka chumbani Kilole alimfuata. “Vipi mpenzi?” “Safi.” “Naona jana jamaa alikuita chemba alikuambia nini, au ndiyo anataka uwahi kumuoa Happy?” “Walaa.” “Alikuitia nini?” “Jamaa anataka kututajirisha.” “Kututajilisha una maana gani?” Kinape alimueleza yote aliyoelezwa na Deus pamoja na kukatazwa kuitoa siri ile nje. Pamoja na kusikia mpango ule wa mabiloni ya shilingi bado Kilole aliona wanamchelewesha. “Kinape hiyo fedha itapatikana lini huoni kama tunachelewa, tuachane na mpango wake tummalize tufikiri mambo mengine.” “Kilole zile ni fedha nyingi zitakazo tufanya tuishi kama peponi, tutakula mpaka tunakufa bila kufanya kazi.” “Kwani huo mpango mwezi gani?” “Wanamsubiri yeye tu watu waingine unga wakati wowote.” “Mmh! Nitavumilia lakini kwa upande wangu naona zilizopo zinatutosha.” “Ni kweli lakini tutafanya kosa kumbwa kuacha mabilioni ya fedha.” “Mmh! Sawa.”
**** Wakati Kilole na Kinape wanapanga mipango ya kummaliza Deus, Jimmy mpiga picha naye alikuwa akipanga yake. Aliamini kupitia picha zile atajipatia fedha na penzi toka kwa Kilole mwanamke aliyempenda kupindukia. Aliamua kumtumia rafiki yake kumtisha ili wapate fedha. Kilole akiwa katika usafi wa kawaida wa nyumba simu yake iliita, namba ilikuwa ngeni kwake. Alibofya cha kupokelea na kusema: “Haloo.” “Haloo, nazungumza na Kilole.” “Ndiyo, nani mwenzangu?” “Naitwa Simon, kumeokota picha zako ambazo zinaonesha unafanya uchafu kwa hiyo ili nisizisambaze nataka milioni tano.” “Picha zangu?” Kilole alishtuka. “Eeh, tena unafanya uchafu na ndugu wa mumeo, kabla picha hazijamfikia mumeo tunaomba huo mzigo.” “Na..na..omba unipigie baada ya dakika tano,” Kilole alichanganyikiwa na kuona Jimmy amemgeuka. Kwa haraka alimpigia simu Jimmy kutaka kujua picha zake zimemfikiaje mtu mwingine. Alipopiga simu iliita kwa muda bila kupokelewa, hakukoma alirudia tena na kupokewa upande wa pili. “Haloo Sister,” Jiimy alipokea upande wa pili. “Nazungumza na Jimmy?” “Ndiyo Sister, lete stori.” “Jimmy nilikueleza nini?” “Kuhusu nini?” “Kuhusu picha.” “Kwani vipi?” “Kuna mtu kanipigia simu anasema ameokota picha zangu kwa hiyo anataka milioni tano la sivyo atazisambaza au kumpelekea mume wangu.” “Ha!” Jimmy alijifanya kushtuka. “Jimmy tulizungumza nini na umefanya nini?” “Samahani Sister, wiki mbili zilizopita nilivamiwa ndani na kuibiwa vitu vingi, nina siku mbili tangu nitoke hospitali.” “Taarifa ulifikisha polisi?” “Niliogopa kwa vile kulikuwa na picha zako.” “Jimmy kwa nini umekaa na picha zangu, kama pesa yako nilikulipa yote?” “Sister niliamini picha zile ulikuwa na umuhimu sana kwako hivyo ungeweza kuzipoteza ndiyo nikaamua kuzihifadhi nyingine kwangu.” “Sasa umeona umenitia hasara?” “Sikujua ingekuwa hivyo.” “Sasa nitafanyaje, utawezaje kunisaidia?” “Dada yangu kama fedha unayo ungempa kwa kweli picha zile siyo nzuri kuonwa na mumeo.” “Nampa lakini kumbuka umenifanyia kitu kibaya sana.” “Najua lakini nia yangu ilikuwa nzuri tu.” “Okay, imekwisha tokea sina jinsi, ila baadaye nitakupa kazi ya kunifanyia.” “Hakuna tatizo dada yangu ila pole sana.” “Bado sijapoa mpaka uifanye kazi yangu kwa asilimia mia.” “Hakuna tatizo.” “Basi baadaye.” Kilole alikata simu na kumpigia aliyempa taarifa ya kuokotwa kwa picha zake. Baada ya kuita ilipokelewa upande wa pili. “Ndiyo, sema.” ”Ulisema?” Kilole aliuliza. “Kuhusu nini?” “Si umesema una picha zangu?” “Ndiyo.” “Samahani kaka angu.” “Samahani ya nini, fedha haipungui hata senti tano kama huna niifanye kazi yangu,” upande wa pili ulimtisha. “Kaka yangu mbona unanifanyia ukatili kama huo, nimekukosea nini mpaka kushindwa kunisikiliza?” “Dada eeh, niambie utatoa mzigo au hutoi nijue moja sikuja kubembelezana.” “Sio kwanza sitoi, nitatoa hata zaidi lakini nilitaka kujua hizo picha umeziokota wapi na zilikuwa kwenye nini?” “Dada yangu eeh, sipo mahakamani kama mshiko upo nijulishe nina mambo mengi, hivi unafikiri nikimweleza mumeo kuwa nina picha hizo ningepata hata mara tatu ya fedha yako.” “Basi naomba unielekeze nizilete wapi hizo fedha?” “Unazo sasa hivi?” “Hapana nakwenda kwenye mashine ya kutolea fedha.” “Basi ukiisha kuwa nazo nijulishe nikuelekeze.” “Nielekeze wala haichuki hata nusu saa.” “Nitakujulisha baada ya dakika tano.” Jamaa baada ya kukata simu alimgeukia Jimmy aliyekuwa pembeni yake. ”Sasa mkuu fedha ndiyo hiyo atuletee wapi?” “Mwambie Sea Green view hotel.” “Poa.” “Yule mwanamke anaonekana ana fedha za kuchezea lazima tumtumie kutengeneza maisha.” “Hakuna noma mkuu.” Baada ya mazungumzo alimpigia simu Kilole. “Haloo Sister tukutane Sea Green view hotel.” “Nje au ndani?” “Aah! Jambo hili si la kitoto tunatakiwa tukabidhiane ndani.” “Mmh! Sawa.” “Mbona unaguna?” ”Si unajua mimi mke wa mtu naweza kuingia kwenye matatizo nikionekana katika mazingira ya kutatanisha.” “Kuachika na kuonekana kipi kibaya?” ”Mmh! Sina jinsi kisu kimegusa mfupa.” “Nikupe dakika ngapi?” “Sidhani itachukua nusu saa, naomba basi nikukute kwani nina haraka.” “Hakuna tatizo.” Kilole alijikuta akiingia katika matatizo ambayo hakuyategemea, moyoni aliapa kumfanyia kitu kibaya Jimmy ambacho hatakisahau maishani mwake. Baada ya kutoka kwenye mashine ya kutolea fedha, alielekea Sea Green view hotel. Alipofika nje ya hoteli alimpigia simu mwenye picha zake. “Haloo nimeisha fika upo wapi?” “Njoo ndani ghorofa ya pili chumba namba 112.” “Mmh! Mbona makabidhiano ndani ya chumba cha hotel?” “Kwa vile wewe ni mke wa mtu.” “Mmh! Sawa nakuja. ” Haikumpa shida kuingia ndani bila kujulikana kutokana na kujitanda kanga iliyomfunika kichwa na kujiziba na miwani nyeusi. Aliingia hadi ndani ya hoteli na kwenda moja kwa moja kwenye chumba namba 112, kabla ya kuingia alipumua kidogo na kugonga mlango. “Pita mlango upo wazi,” sauti toka ndani ilimjibu. Alizungusha kitasa na kusukuma mlango, mlango ulifunguka na kuingia ndani. Alimkuta kijana mmoja aliyekuwa amekaa kwenye sofa akinywa maji yaliyokuwa juu ya meza ndogo. “Karibu,” alimkaribisha huku akitabasamu. “Asante,” Kilole alijibu huku akikaa pembeni yake akiwa hajiamini. “Karibu soda.” ”Hapana nina haraka fedha hii hapa nipe picha zangu niondoke.” “Sikiliza dada yangu kufanya mambo yako kwa pupa utajikuta kila siku unarudia makosa.” “Nimekuelewa kaka yangu ila naomba unipe kwanza hizo picha mambo mengine tutapanga siku nyingine.” “Basi kunywa soda kidogo.” “Hapana kaka yangu nina haraka.” “Ina maana mimi ni mjinga kukununulia soda?” Jamaa alionesha kukasilishwa na kauli ya Kilole. “Basi wacha ninywe kidogo,“ Kilole alisema huku akichukua chupa ya soda iliyokuwa imekwisha funguliwa kabisa. Alikunywa kidogo bila kujua alikuwa amepangiwa mchezo mwingine katika soda, aliona kama inamchelewesha alikunywa yote ili awahi kuondoka. Lakini hakufanya lolote baada ya kupatwa na kuzunguzungu na kujilaza kwenye kochi bila kujua. Joe alimpigia simu Jimmy aliyekuwa nje ya hoteli.
Jimmy aliingia ndani ya hoteli na kumkuta Kilole amejilaza kwenye kochi hakiwa hajitambui. “Ooh! Kazi nzuri sana,” alimpongeza mwenzake. “Mmh! Nilikuwa kwenye wakati mgumu unajua kazi kama hujaifanya hata siku moja lazima utakuwa hujiamini, wasiwasi wangu anaweza kuja na polisi.” “Aje na polisi hajitaki, vipi mzigo amekuja nao?” “Huu hapo,” Joe alimpa bahasha lililokuwa na fedha. Kabla ya kufanya lolote walihesabu fedha na kukuta milioni tano taslimu, Jimmy alimkatia Joe milioni moja kama malipo ya kazi aliyompa. “Mzee nafikiri zinakutosha.” “Asante mkuu, nini kinaendelea?” “Bado sinema inaendelea, sasa hivi tutafanya naye mapenzi kwa zamu huku tukipiga picha ambazo naamini zitazidi kututengenezea fedha.” “Hakuna tatizo.” Walimbeba Kilole aliyekuwa hajitambui na kumlaza kitandani kisha walimvua nguo zate na kuanza kumbaka kwa zamu huku wakimpiga picha za aibu. Baada ya kumaliza zoezi la aibu waliondoka na kumwacha Kilole akiwa amelala hajitambui. ******** Majira ya mchana Teddy alimpigia simu Mr Deus kutaka kujua kama ana nafasi waonane kutokana na baadhi ya washirika wake jioni ya siku ile kuwa na safari kufuata mzigo. “Haloo brother za kazi?” “Nzuri, sijui zako.” “Zangu ziko poa, samahani tunaweza kuonana mchana huu?” “Hakuna tatizo.” “Basi njoo mara moja nikukutanishe na jamaa zangu ili tuianze kazi mara moja.” “Hakuna tatizo, tutakutana wapi?” ”Njoo na gari mpaka sehemu uliyoniacha siku ile.” “Hakuna tatizo ndani ya robo saa nitakuwa hapo.” “Okay, baadaye.” Deus alikata simu na kujiandaa kwenda kuonana na kundi la wauza madawa ya kulevya. Baada ya kupanga vitu katika hali nzuri alitoka na kumuaga msaidizi wake. “Happy natoka kidogo.” “Hakuna tatizo bosi.” Mr Deus alielekea kwenye maegesho kuchukua gari lake na kuelekea kwenye wito, alipofika eneo aliloelezwa alilipaki gari pembeni ya barabara kusubiri maelekezo. Baada ya muda simu yake iliita, alipoitazama alikuta ni Teddy, alibofya cha kupokelea na kuweka sikioni. “Haloo.” “Haloo nimekuona, teremka kwenye gari lako na kupanda kwenye gari litakalo simama mbele yako.” “Na gari langu?” “Liache tu litakuwa katika usalama wa hali ya juu, kwa hilo usihofu.” “Okay,” Mr Deus alikata simu na kuteremkana kulifunga gari lake na kufuata maelekezo. Kabla hajapiga hatua Range Rover Vogue nyeusi yenye vioo visivyoonesha ndani ilisimama mbele yake na kufunguliwa mlango. Hakupoteza muda aliingia ndani ya gari na kufunga mlango na gari liliondoka. Ndani ya gari kulikuwa na watu watatu Teddy aliyekuwa akiendesha gari na wanaume wawili waliokuwa wamekaa siti za nyuma. “Habari zenu?” “Nzuri,” Walijibu kwa mkato. “Samahani brother,” Teddy alisema huku akipaki gari pembeni. “Bila samahani.” “Naomba ufuate utaratibu wetu kabla ya kufika kwetu.” “Hakuna tatizo.” “Utafungwa kitambaa usoni mpaka tutakapofika.” “Hakuna tatizo mnaweza kufanya.” Baada ya kukubali alifungwa kitambaa cheusi usoni na safari iliendelea bila kujua anapelekwa wapi. Baada ya dakika tano gari lilisimama na kuombwa Mr Deus aliteremke, alitii amri na kuteremka kisha alishikwa mkono na kuongozwa hadi sehemu na kufunguliwa kitambaa usoni. Baada ya kufunguliwa alijikuta yupo mbele ya sebule lililokuwa na kila kitu cha thamani. Ndani ya sebule ile kulikuwa na watu zaidi ya nane ukijumlisha watatu aliokuja nao wakawa jumla watu kumi na mbili pamoja na yeye mwenyewe. “Karibu Mr Deus jisikie huru, ila samahani kukuleta kama mateka.” “Kawaida tu wala hakuna baya.” “Karibu kwenye kochi.” “Asante,” alijibu huku akikaa kwenye kochi, baada ya kuketi aliwasalimia aliowakuta. “Habari zenu.” “Nzuri,” Waliitikia kwa pamoja. “Mr Deus hawa ndiyo washirika wangu, huyo hapo ni Mateez anayefuata Sopas, Natalie, Suzy, Moops, Sweet, Pako, Flog, JMS na Poona, nina imani mimi unanifahamu?” Mr Deus alikubali kwa kutikisa kichwa. “Waungwana huyu ndiye mtu niliyewaeleza ana umuhimu mkubwa kwetu, nimeweza kumwelewesha na kanielewa. Kwa vile kazi hii haihitaji kupoteza muda nina imani kuanzia muda wowote biashara ifanyike. “Mr Deus hawa ndiyo washirika wangu niliokueleza kwa bahati nzuri tumekutana sehemu kubwa ya kundi letu. Wengine watatu utawajua kwa vile wiki ijayo wanaingia nimezungumza nao ili wapitie katika mikono yako salama japo wawili wamesema wataanza baada ya sisi ila mmoja atakuja na mzigo ndogo kujaribu.” “Hakuna tatizo kazi itafanyika vizuri kila mmoja ataifurahia,” alisema Mr Deus baada ya kumsikiliza Teddy. “Kwa hiyo kazi rasmi inaanza mwezi ujao kwa mwezi una uhakika wa kutengeneza zaidi ya bilioni mbili.” “Hakuna tatizo nina imani mtafurahia kufanya kazi pamoja japo ni ya hatari.” “Baada ya makubaliano hayo, tunakuonya tena kosa lolote la kizembe litagharimu uhai wako,” Teddy alitoa onyo lingine. “Najiamini kuliko mnavyonidhania,” Mr Deus aliwatoa wasi. “Kumbuka nilikukataza usimwambie siri hii hata mkeo.” “Siwezi kumwambia mtu.” Baada ya mazungumzo Mr Deus aliagwa na kupewa asante wa kukubali kufanya kazi na kundi lile ya milioni 55 kwa kila mmoja kutoa milioni tano. Baada ya mazungumzo yale alifungwa tena kitambaa na kurudisha hadi kwenye gari lake na kumkabidhi huku wakimuacha Mr Deus akiwa hajui alikuwa wapi. ****** Kilole alishtuka na kujishangaa yupo wapi baada ya kushtushwa na mazingira aliyoyaona mbele yake. Alijiuliza pale amefikaje na anafanya nini, kingine kilichomshtua ni kujikuta kitandani akiwa mtupu na pembeni yake kulikuwa na kondomu zaidi ya nne zilizotumika. Alishtuka na kujishika sehemu za siri na kukuta kweli amebakwa, pembeni yake kulikuwa na bahasha mbili zilizokuwa imeandikwa jina lake. Kabla ya kuichukua ile bahasha alitulia na kuvuta kumbukumbu ya kufika pale. Alikumbuka alipeleka milioni tano ili apewe picha alizipiga akifanya mapenzi na Kinape. Aliendelea kuvuta kumbukumbu na kukumbuka baada ya kuonana na yule kijana alikaribishwa soda lakini kilichoendelea hakujua mpaka aliposhtuka na kujikuta akiwa mtupu kitandani huku ikionesha amebakwa zaidi ya mara nne kutokana na mipira minne ya kiume iliyotumika. Alijipa ujasiri na kunyanyuka hadi bafuni na kuoga kisha alirudi chumbani na kuvaa nguo zake kisha alichukua bahasha mbili zilizokuwa na jina lake na kuziweka katika mkoba wake na kutoka nje ya hoteli kurudi nyumbani kwake. Alipofika nje ilionesha kiza kilikuwa kimeingia, alitoa simu yake kwenye mkoba na kuangalia saa ilimuonesha ni saa mbili usiku. Alijikuta akishtuka na kujiuliza utamueleza nini mume wake, katika simu yake kulionesha kuna simu zilizopigwa zaidi ya mara kumi za mume wake pamoja na Kinape. Japo roho ilimuuma kwa kitendo cha kinyama alichofanyiwa na kuapa kulipa kisasi, lakini aliweka pembeni maumivu yale na kutafuta njia ya kukabiliana na mumewe nyumbani atakayetaka kujua alikuwa wapi. Lakini ilikuwa tofauti na alivyofikiria, alipofika nyumbani alishangaa kukuta mumewe hajarudi. Mfanyakazi wa ndani alipomuuliza alisema hajarudi, ile ilimpa nguvu na kumpigia simu mumewe. “Haloo sweet.” “Ooh! Honey vipi mbona napiga simu hupokei mpenzi, kuna nini?” “Nilikuwa nimelala kichwa kimeniuma ghafla.” “Nilitaka kukujulisha kuwa nitachewa tuna kazi moja nzito.” “Mmh! Mume wangu, siyo unanila kisogo,” Kilole alijifanya kulalamika. “Mke wangu siwezi kutoka nje ya ndoa yangu nakupenda sana, hasa mwenetu ambaye ndiye mrithi wetu na yote nayafanya kwa ajili yenu.” “Asante mume wangu, nashukuru kusikia hivyo.” “Nikimaliza tu narudi nyumbani.” “Nakutakia kazi njema, nakusubiri kwa hamu,” Kilole alizidi kumtia ujinga mumewe. Baada ya kukata simu aliingia chumbani mwake na kuziangalia zile bahasha, bahasha ya kwanza ilikuwa na picha alizopiga akifanya mapenzi na Kinape. Bahasha ya pili kulikuwa na picha ambazo zilimmaliza nguvu lakini akijikaza na kuendelea kuzitazama. Alijiona akibakwa na wanaume wawili, alishtuka na kukumbuka soda aliyokunywa ndiyo ilimfanya apoteze fahamu na kumfanya yule mwanaume na mwenzake wambake. Roho ilimuuma kutoa milioni tano bado wamembaka na kumpiga picha chafu. Ndani ya bahasha kulikuwa na karatasi iliyokuwa na ujumbe usemao; Kwa vile unapenda mchezo huo, baada ya kukupa picha zako na kutupa milioni tano, picha hizo zingine zinataka milioni kumi, la sivyo siri ilimfikia mumeo. Tutakupigia simu kujua utatupa lini na wapi? Kilole jasho lilimtoka na kuona kama laana ya matendo yake ndiyo inayomtafuna, alijiuliza milioni kumi akiwapa lazima watatengeneza mpango mwingine. Wasiwasi wake huenda mpango ule Jimmy anaujua, lakini hakutaka kutumia pupa zaidi ya kutumia hata kishawishi cha fedha ili Jimmy amsaidie. Wazo lingine lilikuwa kumuwahi Deus kabla hajajua lolote kwa kumuua ili kuepusha aibu, lakini wazo la kuua bado hakulipa nafasi kutokana na Kinape kuweka pingamizi. Akiwa amechanganyikiwa simu yale iliita, aliipokea na kusema: “Haloo.” “Haloo, bahasha umeiona?” ”Wewe nani?” “Mdau wako, nina imani ujumbe umeuona nieleze hizo fedha nitapata lini?” ”Lakini kaka yangu nimekukosea nini mpaka kunifanyia unyama kama huo?” Kilole alilalamika huku akimwaga chozi. “Hujadhalilishwa na mtu, biashara umeianza wewe, sisi tunaiendeleza.” “Kaka yangu milioni tano nimekupa leo, hizo kumi nitazipata vipi?” “Kama huna pa kuzipata basi salamu utazikuta kwa mumeo,” sauti ya upande wa pili ilimtisha. “Msifanye hivyo, nioneeni huruma.” “Hukujionea huruma sisi tutakuonea vipi?” “Basi nipunguzieni.” “Tulikuwa tunataka milioni hamsini, lakini nimepunguza mpaka kumi bado huoni huruma yangu.” “Basi nipeni muda wa muda ili nizikusanye.” “Tutakupa siku mbili.” “Mbona ndogo?” “Kama ndogo utajuana na mumeo tena tuinampa na za mwanzo ulizopiga na shemeji yako.” “Basi nitawapeni, nakuombeni msimpe mtu.” “Hakuna tatizo timiza haja zetu.” “Hakuna tatizo.” “Kwa heri, usiku mwema.” Baada ya kukata simu alijikuta akirudiwa na maneno ya mtu aliyetaka fedha kwa kusema alifanya mapenzi na shemeji yake ile ilionesha kabisa Jimmy huenda mpango mzima anaujua. Kilole pamoja na kutokewa na tukio zito la kumdhalilisha huku likizidi kumuingiza kwenye mazingira magumu. Lakini hakutaka kuyumba kwani aliamini vita ile ni yake na yeye ndiye anayetakiwa kupambana mpaka tone la mwisho. Alizirudia zile picha na kuuona unyama aliofanyiwa ikiwa pamoja na kuingiliwa kinyume na maumbile. Moyo ulimuuma sana na kujikuta akidondokwa na machozi kutokana na udhalilishwaji kama ule. Aliapa kupigana nayo mpaka hatua ya mwisho hata kwa mtutu kwani alikuwa anajua kutumia vizuri chombo cha moto baada ya kufundishwa na mumewe na kujua kuitumia vizuri. Alikumbuka visasi vingi ambavyo ameviona kwenye sinema hutendeka usiku kwa mtu kuingia sehemu na kufanya mauaji kisha kutokomea bila mtu kujua. Wazo lake lilikuwa kwenda kumbana Jimmy ili amtaje mtu mwenye picha zake na alipanga kuhakikisha anamuua Jimmy na kijana anayemtumia kama mtaji. Wakati akiwaza vile alishtuka kusikia mlango ukigongwa, alificha picha kwenye kabati na kwenda kufungua mlango. Alifuta machozi na kujirudisha katika hali ya kawaida kisha alipofungua akijua mumewe karudi, lakini kumbe alikuwa Kinape ambaye alionekana mwenye jambo zito kichwani mwake kutokana na mwonekano wake. Kilole alizidi kuchanganyikiwa na hali ile ambayo aliona huenda inafanana na yake. “Kilole mbona hivyo?” alimuuliza kwa mshangao. “Kilole umeniweka katika wakati mgumu sana,” Kinape alisema huku akikuna kichwa. “Mungu wangu! Amejua? Kwa nini tusimmalizie mbali?” “Tummalizie mbali nani?” “Si Deus.” “Kwa kosa gani?” “Si amejua.” “Wala si hilo.” “Picha ameziona?” “Kilole hebu acha papala, yote unayouliza siyo.” “Sasa nimekuweka kwenye wakati mgumu kivipi?”
”Happy hanielewi kabisa, kila kukicha naitwa na familia yake naichenga, nikienda nitawaelezea nini wanielewe.” “Kinape unakuwa kama siyo mwanaume, mwambie kuwa humtaki kwani mapenzi ni lazima.” “Si rahisi kiasi hicho, kuvunjika kwa penzi kuna sababu huwezi kuzima chuma cha moto na maji baridi lazima kitapinda na Deus nitamwambia nini mtu niliyempeleka kwa wazazi wa Happy kumtambulisha kama kaka yangu?” “Yote uliyataka wewe, kwa nini hukuniuliza kabla ya kwenda huko?” ”Kilole, wewe ni mke wa mtu na Happy ni mchumba wangu hivyo nilikuwa na haki ya kufanya vile.” “Sasa Deus atakulazimishaje umpende Happy wakati humtaki?” “Nitaanzia wapi ikiwa nilimweleza mengi juu ya mapenzi yangu ya dhati kwa Happy huku akiniahidi kusimamia harusi yangu. Kibaya zaidi Happy na wazazi wake watakuja hapa jioni ya leo ili kujua hatima ya ndoa.” “Kwani wewe ulimjibu nini Happy?” “Nilimueleza asubiri kidogo mzazi wangu mmoja alikuwa na matatizo.” “Sasa yeye anataka nini na ulikwisha mweleza ukweli?” “Anataka kwenda kumuona kwa vile anajua na yeye ni mzazi wake, pia muda wa kuwa naye umepungua si kama zamani. Kingine majibu yako ya mkato yamemshtua kitu ambacho kimemetia wasiwasi huenda tuna uhusiano wa kimapenzi.” “Sasa akijua atafanya nini? Tena mweke wazi ili ajue hana chake.” “Kilole acha kujisahau wewe ni mke wa mtu, kibaya kosa tunalifanya ndani ya kinywa cha simba. Hivi wakija hapa nitamwambia nini Deus na kwa vile huu ni mwisho wa wiki huenda akasema kesho tunakwenda kijijini. Siyo siri tabia ya Happy ilimvutia sana Deus na kusema atanipigania hata kwa fedha kuhakikisha namuoa, hivi niseme simtaki Happy nitaanzia wapi?” “Kinape, Deus hawezi kukulazimisha kuoa mwanamke usiyempenda.” “Unasema tu lakini kauli hiyo kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kuitamka.” “Kwa hiyo unamuogopa Deus?” “Ndiyo.” “Kwa nini tusimpoteze?” “Kilole acha papara nimekueleza tutajipanga.” “Nataka kukueleza kitu kimoja Deus ni kikwazo kwa nini mnamlea?” “Tukifanya kwa pupa tutakosa mwana na maji ya moto.” “Sasa tutafanyaje?” “Nimekueleza niache niangalie tufanye nini?” “Na kuhusu Happy najua ndiye anayeweza kuharibu kila kitu kama ataonekana kijijini?” “Kwa kweli la Happy ndilo linalonichanganya nashindwa nifanye nini, nilipokutana naye leo nimechanganyikiwa jinsi alivyokonda kwa muda mfupi niliokuwa karibu yako na amenitishia nikimuacha lazima atajiua.” “Sasa akijiua wewe utapungukiwa nini, kwanza ndiyo itakuwa safi tunakuwa na nafasi ya kuishi wawili baada ya kumpoteza na Deus.” “Siwezi kufanya hivyo, kama Happy atafariki basi nitakuwa na dhambi kubwa sana ambayo itakuwa kama tone la rangi nyekundu kwenye nguo nyeupe haitanitoka mpaka nitakapo ingia chini ya udongo.” “Mmh! Sasa tutafanya nini?” “Ndiyo maana nikasema umenipa mtihani mzito ambao sikuwahi kuusoma hata siku moja kwangu naona kiza. Kwa nini tusiachane na wazo kama hili?” ”Wazo gani?” “Ukaniachana nioane na Happy na wewe unakie na Deus?” “Kinape huwezi kunivisha kitanzi kisha uniweke juu ya donge la barafu likiyenyuka lazima nitakufa. Heri nife mimi kuliko kuendelea kuishi kwani naamini maisha yangu baada ya zile picha hayana thamani. Kwa hiyo ulitaka kunidhalilisha ili ufurahi kwa vile nimeolewa na Deus kama kweli ulitaka niishi na Deus kwa nini ulinitendea unyama kama ule?” “Happy..Ooh! Sorry Kilole mbona umekosa subira.” “Nimekuelewa Kinape, tutazungumza kesho.” Waliachana na Kilole alirudi chumbani akiwa amechanganyikiwa na kushindwa afanye nini juu ya picha mpya na habari za Happy. Kilole baada ya kuachana na Kinape alirudi chumbani kwake na kujifungia kwa ndani, kila dakika iliyokuja mbele yake ilikuwa na maumivu makali yaliyomfanya akose jibu la haraka afanye nini. Kubakwa hakuona tatizo zaidi ya kusikia habari za Happy kupigania penzi lake ambalo ndilo lililomfikisha katika maumivu yale makali. Alijiona mtu mmoja ambaye alikuwa akipigana na watu wengi bila msaada wa mtu mwingine, alijiuliza atawezaje kumdhibiti Happy kuhakikisha anampata Kinape mwanaume ambaye aliamini ndiye wa maisha yake. Alichukua bahasha na kurudia kuangalia picha alizopigwa akibakwa na wanaume wawili kwa mpigo ambao hawakuonesha sura zao zaidi ya yeye peke yake. Picha zile zilimchanganya sana na kuamini kama zitamfikia Kinape zitamweka katika mazingira magumu ambao utakuwa kama fimbo ya kumpigia ili kumuoa Happy. Alipiga ngumi kwenye godoro kwa hasira baada ya kujiona yupo njia panda asijue aanze na kitu gani ili aweze kuyazima yote na mwisho wa siku awe na Kinape. Akiwa katikati ya mawazo mlango uligongwa, alijua ni Kinape amekuja na wazo jipya, alikwenda hadi mlangoni na kufungua lakini alikuta ni mumewe ambaye alimchanulia tabasamu pana. Kwa mshtuko aliufunga mlango haraka na kufunga na komeo, kwa haraka alichukua picha zake na kuzificha kisha alitoka hadi mlango ambako mumewe alikuwa bado amepigwa na butwaa. “Ha! Kumbe ni mume wangu?” Alijifanya kushtuka. “Unaniona sasa mwanzo ulifikiria nani?” “Mmh! Hata sijui niseme nini, wakati unagonga mlango nilikuwa nimejinyoosha kitandani na kupitiwa na usingizi na kuota nimevamiwa na majambazi. Ulipogonga nilikuwa bado na usingizi nilipofungua na kukuona nilifikiri ni jambazi mpaka uliponiita na kuitambua sauti yako nisamehe mume wangu.” “Kawaida, pole kwa ndoto mbaya.” “Asante mume wangu.” “Vipi mbona kama haupo sawa?” “Mume wangu si nimekueleza naumwa, hata ndoto zangu zilikuwa za kutisha.” “Ooh! Pole sana.” Kilole alijikuta akiangua kilio kilichomshtua mumewe. “Vipi tena?” alimuuliza. “Aah! Basi tu.” “Basi tu nini! Au umezidiwa?” “Walaa, hata sijiui nalia nini.” ”Niambie kama umezidiwa nikuwahishe hospitali, utalia bila kujua unalia nini?” “Nimemeza dawa naomba kitu kimoja.” “Kipi hicho mke wangu?” “Uniache nipumzike nisiamshwe na mtu yeyote na mtoto alale kwa msichana wa kazi.” “Hakuna tatizo mke wangu.” Deus hakutaka kumsumbua mkewe alifanya yote aliyoelekezwa, alitumia nafasi ile ya mkewe kutotaka usumbufu kuzungumza na rafiki yake juu ya mpango aliozungumza na Teddy na wauza unga wenzake. Baada ya kuoga na kupata chakula cha usiku kilichopikwa na msichana wa kazi alikwenda chumba cha rafiki yake. Alimkuta amejipumzisha, alipomuona rafiki yake alimkaribisha kwa furaha. “Ooh! Best karibu.” “Naona umejipumzisha.” “Nifanye nini baada ya mihangaiko ya siku nzima.” “Basi leo tulikuwa na kazi moja nzito ya kukamata gari lililokuwa na madawa kutokana na taarifa za watoa habari. Wenye gari waligoma kufungua mpaka walipokuja wakubwa zetu ambao waliliruhusu bila hata kuuliza. Lakini taarifa zilisema gari lile lina dawa za kulevya.” “Basi hapo kuna rushwa imetembea kwa wakubwa.” “Umeona eeh!” “Ukweli ni huo unafikiri ndani ya gari kulikuwa na mzigo kiasi gani, ndiyo maana walikuwa wabishi kuwafungulia gari kwa vile kuna watu wanawategemea.” “Kitendo kile kimenivunja nguvu kweli, siwezi mkupote muda wangu kwa upuuzi kama ule.” “Nawe kula sehemu yako.” “Sasa kuna dili moja nimeingia leo si mchezo.” “Mmh! Dili gani tena mzee?” “Si nilikueleza yule mwanamke alisema atanikutanisha na wenzake?” “Eeh, ndiyo.” ”Basi leo mchana alinipigia simu na kunikutanisha nao.” “Acha utani! Ehe ikawaje?” “Tumekubaliana kuinza mwezi ujao kwa hiyo mpaka mwezi ukikatika nitakuwa nimetengeneza bilioni mbili.” “Acha utani!” “Ukweli sasa hivi najiona nimekwisha uaga umasikini, kweli! Umefikia wapi mambo yako na Happy?” Swali lilikuwa kama pigo zito moyoni mwa Kinape hakuwa na jibu la haraka, Deus hakujua rafiki yake anawaza nini baada ya kumuuliza na kukaa kimya. “Ni hivi nina fedha kidogo nitakupa ili kuhakikisha unakamilisha harusi yako.” “Kiasi gani?” “Milioni ishirini ambazo nitakupa sasa hivi ufanye maandalizi yako na shemeji, umekwisha mpeleka kwa wazazi kijijini?” “Bado.” “Unasubiri nini? Fanya hivi kesho kutwa hakikisha unakwenda na Happy kwa wazazi ili tupange nipango mingine. Utatumia gari langu sawa pia tafuta nyumba ya milioni hamsini ili nikununulie kwa siri ili shemeji yako asijue kitu.” “Hakuna tatizo nimekuelewa mkuu.” “Mbona kama upo mbali au umechoka?” Deus alimuuliza Kinape aliyeonekana yupo mbali kimawazo. “Ni kweli leo nimefanya kazi kama mbwa, hapa nilipo natamani kulala tu si kitu kingine.” “Basi pumzika tutaonana kesho.” “Usiku mwema.” “Na kwako pia.” Deus alitoka na kwenda sebuleni kutafuta mkanda wa filamu ili kuvuta muda kabla ya kupanda kitandani huku akiwa anaisikia harufu ya utajiri. Alipiga mahesabu hata kama wataingiza mara moja kwa miezi miwili kwa mwaka aliziona bilioni kumi na mbili mbele yake. Alijikuta akicheka peke yake huku akisema kwa sauti ya chini: “Kumbe utajiri hauna njia ndefu.” Wakati akiwaza yale chumbani mkewe alikuwa akigaagaa kitandani kama nyoka aliyemwagiwa mafuta ya taa kutokana na kuwa na maswali yasiyo na majibu juu vitu vilivyopo mbele yake alijiuliza aanze na lipi la Jimmy au la Happy. Alipanga usiku atoroke na kwenda kwa Jimmy kumbembeleza kwa njia yoyote ili tu amjue nani aliyemfanyia mchezo mchafu kama ule tena kujua picha za awali akifanya mapenzi na shemeji yake. Pamoja hakuwa na usingizi alitulia kitandani akisubiri mumewe akilala atumie nafasi hiyo kwenda kwa Jimmy. Naye Kinape baada ya kutoka Deus alijikuta kwenye mtihani mzito wa kutoa uamuzi sahihi ambao hautaleta madhara kati ya Happy na Kilole. Lakini Happy kwake alikuwa muhimu kuliko Kilole ambaye tayari alikuwa mke wa mtu. Swali ambalo kila kukicha lililokuwa likimla akili lilikuwa kuhusu picha alizopigwa akifanya mapenzi na Kilole nani aliyezipiga, alipata wazo la kumtafuta ili kupata ukweli wasiwasi wake huenda mtego ule ulipangwa na Deus. Kingine kilichomkosesha raha kama picha zile zikivuja na kumfikia Deus angekuwa kwenye wakati gani. Wazo la kuua Deus au kumfanyia baya lolote alilipinga kwa nguvu zote japo hakuweza kumweleza ukweli Kilole. Taarifa za siku ya tatu kwenda kijijini kumtambulisha Happy zilizidi kumchanga kwa kujiuliza habari zile akimweleza Kilole atazipokea vipi. Aliamua liwalo na lile lazima amweleze ukweli na hiyo kesho kutwa lazima ampeleke kijijini mengine yatakayotokea atakuwa tayari kukabiriana nayo. Alipuuza mkwara wa Kilole na kujilaza kuitafuta siku ya pili. ***** Majira ya saa saba usiku baada ya kuona mumewe amelala na kukoroma, Kilole alijinyanyua kitandani na kumtazama mumewe aliyekuwa amepitiwa na usingizi hajitambui. Alinyanyuka taratibu kwa kunyata hadi pembeni ya kitanda na kuunyanyua mto aliokuwa amelalia mumewe taratibu na kutoa bastola ya mumewe. Alikwenda hadi kwenye kabati na kuvaa kaptura na fulana, aliichomeka bastora kiunoni kisha alijifunga kanga zilizomziba mwili mzima na kutoka taratibu bila kumshtua mtu yeyote. Aliegesha mlango na kutoka kwa kunyata hadi nje ya geti na kuchepua mwendo kupitia barabara kubwa kuelekea kwa mpiga picha Jimmy ambako hapakuwa mbali sana na kwake. Baada ya mwendo mfupi aliacha barabara ya rami na kuingia kwenye uchochoro ambao ungemfanya atokee nyuma ya nyumba anayoishi Jimmy pia ndipo palipokuwa na dirisha lake. Alishukuru Mungu muda wote hakupata kizuizi chochote alitembea kwa taadhari kubwa, shida yake kwenda kugonga dirisha la Jimmy ili azungumze naye na kutaka msaada wake. Alipokaribia alitembea kwa kunyata ili mtu wa ndani asijue nje ya nyumba kuna mtu anapita. Aliporikaribia dirisha la Jimmy alisikia sauti za watu wawili mwanaume na mwanamke. Mwanaume alimtambua ni Jimmy lakini mwanamke hakujua ni nani, lakini alijua ni mwanamke wake japo Jimmy hakuwa ameoa. Alitulia akijifikiria amwite au afanyeje kwani wasiwasi wake huenda pakatokea tatizo kwa muda ule mwanamke wake akajua yeye ni hawala yake. Wakati akiwaza afanye nini, aliendelea kusikia mazungumzo yaliyokuwa yakizunguzwa ndani. “Sasa mpenzi hiyo fedha utanipa lini?” “Kuna dili moja litatiki muda si mrefu nitakupatia.” “Kumbuka na mimi ninataka kuendesha gari.” “Nimekueleza nitakupatia hiyo fedha baada ya wiki kila kitu kitakuwa tayari.” “Najua unanidanganya.” “Mbona laki nane za kupangia nyumba nilikupa kisha laki nane zingine za kununulia sofa nimekupa nitashindwa vipi milioni nne?” Kauli ile ilimshtua sana Kilole na kujiuliza Jimmy uwezo ya kutoa fedha kiasi kile ameutoa wapi, wakati maisha yake yalikuwa ya kubahatisha mpaka apige picha na muda mwingi alishinda kijiweni. Wakati akijiuliza maswali yasiyo na majibu ndani mazungumzo yaliendelea. “Ha..ha..lafu mpenzi siku hizi unafanya kazi gani maana fedha zimeibuka kama uyoga?”
“Maisha kama kalata ukijua kuzichanga kila kitu kina kwenda kilivyopangwa.” “Au unauza dawa za kulevywa?” “Kwani dia tatizo lako nini?” “Naogopa nisije kukupoteza wakati nakuhitaji.” “Ungekuwa unanihitaji ungeridhika na nilivyokupa.” “Sawa, hata kama unauza unga kuwa makini.” Kilole alijikuta akijawa na maswali juu ya maneno ya Jimmy kuonesha ndani ya wiki ile atampatia yule mwanamke milioni tatu. Pia siku ile alimpa milioni moja na laki sita. Akili ya haraka aliamini fedha hizo huenda ndipo aliziombwa azitoe ili azipate picha zake. Alikubaliana na wazo lake la awali kuwa Jimmy ndiye mhusika mkuu wa mipango yote. Wakati akiwaza vile alisikia simu ya Jimmy ikiita, alimsikia Jimmy akimwambia mwanamke wake. “Samahani nakuja.” “Unakwenda wapi?” “Sipendi maswali ya kijinga nimekueleza nakuja,” Jimmy alijibu kwa ukali. “Najua na wanawake zako tu, “ alimsikia mwanamke akilia wivu. “Wewe si unataka gari sasa kwa nini unapenda kufuatilia mambo yangu?” “Sawa, basi nenda.” Kilole alisikia mlango ukifunguliwa kuonesha Jimmy alikuwa akitoka nje kusikiliza simu. Kilole akiwa ametulia pembeni ya ukuta kwenye choo cha nyumba ya jirani. Alisikia sauti za viatu zikielekea nyuma ya nyumba, kwa haraka alijificha nyuma ya choo. Jimmy bila kujua kuna mtu alisimama pembeni ya choo na kupiga simu iliyopokelewa upande wa pili. “Sema Rich mbona usiku?” “Aisee nina tatizo kubwa ya fedha,” kutokana na utulivu wa hali ya hewa Kilole alisikia mtu aliyekuwa akizungumza upande wa pili. “Shida gani mzee, si leo nimekupatia mgao wa milioni?” “Ni kweli, si unajua nyumba za uswahili baada ya leo kununua sofa nimepandishiwa kodi ghafla na kutakiwa nilipe mwaka mzima na fedha yake anataka kesho. Sasa sijui utanisaidia vipi naomba basi unikope milioni ili kesho kama tukilipwa ile fedha nitakurudishia.” “Sikiliza Rich leo nimempa shemeji yako milioni mbili kwa ajili ya sofa na kulipia nyumba, kwa sasa sina kitu ila jitahidi kumtisha yule mwanamke ili tupate hiyo fedha ikiwezekana hata kesho saa tano asubuhi.” “Okay, nitajaribu kumsomesha.” “Atakuelewa tu, jitahidi kesho tuzipate zote milioni kumi sawa?” “Sawa nimekuelewa.” “Basi usiku mwema, unajua umenitisha sana, wasiwasi wangu yule mwanamke kujua kama ni mimi ndiye namchezea mchezo huu.” “Walaa, nawe usiku mwema.” Baada ya kukata simu Jimmy alirudi ndani na kumuacha Kilole akiwa amepata kitu ambacho mwanzo alikidhania lakini siku ile ukweli ulijulikana. Aliona hakuna haja ya kuendelea kuwa pale. Aliondoka na kurudi nyumbani huku moyo ukimuuma kwa kitendo alichotendewa na Jimmy. Alifika kwake na kuingia ndani bila mtu yeyote kujua kama alitoka, alipanda kitandani na kujilaza. Kutokana na kutingwa na mawazo muda mwingi alifikiria jinsi ya kumuadabisha Jimmy. Moyoni aliapa kabla ya kuwapa hizo milioni kumi lazima wote wawe wamelamba udongo. **** Teddy mwanamke hatari muuza unga baada ya kumaliza kuuza mzigo wake alimuaga Deus na kumweleza kila kitu kitakavyoendelea atamjulisha. Muda wote alikuwa na maswali juu ya mtu aliyemchoma katika kitengo cha madawa ya kilevya. Alijiuliza nani aliyekuwa akijua kuondoka kwake zaidi ya mdogo wa marehemu mumewe ambaye alinyongwa China baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya. Tokea kifo cha mumewe mdogo wa mumewe alikuwa akimfuatilia na kumtaka kimapenzi. Lakini hakuwa tayari kutembea na familia moja kwa vile alikuwa na uamuzi wa kumchagua nani awe mpenzi wake. Muda mwingi kulikuwepo na kutoelewana kwa shemeji yake kulazimisha mapenzi na yeye kumkatalia. Mwanzoni alifanya kazi na mumewe ya uuzaji wa madawa na ndiye aliyemfundisha kuifanya kazi ile. Baada ya kifo cha mumewe alimshirikisha mdogo wa mumewe ambaye baada ya kupata fedha alianza nyodo na kuendelea kumtaka kimapenzi huku akimuahidi kumfanyia kitu kibaya kama ataendelee kumtolea nje. Teddy bado hakutishwa na vitisho vya shemeji yake ambaye bado aliendelea kufanya naye kazi ya kusambaza dawa za kulevya kila kona ya dunia. Hata siku ya kuondoka mara ya mwisho aliyekuwa akijua safari ile ni yeye na washirika ambao wote walikula kiapo cha kuficha siri ya kazi yao na kuwa tayari kumsaidia mwenzao kwa gharama yoyote anapopatwa na tatizo. Wazo lake lilimpekeka huenda ni shemeji yake ndiye aliyefanya mchezo ule ili kumkomoa baada ya kumkataa kimapenzi. Aliapa kumfanyia kitu kibaya kama ni yeye na adhabu yake ilikuwa ni kifo kwa vile nia yake ilikuwa ni kumpoteza. Teddy alipofika Italia alikwenda moja kwa moja kwenye nyumba aliyokuwa akiishi pamoja na shemeji yake. Mara zote alipokuwa akisafiri na kurudi alikuwa akiwasiliana naye hata kumpokea, lakini siku ile alirudi kimya kimya. Alipofika nyumbani kwake aliingia ndani bila hodi, shemeji yake aliyekuwa na rafiki zake wakinywa na kujiachia na wanawake na muziki mkubwa alipomuona alishtuka sana. “Ha! Teddy wewe si ulikamatwa?” “Wapi?” “Si..si.nilisikia umeshikwa Tanzania?” “Nani aliyekuambia?” “Au alinidanganya?” “Nani mbona sikuelewi nani amekwambia mimi nimeshikwa?” “Au umetoa rushwa?” “Ili?” Teddy alimuuliza huku akimtazama usoni kutafuta ukweli. “Tu..tu..achane na hayo, na..na mbona umekuja bila taarifa.” “Tatizo nini? kwa nini umegeuza nyumba yangu club?” “Kwani tatizo nini?” “Mose unanitafuta huwezi kuigeuza nyumba yangu kama kilabu cha pombe ya kienyeji zinazouzwa Afrika.” “Oya washikaji tutimke mambo yamekwisha haribika.” “Sasa sherehe tunaihamishia wapi?” Mwanamke mmoja aliyekuwa amelewa sana na kuvaa nusu uchi aliuliza. “Oya Rose, hii tunakwenda kuimalizia club Royal clasic.” “Sasa kuna faida gani ya kupoteza muda, na huyu nani?” “Shemeji yangu.” “Si ulisema umenyongwa au kafufuka?” “Sitaki maswali hebu tuondokeni.” Mose aliondoka na washikaji wake waliokuwa wamelewa na kwenda kumalizia starehe zao club. Teddy alianza kufanya usafi ili kuirudisha nyumba katika hali nzuri. Macho yake yaliona simu kwenye kochi, aliacha kufanya usafi kuichukua simu ile na kuanza kuipekea kwenye sehemu ya ujumbe. Jicho lake lilikutana na ujumbe ulioonesha shemeji yake alimtumia mtu aje kwenye sherehe ya kupotezwa kwake. Ilisomeka: yule fala nimemmaliza njoo tusherehekee njoo na demu wako. Palepale alipata picha kuwa shemeji yake ndiye aliyemtengenezea mtego ule. Aliapa kummaliza na kutoroka Italia na kwenda kuishi nchi yoyote kutokana na uwezo ya kifedha. ***** Siku ya pili Kilole aliwahi kuamka ili aweze kuzungumza na Kinape kuwa asiondoke ili wazungumze. Kama kawaida Kinape alijichelewesha kwenda kazini. Baada ya Deus kuondoka alimfuata chumbani kwake ili apate muafaka wa jambo walilozungumza jana yake. “Mhu! Umefikia wapi?” Kilole alimuuliza Kinape. “Kuhusu nini?” “Kuhusu huyo mwanamke wako.” “Kwa kweli bado sijapata jibu, tena jana Deus ndio kaniachanganya zaidi.” “Kivipi?” “Amesema kesho niende na Happy kijijini.” “Eti nini?” Kilole alishtuka kusikia habari zile. “Mumeo kasema kesho niende na gari kanipa ili kuhakikisha sina cha kujitetea.” “Wewe ulimjibu nini?” “We unafikiri ningemjibu nini?” “Si ungemwambia umebadili umamuzi kuwa hutamuoa tena Happy.” “Ningeanzia wapi wakati kila siku nimekuwa nikiomba msaada wake kufanikisha ndoa yangu.” “Mmh! Kumbuka akiishafika kijijini mimi sina changu.” “Lakini kwa nini tulazimishe mambo wakati yamekwisha onesha vikwazo?” “Kinape hunielezi lolote nikakuelewa, nimejitoa kwako sitarudi nyuma.” “Sasa nitafanyaje maana leo jioni happy na mama yake watakuja kujua hatima ya uchumba wetu.” “Lakini kwa nini tusimfutilie mbali Deus, huoni anatuwekea kivingu?” “ Ni haraka sana kufanya mambo hayo, kuna kitu kimoja kizuri tukifanya haraka tutakipoteza.” “Kitu gani?” “Mwezi ujao kuna bilioni kama mbili hivi zinaingia kwa hiyo tukizipata tutakuwa na uwezo wa kuishi nchi yoyote tuitakayo.” “Lakini kumbuka kila siku unaongeza siku mwisho wake picha zitamfikia na kuharibu kila kitu.” “Kilole tutakuwa wajinga kuziacha hizo bilioni mbili za bure.” “Tutazitoa wapi?” Kinape alimueleza yote aliyoelezwa na Deus juu ya mpango wa kuhongwa na wauza dawa za kulevya. “Nimekuelewa.” Alimkubalia ili kumaliza mazungumzo lakini moyoni alipanga wiki ile lazima afanye kitu ambacho kitakuwa simulizi midomoni mwa watu. Baada ya Kinape kuondoka kwenda kazini, Kilole alijikuta akizidi kuchanganyikiwa na kujiuliza aanze na nani kati wa watu wote watatu, mumewe, Jimmy na Happy mchumba wa Kinape. Aliamini mtu wa kuanza naye alifaa kuwa Happy kwa kumzima usiku wa siku ile ili kuzuia safari ya kwenda kijiji, kisha Jimmy na mwisho alipanga kummaliza mumewe. Mpango ule aliufanya kwa siri ili mtu yeyote asijue kwa kuamini kama angemshirikisha Kinape angemuharibia kila kitu. Wazo alilopata la kummaliza mumewe aliona anahitaji msaada wa mtu, na mtu wa karibu alikuwa Jimmy. Aliamini msaada wake ulikuwa muhimu lakini mwisho wa yote na yeye angemmalizia mbali. Baada ya kukubaliana na mawazo yake aliamua kumpigia simu Jimmy ili mpaka jioni mpango wake wa kummaliza mumewe ukamilike ibakie kuutekeleza. Baada ya kupiga simu ya Jimmy iliita upande wa pili na kupokelewa. “Haloo.” “Haloo Jimmy.” “Ndiyo sister.” “Samahani Jimmy nina shida na wewe.” “Shida gani?” Sauti ya upande wa pili ilionesha kushtuka. “Nitakueleza tukionana, sema tuonane wapi.” “Njoo nyumbani kwangu.” “Sawa nakuja.” “Nitakuwa nyumbani baada ya nusu saa.” “Hakuna tatizo nitafika kwa muda huo.” Dakika tano baada ya kumaliza mazungumzo na Jimmy, simu ya Kilole iliita alipoitazama ilikuwa namba ngeni. Aliipokea. “Haloo.” “Eeh! Umefikia wapi?” “Kuhusu nini?” Japo sauti iliijua alijifanya kuuliza. “Hiyo milioni kumi ipo tayari?” “Kesho itakuwa tayari.” “Sihitaji kesho nataka leo.” “Okay, hakuna tatizo jioni ya leo nitatimiza kila kitu.” “Na ufanye hivyo, kinyume na kauli yako kila kitu hadharani.” “Wala usihofu, itanibidi nichukue fedha ya ujenzi wa nyumba nitazirudisha kesho.” “Nakutakia siku njema.” “Na wewe pia.” Kilole baada ya kukata simu alishusha pumzi ndefu na kujikuta akili yake ikifanya kazi kama kompyuta kwa kupata jibu. Ilionesha muda alioweka Jimmy ulikuwa ni kuwasiliana na jamaa yake ili kutaka kujua fedha yao. Alicheka kwa uchungu na kuamini siku ile mpaka inakatika itabaki kumbukumbu akilini mwake. Alikwenda kujiandaa kisha alitoka hadi kwenye mashine ya kuchukulia fedha na kuchukua milioni ishirini ambazo aliamini zingemsaidia kuifanya kazi yake vizuri. Baada ya kuziweka vizuri fedha zake aliingia kwenye gari na kwenda moja kwa moja kwa Jimmy. Alimkuta Jimmy yupo nyumbani, kwa vile chumba alikuwa akikijua alikwenda kugonga mlango. “Karibu,” Jimmy alitoka akiwa kifua wazi. “Ooh! Sister karibu.” “Asante nimekaribia,” Kilole alijibu huku akiingia ndani. Ndani ya chumba cha Jimmy hakukuta mabadiliko makubwa zaidi ya tivii ya flati na friji ndogo. Alikaa kwenye kochi wakati huo Jimmy alikuwa akielekea chumbani kuchukua fulana. Macho ya Kilole yaliona kitu kilichomshtua, kiuoni kwa Jimmy kulikuwa na mchoro ambao ulifanana na mchoro aliouona kwenye kiuno cha mtu wa kwenye picha ya watu waliombaka. Moja kwa moja ushahidi wake ulikamilika alijua Jimmy ni mmoja ya watu waliombaka, alijilaumu kwa kuondoka bila siraha ambayo ingemsaidia kumaliza kazi kwani ushahidi wa kutosha kuwa Jimmy ndiye mbaya wake ulikuwa umetimia. Lakini bado aliamini Jimmy alikuwa kiungo muhimu wa kufanikisha mpango wake kabambe utakaomuwezesha kutimiza lengo lake.
Baada ya Jimmy kutoka chumbani akiwa amevaa fulana alikaa pembeni kidogo na Kilole. “Ndiyo sister karibu sana.” “Asante sana, mbona ndugu yangu umenitupa?” Kilole alijifanya kuchangamka japo moyoni alikuwa na hasira za kuua mtu. “Nikutupe wapi wakati kila kukicha mambo afadhari ya jana.” “Samahani sister unatumia kinywaji gani?” Jimmy aliuliza huku akinyanyuka kuelekea kwenye friji. “Walaa usisumbuke nashukuru.” Jimmy alirudi kukaa kumsikiliza Kilole aliyeonekana na haraka. “Sasa ni hivi nahitaji msaada wako wenye malipo mazuri sana.” “Kazi gani tena sister?” “Nina imani michongo ya mjini unaiju vizuri nilikuwa nahitaji unga.” “Unga! Upi?” Jimmy alishindwa kumuelewa. “Kokeni.” “Ha! Wa nini?” alizidi kushtuka. “Dada yako najidunga muda mrefu lakini mtu aliyekuwa akiniletea amesafiri hivyo napata shida sana kubembea.” “Mmh! Wa shilingi ngapi?” “Kwa vile kuna watu wangu nao wana shida nilikuwa nahitaji wa milioni kumi.” “Ha! Mbona mwingi?” “Tatizo mwingi au niupate, mbona kila kitu unashangaa.” “Mmh! Ulikuwa unautaka lini?” “Leo hii na fedha ipo.” “Na kamishina yangu kiasi gani?” “Wewe unataka shilingi ngapi?” “Si unajua kazi za hatari hata laki mbili siyo mbaya.” “Nitakupa milioni.” “Ooh! Asante sana.” “Samahani Jimmy simu yako ina salio nataka nimpigie mtu wa tigo,” Kilole ambaye siku zote alijengwa uwezo wa kufanya mambo na mumewe Deus hata kumfundisha jinsi ya kutumia siraha kwa utimilifu tena kwa uhakika mkubwa. Aliamini kupitia simu ya Jimmy ataweza kuipata namba ya mwenzake ambayo ingemsaidia kumfahamu na kuweza kumtia mikononi. Jimmy bila kujua alimpa simu yake, Kilole aliichukua na kujifanya anaingiza namba, kila alilofanya alimuangalia Jimmy ambaye hakuwa na habari naye. Aliangalia simu iliyoingia jana yake usiku muda ambao yeye alikuwepo pale, baada ya kuiona ili kujiridhisha aliangalia iliyopigwa muda mchache baada ya Jimmy kutoka nje. Jina lilikuwa moja la Rich. Baada ya kunukuu akilini ile namba alimrudishia simu yake, Jimmy naye bila kuhoji aliipokea simu yake. Kilole alinyanyuka kwenye kochi na kuanza kutoka nje. “Basi twende kwenye gari nikakupe hiyo fedha ili jioni nije niuchukue mzigo.” Baada ya kusema vile Kilole alitangulia kwenye gari na kumsubiri Jimmy alipokuja alimuhesabia milioni kumi na moja kisha waliagana. “Jimmy nakutegemea, basi usiniangushe kama zile picha ambazo ninanitia wazimu.” “Ooh! Ina maana bado wanakusumbua?” “Hawana lolote shida yao fedha sina jinsi nitawapa.” “Ooh! Pole sana.” “Ya kawaida, la muhimu nifanyie kazi yangu vizuri.” “Hakuna tatizo sister kazi yako nitaifanya vizuri.” Kilole baada ya kuondoka njiani aliwaza mengi huku hasira zikumpanda kichwani na kutamani kuwafanyia kitu kibaya. Lakini alikumbuka upumbavu wote anaoufanya ni kwa ajili ya kutetea penzi lake kwa Kinape. Hivyo alitakiwa kuwa makini kutekeleza mipango yake bila kumshirikisha mtu moja kwa moja hasa ya mauaji. Kilole alirudi nyumbani kujipanga kuhakikisha kazi yake ya usiku wa siku ile anaifanya kwa umakini mkubwa japo moyo mwingine ulimshauri aachane na mpango ule wa hatari. Lakini upande wingine aliamini maji kaisha yavulia nguo lazima ayaoge na liwalo na liwe. *** Wakati Kilole akipanga mkakati wa kummaliza Happy mchumba wa Kinape ili kuhakikisha haendi kijijini. Kinape naye alikuwa na mazungumzo na mpenzi wake sehemu tulivu waliyochagua, ambaye alikuwa akiteseka na mabadiliko ya mpenzi wake yaliyoonekana kutishia uhusiano wao. Kinape pamoja na kujitahidi kuwa karibu na Happy lakini muda mwingi alibanwa na Kilole ambaye nia yake ilikuwa kuuvunja uhusiano ule. “Kinape pamoja na kusema kesho unakwenda kunitambulisha kwenu bado siamini najua ni kunipoza moyo lakini hunipendi tena.” “Happy kama kusingekuwa na umuhimu wa kwenda kukutambulisha kwetu ningekaa kimya usingejua nini kinaendelea?” “Kinape lakini umegeuka kiasi hiki, nini nimekukosea?” Happy aliuliza kwa sauti ya kilio. “Mambo yameingiliana tu lakini muda si mrefu kila kitu kitakuwa sawa,” Kinape alijitetea. “Kuna kitu unanificha, Kinape una mwanamke mwingine.” “Sina mwanamke mwingine zaidi yako.” Kinape alijitetea japo alijua ana mtihani mzito kwa Kilole, moyoni mwake hakuwa tayari kumsaliti Deus rafiki yake kwa ajili ya mpenzi wake wa zamani. Kilichomuumiza kichwa kilikuwa ni picha za kufanya mapenzi na Kilole ambazo kwake aliamini zilikuwa bomu ambalo kama lingepasuka kusingekuwa na usalama. Moyo alijipanga kuhakikisha anamfahamu aliyefanya mchezo ule, akiwa katikati ya mawazo Happy alimshtua. “Ha..ha..lafu mbona simuelewi shemeji yako?” “Umuelewi kivipi? Kinape alishtuka kidogo. “Asingekuwa mke wa kaka yako ningesema mwanamke wako.” “Kwa nini unasema hivyo?” “Kuna kila dalili za kuwepo siri nisiyojua kuhusu mustakabali wa penzi langu kwako. Mimi si wa kukatazwa kuingia ndani kwenu, hata kama haupo bado nina haki ya kuja kwenu.” “Nimekuelewa lakini kila kitu kitakwenda vizuri, naomba uniamini na kesho ndiyo siku yako ya kuamini kuwa penzi letu lipo hai.” “Mmh! Nitaamini mpaka nitakapokuwa mbele ya wazazi wako na kunitambulisha kuwa mimi ni mpenzi wako mkeo mtalajiwa.” “Tena tumepewa lile lexus kwenda nayo kwa raha zetu.” “Usiniambie!” Happy alifurahi kwa kumkumbatia Kinape na kujisahau kama muda mfupi alikuwa akilaumu. “Hii yote kukuonesha jinsi gani ninavyo kujali na ahadi niliyokuahidi ni ya kweli.” “Asante sana mpenzi wangu.” “Si hilo tu, brother amenipa jana milioni 50 kwa ajili ya maandalizi ya harusi yetu.” “Jamani yaani matamani siku ifike niwe nisimame pembeni yako nikiulizwa: Happy Kinape unakubali kuolewa na Kinape kama mumeo?” “Mmh! Utajibu nini?” “Ndiyooooooo, tena mara mia.” “Basi nikuache akajiandae na safari, kesho alfajiri nakupitia.” “Sawa mpenzi wangu, katika siku ambayo nitakula chakula kiteremke sehemu zake ni leo, na siku tukifunga ndoa sijui itakuwaje bado naona ndoto ya mchana.” “Nina imani kuanzia kesho utakula na kunywa kwa furaha baada ya kukuvisha pete ya milioni kumi.” “Haaaa!” Happy alishika mikono kifuani asiamini masikio yake. “Nataka uamini ile ahadi niliyokuahidi inatimia.” “Kinape amini usiamini mabadiko yako kama yangeendelea kidogo nilikuwa nimewaza kufanya kitu kibaya.” “Kipi tena mpenzi wangu?” “Haki ya nani, leo isingepita salama nilipanga kunywa sumu nifilie mbali.” “Aah! Happy mawazo gani tena hayo mpenzi wangu?” “Hujui tu, nimeteseka sana, nimeumia sana, hebu nitezame mimi ndiye Happy unayemfahamu nimekuwa kama mti uliokauka.” Happy alizungumza huku akiangua kilio ambacho kilikuwa sawa na kukamua uchungu wa moyo kutokana kuteswa na penzi la Kinape baada ya kutekwa na Kilole. “Happy mpenzi wangu yote hayo yatakwisha hata mimi najua kosa langu lilikuwa wapi.” “Naomba usinitende nakupenda sana Kinape, sioni sisikii juu yako, bila wewe mimi sipo,” Happy aliendelea kusema huku akibubujikwa na machozi. “Basi mpenzi nimekuelewa nina imani nilikuumiza lakini nakuahidi kutuliza maumivu yako yote.” Kinape alimpeleka Happy kwao na kuamua kwenda club ili aingie nyumbani usiku sana asionane na Kilole na alfajiri awahi kuamka na kuondoka ili kumkwepa. **** Majira ya jioni akiwa amejipumzisha nyumbani kwake alipokea simu ikiulizia mzigo wao. “Vipi umefikia wapi?” “Kila kitu kipo sawa ila sasa hivi nina wageni muhimu naomba univumilie kidogo.” “Mpaka saa ngapi?” “Sijajua ila lazima usiku huu nikupe mzigo wako wote kwa vile nimekwisha uandaa kabisa.” “Sasa tuambie saa ngapi?” “Nimepanga baada ya mume wangu kulala nitoke mara moja, ila nilikuwa naomba uje karibu na nyumbani ili nikikukabidhi nirudi haraka kabla mume wangu hajashtuka kama nimetoka.” “Kwa hiyo saa ngapi?” “Kuanzia saa sita usiku ila uhakika saa saba.” “Hakikisha muda huo unatupa mzigo wetu ukifanya ujanja wowote picha zako zitasambaa kila kona ya jiji.” “Walaa usitie hofu nilichowaeleza kitakwenda kama nilivyopanga, naomba usikae mbali na simu yako ili nikikupigia utokee na kuchukua.” “Nimekuelewa baadaye.” Kilole baada ya kukata simu alicheka na kuuapia moyo wake usiku wa siku ile utabakia historia nzito moyoni mwake. Majira ya saa moja na nusu usiku Kilole alipigiwa simu ya Jimmy kumjulisha kupatikana kwa mzigo, walielekezana pa kuonana. Alikwenda eneo la tukio na kupewa unga wake wa shilingi milioni moja. Baada ya kuupata aliamini kabisa utamsaidia kuifanya kazi yake kwa uhakika mkubwa. Aliagana na Jimmy na kurudi zake nyumbani na kuuficha sehemu ambayo mumewe hawezi kuiona. Baada ya kuweka mzigo vizuri alichukua bastola ya mumewe na kuichunguza kama risasi, alikuta za kutosha aliamini zitafanya kazi yake ya usiku ule aliiweka vizuri kwa kazi ya usiku ule. Alichota unga kidogo na kuuweka kwenye chakula cha mumewe ili akila alale na yeye aweze kutoka usiku ili akafanye kazi yake nzito ambayo ilimpa mtihani mzito. Baada ya kuipanga mipango yake vizuri, alitulia kusubiri muda. Mumewe baada ya kutoka kazini alimuandalia chakula. Baada ya kula alimuomba waende wakazungumzie chumbani. Waliingia chumbani huku Deus akikisikia kichwa kizito. Hata wakuwahi kuzungumza usingizi mzito ulimpitia. **** Ndani ya jiji Sicily nchini Italia, jiji linalosifika kwa uuzwaji wa dawa za kulevywa,Teddy bado alikuwa na hasira baada ya kugundua shemeji yake ndiye aliyemchoma kwa kitengo cha kuzuia dawa za kulevya Tanzania. Kwake alimuona ni adui mkubwa asiyefaa kuendelea kuishi. Alipanga usiku wa siku ile amuulie mbali na yeye kutimka zake kwenda mji mwingine wa Turin kuanzisha maisha mapya kwa kuamini uwezo wa kifedha ungemwezesha kuishi sehemu yoyote duniani bila tatizo. Baada ya kugundua kuwa shemeji yake ndiye mbaya wake hakutaka kumuonesha kukasilishwa na kitendo kile. Ili kumvuta adui yake alijifanya kubadilisha msimamo kuwa amemkubali kimapenzi. Asubuhi ya siku ile baada ya kifungua kinywa alimwita Mose na kumweleza kitu: “Mose my sweet.” “Teddy kauli hiyo imeanza lini?” Mose alishtuka kusikia anaitwa vile. “Leo mpenzi, nimetafakari na kuona hakuna umuhimu wa kulikataa penzi lako kwa vile wewe ni mwanaume kama wanaume wengine pia kuwa na wewe sawa na kuwa na marehemu kaka yako.” “Umeona eeeh,” Mose alifurahi kusikia vile bila kujua aliyekuwa anazungumza naye si Teddy aliyemzoea bali malaika wa kifo. “Unajua Mose nimekuwa sipati jibu kila nilipojiuliza kwa nini nisikukubalie uwe mpenzi wangu, lakini ujio wa safari yangu Italy ilikuwa kuja kukueleza nimekufungulia moyo wangu kwako.” “Ooh! Asante sana, siamini kwa kweli lazima nikueleze ukweli Teddy nimeteseka kwa muda mrefu juu yako. Nina imani sasa hivi moyo wangu utapoa.” “Najua umeumia kwa muda mrefu, nina imani kama uliteseka juu yangu basi penzi letu litakuwa lenye upendo wa dhati. Mose mpenzi naomba usinitende.” “Teddy amini nitakupa mapenzi zaidi ya kaka, hutajutia kunikubali kuwa mpenzi wako.” Siku ile ilikuwa yenye furaha kwa Mose lakini moyoni kwa Teddy ilikuwa ngumu sana kwake kwa kujipanga kuhakikisha kujirahisi kule kutamlahisishia kummaliza kwa urahisi. Teddy hakuona hiyana kuutoa mwili wake kwa Mose japo alikwisha muapia labda atafanya naye mapenzi akiwa marehemu asiye na fahamu. Siku ile alijitoa ili kumvuta karibu na kuamini kabisa anachokitafuta muda mrefu atakipata. Majira ya mchana Teddy alibuku tiketi ya ndege ya kuelekea Turin saa tatu usiku, baada ya kurudishiwa taarifa ya kupatikana kwa nafasi katika ndege ya usiku ule. Alijipanga kuhakikisha mipango yake inakwenda kama alivyopanga na saa tatu awe kwenye kiti cha ndege akihamia jiji wa Turin kuanza maisha mapya baada ya kummalizia mbali shemeji yake Mose aliyetaka kumpoteza kwenye ramani ya dunia. Baada ya mambo yake kwenda alivyopanga alirudi kwa Mose na kuendelea kunywa katika mahaba mazito. Mose baada ya kulewa sana Teddy alitumia nafasi ile kumpeleleza kupata ukweli. “Mose mpenzi wangu kwa nini ulinichoma?” Teddy alijifanya kulalamika katika mahaba mazito. “Teddy ulinichanganya kimapenzi kwa kweli nilichokifanya hata sielewi nilifanya nini, nilikuwa sawa na mfa maji.” “Lakini usirudie tena, ona sasa kama ningefungwa penzi tamu kama hili ungelipata wapi?” “Nisamehe mpenzi wangu.” Kauli ya Mose ilizidisha machungu moyoni kwa Teddy na kuamini wazo lake na ushahidi aliopata lilikuwa sahihi. Alijitahidi kutengeneza tabasamu la uongo ili kuvuta muda wa kummaliza Mose. Muda wote alionesha mapenzi mazito yaliyomziba masikio asijue nini kilichokuwa kikiendelea.
Majira ya saa moja na nusu Teddy aliamini ule ulikuwa muda muafaka kwake kufanya alichokikusudia, hakutaka kumuua Mose kwa bastora kwa kuhofia sauti yake unaweza kufika mbali. Kwa vile alikuwa amefunga dirisha la chumbani na kuamini sauti haitatoka nje aliona kisu kingefanya kazi yake vizuri kutokana na Mose kulewa sana asingeweza kushindana naye. Wakiwa watupu kitandani Teddy alisema kwa sauti ya mahaba: “Samahani mpenzi.” “Bila samahani,” Mose alijibu kwa sauti ya kilevi. “Nakuja mara moja,” Teddy alisema huku akinyanyuka kitandani. “Basi usichelewe mpenzi, leo moyo wangu una furaha ya ajabu.” “Usihofu leo mimi na wewe mpaka lyamba.” Teddy alikwenda hadi kwenye kabati na kuchukua kisu kikubwa na kurudi nacho kitandani. Wakati huo Mose alikuwa amejilaza chali akiwa amefumba macho kutokana na kunywa kiasi kikubwa cha pombe. Teddy alimkalia tumboni kama anataka kumuandaa kimahaba. Kwa sauti iliyojaa ukatili isiyo na chembe ya huruma alisema: “Wee mbwa Sali sala yako ya mwisho.” “Vipi tena mpenzi?” Mose aliuliza huku alijitahidi kufumbua macho yaliyokuwa mazito kutokana kunywa pombe nyingi kupita kiasi. Macho yake hayakuamini kuona Teddy amemshikia kisu. “Ha! Nini tena?” “Unauliza jibu, nilikueleza nini siku moja?” “Mpenzi mbona sikuelewi.” “Nilikueleza toka mwanzo kuwa hutaugusa mwili wangu labda maiti yangu, lakini leo umeugusa nikiwa mzima ni ishara ya kifo chako.” “Kwa hiyo unataka kuniua?” “Si ulitaka kunipoteza? Sasa nakupoteza wewe.” “Si..si..nimekueleza sa..sa..babu yake,” Mose alijitetea akiwa bado amelala chali mwili haukuwa na nguvu kutokana na kulewa sana. “Fedha yote niliyopoteza baada ya kukamatwa itanunua kifo chako,” Teddy alisema huku akikipunga kisu hewani. “U..u..usi..ni..” hakumalizia alikutana na mapigo ya kisu mfululizo yaliyompiga bila mpangilio. Teddy alimshambulia Mose kwa visu mfululizo kama anatengeneza chujio la nazi. Mose kutokana na ulevi wa kupindukia hakuweza kujitetea. Baada ya kupiga kelele za maumivu kwa muda bila msaada sauti ilizidi kupungua mpaka aliponyamaza kabisa, wakati huo kitanda kizima kilikuwa kimejaa damu kama kachinjwa ng’ombe ambazo zilizomrukia Teddy mwilini. Teddy baada ya kuamini amemaliza kazi, alinyanyuka na kukimbilia bafuni kuoga kisha alibadili nguo na kuchukua vitu vya muhimu na kuhakikisha picha zake zote ameondoka nazo. Baada ya kubeba mizigo yake alikodi gari hadi uwanja wa ndege. Alifika ikiwa imebakia nusu saa ndege iondoke, baada ya kupima mizigo alielekea kwenye ndege na kuketi huku akiomba Mungu aondoke kabla ishu haijashtukiwa. Hakujiamini mpaka ndege alipoondoka katika jiji la Sicily, safari yake ilikwenda vizuri mpaka alipotua katika jiji la Turin salama salimini. Alitafuta hotel yenye hadhi ya nyota tano iitwayo Principi di Piemonte. Baada ya kupata chumba aliagiza chakula na kula kidogo kwani bado picha ya kitendo cha kinyama alichomfanyia shemeji yake ilijirudia akilini mwake. Aliamua kuagiza pombe kali ambayo alikunywa mpaka alipopoteza mawasiliano na kulala alipokuwa amekaa. Alishtushwa siku ya pili na hodi iliyokuwa ikigongwa. Alishangaa kujikuta amelala pembeni ya kitanda kwenye zulia. Aliponyanyuka alizidi kujishangaa kukuta haja ndogo aliimalizia pale bila kujielewa kutokana na kunywa pombe nyingi kupita kiasi. Alinyanyuka na kukimbilia bafuni na kuchukua cha kufutia kisha alifungua mlango. “Za saizi?” mhudumu alimsalimia. “Nzu..nzuri, karibu.” “Asante, nilikua naomba kufanya usafi.” “Kwani sasa hivi ni saa ngapi?” “Saa tano.” “Ooh! Kumbe nimelala sana.” “Inaonesha ulikunywa sana.” “Okay, fanya haraka usafi nataka kupumzika.” Teddy alimwacha mhudumu afanye usafi, baada ya kufanya usafi alioga na kuagiza kifungua kinywa kisha alizimua kidogo. Akiwa amejipumzisha kwenye sofa huku akinywa whisky taratibu, tukio la jana yake lilimjibu kwenye akili na kujikuta akiwasha luninga labda habari za kifo cha Moze kitatangazwa. Alifungua luninga ya taifa, alikuta kuna matangazo ya magazeti na moja ya habari iliyotawala kwenye ukurasa wa mbele ilikuwa yake. Kichwa cha habari kilisomeka unyama wa kutisha, juu kulikuwa na picha ya Mose akiwa amelala kitandani mwili wote ukiwa katika dimbwi la damu. Picha ile ilimtisha alijikuta akifumba macho kwa woga na kuchukua chupa ya whisky na kuipeleka mdomoni kwake na kujaza kiasi kikubwa na kukimeza chote kwa shida huku amefumba macho mpaka mishipa ya kichwa ikamsimama, baada ya kutikisa kichwa alisema kwa sauti ya chini. “Ooh! Mungu wangu, nimemuua Mose kifo kibaya sana.” Akiwa ameinamisha kichwa huku akisikitika na machozi kumtoka kutokana na unyama aliofanya, alinyanyua macho na kushtuka kuona Mose hakufa yupo hospitali ila katika chumba cha wagonjwa mahututi. Akiwa bado anatumbulia macho habari za Mose ambaye alionekana mfu. Alimuona mkuu wa makosa ya jinai akitoa taarifa kuwa mpaka muda ule upelelezi ulikuwa unaendelea ili kujua nani aliyefanya tukio la kikatili kama lile baada ya kukosa ushirikiano wa mgonjwa ambaye alikutwa katika hali mbaya mpaka wakati ule alikuwa akipumua kwa mashine. Taarifa za daktari zilisema mgonjwa kutokana na kupoteza damu nyingi kutokana na kutobolewa na kitu chenye ncha kali aliongezwa damu zaidi ya chupa kumi. Habari zile hazikumfurahisha hata kidogo Teddy na kuamini kama Mose atapona na kutoa ushahidi basi atamtia kwenye matatizo makubwa na akishikwa adhabu yake ni kifo. Wazo la haraka lilikuwa kuondoka ndani ya nchi ya Italy na kwenda kuishi Afrika kati ya nchi ya Tanzania au Kenya. Aliamini upelelezi lazima utajua kuwa ni yeye mhusika aliwasiliana na washirika wake na kukubaliana akajifiche Kenya mpaka hapo mambo yatakapojulikana yamefikia wapi. Bila kupoteza muda alipanda ndege moja kwa moja mpaka Kenya na kwenye kujificha katika jiji la Nairobi katika jumba moja la mshirika wao lililokuwa na kila kitu ndani maeneo ya Kasalani. Mwezi mmoja akiwa anaishi kwa kificho katika jiji la Nairobi aliziona habari na picha yake za kutafutwa kwake kuhusiana na jaribio la kutaka kumuua Mose. Baadhi ya vyombo vya habari na luninga alitoa kila siku sura ya Teddy kutafutwa huku donge nono likitangazwa kwa mtu atakayetoa habari zake na kufanikisha kukamatwa. Taarifa zile zilizidi kumficha Teddy ambaye alikuwa akitoka usiku tu kwenda club za usiku na baada ya hapo alishinda ndani tu. Aliweza kumuona Mose katika hali ya umajeruhi kutokana na shambulio kali la kutaka kumuua. Mwili wake ilionesha kuharibika vibaya hata kuzungumza kwake alizungumza kwa shida. Katika mahojiano na mwandishi wa habari mmoja alimsikia akisema kuwa akipona atamtafuta popote hata kaburini ili kulipa kisasi.
**** Majira ya saa sita za usiku Kinape alijirudisha nyumbani kwa kuamini muda ule Kilole atakuwa amelala. Alipokaribia nyumbani aliona teksi ikisimama mbele kidogo na nyumbani kwao. Aliendelea kusogea kwa vile alikuwa upande wa giza aliweza kuliona lile gari ambalo hata namba zake hazikuwa ngumu kuzinakili kichwani. Kabla ya kupiga hatua alishangaa kumuona mwanamke aliyevaa hijabu na nikabu iliyomziba uso wake akitelemka kwenye teksi na kuelekea kwenye geti la nyumba yao na gari ile kuondoka. Alijuliza ni nani aliyevaa vazi lile kuelekea kwao muda kama ule. Ilibidi atembee kwa taadhari ili kujua yule mwanamke anakwenda kufanya nini kwao muda ule. Alisimama nje ya uzio na kuweza kumuona yule mwanamke akifungua mlango kwa taadhari kubwa, alijiuliza yule mwanamke ni nani au mwizi. Hakutaka kumshtua alitulia kutaka kuona mwisho wake, lakini kilichomshangaza kilikuwa kufungwa mlango kwa ndani. Moja kwa moja alijua yule ni Kilole, lakini swali lilikuwa usiku ule anatoka wapi na katika vazi lile ambalo hakuwahi kuliona hata siku moja. Hakutaka kupitia mlango wa mbale alizunguka nyuma na kuingia chumbani kwake kwa kutumia dirisha. Mara zote anapojua anachelewa kurudi alilitegesha dirisha na aliporudi aliingilia kupitia dirishani. Baada ya kuingia ndani alibadili nguo na kwenda kuoga na kurudi kulala ili alfajiri awahi kuamka kabla Kilole hajaamka. Alikumbuka muda wote alizima simu ili kumkwepa Kilole asimsumbue, alipowasha haikuchukua muda simu iliita. Ilikuwa simu ya dada ya mchumba wake, aliipokea. “Haloo shemu.” “She..she..mu,” hakuendelea kuzungumza alivuta kamasi za kilio kitu kilichomshtua Kinape na kutaka kujua kuna nini, kwani simu ilikuwa hewani kwa mbali alisikia sauti kama za vilio. “Haloo shemu,” aliita lakini upande wa pili haukupokea zaidi ya kuendelea kusikia vilio vya upande wa pili. Aliamua kukata simu na kupiga, iliitaka kwa muda mfupi ilipokelewa upande wa pili na dada ya mchumba wake. “Shemu upo wapi?” aliulizwa. “Nyumbani.” “Una habari gani za Happy?” “Sina! Amefanya nini?” alishtuka. “Amefariki.” “Nini?” Kinape alishtuka. “Amefariki,” kauli ile ilirudiwa. “Muongo acha kunirusha roho shemeji.” “Si kukurusha roho ukweli ni huo mchumba wake ameuawa saa mbili zilizopita.” “Hapana sikubali Happy hawezi kufa kirahisi namna hiyo nimeachana naye jioni akiwa na mzima wa afya.” “Hakufa kwa ugonjwa.” “Nini kimemuua mpenzi wangu?” “Ameuawa.” “Nini?” “Ameuawa.” “Na nani?” “Hatujajua ile sasa hivi tunaupeleka mwili wa Happy hospitali.” “Nakuja sasa hivi.” Kinape alikata simu na kujikuta akichanganyikiwa kwa kuvaa fulana na taulo. Alikwenda moja kwa moja kugonga katika mlango wa Deus kumjulisha taarifa za mchumba wake Happy. Aligonga mlango kwa muda, Deus aliyekuwa kama yupo ndotoni alishtuka na kunyanyuka hadi mlango. Alipofungua alikutana na Kinape aliyekuwa akitokwa na mchozi na macho yalikuwa mekundu kuonesha ana tatizo zito. Deus alishtuka na kutaka kujua rafiki yake kipi kimemsibu usiku mkubwa kama ule. “Best vipi?” Kinape alishindwa kuzungumza alijitupa kifuani kwa Deus na kuangua kilio bila kusema neno. “Best kuna nini?” “Happy.” “Happy amefanya nini?” “Amefariki.” “Wewe! Acha utani, si leo asubuhi mnakwenda kijijini?” Deus alishtuka na kumshika Kinape mabegani na kumsogeza mbele yake ili kumtazama vizuri. “Ndiyo, lakini nimepigiwa simu muda huu amefariki.” “Alikuwa akiumwa?” “Hapana.” “Nini kimemuua?” “Na..na..sikia.. ameuawa.” “Ameuawa! Na nani?” “Hata wao hawajui.” “Mwili wa marehemu upo wapi?” “Wameniambia ndiyo wapo njiani kuupeleka hospitali.” “Unasema kauawa, kivipi?” “Hata najua, nakwenda kujua huko huko.” “Nisubiri basi tuongozane.” Deus alirudi chumbani kumjulisha mkewe habari za Happy. “Mke wangu,” alimwita huku akimtikisa. “A.aa..bee mume wangu.” “Kuna tatizo limetokea.” “Tatizo gani tena?” Kilole aliuliza huku akifikicha macho. “Happy amefariki.” “Nini?” Kilole aliuliza kwa mshtuko. “Happy amefariki.” “Acha utani, Happy mchumba wa shemeji Kinape?” “Ndiyo.” “Muongo, si kesho wanakwenda kijijini kumtambulisha?” “Ndiyo.” “Nini kimemuua?” “Nasikia ameuawa saa mbili zilizopita.” “Sasa inatakuwaje, kwani Kinape yupo wapi?” “Yupo ananisubiri twende hospitali.” “Sasa hospitali kufanya nini ikiwa mnasema amekwisha kufa?” “Wamesema wanaupeleka mwili wa marehemu.” “Kwa hiyo twende wote?” ”Hapana nilikuwa nakutaarifu tu.” Wakati Deus akibadili nguo ili awahi hospitali, Kilole alitoka nje na kilio hadi kwa Kinape na kujitupa kifuani kwake. “Maskini shemeji yangu nini kimemsibu mke mwenzangu?” “Ha..ha..ta sijui.” “Kinape tuwahi nipo tayari,” Deus alisema huku akimtoa Kilole kifuani kwa Kinape. “Okay twende.” “Mbona hujabadili nguo?” “Mbona nipo sawa.” “Sasa utakwenda na taulo?” Kinape alipojiangalia akijikuta amejifunga taulo, alikimbilia ndani kubadili kisha walitoka kuwahi hospitali.
Walipofika walikuta mwili wa Happy ndiyo umefikishwa muda mfupi ukiwa bado upo katika gari la polisi, dada yake Happy alipomuona Kinape alimkimbilia na kujitupa kifuani kwake na kuangua kilio cha sauti. “Ooh! Shemeji mdogo wangu wamemuua.” “Hapana si kweli Happy hawezi kufa kirahisi namna hiyo,” Kinape alisema kwa sauti ya juu huku akimkumbatia shemeji yake. “Kweli mdogo wangu amekufa, yaani wamemuua kama jambaziii…amewakosea nini mdogo wangu mimiii,” dada yake Happy aliendelea kulia akiwa bado amejilaza kifuani. Wakati huo kitanda cha kuuchukulia mwili wa Happy uliokuwa umefunikwa shuka kilikuwa kimesogezwa karibu kabisa na gari la polisi. Kinape alijitoa kwenye mikono ya dada yake Happy na kwenda kwenye gari la polisi wakati huo askari walikuwa wakiushusha mwili wa Happy uliokuwa ulifunikwa na shuka jeupe lililojaa damu. Baada ya kuulaza mwili juu ya kitanda cha magurudumu, Kinape alisogea karibu kabisa akiwa bado haamini kama kweli mpenzi wake Happy amekufa. Aliishika shuka upande wa kichwani na kuanza kuifunua huku mikono ikimtetemeka. Macho yake yalikutana na uso wa Happy aliyeonekana kama umelala. “Happy mpenzi wangu amka,” alimwita kwa sauti huku akimtikisa taratibu. “Shemeji amekufa mdogo wangu,” dada Happy ambaye alikuwa akilia kuliko watu wote waliokuwa pale alikwenda kuungana na shemeji yake ambaye alikuwa bado akiona kama kiini macho kilichokuwa mbele yake. “Happy mpenzi wangu amka huwezi kufa kirahisi mpenzi wangu, huwezi kuniacha peke yangu, leo asubuhi tunakwenda kwa wazazi wangu wakakutambue. Hata kaka Deus yupo hapa ametoa gari ili lake la kifahari ili nikupeleke kijijini…Amka mpenzi amka ni wewe peke yako niliyekuchagua… Hapiiiiiiiiii,” Kinape alimtikisa kwa nguvu ili aamke lakini mwili ule haukuwa na uhai. Kinape alilia kwa uchungu, Deus alimchukua na kumuondoa kwenye kitanda na kumpeleka pembeni kumbembeleza. “Deus niache huu ni unyama wa hali ya juu, inaniuma kwa nini wamuue mpenzi wangu nimewakosea nini?” alisema huku akipiga chini. “Pole rafiki yangu, kazi ya Mungu haina makosa.” “Noooo, hapana hii si kazi ya Mungu ni mashetani wasiopenda kuona Kinape na Happy wanaoana.” “Basi…basi, wewe mwanaume unatakiwa kuyashinda maumivu ya moyo wako,” Deus aliendelea kumbembeleza. “Yaani Happy…hata siamini haiwezekani Happy hajafa,” Kinape alimponyoka Deus na kukifuata kitanda kilichokuwa kikielekea chumba cha uchunguzi kabla ya kupelekwa Mochwali. Alichepua mwendo huku akimwita kwa sauti kama anamsikia, lilikuwa pigo mujalabu ambalo hakulitegemea kipindi kile. “Jamani mnampeleka wapi mpenzi wangu, Happy hajafa amelala mwambieni aamke leo asubuhi nakwenda kumtambulisha kwa wazazi,” kifo cha ghafla cha Happy kilimchanganya Kinape na kuonekana kama chizi. Lakini Deus alimuwahi na kumketisha chini rafiki yake. “Kinape hebu kuna kuwa na moyo wa kiume.” “Siwezi, siwezi Deus inauma sana.” “Najua inauma lakini imekwisha tokea kinachotakiwa kutafuta chanzo cha kifo chake.” Baada ya kuufanyia uchunguzi mwili wa Happy alipelekwa mochwali kwa ajili ya kusubiri kuchukuliwa na kwenda kuzikwa. **** Kilole alijikuta akijigeuzageuza kitandani akiyakumbuka matukio yote aliyoyafanya usiku ule. Moyo ulimuuma kwa kitendo cha kikatili lakini hakuwa na jinsi ilikuwa lazima afanye vile ili kupata anachokitaka. Matukio yalipokuwa yakijirudia kichwani alikwenda hadi kwenye friji ndogo ya chumbani na kuchukua chupa ya pombe kali na kunywa glasi nzima. Baada ya kunywa alijikuta akipitiwa na usingizi na kujilaza nusu ya kitanda, Deus aliporudi toka hospitali alishangaa kumkuta mkewe aliyemwacha amelala akiwa katika hali ya ulevi. Alimshtua toka usingizini kwa kumwita na kumtikisa ili alale vizuri. “Mke wangu.” “Tafadhali, mimi sijamuua Happy,” Kilole alikurupuka usingizini baada ya kumuona mumewe amemsimamia mbele yake. “Nani kakuambia umemuua?” “Sa..sa mahani mume wangu,” Kilole alijibu kwa sauti ya kilevi. “Mbona umekunywa pombe?” “Hivi kweli Happy amekufa?” “Kweli amekufa.” “Basi kila dakika ananijia ndotoni, nikaamua bora ninywe pombe kali nilale fofofo.” “Ooh! Pole sana.” “Umefikia wapi?” “Tumerudi kila kitu kitakuwa asubuhi ya leo.” **** Siku ya pili asubuhi wakiwa sebuleni Kilole na Deus wakimsubiri Kinape atoke chumbani ili wawahi msibani huku macho yao yalikuwa kwenye runinga katika taarifa ya habari ya asubuhi ile. Katika taarifa ile ya habari vilitangazwa vifo vya watu watatu vilivyotokea usiku wa kuamkia siku ile waliouawa kwa risasi. Mmoja wa maiti hizo alikuwemo mchumba wa Kinape, Happy, wengine waliouawa ni Jimmy mpiga picha na rafiki yake Rich. Deus alishtuka kuona na Jimmy amekufa mtu aliyekuwa akimfahamu kwa kumpiga picha nyingi zikiwemo za birthday na mkewe. Taarifa ya habari ilielezea kwa ufasaha vifo vile kuwa mwili wa Happy ilikutwa nje ya geti la nyuma yao na miili mingine ya wanaume wawili Jimmy na Rich ilikutwa katika chumba cha Jimmy wote wakiwa wameuawa kwa risasi. Pia taarifa iliongeza kupitia mashahidi majirani wa nyumba ile kuwa usiku wa saa sita walimuona mwanamke mmoja aliyekuwa amevaa hijabu iliyomziba mwili wote aliyeingia mule ndani. Kwa vile hawakuwa na wasiwasi naye hawakujishughulisha naye lakini baadaye katikati ya usiku waligundua Jimmy hajafunga mlango kitu ambacho hakikuwa kawaida yake. Walipokwenda ndani ndipo walipokuta tukio lile la kutisha. Zilioneshwa picha za Jimmy na Rich zilivyokuwa zimelala kwenye kochi na sakafuni. Lakini maiti ya Happy haikuonekana kutokana na kuchelewa kwa taarifa kufika kwenye vyombo vya habari. Kinape aliyekuwa ndiyo anafika sebuleni aliliona tukio lile. Kilichomshtua ni picha ya Jimmy. “Jamani huyu si Jimmy mpiga picha?” “Ndiye mwenyewe.” “Mungu wangu na yeye kafanya nini?” “Tena nasikia muuaji ni mwanamke,” Deus alimwambia Kinape aliyekuwa amesimama nyuma ya kochi waliokalia. “Mwanamke!” Kinape alishtuka. “Ndiyo, tena alikuwa amevaa hijabu iliyomzima mwili wote.” “Unataka kuniambia ndiye aliyemuua Happy?” “Walaa, mume wangu hawakusema yule mwanamke ni muuaji bali ndiye aliyeingia chumbani kwa Jimmy,” Kilole alipinga kauli ya mumewe. “Kwa nini ujifiche lazima atakuwa muuaji.” “Jamani tuachane na hayo tuwahi msibani tukajue nini kinaendelea,” Kinape alikatisha ubishani wa mtu na mkewe. Wote walinyanyuka kuelea nje kwenye gari, njiani wakiwa ndani ya gari kauli ya Deus kuhusiana na msichana aliyemshtumu kuvaa hijabu ilimshtua na kukumbuka jinsi alivyo mshangaa Kilole aliyekuwa amevaa usiku ule. Alijiuliza kama ni yeye aliyefanya mauaji yale alifanya kwa lengo gani. Alizidi kujiuliza kuhusu kifo cha Happy anaweza kuwa pia ni yeye? ***** Msibani watu walikuwa wengi huku kila mmoja akizungumza la kwake, wengi walikuwa walionekana na huzuni hasa familia ya Happy baba, mama na dada yake ambaye alilia mpaka kupoteza fahamu. Mashoga zake nao walichanganyikiwa kwani walikuwa katika maandalizi ya harusi ambayo walipanga iwe ya kukata na shoka baada ya kuelezwa siku ile ndiyo ilikuwa ya kwenda kutambulishwa kijijini kwa mchumba wake. Kinape naye muda mwingi alikuwa amekaa chini kutokana na kutokuwa na nguvu za kusimama. Deus alitumia muda wake mwingi kuwa karibu ya rafiki yake kumfariji kwani kila rafiki na ndugu wa Happy walipolia naye aliporomokwa na machozi. Kila aliyekuwepo msibani uso wake ulijaa simanzi nzito kutokana na kifo Happy msichana aliyekuwa bado mbichi pia mwenye malengo mazito katika maisha yake. Lakini ilikuwa tofauti kwa Kilole na wote waliokuwepo msibani, moyo wake ulijaa furaha kwa kutimiza lengo lake la kuweza kuuvunja uchumba wa Kinape na Happy ambao aliamini hautaunganika mpaka mwisho wa dunia. Wakati watu wakiendelea kulia huku ibada ikiendelea kabla ya kuuchukua mwili wa Happy haujaenda kupumzishwa Kilole alijikuta akivuta kumbukumbu ya matukio ya kikatili aliyoyafanya jana. Aliamini kabisa kwa Happy alifanya unyama wa hali ya juu, lakini kwa Jimmy na rafiki yake ilikuwa ni kulipa kisasi cha kubakwa kwani aliamini adhabu ya mbakaji Uarabuni au China ni kifo. Pia alikuwa kutimiza kile alichomuahidi Jimmy kama picha zake zitavuja basi angemfanyia kitu kibaya. Aliamini vifo vyao vilibakia simulizi ndani ya vinywa vya watu. Alianza kukumbuka jinsi alivyotoka nyumbani baada ya kuhakikisha mume wake amelala fofofo baada ya kumwekea madawa kwenye chakula. Kwanza alimpigia simu Kinape ajue yupo wapi kwani alipanga na yeye siku ile naye angelishwa chakula kile na kulala fofofo ili aweze kutoka bila kutiliwa wasiwasi na mtu. Lakini simu ya Kinape haikuwa hewani ile haikumsumbua sana japo wasiwasi wake aliwaza huenda wapo pamoja na Happy. Baada ya kuvaa vazi lake lililomziba mwili mzima, alichukua bastora ya mume ambayo aliikagua na kukuta risasi za kutosha. Alichukua na kiwambo cha kuzuia sauti. (bomba linalowekwa mbele ya bastora au bunduki kuzuia sauti) Baada ya kuviweka vitu vyake vizuri alikwenda hadi kwenye bodaboda na kukodi. “Samahani kaka angu, Masaki shilingi ngapi?” “Masaki ipi?” “Mwanzoni kutokea Salenda?” “Kwa vile usiku buku ishirini.” “Naomba uniwahishe.” Baada ya kupanda dereva aliondoa pikipiki kwa mwendo wa kasi kidogo, Alipokaribia nyumba ya kina Happy aliomba ashushwe mbali kidogo. Kwa vile muda ule magari hayakuwa mengi alitumia dakika kumi tu. “Nina imani umewahi?” dereva wa bodaboda alimuuliza huku akipaki pikipiki. “Ndiyo ila naomba unisubiri hapa.” “Dada mbona unanitisha?” aliogopa kukabwa. “Hapana kaka yangu, bado kuna sehemu nakwenda, nafika nyumbani mara moja narudi sasa hivi.” “Na fedha yangu?” “Chuku hii nikirudi tutapatana tena,” Kilole alipa dereva elfu arobaini. “Poa wahi basi.” Kilole alichepua mwendo kuwahi nyumbani kwao na Happy ambapo palikuwa na kipande chenye giza kutokana na nyumba za sehemu ile kuachana eneo kubwa. Alipokaribia alitoa simu yake ambayo aliiseti sauti ambayo muongeaji huwezi kuijua sauti yake mara moja hata laini alikuwa ameinunua siku ileile ambayo ilikuwa haijasajiliwa. Baada ya kujipanga alipiga simu ya Happy ambaye alikuwa amejilaza kitandani akiwaza safari ya kesho yake ambayo alijiuliza sijui itakuwaje atakapo kutana na wazazi wa Kinape mwanaume aliyemkabidhi moyo wake. Happy aliichukua simu yake na kuitazama namba ambayo ilikuwa ngeni kwake, aliipokea. “Haloo.” “Haloo Happy hongera shosti.” “Ya nini?” “Yaani kumbe kesho unakwenda kutambulishwa ukweni hujanijulisha.” “Lakini hiyo si kwenda kutambulishwa lakini mambo bado, nikirudi kila kitu kitakuwa wazi, lakini mazungumza na wewe bado asijakufahamu sauti yako?” “Mimi Betha,” Kilole alimdanganya. “Betha yupi?” “Happy hilo si muhimu kama hili ninalotaka kukueleza?” “Lipi tena hilo?” Happy alishtuka na kujiweka vizuri kitandani. “Najua naweza kuonekana mbeya lakini lazima niseme juu ya tabia za mchumba wako Kinape.” “Tabia gani?” “Japo kweli ni mchumba wako lakini si muaminifu, hivi ninavyozungumza yupo nje ya gari tulilokuja nalo na shoga yangu wakilana denda kibaya zaidi ni jirani na nyumba yenu kweli huu ni ustaarabu?” “U..u..unasema?” Happy aliingia kigugumizi. “Tena kama unaweza wahi uwafumanie ‘live’ ukichelewa hata dakika kumi Kinape ataondoka.” “Okay, nakuja.” Happy bila kumweleza mtu alikurupuka kuwahi kumfumania Kinape, wakati huo Kilole alijiandaa kummaliza baada ya kujua anakuja. Alitoa bastora na kufunga kiwambo na kumsubiri. Mara alimuona akitokeza kwao akiwa na gauni la kulalia bila hata ya viatu kwani aliamini angevaa kiatu angechelewa kufumania. Kwa vile alikuwa kwenye giza alimuona Happy akisogea upande ule akipepesa macho, alitumia nafasi ile kumpiga risasi mbili za kifuani upande wa kushoto kama alivyoelekezwa na mumewe Deus jinsi ya kuua adui kwa risasi. Alimuona Happy akiruka kwa nyuma hakutaka kuona kinachoendelea alichepua kwendo huku akiiweka bastora ndani ya hijabu. Alipofika alimwambia dereva wa bodaboda: “Tuondoke.” “Tunaelekea wapi?” “Mikocheni B.”
Baada ya msiba Kinape alibakia kwenye kaburi na mpenzi wake ambaye usiku wa jana yake alikuwa naye kabla ya kuagana kuonana alfajiri ya siku ile kwa ajili ya safari ya kijijini. Alibakia ameliinamia kaburi huku msiba kwake ukianza upya. Deus na ndugu na jamaa walimbembeleza sana mpaka alipokubali kuondoka makaburini. Moyoni aliapa lazima atamshikisha adabu aliyehusika na kifo cha Happ. Mwanzo alikuwa na wasiwasi na Kilole, lakini kilio alicholia kumlilia mchumba wake aliamini kabisa hausiki kabisa. Usiku wakiwa nyumbani Deus katika kutafuta vitu kwenye kabati alishtuka kuona kiwambo cha bastola yake kipo kwenye nguo. Alishtuka kwani siku zote hukiweka mbali kutokana na kutotumia sana kutokana na matukio ya kijibizana kwa risasi na wauza madawa ya kulevya kupungua. Alikichukua na kukinusa kilionesha kimetumika, alijiuliza mbona kinanuka baruti kama kimetumika. Wazo la haraka lilikuwa kuikagua bastola, alipofungua droo alishtuka kuona haipo kama alivyoiweka. Aliitoa na kuifungua upande wa risasi, alizidi kushangaa baada ya kuzikuta pungufu ya risasi sita. Alijiuliza bila kupata jibu kuwa risasi zile zimekwenda wapi, alinusa mdomo wa mtutu wa bastora na kukuta umetumika. Alijikuta akipata wasiwasi na kumwita mkewe aliyekuwa sebuleni akizungumza na Kinape ili amulize. Kilole aliingia chumbani bila kujua anaitiwa nini. Alishtuka baada ya kumuona mumewe ameshikilia bastora na kiwambo chake. Mshtuko wake ulikuwa dhahili ambao ulionekana wazi kwa mumewe. Mshtuko ule aliuona na kujua kuna kitu anachokijua mkewe kuhusiana na matumizi ya bastola ile. “U..unasemaje mume wangu?” alisita kidogo. “Nani katumia hii bastola?” alimuuliza kwa sauti ya kiaskari. Kilole aliamini kabisa akibabaika lazima atakuwa swali la kujibu, alitulia kwa muda akipanga la kujibu mume wake ambaye alionekana amekunja uso alilirudia swali lake la mwanzo. “Nakuuliza mbona hunijibu nani katumia siraha yangu?” “Si..si..jui.” “Hujui ina maana mimi ndiye niliyetumia?” “Kama hujatumi wewea nani mwingine anaweza kuitumia hiyo bastora, mimi niitumie kwa kazi gani?” “Hujanijibu nani katumia hii bastola na kiwambo chake pia risasi zangu sita hazipo?” “Sijui.” “Mke wangu sitaki utani nieleze ukweli la sivyo leo utanitambua mimi nani, unaweza kuikodisha kwa watu wafanye uharifu ili mimi niingie matatizoni.” “Mume wangu hiyo imeanza lini, niikodishe ili iweje, nina shida gani mimi?” “Kama huna shida nani kaitumia, kumbuka vitu vyote vinakaa sehemu ya siri tunayojua mimi na wewe.” “Kama unataka kufanya lolote juu yangu fanya lakini mimi sijui lolote.” Kauli ile ilimuudhi sana Deus na kuamini kabisa mke wake anajua kila kitu juu ya matumizi ya bastola ile kutokana na kushtuka alipoingia ndani na kumuona ameshika ile silaha. Alimsogelea mkewe kumpa kipigo ili aseme ukweli juu ya matumizi ya silaha ile kwa kuamini kabisa kama silaha ile ikikamatwa inatumika vibaya basi lazima yeye ndiye atakaye julikana anafanya mchezo ule na kufia gerezani. Wakati anamsogelea amzabe makofi, simu yake iliita, aliipokea na kuzungumza “Haloo,” alizungumza huku akitoka nje kutokana na simu kuwa ya kikazi. Taarifa iliyomfikia alitakiwa uwanja wa ndege mara moja kuna ndege iliyosemekana kuna mtu ana madawa ya kulevya hivyo ilitakiwa akamatwe. Taarifa ile ilikuwa inatoka kwa mkuu wake, alibadili nguo harakaharaka na kupitia vifaa vya kazi na kuelekea mlangoni, kabla ya kutoka alisema: “Nakwenda nikirudi nikute jibu la sivyo leo humu ndani patachimbika.” Deus alitoka kutokana na kuchanganywa na matukio ya ndani, alijikuta akimsahau hata Kinape aliyekuwa amejilaza kwenye kochi, alipofika mlangoni alikumbuka hajamuaga rafiki yake aligeuka na kumsemesha Kinape aliyekuwa kwenye dimwi la mawazo mikono kichwani. “Besti…Besti,” alimwita zaidi ya mara mbili ndipo aliposhtuka. “E..ee.eeh,” Kinape alikuwa kama umeamshwa usingizini. “Unaonekana upo mbali sana?” “Wee acha tu, hata sielewi kama nitaweza kuidhibiti hali hii mpaka napata mawazo ya kijinga.” “Mawazo gani tena rafiki yangu.” “Eti nami nijiue nimfuate mpenzi wangu.” “Wewee! Mawazo gani hayo rafiki yangu, baada ya Happy kuna maisha mengine na farijiko lingine.” “Ni kweli, siamini kama nitampata kama Happy, Deus yule mwanamke alinipenda mapenzi ya dhati toka moyoni mwake. Nina imani hata kifo chake kinatokana na kulilinda penzi letu.” “Besti hebu tuache sheria ichukue mkondo wake.” ”Watamkamataje mtu ambaye hajulikani?” “Mkono wa sheria ni mrefu atashikwa tu amini hilo best.” Kauli ile ilimtisha Kilole aliyekuwa kwenye mlango wa chumbani akifuatilia mazungumzo. Wasiwasi kumjaa na kuamini kabisa mumewe kutokana na kazi yake ya kijeshi anajua siri nyingi, pengine hata tukio lile anajua yeye ndiye aliyefanya. Alijikuta akitetemea na kujiona atafia gerezani au kinyongwa, lakini aliendelea kusikiliza kwa kuijificha. Alimuona mume akitoka nje na baada ya muda alisikia gari lake likiondoka. Alirudi chumbani na kukaa kwenye kitanda kutafuta majibu ya maneno ya mume wake. Aliamini ile ni vita alitakiwa kumuwahi mumewe kabla hajafanya jambo lolote baya, wazo la haraka lilikuwa kwenda kwa wakuu wake hasa yule alimweleza hailewani naye baada ya kuzurumiana fedha za rushwa ya madawa ya kulevya. Aliamini kupitia yule bwana atafanikisha mpango wake, kwa vile mumewe alisema akirudi akute jibu na yeye aliamini kabisa hakuwa na jibu la kumjibu hasa akizingatia siraha ile anayejua ni yeye na mumewe tu. Aliona kujiepusha na maswali yasiyo na majibu na mwisho wake kujulikana yeye ndiye muuaji ni kutoroka. Aliamua kutoroka na kwenda kulala nyumba ya wageni ile kesho amtafute yule mkuu wa mumewe na kumweleza kuwa mumewe anajihusisha na dawa za kulevya. Alijua yule bwana atataka kumkomoa na kuja kufanya upekuzi kwa vile atakuwa amwelekeza lazima atatiwa hatiani. Alichukua baadhi ya nguo za kuvaa kesho na kuziweka kwenye mkoba alimuaga mfanyakazi kwa kumwambia siri ile asimwambie mtu. “Marry hakikisha mtoto amekula vizuri.” “Hakuna tatizo dada.” “Na hizi utanunua chochote,” alimpa elfu ishirini. “Asante dada.” Alitoka hadi sebuleni kumuaga Kinape. “Shemu nakuja mara moja.” “Hakuna tatizo, wacha na mimi nikalale,” Kinape alijibu huku akielekea chumbani bila kuuliza safari ile ya wapi. *** Siku ya pili Kilole alifika makao makuu ya kitengo cha kuzuia dawa za kulevya, alimuulizia yule mzee ambaye jina lake alikuwa analijua moja. Baada ya kuingia getini alikwenda mapokezi na kuulizia. “Samahani dada mzee Shamo yupo?” “Wewe nani yake?” “Mtu wake wa karibu.” “Ameingia sasa hivi.” “Naomba nimuone.” “Subiri,” yule dada alisema huku akinyanyua simu, baada ya kuzungumza alisema: “ Nenda chumba namba sita.” Kwa vile hakuwa mgeni sehemu ile alikwenda moja kwa moja chumba namba sita na kugonga mlango. “Ingia,” sauti nzito toka ndani ilisema. Alizungusha kitasa na kuingia ndani, mbele ya meza kubwa kulikuwa na mzee mmoja aliyekuwa na mvi nyingi kichwani zilizompendeza. “Karibu mrembo.” “Asante, shikamoo.” “Asante, nikusaidie nini?” Kilole alitengeneza uongo huku akiusema hata ugomvi wao, baada ya kumsiliza alimuuliza: “Una uhakika na usemacho?” “Mimi si ndiye mkewe sasa unataka uhakika gani zaidi ya huu?” “Okay, muda si mrefu tunakuja kwako.” “Asante mzee wangu.” Kilole aliondoka moyo wake ukiwa mweupe kama seluji, moyoni alijisemea akuanzae mmalize. Baada ya kuhakikisha kila kitu kimekwenda kama alivyopanga alirudi aliamua kurudi nyumbani kwake akiamini muda ule mumewe atakuwa kazini mpaka arudi jioni angekuwa amekwisha wekwa chini ya ulinzi. Alipofika nyumbani alishangaa kumkuta mumewe nyumbani kumbe naye hakurudi jana alipoondoka na kurudi asubuhi ile. Japo alipatwa na mshtuko uliofanya haja ndogo imtoke kidogo alijitahidi kuuficha. “Karibu mke wangu,” Kilole alishangazwa na hali ya mumewe ambaye hakuonesha hasira. Kilole hakujibu alikimbilia chumbani na kuangua kilio kitu kilicho mfanya mumewe amfuate na kumbembeleza. “Mke wangu bado una yaleyale ya jana?” Deus alimuuliza mkewe kwa sauti ya upole. “Siku hizi hunipendi, nimekuwa mke mwema na muaminifu siku zote za ndoa yetu, lakini bado umekuwa huoneshi nina umuhimu kwako,” Kilole alisema kwa sauti ya kilio cha uongo. “Mke wangu, kama kimetokea kitu cha tofauti ndani nimuulize nani kama si wewe mke wangu?” “Ni kweli, lakini kama sijui mimi nitajibu nini, tena ulitaka kunipiga.” “Ni hasira za mpito lakini baada ya kujua kosa langu niliamua kuliacha, lakini muhimu kuwa na uangalizi mzuri wa vitu vyetu usipovitunza wewe nani avitunze…Halafu lile gari lako linaingia mwisho wa wiki.” “Usiniambie! Asante mpenzi wangu.” Kilole alinyanyuka na kumkumbatia mumewe huku akiamini bado ni mshindi na muda si mrefu Deus ataionja joto ya jiwe. Wakati wao wanabembeleza kikosi maalumu cha kupambana na dawa za kulevya kilikuwa nje ya nyumba ya Deus na kugonga hodi. Deus alitoka nje kuwakaribisha alishtuka kumuona mkuu wake mzee Shamo: “Ooh! Mzee karibu naona leo mmenitembelea.” Waliingia wote ndani na kuketi kwenye kochi wakati huo Deus alimwita mkewe awahudumie wageni. “Mke wangu kuna wageni hebu njoo uwasikilize wanatumia nini.” “Tunashukuru, hatuna muda tumekuja kufanya kazi moja hapa kwako.” “Kazi moja! Ipi hiyo?” Deus alishtuka. “Nina imani unaelewa vizuri kazi yetu ni nini?” “Naijua, ndiyo maana hata mimi nimerudi alfajiri kufuatilia mtu mmoja aliyeingiza dawa za kulevya.” “Ni kweli, lakini huwezi kuwa msafi bila kujisafisha.” “Una maana gani?” “Kuna msamalia mwema mmoja amesema kuwa wewe unajishughulisha na uuzaji wa dawa za kulevya.” “Mimi?” Deus alishtuka kusikia vile. “Unashtuka nini, sasa hivi upo chini ya ulinzi na kutuachia kufanya upekuzi.” “Fanyeni tu, hizi ni njama za kuchafuana lakini kila kitu kitafahamika.” Deus aliwekwa chini ya ulinzi na upekuzi ulianza mara moja, Kilole alijifanya kushtuka na kuuliza: “Jamani kuna nini tena?” “Siyo kazi yako,” Mzee Shamo alijibu kwa sauti kali. “Jamani mume wangu kafanya nini?” Kilole aliendeleza usanii. “Wee waache, naona kila siku wananichokonoa lakini ukweli utajulikana,” Deus alisema bila kujua bomu lipo ndani litalipuka muda wowote. “Hebu njoo hapa,” mzee Shamo alimwita Kilole kwa sauti ya ukali. Kilole alimfuata nakumwacha mumewe amekalishwa chini ya ulinzi, alipofika karibu alimuuliza kwa sauti ya chini. “Kuna mabadiliko?” “Hakuna kila kitu kipo vilevile.” “Ipo sehemu gani?” “Ndani ya kabati.” “Okay,” baada ya kusema vile alisema kwa sauti kali kupoteza lengo. “Haya na wewe rudi kwa mwendawazimu mwenzako. ” Kilole alishikwa na askari mmoja na kwenda kukalishwa pembeni ya mumewe, upekuzi uliendelea huku Deus akisema kwa hasira: “Yaani mkikosa hicho mnachokitafuta walahi nitazaa na mtu.” “Mume wangu mbona wanakufuatafuata?” Kilole aliendelea kulalamika kiuongo. “Wee waache, mwaka huu nitakufa mimi au mtu, nimechoka kuchezewa kama mpira,” Deus aliendelea kulalamika kwa hasira. “Wee piga kelele utanyamaza muda si mrefu,” mzee Shamo alisema huku akiendelea kufanya upekezi wa uongo kabla hawajafanya kilichowapeleka pale. Baada kutafuta sehemu nyingine mwisho waliingia chumbani na kufungua kila sehemu na mwisho walichukua briefcase iliyokuwa ndani ya kabati na kuifungua. Ndani ya briefcase kulikuwa na dawa za kulevya zilizokuwa ndani ya mifuko, mzee Shamo alisema kwa furaha: “Amekwisha, hapa hata ateremke masihi kumtetea hatoki.” Waliibeba na kutoka nayo hadi sebuleni na kuifungua mbele ya Deus. “Nilikueleza mapema kuwa huwezi kuwa msafi bila kujisafisha.” “Hiyo nini?” Deus alitaka kunyanyuka kwa hasira lakini alitulizwa na siraha zilizokuwa zimemtazama. “Deus umekwisha, nilikueleza toka zamani kuwa wewe mtoto mdogo huwezi kushindani na mimi, kwa hili utafia gerezani.” “Muongo mkubwa huwezi kuja kuniwekea madawa ili kunitia hatiani, lakini nikitoka nitakuua nakuapia,” Deus alipagawa kuona ndani briefcase yake kuna madawa ya kulevya.
ILIPOISHIA: “Nilikueleza mapema kuwa huwezi kuwa msafi bila kujisafisha.” “Hiyo nini?” Deus alitaka kunyanyuka kwa hasira lakini alitulizwa na siraha zilizokuwa zimemtazama. “Deus umekwisha, nilikueleza toka zamani kuwa wewe mtoto mdogo huwezi kushindani na mimi, kwa hili utafia gerezani.” “Muongo mkubwa huwezi kuja kuniwekea madawa ili kunitia hatiani, lakini nikitoka nitakuua nakuapia,” Deus alipagawa kuona ndani briefcase yake kuna madawa ya kulevya. SASA ENDELEA…
“Jamani tuondoke naye kazi yetu tumemaliza, tunawaachia serikali watafanya nini sisi tena haituhusu.” Deus alitiwa pingu na kutolewa nje kama mhalifu huku Kilole akilia mpaka akagaagaa chini kwa ajili ya kumlilia mumewe, kitu kilichomshtua mzee Shamo na kujiuliza ndiye yule aliyeleta habari za mumewe au mwingine. Deus kabla ya kuondoka alimwambia mkewe. “Nenda kwa Mambo Twalipo mwambie habari hizi, sawa.” “Sawa mume wangu lakini hizo dawa lazima wamekuwekea sisi hatuuzi dawa.” “Itajulikana wewe nenda asubuhi hii.” “Sawa, Kinape yupo wapi?” “Ooh! Kweli alikwenda ofisini kwake, atarudi muda si mrefu, akirudi mweleze na yeye ashughulikie suala hili.” Deus alipelekwa polisi na kufunguliwa mashtaka ya kujihusisha na kuuza dawa za kulevya. Kilole pamoja na kupanga mpango ule alijikuta akijutia uamuzi ule wa kumfunga mumewe kwa ajili ya Kinape. Baada ya kuondoka mumewe alijikuta akilia mpaka macho yalivimba lakini bado aliamini alichokifanya kilikuwa sahihi upande wake. **** Upande wa pili Teddy msichana hatari wa kuuza dawa za kulevya akiwa mafichoni Nairobi Kenya aliwasiliana na washirika wake waliokuwa tayari na mzigo wa kuingiza nchini Tanzania. Baada ya kupewa taarifa zile alimpigia simu Deus kuwa mzigo upo tayari, kwa vile alikuwa na uhakika na kazi yake, alimweleza awaeleze waje. Teddy naye aliwaeleza washirika wenzake wawili waliokuwa wamekuja na mzigo kidogo wa majaribio waingie nao. Hata asubuhi alimpigia kumweleza jamaa wapo njiani naye Deus alimtoa wasiwasi kuwa kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa. Lakini bahati mbaya kabla jioni haijaingia Deus aliangukia kwenye mikono ya polisi na kuwekwa mahabusu kusubiri kufikishwa mahakamani. Akiwa mahabusu alisubiri mtu aje amtume kwa vijana wake kuhusu mzigo utakaoingia jioni ya siku ile. Haikuwa hivyo baada ya kukamatwa mkuu wao vijana wake wote walio chini yake walibadilishwa eneo la kazi, uwanja wa ndege waliwekwa askari wapya. Habari zile zilimkata maini Deus na kuona kama watu wake wakikamatwa atazidi kujiongezea matatizo kutoka kwa wauza dawa za kulevya ambao hawakuwa na dogo. **** Majira ya saa moja jioni ndege ya shirika la Qatar iliwasili jijini, katika abiria waliotua siku hiyo walikuwemo washirika wawili wa Teddy. Wakati huo Teddy alikuwa ameishapiga simu zaidi ya mara kumi kumtafuta Deus. Mwanzo simu iliita bila kupokelewa na mwisho wake haikupatikana tena. Pamoja na kumkosa hewani Deus, Teddy aliamini kutokana na makubaliano ya asubuhi lazima angekuwepo uwanjani. Baada ya ndege kufungua mlango. Tonny na Moppy walitoka taratibu wakiamini wapo kwenye mikono salama ya Deus. Hata mizigo yake ilipowekwa pembeni hawakuwa na wasiwasi kwa kujua ndiyo njia ya kuwatoa kiwanjani salama. Kumbe siku hiyo kulikuwa na usimamizi mpya na mtu waliyekuwa wakimtegea alikuwa akinyea debe. Walishangaa kuwekwa chini na kupewa kashikashi kisha kuchukuliwa na kupelekwa mahabusu. Walishangaa kutomuona mtu wa kuwasaidia. Washirika wenzao waliofika kuwapokea uwanjani pale hali ile iliwashtua na kumpigia simu Teddy. “Haloo Teddy, vipi mbona hatuelewi?’ ”Hamuelewi nini?” “Jamaa ameshikwa wapo chini ya ulinzi.” “Msiwe na wasiwasi watatoka tu,” Teddy alijibu kwa kujiamini. “Kwa hiyo tufanye nini?” “Nendeni nyumbani watakuja wenyewe,” Teddy aliamini kabisa Deus yupo. Kila alipopiga simu ya ya Deus haikupatikana kitu kile kilimtia wasiwasi na kuwaomba waulizie kwa vijana wake mtu anayeitwa Deus. Walifanya vile, lakini jibu lilikuwa hawamfahamu mtu hiyo. Majibu yale yalimfanya Teddy kichwa kifanye kazi kwa kuwaomba kuwafuatilia kwa mpaka mwisho ili wajue nini kinaendelea. Kutokana na uzoefu na kazi ile walifanikiwa kuwatoa kabla hakujapambazuka, lakini mzigo wao wa fedha nyingi ulipotea. Jamaa walijikuta wakimlaumu Teddy kwa kuwaingiza choo cha kike. Teddy kitendo cha Deus kumgeuka kilimuumiza sana na kukumbuka kauli aliyomueleza Deus juu ya kwenda kinyume na makubaliano yao. Siku ya pili Teddy alipanda ndege mpaka Dar kumtafuta Deus, alipofika alijitahidi kumtafuta Deus kila kona lakini hakumpata wala habari zake hazikupatikana. Sehemu zote ya uwanja alimtafuta bila mafanikio, wazo lililomujia ni kumteka sekretary wake ili ajue Deus yupo wapi. Kwa hasara waliyoingia aliapa kumuua kwa mkono wake. Majira ya saa kumi na mbili muda anaotoka secretary wa Deus, ambaye hakuwa mgeni machoni mwake alimuona akiingia kwenye gari na kuondoka. Baada ya kuondoka waliamua kulifuatilia lile gari kwa nyuma. Kutokana na wingi wa magari ilikuwa vigumu kuweza kumteka kwa urahisi. Waliliacha gari lililombeba yule msichana aliyeoneka yupo na mpenzi wake kutokana na muonekano wao ndani ya gari. Japo vioo vyote walifunga lakini walionekana ndani. Gari lilipofika maeneo ya Mbezi beach iliacha barabara kubwa na kuingia njia iliyokuwa haina rami. Teddy aliliacha gari lile litembee kidogo sehemu iliyokuwa wazi. Baada ya kuridhika na kile anachotaka kukifanya alikanyaga mafuta na kulipitisha gari kwenye majani kwa mwendo wa kasi kidogo ili kulipita gari alilokuwa amebebwa secretary na kusimama mbele yao kwa ghafla. Kitu kilichofanya mpenzi wa secretary kuteremka kwa hasira baada ya kumuona aliyefanya mchezo wa kijinga ni mwanamke alimfokea huku akimtishia kumpiga. “Wee malaya unatafutwa bwana.” “Nani malaya?” Teddy aliuliza akiwa anamsogelea bila wasiwasi wowote. “Wewe hapo,” mpenzi wa secretary alisema huku akimnyooshea kidole. “Bahati yako sina shida na wewe, ungejutia maneno yako ya shombo,” Teddy alisema bila hofu kitu kilichomshangaza Secretary na mpenzi wake na kujiuliza yule msichana ni nani. “Ungeniganya nini?” “Nakwambia sina shida na wewe nashida na huyu dada, Deus yupo wapi?” Teddy aliyeoneka akijiamini kupita maelezo alimshtua secretary kwa swali lile. “Deus gani?” “Bosi wako.” “Wewe nani unayemuuliza Deus?” “Umenisahau?” Teddy alisema huku akitoa miwani usoni. “Siwezi kuwakumbuka wote.” “Dear kwanza mambo ya ofini asubiri kesho,” mpenzi wa secretary aliingilia kati. “Sikiliza kaka, nakuheshimu hunijui sikujui, naweza kumchukua sijui mkeo na usinifanye lolote na zaidi ya hapo ni kukupoteza kwa sekunde chache. Mimi si mwendawazimu kuja huku,” Teddy alisema kwa sauti ya kukoroma. “Kwani wewe shida yako nini?” secretary alikuwa mpole kutaka kumsililiza kwani alijua yule dada alikuwa na jambo la msingi. “Shida yangu Deus.” “Nina imani unajua kazi zetu, hebu nieleze shida yako kwa Deus, naweza kukusaidia.” “Shida yangu kuonana na Deus.” “Wewe ni nani kwake?” “Nina imani unanikumbuka niliisha wahi kuletwa ofisini kwa kosa la kukamatwa na dawa za kulevya na tatizo langu lilichukua muda lakini mwisho wa siku Deus alilimalizia.” “Ooh! Nimekukumbuka, kwa sasa huwezi kumuona.” “Kwa nini?” “Taarifa za Deus nilipata juujuu kuwa ana matatizo makubwa sana ambayo yanaweza kumpotezea kazi na kufungwa.” “Tatizo! tatizo gani hilo?” Teddy aliuliza huku macho yamemtoka pima. “Japo si sheria sina budi kukueleza ukweli, Deus jana asubuhi amekamatwa kwake na dawa za kulevya.” “Muongo mkubwa! Mmeamua kupindisha ili kumkinga kwa kitendo alichonitendea?” Teddy alikuja juu hakukubaliana na taarifa ile. “Kwa nini unasema hivyo?” “Juzi nimewasiliana naye na asubuhi ya jana, halafu uniambie eti ana matatizo, usalama wako ni kunipeleka alipo bosi wako la sivyo nitageuka mtoa roho sasa hivi,” Teddy alibadilika na kuwa mwekundu baada ya kuona Secretary akileta ujanja. “Dada hunijui wala sikujui, lakini Deus yupo kwenye matatizo makubwa sana na sijui kama atatoka salama, majuzi alikesha uwanja wa ndege kikazi na asubuhi aliporudi nyumbani kwake hakutulia alikamatwa kwa kukutwa na dawa za kulevya kwenye briefcase yake.” “Kwa sasa yupo wapi?” “Yupo ndani na kesho anapandishwa kizimbani kama unaona nakudanganya njoo kesho mahakamani.” “Kwa nini alinieleza niingine mzigo?” “Tatizo hilo lazima nimtetee ilikuwa ghafla, halafu pigo kubwa lilikuwa kubadili askari wote wa uwanja wa ndege. Kwa tatizo lile bado kuna mabadiliko makubwa yanakuja hata mimi sina maisha marefu kwa vile ndiye niliyekuwa mtu wake wa karibu muda wote aliokuwa kazini. “Hata taarifa za kuingia watu wawili wenye mzigo mimi nilikuwa najua, lakini yaliyotokea walitutisha, kama wangekuwa vijana wake wapo hata mimi ningesimamia kusingeharibika kitu.” “Una uhakika Deus hafanyi kazi ya kuuza unga?” “Afanye ile biashara iwe vipi, wakati kila siku anaingiza fedha nyingi kwa hao wauza unga.” “Unafikiri ni kwa nini amekamatwa na dawa za kulevya?” “Kuna bosi mmoja haelewani naye ndiye aliyemkamata, watu wote tunajua amembambikia ili kumharibia maisha yake.” “Huyo bosi wake anaitwa nani?” “Mzee Shamo.” “Ni mkubwa wake?” “Ndiyo.” “Kwa nini alimfanyia vile?” “Kuna fedha za rushwa ziliingia yule mzee akamzika Deus alipodai ikawa tatizo na kufikia kutishiana maisha. Lakini walimaliza tatizo lao, lakini nashangaa mzee yule alivyommaliza vibaya Deus. Yaani bosi wangu alikuwa mzungu hana tamaa za kijinga kama wazee tunaofanya nao kazi kila kitu wanataka wao.” “Mzee Shamo anakaa wapi?” “Nasikia yupo Kinondoni lakini sijui ni sehemu gani.” “Una namba yake ya simu?” “Ninayo.” “Naomba.” Secretary alimpa namba ya simu, Teddy aliisevu kwenye simu yake na kusema: “Asante, pia samahani kwa kuwasimamisha kijeshi na kuwapotezeeni muda.” “Bila samahani kwetu kawaida,” Secretary alijibu. “Inaonekane kwa shemeji ni ngeni, samahani shemu,” Teddy alimuomba msamaha mpenzi wa secretary. “Kawaida dada yangu.” “Niwaache mkapumzike, lakini hasira zangu kwa Deus zitaishia kwa huyo mzee sijui Shamo lazima atalipa mzigo uliopotea na ziada sitaki mchezo kwenye kazi yangu.” “Haya dada siku njema.” Teddy aliagana na Secretary kwa kuliondoa gari mbele yao na kisha kuligeuza kurudi mjini. Njia nzima alikuwa na hamu ya kuonana na mzee Shamo ili ajue atalipa vipi hasara za kumweka ndani Deus na kuwasabishia usumbufu hasara kubwa. **** Juhudi za kumtoa ndani zilikuwa tofauti kati Kilole na Kinape, Kilole alimweleza Kinape asipoteze muda kwani kesi ya Deus yenye ushahidi kuweka wakili ni kupoteza muda. “Sikiliza Kinape fedha tunayotaka kupoteza kumwekea wakili Deus heri tuiweke kwa ajili ya kumsomeshe mwanaye.” “Japo ameshikwa na dawa ambazo bado siamini kama ni zake, lakini wakili anaweza kupunguza adhabu na kufungwa miaka michache.” “Kinapeee, acha ujinga dawa zimekutwa ndani kwetu tena ndani ya biefcase yake bado unaona atapona?” “Anaweza kupona inawezekana zile zilikuwa za ushahidi na si za kuuza.” “Kinape hata Yesu arudi mara ya pili Deus haponi tena bahati yake ingekuwa Uarabuni angenyongwa.” “Mbona sikuelewi nakuona kama vile una furahia tukio la Deus kufungwa?” “Lazima nifurahie kama angesafiri na mzigo ule kukutwa ndani mimi si ndiye ningenyea debe.” “Lakini hiyo biashara kaianza lini?” “Muda mrefu ila aliifanya kwa siri hakupenda mtu yeyote ajue hata mimi mwanzo alinificha.” “Sasa Deus kwa nini anajiingiza kwenye biashara kama ile wakati alikuwa kwenye mradi mzuri wa kuingiza mabilioni bila fedha.” “Ndio hivyo mshika mawili.” “Lakini bado sikubali nitapigania kuhakikisha Deus anatoka kwa gharama yoyote,” Kinape bado alikuwa na huruma na rafiki yake. “Kinape usiwe mjinga kwa taarifa yako Deus hatoki, hii ni nafasi ya mimi na wewe kuishi pamoja.” “Hapana Kilole haiwezekani lazima nimpiganie Deus, mambo yangu yote haya ni kwa ajili yake sitakuwa mwizi wa fadhira.” “Kinape tulizungumza nini?” Kilole alimshangaa Kinape. ”Kuhusu nini?” “Deus.” “Kuhusu Deus nini?” “Si ulinikataza nisimuue tutafute njia ya kumfanya ili tu atupishe tuwe pamoja, nafasi imepatikana unaleta kiswahili kirefu mbona sikuelewi?” Kilole alizungumza kwa lugha ya ukali. “Pamoja na hivyo lakini tulitakiwa kumsaidia na si kumwacha aangamie, lazima tuoneshe utu katika hili.” “Lakini kwa nini hutaki kuwa mwelewa, kila kilichotokea nimekifanya kwa ajili yako.” “Mmh! Una maana huu mpango wa kukamatwa Deus umeufanya wewe?” “Ndiyo, si ulinikataza nisimuue sasa huu nao unauona mbaya?” “Kiloleee! Mbona unakuwa na roho mbaya kama mnyama, yaani unamfunga mumeo kwa ajili ya penzi haramu?” Kinape alishtuka. “Kinape kulitafuta penzi lako nimepata dhambi kubwa, hili la Deus mbona dogo.” “Kubwa lipi?” “Unajua ila ufahamu, kwa Mungu nina kesi ya kujibu juu ya roho za watu watatu niliowaua kwa ajili yako. Ukifanya mchezo wowote Kinape tutawafuata kina Happy.” “Weweee! Unataka kuniambia wewe ndiye uliyemuua Happy?” “Ndiyo.” “Kwa nini?”
“Kwa nini?” “Kwa ajili yako, ni wewe uliyesababisha nimuue nilikueleza muachane lakini ndiyo kwanza ulitaka kwenda kumtambulisha kwenu. Niliamini akifika kule sina nafasi ya kuwa na wewe tena.” “Kiloleee! Kwanini umemuua Happy mtu asiye na hatia kama kosa nimefanya mimi, si ungeniua mimi Happy amekukosea nini?” Kinape alijikuta akitoneshwa donda lililokuwa bado bichi. “Siwezi kuukata mti wangu wa kivuli, Kinape kumbuka ni wewe ndiye uliyenitoa usichana wangu na ndoto yetu kuwa mke na mume nina imani sasa ndiyo nafasi yetu ya kuwa mke na mume.” “Lakini si kwa ukatiri na unyama kama huu, kwa nini Kilole umebadilika na kuwa na roho mbaya kiasi hiki!” “Kinape mimi na roho nzuri sana tena yenye huruma lakini nilitetea maumivu ya moyo wangu. “Ni wewe ndiye uliyesababisha yote kwa kunipiga picha za aibu mimi nilifanya vile kwa ajili ya kuificha aibu ile kumbuka Deus angejua wewe ungekuwa katika hali mbaya tofauti na mimi. Kila ninachokifanya ni kwa ajili yako bado unaniona mpuuzi. ” “Kwa hiyo unaniambiaje?” “Wiki hii Deus anapandishwa kizimbani na kuhukumiwa kifungo kikubwa, baada ya kifungo chake kila kilicho chake tunataifisha kama tulivyokubaliana tunauza kila kitu tunahama mji.” “Mmh! Sawa,” Kinape alikubali kwa shingo upande huku moyoni akiwa na maumivu makali ya kifo cha mpenzi wake Happy. **** Kikao cha wauza dawa za kulevya kiliendelea chini ya Teddy aliyeoneka mwenye hasira kuliko wote waliokuwepo pale. “Ehe! Vipi huko ulipokwenda?” Moppy aliyekuwa na uchungu wa mali yake iliyokamatwa jana yake. “Sikilizeni watu wangu kuna tatizo limejitokeza ambalo ni dhalula ambayo ilikuwa ni vigumu kuiepuka.” “Kuiepuka vipi Teddy? Usitufanye watoto wadogo,” Moppy alikuja juu kutaka maelezo kamili. Teddy aliwaeleza kazi aliyoifanya kutwa nzima ya kumsaka Deus na majibu aliyoyapata juu ya Deus kukamatwa jana asubuhi muda mfupi baada ya kuwasiliana. “Kwa hiyo unataka kutuambia nini?” “Nia yangu ilikuwa kumuua Deus, lakini nimeamini hana kosa hivyo basi mzeee..sijui nani,” alitoa simu yake kuangalia jina kwenye simu na kulikumbuka. “Mzee Shamo, usiku wa leo anatakiwa kutekwa na kuja kutueleza mzigo wetu tutaupata vipi?” “Tusipoupata tutafanya nini?” Side aliuliza huku akifungua chupa ya Jacky Daniel. “Hilo si swali, si mnakumbuka Mose shemeji yangu nilimfanya nini, pamoja na kumkosa bado namlia taimingi lazima nilibakishe jina. Na huyu mzee lazima afe kama hana maelezo ya kuridhisha.” “Teddy una bahati sana, leo nilikuwa nakuulia hapohapo ulipokaa, niliamini kabisa umeniingiza choo cha kike. Niliamini kama wewe ulitaka kumuua shemeji yako niliona nawe ulistahili hukumu hiyo,” Tonny alisema huku akitoa bastora iliyokuwa kwenye jacket iliyokuwa tayari kukatisha maisha ya Teddy. “Kama ningekuwa nimefanya kwa makusudi ruksa kufanya mtakalo, hata mimi sipo tayari kumsamehe adui yangu,” Teddy alitia nguvu maneno ya Tonny. Walikubaliana usiku wa siku ile kumtafuta mzee Shamo ili wajue wataupataje Mzigo wao. Baada ya kikao Teddy alimpigia simu mzee Shamo baada ya simu kuita ilipokelewa upande wa pili. “Haloo.” “Haloo mzee Shamo, shikamoo,” Teddy alijifanya anamfahamu. “Marahaba, nani mwenzangu?” mzee Shamo aliuliza. “Najua hunijui ila tukikutana utanifahamu vizuri.” “Una shida gani?” “Mzee Shamo haraka ya nini? Tukikutana unajua kila kitu, upo wapi sasa hivi?” “Sasa hivi nipo Sea Cliff Hotel.” “Okay, baada ya dakika ishirini nitakuwa hapo.” “Hakuna tatizo.” Baada ya kukata simu aliwageukia wenzake waliokuwa wakimfuatilia apokuwa akizungumza. “Nakuja sasa hivi.” “Una kwenda wapi?” “Namfuata yule mzee.” “Teddy utamuweza peke yako?” “Akinishinda namtwanga risasi na kutokomea zangu.” “Noo, usifanye hivyo usitumie hasira kila wakati, nenda na Tonny nina imani mtaweza kumfikisha hapa bila kumwaga damu,” Double D alimtuliza Teddy aliyeoneka amepandwa na mzuka baada ya kuona kifo chake kilikuwa usoni kwake kwa kuoneshwa bastora na Tonny iliyotakiwa kuchukua uhai wake. Teddy aliongozana na Tonny kumfuata mzee Shamo, moyoni aliapa lazima atampoteza Tonny baada ya kutaka kumuua yeye alipanga kummaliza siku yoyote bila mtu kujua. Waliondoka katika gari moja kila mmoja akiwa na mawazo yake Tonny akiamini kabisa aliyoyasema yameishia palepale, lakini kumbe mwenzake alikuwa na kisasi kikali moyoni mwake. Walipofika nje ya Hoteli ya Sea Cliff, Teddy alimpigia simu mzee Shamo. “Mzee wangu nimefika.” “Nipo jirani na mlango wa kuelekea baharini.” “Sawa nakuja.” Baada ya kukata simu alimgeukia Tonny aliyekuwa bado yumo ndani ya gari akisubiri maelekezo. “ Tonny mzee anasema yupo karibu na mlango wa kuelekea baharini, sasa fanya hivi.. nenda mpaka eneo lile kisha nibip mimi nitampigia angalia nani anayepokea ili tufanye kazi kwa uhakika.” “Hakuna tatizo.” Tonny aliteremka kwenye gari na kuelekea ndani ya hoteli na kumwacha Teddy akigeuza gari na kuliweka vizuri kusubiri kutaarifiwa. Haikuchukua muda simu yake iliita, alipoangalia ilijua tayari Tonny amefika eneo husika. Alipiga simu moja kwa moja kwa mzee Shamo, baada ya kuita kwa muda ilipokelewa. “Haloo upo wapi mbona sikuoni?” mzee Shamo aliuliza. “Umesimama wapi?” “Nipo hapa mbona unaonekana wewe upo wapi?” “Nipo kwenye mlango wa kuelekea baharini.” “Mbona mimi nimesimama hapa tena nipo wazi.” “Okay nimekuona.” Teddy alikata simu na kumpigia Tonny. “Tonny umemuona?” “Nimemuona.” “Msemeshe na muombe utoke naye huku nje.” “Poa.” Baada ya kukata simu Tonny alimsogelea mzee Shamo na kumsemesha. “Shikamoo mzee.” “Marahaba kijana.” “Nina imani wewe ndiye mwenyeji wetu.” “Una maana gani?” “Sasa hivi sister alikuwa akiwasiliana wewe.” “Eeh! Yupo wapi?” Yupo nje kanituma nikufuate ana mazungumzo na wewe ya dakika tano kisha utaendelea na starehe zako.” “Hakuna tatizo.” Mzee Shamo aliongozana na Tonny nje kuelekea upande wa gari lilipokuwa, Teddy alipowaona wanasogea alilisogeza gari, wakati huo Tonny alikuwa ameisha toa bastora na kumuwekea ubavuni mzee Shamo. “Samahani mzee naomba uwe mpole ingia kwenye gari hilo hapo mbele la sivyo nakumwaga utumbo.” “Jamani kuna tatizo gani?” mzee Shamo alishtuka. “Hakuna tatizo ila tuna mazungumzo ya kirafiki.” Kwa vile gari lilikuwa limekwisha simama na kufunguliwa mlango mzee Shamo aliingia ndani kisha alifuatia Tonny baada ya kufungwa mlango Teddy aliondoa gari kwa kasi. Baada ya kwendo mfupi walimfunga kitambaa cheusi na gari kupelekwa moja kwa moja ndani ya ngome ya wauza dawa za kulevya. Walipofikisha ndani alifunguliwa kitambaa na kujiona yupo mbele ya watu zaidi ya nane. “Karibu mzee Shamo,” Double D alimkaribisha kistaabu. “Asante,” alijibu huku akijenga ujasiri. “Unatumia kinywaji gani?” “Asante, kwa sasa sihitaji zaidi ya kujua sababu ya kuletwa hapa kama gaidi.” “Utajua tu mzee wetu, shida yetu kupata mzigo uliokamatwa juzi.” “Mzigo! Mzigo gani?” “Juzi kuna vijana wawili walikamatwa uwanja wa ndege na dawa za kulevya, na sababu kubwa ni wewe..” “Mimi?” Shamo alimkata kauli kupiga tuhuma zile. “Ndiyo, kumbuka tukio ulilofanya asubuhi ya siku hiyo ndiyo lililoharibu kila kitu, tunajua wewe ni mtu mkubwa tunaomba ule mzigo uurudishe mara moja.” “Usipoteze muda wenu sijui lolote kuhusiana na hicho mnachosema.” “Mzee hatutaki tutumie nguvu, tutakuachia usiku huu kabla hakujapambazuka tunataka mzigo uliokamatwa.” “Sasa mimi nitaupata wapi?” “Utajua mwenyewe la sivyo jina lako litabakia historia.” “Hata mnipe mwaka mzima siwezi kuwapa kitu kilichokamatwa siku zote uharibiwa pia mimi si mtunza stoo.” “Kwa hiyo?” “Sina msaada wowote.” “Teddy nina imani mzee hana jibu, mrudisheni akaendelee na starehe zake.” “Hakuna tatizo, kwa hiyo tunamuacha hivihivi tu?” Teddy alihoji. “Mwacheni tu.” “Siri yetu si itatoka nje?” “Haiwezi, kwanza hapa hajui yupo wapi.” Mzee Shamo alifungwa kitambaa usoni na kupelekwa nje kwenye gari, Double D aliwafahamisha washirika wake kwa nini amemuacha huru mzee Shamo. “Mnajua kwa sababu gani nimeamua kumwacha hai, tukimuua leo lazima tutamuongezea matatizo yule jamaa yetu aliye mahabusu kwa kuamini kifo chake kinatokana na kukamatwa kwake.” “Aisee, sikuwaza vile ingekuwa mimi ningemuua palepale kwenye kochi,” Teddy alisema. “Yule kifo kipo palepale kutokana na maelezo yote inaoneka kabisa jamaa yetu haponi, kwa vile hana msaada wowote kwetu hatuwezi kumsaidia kwa lolote.” “Lakini tunaweza kucheza na hakimu.” “Teddy hata tukimtoa hakuna faida yoyote tutayopata, tusubiri tu akifungwa tumlipie kisasi kwa kuua mbaya wake siamini tuna msaada mwingine zaidi ya huo.” “Mmh! Sawa.” Teddy alikubali shingo upande kwa kuamini alitakiwa aonesha naye ubinaadamu kama alivyofanyiwa na Deus alipokamatwa na mzigo. Kwa upande wake asingeweza kumsaidia kutokana na hofu ya kutafutwa baada ya kushindwa kuua shemeji yake. Baada ya mazungumzo walimtoa mzee Shamo wakiwa njiani kumrudisha walimvutisha dawa ya kulevya zilizomlevya na kulala, kwa vile ilikuwa usiku walimrudisha jirani na hoteli Sea Cliff kumuacha sehemu iliyo salama na kurudi kujipanga upya.
Mzee Shamo aliokotwa pembeni ya hoteli ya Sea Cliff akiwa hajitambui na kukimbizwa hospitali kupata huduma ya haraka. Alipata nafuu baada ya siku mbili, alijua wale ni jamaa zake Deus ambao alikuwa akifanya nao dili la kuvusha dawa za kulevya. Lakini alipoulizwa juu ya kuokotwa hajifahamu ilitokana na nini. Alificha kuhofia onyo kali alilopewa na Double D kama ataitoa siri nje basi wangempoteza. Aliamini kukaa kwake kimya ndiyo salama yake, hivyo kila alipoulizwa mara ya mwisho alikuwa wapi alidanganya alitekwa na watu asiowajua na kujikuta hosipitali. “Unasema walikuteka tu bila kueleza lolote?” Afisa mwenzake alimuuliza. “Yaani wakati nakwenda kwenye gari langu walitokea vijana na kuniteka na kunitupia kwenye gari lao na kuondoka na mimi, baada ya hapo sikujua kilichoendelea mpaka nilipojikuta hospitalini.” “Kwa hiyo hawakukusemesha chochote juu ya kukuteka kwako?” “Hawakunisemesha chochote.” “Sasa kwa nini walikuteka na kukuachia bila kukufanyia lolote?” “Inaonekana huenda waliniteka kimakosa na kuamua kuniachilia baada ya kugundua si mlengwa.” “Lakini upo sawa?” “Nipo sawa, kutokana na maelezo ya daktari nilinusishwa dawa za kulevya tu hakuna kitu kingine kibaya.” “Hukumbuki hata namba za gari.” “Kwa vile nilikuwa sijui nini kinaendelea hivyo sielewi chochote.” Mzee Shamo aliamua kificha siri ile kwa upande wake aliamini ile ni kinga tosha ya wauza dawa za kulevya ya kutommaliza. *** Deusi alipandishwa kizimbani akikabiliwa na kosa la kukutwa na dawa za kulevya. Upande wa msaada Kinape akiweka wakili wa siri baada ya mkewe Kilole kukataa kutumia fedha zake kumwekea wakili akiamini kabisa hawezi kupona katika kesi ile lazima atafungwa kwani ushahidi wote ulikuwepo. Kutokana na kukosa msaada kwa washirika wenzake kumsaidia Deus katika kesi yake Teddy alijitosa kumsaidia kwa kuongeza wakili mzoefu wa kesi nzito kama zile. Kwanza alibadili mavazi na kuvaa ya heshima yenye kuuficha mwili wake kisha alijipaka piko kama mwanamke wa pwani vitu vile vilimfanya aonekane mwanamke mstaarabu mbele ya jamii. “Nahitaji msaada wako Mr Mnyigu ili nimuokoe huyu baba, kesi imemkalia vibaya,” Teddy alimuomba msaada wa wakili wa kujitegemea. “Kutokana na maelezo ya mtuhumiwa kesi imekaa vibaya hasa baada ya ushahidi kukutwa ndani mwake.” “Nina imani kesi kama hizi umekutana nazo sana, chonde msaidie baba wa watu.” “Nitajitahidi lakini hii ni kesi nzito hasa kutokana na kushtakiana wenyewe kwa wenyewe kutokana na maelezo yake hii itakuwa mchezo umechezwa hivyo tusipokuwa makini tutaumbuka.” “Huoni hapo kama unaweza kupata sababu ya kuona ni njama kwa vile kuna rekodi ya kukosana nyuma?” “Teddy hapo utachekesha, wamekosana kwenye rushwa ya madawa ya kulevya, hilo ni kosa lingine ambalo halitakiwi kusemwa mbele ya mahakama.” “Sasa tutafanyaje, kuhakikisha tunamwokoa.” “Labda tuzungumze na mashahidi ambao nasikia ni mkewe na huyo mbaya wake aliyeapa lazima ampoteze.” “Basi hiyo kazi niachie mimi nitakupa jibu leo usiku au kesho asubuhi.” Teddy baada ya kuagana na wakili wa kujitegemea Mr Mnyigu alipanga jioni ya siku ile akasikilize mkewe amejipanga vipi kumuokoa mumewe. ***** Majira ya saa mbili usiku alikuwa nje ya nyumba ya Deus kutokana na maelezo aliyoelezwa hakumpotea nyumba. Ndani ya nyumba kulikuwa na muziki wa rusha roho wa sauti ya juu, ulionesha kama ndani kuna sherehe. Aligonga mlango kwa muda mlango ulifunguliwa na kutoka Kilole ambaye hakuonesha uso wa majonzi. “Karibu,” Kilole alimkaribisha. “Asante,” Teddy alijibu huku akiingia ndani. Baada ya kutulia kwa muda akisoma mandhali ya ndani Kilole alimuuliza: “Ndiyo dada yangu, nikusaidie nini?” “Nina imani wewe ni mke wa Deus?” “Mmh! Kwani vipi?” “Dada nijibu wewe ndiye mkewe au vipi?” “Ndiyo mimi.” “Mpaka sasa kuna juhudi gani za kumuokoa mumeo?” “Kwa kweli hakuna kwa vile amekutwa na ushahidi kabisa, tunasuburi mahakama itaamua nini.” “Hata kama amekutwa na ushahidi bado unaweza kumsaidia.” “Haiwezekani lazima atafungwa mtu kashikwa na ushahidi utamsaidia vipi?” “Naomba ushirikiano wako, nina sikia wewe ulikuwepo mumewe akikamatwa na hayo madawa?” “Unaomba ushirikiano gani?” “Kuhakikisha tunamtoa.” “Ni vigumu kumsaidia hasa kesi yenyewe ipo mikononi mwa serikali, kama una fedha heri unipe ili nimlee mtoto wake.” “Sikiliza, naomba ukane mahakamani kuwa mumeo hauzi madawa ya kulevya nami nitakuwa nyuma yako.” “Siwezi kusema uongo, nitafungwa.” “Huwezi mdogo wangu, wee siku ukipanda kizimbani kutoa ushahidi mteteee mumeo kwa nguvu zote ukisema alikuwa anauza na wewe utakuwemo.” ”Na ule ushahidi?” “Nitashughulika nao mimi.” “Kwanza wewe ni nani?” “Utanijua baada ya kesi.” “Lakini dada kwa vile nami nilikuwa shahidi namba moja kuona dawa za kulevya kwenye brifcase ya mume wangu siwezi kugeuka lazima nitafungwa.” “Huwezi kufungwa.” “Nitafungwa, itanibidi niseme ukweli.” “Hebu kuwa muelewa huwezi kufungwa kwa kutoa ushahidi wa kweli.” “Ukweli si ndio huo wa kuyaona madawa kwenye brifcase ya mume wangu.” “Mume wako anauza dawa za kulevya?” “Mmh! Sijui.” “Hujui nini na wewe ni mke wake?” “Labda alifanya kwa siri.” “Sasa sikiliza ninachokizungumza sasa hivi si ombo bali amri, ukifika mahakamani kana huyajui madawa yaliyokutwa ndani ya brifcase ya mumeo. Wewe hujui kuwa mumeo na mzee Shamo wana ugomvi?” “Najua.” “Sasa kwa nini unakubali mambo kirahisirahisi tu, huoni hizo ni njama za kumpoteza mumeo?” “Sasa mimi akifungwa ananihusu nini?” “Ni kweli mumeo?” “Kweli mume wangu, lakini kilanga haliliwi wala hawekewi matanga kila mtu atazikwa kaburi lake.” “Una ugomvi na mumeo kabla ya tukio hili?” “Hakuna,” wakati huo alikuwa akiingia Kinape ambaye alimsahau Teddy kutokana na mavazi aliyokuwa amevaa. “Kuna mgeni?” Kinape aliuliza baada ya kuingia. “Ndiyo, sijui wakili wa Deus,” Kilole alijibu. “Karibu dada yangu.” “Asante, nina imani wewe ni ndugu yake Deus?” “Ndiyo.” “Unanikumbuka?” “Hataa.” “Naitwa Teddy, najua hujawahi kuniona lakini uliwahi kuisikia sauti hii, uliwahi kutumwa na Deus milioni 75,” Teddy alisema huku akitoa nikabu kichwani na kuweza kuonekana vizuri, Kinape alimkumbuka. “Ooh! Nimekumbuka, karibu sana.” “Ndiyo za siku?” “Nzuri, kama ulivyosikia kaka yupo kwenye matatizo.” “Najua ndiyo maana nipo hapa.” “Lakini hali ni mbaya kila sehemu niliyohangaika imeonekana lazima atafungwa.” “Sasa sikilizeni, humu ndani wangapi wameshuhudia yale madawa?” “Shemeji,” alijibu Kinape. “Nimemueleza msaada mkubwa katika ile kesi ni kukana hayajui yale madawa ile itasaidia kupunguza ukali wa ile kesi.” “Lakini kumbuka kuna mkuu wake ndiye shahidi namba moja,” Kinape alisema. “Hiyo haisumbui, kama ukikana mahakamani kazi nyingine nitajua jinsi ya kuifanya,” Teddy alisema kwa kujiamini. “Mimi siwezi, nitasema kweli,” Kilole alishikilia msimamo wake baada ya kumuona Kinape. “Narudia hili si ombi, kaka unajua kazi yangu, kama mkienda kinyume nitawaua wote kwa mkono wangu,” Teddy alitoa onyo kali. “Uniue mimi?” Kilole alishtuka. “Ndiyo.” “Kwa kosa gani?” “La kumfunga mumeo.” “Sasa mimi nitafanya nini wakati kashikwa na ushahidi?” “Nakuhakikishieni ushahidi utakuwa wa mtu mmoja, mzee Shamo hata panda kizimbani.” “Kwa sababu gani?” “Sitaki maswali ila kesho ukipanda kizimbani toa ushahidi huo.” “Lakin…” “Sitaki maswali, naondoka ila mkienda kinyume mtageuka adui zangu namba moja, kwa herini.” Teddy alisema huku akinyanyuka na kuondoka na kuwaacha Kilole na Kinape wakitazamana. Baada ya kuondoka Teddy, Kilole alimuuliza Kinape. “Yule ni nani?” “Ni yule msichana muuza dawa za kulevya aliyekamatwa na kutoa milioni 75 na ndiye aliyetaka kututajilisha lakini nashangaa papara yako umetukosesha kila kitu.” “Hayo si muda wake sasa.” “Sawa.” “Sasa huyu mwanamke kesi hii inamuhusu nini?” “Sijui.” “Au mwanamke wake?” “Hapana.” “Nakuhakikishia lazima nimfunge Deus kesi hii hatoki nitasema ukweli na aje aniue.” “Kilole yaani nakuomba umsikilize yule dada, usimuone vile ni mafia mbaya anaweza kukuua hata palepale mahakamani baada ya kutoa ushahidi wa kumfunga Deus.” “Sasa tutafanya nini?” “Kwa nini tusimsaidie Deus?” “Deus tayari amenaswa na ndoano hawezi kuruka.” “Sasa sikiliza, hata wewe ukikana bado atafungwa, huenda Deus ana wasiwasi na wewe, ukipanda kizimbani kutoa ushahidi ukane ule ushahidi kuwa huujui lakini akija mzee Shamo atamaliza kazi.” “Mmh! Yule mzee atanielewa kweli ikiwa mimi ndiye niliyetengeneza mpango mzima.” “Fanya hivyo kwa uhai wako yule dada hatanii huenda na mzee Shamo sipande kizimbani.” “Kwa sababu gani.” “Huenda atapewa fedha au auawe.” “Mmh! Inatisha itanibidi nifanya hivyo.” Teddy baada ya kutoka kwa Deus alibadili uamuzi wa kwenda kuonana na mzee Shamo kwa kuhofia kutego baada ya kutendo cha siku chache zilizopita japo hakukuwa na kitu chochote cha kuonesha wanatafutwa. Alipanga kusikiliza utetezi wa mke wa Deus aliyekuwa akipanda kizimbani kesho na kuhakikisha mzee Shamo hapandi kizimbani kutoa ushahidi siku ya mwisho. Siku ya pili Kilole alipopanda kizimbani alikana kuyaona yale madawa ya kusema ameyaona baada ya kuitwa chumbani kwake, lakini mume wake hajawahi kuuza madawa yale. Alipoulizwa inawezekana ni njama za watu za kumchafua mume wake, alijibu inawezekana japo hana uhakika. Majibu ya mke wa Deus yalimshangaza sana mzee Shamo kutokana na yeye kupeleka mchongo ule na kuahidi msaada lakini mwisho wa siku aligeuka kama kinyonga. Kesi iliahilishwa mpaka siku ya pili utakapotolewa ushahidi wa mwisho na mkuu wa kitengo cha kuzuia madawa ya kulevya mzee Shamo. Teddy aliyekuwepo mahakamani alifurahi kuona mambo yamekwenda kama alivyopanga, kazi ilibakia kwake kumaliza kazi. Mzee Shamo alimfuata mke wa Deus na kumuuliza: “Sasa umefanya nini?” “Tutazungumza,” Kilole alijibu kwa sauti ya chini. “Tutazungumza nini, nani aliyeleta taarifa hizi?” “Mimi.” “Sasa kwa nini umenigeuka?” “Lakini wewe si kesho utammaliza.” “Nimmalize kivipi ikiwa umeishapunguza nguvu, wewe ndiye aliyekuwa na kisu kikali cha kumaliza kesi, huoni kama nitabanwa kuwa nimetengeneza kesi?” “Tutazungumza, naomba niondoke eneo hili si salama kwangu.” “Mmh! Nimejua, lakini naapa haponi nitakufa na mumeo.” Kilole aliachana na mzee Shamo aliyemshangaa Kilole kwa kauli yake ya kukana wakati aliapa kutoa ushirikiano wa kutosha na mara ya mwisho usiku kabla ya kukutana na Teddy alimuhakikishia atammaliza Deus. Lakini aliapa lazima ampoteze mbaya wake. Teddy naye alijipanga kuhakikisha mzee Shamo alioni jua la kesho ili kesi ikose nguvu na kumpa nafuu Deus. Baada ya mahakama Kilole na Kinape wakiwa wanajiandaa kuondoka alifika Teddy kwenye gari lao. “Asante mdogo wangu umenifurahisha sana,” Teddy alimpongeza Kilole aliyekuwa akifunga mkanda wa gari. “Lakini kazi bure kesho si anapanda mwenyewe hatujafanya lolote,” Kilole alimjibu kwa sauti ya chini. “Kazi niliyokutuma umeifanya iliyobaki ni yangu, hata akifungwa mumeo hawezi kufungwa miaka mingi.” “Mmh! Siamini.” “Nilimuona anakufuata alikuwa anasemaje?” “Alikuwa akinilaumu kumgeuka.” “Akamjibu nini?“ “ Sikuwa na jibu.” “Najua bado atataka kujua kwa nini umemgeuka.” “Akiniuliza hivyo nimwambieje?” “Mwambie vyovyote vile, lakini kazi itaisha usiku huu.” “Umeishazungumza na hakimu?” “Utajua kesho wakati wa kutolewa ushahidi wa mwisho.” “Haya wacha niende nikapumzike.” Kilole aliondoka huku moyo ukimuuma kushindwa kutoa ushahidi wa kumfunga mumewe. Lakini aliamini mzee Shamo anaweza kumfunga mumewe kwa vile ndiye shahidi namba moja. Mzee Shamo naye alikaa pembeni ya mahakama na vijana wake wakijadiliana juu ya kugeukwa na mke wa Deus mtu aliyefanikisha kukamatwa mume wake. “Sasa mzee tutafanyaje?” “Kwa kweli yule mwanamke kanichanganya sana.” “Sasa tutafanyaje, kesho na wewe ndiye utakayemaliza kutoa ushahidi?” “Dawa iliyopo ni kumshika na kumtesa aseme ukweli ili kesho niweze kupata nguvu katika ushahidi wangu bila hivyo naweza kuonekana kweli nimeutengeneza. Unafikiri wakili wa Deus akisema kuwa nimetengeneza ushahidi ili nimfunge na mkewe amekataa itakuwaje?” “Kwa hiyo kazi tuifanye mara moja kabla hajatoka eneo la mahakamani?” “Hapana anatakiwa akachukuliwe usiku na kupata mateso mazito na kesho atakuja mahakamani akitokea mahabusu.” “Huoni kama anaweza kusema tumemlazimisha?” “Kwa hiyo mnanishauri tufanye nini?” “Mzee inatakiwa tusitumie nguvu tunatakiwa kwanza tujue nini kilichomfanya akugeuke kisha tujue tufanye nini,” kijana mmoja wake mmoja alimpa ushauri. “Halafu kuna kitu alinieleza kuwa usalama wake ni mdogo pale mahakamani.” “Inawezekana kuna watu wanashindana na sisi ambao ni miongoni mwetu.” “Lakini ni yeye aliyeleta taarifa za mumewe kuuza unga sasa anageuka nini kwani tulimfuata?” “Kwa hiyo mzee wangu tunatakiwa kufanya jambo kisomi kuliko kutumia nguvu. Inawezekana kuna kitu kimeingia katikati si umesema jana usiku uliwasiliana naye na kusema kila kitu kipo sawa.” “Hata mimi nashangaa.” “Ukiona hivyo ujue kuna kitu.” “Basi usiku tutakwenda kujua sababu kipi kilichomfanya ageuke kama kinyonga.” **** Majira ya saa kumi na mbili Teddy alikuwa amesimamisha gari lake karibu kabisa na ofisi za kupambana na madawa ya kulevya. Aliwahi makusudi ili aweze kumuona mzee Shamo na kumfuatilia. Baada ya kukaa kwa muda majira ya saa moja kasoro aliliona gari la mzee Shamo likitoka ofisini. Aliliacha lipite kisha alilifuatilia nyuma bila mwenyewe kujua. Mzee Shamo kama kawaida yake alielekea Sea Cliff hoteli, alimfuatilia mpaka alipoingia hotelini. Hakusumbuka sana kumfuata alipaki gari lake pembeni ya gari la mzee Shamo na kumfuata ndani ya baa. Teddy aliagiza wine na kunywa taratibu huku akifuatilia nyendo za mzee Shamo, majira ya saa mbili walitokea vijana wawili na kuondoka naye. Japo alijua ana kazi nzito lakini hakufanya papara. Aliwahi kwenye gari lake walipoondoka aliwafuata taratibu bila wao kujua wanafuatwa na mtu. Waliondoka eneo lililokuwa na taa na kuingia sehemu ya giza aliamini ile ndiyo nafasi aliyokuwa akiitaka. Aliongeza kasi kidogo na kuwapita kisha alilisimamisha gari kwa mbele ghafla iliyosababisha gari la mzee Shamo kulikwangua kwa nyuma. Kilole hakuteremka haraka kwenye gari alitulia bila kufungua vioo. Vijana wa mzee Shamo waliteremka kwa hasira ili wamuadabishe mwenye gari ya mbele. Teddy wakati huo alikuwa amekwisha jiandaa kwa mapigano, bastora yake ilikuwa tayari kufanya kazi. Walifika na kuanza kutukana huku wakigonga kioo kwa ngumi ili afunge. Wakati huo mzee Shamo naye aliteremka na kusogea. Kwa vile ndani ya gari kulikuwa kiza Teddy aliteremsha kioo kidogo na kuachia risasi zilizowapata wote. Hakuondoka haraka aliteremka na kuwaongeza risasi ili kupata uhakika kama kweli wamekufa. Baada ya kumaliza zoezi lake alikimbilia kwenye gari ili aondoke kabla ya kuondoka alisikia king’ora cha polisi kilichomshtua. Alipowasha gari aondoke liligoma kuwaka, aliteremka na kukimbilia sehemu za baharini. Akimbilia na kwenda kujificha nyuma ya mti mkubwa uliokuwa karibu na bahari. Baada ya kujicha alichungulia na kuona gari la doria likisimama eneo la tukio, aliwaona wakiteremka na kuwanza kufanya uchunguzi. “Aisee kuna watu watatu wamelala chini, tuweni makini,” askari mmoja alitoa taadhali baada ya kuona watu wamelala chini. “Tena hii gari kama ya Afande Shamo?” askari mwingine alisema huku akimulika na tochi. “Si huyu!” Teddy alimsikia mmoja akisema kwa mshtuko. “Nani?” “Afande Shamo.” “My God ameuawa?” “Pigeni simu haraka kuongeza ulinzi hali ni mbaya.” “Afande wakati tunakaribia hapa niliona kama mtu anakimbilia baharini.” “Hatuwezi kupambana naye hatujui uwezo wake huenda wapo wengi.” Teddy alitumia nafasi ile kutembea pembezoni mwa bahari mpaka maeneo ya Daraja la Salenda, alichepua mwendo kufuata barabara ya Ali Hasani Mwinyi kuelekea Mwenge. Mbele kidogo gari dogo lilisimama na kushangaa kuitwa jina lake. “Teddy.” “Nani?” “Ingia haraka.” Bila kuuliza aliingia ndani ya gari, haikupita muda gari la polisi lilitokea, lakini halikushughulika nao lilipita huku likipiga king’ora cha hatari. Teddy alishtuka kumuona mbaya wake Tony ndiye aliyekuja kumuokoa. “Vipi Tony unatoka wapi?” “Huwezi kujua, nimetumwa na bosi nikusaidie ameona kila kitu.” “Alikuwa wapi?” “Hiyo haikuhusu ila safari hii moja kwa moja Air Port unatakiwa uondoke na ndege ya saa sita usiku.” “Booking?” “Kila kitu kipo tayari mengine utayajua ukifika chimbo.” Tonny aliendesha gari kwa kasi hadi uwanja wa ndege na kumpatia Teddy tiketi ya kusafiri. Muda ilionesha ni saa tano kasoro sita. Tonny hakuondoka mpaka ndege ilipoondoka kuhofia Teddy kuendelea kuwepo Dar na kuleta tafrani baada ya kukosa uvumilivu wa kutenda mambo. Walihofia huenda akafanya mauaji zaidi kwa vile alikuwa akitumia nguvu bila akili. Teddy aliwasili uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyata saa kumi alfajiri na kwenda moja kwa moja chimbo. *** Siku ya pili Teddy akiwa sehemu yake ya maficho alishtuka kumuona shemeji yake aliyetaka kumuua akiwa mzima wa afya na akikanusha vikali kwamba Teddy ndiye aliyetaka kumuua katika televisheni ya Italy News. Maelezo yake yalimsafisha Teddy aliyekuwa amewekewa WANTED na polisi wa Italia. Maelezo ya shemeji yake yalimchanganya sana Teddy na kujiuliza kwa nini ameamua kumsafisha vile ikiwa amemfanyia kitu kibaya cha kutaka kumuuua lakini alimsafisha mbele ya vyombo vya usalama vya Italia hata kutoka picha za kumuomba radhi Teddy kutokana na kushukiwa na njama za kumuua Moses. Hakiwa bado haamini alipokea simu toka kwa washirika wenzake toka Italia. “Haloo Teddy.” “Ndiyo Jimmy.” “Umepata taarifa za Mose?” “Hapana,” alijifanya hajui kitu. “Mose amekusafisha katika vyombo vya usalama, lakini…” ”Lakini nini tena Jimmy?” “Jamaa amesema yale kwa vile ana uchungu na wewe na amesema atakusaka popote ili alipe kisasi.” “Achana naye hawezi kitu,” Teddy alisema kwa kujiamini. “Teddy humjui Mose! Sisi ndiyo tunamjua, amesema ndani ya mwezi mmoja atakuwa ametia mikononi. Anajua kuna watu wanakukingia kifua eti wanaume zako ataanza kudili na hao na mwisho atakumalizia na hivi ninavyosema anajiandaa kuanza kukusaka.” “Kwani yeye anajua nipo wapi?” “Siwezijua lakini kaa ukijua jamaa kaingia msitari wa mbele kukusaka.” “Poa tutaona mimi na yeye nani atammaliza mwenzake.” “Nataka pia kukueleza Moses ana jamaa zake wanapenda kuua kama hawana akili nzuri, hivyo wakati wowote wataanza kukusaka.” “We mwache aje wala hanitishi kwa jeuri yangu nitamfuata hukohuko.” “Wewe!” “Jimmy hunijui hivi ninavyozungumza nimemlaza mtu mzito serikalini na vijana wake usiku wa kuamkia leo jiji Dar.” “Na sasa upo wapi?” “Jimmy kama umetumwa siwezi kukueleza ila mweleze wala asisumbuke kunitafuta namfuata huko huko,” Teddy alionesha jinsi gani anavyojiamini. “Jamaa amesema anajua sijui upo Kenya sijui sehemu gani, ameniahidi ndani ya mwezi maiti yako itaokotwa barabarani kwanza atakubaka kabla ya kukuua kinyama.” “Umesema amesema nipo Kenya?” Teddy alishtuka. “Ndiyo.” “Mmh! Mwache aje.” “Kuwa makini sitajisikia vizuri nikisikia umeuawa na Mose.” “Sawa Jimmy, nakuahidi nitammaliza yeye kabla hajanigusa.” Baada ya kumaliza kuzungumza na Jimmy simu toka Dar toka kwa bosi wake Double D iliingia.
“Haloo bosi,” Teddy alipokea. “Vipi ulifika salama?” “Nashukuru sana Bosi.” “Basi kuwa makini.” “Sawa Bosi.” “Umezipata taarifa za Mose?” “Kuhusu nini Bosi,” Teddy alijifanya hajui kitu. “Leo amekusafisha kwa vyombo vya usalama ili alipe kisasi, sasa mama vita vya ndani sijui umejiandaa vipi?” “Mkuu utanisaidia vipi?” “Siwezi kuingilia ugomvi wa ndani, ni wewe kuwa makini kwa vile Mose ni mwenzetu.” “Nimekuelewa Bosi kuanzia sasa hivi nitajua niishi vipi naweza nisionekane tena mpaka nitakapomtia mkononi Mose,” Teddy alijibu mapigo. “Kwa hiyo na wewe unamtafuta?” “Nimsubiri animalize, vita siku zote mfuate adui yako, nitatafuta nchi yoyote kuweka kambi ili nimsake hayawani yule wa kiume mbakaji mkubwa.” “Na biashara?” “Sasa hivi nasimamisha kwa ajili ya msako wa huyu hayawani anayetafuta vita na mimi.” “Lakini Mose yupo sawa,” Double D alimtaadharisha Teddy. “Namjua vizuri lakini siwezi kumkimbia akiniwahi basi lakini nitamfanya kitu kibaya zaidi ya kile cha mwanzo.” “Basi kuwa makini, sipendi kukupoteza kwa vile wewe ni mtu muhimu sana.” “Sasa bosi kwa nini usinisaidie kummaliza.” “Msaada labba kukuelekeza sehemu salama, lakini zaidi ya huo siwezi kumbuka kumgeuka Mose sawa na kumsaliti kaka yake ambaye kwangu alikuwa zaidi ya ndugu, nafikiri unafahamu kitu hicho?” “Nafahamu Bosi sina jinsi lakini sifi kikondoo patachimbika,” Teddy alijihami. “Sasa ukihitaji msaada wowote utaniambia.” “Sawa bosi.” Baada ya kukata simu Teddy aliona kimenuka kwani hakukuwa na msaada wowote wa kumlinda kutokana na Mose kuwa ni mwana kikundi na kaka yake aliyekuwa bwana ya Teddy kuwa ndiye mwanzilishi wa kundi lile. Sifa ya kundi lile lilikuwa haliingilii mgomvi wowote wa ndani hata kuuana. Ilikuwa lazima aondoke chimbo alilojificha baada ya kusikia Mose analifahamu, kwake ingekuwa rahisi kuwakimbia polisi wa Italia hata kwa kubadili sura lakini kwa Mose ingekuwa vigumu zaidi ya kutafutana. Kilichokuwa kikimtisha zaidi ni uwezo wa hali ya juu wa Mose kundini katika mapigano, ndiye aliyekuwa akitumiwa kuwaua watu waliokuwa wakiweka kauzibe katika biashara zao. Hivyo suala la kuua kwake lilikuwa sawa na kuzima kibatari. Aliamini kesi ya Deus haina nguvu alijipanga kuondoka mafichoni na kwenda nchi yoyote ambayo aliamini inamfaa kwa muda ule ili kujipanga kumsaka anayemsaka. *****
Jiji Dar kesi iliyokuwa ikimkabiri Deus iliahilishwa kutokana na kifo cha mkuu wa kitengo cha madawa ya kulevya ambaye ndiye aliyekuwa shahidi wa mwisho. Baada ya mwezi mmoja hukumu ilitolewa na Deusi kufungwa miaka saba kutokana na kuonekana kuhusika kwa njia moja ama nyingine japo ushahidi haukumtia hatiani kwa asilimia mia. Baada ya hukumu mkewe Kilole alilia sana kuonesha kuumizwa sana na hukumu ile. Kinape alishangaa kilio cha Kilole, lakini moyoni alimshukuru sana Teddy kuweza kupunguza ukali wa kesi ile ambayo ungefanya Deus aozee gerezani. Baada ya hukumu Deus alichukuliwa na kupelekwa gerezani kutumikia kifungo cha miaka saba. Aliondoka akijua kilio cha mkewe kilionesha jinsi gani ameiachia familia yake maumivu makali. Lakini haikuwa kama alivyofikiria, nyuma ya machozi ya mkewe kulikuwa na kicheko cha furaha cha kummaliza. Mumewe akiwa gerezani Kilole alianza kupanga mipango ya kummaliza kabisa ili akimaliza kifungo chake asikute kitu. Cha kwanza alitaka kumuua mtoto aliyezaa na Deus kitu alichokikataa Kinape kwa nguvu zote. “Sawa tumemfanyia unyama Deus unataka kumuua mtoto wake kwa kosa gani? Kwanza kumbuka hii ni damu yako.” “Ni kweli, lakini anaweza kunigeuka akipata akili na kujua mimi ndiye niliyemfanyia yale baba yake.” “Tafuta njia nyingine lakini si kumuua.” “Sina njia nyingine zaidi ya kumua, nataka mimi na wewe tuanze upya maisha yetu yawe na mtoto wetu wenyewe.” “Kwa hilo sikubaliani nalo.” “Sasa tufanyeje?” “Huyu atakaa hapahapa kama mtoto wako na tutampa matunzo yote na chochote kibaya utachokifanya sitakuwa na suruhu ya kuendelea kuwa na wewe.” “Sawa nitafanyaje lakini simpendi hata kumuona,” Kilole alionesha jinsi gani alivyona roho mbaya hata kwa damu yake. “Kama unaichukua damu yako mimi utanipenda vipi?” “Hapana Kinape nakupenda kuliko nafsi yangu.” “Basi kama unanipenda mpende huyu mtoto mara mbili yangu.” “Nitafanya hivyo kwa ajili yako mpenzi.” MIEZI SABA BAADAYE Katika mapenzi yao haramu Kilole alishika ujauzito Kinape, hapo ndipo Kilole hakutaka kukubaliana na Kinape kuhusiana kuendelea kuwa na mtoto wa Deus. Lakini bado Kinape alikuwa na msimamo makali ikiwa pamoja na kumlazimisha kwenda kumuona Deus gerezani. Kilole kwa vile alikuwa akimpenda sana Kinape alikubaliana naye kwa shingo upande. Mimba ilipoaanza kuonekana alimkataza lakini alikwenda nayo hivyohivyo na kushtua Deus ambaye hakuamini mkewe kumsarti. “Mke wangu hii si mimba?” Deus alishtuka kumuona mkewe aliyemuacha akiwa hana kitu ana ujauzito mkubwa ambao si wake. “Kweli gereza baya, kama kusoma hujui hata kuangalia picha huwezi,” Kilole alijibu kwa nyodo. “Una maana gani mke wangu?” “Hii ni mimba mume wangu.” “Ya nani?” “Ya kwako.” “Si kweli, nimekuacha huna kitu na wala hukuwahi kuniambia una ujauzito.” “Sasa unafikiri ni wa nani?” “Mke wangu mwaka na nusu kuwa gerezani umenisarti?” Deus alisema kwa sauti ya kilio. “Sijakusaliti bali nimempata msaidizi wa kukusaidia mpaka ukitoka gerezani unikute nipo nakusubiri.” “Mke wangu sasa hayo ni maneno gani?’ “Kwani wewe ulikuwa unatakaje?” “Kaitoe hiyo mimba.” “Mume wangu niue kiumbe kisicho na hatia?” “Sasa unafikiri utazaaje mtoto asiye na baba?” “Mume wangu kitanda hakizai haramu, mtoto ni wako.” “Hapana mke wangu pamoja na kufanya kosa la kunisaliti naomba uitoe hiyo mimba.” “Yaani nikae nayo miezi nane niitoe kirahisi nikifa?” “Huwezi kufa mke wangu.” “Hivi huyo mwanaume akisema na yeye amuue mwanao utakubali?” “Nikubali vipi wakati wewe ni mke wangu wa halali.” “Sikuja kwa hayo ila kukufahamisha nimepata msaidizi wa kukutunzia mkeo na mtoto nawe utumikie kifungo kwa amani na mguu huu ni wa mwisho kuja hapa.” “Nooo, usifanye hivyo mke wangu.” “Siwezi kutumikia mabwana wawili.” “Huyo msaidizi ni Kinape?” Deus aliuliza huku amepiga magoti. “Mbona umemtaja yeye ndiye uliyempa kazi ya kukulindia mkeo?” “Hapana mke wangu, mbona unazidi kuniumiza?” “Umejiumiza mwenyewe kwa kufanya biashara haramu kwa siri ningejua si ningeweza kuficha. Nimekutetea mahakamani bado tu unaniona sina maana.” “Nashukuru mke wangu, lakini miaka saba siyo mingi.” “Najua, lakini imetokea hivi unatakiwa ukubali matokeo.” “Nimekubali lakini usiniache bado nakupenda,” Deus alizidi kuumizwa na mkewe. “Basi habari ndiyo hiyo nikitoka leo sitarudi tena labda mwanao,” Kilole alisema huku akiondoka na kumwacha Deus amepiga magoti huku akiendelea kubembeza na machozi kumtoka. Askari magereza alimchukua Deus na kumrudisha ndani, Deus baada ya kurudishwa ndani alijikuta kwenye wakati mgumu maishani mwake. Tokea siku ile aliishia katika maisha magumu huku akiamini yeye ni kiumbe mwenye nuksi. maumivu ya kusalitiwa yalikuwa makubwa zaidi ya yale ya kufungwa gerezani miaka saba. Kitendo cha usaliti wa mkewe kilimuumiza sana kiasi cha kila siku kuonekana mgonjwa mpaka siku alipoitwa na mkuu wa gereza kumkuta mwanaye ofisini na barua yake nzito toka kwa mkewe. **** Kupelekwa kwa mtoto wa Deus gerezani kulifikiwa baada ya mvutano mkali kati ya Kilole na Kinape juu ya kauli ya Deus ya kumlazimisha kuutoa ujauzito wa Kinape uliokuwa na miezi minane. “Hata kama alitaka kuutoa ujauzito huo bado alikuwa na haki ya kusema vile kwa vile wewe ni mkewe.” “Komea hapohapo toka alipofungwa mume wangu ni wewe hivyo na mtoto wake naye hafai kuendelea kuishi.” “Kwa hilo sitakuelewa.” “Sasa nasema hivi kama hutaki tumuue huyu mtoto nitamuua kisha nitajiua na mimi.” “Kwanini umuue, basi tumpeleke wa wazazi wake kijijini?” “Siwezi.” “Basi mpeleke gerezani kwa baba yake.” “Nitampelekaje?” “Mpeleke na kumuacha nje ya gereza na barua mkononi askari wakiumuona watamchukua na kuisoma lazima taarifa zitamfikia.” “Huo si ujinga wakija hapa si nitafungwa.” “Ule mpango umekamilika, nimepata mununuzi wa nyumba na magari.” “Mbona hukuniambia?” “Nilikuwa nikuambie leo.” “Kwa hiyo nitampeleka baada ya kuuza kila kitu.” “Tutabakia na Toyota Land Cruiser tutayoitumia kuuhama mji.” “Tunakwenda wapi?” “Mwanza.” “Ushawahi kufika?” “Sijawahi, lakini nasikia ni mji unakaribiana na Dar kwa ukubwa na mzunguko wa fedha.” “Hakuna tatizo, mauzo saa ngapi?” “Usiku wa leo.” Usiku yalifanyika mauzo ya nyumba za Deus na magari yake tena mbele ya mwana sheria wa mnunuzi. Baada ya makabidhiano walikubaliana waondoke kesho yake, usiku wa siku ile walijiandaa kwa safari ya siku ya pili. Siku ya pili baada ya maandalizi muhimu walimchukua mtoto wa kwenda kumuacha nje ya gereza na kuelekea Mwanza kuanza maisha mapya.
Ndani ya gereza Deusi Ndonga akiwa amejiegemeza kwenye ukuta huku maumivu ya moyo wake yalikuwa makubwa zaidi ya yale ya kufungwa gerezani miaka saba. Lakini kitendo cha usaliti wa mkewe Mwaka mmoja toka aingie gerezani kilimuuliza zaidi. Akiwa bado kaegemea ukuta macho katazama juu alipata ujumbe anaitwa kwa mkuu wa gereza na kwenda kukutana na taarifa zilizozidi kumuumiza na kutamani ardhi ipasuke na kummeza. Deus alimalizia simulizi ndefu sana iliyochukua zaidi ya saa mbili, baada ya simulizi ndefu kwa mkuu wa gereza ya sababu ya yeye kuingia gerezani na kusalitiwa na mkewe na rafiki yake kipenzi Kinape. Mkuu wa gereza aliyekuwa akimsikiliza kwa makini alijikuta akitokwa na machozi ya uchungu bila kujua. (Kwa wasomaji wapya yote hii ni simulizi ya Deus aliyokuwa akimuhadithia Mkuu wa Gereza mwanzo wa hadithi hii baada ya mtoto wake aliyeambatana na barua kuletwa gerezani na mkewe Kilole aliyekuwa tayari ana ujauzito wa rafiki yake kipenzi Kinape.) Mkuu wa gereza baada ya kumsiliza alishusha pumzi ndefu na kusema kwa sauti ya huruma: “Pole sana Deus.” “Sijapoa kila dakika maumivu moyoni mwangu yanazidi mara dufu.” “Ni kweli, lakini wanaume tumeubwa kukabiliana nayo.” “Ni kweli lakini inauma sana.” “Nina imani hawa washenzi wapo nyumbani kwako?” “Ndiyo mkuu.” “Sasa hivi nitaomba msaada wa polisi wakamatwe mara moja.” “Nitashukuru, japo sikupenda tufikie huko zaidi ya kutupatanisha.” “Deus usiwe mjinga kwa hatua hii hakuna suruhu.” “Sawa mkuu, utakachofanya chochote sawa.” Mkuu wa gereza alipiga simu kwa mkuu wa jeshi la polisi na kumweleza kwa ufupi mkasa ule na kuomba msaada wake. Alimuhadi baada ya muda atampa jibu. Deus aliombwa arudi gerezani na mwanaye kwa kipindi kile atakuwa nyumbani kwa mkuu wa gereza. Deus alirudi kichwa chini machozi na makamasi yakimtoka kama mtoto mdogo. Kila dakika kwake aliiona ni mateso mazito na kujiuliza baada ya yale kipi kinafuata. Alipofika alirudi sehemu yake na kuendelea kuegemea ukuta macho alitazama juu lakini hakuna alichokiona zaidi ya maumivu makali ya moyo aliohisi unavuja damu. Mkuu wa gereza aliletewa majibu ambayo aliamini lilikuwa pigo lingine mujarabu kwa Deus. Taarifa zilizotoka polisi ni kwamba Kilole mke wa Deus aliuza nyumba na magari yote na kuondoka. Ila taarifa ilisema itafanya uchunguzi watu hao wapo wapi. Mkuu wa gereza alijikuta akipata wakati mgumu wa kumweleza Deus unyama mwingine aliofanya mkewe. Lakini hakuwa na jinsi alimtuma mtu amwite ili ampe taarifa ambazo aliamini lazima awepo daktari la sivyo wangempoteza. Kabla ya kumwita Deus kumpa taarifa za nyumbani kwake, mkuu wa gereza alimwita daktari mkuu wa gereza na kumwelezea taarifa zile na kumuomba awe karibu kama tukio lolote litatokea aweze kutoa huduma ya kwanza. Baada ya kumwita daktari, mkuu wa gereza alimtuma mtu amfuate Deus gerezani. Deus alikuwa amejiegemeza kwenye ukuta wa chumba cha gereza akiwaza na kuwazua aliyofanyiwa na mkewe Kilole na rafiki yake kipenzi Kinape. Maumivu aliyokuwa akiyapata alitamani dunia imfukie akiwa mzima baada ya kuamini hana thamani yoyote. Alirudisha kumbukumbu jinsi alivyomsaidia Kinape na pia familia ya mkewe Kilole, hakutegemea kama wangemtendea unyama kama ule. Alishtuliwa na sauti ya kuitwa, alinyanyuka na kusogea mlangoni alikukutana na askari: “Mheshimiwa unaitwa na mkuu.” “Sawa,” alijibu kwa sauti ya chini. “Nifuate,” Deus alimfuata bila kusema kitu akiamini Kilole na Kinape watakuwa wamekamatwa. Moyoni hakupenda Kilole akamatwe kwa ajili yake kwa kuamini bado ana nafasi nyingine kwake. Aliongozana na askari mpaka nje ya ofisi ya mkuu wa gereza, kutokana na maelezo ya mkuu kwa secretary wake, walipofika aliruhusiwa kuingia ofisini. “Deus unaweza kuingia,” secretary alimwambia Deus. Deus aliingia ofisini kwa mkuu na kumkuta akimsubiri. “Karibu Deus.” “Asante mkuu,” Deus alijibu kwa sauti ya chini. “Kaa kwenye kiti,” Deus alikaa na kutulia kumsikiliza mkuu wa gereza. Kabla ya kusema mkuu wa gereza alimtazama Deus na kumuonea huruma kwa kuamini moyoni mwake kuna mateso mazito, lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kumwambia ukweli. “Deus,” mkuu alimwita kwa sauti ya upole. “Naam mkuu.” “Najua moyoni mwako upo katika hali gani, lakini kama mwanaume unatakiwa kupambana nayo.” “Ni kweli, lakini nimeshtukizwa sana.” “Ukiwa mwanaume unatakiwa kukabiliana na yote, siku zote mwanaume ni mpambanaji na kutatua matatizo mazito.” “Ni kweli kabisa mkuu, lakini nitawezaje kukabiliana nayo wakati nipo gerezani?” “Unatakiwa kuachana na mambo ya nje ya gereza ili utumikie kifungo chako ukitoka utakuwa na nafasi ya kukabiliana nayo. Lakini ukiwa humu ndani na kufikiria ya nje yatakuchanganya.” “Najitahidi kufanya hivyo lakini kila dakika linazuka zito kuliko la mwanzo.” “Yote hiyo ni mitiani ya maisha unayotakiwa kuikabili hakuna maumivu unayoweza kupokewa na mtu.” “Nimekuelewa mkuu, vipi wamepatikana?” “Kuna taarifa zisizo nzuri, lakini unatakiwa nazo kuzipokea kama mwanaume.” “Taarifa gani?” Deus aliuliza huku moyo ukimlipuka. “Mkeo ameuza kila kitu.” “Ameuza kila kitu una maana gani sijakuelewa?” “Mkeo ameuza nyumba na magari yote.” “Sasa yeye kakaa wapi?” Deus aliuliza swali la kizuzu. “Siwezi kujua.” “Mkuu unasema kweli au unatania?” ”Ni kweli kabisa kutokana na taarifa za kipolisi kuwa zilizofika nyumbani kwako kumekutwa mtu mwingine ambaye amenunua kila kitu jana usiku. Kwa maana hiyo mkeo hajulikani hayupo ila kauza kila kitu.” “Ooh! Mungu,” Deus alisema na kujilaza nyuma ya kiti na kuseleleka mpaka chni alipotua kama mzigo. Mkuu alijitahidi kumuwahi lakini alichelewa Deus alikuwa amekwishafika chini, alipomuangalia alikuta amepoteza fahamu. Haraka alimwita mganga mkuu ambaye hakuwa mbali na kuja kumpa huduma ya kwanza Deus aliyekuwa hajitambui. Walimpatia huduma ya kwanza lakini haikuweza kumsaidia Deus ambaye viungo vya upande mmoja vilionesha kupoteza mawasiliano. “Mkuu hali ni mbaya,” dakta Fukwa alisema huku akijifuta jasho kutokana na kujitahidi kwa muda mrefu kuokoa hali ya Deus bila mafanikio. “Sasa tutafanyaje?” “Hatuna ujanja, tumuwahishe Muhimbili.” “Basi tufanye haraka.” Mkuu wa gereza aliiita gari la wagonjwa lililofika na kumchukua Deus kumuwahisha Muhimbili kupata huduma kubwa. Gari lilimchukua haraka na kumkimbiza hospitali. Walipofika Muhimbili bado Deus alikuwa hajitambui alichuliwa haraka na kukimbizwa chumba cha wagonjwa mahututi. Baada ya kupokelewa alipatiwa huduma ya haraka ili kuokoa maisha yake, walifanikiwa kuyashtua mapigo ya moyo yaliyokuwa yakipungua kila dakika na kuweza kumwekea mashine za kupumulia. Deus alipata ufahamu wa mbali baada ya siku mbili sehemu moja ilikuwa na mawasiliano lakini upande wa pili imepoteza mawasiliano. Hali ile ilimfanya akae hospitali zaidi ya miezi mitano kutokana na kujaribu kuutibu ugonjwa wa kupoteza mawasiliano mwilini. **** Kilole na Kinape baada ya kufika jiji Mwanza na kukaa kwenye nyumba ya wageni huku wakijipanga kutafuta kununua nyumba ya kuishi. Kwa vile walikuwa na fedha waliweza kupata nyumba nzuri maeneo ya shule Isamilo. Haikuchukua muda mrefu walifungua maduka makubwa ya kuuza vitu vya jumla na rejareja mtaa wa Liberty. Kwa muda mfupi maisha yao yalibadilika kutokana na kufahamika haraka kutokana na uwezo wao wa kifedha. Gari walilosafiri nalo toka Dar waliliuza na kununua lingine. Wakati huo Kilole alikuwa amejifungua mtoto wa kike waliyempa jina la Gift. Pamoja na kufanyiwa yote yale Kinape bado alikuwa na kisasi kizito moyoni mwake cha kuuawa mpenzi wake Happy bila sababu. Kila dakika aliyokuwa peke yake alimkumbuka mpenzi wake na kupanga kumfanyia kitu kibaya Kilole ambacho hata sahau maishani mwake. Kilole upande wake aliamini Kinape anampenda sana na ndiye mwanaume wake sahihi maishani mwake. Alipanga kumpigania kwa nguvu zote kuhakikisha hampotezi alikuwa radhi kuendelea kutoa roho ya kiumbe yeyote wa kike atakayemsogelea karibu mpenzi wake. ***** Teddy baada ya kutoka Kenya alikwenda kujificha nchini Ujerumani katika jiji la Hamburg katika hotel ya nyota nne ya Senator. Lakini pale alikaa wiki tatu na kupewa taarifa za tahadhari kubwa. Akiwa amejipumzisha chumbani kwake alipata simu toka kwa bosi wa kikundi Double D. “Haloo Teddy upo wapi?” “Kwa sasa sitaki kumjulisha mtu nipo wapi wacha nipumzike.” “Teddy kuwa serious kuna kitu kibaya kinakukabiri.” “Kitu gani? Acha kunitisha?” Teddy aliamini ni utani. “Mose anakutafuta ile mbaya amefika Kenya kwenye chimbo lako na kukukosa alikuja Dar na kuniuliza juu yako lakini nilisema sijui chochote. Inaonesha kuna mtu katika kundi letu anawasiliana na Mose na kumwambia mimi nafahamu kila kitu kuhusiana na wewe pamoja na kumkatalia lakini alinihakikishia lazima akutie mikononi.” “Hawezi kujua nipo wapi,” Teddy alisema kwa kujiamini. “Kuna taarifa kuwa upo Ujerumani.” “Nani kawaambia?” Teddy alishtuka. “Mtu akitaka kumkamata mtu hashindwi, nimekueleza toka awali kuwa mtu yule anajiamini sana kuna kitu anakitegemea ndiyo maana alifuta ushahidi wa kukutia hatiani ili alipe kisasi kwa mkono wake.” “Kwa hiyo Mose anajua nipo huku?” “Ndiyo.” “Mmh! Nani kamwambia nini nipo huku?” Teddy hakuamini kusikia vile. “Wewe si unaona unafanya siri lakini mambo yako mengi yapo nje, kuwa makini badili mfumo wako wa maisha la sivyo utapotea.” “Kwa hiyo Mose sasa hivi yupo wapi?” “Kwa taarifa nilizozipata sasa hivi Mose na kundi lake wapo Ujerumani tena katika mji wa Humburg.” “Muongo! Acha utani.” “Sasa hivi anafanya msako wa Hotel zote za nyota tano.” “Mungu wangu, sasa nifanyeje?” Teddy alichanganyikiwa. “Fanya uwezavyo uondoke sasa hivi la sivyo mpaka kunapambazuka jina lako litabakia simulizi midomoni mwa watu.” “Niende wapi?”
“Fanya hivi, rudi nchi yoyote ya Afrika nina imani kwake akikukosa atakutafuta kwenye nchi za Ulaya au Marekani. Ukiwa Afrika hata kama msaada wangu utahitajika nitaweza kuja kukusaidia.” “Sasa Afrika niende nchi gani? Maana sasa hivi nimeingia woga.” “Sitaki kukueleza nenda nchi gani wala sitaki kujua atakuwa wapi la muhimu ondoka sasa hivi ukichelewa shauri yako.” Teddy alipakia vitu vyake kwenye begi na kuondoka usiku uleule aliona heri aende moja kwa moja nchini Ghana. Aliamua kukaa palepale mjini Accra katika hotel ya nyota mbili ya East Gate iliyopo maeneo ya East Legon. Taarifa za kusakwa kila kona ya dunia na Mose ilimchanganya sana na kuona muda si mrefu atamtia mikononi na kumuua. Wazo lililomjia ni kwenda kubadili sura ili aweze kumkwepa Mose japo hakupenda katika maisha yake kuibadili sura yake. Kutokana na kuona vita ni kubwa pamoja na kumkimbia bado hakutakiwa kukubali kirahisi kushindwa zaidi ya kupambana. Siku zote aliamini mwindaji hujiamini kuliko anayewindwa naye aliona ile ndiyo nafasi yake maye kuanza kumwinda taratibu. Akiwa chumbani kwake amepumzika kama ilivyokuwa kawaida yake kupenda kutoka usiku na mchana kutulia chumbani kwake. Alipenda sana muda ambao hakuwa na kazi za kufanya kucheza game na alipochoka alilala. Kuhakutaka kufanya chochote kwa wiki mbili ili kupumzisha akili na kuchunguza Mose atakuwa wapi ili asikurupuke na kujiingiza katika mdomo wa mamba. Baada ya wiki mbili kukatika akiwa amejipumzisha chumbani kwake alipatwa na mshtuko baada ya kuona taarifa za kushtusha za kifo cha bosi wake mtu aliyekuwa akimtegemea Double D aliyeuawa na baadhi ya washirika wenzake aliouawa kinyama habari na picha zilizorushwa na shirika la habari la CNN. Yalikuwa mauaji yalioutikisa jiji la Dar na nchi ya Tanzania. Teddy alichanganyikiwa ilibidi ampigie simu Jimmy aliyekuwepo Italia kuhusiana na kifo cha Double D na baadhi ya washirika. Baada ya kuipokea kwanza Jimmy alionesha kushtuka na kuuliza: “Ha! Teddy upo salama?” “Jimmy nipo salama kwani vipi?” “Hali ni mbaya Mose kawa mbogo anaua ovyo.” “Unataka kuniambia yeye ndiye aliyemuua Double D na kina Tony?” “Ndiyo.” “Kwa sababu gani?” “Kwa ajili yako.” “Kwa ajili yangu ndiyo awaue?” “Kwa taarifa zilizonifikia baada ya Mose kujua amejificha wapi nchini Kenya, alipofika na kukukosa. Inasemekana aliyekushtua ni Double D, nasikia walikoromeana sana kuhusiana na yeye kukushtua na kuweza kutoroka kiasi cha kutishiana maisha. “Baada ya Mose kukufuatilia aligundua upo Ujerumani katika jiji la Humburg alifika mara moja na kundi lake, lakini hakufanikiwa kukuona. Kuna mtu katika kundi sijui nani alimweleza kuwa Double D ndiye aliyekubumburusha na kutoroka tena. “Kitendo kile kilimkasirisha sana Mose na kumfuata Double D na kuchimbana mkwara katika kujitupiana maneno Double D alimpiga Mose kama mdogo wake. Mose hakukubali alimtolea bastora na kumlipua kila aliyetaka kumsaidia naye aliuawa kisha walitoroka.” “Mmh! Kazi ipo sasa hivi Mose yupo wapi?” “Amerudi Italia.” “Na ana mpango gani na mimi?” “Siwezi kujua nataka nikuambie kitu kama anataka kumkimbia Mose nenda Tanzania kwa sasa kwa vile hawezi kwenda kwa kuhofia kukamatwa.” “Nitajua mwenyewe niishi wapi lakini wapi nitakuwepo itabakia siri yangu ila nashukuru kwa ushauri wako.” “Take care, Mose kapagawa kawa kama mbwa mwenye kichaa anamuua kila ajae mbele yako sijui akikushika itakuwaje anaweza kukula nyama mbichi.” “Nimekuelewa Jimmy.” Baada ya kukata simu Teddy alijitupa kitandani na kuamini yupo kwenye wakati mgumu na Mose. Pamoja na kuua na kukimbia bado alijua atazidi kumtafuta huenda kamtumia Jimmy ili aweze kumtia mikononi. Lakini bado hakutaka kuitoa siri nje atakufa nayo. Akiwa amejilaza kitandani macho akitazama juu alijikuta akiingiwa na hofu kubwa ya kifo cha Double D na kina Tony kilimchanganya sana na kuamini kama wale watu aliowategemea wameuawa na Mose yeye asingekuwa kitu kwake. Alijilaumu sana kumbakiza duniani na kujiuliza alikosea sehemu gani iliyomfanya Mose aendelee kuwa hai. Aliona kuna umuhimu wa kutafuta jeshi la kumuongezea nguvu kuweza kukabiliana na Mose na kundi lake lililomtishia maisha. Hakutaka kuendelea kumkimbia zaidi ya kujibu mapigo kwa yeye naye kuanza kumwinda adui yake. Wazo la haraka lilimjia lilikuwa kurudi Tanzania kumtafuta Deus kufanya kila awezalo kumtoa gerezani aweze kumsaidia kwa vile alionekana ni mtu mwenye uwezo mkubwa sana wa kutumia siraha kutoka na historia yake aliyoipata toka kwa aliyekuwa sekretary wake. Deus alichaguliwa kujiunga na kitengo cha kupambana na madawa ya kulevya kutokana na utukutu wake na uwezo wa kutumia siraha za moto na mikono kwa ufasaha mkubwa. Teddy aliona kuna haja ya kutumia kiasi chochote cha fedha kumtoa Deus gerezani. Wakati akiwaza hayo muda huo ndiyo Deus alikuwa akitoka hospitali baada ya kupata nafuu kubwa ya kumwezesha kuendelea na kifungo kilichobakia. Pamoja na kurudi gerezani bado kazi ngumu hakuweza kuzifanya, mkuu wa gereza alipanga katika watu watakaopata msamaha wa rais basi mmoja wapo atakuwa Deus. Aliapa kumsaidia Deus mpaka atakapomtoa gerezani kwa kumpa upendeleo wa pekee kwa kula chakula kizuri hata sehemu yake ya kulala ilikuwa nzuri. ***** Teddy aliteremka kwenye gari ka kifahari nje ya gereza la segerea na kwenda moja kwa moja kwenye ofisi za gereza na kuomba kuonana na mkuu wa gereza. Baada ya kujulishwa alimruhusu apelekwe ofisini. “Karibu bibie,” Mkuu wa gereza alimkaribisha msichana mrembo. “Asante mzee wangu, shikamoo.” “Marahaba.” Baada ya Teddy kukaa ulipita ukimya mfupi huku akiwa ameinama kuonesha mwingi wa aibu akichezea vidole, mkuu wa gereza alivunja ukimya. “Ndiyo mama nikusaidia nini?” “Nilikuwa na shida na Deus.” “Deusiii…Deus …yupi?” alimuuliza huku akimkazia macho. “Mfungwa wako aliyefungwa kwa tuhuma za dawa za kulevya miaka zaidi ya miwili iliyopita.” “Sasa mwanangu si ungekwenda gerezani tu ukamuone, huku ni sehemu ya utawala tu mama yangu,” mkuu wa gereza alimjibu kwa ustaarabu. “Kuja huku nina sababu yangu mzee wangu.” “Sababu gani?” “Nataka kuzungumza naye faragha.” “Kuhusu nini?” “Mzee wangu ungenikutanisha naye ningefurahi sana.” “Una muda gani hujaonana naye?” “Mmh! Muda mrefu sana nimeondoka bado hajahukumiwa, taarifa za kufungwa nilizipata nikiwa nje ya nchi. Jana nimefika nataka kumuona na kesho naondoka haitakuwa vizuri kuondoka bila kumuona.” “Sheria za gereza haziruhusu mtu kutembelea katikati ya siku zaidi ya kusubiri siku ya kutembelea wafungwa jumapili.” “Naomba msaada wako nina imani utafurahi mimi kuonana na Deus pia nina mazungumzo mrefu na wewe ambayo pia nina imani tutaelewana na hutanisahau maishani mwako.” “Wewe ni nani wake?” “Ni mtu wake wa karibu sana.” “Unajua yaliyomtokea?” “Zaidi ya kufungwa sijui kingine.” “Ni mengi yamemkuta akiwa gerezani, amekaa hospitali zaidi ya miezi sita.” “Mungu wangu nini tena?” Teddy alishtuka. “Alipooza mwili upande mmoja.” “Ooh! Jesus,” Teddy alisema sauti ya kukata tamaa. “Lakini sasa hajambo japo hawezi kufanya kazi nzito.” Teddy aliinama na kujikuta akipoteza tumaini alilolitegemea bila kutarajia machozi yalimtoka. Hali ile alioona mkuu wa gereza na kuamini kweli yule mtu wake wa karibu aliyeguswa na tatizo la Deus. “Pole sana binti.” “Asante, inauma sana kwani nini kilimsibu mpaka kuwa hivyo?” “Ni historia ndefu ya kusikitisha ya kutoa machozi kwa vile mwenyewe yupo atazungumza naye.” Mkuu wa gereza alimtuma mtu kwenda kumwita Deus gerezani, Deus alikuja akiwa na maswali mengi kwani kila alipoitwa alikutana na kitu kilichouumiza moyo wake. Alipoingia ofisi ya mkuu wa gereza hakuamini kumuona mtu alimpigania kwa nguvu zote lakini alivyopotea hakujua. “Ha! Teddy?” “Ni mimi Deus pole sana.” “Asante, za siku?” “Mmh! Wee acha tu.” “Ukisema hivyo sisi tutasemaje?” Mkuu wa gereza aliwapa nafasi ya kuzungumza, Teddy alitaka kujua nini kilichomsibu Deus kiasi cha kupooza mwili na kulazwa hospitali kwa miezi mingi. Deus hakumficha alimweleza yote baada ya kuondoka jinsi mkewe na rafiki yake kipenzi walivyomtenda. Simulizi ile ilimtoa machozi Teddy na kujikuta akijifuta kamasi nyembamba na mishipa ya kichwa kumsimama. “Amini Deus kwa maelezo yako hata zile dawa za kulevya zimewekwa na mkeo na rafiki yako nina uhakika huo kuna siku nilikwenda kwa mkeo kutafuta njia ya kukutoa gerezani. Nilimkuta mkeo anafuraha amefungulia muziki kwa sauti kubwa, nilishtuka lakini leo nimepata jibu.” “Hata mimi naanza kuamini hivyo.” “Kuna kitu kilinileta na kuwa tayari kutoa kiasi chochote cha fedha ili utoke tuifanye kazi moja ambayo imeniweka katika maisha ya wasiwasi. Lakini hali yako imenikatisha tamaa.” “Kazi gani?” Deus alimuuliza akimtazama usoni Teddy naye ilibidi aeleze mkasa toka alipokamatwa mara ya kwanza uwanja wa ndege na vijana wa Deus na kisasi achokilipa na bahati mbaya adui yake alipona kifo na kuanza kumsaka mpaka kufikia kuua sehemu kubwa la kundi lao akiwemo bosi wao Double D. “Utani huo unataka kuniambia kikosi chote kile kimepukutika?” “Wee acha, nimebakia mimi tu.” “Kweli mwanaume kapania, sasa ulikuwa unahitaji msaada gani toka kwangu?” “Msaada niliokuwa nataka tuunde jeshi la watu wawili wa kumsaka Mose na kummaliza. Lakini hali yako nina imani huwezi kutoa msaada wowote, nitakuwa nimechemka sina jinsi. Mkeo nikimuona nitamuua kwani kama nitakufa mimi sababu ni yeye.” “Kuhusu hali yangu sasa hivi nipo sawa, ila mkuu amenieleza msamaha wa rais utakaotoka mimi nitakuwa mmoja wapo, hivyo kanieleza niendelee kuigiza bado mgonjwa ili watu waamini naumwa hata nikiachiwa wasiwe na wasi na kuachiwa kwangu.” “Mnategemea kuachiwa lini?” “Baada ya sherehe ya uhuru mwezi ujao.” “Kumbe siyo mbali.” “Siyo mbali japo sijui maisha yangu nikitoka yatakuwaje?” “Kuhusu maisha usiwe na wasiwasi kila kitu utapata kwangu na tukifanikiwa kumtokomeza yule nduli nitakupa utajiri mara tatu ya ulioupoteza.” “Japo najua ni kazi lakini nina imani nitamtuliza.” “Mbona unajiamini hivyo?” Teddy alimshangaa Deus.
“Matukio ya hatari kama hayo ndiyo nayataka, tena usisumbuke kuongozana na mimi utanipa picha yake tu, nikitoka sirudi mtupu.” “Deus mbona kama siamini maneno yako?” “Nimepewa kazi na cheo kutokana na kuwatuliza watu kama ninyi. Mkono huu umetoa uhai wa wajinga wengi sijawahi kunyoosha mkono ukarudi mtupu,” Deus alisema kwa kujiamini. “Kama ni kweli natakani utoke hata leo maana sina raha mpaka sasa sijui hatima yangu.” “Vumilia siku zimebakia chache sana.” “Kwa nini nisizungumze na mkuu wa gereza kwa kumpa kiasi chochote ili utoke?” “Acha papara kwa vile njia nzuri yenye uhuru ipo tusuburi, ingekuwa kuna mizengwe ningekuruhusu.” “Hawezi kubadili mawazo?” “Hawezi, kila kitu humu ndani anapanga yeye hivyo hawezi.” “Je, akihamishwa?” “Si rahisi mbona kila kitu kipo sawa usihofu,” Deus alimtoa hofu Teddy. “Nashukuru wazo langu limepata nguvu.” “Wee tulia mbona nitamzima kama kibatari,” Deus alisema kwa kujiamini. Maneno ya Deus yalimpa nguvu na kukubaliana na kauli ya aliyekuwa sekretari wake kuwa Deus ni mtu hatari sana. “Pia nilikuwa naomba ushauri kwa sasa nikakae nchi gani kukusubiri, maana nimechanganyikiwa?” “Kwa nini usumbuke, nenda Mwanza ukapumzike tafuta hoteli yoyote nzuri ukae hapo nina imani muda si mrefu tutakuwa pamoja.” “Hawezi kunifuata huko?” “Sasa hivi kukupata itakuwa ngumu kutokana na mtandao aliokuwa akiutegemea umesambalatika.” “Kwa hiyo unanishauri niende Mwanza?” “Nina imani ni sehemu salama, ningekushauri uende Arusha ule mji wa kitalii sana unaweza kuonekana kwa bahati mbaya, lakini nina imani Mwanza ni sahihi sana kwako.” “Sawa nikitoka hapa nakwenda moja kwa moja uwanja wa ndege hadi Mwanza, vipi una tatizo lolote linalohitaji msaada wangu kwa sasa?” “Kwa sasa sina, nitakuwa nalo nitakapotoka gerezani.” “Sasa nitajuaje umetoka?” “Kila kitu utawasiliana na mkuu.” “Hakuna tatizo.” “Nimepata wazo la haraka.” “Wazo lipi hili?” “Nakuomba ukiweza muombe mkuu upumzike kwake mpaka usiku ndipo uondoke. Mchana si mzuri kiusalama unaweza kuonekana na mtu kisha ukawa hujafanya kitu chochote.” “Atakubali?” “Hawezi kukataa, sasa hivi huyu mzee namuona kama baba yangu mzazi amenisaidi vingi.” Aliitwa mkuu wa gereza na kukaribishwa kwenye mazungumzo ambayo aliisha vizuri kwa kukubaliana kumtoa Deus pia kuwasiliana muda wote kabla ya kutoka. Teddy alimuomba mtoto wa Deus awe naye muda wote wa kumsubiri kutoka gerezani. Deus hakuwa na kipingamizi mtoto wa Rose alipewa Teddy aliyesafiri naye usiku wa siku ile. Shukurani yake kwa msaada wa mkuu wa gereza Teddy alimpatia cheki ya shilingi milioni kumi. “Nashukuru sana mwanangu nakuahidi muda si mrefu Deus utaungana naye, nimefurahi kutokea mtu kama wewe bila hivyo niliamini maisha ya Deus yangekuwa mabaya sana.” “Siku zote akufaae kwa jua mfae kwa mvua.” Usiku wa siku ile Teddy alisafiri na mtoto wa Deus kuelekea Mwanza kupumzika kumsubiri Deus atoke gerezani ili ampe msaada wa kummaliza Mose anayemsaka kama gaidi. JIJINI MWANZA Toka wafike Mwanza pamoja na mapenzi mazito aliyopewa Kinape hakufurahia maisha aliyokuwa akiishi na Kilole. Siku zote alimchukia badala ya kumpenda kutokana na matendo yake mabaya hasa baada ya kumuua mpenzi wake Happy pia hata kumfunga mumewe ambaye ni rafiki yake kipenzi. Aliamini kama Deus atatoka salama basi maisha yake yatakuwa hatarini kwa kujua yeye ndiye adui yake namba moja. Wazo la kwenda kuomba msamaha kwa Deus alikuwa nalo lakini alijiuliza atampokeaje na atamueleza nini amuelewe? Akiwa dukani peke yake baada ya Kilole kwenda nyumbani, alitokea msichana mmoja aliyekuja kununua mahitaji. Macho yake yalipatwa na mshtuko wa ajabu kumuona yule msichana anafanana sana na mpenzi wake Happy. Moyo ulimshtuka baada ya kumuona msichana yule, kwa vile alikuwa amekwenda kununua vitu dukani mwake aliamua kumsemesha. “Habari mrembo?” “Jamani kaka yangu, kweli umechanganyikiwa wakati naingia dukani si tulisalimiana?” “Nitakuwa nimechanganyikiwa.” “Kipi kimekuchanganya kaka yangu?” yule msichana alimuuliza kwa sauti ya upole huku akitabasamu, Kinape alizidi kuchanganyikiwa kuiona picha ya marehemu mpenzi yake mbele yake. “Baada ya kukuona.” “Sasa nini kimekuchanganya baada ya kuniona?” “Umefanana sana na aliyekuwa mpenzi wangu.” “Labda ndiye mimi.” “Hapana, yeye alifariki zaidi ya mwaka na nusu.” “Ooh! Pole sana.” “Asante.” “Kwa hiyo baada ya kufariki hukutafuta mpenzi mwingine?” “Ninaye.” “Basi, usingekuwepo ningeichukua miye,” yule msichana alimtania. “Kwani wewe upo singo?” “Kwa ajili yako ningekuwa singo.” “Wewe mwenyeji wa wapi?” “Singida.” “Wawoo, mkoa aliotoka marehemu mpenzi wangu.” “Inaonekana ulikuwa unampenda sana?” “Tena sana.” “Nini kilichomuua?” “Ni historia ndefu sana ila hatanitoka moyoni mwangu mpaka nakufa.” “Ooh! Pole sana.” “Asante.” “Basi inaonekana una bahati wa wasichana wa mkoa huo?” “Inawezekana, unaitwa nani mrembo?” “Happy.” “Noo, serious?” Kinape alishtuka. “Ndiyo, mbona umeshtuka hivyo?” yule msichana aliuliza. “Siamini, mfanane sura, umbile na jina hata sauti….siamini.” “Muongo! Mpenzi wako alikuwa akiitwa Happy?” “Ndiyo! Inawezekana kabisa Mungu kakuleta ili upoze maumivu yangu.” “Lakini wewe si una mke?” “Ninaye kama kivuli nina imani kabisa wewe ni mtu sahihi kwangu.” “Lakini mimi si mkaaji Mwanza natarajia kuondoka leo na ndege ya mchana mpaka Dar kisha nirudi kwangu Arusha.” “Arusha unafanya nini?” “Nipo katika shirika moja la kitalii.” “Na hapa Mwanza?” “Nimekuja kwa shangazi yangu mmoja anakaa maeneo ya Kilimahewa.” “Kwa nini usiondoke kesho ili jioni tuzungumze zaidi, yaani siamini nakuona kama ni mpenzi wangu Happy uliyefufuka ili kunipoza machungu ya kila siku kila nimkumbukapo.” “Itakuwa ngumu kwa vile tayari nimeishatoa taarifa yakuondoka na ndege ya mchana huu.” “Usihofu Happy, kila kitu kuanzia sasa nitakuwa juu yangu gharama ya tiketi yako itakuwa juu yangu.” “Hakuna tatizo, basi kuwa na ahadi za ukweli nisije ahirisha safari yangu kisha nilale pele yangu. Nitakuja kukutoa nishai mbele ya mkeo.” “Mimi ndiye niliyekuomba ubakie hivyo siwezi kwenda kunyume.” “Haya nipe namba ya simu.” Kinape alimpa Happy namba ya simu kisha yule pacha wa Happy alimbeep Kinape ili kumpa namba yake na kuondoka na kumuacha Kinape akimsindikiza kwa macho asiamini kumuona Happy mbele yake. Baada ya kuondoka aliamini kabisa ile ndiyo nafasi yake ya kulipa kisasi kwa Kilole kutokana na pigo alilompiga la kumuua mpenzi wake Happy. **** Teddy baada ya kufika jijini Mwanza alikwenda kukaa sehemu za Nyakato katika Hoteli iliyokuwa ndani kidogo ya Green Motel iliyopo maeneo ya Nyakato Nundu. Japo ilikuwa ya nyota moja aliamini kwa muda wa kumsubiri Deus kukaa sehemu ile si pabaya sana. Vazi lake kila alipotoka lilikuwa hijabu iliyomuacha wazi usoni na kuvaa miwani, siku nyingine alivaa wigi na miwani kubwa kila alipotembea alikuwa na Rose mtoto wa Deus ambaye alimfanya kama mtoto wake kwa kumpa matunzo ya hali ya juu. Akiwa amekwenda benki kubadili fedha kwa ajili ya matumizi, wakati anatoka kamshikilia mtoto mkono wakielekea kwenye gari alikutana na Kilole aliyekuwa akiingia benki. Kilole alipomuona Rose alishtuka lakini aliamini kabisa kamfananisha mwanaye, alisimama na kumuangalia yule mtoto aliyeamini kabisa ni mwanaye Rose. Aliangalia aliyenaye bado hakuwa na uhakika kutokana na mwili wote kufunikwa na hijabu. Alipotaka kuendelea na safari alimsikia yule mwanamke akimwita yule mtoto: “Rose nikununulie ice cream.” “Yes mamy.” Teddy alitoa fedha na kumwita mwenye kigari cha Ice Cream, alinunua mbili kisha waliingia kwenye gari na kuondoka. Kilole alishtuka na kuliangalia lile gari ambalo lilikuwa la kukodi katika makampuni ya magari mpaka lilipotea kwenye macho yake. Hakuingia tena benki alikimbilia hadi kwenye gari lake na kujifungua kwa ndani kisha alitoa simu na kumpigia Kinape. “Haloo baby,” Kinape alipokea upande wa pili. “Kinape..Kinape,” alimwita kwa sauti ya muhemo kitu kilichomshtua Kinape. “Vipi, mbona unaniita hivyo?” “Nimemuona Rose.” “Rose! Rose gani?” “Mwanangu.” “Mwanao! Kafika vipi huku?” “Hata sijui.” “Umemuona wapi?” “Hapa nje ya benki.” “Nje ya benki! Anafanya nini?” “Yupo na dada mmoja amevaa hijabu nina wasiwasi na yule aliyejitolea kumtetea Deus.” “Hapana, umemfananisha tu.” “Nooo, Kinape ni yeye damu yangu siwezi kuipotea.” “Kama unajua damu yako kwa nini ulitaka kuitoa uhai?” “Kinape acha utani nina wasiwasi Deus yupo jiji Mwanza inawezekana kabisa amekuja kulipa kisasi.” “Aje Mwanza kwani kifungo kamaliza? Na huu ndiyo mwaka wake wa pili na yeye kafungwa miaka saba. Ndiyo maana nakueleza umemfananisha tu,” Kinape bado aliamini mpenzi wake amefananisha mtu. “Kinape haki ya nani ni Rose mwanangu tena yupo na yule dada, yaani tumepishana nikashtuka kumuona Rose nilipomuangalia vizuri yupo na nani nusra haja ndogo initoke baada ya kumuona yule dada uliyesema ni mafia akiwa na Rose tena kwa mdomo wake alimwita jina lake kumuuliza amnunulie ice cream, kwa sauti ya mwanangu ninayoijua alikubali tena akikubali kwa kuitika yes mamy.” “Bado sijakubali, utakuwa umemfananisha tu,” Kinape alizidi kukataa. “Kinape acha ubishi Deus huenda yupo Mwanza na yule mwanamke ni mwanamke wake tu, nilikueleza mapema ukabisha tulitakiwa tumuue Deus na mtoto wake mapema yote haya yasingetokea.” “Kilole una uhakika gani kuwa uliowaona ni wenyewe Rose?” “Kinape sijawa kukueleza jambo hili hata siku moja, amini nilichokiona ni kweli kabisa nimemuona Rose na Deus yupo Mwanza.” “Mmh! Sasa umeisha maliza kilichokupeleka hapo benki?” “Hata nguvu ninazo za kuingia tena benki narudi tu nyumbani kupumzika nitarudi kesho.”
“Basi wewe rudi, lazima nipate ukweli wa kitu ulichokisema.” “Ukweli upi?” “Kuulizia habari za Deus kama kweli ametoka au vipi.” “Kama ametoka?” “Tutajua cha kufanya hebu rudi basi tujue tufanye nini.” “Yote umeyataka wewe kama ningemuulia mbali yote haya yasingetukuta, sasa tutakwenda wapi?” “Acha kupagawa njoo tutazungumza nyumbani haya si ya kuyazungumza mbele za watu.” “Nimo ndani ya gari.” “Mimi nipo dukani.” “Basi funga duka tukutane nyumbani.” Deus alifunga duka na kutangulia nyumbani kumsubiri mpenzi wake, haikuchukua muda Kilole naye alifika nyumbani kijasho kikimtoka japo alitoka ndani ya gari lenye kiyoyozi kikali. “Vipi mbona jasho jingi?” “Unafikiri lililopo mbele yetu dogo?” “Una uhakika gani kuwa ni wenyewe?” bado Kinape aliamini Kilole amefananisha. “Kilole acha ubishi, Rose mwanangu siwezi kumpotea.” “Kabla ya yote wacha nipate ukweli wa Deus kisha tujue tufanye nini,” Kinape alimueleza Kilole aliyekuwa bado amesimama toka aingie ndani. “Utaupaje ukweli, Kinape mbona na wewe unanichanganya?” “Nitampigia mtu simu wa Dar atanipa habari zote za Deus.” “Mtu gani? Una namba ya nani?” “Wapo rafiki zangu nitawapigia simu.” “Utawaeleza upo wapi huoni kama hiyo ni njia ya kutujulisha tupo wapi,” Kilole alimtaadharisha. “Si kuna kile kitabu cha Deus cha kumbukumbu zake, mule kuna namba nyingi za rafiki zake nitampigia mmoja kumuulizia lazima atakuwa anajua habari zake.” “Utajitambulishaje?” “Kwa jina la uongo na kujifanya ni mmoja wa mtu wake wa karibu ili niweze kumdodosa bila kujua.” Kilole alikwenda chumbani kwenye kabati ya nguo na kutoa kitabu chenye kumbukumbu muhimu za Deus na kumpelekea Kinape. Alitafuta namba za kupiga jina la Best aliamini ndilo lililofaa kupigwa. Baada ya kuandika namba alipiga lakini haikuwa hewani, walijaribu namba zaidi ya tano ya sita ilikubali. Baada ya kuita kwa muda ilipokelewa upande wa pili. “Haloo.” “Haloo Mr Mabina za siku?” “Nzuri tu, nani mwenzangu?” “Naitwa John Mwenge.” “Ndiyo bwana Mwenge, jina lako kama geni, samahani hebu nikumbushe tulionana wapi?” “Tulionana hapohapo Dar siku moja nilikuwa na Mr Deus.” “Mr Deus yupi?” “Yule jamaa aliyekuwa mkuu wa kitengo cha kuzuia dawa za kulevya kituo cha uwanja wa ndege.” “Ooh! Kweli basi itakuwa muda sana, ehe lete habari.” “Nilikuwa nataka kujua habari za Deus, maana niliondoka kabla kesi yake haijaisha.” “Kwani upo wapi?” “Nipo Mtwara karibu kabisa na mpaka wa kuingia Msumbiji.” “Mmh! Kwa sasa hata sijui habari zake japo nina wasiwasi huenda amekwisha fariki.” “Deus amekufa?” Kinape alishtuka. “Alinyongwa?” “Hapana, alipata stroke.” “Kwa sababu gani?” “Rafiki yangu mwanamke watu wabaya sana tunalala nao na kujifunika shuka moja lakini ni maadui zetu wakubwa. Mkewe aliyekuwa naye alikuwa zaidi ya nyoka kamfanyia kitu kibaya sana rafiki yangu. Baada ya kuhukumiwa miaka saba nasikia yule mwanamke alianzisha uhusiano na rafiki kipenzi wa Deus na kufikia hatua ya kumpatia ujauzito hiyo ikawa haitoshi wakaenda kumuachia mtoto gerezani kubwa zaidi ilikuwa ni taarifa za kuchukuliwa kila kitu nyumba na magari yake ambayo yule mwanamke aliuza na kukimbia. “Taarifa ilipomfikia ndipo alipoanguka na kupoteza fahamu na muda huohuo akapata stroke.” “Mungu wangu!” Kinape alipata mshtuko wa kweli toka moyoni baada ya kusikia madhara ya ubaya waliomfanyia Deus chanzo wakiwa wao hasa Kilole. “Basi Deus kakaa hospitali miezi miwili hajui anayeingia wala anayetoka, baada ya hapo nilisafiri nje ya nchi kama miezi minne. Niliporudi nilikwenda moja kwa moja hospitali kumjulia hali yake. Nilikwenda moja kwa wadi aliyokuwa Deus nilipofika kitanda alichokuwepo nilikuta mgonjwa mwingine. “Ilibidi niulize mgonjwa aliyekuwepo kitanda kile yupo wapi, alielezwa ana wiki tatu toka afariki.” “Ooh! Maskini rafiki yangu Deus,” Kinape alisema kwa uchungu wa kweli toka moyoni huku machozi yakimtoka, “Si wewe hata mimi kaniuma sana jamaa alikuwa mtu safi sana sijawahi kuona.” “Asante kwa taarifa yako.” Kinape baada ya kukata simu aliinama na kuanza kulia baada ya kusikia rafiki yake kipenzi amefariki na chanzo ni yeye na Kilole. Kilole aliyekuwa pembeni yake alimuuliza: “Vipi mbona hunipi jibu unainama na kulia nani kafa?” “Deus.” “Deus?” Kilole alishtuka. “Ndiyo.” “Lini?” “Miezi sita baada ya sisi kuondoka.” “Nani kakueleza kafa na nini kimemuua?” Kinape alimweleza yote aliyoelezewa kwenye simu na Mr Mabina, baada ya kumsikiliza alisema: “Sasa Rose kafikaje Mwanza?” “Nimekueleza utakuwa umemfananisha tu.” “Labda, lakini ni yeye Rose na yule msichana ulisema anaitwa nani?” “Teddy.” “Lakini naomba ufanye upelelezi zaidi juu ya ukweli juu ya kifo cha Deus ili tusiwe na wasiwasi tuishi kwa kujiachia,” taarifa zile kidogo zilishusha presha ya Kilole. “Hakuna tatizo mpenzi.” “Yaani huwezi kuamini nilikuwa nimeisha changanyikiwa, sasa kama Deus amekufa bado nina kazi moja muhimu.” “Ipi hiyo?” “Ya kumsaka Rose na kuua.” “Kwa nini?” “Unafikiri Rose akikuwa na kujua chanzo cha kifo cha baba yake ni sisi kutakuwa na usalama?” “Hizo taarifa atazipata wapi?” “Hujui dunia hii, ipo siku tutaumbuka, nitamsaka sehemu yoyote mpaka nimuue.” “Kumbuka ni damu yako.” “Lakini ndiyo itakayokuwa adui yangu namba moja.” “Tena Mpenzi nilisahau kuna sherehe ya Send of ya rafiki yangu leo usiku La Cairo hotel.” Kinape aliingiza na miadi yake na Happy ya usiku ule. “Mbona hukuniambia mapema?” Kilole alihoji taarifa zile za ghafla. “Huwezi amini hata kadi nimeelezwa atapewa nikifika mlangoni.” “Twende wote.” “Noo, mtoto bado mdogo hatakiwi kutoka usiku.” “Mmh! Sawa.” Kilole alikubali lakini moyoni alikuwa na wasiwasi na taarifa ya ghafla aliyopewa na mpenzi wake kuhusu kwenda kwenye sherehe. Kwa vile alikuwa analea alikuwa mpole. ***** Kinape baada ya kupata ruhusa kutoka kwa mpenzi wake alimjulisha Happy watakutana hoteli ya Gorden Crest majira ya saa tatu usiku ili wale chakula cha pamoja kabla ya kujuana zaidi. Happy naye alimweleza yeye atawahi mapema na kuchukua chumba kwa fedha yake. Majira ya saa tatu usiku Kinape alijiandaa kama kweli anakwenda kwenye sherehe ya harusi. Baada ya mkewe kumkagua alimsifia amependeza. “Asante mpenzi.” “Lakini chonde mpenzi ulivyopendeza hivi nisiibiwe tu,” Kilole alilia wivu. “Usiwe na wasiwasi najua tumetoka wapi.” ”Ukilijua hilo nina imani mali zangu zitarudi salama.” Kinape alimbusu Kilole pande tatu kisha alitoka, alichukua gari dogo kuelekea hoteli ya Gorden Crest. Kwa vile alikuwa ameelekezwa chumba alipofika pale hotelini hakumuuliza mtu alikwenda moja kwa moja kwenye mlango wa chumba na kuingia ndani na kumkuta Happy amejaa tele katika vazi la kanga moja bila kitu ndani. Alipomuona alifurahi na kumrukia na kumkumbatia. “Wawooo baby kweli una uhadi za kweli pia nimeamini ulikuwa ukimpenda wa jina wangu kama unavyosema tulikuwa tunafanana sina budi kusema pacha wangu.” Happy alisema kwa furaha. “Ni kweli, ninavyokuona leo kama namuona Happy amefufuka kuja kunipoza machungu yasiyo na kifani moyoni mwangu.” “Nina kuhakikishia hutajutia kuonana na mimi, nitajitahidi kukufurahisha japo sina uhakika kama nitamshinda pacha wangu.” “Nina imani utaziba pengo lake, si rahisi moyo wangu kumuamini mtu lakini kwako nimekumeza mzimamzima.” “Na mkeo?” “Happy nakuahidi wewe ndiye mke wangu wa ndoa nitakaye kukabidhi moyo wangu na kila kitu changu ni halali yako.” “Na dada?” “Nitakapokuoa utajua kila kitu kwa sababu gani simpendi yule mwanamke.” Happy aliondoka nguo zote alizovaa Kinape na kwenda wote pamoja kuoga. Ulikuwa usiku wa raha katika maisha ya Kinape toka afariki kipenzi chake Happy. *** Kilole roho ilikuwa haimpi muda wote aliwaza anaibiwa, pamoja na mpenzi wake kutoka kisherehe bado hakumuamini kwa asilimia mia. Baada ya kunyonyesha mtoto wake na kuamini ameshiba hawezi kuamka mapema. Alibadili nguo na kuvaa track suti na raba kisha alitoka hadi kwenye gari kuelekea Hotel La Cailo iliyokuwepo maeneo ya Kirumba. Kutoka Isamilo hadi Kirumba hakukuwa na umbali mrefu hasa usiku ule wa saa nne magari yalikuwa machache sana njiani. Alikanyaga mafuta kwa dakika saba alikuwa ameegesha gari kwenye maegesho ya Hotel La Cailo. Aliteremka na kutembea taratibu hadi kwenye ukumbi unaoshughulika na sherehe. Ukumbi ulikuwa mtupu alizunguka kila kona hakukuwa na sherehe yoyote. Alimfuata mfanyakazi mmoja wa kike na kumsalimia. “Samahani dada yangu, za saizi?” “Bila samahani dada yangu, nzuri tu,” alimjibu huku akijiandaa kuulizwa swali. “Eti leo kulikuwa na sherehe ya send of hapa?” “Mmh! Hapana,” alijibu huku akitikisa kichwa. “Kwani hapa Mwanza kuna La Cailo ngapi?” “Moja.” “Asante.” “Kwani vipi dada kuna mtu unamtafuta?” “Hapana.” Baada ya kusema vile aligeuka na kwenda moja kwa moja kwenye gari na kuondoka kwa mwendo wa kasi mpaka nyumbani. Kutokana na kwenda kwa kasi alijikuta akiligonga geti na kulivunja. Baada ya kuteremka aliingia chumbani na kuanza kulia huku akisema: “Huyu mpumbavu hanijui mimi ni nani, mapenzi yote dhambi zote nilizozipata kwa ajili yake anaona bure. Sasa tutaona mimi na yeye nani zaidi,” Kilole alisema huku akipiga ngumi kitandani. Wazo la kumuua aliliondoa kwa vile aliamini hakuna mwanaume chini ya jua anayempenda kama Kinape. Ila aliapa kila atakayeonja asali yake itageuka sumu na kuapa kumsaka aliyemtoa usiku mpenzi wake na kuhakikisha anampoteza kama alivyompoteza Happy.
ILIPOISHIA: Wazo la kumuua aliliondoa kwa vile aliamini hakuna mwanaume chini ya jua anayempenda kama Kinape. Ila aliapa kila atakayeonja asali yake itageuka sumu na kuapa kumsaka aliyemtoa usiku mpenzi wake na kuhakikisha anampoteza kama alivyompoteza Happy. SASA ENDELEA… Pia alipanga kutomuuliza chochote hata akirudi asubuhi lakini atafanya uchunguzi wa siri na akimjua lazima amuue. Alishindwa kulala na kujikuta akizunguka nyumba huku akilia akiuapia moyo wake kuwa ataendelea kubeba dhambi mpaka hapo Kinape atakapojua thamani ya penzi lake. Alishinda amekaa sebuleni macho muda wote alilia kwa hasira, alikumbuka Kinape akirudi na kumkuta analia lazima angehoji hapo angekosa la kujitetea. Alifuta machozi na kunawa kisha alipanda kitandani na kujilaza japo usingizi hakuwa nao kifua kilivimba kama kinataka kupasuka kwa hasira. Kinape alirudi nyumbani alfajiri akioneka amelewa, Kilole alipokea bila kumwambia kitu. Kwa vile alikuwa amechoka baada ya kuoga alipanda kitandani kulala. Kinape akiwa njiani akirudi nyumbani alifuta meseji zote hata simu alizompigia Happy. Akiwa amelala Kilole alitumia nafasi ile kuipekua simu ya mpenzi wake lakini kila alipofungua hakukuta kitu. Aliamini mtihani wa kwanza ameshindwa lakini hakutaka kuwa mkali kwani aliamini muonja asali haonji mara moja lazima atarudi hapo lazima atamkamata na kufanya alichokipanga.
DEUS GEREZANI Baada ya Teddy kuondoka gerezani, mkuu gereza alikuwa na mazungumzo na Deus ili kujua kipi kinatakiwa kabla ya kutolewa gerezani. “Deus kwanza nashukuru kwa mgeni wako, yaani na mimi nitamalizia nyumba yangu na kupata kigari cha kutembelea, si unajua bado miaka miwili nistaafu, mbona kaniokoa.” “Yote inatokana na wema ulionitendea, na mimi nakuahidi nikirudi safari yangu salama nitakupa zawadi kubwa.” “Usiwe na wasiwasi, kuna kitu nilitaka kujua kutoka kwako.” “Kitu gani hicho mzee wangu?” “Kwa muda huu unataka nikufanyie kitu gani ambacho unaamini kitakuweka katika hali nzuri kwa muda uliobaki.” “Tena umeniuliza swali zuri ambalo lilikuwa likiniumiza kichwa.” “Kitu gani? Niambie nipo tayari kukusaidia, unataka ukae nje ya gereza muda huu?” “Hapana, kupata muda wa mazoezi ya kujiweka sawa kabla ya safari yangu ya Italia.” “Hayo mazoezi saa ngapi?” “Usiku.” “Hakuna tatizo, usiku nitakuchukua mwenyewe kukupeleka kwenye gim na kukurudisha.” “Nitashukuru.” Baada ya mazungumzo Deus alirudi gerezani kwa mwendo wake wa kuvuta mguu kuonesha bado ugonjwa unamsumbua. Mkuu wa gereza alipanga mpango ule kuhakikisha Deus anatoka mapema kwa kuhofia yaliyomkuta kama angekaa gerezani kwa muda mrefu lazima atakufa kwa mawazo. Usiku majira ya saa nne wakati wafungwa wote wamelala Deus alitolewa kwenye chumba alichotengewa na kuongezwa baadhi ya vitu vya kumliwaza toka Teddy alipompa mkuu wa gereza asante la milioni kumi. Deus alipelekwa gim muda ambao watu walikuwa wamemaliza na kufanya mazoezi peke yake kwa saa mbili kisha alirudishwa gerezani na kujipumzisha huku akila chakula kizuri kilichokuwa kikipikwa kwa mkuu wa gereza.
JIJI MWANZA Penzi la Kinape na Happy alilizidi kuota mizizi kiasi cha Kinape kumuongezea wiki nzima kuwepo jiji Mwanza kuendelea kuwa naye akiamini ndiyo njia pekee ya kumuenzi mpenzi wake marehemu Happy aliyeuawa na Kilole. Mabadiliko ya Kinape yalimfanya Kilole kuendelea kupelelezi bila kuonesha ameshtukia kitu. Kwa vile ilikuwa ni vigumu kugundua huwa anakwenda wapi, ilibidi amkodi mtu kumfuatilia Kinape kila kona ili ajue anakwenda wapi kila apoondoka nyumbani. Kijana mmoja aliifanya ile kazi kwa kufuatilia nyendo za Kinape na kufanikiwa kumuona akiingia hoteli ya Gorden Crest. Baada ya kumuona katika hoteli ile zaidi ya mara mbili alimpigia simu Kilole kumjulisha. “Sister huwa anakuja hoteli ya Gorden Crest.” “Umemuona hapo mara ngapi?” “Zaidi ya mara mbili na akiingia huchukua muda mrefu kutoka.” “Umemuona kaongozana na nani?” “Kwa kweli mara zote nimemuona peke yake.” “Na akitoka huwa ameongozana na nani?” “Hutoka peke yake.” “Nitakuongeza fedha chunguza huingia wapi na huwa na nani.” “Hakuna tatizo nitakuwa jibu muda si mrefu.” Anko Jay Jay kijana aliyepewa kazi ya kumchunguza Kinape alipokata simu aliingia ndani ya hoteli ya Gorden Crest lakini alishindwa aanzie wapi na amuulize nani. Kwa vile ilikuwa vigumu kujua yupo mule kwa ajili ya mazungumzo au chumbani na mwanamke. Akiwa amesimama kwenye korido akiwaza alimuona Kinape ameongozana na msichana mmoja mzuri. Walimpita wakizungumza na kusimama pembeni yake, aliwasikia wakizungumza: “Sasa baby wacha nikimbie nyumbani si unajua yule mtu machale yameanza kumcheza ila nikija Arusha utanichoka.” “Siwezi baby, yaani nitanenepa.” “Kapumzike basi baby, kesho.” Anko Jay Jay alishuhudia Kinape akilishana mate mbele yake kisha waliagana na Kinape kutoka nje ya hoteli na yule msichana kurudi chumbani. Anko Jay Jay aliachana na Kinape na kumfuatilia yule mwanamke aliyepanda ngazi kuelekea juu. Alimfuata mpaka alipomuona akiingia katika chumba ambacho alinakili namba zake kisha aligeuka na kuteremka hadi chini kisha alimpigia simu Kilole. “Haloo sister itabidi uniongeze mshiko.” “Ukifanya kazi nzuri sitakuwa na hiyana nitakuongeza nyingine kama niliyokuahidi.” “Basi sister nimefanya bonge la kazi.” “Usiniambie!” Kilole alishtuka kusikia vile. “Nimemaliza kila kitu kazi kwako.” “Mmh! Niambie umefikia wapi?” Anko Jay Jay alimweleza yote na kumfanya Kilole afurahie kwa kuruka juu na kusema: “Anko Jay Jay umefanya kazi nzuri sana.” “Kwa hiyo?” “Njoo uchukue chako, nikiwa na shida nitakutafuta ila nakuomba siri hii usimwambie mtu,” Kilole alimuonya Anko Jay Jay. “Siwezi sister.” *** Kinape kutokana na kubadili ratiba yake ya kuwahi kurudi nyumbani pia mpenzi wake kutoonesha wasiwasi wowote aliamini mambo yake yanakwenda vizuri. Ilikuwa lazima aende mchana hotelini na kula chakula cha pamoja na Happy na jioni kuwa pamoja hadi saa nne usiku na kurudi nyumbani huku akimweleza Kilole kuwa na mazungumzo na rafiki zake. Siku ya pili kama kawaida Kinape majira ya saa sita mchana alikwenda hotelini kwa Happy kwa ajili ya chakula cha mchana. Mlango ulikuwa umerudishwa kama kawaida alifungua mlango huku akiita: “Sweetiiiii.” Kama kawaida yao kila alipofika na kumwita vile Happy hukurupuka na kwenda kumrukia kwa furaha. Lakini siku ile alishangaa kutopokewa alipoingia ndani alimkuta Happy akiwa amelala kifudifudi kitandani akiwa katika mavazi ya kulalia. “Babiiii,” Kinape alimwita huku akimsogelea kitandani. “Babiii kulala gani huko, amka tukapate lunch.” Happy hakujigeuza wala kuitikia, ilibidi amtikise huku akimwita. “Happy..Happy, wake up baby.” Lakini vilevile hakuonesha kushtuka kitu kilichomshtua Kinape na kumgeuza kwa nguvu ili kumshtua. Happy aligeuka mzimamzima akiwa amelegea kifuani kukiwa na damu na sehemu aliyolala kulikuwa na damu nyingi. Kinape alishtuka na kutaka kupiga kelele za kilio lakini alishika mdomo asitoe sauti. Alipomchunguza aligundua mpenzi wake mwingine kauawa kwa risasi. Kwa haraka alitoka nje ya chumba na kukimbilia nyumbani huku akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa. Kilole alishtuka kumuona yupo katika hali ile alimfuata chumbani na kumkuta Kinape machozi yakimtoka huku mikono ikikosa pa kushika kila alipojishika aliona hapafai. “Honey vipi?”Kilole alimuuliza. “Safi.” “Mbona hivyo?” “Wee acha tu,” alijibu huku akigeukageuka kitandani kama kuna miba. “Kuna nini honey? Kilole alimuuliza kwa sauti ya upole. “Hakuna kitu naomba uniache,” Kinape alijibu kwa hasira mikono ikiwa kichwani. “Mmh! Haya ukihitaji msaada wangu utanifuata,” Kilole alisema huku akitoka nje. Kinape alianza kulia kilio cha sauti huku akisema: “Kwa nini lakini…Ooh! Happy kwa nini lakini? Uuuu aaa..sikubaliii Happy hawezi kufa kirahisi namna hii,” alilia huku akipiga ngumi kifuani kwa nguvu. Kinape alijua lazima aliyefanya kitendo kile cha ukatili atakuwa Kilole tu hakukuwa na mtu mwingine ambaye angefanya mauaji kama yale. Alikumbuka kifo cha mpenzi wake wa kwanza hakikuwa na tofauti na kile cha Happy wa pili. Moyoni alijiuliza Kilole ataendelea kuua mpaka lini. Alitoka chumbani kama mbogo na kwenda sebuleni kumfuata Kilole amueleze kwa nini amemuua Happy. Aliapa bila majibu mazuri angemfia mikononi, alipofika alipokuwa amekaa Kilole akisoma ujumbe kwenye simu wakati huo katika luninga kulikuwa kunaoneshwa tukio la mauaji katika hoteli ya Gorden Crest. Kinape kwanza alitulia kusikiliza nini kinaendelea baada ya kifo cha Happy. Mtangazaji alielezea tukio la kifo cha msichana aliyefahamika kwa jina la Happy Simoni Mfanyakazi katika kampuni ya Utalii Arusha aliyeuawa kwa risasi majira ya saa nne na saa tano asubuhi katika hoteli ya Gorden Crest. Mtangazaji aliendelea kusema kuwa msichana yule alikuwa amepanga pale siku ya tatu akiwa na mpenzi wake wa kiume ambaye alikuwa halali pale na kukutana mchana na usiku kisha mpenzi wake huondoka. Taarifa ziliendelea kusema siku ya tukio mpenzi wake alionekana pale hotelini na kwenda kuweka oda ya chakula cha mchana kama kawaida, baada ya wahudumu kuona anachelewa ndipo walipokwenda chumbani na kukutana na tukio lile la kutisha bila kumuona yule mpenzi wake. Taarifa zilizidi kuelezwa kuwa baada ya hapo walitoa taarifa katika uongozi wa hoteli kisha kuitaarifu polisi waliofika na kuichukua maiti kwa uchunguzi zaidi huku mpenzi wake akiendelea kusakwa na polisi. Baada ya taarifa ile Kinape alimgeukia na kuuliza kwa sauti kali: “Nani kamuua Happy?” “Happy! Ndiye nani?” Kilole alijifanya kushangaa. “Unajifanya hujui siyo?” Kinape alimtolea macho yaliyokuwa mekundu kwa ajili ya kulia. “Baby mbona unataka kuniingiza katika matatizo, nimuue Happy mara mbili?” Kilole alizidi kuruka. “Siyo mpenzi wangu wa Dar huyu aliyekufa leo hii.” “Kinape…Mimi na sijui huyo Happy wapi na wapi, kwanza nimuue kanifanya nini?” Kilole alijifanya kushangaa. “Nitajua tu muda si mrefu.” “Kujua nini, kwanza nataka uniambie huyo Happy ni nani? Kinape ulikuwa na mwanamke wa pembeni?” Kilole naye alikuja juu huku akimfuata Kinape na kumvuta shati. “Niambie Kinape kumbe ulikuwa na mwanamke unaona Mungu kakuumbua.” Kilole alisema huku akilia kwa uchungu. “Nitajua tu.” “Kujua nini mpenzi wangu, anayetafutwa ni wewe?” Kinape alikaa kwenye kiti na kuanza kulia kwa sauti ya kwikwi huku akisema: “Nini hatima ya yote.” Kilole alimfuata na kukaa pembeni yake na kumsemesha kwa sauti ya upole: “Baba Junior hebu nieleze kifo cha huyu msichana wewe kinakuhusu vipi?” “Ni rafiki yangu ambaye alikuwa mfanya biashara na nilikuwa nakwenda pale kwa ajili ya mazungumzo ya kufanya biashara Mwanza na Arusha. Leo nilipofika nikakuta ameuawa kwa kupigwa risasi kifuani.” “Anafanya biashara gani? Kama madini huenda ameuawa na majambazi, hakuibiwa kitu chochote?” “Hata sijui huoni kama mimi nipo hatarini.” “Nitakusaidia mpenzi wangu, itabidi uondoke kajifiche Afrika ya Kusini mpaka matatizo yakiisha urudi ukiweezekana tuhamie huko wote.” “Yaani ikiwezekana hata leo niondoke maana nikishikwa nitanyongwa au kuozea gerezani.” “Hakuna tatizo mpaka jioni utapata jibu la safari kuna mtu nitampigia simu ili uondoke na ndege ya saa sita usiku.”
Tarehe Tisa Desemba siku ya uhuru mheshimiwa rais alipotangaza msamaha kwa wafungwa wenye vigezo vya kuachiwa, Deus alikuwa mmoja ya watu walionukaika na msamaha huo. Kama kawaida walisomewa majina wafungwa watakao achiwa na kutolewa gerezani kwa msamaha wa rais. Baada ya kusomewa Deus alitoka katika mwendo wake wa kuvuta mguu wa kushoto kama kweli ni mgonjwa. Wafungwa wenzake walimuaga wakiamini kabisa jamaa yao ni mgonjwa ambaye hakuwa na faida yoyote kuendelea kuwepo gerezani. Baada ya kutoka gerezani, nje ya gereza alimkuta Teddy akimsubiri na kuondoka naye ndani ya gari lililokuwa na vioo vyeusi mchana ule moja kwa moja mpaka uwanja wa ndege na kwenda naye kwenye maficho yake jijini Mwanza. Walifika Mwanza majira ya saa tisa alasiri, baada ya kufika tu Mwanza hakutaka kupoteza muda alimuuliza Teddy. “Ipe information ili kazi ifanyike mara moja.” “Deus mbona haraka sana kwa nini usipumzike kwa siku mbili tatu, nina wasiwasi ulitakiwa upumzike mwezi mzima kuuandaa mwili. Kifungo si mchezo hasa magereza ya kibongo.” “Teddy nipo fiti huu mwili unauonaje?” Deus alitoa shati kuonesha mwili uliojengeka kimazoezi. “Ha! Deus, mwili umejengeka kimazoezi umefanya muda gani? Tena unaonesha upo fiti.” “Ile mbaya, nimejiandaa kuifanya kazi kwa aina yoyote ya mapigano kwa siraha au mkono mtupu.” “Kwa hiyo ulitaka twende lini?” “Kesho.” “Keshooo?” Teddy alishtuka. “Teddy hebu tumalize kazi hii mara moja ili nifanye nyingine, una picha ya huyo mshenzi?” “Sina, labda tuangalie kwenye Facebook.” Waliwasha Lap top na kuiweka moderm na kumsachi jina la Moses Chris, lakini ilionesha ameondoa picha zake zote na kuacha kivuli tu kwenye jila lake. “Sasa tutafanyaje?” Deus alimuuliza Teddy. “Nimekumbuka hebu sachi jina la Jarome Moore.” Walitafuta jina la Jarome Moore na kufunguka kisha walifungua kwenye picha zake, baada ya kutafuta kwa muda Teddy alisema. “Huyu hapa,” alimuonesha kwenye picha aliyopiga pamoja na Jarome Moore. “Okay, tuisevu kwenye desktop.” Baada ya kuiweka desktop Deus aliikuza na kuitazama kwa muda kisha alisema: “Okay, nimemuona.” “Kwa hiyo?” “Tayari.” “Ina maana huchukui picha yake?” Teddy alishangazwa na uchukuaji wa picha ya Moses. “Kazi yetu haitakiwi kutembea na picha ya mtu unaweza kutuweka katika matatizo.” “Kwa hiyo unataka kuniambia umeisha mtambua hata ukikutana naye?” “Wee utasikia nimefanya nini, fanya mipango ya hati za kusafiria nianze kazi mara moja ambayo nina imani itachukua siku chache kabla sijaanza msako wa kufa mtu wa wale mashetani.” “Ukiwashika utafanyaje?” “Nitajua nikiwashika, ila nitakachowafanya Mungu anajua.” “Hiyo kazi nitaifanya miye.” “Nilitaka kusahau nitaondoka peke yangu hii kazi sitaki msaada ni ndogo sana.” “Kwa nini? Utawaweza peke yako nasikia wapo wengi.” “Mimi peke yangu sawa na jeshi la watu mia.” “Mbona unajiamini sana?” “Kwa vile najiamini.” “Kwa hiyo unataka ondoke lini?” “Teddy, huu si muda wa kupoteza, natakiwa niondoke kesho usiku.” “Visa nitapataje?” “Mpigie mtu huyu.” Deus alimpa namba ya rafiki yake kipenzi anayefanya kazi uhamiaji. Baada ya kuita alizunguza naye. “Haloo.” “Haloo.” “Nani mwenzangu?” “Deus.” “Deus! Deus gani?” “Mpolipoli.” “Wee Acha utani, Deus mpolipoli ni mmoja tu ambaye mpaka sasa sijui yupo hai au amekufa.” “Hajafa yupo hai na ndiye unayezungumza naye.” “Wewee, acha utani! Ni wewe kweli?” “Sasa kiliza Bon ni hivi nitafutie visa ya kusafiri kesho jioni.” “Lakini mbona kama siamini.” “Bon, ni hadithi ndefu unayoijua na usiyoijua, kama nikirudi salama safari yangu ya Italy tutazungumza mengi.” “Unajua siamini.” “Best camooon.” “Kweli nimeamini ni wewe, nipe muda upo wapi?” “Nipo Mwanza, usiku wa leo nitakuwa Dar kwa ajili ya safari ya Italia.” “Siamini mpaka nikuone.” “Utaniona la muhimu nifanyie hiyo kazi mara moja.” Deus alikata simu na kumgeukia Teddy aliyekuwa bado ameshangaa. “Vipi mbona unanishangaa?” “Siamini, visa utapata kesho.” “Kesho ni safari ya kifo.” “Deus kwa nini tusiende wote? Unajua moyo wangu haunipi kabisa wewe kwenda peke yako.” “Hapana kazi hii si ya kitoto.” “Deus unanidharau kwa vile mwanamke?” “Walaa, kazi hii tukienda wawili tunaweza kumpoteza mtu, sitaki nikuone akifa.” “Siwezi Deus.” “Nina uzoefu na safari za aina hii, kama jamaa anakuwinda utakuwa umepata nafasi ya kukupata kwa urahisi. Niache nicheze naye kwa vile hanijui nitamumaliza kama kuzima kibatari.” “Deus ukifa nami nitakufa nakupenda sana.” “Asante.” “Sio siri nilikupenda toka siku ya kwanza na ulichonifanyia ndiyo ulizidi kunimaliza. Naomba nipasue siri yangu ambayo ilinitesa muda mrefu Deus nakupenda sana tena sana.” “Asante.” “Deus mbona kila kitu unasema asante au hunipendi?” “Utajua nikirudi Italia.” “Hapana Deus naomba uniambie kama kweli nami unanipenda, nina imani nina nafasi kubwa moyoni mwako baada ya mkeo kukutenda.” “Nami nilikupenda toka nilipokuona lakini sikuweza kusema ningeweza kuharibu kazi.” “Kweli Deus, nimefurahi sana kusikia kumbe na wewe ulikuwa ukinipenda.” Walijikuta wamesahau mambo ya safari na kuingia dunia nyingine iliyoandikwa historia mpya kwa siku ile. “Deus naomba unioe.” “Hiyo ndiyo itakayofuata kama nikirudi salama.” “Deus mpenzi utarudi salama nakusubiri kwa hamu kubwa.” Kila mmoja alimpa uhuru mwenzake mikono yake uzuru pande zote za mwili, ilikuwa raha kwa wote huku Teddy akitimiza ndoto yake ya kumtamkia Deus kuwa anampenda. **** Mpango wa Kilole kumtorosha Kunape uligonga mwamba baada mtu waliyekuwa wakimtegemea kufanya mpango wa safari kusafiri kuwa nje ya nchi kwa wiki nzima. “Sasa itakuwaje mpaka arudi si nitakuwa nimekamatwa?” Kinape aliuliza akiwa amejawa na hofu. “Kinape usihofu kwa vile hawakujui, we kaa ndani usitoke mpaka soo litakapoisha,” Kilole alimpa moyo. “Kumbuka wamesema wamechukua mkanda unaochukua matukio yote ya hotalini siku ile huoni nitaonekana?” “Hata kama utaonekana bado hujaua.” “Hata kama sijaua huenda wakasema nimeshilikiana na muuaji?” “Kwanza kamera zile hazina uwezo mkubwa wa kuiona picha kwa ufasaha, pia muuaji ataonekana si wewe hivyo hawatashughulika na wewe zaidi ya kumsaka muuaji.” “Mmh! Usalama wangu ulikuwa kuondoka hapa tu,” Kinape alihofia kukamatwa na kufunguliwa mashtaka. “Jamaa anarudi baada ya wiki usiwe na wasi akirudi tu unaondoka.” “Itabidi nivumilie sina ujanja.” Wakiwa wamekaa sebuleni wakisikiliza taarifa ya habari, taarifa kutoka polisi zilisema kuwa kamera la hoteli ambazo huonesha mwisho nje ya mlango wa kuingia chumbani. Majira saa saa tano na dakika tano asubuhi alionekana mtu kama mwanamke aliyekuwa amevaa hijabu akiingia katika chumba cha marehemu na kutoka baada ya dakika kumi. Taarifa ziliendelea kusema muuaji ndiye aliyevaa jazi refu la kumziba mwili mzima. Jeshi la polisi lilikuwa likiomba mpenzi wa mwanamke yule ambaye alikuwa Kinape kwenda kujisamilisha ili kutoa msaada kwa polisi kwa kuonesha muuaji anamjua. Kauli ya mtangazaji ilimfanya Kinape alalamike kwa sauti. “Jamani mimi nimjue wapi muuaji?” Kinape aliuliza huku akizidi kukata tamaa. “Hebu acha kujitia presha, usijitokeze tuone watakuona wapi kwa muda huu matembezi yako yatakuwa usiku tu.” Wakiwa katikati ya mazungumzo mtoto ndani alilia na kumfanya Kilole amfuate ndani na kumkuta amejisaidia, ilibidi amfanyie usafi kwanza. Sauti ya kuonesha katika simu ya Kilole ujumbe umeingia ulilia na kumfanya Kinape kuiona simu ya Kilole aliyoiacha kwenye kochi. Kwa haraka aliichukua na kuufungua ujumbe ulioingia uliokuwa unasomeka. “Sawa sister sitamwambia mtu, unatisha lakini kumbe we mafia mbaya.” Alisoma mwingine uliotangulia ambao ilionesha Kilole aliosoma na kuujibu: “Sister yule demu anayetembea na mumeo nimesikia ameuawa, vipi umemuua wewe?” Ulikuwa ujumbe uliotangulia ambao Kilole aliujibu na kutumiwa mwingine ambao nao aliamini angeujibu. Aliichukua namba ya simu ya aliyetuma ujumbe na kuufuta ujumbe ulioingia ili Kilole asijue kama ameshika simu yake na kuirudisha simu juu ya kochi kama ilivyokuwa. Moyoni alitamani kumuuliza lakini alivuta subira isionekane kama anampekua baada ya kuwekeana mipaka kwenye simu zao. Kilole akiwa chumbani alikumbuka amesahau simu juu ya kochi sebuleni. Alimweka mtoto kitandani na kutoka haraka. Simu yake aliikuta alipoiacha aliichukua na kurudi nayo chumbani, kabla ya kuingia chumbani Kinape alimwita. “Kilole.” “Abee,” aliitika huku akigeuka kumtazama. “Mbona umefuata simu kwa haraka?” “Nilisikia ikiita kumbe masikio yangu.” “Mmh! Haya.” “Kwani umewaza nina mwanaume wa nje?” “Basi tu.” Kilole hakuongeza neno alielekea chumbani kumvisha nguo mtoto kisha alitoka naye na kukaa pembeni ya mpenzi wake ambaye aliamini ana mawazo ya kukamatwa kumbe alikuwa amepata nusu ya ushahidi wa kifo cha mpenzi wake Happy.
Akiwa amekaa akimuangalia Kinape alijikuta akikumbuka jinsi alivyomuua mpenzi wa Kinape. Baada ya kukamilisha uchunguzi wa mabadiliko ya mpenzi wake na kufahamu ana mpenzi aliyempangia Gorden Crest alijipanga kwenda pale. Majira ya saa nne asubuhi baada ya kumlisha chakula mtoto wake alimlaza kitandani na kuvalia baibui lililouficha mwili na uso na kuchukua bastora aliyoichomeka kwenye suruali na kutoka. Alitumia gari dogo na kwenda kulipaki pembeni ya ofisi za Tanesco, gari lake lilitazamana na Maktaba kuu. Alikodi bodaboda na kuteremkia karibu na hoteli ya Gorden Crest. Baada ya kumlipa fedha dereva wa bodaboda alimuomba amsubiri. “Samahani kaka yangu, kunisubiri kwa dakika kumi utanitoza kiasi gani?” “Baada ya kukusubiri utaelekea wapi?” “Nitarudi uliponitoa.” “Ukinipa buku tatu haitakuwa mbaya.” “Basi mimi nitakupa tano unasemaje?” “Utakuwa umecheza sister.” “Poa, wacha niwahi.” Kilole alichepua mwendo kuingia ndani ya hoteli na kuelekea upande wa vyumba, kutokana na elekezo aliyopewa kuhusu jografia ya hoteli ile haikumpa kazi kufika kwenye ngazi za kupanda juu na kwenda hadi ghorofa la pili. Alipofika kabla ya kuelekea chumbani kwa mbaya wake alitulia kwa muda kuangalia kama kuna mtu anamfuatilia. Hali ilikuwa ya tulivu hakukuna na watu sehemu ile, kabla ya kuchepua mwendo aliipapasa bastora yake kupata uhakika kuwa ipo. Taratibu alikwenda hadi mlangoni na kuzungusha kitaza kama mlango umefungwa kwa ndani. Mlango ulitii amri na kufunguka aliingiza mkono ndani ya hijabu na kutoa bastora yake na kuingia nayo kaishikilia mkononi. Alimkuta Happy amejilaza kwa kulalia tumbo akiwa katika vazi la kulalia, nguo ilivyokuwa ilionesha hakuwa na kitu ndani kumaanisha alikuwa akimsubiri mpenzi wake ampe burudani. Baada ya kuingia ndani alitulia akimuangalia yule msichana kwa hasira, aliamini muda ulikuwa unakwenda kwa vile kamuona mbaya wake ilitakiwa kazi moja na kuondoka. Alifunga mlango kwa sauti kidogo kitu kilichomshtua Happy kuamini mpenzi wake amefika. Alipogeuka alikutana na mwanamke aliyekuwa amevaa hijabu bastora mkononi iliyokuwa imemwelekea yeye. “Vipi dada?” Happy alishtuka. “Unashtuka nini ulipomchukua mume wangu mbona hukushtuka?” “Sa..sa..mahani dada mi..mi..si..jachukua mume wa mtu!” Happy alijitetea huku akitetemeka. “Kinape mumeo?” “Si..sijajua kama ni mumeo..ni..nisamehe.” “Sina muda wa kubishana na mwizi wangu.” “Sasa unataka kunijfanya nini dada yangu?” “Unataka kujua, Sali sala yako ya mwisho utajua muda si mrefu.” “Tafadhali dada usiniue.” “Lazima ufe kwa vile niliapa kila nitakayemkamata na mume wangu lazima nimtangulize mbele na Kinape anajua hivyo si kosa langu aliyekuponza ni huyo aliyekudanganya.” “Dada yangu nakuapia kwa miungu yote sirudii te…” Kilole aliona muda unachelewa alifumba macho na kuminya kifyatulio mara mbili kwa haraka, risasi mbili zilitua kwenye kifua cha Happy na kumrusha kwa nyuma. Baada ya kukata roho, kwa moyo wa ujasiri Kilole aliuchukua mwili ule na kuulaza kitandani kisha alitoka taratibu kuelekea nje ya hoteli. Alimkuta dereva wa bodaboda akimsubiri alipanda hadi alipopaki gari lake, baada ya kumlipa alipanda ndani ya gari lake na kurudi nyumbani kwake. Alipofika alijikausha kusubiri taarifa ya kifo cha mpenzi wa Kinape na jinsi mpenzi wake atakavyokipokea. Baada ya saa mbili ndipo aliporudi Kinape akiwa amechanganyikiwa na kumuuliza na yeye kukataa kujifanya hajui kitu. Alipanga kumweleza baada ya kila kitu kutulia. “Kilole,” Kinape alimwita baada ya kumuona mpenzi wake amehama kimawazo. “A..abee,” Kilole alishtuka kutoka katika dimbwi la mawazo. “Vipi mbona kama upo mbali?” Kinape alimshtua Kilole. “Aah! Ni..ni..po sawa kwani vipi?” Kilole alishtuka kama anatoka ndotoni na kubabaika. “Mbona kama upo mbali?” “Aah! Nipo sawa.” “Basi nataka kutoka mara moja,” Kinape alisema akinyanyuka. “Wewee! Unataka kwenda wapi umesahau unatafutwa?” “Ooh! Nilijisahau yaani nimechanganyikiwa ile mbaya.” Kinape alielekea chumbani kulala na kumuacha Kilole akiwa amekaa sebuleni, baada ya Kinape kwenda chumbani Kilole aliipekua simu yake labda kuna ujumbe umeingia lakini hakukuta na ujumbe wowote. Alimtumia ujumbe yule Jay Jay asimwambie mtu pia asitume tena ujumbe wowote muda ule ili aende ndani akamliwaze mpenzi wake aliyekuwa kwenye lindi la mawazo. **** Majira ya saa tatu usiku Kinape alimuaga Kilole kuwa anatoka mara moja. “Safari ya wapi tena baba?” “Si unajua leo nimekaa ndani kama utumbo ngoja nikanyooshe mwili.” “Sawa baba, kuwa makini tu si unajua sasa hivi wewe ni lulu?” “Hilo nalijua.” “Unarudi saa ngapi?” “Sichelewi.” “Au twende wote?” “Na mtoto umuachie nani?” “Tutatoka naye, si hatufiki mbali?” “Kuna baridi, huu si muda wake wa kumtembeza usiku, akikuwa tutatoka naye.” “Haya baba, basi uwahi kurudi si unajua bila wewe nyumba inapwaya.” “Nalijua hilo mpenzi wangu nitawahi, si unajua leo siko vizuri nahitaji kuwa karibu yako.” “Ni kweli baby wangu.” “Basi baadaye, nitachukua gari ndogo.” “Mume wangu lolote ulitakalo.” “Lazima nikujulishe,” siku ile Kinape alikuwa mpole sana lakini moyoni palifukuta kwa hasira. Kinape alitoka na gari ndogo hakufika mbali alisimama gari na kuipiga namba iliyomtumia ujumbe Kilole. Kabla ya kupiga alikumbuka kama ataipiga huenda akashtukiwa alijaribu kwanza kutuma ujumbe kama watashindwa kuelewana basi angempigia. Alituma ujumbe unaosema: “Oya Anko Jay Jay upo anga zipi mida hii?” Baada ya muda ujumbe alirudi. “Nipo Kapili Kabana, nani mwenzangu?” “Unatoka saa ngapi huko?” aliongeza swali badala ya jibu. “Mmh! Mpaka saa tano vipi una ishu?” “Ndiyo.” “Ishu gani?” Kinape hakumjibu tena aliwasha gari na kuwahi Kapili Kabana, alipofika alipakia kwenye maegesho na kupiga simu huku macho yake yakitazama mlango wa kutokea. “Oya, nipo nje njoo mara moja nina haraka.” Anko Jay Jay alitoka nje haraka akiamini kuna ishu ameletewa, kwani mjini yeye alikuwa akiishi kwa misheni tauni kila kazi iliyokuja mbele yake aliifanya ikiwemo ya udalali wa kila kitu mpaka wake na waume za watu kwake ilikuwa kazi ndogo. Alipotoka alitazama kulia na kushoto labda atamuona mtu aliyekuwa akimwita, kuhangaikakwa Jay Jay kumtafuta aliyempigia simu kumfanya Kinape amuone kwa urahisi. Akiwa na simu mkononi alipiga ili kumuuliza mtu anayemtafuta yupo wapi. Baada ya muda simu iliita na kumuamini ndiye mhusika, alikuwa kijana mmoja aliyeoneka brother men. Hakuipokea aliteremka na kumfuata alipokuwa amesimama kwa vile alikuwa amevaa kapelo ilikuwa vigumu Anko Jay Jay kumfahamu, alipomkalibia alimpa mkono na kumsalimia. “Habari Anko Jay Jay.” “Nzuri, nina imani ni mtu uliyekuwa ukitafuta?” “Kweli kabisa,” Kinape alijibu huku akitoa kofia kichwani. ‘Ha!” Anko Jay Jay alipomuona alishtuka na kutaka kukimbilia lakini hakuweza kwa vile Kinape alikuwa amemshika mkono kwa nguvu. “Sasa unataka kukimbia nini?” Kinape alimuuliza kwa sauti ya chini. “Siyo hivyo brother.” “Basi sikiliza naomba uwe mtulivu tuzungumze taratibu bila hivyo nitakufanya kitu kibaya.” “Sawa Brother,” Ako Jay Jay ilibidi awe mpole. “Naomba twende kwenye gari langu tuzungumze kirafiki.” “Hakuna tatizo brother.” Waliongozana hadi kwenye gari na kuingia ndani, muda wote Anko Jay Jay alikuwa na wasiwasi mwingi. Baada ya kutulia Kinape alimuuliza kwa sauti ya chini. “Unanifahamu?” “Ha..hapana.” “Kuwa mkweli, kwa nini ulitaka kunikimbilia?” “Ulinishtua.” “Naomba uniambie ukweli la sivyo kifo cha mwanamke aliyefariki leo wewe ndiye utakaye kuwa mtuhumiwa namba moja.” “Siyo mimi brother, mi nilitumwa nikuchunguze tu kama una mwanamke, zaidi ya hapo sijui lolote, hata mimi nimeshtuka kusikia yule mwanamke ameuawa.” “Nani alikutuma?” “Mkeo.” “Umemjuaje mke wangu mimi usinijue?” “Nakujua brother.” “Alikutuma nini?” “Alinikutuma nikuchunguze kama una mwanamke wa nje, baada ya kazi yangu kwisha nilimpa ripoti na kunipa changu na mimi kuendelea na mambo yangu mengine. Leo mchana nimeshtuka kusikia yule mwanamke ameuawa kwa risasi, kwa kweli sijui lolote zaidi ya kazi ya kukuchunguza tu brother.” “Kwa hiyo mke wangu ndiye aliyekutuma?” “Ndiyo brother.” “Kama yeye alikutuma nani alimuua yule mwanamke?” “Sijui, labda yeye mwenyewe.” “Baada ya taarifa ya kifo yeye alikuambiaje?” “Amesema nisimwambie mtu juu ya kifo kile pia hata mpango wetu wa kuwachunguza.” “Asante, naomba taarifa hizi usimwambie mke wangu kama tumeonana, sawa?” “Sawa brother, nitafanya kama nilivyokueleza.” “Okay endelea na burudani,” Kinape alisema huku akimshikisha noti mbili za elfu kumi. “Asante brother,” Anko Jay Jay alipokea huku akiwa haamini kama ametoka salama. Baada ya kuachana na Kinape alimpigia simu Kilole kumweleza kuhusiana na kufuatwa na mumewe usiku ule. Baada ya simu kuita sana ilipokelewa. “Anko Jay Jay si nimekuambia usinipigia simu mpaka nikupigie mbona unakuwa si mwelewa?” “Sister kuna jambo la muhimu limenifanya nikupigie simu usiku huu.” “Jambo gani?” “Mumeo kanifuata na kunibana juu ya kifo cha yule msichana na kuniomba nisikuambie.” “ Anko Jay Jay acha utani?” Kilole hakuamini. “Kweli sister.” “Amevaaje?” “Jinsi ya bluu na tishet nyekundu na kofia nyeusi na chini kavaa raba nyeupe.” “Mmh! Ni kweli,” Kilole alishusha pumzi ndefu. “Yaani huwezi kuamini nilishtuka kidogo haja ndogo initoke.” “He, makubwa! Amekuuliza nini?” Kilole alishtuka sana. ”Eti nani kamuua yule mwanamke.” “Mmh! Kwanza wewe umekujuaje?” “Nikuulize wewe, kwa vile siri ilikuwa ya watu wawili.” “Kosa limetendeka wapi?” “Lazima litakuwa kwako tu.” “Mmh! Umemjibu nini?” “Nimwambia sijui lolote.” “Halafu.” “Alinibana na kutishia kunipeleka polisi kuwa mimi ndiye muuaji.” “He! Ikawaje?” “Nilimchoropoka na kukimbia, sasa usalama wangu utakuwaje?” “Okay, Jay Jay nimekuelewa nitakujulisha muda si mrefu.” “Poa sister jambo hili lifanyie kazi naweza kuozea gerezani wakati sijui lolote kuhusiana na kifo hicho.” “Anko Jay Jay hebu niachie kazi hiyo maana hata mimi suala hilo limenishtua sana, lakini nakuapia huwezi kukamatwa nitamtuliza huyu mshenzi kabla hajafanya lolote.”
“Sawa sister nakutegemea wewe.” “Usikonde.” Kilole alikata simu na kukaa kwenye kochi akiwa amechoka na kuamini itakuwa vigumu kwa Kinape kumwelewa akijua yeye ndiye aliyemuua mpenzi wake mwingine. Aliamini kama Anko Jay Jay alikimbia lazima Kinape atamtafute na kumlazimisha kusema ukweli kwa vile ameishaonesha woga lazima angesema kweli. Alijua usiku ule ulitakiwa kila mtu amzidi akili mwenzake kama Kinape aliweza kumzidi akili kwa kumgundua mtu aliyemtumia kumchunguza lazima atataka kujua nani kamuua mpenzi wake. Baada ya kuwaza na kuwazua alipata jawabu ya kitu kilichokuwa kikimsumbua kuificha siri ile kabla Kinape hajajua ni kumuua Anko Jay Jay usiku uleule. Alichukua simu yake na kumpigia Anko Jay Jay, baada ya kuita ilipokelewa upande wa pili. “Vipi Sister?” “Umesema upo wapi sasa hivi?” “Nakaribia home siku imeishaingia nuksi.” “Tunaweza kuonana?” “Wapi?” “Tukutane daraja la Nyakabungo.” “Poa nakuja.” Anko Jay Jay alikuwa anakaa jirani na shule ya Mirongo kufika Daraja la Nyakabungo isingechukua dakika tano. Kilole alikata simu na kwenda ndani kuchukua bastora na kuifunga kiwambo cha kuzuia sauti na kuichomeka kwenye suruali ya jensi na kuvaa vazi lake analolitumia kwenye matukio kama yale. Alitoka kwa haraka kabla Kinape hajarudi, kwa vile kutoka kwake mpaka kwenye daraja la Nyakabungo hakukuwa mbali hakuitaji kutumia gari alitembea kwa miguu kwa mwendo wa haraka kumuwahi Anko Jay Jay. Njiani kila gari lililokuja mbele yake na kumuulika na taa aligeuka na kulipa mgongo mpaka lilipopita. Aliliona gari lao dogo na kujua Kinape ndiyo anarudi lazima angemtafuta. Alichepua mwendo hadi karibu ya daraja na kumuona Anko Jay Jay akija kwa mbele akipepesa macho huku simu ikiwa sikioni. Kilole hakutaka kupoteza muda kwa vile alikuwa kwenye giza alitoa bastora yake na kumlenga kifuani na kuachia risasi mbili zilizomrusha Anko Jay Jay chini ya daraja. Kwa haraka aligeuka na kurudi alipotoka. Wakati anafanya kitendo kile mlinzi mmoja aliyekuwa kwenye nyumba zilizokuwa upande wa shule ya sekondari ya Lake aliona. Kwa vile alikuwa kwenye kiza aliona tukio lile ambalo lilimshtua lakini alikaa kimya kihofia uhai wake. Kilole baada ya kutimiza dhamila yake alirudi nyumbani, alipofika alizificha nguo kwa nje na kuelekea kwenye Bar ya karibu na kununua chips mayai kisha alirudi nyumbani. Kinape aliyefika kitambo na kushangaa kutomkuta mpenzi wake. Alipoingia chumbani alimkuta mtoto amelala kitu kile kilimuonesha hayupo mbali. Alitulia kwenye kochi akiwa na hasira kwa Kilole, alijikuta akipata kigagaziko cha kumuuliza usiku ule. Alipanga kujifanya ametoka kutembea ili asijue chochote. Baada ya nusu saa Kilole alirudi na chipsi kwenye mfuko. “Vipi baby umerudi zamani?” “Kiasi, vipi ulifuata chipsi?” “Ndiyo mpenzi, ulifika mbali?’ “Si sana.” “Karibu chipsi.” “Sijisikii kula mpenzi naomba nikapumzike,” Kinape alisema huku akielekea chumbani na kumuacha Kilole akimsindikiza kwa macho. *** Baada ya kupewa maelekezo ya awali na taarifa kutoka Dar es salaam kuwa kila kitu kimekwenda vizuri anasubiliwa yeye kusafiri tu. Jioni ya siku ile walipanda ndege mpaka Dar. Waliwasili uwanja wa ndege wa J.K .Nyerere jijini Dar majira ya saa moja usiku akiongozana na Teddy pamoja na mwanaye kipenzi Rose. Walipofika walimkuta mwenyeji wao akiwa na kila kitu, mwenyeji wake alipomuona alifurahi na kumkumbatia kwa furaha asiamini kama rafiki yake yupo hai. “Siamini…siamini Mungu mkubwa,” Bon alimkumbatia Deus kwa furaha mpaka machozi yakamtoka. “Deus siamini naona kama ndoto yaani ninachokiona siamini,” Bon alisema huku akibubujikwa na machozi ya mshangao. “Bon ni mitihani ya maisha ni histori ndefu.” “Unajua siamini naona kama nimeona mzimu wako, wakati wa matatizo yako nilikuwa nje ya nchi na niliporudi nilikutana na Mr Mabina na kunieleza ukiwa gerezani ulipatwa na tatizo lililosababisha upate stroke lililosababisha ulazwe hospitali kwa muda mrefu na mara ya mwisho alikuja kukutembelea aliambiwa amefariki. “Niliulimia sana rafiki yangu, uliponipigia simu sikuamini baada ya kunifahamisha nilifanya uliyonituma lakini hamu yangu kubwa kukuona leo. Nimefurahi sana mtu niliyelezwa alipooza sehemu mmoja na kusikia umekufa upo hai katika afya njema kweli Mungu mkubwa. Ilikuwaje maana bado naona kama ngamia kapita kwenye tundu la sindano mbele ya macho yangu.” “Kabla ya yote kwanza nashukuru kwa kazi nzuri uliyonifanyia, naomba tusizungumze lolote niombee Mungu safari yangu nirudi salama nitakupa picha kamili.” “Naomba hata unidokeze kidogo kwani utaniacha kama mtu aliyeota usiku alipoamka asubuhi aliyoyaona yakabakia ndotoni na si kweli.” Deus alimdokeza kidogo lakini safari ya Italia hakumweleza anakwenda kufanya nini. Baada ya mazungumzo ya marafiki wawili waliofanya kazi pamoja kwa muda mrefu kabla Deus hajaingia kwenye matatizo walitafuta sehemu yenye tulivu kuzungumza. Deus alikuwa anaondoka usiku ule na ndege ya British Air ways saa nne usiku. Muda mwingi walikuwa sehemu yenye mwanga hafifu ambayo ilikuwa vigumu kwa watu kuwatambua kwa urahisi. Hawakupenda kuonekana kwa ajili ya usalama wa Teddy. Majira ya saa tatu Deus kabla aliingia chumba cha wageni kujiandaa kuondoka. Walimuomba Bon awapishe kidogo wazungumze, baada ya kusogea pembeni wapenzi wawili na mtoto wao walizungumza ya mwisho kabla ya safari. “Sasa mpenzi naomba nikupe maelekezo ya mwisho,” Teddy alimweleza Deus. “Sawa.” “Ukifika katika mji wa Sicily kuna Cassino nyingi katika zote nilizokueleza, anazopenda Mose zipo mbili, ni mpenzi sana wa kucheza kamali anazozipenda ni Piedimonte San Germano na Liola Hotel (Aquino) hii Liola ndiyo yenye gharama sana na hata kamali yake ni kubwa. Kama Mose ana fedha hupendelea hoteli hii ambayo ina cassino ndani lakini akiwa ana fedha kidogo japo biashara yetu inakufanya uwe na fedha mpaka kufa, hupenda kwenda San Germano.” “Nimekuelewa.” “Unaweza kutembelea Cassino zingine lakini hizi huwa hakosi.” “Kwa vile mji wa Sicily si mgeni kwangu haitanipa wakati mgumu, hii kazi ni ndogo sana kwangu.” “Inaweza kuwa ndogo lakini jamaa wale ni wabaya kuua kwao jambo la kawaida, ukikosea mahesabu wanaweza kukupoteza.” “Si rahisi.” “Mpenzi mbona unajiamini sana?” “Watu sampuli ya huyo mshenzi nimepambana nao sana.” “Nina imani fedha uliyonayo inatosha sana.” “Inatosha sana, hii kazi nataka kuifanya ndani ya saa 24 niwe nimemaliza kila kitu.” “Basi nakutakia kila la heri katika safari yako.” “Nashukuru sana, ila kama mambo yatakwenda kinyume naomba unitunzie mwanangu.” “Bila shaka nitamlea kama mwanangu wa kumzaa, lakini sitaki ufe bado nakuhitaji baada ya maisha ya mateso nina imani tunahitaji faraja ya mioyo yetu.” “Mwanadamu amezaliwa na kufa, hivyo hatuwezi kuepuka kufa kama tumezaliwa.” “Ni kweli lakini Mungu atakutangulia.” Walikumbatiana kisha alimbusu Teddy na mwanaye Rose, alimwita Bon. “Best wacha nikajiandae na safari, shemeji yako anarudi Mwanza kesho asubuhi.” “Hakuna tatizo nikutakie kazi njema, nakubiri kwa hamu najua una mengi ya kunieleza.” “Tumuombe Mungu anirudishe salama.” “Nina imani kwa dua zetu wote atakutangulia.” “Amina. Aliagana na wote kisha alielekea kwenye ndege kwa ajili ya safari ya kuelelea Sicily Italia. **** Kinape aliamka siku ya pili akiwa mtu mwenye mawazo mengi kutokana na tabia ya Kilole kuwaua watu wake wa karibu kila kukicha. Alijiuliza hali ile itaendelea mpaka lini, kuwaua watu wasio na hatia. Akiwa sebuleni akitazama taarifa ya habari ya saa kumi na mbili asubuhi, katika taarifa ule ya habari alishtushwa na taarifa ya sikitisha ya kifo cha mtu aliyeamini kwake ni muhimu kuhusiana na kifo cha mpenzi wake Happy. Katika taarifa ile habari moja ilimshtua baada ya mtangazaji kusema: Kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Anko Jay Jay mkazi wa maeneo ya Mirongo jiji Mwanza, ameuawa usiku wa kuamkia siku ile kwa kupigwa risasi mbili za kifuani na mtu aliyekuwa amefunika mwili nzima. Taarifa iliendelea kusema, mlinzi wa nyumba za jirani ndiye aliyeshuhudia mtu aliyekuwa ameuziba mwili mzima mithiri ya ninja, akimpiga risasi kijana aliyekuwa akija kwa mbele huku akiuliza kwa sauti “Uko wapi?” Bila ya kujua alikuwa akimpigia nani yule mwanamke alitoa bastora na kumpiga risasi iliyomrushia darajani kisha kugeuka kurudi alipotoka. Taarifa iliendelea kusema: Mlinzi baada ya kuona kitendo kile alikaa kimya kuhofia uhai wake na baada ya kuondoka muuaji alimjulisha bosi wake na kupiga simu polisi, baada ya polisi kufika waliuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka hospitali ya Sekou Toure kwa uchunguzi zaidi. Mkuu wa polisi aliwataadharisha watu wote kuhusiana na mauaji ya kutisha yanayoendelea nchini hasa jiji Mwanza yanayofanywa na mwanamke anayevaa vazi refu la kumficha kama ninja ambaye amekuwa tishio jijini baada ya kufanya mauaji mawili ya kufuruliza. Mkuu wa polisi amewaomba watu kutoa ushirikiano pale anapoonekana mtu wa aina hiyo ili kumtia nguvuni. Wakati taarifa ya habari ikiendelea Kilole naye alisimama kwa muda kusikiliza taarifa za kifo cha Anko Jay Jay. Baada ya taarifa ili aliondoka kuendelea na shughuli zake. Kinape aliamini aliyefanya vile alikuwa Kilole lakini ushahidi hakuwa nao hivyo ingekuwa vigumu kumtia hatiani moja kwa moja hasa baada ya mtu aliyemtegemea kutoa ushahidi kumuua. Alijuliza Kilole kamuua Anko Jay Jay kwa ajili gani? Aliamua kutoka nje ya nyumba akiwa na mawazo mengi sana na kujiuliza hali ile itaendelea mpaka lini. Aliamini mwisho wake angekuwa kama Deus ambaye kwake aliamini amekwisha fariki. Akiwa anatembea taratibu kichwa chini mikono nyuma kuzunguka nyumba yao alishtuka kuona kitu kama furushi jeusi likiwa pembeni ya maua. Aliinama na kulitazama kwa kulipekua na kipande cha mti kwa kukinyanyua. Aliponyanyua alishangaa kuona bastora ukidondoka chini, aliiokota na kuichomeka kwenye bukta aliyokuwa amevaa na kuificha kwa fulana aliyovaa juu. Alitupa kipande cha mti na kuinyanyua nguo iliyokuwa kimezungushiwa bastora na kugundua lile ni gauni lefu lenye mtandio wake na kutambaa cha kujifunika usoni na kuwa kama ninja. Kwa mara ya kwanza alipata ushahidi wa nani muuaji japo mwanzo alikisia bila kuwa na ushahidi. Aliviangalia vitu vile na kukumbuka vitu vingi kuanzia kifo cha mchumba wake na mpenzi wake wote wenye majina ya Happy pamoja na Anko Jay Jay ambaye aliuawa muda mfupi baada wa yeye kuzungumza naye kwa mujibu wa shuhuda. Aliishika bastora mkononi na kuitazama kwa muda hasira zilimpanda mpaka akaanza kutetemeka. Moyoni alijiapiza siku ile ndiyo ungekuwa mwisho wa kumvumilia muuaji mkubwa asiye na chembe ya huruma aliyemkosanisha na rafiki yake kipenzi Deus na kusababisha kifo chake. Aliamini baada ya Anko Jay Jay anaweza kufuata yeye aliona dawa ni kumuwahi kabla hajawahiwa. Alibeba zile nguo mkono wa kushoto na mkono wa kulia alishikilia bastora na kuingia ndani kama askari aliyetumwa kumkamata mtuhumiwa wa mauaji. “Kilole,” aliita kwa sauti kubwa. Kilole aliyekuwa jikoni akiandaa maziwa ya mtoto, alipotoka alishtuka kukutana na mdomo wa bastora ukimtazama huku mkono mwingine ameshilikia nguo zake za kazi. “Kinape vipi?” alimuuliza macho yamemtoka pima. “Kilole kwa nini umemuua Happy?” “Hilo jibu uliza swali,”Kilole alijibu kwa kujiamini. “Kwa nini umemuua Anko Jay Jay?” alibadili swali. “Alistahili kufa.” “Kwa nini?” “Sina jibu zaidi ya nililokujibu.” “Kilole, umesababisha Deus kufungwa, umesababisha nimgeuke rafiki yangu umesababisha kifo chake na kumuacha Rose yatima. Umemuua mchumba wangu Happy umemuua mfanya biashara mwenzangu Happy na mwisho umemuua Anko Jay Jay.” “Kinape kina kitu unajua unataka nikujibu nini?” “Naomba jibu kwa nini umewaua?” “Sina jibu, unataka kunifanya nini wakati unajua kila kitu?” “Nataka na wewe uwafuate wenzako,” Kinape alisema huku akitetemeka na jasho kumtoka bastora kaielekeza kwa Kilole. “Kwa hiyo unataka kuniua?” “Lazima ufe Kilole, siwezi kuishi na mwanamke mwenye roho mbaya kama wewe.” “Haya niue,” Kilole alisema huku akisogea mbele ya mdomo wa bastora. Baada ya kusimama mbele ya bastora bila kufanywa jambo lolote alishika bastora na kuanza kunyang’anyana. Kila mmoja alitumia nguvu kwa Kilole kutaka kunyanyang’anya na Kinape kuing’ang’ania. Kwa bahati mbaya katika kugombea kidole cha Kinape kilichokuwa katika kifyatulio kiliminya kifyatulio kilicho fyatuka na kusababisha risasi mbili zitoke na kumuingia mtu chini ya kifua. “Aah!” ilikuwa sauti iliyoonesha risasi kumuingia. Taratibu mmoja aliteremka chini huku damu zikimtoka chini ya kifua, mwingine alishtuka na kutaharuki na kumtazama mwenzake aliyekuwa ametoa macho pima huku akisema kwa sauti ya mawimbi. Alimuwahi na kumpakata huku mkono ukijitahidi kuziba sehemu zilipoingia risasi na kuufanya mkono mtote damu. “U.u..u..me..ni..ua…,” ilikuwa sauti ya mawimbi. “Nooo…samahani… bahati mbaya.. hu..wezi kufa,” alisema kwa sauti ya kilio ikifuatiwa na machozi. “Na..na..kufa…ume..ni..ni..,” alisema kwa shida huku damu ikimtoka mdomoni na kuweka michirizi pembeni ya mdomo iliyoteremka mpaka kwenye mapaja ya aliyemkumbatia.
“Huwezi kufa…usife… mpenzi wangu kazi yote niliyofanya imekuwa bure.” “Naomba Deus a..ni..ni..samehe sana, ni..ni..na imani nina deni zito kwa..kwa..a ke.” “Jamani huu mkosi gani….Ki..Ki..Ki..,” alishindwa kumalizia jina kwa uchungu ulikuwa mkubwa moyoni. “N.n.na..na..ku.ku.f..f.,” damu ilijaa mdomoni na sauti ilishindwa kutoka nuru ya macho ilipotea taratibu roho iliachana na mwili. Alimtikisa kwa nguvu huku akimwita jina lake lakini hakuwa na jibu macho yalikuwa yametulia kama alikuwa akimtazama lakini tayari roho iliachana na mwili. **** Sauti ya tamu ya kike ya mhudumu wa ndege ya British Air ways ilimshtua Deus aliyekuwa amepitiwa na usingizi: “Ndugu abiria wa ndege yetu ya British Air ways, ndege yetu ndiyo inakaribia kutua katika uwanja wa Sicily, tafadhali mnaombwa mfunge mikanda, tunawatakia safari njema yenye furaha, asanteni.” Deus alifumbua macho na kuangalia saa yake ilimuonesha ni saa mbili na nusu za usiku. Alichukua mkanda wake na kujifunga kisha alitulia huku abiria wengine nao wakijifunga mkanda. Baada ya muda ndege iliteremka uwanjani na matairi kugusa rami na kutembea kwa muda kabla ya kusimama. Deus alikuwa wa mwisho kuteremka kwenye ndege, alitoka taratibu na Brifcase yake mkononi. Baada ya kufanyiwa upekuzi alitoka nje ya uwanja wa ndege na kupokewa na dereva wa teksi. “Habari ndugu.” “Nzuri.” “Karibu Sicily,” Dereva mwenye asili Kichotara alimkaribisha Deus. “Asante.” “Unaelekea wapi?” “Liola Hotel (Aquino).” “Hakuna tatizo.” Deus aliingia kwenye gari na kuelekea mjini akilakiwa na mataa yaliyoupendesha mji wa Sicily kwa taa. “Pole na safari?” dereva alionekana mcheshi alimsemesha Deus aliyekuwa kimya akitafakari safari yake. “Asante.” “Kaka wewe ni mgeni mji huu?” “Kwa nini?” swali lile lilimfanya Deus aache kuangalia mitaa na kumtazama dereva. “Mbona hapa jijini kuna hotel tulivu zipo pembeni ya mji karibua na upepo wa bahari unakwenda hotel ile.” “Ni uamuzi tu, shughuli zangu huzifanyia karibu na ninapokwenda.” “Na kweli, kuwa katika hoteli ya karibu na shughuli zako ni vizuri.” “Nashuku kwa kulielewa hilo.” “Umekuja kibiashara?” “Ndiyo.” “Biashara gani? Naweza kuwa msaada kwako.” “Biashara yangu aihitaji msaada wa mtu.” “Okay, nilidhani utahitaji mwenyeji.” “Mi mwenyewe ni mwenyeji hivyo sihitaji mwenyeji mwingine.” Wakati huo teksi ilikuwa ikikata kona kuingia Liola Hotel (Aquino), baada ya kuegesha kwenye maegesho dereva alimwambia mgeni wake. “Nina imani tumefika salama?” “Nashukuru.” “Hata uendeshaji wangu nina imani umeupenda?” “Ni kweli, wewe ni dereva mzuri.” “Basi ndugu yangu atakapokuwa ukija hapa kwa shughuli zako usiache kunitafuta ndugu yako, kadi yangu hii hapa, naitwa Abdul.” “Hakuna tatizo, nitakutafuta,” Deus alisema huku akipokea ile kadi ya biashara ya Dereva Abdul. “Hakuna tatizo, vipi totoz?” “Nikihitaji nitakutafuta.” “Usiwe na wasiwasi sisi ndiyo wenyeji wa mji huu, ukiingia kichwa kichwa unaweza kukombwa kila kitu.” “Hakuna tatizo.” Baada ya kumlipa chake aliteremka kwenye gari na kuingia ndani ya hoteli na kwenda moja kwa moja mapokezi na kupokewa na msichana mrembo. “Karibu kaka.” “Asante.” “Unahitaji msaada?” “Ndiyo, nataka chumba.” “Unataka cha juu au chini?” “Nataka ghorofa ya pili.” “Umepata.” Baada ya kuandikisha mapokezi alipewa msichana aliyempeleka mpaka chumbani kwake. Baada ya kumfikisha msichana aliyempeleka alimwambia kwa sauti tamu: “Karibu sana.” “Asante.” “Nina imani imeridhishwa na huduma yangu pia vyumba vyetu?” “Ni kweli, huduma yako ni nzuri pia chumba ni vizuri sana.” “Utahitaji huduma zaidi?” “Kama ipi?” “Najua usiku utakuwa mrefu sana kama ukilala peke yako, ukiniihitaji nikupe kampani nitakuwepo leo kwa ajili yako,” binti mrembo alisema kwa sauti ya wizi. “Nashukuru, nikuhitaji nitakujulisha.” “Naitwa Loveness na namba yangu ya simu hii piga muda wote usihofu,” yule msichana alimpa kikaratasi alichokuwa kimeandikwa namba ya simu na kumfanya Deus ajiulize ameandika muda gani ikiwa muda wote walitembea pamoja kupanda juu. “Nashukuru,” Deus alikipokea kile kikalatasi na kumwacha yule msichana aondoke. Baada ya kuondoka alifunga mlango na kwenda kujitupa kitandani kama mzigo macho yake yakitazama juu. Aliusikia mwili wake ulivyochoka kutokana na kusafiri saa 24 bila kupumzika. Uchovu aliousikia aliamini akijiegesha lazima atalala na yeye alitaka kazi ile aianze usiku ule. Japokuwa alikuwa amechoka sana hakutaka kupumzika Alijinyanyua kitandani na kukaa kitako, alipoangalia saa yake ilimuonesha ni saa nne na dakika saba, baada ya kuweka mizigo yake aliteremka upande wa Cassino. Alipofika upande wa Cassino kila mtu alikuwa yupo bize na mambo yake. Alielekea upande watu wakiokuwa wakicheza kamari huku wakinywa pombe, alizunguka taratibu kila kona bila kumuona mtu aliyemfuata. Alitulia kwa muda wa saa nzima akizunguka kila kona. Saa tano iliingia bila kumuona, alitoka hadi hotelini na kuagiza chakula kutokana na njaa aliyokuwa akiisikia. Baada ya kula alirudi tena Cassino lakini hakumuona mtu wake, alisubiri mpaka saa sita bila dalili za kuonekana Moses. Aliamua kwenda kuoga ili amtafute Abdul ampeleke hoteli nyingine. Baada ya kuoga alimpigia simu Abdul dereva wa teksi. Baada ya siku kuita ilipokelewa: “Haloo.” Simu ilipokelewa upande wa pili. “Haloo mr Abdul.” “Haloo, nani mwenzangu?” Abdul aliuliza. “Aah! Bwana Abdul si tumeagana muda si mrefu?” Deus alishangaa kuulizwa jina, lakini alikumbuka alichukua namba ya dereva bila kumpa yake. “Nimeagana na watu wengi, hebu nikumbushe.” “Ndugu yangu hata sauti huijui?” “Ooh! Mgeni wangu wa Liola Hotel (Aquino)?” “Ndiyo.” “Okay, unahitaji huduma gani kwa sasa?” “Kwani una huduma ngapi?” “Kaka si tulizungumza kama unahitaji mtoto wa kukusaidia kuuvusha usiku na usafiri.” “Kwa sasa nahitaji usafiri.” “Unataka kwenda wapi usiku wote huu?” “Utajua ukifika.” “Poa, nakuja muda si mrefu.” Japo mwili wa ulikuwa umechoka Deus aliamini siku ile hakutakiwa kuupitisha bila kufanya kazi iliyompeleka, alikuwa radhi ya siku ile ashinde kama popo kwenye kwenye Cassino zaidi ili tu kumtafuta Moses bila kuwa na uhakika kwa kumpata kwake aliona akicheza pata potea. Baada ya muda simu yake iliita ilikuwa namba ya Abdul, alichukua bastora yake na kuipachika kiunoni kisha aliteremka chini. Alimkuta Abdul anamsubiri alipomuona alisogeza gari karibu yake na kumfungulia mlango. Deus aliingia na kumueleza: “Nipeleke Piedimonte San Germano.” “Hakuna tatizo, inaonekana mzee mtu wa kujirusha, eeh?” “Hapana kuna mtu namfuata.” “Hakuna tatizo,” dereva alisema huku akikanyaga mafuta baada ya gari kuingia barabara kuu. Kutokana na uchache wa gari barabarani walitumia dakika kumi kufika Piedimonte San Germano. Abdul alipaki gari kwenye maegesho na kumgeukia Deus aliyeoneka anawaza kitu. “Mheshimiwa tumefika.” “Okay nashukuru,” Deus alijibu huku akifungua mkanda na kutoa bochi ili amlipe. ”Kiasi gani?” “Kwani si nakusubiri au nakuacha?” “Sijui nitachukua muda gani lakini nahitaji huduma yako kwa muda wote nitakaokuwa hapa.” “Kwa hiyo nikusubiri?” “Ndiyo maana yake.” “Kumbuka kuna chaji ya kukusubiri.” “Usihofu nitalipa.” “Nikusibiri hapa au tuingie wote.” “Siyo mbaya tunaweza kuingia wote.” Walitoka ndani ya gari na kulifunga gari kwa rimoti kisha waliongozana ndani ya ukumbi. Kwa vile hakuwa mgeni wa sehemu zile alitafuta meza moja na kukaa na Abdul kisha waliagiza vinywaji. Deus alitumia nafasi ile kumuacha Abdul mara moja na kuelekea upande wa cassino. “Mzee nakuja,” alisema huku akinyanyuka. “Hakuna tatizo.” “Suala la malipo usiwe na wasiwasi nitamaliza mimi.” “Najua nipo na mtu mzito.” Deus aliachana na Abdul na kuelekea upande cassino ambako kulikuwa kumechangamka kulikuwa na watu wengi kila mtu alikuwa bize na kucheza kamali huku akinywa pombe. Alizunguka kila sehemu bila kuiona sura ya Mose, alirudi alipokuwa amekaa Abdul akiamini sehemu ile ilikuwa ndiyo karibu na njia ya kuelekea upande wa kuchezea kamali hivyo angeweza kumuona kila aliyeingia na kutoka ndani. Muda ulikatika bila Mose kutokea kitu kilichozidi kumchanganya na kuona njia waliyotumia kumtafuta Mose ilikuwa ya kitoto heri angemuelekeza anapoishi kuliko kumtafutia cassino. Alianza kuiona kazi inaanza kuwa ngumu, lakini hakukata tamaa aliendelea kukaa pale kuangalia waliokuwa wakiingia na kutoka. “Mzee unaonekana haupo sawa?” Abdul alimuuliza baada ya kumfuatilia kwa muda mrefu. “Kivipi?” “Toka timefika unaonekana kuna kitu unakitafuta.” “Nakuja,” Deus alisema huku akinyanyuka baada ya kumuona mtu mmoja anayefanana na Mose akipita akielekea upande wa kaunta. Kwa vile alikuwa amempa kisogo hakuwa na haraka ya kumfuata. Alimwacha asogee mbele kidogo kisha alimfuata nyuma taratibu ili amuone mtu yule anayefanana Mose anakwenda upande gani. Alimuona amesimama kaunta na kuagiza kinywaji, hakuwa na haraka naye alimwacha mpaka atulie. Japo mtu yule alimfananisha na Mose kilichomshangaza alikuwa peke yake tofauti na maelezo ya Teddy kuwa Mose alitembea na kampani ya vijana wa kihuni. Alimuona yule mtu akihama kwenye kaunta na kusogea sehemu ya kuchezea kamali alisogea taratibu hadi alipokuwa na kumtazama usoni kwa chati. Alipomtaza vizuri aligundua kumbe siye mwenyewe, alijikuta akijifyonza na kurudi sehemu yake. Pamoja kuwa na Abdul mawazo yake yalikuwa mbali kila muda aliangalia saa yake ya mkono na kuuona muda ukizidi kukatika bila mhusika kutokea.
Mpango wa kumtafuta mtu kwenye Cassino aliuona wa kitoto badala ya sehemu anayoishi ambayo ingemfanya aifanye kazi ile kwa uhakika mkubwa, japokuwa Teddy alimweleza Mose ana tabia ya kujesha club kuliko kuwepo nyumbani. Kila dakika alitupia jicho kwenye saa na kumuonesha muda unazidi kutaradadi, mishale ilimuonesha ni saa nane kasoro usiku. Alijikuta akijifyonza mwenyewe kila dakika kitu kilichomfanya Abdul kumuuliza. “Kaka vipi mtu aliyemfuata amechelewa nini?” “Aah! Kuna Cassino ngapi maarufu kwa kamari jijini?” “Mmh! Zipo nyingi tofauti na ulipopanga na hapa kuna Piazza Marcom, Gari, Forum Palace na nyingine nyingi ila kati ya hizi moja utafurahi.” “Sasa fanya hivi nirudishe mara moja hotelini ili unipeleke ya karibu.” “Ya karibu ni Piazza Marcom.” Walilipa vinywaji na kutoka huku moyoni Deus akianza kuona ugumu wa kazi iliyopo mbele yake, mwili nao ulikuwa umechoka kutokana na safari ya saa 24 angani. Alitamani kurudi hotelini kulala lakini hakukubaliana na hali ile. Abdul alikimbiza gari na kutumia muda mfupi kurudi hotelini. “Niteremshie hapa wee kageuze,” Deus alimwambia Abdul aliyelisimamisha gari katikati ya barabara. Gari lililokuwa kija mbele lilisimama na kupiga hodi, Abdul alipotaka kuliondoka gari Deus alimwambia: “Waache wasubiri,” alisema huku akiteremka kwenye gari. Waliokuwa kwenye gari la mbele walianza kutukana: “Wee fala ondoa uchafu wako barabarani.” Kauli ile ilimfanya Abdul azime gari kabisa na kumfanya Deus amshangae. “Vipi Abdul,” Deus alimuuliza akiwa bado amesimama pembeni ya gari. “Hawa watoto hawanijui, kuuza midawa yao ya kulevya haiwezi kuwafanya watudharau wakubwa zao.” “Unawajua?” “Nawajua si wazungu wa unga hawa.” “Oyaa wee fala ondoa kopo lako, “ aliteremka kijana mmoja aliyekuwa amevaa kofia kwa kuigeuza nyuma na kupiga ngumi kwenye boneti ya gari. “Ondoaa Ondoaaa.” Kitendo kile kilimfanya Abdul kutoka kwenye gari na kwenda kumbeba mzimamzima na yule kijana na kwenda kumtupa kwenye gari lao. Wenzake walitoka kishari. “Nyie paka hakuna hata mmoja anaweza kunigusa au mnataka nilipasue gari lenu?” Abdul aliyekuwa amejengeka kimazoezi akitamba mbele ya wale vijana. “Basi brother unajua mwenzetu amelewa,” jamaa mmoja alisema huku akimvuta mwenzake aliyeoneka amekunywa kidogo. “Mose waambie wenzako mimi nani?” Abdul aliendelea alijitapa. Wakati Deus akisogea karibu na Abdul ili kumsaidia kwa lolote macho yake yalipata mshtuko baada ya kumuona mtu aliyekuwa akimtafuta sana. Mose aliwatuliza wenzake na kurudi ndani ya gari lao. Abdul aliingia ndani ya gari lake na kuitoa gari njiani. Deus alipata wazo la haraka na kurudi kwenye gari na kumfanya Abdul amhoji: “Vipi mbona umerudi?” ”Naomba tuwafuate hawa popote wanapokwenda.” “Achana nao watatupotezewa muda.” “Kuna kitu nataka kujua.” “Gharama zinaongezeka.” “Usiwe na wasiwasi wee fanya kazi fedha siyo tatizo.” “Kama bado unayo yangu achana nao,” Abdul alisema huku akiliacha gari la kina Mose likiingia barabarani na kuondoka kwa kasi. “Abdul utaniudhi ifuate ile gari hakikisha hulipotezi,” Deus alisema kwa sauti ya amri. Abdul aliwasha gari na kuliondoa kwa kasi kulifukuza gari la kina Mose lililokuwa likimbizwa kwa kasi ya ajabu na kushindwa kuliona kila walivyokanyaga mafuta hakufanikiwa kuliona. “Abdul tutawaonaje wale watu?” “Mmh! Kwa kweli sijui, si unajua uwezo wa gari lao na langu, hata kama tungewafuata nyuma wangetuacha lile gari habari nyingine hata bei yake mbaya wananunua wazungu wa unga tu.” “Sasa watakuwa wamekwenda wapi?” Deus alianza kuchanganyikiwa. “Lazima watakuwa wamekwenda Piedimonte San Germano, ndiyo club iliyopo mbele,” Abdul alimtoa wasiwasi. “Basi twende tuwawahi.” “Kwani kuna nini? Wewe ni polisi?” “Hapana, kuna mtu nina shida naye katika wale vijana.” “Hakuna tatizo.” “Yule anayeitwa Mose unamfahamu?” “Ndiyo.” “Anakaa wapi?” “Kwa kweli sijui huwa tunakutana sehemu hizi.” “Unamjua vipi Mose.” “Mmh! Yule kijana ana historia ndefu kwanza inasadikiwa na fedha sana hata lile gari ni lake, pili ameponea tundu la sindano kwenye kinywa cha mauti. Inasemekana walidhulumiana mshiko na wenzake, si unajua wale wazungu wa unga.” “Nani aliyemfanya vile?” “Wengi walijua labda shemeji yake, lakini baadaye alikataa, mpaka sasa haijajulikana nani aliyemfanyia kitu kama kile, Kwa sasa imekuwa kimya hakuna tena habari zile.” Abdul alipunguza mwendo ili akate kona kuingia Piedimonte San Germano, bahati nzuri lile gari waliliona na kwenda kupaki pembeni yake. “Imekuwa vizuri tumewakuta,” alisema Abdul huku akizima gari. “Kazi nzuri,” Deus alijibu huku akiteremka kwenye gari na kuelekea ndani ya Cassino haikupita muda Abdul alikuwa pembeni yake. Walitembea kwa mwendo wa haraka mpaka ndani ya cassino. “Abdul nisubiri hapa,” Deus alimuacha Abdul sehemu ya mwanzo na kuelekea kwenye kamali. Alipofika alimkuta Moses akiwa ameshikilia bunda la dola mkononi akijiandaa kucheza, pembeni alikuwa na rafiki zake ambao walionekana ni wapambe wake. Kwa hali ile aliamini anaweza kukesha bila kufanya jambo lolote, ilibidi atumie akili za kuzaliwa kuweza kumtoa Mose sehemu ile kabla hajaingia kwenye kamali. Alirudi hadi kwa Abdul aliyekuwa amekaliwa na mwanamke mmoja aliyekuwa sehemu ya mwili wake wazi na kuchezeana. Alisogea mpaka karibu ya Abdul na kuishika siraha yake kwa kuamini muda si mrefu itakuwa ama zao ama zake na damu itamwagika. Alipoangalia saa yake ilimuonesha ni saa tisa na nusu za usiku ulikuwa umebakia muda mchache kuingia alfajiri ambayo ingemuharibia shughuli yake ya siku ile. JIJI DAR ES SALAAM Akiwa bado ameishikili mwili ambao aliamini kabisa ulikuwa umetengana na roho, aliutikisa tena huku akijiona kama amefanya kazi ya bure ya kubeba maji kwenye gunia. Akiwa kama mtu aliyekuwa akizungumza na mtu aliye hai kwa kuutikisa mwili usiokuwa na uhai. “Mpenzi amka…amka mpenzi wangu…kuna faida gani ya mimi kuendelea kuishi kama wewe niliyekutegemea umekufa….Wewe ndiye aliyefanya nifanye yote haya.” Aliukumbatia mwili wa mpenzi wake kama amempakata mtoto mdogo, machozi yake yaliangukia kwenye paji la uso wa marehemu. “Mpenzi…bahati mbaya..Ki..Ki.. samahani… sikukusudia kukuua bahati mbaya…Eeh! Mungu kwa nini umemchukua mtu huyu wakati bado namhitaji sana.” Wakati huo mtoto ndani alikuwa akilia kwa sauti kwani ndiyo alikuwa akiandaliwa maziwa. Aliuweka mwili chini bila kujifuta damu alikwenda chumbani na kumchukua mtoto na kumbeba akiwa na damu zake mkono. Alitoka naye hadi pembeni ya mwili wa marehemu alipiga magoti na kumweleza mwanaye ambaye alikuwa hajui chochote. “Gift mwanangu huna tena baba tena… Baba yako amekufa.. Kinape amka umuone mtoto wako ataishije bila baba?” Kilole machozi ya majuto yalimtoka kama maji. Gift kama alisikia alichoelezwa na mama yake, aliangua kilio kama kauguzwa moto, kila alivyombembeleza hakunyamaza. Kilole alijikuta naye akiangulia kilio akiwa bado amepiga magoti mbele mbele ya mwili wa Kinape aliyekuwa amefariki muda mrefu. Akiwa hajui afanye nini, sauti ya mlango kugongwa ilimshtua, kwa haraka alikwenda hadi mlangoni na kufunga kwa ndani badala ya kufungua kisha alishusha mapazia yote. Aliuvuta mwili wa Kinape hadi chumbani na kutengeneza michirizi ya damu toka sebuleni hadi chumbani. Kwa haraka alichukua dekio na ndoo ya maji ya kuanza kuifuta damu, wakati huo mlango uliendelea kugongwa na kuzidi kumuweka Kilole kwenye wakati mgumu na kujiuliza atakuwa nani. Alijikuta akipata wazo baya na kwenda chumbani kuchukua bastora ili kumzimisha anayegonga mlango moyoni aliapa hatakubali kushikwa kirahisi lazima afe na mtu. Alipotaka kwenda kufungua mlango alisita kwanza alirudi ndani na kusafisha damu iliyokuwa kwenye zuria aliubeba mwili wa Kinape kwa shida na kuulaza kitandani kisha aliufunika shuka na kuhakikisha nguo zote zenye damu anaziweka bafuni. Baada ya kuhakikisha hakuna damu sehemu zote alipuliza pafyumu ili kuondoa harufu ya damu mbichi. Baada ya kupulizia manukato kila kona alitoka hadi mlangoni na kufungua mlango. Lakini nje hakukuwa na mtu yeyote alizunguka nyumba lakini hakumuona. Alirudi ndani na kujiuliza atafanya nini baada ya kumuua bila kukusudia mwanaume aliyemfanya afanye yote yale. Moyoni alitamani awatafute wote aliowaua kwa ajili ya Kinape ili awaombe msahama. Alitamani kulijua kaburi la mume wake Deus ili akamuombe msamaa kwani nguvu zote alizotumia ilikuwa kazi bure. Wazo lililomjia lilikuwa kutafuta vijana wa wamchimbie shimo ili usiku amzike mwili na Kinape, kwa kuhofia kama akikaa sana na mwili unaweza kuharibika na kutoa harufu na kusababisha kutiliwa mashaka. Wazo lile lilimpa ujasiri na kumbeba mtoto wake na kufunga nyumba kisha alielekea kijiweni kutafuta vijana wa kumchimbia shimo ambalo ndilo litakuwa kaburi la Kinape **** Nyuma ya meza kubwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai DCI Karimu Swago aliyekuwa kimya akiisoma ripoti ya mauaji ya kutisha yaliyotokea kwa muda mfupi Jiji Mwanza na muuaji alikuwa mwanamke anayevaa vazi refu jeusi linalouziba mwili wake na kuwapa wakati mgumu jeshi la polisi kumjua ni nani. Baada ya kuisoma alimgeukia mkuu wa upelelezi Athumani Fukwa. “Fukwa,” alimwita huku akimkazia macho. “Mkuu.” “Mpaka sasa mmefikia wapi mauaji haya?” “Mkuu kwa kweli bado tunapambana lakini bado hatujajua ni nani anayefanya mauaji haya.” “Kwa hiyo mnataka kuniambia chombo cha dola tumeshindwa?” “Hapana mkuu, bado tunaendelea na upelelezi.” “Hapa naona kuna mtu anaitwa Kinape, mmesisha mtia mikononi?” “Mkuu simu yake haipatikani.” “Kama haipatikati mmetumia mbinu gani kumpata?” “Mkuu bado tunaendelea na upalelezi ikiwa pamoja na kuhoji waliokuwa wapenzi wa marehemu Happy aliyeuawa Gorden Crest.” “Mmh! Na kuhusu familia ya Anko JayJay inasemaje?” “Kwa kweli hawajui lolote kutokana na marehemu kufanya mambo yake kivyakevyake bila kumshirikisha mtu yeyote.” “Alikuwa akifanya kazi gani?” “Wanamwita martpapas.” “Wana maana gani?” “Hakuwa anachagua kazi kila kazi uliyokuja mbele yake aliifanya.” “Hakuwa na rafiki wa kike?” “Hilo tuliuliza, tuliambiwa hakuwa na mwanamke mmoja hivyo ilikuwa vigumu kumjua nani aliyekuwa akijua habari zake kwa siku ile.” “Mliwatafuta na kuwahoji?” “Ndiyo,tuliwapata wachache, wote walisema walikuwa na muda mrefu bila kumtia machoni.” “Hana mtu wake wa karibu?” “Yupo lakini inaonesha aliondoka siku tatu kabla ya kifo cha Anko Jayjay.” “Alikuwa na umuhimu wa kumuhoji, inawezekana kuna vitu anavijua vinaweza kutusaidia kupata mwanga.” “Hakuna tatizo mkuu tulimueleza tukiwa na shida naye tutamtafuta.” “Basi atafutwe mara moja nataka jioni nipate jibu mmefikia wapi, haiwezekani tuchezewe kiasi hiki tumekaa kimya. Hamjui tunaiabisha sifa ya jeshi letu makini lenye nguvu,” DCI Swago alisema kwa sauti ya amri. “Sawa mkuu.” “Basi naomba kazi ifanyike mara moja naamini hatujashindwa kama hamuwezi nitaingia mwenyewe mstari wa mbele.” “Kazi itafanyika mkuu,” Mkuu wa upelelezi Fukwa alimhakikishia mkuu wake kazi itafanyika. Baada ya kutoka kwenye kikao na mkuu wake wa kazi, Fukwa aliwaita vijana wake wa kikosi maalumu na kutoa amri ya kijeshi. “Nina imani mmemsikia mkuu, kwa hiyo sitaki kusikia tena muuaji bado anatamba, mpaka kesho jioni nataka tuwe tumemkamata. Sijui mtamkamata vipi, hiyo si juu yangu bali kusikia yupo mikononi mwa polisi, sawa?” Mkuu wa upelelezi Fukwa. “Sawa mkuu,” vijana aliitikia kikakamavu.
“Nina imani mmepata pa kuanzia?” “Ndiyo mkuu.” “Haya tawanyika mkimkosa na ninyi msirudi hapa.” Ilikuwa kauli iliyowapa wakati mgumu kikosi cha kazi kinachodili na mtukio kama yale. Walikubaliana kutawanyika huku kila mmoja akijipa jukumu lake ili wakikutana wajue wamefika wapi. *** Kachero Mzengwa alitembea taratibu maeneo ya Mirongo kwa kupita katika vijiwe vya Anko Jay Jay. Kwa vile alikuwa katika vazi la kawaida alifika kwenye uwanja wa mpira wa shule ya Mirongo na kuwakuta vijana wakicheza kamali huku wakivuta bangi hakufanya kitu na yeye alijichanganya. Na yeye aligongea sigara ya kawaida na kuvuta huku akifuatilia kamari. Mara alisikia jamaa mmoja akisema: “Washikaji tumempoteza mwanetu Jay kama utani,” jamaa aliyekuwa akivuta bangi alisema. “Mmh! Unajua naye alizidi kila kazi alifanya unakumbuka Tom nilimweleza Jay kwa kazi yake ya ukuwadi ipo siku atakufa. Jamani Jay kufa kwa risasi kama siyo kumkuwadia mume wa mtu ni nini?” mwingine aliongezea huku akilamba lizila unyonge bangi. “Na kweli jamaa alizidi, mi nilijua mwisho wake mbaya.” “Tena Side bahati yake alikwenda bushi la sivyo na yeye angekufa.” Wakiwa katikati ya mazungumzo alitokea jamaa mmoja na wote waligeuka na aliyekuwa akinyonga alisema: “Sideeee wapi Jay, jichanganye na wewe utamfuata mwenzako, fanya kazi zote lakini ya ukuwadi ni kifo.” “Mwambie, hivi wewe mkeo akikuwadiwa utajisikiaje?” “Jamani mbona umekosa ya kuzungumza, naona kijiwe hakinifai nikajichanganye na masela wa Lake sekondary,” Side alisema huku akiondoka taratibu na kuwaacha jamaa wakiendelea kumpaka mbovu. “Side kuondoka siyo dawa, kama utafanya kazi ya rafiki yako nawe si muda mrefu utamfuata.” “Ninyi mnajuaje kama kauawa na mke wa mtu?” Side alisimama na kuuliza. “Side hata kama mimi siyo mpelelezi lakini ukiangalia mauaji yalivyotokea picha nzima inaonesha kauawa mwanamke aliyekuwa nyumba ya wageni. Hata siku mbili hazijapita kauawa Jay tena na mtu wa aina moja mwanamke anayevaa vazi refu la kumziba mwili na uso. “Huyo mwanamke lazima amegundua yule mwanamke aliyemuua hotelini anatembea na mumewe na mtengeneza mipango ni Jay na yeye kumuua. Sasa nawe jipendekeze moto ukuwakie sisi siyo wajinga kukomaa na kazi za upusha, tunapenda maisha mazuri lakini mwisho wake kufa kama jambazi.” Jamaa mmoja aliyekuwa akisema kwa sauti nzito huku akinyonga ganja. Machero Mzengwa alijikuta akipata kitu kipya ambacho hakuwahi kukiwaza, alichosema jamaa aliyekuwa akinyonga ganja. Japo alifurahi kumuona Side mtu muhimu kwake lakini pia alipata mwanga mwingine ambao aliamini utamsaidia atakapozungumza na Side. Alimpigia simu dereva wa defenda ili apate usafiri wa kuondoka na Side. “Poa, lakini mnanionea bure,” Side alizidi kujitetea. “Tukuonee vipi ikiwa wewe na Jay mlikuwa mnatutenga na kutuona sisi sio kwa vile mnakamata fedha ya ukuwadi.” Mara ghafla kulizuka ugomvi baada kudhulumiana kwenye kamali, ile ilimpa nafasi kachero kumfuata Side aliyekuwa amesimama pembeni na kumsalimia. “Side vipi?” ‘Poa mkubwa.” “Sasa Side tuzungumze kidogo.” Walisogea pembeni kidogo ili wazungumze, ghafla lilitokea defenda na kuwafanya waliokuwa wakicheza kamali na kuvuta bangi kukimbia. Side naye alitaka kukimbia lakini alishikwa na kachero Mzengwa na kushindwa kukimbia. “Vipi Brother?” alilalamika ili aachiwe. “Tulia,” Kachero Mzengwa alisema kwa sauti ya amri. Baada ya gari kusimama Side alipakiwa na gari lililokwenda moja kwa moja hadi kituo cha makosa ya jinai. Waliteremka na kuingia naye kwenye chumba cha mahojiano. Kwa vile Side alikuwa na wasiwasi sana kachero Mzengwa alimuagizia soda ya baridi kwanza. Baada ya kutulia alianza kumuhoji. “Side ondoa wasiwasi hutafanywa kosa lolote ila nahitaji msaada wako,” Mzengwa alianza kwa kumtoa wasiwasi. “Msaada gani?” “Anko Jay Jay alikuwa nani yako?” “Rafiki yangu sana.” “Kabla ya wewe kwenda shamba alikuwa na dili gani?” “Mmh! Nakumbuka alipewa kazi na dada mmoja ya kumfuatilia mume wake.” “Mume wake alikuwa na tatizo gani?” “Alikuwa na wasiwasi anatembea na mwanamke mwingine.” “Mmh! Baada ya hapo nini kiliendelea?” “Aliniambia amegundua kweli yule mwanaume alikuwa na mwanamke kampangia hotelini.” “Baada ya hapo?” “Alipomaliza kazi yake alilipwa chake na mimi kesho yake nilisafiri, nikiwa bushi nilipopata taarifa za kushtusha kuwa mchizi wangu Jay ameuawa,” Side alisema kwa uchungu. “Unakumbuka huyo mwanamke alikuwa amepangiwa hoteli gani?” “Gorden Crest.” “Na hiyo mwanamke unamjua?” “Kwa kweli sikuwahi kumuona.” “Sehemu anapokaa unapajua?” “Ni Isamilo lakini nyumba siikumbuki vizuri kwa vile tulikwenda usiku ila nakumbuka nilimsubiri sehemu na kuingia kwenye nyumba yenye geti.” “Hukumbuki hata kidogo?” “Nikifika nitaijua japo sikuangalia vizuri siku tuliyokwenda.” “Nafikiri twende muda huu ukatuoneshe hiyo nyumba.” “Sawa.” Walikubaliana kwenda kuitafuta nyumba ya mwanamke aliyempa kazi Anko Jay Jay ambayo waliamini anaweza kuhusika kwa asilimia kubwa katika mauaji yale. ***** Majira ya saa kumi na mbili za jioni Land Cruser ilitembea taratibu katika mitaa ya Isamilo. Walilipaki sehemu na kuteremka kisha kutembea taratibu kufuata mtaa ambao Side alikuja siku moja na marehemu Anko Jay Jay kufuata malipo ya kazi aliyopewa ya kumchunguza mume wa mtu. Sehemu aliposimama kumsubiri ilimchanganya kidogo kutokana na nyumba zile kufanana kidogo katika nyumba aliyoingia Jay. “Vipi umeikumbuka?” kachero Mzengwa alimuuliza. “Kati ya nyumba hizi mbali moja wapo, sikumbuki nilisimama wapi kwa vile ilikuwa usiku.” “Joe unasemaje?” Mzegwa alimuuliza mwenzake. Kabla hajamjibu lilikuja gari na kusimama kwenye nyumba moja kati ya zile mbili na kupiga honi. Baada ya muda alitoka mama mmoja mwenye mwili mkubwa kufungua geti huku akisema: “Mume wangu leo nimekuwa mlinzi.” “Mlinzi yupo wapi?” “Nimemtuma mara moja.” Baada ya kufungua geti gari lilingia ndani na kulifunga, baada ya kufungwa geti Side alisema: “Itakuwa nyumba hii.” aliionesha nyumba jirani na gari lilipoingia gari. “Kwa nini?” “Jay alinieleza yule mwanamke anaishi na mume na mtoto mchanga hii inaonekana wenye nyumba ni watu wazima pia nyumba ile alinieleza haina mlinzi.” “Una uhakika?” “Ndiyo ni nyumba hii.” “Basi tuondokeni tukajiandae kuja usiku nina imani kazi itakuwa si ngumu sana.” “Na huyu?” Joe aliuliza kuhusu Side. “Huyu tutakuwa naye mpaka zoezi la leo usiku liishe kisha atarudi kwake.” Walirudi kwenye gari lao na kurudi ofisini kwa ajili ya operesheni ya kumtia mikono Kilole ambaye waliamini ndiye aliyekuwa akijua kila kitu juu ya kifo cha msichana aliyeuawa Gorden Crest na Anko Jay Jay japokuwa hawakujua muuaji ni nani, lakini waliamini kumtia mikononi yule mwanamke angewasaidia upelezi wao kwa kiasi kikubwa. ***** Deus baada ya kuikagua siraha yake alisogea mpaka karibu ya dereva teksi Abdul aliyekuwa amezama kwenye penzi na mwanamke wa usiku. “Mzee vipi?” Deus alimshtua Abdul. “Poa mkuu.” “Naona upo kazini?” “Hapana nimemwita huyu baada ya kuona maboweka.” “Njoo basi nje mara moja.” Walitoka mpaka nje pamoja hadi ya cassino. “Vipi mzee?” Abdul alimuuliza Deus akimtazama usoni. “Mose unafahamiana naye sana?” “Kiasi ila tunaelewana sana.” “Kuna kazi nataka kukupa ukiifanya vizuri nitakupa fedha nzuri.” “Kazi gani mkubwa?” “Nina shida Mose ila nataka ukamtoe bila wapambe wake kuja nina mazungumzo naye.” “Hilo mbona dogo.” “Lakini usimwambie kama kuna mtu anamwita.” “Hiyo kazi niachie mimi, akili yangu ukisikia fedha huwa haishindwi na kitu chochote hata kumfukua marehemu.” “Basi nifanyie hiyo kazi mara moja, ila ukija hakikisha wewe unasimama huku na yeye huku.” “Hakuna tatizo bosi wangu.” Abdul aliingia ndani mara moja hadi kwenye meza za kamali na kumkuta Mose bado kashikilia bunda la dola akisubiri kuingia kucheza kamali. “Mose,” Abdul alimwita alipomkaribia. “Unasemaje Brother Abby?” “Samahani nakuomba mara moja.” “Una shiga gani brother? Zungumza nakusikiliza.” “Naomba tutoke nje mara moja.” “Si unajua muda wangu wa kuingia kwenye gemu umekaribia, jana walinila leo nina usongo nao,” Mose alijitetea ili asiende mbali. “Dakika tano tu, waachie washikaji wakushikie unarudi sasa hivi.” “Paul shika mkwanja huu narudi.” “Poa mkubwa.” Walitoka hadi sehemu ya kupakia magari, Deus alipomuona anakuja alizunguka nyuma ya gari. Walichomoa bastora tayari kwa tukio, walipofika walisimama Mose akiwa amempa mgongo Deus kama alivyomuelekeza Abdul. Aliiweka bastora yake tayari na kumsogelea taratibu hadi waliposimama na kumwekea bastora Mose kisogoni huku akisema kwa sauti ya chini yenye amri. “Fungua mlango wa mbele wa gari na uingie ndani bila kuleta ujanja la sivyo nitakufumua ubongo.” “Mheshimiwa vipi?” Abdul alishtuka kuona Deus ameshikilia bastora. “Sitaki swali nawe ingia upande wako mara moja.” Abdul hakutaka kubishana alizunguka upande wake na kuingia ndani na Mose naye alifanya kama alivyoelekezwa. Deus aliingia mlango wa nyuma na kusema kwa sauti ya amri. “Elekea baharini mara moja.” “Sawa,” Abdul alijibu huku akiwasha gari na kuondoka. “Kaka mkubwa nimefanya nini?” Mose aliuliza kwa sauti ya upole. “Utajua muda si mrefu.” Gari lilitoka hoteli ya Piedimonte San Germano na kuingia barabara kubwa na kuelekea upande wa baharini. “Abdul nataka gari likimbie kama linapaa,” Deus alitoa amri ya kijeshi. “Hakuna tatizo mkubwa.” Abdul alibadili gia na kukanyaga mafuta na kulifanya gari liondoke kwa mwendo wa kasi. Kabla ya kulivuka daraja refu gari la kina Mose lilikuja nyuma kwa kasi na kuwavuka na kusimama mbele yao kwa ghafla na kumfanya Abdul kufunga bleki kwa nguvu zote. Lakini gari lao liliseleleka na kwenda kuligonga gari la kina Mose wakati huo wapambe wa Mose walikuwa wametoka ndani ya gari na bastora mkononi tayari kumsaidia bosi wao. Deus akili ilimchemka na kuona kafanya makosa ya kutoka naye mbali sana, lakini aliamini atapambana nao mpaka tone la mwisho la damu yake japokuwa alikuwa peke yake akipambana na kundi la zaidi ya watu sita wote wana siraha. Deus naye kwa wepesi wake alitoka nje na kujificha nyuma ya teksi ya Abdul ambaye alikuwa hajui afanye nini. Wapambe walikuwa amekwisha ivamia gari na kumtoa bosi wao. Jamaa aliyetupwa juu ya gari na Abdul naye aliona ile ndiyo sehemu ya kulipa kisasi kwa Abdul. Bila kuuliza alimjaza Abdul risasi za kichwa mpaka alipoamini amekata roho na kichwa hakitamaniki. “Jamani mbaya wetu asikimbie,” Mose alisema kwa sauti ya juu. “Hatoki lazima tumtie mikononi.” “Nataka tusimuue tumshike akiwa hai,” Mose alitoa amri wa wapambe wake. “Huyu hatoki hapa.” Ilikuwa kauli ya kumuunga mkono Mose ambaye alikuwa na hasira na Deus. Deus aliinama kwa chini ili asionekane, wakati huo risasi zilikuwa zikirindima sehemu aliyojificha naye alijitahidi kujihami kwa kurudisha mashambulizi. Risasi ya bega iliyompata Deus ilimfanya adondoshe bastora chini. Alipotaka kuiokota kwa mkono cha kushoto alikuwa amechelewa teke zito lilitua usoni kwake na kumrudisha nyuma.
Hakutaka kufa kikondoo alipambana kiume kwa kutumia mkono mmoja na mateke. Alijitahidi kuwadhibiti huku Mose akiendelea kuwakataza wenzake kutotumia siraha ili kumkamata akiwa hai. “Jamani tusimuue lazima tujue nani kamtuma,” Mose alipaza sauti. “Bosi usiwe na wasi atalegea muda si mrefu.” Kauli ile ilimpa nguvu Deus ya kuendelea kupambana huku akishangaa ujasiri wa Mose wa kuwakataza wenzake wasitumie siraha na kuendelea kupambana kwa mikono. Kitu kizito kilichompiga Deus kisogoni kilimpoteza fahamu na kuanguka chini kama mzoga. Mose na vijana wake kwa haraka alimchukua Deus na kumweka kwenye gari lao na kuelekea naye baharini. “Mkuu wapi hii?” mmoja wa wapambe wake aliuliza. “Huyu lazima tukamhoji bahari baada ya kupata ukweli tunamuua na kumtupia majini ili kuondoa ushahidi, pia inatakiwa usiku huu tuondoke Sicily twende Torino kwa muda ili sakata ili lipite lazima watatulitilia mashaka kwa vile gari letu linaweza kuonekana kwenye kamera zao.” “Hakuna tatizo.” Walimbeba Deus kuelekea ufukweni kwa ajili ya kumhoji na kumuulia mbali. ****** Kilole baada ya kufanikiwa kuwapata vijana waliomchimbia shimo nyuma ya nyumba. Aliwalipa ujira wao na kusubiri muda wa usiku auzike mwili wa mpenzi wake Kinape aliyemuua kwa bahati mbaya wakati wakigombea bastora. Akiwa amesimama kwenye uzio kwa ndani aliona watu wakielekezana nyumba yake, ile ilimtisha sana na kuona bwawa linaweza kuingia luba. Mapigo ya moyo wakiwa yana mwenda mbio alitulia akiwachungulia awaone wanataka kufanya nini. Baada ya muda aliwaona wakiondoka, alijikuta akijiuliza watu wale walikuwa na shida gani. Baada ya kuondoka alirudi ndani na kutafuta pombe kali na kunywa ili kupunguza maumivu ya moyo baada ya kumuua mtu muhimu maishani mwake. Majira ya saa tatu na nusu usiku Kilole alitoka mpaka nje ya geti kuangalia hali ya hewa ambayo ilikuwa tulivu. Aliamini hakukuwa na mtu aliyekuwa akimtilia mashaka alirudi hadi ndani na kwenda moja kwa moja chumbani na kuufunga vizuri mwili wa mpenzi wake katika shuka ambao ulikuwa amepoa na kuanza kukauka. Aliuvilingisha shuka kisha aliuvuta mpaka chini na kuanza kuburuza kuupeleka nje kwenye shimo. Aliuburuza mwili hadi nje na kupumua kidogo kutokana na uzito wa mwili wa mpenzi wake. Alijifuta jasho kwa mkono kisha aliendelea kuuvuta mpaka karibu na shimo ili autumbukize na kuufukia. “Hapo hapo… Upo chini ya ulinzi,” Sauti kali ya amri ilimshtua Kilole na kumfanya adondoke chini kwa hofu. Alipoangalia aliwaona watu zaidi ya wanne wakiwa na silaha mkononi. “Unafanya nini?” sauti kali ilimuuliza. “Si.si..si..” Kilole aliingiwa kigugumizi huku haja ndogo ikimtoka kwa hofu. “Unaburuza nini?” “Jamani bahati mbaya sikukusudia.” “Hukusudia nini?” “Jose mbona kama mtu huyu?” Kachero Mzengwa aliuliza baada ya kuuona kilichokuwa kikiburuzwa kilikuwa kama mtu. Wakitumia tochi kukichunguza kilichokuwa kikiburuzwa na Kilole, askari aliyeimana kuangalia alisema kwa sauti ya juu. “Ha! Mtu?” “Eti?” walishtuka. “Bwana we, mwili wa mtu huu.” “We mwanamke unaupeleka wapi huu mwili?” “Samahanini jamani…ba..ba..ha..” “Huyu nani?” “Mu.mu..mu..me ..wa..wa..ng…” Presha ya Kilole alikuwa kubwa sana kiasi cha kumfanya aishiwe nguvu na kupoteza fahamu. Walimpatia huduma ya kwanza lakini haikusaidia waliteuliwa askari wawili kumuwahisha Kilole hospitali ya Seko Toure katika ulinzi mkali. Kabla ya kuupeleka mwili wa marehemu hospitali walifanya upekuzi kila kona ya nyumba ile. Ndani ya nyumba waligundua vitu vingi vikiwemo vifaa vya Kilole vya kufanyia mauaji. Pia bastora na risasi vyote vilivyokutwa ndani. Baada ya kukamilisha upekuzi walimchukua mtoto wa Kilole aliyekuwa amelala hajui lolote ili kumpeleka kwa mama yake. Mwili wa marehemu waliupeleka hospitali ya Seko Toure kwa ajili ya uchungu kabla ya kufanya taratibu zote za kuwatafuta ndugu wa marehemu. Baada ya taratibu zote walimpeleka mtoto kwa mama yake wadini, walimkuta Kilole ameamka akiwa amejilaza mkono wake mmoja ukiwa na pingu iliyofungwa kwenye kitanda alicholala. Aligeuka na kuwangalia askari na mtoto wake na kujikuta akiangua kilio, mtoto wake naye aliamka na kuanza kulia ilibidi anyanyuke na kunyonyesha ili anyamaze. **** Deus alipepesa macho kuangalia sehemu aliyokuwepo alishtuka na kujiuliza pale alikuwa akiota au kweli. Alirudisha kumbukumbu kilimtokea mara ya mwisho ni kweli huku akijipapasa, mkono wake ulitua kwenye bega la mkono wa kulia na kukutana bandeji. Alizidi kushtuka aligeuza shingo taratibu na kukutana na tabasamu pana. “Pole mpenzi,” sauti tamu ya Teddy ilitua kwenye ngoma za masikio ya Deus. “Teddy!” Deus alimwita akiwa bado anajipapasa. “Abee mpenzi.” “Ninachokiona mbele yangu ni kweli au naota?” “Huoti mpenzi ni kweli mpenzi.” “Hapana hii ni ndoto tu,” alisema huku akirudisha mkono kwenye bandeji na kuanza kukandamiza kwa nguvu. Lakini Teddy aliwahi kumshika mkono. “Deus unataka kufanya nini?” “Teddy hii ni ndoto tu.” Alipoangalia pembeni alimuona mwanaye kipenzi Rose akiwa amelala usingizi, alizidi kujishangaa. “Hapa ni wapi?” “Ndani ya ndege,” Teddy alimjibu huku akimshika mkono aliouondoa kwenye jereha na kuanza kuupapasa taratibu. “Ndani ya ndege! Tunatoka wapi na tunakwenda wapi?” “Tunatoka Italia na tunarudi Tanzania.” “Hapana…Hapana hii ni ndoto si kweli,” Deus alizidi kukataa. “Kwa nini mpenzi?” “Teddy nimekuacha Tanzania umefikaje Italia na umewezaje kuniokoa kwenye kinywa cha mauti?” “Ni historia ndefu naomba kwanza tufike nyumbani, la muhimu mshukuru bwana Mungu wako kwa kukuwezesha kuendelea kuvuta pumzi yake mpaka muda huu.” Pamoja na kuelezwa yote bado Deus aliamini ile ni ndoto kutokana na hali aliyokutananayo ya kuwa ndani ya kinywa cha mauti. Pamoja na kuamini ile ni ndoto lakini bado hakujua yupo wapi japokuwa ndoto ilimuonesha yupo sehemu salama. Teddy aliamini kabisa Deus yupo katika wakati mgumu kuamini kilichomkuta na sehemu aliyokuwepo ilibidi amrudishe katika hali ya kawaida. “Deus,” alimwita kwa sauti ya chini huku akitembeza mkono yake kichwani kwa Deus aliyekutana na joto la kumsisimua. Deus hakuitika japo alisikia akiitwa aligeuza shingo na kumtazama Teddy aliyekuwa amekaa pembeni yake akitembeza mikono yake taratibu. “Deus, najua ni vigumu kuamini hali iliyokutokea na sehemu uliyopo sasa ndiyo inakuchanganya sana.” “Hapana Teddy si hicho.” “Nini sasa kinachokufanya usiamini kama ni kweli?” “Mimi na wewe tumeachana lini?” “Juzi usiku.” “Wapi?” “Dar.” “Ukijiandaa kwenda wapi?” “Mwanza.” “Huoni kuwa mbele yangu ni ndoto usiyokubalika?” Deus alisema akiwa amemkazia macho. “Deus mpenzi wangu, najua hicho ndicho kinacho kutatiza, ni kweli uliniacha Dar lakini sikwenda Mwanza kama nilivyo kuahidi bali nilikufuata Italy.” “Muongo!” “Kweli mpenzi wangu, sema tu tumeomdoka ndege tofauti ya Italy mimi ndiye niliyewahi saa moja kabla yako niliondoka na ndege ya Fly Emirates.” “Teddy mi si mtoto mdogo wa kudanganywa namna hiyo, Italy si sawa na kutoka Ubungo kwenda Kariakoo, kuna maandalizi yake hasa kutoka nje ya nchi kuna taratibu zake si za saa zaidi siku nzima hata siku mbili.” “Ndiyo maana nikakueleza ni historia ndefu, moyo wangu haukukubali kukuamini moja kwa moja uende peke yako. Nilichowaza ndicho kilichotokea bila kufanya hivyo lazima ungekufa na mimi kusakwa mpaka kukamatwa kisha kuuawa kifo kibaya sana namjua vizuri sana Mose ana roho mbaya sana.” “Mmh! Bado siamini.” “Kweli Deus moyo wangu ulikataa kukuacha peke yako kwa vile namjua vizuri Mose. Nilijua kama ningekueleza tuongozane ungekataa hivyo nilifanya mipango yangu kwa siri bila wewe kujua ulipofika Italy nilikufuatilia kila hatua.” “Uliwezaje kuniokoa katika kundi la vijana hatari kama wale?” Deus alikubaliana na hali halisi ilibidi awe mpole. “Kwa vile niliwahi kufika Italy nilisubiri wageni watakaoingia na ndege uliyopanda na kuweza kukuona. Kabla sijaja niliwasiliana na mtu mmoja katika kampuni ya magari ya kukodi aniandalie gari atakalo liweka uwanja wa ndege na kunieleza lipo sehemu gani. “Nilipofika nililikuta aliponielekeza likiwa katika hali nzuri, nililikagua na kukuta lipo kama nilivyoitaka. Huwezi kuamini nilikuwa tayari kwa lolote niliamini kama sikufa mimi basi Mose.” “Na Rose?” “Rose nilimuacha Hotelini.” “Hoteli gani?” “Liola Hotel (Aquino.” “Muongo si ndiyo hoteli niliyopanga mimi?” “Nilibahatisha kati ya hoteli mbili, niliamini utapumzika lakini sikukuamini bado nilikufuatilia kwa kukaa mapokezi. Ulipotoka nilikufuatilia mpaka Piedimonte San Germano bila wewe kujua. Hata uliporudi bado nikuwa na wewe mpaka mlipokutana na Mose na kundi lake bila wewe kumjua Mose haraka . “Ilionekana ulimtambua na baada ya kashikashi ndogo mliachana nao kisha niliona mkiwafuata hapo ndipo nilipojua shughuli imeanza. Mpaka unamteka Mose na kuondoka naye niliamini umefanikiwa lakini kuna mpambe mmoja aliona mchezo ule na kuwafuata wenzake ndani. “Hapo ndipo nilipojua kazi imeiva, niliwaacha watangulie nami niliwafuata nyuma huku moyoni nikijiapia ama zao ama zangu. Nikiwa kwa mbali niliona mchezo mzima. Lazima nikusifu wewe ni mwanaume wa shoka mpaka kukushinda walitumia nguvu ya ziada. “Sikuweza kuingilia mapigano yenu baada ya kuanguka moyo uliniuma sana mpaka machozi ya uchungu yalinitoka nikajua wamekumaliza. Walipo kuchukua na kuondoka na wewe sikujua wanakupeleka wapi, niliwafuatilia na kuwaona wanakupeleka ufukweni. “ Kwa vile sehemu ilikuwa ya uwazi niliwaacha niwaone wanaenda wapi. Nilipowaona wamesimama niliamua kuwafuata kwa kuingia ndani ya maji. “Namshukuru Mungu nilikuwa mtundu toka nilipoingia kwenye kazi hii ya hatari. Niliogelea hadi karibu yao na kutokeza kwa taratibu na kuwaona wanakumwagia maji uamke. Nilitumia nafasi ile kuwaua wote kwa risasi kisha nilitoka na kukuta hujafa ila una jeraha la risasi begani. “Nilitumia gari lao kukubeba mpaka nilipopaki langu na kukuhamishia kwenye gari langu. Nilikupeleka kwa daktari wangu ambaye alikushughulikia na kusema huna tatizo kubwa zaidi ya jeraha tu. Nilitaka nisafiri naye mpaka Tanzania lakini alisema hakuna sababu ya yeye kusafiri na sisi kwa vile huna tatizo kubwa sana. “Kwa vile nilijua kimenuka sikuwa na jinsi ilibidi nikodi ndege kwa gharama kubwa sana ili kuhakikisha usiku uleule tunaondoka Italy. Nilimfuata Rose hotelini na kuondoka mpaka uwanja wa ndege kisha tukaondoka. Hivi ninavyozungumza tuna saa sita tupo angani toka tutoke Italy.” “Kwa hiyo Mose umemuua?” “Yeye ndiye wa kwanza nilimpiga risasi tatu za kichwa kisha wenzake. Yaani hakuna siku niliyofurahi kama leo,” Teddy alisema kwa furaha huku akiubusu mkono wa Deus aliyekuwa bado amegandisha macho kwake. Imauhakika gani kama Moses amekufa?” “Baada ya kutoka ndani ya maji nilichukua bastora yake iliyokuwa na risasi kumi na kukisambaratisha kichwa chake kama atakuwa mazima tena basi nitajua ni mzimu.” “Kwa hiyo kazi yangu imekuwa ya kitoto?” Deus aliuliza kiunyonge. “Hapana mpenzi, kazi uliyofanya wewe ilikuwa kubwa sana mimi nimemalizia tu, nisingeweza kupambana na mijitu kama ile ambayo umeitoa jasho.” “Unafikiri kwa nini Mose hakutaka kuniua?” “Nina imani alitaka kujua umetoka wapi na nani kakutuma, anaamini mtu wa pale hawezi kumfanyia kitendo kama kile.” “Baada ya kunihoji nini kingefuata?” “Baada ya kupata ukweli wangekuua na kukutupia baharini.” “Nashukuru sana Teddy kuyaokoa maisha yangu.” “Nikushukuru wewe mpenzi kwa kuyatoa maisha yako kwa ajili yangu, Deus sijawahi kuona mwanaume mwenye mapenzi mazito na mimi kama wewe umekubali kuyatoa maisha yako kwa ajili yangu, umekubali kupoteza kazi yako kwa ajili yangu. Sina cha kukulipa zaidi ya kukuahidi upendo wa dhati na maisha mazuri mpaka kufa kwako, nife unizike ufe nikuzike.” “Nashukuru kwa kulitambua hilo, ila nami nina kazi yangu.” “Ipi?” “Ya kumsaka Kilole na Kinape.” “Nitakusaidia mpenzi wangu mpaka tuwatie mkononi na hakuna hukumu nyingine zaidi ya kifo.” Ndege iliingia Dar es salaam Tanzania majira ya saa tano usiku, Deus alichukuliwa na kupelekwa kwenye moja ya jumba lililokuwa likitumiwa na kikundi cha wauza dawa za kulevya ambalo lilikuwa lipo mikononi mwa Teddy ambalo alilikimbia kumkimbia Mose lakini baada ya kumuua hakuwa na wasiwasi tena na lilikuwa kwenye hali nzuri. Alimpigia simu daktari wao ambaye alifika kumhudumia Deus aliyekuwa na jeraha ambalo lililonekana lipo katika hali nzuri hakutakiwa kupewa huduma zaidi alitakiwa kupumzika.
Siku ya pili Deus wakiwa sebuleni amejilaza kwenye sofa akiangalia tivii taarifa ya habari ya saa sita mchana. Deus alishtuka kumuona Kilole akiwa anatoka mahakamani chini ya ulinzi. Macho yalimtoka kumuona mbaya wake akiwa mikononi mwa chombo cha dola. Alijikuta akinyanyuka na kukaa kitako huku macho yakemtoka pima, mtangazaji alisema kesi ile itaendelea tarehe iliyopangwa kufikishwa tena mahakamani kusikizwa kesi yake ya mauaji ya watu wa tatu. Mwanamke mmoja aliyekuwa akifanya kazi katika kampuni za kitalii mkoani Arusha aliyefahamika kwa jina la Happy pia mvulana mmoja aliyekuwa akifanya kazi za misheni tauni aliyefahamika kwa jina maarufu Anko JayJay pia mwanaume mwingine aliyefahamika kwa jina la Kinape ambaye inasadikiwa alikuwa mumewe wote aliwaua kwa risasi. “Vipi mbona unaoneka umeshtuka na kukaa kitako wakati nimekueleza hutakiwi kuimana kwa mbele?” Teddy alimuuliza Deus baada ya kutoka chumbani na kumkuta amekaa kitako tofauti na alivyomuacha akiwa amejilaza. “Aisee Kilole,” Deus alijibu kama anatoka usingizini. “Kafanya nini?” “Kumbe alikimbilia Mwanza, ameua.” “Ameua?” “Ndiyo, yupo mikononi mwa polisi ana kesi ya mauaji ya watu watatu.” “Mauaji?” “Ndiyo, ha..ha..rafu kuna jina sijaelewa vizuri sijui nimesikia vibaya.” “Jina gani?” “La Kinape.” “Limefanya nini?” “Ameuawa na Kilole.” “Utani huo, si ndiye aliyeondoka naye kamuua kwa kosa gani?” “Kwa kweli sijui kitu ila katika majina ya watu aliyowaua nimesikia jina kama hilo lazima atakuwa yeye kwa vile wamesema ni mume wake.” “Kesi ipo wapi?” “Mwanza.” “Umesema imeahirishwa mpaka lini?” wakati huo Teddy alikuwa akimlaza Deus kwenye sofa taratibu asimtoneshe jeraha. “Hata najua baada ya kuiona picha ya Kilole nimechanganyikiwa.” “Kwa vile umejua yupo Mwanza kazi hiyo niachie mimi.” “Hapana tusimuue nzi kwa nyundo wakati kajifia mwenyewe.” “Kwa nini unasema hivyo?” “Yule yupo chini ya mikono ya dola pia kesi yake ni nzito lazima atanyongwa kwa nini tutumie nguvu tukikosea mahesabu tuanze kukimbia upya.” “Deus watu wale hawaaminiki anaweza kupona kimaajabu na kuanza kutusumbua. Nitamuua kwa mahesabu makali sana hakuna mtu atakayejua. Japokuwa najua kakuumiza lakini ndiye chanzo cha matatizo yote yako na yangu.” “Mpenzi hebu kwanza tuiache mahakama ifanye kazi yake kisha tutajua tufanye nini?” “Kwa hiyo tarehe ya kufikishwa mahakamani huijui?” “Itabidi uulizie Mwanza.” “Hakuna tatizo,” Teddy alisema huku akichukua simu na kupiga sehemu aliyokuwa amepanga. “Haloo.” “Haloo Juma mambo vipi?” “Poa sister.” “Eti Juma kuna mwanamke anashtakiwa kwa makosa ya mauaji hapo jijini?” “Ndiyo dada, leo alipandishwa kuzimbani kwa mara ya kwanza.” “Tarehe ya kurudi unaijua?” “Mmh! Hebu subiri nikuulizie usikate simu.” “Hakuta natatizo,” Teddy alisubiri baada ya muda sauti upande wa pili ilisema. “Mpaka tarehe 22 ya mwezi ujao.” “Asante.” “Upo wapi dada?” “Nipo Dar.” “Utarudi lini?” “Nitakujulisha.” Teddy alikata simu na kumueleza Deus tarehe ya Kilole kupandishwa tena kizimbani. “Nina imani mpaka siku hiyo nitakuwa nimepona.” “Kwa hiyo tutakuwa mahakamani siku hiyo?” “Itakuwa vizuri.” *** Siku ya kupandishwa tena kizimbani Kilole ilifika, mahakama ilikuwa imejaa kusikiliza kesi ya mauaji yaliyotikisa jiji la Mwanza mwanamke mwenye vazi refu jeusi. Deus, Teddy na mtoto wao Rose walikuwa miongoni mwa watu waliokuwepo mahakamani pale. Baada ya hakimu kuingia na kukaa kwenye kiti chake na watu wote waliokuwa wamesimama kuelezwa wakae chini mahakama ilianza. Kesi ilianza mara moja kwa kuitwa kesi ya kwanza ilikuwa ya uchomaji wa nyumba na kusababisha mauaji ya mtu mmoja na uhalibifu wa mali. Mtuhumiwa alisomewa shtaka na kurudishwa rumande bila kujibu kitu. Kesi ya pili kutajwa ilikuwa ya Kilole. Kama kawaida alitoka rumande na kupandishwa kizimbani. Alipanda taratibu akiwa ameinama huku moyoni akijutia kitendo cha kuua mpenzi wake Kinape bila kukusudia. Baada ya kupanda alisimama na kutulia kusubiri kusomewa mashtaka. Akiwa ameangalia chini kusubiri kusomewa mashtaka yake kwa mara ya pili, kwa vile hakutakiwa kujibu lolote mpaka upelelezi utakapokamilika alitulia kusubiri kusomewa ili arudishwe rumande. Akiwa ameangalia chini alinyanyua macho yake taratibu na kuwaangalia watu waliokuwa mahakamani. Macho yake yalipogongana na Deus, alishtuka na kuyarudisha tena sura ilikuwa ileile ya Deus mtu anayejua amekwisha kufa. Aliyatuliza macho yake huku mapigo ya moyo wakienda kwa kasi, alijiuliza anaota au ni kweli. Akili yake anajua Deus aliisha kufa yule aliyesimama mbele yake ni mzimu wake au nani. Kingine kilichomchanganya zaidi kilikuwa mwanamke aliyekuwa amekaa naye ambaye alikuwa akimkisia ni mpenzi wa Deus, alikuwa pembeni yake na mtoto wake Rose. Pale ndipo alipoamini yule ni Deus ambaye alidanganywa amekufa kumbe alikuwa hai. Hata alipoanza kusomewa mashtaka akili haikuwa pale yote ilikuwa kwa Deus na kujiuliza ni kweli au yupo ndotoni. Alijaribu kujifinya alihisi maumivu na kugundua si ndoto ni kitu cha kweli. Moyoni alijiapiza kwa vile alijua kesi ile hawezi kupona lazima atanyongwa kutokana na ushahidi wote aliamini ile ndiyo nafasi ya pekee ya kutimiza azima yake ya kumuua Deus. Alimuangalia askari aliyekuwa pembeni yake ametulia akiangalia watu. Alipoangalia kiunoni kwake aliiona bastora amekaa kihasarahasara. Alipiga hesabu zake na kuamini ataipata na kufanya mauaji ya mwisho mulemule mahakamani kabla ya hukumu yake ya kunyongwa. Baada hesabu zake kukamilika alichomoka kama mshale na kumpiga kikumbo askari mpaka chini na kuipokonya bastora iliyokuwa kiunoni. Kwa wepesi wa ajabu aligeukia upande alipokuwa amekaa watu waliokuwa wamekaa watu sehemu yaliyokuwepo wabaya wake. Deus na Teddy kwa pamoja waliliona tukio lile na wote kulala chini, watu wengine nao wamelala chini kuhofia kupigwa risasi. Kuchanganyikana na watu ilimpa Kilole wakati mgumu kuwapiga risasi wabaya wake. Kwa hasira alipiga risasi mfululiza eneo waliokuwepo na kuua watu ovyo na wengine kuwajeruhi. Askari aliyepigwa kikumbo na kunyang’wa bastora, alinyanyuka kishujaa baada ya Kilole kumpa mgongo. Alimvaa na kuanguka naye chini. Kwa wepesi wake aligeuza batora na kumpiga yule askari kifuani. Hali ya mahakamani ikawa tafrani kila mmoja alishikilia roho yake kutokana na milio ya risasi. Teddy akiwa amejilaza alitoa bastora kwa siri na kumlenga Kilole sehemu ya kichwa ili ammalize kabisa. Wakati huo Deus alikuwa ameisha muona Teddy anataka kufanya nini, kabla hajafyatua alimsukuma kwa miguu na risasi aliyopiga Teddy ilimkosa Kilole na kwenda kupiga ukutani. Wakati huo askari wa kikosi maalumu walikuwa amefika kwa vile Kilole alikuwa amepagawa askari mwenye shabaha alimpiga risasi ya bega aliloshika bastora na kuidondosha na kuwapa nafasi ya kumvamie. Kilole aliyekuwa akitokwa na damu begani huku akipiga kelele wamuue kabisa aliwekwa chini ya ulinzi mkali. Askari walisaidia kuondoa maiti za watu watatu na askari mmoja na majeruhi zaidi ya ishirini. Mahakama haikuweza kuendelea ilibidi iahilishwe kutokana na tukio lile zito. Wakiwa nje ya mahakama baada ya kukamatwa Kilole na kuwekwa chini ya ulinzi mkali. Teddy alimlaumu Deus kumkanyaga wakati alijua ile ndiyo ilikuwa nafasi ya kumuua mbaya wao bila tatizo. “Deus umefanya nini?” “Hapana, haikuwa na haja kulipa baya kwa baya.” “Deusiiii! Angetuua huoni kama alitukusudia?” “Ni kweli lakini bado siamini natakiwa kumhukumu kifo.” “Kwa nini Deus?” “Kesi aliyonayo bado ni hukumu nzito kumbuka kaua watu wengi na leo ameongeza kosa lingine la kuua watu wengine mahakamani.” “Deus hayo hayaniingii akilini, tulikubaliana tumfanye nini?” Teddy alimuuliza huku machozi yakimtoka. “Teddy unanipenda?” Deus alimuuliza akiwa akimkazia macho. “Tena sana mpenzi wangu wewe kwangu ni kila kitu.” “Basi nakuomba nisikilize mimi, tuachane na Kilole nina imani nisingefurahi kumuona anakufa mbele yangu. Sitakiwi kuwa na roho ya kisasi kwa vile Rose ni mwanangu mtoto wa Kilole.” “Lakini si alikusudia kuua?” “Ni kweli, tushukuru Mungu tumepona.” ***** Kilole alipelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu ya jeraha la bega kisha hospitali ya wagonjwa wa akili ili kupimwa akili. Baada ya matibabu na vipimo vyote Kilole alikutwa akili yake ipo timamu hivyo alipandishwa tena kizimbani baada ya kupona jeraha katika ulinzi mkali. Kesi yake haikuchelewa alihukumiwa jela maisha na kazi ngumu. Teddy alioana na Deus na kuwa mke na mume Rose alilelewa na Teddy ambaye tayari aliishajua ndiye mama yake wa kumzaa huku akisubiri wa kwake kuongeza familia. Waliamua kuhamishia maisha yao Mwanza na kufungua miradi na Teddy kuachana na biashara ya dawa za kulevya.
Simulizi : Kitanzi, Kisu Na Bastola Sehemu Ya Kwanza (1)
ANATEMBEA akiwa anapepesuka kwa ulevi uliomjaa kichwani. Amelewa chakaliii, pombe zikimdanganya na kumfanya asiwe na hofu hata kidogo kukatiza kona hatari za mitaa ya Songasonga. Laiti kama angekuwa na akili zake timamu asingediriki hata kuwaza kupita peke yake usiku huo kwa kuwa anazijua vema sifa za mtaa wake. Roba za mbao, ubakaji na mara nyingine kesi za mauaji ndiyo mambo makubwa yanayozifanya hata serikali za mitaa na wilaya ziuangalie kwa jicho la tatu pekee mtaa huo. Lakini usiku wa leo, saa nane hiyo, Dedan Magesa anapita bila wasiwasi wowote, mkononi akiwa amekumbatia kopo la pombe ya kienyeji maarufu kama mataputapu. “Muuuvu bichii geliatu weiii. Muuuvu bichii geliatu weiii,” alijiimbia wimbo wake aliokuwa akiurudiarudia kiitikio tu tena kwa sauti mbaya ya kilevi kinachotia kichefuchefu hata kukisikiliza. Taratibu Magesa aliyoyoma akipita karibu kabisa na kona na vichochoro kadhaa vyenye sifa mbaya sana za uhalifu. Kama vile mkono wa Mungu ulikuwa juu yake siku hiyo, alifika nyumbani salama salimini. Akafungua na kufunga mlango wa chumba chake kwa umakini mkubwa kisha akajitupa kitandani kwa nguvu na kulala fofofo akiwa na viatu na nguo zake zote. Kwa mbali kabisa, moyo wake ulilia na kuomboleza. “Uko wapi mpenzi wangu, kwa nini umeniacha peke yangu leo? Ina maana hukunipenda hata kidogo kiasi cha kuamua kunifanyia hivi? “Najua sitampata msichana mwingine mzuri kama wewe…Ooh Carolina! Nini nimefanya hadi kustahili adhabu hii?”
*** Asubuhi iliyofuata, Dedan aliamka kama kawaida yake na kufungua ofisi yake, kibanda kidogo pembezoni mwa nyumba kubwa aliyopanga, akiuza vifaa vya simu, kuchajisha simu, kutengeneza na kuingiza nyimbo kwenye simu kwa kutumia kompyuta Kwa maisha ya kujinyima na kutopenda starehe, kazi yake hii ilimnufaisha kiasi cha angalau kujikimu kimaisha na pengine kumfanya hata asiwaze kabisa kufikiria kufanya kazi nyingine yoyote. Tofauti na siku nyingine, siku hiyo ilianza vizuri sana kwa upande wake, alipata wateja wengi kupita kiasi. Kama mjasiriamali mwingine mzoefu, alifanya kazi zake kwa umakini mkubwa na kuhakikisha wateja wake wanavutiwa na huduma zake kwa kuongeza ukarimu na kuongea lugha yenye bashasha na hata ikamlazimu kuwajua na kuwaita kwa majina wateja wake ambao walijipanga kwa michapo ya hapa na pale huku akiendelea kuwahudumia. Hakika mtu yeyote alijisikia huru kukaa kwenye benchi dogo lililopo pembeni ya kibanda cha Dedan, akipiga soga na kupoteza muda, akinywa kahawa au pengine akijiunga na kikundi cha vijana wachache kwenye vikao visivyo rasmi wakibadilishana mawazo ya siku. Ndiyo, kila mtu hulalamikia ugumu wa maisha wa siku hizi, kiasi cha furaha au jambo jema kutokea kwa nadra sana na pengine lisitokee kabisa hata kufikia mtu kukushirikisha walau punje ya neema yake. Umasikini ulisababisha kila mtu ajifungie peke yake kwa uchoyo akila matunda ya kazi zake. Hivyo, iwe asubuhi, mchana au jioni, wakazi wa Mtaa wa Songasonga hukutana kwa unyonge si kwa jambo lingine, bali kuzungumzia mawazo dhaifu ya siasa za kupindua nchi na mara nyingine wakisimuliana hadithi za nani kafanya nini, lini na wapi! Kwa kifupi Dedan alikuwa ndiyo kitovu cha mkusanyiko wa watu katika mtaa mzima wa Songasonga. Kwa sababu hiyo na sifa nyingine kedekede, alitokea kupendwa na kila rika kiasi cha kujulikana vizuri na kila mtu mtaani kwake. Japokuwa alionekana mwenye furaha kubwa machoni mwa watu siku hiyo, ndani ya moyo wake kwa kificho alikuwa amebeba maumivu makali kiasi kwamba kama hali hiyo ingemkuta mtu mwingine kwa hakika asingekuwa hata na nguvu ya kusimama na kuongea kwa furaha mbele za watu. Siku zote Dedan aliamini katika kuyamaliza matatizo yake yeye mwenyewe bila kuathiri mwenendo wa shughuli zake au wa watu wengine. Akaamua kutowashirikisha kabisa ndugu wala marafiki zake majonzi na matatizo yake. Mara nyingine aliweza hata kulala na njaa bila kusema wala kuomba msaada kwa mtu yeyote. Huenda misimamo hiyo ndiyo sababu kubwa iliyomfanya ajikaushe muda wote huo, akiigiza kucheka na watu hali moyoni akilia kwa sauti akimuwaza mpenzi wake, hapana, aliyekuwa mpenzi wake, zamani “…ooh! Carolina, maisha gani nitaishi bila wewe? Naumia…naumia, ee… Mungu naomba nirudishie Caro wangu.” Tenzi zilipokwamia hapo alitamani kupiga kelele na kulia kwa nguvu. Huenda angepunguza maumivu walau kwa kiasi kidogo, si ndiyo wanavyosema hao wanaojiita wanasaikolojia, eti kulia kunapunguza msongo wa huzuni na kulainisha mrundikano wa dukuduku lililofungamana rohoni. Waongo wakubwa! Kinyume na wote hao yeye aliamini kulia si punguzo wala suluhisho la matatizo yake, hasahasa tatizo la mapenzi. Alihakikisha kwamba hatoi mwanya wa hata chozi moja kumdondoka wala kumlengalenga kutoka machoni mwake. Mwanaume rijali hamlilii demu bwana!
TARATIBU zimwi la upweke likamzonga na kuushinda kirahisi ustahimilivu wa moyo wa Dedan. Kama mfungwa kwa mawazo yake akajikuta hajielewi kabisa. Kichwani akiwaza mara ya kwanza alipoongea na Caro kwa njia ya simu
“Mungu wangu! Msichana mrembo wa ajabu huyu,” alisema moyoni Dedan. Akakumbuka pia alipoamua kumfungulia kurasa mpya za mapenzi ndani ya kuta za moyo wake. Alikumbuka vyema kila zuri walilofanya pamoja, wakicheza baharini na kurushiana mito kitandani. Walilishana chakula na kubusiana kimahaba. Lakini hayo yote yalitoweka ghafla baada ya kukumbuka sauti kali ya Carolina kwenye simu ikimtosa bila huruma na pasipokuwa na sababu yoyote. Akasikia sauti nyingine ya mwanaume wake wa sasa ikimchimba mkwara kwamba atakiona cha mtemakuni endapo atajipendekeza kwa hali yoyote ile kumtafuta Carolina. “Hapana,” alijishtukia akiweweseka kwa sauti ya ukali mbele ya mteja wake mkubwa, Salima ambaye muda mwingine alikuwa akimsemesha huku akimkabidhi simu yake ya mkononi kwa ombi la huduma ya kuchajisha lakini bila mafanikio. “Ooh! Samahani sana Salima, ulikuwa unasema nini?” Dedan aligutuka kutoka katika vita ya nafsi na kushusha pumzi ndefu akimwomba Salima arejee maongezi yake ya awali. “Dedan, mzima kweli leo wewe?” Salima aliuliza baada ya kugundua hali ya kubabaika ya Dedan. “Mi mzima tu…lete stori,” kwa uchangamfu Dedan aliongea kiasi cha kumshawishi Salima aamini kwamba kila kitu kilikuwa sawasawa. “Hata hivyo, siku zote ni nzuri kwa Dedan, ni kama anaishi katika ulimwengu wa pekee, japo ni maskini mwenzangu, anaonekana haumizwi na kitu. Shida hizi anazichukulia kama changamoto kwa kupigana kwa nguvu zake zote kupata maendeleo tofauti na vijana wengi wa rika lake. “Kweli ninatamani sana niwe na mwanaume kama huyu. Hapana si kama, bali ni huyu huyu…Mh! Lakini namwogopa kumuanza, sijui atanichukuliaje? Mtu mwenyewe ni mwingi wa shughuli! Ila nitamwambia kesho asubuhi nikija kuchukua simu yangu. “Nitamtumia meseji nzuri ya mapenzi. Nimejaribu kumfanyia mambo mengi ilimradi azisome hisia zangu, lakini mtu mwenyewe wala haoni,” aliwaza Salima huku akiwa amesimama na kujichekesha na kuweka tabasamu pana mbele ya Dedan aliyekuwa akimtazama tu bila kuona chochote. Mawazo yake yalikuwa mbali, kama vile ana macho lakini haoni na ana masikio lakini hasikii. “Usiku mwema Dedan,” aliongea Salima kwa huruma na upole baada ya kugundua ameshindwa kulinasa windo lake kwa siku hiyo. Mbinu alizofundishwa na kungwi wake, Bi. Hamdani wa Masasi hazikufua dafu mbele ya Dedan. Alitamani amrukie na kumbusu kwa nguvu ili amjulishe hisia zake, lakini alihofia akiamini ataonekana msichana malaya kama si aliyekosa maadili mema. “Nitasubiri nafasi yangu, sitaki niharibu yote niliyoyaanza. Kwa Dedan nitakuwa mwanamke mstaarabu, mwema na mwaminifu daima naamini atanipenda tu,” alijiapiza na kujiondokea zake moyoni akilia na kumlaumu mwanaume huyo kwa kutojua windo lake. “Usiku mwema Dedan…usiku mwema mpenzi wangu…” chochote asichokisema kwa sauti kumwambia Dedan moja kwa moja, aliamua kukimalizia kwa kuongea kwa sauti ndogo akitumaini ipo siku atamjibu na kumuuliza mambo mengi wakiwa kama mke na mume. Baada ya kuhakikisha amemaliza na kuweka vizuri kila kitu, Dedan aliitazama saa juu ya kioo cha simu yake iliyoonesha namba ishirini na moja, ikiashiria saa tatu usiku kwa urekebisho wa saa ishirini na nne za siku moja. Alifunga vyema ofisi yake kisha akatokomea huko vichochoroni ambako aliwahi kusikia vinauzwa hivyo vinavyopoteza mawazo, eti pombe! “Hakuna muda mzuri wa kuamua kuwa chakari kama huu,” Dedan alijisukuma kwa mara ya kwanza kwenye vilabu vya pombe za kienyeji. Aliamini atalewa kwa gharama ndogo sana huku akifanikiwa angalau kuvuka makali ya upweke kwa usiku huo wa kwanza akilala akiwa anajua kabisa hataishi na Caro wake tena. *** Asubuhi aliamka na kujinyoosha na kupiga miayo mfululizo. Alionekana mwingi wa uchovu kutokana na pombe kali za jana yake. Ghafla alijishangaa machozi yakimbubujika. Alitaka kuamka, lakini akashindwa. Jasho jingi lilimtoka mwilini huku mapigo ya moyo yakienda kwa kasi ya ajabu. Kama mzigo alidondoka chini na kupoteza fahamu.
Jasho jingi lilimtiririka na kufuatiwa na maumivu makali ndani ya kifua chake. Mapigo ya moyo yalimuenda kwa kasi na kusimama kwa mara moja. Ghafla nguvu zake zilimuishia akadondoka na kuzirai akiwa peke yake chumbani. Salima alitembea haraka akielekea dukani kwa Dedan. Moyoni akiwa na malengo makuu mawili, kuichukua simu yake aliyoiacha kwenye chaji usiku wa jana yake na kumfungukia Dedan kuhusu dukuduku aliloliweka rohoni kwa muda mrefu Njiani kote moyo wake ulimdunda kwa kasi akihofia ni nini Dedan atamjibu kama atamwambia hisia zake. Kile kiroho cha nighairi leo nimwambie kesho kilizidi kuisumbua nafsi yake. Akaona kama kila siku ataendelea kuogopa na kuishia kusema atamwambia kesho, basi kwa hakika hatamwambia daima na zaidi ataendelea kuumia tu na kesho zisizofika. “Leo lazima kieleweke,” Salima alijipa moyo huku akijiangalia vizuri kuanzia juu mpaka chini jinsi alivyopendeza. Akahakikisha anatembea mbali na barabara akihofia vumbi la magari lisije likamchafua. Hakuwahi kujisikia hali hii kwa mwanaume yeyote kabla hajakutana na Dedan, lakini siku hiyo alishindwa kabisa kujizuia kujipodoa na hata kupitiliza. Asubuhi alipokuwa bafuni alitumia takriban nusu saa kuhakikisha alikuwa msafi kila kona ya mwili wake. Hata alipokuwa chumbani mwake, alijishangaa akitumia muda mwingi kucheza mchezo wa vua vaa kwa kila aina ya nguo mpaka alipoipata suruali yake adimu aliyoiandaa rasmi kwa tukio muhimu kama hilo. Kwa kuwa alikuwa mgeni wa mavazi ya kubana, alijishangaa baada ya kuona ukubwa wa hipsi zake na jinsi zilivyojichora vema nje ya suruali. Alitembea huku akijiangalia kila hatua aliyoipiga. Juu alivaa kiblauzi cha pinki kilichoendana vizuri na rangi ya ngozi yake ya kahawia. Kifua chake kilikuwa wazi sehemu kubwa na kukifanya kivutie maradufu huku kichwani akiwa amevaa wigi la rangi nyeusi akizifunika nywele zake zisizoijua saluni kwa muda mrefu. Ilikuwa wazi kwamba uzuri wake siku zote ulijificha kutokana na jinsi alivyokuwa akijiweka, lakini siku hiyo hata yeye mwenyewe alijishangaa na kujikubali kwamba wakiitwa warembo kumi hakika na yeye ataitika. Njiani kila mtu alikuwa akimuangalia kwa mtazamo mpya. Yeye pia alionekana akiupenda sana muonekano huo. Akazidisha mikogo na kujifanya kama ameizoea hali hiyo japo moyoni alijaa aibu tele kwa ugeni wa kila alichokivaa siku hiyo. Akiwa njiani alifungua kipochi chake na kutoa kioo kidogo akihakikisha poda na rangi aliyoipaka mdomoni imesambaa vizuri. Akajilazimisha kutabasamu ili kuondoa mikunjo yoyote ya huzuni kwenye uso wake japokuwa haikuwepo. Akiwa anakaribia kona ya mwisho kutokea kwenye kibanda cha Dedan, Salima alibana kwenye kona na kuhema kwa nguvu. Akajipulizia marashi kwa mara ya mwisho. Akajitokeza na kuanza kutembea taratibu huku akiangalia ni wapi alipo Dedan ili amroge kwa muonekano wake alioenda nao siku hiyo. Kwa mbali, alishangaa kuona kibanda kimezungukwa na watu wengi ambao bila shaka walikuwa wateja wa Dedan, kwani wengi huwa na mazoea ya kuacha simu na betri zao usiku mzima kwenye chaji kwa ahadi ya kwenda kuzichukua siku itakayofuata. Salima alishangaa kuona mpaka saa nne, bado ofisi ya Dedan ilikuwa haijafunguliwa. Alihisi kuna walakini kwani kwa jinsi alivyomjua Dedan, hakuwahi kumwona hata siku moja akikosa kufungua ofisi yake mapema pasi na sababu maalumu. “Pengine anaumwa!”alistaajabu Salima huku akiukaribia umati uliojaa nje ya duka la kijana huyo ili angalau ajue nini kilichokuwa kikiendelea. “Huyu jamaa vipi leo? Kuna mtu anayepajua nyumbani kwake? Sisi tunachelewa kazi zetu bwana!” Hayo ndiyo maneno aliyosikia yakisemwa na watu walioshindwa kuvumilia huku wengine wakidiriki kuyapuuza mema yote waliyofanyiwa na Dedan kwa kumtuhumu huenda akawa amewatia changa la macho na kutoroka na fedha na simu zao. Presha ikaanza kumpanda Salima. Akapitiliza bila hata kupiga hodi na kuingia moja kwa moja hadi ndani ya nyumba kubwa yenye vyumba vingi vilivyotenganishwa na varanda nyembamba. Akahesabu vyumba kuanzia mkono wa kulia na kugonga mlango wa chumba cha tatu. Akagonga tena na tena bila mafanikio. Hofu ikaanza kumpanda kadiri alivyokosa majibu ya hodi zake. Akachungulia kwenye kitasa akaona ufunguo ukiwa ndani ya kitundu cha mlango. Je, Dedan amepatwa na nini? Akahisi huenda Dedan alijifungia kwa makusudi kabisa na pengine alikuwa amelala na mwanamke mwingine ndiyo maana alishindwa kumfungulia mlango. Hasira na wivu vilimjaa Salima, akaanza kujilaumu kwa kila kitu alichojisumbua kwa ajili ya Dedan kwa siku hiyo. Nguvu za miguu zilimuishia, akajikuta akikaa chini na kuuegemea mlango wa chumba cha Dedan akilia. Machozi yalimtoka mpaka yakamkauka kwa mapenzi yaliyozidi kipimo. Kwa mara ya kwanza katika maisha yake, akawa hajitambui kabisa. Akawa kama mtu aliyechizika, huku mapenzi yakiwa ndiyo sababu kubwa ya uchizi wake. Akaona hapana, ni lazima ahakikishe ukweli wa kile alichokuwa akikiwaza. Akajibanza pembeni kwenye kona akitega sikio juu ya ubao wa mlango akikusudia kusikiliza kila tendo lililokuwa likifanyika mle chumbani. Japokuwa kulikuwa kumetawala ukimya wa hali ya juu, lakini kwa upande wake alisikia sauti kubwa zikitoka chumbani tena kwa ufasaha kabisa. Aliisikia sauti ya huyo mwanamke aliyeamua kumpachika jina la malaya na ile ya Dedan zikisemezana kwa maneno ya faragha kana kwamba walikuwa kwenye mapenzi mazito sana. Kwa sikio lake alimsikia vyema huyo malaya akizungumza kwa lugha laini na kwa sauti ya kubana pua. Wakati huo akili ya Salima ilikuwa ikimpeleka kama aliyokuwa akitaka mwenyewe, ilimtoa kutoka kwenye ulimwengu wa uhalisia na kumtupa sehemu mbali kabisa kwenye ulimwengu wa dhahania ambao laiti kama ungepewa jina ungeitwa Ulimwengu wa Watu Wenye Wivu wa Kipumbavu. Ulimwengu ambao wenye wivu usio na maana wote wangekutana huko na pengine kuanzisha serikali huku Salima akiwa rais wao. Akawa akiwaza kitu na mara moja kinakuwa kweli, sawa sawa na kuwaza bahari na ghafla mbele yako inatokea. Macho ya Salima yakaanza kujaa ukungu huku machozi yakimlengalenga kwa hasira na wivu, ingawa hakuwa mpenzi wa Dedan rasmi, lakini aliumia sana. Alijihisi kama vile alikuwa akiibiwa mali yake. Siku zote alitamani kuwa mwenye haki juu ya mwili na akili ya Dedan na siyo mwanamke mwingine yeyote. Aliamini amezaliwa si kwa ajili ya mwanaume mwingine zaidi ya Dedan Magesa. Moyo wake ulikuwa huko na daima aliapa kulipigania penzi lake. Alijikuta akiwaza mambo mengi ambayo kiukweli yote yalikuwa ya kuhisi tu na laiti kama angejua yaliyomkuta Dedan huko chumbani hakika nafsi yake ingemsuta kwa kumuhukumu kwa uongo bila kujua ukweli; na hata kama ingekuwa kweli kwamba Dedan alikuwa na mwanamke chumbani kwake, yeye Salima alikuwa ni nani mpaka aingilie maisha yake? Hakuwa mpenzi wake, wala rafiki yake. Alikuwa mteja wake tu hapo dukani, sasa kwa nini ajifanye anajali sana? Alifikia kipindi akawa hawezi kabisa kuuzuia uchizi wake, akasimama na kurudi nyuma hatua kadhaa na kuurukia kwa nguvu mlango ambao tayari ulikuwa umeshaanza kuliwa na mchwa. Mlango ukajiachia kwa kukatika katikati huku vipande viwili vikining’inia kwenye bawabu,“ lolote na liwe,” aliwaza Salima. Ilimchukua dakika kadhaa kuzinduka katika bumbuwazi alilokuwa nalo. Hakukuwa na huyo mwanamke malaya aliyekuwa akimuwaza wala hakukuwa na Dedan hapo kitandani, ila kuna kitu mfano wa mtu upande wa pili chini ya kitanda. “Ni nini…Ah! Ni nani… Dedan! Dedan! Nini tena? We Dedan!” Salima alijikuta akipiga makelele yaliyochanganyika na kilio baada ya kumuona Dedan akiwa hajitambui huku akitokwa na mapovu mdomoni. *** “Mimi ni Salima unanikumbuka?” “Mmm…” “Mimi ni mpenzi wako Salima, haunikumbuki?” “Mmm…” “Jana tu nilikukumbusha jina langu, kwa nini unanisahau jamani!” “Mmm…” Kila alichokiongea alijibiwa: “Mmm…” Mpaka akachoka, akaamua kukaa kimya akimwangalia tu. Hakuna rafiki wala ndugu yake hata mmoja aliyejua kama anaishi na mwanaume. Aliifanya siri kubwa moyo wake ukawa sanduku pekee la kuihifadhi. Pamoja na furaha yake mpenzi wake hakuwa na uwezo wa kufanya kitu chochote. Siku nzima alishinda amekaa au amelala kitandani kama zezeta…
Simulizi : Kitanzi, Kisu Na Bastola Sehemu Ya Pili (2)
SALIMA alishtuka kutoka usingizini baada ya kuhisi alimsikia Dedan akitamka maneno ambayo hakuwa na uhakika nayo Akaamka kitandani na kumsikiliza kwa makini kama ni kweli Dedan ndiye aliyekuwa akiyatamka maneno yale. Akagundua kuwa kweli alikuwa yeye. Alipomsikia mara ya pili na ya tatu, akagundua moja kwa moja kwamba, Dedan hakuongea maneno yale kwa bahati mbaya. Ni wazi kuwa alianza kurudiwa na kumbukumbu zake. Salima alifurahi kidogo alipomsikia kijana huyo kwa ufasaha zaidi akitamka ‘Caro,’ neno ambalo bila shaka lilikuwa jina la mwanamke. “Caro!” Salima alistaajabu kimoyomoyo huku akimuangalia Dedan aliyekaza macho akiliangalia pazia lililokuwa likiyumbishwa kila upande na upepo uingiao ndani kupitia dirisha. Awali, Dedan alikuwa akitamka neno moja tu, “mmm’’ kila alipokuwa akiulizwa swali. Ajabu ni kwamba neno hilo limebadilika ghafla kwa usiku mmoja na kuwa Caro. Kwa wakati huo kila alipokuwa akiulizwa kitu alitamka jina hilo huku machozi yakimtoka hali iliyosababisha Salima ahisi kuna uhusiano mkubwa kati ya Dedan na Caro. “Labda ni ndugu yake,” aliwaza kwa wasiwasi huku akishindwa kuzizuia hisia zake kwamba huenda Caro alikuwa ndiye chanzo cha Dedan kuwa katika hali ile na labda ilikuwa bora aendelee kukaa kimya tu asije akayaibua mambo mengi ambayo yalikuwa yametulia. Salima alitambua kuwa ni lazima afanye utafiti binafsi kuhusu huyo mwanamke Caro. Aliamini lazima kutakuwa kuna kitu kati ya wawili hao. Akawa kama anakumbuka kitu fulani, akainuka na kulivuta sanduku moja kutoka chini ya uvungu wa kitanda akafungua zipu yake na kulitazama ndani. Aliviweka pembeni vyeti na picha za Dedan na kupekuapekua kila upande akilenga kutafuta kiashiria chochote kuhusu namna gani Caro na Dedan walikuwa wakifahamiana. Alitafuta mpaka akachoka, hakukuwa na cheti wala karatasi iliyokuwa na jina la Caro. Alitazama kila mahali akijitahidi kukumbuka kama kuna kitu cha Dedan alikiweka mahali pengine zaidi ya hapo, kwani tangu wahamie hapo alihakikisha kukitunza kila kitu cha Dedan bila ya kuvifungua ili kama mwenyewe atapona ampatie vitu vyake vikiwa salama. Kwa wasiwasi aliokuwa nao alikubali kwa siku hiyo kuivunja kanuni aliyojiwekea na kupekua vitu vya Dedan bila ya ruhusa yake. Akainama na kulivuta furushi jingine. Ndani yake akatoa chaja, vifaa vya umeme, simu mbovu na nzima, vyote vikiwa ni vifaa vya dukani kwa Dedan. Alipoziona simu ndipo akaikumbuka simu ya Dedan ambayo wala hakuwahi kuifikiria kwa muda wa takriban miezi mitatu tangu Dedan alipoanza kuumwa. Akaiwasha na kushusha pumzi akisubiri utitiri wa meseji uanze kuingia. *** Side alikuwa akimfuatilia kwa karibu sana msichana huyo aliyekuwa adimu sana kuonekana mitaani, alihakikisha anaijua vema nyumba aliyokuwa akiishi. Alipomwona akiingia chumba kimoja kati ya vile vya mkono wa kulia, akatabasamu na kuingia ndani ya gari lake aina ya Toyota Hilux na kuondoka eneo lile. Huku akiendesha gari, Side aliipokea simu yake iliyokuwa inaita na kuiweka loudspeaker. “Vipi? “ sauti nzito ilisikika kutoka kwenye simu. “Bro, nimeshapajua anapokaa,” Side alijibu huku akitabasamu kana kwamba alikuwa amefanikisha jambo muhimu sana. “Kweli?” “Huamini kesho nikupeleke?” “Duh! Kweli dogo we ni noma aisee, njoo basi haraka unipe fulu stori.” “Nipo njiani nakuja usiende sehemu yoyote kaka,” aliongea Side huku mikono yake ikiwa bize na kuzungusha usukani wa gari akikwepa vidimbwi vilivyojazana katikati ya barabara. *** Baada ya muda, simu ya Dedan iliunguruma mara mbili kuashiria meseji mpya imeingia. Akatulia kimya asiifungue akitaka meseji zote ziingie kwanza ili aanze kuzisoma taratibu. Alihesabu moja mpaka ishirini haikuingia meseji nyingine, akaamua kufungua na kuisoma. Cha ajabu haikuwa na jina la mtumaji na ilikuwa fupi sana isiyoonesha hali, dhamira wala jinsia ya mtumaji. Iliandikwa tarakimu ‘90’. Salima aliisoma mara nyingi bila kuijua maana yake kiundani, akaipuuza na kuanza kuzisoma meseji nyingine zilizokuwepo ndani ya simu hiyo tangu awali. Akagundua meseji nyingi zilitumwa kwa namba ileile iliyotuma meseji muda ule. Akiwa haamini alichokigundua ghafla simu yake ikaanza kuita, alipoiangalia aliona namba ile aliyotumiwa ujumbe. Ilikuwa kama vile mpigaji alikuwa akiiangalia simu yake muda wote, maana kama isingekuwa hivyo angewezaje kujua kama ujumbe wake umefika kwa mtu aliyemtumia? Salima alikuwa makini, alitafakari kwanza kabla ya kuipokea simu ile kwa vile ndiyo kwanza alikuwa ameanza kuzisoma meseji zilizokuwa zimejazana kwenye simu ya Dedan. Aliamini kwamba ni vyema kama angejua kwanza jambo lolote kuhusu mpigaji simu huyo kabla hajaipokea na kuongea naye akihofia asije akajianika yeye na Dedan wake kwa watu wabaya ambao huenda kwa njia moja ama nyingine walishiriki kumfanya jamaa yake huyo kuwa katika hali ile. Kwanza alimtazama mgonjwa wake ambaye alikuwa ameshaanza kusinzia kwa uchovu wa chai na mihogo ya kukaanga aliyokuwa amemlisha, kisha akaipokea ile simu na kusikilizia sauti ya mpigaji. “Haloo!” sauti ya kike ilisikika… “Halo Dedan!” mpigaji aliendelea kuita huku Salima akiwa amejikausha. “Haloo, mimi ni Carolina. Najua nimekuumiza sana kwa yote niliyokufanyia, tafadhali naomba unisamehe mpenzi wangu, haikuwa dhamiri yangu kukuumiza. Please Dedan naomba unijibu basi,” aliongea msichana huyo kwa huzuni huku kwikwi na kilio vikisikika kwa mbali. Baada ya kulisikia jina la Caro, Salima akahisi kama vile alikuwa akitaka kupasuka kwa jinsi alivyovimba kwa hasira. Ule uchizi na jazba alizokuwa nazo zamani zilianza kumpanda kichwani na kujikuta akishindwa kujizuia kwa ghadhabu alizokuwa nazo. Msichana huyo akasonya na kukata simu kwa kuizima kabisa huku mishipa ya damu ikiwa imemsimama kichwani. “Hakuwepo wakati unaumwa, leo anajifanya anakupigia simu akiomba msamaha. Kama yeye mwanamke kweli tutaona kama atakupata. Eti oooh! Mimi Carolina mpenzi wako, anajua nimekugharamia vingapi? Mbona hakujitokeza siku zote hizo. Anachezea moto, we muache tu!” Salima aliongea kana kwamba alikuwa akimwambia Dedan badala ya Carolina mwenyewe. Kipindi chote hicho Dedan alikuwa amelala, lakini alipolisikia jina la Carolina likitajwa na Salima akashtuka na kukaa kitandani akimkazia macho bila kuyafumba huku akihema kwa kasi kama amekutana na jinamizi. Salima aliogopa kumuona Dedan katika hali ile, akamfuata na kumbembeleza taratibu hatimaye akalala tena kitandani. Salima alishindwa kujizuia kustaajabu jinsi Caro alivyouteka moyo wa Dedan, yaani hata katika hali ile ya kutojielewa, lakini alimkumbuka vizuri kiasi cha kumtajataja kila mara. *** Ilipofika saa tano juu ya alama, Side alikuwa tayari ameshafika kwa John Chakos kumpa kila kitu alichokuwa akikifuatilia asubuhi na mapema ya siku hiyo. Ndani ya chumba kizuri katika Hoteli ya Toptown Wild Wind mwanaume mrefu mwenye rangi ya kitasha alitokea kutoka maliwatoni akiimba kwa mikogo huku akiwa na kitaulo tu. Alimtazama Side aliyekuwa amekaa kwenye sofa bila wasiwasi akiitazama sehemu ya jiji zima la Dar kupitia dirisha kubwa la kioo kwa mwonekano wa juu. Ilikuwa ni ghorofa ya kumi na saba. Mtu yeyote anayepanga vyumba vya hoteli hiyo kwa vyovyote vile huwa na utajiri wa mabilioni ya fedha kiasi kwamba haimuumi kulipa laki sita kwa siku moja kama gharama ya kukaa hotelini hapo. Japo Side ni mtoto wa mjini kiasi cha kulijua vyema Jiji la Dar na vichochoro vyake, lakini siku hiyo alikubali kutolewa ushamba kwa kuingia katika hoteli yenye hadhi kama hiyo. John Chakos ni mmoja kati ya matajiri wachache walionufaika kwa kuwatumia wasichana wachache wa tabaka la chini kwa biashara ya ngono. Kwa mujibu wa uchunguzi wake, Side alibaini kuwa wasichana wachache walioonekana warembo, hupangiwa kulala na wageni mbalimbali wa kiume wajao nchini kwa malipo ya kiasi fulani cha fedha. Kwa donge nono, Side alipewa kazi ya kuhakikisha kila mara alikuwa akiwatafuta wasichana hao kutoka mitaani. Alianza kazi yake taratibu na sasa amekuwa mzoefu na mwenye mafanikio makubwa. Alikuwa akipiga picha za wasichana kadhaa na kuzinadi kwa bosi wake, ikiwa picha ya mrembo mmoja ilikubaliwa basi lilikuwa ni jukumu lake kumfuatilia na kumpeleka kwa bosi wake kwa kumlaghai kwa pesa kidogo. Siku hiyo Side alikuwa amekwenda kukabidhi ripoti ya uchunguzi wake wa awali kuhusu mmoja wa wasichana warembo aliyekuwa akimfuatilia kwa muda mrefu. Tofauti na wasichana wengine ambao Side alikuwa akiwapeleka kwa bosi wake, msichana huyo alionekana kuzitawala fikra za bosi wake, Mr. John Chakos. Alimuulizia kila mara na kumtaka aharakishe kukamilisha ripoti yake na kumpelekea chumbani mwake tofauti na utaratibu wa kawaida. Kiasi fulani machale yalimcheza Side na kuanza kuhofia juu ya hatima ya msichana huyo aitwaye Salima Rajab.
HAKUWAHI kuwa na rafiki wala ndugu aliyepajua alipokuwa akiishi tangu ahamie kwenye mtaa huo mpya. “Huyu atakuwa ni nani?” aliwaza Salima.
Kengele ya hatari ikalia kichwani mwake, akausogelea mlango na kufungua kidogo akichomoza kichwa chake kwanza ili kutotoa mwanya wa mtu huyo kuchungulia ndani ya chumba chake ambacho pasipo ubishi kilikosa hadhi ya kuitwa chumba, ingawa Salima mwenyewe alifanya hivyo ili kumficha Dedan asionekane. “Habari yako,” alisema mwanaume mrefu kidogo mwenye kila sifa ya kuitwa bosi au mkuu wa kitengo fulani kwa jinsi alivyovalia kiofisi na haiba yake. “Sa…salama tu…nikusaidie nini?” alisema Salima kwa kigugumizi. “Naitwa Saidi Hamis Kibona, eee.. Wewe ni Salima?” “Haa…hapana haa..no, ni mimi, unashida gani?” kwa woga Salima alijikuta akikataa na kukubali kwa pamoja. “Usiwe na hofu dada yangu, mimi ni wakala kutoka kwenye Kampuni ya kigeni iliyoingia nchini Tanzania. Mmm… Mara nyingi tumekuwa tukitembelea nchi kadhaa tukifanya sanaa ya urembo na wasichana mbalimbali hasa tunaowaona wana vigezo.” “Kwa hiyo nikusaidie nini?” “Kama nilivyokwambia awali, huwa tunafanya kazi na msichana tunayemwona ana vigezo, eee.. Salima nadhani bahati hii imekuangukia wewe.” “Mbona sikuelewi! Hebu kwanza niambie jina langu umelijuaje?” “Kwani una wasiwasi gani, nimeuliza nikatajiwa au kuna ubaya wowote dada yangu?” “Hapana sikuwa na maana hiyo,” alijibu Salima akiwa bado na wasiwasi mkubwa. “Usijali Salima, nadhani utanielewa vizuri, kwa sasa naomba nikupe fomu hii ambayo ina maelekezo yote kuhusu historia na jinsi kampuni yetu inavyofanya kazi zake.” Side alifungua begi lake na kutoa bahasha ndogo akamkabidhi Salima. “Maelekezo yote yapo humo. Tafadhali yasome taratibu na kama umevutiwa kufanya kazi na sisi, tuwasiliane,” alisema Side na kuondoka. Salima alipokea bahasha ile kwa mshangao na kurudi chumbani kwake, lakini akaona siyo vizuri mgeni aondoke bila kumsindikiza. Akajitanda kanga mabegani na kutoka nje haraka akimuwahi Side. “Ngoja nikusindikize mgeni,” alijibaraguza Salima kwa aibu baada ya nafsi yake kumsuta kwani awali hakuweza kumchangamkia wala kumkaribisha ndani kwa ukarimu, lakini hata kumsindikiza pia asiweze! Aliona siyo picha nzuri kwa mgeni huyo na pengine angeweza hata kuikosa kazi nzuri kutoka katika kampuni hiyo kwa kuwa tu hakuwa mkarimu kwa mtu huyo. Side aligeuka na kumtazama Salima aliyemkimbilia. Wakatembea wakiongozana bila ya kuongea jambo lolote kimyakimya mpaka nje ya nyumba. Kwa mshangao Salima alimuona Side akiutoa ufunguo na kufungua mlango wa gari moja zuri na kuingia ndani yake. “Salima, nafasi ni chache sana fanya maamuzi haraka sana hata leo jioni nijulishe kama umevutiwa na kazi yetu,” alisema Side huku akiwasha gari lake na kuondoka, moyoni akifurahi kwa mtego aliomtega Salima. Watano kati ya wasichana aliokwisha wakabidhi kwa Mr. Chakos walikuwa wepesi sana kuwapata. Kwa maisha mabovu waliyokuwa wakiishi, hakupata tabu kunasa kwani wengi walipotajiwa tu kiwango cha fedha watakazolipwa waliruka kwa furaha bila kujali wangedhalilishwa kwa kiasi gani. Pesa ilikuwa na thamani hapa kuliko hata uhai wa mtu katika jiji hili na Side alilijua hilo fika. Salima tu ndiye aliyekuwa tofauti na wasichana wenzake na kumfuata kwa njia ya kawaida kungesababisha kumpoteza msichana huyo. Kutokana uzuri wa sura na hata umbo lake. *** Salima aliifungua haraka bahasha hiyo, akasoma na kuvutiwa na hadhi na mshahara mkubwa wa kazi hiyo. Akafurahi kuona hatimaye angeweza kupata fedha za kumtibia Dedan na kufanya mambo mengi ya kimaendeleo. Moyoni mwake alikubali kuajiriwa na kampuni hiyo akaitafuta simu ya Dedan na kuiwasha akidhamiria kumtaarifu Side ili asije akaipoteza nafasi ya kazi hiyo adimu. Alipoiwasha simu mara meseji ziliingia kwa fujo, zote zikiwa zimetumwa na Caro moja ilisomeka kwa tarakimu ’91.’ “Huyu mwanamke mchawi hizi namba ana maanisha nini!” alistaajabu Salima na kuzipuuza. *** Side akiwa na wasiwasi kama mtego wake utanasa au lah, alisimama kama punguwani akipiga hatua mbele na nyuma huku macho yake kila saa yakiiangalia saa yake ya mkononi. Alitaka amalize kila kitu kabla hajampeleka Mr. John Chakos kuhakiki makazi ya Salima. Alitaka amshtukize bosi wake na pengine kwa kutaka kuonekana mfanyakazi bora kwa kukamilisha kazi zake mapema. Kwa muda wote huo alikuwa akiisubiri simu kutoka kwa Salima kwani kwa mkwara aliomuonesha msichana huyo, isingekuwa rahisi kutobabaika na kuamini kwamba alikuwa hatanii kuhusu kazi hiyo. Majira ya saa tano na nusu asubuhi, Dedan aliamka akihisi maumivu makali ya tumbo. Laiti kama angekuwa na ufahamu basi angetambua kwamba alisumbuliwa na njaa kali. Kila siku alikuwa akilishwa na kufanyiwa kila kitu na Salima. Bado hakuwa na kumbukumbu kuhusu kitu chochote katika maisha yake na mbaya zaidi hata kutembea na kuongea ulikuwa mtihani. Ingawaje alikuwa hakumbuki vitu vingi sana, lakini tabia ya asili ya kibinadamu ilimfanya kuwa na utambuzi juu ya matendo yote ambayo huleta maumivu na yale yaletayo furaha, kwa hiyo alilia kwenye maumivu na kutabasamu au kucheka kwenye furaha. Kwa mara ya kwanza Dedan akasimama na kutembea akikisogelea kiberiti kilichokuwa juu ya meza, akatoa njiti moja na kuisugua upande wenye baruti. Huenda jambo hilo alijifunza kwa kumuona Salima alipokuwa akiwasha moto kila alipokuwa akitaka kupika. Moto ukawaka huku ile njiti ya kiberiti ikiwa mkononi mwake. Iliwaka huku moto ukishuka taratibu na kuongeza joto kwenye vidole vyake. Kwa maumivu ya kuungua akaitupa njiti ile chini kwa bahati nzuri ilizimika pasipo kuunguza kitu chochote. Kwa kiasi fulani mwanga wa kumbukumbu za kale ukapita akilini mwake. Siku hiyo akaanza kutambua kwamba kuna kitu kuhusu yeye hakijui. Akaangaza macho yake kila kona ya chumba kile kama mgeni huku akikosa majibu ya maswali kibao aliyokuwa nayo kichwani. Akastaajabu yeye ni nani na alikuwa akifanya nini humo ndani! Kanga na nguo za kike zilizokuwa zimesheheni humo chumbani, kwa kiasi fulani zilimuogopesha. Hisia zake zikamtuma kwamba kulikuwa na mwanamke aliyekuwa akiishi, mwanamke huyo ni nani? Alijiuliza. Kitu ambacho pengine mwanadamu wa kawaida hukichukilia pasipo na uzito kwenye nyumba, ‘mlango,’ kwa Dedan mtazamo wake ulikuwa tofauti sana juu ya kifaa hicho muhimu kiasi kwamba alipouona tu aliutambua mara moja. Mbao nne zilizounganishwa pamoja, bawaba na kitasa chenye tundu la ufunguo ndiyo vilikuwa vitu muhimu sana kwa muundo wa milango mingi ya uswazi. Kwa Dedan, mlango haukuwa njia ya kutoka nje na kuingia ndani tu. Hata katika ulimbukeni aliokuwa nao, bado aliuona mlango kama alama ya tumaini baada ya kiza cha utumwa na ufungwa. Ndani kulikuwa ni kizuizi chenye upweke wakati nje ilikuwa ni uhuru na furaha hatimaye. Haya yote alijifunza alipokuwa mvulana mdogo sana. Shangazi yake Bi. Tabia alikuwa akimfungia mara kwa mara ndani, mchana na usiku bila kutoka nje huku adhabu kubwa aliyopewa na shangazi yake huyo ikiwa ni kuchomwa na moto mikononi. Mambo hayo yote aliyavumilia kwa kuwa hakuwa na mzazi aliyekuwa hai kumtetea. Kwa hiyo aliishi katika mazingira hayo mpaka siku moja alipoweza kutoroka kwa kuufungua mlango kuelekea kwenye uhuru na furaha ya kuwa nje aliyokuwa akiitamani siku zote. Nje ya mawazo hayo, Dedan aliutazama ule mlango kwa muda kisha akaukimbilia haraka, akauzungusha mkono wa kitasa na kujaribu kufungua, lakini haukufunguka. Akauvuta kwa nguvu; haukufunguka pia. Moyoni alijua halikuwa jambo rahisi kwani hata alipokuwa mtoto mdogo, pindi alipofungiwa mlango na shangazi yake alikuwa akitumia waya au msumari kuchokonoa tundu la mlango mpaka ufunguke. Akaanza kuutafuta waya au msumari ndani ya chumba hicho, kwa bahati nzuri akaupata msumari mkubwa wa bati. Akausuguasugua ardhini na kuufanya bapa kisha akaupenyeza kwenye tundu la kitasa na kuanza kuchokonoa taratibu huku akiwa amefumba macho yake kana kwamba alikuwa akivuta hisia. Kwenye mawazo yake aliiona sura mbaya ya shangazi yake ikimkaripia, hofu ikaanza kujijenga taratibu huku kila kitu ndani ya chumba hicho kikigeuka na kuwa kama vile cha shangazi yake huyo. Kwa mara nyingine mlango ukawa alama ya uhuru kwa Dedan, kwa muda huo alitaka sana kuwa huru tena. Akajitahidi kuchokonoa kitasa hicho na mara kikazunguka na kichuma cha loki kikajiachia na kurudi ndani kadiri alivyokuwa akiunyonga msumari huo. Akaufungua mlango na kutoka nje kwa kupita koridoni hadi nje ya nyumba. Njiani akikutana na sura tofauti za watu wengi wakimtazama na kumshangaa kwa jinsi alivyovaa vibaya na jinsi uso wake ulivyomvimba kwa usingizi na njaa. Akakatiza mitaa kama chizi kwa bahati mbaya alikoswakoswa na magari mengi barabarani. Tangu alipofika asubuhi, alikuwa akitolewa chumba kimoja na kupelekwa chumba kingine. Alishangaa sana alipoingia kwenye chumba kidogo chenye mvuke wenye joto kali kiitwacho ‘Sauna’, aliambiwa mvuke huo humsafisha mtu kuzidi hata maji ya kawaida ambayo tumezoea kuyaoga. Kisha akapelekwa chumba cha ‘massage’, humo alikandwakandwa na warembo wenye mikono laini utadhani mikono yao haifanyi kazi nyingine yoyote zaidi ya hiyo, kwani kwa jinsi mikono yao ilivyokuwa laini hakuna aliyeonekana kuwa na uwezo wa kushika shoka na kukata kuni au hata kusugua majungu yenye ukoko na masizi. Akapelekwa chumba kingine ambacho kwa huduma alizozipata humo alikitambua kama saluni ya kike. Humo alisetiwa nywele na kufanyiwa ‘facial’, ‘manicure’ na ‘pedicure.’ Kwa mambo hayo Salima alijikuta akisahau kabisa kuhusu Dedan ambaye kwa wakati huo alikuwa akitembea toka mtaa mmoja hadi mwingine bila kuelewa mahali alipokuwa akielekea au hatari iliyokuwa ikimkabili. Wasichana wengi wazuri na warembo walimzunguka kila mmoja akifanya kazi fulani katika mwili wake. Alitumia muda mwingi sana akistaajabu, jinsi gani urembo wa mwanamke ulivyokuwa na gharama! Alishukuru tu kwamba kila kitu kilikuwa kikilipwa na kampuni hiyo aliyoitambua kwa jina la ‘Serenity’ . Kwa muda wote huo Madam Flaviana alikuwa amekaa pembeni ya Salima akimtazama kana kwamba alizidi kuwa mpya kwa kadiri alivyokuwa akipambwa. Ilisemekana kuwa mwanamke huyo alikuwa na uwezo wa kumpima mtu kwa kumtazama tu na kujua haraka vipimo vyote vya nguo yake, kuanzia ukubwa wa kiuno, urefu, mpaka upana wa mabega. Inawezekana kabisa Madam Flaviana alikuwa akimtazama Salima kwa lengo hilo, lakini kuna kitu cha ajabu ambacho Salima alihisi baada ya kumtazama jinsi Madam Flaviana alivyokuwa akimuangalia, lakini alipuuzia na kukaa kimya. “Salima, unajua kama wewe ni mrembo sana?” alisema Madam Flaviana huku akimwangalia Salima kuanzia chini mpaka juu. “Mbona mi wa kawaida sana,” Salima alijibu kwa aibu kidogo. Ukweli ni kwamba Salima hakujali sana urembo kama wasichana wengine kiasi cha kujijua na kujua watu wengine wanamuonaje. Alikuwa msafi na mzuri wa asili asiyependa kuupoteza muda wake mwingi mbele ya kioo, hivyo hakuwa akijifahamu kama ni mzuri kiasi hicho cha kusifiwa na Madam Flaviana, kilicho kuwa akilini mwake wakati huo ni harakati za kutoka kimaisha tu. “Oke, twende nikakuchagulie nguo,” alisema Madam Flaviana bila kutaka kuendeleza ubishi kwa mtu ambaye haifahamu thamani ya uzuri wake. Alichowaza akilini ni kumtumia kwa manufaa ya kampuni yao haramu. Salima kwao alikuwa ni kama ndege mjinga asiyejua thamani ya mlio wa sauti yake, hilo lilikuwa jambo la kujivunia kwa Madam Flaviana, akapenda abakie hivyohivyo. Akiwa katika chumba kilicho sheheni nguo mbalimbali, alichaguliwa nguo moja baada ya nyingine na kutakiwa kuzijaribu. Nyingi zilikuwa fupi, zenye kubana. Kila mara alivyotoka kwenye chumba cha kubadilishia nguo na kuvaa nguo nyingine, Madam Flaviana alionekana kumuangalia sana bila kusema chochote zaidi ya kumkabidhi nguo mpya badala ya ile ya mwanzo na kumtaka aendelee kuzijaribu. Hatimaye zoezi hilo la kuchosha lilimalizika kwa Salima na kuvaa nguo moja iliyombana sana kisha wakaelekea kwenye mgahawa kwa ajili ya chakula cha mchana. Kila kitu kilikuwa kipya sana kwa Salima, akafundishwa jinsi ya kuketi kistaarabu, jinsi ya kula kwa kutumia uma na kisu, akafundishwa jinsi ya kufungua shampeni na kuzungumza kwa staha na haiba za kike. Yote alionekana kuyashika haraka sana kiasi cha kumfurahisha Madam Flaviana. “Mama yangu!” Salima alishtuka baada ya kugundua kuwa muda mrefu ulikuwa umepita tangu amuache Dedan peke yake. Akasimama na kutaka kuondoka kama mtu aliyechanganyikiwa. “Salima nini tatizo?” aliuliza Madam Flaviana baada ya kugundua kubadilika ghafla kwa hali ya Salima. “Nimemuacha mgonjwa peke yake tangu asubuhi nilipokuja huku, nilipitiwa na kumsahau kabisa, sijui hali yake itakuwaje maana hawezi hata kusimama na kula mwenyewe.” “Usihofu sana, hii ni saa nane tunaweza kumuwahi kwa gari langu. Twende haraka,” aliongea Madam Flaviana kisha wote wakaondoka.
Wasiwasi ulimjaa sana Salima, akaona hata gari lenyewe lilikuwa halikimbii kwa kasi aliyokuwa akiitaka, lakini alijikaza na kuvumilia bila kuteremka. Kimoyomoyo alisali sala zote bila kujali dini wala lugha aliyoitumia ilimradi tu sala hizo ziweze kumfanya Dedan awe mzima mpaka saa atakayofika. “Usihofu Salima, utamkuta tu akiwa mzima,” alisema Madam Flaviana kwa huruma huku akiuzungusha usukani na kuongeza spidi kila ilipompasa kufanya hivyo. “Madam, hujui tu Dedan ana umuhimu gani kwangu ndiyo maana unasema kirahisi hivyo,” aliongea Salima huku machozi yakimtoka bila kujua kama alilitaja jina la Dedan kimakosa katika maneno yake aliyoyasema. “Kwani mgonjwa wako anaitwa Dedan? Mmm…ni nani yako?” Madam Flaviana alimuuliza maswali mfululizo Salima. “Aahh…ni mpenzi wangu tu,” aliongea Salima kwa kigugumizi baada ya kujishtukia kwamba alilitaja jina la Dedan kimakosa. “Oooh! pole sana, kwani anaumwa nini?” Kwa swali hilo Salima akawa kimya akijishauri kumwambia au kutomwambia Madam Flaviana, hata hivyo aliamua kumsimulia ukweli wote kwani kwa hali ilivyokuwa asingeweza kuyazuia maswali kutoka kwa mwanamke huyo kwa wakati huo kwa kuwa alijikoroga mwenyewe kwa kumtaja Dedan mbele yake. Alihisi asingekuwa muungwana kwa kuficha kila kitu mbele ya Madam Flaviana ambaye alijitolea kumpeleka kwa gari lake mpaka nyumbani kwake bila hiyana. Basi Salima alijikuta akimsimulia Madam Flaviana mwanzo mpaka mwisho kuhusu Dedan na yeye. Akamwambia kila kitu bila kuficha. Akabainisha pia hata dhumuni la kuamua kufanya kazi katika kampuni hiyo, ilikuwa ni kwa ajili ya mpenzi wake aliyekuwa akihitaji tiba na matunzo. Madam Flaviana alishindwa kulizuia chozi lisimdondoke mara baada ya Salima kuhitimisha simulizi yake kwa kusema alikuwa akimpenda sana Dedan kiasi cha kufanya kitu chochote ili awe naye. Madam Flaviana alimuonea huruma sana msichana huyo mdogo ambaye maisha hayakuwa mazuri sana kwa upande wake. Akaishia kumwangalia tu moyoni akitamani amuokoe na janga ambalo yeye pamoja na kampuni yake walikuwa wamemwandalia, lakini akasita na kuamua kumuacha tu katika bumbuwazi alilokuwa nalo kwa kuhofia kuwa kama angemwambia angesababisha hata uhai wake yeye mwenyewe kuutia mashakani kwani alimjua vyema Mr. John Chakos. Mwanaume mtanashati sana ambaye ukatili wake ulijificha vyema nyuma ya uzuri wa sura na umbo lake. Madam Flaviana mwenyewe alikuwa kama mmoja wa wasichana waliokuwa wa kwanza kabisa kuuzwa katika biashara hiyo, ndiyo maana hakukuwa na mtu wakumshangaa kwa nini alikuwa mrembo sana. Tuseme bahati tu ilikuwa upande wake. Uzuri wake ulimletea mafanikio makubwa na kujuana na watu wengi kutoka nchi mbalimbali. Pengine hiyo ndiyo ilikuwa salama yake kwani kampuni ingepata hasara kubwa kama ingemwachisha kazi baada ya umri wake kumtupa mkono kwa kuhofia kupoteza mtandao wa marafiki na wateja ambao Madam Flaviana aliutengeneza. Kwa kugundua hilo wakampandisha cheo na kuitwa ‘Madam’ ama ‘Bibi Mkuu,’ kazi yake ikiwa ni kuwafunza ustaarabu mabinti wapya na kuhakikisha wanatii sheria na taratibu zote za kazi yao huku akiripoti maendeleo ya kila msichana aliyekuwa akiishi kwenye lile jumba. Kwa miaka kumi na mbili aliyoishi katika kampuni ya ‘Serenity’ alipata kushuhudia mambo ya kutisha sana yakiwatokea wote ambao walikuwa wakikaidi kanuni za kazi na kutaka kutoa siri za kampuni hiyo nje. Kwa kifupi hata yeye mwenyewe alishapoteza marafiki wengi sana aliokuwa nao katika jumba la ‘Serenity’. Hakuna mtu wa nje aliyekuwa akifahamu vizuri nini kilichokuwa kikiendelea ndani ya kuta za jengo hilo ambalo yeye aliliona kama ‘Danguro la kimataifa.’ “Kwa hiyo vipi! Kama Caro atakuja kumfuata bwana ‘ake, wewe utafanyaje?” aliuliza Madam Flaviana huku akikata kona ya kuingia vibarabara vya uswahilini. “Sipo tayari kumuachia, labda nisiwe hai,” “Nilishawahi kupenda kama wewe Salima, sishangai hata kido…” “Ishia hapohapo!” Salima alisema akimkatiza usemi Madam Flaviana na kushuka haraka akikimbilia moja kwa moja hadi ndani ya nyumba. Macho yake yakakutana na mlango wa chumba chake ukiwa wazi huku kila kitu ndani ya chumba chake kikionekana isipokuwa Dedan.
Simulizi : Kitanzi, Kisu Na Bastola Sehemu Ya Tatu (3)
“Simama hapohapo!” Salima alisema akimkatiza usemi Madam Flaviana na kushuka haraka akikimbilia moja kwa moja hadi ndani ya nyumba, macho yake yakakutana na mlango wa chumba chake ukiwa wazi huku kila kitu ndani ya chumba chake kikionekana isipokuwa Dedan. Songa nayo… Salima hakuwa na muda wa kumshukuru Mungu baada ya kuona kila kitu chake kilikuwa salama, badala yake alizidi kupata wasiwasi na hofu baada ya kubaini kuwa Dedan hakuwepo ndani ya chumba hicho. Madam Flaviana alimfuata kwa nyuma na kuingia katika nyumba hiyo ambapo watu na majirani walishaanza kutokeza vichwa vyao wakimshangaa Salima na huyo mgeni aliyeambatana naye kwa jinsi walivyopendeza huku watoto wa uswahilini wakilichezea gari la Madam Flaviana kila moja akidai ni la kwake. Salima alishindwa kujizuia, alikaa chini na kuangua kilio akilitaja jina la Dedan. Madam Flaviana hakuwa akijua kilichokuwa kinaendelea, lakini kwa hali aliyoiona akajua kwamba huyo Dedan aliyekuwa akiishi na Salima hakuwepo chumbani humo jambo ambalo lilikuwa kweli. Akajitahidi kumkokota Salima huku akimbembeleza hadi ndani ya chumba chake na kumwacha akilia kama mtoto kisha akatoka nje na kuulizia watu kama walimuona mwanaume yeyote akitoka ndani ya chumba hicho. Watu wote walikuwa kimya wasijue kama Salima alikuwa akiishi na mwanaume mle ndani na wengine wakishangazwa na taarifa za kupotea kwa mtu aliyekuwa akiishi ndani ya chumba hicho na Salima bila ya wao kujua. Madam Flaviana akiwa katika hali ya kukata tamaa, mtoto mmoja wa kiume alimfuata na kusema alimuona mwanaume mmoja akitokea chumba kilekile alichokuwemo Salima na kuelekea barabara ya Machinjioni. Kwa siri kubwa Madam Flaviana akamvuta mtoto yule pembeni na kumuuliza kama kuna mtu mwengine alimwambia kuhusu jambo hilo, mtoto yule alijibu kuwa hakuna mtu yeyote aliyemwambia isipokuwa yeye tu. “Safi sana, sasa usiseme kwa mtu umesikia eeeh!” alisema Madam Flaviana na kuchomoa noti ya shilingi elfu kumi na kumpa, lengo lake likiwa ni kumtenga Salima na jambo lolote litakalomtoa kwenye akili ya kazi waliyotaka aifanye. Madam Flaviana alijua fika kuwa uhusiano wa mapenzi na kazi zao jinsi zisivyochangamana. Tangu mwanzo alipopata taarifa kuwa Salima alikuwa akiishi na Dedan alikuwa akifikiria jinsi ya kuwatenganisha na siku hiyo ilikuwa kama bahati kwake, ikiwa kama Dedan alitoka humo ndani mwenyewe au lah! Salima hakupaswa kuujua ukweli. Kwa kificho akatoa simu yake na kumpigia Side akitoa maelekezo amfuatilie mwanaume fulani barabara ya Machinjioni na ikiwezekana ammalize mara moja. Side alifanya kama alivyoamrishwa, akakitonya kikosi kazi chake na mara moja wakaingia mtaani kumsaka Dedan wakati kwa upande wa pili, Madam Flaviana alimdanganya Salima kuwa kampuni imewataarifu polisi na tayari walikuwa wakimtafuta. Akamshawishi waondoke maeneo hayo kwa usalama wake kwani alimfanya Salima aamini kuwa watu waliotumwa na Caro ndiyo waliomteka Dedan. Salima alikubali kwa kuwa aliamini Dedan hakuweza kusimama wala kutembea mwenyewe na hata kama angeweza kufanya hivyo isingekuwa rahisi kuufungua mlango kwani alikumbuka vyema alivyoufunga, tena kwa ufunguo. Ni wazi aliyoyasema Madam Flaviana yalikuwa na ukweli ndani yake, akakubali kuondoka maeneo hayo huku akichukua baadhi ya vitu muhimu. *** Ndani ya jengo kubwa la ‘serenity’ salima alikuwa ndani ya ‘lifti’ akiongozwa na Madam Flaviana mpaka kwenye chumba kilichokuwa ghorofa ya sita alichooneshwa kuwa makazi yake mapya. Mazingira mazuri ya chumba hicho hayakumfanya amsahau Dedan hata kidogo. Katika mawazo yake alishawishika kuwa kutoweka kwa Dedan ulikuwa ni mchezo aliochezewa na Carolina kama alivyodanganywa na Madam Flaviana. Uoga na hasira vyote vilimjaa kwa pamoja akashawishika kuwa ‘Serenity’ ni mahali salama kwake kwa muda huo japo hakukubali kama amempoteza Dedan moja kwa moja kiasi cha kutoonana naye maisha yake yote. “Siku moja nitakuona mpenzi wangu, utakuwa wangu tena,” alijiliwaza Salima huku machozi yakimlengalenga. Akapitiwa na usingizi huku akiombea yote yaliyotokea yawe ndoto ya mchana isiyo na ukweli wowote wakati atakapoamka. *** Usiku uliingia, Dedan alizidi kutokomea mitaani huku njaa ikizidi kumuuma. Hakuna mtu aliyekuwa akimjali hata pindi alipojibana kwenye kona ya Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mwanakwetu akiugulia njaa kali asijue dawa yake. Kama angelijua kuwa chakula ndiyo tiba ya ugonjwa wake si ajabu angeishajiunga na mapunguwani wenzake waliojazana karibu na jalala kubwa la jiji wakigombania mabaki ya vyakula jirani kabisa na mahali alipokaa, lakini Mungu wake kwa siku hiyo hakuwa kabisa na mja wake huyo. Kiu na njaa kali vilimfanya adhoofu na kupoteza fahamu kabisa, akalala kifo kikimnyemelea, ubongo wake ukiimba nyimbo za huzuni huku taswira na jina la msichana mzuri aitwaye Carolina ikififia kichwani mwake..
Usiku huo giza lilikuwa nene kupita kiasi. Watu wengi tayari walisharudi kutoka kwenye mihangaiko ya kila siku na kujifungia majumbani mwao. Hakuna hata mmoja aliyejua kama kuna mtu aliyekuwa akitaabika na njaa huko nje pasipo kuwa na msaada wowote. Kadiri muda ulivyozidi kwenda mbele, ndipo kibaridi cha usiku kilizidi kuvuma na kumfanya Dedan azinduke kutoka katika usingizi wa kifo uliompitia. Kidogo fahamu zake zilirejea, akasimama na kutazama kila kona kama vile hakumbuki kama alienda mahali hapo mwenyewe. Ghafla, tone zito la maji ya baridi lilimwangukia mkononi, akalitazama na kulipangusa mara moja. Mara matone mengi zaidi yalizidi kumwangukia kila sehemu ya mwili wake huku upepo mkali ukiyumbisha miti na mapaa mahali hapo. Kufumba na kufumbua ilizuka mvua kubwa ya upepo. Dedan akiwa hafahamu lolote, akasimama mahali hapo amejikunyata kwa baridi huku akilowa na mvua pasipo kujua jinsi ya kujikinga nayo. Mvua ilinyesha na kuilowanisha midomo yake mikavu, kidogo maji yaliyopenya yalimpa ladha nzuri katika ulimi wake. Akaachama mdomo huku akiyameza maji ya mvua yaliyokuwa yakitiririka kwa wingi usoni mwake. Aliendelea kunywa mpaka tumbo lake likagoma kupokea maji tena. Hapo ndipo alipogundua tiba ya kiu chake japo tumbo lilianza kumuuma huku baridi kali likimpiga kila kona, alianza kutetemeka. Kwa mwendo wa kasi gari moja lilipita maeneo hayo na kufunga breki mbele ya Dedan. Mara moja watu watatu waliovalia makoti makubwa ya mvua walishuka na kumsogelea Dedan. Mkubwa kuliko wote ambaye alionekana kama kiongozi wao, alitoka na kusimama karibu kabisa na gari lile huku wale wawili wakimfuata Dedan. “Wewe kwa nini upo hapa peke yako?” alisema mmoja wao kwa ukali akimwambia Dedan huku akitazama kila upande kuhakikisha kwamba hakukuwa na mtu karibu. “Una uhakika ni huyu?” yule mwingine alimuuliza mwenzake huku akionekana kuchoka sana kwa kazi fulani waliyoifanya siku hiyo. “Funga domo lako bwana we huoni ninajaribu?” alijibu kwa hasira mtu yule wa mwanzo na kumtikisatikisa Dedan aliyesimama akiwatazama kwa uwoga. “Lazima atakuwa ndiye huyu, angalia!” yule mtu wa mwanzo alimwambia mwenzake baada ya kugundua kucha fupi na ndevu zilizokatwa vizuri usoni kwa Dedan japokuwa alikuwa mchafu kama chizi wengine. Wote wawili walikubaliana kuwa huyo ndiye mtu waliyetumwa kumtafuta na Side, wakamuangalia yule mtu mwingine aliyesimama nyuma yao akatoa ishara fulani. Mara moja Dedan akapigwa mtama na kufungwa kamba mikono na miguu kisha wakamtupa ndani ya buti la gari na kupotea maeneo hayo. *** “Haloo (kimya kidogo) ndiyo lakini lazima tuhakikishe kama huyu ndiye Dedan kweli kabla hatujafanya jambo lolote (kimya kidogo..) okey, basi kama Salima atakuwa na picha yake litakuwa jambo zuri (kimya kidogo..) kama atakuwa ni huyu tuliye naye basi hesabu kama kazi imekwisha tayari,” aliongea Side kwa njia ya simu na mtu mwingine. “Wewe ni Dedan au siyo?” aliongea Side akimtazama Dedan aliyekuwa akifakamia chakula kwa pupa baada ya kuiga mfano kutoka kwa mtu fulani aliyemuona akila pembeni yake. Kwa jinsi Side alivyosimuliwa na Madam Flaviana kuhusu Salima alivyosahau kumpa chakula Dedan kwa siku nzima, alimuonea huruma mtu huyo na kumpa chakula. Side alikuwa na amekuwa akishuhudia mara nyingine kusababisha au kufanya mauaji ya watu wengi kwa manufaa ya ‘Serenity.’ Hakufikiria kama angetumwa tena kumuua mtu mwingine ambaye hana hatia kwa masilahi ya kampuni hiyo. Dhamira yake daima imekuwa ikimsuta kwa yote aliyoyafanya. Akaamua lolote na liwe, lakini kwa mikono yake hata mwaga damu ya mtu mwingine tena lakini lazima atafute njia ya kumficha mtu huyo ikiwa ni Dedan kweli. *** Kama kuna mtu alifahamu kuwa ndani ya vyumba vya ‘Serenity’ kulikuwa na siri basi alikuwa amekosea. Kuanzia sakafuni mpaka kwenye paa, jengo zima lilikuwa limesheheni vinasa sauti na kamera za ‘CCTV.’ Kwa hiyo kila kitu kilichokuwa kikifanyika na kuongelewa humo ndani, kilikuwa kinasikiwa na kuonwa na Mr. John Chakos aliyekuwa maili mia moja kutoka katika jengo hilo. Chakos alijua vema yupi kati ya wasichana walioingia humo mjengoni hana ari ya kazi na yupi kwa pesa alizopata kwa kazi hiyo alikuwa radhi kukaa hapo ‘Serenity’ kwa miaka yote ya maisha yake. Tangu Salima alipoingia ndani ya jengo hilo Mr. John Chakos, alikuwa akimtazama kupitia kompyuta yake. Alimtazama usiku mzima jinsi alivyokuwa amelala, mpaka asubuhi ya siku hiyo mpya. Alishinda akimuangalia Salima alivyokuwa akioga na kuvaa nguo zake na hata akitembea ndani ya korido za jengo hilo. Nafsi yake ilianza kujaa tamaa ya kufanya mapenzi na msichana huyo.
Salima kwa upande wake aliamka asubuhi na mapema akiwa na nia ya kumuuliza Madam Flaviana kama mpenzi wake, Dedan alikuwa amepatikana. Akatembea akikatiza korido kadhaa akikielekea chumba ambacho alielekezwa tangu jana yake kuwa ni cha Madam. Kama vile Madam Flaviana na Salima walikuwa na fikra sawa, kabla hata Salima hajabisha hodi kwenye mlango wa chumba hicho, Madam Flaviana naye alikuwa akitoka mlangoni. Wote wakakutana kwenye korido. “Waoh! Salima, umeamkaje leo? Nifuate tukapate kifungua kinywa,” alisema Madam Flaviana kwa mshtuko kwani hakutegemea kama Salima angekuwa hapo mlangoni kwa wakati huo. “Madam, polisi wamepata taarifa zozote kuhusu Dedan?” Salima alimuuliza Madam Flaviana bila kupepesa macho yake. “Hapana mpaka sasa bado hatujasikia lolote, lakini polisi walikuwa wakihitaji picha zake ili wamtafute kiurahisi, si unazo?” “Ndiyo ninazo ngoja nikuletee,” alisema Salima na kukimbilia chumbani kwake mara moja ambapo alirudi na picha kibao za Dedan na kumkabidhi Madam Flaviana achague ipi moja wapo iliyokuwa ikionekana vizuri ili aipeleke haraka polisi wakamtafutie mpenzi wake. Mara baada ya Madam Flaviana kuzipata picha hizo alifurahi kimoyomoyo akijua kuwa kama Dedan ndiye yule mtu aliyekamatwa na kikosi kazi kilichoongozwa na Side jana yake, basi huo ndiyo ulikuwa mwisho wake. Akamsikitikia Salima kwa kutokujua dhumuni lake kisha akainua simu na kumpigia Side akimtaka aonane naye mara moja ili amuoneshe picha hizo kama zilikuwa zikifanana na huyo mtu waliye naye huku Salima akizugwa kuwa Madam alikuwa akiongea na ofisa fulani wa polisi. Baada ya kunywa chai, Madam Flaviana alimpeleka Salima kwenye jukwaa kubwa na kumfundisha jinsi ya kutembea kama mamiss ‘catwalk.’ Akamfundisha pia na maneno machache ya kumkarimu mtu kwa lugha ya Kiarabu bila Salima mwenyewe kujua kusudi la somo hilo kuwa ni kumuandaa kwa ujio wa Prince Khalfan, mgeni kutoka Falme za Kiarabu. Kwa kuwa Salima alionekana na mawazo mengi kuhusu Dedan, Madam Flaviana aliona ni vyema amshawishi Salima kunywa pombe ili angalau apoteze mawazo. Madam Flaviana akajifanya kama vile alikuwa akimfundisha Salima majina mbalimbali ya vinywaji vikali na ladha yake, ambapo ilibidi Salima aonje na kutambua ladha ya kila pombe aliyopewa, somo ambalo Salima alivutiwa nalo na kujikuta siyo tu akionja, bali akinywa pombe hizo kwa kiwango kikubwa hadi akapoteza fahamu. Haraka wasichana waliokuwa wakihudumia mahali hapo wakambeba Salima na kumpeleka chumbani kwake kisha wakarudi na kuendelea na shughuli zao. Madam Flaviana akautumia muda huo kukutana na Side ili amuoneshe picha za Dedan alizozipata kutoka kwa Salima. ** “Vipi mume wangu mbona haupo sawa leo?” aliongea Sonia akimtazama mumewe Side ambaye tangu alipopokea simu ya Madam Flaviana aliyemtaarifu kuwa picha za Dedan zilikuwa zimepatikana alikuwa na wasiwasi mkubwa huku mikono yake ikitetemeka. Side alikuwa akiomba kimoyomoyo huyo kijana waliyemteka na kumhifadhi kwenye godauni la kiwanda cha vyuma ‘BIASI,’ asiwe Dedan kweli, kwani kwa vyovyote kama ni yeye basi kifo chake kilikuwa kikimkaribia. Akajikaza na kuvaa shati lake ambapo alikosea kufunga baadhi ya vifungo kwa uoga na wasiwasi. “Niambie ni nani sasa waliyekutuma ukamuue?” Sonia alizidi kumtwanga maswali Side, utadhani alikuwa akimfahamu vyema Side kiasi cha kutambua hata baadhi ya siri zake za kazi. “Nitakwambia nikirudi,” Side aliondoka na kufunga mlango kwa nguvu huku Sonia akibaki njia panda asijue ni kipi kilichokuwa kikimsumbua mumewe japo kuwa alipatwa na hisia kuwa lazima damu itamwagika mahali fulani. *** Sonia alikumbuka vyema siku ambayo alimuona Side akitetemeka kwa hofu ya kuua kama alivyomuona siku hiyo. Alikumbuka ambavyo alitamani kuifutilia mbali tarehe na mwezi ule ili isahaulike kabisa kutoka kwenye kalenda. Siku hiyo yeye Sonia, alikuwa ndiye mtu aliyetakiwa kuuawa na Mr. John Chakos.
Side aliyeiseti vyema bunduki yake katikati ya paji la uso wa Sonia, hakuweza kufanya chochote zaidi ya kumtazama kwa huruma. Sonia alikumbuka kuwa katika saa hizo zilizokosa nuru, ndipo alipomuona Side akiwa katika hali kama hiyo aliyomuona nayo muda mfupi uliopita. Ni wazi Side alikuwa akitetemeka kwa hofu ya kutekeleza kile alichotumwa na bosi wake. Hatimaye Side aliishusha silaha yake na kumtorosha Sonia kwa siri akimficha hapo katika Kijiji cha Ulongoni, nje kidogo ya mji na kuanza maisha mapya. Kwa msaada wa Side, Sonia alikuwa hai mpaka siku hiyo, hivyo Sonia hakusita kulipa fadhila kwa kukubali kuishi na mwanaume huyo kwa kuwa ni siku nyingi alikuwa akimuonesha wazi kuwa alikuwa akimpenda, lakini hakuweza kumwambia kutokana na hali ya maisha ilivyo ndani ya jumba la ‘Serenity.’ Kanuni zilijieleza wazi; Sonia alipaswa kuwa malaya wa kimataifa na Side alikuwa kibaraka wa kuhakikisha hayo yalifanyika bila kuuliza swali au kuingilia upande usiomhusu, kwa hiyo chochote alichojisikia moyoni mwake kuhusu Sonia kilipotea na upepo mpaka siku hiyo. Kwa vile Side alikuwa akiaminiwa sana na Chakos, hakukuwa na mtu yeyote aliyefuatilia kama alikuwa ameshafanya mauaji kama alivyokuwa ameagizwa au lah, kwani kwa kufoji maiti ya msichana mwingine, Side aliweza kumshawishi Mr. Chakos kuwa alitekeleza kila kitu kama alivyotumwa na bosi wake. Tangu siku hiyo, Sonia alikuwa ni mtu wa kukaa nyumbani tu huku muda wote akiufunika uso wake kwa baibui na nikabu ili watu wasijue kuwa yupo hai kwa kuwa kama angetambulika, hatari isingekuwa kwake pekee, bali hata kwa mumewe na watoto wake pia. Kwa uoga, Sonia alikaa chini na kusali akiomba kwa Mola wake kila kitu kiende salama kwa mumewe na huyo mtu aliyekuwa katika hali ya kuitetea roho yake. *** Diana na Zubeda walikuwa katika vyumba vyao chini ya Madam Bernadeta ambaye alikuwa ni kiongozi wa hosteli yao. Katika kila upande wa jengo kulikuwa na hosteli moja na kiongozi wake ambaye kazi yake ilikuwa ni kuhakikisha kila msichana alifanya kama alivyokuwa akiagizwa kutoka ngazi ya juu ambayo ni Madam Flaviana, naye akiongozwa na Mr. John Chakos. Chakos naye alikuwa chini ya Mr. George japokuwa hakuna mtu yeyote aliyewahi kuiona sura yake, hakuna, hata Chakos mwenyewe hakuwa akimfahamu mbali na kupewa maelekezo ya sauti na maandishi. Siku hiyo, Madam Bernadeta alikuwa na ujumbe kwa msichana Diana ambaye alikuwa akihitajika mara moja na utawala. Pasipo kujua jambo aliloitiwa, Diana alisimama na kumfuata Madam Bernadeta mara moja na kufungua mlango wa chumba kilichokuwa ghorofa ya juu kabisa. Mara milio ya risasi ikifuatiwa na sauti kali iliyoashiria maumivu makali ilisikika kwa mbali kutoka ndani ya chumba hicho. Kufumba na kufumbua kukawa na damu kila mahali, zikichirizika kutoka katika mwili wa Diana. “Safisha chumba na hakikisha hakuna mtu atakayejua kuhusu jambo hili, sawa!” Iliongea sauti ya kiume kutoka kwenye spika zilizokuwa ukutani ikimwambia Madam Bernadeta aliyekuwa amejibana nyuma ya chumba alichoingia Diana. “Ha…hakuna mtu atakayefahamu bosi,” alijibu Madam Bernadeta kwa uoga. “Vizuri, kesho asubuhi atakuja msichana mpya, jina lake ni Salima. Mpokee na mfahamishe kila kitu anachotakiwa kukifanya, nitakuwa nikifuatilia kila kitu!” “Sawa Mr. Chakos,” alijibu Madam Bernadeta huku sauti kali ya Mr. John Chakos ikipotea taratibu kwa njia ya mwangwi na kukiacha chumba alichoingia Diana kikiwa na ukimya wa hali ya juu. “Ooh, my God!” alihuzunika kimoyomoyo Madam Bernadeta mara baada ya kuuona mwili wa Diana ukiwa sakafuni hali ukiwa na matundu mengi ya risasi. Aliyafumba macho ya Diana ambayo bado yalikuwa yakitazama kisha akaiburuza maiti yake mpaka kwenye sinki kubwa lililojaa uji wa shaba iliyoyeyushwa na kuitumbukiza humo mpaka ikayayushwa na uji huo wa moto. “Ulichokitaka umekipata, si ulitaka kurudi nyumbani?” aliongea peke yake Madam Bernadeta huku akichora ishara ya msalaba hewani kama padri aombeavyo maiti. *** “Angalia!” aliongea Madam Flaviana huku akimpatia bahasha ndogo Side aliyeipokea kwa mashaka na kuifungua. “Ndiye, siye?” aliuliza Madam Flaviana akimtazama Side aliyekuwa akizikodolea picha alizozitoa ndani ya bahasha ile. “Vipi?” Madam Flaviana aliuliza tena baada ya kumuona Side akitetemeka kwa hofu kama mtu aliyeona jini. Picha zilikuwa sawa kabisa na mtu waliyemkamata usiku wa jana yake, isipokuwa tofauti ilikuwa ni unene na nywele ambazo kwenye picha alikuwa nazo tofauti na alivyomuona. Akili ya Side ikafanya hesabu za harakaharaka na kujipongeza kwa kile alichokiita kujihami, kwa kuwa alikuwa tayari ameishafikiria jinsi ya kumtorosha Dedan mapema kabla ya kufika hapo kwani alijua lazima Dedan atakuwa ni mtu yuleyule waliyemkamata jana yake. Kikwazo kikabaki kuwa Madam Flaviana. Side alijiuliza ikiwa mwanamke huyo atataka akamuone huyo mtu waliyemkamata jana yake wangempeleka nani tofauti na Dedan? Hata kama wangempeleka mtu mwingine ambaye Side tayari alikuwa ameshamuandaa badala ya Dedan je, Madam Flaviana atamwacha mtu huyo akiwa hai? Side alijiuliza maswali hayo kwanza kabla hajajibu swali aliloulizwa na Madam Flaviana. Hakutaka kuona damu ya mtu mwingine ikimwagika kwa ajili yake. Muda wa kufikiri ulikuwa umekwisha kwa Side, alihofia pengine angempandisha hasira Madam Flaviana kwa kuchelewa kujibu maswali yake haraka iwezekanavyo, kwa ujasiri akafungua kinywa chake. “Siye,” alijibu Side huku akishindilia picha zile ndani ya mifuko ya suruali yake. “Siye!..twende ukanioneshe huyo mtu uliyenaye,” aliongea Madam Flaviana kwa hamaki huku akipiga hatua kuelekea mahali lilipo godauni. Side alikuwa makini akiitegemea hatua hiyo ya Madam Flaviana, kwa pamoja wakaelekea ndani ya godauni hilo ambalo mara nyingi hulitumia kwa mambo yao ya kikatili. “Ooh shit! Namtaka Dedan haraka sana siyo chizi huyu!” aliwaka Madam Flaviana baada ya kumuona mtu asiyefanana hata chembe na Dedan akiwa amefungwa kitambaa kizito usoni na mikononi. Kwa hasira Madam Flaviana akaikoki bastola yake akitaka kumuulia mbali mtu huyo. Ghafla Side akamuwahi Madam Flaviana na kuukwepesha mkono wake, risasi mbili zikatua pembeni bila kumpata huyo chizi. “Madam, mtu mwenyewe ni chizi asiyejitambua unapoteza nguvu zako bure,” aliongea Side akimpooza Madam Flaviana aliyefura kwa hasira. Kwa ushawishi huo Side alifanikiwa kumuondoa Madam eneo hilo bila ya damu ya mtu yeyote kumwagika. Akamfungulia chizi huyo na kumuacha huru aondoke zake, cha kushangaza ndiyo kwanza alikuwa aking’ang’ania kubaki maeneo hayo bila uoga wowote. *** Salima aliamka katikati ya usiku akiwa mchovu sana kutokana na wingi wa pombe alizokunywa mchana wa siku hiyo. Akiwa amechanganywa na giza la usiku, alihisi huenda alipitiliza siku nzima akiwa kitandani. Akilini mwake alihitaji kujua nini kilikuwa kikiendelea muda wote alipokuwa amelala. Akaamka na kuufungua mlango wa chumba chake akaelekea kwenye korido kuu inayovitenga vyumba vingi katika upande wa kulia na kushoto. Ukimya wa hali ya juu ndani ya jengo hilo haukumtisha na kumfanya asitembee huku na huko akichunguza kila sehemu ya jengo hilo ambalo tangu ahamishie makazi yake humo hakuwahi kulichunguza. Akiwa katika kutembea huko, ghafla alihisi kuna mtu alikuwa akimfuata nyuma yake. Mwili wake ukasisimka kwa mtindo wa ajabu. Akageuka nyuma na kutazama, lakini hakukuwa na mtu yeyote. Bila hofu Salima akaendelea kutembeatembea, bila kujua kuwa hisia zake zilikuwa kweli, kwani Mr. John Chakos ndiye mtu pekee aliyekuwa akimtazama kupitia kamera zilizotegwa humo ndani akimfuatilia kila alipokuwa akielekea usiku huo. Alimaliza kuzunguka kila mahali katika ghorofa hiyo, akapanda ngazi inayoelekea ghorofa ya juu yake na kushangazwa na muundo uleule wa vyumba kama ulivyokuwa katika ghorofa aliyoitazama mwanzoni. Vyumba vingi katika ghorofa hiyo vilikuwa havina madirisha wala milango iliyoruhusu kutazama mazingira ya nje. Kwa namna moja ama nyingine Salima alistaajabishwa na ramani ya jengo hilo lililokaa kama aina fulani ya gereza. Akiwa katika mawazo hayo mara alisikia muungurumo wa lifti ikishuka kutoka ghorofa ya juu na kusimama. Mara akasikia sauti ya mlango wa umeme ukifunguka na kufuatiwa na hatua za watu. Hakutaka kukamatwa akichunguzachunguza mambo ya watu usiku kama alivyokuwa akifanya. Hatua zilizidi kusogea kuelekea mahali alipokuwa. Laiti kama angechelewa kujificha kwa dakika moja tu, basi watu hao waliokuwa wakipita maeneo hayo wangemkuta hapo. Kwa muda huo kona ya korido tu ndiyo iliyokuwa ikimfanya asionekane. Bila kupoteza muda Salima alijaribu kufungua mlango wa chumba kilichokuwa karibu yake mara moja ukafunguka kisha akajitosa ndani yake asijue kama chumba hicho kilichotanda kwa kiza totoro kilikuwa ni cha nani!
Hatua zile zilifika na kukomea hapohapo kwenye chumba alichoingia Salima. Mara akasikia mlango ukifunguliwa na kufungwa huku sauti za minong’ono na miguno ya kimahaba zikisikika kutoka kwa watu hao ambao kwa sauti zao, Salima aliwatambua kuwa wote walikuwa wanawake. Salima alikuwa ameshajua jinsi gani alivyojiweka matatani kwa kuingia ndani ya chumba hicho, kwani kama angelikubali aibu ya kukamatwa akizungukazunguka kwenye vyumba vya ghorofa isiyomhusu, ingelikuwa afadhali kuliko kujitokeza muda huo, tena akiwa ameshaingia kwenye chumba cha watu. Akaendelea kujificha nyuma ya sofa kimya bila kutikisika wala kutoa sauti akisubiri nini kitakachofuatia. *** Wakati huo Mr. John Chakos alikuwa akikosa uhondo wa kuona kile kilichokuwa kikiendelea ndani ya kile chumba. Kamera zake zilishindwa kupata picha angavu kutokana na kiza kilichotanda ndani ya chumba hicho. Mara ya mwisho alimuona Salima akijificha na kukimbilia humo ndani ambapo baada ya dakika chache, aliwaona Madam Bernadeta na Julieth nao wakiingia huku wakiwa wamekumbatiana na kupigana mabusu mfululizo. Mara nyingi amekuwa akiwaona wakiwa katika hali hiyo na pengine hata wakifanya mapenzi ya jinsi moja. Jambo hilo halikumsumbua Chakos hata kidogo kwa kuwa Madam Bernadeta na Delilah walikuwa wakifanya kazi zao vizuri. Mr. Chakos alitaka kushuhudia jinsi ambavyo Salima atajiokoa na kutoka humo chumbani bila kuonekana. Akawa makini kuangalia video ya chumba kile bila kupepesa macho kwa kuhofia kupitwa na shoo ile. “Wawili kwa mmoja, Salima! Mtoto mzuri utatokaje?” Mr. Chakos alijikuta akizungumza mwenyewe huku macho yake yakiangalia kwa makini giza nene la chumba kile kwa kutumia televisheni kubwa zilizounganishwa kitaalamu na kamera za jengo zima la Serenity, lakini aliambulia kusikia sauti za akina Madam na Delilah tu wakiwa katika mambo yao. *** Usiku huo, Madam Flaviana akiwa kwenye gari lake tayari kwa kuondoka, machale yakamcheza. Akairudisha siku nyuma na kutafakari, taratibu akaona shaka juu ya tabia ya Side. Alikumbuka jinsi Side alivyokuwa na wasiwasi alipomkabidhi azitazame picha za Dedan, pia alishindwa kujua kwa nini Side alikuwa na huruma kiasi kile hata akamkwepesha mkono wake alipotaka kumfyatulia risasi yule mwendawazimu aliyefungwa ndani ya godauni! Madam Flaviana alihisi kuna kitu kilichokuwa kikiendelea nyuma ya pazia. Akaanza rasmi kumtilia shaka Side. Akainua simu yake ya mkononi na kubofya namba kadhaa kisha akaiweka sikioni na baada ya muda kidogo “Haloo Henry,” aliongea Madam Flaviana kwa madaha huku akivuta sigara kubwa maarufu kama ‘cigarette.’ “Haloo Madam,” ilisikika sauti nzito kutoka upande wa pili wa simu. “Ninahitaji kukupa kazi nzito, upo tayari?” “Sema ni nani nikammalize!” “It’s a rat out mission, no one in particular people (ni mpango wa kumfichua msaliti, siyo mtu fulani moja kwa moja).” “Guess it’s like old times, is it! (Nadhani ni kama enzi zile au siyo!)” “Yeah! It’s like old times (Ndiyo, sawia kabisa)” “Hesabu kazi yako imekwisha. Ni nani mtu huyo?” “Unamkumbuka Side?” “Yeah, unahitaji nini kuhusu yeye?” “Kikubwa nahitaji kujua kila kitu anachokifanya, narudia tena kila kitu!” “Mh! Nahisi itakugharimu kidogo. Nadhani unajua kuwa mimi ni muuaji siyo paparazi?” “Usihofu kuhusu malipo, nusu kabla na nusu ukimaliza kazi, sawa?” “Ok sawa.” Baada ya kumaliza kuongea na mtu huyo, Madam Flaviana akawasha gari lake na kutokomea gizani, akifikiria jinsi gani Side ataliepuka hilo zimwi aliloliamsha juu yake. “Better be without any secret Side, otherwise you will be dead (Bora usiwe na siri Side, la sivyo utakufa).” *** Baada ya purukushani za muda kwenye kitanda, hatimaye muda ulifika na watu hao wakawa kimya kabisa huku sauti pekee Salima aliyokuwa akiisikia ni mlio wa moyo wake tu ambao ulikuwa ukidunda kwa nguvu. “Madam, nitakuja kesho mi naondoka bwana,” aliongea Julieth na kusimama akiwa na nguo zake mkononi. “Subiri kwanza kwani unawahi nini?” alisema Madam Bernadeta akimvutia Julieth ndani ya kitanda chake. “Unamjua yule msichana mpya?” alisema Madam Bernadeta kwa kunong’ona huku akiendelea kumtomasatomasa Julieth. “Namjua yule anayeitwa Salima?” Salima alishtuka baada ya kusikia jina lake likitajwa, akatega masikio yake ajue ni nini kilichokuwa kikitaka kuongelewa kuhusu yeye.
Simulizi : Kitanzi, Kisu Na Bastola Sehemu Ya Nne (4)
ILIPOISHIA “Unamjua yule msichana mpya?” alisema Madam Bernadeta kwa kunong’ona huku akiendelea kumshikashika Julieth. “Namjua si yule anayeitwa Salima?” Salima alishtuka baada ya kusikia jina lake likitajwa, akatega masikio yake ajue ni nini kilichokuwa kikitaka kuongelewa kuhusu yeye. Songa Nayo… “Unamwonaje mzuri eee?” aliongea Madam Bernadeta huku mikono yake ikiwa kifuani kwa Julieth. “Usiniambie kama tayari umeshampenda ukaniacha mimi!” Julieth alijibu kwa hasira zilizochanganyika na wivu huku akijitoa mikononi mwa Madam Bernadeta na kuketi kitandani. “Aaa…hapana siyo hivyo ni hivi, kesho atahamia chumbani kwa Diana, ninataka uwe naye karibu. Hakikisha anafuata kila kitu atakachotakiwa kukifanya. Kikubwa ninataka uwe rafiki yake. Mpeleleze na uniambie kila kitu atakachokuwa akikifanya wakati mimi sipo karibu naye.” “Usijali, ni hilo tu?” aliuliza Julieth na kushusha pumzi ndefu kifua chake kikiyeyusha chuki nzito na wivu ulioanza kujijenga moyoni mwake baada ya kumsikia Madam Bernadeta akimtaja huyo msichana mpya mbele yake. Akasimama na kuufungua mlango, taratibu akatoka nje ya chumba hicho kisha akaufunga kama ulivyokuwa awali na kutembea hatua kadhaa hadi chumbani kwake, bila kujua kama kuna watu walikuwa makini wakiwasikiliza kila kitu walichokuwa wakizungumza Mr. John Chakos na Salima. Ni wazi kuwa Salima alikuwa msichana mzuri wa umbo na sura, kila mtu aliliona hilo. Kwa Julieth uzuri wa Salima ukawa kikwazo kikubwa kwa kuwa alianza kuhofia taji lake la urembo wa ‘Serenity’ kunyakuliwa na msichana huyo mpya. Siku zote yeye ndiye aliyeonekana msichana mrembo kuliko wote humo ndani. Uzuri wake uliifanya thamani na hadhi yake iwe juu zaidi ya wasichana wote ambao huuzwa ndani ya jengo hilo. Kila mgeni muhimu alipoingia nchini Tanzania, Julieth ndiye aliyepewa kipaumbele kutembea naye kuliko msichana mwingine yeyote. Hivyo ujio wa msichana mrembo na mzuri zaidi yake ulikuwa kikwazo kwake, alihisi kila kitu alichokuwa akiringia kilikuwa mashakani kuchukuliwa na Salima; kuanzia wateja, hadhi, marafiki na mwisho kabisa, penzi la Madam Bernadeta. Julieth hakufikiria kuruhusu hayo yote yatokee, aliwaza kufanya kila atakachoweza kupambana na adui yake. *** Muda wote huo Salima alikuwa akitafakari kitu gani kilichowapa haki wasichana hao wawili wapange kumbembeleza yeye. Alijiuliza kwa nini alikuwa akitakiwa kuhama chumba chake kesho asubuhi na kuhamia chumbani kwa msichana waliyemtaja kwa jina la Diana? Akili yake haikuweza kufikiria sawasawa katika hali hiyo, alitaka kuwa huru kwa kutoka humo ndani kwanza na kurudi chumbani kwake kabla muda haujazidi kuyoyoma. Kama vile paka mwizi, aliinua shingo yake na kumchungulia Madam Bernadeta ambaye alionekana kuanza kukolea usingizi mzito kwa uchovu mwingi wa yote waliyoyafanya dakika chache zilizopita na Julieth. Wataalamu wa saikolojia husema kwamba mtu akiwa katika dakika arobaini za mwanzo za usingizi, mfumo wake wa fahamu huwa katika hali isiyoeleweka kiasi kwamba mtu huyo hawezi kuamka mwenyewe wala kuamshwa hata kama kungetokea kitu cha kushtusha kiasi gani. Salima alijifunza kuhusu hilo sehemu fulani lakini hakujua ilikuwa wapi moja kwa moja. Akilenga kutumia mbinu hiyo alisimama na kunyata taratibu akikipita kitanda cha Madam Bernadeta aliyekuwa akijigeuza mara kwa mara na kuusogelea mlango. Kama mahesabu yake yalikuwa sawa, Madam Bernadeta hata kama angejigeuza vipi asingeweza kuamka muda huo, lakini kama mahesabu yake yalikuwa na hitilafu basi siku hiyo ndiyo ingekuwa arobaini yake japo kuwa siku thelathini na tisa zilizopita hakuzitumia kuchunguza vitu vya watu kama ilivyokuwa siku hiyo. “Mungu nisaidie,” Salima alijikuta akisema kimoyomoyo na kunyonga komeo la mlango kisha akafungua haraka akatoka nje na kushuka ghorofa hilo isiyomhusu ambapo moja kwa moja aliingia chumbani kwake na kujifungia huku akihema kwa nguvu. *** Asubuhi ya siku iliyofuata Side alijua lazima atakuwa na la kujibu kwa mkewe Sonia, hasa kumueleza kuhusu kila kitu ambacho kilitokea usiku wa jana yake na kuhusu huyo mwendawazimu aliyemhifadhi siku nzima ndani ya chumba cha wageni kwenye nyumba yao. Huku macho yake akimkazia Side, Sonia alichukua sahani kubwa ya matunda na kumsogezea Dedan ambaye alitazama ulaji wake kwanza na kuiga mfano kutoka kwa mwenyeji wake Side ambaye aliyazoa matunda hayo na kuyameza huku mbegu tu akizitema kama sehemu isiyofaa kuliwa ya tunda hilo la zabibu. Kwa utamu wa matunda hayo Dedan alijikuta akimaliza sahani nzima na kutaka tena na tena jambo ambalo liliendelea kumfanya Sonia azidi kumkazia macho mumewe Side. Ghafla alamu ya mlango ikalia. Sonia akakimbilia chumbani kwake na Side akamficha Dedan mahala kisha akaenda kufungua mlango.Kwa kuwa kuua kulikuwa ndani ya damu yake, Henry hakuona shida yoyote zaidi ya kufurahia amri hiyo. Tofauti na zamani, siku hiyo wala dhamira yake haimsuti juu ya damu za watu alizozimwaga kwa mikono yake. Alikuwa akizidi kuendelea kufanya ushetani wake kwa furaha kabisa kama vile kuua ilikuwa ni aina fulani ya mchezo. Si kilio cha Sonia wala machozi ya Dedan yalimfanya awaonee huruma na kuwaachia mateka wake hao. Badala yake Henry alikuwa akiwaangalia na kucheka kila mara Sonia alipolia kwa uwoga baada ya kumgusagusa na mdomo wa bastola yake. Henry alichagua sehemu nzuri mbali kabisa na makazi ya watu kiasi kwamba hakupata bugudha yoyote kuwahifadhi mateka wake. Sauti ya vilio vya kimyakimya ndivyo ambavyo vilisikika eneo hilo kutoka kwa Sonia ambaye huenda angepiga makelele kwa nguvu kama tu asingefungwa kwa kitambaa kizito mdomoni. ** Side aliingia kila chumba ili kuhakikisha kama kweli mkewe Sonia hakuwemo ndani; kitu ambacho kilikuwa sahihi. Akawaza labda alikuwa nje mahali fulani. Labda aliondoka bila kuaga! Alitafakari wazo hilo na kutolipa uzito kwani Sonia hakuwa na tabia ya kutoka nje, alikuwa ni mtu wa kukaa ndani muda wote akihofia kujulikana na watu. Hata mavazi yake yalikuwa ni yale yaliyomficha mwili mzima na kuacha macho tu. Alipokuwa akitembea kuelekea mlango wa nyuma ambao ndiyo ulikuwa umefunguliwa, Side aligundua alama za viatu asivyovifahamu kwenye ardhi ya mlango wake. Ni wazi mtu asiyemjua aliingia na kutoka ndani ya nyumba yake. Kama vile mchunguzi wa masuala ya uhalifu (forensic), Side alitafuta kila mahala alama yoyote itakayomdhihirishia alichokuwa akikiwaza, kuwa jambo lililotokea muda mfupi nyumbani kwake lilikuwa ni utekaji nyara na si vinginevyo. Mara akagundua kuchunika kidogo kwa rangi kwenye kichuma cha loki ya mlango ulioachwa wazi jambo lililomfanya agundue kuwa mlango huo ulisukumwa kwa nguvu na aliyeingia ndani. Moyo wa Side ukaanza kudunda kwa kasi kiasi cha jasho jingi kumtoka kama vile mtu aliyechanganyikiwa. Side alishindwa kutoa taarifa polisi wala sehemu yoyote ya usalama kwa kuwa alihofia kwa kufanya hivyo atamuanika Sonia mbele ya wabaya wake. Kuna ule muda mtu huwa hafikirii chochote zaidi ya kuwa na hofu isiyokuwa na mfano, muda huo ulikuwa juu ya Side kwa siku hiyo akaanza kutetemeka kwa woga. Moyo wake mara ulifanya pah! Aliwakumbuka watoto wake mapacha ambao alizaa na mkewe Sonia wote walikuwa katika shule ya malezi ya awali kwa watoto ‘Msami Day Care.’ Kwa kasi ya ajabu Side alifika shuleni lakini jibu ni kwamba hawakuwepo hapo na walimu hawakujua wapi walipokwenda ingawa ushahidi wa watoto hao kuripoti shuleni asubuhi ulikuwepo. Kwa uchungu Side alifumba macho yake kwa nguvu, machozi yakimtiririka mashavuni kama mtoto mdogo. Kitu alichokuwa akikitaka kujua zaidi ni nani aliyekuwa akimfanyia mambo yote hayo? Akiwa mwenye kukosa matumaini, simu yake ya mkononi iliita kwa namba asiyoifahamu akaipokea na kusikiliza: “Haloo Side, kama unamthamini mkeo na watoto wako rudi nyumbani kwako haraka sana, nina zawadi yako,” iliongea sauti ya mtu asiyemfahamu kwa kujiamini. “Sema unataka shilingi ngapi nikupatie, naomba uniachie familia yangu,” alisema Side kwa pupa huku machozi yakimtoka. “Usiwe kama mwanamke Side, inuka uje mara moja na nikukumbushe tu, uje peke yako ukifanya ujanja wowote mkono wangu sitauzuia juu ya watoto wako.” “Nakuja naomba usiwafanyie jambo lolote baya.” “Kuna usemi unaosema kuwa muuaji akilia hulia machozi ya kweli siyo bandia unajua maana yake? Ngoja nikwambie ni vile tu muuaji hujua maumivu ya mateso kuliko mtu yeyote yule, naamini unafahamu fika jinsi inavyokuwa. Una dakika kumi au nitaanza na mkeo,” alisema muuaji huyo na kukata simu. Bila kupoteza muda, Side alikimbilia nyumbani kwake pasipo kujali hatari itakayomkuta. *** Salima aliburuzwa mpaka ghorofa ya tatu, safari yake wakati huu ikaishia ndani ya chumba kimoja ambacho aliamini ndicho kilichokuwa kinakaliwa na msichana aliyesikia akizungumziwa usiku wa jana yake, Diana. “Kuanzia leo hautaruhusiwa kukaa na simu wala kitu chochote kitakachokuwezesha kufanya mawasiliano nje ya jengo hili, mimi ndiye utakayepaswa kunisikiliza na kuniuliza kila kitu unachokiona haujakielewa. Sheria zetu zipo kila mahali ndani ya jengo hili kuwa makini uzisome kwanza kabla ya kufanya jambo lolote mahali popote, jambo la mwisho kuanzia leo jina lako litakuwa Carolina,” alimaliza kusema mwanamke huyo ambaye sauti yake, Salima aliikumbuka vyema kwa kuwa aliisikia jana yake. “Huyu lazima atakuwa Madam Bernadeta,” aliwaza Salima masikio yake yakishindwa kuamini kama alipewa jina la mwanamke ambaye alikuwa hasimu wake wa muda mrefu kabla ya kuelewana naye dakika chache zilizopita. Kwa kuwa kuua kulikuwa ndani ya damu yake, Henry hakuona shida yoyote zaidi ya kufurahia amri hiyo. Tofauti na zamani, siku hiyo wala dhamira yake haimsuti juu ya damu za watu alizozimwaga kwa mikono yake. Alikuwa akizidi kuendelea kufanya ushetani wake kwa furaha kabisa kama vile kuua ilikuwa ni aina fulani ya mchezo. Si kilio cha Sonia wala machozi ya Dedan yalimfanya awaonee huruma na kuwaachia mateka wake hao. Badala yake Henry alikuwa akiwaangalia na kucheka kila mara Sonia alipolia kwa uwoga baada ya kumgusagusa na mdomo wa bastola yake. Henry alichagua sehemu nzuri mbali kabisa na makazi ya watu kiasi kwamba hakupata bugudha yoyote kuwahifadhi mateka wake. Sauti ya vilio vya kimyakimya ndivyo ambavyo vilisikika eneo hilo kutoka kwa Sonia ambaye huenda angepiga makelele kwa nguvu kama tu asingefungwa kwa kitambaa kizito mdomoni. *** Side aliingia kila chumba ili kuhakikisha kama kweli mkewe Sonia hakuwemo ndani; kitu ambacho kilikuwa sahihi. Akawaza labda alikuwa nje mahali fulani. Labda aliondoka bila kuaga! Alitafakari wazo hilo na kutolipa uzito kwani Sonia hakuwa na tabia ya kutoka nje, alikuwa ni mtu wa kukaa ndani muda wote akihofia kujulikana na watu. Hata mavazi yake yalikuwa ni yale yaliyomficha mwili mzima na kuacha macho tu. Alipokuwa akitembea kuelekea mlango wa nyuma ambao ndiyo ulikuwa umefunguliwa, Side aligundua alama za viatu asivyovifahamu kwenye ardhi ya mlango wake. Ni wazi mtu asiyemjua aliingia na kutoka ndani ya nyumba yake. Kama vile mchunguzi wa masuala ya uhalifu (forensic), Side alitafuta kila mahala alama yoyote itakayomdhihirishia alichokuwa akikiwaza, kuwa jambo lililotokea muda mfupi nyumbani kwake lilikuwa ni utekaji nyara na si vinginevyo. Mara akagundua kuchunika kidogo kwa rangi kwenye kichuma cha loki ya mlango ulioachwa wazi jambo lililomfanya agundue kuwa mlango huo ulisukumwa kwa nguvu na aliyeingia ndani. Moyo wa Side ukaanza kudunda kwa kasi kiasi cha jasho jingi kumtoka kama vile mtu aliyechanganyikiwa. Side alishindwa kutoa taarifa polisi wala sehemu yoyote ya usalama kwa kuwa alihofia kwa kufanya hivyo atamuanika Sonia mbele ya wabaya wake. Kuna ule muda mtu huwa hafikirii chochote zaidi ya kuwa na hofu isiyokuwa na mfano, muda huo ulikuwa juu ya Side kwa siku hiyo akaanza kutetemeka kwa woga. Moyo wake mara ulifanya pah! Aliwakumbuka watoto wake mapacha ambao alizaa na mkewe Sonia wote walikuwa katika shule ya malezi ya awali kwa watoto ‘Msami Day Care.’ Kwa kasi ya ajabu Side alifika shuleni lakini jibu ni kwamba hawakuwepo hapo na walimu hawakujua wapi walipokwenda ingawa ushahidi wa watoto hao kuripoti shuleni asubuhi ulikuwepo. Kwa uchungu Side alifumba macho yake kwa nguvu, machozi yakimtiririka mashavuni kama mtoto mdogo. Kitu alichokuwa akikitaka kujua zaidi ni nani aliyekuwa akimfanyia mambo yote hayo? Akiwa mwenye kukosa matumaini, simu yake ya mkononi iliita kwa namba asiyoifahamu akaipokea na kusikiliza: “Haloo Side, kama unamthamini mkeo na watoto wako rudi nyumbani kwako haraka sana, nina zawadi yako,” iliongea sauti ya mtu asiyemfahamu kwa kujiamini. “Sema unataka shilingi ngapi nikupatie, naomba uniachie familia yangu,” alisema Side kwa pupa huku machozi yakimtoka “Usiwe kama mwanamke Side, inuka uje mara moja na nikukumbushe tu, uje peke yako ukifanya ujanja wowote mkono wangu sitauzuia juu ya watoto wako.” “Nakuja naomba usiwafanyie jambo lolote baya.” “Kuna usemi unaosema kuwa muuaji akilia hulia machozi ya kweli siyo bandia unajua maana yake? Ngoja nikwambie ni vile tu muuaji hujua maumivu ya mateso kuliko mtu yeyote yule, naamini unafahamu fika jinsi inavyokuwa. Una dakika kumi au nitaanza na mkeo,” alisema muuaji huyo na kukata simu. Bila kupoteza muda, Side alikimbilia nyumbani kwake pasipo kujali hatari itakayomkuta. *** Salima aliburuzwa mpaka ghorofa ya tatu, safari yake wakati huu ikaishia ndani ya chumba kimoja ambacho aliamini ndicho kilichokuwa kinakaliwa na msichana aliyesikia akizungumziwa usiku wa jana yake, Diana. “Kuanzia leo hautaruhusiwa kukaa na simu wala kitu chochote kitakachokuwezesha kufanya mawasiliano nje ya jengo hili, mimi ndiye utakayepaswa kunisikiliza na kuniuliza kila kitu unachokiona haujakielewa. Sheria zetu zipo kila mahali ndani ya jengo hili kuwa makini uzisome kwanza kabla ya kufanya jambo lolote mahali popote, jambo la mwisho kuanzia leo jina lako litakuwa Carolina,” alimaliza kusema mwanamke huyo ambaye sauti yake, Salima aliikumbuka vyema kwa kuwa aliisikia jana yake. “Huyu lazima atakuwa Madam Bernadeta,” aliwaza Salima masikio yake yakishindwa kuamini kama alipewa jina la mwanamke ambaye alikuwa hasimu wake wa muda mrefu kabla ya kuelewana naye dakika chache zilizopita.
Baada ya kuongea hayo, Madam Bernadeta na hao wanawake alioingia nao wakaondoka na kumuacha Salima peke yake. Akili yake ikiwa juu ya maneno makali aliyoambiwa na Caro kupitia ujumbe wa simu dakika chache zilizopita, alihisi yalikuwa yakianza kutimia kwa kuwa walishaanza kumkataza kuwa na mawasiliano na mtu yeyote wa nje bila kuambiwa sababu za msingi pia sauti ya Madam Bernadeta ilikuwa yenye mamlaka na amri tofauti na vile alivyoongeleshwa na mtu yeyote tangu alipoingia mara ya kwanza katika jengo hilo. “Labda wamenisikia nikiongea na Caro?” alijiuliza Salima huku akiyakumbuka vyema maneno aliyotumiwa na Caro kwa njia ya ujumbe mfupi muda mchache uliopita ukisomeka: “Kila unachokiongea na kukifanya kuna mtu anakutazama.” *** Kama ilivyo kwa mwanaume yeyote, akili ya Dedan iliwaka ari ya kutaka kujiokoa toka kwenye kifungo alichomo. Japo alikuwa amefungwa vyema mikono na miguu yake, tena akiwa na kitambaa kizito mdomoni, alihisi lazima afanye jambo ili kujisaidia yeye na mwanamke aliyekuwa mkarimu kwake tangu alipofika nyumbani kwake usiku uliopita. Mwanamke huyo hakuwa mwingine zaidi ya Sonia ambaye ingawa Dedan hakujua vyema wasifu wake, lakini aliamini hakustahili kupitia mateso hayo pamoja naye siku hiyo. Moyoni aliazimia kuurudisha wema wa Sonia na mumewe Side kwa kuwaokoa na hatari yoyote ambayo ingewakuta siku hiyo bila kujua kuwa yeye ndiye alikuwa chanzo cha yote kwani kama Side asingejihangaisha kumuokoa yeye, Madam Flaviana angejuaje kama alikuwa akificha siri hadi kumtuma Henry amchunguze? Dedan alijitahidi kwa shida kujinyonganyonga mpaka akafanikiwa kuigeuza mikono yake iliyofungwa kwa nyuma na kuwa mbele kama ambavyo huwa kwa kawaida. Kwa muda mrefu Dedan aliisuguasugua kamba ngumu aliyofungwa mikono yake kwenye ncha ya gogo la mti lililokuwa karibu yake mpaka ikalainika na kukatika. Kwa kuwa mikono yake ilikuwa huru aliweza kuifungua kwa wepesi kamba iliyokuwa miguuni mwake na baadaye kumfungulia Sonia kisha wote wakaondoka maeneo hayo. “Fanya haraka tuondoke asije kurudi hapa na kutukuta,” Sonia alisema kwa hofu wote wakielekea nyumbani kwao bila kujua kama Henry alikuwa huko tayari na watoto wake. *** Side alifika nyumbani kwake mara moja. Hakuwa na muda wa kujihami hata kidogo. Kitu alichokifikiria mbele yake ni jinsi atakavyoweza kuiokoa familia yake toka kwa bedui mmoja aliyetumwa na Serenity mara baada ya siri zake kufichuka. Kwa kuwa alikuwa akifanya nao kazi kwa muda mrefu, alijua fika kiwango cha adhabu yake kwa makosa aliyoyafanya. Alijua hakuna hata chembe hai moja katika mwili wake itakayosalia. Kifo chenye maumivu makali ndiyo adhabu ndogo aliyojikadiria kupewa pindi Madam Flaviana na Mr. Chakos atakapomtia mkononi. Side alijua hakuwa na cha kufanya. Alitambua wajibu wake ni kuitetea familia yake kuliko kitu kingine chochote. Akapiga moyo konde na kuvuka barabara ya mwisho kuingia nyumbani kwake, saa yake ya mkononi ilionesha kuwa aliwahi kwa dakika nne kati ya kumi alizopewa na mtekaji nyara. Hatua mbili kabla hajafika kwenye geti la nyumba yake alihisi mkono mzito ukimshika begani alipogeuka tu! *** Side hakukumbuka kitu chochote tokea hapo zaidi ya kushtuka akiwa katika moja ya vyumba vyake huku mikono na miguu yake ikiwa imefungwa hali kadhalika midomo yake. Masikio yake yaliruhusiwa kusikia sauti za watoto wake wadogo wakilia chumba cha pili kutoka kile alichopo. Kwa upendo uliopitiliza juu ya wanae, Side alijikuta akimwaga machozi kama mtoto mdogo akijilaumu kwa kila jambo alilolifanya. Akiwa katika hali hiyo, mara mlango ukafunguliwa na mtu asiyemfahamu. Alipoangalia kiatu chake aligundua kuwa ndiyo kiatu chenye soli alizoziona mapema siku hiyo nje ya nyumba yake. Alipomsikiliza sauti yake kwa makini, aliitambua kuwa ndiyo ileile iliyozungumza naye muda mfupi ikimtaka arejee nyumbani kwake mara moja. Woga ulimshika akatulia kimya akisubiri nini kitafuatia kwani alishamjua mtekaji wake kuwa ni Henry ‘Ze Deader’ maana yake ni ‘Muuaji Wauaji’ kama ambavyo aliwahi kumsikia Madam Flaviana na Mr. Chakos wakimzungumzia mara kadhaa huko nyuma. Akiwa amekosa msaada wowote, Side alijigaragaza sakafuni kila muuaji wake alivyozidi kumsogelea. Kwa mikogo, Henry aliichukua simu yake na kupiga kutoa maagizo kwa mtu fulani. “Muda ndiyo huu, hakikisha unaipeleka hiyo mizigo Serenity mara moja ikiwa kama ilivyo. Wakikuzidi nguvu ua!” alisema Henry bila kujali jinsi gani Side aliumia kwani alishajua kuwa mizigo iliyokuwa ikizungumziwa ni mkewe Sonia na Dedan. “Inaonekana Madam Flaviana anakupenda sana. Eti ameniambia nikumalize mara moja ila hakuniambia kwa njia gani, so i will make it faster and painless (kwa hiyo nitafanya haraka bila maumivu) kwa ajili ya heshima yake,” alisema Henry huku akimtazama Side aliyekuwa akihangaika kujaribu kujifungua kamba alizofungwa baada ya kujua hatima yake. Bila huruma, Henry aliichomoa bastola yake na kuifunga ‘silenser’(kidhibiti sauti) kisha akafyatua risasi kadhaa zilizotua vyema katika mwili wa Side. Mithili ya paka shume Henry akaondoka ndani ya jengo hilo akiwa tayari ameliwasha moto akilenga kuwateketeza watoto wa Side ndani yake. *** Wakiwa bado mbali na makazi ya watu, Dedan na Sonia walihangaika huku na huko kuitafuta barabara na makazi ya watu. Kila kona walikuwa wamezungukwa na vichaka wasijue waendako. Dedan ndiye alikuwa wa kwanza kusikia mngurumo wa gari upande wake wa kushoto. Akamshika mkono Sonia na wote wakakimbilia upande huo na kulisimamisha gari hilo wakapanda bila kujua muendeshaji wake kuwa ni mtu yuleyule aliyetumwa na Henry dakika chache zilizopita. *** Madam Flaviana aliketi pembezoni mwa Mr. Chakos, kama kawaida yao walikuwa wamezungukwa na kompyuta nyingi zilizounganishwa na kamera za CCTV zilizotegwa vyema ndani ya jengo la Serenity wakiangalia kila kitu kilichokuwa kikifanyika ndani ya jengo hilo. Hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa akiijua siri ya kamera hizo isipokuwa wao tu na bosi wao Mr. George ambaye bado hakuna hata mmoja kati yao aliyekuwa akimjua kwa sura. “Haya Sonia ameishapatikana vipi kuhusu Caro?” Madam Flaviana alimuuliza Chakos. “Caro atapatikana tu. Nimewatuma watu wamtafute kwenye mtandao kupitia simu ya mwisho aliyompigia Salima. Wewe hakikisha hakuna kinachoharibika, tumebakiza mwezi mmoja tu kabla Prince Khalfani hajafika jijini,” alisema Chakos na kunyamaza ghafla macho yake yakiangalia kwa makini video iliyomuonesha Julieth akigonga mlango wa chumba cha Salima aliyepewa jina la Carolina muda mfupi uliopita. *** Salima aliufungua mlango na kushtushwa na msichana mrembo aliyekuwa amesimama mbele yake. “Naitwa Julieth nimesikia wewe ni mgeni hapa. Unaitwa Caro si ndiyo?” alisikika Julieth huku akijikaribisha mwenyewe ndani ya chumba cha Salima na kukaa kitandani. Kwa sauti ile, Salima aligundua mara moja kuwa mwanamke huyo ndiye aliyekuwa chumbani kwa Madam Bernadeta siku ile. “Njoo huku,” aliita Julieth na kusimama. Bila ubishi Salima akamfuata kwa nyuma. Walipita korido ndefu na kuingia ndani ya chumba kimoja kilichoandikwa ‘Restroom.’ Salima alipigwa na butwaa baada ya kuwaona wasichana wengi wasiopungua thelathini wote wakiwa wamevalia nguo zinazofanana na zile alizovaa yeye na Julieth. Wasichana wote waliokuwa ndani ya chumba hicho walikuwa wakimtazama yeye peke yake huku wengi wao wakionekana kumtazama zaidi mpaka akainama chini kwa aibu akitamani kujificha nyuma ya Julieth. “Jamani huyu ni Caroline. Atakuwa na sisi kuanzia leo,” Julieth alimtambulisha Salima huku wasichana wale wote wakimsikiliza kwa makini. “Vipi amepitia ‘initiation’ au bado?” aliuliza msichana mmoja, kufumba na kufumbua macho wote wakamvamia Salima wakimshambulia. “Pole Caro sote tumepitia hilo,” alisema Julieth huku naye akijiunga nao. Salima alibaki akipiga makelele akiomba msaada na kujitetea kila alivyoweza lakini hakuna hata mmoja aliyemuogopa zaidi ya kuzidi kumuandama Ilikuwa kama jambo la utamaduni, endapo msichana mpya atatambulishwa basi lazima apitie sharti gumu la kuvuliwa nguo zake zote na wasichana waliomtangulia kama utaratibu wa kuingia ndani ya jengo hilo. Shughuli hiyo ndiyo huitwa ‘initiation.’ Akiwa hajui kuhusu jambo hilo, Salima alipiga makelele bila msaada wowote huku wasichana hao wakimvua nguo zote na kumuacha kama alivyozaliwa akitetemeka kwa hasira. Cha ajabu baada ya kuhakikisha Salima hakuwa na nguo yoyote mwilini mwake, wale wasichana wote wakaangua vicheko na kumfafanulia maana ya kitendo walichomfanyia ambapo Salima mwenyewe alijikuta akicheka pamoja nao huku na yeye akiapa kulipiza kisasi kwa msichana mwingine mgeni atakayetambulishwa siku zijazo. *** Dereva wa gari walilopanda akina Dedan aliendelea kukata kona toka mtaa mmoja kwenda mwingine. Mwanzoni Sonia alifikiri mtu huyo alikuwa akiwapa lifti kwa kuwapeleka nyumbani kwao kama alivyowaahidi saa chache zilizopita, lakini haikuwa hivyo. Sonia alipomtazama vizuri dereva yule aligundua kuwa alikuwa makini sana akiwaangalia kwa kioo cha juu yake kilichomruhusu kuwaona abiria wote waliokaa kwenye siti za nyuma yake ambao ndiyo yeye Sonia na Dedan. Bila kuonesha hofu yake, Sonia aligeuza shingo na kuitazama milango ya gari hilo na kugundua kuwa ilikuwa imelokiwa. Akaangalia aina ya viio vyake akagundua kuwa vilikuwa vile vya ‘tinted’ ambavyo mtu wa ndani huweza kuona nje pasipo wa ndani kuonekana. kwa mazingira hayo Sonia alihisi yalikuwa mazuri kwa utekaji nyara kama akili yake ilifikiri kwa usahihi. Kwa uoga Sonia alishindwa kuhoji wapi walikuwa wakipelekwa maana hata Dedan mwenyewe alianza kupatwa na wasiwasi na kugeuka mara kwa mara akimwangalia Sonia. Sonia alizidi kupepesa macho yake akiangalia vyema kila kitu ndani ya gari hilo. Zaidi alikuwa akiangalia kitu chochote kitakachoweza kugeuka silaha kama tu dereva huyo atageuka na kuwa mmoja kati ya majambazi waliotumwa kuwadhuru. Alipopapasa juu ya kiti alichokaa, akagundua kulikuwa na peni. Akaificha akitumaini kuitumia baadaye kama silaha yake. Akaendelea kupapasa zaidi kwa kificho ili asije kushtukiwa na dereva yule aliyekuwa makini kila saa akitupia jicho lake kwenye kioo akiwaangalia Sonia na Dedan nyuma yake. “Sonia najua mpaka sasa utakuwa umeshajua ninatokea wapi, kwa hiyo hakuna haja ya kuhangaikahangaika. Mimi ni dereva tu na jukumu langu ni kukurudisha nyumbani,” aliongea dereva huyo akiuvunja ukimya baada ya kushtukia mbinu za Sonia. “Sonia ni nini kinaendelea?” Aliongea Dedan akimgeukia Sonia aliyekuwa amepigwa butwaa akishangaa ‘Serenity’ wamejuaje kama alikuwa hai! “Usiogope Dedan, usiogope..” aliongea Sonia akizama kwenye siti ya kiti alichokaa, taratibu akaishiwa nguvu na kuzirai. “Sonia!” Dedan alimwita Sonia kwa kumtingishatingisha huku akiwa katika bumbuwazi asijue nini kilichokuwa kinaendelea kwenye maongezi ya Sonia na dereva huyo kiasi cha Sonia kuwa katika hali hiyo. Baada ya mwendo mfupi, dereva alikunja kona na kuingia ndani ya geti kubwa lililojifungua na kujifunga lenyewe na kuzidi kutokomea ndani zaidi na baadaye kupaki. Mara mlango wa siti aliyokaa sonia ukafunguliwa kisha mtu mwingine akatokeza mikono yake na kumtoa nje Sonia akiwa bado amezirai. “Wewe shuka unifuate!” Ilisikika sauti yenye amri kutoka nje ya gari ikimwamrisha Dedan ashuke mara moja, jambo ambalo alilifanya haraka bila kupoteza muda. Mbele kulikuwa na mlango mwingine mkubwa uliokuwa ukiingia ndani ya ghorofa refu lililopambwa kwa rangi nzuri huku juu ya mlango maandishi yaliyoandikwa ‘Serenity’ yakionekana kwa ukubwa. “Huyo ndiyo Dedan na hatimaye Sheila amepatikana umemuona jinsi alivyo?” Aliongea Madam Flaviana akimwambia Mr.Chakos kama kawaida yao wakiwa hawabanduki kwenye kompyuta zao. “Nasikia alikuwa akijiita Sonia, tumpe haki yake tumwite hivyohivyo,” aliongea Chakos mara simu yake ya mkononi ikaita, akaongea kwa muda kidogo kisha akageuka na kumtazama Madam Flaviana akiongea kwa sauti: “Carolina naye amepatikana andaa mchezo!”
“Carolina! umempataje?” aliuliza kwa mshangao Madam Flaviana. “Usishangae sana hakuna kitu kinachonishinda nikiamua,” alijibu Mr. Chakos kwa kujiamini huku akikenua meno yake meupe huku meno mawili ya pembeni yakiwa yenye
kuchongoa kama yale ya wanyonya damu; kama umeishawahi kuona filamu za ‘Dracula.’ “Yupo wapi?” aliuliza kwa shauku Madam Flaviana. “Subiri muda mfupi ujao atapelekwa Serenity kama wenzake.” ** Iliwachukua takriban nusu saa majirani wa Side kugundua kuwa moto mkali ulikuwa ukiwaka ndani ya nyumba ile. Taarifa zilienea kila mahali kwa kasi ya ajabu huku watu
wakimiminika toka kila kona ya Ulongoni. Watu wachache walio jasiri walijitolea kumwaga maji na mchanga ili waupunguze moto ule au kuuzima kabisa. Wengine walitoa taarifa kwa kitengo cha zimamoto na polisi
ambao kama kawaida yao walitumia muda mrefu kufika kwenye tukio. “Nani mmiliki wa nyumba hii?” aliuliza afande Luka akichukua maelezo kutoka kwa mmoja wa jirani zake Side. “Samahani afande, sikufundishi kazi lakini kwa nini tusitoe msaada kwanza hayo mambo mengine yafuate baadaye?” aliongea afande John na kupata sapoti kubwa kutoka kwa
wakazi wa eneo hilo. “Unataka kufanya nini John! Wewe huoni huo moto ulivyo? Hakuna kiumbe chenye uhai humo. Subiri amri toka kwangu siyo unapayuka tu. Kama unataka kuingia ukafe, nenda!”
Aliongea afande Luca kwa ghadhabu. Kufumba na kufumbua, afande John alijitosa ndani ya nyumba hiyo iliyochachamaa kwa moto bila uoga wowote huku kila mmoja akimshangaa. “Mwanaharamu huyu anataka kufanya nini?” alisema afande Luca kwa hasira akikunja kitabu chake alichokuwa akiandika maelezo huku jasho likimtiririka kwa hofu. Baada ya dakika chache… “Njooni huku,” ilisikika sauti ya afande John ikitokea ndani na kumfanya kila mmoja ageuke na kuelekea upande ambao ilisikika sauti hiyo. Katikati ya moshi mzito alichomoza afande John mkononi mwake akiwa amewabeba watoto wawili aliopokewa na polisi wenzake kwa ajili ya huduma ya kwanza na kuwahishwa
hospitali mara moja. “Nyumba nzima sijamuona mtu yeyote zaidi ya hao watoto wawili,” aliongea afande John kwa taabu akimwambia afande Luca ambaye aliachama mdomo kwa mshangao akizitazama
nguo za afande mwenzake zikifuka moshi, akili yake ikikataa kuamini ujasiri uliooneshwa na afande mwenzake. Wakati watoto wale wanapakizwa kwenye ‘ambulance’, afande John aliweza kuona kamba zikiwa mikononi mwao na vitambaa vizito midomoni mwao. Haraka akahisi kwa vyovyote
vile tukio la kuungua kwa nyumba kumefuatia baada ya uharifu fulani kufanyika. Kwa muda mfupi aliokuwa hapo, aligundua kuwa wakazi wa nyumba hiyo iliyotajwa kuwa ya bwana Saidi maarufu kama Side hawakuwa na ushirikiano mzuri na majirani zao kiasi
cha watu hao kujulikana sana. Maelezo ya jirani mmoja yalionesha kuwa familia hiyo ni ya baba na watoto wadogo wawili wa kike, lakini mara nyingine kumekuwa na maelezo
kuhusu kuonekana kwa mwanamke mwenye ushungi kuanzia juu mpaka chini ndani ya nyumba hiyo. Kwa maelezo ya majirani hao, walisema ni nadra sana mwanamke huyo kuonekana hadharani na mara kadhaa huisikia sauti yake kutoka ndani. Kwa maelezo hayo afande John alihisi kwa vyovyote Side na huyo mwanamke aliyekuwa akiishi naye kwa siri walikuwa wakihusika katika mpango wa kutaka kuwaua watoto wao
kwa kuwasha moto kwa makusudi. Akafungua kitabu chake kisha akachora michoro kadhaa na kuweka alama ya viulizo katika jina la Side na katika jina jingine alilolipachika ‘nani.’ Kikosi cha zima moto hatimaye kikafika na kuanza kazi yake. Muda huo nusu ya nyumba ilikuwa imeteketea pamoja na mali zote huku kuta zenye masinzi mazito zikibakia
kama kumbukumbu kuwa eneo hilo awali liliwahi kukaliwa na jengo zuri. Upesi askari wakawatawanya watu na kulizungushia eneo hilo utepe kama kidhibiti na kuwatenga raia wa kawaida kutoka sehemu hiyo ili wafanye uchunguzi wa chanzo cha
tukio hilo. *** Salima alirudia na hali yake ya furaha na kwa mara ya kwanza akapata marafiki wapya ndani ya jengo hilo. Katika hayo kamwe hakusahau kuwa Julieth alitumwa kumpeleleza
kama ambavyo aliwasikia wakizungumza chumbani na Madam Bernadeta. Usiku ule Salima alilala kwa amani kana kwamba hakuwahi kulala kama vile maishani yake yote, lakini ghafla katikati ya njozi zake doa la giza liliingia na kusambaa
likiharibu weupe wote ulioangaza juu ya ndoto yake. Mapigo ya moyo yakapiga kwa kasi, mara akazinduka kitandani akiwa na hofu asijue maana ya ndoto ile. Akiwa hana hata lepe la usingizi, akawasha taa ya chumbani na kubaki akizungukazunguka kama vile alikuwa akikatafuta kitu alichokipoteza. Ghafla macho yake yakatua pembeni ya kitanda chake na kuuona mchoro wa ajabu ulioonekana nyuma ya ubao wa kitanda kile. Mwanzoni alishindwa kuelewa maana ya mchoro ule ulioonekana wazi kuchorwa kwa kitu chenye ncha kali. Lakini alipobadilisha mtazamo yaani kwa kuuangalia tokea upande wa
kulia kwenda kushoto alianza kuuelewa taratibu. Shepu ya mchoro huo ulikuwa ni ramani ya chumba, kama vile wachoravyo wataalamu wa majengo. Ramani hiyo ilikuwa na sehemu ya wazi katikati, mara moja Salima aliigundua
sehemu hiyo iliwakilisha mlango wa chumba hicho. Kwenye kona ya mchoro huo, alama mfano wa jicho ilionekana na kona nyingine kulikuwa na alama mfano wa sikio. Kwa tafakari ya harakaharaka, viungo hivyo huwa na kazi ya kuona na kusikia ni wazi kuwa mchoraji wa ramani hiyo alikuwa na maana yake ambayo Salima hakuijua. Hofu
ikaanza kumpanda huku akiukumbuka ujumbe wa mwisho aliotumiwa na Carolina kuwa chochote atakachofanya kuna mtu anamuona na kumsikia. Akazima taa na kuanza kufuatilia kimyakimya maana ya jicho na sikio kama alivyoiona kwenye ramani. Akaelekea upande wa kushoto kama mchoro ulivyoonesha. Kwa mshangao
akakiona kitufe kidogo chenye lenzi kikiwa kimefichwa vyema katika ua la plastiki lililopambwa ukutani. “Mungu wangu, kamera!” alijisemea Salima kimoyomoyo huku akiiacha kama ilivyo na kuelekea upande mwingine ambapo alikiona kinasa sauti. Fumbo lote lilikuwa limefumbuliwa mbele yake, akatambua kuwa jicho ilikuwa ni kamera na sikio kilikuwa ni kinasa sauti. Kwa uwoga na aibu, Salima aliishia kusikitika
na kujilaza kitandani akiwaza juu ya kila kitu alichokifanya kuwa alikuwa akionwa na kusikiwa na mtu mahali fulani. *** Baada ya huduma ya kwanza, hatimaye Sonia alishtuka akiwa katika chumba asichokifahamu. Akavuta kumbukumbu zake na kugundua kuwa kabla hajazirai alikuwa akizungumza na
dereva wa gari alilolipanda akiwa na Dedan. Kuanzia hapo hakukumbuka chochote zaidi. Moja kwa moja akajua tayari ameshaingia katika mikono ya Serenity. Akiwa bado amejilaza kitandani kwa uchovu mwingi, Sonia alijigeuza taratibu upande wake wa kushoto na kumuona msichana mwingine akiwa amelala kitanda cha pembeni yake akihema taratibu mfano wa mgonjwa mahututi. Haukupita muda mrefu msichana huyo akashtuka na kugeuka akishangaa huku na huko na mara macho yake yakatua kwa Sonia. “Naitwa Sonia, nani wewe?” Kwa tabu Sonia alianza kujitambulisha yeye mwenyewe. “Caro,” alijibu msichana huyo kwa shida huku akijipapasa shingoni mwake kana kwamba kuna kitu alikuwa anakitoa bila mafanikio. “Kwa nini upo hapa?” Sonia aliendelea kuuliza kwa shauku huku akijaribu kukaa kitandani lakini alishindwa na kulala tena. “Shhh!” Caro alimkatiza usemi Sonia. Mara sauti ya viatu vilisikika vikisogea kwenye chumba hicho. Ghafla Madam Flaviana akaingia na kujongea taratibu mpaka kwenye
vitanda walivyokuwa Caro na Sonia. “Karibuni warembo, I’m so happy to see you again (ninafuraha kuwaona tena),” aliongea Madam Flaviana kwa mbwembwe huku akiwatazama Caro na Sonia jinsi walivyopigwa na
butwaa. “Najua mnajisikia uchovu sana, hiyo inatokana na nusu kaputi tuliyowawekea kabla ya kuwafanyia oparesheni maalumu.‘Infact’ tumewawekea vipandikizi karibu kabisa na uti
wa mgongo upande wa shingo. Vipandikizi hivyo ni hatari kama mtataka kuviondoa kwa kuwa tumevishikiza karibu kabisa na sehemu ya uti wa mgongo. Niwaambie tu kwamba hakuna daktari yeyote
atakayeweza kuviondoa vipandikizi hivyo bila kuutoa na uhai wenu pia. Tunahitaji jambo dogo sana kutoka kwenu. Nina uhakika hamuwezi kukataa,” aliongea Madam Flaviana
kwa nyodo huku akiondoka. “Oh! Nimesahau kuwaeleza kuhusu hivyo vipandikizi tulivyovifunga miilini mwenu. Kama mtajaribu kutoroka kwa hali yoyote ile ndani ya jengo hilo vipandikizi hivyo
huweza kuripuka na kukumaliza moja kwa moja. So be careful,” alimalizia Madam Flaviana na kuondoka akiwaacha Sonia na Caro wakilia kwa uchungu. Hakuna ubishi wote
walijijua wapo ndani ya mikono ya Serenity. *** Kama askari wa kitengo cha upelelezi, Afande John alijitahidi kufanya kila kitu kwa ustadi mkubwa. Ubaya wa kazi yake ni kwamba kila siku amekuwa akishughulika na
upande hasi wa mwanadamu kwa maana ya maovu wanayoyafanya watu kila siku iendayo kwa Mungu. Siku hiyo pia alikuwa akishuhudia matokeo ya maovu hayo. Mbele yake kulikuwa na maiti ya mwanadamu iliyoiva kwa moto kiasi cha kutotambulika hata kidogo. Kama maelezo yatakuwa sahihi basi mtu huyo atakuwa ndiye Side aliyetajwa kama mmiliki wa nyumba hiyo iliyoungua. Kwa umakini mkubwa alivaa glovu zake na kuugeuza mwili huo. Mara akaona matundu ya risasi katika maiti hiyo. “Huyu alikuwa ameuawa kabla ya moto kumuunguza,” aliwaza Afande John huku akiendelea kuchorachora kwenye kitabu chake, saa hiyo juu ya yale jina la Side likaunda
kiboksi kingine na kuweka kiulizo. “Huyu alikuwa ameuawa kabla ya moto kumuunguza,” aliwaza Afande John huku akiendelea kuchorachora kwenye kitabu chake. Saa hiyo juu ya jina la Side akaunda kiboksi
kingine na kukiwekea kiulizo.
“Vipi kuna maiti nyingine zaidi ya hiyo?” Afande Luca alimuuliza Afande John huku akipiga miayo mfululizo kutokana na uchovu uliochanganyika na usingizi kwani tayari
kiza kilikuwa kimeshaanza kutanda. “Hapana, ni hii tu,” alijibu Afande John. “Fasta tuipakize kwenye gari tuondoke hapa,” alisema Afande Luca. Baada ya kumaliza zoezi la kuibeba maiti ile, Afande John aligeuka kana kwamba machale yake yalimtuma afanye hivyo. Mara macho yake yakakutana uso kwa uso na mtu mmoja
aliyepotelea haraka kwenye vichaka vilivyokuwa karibu yake huku giza la usiku likimficha. “Kuna mtu anatutazama upande ule haraka tumfuatilie,” alisema Afande John na kukimbilia huko mara moja akimwacha Afande Luca aliyebakia akimlaani kwa kujifanya
kiherehere kwenye kila jambo. Japo kuwa mtu yule alikuwa na spidi kali, lakini hakuweza kufua dafu mbele ya Afande John aliyekuwa akiruka viunzi kama vile hakuwa na akili nzuri. Kwa kasi ya ajabu, Afande John alifanikiwa kumfikia na kulidaka shati lake akijaribu kumvuta ili kumpunguza kasi. Kama vile mtu yule alikuwa akiyasoma mawazo ya Afande
John, upesi akabonyea chini kidogo, kufumba na kufumbua shati pekee ndilo lililobakia mikononi mwa Afande John, huku mtu yule akipepea kifua wazi na kutokomea
vichakani. “Yuko wapi sasa huyo mtu?” alitamka Afande Luca huku akihema bila mpangilio baada ya kufika kwenye tukio. “Nusu nimkamate, lakini amefanikiwa kunitoroka afande.” “Umeona eee! Nilishakuambia tuondoke, wewe unang’ang’ania kufanya mambo yasiyokuhusu. Sitaki urudie upuuzi kama huo ukiwa unafanya kazi na mimi.” “Sawa afande tuondoke,” alijibu Afande John huku mikono yake ikiwa bize ndani ya mifuko ya shati alilolipata kutoka kwa mtu yule aliyemchoropoka. Mara akachomoa kadi
fulani na kuanza kuikagua. “Tazama afande!” alisema Afande John akimwonesha Afande Luca ambaye alikuwa bado amekunja ndita kwa hasira kama vile mtu aliyekusudia kulamba ndimu lakini kwa bahati mbaya ndimu ikamlamba yeye. “Nini? Giza limeingia tuondoke bwana!” Alifoka Afande Luca kwa hasira. “Angalia ni kadi ya kampuni, halafu hii nembo nadhani nimeishawahi kuiona mahali lakini sikumbuki ni wapi,” “Hebu leta kwanza,” alisema Afande Luca hasira zake zikiwa zimepungua kidogo na kuipokonya kadi ile akijifanya hodari kutoa majibu mambo yaliyoshindikana. “Mh! Hata mimi alama hii nimeshawahi kuiona kwenye jengo moja, ngoja tufike ofisini kwanza.” Wote wakakubaliana kuihifadhi kadi hiyo na kuondoka eneo hilo. Kama kawaida yake, Afande John alifungua kitabu chake, akaandika neno ‘mvamizi’ pembeni ya jina la Side kisha akakifunga vizuri na kukirudisha mfukoni. *** Mr.Chakos, Madam Flaviana na mwanaume aliyeonekana kula chumvi nyingi walionekana wakimtazama kwa umakini mkubwa Dedan kupitia kompyuta zao. “Kwa kumuangalia unamwonaje, ni mzima au?” aliuliza Mr.Chakos akimtazama huyo mzee aliyekuwa pembeni yake. “Yap, vipimo vya nje vinaonesha kuwa ni mzima, ila bado hana kumbukumbu ya mambo ya zamani. Katika hatua aliyopo anaweza akapandikizwa uongo wowote na kuuamini kuwa ni
kweli kwa kipindi chote cha maisha yake,” alijibu mwanaume huyo ambaye kitambulisho chake kiliandikwa ‘Dr. Eugene Harry’. “Madam, kafanye kazi yako,” Mr. Chakos alimgeukia Madam Flaviana aliyesimama na kutoka mle ndani. *** Akiwa hajui nini kilichokuwa kikiendelea, Dedan alitulia tuli akisubiri hatima yake. Masaa yalikuwa yakienda taratibu sana ndani ya chumba alichofungiwa. Chumba kizima kilikuwa na kitanda na televisheni peke yake. Kwa muda huo alitamani kuwaza kitu fulani kuhusu maisha yake, lakini hakuwa na kitu chochote katika
kumbukumbu zake zaidi ya Sonia na Side watu aliowafahamu siku moja tu iliyopita kabla hawajatengana. Mara sauti ya ufunguo ilisikika mlangoni pake. Mlango ukafunguliwa na mwanamke wa makamo aliingia ndani kwa kujiamini akimfuata mahali alipokaa Dedan huku akimwachia
tabasamu pana kana kwamba walikuwa wakifahamiana. “Hallow Dedan! Naitwa Madam Flaviana,” alisema Madam huku akimpa mkono wa salamu Dedan ambaye aliupokea kwa heshima. “Nafahamu haujui uko wapi na kwa nini upo hapa, ila tambua tu kuwa upo sehemu nzuri na salama, ondoa hofu,” alisema harakaharaka Madam Flaviana akimtoa uwoga Dedan
aliyekuwa kimya akimsikiliza. “Nafahamu una maswali mengi sana kichwani mwako, nipo hapa kukujibu machache ambayo nina imani ndiyo ya msingi. Najua umemsahau Salima lakini ngoja nikukumbushe,” alichombeza Madam Flaviana huku akichomoa ‘laptop’ yake. Akafungua upande wa picha na kuanza kumuonesha Dedan picha
za Salima huku akimpa mkanda mzima kuhusu uhusiano wake yaani yeye Dedan na msichana huyo. Baadaye alimsimulia kuhusu Caro kama chanzo cha matatizo yake huku akidanganya kuwa mara kadhaa hapo zamani msichana huyo alijaribu kumuua na kuokolewa na Salima jambo….
Simulizi : Kitanzi, Kisu Na Bastola Sehemu Ya Tano (5)
Wakaingizwa ndani ya lifti na kupelekwa hadi ghorofa nyingine, huko wakakabidhiwa kwa Madam Bernadeta na kupewa nguo zenye rangi sawa kisha wakapelekwa kwenye jukwaa kubwa ambalo ndani yake kulikuwa na wasichana wengi wakiwa na nguo kama zao. Kwa harakaharaka, Carolina na Sonia wakajua kwamba tayari wamerudishwa tena kutumika ndani ya jumba la Serenity kwa kuwa hawakuwa wageni ndani ya mazingira hayo.
Wakati huo, Sonia alikuwa akitokwa na machozi mfululizo kwa kuwa alimkumbuka sana mume wake Side na watoto wake ambao mpaka siku hiyo hakujua nini kilichokuwa kikiendelea kwa upande wao. Wakati huohuo, Carolina alikuwa akiwaza jinsi ya kumpata Salima msichana ambaye aliongea naye siku chache zilizopita. Moyoni mwake alijua kama akionana na msichana huyo basi kila kitu kinachomhusu Dedan atakifahamu. “Niambie, unamfahamu Salima?” Carolina alimuuliza Julieth bila kutoa salamu yoyote ya kiungwana. “Salima! Unamaanisha Caro?” aliuliza Julieth. “Mimi namfahamu kwa jina la Salima tu na si vinginevyo.” “Kwani mnafahamiana?” “Sijawahi kumuona hata siku moja. Naomba unioneshe kama yupo hapa tafadhali.” “Tangu leo asubuhi sijamuona… labda nikupeleke kwenye chumba chake,” alisema Julieth na kumuongoza Carolina huku Sonia naye akifuatia kwa nyuma. “Hiki ndiyo chumba chake,” alisema Julieth huku akiufungua mlango wa chumba cha Salima bila kubisha hodi. Wakiwa wanajishauri waingie au wamsubiri, mwenyeji wao awakaribishe, mara wakasikia kicheko kikali kikitoka ndani ya chumba hicho. Walipoingia walimkuta Salima akirukaruka juu ya kitanda chake huku masikioni akiwa na ‘headphone’ alizozichomeka kwenye ‘ipod’ yake. Ni wazi kwamba alikuwa akisikiliza na kucheza nyimbo fulani kwa fujo. Salima alipowaona, akaacha uchizi aliokuwa akiufanya na kuteremka kitandani kisha kwa mashauzi akamfuata Julieth na kumtazama kwa madaha kabla ya kufanya vivyohivyo kwa Carolina na Sonia. “Caro, una nini leo? aliuliza Julieth kwa mshangao baada ya kuhisi mabadiliko makubwa kwenye tabia ya Salima tofauti na alivyokuwa akimfahamu. “Kwani vipi! Hawa akina nani?” Salima aliongea kwa dharau huku macho yake yakitua kwenye uso wa Carolina na kumuangalia kwa muda huku akisubiri jibu la swali lake. “Hawa ni wageni wako. We wasikilize mwenyewe bwana!” Julieth alijibu kwa hasira na kutaka kuondoka, lakini aliamua kusubiri asikilize kitu gani wasichana hao walitaka kuongea na Salima au Caro kama alivyokuwa akiitwa. “Mimi naitwa Carolina, tuliongea wote kwenye simu siku chache zilizopita,” aliongea Carolina kwa sauti ya chini baada ya kubaini kamera iliyokuwa imetegwa kwa kificho pembeni ya ua, akahisi lazima kutakuwa na kinasa sauti mahali fulani karibu na waliposimama. “Carolina? Mbona mimi sikufahamu,” Salima alijibu kwa sauti na harakaharaka bila ya kuipa nafasi akili yake ifikirie. “Tulikuwa tumuongelee Dedan. Bado haujakumbuka?” Carolina alisisitiza. “Sikia dada, mimi sikukumbuki hata kidogo…naomba tusipotezeane muda. Kama hauna kitu cha msingi, ondoka.” “Lakini…wewe si ndiyo Salima?” “Hapana, mimi naitwa Caro,” aliongea Salima na kuvaa headphone zake huku akiendelea kucheza wimbo aliokuwa akiusikiliza. Carolina alivunjwa nguvu na kauli hiyo ya Salima kwa kuwa alimtegemea msichana huyo kama mtu pekee atakayeweza kumsaidia kukutana na Dedan wake kwa mara nyingine. *** Afande John akiwa kwenye haraka, alikatiza wodi ya watoto, Muhimbili akielekea kwa daktari mkuu wa kitengo hicho, Dr. Denis Mtima ambaye alimpeleka moja kwa moja mpaka kwenye chumba walicholazwa watoto wa Side. Watoto ambao walinusurika kifo kwenye ajali mbaya ya moto. Mengi yalikuwa yakiongelewa kuhusiana na tukio hilo, lakini ukweli ulikuwa ndani ya mioyo ya watoto hao ambao kama walikuwa wamerudiwa na fahamu basi watawataja wahusika wote pamoja na chanzo cha moto ule. Kwa mujibu wa daktari huyo, watoto hao walikuwa wameanza kupata nafuu na kuweza kuongea, hivyo hiyo ilikuwa ni nafasi pekee ya afande John kuwauliza maswali ili kujua nini kilichokuwa kimetokea siku ile. “Hamjambo watoto wazuri?” aliongea afande John huku akiwapatia pipi na chokleti watoto wale ambao walikuwa wamelala kwenye vitanda tofauti. Wakapokea na kushukuru. “Eti mama na baba wapo wapi?” aliuliza Habida, mtoto wa kwanza wa Side na kumfanya mwenzake aitwaye Safia ageuze shingo yake haraka na kumtazama afande John kwa makini. “Baba na mama wanakuja sasa hivi. Wamenituma niwaletee hizo zawadi kwanza,” aliongea afande John huku moyo wake ukimuuma kwa kuongea uongo Akafungua mkoba wake na kutoa picha za watu kadhaa. Akawaonesha wale watoto picha moja baada ya nyingine akitaka wachague picha za watu waliowahisi kuwaona siku ya tukio. Picha ya kwanza kuchaguliwa ilikuwa ya Dedan na baada ya kuchambua picha nyingine ilionekana picha ya Henry. Wa kwanza kushtuka alikuwa ni Safia ambaye alipoitazama picha ile alifumba macho kwa woga na kugeuza shingo yake kana kwamba aliiona taswira mbaya ya ‘Lusifa’ mwenyewe. Baada ya kugundua hilo, afande John akaigeuza picha hiyo haraka na kuirudisha kwenye mkoba wake ili asiwaumize watoto hao walioonekana kupitia maumivu makali tofauti na umri wao. Kwa kitendo cha watoto hao kuiogopa picha ya Henry, tayari afande John aligundua kuwa mtu huyo hakuwafanyia jambo jema watoto hao tofauti na Dedan ambapo walipoiona picha yake walitazama bila woga wowote. Akawageukia tena watoto wale na kuanza kuwahoji. Walisimulia kila kitu kilichowatokea ikiwemo jinsi Henry alivyowachukua shuleni kwao kwa kujifanya mjomba wao. Pia wakasimulia walivyopelekwa nyumbani na kufungwa kamba ambapo chumba cha pili walisikia sauti ya baba yao, yaani Side akilia kwa uchungu kabla ya baadaye kusikia mlio wa kuogofya ambao afande John alitambua kuwa walikuwa wakimaanisha mlio wa risasi. Mwisho kabisa wakaelezea jinsi moto ulivyowaka na kuwazingira kila kona. “Aliyeyafanya yote hayo ndiye huyu?” aliuliza afande John kwa mara nyingine huku akitoa picha ya Henry na kuwaonesha watoto wale jambo ambalo liliwashtua sana na kuwafanya wapige kelele kwa nguvu. “Afande, mahojiano gani hayo ya kuwatisha watoto kiasi hicho? Naomba uondoke mara moja!” Dk. Denis aliongea kwa jazba akimtimua afande John. Kwa kutambua hilo, afande John akatekeleza agizo la daktari bila ubishi kwa kuwa alitambua fika kuwa watoto wale walikuwa bado kwenye mfadhaiko kwa yote yaliowatokea, hivyo kama Dk. Denis asingemkataza angeweza kuwasababishia presha na matatizo mengine. Afande John aliondoka mara moja katika wadi hiyo, safari hii angalau alikuwa na uhakika kuwa amepata mahali pa kuanzia. “Hallow afande Prisca! Umepata chochote?” aliongea afande John kupitia simu yake ya mkononi huku akitembea kuelekea mahali alipoipaki pikipiki yake. “Ndiyo mkuu, wengi kati ya hawa wasichana waliopo pichani, wamewahi kuripotiwa wamepotea mitaani mwao. Sasa sijui kama walitoroka makwao kwa makusudi au vipi?” alizungumza afande Prisca ambaye ni afisa upelelezi kitengo cha uhalifu kwa njia ya mtandao. “Mh…Hapo kuna tatizo, nakuja sasa hivi,” alijibu afande John na kuondoka hospitalini hapo. Kwa mbali Henry aliyekuwa amejibanza kwenye foleni za wagonjwa, alimtazama afande John akiondoka. Akaishusha kofia yake chini zaidi na kuficha sehemu kubwa ya uso wake kisha akaingia ndani ya hospitali ileile aliyotoka afande John, mkononi mwake akiididimiza bastola yake aina ya ‘revolver’ ndani ya mifuko ya koti lake. Bila kutiliwa mashaka na mtu yeyote, Henry akaingia mpaka kwenye varanda kuu na kuelekea chumba walichokuwamo watoto wa Side. *** Akiwa mwenye kukosa tumaini, Carolina alimtazama Salima kuanzia chini mpaka juu kana kwamba hakutaka amsahau kabisa katika kumbukumbu zake.
Katika kutazama huko, mara akagundua kidoa chekundu katika kiganja cha mkono wa Salima. Ghafla akamfuata na kumshika mkono wake akikitazama kidoa kile kilichofanya kipele kidogo juu ya mshipa wake wa damu.
Kwa hasira Salima akamsukuma Carolina na kumtaka aondoke chumbani kwake mara moja. Kwa tahadhari ya kutoharibu mipango yake, Carolina alitoka nje ya chumba cha Salima akiongozana na Sonia na Julieth ambao wote walipigwa na butwaa wakiwa hawajui maana ya kitendo alichokifanya Carolina.
“Wewe una uhakika kama yule ndiye Salima?” aliongea Carolina kwa ghadhabu akimwangalia Julieth usoni kana kwamba alidanganywa na kupelekwa kwa mtu mwingine mbali na Salima. “Ndiye yeye mwenyewe…kama huamini waulize wote humu ndani.” Julieth alijitetea baada ya kuona uso wa Carolina ukiwa umefura hasira. “Umeshawahi kumuona Salima akiwa katika hali ile au amebadilika?” “Salima ni mpole na mwenye aibu nyingi, leo amebadilika sana, hata mimi mwenyewe amenishangaza.” Kwa jibu hilo la Julieth, tayari Carolina alielewa kuwa huenda msichana huyo alikuwa amechomwa sindano ya dawa za kulevya ‘Ecstasy 33’ iliyomfanya apoteze haiba na kumbukumbu zake za awali. Carolina alilijua hilo kwa kuwa hata yeye mwenyewe alishawahi kuchomwa sindano hizo na mtu ambaye si mwingine zaidi ya Dr. Church; Mkemia hatari ambaye kipaji chake alikitumia vibaya kwa kuumiza kundi fulani la watu na kujinufaisha mwenyewe. Miaka kadhaa iliyopita, Mzee huyo aliajiriwa na ‘Serenity,’ huku kazi yake kubwa ikiwa ni kutumia dawa zake kwa msichana yeyote aliyeonekana kutoendana na taratibu za ‘Serenity,’ hasa katika suala la kutumika kimapenzi. “Bila shaka Salima ni msichana mwenye msimamo sana kiasi cha kudungwa madawa. Kwa sasa sina la kufanya. Itanilazimu nimsubiri mpaka atakapopata ahueni,” Carolina alijisemea kimoyomoyo akikumbukia jinsi alivyokuwa akichomwa sindano hizo kila mara alipovunja kanuni za jumba hilo. Akajiangalia mikononi na kuona alama za makovu ya sindano zile yakiwa yameanza kufifia. Akashusha pumzi kwa nguvu akitafakari jinsi ya kutoka ndani ya jengo hilo akiwa na Dedan, mwanaume aliyedhamiria kumpata kwa hali yoyote. *** Wakati huo Dedan alikuwa akipata huduma nzuri tofauti na wenzake. Yeye alipata nafasi ya kuwa karibu zaidi na Madam Flaviana. Wakazungukia kila kona ya jumba la ‘Serenity’ isipokuwa upande wa vyumba vya wasichana waliowekwa tayari kwa ajili ya kuuzwa kwa wanaume Wakizungu. Kwa hali hiyo, Dedan akawa kama mmoja wa wafanyakazi wa karibu wa madam Flaviana huku mwanamke huyo akiwa makini kutomkutanisha na Salima wala Caro akiepuka kuharibu mipango yao. *** Henry bila kusuasua, aliufungua mlango wa chumba walichokuwemo watoto wa Side huku mkono wake wa kulia ukiishika vyema bastola yake. Akaingia ndani na kutupa macho yake juu ya vitanda na kuwaona watoto wote wawili waliokuwa wamelala kwa kujifunika kwa mashuka mwili mzima. Akakenua meno yake na kuwafuata taratibu huku akiufunga mlango kwa nyuma. Akajongea mpaka kwenye kitanda cha mtoto wa kwanza na kufunua shuka kwa kutumia mdomo mrefu wa bastola yake, akitumaini hapo atakiona kichwa cha mtoto mmoja wapo ili amuulie mbali lakini badala yake akauona mto. Alipofunua shuka lote alikutana na mito na mashuka yaliyopangwa vizuri na kufanya shepu kama ya watu waliolala. Kabla hajafanya chochote alishtukia mdomo wa bastola ukimgusa nyuma ya kichwa chake. “Taratibu rusha bastola yako pembeni na uinue mikono juu. Ukijaribu kufanya chochote nakufumua ubongo wako,” ilisikika sauti ya afande John. “Kivyovyote huyu mtu atakuwa anajua vyema kuitumia bastola yake. Hapa sina ujanja zaidi ya kutii maagizo yake,” Henry alijionya mwenyewe kimoyomoyo na kufanya kama alivyoagizwa. Kufumba na kufumbua Henry alishtukia yupo chini huku mikono yake ikiwa imefungwa pingu kwa nyuma. Pamoja na mwili wake wa miraba minne, Henry hakuwa na ujanja wowote mbele ya afande John. Kwa mshangao, Henry akabaki akistaajabu jinsi ambavyo afande John alirudi hospitalini hapo haraka kiasi kile, wakati kwa macho yake alimshuhudia akiondoka? Baada ya dakika chache, askari wengine walifika katika eneo hilo na kumpeleka Henry kituoni kwa ajili ya mahojiano. *** Siku zikazidi kuyoyoma huku Salima akiwa amebakiza siku tatu kabla ya ujio wa Prince Khalfani; mgeni ambaye yeye na Julieth walipangiwa kuwa naye katika kipindi chote cha ziara atakayoifanya nchini. Mr. Chakos na Madam Flaviana chini ya usimamizi wa Madam Bernadeta, walikesha wakifanya kazi kuhakikisha Salima au ‘Caro’ kama walivyomwita anakuwa katika afya nzuri na kupatiwa mafunzo yote muhimu ilimradi asiwaangushe wakati wa ziara hiyo. Wakahakikisha anakariri vyema maneno mengi ya kiarabu na kuelewa baadhi ya tamaduni zake. Baada ya kuhakikisha kila kitu kinaendelea vizuri wakakaa kimya wakisubiri ugeni huo.
“Madam Flaviana, amekuja kunifuata mimi au?” alijiuliza Salima kwa shauku kwani zilikuwa zimepita siku nyingi bila kuonana naye.
Salima aliingia ndani na kusimama kwa furaha baada ya kumuona Madam Flaviana pembeni ya Madam Bernadeta. Moyoni aliamini Madam Flaviana atakuwa na habari mpya kuhusu mpenzi wake, Dedan. Akahisi huenda atakuwa amepatikana. “Caro, nina habari nzuri na mbaya, ipi nianze kukwambia kwanza?” Madam Flaviana alimuuliza Salima bila uso wake kuonesha alama yoyote ya furaha. “Aaah…anza na habari njema kwanza,” Salima aliongea kwa wasiwasi hasa baada ya kumsikia Madam Flaviana naye akimuita kwa jina la ‘Caro’ na si Salima kama ilivyokuwa zamani. Kauli ya habari nzuri na mbaya ilizidi kumtia hofu Salima. “Baada ya wiki mbili kutoka sasa, kuna ugeni kutoka Uarabuni utafika nchini kwa ziara binafsi ya kibiashara na kampuni yetu. Kwa niaba ya ‘Serenity’ tumekuchagua wewe kuwa mwenyeji wao kipindi chote watakapokuwa katika ziara yao… Hongera sana Caro,” alisema Madam Flaviana akirudia tena kutumia jina hilo Caro badala ya lile la Salima, akaachia tabasamu pana huku Madam Bernadeta na Julieth wakimpigia makofi. Kipindi chote hicho Salima alitulia kimya, maswali mengi kuhusu uhusika wake kwenye hiyo ziara yalitawala akilini mwake huku akishangazwa kwa jinsi gani hiyo ilikuwa habari nzuri! “Usiwe na wasiwasi hautakuwa peke yako. Kipindi chote utakuwa na shoga yako Julieth. Mwenzako ana uzoefu sana,” Madam Flaviana alisema huku akimwangalia Julieth ambaye alikuwa amesimama nyuma ya Salima huku uso wake ukiwa umejikunja kwa kutajwa kama msindikizaji wa Salima. “Na habari mbaya ni ipi?” Salima aliuliza kwa hofu akimtazama Madam Flaviana machoni kana kwamba alitegemea kusoma macho yake zaidi ya kusikiliza. “Jamani naomba mtupishe,” aliongea Madam Flaviana, mara moja Julieth na Madam Bernadeta wakatoka nje na kumuacha yeye (Madam) na Salima. Madam Flaviana alijua fika kuwa lazima abuni uongo mpya ambao Salima hatoweza kuugundua kwa haraka kwa kuwa, awali yeye ndiye aliyemdanganya Salima kwamba Dedan alikuwa amechukuliwa na Caro jambo ambalo halikuwa sahihi. Mbaya zaidi Salima alishaongea na Caro mwenyewe, kwa hiyo isingekuwa rahisi kumdanganya Salima kuwa Dedan bado alikuwa kwa Caro. “Habari mpya ni kuhusu Dedan,” alianza kuongea Madam Flaviana kwa umakini mkubwa. “Dedan! Vipi amepatikana?” Salima alijikuta akiuliza kwa hofu kwani tayari kichwani mwake alishajiwekea kuwa hiyo ndiyo habari mbaya kama alivyotahadharishwa. “Ndiyo amepatikana na ni mzima wa afya, lakini…”Madam Flaviana alinyamaza kidogo na kumtazama Salima kwa kuibia akitarajia kumuona akiwa ameanza kuchanganyikiwa jambo ambalo lilikuwa sahihi. “Siku zote tulizodhania alikuwa kwa Caro kumbe alikuwa na mwanamke mwingine anayeitwa Sonia. Kibaya zaidi ni kwamba, Sonia ndiye mke wake wa ndoa na wana watoto wawili siku nyingi. “Kwa kifupi Dedan alikuwa na uhusiano na wanawake wawili, ambao mmoja tu ndiye uliyemtambua, yaani Caro.” alisema Madam Flaviana kwa umakini mkubwa ili asije kukosea. Siku zote msema uongo hupaswa kuwa na kumbukumbu nzuri ili asije akajisahau na kuchanya madawa. Kwa hilo, Madam Flaviana alijipanga kutofanya makosa kwani alishakariri kila neno alilopanga kumwambia Salima na kuhakikisha analirudiarudia kabla ya kukutana na Salima siku hiyo. “Sina haja ya huyo mkewe wala watoto wake, Dedan yupo wapi?” Salima aliuliza kwa hasira kidogo kwani alishaanza kuhisi kuumizwa na kila neno ambalo Madam Flaviana alikuwa akiliongea kuhusu Dedan. “Ubaya ni kwamba mimi mwenyewe nilijitahidi kumtaka Dedan angalau aongee na wewe yeye mwenyewe, lakini alikataa na kusema kuwa hakufahamu na mbaya zaidi amenipa ujumbe huu akitegemea kuwa baada ya kuusoma, hautamsumbua tena,” aliongea Madam Flaviana huku akimkabidhi Salima bahasha ndogo. ** Baada ya kushinda siku nzima ya jana yake wakiwa na uchovu uliopindukia, siku hiyo waliamka wakiwa na nguvu kama kawaida. Kwa mara ya kwanza Sonia naye alianza kuhisi maumivu shingoni mwake, akajua kwamba Madam Flaviana hakutania kuhusu kuwawekea vipandikizi ndani ya miili yao. Akageuka na kumtazama msichana aliyejitambulisha kwa jina la Caro na kumuongelesha. “Caro, unamfahamu Dedan?” aliuliza Sonia kimasihara baada ya kuhisi huenda Caro aliyewahi kusimuliwa na Side alikuwa ndiye huyo. “Ndiyo namfahamu. Nafahamu pia kuhusu Salima msichana aliyekuwa akiishi naye baada ya wewe kumsababishia Dedan matatizo.” “Jamani Dedan wangu ana matatizo gani! Yupo wapi?” alinong’ona Caro kwa simanzi kubwa huku machozi yakianza kumtiririka. “Tulitekwa wote na kuletwa hapa, lakini sijui amewekwa sehemu gani!” “Unataka kusema Dedan yupo hapa Serenity! Alipatwa na matatizo gani?” “Kwani wewe hujui? Nimeambiwa alikuwa zezeta, lakini alipona akiwa kwa huyo Salima ambaye naye nimesikia ameletwa hapa Serenity kama msichana wa kuuzwa.” “Unasemaje! Dedan alikuwa zezeta?” alihoji Caro huku machozi yakimtiririka kwa kasi, safari hii yakifika hadi mashavuni mwake. Hakutegemea kama Dedan angefikia hali hiyo baada ya kummwaga enzi zile. Akakosa hoja na kubaki akijilaumu kwa yote aliyomfanyia Dedan, hata hivyo alitamani kupata nafasi ili amuombe msamaha kwa kitendo alichomfanyia na kuamini angesamehewa kwani alijua alikuwa na sababu ya msingi ya kufanya vile. *** “Umefanya kazi nzuri sana Madam,” Mr. Chakos alimpongeza Madam Flaviana huku akimmiminia ‘wine’ kwenye glasi yake. “So nini kinafuata?” aliongea Madam Flaviana huku akiipokea glasi kutoka kwa Mr. Chakos na kuonja kidogo. “Njoo uangalie, nilichokigundua,” Mr. Chakos alimvuta Madam Flaviana mpaka upande wenye kompyuta moja kubwa na kuicheza video aliyorekodi muda mfupi uliopita. Kwenye video ile, Salima alionekana akitembea kwenye korido huku macho yake yakiziangalia kamera zilizotegwa kwenye dari kana kwamba alikuwa akifahamu uwepo wa vifaa hivyo. “Angalia na hii,” Chakos alibofya ‘kipanya’ cha kompyuta yake na kuicheza video nyingine ambapo ndani yake walionekana Caro na Sonia wakiongea kwa kunong’ona kana kwamba walikuwa wakijua uwepo wa kinasa sauti ndani ya chumba chao. “Dirty bitch (mbwa jike mchafu)! Lazima Caro alimwambia Salima kuhusu jambo hili, si unakumbuka siku ile Caro ndiye aliyeongea naye mara ya mwisho kwenye simu?” alifoka Madam Flaviana. *** Ndani ya chumba chake, Salima alikuwa amejifungia kimya akitafakari jinsi gani Dedan aliweza kufanya mambo hayo yote kwa muda mfupi. Ujumbe aliopewa ulijieleza vizuri kama Madam Flaviana alivyomwambia, lakini hakuamini moja kwa moja kama maneno hayo yaliandikwa na Dedan mwenyewe. Akiwa na hasira zilizochanganyika na wivu, Salima alifikiria jambo moja tu ambalo ni kuondoka ndani ya jengo la Serenity na kuhakikisha anamsaka Dedan popote alipo ili angalau amsikie akitamka maneno hayo kwa kinywa chake mwenyewe. Akasimama na kuweka nguo zake kwenye begi bila kujali kamera iliyokuwa ikimmulika. Baada ya kumaliza zoezi hilo, akafungua mlango wa chumba chake na kuanza kutembea kwa kujiamini akielekea kwenye korido na hatimaye kuteremka kwa lifti mpaka chini na kufika nje. Akavuka vizingiti vyote na kutembea kuelekea kwenye geti kubwa lililotenganisha ulimwengu wa nje na mle ndani. Kwa hasira alizokuwanazo, hakujali chochote, akazidi kukaribia geti hilo, lakini ghafla kitu mfano wa sindano kikamchoma mgongoni, Salima akajikuta akilegea ghafla na kudondoka chini kama mzigo, ‘puuh’. *** Kufanya kazi kwa bidii ndiyo sababu iliyomfanya Mkuu wa Upelelezi amkabidhi kesi ile Afande John. Alijua baada ya siku chache watuhumiwa watakuwa wamepatikana kwa kuwa alimuamini sana kijana wake huyo tofauti na maaskari wengine. Bila hiyana, Afande John naye alilichukua jukumu hilo na kuanza kulifanyia kazi ambapo kwa muda mfupi tu alifanikiwa kupata taarifa za watu wawili ambao ni: Henry ‘Ze Deader’ yaani yule muuaji wa Side, na mtu mwingine ambaye alionekana mara moja tu akiwa na marehemu, wakimaanisha Dedan. Kwa maelezo ya watu wachache aliowafanyia mahojiano, Afande John alifanikiwa kufika hadi kwenye kichaka ambacho awali alifungiwa Dedan na Sonia na kugundua kamba zikinin’ginia kwenye magome ya miti miwili. Baada ya kuchunguza, aligundua kuwa mahali hapo watu wawili walikuwa wamefungwa kabla ya kuhamishwa ama kutorokea sehemu nyingine. Kama kawaida yake, Afande John akatoa kitabu chake na kuchora michoro aliyoifahamu yeye mwenyewe. Ghafla wazo likamjia. Kwa kasi ya ajabu akairukia pikipiki yake na kuiwasha kana kwamba alikuwa akiwahi jambo fulani alilolikumbuka. Akiwa njiani, aliiacha barabara ya lami na kuingia ya vumbi ambayo haikuwa ikielekea sehemu yoyote nyingine zaidi ya kwenye jengo moja kubwa la ghorofa lenye fensi ya ukuta mrefu kupindukia. Akasimamisha pikipiki yake na kuificha mita chache karibu na jengo lile. Akaitoa mfukoni ile kadi aliyoichomoa kwa yule mhalifu aliyekurupushana naye usiku wa jana yake na kujaribu kuifananisha na alama iliyopo kwenye kadi hiyo na ile aliyoiona kwenye lile geti. Akaitazama na kubaini kuwa alama zile zinafanana. “Kumbe herufi ‘s’ ni kifupi cha neno ‘Serenity’!” Afande John alistaajabu kimoyomoyo. Moja kwa moja akatambua kuwa kwa vyovyote yule mtu aliyekurupushana naye alikuwa akifanya kazi ndani ya jengo hilo. Kwa kutumia simu yake ya kisasa akaandika neno ‘Serenity’ akidhamiria kutafuta maana yake kwenye mitandao akiamini huko atapata maelezo sahihi kuhusu kampuni hiyo na shughuli zake. Baada sekunde chache za kuperuzi kwenye kurasa za ‘google,’ alibaini kuwa jengo hilo lilijihusisha na masuala ya kukuza vipaji vya urembo na lina matawi mengi duniani. Alipojaribu kuchimba zaidi kuhusu watu wanaoiendesha kampuni hiyo, kurasa ziligoma kufunguka na kuhitaji anuani ya barua pepe na ‘pasiwedi’ ili kuweza kufunguka. “Kwani kuna siri gani humu!” alijisemea Afande John huku akiingiza anuani yake ya barua pepe na ‘pasiwedi’ akijaribu kama kurasa hizo zingefunguka. Taratibu kurasa mpya ilianza kufunguka kwenye simu yake huku zikionekana baadhi ya picha za wasichana kadhaa warembo wakiwa katika pozi tofauti. ‘Akazidownload’ haraka picha hizo na kuzihifadhi ndani ya simu yake, lakini zaidi ya hapo hakufanikiwa kupata kitu chochote ndani ya kurasa hizo, aliona maandishi mekundu yaliyosomeka: MEMBERS ONLY (Wanachama pekee)! Baada ya jitihada za kuzifungua kurasa zile kugonga mwamba, Afande John aliketi hapo kwa muda kidogo akiangaza kila kona ya jengo hilo lililokuwa kimya sana. Kwa kujificha akapiga picha chache na kupotea eneo hilo moyoni akiweka azma ya kufuatilia zaidi namna kampuni hiyo inavyoendeshwa. *** Salima akiwa hajielewi alibebwa na kukokotwa na mabaunsa walioonekana kujizatiti katika kazi yao. Wakapita naye karibu kabisa na mahali walipofungiwa akina Sonia. Moja kwa moja wakambwaga juu ya kitanda cha chumba ambacho ndani yake walionekana Madam Flaviana na mzee mmoja wa Kizungu aliyejulikana kwa jina la Dr. Church kisha wakaondoka. Haraka Dr. Church alifungua begi lake na kuchukua sindano, kisha akaifyonza dawa iliyokuwa ndani ya chupa moja wapo na kumchoma Salima kwenye mshipa wa kiganja chake na kutulia kwa muda. “Itasaidia kweli?” aliuliza Madam Flaviana ambaye kipindi chote hicho alikuwa kimya akimwangalia Dr. Church alipokuwa akifanya vitu vyake. “Hii ni moja kati ya dawa zangu chache zilizonigharimu sana katika ugunduzi wake, nimeipa jina la ‘Ecstacy 33’ kutokana na uwezo wake wa kumfanya mtu asahau mambo yote ya awali na kukubali kila kitu atakachoamrishwa kufanya. Sibahatishi katika hili, kama utakuwa tayari tutamjaribu mtu wako baada ya saa moja.” alisema Dr. Church kwa kujiamini tena kwa Kiswahili fasaha. Kwa maelezo yake, dawa hiyo aliigundua kwa kutumia dawa za kulevya aina ya ‘Ecstasy’ ambayo ina uwezo wa kumfanya mtu asahau mambo na kumchangamsha saa zote. Dr. Church alichoweza kukifanya ni kuiweka dawa hiyo katika kiwango sahihi cha dozi huku akiichanganya na kemikali nyingine zilizokuwa na uwezo wa kumfanya mtu kuwa katika hali hiyo kwa muda mrefu tofauti na ‘ecstasy’ ya kawaida. Kwa hiyo, baada ya muda mfupi ujao, dawa hiyo ingeweza kumfanya Salima amsahau Dedan na kukubali kufanya kila kitu atakachotumwa na Madam Flaviana hasa wakilenga kufanikisha kumtumia katika ziara ya Prince Khalfani kutoka Falme za Kiarabu. *** “Caro, kwa nini kila mara ukiongea unataka tuzungumze kwa sauti ya chini kwani kuna nini?” aliuliza Sonia kwa kunong’ona baada ya kila mara kuzuiwa na Caro kuongea kwa sauti ya kawaida. “Shh! kuna vinasa sauti na kamera ndani ya jengo zima,” alijibu Caro bila kumtazama Sonia. Bado moyo wake ulikuwa na donge zito kwa aliyoyasikia muda mfupi kuhusu Dedan. Ghafla wakasikia vishindo vya watu vikipita karibu na chumba walichomo, kwa sauti za hatua zao Caro aligundua mara moja kuwa watu hao walikuwa wakielekea upande wao, jambo ambalo lilikuwa sahihi. Kufumba na kufumbua wanaume watatu wenye miraba minne waliingia ndani ya chumba hicho. Kwa uoga Sonia alijikuta akimkumbatia Carolina. “Tufuateni mara moja!” alitoa amri mmoja wa wanaume hao aliyeonekana kama kiongozi wao. Bila kukaidi, Caro alisimama na kuanza kutembea akiwafuata watu wale huku Sonia naye akifuatia kwa nyuma kama vile mbwa amfuatavyo chatu hali akijua hatoweza kupona.
********
“Ni mbinu za kikazi, siwezi nikakueleza. Cha msingi naomba unijibu maswali nitakayo kuuliza,” afande John aliyeyusha swali la Henry kwa kuhamisha mada.
“Haya uliza!” Henry alijibu kwa hasira baada ya kuona hakupata jibu zuri kutoka kwa afande John. “Serenity inajihusisha na nini?” “Come on! Afande John, nilidhani unajua kuhusu hilo, kwani hujui kama Serenity inawauza wasichana kwa wageni wa kizungu wanaokuja nchini?” “What! Mimi nilitambua inahusika katika shughuli za urembo na kuwapromoti mamiss.” “Wasichana wote wanaoonekana kama mamiss hutumikishwa kingono, Serenity ni danguro kubwa linalojiendesha kwa kivuli cha masuala ya urembo, hakuna lolote!” “Mh! unauhakika na unachokiongea?” “Yah, asilimia mia mbili,” “Mmiliki wake ni nani?” “afande mimi nawafahamu watu wawili tu; Mr. Chakos na Madam Flaviana lakini mmiliki wake nimewahi kusikia kuwa anajulikana kwa jina la Mr. George. Hakuna mtu yeyote ambaye amewahi kuuona uso wake, hata Mr.Chakos mwenyewe hajawahi kuonana naye hata siku moja. Wanasema kuwa yeye ndiye hutafuta amtakaye na siyo wewe umtafute yeye. Mara zote Mr. George huongea kwa simu kwa sauti tofautitofauti au hutuma ujumbe kwa njia ya mtandao kwa watu maalumu tu. Kwa hiyo kumtafuta ni sawa na kuitafuta njia ya mauti,” alisema Henry ambaye maelezo yake yalizifanya nywele za afande John zisimame kwa hofu. Mara nyingi nywele zake zinaposimama na kwa mtindo huo, afande John hukosa amani kwa kuwa hujua kuna hatari inamnyemelea, hatari yake kwa wakati huo ilikuwa ni hilo suala la Serenity. *** NDANI YA UWANJA WA NDEGE, MAHALI FULANI Waarabu wawili waliovalia suti na miwani myeusi walionekana kuteremka ngazi za ndege moja iliyoonekana kutua muda mchache uliopita. Mavazi na mienendo yao ilionekana wazi kuwa ni walinzi wa mtu au kitu fulani cha gharama. Kwa umakini mkubwa wakaangalia kila upande kisha mmoja wao akajongea mbele kidogo ambapo hapo walionekana Mr. Chakos na Madam Flaviana wakiwa na kundi la wasichana warembo waliokuwa wakitabasamu muda wote isipokuwa wasichana wawili pekee ambao ni Sonia na Carolina. Baada ya Mwarabu yule aliyeonekana kama bodigadi kuwaona wenyeji wake, akatoa ishara kwa yule mwingine ambaye alichomoa simu yake na kupiga mara moja. Sekunde chache baadaye walionekana kuteremka Waarabu wengine ambao idadi yao ilifikia wanaume kumi na moja. Wengi walionekana kuvalia kanzu na vilemba vichwani isipokuwa mmoja tu kati yao ambaye alivalia kizibao cha rangi ya kahawia, miwani ya jua na kanzu nyeusi kiasi cha kuonekana nadhifu kuliko wote waliokuwa hapo. “Bila shaka yule ndiye mgeni wao,” alisema Henry aliyejificha ndani ya gari la vioo vya tintedi akimwambia afande John ambaye alikuwa bize akiliangalia tukio zima kwa darubini yake huku akivuta lenzi yake kuelekea upande waliosimama warembo wale. Kwa umakini mkubwa akapiga picha kadhaa za wasichana hao kwa kubonyeza kitufe fulani cha darubini hiyo ya kisasa na kusevu ndani yake kama picha za mnato. “Unaweza kumtambua mmojammoja kama nikikuonesha picha zao?” aliuliza afande John baada ya kumaliza kuchukua picha ya kila mrembo aliyekuwa katika kundi lile. “Yah,” alijibu Henry huku akiangalia kwa makini nje ya kioo chake. Yule Mwarabu nadhifu kuliko wote alionekana kujongea mbele na kuongea kwa muda na Mr.Chakos kisha wakapeana mikono na kukumbatiana kwa furaha kabla ya kila mmoja kumbusu mwenzake shavuni kama desturi ya Waarabu ilivyo. Baada ya kitendo hicho Kwa unyenyekevu, Mr. Chakos na Madam Flaviana waliwaongoza wageni wao mpaka kwenye msururu wa magari ya kifahari yaliyoegeshwa nje ya uwanja huo na kuwabeba wageni hao wakielekea kuponda raha ndani ya jengo la Serenity. Kila msichana aliyekuwa uwanjani hapo alipangiwa gari atakaloingia na kuketi akiwa na mgeni wake kabla ya baadaye kununuliwa na wageni hao ambao kwa huduma ya kila mrembo watapaswa kulipa fedha zisizopungua dola elfu mia tano kwa siku. Wakati wakielekea Serenity, Sonia alikuwa ameketi siti ya nyuma kabisa na Mwarabu mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Awadh Sayeed. Muda wote Awadh alionekana kumsumbua Sonia kwa kumpapasapapasa kila mara. Wakati mwingine alitumia nguvu kutaka kumvua blauzi yake kitendo ambacho Sonia alikichukia na kubaki akijisitiri mwili wake huku machozi yakimtoka. Bila kujali, Awadh aliendelea kumnyanyasa mrembo huyo huku akionekana kuvutiwa na kitendo alichokuwa akikifanya. Kuna wakati alimshika na kumpiga makofi huku akimtanua miguu yake kwa nguvu ili amalize haja zake humohumo kwenye gari, lakini Sonia alibana miguu yake kwa kadiri alivyoweza asiruhusu kudhalilishwa. Walipofika Serenity, wengi kati ya waarabu hao waliondoka na warembo hao huku kila mmoja akielekea katika vyumba maalumu ambavyo vilikuwa tayari vimeandaliwa kwa ugeni huo. Bila kupoteza muda Awadh aliyeonekana kuvutiwa na Sonia alikuwa wa kwanza kumbeba msichana huyo na kuingia naye ndani ya chumba chake tayari kwa kutekeleza azma yake mbaya. Kwa mbali Carolina aliyekuwa akiingia chumbani kwake na Mwarabu mwingine aliyejitambulisha kama Omar Kareem, alimuona Sonia akihangaika kujinasua maungoni mwa Mwarabu huyo, moyo wake ulimuuma sana kwa kitendo kile lakini katika mazingira hayo hakuwa na cha kufanya zaidi ya kutafakari jinsi ya kuyaepuka matatizo yake kwanza kabla ya kumsaidia mwenzake. *** Salima alionekana kuvinjari na Prince Khalfani kwa mtindo wa pekee. Mara alimkumbatia na kumbusu, mara alisimama na kuzungusha kiuno chake laini akicheza ala za kiarabu na mara nyingine aliongea kwa lugha laini na Prince Khalfani ambaye muda wote huo alikuwa mtulivu sana kama vile buibui atuliavyo akisubiri mdudu ajipeleke katika utando wake aanze kumshambulia. *** Wakati mambo yote yakiendelea kama yalivyopangwa, Madam Flaviana na Mr. Chakos wote walikuwa makini kuhakikisha hakuna kitakachoharibu ugeni wao. Wakakaa kwenye kompyuta zao wakiangalia kila kitu kinachofanyika katika vyumba hivyo. Katika kuonesha kwamba suala hilo lilikuwa na umuhimu, Mr. George mwenyewe alipiga simu kuulizia kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Wakati mwingine yeye mwenyewe ndiye alikuwa akitoa maelekezo ya nini kifanyike, wapi na wakati gani. *** Carolina akiwa chumbani na Omar, alivua nguo zake taratibu na kuvaa mavazi mepesi ya usiku kama alivyotakiwa kufanya. Wakati huo Omar alikuwa kitandani ameegemea kitanda chake akivuta sigara yake kwa pupa huku akimtazama Carolina kwa jicho la husuda, Carolina alilishtukia na kuzidisha manjonjo. Akili ya Carolina muda huo ilifanya kazi haraka sana kwani kadiri muda ulivyozidi kuyoyoma, ndivyo alivyozidi kupata wasiwasi juu ya rafiki yake Sonia ambaye kwa muda huo alikuwa katika wakati mgumu na Awadh. Harakaharaka lakini kwa mpangilio, Carolina aliuchomoa udi wake ndani ya boksi maalumu, akauwasha kisha akaanza kuufukiza chumba kizima kama wafanyavyo watu wa Pwani. Taratibu akajongea mahali alipolala huku akilipandisha gauni lake taratibu kana kwamba alijitoa kumpatia mwili wake. Lakini kadiri alipokuwa akimsogelea ndivyo Omar alivyozidi kutetemeka kwa hofu, mara akadondoka kitandani kama gogo huku akitoa sauti ya kukoroma kana kwamba alipitiwa na usingizi mzito. Baada ya zoezi hilo, Carolina alikimbilia bafuni ghafla na kunawa uso wake huku akijiziba pua kuuepuka moshi wa udi uliotanda ndani ya chumba hicho. Haraka pasipo kupoteza muda aliuzima udi ule ambao vielelezo vyake vilionesha kuwa ulitengenezwa kwa sumu aina ya ‘Carbon Monoxide.’ Sumu ambayo huanza kwa kulegeza fahamu za mtu kisha kufuatiwa na usingizi mzito kabla ya kifo. Kama mzimu, Carolina akazima taa na kurudi taratibu mpaka kwenye mabegi ya Omar. Akachambua nguo zake akitafuta simu au kifaa chochote cha mawasiliano ambapo kwa bahati aliipata simu ya kisasa ‘Smart Phone’ ambayo aliiwasha na kutuma ujumbe mfupi kwa mtu aliyemfahamu mwenyewe. *** “Sikilizeni, nimetumiwa meseji ya hatari kutoka kwa afande Beatrice. Haya kaeni tayari kwa kuvamia!” alisema Afande John akiwaambia makachero wenzake ambao tayari walikuwa wameishaizingira ngome ya ‘Serenity.’ “Samahani kidogo, Beatrice ndo nani?” Henry alishindwa kujizuia na kuamua kuuliza baada ya kusikia jina la afande Beatrice likitajwa kama mtu aliyetuma ujumbe wa hali ya hatari muda mfupi uliopita. “Ni afisa upelelezi ambaye alijipenyeza ndani ya Serenity bila kujulikana,” alijibu afande John lakini jibu hilo lilizidi kumwacha Henry njia panda badala yake akauliza tena. “Nini? Ina maana kumbe mlikuwa mnaifuatilia hii inshu kwa muda mrefu? Hivi huyo Beatrice ni nani humo ndani?” “Ni siri za kikazi. Kukusaidia tu ni kwamba, ‘Beatrice’ siyo jina lake halisi kwa hiyo usijisumbue kufikiria kama unamfahamu au la. Hima tuoneshe njia,” “Tuelekee huku,” aliongea Henry na kuingia kwenye mtaro wa majimachafu uliopita chini ya ukuta na kuibukia ndani ya uzio wa jengo hilo nyuma yake akifuatiwa na makachero ambao wote waliingia huku macho yao yakiwa makini kuangalia kila upande tayari kukabiliana na adui yeyote. Kwa namna fulani waliweza kupenya hadi ndani kabisa ya jengo hilo bila kuonekana kwa kuwa kulikuwa na giza nene sana usiku huo. Mwanga pekee ulioonekana hapo ni ule uliotokana na taa zilizoonekana kutokea vyumba vya ghorofani na juu ya ukuta wa fensi ile ndefu. *** Akiongozwa na hisia zake, Carolina alitoka chumbani kwake na kupita koridoni haraka kisha akaingia bila hodi ndani ya chumba alichokuwemo Sonia na yule Mwarabu Awadh.Wote walishtuka baada ya kumuona Carolina akiwa amesimama mbele yao. Aliyeshtuka zaidi alikuwa ni Awadh ambaye kwa wakati huo alikuwa kama alivyozaliwa. “Maadha turidu (unataka nini)?” Awadh alifoka kwa kiarabu huku akimtazama Carolina kwa hasira. “Laashakka (hakuna shaka),” alijibu Carolina kwa kiarabu pia huku akavifungua taratibu vifungo vya gauni lake jepesi akijaribu kumlaghai Awadh kwa mwili wake kana kwamba alikuwa na nia ya kufanya mapenzi ya watu watatu. Wakati huo Sonia aliyekuwa amejikunja pembeni ya kitanda, akikikumbatia kipande cha nguo yake ambacho ndiyo pekee kilichokuwa kimebakia kumsitiri maungo yake, alibaki akimshangaa rafiki yake asijue kusudio lake.
Taratibu fahamu za Salima zilianza kumrudia. Aliweza kukumbuka kila kitu kilichokuwa kimetokea. Mbali na kumbukumbu hizo pia alimkumbuka Dedan na Carolina. Wasiwasi ulianza kumjaa kila mara alipowaza uwezekano wa Dedan kurudiana na msichana huyo ambaye muda huo ndiyo kwanza alianza kumkumbuka kuwa aliwahi kuonana naye mara kadhaa alipokuwa ‘Serenity.’
Akiwa katika mawazo hayo, mara mlango wa wodi aliyolazwa ulifunguliwa. Ndani yake akaingia Dedan aliyeongozana na Carolina. Ikawa kama vile Salima alivyowaza. Kweli Dedan alikuwa mikononi mwa Carolina tena huku wakionekana wenye furaha juu ya maisha yao mapya, japokuwa walijitahidi kuificha hali hiyo mbele ya Salima.
“Salima unaendeleaje?” Carolina alitangulia kuuliza baada ya kumuona Dedan akisitasita kumsalimia Salima ambaye hakujibu chochote zaidi ya kufumba macho yake huku machozi yakimlengalenga.
“Salima, najua uliteseka sana juu yangu kiasi cha kujiingiza katika matatizo makubwa ili unisadie. Kwa moyo wangu wote, naomba radhi kwa hilo. Nipo tayari kurudisha wema wako kwa kukupatia chochote utakacho, tafadhali niambie nikupe nini ili angalau nirudishe nusu ya fadhila zako,” aliongea Dedan akijitahidi kuikaza sauti yake huku akijaribu kutoathiriwa na machozi ya Salima.
“Naomba unipe kitanzi, kisu au bastola!” alijibu Salima kwa hasira. “Una maanisha nini Salima?” aliuliza kwa mshtuko Dedan.
“Baada ya kupitia yote haya unadhani nitaishije? Si ni bora niukatishe uhai wangu kuliko kuishi kwa fedheha? Najua haukunipenda hata kidogo na najua siwezi kuubadilisha moyo wako ukanipenda mimi kama unavyompenda Carolina. Nyote wawili mna maisha mapya mbele yenu na mnapendana kwa dhati je, mimi nitabaki na nani? Niache nijiue,” aliongea Salima na kuangua kilio kikubwa. Dondoo:
-Kwa msaada wa Carolina, Salima aliweza kupatiwa kazi na nyumba ya kuishi, lakini mbali na yote hayo bado upendo wake kwa Dedan ulikuwa palepale. Kitu cha ajabu ni kwamba Salima alianza kubadilika kitabia. Alianza kukopi kila kitu kutoka kwa Carolina, kuanzia muonekano wake hadi utembeaji. Moyoni akitarajia kuuteka moyo wa Dedan.
-Carolina na Dedan walishtukia tabia ya Salima, ili kuepuka kumuumiza msichana huyo, wakahamisha makazi yao na kuelekea mkoani Arusha ambapo walianza maisha mapya kwa kufunga pingu za maisha na kuishi kwa raha mustarehe kama mume na mke.
-Sonia alifanikiwa kukutana na watoto wake na kuanza maisha mapya. Kutokana na akiba ya fedha aliyoiacha mumewe, Sonia aliweza kuanzisha biashara mbalimbali jijini na kuweza kujikimu. -Mr. Chakos na Madam Flaviana wote wawili walitupwa jela na kutumikia kifungo cha miaka 40 kila mmoja kwa makosa ya mauaji, utumwa na kukwepa kodi. Polisi nao wakiongozwa na Afande John bado walikuwa wakiendelea kumtafuta Mr. George wakiwa na matumaini ya kumtia nguvuni.
ILIKUWA ghafla, kama pigo la kisu ambalo lilipenya mwilini na kuujeruhi moyo wa Inspekta Kombora. Kati ya yote aliyoyatarajia jioni ya leo, simu kama hiyo, ya maafa, haikuwamo kabisa akilini mwake. Kwa jumla, ilikuwa kama iliyopigwa muda huu kwa ajili ya kumsimanga au kumdhihaki. Muda mfupi uliopita alikuwa akiitazama kwa furaha kubwa chati yake ya taarifa za wizi, ujambazi na mauaji nchini. Ingawa tabasamu ni kitu ambacho huutembelea uso wa Kombora kwa nadra sana, lakini leo liliutawala uso huo kwa muda mrefu wakati akiitazama chati hiyo. Furaha iliyotokana na jinsi idadi ya vitendo hivyo ilivyokuwa ikishuka kwa kasi. Ukiacha udokozi mdogomdogo, wizi wa kuaminiana na ule wa kalamu vinginevyo rekodi hiyo ilikuwa ikielekea kwenye sifuri. Wakati wowote Tanzania ingeweza kujitangaza duniani kama taifa pekee ambalo limeushinda kabisa ujambazi. Kombora alikuwa mtu wa kwanza aliyestahili kuifurahia hali hiyo kwani alikuwa mstari wa mbele kati ya wale wachache ambao huumiza vichwa vyao na kukesha usiku na mchana pindi linapotokea tukio lolote ambalo hutishia usalama wa taifa hili. Hivyo, alichekelea huku akimpongeza kimoyomoyo Waziri wa Mambo ya Ndani, Augustine Mrema, ambaye alisimamia kwa dhati ulinzi wa sungusungu ambao uliwajumuisha raia wenyewe kujilinda usiku. Kombora aliamini kabisa kuwa hilo lilichangia sana kupunguza wizi, uvunjaji wa majumba na mauaji ambayo yalifikia kiwango cha kukatisha tamaa. Hata hivyo, tabasamu la Kombora lilitoweka. Lile wazo lililokuwa likimpekecha ubongo mara kwa mara lilipomjia tena, wazo la kwamba, kama imefikia hatua ya raia wenyewe kukesha nje wakijilinda, vyombo ambavyo vina jukumu hilo vinafanya nini? Havitoshi? Haviwezi? Havifai? Haviaminiki? Na kama jibu limo katika moja ya maswali hayo kuna umuhimu gani wa kuwa na vyombo hivyo na kuvitengea mamilioni ya pesa kila mwaka? Akiwa askari mwaminifu, anayeipenda na kuiamini kazi yake Kombora alijisikia haya. Angefurahi zaidi kama idadi hiyo ya matukio ya kijambazi ingekuwa inashuka kutokana na uwezo wa polisi au usalama. Angefurahi zaidi kama raia wote wangelala usingizi wao kwa amani kama ilivyokuwa miaka michache iliyopita. Pamoja na hayo, aliendelea kuifurahia hali ya usalama. Alijiona kama kwamba wanausalama wako mapumzikoni au chuoni wakiandaa mkakati ambao utawafanya warudipo kazini watimize jukumu lao kwa uhakika zaidi. Ni wakati alipotoka mbele ya jedwali hilo na kuketi juu ya kiti chake pindi ilipolia simu hii na kuupasua moyo wake kwa habari za mauaji. “Unasema unaitwa nani vile?” Kombora aliuliza kwa ukali kidogo. “Sajini Brashi, mzee. Wa kituo Kikuu… Ni kweli hunifahamu. Lakini mimi nakufahamu…” Kombora alimkatiza tena, safari hii kwa ukali zaidi, “Kwa nini unipigie mimi? Huna mkuu wako wa kazi? Sikiliza, Sajini. Kama hadi leo hujafahamu taratibu za kazi yako nadhani njoo zako hapa tukupe barua ili urudi tena chuoni.”
“Sivyo, mzee,” upande wa pili ulijibu, kiasi sauti yake ikiwa na hofu. “Naufahamu wajibu wangu. Lakini kuna jambo katika mauaji haya, ambalo nadhani ungependa kuliona kabla ya mtu mwingine yeyote.” “Jambo lipi hilo?” “Labda nikuombe uje mara moja. Ni mwendo wa dakika tano tu, mzee…”
*** PONGWE Hotel ni moja kati ya yale mamia ya hoteli za kitalii ambazo ziliibuka kama uyoga huku na huko nchini, mara baada ya kutangaza ule uhuru wa kiuchumi. Hii ipo katika Mtaa wa Livingstone, Kariakoo. Ina ghorofa sita, vyumba mia na ishirini vya kulala, vyote vikiwa vinajitegemea kwa bafu, choo na mashine ya kurekebisha hewa. Kwa nje hoteli hii inaonekana kama hoteli nyingine nyingi za mji huu, kana kwamba wajenzi wake walikusudia kumfanya mpitanjia asivutiwe kabisa na majengo, rangi wala mandhari yake. Lakini ndani, hali ilikuwa tofauti kabisa. Utaalamu na utajiri vilijumuishwa kiasi cha kumfanya Kombora, ambaye hapati nafasi ya kutembelea hoteli mara kwa mara, atikise kichwa chake. Zilimchukua dakika tisa, badala ya tano, kutoka ofisini kwake hadi hapa, hali ambayo ilisababishwa na msongamano wa magari na ubovu wa barabara. Alimkuta Brashi, kijana mwembamba, mrefu, mwenye nywele nyingi aliyevalia kiraia, akimsubiri mlangoni. “Hadi sasa, zaidi ya mhudumu wa chumba hicho na meneja wa hoteli, hamna mtu mwingine anayejua kilichotokea,” Brashi alimweleza Inspekta akimwongoza ndani. “Ni katika ghorofa ya tano, chumba namba 108.” Walipita mapokezi ambapo mhudumu wa kike alikuwa akiwakaribisha wageni wanne kwa maneno na tabasamu lililotosha kabisa kuwashawishi wakae hotelini hapo kwa miaka. Kutoka hapo waliingia chumba cha vinywaji. Huko nusu ya viti vyote tayari ilimezwa na wateja walioonekana wachangamfu zaidi kutokana na bia nyingi zilizokuwa wazi mbele yao. Wawili kati ya wateja hao waligeuza nyuso zao kuwatazama Brashi na Inspekta Kombora, waliokuwa katika mavazi yao ya kawaida. Watumiaji hao waliwapuuza mara moja kwa kuwachukulia kama wanywaji wenzao. Brashi alimwongoza Kombora kuifuata ngazi ya kupandia juu. Mbele ya chumba walichokihitaji walimkuta meneja akinong’ona na mzee mmoja mwenye tumbo nene na uso wa mtoto mdogo ambaye, kwa kumtazama tu, Kombora alifahamu kuwa ni Mchaga. Nyuso zao zilijawa na wasiwasi. “Karibu mzee,” Meneja aliwakaribisha. “Huyu hapa ni bwana Mmari, ndiye tajiri wa hoteli hii. Nilikuwa nikimfahamisha mkasa uliotukuta.” Walishikana mikono. Kisha, wote wakaingia katika chumba hicho ambacho kwa mtazamo wa kawaida kilikuwa kama kawaida. Shuka zilitandikwa vizuri kitandani. Juu ya kitanda hicho alilala kifudifudi msichana mwembamba, mweupe, ambaye huhitaji kumtazama usoni ili ujue kuwa ni mzuri. Alivaa nguo zake zote; gauni jepesi, refu japo lilifunua paja moja na kuonekana kutokana na kulala vibaya. Mikono yake laini ilijaa bangili na pete ya dhahabu. Shingoni pia alikuwa na mkufu wa dhahabu ambao ulioana na nywele zake ambazo pia zilibeba rangi ya dhahabu. Kwa kila hali alikuwa msichana mzuri wa kileo. Angeweza kuwa amelala… angeweza kuwa amejipumzisha. Kombora alimtazama Brashi kama anayetaka ufafanuzi wa hayo. “Amekufa mzee,” Brashi alijibu swali hilo ambalo alilisoma katika macho ya kombora. “Amekufa kifo cha kikatili kupita kiasi.” Kombora hakuelewa. Alimwonyesha hivyo Brashi katika macho yake. “Labda nikuonyeshe, mzee,” alisema akimsogelea marehemu. “Nikuonyeshe jeraha mzee?” Kombora alipotikisa kichwa kukubali, Brashi alichukua kitambaa cha meza ndogo kando ya kitanda hicho na kukifunga katika mkono wake wa kushoto. Kisha, akautia mkono wake tumboni mwa marehemu na kumgeuza taratibu huku akiyafumba macho yake na kusema taratibu, “Jiandae kwa mshituko.” Kwanza Kombora hakuelewa. Ilikuwa kama anaota ndoto ya ajabuajabu inayotisha kuliko vitisho vyote. Kisha, akadhani kuwa haoti, bali anatazama sinema ya kuogofya kupita kiasi. Alipotanabahi kuwa hayuko pichani wala ndotoni alihisi alishikwa na kichefuchefu. Hakuhitaji kutapika kwani bwana Mmari alikuwa akitapika badala yake huku akitokwa na sauti ya kilio cha ghafla. Ilikuwa picha ya kutisha, picha isiyoelezeka wala kutazamika. Yeyote aliyefanya kitendo hiki hakuwa binadamu wa kawaida isipokuwa mnyama. Vinginevyo, hangewezaje kuthubutu? Angewezaje kufikiria hilo? Bila kujua atendalo, Kombora alijikuta akimshika Sajini Brashi mkono kwa vidole vyake vikubwa na kumbana huku akimuuliza kwa sauti ndogo, “Mimi nahusika vipi na maiti hiyo Sajin? Kitu gani hapo ambacho uliona kitapendeza sana niskikiona?” Brashi alijaribu kujitoa katika mkono wa kombora. Ilikuwa kama kujaribu kujikwatua toka katika pingu. Badala yake ndiyo kwanza vidole hivyo vilizidi kudidimia katika ngozi yake. Japo maumivu yalikuwa makali, lakini hayakumzuia kushangazwa na nguvu za mzee huyu. “Anakula nini?” alijiuliza akimtazama usoni. “Kitu gani ulichodhani kitanipendeza hapa?” Kombora aliuliza tena. “Unaniumiza Inspekta.” Ndiyo kwanza Kombora akafahamu kuwa alikuwa amemshika Brashi mkono. Akamwachia na kuiona damu ambayo ilianza kutoka katika michubuko iliyosababishwa na vidole vyake. Angeweza kumwomba radhi, lakini hakufanya hivyo. Rohoni mwake, aliona adhabu hiyo ndogo inatosha kabisa kumfunza adabu sajini huyu kwa kosa lake la kuivuruga amani na starehe aliyokuwa nayo moyoni kwa siku chache zilizopita bila misukosuko ya kutisha. Kumwita hili atazame maiti hii iliyokuwa katika taswira ya kutisha kupita kiasi, maiti ambayo haitamtoka akilini wala katika ndoto zake, kwa muda mrefu bila sababu ya maana, aliona ni ufedhuli wa hali ya juu. Alimkazia Brashi macho akifikiria adhabu ipi ya pili ambayo ingemfaa zaidi. Brashi hawezi kuwa mbumbumbu kiasi hicho. Hawezi kuwa mtu pekee nchini na duniani ambaye hafahamu kuwa Kombora alikuwa akiongoza idara maalumu na pekee ambayo hushughulikia yale masuala mazito na yanayotishia usalama wa serikali na taifa, si masuala madogomadogo, ya kawaida ambayo yangeweza kushughulikiwa na polisi wa kawaida. Kana kwamba anayasoma mawazo yake, Sajini Brashi alisema, “Samahani sana Inspekta, nilidhani wewe na Joram Kiango mna aina fulani ya uhusiano. Sijui namna yoyote ya kumpata Joram, ndipo nikaona nikuarifu wewe kabla ya kulipeleka suala hili kwa wakuu wangu ambako linaweza likatangazwa ovyo au kupuuzwa. Kama nimekosea, Inspekta, naomba radhi…” “Sijakuelewa Joram anahusika vipi na huyu marehemu?” Kombora aliuliza, moyoni akitetemeka kidogo kwa jibu atakalopata. “ Yawezekana huyu marehemu ni Nuru, yule mwenzi na mpenzi wake Joram Kiango. Kama ndiye…” “Hukuona mzee?” Brashi alikatiza mawazo yake. “Hukuona? Basi nitalazimika kumfunua tena marehemu.” “Kuona nini?” Kombora alijaribu kumzuia, lakini alichelewa. Tayari alikwishamgeuza maiti chali. Kombora alilazimika kulitazama tena jeraha hilo. Bado lilikuwa halitazamiki. Utalitazamaje jeraha ambalo lilikuwa zaidi ya jeraha? Pale ambapo palitakiwa kuwa na uso wa msichana huyo, toka sikio hadi sikio, na paji la uso hadi kidevu, badala yake palikuwa na shimo la kutisha lililokuwa limekula nyama zote na kuacha mifupa mitupu. Pale yalipostahili kuwepo macho, pua, midomo na ulimi sasa yalikuwa mashimo ambayo yaliacha wekundu wa nyama na damu uonekane kiasi cha kutisha zaidi ya fuvu lolote la binadamu. Safari hii, akitazama kwa makini zaidi, Kombora aliweza kubuni kilichokula nyama hiyo. Kama si biological weapon ya kisasa zaidi ambayo inatoa wadudu wadogo na wengi sana ambao wanashambulia nyama ya binadamu kwa dakika kadhaa kabla ya kufa, basi ni aina kali sana ya asidi ambayo ilimchoma binti huyo uso mzima na kuacha mifupa mitupu. “Unaona mzee?” Brashi alimzindua. “Nini?” “Tazama hapa,” alielekeza mkono wake pale ambapo palistahili kuwa kinywa, ambapo sasa palikuwa na meno yaliyotokeza kana kwamba yanalia au yanacheka. Kombora aliinama na kuchungulia. Ndipo alipoweza kukiona kipande cha karatasi kilichokuwa kimelazwa humo kinywani. Kilikuwa na maandishi. Kombora aliinama na kuyasoma. “TUNAMTAKA JORAM KIANGO” Kombora aliyasoma kwa mara ya pili kabla hajaupata ujumbe huo. Alipoupata aliingiza mkono wake mfukoni na kutoa kitambaa. Akakizungushia katika vidole vyake na kuvididimiza humo kinywani hadi alipofikia hicho kipande cha karatasi. Alikichukua na kukizungushia katika kitambaa hicho na kisha kukitia mfukoni mwake. Baada ya hapo alimgeukia Brashi na kumwambia, “Sikia sajini, umefanya kazi nzuri. Wanamtaka Joram Kiango. Tutampa ujumbe wao.” Alimkazia macho kabla hajaendelea, “Sasa unaweza ukaendelea na taratibu zako zote, kama kawaida. Tafadhali nitaomba unipe taarifa kamili ya upelelezi wenu juu ya mauaji haya mara mtakapokuwa tayari. Sawa?” Brashi alitikisa kichwa. “Na unajua sajini? Sikio la mtu yeyote nje ya chumba hiki lisisikie kuwa mauaji haya ni salamu tu kwa Joram Kiango. Nataka iwe siri, tafadhali.” “Bila shaka Inspekta.” “Ngoja nikuonyeshe,” alisema akiinama tena kitandani na kumshika maiti.
*** HADITHI ilikuwa fupi na nyepesi. Kwa jina aliitwa Sofia Ali, mzaliwa wa huko Dodoma, wilayani Mpwapwa. Alikuja Dar es Salaam kama ilivyowatokea wasichana wenzake wengi wa hirimu yake. Amemaliza shule darasa la saba hana kazi wala mchumba. Jirani, mke wa bwana fulani huko Dodoma mjini anatokea na kumshahuri wafuatane naye mjini kumtunzia nyumba. Mshahara? Mia tano kwa mwezi. Chakula bure, malazi bure, nguo alizochoka nazo mama mwajiri bure, Akatae? Kama wengi wengine Sofia alijikuta yuko mjini. Maji ya bomba ya mara kwa mara, chai ya maziwa kila asubuhi, chakula chenye viungo vyote; pamoja na ile dokoadokoa ya vipodozi vya mama ilifichua kiumbe mrembo aliyejificha katika umbo lile lililochakaa la Sofia Ali. Badala yake, miaka miwili baadaye, aliyesimama mbele ya mama mwajiri alikuwa Sofia mwingine kabisa, Sofia aliyewiva, Sofia aliyejaza, Sofia ambaye alimfadhaisha baba mwenyenyumba na kumtisha mama. Matokeo yake Jumapili moja alipewa tiketi ya kurudi Mpwapwa. Kufanya nini? Kazi basi. Hakurudi Mpwapwa. Akafuate nini? Jembe na mpini wake? Amwachie nani starehe za sinema na muziki ambazo ndio kwanza alikuwa ameanza kuzionjaonja? Rafiki yake aliyekuwa akiishi Tambuka Reli, ambaye alikuwa ameanza kujitegemea baada ya kupitia mkondo huohuo, alimpokea. Chumba chao chenye upana wa futi tano kilibeba kitanda chao cha futi tatu na majukumu yote ya jiko, ghala; na mengineyo. Ungewatembelea mchana wakati wa joto, huku moshi ukiwaadhibu, usingekosa kuwahurumia. Lakini waone jioni, wakati tayari wameoga, wamevaa na kujitengeneza usingekosa kujiuliza kwa nini hawajatokea wachumba wakawaoa. Mwaka mmoja baadaye, Sofia alikuwa Sofia hasa. Hata shoga zake walianza kumchukia kwa wivu. Hakujali, kwani alikuwa na marafiki wengi wa kiume kuliko wa kike. Na ni hao ambao aliwahitaji. Wakati huo hata jina alianza kulibadili. Badala ya Sofia sasa alijiita Soffy. Na alipenda sana baba yake aitwe Ally badala ya Ali. Hata lugha yake ilianza kubadilika. Katika kila sentensi alijikuta akiweka walau neno moja la Kiingereza. Hakujua kilipotokea hicho Kiingereza chake Lakini alikuwa na hakika nacho. Sofia alifanya kosa. Mimba iliingia bila taarifa wala hiyari. Bwana hakumjua wala hakuhitaji mtoto. Alimeza vidonge mimba ikafa. Miezi miwili baadaye mimba ya pili ilimkamata. Hii haikusikia vidonge. Miezi mitatu, minne, mitano! Kila mtu alianza kumshuku. Elfu tatu zilimaliza kazi. Daktari mmoja asiye na huruma, alifanya kazi hiyo na kutupa mtoto anakokujua. Sofia aliponea chupuchupu. Baada ya miezi mitatu ya maumivu, afya yake ilimrudia. Mji wa Dodoma akauona nuksi. Huyoo, akaingia Dar es Salaam. Dar ilimlaki juujuu. Rafiki yake mmoja wa Kinondoni, akijua kuwa umbo la Sofia lingemwongezea riziki, alimkaribisha kwake na kumwonyesha mji. Madisko ya Lang’ata na Ushirika yaliwakoma. Madansi ya DDC na Friend’s Corner yaliwatambua. Mabaa ya Sky Way na Kilimanjaro, yaliwaheshimu. Mabwana walikuwa tele, wa kila kabila na kila rangi. Sofia hakujua kumkataa mtu. Ni yeye aliyeanzisha msemo wa “… Ni pochi yako tu.” Jioni ya leo alikuwa katika Hoteli ya Sky Way, ndipo alipomwona yule kijana mrefu, mnene, ambaye alikuwa akinunua vinywaji kwa fujo kuliko mtu mwingine yeyote hotelini hapo. Na mifuko yake bado ilionekana kuwa imetuna. Wasichana wengi waliokuwa wakimzengeazengea walipewa bia na kufukuzwa toka mezani pake. Sofia hakuwa mtu wa kuomba bia. Yeye huitwa au kufuatwa. Alimtupia jicho moja tu kijana huyo na kuona tayari ameimeza ndoano yake. Hakukosea kwani dakika mbili baadaye alianza kuletewa bia, oda ya kijana huyo. Na dakika kumi baadaye tayari waliketi pamoja, na kuanza kushikanashikana. “Unasemaje? “Pochi yako tu, darling “Kiasi gani?” “Hata wewe? Nilidhani umesoma, brother.” Maongezi yao yaliishia katika kimojawapo cha vyumba vya hotelini. Baada ya nusu saa ya vilio na vicheko vya uongo na kweli Sofia alipokea “pochi” yake. Wakati akijiandaa kuondoka kijana huyo alimshika mkono na kumwambia, “Unajua Soffy, ni tamaa tu iliyonifanya niamue kuanguka nawe. Kwa kweli, nina rafiki yangu mpenzi, mwenye kitita cha pesa, kuliko hiki changu ambaye amenituma hapa Sky Way kumtafutia mwanamke mzuri. Kweli, hata hizi pesa nilizokuwa nikizinywa ni zake, kama hujachoka nikupeleke.” “Kuchoka!” Sofia alicheka. “Nani aliwahi kuchoka kupokea pochi? Kama una wivu, I can understand, kama huna nipeleke.” Kisha, Sofia alishituka na kusita kidogo wazo jipya lilipomjia. “Huyo, rafiki yako, What is his name?” aliuliza. “Jina simfahamu.” “Why! Ni binadamu kweli?” “Sema, maana mambo ya siku hizi you can’t understand. Mimi sijachoka kiasi cha kumvulia underware yangu mnyama.” Kijana huyo alicheka. “Unadhani mimi ni crazy kiasi hicho? Huyo ni mtu mwenye hadhi na heshima zake. Naamini hujapata kukutana na mtu mzito kama huyo.” Bado Sofia alisitasita kidogo. “Jina humjui. Wewe mwenyewe unaitwa nani, honey?” “Niite Ram Shog.” “Na huyo friend wako yuko wapi?” Alipomalizia kuvaa, Ram alimshika mkono Sofia na kumwambia, “Twende nikupeleke. Amepata chumba katika Hoteli ya Pongwe.”
*** ***
Kiti cha Kombora kilikuwa kama chenye moto. Hakikukalika, mara aliinuka mara aliketi kana kwamba alikalia kaa ambalo lilikuwa likimchoma. Mkononi alikumbatia redio call yake kwa utulivu kama roho yake. Aliitazama na kuitingisha kama yai ambalo hakuwa na hakika kama ni zima au bovu.. Hata hivyo, alikuwa na kila hakika kuwa haikuwa mbovu. Ni ile ya upande wa pili ambayo alihitaji kuitilia shaka.
Muda mfupi tu uliopita alikuwa akiwasiliana na Koplo Shoka toka Lang’ata. Mara mawasiliano hayo yakakatika. Hakujua kama ilitokana na ubovu wa chombo hicho au Shoka alikata ghafla maongezi kuepuka mtu ambaye angeweza kuyasikia. Alichokuwa ameambulia ni “…Afande … tumempata…” na kisha “ amefika…” kisha chombo kikazimwa. Juhudi zote za Kombora kumpigia tena hazikuzaa matunda.
Wazo la kufanya uchunguzi kwa makini hapo Lang’ata lilimjia Kombora kutokana na uzoefu wake juu ya tabia za muuaji. Mara kwa mara katika kesi nyingi za mauaji hutokea muuaji akapenda kutembelea eneo na hata nyumba yalimotokea mauaji hayo.
Mara nyingine hutokea muuaji akadiriki hata kuhudhuria mazishi ya mtu aliyemuua. Kitu ambacho Kombora alikuwa haelewi ni sababu ipi ambayo hufanya wauaji hao wafanye hivyo. Hakujua kuwa walikuwa katika upelelezi wa kuelewa polisi wamefikia wapi katika uchunguzi wao, ama ni yaleyale waliyosema wahenga kuwa “damu nzito…” kwani mara kadhaa wauaji wengi wamepatikana kutokana na makosa hayo. Ni hilo tu ambalo lilimfanya amwamuru Shoka kuendelea na uchunguzi wake hapa Lang’ata ingawa siku mbili zilizopita hazikuwa na mafanikio.
Hivyo basi, redio yake ilipopata uhai na sauti ya Shoka ilipojitokeza na kusema “Tumempata” alijisikia kulia kwa furaha. Mara ukimya huu ukazuka. Dakika saba sasa zilikuwa zimepita. Aliendelea kuisubiri redio ya Shoka ipate uhai, aendelee kumwarifu alichogundua.
Dakika nane.
Dakika tisa.
Mara Kombora akaruka kama aliyeguswa na waya wa umeme. Akapiga ngumi kwa nguvu juu ya meza. Ameanza kuwa mzee? alijiuliza kwa hasira akiutia mkono katika fungati la meza yake na kuutoa ukiwa umeshikilia bastola yake kubwa ambayo aliitia mfukoni mwake.
Akatoka nje ya ofisi yake na kuchungulia ofisi ya msaidizi wake. Hakuwepo. Chumba cha pili alimpata askari mmoja ambaye alimtumia kuwakusanya askari wote waliokuwa ofisini wakati huo. Ukiwa usiku wa saa tano kasoro kituo kilikuwa na askari wanne tu. Wengine walikuwa katika shughuli nyinginezo au mapumzikoni. Kombora aliwachukua askari wawili na kumwamuru mmojawao aendeshe gari kasi iwezekanavyo kuelekea Lang’ata.
Gari lilikuwa likiruka, nusura lipae, lakini Kombora alizidi kumhimiza kijana huyo akanyage mafuta. Mara mbili askari mmoja alijaribu kumdadisi Kombora Lang’ata kulikoni lakini hakupata jibu lolote. Si kwamba Inspekta hakupenda kuzungumza, la! Isipokuwa hakuiamini sauti yake.
Hisia za hatari zilikuwa zikichemka akilini mwake na kumjaza hofu kila alipoyakumbuka maneno ya Shoka “…tumempata…” na kisha maongezi kukatika. Ni hili la mwisho lililomtisha zaidi. Amefika! Bila shaka ni Kakakuona. Amefika wapi? Alikuwa amefika katika ukumbi au alimfumania Shoka akiipiga redio hiyo? Kama ni hivyo kipi kinachofuata? Kombora alimwamini Shoka. Lakini pia aliamini kuwa Kakakuona yu kiumbe hatari zaidi ya simba aliyejeruhiwa. Ni hilo lililomtoa kasi ofisini.
Wakati wanafika mbele ya lango la ukumbi huo walisikia muziki ukikatika ghafla na kimya kikubwa kuzuka ndani ya ukumbi.Kombora aliruka nje ya gari na kumwambia askari mmoja alinde lango, asiingie wala kutoka mtu yeyote. Askari wa pili aliamriwa kufuatana naye.
“Kakakuona,” Kombora aliwanong’oneza. “Inawezekana yumo humu ndani. Picha zake mnazo. Mkimwona, kama hana silaha, msisite kumuua kwanza, maswali tutamuuliza baadaye. Okey?”
Ndani aliwakuta watu wakizungumza kwa sauti ya hofu na minong’ono. Umati mkubwa ulikuwa ukipambana kuingia choo cha wanaume ambako kila aliyetoka huko alikuwa kimya, aliyeduwaa kama aliyeona mzimu.
Ilimchukua Kombora na msaidizi wake dakika tatu nzima kuweza kupenya umati huo kuyafikia maiti. Hakuwa na haja ya kuyatazama kwa makini kabla ya kumtambua Shoka ambaye alilala kifudifudi kama anayechungulia kitu katika shimo la choo huku damu ikiendelea kutiririka na kufanya bwawa dogo jekundu liendelee kupanuka.
Kombora aliyasaga meno yake kwa hasira. Kisha alimwamuru mgambo ambaye alikuwa mbele ya mlango huo wa choo, akijaribu kuwazuia watu, kuufunga mlango wa choo hicho na kuulinda. Akarudi mlangoni ambako alitoa amri mpya. Watu wote watoke ukumbini humo, lakini si kabla ya kukaguliwa kila mmoja, tangu mifuko hadi vitambulisho.
Polisi wa Kituo cha Magomeni ambako tayari walikuwa wamepigiwa simu walipewa amri hiyo pia na kusaidiwa kuitekeleza. Wasichana, watoto na watu ambao hawakuwa na haja ya kushukiwa walitoka kwa urahisi. Watu wenye vitambulisho halali na shughuli zinazofahamika pia waliachiwa bila tabu. Lakini kuna wale ambao hata wao wenyewe hawazifahamu kazi zao, wale wenye zaidi ya kitambulisho kimoja, wao walitokwa jasho kwa maswali.
Baadhi yao walijikuta wakitupwa katika magari ya polisi na kupelekwa kituoni ambako waliendelea kuchunguzwa.
Muda wote huo Inspekta Kombora alikuwa nje ya ukumbi, kaegemea gari lake, mkono mfukoni ukiipapasapapasa bastola yake. Macho yake yalikuwa makini yakiuangalia kila uso na kila sura. Hakuiona dalili yoyote ya Kakakuona. Wala hakuwa na matumaini makubwa ya kuiona. Alivyomfahamu, kama mauaji hayo alikuwa kayatenda yeye, kwa vyovyote muda huo alikuwa maili kadhaa nje ya eneo hilo. Hata hivyo, yawezekana akawa hakuyafanya yeye. Mtu aliyeyafanya anaweza akazubaa humo ukumbini, au akawa ameshirikiana na mtu ambaye atazubaa. Hilo ndilo lililomfanya asisitize uchunguzi wa makini kwa kila mtu.
Baada ya muda alimwita mgambo mwingine aliyekuwa akilinda magari na kumuuliza taratibu, “Ulikuwepo muda wote au ulitoka?”
“Nilikuwepo mzee.”
Unaweza kukumbuka ni magari mangapi yameondoka dakika kumi kabla ya tukio hili.”
“Kama sikosei, ni magari matano tu mzee.”
“Jaribu kukumbuka taratibu, unieleze magari hayo ni ya aina gani, yaliwachukua kina nani na yaliwapeleka wapi?”
Mgambo huyo alikuwa na kumbukumbu kali ambayo ilimfurahisha sana Kombora. Aliweza hata kukumbuka namba za magari matatu kati ya hayo, mawili ya kwanza yakiwa ya wenye disko hilohilo lililokuwa likipigwa hayakumvutia Kombora. Gari la tatu ambalo lililokuwa na wavulana wawili na wasichana wao pia halikumsisimua. Magari mawili ya mwisho ndiyo yalimfanya amtazame mgambo huyo kwa makini zaidi huku akitoa daftari lake dogo.
“Datsun nyekundu! Unasema ilikuwa na shombe wawili tu! Ambao walifika wakakaa dakika tano na kuondoka?”
“Ndiyo, mzee.”
“Namba yake…”
“TZA 42112”
Kombora aliinakili na kuuliza “Ilielekea wapi?”
“Sikumbuki vizuri nadhani ilielekea mjini.”
“Na hii nyingine unasema ni TZB 414, sio?”
“Ndiyo.”
“Toyota Corolla?”
“Ndiyo.”
“Ilikuwa na mtu mmoja tu! Ulimwangalia vizuri?”
“Sikupata nafasi ya kumwona vizuri. Lakini kwa harakaharaka nilimwona kama afisa hivi. Hata mavazi yake yalikuwa ya bei. Alitembea taratibu sana mkono mmoja mfukoni na kuingia katika gari lake. Nilitegemea atanipa walao asante kwa kumlindia gari lake, lakini hata kuniaga hakuniaga. Nadhani hiyo ndiyo sababu iliyonifanya niitazame gari yake na kuiweka namba akilini.”
Kombora alimsikiliza kwa makini na kunukuu hili na lile. Wakati akitaka kumtupia swali lingine, aliitwa mlangoni haraka. Mtu mmoja alikuwa amekamatwa na bastola. Alijaribu kuificha katika mapaja yake lakini mikono ya askari hao, ambayo imeelimika, ikaifikia.
Akapelekwa katika chumba cha ofisi ambamo aliendelea kuhojiwa huku Kombora akiifungua bastola hiyo na kuangalia risasi. Ilikuwa na risasi sita. Haikuwahi kufyatuliwa. Kibali cha kuwa na silaha? Hakuwa nacho. Kazi anayoifanya? Hakuijua. Kwa nini alikuja kwenye starehe na silaha? Hakujua. Kwa mtazamo wa harakaharaka, Kombora hakumwona kama mtu wake. Hivyo, aliamuru apelekwe kituoni pamoja na watuhumiwa wengine.
Hadi anahojiwa mtu wa mwisho ilikuwa yakaribia saa tisa alfajiri. Ndipo Kombora aliporudi ofisini baada ya kuhakikisha maiti yanapelekwa Muhimbili na familia yake kuarifiwa.
Ofisini Kombora aliinua simu na kumpigia Mkuu wa Usalama Barabarani, Mkoa wa Dar es Salaam. Bosi huyo, akiwa na usingizi mzito, alikoroma kwa hasira katika chombo cha simu “Nani?”
Lakini aliposikia jina na sauti ya Inspekta Kombora usingizi ulimtoka mara moja, akakiacha kitanda na kuuliza kwa upole, “Nikusaidie nini, mzee?”
“Samahani kwa kukusumbua,” Kombora alimwambia. “Ni suala ambalo haliwezi kulala. Naomba uwaambie vijana wako ambao wako zamu wanitafutie habari za magari haya mawili. TZB 414 na Datsun TZA 42112. Ikiwezekana waambie wayafuatilie kuona sasa hivi yako wapi. Waonye wasiwaulize wenyewe swali lolote ambalo linaweza kuwafanya washukiwe. Sawa?”
“Sawa.”
“Naweza kuyapata maelezo haya ofisini hapa kesho kabla ya saa moja asubuhi?”
“Tutajitahidi… nadhani tutapata.”
Kombora akaizima simu na kumtazama kijana wake mmoja ambaye alikuwa ameingia chumbani humo na kusimama kama aliyeitwa.
“Enhe?” Kombora akamtupia.
“Nimepokea simu kwa niaba yako mzee, baada ya kuona una simu nyingine. Imetokea Central ambako wanasema wamearifiwa na wavuvi juu ya maiti ya msichana mcheza disko ambayo wameiokota ufukweni. Wanasema amenajisiwa na kulawitiwa…”
“Kwa nini waniarifu mimi?” Kombora alimkatiza kwa ukali kidogo.
“Sura”
“Sura?”
“Wameniambia kwamba nikikwambia sura yake…”
“Inatosha!” Kombora alimwambia akiinua mkono wake kuuegemeza kwenye kichwa chake. Kwa mara ya kwanza katika maisha yake alihisi uzee ukianza kumshinda nguvu.
AKIWA mgeni katika hoteli hiyo, Sofia alivutiwa mara tu baada ya kushuka toka katika teksi iliyowaleta. Ram akamwongoza hadi mapokezi ambako aliomba ufunguo wa chumba namba 108. Walipanda ngazi hadi ghorofani ambako walifungua na kuingia hadi chumbani. “Itabidi umsubiri,” Ram alimwambia Sofia ambaye alikwishajitupa juu ya kitanda na kujilaza. Usingizi wa pombe ukamchukua. Hakuamka tena hadi majuzi, meneja wa hoteli alipojaribu kumwamsha na, hatimaye, Sajini Brashi alipomgeuza na kukutana na uso ule ambao aliokutana nao.
GARI lilimteremsha Joram Kiango mtaa wa pili. Kama ilivyo Dar es Salaam nzima, pamoja na kwamba sasa ilikuwa usiku wa manane, bado mitaa yote ilikuwa na watu waliokuwa na shughuli zao. Wako walioketi kwa makundi wakinywa pombe mbele za nyumba mbalimbali ambazo zimetokea kuichukulia biashara hiyo kama kitegauchumi muhimu.
Wengine walikuwa wakiuza chipsi, chai, au kahawa katika magenge. Baadhi walikuwa wamekaa tu kuepuka joto na mbu waliokuwa wakiwasubiri vyumbani mwao. Hivyo, ilikuwa rahisi kwa Joram kujipenyeza hapa na pale hadi alipoupata uchochoro uliomfikisha nyuma ya nyumba yake.
Alisikiliza kwa makini hadi alipohakikisha kuwa nyumba ilikuwa tupu kama alivyoiacha kisha, kama mwizi alifungua mlango taratibu na kujipenyeza ndani. Kama mwizi, vilevile hakuthubutu kuwasha taa. Badala yake alitumia tochi yake ndogo kufanya uangalifu mkubwa kuepuka asiguse kiti kilichotegwa bomu. Alilifikia kochi. Akaketi na kuanza kusubiri.
Kusubiri, ikiwa kazi ngumu kuliko zote kwa Joram Kiango, kulianza kumkinaisha dakika tano tu baadaye. Hata hivyo, alijua hiyo ilikuwa silaha yake pekee ambayo ingemfanya akabiliane na adui ana kwa ana. Maadui hao wakiwa wanaamini kuwa wamemlazimisha kuketi juu ya kiti chenye bomu, alikuwa na hakika kuwa baada ya muda wangependa kujua matokeo ya kikao hicho. Hivyo, wangetuma watu au mtu kuangalia. Ni mtu huyo ambaye Joram alikusudia amfikishe mbele ya bosi wao na mbele ya Nuru ambaye wamemteka nyara, apende asipende.
Subira ilikuwa dawa pekee.
**
Nuru pia alikuwa akivuta subira. Walikuwa wametua mahali fulani katika pwani ya Zanzibar kitambo. Lakini yeye aliendelea kujifanya hana fahamu adui zake hao walipokuwa wakiufunga vizuri mtumbwi wao na kisha kujitenga kando ambapo walipanga mambo yao kwa sauti za mnong’ono. Baada ya muda walimrudia Nuru, mmojawao akimtikisa.
“Bado amezirai?” mwenzie alijiuliza kwa mshangao.
“Asidanganye huyu,” yule ambaye alikuwa amemshika mkono alisema.
“Dawa yake ndogo sana.”
Aliupeleka mkono wake mfukoni na kutoa kibiriti, akawasha njiti moja na kukichoma kidole cha Nuru. Maumivu yalikuwa makali kupita kiasi. Lakini Nuru alijikaza kisabuni, bila kutikisika wala kufumbua macho.
“Au amekufa?” mwenzie aliuliza tena. “Angalia usimtie jeraha. Bosi hatafurahi. Angependa sana kumpata akiwa kamili. Mpe Konyagi kidogo itamzindua.”
Kiberiti kikazimwa na Konyagi kutolewa kutoka katika mfuko wa koti la mmojawao. Nuru aliponyweshwa fundo la pili alijitia kupiga chafya huku akifumbua macho.
“Ni… ni…niko wapi?” alijitia kuuliza.
Adui zake wakaangua kicheko.
“Uko wapi?” Chongo alimdhihaki. “Uko kisiwani. Uko katika kisiwa cha karafuu. Uko likizo ndogo.” Kisha, akazungumza kwa sauti ya amri. “Ni hivi. Tuko Zanzibar kwa ajili ya mapumziko kidogo. Tunataka kukuburudisha kwa wiki moja hivi kabla ya kurejea Dar. Mimi na rafiki yangu hapa tumeafikiana kuwa wewe ni msichana mzuri.”
“Na mtamu,” mwenzie alidakia.
“Ndio, mtamu tosha,” aliendelea. “Hatuna shaka kuwa tutakuwa kama wewe. Tumeafikiana, itakuwa mmoja anaburudika mmoja anashuhudia, ni mchezo mzuri… tunaamini utapenda.”
Nuru alihisi akiingiwa na hofu kubwa zaidi. Atafanya nini na watu hawa wenye wazimu? Alijiuliza. Apige kelele? La! Ni aibu kwake. Vilevile, kabla sauti yake haijafika popote risasi zingekuwa tayari zimeifumua kichwa chake. Hawakuwa watu wenye hata chembe ya simile.
Alichohitaji ni subira. “Tunaye rafiki yetu mmoja anayeishi hapahapa,” yule mwenye chongo aliendelea kueleza. “Tutakufungua kamba za miguu na kukufunga za mikono kwa namna ambayo itakuruhusu kutembea kwa urahisi zaidi. Mimi nitakuwa nyuma yako, ndugu yangu. Lazima utembee kama kawaida kana kwamba tupo pamoja. Sawa?”
Nuru alitikisa kichwa.
“Sina mchezo! Sina mchezo kabisa!” Chongo aliendelea kubweka. “Unaiona hii?” aliitoa bastola yake na kumwonyesha Nuru. “Unaona kuwa ina kiwambo cha kupotezea sauti! Kwa taarifa yako, mara tu utakapojitia unaanza umalaya wako mimi nitabonyeza. Kwangu ni rahisi sana. Unaonaje?” alisema akilenga bastola hiyo kwenye uso wa ajabuajabu wa mwenzie na kuifyatua.
Nuru hakuyaamini macho yake. Alimtazama adui huyo anavyotapatapa na hatimaye kuanguka chini kama gunia, huku tundu kubwa lililojitokeza hapo usoni likivuja damu nyingi.
Nuru alipomtazama tena mwenye chongo alimwona akitabasamu. Kwa sauti inayotabasamu vilevile alimsikia akijigamba, “Unadhani ningekubali kuchangia mtoto mzuri kama wewe na dude hilo? Usiwe na shaka mpenzi, ni mimi na wewe tu.”
Baada ya maneno hayo alianza kufanya kazi harakaharaka. Alimzoa Nuru na kumbwaga chini. Kisha akamzoa mwenzie huyo ambaye alikuwa akipapatika na kumbwaga ndani ya mtumbwi. Akautia mkono wake mfukoni na kuutoa ukiwa na kititita cha pesa na kukididimiza mfukoni mwake. Kisha, akaufungua mtumbwi na kuuelekeza baharini. Akautega usukani vizuri na kuufunga kwa kamba halafu aliwasha mashine, mtumbwi huo uliondoka kasi kuelekea baharini. Akamrudia Nuru na kumfungua kamba za mikononi na miguuni.
‘Sasa!’ Nuru aliwaza na kujiandaa kupambana. Hata hivyo, alisita. Hakuona kama ulikuwa usiku wake, kwa jumla ulikuwa usiku wa adui yake. Wangeweza kufanya chochote walichotaka. Hata ukimya na uhaba wa anga lao, mvuvi mmoja katika pwani yote hiyo ilikuwa dalili ya ushindi wa maadui. Ni hilo lililomfanya Nuru asite, azidishe unyonge na ulegevu, pindi kamba zikifungwa upya ubavuni mwake.
“Twende zetu,” Chongo alisema baada ya kuhakikisha ubora wa kazi yake. “Kama nilivyosema, kumbuka hila ndogo tu ni mauti yako.”
Wakaondoka, Nuru mbele, Chongo nyuma. Ulikuwa sawasawa na msafara wa malaika wa shetani.
***
Saa kumi na mbili kamili ilimkuta Kombora akiwa tayari ofisini mwake. Alikuwa amejiiba kwa dakika arobaini tu kwenda nyumbani kwake ambako alioga na kubadili mavazi. Akajaribu kunywa kifungua kinywa ambacho kilikataa kushuka, akaishia kunywa kahawa kikombe kimoja na kuipooza kwa glasi ya maji ya kunywa.
Ofisini alikuta majalada kadhaa yakiwa juu ya meza yake. Moja ilikuwa taarifa ya magari aliyoyahitaji, ambalo lilifika nusu saa iliyopita. Nyingine ilikuwa taarifa ya uchunguzi mbalimbali la watu waliokuwa wamekamatwa pale Lang’ata. Jalada la tatu lilikuwa la taarifa ya kifo cha Doll.
Shingo upande, Kombora alianza na jalada hilo la mwisho, mara tu alipolifunua macho yake yalikutana na ile picha ya kusikitisha ambayo hakutaka hata kuiona. Picha ya marehemu, msichana mzuri, ambaye alilala juu ya mchanga, ufukoni, uchi kama alivyozaliwa, mavazi yake yakiwa yametupwa kando. Umbo lake lilikuwa zuri, la kuvutia toka miguuni hadi shingoni, usoni kulikuwa hakutazamiki. Sura yake ilikuwa imeharibiwa kinyama kama wale marehemu waliotangulia. Kombora alifunika huku akisaga meno yake kwa hasira kisha akayasoma maelezo yalioambatana na picha hiyo.
Ilikuwa kama ilivyotarajiwa maiti aliokotwa na wavuvi mnamo saa sita na robo usiku akiwa kama alivyo pichani. Taarifa ya madaktari ilithibitisha kuwa aliuawa kwa aina ileile ya sumu iliyowaua waliotangulia, sumu ambayo hadi sasa wanamaabara walikuwa hawajapata kuifahamu. Taarifa hiyo ilieleza jina la marehemu, wazazi wake, marafiki zake na kwamba jioni hiyo alionekana katika ukumbi wa Lang’ata muda mfupi kabla ya kifo chake.
Kombora aliliweka kando jalada hilo na kutwaa lile lenye maelezo ya watu walioshukiwa usiku huo. Alifunua harakaharaka akitafuta maelezo ambayo yangemfanya ayape uzito mkubwa zaidi. Kama alivyotarajia, hakuona kuwa kati ya hao kuna yeyote ambaye angeweza kuwa mtu wake.
Yule aliyekamatwa na bastola alitambulika baadaye kama jambazi mkubwa ambaye alikuwa akitafutwa muda mrefu kwa kosa la mauaji ya tajiri mmoja wa Kihindi huko Mwanza. Watu wawili waliokuwa na vitambulisho vya bandia walifahamika kama matapeli wenye tabia ya kughushi hundi za bandia. Mmoja hakuwa na akili timamu. Alikuwa kavaa vizuri anazungumza kama kawaida. Hata hivyo, iliwachukua polisi saa nzima kugundua kuwa wanazungumza na punguani.
Inspekta Kombora aliandika maelezo mafupi ya jalada hilo. Aliagiza wasio na hatia waachiwe mara moja. Kisha, akalitupa kando na kuvuta jalada la mwisho ambalo ndilo hasa alilolihitaji, taarifa ya mienendo ya magari mawili ambayo aliyatilia shaka. Maelezo yalikuwa mafupi, lakini yakiwa wazi kabisa.
Datsun TZA 42112 ni mali ya Swaleh Akbar, Mwarabu mwenye damu mchanganyiko, mama mswahili wa Rufiji, aliondoka nchini zaidi ya miaka kumi iliyopita na kuhamia Oman ambako amerudi juzi na malori matatu, basi kubwa la abiria na gari hilo dogo la kutembelea.
Akiwa na umri wa miaka ishirini na mitatu tu, Swaleh ni mtundu na mtumiaji kupita kiasi. Kila jioni gari lake huwa liko njiani, katika majumba ya starehe. Katika usiku mmoja gari lake linaweza kuonekana katika majumba kumi ya starehe. Si mnywaji sana, lakini anapenda sana kunywa katika makundi huku akinunua bia kama maji.
Baada ya kupokea amri ya kulisaka gari hilo askari wa barabarani walilipata mnamo saa kumi kasoro, likitokea Buguruni. Lilikuwa likielekea Kariakoo. Ghafla waliliona likibadili njia na kuelekea Keko. Sasa hivi gari hilo liko mbele ya nyumba moja mbovumbovu, hukohuko Keko. Askari mmoja wa Kombora ameichukua kazi hiyo toka mabegani mwa polisi wa Usalama Barabarani. Analitazama gari hilo toka mbali, akiisubiri amri ya Kombora.
Kombora aliwaza kwa muda, kisha, akaichukua kalamu yake na kuandika juu ya karatasi hiyo, “Watu wawili zaidi waende huko. Watumie njia yoyote kuingia humo ndani, kuona wanafanya nini na kama ni watu wetu waletwe mara moja.”
Taarifa ya pili ilikuwa fupi zaidi, lakini Kombora aliisoma kwa makini zaidi. Si kwa ajili ya hisia ambazo zilikuwa zikichemka katika roho yake tu, bali kwa kuwa aliona taarifa nyingine zote hazikumpa hali aliyotarajia.
Gari dogo aina ya Toyota Corolla TZB No. 414 lilionekana katika Barabara ya Ocean likitembea taratibu. Lilipofika mbele ya Hoteli ya New Africa, lilipaki na dereva wake kuingia hotelini ambamo alionekana kuchukua ufunguo mapokezi na kupanda lift hadi ndani ambako yaelekea amelala.
Gari hili ni mali ya kampuni moja ya ukodishaji magari iitwayo Shabir Safaris Limited ya Morogoro. Kwa mujibu wa mwenye kampuni hiyo, Shabir Datoo, gari hilo lilikodishwa wiki mbili zilizopita kwa Mmarekani mweusi mmoja na mkewe, hati ya usafiri namba… iliyotolewa mjini Miami miaka minne iliyopita chini ya jina la Morrice Juakali.
Huyu ni mtu wetu! Kombora aliwaza akiisoma tena taarifa hiyo. Alitafuna ncha ya kalamu yake kwa muda kabla hajainama na kuandika katika jalada hilo.
“Ongezeni ulinzi nyuma na mbele ya hoteli. Kila mmoja awe na silaha na awe na picha halisi ya mtu wetu akilini. Kila hadhari ichukuliwe kumfanya mtu huyu asishuku anachunguzwa. Na mara tu atakapoonekana akitoka nitaarifiwe mara moja.”
Baada ya hayo Kombora alijaribu kutulia kwa kuagiza aletewe kahawa huku akivuta jalada la Kakakuona na kuanza kulipekua tena. Japo alilisoma mara kadhaa swali lilelile lilikuwa wazi, bila majibu yoyote, rohoni na akilini mwake; Kakakuona anahitaji nini kwa Joram Kiango? Kwa mara nyingine aliamua kuliweka swali hilo kando na kuendelea kusubiri kukamatwa kwa Kakakuona.
Alipoikumbuka kahawa yake tayari ilikuwa imepoa tena.
***
‘Mchezo umeanza kuwa mtamu,’ Kakakuona aliwaza akichungulia dirishani katika tundu dogo aliloliunda kwa kutoboa pazia la dirisha. Akiwa mtu mwenye uwezo wa kumnusa polisi hata awe wapi, hakuwa kipofu wa kushindwa kuwatambua watu walioiinamia injini ya teksi aina ya BMW, iliyoegeshwa mbele ya hoteli hiyo, kando ya gari lake, kuwa ni polisi.
Mtu wa tatu alikuwa ameongezeka, polisi pia. Chumba chake kikiwa upande mzuri, ghorofa ya tano katika hoteli hii, alikuwa na nafasi nzuri sana ya kuwatazama.
Tangu usiku alipokuwa akirejea toka ufukoni, ambako alimshughulikia kikamilifu yule msichana na kumwacha maiti baada ya kuiharibu sura yake, Kakakuona alihisi kuwa anafuatwa. Hakuwa na hakika.
Hivyo, alifanya hila za kupita hapa na pale, kupinda kona hii na ile, kupunguza na kuongeza kasi n.k. Wakati alipoamini kuwa amelipoteza gari hilo aligeuza njia na kuja New Africa. Alipokuwa akivikusanyakusanya vifaa vyake na kuvitia katika briefcase ndipo alipoliona gari hili likizimika katikati ya barabara na watu wawili kushuka. Walilivuta hadi kando ya gari lake na kulifunua boneti. Kisha, wakafunga hiki na kufungua kile. Hawakuinua uso kumtazama, lakini Kakakuona alijua kabisa kuwa wako pale kwa ajili yake. Alitulia katika gari kwa dakika kadhaa akivuta sigara huku mkono wake ukiipapasa bastola yake, Alipoona hawamjii alifahamu kuwa askari hao hawakuwa na amri ya kumkamata. Hivyo, aliingia chumbani ambako, alioga akaweka vifaa vyake sawa na kisha akazima taa na kujilaza kitandani.
Nusu saa baadaye aliamka na kuwachungulia. Mtu mmoja alikuwa ndani ya gari wa pili akiendelea kuhangaika na injini ‘Watasubiri sana’ aliwaza akijilaza tena na kujaribu kuwaondoa akilini.
Hata hivyo, akili yake haikumruhusu kustarehe. Hisia za hofu, kitu ambacho kwa kawaida hakimo kabisa katika damu yake, zilikuwa zikimnyemelea. Alijihisi akijilaumu na kujutia uamuzi wake wa kwenda Lang’ata na kumfuata yule msichana ambaye aliamini kwa namna moja au nyingine amekuwa chanzo cha polisi kumnusa mapema namna hiyo.
Pamoja na ukweli kuwa hakuwa hata na chembe ya hofu ya kukamatwa na polisi hao, bado hakuona kama ilimstahili kushukiwa mapema hivyo, jambo ambalo lingemfanya aanze upya maisha ya kujifichaficha hata kabla ya kwenda kuyazoa yale mamilioni ambayo yanamsubiri pindi atakapomfikisha Joram Kiango au mzoga wake mbele ya wadhamini wake.
‘Hawana lolote la haja wanalofahamu juu yangu,’ aliwaza. ‘Wangekuwa nalo wangekuwa wamekwishanipigia hodi. Nitalala zangu kwa amani. Kesho mchana nitamshughulikia Joram na kisha kumfuata Chongo popote alipojichimbia.’
Sasa ilikuwa saa mbili asubuhi. Gari lile lilikuwa likiendelea kuchokonolewa. Mara liliwaka. Wale watu wawili wa mwanzo walitabasamu. Baadaye walionekana wakimlipa yule mtu wa tatu na kisha kuondoka zao. Yule mtu wa tatu alitazama huku na huko, kisha, akavuka barabara na kuanza kutembea taratibu kando ya Benki ya City Drive hadi alipotokomea, miongoni mwa watu wengine.
Kakakuona hakuwa mtu wa kuingia katika mtego mdogo kama huo. Alijua fika kuwa kuondoka kwa watu hao ni kubadili zamu tu. ‘Wako wengine sehemu nyingine, ambao wananichunguza kwa makini. Acha waendelee kupoteza muda wao,’ aliwaza akiingia bafuni ambako alioga, akabadili nguo na kisha kupakia vitu vyake vyote muhimu katika briefcase yake maalumu. Kisha, akawaita wahudumu wa vyumba na kuagiza kifungua kinywa na gazeti la Daily News. Alikunywa chai yake kwa utulivu huku akilipekuapekua gazeti hilo.
Mara macho yake yakavutwa habari fupi iliyopachikwa kando katika ukurasa wa nne. Ilieleza juu ya mtumbwi wa mashine ambao uliokotwa baharini na wavuvi wa Zanzibar, ukiwa na maiti ya mtu mwenye jeraha la risasi. Habari hiyo iliendelea kueleza kuwa marehemu huyo alikutwa na bastola mfukoni mwake, jambo ambalo lilifanya iaminike kuwa alijiua mwenyewe.
Maelezo juu ya umbile na mavazi ya hayati huyo, yalimfanya Kakakuona amtambue mara moja. ‘Chuchu’ alinong’ona. ‘Chongo amemuua. Sasa bado zamu yake.’
Alitazama saa yake, tatu kasoro. Akainuka, akauchukua mkoba wake na kutoka nje ya hoteli. Baadaye akamtupia macho msichana wa mapokezi ambaye alikuwa akimchekea kana kwamba yuko katika mashindano ya kutabasamu. Akalifuata gari lake na kuingia.
Alhaji Salum Banduka ni mmoja kati ya watu wanaojiheshimu na wanaoheshimika sana mjini Zanzibar. Tangu alipohamia hapa toka Bara, aliondokea kuwa mtu ambaye kila mtu alipenda kumtolea mfano.
Tazama aliingia hapa hana kitu zaidi ya mtaji wake wa shilingi elfu ishirini, kanzu moja, suruali ya pili na makubazi miguuni. Tripu nane za Bara na Pemba zilimfanya aache biashara ya chakula na kuanza kwenda zake Uarabuni. Leo hii tayari anayo maduka matatu, daladala nne na hoteli kubwa ya kitalii!
Tazama! Pamoja na utajiri wote huu hata sala moja haimpiti. Tayari amehiji Makka mara tatu na anatarajia kwenda tena mwaka huu. Wala hana kiburi. Kila siku huwa yupo katika magenge ya vijana na wazee akisimulia jinsi shilingi elfu ishirini zilizomfanya awe tajiri.
“Hawakukosea wazee waliposema, “Akili ni mali…” Banduka alipenda sana kuitumia methali hiyo mwisho wa maelezo yake, kwa sauti ya kicheko.”
Huyo alikuwa Banduka wanayemjua wao; mtu mfupi, mnene, mwenye tumbo la kutosha na kovu lililomeza nusu ya shavu lake la kushoto, mtu ambaye alitulia na wake zake wawili, mmoja akiwa na damu ya Kiarabu wa pili ya Kimvita.
Kama wangefahamu kuwa Banduka huyuhuyu ndiye yule aliyevuma sana huko Bara zaidi ya miaka kumi iliyopita kwa ushiriki wake katika wizi, ujambazi na mauaji, kamwe wasingempa hadhi msikitini wala heshima mtaani.
Kama wangejua kuwa kuja kwake visiwani ilikuwa ni kujificha baada ya kushiriki katika kazi nzito ambayo iliacha familia nzima ya Mhindi mmoja mahututi hali wao wakiondoka na milioni saba kamwe visiwa hivi vya amani na utulivu visingempokea.
Banduka alikuwa na bahati ya mtende. Siku hiyo kazi yake ilikuwa ndogo tu, kukaa chonjo, bastola mkononi, akilinda mtu yeyote ambaye angetokea kuitibua kazi yao katika nyumba hiyo. Kazi ilikwisha kwa amani. Yeye, ambaye hakujitokeza mbele ya uso wa Mhindi, akapewa jukumu la kulinda furushi hilo la fedha ili ikipoa wagawane. Kama muujiza, usiku huohuo wenzake wote walikamatwa. Yeye akatoroka na jahazi la makasia hadi hapa ambapo alijichimbia. Kwa kuwa haukupatikana ushahidi wa kutosha wenzake walichukua miaka saba, saba. Hakuna aliyemtaja.
Ndipo alipolivua jina lake la Bandua na kujiita Banduka. Akauvua ujambazi pia katika fikra zake na kuapa kuwa kamwe asingejihusisha nao tena kwa namna yoyote.
Lakini kiapo chake hicho hakikudumu muda mrefu. Mara tu alipoanza kuipanua miradi yake alijitokeza askari kanzu mmoja ambaye jioni moja alijipenyeza hadi katika chumba chake cha sala. Banduka alishtukia mtu kasimama mbele yake akitabasamu kifedhuli.
“We’ nani?” alifoka.
“Usitake kunifahamu. Suala ni kwamba mimi nakufahamu wewe. Unaitwa Alhaji Banduka. Mimi najua kuwa wewe ni Bandua, mwizi, muuaji na tapeli mkubwa ambaye unasubiriwa Bara kwa hamu kubwa sana. Kataa…”
Banduka aliduwaa. Hakutarajia kuwa kisiwani hapa kulikuwa na binadamu yeyote anayehifahamu rekodi yake.
“Usishangae,” askari huyo alimzindua “Wewe una pesa, mimi ninayo siri yako. Leta pesa nikufichie siri. Vinginevyo, kesho hutakuwa huru.”
Baada ya ubishi mrefu, Banduka akijaribu kukanusha, aligundua kuwa kidudumtu huyo alikuwa na ushahidi tosha dhidi yake.
“Unataka kiasi gani?” alimuuliza.
“Milioni tatu tu.”
“Milioni tatu!” Banduka alifoka. “Una wazimu!”
“Labda. Lakini ni milioni tatu au roho yako. Mimi pia nimechoka kukesha usiku na mchana nikiwalinda wenye pesa zao. Nataka kupumzika kama wewe.”
Baada ya ubishi mwingine mfupi Banduka aliafiki. “Njoo kesho kuchukua.”
Kauli hiyo ilimfanya askari huyo aangue kicheko. “Nina akilia bwana Banduka. Mara tu nikiondoka utaanza kubuni mbinu za kuniangamiza. Pesa hizo nazitaka leo. Sasa hivi. Nimeingia humu kwa siri bila ya mtu yeyote kuniona ili tumalizane kabisa. Nikitoka kila mtu ajue lake.”
Kipande hicho cha habari kilimsaidia sana Banduka. Alikuwa amechoka kusumbuka. Alikuwa ameishiwa na hamu ya kufungwa na kuwakimbiakimbia polisi. Alivuta droo yake ndogo kama anayetaka kuchukua ufunguo. Alipoutoa mkono wake ulikuwa umeshikilia kisu chake kirefu ambacho dakika hiyohiyo kilipotelea katika kifua cha askari huyo, ambaye hakuwahi kupiga hata kelele. Alianguka hali katokwa macho kwa mshangao na maumivu.
Banduka aliifanya kazi ya kufuta damu na kumzika marehemu kwa siri sana. Kisha, akatulia kusikiliza kama kuna mtu yeyote ambaye angemuunganisha yeye na “kutoweka” kwa askari mgeni aliyetokea Bara. Wala.
Ikafuata miaka ya starehe, amani na utulivu. Banduka akaweka kiapo kingine cha kutojihusisha tena na aina yoyote ile ya ujambazi, kiapo ambacho leo hiihii alikikumbuka na kuanza kukitilia shaka kama kweli atatimiza.
Alfajiri hii aliamka mapema, kama ilivyokuwa kawaida yake ili aende zake msikitini. Alipoitazama saa yake aligundua kuwa alikuwa ameamka nusu saa kabla ya muda wa sala. Akiwa chumbani peke yake, baada ya mkewe mkubwa kwenda zake Bara, aliamua kuamka na kuoga. Akajaza maji baridi katika beseni la kuogea na kuyapoza kwa maji moto kidogo. Wakati akivua taulo alilojifunga kiunoni ili ajitumbukize alihisi mlango wa bafuni ukifunguka na umbo la mtu kujipenyeza.
“Nani?” alifoka kwa mshangao.
“Taratibu, aisee. Mie wako. Tuseme umenisahau?”
Banduka alimtazama mtu huyo aliyeingia kama kivuli. Roho ikamlipuka. Miaka zaidi ya kumi iliyowatenganisha katu isingemfanya amsahau Chongo, mmoja kati ya watu ambao Banduka hakupenda kabisa kuwatia machoni. Hisia za hatari zilimwingia. Aliduwaa kwa muda kabla hajauliza kwa sauti ya unyonge, japo ilijaa hasira, “Umeingiaje humu?”
“Nimeingiaje? Mimi na wewe! Usiniambie kuwa umekuwa bwege kiasi hicho Banduka. Jumba lako hili halina kufuli hata moja. Kila nilipokuwa nikija hapa Zanzibar kutumia, nilikuwa naitembelea nyumba yako kuichunguza. Nilishangaa unavyoishi kama ndege ukijifanya mswahilina. Nasikia hata Makka umekwenda. Si umekwenda tu kuutia nuksi mji ule takatifu? Wewe ni wa kwenda Maka!”
Hofu ilianza kumtoka Banduka. Akijua kila dakika anayokaa na mshenzi huyo ilikuwa ikihatarisha usalama wake, alimwambia kwa ukali kidogo, “Sijui umefuata nini hapa. Sina hamu ya kuisikiliza sauti yako mbovu wala kuitazama sura yako nzuri. Inatosha. Sasa ondoka niendelee na sala zangu.”
“Sala!” Chongo alicheka. “Sala! Ha! Ha! Wadanganye binadamu usimdanyanye Mungu. Sala zako hazitoki nje ya chumba hiki, Banduka,” alisema na kuongeza, “Unajua Banduka nakudai pesa nyingi, mamilioni. Nafahamu kuwa ulitusaliti ukituacha tuozee gerezani hali wewe unatumia pesa zetu. Lakini hakuna anayekulaumu. Hakuna mwenye shida kati yetu. Kwa upande wangu mimi sihitaji utajiri. Nahitaji pesa kidogo za kula. Lakini kwako sihitaji pesa. Nahitaji hifadhi kwa siku mbili tatu tu. Niko na mpenzi wangu.” “Siwezi kukupa hifadhi. Katafute pengine.”
“Usinilazimishe kukulazimisha,” Chongo alifoka. “Mbona huna shukrani, mtu wewe? Ombi dogo kama hilo likushinde wakati unanenepa tumbo kwa mamilioni yangu?” alimaliza kwa kicheko chake cha kikohozi.
Banduka alipoona kuwa hana uwezo wa kumkana alijitia kuafiki huku akibuni mbinu zaidi ambazo aliamini zingemfanya Chongo ajute milele kumtibulia maisha yake ya amani ambayo amekuwa akiishi miaka nenda rudi.
“Nitakuhifadhi,” alimwambia, “lakini kwa masharti kwamba hutatoka nje ya nyumba hii mchana, na utakapokamatwa usithubutu kunitaja kwamba tunafahamiana. Upo?”
Chongo alipochelewa kujibu aliongeza, “Usijidanganye kuwa ushahidi ulionao utakusaidia chochote. Nina marafiki wakubwa hapa. Ukikorofisha ukamatwe elewa kuwa utakufa na ushahidi wako hata kabla hujafika mbele ya mahakama.”
Hilo lilimchekesha Chongo. Baada ya kicheko chake alisema, “Kabla sijafa mimi elewa kuwa wewe utakuwa na risasi sita kichwani mwako. Hilo nakuomba ulitie maanani. Hila yoyote itakuletea balaa. Unaiona hii?” kwa wepesi wa ajabu, bastola yake ilitolewa na kuzungushwa angani, akairusha mara mbili na kuidaka huku ikizunguka. Kisha, aliipunga kumwelekea Banduka
“Unaona?” alimuuliza. “Sina mchezo, sitaki mzaha. Na kuanzia sasa hivi ni mimi nitakayetoa amri zote katika nyumba hii hadi nitakapoondoka. Tumeelewana?”
Muda mfupi baadaye, kwa amri ya Chongo, Nuru ambaye alikuwa amelazwa nje ya mlango kwa nyuma, aliingizwa humo akiwa amebebwa na Alhaji Banduka. Nuru akiwa taabani kwa uchovu. Alijifanya mgonjwa zaidi kiasi kwamba hata alipoongea kuomba maji iliwachukua dakika mbili kumwelewa. Alipatiwa maji. Kisha, Banduka aliamriwa kuleta chakula. Ulipatikana wali mkavu kwa kahawa. Nuru alifunguliwa mkono mmoja na kutakiwa ale. Kwa jinsi alivyokuwa na njaa aliusikia wali huo kama biriani ya kuku.
“Unaweza kwenda kulala,” Banduka aliambiwa. “Nitakuhitaji kesho saa mbili. Kumbuka ukijitia akili utajuta kuzaliwa. Nenda.”
Banduka akatoka.
Chongo akaufunga mlango nyuma yake na kuutia ufunguo. Kisha akamgeukia Nuru na kusema, “Mpenzi… tupo peke yetu kama nani na nani vile?… Adamu na Hawa,” akajijibu mwenyewe. “Wapi ilikuwa vile?… Bustani ya Edeni… au sio?…”
Nuru hakujua kama ilimpasa kulia ama kucheka kwa kipande hicho cha habari. Kufanya mapenzi na dude hilo, rohoni mwake ilikuwa ni aibu na tusi lisilostahimilika. Kwa mara nyingine akafanya uamuzi kuwa ni maiti yake tu ambayo ingelala na chongo. Yeye hapana.
“Unasemaje mpenzi?” Chongo alikuwa akiendelea. “Si unajua kuwa roho yako iko mikononi mwangu? Basi uweke pia mwili wako miguuni mwangu. Ukifanya kazi nzuri naweza kukuachia roho yako. Tuna muda wa saa tatu za kusubiri. Nataka tutumie kwa kujiburudisha. Baada ya hapo nitapiga simu moja Dar es Salaam. Majibu yakiwa mazuri utatoka chumba hiki ukiwa na sura nyingine kabisa, yakiwa mabaya utatoka kama ulivyo, pengine na mtoto wetu tumboni mwako. Upo?” Nuru alimtumbulia macho, hasira zikichemka rohoni mwake.
“Sema,” Chongo alisema akimsogelea na kumminya titi. Nuru alitazama kwa makini zaidi.
Kabla hajaliwasha, alichunguza kila kitu kwa makini. Hakuona kasoro yoyote. Akaliwasha na kuliondoa kufuata Mtaa wa Samora. Macho yake yalikuwa makini. Alisimamisha gari hilo mbele ya duka moja na kuingia. Hakuona gari lolote. Alipotupa macho mbele aliona gari moja dogo jeupe likisimama, magari manne mbele yake. Alipomfikia dereva wa gari hilo, alimtazama kiujanjajanja katika kioo chake cha ndani. Akatabasamu na kumpita huku yeye pia akijitia hamwoni.
Aliendesha gari moja kwa moja hadi Mtaa wa Lumumba. Mbele ya Jengo la Ushirika. Hapo alishuka na kukiendea kikundi cha watu ambacho kilikuwa kikisubiri lifti. Yeyote aliyekuwa akimfuata Kakakuona aliamini kuwa hakuwahi kuipanda lifti hiyo kwani mara tu alipofika lifti ilifika, naye akawa mtu wa mwisho kuingia.
Alipanda hadi ghorofa ya mwisho kisha akashuka nayo hadi mwisho wa lifti hiyo ambako ni ghorofa moja zaidi chini ya ardhi. Huko aliacha lifti na kufanya haraka kuifuata ngazi ambayo inatokea upande wa pili wa jengo hilo. Huko alitembea hadi mtaa wa pili ambapo alikodi teksi iliyomfikisha Kariakoo ambako alishuka na kukodi teksi nyingine iliyompeleka Ilala.
Akaingia ofisi ya ndege za kukodi, AirTanzania, na kuomba usafiri wa haraka kwenda Zanzibar. Akitumia pesa nyingi na hati zake za bandia dakika ishirini baadaye alikuwa akielekea juu ya anga ya Zanzibar.
***
Ulikuwa usiku mrefu mno kwa Joram Kiango, usiku unaochosha na kukinaisha kupita kiasi. Kwa mtu wa vitendo kama yeye, ilikuwa kama adhabu kukesha wima, ndani ya chumba chako, kando ya kitanda chako, ukisubiri jambo ambalo halitokei.
Kucha aliyatega macho yake yakipasua kiza kuchunguza chochote ambacho kingekuwa kigeni chumbani humo. Kadhalika, masikio yake yalikuwa makini, tayari kunasa mchakacho wowote ambao angeusikia. Lakini hadi kulipopambazuka hakusikia wala kuona chochote, jambo ambalo lilimfanya ajikute akipandwa na hasira kali zaidi dhidi ya yeyote aliyekuwa akimtendea kitendo hicho, hasira ambazo kiasi zilimfanya ajione mpumbavu kwa uamuzi wake wa kuwasubiri adui hao.
Ilikuwepo haja gani ya kupoteza usiku mzima akiwa ameketi akiwasubiri badala ya kuwa mitaani akipambana nao? ‘Haiwezekani kuwa kitendo chake cha kukesha hapo bila ya kushughulika ndicho hasa walichokihitaji ili waendelee na unyama wao mitaani? Wamenifanya mpumbavu!’ aliwaza kwa uchungu na hasira. Na kwa hasira hizo alitabasamu.
Hata hivyo, hakujilaumu sana. Alijua kama siyo leo, kesho wangekuja kuhakikisha mauti yake. Na alikusudia wamkute akiwa anajua adui yake ni nani na anakusudia nini. Hivyo, asubuhi hiyo aliamua kuitumia kwa uchunguzi.
Kulipopambazuka kikamilifu, Joram akaingia bafuni kuoga. Kisha, akaliendea kabati la nguo na kutafuta moja kati ya mavazi yake ambayo humfanya asitambulike kwa urahisi wala kumtazama kwa makini. Leo alivaa kanzu nyeupe, kijikoti cheusi juu, ndala miguuni, kofia pana kichwani na miwani myeusi.
Akachukua fimbo yake ya kutembelea na kutoka nje akitumia mlango wa nyuma. Baada ya kupenya hapa na pale, aliifikia barabara kuu ambako alikodi gari lililomfikisha mjini. Huko alitafuta hoteli na kujipatia kifungua kinywa. Kutoka hapo alikwenda Mtaa wa Mkwepu kwenye duka moja ambalo wanaruhusu wapita njia kupiga simu kwa malipo. Alimwomba Mhindimwenye simu hiyo aitumie nusu saa huku akimpa shilingi elfu tano.
“Napiga hapahapa mjini zikiisha, nitaongeza,” alimwambia.
Huku akiwa na mshangao, mwenye duka huyo alipokea harakaharaka na kumpisha Joram kiti.
Polisi ni watu wanaojua sana kufumba midomo. Kujaribu kunyofoa ukweli toka katika mikono ya polisi ni kazi ngumu kama kujaribu kung’oa ulimi wa jabali. Lakini si kwa mtu kama Joram Kiango. Hadhi yake katika masuala ya mapambano ilimpatia marafiki wengi katika jeshi hilo. Aidha, alikuwa na marafiki zake wawili, watatu ambao humuuzia siri na habari mbalimbali anazohitaji, kama vile ambavyo yeye huwapa ‘tip’ wanapofuatilia masuala fulanifulani anayoyafahamu.
Akiwa na hakika kuwa mauaji ya wasichana wote wawili yalikwishagundulika na polisi, simu yake ya kwanza aliielekeza Idara ya Upelelezi ya kituo kikuu. Alikuwa na bahati ya kumpata mtu wake.
Baada ya maongezi mafupi ya mafumbo-mafumbo, Joram aliweka simu chini. Habari alizopata licha ya kuwa hazikumnufaisha sana bado zilimwongezea hasira. Mpelelezi huyo alikiri kuwa bado kuna jambo la ‘moto sana’.
Anachofahamu ni kwamba, raia watatu na askari kanzu mmoja wamekwishauawa. Ni hilo lililomsikitisha Joram Kiango. Watu zaidi wameendelea kufa wakati yeye ameketi juu ya kochi akisubiri adui ajilete. Aibu iliyoje!
Maswali yake yaliyofuata hayakupata majibu zaidi. Hivyo, Joram akakata na kupiga kwenye simu ya Kombora. “Namtaka Shoka,” aliomba.
“Hayupo”
“Yuko wapi?”
“Amehama.”
Moyo wa Joram ulidunda kwa nguvu. Hakuwa mgeni wa msamiati huo. Askari anapotamka moja kwa moja kuwa askari fulani amehama, huwa haina maana nyingine zaidi ya kufa. Yawezekana ni yeye aliyekufa kwa ajili yake? Joram alijikaza na kutaja jina la pili. “Hayupo,” mtu wake wa tatu pia hakuwepo.
Wakati Joram akiwa ameduwaa, mtu aliyekuwa upande wa pili wa simu alimshangaza alipomwambia, “Au nikupe Inspekta Kombora mwenyewe Joram?”
“Najua Inspekta hana muda wa kukuona. Wala asingependa kukushirikisha. Hata hivyo, mimi nitakuibia siri. Suala hili ni zito na gumu. Watu wanaendelea kuteketea kwa ajili yako, wakati uko gizani. Mwiba hutokea ulikoingilia. Tunaweza kuonana wapi nikudokolee hicho tulichonacho?”
“Tukutane New Africa…”
“Hapana.”
“Embassy.”
“Haifa?”
“Wewe unadhani wapi panafaa?” Joram alimuuliza.
“Hapohapo ulipo. Dakika tano baadaye. Uko wapi?”
Joram akaeleza.
Kama walivyo vijana wote wa Inspekta Kombora, kijana huyu ambaye alimtokea Joram Kiango dakika saba baadaye, alikuwa mkakamavu, mtulivu na mstaarabu kiasi kwamba haikuwa rahisi kumshuku kuwa ni kachero. Lakini si kwa Joram. Alitambua mara tu alipoingia katika mgahawa huo, gazeti mkononi na kuketi kama wateja wengine, akimsubiri mhudumu ambaye aliagizwa kuleta soda. Joram aliiacha meza yake na kuhamia meza aliyoketi bwana huyo.
“Ningeomba kuwa mwenyeji wako,” alimnong’oneza.
Mgeni huyo alimtazama Joram kwa mshangao kidogo, mshangao ambao uligeuka kuwa tabasamu baada ya kumtambua, licha ya mavazi yake bandia.
“Kwanza, ningeomba unielewe kuwa kwa kuzungumza nawe navunja amri zote za kazi yangu. Jambo ambalo natarajia kuzungumza ni siri kubwa sana ambayo haikutakiwa kuyafikia masikio ya raia yeyote yule. Mzee Kombora ataninyonga kwa mkono wake kama atasikia kuwa nimekudokezea. Natumaini unanielewa.”
“Vizuri sana,” Joram alimjibu.
“Hata hivyo, kama nilivyoeleza awali, sioni umuhimu wa kutokukuhusisha. Hakuna asiyefahamu mchango wako katika kupambana na udhalimu hapa nchini na kote duniani. Zaidi, sioni kwa nini watu wasio na hatia waendelee kuuawa kinyama wakati wewe umestarehe. Sidhani kama wewe u mvivu kiasi hicho. Natumaini tutakuwa bega kwa bega kupambana naye. Sawa.”
Joram aliona kama anayepotezewa muda kwa maelezo yasiyo ya msingi. Alichohitaji ilikuwa ni kitu kidogo sana. Kuelewa makachero wanaelewa nini juu ya adui huyo, ili aanze harakati. Kulala ndani kulikuwa kumemchosha.
“Unaonaje ukikata mahubiri na kunieleza kile ulichopanga kunieleza. Huoni kama tunapoteza muda?” alimuuliza.
“Yote ambayo naweza kukueleza yako katika gazeti hili. Ambacho hakimo ni kwamba sasa hivi Kakakuona yuko Zanzibar.”
“Kakakuona?”
“Inaonekana humfahamu,” kachero huyo alieleza. “Huyo ndiye mbaya wako. Anaweza kuwa ni mtu hatari zaidi ya kifaru aliyejeruhiwa. Anaua huku ametulia kama anakunywa maji baridi. Kifo chake ni muhimu kitokee kabla hajatuathiri,” alimaliza akiinuka huku akiliacha gazeti lake mezani.
“Wazulu wa kale hawakuwa na neno ‘asante’ katika msamiati wao, wala samahani, mimi na wewe tunaishi katika dunia na kucheza na kifo. Hatuna tofauti yoyote na Wazulu hao. Hivyo, sina la kusema…” Joram alimwambia kachero huyo huku akijaribu kumpa mkono ambao ulipuuzwa.
“Hunijui, sikujui. Sawa?”
“Sawa,” alijibu akitabasamu. Kisha, akalichukua gazeti hilo na kuhamia hoteli nyingine ambako nako pia alichukua meza ya kando, isiyo na mtu. Baada ya kupata kinywaji chake alitoa nakala sita za kopi za maandishi yaliyoonekana kama yaliyotoka kwenye faili.
Alizisoma kwa makini. Dakika mbili baadaye alizichanachana huku akiwa tayari amezichora akilini.
‘Kakakuona!’ aliwaza kwa hasira. ‘Anamtaka nini? Ameibuka kutoka wapi? Nani anamtumia? Kwa nini? Kwa nini? Kwa nini?’ alifoka kimoyomoyo.
Maswali yalikuwa mengi na marefu. Majibu yalihitaji muda. Kuwasiliana na wenzake wa nje. Kuwasiliana na benki, kujadiliana na nyumba za wageni, kufuata nyayo zake zinakotokea, kuwalipa maajenti wa nje, wenye kompyuta ambazo zinaweka kumbukumbu za vitendo vya watu kama hao n.k. Yote hayo yalihitaji muda, kitu ambacho Joram hakuona kama kilikuwepo. Kilichohitajika ni kumuua Kakakuona kwanza, na kuuliza maswali baadaye.
Baada ya kuwaza hayo, alifanya haraka kwenda Air Tanzania ambako walimvunja moyo kwa kutokuwa na ndege ambayo ingeondoka muda huo isipokuwa “Saa kumi na mbili za jioni.”
Shingo upande, akageuza njia na kuifuata Sea Express. Boti ambayo ingeondoka mapema zaidi ilikuwa ni ya saa tisa mchana, saa nne baadaye. Joram alikata tiketi yake. Kisha, akatafuta simu ambapo alipiga moja Zanzibar na ya pili Nairobi. Zote hazikuwa na majibu ya mara moja. Akaahidi kupiga tena usiku huo.
Muda wa kusubiri Joram aliuona mrefu kupita kiasi. Kila dakika iliyopita ilizidi kumtia wasiwasi. Mara kwa mara akilini ilimjia picha ya Nuru akiwa na uso kama ulioteketezwa kinyama kama nyuso alizoziona katika picha alizotumiwa, jambo ambalo lilizidi kumtia hasira na kumfanya atamani kuruka, apae hadi Zanzibar, mbele ya Kakakuona.
***
“Ndege yake inatua mzee.”
Kombora aliarifiwa katika simu, kutoka Uwanja wa Ndege Zanzibar.
“Vizuri,” alijibu.
“Anashuka. Abiria ni mmoja tu. Amebeba mkoba. Mavazi yake ni kama uliyoyaeleza. Haonekani kama mtu mwenye wasiwasi wowote. Sasa hivi amefika meza ya Uhamiaji. Tumkamate?”
“Nimesema msimsogelee hadi nitakapotoa amri nyingine. Ni mtu hatari kuliko mnavyoweza kufikiria nyie,” Kombora alifoka. Kisha akaongeza “Endelea kuniarifu kila tukio na wekeni makachero wengi waangalie kila hatua yake. Angalieni asifahamu kuwa anafuatwa. Sawa?”
“Sawa”
Baada ya muda, “Amekodi teksi. Anaelekea mjini. Magari yetu mawili ya teksi yanamfuata kwa uangalifu.” Na baadaye “Inaelekea kama anafahamu kuwa anafuatwa. Lakini yaelekea hajali.”
Dakika kumi baadaye Kombora aliarifiwa ghafla, “Ameshuka mzee! Amechoropoka ghafla sehemu za Darajani. Haonekani alipo. Yaelekea amejichanganya katikati ya watu na kuingia mitaa ya Mji Mkongwe. Tufanyeje?”
“Asipotee.” Kombora alinguruma “Makachero wote wafanye kazi ya kumtafuta ili awe chini ya miwani yenu kila dakika. Nataka kujua anafanya nini, anakutana na nani, na kadhalika, na bado naonya asisogelewe wala kushtuliwa. Sawa?”
“Sawa, Afande.”
“HUWEZI kulala na mwanamke aliyefungwa kamba mikononi na miguuni, ukafaidi, huwezi ukatamba mbele ya marafiki zako kuwa mwanamke yule nimefanya naye mapenzi, wakati alikuwa kafungwa mikono na miguu, ambapo hakukukumbatia, hakukubusu wala hakukufurahia. Ni aibu. Ni kitendo cha kihanithi.”
Nuru aliyasema hayo kwa sauti aliyoifanya dhaifu kuliko ilivyokuwa, macho yake yakimtazama Chongo kwa ulegevu huku akiruhusu tabasamu dogo kuutembelea uso huo.
Ilimgharimu kila kitu kuyatamka maneno hayo. Tangu kiumbe huyo alipoonyesha dalili za kumtaka mapenzi roho ilipasuka na akili kufadhaika. Alijisikia kulia, alijisika kucheka na alijisikia kutapika. Yote hayo hakuyafanya. Badala yake alijikaza kisabuni na kuyatamka hayo kwa nia ya kumlaghai Chongo.
Chongo hakuwa mpumbavu kwa namna ambavyo Nuru alimkadiria. Kama jibu kwa maelezo ya Nuru alikitoa kitu kile ambacho alikusudia kuwa tabasamu usoni mwake. Kisha, alimwambia, “Una hila kama kinyonga, mpenzi. Ningeweza kukukomoa zaidi kwa kunifikiria bwege kiasi hicho. Bahati mbaya muda wa kuketi chumbani humu ni mrefu mno. Siwezi kuvumilia kukuachia. Ila tu nakuomba wakati nikifanya vitu vyangu usiote kabisa kunivamia. Nitakufungua miguu. Na nitakuwa na bastola mkono mmoja.”
“Na mikono?”
“Siwezi kukufungua.”
“Nitakukumbatia vipi? Au unaniogopa? Mwanamke mmoja tu katika chumba kilichofungwa, huku una bastola mkononi! Nilidhani wewe ni mwanaume..!”
Sauti hiyo yenye dhihaka ilimwingia Chongo. Akiwa mtu ambaye hana asili ya kukubali kudharauliwa, alimwambia Nuru, “Vizuri. Nitakufungua mikono na miguu. Lakini nakuonya. Kama nia yako ni kujaribu ushangingi, kwangu sina lawama. Nitakuharibu bila kujalI kuwa nitakuuza kwa mamilioni. Upo?”
Kitu kimoja Chongo hakuelewa. Hakuelewa kuwa Nuru alikuwa ameamua kitambo kuwa alikuwa tayari kuacha maiti yake ilale na Chongo, siyo yeye! Hivyo, alitulia pindi Chongo alipokuwa akizikata kamba za miguuni na mikononi. Akatulia pia wakati nguo zake zikipambuliwa moja baada ya nyingine na kuwekwa kando ya kitanda.
Na alizidi kutulia alipolazwa chali juu ya kitanda hicho, miguu yake ikipelekwa mmoja huku mwingine kule. Kisha, bila ya kuitua bastola iliyokuwa imara mkononi mwake, Chongo akaanza kufungua vifungo vya suruali yake.
Ni kitendo hicho ambacho Nuru alikuwa akikisubiri. Aliifyatua miguu yake kama mshale, akailenga shingo ya Chongo!
Lilikuwa pigo zuri. Lakini Nuru naye alikuwa gizani. Hakuwa na habari kuwa Chongo alikitarajia kitendo hicho. Hivyo, teke hilo zuri lilipepea angani na kuikosakosa shingo hiyo iliyokusudiwa kwa nusu inchi. Wakati huohuo, Chongo aliachia ngumi nzito ambayo pia ilimkuta Nuru ameviringika kutoka kitandani na kusimama, akiwa tayari kwa lolote.
Tayari kufa.
Tayari kuua.
Ilikuwa dhahiri kuwa Chongo hakupenda kutumia bastola. Aliididimiza mfukoni na kumsogelea Nuru huku akiyumba kwa mbinu. Nuru alimsubiri. Ngumi mbili za Chongo zilimkosa Nuru, kitendo ambacho kilikuwa kosa kubwa katika maisha yake, kwani wakati huohuo vipigo vya Nuru vilimnyeshea kama mvua kiasi cha kumfanya aanguke kitandani. Nuru alipojaribu kumfuata kitandani hapo alisita baada ya kuona Chongo akiichomoa bastola yake na kumwelekezea huku akinguruma “Naua!” Mauaji yalikuwa wazi katika macho yake. Huku uso wake ukitetemeka kwa hasira na maumivu, aliilenga vizuri bastola yake. Kwa sauti nzito akasema, “Malaya mkubwa nimejaribu kukuhurumia hadi dakika hii bado unanionyesha ushangingi. Sasa sina budi kukuondoa duniani.”
Kwa mara ya kwanza maishani Nuru alijikuta hana la kufanya. Kana kwamba mwili mzima umeshikwa na ganzi alijikuta katulia kimya akiisubiri risasi!
***
Baada ya kuuacha uwanja wa ndege huku akiwa na hakika kuwa anafuatwa, Kakakuona alimwamuru dereva wa gari alilokodi kumshusha katika kundi la watu eneo la Darajani. Alipiga chenga mbili tatu za mwili na kuingia sokoni. Kutoka hapo akapenya hadi mbele ya duka mashuhuri la vitabu, ambako alijinunulia gazeti la Heko na kisha kuingia katika mgahawa mdogo ulioelekeana na duka hilo.
Akiwa katika mji huo mkongwe wenye vichochoro vingi, alikuwa na hakika kuwa amewapiga chenga ya mwili makachero waliokuwa wanamwandama. Hata hivyo, alijua hiyo ni chenga ya muda mfupi tu. Mji wa Zanzibar ulivyo mdogo, na mkongwe kiasi kwamba karibu raia wote wanafahamiana alijua baada ya saa chache atakuwa tena machoni mwao, akichunguzwa kwa kila kitendo chake. Hivyo alitaka atumie muda huo mfupi wa Uhuru kukamilisha suala la kumuua Chongo na kumtia Nuru mikononi mwake. Mengine yangefuata baadaye.
Hofu ya kukamatwa kabla ya kutimiza azma yake haikuwa na nguvu akilini mwake. Alikuwa na hakika kuwa japo polisi walikuwa wanamshuku bado hawakuwa na ushahidi wowote wa haja ambao ungemfanya asimamishwe kizimbani kwa kosa la mauaji. Na ni hilo peke yake lililowafanya wasite kumvamia wakati walipopata mwanya.
Kwa utulivu alifikiria wapi ambapo mtu kama Chongo angeweza kujichimbia. Suala la kwamba angeweza kwenda hotelini alilitupia mbali. Akiwa na “mateka” ambaye ni msichana mzuri na maarufu kama Nuru kwenda hoteli yoyote ingekuwa sawa na kwenda Central Police. Lazima atakuwa amejificha katika majumba ya majambazi wengine, ambao ni haba sana Zanzibar. Kakakuona akiwa mtu ambaye alikuwa nje ya nchi kwa muda mrefu, hakumjua jambazi hata mmoja.
Baada ya kuwaza sana alimkumbuka Alhaji Banduka. Akakumbuka kuwa aliwahi kusikia maongezi juu ya mzee huyo ambaye aliamua kubadili maisha yake kabisa na kuondokea kuwa mmoja kati ya matajiri wakubwa mjini hapo. Aliyeogelea hafi maji. Aliwaza. Banduka atamsaidia walao kwa kumwelekeza wapi aanzie kumtafuta Chongo. Alikuwa hafahamu Banduka anakaa upande gani wa kisiwa hicho.
Lakini hilo halikumsumbua. Alikuwa na hakika kuwa kama angeuliza mtu yeyote angeweza kumsaidia.
Akiwa na wazo hilo kichwani, aliuacha mgahawa huo na kujichomeka ndani zaidi ya Mji Mkongwe. Ikamshangaza zaidi kuona hoteli za kitalii zilizokuwa zikifunguliwa katika majumba hayo makuukuu. Alichagua hoteli moja ndogondogo ambamo alijipatia chumba na kulipia. Alichofanya chumbani humo ilikuwa kuyabadili mavazi yake ili aweze kuwachanganya polisi walau kidogo.
Macho yake akayafunika kwa miwani myeusi na kuweka kofia kichwani. Kisha, akazikagua silaha zake. Akatoa bastola yake ndogo na kuifutika katika mfuko wa suruali. Dakika kumi baadaye alikuwa tena mitaani, briefcase mkononi, akiuliza iliko nyumba ya Banduka.
Baada ya kuwauliza watu wawili watatu, mtoto mdogo aliamua kumpeleka. Walipenya vitongoji hivyo vya kihistoria hadi walipotokea mbele ya hoteli ya kitalii iitwayo Africa House. Kutoka hapo mtoto huyo alimwelekeza uchochoro unaoteremka ufukoni ambao ungemfikisha mbele ya nyumba aliyoihitaji, ambayo aliiona meta mia tatu toka hapo walipokuwa. Kakakuona alimshukuru kijana huyo na kuondoka.
Akiwa mbele ya nyumba hiyo alisikia sauti za minong’ono. Lakini mara tu alipogonga mlango alishangaa kusikia akijibiwa kwa ukimya wa ghafla. Akagonga tena. Kimya. Alipogonga kwa mara ya tatu alisikia sauti ya kiume ikiitika toka katika chumba kimojawapo, “Nani?”
“Mimi.”
“Wewe nani?”
Kakakuona alipochelewa kujibu alisikia hatua za mtu zikiujia mlango. Ukafunguliwa kidogo na uso wa mwanamume wa makamo kuchungulia nje.
“Nikusaidie nini?” aliulizwa.
Kakakuona hakuwahi kuhusiana sana na Banduka enzi za ujambazi. Hivyo, alikuwa hamfahamu, japo aliwahi kumwona mara mbili, tatu katika vikao vya matumizi na kuonyeshwa kwa mbali kuwa “Yule ni wetu kabisa.”
Sura hiyo haikumkaa sana akilini. Lakini hakuhitaji kutambulishwa kufahamu huyu hapa mwenyeji wake. Hata hivyo, alisita baada ya kumwona mwenyeji huyu akiwa katika hali ambayo hakuitarajia. Macho yake yalijaa wasiwasi, uso wake uliloa jasho, sauti yake ilikuwa ya mashakamashaka na kwa mbali alikuwa akitetemeka. Macho makali ya Kakakuona yaliona kitu kingine zaidi katika mkono wa Banduka, damu.
Damu mbichi! Ikilowesha kiwiko cha mkono huo na kusahaulika katika juhudi za kufutwa.
“Unataka nini?” Banduka aliuliza tena akitaka kufunga mlango.
“Nina shughuli ndani.”
“Naomba unikaribishe ndani. Mimi mgeni wako,” alisema akiuzuia mlango huo kwa mguu
“Mimi sikufahamu”
“Mimi nakufahamu. Kwani wewe si Banduka?”
Banduka alionekana kaduwaa. “Pamoja na hayo” akamwambia,
“Sina nafasi ya kupokea mgeni yeyote leo. Labda uje jioni naweza kukusikiliza.”
Kakakuona aliusukuma mlango huo na kuingia ndani. Kitendo ambacho kilimfanya Banduka apepesuke na kutaka kuanguka. Wakati anajiweka vizuri Kakakuona alikuwa akiufunga mlango kwa utulivu kabisa nyuma yake. “Kuna nini humu ndani?” alimuuliza Banduka ambaye alitokwa na macho ya hasira na mshangao.
Kakakuona aliyatupa macho yake huko na huko ukumbini hapo na kuona dalili nyingi za mshughuliko usio wa kawaida. Kochi moja lilikuwa limevutwa upande, kiatu kimoja cha kiume kilikuwa juu ya kochi hilo na glasi iliyovunjika ilikuwa haijazolewa toka juu ya meza ilipovunjikia. Akapiga hatua mbili tatu kukiendea chumba ambacho aliona macho ya mwenyeji wake yakielekezwa mara kwa mara. Banduka alimfuata na kujaribu kumzuia, lakini alisukumwa kando na kupepesuka kama kishada, jambo ambalo lilimfanya apandwe na hasira na kuingiza mkono wake katika mfuko wa suruali ambamo aliificha bastola yake yenye kiwambo cha kupotezea sauti ili amwadhibu mgeni huyu “mkaidi”. Lakini hakujua kiasi gani ameondokea kuwa mzito. Hata kabla mkono huo haujatoka mfukoni alijikuta tayari yumo ndani ya kabali ngumu ya Kakakuona huku mkono huo ukinyongwa hadi bastola ilipopokonywa. Aligugumia kwa maumivu na kutapatapa, nusura pumzi imwishie kama asingeachiwa na kuanguka chini kama mzigo.
“Tatizo lako wewe huelewi kama u steki tupu,” alimsikia mgeni huyo akimwambia. “Huna uwezalo kufanya. Unaiona bastola yangu hii? Dude la uhakika. Sio hili toi lako unalochezea. Kwa hii naweza kufumua bichwa lako kwa urahisi kama kuvunja yai. Upo?”
Banduka, kinywa wazi, akitetemeka, hakuwa na la kujibu zaidi ya kutokwa na jicho la hofu; macho kayakodoa kuitazama bastola hiyo ambayo ilimlenga paji la uso.
“Nadhani unanielewa,” Kakakuona alimwambia. “Sasa niambie kuna nini nyumba hii.”
Alipochelewa kujibu Kakakuona alimwinua na kumshurutisha kutangulia katika chumba hicho alichokuwa akikiendea.
Banduka alifungua mlango na kusita mlangoni. Macho ya Kakakuona yalimpita hadi chumbani humo. Kinyume na matarajio yake alikiona chumba kikiwa kitupu ingawa kulikuwa na dalili zote za vurumai. Alimtazama Banduka kwa namna ya kudai maelezo. Macho yake yalimsaliti tena. Yalikuwa yakilitazama kabati kubwa la ukutani kiwiziwizi kwa namna ya wasiwasi. Kakakuona aliliendea kabati hilo na kulifungua.
Kama asingekuwa mzoefu wa masuala hayo angeweza kushtuka sana kwa kukabiliana ghafla na maiti ambayo ilisimama ndani ya kabati hilo, damu ikiendelea kumvuja toka katika jeraha la risasi ya kifo. Jicho pekee la marehemu huyo lilikuwa wazi, kama linalomtazama Kakakuona kwa namna ya kuomba radhi.
Kakakuona alimgeukia Banduka na kumwona jinsi alivyokuwa akitetemeka mwili mzima kama mgonjwa wa homa. Kwa kumtoa wasiwasi Kakakuona alimwambia, “Kama ni wewe uliyemuua mtu huyu umekuwa rafiki yangu. Kwa kweli nilikuja hapa kwa kazi moja tu ya kumtia risasi ya kifua. Umenitangulia.”
Kiasi Banduka alipata ahueni.
“Ni wewe uliyemuua?” Kakakuona aliuliza ghafla.
Huku akikerwa na mgeni huyo alivyotamka neno “kuua” kwa urahisi kama “kula” au “kunywa Banduka alitikisa kichwa kukubali.
“Alifuatana na mwanamke?”
“Ndiyo…”
“Mwanamke huyo ni mpenzi wangu. Mshenzi huyu alifanya kumtorosha tu. Ningemuua kwa tabu kuliko ulivyomuua wewe.”
Alisita kidogo akiitazama maiti ya Chongo ndani ya kabati hilo na kumrudia Banduka. “Ebu nieleze kila kitu. Toka mwanzo hadi mwisho,” aliamuru. “Nadhani ukiketi tutazungumza kwa urahisi zaidi.”
Banduka alijibweteka juu ya kochi. Kwa suti hafifu, alimweleza jinsi alivyoingiliwa na marehemu huyo alfajiri hiyo akiwa amefuatana na “mateka” ambaye ni mwanamke mzuri. Ili kuifanya habari yake ikubalike zaidi Banduka alilaghai kwa kueleza kuwa marehemu alitishia maisha yake kwa kumwelekezea bastola na kudai pesa.
“Kama si mwanamke huyo kupiga teke bastola hiyo na mie kuidaka sasa hivi tungekuwa marehemu badala yake. Sikukusudia kumuua.” Banduka aliongeza. “Ilikuwa katika kumtishia kwani alikuwa akiendelea kunifuata, ndipo nilipolenga na kusikia ikifyatuka.”
“Usijali. Alistahili kufa,” Kakakuona alisema na kuuliza, “Yu wapi Nuru?”
“Nuru! Nuru yupi?”Banduka alishangaa.
“Yule msichana… mpenzi wangu. Yuko wapi sasa hivi?”
Banduka alielekeza mkono wake mlango wa bafu na kusema, “Anaoga, ili kuondoa uchovu. Yaelekea amepata shida nyingi sana…” Kisha, alisita na kujiuliza huyu mgeni ni nani na ana uhusianao gani na mkasa huu wa ajabu ambao hakujua umemfikisha wapi na kuishia wapi?” alimuuliza.
“Wewe ni nani?”
Kakakuona alitabasamu na kumwambia, “Usijali kunifahamu.” Na kisha, aliongeza “Nadhani ameoga kwa muda mrefu. Mgongee mwambie mpenzi wake anamsubiri hapa nje. Una hakika hana silaha?”
Banduka aliduwaa, “Silaha…mpenzi wako…”
“Usijali. Mgongee.”
***
‘Una hakika hana silaha?’ Hilo lilitosha kabisa kumdhihirisha Nuru kuwa kifo cha Chongo kwake kilikuwa sawa na kuruka jivu na kukanyaga moto. Hakuwa na shaka tena kuwa kijana huyu mtanashati, ambaye amekuwa akimsikiliza na kumchungulia katika tundu la ufunguo, hakuwa rafiki bali adui yake mkubwa; adui ambaye bila ya shaka yoyote ndiye aliyekuwa akimtumia Chongo na marehemu wenzake wote.
Hofu, ambayo ilimtinga saa mbili zilizopita alipokata tamaa kabisa ya kuendelea kuishi mara Chongo alipomlenga bastola tayari kabisa kuifyatua, ambayo ilianza kumtoka, ilimrudia tena. Akiwa hana la kufanya Nuru alikuwa akiisubiri risasi hiyo wakati jambo ambalo hakulitarajia lilipotokea. Picha iliyokuwa katika ukuta mmoja wa chumba hicho iliteleza ghafla na kuanguka. Papohapo bastola ambayo ilikuwa na kiwambo cha kupotezea sauti ilichungulia na kufyatuka. Risasi mbili zilimpata Chongo kifuani na kumfanya aanguke chini ambapo alitapatapa kwa muda kabla ya kukata roho.
Nuru alipotazama ilipotokea risasi hiyo aliuona uso wa Banduka ukichungulia na sauti yake kumfikia ikisema, “Usiogope, nakuja.” Baada ya muda alisikia funguo zikichomekwa katika kitasa cha mlango. Harakaharaka, Nuru aliinama na kuiokota bastola ya Chongo akaifutika katika vazi lake la ndani. Banduka alipofungua mlango na kuingia chumbani humo huku akitetemeka alimkuta Nuru kaketi juu ya kochi akimtazama marehemu.
“Nimeua. Sikutegemea kuua…” aliropoka. Kisha, kana kwamba ndio kwanza anamwona Nuru alifoka, “Msichana, huu nani wewe?? Nilikuwa nikichungulia unavopigana. Sijaona mtu akipigana kama wewe.”
“Ni hadithi ndefu, isiyo na kichwa wala miguu,” Nuru alimwambia “Nadhani kwa wakati huu ningekushauri tuwapigie simu polisi ili waje wamwondoe huyo,” alisema akielekeza mguu wake kwa marehemu.
Polisi? La! La! La! Siwezi kuwashirikisha.”
“Lakini umeua katika kujihami. Amekuvamia na angeweza kuniua mimi na wewe pia… Mimi nitakuwa shahidi,” Nuru alijaribu kumwelimisha.
“Na wakati huo nitakuwa mahabusu wanangu wakifa njaa na biashara zangu kuharibika. Polisi hapana” Alisita kidogo akiwaza. Kisha akaongeza. “Labda nikuombe unisaidie tuufiche huu mzigo ndani ya kabati, wakati nafikiria la kufanya. Baada ya hapo unaweza kwenda zako.”
Waliifanya kazi hiyo kwa tabu kuliko Nuru alivyotarajia. Kuua ni jambo moja, kubeba maiti ni jambo lingine. Kwa Nuru ilikuwa kazi ya kutisha na ilimtia kichefuchefu. Alijikaza kisabuni na kustarehe pale tu ambapo maiti hiyo ilifungiwa kikamilifu ndani ya kabati hilo.
Baada ya kazi hiyo ndiyo kwanza Nuru alijitazama na kuona alivyokuwa mchakavu. Nguo hizo chafu pia zilikuwa zimetatuka ovyo hapa na pale. Kwa jumla, nguo zilimfanya awe nusu uchi. Alimtazama Banduka kwa aibu na kumwomba msaada wa kuazimwa nguo za mkewe ili aondoke akiwa katika hali nzuri kiasi.
Bila kusita Banduka alimletea gauni moja zuri, jozi ya viatu na khanga mbili. Nuru alimshukuru na kuingia bafuni ambako alivua na kuufariji mwili wake kwa maji baridi.
Ni wakati alipomaliza kuvaa aliposikia hodi na hatimaye, kuchunguliwa na mtu huyo ambaye alikuwa akizungumza kwa kujiamini; mtu ambaye alionekana hatari zaidi.
Afanye nini? Alijiuliza. Apige kelele? Hilo alilipuuza mara moja. Yeye si msichana wa kufanya hilo. Zaidi, udadisi ulikuwa umeipiku hofu katika moyo wake. Alijisikia hamu ya kufahamu ni kina nani wanaofanya mambo haya yasiyoeleweka na kiini chake. Kujificha bafuni kusingemsaidia. Aliipapasa tena bastola yake na kuhakikisha kuwa imefichika vilivyo. Kisha, alijitazama katika kioo na kurekebisha nywele zake. Baada ya hapo alifungua mlango wa bafu na kutoka taratibu.
Picha za Nuru ambazo Kakakuona alikuwa nazo zilimdhihirishia kuwa binti huyo ni “kipande kizuri cha kazi ya sanaa ambayo mungu aliifanya kikamilifu.” Hayo aliwahi kuyasema kimoyomoyo. Hata hivyo, hakujua kuwa msichana huyu alikuwa mzuri kiasi hiki. Alimwangalia kwa mshangao tangu alipoufungua mlango na kutoka taratibu kana kwamba anafanya majaribio ya kupigwa picha za sinema. Alimtumbulia macho pia wakati alipowasogelea na kuwasalimu kwa sauti dhaifu, ambayo Kakakuona aliiona tamu. Kisha, alijikusanya na kuukumbuka wajibu wake.
“Pole sana, darling,” alimwambia.
Nuru alimtumbulia macho yake mazuri, huku akiliweka vizuri gauni lake la kuazima, ambalo alihisi linampwaya japo lilimkaa kana kwamba mshonaji alimfikiria yeye.
“Pole kwa misukosuko yote iliyokukumba. Maadamu nimefika hakuna lingine litakalotokea,” aliendelea.
Nuru hakumjibu. Hakuwa na la kumjibu, jambo ambalo lilimfanya Kakakuona ahisi kuwa anamwogopa Banduka. Hivyo, alimwomba akatayarishe chakula ili azungumze faragha na mpenzi wake.
Walipobaki peke yao, Nuru alimuuliza, “Wewe ni mmoja wao?”
“Ndiyo na hapana.”
“Una maana gani?”
“Nina maana hiyohiyo. Ndiyo, mimi ni mmojawao na hapana; mimi si mmojawao.”
Alipoona Nuru hajamwelewa aliongeza baada ya kutoa tabasamu pana, “Maana yangu ni kwamba, mimi ndiye niliyewatuma wakulete. Amri ya kufa au kuishi kwako iko mikononi mwangu. Niliwalipa vizuri sana ili wafanye kazi ndogo sana ya kukuchukua na kukuleta kwangu. Kwa bahati mbaya wamekuwa kundi kubwa la wapumbavu watupu. Wote sasa ni marehemu. Mmoja anaoza humo ndani ya kabati. Sio?”
Nuru hakumjibu.
“Wamekufa wote. Wanaume wanne. Wewe huko hai. Umetulia huna wasiwasi wowote. Ndio kwanza unatoka zako kuoga. Sivyo?”
Nuru alipochelewa kujibu Kakakuona aliongeza, “Sijui una kitu gani. Sielewi umetumia hila gani kuwaangamiza watu wote wale. Ila ninachokuarifu ni kitu kimoja. Naitwa Kakakuona. Mimi na kifo hatutofautiani sana. Nikisema kufa, lazima utakufa. Upo?”
Nuru aliamua kutomjibu.
“Napenda uelewe hivyo. Wala usidhani kuwa najipendekeza kwako. Ngoja nikuonyeshe.”
Aliinama na kuichukua briefcase yake. Akaifungua na kuipekua hadi mkono ulipotoka ukiwa umeshikilia picha ya yule msichana aliyeharibiwa uso.
“Unaona?” alisema akimkabidhi Nuru. “Unaona? Hiyo ni kazi yangu.” Ilikuwa haitazamika mara mbili. Nuru alimrudishia upesiupesi huku akijisikia kutapika.
“Hiyo ni kazi yangu,” Kakakuona alirudia akicheka. “Nafurahi kuwa umeipenda picha hiyo. Unaonaje hapo utakapojikuta na sura kama hiyo? Utafika mbele ya yule hawara yako, Joram Kiango? Si atakufa kwa uchungu?”
Kutajwa kwa jina la Joram kuliisisimua damu ya Nuru. Alijikuta akirudiwa na maswali ambayo yamekuwa yakimsumbua sana juu ya usalama wake. Alitamani amuulize mtu huyo kama wamemkamata au la. Kwa jumla, alikuwa na maswali mengi ya kumuuliza. Lakini aliamua kutumia silaha ya ukimya na utulivu ili kupambana na mtu huyo ambaye alikuwa akijaribu kupandikiza hofu katika moyo wake, mchezo ambao Nuru hakuwa mgeni nao.
“Nasikia Joram ni shujaa na ana roho ngumu. Nasikia hakutokwa hata na chozi moja baba yake alipofariki. Hivyo, bila shaka hatashtushwa na kifo chako. Lakini atakapokuona uko hai, ukiwa na sura kama hii, hatalia kweli?”
Kana kwamba anajijibu mwenyewe aliongeza harakaharaka, “ Lakini haitatokea, labda kama utakuwa mbishi. Jitahidi akija mwenyeji wetu tuwe kama mtu na mpenzi wake. Baada ya kula tutaondoka zetu kwenda Dar es Salaam, mkono kwa mkono hadikwenye chombo. Tutakaa mkono kwa mkono hadi tuendako. Ukijitia kujua umeumia. Iwe mbele ya watu, iwe mimi na wewe, upo?”
Penye wengi hapakosi mengi. Katika mkusanyiko wa wasafiri waliokuwa wakiisubiri Sea Express bandarini Dar es Salaam, ili iwapeleke Zanzibar kulikuwa na pilikapilika nyingi ambazo hazikuwa na msingi wowote. Kwa mfano, pamoja na ukweli kwamba kila msafiri alikuwa na tiketi yake mkononi, yenye namba ya kiti chake, bado kuna wale waliojifanya kuwa wana haraka zaidi ya wengine. Hawa walikuwa wakikimbia huku na huko, mizigo mikononi, na kisha hukaa katika ukingo wa kivuko tayari kuivamia meli hiyo ambayo ndio kwanza ilikuwa inatia nanga.
Milango ilipofunguliwa na abiria watokao Zanzibar kuanza kushuka taratibu abiria hawa “wenye haraka” walikuwa kikwazo kwa jinsi walivyosababisha msongamano mkubwa mlangoni hapo. Watumishi wa Bandari walifanya kazi ya ziada kuwadhibiti abiria hao ili wenzao washuke kwa utaratibu.
Kati ya abiria hao wenye haraka alikuwamo Joram Kiango. Pengine yeye alikuwa na haraka zaidi ya watu wote katika msafara huo. Lakini, kama kawaida yake haraka au shauku yake ya safari hiyo ilikuwa siri yake binafsi. Usoni alionekana mtulivu, ambaye isingekuwa rahisi kufahamu kama anasafiri, amekuja kupokea mgeni, au anasindikiza.
Aliketi juu ya kiti cha mbao, ambacho wasafiri wengi walikiacha na kusimama wima na mizigo yao. Akiwa katika mavazi yake yaliyomfanya awe mtu asiyetazamika sana, yaani kanzu ya kawaida, kijikoti juu ya kanzu hiyo, kilemba kichwani na ndevu za bandia huku kijimfuko kidogo kikiwa miguuni pake, hakuna aliyejisumbua naye.
Lakini yeye alikuwa akijisumbua na kila mtu. Macho yake yenye uzoefu yalimpitia karibu kila mtu katika umati huo. Watu wawili katika umati huo walimsumbua. Ingawa walikuwa wageni kwake, lakini macho yao na tazama yao ilimfanya Joram aone kuwa si wasafiri wa kawaida. Neno “kachero” lilikuwa wazi katika tazama yao, zungumza yao na simama yao.
Joram alihisi kuwa hawa pia wako safarini kwenda Zanzibar kumfuatilia Kakakuona, jambo ambalo halikumpendeza kwani alitamani sana ngoma hiyo aicheze peke yake. Hata hivyo, alitulia kimya, akiendelea kutazama kwa makini zaidi, aone nani mwingine yumo katika msafara huo.
Kwa uzoefu wake wa upelelezi hiyo haikuwa kazi kubwa kwake. Alifuatilia tazama ya makachero hao wawili. Kila walipoelekeza macho yao kwa hila, yeye pia aliyaelekeza huko kwa mbinu, akichunguza ishara zote.
Haukupita muda mrefu kabla Joram hajakipata hicho alichokusudia. Macho ya makachero hao yalikosea kulitazama gari moja, aina ya Toyota Land Cruiser, lililokuwa limepaki nje kidogo yabandari, ndani yake mkiwa na watu watatu. Joram Kiango alimtambua mmoja kati yao mara moja. Alikuwa Inspekta Kombora.
‘Kombora pia anakwenda Zanzibar!’ Joram alijiuliza kwa mshangao. Ndio kwanza akahisi kuwa Kakakuona ni mtu hatari sana. Awali ya hapo alimchukulia kama mtu kichaa tu, ambaye anaua watu wanyonge na kumteka mtu asiye na hatia, kama Nuru, kwa sababu zake anazozijua yeye mwenyewe, ambazo Joram Kiango hakuona kama angepata muda wa kuzifahamu kwani alichokusudia, mara tu baada ya kukutana na kichaa huyo ana kwa ana, ilikuwa kumuua kwanza, kumuuliza maswali baadaye.
Akaamua kumpuuza Kombora na makachero wake wote na kuendelea kuwasubiri abiria waliokuwa wakiendelea kushuka kutoka katika chombo hicho waishe ili awe miongoni mwa watu wa kwanza kuingia.
Kama kawaida ya abiria wa meli, ile haraka yao ya kupanda waanzapo safari, haitofautiani sana na ile ya kushuka wanapofika mwisho wa safari. Hivyo, pilikapilika zilikuwa nyingi. Joram alitulia akiwatazama abiria hao, hali fikra zake zikiwa nje kabisa ya eneo hilo. Hakuwatilia maanani watu mbalimbali waliopita mbele yake, mizigo yao mikononi.
Lakini haukupita muda kabla hajashuka abiria mmoja aliyemfanya agutuke ghafla kama aliyenaswa na waya wa umeme. Kama si mzoefu katika masuala ya upelelezi angeweza kuinuka na kumkimbilia abiria huyo. Angeweza kumkumbatia na kumbusu. Lakini si yeye. Pamoja na kushtuka kwake, pamoja na kutoyaamini macho yake, alitulia kwa utulivu kana kwamba abiria huyo ni miongoni mwa abiria wa kawaida machoni mwake; kana kwamba hamfahamu na wala hajapata kumwona maishani mwake.
Abiria huyo alikuwa msichana mzuri kupita kiasi, mwenye umbo zuri kupindukia, alilolificha katika baibui alilojitanda juu ya mavazi yake. Mkono mmoja wa abiria huyo ulikuwa umeshika briefcase ya kiume hali mkono wa pili umeshikana na ule wa kijana mmoja ambaye alionekana kama mpenzi wake. Mkono wa pili wa kijana huyo wa kiume ulikuwa ndani ya mfuko wake wa koti.
Abiria huyo wa kike hakuwa mwingine zaidi ya Nuru.
Wala Joram hakuhitaji kuambiwa kwamba mtu huyo aliyeandamana naye alikuwa mtu baki zaidi ya Kakakuona.
Kwa mtazamo wa kawaida, mtu yeyote angepata hisia kuwa abiria hao walikuwa wapenzi wawili ambao ndio kwanza wameoana, hivyo, wanatoka zao Zanzibar kusheherekea ndoa yao. Lakini kwa mtazamo wa mtu kama Joram alifahamu fika kuwa uhusiano wa kimapenzi baina ya viumbe hao wawili ulikuwa sawa na ule wa kondoo na mbwa mwitu. Joram aliona wazi kuwa Nuru alikuwa ametekwa nyara na mtu huyo. Aliona wazi vilevile kuwa mkono wa mtu huyo uliofutikwa mfukoni ulikuwa umeshikilia bastola iliyomlenga Nuru kikamilifu na asingesita kuifyatua iwapo lolote lingetokea. Adui huyo alikuwa akitembea kwa mwendo wa kujiamini kwa kiwango kilichomshangaza Joram. Hakutarajia muuaji mwoga, kiasi cha kuua watoto wa kike wasio na hatia, angeweza kuwa na moyo sugu kiasi hicho.
Macho ya Joram yaligongana na ya Nuru. Mavazi bandia aliyoyavaa hayakuwa kipingamizi cha kumfanya Nuru asimtambue mara moja. Joram alihisi kitu kama faraja ikichepuka ghafla katika macho yake mazuri.
Hata hivyo, akili yake ilikuwa nzuri vilevile kwa kiwango ambacho kilimfanya Joram Kiango azidi kumheshimu. Zaidi ya kumtupia jicho hilo moja la kawaida kama ilivyokuwa kwa watu wengine, Nuru aliendelea na safari yake kama kawaida.
Pamoja na uduni wa mavazi yake, Joram alikuwa kamili kikazi. Isingemchukua sekunde moja kuifikia bastola yake na kuufumua ubongo wa Kakakuona. Hali kadhalika, maungo yake yalikuwa yakichemka kwa hamu ya kumfanyia mazoezi ya judo mpuuzi huyo.
Hata hivyo, kwa kuchelea kuyanadi maisha ya Nuru, hasa baada ya kukumbwa na misukosuko yote ile isiyokadirika, Joram aliamua kuacha mchezo huo uendelee kidogo.
Jambo lingine lililomfanya Joram aahirishe kumchukulia hatua muuaji huyo ni ile heshima au hadhi mpya ambayo alijikuta akimpatia muuaji huyo kutokana na kitendo chake hicho cha aina yake. Halikuwa jambo la kawaida muuaji ambaye anafahamu fika kuwa anawindwa zaidi ya kifaru mwenye kichaa, kujitokeza hadharani, mchana kweupe, akiwa na mateka ambaye ni mwanamke hatari zaidi ya nyoka aina ya swila. Hivyo, Joram alijikuta akiamua kujionea kitu kinachomtia ujeuri huo.
Kisha, akamkumbuka Kombora na makachero wake. Ndio kwanza akafahamu kuwa hawakuwa safarini, bali walikuja kwa ajili ya kumlaki mwuaji huyo kwa matumaini ya kumkamata.
Akageuka kuwatazama makachero hao. ‘Polisi ni polisi, avae magwanda asivae,’ Joram aliwaza alipoona hali ya makachero hao. Japo walijitahidi kujikaza, kana kwamba hakuna kinachoendelea, lakini hakushindwa kusoma ramani ya misukosuko katika nyuso zao.
Kila mara mikono yao ilichopoka na kupelekwa mifukoni, kuzipapasa bastola zao; miguu yao ikichezacheza kwa namna ya ukosefu wa utulivu mioyoni mwao. Mara kwa mara waliyatupa macho yao katika gari alilokuwemo Kombora kwa namna ya watu wanaosubiri amri ili wafanye jambo, amri ambayo Joram hakuona kama Kombora alikuwa tayari kuitoa kwa jinsi alivyopigwa butwaa ingawa alijifanya mtulivu; akivuta sigara yake, gazeti mkono wa pili.
Wakati huo Kakakuona na Nuru walikuwa wakimaliza ngazi na kuanza kutoka nje ya banda. Kakakuona aligeuka kumtazama mmoja kati ya makachero wa Kombora kwa namna ya kumwambia, “Nimekutambua.”
Joram alihisi kuona tabasamu la kebehi katika macho hayo.
***
Kama kuna siku ambayo Inspekta Kombora aliwahi kuhisi akili yake imeduwaa, huku fikra zake zikiwa zimedumaa, ni hii. Mwili mzima ulimlegea, mikono ikamtetemeka kwa kitu ambacho asingeweza kukipambanua kati ya hasira na aibu. Sigara ambayo aliiwasha kitambo iliendelea kuteketea mdomoni mwake.
“Mzee… anakwenda zake… Tufanye nini mzee?” mmoja kati ya wasaidizi wake, aliyekuwa kiti cha nyuma cha gari hilo alimuuliza Kombora akigeuka kumtazama, ingawa macho yake yalidhihirisha kuwa alikuwa hamwoni
Akili yake bado ilikuwa imepaa au kuzama katika lindi refu la mshangao na kutoyaamini macho yake. ITAENDELEA
Zaidi ya saa moja iliyopita alipokea habari toka Zanzibar kuwa Kakakuona ambaye alitoweka ghafla, aliibuka toka katika mitaa ya mji huo akiwa amefuatana na msichana ambaye alionekana kama Nuru. Kombora aliwakumbusha waendelee kumchunguza bila kumshtua. Lakini dakika tano baadaye, alipoambiwa kuwa Kakakuona alikuwa akija Dar es Salaam kwa Sea Express na kwamba Nuru alionekana kama ambaye yuko chini ya ulinzi, aliongoza kikosi cha vijana wake wazuri, sita, ambao walikuwa tayari; wakisubiri amri yake.
Kombora alisita kuitoa amri baada ya kuona kile ambacho hakutarajia kukiona katika macho ya Kakakuona. Kitu kisichoelezeka kwa jinsi kilivyofungwa pamoja katika fungati la ukatili, dharau, unyama na dhihaka ya hali ya juu.
Kombora alishangaa alipoona kuwa Kakakuona alijua fika kuwa amezingirwa na makachero wengi, ambao walikuwa tayari kumuua mara tu wapewapo ishara, lakini bado alipita kwa kujiamini. Dharau yote hiyo ya Kakakuona ilitokana na ukweli kuwa asingekufa kabla hajamuua Nuru, jambo ambalo alifahamu kuwa yeyote duniani asingelifanya kwa urahisi.
Kwa ajili ya unyama wa mtu huyo, kwa jinsi ambavyo alikuwa anaendelea kuteketeza maisha ya watu wasio na hatia, Kombora angekuwa tayari kutoa amri avamiwe na kuuawa bila kujali ambacho kingemtokea msichana huyo.
Ndiyo, angefanya hivyo, iwapo tu msichana huyo asingekuwa Nuru.
Nuru ni mmoja kati ya wasichana wachache wenye nafasi ya pekee katika moyo Kombora. Ingawa hakupata kumwambia hivyo waziwazi, lakini aliheshimu sana mchango wake katika harakati za yule mpenzi wake Joram Kiango.
Kombora asingeweza kusahau jinsi msichana huyo alivyobadilika kutoka katika umbile laini la kike na kuwa jabali la chuma tangu aliposhirikishwa katika ule mpango wa kinyama wa kuwaua viongozi wa nchi huru za Kiafrika mjini Arusha, mkasa ambao tayari umehifadhiwa katika kitabu kinachoitwa Salamu Toka Kuzimu ambao kwa jinsi unavyotisha hata baadhi ya watu wanauchukulia kama riwaya ya kubuni.
Baada ya hapo ndipo Nuru alipoamua kuudhihirisha uanamapinduzi wake katika visa na mikasa kadha wa kadha ambavyo pia vimetolewa vitabu vinavyoitwa Tutarudi na roho zetu? Malaika wa Shetani na vinginevyo.
Kazi ya Nuru katika mikasa hiyo ilikuwa kubwa kiasi kwamba bila ya yeye pengine Joram Kiango asingekuwapo duniani leo hii.
Kombora hakuona kama inayumkinika kutoa amri msichana kama huyo afe kwa ajili ya kumwogopa Kakakuona na unyama wake. Akaendelea kuduwaa.
“Mzee… wanaondoka,” msaidizi wake aliendelea kumkumbushia.
Wakati huo Kakakuona alikuwa akimaliza kuingia katika gari la kukodi, aina ya Datsun, baada ya kumtanguliza Nuru kukaa na dereva mbele, yeye, nyuma. Dereva akiwa haelewi lolote alitia gari moto na kuondoka taratibu. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Wakati gari hilo likiondoka, kijikaratasi cheupe kilidondoka toka dirisha la nyuma. Mmoja kati ya makachero wa Kombora alikiokota. Baada ya kusoma alikileta kwa Kombora huku akiwa na dalili za mshtuko mkubwa. Alimkuta Kombora akiongea katika Redio call kuwaarifu watu wake waliokuwa nje ya eneo hilo walifuate gari hilo kwa hila. Aliwapa namba za gari na rangi yake.
Kisha, aliitupa sigara yake ambayo ilikuwa imekwisha na kujiwashia nyingine.
“Ni nini?” alimuuliza askari huyo huku akipokea kipande cha karatasi.
“Ujumbe.”
“Ujumbe gani?”
Ulikuwa ujumbe mfupi ambao uliandikwa kwa peni ya wino mweusi;
Fanyeni upumbavu wa aina yoyote ile mtashangaa kuiokota maiti ya msichana huyu barabarani ikiwa na sura ya wale waliotangulia. Na sipendi kufuatwafuatwa.
Kakakuona.
Kombora aliisoma kwa mara ya pili. Kisha, akaitumbukiza katika mfuko wa koti, hasira zikichemka kichwani mwake, kutokana na dhihaka hiyo ya Kakakuona. Kombora alijikuta akizungumza peke yake kwa minong’ono, “It’s too much. Kama anajua anafuatwa ya nini kuendelea kujificha?”
Kwa sauti alikoroma, “Ok, twendeni.”
“Wapi?”
“Mfuateni,” aliamuru. “Usijali kama atafahamu kuwa anafuatwa au la,” alimwambia dereva. “Anaonekana kama anayetaka tumfuate.”
Magari mengine matatu ya polisi, yenye namba za kiraia, ambayo yaliegeshwa katika eneo hilo yalianza kuondoka moja baada ya jingine, kwa maelekezo ya Kombora kupitia Walkie talkie yake magari mawili kati ya hayo yalilipita gari la Kakakuona, ambalo lilikuwa likienda kwa mwendo wa wastani, na kulitangulia. Mbele ya safari gari moja lilichepuka kama vile halina habari na msafara huo, la pili likiendelea taratibu.
Gari la Kakakuona liliifuata Barabara ya Sokoine na lilipoifikia Barabara ya Morogoro likaifuata, jambo ambalo lilifanya gari la makachero wa Kombora lililotangulia lipitilize hadi katika mzunguko wa Mnara wa Saa ambapo lilipinda na kuingia samora hadi walipopishana na Kombora, ambaye aliwaashiria kurudi ofisini kazi yao ilichukuliwa na teksi moja yenye namba za TX ambayo ilionekana kama imechukua abiria watatu.
Kichwa cha Kombora kiliendelea kusumbuliwa na hali ya kucheza na mtu kama Kakakuona. Alijihisi kuwa yeye na askari wake wote wako katika duru wakicheza ngoma wasiyoifahamu, ngoma ambayo mpigaji hakuwa mwingine zaidi ya Kakakuona mwenyewe. Jambo hilo lilizidisha hisia za hatari kichwani mwa Kombora.
Ingekuwa rahisi sana. Kati ya magari yake yaliyotangulia, moja lingeweza kusababisha ajali ya ghafla kwa lile lililomchukua Kakakuona, papohapo, yeye na askari wake kuivamia ili kumuua Kakakuona na kujaribu kumwokoa Nuru. Ni moja kati ya mambo ambayo yamekwishafanywa sana. Hata hivyo, ilikuwa kama kamari ambayo Kombora hakuwa tayari kuicheza. Hivyo, ikabidi aendelee kustahimili, akiruhusu magari yake yaendelee kumsindikiza Kakakuona kama shujaa anayepelekwa Ikulu kuchukua wadhifa wa nchi.
***
Kwa Joram Kiango ilikuwa kazi rahisi kuliko alivyotarajia. Mara tu alipomwona Inspekta Kombora akishindwa kuchukua hatua dhidi ya Kakakuona, badala yake akianzisha msafara wa kumfuata, yeye pia alifanya hima kuliendea mojawapo ya magari mengi yaliyokuwa yakisubiri abiria nje ya stesheni.
Alichagua gari jipya, aina ya Suzuki, lenye namba za Posta, ambalo ingawa dereva alidai kuwa yuko kazini, lakini Joram hakuchelewa kugundua kuwa alikuwa akisubiri abiria yeyote ambaye angemkodi ili ampatie chochote cha kutia mfukoni.
“Una petroli ya kutosha?” alimuuliza.
“Kwani unakwenda mbali mzee?”
“Itategemea,” Joram alijibu akizunguka upande wa pili ambako alifungua mlango na kuingia ndani. “Ifuate ile. Ifuate taratibu wasijue kuwa wanafuatwa.”
Dereva huyo alionyesha wasiwasi kidogo. “Gari ile, mzee! Kwa nini tuifuate? Unajua…” alisita kidogo. Lakini alipoona kitita cha shilingi elfu tano kikiwekwa juu ya mapaja yake alionekana kubadilika kidogo.
“Wakienda mbali zaidi nitakuongeza,” Joram alisisitiza, huku akimhimiza kuondoa gari.
“Tatizo ni kwamba ile gari naijua brother,” alisema akiondoka shingo upande. “Ile ni gari ya wenyewe ile. Inatumiwa na manjagu, pamoja na kuwa na namba za kiraia. Naogopa wasije wakaniletea matatizo wakijua kuwa wanafuatwa.”
“Usijali, hawatafahamu.”
Akili ya Kakakuona ikiwa juu ya magari ya Kombora ambayo alikwishayakariri namba zake vizuri sana kichwani, hakujishughulisha na gari dogo la Posta ambalo lilionekana kwa mbali sana miongoni mwa magari mengine.
Aidha, Kombora vilevile fikra na hisia zake zote zikiwa katika gari la mbele yake, ambalo lilimchukua muuaji hatari kama Kakakuona, hangeweza kulitazama gari hilo la Posta lililokuwa nyuma yao. Hali kadhalika, ikiwa tabia ya polisi ni kufuata badala ya kufuatwa, kusaka badala ya kusakwa, wazo la kugeuka nyuma mara kwa mara halikumjia akilini kabisa. Tabia hii ilifanya kazi ya Joram na dereva wake iwe nyepesi kama ilivyokuwa.
***
Ulikuwa ni msafara usio na kona nyingi wala mizunguko mingi. Ilielekea kama Kakakuona alikuwa hana haja ya barabara nyingine zaidi ya ile ya Morogoro, Hata hivyo, walipofika Mtaa wa Jamhuri, gari hilo lilionekana likipinda kulia kuufuata mtaa huo. Gari la Kombora likafanya hivyohivyo. Joram pia akamwamuru dereva wake kuwafuata.
Njia hiyo ilikuwa na msongamano mkubwa wa magari hivyo, safari yao ilikuwa ya taratibu, jambo ambalo lilimtia hofu Kombora kuwa Kakakuona angeweza kuitumia fursa hiyo kuchepuka ghafla mahala ambapo asingekuwa mwepesi wa kuona alipoelekea.
Lakini Kakakuona hakuonekana kama mwenye haraka ya kufanya hivyo. Aliendelea na safari yake taratibu kama ambaye alikuwa na nia njema sana ya kumwongoza Kombora na msafara wake hadi alipoufikia uchochoro ambao unachepuka na kuunga mtaa huo hadi Mtaa wa Kisutu ambapo alionekana akisogea kulia na kuliingiza gari katika ukumbi wa jengo moja jipya, ambalo liliacha eneo zuri la kupaki magari chini yake kwa meta kama kumi ndani yake.
Kombora alilitazama gari hilo likipaki kwa utulivu. Alitumia dakika mbili tatu za kuduwaa, akijiuliza afanye lipi, kwa makini. Jengo hilo lenye ghorofa nne lilikuwa moja kati ya majengo mapya yaliyokuwa yakiibuka huko na huko jijini Dar es Salaam.
Vibao vya kampuni na biashara mbalimbali vilionekena katika kuta mbalimbali za jengo hili chini ya kibao kilichoandikwa Sunrise Modern Club. Kibao hiki kilimeza karibu robo ya ghorofa zima ya chini. Maandishi yake yalikuwa juu ya kioo kikubwa, kwa rangi mbalimbali ambazo usiku ziliwaka kwa namna ya kuchezacheza katika hali ya kuvutia macho. Kombora aliwahi kupita hapa mara nyingi usiku na kuvutiwa, kama watu wengine, lakini hakuwahi kuingia ndani. Kumwona Kakakuona akipaki hapo aliyakumbuka mauaji ambayo amekuwa akiyafanya katika hoteli na kumbi za starehe kama yale ya Lang’ata; akajikuta akipatwa na hisia za hatari kuliko awali.
“Liwalo na liwe,’ aliwaza. “Tunamfuata hukohuko ndani,” aliamuru, “Angalieni. La msingi ni kuyaokoa maisha ya Nuru. Hivyo, risasi za kwanza, kama itabidi, ziwe za kumvunja mabega, ili asiweze kuitumia mikono yake. Aliye kulia, alenge mkono wa …”
Kombora alilazimika kuyakatisha maongezi yake alipomwona Kakakuona akishuka huku akifuatiwa na Nuru ambaye alikumbatiwa kiuno kama wapenzi wa damu.
Walishuka harakaharaka na kuingia ndani ya jengo hilo.
Kombora, akiwaongoza askari wake wawili, pia alishuka na kumfuata. Alipolifikia gari lililokuwa likitumiwa na Kakakuona nusura atokwe na ukelele wa mshtuko, mshangao na hasira, alipomtazama dereva.
Alikuwa amelalia usukani wake akitapatapa; tundu kubwa la risasi likiwa limekifumua kichwa chake kisogoni, na kuruhusu damu nzito iliyochanganyika na ubongo iendelee kumwagika kama uji mwekundu unaomwagika toka katika birika.
“Haraka… ndani,” Kombora alinguruma akiitoa bastola yake na kutangulia ndani ya jengo hilo. Mlango uliwaongoza katika korido nyembamba iliyowafikisha katika chumba cha mapokezi, ambacho kilikuwa na makochi manne makubwa yaliyokuwa matupu. Makochi hayo yalikielekea chumba cha kioo ambamo hamkuwa na mtu. Kombora alitazama huku na huko kama anayeomba msaada. Aliiona lifti, na upande wa pili aliiona ngazi iendayo juu.
“Mmoja atumie lifti, mwingine apande kwa ngazi. Upesi. Kama nilivyosema, mkimwona msizungumze naye. Acheni risasi zizungumze. Ok?”
Wakati yule aliyeamriwa kwenda kwa miguu alipoanza kupanda ngazi harakaharaka na yule wa lifi akiita kwa kubonyeza tufe, Kombora aliitoa walkie talkie yake na kuwaamuru makachero wengine kuja mara moja. Kisha, akasogea kaunta bila kujua alihitaji nini. Kama awali alijisikia kupiga kelele, safari hii akijisikia kuzimia kwa kile ambacho alikiona chini ya meza hiyo ya kaunta.
Mzoga wa mtu ulikuwa umelala kifudifudi katika dimbwi la damu nyingi ambayo ilikuwa ikiendelea kujaa sakafuni. Dalili yoyote ya uhai haikuwamo katika umbile hilo ambalo sare alizovaa msichana huyo zilionyesha kuwa alikuwa mhudumu wa mapokezi.
Akili ya Kombora ilidumaa kwa kitambo cha robo dakika. Watu wawili, wasio na hatia, kuuawa huku yeye anashuhudia…! Aliwaza kwa uchungu. Alishindwa kuendelea kuwaza. Badala yake alikurupuka mbio kuiendea ngazi ambayo aliipanda kwa kuruka ngazi tatu tatu, bastola ikiwa imemtangulia.
***
Kwa Nuru ilikuwa kama mtu anayeshuhudia mchezo wa sinema ya kusisimua ambao yeye mwenyewe ndiye mtazamaji, wakati huohuo mwigizaji. Naam, ilikuwa kama ndoto tu; tangu alipojikuta akihama kutoka katika mikono ya yule muuaji Chongo na kuangukia katika milki ya Kakakuona. Kama kondoo, aliafiki kila alichoelekezwa. Aliafiki kuushika mkono wa muuaji huyo huku akitabasamu.
Kadhalika, aliafiki kupita kote huku akijua kabisa kuwa kila hatua anayopiga na muuaji huyo inamsogeza karibu zaidi na mauti yake mwenyewe.
Hata hivyo, ile kiu yake ya kufahamu kwa undani zaidi kiini cha mauaji haya ilikuwa sababu nyingine iliyomfanya aendelee na ukondoo huo. Aidha, ile bastola yake, ambayo aliificha vyema alipokuwa akioga bafuni ilimpa moyo na kumpa matumaini ya kupata fursa nzuri ambayo ingemwezesha kuyaokoa maisha yake mara mambo yatakapovuka kina.
Matumaini hayo yaliongezeka maradufu mara aliposhuka bandarini na kumwona Joram Kiango akimsubiri, bila ya Kakakuona kumtambua. Nuru alizidi kupata moyo.
Ilikuwa mara yake ya kwanza kumtia Joram Kiango machoni. Ile hofu yake kuwa tayari wauaji hawa wamempata ikatokomea. Ingawa hawakuongea wala kupeana ishara yoyote, lakini bado kule kumwona akiwa hai na kuyaona macho yake yaking’ara kama ilivyo kawaida yake kulimwongezea ari na kumpa matumaini makubwa ya ushindi.
Hivyo, hakuwa na hofu kubwa sana pindi walipochukua gari na kuondoka huku domo la bastola ya Kakakuona, iliyofichwa mfukoni, likiendelea kumtekenya ubavuni. Wala hakubabaika Kakakuona alipouandika ule ujumbe wa kejeli kwa Kombora, ambao ulikusudiwa kumwongezea hofu.
Lakini, mara tu baada ya gari kusimama hapa na Kakakuona kufanya kile kitendo ambacho Nuru hakukitarajia, alijikuta akiingiwa na hofu kubwa iliyochanganyika na hasira.
Ndiyo, Nuru ameshuhudia mara nyingi watu wakiuawa. Kamwe hakuwa mgeni kwa hilo. Lakini kuuawa kwa kijana huyu wa Kipemba, asiye na hatia, ambaye aliwaendesha bila hofu wala hisia zozote za hatari, kuliufanya moyo wake ukose baadhi ya mapigo yake, hasa pale alipoona kijana wa watu akianguka ghafla juu ya usukani kama mbuzi.
KAKAKUONA alitenda kitendo hicho kwa wepesi wa ajabu. Sekunde ya kwanza alitulia akiupima mwendo wa gari la Kombora lililokuwa nyuma yao. Sekunde ya pili tayari alikuwa ameua na kuirejesha bastola yake mfukoni, huku akimwamuru Nuru kutoka nje ya gari haraka.
Mshangao, kutotarajia na wepesi huo wa ajabu ulimfanya Nuru aduwae kwa hofu; kama mtazamaji asiye na uwezo wa kufanya lolote. Jambo hilo lilimuumiza sana rohoni. Kama angejua kinachokaribia kutokea angemuua Kakakuona kwanza, yeye binafsi kufa baadaye, badala ya kushuhudia kijana huyo asiye na hatia akiuawa mbele yake, kwa ajili yake.
“Fanya mzaha, kifo kitakachofuata kitakuwa chako,” Kakakuona alimwonya wakati wakiingia ndani ya jengo hilo, akiwa mtulivu.
Tabasamu laini lilitanda usoni mwake kama mtu aliyeua mbu tu. Akiwa na tabasamu hilohilo, huku kashikilia kiuno cha Nuru, alimsogelea msichana wa mapokezi. Nuru alihisi nia yake huku tayari akiwa amechelewa sana kwa nusu sekunde nzima. Wakati huo risasi ilikuwa imekwishapenya katika paji la uso mzuri wa msichana huyo. Kwa wepesi uleule aliupenyeza mkono wake ndani ya vazi lake la ndani na kuishika bastola yake. Lakini hakuwahi kuitoa. Kitako cha bastola iliyomuua msichana huyo tayari kilikuwa kimepigwa upande mmoja wa kichwa chake na kumfanya arukwe na fahamu na kupepesuka. Aliongezwa kipigo cha pili ambacho kilimmaliza kabisa. Kama ndoto, alihisi akididimia katika shimo lenye kiza na kina kirefu kisicho na mwisho.
Wakati hayo yakimtokea Nuru, kikosi cha makachero wasiopungua kumi, wakiongozwa na Inspekta Kombora walikuwa tayari wamelivamia jengo hilo, wakichungulia kila uchochoro na kuchunguza kila chumba. Wenzi wao, vijana sita machachari, walikuwa nje ya jengo wakichungulia kila kona na kila uchochoro. Wote walikuwa makini, silaha zao mikononi, tayari kwa lolote.
Inspekta Kombora alikuwa makini zaidi ya wote. Akiwa na hasira ambayo iliimeza kabisa hofu ya kifo dhidi ya muuaji huyu, aliwaongoza askari katika kila chumba, akiamuru kupekuliwa kila kabati. Kila jokofu na kila sanduku; kuchungulia kila choo na kufunua kila kitanda na kadhalika.
Bastola yake ikiwa wazi mkononi, mikunjo ya hasira tele usoni, iliwafanya wapangaji wa jengo hilo kushindwa kumwuliza lolote. Badala yake waliduwaa, wakimtazama, kama ambavyo hawakuyaamini macho yao.
Baada ya dakika kumi za kuepuka hapa na pale, Kombora na kikosi chake kizima walijikuta wamerudi tena katika ukumbi wa disko wa Sunrise huku wakitazamana kwa namna ya kukata tamaa; kila mmoja akitokwa na jasho jingi lililotokana na mbio walizozipiga katika jengo hilo.
“Haiwezekani,” Kombora alinong’ona kama anayezungumza peke yake. “Nilimwona kwa macho yangu mwenyewe akiingia katika jengo hili. Na ameua watu wawili, wasio na hatia, mbele ya macho yangu katika jengo hilihili. Haiwezekani kuwa ametoweka.”
“Kwani kuna nini mzee?” aliyeuliza ni mzee wa makamo aliyekuwa nyuma ya kaunta, ambayo alimezwa na kila aina ya pombe ipatikanayo katika sayari hii, katika karne hii. Mzee huyu pamoja na wateja wake watatu, Mhindi na waswahili wawili, ambao alikuwa akiwahudumia, walishikwa na bumbuazi walipoliona kundi la watu wenye silaha, likiuvamia ukumbi huo na kuanza kuchungulia kila mahali huku nyuso zao zikionyesha wazi kuwa walikuwa tayari kwa lolote, tayari kuua, tayari kufa.
“Kuna nini?” mmoja wao aliuliza.
Alijibiwa kwa swali la harakaharaka, “Yuko wapi?”
“Nani?”
Kombora alihisi kama anayezungumza na ukuta. Alimwacha huyo na kujishughulisha kikamilifu katika msako huu wa aina yake, ambao hakumbuki lini amewahi kuufanya tena. Baada ya kukata tamaa ndipo aliporudi chumbani humu na kujumuika na askari wake. Alimtazama mhudumu huyo wa baa na kugundua kuwa alikuwa hajui lolote, wala hakumwona mtu yeyote akiingia au kutoka.
Hivyo alimpuuza na kuwatazama wasaidizi wake, akisubiri mawaidha yao. Alipowaona kimya alizungumza tena kwa sauti dhaifu, “Haiwezekani kuwa ametoweka, lazima yumo humu ndani. Chumba gani ambacho hatujakikagua?”
“Nadhani hakuna chumba tulichokiacha mzee,” mmojawao alimjibu. “Kama yumo katika jengo hili tungekuwa tumempata…” Alisitasita maneno yake aliposhuhudia macho maangavu ya Kombora yakimtazama kwa ukali.
“Yumo humu…” alifoka. “Yuko humuhumu. Lazima apatikane leo hiihii. Ikibidi kila tofali la jengo hili lifunuliwe hadi apatikane. Mnanielewa?”
Kimya kilichofuata, baada ya kauli hiyo nzito ya Kombora, kilifuatiwa na mshindo mkubwa wa ajabu ambao ulisikika ghafla na kumeza anga nzima. Ulikuwa mshindo wa aina yake ambao Kombora hakupata kamwe kuusikia maishani mwake, mshindo ambao ulilifanya jengo hilo zima litikisike kama ambalo lilikaribia kubomoka. Mshindo ambao ulidumu kwa nusu dakika tu, nusu iliyofuata, kila kitu kilikuwa shwari kana kwamba hakuna kilichotokea.
Kombora na vijana wake walitazamana kwa mshangao.
“Ni nini hicho?” mmojawao aliuliza kwa mshangao.
Wenzake wote walimtumbulia macho.
***
Joram alipoliona gari hilo likipaki katika mtaa huo wa Kisutu, alimshauri dereva wake kupitiliza kana kwamba hana shughuli nao. Alimwelekeza dereva huyo kufuata barabara ya umoja wa wanawake, upande wa pili wa mtaa huo, ambapo alishuka na kumruhusu dereva huyo kuondoka.
Kijana huyo hakuamini, shilingi elfu tano kwa kazi ndogo kiasi hicho! Alionekana kama aliyetaka kumwambia hivyo Joram. Lakini Joram hakuonekana kama yuko tayari kwa maongezi zaidi. Alikwishashuka garini na kuliacha hatua kadhaa huku macho yake yakitazama jengo refu lenye maandishi makubwa: Kangaroo Enterprises Ltd, ambalo alihisi lilielekeana na Sunrise Club ambapo Kakakuoa alishukia.
Nia ya Joram ilikuwa kutafuta upenyo au uwezekano ambao ungemwezesha kuifikia klabu ile kwa njia ya mkato badala ya kufuata njia aliyojia.
Uwezekano ulikuwa mdogo. Jengo hilo lenye ghorofa nne lilikuwa limeungana na majengo mengine kwa ukuta mkubwa wenye chupa zilizobandikwa juu. Magari ya watumishi, wateja wa ofisi hiyo walikuwa nje badala ya ndani ambako Joram angeweza kutumia hila kuingia.
Wakati Joram akiendelea kutafakari afanye nini, hakuyaamini macho yake alipomwona mtu aliyekuwa akitoka nje ya jengo akiwa ameshikilia briefcase mkononi. Ingawa macho yake alikuwa ameyafunika kwa miwani, Joramasingeshindwa kumtambua maramoja. Alikuwa Kakakuona. Alikuwa akitembea kwa mwendo wa harakaharaka kuliendea moja ya magari yaliyopaki hapo ambalo alilifungua na kuingia. Kisha, kama aliyekumbuka jambo,Kakakuona alitoka nje ya gari hilo na kuufunga mlango. Akaanza kurudi ndani harakaharaka kama alivyokuja.
Joram Kiango hakuweza kuamini bahati yake. Ilikuwa kama mungu kamleta kwake moja kwa moja. Alikuwa na nafasi nzuri ya kumtia risasi ya kisogo. Lakini kwakuwa alimhitaji alimfuata, rohoni akijua kuwa wakati wa kukijaribu kile ambacho alikuwa akijikumbushia huko kisiwani umewadia.
Ni wakati huohuo anga lilimezwa na mlio mkubwa wa ghafla ulioitetemesha ardhi. Joram alipepesuka na kujikuta akiliegemea gari la Kakakuona. Alifanya harakaharaka kujiweka sawa ili asimpoteze muuaji huyo. Hakumwona.
Kakakuona alikuwa ametoweka mbele yake kama muujiza. Pale ambapo alikuwa hatua kumi tu aliposimama Kakakuona, palikuwa patupu bila dalili yoyote ya binadamu wala uhai. Joram alitazama huku na huko na kuambulia macho ya mshangao ya wapiti njia ambao waliduwaa, baadhi wakitetemeka kwa tukio hilo ambalo hawakuweza kulitafsiri.
“Ni kitu gani?” mpita njia mmoja aliuliza, akimtazama mwenzie ambaye kapu alilokuwa amelibeba lilikuwa limedondoka chini.
“Tetemeko la ardhi…”
“Wala!” alidakia, “Tetemeko gani lenye mlio wa kutisha kama huu.”
Walitazamana. Wakatazama huku na huko kisha wakaachana. Kila mmoja alishika njia yake.
***
“Kuna nini jamani?” Fidels Sembera, mfanyakazi wa Shirika la Maktaba ya Taifa ambayo iko katika barabara hiyo, nyumba kadhaa toka aliposimama Joram, alifoka.
“Nani anayejua?” mtu mmoja alimjibu. “Au ndio mwisho wa dunia?”
Kicheko.
***
“Nini tena hicho?” Muhidini Michuzi, mwandishi wa habari wa Daily News alimwuliza Wilson Kaigarula ambaye waliketi meza moja wakijadili jambo.
“Mwangwi.”
“Mwangi, toka wapi!”
“Labda mvuayataka kunyesha!”
“Mvua kweupe hivi!. Hata hivyo mvua za Dar es Salaam tangu lini zikaanza kunguruma?”
Mhindi, dereva wa daladala ambaye alikuwa akipinda kona kuiacha Umoja wa wanawake aingie Maktaba, alijikuta akisimamisha gari ghafla na kushuka chini huku akitetemeka. Aliamini kuwa amegongana au kagongwa. Alipoona gari likiwa halina dosari, huku kila mtu kaduwaa akauliza, “Nini hiko nalia?”
Hakupata jibu.
***
Jibu alikuwa nalo mtu mmoja tu, Joram Kiango. Ni yeye aliyeona na kujua kilichotokea. Kakakuona alikuwa ameuawa! Mlio uliosikika ni silaha ya aina yake, ambayo tangu ilipogundulika iliaminika kuwa ilikuwa imekwisha tumiwa mara mbili tu. Mara ya kwanza ilitumika nchini Urusi, kwa amri ya Stalin. Ilitumiwa kumwondoa duniani mjerumani mmoja ambaye alijipenyeza hadi katika jeshi la Urusi , miaka nenda miaka rudi akiiba siri mbalimbali ambazo alikusudia kuzipeleka kwao. Wakati huohuo Urusi na Ujerumani ikiwa katika vita, Stalin aliamuru bunduki hiyo itumike juu yake ikiwa pia kama sehemu za majaribio kwa silaha hiyo. Matokeo yake yaliwasisimua sana warusi.
Lakini matokeo hayo yaliwavutia pia Wamarekani ambao walifanya jitihada zote hadi baada ya miaka kumi wakawa wameiba mbinu za kuitengeneza. Na walijikuta wakilazimika kuitumia miaka saba baadaye.
Kijana mmoja aliibuka kusikojulikana na kutangaza kuwa aliwahi kufanya mapenzi ya kimwili na mke wa Rais wa Marekani ambaye alikuwa madarakani wakati huo. Alidai kuwa anamtaka Rais huyo ajiuzulu, vinginevyo angezitoa hadharani picha za video alizopiga akifanya mapenzi na mama huyo. Siku chache baada ya madai hayo, kijana huyo alipokuwa akitoka nje ya nyumba yake, alisikia akiitwa na watu waliokuwa ndani ya gari lililosimama mbele ya nyumba hiyo. Wakati akilisogelea ulisikika mlio kama huu. Ukawa mwisho wake na mwisho wa madai yake.
Silaha hii, ambayo wenyewe huiita ‘kifutio’ ilikuwa kali kiasi kwamba mara unapopokea kipigo chake unasambaratika katika vipande vidogovidogo zaidi ya milioni mbili.Matokeo yake ni kwamba hakionekani kipande cha mfupa, nyama wala tone la damu. Unakuwa umefutika katika uso wa dunia kana kwamba hukuwai kuwepo.
Ni silaha hiyo iliyotumiwa kwa Kakakuona, mbele ya macho ya Joram Kiango. Sekunde moja alikuwa hai mbele ya macho yake, sekunde iliyofuata haikuwepo hata dalili yake.
Joram alilitazama jengo hilo kwa makini. Hakuona mtu wala kitu. Yeyote Yule aliyeifyatua bunduki hiyo alitumia mfadhahiko uliowakumba. Joram pia aliamua kuitumia fursa hiyo. Alitumia funguo zake Malaya, akalifungua gari la Kakakuona na kuichukua ile briefcase yake aliyokuwa nayo mkononi. Akaurudishia mlango na kuondoka taratibu.
***
Akiwa na shahuku kubwa ya kufahamu chochote ambacho angeweza kufahamu juu ya hayati Kakakuona, Joram Kiango hakwenda mbali. Aliivuka barabara hiyo ya UWT na kuingia katika moja ya majengo ya SIDO ambayo baadhi yamepangishwa kwa watu wanayoyatumia kama ofisi.
“Naomba kwenda haja,” alimweleza mtu wa kwanza ambaye alimkuta mbele ya ofisi mojawapo, msichana mtanashati ambaye alimchekea na kisha kumwelekeza kwa mkono.
Joram aliufuata mkono huo na kujikuta katika choo ambacho bila shaka hakikuwa na mwangalizi kwa jinsi kilivyokuwa kichafu. Hata hivyo, alijifungia kwa komeo, kisha akajibanza nyuma ya mlango huo na kuanza kuishughulikia ile briefcase ya Kakakuona. Kwa mtu wa kawaida, briefcase hizi zinafunguliwa kwa namna maalumu, ingemchukua miaka kuifungua. Lakini si kwa Joram Kiango. Yeye alikuwa na mbinu zake ambazo alizitumia kucheza na namba hizo. Dakika mbili baadaye tayari ilikuwa wazi ikimchekea. Kati ya yote aliyoyategemea katika mfuko huo, kamwe hakutegemea kukuta mabunda mengi ya pesa za kigeni kiasi hicho. Kwa hesabu ya harakaharaka zilikuwa paundi za kiingereza laki moja. Zaidi ya pesa hizo ilikuwemo hati ya kusafiria yenye jina la Bruno Malapaka ambaye alielezewa kuwa raia wa Naijeria ambaye alikuwa ni mfanyabiashara. Picha ilikuwa ya Kakakuona. Chini ya vitu hivyo kulikuwa na bastola.
Joram alivitazama vitu hivyo kwa mshangao. Kwa kiasi fulani, mategemeo yake katika kuuchukua mfuko huo yalididimia. Alitegemea kupata maelezo ya kutosha ambayo yangemwezesha kufahamu mengi juu ya Kakakuona; aliajiriwa na nani, mwajiri yuko wapi, kwa nini anafanya mauaji hayo, na mengine mengi. Badala yake alichoambulia ni hati ya usafiri ambayo bila shaka yoyote ni ya bandia, bastola ambayo hakuihitaji sana na pesa ambazo bila ya Nuru kupatikana mapema, akiwa hai, kamwe zisingeweza kumfariji.
Kulifikiria kwake jina la Nuru kulimrejeshea hasira na hofu aliyokuwanayo juu ya usalama wake. Hisia zilimfanya ashuku kuwa waliomuua Kakakuona ni watu haohao waliotumwa kumkamata Nuru. Hisia zilionyesha kuwa mara baada ya Kakakuona kumfikisha Nuru mikononi mwao hawakuuona tena umuhimu wake. Hivyo, walichofanya ilikuwa kumlipa malipo waliomwahidi na kisha kumshawishi aondoke mara moja. Wakati akiondoka ndipo walipoamua kumfuta duniani kwa matumaini kuwa hakuna ambaye angeona wala kuelewa kilichotokea, jambo ambalo lingewafanya polisi waendelee kumsaka Kakakuona ambaye hayuko tena duniani hali wao wakiwa wametulia zao raha mustarehe.
Kuwa kwao na silaha hatari kama hiyo, ambayo ni wachache tu waliowahi kuisikia na uwezo wao kiuchumi, ni miongoni mwa mambo yaliyomfanya Joram azidi kuamini kuwa hawa hawakuwa watu wa kawaida. Licha ya kujizatiti kwao kwa kiwango hicho bado walikuwa wakatili kupindukia. Kitendo chao cha kumwua mtumishi wao, Kakakuona, kikatili kiasi kile, na kupuuza mamilioni ya pesa walizompa kulimfanya Joram aamini kuwa walikuwepo kwa kazi moja tu, kuua.
Hali hiyo ilimfanya ataabike sana moyoni kila alipowaza kuwa Nuru yuko mikononi mwao, mikononi mwa viumbe wasihofahamika, katili kuliko shetani mwenyewe.
‘Lazima atoke mikononi mwao… mapema iwezekanavyo…’ Joram aliwaza huku akiyasaga meno yake kwa hasira. Hata hivyo, alijirudi mara moja na kujaribu kuituliza hasira yake alipojikumbusha, kwa mara nyingine, kuwa dhamira kubwa ya watu hao, kwa kila aina ya ukatili wanaoufanya, ilikuwa kumtia uchungu na hasira, ili ashindwe kufikiri kikamilifu, jambo ambalo litamfanya akurupuke na kuangukia katika mikono yao kama kinda la ndege.
‘Lazima nitulie… nipange kila kitu kwa tuo…’ alijinong’oneza moyoni.
Akiwa ameituliza akili yake alijiuliza anafahamu nini juu ya maadui hao. Hakuna! Aliwaza kwa uchungu muda wote alikuwa akihangaika na Kakakuona ambaye sasa ni marehemu. Hivyo, alikuwa hajui chochote zaidi ya ukweli kuwa anapambana na watu wenye nguvu zote: kiuchumi, kiulinzi na kiukatili.
Chanzo pekee cha kufahamu juu ya watu hao ni katika jengo hilo la kampuni ya Kangaroo ambamo silaha iliyomwua Kakakuona ilitokea. Alijua kuwa jumba hilo au chumba katika jumba hilo kilihusika, kwa namna moja au nyingine, na mkasa huu. Ni hapo ambapo angeanzia. Hata hivyo, Joram alifahamu fika asingekurupuka na kwenda huko kwani ingekuwa sawa na kujitumbukiza wakati moto anauona, hakuwa na shaka kuwa maadui hao wanamsubiri kwa hamu.
Kwamba angehitajika kushughulika mara moja ili kumtoa Nuru katika mikono yao, hilo halikumsumbua tena. Alikuwa na uhakika kuwa Nuru alikuwa akitumiwa kama chambo cha kumfanya aharakishe kuwaendea, jambo ambalo lilimtia moyo kuwa wasingemdhuru kabla hajatokea.
‘Nitatokea… nikiwa tayari…’ aliwaza.
Wazo lake lilikatizwa kwa mlango kusukumwa kwa nguvu nyuma yake. Kitendo hicho kilifuatiwa na sauti nzito ya kiume iliyoita toka njeikiuliza, “vipi braza, bado tu?”
Ndio kwanza Joram akakumbuka kuwa alikuwa chooni. Akaitazama saa yake na kugundua kuwa alikuwa ametumia zaidi ya robo saa, akiwa amejifungia katika choo hicho cha watu. Sasa aliweza hata kusikia harufu kali ya mchanganyiko wa kinyesi na mkojo chooni humo.
Akahakikisha kuwa ameifunga briefcase hiyo kama ilivyokuwa na kutoka nje ya choo huku akijitia kufunga vifungo vya suruali yake. “samahani ndugu yangu.” Alimwambia kijana wa kiume aliyekuwa amenyoa panki, ambaye alikuwa kasimama nje ya choo hicho katika hali ya kubanwa sana na haja ndogo. “Tumbo lilikuwa likinisumbua sana,” alimlaghai.
“Shauri ya bia za Mtikila.” Kijana huyo alimjibu akiingia na kujifungia.
Joram aliduwaa hapo nje kwa muda. Kisha, akajiwashia sigara na kuipachika mdomoni. Kwa mwendo wa utulivu, alivuta hatua moja baada ya nyingine akielekea katika hoteli ya Mawenzi ambako alipanga achukue chumba na kuziifadhi zile pesa. Mengine yangefuata baadaye.
***
Wakati Joram Kiango alipokuwa ameduwaa chooni, Inspekta Kombora alikuwa pia ameduwaa robo kilomita toka hapo. Yeye aliduwaa akiwa ameliegemea gari lake kwa mgongo, katika hali ya kukata tamaa.
Hakutaka kuamini kuwa Kakakuona alimponyoka katikati kabisa ya mtego wake kama samaki katika mdomo wa mamba. Hakupenda kuamini ingawa hali iliashiria hivyo. Upekuzi wa hali ya juu kupita kiasi tayari ulikuwa umefanyika katika jengo zima.
Tayari Kombora alikuwa na malalamiko ya baadhi ya wapangaji hao, mmoja akidai kuwa alilazimishwa kutoka bafuni akiwa uchi,mwingine akidai kuwa kapigwa ngwara bila sababu; watatu wakilalamika kusukumwa na kusachiwa bila maelezo. Halikadhalika, kulikuwa na malalamiko ya kuvunjwa kwa kabati moja ambalo funguo wake ulichelewa kupatikana, kubomolewa kwa tundu la ndege, kuharibiwa kwa mafriji matatu na friza moja; kuchanwa kwa mazulia na mapazia yasiyo na idadi, n.k. yote hayo Kombora alijua yangeletwa kwake kwa maandishi. Hakujali.
Ambacho alijali, ambacho kilimtisha ni kule kutopatikana kwa dalili yoyote ya Kakakuona. Alikuwa ametoweka! Nuru akiwa mikononi mwake! Ni hilo lililomfanya Kombora aduwae, Na kwa mara ya kwanza maishani mwake alijikuta akiwa hajui la kufanya kwa dakika kadhaa.
Alipotanabai kuwa karibu vijana wake wote walikuwa wamerejea na kumzunguka kwa namna ya kusubiri maelekezo zaidi ndipo alipojiinua toka kwenye gari na kupiga hatua mbili tatu za taratibu, huku akiwaza. Mara akagundua kuwa hakujua awaze lipi zaidi. Ndipo ikamjia akilini kuwa alihitaji kupata muda wa kutuliza akili yake ili aweze kuwaza kwa makini zaidi.
“Wanne wabaki hapa na kulilinda jengo hili kwa uangalifu mkubwa kila dakika, kila upande wa nyumba uwe katika macho yenu; mpo?” alisema. “Tupo.” Msaidizi wake wa karibu alijibu
“Vizuri. Nitarudi ofisini kwa muda. Baadaye nitaleta maelekezo mapya. Bado naamini mshenzi huyu yupo humuhumu ndani. Na sitamruhusu aiachie nyumba hii akiwa hai, alisema akigeuka kuliendea gari lake.
“Hayumo mzee, kama angekuwemo hata kama angekuwa amejigeuza sisimizi tungempata. Naamini hayo…” kachero kijana aliyeyasema hayo alilazimika kusita ghafla huku akiulaani ulimi wake baada ya kuona Kombora akimgeukia na kumtupia jicho kali, ambalo lilipenya uso wake na kuunyanyasa moyo wake kiasi cha kumfanya atetemeke miguu, jicho ambalo kamwe hatalisahau.
Kombora alipanda gari na kumwamuru dereva kuelekea ofisini. Lakini kabla dereva hajalitia moto wazo jipya lilimjia. Akashuka garini na kumwita tena sajini Kangua, msaidizi wake wa karibu “Nadhani tunahaja ya kutupia macho majumba ya jirani kabla ya kuendelea na ulinzi wa nyumba hizi. Unasemaje?”
“Wazo zuri afande,” Kanguru alimjibu “Kwasababu kama angekuwa humu ndani kwa vyovyote angekuwa amepatikana.”
Walifuatana kuiendea nyumba iliyokuwa kushoto mwa jengo hilo. Lilikuwa duka kubwa, la Mhindi mmoja aliyenenepa kupita kiasi. Mhindi huyo, ambaye bila shaka yoyote alikuwa anafahamu kuwa kwa jirani kuna jambo, alijizoazoa kwa tabu na kumfuata Kombora kaunta.
“Ndio bana kuba, iko taka nini?”
Kombora alimvuta nje ya wateja na watumishi wake, ambao walitega masikio yao kwa makini ili wasikie kinachoendelea. “Tungependa kuikagua nyumba yako hii.”
“Iko kosa gani? Mimi niko fanya biashara lali bana kuba. Bana Rema iko jua ivo. Iko toa michango mingi. Iko lipa kodi pato. Iko…” alisema huku akitetemeka.
Kombora angeweza kumwacha aropoke hadi mwisho wa maelezo yake, akiwa na hakika kuwa wafanyabiashara hawa hawakosi madhambi. Lakini kwa kuwa hakuwa na nafasi hiyo alimkatiza kwa kumwambia kwa upole, “Hatuna haja na wewe wala biashara zako. Tunataka tuone kama kuna uwezekano wowote wa mtu kupenya toka jengo hilo la jirani yako kupitia hapa kwako.”
“Hakuna mitu pita hapa,” alijitetea
“Tunajua. Lakini tunataka kuwa na hakika,” Kombora alisema akianza kuingia ndani. Mhindi huyo alimzuia kwa kono lake zito lililolowa jasho.
“Hapana taka… Ngoja mimi iko piga simu kwa waziri Rema ulizia yeye. Iko subiri.”
Kauli yake ilipandisha hasira za Kombora. Aliutoa mkono huo kifuani pake kwa pigo moja la kiganjakwa mkono wake wa kushoto. “Sikia,” baadae alifoka huku kamkazia macho makali mhindi huyo, “Ukiendelea kunipotezea muda wangu nitaruhusu vijana wangu ishirini waingie humu na kuipekua nyumba hii. Na nakuhakikishia baada ya dakika ishirini tu utakuwa mahabusu kwa makosa yasiyo na idadi.”
Ukali wa Kombora ulifikisha ujumbe katika kichwa cha Mhindi huyo. Kwa unyonge, huku akijitia kutabasamu, alimpisha Kombora na kumfuata taratibu huku akisema, “Mimi iko mitu mema iko penda saidia…”
Kombora hakumsikiliza alimwita hadi uwani akifuatiwa na msaidizi wake. Huko walikutana na ukuta mnene, mrefu ambao ulikingwa na vipande vya chupa. Kombora hakuona uwezekano wa mtu kuupanda ukuta huo katika muda mfupi kama ule. Akageuka kumtazama msaidizi wake ambaye macho yake yalionekana kuwa na wazo hilohilo.
“Kwa mtu kama Kakakuona ukuta huu unapandika. Lakini apande yeye, ampandishe na mateka wake kwa nguvu, huku akiwa na bastola mkononi sio rahisi.”
Hata hivyo, Kombora na msaidizi wake, bastola zikiwatangulia, walianza ziara ya chumba hadi chumba. Mhindi huyo ambaye tayari alikuwa ameamuru kufunga duka alikuwa akiwafuata nyuma huku akitetemeka na kulalamika kwa maneno mengi ambayo Kombora aliyapuuza.
Karibu kila chumba kilikuwa na vitu mbalimbali vya thamani kubwa kama mashine za kupozea hewa, TV, deki za video, mazulia, nguo na vitu mbalimbali. Kwa jinsi Mhindi huyo alivyokuwa akitetemeka Kombora alijua fika kuwa kama angehoji mengi juu ya vitu hivyo angegundua kuwa nyingi zilikuwa mali za magendo au hazikulipiwa ushuru bandarini, au zimelipiwa nusu n.k. hata hivyo hakuwa na muda huo hadi alipofikia chumba ambacho Mhindi alitetemeka hadi kutokwa na machozi wakati Kombora akimshurutisha kukifungua.
“Iko kupa pesa milioni, sawa?” alibembeleza.
Kombora alimshika ukosi wa shati na kumsukasuka kwa hasira hadi funguo zikamtoka mkononi. Sajin kangua alizidaka na kuufungua mlango huo. Huku bastola ikimtangulia alitangulia kuingia, Kombora akimfuatia, na kumvuta mhindi huyo ambaye baada ya kuona hana hila alijikaza kisabuni na kuendea sefu la chuma lililokuwa katika kona moja ya chumba hicho. Alilifungua na kutoa mabunda ya pesa za kigeni na kumkabidhi Kombora.
“One hundred thousand dollars. Please…”
Kombora alizichukua fedha hizo na kuzikabidhi kwa msaidizi, “Yaani hata benki ya fedha za kigeni unayo katika chumba hikihiki, sio?” alimwuliza “Very well. Suala lako litamalizwa na polisi,” aliongeza akizungumza katika redio call yake na kuombwa aunganishwe na kituo kikuu cha polisi. Kilipopatikana aliwataka kuja kumchukua mtu wao mara moja.
Alipomgeukia Mhindi huyo nusura amhurumie kwa jinsi alivyolowa jasho na mkojo ambao ulikuwa ukimtoka kama mtoto hali mwenyewe hana habari. Kombora alimtazama kwa dharau na kumwacha mikononi mwa kachero wake mmoja kuwasubiri polisi. Kisha, akaongoza kutoka akiifuata nyumba ya upande wa kulia.
Nyumba hiyo haikuwasumbua. Lilikuwa jengo la ofisi ya idara moja ya serikali moja ambayo wafanyakazi wake wote tayari walikuwa wameondoka na kumwacha mlinzi ambaye hakuwa na funguo. Baada ya kutazama Kombora aliona mara moja kuwa Kakakuona hakuwa katika jengo hilo pia. Kuta zilikuwa ndefu, imara, ambazo pia zilipambwa kwa vipande vya chupa.
“Turudi ofisini,” aliamuru kwa sauti ya unyonge.
Nyumba hiyo haikuwasumbua. Lilikuwa jengo la ofisi ya Idara moja ya serikali ambayo wafanyakazi wake wote tayari walikuwa wameondoka na kumwacha mlinzi ambaye hakuwa na funguo. Baada ya kutazama Kombora aliona maramoja kuwa Kakakuona hakuwa ndani ya jengo hilo pia. Kuta zilikuwa ndefu, imara ambazo pia zilipambwa kwa vipande vya chupa. “Turudi ofisini,” aliamuru kwa sauti ya unyonge.
Wakati wakipanda magari yao walipishana na polisi wengi wenye magwanda ambao walikuwa wakimburura Yule Mhindi mwenye duka huku tayari alikuwa ametiwa pingu “Tutawaandikieni ushahidi mdogo tulionao dhidi yake.” Kombora alimwambia kiongozi wao ambaye alikuwa amesimama kwa ukakamavu mbele yake baada ya kupiga saluti ambayo Kombora aliipuuza.
Msafara wa Kombora ulitanguliwa na gari lake. Waliuacha mtaa huo na kuingia barabara ya umoja wa wanawake. Walipopinda kushoto na kuelekea hatua kadhaa Kombora alitupa macho kulia na kuliona jengo ambalo kwake limekuwa kama fumbo la aina yake, fumbo lililomtia aibu na hasira kubwa kwa kushindwa kulifumbua.
Jengo hilo lilionekana nyuma ya jengo jingine la ghorofa mbili lililobeba maandishi yaliyosomeka Kangaroo Enterprises. Kampuni hiyo ilikuwa sambamba mgongo kwa mgongo na Sunrise Modern Club. Hisia zilimfanya Kombora ashuku kuwa inawezekana kabisa Kakakuona alitorokea katika jengo hilo. Akaamuru gari lisimamishwe mara moja. Huku akimwashiria Kanguru kumfuata, alishuka na kuliendea lango la kampuni hiyo.
Mlango ulifunguliwa hata kabla hawajaugusa. Aliyeufungua alikuwa askari aliyevaa magwanda ya mgambo ambayo ilionyesha ni moja ya kazi yake kuwafungulia wageni wote mlango waingiapo na watokapo.
Ilikuwa moja ya zile ofisi nyingi ambazo unaweza kudhidharau kwa nje lakini ndani ukaziogopa. Ndio kwanza Kombora na msaidizi wake wakagundua kuwa walikuwa wamechakaa kwa jasho baada ya kujikuta katika chumba hicho cha mapokezi, chenye vioo kila upande ambavyo viliwafanya wajitazame. Chumba kilikuwa na hewa safi ambayo ilikuwa ikitokea katika vipozea hewa. Mbele yao, nyuma ya meza ya mapokezi kulikuwa na wasichana wazuri watatu. Kushoto kwao kulikuwa na msichana mwingine, nyuma ya ukuta wa kioo, ambaye alikuwa akiendelea kuwachekea huku akisema kwa mara nyingine, “Karibuni kwenye viti.”
Kombora alianza kujiona mpumbavu kwa uamuzi wake wa kuingia humo. Kati yao hakuna aliyeonekana kuwa na wasiwasi wowote juu ya lolote ambalo lilitokea nje ya ofisi hiyo.
Kakakuona hakuwa amepita hapo. Alishawishika kuketi kwenye makochi ya kuvutia chumbani humo, kutokana na uchovu aliokuwa nao.
“Kangaroo Enterprises shughuli zenu hasa ni zipi?” Alimwuliza msichana huyo ambaye alianza kupoteza tabasamu lake kutokana na jinsi alivyomwona mgeni wake.
Kabla ya kujibu msichana huyo aliinama na kuinuka huku mkono wake ukiwa umeshikilia kijitabu chenye kurasa zaidi ya ishirini zilizochapwa kwa rangi mbalimbali ndani na nje. Juu ya kijitabu hicho lilitajwa jina la kampuni hiyo na nenoCatalogue chini yake. Kombora alikipokea na kukididimiza mfukoni mwake. Msichana huyo alipoona hana walau nia ya kukitupia macho alisema kwa sauti ya kibiashara “Tuna fanya mambo mengi, tunajenga viwanda, tunasafirisha watalii, tunaagiza na kuingiza mali nje ya nchi, tuna maduka ya kubadili fedha n.k. Hii ni ofisi kuu hapa nchini. Ni tawi la kampuni ya Kangaroo yenye makao yake makuu nchini Marekani na matawi katika nchi mbalimbali za dunia” msichana huyo alieleza kwa ufasaha. Alipoona maelezo yake hayaelekei kumvutia. Kombora aliongeza harakaharaka.
“Sijui nikusaidie nini mzee wangu?”
“Naweza kumwona bosi wako?” lilikuwa jibu la Kombora
“Bosi huwa hapatikani kwa urahisi, labda ueleze shida yako ili tumwulize kama anahitaji kukuona..”
“Shida yangu ni kumwona yeye!” Kombora alijibu kwa sauti nzito iliyoonyesha madaraka. Alipomwona msichana huyo kaduwaa aligeuka na kuufuata mlango ulioandikwa Mkurugenzi Mkuu.
Akifuatana na msaidizi wake, walipanda ngazi ambazo ziliwachukua hadi ghorofa ya kwanza ambapo walijikuta ndani ya ofisi nyingine iliyojaa watu ambao pia walikuwa katika mishughuliko mingi. Alikuwepo msichana mwingine wa mapokezi. Kwa mshangao wa kombora msichana huyo aliwaelekeza kwa adabu katika chumba kilichoandikwa Mkurugenzi Mtendaji. Nje ya ofisi hiyo kulikuwa na chumba cha kusubiria chenye makochi bora zaidi, ambayo yaliizunguka meza ndogo iliyojaa makabrasha ya kujisomea. Kombora hakuketi. Aligonga mara moja mlango wa mkurugenzi na kisha kuusukuma. Ulifunguka na kumruhusu kuwa ndani ya chumba kipana nadhifu, ambacho kilinukia kila dalili ya pesa. Zulia lililotandikwa hapo sakafuni lingetosha kujenga madarasa matatu ya shule ya msingi, meza kubwa iliyokuwemo ingeweza kuwafanya ombaomba kuwa matajiri kwa miaka mitatu. Viti vilivoizunguka meza hiyo vingewafanya watoto wa mitaani wanane wasahau kuwa hawana wazazi.
Lakini vitu hivyo havikumvuta Kombora kama alivyovutwa na mtu aliyeketi nyuma ya meza hiyo pana akiwatazama. Kombora alitegemea kumkuta Mkurugenzi wa kampuni iliyonona kama hiyokuwa mtu aliyenona, mtu ambaye hakuhitaji kujitambulisha ili umtambue.
Badala yake aliyeketi nyuma ya meza hiyo alikuwa mtu wa kutisha au kutatanisha. Haikuwa rahisi kujua kama alikuwa mzungu au mwafrika kutokana na kovu kubwa jeusi ambalo lilikula nusu ya uso wake, kuharibu jicho lake moja na kuchoma robo tatu ya nywele zake kiasi cha kumfanya awe katikati ya mataifa hayo mawili.
“Yes. Sir what can l do for you?” mwenyeji huyo alimwambia Kombora ambaye tayari alikuwa ameketi mbele ya kimojawapo ya viti hivyo. Kabla hajajibu Kombora alitia mkono mfukoni mwake na kutoa moja ya kadi zake, ambazo humfanya awe na cheo kidogo kuliko kile cheo chake kamili, kile ambacho ni siri yake yeye pamoja na mkuu wa nchi. Meneja huyo alipokea kwa mkono wake wa kushoto, jambo lililomfanya Kombora aamue kuutazama mkono wa kulia na kugundua kuwa ulikuwa wa bandia ambao ulitengenezwa kwa mbao au plastiki kwa ufundi kiasi cha kufanana na ule wa kawaida.
“Vita… vita sio mchezo. Vita vya Angola ndiyo ilinifanya hivi,” alisema ghafla kana kwamba alikuwa akiyafuata macho na mawazo ya Kombora. “ Kwa hiyo wewe ndiyo Inspekta Kombora? Tumekuwa tukizisikia jitihada zako. Hongera sana.”
Kombora hakujua ni jitihada zipi hizo, na huyo bwana alizifahamu vipi, “Sijui na wewe mwenzangu unaitwa nani?” aliuliza badala yake.
“Naitwa Paul Powel. Ni mkurugenzi mwendeshaji wa kampuni hii. Sina budi kushukuru sana kutembelewa na mtu mzito kama wewe.”
Kombora alihisi kitu kama kebehi katika sauti yake. Naam, aliweza hata kuiona waziwazi katika jicho lake moja ambalo lilikuwa likimcheka ingawa mdomo wake ulikuwa hauna tabasamu lolote.
“Vizuri.” Alimjibu kwa utulivu. “Shida yetu ilikuwa ndogo sana. Kuna mtu wa hatari ambaye ametoroka jengo la jirani yenu upande wa pili wa mtaa. Tulichohitaji ni kukagua jengo zima ili tuwe na hakika kuwa hayuko humu ndani.”
Powel alicheka. “Jengo hili haliingiliki hovyo. Tuna biashara ya mamilioni hapa, hivyo tumelijenga kwa usalama wa hali ya juu. Mtu atakayeingia hapa itambidi kupitia mlangoni peke yake…”
“Hilo tunaelewa. Lakini kiutaratibu lazima tuhakikishe kwa macho yetu wenyewe, kwa usalama wenu…” Kombora alilazimika kusita ghafla alipoona pazia lililokuwa nyuma ya Powel likifunuka
taratibu na Powel mwingine kuingia ghafla kama kivuli na kuketi kwenye kiti kilichomuelekea Kombora.
Kombora alimfikiria kama Powel mwingine, kwa jinsi walivyofanana kimaumbile na kimavazi.Yeye pia alikuwa ameungua uso na sehemu mbalimbali za mikono yake. Yeye pia alikuwa na jicho moja, ingawaje lake lililoungua lilikuwa wazi nyuma ya kovu kana kwamba linaona. Badala ya mkono wa bandia yeye alikuwa na mguu mmoja wa mbao. Hilo Kombora aliligundua wakati alipoukunja kwa mikono yake yote miwili pindi akiketi chini, vinginevyo isingekuwa rahisi kugundua.
Powel aliyaona macho ya Kombora yakitembelea uso huu hadi ule kana kwamba yanadai maelezo. Kwa sauti ilelile inayocheka Powel alisema, “Watu wengi wanasema tumefanana. Wengine wanadhani tu mapacha. Lakini wanakosea sana. Hatujafanana hata kidogo. Ukishatuzoea, utagundua kuwa huyu mwenzangu ni mrefu kuliko mimi, mnene kuliko mimi.” Alipoona maelezo hayo hayajamridhisha Kombora aliongeza, “ kinachotufanya tufikiriwe ndugu ni haya masahibu yaliyotukuta, siku moja, saa moja, kwa bomu moja. Ilikuwa tufe pamoja, kwa bahati mungu alitunusuru pamoja. Tungeweza kuwa ombaomba barabarani, lakini mungu ametusaidia vilevile na kutuwezesha kuwa wafanyabiashara wakubwa duniani…”
“Oh kweli anaitwa Philip Benjamin. Yeye ni Mkurugenzi wa Fedha” alimgeukia mwenzake huyo na kumwambia, “Philip, huyu hapa ni Inspekta Kombora bila shaka umepata kumsikia”
Philip alitikisa kichwa kukubali.
Powel aliendelea “Inspekta Kombora anadhani kuna mwizi ambaye amejificha katika jengo hili. Unadhani inawezekana Philip?”
Badala ya kujibu Philip aliangua kicheko. “Unaona Inspekta? Unapoteza muda wako bure.” ITAENDELEA
Kombora alianza kupandwa na hasira juu ya watu hawa. Aliona wazi kuwa ama walikuwa punguani wa akili kama ilivyokuwa kwa baadhi ya viungo vyao, ama walikuwa wakimdhihaki. Akaamua kucheza mchezo waliotaka wao. Aliinuka akawashukuru na kutoka nje huku akihisi kila jicho linaloona, la kila mmoja kati yao, likiwa limemganda mgongoni huku linamcheka.
Alipanda gari na kuamuru liondoke. Baada ya kupinda kona moja alisimamisha gari na kumwamuru kachero mmoja arejee na kutafuta uwezekano wa kuilinda ofisi hiyo kwa makini bila ya yeye mwenyewe kuonekana.
11
Ilikaribia saa kumi na mbili Kombora aliporejea ofisini kwake kama mgonjwa aliyeruhusiwa kutoka hospitali baada ya kukata tamaa ya kuendelea kuishi. Alijibweteka juu ya kiti chake na kujiinamia kwa muda, mikono yake yote miwili ikiwa imekilea kichwa chake.
‘Msichana mzuri, asiye na hatia yuko mikononi mwa muuaji wa hatari, aliwaza kwa uchungu, mbele ya macho yangu mwenyewe jambazi huyohuyo ameua watu wawili wasio na hatia… Na ametoweka…mbele ya macho yangu mwenyewe. Mimi … ambaye najiita mkuu wa kikosi hiki…’ alishindwa kuendelea kufikiri. Hasira zilikuwa zimefura katika kichwa chake kiasi cha kufanya ubongo wake ukitishia kuchemka. ‘Lazima nitunze kichwa changu,’ alinong’ona kimoyomoyo huku akiiitoa mikono yake kichwani na kuipeleka mezani ambako ilirudi na faili ambalo hakulihitaji. Alilitupa mezani hapo na kuiingiza mikono mfukoni ambamo alitoka na kile kijitabu cha maelezo ya kampuni ya Kangaroo. Alikipekuapekua kwa dakika chache kabla hajainua simu na kumpigia mmoja wa wasaidizi wake, ambaye alifika mbele yake mara moja na kupiga saluti ambayo haikujibiwa.
“Fanya kila unaloweza nipate taarifa za kampuni hiyo kabla ya saa mbili,” alimwamuru akimwonyesha kijitabu hicho. “Nataka kujua imeanzishwa lini na wapi, hapa nchini imeingia lini, nani hasa mwenye kampuni hiyo, shughuli zake hasa ni zipi na kila unachoweza kupata. Zaidi, jitahidi nipate kila ambalo linaweza kupatikana juu ya wakurugenzi wake wawili walioko hapa, Paul Powel na Philip Benjamin. Tumia watu wote unaoweza kuwapata. Upo?
“Nipo afande.”
“Haya! Bado unasubiri nini zaidi?”
Amri ya pili ambayo Kombora aliitoa na kumtaka Sajin Kangura mwenyewe kuhakikisha inatekelezwa mara moja ni ile ya kupata ramani ya majengo ya Sunrise Modern Club na Kangaroo Enterprises katika muda wa saa mbili.
“Ni zaidi ya saa mbili sasa, afande. Ofisi ya Ardhi na jiji zitakuwa zimefungwa…”
“Zinaweza kufunguliwa. Kama wanaohusika hawapatikani mtafute waziri wao azifungue. Na kama hana funguo mwambie azivunje.” “Ndiyo, afande.”
Kombora alipobaki peke yake alijaribu tena kukisoma kijitabu cha maelezo ya kampuni ya Kangaroo. Maelezo yalikuwa mengi, marefu yaliyowekwa katika mpangilio ambao ungemfanya msomaji yeyote ahisi kuwa kampuni hiyo ilikuwa moja ya makampuni makubwa sana duniani. Yalitaja matawi yake katikasehemu mbalimbali za dunia. Hata hivyo, ilimshangaza Kombora kuona kuwa anuani za matawi hayo hazikutajwa wala makao makuu, ambayo yalidaiwa kuwa yako New York, Marekani. Hali kadhalika, zaidi ya Powel na Philip, kijitabu hicho hakikuwa na jina jingine la Mkurugenzi yeyote.
Hayo yaliyoongeza mashaka ya Kombora juu ya kampuni hiyo, mashaka ambayo yalianza tangu alipowatia machoni wakurugenzi hao wawili, ambao pamoja na kutojiweza kwao hawakuonekana kuwa na lugha ya biashara hata chembe. Kwa ujumla, Kombora hakuwaona kama wafanyabiashara. ‘Kama wanafanya biashara, lazima biashara hizo zitakuwa haramu,’ aliwaza. ‘Si biashara walizoziorodhesha hapa.’
Kombora alijua ambacho angefanya kesho. Alijua kuwa angehitajika kuwataka msaada polisi wa kimataifa, Interpol, toka nchi zote ambazo Kangaroo ilizitaja kuwa ina matawi yake na kumwomba juu ya uhalali wa makampuni hayo, biashara halisi wanazozifanya na taarifa kamili za wakurugenzi wake.
Hilo lilikuwa la kesho. La leo ambalo lilikuwa likimsumbua Kombora na ambalo lisingesubiri kesho lilikuwa la kumtoa Nuru mikononi mwa Kakakuona, akiwa hai. Alitazama saa yake na kuona ikikaribia moja na nusu usiku; lakini hajapata bado jibu toka kwa watu aliowataarifu kupata taarifa za Kangaroo, jengo lao na lile la Sunrise. ‘Wako wapi hawa’ alinung’una akiinua uso wake kutazama mlangoni.
Juu ya meza yake Kombora alishukuru kuona kuwa mtu mmoja alimwekea chupa ya chai au kahawa na mayai matatu ya kuchemsha. Ndio kwanza akahisi kuwa alikuwa na njaa kali. Akavunja yai moja na kulitafuna. Yai la pili vilevile alilila kavukavu. La tatu ndilo aliloshusha kwa chai nzito ya maziwa toka katika chupa. Baadaye, aliinuka na kuukamilisha mlo wake kwa glasi mbili za maji toka katika friji yake ndogo ya ofisini. Wakati akirudi mezani simu ililia. Kombora aliinyakua na kuidaka masikioni mwake.
“Afande, Kabweka hapa.”
“Najua, uko wapi?”
“Napiga toka bandarini, nilikuwa katika kuhakikisha kama kweli hawa Kangaroo wanaingiza vitu toka nje.”
“Enhe!”
“Ni waingizaji maarufu wa vitu vya nje, Mzee, nimeona mizigo yao mingi ambayo haijatolewa. Nimeambiwa pia kuwa safari hii wamekodi meli mbili. Moja inatarajiwa kuanza kushusha mali zao wakati wowote. Ya pili haijapata nafasi ya kuingia bandarini, imetia nanga nje kidogo ya pwani.”
Hazikuwa habari nzuri sana kwa Kombora. “Ni hayo tu uliyoyapata?” Kombora aliuliza akitaka kuthibitisha kama hakukuwa na habari nzuri zaidi.
“Ndiyo mzee, lakini…”
“Lakini nini?”
“Kuna jambo moja ambalo limenitatanisha.”
“Lipi?”
“Hawa wakurugenzi wake. Idara yetu inayoshughulikia taarifa za wageni haina lolote kabisa juu ya Philip na Powel. Hakuna kinachofahamika zaidi ya kuwa ni raia wa Urusi ambao walikwenda Angola kuwasaidia wazalendo dhidi ya Wareno, wakati walipokuwa wakipigania uhuru wao. Taarifa hizo hazionyeshi maisha yao huko Urusi, waliondoka lini na walikuwa wakipigana kikosi kipi. Zinaonyesha kuwa MPLA tayari wameulizwa juu ya watu hawa na wakashindwa kutoa majibu. Wanasema kwa kuwa watu wengi vitani hupenda kutumia majina ya bandia huenda watu hao walishiriki. Urusi nako, kikosi chao cha KGBkimesema hakina majina hayo katika kumbukumbu zao.”
Kombora alimsikiliza kwa makini, “Kwa hiyo, unawafikiriaje watu hawa, Kabweka?” Kombora alimwambia.
“Nahisi kuna kitu wanaficha na kuna kitu zaidi wanafanya. Inawezekana hawa ni wanachama wa kikundi cha Mafia ambao wanajishughulisha na biashara haramu za dawa za kulevya au nyara za serikali,” alieleza na kuongeza kwa sauti ya kujiamini. “Inawezekana mzee, hawa ni maadui wa Joram Kiango.”
“Ahsante kwa mchango wako. Endelea na usikose kuniarifu kila utakapopata kitu kipya,” Kombora alisema akiitua simu chini.
Papo hapo ikaita tena. Safari hii aliyepiga alikuwa Sajin Kangura. Alikuwa akipiga toka Halmashauri ya jiji. Alimwarifu Kombora habari ambazo zilimsisimua zaidi. “Inashangaza, afande. Si wizara ya Ardhi wala jiji ambao wana nakala ya ramani ya majengo hayo yote mawili.”
“Kwanini?”
“Haieleweki. Jiji wanadai kuwa wana hakika walikuwa na nakala za majengo hayo lakini hawazioni. Hata hivyo, mmoja wa maafisa wa jiji ananieleza kuwa jengo la Sunrise lilikuwa dogo la ghorofa moja lakini liliibuka ghafla na kupanuliwa hata kabla ya kukamilisha taratibu za ujenzi. Kuwa waliingia katika mgogoro na mwenye jengo hilo ambapo baadae ulitatuliwa na akaruhusiwa kundelea.”
“Hamkuweza kumpata mwenye jengo hili awapeni ramani hiyo?” Kombora alimwuliza.
“Yeye pia yalimkuta makubwa,” Kombora aliambiwa “Inadaiwa kuwa huu mwaka wa tatu tangu alipotoweka”
“Katoweka!” “Ndiyo, afande. Tumeambiwa kuwa bwana huyo, Fabian Kalila, ambaye alikuwa maarufu kwa ujenzi mara tu baada ya kukamilisha jengo hilo la Sunrise aliaga siku moja kuwa anakwenda Kigamboni kukagua uwanja mpya ambao ulihitajiwa kujengwa nyumba ya pili. Bwana huyo alifika hadi Ferry ambapo alionekana akizungumza na watu anaofahamiana naye.Watu waliomwona kwa mara ya mwisho walidai alipanda na kwenda ng’ambo. Lakini huko ng’ambo hakuna aliyemwona, yametolewa matangazo magazetini na maredioni lakini hazijafika taarifa zozote juu yake, wala maiti yake.”
“Naam, iko namna,” Kombora aliropoka kwa namna ya mtu anayezungumza peke yake.
Kangura alikuwa akiendelea, “pamoja na hayo, afande, tumefanya upekuzi mkubwa katika makabrasha yake yote, tumeweza kuona karibu nakala za majengo yote aliyowahi kushughulikia isipokuwa hili la Sunrise na Kangaroo. Hatukuweza kupata hata zile za majaribio.”
“Ni yeye aliyeshughulikia jengo lile pia?”
“Ndio, afande”
Kombora hakujua afanye nini zaidi. Alichanganyikiwa kupita kiasi. Kwa ujumla, hakujua kama anakwenda mbele au anarudi nyuma katika suala hilo. Alitua simu chini bila kusema neno lolote zaidi.
***
Mtu mwingine aliyekuwa jengo Fulani mtaa fulani, wa jijini hapo, baada ya kuyasikiliza maongezi hayo ya Kombora na wasaidizi wake aliitua simu yake chini taratibu. Kisha, akakichunguza chombo chake cha kunasia sauti kuona kama kilikuwa kinafanya kazi vizuri.
“Not so bad” alitamka, akitabasamu. Aliitoa kanda hiyo na kuitia mfukoni mwake. Akategesha upya chombo chake na kisha kuondoka zake toka chumbani humo, tabasamu likiwa bado usoni mwake.
***
Mtaa wa tatu toka hapa mtu mwingine alikuwa akitabasamu. Lakini hili lilikuwa tabasamu lake la kwanza kwa siku hiyo, na pengine kwa wiki hiyo. Mtu huyo aliitwa Joram Kiango.
Kama ungemtazama harakaharaka alivyoketi juu ya kochi, ndani ya chumba alichokodi katika hoteli hii ya Mawenzi usingemfikiria kabisa kuwa alikuwa na tatizo kubwa la kutisha ambalo lingetosha kabisa kumtia kichaa. Badala yake ungemwona kijana mtanashati, aliyevaa suti yake nyeusi iliyomkubali vilivyo; akiwa ameketi juu ya kochi pana glasi ya wiski ikiwa mbele yake, sigara mkono mmoja na simu mkono wa pili.
Hali hii ilimrejea joram baada ya kujiaminisha tena na tena kuwa alihitaji kutuliza kichwa chake ili kupambana kikamilifu na janga hilo. ‘wewe ni Joram Kiango’ nafsi yake ilimwambia, ‘Endelea kuwa Joram Kiango vinginevyo Nuru utampoteza na maisha yako yatapotea.’
Hakujali sana juu ya maisha yake lakini alipomkumbuka Nuru na ukatili wa watu wanaomshikilia, alituliza akili yake na kuwa Joram Kiango. Na kwa mshangao wake alikuta akili yake ikichemka kwa ukamilifu kama betri zilizochajiwa upya.
Aliwakumbuka marafiki zake wote, wa nje na ndani. Namba zao za simu teleksi na faksi ziliibuka kama chemichemi akilini mwake. Akiwa na pesa za kutosha haikumchukua muda kukifanya chumba hicho kidogo kigeuke ofisi kubwa ya mawasiliano ambayo yalitoka huku na huko.
Simu yake ya kwanza ilimwendea rafiki yake mmoja anayemiliki kampuni yake binafsi jijini. Huyu akiwa ni mtu ambaye kila kitu kwake ni biashara, alikuwa anafahamu kila mtu na kila kampuni jijini Dar es Salaam. Hivyo, Joram alipomwuliza anafahamu nini juu ya Kangaroo Enterprises rafiki yake aliangua kicheko.
“Vipi? Sioni kama jina hilo linachekesha,” Jorama alimsaliti.
“Sio jina braza, ni pesa” Sauti ilijibu toka upande wa pili.
“Pesa?”
“Pesa hazina macho,” alieleza na kuongeza “pesa, kwa kweli mara nyingine inapotea njia.”
“Sijakuelewa?” Joram alimkumbusha.
“Kwani hujawaona wakurugenzi wa kampuni hiyo?”
“Wakurugenzi gani?”
“Powel na Philip.”
“Wanakasoro gani?”
“Swali sio wana kasoro gani , ila kasoro gani hawana” kicheko “Wale mabwana ukiwaona utafikiri pacha. Wenyewe wanadai hawana undugu wowote. Ukiwaona utadhani ndio kwanza wanaibuka toka kaburini; utafikiri waliwekwa katika pipa wakachemshwa na kisha kutolewa kabla ya kukata roho. Mmoja ni nusu kipofu asiye na mkono wa pili, mwingine nadhani kiziwi na hana mkono mmoja. Kwakweli mabwana wale ni watu wa kuchekesha sana.”
“Sioni wamewezaje kupata pesa,” Joram alichochea.
Baada ya maswali mengi alibaini kuwa kampuni ya Kangaroo Enterprises ni mpya inayoongozwa na watu wasiojiweza, Paul powel na Philip Benjamin. Pamoja na kwamba kampuni hiyo ilidai inajishughulisha na mambo mengi, lakini taarifa alizozipata ni kuwa kazi kubwa ambayo kampuni hiyo imekwishafanya ni uingizaji wa pickup, bidhaa toka nje na kuzisambaza kwa wauzaji mbalimbali wa jumla jijini. Bidhaa yao kubwa, Joram aliarifiwa, ni vipodozi vya aina kwa aina, hasa kwa kina mama.
Alifahamishwa kuwa kampuni hiyo ilijenga maghara yake kando ya barabara ya Nelson Mandela katika eneo la Tabata.
Joram alimshukuru rafiki huyo na kumtaka amwarifu kila atakachokipata juu ya wakurugenzi hao wawili.
Rafiki yake mwingine alikuwa miongoni mwa vijana wa Inspekta Kombora. Kila alipopata wasaa aliwatoroka wenzake na kumdokeza Joram juu ya kila tukio. Alimfahamisha jinsi ambavyo Inspekta Kombora alikuwa taabani baada ya watu wawili wasio na hatia kuuawa mbele yake na Nuru kutoweka mbele ya macho yake. Aidha, alimfahamisha juu ya harakati zote ambazo zilifanyika kulikagua jengo hilo na majengo yote ya jirani bila mafanikio yoyote.
“Sasa hivi ukimwona mzee Kombora utadhani ana umri wa miaka mia moja, kwa jinsi alivyozeeka ghafla,” Rafiki huyo alidokeza katika maongezi hayo.
Baada ya Joram kuuliza kwa makini ukubwa wa jengo la Sunrise Modern Club, Kangaroo Enterprises zilivyojengwa ndani na nje, sehemu ambayo Kakakuona alimwua dereva wa taksi na alipomwua msichana wa mapokezi, na mengine mengi, alipatiwa majibu yote aliyoyahitaji kwa kiwango cha kuridhisha. Maelezo hayo yalifuatwa na onyo, “Joram kama unakusudia kufuata nyayo za Kakakuona, lazima ujihadhari sana. Huyu sio mtu wa kawaida. Mambo aliyoyafanya hapa ambayo nimeyaona kwa macho yangu sio mambo ya kawaida. Labda tunayoona katika filamu baada ya watu wa studio kuweka utaalamu wao. Huyu si binadamu ningekushauri ufikirie mara mbili.” Ni hilo ambalo lilimfanya Joram atabasamu kwa mara ya kwanza siku hiyo. Yalimchekesha mengi. Moja likiwa lile la kujua kuwa nje ya maadui, ni yeye peke yake ambaye alifahamu kuwa Kakakuona hayuko duniani tena. Jingine alipoona rafiki yake huyo asivyomwelewa kikamilifu kwa kumtahadharisha kumfuata Kakakuona. Laiti angejua kuwa alikuwa tayari kumfata hadi kuzimu, na kuhakikisha akirejea na Nuru, akiwa hai au salama! Hata hivyo, Joram alimshukuru rafiki huyo na kumtaka aendelee kuwa macho.
Joram alipata msaada mkubwa zaidi toka kwa rafiki yake mmoja wa kampuni ya simu. Huyu, alimwezesha kupata moja kwa moja mawasiliano yote ya simu yaliyokuwa yakiendelea katika ofisi ya Kombora kwa kuiunganisha na laini moja ya hoteli ambayo Joram aliikodi kwa bei mbaya.
Mawasiliano hayo yalimpunguzia Joram kazi kwa kiasi kikubwa. Hakuhitaji tena kujishughulisha na uraia wa watu hao kwa wakati huo kutokana maongezi baina ya Kombora na msaidizi wake. Hakuwa na haja tena ya kutafuta ramani ya majengo hayo wala ujenzi wake kutokana na taarifa hizohizo. Hali kadhalika, asingepoteza muda wa kutafuta habari za kampuni hiyo huko nje kwani tayari ilionyesha kuwa taarifa zao sio za kweli. Zaidi, Joram hakuwa na wasiwasi juu ya Nuru kuhamishwa toka jengo hilo kwa kujua kuwa vijana wa Kombora walikuwa wakilinda doria na kumtaarifu juu ya kila tukio lililotendeka, taarifa ambazo yeye pia alikuwa akizipata.
Kitu ambacho kwa sasa kilisumbua sana akili ya Joram Kiango kilikuwa kushindwa kuoanisha maelezo juu ya maumbile ya wakurugenzi hao wa Kangaroo na mkasa huu mzima. Kama kweli ni watu wasiojiweza,wenye biashara zao halali, vipi wajihusishe na ujasusi huo wa kimachomacho? Watakuwa wanajiamini nini?
Kitendo chao cha kumteketeza Kakakuona hata kabla hajakamilisha jukumu alilopewa pia lilimtatiza. Kama wangemwua Kakakuona na kisha kumwachia Nuru angeweza kuelewa. Ingekuwa ishara ya kukubali kushindwa. Lakini kumwua Kakakuona, na kuendelea kumshikilia Nuru kwa vyovyote vile ni dalili ya kutangaza shari zaidi, shari ambayo kwa maumbile yao yalivyo, wasingeweza kuitekeleza bila msaada wa mtu mwingine mwenye uwezo na akili timamu zaidi ya Kakakuona.
Joram alihitaji kumfahamu mtu huyo kwa gharama yoyote ile kwani ni yeye tu aliyekuwa kipingamizi baina yake na Nuru. Vinginevyo, angeweza kwenda zake, mchana kweupe, na kumpokonya Nuru toka mikononi mwao.
Simu ililia. Akaipokea na kuisikiliza, kisha akaitua, haikuwa na kitu cha muhimu.
Teksi ikapata uhai. Taarifa ilitoka katika tawi moja wapo la NBC mjini hapo, ilimtajia namba ya akaunti ya Kangaroo Enterprises na kitita cha pesa kilichokuwemo. Kwa kampuni kama hiyo, bilioni moja na nusu si ela nyingi. Kilichomsisimua Joram ni habari kuwa pesa hizo ziliingia toka katika akaunti moja ya mjini New York, Marekani.
Joram aliitazama saa yake. Ilikuwa saa kumi kasoro. Aliandika ujumbe harakaharaka na kuutuma kwa faksi kwenda kwa rafiki yake mmoja mwenye kampuni ya upelelezi wa kujitegemea mjini humo, akimtaka kuichunguza akaunti hiyo kuona ina pesa kiasi gani na nani anamiliki. Ujumbe ulichukua nusu dakika kufika na baadaye kupata jibu ambalo lilimfahamisha kuwa anashughulikiwa.
Nusu saa baadaye alipata majibu ya maswali yake. Benki hiyo haikuwa na akaunti yoyote yenye jina la Kangaroo wala namba zilizotajwa si za benki hiyo.
‘Haya.’ Joram aliwaza baada ya kuisoma faksi hiyo, ambayo pia iliandikwa kwa mkono, kazi ndio kwanza inaanza! Hata hivyo, hilo alikumsumbua sana Joram. Kitendo cha kuficha ukweli wa pesa zao ni jambo la kawaida kwa wafanyabiashara kote duniani. Alipoitazama tena saa yake aligutuka kugundua kuwa imetimia saa tatu za usiku akiwa ameketi kwenye kochi hilohilo. Akiwa si mtu wa kuketi alifurahi kuona usiku umeingia. Kwake giza ni mali, giza ni uhai; hali ambayo alihitaji sana.
Akavuta kabati na kutoa vifaa vyake vyote muhimu alivyokuwa ameviandaa kwa safari yake ya Zanzibar; bastola moja, visu viwili, funguo zake Malaya, bomu moja la mkono alilolitengeneza mwenyewe na vikorokoro vingine vingi. Vyote alivifutika katika mifuko ya siri baada ya hapo alichukua kitita cha pesa na kukifutika mifukoni. Kabla ya kutoka alitegesha chombo cha kupokelea simu ambazo angepigiwa. Wakati akikamilisha kufanya hivyo, simu iliyomwunga na redio call ya Kombora ilipata uhai. Joram akainua chombo cha kusikilizia na kulitegesha sikio lake.
“Ni mimi afande koplo Shomari. Bado nilikuwa nikilinda ofisi ya Kangaroo ninamashaka kuna kitu wanafanya mzee…”
“Kitu gani?”
“Ni sanduku kubwa ambalo linatosha kupakia watu watatu wazima. Sioni kwanini mzigo huo usafirishwe saa hizi…”
“Nisubiri nakuja.” Sauti ya Kombora ilisikika. “Usiache mzigo huo ukupotee machoni. Kadhalika, usiruhusu wajue kuwa unawatazama.”
“Sawa, afande…”
Jibu hilo la mwisho halikumfikia Joram. Alikuwa tayari amekwisha funga mlango na kukimbia hadi nje ambako alimwomba dereva wa teksi bubu moja, aina ya Toyota Corolla, aliyekuwa amepaki nje ya hotel hiyo, amwazime gari. Ili mtu huyo asiwe na shaka Joram alimkabidhi laki tano. “Nikirudisha gari salama laki mbili zako, laki tatu utanirejeshea,” alimwambia baada ya kumwelekeza namba ya chumba chake na kumtajia jina lake la bandia.
Dakika tano baadaye gari hilo likawa limepaki jengo moja toka ilipo ofisi ya Kangaroo, boneti ikiwa imefunguliwa huku dereva wake akihangaika, mara achungulie ndani ya injini mara aingie ndani na kujaribu kuwasha, mara ajitie kulisukuma. Lakini wakati wote huo macho yake yalikuwa yakiangalia kwa umakini kila kinachoendelea katika ofisi hiyo.
Utulivu wake na jinsi alivyokuwa akiitazama saa yake mara kwa mara vilimfanya Joram aanze kuhisi kuwa chochote kilichomo ndani ya sanduku hilo hakikuwa na thamani yoyote kama alivyotarajia. Hakuamini kama Nuru alikuwa ndani ya sanduku hilo. Badala yake alihisi kuwa zilikuwa zinafanyika njama za kuwaita polisi nje ya eneo hilo ili aweze kuhamishwa kwa utulivu zaidi.
Wakati Joram alipokuwa akiwaza hayo, aliona gari ya Inspekta Kombora likifika katika eneo hilo. Lilikuwa Rangerover lenye namba za kiraia. Lilijipitisha katika eneo hilo kama ambalo halina shughuli yoyote na jengo hilo, kwa mwendo wa taratibu na kutokomea mitaani.
Kana kwamba dereva wa pickup yenye ‘mzigo’ alikuwa akisubiri ishara hiyo, aliingia ndani ya gari lake na kulitia moto. Alifuata barabara ya UWT na baadaye kuingia ya Morogoro. Dakika mbili baadaye Joram aliona gari ya Kombora, likiwa na watu wawili zaidi, waliovaa sare za polisi wakilifuata gari hilo.
Joram alisita kabla ya kuamua kulifuata gari hilo au la. Lakini, shingo upande alilifanya gari lake Lionekane kama limepona, akaliwasha na kuyafuata magari ambayo yalikuwa yakitokomea mbele yake.
Saa hizo, magari yakiwa yamepungua barabarani, haikumchukua muda kuyapata magari hayo. Aliacha magari mawili, moja likiwa daladala yamtenganishe na Kombora ambalo lilikuwa nyuma ya ile pickup. Waliipata kariakoo wakaivuka jangwani na kuingia magomeni ambapo pia waliinuka hadi Manzese.
Wakati wakikaribia kiwanda cha urafiki, Joram alimwona Inspekta Kombora akilipita gari hilo na kisha kulisimamisha kwa mkono. Liliposimama yeye na wenzake wawili, bastola zikiwa wazi mikononi, walishuka na kumfuata dereva wa pickup hiyo.
“Una nini ndani ya sanduku…? Joram alimsikia Kombora akiuliza alipokuwa akiwapita taratibu. Asingeweza kusimama hapo. Hivyo, aliwapita kama hatua mia moja na kisha kulisimamisha gari lake kando ya barabara. Huku akijifanya anakagua matairi ya gari, macho yake yalikuwa makini yakitazama kinachoendelea baina ya Inspekta Kombora na dereva wa pick up. Alimwona dereva akishuka na kuzunguka nyuma ya gari. Alihangaika kama anayetaka kulifungua sanduku hilo. Kisha, jambo la ajabu lilitokea. Joram alimwona Inspekta Kombora akipaa angani na kisha kuanguka chini kama mzoga. Alipojaribu kuinuka alipokea kipigo kingine ambacho kilimfanya apepesuke na kurudi chini huku bastola yake ikifyatuka na askari wengine walikuwa wakigalagala chini, mmoja kashikilia mbavu zake, wa pili shingo ikiwa haifanyi kazi.
Tukio hili lilifanyika kwa muda mfupi sana kiasi kwamba ilimchukua Joram Kiango nusu dakika kuelewa kinachotokea. Baada ya hapo alikuwa ameliacha gari lake na kutimka mbio kuelekea eneo la tukio. Alikimbia kwa kunyata kama chui. Alimfikia dereva huyo ghafla na kuachia teke ambalo lilitua tumboni barabara. Dereva huyo alipepesuka na kutokwa na macho ya mshangao. Hata hivyo, Joram aliporusha teke la pili lilidakwa na mguu wake kuanza kupindwa. Alitumia mguu wake wa pili kuruka tiktak ambayo ilimpata barabara dereva huyo usoni na kumfanya aanguke na kumwachia Joram ambaye aliviringika! Waliinuka kwa pamoja na kuanza kunyatiana kwa mwendo wa chui walio mawindoni. Macho yao yalitazamana. Hayakuwa macho ya kawaida. Kila mmoja aliona kitu katika macho ya mwenzie, kitu kisichoelezeka, kinachoonyesha waziwazi wao ni nani katika dunia hiyo.
Joram alihisi kupata kuyaona mahali fulani macho hayo. Macho ambayo yana dalili zote za tamaa ya kuwa kiu ya mauaji. Wapi aliyaona macho haya? Alijiuliza wakati akinyata kutafuta fursa nzuri ya kummaliza adui yake, huku akijua fika adui huyo pia anatafuta nafasi ya kumwua.
Wakati huo kikundi cha wapita njia kilikwisha wazingira, kila mmoja akiwa mdomo wazi kwa mshangao na kutoelewa kinachotukia. Dereva huyo alitazama huko na huko kisha akatia mkono wake mfukoni na kuutoa ukiwa umeshikilia tufe ambalo alilipiga chini kwa nguvu. Papo hapo ulitokea moshi mzito unaowasha zaidi ya bomu la machozi. Joram alilazimika kufumba macho huku akiruka upesi kutoka eneo hilo, kitendo ambacho kilimwokoa na pigo la judo ambalo lingemmaliza. Akiwa ameyafumba macho yake yaliyojaa machozi, huku watu wengi wakilia na kukimbia ovyo, hakuwa na uwezo wa kufanya lolote kuizuia pick up hiyo kuondoka kwa mwendo wa kasi.
‘Ninja’ aliwaza kwa mshangao. ‘Ninja Tanzania!’
Fahamu zilipomrudia Kombora alijikuta kaketi juu ya sakafu hali kaegamia ukuta, wasaidizi wake wawili wamelala chali; kila mmoja akiwa amekilaza kichwa chake juu ya paja lake moja. Walilala kwa utulivu, kila mmoja akiwa amekiacha kinywa wazi na kutokwa na macho nje. Haikimchukua Kombora muda kuelewa kuwa wote wawili walikuwa maiti. Alipatwa na mshituko mkubwa na kukurupuka wima huku akitazama huko na huko.
Ndio kwanza akagundua kuwa alikuwa katika chumba kisichokuwa cha kawaida, chumba kipana chenye kuta za chuma kisicho na mlango wala dirisha. Hewa chumbani humo ilikuwa nzito iliyojaa harufu ya kifo au maiti. Kombora alitazama huko na huko, akitafuta uwezekano wa kutoka katika chumba hicho. Hakuuona. Kwa kila hali, kilionekana chumba madhubuti kilichojengwa chini ya ardhi maalumu kwa ajili ya kumfanyia binadamu unyama.
Akayarudisha macho yake kuwatazama wasaidizi wake ambao sasa walikuwa marehemu. Kila dalili ilionyesha kuwa walikufa baada ya mateso makubwa ya kinyama. Mmoja alikuwa kavunjika shingo, jambo ambalo lilimfanya alale kama mzoga wa mbuzi. Na wa pili alikuwa na jeraha kubwa kifuani, ambalo lilionyesha kitu kigumu kilipenya humo na kuzifumua figo zake.
Kombora aliitazama saa yake. Dakika arobaini tu zilikuwa zimepita toka alipotoka ofisini kwake kufuata wito wa Koplo Shomari, ambaye sasa ni marehemu, ikimwarifu juu ya sanduku lililokuwa likisafirishwa toka ofisi Ya Kangaroo. Tayari watu wawili ni marehemu hali yeye akiwa hai kwa fadhila au kebehi ya wauaji hawa. ‘Kwanini hawakumwua yeye pia? ’ kwa nini?’ alifoka kimoyomoyo akitembea huku na huko chumbani humo kwa uchungu. Hasira zilianza kumpanda zikamfanya asahau hofu aliyonayo juu ya maisha yake na kujikuta akijenga chuki kwa yeyote Yule aliyekuwa akimtendea haya. Alitamani ampate papo hapo, amchanechane kwa mikono yake na kuacha viungo vyake vikiliwa na fisi.
Hasira zilikuwa zikimcheka kichwani mwa Kombora, hasa zikisababishwa na unyama wa binadamu huyu ambaye hakuwa na shaka ni Kakakuona mwenyewe; bali jinsi alivyoufanya unyama wake mbele ya macho yake, hadharani, kana kwamba Kombora hakuwa lolote wala chochote mbele yake. Yeye, ambaye historia ya Tanzania na dunia kwa ujumla haitamsahau kwa mengi aliyoyatenda kuifanya serikali iendelee kuwepo na amani izidi kutawala nchini! Yeye ambaye jina lake tu lilikuwa sumu kali kwa yeyote aliyekuwa na ndoto za kuidhuru Tanzania!
Kamwe asingejisamehe kwa tukio hili la leo ambalo lilimfanya atoke ofisini bila kuaga, na kujikuta akisindikiza mzigo ambao hakujua ni wa nini. Asingejisamehe kuruhusu dereva wa pick up hiyo atoke nje na kuwazubaisha kwa maelezo marefu ya kebehi na mara ageuke kama chui ambaye alipaa angani na kuanza kuwachalaza kwa kong fu, judo na kareti kwa namna ambayo Kombora na umri wake wote katika ukachero hakupata kuiona.
Ilikuwa kama hadithi ambazo hutokea katika michezo ya sinema. Dakika moja walikuwa wima wakizungumza naye, dakika ya pili walikuwa wakigalagala chini kwa maumivu yasiyosemeka. Kwa mbali, kama ndoto, Kombora alihisi kumwona mtu mwingine akipambana kwa kiwango kama kilekile, kana kwamba hayati Bruce Lee amefufuka na anafanya vitu vyake. Lakini tukio au ndoto hiyo ilitoweka ghafla kwa mlio wa kutisha uliofuatwa na moshi mzito unaowasha, ambao ulimfanya Kombora aishiwe nguvu kabisa. Hakuwa na la kufanya wakati alipobebwana kutupiwa nyuma ya gari kama mzoga.
Wala hakuwa na neno alipohisi akinukishwa kitu fulani ambacho kilimfanya apoteze kabisa nusu ya fahamu alizobaki nazo. Na zilipomrudia ndipo alijikuta kaegemea ukutani. Maiti za vijana wake zikiwa zimelazwa juu ya mapaja yake kwa namna ya kumdhihaki.
‘Nitalipa kisasi’ kosa moja wamefanya kuniacha hai. Kwa vyovyote watalijutia.’
Wakati akiwaza hayo, alikuwa akitembea huko na huko kukikagua chumba hicho. Alikuwa na hakika kuwa kina mlango na dirisha, vinginevyo wao wasingeingizwa chumbani humu. Alikagua kwa makini kila sentimita ya chumba hicho. Haikumchukua muda kugundua sehemu aliyotaka. Nusu ya ukuta huo ulikuwa pande zito la chuma ambalo lilionekana kama mlango. Hata hivyo ilikuwa dhahiri kuwa lango hilo lilifunguliwa kwa umeme, toka nje ya chumba hicho.
‘Watafungua tu na watanikuta tayari nikiwasubiri.’ Kombora aliwaza akiupeleka mkono wake kuitafuta bastola kama alivyotegemea ilikuwa tayari imetoweka. ‘No problem, nitawasubiri na kupambana nao hata kwa meno.’
Mara taa ya umeme iliyokuwa inawaka chumbani humo ilizimwa, likafuata giza nene la kutisha. Kisha, ziliwashwa taa nyingi zaidi zenye Nuru kali kuliko giza lililokuwemo. Nuru hiyo ikafuatwa na joto kali ambalo dakika moja baadae lilimfanya Inspekta Kombora aanze kutapatapa huku tayari ameloa jasho.
“Karibu sana Inspekta Kombora’ sauti nzito ambayo haijulikani inapotokea, ilitamka ghafla kwa kiingereza. “Karibu kwetu. Karibu katika chumba cha mauti. Hajawahi binadamu yeyote kuingia humo akiwa hai na kutoka hai”
Sauti ikafuatiwa na kicheko ambacho binadamu yeyote asingekiita kicheko kwa jinsi kilivyokuwa hakina hisia zozote za binadamu.
Haikuwa sauti ngeni kwa Kombora. Wala Kombora hakuhitaji kufikiri sana ili kukumbuka alipata kuisikia wapi. Ilikuwa sauti ya mmoja kati ya wale wakurugenzi wawili wa Kangaroo, Paul na Philip.
“Nilijua kitambo kuwa mna kasoro fulani akilini mwenu” Kombora alifoka bila kujua kama anasikika au la. ‘Kama mlivyo na kasoro katika miili yenu.’ Alitamani kuongeza kwa hasira lakini hakufanya hivyo. Badala yake alisema “Kwahiyo mtindo wenu ndio huu, wa uoga na kujificha nyuma ya ukuta ndipo muweze kumkabili binadamu? Ni hili ambalo pia mmelifanya kwa msichana wa watu asiye na hatia.”
Kicheko kingine kibaya kilifuata. Kikafuatwa na sauti ileile ikisema, “Hatujifichi Inspekta, hatuna haraka ya kuonana nawe, kwa ujumla hatukuhitaji sana. Orodha yetu ilikuwa na watu wawili tu katika Tanzania. Wewe umejilazimisha na kuwa wa tatu. Hivyo, bado mmoja, Yule kijana mtukutu ambaye nyie mnamwita Joram Kiango. Baada ya muda mfupi tutakuwa naye hapa. Na hapo ndipo tutaanza kufanya vitu vyetu ambavyo mtavishuhudia kwa macho yenu wenyewe.”
“Mnataka kufanya nini?” Kombora hakustahimili kuuliza. Kicheko kingine cha kebehi kikafuata.
“Usiwe na haraka Inspekta. Uko hapa utajionea mwenyewe. Kwanza, lazima ujihesabu kama mtu mwenye bahati kuwa hai hadi sasa hivi. Ungeweza kuwa marehemu kama hao kuku wenzako waliolala hapo. Kwa bahati, bado tunakuhitaji. Tunahitaji uwe shahidi, uone kwa macho yako mwenyewe kile ambacho kitatokea nchi yako. Baada ya hapo utakufa kwa amani utapumzika kuzimu hali ukiwa na picha halisi akilini mwako, picha ya kupendeza ambayo kamwe haitafutika akilini mwako.”
Kombora hakuweza kumsikia vizuri. Joto kali lilimzidi kimo na kumfanya aanze kutapatapa kama samaki anayekaangwa akiwa hai. Aliruka huko na huko akiyavua magwanda yake, mishipa ya fahamu ikikaribia kupasuka, macho yake yalipoteza nuru na kizunguzungu kumshika ghafla. Polepole alijikuta akiteleza na kuanguka sakafuni, kando ya maiti ya vijana wale. ***
“Twende huku, ukamwone hawara yako mwingine aliyekuja kukusalimu,” Nuru aliamrishwa akiinuliwa toka sakafuni alipojibweteka na kusukumwa kama mzigo.
Mikono iliyomwinua toka sakafuni hapo ilikuwa mikakamavu yenye nguvu kama chuma. Hakuwa na hali ya kupingana nayo ingawa moyo wake ulimtaka sana kufanya hivyo. Mwili wake haukuwa na uwezo wala akili yake hakuiona kama ilifanya kazi kwa kiwango chake. Kwa ujumla alijiona kama kondoo au zezeta lililokuwa tayari kufuata amri yoyote ambayo alipewa na viumbe hawa wawili, amri yoyote ile; hata kama ingekuwa kujitumbukiza mwenyewe katika shimo ambalo lingempeleka moja kwa moja hadi kuzimu.
Kitu kimoja Nuru alikuwa na hakika nacho. Ukondoo au uzezeta haukumjia hivihivi kutokana na ukatili usioelezeka ambao aliushuhudia kwa macho yake mwenyewe ukifanywa na Kakakuona mbele yake, la hasha! Aliamini kabisa kuwa uzezeta huu ulitokana na sindano alizokuwa akichomwa mara kwa mara zilimfanya apoteze fahamu na zilipomrejea akajikuta mzembe akilini na mwilini kiasi cha hata kuwa mvivu na kukumbuka yote yaliyomtokea.
Kwa namna ya ndoto tu, alikumbuka yaliyomtukia kisiwani mara moja tu Joram alipoondoka. Alikumbuka jitihada zake ambazo zilisababisha vifo vya watu wawili kati ya wale waliokuja kumkamata, lakini waliobaki wakafanikiwa kumteka nyara. Alikumbuka alivyopelekwa Zanzibar na chongo kumwua mwenzie na kisha yeye mwenyewe kuuwawa. Alikumbuka pia kuwa mwenyenyumba Banduka, alivyouawa na kufichwa na Kakakuona ambaye alimrejesha Dar Es Salaam kwa mtutu wa bastola huku watu waliosafiri nao wakiwa hawana habari. Na alikumbuka alivyofika forodhani na kumwona Joram Kiango akiwa katika mavazi bandia yaliyomfanya asifahamike na yeyote zaidi yake.
Matukio ya kutisha zaidi, ambayo Nuru aliyakumbuka kama mabaya zaidi ni yale ya kuuawa kwa dereva wa teksi na msichana wa mapokezi, hadharani, mbele yake bila ya yeye kuwa na uwezo wa kufanya lolote. Mkono wake ambao aliutia haraka katikati ya miguu yake ili kuichukua bastola yake mbayo alikuwa ameificha mahali hapo, haukuweza kutoka na silaha hiyo kama alivyokusudia kwani ni wakati huohuo alipopigwa kitako cha bastola kilichomfanya azirai na kupokonywa bastola hiyo.
Na alipozinduka ndipo akajikuta katika chumba hiki, ambacho kwa kila hali, kilionekana kuwa kilichojengwa chini ya ardhi, maalum kwaajili ya kufanyia maasi au maovu. Na baada ya hapo ndipo alipoanza kudungwa sindano zilizomlewesha na kumpumbaza hata akawa hajiwezi, hajitambui. Kila dawa hizo zilipoisha nguvu alidungwa tena, jambo ambalo lilimfanya awe taabani daima.
Wakati akiwa taabani, kama ndoto vilevile, Nuru aliwaona watu wawili wenye maumbo ya ajabu wakimjia na kumtazama kwa muda mrefu. Mara mbili tatu watu hao walimvua nguo na kumchezea matiti na sehemu zake za siri kwa vidole vyao vikavu. Mara moja mmoja wao alijaribu kumnajisi, lakini Nuru alihisi kuwa alishindwa kwani hakuuhisi uume wake mwilini mwake. Hata hivyo waliendelea kumchezea wakifurahia kila kitendo chao.
Nuru alihisi kupata kuwaona watu hawa, lakini hakumbuki wapi. Watu wasiojiweza, wasio na viungo kamili, wanaoonekana kama walipata kutupwa katika tanuru la moto na kisha kutolewa kabla hawajateketea kabisa; aliwaona wapi? Mara kwa mara aliituma akili yake nzito kumfahamisha, lakini nayo haikuwa na jibu. Hivyo, alijikuta akiamua kuamini kuwa hakuna mahala popote ambapo aliwaona isipokuwa usingizini, katika moja ya zile ndoto zake mbaya ambazo humtokea binadamu mara chache katika maisha yake; ndoto za viumbe wa ajabuajabu wanaotisha ambao humwandama mtu usingizini na kumfanya aamke huku akitweta, jasho likiwa limemjaa mwilini tepetepe.
Kitu kikubwa kilichoisumbua zaidi akili iliyodumaa ya Nuru ni dawa hizo alizokuwa akilazimishwa kutumia. Baada ya kudungwa mara tatu alihisi mwili wake ukizitamani na kutaka apewe mara kwa mara. Ni jitihada kubwa sana zilizomfanya asitamke kwa sauti, kuomba tena au kuzidishiwa
Hili lilimtisha sana kwani alijua fika kuwa anachotumia ni kitu hatari kwa maisha ya binadamu. Kama haikuwa Cocaine basi ilikuwa Heroine au Mandrax. Hakuwa mtaalamu sana katika masuala ya madawa ya kulevya, lakini hicho kidogo alichofahamu kilimfanya aelewe kuwa alikuwa katika hatari kubwa wa kuwa teja wa dawa hizo, jambo ambalo lingemfanya apoteze akili, afya na hata uhai wake.
“Nimekwambia inuka, nenda kule ukamwone hawara yako mwingine,” sauti ilimwamrisha tena Nuru akizidi kusukumwa kwenda mbele. Msemaji alikuwa akizungumza kiingereza.
Macho ya Nuru yalikuwa mazito kufunguka. Lakini alitumia akili yake kufikiri sauti hiyo. Haikuwa sauti ya Kakakuona. Ilikuwa sauti ya mtu mwingine. Hata lafudhi yake haikuwa ya Kiafrika. Nuru alihisi kuwa msemaji alikuwa Mjapan au Mchina. Akajilazimisha kufungua macho yake. Kwa taabu, aliweza kumwona mtu huyo. Alikuwa mrefu mwenye kifua cha simba ingawa alitembea kwa kunyata kama chui aliye mawindoni.
Nuru hakujisumbua kuwaza uwezo wa kupambana naye. Hali haikumruhusu. Hivyo, aliruhusu kusagwa kikondoo hadi katika chumba kingine ambacho kilifunguka baada ya mtu huyo kubonyeza tufe la umeme na sehemu ya ukuta huo kumeguka. Alisukumwa chumbani humo na kujikuta ameangukia mwili wa mtu mnene, wa makamo ambaye Nuru alimtambua mara moja.
“Inspekta Kombora.’ Alinong’ona. Sauti haikutoka. Kando ya Inspekta huyo ambaye alilala nusu uchi, baada ya kuitupa suruali na shati yake huku na huko kupunguza joto kali ambalo lilimfanya azirai, Nuru aliona miili ya watu wawili ambao hakuhitaji kuambiwa kuwa wamekufa.
Hakushituka. Wala hakushangaa. Alikwisha vuka kiwango hicho.
***
Kwa Joram Kiango, ulikuwa usiku mfupi kuliko matarajio yake. Angependa sana uwe mrefu zaidi. Usimame, kama Biblia inavyodai jua lilisimama wakati Waisrael wakiwateketeza wapalestina ili waweze kushinda vita vile ambavyo viliwawezesha kuichukua nchi ya Ahadi. Lakini Joram hakuwa na bahati hiyo. Alipoitazama saa yake ilimwambia kuwa ilikwishatimia kumi na robo za usiku. Alihitaji saa sita zaidi ya kiza ili aweze kukamilisha awamu ya pili ya kazi yake.
Awamu ya kwanza alihisi kuwa ameitimiza. Ilikuwa kumtia adui jeraha la moyo ili naye apate uchungu na kuanza kutapatapa, kama ambavyo adui huyo aliamini Joram anatapatapa, kwa kuteketeza watu wasio na hatia, kumteka Nuru na hatimaye Inspekta Kombora.
“jeraha” ambalo litausononesha moyo wa adui huyo ni pale alipoamua kuteketeza maghala yake yote ambayo yalikuwa na mali ya mamilioni ya pesa za kigeni. Joram alihakikisha kila kitu kinateketea na kuwa jivu kwa moto aliouanzisha.
Hatua ya kutenda kitendo hicho, ambacho kilikuwa kinyume na desturi yake, Joram aliichukua ghafla mara baada ya tukio la saa chache zilizopita Barabara ya Morogoro.
Akiwa taabani kwa maumivu ya Moshi ule, ambao ulipenya hata kooni na kukwaruza, Joram alifanya haraka kukimbilia nyumba za jirani ambako aliomba maji na kunawa. Wakati akiondoka eneo hilo, alisikia kishindo cha watu waliozolewa na kutupwa katika pick up, na kisha kusikia ikiondoka kasi. Hakuwa na uwezo wa kufanya lolote.
Baada ya kunawa na macho yake kurudia hali ya kawaida alilirudia gari lake huku akipishana na watu waliokuwa wakitapatapa, baadhi yao wakipiga mayowe kwa maumivu na taharuki. Alilitia moto gari lake na kuifuata njia hiyohiyo ya Morogoro hadi alipofika ubungo ambako alipinda kushoto na kufuata barabara ya Mandela. Haikumchukua zaidi ya dakika kumi kabla hajaona kibao ambacho kiliashiria kuwa ameyafikia maghala ya kiwanda hicho.
Alisimamisha gari lake toka hatua kadhaa toka kibao hicho. Kisha, akavuka barabara kuyafuata majengo hayo ambayo toka hapo alipokuwa aliyaona kuwa yalikuwa makubwa kuliko alivyotegemea, alipoyafikia, kama alivyotegemea, alikutana na ukuta mkubwa uliyoyazunguka. Mbele ya ukuta huo kulikuwa na lango kubwa la chuma ambalo lililindwa na watu wawili waliovaa mavazi ya Jeshi la Mgambo. Joram alisita kwa muda akiwatazama. Tangu alipoipata safari hii, hata kabla hajaamua kuifuata pick up ambayo iliwatorosha Kombora na wasaidizi wake, Joram alijua kuwa ingekuwa safari ya hatari. Alikuwa na kila hakika kuwa viumbe wale, kwa mujibu wa maelezo aliyoyapokea toka pande zote, hawakuwa watu wa kawaida na hivyo hawakuwa wakifanya biashara za kawaida. Hivyo, dhamiri yake kuu ilikuwa kuikagua biashara hiyo ili aelewe kabla ya kuwakabili viumbe wenyewe.
Hali kadhalika, alikuwa na mashaka kuwa mabohari hayo yalitumiwa kuficha maovu yao mengi, ambayo yaliwafanya wajiamini na kufanya maovu yao kwa dharau, bila hofu wala wasiwasi wowote. Kwa ujumla, licha ya biashara haramu kama dawa za kulevya au nyara za serikali, Joram alitegemea maghala hayo kuwa maficho ya kikosi cha mauaji ambayo yalikuwa yakiendelea nchini. Na alijiandaa kwa hilo.
Ambacho hakujiandaa nacho ni kukutana na ninja. Kamwe hakutarajia kuwa watu hao, ambao pamoja na ukatili wao walionekana wapuuzi, wangefikia hatua ya kumleta ninja nchini, ili waweze kufanikisha adhma yao.
Sio kwamba Joram alimwogopa ninja. Kinyume na watu wengi yeye alifahamu kuwa ninja ni binadamu kama binadamu wengine. Kilichowapa umaarufu, licha ya ukatili wao, ni upya wa taaluma yao machoni mwa watu kiasi cha watu kuondokea kudhani kuwa ninja ni zaidi ya kuwa binadamu wa kawaida.
Joram hakuwa ninja, lakini taaluma ya uninja iliiva kichwani mwake sawa na ninja yeyote yule. Alichokosa ni Master ambaye angeweza kumtangaza U-ninja kwa kumpa baraka ambazo angeambatana nazo maishani.
Lakini hilo halikumsumbua hata chembe. Kwa kiwango chake, baada ya visa na mikasa yote iliyomkumba wakati akiishi nchini Marekani, hakuhitaji mwalimu ambaye angemtangaza rasmi kwani hakuwa katika kikundi chochote wala ukoo wowote ambao ulihitaji kumkubali au kumkataa.
Joram aliipata taaluma ya u-ninja kwa gharama ya sehemu kubwa ya jasho na damu yake, nusura imgharimu roho yake. Alianza kwa kujiunga na vyuo vidogovidogo vya kareti na judo, ambavyo wakati huo vilienea sana nchini Marekani. Jitihada zake kubwa zilifanya apendwe na walimu wake ambao baada ya kumfundisha kila walichojua walipendekeza vyuo vingine hadi alipojikuta katika chuo kile ambacho kilikuwa kikifundishwa na hayati Bruce Lee mwenyewe.
Joram alikuwa mtoto mweusi pekee katika darasa hilo. Lakini jitihada zake na uwezo wake wa kuzingatia kila alichofundishwa kilimfanya awe kipenzi cha hayati huyo, jambo lililomfanya achukiwe na wanafunzi wenzake wote shuleni hapo.
Kifo cha kutatanisha cha hayati Bruce Lee kilipotokea, Joram alihisi kama aliyepotelewa na baba au kaka yake wa damu. Alikosa raha kwa siku kadhaa. Baada ya msiba alijaribu kutafuta chuo kingine ambacho kingemfaa, lakini alijikuta akipoteza muda wake bure kutokana na jinsi mbavyo alijiona amevuka kiwango cha mafunzo mengi yaliyotolewa kitaaluma na kivitendo. Hivyo, mafunzo mengi kwake ilikuwa kujikumbushia tu.
Hali hiyo ilimwongezea uadui hata miongoni mwa walimu. Wako walimu wa Kichina na Kijapan ambao waliamini kuwa taaluma hiyo ni maalumu kwa ajili yao tu. Hivyo, hawakuona haki ya mgeni kuifahamu kama wao au zaidi ya wao. Na wamarekani hawakuona haja ya mtu mweusi kutamba mbele yao. Hivyo, kila ilipotokea nafasi, Joram alijikuta akiingia katika ugomvi ambao hakuujua chanzo chake. Lakini aliibuka mshindi katika kila tukio. Baadaye walianza kumshambulia katika vikundi. Bado mara kwa mara Joram alivisambaratisha au kutoroka bila matarajio yao.
Lakini ilitokea jioni ya siku moja, akiwa katika viwanja vya mazoezi peke yake, Joram alijiwa na mtu aliyevaa mavazi meusi kiasi cha kufunika mwili mzima isipokuwa macho tu. Alikuwa akitembea harakaharaka lakini kwa kunyata kama kivuli. Joram hakuitaji kuambiwa kuwa alitembelewa na ninja. Alikwisha soma habari zao katika vitabu vingi, ingawa hakupata kukutana ana kwa ana.
“Joram Kiango?” mgeni huyo alimwuliza.
“Kama ndiye?” Joram alimjibu kwa swali jingine.
Mgeni huyo alimtazama toka miguuni hadi utosini. Akaonyesha kuridhika na alichokiona, “Nimekuwa nikizisikia sifa zako. Nimekuja nione kama ninachokisikia ni kweli. Uko tayari?”
Joram hakuwai kukataa kupambana na mtu yeyote, hasa anapoonyesha shahuku ya kumjaribu kama huyo. Alimkubalia na kujiandaa. Adui yake alimtazama kisha akaanza kunyata huku na huku, kabla hajapata fursa ya kuachia pigo ambalo lilikingwa na Joram kirahisi. Pigo hilo lilikuwa kama la kumzindua tu kwani wakati huohuo alifyatuliwa miguu kwa namna ambayo hakuitegemea na kujikuta akiviringika. Mara tu alipoinuka alifyatuliwa tena. Wakati huohuo akiwa amekwisha jiandaa alianguka hali akiachia teke ambalo lilimpata adui yake tumboni na kumfanya apepesuke. Aliviringika toka sakafuni hapo na kumfuata adui yake ambaye aliruka na kudaka miti ya mazoezi ambayo aliitumia kukimbia kwa mikono kama nyani. Wakati Joram akiwa ameduwaa kwa hilo adui huyo alichupa hewani kama chui na kutua juu ya kifua chake.
Kilichofuata ni kitu ambacho Joram hatokisahau hadi leo. Vipigo vilimnyeshea kama mvua. Hakupata fursa kujitetea kwani alipouinua mkono wake ulikuwa hauna kazi, hauna nguvu. Walimwokota hapo, dakika ishirini baadaye, walimpeleka hospitali moja kwa moja, ambako alipimwa na kugundulika kuwa alivunjika mkono, mbavu tatu na kuteguka mguu.
Alikaa hospitali mwezi mmoja. Aliporuhusiwa kutoka, hata kabla ya POP halijaondolewa alianza mazoezi. Na mara lilipoondolewa, wiki tatu baadaye, alikuwa safarini toka mjini Washington kuelekea mjini Carfornia ambako alisikia kuna mwalimu wa kichina aliyekuwa akitoa mafunzo ya U-ninja kwa “wateule” wachache aliodhani kuwa wanafaa. Joram aliondoka bila kuwaaga wazazi wake ambao walipinga hatua yake ya kujihusisha na mambo hayo.
Ilimchukua wiki nzima kugundua kilipojificha. Chuo hicho kilikuwa katika moja ya misitu mikubwa iliyokuwa haijaanza kutumika ya mtengenezaji mmoja mashuhuri wa filamu katika mji wa Hollywood. Chuo hicho kilikuwa kinaongozwa na mzee mmoja mfupi, mnene mwenye upara uliomeza robo tatu ya kichwa chake. Mzee huyo alimtazama Joram kwa macho yaliyojaa chuki na dharau dakika mbili nzima kabla ya kumjibu kwa swali, “alikuambia nani kuwa nafundisha taaluma hiyo? Na hata kama, nitamfundishaje panya mchezo wa paka?”
Joram alitumia hekima yake kubembeleza na kusihi hadi alipoona mwalimu huyo akianza kumsikiliza kwa makini “Unadhani unafahamu nini juu ya taaluma hii?” mwalimu huyo aliuliza.
“Sifahamu chochote”
“Kwa hiyo, unifahi, sifundishi watu mbumbumbu.”
Joram alipozidi kumbembeleza mzee huyo alipiga makofi. Mara miti iliyokuwa imeenea eneo hilo ikapata uhai. Zaidi ya vijana sita, ambao Joram hakujua kuwa walijificha juu ya matawi hayo wakimtazama, waliruka na kutua chini wakiwa wamemweka kati. Joram alimfahamu mmoja wao. Alikuwa Yule ambaye majuzi tu alimfanya alazwe hospitali kwa mara ya kwanza maishani mwake.
“Niondoleeni mbele yangu hii takataka” mwalimu huyo aliamrisha.
Mara vijana hao wakageuka mbogo. Kwa pamoja walimvamia joram na kuanza kumshambulia. Akijua kuwa huu ulikuwa mtihani mbele ya mkufunzi huyo Joram alichachamaa na kupigana kwa nguvu zake zote na moyo wake wote. Dakika mbili baadaye watatu kati ya hao walikuwa wakigaragara chini, hawajitambui. Joram mweyewe akiwa taabani, lakini hakukubali kushindwa. Muda si mrefu aliwatupa wawili wengine na kujikuta amebakiwa ana kwa ana na yule mkuu. Wote walitweta kama majogoo yanayoogopana baada ya Joram kuikwepa kila hila iliyofanywa na kijana huyo.
“Inatosha.” Mkufunzi huyo alisimamisha pambano, uso wake ukionyesha kufurahishwa sana na alichokiona “Pumzikeni, kesho tutaangalia ambacho tunaweza kufanya kwa mgeni wetu huyo machachari.”
Joram aliliona jicho la chuki likimtazama toka kwa kijana huyo. Kesho yake, bila ya mwalimu huyo kujua chuki baina yao bado alimkabidhi Joram kwa kijana huyo ili ampe zoezi kabla hajaanza kumfundisha mwenyewe.
Kijana huyo ambaye baadaye Joram alifahamu kuwa anaitwa Adrian, mchina aliyechanganyika na Mmarekani, aliondokea kuwa mwalimu, hasa kwa Joram. Kutwa nzima ambayo alimchukua porini alimtesa kwa kumpa adhabu za kutisha, huku akitamba kwa kumwonyesha Joram ujuzi wake katika hila ambazo wengi hudhani ni mazingaombwe, mbinu za kuruka ambazo wengi hudhani ni miujiza, kuparamia miti ambako baadhi wanafikiri ni uwezo utokanao na mitishamba, kuzua moshi ambako hata Joram alidhani ni uchawi n.k.
Yote hayo Adrian aliyafanya kwa kujisifu, kwa nia ya kumwonyesha Joram kuwa hajui kitu. Lakini hakujua kiasi gani Joram alikuwa akiyafuatilia yote hayo na kuyachora katika ubongo wake.
Jioni moja Master alitangaza mwenyewe kuwa angeanza kumfundisha Joram. Usiku huohuo Adrian alimnong’oneza Joram, “Hii sio taaluma ya nyani weusi. Kesho alfajiri ondoka urudi kwenu. Ukiendelea kukaa hapa mpaka jioni nitakuua.”
Joram alimpuuza lakini kilichotokea mchana huo kilimfanya aamini kuwa Adrian hakuwa na mzaha. Mwalimu alikuwa amekwenda nje ya kambi na kuwataka waendelee na mazoezi. Adrian alimwita Joram na kumtaka amfuate ili amwonyeshe kitu ambacho hakupata kukiona huko nyuma. Walipofika katikati ya kichaka, Adrian ghafla aligeuka mbogo na kuanza kumshambulia Joram. Mapigo yake yote yaliashiria kuua. Kwa bahati mbaya hakujua Joram amejizatiti kiasi gani. Baada ya dakika arobaini za mapambano, Joram alikuwa amelowa jasho na damu, mkono wake mmoja ukiwa haujiwezi. Lakini Adrian alikuwa chini, chali, nusu maiti.
Joram alijikongoja na kumburuza hadi kambini ambako alikutana na macho makali ya Master akimsubiri kwa ukali.
“Wewe ni mnyama. Huyu ni mwanangu, mwanangu wa pekee. Tazama ulivyomfanya! Sasa nakuamuru uondoke mara moja katika kambi yangu. Ukiendelea kukaa, dakika moja zaidi nitakuua kwa mikono yangu mwenyewe.”
Joram hakuwa na hili wala lile zaidi ya kuondoka.
***
Naam, Joram hakuwa mgeni wa maninja. Hata hivyo, kitendo cha ninja huyo kumdhihaki na kuondoka na mtu mkubwa kamaa Inspekta Kombora mbele ya macho yake, kilimwongezea hasira na kumpa ari ya kuteketeza bidhaa hizo bila huruma.
Wale walinzi wawili waliovaa mavazi ya mgambo hawakumpa shida. Alichofanya ilikuwa ni kuwanyemelea hadi mita nne nyuma yao, kisha akachupa hewani na kutua huku wote wawili wakiwa chini yake. Kabla hawajafahamu kinachotokea alikwishawagonganisha vichwa mara kadhaa hata wakapoteza fahamu. Baada ya hapo aliwafunga kamba za mikono na miguu, akawatia matambara mdomoni ili watakapozinduka, wasiweze kupiga kelele na kisha akawavuta na kuwalaza katika kibanda chao cha ulinzi.
Kwa kutumia funguo zake malaya aliufungua mlango wa geti na kisha kushughulika na makufuli ya kuingilia ghalani. Ilimgharimu dakika kumi, ambazo Joram aliona kama miaka kumi hadi makufuli yalipokubali. Alipigwa na butwaa kwa wingi wa mali zilizokuwemo humo ndani. Jengo zima lilifurika kwa makatuni yaliyopangwa vizuri hadi kufikia kabati. Joram alishusha baadhi ya makatuni na kutazama majina yake, Glamorous Perfume, Glamorous Cream, Glamorous toilet soap, Glamorous powder, n.k.
Joram alikumbuka kuona matangazo ya bidhaa hizo katika magazeti na televisheni. Aidha, alipata kusikia yakitangazwa pia katika redio. Akiwa mtu ambaye hajishughulishi na vipodozi, hakuyatilia maanani matangazo hayo.
Hata hivyo, alikuwa na uhakika kuwa hazijaanza kuuzwa nchini kwakuwa tangazo moja lilikuwa likitangaza tarehe ambayo bidhaa hiyo ingeanza kusambazwa kote nchini. Hakutegemea kama bidhaa inayoingia nchini kwa majaribio, ambayo ilitajwa wazi kuwa ingeanza kutumika duniani kwa mara ya kwanza, ingeweza kuletwa kwa wingi kiasi hicho.
‘Bahati yao mbaya, itabidi walete mali mpya,’ aliwaza wakati akipanda juu ya masanduku hayo na kuchokonoa umeme. Kuanzisha moto ukiwa mchezo mdogo kwake, haikumchukua nusu saa kuona nyaya za umeme alizozitegesha zikianza kusafirisha moto ambao utakapokutana mlipuko usingekuwa wa kawaida.
Alifanya hivyo katika jengo la pili pia. Kisha, akatoka nje na kuwaburuza walinzi wale wawili hadi barabarani ambako aliwafungua kamba na kuwaacha wakiwa wameduwaa. Akapanda gari lake na kulitia moto, akilielekeza mjini.
Kabla hajafika popote mlipuko wa kwanza ulitokea. Ulifuatiwa na moto mkubwa ambao ulifanya usiku ugeuke mchana. Mlipuko wa pili ulimkuta keshafika mjini.
Ukubwa wa mlipuko na ukali wa moto toka katika maghala hayo ulimshitua karibu kila mtu katika maeneo ya Tabata, Buguruni, Ubungo na kwingineko. Watu wengi waliamka na kuutazama kwa hofu, huku vibaka wakifukuzana kwenda katika eneo hilo kwa matumaini ya kujipatia chochote. Hakuna kilichopatikana. Hata zima moto ambao walifika katika eneo hilo, nusu saa baadaye, waliduwaa wakiutolea macho moto huo jinsi ulivyokuwa unatafuna na kuteketeza kila kitu katika majengo hayo. Hakuna aliyethubutu kuusogelea.
Taarifa za kuungua kwa maghala ya Kangaroo iliwafikia wakurugenzi wa kampuni hiyo, Paul na Philip, dakika arobaini baadaye. Walikurupuka toka katika ofisi yao, ambayo kwa juu yalikuwa makazi yao na kujikongoja kulielekea gari lao.
“Number One!” mmoja aliita. Alipoita mara ya pili kile kilichoonekana kama kivuli, ambacho kilisimama katika kivuli cha mchongoma ulioizunguka ofisi hiyo, kilipata uhai na kuwaendea kwa mwendo wa kunyata.
“Tulikuajiri kwa kazi moja tu” Philip alisema kwa sauti yake ya mkwaruzo. “Kumpata Joram Kiango na kumleta kwetu akiwa hai, wewe umekaa hapa kivulini wakati yeye anatufanyia madhara ghalani. Twende tuone ni kiasi gani cha madhara alichotufanyia” Number One hakuwajibu. Hakuwa mtu wa maneno mengi isipokuwa vitendo. Zaidi, alikuwa na mashaka kuwa waajiri wake hawa walikuwa na dosari katika vichwa vyao kama ilivyokuwa katika miili yao. Hakupata kuwaelewa hata mara moja. Hata hivyo, alilazimika kuwatii kwa kuwa tu alihitaji pesa zao ambazo aliziona kama za bure kwa wepesi wa kazi waliyomtajia.
Si kawaida ya ninja kukodiwa kwa kazi ya aina hii. Lakini dunia ilikuwa imebadilika kitambo. Akiwa ametulia hotelini kwake mjiniCalifornia, asubuhi hiyo alifuatwa na ajenti wake ambaye alimwambia kuwa kuna kazi ya kufanya nje ya nchi.
“Wapi?”
“Afrika”
“Nchi gani?”
“Tanzania”
Hakujua Tanzania. Kwa ujumla nchi za Afrika alizozifahamu ni Naijeria na Cameroon kwa ajili ya mpira; Uganda kwa ajili ya vituko vya Idd Amin, Kenya kwaajili ya utalii na Afrika Kusini kwa ajili ya Mandela Tanzania haikuwemo kabisa katika ramani ya kichwani.
Lakini baada ya kukutana na watu hao waliomuhitaji, ambao nusura wamfanye aangue kicheko kwa maumbile yao, alijikuta akiijua Tanzania. Ilikuwa baada ya kutajiwa jina la mtu ambaye alitakiwa wamkamate, Joram Kiango, alikuwa hajamsahau. Hakuwa na uwezo wa kusahau kipigo ambacho “nyani” huyo anayejiita Joram Kiango alimpa, kipigo cha kwanza katika maisha yake. Hivyo, aliafiki mara moja.
Kumkamata Joram lilikuwa jukumu la pili la kwanza lilikuwa kumfuta duniani “nyani” mwingine anayeitwa Kakakuona, kwa kosa la kushindwa kumpata Joram na kuhatarisha harakati zao kwa kufanya mauaji kwa fujo, kimachomacho. Jukumu hilo alilitekeleza kwa urahisi sana, hasa baada ya kuandaliwa silaha safi ya aina yake, ambayo alikuwa akiisikia tu katika simulizi za kihistoria. Kidole chake cha shahada kilipoifyatua bunduki hiyo na kumfanya binadamu, ambaye alikuwa kando ya barabara, atoweke kama tufe la barafu, lililoyeyuka ghafla, alijisikia kama mungu. Baada ya kazi hiyo ndipo alipotakiwa kumnasa Inspekta Kombora ambaye waajiri wake walidai kuwa anajitia “kimbelembele” ambacho kinawea kuwaharibia mipango yao kabla hawajampata Joram. Haikuwa kazi kubwa kumtia mikononi. Wakiwa na hakika kuwa makachero wake wanaichunguza nyumba hiyo kwa uficho, na wakiyasikiliza maongezi yake baina yake na vijana wake, ingawa walitegemea mfasiri kuwafahamisha kwa kiingereza, iliwagharimu kutumia hila za kizamani, ya kupakia sanduku katika pick up na mara wakamsikia akimwambia kachero wake kuwa anakuja.
Tatizo pekee katika kumnasa Kombora ni pale alipotokea mtu ambaye hakujulikana na kuanza kupambana naye. Number one hakumtegemea. Na zaidi alishangazwa na uwezo wake wa kupigana ambao ulimfanya ashindwe kuamini kuwa anapambana na binadamu wa kawaida kwani hakuna binadamu wa kawaida ambaye alipata kumpa shida kama huyu. Wingi wa watu ambao walianza kujazana na ufupi wa muda aliokuwa nao, vilimfanya Number one atumie njia ya uoga, ya kupiga lile bomu la moshi unaowasha, na kuitumia fursa hiyo kuwachukua mateka wake na kuwarejesha mjini.
Ni wakati alipokuwa akiendesha pick up hiyo kurudi mjini, ndipo ilipomjia akilini kuwa aliyekuwa akipambana naye hakuwa mwingine ila ni Joram Kiango. Miaka mingi waliyotengana ilimfanya aanze kumsahau lakini asingeusahau upiganaji wake usio kifani. Alijilaumu kuruhusu, kwa mara nyingine, aponyoke toka mikononi mwake kama samaki aliyepenya toka kinywani mwa mamba. ‘mwanaharamu yule, ama zake ama zangu,’ aliwaza akiwageukia Philip na Paul ambao walikuwa wakiendelea kusema kitu ambacho hakuwa amekisikia.
“Tunasema twende huko ghalani tukaone madhara yaliyosababishwa.” Paul alisema akiingia nyuma ya benzi lao na kufuatiwa na Philip. Number one ambaye jina lake lingine la bandia katika hati ya usafiri lilikuwa Newton Kelly, aliingia mbele na kulitia moto gari.
Ingawa alikuwa na siku tatu tu tangu alipoingia Dar es Salaam, lakini ramani alizopewa na jinsi alivyoutumia muda huo mfupi kulivinjari jiji tayari alikwishakuwa mwenyeji. Hakuhitaji kuelekezwa, wala hakusubiri kuamriwa afuate njia ipi. Badala yake alikanyaga petrol na kuacha gari liteleze kuifuata UWT na baadaye, Maktaba, hadi Samora ambako aliichukua uhuru na kuambaa nayo hadi Buguruni. Alipofika Mandela alipinda kulia na kuelekea Tabata.
Toka hapo macho yao yalivutwa na moto mkubwa ambao uliufanya usiku huo uonekane mchana. Philip na Paul hawakuyaamini macho yao walipoona kuwa moto huo ulikuwa ukiiteketeza hazina yao yote, hazina ambayo pia ilikuwa ndoto yao pekee ambayo waliiweka akilini kwa miaka zaidi ya sita na kuigharamia kwa kila senti waliyokua nayo. Waliutazama moto huo kwa huzuni, hisia zao zikionyesha ni miili yao inayoteketea katika majengo hayo, badala ya mafuta ya kujipaka na vipodozi. Mmoja wao alitokwa na sauti ya kilio bila machozi, hali mwingine alitokwa na machozi bila kilio.
Number one aliwatazama kwa mshangao jinsi walivyobadilika. Alitamani kucheka lakini hakuthubutu. Alitamani kuwahurumia, lakini hakujisikia. Hakuona vipi tukio kama hilo, kwa wafanyakazi wakubwa kama wao, liwe kama mwisho wa dunia. “Kwani hamna bima?” aliwauliza. Hakuna aliyemjibu. Badala yake Philip alimgeukia na kumkazia macho. Baada ya muda, kama anayezungumza peke yake, alisema, “Najua hii ni kazi ya Joram Kiango. Mwanaharamu, kwa mara nyingine ametutia kilema. Kwa bahati mbaya safari hii ametutia kilema cha moyo badala ya mwili. Unasemaje Paul?”
Paul aliendelea kulia.
Philip akamrudia Number one, “Kelly” kwa mara ya kwanza alimwita kwa jina lake, kinyume na maafikiano yao.
“Tumekuhaidi ngapi kwa kutuletea Joram Kiango?”
Number one hakukumbuka. Tangu alipojua kuwa mtu wake ni Joram kiango alijikuta amesahau malipo ya kazi hiyo na kuifanya yake binafsi, kwa nia ya kulipa kisasi.
“Ngapi?” Philip alirudia. “Okey pengine hamna haja ya kutaja. Ninachosema ni hiki. Tunamtaka Joram Kiango usiku huu huu; awe hai au amekufa. Tutakulipa mara kumi ya chochote tulichokuhaidi. Upo?”
Number one alikubali kwa kichwa.
“Usiku wa leo.” Philip alisisitiza. Kabla ya kesho tutakuambia wapi amejificha. Unasemaje Paul?
***
Joram Kiango pia alikuwa ameapa kuwa usiku huohuo angemaliza “unyama huu wa kipuuzi.” Mara tu alipohakikisha moto aliouanzisha umepamba moto, alifika mjini na kuliegesha gari lake mbele ya kiwanda cha printpak. Kisha, akatembea kwa mguu kurudi hotelini kwake ambako alikisikiliza chombo chake cha kupokelea ujumbe wa simu zake.
Akafahamu kuwa Inspekta Kombora alikuwa hajarudi na kwamba vijana wake walikuwa wakitapatapa kwa “kutoweka” huko kwa afande wao. Aidha, mtu wake wa kampuni ya simu alimwarifu kuwa bado ilikuwa vigumu kunasa maongezi ya ofisi ya Kangaroo kutokana na mitambo iliyotengwa kuepusha jambo hilo. Habari alizotegemea toka nje juu ya wakurugenzi wa Kangaroo zilikuwa bado hazijapatikana. Akakitegesha tena chombo hicho na kusimama.
Uchovu aliokuwa nao haukuwa na kifani; alitamani kuingia bafuni aoge. Alikitamani kitanda chake, lakini hakuweza kufanya lolote kati ya hayo kila alipokuwa akiitazama saa yake ilikuwa ikimkera kuona mapambazuko yakikaribia. Hivyo, alijinyoosha, akachunguza vifaa vyake vyote vilikuwa kamili katika mifuko yake ya siri. Kisha, akakifunga chumba chake na kutoka.
Hakuhitaji gari, alipenya vinjia vya uchochoroni na akiiendea ofisi ya Kangaroo. Nyumba mbili kabla ya kuifikia ofisi hiyo, alitafuta uchochoro na kujificha, macho yake yakiwa kazini kulitazama jengo hilo kwa makini.
Matumaini ya Joram yalikuwa kwamba taarifa za kuungua kwa maghala yao zitakapowafikia wakurugenzi hao wasingesita kutoka kwenda kutazama uharibifu uliotokea. Fursa hiyo alihitaji ili aingie katika jengo hilo na kumtoa Nuru kabla hajawashughulikia wendawazimu hao.
Kama alivyotegemea, haikupita robo saa kabla hajaona benzi likitoka eneo hilo kwa mwendo wa kasi kuifuata UWT. Aliwapa dakika tano kisha aliiendea ofisi na kushughulikia geti ambalo halikumchukua dakika mbili. Alilifunga nyuma yake na kuliendea lango akipenya katika kivuli cha michongoma. Joram alikuwa na taarifa zote jinsi jengo hilo linavyolindwa kwa umeme. Alifahamu fika kuwa kwa kugusa mlango au dirisha ovyo angekuwa amejichongea kwa kutoa ishara ambayo ingeweza kuwafikia wakurugenzi hao huko huko waliko na hata kituo cha polisi. Hali kadhalika, alijua kuwa ndani ya jengo hilo kuna milango ya siri ambayo isingeweza kufunguka bila ya kujua hila ambazo hutumiwa. Ni hayo ambayo yalimfanya Joram ahitaji ramani za jengo hilo au mhandisi aliyelishughulikia. Lakini baada ya kusikia kilichomtokea mhandisi huyo, na kunasa maongezi ya kikosi cha Kombora juu ya ramani ya jengo hilo, hakuona kama alikuwa na muda wa kutosha zaidi ya kufanya kile ambacho waingereza ukiita short in the dark, kujituma kazini.
Kwa mujibu wa taarifa za kikosi cha Kombora, na kile alichokiona mwenyewe Kakakuona alipojituma kupitia jengo la Sunrise na kutokea Kangaroo, Joram alikuwa na uhakika kuwa nyuma au chini ya meza kulikuwa na njia ya siri ambayo ama ilifunguka kwa kubonyeza tufe lililofichwa ukutani au kwa chombo maalumu cha mkononi. Joram hakupenda kupitia njia hiyo kwa kuhofia kupotezewa muda na makachero wa Kombora ambao pia wangeweza kumharibia mambo. Hali kadhalika, alijua jicho la adui linatazama upande huo baada ya Kakakuona kukorofisha. Hivyo, aliamua kutumia mlango wa mbele.
Akiwa amejiandaa kwa vifaa vya umeme, Joram alitafuta hadi alipopata nyaya za umeme. Alizifuata hadi zinapoungana na zile za ndani. Akashughulika nazo kwa dakika kadhaa na kufanikisha kutegesha chombo chake maalumu ambacho kina nguvu ya kuvuruga mpangilio wote wa vifaa vya umeme katika jengo kiasi cha mitambo iliyotegeshwa kushindwa kufanya kazi. Baada ya hapo alitumia funguo zake malaya kufungua ofisi hiyo na kuingia. Alihofia kuwasha taa za umeme ambazo zilikuwa zimezimwa. Akatumia tochi yake ndogo yenye ukubwa wa kalamu kumulika hapa na pale hadi alipoipata ofisi ya wakurugenzi. Alihangaika na makasha mbalimbali na kupekua nyaraka hizi na zile hadi alipoona kuwa alikuwa akiupoteza bure muda wake. Akageuka ukutani na kumulika hapa na pale, akipapasa hapa na kutomasa pale hadi alipata kitu alichokuwa akikihitaji. Picha moja ukutani hapo ilikuwa imficha tufe moja lenye namba toka 0 hadi 9. Joram alicheza na namba hizo kwa dakika kama kumi. Wakati akikaribia kukata tamaa, kama ndoto, aliona nusu ya ukuta huo ikimeguka na kumruhusu kuingia katika chumba kipana, cha siri. Hicho ndicho chumba alichokihitaji.
“wewe malaya, inuka hapo ulipo, kuja hapa,” sauti yenye mkwaruzo , iliyojaa chuki na hasira ilimwashiria Nuru.
Ilikuwa sauti Philip, Paul akiwa nyuma yake. Ndio kwanza walikuwa wamerejea toka kushuhudia hasara kubwa waliyoipata. Wakiwa wamejawa na hasira, akili yao ilikuwa najambo moja tu akilini, kuua, hawakuweza kushuku chochote walipoingia katika jengo lao hilo; kupita katika ofisi ya siri hadi katika chumba cha mateso.
Nuru alijikongoja kuinuka toka sakafuni alipolala, kando ya Kombora. Akawaendea na kusimama mbele yao akitetemeka. Hasira zilimjaa moyoni, lakini macho yake yalijaa upole yakiomba kitu ambacho akili yake haikumruhusu kutamka. Kilio chake kilikuwa wazi machoni mwa Philip na Paul. Pamoja na hasira zilizowajaa rohoni, walitazamana, wakacheka.
“Unataka chakula chako sio?” Philip alimkebehi, “Leo hutapata chakula chako, mama. Tunakutaka uwe mzima na akili zako zote ili ufe huku unaona. Usikie kila ladha ya kifo hadi roho yako itakapokutoka. Upo mpenzi?”
“Na nitakuambia jambo jingine la kupendeza,” Paul aliongeza. “Kabla hujafa utashuhudia kifo cha hawara yako Joram Kiango. Wakati wowote kuanzia sasa ataletwa hapa akiwa hai au maiti. Tutapenda umpatie busu la mwisho kabla hamjaagana na kuanza safari yenu ya mwisho ya kwenda motoni.”
Inspekta Kombora aliyasikia yote hayo hali kalala chali juu ya sakafu. Alikuwa akilaani kila dakika ambayo ilikuwa ikimfanya aendelee kuwa shahidi wa unyama huo bila uwezo wa kufanya lolote. Aliiona bastola moja iliyoshikwa kizembe katika mkono mmoja wa Paul. Angeweza kabisa kuipokonya bastola hiyo kirahisi na kisha kuvifumua vichwa vyao wote wawili kabla hawajajua kinachowatokea. Kilichomzuia kufanya hivyo ni hali aliyokuwa nayo. Sindano waliyomchoma mara tu alipozinduka baada ya lile joto la kutisha ilimlegeza kila kiungo na kumlegeza akili. Alijiona kama dubwana ambalo lingeweza kuambiwa “lala vizuri tukuchinje” likalala bila kipingamizi. Pamoja na ukweli kwamba alijaribu kupambana na hali hiyo, bado alijua fika kuwa anajidanganya. Hakuwa na hali.
Hilo Kombora alilifahamu tangu alipoona miili ya vijana wake ikiburuzwa kama mizoga ya mbwa na kutumbukizwa ndani ya shimo chumbani humo. Shimo hilo, mara tu lilipofunuliwa liliruhusu harufu mbaya isiyostahimilika ambayo iliashiria kuwepo kwa maiti nyingine nyingi zilizoachwa kuozea humo. Alijaribu kuinuka awatetee vijana wake. Hakuweza. Alipojaribu kufoka sauti haikutoka. Alichoambulia ni kutoa macho tu, kama kondoo.
“Unajua kwanini mnakufa leo?” Philip aliendelea kumsimanga Nuru, “Mnakufa kwaajili ya roho zenu mbaya. Mnakufa kwaajili ya tamaa yenu ya fisi. Mnakufa kwakua nyie sio watu, ni mijibwa tu isiyostahili kuishi.”
“Inatosha Philip, inatosha sana. Huna haja tena ya kuendelea kumnyanyasa msichana huyo asiye na hatia yoyote,” Sauti kubwa, iliyowazi na inayojiamini ilisikika ghafla chumbani humo na kuwafanya Philip na Paul watazamane kwa hofu kubwa.
Ilikuwa sauti ambayo kamwe Nuru asingeweza kuisahau, sauti ya mtu aliyempenda zaidi ya alivyojipenda mwenyewe. Sauti ya Joram Kiango. Ilimfanya Nuru ahisi akipata nguvu mpya.
Mara sehemu ya ukuta chumbani humo ikamenyeka. Umbo refu, lililokakamaa; la Joram Kiango likaingia taratibu, hatua moja baada ya nyingine. Akiwa amevaa suti yake nyeusi, iliyochafuka kwa mavumbi machoni mwa Nuru alionekana mchovu kupita kiasi, lakini macho yake yalikuwa maangavu yakitoa nuru ambayo Nuru asingeweza kuisahau kila aionapo; Nuru ya ushindi. Mkononi alikuwa na bastola ambayo ilimwelekea Philip, lakini hakuijali sana. Alimwendea taratibu na kusimama mbele yake. Akamtazama kwa muda mrefu. Kisha alikizungusha kichwa chake na kumpokonya bastola hiyo ambayo aliitumbukiza katika moja ya mifuko yake. “wewe, umeingiaje humu ndani?” Philip alifoka baada ya kupigwa na butwaa muda mrefu.
“Wewe ni Joram kiango?” Paul naye alipata sauti yake.
“Naam, nadhani mlikuwa mkinitarajia kwa muda mrefu. Sioni kwanini mshangae kuniona,” Joram aliwajibu kwa kebehi huku akiwatazama.
Macho yao yalijaa chuki, hasira na kisasi kwa kiwango ambacho Joram hakupata kukiona. Hata hivyo, ilikuwa dhahiri kuwa hawakuwa na uwezo wa kufanya lolote, hasa baada ya ngao yao kubwa, ambayo ilitokana na mitambo yao ya umeme waliyoiamini kubomolewa. Walitazamana. Kisha, wakatazama huko na huko kama wanaotarajia msaada. Mmoja wao alifyonza na kutema mate. Joram aliwapuuza akamwendea Nuru na kumkumbatia. Alichokiona katika macho yake kilimtisha. Hakuwa Nuru aliyemfahamu, Nuru ambaye siku zote alikuwa sharp kwa maneno na vitendo. Nuru huyu macho yake yalionekana kana kwamba yuko maili elfu moja nje ya chumba hicho. Ingawa alimtambua Joram lakini alionekana kama amemwona katika ndoto, si katika dunia halisi. Hata mwili wake, Joram alipomkubatia ilikuwa kama aliyekumbatia zombie au maiti yanayotembea.
Hali hiyo iliamsha upya hasira za Joram “Mmemtendea haya msichana huyu?” alimwuliza kwa sauti ndogo ambayo, kwa anayeifahamu ilikuwa kali, yenye hasira zake siku zote. Mmemfanya nini mpenzi wangu? Vizuri. Muda si mrefu baadaye mtajuta kuzaliwa. Nilitegemea niwafikishe katika vyombo vya sheria, lakini sioni kama kuna haja ya kufanya hivyo. Nitawaadhibu mimi mwenyewe, kwa njia ninazofahamu mimi.”
Alimwendea inspekta Kombora na kumtazama machoni. Hali yake haikutofautiana sana na ya Nuru. Kombora aliduwaa, akamtazama Joram bila kuonyesha dalili zozote za kuelewa kama amekuja kummaliza au kumwokoa.
Joram hakuhitaji kuambiwa kuwa walikuwa wamepewa kiasi kikubwa cha dawa za kulevya,Sedative Hyprotics, kama Mandrax na mengineyo ambayo yaliwapumbaza miili na akili. Baada ya kuitazama hali yao kwa muda, Joram alijikuta akibuni njia ya kuweza kuwachangamsha walao kwa muda. Miongoni mwa vitu vyake vya siri ambavyo hutembea navyo siku zote ni pamoja na vidonge vya kuongeza nguvu, kuhamasisha mwili na kutoa maumivu, vichocheo ambavyo ni mchanganyiko wa Cocaine, Amphetamine, Heroine na mengineyo. Ingawa matumizi ya dawa hizo pia hayaruhusiwi bila ushauri wa daktari, Joram, kwa nadra sana alizitumia kila ilipobidi; na mara nyingi zilimsaidia. Alitoa vidonge viwiliviwili kati ya hivyo na kuwapa Nuru na Kombora.
Philip na Paul walijaribu kutumia fursa hiyo kutoroka. Walinyata kuiendea sehemu ya kubonyeza tufe ili wafungue lango na kutoka. Hawakujua jinsi Joram alivyo mwepesi. Aliwaona bila kugeuza kichwa chake. Na kabla hawajabonyeza tufe hilo, alikwisha ruka na kuwachota teke moja ambalo liliwapeleka chini wote wawili, kama magunia.
“Bado nina shughuli na nyinyi,” aliwaambia akiwaburuza katikati ya chumba.
Alipowarejea Nuru na Kombora walionekana wakianza kuchamgamka. Dakika moja baadaye Nuru alitamka kile ambacho roho yake ilitamani kukitamka muda mrefu “Joram!”
Alisogea na kumkumbatia tena, machozi yakianza kumtiririka.
Joram alimbusu na kumfuta machozi huku akisema, “Wewe ni msichana mkubwa Nuru. Unafahamu kabisa kuwa huu sio muda wa kutokwa na machozi. Bado tuna kazi ya kufanya.”
Pamoja na kuanza kuchangamka, Inspekta Kombora alionekana mnyonge sana. Alijitahidi kukwepa macho ya Joram, kila alipomtazama. Joram akiwa mtu anayemfahamu fika mzee huyo, alijua kuwa alikuwa akikionea aibu kitendo chake cha kupatikana kirahisi na maadui hao kuruhusu vijana wake wauwawe mbele yake na kuaibishwa mbele ya Joram na Nuru. Joram alimpa maneno ya mzaha ambayo yalimfanya asahau aibu hiyo, aamke na kuanza kuwachunguza maadui hao. “Viumbe duni na dhaifu hawa wamewezaje kufanya unyama wote huu” Kombora aliuliza na kumtazama Joram kwa mshangao.
“pesa.”
“pesa?”
“Wanapesa nyingi sijapata kuona. Katika ofisi yao nimepata akaunti yao ya siri ambayo ina pesa inayotosha kulisha jeshi letu zima kwa miaka miwili.”
Alimsimulia Kombora uchunguzi alioufanya katika chumba hicho ambao ulimfanya atetemeke baada ya kugundua kuwa walikuwa wakipambana na watu ambao wanaweza kuiharibu Tanzania na kuiweka katika msiba usiomithilika hapa duniani.
“Sijapata kuona binadamu wenye mioyo ya kinyama kama hawa, Inspekta Kombora. Wangeifanya Tanzania liwe taifa la kusikitisha, lenye machozi na majonzi yasiyo na mwisho kwa miaka nenda rudi. Mbinu waliyobuni, ambayo haijapata kutumiwa na mtu yeyote duniani, kwa kiwango kikubwa, ilikuwa imekwishafanikiwa. Hasira na chuki waliyonayo dhidi yangu pengine ndiyo iliyowaharibia. Walitaka wahakikishe wanashuhudia kifo au maiti yangu kabla hawajaanza rasmi harakati zao za kishetani,” Joram alieleza na kumwuliza Kombora, “Inspekta si unawakumbuka wale marehemu ambao mlipata maiti zao na kukuta nyuso zao zikiwa zimeliwa nyama na kubakia mafuvu?”
Kombora aliitikia kwa kichwa.
“Basi yale yalikuwa majaribio tu. Ama yalifanywa kimachomacho mno ili kufikisha ujumbe kwangu. Hali ya marehemu wale ndio ingewatokea watanzania wengi, wake kwa waume, katika sura na miili yao. Lakini ingetokea taratibu, hatua kwa hatua, baada ya miezi mitatu au minne ya matumizi ya perfume, mafuta, sabuni, poda na vipodozi vingine mbalimbali ambavyo viumbe hawa wameingiza nchini.” Joram alisita kidogo na kutazama jinsi taarifa hiyo ilivyopokelewa na Kombora kwa hasira iliyochanganyika na hofu. “Vipodozi hivyo ambavyo wamevipa jina Glamour ni sumu kali sana ambayo imefanyiwa utafiti wa miaka mingi, kwa gharama kubwa, hadi ilipoonekana ipo tayari ndipo imewekwa katika mafuta, perfume, cream, sabuni n.k ambazo zina harufu nzuri sana tofauti kabisa na matokeo ambayo yatafuata baada ya miaka mitatu, yasiyo na dawa, ikizingatiwa kuwa tayari sumu hiyo itakuwa imeenea mwilini na hakuna daktari ambaye amejiandaa.”
Kwa Kombora ilikuwa kama ambaye tayari ameshuhudia maafa hayo, kama ambaye tayari anauona msululu wa watu waliokata tamaa mbele ya madaktari walioduwaa, huku vilio vikisikika toka katika kila nyumba na kila mtaa. Aidha, aliona majeneza mengi yakipelekwa katika viwanja vya makaburi ambayo tayari vilikuwa vimefurika.
Kombora aliweza hata kuhisi harufu iliyotapakaa katika kila nyumba harufu ya uozo, harufu ya nyama, sura na miili ya wasichana wazuri ambao wanaoza taratibu huku wakiwa hai, hadi pale wanapokata tamaa na kusalimu amri ya kifo. Kana kwamba anayasoma mawazo yake, Joram kiango aliongeza ghafla, “Naamini mpango wao haukufanikiwa. Maghala yao mawili ambayo yalikuwa yamefurika mali zikisubiri zianze kutawanywa kote nchini, baada ya matangazo mengi katika vyombo vya habari, nimeyateketeza kwa moto. Kila kitu kimegeuka jivu, mizigo yao ambayo ipo bandarini, ambayo nashuku pia ina bidhaa za aina hii, kama nilivyoona katika hati zao za siri, pia haitawafikia wananchi. Itateketezwa kabla vibaka hawajaiba hata kopo moja.”
Kombora alishusha pumzi kabla hajasema, “Mambo yote umenieleza, Joram, kama ilivyokawaida yako umenitafunia na umeacha nimeze tu. Hata hivyo, kuna mawili hujaniambia. La kwanza hujaniambia adui yangu mkubwa zaidi ni nani, Kakakuona yuko wapi. Usiniambie kuwa amekuponyoka kwasababu ningependa kushuhudia kifo chake kwa macho yangu, kama si kumwua kwa mkono wangu.”
“Kakakuona tayari amekufa,” Joram alimjibu.
“Amekufa! Amekufa lini?
“Ni hadithi ndefu Inspekta. Tutaizungumza baadaye. Kuhusu swali lako la pili, nadhani unataka nikwambie hawa viumbe ni kina nani na wanahusika vipi na mkasa huu wa kutisha. Au sio Nuru?” alisita akimtazama Nuru na Inspekta Kombora kwa zamu, kisha akaendelea, “Hiyo ni hadithi nyingine ndefu, ningeshauri tutoke katika chumba hiki cha mauti twende katika ofisi ya kifahari ya wakurugenzi hawa ambamo tutaketi na kuzungumza kwa utulivu kabla hatujawakabidhi watu hawa kwa vijana wako ambao watajua la kuwafanya.”
“Kuwakabidhi?” Kombora alifoka ghafla. “Niwakabidhi kwa mtu mwingine watu kama hawa! Sikiliza Joram, mwanangu. Naweza kuwa mtu ninayeheshimika sana kisheria. Naweza pia kuwa mtu aliyeajiriwa kwa kuhakikisha sheria zinafuatwa. Lakini sio kwa suala la mashetani kama haya. Hawa, niliapa nitawauwa kwa mikono yangu,na ni hilo nitakalolifanya.” Aliwatazama Nuru na Joram kwa zamu. kisha, akauelekeza mkono wake kwenye shimo ambalo lilikuwa likiendelea kutoa harufu mbaya za maiti.
“Mnaliona shimo lile? Watu hawa wamelitumia shimo lile kuangamiza watu wengi wasio na hatia. Shimo lilelile litakuwa kaburi lao. Na nitawazika ili waisheherekee kila kila dakika ya safari yao kuelekea kuzimu.” Baada ya kusema hayo, bila kutaka ushauri wa Joram wala Nuru, alimwendea Philip na kumpiga teke moja ambalo lilimfanya aanguke kando ya shimo hilo, damu zikimvuja puani na mdomoni. Teke la pili, ambalo bila shaka liliuvunja mguu wake mzima, lilimfanya aviringike na kutumbukia shimoni humo kuungana na maiti nyingine.
Paul alianza kutetemeka hata kabla ya Kombora hajamfikia. Kwa jicho lake kali, ambalo lilijaa kisasi, alimtazama Joram kwa muda mrefu hadi Kombora alipompiga ngumi iliyomfanya ateme meno mawili na kuvunjika pua. Huku bado akimtazama Joram, badala ya Kombora aliyekuwa akimwadhibu, aliangukia shimoni kama mzoga. Kwa msaada wa Joram, Kombora aliitoa miili ya vijana wake wawili. Kisha, wakafunga mlango wa shimo hilo ambao ulifanya ionekane kama sakafu ya kawaida.
“Msijali” kombora aliwaambia, akiwatazama Jorama na Nuru. “Kwa hili nipo tayari kujieleza hata mbele ya mungu.”
Nuru na Joram walitazamana kisha, kwa sauti ndogo Nuru akamwambia, “Tuondokeni katika chumba hiki. Ni chumba cha mauti, hakitufai.”
Joram aliendea tufe la ukutani na kulibonyeza. Ukuta ukafunguka na kuwaruhusu kuingia katika ofisi safi ya wakurugenzi hao ambao walikuwa wakitapatapa chini ya ardhi kwa kukosa hewa safi. Wakaufunga nyuma, Joram akiwa amemshika Nuru mkono, aliwaongoza hadi juu ya viti ambako waliketi.
Ndio kwanza wakafahamu kuwa kulikuwa kumepambazuka. Nuru toka nje kupitia katika vioo, ambavyo viliruhusu kuona nje hali mtu wa nje hawezi kuona ndani, iliwawezesha kuona kundi dogo la polisi wenye silaha wakiwa wamelizingira jengo hilo. Kiongozi wao, akiwa na kipaza sauti mkononi, alikuwa akizungumza kitu fulani mara kwa mara kabla hawajalivamia. Kundi kubwa la raia walionekana wakiwa wamesimama nyuma ya askari hao wakitazama kwa macho yanayouliza, kulikoni!
Joram aliwapuuza watu hao wa nje. Akainuka na kuiendea ofisi ya mkurugenzi mtendaji na kuketi juu ya kiti chake cha starehe. “Kisasi ni kitu cha ajabu sana” Joram alianza kuamini.
“Nuru” alimwita akimtazama. “Unaweza kuamini kuwa hawa watu wawili ni binadamu pekee walionusurika katika jengo ambalo lilikuwa na ile mitambo iliyokuwa ikiendesha satelaiti ya ajabu ya Afrika Kusini ambayo ilikuwa isababishe ile mioto ya ajabu ajabu katika nchi za mstari wa mbele?”
“Philip na Paul walikuwa miongoni mwa mainjinia waliokuwa wakiiongoza mitambo hiyo. Ni wao pekee walionusurika kufa, baada ya moto tuliouanzisha kuteketeza kila mtu na kila kitu,” aliogeza.
Hakuna mtu ambaye angeweza kulisahau tukio hilo. Kombora asingesahau jinsi yeye, na kila Mtanzania, alivyokuwa roho mkononi, akisubiri maafa ambayo yaliandaliwa na serikali ya kidhalimu iliyokuwa ikiongoza nchi wakati huo. Nuru asingeweza kusahau yaliyomkuta. Asingesahau alivyoonja kifo baada ya mateso na kudhalilishwa kusiko na kifani. Ingawa yeye na Joram walitoka kama washindi na mashujaa wa Afrika na dunia nzima, bado tukio hilo ambalo limeandikwa vitabuni kwa lugha mbalimbali kama Tutarudi na Roho Zetu? Na Zero Hour bado kila anapolikumbuka, Nuru hujisikia kichefuchefu.
“Kwa nini hukuniambia kabla Joram?” aliuliza taratibu. “Nisingeacha wabakie hai humo shimoni.”
“Hawako hai.” Kombora alijibu. “Wamekufa taratibu, kifo ambacho kinawastahili kabisa.”
Joram aliendelea, “Ilivyotokea ni kwamba, baada ya wale jamaa kupona majeraha yao walijaribu kujihusisha tena na mipango ileile. Na kwakuwa jambo lile lilikuwa la siri sana likiwa limetengewa mamilioni ya pesa ambazo wao walikuwa miongoni mwa walioruhusiwa kuzitumia benki, walichofanya ilikuwa kuhamisha pesa hizo na kuziweka Marekani kwa majina yao. Wakati huo harakati za ukombozi nchini humo zilizidi kupamba moto, na hatimaye Mandela kuchukua urahisi baada ya kutoka kifungoni. Hasira zao juu ya mtu mweusi zilizidi. Na walizielekeza hasira hizo kwangu kwa kudhani kuwa nimesaidia kuwafanya washindwe na Watanzania wote kwa kuamini kuwa wamechangia kuwezesha ubaguzi utokomezwe, hivyo, wakabuni njia mbalimbali hadi walipopata msaada wa wanasayansi ambao walifanikisha jaribio la kutengeneza sumu ambayo ilikuwa almanusura iangamize Tanzania.”
“Nadhani wameona kuwa Tanzania bado si nchi ya kuchezea,” Kombora alisema.
“Nadhani,” Joram alisema akijiuliza mangapi zaidi amweleze Kombora. Katika uchunguzi wake alipata namba za akaunti za watu hao ambazo alikuwa tayari kumpa Kombora. Pia alipata nyaraka nyingi za siri ambazo angempa ili zimsaidie kukamilisha kazi yake.
Lakini katika uchunguzi huohuo aligundua uficho wa siri katika ofisi hiyo, ambao ulikuwa na mamilioni ya pesa taslimu za nje na za kigeni. Hilo asingemwambia Kombora kwani alipangakuzihamisha usiku utakapoingia. Aidha, kwa kumuhurumia mzee huyo alivyochoka hakupenda kumsimulia muda huo juu ya kiumbe wa hatari kuliko Kakakuona, mwenye taaluma kamili ya ninja, ambaye yuko mahali fulani, akisubiri. Joram aliamua kuwa hilo pia liwe siri yake hadi atakapolishughulikia.
Akiwa na hakika kuwa Kombora na jeshi lake hata wapekue jengo hilo mara ngapi wasingeweza kuzifikia pesa hizo aliinuka na kumshika Nuru mkono. “Nadhani huyu msichana amechoka. Anahitaji kupumzika. Kila kitu unachohitaji kiko humu. Kwa hiyo, nadhani utaturuhusu twende zetu.” Alipiga hatua mbili tatu kuuendea mlango, kisha akamgeukia Kombora na kumwuliza, “Kwa jinsi watu walivyojaa huko nje, unaonaje, nani aanze kutoka. Wewe au mimi na Nuru?”
Mamia ya watu walioduwaa nje ya jengo hilo walishangaa kuona mlango ukifunguka taratibu na kumruhusu kijana mmoja mkakamavu na msichana kuanza kuondoka. Mvulana akiwa katika suti yake nyeusi, isipokuwa kwa vumbi kidogo, katika mavazi yake alionekana mtanashati kama ambaye anatoka katika jumba la starehe kinyume na watu waliokuwa nje walivyoamini. Lakini msichana alikuwa taabani, kachakaa mwili na mavazi kama aliyetoroka kuzimu. Alitembea kwa kujikongoja huku akipata msaada wa mkono wa mvulana uliomshika kiuno.
Sura za vijana hawa zilikuwa maarufu nchini kama zilivyomashuhuri kote duniani. Haukupita muda kabla ya watu waliokuwa hapo nje hawajaanza kunong’ona, “Ni joram Kiango!”
“Ndiyo. Na Nuru”
Polisi ambao walianza kuziweka silaha zao sawa kuwaelekea, walipowafahamu walizirudisha makwapani na kusimama kwa utulivu. Mmoja wao saluti ilimtoka, na Joram akapokea kwa kutabasamu kidogo. Kabla askari hao hawajajua wafanye nini na Joram, bosi wao, Inspekta Kombora, alitokea, na askari wote wakamkimbilia.
Yeye pia alikuwa taabani kama Nuru. Nguo zake zilichakaa na kuchafuka, mwili wake ulijaa marejaha, macho yake yalilegea kana kwamba alikuwa amekesha akinywa pombe kali. Akiushikilia ukuta alitembea taratibu na kuzipuuza saluti ambazo zilielekewa kwake.
“Pole sana mzee.”
“Nipelekeni ofisini… hapana nyumbani,” alisema kwa udhaifu
“Tukupeleke hospitali afande?”
“Nimesema nyumbani.”
Dereva mmoja alimsogezea gari. Kabla hajalipanda alitoa maelekezo kwa askari hao, akiwataka wahakikishe jengo hilo linalindwa kwa makini usiku na mchana hadi atakapokuwa tayari kukamilisha suala hilo ambalo alidai limekwisha!
Joram alitumia fursa hiyo kuutoroka umati wa watu. Alimfuata mtu mmoja aliyekuwa ameketi ndani ya gari lake, Toyota Saloon, na kumwomba lifti. Mtu huyo, kwa furaha, aliwafungulia milango na kuwakaribisha ndani. Joram akamwingiza mgonjwa wake kisha yeye akaingia na kumtaka awapeleke hotel ya Mawenzi.
“Nina bahati sana leo” msamaria alisema.
“Bahati gani?” Joram alimwuliza
“Kukutana ana kwa ana na wewe. Ni jambo ambalo sikulitegemea kabisa. Nimekuwa nikikusoma katika vitabu na magazeti tu. Hivi huko ndani kulikuwa na nini?”
“Ngoja gazeti la kesho utaelewa, ni hadithi ndefu sana”
“Hivi haya wanayoyaandika juu yako ni ya kweli? Sio kwamba waandishi wanatia chumvi sana ili magazeti na vitabu vyao vinunuliwe?”
Joram, akiwa hana hamu na magazeti, alijikuta akimwambia, “Hayo unayoyasikia yazidishe mara nne, utoe nane na kuongeza mbili ndipo utapata ukweli wenyewe”
Akiwa amechanganyikiwa, dereva huyo aliendesha gari bila maongezi zaidi mpaka alipowafikisha mbele ya hoteli yao.
Joram alimshukuru kwa ukarimu wake, akamzoa Nuru ambaye alianza kulala na kumwingiza hotelini. Watu waliokuwa mapokezi walitokwa na macho ya mshangao, hasa kutokana na hali ya Nuru, lakini Joram hakuwapa nafasi ya maswali. Badala yake alichukua ufunguo wake na kwenda chumbani kwake, akiwa bado amemshikilia Nuru kiuno. Hakuhitaji funguo huo, chumba kilikuwa wazi, kinyume na alivyokiacha. Jicho lake moja chumbani humo lilimfanya afahamu kuwa alikuwa ametembelewa. Ingawa karibu kila kitu kilikuwa kama alivyokiacha, lakini bado dalili zilimwonyesha kuwa kila kitu kilikuwa kimekaguliwa na kuvurugwa kwa uangalifu mkubwa.
Joram akamtua Nuru kwenye kitanda na kumlaza taratibu. Alipovuta mto ili amweke vizuri, aligutuka kuona mto huo ulikuwa umetumiwa kuficha maiti ya paka mnene, aliyenawiri, ambayo yalilazwa kitandani hapo. Kando ya mzoga huo, Joram aliona maandishi mekundu yalioandikwa juu ya shuka kwa lugha ya kiingereza ‘you’re next’ yakimaanisha kuwa ni yeye Joram atakayefuatia.
Alipomgeukia Nuru kuona kama naye pia alikuwa ameuona mzoga huo, alifurahi kumwona tayari kalala kwa utulivu, akikoroma taratibu. Akainama na kumchunguza paka huyo kwa makini zaidi. Akabaini kuwa aliuawa kwa kunyongwa kwa kwa mkono muda mfupi uliopita kwani alikuwa bado ana joto. Lakini Joram alipozidi kumchunguza aligundua kuwa bado alikuwa akipumua taratibu. Badala ya kumtupa dirishani kama alivyokusudia, Joram alimwinua polepole na kumweka nje ya chumba, upande wa mapumziko.
Baada ya kuduwaa kwa mara ya pili, Joram alimnusisha paka huyo dawa ya kulevya, jambo ambalo lilimfanya mnyama huyo mdogo apige chafya na dakika chache baadaye ainuke na kujikongoja taratibu kuelekea nje.
Joram hakuhitaji kuambiwa paka huyo ameletwa na nani chumbani humo. Adrian!… Ni yeye pia aliyekipekua chumba chake ambamo dalili zilimwonyesha Joram kuwa alikaa muda mrefu akimsubiri.
Kitendo cha kupata uhai kwa paka huyo, ambaye Joram alijua fika aliwekwa hapa kwa njia ya kumtisha huku adui huyo akiamini kuwa ni mzoga, kilimdhihirishia Joram kuwa mapambano bado yalikuwa yanaendelea. Hata hivyo, ilimtia matumaini makubwa ya kuibuka mshindi akizingatia uhai wa paka huyo ulivyorejea baada ya muuaji kuamini kuwa ametimiza kazi yake.
Akifahamu fika jinsi roho ya Adrian ilivyolemaa kwa chuki na fikra zake zilivyomezwa na kiasi Joram alijua kuwa alikuwa na wajibu mkubwa kumteketeza kiumbe huyo kabla hajafanya madhara zaidi. “Ni yeye, au mimi!” aliwaza akiondoka kurudi kitandani ambako Nuru alilala kwa utulivu.
Joram alimtazama msichana huyu alivyolala na mavazi yake yote. Aliitazama sura yake nzuri na umbo lake la kuvutia lilivyopendeza katika mavazi hayo yaliyochakaa na kuchafuka.
***
Pamoja na hasira zake, Adrian alichukua wasaa wa kujilaumu kimoyomoyo. Kwa kiasi kikubwa alihisi alishiriki kuwaangusha waajiri wake ambao alikwisha amua kuwa wana aina fulani ya kichaa. Kitendo chake cha kupenya toka katika eneo hilo la ofisi hadi katika hoteli ya Joram Kiango ili akammalize hukohuko, badala ya kumsubiri, kama wenyeji wake walivyomwelekeza, kwa kila hali kimechangia kumfanya awe hai hadi sasa na awaokoe mateka wake.
Jambo hili, limezifanya jitihada zake zote, za kupenya katika uchochoro wa hoteli hiyo, hadi nyuma ambako alitumia kamba kupanda hadi juu na kisha kwa kutumia tundu la moshi kujipenyeza hadi ndani ziwe za bure.
Chumbani mwa Joram, Adrian alipekua kila sehemu bila kujua anatafuta nini. Hakupata chochote. Hata hivyo, ili asiondoke bila zawadi yoyote, ndipo alipochukua mkufu wa dhahabu uliokuwa kama umesahauliwa katika begi mojawapo.
Adrian alijua ingemchukua muda Joram kugundua upotevu huo, lakini kwake ingekuwa fahari kubaki na kumbukumbu ya kumfuta duniani.
Ni wakati alipokuwa akitoka nje ya chumba hicho alipokutana na paka yule ambaye alipita akinusa huko na huko. Adrian hakuchelewa kumdaka na kumminya koo kwa vidole viwili hadi paka alipokata roho, kisha akamlaza juu ya kitanda cha Joram kama salamu ambazo alijua zitamsisimua zaidi ya kupotea kwa mkufu mdogo wa dhahabu. Adrian akaamua kurudi kwa waajiri wake. Akiwa nje ya jengo hilo la Paul na Philip, alimwona inspekta Kombora, pamoja na uchovu wake mwingi, akitoa maelekezo juu ya ulinzi wa jengo hilo. Akiwa na hakika kuwa mambo yalikuwa yamewaendea kombo waajiri wake, Adrian alitazama kwa makini jengo hilo huku rohoni akijua wazi kuwa japo jeshi zima la polisi liletwe kulinda usiku huo lazima angeingia katika jengo hilo na kuchukua kila kilicho chake.
Hakukuwa na mtu yeyote, duniani na mbinguni, ambaye angemzuia.
Kwa miji yote mikubwa ilivyo kote duniani, jiji la Dar es Salaam pia halijui usiku. Mara tu jua linapozama na kiza kutanda, wako baadhiya watu ambao huona kana kwamba ndio kwanza kumepambazuka. Hivyo, wakati wenzao wakijiandaa kulala wenzao hujiandaa kutoka tayari kwa shughuli zao mbalimbali, baadhi wakiwa wafanyakazi wa zamu za usiku, baadhi watumiaji tu wa pesa zao, hali wengine wakiwa waviziaji tu, wezi na Malaya wa bandarini.
Usiku wa leo Joram alikuwa mmoja wao. aliporejea toka muhimbili akiwa na aina mbalimbali za dawa ambazo alielekezwa jinsi ya kumpa Nuru, alimwamsha na kumshurutisha kuzinywa.
Kama alivyokuwa ameambiwa na daktari yule, mara tu baada ya kuzinywa, Nuru alichukuliwa tena na usingizi, usingizi mzito ambao ungempumzisha kwa saa ishirini na nne wakati dawa zikifanya kazi.
Baada ya kuhakikisha Nuru amelala kwa utulivu, ndipo Joram pia alipolala kando yake na usingizi mnono, usio na ndoto, kumchukua. Alizinduka saa moja usiku. Akafanya haraka kuoga, kisha kuvaa suti yake.
Baada ya hapo aliichukua bastola yake, bomu moja la mkono, kisu na silaha zake nyingine akazitokomeza katika mifuko yake ya siri. Alipojitazama katika kioo na kuridhika kuwa hata askari mdadisi kiasi gani asingemshuku kuwa anakwenda vitani badala ya kwenda kufanya matumizi, ndipo alipombusu Nuru, akamfunika vizuri na kisha kuondoka baada ya kuufunga mlango vyema nyuma yake.
Hakuwa na haraka. Alipita katika chumba cha maakuli ambako aliagiza ugali kwa kuku wa kuokwa. Wakati akisubiri chakula hicho alijipongeza kwa bia mbili za stella. Chakula chake kilipofika alikula kwa utulivu, huku akiteremsha kwa kopo la tatu la stella. Alipomaliza aliwasha sigara na kuivuta taratibu huku kopo la nne lilkikoza moshi. Saa yake ilipomwashiria kuwa imetimia nne kasorobo za usiku ndipo alipolipa bili yake na kuingia mitaani.
Kwa mwendo ule ule wa taratibu, alivuta hatua moja baada ya nyingine kuziendea ofisi za Kangaroo. Alijua fika kuwa watakuwepo na silaha zao mikononi. Hata hivyo, akiwa amedhamiria kuingia alikwishajiandaa kwa njia moja au nyingine ambayo ingemwezesha kuingia. Hivyo, hilo hakulitilia wasiwasi. Ambalo lilimtia wasiwasi na kumwongezea shahuku ya kufika aendako ni Adrian. Alikuwa na hakika kuwa Adrian, alivo kichwa maji, lazima pia angebuni kuingia katika jengo hilo. Na ni hilo lililomfanya awahi. Alitaka awe wa kwanza kufika katika jengo hilo ili amsubiri na kumpokea. Alijua fika kuwa mkutano wao wa ana kwa ana ulikuwa na maana moja tu, ya kumwacha mmoja hai, mwingine maiti. Joram alikuwa na uhakika kuwa huyo maiti asingekuwa yeye.
Wakati akikaribia ofisi hiyo, Joram aliichomoa tai yake nyeupe na kuisokomeza mfukoni. Kuondolewa kwa tai hiyo, kulimfanya abadilike ghafla na kuwa kama kivuli au sehemu ya kiza. Aliubadili pia mwendo wake na kuanza kunyata kwa uangalifu, toka ukuta hadi ukuta; kichaka hadi kichaka. Wapita njia waliomtazama kwa macho ya udadisi aliwapumbaza kwa kujifanya ama anajisaidia haja ndogo au anafunga kamba za viatu vyake, ama amelewa na hivyo, anakwenda bila mpangilio wowote.
Alipofika mbele ya Kangaroo, kama ivyotegemea, alimwona askari mmoja mwenye silaha na magwanda akiwa amesimama kuuegemea ukuta, bunduki yake kaishika mkono mmoja, wa pili ukiwa mfukoni. Joram alimtazama kwa makini. Akashangazwa na utulivu wa askari huyo. Alipotupa macho kutazama huko na huko hakumwona askari mwingine.
Akaitazama saa yake ambayo ilimuashiria saa nne na dakika kumi. Alihitaji kuwa katika jengo hilo mapema. Hivyo, alipoona askari huyo hatoki hapo aliposimama, aliamua kumfuata. Aliiwasha sigara yake na kuipachika mdomoni, akakohoa, kisha akaanza kumsogelea. Alitegemea kuambiwa simama au kupewa amri yoyote ile. Haikutoka. Joram alizidi kumsogelea hadi alipomfikia na kumsalimu. Hakuitikia.
“Hujambo, brother?” Joram alisalimu tena.
Bado hakuitikiwa, jambo ambalo aliona halikuwa la kawaida. Alimtazama askari huyo kwa makini zaidi na kubaini kuwa alikuwa hatingishiki, haoni wala hasikii. Alipojaribu kumtikisa aliporomoka na silaha yake na kuanguka sakafuni.
Ndio kwanza Joram akabaini kuwa alikuwa anaongea na maiti. Akainama na kumshika kifuani ambako alimkuta kapoa kitambo. Kiasi Joram alitahayari. Alitegemea ukatili. Lakini hakutegemea ukatili wa kiasi hicho. Kwa ujumla, aliondokea kuamini kuwa kipindi cha mauaji ya kinyama kilikuwa kimepita, wazo ambalo sasa alilijutia.
Hakuhitaji kuambiwa kuwa mauaji hayo yamefanywa na nani. Wala hakuiona haja ya kujiuliza kwanini yamefanyika. Adrian alikuwa amemtangulia. Akamwua askari huyo, bila shaka kwa hila, ili asiwe kipingamizi cha kumfanya ashindwe kuingia ndani. Hivyo, ama alikuwa ndani ama ametoka.
Wakati akiyafikiri hayo Joram Kiango tayari alikuwa ameusimamisha mzoga huo wa askari kama alivyoukuta na kuirejesha bunduki mkononi mwake na kuanza kunyata akielekea mlangoni. Kando ya mlango huo, kwenye kibanda kidogo cha mapokezi, Joram aliikuta maiti ya askari wa pili. Huyu alikuwa ameketishwa juu ya kiti na kuiinamia meza, bunduki mkononi. Joram hakuitaji kumgusa kujua kuwa amekufa.
Aidha, hakuwa na haja ya kumshika shingo ili kubaini kuwa lilikuwa limevunjwa kwa pigo kali la judo. Alichofanya ni kukimbilia ndani, ambako aliukuta mlango ukiwa wazi, kama unaomsubiri. Harakaharaka bastola yake ikiwa mkononi, alinyata toka chumba hadi chumba. Akitumia tochi yake yenye ukubwa wa kalamu, alichungulia kila kona, kila uvungu wa meza, kila kabati, kila uvungu wa friji, bila mafanikio. Kila dalili ilimwonyesha kuwa Adrian amekuja na kuondoka.
Joram akaziacha ofisi za kawaida na kuzifuata zile za siri ambako waliwazika hai Paul na Philip. Huko pia Adrian alikuwa amemtangulia na alichokifanya hakikustahili kutazamwa. Mateka hao wawili ambao yeye na Kombora waliamua kuwafungia hai, Adrian alikuwa amewachoropoa toka shimoni humo na kuwachinja kama kuku, mmoja baada ya mwingine. Miili yao, aliitupa juu ya sakafu na kuwafanya walale wakiwa wamekumbatiana ndani ya dimbwi la damu yao wenyewe.
Joram alikiacha chumba hicho na kukimbilia kile ambacho kilihifadhi mamilioni ya pesa za kigeni. Alisogeza sefu ambalo liliwekwa kwa geresha na kulifikia lile la siri ambalo liliunganishwa na ukuta kwa hila. Alipojaribu kulifungua alishangaa kulikuta likiwa wazi. Pale ambapo palikuwa na vitita vya noti za ndani na nje sasa hapakuwa na kitu chochote. Hapana, palikuwa na kitu fulani, kitu kidogo, cheusi. Joram aliisogeza tochi yake na kutazama. Kama macho yake yalichelewa kumwashiria yanatazama nini, pua yake haikuchelea kufanya hivyo. Kitu hicho kilikuwa kinyesi. Baada ya kuchukua pesa hizo, kwa kuonyesha dharau, Adrian, akijua mtu yeyote angetamani kuzipata pesa hizo ndipo alipoamua kufanya hivyo. Mara ya kwanza maishani mwake hasira hizo zilimfanya atetemeke mwili mzima. “Mshenzi” aliropoka kwa mara ya pili. “Haendi popote! Kamwe haondoki nje ya nchi hii akiwa hai,” alinguruma akigeuka kuanza kutoka nje ya chumba hicho taratibu kwa mwendo wa sismba aliyejeruhiwa mwili na roho.
Simulizi : Sikutegemea Sehemu Ya Kwanza (1) Ama kweli mwanaume wa kweli hakimbii shida, kwa jina naitwa Adam. Ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto wawili, yaani mimi na kakaangu. Sio kwamba tulikuwa na maisha mazuri sana lakini kila nilichokitaka nilikipata kutoka kwa wazazi wangu. Wakati nikiwa kidato cha pili kakaangu alioa na kuondoka, aliishi na mkewe sehemu moja inayojulikana kama Kijichi kisiwani Zanzibar. Maisha yaliendelea kuwa mazuri huku nikiwa na ndoto za kuwa mtu wa maana sana katika jamii, lakini ndoto zote hizo zilizima baada ya wazazi wangu wote wawili kuaga dunia katika ajali ya meli.
Wakati huo nilikuwa nimeshamaliza kidato cha nne na nilikuwa nasubiria majibu, lakini hata yalipotoka sikuweza kuendelea kusoma kwa sababu hakukuwa na mtu wa kunisomesha. Nilitegemea labda kaka angeniendeleza lakini yeye mwenyewe maisha yake yalikuwa duni sana. Nilikaa nyumbani nikisubiria fungu langu la urithi ambalo ndani ya akili yangu nilidhamiria nikilipata nijiendeleze mwenyew. Ama kweli dunia hadaa ulimwengu shujaa na na ukistaajabu ya Mussa utayaona ya firauni.
Jamaa zetu walizigombania hizo mali kidogo zilizoachwa na wazazi wetu na kugawana wao kwa wao. Na hilo pia lilipelekea kufukuzwa nyumbani na nyumba ile kuuzwa. Kiufupi sikubakiwa na kitu chochote kile zaidi ya nguo nilizokuwa nimevaa. Taarifa zilimfikia kakaangu na hapo akaamua kunichukua nikaishi kwake, nilishukuru Mungu japokuwa sikujua kumbe huko nako kuna majanga mengine.
Kaka alikuwa akijishughlisha na masuala ya uvuvi hivyo muda mwingi hakuwa nyumbani, nilibaki mimi na shemeji yangu tu. Nae alianza kunifanyia vitimbi, kuna wakati hakunipa chakula kutokana na sababu anazozijua yeye mwenyewe. Hilo halikuniumiza sana kwani kula hata mtaani nilikuwa napata kutoka kwa marafiki zangu niliowakuta eneo hilo. “kaka kwanini na mimi usinichukue bahari usiku nikajifunze kuvua” siku kaka alikuwa nyumbani na nikapata muda wa kuongea nae. “mdogo wangu bahari isikie kama ilivyo” alinijibu, “ah unajua kukaa nyumbani kama mtoto wa kike nimeshachoka na mimi nataka niende baharini nikajifunze uvuvi, pia hio itasaidia na hapa nyumbani” nilijaribu kuwa mbishi mpaka mwisho akanikubalia.
Maisha yangu mapya kama mvuvi yalianza, siku za mwanzo nilipata sana shida hasa ukizingitia uvuvi wetu ulikuwa ni wa usiku sana. Lakini kadiri siku zilivyokwenda nilianza kuzoea mpaka na mimi nikawa bingwa sasa. Miaka miwili ilipita kama upepo na vitimbi vya shemej yangu vilizidi ndani ya nyumba. Sasa alikuwa akinitaka kimwili jambo ambalo sikuwa tayari kulifanya, mara kadhaa alinitishia kuwa akirudi kaka atamwambia namtongoza.
Nilivumilia mwanzo lakini mambo yalizidi kuwa mabaya maana alikuwa akinifata chumbani kwangu hata kama kaka yupo. Mshare wa hatari ukagonga kichwani mwangu na hapo ukawa umefika muda wa kufanya maamuzi magumu. Siku hiyo nilijifanya naumwa ili nibaki nyumbani, baada ya kaka kuondoka kuelekea baharini nilichukua begi langu na kuchukua nguo kadhaa. Kimya kimya bila hata kuaga nilitoroka nyumbani.
Moja kwa moja mpaka bandarini, nilikata tiket ya meli ya usiku huo kuelekea jiji lenye heka heka za kila aina za maisha nalo si jingine bali ni jiji la Dar-es-salaam. Meli iling’oa nanga saa nne usiku na safari mpya ya maisha yangu ikaanza, “oi mwanangu niaje” wakati nikiwa nimepumzika nilisikia mtu akinisalimu. “shwari kama kawa” nilimjibu, “mimi naitwa Frank” alijitambulisha. “nashukueu kukugahamu Frank, mimi naitwa Adam” nilimjibu huku nkimpa mkono. Hapoo ndio ulikuwa mwanzo wa urafiki wetu.
Tuliongea mengi sana na kumwambia kuwa mimi ni mgeni huko ninapo kwenda, “usijali ndugu yangu sisi wote tunakwenda huko kutafuta” aliongea Frank kisha akaendelea “mimi ni dereva wa bodaboda huko sehemu moja inaitwa mbezi makonde”. “mimi hata sikuaham huko napasikia tu” nilimjibu, “tukishuka tufatane huenda ukapata shavu huko, kuna vibosile vingi tu vinatafuta vijana wa kazi hasa madereva wa bodaboda” alinijibu na kunipa moyo. “lakini ndugu yangu mimi hiyo pikipiki kuendesha sijui”. “usijali ndugu nitakufundisha kisha ntakusaidia kutafuta ajira” aliongea huku akinipiga begani. “ama kweli dunia bado ina watu wenye huruma” nilijiesemea moyoni, meli ilitia nanga saa kumi na mbili asubuhi. Abiria wote tukashuka, niliongozana na Frank mpaka nje ya bandari na kuchukua kibajaji mpaka kariako. Huko tulipanda magari kuelekea tegeta na kushuka mbezi, 2karibu nyumbani aisee” Frank aliongea wakati tunaingia katika chumba kimoja kidogo sana cha kupanga. Hata hivyo nilishukuru sana maana sikujua hata nikifika nitakaa wapi lakini kama ilivyo Mungu hamtupi mja wake, akaniletea muokozi.
Maisha yalianza hivyo hivyo japo yalikuwa magumu sana kutokana na mimi kutokuwa na kazi, wakati huo Frank alikuwa akinifundisha kuendesha pikipiki. Baada mwezi mmoja nilikuwa nimeiva vizuri sana, bila kuchelewa nilianza kufatilia mchakato wa leseni na kufanikiwa kuipata. Franka alinitembeza kwa mabosi anaowajua na kufanikiwa kupata ajira kwa mama mmoja hivi wa kizaramo. Kuanzia hapo maisha yangu yaliingia tumaini jipya, nilifanya kazi kwa bidii sana huku nikijathidi kuweka pesa kwa ajili kuja kununua pikipiki yangu mwenyewe.
Kwa wakati huo nilikuwa na miaka ishirini na mbili, uaminifu wangu ulimpendezesha bosi na kuniacha pikipiki nifaye kazi hadi usiku. Maisha yalizidi kuwa mazuri huku mimi na Frank urafiki wetu ukizidi kuota mizizi, “oyaa, wewe mpemba kichaa”mtu mmoja aliniita. “halafu we si nmekwambia usiniite hilo jina” nilimlibu huku nikikaza macho. “ah wapi, mimi ntaendelea kukuita jina hilo hata kama hulipendi, we umesikia wapi mpemba akawa dereva wa bodaboda. Nyinyi kazi yenu uvuvi huko na si kuvamia kazi za watu” alizidi kuongea. “Jackson acha utani wewe, eti wapemba kazi yao uvuvi” Frank aliongea huku akicheka.
Hayo yalikuwa ni matani ya kawaida kila siku, walizoea kuniita mpemba kichaa mpaka jina hilo likazoeleka maeneo yote ya karibu. Ukweli nilipata marafiki wengi sana tafauti na nilivokuwa nikifikiria kipindi niko kisiwani. Nilikuwa najua Dar kuna wezi na matapeli ile mbaya lakini kumbe zilikuwa stori tu japo zilikuwa na ukweli ndani yake. Lakini niliowapata mimi walikuwa marafiki wa kweli na kila siku nilikuwa nikimshukuru muumba wa mbingu na ardhi.
Siku moja nikiwa kijiweni nasubiria, niliwasikia washkaji wakiongelea mchakato wa kuzamia nchi za magharibi. Maongezi yao yalinifanya nitege masikio vizuri maana na mimi nilikuwa nina hamu ya kuwa na maisha mazuri. Na nilidhani ukifika tu huko nchi za magharibi basi ndio unasahau kabisa shida. “unasikia mtu kuna meli huwa inakuja Tanzania kwa mwezi mara moja tu, na ktika hiyo meli kuna mzungu ukichinga nae fresh tu basi anakupenyeza halafu ndio kwa heri shida2 aliongea kijana mmoja. “mwanangu wasema kweli au watania wewe” James aliuliza kwa lafudhi yake ya kitanga.
“sasa mtu wangu nikutanie vipi wakati mifano hai ipo, si munamkumbuka yule mshkaji alikuja kutoka Tabora”, “ndio halafu yule dogo kapotea mwaka wa pili huu”. “ah kapotea wapi yule, dogo anakula shavu kwa Obama huko”, “ebwnaee”. “unataka kusema dogo kazamia mbele huko”, “ndio mimi ndo nilimfanyia mpango”. “sasa mbona wewe uko hapa leo”, “ndugu yangu wee, nilikuwa sina hela ya muhonga mzungu”. Kwa kweli mazungumzo hayo yaliniingia akilini kisawa sawa na kujikuta nikitamani na mimi niende huko wanapopaita kwa Obama sijui kwa malikia.
Niliendelea kufanya kazi huku nikiwa nawaza ntampataje mshkaji ili anipe mchongo kama vipi na mimi nizamie kwa ngozi nyeupe huko nikale bata. Baada siku mbili wakati nasubiria wateja usiku nilimuona yule mshkaji alieongelea kuhusu kuzamia. Niliwasha pikipiki na kusogea alipo, nilimpa ishara apande kisha nikaondoka eneo hilo. Nilipofika sehemu ambao niliami tutaongea wa faragha nilisimamisha pikipiki. “mambo niaje mwanagu” nilimsalimu, “Shwari tu kama kawaida” alinijibu huku akishuka.
“ebwana juzi wakati unaongelea kuhusu kuazamia aisee ulinivuta sana” nilimwambia bila kuficha, “kwa hiyo ndugu yangu unataka kuibuka kwa Obama sio” aliniuliza. “ndio maisha bongo magumu sana”, “una hela ya kutosha kumuhonga huyo mzungu”. “kwani ni kiasi gani?”, “ah sio hela ndefu sana, ni milioni mbili na kidogo tu”. “dah kwani hiyo meli inakuja lini?”, “hiyo itaingia bandarini mwezi wa sita huko”. “basi mpaka muda huo hela itakuwa ishakamilika”, “hamna noma we ukiwa tayari unaweza kunishtua tu”. Tulimaliza kuongea na kubadilishana namba za simu na kuahidi kuwa hiyo iwe siri kati yetu. Niliondoka hapo na kuendelea kazi yangu huku nikipania kufanya kazi ya ziada ili kutimiza kiasi cha fedha kinachotakiwa. Kwa wakati huo nilikua na kama milioni na nusu hivi, niliiweka pesa hio ili nije kununua pikipiki yangu. Lakini wazo hilo lilikufa baada ya kuingia tamaa ya kwenda huko kwa Obama. “ama kweli tamaa mbele mauti nyuma” niliusahau kabisa msemo huo, nilinza kupiga kazi kwa bidii mpaka Frank akawa ananishangaa lakini aliponiuliza nilimdanganya kuwa nataka kununua pikipiki yangu. Miezi ilikatika haraka na hatimae mwenzi wa sita nilimtafuta yule jamaa, “mzigo nnao wa kutosha sasa bipi kuhusu ile ishu tulioongea”. “hakuna noma meli imeingia juzi na sasa hivi wanapakuwa mizigo, inabidi kwanza tukaongee na huyo jamaa maana haikai sana itaeleekea kwa Mandela”.
Nilikubaliana nae na kuchoma mafuta mpaka Oysterbay ambapo ndipo anapokaa huyo baharia wa kizungu, jamaa alitoa simu na kuwasiliana nae na baada ya muda alitoka na kutonyesha ishara tumfate. Tulitafuta sehemu iliotulia na kuanza kuongea, muda wote mimi nilinyamaza kimya kwasikiliza wao wakionge. Baada robo saa jamaa aliniita pembeni, “mwanang mchono umetiki” alipoongea hivo nilitamani kumkumbatia lakini si unajua tena. “sasa nipe hiyo bahasha nimkabidhi” aliongea na hapo nikatoa bahasha na kumkabidhi. yule mzungu alizito zile pesa na kuanza kuzihesabu, na alipomaliza alitabasamu na kunionyesha dole gumba akimaanisha zinatosha. Yaani niliztoa milioni mbili na laki sita ambazo nilizitolea jasho kuzipata kirahisi rahisi sana.
Yule jamaa alienipeleka alirudi na kunambia tuondoke, niliwasha pikipiki na safari ya kurudi mbezi ikaanza. “safari lini?”nilimuuliaza, “jumamosi inayofuata, na unatakiwa ufike pale pale tulipokutana nae saa tatu usiku” alinambia na hapo nikafunga mdomo kuwa makini na barabara nisije kufa kabla sijafika nnapopataka. Tulifika mbezi na kumuacha jamaa sehemu ambayo ni mbali na kituo, niliendelea na mizunguko ya kawaida huku nikiwaza safari tu.
Hatimae siku ya safari ilifika, siku hiyo nilirudisha pikipiki kwa bosi mapema kwa kisingizio nimepata simu ya ghafla kutoka kwa mtu ninae mfahamu kutoka Zanzibar. Alinielewa na kunipa laki tano kwa ajili ya safari. Nilijisikia vibaya sana lakini sikuwa na jinsi, akili yangu ilikuwa ikiwaza mambo mazuri yanayonisubiri nchi za magahribi. Niliaga nakuondoka kurudi nilipopanga, “oya mbona unapanga, vipi kaka?” Frank aliniuliza. “ah nakwenda Zanzibar kidogo, nimepakumbuka sana” nilimdangaja, “afadhali hata unataka kurudi kwenu, ni miaka takriban miwili sasa imepita hujapatia mguu” Frank aliongea huku akitabasamu.
Nilimaliza kupanga nguo mbili tatu, nikafunga begi. Nilimuaga Frank na kuondoka, nilipanda boda boda mpaka maeneo ya Posta. Nilifanya hivo ili nisishtukiwe, baada yule jamaa kuondoka niliita bajaji na kuelekea Osterbay ambapo ndipo nilikubaliana nikutane na yule mzingu. Nilifika Osterbay na kushuka, nilimlipa mwenye bajaji na kuanza kutmbea. Na kwasababu ilikuwa saa tisa, ilibidi niatafute pahali nikae kwanza kwa ajili ya kuusongesha muda mbele. Nilikaa sana huku mara kadha nikizungunguka, nilikumbuka kuwa maji ni muhimu. Hivyo nilinunua chupa kadhaa za maji na kuzitia kwenye begi langu. Niliendelea kusubiri mpaka saa tatu ilipotimia, nilimuona yule mzungu akija upande wangu.
Wala hakufika sehemu niliopo, alinipa ishara nimfate. Niliinuka haraka na kuanza kumfata, alitangulia mbele huku akiwa makini sana. Tulifika mpaka kwenye gari yake, tulipanda na safari ikaanza. Tulipofika katika geti la kuingia bandarini alinipa ishara niiname kujificha, nami nikafanya hivo. Baada ya maongezi ya sekunde kadhaa na walinzi pale getini, aliruhusiwa kupita. Moja kwa moja mpaka kwenye meli moja kubwa sana, aliipandisa gari mpaka ndani ya meli kuendelea mpaka sehmu moja ambayo nahisi ilikuwa ni ya kuwekea magari.
Alishuka kisha akanambia na mimi nishuke, tulitembea kwa umakini mkubwa mpaka kwenye mlango mmoja hivi. Aliufungua na kuanza kushuka ngazi kuelekea chini, tulifika kwenye chumba fulani hivi na kufungua mlango. Macho yalinitoka kukuta vijana wengine kama mimi, wavulana kwa wasichana wakiwa wamejazana ndani ya chumba hicho. “kijana utakaa humu na wenzako” aliongea hivo na kunikabidhi box dogo la biskuti, “hichi ndio kitakuwa chakula chako, utakuwa unakula moja kila baada ya siku tatu na maji nitakuwa nawaletea mimi” alimaliza kuongea na kukifunga chummba hicho.
Niliwaangalia wale wenzangu na kutabasamu kidogo, niliona tayari nimeshapata marafiki wa kuanza nao maisha tukifika. Mashine za meli ziliwaka mnamo saa nane usiku, na baada muda kidogo nilisikia ikipiga honi kuashiria kuwa ilikuwa inang’oa nanga. Moyo wangu uliingiwa na amani na kuhisi kuwa nimetuwa mzigo mkubwa wa dhiki. Ama kweli usilolijua ni sawa na usiku wa giza na ng’ombe wa masikini hazai. Meli hiyo ilikuwa ikitembea taratibu sana, kuna baadhi ya wakati vijana wengine walitapika kutoka na kuchafuka kwa bahari.
Kuna wakati ilisimama na nilihisi kuna vijana wengine waliingizwa katika vyumba vingine, safari hiyo ilendelea huku kila siku nikipanga mipango mingo sana. Kuna wakati mawazo kama “nikifika huko niwe msanii au niwe muigizaji”, “nikifika huko niwe muuza madawa ya kulevya maana ya hela sana” yalipita katika akili yangu. Meli ilisimama tena sehemu na baada masaa kadha nilisikia milango ikifunguliwa, hiyo iliashiria kuwa vijana wengine waliingizwa kwa siri.
Kadri siku zilivyokwenda ndio hali ya bahari ilizidi kuwa mbaya, huku vijana wengi walitapika hadi kupoteza fahamu. Wengine walitapika mpaka kujisaidia haja ndogo na kubwa hapo hapo, ilimradi ilikuwa ni karaha ndani ya chumba hicho. Harufu ilikuwa mbaya sana, utasema tulikua tunaishi katika karo la mavi. Hata hivyo ilifikia wakati hiyo harufu sikuisikia tena, masikini mimi nilipojiangalia niligundua kuwa nilikuwa nimekonda sana.
Hapo sasa nikaanza kujuta kwanini nimefanya maamuzi ya kijinga namna ile, lakini ningefanyaje na wakati maji nilishayavulia nguo na sikuwa na budi kuyaoga. Mwili wangu ulijaa ukurutu kutokana kutooga kwa muda mrefu sana. Yaani tulikaa ndani ya chumba hicho mpaka tukasahau siku zinaendaje huko duniani maana hata jua tulikuwa hatulioni. Ukweli hali ilizidi kuwa mbaya katika vyumba hivi tulivyofichwa, isitoshe tulikuwa wengi sana lakini tungefanyaje na kila mmoja alikuwa ya kufika magharibi. Tukiwa humo ghafla meli ilisimama, tulidhani kuwa tushafika. Wengi tulianza kutabasamu lakini tabasamu hizo zilipotea baada ya kufunguliwa na kuingia wanaume watatu wakiwa na mitutu mkononi. Walituamuru tusimame na kuongoza njia kuelekea nje ya vyumba hivyo. walitupeleka mpaka juu kabisa kwenye deki na huko sasa nilipigwa na mshangao mzito baada kuona idadi yetu ilikuwa kubwa sana.
“nyinyi ndio munaopenda kuzamia, si ndio?” aliongea mtu mmoja aliekuwa katika mavazi ya kinahodha. Moyo ulianza kunienda mbio na hapo nikaanza kukumbuka hadithi za mtaani, eti ukikamatwa na mabaharia aidha ufanywe mwanamke au wakutose majini uliwe na samaki au ufe mwenyewe. Na asikwambie mtu kifo cha maji kibya sana, kwasababu hufi mpaka pale utakapokuwa ushakunywa maji mengi sana na mwili hauna tena pumzi. Yaani unakufa taratibu huku unajiona kabisa lakini huwezi fanya chochote.
“si nimewauliza nyinyi” alifoka tena kisha akaendelea “sasa ni hivi, hapa inadidi uchague kuwa mke wetu au tukutoe sadaka baharini ukaliwe na samaki”. “halafu mimi huwa napenda sana makalio ya kiume” aliongea baharia mmoja amabe alionekana kuwa na uchu wa ngono. Ilikua ni rahisi kumjua kutokana na kuwa tayari suruali yake ilishatuna maeneo ya zipu. “eti mwanaume mzima nikubali kulawitiwa” nilijisemea moyoni, nilipoangalia pembeni nilmuona binti mmoja mrembo sana wenye asili ya kisomali. Alikuwa kitetemeka si mchezo, mimi mwenyewenilikuwa nikitetemeka lakini nilijikuta nikimuonea huruma. “masikini sijui amekimbia vita huko kwao, na huku anakutana na msala mwengine” nilijisemea moyoni.
Nilianza kuangaza huko na kule kutafuta kama kuna kisiwa karibu, kutokana na uzoefu wangu baharini niliweza kugundu kuwa kipo kisiwa japo kuwa kilikuwa mbali kidogo. “ehe nani nani yuko tayari kuwa chombo chetu cha starehe?” aliuliza baharia mmoja. Hapo niliwaona wadada wawili wakisoge mbele kuashiria walikuwa tayari kutumika kama chombo cha starehe ili kuokoa maisha yao. Mabahria wawili walishaki wale wadada na kuwavua nguo kisha wakaanza kuwafanyia ushenzi wao mbele yetu. Na mbaya zaidi waliwaingilia sehemu zote mbili huku mmoja wao akiwa na camera akirikodi uchafu ule.
Masikini wadada wa watu walipiga sana kelele na kulia kwa nguvu kutokana na maumivu wanayoyapata pale walipongiliwa kinyume na maumbile. Hata hivyo wale jamaa hawakuacha kuwafanyia walichokuwa wanakifanya mpaka pale walipofika mshindo mkuu. Waliwapiga risasi na kuwatosa baharini, “unapopakuliwa hutakiwi kulia” aliongea mmoja miongoni mwa wale washenzi wawili. “kama mbwai na iwe mbwai tu, mimi mtoto wa kiume siwezi kufanya shoga bora hata nife majini ili nipate kujitetea mbela za Mungu” nilijisemea moyoni na kumwangalia yule binti wa kisomali. Nilimfanyia ishara kama anajua kuogelea nae akatikisa kichwa kuashiria kuwa alikuwa anajua.
Nilivuta pumzi kwa nguvu kwa maana nilielewa kitendo ninacho kwenda kukifanya kinaweza kunigharimu maisha yangu. Nilimshikia mkono yule binti na kukimbia nae, nilipofika mwisho sikujishauri, nilimvuta kwa nguvu na kuruka nae majini. kwa mbali nilisikia milio ya risasi lakini wala sikujali, kutokana na uwezo wangu mkubwa wa kuogelea pia na wa yule binti tulifanikiwa kufika mbali na kuibuka. Nilipoangalia kule kwenye meli niliwaona vijana wengine wenye roho za paka kama mimi wakijitosa majini.
Sikutaka kupoteza muda hapo maana nilielewa tukiendelea kung’aang’aa macho macho sehemu hiyo huenda wale jamaa wakatufuata. Nilimpa ishara yule binti anifuate na kuanza kuogelea, tuliogelea kwa muda mrefu sana. “mimi nimeshachoka” aliongea yule binti, “jitahidi tu muda si mrefu tutafika” nilimjibu uongo ili mradi tu asikate tamaa. Alikubali na tukaendelea kukata maji, sasa kiza kilishaanza kuingia. “naomba niache nife wewe endelea na safari na nshkuru kwa msaada wako” yule binti aliongea kwa tabu sana na kabla sijamjibu alianza kuzama. “mimi sijakuokoa uje kufia mikononi mwangu” nilijisemea na kumshika kisha ni
Sijui hata saa ngapi nilipoteza fahamu ila nilikuja kushtuka baada kuhisi kitu baridi kikinigusa mdomoni na kunisaidia pumzi, wenzetu wanaita busu la kuokoa maisha (kiss of life). Nilipoangalia vizuri niligundua kuwa nilikuwa ufukweni, na yule binti alikuwa pembeni yangu ananiangalia. “sijawahi kuona mtu mbishi kama wewe, yaani unathubutu kupambana na kifo” aliongea binti huyo huku akitabasamu. Tabasamu ambalo liliuchanua uso wake na kuuthibitsha urembo wake, “siku yetu ya kufa ilikuwa bado” nilimjibu huku nikijizoa zoa na kukaa kitako.
“mimi naitwa Adam” nlijatmbulisha maana mpaka muda huo tulikuwa hatujuani majina, “mimi naitwa Latfina au Latifa kama wengi walivyozoea kuniita Tanzania” alijibu akitabasamu. “hivi ulijuaje kama kuna kisiwa maeneo haya” aliniuliza, “ah niliwahi kuwa mvuvi huko nyuma, so nilijifunza kusoma mazingira ya bahari poja na mwenendo wa mawimbi na hicho ndicho kilichonisaidia kujua kama kuna kisiwa karibu japo sio karibu kama nnavyokusudia” Nilimjibu huku nikisimama. Lakini nilishanga kujikut sina nguvu hata kidogo, “pumzika kwanza, umechoka sana” Latifa alinambia.
Tulikaa ufukweni kwa muda mrefu kabla kuanza kuona miili ya watu ikisukumwa ufukweni na mawimbi. Sijui hata nguvu nilito wapi, nilisimama na kukimbilia kwenye maji na kuanza kuwavuta mmoja mmoja na kuwaweka ufukweni. Nilishangaa kumuona Latifa akiwashika mikono chini kidogo kwenye kiganja, “unafanya nini?” nilimuuliza. “inawezekana wengine hawajafa hawa” alinijibu huko akisilizia kwa makini, ghafla alianza kumgandamiza kifua na kufanya kama anasukuma hivi. Ghafla alizinduka huku akikohoa na kutema maji.
Basi tuliendelea hivo huku mimi nikijatahidi kuwaleta nchi kavu, Latifa akiwapatia huduma ya kwanza wale waliobahatika kuwa hai. Wakati nikiendelea kusubiri miili ifike nchi kavu kwa mbali nilimuona mmoja akiwa anapapatuana na maji, na alionekana kuchoka sana. Nilipiga mbizi na kumfuata alipo, nilimshika na kurudi nae nchi kavu. Tulipofika kwanza wote wawili tulilala chali huku tukihema kwa nguvu, baada ya mua kidogo niliinuka na kumpa mkono. kwa msaanda wangu alisemama na kuelekea walipo wenzetu. “kati ya watu mia waliokuja nchi kavu ni watu ishirini na mbili tu ndio wamepona, wengine wote wamepoteza maisha” Latifa aliongea kwa huzuni kidogo.
“samahani bro, nashkuru kwa msaada wako, kwa jina naitwa Louise” aliongea yule kijana nilieenda kumuokoa, “usijali Louise tushukuru Mungu kwa kutupa uwezo wa kuwa hai mpaka saa hivi, mimi naitwa Adam na huyo nesi hapo anaitwa Latifa” nilimjibu na kujitmbulisha pamoja na kumtambulisha Latifa. Wakati huo njaa ilikuwa inanisumbua kweli kweli, taratibi nilianza kusogea kwenye miti. Niipofika nilianza kukata majani na kula, asikiwambie mtu njaa mwanakharamu. Wale wengine wote walivyoona nakula majani na wao walikuja mbio na kuanza kufakamia majani ya miti amabyo wengi wetu tulikuwa hatuijui.
“unajua Adam kukaa hapa ufukweni ni hatari sana” aliongea Louise kunambia, “kwanini?” nilimuuliza. “bora tuingie humo msituni huenda tukawa salama zaidi” aliongea, na kwa upande mmoja wazo lake lilikuwa la msingi sana. Baada jushiba majani tuliitana wote na kushauriana kama vipi tuingie msituni. Wengi waliliunga mkono wazo hilo na bila kuchelwa tunajongea na msitu huo ambao hatukujua tungeishi kwa muda gani. Tulitembea kwa dakika kama ishirini hivi mpaka tulipofika pahali kwenye uwazi kidogo, kwa kweli sikuwahi kuona sehemu nzuri kama ile. Kulikuwa na maporomoko ya maji safi yasio chumvi hata kidogo, kulikuwa na miti yenye matunda pamoja na ndege wa aina mbali mbali. Kila mtu alikimbili katika bwawa ambalo maji yalikuwa yakimwagika kutoka katika bonde la karibu. Wakati wenzetu wakifurahia maji; mimi, Louise na Latifa tulikaa tuli tunawaangalia. Wengi walionekana kufahamiana lugha tafauti na sisi ambao tulikuwa pekeetu. Mimi ndie mtanzania pekee niliokoka kutoka katika ile meli, Latifa ni msomali na Louise ni mnamibia. Tuliongea Lugha tatu tofauti lakini hawa wawili walikuwa wakikifahamu kiswahili japo si sana.
Kiza kilianza kuingia na hapo tugawanyika katika makundi kadhaa, huku kundi letu ltukiwa sisi pekeetu. “unajua kwa hii hali ilivyo, huenda baadae ikanyesha mvua” aliongea Louise, “dah na hakuna hata sehemu ya kujikinga” aliongea Latifa. “msijali marafiki zangu mimi najua kutengeneza vibanda kwa kutumia vichaka na vina uwezo kutukinga na mvua bila tatizo” Louise aliongea hukua akiangaza huku na kule. Alipona kichaka kilichoshona miti mingi alikisogelea na kuingia ndani japo kwa shida kidogo, nipeni dakika kama ishirini hivi kitakuwa tayari” aliongea akiwa ndani ya kichka hicho.
Tulianza kusikia miti ikikatika katika, kichaka hicho kilikuwa kikitingishikwa kwa juu. Lakini maajabu ni kwamba, haukuonekana hata mti mmoja ukikatika kwa juu. Baada kama dakika kumi na tano hivi alitoka na kuniambia nimfuate. Tulitembea mpaka kwenye miti fulani hivi inafanana na migomba, tulikata majani kadhaa na kurudi nayo kwenye kile kichaka. Aliingia ndani na kuendelea na kazi yake, baada muda kidogo alitoka na kutuamabia tuingie. Loo sikuamini macho yangu kwa jinsi kile kichaka alivyokichonga ndani. Kilikuwa kam kijichumba flani hivi kidogo kidogo, “mimi na wewe tutalala hapo” aliongea huku akininyooshe kidole. “na mimi je?” Latifa aliuliza, “wewe utaingia hapo kwenye hiyo kuna, ndio kuna kijisehemu chako. Wewe unahitaji uhuru wa kutosha so nimekuandalia hico kijisehemu ambacho utakuwa unaweza kufanya mambo yanayokuhusu wewe na kulala unavotaka” alijibu Louise.
“hivi kweli maji hayawezi ingia humu?” nilimuuliza kwa mshangao kidogo, “ndio na kama huamini subiri mvua inyeshe” alinijibu. “sasa huko nje mtu si ataona mlango wa kuingilia ndani?” aliuliza Latifa, “hapana mtu hawezi gundua kama katika hichi kichaka kuna watu wanaishi labda aone alama za miguu. Na hilo ni gumu sana kutokana na kuwa mvua katika sehemu kama hizi hazikati hivyo hata hizo alama za miguu zitakuwa zinafutika” alijibu Louise. Wakati tukiendelea kuongea ghafla mvua ilianza kunyesha, nilisubiri kwa hamu ili kuthibitsha maneno ya Louise. Na kweli halikupa hata tone moja la maji ndani ya kichaka hicho.
“hivi umewezaje kutengeza hivi?” ilibidi niulize ili kutoa dukuduku langu, “mimi ni mwanajamii wa jamii za kiwindaji zinazopatikana Namibia, kabila langu ni Khosa ama san kama wanavoita watu wengine. Pia vijana wengi wa siku hizi wanatuita Bushman baada ya kuona ile filamu ya the gods must be crazy” alipofika nilitamani kucheka lakini Latifa alinifinya na kunifanya nitulie. “wazazi wangu walitaka nijifunze mila zetu hivyo wakaamua kuniondoa mjini na kunipeleka kwa babu yangu ambae bado yeye alikuwa anaishi kimila zaidi, huko nilifundishwa kuwinda. Pia nilifundishwa jinsi ya kugundua miti ambayo ni dawa na miti ambayo ni sumu. Pia nilifundisha jinsi ya kutengeza makazi ya muda mfupi ikiwa usiku utanikuta porini na mambo mengine mengi tu” aliendelea kutusimulia.
“sasa kwanini umeamua kuzamia” ilibidi nimuulize, “ah si unajua tena kila mtu siku hizi anataka maisha ya kisasa yaliojaa starehe, na hicho ndicho kilichonifanya nitoroke kule kwa babu. Na mpaka sasa wazazi wangu wanajua niko kwa babu yangu kwa sababu hakuna njia ya mawasiliano isipokuwa kufika tu huko anapoishi babu. Kwa kweli najuta kwanini nimefanya maamuzu ta kipumbavu sana wakati kila kitu ninachokitaka nilikuwa napata” alipofika hapo alianza kulia, ilibidi tumnyamazishe na hapo ndio ukawa mwisho.
Kwa vile kiza kilishaingia wala hatukutoka tena kwenye kichaka hicho ambacho ndicho tulikifnya kama nyumba yetu. Asubuhi na mapema tulitoka na kuelekea kwenye lile bwawa ambapo tulikuta wenzetu kadhaa wakiwa washaamka. Kila mtu alitafuta upande wake wa kuoga na kumaliza haja zake zote. “sasa hapa tatizo linabaki chakula” niliongea kwa sauti ndogo kama mtu aliekuwwa hataki kusikika. “ah na matunda na miti yote hii iliojaa ufe njaa kweli, utakua huna akili” Louise alinisikia na kunijibu.
Wakati tukiendelea kuongea, Latifa alifika na kuunga maongezi. “Tuingie ndani zaidi huenda tukapata matunda mazuri” Louise aliongee na kusimama. Mimi na Latifa tuligate kwa nyuma, tulitembea huku tukichuma matunda aina tofuti na kubugia. Tuliposhiba tulibeba na mengine kisha tukarudi walipo wenzetu. Kwa kweli hata tulikuwa hatujui siku zinaendaje, maana sisi tulikuwa tunaishi tu ili kuokoka. Pia tulikuwa na matumaini kama huenda meli nyingine ikapita na kupata msaada wa kuondoka katika kisiwa hicho, hivyo hatukuacha kutembelea ufukweni.
Wiki ilikuwa ishakata huku wenzetu wengi wakionekana kujisahau kama wapo kwenye dhiki, kuna wakati walikuwa wakifanya mapenzi kama wanyama tu. Walifanya kweupe huku wengine wakishuhudia na kushangilia. Tulijaribu kuwaonya kuwa huenda tukawa hatupo pekeetu kwenye kisiwa hicho lakini walionekana kutoelewa kabisa. Ilibidi tuwaache wafanye wanavyotaka maana ilifika wakati mpaka tukawa tunagombana.
` Siku moja wakati tukiwa tunaongea mawili matatu, nilianza kusikia harufu fulani hivi ya moshi. Harufu hio haikuwa ngeni puani mwangu, “tungieni ndani haraka” nilipiga kelele huku nikionesha ishara ya hatari. Bila kupoteza muda mimi, Louise na Latifa tuliingia ndani ya kichaka chetu na kujificha. Haukupita muda nilianza kuhisi maruweruwe na kuanganguka sehemu niliokaa na kupoteza fahamu
Nilishtusha na mangurumo mazito huku yakiambatana na mvua kali sana, niiangaza pembeni ambapo niliwaona Louise na Latifa. Kila mtu alikuwa amelala anavojua mwenyewe, “Louise, Louise…Latifa amkeni” niliwaita huku nikiwatikisa. Louise alikurupuka kama mtu aliechomwa na mweba, “kuna nini?” na kuuliza, “mimi mwenyewe sijui lakini nahisi tumelala muda mrefu sana” nilimjibu. “Latifa amka” nilimuamsha na Latifa ambae aliamka kwa kujizoa zoa na alionesha amechoka sana.
“hivi imekuaje tukalala bila kujitambua” aliuliza Latifa punde tu baada ya kuamka, “ni ile harufu ya moshi” nilijibu na kuwafanya wote waniangalie. “ule moshi ni kemikali aina chlorofom au nusu kaputi, inavyoonekana katika hichi kisiwa kuna watu wengine” nilifafanua na kuongezea. “unamaanisha hatuko pekeetu?” Louise aliuliza huku ametoa macho, “ndio maana yake hiyo, na inavyoonekana hawa watu si wa kawaida” alijibu Latifa.
“hapa hapatufai tena itabidi tuhame” Louise aliongea kwa msisitizo.
“tusubiri pakuche kwanza tuangalie hali ikoje huko nje” niliongea na wote wawili wakakubaliana na mimi. Ila hakuna hata mmoja aliepata lepe la usingiz, kwanza kutokana na hofu, pili ni kwamba tulikuwa tumelala muda mrefu hivyo usingizi wenyewe ukagoma kuja. Palikucha na kwa umakini wa hali ya juu tulitoka kwenye kichaka chetu kama visungura hivi, tuliwakuta baadhi ya wenzetu wakilia na tulipowauliza kwanini wanalia. Wakasema kuwa kuna wengine wamechukuliwa na watu wasijulikana. Ilibid tutane wote ili tujue tumebakia wangapi, na ukweli kwamb wenzetu tisa walikuwa hawapo.
“huu mtihani mkubwa” nilijisemea moyoni, wakati tukiendelea kujadili nini tufanye. Kwa mbali nilisikia kama mlio wa gari. “Louise unausikia huo mlio wa gari” nilimuuliza ili kuthibitisha, “shit! huo ni mlio wa gari tena kubwa” Louise alinijibu. “itabidi kwanza tujue hawa watu ni wa aina gani” nilisema kwa nguvu kidogo. “acha utani wewe” Louise aliongea, “kweli tena Louise bila kujua tunacheza na nani itakuwa vigumu sana kutoroka katika eneo hili” niliongea kwa msisitizo kuonesha kuwa sikukosea mwanzo.
“haya master plan tueleze tunafanyaje sasa” Latifa aliongea na Louise akacheka kidogo, “inabidi tupande hilo bonde, huenda juu tukapata mwanya mkubwa kulijua eneo hili na kila kitu chake” nilitoa wazo ambalo Louise aliliongea kwa tena kwa lugha tatu tofauti ambazo zilikuwa kiingereza, kijerumani na kifaransa. Hapo wale wengine waliguna kidogo na hiyo ilikuwa ishara kuwa wamelielewa. Mmoja wao aliongea kwa jambo kwa kifaransa, Louise alinigeukia na kunambia “anasema ni wazo zuri lakini ni hatari pia, ila kama litapita basi yeye amejitolea kuwemo miongoni mwa watakaopnada hilo bonde”
Tuliendelea kujadiliana huku Louise akinisaidia kuwatafsiria wale ambao hawanielewi, mwisho tulifikia lengo moja tu kuwa watoke vijana watatu miongoni mwetu wapande lile bonde. Nilijitolea mimi, Louise na yule jamaa mwengine ambae aliitwa Akinola. Alikuwa ni mtu wa Nigeria, tuliwaaga wenzetu na kuanza safari. tulitembea mpaka kwenye bonde kabisa na kuanza kupanda. Kwa kweli haikuwa kazi rahisi hata kidogo na mara kadhaa tlikosea kuteleza na kuangulka, hata hivyo tulipiga moyo konde na kuendelea kupanda.
Ilituchukua takribani masaa matatu mpaka kufika juu huku tukipumzika mara nne njiani, tulitafuta sehemu na kujificha ili tupumzike. Maana ilikuwa balaa si dogo mpaka kufika juu, kama ingelikuwa si kupigania maisha yangu naapa kwa Mungu ningeishia njiani. Baada ya kupata mapumziko kama ya dakika kumi hivi, tuliinuka na kuanza kusonga mbele. Macho yalitutoka baada kuona mahoteli makubwa upande wa pili wa kisiwa hicho. “yaani sisi tunapigika huku, tunaishi kama ngedere kwa kushindia matunda. Lakini upande wa pili wa kisiwa hicho hicho kuna watu wanaponda starahe” nilijisema huku nikiuma meno. Tuliendelea kusonga mbele kwa kuufata mto huo unapotoka lakini tukiwa makini sana tusije tukakamatwa. Kwa mbali tulianza kusikia miguno lakini hakuwa ya kawaida maana yote ilikuwa ya kiume. iliidi tusogee karibu zaidi ili tujue kitu gani kinaendela, La haula tulimuona mzungu mmoja akiwa anamuingilia kijana tena wakiume. Alikuwa amemfunga kamba katika mti kiasi cha kushindwa kujitetea, nilijikuta hasira zikianza kunipanda hasa pale nilipogundua kuwa yule mzungu ndio yule mpumbavu alienifanyia mchongo wa kuingia katika meli yao. Nilinyata kama simbi na kuokota gongo kubwa.
Bila kusita nilipomkaribia, niliinua gongo juu na kumsindika nalo la kichwa. Alipigwa ukwenzi mara moja tu na kabla hajakaa sawa nikamtwanga la pili na kuendelea kumtandika magongo ya kichwa bila huruma hata kidogo. Mwisho Louise alilishika gongo na kunambia basi maana tayari alikuwa kashakufa, tulimfungua yule kijana lakini kwa aibu aliinuka kukimbilia gogo lenye ncha kali na kujichoma. Iliniuma sana kuona kijana mwenzangu kama yule amejiuwa lakini angefanyaje na ndivyo akili yake ilivyomtuma ili kueouka aibu. Wakati tukiendelea kushangaa eneo hilo, tulianza kusika mivumo ya gari ikija upande wetu.
Haraka tulitafuta sehem ya kujificha kwa usalama wetu, lilipita gari moja kubwa kama yale yanayobeba petroli. Ilisimama mbali kidogo na tulipo sisi lakini tulifankiwa kusikia walichokuwa wanakiongea, “hii kemikali ni sumu na endapo mtu yoyote atakunywa haya maji baada kutia kemikali hii basi atakufa” nilisikia vizuri sana. Hapo akili yangu ikawa inamuwaza Latifa tu, nilijikuta nikichomoka kama mshale huku wenzangu wakinifata nyuma kwa lwengo la kunizuia kwa maana ilikuwa ni vigumu kufikisha ujumbe huo kwa wengine. Kwasababu hata nikifika huko chini basi watakuwa tayari wameshakufa kwa sababu tulikuwa tukinywa sana.
Jambo ambalo hawakulijua wenzangu ni kwamba, sikuwa na mpango wa kushuka bonde hilo kama nilivyopanda. Nilipofika karibu na maporomoka, niliruka tu bila hata kufikiria huko chini ntakutana na nini. Nilichoma kwenye maji na nilipoibuka tu nilianza kupiga kelele watu watoke kwenye maji. Sekunde kadhaa baadae alichoma Louise na Akinola, nao pia walipoibuka walipiga kelele watu watoke kwenye maji.
Baada wote kutoka kwenye maji, Louise alitupa ishara kuwa tuondoke eneo hilo haraka sana maana palikuwa si salama tena hata kwa dakika moja. Tuliongozana na kuzama msituni zaidi kwa lengo la kuokoa maisha yetu, tulikuwa tukikimbia tu bila kufata njia maalum. Mara kadhaaa baadhi yetu tulijikwaa lakini tuliokotana na kuendelea na safari huku tukihakikisha hatumuachi mtu nyuma. Tuliendelea kukimbia bila kusimama kwa muda kama wa nusu saa hivi, “jamani tupumzike kidogo” aliongea mschana mmoja huku akisogea kwenye mti na kuegemea.
“Jamani inatosha tumekimbia sana na wenginie wamechoka sana” aliongea Akinola, “hakuna shida, tutapumzika hapa kwa muda kisha tutaendelea na safari” aliongea Louise na hapo karibu kundi zima tukakaa chini. “Tuelezeni basi mumekutana na nini huko juu na kutufanya tukimbia kama panya darini wakimkimbia paka” aliongea mtu mmoja. “Nyine acheni tu tulichokikuta huko ni hatari kabisa” niliongea kwa kiingereza ili kila mtu anielewe japo sikuwa nikikijua vizuri. Wala sikuogopa kwasababu hapo walikuwepo wengine ambao walikuwa wakiongea kingereza kibovu kuliko mimi.
“Yaani tumejitahidi kutoroka kwenye ile meli tukiamini ndio salama yetu lakini haikuwa hivyo. Inaonekana hapa kisiwani ndipo tulipokuwa tunaletwa kwa ajili ya kutumika kama vyombo vya starehe. Upande wa pili wa kisiwa hichi kuna mahoteli makubwa sana tena ya kifahari kuliko tunavyofikiria. Yaani hawa jamaa wanazunguka katika nchi masikini na kutuchota watu kama sisi ambao tunajaribu kukimbia matatizo. Wanatudanganya eti watatufikisha nchi za magaharibi huku wakitupa matumaini yasiopingika. Lakini ukweli ni kwamba wanatuchukua kilaini sana na kuja kutfanya watumwa wa ngono huku katika kisiwa hichi” nilimaliza kuongea na kuwaangalia wenzangu. Wote waliokuwepo hapo walikuwa wamejiinamia na kujiona wajinga wa hali ya juu.
“Lakini tukikaa pamoja na kusaidiana tunaweza tukaondoka hapa kisiwani” aliongea Louise na kuwa kama alirudisha uhai katika moto ulianza kuzima. Kila mtu alianza kunong’ona na mtu aliekaribu nae huku wakionekana kubadilishana mawazo. Wakati kila mtu akiwaza lake, ghafla Louise alishtuka na kulaza sikio lake la kulia kwenye ardhi. Hakuishia hapo tu, alichota tope kidogo mkononi na kuliramba kisha akawa kama anasikilizia utamu fulani hivi.
“Shit! Adam hii sehemu si nzuri kabisa” aliongea hukua akisimama na kuanza kuangaza huku na kule.
“kivipi mbona sikuelewi Louise” niliuliza, “hii njia inavyoonekana kuna myama mkali anapita mara kwa mara” alijibu huku akizidi kuwa makini. Kwa kweli huyu jamaa alikua na kipaji cha uwindaji, mimi naweza sema yeye mwenyewe alikuwa kama mnyama katika kushtukia mambo. Aliinua kichwa na kuangalia miti iliotuzunguka, alionekana kama kupiga mahesabu yake bila kupepesa macho.
“Jamani kwa mazingira haya tumeumia” aliongea na kukata majani kadhaa kisha akauarusha juu kuangalia muelekeo wa upepo unapuliza wapi.
“Adam nahisi mnyama anaepita njia hii ni jamii ya paka wa kubwa” aliongea huku akisogea kwenye mti na kuangalia kwa makini.
“Na kama ni jamii ya paka wa kubwa, huenda akawa chui mweusi au chui mwenye mistari maana ndio mazingira yao haya” niliongea bila kutarajia. Kilichonifanya niongee hivyo ni baada ya kukumbuka filamu fulani hivi inaitwa apocalipto au vijana walikuwa wanaiita filamu ya Ronaldinho wa msituni.
“Hapana chui mwenye mistari hawezi kusihi katika msitu huu ndani ya kisiwa kama hichi” Louise aliongea huku akirudi nyuma kwa woga kidogo. Hapo wenzetu wote walikuwa wakituangalia bila kujua nini kinaendelea maana tulikuwa tunaongea Kiswahili.
“unataka kunambia hapa anapita chui mweusi au” niliongea huku nikimeza funda kubwa la mate.
“ndio maana yake na kwa kukadiria hivi sasa kunaelekea jioni, kutokana na upepo unavyo vuma. Huyu kiumbe atakuwa anarudi kutoka mawindoni muda si mrefu” Louise aliongea.
“umejuaje” niliuliza sasa wasiwasi wangu ukiwa wazi,
“kawaida ya wanyama wanamna hii mara zote hutembea kupingana na upepo, hiyo inawasaidia harufu yao kutohisika na wanyama wengine” alijibu.
Kutokana na nilivyomuangalia kwa haraka nikagundua kuwa alikuwa akijipanga kukimbia, niliwageukia wengine na kuwaonesha ishara kuwa wakimbie lakini kimya kimya sana. Nilipogeuka mbele Louise alipita pembeni yangu kwa kasi ya hali ya juu sana. Bil kuchelewa nilimshika mkono Latifa na kuanza kutimuka. Hapa sasa ilikuwa si kuwakimbia watu bali ni kuokoa maisha yetu, nyuma yangu vilifuata vishindo vilivyoandama na kelele za woga. Nilichokifanya ni kukaza mkono wangu niliomshika Latifa na kuongeza mwendo. Mbele yangu alikuwa Louise ambae alikimbia kadiri miguu yake ilivyotoa ushirikiano.
Wakati tukiendelea kukata mbuga tulisikia ukwenzi mzito uliofuatiwa na ungurumo mzito sana. Hapo nilielewa kuwa tayari kuna mmoja wetu kashakamatwa na kiumbe hicho kilichokuwa nyuma yetu. Ungurumo ule ulikuwa ni kama gia kwa Latifa ambae alinichia mkono na kunipita kwa kasi hali ya juu sana, na mimi sikubaki nyuma niliongeza mwendo hasa ukizingatia sasa nimekuwa mwepesi zaid. Louise alikibia mpaka sehemu yenye mlima wa mawe na kuanza kupanda, Latifa nae alifuata huku mimi nikiunga mkondo huo. Nyuma yangu nilisikia pumzi nzito na kunifanya niongeze kasi ya kupanda mlima huo.
Tulipofika juu Louise alisimama ghafla na kumzuia Latifa ambae alionekana kukosa breki kabisa, mimi niliwapita kidogo na kusimama kwa mbele. Nilipogeuka nyuma nilimuona mschana mmoja akimalizia kupanda mlima huo. “Hapa tutakuwa salama, hawezi kutufata huku” Louise aliongea na kukaa kitako. “kumbe wewe ndo ulikuwa nyuma yangu” nilimwambia yule mschana huku nikicheka kidogo. “ndio” alijibu, “mi nilidhani ni yule kiumbe ndio maana nilikuwa nakaza mwendo tu. Tulipoteana na wengine na wala hatukujua hatma yao ilikuwa nini, tulibakia wanne tu yaani mimi, Louise, Latifa na yule mwanadada aliejitambulisha kwa jina la Linda. Tulibaki kimya tunatazama kwa muda huku kila mtu akihema kama farasi aliesafiri masafa marefu. “Sasa tunaganyaje” aliuliza Latifa, “hakuna cha kufanya zaidi ya kutafuta sehemu ya kujificha kwa muda kabla kiza hakijachanganya” nilijibu. “Eneo hili halina hata maji, inabidi tutafute sehemu iliokaribu na chanzo cha maji” aliongea Louise akijikaza na kusimama. “Ah bora tupumzike tu, kesho ndio tutaanza kusaka sehemu yenye chanzo cha maji” nilongea kwa uvivu sana. Tulibishana sana ila mwisho alikubali tutafute sehemu ya kulala, siku ya pili ndio tutaanza safari.
Tulitembea kwa nusu saa mpaka kufika sehemu ambayo tulihisi ni salama kwa kuupitisha usiku. Sehemu hiyo ilikuwa na majani makubwa sana kiasi cha kutoonekana kirahisi hata kama mtu angetokea ghafla. Louise alifanya mandingo yake ya kukunja majani hayo na kufanikiwa kutengeza vibanda viwili vidogo. Kimoja kilikuwa kwa ajili ya waschana na kimoja kwa ajili yetu sisi wavulana, tulikaa nje ya vibanda hivyo kwa muda huku tukipiga soga za hapa na pale. Tulifanya hivo ili kujaribu kuutoa woga uliokuwa umejirundika ndani ya mioyo yetu.
Tuliongea sana mpaka tukaanza kusinzia, hapo sasa kila mtu aliingia kwenye kibanda kinachomuhusu kwaajili ya kuupitishwa usiku huo ambao ndani yake ulikosa amani kabisa. Wakati tukiwa tumejilaza mimi na Louise, tulisikia kibanda chetu kikitiswa. Louise alinipa ishara nitulie tuli kama maji mtungini,
“jamani nyie mbona hamuitiki” tulisikia sauti ya Latifa. Kwa pamoja tukashusha pumzi kisha tukatoka.
“Mnataka nini si mkalale” niliongea kwa uvivu kidogo, “sisi tunaogopa kulala pekeetu” aliongea Latifa huku akionesha wazi alikuwa akitetemeka.
“Sasa tunafanyaje na kibanda kimoja hatutoshi sote” aliongea Louise akiwa ameshangaa kidogo.
“Kama vipi mimi ntalala na Latifa na wewe lala na Linda” niliropokwa tu bila hata kufikiria maana usingizi ulikuwa umenishika vilivyo.
“Bora hivyo” Linda aliniunga mkono, basi hatukuwa na jingine la kufanya. Louise aliingia kwenye kibanda kimoja pamoja na Linda na mimi nikalala na Latifa. Sikujua huko kwa mwenzangu mambo yameendaje lakini kwangu mambo yalikuwa magumu kuliko nilivyotegemea.
“Wewe si ulale huko na mimi huku” niliongea baada kuhisi nimeguswa mgongo,
“Adam mimi naogopa sana kwa kweli, kama ungekuwa shuka basi ningejifunika” aliongea Latifa huku akizidi kujisogeza kwangu.
“Sasa wewe unaogopa nini wakati hapa tumejiridhisha pako salama kupumzikia” niliongea huku nikijaribu kumsukuma kwa sababu alikuwa tayari kashanibana sana.
“Adam tafadhali bwana usinisukume, si nimeshaakwambia naogopa” aliongea Latifa huku akiishika mikono yangu nisiendelee kumsukuma. Bila kutarajia aliitanua mikono yangu na kurudi nyuma kwa nguvu kisha akauzungusha mkono wangu na kuulaza tumboni kwake. Hapo sasa tulikuwa tumegusana kabisa, niliona hakuna haja ya kuendelea kubishana nae wakati hapo na mimi ningepata faida ya joto. Nilichokifanya ni kuupenyeza mkono wangu kwa chini na kuukutanisha na mkono wangu ambao ulikuwa tumboni kwake. Kila mtu alifunga macho kwaajili ya kulala, kutokana na uchovu hazikupita dakika nyingi mimi nikalala.
Usingizi huo uliambatana na vijindoto vitamu vitamu na vya kufurahisha sana, na hiyo ilitokana na joto liliyokana na kugusana kwa miili yetu. Nilikuja kushtuka baada kupigwa na mwangaza wa jua usoni. Nilimsogeza Latifa pembeni ambae bado alionekana yupo katika ulimwengu mwingine kabisa. Nilitoka kwenye sehemu niliolala na kujinyoosha kidogo, “Louise, Louise pamekucha mtu wangu” niliita na baada ya sekunde kadha alitoka. Alionekana ni mwenye kuchoka sana “vipi jamaa yangu mbona mapema sana” aliniuliza. “Sasa ulitaka tukae hapa mpaka saa ngapi wakati unaju kabisa bila shaka tutakuwa tunatafutwa” nilimjibu,
“basi sawa tuwaamshe hawa waschana halafu tuondoke eneo hili”. Niliingia nilipolala na kuamsha Latifa, alikuwa hataki kabisa kuamka lakini nilimkomalia mpaka akaamka. Tulitoka na kuwakuta kina Louise na Linda wakitusbiri, baada kapigwa na jua kidogo tulianza safari ya kuelekea tusipopajua. Tulitembea kwa muda mrefu sana mapaka tukafika sehemu ambayo tulihisi itakuwa salama kwa kupumzika kabla ya kuendelea na safari.
“Jamani mimi nina njaa sana” Linda alilalamika, “hata sisi tunanjaa lakini hapa tulipo hatuwezi pata chakula” nilimjibu huku nikishika tumbo langu ambalo lilikuwa linakoroma kama paka.
“Tukifanikiwa kufika sehemu yenye maji huenda tukapata na matunda ya kula” Louise aliongea, wote tulikubaliana nae japo njaa ilikuwa ikitula ndani kwa ndani. Baada ya mapumziko mafupi safari iliendelea, tulitembea karibu siku nzima huku mara kadhaa tukipumzika.
“Jamani naona kama maporomoko ya maji kwa mbali” Louise aliongea. Wote tuliinuka na kuangalia na bila kuuliza kila mtu alianza kutimua kuelekea kwenye maporomoko.
Tulikimbia kwa muda kidogo mpaka tukafika sehemu hiyo, mimi wala sikusimama nilipitiliza mpaka kwenye maji na kuanza kunywa. Nilikunywa mpaka niliporidhika ndio nikapumua, baada ya hapo niligeuka na kuingalia sehemu hiyo. Nilichogundua kuwa sehemu hiyo ilikuwa ni vigumu mtu kuiona akiwa karibu kutokana na kuzungukwa na miti miti mirefu sana. Miti hio ilikuwa na matunda ambayo wala sikuwahi kula hata siku moja. Niliokota jiwe na kurusha mara kadhaa, nilifanikiwa kupata matunda na kuanza kula.
Yaani tulikuwa tukigombania matunda hayo utasema yalikuwa dhahabu, yaani mtu anakula hili akimuona mwenzake anakula jingine. Anaacha lile analo kula na kunyang’anyiana lile jingine. Ama kweli aliesema
“njaa mwanaume hajakosea hata kidogo, wakati wengine wanaendelea kula. Mimi au Louise mmoja wetu aliangua mengine. Tulikula mpaka mwisho tukawa tunayaangalia tu matunda ambayo tulikuwa tumeyazunguka.
“Sasa afadhali” nilisema huku nikiegemea mti ulikuwa nyuma yangu.
“Tumepotezana na wenzetu wote na hatujui wako katika hali gani” Latifa alioengea baada ya kushiba.
“Hilo lishatokea na tunachotakiwa kufanya saa hivi ni kuhakikisha tunakaa pamoja mpaka pale tutakapo pata msaada” Louise aliongea.
“Sasa mkandarasi vipi mpango wa kulala” nilimuuliza kiutani. “Ahaa hakuna shida subiri kidogo chakula kishuke ndio tuanze kazi” alijibu huku akipapasa tumbo lake.
Tulikaa kwa muda tukiongea huku tukisaidia na mwanga hafifu kwa mwezi kutokana na kiza kilishaachanganya.
“Muda wa kutengeza vibanda vya kulala” Louise aliongea na kuinuka lakini ghafla alishika kichwa.
“Kuna nini tena mbona unahika kichwa” nilimuuliza, “sasa unadhani tuanakataje miti ya kutengezea na miti yenyewe minene kweli kweli” alinijibu na kunifanya na mimi kushika kichwa pia.
“Kwa nini tusitafute ilianguka tu” nilitoa wazo, “hilo wazo zuri lakini pia ina matatizo yake” alinijibu.
“Matatizo gani” niliuliza, “vijidudu, si unajua imeshakaa chini na mengine ishakaa sana na wadudu washaanza kujenga nyumba zao”. Nilikaa kidogo kidogo nikawa natafakari huku nikiangaza huku na huko, nilijikuta nikitabamua bila kutaka. “Mbona unacheka mwenzetu” aliuliza Latifa, “unajua nimeona miti ambayo itatusaidia kujengea” nilijibu. “Mti gani huo” Louise aliuliza, “ni hio minazi” nilijibu huku nikisogelea mnazi uliokaribu kabisa. Haukuwa mrefu sana kiasi cha kutishia amani kuupanda, nilipanda mpaka juu na kuanza kushindana na makuti yaliojishilikialia vizuri katika mti huo. Mara kadhaa nilikosea kuanguka lakini hilo wala halikuniogopesha kabisa. Baada kungo’a makuti kadhaa nilishuka na kupanda mnazi mwngine mpaka pale nilipohakikisha makuti yametosha. Unajua kitu kingine ambacho nimejifunza kipindi cha uvuvi na kusuka makuti na kutengeneza sehemu ya muda mfupi ya kuishi. Kwa utashi nilokuwa nao juu ya sanaa ya kucheza na makuti nilifanikiwa kujenga vijisehemu ambavyo tungeweza kuupitisha usiku huo mpaka sikui inayofuata. Kutokana na uchofu safari ndefu tuliokuwa nayo tulipoweka tu vichwa chini tulipitiwa na usingizi mzito.
Siku ya pili mapema tulianza kazi ya kutafuta miti ya kujengea, japo tulikuwa wageni eneo hilo lakini kwasababu tulikuwa na Louise kazi haikuwa ngumu. Tulipata miti ya kutosha ya kujengea na tukaanza kazi, tulijenga kwa kasi sana maana usiku ukiingia ni shida. Kulikuwa na baridi kupita malelezo, tulufanikiwa kumaliza mapema tu. Tulipohakikisha vibanda hivyo vimesimama na vinafaa kuishi kwa binaadamu tulipongezana sana.
“Jamani kwa sasa itabidi tuzoe mazingira kwanza maana kurudi ufukweni ni kujitafutia kifo tu” niliongea wakati tuna tunapata kula. Usije ukadhani ni kula ipi, tulikuwa tunakula matunda mwitu tu.
“Ni kweli kabisa, kwa sasa itabidi tukae huku, baada ya muda kupita ndio tutarejea ufukweni kuangalia uwezekano wa kurudi uraiani” Louise aliniunga mkono.
“Pia maisha hapa hayatokuwa magumu kwa sababu tunapata kila kitu, matunda na maji na ndivyo tegemezi letu kwa sasa maana hata kuwasha moto ni hatari” aliendelea kuongea. Tuliendelea kupiga domo, kwa muda tulisahahu kabisa kama tupo katika wakati mgumu sana wa maisha.
Kasheshe ilikuwa kwenye kuoga sasa, sio kwamba maji yalikuwa hayatoshi. Laa, japo kulikuwa na maporomoko ya maji lakini hapakuwa na sehemu kubw sana. Hivyo ulipoika wakati wa kuoga kila mtu alikuwa anaona aibu kuvua nguo mbele ya mwenzake. Kutokana na hilo ilibidi sisi wanaume tuingia vibandani ili kuwaachia wanawake waoge kisha ndio tuende sisi. Si unajua kuoga ya wanawake, wanaoga utadhani hiyo ndio mara yao ya mwisho kuoga. Walipomaliza wao ndio tukaingia mimi na Louise, dakika kadhaa tu tulikuwa tumemaliza. Baada ya hapo tulikaa sehemu na kuanza kuongea mawili matatu. Kiza kilianza kuingia hivyo tulipata chakula cha usiku na kila mtu akaingia kwenye kibanda chake kwa ajili ya kupisha usiku huo ulioandamwa na rasha rasha za mvua. “Hivi tunalalaje” Latifa aliniuliza, “ah kama kawaida tunalala mzungu wa nne” nilimjibu kisha nikageuka upande wangu na kujilaza. “Adam mwenzio nasikia baridi” kabla hata sijafumba macho nilimsikia Latifa akiongea, “ah na huku hata blanket” nilimjibu bila kugeuka. Ghafla akaniwasha kofi zito, “sasa mbona umenipiga” niliongea huku nageuka. “Mimi nakwambia kitu cha maana wewe unadhani masihara” aliongea kwa sauti iliojaa deko. “Ah sasa mimi nakusaidi..” kabla sijamaliza hata kuongea, nilishangaa kashanivamia. Wakati nataka kumtoa aliniwahi mikono na hapo akasogeza midomo yake laini na kukutanisha na ya kwangu. Hapo mtoto wa kiume nikaishiwa ujanja kabisa na kumpokea kwa mikono miwili. Naam na baridi niliisahau kabisa na ulimwengu nikahama na kuelekea ulimwengu wa huba uliojaa rasha rasha za upendo na kibaridi cha kukonga moyo. “Adam nakupenda sana” alininong’oneza maneno hayo wakati tukindelea na starehe yetu ambayo ni haramu kuifanya kabla ya ndoa. Bila kusita nilimuekea kidolo mdomo kama ishara anyamaze na tuendelee na furaha yetu. Hata sijui saa ngapi nilipitiwa na usingizi baada ya kumaliza tendo hilo, nilikuja kushtuka asubuhi baada ya kupigwa na miale ya jua. Ndege pia walionekana kulifurahia jua hilo la asubuhi huku wakiimba kwa sauti zao walizoajaaliwa na muumba. Bado Latifa alikuwa maungoni mwangu na alionekana kuchoka sanan. Hivyo sikutaka hata kumuamsha na mimi nikafunga macho kwa ajili ya kuongeza masaa ya kulala. Maisha yetu yaliendelea hivyo huku tukiishi kama watu wa msituni, maana mwisho aibu ilitutoka kabisa. Kiufupi hatukua na tofauti na wanyama kwa sababu kuna wakati tulifanya mamabo ambayo hayaykustahiki kufanywa hadharani kabisa. Lakini tungefanyaje maana utu ulikuwa umeanza kutuvuka, hiyo ilitokana na kukaa ndanu ya pori hilo kwa muda mrefu huku tukihesabu masiku tu. Nakumbuka siku hiyo niliamka mapema kuliko wenzangu wote, nilitoka ndani ya kipanda changu na kuelekea mtoni kwa ajili kutimiza yale mahitaji yangu ya asubuhi. Wakati nikiwa katikati ya shughuli nilihisi kitu kama mwiba kikinichoma mgongoni na ghafla nilianguka na kupoteza fahamu na sikujua nini kilindelea. Wakati nikiwa katika usingizi mzito nilihisi kama watu wakipiga kelele huku wakicheza ngoma. Nilifumbua macho kivivu ili kuangalia ni kitu gani kinaendelea maana nilihisi niko ndotoni, lakini haikuwa hivyo kila nilichokiona mbele yangu kilikuwa kweli tupu. Niliona watu wengi wakicheza na kururuka huku wakizunguka moto mkubwa sana uliokuwa unawaka na kutoa mgurumo mkubwa kuonesha n jinisi gani ulivyokuwa mkali. “Kumbe ni kweli watu aina hii wapo duniani” nilijisemea mwenyewe huku nikiushidi kabisa moyo ukipiga kwa nguvu na kusababisha kifua changu kupanda na kushuka kwa kasi sana. Maisha yangu yote nilidhani kuwa jamii za watu wa aina hii haipo tena duniani. Najua utakuwa unajiuliza watu aina gani, usijali nitakwambia tu. Inasadikika zamani kulikuwa na watu wanaokula watu nyama za watu wengine, wanajulikana kama canibals. Kwa kweli siku hiyo nilidhani nimeshaageuka kitoweo maana kwa zile staili walizokuwa wakicheza, wazi kuwa walikuwa wakisheherekea kwa kupata kitoweo safi. Nilijaribu kuangaza huku na kule ili kutafuta kama kuna uoenyo wowote wa kutoroka hatari iliokuwa mbele yangu. Lakini hakukuwa na upenyo wowote ule, nilikuwa nimefungiwa ndani ya banda la miti. Nilivyogusa ilikuwa migumu kwelikweli, bila shoka kulikuwa hakuna uwezekano wa kutoroka eneo hilo. Nilihisi haja ndogo na kubwa zikitaka kutoka, tena zilitaka kutoka kwa wakati mmoja zote. Aisee japo kulikuwa na baridi usiku huo lakini kijasho chembamba kilikuwa kikinitoka usoni. Wakati nikiwa katika dimbwi la mawazo ghafla niliskia mlango ukifunguliwa, waliingia wanaume wanne walioshiba. Walinishika kwa nguvu na kunifunga kamba mikononi na miguui, kisha wakanibeba na kunitoa nje ya banda kisha wakachukua gongo na kulipitisha miguuni mpaka mikononi na kunining’iniza. Yaani kama umewahi kuona wawindaji wa zamani wanavomuweka mnyama baada ya kumuwinda basi ndivyo hivyo hivyo nilivyokuwa nimening’inizwa. Nilijaribu kuomba msamaha waniachie lakini ilikuwa ni kama napigia mbuzi gita maana hata lunga niliokuwa naongea walikuwa hawaifahamu. Walinipeleka mpaka karibu na moto na kuniweka pembeni kabisa na moto huo. Baada ya hapo walikaa pembeni na kuinamisha vichwa vyao, hapo sasa nilimuona mmoja kati yao akiinuka kutoka katika kiti kikumbwa kilichotandikwa ngozi ya chui, Mtu huyo alikuwa na kofia kubwa iliosukiwa manyoya fulani hivi ya ndege nisiemfahamu. Alikuwa na mwili mkubwa kidogo, alikuwa mweusi tii kama nyungu inayopikiwa kwa kuni, alikuwa ni kiongozi wao. Aliinua mikono juu na kuongea kitu kwa nguvu sana, wengine wote walishangilia kwa nguvu. Hasa wanawake waliruruka kwa nguvu na kufanya vifua vyao vilivyoshiba chakula cha mtoto kutii miruko hiyo na kwenda chini na juu. Yaani mimi wakati huo nilikuwa nalia kama mtoto mdogo alienyimwa ziwa na mamae. Kilio hicho kiliambatana na kamasi laini iliotengeza njia yake na kutoka nje ua nuymba yake. “Ee Mungu wangu, niokoe na hili janga. Najua kama nimekukosea lakini sistahili adhabu ya aina hii” nilijisemea moyoni huku nikianza kuomboleza kifo changu mwenyewe. Lakini ghafla wakati akiendelea kuongea kile nisichokielwa, mvua ilianza kunyesha tena ilikuwa kubwa sana na kila muda ulivyozidi kuenda ndivyo ilivyozidi kunyesha. Moto ulianza kufifia na mwisho ukazima kabisa na hapo nikaanza kusikia vilio. Yule aliekuwa kiongozi wao aliongea kitu kwa nguvu na hapo wale jamaa waliokuja kunitoa kule bandani wakanabeba na kunirudisha tena kule kule. Yaani kunyesha mvua ndio imekuwa pona pona yangu, kweli Mungu alikuwa amesikia kilio changu. Walinifungia na wao wakaondoka, wakati huo machozi yalishakata. Nilitafuta kona katika banda hilo na kujikunyata kama paka aliemwagiwa maji ya baridi. Hapo sasa ndio mawazo ya wenzangu yakanirudia kichwani, picha ya Latifa mschana niliempenda kuliko wanawake baada ya mamaangu mzazi ambae alikuwa tayari ni marehemu. Pia niliwakumbuka Louise na Linda, kwa kipindi kifupi ambacho nimekaa nao basi wameweza kutenengeza makazi yao ya kudumu. Nilihisi moyo wangu ukimenyeka na kukatika vipande, nikiwa katika hio usiingizi ulinipitia na kunihamisha ulimwengu. Nikiwa usnigizini nilianza kuota ndoto mbaya sana, ndoto ilionionesha nimekatwakatwa vipande na kupikwa vizuri. Watu walikuwa wakila nyama yangu huku wakifurahi sana, tena walikuwa wakicheka sana. Nilikurupuka kutoka usingizni huku nikihema kwa kasi sana, kitu cha kwanza nilijiangalia kama kuna kiungo chochote kimepungua mwilini mwangu maana ile ndoto haikuwa ya kawaida hata kidogo. Nilipoangaza vizuri tayari kulikuwa kumeshaanza kukucha, wanajamii wa sehemu hiyo walikuwa wakiendelea na shughuli zao za kawaida. Hawakunyesha kujali kabisa uwepo wangu eneo hilo isipokuwa watoto tu ndio walikuwa nje ya banda hilo wakinishangaa na kucheka cheka. Kiu ilikuwa imenibana sana na nilitani kuomba maji lakini nikawa sijui nianzie wapi maana ni sawa na kuku kuongea nabata kitu ambacho hakiwezekani. Mwisho nikaona bora ninyamaze tu maana sikuwa na jinsi. Siku hiyo iliisha kwa mtindo wa kushinda na kiu yangu, usiku uliingia na baridi siku hiyo ilizidi kuwa kali. Sitoweza kusahau nilivyoteseka na baridi siku hiyo, nilihisi ngozi kama inataka kuchanika. Wakati nikiwa nimejikunyata katika pembe moja wapo ya banda hilo, nilisikia mruzi wa sauti ya chini. Niliangaza kutafuta wapi mruzi huo ulipotoka, “Adam” nilisikia jina langu likiitwa. “Louise unafanya nini hapa” niliuliza baada ya kutambua kuwa sauti hiyo ni ya Louise. “Nimekuja kukutoa mtu wangu, marafiki hawaachani nyuma” Louise aliongea kwa sauti ya chini. “Hii miti migumu sana, na huwezi kuivunja kama huna silaha” nilimjibu huku nikisogea alipo. “Ah kuna sehemu itakuwa imelegea tu, tukiipata hiyo sehemu utaweza kutokan ndani ya banda” alinijibu na papo hapo tukaaanza kutafuta sehemu iliolegea. “Hii hapa nimeipata” nilimsikia Louise akiongea, nilsogea sehemu aliopo na tukasaidiana kuusogeza mtu uiolegea. Kweli nilpata nafasi ya kutoka, sijui nguvu niliizipata wapi. Yaani baada ya kutoka tu nilitoka mbio, hata kama kungekuwa na chui au simba au mnyama mwengine yeyote basi aingenikamata badala yake angeambulia vumbi tu. Louise alikuwa nyuma yangu na alijitahidi kuashikamana na mwendo wangu, kweli mlemavu kaponyoko meno ya simba usiulize kaponyokaje maana jibu utakalopewa halitokurdhisa kabisa. Baada ya kukimbia kwa muda mrefu hatimae nilisimama na huku nikihema kama mbwa, “duh, ndugu unakimbia” Louise aliniambia huku akiwa ameshika magoti kuashiria kuwa alikuwa amechoka sana. “Kina Latifa wako wapi” nilimuuliza, “nimwaacha kule tunapokaa” Louise alinijibu. “Ile sehemu haifai tena twende haraka tukawachukue tuondoke” nilimjibu nikijaribu kuchora ramani kichwani mwangu jinsi ya kufika kule tulipokuwa tunakaa. “Poa nifuate” Louise aliongea na kuongoza njia, tulitembea kwa muda kidogo. Latifa alikuwa amekaa karibu na mto, na aliponiona tu alikuja mbio kunikumbatia. Jamani kupendwa raha acheni kabisa, kwa sekunde kadhaa nilisahau kabisa kama nimechoropoka kifo. Tuliwaeleza hali halisi na wao waliubaliana na sisi na muda huo huo safari ikaanza. “Sasa tunaelekea wapi” Linda aliuliza, “tunaelekea ufukweni tujaribu bahati yeti kama itapita meli yeyote” nilimjibu huku nikikzana. “Hivi Louise umejuaje kama nilikuwa kule” lilinitoka swali hilo kinywani mwangu maana lilikuwa limenikaa sana. “Siku uliochukuliwa nilikuona, lakini nikashindwa kufanya chochote kutokana na wale watu walikuwa wengi. Hivyo nilianza kufatilia kwa siri mpaka ulipofikishwa kule kijijini. Hata hivyo ilibidi nitulie sikuwa na uwezo wa kufanya chochote kwa wakati ule. Nilirudini kambini kujipanga kwanza kabla kurudi tena kwa mara ya pili. Lakini usiku wake siku ile nikasikia ngoma, kwa kweli nilijua kabisa kuwa rafiki yangu unakuwa kitoweo. Lakini bado Mungu alikuwa upande wako, ile mvua ndio iliokuokoa.Nilirudi tena kijijini usku wa kuamkia leo na ndio nikafanikiwa kukutorisha” alimalizia hapo. “Yaani ndugu yangu nahisi kama usingeniokoa, saa hivi wale viumbe wangekuwa wanachezea matumbo yao huku wakimalizia kulamba mifupa yangu” niliongea na kuwafanya wote wacheke. “Kama si tamaa za kimaisha leo nisingekuwa hapa” nilijisemea moyoni, “Sikutegemea, ama kweli matatizo hayakimbiwi”. Tulitembea kwa muda mrefu sana mpaka miguu ikaanza kugoma kutoa ushirikiano, “jamani tupumzikeni maana hii miguu nahisi inawaka moto” Linda aliongea na kukaa kitako kabisa. “Sawa tutapumzika hapa kwa muda kisha tutaendelea na safari” Louise aliongea na yeye akakaa. Mimi sikukaa tu bali nililala kabisa maana mwili wangu wote ulikuwa unauma kama kidonda Kwa bahati nzuri pia tuliondoka na matunda kadhaa, hivyo tukapata matunda kidogo ili kuyafurahisha matumbo yalioonekana kunguruma kama gari kwa njaa. Baada ya mapumziko ya kutosha, safari ilianza tena. Tulitembea siku nzima huku tukipumzika mara kadhaa, usiku nao ulianza kuonyesha nguvu zake kwa kusambaza kiza chake. Bila hata kufikiria tayari kiza kilishaatanda kabisa, hatukua na kipanda wala nini. Na sehemu tulikuwepo ilikuwa tambarare kabisa, “leo tutalala hapa, na tuombe mungu tu mvua isinyeshe” Louise aliongea. “Hata ikinyesha ntalala hivyo hivyo” nilijikuta nikisema kwa nguvu na kukaa kwenye nyasi. Latifa alikaa pembeni yangu na kunishika mkono, “tuombe Mungu tuokoke na hili janga” aliongea kwa sauti ya chini. Nilimsogeza karibu na kumkumbatia kisha tukajilaza chini kwaajili ya kuupitisha usiku. Kutokana na uchovu sikuwaza kufanya chochote zaidi ya kulala tu maana nilikuwa nimechoka kuanzia akili mpaka kiungo kidogo chao mwilini. Japo kulikuwa na baridi sana lakini sikuihisi kabisa, yaani nililala kama mtu aliepuliziwa dawa ya usingizi. Wakati nikiwa usiningizini nilihisi mtu akinitingisha. “Adam amka kaka, kuna msala unakuja” japo nilikuwa usingizini lakini niliifahamu fika kuwa asuti hiyo ilikuwa ni ya Louise. Nilifungua macho kivivu na kuuliza, “mbona tunakatiashiana usingizi”. “Nasiki sauti za magari zinakuja upande huu” Louise aliongea kwa sauti ya chini, hapo sasa usingizi wote ukaniruka na kuinua masikio kama mbwa kusikiliza kama ni kweli. “Ni kweli kaka, waamshe hao tuondoke” niliongea huku nikisimama na kuanza kumuamsha Latifa. Louise nae alimuamsha Linda, walipoamka tuliwaonesha ishara watulie. “Kuna gari zinakuja upande huu, inabidi tuondoke sasa hivi” niliongea huku nikimshika Latifa mkono. Kwa mwendo wa haraka tulianza kutembea huku tukiwa makini sana, ghafla Linda alikaja mwiba na kutoa ukwenzi wa maumivu kabla Louise hajamuwahi. Lakini keki ilikuwa ishaingia mchuzi, maana tuliona taa za gari hizo zikija upande wetu. Gari hizo zilikuwa zinakuja kasi sana, huku mataa makali ya juu katika gari hizo zikimulika sehemu tulipo na kutufanya tuonekane vizuri zaidi. Ngoja nikueleze kitu ndugu msomaji, sifa yangu moja nzuri sana na nashukuru mungu kwa kunipa sifa kama hiyo, Mimi ni mwepesi sana wa kufanya maamuzi hasa nikishaona hatari inakuja. Kabla hata wenzangu hawajafikiria wafanye nini, niliukaza mkono wangu uliokuwa umeshika mkono wa Latifa na kuanza kuchapa ndala. Louise nae aliniunga akiwa kamshika Linda ambae alikuwa akilia kutokana na maumivu aliokuwa anayapata. “Simameni au tunafyatua risasi” tulisikia sauti hiyo lakini mimi sikuijali kabisa, niliendelea kuchanja mbuga tu. “Adam tusimame watatuua hawa watu” Latifa aliniongelesha wakati tunakimbia. “Mimi bora waniue kuliko kuniepeleka kule kambini kwao” niliongea kwa nguvu huku nikiendelea kuchana upepo. Wakati tunakimbia sikuwasikia kina Louise nyuma yangu, lakini hilo halikunifanya nisimame. Nilidhamiria kufanya maamuzi magumu sana ya kuendelea kutetea roho yangu. “Nyinyi ndio hamusikii, si ndio” nilisikia sauti ikiongea tena. “Wewe piga tu risasi lakini mimi sisimami” nilijisemea moyoni, lakini ghafla nilishangaa Latifa kuutoa mkono wake kwa nguvu jambo lililopelekea yeye kuanguka kutokana na kasi niliokuwa namvuta. Nilisimama ili kumrudia lakini nilimsikia akisema “Adam mimi siwezi tena kukimbia, nimechoka. Wewe endelea na safari”. Na nilipoangalia vizuri wale jamaa walikuwa washamkaribia sana, “ni mwendo wa maamuzi magumu tu” nilijisemea moyoni na kugeuka na kuanza kukimbia tena. “Adam jitahidi kidogo tu, msitu huo hapo mbele yako. Hiyo ndio salama yako” sauti yangu mwenyewe iliniongelesha na kunifanya nizidi kuchochea miguu. Najua utajiuliza kwanini nilikuwa nawaacha mbali, hiyo ilitokana na sehemu hiyo kuwa na miinuko na mashimo mengi sana kiasi kwamba ukiendesha gari kasi lazima utapinduka.
Nilifanikiwa kuingia msituni ndipo nikasimama kuvuta pumzi maana kifua kilikuwa kinawaka moto. Niliegemea kwenye mti huku nikihema kama chui alieukuza windo na kulikosa, kabla hata sijakaa sawa niliona miale ya taa ikija msituni. “Yule pale” nilimikia mmoja wo akisema, kabla hata sijafikiria nifanye nini ghafla nilisikia mlio wa risasi lakini haikunipa ilipiga kwenye mti. Akili yangu ikatuma taarifa miguuni kuwa ifanye kazi yake. Na bila kujishauri mara ya pili nilianza kutimuka tena, yaani kiukweli hasa sijui pumzi zile za kukimbia muda mrefu nilizitoa wapi.
“Wewe si ndio nunda sio” nilimsikia mtu akiongea kwa mbali,
“bora niliwe hata na mnyama kuliko kukamata na nyinyi mkanifanya shoga” nilijisemea na kuongeza mwendo. Wakati nazidi kuruka vihunzi na vituta, mashimo na mizizi ghafla nilishtuka nimekanyaga hewa na kuanza kuanguka. Kumbe nilikuwa nimefika mwisho wa bonde nililokuwa nakimbia, katika maisha yangu sijawahi kuanguka umbali kiasi kile. Nilitamani nitoke mbawa niruke lakini wapi, hata hivyo bahati ilikuwa kwangu. Maana chini kabisa kulikuwa kunapita mto, hivyo nilichoma ndani ya maji lakini kutokana na kasi niliofika nayo. Nilikwenda moja kwa moja mpaka chini kabisa na kupiga kichwa katika sakafu ya mto huyo japo haikuwa na mawe lakini nilikata mawasiliano na mwili mzima na kupoteza fahamu.
Nilikuja kushtuka nimo ndani ya kipanda, niliangaza pande zote kuangalia kama kuna mtu yeyote. Na nilipojaribu kusimama nilishindwa kutokana na kichwa kuuma kama kinachogongelewa msumari. Hivyo sikuwa na budi nilirudi tu chini na kuendelea kulala, wakatia natafakari niko wapi. Ghafla aliingia mwanaume mmoja mzee sana, sura yake likuwa ina michoro kadhaa. “Tobaa nimerudi kule kwa wale wanaokula nyama au” nilisemea moyoni, lakini hofu ilinitoka baada ya yule mzee kunisogelea pale nilipolala na kunishika kichwa. “Unajisikiaje kijana” nilishtuka aliponiuliza hivyo, tena cha ajabu sana aliniuliza kwa kiswahili.
“Hivi mimi naota ama vipi” niliongea kwa sauti kubwa kidogo mpaka yule mzee akanisikia, “hapana kijana wala huoti kila kitu unachokiona ni kweli” alinijibu na hapo nilithibitisha kuwa sioti. Baada ya hapo alitoka na nje kurejea baada ya dakika muda kidogo akiwa na bakuli mkononi. “Kunywa hii dawa itakusaidia kupunguza maumivu ya kichwa” alinikabidhi bakuli hilo na kuongea. Aisee sijawahi kuja dawa chungu kama ile tokea nizaliwe, ilikuwa chungu kiasi kwamba kila nlivykuwa nikipiga mbwewe uchungu niliuhisi mdomoni. Na kweli baada ya muda kupita kichwa kiliacha kuuma kabisa na hapo ndio nikapata uwezo wa kusimama na kutoka nje. Nilishangaa kukuta watu wengi wakinisubiri hapo nje. Yule mzee aliongea kwa lugha nisioifahamu, alipomaliza baadhi yao walinifuata na kunishika mkono na kunisogeza kwenye kiti kizuri kilichotengenezwa kwa ngozi ya chui mweusi. “Unawitwa nani?” mmoja wao aliniuliza akimaanisha naitwa nani, “Naitwa Adam” nilimjibu na hapo aliangua kicheko na kumfata yule mzee na kumwambia kitu. “Amekwambia nini” nilimuuliza, “anasema anataka umfundishe kiswahili” alinijibu huku akicheka. “Kijana ilikuwaje ukafika huku?” swali hilo lilifuata, “kwa kweli mzee wangu ni hadithi ndefu sana inayonifanya nijione mjinga na mpumbavu mwenye PHd, sikutegemea ila kwa kweli matatizo hayakimbiwi. Laiti kama ningeliridhika na kipato alichonijaalia Mungu leo nisingekuwa hapa” niliongea huku nikitiririkwa na machozi.
Nilimueleza kila kitu kilichonikuta mpaka nikafika pale, “kijana haya ndio maisha, usipofunzwa na mamayo basi utafunzwa na ulimwengu” alianza kwa methali hiyo. Ila kabla hajaendelea nilimkatisha kwa kumuuliza imekuwaje mpaka yeye akawa sehemu ile kwa wakati ule. “Mimi sikufika hapa kwa kutaka kuzamia kama wewe, miaka takribani thalathani ilopita nilikuwa mwanafunzi wa chuo cha Muhimbili. Nilikuwa nikisomea udaktari, hakika niliupenda sana hivyo nikawa nashiriki semina nyingi sana za ndani ya nchi na nje ya nchi. Siku moja nilipata bahati ya kushiriki katika uchunguzi maalum, nakumbuka kipindi hicho nilikuwa nachukua shahada ya uzamili.
Tulichaguliwa wanafunzi watatu kutoka Afrika Mashariki, tulisafirishwa mpaka nchini Marekani ambako tulipewa mafunzi kwa muda wa miezi mitatu kabla ya kuanza uchunguzi. Tulizunguka visiwa vingi sana kusaka miti mizuri ya kutenegezea dawa, na ndipo tukafika katika kisiwa hichi. Hapa ndipo tulipoupata mti tuliokuwa tunautafuta, na mimi ndie mtu wa kwanza kuugundua lakini kama unavyojuwa wenzetu hawataki wawe chini yetu. Hivyo walipanga mbinu za kutuuwa, mbinu hiyo ilifanikiwa kwa wenzangu wawili lakini mimi nilifanikiwa kutoroka.
Baada ya hapo waliondoka kabisa kisiwani hapa na kuniacha nikiwa natanga tanga nisijue nini cha kufanya. Mwisho nilikata tamaa ya kabisa ya kurudi tena katika ulimwengu wa kawaida, hivyo nikaamua kuanzisha makazi yangu huku huku. Na kazi yangu kubwa ilikuwa n kutafuta miti shamba ambayo ni dawa. Baada ya miezi mingi sana kupita, siku moja wakati nazunguka msituni ndipo nakijikuta mikononi mwa jamii hii. Walinikamata na kunileta huku kijijini kwao, walikuwa na lengo la kuniua. Lakini kwa bahati nzuri au mbaya mtemi wao aliumwa ghafla na jitihada za kuokoa maisha yake ziligoma kabisa.
Sijui hata ujasiri nilitoa wapi lakini niliwaomba kwa lugha ya ishara kwa sababu tulikuwa hatufahamiani lugha ya maongezi kuwa ninia uwezo wa kumtibu kiongozi wao. Walinikubalia na kweli kwa elimu alionipatia mungu nilifanikiwa kujua tatizo na kufanikia kumtibu. Alipopona tu alinifanya kuwa muuguzi mkuu wa jamii yao na kuniozesha binti yake. Walinifundisha tamaduni na miendendo ya maisha yao na tokea siku hiyo nikiwa miongoni mwao” alimaliza kunieleza mzee huyo. Muda wote nilibakia mdomo wazi huku nikiwa na maswali kadhaa kichwani.
“Hivi huku upo kwa muda gani sasa” nilimuuliza, “huu ni mwaka wa thalathini na tatu sasa” alinijibu. Nilibaki nimekodoa macho kama mjusi aliebanwa na mlango, hapo ndio nikathibitisha ule msemo wa kimtaani “hakuna sehemu ambayo wabongo hawapo”. Msemo huo nilikuwa nikiusikia tu kwa vijana wenzangu lakini siku ndio siku niliothibitisha siku hiyo. “Samahani mzee wangu lakini sijakujua jina bado” nilimuuliza tena, “mimi naitwa Robert Augistino au wazee na wanafunzi wenzangu walipenda kuniita Robby” alinijibu huku akitabasamu.
Katika vitu ambavyo sikutegemea kukutana navyo katika masiha yangu, moja ni hii safari ya kwa obama iliobadilika na kuwa ya mwituni. Pili ni kukutana na mtanzania anaeishi miongoni mwa makabila yanayosadikika kutokuwepo tena duniani. Kutokana na hali yangu kutokuwa nzuri sana niliamua kukaa na jamii hiyo bila kuuliza njia ya kuondoka katika kisiwa hicho. Maisha ndani ya jamii hiyo hayakuwa magumu kabisa, watu wake walikuwa wakarimu tofauti na wale walionikamata mara iwa kwana kutaka kunifanya supu. Baada ya muda kidogo kupita ndio nikaanza kumuuliza Mzee Robert kama kuna uwezekano wa kuondoka kisiwani hapo. “Kijana kuondoka katika kisiwa hichi ni kama ndoto” alinipa jibu lilikuwa mwiba moyoni mwangu. “Lakini kuna boti upande wa pili wa kisiwa hiki japo sina uhakika kama ni nzima au mbovu. Boti hiyo kama itakuwa nzima ndio itakuwa njia pekee ya kutoroka hapa kisiwani” alinipa maelezo hayo kidogo yakarudisha matumaini. Kichwa changu kilianza kupiga mahesabu ya kutoroka, lakini kabla sijafika mbali katika mipango yangu niliwakumbuka wenzangu ambao sijui maisha yao yakoje huko walipopelekwa baada ya kukamatwa.